Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

X SEHEMU YA 6/10

   


X  

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA


WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 6 KATI YA 10


“Huyo na makamu wa raisi ni kma pete na kidole hafai muheshimiwa raisi”

“Kweli?”

“Ndio na tuna faili lake ni mtu mchafu sana, ana kampuni yake ya malori ya kubeba mafuta ana zaidi ya deni la kidi trilioni moja pointi nane hajalipa na alikuwa ana kingiwa kifua na makamu wa raisi aliye pita”

“Aisee kumbe watu wana madeni hivyo?”

“Ndio muheshimiwa raisi ndio maana tume kuomba uwe wewe. Simama na sisi sote tuta kuwa nyuma yako”

Nikashusha pumzi huku nikimtazama Judy usoni mwake na nina imani ana tamani kuniona hata leo hii nina kuwa raisi.

“Nawapa siku mbili, mutafakari nani wa kumuachia hichi kiti. Nani asimame kwenye hichi kiti ila kwa nini safari hii asisimame mwanamke”

“Mwanamke kuongoza hii nchi muheshimiwa raisi?”

“Ndio, wanawake wana uwezo na wana jua nini wanafanya. Na ninampendekeza madame Caro kwanza ni jasiri, mahiri na mpambanaji.”

“Ahaaa muheshimiwa raisi mimi sio mwana siasa na sija panga kabisa kuwa mgombea wa chama chochote na kama unavyo jua hatuna vyama sisi”

Madam Caro alijitetea.

“Una uwezo, una wajua maadui wa taifa, una jua taifa hili kinaga ubaga, wapi tuna feli na wapi tuna patia. Kwa pamoja tumuunge mkono madame Caro”

“Ni kweli muheshimiwa raisi tumuunge mkono”

“Au muna hitaji tupige kura ya siri kukuunga mkono”

“Muheshimiwa raisi hakuna haja ya kupiga kura. Mama yetu hapa ana uwezo na tuna jua kwamba ana uwezo huo. Basi kwa pamoja tumuunge mkono”

Sote tukapiga makofi kumpitisha madame Caro kuwa mgombea uraisi baada ya mdua wangu wa kuisha.

“Nchi ina hitaji mwana usalama. Kama uchumi tunao, kama ni silaha tunazo, hatuwezi kuja kuongozwa na tahira ambaye hata maswala ya silaha hawezi, hajui mlio wa hizi bunduki wala hajawahi kuingia uwanja wa vita. Tuna kuhitaji madame”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama madame Caro usoni mwake.

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz .EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

*********************************************************************

“Ila jamani kiti cha uraisi ni nafasi ya juu kabisa. Kuongoza taifa lenye nguvu kweli nita weza?”

“Mama ni mtu mmoja wa kipekee sana kwenye hii dunia. Mama hawezi kushindwa kuishi na mwanaye hata kwenye hali yoyote ile. Japo sijui kwa upande wa mama yangu na huwa nina jiuliza kwa nini alinitupa mtaroni na nikalelewa na kituo cha yatima. Ila nina uhakika wewe una weza madem. Timu yako hii ya watu ita kuwa pamoja nawe”

Nilizungumza kwa msisitizo na watu wote wakakaa kimya huku wakinitazama.

“Pole muheshimiwa”

“Pole ya?”

“Kutelekezwa na mama yako?”

“Aha nilisha sahau hayo ni mambo ya miaka ya nyuma na sijutii kufanyiwa hivyo na mtu aliye niweke tumboni miezi tisa. Labda alikuwa na sababu zake zilizo pelekea yeye kufanya hivyo, sisi wote hapa hatujui hivyo madame nafasi ni yako na sisi ndio wenye nchi. Uta ingia kwenye siasa na uta chagua watu wako wa kukulinda ambao una jua ni watu wako”

“Na utapendezea sana kuwa raisi madame”

“Kubali”

“Kubali madame Caro”

“Nipo na wewe madame kubali”

Watu wote kumi na mbili tuka muunga mkono madame Caro na akatoa jibu la kukubali na kilicho salia sasa hivi ni kuhakikisha kwamba ana ingia kwenye kinyang’anyiro cha uraisi. Majira ya saa kumi na moja asubuhi kikao hichi kikakamilika na viongozi hawa wakaanza kuondoka. Nikaongozana na madame Caro pamoja na Judy hadi ofisini kwangu.

“Muheshimiwa raisi una hatari sana wewe”

Madame Caro alizungumza.

“Kwa nini?”

“Yaani kunipendekeza kuwa raisi una jua hili swala ni gumu sana kwangu kulikubali”

Tukaka kwenye sofa zilizopo eneo hili.

“Kwa nini gumu?”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz .EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

*********************************************************************

Nilizungumza huku nikifungua vifungo vya koti langu la suti na nikakunja nne kumtazama madame Caro usoni mwake.

“Nchi hii ni kubwa muheshimiwa. Ina nguvu kweli jeshi na watu wengine wata ielewa kauli yangu?”

“Una jua mamlaka ya raisi ni sawa na mfalme au malikia?”

“Nalijua”

“Kauli ikisha tolewa kinacho fwata ni utendaji, asiye hitaji kufwata unacho kihitaji una mpiga chini tu. Tatizo lipo wapi”

“Ila madame nafasi ina kufaa kweli nina imani huto tuangusha wanawake wezako”

“Jamani daaayaani nawaza nitakavyo kuwa nina simama kwenye majukwaa ya kisiasa ikiwa sina ujuzi wowote wa kisiasa”

“Wiki mbili tu una weza kusoma siasa ukaielewa madame. Ach akuwa na woga, hadi kukupendekeza wewe nina imani nimechagua mwanamke wa shoka na sio mwanamke lege lege.”

Madame Caro akashusha pumzi na kukubaliana na tulicho kiamua.

“Sawa muheshimiwa raisi acha nikalifanyie kazi”

“Nashukuru”

Madame Caro akatoka ndani hapa na nikabaki na Judy.

“Judy una taka kuwa nani wewe baada ya mimi kuondoka?”

“Nahitaji niwe kwenye hicho kikosi cha X”

“Ila ni kikosi hatari?”

“Mkuu mikono yangu haijazoea kushika mwiko wala sufuria. Mikono yangu ime zoea kushika bunduki, vidole vyangu vimezoea kuvuta triga na kubadilisha magazine za bunduki. Hivyo nahitaji kuingia huko najua umetupiga rasha rasha ila nahitaji kuwa huko nikawa zaidi ya hapa”

“Sawa kikubwa nina imani uta kwenda kufanya na kuwa best na nina imani ukikata uta kuwa kiongozi wao”

“Nakuhakikishia sinto kuangusha kabisa”

“Nitahitaji na Gody naye kuingia huko ikiwezekana na Willy”

“Mmmm Willy ata weza kweli?”

“Ndio ata weza kwa maana mukienda muna kuwa wapya na muna anza moja”

“Mafunzo ni hapa hapa Tanzania au?”

“Mafunazo yapo ya ndani na nje hivyo jiandaeni tu”

“Sawa muheshimiwa raisi. Ila ninge penda kufahamu, baada ya kuachana na uraisi uta rudi serikalini au?”

Nikatingisha kichwa nikimaanisha hapana.

“Sihitaji kukuficha Judy nahitaji ujiandae kisaikolojia mapema maisha ya kuishi bila mimi. Najua ita tuumiza sisi sote kwa maana kuishia kama mtu na kaka yake tuliweza kulifaulu wa asilimia mia moja. Hivyo sinto kaa Tanzanai tena, nita hitaji kwenda sehemu ambayo nita sahau mambo yote ya nyuma na nita anza maisha mapya kama mtu wa kawaida na mtu wa kujifunza taratibu za nchi hiyo”

“Daaa!! Inaumiza sana, uta kwenda nchi gani?”

“Nchi yoyote ile ambayo nita amini nina weza kuaa ila nchi ambayo ni namba moja nina iwazia kwenda kuishi na Japani”

“Japani?”

“Yaa nina ijua vizuri ile nchi na muta kuja Japan kwenye mafunzo yenu ni lazima mupitie mafunzo ya kininja. Wala jamaa tulio kuja nao ni maninja wezangu. Hivyo mukija tuta pana nafasi na wasaa wa kukaa na kuonana tena ila sehemu sahiahi ya mimi kuishi mimi na mke wangu ni Japan”

Nilizungumza kwa sura ya upole na kumfanya Judy kukaa kwa unyonge na machozi yakaanza kumbubujika, hapa ndio nikaamini Judy ana mapenzi ya dhati ya kama ndugu kwangu mimi na kukaa mbali nami ni jambo ambalo lita muumiza kwa kipindi kirefu hadi kuja kukubaliana na hali halisi kwamba sipo tena upande wake wa kazi.


************************************************

“Usihuzunike Judy, kwenye maisha kuna wakati wa kuwa pamoja na kutengana sasa huu ni wakati wa sisi kutengana”

“Ina uma Eddy”

“Najua ni heri nipo hai je nikifa itakuwaje kwa upande wako?”

“Yaani ukifa haki ya Mungu na mimi nina weza kufa. Sijawahi kuwa na kaka, bosi bora kama wewe, kaka unaye mruhusu mdogo wako kukujua vizuri kuliko hata watu wengine. Ina niuma sana Eddy”

Judy alizungumza huku machozi yakizidi kumwagika. Taratibu nikanyanyuka, nikamnyanyua Judy na kumkumbatia na kumfanya azidi kulia kwa uchungu. Kilio cha Judy kikazidi kunipa simanzi kiasi kwamba nikatamani kubadilisha mawazo yangu ila kusema kweli siwezi kuishi Tanzania mara baada ya maisha yangu ya uraisi kuisha. Baada ya muda kidogo nikamuachia Judy, nikamfuta machozi mashvuni mwake kwa kutumia vidole vyangu.

“Mkuu naomba siku ya leo nikapumzike nyumbani”

“Hakuna shaka, una weza kupumzika hadi kesho kutwa”

“Nashukuru”

Judy akanitazama kwa masikitiko kisha akatoka ofisini kwangu. Kutokana tupo kwenye wiki ya maombolezo sikuona haja ya kukaa ofisini kwangu. Nikarudi nyumbani kwangu, nikamkuta Cauther akiwa sebleni pamoja na Maria mtoto wa raisi. Nikasalimiana nao kisha nikaa kwenye moja ya sofa.

“Mume wangu leo nina jisikia kutoka out nime choka sana kukaa humu ndani”

“Una taka kwenda wapi?”

“Sehemu yoyote tulivu nikatulize akili”

“Kuna mbuga nyingi za wanyama nina imani zime tulia sana. Una onaje ukaenda huko wifi?”

“Hapana nahitaji yaani sehemu ambayo ina milima mingi na mapori yaliyo tulia”

“Kuna milima ya Udzungwa wifi huko kume tulia sana”

“Mke wangu tuna miezi miwili na siku kadhaa kuwepo hapa mjengoni. Vumilia kwa maana ukihitaji kwenda huko, huwezi kwenda au hatuwezi kwenda kama tulivyo zoea kutembelea maeneo mbalimbali tukiwa na gari letu binafsi. Sasa hivi kwenda maeneo hayo ni lazima twende na walinzi pamoja na timu nzima. Hatuwezi kutembea sisi wenyewe jambo ambalo ni matumizi mabaya ya pesa za serikali”

“Sawa mume wangu”

“Dokta amekuja kukuona leo?”

“Bado ila ameniambia yupo njiani”

“Sawa, niandalie chai, ninywe nikapumzike kidogo kwa maana sija pata usingizi kabisa”

“Sawa mume wangu”

“Au pumzika, ngoja nilale kwanza kisha nikiamka ndio nile”

“Unge kula kwanza”

“No nikila nina weza kufanya mambo mengine. Atakaye kuja kuniulizia muambieni raisi amelala”

“Sawa”

Nikaingia chumbani, nikavua nguo zote na nikabaki na boksa. Nikajirusha kitandani huku nikihisi jinsi mwili wangu ulivyo choka kwani usiku nilikuwa na mambo mengi yaliyo chosha mwili wangu. Hazikuisha hata dakika tano Cauther akaingia ndani hapa, akaka pembeni yangu.

“Unajisikiaje?”

“Nime choka sana”

“Ngoja nikuafanyie masaji”

“Sawa mke mwangu”

Cauther akachukua kichupa cha mafuta maalumu kwa ajili ya kumfanyia mtu masaji. Nikalala kifudi fudi kisha taratibu akaanza kuuchua mgongo wangu, kuanzia kiunoni hadi mabegani.

“Nikanyage”

Nilizungumza kwa sauti ya uchovu na taratibu Cauther akapanda juu ya mgongo wangu na kuanza kunikanyaga kanyaga taratibu.

“Yaani ninge kuwa kibonge ningekuwa nimesha kumwaga utumbo”

“Hahaaa ndio maana nime kuchagua wewe, yaani hata ikitokea hatari nina kubeba na kukimbia nawe sasa kama ungekuwa ni kihonge sijui nakubebaje”

“Ila huyu mwanao amenifanya nime nenepa kiasi na nime kuwa mzito”

“Mazoezi yale madogo madogo ume acha kufanya?”

“Nina fanya ila uvivu muda mwengine mawazo ya hapa na pale”

Taratibu Cauther akashuka mgongoni mwangu na akalala pembeni yangu. Nikamfunua dera lake hadi eneo la tumboni mwake. Nikaanza kulipapasa tumbo lake ambalo tayari limesha kuwa na bado miezi michache tu ajifungue mtoto.

“Naamini mwanao ana furahia tumboni humu”

Cauther alizungumza huku akitabasamu.

“Yaa lazima afurahie kwa maana yupo kwenye tumbo la mama bora. Leo usiku nataka tukale chakula mtaani”

“Wapi?”

“Kwa kina Sudy pale Sinza hivyo usipike”

“Tena nilikuwa nime mis wale kuku wao”

“Mpigie simu Nadia na umuambie leo kuna mtoko huo ni lazima ata kuja”

“Sawa mume wangu kipenzi nina kupenda hapo. So tuna kwenda na walinzi?”

“Ndio hatuwezi kutoroka kwa maana nitakuwa nime vunja sheria. Sasa nikivunja sheria na lolote litakalo tokea basi itakuwa ni juu yangu”

“Ngoja nikuulize mume wangu najua mambo mengine ni ya siri na ya nchi sipaswi kuyafahamu ila samahani?”

“No una haki ya kujua wewe ni mke wangu, japo kweli kuna vitu vya nchi ni siri”

“Kwani raisi hawezi kuishi maisha ya kawaida na kutembea pasipo kuongozana na walinzi?”

“Hawez. Labda nikufafanulie. Raisi ni mtu muhimu sana kwenye nchi yoyote inayo ongozwa kwa mfumo wa maraisi kuliko mtu yoyote ndani ya nchi. Uhai wa raisi ni wa kwanza na muhimu kuliko hata walinzi wake ndio maana mlinzi wa raisi yupo tayari kufa kwa ajili ya kuokoa maisha ya raisi wake”

“Kwa nini ina kuwa hivyo. Inaonyesha tuna wasujudia?”

“Hatuwasujudii au hasujudiwi ila raisi ni mtu ambaye akitamka neno lake lina angaliwa kuliko la mtu yoyote. Mfano mmoja ni ule nilio sema kwamba tuta omboleza kwa wiki moja msiba wa raisi aliye pita. Maofisi ya serikali yote yamefungwa na hayakufanya kazi kasoro jeshi na hospitali, ila watu wengine wote walikuwa majumbani. Hivyo hivyo pia maofisi ya watu binafsi kadhaa walifunga ila ile siku ya msiba haikuwa siku ya kufanya kazi kwa nchi nzima. Umeona kauli yangu jinsi ilivyo kuwa na nguvu kubwa katika jamii. Laiti ningekuwa mtu wa kawaida hata ningesema hivyo kusinge kuwa na wakunisikiliza.”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz .EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

*********************************************************************

“Ahaa kwa hiyo raisi ni kama baba kwenye familia”

“Ewalaa, baba akisema leo makande wote tuna kula makande, leo ubwaba wote tuna kula ubwabwa. Ila mama anaweza akasema leo tuna kula chipsi ila baba akasema tuna kula ugali, basi hakuto pikwa chipsi na ugali ila kutapikwa ugali peke yake”

“Mmm ila mimi huwa najisikia kama mtu wa ajabu pale ninapo ona watu wamenizingira zingira. Una jua nilisha zoea maisha kama nikitaka kwenda Kariakoo naingia ndani ya gari huyo naishia zangu kariakoo ila sasa hivi yaani hata mtu akitaka kunisalimia lazima walinzi wawili wasimame mbele yangu”

“Ndio hivyo mke wangu. Mambo yana badilika, ila baada ya uchaguzi kufanyika tuna timka zetu nikisha kabidhisha ofisi kwa raisi ajaye”

“Sawa mume wangu. Ngoja nikuache ulale kwanza ume choka”

“Mpigie kwanza Nadia”

“Tena nilikuwa nime sahau”

Cauther akampigia simu mdogo wake.

“Shosti upo wapi?”

“Basi leo kuna mtoko, njoo basi”

“Ndio tumesha rudi, tulirudi jana ile ile”

“Wahi leo tuna kwenda kula kuku”

“Hahaa”

“Hembu lete niongee naye”

Cauther akanikabidhi simu.

“Wee mwanamke”

“Niambie mume wangu”

“Poa mke, njoo basi tukale kuku”

“Nakuja shem na hembu muache maagizo hapo getini kwenu kwa maana si kwa ulinzi huo”

“Kwani una kaguliwa?”

“Ndio wana nikagua”

“Basi nita waleza wasikusumbue”

“Sawa mume wa mimi, nime wamisije”

“Sisi tupo”

“Naoga fasta nina kuja”

“Haya”

Nikamrudishia Cauther simu yake.

“Ehee”

“Alafu muambie mama akupe ile dawa ya chango niliyo kuambia uje nayo”

“Sawa”

Cauther akakata simu.

“Una chango mkewangu?”

“Hapana ila si una jua kipindi hichi ina bidi uwe tayari kwa lolote linalo kwenda kutokea”

“Hapo sawa mke wangu, naomba simu yangu”

Cauther akanikabidhi simu yangu, nikampigia mlinzi wangu mkuu na kumueleza aandae mazingira ya mimi kwenda kula chakula cha usiku, nikampigia mlinzi wa getini na kumueleza juu ya ujio wa shemeji yangu na nikawaomba wasimkague sana, kisha nikaanza kuutafuta usingizi ambao tayari ulisha anza kupotea. Haikunichukua muda mrefu nikapitiwa na usingizi fofofo.

Gafla nikahisi kitu kikininyonya sikoni mwangu, nikafumbua macho na kumuona Cauther akiwa ame niinamia.

“Muda umekwenda mume wangu”

“Ume nistua. Saa ngapi sasa hivi?”

“Ni saa kumi na mbili na dakika kumi”

“Nimelala”

“Yaa ume lala sana na hujakula siku nzima”

Cauther alizungumza huku akiendelea kuniinamia. Taratibu akanikalia kiunoni mwangu, akavua dera lake na kubaki na chupi tu.

“Nina hamu naye sana”

Cauther alizungumza huku akichezesha chezesha kitumbua chake juu ya jogoo wangu ambaye amelala. Taratibu jogoo wangu akaanza kuitikia mualiko wa Cauther na ndani ya muda mfupi akasimama. Cauther akamshika taratibu na kuisogeza chupi yake pembeni kidogo na akaanza kumkalia. Kitu ninacho kipenda kwa mke wangu ni jinsi kitumbua chake kilivyo jaliwa kuwa na joto kali sana na jinsi alivyo mjamzito, joto ndio limezidi kuongezeka mara dufu. Japo ni mjamzito ila Cauther kitandani sio mzembe, akazidi kumkatikia mauno ya taratibu jogoo wangu hadi sote tukafika mwisho wa safari yetu tuliyo ianza dakika arobaini zilizo pita pamoja.

“Yaani mke wangu una niwezea sana.”

“Nakuwezea kivipi?”

“Yaani una nikojoza mapema”

“Si nina jua namna ya kuikuna mbo** yako”

“Ndio maana nina kupenda mke wnagu. Yaani hata ikiwa ni staili moja ila una nimudu hadi nina fika mwisho”

“Ndio hivyo, sasa ole wako nisikia una mpa utamu wangu mwanamke mwengine. Haki ya Mungu nina kuapia Eddy nita muua huyo mwanamke na maiti yake wala hauto iona”

“Una hisi ume wako nina chepuka?”

“Sikuhisi ila najua lazima wanawake wa ajabu ajabu wata kuwa wana kunyemelea. Kipindi kile una endesha taksi tu wanawake walikuwa wana jigonga gonga sana kwako. Kipindi hichi ni raisi ita kuwaje”

“Usijali mimi ni wako tu”

“Eddy una nijua mume wangu. Nina wivu na wivu wangu una ujua ni mbaya sana”

“Nimekuelewa mama watoto”

Cauther taratibu akaninyonya denda kisha akashuka kiunoni mwangu. Nikamtazama kwa umakini na nikakumbuka maisha ya nyuma alisha wahi kutumia msichana mmoja majambazi wakampiga nusu ya kumuua na kumtupa mtaroni kisa tu ni kukuta meseji ya msichana huyo akinitongoza na sikuweza kumfanya kitu chochote kwa kipindi kike kutokana mapenzi yalisha kolea kwake na sikuhitaji ayajue maisha yangu ya nyuma nilikuwa ni mtu wa aina gani.

“Mbona una niangalia sana mume wnagu?”

“Naangalia uumbaji wa Mungu mama watoto. Kweli Mungu fundi, ana jua kuunda wanawake wazuri sana”

“Asante njoo tuoge”

Tukaoga kwa pamoja kisha tukajianda kwa ajili ya kuelekea Sinza. Tukatoka ndani hapa na kumkuta Maria na Nadia nao wakiwa wamesha jiandaa. Mlinzi wangu namba moja akaingia ndani hapa.

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz .EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

*********************************************************************

“Muheshimiwa raisi kila kitu kipo tayari”

“Sawa nina kuja”

Mzee ambaye ni mshauri wangu naye akaingia sebleni hapa, tukamsalimia, kisha tukaka kwenye meza ya chakula kwa ajili ya mazungumzo.

“Muheshimiwa raisi kesho kuna dhiara yako ya kikazi ina bidi uelekee kule mkoani Singida ukawafariji wale wana ndugu ambao wamefiwa na ndugu zo kutokana na madhara ya kile chungu cha nyuklia”

“Mbona ume nieleza saa hizi?”

“Nilikuja na mama aliniambia kwamba ume lala hivyo nilishindwa kuleta ripoti ya kueleweka”

“Sawa, tuna kwenda kwa ndege au magari?”

“Magari mkuu”

“Ila kila kitu kimesha andaliwa vizuri?”

“Ndio muheshimiwa”

“Sawa, niandalieni ratiba nzima ya sehmu tunayo kwenda kisha utaniwekea hapa mezani kwani nina nitakapo kuwa nime rudi uta kuwa umesha ondoka”

“Ratiba ipo tayari na tuna kwenda pamoja kwenye hii safari”

“Ohoo sawa, uta nipatia ndani ya gari”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Mzee huyu akaondoka kisha nami nikarudi sebeleni.

“Twendeni”

“Ila raisi ana vaaje pensi”

Nadia aliniuliza kwa maan nime vaa pensi na tisheti pamoja na kofia nyeusi.

“Kwani kuna shida, nina toka kifamilia si kikazi mke”

“Umependeza bwana mume wangu. Twendeni”

Tukatoka na kuongozana na walinzi wetu hadi kwenye gari ya raisi ambayo ina uwezo wa kuingia hata watu nane kwa wakati mmoja na ni gari iliyo tengenezwa kwa uhimara wa kuto ingiza risasi wala bomu la ina yoyote pale inapo shambuliwa. Msafara wa gari kama kumi na mbili ukaanza pamoja na pikipiki.

“Muheshimiwa ratiba hii hapa”

Mshauri wangua linikabidhi ratiba ya safari nzima ya kuelekea mkoni Singida. Nikaisoma kisha karatasi hii nikaiweka mfukoni.

“Vipi mume wangu”

“Kesho nina ziara ya kikazi Singida”

“Ohoo sawa sawa”

“Ila hii gari ni nzuri jamani”

Nadia alizungumza huku akitazama mandhari ya gari hili ambalo kwa Maria mtoto wa raisi sio mara yake ya kwanza kulipanda ila kwa Nadia ni mara yake ya kwanza kulipanda.

“Ndio gari ya raisi mke”

“Ina itwaje hii mume nami nijichange ninunue”

“Hahaa best hii gari ni maalumu kwa raisi tu. Ina itwa Cadillac One, gari hili lime garimu kama milioni mbili hivi za Kimarekani”

“Duuu kweli ina mfaa raisi peke yake”

“Hahaaaa”

Uwepo wa Nadia ndani ya gari hili, inatufanya tuchangamke sana kwani uzuri wa Nadia ni muongeaji na uongeaji wake haumkeri mtu. Tukafika Sinza na tukakuta walinzi wakiwa tayari wamesha lizingira eneo ambalo mimi na familia yangu tuta pata chakula cha usiku hapa. Watu wengi wapo eneo hili kushuhudia ni nani anaye shuka kwenye gari hili kwani ime kuwa ni kama suprize kwao. Nikafunguliwa mlango na mlinzi wangu nikashuka pamoja na mke wangu. Watu wakaanza kushangilia hata walio kuwa kwenye viti vyao wakiendelea kula nao wakaacha kula na kutushangilia. Upendo huu ukanifanya nishangae sana kwani sijatarajia kama watu wana weza kunipenda namna hii ikiwa ni juzi juzi tu hapa nilikuwa ni dereva taksi na ni mara nyingi nilikuwa nina kuja eneo hili na wala sikushangiliwa na hata mfuta meza.



Nikawapingia watu mkono huku wengine wakujitahidi kupiga picha na waandishi wa habari hususani wa ikulu hawakuwa mbali kuhakikisha wana piga picha ya kila kinacho endelea eneo hili. Mimi na Cauther tukaelekea moja kwa moja hadi eneo walipo Sudy na wezake. Uchangamfu leo kidogo umeyumba na sura zao zina onyesha kujawa na woga kwani hawajazoea kuniona hivi.

“Nini mbona hamjachangamka?”

Niliwauliza huku nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu.

“Ahaa kaka tuna ogopa aisee. Ume kuwa mtu wa tofauti kabisa aisee”

Sudy alijikaza kuzungumza.

“Yaani shem Sudy leo ume poa kama maji ya mtungini. Changamkeni bwana, hatujakuja kuwadhuru. Leo kajomba kenu tumboni kalikuwa na hamu ya kula chakula chenu ndio maana mume ona tupo hapa”

“Hahaaa sawa ehee niwapatie nini?”

“Kama kawaida Sudy au hujui ninacho penda?”

“Najua”

“Sudy muna chakula cha kutosha?”

“Ahaa yaani?”

“Nahitaji mimi na timu yangu hapa sote tule pamoja na watu wote walipo hapa nao wapate chakula. Je ina wezekana?”

Sudy na bosi wakae wakatazama idadi ya watu walipo hapa kwa haraka haraka ni kama watu mia na ishirini na jinsi dakika zinavyo zidi kusonga ndivyo jinsi idadi hii inavyo zidi kuongezeka kwani kila mtu ana hitaji kumuona raisi.

“Labda tuongeze gunia jengine la viazi”

“Basi fanyeni hivi. Nalipoa chipsi yai sahani mia tano kwenye kila chipsi yai moja kuwe na miskaki miwili, ita kuwa bei gani?”

“Duuu ngoja tupige hesabu kaka”

“Fanya hivi nalipa milioni mbili sasa hivi na hakikisheni watu wote wana pata chakula, kama ni kuwafungia kwenye mifuko muta wafungia na kama kuwawekea kwenye take away muta waweka. Ila kwanza hakikisheni kwamba chakula changu na familia yangu kina kuwa bora kama kinavyo kuwa siku zote”

“Usijali muheshimiwa raisi”

Sudy alizungumza huku meno yote thelathini na mbili yakiwa nje kwa furaha. Nikatoa kiasi cha milioni mbili na kumkabidhi bosi wa Sudy.

“Sudy ina bidi siku nikualike ikulu bwana uje kupike”

“Wee kaka si nita kufa mimi”

Kiswahili cha kipemba ambacho ndio lafudhi ya Sudy ikatufanya tucheke sana.

“Ndi kaka, utanifanya nife hata kabla sijafika hapa ikulu.”

“Sudy acha kunichekesha bwana, mtoto wangu asije akatoka bure tumboni. Kwa nini sasa uta kufa”

“Ahaa una jua Cauther yaani naona kama ndoto ambayo siamki vile. Kipindi kile muna kuja kula chipsi hapa na sasa hivi ni tofauti kwa kweli. Sasa hivi muna lindwa na mabundiki”

“Hahaaa maisha yana kwenda, ila nita kuhitaji weekend hii ikulu. Ngoja nikukutanishe na mtu atakaye kusaidia kuingia ikulu”

Nikamuita mshauri wangu kwa ishara na akatufwata sehemu tulipo simama.

“Mzee wangu huyu kijana juma mosi nahitaji aje ikulu kutuchomea nyama. Ni mtaalamu kwenye maswala ya nyama na kupika pika”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Uta chukua namba yake na jumamosi ata kuja ikulu”

“Hakuna tabu muheshimiwa raisi”

Sudy macho yakamtoka kwa mshangao kwa maana haamini kile nilicho kifanya.

“Wee Sudy”

Cauther alimuita Sudy na akastuka.

