Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

DAPHINE SEHEMU YA 8/10

 

 


DAPHINE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 8 KATI YA 10

 


“Weee,weka chai hapo na chapati mbili!Chai ya maziwa”

“Nipatie supu ya kuku”

Zilikuwa ni kelele nyingi ndani ya mgahawa uliopo Sakina,ambapo mabasi ya kampuni ya Kampala Coach,husimama ili abiria wapate kifungua kinywa!Kelele hizo zilifanya watu wasielewane kwani kila mmoja alitaka awe wa kwanza kupata huduma,hata hivyo kulikuwa na wasaidizi ili kurahisisha huduma hiyo.Abiria walipewa dakika kumi kupata kifungua kinywa ili safari iendelee,wenye kufunga walifunga na waliotaka kulia hapohapo walikaa kwenye viti.

Ngesa,alitulia kwenye siti ya mwisho,amevaa sweta lililomfunika mpaka kichwani,anamtizama kila mmoja kwa umakini.Hakuwa ana uhakika kama alikuwa salama eneo hilo sababu alijua kivyovyote vile anasakwa kwa wudi na uvumba,kujiachia na kujisahau kulimaanisha kukamatwa kizembe, kabla ya kufanikisha jambo lake!

“Umesikilizwa?”

Mzee mmoja,aliyevalia koti jeupe kwa mbele na kofia nyeupe kichwani alimfikia kwenye meza yake na kumuuliza,kumaanisha kwamba alikuwa ana husika na huduma zote za jikoni.

“Niletee supu ya Ng’ombe na chapati tatu.Na pepsi ya baridi”

“Sasa hivi utapata”

Macho ya Ngesa hayakutulia hata kidogo,alikuwa makini kwa kila mmoja!Alivyohakikisha kuna usalama na kila mtu ana hamsini zake,kidogo akatulia na kuanza kufikiria mipango yake kabambe!


Hakuna watu waliokuwa makini kama wanausalama waliotumwa na Ramadhan Nurdin,ilikuwa ni vigumu kuwatambua sababu wawili walikuwa ndani ya mgahawa huo na wengine watano walikua nje,kila alichokifanya Ngesa walikiona, hata alivyoanza kunywa supu aliyoagiza walimuona pia,niya yao ilikuwa kumsubiri afike mkoani Kilimanjaro ili wamchukuwe kiurahisi,mwanausalama mmoja aliyekuwa kwenye kona, aliyefahamika kwa Jina la Dickson Mwaipopo alikuwa makini kumchora Ngesa!

“Anasimama anaelekea chooni!Luka,umenisoma?”

Dickson aliongea,masikioni aliweka ‘headphone’ ungemuangalia ungedhani anasikiliza mziki kumbe anazungumza na mwenzake,ambaye alikuwa kwenye kona ya mwisho karibu na friji.

“Ndio,nimemuona”

“Asikutoke”

Kufikia hatua hiyo,Lucas akasimama na kuliendea friji ambapo walipishana na Ngesa,kwa kuzuga akajifanya ananunua maji,alivyoona Ngesa kaelekea chooni nayeye akaenda hukohuko ili kumlinda asitoroke!Ngesa hakuwa mwenye habari,baada ya kushiba alichowaza ni kufika jijini Dar es salaam lakini kuna kitu alikikumbuka kikaanza kumtia mashaka!Askari walioingia ndani ya basi na kushuka bila kumuhoji,jambo hilo lilimfanya ahisi kuna hatari mbeleni,kutokana na uzoefu wake wa kijasusi alielewa namna ya kazi za kipelelezi zinavyofanywa!Alivyomaliza kutoa haja ndogo akaliendea sinki na kuanza kunawa mikono huku akimtizama kila mmoja anayeingia bafuni kwa namna ya kuhakikisha hakuna mtu anayemfuatilia,alivyoona hali ipo sawa akarudi na kuketi kwenye kiti chake cha awali.

“Abiria wanaoondoka na Kampala Coach,anzeni kuingia kwenye basi!”

Kipaza sauti kilisikika,Ngesa akasimama ili aliendee basi lakini kuna kitu kilimfanya asite.Mwanamme mmoja aliyekaa kushoto kwake,alimfananisha lakini hakuwa ana uhakika hata hivyo hakutaka kulipa wazo hilo kipaumbele kwani duniani watu wawili wawili.

Lakini mbaya zaidi, alivyosimama ili atoke kupitia kioo cha friji la soda,akamuona jamaa huyo nayeye anasimama huku anaongea na simu!Kuna hatari mbeleni alianza kuhisi baada ya kuona wanaume wengine watatu mbele yake wanamtizama alafu ghafla wakaangalia pembeni,tukio hilo lilifanya awe makini zaidi.

Badala ya kufata usawa wa basi lilipo,akaelekea kulia ambapo upande wa pili akaona taxi nne zinamtizama akavuka barabara,alivyoizunguka taxi kwa mbele akageuka nyuma huku akiwa amejificha!

Akawaona wanaume hao wanavuka barabara,hapo akawa ana uhakika kama anafuatiliwa!

“Kiongozi,vipi mambo”

Ngesa akamsalimia dereva taxi,kijana mmoja aliyekuwa ndani, nyuma ya usukani amevaa zura jekundu kichwani.

“Aisee safi chalii yangu”

“Naenda Moshi mjini,Majengo!”

“Twende tu chalii angu”

“Bei gani?”

“Usijali,wee ingia tu chalii.Tutapata tu bei”

Ngesa akafungua mlango wa nyuma kwa niya ya kupanda lakini kabla ya kuingiza mguu wake mmoja ndani,akahisi kuna kichuma kizito kimemkandamiza kwenye mbavu zake!

“Ngesa,usifanye kitu chochote!Tulia”

Kabla ya kugeuka nyuma,akajua tayari wamemkamata,alivyoangalia upande wa pili,akaona dereva kawekewa bastola nayeye usawa wa kichwani,akipewa amri ya kukaa kimya!

“Ingia ndani,tumalize ili zoezi kimyakimya Ngesa”

Hakuwa na ujanja,wanaume wanne walikuwa wamezunguka gari!Wanatizama huku na kule huku wakiwa wameziba gari ili wapita njia wasione mchezo huo wa kutishia amani!

“Ngesa,usilete ubishi”

“Mnataka nini?”

Ngesa akauliza huku akitaka kugeuka nyuma,lakini alirudishwa na ngumi nzito ya shingo, kichwa chake kikapiga kwenye bodi ya gari, kabla hajakaa sawa,akasukumwa ndani ya gari!Mmoja akaingia upande wa kulia mwingine kushoto,wakamuweka mtu kati.Yule aliyekuwa kamuwekea bastola kichwani dereva,akakaa siti ya mbele kushoto!

“Ngesa,ukifanya upumbavu.Nakuuuwa”

Ilikuwa ni sauti kali na nzito,iliyoambatana na hasira za waziwazi.Mbaya zaidi jamaa huyo aliyekuwa mbele,mkononi alishika bastola kageuka nyuma huku akiwa amemuwekea Ngesa usawa wa kichwa.

Kilikuwa ni kitendo kilichomuogopesha Ngesa na katika harakati zake za kijasusi, alizopitia alielewa kabisa sauti hiyo haikuwa na utani,kufanya mjongeo wowote wa ghafla tafsiri yake ingekuwa kifo,hiyo ilimfanya aogope na kutetemeka kwa wakati mmoja!Kutulia kwa Ngesa kulimfanya Jamaa mwingine aliyekuwa pembeni yake,aanze kumpekua ambapo walimkuta na bastola mbili,kisu cha kukunja na ‘magazine’ moja iliyojaa risasi.

“Dereva washa gari,tuondoke!Luka mpigie bosi mwambie Ngesa tunaye”

Kila kilichotokea kwa Ngesa,kilikuwa kama mazingaombwe jinsi walivyomvizia na kumkamata kama kuku ndani ya banda ilimuogopesha,akaamini watu hao walikuwa wana mafunzo ya kutosha,wapo makini na wajanja!

“Mnanipeleka wa….”

Ngesa akataka kuhoji lakini kabla ya kumalizia swali lake,akanyamazishwa kwa kupigwa na kitako cha bastola mdomoni,akaachia yowe kali la maumivu,alivyojiramba akahisi kama ladha ya chumvichumvi akarudisha ulimi wake ndani na kutema mate pembeni,alivyoyaangalia akaona yamechanganyika na damu.

“Dereva,nimekwambia washa gari”

Hapohapo gari,likawashwa na safari ikaanza wakiwa na ushindi wa kumkamata Ngesa,tayari kwa kwenda kumuuwa!




Kukamatwa kwa Ngesa ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kwao,wakiamini kwamba huo ungekuwa mwisho wake na asingeweza kutumia ujanja wa aina yoyote ule kufurukuta, hiyo ni kutokana na kuongeza umakini sana kumlinda!Walijua hatari yake endapo wangefanya uzembe kwani walijua historia yake kipindi cha nyuma namna alivyokuwa anawatoroka mamia ya maaskari,sio siri Ngesa alikuwa mwenye mafunzo ya kijasusi ambayo hakusomea nchini Tanzania,hiyo ndiyo ilimfanya awe mjanja na makini katika kila maamuzi anayofanya!

Akiwa ndani ya gari,amewekwa mtu kati aliisumbua akili yake lakini aliona asingeweza kufanya kitu chochote kile sababu mbele yake alitizamana na mdomo wa bastola,ikiwa imeshikiliwa na mwanamme mwenye usongo aliyeweka mzaha pembeni,kuleta ujanja wowote kulimaanisha kuharakisha kifo chake ambacho mpaka wakati huo hakuelewa angeenda kufa vipi!Gari lilitembezwa kwa kasi ya kimondo, mpaka walipofika mkoani Kilimanjaro,Njia panda na kupaki pembeni wengine wakashuka,ndani wakabaki wanausalama wengine wawili wakiwa makini,hata hivyo baada ya wengine kushuka wengine watano wakafika kwa namna ya kuhakikisha kama kweli Ngesa yupo chini ya ulinzi.

“Kweli,nimeamini”

Mmoja wao alisema,baada ya kuchungulia dirisha la mlango wa nyuma.

“Mkuu anajua?”

“Hapana,simpati kwenye simu nilimpigia Muna.Ameniambia yupo kwenye kikao na Rais”

“Hakuna shaka,sasa tunamfanya nini?”

“Inabidi tusubiri maelekezo”

“Wakati tunasubiri maelekezo kwanini tusianze safari ya kurudi Dar?”

“Ni wazo zuri”

Maongezi hayo yote Ngesa,aliyasikia akiwa kiti cha nyuma bado mbele yake kuna mdomo wa bastola unamuangalia,hakuweza kufanya chochote kile kwani watu wa usalama walikuwa wengi mno!

Hata hivyo alijionya kujaribu kufanya mjongeo wowote ule!Dakika moja baadaye baada ya kikao kifupi kufanyika,wakamshusha ndani ya taxi na kumpakia kwenye gari lingine,ulinzi ukawa vilevile tena safari hiyo ulizidi.Bastola tatu zilimuangalia,moja mtu wa mbele nyingine kushoto na kulia!

“Mbona kama hamjiamini,hamuamini kama mmenikamata?”

Ngesa,akavunja ukimya kuna jambo alitaka kujaribu kama lingefaa kwa wakati huo!

“Usijidanganye,mwisho wako umefika”

“Niueni basi”

Akasema makusudi ili kupima maji nakujua ni muda gani,angetumia kabla ya kumuua!

“Wala usijali,simple sana”

“Mnasubiri nini?Simu ya bwana enu?Mnakuwa kama wanawake Malaya”

“Jeuri yako,imefika tamati Kenge wewe”

Ngesa akatulia kidogo na kujitafakari,alishaelewa kivyovyote vile huko mbeleni anaenda kukutana na kifo hata angefanya nini.

Katika harakati zake za kijajusi alishakumbana na misukosuko mingi sana,mbali na hapo alivyokuwa mafunzoni kitu kufa kikondoo kichwa chini ulikuwa ni mwiko ilikuwa ni bora kijerumani tai shingoni,akapata muda kidogo wa kutafakari siku ya mazishi yake akiwa kama shujaa aliyeipigania nchi yake, jeneza lake limefunikwa na bendera ya Tanzania na baada ya hapo kupigiwa mizinga na jina lake kuandikwa kwenye vitabu mbalimbali!Hiyo ilimpa moyo na kumfanya apate nguvu mpya,akatafakari kidogo na kujigeuza kama mwanafunzi aliyekalia banseni bana kwenye daladala.

“Mbona hautulii?Au umevaa chupi mbichi”

Mmoja wa wanausalama,aliyekuwa kushoto kwake aliuliza kwa kejeli huku akiweka tabasamu fulani la dharau usoni.

“Ndio,chupi yangu imelowa”

Ngesa nayeye akajibu.

“Basi,usijali tutaenda kuikausha”

“Tunaenda wapi?”

“Utajua ukifika”

Gari lilizidi kusonga mbele kwa kasi sana!Ngesa alivyoangalia pembeni akaona kuna shamba la katani,mitaa hiyo aliijua sana walikuwa wamefika Same!Akanyanyua kidogo shingo yake ili kutizama kioo cha ubavuni,akaona nyuma kuna magari mengine matatu,akatuliza akili yake na kushindwa kuelewa ni kwa njia gani,angewatoroka watu hao wenye roho mbaya wanaotaka kumuuwa!

“Mkuu,anapiga”

Mmoja wao akasema!

“Pokea”

Simu,ikapokelewa na kuwekwa sikioni!

“Ndio mkuu,tunaye tunakuja naye huko Dar!Tulishindwa,tulitaka kusikia kwanza kauli yako…Sasa,hakuna shaka!Sawa mkuu,kila kitu kitaenda sawa”

Upande wa pili haukusikika lakini kila mtu alifatisha maongezi hayo,Ngesa pia alikuwa makini kusikiliza kila kitu kinachoongelewa na baada ya simu kukatwa kuna ishara fulani aliona anawapa wenzake,jambo hilo lilikuwa la hatari sana!Hakukua na usalama mbeleni.

“Boma,kunja kona hapo!Twende kule katikati”

Sentensi hiyo ilimfanya Ngesa ajuwe nini maana yake!

Dereva akapunguza mwendo,wakaanza kuifata barabara yenye vumbi, mbaya zaidi akamuona mmoja wao anaweka bastola yake kiwambo cha kuzuia sauti isitoke,sio siri katika siku alizowahi kuogopa ni hiyo!Moyo wake ulipoteza utulivu,hofu ya kifo ilimtanda hakuelewa ni kitu gani akifanye hata hivyo hakuacha kuisumbua akili yake kuwaza namna ya kujinasua!Alivyogeuka nyuma,akayaona yale magari matatu yanafuata!Hapo ndipo alipochoka zaidi, ilikuwa ni lazima achukuwe maamuzi ya haraka kabla mambo hayajaharibika!

Gari lilizidi kusonga mbele mpaka walipofika katikati ya shamba hilo la katani,kisha kusimama!Jamaa mmoja wa upande wa kushoto akafungua mlango na kushuka akiwa na bastola mkononi,mbaya zaidi amemuelekezea Ngesa!

“Teremka,umefika mwisho wa safari”

“Mnataka kuniua?”

Sio siri Ngesa aliuliza kwa hofu na sauti yake,ilionekana kupwaya kwa uwoga!

“Shuka,shuka nimekwambia”

Watu hao,hawakuwa na utani hata kidogo na nyuso zao zilikuwa tayari kutoa roho yake!Akamtizama dereva ambaye alikuwa anamalizia kuzima gari,akaangalia pembeni yule mtu aliyekaa naye kulia kumlinda,akawa anajiandaa kushuka!

Ilikuwa ni lazima ajaribu nafasi ya mwisho kupigania roho yake,katika mafunzo yake ya ujajusi nchini Cuba alishawahi kufundishwa kujihami na mtu aliyeshika silaha!Sharti la kwanza aliambiwa alitakiwa kujifanya fala katika namna ya kumpumbaza ili ajione mshindi alafu kingine kuuwahi mkono wenye silaha,hicho ndicho alichokifanya.Akateremka mikono yake ikiwa juu lakini akili yake ikiwa kwenye mkono wenye silaha!Kitendo cha kufumba na kufumbua akamvaa na bega jamaa huyo mwenye bastola,kabla ya kutua chini,akajigeuza kama kambale kwenye tope,mkono wenye bastola akauzungusha kwenye kiuno chake,jamaa huyo akawa nyuma yake,bila kumpa nafasi akampiga kiwiko cha mbavu huku akinyanyua goti lake kidogo na kuupigiza mkono wenye bastola juu ya goti.

“Pyuuuuu”

Risasi moja,ikachomoka na kupasua kioo cha gari!Sauti ile ikawashtua wenzake!Jambo hilo likamuogopesha Ngesa, akamuona mmoja wao upande wa kulia,kashika bastola anamlenga alichokifanya ni kumgeuza yule jamaa aliyemshika akamfanya kama ngao!

“Paaaaaaa”

Risasi moja ilifumuka kwa niya ya kumpata Ngesa lakini ilionekana mlengaji hakuwa makini sababu ilimpiga mwenzake kifuani, ambaye Ngesa alimtumia kama ngao, jamaa huyo akaachia yowe kali la maumivu na kutulia,hapo ndipo Ngesa akapata mwanya wa kuchukua bastola iliyokuwa chini,akajibiringisha huku risasi zikimkosakosa na kuchimba mchanga,akajisogeza mpaka pembeni ya gari na kutulia!

Alivyochungulia kidogo, risasi ikapiga kwenye bodi mlengaji akawa amemkosa hiyo ilimfanya atambae na makalio mpaka upande wa mbele wa gari!Akamuangalia kwa makini mwana usalama mmoja,aliyekuwa ananyata kizembe huyohuyo akaanza naye kwa kumpiga risasi moja ya kichwa,habari yake ikaishia hapohapo!Katika ulengaji wa shabaha kwa kweli alijisifu, kwake ilikuwa kama kipaji ndiyo maana alitamba. Kwa haraka akatambaa na tumbo na kuingia uvunguni mwa gari,akabana jicho moja baada ya kuona miguu ya mtu!

“Paaa paaaa”

Risasi moja,ikamvunja mfupa akadondoka ya pili Ikamfikia tumboni akamuongeza nyingine ya utosi,tayari wa pili akawa amekufa!Alivyoona hivyo,akachomoka uvunguni kwa namna ya kutambaa na tumbo mpaka kwenye tairi!

“Paa! Paaa! Paaaa! Paaa! Paaaa!”

Ilikuwa ni milio ya risasi,kutoka upande wa pili kwa walengaji waliokuwa wanapiga risasi hovyo, hiyo ilionesha dhahiri wamepagawa tayari,ndiyo maana walirusha hovyo!

Nyingi zilipasua tairi nyingine zilipita hewani,hiyo ikamfanya Ngesa ajiinue kidogo na kuchungulia kwenye dirisha,akamuona mmoja wao yupo kwenye bodi ya gari pembeni!Akaishika bastola yake vizuri na kubana jicho moja,akavuta kilimi cha bastola,risasi moja tu ya kichwa ikamtupa hewani akadondoka chali!Mwenzake akawa amepagawa,hajui afanye nini!

“Suka,zunguka kule!Yuko pale”

Mtu mmoja,aliwatoa jasho na sasa walibaki watano tu,hesabu zao zikashindwa kufanya kazi!Risasi ziliendelea kurushwa na kila risasi moja ya Ngesa haikupotea bure,ilimdondosha mtu!Hatimaye,akabaki mmoja,anahema juujuu haamini anachokiona mbele yake!

“Tupa,bastola yako chini”

Hakutarajia kabisa kitendo hiko,Ngesa alikuwa nyuma yake na bastola imegusa kwenye kisogo chake!Bila ubishi wowote,akaweka bastola chini.

“Simama”

Akatii amri,mikono yake ikiwa kichwani!Anatetemeka.

“Nina watoto ndugu yangu,usiniue”

“Sijakuuliza.Nani,kawatuma?”

“Nurdin,kasema tukuuwe”

“Nurdin?Kwanini sio Rais?”

“Mimi sijui”

Ngesa,akatulia kidogo na kurudi nyuma akijaribu kutafakari lakini lilikuwa ni kosa kubwa la jinai kwani kufumba na kufumbua,alipigwa teke kali la kifua aina ya roubnd kick,akayumba na kupepesuka!Kabla ya kufanya lolote akapigwa teke lingine la tumbo akadondoka chali mzimamzima, bastola ikadondoka kando,bila kukawizwa akaanza kushushiwa kipigo cha mateke makali ya tumbo!Sio siri alihisi maumiviu makali sana!

“Mimi ndio Manyiko”

Jamaa huyo alijigamba huku akimtizama Ngesa kwa dharau,akamkwida shati na kumpiga kichwa puani!Hakuishia hapo,akamshika shingo na kumpigiza kwenye bodi la gari!

Hiyo ilimfanya Ngesa apige yowe kali la maumivu huku kichwani kwenye paji la uso akiwa anavuja damu!Kwa kiasi kikubwa alihisi maumivu makali na kichefuchefu cha kutapika,akarusha ngumi kwa niya ya kujitetea lakini ikapita hewani kwani bwana Manyiko,aliinama kidogo na kumtandika ngumi tatu nzito za mbavu zilizomuingia kisawasawa na kuhisi labda mbavu zake zimevunjika!Bwana Manyiko,akajiona mshindi kwa mbwembwe na madoido akaanza kuchezesha miguu yake kama wapigana boxa,mtu huyu alijiamini na alikuwa mtaalam sana kwenye mchezo wa karate na Judo ndio maana alimchanganya Ngesa na kuweza kummudu ipasavyo!Hiyo ilimfanya Ngesa,atulize akili sana kumsoma,teke moja lililokuja hewani akaliona akainama kidogo na kulidaka,hakutaka kumkawiza akampiga ngumi moja sehemu za siri na kumchota mtama ule mguu mmoja uliobaki,bwana Manyiko akadondoka mzimamzima kama embe lililoiva mtini,mbaya zaidi alifikia shingo!