“Acha kushangaa shangaa, nime kueleta mdogo wangu umtongoze”

“Aahaa Cauther wewe, wataka nipate mstuko wa moyo sasa. Huku ikulu huku mdogo wako ndio nitakufa zaidi”

“Hahaa chizi kweli wewe. Jamani mimi ngoja nikakae na wezangu. Sudy njoo basi uwasikilize”

“Sawa sawa”

Sudy akaongozana na Cauther hadi eneo walipo kaa Nadia na Maria.

“Muheshimiwa raisi una lisaa moja la kukaa eneo hili ina bidi urudi ikulu kwa ajili ya safari ya kesho”

Mlinzi wangu alininong’oneza sikioni mwangu.

“Sawa jes nina weza kupiga picha na hawa watu wanao tamani kupiga nami picha?”

“Ngoja tuandae mazingira”

Waalinzi wakajipanga moja ya eneo vizuri kisha nikaruhusiwa kukutana na mtu mmoja au wawili kwa ajili ya kupiga nao picha. Kila mwananchi akafurahia uwepo wangu eneo hili. Chakula chetu kikaandaliwa vizuri na tukaanza kula.

“Mmmmm kumbe chakula chao hapa ni kitambu ehee?”

Maria alizungumza hukua akiendelea kula.

“Yaa ni kitamu sana ni ufundi wa Sudy huo”

“Sudy ndio yupi?”

“Yule aliye vaa tisheti ya njano”

“Ahaa yule mpemba uliye kuja hapa na Shem?”

“Ndio”

“Aisee ana pika vizuri jamani”

“Juma mosi tuta kuwa naye ikulu. Hivyo musio jua kuchoma nyama mujiandae kwa darasa”

“Ila tatizo la Sudy sijui nini?”

Cauther alizungumza huku akiendelea kula.

“Kwa nini?”

“Ana mkono mzuri kama huu. Sasa kwa nini asitafute sehemu yake akafungua. Ana kazi ya kuajiriwa weee”

“Huwezi jua makubaliano waliyo ingia. Isitoshe hawa wote ni Wapemba na wana toka sehemu moja hivyo una weza kukuta wame kubaliana mambo yao huko ndio maana ana shindwa kuondoka”

“Shem”

“Naam”

“Kwenye zile fremu tulizo panga kufungua duka, kwa nini tusifungue mgahawa wa kisasa alafu tukamuajiri Sudy kama mpishi mkuu na tukamlipa mshahara mkubwa ambao uta mkidhi hata yeye kufungua sehemu yake kwa maana hapa ni siku ya pili tuna kuja, nina mkuta na tisheti yake ile ile ya njano sasa sijui hana pesa ya kununua”

Nadia akatufanya tucheke.

“Una jua nini Nadi. Sudy ana kupenda na alisha muambia shemeji yako hapa. Sasa ukimshawishi juu ya hilo wazo lako nina imani ata kuelewa haraka sana kuliko nitakavyo mueleza mimi au shemeji yako”

“Dooo mwanaume kama Sudy mimi hapa, muda wote ana tabasamu tabasamu”

“Hahahaa sasa shem hutaki mwanaume mcheshi kama Sudy”

“Aha…ucheshi ukizidi sana una onekana kama Zuzu”

“Utabiri wangu kwako Shem. Yule Sudy unaye muona kama Zuzu, ata kuoa na ata kuwa mumeo”

“Shem tema mate chini, sitaki utabiri wako huo”

“Ahaa mimi nasema ukweli kwa maana naona kama una mchukulia poa Sudy ila hilo wazo lako la mgahawa ukilikamilisha na ukawa karibu naye uta jua umuhimu wake na uzuri wake”

Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kuona namba ya Willy.

“Dogo niambie”

“Safi kaka naona una pata chakula cha usiku na familia”

“Ndio mdogo wangu, vipi huyo bibie ana endeleaje?”

“Yupo poa. Tumepokea taarifa kwamba kesho kuna safari ya kwenda Singida?”

“Ndio ndugu yangu asubuhi na mapema muwe ikulu”

“Sawa kaka”

“Msalimie Judy”

“Zimefika”

Nikakata simu. Tukamaliza kula, tukaagana na Sudy na wezeke ambao tayari wamesha anaza kugawa sahani za chakula kama nilivyo toa maelekezo, nikawapungia mkono wananchi na tukaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hili.

“Wananchi wana kupenda Eddy, kwa nini usiendelee na hii nafasi”

Maria alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ahaa baso sijawaza au kufikiria juu ya kuendelea kuwa madarakani”

“Ila upendo ambao wame kuonyesha wananchi sio mdogo Eddy. Jaribu kulifikiria hilo”

“Ila ni kweli shemeji uraisi ume kupendeza sana. Kwani si miaka mitao una chaguliwa tena una malizia mitano baada ya hapo ina kuwa kumi”

“Ngoja niwaambie siri moja. Hakuna kazi ngumu na inayo chosha kama kuwa raisi. Musione hivi tuna tembea kwenye magari makubwa, walinzi wengi ila hii kazi ni ngumu mmno. Mke wangu ndio anaye jua, kuna wakati kichwa kina pata moto hadi una tamani uvute hata bangi. Kuna wapuuzi wa kila aina, seme Maria hukukaa sana na mzee ila leiti ungekuwa una mshuhudia hayo mafaili jinsi yalivyo pangaa ofisini kwake, nina imani unge mshauri Aachen tu na kasi hiyo”

“Ila mzee aliipenda kutoka moyoni mwake”

“Yaa yeye alikuwa ni mwana siasa. Mimi ni mwanajeshi tupo njia mbili tofauti. Sisi tumezoea kufanya kazi inayo kwisha na watu kufwata amri. Ila huku kwenye siasa ukiwapeleka watu kiamri amri uta ambiwa hauna demokrasia. Ukiwapelekea kiupole wata kuambia raisi hana nguvu ya kutawala ni mpole. Ukiwa kawaida wata kuambia raisi gani mbona ana fwata bendera kama upepo. Sasa hapo ndipo kwenye shida, sisi wengine hatuwez I kuvumilia kma hivyo, mtu akikukashifu una malizana naye, sasa haijalishi ni kwa njia salama au sio salama”

“Shemu una onekana ni mtu ambaye hupendwi kusemwa vibaya?”

“Yaa kwa sababu sipendi kumsema mtu yoyote vibaya.”

Tukafika ikulu, mke wangu na wadogo zake wakaelekea eneo tunalo ishi huku mimi na mshauri wangu tukielekea ofisini kwangu.

“Ehee mzee wangu kesho tuna ondoka saa ngapi ikulu?”

“Saa mbili asubuhi, tayari wana usalama wamesha imarisha ulinzi barabarani pamoja na eneo ambalo uta tembelea”

“Hivi hawa wananchi ambao familia zao zilikumbwa na vifo vya ndugu zao wamepata kifuta machozi?”

“Bado serikali haijaweza kutoa chochote kwao kwa maana kama unavyo jua hapa katikati mambo yametokea haraka sana hivyo tume shindwa kuwapangilia ni namna gani ya kuwapa”

“Idadi yao ina julikana?”

“Ndio”

“Hembu mpigie mkuu wa mkoa wa Singida”

“Sawa”

Mshauri wangu akampigia simu mkuu wa mkoa wa Singida.

“Muheshimiwa amesha pokea”

Nikaipokea simu hii ya mshauri wangu na kuiweka sikioni mwangu.

“Habari yako mama Bughe”

“Salama muheshimiwa raisi”

“Nina umani kila jambo lina kwenda vizuri ndani ya mkoa wako?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Ehee hembu niambie familia zilizo kumbwa na misiba ya sumu ya nyuklia zina fahamika?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Basi andaa mazingira ya mimi kesho kukutana na hao wana ndugu muhimu, kama ni baba au mama au mtu sahihi wa familia na kwenye kila familia watoke watu wawili nahitaji kuongea nao”

“Sawa muheshimiwa raisi nita likamilisha”

“Nashukuru kwa hilo, je kuna lolote ungependa kuniomba binafsi kabla sija fika mkoni kwako?”

“Tuta zungumza tukikutana muheshimiwa raisi”

“Sawa nashukuru”

Nikakata simu na kumrudishia mshauri wangu.

“Hembu nitafutie faili la waziri mkuu, nahitaji kufahamu mali zake zote na deni analo daiwa na pia mpigie mkuu wa TRA nahitaji kuonana naye usiku huu”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Mzee huyu akatoka ofisini hapa, taratibu nikarudisha nyuma kiti hichi cha kuzunguka na nikaiweka miguu yangu juu ya meza huku nikitafakari namna nchi hii ilivyo jaa matobo matobo makubwa ya wala rushwa, wasaliti na watu wanao jipendelea wao wenyewe kiuchumi na kuwadhulumu hata wenye kidogo.

‘Sema muda mchache ila ninge wanyoosha wapuuzi hawa’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kutafakri. Baada ya muda mfupi mzee akaingia na faili la waziri mkuu akanikabidhi.

“Mzee wangu ninajambo nahitaji kukuuliza”

“Bila shaka muheshimiwa raisi”

“Wezako wote baada ya sekeseke lililo wapata waliamua kuomba likizo na kupumzika kwa nini wewe upo na mimi kila wakati ikiwa nawe ulikuwemo kwenye sekeseke za kutekwa”

“Aaaha muheshimiwa raisi mimi ni mtu ninaye ipenda kazi yangu na nina jua thamani ya hii kazi kwenye taifa langu. Raisi alisha wahi kuniambia kwamba ana tamani sana siku moja wewe uje kuwa raisi wa hii nchi na alikuwa ni mtu kama aliye weza kuona maono ya kifo chake. Alisha wahi kuniambia kwamba sinto maliza kipindi cha uongozi wangu.”

“Alisema hivyo?”

“Ndio aliniambia miezi miwili nyuma kabla ya kifo chake na akasema kwamba endapo siku uta kufa. Haijalishi ita kuwaje ni lazima nihakikishe nina kusaidia una kuja kukamata uongozi wa hii nchi na nina kuwa na wewe bega kwa bega hata kama ni kwa muda mfupi wa kuongoza ila niweze kukukuza kwenye mazingira ya kuja kuwa kiongozi bora pale muda utakapo wadia”

Nikatulia kimya kwa dakika kama mbili hivi nikitafakari maneno ya mzee huyu.

“Nikuulize kitu?”

“Ndio”

“Una hisi mimi kweli ni kiongozi mzuri?”

“Ndio, kiongozi mzuri ni yule mwenye msimamo. Anayeitanguliza nchi kwanza na mambo mengine yana fwata. Kiongozi ambaye hajali maumivu ya watu wachache au wengi. Yeye anacho jali ni kwamba ana simamia misingi ya haki na sheria inavyo paswa kufwata na ana waeleza watu ukweli juu ya kila kinacho wahusu kuambiwa ukweli na sio kubembelezana. Hicho ndio nilicho kiona kwako, ukiendelea kuwa hivi, hili taifa lita zidi kuwa imara na hakuna ambaye ataweza kuliangusha wala kulifikia”

“Ila mzee wangu una jua sina ndoto kabisa ya kuwa kiongozi wa hii nchi na hichi cheo kime kuja kama ajali tu, yaani sikutegemea wala kufikiria kwamba nita kuwa hapa sasa hivi”

“Muda wako bado Eddy, uta fika muda na wakati wa wewe kuwa kiongozi wa hii nchi. Sasa hivi ime tokea kama ajali kama ulivyo sema. Acha Caro awe kiongozi kisha baada ya miaka yake kumi uta kuwa kiongozi wewe”

Nikashusha pumzi.

“Ila sijui kama nita kuwa hivi mzee wewe una mri gani?”

“Miaka stini na saba”

“Baada ya miaka kumi uta kuwa na miaka sabini na saba?”

“Ndio, tuombe uzima kwa Mungu”

“Nina imani kuna mambo mengi sana una weza kuyafahamu kuhusiana na raisi pamoja na makamu wa raisi”

“Ndio nina wafahamu vizuri sana na walikuwa ni watu marafiki wa kipindi kirefu sana na hata kipindi kile mupo wadogo wewe na wezako muna ingizwa kwenye jeshi tulipendekeza wazo hilo kwa pamoja la kutengeneza kitengo maalumu cha watu wachache na hatari na tuka wapendekeza nyinyi. Ungomvi mkubwa wa raisin a makamu waraisi na kupelekea raisi kuishi kwenye maisha hofu na woga ni pale tulipo gundua siri ya vifo vya wezako, nani ana husika na nani yupo nyuma ya tukio zima”

“Mulimfahamu ni nani?”

“Ni kamau wa raisi na mbaya zaidi tuka gundua kwamba ana miliki organization kubwa ya kuhalifu inayo dili na viongozi wa ngazi za juu nani genge ambalo ndio lilihusika pia na vifo vya wezako naamini una litambua hilo?”

“Ndio nina litambua na nina hitaji kuendesha oparesheni ya kuhini”

“Una maanisha nini?”

“Nina hitaji kumsaka mmoja baada ya mwengine na wote kuwangamiza”

“Eddy kundi la Scropion ni kubwa sana na sio dogo”

“Najua na kwa muda wote huu nina fanya upelelezi wangu ndio maana una niaona nipo kimya. Nahitaji kutoka kabisa kwenye serikali na hii nchi. Nina hitaji kufanya kazi mimi kama mimi”

“Huitaji msaada wa nchi?”

“Hapana kwa maana mimi nikiwapiga wao. Wao wata kuwa wana ipiga nchi na kuwaua wananchi wasio na hatatia”

“Eddy”

“Naam mzee”

“Nita kusubiria hadi wakati wako utakapo fika. Una miaka kumi ya kujipanga na kuamua nini ufanye juu ya hii nchi. Sawa”

“Sawa mzee wangu”

Ujumbe mfupi ukaingia katika simu ya mshauri wangu, akausoma kwa sekunde kadhaa kisha akanitazama.

“Mkuu wa TRA amefika”

“Mauambie aingie”

Baada ya dakika chake akaingia mzee mmoja mnene kiasi na mwenye nywele nyeupe kichwa kizima. Tukamsalimia kisha nikamkaribisa.

“Pole kwa kukusumbua bwana nani vile…..”

“Bwana Mayai”

“Sawa bwana Mayai. Nina imani una fahamu deni analo daiwa waziri mkuu kutokana na kampuni zake na kukwepa kulipa kodi. Una lifahamu?”

“Ahaa labda nikaangalie kwenye taarifa zangu muheshimiwa raisi”

Nikamsogezea faili la waziri mkuu aliye jiudhuru yeye mwenyewe.

“Najua una jua kwamba ana daiwa ila mume fumba macho. Nahitaji ndani ya wiki moja hiyo pesa iwe imeingia BOT, la sivyo huna kazi na nitakusweka ndani. Tuna elewana”

Nilizungumza kwa sauti ya upole ila yenye msisitizo na kumfanya mkuu huyu wa shirika muhimu sana la mapato nchini Tanzania bwana Mayai kutokwa na macho ya mshangao hadi akaanza kutetemeka kwa woga ulio tufanya mimi na mshauri wangu tujiulize maswli mengi sana juu ya woga na wasiwasi wake huo.


“Mzee wangu mbona una tetemeka kuna shida?”

“Aha…hakuna muheshimiwa raisi”

“Basi fanya kazi, sijakuita kukutisha ila nime fwata taratibu za kisheria.”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Una weze kwenda na pole kwa kukusumbua usiku huu”

“Nashukuru”

Mzee Mayai akanyanyuka na kuondoka eneo hili.

“Ukioa mtu ana hali kama hiyo basi amehusika kwenye huo ulaji wa hizo pesa”

Mshauri wangu alizungumza.

“Kweli?”

“Ndio hapo nina imani ata kuwa ana wazia namna ya kurudisha hiyo pesa aliyo hongwa kwa maana huwa wana pozwa pozwa na pesa na kuisababishia nchi hasara kubwa kama hii”

“Raisi ajeye ana kazi kubwa ya kudili na watu kama hawa”

“Kwa Caro uliye mchagua nina uhakika ana uwezo wa kupambana na haya yote”

“Mungu amsaidie kwa maana si kwa vituko kama hivi”

“Ni kweli aisee muheshimiwa”

“Mzee wangu nenda kapumzike kwa kweli kwa maana muda ume kwenda na kesho tuna safari ndefu sana”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Nikaagana na mzee huyu kisha mimi nikaelekea eneo ninalo ishi. Kutokana muda umesha kwenda, sija kuta mtu yoyote sebleni, moja kwa moja nikapitiza hadi chumbani na kumkuta Cauther akiwa amelala fofo, kutokana na uchovu nikajilaza pembeni yake na hazikupita hata dakika tano usingizi mzito ukanichukua.

Asubuhi na mapema nikaanza kufanya maandalizi ya safari ya kikazi kuelekea mkoani Singida.

“Ni ziara ya muda gani mume wangu?”

“Siku mbili, ungekuwa vizuri tunge enda ila kutokana na hali yako hiyo siwezi kukuruhusu”

“Hata hivyo sina uwezo wa kuaa ndani ya gari kwa muda mrefu mume wangu”

Cauther alizungumza huku akinibandika kijinembo chenye alama ya Tanzania katika koti langu hili la suti nililo vaa.

“Sasa umekamilika mume wangu. Kuwa makini kwenye safari yako”

“Nashukuru mke wangu”

Taratibu tukanyonyana denda kwa hisia kali sana kisha nika bebeba brufcase yenye suti mbili alizo niandalia mke wangu, pamoja na soksi na boksa. Tukatoka sebleni na kumkuta Nadia akiwa tayari amesha amka, nikasalimiana naye.

“Afadhali nime kuwahi shemeji. Mama alikuwa na ombi, kama ita wezekana dada arudi nyumbani, kwani hali yake hii ina hitaji ungalizi wa wanawake watu wazima kama yeye. Nilimuuliza kama ana weza kuja kuishi hapa ikulu akasema hilo sio jambo zuri kwa mila zetu sisi waarabu wazazi wa kike hawajazoea sana kuishi kwa wakwe wa watoto wao”

“Sawa hakuna tatizo kikubwa ata ongoza na walinzi wa ikulu hivyo wasije wakaogopa kuona idadi ya walinzi ime ongezeka”

“Sawa shemeji nashukuru”

“Usijali, mke wangu umeridhia hilo?”

“Ndio baby”

“Sawa msalimieni mama”

“Poa mume wangu”

Cauther akanikumbatia tena kisha nikatoka ndani hapa. Mlinzi wanagu namba moja akaipokea brufcase hii na tukaanza kutembea kuelekea ofisini kwangu. Nikakutana na Maria secretary wa raisi aliye pita.

“Habari ya asubuhi muheshimiwa raisi”

“Salama, si upo likizo wewe vipi mbona hapa?”

“Sijazoe kukaa nyumbani hivyo nimerudi kazini rasmi mkuu”

“Ila upo salama?”

“Ndio”

“Si upo kwenye msafara?”

“Ndio”

“Sawa karibu kazini mtoto mzuri”

Maria akatabasamu, nikaingia ofisini kwangu, hazikupita dakika tano mshauri wangu akaingia akiwa ameongozana na Willy pamoja na Judy. Nikasalimiana nao huku wote wakionyesha kuwa na sura za furaha.

“Ziara yako ya kwanza muheshimiwa raisi hongera”

Judy alizungumza huku akitabasmau”

“Yeah ngoja tukaangalie mambo yalivyo. Kila kitu si kipo tayari?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Muite Maria”

Judy akamuita Maria na akaingia ofisini hapa.

“Maria tuongozee sala ya safari yetu si una jua bwana”

Nilimuambia Judy na akakubaliana na nilicho kisema kwa pamoja tuka simama na kushikana mikono yetu huku tukizunguka duara moja. Maria akaanza kusali sala ya nguvu ilicho chukua dakika mbili, baada ya sala hii tukatoka ndani hapa, tukaongozana na walinzi hadi nje ya ikulu. Nikafunguliwa mlango wa gari na kuingia katika gari nyingine ya raisi ambayo hutumika katika safari za masafa marefu na ina uwezo wa kukimbia kilomita mita mia tatu kwa saa. Katika gari hii nikapanda na Judy, mlinzi wangu namba moja akaka mbele pamoja na dereva na wengine wakaingia katika magari megine ya msafara.

“Duu haya maisha yalikuwa kama ndoto vile”

Judy alizungumza huku akinitazama.

“Ndoto kivpi?”

“Sikutegemea kama nita kuwa kuwa mshauri wa raisi”

“Ila kwa muda”

“Ni kweli ila nina furahia furahia”

“Hahaa,raha ya kuwa raisi ni kwamba husimami foleni”

“Hahaaaa hicho ndio unacho furahia?”

“Ndio, si unaona jinsi barabara ilivyo nyeupe gari zote zimekaa pembeni”

“Haya bwana. Mmmmm”

Judy aliguna huku akiwa ameshika simu yake.

“Kuna gazeti la simu, Willy amenitumia hapa, kichwa cha habari kina sema ‘BAADA YA RAISI OG KUFA, RAISI FEKI ALA BATA NA WATOTO WA KIARABU KABLA HATA YA MASAA AROBAINI NA NNE YA MSIBA WA RAISI OG KUMALIZIKA”

“Gazeti gani limeandika huo upuuzi?”

“Linaitwa UDAKU WA MJINI”

“Nitafutieni huyo muandishi na mmiliki wa gazeti na hembu nione”

Judy akanikabidhi simu yake, nikaona picha zangu za familia yangu, jambo ambalo kusema kweli limeniudhi, huwa sipendi kabisa kwa mtu kuingilia maswala yangu binafsi ya familia.

“Hembu tafuta habari ya ndani ya hilo gazeti kisha unisomee”

“Dakika moja”

Judy akapekua simu yake na akaipata habari hiyo.

“Habari ina sema hivi”

“Ehee”

“Baada ya raisi aliye pigiwa kura na wananchi zaidi ya milioni arobaini na kupita kwa kishindo kufariki dunia. Raisi kajanja a.k.a raisi feki ambaye hajachaguliwa na hata kuku au bata mmoja wa Tanzania”

“Kuku au bata?”

“Ndio muheshimiwa”

“Endelea”

“Ameonekana kuanza kuzitumbua mali za serikali bila ya huruma. Raisi huyu Eddy Jr alimaarufu X, usiku wa kuamka leo ameonekana viunga vya Sinza akila bata na watoto wawili wa kiaruabu pamoja na mtoto wa marehemu raisi aliye fariki dunini. Tukio hilo limetokea hata masaa arobaini na nate toka kuzikwa kwa aliye kuwa raisi wa watu. Raisi Eddy Jr amezidi kutumbua mali za serikali kwa kuwanunulia wananchi wote chipsi na miskaki ili mradi watu wampende.”

“Gazeti letu la udaku lilifanikiwa kuwahoji wananchi wawili watatu kuhusiana na raisi huyu ambaye kiumri ni mdogo na hafai kuwa raisi. Mwananchi wa kwanza, kusema kweli huyu kiana sidhani kama ana weza kuongoza nchi tajiri kama hii, bado ana akili za kitoto.”

Judy akanitazama jinsi uso wangu ulivyo jawa na ndita za hasira.

“Endelea”

“Mwananchi wa pili. Raisi huyu hajachaguliwa na watu hivyo acha aponde mali kwani hato kuwa tena raisi wetu. Mwananchi wa tatu, hapa hatuna raisi, huyu ni raisi maandazi hatufai na akili yake nina hisi ni ndogo kama tumba ya ubuyu, hakuna kitu mule. Hayo ni baadhi ya maoni mengi ya wananchi, na sisi udaku tuna sema hatuwezi kuongozwa na raisi ambaye akili zake ni punje za ubuyu isitoshe ana tembea na mwanamke wa kiarabu tena mjamzito na kumleta maeneo ambayo hapaswi kuonekana, isitoshe mke wake ni mbaya hana tako kama la mke wa raisi aliye pita.”

Nikaachia msunyo mzito hadi Judy akasitisha kusoma.

“Endelea”

“Ila mkuu uta zidi kukasirika”

“Wewe endelea”

“Haya…Mwanamke wake ni wale wanawake wa kigaidi wa Al-quida hivyo hatumtaki raisi anaye ongozwa na wanawake wa kiarabu tuna taka raisi anaye muoa mtanzania mwezetu ili ampe changamoto za maisha yetu. Sasa muarabu huyo ana tujuaje sisi na wakilala kitandani wana shawishiana nini zaidi ya kutulipua lipua kwa mabomu hivyo raisi maandazi asidhubutu kugombania uraisi kwani ita kuwa ni anguko kwa chama tawala. Imeanzikwa na Mzee wa Udaku”

“Imeisha?”

Nilimuuliza Judy kwa sauti nzito kidogo iliyo jawa na hasira?”

“Ndio mkuu”

“Mpigie RPC”

“Wa Dar?”

“Ndio”

Judy baada ya kupiga simu hiyo akanikabidhi.

“Ni mimi”

“Muheshimiwa raisi habari za asubuhi”

“Salama. Kuna habari ime andikwa kwenye gazeti linaitwa nini Judy?”

“Udaku”

“Gazeti la udaku, nina omba kuanzia muandishi na mmiliki pamoja na muhariri wa hilo gazeti wakamatwe hadi nitajapo rudi nita waona”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Hakikisha ulinzi wa mkoa una kuwa salama”

“Hakuna shaka”

Nikakata simu na kumrudishia Judy simu yake.

“Ila muheshimiwa, kwa habari kama hizi zisikuumize kichwa kwa maana ime zoeleka hii ni nchi huru na kila mtu ana haki ya kuzungumza anacho kitaka”

“Si kwa utawala wangu. Mimi sio mwana siasa Judy siwezi kuishi maisha ya kusemwa hususani mke wangu. Una jua hapo wamemuita gaidi, akiona hiyo habari au akisoma ata jisikiaje kwa mfano na ile hali yake mawazo yake yata kuwaje?”

“Hapo kweli wame kosea”

“Basi kwa kuniita raisi maandazi nime kubali, sijui nina akili ndogo kama tumba za ubuyu nime kubali ila kwenye hili la kusema kwamba mke wangu ni gaidi wa Al-quida aisee wata juta”

“Sawa mkuu ila punguza jazba bwana. Tuna kwenda kutembelea eneo lenye maafa na watu wana hitaji ufariji wako kama raisi, achana na hawa wapuuzi wa magazeti ya udaku”

Judy alinifariji huku akinitazama.

“Kwanza tupo wapi?”

“Tuna karibia Msamvu Morogoro”

“Sawa”

Safari ikazidi kusonga mbele huku magari yakienda kwa mwendo wa kasi sana huku ulinzi ukiwa mkali sana na tukisindikizwa na helicopter mbili za jeshi.

“Muheshimiwa raisi kuna wananchi mkuani Dodoma wana hitaji uwasalimie”

Mlinzi wangu namba moja alizungumza huku akiwa amenigeukia.

“Sawa”

Msafara ukazidi kusonga mbele huku nikianza kutafakari ni kitu gani ambacho nita kwenda kukizungumza mbele ya wananchi hawa.

“Hivi Dodoma ina changamoto gani?”

“Muhshimiwa raisi, kinacho wasumbua ni bei ya Zabibu”

“Ime fanyaje?”

“Imeshuka kwa kiasi fulani, hivyo nina imani ndio watakacho anza nacho”

Mlinzi wangu namba moja alizungumza huku akiwa amenigeukia.

“Sawa”

Tukaingia mkoani Dodoma na kweli tukafika eneo la katikati ya jiji na tukakuta wananchi wengi wakinisubiria kwa hamu huku wakiwa wameshika mabango.

“Muheshimiwa usisimame kwanza”

Mlinzi wangu alizungumza huku akiniomba nisisimame kwenye siti hii ambapo kwa juu gari hililina funguka na huniwezesha kutokeza kwa juu.

“Maiki hii ya kuzungumza”

Mlinzi wangua kanipa maiki, kisha akashuka ndani ya gari.

“Judy niongee nini?”

“Chochote tu”

“Nianze kuwaambiaje”

“Dodomaa hoyeee”

“Hahaaa aisee siasa kweli kazi. Hivi habari za mchana kwa Kigogo wana semaje?”

“Duuu sijui mkuu”

“Dereva wewe ni kabila gani?”

“Mkuu mimi ni Mfipa”

“Una jua wanavyo salimia kwa Kigogo”

“Hapana muheshimiwa”

Baada ya ulinzi kukamilika nikaruhusiwa kutokea katika gari hili. Wananchi wakanishangilia jambo ambalo sikulitegemea kabisa. Nikawasalimia huku nikiwatazama kwa umakini kwa maana mimi mwenyewe nilisha kuwa mlinzi wa raisi hivyo kwenye eneo lenye watu wengi kama hivi ni lazima macho na machale yawe makini sana.

“Nashukuru kwa mapokezi yenu kwa kweli ni jambo ambalo sikulitarajia kuliona kwa watu wa Dodoma. Niambieni muna hitaji nini niwafanyie watu wa Dodoma kabla ya muda wangu huu mfupi haujaisha”

Akapewa maiki mwana mama mama mmoja.

“Muheshimiwa raisi mimi nina itwa mama Mwajuma. Muheshimiwa, hapa Dodoma changamoto yetu kubwa ni zabibu. Zabibu imeshuka bei sana, hivyo tunge uomba muheshimiwa raisi, ulisimamie soko letu kwa maana makanjanja ni wengi sana”

“Usijali mama yangu hilo lime kwisha. Ehee jambo jengine”

Akapewa maiki bibi kikongwe ila ana jimudu japo ana tembea kwa mkongojo.

“Muheshimiwa raisi kuna mengi sana ya siri ambayo ninge penda kukuambia wewe peke yako. Hivyo kama ina wezekana nina omba nikuambie wewe kama wewe, na tuwe sisi wawili tu”

Karibia wananchi wote wakamcheka bibi huyu ila nikahisi jambo kwake. Mlinzi mmoja akajaribu kumpokonya maiki ila nikamzuia.