Hapo ndipo Ngesa alipata nafasi ya kumsulubu akiwa chini!Ilielekea bwana Manyiko alikuwa mtaalam wa michezo hiyo kwani aliudaka mguu wa Ngesa na kumpiga ngwala,akamdondosha chini. Alivyotaka kusimama Ngesa akawa amemsoma akamrudisha na teke!Wote wakasimama na kukunja ngumi huku wakihema juujuu kama wana riadha!

Kosa namba moja alilofanya Bwana Manyiko ni kumfuata Ngesa kwa kasi huku akipiga kelele nyingi,Ngesa akaona hilo akamkwepa kidogo na kumsindikiza na teke la mgongo!Kwa kasi ya upepo akamfuata nyuma yake na kumpiga kabali moja matata sana!Kila alipohangaika kuitoa,akashindwa Ngesa akazidi kukaza mkono mpaka Bwana Manyiko alipoanza kuishiwa nguvu huku akijaribu kuutoa mkono wa Ngesa!

“Kaaaaa”

Kilichosikika ilikuwa ni sauti mithili ya mti mkavu uliovunjika,Shingo ya Bwana Manyiko ikawa imevunjwa,akatulia hapohapo na kusukumizwa,akadondoka chini,alichokifanya Ngesa ni kujishika shingo kwa namna ya kujinyoosha kutokana na maumivu!

Hakuwa na muda wa kupoteza,akachukua bastola moja wapo na kuingia ndani ya gari.Akawasha na kukanyaga mafuta mengi,tairi zikazunguka kwa kasi akafunga mkanda vizuri kwenye kiti huku shabaha ya safari yake ikiwa ni kufika jijini Dar es salaam,amfuate mpenzi wake Jaqlin Mfinanga baada ya hapo amsake Daphine pamoja na Dustan ili ‘ambush’ ianze!




Japokuwa alijitahidi kujitetea na kuelezea mkasa mzima jinsi ilivyokuwa tangu Brigedia Karanje,amchukue akiwa mtoto mdogo na kumpeleka Urusi lakini hawakumuelewa,walimchukulia moja kwa moja ni muuaji na ilitakiwa ashtakiwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kosa hilo zito la kuuwa watu,hakuwa na jinsi wala ujanja!Alikubali kila kitu na kuwa tayari kwa lolote lile litakalo tokea mbele!

“Daphine”

“Abee”

“Una uhakika ulikuwa hujui chochote?”

Ndani ya chumba kidogo cha mahojiano Daphine aliwekwa, mbele yake alitizamana na mpelelezi anayeshikilia faili lake.Siku hiyo alivaa dera akabana nywele zake vizuri kwa nyuma.Uzuri wake ukaonekana,Daphine alikuwa msichana mrembo pengine ungeambiwa alishawahi kuuwa ama ni hatari ungebisha,sura yake ilikuwa ya duara iliyobeba macho makubwa kiasi ya kusinzia na pua ya kiajemi,midomo yake ilikuwa midogo hiyo ilitokana na mashavu yake kuwa manene kiasi!Kifua chake kilibeba vizuri matiti madogo ya wastani,yaliyoendana na mwili wake,sio mnene wala mwembamba saizi ya kati!Hiyo ilimfanya Mpelelezi Abraham Odiero,aweke alama ya kujiuliza kichwani hakuwa ana uhakika kama ni kweli Daphine muuaji ama alibambikiwa kesi.

“Ndio,nilishawahi kuuwa.Lakini Mungu anisamehee!”

“Kwanini uliua?”

“Shinikizo la Brigedia Karanje”

“Lakini haikuwa kwa ridhaa yako?”

“Ndio”

Baada ya mahojiano mafupi,askari akafika na kumfunga pingu ili wamrudishe maabusu kusubiri hukumu yake!Daphine alisikitika sana na hakuacha kumkumbuka Ngesa huko alipo na kumuombea kwani alielewa gereza la Quantamo lilivyokuwa na ulinzi mkali hata hivyo hakuwa ana uhakika kama Ngesa yupo hai,hilo ndilo liliomfanya awe mpole na kutii amri zote,ghafla picha mbaya za wazazi wake kuuwawa kinyama ndani ya mbunga ya Mikumi ilianza kujijenga kichwani,ikaumba kama taswira fulani.

Japokuwa hakuwepo kipindi hiko wazazi wake wanauwawa na jeshi la Brigedia Karanje lakini alisimuliwa na kumfanya kila wakati akumbuke!Akaona jinsi wazazi wake wanavyopigwa risasi nyinginyingi!Moyo ukamuuma,baada ya kugundua kwamba hana ndugu hata mmoja anayemfahamu sababu aliokotwa akiwa mdogo sana!Mawazo yaliteka hisia zake,akapata muda mfupi kukumbuka mafunzo ya kijasusi alivyokuwa nchini Urusi,akashusha pumzi nyingi na kubana meno yake kwa hasira huku neno Kisasi likipita ndani ya ubongo wake!


****

Mwendo wa gari aliloendesha Ngesa ulikuwa ni kilomita kumi kwa dakika,gari lilikimbia mno kiasi kwamba kila mtu alilishangaa njiani, hata hivyo Ngesa alikuwa makini mno barabarani akiwa ameshikilia usukani kwa mikono miwili,anakimbiza gari kama chizi ili awahi jijini Dar es salaam aanze operesheni yake!Alielewa ni lazima angekumbana na vikwazo vingi sana kwani vita aliyoianza ilikuwa nzito na ilikuwa ni lazima aimalize!Kitu cha kwanza kumjia kichwani kwake alikuwa ni mpenzi wake Jaqlin Mfinanga,hakuelewa ni wapi amfiche ili yeye aendelee na harakati zake lakini alipokumbuka gala la mzee Lusubilo huko Vingunguti,akapata jibu akapandisha gia na kuzidi kusonga mbele huku akifikiria jinsi ya kuingia Ikulu ama kumteka Brigedia Karanje,ilikuwa ni kazi ngumu mno kuifanya peke yake, ndiyo maana alihitaji watu makini kama Daphine na Dustan ili operesheni hiyo iwe nyepesi kwake!Masaa manne baadaye alikuwa Mombo mkoa wa Tanga,hapo hakutaka kusimama sababu alishakula tayari,akapunguza mwendo ili kukunja kona!Kama kawaida ya wauza matunda na mikate,wote wakawa wanakimbiza gari lake wakitafuta mkate wao wa kila siku lakini Ngesa hakua na muda nao,akapandisha gia na kuongeza mwendo!


*****

Mbele yake walisimama wanaume watano na mwanamke mmoja katili, aliyejitambulisha kwa jina la Hawa,hawakutaka kusema wanatokea wapi lakini walitaka kujua nini Ngesa alizungumza naye!Hata hivyo maswali yao yaliambatana na mateso makali!Jaqlin Mfinanga aliteseka akiwa juu ya kiti amefungwa kamba miguuni na mikononi mdomoni kabandikwa gundi kali, iliyomfanya asiweze kupiga kelele.Ilikuwa kila wakimuhoji wanaitoa kisha kuirudisha tena huku wakimpa mateso makali sana!

“Ngesa alikwambia nini?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa mwanamme mmoja mrefu mweusi,aliyevaa kadeti ya kaki.Huyo alijitambulisha kwa jina la Dunga,sura yake ilikuwa nyeusi tii, mwili wake umejazia kwa juu, hakuonesha mzaha hata kidogo!

“Nimekuuliza, Ngesa alikwambia nini?”

Akauliza tena lakini badala ya Jaqlin kujibu alitingisha kichwa akimaanisha hakuna chochote anachoelewa,hapohapo alipokea ngumi nzito ya mdomo ikafanya mpaka kiti alichokalia kiyumbe kidogo,haikuishia hapo wakamtoa gundi mdomoni na kuendelea na maswali yao!

“Hatutoshindwa kukuuwa,hapahapa juu ya kiti na kifo chako kitakuwa kibaya sana!Upo tayari?”

Yalikuwa ni maneno ya kutisha mno,mateso yaliambatana na hakuwahi kuumizwa na kunyanyaswa namna hiyo,wakati mwingine alijuta kujiingiza katika mahusiano na Ngesa kutokana na matatizo kufuatana!

“Haku..niambia kitu chochote.Zaidi ya kuniaga tu”

“Unatudanganya,tuambie ukweli.Jiokoe,tuambie alichokuambia tunakuachia”

“Huo ndio ukweli…”

Jaqlin Mfinanga akajibu,mdomo wake ulikuwa mzito na ulivimba,damu zinamtoka puani anahisi maumivu makali mno!Kitendo cha kujibu hivyo,wakamfunika na kipande cha taulo puani,mmoja wao akaleta maji na kuanza kumimina juu ya kipande cha taulo,ndani ya sekunde sabini akaanza kutupatupa miguu na mikono akitafuta hewa ya oxijeni,taulo likatolewa.Akaanza kuhema kwa pupa!

“Tutaendelea hivi,mpaka utakapo kufa!Ngesa alikwambia nini?”

“Si..jui”

Zoezi likaendelea!Ndani ya dakika moja wakatoa tena taulo.

“Na..waambia nasema nawaambia”

Hakuweza kuvumilia tena baada ya kuona mateso yanazidi,kuendelea kubaki kimya aliamini ni lazima zoezi lingeendelea tu.

“Sema”

“Aliniambia nije hapa Baga..moyo!Nimsubiri atakuja”

“Lini?”

“Hajaniambia ni lini”

“Una uhakika?”

“Ndio”

Hawakuwa na sababu tena ya kuendelea na zoezi hilo wakiamini ni lazima Ngesa angefika mahali hapo,hata hivyo walipewa taarifa kwamba tayari yupo Tanzania mkoani Arusha!Na mpaka wakati huo hawakuweza kupata mawasiliano na wanausalama wenzao,dalili ilionesha kwamba Ngesa kawazidi nguvu,walichokifanya ni kutega mitego yao!Wakamfungua kamba Jaqlin Mfinanga na kumkalisha kwenye kiti.

“Sisi tunaondoka,akija Ngesa tupigie simu namba zetu hizi hapa”

Baada ya hapo wakatoka nje,ambapo huko walitega mita mia kutoka kwenye nyumba hiyo ili wamvizie Ngesa,wamnase!


******

Saa tisa ya Alasiri,Ngesa aliingia Msata akakunja kona na kunyoosha mzimamzima bila kupunguza mwendo, akiifuata barabara ya Bagamoyo,ambapo huko alinyoosha moja kwa moja!Baada ya masaa machache akafika Bagamoyo mjini,sasa akawa amekaribia kufika!Kivyovyote vile alielewa ni lazima atakuwa anafuatiliwa, alichokifanya ni kuweka gari kando,akachukua bastola na kuiweka kiunoni!Akapata muda kidogo wa kukagua gari,kwa maana ya kuangalia kama angekuta kitu chochote ambacho kingemfaa!Akaona bastola moja iliyojaa risasi,pamoja na magazine tatu, pia zilikuwa na risasi za kutosha!Akazidi kupekua lakini hakukuta kitu kingine chochote cha maana,akafunga mlango na kuanza kutembea kwa tahadhali huku akigeuka nyuma akiangalia usalama,akaamba na ukuta taratibu akatokea kwenye kichochoro,hapo akatulia na kuchungulia, jambo lililomfanya apigwe na butwaa,moyo wake ukapiga kwa nguvu!Gari aina ya Prado,lilikuwa upande wa kushoto na kando kulikuwa na wanaume watatu,mbaya zaidi wanaitizama nyumba aliyomwambia Jaqlin Mfinanga amsubiri!

Hisia zake zikamwambia watu hao ni lazima watakuwa usalama wa taifa,alichokifanya ni kuambaa na kichochoro mpaka kwenye mti mkubwa,hapo akajificha akitafakari atumie njia gani ili asisababishe purukushani yoyote ile.Akapata wazo baada ya kukumbuka kuna mlango wa nyuma wa uani,isingekuwa rahisi kwa mtu kupenya sababu kulikuwa na miti mingi iliyotengeneza kichaka kizito,akajitosa na kuingia kwenye miti hiyo,ambapo kulikua na miiba mingi sana!Akafanikiwa kupita akaruka ukuta na kutua uwani bila kutoa kishindo chochote kile,akachomoa bastola yake na kuishika vizuri,mkononi!Kwa tahadhali akaanza kunyata akatizama huku na kule.Kwa kuwa ilikuwa ni nyumba ambayo haikumaliziwa ilikuwa ni rahisi kwake kuingia,akanyata tararibu na kumuona Jaqlin Mfinanga akiwa juu ya kochi,analia kwa kwikwi!Alivyotaka kujitosa kumfuata,akajionya asifanye hivyo kwani ingekuwa ni hatari kwa usalama wake!Akapata muda kidogo wa kutizama huku na kule!Alivyohakikisha usalama upo,akajitosa mpaka seblen!

“Jaqlin”

Kitendo cha kusikia jina lake,alishtuka mno!Alivyogeuka nyuma akapigwa na butwaa lisilokuwa na mfano,hakuamini kama anayemuona ni Ngesa mpenzi wake!Kwa furaha ya ajabu akasimama na kumrukia,wote wakakumbatiana, Jaqlin akazidi kulia kwa kwikwi.

“Wana..kutafuta mpe..nzi..Wanataka kukuuwa”

“Naelewa,tuondoke mahali hapa”

Hakukuwa na muda wa kupoteza.Wakaanza kutembea kupitia mlango wa nyuma,huko kulikuwa na ukuta uliochoka, Ngesa akaelewa kabisa Jaqlin asingeweza kuruka alichokifanya ni kuiweka bastola yake kiunoni na kuanza kumpandisha!

“Weka mguu mmoja hapa!”

Kwa usaidizi wa Ngesa,akaweka mguu mmoja juu ya tofali.Akajishika vizuri kwa juu ili arukie upande wa pili!

“Pyuuuuuu”

Risasi moja,ilipunyua ukuta na kumkosa kosa Ngesa kichwani!Akainama na kujitupa upande wa pili chali, baada ya kugundua kuna hatari na kuna mtu yupo nyuma yao anarusha risasi!

“Pyuu pyuuu”

Kuendelea kusikilizia risasi zinazorushwa bila kujibu ilikuwa ni sawa na kusubiri kifo,akachomoa bastola yake kutoka kiunoni!

“Paaaaaa”

Risasi moja tu aliyofyatua Ngesa,ikamuondoa jamaa huyo mlengaji ikamtupa mbali na kukichengua kichwa chake vibaya sana, hata hivyo Ngesa akajua ni lazima wangeingia wengine kwa kusikia mlio wa bastola!Kwa kasi,akatoka mafichoni na kuparamia ukuta na kutua upande wa pili,ambapo kwa nje alimkuta Jaqlin amepagawa tayari!

“Twende huku”

Akasema huku akimshika mkono wakaanza kutembea kwa haraka,mpaka kwenye kichochoro chembamba hapo Ngesa akachungulia kwa namna ya kuangalia usalama!Kila kitu kilivyokuwa sawa,wakatembea mpaka kwenye gari wote wakaingia!

“Funga mkanda”

Gari likapigwa norinda,likageuzwa kwa kasi na kuingia barabarani kwa niya moja tu,kwenda nyumbani kwa Dustan,Masaki! Ili aonane naye wapange mikakati, zikiwemo mbinu za kumteka Rais Leslie na baada ya hapo amsake Daphine popote pale alipo, waungane!



Shingo ya Ngesa ilikuwa nyuma muda wote,kakanyaga mafuta mengi gari linarudi kinyumenyume kwa kasi lakini kabla ya kukaa sawa akasikia mlio mkubwa wa risasi,alivyogeuka mbele akawaona watu wawili wameshika bastola mikononi na mmoja kati yao ndiye aliyefyatua risasi lakini ilipita hewani,alivyoona wanataka kuachia risasi nyingine akageuza gari kwa haraka!

“Weka kichwa chako chini”

Ngesa alitoa amri,Jaqlin Mfinanga kwa hofu akaweka kichwa chake chini huku akihema,risasi zilizidi kurushwa lakini ilishindikana sababu Ngesa alikunja moja ya kona na kuzidi kukimbiza gari!Akaanza kutafakari kama ni salama kwake kuwasubiri ili apambane nao lakini alijionya kufanya hivyo kwani angepoteza muda alafu kingine kilichomfanya asite hakujua watu hao wamejipanga vipi, kwake ikawa bora nusu shari kuliko shari kamili.Kwa umakini wa hali ya juu akawa ana kazi ya kutizama vioo vya ubavuni kama kuna dalili yoyote ile ya gari linalomfatilia,alivyohakikisha kila kitu kipo shwari akashusha pumzi na kumtizama mpenzi wake!

“Pole mpenzi”

Akasema huku akimwangalia kidogo,kwa haraka alikiri kwamba Jaqlin Mfinanga ni msichana mrembo mno,alikua ni mrefu kiasi mwenye mwili mdogo kimtindo!Macho yake makubwa yalimkaa vizuri na kumfanya azidi kuvutia,sio hivyo tu rangi ya msichana huyo ilikuwa maji ya kunde naya kung’aa!Ingawa alikuwa anaendesha gari lakini alipata muda mfupi wa kumkagua mpenzi wake hata yeye alikiri siku hiyo Jaqlin Mfinanga ni msichana mrembo,wakati mwingine alimuonea huruma baada ya kujiingiza naye katika mahusiano,ambayo yalimpelekea mpaka maisha yake yawe hatarini.

“Walikuwa wanataka nini?”

Ngesa akaweka kwanza mawazo hayo pembeni sababu alijua athari yake kwani mwili wake ulianza kuchemka,alichotaka kujua watu waliomfuata nyumbani walimuuliza kitu gani.

“Sijui,lakini waliniuliza maswali”

“Maswali gani?”

“Kwamba wewe uko wapi?”

“Uliwajibu?”

“Hapana,baada ya hapo wakaniambia wanaondoka kumbe walikua nje”

“Walijuaje,upo pale?”

“Hata mimi sielewi”

Kwa akili ya Ngesa na mambo yalivyoenda alijua fika kwamba ni lazima watu wake wote wa karibu wanafuatiliwa,hilo alilipa asilimia zote mia moja bila kipingamizi!Akabana meno kwa hasira na kuzidi kuchanja mbuga,akisonga mbele!

“Shiiit”

Ngesa akakema baada ya kuona mbele yake kilomita mbili kuna askari walioshika bastola na mitutu, mbaya zaidi walikuwa wameziba barabara kwa kuweka ‘Barrier’ iliyokuwa na chuma,haikuwa rahisi kuvuka eneo hilo bila kukaguliwa!

Hilo lilimfanya aingiwe na mashaka sana,akashika bastola yake vizuri lakini katika kutafakari kwa muda akajua kivyovyote vile hatoweza kupita eneo hilo sababu askari walikuwa wengi!Alichokifanya ni kumtizama Jaqlin Mfinanga!

“Shika usukani”

“Unasemaaa?”

“Shika usukani”

Ngesa alizungumza huku akichomoa bastola yake kiunoni,mkono wa Jaqlin ukawa umeshika usukani!

“Pita huku”

Ngesa akawa anajitoa taratibu niya yake ikiwa ni kubadilishana siti,Jaqlin Mfinanga aendeshe gari yeye akae kushoto,zoezi hilo lilivyofanyika baada ya kubadilishana siti!Ngesa akatulia kidogo ili kupiga hesabu,kivyovyote vile alijua askari hao wanamtafuta yeye!Gari analoendesha lilikuwa ni pickup hardboard nyuma lilikuwa na uwazi na umbali wa mita mia mbili kulikuwa na maaskari,hiyo ilimaanisha achomoke kikomandoo!

“Punguza mwendo”

Jaqlin alivyopunguza mwendo Ngesa akafungua mlango,akajitupa upande wa nyuma ambapo kulikuwa na turubai,akajifunika huku akiwa na bastola mkononi akijihami kwa askari yoyote yule atakayejifanya kiherehere kufungua turubai.Gari likazidi kusonga mbele,walivyokaribia kwenye ‘barrier’ askari mmoja aliyevaa mtutu begani akasogea barabarani na kupunga mkono kwa ishara ya gari lisimame,Jaqlin akasimamisha gari lakini askari huyo akapunga mkono kwa ishara kwamba apaki pembeni!Hilo halikuwa tatizo ingawa alikuwa mwenye hofu sana moyoni mwake!Askari huyo aliyekuwa mrefu kiasi,mwembamba akatembea mpaka kwenye gari taratibu, akagonga kioo,kikateremshwa!

“Habari yako dada”

Afande akasalimia huku akitupia macho ndani ya gari,kwa namna ya kufanya ukaguzi!

“Salama afande poleni na kazi”

“Unatoka wapi?Unaelekea wapi?”

“Natoka Bagamoyo!Naelekea Mjini”

“Kufanya nini?”

Lilikuwa ni swali lililoulizwa na Afande.

“Mama yangu anaumwa”

“Mbona kama una wasiwasi?Upo sawa?”

“Sipo sawa,mama anaumwa”

“Teremka ndani ya gari”

Moyo wa Jaqlin Mfinanga ukapiga paaa!Ukapoteza uelekeo,akaanza kuhema kwa kasi jasho linamtoka mbaya zaidi alivyoona askari mwingine kasimama analifuata gari,akatafakari kwa muda na kumtizama afande huyo aliyekuwa karibu na mlango wake!

“Afande,Mama yangu anaumwa naomba niwahi”

“Nimekuelewa dada,shuka kwenye gari”

“Namuw….”