“Bibi una hitaji kweli kuzungumza na mimi?”

“Ndio nina hitaji kuongea na wewe, ni muhimu muheshimiwa raisi”

“Sawa mleteni huyo bibi nizungumze naye humu ndani ya gari”

Kila mmoja akashangaa hadi Judy aliye kaa ndani ya gari akashangaa na kunishika mguu, nikamtazama na akatingisha kichwa akimaanisha nisimruhusu bibi huyo kuingia ndani ya gari hili.



“Acha nimsikilize, una weza kutupisha”

Nilizungumza huku nikikaa katika siti, Judy akanitazama machoni mwangu kisha akafungua mlango wa gari na akashuka ndani ya gari hili pamojana dereva. Bibi akafunguliwa mlango na mlinzi wangu na akaingia ndani.

“Shikamoo bibi”

“Marahaba mjukuu wangu. Kwanza nina shukuru sana kwa kukubali kuniona”

“Nashukuru nawe pia, ehee niambie nini unahitaji kuzungumza nami?”

“Najua nikizungumza hivi nita kufa na nita uwawa. Ila ni bora kuongea ili kuisaidia nchi yangu niliyo ishi kwa mwaka wa tisini sasa”

“Mimi nimetoroka kwangu Singida kwa hofu ya kuuwawa na mjukuu wangu”

“Kwa nini ana hitaji kukuua mjukuu wako?”

“Kwa sababu nime gundua siri yake”

“Siri gani?”

“Mjukuu wangu amehusika na ulipuaji wa bomu sijui kwenye kisima sasa sijui ni kisima gani na ameiba bomu jengine na alikuja nalo nyumbani, lipo kwenye sanduku kubwa na lina baadhi ya vibatani kama vya simu”

‘Ohoo Mungu wangu’

Nilizungumza kimoyo moyo kwani hilo ni bomu la nyuklia na kweli kwa uzito wa hili jambo bibi asinge weza kuropoka hadharani na jambo la kumshukuru Mungu ameweza kutumia hekima kubwa sana.

“Mjukuu wako ana itwa nani?”

“Khalidi Salumu”

“Ana jishuhulisha na nini?”

“Wala sifahamu kwa maana ni mtu wa kutoka asubuhi na ana rudi usiku hivyo miaka yote sijui ana fanya kazi gani na hadi siku nilipo sikia usiku akizungumza na simu chumbani kwake kwamba zoezi la kutega mabomu ya siri kwenye kisima cha nyuklia imefanikiwa hivyo kuanzia muda wowote kila kitu kita kwenda vizuri. Hapo mwanzo nilihisi ni kama jambo la kawaida, ila kesho yake ulipo tokea ule mlipuko ndio nikaweza kuunganisha matukio na maneno yake. Nilikwenda chumbani kwake na chini ya kitanda chake ndio nika kuta hilo sanduku na nilipo lifungua ndani nikaona hilo bomu. Niliogopa sana hivyo kaela kangu kadogo niliko kuwa nako ka akiba kalinisaidia kuondoka Singida na kuja hapa Dodoma na nina ishi kwa kuomba omba”

“Aisee pole sana bibi yangu. Ulitoa ripoti polisi?”

“Hapana niliogopa na niliishi kwa woga na hata kama ningeenda polisi na uzee wangu huu wasinge niamini kwa jambo kama hilo na ninavyo wajua polisi jinsi wanavyo penda rushwa labda wangenisaliti na isitoshe yule kijana wangu ni rafiki mkubwa sana wa RPC wa hapo Singida”

Nikashusha kioo cha gari na nikamuita Judy nikampa ishara ya kuingia na kukaa siti ya mbele.

“Ndio mkuu”

“Katika mlipuko wa kisima cha utengenezaji wa silaha za nyuklia bibi ana mfahamu muhusika”

“Weeee?”

“Ndio kijana wake ana itwa Khalid, mkutanishe huyu bihi na mchoraji wa serikali, pia mkabidhishe kwa vijana wetu tuna kwenda naye Singida na oparesheni hii nina hitaji uisimamie kikamilifu sawa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Muheshmiwa raisi mukinirudisha Singida wata niua?”

“Niamini mimi bibi hakuna atakaye kuu. Umri wako ume kwenda huwezi kuishi kwa maisha ya kukimbia namna hii ni lazima tuhakikishe kwamba una kuwa salama. Utapata ulinzi na aliye husika ata kamatwa, wewe uta ondoka na huyu binti na muta ingia katika gari nyingine kisha uta wapatia maelezo ya namna kijana wako alivyo na mabo yata kwenda vizuri wala usijali.”

“Kwa sababu ni wewe ume sema basi nita kumini”

“Nashukuru kwa kuniamini bibi yangu. Judy uta mpatia bibi milioni moja ya matumizi na uhakikishe kwamba nyumbni kwake ana kuwa salama na ulinzi una kuwa ni imara”

“Sawa mkuu”

Bibi akaomba anikumbatie na bila hiyana nikamkumbatia hadi machozi yakaanza kumwagika kwa huzuni. Akashuka ndani ya gari kisha nikasimama tena kwenye siti, nikasikiliza kero za wananchi wawili wa mwisho kisha tukaondoka mkoani hapa na safari ikaendelea. Tukafika mkoani Singida na tukapokelewa na mkuu wa mkoa pamoja na RPC na wafanyakazi wengine wa serikali.

“Niitie Judy”

Nilimnong’oneza mlinzi wangu wa upande wa kushoto, akawasiliana na Judy baada ya muda akafika.

“Umefikia wapi?”

“Tayari picha nimesha ituma kwa wapelelezi wote tulio ongozana nao na wale walio tangulia hapa na kazi imesha anza”

“Je una hisi kwamba ana weza kuwepo hapa Singida bado?”

“Sija jua mkuu”

Willy akanifwata sehemu nilipo kaa huku tukitazama ngoma za wanyaturu wakicheza kwa kunikaribisha mkoani kwao.

“Kaka muhusika ameweza kukamatwa na vijana wetu”

“Kazi nzuri. Bomu?”

“Amekamatwa na bomu hilo alikuwa ana litega eneo la karibu kabisa na sehemu uliyo kuwa una kwenda kuitembelea hivyo iinavyo onyesha ilikuwa ni mahususi kabisa kwa kukuangamiza”

“Kazi ipo, hakikisheni muna mkamua na hakikisheni macho yenu yana kuwa kwa huyu PRC wa polisi”

“Sawa mkuu”

Baada ya sherehe hii fupi ya kupokewa moja kwa moja tukaelekea hadi katika eneo ambalo vipo visima vya kutengeneza silaha za nyuklia.

“Mulichukua hatua gani za kiupelelezi ili kufahamu juu ya hili tukio?”

Nilimuuliza mkuu wa mkoa huku tukitazama uharibifu mkubwa ilio tokea hapa.

“Muheshimiwa raisi, upelelezi bado una endelea na nina uhakika tuta mbaini aliye husika?”

“RPC yupo wapi?”

“Nipo hapa mkuu”

“Ehee niambie jeshi la polisi hadi sasa limempata nani au kumtilia mashaka nani kwa maana hivi vyungu sio rahisi kulipuka pasipo mtu au watu kutegesha bomu lenye uwezo wa kushusha kinu kikubwa kama hichi”

“Ni kweli muheshimiwa raisi. Jeshi la polisi lime jipanga kidhatiti kuhakikisha kwamba tuna wakamata wahusika”

“Wiki ya pili sijui ya tatu hii, hakuna kilicho fanyika ina kuwaje hapo ndugu yangu au muna hata Profile ya aliye husika au kuhisi tu ana weza kuwa ni mtu fulani?”

“Kusema kweli muheshimiwa raisi, jeshi la polisi halifanyi kazi kwa ajili ya kuhisi ila wapelelezi watu wapo kazini na kazi wana ifanya”

Jibu la RPC likanifanya nitabasamu kidogo. Willy akanisogelea na kuninong’oneza.

“Kwa ripoti niliyo pewa, RPC anahusika na tukio hilo na siku ya tukio alikuwa mkoani Shinyanga kwa mapumziko yake binafsi ikiwa ni siku ya kazi na aliondoka na familia yake”

Willy alininong’oneza kwa maana naa fwalitia mahojiano ya moja kwa moja na vijna walio mkamata Khalidi.

“Na picha za satelate za wiki iliyo pita majiara ya saa nane usiku gari yake binafsi ilifika nyumbani kwa bibi yule na kubeba sanduku hilo lenye bomu la nyuklia”

Willy aliendelea kuninong’oneza kisha akanikabidhi simu yake na nikaanza kuangalia picha hizo.

“Shukrani dogo. Ehee ume sema kwamba polisi hamuwezi kufanya kazi kwa kuhisi?”

“Ndio muheshimiwa”

Nikamtazama RPC kisha nikamgeukia mkuuwa mkoa.

“Siku tukio lina tokea mkuu wa mkoa ulikuwa wapi?”

“Nilikuwa hapa hapa Singida muheshimiwa raisi”

“Wewe na familia yako?”

“Ndio mkuu”

“RPC ulikuwa wapi hiyo siku?”

“Nilikuwepo hapa hapa na mimi mkuu”

“Masaidizi wa RPC njoo”

Akaja msaidia wa PRC na kusimama pembeni alipo simama RPC.

“Siku hili tukio lina tokea wewe ulikuwa wapi?”

“Nilikuwa ofisini mkuu nikikaimu nafasi ya PRC”

“Kwa hiyo RPC hakuwepo?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Nikasoma beji yenye jina la RPC.”

“Bwana Mvungi mbona una niongopesa sas ndugu yangu. Ina kuwaje msaidizi wako akaimu nafasi yako ikiwa wewe upo?”

RPC akakosa jibu.

“Una taka kuniambia kwamba msaidizi wako ana nidanganya?”

“Aha…muheshimiwa ila nilirudi”

“Ukitokea wapi?”

“Shinyanga”

“Ulikwenda kufanyaje Shinyanga?”

“Ku…ku kulikuwa na kikao cha wakuu wa polisi kanda ya ziwa”

“Mkuu wa mkoa ilikuwa tarehe ngapi tukio lina tokea?”

“Nane mkuu”

“Nane?”

“Ndio”

“Mpigie RPC wa Shinyanga”

Nilizungumza kwa upole kwa maana njia ya ufupi ni ndogo. Mlinzi wangu namba moja akampigia simu RPC wa mkoa wa Shinyanga mbele ya kila mtu na akanikabidhi simu yake na nikaweka loud speaker.

“Haloo”

“Unazungumza na raisi”

“Heshima yako muheshimiwa raisi”

“Nashukuru, nipo Singida hapa kwenye hiki kinu cha Nyuklia kilipo lipuka. Siku kina lipuka ulikuwa wapi?”

“Nilikuwa ofisini mkuu”

“Shinyanga?”

“Ndio mkuu”

“Kulikuwa na kikao gani hiyo siku zima kwenye ofisi yako?”

“Hapakuwa na kikao chochote mkuu”

“Kweli?”

“Nina kuapia kwa jila ya Mungu wangu, hapakuwa na kikao chochote”

“Una fahamu kwamba RPC wa hapa Singida alikuwa mkoani kwako?”

“Ndio alikuja na familia yake kwa ajili ya mapumziko mkuu”

“Sawa nina shukuru kwa muda wako”

“Asante muheshimiwa raisi”

Nikakata simu na kumrudishia mlinzi wangu.

“Kuanzia hivi sasa wewe ndio RPC wa mkoa huu. Huyu Mvungi mkamateni na mumuweka ndani. Ngoja nimueleze kila mtu ili ajue kwamba hatujakuonea kukukamata. Wewe na Khalidi nikizungumza hivyo nina imani kwamba una mfahamu. Mulihusika katika kulipua hichi kinu kilicho garimu mabilioni ya pesa pamoja na maisha ya watu. Isitoshe gari yako ilibeba bomu jengien la nyuklia na ulitaka tulipuke sote hili eneo. Kwenye nchi hatuwezi kuwa na watu wapuuzi kama nyinyi. Mkuu wa jeshi huyu asikamatwe na askari wake, huyu muna jua wapi kwa kumpeleka na hakikisheni ana toa ushirikiano wa kumjua mkuu wa mpango huo”

“Sawa muheshimwia raisi”

“Ila mkuu mimi sijui kinacho endelea”

Bwana Mvungi alijitahidi kujitetea ila tayari alisha chelewa kwa wanajeshi wawili vipande vya watu tayari vimesha mdhibiti na kumuondoa eneo hili na kuwafanya wanadishi wa habari kuendelea kupiga picha na wana rekodi kila kitu kinacho tokea hapa. Baada ya kukamilisha ziara yangu ya eneo hili moja kwa moja tukaelekea katika ukumbi maalimu ambapo wana ndugu wa wafiwa wameandaliwa kwa ajili ya kuzungumza nao. Tukaingia ukumbini hapa na sikuhitaji kupoteza muda kwani wamenisubiria kwa muda mrefu sana.

“Habari zenu”

“Salama”

“Kwanza niwape pole kwa kila jambo lililo tokea kwa familia zenu. Kusema kweli ulikuwa ni msiba wa taifa kama munavyo fahamu ni mambo mengi sana yaliweza kutokea kwenye ile wiki ikiwemo kufariki kwa raisi wetu.”

“Nikiwa kama raisi wa muda nimeona si vyema hili jukumu nika muachia raisi atakaye kuja kuchukua nafasi hii. Serikali yangu ya mpito ita toa kiasi cha milioni mia moja kwa kila familia, nina imani walio ondoka kwenye familia ni watu muhimu sana kuliko hizo pesa ambazo serikali ita zitoa. Ila tuna imani hiyo ita kuwa moja ya rambirambi itakayo saidia familia zetu kuweza kuishi katika mazingira ya faraja”

“Utoaji wa pesa hizo uta simamiwa na mkuu wa mkoa na kila familia iliyo poteza mfiwa wake itapewa hicho kiasi cha pesa. Mkuu wa mkoa, tafadhali mama yangu, hizi pesa ni kodi zinazo kusanywa kutoka kwa hawa wananchi hivyo sinto hitaji mchezo wowote wa kuwadhulumu au upigaji wa pesa hizi. Endapo ita tokea na nika jua. Una jua nini kiancho fwata. Ndugu zangu nirudie tena kuwapa pole na Mungu azidi kuwapigania na kuwapa mioyo ya faraja kwenye kipindi hichi kigumu munacho endelea kukipitia. Asanteni sana na nisiwe muongo ratiba yangu kidogo ina bada hivyo kuna sehemu ina bidi kuelekea.”

Mwanamaam mmoja akanyoosha mkono.

“Ndio mama yangu”

Akapewa kipaza sauti ili niweze kumsikia vizuri.

“Muheshimiwa raisi kusema kweli una moyo wa kipekee sana. Mungu azidi kukubariki na jinsi ulivyo mdogo endelea kuwa na moyo huo huo kwa maana mimi nime mpoteza mume wangu na ameniachia watoto saba. Nina imani kwa kiasi hicho cha pesa ambacho utatupatia kwa kweli uta kuwa ume itoa familia yangu kwenye umasikini na kuiweka kwenye hali ambayo tuna wez akufungua miradi mingine na ikatusaidia sisi kama familia”

“Nashukuru nawe pia mama yangu, Mungu ata zidi kuwapigania kwenye kila jambo”

“Asante muheshimiwa.”

“Asante, ehee mzee wangu”

“Kijana nina kuomba sana uendelee kuwa raisi wa hii nchi hadi pale Mungu atakapo kuchukua. Kwa kweli ume tufuta machozi. Mungu akubariki zaidi na zaidi. Ni hayo tu mwanangu”

“Nashukuru sana mzee wangu. Nawashukuru kwa muda wenu na poleni sana kwa kunisubiria na pia nina waomba munisamehe kwa kuchelewa kama munavyo fahamu maswala ya kiserikali ni mengi na muda ni mchache. Asanteni sana”

Baada ya kuzungumza hivyo nikaondoka ukumbini hapa na moja kwa moja nikaelekea hadi katika kitengo cha upelelezi ambapo ndipo Khalid alikamatwa.

“Hali yake ipo vipi?”

Nilimuuliza mpelelezi aliye ongoza oparesheni ya kumsaka Khalid.

“Tumempa mateso ya kutosha”

“Ana weza kuzungumza?”

“Ndio mkuu”

“Nahitaji kumuona”

Nikavua koti langu la suti. Nikamkabidhi Judy kisha nikaingia ndani humu huku nikikunja mikono ya shati langu hili refu. Nikamtazama Khalid ambaye alichorwa kwenye picha na jinsi alivyo ana fanania ndio maana ime kuwa raisi kumkamata.

“Una nijua mimi ni nani?”

Nilizungmza huku nikimtazama Khalid aliye inamisha kichwa chini. Akanyanyua kichwa chake taratibu, uso wake umesha vimbishwa kwa kipigo.

“Nataka kujua jambo moja nani alikupatia oder ya kulipua kile kinu?”

“Ni makamu wa raisi”

“Alikulipa kiasi gani hadi utekeleze unyama wa kiasi kile na wewe ni nani na una fanya kazi gani?”

“Mimi nilikuwa ni mmoja wa wana sayansi kwenye vile vinu vya kutengeneza Nyuklia na tulipwa milioni mia moja kila mmoja”

“Na nani mwenzako alilipwa?”

“RPC Mvungi”

“Hivi una jua adhabu ambayo unapaswa kuipata?”

Nilimuuliza Khalidi huku nikimtazama usoni mwake.

“Naombeni munisamehe ni tamaa tu”

“Tamaa ya kuingizia nchi hasara kubwa kama hii, nchi imepoteza nguvu kazi kwa ajili ya upuuzi wa vichwa vyenu viwili?”

Nilizungumza kwa kufoka hadi Khalid alizungumza akilia kwa uchungu.

“Umenufaika na nini na hizo milioni mia moja ikiwa ulimfanya bibi yako kuwa ombaomba.”

“Muheshimiwa raisi nina omba unisamehe, ni tamaa tu”

“Tamaa una ua watu una ingizia taifa mabilioni ya pesa. Nisikilize, una dakika tano ya kusali sala yako ya mwisho”

“Ehee?”

“Nime kuambia una dakika tano ya kusali sala ya mwisho. Nina kuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe kwa sasabu hata Mungu wa mbinguni ata kuwa hajanihesabia dhambi juu ya watu kama nyinyi. Kuna wababa, wamama, watoto na vijana walikufa kutokana na ile simu kwa ajili ya upumbavu wenu. Hivyo salia na tubu dhambi zako kabla sija kuua na sina utani katika hili”

Nilizungumza huku nikichomoa bastola yangu niliyo ichomeka kwenye soksi ya upande wangu wa kushoto nikaikoki na kumuelekezea Khalid usoni mwake hadi akafumba macho huku mwili ukimtetemeka kwa woga.



Nikamtazama Khalid kwa muda kidogo kisha nikaishusha bastola chini na nikatoka ndani hapa kimya kimya na kumuacha akiendelea kutetemeka kwa woga.

“Mkuu tumfanye nini?”

Mkuu wa wapelelezi aliniuliza huku akinitazama,

“Aletwe RPC nahitaji kuzungumza naye”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Agizo langu likatekelezwa haraka kama nilivyo hitaji. RPC akaletwa akiwa tayari amesha ivishwa mwili wake, sehemu kadhaa za mwili zimejaa manundu kisawa sawa. Vijana wangu hawakuhitaji kumuonea huruma hata kidogo. Akaingizwa katika chumba cha mahojiano kwa ajili ya mazungumzo yetu sisi wawili. Nikaingia katika chumba hichi, nikavuta kiti kisha nikaketi.

“Laiti kama ninge kuwa na muda mrefu wa kukaa madarakani basi ningeifanya hii nchi kama Korea Kaskazini. Yaani kusinge kuwa na kisingizio cha haki za kibinadamu. Yaani kwa makosa kama haya ingekuwa ni kutandikwa chuma hadharani wewe na familia yako ili wakati mwengine mujifunze na kuacha uroho wa pesa kuliko roho za watu.”

Nilizingumza huku nikimtazama RPC usoni mwake.

“Sijui una nielewa?”

“RPC hakunijibu chochote zaidi ya kunitazama kwa macho ya huruma.

“Kwa nini muliamua kupeleka bomu kwenye eneo ambalo ulitambua kabisa nina kwenda kutembelea?”

“Nilihitaji ufe”

RPC alizungumza kwa kujiamini hadi nikashangaa.

“Naamini kifo changu kingekuwa ni sherehe sana kwenu?”

“Ndio hufai kuishi hata kwa dakika moja kwenye hii dunia. Na nina kuahidi nikipata nafasi ya kuishi tena ni lazima nita kuua”

Mlango wa chumba hichi ukafunguliwa na Judy akaingia, akainama nyuma yangu kidogo na kuninong’oneza.

“Mke wake na watoto wake wapo chumba kinacho fwata tufanyaje?”

“Nitumie video yao”

“Sawa”

Judy akanitumia video inayo muonyesha mke wa RPC pamoja na watoto wake watatu wakiwa katika chumba kingine katika jengo hili. Nikaitazama video hii yenye sekunde hamsini na tisa kisha nikamgeuzia simu RPC, macho yakamtoka na hofu ikamuingia.

“Ngoja nikuambie unakuwa ni mwanaume wa kipumbavu sana kuandamana katika kifo pamoja na mke wako na wanao. Sasa nahitaji kukuonyesha kwamba mimi sio mtu wa kuchezea kwa maana nikama niliweza kutekeleza agizo la kumua mtoto mdogo kwa kupewa oder maalumu basi na wewe siwezi kushindwa kuiteketeza familia yako ukishuhudia na nikuambie huto weza kupata nafasi ya kutoka eneo hili wala kuliona jua la kesho. Una kufa”

Machozi yakaanza kumwagika RPC.`

“Ina subiriwa amri yangu kutekeleza agizo”

“Mimi ndio mwenye dhambi familia yangu haina la kufanya juu ya hili. Tafadhali mkuu nina kuomba usiwaue vijana wangu wala mke wangu”

RPC alizungumza kwa sauti ya unyonge, jeuri na kiburi vyote vimeyayuka mithili ya barafu juani.

“Ulihisi ungeniua mimi familia yangu isinge rudisha kisasi kwako au endapo wangefahamu ukweli, ila kutokana na wewe ni msalitii katika mchi nyote muna kula chuma. Utashuhudia kuona wanao na mke wako wakiuwawa kisha utamaliziwa wewe”

Mara baada ya kuzungumza maneno hayo nikavuta kiti nyuma kisha nikasimama.

“Mkuu nina kuomba, nakuomba sana usifanye hivyo, wanangu wana ndoto kubwa kwenye maisha yao. Tafadhali?”

RPC alizungumza huku akilia mithili ya mtoto mdogo,

“Hata wale mulio waua walikuwa na ndoto zao pamoja na familia yao. Hivi nyinyi ni watu wa aina gani, kwa nini muna kuwa wabinafsi sana. Eheee?”

Nilifoka kwa hasira huku nikipiga piga ngumi juu ya meza.

“Kila mmoja ana haki ya kuishi, ila kwa tamaa za kipuuzi na upuuzi mukasababisha nchi kuingia kwenye shida na hasara kubwa. Hivi unalitambua hilo eheee?”

Nilizidi kuwa mkali na RPC safari hii akashindwa hata kuzungumza. Nikatoka ndani hapa huku macho yakiwa yametawaliwa na machozi ya hasira. Walinzi, washauri wangu wote wakabaki wakinitazama pasipo kunisemesha chochote.

“Nahitaji hewa”

Nilizungumza huku nikianza kupandisha ngazi zinazo elekea gorofa ya juu kabisa. Walinzi wangu wakaambatana nami, tukafika juu ya gorofa, nikasimama katika eneo ambalo nina weza kuuona mji huu wa Singida vizuri kwa maana jengo hili lipo katikati ya mji huu.

“Muheshimiwa”

Judy aliniita huku akiwa amesimama pembeni yangu. Nikamtazama tu pasipo kumjibu chochote.

“Ahaa kuna simu yako hapa kutoka kwa mke wako”

Nikaipokea simu ya Judy na kuiweka sikioni mwangu.

“Honey”

Cauther aliniita kwa sauti nyororo ambayo kidogo nikajikuta nikipata hata nafuu ya kuilainisha hasira yangu. Nikashusha pumzi nyingi kabla ya kuzungumza.

“Niambie mke wangu”

“Mbona una zungumza kama una hasira kuna nini tena?”

“Ni mambo tu madogo madogo mke wangu.”

“Pole sana mume wangu. Mimi nimesha fika kwa mama na hapa bibi alihitaji kuzungumza na wewe, nimemuambia upo kazini ila bado ana endelea kusisitizia hadi imebidi nimpigie Judy nilihofia kwamba una weza kuwa katika mkutano ndio maana nimeshindwa kukupigia”

Judy alizungumza kwa sauti laini na yenye kuvutia.

“Mpatie simu”

“Sawa mume wangu”

“Halloo mume hujambo wewe”

Niliisikia sauti ya bibi Cauther akizungumza kwa furaha.

“Sijambo bibi, shikamoo”

“Marahaba, umeniacha mume, sikuoni huku siku hizi kuna nini?”

“Bibi ni majukumu, ila nita kuja”

“Njoo bwana mume wangu, si unajua umemuona niliye mrithisha jina langu. Nahitaji kukuona bwana”

“Usijali nikirudi tu Dar es Salaam nita kuja hapo”

“Sawa mume rudi mapema bwana nime miss kupiga story na wewe”

“Hahaaa sawa bibi”

“Haya hapa roho yangu ime ridhika kwa maana si muna jua nyinyi vijana ukiona binti ana rudi rudi sana kwao una weza kukuta ndio tayari”

“Tayari nini bibi?”

“Tayari ameshaachwa, hivyo nilitaka kujua kwamba muna endeleaje?”

“Hahaa bibi nina mpenda sana mke wangu. Hivyo siwezi kumuacha hata moja”

“Sawa mume wangu. Kazi jema”

“Nawe pia bibi”

“Baby”

“Aisee bibi mameno yoye hayo amayatolea wapi?”

“Yaani wee acha tu mume wangu ana zungumza siku hizi sijui amekula na kitu gani”

“Aisee kazi kweli kweli. Ila mume wangu upo salama?”

“Nipo salama mke wangu. Tuta zungumza baadae”

“Sawa mume wangu, nina kupenda.”

“Nina kupenda pia mume wangu”

Nikakata simu na nikamrudishia Judy simu yake.

“Muheshimiwa raisi muda wa kwenda ikulu ume wadia sasa”

Mshauri mkuu alinieleza huku akinitazama usoni mwangu kwa maana maisha ya raisi yana kwenda kwa ratiba na siishi ninavyo hitaji mimi kuna baadhi ya mambo huwa ni lazima kufwata ratiba kwa ajili ya usalama wangu.

“Ila muheshimiwa raisi bado hajamalizana na hawa watu wawili. Khalid na RPC, muheshimiwa wale watu ni virusi kwenye hii nchi. RPC amekiri kabisa kwamba ni lazima ata kuu, tuna fanyaje?”

Judy aliuliza huku akinitazama machoni mwangu.

“Ila hayo ni maamuzi magumu ambayo raisi ana paswa kuyafikiria kwa mara ya pili”

Mashauri mkuu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nahitaji kupumzisha kichwa changu. Haya mambo ya kiswahili yata nizeesha bado mdogo sana”

Nilizungumza na kuondoka eneo hili. Tukaanza safari ya kuelekea katika ikulu ndogo iliyopo mkoani hapa Singida. Nikapokelewa vizuri na watu wa hapa, nikanyeshewa chumba cha kupumzika.

“Natamani uchaguzi ufike aisee”

Nilizungumza huku nikikaa kwenye moja ya sofa humu chumbani kwangu, Judy akakaa kwenye sofa jengine huku mshauri wangu na Willy wakikaa katika sofa jengine.

“Kwa nini kaka?”

“Haya maisha yamenichosha munajua. Yaani muda mwengine una weza kufanya maamuzi ambayo yanaweza kukuleta shida baadae”

“Ila ndio uongozi huo mkuu. Kuna wakati ina bidi ufanye tu maamuzi magumu kwa ajili ya kuinusuri amani ya nchi”

Mshauri wangu alizungumza huku akinitaza.

“Hapo ndipo kunapo washinda viongozi wengi wa Kiafrika. Wengi wana fanya maamuzi ambayo huleta shida kwenye nchi zao”

“Hivi lile swala la Somalia limefikia wapi?”

Niliuliza.

“Somalia bado kina nuka, jeshi la serikali ya sasa ambalo ndio hilo la Al-Shabab lina jitahidi kupambana na jeshi la raisi aliye tolewa madarakani ambaye kwa sasa yupo kwa uhamisho nchini Afrika Kusini”

Willy alijibu kwa maana yeye muda mwengi yupo kwenye maswala ya mtandao na ana fahamu mambo mengi sana yanayo endelea huko duniani.

“Ila muheshimiwa raisi hii ina weza kuwa nafasi kwetu sisi kama nchi kunufaika na vita hiyo”

Mshauri wangu alizungumza huku sote tukimtazama machoni.

“Una maanisha nini?”

“Nchi kama sasa hivi ipo kwenye vita. Sisi tuna silaha za kisasa na zenye nguvu. Tuna weza kuwauzia jeshi la huyu raisi aliye chaguliwa na watu na akaenda kupambana na sisi tukapata pesa”

“Kama ametolewa madarakani ina maania alikimbia kila kitu, hivyo sidhani kama ata kuwa na pesa ya kutupa sisi ili kumuuzia silaha.”