Afande alivyoona hakuna maelewano,akashika kitasa cha mlango na kuvuta,mlango ukafunguka!

“Shuka dada,tufanye kazi yetu au unataka nitumie nguvu?”

Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana,kubwa kuliko kandokando kulikuwa na shati la Ngesa lenye damu, kabla ya askari kuliona Jaqlin akalivuta na mkono wake wa kushoto akalitupa chini ya siti.

“Nyuma kuna nini?”

“Hakuna kitu”

Maongezi ya Askari yalimfikia Ngesa akiwa ndani ya turubai,amejifunika yupo chali bastola yake kaishika mkononi tena ameikoki kidole kimoja kipo kwenye triga,ametulia kama maji ya kisima!Akasikia hatua za askari anakuja upande wa nyuma yake.Hakukosea kwani askari mmoja wapo alifika mpaka nyuma akatizama turubai kwa kama sekunde tatu,akionekana kama anataka kulifungua!

“Kuna kitu gani humu?”

Akauliza afande huyo huku akilishika,hakuelewa kwamba kwa sekunde hiyo Jaqlin Mfinanga anaomba Mungu hatari itakayotokea mbele yake aiepushe!Afande akashika turubai ili alifungue lakini kilichomshtua ni nyuma yake umbali wa mita mia mbili baada ya kuona kuna gari linakuja kwa kasi ya risasi,hiyo ilitosha kabisa kushuku kwamba hakukuwa na usalama!

“Afande…Tizama”

Lilikuwa ni jambo lililomshtua Jaqlin Mfinanga pia,gari aliloliona linakimbia kwa kasi lilimuogopesha kwani ndio lile lililokuwa nyumbani lililobeba watu waliotoka usalama wa taifa,hapo wakajua tayari wamekwisha alichokifanya Jaqlin ni kujiongeza!

“Afande….”

Jaqlin Mfinanga akaita huku akiweka sura ya huzuni alielewa nini maana yake endapo gari hilo la wanausalama lingefika mahali hapo!

“Dada washa gari,ondoka eneo hili”

Lilikuwa ni kosa kubwa la jinai kwa askari kutoa ruksa hiyo kwani Jaqlin hakutaka kuangalia nyuma tena ‘barrier’ ikatolewa barabarani,akawasha gari na kuliondoa kwa kasi huku akiangalia kwenye vioo vya ubavuni, ambapo aliliona gari la wanausalama linasimamishwa na askari zaidi ya watano walioshika silaha!

Alivyotaka kuendelea kuangalia ili kujua nini kingetokea akajionya asifanye hivyo kwani ingekuwa rahisi kwao kukamatwa kabla hawajafika mbali,walizidi kusonga mbele na walivyofika Bunju akaweka gari kando na kushuka,akatembea mpaka nyuma ya turubai.

“Mpenzi shuka”

“Tuko wapi?”

“Bunju B”

Ngesa akatembea na kuingia kwenye usukani huku akimshukuru sana mpenzi wake kwa ujasiri aliokuwa nao!Hakukuwa na muda mwingine wa kupoteza sababu alitaka kupanga mikakati hiyo kabambe kabla ya jua alijazama na alivyoangalia saa yake alijipongeza kiasi, sababu alikuwa ndani ya muda ingawa ulimtupa mkono kidogo!


*****

Baada ya kufika Masaki,Bridgestone Street!Akaweka gari kando,ulikuwa ni mtaa uliotulia na kwa haraka walikuwa wakiishi watu wazito ama wenye pesa zao kwani yaliambatana magorofa na mageti makubwa huku pembeni kukiwa na kuta zilizozungukwa na nyaya za umeme!Ngesa alikuwa karibu na nyumba anayoishi Dustan,hakutaka kuingia kichwakichwa ndiyo maana akaweka gari umbali mrefu kidogo, nyumba akawa anaitizama kwa mbele!

“Kacha kacha”

Akakoki bastola na kumtizama Jaqlin Mfinanga kwa macho fulani hivi,yasiyokuwa ya kawaida.

“Kamati hii”

“Mpenz…”

“Hapa ni kupiga risasi,nimeikoki tayari.Kua makini mpenzi narudi sasa hivi”

Katika siku ambayo Jaqlin Mfinanga alitetemeka ni hiyo,hakuelewa itakuwaje kwani hakuwahi kutumia silaha kabla hata hivyo akaishika na kutamani kumwambia Ngesa abaki,lakini alikuwa tayari amechelewa sababu Ngesa alitoka nje tayari kuelekea mbele,akamuona jinsi anavyotembea mpaka kwenye moja ya kona na kukunja!

Uchunguzi wa Ngesa uliendelea huku akiwa anatembea,alilitizama geti ambalo ndani yake kulikuwa na nyumba ya Dustan,akauangalia ukuta ulivyokuwa mrefu kwenda juu!Hakuelewa ndani kulikua na walinzi wangapi lakini alijua ni lazima nyumba hiyo ilikua inalindwa siku zote!Alichokifanya ni kutembea mpaka mwisho wa ukuta ambapo huko kulikuwa na mti mdogo uliokatwa vizuri,hilo likamfanya Ngesa atabasamu na kushukuru!Kabla ya kupanda,akatizama huku na kule akatembea kwa kasi na kudandia,akapanda kwa kasi na kuushika ukuta vizuri ambao ulikuwa una nyaya za umeme,alivyochungulia chini ndani ya nyumba hakuona mtu hata mmoja!Kwa tahadhari akashika ukuta vizuri,akapitisha miguu yake upande wa pili!Kazi ikawa kwenye kushuka kwani ukuta ulikuwa ni mrefu,hata hivyo hakutua vizuri kwani alitoa kishindo kikubwa kidogo!

“Wooow! Woooow! woooooow!”

Sauti ya mbwa kubweka ikasikika,hiyo ilimuogopesha akajua kivyovyote vile kama kuna mtu ndani ni lazima angetoka kutizama nje!Kwa kasi akakimbia kwenye kona na kujificha,hakukaa sana akamuona mwanamke akiwa gorofani anatizama chini,sura hiyo haikuwahi kumtoka alikua ni mke wa Dustan!Mke wa Dustan alivyoingia ndani,Ngesa akatoa bastola yake kutoka mafichoni kwa kunyata akatembea na kuingia ndani,ambapo alikuta mlango upo wazi!

Akatokeza jikoni,kulikuwa na ukimya wa hali ya juu,akazidi kutupa hatua zake!Mbele yake kulikuwa na mlango, huo aliujua wa kuingilia seblen,akanyata taratibu mithili ya paka shume akasukuma mlango wa jikoni huku bastola yake ikiwa mbele,alivyopiga hatua ya kwanza kuingia seblen akakuta utulivu uleule.Ilikuwa ni seble kubwa yenye vitu vya gharama na imepangiliwa vizuri,televisheni kubwa ukutani na masofa ya kisasa!Akazidi kusonga mbele, alivyokanyanga ngazi ya kwanza ili apande gorofani,akahisi kichuma cha baridi kimemgusa kisogoni moyo wake ukakosa utulivu!

“Derrick Ngesa, tupa bastola chini”

Ilikuwa ni sauti iliyotokea nyuma yake,ikimuonya asifanye kitu chochote cha kijinga isipokuwa kutupa bastola chini na kusalimu amri.Kilichomuogopesha zaidi sauti hiyo haikuwa ya Dustan,hiyo ilimaanisha tayari ameingia kwenye mikono ya watu hatari kwa mara nyingine!

“Nimekwambia tupa bastola chini,mwisho wako umefika Ngesa hauna ujanja”

Hakuwa na jinsi zaidi ya kutupa bastola chini,akaweka mikono hewani.

“Unataka nini?”

“Songa mbele”

Hatua za taratibu akaanza kutembea huku bado bastola ikiwa imegusa kisogo chake. Siku zote huwezi kukwepa kifo lakini kamwe katika maisha yake aliapia kwamba hatokuja kufa kifo chochote akiwa vitani bila ya kumuona adui yake!

Alivyofika seblen,alishtuka na kupigwa na bumbuazi baada ya kumuona Dustan kawekwa juu ya kiti cha mbao,uso wake una vuja damu!Kichwani amepasuka vibaya sana,pembeni ya Dustan yupo mtu aliyeshika bastola anamtizama yeye,sura yake ilifanana na mtu anayetaka kupiga chafya ikaishia katikati.Ngesa alipandwa na hasira kwani Dustan alitia huruma na alionekana alikuwa akiteswa kwa muda mrefu sana.

“Mmemfanya nini rafiki yangu nyie wapumbavu?”

Ngesa akauliza kwa jazba,akashindwa kuzuia hasira zake, akataka kugeuka ili afanye fujo lakini akatulizwa na kitako cha bastola kichwani,akajitupa makusudi kwa mbele akiwa hivyo hivyo na maumivu ili aione sura ya mtu aliyemuwekea bastola kwa nyuma,hakuamini mtu aliyemuona! Hapo ndipo akajua kwamba duniani kuna watu na viatu!




Mwanamme aliyemuona mbele yake kamshikia bastola anashirikiana na usalama wa taifa kumuangamiza hakuamini kabisa,alikuwa ni rafiki yake wa kufa na kuzikana aliyefahamika kwa jina la Mbita,alikuwa ni mfupi kiasi mwenye misuli ya mazoezi mikononi, akiwa katika dimbwi la mawazo akikumbuka jinsi walivyokuwa pamoja na kucheza wote utotoni,akashtukia amepigwa teke zito la shingo na mtu aliyekuwa kando,sio siri maumivu aliyohisi akadhani wenda shingo yake imevunjika sababu alijipigiza kwenye meza na kutulia chali,akiwa anahema kwa pupa!Baada ya utulivu wa sekunde mbili,akamuona mtu mwingine anaingia, hapo akaamini kwamba ulikuwa ni mtego wa kumsubiri yeye na walimtumia mke wa Dustan kuchungulia kila mtu anayeingia ndani ya nyumba hiyo,ghafla moyo wake ukapoteza utulivu baada ya kumkumbuka Jaqlin Mfinanga aliyekuwa nje peke yake!Hakuwa ana uhakika kama huko alipo alikuwa salama ama tayari watu hao hatari wamemuweka chini ya ulinzi!

“Mnataka nini?”

Ngesa akauliza kwa niya ya kununua muda kidogo!Lakini badala ya kujibiwa mmoja wapo mbele yake,akacheka kicheko cha dharau na kebehi.

“Ngesa,sidhani kama hujui ni kitu gani tunataka”

“Sijui”

Hapohapo akapokea teke lingine mithili ya shuti lililomfanya ahisi kichefuchefu cha kutapika,hakika yalikuwa mateso makali mno kuwahi kutokea,mmoja wapo kati ya watu wale akamsogelea karibu na kumuinua kwa namna ya kumkwida akamsimamisha na kumtizama kwa hasira za waziwazi.

“Unajifanya mjanja sana lakini huu ndio mwisho wako Ngesa”

“Mnachelewa nini?”

Sio kwamba alijibu kwa kiburi kutoka moyoni,lakini ukweli Ngesa alikuwa mwenye hofu mno!Alitetemeka ndani kwa ndani,sababu kifo siku hiyo kilikuwa nje nje na hakuwa ana uhakika kama angefika kesho kwani sura za watu waliokuwa ndani wanamuangalia walikuwa na uchu,hakukuwa na masihara yoyote na kile walichokiongea walimaanisha!

“Usijali,mikakati ya kifo chako ndio kinasubiriwa nyumbu wewe”

Baada ya mtu huyo,kumalizia sentensi yake akamtwanga kichwa kikali Ngesa puani kilichomfanya ayumbe na kudondoka chini kama mzigo,akahisi maumivu makali na nyota nyingi sana mbele yakiambatana na maluweluwe,hakika yalikuwa maumivu makali mno!Hakuishia hapo,akainuliwa na kupigwa ngumi tatu za mbavu zilizomuingia kisawasawa kama sindano,alivyotaka kuleta upinzani akaona midomo ya bastola inamtizama hiyo ilimuonya na kumfanya awe mpole mbele ya manati hizo za mzungu!

Akiwa chini anaugulia maumivu,akajigeuza pembeni na kumuona Dustan alivyoumizwa vibaya sana usoni,yupo hoi jicho moja limeumuka ana majeraha shingoni na mikononi, hasira zilimpanda lakini alivyotaka kukurupuka kama swala,akasita akiamini kwa kufanya mjongeo wowote usio rasmi angechapwa risasi,akatulia akitafakari cha kufanya!Alivyokuwa chini,akasikia simu ya rafiki yake kipenzi ambaye kwa wakati huo alionekana Yuda na kivyovyote alijuwa ndiye mkuu wa operesheni hiyo.

“Halloo,ndio tupo nao wote!Na mwenzake?Sawa hilo halina shida,okay”

Upande wa pili wa simu haukusikika lakini kupitia macho yake kulikuwa na mpango hatari mno!Akamshuhudia Mbita anawaita wenzake wakawa kama wanajadili kitu fulani cha siri,baada ya hapo wawili kati yao wakavaa gloves nyepesi!Kulikuwa kuna kila sababu ya kuamini hatari mbeleni kwani aliyekuwa mbele akaweka bastola mezani na kuchukua kamba nyembamba,akaisokota ikafanana na kitanzi,akasogelea meza na kuirusha kwa juu ambapo ilijizungusha juu ya chuma kizito,akaifunga vizuri na kumuendea Dustan,aliyekuwa kwenye kiti akamuinua!Moyo wa Ngesa ulipoteza utulivu kabisa,alisikia uchungu na alitamani amuokoe rafiki yake kipenzi kutoka kwenye kifo chenye mateso ambacho kingesababishwa na kitanzi!Hakuwa na ujanja zaidi ya kutulia,akishuhudia wanamuinua Dustan,wakamvalisha kitanzi shingoni!Mkewe akaangua kilio lakini alitulizwa na kibao kikali kilichompeleka chini mzima mzima,jambo lililomfanya Ngesa azidi kupandisha mashetani,hata hivyo hakuwa na namna akatulia!

“Vuta kamba vizuri na huyu Ngesa mfungeni tuondoke naye”

Sentensi hiyo ilitoka kwa Jamaa mmoja,aliyekuwa mlangoni mkononi ana bastola!

“Mnataka kunipeleka wapi?”

Sasa akawa ana uhakika kwamba hakutakiwa kuuwawa hapo,alichoelewa yeye ilitakiwa apelekwe sehemu fulani ambapo huko angepata mateso bila shaka kabla ya kuuwawa kifo cha kinyama sana!

“Kelele,tutakuuwa”

“Mngetaka kuniua,mngeshaniua tayari”

Hapo alitulizwa na kofi aina ya kelbu na kunyamaza kimya,wakamvuta kwa nguvu na kuibana mikono yake kwa nyuma!Kama utani,akamuona Dustan anapandishwa juu ya meza ili anyongwe jambo ambalo hakuwa tayari kuliona ilikuwa ni bora yeye aanze kufa kuliko kushuhudia kifo kama hiko cha kinyama tena chenye mateso makali mno!Dustan,alivyopandishwa juu,meza ikapigwa teke, akaanza kuning’inia kama nyama buchani,mkewe alilia kwa uchungu Ngesa akapandwa na hasira huku akimtizama Dustan aliyekuwa juu ya kamba anatupa tupa miguu hewani,ndiyo hapo akapata wazo na kukusanya nguvu nyingi!

Nyuma yake kulikuwa na mtu anamfunga kamba vizuri,alivyoangalia mbele yake akaona watu walioshika bastola wamepoteza umakini wanamtizama Dustan,nafasi hiyo hakutaka kuipoteza hata kidogo kwa kasi na nguvu za ajabu akarudisha kichwa nyuma na kikampiga jamaa cha pua,akaachia yowe na tusi juu!Alivyogeuka mbele akawaona wenzake,wamegeuka ghafla kitu ambacho alikuwa tayari kajiandaa nacho!Kwa haraka akageuka na kumvuta mtu aliyempiga kichwa na kumuweka mbele yake!

“Paaaaaa”

Risasi moja ikaachiwa,badala ya kumpiga Ngesa ikampata mwenzao!Hiyo ilimfanya Ngesa ajitupe nyuma ya sofa ambapo huko zilisikika risasi tu,akawa amelala chali risasi zinapita juu yake!Pembeni yake kulikuwa na stuli ndogo,mbele kidogo kuna bastola iliyokuwa chini, ipo karibu na mke wa Dustan,ambaye kwa wakati huo alikuwa anatetemeka yupo nyuma ya sofa la pili,wanaangaliana!

“Bastolaaaa”

Ngesa alisema kwa vitendo huku akimwambia Mke wa Dustan aisukume bastola upande wake,haikuwa rahisi kama anavyodhani hiyo ilimchukiza Ngesa,taratibu akaanza kutambaa,alivyochungulia kwenye kingo ya sofa risasi ikamkosa kosa,akarudi tena na kutulia, hakika lilikuwa ni jambo la hatari sana ukizingatia hakuwa na silaha yoyote ile!Kuna kitu kilimfanya atabasamu baada ya kukumbuka ana kisu kwenye buti,akakichomoa taratibu na kurudi upande wa chini,akachungulia na kuwaona watu hao hatari wakiwa na bastola mkononi,hakuwa ana uhakika na jaribio analotaka kulifanya lakini alijipa matumaini kwamba lingefanya kazi,katika mafunzo ya kijasusi alijikubali sana hususani katika swala zima la kutumia visu,ndiyo maana alikishika kisu vizuri kwenye ncha ya makali na kuanza kumpigia hesabu jamaa wa mbele aliyekuwa makini kulitizama sofa!Hapo hapo kitendo cha kufumba na kufumbua akajitokeza na kurusha kisu kisha kurudi chini,hakufanya makosa kisu kilimfikia jamaa wa mbele cha shingo, kilimuingia vizuri ndani mpini ukabaki nje,kutokana na maumivu makali,akaachia risasi kadhaa hewani huku akiwa ameshika shingo yake inayovuja damu hapohapo akadondoka chini akiwa anakoroma kama kondoo anayechinjwa,wenzake kwa kiwewe wakaanza kurusha risasi hovyo kama waliopagawa,hayo ndiyo yalikuwa mahesabu ya Ngesa,akachepuka upande wa pili kwa mtindo wa kubiringika kama Ninja na kuiokota bastola.

“Paaaaa”

Cha kwanza tu,alilenga chuma lililokuwa juu lililokuwa na kamba iliyomfunga Dustan kwa juu,akadondoka kama mzigo risasi nyingine ikamfikia mwingine na kumtupa chini!Kuhusu swala la shabaha alikuwa vizuri na alilijua hilo,ndiyo maana akatulia kidogo na kusikiliza milio kadhaa ya risasi na ilikuwa kila akitoka mafichoni anaondoka na mtu mmoja!Mpaka alivyobaki mmoja,ambaye huyo alikuwa Yule rafiki yake Mbita,sio siri alikuwa na usongo naye baada ya kukumbuka walivyomuweka Dustan juu ya kamba wakitaka kumnyonga!

“Paaa paaaaa”

Risasi mbili,zilipiga kioo akawa ana uhakika kabisa mlengaji hakuwa makini sana!Alichokifanya ni kusikiliza kwanza,akachungulia kidogo na kumuona Bwana Mbita katokeza anataka kuhama upande hapohapo akavuta kilimi na kumtandika risasi ya mguu,kabla hajadondoka chini akamchapa risasi nyingine begani iliyomuachia maumivu makali sana akiwa chini!Ngesa hakutaka kutoka kwanza mafichoni,akatulia kama dakika moja nzima ili kuangalia usalama!Alivyoona kupo shwari akasimama akiwa na bastola mkononi,akamsogelea Mbita aliyekuwa chini anaugulia maumivu,akaipiga bastola iliyokuwa karibu yake teke,akamchapa risasi nyingine ya paja!

“Mbita”

“Nge……s….a usiniu..e tafadh..ali”

Ngesa akamtizama kwa hasira kabla ya kugeuka na kumuangalia Dustan aliyekuwa amelala chali,mkewe yupo juu yake analia machozi!Hakuwa ana uhakika kama Dustan yupo hai ama amekufa lakini alipandwa na hasira za waziwazi,akatembea taratibu mpaka kwa maiti iliyotoa macho,kisu kipo shingoni akakichomoa na kumsogelea Mbita.

“Huu ndio ujira wa kazi yako”

Kama utani,Ngesa akamkata jicho kali Mbita na kukitumbukiza Kisu tumboni mwake hakuishia hapo,akaubararua utumbo mzima kwa hasira huku akitetemeka,alivyohakikisha kamaliza hasira zake,akamchapa risasi nyingine ya kichwa iliyofanya ubongo wake umwagike kisha akamtemea mate!Hakukua na muda wa kupoteza tena,akaamini kwamba muda wowote wangeingia wengine!Akamsogelea Dustan kwa kasi na kuinama kidogo!

“Sogea apate hewa”

Ngesa akasema ili kutoa huduma ya kwanza,akachana shati lake na kusikiliza mapigo ya moyo kwa namna ya kuweka sikio kifuani mwa Dustan!

“Anahema kwa mbali,tuondoke”

Kwa usaidizi wa Ngesa pamoja na mkewe wakambeba Dustan huku na kule huku bastola ya Ngesa ikiwa mkononi tayari kwa shambulizi lolote lile,mbeleni!Wakatoka mpaka nje wakiwa makini mpaka kwenye gari,kilichomfanya Ngesa apigwe na butwaa ni baada ya kumkosa Jaqlin Mfinanga ndani ya gari,kwa kweli moyo wake ulikosa utulivu kabisa.

Akatulia kwa muda wa sekunde mbili na kumuacha Dustan ndani ya gari,akaanza kutembea kwa mguu huku akimtafuta!Hisia mbaya zilimtuma wenda Jaqlin Mfinanga alikuwa ametekwa tayari na watu hatari,akakosa raha kabisa na kuamini kivyovyote vile zoezi lake lingeanza kuwa gumu sana!

“Jaqlin,Jaqlin,Jaqlin”

Ngesa aliita kwa sauti ya chini,akatizama huku na kule!Ghafla kwenye maua akaona kuna kitu kinacheza cheza akakamata bastola yake vizuri,kulikuwa na kichungu kikubwa sana kinachotingishika, kwa umakini na taadhali akakisogelea lakini ghafla akakutana na mlango wa bastola!

“Usiniue, usiniue”

Sauti hiyo ilitoka kwa Jaqlin Mfinanga akiwa na hofu kubwa huku akiwa amefumba macho anaogopa na kutetemeka kwa wakati mmoja!

“Ni mimi Derrick,weka bastola chini taratibu Jaqlin.Upo salama!Mimi Derick Ngesa mpenzi wangu”

Kwa utulivu Ngesa akasema akiamini kivyovyote vile kama Jaqlin angevuta kilimi cha bastola angechapwa risasi ndio maana akawa mpole akitumia diplomasia kama anayeomba!Jaqlin alivyosikia hivyo akafumbua macho yake na kumkumbatia Ngesa kwa nguvu zake zote!

“Mpenzi naogopa”

“Usiogope,upo salama tuondoke”

Muda wa kukaa hapo na kuoneshana mahaba,haukuwepo tena!Walichokifanya ni kuanza kutembea kwa haraka mpaka walipopaki gari,Ngesa akaingia ndani ya gari akawasha wakaanza safari ya kuondoka.


******


Waliingia mtaa wa Mchikichini saa mbili kasoro usiku,walishukuru Mungu hakukuwa na tabu yoyote ile njiani, Ngesa alikuwa nyuma ya usukani akakunja na kutokezea mtaa wa Gonga akasonga mbele na kukunja kulia ambapo alishika barabara inayoelekea mtaa unaoitwa Nyota,hapo Ngesa akazima taa ili kuepuka macho ya watu waliokuwa vibarazani wanamtizama!Akaweka gari kando na kuwageukia Dustan na mkewe!

“Nisubirini,nakuja”

Ngesa akatoka,akiwa ana uhakika alipo kulikuwa na giza lililotokana na miti mikubwa ya mikorosho,akaanza kutembea na kukunja kona ambapo kulikuwa na uchochoro mwembamba,akaivuka nyumba ya kwanza!Ya pili,akagonga huku mkono wake mmoja ukiwa ndani ya mfuko umekamata bastola yake vizuri kwa chochote kitakachotokea!Baada ya kutulia akasikia mlango unafunguliwa,mbele yake akamuona mzee mwenye mvi amefunga msuli na kavaa kibalagashea kichwani!

“Derick mjukuu wangu”

Mzee alihamaki kwa mshangao wa waziwazi.

“Ndio mimi babu,shikamoo”

“Marahaba”

Alikuwa ni mzee mwenye umri kati ya miaka 75-77,ndiyo maana sauti yake ilikuwa ya kitetemeshi kidogo.

“Babu,nina matatizo”

“Mjukuu wangu,nashukuru nimekuona kabla sijafa!Karibu ndani”

“Ahsante,nina ndugu zangu kule wamepata matatizo”

“Wako wapi?”

Babu akauliza huku akitizama nje kwa namna ya kuwaona hao ndugu zake na Ngesa!

“Kwenye gari”

“Kwenye gari?”

“Ndio babu”

“Wakaribishe ndani”

Kwa kasi Ngesa akatoka mpaka gari lilipo,wakambeba Dustan vizuri wakisaidiana na Jaqlin Mfinanga mpaka kwenye kijumba hiko cha Babu,wakaingia ndani na kufunga mlango!

Kabla ya yote Ngesa akapata muda mfupi kutoa utambulisho wa babu yake mzaa Mama,aliyefahamika kwa jina la Mzee Mirobo!Kwa kuwa Ngesa aliwahi kuishi ndani ya nyumba hiyo miaka mingi iliyopita,hakuwa mgeni na mazingira, akaingia jikoni na kuwasha jiko la mkaa ambapo alibandika maji mengi kisha kurudi seblen na kumtizama Dustan,aliyekuwa kidogo ana nafuu sasa aliweza kufumbua macho yake ingawa kwa tabu sana!

“Pole rafiki yangu Dustan”

“Ng…esa ahsante sana,umeyaokoa maisha yangu!Mungu akubariki,hapa ni wapi?”

“Kwa babu yangu,mzee Mirobo!Kua na amani”

“Wale watu ni hatari sana”

“Naelewa,pumzika kwa sasa”

Hapo Ngesa,akatulia kisha kukapita ukimya!Akamtizama Jaqlin Mfinanga na kumpeleka mpaka chumba kimoja kilichokuwa na godoro dogo,pembeni kuna ndoo ya maji na kabati lililochoka,kifupi ilikuwa ni nyumba ya kizee kutokana na mazingira yaliyokuwepo!

“Utapumzika humu ngoja nikuwekee maji ya kuoga”

“Derrick naogopa”

“Usiogope tutakuwa wote”

“Tafadhali usiniache”

“Siwezi kukuacha tena Mpenzi”

Ngesa akamtoa wasiwasi kisha kurudi jikoni ambapo huko,alichukua maji kidogo akamuwekea Jaqlin bafuni,akaoga kisha yeye baadaye akaoga pia!Kwa mara ya kwanza kutuliza akili yake tangu atoke nchini Rwanda ilikuwa ni hiyo,kwa kweli alijihisi sasa amekuwa binadamu kamili,akapata muda wa kumuhoji Dustan!

“Daphine yupo Central ana kesi na kifungo chake cha maisha,atahukumiwa”

“Nani anasimamia kesi yake?”

“Sijajua,nilivyotaka kufuatilia ndio kama ulivyoona walinifuata nyumbani kwangu”

“Nani kawatuma?”

“Hata sielewi”

“Karanje yuko wapi?”

“Huyo ndio sijui hata alipo ana ulinzi mkali,ukitaka kufahamu alipo Karanje mtafute IGP Abubakar Mboya”

“IGP,anahusika vipi na mkasa huu?”

“Ndio yupo karibu sana na Rais Leslie siku hizi,Ngesa kuna siri kubwa sana Karanje anayo kuhusu Rais Leslie!Ndiyo maana hataki aguswe”

Kitu hiko kiliibua hisia kali sana kwa Ngesa,akahisi kama amepigwa na ubaridi mgongoni akashusha pumzi nzito,sasa akaanza kupata picha kamili ya matukio mbalimbali yaliyotokea na kwanini Rais Leslie alitaka kumrudisha gereza la Quantanamo!

Usiku huo waliongea vitu vingi,baadaye wakala ugali na matembele wakashushia na maji!Kila mtu akaingia chumba alichooneshwa,Ngesa alivyofika chumbani kwake akamkuta Jaqlin Mfinanga amelala muda mrefu sana anakoroma kwa mbali,akavua nguo zote na kushika bastola yake vizuri akajitupa kwenye godoro na kuiweka bastola chini,kandokando kabisa ya kichwa!Akabaki kutizama juu,hakutaka usingizi umchukue sababu aliamini hakuwa salama kabisa.

“Mbona hulali mpenzi?”

Jaqlin akauliza baada ya kujigeuza.

“Sina usingizi”

Kitendo cha kusema hivyo,Jaqlin akamsogelea karibu miili yao ikagusana.Ki ukweli walihisi kama shoti zimewapiga,Jaqlin akajisogeza karibu zaidi na kuanza kumnyonya Ngesa mdomo mkono wake taratibu akaupeleka kwenye malighafi, jambo lililomfanya Ngesa atulie na ujasusi wake wote akawa kama mwanakondoo anayeenda kuchinjwa,Jaqlin hakuishia hapo!Akaanza kumpapasa kifuani na mwili mzima huku wakibadilishana mate,akatoa kanga na kubaki kama alivyozaliwa!Hapo ndipo Ngesa,akapata kuuona vizuri uzuri wa Jaqlin Mfinanga na kifua chake kilichosimama kama miba ya michongoma,akamvuta kwa nguvu akimkwaruza mgongoni huku mkono mmoja ukiwa taratibu unayabinya makalio yake!Hata hivyo hawakuchukua muda mrefu,wakaingia katika tendo lililowaleta duniani!




Kwa mara ya kwanza tangu aanze pilika na kashkash za kutafutwa na watu wa Rais Leslie kutoka usalama wa taifa,alikuwa amelala usingizi mtamu wa kueleweka!Alijihisi ni mwepesi na akili yake imetulia kwa kufikiria vizuri!Penzi tamu alilopewa na mpenzi wake, ghafla lilimsahaulisha matatizo yote aliyopitia!Saa kumi na moja alifajiri alikurupuka kutoka kitandani,akatizama huku na kule akamuangalia Jaqlin Mfinanga,ambaye kwa wakati huo alikuwa amelala hoi anatoa sauti ya mkoromo kwa mbali,akatafakari kwa muda na kuutoa mkono wake uliokuwa kifuani kisha kusimama mpaka dirishani ili kuangalia usalama kwanza,alivyohakikisha hakuna kiumbe yoyote anayemfuatilia akafungua mlango na kuingia bafuni ambapo huko alioga na kunawa vizuri,akarudi chumbani na kuvaa nguo!Akachukua bastola yake na kuiweka kiunoni,hapo ndipo Jaqlin Mfinanga alishtuka na kumuangalia kwa macho fulani ya uchovu.

“Unaenda wapi mpenzi?”

“Nitarudi muda sio mrefu”

“Unaniacha mwenyewe?”

“Upo sehemu salama,nitarudi lakini mpenzi wangu!Sio kwamba napenda kukuacha,sitaki kukuingiza kwenye matatizo mengine zaidi”

Ngesa akatumia diplomasia akiongea kwa utulivu wa hali ya juu akimshawishi Jaqlin Mfinanga abaki huku akimtoa wasiwasi kabisa!Hilo halikuwa tatizo kwani msichana huyo alimuelewa ingawa kwa shingo upande,alichokifanya Ngesa ni kutoka na kunyoosha mpaka chumba alicholala Dustan huko alichotaka kujua ni wapi Daphine alipo na wala sio kitu kingine!

“Central”

“Yupo Central uliniambia,ulinzi wa pale upoje?”

“Mkali,nadhani unajua historia ya Daphine”

“Naelewa”

“Uwe makini Ngesa”

Badala ya Ngesa kujibu akamtizama Dustan kwa macho fulani yanayosema ‘Usijali’ akamtizama mke wa Dustan ambaye alionesha kila dalili ya kuwa na wasiwasi sana!Kuanzia hapo,hakukua na maongezi mengine zaidi ya kumuaga babu yake na kutoka nje,ambapo huko aliingia ndani ya gari na safari ya kwenda kituo kikubwa cha polisi kilichopo mjini Posta, kuanza mara moja!


****

Haukuwa utani,Daphine alilindwa kuliko mtuhumiwa yoyote yule,askari walipokezana zamu na walikuwa na silaha za moto!Kutoroka kwa Daphine akiwa rumande ilimaanisha vibarua vyao kuota nyasi, ndiyo maana Rais Leslie alitaka Daphine awekwe chini ya ulinzi mkali mno!Na hicho ndicho kilichotokea,askari hawakulala usiku na mchana,akitoka huyu anaingia yule!

“Mimi ndio natoka sasa hivi Kamanda,nakukabidhi ofisi”

Askari mmoja alisikika akimwambia mwenzake,asubuhi hiyo kulivyo pambazuka!

“Sawa afande mimi nipo”

“Hakikisha,una saini hapa”

Daphine alikuwa nyuma ya nondo,amekaa ameegemea ukuta hana hili wala lile,aliwaza vitu vingi sana hususani maisha yake ya gerezani yangekuwaje,aliumia moyo zaidi baada ya kubaini kwamba anaenda kufungwa bila ya kuwajua ndugu zake!Kitu ambacho hakikua cha kawaida kabisa,alivyomkumbuka Brigedia Karanje akaumia mtima,akatamani atoke alipo akamvae amuue!Licha ya yote kila kitu alikiacha kama kilivyo,hata hivyo alimkumbuka sana Derrick Ngesa huko alipo alimuombea Mungu amlinde na kila kitu,machozi yalimlenga na alikuwa ana kila sababu ya kudhani tayari Ngesa amekufa!Alisikitika na kujikuta anainamisha kichwa chake chini, akimwaga machozi!


*****

Mzee wa kazi Ngesa alikuwa tayari ameshaingia mjini Posta,yupo ndani ya gari anatizama mazingira ya jinsi atakavyoingia ndani ya kituo hiko cha polisi kinacholindwa mno!Mbele aliona magari ya polisi yakiwemo Diffenda na magofu makubwa ya mapolisi,kando kando aliwaona maaskari wakiwa katika jezi zao na trafiki wa barabarani,akaendelea kupiga hesabu jinsi atakavyoingia ndani ya kituo hiko!Macho yake yakavutiwa na askari mmoja aliyetoka ndani ya kituo hiko anavuka barabara,akamtizama kwa kama sekunde tisa na kumuona anaingia ndani ya kantini,alichokifanya Ngesa ni kuwasha gari na kulisogeza stendi ya mabasi ili amsubirie vizuri!Akamsuburi mpaka atoke ambapo hapo alimuona anatembea mpaka kwenye gari ndogo akazidi kumdadisi!Ghafla akamuona amebadili mawazo na kuliacha gari,ilielekea kuna kitu alisahau ndani. Hapo ndipo Ngesa akateremka kwa kasi,akatizama huku na kule kichwa chake kikiwa chini mpaka kwenye gari alilokuwa askari,alivyolifikia akasimama kwa pembeni huku akichungulia huku na kule kama kuna mtu yoyote anafuatilia nyendo zake,alichoshukuru Mungu kila mtu asubuhi hiyo alikuwa na hamsini zake za kutafuta rizki,jambo hilo lilimfurahisha zaidi!Alivyomuona askari huyo mnene mwenye kitambi analifikia gari,akabonyea kwa chini!Alielewa mfumo wa gari hilo kwamba dereva akifungua mlango wake ni lazima loki zote za milango ziachie, ndiyo maana mkono wake ulikuwa kwenye kitasa cha mlango wa nyuma,askari bila kuangalia akaingiza funguo kwenye kitasa cha mlango akafungua Ngesa akawahi kuingia na kuchomoa bastola,askari alivyoingia alipigwa na butwaa baada ya kukutana na mlango wa bastola!

“Kaa kimya”

Ngesa alizungumza kwa sauti isiyokuwa na mzahaa, macho yake ameyakaza bastola ipo mkononi!

“Wee ni nani?”

Askari akauliza kwa sauti ya kitetemeshi huku akihema kwa uwoga!

“Funga mlango,weka mikono yako juu ya usukani”

Zilikuwa ni kauli za kitemi,zilizomfanya askari huyo aogope mno!Mbaya zaidi gari lake lilikuwa ‘tinted’ yaani vioo vyeusi,hivyo hakukua na mtu yoyote ambaye angeweza kujua nini kinaendelea ndani ya gari.

“Toa bastola yako taratibu ukitumia vidole viwili”

Hakukua na namna ya kukahidi amri ya Ngesa aliyekuwa nyuma yake,anamtizama kwa hasira!Alichokifanya afande huyo ni kutumia vidole viwili kuchomoa bastola yake na kumpatia Ngesa!Alivyoangalia vizuri,akahisi kama kinyesi kinataka kumtoka,sura hiyo haikuwa ngeni kwake alishawahi kuiona siku kadhaa zilizopita kwamba mtu huyo anahusika na ugaidi sasa leo hii yupo naye ndani ya gari,katika siku ambayo alikuwa katika wakati mgumu ni hiyo!

“Usiniue ndugu yangu,nitafanya chochote unachotaka mimi sio mmbaya wako”

“Sina shida ya kukuua,nataka kujua Daphine yupo wapi?”

“Daphine gani mi…..”

Kabla ya askari kumalizia sentensi yake alipigwa na kitako cha bastola kichwani,hiyo ilikuwa ni kama kumshtua kidogo akili yake ikae sawa!Kufumba na kufumbua,damu zikaanza kumtoka kwenye paji la uso!

“Daphine yuko wapi?Sitorudia tena kuuliza kwa mara nyingine!Niambie alipo”

Safari hii,akajua kweli hakukua na utani kwani bastola iligusa utosi wake!

“Yupo ndani na afande Faraji,mimi nimetoka zamu sasa hivi”

“Nafikaje ndani?”

“Mimi sijui”

Ngesa akawa na wakati mgumu kidogo,akatizama kituo cha polisi akaona jinsi gani maaskari wanavyoingia na kutoka bila kuangaliana usoni,akapata wazo kabambe na kumtizama askari anayelia lia kama mtoto wa kike,alichokifanya ni kuizungusha mikono yake shingoni na kuanza kumkaba kwa nguvu huku aking’ang’ania mshipa mmoja unaotoa hewa!Hiyo ilimfanya askari huyo atupe tupe miguu kama kuku anayechinjwa,ndani ya dakika tatu akawa amezirai Ngesa hakutaka kumuua!Kwa kasi,akajipinda vizuri na kuanza kumvua nguo zote mwilini,akazivaa yeye!Akachukua na kofia!Akaiweka kichwani,akaivuta mpaka chini kidogo!Nguo za askari zilimpwaya kidogo ingawa zilimtosha,akashuka ndani ya gari kichwa chake kikiwa chini!

“Afandee…..”

Sauti ya nyuma yake ilimshtua kidogo,akapiga hatua mbili mbele zaidi lakini akasikia hatua za mtu zinamjia kwa kasi,akasimama huku akiingiza mkono wake mafichoni,akaishika bastola vizuri.

“Afande,naomba nisaidie kitu”

Hapo Ngesa alishusha pumzi ndefu baada ya kuona sura ya kijana mmoja anayetaka msaada wa ki usalama.

“Kuna nini?Ebu nenda pale kituoni kuna mwenzangu atakusaidia”

Ngesa akazungumza kama askari aliyefuzu,licha ya hayo yote katika mafunzo yake ya kijasusi alifundishwa jinsi ya kubadilika kutokana na mazingira,ndiyo maana kwake ikawa rahisi akaingia mpaka mapokezi!

“Jambo afande…”

“Jambo..”

Ngesa nayeye akaitikia,akaanza kutembea huku akikagua chumba kimoja baada ya kingine,alivyokunja kona akamuona askari amesimama nje ya maabusu!Akamtizama akajua ni lazima hapo Daphine angekuwepo sababu ilikuwa tofauti na ‘Lockup’ nyingine ambazo hazikuwa na ulinzi wowote ule!Akamuendea askari huyo,mpaka karibu kabisa!

“Kamanda Faraji”

Ngesa,akatingisha kiberiti hakua ana uhakika kama Kamanda Faraji ni huyo,jina hilo alipewa na askari aliyekuwa ndani ya gari ambaye mpaka wakati huo hakuelewa angepata fahamu muda gani,alichotakiwa kufanya ni kupeleka mambo harakaharaka ili kitumbua kisiingie mchanga!

“Naam afande”

Haikuwa rahisi kugundulika kwani kulikuwa na giza totoro!Hiyo ilimpa Ngesa nafasi ya kuchungulia ndani,ambapo kulikuwa na chuma mithili ya nondo ngumu, kwa mbali akamuona msichana ameinamisha kichwa chini,hakua ana uhakika kama ni Daphine lakini alitaka apate uhakika zaidi,akachomoa bastola yake na kuigonga kwenye nondo ikatoa mlio!

“Arooooo”

Ngesa akapiga mkwara kwa namna ya kutaka Daphine ainue kichwa lakini badala yake,zoezi hilo likaonekana kuwa gumu kwani Daphine aliendelea kulia kwa kwikwi kichwa chake kipo chini.Ngesa,akawa ana kazi ngumu kidogo akasogea upande wa pili,kilichomfanya agundue kuwa ni Daphine ni baada ya kuona kovu kwenye mkono wake wa kushoto,akapata uhakika na kumtizama Mlinzi, akamuangalia kiunoni ambapo kulikuwa na funguo nyingi mno!Hakutaka kumkawiza,akamvuta kwa nguvu na kumpiga pigo moja la judo shingoni,askari hakuomba maji mdogo mdogo akaanguka chini na kutulia.Hakukuwa na muda wa kupoteza zaidi ya Ngesa kuchukua funguo na kuanza kujaribu moja baada ya nyingine.

“Ngesa!”

Butwaa alilopigwa Daphine,halikuwa na kipimo chake!Kwa kasi akasimama na kuzisogelea nondo, ambapo hapo Ngesa alikua bize,kujaribu funguo kwenye kufuli mara aichomeke hii mara ile ‘Kacha’ sauti ikasikika ya kufuli kuachia,Daphine hakuchelewa akafungua mlango na kumkumbatia Ngesa kwa nguvu na hisia zote!

“Ngesa”

“Daphine,pole sana!Tuondoke,hatuna muda tena wa kukaa hapa”

Hakua na lingine zaidi ya Daphine kujiongeza na kuchukua mtutu wa askari aliyekuwa chini,akaukoki na kuongoza mbele akiwa na ujasiri mkubwa mno!Jinsi alivyoushika mtutu mkononi, hakutofautishwa na mwanajeshi vitani,alivyofika kwenye kona akatulia na kumuonya Ngesa asimame!

“Twende”

Daphine akasema kikomandoo,akanyata na kumuona afande mmoja anakunywa chai,akamtwanga na kitako cha mtutu utosini,puu chini!Wakasonga mbele na kutulia kidogo!