“Muheshimiwa raisi ni kweli ata kuwa hana pesa ila hii tuna ingia naye mkataba wa kumsaidia na ndani ya kipindi fulani nchi yetu ita kuwa ina nufaika na baadhi ya maliasili zilizopo Somalia”

“Kwani Somalia wana maliasili gani kwa maana ile nchi maeneo mengi niliyo pita yapo chini sana kiuchumi”

Niliuliza kwa maana Somalia nilisha wahi kwenda kipindi cha nyuma kwenye baadhi ya oparesheni za kundi langu la X.

“Muheshimiwa raisi ina mali nyingi, wana mafuta wale, wana gesi, wana Uranium, iron one, tin, gypsum, bauxite, copper na chumvi”

Mshauri wangu mkubwa alizungumza.

“Duu!!”

“Ndio muheshimiwa raisi, hawa tukiwasaidia kwa siri, tuna weza kupiga pesa nyingi sana kutoka kwenye hizo maliasili zao na nchi yetu ikazidi kupanda kiuchumi na kuwa na nguvu zaidi ya hii na pia madini hayo ya Uranium yana msaada mkubwa sana kwetu kwenye nyuklia.”

Nikakaa kimya huku nikiwatazama hawa washauri wangu.

“Muheshimiwa raisi tuna uwezo wa kushinda hii vita. Maamuzi ni kwako tu, tuna wapiga Al-Shabab na wana anchia madaraka na tuna yarudisha kwa raisi aliye tolewa”

“Hofu yangu hawa jamaa huwa hawatabiriki jamani. Una jua Kenya wana teswa sana na hawa jamaa sasa nahofia hiyo vita ikaletwa hapa kwetu. Nchi kubwa hii jamani, ina amani na wananchi hawajazoea hayo mambo ya kulipuliwa lipuliwa na watu walio choka kula ugali na wana amua kujitoa tu muhanga”

“Ila ni kweli muheshimiwa raisi ila tuna jeshi na tuna uwezo wa kuilinda nchi. Nafasi hii tuitumie kabla Marekani hajakamata fursa hiyo na kama unavyo jua Mmarekani akipata hizo Urenium, ata tupia kwenye soko la nyuklia”

“Mshauri wangu aliendelea kuzungumza kwa kunishawishi”

“Willy nime bakisha siku ngapi kabla ya kumaliza kazi yangu?”

“Siku sabini na tano?”

Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari siku hizi sabini na tano.

“Siku kumi zina tosha kuwapiga ehee?”

Niliuliza.

“Sio kumi tu mkuu. Siku mbili tu tuna iteka miji yao waliyo ishikilia hususani Mogadishu kisha tuna rudisha serikali madarakani”

“Ila watatuona wazinguaji sana kwa maana walituomba msaada tuka wachomolea?”

“Lawama hizo zita pelekwa kwa raisi aliye pita ila sio wewe. Muheshimiwa raisi hii ninafasi kwetu kukuza uchumi mara dufu”

“Ila nina ushauri jamani”

Willy alizungumza.

“Ushauri gani?”

“Kama tuna kuwasaidia hawa jamaa ina bidi iwe ni kwa siri sana kwa maana endapo tukijionyesha kama Wamarekani, wana weza kuweka visasa na kumbukeni hawa jamaa visasi vyao ni vya kuambukizana kutoka kizazi kimoja hadi kingine hivyo, sisi tuna weza tusiwe hai duniani ila watoto na wajukuu wetu tukawaachia majanga ambayo wata yalaani kwa maana yamesababishwa na sisi watatu wanne humu ndani”

“Hiyo nayo ni pointi dogo. Yaani hao ni kama Al-quida. Hawafai kabisa na hawana huruma kabisa, una kuta mtu ana rithi kisasi cha Marekani na Osama Bin Laden ikiwa watu hao walisha fariki”

“Ila tukisema mkuu tuangalie hivyo hatuto zidi kuwa wakubwa. Nini maana ya kuwa nchi tajiri na yenye nguvu duniani? Maana yeka ni kuhakikisha kwamba tuna fanya vitu ambavyo nchi nyingine haziwezi kufanya hivyo vitu”

“Judy upo kimya changia basi mada”

Nilimuambia Judy huku nikimtazama usoni mwake.

“Ukiona kobe ame inama basi uje ana tunga sheria. Ngoja nita wapa pointi ya muhimu”

“Sawa, ila….”

Maria akafungua mlango na kuingia ndani hapa.

“Aha..muheshimiwa raisi kuna video call yako”

“Kutoka wapi?”

“Raisi wa Marekani ana hitaji kuzungumza na wewe”

“Mimi?”

“Ndio”

“Ila mimi sina urafiki naye kabisa ina kuwaje?”

“Urafiki una sehemu ya kuanzia hivyo ina bidi uende kumsikiliza”

Mshauri mkuu alizungumza na nikakubaliana na hilo. Nikanyanyuka na kuelekea katika ofisi iliyopo hapa. Nikaaa kwenye kiti na kuwasha computer hii yenye kamera inayo niwezesha kuonekana na kuweza kufanya mazungumzo na raisi wa Marekani.

“Muheshimiwa raisi Eddy habari yako”

“Salama muheshimiwa raisi habari ya wewe?”

“Mungu ana bariki. Nina ajenda ndogo ningependa tuweza kuijadili kwa maana nimeona wewe ni mtu mwenye msimamo na tuna weza kuendana katika fikra za ajenda hii”

“Karibu nina kusikiliza muheshimiwa raisi”

Washauri wangu wote wapo nyuma ya computer hii wakifwatilia kile ninacho zungumza na raisi wa Marekani.

“Dunia ime yumba kwa kupoteza viongozi wao nchini Ujerumani. Al-quida waliidhihirishia dunia kwamba wana husika kwenye ulipuaji wa bomu lile. Ningependa tuunde timu itakayo husika na oapresheni ya kulipiza kisasi kwa hao Al-Quida kwa maana sisi tukikaa kimya ni ishara ya kukubaliana na lile walilo litenda kwa viongozi wengine”

Nikaka kikmya kwa sekunde kama ishirini hivi.

“Ni wazo zuri. Ila nitaomba muda wa kulifikiria kisha nita kurudishia jibu”

“Nita shukuru sana muheshimiwa raisi, nina imani utanipatia jibu zuri”

“Usijali”

Nikakata simu hii na katika kioo cha computer hii ikatokea nembo ya raisi. Nikawatazama watu wote waliomo ndani hapa.

“Huu ni mtego kaka, Marekani hawezi kufanya jambo bure bure kwa hisia zangu tu hizi ndogo nina imania ana hitaji kutupeleleza juu ya nyuklia na anedapo akajua basi tumekwisha kaka”

Willy alizungumza kwa msisitizo kiasi cha kunifanya nitingishe kichwa kama ishara ya kukubaliana naye kwa maana Marekani hawezi kuungana na mtu au kumsaidia mtu bila ya kuwa na faida nyuma ya muungano huo kwa jinsi walivyo wajanja kwa kujipatia pesa zisizo halali na sisi ni wajanja namna hiyo hiyo hivyo hapa ngoma ndroo.



“Siwezi kukubali dili kwa watu wajanja kama hawa. Sasa hivi tuliangalie kwanza hili swala la Somalia.”

Nilizungumza huku nikibadilisha mada ya kuwazungumzia hawa Wamarekani.

“Kwa hiyo muheshimiwa raisi ume kubaliana na swala la kuwasaidia Wasomali?”

“Ndio ila kwa faida, kama hatuto pata faida basi hatuwezi kufanya nao kazi. Nahitaji kuiacha hii nchi kwenye nafasi nzuri ya kuipatia pesa na mali nyingi”

“Ni maamuzi mazuri hayo muheshimiwa raisi.”

“Sasa andaeni mazingira ya kuonana na raisi aliye pinduliwa ili nikae naye mezani kwa ajili ya mazungumzo”

“Nita lishuhulikia hilo muheshimiwa raisi”

Mshauri wangu mkuu alizungumza na kutokana nina muamini sikuona haja ya kumpa maelezo ni wapi na muda gani wa kuonana na huyo raisi wa Somalia. Siku ikaisha kwa kupitia mafaili yanayo husu changamoto za mkoa huu wa Singida.

Siku iliyo fwata nikafanya ziara kwenye miradi miwili ya uchimbaji wa madini kisha safari ya kurudi jijini Dar es Salaam ikaanza.

“Judy”

“Ndio mkuu”

“Nahitaji msafara huu uende moja kwa moja kwa wakwe zangu”

“Sawa muheshimiwa”

“Nalala kidogo”

Taratibu nikaikunjua siti yangu na nikajilaza huku safari ikizidi kusonga mbele.

“Mkuu”

“Naam”

“Tupo Morogoro”

“Duu safari imekwenda kasi sana”

“Ndio”

“Si hakuna kizuizi cha kusimama njiani?”

“Ndio”

“Naomba maji”

Judy akafungua kifriji kidogo kilochopo ndani ya gari hili, akanikabidhi chupa ya maji.

“Aisee nilichoka sana”

“Pole sana mkuu”

Safari ikazidi kusinga mbele na tukafika jijini Dar es Salaam. Moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwa wakwe `zangu pasipo kuwapa taarifa. Tukapokelewa kwa furaha sana na mama mkwe huku akishangaa jinsi walinzi wangu walivyo makini kuhakikisha kwamba nina kuwa salama.

“Karibu sana mume wangu”

Cauther alizungumza huku akinikumbatia, akanaipiga mabusu kadhaa mdomoni mwangu.

“Shukrani sana mke wangu, vipi hali yako?”

“Ninamshukuru Mungu nipoo salama mume wangu. Nimekumiss tu”

“Nimekumiss pia. Bibi yupo wapi?”

“Yupo chumbani kwake, amejipumzisha”

“Nimeamka”

Bibi Cauther alizungumza huku akitoka hapa sebleni, akanikumbatia kwa furaha.

“Umependeza sana mume wangu”

“Nashukurukuru mke wangu”

“Leo nataka kuondoka na wewe twende ikulu nami nikapaone jamani kabla sijakufa”

“Hahaaaa usijali mke leo tutaondoka wote”

Bibi Cauther akajawa na furaha sana. Kikaandaliwa chakula cha usiku na kwa pamoja tukala.

“Sijamuona baba yupo wapi?”

“Amekwenda Dubai”

Mama mkwe alinijibu.

“Aahaa sawa sawa”

Tukamaliza kupata chakula cha usiku na majira ya saa tatu usiku tukaondoka nyumbani hapa na kuelekea ikulu huku bibi Cauther akiwa haamini anacho kiona kwani sio jambo la kawaida kwa raia wa kawaida kupanda gari la raisi. Tukafika ikulu na kumkaribisha nyumbani bibi Cauther.

“Muheshimiwa raisi una hitajika commanding room”

Mshauri wangu mkubwa alininong’oneza sikioni mwangu.

“Baby tangulia na bibi nina kuja”

“Sawa mume wangu”

“Mke nina kuja mara moja”

“Una enda wapi tena?”

Bibi Cauther alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia.

“Kuna swala nina kwenda kulishuhulikia mara moja”

“Ila si uta rudi?”

“Ndio”

“Sawa mwenyezi Mungu akuongoze”

“Amen”

Nikaondoka eneo hili na walinzi wangu pamoja na washauri wangu.

“Kuna nini kilicho tokea?”

“Kuna shambulizi limetokea nchini Kenya na walio fanya shambulizi hilo ina sadikika ni wanajeshi wa Tanzania?”

“Tanzania? Imekuwaje na ni shambulizi la nini?”

“Kuna mji upo mpakani mwa Tanzania na Kenya ndio hicho wanacho dai kwamba kime vamiwa na wananchi karibia mia nane na tisini wameuwawa kwa risasi na mabomu”

“Mungu wangu! Ni mji tukio hilo limetokea?”

“Mji wa Marindi”

“Napafahamu”

Nilizungumza huku nikifungua vifungo vya koti langu, tukaingia katika ukumbi huu wa kuendesha oparesheni zote za kiusalama. Nikavua koti langu la suti na kuliweka nyuma ya kiti anacho kaa raisi, nikakuta washauri wengine wakiwemo wa kuu wa vyombo vya usalama. Baada ya kukaa kila mtu akakaa.

“Picha za video pamoja na picha za kawaida zina onyesha namna gania ambavyo wanayeshi walio valia mavazi ya Tanzania wakiwaua wananchi.

“Hawa sio wanajeshi wangu”

Nilizungumza huku nikitazama video inayo onyesha jinsi wanajeshi wakifyatua risasi kwa wananchi walio kwenye mgahawa mmoja.

“Muheshimiwa raisi, raisi wa Kenya anahitaji kuzungumza na wewe”

Maria alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ni video call?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Pokea”

Ikaunganishwa video call hiyo kwenye tv kubwa iliyopo ndani ya chumba hichi.

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Jeshi lako limeua watu wangu na sinto rudi nyuma kwenye hili ni lazima nitwashuhulikie”

“Ngoja ngoja kwanza muheshimiwa raisi. Punguza jazba na kumbuka una zungumza na raisi mwenzako wa nchi.”

“Siwezi kupunguza jazba ikiwa wamama, watoto, wanaume watu kibao wamekufa kwenye ardhi yangu. Marindi nzima ina vuja damu, upo wapi ujirani mwema, Ehee?”

Raisi wa Kenya aliendelea kufoka, nikashusha pumzio huku nikimtazama.

“Muheshimiwa raisi nikuhakikishie jambo moja. Nchi yangu ina heshimu kila nchi iliyopo jirani nasi na hata walipo mbali sana. Hatujafanya huo upumbavu kwa maana siwezi kutoa amri ya kipuuzi namna hiyo, hilo ni moja. Mbili jeshi langu ni jeshi tiifu na lipo kwa ajili ya kulinda nchi na kusaidia mataifa mengine, jeshi langu halipo kwa ajili ya kuvuruga amani katika nchi yoyote hapa duniani. Tuna elewana muheshimiwa?”|

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama raisi wa Kenya ambaye mazungumzo haya yana fwatiliwa na watu wote ndani ya chumba hichi.

“Kwa hiyo kilicho onekana na video inayo samba ni filamu na maigizo?”

“Sio magizo wala filamu, ila ukweli ni kwamba hao sio wanajeshi wangu japo mavazi yaliyo valiwa ni ya kama wanajeshi wa nchi yangu. Jambo la msingi ni sisi kushirikiana ili kufahamu ni nani na nani ambaye ana weza kubebe hili swala”

“Muheshimiwa raisi sikuelewi. Watu wangu wamekufa una niambia nitulie ehee?”

Raisi wa Kenya aliendelea kuzungumza kwa kufoka hadi nikajikuta nikianza kujawa na gadhabu.

“Muheshimiwa raisi tafadhali nime kuambia tushirikiane kwenye hili na kujua ni nani muhusika. Hapa tume chonganishwa sisi kwa maana hapa sisi kama nchi hatuna kosa.”

“Nina kupa masaa mawili ya kunipatia maelezo ya kina na nani amehusika la sivyo tuna tangaza vita dhidi yenu”

Video hii ikakatwa na kila mtu aliye kuwa kawatia wakati wa wasiwasi akashusha pumzi nzito.

“Luteni Jenerali, andaa jeshi tayari kwa kupiaga vita. Nahitaji vifaru vya kijeshi vipelekwe kwenye mipaka yote ya Kenya na Tanzania. Mabomu ya nyuklia makubwa manne, yaelekezwe Kenya. Hakikisheni yana piga pande nne zote za Kenya na ndani ya dakika ishirini, tuna ifuta kwenye ramani ya dunia. Tuna elewana?”

Nilizungumza kwa kujiamini na kuwafanya watu wote macho kuwatoka kwa mshangao.

“Ndio muheshimiwa raisi”

Luteni Jenerali alikubaliana na amri yangu.

“Hakikisha kwamba battle ship zote zina wekwa tayari. Hakikisha ndege zote za kijeshi zina kuwa tayari kwa mashambulizi ya anga na kuanzi sasa hivi natangaza hali ya hatari. Kila mwana usalama atangaziwe hali hiyo”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Luteni Jenerali alijibu kwa ukakamavu.

“Ila muheshimiwa raisi hili jambo tuna weza kulimaliza kidiplomasia tu.”

Mshauri wangu mmoja wa mambo ya nje ya nchi alizungumza huku akinitazam usoni mwangu.

“Diplomasia kweli ina weza kufanya kazi ndani ya masaa mawili tuliyo pewa. Nilipo kula kiapo cha nchi yangu niliahidi kuilinda nchi yangu. Hivyo kwanza kujiandaa ni lazima kisha diplomasia ita fwata. Nishaurini nini nifanye”

“Muheshimiwa raisi ina bidi tuweze kufanya utambuzi wa sura za wanajeshi hao kwamba rekodi zao zina soma wapi kwani kuna wanjeshi wawili sura zao zime naswa kwenye ile video hivyo vijana wangu wana zifanyia scaning ili kuweza kuwatambua”

Madame Caro alizungumza.

“Ita chukua muda gani?”

“Muda si mrefu mkuu?”

“Nipatie muda maalumu?”

“Dakika kumi hadi kumi na tano muheshimiwa”

“Hembu play tena ile video?”

Video ikachezwa tena na nikaanza kuitazama upya.

“Moja jeshi langu la Tanzania hatutumii bundiki hizo kwa maana sisi tuna zalisha bundiki zetu sisi wenyewe na hizo bundiki zilikuwa zina tumika miaka thelathini iliyo pita. Mbili kombati za jeshi langu zimekolea rangi na hizo zime pauka na zina onyesha ni chakavu.”

Nilizungumza huku nikitazama wanajeshi walio funika sura zoa ila wana mavazi ya nchi yangu ya Tanzania.

“Hembu simamisha?”

Video ikasimamishwa.

“Zoom viatu vya mwanjeshi aliye simama kule mbele”

Nilitoa maelekezo na kijana wa IT akavivuta kwa ukaribu viatu hivyo.

“Mumeona, jeshi langu hazivai buti kama zile. Hembu scan na ujue hivyo viatu vina valiwa na wanajeshi wa nchi gani?”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Baada ya dakika mbili kijana huyu akatugeukia.

“Muheshimiwa raisi viatu hivo vina tumiwa na wanajeshi wa nchi ya Somalia hawa wa sasa”

‘Makamu wa raisi sasa nime kupata umawasaidia waasi kuingi madarakani alafu una taka watuchonganishe na Kenya”

“Ina maana ni Al-Shabab?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

Nikashusha pumzi huku nikitafakari nini cha kuzungumza. Nikamuita kwa ishara mshauri wangu mkuu na akanifwata nilipo kaa.

“Raisi aliye tolewa madarakani umefikia wapi kumpata?”

“Kesho ana fika hapa Tanzania kimya kimya”

“Sawa”

Mazungumzo yetu ya kunong’onezana hayakusikiwa na mtu wa aina yoyote zaidi ya sisi wawili.

“Muheshimiwa raisi ina bidi tutume huu ushahidi kwa nchi ya Kenya na kuwaeleza ni hao Al-Shabab ndio wana endelea kuwatesa”

Mashauri mwengine alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Mpigieni raisi wa Kenya video call”

“Sawa”

Ikapigiwa video call na ikapokelewa kwa muda mfupi na tukamuona raisi akiwa na kamati yake ya viongozi wa ngazi za juu za kiusalama.

“Umefika wapi?”

Raisi huyu wa Kenya alizungumza kwa kujiamini na kiburi kidogo.

“Tumepata ushahidi wa kudhibitisha kwamba walio husika sio wanajeshi wangu. Tuna tuma picha na udhibitisho wa kwanini tuna sema sio wanajeshi wetu.”

Picha zikatumwa na kijana huyu wa I.T.

“Hizo picha hapo zina onyesha bundiki hizo ambazo Tanzania jeshi langu waliacha kuzitumia zaidi ya mika thelathini iliyo pita. Tuna tengeneza silaha zetu sisi wenyewe na ndio zinazo tumika kwenye majeshi yetu. Kombati zetu za jeshi zime kolea rangi yake ya mabaka baka, ila hizo ukizitazama rangi yake ime pauka. Tatu wanajeshi wangu hawavai buti za aina hiyo na tumegundua buti za aina hiyo zina valiwa na wanajeshi wa nchi ya Somalia hawa walio pindua serikali yao”

“Una hisi huo ushahidi wako una tosheoleza sisi kuwaamini ikiwa mume ua watu wetu ehee?”

Raisi alizungumza kwa kufoka sana.

“Muheshimiwa raisi kabla hatujasonga mbele nikuambie jambo moja tu. Sitaki unifokee, zugumza kwa heshima na upole nita kuelewa, unavyo payuka usihisi kwamba mimi siwezi kupayuka, nina uwezo wa kukufokea hata kama umenipita umri. Hivyo heshima ya kirahisi ifwate mkondo wake.”

“Siwezi kukaa kimya au kuzungumza kwa upole kwa ajili yako. Masaa yana zidi kuzonga mbele hivyo nina hitaji munipatie ushahidi wa kueleweka na sio upumbavu upumbavu kama huu. Hivi una jua uchungu wa vifo vya wananchi wewe ehee?”

Raisi wa Kenya aliendelea kufoka kana kwamba ana zungumza na mwanaye wa kumzaa.

“Muheshimiwa raisi kuwa na heshima na raisi wangu. Tunazungumza na wewe kiustarabu kwa sababu tuna hitaji urafiki ulipo katika nchi zetu uendelee kudumu milele na milele. Sasa unapo zungumza hivyo una mvunjia heshima raisi wetu.”

Judy alizungumza kwa msisitizo na kujiamini.

“Wewe malaya wa kike unaye ingilia mazungumzo ya viongozi wako ni nani haswa?”

Tusi hili kikawa ni kama mkuki wa mto ulio penya katika moyo wangu. Nikajikuta nikifumba macho kwa sekunde huku nikimnyooshara Judy ya kuto kujibu chochote na wala mtu yoyote kuzungumza chochote kwenye hili.

“Ninacho kihitaji ni nyinyi kulipa kwa hili mulilo lifanya”

Raisi wa Kenya aliendelea kufoka.

“Kabla hujakata simu yako nahitaji kukuonyesha kitu raisi. Heshima ni jambo moja kubwa sana kwenye maisha ya kila binadamu. Umeshindwa kumuheshimiwa mshauri wangu binafsi na kumuita malaya mbele ya kamati yangu ya ulinzi na kamati yako ya ulinzi hili tusi nina kuapia kwa jila la mama yangu, halite kwenda bure. Nimekuvumilia ime tosha sasa nina ona masiko yana kwenda kuvuka ukubwa wa kichwa. Sasa ni hivi, hatutoi ushahidi wowote juu ya tukio hilo. Kwa sababu umesema ushahidi wa awali ni upumbavu.”

“Ndio ni upumbavu…..”

“Sijamaliza na ninapo zungumza usinikatie na funga kinywa chako”

Sasa nikaanza kubadilika na hasira niliyo ificha kwa muda mrefu ikaanza kunitawala.

“Una niambie nini?”

“Funga bakuli lako na usi jaribu kuzungumza tena ninapo zungumza. Luteni Jenerali umefikia wapi?”

Nilizungumza huku nikimtazama Luteni jenerali.

“Kila kitu kipo tayari mkuu”

“Tuma video ya kila kitu?”

Ndani ya sekunde kumi video za jinsi hali inavyo endelea mipakani, baharini, angani na mabomu ya nyuklia yakiwa tayari kwa mashambulizi ikaonekana kwenye tv kubwa zilizopo humu ndani.

“Una ona kinacho endelea ndani ya nchi yangu, kama wewe una kaa na hao watu wako kupanga ni namna gani ya kuishambulia Tanzania, kabla ya kikao chenu kuisha nita kuwa nimesha waua wote. Nitaisambaratisha nchi yako ndani ya dakika kumi tu na hakuna atakaye weza kuitafuta hata mabaki ya nchi yako. Sasa wewe leta bangi, uone kama sijawapiga kuanzia ardhini, majini na angani na nikiwashindilia na bomu hizo nne za nyuklia ambazo ni megatons 50 za TNT(210PJ) Sasa wewe fanya fweeeee mimi nitafanya fwiiiiiii. Uta kwenda kusimulia kuzimu”

Nilizungumza kwa sauti nzito na iliyo jaa mikwaruzo ya hasira hadi nikamuona raisi wa Kenya na kamati yake macho yakiwatoka kwa maana wakijichanganya tu, nina wafanya kama Hiroshima.



Ukimya utakawala ndani ya chumba hichi huku raisi wa Kenya na viongozi wake wakikaa kimya wakinitazama machoni mwangu kwa wasi.

“Aha samahani muheshimiwa raisi mimi ninaitwa Otieno ni mshauri wa maswala ya kidiplomasia. Ningependa hili swala tuweze kulizungumza kwa amani na tusifikie kwenye maswala ya kivita kwa maana sisi na nyinyi ni marafiki kwa miaka mingi sana toka miaka ya stini na kitu. Hivyo muheshimiwa raisi nina kuomba sana tuzungumze kwa amani”

Mzee Otieno alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyenyekevu.

“Mimi sina shida na nchi yenu ila nime chukizwa na kitendo cha raisi wenu kunijia juu na kumtukana mshauri wangu binafsi hivyo tumewapa ushahidi wa kila kitu kwamba wanajeshi hao hawajatokea nchini Tanzania na hatujahusika, miaka mingapi nyinyi na sisi tumekuwa marafiki, je kuna hata raia wenu aliye uwawa ndani ya nchi hii. Kwa nini tuvamia mji huo kwa jambo gani haswa tunalo lihitaji. Ehee?”n

Nilihoji huku nikitazama.

“Ni kweli muheshimiwa raisi ila tunaomba mazungumzo ya amani yafanyike”

“Kabla hatujasonga mbele, raisi wenu ina bidi aombe msahama kwa mshauri wangu na kamati yangu nzima iliyo kaa hapa kwa maana hapa hakuna mototo wake ambaye ana weza kumfokea na kumkaripia mithili ya mototo mdogo”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama raisi wa Kenya. Nikamuona kifua chake jinsi kinavyo panda akionekana akivuta pumzi na kuishusha.

“Binti nina omba unisamehe, ni hasira ndio zime nifanya niwe hivi. Pia nina waomba wote munisamehe kwa maana hata kama ingekuwa ni nyinyi mupo kwenye hali hii ni lazima munge kuwa wakali sana ila. Nina waomba sana tuweze kusamehana”

“Mimi nime kusamehe muheshimiwa raisi”

Judy alijibu na kila mmoja akakiri kwamba watumesamehana na mazungumzo ya amani sasa yakaanza kwa maana mambo yalisha vurugika na amani baina yetu ilisha anza kupotea.

“Ni miaka mingi tumekuwa tukipiga na kundi hili la kigaidi la Al-Shabab, tumekuwa tuna pambana nao usiku na mchana kuhakikisha kwamba tuna washinda ila kwa bahati mbaya kwa sasa wanaongoza nchi hivyo wamezidi kuwa na nguvu kubwa tofauti na pale mwanzoni walipo kuwa. Je nyinyi wezetu mumejipangaje juu ya hawa watu kwa maana kwa hili walilo lifanya ni uchonganishi mkubwa sana ambao una weza kusababisha mafarakano katika nchi zetu”

Raisi wa Kenya alizungumza kwa sauti ya upole sasa. Maria akanisogelea na akaninong’oneza sikioni mwangu.

“Muheshimiwa raisi kuna habari inayo endelea kwenye vyombo vya habari juu ya hili tukio”

“Hembu washa tv”

Maria akawasha tv nyingine na tukaona kutuo cha CCN kikitangaza juu ya kutokea kwa uvamizi wa jeshi la Tanzania katika mji wa Marindi Kenya.

“Hii habari nyinyi ndio mumeiachia?”

Nilimuuliza raisi wa Kenya kwa maana ana tazama hichi tunacho kitazama sisi.

“Hapana sio sisi na ndio maana tuliweza kuwasiliana nanyi wakatu tykio hili lina tokea, hatukutaka kutangaza moja kwa moja ndio maana vyombo vya habari vya ndani ya nchi yetu havijatangaza kabisa juu ya tukio hilo”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikiwatazama watu wangu.

“Muheshimiwa raisi muna onaje mukatoa statement juu ya kwamba sisi hatuhusiki kwenye hili kwa maana kama hivi vyombo vya habari vya kidunia vimeanza kutangaza hili jambo basi hali ina weza kuwa mbaya kwa upande wetu”

Waziri wa mambo ya nje alizungumza.

“Hilo halina tatizo. Tutahakikisha kwamba tuna ieleza dunia kwa kila jambo ambalo lina endelea na nyinyi tungependa muweze kulikataa hili jambo.”

“Tuna wahakikishia kwamba sisi tuta lifanya hilo hakuna tatizo lolote. Ehee turudi kwenye biashara, hawa magaidi tuna kwenda kuwafanya nini?”

“Tungeomba vikosi vyetu viungane kwa pamoja na kuwashambulia hao Al-Shabab na tuweze kuwatoa madarakani na nina imani ita kuwa ni jambo zuri kwa upande wetu kwa maana sisi wana tusumbua sana”

Nikaka kimya huku watu wakinitazama na kunisikilizia kama nina weza kukubaliana na jambo hilo.

“Nimepigana vita nyingi sana hususani na makundi ya magaidi kama Al-quiada, Islamic State na hao Al-Shabab wenyewe. Kitu ambacho nina kifahamu, visa huwa wana virithisha kwa vizazi hadi vizazi ndio maana una weza kuona nyinyi hadi leo hii hamna amani kwa watu hawa. Labda niweze kushauri jambo moja ambalo lina weza kutusaidia kuimaliza vita hii”

Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nikaendelea kuzungumza.

“Tunapaswa kuwafuta hawa Al-Shabab kwenye uso wa dunia. Tusiwapige wakatoroka, ila tuwapige na kuwaua wote. Akitoroka hata mmoja ana kwenda kuanzisha kundi lake taratibu na wana kuwa wengi kwa maana hawa wamejengewe uwezo na mafunzo ya kuweza kuunda vikundi na watendelea na misimamo yao ile ile ambayo kwa hapo baadae ita kwenda kututesa kama inavyo tutesa sasa hivi. Jambo la msingi na kubwa ni kuhakikisha kwamba tuna waua wote na hatoto peleka jeshi kubwa ina tupasa kupeleka makomandoo. Makomandoo wenye uwezo wa kupiga kimya kimya hadi wakaisha”

“Ila muheshimiwa raisi tukumbuke kwamba jamaa wameshikiliz nchi nzima na sidhani kama makomandoo wana weza kuikamilisha kazi hiyo kwa nchi nzima na ile nchi ina ukubwa wake muheshimiwa raisi na isitoshe wana bahari hivyo ukisema kwamba hawato kukimbia, ita kuwa ni ngumu wana weza kutumia hata bahari na wakatoroka”

Raisi wa Kenya alishauri.

Mshauri wangu akanisogelea na kuninong’oneza.

“Muheshimiwa raisi, una onaje hili swala tungeliacha kwanza hadi tunge kutana na raisi wa Somalia aliye pinduliwa madarakani kwa maana ni asubuhi tu ndio ana fika hapa”

“Sawa. Muheshimiwa raisi hili swala la mashambulizi ya hilikundi la Al-Shabab tungependa nizungumze na vikosi vyangu kisha tuta warudia na kuwaeleza ni wapi tulipo fikia.”

“Sawa muheshimiwa raisi na tuna omba amani izidi kutawala kati yetu na tusamehane kwa kila jambo”

“Hakuna shaka kila jambo litakuwa vizuri”

“Asante”

Mazungumzo ya kikao chetu kwa njia ya video call yakaishia hapa.

“Waziri wa mambo ya nje hili swala la kukanusha uta lishuhulikia usiku huu”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Hongera sana muheshimiwa raisi”

Chief secretary alizungumza huku akinitazama kwa furaha.

“Hongera ya nini madame”

Nilimuuliza mwana mama huyu.

“Ujasiri wako na kujiamini kwako na ufanyaji wako wa maamuzi ume weza kulifanya hili swala liende kwenye mstari tofauti na vile tulivyo kuwa tuna dhani. Wewe ndio raisi tunaye muhitaji kwenye hii nchi”

“Nashukuru ila wakati wa mimi kuwa raisi bado sana. Ila tuombeane kwa mwenyezi Mungu kila jambo lita kuwa vizuri”

“Mungu akubariki”

“Amen. Ndugu zangu nina imani kikao chetu kimeisha hapa, nina shukuru kwa kuja kwenu kama kuna mtu ana ushauri au wazo lolote ana weza kuzungumza”

“Muheshimiwa raisi mimi nina ushauri”

“Karibu ndugu yangu”

“Kwa kipindi hichi kidogo ulicho ongoza hii nchi, kuna heshima imerudi kwenye hii nchi. Heshima ya kuwa nchi ya kuogopwa sasa imerudi, kwa ushauri wangu ningependa katiba ya kumruhusu raisi kugombania uraisi ivunjwe na irekebishwe upya na raisi ashushiwe umri hadi afikishe miaka thelathini”

“Hahaaa mutakuja kupata viongozi vichaa. Musiangalie kwa maisha ya sasa hivi angalieni kwa maisha ya baadae kwa hao tutakao waachia hizo nafasi wata zitumiaje. Sasa hivi acheni madame Caro asimame kwenye kugombania uraisi na baada ya kipindi chake kuisha nina imani kwamba mambo yana weza kuwa mazuri.”

“Ila muheshimiwa raisi, uwezo wa kuongoza unao ila kikwazo ni umri tu”

“Ni kweli jamani ila tuombe uzima na afya nina imani sinto waangusha”

“Amen”

Jambo la kumshukuru Mungu watu hawa wananielewa na wana weza kuendana na misimamo yangu. Baada ya kikao hichi kuisha nikaagana na kila mmoja na kurudi eneo ninalo ishi. Nikamkuta Nadia akiwa peke yake sebleni.

“Hujalala?”

“Leo sina hata usingizi shem”

“Bibi na dada yako?”

“Wamelala toka saa tano usiku”

“Aise ehee niambie shemeji yangu”

Nilizungumza huku nikikaa kwenye sofa linalo tazamana na sofa alilo kaa Nadia, nikatazama saa yangu ya mkononi ina onyesha sasa hivi ni saa nane usiku.

“Safi shem nina hamu na wewe ile mbaya”

“Mmmm mazingira sio rafiki?”

“Jamani shem eneo lote hili jamani, kidogo”

“Ngoja nitazame mazingira kisha nita kukuja”

“Usiniangushe shemeji”

“Usijali”

Nikaingia chumbani kwangu, nikamkuta Cauther akiwa anauchapa usingizi kisawa sawa. Nikamsogelea na kubusu shavuni mwake. Nikamtandikia neti kisha nikaingia bafuni, nikaoga na nikavaa bukta pamoja na tisheti. Nikahakikisha mke wangu yupo kwenye usingizi fofofo, nikarudi sebleni na kumkuta Nadia akiwa bado yupo usingizi. Nikamuita kwa ishara na nikaingia naye katika ofisi yangu ya hapa ninapo ishi. Nikaufunga mlango kwa ndani kisha taratibua Nadia akaanza kuvua nguo zake na akabaki kama alivyo zaliwa. Nikambebe na hadi katika sofa iliyomo humu ndani, nikakaa kitako na akanikalia mapajani mwangu.

“Hivi una jua hichi tunacho kifanya ni kosa kwa dada yako na hata mwenyezi Mungu”

Nilizungumza kwa sauti ya kunong’oneza

“Najua shem ila nina kupenda sana natamani na mimi nikubebee ujauzito”

“Mimba hapana, uta fanya kila kitu kijulike”

Nadia taratibu akamchomoa jogoo wangu ndani ya bukta hii, akaanza kukisugua kichwa cha jogoo wangu kwenye kitumbua chake hadi kikalowana. Taratibu akamkalia na mtanange huu ukaanza taratibu huku ukiwa ni mtanange wa kimya kimya.

“Mmmmm….aiiisii….”

Nadia alitoa miguo huko tukiendelea kupeana kitu roho ina penda. Hadi tuna maliza mtanange huu, ni zaidi ya mara tatu Nadia alifika kileleni.

“Asante mume wangu”

Nadia alizungumza huku akiwa amenikumbatia.

“Asante nawe pia. Ina bidi sasa ukulele kwa maana ni saa kumi usiku sasa”

“Sawa mume wangu”

Nadia akavaa nguo zake zote, nikafungua mlango wa ofisini hapa, nikahakikisha mazingira ya eneo hili hayana mtu nikamruhusu Nadia kukimbilia chumbani kwake kisha name nikalekea chumbani kwangu, nikaingia bafuni nikaoga na nikapanda kitandani na taratibu nikamkumbatia Cauther kwa nyuma na kuanza kuutafuta usingizi.

‘Aisee sisi wanaume ni wauaji sana’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikilipapasa tumbo la mke wangu ambaye kusema kweli ana nipenda kuliko kitu chochote ila mume wake ndio kwanza nina kuwa mstaliti hadi kwa mdogo wake.

‘Mungu nisamehe tu, si una jua ndoa ya mke mmoja nayo ni ngumu sana kwa sisi wakristo.’

Niliendelea kuomba kimoyo moyo huku nikiwa sina uhakika kama maombi yangu haya yana weza kupokelewa kwa mwenyezi Mungu.

“Baby”

Niliisikia sauti ya Cauuther kwa mbali kidogo. Nikafumbua macho yangu na kumtazama.

“Umeamkeje mume wangu”

“Salama baby, niambie”

“Safi, mshauri wako yupo sebleni ana kuhitaji”

“Saa ngapi sasa hivi?”

“Ni saa mbili na nusu”

“Aisee nimelala sana ehee?”

“Ndio mume wangu, ila umechoka sana”

“Weee acha tu hizi kazi nyingine hazina tofauti na mwanafunzi anaye paswa kuwahi namba shuleni”

“Ndio hivyo mume wangu ila muda umebaki mchache uta rudi kwenye maisha yako”

“Natamani hata leo nirudi kwenye maisha yangu. Anasemaje Yule mzee?”

“Yeye ameniomba tu nikuamshe”

Nikavaa suruali ya mazozi na tisheti kisha nikatoka ndani hapa na nikakutana na mshauri wnagu, nikasalimiana naye.

“Muheshimiwa raisi. Raisi wa Somalia amesha fika?”

“Amefika?”

“Ndio yupo hapa ikuku”

“Mungu wangu, hata kuoga sijaoga?”

“Usijali, nilimuambia una kikao kidogo hivyo una weza kutumia muda huu kujiandaa kwa ajili ya kuonana naye”

“Ume fanya jambo zuri kwa maana ukichanganya uchovu wa safari, kikao hapa nina ona maruwe ruwe balaa”

“Pole sana muheshimiwa ina bidi upate kawaha”

“Ni kwel, sawa nina kuja”

“Una dakika arobaini”

“Hakuna shaka”

Nikarudi ndani huku nikipiga miyayo ya usingizi.

“Mke wangu kuna raisi nina kwenda kuonana naye naomba uniandalie kahawa”

“Sawa mume wangu, una kwenda kuonana naye nje ya ikulu?”

“Hapana ni hapa hapa, ni raisi aliye pinduliwa huko Somali hivyo amekujak uomba msaada”

“Alafu mume wangu leo asubuhi nime ona taarifa kwenye tv zinasema kwamba jeshi la Tanzania lime shambulia Kenya kwenye mji wa Marindi?”

“Yaa ila sio wanajeshi wetu wale walikuwa ni wanajeshi wa Al-Shabab ambao walivalia mavazi ya Tanzania hivyo walikuwa na lengo la kutuchonganisha. Ila nina tambua kuna mtu yupo nyuma ya hili na nina uhakika wa asilimia mia moja lita kuwa ni wazo la makamu wa raisi aliye toka madarakani”

“Ila ni kwa nini Yule baba ana fanya hivi jamani”

“Amechanganyikiwa, ila siku nikimkamata, aisee ata nitajia jina la mama yangu”

“Mmmm ila pole mume wangu. Sasa hiyo si ina weza kuleta vita?”

“Yaani ilikuwa bado kidogo tu tuzichape na majirani zetu. Ila tunamshukuru Mungu shetani aliweza kupita kushoto”

“Masikini pole mume wangu. Ni bora tu achane na hiyo kazi”

“Itakwenda kuishi tu”

“Naamini hivyo mume wangu. Ngoja nikuandalie kahawa usije ukachelewa bure”

“Shukrani mke wangu”

Nikajiandaa na kuvaa suti nyeusi aliyo niandalie mke wangu, nikatoka sebleni nikanywa kikombe hichi cha kahawa, kisha nikaagana na mke wangu na nikaelekea ofisini kwangu. Nikasalimiana na Maria ambaye tayari amesha fika.

“Umependa Maria”

“Nashukuru Eddy”

“Raisi yupo wapi?”

“Yupo ofisi ya wageni V.I.P tumependekeza kikao kikafanyikie kule”

“Sawa twende”

Nikaongozana na Maria pamoja na walinzi wangu kwenye ofisi ambayo ni kwa ajili ya wageni wale wenye hadhi ya juu. Nikawakuta Judy na mshauri wangu wakiwa wana zungumza mambo mawili matatu na raisi huyu wa Somalia ambaye amepinduliwa madarakani. Tukasalimiana kwa kupena mikono na kukumbatiana kidogo kisha nikakaa kwenye kiti change kwa ajili ya mazungumzo.

“Karibu sana nchini Tanzania”

“Nina shukuru sana raisi Eddy nime karibia”

“Pole kwa kila kitu ambacho kimekupata kwa maana hizi ndio changamoto za kuongoza nchi za kiafrika”

“Ni kweli muheshimiwa raisi kwa maana nilikuwa nina waadithi namna tukio zima la mapinduzi lilivyo tokea hadi nikapinduliwa”

“Ehee ilikuwaje hadi ukapinduliwa kwa maana ulikuwa na jeshi na walinzi wa kutosha?”

“Ni story ya kusikitisha muheshimiwa raisi kwa maana mapinduzi yaliongozwa na damu yangu”

“Damu yako kivipi?”

“Mwanangu wa kumzaa ambaye ndio mwanangu wa kwanza nilimpa uwaziri wa ulinzi na kupitia nafasi hiyo akaitumia na akanisalititi yeye na wanajeshi walio kuwa wana msikiliza na kumtii akanipindua madarakani na akataka kuniua ila nina shukuru Mungu niliweza kutoroka na hapa ninavyo zungumza habari za kipelelezi zina sema kwamba yeye ndio ata chaguliwa kuwa raisi wa Somalia na ni jana tu amemuoa mtoto wa mkuu wa kundi hilo la Al-Shabab ili kuzidi kudumisha mahusiano kati yake yeye na magaidi hao wa Al-Shabab”

Nikashusha pumzi huku nikimtazama raisi huyu nikatazamana na Judy pamoja na mshauri wangu mkuu kwa maana hii vita iliyopo Somalia kumbe ni ya baba na mwana tofauti na jinsi sisi tulivyo kuwa tunahisi kwamba ina husisha magaidi wa Al-Shabab na serikali ya nchi ya Somalia.



“Kwa hiyo ni mwanao ndio amekufanyia mapinduzi?”

Niliuliza huku nikikunja nne miguu yangu.

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Nini tukufanyie?”

“Muheshimiwa raisi mimi ningependa sana kuirudisha serikali yangu mikononi.”

“Kwenye kuirudisha mikononi kuna garama zake muheshimiwa raisi. Ni lazima ujue hapo damu ita mwagika na kuna uwezekano mkubwa wa vijana wangu kufariki dunini. Sisi kama sisi una tuahidi nini?”

“Muheshimiwa raisi kusema ukweli nipo tayari kuwapatia chochote mutakacho kihitaji kutoka katika nchi yangu”

“Chochote?”

“Ndio chochote ukitakacho”

Nikatazamana na Judy pamoja na mshauri wangu mkuu kwa maana tulicho kuwa tuna kuhitaji sasa kina kwenda kukamilika.

“Je una idadi gani ya wanajeshi ambao ni watiifu kwako?”

“Sio idadi kubwa wengi waliuwawa kipindi cha mapinduzi na hadi nilio nao sasa hivi hawazidi kmia moja”

“Duuu kama hawazidi mia moja ina maana huna jeshi la kuweza kukulinda, itakuwaje ukichukua nchi kwa mara nyingine na idadi ya jeshi lako ni dogo namna hiyo?”

“Ni kweli muheshimiwa raisi ila nipo tayari kuhakikisha kwamba nina lilipa jeshi lako liweze kunilinda huku nikiendelea kujenga jeshi langu hadi pale nitakapo simama mimi kama mimi”

Tukakaa kimya huku nikimtafakari raisi huyu anaye tia huruma.

“Muheshimiwa raisi kabla mwanao hajakusaliti na kujiunga na Al-Shabab kuna viashiria gania ambavyo hapo awali ulikuwa ukimtilia mashaka?”

“Kitu ambacho yule mtoto aliniweza ni kuficha usiri wa mambo yake ya nyuma. Alikuwa ni mkono wangu kulia na nilimuamini kwa kila jambo ndio maana nilimpa wizara nyeti kama ya ulinzi. Kila jambo langu nilimueleza na kila jambo lake alinieleza. Kiufupi ni jambo gumu sana kuto muamini mwanao kama wote muna kwenda njia moja ila alivyo badilika na kubadilika sikuamini na hadi sasa hivi siamini kabisa”

Raisi wa Somalia alizungumza huku machozi yakimlenga lenga machoni mwake.

“Ningeomba sana muheshimiwa raisi uweze kunisaidia. Nina imani sinto fanya makosa tena, niwahakikishie nita walipa kiasi chochote cha pesa au hata nitoa visima vya mafuta au gesi muwezew kupata pesa”

“Nimekusikia muheshimiwa raisi. Ila nina omba niweze kuzungumza na mtu ambaye uta kuwa naye kwenye kipindi kijacho na ata weza kusimamia mikataba tutakayo ingia”

“Hakuna shaka”

“Judy mpigie madame Caro na umueleze afike hapa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Madam Caro akapigiwa simu na tukamuhitaji kwa haraka, ikambidi kutumia helicopter kutoka makao makuu ya NSS ambayo hadi sasa bado ina fanya kazi tukisubiria mchakato wa kutengeneza kundi jipya na kubwa litakalo itwa X.

“Karibu sana”

“Nashukuru sana muheshimwa raisi”

“Kutana raisi Abas, naamini una mtambua alikuwa raisi wa Somalia. Raisi Abas huyu ni mkuu wa kitengo cha NSS anaitwa madame Caro”

Wakasalimiana kwa kupeana mikono. Kisha kwa ufupi nikamueleza madame Caro juu dhima yote ya kikao hichi na akaelewa kabisa.

“Ila hofu yangu muheshimiwa raisi, nyinyi Wasomali muna weza kutubadilika na hamuamini?”

Madame Caro alizungumza.

“Nina kuapia kwa Allah sinto weza kubadilika hata siku moja. Na isitoshe makubaliano tunayo ingia yana weza kunifunga na kunihukumu”

“Muheshimiwa raisi mimi nisikufiche nikiingia madarakani, na endapo muta kiuka makubaliano yetu. Ninataipiga nchi yako na nita kutoa madarakani “

Madame Caro alizungumza kwa kujiamini.

“Wala usijali hatuto weza kufika huko, wewe niamini mimi”

“Kweli?”

“Ndio wewe niamini mimi”

Maria akatuandalia mikataba inayo husiana na makubaliano baina ya Tanzania na Somalia na tukakubaliana jeshi la nchi ya Tanzania litakaa Somalia kwa miaka kumi huku Tanzania ikijipatia asilimia stini kwenye uzalishaji wa gesi pamoja mafuta yapatikano katika nchi ya Somalia. Pia tukampatia hifadhi ya siri raisi Abas hapa nchini Tanzania yeye na walinzi wake ishirini huku wanajeshi wake wanao mtii wakibaki nchini Afrika kusini ili kuwapoteza maboya watu wanao muwinda. Baada ya raisi Abas kuondoka ikulu na kupelekwa kwenye nyumba salama ambapo ata ishi hapo hadi jeshi langu litakapo ifanya kazi ya kupindua utawala wa Al-Shabab basi ata rudishwa nchini kwake na ata kuwa chini ya ungalizi wa jeshi la Tanzania kwa miaka kumi kama mkataba wetu unavyo weza kuzungumza na katika kipindi cha miaka kumi faida ambayo tutaipata kwenye gesi pamoja na mafuta ita fikia dola za kimarekani trilioni kumi ambazo zita zidi kuifanya nchi ya Tanzania kuwa tajiri na nguvu kubwa duniani.

Washauri wa maswala ya usalama pamoja na meja jenerali wa jeshi wakahusika katika kikao hiki cha kupanga mkakati wa kuhakikisha kwamba tuna peleka jeshi litakao kwenda kuifanya kazi ya mapinduzi kimya kimya. Vikosi vya wanajeshi elfu moja huku mia mbili wakiwa ni makomandoo vikaandaliwa. Hadi ina fika saa sita usiku vikosi vyote vipo tayari kwa ajili ya vita hii ya kimya kimya. Nikapewa nafasi ya kuwahutubia kupitia televishion ambayo moja kwa moja ina wafikia kwenye kambi ambayo wapo kwa ajili ya maandalizi ambayo yalianza kuanzia saa sita mchana wa siku ya leo hadi sasa hivi saa sita usiku.

“Sisi sote ni wa Afrika. Waafrika ambao tuna rangi nyeusi japo lugha na uhalisia ni tofauti. Wasomalia ni ndugu zetu, wana wake, watoto na wazee ambao wana hitaji msaada wetu wa kijeshi na nchi kurudishwa kwenye mfumo wa kidemokrasia”

“Vita hii ni kwa ajili ya ndugu zetu. Tupambane na tuhakikishe kwamba ndugu zetu wana weza kuwa hai tena, ndugu zetu wana weza kuishi kwa furaha na amani tena ili wao waweze kufaida na nchi yao kama sisi tunavyo faidia na nchi yetu.”

Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha nikaendelea kuzungumza huku washauru wangu na wakuu wote wa vitengo vya usalama wakiwa nyuma ya kamara hizi zinazo nirekodi.

“Nchi ya Somalia ina ukubwa wa 637,657 km. Hivyo hilo eneo zima tuna takiwa kulitoa mikononi mwa Al-quida na tuta ipandisha upya bendera ya Somalia yenye rangi ya blue na nyota nyeupe. Vikosi vya majini muta hakikisha kwamba hakuna anaye toka kupitia bahairini. Vikosi vya ardhini muta hakikisha hakuna anaye jificha kwenye mahandaki wala kupita kwenye njia za chini ya ardhi. Vikosi vya angani hakikisheni hakuna ndege hata moja ya kijshi inayo ruka juu ya anga la nchi ya Somalia. Nina hitaji ushindi mkubwa na nina hitaji huu uwe ni usiku wa kundi la Al-Shabab tuna elewana?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

Wanajeshi wote walijibu kwa ukamavu, wakanipigia saluti kwa maana nina waona kupitia tv na wao wana niona kupitia tv hii. Majukumu yakaanza huku wanajeshi wakianza kukimbilia kwenye ndege kubwa za kivita pamoja na helicopter. Wanajeshi wa majini wakapelekwa kwenye meli kubwa za kivita zilizopo baharini. Makomandoo wote mia mbili wanao ongoza vikosi vya wanajeshi, katika kofia zao wamefungwa kamera maalumu zinazo tuonyesha kila kinacho endelea kwenye oparesheni hii ya kivita. Viongozi wote tulio jadiliana katika mpango huu wa kijeshi tupo kwenye ukumbi huu wa kuongozea oparesheni hizi za kiusalama huku kila mtu akiwa makini kufwatilia namna gani vita hii ina inafanyika.

“Maria niletee kahawa”

“Sawa mkuu”

Toka nilipo asubuhi nyumbani kwangu hadi sasa hivi sijarudi kabisa nyumbani na hata sijapata chakula cha kueleweka zaidi ya kula bistkuti na juisi. Hapakuwa na mtu aliye ingia kwenye ukumbi huu na akatoka au kwenda nyumbani kwake, kila humu ina patikana humu ndani na leo tupo kwa ajili ya kazi hii tu, kama vita itachukua siku moja au mbili basi hatuto toka hii ina saidia kuwapa nguvu wanajeshi wetu ambao wanaelekea katika uwanja wa vita.

“Hii hapa muheshimiwa”

Maria akanikabidhi kikombe kilicho jaa kahawa ya moto.

“Shukrani”

Nilimjibu huku nikiendelea kutazama tv kubwa ambayo imegawanyika katika picha ndogo ndogo zinazo onyesha idadi ya kamera za wanajeshi wetu na tuna wasiliano nao moja kwa moja. Wanajeshi wanao husika na maswala ya I.T nao wapo katika kambi kuu ya jeshi kuhakikisha kwamba mawasiliano yetu na wanajeshi wetu hayapotei na kingine tayari Satelaite za nchi ya Tanzania zina imulika nchi ya Somalia yote hivyo tuna weza kuona kila kinacho endelea katika nchi ya Somalia. Jambo la kumshukuru Mungu majirani zetu wa nchi ya Kenya wameturuhusu ndege zetu za kijeshi kupita kwenye anga la nchi yao kuhakikisha kwamba tuna kwenda kuwatandika Al-Shabab kisawa sawa na vita hii nina imani hawajawahi kupigana nayo kwani idadi ya wanajeshi elfu moja ambao wamegawanyika kwenye vikosi karibia hamsini sio jambo dogo.

‘Mungu wasaidie’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kutazama namna wanajeshi walipo kwenye helicopter arobaini jinsi zinavyo zidi kuchanga mbuga. Wanajeshi walio tangulia kwa ndege kubwa za kijeshi wakaanza kushuka kwa maparachuti katika mji mkuu wa Mogadishu kimya kimya, ndege hizi za kijeshi kubwa zime weza kupenya hadi Mogadishu kutokana na kwamba moja hazinaswi na mitambo yoyote ya nchi ya Somalia. Mbili hatoi mlio wowote ambao una weza kumstua adui. Wanajeshi thelathini wakiwa makomandoo watano, wakafanikiwa kutua salama kwenye mji huu mkuu majira ya saa tisa usiku na wakagawanyika kama vile mpango wa vita unavyo hitaji.

Wanajeshi hawa kazi yao kubwa ni kuhakikisha kwamba wana iteka ikulu yote na kumkamata mkuu wa kundi la Al-Shabab na mtoto wa raisi Abas. Wakanza kuua wanajeshi wa Al-Shabab mmoja baada ya mwengine.

Wanajeshi hawa wakazidi kusonga mbele huku wakipata maelekezo kutoka kwa wanajeshi wengine wa I.T ambao wana watumia video maelekezo maalumu ya wapi wapite kuhakikisha wanajeshi wanao linda ikulu hiyo hawastuki. Wanajeshi wa Tanzania ndani ya nusu saa wakafanikiwa kuiteka ikulu nzima ya Somalia na wakamuweka chini ya ulinzi mku wa kundi la Al-Shabab pamoja na mtoto wa raisi Abas wote walikutwa wakiwa wamelala na wake zao.

“Muheshimiwa raisi tume wakaata wahusika”

Karibia kila mtu akashangilia ndani ya chumba hichi, Judy akanikumbatia kwa furaha kwa maana mafanikio ya oparesheni hii kwa asilimia sabini nilitoa mbinu zinazo tuwezesha kuishinda vita hii kwa muda mfupi na bila ya kuua raia wasio na hatia. Sasa nikatoa amri majeshi yanayo subiria mipakani kuvamia sasa nchi nzima, jambo ambalo wanajeshi wa Al-Shabab walijikuta wakiishiwa uwezo wa mashambulizi kwani jeshi kubwa lilikuwa lipo katika mji wa Mogadishu kumlinda mkuu wao na wengi wameuwawa hivyo hawa walio mikoani na mipakani ni sawa na kumsukuma mlevi kwenye mteremko. Mashambalizi ya kustukiza na ya nguvu yakazidi kurindima nchi nzima. Ndege za kijeshi za waasi lizi jaribu kuruka angani zote zilichanguliwa kabla hata hawajafanya mashambulizi. Wanajeshi wangu wa anga wanao endesha ndege za mapigano aina za Jet F-35 Lightning II hawakuwa huruma hata kidogo kwani si kwa kuwaangamiza hivi waasi. Walio jaribu kukimbilia baharini walikutana na majeshi ya majini ambao kazi yao ilikuwa ni kuwamalizia kwa kuwashindilia risasi nyingi zisizo na idadi. Walio jaribu kupita njia za ardhini kutoroka nchi walisindikizwa na mabomu ya ardhini yaliyo waua na kuwazika huko huko.

“Muheshimiwa raisi nchi ya Somalia sasa ipo mikononi mwetu”

Mkuu wa oparesheni alirusisha ripoti na kutufanya tushangilie hadi kwa furaha machozi yakaanza kunimwagika. Kwa kweli ukitazama uzito wa kazi na masaa yaliyo tumika kwa kweli tuna haki ya kuitwa taifa kubwa na lenye nguvu duniani. Kwani sasa hivi ni saa mbili na dakika ishirini asubuhi na kazi imekwisha na nchi ya Somalia tumesha ikomboa.

“Kazi nzuri nipatie taarifa ya vifo na majeruhi?”

“Tuna majeruhi kumi na mbili muheshimiwa raisi na katika majeruhi hao wote wana endelea vizuri na hakuna aliye poteza kiungo cha mwili wake. Pia habari nzuri ni kwamba hatuna vifo muheshimiwa raisi”

Shangwe zikazidi kutawala ndani ya ukumbi huu.

“Hongereni sana”

“Tuna shukuru muheshimiwa raisi. Je mkuu wa Al-Shabab pamoja na mtoto wa raisi Abasa na wake zao tuwafanye nini?”

Nikashusha pumzi kidogo huku nikitafakari cha kufanya.

“Waleteni nchini Tanzania. Kama ni hukumu ita tolewa na raisi wao”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Kila mmoja akanipongeza kwa oparesheni hii namna ilivyo endeshwa kwa kweli ni oparesheni iliyo tumia akili kubwa sana kuhakikisha nchi hii tuna ipigaa na kuikomboa. Raisi wa Somalia akaletwa ikulu hapa na nikampatia habari njema ya namna nchi yake tulivyo ikomboa. Raisi Abas akajikuta akipiga magoti chini na akanishika miguu yangu huku akilia, jambo lililo nifanya nimnyanyue kwa haraka kwa maana sihitaji kusujudiwa.

“Nashukuru sana muheshimiwa raisia, mwenyezi Mungu akulipie mara elfu moja, jina lako halite saulika kwenye historia ya nchi ya Somalia. Ulilo lifanya hata mwenyezi Mungu amelipitisha ndio maana kazi iliyo shindwa na wanajeshi wangu ime kamilika kwa wanajeshi wako nashukuru sana”

Raisi Abas alizungumza huku akiendelea kulia mithili ya mtoto mdogo.