******

Afande Chilumba,alizinduka dakika saba baadaye!Shingo yake ilimuuma mno!Akaizungusha kwa namna ya kujinyoosha,alivyotulia vizuri akagundua hana nguo hata moja!Taa nyekundu ikawaka kichwani kwake,akajua kabisa kuna kitu kibaya kimetokea kwani hakuwa na jezi hata moja mwilini,alichokifanya ni kuvuta suruali ya Ngesa aliyoiacha na kutoka bila shati mkuku mkuku mpaka kituoni huku akipiga kelele nyingi!Ngesa na Daphine wakiwa bado kituoni wanataka kutoka walisikia kelele hizo kutoka kwa afande,hapo hakukuwa na jinsi zaidi ya kuchomoka kwa kasi lakini walikuwa tayari wamechelewa sababu walisikia milio ya risasi,wakainama kidogo na kupenya penya mpaka kwenye moja ya Diffenda na kuingia!Askari walirusha risasi nyingine zikapasua vioo vya Diffenda,hiyo iliwatia mashaka sana ya kukutwa mahali hapo, ilibidi washauriane waingie ndani ya gari,hilo likafanyika!

“Cover me”(Nilinde)

Ngesa alisema,alichokifanya Daphine ni kumimina risasi nyingi upande waliokuwa maaskari mpaka Ngesa alipofanikiwa kuvunja swichi ya gari na kugusisha waya,diffenda ikawaka Daphine akaingia ndani.Gia ikapigwa,gari likaanza kurudi kinyume nyume kwa kasi huku wakirushiwa risasi!Kazi ya Daphine ilikua ni kuwajibu kwa kufyatua risasi mfululizo huku gari likiwa linarudi kinyume nyume.




Katika swala zima la kucheza na magari Ngesa alikuwa hodari mno,akiwa mafunzoni pia alifundishwa jinsi ya kupambana na adui yoyote huku akiwa nyuma ya usukani,jambo hilo lilimfanya awe mwepesi kama kambale kwenye tope ndiyo maana alirudisha gari kinyume nyume huku shingo yake ikiwa nyuma,alivyopata upenyo wa barabara pana akavuta hendi breki na kukanyaga breki,hapohapo kwa kasi ya upepo akazungusha usukani,gari ikazunguka kitaalam kama sinema jambo lililowashangaza hadi mapolisi waliokuwa ndani ya difenda,katika maisha yao mambo hayo waliyaona kwenye video lakini siku hiyo ilikuwa mubashara,hata hivyo hawakutaka kumuacha wakarusha risasi hovyo, lakini hazikuzaa matunda kwani baadhi zilipita hewani na nyingine kupasua taa za gari,ilielekea walengaji hawakuwa na shabaha nzuri.

“Risasi zimeisha”

Daphine aliyekuwa kiti cha pembeni akarudisha shingo ndani baada ya risasi kumuishia ndani ya mtutu,alichokifanya Ngesa bila kusema chochote akachomoa bastola kutoka kiunoni na kumkabidhi!Kabla ya kuanza kufanya mashambulizi akachomoa magazini na kukuta kuna risasi sita tu zilizosalia,hiyo ilimaanisha awe makini katika utumiaji wake!Askari wakiwa na diffenda walizidi kupamba moto,sasa walikuwa wenye uhakika kwamba wanayemfukuzia ni mwanaume hatari anayeitwa Ngesa,aliyetokea kulisumbua jeshi la polisi pamoja na serikali nzima,mbaya zaidi tayari alikuwa ameungana na mwanamke jasusi,Daphine!Hiyo ilikuwa ni hatari kubwa sana kwao endapo wangechomoka bila kuwatia nguvuni.

“Tunahitaji difenda nyingine,unaongea na Meja Kamali!Staki shari,nahitaji askari ishirini sasa hivi”

Kupitia redio upepo askari waliomba msaada baada ya kuona patashika hiyo kali!Wakazi wa Posta na sehemu jirani,walitandwa na hofu, maeneo hayo tayari yalikuwa meupe,kila mtu alitaka kunusuru roho yake!Vilema waliokuwa kandokando ya mitaa ya Posta wamekinga mikono na vibakuli wanaomba, walisimama na kutimka,milio ya risasi iliwatisha hiyo ilifanya wakazi wa eneo hilo, wagongane vikumbo kama siafu waliomwagiwa majivu ya moto!Daphine alikuwa makini,shingo yake ipo nje kashika bastola vizuri,risasi moja tu aliyoachia haikufanya makosa,ikatoboa tairi la diffenda lililokuwa katika kasi sana,hiyo ilifanya gari hilo liache njia na kugonga ukuta mkubwa,likabiringika na kutulia!Milio ya risasi ilisikika na kwa muda mfupi habari hizo zilienea kwa kasi ya moshi wa kifuu,Ramadhan Nurdin alitetemeka kwa hofu kwani alishaelewa nini chanzo cha mirindimo ya risasi.

“Shiiit,this is bullshit!Kwanini iwe hivyo?”

Ramadhan Nurdin,Mkurugenzi katika kitengo cha usalama wa taifa alizipokea taarifa hizo kwa mshtuko mkubwa sana,bado hakuamini kama watu wake walizidiwa nguvu na Ngesa mpaka akaingia jijini Dar es salaam,akiwa ndani ya ofisi yake alijihisi kuchemka kila kitu kuanzia damu mpaka mwili,akahisi kama miguu yake imeishiwa nguvu za kutembea ghafla akahisi kama joto kali,akalegeza tai yake shingoni.

“Mpumbavu mkubwa nataka maelezo vizuri,imekuaje”

Ramadhan Nurdin,alizungumza kwa sauti ya juu simuni akiwa mwenye hasira za waziwazi!Wakati akifoka mlango wake ukagongwa,akasita kidogo na kutembea!Alivyofungua alikutana na sekretari wake akiwa na simu mkononi!

“Rais Leslie,anataka kuzungumza nawewe”

Sekretari akasema huku akiwa ameganda bado mlangoni,hata yeye alimshangaa sana bosi wake Ramadhan namna anavyohema na alionekana kama mtu aliyekosa utulivu kabisa!

“Sawa,kaendelee na kazi”

Ramadhan Nurdin akajibu kwa sauti ya juu akimruhusu Sekretari aondoke,akafunga mlango na kushusha pumzi ndefu,alishaelewa ni kitu gani Raisi Leslie anataka kujua,alikuwa na asilimia zote mia moja kwamba angeulizwa habari za Ngesa!

“Halloo Mheshimiwa Rais”

“Nakusikiliza”

Sauti ya upande wa pili ilionesha ni jinsi gani Rais Leslie amechukia kwani hakutaka salamu ya aina yoyote!

“Mheshiw..”

“Nurdin,imekuaje?”

“Ah aaaah,ndio ndio tunafanya utaratibu wa kumka…”

“Stupid….Unajua nini maana yake?Unajua madhara yake nilikuamini sana na ulinihakikishia kila kitu kitakua salama na..”

“Mheshimiwa Rais a…”

“I’m still talking, shut up”(Bado nazungumza nyamaza)

Mkwara na vitisho vyote vilimfanya anywee na kuwa mpole mbele ya bosi wake Rais Leslie,hakuelewa amjibu nini wakati alipanga jambo hilo liwe siri kubwa sana,lakini matokeo yake alishindwa kumzuia Ngesa mpaka anaingia jijini Dar es salaam mbaya zaidi fununu alizosikia ni kwamba kamtorosha Daphine!

“Kwanini hukuniambia mapema?”

“Niliogopa kukusumbua Mheshimiwa Rais”

“Kwahiyo una mpango gani?”

“Mheshimiwa nipe leo,atakuwa mikononi mwangu”

“Nurdin,hii nafasi umeipoteza!Nampa mtu mwingine”

“Hapana,naomba unipe nafasi nyingine sitofanya makosa”

“Nakupa masaa Ishirini na mbili,Ngesa awe chini ya ulinzi pamoja na Daphine”

Masaa aliyopewa kufanya kazi hiyo,yalikuwa machache kumsaka mtu kama Ngesa mwanamme hatari na jasusi,licha ya yote aliitikia huku akiapia kwamba angempata Ngesa ndani ya masaa manne tu,hata hivyo alijiamini ndiyo maana baada ya kukata simu akatembea mpaka kwenye ‘draw’ yake na kuchukua bastola yake ndogo,iliyojaa risasi!Akabana meno yake kwa hasira akiwa mwenye usongo wa kumpata Ngesa awe mfu au hai.Hakutaka kupoteza muda,akanyanyua mkonga wa simu akabonyeza namba fulani kisha kusikilizia!

“Niunganishe na IGP,sasa hivi”

Simu hiyo ilimfikia Sekretari,ambapo bila kupoteza muda akafanya alichoambiwa IGP akawa kwenye laini na mkurugenzi wa usalama wa taifa!

“Zoezi linaendeleaje?”

“Bado vijana wangu,wanafukuzana naye!Sijapata taarifa ya uhakika mpaka sasa hivi”

“Wako wapi?”

“Kwenye redio call yangu hapa naona wamefika,Vingunguti”

“Umefanya jitihada gani,kuwasiliana na askari wa Vingunguti?”

“Barabara imezibwa tayari”

“Niunge na redio 097 nataka kusikia kila kinachoendelea”

“Hakuna shaka”

Ramadhan Nurdin,alishikwa na hasira ajabu mbaya zaidi shabaha yake haikuwa kumtia Ngesa chini ya ulinzi bali kumuua,alichokifanya ni kushuka ngazi kwa kasi mpaka kwenye maegesho ya magari na kuchukua gari aina ya Volkswagen comb,pembeni alishika redio upepo ambayo aliweza kusikia mawasiliano yote yanayofanywa na jeshi la polisi,ilikuwa rahisi kwake kujua Ngesa anaelekea upande gani,ndiyo maana baada ya kuwasha gari aliwaza jambo moja tu,kuitafuta Vingunguti

ilipo!


******

Diffenda iliyokuwa inaendeshwa na Afande Anthony Wabike,ilikuwa sambamba na gari la Ngesa!Dereva huyo,alionekana nayeye alikuwa mtundu mno ndiyo maana aliweza kula sahani moja na gari la mbele yake,ilikuwa kila Ngesa akikata kona nayeye yupo pembeni,haikuwa hali ya kawaida, hata Ngesa aliingiwa na mashaka na wasiwasi wa kukamatwa ulimuingia sababu tayari waliishiwa risasi!Hiyo ilimfanya Ngesa atumie akili ya ziada lakini katika kutafakari akasikia mtikisiko mkubwa wa gari,alivyoangalia kioo cha ubavuni akaona hatari kubwa, Difenda iliyokuwa sambamba nao iliwagonga kwa nyuma,akaishuhudia inataka kuwapita lakini jambo hilo hakutaka litokee ndiyo maana akazungusha usukani kulia ili kuzuia asipitwe,ilielekea dereva wa Difenda kamanda Anthony Wabike,alishtukia hila hiyo akawahi kurudisha gari kushoto akawa upande wa Daphine,akakanyaga mafuta mengi na kuligonga gari la Ngesa ubavuni,ambapo lilipoteza uelekeo hiyo ikamfanya Ngesa atumie jitihada nyingi kulirudisha barabarani!Hakukuwa na kitu kingine ambacho kingeweza kuwanasua kwenye hatari hiyo mbaya,isipokuwa kukimbiza gari na kucheza na usukani!

“Nikikwambia fungua mlango,unafungua”

“Unasemaje Ngesa?Sijakusikia”

Daphine akauliza hakusikia vizuri kutokana na sauti ya upepo mkali na milio ya honi,Ngesa akatoa maelekezo tena akijaribu kufanya hesabu zake lakini bahati haikuwa kwake,Kwani Diffenda iliwapita ubavuni wakawa sambamba,wakamshuhudia dereva anatoa bastola ili awafyatue,alichokifanya Daphine ni kuinama chini kwa kasi,Ngesa akapigwa na butwaa lakini akawahi kukanyaga breki za gari,lile difenda likapitiliza risasi ikapunyua kioo,ilikuwa ni shabaha isiyokuwa na hesabu!Hapo ndipo Ngesa akazungusha usukani na kuingia barabara nyingine ya Vumbi,inayoelekea Kipawa!Sio siri,hawakua na uhakika kama wangeshinda vita hiyo ambayo maaskari walizidi kuongezeka!Safari ilizidi kupamba moto,wakizungushana mara huku mara kule!


******

Taa za gari la Ramadhan Nurdin,zilikuwa ‘full light’ kuashiria ana dharura hivyo apishwe barabarani, anakimbiza gari kwa kasi ya ajabu!Huku akipiga honi mfululizo bastola yake ipo pembeni ya gia,usongo aliokuwa nao ulikuwa wa kuua,hakua tayari kumuacha Ngesa hai hata kidogo hilo alijihaidi mwenyewe na hiyo siku aliapia kama asingemuua Ngesa na kazi ataacha kwani alitokea kujiamini sana!Masikio yake yalikuwa makini sana kusikiliza redio upepo,mara ya mwisho akasikia Ngesa yupo Barabara ya Msimbazi centre,butwaa alilopigwa halikuwa la kawaida haikuwezekana hata kidogo dakika chache atoke Vingunguti mpaka alipo,hata hivyo hakutaka kujiuliza mara mbilimbili,akavunja sheria na kupanda katikati ya barabara ambapo kulikua na msingi mkubwa akaingia upande wa pili na kurudi alipotoka niya yake ilikuwa atokee kwa mbele,yaani amlie Ngesa denge,hila yake ilikuwa karibu kufanikiwa sababu baada ya muda mfupi alikuwa tayari amefika Mataa ya Magomeni,bila kusimama akakunja mzimamzima,akachukua bastola yake iliyokuwa pembeni ya gia!

“Kacha kacha”

Akaikoki na kuishika mkononi vizuri,tayari kwa kumuua Ngesa!Masikio yake akayatega kwenye redio upepo ambapo alisikia maaskari wakisema amefika Kigogo!Hiyo ilimfanya atabasamu na kukunja mdomo kwa uchu wa kuua,akazidi kukanyaga mafuta,alivyofika round about ya Kigogo akahepa kushoto ili akutane na Ngesa uso kwa uso!Kwa mbali aliona msururu wa diffenda nne,mbele yake kuna gari ndogo iliyovunjika vioo!Akawa ana uhakika bila kuuliza ni lazima angekuwa Ngesa tu,hapohapo akapiga msele gari ikasimama na kuzunguka ikakaa katikati ya barabara, bila kujifikiria akashuka na kupanda juu ya boneti, akashika bastola yake vizuri.

“Paa! Paa! Paa! Paa! Paa! Paa! Paa! Paa! Paa! Paaa! Paaaaa!”

Ramadhan Nurdin,aliachia risasi zisizokuwa na idadi kamili,nyingi zilipita hewani nyingine zikapasua kioo cha mbele,tatu zikapiga tairi za mbele Ngesa akashindwa kulimudu gari likahama upande na kupiga ukingo wa daraja la mto Msimbazi,likabiringika mpaka chini na kutumbukia ndani ya mto huo wenye maji,difenda zote zikapiga msele askari wakatua ardhini kama makomandoo na mitutu yao mikononi!Ramadan Nurdin,akakimbia kwa kasi mpaka kando kando ya daraja hilo,akalishuhudia gari linapelekwa taratibu,macho yake yakawa juu akiwa mwenye usongo bastola yake mkononi,anamsubiri Ngesa aibuke amshindilie risasi nyingi mpaka afe!




Ramadhan Nurdin,alisimama juu ya ukingo wa daraji kwenye chuma pembeni akitembea huku na kule bastola yake mkononi macho yake yapo chini kwenye maji yanayotembea,usongo aliokuwa nao juu ya Ngesa haukuelezeka!

“Pita kule,ruka chini.Kakae pale kamanda”

Ramadhan Nurdin,alitoa amri hiyo!Akapanda juu ya kingo na kuweka bastola yake kiunoni ili ateremke chini akakae kando kabisa ya maji ya mto huo,alielewa kabisa ni lazima Ngesa angeibuka na hapo ndio ungekua mwisho wake duniani,hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee ya kummaliza,gari lililozama likaanza kuibuka juu taratibu hapo akajitupa na kutua kwenye majani akateleza kidogo na kukaa sawa,akachomoa bastola na kulitizama gari lililoanza kutokeza kwa juu,akajua ni lazima Ngesa ataibuka muda mfupi ujao!Askari wote walitanda kila kona wakiwa na mitutu yao mikononi tayari kwa kupambana na mtu aliyekuwa hatari,baadhi yao wakatega kwenye magari na wengine walikuwa barabarani wanazuia magari yasipite eneo hilo kwani muda mfupi ujao risasi zingerushwa,kwa tahadhari wakawaambia raia wasogee mbali na eneo hilo,dakika moja baadaye kukawa kweupe kilichokuwa kinasikika ni sauti za redio upepo!

“Atakuwa wapi huyu?”

Ramadhan Nurdin akajiuliza,kidole chake kikiwa kwenye kilimi cha bastola macho yake kwenye gari,bado Ngesa hakutoka!

Ilikuwa ni lazima askari wawe juu ya daraja hilo,ndiyo maana alibana pumzi zake na kumshika Daphine wakiyakata maji chini kwa chini,walivyofika chini ya daraja wakaibua shingo zao na kuwaona jinsi askari walivyozagaa eneo hilo kama siafu,ilikuwa ni hatari kubwa kama wangeonwa ndiyo maana baada ya kuhakikisha wamevuta hewa ya kutosha wakazama chini na kuendelea kuyakata maji wakipiga mbizi,wakasonga mbele zaidi na walivyohakikisha wamewaacha askari mita kadhaa wakaibuka na kuhakikisha tena,wakatembea kwa tahadhari mpaka kando ya maji ambapo walitoka kabisa wakiwa chapachapa wamelowana,hakika ilikuwa ni bahati kubwa sana kuponea chupuchupu na kifo kibaya,uzuri hakukuwa na watu eneo hilo, walielewa fika ni kutokana na risasi zilizorindima muda mfupi uliopita,walichoshukuru Mungu ni kuona baadhi ya magari yaliyotelekezwa na madereva,wakachagua gari moja wapo Ngesa akaingia nyuma ya usukani na safari ikaanza hapohapo!Katika wakati waliokuwa makini ni huo,macho yao yote yalikuwa nyuma kuhakikisha kama hakuna kiumbe yoyote anawafuatilia,walivyohakikisha kila kitu kipo sawa,wakazidi kusonga mbele!

“Tunaelekea wapi?”

“Kwa babu yangu”

“Una uhakika kuna usalama?”

“Ndio upo”

Ngesa hakujibu tena swali lingine zaidi ya kuwa makini kuangalia mbele na vioo vya ubavuni,alivyofika Ilala Boma akakunja kushoto akatafuta kichochoro kimoja na kuingia,ambapo kulikuwa na miti mingi ya miembe,akasimama kandokando ya ukuta mrefu akashuka ili kuangalia utulivu wa eneo hilo!Kilichomfanya ashikwe na hofu hakuwa na silaha mkononi,lakini hata hivyo hilo halikumfanya ashindwe kusonga mbele!

“Shuka,tumefika”

Akaingia ndani ya gari na kumwambia Daphine,baada ya hapo akaanza kupekua akifungua fungua dro kama angekuta kitu chochote ambacho kingemsaidia,bahati nzuri chini ya kiti akakuta sime yenye makali kotekote,akaisunda kwenye ‘jeans’ kiunoni na kufunika shati, nyuma akafuata Daphine akiwa makini kabisa kutizama huku na kule kwa ajili ya usalama!Wakatizama kichochoro cha kwanza ambapo pembeni kulikua na miti ya michongoma,walivyovuka mtaa wa kwanza wakaingia wa pili,kushoto kulikua na nyumba ya baba yake Ngesa,ukimya wa nyumba hiyo ulimfanya Ngesa ahisi hali ya hatari!Akasita kidogo kugonga mlango, alichomtaarifu na kumwambia Daphine atulie chini ya mti,alichokifanya Ngesa ni kuzunguka nyuma ya nyumba huku akinyata taratibu mpaka mlango wa nyuma ambapo hapo aliufungua taratibu kwa tahadhari,akapenyeza shingo kidogo na kupitisha mkono,akachomoa komeo na kuingia,alivyozama ndani akachomoa sime yake!Milango yake ya fahamu yote ilikuwa makini kuanzia ngozi,pua,mdomo na masikio!Akanyata taratibu na kusukuma mlango mwingine wa nyuma,kwa utaalam wa kuhisi akaingiwa na mashaka baada ya kuzama ndani,alikuwa ana kila uhakika kwamba kuna mtu nyuma yake ndiyo maana akatulia,ni kweli alikuwa kama ametabiri sekunde zilikuwa nyingi akapigwa kikumbo kikali cha kibabe kilichomfanya apepesuke,alivyojitahidi kukaa sawa akapokea teke la mbavu likampeleka chini mzimzima,kabla ya mtu huyo kumfuata akajibetua ili asimame lakini alichelewa kwani alipokea kikumbo kingine kikali kilichomyumbisha na kuparamia stuli!

“Ngesaa”

Kumbe alikuwa ni Dustan,bila kuelewa alikua anapambana na Ngesa hiyo ilitokana na kutandwa na hofu,Ngesa alikuwa chini kashika shingo yake yenye maumivu makali baada ya kudondokea stuli.

“Umeniumiza shingo yangu”

“Pole sana bwana,sikujua”

“Fungua mlango Daphine yupo nje”

Bado Dustan alikuwa na maumvivu,akatembea kwa kuchechemea mpaka mlangoni ambapo alifungua na kumkuta Daphine yupo,akamkaribisha ndani na wote kutulia seblen!Ilikuwa ni furaha kubwa kukutana kwa mara nyingine wakiwa na afya, tena wazima!