“Amen. Pia usijali muheshimiwa raisi nina shukuru kwa uvumilivu wako na sasa watuhumiwa wako njiani wana letwa tuna shukuru tuliwakamata wakiwa hai”

“Asante sana na nina hamu ya kuwaona hao watu”

“Usijali wata fika muda si mrefu. Jambo kubwa ni kuhakikisha nchi yao una iongoza kwenye misingi ya kidomokrasia na uachane na tamaa za madaraka. Kwani kukaa sana madarakani hupelekea vikundi vya waasi kujiunda na kuipinga serikali yako. Uwe mwema kwa watu wako, upo madarakani si kuwagandamiza au kuwaongezea ufukara wafanya kazi wako. Upo kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi wako ili nchi yako nayo itoke mavumbini na kupanda juu”

“Nashukuru sana muheshimiwa raisi na Mungu akubariki. Kwa kweli umenipa funzo kubwa sana maishani. Nina kuahidi nita kuwa raisi bora na nitaunda serikali nzuri pasipo upendeleo wa kifamilia wala urafiki”

“Hilo ndio ninalo penda kulisikia. Nitafurahi siku Somali iwe ni sehemu salama kama unavyo tembea hapa Tanzania, natamani iwe ni sehemu ambayo uchumi wake uta panda na kuimarika kama hapa Tanzania. Vizazi na vizazi viweze kujifunza historia nzuri na sio historia mbaya. Kama mulishindwa kujijenga pale awali sasa ni wakati wa nyinyi kujijenga upya”

“Nimekuelewa muheshimiwa raisi na nina shukuru sana kwa ushauri wako ulio mwema na wenye kuitakia mema serikali yangu”

“Nashukuru sana ombi langu usisahau wapi tulipo kutoa na wapi tulipo na wapi tutakapo kupeleka. Mimi sina muda mrefu kama unavyo jua au kusikia mimi ni raisi wa muda na ilinizalimu kuwa raisi mara baada ya viongozi wa ngazi za juu wote watatu kutokuwepo madarakani. Hivyo atakaye kuwepo ni yule mama naamini ita bidi uwe muangalifu kwenye kila jambo sawa ndugu yangu”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Judy akaingia hapa ofisini kwangu kwa maana nilitoka katika ukumbi wa kuendeshea oparesheni na kuingia ofisini ili kuzungumza na raisi huyu wa Somalia.

“Ndio”

“Muheshima raisi wahalifu wamesha fikishwa na wapo kambi kuu ya jeshi”

“Sawa, muheshimiwa raisi tuna ambatana kwa pamoja hadi kwenye kambi hiyo. Kisha mambo mengine yata fwata”

“Sawa”

Msafara wa kuelekea kambi ya jeshi ya Kigamboni ukaanza kupangwa. Kutokana bado sijamaliza majukumu ya kikazi ikanilazima kuto kwenda kumuona mke wangu. Tukaondoka ikulu na moja kwa moja tukaeleka katika kambi kuu ya jeshi. Tukapokelewa na mkuu wa kambi na moja kwa moja tukapelekwa hadi alipo hifadhiwa waalifu. Tukafika katika mlango wa chumba cha kuingia eneo walipo fungwa, nikamsimamisha kwanza raisi Abas kwa maana uso wake tayari umesha jawa na ndita za hasira.

“Kabla hatujaingia ndani, niambie una taka kuwafanya nini?”

“Muheshimiwa hata sijui ila naomba tu tuingie”

Tukaingia ndani ya chumba hichi na kuwakuta mkuu wa kundi la Al-Shabab pamoja na mtoto wa raisi Shabani wakiwa wamepigika kisawa sawa.

“Babaaaa!!”

Mtoto wa raisi Abas aliitwa huku akipatwa na mstuko huku akimtazama baba yake kwa woga.

“Baba yako ni nani eehee?”

Raisi Abas alizungumza kwa kufoka huku akimwata mwanaye huyu aliye pugwa pingu mikononi na mguuni amefungwa minyororo ambao sio rahisi kukatika. Akaanza kumpiga mangumi, mateke hadi mwanaye huyo akaanza kutapika damu.

“Sikukuzaa wewe uje kuw amsaliti. Ulikosa nini kwangu wewe, umeshawishiwa nini na huyu mpuuzi hadi ukaamua kuharibu mfumo mzima wa serikali yetu eheee?”

Raisi Abas alizungumza kwa kufoka huku akimuinamia mwanaye aliye lala chini akiendelea kuugulia kwa maumivu.

“Kama nilikutoa kiunoni mwangu sioni hasara kukuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”

Raisi Abas akanza kumpiga mateke ya kichwa kijana wake ambaye hana uwezo wa kujitetea kwani miguu na mikono yote imefungwa kisawa sawa. Raisi Abas akaona hiyo haitoshi akavua mkanda wake akamkalisha mwanye kisha akaanza kuuzungusha mkanda huo shingoni mwa mwanaye na akaanza kumkaba shingo yake kwa nguvu na kumfanya mwanaye kuanza kurusha rusha miguu ya kukata rogo na baada ya muda miguu ikatulia na akamalizia kumvunja shingo yake kwa mikono kuhakikisha kwamba amemuua kabisa jambo lililo nifanyasha nishushe pumzi ndefu kwa maana si kwa ukatili huu sidhani kama mimi nina weza kumua mwanangu wa damu kwa mateso kama huyu mzee alivyo fanya.

***************************************************

Raisi Abas akasimama huku akihema mithili ya mtu aliye toka kukimbia ziara ndefu.

“Samahani muheshimiwa raisi kwa kufanya mauaji katika nchini yako, ila siku zote wasaliti huwa hawapaswi kuishi.

“Ni kweli”

“Nina kuomba huyu nimuue kinyama hadi asikie maumivu makali”

“Nina kushauri jambo moja. Una onaje ukambeba na kurudi naye Somalia na kumuua mbele ya wananchi wakishuhudia ili iwe funzo kwa wengine”

“Hilo ni jambo zuri muheshimiwa nashukuru sana muheshimiwa raisi”

“Karibu sana”

Utaratibu wa raisi Abas kurudi nchini Somalia ukaanza kupangwa na jeshi huku akiwa ana wekewa ulinzi na wanajeshi wa nchi ya Tanzania pamoja wanajeshi wake wachache alio kuja nao nchini Tanzania. Baada ya raisi kuingia katika helicopter ya jeshi pamoja na wanajeshi huku muhalifu wake pamoja na maiti ya mwanaye wakipakizwa kwenye helicopter ya pili huku ulinzi ukiwa mkali sana. Nikaondoka kambini hapa na walinzi wangu na kurudi ikulu.

“Nahitaji kulala sasa kwa maana ni siku ndefu sana imekuwa”

Niliuzungu huku nikishuka katika gari. Kabla sijaelekea nyumbani kwangu Maria akanifwata huku akiwa katika mwendo wa haraka.

“Muheshimiwa raisi kuna tatizo”

“Tatizo gani?”

“Kuna mgomo wa madaktari nchi nzima umeanza majira ya saa tano asubuhi.”

“Mgomo wa madaktari!?”

Niliuliza kwa mshangao mkubwa sana kwani hili jambo ni adimu sana kulisika kwenye nchi tajiri na kubwa kama hii.

“Ndio muheshimiwa”

Ikanibidi kughairi mpongo wa kuelekea ninapo ishi na moja kwa moja nikaeleka ofisini kwanguna kuwakuta washauri wangu pamoja na waziri wa Afya.

“Ehee nini shida”

Niliuzungumza huku nikikaa katika kiti change.

“Muheshimiwa raisi kuna malimbikizo ya shilingi trioni kumi na moja ambazo madaktari walikuwa wamelimbikiziwa kipindi cha miezi sita na serikali iliyo pita na serikali ilihaidi kulipa deni hilo ndani ya miezi miwili ila kwa bahati mbaya haikuweza kulipwa.”

Waziri wa Afya alizungumza kwa unyenyekevu.

“Umesema ni malimbikizo ni ya nini?”

“Mishahara mkuu, wapo walio ongezwa madaraja na bado mishahara yao haijapanda na pia serikali iliongeza misharaha ya wafanyakazi pia mishahara yao haijaweza kupandishwa kwa kipindi hicho”

“Na hii ni hatari muheshimiwa raisi kama muda wa madaktari wakiendelea kugoma. Wagongwa wengi wana weza kukumbwa na matatizo makubwa wakikosa huduma”

“Nani kiongozi wa huo mgomo?”

“Ni mwenyekito wa chama cha madaktari taifa.”

“Muheshimiwa raisi kuna picha za mabangoa hapa. Madaktari wana hitaki kuonana na wewe”

Judy alizungumza huku akinionyesha picha za mabango hayo. Nikazitazama kwa muda huku bango moja likisomea, raisi Eddy tuna kuomba usikilize kilio chetu. Nikavuta pumzi nyingi na taratibu nikashusha pumzi.

“Hii pesa ipo?”

“Muheshimiwa raisi labda tumuulize gavana mkuu”

Mashauri wangu mkuu alizungumza.

“Piga simu”

Mshauri wangu mkuu akapiga simu kisha akanikabidhi simu nizungumze na gavana.

“Unazungumza na raisi hapa”

“Habari muheshimiwa raisi”

“Salama, nahitaji kufahamu juu ya madai ya madaktari ni trilioni kumi na moja. Je hii pesa ipo benki kuu?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Kwa nini kipindi chote haijalipwa?”

“Hatukupata idhini yoyote kutoka kwa muheshimiwa raisi aliye pita ndio maana tuliendelea kuifadhi tu benki”

“Nahitaji iweze kuandaliwa ina kwenda kukutana na madaktari nahitaji kila mwenye deni lake aweze kulipwa leo. Tuna elewana?”

“Ndio muheshimiwa raisi. Pia ningependa uweze kuidhinisha kwa maandishi?”

“Hakuna tatizo”

Nikakata simu.

“Ehee wapi kwa kuidhinisha?”

Nikkakabidhiwa ipad yenye fomu inayo niwezesha kuidhinisha kiasi hicho cha pesa kutoka benki kuu. Nikaisoma na nilipo jiridhisha nikatia saihi na ikatumwa benki kuu.

“Madaktari wamekusanyika wapi?”

“Viwanja vya karimjee”

“Anadeni msafara nahitaji kwenda kuwaona”

“Una onaje muheshimiwa raisi ukabadilisha suti?”

Judy alizungumza.

“Alafu kweli, naenda kuoga na kubadilisha suti baada ya dakika ishirini tuna ondoka”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Nikanyanyuka na kutoka ofisini kwangu huku nikiongozana na walinzi wangu, hadi nikafika eneo ninalo ishi. Cauther akanikumbatia kwa furaha, huku akinipiga mabusu tele.

“Pole mume wangu kwa uchovu”

Cauther alizungumza huku akinivua koti langu hili la suti.

“Nashukuru mke wangu. Nimerudi mara moja kuoga na kubadilisha nguo nahitaji kwenda kuzungumza na madaktari.”

“Pole mume wangu. Nimesikia mgomo wao kuna rafiki yangu ilimlazimu kutoka hospitali ya serikali na kuelekea hospitali binafsi kutokana na mgomo huo”

“Yaa. Ila kazi hii ni ngumu sana mke, huwezi amini sijala kiti cha kueleweka toka jana.”

“Masikini, basi subiri nikupikie mume wangu ule ndio uende”

Cauther alizungumza huku akinivua shati kwani tayari tumesha ingia chumbani.

“Hapana mke wangu. Nita pata uvivu, niandalie ndizi nyama, na maharage ya nazi. Najisikia kula hivyo leo”

“Sawa mume wangu, nikuandalie suti gani?”

“Ile darkblue”

“Sawa”

Nikaingia bafuni na kuaoga haraka haraka, nikatoka na kukuta Cauther amesha andaa kila kitu cha kuvaa. Jambo ninalo mshukuru Mungu kutoka kwa Cauther ni mwanamke anaye jua nini maana ya kuwa na mume. Japo amekulia maisha ya kitajiri na hajawahi kuisikia shida ya pesa toka alipo zaliwa. Ila ana jua jinsi gani ya kufanya shuhuli zake za ndani kama mwanamke, ana pika na ana fanya usafi kama wanawake wengine tofauti na wale wanawake wenye vipesa vya kununua maandazi kazi zote huwaachia wafanyakazi wa ndani hadi kutandika vitanda vyao wanavyo lala na waume zao.

“Nina kupenda sana mke wangu”

Nilizungumza huku nikitabasamu. Cauther akatabasamu kidogo huku akinivalisha shati langu.

“Una jua mimi ndio nina kupenda kuliko chochote mume wangu hivyo siwezi kuongea zaidi ya kukuonyesha kwa vitendo.”

“Nina shukuru sana mke wangu. Kwa kweli wewe ni mwanamke muhimu na bara kwenye maisha yangu”

“Hata wewe ni mwanaume bora mume wangu na nina jivuani sana kuwa na wewe”

Nikamaliza kuvaa suruali na nikaka kitandani na taratibu Cauther akanivisha soksi pamoja na viatu.

“Ila hii kazi imekupendeza sana mume wangu”

“Kwa nini?

“Yaani hii kazi ukiwa hata haupo karibu nami nina kuwa na amani asilimia mia moja. Tofauti na kazi ya ujasusi, ile ukienda sehemu huku nyuma nina kazi ya kusali tu Mungu akuepushe na malaika wabaya”

“Una taka niendelee kuwa raisi?”

“Hapana, sasa hivi nina miss uwepo wako. Kuna wakati nina tamani kucheka na wewe, kukulalia, kudeka, kufanya michezo yetu ya kitandani ila ninapo kumbuka upo ofisini basi nina heshimu sana ofisi yako. Ndio maana muda mwengine nikiona upo bize nina mpigia simu Judy”

“Ila hata niwe bize vipi wewe ni mke wangu na kama una shida na mimi nipigie kwenye simu yangu kwa maana wewe ni wangu na mimi ni wako hivyo sinto hitaji kazi iweke daraja la mawasiliano baina yetu saawa mke wangu”

“Sawa baba kijacho nimekuelewa”

Cauther akanipiga busu la mdomoni na akanivalisha saa mkono wangu wa kushoto.

“Eiii nimeshau jambo moja. Wallet”

Cauther akanitolea Wallte katika suruali niliyo ivua na akanikabidhi.

“Asante mke wangu. Vipi bibi na Nadia wapo wapi?”

“Ohoo nilisahau kukuambia. Walielekea Agakhan kuna dawa za kisukari bibi amekwenda kuzichukua ila wapo na walinzi”

“Ohoo sawa sawa, nita onana nao nikirudi”

“Sawa mume wangu”

Nikamnyonya denda Cauther kidogo kisha nikatoka ndani hapa, moja kwa moja nikaelekea nje kwa maana msafara una nisubiria mimi tu. Tukaingia ndani ya magari huku nikiwa na mlinzi wangu, washauri wangu ambao ni Judy na mzee huyu, safari ya kuelekea katika viwanja vya Karimjee ikaanza. Hatukukuchuku muda mwingi tukafika katika viwanja hivi, nikawakuta madaktari na wauguzi wakiwa wengi huku wakiwa wamevalia makoti yao.

“Hivi wamesha ingiziwa pesa zao?

“Bado muheshimiwa tuna subiri uzungumze nao kwanza kisha tuna wapa ruhusa benki kuu kuwaingizia pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao.”

“Sawa sawa”

Gari zikasimama na walinzi wakaimarisha ulinzi, nikafunguliwa mlango wa gari hili nikashuka pamoja na washauri wangu. Moja kwa moja nikaelekea hadi kwenye eneo nililo andaliwa kwa ajili ya kuzungumza. Nikapeana mikono na viongozi hawa wa madakatri na nikakaribishwa eneo nililo andaliwa kukaa. Mlinzi wangu namba moja akakiweka kiti change vizuri kisha nikaa.

“Muheshimiwa raisi tuna shukuru sana kwa kuweza kuja. Kwa kweli wewe ni raisi msikivu na raisi ambaye unas ikiliza haja za wafanyakazi na kuzitendea kazi kwa haraka. Kwa jina langu ninaitwa Dismas Komba ni mwenyekiti wa chama cha madaktari nchini nzima.”

Dokta Komba alizungumza huku akiwa amesimama eneo lenye kipaza sauti.

“Muheshimiwa raisi, sisi ni watumishi waadilifu ambapo muda mwingi tunakuwa kazini kuhakikisha tuma okoa maisha ya wananchi wanao letwa mahospitalini kwa ajili ya matibabu.”

“Muheshimiwa raisi shida yetu sisi ni madai yetu kwa serikali. Tuna deni kubwa kwa serikali linalo fika trilioni kumi na moja. Tuliweza kuandika barua wazara ya Afya na kuwaleza juu ya duni hilo ila hatukupata ushirikiano. Mimi niliweza kuonana na makamu wa raisi aliye pita na nikamueleza juu ya deni letu kwani ni malimbikizo ya misharaha, promosheni pamoja na malipo ya likizo kwa baadhi ya madaktari. Muheshimiwa raisi hatukupewa ushirikiano wa kueleweka.”

“Muheshimiwa raisi hadi tumefikia hatua ya kugoma sio kwamba hatuwapendi wagongwa wetu. Tuna wapenda ten asana, ila nasi sisi ni binadamu. Tuna mahitaji yetu binafsi kama binadamu na sidhani kama daktari ana weza kuifanya kazi iliyo tukuka endapo ata kuwa ana njaa. Hii ina pelekea mianya ya rushwa kupenyeza ili daktari apate mia mbili mia tatu ili akakidhi mahitaki katika familia yake.”

“Hivyo muheshimiwa raisi nina kuomba sana uweze kusikia kilio cha sisi madaktari wako ambao tumeyatoa maisha yetu kuhakikisha kwamba wagonjwa wana weza kupatiwa huduma nzuri na huduma itakayo tusaidia kushusha vifo kwa wagonjwa kwa asilimia kubwa. Hivyo muheshimiwa raisi naomba kuwasilisha.”

Nikatabasamu kidogo kisha nikasimama, nikatembea hadi sehemu kilipo kipaza sauti na kuwatazama wafanyakazi hawa.

“Habari za mchana?”

Wote wakaitikia.

“Kusema kweli nyinyi ni watu muhimu sana kwenye hili taifa kubwa. Kwani nguvu kazi ya wananchi ikipungua basin chi haito kuwa na nguvu kama tuliyo nayo sasa hivi.”

Judy akanifwata na kuninong’oneza sikioni mwake.

“Wanauliza waanze kutuma pesa?”

Nikamjibu Judy kwa kutingisha kichwani kimaanisha ndio.

“Serikali yangu ya mpito ime weza kusikia ombi lenu na kusema kweli sinto weza kulidharau ombi lenu kwani najua umuhimu wenu. Kila mmoja ata kwenda kulipwa deni lake leo hii na sasa hivi”

Madaktari wakaanza kupiga makofi kwa kushangilia.

“Maana ya kuwa nchi yenye nguvu duniani maana yake tuna paswa kuhakikisha kwamba wafanyakazi wa sekta zote wana jaliwa kwa kupata stahiki zao katika muda muafaka.”

Nikaanza kuwaona madaktari wakitoa simu zao mifukoni na kutazama meseji zinazo ingia kwa kasi. Sura za madaktari hawa zikajawa na furaha kubwa sana kwani kila mmoja sasa ana lipwa pesa yake.

“Huwa sipendi madeni na wala sipendi kuzunguka kwa maana mimi sio mwana siasa. Serikali imewalipa deni kila mmoja, nina hitaji mukitoka hapa kila mmoja aelekee kwenye kituo chake cha kazi na akafanye kazi. Kuna wamama wana hitaji wakunga sasa hivi ila hawawaoni, kuna watu wana hitaji oparesheni ila hawaipati, kuna watu wana hitaji dawa ila hawazipati. Tafadhali mukafanye kazi kwa weledi mkubwa na unyenyekevu. Sinto penda kupata malalamiko kwa wagonjwa kwamba kwa kutumia pesa hizi, imekuwa chanzo cha madaktari kuelekea kazini mukiwa mumelewa. Siwakatazi kulewa, ila sio wakati wa kazi. Nita jaribu kukaa na viongozi wenu siku nyingine ili kuhakikisha hili jambo halijitokezi tena kwani ni aibu kwa serikali na nchi kwa ujumla”

“Sina maneno mengi na Mungu awabariki, ila nasisitiza ninaopo ondoka hapa uwanjani kila mmoja arudi kituo chake cha kazi. Asanteni”

Nikarudi kwenye kiti change na nikapena mikono na viongozi hawa.

“Asante sana muheshimiwa raisi. Wewe ndio raisi unaye paswa kuendelea kuwepo kwenye hii nchi. Huna kona kona ume nyooka”

Dokta Komba alizungumza huku akicheka.

“Nipo hivyo kwa sababu mimi sio mwana siasa, nimezoea jeshi kufwata amri ndio maana nime nyooka. Nami nimewapa amri mukitoka hapa wote murudi kazini. Nita lifwatilia hili sasa wewe waambie watu wako endapo mtu akakaidi na akaenda kugambeka saa hizi na hili jua la utosi, basi kitakacho mkuta ata shangaa na roho yake. Tumeelewana?”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama dokata Komba machoni mwake.

“Sawa muheshimiwa raisi hakuna shaka juu ya hilo. Madaktari wana endelea kupokea miamala yao”

“Haya mimi sina jengine la kufanya. Nina waomba niondoke, ili tokoe muda”

“Raisi tuna kupendaa….Tunaomba ugombanie uraisi”

Madaktari wamama walizungumza huku wakipunga juu kofia zao, nikasimama na kuinama kidogo ikiwa ni ishara ya kutoa heshima kwao. Nikawapungia mkono kisha nikaanza kuondoka viwanjani hapa ulinzi ukiwa ni mkali sana.

“Kichwa kina niuma aise”

Nililalama huku nikifunga mkanda wa siti ya gari hili.

“Vipi tukupeleke hospitalini”

Mshauri wangu mkuu aliniuliza.

“Hapana nahitaji kurudi nyumbani. Ni uchovu tu”

Tukarudi ikulu, nikawapa ruhusua Judy na mzee huyu kuelekea mapumzikoni kwani wamechoka sana. Nikaelekea ninapo ishi na kumkuta bibi Cauther na Nadia wakiwa wamesha rudi.

“Mume leo nimeamka sija kuona?”

“Yani mke toka nilipo toka jana ndio nina rudi leo”

Nilimjibu bibi Cauther huku nikikaa pembeni yake.

“Umependeza, tumekuona hapo kwenye tv”

“Nilikuwa nina tuliza tuliza presha za madaktari”

“Yaani shem huko tulipo toka wagonjwa ni wengi sana. Yaani kugoma kwa madaktari kumeifanya ile hospitali kufurika wagonjwa hadi wengine wana kosa kwa kulaza”

“Naamini watarudi kwenye hospitali zao za kawaida.”

“Mume mikono yako ni ya moto”

Bibi Cauther alizungumza huku akinishika viganja vyangu.

“Ahaa ni kutokana na kutoa kupata muda wa kupumzika”

“Pole ila hii ni homa una joto kali sana hadi shingoni”

Bibi Cauther alizungumza huku akinishika shingoni mwangu.

“Yaa ngoja nikapumzike kidogo naamini nikiamka nita kuwa nimesha pona”

“Sawa nenda kalale kidogo”

Nikanyanyuka nikapiga hatua mbili, kizunguzungu kikali kikanikamata hadi macho yakapoteza uwezo wa kuona, nikajaribu kujikaza na kutembea ili nisiwaonyeshe udhaifu wowote bibi Cauther na Nadia ila nikayumba na nikaanguka chini kama mzigo na nikaanza kusikia kelele kwa mbali za Cauther na bibi yake wakiomba msaada na baada ya muda kelele hizo zikakatika kabisa masikoni mwangu na hata sikuweza kuona chochote kinacho endelea mbele.



“Usilie mjukuu wangu, ata amka tu”

Niliisikia sauti ya bibi Cauther kwa mbali sana. Nikafumbua macho yangu taratibu, nikamuona Cauther akiwa amejiinamia pembeni yangu huku bibi akiwa amekaa pembeni yake. Nikatazama maizingira haya na nikagundua kwamba hapa nilipo ni hospitalini. Mkono wangu wa kushoto umechomwa sindano ya dripu ambalo baada ya kulichunguza vizuri nikagundua ni dripu la maji.

“Hei”

Niliita kwa sauti ya unyonge na iliyo jaa ukakasi wa na mikwaruzo.

“Umeamka mume wangu”

Cauther alizungumza kwa furaha huku akinishika mkono wangu wa kulia.

“Ndio mbona una lia”

“Yaani wee acha tu mume. Ulivyo anguka yaani mke wako ni kulia tu kama mtoto mdogo alihisi una kufa, ila nilimuambia kwamba uta rudi na kuwa sawa tu”

“Nina sumbuliwa na nini?”

“Malaria mume wangu, ilikuwa ni kali sana na uchovu pia umechangia ndio maana mwili uliishiwa nguvu”

“Duuu hivi una jua sikumbuki mara ya mwisho kuumwa malaria ni lini?”

“Ndio maana hii ilivyo kukamata tu imekulaza”

Bibi Cauther naye alizungumza.

“Ni kweli mke. Tupo hospitali gani?”

“Hospitali ya taifa. Aisee madaktari wamakuhudumia kwa haraka sana mume”

“Ni kawaida kwa raisi akiumwa huwa ni lazima ahudumiwe kwa haraka. Walinzi wapo wapi?”

“Wote wapo nje, na washauri wako, na rafiki zako wa karibu”

“Duuu ina maana hii habari imesambaa kwenye vyomba vya habari?”

“Hapana”

“Mumenileta hapa saa ngapi?”

“Sasa hivi ni masaa kama sita hivi”

“Duuu nimezimia kwa muda mrefu ehe?”

“Sio sana mume. Ila unajisikiaje?”

“Bado nasjikisikia mzito mzito kidogo”

“Ngoja nimuite daktari”

Cauther akapiga simu kwa daktari kwa kutimia simu iliyopo mezani na baada ya muda daktari akaingia hapa na daktari huyu ndio yule mwenyekiti wa madaktari ambaye mchana nilikuwa naye kwenye mkutano wao wa dharura.

“Unajisikiaje muheshimiwa raisi?”

“Ahuweni nime toka kwenye shimo la mauti. Kumbe upo hospitali hii?”

“Ndio muheshimiwa raisi, nina fanya kazi hapa ndio daktari mkuu msaidizi”

“Ohoo safi sana. Ehee tofauti na malaria ni kitu gani kingine mulicho kiona?”

“Upungufu wa maji muheshimiwa. Ina onekana una kimbia kimbia sana kunywa maji. Laiti maji yangekuwa ni mengi sana mwilini nahisi hii malaria isinge kulaza. Ila jitahidi sana kunywa maji, kula kwa wakati naamini kwenye swala la mazoezi hapo huwa unazingatia?”

“Yaa nina zingatia ila toka niwe kwenye hii kazi nimekuwa mvivu sana wa kufanya mazoezi.”

“Ujitahidi muheshimiwa kwa maana mazoezi pia ni dawa”

“Ni kweli, nita jitahidi”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz? .EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

“Itakuwa viruzi muheshimiwa hivyo ina bidi tuangalie afya yako kwa leo naamini kesho tuta kuruhusu”

“Asante”

“Pia kuna sindano nita kuja kukuchoma baadae saa sita usiku”

“Hakuna shaka”

Daktari akatoka ndani hapa, Judy, Willy na mshauri wangu mkuu wakaingia ndani hapa, nikasalimiana nao kwa furaha.

“Unajisikiaje sasa?”

“Nipo poa”

“Aise unajua nilipo pigiwa simu na mlinzi wako, hata mapumziko yangu niliyakatisha na mara moja nikawahi hapa hopsitalini”

“Pole sana mzee wangu, ila ni Malaria tu ndio kidogo imenisumbua sumbua”

“Ila pole Mungu ni mwema ata kusaidia uta pona”

“Aise kaka toka nikufahamu leo ndio nina sikia una umwa?”

“Haahaa Willy kwani mimi pia si binadamu. Kuumwa ni jambo la kawaida kwa kila binadamu mwenye pumzi”

“Ila jambo la msingi sio ugonjwa mkubwa”

“Shem Malaria ni ugongwa mkubwa. Yaani hadi amezimia sio jambo dogo una jua, angekufa mwenzenu”

“Mungu alikuwa pamo naye ndop maana hadi sasa hivi yupo salama salmini”

“Ni kweli, kwa hiyo una toka lini?”

“Kesho, si ndio hivyo alivyo sema dokta mke wangu?”

“Ndio alisema keso uyapewa ruhusa.”

“Mkuu wale waandishi wa lile gazeti hivi una jua bado wapo ndani?”

“Weee nilisha washahai kabisa”

“Wapo ndani”

“Ngoja nikitoka hospitalini nita kwenda kukutana nao. Ehee Willy nipe maoni wanayo toa wananchi kwenye maswala ya uongozi wangu huu wa muda mfupi?”

“Kusema kweli kaka kama una amua kugombania uraisi, basi una asilimia themanini na tano za kushinda. Wananchi wengi wana toa maoni mazuri juu yako. Wengi wana pendezwa na uongozi wako jinsi namna unavyo jail kero na shida zao kwa uharaka sana. Pia hili swala la madaktari limzeidi kukuongezea sifa huko mitaani?”

“Willy usitake kumuambia mume wangu agombanie uraisi jamani, siihitaji kazi hiyo”

Cauther alilalama.

“Hapana shem ni maoni tu tunatoa”

“Mke wangu siwezi kuwa raisi, sijakidhi vigezo vya kikatiba. Kwa hiyo Willy wananchi sasa hivi wana nielewa?”

“Sana na sasa hivi vyombo vya nje ya nchi vina rusha habari juu majeshi ya Al-Shabab kupinduliwa na majeshi ya Tanzania na uongozi kurudishwa kwenye serikali ya Somalia. Yaani una zidi kukonga mioyo ya watu”

“Aisee kama nashawishika vile kuwa kiongozi”

“Eddy sitaki”

“Nakutania bwana mke wangu”

“Ila mume uta kuja kuwa kiongozi. Cauther atake au asitake uta kuja kuwa kiongozi kwani nguvu ya wananchi ni kubwa kushinda nguvu ya mke wako.”

Bibi Cauther alizungumza huku akinitazmaa machoni mwangu.

“Bibi sitaki mume wnagu awe raisi jamani. Hii kazi mtu una kosa hata uhuru. Zamani nilikuwa nina weza kwenda Kariakoo mwenyewe, nikazunguka wee bila hata hata ya mlinzi ila sasa hivi, yaani kila ninapo kwenda, walinzi wana nifanya nyuma nyuma nyuma kama mkia jamani. Mimi hayo maisha wala siyawezi mwenzenu”

“Ila iba bidi kuyazoea shem”

Mshauri mkuu alizungumza.

“Ita nichukua muda mwingi sana. Huwa nimezoea kuwa huru na mume wangu, maisha ya kubanwa banwa siyawezi kabisa”

“Una jua tatizo la mjukuu wangu kama hamjalijua ana mpenda sana mume wake, hivyo mume wake anapo kuwa mbali naye au bize huku ana kuwa ana jisikia vibaya. Hiyo ndio shida yake, ila nawaahidi akiwa na mtoto basi ataweza kuugawa upendo wake, nusu utakuwa kwa mtoto na nusu kwa mume wake”

“Mmmm bibi yaani siwezi kuugawa upendo wangu. Nita wapenda wote na kila mmoja ata kuwa na nafasi yake kwenye maisha yangu”

“Haya uta kuja kuniambia”

Tukaendelea kuzungumza mambo mengi hadi Nadia akaja na chakula alicho kuwa amegizwa. Kwa pamoja tukapata chakula hichi huku tukiendelea kuzungumza. Majira ya saa sita usiku, Judy akaondoka na wezake huku Nadia na bibi nao wakirudi ikulu na mimi hapa nikabaki na Cauther pamoja na walinzi wangu. Daktari kama alivyo ahidi akanichoma sindano na wakaniwekea dripu jengine la maji.

“Hii dripu ya ngapi?”

Nilimuuliza daktari.

“Ni ya kumi na mbili mkuu kwa maana tulikuweka dripu muda ule ulivyo za haraka haraka ili kiwango cha maji mwilini mwako kiweze kuongezeka”

“Ahaa sawa asubuhi mutanitoa saa ngapi?”

“Saa nne muheshimiwa raisi”

“Nashukuru”

“Shemeji kama huto jail na wewe upumzike kwa manaa hali yako hiyo jinsi livyo tusije tukapandikiza tatizo juu ya tatizo”

“Usijali dokta nilalaa”

“Sawa shemeji”

Daktari akatoka na nikabaki na mke wangu.

“Njoo ulale hapa kitandani. Mimi kutokana nipo vizuri nita lala hapo kwenye kochi”

“Jamani mume wangu. Wewe una umwa?”

“Siumwi kusema nimekuwa hoi mahututi bwana. Njoo ulale”

Taratibu nikashuka kitandani huku nikishikilia bomba maalumu iliyo ning’iniziwa dripu hili la maji. Mke wangu akapanda kitandani, nikakaa kwenye kiti kilichopo pembeni ya kitanda hichi.

“Mbona huendi kulal mume wangu?”

“Nimelala sana. Nipo hapa kwa ajili ya kukulinda kama ulivyo nilinda nilipo kuwa nime kaka”

“Mmmm jamani mume wangu”

“Ndio, nina kulinda mke wangu. Hivyo lala vizuri na kwa amani”

“Hahaa haya bwana. Nina kupenda sana Eddy”

“Nina kupenda pia mke wangu”

Cauther hakuchukua muda mrefu akapitiwa usingizi na akalala fofofo. Nikasimama huku nikiwa nimevalia nguo za hapa hospitalini. Nikasukuma bomba hii yenye dripu huku ikwia na matairi. Nikafungua mlango na nikawaona walinzi wangu wakiwa wamesimama huku ulinzi ukiwa ni mkali sana.

“Muheshimiwa raisi”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz? .EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

Mlinzi wangu namba moja aliniongelesha.

“Niambie Lube”

“Safi mkuu unajisikiaje?”

“Namshukuru Mungu, nataka nipunge punge upepo kidogo”

“Sawa sawa”

“Lube una familia?”

“Ndio muheshimiwa raisi, nina mke na watoto wawili”

“Safi sana. Hivi mwanamke anapo jifungua mtoto wake wa kwanza ina kuwaje kuwaje mapenzi yake yanakuwa sawa sawa na vile mulivyo kutana kwa mara ya kwanza au yana pungua”

Ilibidi nimuulize Lube kwa maana yeye anamuda mwingi kwenye ndoa.

“Ahaa muheshimiwa raisi wana wake huwa wana tofautiana. Kuna wanawake wana weza kukupenda sana kipindi ambacho huna ujauzito ila pale anapo pata ujauzito tu basi ana badilika, anajawa na chuki na hasira dhidi yako na baada ya kujifungua mambo yana rudi kwenye mstari. Ila kuna mwengine ata kupenda kipindi cha ujauzito ila akisha jifungua basi mapenzi yeka yote huyaamishia kwa mtoto”

“Okay kumbe ina kuwa hivyo ehee?”

“Yaa ila kuna mwengine ana weza ku balance upendo wake, kwa mume na watoto. Ila wa aina hiyo ni wachache sana tena sana”

“Mke wako ana jisikiaje unapo kuwa bize namna hii popote raisi anapo kwenda na wewe upo?”

“Kusema ukweli nilisha mzoesha, kipindi ni wachumba na ana elewa kazi yangu na jambo zuri ni kwamba huwa ana niona ona mara kadhaa kwenye tv hivyo moyo wake una kuwa na amani kabisa.”

“Hembu tutembee tembee”

Tukaanza kuondoka eneo hili huku walinzi wengine wakiongozana nasi huku wengine wakibaki kuhakikisha wana imarisha ulinzi wa chumba alicho lala mke wangu.

“Kuna tofauti gani kati ya uongozi wangu na raisi aliye pita kwa maana umetulinda sote?”

“Ni kweli, utofauti upo mkubwa sana”

“Upi?”

“Upendo”

“Una maanisha nini kusema upendo?”

“Wewe una ongoza nchi kwa upendo kutoka moyoni. Ila raisi aliye pita alikuwa ana ifanya kazi hii kama ajali tu ambayo imetokea. Aliweza kutawaliwa na makamu wake wa raisi pamoja na mke wake. Kuna wakati alitamani kabisa kuachana na hii nchi ila alipo jaribu kuniomba ushauri nilimtia moyo na akaiongoza ongoza nchi hadi mauti yalipo mkuta. Ila wewe hii kazi umekutana nayo kama ajali ila umeishika na kuipeleka mbele hutetereki na una fanya maamuzi sahihi na wakati sahihi. Hutegemei sana ushauri wa watu wako wa pembeni ila kinacho kuja kichwani mwako ndio unahco fanya. Huo sasa ndio uongozi muheshimiwa raisi”

“Una jua mimi sijawahi kuwa mwana siasa na wala sikuhitaji kuwa kwenye hii nafasi hivyo hata uongozi wangu nina uongoza kwa namna ile nilivyo kuzwa kijeshi jeshi hadi hapa nilipo”

“Ni kweli muheshimiwa. Una jua kuna wakati siasa isiongoze nchi ila maamuzi sahihi ndio yaongoze nchi. Nchi inayo tawaliwa na siasa mara nyingi huwa nyuma sana kimaendeleo kwa maana wana siasa wapo kama wawamba ngozi. Kila mtu ata vutia kwake ili mradi mambo yawawie vizuri kwenye vyama vyao vya kisiasa. Laiti ingekuwa ni amri yangu basi unge endelea kuongoza hii nchi hadi pale utakapo sema ina tosha”

“Hahaaa, hii ni wadi ya nini?”

“Wamama na watoto”

Nikatazama wodi hii kisha taratibu nikaingia humu. Nikawakuta wamama wakiwa na watoto wao, baadhi ambao hawajalala wakastuka sana kuniona nimeingia humu kwani wananchi wa kawaida hawana habari ya uwepo wangu katika hospitali hii.

“Habari zenu”

“Salama muheshimiwa shikamoo”

Baadhi ya wamama walinisalimia pasipo kujua umri wangu.

“Nashukuru”

Nilijibu kwani huwa sipendi sana kusalimia kwani maana ya shikamoo ni sawa na kumuambia mtu nipo chini ya miguu yako.

“Niambieni. Mupo salama?”

“Ndio muheshimiwa raisi tuna endelea salama”

“Huduma muna zionaje, zungumzeni taratibu watoto wasije wakaamka”

“Muheshimiwa raisi, kusema kweli huduma zina mapungufu kwa baadhi ya watenda kazi wa hii hospitali”

“Ehee niambieni”

“Manesi wana lugha chafu na za matusi juu yetu. Au kwa sababu sisi kina mama tuna hudumiwa bure pamoja na watoto wetu ndio maana hawatuthamini?”

Mwana mama huyu mwenye watoto wake mapacha wa kike alizungumza.

“Ni nesi gani mwenye lugha chafu dhidi yenu?”

“Karibia wote muheshimiwa raisi, ila kuna mama mmoja anaitwa bi Mwamvita, yeye ana roho nzuri sana yule mama ana jua kuzungumza na sisi. Pia ana jazibu kuwakanya wezake ila hawamsikii”

“Huyo mama yeye ndio mkuu wao?”

“Hapana ni nesi wa kawaida na ana miaka mingi sana hapa hospitali. Ila hivi vibinti vinavyo anza anza maisha na hata wahajui maumivu ya kuzaa. Wana dharaua kama nini muheshimiwa raisi”

Nikashusha pumzi.

“Sasa hivi ata kuwepo?”

“Tena ametoka kututembelea muda si mrefu yupo. Yaani huyo mama ni mtu mwema sana muheshimiwa raisi”

“Lube hembu mpigie simu dokta mkuu na muambie aje na huyo mwana mama”

“Sawa muheshimiwa”

Ruben akampigia simu daktari mkuu msaidizi bwana Komba na baada ya dakika tano wakafika wodini hapa akiwa ameongozana na nesi huyo wa kike.

“Nimepata malalamiko bwana, wauguzi wako wana lugha chafu kwa hawa mama zetu. Je tuhuma hizo una zijua?”

“Hapana muheshimiwa raisi, ndio nina zisikia kwako”

“Eti mama Mwamvita una jua hilo tatizo la wauguzi wezako kuwa na lugha chafu na mbovu kwa hawa wamama?”

“Ahaa muheshimiwa raisi ni kweli, ila tuna endelea kukanyana taratibu taratibu”

“Kwa hiyo wana watukana na kuwanyanyasa hawa wamama?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Mkuu wenu ni nani, yaani mkuu wa manesi?”

“Ni bi Magreth”

“Ana lijua hilo?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Amechukua maamuzi gani?”

“Hajachukua maamuzi yoyote muheshimiwa”

“Komba”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Nahitaji huyu mama kuanzia sasa hivi ndio awe mkuu wa wauguzi wote. Pia awe na mamlaka ya kuf ukuza na kuajiri wauguzi wenye weledi. Hawa ndio wake zetu, wana tulelea watoto wetu. Mimi sinto furahia siku nesi ana mtukana mke wangu na nikamsikia kwa kweli nita mzaba makofi hadharani. Hivyo mama Mwamvita.”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Kuanzia sasa hivi wewe ndio mkuu wa wauguzi wote, hapa hospitalini, atakaye tukana, au utakaye pokea malalamiko yoyote kutoka wagonjwa zaidi ya mara tatu na wagongwa watatu tofauti. Futa kazi, hatuwezi kuona wamama wana nyanyasika kisa wapuuzi wachache ambao wana chafuta taswira ya kitengoc chunu cha afya. Usiwe na huruma sawa”

“Sawa muheshimiwa raisi nina shukuru kwa hilo na Mungu akubariki”

“Amen”

Wamama wote wakapiga makofi na kushangilia hadi watoto kadhaa wakaanza kulia kwa kuamshwa kwa shangwe hizi za mama zao juu ya maamuzi yangu niliyo yachukua pasipo upendeleo kwa mtu yoyote yule.



“Kuna shida nyingine?”

Niliwauliza wamama hawa huku nikiwatazama.

“Tunashukuru muheshimiwa raisi Mungu akijalia kura tutakupa wewe”

Wamama hawa walizungumza kwa furaha na kunifanya nitabasamu. Sikuhitaji kuwakatisha tamaa kwamba sina mpanmgo wa kugombani uraisi wala kuishi tena nchini Tanzania mara baada ya muda wangu wa madaraka kuisha. Nikagaagana na wamama hawa kisha tukatoka katika wodi hii.

“Muheshimiwa raisi kwa dawa niliyo kuchoma ina bidi upate muda wa kupumzika”

Dokta Komba alinishauri huku tukiendelea kutembea taratibu kwenye maeneo ya hospitali hii.

“Usijali Komba, mimi ni mwanajeshi tena ni zaidi ya Komandoo. Sijazoea maisha ya kulala kitandani kwa muda mrefu hivyo, hivi ninavyo tembea tembea basi mwili wangu unazidi kurudi kwenye umara wake”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Hii ni wodi ya nini?”

“Wagonjwa wa mifupa mkuu”

“Tuingie”

Tukaingia katika wodi hii ya wagonjwa walio pata ajali na kuvunjika mivingo vya miili yao. Hali niliyo ikuta humu japo ni jasiri ila kusema kweli ina ogopesa kwa kiasi kwani kuna baadhi ya watu wamekatwa miguu, huku wengine wakiwa wamekatwa mikono. Kutokana na hali zao kuwa hoi nikashindwa hata kuzungumza nao, tokatoka ndani hapa na kurudi katika wodi yangu. Nikamkuta Cauther akiendelea kuutandika usingizi. Kutokana na kulala muda mrefu, usingizi umegoma kabisa kuninyemelea. Kutokana sina kazi ya kufanya nikaanza kucheza baadhi ya games nilizo zihifadhi kwenye simu yangu ili kusogeza sogeza muda uzidi kusinga mbele. Majira ya saa kumia na moja alfajiri Cauther akaamka na akaingia chooni akajisaidia haja ndogo na kurudi chumbani.

“Hujalala tu mume wangu?”

“Sijalala mke wangu”

“Saa ngapi sasa hivi?”

“Kumi na moja na dakika kumi”

“Kumbe bado bado, ngoja nilale tena”

Cauther alizungumza na taratibu akapanda kitandani na kuumalizia usingizi wake. Majira ya sa mbili asubuhi daktari Komba akaingia chumbani hapa. Tukasalimiana naye kwa maana hata Cauther naye tayari amesha amka.

“Unajisikiaje muheshimiwa?”

“Nipo vizuri dawa imenisaidia kwa asilimia kubwa sana sasa nina weza kurudi kwenye majukumu yangu ya kawaida”

“Ni jambo la kumshukuru Mungu. Ina bidi tukupime kwa mara ya mwisho kuhakikisha kama hali yako imekuwa imara”

“Sawa hakuna shaka”

Dokta Mkumbo akanichoma sindano na kuchukua kiasi cha damu kiasi kisha akaondoka. Baada ya lisaa akarudi na kunipatia habari kwamba malari ina pungua hivyo nikapatia ruhusa ya kutoka hospitalini hapa. Tukarudi ikulu na siku hii nzima nikaitumia kwa mapumzikio.

“Baby”

Cauther aliniita huku akinitazama usoni mwangu.

“Naam”

“Umesema kwamba baada ya muda wako wa kuongoza nchi ukiisha tuna ondoka. Ila zimebaki siku chache kabla ya sisi kuondoka. Ila hujaniambia ni wapi tuna elekea, tukifika huko tuta ishije, utafanya kazi gani na mimi nita fanya kazi gani kwa maana ni maisha mapya. Maisha ambayo naamini yatakuwa ni maisha ya furaha na Amani. Hivyo ni vyema tukashirikiana kwenye hilo”

“Ni kweli mke wangu. Ila nchi ambayo nime ipendekeza ni Japani, kule tuta ishi kwa furaha na Amani, ukiachilia uzoefu wa mimi kuishi kule japani ila nina marafiki ambao ni kama ndugu kwangu. Hivyo tutapata wakati mzuri wa kuishi na kuanza maisha mapya”

“Sawa mume wangu nime kuelewa”

“Au hujapapenda Japani?”

“Sijawahi kuishi Japan, tukienda huko tuta jua kila kitu wala usijali kwenye hilo”

“Sawa mke wangu”

“Ila mume wnagu nime bakisha mdua mchache wa kujifungua. Una onaje kama nikijifungulia hapa Tanzania, nikapata msaada wa kina mama na hali ikitengemaa mimi na mtoto ndio twende Japani kwa maana huko Japani kwanza ni nchi mpya kwangu, sijajua maisha ya kule yapo vipi hususani kwa sisi wa mama wajawazito. Hivyo ningepeda nijifungue hapa kisha ndio twende na mtoto”

“Sawa mke wangu. Nitafanya mpango wa kununua nyumba kule ili tukifika tufikie tu kwenye nyumba yetu na maisha ya ende sawa”

“Hapo sawa mume wangu. Ehee leo utakula nini?”

“Nina hamu na nyama choma”

“Ulimuambia Sudy kwamba uta mleta huku ikulu siku”

“Yaa tena nimekumbuka hembu nipe simu yangu nimpigie”

Cauther akanipatia simu yangu ambayo niliiweka juu ya meza na nikampigia Sudy, simu ikaita kidogo na akapokea.

“Sudyyyyyy!!”

“Ahaa muheshimiwa heshima yako”

“Shukrani aisee upo wapi?”

“Nipo ofisini hapa ndugu yangu ndio tuna fungua fungua ofisi”

“Sasa nina tuma walinzi wangu wana kuja kukuchukua na kukuleta ikulu”

“Ndugu yangu mbona wanifanyia suprize hivyo, mi mwenzio sijaozea”

“Hahaaaa dogo acha woga”

“Haki ya Mungu vile na hapa nguo nilizo vaa ni za kazi sijui kama hata zapendeza mimi kuja nazo huko ikulu”

Sudy alizungumza kwa lafudhi yake ya kipemba huku akiwa amejawa na woga.

“Acha visingizio, wata kununulia nguo na utapigwa sop sop na kuletwa huku”

“Mmmm sawa ndugu yangu ila naogopa”

“Una ogopa nini, wewe kaa hapo natuma vijana wangu wana kuchukua watakupisha dukani, chagua nguo unazo hitaji kuvaa kisha utaletwa huku”

“Sawa kaka”

Nikakata simu.

“Ana ogopa kuja?”

“Ndio mpemba yule mshamba ana woga kama nini, badala ya kufurahi kama bibi yeye ana ogopa”

“Haaaha yaani bibi siku ile alifurahi sana kuingia ikulu, tena ana sema nimekuja kwa mume wangu yaani ahaa…kweli uzee nao una weza kukurudisha ukawa mtoto”

“Ni kweli, ngoja niongee na walinzi”

“Sawa mume wnagu”

Nikatoka ndani na kumpa maagizo mlinzi wangu namba moja na akawaagiza walipo chini yake kuelekea eneo ambalo Sudy anafanya kazi.

“Unaendeleaje mume?”

“Namshukuru Mungu sasa nipo salama”

“Pole bwana, jana ulitutia wasiwasi hadi tukahisi wakati wetu wa kuishi hapa ikulu umefika kikomo weee”

Bibi Cauther alizungumza na kunifanya nicheke.

“Muda wetu ni mchache ila siwezi kuondoka kwa staili kama ya jana”

“Mwenyezi Mungu akupe afya njema na bora”

“Amen”

Sudy akafika ikulu hapa, nikamkaribisha vizuri kwa maana ni mtu ambaye tume fahamiana naye kwa muda mrefu sana.

“Yaani una jua hadi sasa hivi siamini yaani”

“Haumini nini?”

“Kama nimekanyaga white house”

“Sudy karibu”

Cauther alizungumza huku akitoka ndani.

“Nashukuru shemeji. Naona mambo yanazidi kunoga”

“Yaa kabamdogo kenu siku si nyingi nina kaleta duniani”

“Aisee tuta furahi sana.”

“Leo Sudy umependeza”

“Asante shemeji, kidogo watu wa kaka wamenipatia vitu vipya”

“Usijali ni vitu vya kawaida tu. Bwana leo nahitaji unichomee nyama moja fresh sana nina umwa”

“Sawa kaka, ila majiko yenu ya hapa si ya kisasa kweli nita weza kuyatumia kwa maana niemsha zoea jiko la mkaa”

“Hakuna shaka hakuna kinacho kosekana kama ni majiko ya kupikia yapo ya kila aina”

“Basi hakuna shaka”

“Kwanza sijakutambulisha huyu ni mke wangu mkubwa”

“Bibi shikamoo”

“Marahaba”

“Bibi huyu ni kijan ambaye kipindi hicho bado sijafunga ndao na Cauther tulikuwa tuna kwenda kula chakula eneo lake mara kwa mara”

“Ahaaa sawa anaitwa nani?

“Soudy”

“Karibu Soudy”

“Nashukuru bibi naona umefanana sana na shem Cauther”

“Yaa mimi ndio mzaa baba yao hivyo wote wana fanana sana na mimi”

“Sawa sawa bibi”

Soudy akaanza kusaidiana na mpishi mkuu kuandaa chakula. Ng’ombe mzima akachinjwa kwa ajili ya kuandaa tu nyama choma.

“Naona leo ni sherehe mume wangu”

“Yaani wee acha tu”

“Kwa nini visiwekwe vinywaji na kila mtu akala na kunywa”

“Eti ehee?”

“Ndio”

Nikalikabidhi wazo la Cauther kwa walinzi wangu, vinywaji vikaandaliwa huku nyama ikiendelea kuchomwa na mpishi mkuu pamoja na Soudy. Tukaalika wafanyakazi wote wa ikulu kujipatia nyama hii ambayo imechomwa kwa utaalamu mkubwa na wahali ya juu. Japo haikuwa ni sherehe ramsi ila kila mtu akaonekana kufurahia ulaji wa nyama hii. Kutokana na watu wengi tukaongeza ng’ombe wa pili na burudani ikaendelea.

“Shukrani sana muheshimiwa raisi”

“Nashukuru”

Kila mtu akanishukuru kwa muda wake. Hadi ina timu saa nne usiku ulaji wa nyama choma hizi ukaisha na wakuondoka wakaondoka na wakubaki wakabaki hapa ikulu kuendelea na majukumu mengine ya kikazi.

“Soudy nashukuru sana kwa kuja kwa kweli kila mtu ameipenda nyama yako”

“Nashukuru sana kaka, nimefurahi kwa kweli”

“Laiti kama ningekuwa na muda mrefu kukaa hapa ikulu ningekupatia ajira ya kudumu. Sema ndio hivyo”

“Mwenyezi Mungu atakujalia kaka utapata ajira ya kudumu”

“Amen”

“Baby kalete ule mzigo”

“Sawa”

Cauther akaingia ndani, kisha akatoka akiwa na bahasha ya kaki ambayo ndani ina kiasi cha shilling milioni moja.

“Ndugu yangu huu mzigo utakusaidia saidia siku mbili hizi”

“Shukrani sana ndugu yangu”

“Alafu kuna wazo moja nilisahau mume wangu. Soudy, Nadia anahitaji kufungua mgahawa, hivyo alikuwa ana kutegemea ukawe chied cooker wake?”

“Hakuna shaka juu ya hilo. Mimi nipo tayari kwa kila jambo, ila sijamuona leo”

“Hayupo, wana mitihani chuo hivyo alichelewa kutoka na yupo nyumbani kwa wazazi”

“Ahaa basi akiwa tayari tuta wasiliana”

“Sawa sawa”

Nikamkabidhi Soudy kwa walinzi na nikawapa maagizo wampelekea hadi nyumbani kwake na akaondoka hapa. Judy akanifwata na kuninong’oneza sikioni mwangu.

“Mkuu kuna tatizo kidogo la kiofisi”

“Sawa nina kuja”

Judy akaondoka sebleni hapa.

“Mke wangu kuna tatizo kidogo ngoja nikalishuhulikie.

“Jamani mume wangu, tambua kwmaba hali yako haijatengemaa”

“Najua hilo mke wangu ila nakuomba nikalishuhulikie kwanza”

“Sawa mume wangu”

Nikambusu Cauther mdomoni mwake kisha nikaelekea ofisini kwangu, nikamkua Cauther na mshauri wangu mkuu wakinisubiria.

“Ehee niambieni kuna shida gani?”

“Ahaa muheshimiwa raisi kuna shehena ya dhahabu tani mia moja zina mpango wa kiibiwa na kutoroshwa kutoka nje ya nchi na mtendaji mkuu wa hili jambo ni waziri mkuu mstafu”

“Ngoja kwanza si niliwaambia kwamba malizake zina paswa kuchunguzwa na lile deni aliko kuwa ana daiwa na TRA si alipaswa kulipa?”

“Ndio muheshimiwa raisi alipaswa aweze kulipa, ila ndio hivyo bado hajalipa na hizi habari ni za kipelelezi ndio zimeletwa”

“Hizo dhahabu zipo mkoani gani?”

“Arusha mkuu”

“Mpigie simu mkuu wa mkoa wa Arusha na nipe simu niongee naye”

Mshauri wangu mkuu akafanya hivyo na akanikabidhi simu.

“Haloo nani mwenzangu”

“Ni mimi”

“Wewe nani?”

Mkuu wa mkoa alizungumza kwa sauti ya kilevi. Nikatazama saa yangu ya mkononi na ina soma sasa hivi ni saa tano usiku.

“Mimi raisi wako”

“Raisi? Raisi gani wa chama cha mpira au raisi wa nchi?”

Mkuu wa mkoa aliendelea kubwabwaja. Na simu hii ime wekwa loud speaker na sote tuna sikia. Mshauri wangu mkuu akataka kuichukua simu ili azungumze vizuri na mkuu huyu wa mkoa ila nikamkataza.

“Unazungumza na raisi wa jamhuri ya Muungano Eddy Jr”

Nilizungumza kwa hasira na kwa msisitizo mkali sana.

“Mungu wangu! Mu…mu….h….ehshimiwa, shikamoo, marahaba. Za jioni”

Mkuu wa mkoa alibabaika na kuzungumza vitu ambavyo havifai.

“Kama kiongozi wa mkoa sasa hivi umelewa chakari na kujibu upuuzi upuuzi kwa mkuu wako wan chi hivi una uweza kuongoza mkoa na kesho ni siku ya kazi, sasa hivi saa tano ume lewa hivyo. Sasa ni hivi, kuanzia hivi sasa huna kazi shenzi wewe”

“Muheshimiwa sama…..”

Nikakata simu.

“Andaeni helicopter tuna kwenda Arusha sasa hivi. Judy kanichukulie koti la kuzuia baridi kwa mke wangu. Wape taarifa walinzi wangu tuna kwenda Arusha”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Mara baada ya kutoa maagizi hayo washauri wangu wakatawanyika kwa ajili ya maandalizi ya safari hii kuhakikisha tani mia moja za vipande vya dhahabu hazitoki ndani ya nchi ya Tanzania kwani endapo zikitoka basi ni hasara kubwa sana kwa taifa.



Baada ya dakika tano Judy akatangulia ofisini hapa huku Cauther akimfwata kwa nyuma.

“Mume wangu una kwenda wapi sasa?”

Cauther aliuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana Judy taratibu akatoka ofisini hapa na kuniacha mimi na Cauther.

“Mke wangu nina kwenda Arusha mara moja kuna tukio la kusafirisha zaidi ya tani mia moja za dhahabu. Hivyo ina bidi kwenda kulishuhulikia?”

“Jamani mume wnagu hujionei huruma. Una umwa, una dozi ila bado una hangaika kwa nini lakini jamani. Hembu pumzika mume wangu, kwani hapa nchini upo wewe peke yako. Si kuna watu kama wakuu wa mikoa na wakuu wa polisi kwa nini usiwaambie wafanye hivyo hadi uende wewe?”

Cauther alilalama huku machozi yakimlenge lenga. Taratibu nikamshika mke wangu mkono na kumsogeza karibu ya kifua changu na kumtazama machoni mwake.

“Mke wangu najua una umia kwa mimi kufanya majukumu makubwa kama haya. Ila hili ninalo kwenda kulifanya ni kwa ajili yah ii nchi. Naomba nikafanye hii kazi kisha nina rudi usiku huu huu pia tuna tumia usafiri wa helicopter na sio magari”

“Sawa mume wangu ila kumbuka umekunywa dawa nab ado hali yako haijawa sawa, tafadhali mume wangu”

“Nakuomba mke wangu nikashuhlike hili”

Mlango ukagogwa na sote tukautazama.

“Ingia”

Akaingia mshauri wangu mkuu. Akasogea hadi tulipo simama mimi na Cauther.

“Muheshimiwa raisi kila kitu kipo tayari”

“Sawa”

Mshauri wangu mkuu akatoka ndani hapa na kutuacha na mke wangu.

“Mke wangu sasa hivi nenda kapumzike tu. Acha mimi nikaifanye hii kazi nakuahidia nita wahi kurudi na wala usiwe na shaka”

“Sawa mume wangu ila kuwa makini sana huko uendapo”

“Usijali”

Cauther akaninyonya denda kisha kisha tukatoka ndani hapa, moja kwa moja akaeleka tunapo ishi huku nami nikielekea katika kiwanja cha helicopter. Nikaingia kwenye helicopter yangu nikiwa na washauri wangu pamoja na mlinzi wangu mkuu Ruben. Taratibu helicopter hizi tatu zikaondoka uwanjani huku helicopter mbili zikiwa za walinzi. Na endapo kuna tokea tatizo lolote hewani basi wana weza kunilinda. Tukafika Arusha na moja kwa moja helicopter zikatua katika chuo cha maofisa wa kijeshi.