“Dustan,ilikuaje mbona upo hivyo?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Daphine,uso wa Dustan ulimfanya aulize kutokana na majeraha na baadhi ya vidonda ambavyo bado vilikuwa vibichi!Hakukua na sababu ya kukaa kimya,ilibidi Dustan aseme kila kilichotokea mpaka Ngesa akaamua kufanya ukombozi!


****

Zoezi zima liliendelea mpaka jioni,bila ya kuwa na dalili yoyote ile ya Ngesa kuonekana wala Daphine!Hiyo ikawa ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege,Ramadhan Nurdin hakutaka kukubali jambo hilo kwani alilifananisha na kiini macho,alishindwa kuelewa Ngesa kachomoka kwa mtindo gani eneo kama hilo lililowekwa vizuizi kila kona,alivyopiga jicho kushoto kwake upande wa pili wa daraja akaona kuna upenyo fulani,wasiwasi ukamuingia akaingiwa na hisia kwamba ni lazima Ngesa atakua ametumia mwanya huo kuwachenga askari,akatembea mpaka eneo hilo!Uhakika akawa nao baada ya kuona nyayo za viatu zimetitia kwenye tope,akazifuatisha mpaka zilipotokea barabarani,hapo akawa na uhakika Ngesa aliingia barabarani na si ajabu akachukua usafiri,kazi ikawa nzito kuliko anavyodhani kwani mpaka hapo hakujua Ngesa alichukua uelekeo upi!Jambo lililomuogopesha na kumtisha zaidi ni simu kutoka kwa Rais Leslie akitaka kujua ni wapi amefikia!

“Ndio tupo kwenye msako”

“Nimekuuliza amepatikana?”

“Hapana Mheshimiwa Rais”

“Kwanini kazi inakuwa ngumu kwako?”

“Haijawa ngumu”

“Ila?”

“Atapatikana sasa hivi”

“Uliniambia leo kabla jua halijazama Nurdin,kuna shida gani?”

“Hakuna shida mheshimiwa”

“Nahitaji huyo mwanaharamau apatikane le oleo,umenielewa?”

“Ndio Mheshimiwa Rais”

Simu ilivyokatwa ilimuacha Ramadhan Nurdin,akiwa katika wakati mgumu mno,hakuelewa aanzie wapi aishie wapi!Jasho jembamba lilimtoka,akashika kiuno huku akitizama magari na watu wanavyopita huku na kule,ghafla kuna kitu akakikumbuka akatoa simu yake na kubonyeza namba fulani!

“Uko wapi?....Kuna kazi nataka kukupa,ndio leo hii hii…Njoo ofisini kwangu”

Alivyomaliza kutoa maelekezo,akakata simu na kuiweka mfukoni akiwa bado haamini kama Ngesa,amechomoka kwenye mtego huo!


*****

Picha mbaya bado ilimsumbua ya kupigwa risasi nyingi mwilini!Hakika alimchukia sana Daphine na kwa wakati huo hata angeokota bastola,angemmaliza!Macho yake yalikua makali kwa Daphine,kwa kasi ya ajabu bila kuuliza chochote akaokota kisu na kutaka kumvaa Daphine,bahati mbaya akamkosa kosa kwani Daphine kwa utaalam wa hali ya juu,akamkwepa na kuudaka mkono ulioshika kisu,akauzungusha kwa mtindo wa judo akaubana mkono wa Jaqlin Mfinanga, vizuri!

“Unataka kufanya nini?”

Daphine akauliza hapo ndipo Ngesa akatokea,picha nzima akawa ameiona!Akamtoa Jaqlin Pembeni ambaye alikuwa anatukana akilalamika kwanini Daphine bado yupo hai mpaka wakati huo!

“Nisikilize mpenzi,sahau yote yaliyopita”

“Siwezi Derrick,mimi nitamuua”

“Punguza hasira tafadhali,yote yalishapita jaribu kusahau kabisa”

“Nitasahau vipi kirahisi namna hiyo?”

Kelele hizo,zikaenea chumba kizima!Alichokifanya Ngesa kwa busara akamtoa Jaqlin Mfinanga mpaka seblen ambapo huko,walikutana na Dustan pamoja na mkewe!Ulikuwa ni usiku wa saa nne,wakiwa katikati ya kikao kidogo lakini kizito!Kila kitu walichokifanya walikua makini nacho,ndiyo maana Dustan akawa mstari wa mbele akichora ramani jinsi ya kupata silaha ili kazi ianze usiku huo!

“Hapa wa kumuweka chini na kumkamata kwa wakati huu ni Karanje sio Rais Leslie”

“Karanje yuko wapi?”

“Sijui yuko wapi!IGP ndio anaweza kujua hilo…”

“IGP Mahugo?”

“Ndio,anaelewa kila kitu”

“Kwake ni wapi?”

“Mbezi”

“Tunaweza kwenda?”

“Tutaenda vipi bila silaha,analindwa mno”

“Silaha tutatoa wapi?”

“Kuna Karakana moja ipo Tazara pale,ndipo wanahifadhi silaha pale Depo!Ulinzi wake,sio mkali sana tutawamudu askari”

“Tunaweza kwenda usiku huu?”

Ngesa akauliza swali,hiyo ilimfanya Dustan ajipime kwanza kwa kujiangalia kama afya yake ingeruhusu!

“Tutaenda”

“Jiandae”

Kikao,kikawa kimeisha!Ajenda ilikuwa waingie kwenye Karakana waibe silaha kisha waende kumkomboa Brigedia Karanje,kufuatia hapo wangejua ni kitu gani wafanye!Hakukua na muda wa kupoteza zaidi.Ngesa alivyoingia chumbani akamfuata Daphine ambaye alikua anamalizia kuvaa fulana,ambayo ilimkaa vizuri na jeans ya kijani,umbo lake likajichora vizuri!Nywele zake,amezibana kwa nyuma!

“Daphine,inabidi ubaki”

“Kwanini?”

“Hakuna ulinzi hapa”

“Mkeo anabaki?”

“Ndio”

“Unadhani nitaweza kubaki naye?Atanielewa?”

“Nishaongea naye”

“Sina silaha”

“Kuna bastola moja ya Dustan,nitakupa!Kua makini sana,mzee amelala”

“Ondoa shaka Ngesa,alafu mnaenda wapi kwani?”

“Karakana,kuchukua silaha alafu baada ya hapo tunaweza kurudi”

Daphine,akawa yupo tayari kwa kila kitu,akamsogelea Ngesa akamkumbatia kwa nguvu zake zote huku akiyafumba macho yake kwa ishara ya kuagana,lakini kitendo hiko kilimfanya Jaqlin Mfinanga aingiwe na wivu baada ya kufungua mlango na kuwakuta wamekumbatiana,moyo ulimuuma ajabu taa nyekundu ikaanza kuwaka kichwani kwake kwamba Ngesa na Daphine,wanamegana kisela!

“Jaqlin mpenzi,utabaki na Daphine!Sisi tunaondoka!Mtabaki hapa,naomba muweke tofauti zenu kando”

Ngesa akamaliza kuongea,akamsogelea Jaqlin na kumpiga busu la mdomoni kwa ishara ya kumuaga,alivyofika Seblen akamkuta Dustan yupo tayari wote wakatoka nje na kuingia ndani ya gari na safari ya kwenda Karakana kuanza mara moja!


******

“Ssshssssssss”

Ilikuwa ni kama mtu aliyekurupuka kutoka lindoni,usiku huo mnene!Alikuwa ni Daphine baada ya kuhisi nje kuna vishindo vya watu,akamnyamazisha mke wa Dustan na Jaqlin Mfinanga,pamoja na babu!Bastola ipo mkononi,akatembea mpaka dirishani na kuchungulia,alichokiona kilimfanya moyo wake ukose utulivu!Hakuona watu vizuri lakini aliviona vivuli vya watu watatu,vikitembea kuufuata mlango!Akanyata taratibu mpaka mezani ambapo kulikua na kisu kidogo!Akatulia nyuma ya mlango,kisha akakishika vizuri mkono wa kushoto bastola mkono wa kulia!Watu waliokua nje,mmoja wapo akachungulia dirishani mbaya zaidi alikuwa na tochi,akaanza kumulika huku na kule,hazikupita sekunde moja wakasikia mlango unachezewa,hapohapo ukafunguka mguu ukaingia ndani bastola ikatangulia mbele,Daphine akasubiri nyuma ya mlango!Akili yake ikaanza kufanya kazi kwa kasi,alivyoona mtu wa pili kaingia,akasubiri mpaka wa mwisho ili aanze ambush!

“Kimya,mkijitingisha nammwaga mtu ubongo”

Jamaa aliyekuwa mbele,akawapiga mkwara wakina Jaqlin Mfinanga waliokua na hofu seblen!Wa pili nayeye akafuata nyuma,sekunde tatu zikapita bila ya mtu wa tatu kutokeza!Hiyo ilimfanya Daphine ajue ni lazima,wa tatu kabaki nje analinda usalama.Bila kupoteza muda akakishika kisu vizuri kikomandoo,akakirusha kwa kasi kikakita shingoni mwa Jamaa wa kwanza,chote kikazama ndani ya shingo mpini ukabaki nje,wa pili alivyogeuka akarudishwa na teke la hewani la mtindo wa kong fuu,kabla hajatua chini,Daphine akauwahi mkono wake!Ki utaalam zaidi,akaukunja vizuri na kuuvunja kama mua,jamaa akapiga yowe kali lakini alinyamazishwa na kifuti cha mdomo,akadondoka chali mzima mzima,hiyo haikufanya Daphine amuachie akamsogelea na kumpiga teke kali la korodani,jamaa akabweka kama mbwa na kutulia!

“Mpo wangapi?”

Daphine aliuliza kitemi bastola mkononi,tayari kwa kuua!

“Sijui”

Kwa hasira Daphine akainua mguu na kumkanyaga shingoni kwa nguvu!

“Nitakuuuua”

“Ma….layaaa weee na kifo chak…ooo kipo mlangonii utakufa kifo kiba…yaa sana”

Aliyekua anapiga mkwara huo,alikuwa mahututi chini yupo hoi mguu upo shingoni!Daphine yupo juu yake kashika bastola anamtizama kwa hasira,katika hali ya kushangaza,akashtukia amepigwa teke kali mgongoni,akapepesuka kabla ya kutulia,akapigwa teke lingine kiuoni,hapo hapo akashikwa shingo alivyotaka kutumia bastola,mkono wake ukakamatwa na mtu aliyekuwa nyuma yake!Akajitahidi kufurukuta lakini hakua na jinsi,shingo yake ikazidi kuminywa na mtu aliyekuwa nyuma ambaye mpaka wakati huo hakuona sura yake!Kuendelea kubaki hapo,kulimaanisha kifo chake akatulia kidogo ili ajipime,akakusanya nguvu za kutosha na kukanyaga stuli iliyokuwa mbele yake wakarudi nyuma kwa kasi,aliyekuwa nyuma yake,akafikia kwenye ukuta na kujikita,Kwa wepesi aliokuwa nao Daphine akarusha kifuti kikali kilichomfikia mtu huyo,puani!Hapo ndipo akatoa mikono yake,Daphine akajigeuza na kuhepa kulia baada ya kuona ngumi inakuja mbele yake,akaona teke akalizuia lakini lilimshinda nguvu kwani lilimyumbisha kidogo kabla ya kukaa sawa,akapigwa ngumi mbili za mbavu zilizomfanya ahisi maumivu makali sana,sasa akaelewa anayepambana naye hakuwa mtu wa kawaida!Akawa makini mno kusoma mchezo wa adui yake,ilielekea mtu huyo alikuwa mzuri katika michezo ya boxa ndiyo maana alikuwa anadunda kama kitenesi akirusha ngumi huku akihama upande,kwa kuwa Daphine alilijua hilo,akawa anamchora anavyonesa,akasogea huku anahama kule,akirusha ngumi anainama na kuibukia upande wa kule ukawa kama mchezo kumbe anamlia ‘timing’!Ndani wakawa kama watoto,mara huku mara kule!Ngumi ya sita,aliiona vizuri akainama kidogo na kuushika mkono akazungusha na kumpiga pigo la Karate kwenye chemba,hiyo ilimfanya jamaa huyo atoe macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango!Hakukaa sawa,Daphine akakanyaga ukuta na kujibetua teke moja la fly kick lililomdondosha jamaa huyo chini,alivyojitahidi kusimama Daphine tayari akawa amefika,akamtandika ngumi mbili za pua na kumzaba kibao kikali cha uso kilichomfanya jamaa huyo,aone nyota!Hakika Jaqlin Mfinanga na mwenzake,hawakuamini wanachokiona jinsi Daphine alivyopambana,ilikuwa kama sinema ya kuigiza!

“Nani kawatuma?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Daphine lakini jamaa huyo akacheka kwa sauti kana kwamba kaona kibonzo,alichokifanya Daphine ni kuchomoa kisu kutoka shingoni mwa maiti akamfuata jamaa aliyemuacha mara ya kwanza chini anahema,akamchoma kisu cha kifua,akakichomoa na kumchoma shingoni,kisha akamrudia.

“Nadhani,umeona nilichomfanya mwenzako”

Daphine akasema,hiyo ilimfanya jamaa huyo atetemeke,sasa akawa tayari kusema kila kitu baada ya kuona unyama wa Daphine.




Gari aina ya pickup double kebeni walioiba ilipaki ng’ambo ya upande wa pili,kulia kwao kulikua na Karakana kubwa ya kuhifadhi silaha za kivita,humo ndimo Dustan na Ngesa walitakiwa kuingia na kuiba silaha hizo za moto!Halikuwa jambo rahisi sababu hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa na silaha mkononi ya kujihami!Hata hivyo walijiamini!

“Ndio pale?”

Ngesa akauliza huku akilitizama geti kubwa,ambalo lilikuwa na ukuta mrefu kwenda juu!

“Yes,upande wa kushoto kule ndio kuna hiyo Karakana!Ya vifaru na kila aina ya silaha”

“Ulinzi wake upoje?”

“Panalindwa sana,sio rahisi lakini mara nyingi walinzi wanakuwa mlangoni pale”

“Wangapi?”

“Watatu,kule kwenye Karakana yenyewe!Sina uhakika”

“Okay,tutapata uhakika tukiingia ndani!Pitia getini,mimi nitaruka ukuta ule”

“Nipite getini?Kivipi?”

Dustan akauliza,jambo hilo lilimshtua mno!

“Gonga getini,ongea nao chochote kuanzia hapo niachie mimi”

Yalikuwa ni maelekezo kutoka kwa Ngesa,akiwa siriazi na kitu anachokifanya baada ya hapo akatizama ukuta kwa namna ya kuutathmin kama angeweza kuruka kwani ulikuwa mrefu mno!Akamgeukia Dustan kwa mara nyingine!

“Upo tayari?”

“Nipo tayari”

“Sawa,tangulia”

Kwa tahadhari,Dustan akateremka kutoka ndani ya gari akatizama huku na kule na kuingiza mikono mfukoni,akavuka upande wa barababara kwenda upande wa pili,alivyogeuka pembeni akamuona Ngesa kwa mbaali,anazunguka ukuta!Akashusha pumzi ndefu na kuzidi kusonga mbele mpaka alipolikaribia geti,kitendo cha kulifikia tu walinzi wawili wenye mitutu wakamsogelea kwa kasi!

“Vipi?”

Mlinzi mmoja akamuuliza kwa sauti ya juu,kwa namna ya kumpiga mkwara!

“Poleni kazi”

“Una shida gani?”

“Kuna jambo nataka kuuliza”

“Hapa sio bungeni ni sehemu hatari,kaulize huko mbele ya safari, potea”

Wakati Dustan akiendelea kumzuga mlinzi wa getini yeye Ngesa alikuwa kazini anatafuta saiti nzuri ya kupanda ukuta,hakika ulikuwa ukuta mrefu kumzidi kimo chake!Akazidi kuuzunguka kwa nyuma zaidi,akafurahi baada ya kuona geti dogo la chuma akajua kabisa hilo lingempa sapoti ya kupanda ukuta,akakamata chuma vizuri na kukanyaga kwenye kingo zake,mikono yake ikagusa ukuta!Taratibu akainua shingo na kutizama ndani,akaliona geti lingine ambalo Dustan yupo na walinzi wawili wanamuhoji,mmoja yupo kando anavuta sigara!Akajivuta taratibu kwa juu,alivyohakikisha stamina zipo vizuri,akatua ndani bila kutoa kishindo kama paka!Huo ulikuwa utaalam aliofundishwa katika mafunzo ya kijasusi,alivyotulia akasikilizia ili kupima utulivu!Alivyohakikisha kila kitu kipo sawa na eneo hilo lipo shwari kabisa,akamtizama mlinzi aliyekuwa anavuta sigara hana habari mtutu wake upo begani,akaambaa ambaa na ukuta wa pembeni ambapo kulikuwa na giza totoro!Alivyomsogelea karibu,akampiga kabali kali la shingo na kumziba mdomo huku akimvutia kwenye giza,mlinzi akajitahidi kukukuruka lakini alitulizwa na jebu la shingo,akatulia chini!Alichokifanya Ngesa ni kuuvuta mtutu,akamtwanga nao kwa kutumia kitako kichwani na kumsogeza pembeni kabisa,akashika mtutu vizuri akasogea taratibu mpaka karibu kabisa na walinzi nyuma yao!

“Tupeni silaha zenu chini,fanyeni haraka”

Ilikuwa ni kauli iliyowafanya walinzi hao waogope na kutandwa na hofu,hata hivyo hawakutaka kuuliza mara mbilimbili baada ya kumuona Ngesa mzee wa kazi,walielewa mziki wake na wasingetii amri asingekuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kuwachapa risasi!Kwa tahadhari wakaweka mitutu chini na kupiga magoti mikono yao ikawa hewani kama wanafunzi wa shule ya msingi waliopewa adhabu!

“Ndani kuna walinzi wangapi?”

Ngesa akahoji,mtutu upo mkononi hacheki sura yake imechora makunyazi!Alivyoona hajibiwi kwa wakati,akamsogezea mtutu mmoja wa walinzi, mpaka kichwani kabisa ukagusa paji la uso!

“Hua sipendi kupotezewa muda!Ala..”

“Wapo wanne”

Kilichofuata hapo,ilikuwa ni kazi ndogo tu!Kuwafunga kamba walinzi na kuwaweka ndani ya kibanda chao,wakafunga mlango kwa nje!Sasa wote wakawa na silaha mikononi mwao ingawa hawakupenda kuzitumia wakihofia zingetoa kelele na kusababisha purukushani ambazo zingewapotezea muda wa kuendelea na harakati zao!Kimya kimya wakatembea mpaka kwenye moja ya jengo kubwa ambalo pembeni kulikuwa na mti mrefu na mpana,kila mtu akajigawa upande wake!Ngesa akaenda kushoto ambapo huko alikutana na mlinzi amelala juu ya kiti,anakoroma!Akamsogelea karibu na kumzaba kibao cha nguvu shavuni,alivyokurupuka akamtuliza na cross jebu ya mbavu, mlinzi akarudi kwenye kiti bila kupenda,alivyotulia mbele yake akaona mlango wa mtutu!

“Tulia hivyo hivyo,tupa silaha yako chini!Simama ongoza mbele”

Mambo yalikuwa kimyakimya,hakuna mtu yoyote aliyetumia nguvu!Walivyoufikia mlango akakutana na Dustan,ambaye tayari aliwathibiti walinzi wengine ipasavyo!

“Fungua mlango,naomba nikuonye”

Kabla ya kuendelea na zoezi la kufungua mlango Ngesa akamgeuza mlinzi,wakawa wanatizamana uso kwa uso!

“Hii sura sio ngeni kwako nina uhakika huo!Ukienda kinyume,sitoshindwa kuuumwaga ubongo wako chini!Umenielewa?”

“Ndi…ndio mkuu”

“Fungua mlango”

Bila ubishi na utata wowote ule Mlinzi akachukua funguo na kufungua,macho yao yote wakatupa ndani!Ilikuwa ni eneo lenye uwazi mkubwa uliojaa silaha za kutosha,kuanzia mabomu magari ya kivita mpaka makombora,kila aina ya silaha ilikuwepo!Ngesa akamtizama Dustan na kutabasamu,kwake ilikuwa furaha kubwa sana kupata vitendea kazi!Wote wakaingia ndani na kuchukua begi kubwa na kuanza kupakia silaha,kazi yao ilikuwa ni kuchagua mithili ya mtu anayechagua bidhaa sokoni,wakapakia ndani ya begi na kuliweka vizuri!Lilikuwa begi zito mno.Alichokifanya Ngesa ni kuchukua pia bastola na magazine tano zilizojaa risasi akaziweka kiunoni na nyingine akazisunda kwenye buti,bastola nyingine akaiweka nyuma ya kiuno chake!

“Geti lingine liko wapi?”

Ngesa akahoji,hakutaka kutumia geti waliloingilia hiyo ndiyo ilikuwa prinsipo ya kijasusi siku zote ili kumchanganya adui aliyekuwa anakufatilia!

“Lipo kule mwisho”

“Ongoza mbele,tunaondoka na nyie”

“Wapi tunaenda?”

“Ongoza mbele”

Hakukuwa na ubishi mwingine, zaidi ya walinzi hao kuongoza mbele wakiwa na hofu,wakafungua geti la nyuma na kutoka nje ambapo huko waliingia ndani ya gari moja wapo wanalotumia kupiga doria!

“Tunaenda Kinyerezi,nipeni simu zenu haraka”

Wakapokonywa kila kitu,walivyofika karibu na Magengeni,wakaambiwa wajitupe nje huku gari likiwa katika mwendo wa kasi,hakuna aliyediriki kupinga kwani uhai ulikuwa ni muhimu kwao kuliko kuendelea kubaki ndani ya gari,wote wakaruka nje Ngesa akazungusha usukani na kuzima taa za gari,akaingia kwenye moja ya kichochoro ili kuwapotezea umakini walinzi, wasiweze kujua ni wapi wameleekea!Lilikuwa ni tukio la hatari lililofanyika ndani ya muda mfupi tu.


*****

Jinsi mtuhumiwa Brigedia Karanje alivyolindwa ilitisha,ilikuwa ni rahisi sana kuingia Ikulu na kuvamia lakini sio kuingia katika chumba alichokuwa Brigedia Karanje,zaidi na hilo alipewa chakula kizuri akala na kushiba kifupi hakutofautishwa na mfungwa huru!Alichokuwa anahitaji Rais Leslie ni kaseti iliyokuwa na sauti yake ndiyo maana alimtunza namna hiyo lakini pia alimuwekea walinzi wenye silaha za kutisha,wakihofia wafuasi wa gaidi huyo kuvamia hata hivyo kuwekwa ndani ya chumba hiko ilikuwa ni siri kubwa mno ambayo mtu yoyote asingeweza kujua kirahisi!Katika kitu ambacho Raisi Leslie,alitaka kujua ni wapi kaseti ilipo!

“Nakuhakikishia ukinipa hiyo kaseti,unakuwa free nakuhamisha hii nchi!Kwa kutumia madaraka yangu”

Siku hiyo Rais Leslie alikuwa ndani ya hiko chumba,anamsihisi Brigedia Karanje aseme ukweli!

“Leslie,sitorudia tena!Siwezi kukupa chochote mpaka niwe huru kwanza, hilo moja jambo la pili,Mzee Ngesa aachiwe huru pamoja na mwanangu”

“Ni jambo gumu hilo,haliwezekani”

“Kama kitu rahisi kama hicho unashindwa kufanya,huwezi kunihamisha nchi.Hukumu yako ni kunyongwa tu nadhani unajua kilichokuwa ndani ya ile kaseti”

“Naelewa”

“Kwahiyo kafikirie mara mbili”

“Na mabomu yako wapi?”

“Tena una masaa machache,moja lilipuke”

Namna Brigedia Karanje alivyozungumza kwa kujiamini iliogopesha hiyo ikamfanya mpaka Rais Leslie,aishiwe pozi akashusha pumzi ndefu za kuchoka,hakuwa nala kufanya zaidi ya kutoka nje na kumtafuta Ramadhan Nurdin kwenye simu akitaka kujua mchakato wa kumpata Ngesa umefikia wapi!

“Bado Mheshimiwa Rais”

“Kazi itakushinda Rama”

“Sio hivyo,tupo mbioni kumkamata!Usiwe na wasiwasi kabisa”

“Mkamateni,haraka sana”

“Mheshimiwa Rais,nitafanya hivyo naomba nikuhakikishie”

Wakati simu inakatwa ilimuacha Ramadhan Nurdin,amepigwa na ganzi yupo ndani ya karakana baada ya kusikia watu wawili wamevamia na kuchukua silaha za moto na mmoja wao alikuwa ni Ngesa,kwa kweli alichoka na kila kilichotokea hakuamini bado!

“Ilikuwa vipi mmeniambia?”

Ramadhan Nurdin,akauliza kwa mara nyingine tena!Mikono kaiweka kiunoni,bado haamini anachokiona,alishindwa kumuelewa Ngesa ni binadamu mwenye mafunzo ya aina gani!Walinzi wakajielezea na kusema jinsi walivyovamiwa na wenzao kutupwa barabarani hakika ilikua ni simulizi ya kimafia sana!

“Shiiit!”

Ramadhan akakema kwa hasira za waziwazi na kubana meno yake kwa jazba hakika Ngesa,alizidi kumtia hasira sana!


******

Mipango ya Ngesa ilikuwa kwanza kumteka Nyara IGP ili ajue ni wapi Brigedia Karanje alipo kisha mambo mengine yaendelee,ilikuwa ni lazima ayategue mabomu yote kwanza ili kuikomboa nchi yake ambapo baada ya muda mfupi mamia na maelfu wangekufa kwenye mlipuko,hakutaka tena kushirikiana na Serikali akiamni kwa kufanya hivyo angekamatwa kwani alikuwa akitafutwa kwa wudi na uvumba kila pembe ya nchi kama shilingi!Daphine alikuwa pembeni anasikiliza kwa makini kikao hiko kilichokuwa kinafanywa na Ngesa,pembeni yupo Dustan, pia yupo makini!

“IGP inabidi tujue alipo,tumteke yeye ama familia yake!Tunataka tujue ni wapi,Karanje alipo!Na kuna mtu anaitwa Ramadhan Nurdin,Daphine umeniambia hawa watu wametumwa!Hapa tuhame ni hatari kwa sasa hivi”

Katika mazungumzo yake,alitoa maelekezo huku akiwa amesimama anamtizama kila mtu,Ngesa hakutofautishwa na mwalimu wa hisabati!

“Karanje atatutajia ni wapi mabomu yalipo,kwa njia moja ama nyingine!Lakini hatuwezi kumpata huyo mtu bila ya IGP,kuna mwenye swali?”

Katikati ya kikao hiko Daphine kuna kitu alihisi ambacho hakikuwa cha kawaida,nje aliona vivuli vya watu alivyoangalia dirishani akaona mtutu wa bunduki umepenyezwa unamuangalia Ngesa aliyekuwa kasimama wima,kupiga kelele kungemchelewesha na Ngesa angemiminiwa risasi na kufa!Alichokifanya kwa kasi,akasimama na kumpiga kikumbo kikali Ngesa akitumia bega lake,kabla ya kutua chini zilisikika risasi kutoka kwenye mtutu!

“Griiii griiii griiiiiii”

Mirindimo ya risasi pamoja na mitutu ilisikika kutoka nje,risasi zikawa zinapiga ukuta wote wakalala chini zikawa zinapita juu!Ndani kukawa na vumbi kali,walengaji hawakuacha walizidi kumimina risasi nyingi mno na ilielekea walikuwa wengi,hiyo iliwafanya watu wote watandwe na hofu mpaka Ngesa mwenyewe akashindwa kuinuka kwani risasi zilikuwa zinarushwa kama mvua!




Risasi zilirindima,kila pembe ya kona na wapigaji waliokuwa nje walizidi kuzirusha kwa fujo hiyo ilimfanya Ngesa aliyekuwa kifudifudi atambae kama nyoka akitumia tumbo kwani angeinuka kidogo mwili wake ungemiminiwa risasi na kuwa kama neti ama chujio la chai,kila alipojaribu kutafuta saiti nzuri ya kukaa alishindwa hiyo yote ilitokana na vumbi kutawala ndani,viti na stuli vilirushwa rushwa kuta zote zilitoboka toboka, Jaqlin Mfinanga alilia machozi,milio mikubwa ya risasi ilimtisha!Daphine aliendelea kulala kifudi fudi mikono yake kaifumbata kichwani,risasi zinapita juu ya mgongo wake kuinua shingo yake ingemaanisha ndio ungekuwa mwisho wake duniani,ndani hakukuwa na mtu yoyote mwenye tumaini la kutoka salama japokuwa hawakukata tamaa hata hivyo ilikuwa afadhali kwa Dustan, sababu pembeni yake kulikuwa na begi lenye silaha walizoiba kwenye Karakana,alichokifanya ni kujitoa kimasomaso,akavuta begi kwa mguu na kuingiza mkono ndani akaanza kupapasa,akatoa kitu kama kiazi chenye kipini,hilo lilikuwa ni bomu aina ya ‘grenade’ akachomoa kichuma kidogo cha juu na kulirusha nje,kilichosikika muda mfupi ujao ulikuwa ni mlipuko mkubwa,watu wa nje wakapiga yowe kumaanisha shabaha yake ilifanya kazi!Huo ndio ulikuwa upenyo pekee wa Dustan kuchomoa bastola ndogo, akiwa hivyo hivyo amelala,kwa umakini wa hali ya juu akaangalia risasi zinapotokea!Akabana jicho lake moja ili atafute shabaha nzuri.

“Paaa paaaa”

Risasi mbili tu,zilimtosha mdunguaji aliyekuwa dirishani zikamuondoa, akamlenga mwingine aliyekuwa karibu na mlango,kasi ya watu wa nje ikapungua,hiyo ilimfanya Dustan ajiburuze kama nyoka na kumtupia Ngesa begi la silaha,hapo ndipo mwanaume huyo akawa kama mwehu baada ya kulishika begi na kuchomoa bastola moja wapo,akaanza kurusha risasi moja baada ya nyingine kwa kuwa alishaelewa ni wapi walengaji walipo,alivyoona haitoshi akachukua bomu lililofanana na kiazi,akayarusha mawili nje!

“Pokeeni hayo”

Akasema na kutulia,ulivyotokea mlipuko akasimama wima akiwa na mtutu mrefu mkononi!

“Grii griiii”

Mashambulizi yalianza mara moja,kuendelea kulala chini ilimaanisha kufa kikondoo hakua tayari kwani kwake ilikuwa ndio kwanza picha limeanza,alivyoona kuna utulivu akatulia nyuma ya mlango kwani alihisi kuna mtu anataka kuingia,mlango ukapigwa teke kibabe kwa nguvu,ukavunjika mwanamme mrefu akaingia hakuweza kumuona vizuri lakini alivyotuliza akili yake,akamtambua alikuwa ni Mkurugenzi kutoka idara ya usalama wa taifa Ramadhan Nurdin Mpelembe,akashtuka sana kwani hakuelewa alijuaje maficho hayo,kilichomtisha ni baada ya kumuona kashika bastola mkononi kamuelekezea mpenzi wake Jaqlin Mfinanga,akaweka mtutu vizuri begani ili amfyatue!

“Karakacha karacha!Shiit”

Mtutu haukuwa na risasi hiyo ilimfanya Ngesa akeme kwa mshtuko,akaugeuzia kwenye kitako ili amtwange nao Ramadhan Nurdin kichwani lakini haikuwa rahisi kwani Ramadhan alichezwa na Machale,akageuka na kuhepa kushoto mtutu ukapita vuup hewani,akaudaka mkono wa Ngesa na kumvuta kulia alivyotaka kumpiga kifuti Ngesa akazuia na mkono,akaushika mkono wa Ramadhan ulioshika bastola na kuubamiza kwenye kingo ya ukuta,bastola ikadondoka kando akamtandika ngumi kavu ya shingo,maumivu aliyohisi Ramadhani yalimfanya apige kelele lakini hilo halikumfanya akubali,akachezesha miguu yake mara mbili mara ya tatu akaruka hewani kama ngedere,Ngesa akayaona moja akalizuia lakini moja lilimfikia usoni akapepesuka na kujigonga ukutani!Ramadhan Nurdin Mpelembe,alikuwa mwepesi na alichanganya mapigo mara judo mara kick boxa,hiyo ilimfanya Ngesa ashindwe kumsoma vizuri ki ukweli alikiri, hakuwahi kukutana na mpiganaji hodari kama Ramadhan,licha ya hayo hakukubali kushindwa akamuacha kwanza aruke ruke kama kitenesi,alichokosea Ramadhan ni kurusha teke la hewani,Ngesa akainama kidogo na kumchapa ngumi kali ya korodani,iliyomfanya Ramadhan abweke kama mbwa koko aliyepigwa na jiwe la kichwa,alivyotaka kumsogelea ili amshindilie teke,akahisi kichuma kimemgusa shingoni!

“Tulia Ngesa kama unanyolewa,ukifanya upuuzi wowote nakuua”

Katika vitu ambavyo Ngesa alikuwa makini navyo ni sauti ambazo zipo mbali na mzahaa,sauti ya nyuma yake ilikuwa kavu haina masihala hata kidogo kwenda kinyume kulimaanisha kuuliwa mara moja, ndiyo maana akatulia na kuwa mpole ghafla!Hata hivyo alipata nafuu baada ya mtu wa nyuma yake aliyemuwekea bastola kichwani nayeye kuwekewa bastola utosini na Daphine!

“Tupa bastola chini, Comrade”

Baada ya Daphine kusema hivyo,Dustan nayeye akasimama na bastola mkononi,zoezi likawa limebadilika Jeshi la Ramadhani Nurdin likawa limewekwa mateka, tayari!

“Tupa bastola chini,kacha kacha”

Daphine akakoki bastola alivyoona jamaa huyo anakahidi amri,kwa hofu ya kifo akaitupa chini na kuiweka mikono yake kichwani!

“Sasa hapa tunaweza kufanya mazungumzo vizuri,piga magoti fanya haraka”

Hasira za Daphine,zilikuwa nje nje!Hakuwa na utani hata kidogo,akampa bastola nyingine Ngesa sasa wote wakawa na silaha mikonni!

“Nurdin,kwanini unanifuatilia fuatilia namna hii? Mimi sipendi kufuatwa fuatwa hasa nikiwa kwenye misheni zangu?”

Ngesa akauliza,sauti yake ilikuwa mbali na utani!Bastola ipo mkononi,kamuwekea kichwani mbaya zaidi iligusa kabisa paji la uso wake!

“Nipo kazini…Puuuuu!”

Kitako cha bastola kilimfikia Ramadhani mdomoni,kikamchana akaanza kuvuja damu!

“Chunga majibu yako”

“Ngesa”

Daphine akaita,akamuangalia kwa makini Ramadhan, alionekana kuna kitu anataka kuchangia!

“Yes”

“Huyu atatufaa kufika kwa IGP Mahugo,tusipoteze muda!Twende naye”

“Kweli?”

“Ndio,anaishi Ukonga mkewe anafanya kazi Kipawa Airport nitawashikilia mkewe na watoto wake mateka!Asipoonesha ushirikiano,nawaua”

Wazo hilo lilimuingia vizuri sana Ngesa lakini lilimfanya Ramadhan Nurdin,atoe macho kwa hofu familia yake ilikuwa ndio kila kitu katika maisha yake,ndiyo maana alianza kutetemeka!

“Mnataka kuifanya nini familia yangu?Dilini namimi sio familia yangu”

“Uhai wa familia yako,utakuwa mikononi mwako nachotaka kujua ni wapi Brigedia Karanje alipo!Najua sana kwamba IGP Mahugo,anajua siri hiyo!Wewe ndio utatusaidia kujua”

“Nitatumia njia gani?”

“Wewe ni mtu mzima,hatuwezi kukufundisha kazi!Daphine….”

Ngesa akaita, Daphine akageuka!

“Abee”

“Anza kazi”

Jambo lililofanya Daphine achukue bastola kadhaa pamoja na visu,Dustan nayeye akaunga tela!Wote wakatoka nje kwa niya ya kwenda kuiteka nyara familia ya Ramadhan Nurdin ili iwe rahisi kwao kuingia ndani ya jumba la IGP bila kutumia nguvu yoyote ile,jambo hilo waliamini lingefanikiwa kwa asilimia zote mia moja!Ramadhan Nurdin Mpelembe pamoja na wenzake wawili,waliwekwa mateka wakafungwa kamba na kuzibwa midomo na gundi nzito,hilo likafanyika ili wasubiri simu kutoka kwa Daphine!

Baada ya lisaa limoja,simu ikapigwa kwamba wamefanikiwa kuwaweka mateka Mke wa Ramadhan Nurdin na Watoto wake watatu!

“Ongea na mkeo”

Ngesa akasema na kuweka simu loudspika!

“Asia mke wangu”

“Abee,kuna nini..Naogopa naogopa!Kuna nini Mme wangu?Kama wanataka pesa wape”Upande wa pili wa simu ulienea!Mke wa Ramadhan Nurdin, alikuwa kwenye laini!

“Sio hiv….tititi”

Ngesa akakata simu,hakutaka kusikiliza vilio vya mapenzi kwani alikuwa yupo kazini!

“Nadhani umewasikia,wapo hai kwa sasa hivi!Ukienda kinyume maiti zao utazikuta Posta pale feli,zimekatwa katwa,nakuhakikishia,kifo chao kitakuwa cha mateso nacha taratibu mno!”

Sauti ya Ngesa ilikuwa mbali na mzaha,alikuwa ana kila sababu ya kuongea hivyo kwani moyoni alikuwa na visasi mno!Akamfungulia kamba na kumuwekea Bastola kichwani!

“Tunaongozana mpaka nyumbani kwa IGP,ukijaribu kuwataarifu polisi ama kufanya tofauti na ninachokitaka,naanza na mtoto wako wa kwanza kumuua!Nadhani unajua nani atakayefuata,twende”

Mkwara aliochimbwa Ramadhan Nurdin Mpelembe ulitisha na alihofia,hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali kuvunja sheria sababu kwake familia yake ilikuwa ndio kipaumbele cha kwanza!Wakaingia ndani ya gari akiwa na Ngesa na safari ya kwenda Masaki kuanza mara moja!

“Kwanini unafanya hivi Ngesa?”

Akiwa ndani ya gari,Ramadhan alivunja ukimya nayeye ndiye alikuwa akiendesha gari!Ngesa hakuwa na sababu ya kumfunga tena akiamini angekuwa na hofu juu ya familia yake!

“Unataka kujua kwanini?”

“Ndio”

“Nafanya hivi kwa ajili ya nchi yangu ya Tanzania,sio kwa ajili ya watu wachache”

“Ili upate nini?”

“Wananchi wawe huru,hii nchi inaongozwa kisiasa na watu wachache wenye uchu wa madaraka akiwemo Rais Leslie,kwanini hataki nimuhoji Brigedia Karanje?”

“Ni sababu za kiusalama zaidi”

“Hujui kitu Rama,bora unyamaze tu!Nachotaka kujua ni wapi Brigedia Karanje alipo”

“Kwanini tunaenda kwa IGP?”

“Ndio anajua ukweli”

“Nani amekwambia?”

“Ndio maana nakwambia hujui kitu!IGP,Ndio anajua”

Maongezi yakakoma,hatimaye wakafika Masaki!Kandokando ya nyumba ya IGP Mahugo,Ramadhan alivyotaka kushuka Ngesa akamzuia!

“Kumbuka kitu kimoja nina familia yako,usijaribu kufanya kitu chochote cha kipumbavu!Nitawaua,sitanii”

Ramadhan hakujibu kitu,akawa mpole na kushuka ndani ya gari ambapo ilikuwa rahisi sana kwake kuingia baada ya kuonesha kitambulisho kwa walinzi getini,akaingia mpaka ndani ambapo alimkuta IGP anatizama Taarifa ya habari!

“Kijana karibu”

IGP akasema,ufupi na kitambi chake vilitosha kabisa kugundua kwamba ni mambo safi na pengine anakula kodi za wananchi kiholela!

“Ahsante,nina mazungumzo nawewe kidogo!Tunaweza kupata sehemu yoyote nzuri?”

“Zungumza tu”

“Hapana sio hapa”

“Ulitaka wapi?”

“Ni mambo ya kiusalama zaidi”

“Sawa nifuate”

IGP Mbele Ramadhan Nurdin nyuma,wakaongozana mpaka kwenye chumba maalum kidogo,Ramadhan akafunga mlango kwa ndani,akavuta chuma kidogo kandokando na kumponda nacho kichwani!

“Brigedia Karanje yuko wapi?”

Ramadhan Nurdin,akauliza kwa ukali bila mzaha!Swali hilo likamshtua sana IGP akiwa chini anaugulia maumivu anavuja damu kichwani!

“Unaongelea nini?”

“Sitokuuliza tena”

Alichokifanya ni kuchukua mfuko wa nailoni,akamimina vitabu chini na kumpiga teke la tumbo kisha kumkaba na kumvalisha mfuko usoni,alifanya hivyo huku akimshindilia ngumi za shingo zilizomfanya IGP ajambe ndani ya suruali,alivyoutoa mfuko akawa anahema kama mtu mwenye presha ya kushuka!

“Yuko wapi?”

“Sijuiiii”

“Okay”

Ramadhan alivyotaka kurudia zoezi,IGP akawa tayari kuzungumza,anahema huku anamtizama Ramadhan Nurdin ambaye hakuwa rafiki tena ile sura ya tabasamu aliyoingia nayo ilibadilika kabisa!

“Yupo Mbweni,Tegeta kule!Kambi kuu ya maaskari”

“Nitampata vipi?”

“Yupo pale pale”

“Chomekea vizuri twende,ukijaribu kwenda kinyume sitokuacha salama”

IGP hakua na chaguo lingine zaidi ya kuchomekea na kuweka kila kitu sawa ili atengeneze mazingira kwamba hakuna kitu kinachoendelea,akatoka nje ambapo huko walinzi wake walitaka kumsindikiza kwa niya ya kumlinda,akawakataza akidai kwamba kila kitu kipo shwari!Wakatoka nje na kuingia ndani ya gari alilokuwa Ngesa!

“Kumbe upo na huyu mwanaharamu,nishaanza kupata picha al…”

“Kelele”

Ramadhan akamnyamazisha na kofi kali,Ngesa alikuwa pembeni hasemi chochote anawatizama!

“Tunaenda wapi?”Akauliza!

“Mbweni”

Gari likawashwa na safari kuanza mara moja,ilikuwa ni lazima Brigedia Karanje!Akombolewe kwa ajili vitu viwili,aseme mabomu yalipotegwa na kutaja ni wapi mkanda wa video unaoonesha ukatili wa Rais Leslie, ulipo!




Safari ya kuelekea Mbweni,Tegeta!Ambapo IGP alisema huko ndipo Brigedia Karanje alipo,ilianza dakika hiyohiyo bila kupoteza muda!Ramadhan Mpelembe Mkurugenzi wa kikosi cha usalama wa taifa,alikuwa mwenye kila sababu ya kupeleka mambo harakaharaka ili aikomboe familia yake ambayo ilikuwa mateka kwani ilikuwa ndio kitu cha kwanza katika maisha yake,alivyomkumbuka mke wake mrembo wa kitusi,alizidi kuumia zaidi moyo ulimuuma baada ya sura za watoto wake kumjia kichwani!Hakutaka siku moja,watoweke kwenye upeo wa macho yake!Hiyo ilimaanisha afuate kile Ngesa, anachosema!