“Nahitaji kuvaa kombati za jeshi”

Nilimpa maagizo Judy huku tukishuka kwenye helicopter mkuu wa chuo akanipokea kwa kunipigia saluti.

“Karibu sana muheshimiwa raisi”

Alizungumza huku akinipatia mkono wa salamu.

“Shukrani sana ndugu. Naamini ume pokea ripoti?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Ehe hadi sasa hivi mitego imekamilika?”

“Ndio muheshimiwa raisi mitego yote tumesha iweka tayari, tunasubiri samaki kunasa kwenye chambo”

“Sawa, nahitaji kupiga gwanda nime zikumbuka sana”

“Hakuna shaka mushimiwa raisi”

Nikasalimiana na maofisa kadhaa wa zamu kisha nikaingia katika chumba cha kuhifadhia kombati mpya za kijeshi. Nikachagua kombati mpya inayo nikaa vizuri mwilini mwangu. Baada ya kuvaa kila kitu kama mwanajeshi mwengine nikatoka ndani hapa na kumkuta Judy naye akiwa amevalia mavazi ya kijeshi. Akanikabidhi bastola yenye magazine iliyo jaa risasi.

“Zimejaa?”

“Ndio”

Tukaingia katika gari mmalumu ya kijeshi aina ya Jeep na tukaondoka hapa huku gari nyingine nne za jeshi zikiwa katika msafara huu.

“Nilizikumbuka sana hizi nguo”

Judy alizungumza huku akitabasamu.

“Kweli?”

“Yaa ukizoea kuvaa suti kila siku alafu ukaja ukavaa hizi kuna kitu kipya kina ongezeka mwilini. Yaani hapa najihisi mwepesi sana, kuliko ninapo kuwa na suti.

Judy alizungumza kwa furaha. Moja kwa moja tukaelekea hadi kwenye mitego ambayo taarifa za kipelelezi zina tuelekeza gari hizo zita pita kwenye eneo hilo. Nikasalimiana wanajeshi walio tangulia eneo la mtego na kila mmoja hakuamini kuniona hapa.

“Tuna shukuru sana muheshimiwa raisi kwa kuja”

“Musijali mimi na nyinyi ni kitu kimoja. Sote ni wanajeshi tuna pambana kwa ajili ya kulinda nchi yetu”

“Ni kweli muheshimiwa raisi”

“Gari zina kuja kutokea kaskazini mwa mlima Over”

Tulipata habari kwa simu ya upepepo na vijana wakajipanga vizuri huku wenye bundiki za udunguaji wakiwa wamejitega maeneo mbalimbali, nikakabidhiwa earphone maalumu kwa ajili ya mawasilino na vijana wote walipo kwenye oparesheni hii.

“Naomba bunduki yako”

Nilimuambia kijana mmoja na akanikabidhi bunduki aina ya L115A3 AWM, nikaikoki vizuri na kuiweka nigh vision kwenye lenzi yake ambayo huonyesha rangi ya kijana inayo niwezesha kumuona adui hata eneo la giza nene.

“Gari zinazo kuja zipo ngapi?”

Niliuliza huku nikiwa na nimelala chini huku bunduki hii nikiielekezea aneo la barabara ambapo gari hizi tumeelezwa zina pita.

“Ni Scania tao mkuu na katika moja ya Scania ya tatu kutoka mbele yupo waziri mkuu mstafu”

“Sawa”

Tukasubiri kama kwa dakika tano hivi tukaanza kuona gari hizo zikija kwa kasi eneo hili ambalo ni kiporomoko na kuna tambalale na sisi tupo mlimani hivyo tuna weza kuziona gari hizo.

“Nahitaji waziri mkuu awe hai. Ila wengine wakidhubutu kufyatua risasi wote pigeni risasi na wafe”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Vijana wangu wakapokea amri hii. Dereva wa lori la mbele nikamuweka vizuri kwenye tageti ya bunduki hii. Nikamvuta kwa ukaribu kabisa eneo la kichwa chake.

“Nahitaji madereva wote wauwawe”

“Sawa muheshimiwa”

“Mimi nina chukua dereva wa mbele na nyingi jigaweni na madereva wa gari zinazo fwata”

“Sawa mkuu”

“Moja, mbili, tatu”

Sote kwa pamoja tukapatandika risasi madereva wa malori haya matano na gari hizi zikaanza kupoteza muelekeo huku nyingine mbili zikianguka na gari nyingine zikisimama kwa kuzigonga gari nyingine kwa nyuma. Kwa bahati nzuri gari aliyo panda waziri mkuu haijaanguka.

“Tulieni”

Niliwaeleza vijana huku tukitazama ni hatua gani watakayo chukua. Gari tatu ambazo hajijaanguka tukaona watu wenye bunduki wakitoka ndani ya gari hizo. Huku wakitazama tazama milimani. Nikawahesabu vijana hao wana kwa haraka na wapo ishirini.

“Waueni”

Mvua ya risasi ikawamwagikia vijana hawa na wote wakauwawa. Tukaanza kuyasogelea magari haya kwa umakini wa hali ya juu.

“Nyoosha mikono juu”

Mwanajeshi mmoja alimuamrisha waziri mkuu akiwa ndani ya gari hili.

“Muna jua mimi ni nani?”

Makamu wa raisi alizungumza kwa ukali huku mikono ikiwa juu.

“Mimi ni waziri mkuu wa hii nchi”

“Mshusheni”

Niliwaambia vijana hawa na wakaingia ndani ya gari na kumshusha waziri mkuu kwa haraka.

“Muheshimiwa mali ipo”

Mwajeshi mmoja alizungumza.

“Ni original au feki?”

“Ni dhahabu yenyewe mkuu”

Mwanajeshi mmojaa akanikabidhi kipande cha dhahabu ambacho kimetengenezwa kama mche mdogo wa sabuni.

“Musinimulike machoni, hamjui mimi nani?”

Nikampa ishara mwanajeshi mmoja kuzima tochi aliyo kuwa ana mmulika waziri mkuu mwabochoni mwake na kumfanya kuto ona watu walio mbele yake. Ikamchukua dakika waziri mkuu kutuona vizuri hususani mimi.

“Ehee wewe ni nani?”

Nilimuuliza waziri mkuu huyu mstafu.

“Ahaa mkuu”

Waziri mkuu alizungumza huku akitabasamu akihisi akinionyeshea uso wa tabasamu basi adhabu yake haito kuwepo.

“Nimekuuliza wewe ni nani?”

“Ahaa mkuu, habari za usiku”

“Mkalisheni chini kwanza huwezi kuzungumza na mimi ukiwa ume simama”

Mwanajeshi mmoja akampiga mtama mkali waziri mkuu mstafu na akaka chini pasipo kupenda huku akitoa yowe la maumivu. Nikachuchumaa na kumtazama vizuri usoni mwake.

“Una hisi hii nchi ni ya baba yako au ni mali yako una kwenda kusafirisha tani mia moja za dhahabu kwa njia za magendo si ndio?”

“Muheshimiwa naomba tuzungumze basi”

“Zungumza mbele ya hawa wapiganaji ambao waliacha majukumu yao ya msingi na kuja kukukamata wewe. Mrekodini aise, wananchi wasije wakasema tume muonea?”

“Nawarekodi mbona”

Judy alizungumza huku akiwa ameshika simu yake na kuendelea kurekodi kila kinacho endelea hapa.

“Muheshimiwa raisi nakuomaba unisamehe”

“Hivi una jua una hujumu uchumi wa taifa wewe. Nyinyi ndio watu munao rudisha nchi nyuma sasa kwa kipindi change hichi kidogo musahau. Haijalishi uwe ni waziri mkuu, makamu wa raisi au panya yoyote. Endapo uta toa mali ya nchi, kuanzia dhahabu, sijui pembe za ndovu na mambo mengine yanayo fanania na hayo aisee tuta dili na wewe na si kwa kukuonea ila sharia ndio itakayo kupatia hukumu. Mpigeni pingu na mpekekeni kambini.

“Muheshmiwa raisi mimi sipo mwenyewe nimeshirikiana na watu”

Nikampa ishara mwanajeshi ambaye alianza kuikamata mikino ya waziri mkuu kwa ajili ya kumpiga pingu.

“Upo na nani?”

“Mzigo wangu hapa mimi ni nusu tu ila robo tatu inayo baki ni mzigo wa waziri mkuu mstafu”

“Ohoo kwa hiyo mumeshirikiana?”

“Ndio muheshimiwa”

“Basi una mambo mengi sana ya kujibu. Muondoeni hapa. Mzigo ulipo kwenye gari zlizo anguka hakikisheni una pakizwa kwenye gari hizi tatu na zina rudishwa jeshini. Hakikisheni hakuna kipande hata kimoja kina potea nita zipima sasa hata ikipungua gramu mmoja muta jibu ni wapi imekwenda”

Niliwachimba mkrwa wanajeshi hawa kwani kwenye mali kama hizi sio kila mtu huwa ni muaminifu. Nikasimamia mzigo wote kuingizwa kwenye magari haya na tukaondoka huku eneo la tukio tukiacha wanajeshi kadhaa kuikusanya miili ya watu wa waziri mkuu.

“Tuna elekea kwa mkuu wa mkoa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Majira ya saa kumi na moja alfajiri tukafika nyumbani kwa mkuu wa mkoa. Askari polisi wanao linda nyumbani kwake hapa wakastushwa sana na ujio wangu, tena nikiwa nime valia gwanda za jeshi.

“Mkuu yupo?”

“Toka alipo ondoka jana usiku hajarudi”

“Saa ngapi aliondoka?”

“Saa mbili mkuu, alikuja akabadilisha nguo na kuondoka”

“Namba ya dereva wake munayo?”

“Ndio”

“Wewe mpigie simu na muulize yupo wapi na mkuu”

“Sawa”

Askari huyu akampigia simu dereva wa mkuu wa mkoa.

“Ehee Mashaka, afande Sele hapa”

“Ahaa niambie ndugu yangu”

“Safi aisee upo wapi na mkuu?”

“Ahaa mkuu nipo naye huku Ngarenaro kuna nyumba ndogo yake bwana ame kuja huku. Vipi lakini?”

“Ahaa safi, nilitaka kujua tu”

“Poa aisee hapa nilikuwa nimelala ndani ya gari”

“Poa poa”

Afande huyu akakata simu.

“Wapo Ngarenaro mkuu”

“Hembu itrack hiyo namba”

Mwanajeshi mmoja akafungua compture maalumu za jeshi na kweli tukajua eneo alipo mkuu wa mkoa. Tukaingia ndani ya gari na kuelekea eneo hilo. Saa kumi na moja na dakika arobaini tukafika katika nyumba hii yenye geti jeusi. Gari zikasimama nje na sote tukashuka, mlango ukagongwa na mmasai akaufungua geti.

“Yesuuuu”

Mmasai huyu alijikuta akistuka mara baada ya kuona gwanda za jeshi zikiwa zimetapaka nje ya nyumba hii.

“Mkuu wa mkoa yupo humu?”

Judy alimuuliza mmasai huyu anaye endelea kutetemeka kwa wasiwasi.

“N…dio…yupo”

“Fungua sasa geti una shangaa shangaa nini?”

Judy akatangulia kuingia huku nami nikifwatia nyuma na kofia yangu nikiwa nimeishusha. Dereva wa mkuu wa mkoa akakurupuka ndani ya gari na akashuka.

“Bosi wako yopo chumba gani?”

“Dirisha la pili kushoto”

Dereva alijibu swali nililo muuliza huku akitetemeka. Nikashika kitasa cha mlango wa kuingilia sebleni na kwa bahati nzuri mlango huu tukaukuta upo wazi. Tukaingia sebleni huku walinzi wangu pamoja na wanajeshi nilio ambatana nao wakiwa wameshika bunduki zao vizuri. Nikapiga hatua hadi katika mlango wa chumba tulicho elekezwa. Nikagonga mlango huu taratibu.

“Nani?”

Tulisikia sauti ya kike. Sikujibu chochote zaidi ya kugonga mlango huu, nikageuka nyuma na kumuona Judy akirekodi tukio la hapa.

“Mmmm wewe dada leo si weekend mbona una una tugongea asubuhi yote hii”

Mwana mama anaye ongea kwa ukali nina hisi anahisi anaye gonga hapa ni dada wake wa kazi.

“NIN…….”

Mwana mama huyu mweupe na aliye jifunga tenge kifuani mwake alishindwa kumalizia sentensi yake mara baada ya kuniona mimi huku nikiwa nimevalia gwanda za jeshi. Kwa ishara ya kidole nikamuambia asogee pembeni na nipite na akatii huku akitetemeka.

“Ni nani huyo baby”

Nikaingia ndani na kumukuta mkuu wa mkoa akiwa amelala uchi wa mnyama huku tumbo likiwa juu juu kama kichuguu.

“Mkuu”

Akakurupuka huku akijifunika shuka na akaka kitako.

“Ahaa mkuu habari za za…..”

“Zaa zaa nini. Hivi nyinyi viongozi wa serikali muna matatizo gani? Mishahara yenu ndio muna kuja kuwapangishia malaya hawa si ndio na wana wafanya munashindwa kufanya kazi za msingi na una leta tumbo kama bakuli la supu eheee?”

Nilizungumza kwa kufoka huku nikimtazama mkuu wa mkoa.

“Unatumia gari ya serikali kuja kuisimamisha kwenye nyumba ya kimada. Una akili wewe?”

“Muheshimiwa raisi nakuomba unisamehe”

Nikatazama mezani na kuona chupa za pombe kali.

“Leo ni lini?”

“Juma nne mkuu”

“Kwa hiyo Jumatatu uliitumia kunywa pombe si ndio?”

Mkuu wa mkoa akashindwa kujibu swali langu.

“Hapa ni nyumba ambayo umepewa na serikali ili uishi?”

“Hapana mkuu”

“Mke wako ana jua upo hapa?”

“Hapana mkuu”

“Nipe namba ya mke wako”

“Ehee?”

“Umenisikai nipe namba ya mke wako”

Mkuu wa mkoa hakuwa na namna zaidi ya kunipa namba ya mke wake wa ndoa. Nikampigia na simu ikapokelewa.

“Asubuhi za asubuhi mama”

“Salama nani mwenzangu?”

“Mimi ni raisi”

“Ohoo habari muheshimiwa raisi”

“Salama kabisa nashukuru kwa kuweza kuitambua sauti yangu. Nimejaribu kumpigia simu Mr ila naona hapatikani je una weza kujua ni wapi alipo kwenda?”

Niliweka loud speaker na watu wote wana siki hichi ninacho kizungumza.

“Kusema kweli muheshimiwa jana alirudi akaniambia kwamba ana kwenda kwenye oparesheni na vijana wake hivyo hadi sasa hajarudi nina Imani ata kuwa porini”

“Ohoo sawa sawa mama yangu. Nikutakie asubuhi njema”

“Nashukuru sana muheshimiwa raisi kwa kuzungumza nami”

“Nami pia nina shukuru”

“Mwenyezi Mungu aendelee kukubariki na kuifanya kazi yake iliyo tukuka”

“Amen”

Nikakata simu huku nikimtazama mkuu wa mkoa jinsi anavyo tetemeka hadi jasho lina mwagika.

“Mleteni huyo malaya wake”

Judy akamshika mkono mwana mama huyu na kumsimamisha pembeni ya mkuu wa mkoa. Nikawapiga picha kadhaa wakiwa pamoja.

“Sasa hizi picha nina ziposti kwenye mtandoa ili iwe funzo kwa wapuuzi kama wewe. Muna pewa pesa na serikali, magari yana jazwa mafuta, fanyeni basi kazi za nchi. Wewe una kuja kufanya kazi ya kutomban** na baada ya hapo una mpelekea Ukimwi mke wako nyumbani si ndio?”

Nilizungumza kwa ukali na kumfanya mkuu wa mkoa kuangua kilio cha uchungu na akapiga magoti chini na akaanza kuniomba msamaha huku akiniomba nimfute kazi ila nisimchomee kwa mke wake kwani akimpoteza mke wake wa ndoa ana weza kufa kwa mawazo.



“Wee mama si una jua huyu ni mume wa mtu”

“Ndio mkuu ila tunaomba utusamehe?”

“Jibu ni ndio au hapana”

“Ndio najua”

“Kwa nini muna mdhulumu mwana mama wa watu penzi lake. Sawa kama una chepuka chepuka basi kwa akili, si hadi una kuja kulala kwa mwanamke ukisingizia kazi. Endapo una kufa galfa ndani humu na kitambi chako hicho una hisi huyo mama ata iambia nini serikali na familia yako. Ngoja niwaambie jambo moja wanaume asilimia tisini na tisa pointi tisa ni wachepukaji ila wewe una singizia kazi kama kigezo cha uovu wako. Ehe ni oparesheni gani ulikwua una kwenda”

“Hakuna mkuu, naomba unisamehe”

“Kwanza nyanyuka na ukae hapo juu ya kitanda chenu”

Wakakaa, nikasogelea chupa hizi za wisky.

“Hennessy Very Special Cognac ni bei gani hii?”

Nilizungumza huku nikishika chupa hii ya wisky yenye ujazo wa ujazo wa 750ml”

“Dola thelathini na tisa mkuu”

Mkuu wa mko alinijibu kwa sauti ya kinyonge.

“Vaa uta nikuta ofisini kwako”

Nikatoka ndani hapa, tukaingia ndani ya gari na kuelekea moja kwa moja ofisini kwa mkuu wa mkoa. Wafanyakazi wengi wakastushwa na ujio wnagu. Wakanisalimia kwa heshima kubwa, baada ya dakika tano mkuu wa mkoa akaingia ofisi huku akihema.

“Nahiraji ripoti ya biashara za waziri mkuu za ndani ya mkoa wako wa Arusha. Nahitaji kujua kampuni zake zina changia vipi pato la mkoa wa taifa”

“Sawa mkuu”

“Pia mpigie RPC hapa aje”

Mkuu wa mkoa akanzana kupekua pekua mafaili yake huku akionekana kuchanganyikiwa.

“Mkoa wako kwa mwenzi una kusanya kodi kiasi gani?”

“Nia milioni mia mbili mkuu”

“Milioni mia mbili tu?”

“Ndio mkuu”

“Yaani jiji hili la biashara alafu muna ingizia milioni mia mbili seriously broo. Mzee mpigie RPC, mpigie mkurugenzi wa mkoa, mpigie mkuu wa TRA wa mkoa. Wote waje hapa muda huu”

Nilimpa maagizo mshauri wangu mkuu na akatekeleza agizo la kuwapigia viongozi hao. Ndani ya dakika ishirini wote wakafika haapa ofisini. Kila mmoja uso wake una onyesha kujawa na woga kwani hakuna aliye jua kama nipo ndani ya mkoa huu kwani nimekuja kimya kimya.

“Mkurugenzi wa TRA muna kusanya kiasi gani kwa mwenzi kodi?”

“Ahaa….mkuu tuna kusanya…..”

Wakaanza kutazamana usoni na mkuu wa mkoa.

“Aisee tusichezeane akili. Nimekuuliza swali wewe una mtazama mkuu wa mkoa yeye ndio aliye kuuliza?”

Nilizungumza kwa ukali hadi mzee huyu akaanza kutetemeka.

“Nijibu aisee sijaja kukuaa hapa?”

“Milioni mia mbili hamsini mkuu”

“Mkurugenzi ni kiasi gani kina kisanywa na halimashauri zako unazo zisimamia?”

“Zote?”

“Aisee mbona swali juu ya swali?”

“Muheshimiwa raisi tuna kusanya kama alivyo sema mkuu wa TRA”

“Kiasi gani?”

“Milioni miambili na hamsini”

“Hivi muna akili nyinyi. Yaani muna kusanya milioni mia mbili hamsini ikiwa muna viwanda, muna utalii, muna mambo chungu nzima ya kuwaingizia kodi kubwa. Mzee kwa wastani wa makadirio wana paswa kukusanya kiasi gani?”

“Kuanzia bilioni mia moja na kuendelea”

Mshauri wangu alizungumza.

“Aisee kamanda una watu wa mahesabu kwenye kiosi chako?”

Nilimuuliza mkuu wa chuo cha jeshi ambaye toka jana usiku nime ongozana naye.

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Wapo viziuri si ndio”

“Ndio mkuu”

“Aise niletee vichwa hapa wafanye tathmini ya haraka juu ya kodi inayo kusanywa. Sasa nyinyi leo sijui nita wafanya nini”

“Sawa muheshimiwa raisi dakika kumi wata kuwa wamesha fika hapa”

“Nashukuru. Ehee wewe RPC itelejensia yako ina jua nini hadi sasa kinacho endelea ndani ya mkoa wako?”

“Ahaa muheshimiwa raisi kuna majambazi walikuwa wana mpango wa kuvunja maduka ya wafanya biashara ila tuliwawahi kabla ya kutekeleza tukio hilo na wapo mikononi mwetu.”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama mkuu huyu wa polisi wa mkoa.

“Hilo tu?”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

“Ndio muheshimiwa?”

“Hili eneo lina shida kubwa sana Judy hembu niambie niwafanye nini hawa watu ambao wamenenepeana kama nguruwe anaye pelekwa machinjioni. Mzee wangu wewe ni RPC hivi na hilo tumbo na uenene kweli jambazi hapa akitokea una weza kupigana naye?”

“N…dio mkuu, nipo ngangari”

“Wewe una uwanja hapa ofisini kwako?”

“Ndio”

“Mzee si upo ngangari, nahitaji umpige huyu mwanamke. Twendeni nje tukashuhudia akikupiga, nina kuvua cheo na nita kupa mwenzi mmoja uwe umepungua mwili huo. Hatuwezi kuwa na askari wanene kama vitembo watoto aisee. Hivi kati ya hawa wanajeshi nilio ongozana nao au hawa vijana wangu wanao nilinda umesha muona mwenye hata kitambi?”

RPC jasho likaanza kumchuruzika usoni mwake.

“Nakuuliza?”

“Hapana mkuu”

“Haya nyanyukeni tukashuhudia pambano”

Kila mtu akahisia masihara kitendo cha mimi kusimama na kutoka nje wakakurupuka ndani na kuanza kunifwata kwa haraka.

“Usije ukaniangusha”

Nilimnong’oneza Judy sikioni mwake.

“Usijali mkuu nipo vizuri”

Tukafika katika kiwanja kilichopo katika ofisi hizi za mkuu wa mkoa. Judy akanikabidhi simu yake pamoja na saa yake.

“Ila muheshimiwa sidhani kama hili ni jambo sahihi”

Mshauri wangu alizungumza kwa sauti ya chini huku akiwa amesimama pembeni yangu.

“Sisi ni wanajeshi, muda wote tuna paswa kuwa tayari kwa vita. Hivyo watu wa aina hii wanao kaa ofisini na kula rushwa huku wengine wakiminyika kwa kulinda amani ya nchi. Dawa yao ni hii”

RPC akajiweka sawa kisha akaanza kurusha ngumu kumshambuliua Judy ambaye kwa umahiri mkubwa ana zikwepa huku akiendelea kumsoma mpinzani wake namna anavyo mshambulia.

“Ona tumbo linavyo mtikisika, una hisi kwa staili ile ana weza kweli kupigana na jambazi kama wamekutana uso kwa uso. Judy hajampiga ngumi hata moja ila tazama anavyo hema kwa shida. Huyu ni kiongizi wa polisi wa mkoa, hawa ndio wale wanao toa maagizo ofisini halafu hawajui maumivu wanayo pitia vijana wao. Wana furahia kupanda mashangingi na kuto kukaa kwenye foleni. Sasa acha leo wafundishwe adabu”

Nilizungumza kwa msisitizo huku mkuu wa chuo cha jeshi akiwa amesimama kulia kwangu na mshauri wangu wamesimama kushoto kwangu. Judy akanipa ishara ya kuniuliza je nianze kumshambulia. Nikamnyooshea dole gumba nikimaanisha ndio nimempa ruhusa. Judy akaanza kurusha mateke na ngumi mfululizo, kila RPC alivyo jaribu kuyazuia ila alishindwa na kujikuta akiangushwa chini. Akasimama haraka haraka ili asionekaje mjinga. Kila anavyo jaribu kumzuia Judy ila binti ni kama mbwa wa jeshi aliye pewa ruhusa ya kumshambulia adui. Hali ikazidi kuwa mbaya kwa RPC. Mateke, ngumi ambazo Judy anampekekea zikamfanya achoke sana. Judy akaruka hewani na kumpiga round kick(Teke la mzunguko) ambalo likempata barabara shingoni mwake na RPC akaanguka chini na kutulia tuli. Nikaitazama saa yangu ya mkononi na kuona Judy ametumia dakika tano toka alipo anza kumshambulia RPC na kumpiga. Judy akachuchumaa na kumuwekea vidole RPC shingoni mwake kisha akasimama na kuja eneo nilipo simama.

“Amezimia”

Judy alizungumza huku akijifuta futa vumbi.

“Kazi nzuri. Mzee wangu umeona madhara ya kuwa legelega alafu una jiita afande. Mshuhulikieni na akiamka sio RPC tena mpatie maelezo IGP na umuambie kwamba achague kijana aliye bora kuja kuwa RPC wa huu mkoa. Mtumie video clip ya pambano hili na muambie au nitamuambia mwenyewe. Wazee wangu mumeangalia pambano sasa turudi kwenye kikao chetu na nyinyi jiandaeni”

Mkuu wa mkoa akatazamana na mkurugenzi wake wa mkoa. Tukarudi ofisini kwa mkuu wa mkoa huku RPC tukimuacha akipatiwa huduma ya kwanza na wanajeshi.

“Muheshimiwa raisi vijana wamesha fika”

Mkuu wa chuo cha jeshi alizungumza.

“Waambie waingie”

Wakaingia vijana wanne, wawili wakiwa ni wanawake warembo sana na wawili wakiwa ni wanaume. Wakapiga saluti huku wakiwa katika mavazi yao ya kijeshi.

“Nina Imani mumeambiwa muna kuja kufanya nini?”

“Ndio muheshimiwa raisi na kipindi tupo njiani tukija huku tumeshafika nusu ya mehesabu hivyo ukitupatia dakika kumi tu. Tunaweza kumalizia kazi yetu”

“Muda ni wenu ndugu zangu”

Wakafungua laptop zao na kuanza kuminya minya. Nikakaa kimya huku nikimtazama mkuu wa mkoa, mkurugenzi wa TRA wa mkoa huu pamoja na mkurugenzi wa mkoa. Kabla hata dakika kumi hazijaisha akasimama mwanamke mmoja.

“Muheshimiwa raisi kazi imekamilika”

“Ehee tusomeeni”

“Kwa mwezi kutokana na vyanzo vya kibiashara vinavyo patikana katika mkoa, ina paswa kuingiza shilingi bilioni mia sita na hamsini. Vyanzo vyenyewe ni hivi na mapato yanayo paswa kuingia kwa kila chanzo hi hizi”

Binti huyu akanikabidhi laptop mmoja na nikaanza kutazama kuanzia vyanzo vya utalii, biashara kubwa na ndogo ndogo. Viwanda, viwanja vya mpira, majengo na hesabu kweli ina kuja kutoka billion mia sita na hamsini kwa mwezi”

“Mkuu wa TRA niambie haya mahesabu yana hongopea au?”

Nilizungumza huku nikimgeuzia laptop hii, akaanza kusoma neon moja baada ya jengine na kila anavyo zidi kusoma jasho lina mwagika.

“Vipi zina danganya?”

“Mu…h…e…shimiwa raisi kuna baadhi ya makampuni yame futiwa kodi”

“NINI?”

*******************************************************************

Ili uwe wa kwanza kupata episode za mbele za hadithi hii kabambe ya X unacho paswa kufanya ni kuwasiliana nami whatsapp 0742334453 au 0657072588. Kama upo Facebook uta ipata kupitia facebook inbox kwenye page yangu ya Story Za Eddy-tz EPISODE MOJA NI SH 250/= TU. Wahi sasa

********************************************************************

“Ndio mkuu yalifutiwa”

“Na nani na kwa nini wafutiwe na ni yapi kati ya haya yaliyo orozeshwa hapa?”

“Ahaa….muheshimiwa…..ni….”

“Acha kujingata ng’ata ni yapi hapa?”

“Haya ya kitalii”

“Mungu wangu. Hawa ndio wanapaswa kulipa kodi nyingi sana kwa maana wanacho kiingizi ni kitu kikubwa cha pesa za kigeni. Hivi kumbe kuna madudu mengi, ni sharia gani imefuta kwa makampuni ya kitalii kufitiwa kodi?”

Mkurugenzi wa TRA akatokwa na macho kama amabwana na mlango.

“Mzee mpigie mkurugenzi mkuu wa taifa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Simu ikapigwa kisha nikakabidhiwa na mshauri wangu.

“Haloo”

“Ni mimi. Kwanza ulifikia wapi kwenye swala zima la madeni ya waziri mkuu?”

“Aha…muheshimiwa raisi aliahidi ndani ya mwenzi mzima ata lipa”

“Ehee makampuni ya watalii kwa nini hayalipi kodi?”

“Nani kasema?”

Nikamtazama mkurugenzi huyu.

“Mkurugenzi wako wa Arusha”

“Mungu wangu, muheshimiwa hakuna kitu kama hicho”

“Kwa hiyo wana lipa”

“Ndio kwa maana pato la taifa lina tegemea pia utalii”

“Sawa”


ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

BLOG