“Kwanini unafanya hivi Rama?”

Akiwa katikati ya mawazo IGP alimshtua kwa swali,jinsi picha lilivyoenda alijua fika kwamba Ramadhan Nurdin,anashirikiana na Ngesa!

“Unachotakiwa ni kukaa kimya”

Wakati Ramadhan na IGP wakijibizana yeye Ngesa akili yake ilikuwa kazini,alikuwa akiwaza vitu chungu mzima hususani nchi yake ya Tanzania na watu wake kwa ujumla,wakati mwingine alianza kujuta ni kwanini kajiingiza kwenye mkasa mzito namna hiyo tena wa kutisha,wakati muda kama huo alitakiwa awe na mpenzi wake faragha wanachapana mabusu,aliwaza siku za nyuma alivyokuwa rafiki mkubwa wa rais Leslie,lakini leo hii wamekua kama paka na Panya,hapo ndipo akakumbuka msemo unaosema rafiki yako wa leo ndio adui mkubwa wa kesho,hata hivyo aliamini kila kitu kitaenda sawa kama mambo yangeenda vizuri!Katika kutafakari,akapitisha kiganja cha mkono usoni,akashtuka zaidi baada ya kugundua ana nywele nyingi kwenye mashavu na ndevu nyingi,kumaanisha kwamba siku nyingi sana hajakata nywele,lakini kwake hilo hakuzingatia sana alichotaka kujua ni wapi Brigedia Karanje alipo na baada ya hapo,angesema ni wapi mkanda wa kaseti ulipo pamoja na mabomu mengine aliyotega!Walivyowasili Tegeta kwa ndevu IGP akatoa maelekezo,waikaingia upande wa pili,hapo Ngesa akawa makini kwani alielewa wanakaribia kufika.

“Kuna umbali gani?”

Ngesa akauliza,akitaka kupanga mahesabu yake kichwani.

“Mtaa wa nyuma”

IGP,akajibu kwa adabu kwani mdomo wa bastola ulikuwa kichwani kwake,kujibu utumbo utumbo ama pumba kulimaanisha ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yake siku hiyo!

“Ulinzi upoje?”

“Analindwa na askari nane”

“Nadhani sura yangu sio ngeni kwako,historia yangu unaifahamu vizuri.Sitotaka uzembe wowote kwenye hili zoezi,umenielewa?”

“Ndio,nimekuelewa”

Mkwara na sauti ya kitisho aliyotoa Ngesa kujumlisha na bastola aliyoshika mkononi,ilikuwa ni dalili tosha kwamba hataki utani na yupo kazini,kwenda kinyume na zoezi lake kifo ingekuwa halali yake,hilo IGP alilitambua ndio maana alijibu huku akihema kwani aliijua sana historia ya Derick Ngesa,tangu miaka ya tisini alivyoenda mafunzoni kisha kujiingiza katika jeshi la polisi lakini katika kitengo cha Upelelezi wa kujitegemea,kumbukumbu za kulisumbua jeshi la polisi huku akiwaua alizijua vilevile,ndio maana akawa mpole na mdogo kama kidonge cha pilton!

“Ni nyumba ile pale,yenye geti jeusi”

IGP,akasema!Baada ya mbele yake kuona nyumba hiyo yenye geti jeusi,ukuta mweupe ambapo juu kulikuwa na nyaya maalum za umeme,pamoja na urembo wa taa!Lilikuwa ni jumba kubwa sana,ambapo ilielekea ndani aliishi kigogo ama mfanyabiashara mkubwa.

“Kwanini mmemuweka huku?”

Ngesa,akahoji akitaka kudadisi kitu.

“Rais,hataki mtu yoyote amuhoji”

“Kwanini?”

“Hakusema”

“Kivipi kakuamini wewe?”

“Hapo sijui”

Alichiokifana Ngesa ni kutoa begi lake dogo la mkanda mmoja mgongoni,akaingiza ndani na kutoa darubini ndogo akaweka machoni na kutizama geti,ilikuwa ni darubini yenye lensi kali mno!Wanaume watatu walioshiba na kwenda hewani futi nyingi walikuwa getini,wanatembea huku na kule akajua ni lazima wangekuwa wanalinda,alichokifanya ni kuchukua bastola yake,akachomoa ‘magazine’ ili kuikagua kama ina risasi,alivyohakikisha ina risasi zimejaa akaikoki na kuiweka kiunoni,hakuishia hapo akachukua ‘magazine’ nyingine iliyojaa risasi na kuiweka ndani ya kiatu!Akashusha pumzi ndefu na kumgeukia IGP.

“Yupo kwenye chumba kipi,ukiingia ndani?”

“Gorofani,ukipanda ngazi!Kule bafuni,kuna chumba kwa ndani yake”

“Una uhakika?”

“Ndio,sina sababu ya kukudanganya”

“Twende”

Jinsi IGP alivyotoa macho,iliogopesha alikuwa ni mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango,hakutaka kuamini kama Ngesa ana ujasiri wa namna hiyo,hata hivyo wote walishuka kutoka ndani ya gari!

“Nisikilize kwa makini IGP,sitaki mtu yoyote ajue!Kinachoendelea”

“Sawa”

Ngesa,aliweka sura yake chini Ramadhan Mpelembe kando yake, wakaanza kuongozana mpaka ilipo nyumba iliyosadikika kwamba Brigedia Karanje yupo!

“Nahitaji kuingia ndani”

IGP,akasema kwa kuwa walimtambua hakukuwa na tatizo,maswali waliyojiuliza walinzi hao wanaume wawili waliokuwa naye ni akina nani,hawakutaka kubaki kimya!

“Hawa ni nani?”

“Nipo nao”

“Mbona hatuna taarifa?”

“Nimekwambia nipo nao ni dharura au nimpigie Rais,nimwambie hamtaki nipite?”

IGP Mahugo akatingisha kiberiti,akawapiga mikwara akijifanya kufoka!Ngesa alijitahidi kadri anavyoweza asiinue sura yake!

“Mpigie Rais simu”

Mmoja wa walinzi,akaweka mkazo hiyo ilimfanya Ngesa aanze kupeleka mkono taratibu nyuma ya kiuno chake,akakamata bastola vizuri ili aanzishe kitimtim kwani aliamini hakuna njia nyingine yoyote isipokuwa ‘plan B’ tu!

“John,waruhusu wapite”

Mmoja wapo,akatoa kauli hiyo baada ya kuona mzozo huo, ilielekea alijua nini maana ya Rais Leslie kuambiwa IGP Mahugo kuzuiliwa kuingia ndani.Hilo ndilo lilikuwa ni kosa kubwa la jinai lakini kwa upande mwingine alikuwa amefanya la maana kuokoa maisha yao, sababu Ngesa alikuwa tayari,kuwachapa na risasi.

Kitendo cha kuingia ndani,walikumbana na uwazi mkubwa, nje kulikuwa na magari ya kifahari kama HAMMER III original,Range Rover na BMW X5,hakika mwenye jumba hilo alikuwa ana pesa nyingi sana,macho ya Ngesa yalizidi kudadisi kila pembe ya eneo hilo,ambapo kwa nyuma pembeni aliona bwawa la kuogelea kubwa sana,kando kando kuna bustani ya maua,iliyokarabatiwa vizuri na kuchongwa.Walivyoigia ndani wakakutana na wanaume wengine wawili, kwenye makochi wanacheza gemu aina ya playstation,tena mpira hawa hawakuwa na habari nao,wakapandisha ngazi mpaka juu,ambapo mpaka hapo hakukuwa na mtu yoyote yule waliyepishana naye!

“Chumba kipi?”

Ngesa,akahoji!

“Kile pale”

Kwa kasi,Ngesa akachomoa bastola yake kutoka mafichoni akaishika mkononi akamtizama IGP Mahugo machoni!

“Namtaka Karanje,naomba nikwambie kitu kimoja!Hii bastola ina risasi kumi na nane,zote nitazifyatua mwilini mwako kama ukienda kinyume”

Yalikuwa ni maneno ya kutisha yaliyomfanya IGP ameze fundo la mate kwa uwoga na katika kuamini hilo mdomo wa bastola ya Ngesa uligusa juu ya paji la uso wake,kidole cha Ngesa kipo kwenye kilimi cha kufyatua risasi yaani triga!Jambo hilo lilimfanya ahisi tumbo linamuuma ajabu hata hivyo kilichotakiwa hapo ni utekelezaji na sio kusimama kama mlingoti!

Ramadhan Mpelembe pamoja na IGP wakanyonga kitasa na kuingia ndani ya chumba hiko huku nyuma wakimuacha Ngesa,anawasubiri kwani aliamini kivyovyote vile angeingia ndani wangemgundua na kusababisha patashika, jambo ambalo kamwe hakutaka litokee mwanzoni kabla hajamtia Brigedia Karanje mikononi mwake!

IGP Mahugo pamoja na Ramadhan Mpelembe,sasa walikuwa ndani ya chumba kikubwa chenye kitanda!Kwa kuwa IGP alijua mchoro wote,akaingia bafuni ambapo huko kulikuwa na kabati,dogo kiasi,akalisukuma pembeni kukatokea uwazi mkubwa sana!Ndani ya chumba,kulikuwa na giza kwa mbali wanaume wawili wapo kandokando,pembeni yupo Brigedia Karanje amekaa anavuta sigara bila wasiwasi wowote ule!

“Nimetumwa na Rais,kuja kumchukua!Mfungue”

Ilikuwa ni kauli kutoka kwa IGP,iliyofanya walinzi wote wamtupie macho!

“Kakutuma?”

“Ndio”

“Mbona hatuna hizo taarifa na katoka hapa jana usiku?”

“Mimi ndio nakwambia,ameniagiza!Fanyeni haraka”

Ilikuwa ni kauli iliyomfanya mlinzi mmoja aliyekuwa pembeni amekaa kwenye kiti,anavuta sigara asimame na kumuendea kwa haraka!

“MPIGIE SIMU”

Akasema kwa dharau huku akipuliza moshi hewani,akarudisha kipisi cha sigara mdomoni tena!

“Naona hutaki kazi Sam”

“Nimesema mpigie simu,nina maongezi naye”

Mtihani ukaanza kuwa mgumu jambo hilo likamfanya IGP amtizame Ramadhan Nurdin Mpelembe,haikueleweka kama anampa ishara ama mambo tayari yameharibika!

“Simu yangu haina airtime,nipatie yako”

Ilikuwa ni lazima Ramadhan Mpelembe ajiongeze,akili yake ilifanya kazi kwa kasi ya umeme akamtizama mlinzi aliyefahamika kwa jina la Sam,anatoa simu mfukoni kiunoni kwake akaona bastola,akatizama kwa makini!Kama ngedere,akamrukia na kumpiga kifuti cha mbavu akauvuta kwa kasi mkono wake na kuchomoa bastola iliyokuwa kiunoni kwake!

“Paaaaa”

Kabla ya kufanya chochote,ukasikika mlio mkubwa wa risasi mlinzi wa pembeni alifyatua baada ya kuona patashika lakini hata hivyo,hakuwa na shabaha nzuri kwani ilipiga ukutani ,Ramadhan Mpelembe akaruka upande wa pili kama swala na kubiringika kwa mtindo wa ninja,risasi zikawa zinamkosa kosa!Ngesa aliyekuwa nje alivyoona milio hiyo,akajua tayari mambo yameharibika akapiga mlango teke kwa nguvu na kuzama ndani,ambapo wa kwanza kumuona alikuwa mlinzi mmoja,akamchapa risasi ya kichwa ambayo ilimrusha hewani akadondoka,kabla ya kutulia akamchapa nyingine!

Akanyata taratibu mpaka bafuni,ambapo huko aliona uwazi mkubwa akaingia lakini alikoswa koswa na risasi baada ya kurudi nyuma,zikawa zinapiga mlangoni!Alichokifanya ni kutambaa chini,katika swala zima la kulenga shabaha alijiamini ndio maana,akabana jicho lake na kuanza kumfyatua mmoja wapo aliyekuwa dirishani,akapiga yowe kali na kutulia!Kuna kitu kilianza kumshangaza baada ya kusikia vishindo vinatokea kwenye ngazi akajua lazima kuna kundi la watu linakuja,akajivuta mlangoni kwenye kona kwani alijua tayari mambo yameharibika alichokifanya ni kumtizama Brigedia Karanje kwa umakini huku akipiga hesabu za namna ya kumtoa,akaona mbele yake kuna dirisha la kioo kikubwa ,hapo ndipo akakumbuka kwamba upande huohuo kulikuwa na bwawa la kuogelea,hakua ana uhakika kama hesabu zake zingefanya kazi!

Kishindo cha mtu,aliyekuwa anakuja pembeni yake kilimfanya ajiandae vizuri,alivyofika tu akamtuliza na kiwiko cha pua,akamvuta kwake na kumtwanga kichwa cha mdomo!Alichokifanya hapohapo ni kumuweka mbele yake,akawa anamtumia kama ngao,risasi walizokuwa wanarusha walinzi,nyingine zilimpiga mwenzao na baadhi zikapita pembeni!

“Paa paa paaa”

Ngesa akawa anajibu nayeye akiwa nyuma ya jamaa aliyemfanya ngao,alivyomkariba Brigedia Karanje,akajitupa na kutambaa kama nyoka,akaanza kumfungua kamba za miguu,alivyohakikisha Brigedia Karanje yupo huru akamchota mzobemzobe huku akilifyatulia risasi dirisha la kioo,ndani ya sekunde tano akawa tayari kakikaribia akamshika Brigedia Karanje vizuri na kujipindua kitaalam,ambapo alikuwa tayari amefika kwenye dirisha na kujitupa nje huku akiwa amemkumbatia Brigedia Karanje ‘Chubwiiii’ sauti ya kitu kizito kutua kwenye bwawa la kuogelea ikasikika,Ngesa na Brigedia Karanje wakawa wametumbukia ndani ya bwawa hilo la kuogelea huku juu wakiwaacha walinzi wametoa shingo nje,wanamimina risasi nyingi kwa chini ndani ya bwawa hilo!




Katika maswala ya kupiga mbizi,halikuwa tatizo kwake ndio maana akatulia ndani ya bwawa akishuhudia risasi zinapita ndani ya maji,hata hivyo aliamini silaha wanazotumia hazikuwa na nguvu sana ndiyo maana zilivyopita chini ya maji zilipungua nguvu,akiwa amefumbua macho yake kamshika Brigedia Karanje vizuri huku mkono wa kulia kashika bastola,akaibua shingo na kurusha risasi moja dirishani,ambayo haikufanya makosa hata kidogo!Kitu cha kwanza alichosikia ni yowe,akamshuhudia mmoja wa watu hao,akiporomoka kutoka juu hata hivyo hakutaka afike chini kistarehe akiwa hewani hukohuko akamsindikiza na risasi tatu,mpaka chini!Ubongo wake pamoja na utumbo vikawa vimesambaratika vibaya sana,ilikuwa ni maiti iliyotisha sana!Akiwa ndani ya bwawa la kuogelea akapima utulivu,akajiuliza maswali mmoja aliyekuwa anarusha risasi ameleekea wapi kwani walikuwa wawili.Alichokifanya ni kutizama kwa umakini madirisha yote,akayachapa maji huku akiwa na Brigedia Karanje pembeni,wamelowa chapachapa!Kwa usalama zaidi,akamtanguliza mbele huku akiwa anaangalia juu kwa umakini!

“Paa! Paaaa!”

Risasi mbili zilimkosa kosa,akawahi kujitupa kwenye maua!Mlengaji akakosa shabaha yake,hiyo ilifanya Ngesa atulie na kusikilizia kwanza kwani aliona risasi zinatokea mlangoni,akajua ni lazima mlengaji huyo atakuwa karibu na hapo,alichokifanya ni kuanza kutembea taratibu kabisa!Mlengaji alivyotokeza ili afyatue risasi kwa mara nyingine,akawa amechelewa tayari kwani risasi moja ya kichwa ilimtupa mbali na kufumua ubongo wake vibaya sana,huo ndio ukawa mwisho wake!Vifo vya watu mbalimbali tena vya kinyama kwake lilikuwa ni jambo la kawaida sana kushuhudia,ndiyo maana hakujisumbua kubaki na kuitizama maiti hiyo inayotisha,alichotaka yeye kwa wakati huo ni kuondoka na Brigedia Karanje,ndiyo maana muda wote alimshika mkono akiwa naye makini!

“Tulia hapo”

Ngesa akasema,akimuonya Karanje asiende popote hiyo ni baada ya kulifikia geti na kutoa kichwa nje ili kuangalia kama usalama upo,alivyoona kila kitu kipo sawa,akamvuta Karanje na wote kuingia ndani ya gari,ambapo hapo alichukua simu ya mkononi na kumtafuta Dustan hewani!

“Tukutane Kibo,karibu na Lamada Hotel!Ndio,pale Open beach!Nipo naye tayari”

Alivyokata simu,akamtizama Karanje kwa jicho kali la hasira, alitamani kum-miminia risasi zote zilizobaki ndani ya bastola lakini hilo asingeweza sababu alitaka kujua vitu vingi kutoka kwake,kwa kupigilia msumari hilo akamsisitiza kwamba ni lazima atasema tu!

“Leo,utaongea lugha zote!Mwisho wa siku nahitaji kujua,mambo nitakayokuuliza”

Ngesa akasema,akapiga gari moto na kukanyaga mafuta mengi, jambo lililofanya matairi yazunguke kwa kasi!

****

Hakuna kitu kilichomsumbua akili kama binadamu anayeitwa Derick Ngesa,tangu azaliwe hakuwahi kukutana na changamoto kubwa namna hiyo, tena kutoka kwa mtu mmoja!Hakuelewa jeshi lake linakwama wapi wakati kila kitu alitoa kuanzia silaha na vyombo vyote vya kijasusi lakini mwisho wa siku mambo yalienda ndivyo sivyo,hakua na raha kabisa hata usiku hakupata usingizi!

“Kwanini hulali Leslie?”

Mkewe,alimuuliza siku hiyo wakiwa ndani ya shuka moja usiku,baada ya kumuona mmewe mwenye mawazo,alikuwa ana kila sababu ya kuhoji!

“Nipo sawa”

Rais Leslie akajibu,kitu ambacho hakikuwa cha ukweli kabisa,mkewe akamsogelea karibu na kuanza kumpapasa kifua,akijaribu kumfariji ili ampe haki ya ndoa aliamini wenda ingesaidia kupunguza mawazo!

“Sipo kwenye mudi,sijisikii kufanya chochote”

“Kwanini lakini?”

“Basi tu”

“Leslie,una nini?!Mimi ni mkeo lakini”

“Nilishakwambia hakuna kitu”

Hapo Rais Leslie,akasimama wima akiwa hana nguo hata moja,kilichomshangaza mkewe ni kumuona yupo katika hali ileile yaani jogoo hajapanda mtungi,jambo ambalo halikuwa la kawaida hata kidogo kwa mwanaume kamili kama Rais Leslie!

“Leslie”

Mkewe nayeye akasimama huku akiita,akavuta kanga na kuiweka mwilini,akamfuata mumewe na kumkumbatia kwa nyuma!

“Una nini mme wangu?Ninaweza kukusaidia hata kwa mawazo”

Mke,akadeka na kumpiga busu shavuni!

“Nina matatizo makubwa sana”

“Yapi?”

“Mengi tu,nitakwambia siku moja”

“Lini?Niambie leo”

“Usijali….”

Alichokifanya Rais Leslie ni kuvaa taulo kisha kutoka chumbani na kunyoosha mpaka seblen,ambapo huko alichukua simu ya mezani na kuanza kumtafuta Mkurugenzi wa usalama wa Taifa Ramadhan Nurdin Mpelembe!Simu iliita sana bila kupokelewa,ikaita tena na tena!

“Rama”

Simu ilivyopokelewa,Rais Leslie akasema!

“Naam Mheshimiwa Rais”

“Mbona sipati ripoti?”

Lilikuwa ni swali la kwanza kuuliza.

“Mkuu”

“Nakusikiliza”

“Brigedia Karanje pia,ametoroshwa na Ngesaa”

Jibu hilo lilimfanya Rais Leslie,aishiwe nguvu akahisi kama amepigwa sindano ya ganzi mwilini,akawa ameganda kama barafu!

“Rama,Whaaaat?Katorokaje?Imekuaje?”

“Tupo kwenye jitihada za kumdhibiti,hawezi kwenda mbali hapa ninavyoongea nawewe!Nipo barabarani namsaka”

“Sasa hivi,ukimpata muue Ngesa pamoja na Karanje,alafu weka hilo Low profile,asijue yoyote yule!Umenielewa Rama?”

“Ndio mkuu”

“Angalia,asijue mtu yoyote yule”

Rais Leslie,alizungumza kwa sauti ya chini bila kujua pembeni nyuma ya kabati mkewe kajificha na amesikia kila kitu,sasa akaanza kupata picha ni kwanini mumewe hayupo sawa!

Kitu,kilichomjia kwa haraka ni kutafuta namba ya Ngesa ili kumuokoa na kifo hicho kwani aliamini ni mtu ambaye hana hatia hata hivyo huko nyuma,alishawahi kuwasaidia kipindi mtoto wake ametekwa nyara,hakika Ngesa hakustahili anachopitia,hata hivyo kuna maswali mengi sana alijiuliza mwanamke huyu!Ni kwanini Ngesa auwawe?Kwanini Karanje awekwe kwenye maficho?!Alama kubwa ya kiulizo ikamjia kichwani.


***

  ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG