Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

SIN SEASON 2 SEHEMU YA 5/10

   


SIN SEASON 2

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 5 KATI YA 10


“Una tamba mimi ni mume wa mtu?”

Swahi la Jery likampa Shani kiguhumizi, akajaribu kujitoa mikoni mwa Jery ila Jery akaikaza mikobo yake na kujikuta akiendelea kugugumia kifuani mwa Jery.

“Nd..io..”

“Una taka kumuibia mke wangu penzi lake”

“Ha…ha…a.ha…p…..a…..n….a bo…s….s…”

Shani alizungumza kwa woga pasipo kujua kwamba Jery ana tabasamu kimoyo moyo. Akamuachia Shani na kumtazama kwa sekunde kadhaa.

“Hatuwezi kufanya mapenzi kwenye kitanda ninacho lala na mke wangu, wala humu ikulu. Nina iheshimu sana nyumba hii eneo. Sasa fanya hivi, kwako ni wapi?”

“Kwangu ni Kimara?”

“Ume panga nyumba nzima?”

“Hapana nina chumba na sebule”

“Sawa, nita kuambia ni wapi uje sawa, ikremishe namba yangu”

Jery akamtajia Shani namba yake ya simu kisha, Shani naye akamtajia Jery namba yake ya simu na Jery akaingia chumbani kwake na Shani akaendelea na majukumu yake ya kawaida huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Jery akajilaza kitandani huku akitafakari mambo mengi sana, akaitafakari ndo yake ambayo ndio kwanza bado ni mpya.

‘Ila huyu demu ni mzuri aisee, siwezi kumukosa’

Jery alijisema kimoyo moyo. Akashuka kitandani, akaingia bafuni na kuaoga kwa haraka, akavaa nguo zake kisha akatoka chumbani hapo na kumkuta Shani,akifuta futa meza ya hapo sebleni, akamsogelea na kumshika kidevu chake, akamtazama macho yake malegevu kisha akaanza kumnyonya lipsi zale kwa sekunde kadhaa na kumfanya Shani ahasi kama mwili wake una nyong’onyea kwa furaha.

“Usimuambie mtu”

Jery mara baada ya kuzungumza hivyo akatoka ndani hapo. Akampigia simu mlinzi wake ambaye alikwa naye kipindi chote toka alipo kuwa masomoni Marekani, japo alipata matatizo kwa kumsaidia bosi wake huyo kwenye maswala ya kutumtumia Evans majambazi ila, hakuacha kuwa mnyenyekevu kwa Jery na siku zote ame kuwa ni mtunza siri mzuri sana wa Jery.

“Niambie Devi”

“Safi kaka”

“Hivi una fahamu dalali ambaye ana weza kunisaidia kutafuta nyumba nzima, eneo ambalo lime tulia na lisilo na mambo mengi kwa siku hii hii ya leo?”

“Ndio madalali wapo wengi sana. Je una hitaji kuhama hapa ikulu?”

“Hapana sihami”

“Ila nyumba ya nini tena kaka?”

“Nahitaji kumpangishia mmoja wa wasichana hapa ikulu nahitaji awe mke wangu wa pembeni”

“Jery Jery Jery ndugu yangu, bado huja acha hizo tabia rafiki yangu. Kumbuka kwamba ume oa tena mwanamke mkali sana, why una taka kuhangaika na wasichana kama ulivyo kuwa Marekani kule”

“Kaka huyu ata kuwa ni mwanamke wangu wa mwisho kabisa”

“Hapana huwezi kumfanyia hivyo mke wako. Kumbuka ni mambo mangapi tuliyafanya juu ya yule manzi, ilibakia kidogo nipoteze ajira yangu. Hembu tulia kwanza achana na huyo manzi”

Jery akaka kimya kwa sekunde kadha huku akimtazama Devi usoni mwake.

“Namuhitaji yule msichana, una nisaidia au hutaki?”

Jery alizungumza kwa jazba kidogo na kumfanya Devi akubali kishingo upande. Wakatafuta dalali mzuri na mwenye sifa nzuri katika utendaji wake wa kazi, wakaona picha jumba moja la gorofa lililopo Mbezi Lous Dar es Salaam.

“Mpigie simu”

“Kaka hii nyumba ni milioni mia sita una taka kuichukua”

“Fanya hivyo Devi, pesa yangu ipo nyingi na haina kazi, acha ninunua hii nyumba”

Devi akafwata maelekezo ya mkuu wake huyo ambaye ana mjua A to Z, na ana mtambu kwamba Jery ni king’ang’anizi na endapo ata amua kufanya jambo lake lolote basi hawezi kusikiliza jambo la mtu ni lazima alitimize kwa wakati anao uhitaji yeye. Dalali huyo aka wahakikishia kwmaba jumba hilo lipo na walicho kifanya ni kuondoka na kueleka lililo hilo. Jumba, wakiwa wawili tu. Wakakutana na dalali na kuanza kulikagua hilo jumba.

“Mwenye hili jamba ni mzungu, muda wake wa kuondoka nchini ume kwishi hivyo ana iuza kwa uharaka sana.”

Dalali alizungumza huku akiwatazama Jery na mlinzi wake huyo.

“Una weza kuwasiliana na muhusika?”

“Ndio”

Dalali huyo akawasiliana na mzungu huyo ambaye baada ya dakika ishirini akafika hapo wakakubaliana na Jery katika kuinunua jumba hilo la kifahari, Jery akafanya malipo kwa njia ya benki na wakaandikishiana na mzungu huyo kisha akakabidhiwa hati za jumba hilo na kuanza hapo akawa ni mmiliki halali wa juma hilo.

“Sasa kaka yule demu akija kuishi kwenye hili jumba nina imani lita mfaa sana. Jambo la kwanza nina mpiga mimba anizali mtoto kabla ya mke wangu ambaye kuna mambo nina hisi kwake”

“Mambo gani?”

“Nina hisia mbaya na mke wangu na nina hisi ana hitaji kutumia ndoa yetu kama daraja la kufanikishia mambo yake na familia yake”

“Mmmm mambo gani hayo kaka?”

“Bado sijayajua, ila kwa sasa nina jifanya ni mjinga kwake, ila nina mpeleleza taratibu endapo nikipata uhakika wa kile ninacho kihisi PUUUUUUU, nita muua”

Devi akastuka sana huku akimtazama Jery usoni mwake kwa maana endapo Jery ana sema jambo la kumuua mtu huwa ana dhamiria kufanya hivyo na sio mtu muoga wa kumuua mtu kwa maana ana roho mbaya na ngumu kumpita hata baba yake japo amepewa sura nzuri, yenye ucheshi na tabasamu la plastiki.

**************


“So una muua mke wako wa ndoa?”

Swali la Devi likamafanya Jery kumtazama kwa sekunde kadhaa.

“Una jua nikizungumza huwa nina maanisha. Sina ukoo naye wala undugu naye. Nilitengena naye kwa miaka kama kumi hivi, na mbaya alinidanganya kwamba ni bikra na majibu ya dokta yalivyo toka nika ambiwa ni kweli ana bikra. Hadi jana tulivyo fanya mapenzi nilimkuta ni bikra”

“So kama ume mkuta na usichana wake, ina kuwaje sasa una taka kumuua?”

“Ila ni bikra feki. Am the doctor tena professional doctor. Sikwenda Marekani kucheza nilisoma na nina ujua vizuir sana mwili wa binadamu, kuanzia ndani hadi nje. Nilimuonyesha fura ya nje ila ukweli, nina hitaji ni kufahamu ni kwa nini aliweka bikra ya bandia na ana mpango gani katika maisha yangu na baba yangu”

Devi alikabaki akiwa amejawa na mshangao pasipo kujua achangie nini kwenye hilo jambo kwa maana ni swala la kusghangaza sana.

“Sikia nahitaji nyumba ijazwe fenitures sasa hivi ni saa sita kanitafutie sofa za kisasa, vitanda vitatu vya kisasa. Naamini una jua nini napenda, tulipo kuwa tuna ishi Marekani ulikuwa una tambua jinsi gani ninavyo ipamba nyumba yangu”

“Ndio nina weza kusema ni mtu ambeye nina kujua vizuri kuliko mtu mwengine”

“Yaaa, ila jambo moja hili eneo litakuwa ni la siri sana. Mimi na wewe tu ndio tuta kuwa tuna jua. Credit card yangu hii kanitafutie hivyo vitu”

“Sawa mkuu”

Devi akaondoka na kumuacha Jery peke yake akiendelea kukagua mazingira ya jumba hilo. Hakika ni jumba lililo jengwa kisasa. Lina viwanja viwili vya michezo, kimoja ni kiwanja cha Tennes na kiwacha kingine ni cha Basketball. Sweeming pool lake ni kubwa kiasi cha kuweza kutosheleza watu hamsini wakaogelea kwa wakati mmoja. Kuna chumba maalumu cha mazoezi pamoja na chumba maalumu cha kutazamia filama kwa mfumo wa Sinema.

“Wooo huyu mzee alijenga”

Jery alishangaa huku ekihesabu viti vilivyomo katika chumba hicho. Akapata idadi ya viti ishirini, hivyo akiwa na marafiki zake kumi na tisa basi wana weza kutosha katika chumba hicho. Baada ya masaa mawili na nusu, Devi akafika nyumbani hapo huku akiwa ameongozana na gari mbili aina ya Scania zenye tela mbili zilizo jaa mizigo ya vitu vya ndani. Vitu hivyo vikashushwa na kuanza kupangwa ndani ya jumba hilo na wafanyakazi wa kampuni hiyo ambayo Devi alinunua viti hivyo vya ndani. Baada ya lisaa moja kila kitu kikawa kime wekwa sehemu yake. Hapakuwa na kitu kilicho kosekana hapo.

“So una kwenda kumuita yule demu hapa?”

Devi alizungumza huku akimkabidhi Jery kadi yake ya malipo(credit card).

“Hapana”

“Kwa nini?”

“Nahitaji kumpima akili yake kwanza ipo vipi si una jua sipendi kukurupuka. Nilimpatia ahadi ya kuonana naye ila sinto mpigia wala sinto muambia chochote. Turudi ikulu, na nikimaliza mazishi ya mama ndio nita kuja naye huku”

“Sawa na hizo document vipi una rudi nazo ikulu?”

“Ndio ila hato ziona”

“Sawa”

Jery na Devi wakarudi ikulu. Moja kwa moja Jery akaelekea ofisini kwa baba yake.

“Shikamoo hatuja onana baba leo?”

“Marahaba, yaa niliwahi kuamka mapema sana kuna majukumu nilipaswa kuya weka sawa”

“Okay kuna jambo moja nahitaji kukushirikisha kwa maana wewe ndio uliye baki kwenye maisha yangu.”

Jery alizungumza huku akiweka nyaraka hizo za ununuzi wa jumba hilo la kifahari juu ya meza ya baba yake.

“Ni nini hizo?”

“Nime nunua jumba moja la kifahari lipo Mbezi Louis”

Raisi Mtenzi akazichukua nyaraka hizo na kuanza kufunua moja baada ya nyingine. Katika nyakaraka hizo kuna picha za juma hilo.

“Waooo ni zuri. Ume kua sasa”

“Ni kweli baba, nami nahitaji kuw ana mji wangu kwa maana endapo muda wako ukiishia hapa ikulu, siwezi kwenda kuishi kwenye ile nyumba yako kule, ni lazima nikaishi kwangu”

“Yaa huo ndio uwanaume, kama umeweza kufikiria jambo kama hilo, ni kitu kivuzi sana”

“Ni kweli, ila sinto kwenda kuishi kwenye hii nyumba na mke wangu”

“Nini, una taka kwenda kuishi na nani!!?”

Raisi Mtenzi aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana usoni mwake.

“Nime jikuta nikianza kuwa na mashaka na mke wangu baba, toka nilivyo pata ile hasira, sina amani naye kabisa. Yaani nina fikiria kuwa na mwanamke mwengine kabisa”

“Ume changanyikiwa wewe?”

Raisi Mtenzi aliuliza kwa msisitizo kidogo.

“Sijachanganyikiwa baba ila nina zungumza kitu ambacho kipo moyoni mwangu. Kuna vitu nina endelea kumpeleleza mke wangu, endapo niki mkuta na huo ushahidi basi nita kuambia.”

“Vitu gani?”

“Kwa sasa siwezi kukuambia ila nitakapo kamilisha ushahidi wangu basi nita kueleza. Jambo la msingi nina kuomba sana usimuonyesha mkweo dalili yoyote ya kwamba nimesha anza kumtoa kwenye ufahamu wangu wa akili”

“Jery ngoja kwanza nikuambie kitu mwanangu”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akinyanyuka na kukaa kwenye moja ya sofa na Jery akamfwata sehemu alipo kaa.

“Ndoa ina pande kuu mbili. Upande wa kwanza kabisa ni furaha ambayo ndani yake ina sababishwa na mambo mengi sana yatokanayo na amani munayo jaribu kuitengeneza. Upande wa pili ni majonzi, ambayo yana sababishwa na mchafuko wa amani ndani ya watu wawili. Mke wako kukukatalia kufanya tendo la ndoa haimaanishi kwamba yeye ni malaya, hapana ni mwana mke anaye kupenda sana. Aliweza kutazama hichi kipindi tunacho kipitia cha kumpumzisha mama yako, ndio maana liweza kumaptia heshima. Je ulivyo fanya naye jana hukumkuta na usichana wake”

Jery akatabasamu kidogo huku akimtazama baba yake.

“Nili mkuta nao”

Jery alijibu kwa kuadangana kwa maana ana tambua kwamba alimkuta mke wake na bikra ya bandia.

“Basi kama uli mkuta nao ni kwamba alijituza siku zote”

“Baba bikra ina weza kusababisha mwanaume au mwanamke aka mpenda mmoja wapo?”

“Ndio hususani ikitolewa katika ndoa.”

“Ila baba ni wanawake wangapi wana olewa pasipo kuwa na bikra na hao walio wavunja uta kuta nao wana familia zao”

“Ni hao, ila kwenye mfumo wangu wa maisha, niliweza kumtoa mama yako usichana wake, ndani ya ndoa yetu. Kitendo hicho kime tufanya tuishi kwa upande hadi alivyo tutoka duniani. Hivyo kwa changamoto ya juzi isije kukufanya uka uka muacha mtoto wa watu kisa ni hisia zako. Tume elewana”

“Ndio baba nime kuelewa, ila nina ufanya upelelezi wangu ukikamilika sawa nita kuambia. Ila nina kuomba sana uni tunzie hizo nyaraka, kwa maana nahitaji iwe siri juu ya ununuzi wa ile nyumba kule”

“Sawa nime kuelewa, ila hakikisha humu achi mtoto wa watu na ukifia wakati muafaka wa kumueleza juu ya hii nyumba ufanye hivyo”

“Sawa baba”

Jery alipo maliza kuzungumza na baba yake akanyanyuka na kutoka ndani hapo.

Julieth akafungua akaunti yake ya mtando wa Facebook. Akajifikiria kwa muda na kutafuta jina la Evans Shika. Wakatokea watu kadhaa, ila mtu aliye kuwa ana mtafuta, ni wa tatu kutoka kwenye hiyo listi ya watu alio waorodhesha hapo. Akaingia upande wa picha za Evans na kuanza kuzitazama moja baada ya nyingine.

‘Nakupenda sana Evans, natambua nime kuacha kwenye kipindi ambacho hukupaswa kuachwa na mimi n anime fanya hivi kwa ajili ya maisha ya familia yangu. Ila moyo wangu na hisia zangu zote zipo kwako. Nipo na mwanaume kimwili tu mpenzi wangu’

Julieth alijisemea kimoyo moyo huku machozi yakimlenga lenga. Kusema ukweli ni kwamba ana mpenda sana Evans kwa maana ndio mwanaume wake wa kwanza kumuingiza kwenye dira ya mapenzi. Isitoshendio mwanaume ambaye aliweza kumshirikisha vitu vyake vingi sana kuliko hata mume wake wa ndoa ambaye waliharakisha sana katika kuifunga ndoa hiyo.

‘Upo wapi mpenzi wangu. Tafadhali niambie upo wapi?’

Julieth aliendelea kulalama, gafla mlango wake ukafunguliwa, alipo iona sura ya Jery, moyo wake uka anza kumuenda kasi. Akafuta faili facebook kwenye laptop yake hiyo iliyopo mezani hapo.

“Hei baby”

Jery alizungumza huku uso wake ukiwa umejawa na furaha kubwa sana.

“Vipo honey”

Julieth alizungumza huku akijiweka vizuri uso wake.

“Safi”

Jery akambusu Julieth mdomoni mwake, kisha akaka kwenye kiti cha mbele ya meza hiyo ya Julieth na kaunza kuangaza angaza ndani ya ofisi hiyo.

“Ofisi ime kupendeza ehee?”

“Yaa nime ipenda kwa kweli mume wangu”

“Vipi macho yako mbona ni mekundu?”

“Mafua mpenzi wangu”

“Ooohoo pole sana mke wangu, yame kuanza muda gani?”

“Mchana huu”

“Pole sana mama watoto. Vipi lunch una hitaji kula nini?”

“Mmmm chochote”

“Basi kachukue kantini nahitaji tule hapa hapa ofisini kwako”

Julieth akajifiria kwa sekunde kadhaa kisha wakakubaliana na mume wake, aende kuchukua chakula hicho. Julieth akachukua simu yake, wakanyonyana denda kidogo na mume wake kisha akatoka ndani hapo na kuelekea kwenye kantine ya ikuku kuchukua chakula wanacho kipenda yeye na mume wake.

Jery kwa haraka akainyanyuka na kutoa kifaa kidogo alicho kabidhiwa na Devi ambacho kina uwezo wa kunasa mazungumzo yote yanayo weza kufanywa ndani ya ofisi hiyo. Akakinatisha kifaa hicho chini ya meza hiyo kubwa ya mke wake. Akia ana taka kurudi kwenye kiti chake, akaitazama laptop hiyo ya Julieth. Akafungua faili la Mozila. Moja kwa moja akaenda upande wa ‘History ili kuweza kujua ni kitu gani alicho kifanya kifungua magreth kwenye faili hilo. Moyo wake uka mstuka mara baada ya kuona maandishi yanayo someka EVANS SHIKA FACEBOOK na mbaya zaidi faili hilo lime funguliwa kama dakika sitazilizo pita. Jery akafilifungua faili hiyo na kukutana na picha ya Evans.

‘Ahaa huyu mshenzi bado ana mfikiria mjinga wake?’

Jery alijisemea kimoyo moyo huku hasira na chuki dhidi ya Julieth vikizidi kumtawala. Akalifunga faili hilo vizuri kisha akarudi kwenye kiti chake na kukaa. Hazikupita dakika tano, Julieth akarudi akiwa na vyakula hivyo.

“Karibu chakula mume wangu”

“Nashukuru, kuna jambo moja nahiyaji tuzungumze mke wangu”

Jery alizungumza huku akimtazama mke wake kwa tabasamu ambalo kwa haraka haraka ukimtazama una weza kuamini kwamba moyo wake ume jawa na furaha nyingi sana.

“Jambo gani baby”

“Nahitaji tutafute mtoto sasa”

Julieth akastuka kidogo huku akimtazama mume wake.

“Nahitaji tusimalize hata mwaka huu, ume umesha pata mimba”

“Jery mume wangu, ndoa yetu bado change una onaje kwanza uka nipa muda wa kuzoea maisha ya ndoa kisha ndio nika beba mimba”

“Kwani huwezi kuzoea maisha hayo pasipo kuwa na mtoto tumboni mwako?”

“Siwezi mume wangu”

Julieth alijibu kwa msisitizo pasipo kujua kwamba Jery kuuliza maswali ya namna hiyo ana maana yake ikiwa ni njia moja wapo ya kuendelea kumpeleleza mke wake ambaye hadi sasa hajui kama mume wake ana endelea kumpeleleza.

***

“Yule pale yule pale”

Samson alizungumza huku akimuonyesha Magreth mtoto huyo aitwaye Mathayo. Samson akachukua kamera na kuanza kumpiga picha mtoto hyo huku wakiwa katika gari maalumu walio pewa na raisi kwa ajili ya kazi hiyo na gari hilo halijasajiliwa kwa namba za ikulu. Mtoto huyo aliye toka kwenye geti la shule hiyo huku akiwa emevalia begi mgongoni mwake pamoja na sare za shule, akaingia kwenye gari moja ina ya Benz CLASS C.

“Ni nani yule?”

Magreth aliuliza huku akitazama gari hilo linavyo anza kuondoka getini mwa shule hiyo taratibu.

“Ile gari ina tumiwa na house boy”

“House boy ana tumia Benz?”

“Yaa ana kuja kumchukulia mtoto wa bosi, huwa halali hapa shule”

“Ahaa sawa”

Gari hili likapita pembeni yao kwa mwendo wa taratibu. Magreth akawasha gari hilo na kuligeuza gari hilo na kuanza kulifwatilia gari alilo panda Mathayo. Wakia katika barabara iliyo tulia na isiyo na nyumba zozote. Magreth akaongeza mwendo wa gari hilo na kulipita gari hiyo kisha akalizibia njia kwa mbele na kumsababisha kijana huyo wa kazi kufunga breki za gafla pasipo kujua ni nini kinacho endelea.

“Una fanya nini?”

Samson aliuliza huku mapigo ya moyo yakimuende kasi.

“Tulia”

Magreth alizungumza huku akichomoa bastola yaka. Akajifunga kitamba chake nusu uso, akavaa miwani nyeusi na kushuka kwenye gari. Akatembea kwa mendo wa haraka na kumuhimiza dereva kushuka kwenye gari. House boy huyo akashuka kwenye gari huku mikono yake akiwa emeinyoosha juu. Magreth akamuhimiza kulala chini na akatii amri. Magreth akafungua mlango wa nyuma na kumkuta kijana huyo akiwa ana tetemeka.

“Una…ju….a mam….amm…..a yan….g…u ni…..ni…..nani?”

Kijana huyo alijitahidi kujibaragazua mbele ya Magreth, ambaye hakutaka kumtazama sana, akampiga shingoni mwake kwa ubapa wa kiganja chake cha kulia na akazimia. Akamchomoa kwenye gari hili na kumuingiza kwenye gari walilo nalo na kuondoka eneo hilo huku wakiwa wamemuacha house boy huyo akiwa ameendelea kulala kifudi fudi.

“Ame kufa?”

“Ata kufaje ikiwa tuna haja naye”

“Sasa mbona ame tulia kimya?”

Samson aliuliza huku akiwa na wasiwasi.

“Samson kwani hujawahi kufanya hii kazi?”

“Hata siku moja, kwenye maisha yangu ninacho kijua ni computer tu”

“Basi tulizana, ume shirikiana na mimi katika hii kazi na uta fanya kile nitakacho kuambia. Sawa”

“Sawa”

Magreth akasimamisha gari kwenye nyumba yake ambayo ana itumia kwa ajili ya kazi zake za siri. Akafungua geti la nyumba hiyo iliyo jitenga pembezoni mwa bahari na eneo hilo halina mtu yoyote anaye ishi.

“Ingiza gari”

Samson akahamia kwenye siti ya pembeni na kuendesha gari hilo hadi eneo maegesho. Magreth akafunga geti huku akihakikisha hakuna anaye wafwatili.

“Hapa ni wapi?”

Samson aliuliza huku akishangaa mazingira ya majani mengi katika eneo hilo la nyumba hiyo.

“Hapa ni kwangu, mshushe huyo dogo”

Samson akambeba Mathayo na wakaingia ndani. Akamalaza mtoto huyo kwenye moja ya sofa lililo jaa vumi.

“Hii nyumbana haitumiki ehee?”

“Ndio. Samson fanya hivi nahitaji kumpigia simu yule mama.”

“Una hitaji kumuambia nini?”

“Nahitaji kumpa onyo la kuhakikisha kwamba nina mpima ana toa siri yote ya wapi alipo rafiki yangu”

“Nina wazo”

“Wazo gani?”

“Una onaje uka mrekodi video huyu kijana kisha ukaituma kwenye namba yake na utampatia maelezo ya kuhitaji kujua alipo Josephine”

“Wazo zuri”

Magreth kwa haraka akamnyanyua kijana huyo na kumkalisha kwenye kiti, akamfunga miguu yake na mikono yake kwa nyuma. Akamziba mdomo kwa kumfunga kitambaa kisha akamfunga macho yake na kumwagika maji na kumfanya kijana huyo akazinduka. Akaanza kugugumia kwa woga, kwa maana hajui hapo alipo ni wapi. Samson akarekodi video ya sekunde thelathini, kisha akaindika maandishi mfupi yanayo someka, ili mwanao apone, tuna muhitaji Josephine la sivyo ata kufa ndani ya masaa kumi na mbili. Baada ya kufanya hivyo akaituma video hiyo kwenye namba ya mwana mama Sia Kamara na ubaya ni kwamba video hiyo hiyo hiyo iliingia pasipo kuonyesha namba ya Samson aliye ituma.



“Nimesha mtumia?”

“Ume mtumia kwa namba yako?”

“Ndio ila hawato weza kuina kwa maana kule ata ona ni private number. Hata wakijaribu kuitafuta hawato weza akuiona”

“Kazi nzuri, je akihitaji kuwasiliana nasi ita kuwaje?”

“Ata tuma ujumbe hapo hapo whatsapp na tuta upata”

“Kazi nzuri”

Magreth mara baada ya kuzungumza hivyo akatoka, nje akaitafuta namba ya raisi Mtenzi na kumpigia.

“Ndio Mage”

“Tume fanikiwa kumpata kijana wake na tume mtumia clip yenye maelezo ya kwamba atoa maelezo ya wapo alipo Josephine”

“Kazi nzuri je ahto weza kufahamu kwamba ni nyinyi?”

“Hapana haja weza kufahamu na Samson ame nihakikishia hilo”

“Safi uwe una nipatia ripoti ya kila linalo endelea”

“Sawa muheshimiwa”

Magreth akakata simu huku akishusha pumzi taratibu kisha akarudi ndani na kumkuta Samson akiminya minya laptop yake.

“Una njaa?”

“Hapana nipo vizuri”

Magreth akafungua friji na kutoa sofa ya kopo aina ya Cocacola, akaka kwenye moja ya sofa na kuanza kunywa taratibu huku akiendelea kusubiria majibu kutoka kwa mwana mama Sia Kamara.

***

Koti la suti alilo liavaa hakika alilihisi ni zito kwa kipindi hicho. Video ya mwanaye kutekwa hakika ime mchanga kiasi cha kumfanya kuacha kufanya kazi aliyo kuwa ana iandika kwenye laptop. Akatamani kunyanyuka na kueleeka ofisini kwa mkuu wake japo kumueleza juu ya jambo hilo ila akashindwa kwa maana ni lazima ata paswa kutoa maelezo ya kwa nini watekaji wana mlazimisha kumtoa Josephine na moja moja atakuwa ameingia kwenye shutma hizo. Akampigia simu house boy wake, simu yake ikaiata kwa mara kadhaa pasipo kupokelewa. Jambo hilo likmampa udhibitisho kwamba kuta kuwa na tatizo. Akamfikiria nabii Sanga aliye mpatia kazi hiyo ambayo kwa sasa ime muingiza kwenye matatizo . Akaitafuta namba yake kwenye simu yake alipo ipata akataka kumpigia, ila akasitisha zoezi hilo. Akarudia kuiangalia video hiyo na maelezo ya kumuhimiza ataje ni sehemu gani Josephine alipo.

‘Nisikurupuke’

Sia Kamara alizungumza huku akijiweka sawa kwenye kiti chake. Alicho kifanya ni kuandika ujumbe mfupi kwenye private number hiyo iliyo mtumia clip ya mwanaye.

‘SIFAHAMU CHOCHOTE JUU YA MAGRETH.’

Ujume huo ukaweka tiki mbili za blue ambazo zina ashiria kwamba ujumbe huo ume soma. Sia Kara, akampigia simu body gurd wkae ambaye alishirikiana naye kwenye kazi ya kumteka Josephine.

“Wame mteka mwanangu”

Sia Kamara alizuguma mara baada ya kijana huyo kuingia ofisini kwake.

“Kina nani hao?”

Akammabidhi kijana wake simu, akatazama clip hiyo iliyo ambatana na maandishi.

“Duu sasa ina kuwaje bosi?”

“Hata sijui ita kuwaje. Hapa najaribu kutafakari nini tufanye?”

“Na hili swala tukisema tushirikishe ofisi lazima lawama zita kuangukia”

“Ni kweli”

“Una muhisi ni nani ambaye ana fahamu juu ya hii ishu?”

“Siisi watatu ndio tuna fahamu. Mimi, wewe na nabii Sanga, ila nina kuhakika kabisa hakuna mtu ambaye ana fahamu juu ya hili swala”

“Mmmm sasa tuna fanyaje mkuu”

“Ina bidi kuonana na nabii Sanga”

“Alafu?”

“Kumshirikisha. Haya ni maisha ya mwanangu na hakuna mt aliye wahi kunifanyia mchezo kama huu, hususani kwa mwanangu”

“Sawa mkuu tufanye hivyo kabla ya haya masaa yao elekezi hayajaisha.”

Wakawasiliana na nabii Sanga na akawaeleza sehemu alipo na wakaondoka na kumfwata huko huku. Haikuchukua muda mwingi wakakutana na nabii Sanga kwenye mija ya moja ya maegesho ya magari. Sia Kamara akashuka kwenye gari na kuingia kwenye gari la nabii Sanga.

“Vipi ume weza kuiakamilisha kazi niliyo kupa”

“Sija ifanya kuna tatizo?”

“Tatizo gani?”

“Mwanangu ame tekwa na watu wasio julikana na watu hao wana muhitaji Josephine”

“What?”

“Ndio”

Sia Kamara akamuonyesha nabii Sanga video hiyo.

“Naamini huja mdhuru yule binti si ndio?”

“Usitake kuniambia kwamba nimrudishe kwa ajili ya hii clip ya mchezo?”

“Mchezo. Sanga huyo ni mwanangu na sio mwanao ume nielewa. Nita fanya chochote kuhakikusha nina muokoa mwanangu. Hili swala lipo very simple kwako. Mrudishe Josephine ili mwanangu aweze kuachiwa huru. Una masaa mawiwi la sivyo nita fanya kitu ambacho wewe na familia yako muta kwenda kuiona hii Tanzania ni chungu”

“Kwa hiyo una nitisha au?”

“Sikutishi ila nina kueleza nikiwa kama mama jasiri na mwenye uwezo wa kuilinda familia yake. Sanga una masaa mawili, sasa hivi ni saa tisa mchana. Ikifika saa kumi na mbili nahitaji mwanangu awe mikononi mwangu la sivyo nina mwaga ugali wako pamoja na mboga zangu ili sote tukose”

Sia Kamara baada ya kuzungumza hivyo akafungua mlango na kushuka kwenye gari la nabii Sanga na akaingia kwentye gari lake.

“Ana semaje?”

Kijana wake alimuuliza huku akiliondoka gari hilo eneo hilo taratibu.

“Mkrwara nilio mpiga nina uhakika ata nijua mimi ni nani?”

Nabii Sanga akanilitazama gari hilo likiondoka eneo hilo hapo huku akiwa amejawa na hasira sana kwa maana mwana mama huyo ame mbadilikia na ana hitaji kuvuruga mpango wake kabla hata haja ukamilisha.

***

Josephine akaendelea kusali huku akiwa amekaa kwenye kona ya kitanda cha chumba hicho.Kila alivyo jaribu kumuomba Mungu ili amuonyesha ni kina nani wame husika na kumteka kwake, hakuweza kupata jibu la moyo kwa moyo. Machozi yaliendelea kumwagika usoni mwake huku woga ukiendelea kumuandama. Mlango huo ukafungulia na akaingia mwanaume aliye usiku pamoja na asubuhi ya siku hiyo kwa ajili ya kumleta chakula.

“Usipo kula uta kufa na njaa”

Mwanaume huyo kwa mara ya kwanza alizungumza huku akiweka sahanu yenye chipsi, nyama ya kuku pamoja na glasi ya juisi. Akavitazama vyakula hivyo kisha akaanza kutembea kuelekea mlangoni.

“Samahani kaka. Uso wako dhahiri una onyesha kwamba wewe sio mtu mbaya. Naomba uniambie hapa nilipo ni wapi jamani?”

“Ume pigwa toka uingiee hapa?”

“Hapana?”

“Ume kosa chakula?”

“Hapana”

“Basi kaa kwa amani hatu hapa kwa ajili ya kukudhuru. Ukihitaji kutizama tv, rimoti ipo hapo”

Mwanaume huyo baada ya kuzungumza maneno hayo akafunga mlango na kutoka ndani hapo. Njaa ikamfanya Josephine ashuke kitandani taratibu. Akavuta sahani hiyo yenye chipsi na kuanza kula taratibu. Alipo hakikisha kwamba ame shiba vizuri, akanywa juisi hiyo ya nanasi kisha akaingia bafuni.Akajisaidia haja zake ndogo pamoja na kuoga kisha akarudi na kujilaza kitandani.

‘Mungu wangu, nina jua kwamba una makusudi ya mimi kuwepo katika meli hii, muda na wakati kama huu’

Josephine alizungumza kimoyo moyo.

‘Nina imani kulia kwangu hakuto nisaidia ila wewe wa pekee ndio unaye weza kunisaidia. Tafadhai Mungu baba nina kuomba unipe japo ishara ya kumfahamu huyo aliye husika na jambo hili nami nina imani nita kuwa ni balozi mzuri wa kuhakikisha ana kwenda jela kwa makosa yake yote aliyo yafanya’

Josephine aliendelea kuomba kuomba ila hakupata ishara yoyote.

“Nani?”

“Mkuu”

Kiongozi wa meli hiyo ya nabii Sanga ambayo ina wafanyakazi wake wana jishuhulisha na mambo mengi hususani ya kijambazi na usambazaji wa madawa ya kulevya, akaichukua simu hiyo aliyo pewa na kijana wake na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio muheshimiwa”

“Huyo msichana ana endeleaje?”

“Yupo vizuri tu mkuu”

“Sasa nina hitaji mumrudishe Tanzania”

“Lili?”

“Leo hii na muta mfikisha katika fukwe za koko na kuanzia hapo ata jua mwenyewe wapi kwa kwenda”

“Ila samahani muheshimiwa, je nina weza kujua ni kwa nini ana rudishwa mapema kiasi hichi ikiwa tulipanga akae hadi mpango utakapo kwisha?”

“Ndio ila yule aliye tufanyia kazi kijana wake ame tekwa na wana hitaji kubadilishana na Josephine ili kumuachia kijana huyo”

“Kutwekwa kwa mwananye ndio kukufanye uvuruge mpango wako muheshimiwa?”

“Ndio sina jinsi. Fanya hivyo”

“Nina wazo mkuu”

“Wazo gani?”

“Una onaje tuka muua huyo mwana mama”

Nabii Sanga akaka kimya huku akitafakari juu ya jambo hilo alilo shauriwa.

“Kwa maana hayo sio makubaliano yenu isitoshe kazi haijakamilika na makamu wa raisi wa Marekani ana kuja kesho. Una onaje leo hii hii nika tuma vijana waka muondoka huyo mwana mama”

“Tukimuua huyo mwana mama serikali nzima ya Tanzania ita tujia juu yetu. Fanya hivyo nilivyo kuambia ume nielewa”

“Ndio muheshimiwa”

Simu ikakatwa na jaama huyo akawaamrisha vijana wake wawili kumtoa Josephine katika chumba chake. Wakamchoma sindano ya usingizi, wakampandisha kwenye boti na wakaanza kurudi naye nchini Tanzania. Ndani ya lisaa moja na nusu wakamfikisha Josephine pembezoni mwa fukwe za Koko beach, kwa bahati nzuri eneo hilo halina watu. Wakachoma sindano ya kumzindua kisha wakaondoka, Josephine taratibu akamfumbua macho yake huku akiwa amejawa na uchovu mwingi sana. Akatazama eneo hilo na kulifahamu vizuri, akaanza kutembea hadi kwenye kibanda kimoja wapo cha msajili wa laini.

“Mambo”

Josephine alizungumza kwa sauti ya upole.

“Safi sister vipi?”

“Poa. Una weza kuniazima simu yako nika mpigia rafiki yangu akafika hapa kunichukua”

“Wewe ni mgeni na hapa Dar es Salaam?”

“Hapana ila nime poteza simu yangu”

Msajili laini huyo akamtazama Josephine kwa sekunde kadhaa kisha akamkabidhi Josephine simu ndogo aina ya Tecno. Josephine akaiandika namba ya Magreth na kumpigia, simu ya Magreth ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.

“Haloo”

“Josee”

Magreth aliita kwamshangao mkubwa sana.

“Yes Mage, nipo Coco beach njoo unichukue”

Josephine alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Okay nina kuja sasa hivi upo na nani?”

“Peke yangu, nime kaa hapa tu kwenye kibanda cha kusajili laini”

“Poa usiondoke hapo nina kuja sasa hivi”

“Sawa”

Josephine akakata simu huku akijipangusa machozi usoni mwake. Akamkabidhi muuza laini simu yake.

“Kaa kwenye benchi hapa sister”

Muuza laini huyo alizungumza huku akisogea pembeni kidogo na Josephine akaka kwenye benchi hilo huku akiw ana wasiwasi. Baada ya dakika ishirini nane Magreth akafika kwenye fukwe hizo za Coco beach, akashuka kwenye gari na kuanza kuangaza kila eneo na kumuona Josephine akiw aamekaa huku amempa mgongo. Akakimbia hadi kwenye eneo hilo, kwa haraka Josephine akanyanyuka na wakakumbatiana na furaha hadi msajili wa laini hizo akashangaa.

”Pole rafiki yangu”

“Nashukuru, huyu kaka ndio amenisaidia kwa kunipa simu yake nika kupigia”

Magreth akaingiza mkono mfukoni na kutoa noti tatu za shilingi elfu kumi kumi na kumkabidhi kijana huyo kama asante. Wakaondoka kwa haraka katika fukwe hiyo na kuanza kuelekea katika nyumba alipo muacha Somson na mtoto wa Sia Kamara.

“Ume weza kuwaoan walio kuteka?”

“Ni wazungu tu hao watu sija muona muafrika hata mmoja”

“Mmmm kweli?”

“Ndio na wapo kwenye meli ila sija weza kjua ni meli gani na wala ina itwaje. Ila kwa kuwatazama haraka haraka ni watu wana fanya kazi chini ya mtu mkubwa sana”

“Sio wa Marekania?”

“Hapana ni wazungu wenye mchanganyiko wa asili tofauti”

“Duu, ila kuna mtoto wa mwana mama mmoja ni kiongozi wa kitengo cha NSA. Nime mteka mwanaye nime weza kuma amri ya kukurudisha na ime kuwa hivyo. Hapa sasa nina weza kupata ushahidi kwamba mwana mama huyo ndio aliye kuteka”

“Yupo yupoje huyo mwana mama?”

Magreth akamuonyesha Josephine pich ya Sia Kamara na kujikuta macho yakimtoka.

“Huyu mwana mama alikuwa amekaa nyuma yangu pale kanisani kwa nabii Sanga”

“Basi huyu ndio ana husika na tukio la kutekwa kwako. Tuna shukuru Mungu upo salama, sasa kwa kuendelea kumshikilia mwanaye basi tuta weza kufahamu ni nani na nani ambao ana fanya nao kazi na hao wote ni lazima wafungwe kwa mujibu wa sheria ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania”

Magreth alizungumza kwa kujiamini huku moyoni mwake akiwa amejawa na furaha kubwa sana kwa maana amesha mpata rafiki yake na mtu wa pekee aliye salika katika kumshuhulikia ni Sia Kamara na yeye ndio ata mtaja muhusika mmoja baada ya mwengine.



Wakafika sehemu walipo muacha Samson pamoja na Mathayo.

“Dogo vipi?”

Julieth alimsalimia Samson huku wakipeana mikono.

“Safi pole kwa matatizo”

“Nashukuru.”

“Vipi huyo dogo ana endeleaje?”

Magreth alizungumza huku wakiwa wamesimama nje ya nyumba hiyo.

“Ana lia lia tu”

“Bado tuna kazi naye. Hatuwezi kumuachia kwa maana mama yake ana paswa kujibu maswali yetu. Vipi ame kuona uso wako?”

“Hapana, nime jifunga kitambaa na hajaweza kuniona uso wangu”

“Sasa fanya hivi mtumie meseji nyengine umuambie tuna hitaji jina la aliye muagiza kumteka Josephine. La sivyo ifikapo saa mbili asubuhi kesho, kichwa cha mwanaye kita kuwa zawadi yake”

“Sawa”

Samson akajifunga kitambaa hicho kisha akarudi ndani. Akachukua laptop yake na kutoka nje, akautuma ujumbe huyo kwa Sia Kamara kama alivyo elezwa na wakakaa kwa ajili ya kusubiria majibu.

“Mpigie muheshimiwa raisi”

Josephine alizungumza huku akimtazama Magreth, akampigia simu raisi Mtenzi.

“Muheshimiwa mpango ume kwenda vizuri. Tume fanikiwa kumpata Josephine”

“Wee hembu mpatie simu”

“Habari muheshimiwa”

“Salama…Ohooo asante Mungu upo salama kwa kweli. Vipi wame kudhuru?”

“Hapana muheshimiwa”

“Je una weza kutambua sura za hao walio kuteka?”

“Nina ikumbuka sura ya mmoja wao ambaye yeye ndio aliye kuwa akinihudumia katika kunipatia chakula”

“Sawa, fanya hivi njooni ikulu sasa hivi”

“Sawa muheshimiwa”

“Hembu mpatie simu Magreth”

Magreth akakabidhiwa simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Mage hongeneni kwa kazi mulio ifanya.Vipi huyo kijana bado upo naye?”

“Ndio bado nime mshikilia mtoto wake. Ila sinto hitaji kumuachia hadi niweze kupata jibu la nani ambaye ame mtuma kwa ajili ya kumteka Josephine”

“Basi fanya hivyo ita kuwa ni jambo zuri sana”

“Sawa muheshimiwa ila Josephine ina bidi aje peke yake huko ikulu kwa maana huyu kijana ina bidi nimuwekee uangalizi”

“Sawa”

Magreth akakata simu kisha akamkabidhi Josephine funguo za gari na akaondoka eneo hilo na kuelekea ikulu.

***

Nabii Sanga akaitoa simu yake mfukoni na kuifungua meseji kutoka kwa Sia Kamara. Meseji hiyo ika mstua sana kwa maana kama ni kumuachia Josephine tayari alisha muachia ina kuwaje watekaji wana endelea kumshikilia mtoto wa Sia Kamara. Kwa haraka nabii Sangaa kamapigia simu Sia Kamara.

“Una maanisha nini unavyo sema kwamba upo tayari kunitaja kwa ajili ya mwanao?”

“Nina hisi kwamba hapo hakuna kitu kilicho jificha, mzee kama ni pesa yako nina kurudishia na nita kutaja tu, ili mwanangu awe salama”

“Ila nimesha muachia Josephine”

“Mbona huja niambia?”

“Nilihisi kwamba uta kuwa ume pata habari. Alafu Sia kumbuka ni kazi ngapi tume fanya pamoja ila mbona kwenye hii ume kuwa una nyumba nyumba”

“Hivi angekuwa ni mwanao ndio ame shikiliwa je unge fanya nini wewe?”

“Tazama wewe una watu wengi sana kwenye hicho kikosi chako. Una shindwa vipi kuwatumia kwa ajiliya kukusaidia katika kazi hiyo. Hembu jiongeze bwana kwenye hilo na fanya jambo katika hilo”

Nabii Sanga alimshawishi Sia Kamara katika kuhakisha ana jitahidi kumtafuta mwanaye.

“Aisee hii ishu ime kaa vibaya. Nipatie nyongeza ya pesa ili niweze kuifanya kazi hiyo.”

“Kiasi gani una hitaji”

“Dola milioni moja”

“Nyingi sana hiyo Sia”

“Okay kwa sababu ni nyingi siwezi kwenda chini mimi mwenyewe. Nita hakikisha kwamba tuna kwenda chini pamoja”

Baada ya kuzungumza hivyo Sia Kamara akakata simu jambo ambalo lilizidisha hasira kwa nabii Sanga. Akaichukua simu yake na kumpigia kiongozi wa vijana wake.

“Nisikilize jambo moja”

“Ndio mkuu nina kusikiliza”

“Nahitaji huyu mwanamke aondolewe, ana nitishia haniji mimi ni nani?”

“Una hitaji afe kifo cha aina gani?”

“Kisicho na ushahidi”

“Sawa muheshimiwa”

Nabii Sanga akakata simu, kabla hajairudisha mfukoni mwake, ikaingia simu kutoka kwa Julieth.

“Baba simu yako ipo bize sana”

“Kuna watu nilikuwa nina zungumza nao. Vipi?”

“Baba nina hisi mpango wetu una kwenda kuyumba”

“Una maana gani?”

“Mume wangu ana hitaji nizae naye”

“Shitiii!! Ume mjibu nini?”

“Sija mpatia jibu la moja kwa moja, sasa tuna fanyaje?”

“Upo wapi kwa sasa?”

“Nipo ofisini kwangu”

“Nita kuambia nini cha kufanya, ngoja nifikirie kwanza”

“Sawa baba nina subiria jibu lako”

Nabii Sanga akashusha pumzi huku akijaribu kuchanganua ni nini ana weza kufanya. Galfa meseji ikaingia kwenye simu yake kutoka upande wa whatsapp. Akaifungua kwa haraka na kukuta ina toka kwa mmoja wa wachungaji wake walipo mkoani Tanga. Macho yakamtoka mara baada ya kuona picha ya mke wake akiwa amekaa na kijana mmoja katika mkao wa kimahaba. Hasira taratibu ikaanza kumpanda huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana. Akampigia mchungaji huyo simu na akaipokea.

“Ume muonaa wapi mke wangu?”

“Mtumishi nime muona Lushoto. Nimie ituma hiyo picha ili kudhibitisha kwamba ni yeye au si yeye kwa maana mke wako ninaye mtambua ni mtu mwenye heshima sana”

“Lustoto Tanga si ndio?”

“Ndio mtumishi”

“Ame kuona?”

“Hapana ili bidi nijifiche”

“Sasa nina kuja usiku huu huu”

“Sawa mtumishi”

“Hakikisha huondoki kwenye hiyo hoteli na una wafwatilia ipasavyo”

“Sawa mtumishi”

Nabii Sanga akakata simu, akafungua shelf yake na kutoa bastola yake pamoja na magazine ambayo ipo pembeni. Akataka kutoka ndani hapo, ila akapata wazo moja, akaona akitumia usafiri wa gari kuelekea mkoani Tanga ita mchukua masaa mengi na isitoshe ana jazba kubwa sana.

‘Mke wangu ana nichukuliaje hadi atembee nia vijitoto vidogo?’

Nabii Sanga aliwaza huku jasho litokanalo na hasira likiendelea kumchuruzika mwili mzima.

“Nahitaji usafiri wa helicopter nina elekea Tanga Lushoto muda huu”

Nabii Sanga alizungumza na mmoja wa mawakala wa shirika moja la ndege za kukodisha.

“Sawa mzee una weza kufika ofisini. Helicopter zipo”

“Nakuja sasa hivi”

Nabii Sanga akatoka ndani kwake na moja kwa moja akaelekea katika ofisi hizo ambazo zina husika na usafiri wa anga. Akalipa kiasi anacho takiwa kulipa kwa safari hiyo ya kwenda, kisha safari ya kuelekea mkoani Tanga.

‘Huyu mwanamke lazima nimfundishe adubu’

Nabii Sanga alozungumza kimoyo moyo huku akigusa gusa eneo la kiunoni mwake alipo ificha bastola yake hiyo. Nabii Sanga akamtumia meseji mchungaji wake huyo na kumuelekeza ni wapi ampokee kwa maana yupo njiani kuelekea Lushoto.

***

“Haki ya Mungu nime yapenda sana haya mazingira.”

Mrs Sanga alizungumza huku miguu yake akiwa ameiweka mapajani mwa Tumaini.

“Nilikuambia Lushoto ni pazuri sana. Hata hii hoteli wazungu ndio wana pendelea kufika.”

Tumaini alizungumza huku akiipapasa papasa miguu hiyo ya mrs Sanga huku wakiwa wamekaa kwenye moja ya kibanda kidogo cha mapumziko huku wakiendelea kupata vinywaji.

“Ila sio mbali sana. Zile kona za pale chini kidogo ulivyo kuwa una zikata zilikuwa zina nipa wasiwasi sana”

“Hahaa zile zina itwa Kona za Soni. Pale ukiwa ni mgeni wa hii barabara ni lazima ulidumbukize gari chini”

“Kweli aisee. Malizia kinywaji chako mpenzi wangu uka nipatie mautamu, si tume pumzika vya kutosha”

“Yaa”

Tumaini akapigwa fumba la bia yake na kuimaliza. Wakasimama na kuondoka eneo hilo huku wakiwa wameshikana mikono. Mchungaji Smith alijikuta akitingisha kichwa huku akitamani sana kumstua mrs Sanga na kuma habari juu ya ujio wa ume wake, ila akashindwa kwa maana tayari alisha uza picha kwa nabii Sanga. Akawafwatila kwa umakini hadi kwenye chumba walicho ingia, kisha akarudi kwenye kibanda alicho kuwa amekaa huku akisubiria simu ya nabii Sanga.

Tumaini hakuhitaji mazungumzo mengi, akamsukumia Mrs Sanga kitandani, na taratibu akaanza kumvua nguo moja baada ya nyingine.

“Baby ngoja kwanza”

“Noo baby nina hamu”

Tumaini alizungumza huku akiipanua miguu ya mrs Sanga. Akaanza umlamba kitumbua chake na kumfanya mrs Sanga kuanza kujisikia raha ambayo ime sababisha achanganyikiwe na penzi la kijana huyo. Tumaini akaendelea na mautundu yake, alipo jiridhisha na uandaaji wa kitumbua cha mrs Sanga, akampaka jogoo wake mate kiasi kisha taratibu akaanza kumuingiza ndani ya kitumbua cha mrs Sanga na kumfanya ajihisi raha ambayo hakuwahi kupewa na mwanaume yoyote duniani.

‘Tumekaribia una weza kujiandaa’

Meseji hiyo ikamfanya mchungaji Smith kunyanyuka kwenye kiti alicho kikalia. Akakimbilia hadi lilipo gari lake, akaingia na kuondoka. Haikumchukua hata dakika kumi akawa amefika eneo ambalo kuna kiwanja cha helicopter, akasubiri hapo kwa dakika tano na akaishuhudia helicopter yenye rangi nyekundu, ikishuka taratibu. Ilipo tulia, mlango wa helicopter hiyo ukafunguliwa na nabii Sanga akashuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka.

“Bado wapo?”

Nabii Sanga alimuuliza mchungaji Smith.

“Ndio”

“Twende”

Wakaingia kwenye gari na kuanza kurudi hotelini. Mchungaji Smith muda wote alikaa kimya kwani hakuwahi kumuona hata siku moyo kiongozi wake huyo wa dini akiwa amekasirika kiasi hicho.

“Huyu mwanamke nimpe nini jamani?”

Nabii Sanga alilalama kana kwamba yeye sio mchepukaji. Wakafika hotelini hapo na moja kwa moja wakaelekea hadi kwenye chumba hicho. Mchungaji Smith akagonga mlango taratibu.

‘Baby ni nani?”

Tumaini alimuuliza mrs Sanga huku akiwa emembong’olesha na yeye akiwa kwa nyuma.

‘Ahaa sijui ni nani, endelea bwana kunitomb**”

Mlango uka gongwa tena na kuwafanya watazamane.

“Ngoja nikamuangalie anaye gonga”

Tumaini alizungumza huku akimchomoa jogoo wake katika kitumbua cha mrs Sanga.

“Sawa”

Mrs Sanga alijilaza kifudi fudi huku akiwa amechoka sana kwa maana mpite mpute anao pelekwa na kijana huyo hakika sio wa kawaida.

“Habari zenu?”

Tumaini alizungumza huku akiwatazama mchungaji Smith pamoja na nabii Sanga. Nagii Sanga, akapiga kikombo mlango huo na kuingia ndani huku akiichomoa bastola yake. Mchungaji Smith akamsukumia Tumaini kwa ndani na akauwahi kuufunga mlango huo kwa ndani. Mrs Sanga mapigo yake ya moyo yakamstuka sana mara baada ya kumuona mume wake akiwa amesimama huku mkononi mwake akiw aameshika bastola. Akaliwahi shuka kwa haraka na kujifunika huku akitetemeka kwani hakutaraji kumuona mume wake katika mazingira kama hayo.

***

“Mpango ni mpango gani ambao wanao yeye na baba yake?”

Jery alizungumza huku akimtazama Devi mara baada ya kusikiliza mazungumzo hayo ya Julieth aliyo kuwa ana zungumza na baba yake.

“Devi ndio maana nilikuambia kwamba huyu demu alizitumia hisia zangu ili kufanikisha mipango yake na familia yake”

“Jery tusi muhukumu moja kwa moja. Hembu endelea kumfwatilia na kile kifaa ulicho kiweka nina imani kwamba kita rekodi kila jambo”

“Kaka nili ingia cha kike, leo nilikuta alikuwa ana angalia picha za yule fala wake Evans kwenye laptop yake. Pili nilimueleza swala la kumuo, hakunipa jibu la kueleweka, mara kaingia huku mara katokea huku, huoni huo ni ubabaishaji”

“Wanawake ina bidi uwajue, hembu jaribu kuliwekea umakini hili jambo nina imani kwamba kila kitu kita kuwa sawa”

“Nita hitaji yule demu leo nika lale naye kule”

“Hapana bado mapema, kaka usije ukaruka majivu ukakanyaga moto. Muda ume kwenda sasa ingia ndani uka tulie na mke wako”

Devi alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Jery ashushe pumzi, kisha akashuka kwenye gari hilo bila hata ya kuaga na akaelekea ndani.

***

Vijana wa nabii Sanga wakaendelea kulifwatilia gari la Sia Kamara kwa umakini sana pasipo yeye mwenyewe kutambua chochote. Akafika kenye moja ya mgahawa akasimamisha gari hilo pembeni kisha akashuka huku akiwa na mawazo mengi sana kichwani mwake. Kutekwa kwa mwanaye na kulazimishwa kumtaja muhusika aliye muahiza kumteka Josephine hakika ni jambo linalo muumiza sana kichwa chake. Nafsi moja ina muhimiza kwa nguvu zote azungumze ukweli ili kumuokoa mwanaye, huku nafsi ya pili ikimshaiwishi kuto kuzungumza chochote kwa maana watekaji hao wanacho kifanya ni vitisho tu. Kijana mmoja akashuka kwenye gari na kutembea kwa mwendo wa umakini hadi pembezoni mwa gari la Sia Kamara, Akachuchumaa kidogo na kubandika bomu la kutega chini ya gari hilo, kisha akarudi kwenye gari alilo toka.

“Ume liweka vizuri?”

Mwenzake aliye ambatana naye alimuuliza huku akitazama gari hilo.

“Ndio”

Hawakuondoka hapo, hadi walipo muona Sia Kamara akitoka ndani ya mgahawa huo, akasimama nje ya gari lake kabla hajafungua mlango, simu yake ikaanza kuita. Akaitazama na kukuta ni namba ngeni, akaipokea na kuiweka sikioni mwake.

“Haloo”

“Una zungumza na Magreth nina imani kwamba una nifahamu?”

“Ndio Mage, una hitaji nini?”

“Mwanao ninaye na mimi ndio nime mteka. Yupo mikono salama kabisa na nina tambua wewe ndio ume mteka Josephine. Sihitaji tuzunguke mbuyu kwenye hili, ila nina hitajiuweze kuniambia ni nani aliye kupa kazi ya kumteka Josephine, usipo niambia, basi nina imani kwamba ume muona nilicho mfanya yule Jackline, basi mwanao naye nita mfanya hivyo hivyo”

Sia Kamara hasira ikamapanda, akafungua mlango wa gari lake na kupanda huku simu yake ikiwa mkononi mwake.

“Wewe mpumbavu endapo uta mfanya chochote mwanangu, nita kuua mshenzi wewe”

“Kweli mimi nimshenzi, nipe jina la aliye kutuma nami nikuletea baby boy wako akiwa salama salmini”

Sia Kamara akaiweka loud speaker simu yake, akaingia upande wa kuitafuta namba hiyo kwa kutumia satelaite na akafahamu ni wapi inapo tokea, akawasha gari lake na kuanza kuondoka kwa mawendo wa kasi sana.

“Sia nipe jibu”

Magreth aliendelea kuzungumza na kumfanya Sia kuzidi kukanyaga mafuta. Kijana mmoja wa nabii Sanga mara baada ya kuliona gari la Sia Kamara lime fika mbali kidogo, akatoa rimoti ya kulipulia bomu hilo kwenye koti la suti yake. Akalitazama kwa sekunde gari hilo linalo kwenda kwa kasi sana, kisha akaminya batani nyekundu katika rimoti hiyo na kusababisha gari la Sia Kamara kurushwa juu mita kadhaa huku likichanguka vipande vipande na kusababisha Sia Kamara kufa katika mlipuko huo bomu.



Magari yaliyopo pembezoni mwa eneo lilipo tokea shambulio la mlipuko wa gari la Sia Kamara nayo hayakuwa salama, mengi ya magari hayo nayo yalianza kuwaka moto huku mengine yakiwa na watu ndani. Watu walio kuwa wana tembea kwa miguu nao waliweza kuathiriwa na bomu hilo huku wengi wao wakipoteza maisha.

***

“Pole sana Josephine”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama Josephine aliye kaa katika moja ya ofisini hapo ofisini kwake.

“Nashukuru.”

“Ila hiyo meli nina imani kwamba haipo nchini Tanzania?”

“Sijajajua muheshimiwa raisi”

Gafla mlango ukafunguliwa na akaingia sekretari wake.

“Muheshimiwa kuna tukio la mlipuko wa bomu”

Kauli hiyo ikawastua sana raisi Mtenzi pamoja na Josephine.

“Waa..pi?”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Wakatoka ofisini hapo na moja kwa moja wakaelekea kwenye katika chumba cha mawasiliano. Wakakuta habari ya mlipuko huo kwenye tv.

“Ime kuwaje?”

Raisi Mtenzi aliuliza huku akikodolea macho tv hiyo.

“Muheshimiwa ni mlipuko wa bomu umetokea maeneo ya Kinondoni na gari iliyo lipuka ni ya mmoja wa wapelelzi wa kitengo cha NSA”

“Nani?”

“Bi Sia Kamara”

Raisi Mtenzi akatazamana na Josephine huku wakiwawamejawa namshangao. Raisi Mtenzi akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Magreth.

“Muheshimiwa raisi”

“Aisee kuna mlipuko ume tokea na inavyo sadikika Sia Kamra ndio amelipuka kwenye mlipuko huo”

“Mungu wangu, unajua nime toka kuzungumza naye muda mchache ulio pita na simu yake ilikatika galfa kumbe ndio mlipuko huo”

“Ndio ulikuwa una zungumza naye nini?”

“Nilizungumza naye kuhusiana na nani ambaye ame husika katika kumteka Josephine ila hakuweza kumtaja ni nani”

“Nina hisi kuna mchezo mchafu. Hakikisha huyo kijana una mrudisha nyumbani kwao pasipo mtu yoyote kuweza kujua hilo na hakikisha kwamba una fika eneo la tukio na ili uweze kujua ni nini kinacho endelea”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Raisi Mtenzi akakata simu huku akiendelea kutazama taarifa hiyo.

“Jose ume weza kuona chochote juu ya hili tukio?”

Raisi Mtenzi alimuuliza Josephine kwa sauti ya chini kidogo.

“Kuna watu wawili nina waona wapo kwenye gari aian ya Toyota Mark , ina rangi nyeusi.”

Josephine alizungumza huku akiwa amefumba macho yake.

“Ina elekea kwa sasamaeleo ya Kawe”

“Tafuteni gari nyeusi aina ya Mark X katika njia ya Kawe”

Raisi Mtenzii alizungumza na wataalamu wake wanao dili na maswala ya computer wakaanza kuifanya kazi hiyo.

“Muheshimiwa raisi tume pata Mark X mbili, moja ikiwa ina elekea Kawe na moja ina tokea Kawe na zote ni nyeusi”

“Hiyo inayo elekea Kawe”

Josephine alizungumza na kijana huyo akaanza kuivuta karibu gari hiyo kwa kutumia Kamera zilizo fungwa kwenye kila nguzo ya barabara hiyo. Waka iscan gari hiyo na kuona ndani ikiwa na watu wawili wote wakiwa ni wanaume.

“Hao ndio wana husika muheshimiwa”

Josephine alizunguzma huku akitazama watu hao wanao endesha gari hilo kwa mwendo wa kasi sana. Raisi Mtenzi akapiga simu kwa RPC bwana Karata na kumpa agizo la kuhakikisha wana izuia gari hiyo.

***

“Hei hichi kizuizi vipi?”

Kijana mmoja alizungumza mara baada ya kuona mbele kuna kizuizi cha gari tatu za polisi zikiwa zime ifunga barabara.

“Hata sielewi mwanangu”

“Wana silaha jamaa yangu na ina onyesha wana tuhitaji sini”

Kijana huyo anaye endesha gari hilo alizungumza huku akipunguza mwendo na mwishowe akasimamisha gari hilo.

“Hatuwezi kukamatwa”

Kijana aliye kaa siti ya pembeni alizungumza huku huku akichomoa bastola yake kiunoni. Gafla gari mbili nyingine za polisi zikasimama nyuma yao na kuwaweka katikati.

“Wama tambua ni sisi”

“Poa hapa ni kufa kiume”

Wote wakachomoa bastola zao kisha wakaanza kushambulia gari za polisi zilizopo mbele yao.

“Musifyatua risasi”

Mkuu wa kikosi hicho cha polisi aliwaamrisha askari wake na walicho kifanya wao ni kujificha kwa maana watuhumiwa hao wata hitajika wakiwa hai. Vijana wa nabii Sanga wakaendelea kushambulia kwa risasi hadi wakajikuta risasi zikiwaishisa. Askari walipo sikia ukimya wa sekunde arobaini na tano wakatambua kabisa kwamba risasi zime waishia majambazi hao. Askari walio nyuma ya gari hilo wakaanza kunyata kwa umakini huku mikononi mwao wakiwa wamezishika vizuri bunduki zao aina ya SMG. Askari wawili wakaisogelea vizuri milango ya gari hilo, askari hao wakashangaa mara baada ya kuwaona watu hao wakitokwa na mapovu midomoni. Wakavunja vioo vya milango ya gari hilo kwa kutimia vitako vya bunduki kisha wakawatoa watu hao ambao wame kunywa vidonge vya sumu kwa ajili ya kuficha siri ya kile walicho kifanya.

“Shitiii”

Askari mmoja alizungumza mara baada ya mmoja wa vijana hao na kukuta akiwa amesha poteza maisha.

“Vipi?”

Mkuu wao aliuliza huku akimtazama askari wake huyo.

“Wame jiua kwa sumu”

“Duu, wasachini muangalie kama wana simu au kitu chochote ambacho kina weza kuleta ushihidi”

“Sawa”

Askari wanane wakavaa gloves nyeupe mikononi mwao na kuanza kuwapapasa watu hao kwenye mifuko yao na kwa bahati mbaya hawakukuta simu wala kitu chochote ambacho kina weza kuwawezesha kwenye upelelezi wa kufahamu ni nani aliye nyuma ya tukio la mauaji ya SIA Kamara.

***

Nabii Sanga akamvuta Tumaini kwa mkono mmoja hadi taulo alilo jifunga kiunoni mwake, likamuanguka. Akamsimamisha mbele yake huku akimtazama kwa macho makali yenye hasira mithili ya simba aliye yeruhiwa kwa mikuki ya wawindani. Akamuwekea bastola ya paji lake la uso huku mwili ukimtetemeka, mchungaji Smith akatamani kuzungumza jambo ila akajikuta akishindwa kutoka na hasira kali ya nabi Sanga. Mrs Sanga alitamani arthi ipasuke na imeze ila hilo halikutokea. Nabii Sanga akamtazama Tumaini ambaye kwa muonekano bado ni kijana mdogo sana na ambaye ana amini kwamba sio yeye aliye mfwata mke wake. Akamsukumia Tumaini kwenye sofa na kumgeukia mke wake.

“Ni nini ambacho ume kosa kwangu wewe mwanamke?”

Nabii Sanga alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Leo hii una tembea hadi na watoto hawa wadogo. Huyu mbona hata Julieth wetu hamfikii kwa umri, eheee?”

Mrs Sanga alikaa kimya huku akilia kwa uchungu, kipindi alipo fumaniwa na Tomas alimuahidi mume wake kwamba hato weza kurudia tena kosa hilo ila leo hii ame fanya kosa hilo hilo.

“Niambie au ni utumishi wangu ndio una hisi kwamba una utumia kama ngao ya kuniumizia. Juzi tume toka kwenye misiba ya vijana wetu. Leo hii ume ona uniumize zaidi na zaidi”

Nabii Sanga alizungumza maneno ambayo hakutaka mchungaji Smith amjue ni mtu wa aina gani. Laiti kama angekuwa yupo peke yake basi ange hakikisha kwamba ana mfanyia kitu kibaya kijana huyo.

“Pesa nina kupa, tuna kila aina ya mali hapa duniani. Niambie nikupe roho yangu si ndio?”

“M…u…u….m….e…..me…..wang…..”

Mrs Sanga alishindwa kabisa kuzungumza kutokana na aibu iliyo mjaa. Hakuamini kama angeweza kufumaniwa kwa mara nyingine.

“Mchungaji ndo ni mzigo. Sisi tunao simama kila siku madhabahuni mwa Mungu na kuwaimiza watu waishi vizuri kwenye ndoa zao, ila sisi malipo yetu ndio haya. Sijui kwa nini Mungu ana nipitisha kwenye kipindi kama hichi”

Tumaini akazidi kuogopa sana mara baada ya kuikumbuka vizuri sura ya nabii Sanga. Ni mchungaji ambaye mara nyingi ana muona kwenye baadhi ya clips za youtube na whatsapp akitoa mafunzo mbalimbali ya kindoa na maisha.

“Kijana hongera kwa kuona utupu wa mke wangu. Vaa nguo zako na uondoke”

Tumaini hakutegemea kupata msamaha kama huo.

“Una shangaa nini, vaa ondoke nita kuzaba makofi”

Mchungaji Smith naye alizungumza kwa ukali na kumfanya Tumaini kusimama, akaokota jinzi yake sehemu alipo kuwa ameitupa na kuivaa. Akachukua tisheti yake, simu pamoja na begi lake la nguo na kuanza kuelekea mlangoni.

“Kijana simama”

Nabii Sanga alizungumza kwa sauti ya mikwaruzo na kumfanya Tumaini kusimama huku akitetemeka.

“Mke wangu alikuahidi nini na nini?”

“Ehee?”

“Alikuahidi kukupatia nini na nini?”

“Du…u….k….a”

“Una akaunti ya benki?”

“Ehee???”

“Una akaunti ya benki?”

“Hapana ila nina tigo pesa”

Nabii Sanga akatoa simu yake mfukoni na kuingia kwenye upande wa kuhamisha pesa.

“Nitajie namba yako?”

Tumaini akaanza kutaja namba yake huku akiwa na wasiwasi mingi sana.

“Nime kuingizia milioni tano. Nenda kafungue hilo duka na ole wako utos siri hii, maisha yako yatakuwa halali yangu”

Mrs Sanga macho yakamtoka kwa mshangao. Akajaribu kulinganisha matukio ya kipindi amefumaniwa na Tomas na tukioa hili, akahisi lazima kuta kuwa na jambo kwa maana hakuna mwanaume hata mmoja duniani ambaye ana weza kumkamata mtu anaye kula utamu wa mke wake kisha akampatia kiasi hicho cha pesa.

“Nashukuru”

Tumaini baada ya kuzungumza hivyo akatoka chumbani hapo. Kitendo cha kuufunga mlango huo, akatimua mbio na kuondoka hotelini hapo huku akiwa haamini kama ile bastola aliyo kuwa amewekewa usoni mwake haija muondoa maisha yake.

“Mchugaji nina kuomba unisubiri hapo nje”

“Sawa mkuu”

Mchungaji Smith akatoka ndani hapo na nabii Sanga akamtazama mke wake ambaye muda wote hana hata cha kujitetea kwa maana ame mkamata na ushahidi kamili.

“Vaa nguo zako”

“Ehee?”

“Vaa nguo zako turudi nyumbani mke wangu”

Mrs Sanga taratibu akashuka kitandani hapo na kuelekea bafuni huku akiwa haamini juu ya matendo hayo anayo yaonyesha mume wake. Akamaliza kuoga na kurudi chumbani, akavaa nguo zake kisha akakusanya kila kilicho chake na wakatoka ndani hapo.

“Mtumishi nina shukuru sana, acha sisi turudi Dar es Salaam”

“Usiku huu?”

“Ndio”

“Hapana mkuu, una onaje ukakaa kwenye hoteli nyingine hadi asubuhi ndio muondoke?”

“Hapana kuna mambo ambayo asubuhi nina hitaji kuyafwatilia. Hivyo nina kuomba sana ndugu yangu niweze kwenda”

Mchungaji Smith akamtazama nabii Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa ikiwa ni ishara ya kukubaliana na hilo ambalo mkuu wake huyo wa kanisa ana muambia. Hakika alimuona nabii Sanga ni mtu wa tofauti kwani hata kama ni yeye angemkuta mke wake, basi ange mchangamsha na makofi kadhaa. Moyoni mwake, chuki dhini ya mrs Sanga ikamtawala. Hapo awali aliweza kumuona ni mama mwema na wakuigwa na wanawake wengine katika kanisa hilo, kumbe ni mchafu. Wakaagana na mchungaji Smith kisha nabii Sanga namke wake wakingia kwenye gari la mke wake na kuianza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam huku mrs Sanga moyoni mwake akiwa amejawa na wasiwasi ambao hakujua ni kitu gani ambacho mume wake angekwenda kukifanya wakifika jijini Dar es Salaam.

***

Jery akamtazama mke wake ambaye amejilaza pembeni yake. Akamshika kiuno chake taratibu ila Julieth akajigeuzia ukutani akionyesha kuto hitaji kufanya jambo lolote kwa wakati huo.

“Mke wangu huku nipa jibu juu ya kutafuta mtoto?”

“Mume wangu, tuta zungumza hilo sio swala la kukurupuka”

“Ahaa sio swala la kukurupuka?”

“Ndio”

Jery akashusha pumzi huku akimtazama Julieth ambaye hapo awali aliamini kwamba ame pata bonge la mke wa ndoa kumbe ni balaa tupu.

“Hivi Julieth una nichukuliaje mimi?”

Jery alizungumza kwa hasira huku akikaa kitako. Kitendo hicho kikamfanya Julieth kugeuka na kumtazama kw amshangao.

“Kivipi mume wangu”

“Kivipi au uliolewa na mimi kwa ajili ya jambo fulani kwenye maisha yako au?”

Jery aliendelea kuzungumza kwa hasira na sentensi hiyo kidogo ika mstua Julieth.

“Kwa maana kama ni mahari kwenu sidaiwi hata shilingi mia moja, nime kuoa kwa harusi ya kifahari. Leo hii nina kuambia swala la kuzaa una anza kuingia huku na kule. Kama ume kuja kwenye familia hii tambua hukuja kutembea na kushangaa ofisi za hapa ikulu. Ume kuja kuwa mke wangu na kunizalia watoto. Familia yangu ni ndogo sana, mama yangu amekufa, kaka yangu ame kufa. Nipo mimi na baba, je mmoja wetu akifa au tukifa wote si tutakuwa tumeisha. Sasa jifikiria, kama upo tayari kuzaa na mimi, nijibu, kama haupo tayari kuzaa na mimi pia uzungumze. Umenielewa?”

“Mume wangu unavyo zungumza hivyo una kosea?”

“Nina kosae nini, nina zungumza kama haki yangu kwamba nina taka mtoto ndani ya familia yangu ume nilewa?”

“Ndio”

Julieth alijibu huku akiwa na wasiwasi kidogo.

“Jambo jengine, sitaki urudie kufanya ulicho kifanya”

“Sija kuelewa mume wangu”

“Uta nielewa siku ambayo nita kukamata”

Julieth akajawa na mshangao kiasi cha kumfanya akae kimya huku akimtazama mume wake.

“Ume nielewa?”

“Ila Jery ni heri unge kuwa muwazi kwenye hilo jambo lako”

“Una penda niwe muwazi si ndio?”

“Ndio mume wangu, hiyo ndio misingi ya ndoa yetu”

“Ni hivi, sitaki uingie tena Facebook na kutazama picha za yule fala wako. Endapo siku nyingine nika gundua kwamba bado una mfwatilia nita kufanya kitu ambacho huja wahi kufanywa kwenye maisha yako. Kama bado una mpenda na kumtamani, basi usinge kanyaga hapa ikulu ume nielewa?”

Jery alizungumza huku jasho likimwagika mwili mzima kwa hasira. Julieth mwili mzima ukaanza kumtetemeka.

“Na jambo jengine usijaribu tena siku nyingine kuni danganya kwa kuni weka BIKRA FEKI ya kupandikizwa na madaktari, ume sahau kwamba mimi ni dokta. Usiku mwema”

Jery mara baada ya kuzungumza hivyo akashuka kitandani hapo na kutoka chumbani hapo huku akiwa amevaa boksa tu na kuelekea sebleni na kumuacha Julieth mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi huku naye akitamani ardhi impasuke immeze kwani si kwa aibu hiyo.



Julieth akatamani kushuka kitandani na kumfwata mume wake sebleni, ila akashindwa kwa maana uongo wote alio kuwa ameutengeza yeye na familia juu ya bikra yake leo hii Jery ame weza kuufahamu, isitoshe amagundulika alikitazama picha za Evans Shika mwanaume ambaye bado moyoni mwake ana mpenda japo kuwa alimuacha kutokana na kuheshimu penzi lake la kale. Julieth akatamani kumpigia baba yake na kumueleza hali hiyo ila akashindwa akihofia kwamba Jery ana weza akawa ana msikiliza mlangoni hapo. Gafla mlango ukafungulia na Jery akaingia ndani hapo, moja kwa moja akapitiliza hadi kabatni, akafungua na kutoa pensi yake pamoja na tisheti. Akafungua kabati la viatu na kutoa kobazi anazo zipenda kuvaa na kutoka ndani hapo pasipo kumuongelesha chochote Julieth anaye endelea kumwagikwa na machozi.

“Upoa wapi?”

Jery alimuuliza Devid kwa kutumia simu yake.

“Nime pumzika mkuu”

“Nahitaji uniepele sehemu sasa hivi”

“Wapi tena”

“Wewe njoo kwenye maegesho ya magari”

“Sawa”

Jery akakata simu huku kifua chake kikiwa kina chemka kwa hasira. Baada ya dakika tano Devi akavika huku akichomeka vizuri Shati lake lenye rangi nyeupe, akaichomeka bastola yake vizuri kiunoni na kuvaa koti lake la suti kisha akaingia ndani ya gari analo litumia Jery.

“Vipi tena mbona muda huu?”

“Nime mchana makavu yule demu”

“Nani?”

“Si mke wangu”

“Mke wako ndio una muita demu rafiki yangu?”

“Ahaa ni demu ndio, kwa maana nina pata shida, ni kwa nini anidanganye juu ya bikra feki. Kama unavyo nifahamu ni kwamba huwa siwezi kuweka kitu moyoni ndugu yangu, ndio maana nime amua kumpa makavu yake”

“Sasa yeye ume msikiliza?”

“Azungumze nini amekaa kimya na kulia lia huku akitetemeka. Sina hamu ya kulala kabisa ndani hapa. Hembu nipeleke kule kwenye ile nyumba”

“Ila ni usiku sasa hivi?”

“Wewe twende una ogopa nini?”

“Ume muaga mzee?”

“Mzee hana haja ya kuagwa kwa maana mimi ni mtu mzima na nina maisha yangu sasa hivi. Hivyo nina amua kufanya ninacho kiona ni sahihi kwenye maisha yangu”

Majibu ya Jery yakamfanya Devi kukubali kishingo upande japo ana tambua kwamba endapo kuta tokea tatizo lolote juu ya Jery basi yeye ndio atakaye wajibishwa. Taratibu wakaanza kuondoka eneo hilo la ikulu huku Jery akiwa kimya kabisa. Akamkumbuka Shani, akatoa simu yake mfukoni na kuiandika namba ya Shani na kumpigia, simu ya Shani ikaanza kuita hadi ikakata.

“Una mpigia nani?”

“Yule demu”

“Yupi tena?”

“Yule mfanya usawi wetu”

Jery alizungumza huku akiiweka tena simu hiyo sikioni mwake. Simu ya Shani, ikaita kwa sekunde kumi na tano kisha ikapokelewa.

“Haloo”

Shani alizungumza kwa sauti iliyo jaa uchovu wa usingizi.

“Upo wapi?”

“Mmmmm”

“Upo wapi?”

“Nipo nyumbani kwangu.Jery?”

“Ndio ni mimi”

“Nipo kwangu”

“Nielekeze nina hitaji kuja sasa hivi kukuchukua”

“Usiku huu!!?”

“Ndio, mbona una shangaa au vibaya?”

“Hapana, ila naona muda ume kwenda sana”

“Ndio ila nina hitaji kuja kukuchukua jiandae kabisa”

“Sawa”

Shani akamuelekeza Jery sehemu anapo ishi na kutokana Devi ni mwenyeji na eneo hilo la Kimara, haikuwawia ugumu kufika katika nyumba hiyo. Jery akapiga simu tena na Shani akatoka huku akiwa amesha jiandaa japo hafahamu ni wapi anapo elekea. Akapanda na kukaa siti ya nyuma ya gari.

“Habari zenu”

Shani alisalimia huku akiwa na aibu kidogo.

“Salama”

Devi pekee ndio aliitikia, ila Jery muda wote alikuwa kimya huku akiwazia ni jinsi gani atakavyo fanya kuhakikishaana mtoa Julieth kwenye maisha yake.

“Jery habari yako”

“Salama, Devi twende kule”

“Sawa”

Safari ya kuelekea Mbezi Luis ikaanza wakafika katika jumba ambalo Jery amelinuna.

“Tunaweza kushuka”

Jery alimuambia Shani huku akimtazama. Kabla hawajashuka Jery akazima simu yake kuepuka usumbufu. Wakaingia ndani huku wakimuacha Devi kwenye gari kuhakikisha ana imarisha ulinzi wa eneo hilo.

“Hapa ni kwako?”

“Ndio, uta kuwa una ishi hapa”

“Mimi!!?”

“Ndio”

“Na mke wako je?”

“Hayo mambo ya mke wangu sitaki kuyasikia ukiwa na mimi”

Jery alizungumza kwa ukali kidogo na kumfanya Shani kukaa kimya kwa sekunde kadhaa. Akakumbuka aliweza kumshuhudia Jery akiwa na hasira na dawa ya pekee aliyo ifanya ni kumkumbatia na hasira zake yanyuka mithili ya barafu. Shani pasipo kuzungumza kitu chochote, kwa haraka akamkumbatia Jery kwa nguvu na kuanza kuyasikilizia mapigo yake ya myo yanavyo muenda kasi. Hasira na chuki yote iliyo kuwa ndani ya moyo wa Jery ikaanza kuyayuka taratibu hadi akarudi katika hali yake ya kawaida. Taratibu wakatazamana, Jery akayashika mashavu ya Shani kwa viganja vyake viwili kisha tartaibu akaanza kuzinyonya lipsi zake msichana huyo aliye barikiwa uzuri wa kipekee. Shani hakuwa na kipingamizi zaidi ya kupokea denda hilo la Jery na wakaanza kugonganisha ndimi zao, zilizo wafanya wapandwe na hisia kali sana. Wakaanza kuvuana nguo huku kila mmoja akiwa katika shahuku kubwa ya kutaka kufanya mapenzi. Jery akamlaza Shani juu ya sofa na kuendelea kumnyonya maeneo mbali mbali ya mwili wake, alipo hakikisha amemuandaa vya kutosha akaanza kumpa penzi takatifu, ambalo lilimfanya Shani na yeye kuonyesha ujuzi wake wote kuhakikishakwamba ana mpagawisha mwanaume huyo ambaye tayari amesha zama moyoni mwake.

***

Magreth mara baada ya kumrudisha mtoto wa Sia Kamara nyumbani kwao, moja kwa moja wakaelekea eneo la mlipuko wa gari na kukuta tayari magari ya zima Moto pamoja na vikosi vya polisi vikiwa vime kusanyika eneo hilo huku barabara ikiwa ime fungwa. Samson pekee ndio ana kitambulisho kinacho muwezesha kuingia katika utepe huo wa polisi ulio andikwa kwa maandishi ya rangi nyeusi ‘NO CROASING’.

“Nani ni kiongozi hapa”

Samson alimuuliza mmoja wa askari mara baada ya kuonyesha kitambulisho chake kwa askari huyo na kuruhusiwa kuingia kwenye utepe huo wenye rangi ya chugwa iliyo kolea.

“RPC yupo pale”

Samson akamfwata RPC Karata ambaye ana wasimamia vijana wake katika kupima jinsi shambulizi hilo la bomu lilivyo tokea.

“Shikamoo kaka”

“Marababa dogo vipi mbona hapa muda huu?”

“Nime kuja na Magreth. Raisi ame tuagiza hapa”

“Yupo wapi? Muambie aingie”

RPC Karata alizungumza huku akiangaza angaza huku na kule na akampatia ishara Magreth ya kuingia katika utepe huo na askari wengine hawakuweza kumzuia.

“Kaka za masiku”

“Salama aisee. Tume poteza mtu muhimu sana kwenye vitengo vyetu vya usalama”

“Poleni sana, hivi mume weza kupata chochote kutoka kwake?”

“Kila kitu kime ungua, yaani tulivyo fika hapa tulikuta majivu tu. Wewe mwenyewe una shuudia gari lake jinsi lilivyo ungua?”

RPC Karata alizungumza huku akimuonyesha Magreth la Sia Kamara.

“Aisee ina tisha sana. Mabaki ya mwili wake yapo wapi?”

“Tumesha yapeleka Mochwani ya Muhimbili”

“Sawa sawa”

Simu ya upepo ya RPC Karata ikasikika sauti ikizungumza kwamba wamefanikiwa kuwapata wahusika walio tegesha bomu kwenye gari la Sia Kamara ila wameweza kumeza vidonge vya sumu na kufa kabla ya kukamatwa na polisi.

“Wapi hiyo ime tokea?”

Magreth aliuliza kwa shahuku huku akimtazama RPC Karata usoni mwake.

“Afande mupo wapi kwa sasa? Over”

“Tupo hapa Kawe bado mkuu. Over”

“Basi nina kuja hapo sasa hivi. Over”

“Sawa mkuu”

Magreth na Samson wakakimbilia kwenye gari walilo jia hapo eneo la tukio na kuanza kuongozana na gari la RPC Karata kuelekea kwenye eneo la Kawe. Hawakuchukua dakika nyingi barabarani, wakafika eneo la tukio na kukuta askari wengi wakiwa wana imarisha ulinzi katika eneo hilo. Wakashuka kwenye magari na kuelelekea aneo hilo. Askari wakampigia saluti RPC Karata kwa maana ndio mkuu wao wa kazi kwa hapa Dar es Salaam.

“Ime kuwaje?”

“Kama tulivyo pewa agizo, hatukuwashambulia kwa risasi, japo wap walitushambulia kwa risasi tulicho kifanya sisi ni kujihami tu. Ina onekana walikuwa na uhaba wa risasi hivyo waliweza kuishiwa, tulivyo wanyatia tukawakuta wakimwagikwa na povu. Tulivyo jaribu kuwawahi, ila hatukufanikiwa mkuu”

Mkuu wa kikosi hicho alizungumza huku akimtazama RPC Karata usoni mwake.

“Simu au kidhibitisho chochote kinacho waonyesha wao ni wahusika wa tukio, je mume weza kupata?”

“Hapana mkuu, hatujakuta simu wala kitu chochote”

“Mume pekua gari hilo vizuri?”

Magreth aliingilia mazungumzo hayo huku akimtazama askari huyo.

“Ndio tume kagua kila eneo ila hatuja weza kupata kidhibitisho chochote.”

Magreth akachuchumaa pembeni ya maiti za vijana hao huku akiwachunguza kwa umakini sana. Vijana hao wenye asili ya kiarabu kidogo wakamzidi kuliweka jambo hilo la Sia Kamara katika wakati mgumu, isitoshe Josephine alimuambia kwamba walio mteka ni wazungu.

“Maiti zao muzichukue na muzipelekea Muhimbili, gari lao mulipeleke Central kwa ukaguzi zaidi”

“Sawa mkuu”

“Ngoja kwanza”

Magreth alizungumza huku akimtazama RPC Karata.

“Naombeni Gloves”

Magreth akakabidhiwa glovers nyeupe na akaziva mikononi mwake. Akachuchumaa tena na kuanza kufungua vifungo vya mashati ya vijana hap na kuwakuta wakiwa na tattoo(michoro) ya uwa jeusi aina ya ROSE. Alama hizo zipo katika vifua vyao eneo la kushoto.

“Hii ni chapa yao”

Magreth alizungumza huku akitazama alama hizo taratibu.

“Samson hembu piga picha hizi alama”

Samson akatoa simu yake mfukoni na kuanza kupiga picha michoro hiyo ya hao vijana. Magreth akamgeuza kijana mmoja na kumtazama maeneo ya mgongoni mwake na hakuweza kuona chochote. Akamgeuza kijana wa pili na kumchunguza na yeye hakuweza kuona kitu chochote.

“Vipi ume maliza?”

RPC Karata alimuuliza Magreth mara baada ya kumuona akinyanyuka huku akivua gloves hizo.

“Sijamaliza bado, ina bidi niende nazo mochwari hizi maiti. Haiwezekani wakawa hawana simu au kifaa chochote cha mawasiliano. Inavyo onyesha ni kundi kubwa la watu ambao wana mtandao mkubwa. Na wamejia kwa ajili ya kuficha siri ya mtandoa wao. Laiti ingekuwa ni wahalifu wa kawaidaa basi wangekubali kukamatwa na wangejua mbele ya safari kinacho kwenda kuwatokea”

“Hapo na mimi nina anza kupata picha. Nime fanya kazi hapa Tanzania ya kudili na wahalifu, sasa ni mwaka wa ishirini na tatu sijawahi kuona muhalifu akimeza kigonge cha sumu na kumuua haraka kama hivi”

Kiongozi wa kikosi hicho cha polisi alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Miili hiyo ikapakizwa kwenye defender ya polisi na safari ya kuelekea Muhimbili ikaanza huku, Samson na Magreth wakiwa katika msafara huo.

***

Simu ya nabii Sanga ikaanza kuita, akamtazama mke wake kwa jicho la hasira kidogo kisha akaitoa mfukoni mwake na kutazama jina la anaye mpigia. Akakuta ni kijana wake, akaipokea na kuiweka sikioni huku akipunguza mwendo kasi wa gari lake.

“Ndio”

“Mkuu tume fanikiwa kumuondoa duniani Sia Kamara”

“Safi sana ila si hakuna ushahidi?”

“Ndio, ila vijana nilio watuma nao wameweza kujiua”

“Kwa nini?”

“Walizingirwa na polisi. Hatukujua ilikuwaje mpaka polisi wakawajua, amri ya mwisho nilio weza kuwaambia ni kuhakikisha wana meza vidonge vya sumu na wana jiua.”

“Shitii, je simu zao zipo wapi kwa maana zikikamatwa si zina weza kutuletea matatizo”

“Ndio, ila hawakwenda na simu?”

“Walikwenda na nini?”

“Vinasa sauti ambayo walisha vivunja na hakuna chochote ambacho kita wawezesha kujua ni nani ambaye aliwaagiza”

“Ni jambo zuri. Sasa kama kawaida. Atakaye fia kazini familia yake iweze kuingiziwa dola milioni moja”

“Sawa mkuu nina fanya hivyo kwa maana wame kuwa ni waaminifu kwenye kazi yetu”

“Hakuna shaka. Juu ya makamu wa raisi wa marekani nita waambia nini cha kufanya kukipambazuka”

“Sawa muheshimiwa, usiku mwema”

“Nawe pia”

Nabii Sanga akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake. Akaendelea kukanyaga mafuta ya gari hilo ambalo hakika lina kwenda kwa kasi, kiasi kilicho mfanya mrs Sanga kujawa na wasiwasi wa kifo kwa maana endapo wata pata ajali basi wata kufa vibaya sana.

“Baba J punguza mwendo ni Wami hapo”

Mrs Sanga alizungumza huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana kwa maana kuna daraja la Wami ambalo ni jembamba sana na lina pitisha gani moja kwa wakati mmoja kwani magari mawili hayawezi kupishana katika eneo hilo. Nabii Sanga hakujibu chochote zaidi ya kuukaza mguu wake ambao umekanga pedeli ya gari hiyo na kuufanya mshale unao soma spidi mita kuhama kutoka mia mbili na ishiri na kuelekea miambili na arobaini. Wakiwa katikati ya daraja hilo, lori moja la mizigo ambalo lime feli breki nalo likaanza kushuka kwenye kiporomoko chakuelekea kwenye daraja hilo na endapo gari hilo zitakutaka katikati ya daraja hilo basi zita gongana uso kwa uso ita sababisha gari la nabii Sanga kupondwa vibaya sana, kwanza ni kutokana na mwendo wa kasi pili ni udogo wa gari hiyo ukilinganisha na ukubwa wa lori hilo aina ya Scania lililo sheheni matanki mawili makubwa yaliyo jaa mafuta aina ya Petroli.


Nabii Sanga akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari lake na kumfanya dereva wa lori kujikuta akikunja kona iliyo pelekea lori hilo kuanza kuelekea kwenye kiporomoja kilichopo pembezoni mwa daraja hilo na kikaanza kutangulia kichwa cha lori hilo kudumbukia kwenye mto huo mkubwa ambao una sifika una kina kirefu kwenda nchini pia na uwepo wa mamba wakali sana. Mlipuko mkubwa wa gari hilo haukumfanya nabii Sanga kupunguza mwendo au kusimama kutazama, alicho kifanya ni kuushikilia mskania wake vizuri huku naye akiyasikililizia mapigo yake ya moyo yanavyo kwenda kwa kasi kwani laiti ingekuwa sio kujichanganya kwa dereva huyo wa roli basi sasa hivi wangekuwa katika hali nyengine. Mrs Sanga alikaa kimya huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake, hakuamini kama wame weza kuvuka kwenye kifo hicho.

Majira ya saa tisa usiku wakaingia jijini Dar es Salaama na hawakuwa na sehemu yoyote ya kupitia zaidi ya kufika nyumbani kwao. Wakashuka kwenye gari huku nabii Sanga akiliacha gari hilo likiendelea kunguruma. Nabii Sanga akamtazama mke wake anaye tembea kwa uchovu huku akijivuta vuta kuelekea ndani akiwa na mashaka mengi sana.

‘Nitakacho kufanya wewe malaya uta juta kuolewa na mimi’

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake kwa macho yaliyo jaa hasira ali sana. Nabii, Sanga akakumbuka jambo moja alicho kifanya ni kuitafuta namba ya kijana wake.

“Ndio mkuu”

“Kuna meseji ya tigopesa nina kutumia hapo. Mtafuteni huyo niliye watumia pesa na hakikisheni mukimpata muna mkamata na kumuweka hadi nitakapo muona. Mume nielewa?”

“Ndio”

“Usiku mwema”

Nabii Sanga akakata simu na kuingia ndani kwake. Akamkuta mke wake akiwa amekaa sebleni huku amejiinamia, nabii Sanga hakumsemesha chochote zaidi ya kupandisha ngazi na kuelekea gorofani kilipo chumba chao.

***

“Muna weza kuingia”

Muhifadhi maiti wa hospitali ya Muhimbili, alimuambia RPC mara baada ya maiti hizo kuingizwa ndani ya chumba hicho.

“Ahaa mimi siingii”

Samson alizungumza huku akiwa ametawalaiwa na woga kwa maana hadi kumuona mtu ana ingi ndani ya chumba hicho basi utambue ana moyo wa kijasiri sana.

“Huja jua chochote juu ya hiyo michoro ya mauaa?”

Magreth aliuliza huku akimtazama.

“Hapana”

“Poa baki hapa”

Magreth na RPC Karata wakaingia ndani ya jengo hilo. Wakapelekewa hadi sehemu maiti hizo zilipo lazwa zikisubiria kuingizwa kwenye mafriji ili zisiharibike. Wakafungua mashuka hayo na kukuta wakiwa uchi kabisa, wakavaa gloves na kuendelea kuzikagua.

“Ila kwa nini wame muua Sia Karata?”

RPC Karata alizungumza kwa maana haelewi ni jambo gani linalo endelea.

“Yaani wewe acha tu”

“Una fahamu sababu?”

“Ndio”

“Ehee ni sababu gani?”

“Josephine alitekwa tukiwa kanisani kwa nabii Sanga”

“Weee?”

“Ndio, ila nilivyo fanya upelelezi wangu wa kina nikatambua kabisa kwamba Sia Kamara ana husika na kutekwa kwa Josephine. Nilicho kifanya nikamtekamwanaye, na nika mueleza ukweli kwamba nime mteka mwanaye”

“Ehee ikawaje?”

“Josephine aliachiwa siku hiyo hiyo baada ya Sia Kamara kufahamu kwamba mwanaye ametekwa.”

“Duu sasa kwa nini ame mteka?”

“Sijajua na Josephine ana dai kwamba alipelekwa kwenye meli ambayo meli hiyo ina wazungu na watu wa mataifa mchanganyiko ila wenye uwasili wa weupe tu. Sasa Kama unavyo wauaji wana asili ya Asia, sasa hapa ndipo tunapo pata kizungu mkuti ni nani ambaye alimtuma Sia Kamara”

“Ulisema ame tekwa akiwa kanisani kwa nabii Sanga?”

“Ndio”

“Mmmm”

“Mbona una guna?”

“Kumuhisi mtu sio jambo zuri ila ninavyo hisi nabii Sanga ata kuwa ana husika?”

“Hapana kwa maana nili muhoji na nina mjua yule mzee vizuri kama unavyo tambua kwamba nilikuwa nina mahusiano naye ya kimapenzi, hivyo kwa asilimia kadhaa nina hisi kwamba hajahusika”

“Magreth una weza kumjua nabii Sanga kwa utandani ila uka shindwa kutambua mambo yake.Ile familia ni watu wabaya sana, wapo kufanya chochote, ikiwa kutumia pesa kwa ajili ya kufanya wanacho kitaka. Ninapo kumbuka hili swalala la kutekwa kwa Josephine, tena akatumia kiongozi mkubwa ndani ya kitengo cha NSA. Ina nikumbuka tukio langu la nyuma. Nabii Sanga aliweza kunilipa pesa nyingi sana kwa ajili ya kumtorosha Tomas mahabusu. Ila lile jambo raisi aliweza kulifahamu, ilisalia kidogo raisi anifukuze kazi. Kuanzia siku hiyo nilijitenga na yule mzee na nikamchukia sana kwa maana nilimfichia siri yake ambayo kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni shuhuli kubwa sana.”

“Ila yule Tomas si alikuwa na mahusiano na mke wake?”

“Ndio, ni the same na wewe angekuja kunilipa mrs Sanga ili nikuteke au nikupakazie kesi yoyote. Ume nielewa hapo”

“Yaa kwa hiyo huwa wana watumia viongozi wa vitengo vya usalama?”

“Ndio tena wana watumia sana”

“Sasa kwa nini amteke Josephine ikiwa hana bifu naye ni muumini wake na yeye ndio alimpigia simu ili aweze kwenda kwenye kongamano la kuiombea nchini. Hivyo sioni doti yoyote ya kuunganisha kwamba nabii Sanga ana husika katika hilo”

“Sawa”

“Ila nina hisi ni Wamarekani”

“Kwa nini Wamarekani?”

“Kwanza nahisi wamesha anza kuutambua uhusika kwa Josephine, hivyo waliweza kumtumia Sia Kamarakatika kumteka ili kukamilisha mambo yao ikiwema kutafuta baadhi ya adhini ambayo ipo nchini Tanzania, ndio maaana una ona kwa sasa uhusiano wetu na nchi yao ume yumba”

“Ila kesho makamu wao wa raisi ana kuja?”

“Ndio ana kuja nahisi kuna mambo yana ingiliana hapo. Yaani nilikifikiria jambo hili nina hisi kichwa changu kuchanganyikiwa kwa maana asubihi ya siku ambayo Josephine anatekwa nini imani uliwez kusikika kwambakuna mtu alikuwa ana hisiji kuniua?”

“Yaa niliipata ile bahari pole ssana”

“Nashukuru, na yule anaye taka nikiua ni jasusi kutoka Kenya, alikuwa ana fanya kazi katika jeshi la Kenya ila akastafu. Yaani bado nina pata tabu tupu kulitafakari jambo”

“Tuyaache kama yalivyo. Ina bidi uende kupumzika sasa ni usiku na muda umwe kwenda sana”

RPC Karata alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Wakatoka katika jengo hili paasipo kupata ushidhi wowote. Samson na Magreth wakarudi ikulu na wakamtaarifu raisi Mtenzi kwamba hawajapata chochote katika waty hapo.

“Poleni kwa kazi ndefu, hivyo pumzikeni, kesho nita kuwa bize kuwapokea viongozi wa mataifamengi hivyonina waomba muweze kupumzika tuta kutana kesho kutwa kanisani kwenye sala ya kumuombea mke wangu na makamu wa raisi”

“Sawa muheshimiwa”

Josephine, Magreth na Samson wakaondoka ikulu, wakampitia Samson nyumbani kwake kisha wakaelekea nyumbani kwa Magreth. Hapakuwa maongezi mengi kwani kila mtu ame choka sana na uchovu wa mishemishe ya siku mbili mfululizo kila mmoja akapitiliza ndani kwake na kulala.

***

Ulinzi wa nchi ya Tanzania, hususani kaytika jiji la Dar es Salaama ukazidi kuimarishwa. Vikosi vya makomandoo wa nchi ya Tanzania kutoka miko mbalimbali, wakachukua nafasi ya pekee katika kulinda maeneo maalumu ambayo viongozi wa mataifa mbalimbali wata fikia. Viongozi wengi kutoka mataifa mbalimbali wakazidi kumiminika huku kazi ya raisi Mtenzi ikiwa ni kuhakikisha ana wapokea katika uwanja wa mwalimu J.K Nyerere.

Jery akaingia sebleni na kumkuta Julieth akiwa ana tazama tv huku akiwa hana furaha kabisa usoni mwake. Akaka kwenye moja ya sofa huku akitazama jinsi baba yake anavyo salimiana na raisi wa Ghana aliye fika uwanjani hapo. Jery akachukua rimoti juu ya meza na kuzima tv hiyo.

“Ulilala wapi?”

Julieth aliuliza kwa sauti ya upole huku akimtazama Jery usonim wake.

“Ninapo pamjua mimi”

“Jery tambua mimi ni mke wako, sikuhitaji kumuambia baba yako juu ya hili jambo la wewe kuondoka usiku”

“Ohoo kama ulikataa kumuambia ni jambo zuri kwa maana ungeunganisha kwamba bikra yako ni feki”

“Jery Jery kwa nini una nitukana?”

Julieth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Nakutukana sasa hivi?”

“Ndio una nitukana, kwa hiyo mama yangu alinilea vibaya. Kwa hiyo alinilea na bikra feki si ndio?”

Julieth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Usijifanye una lia kinafki ume nielewa. Yaani nikukute na usichana feki, hivi ume sahau kwamba mimi ni daktari”

“Nina mashaka na udaktari wako. Kama ulijijua wewe ni daktari ni kwa nini usinge nipima kabla ya kuniua. Una kuja kunipima baada ya kuniingilia ehee?”

Julieth naye alikuja juu ili kutetea uongo wake uweze kuonekana kama ni kweli”

“Kama ume nioa kwa ajili ya kunichezea, acha niondoke zangu, nipo tayari hii ndoa ife kuliko niyanyanyasike kiasi hichi, kwetu hatuna shida na kama ni hii kazi aliyo nipa baba yako nina weza kuiacha pia na tusijihusishe na chochote kuhusiana na familia yako”

Julieth alizungumza kwa hasira huku akimkazia macho Jery, machozi yanayo mwagika hakika yana dhamiria na kudhibitisha kwamba anacho kizungumza ni kitu kinacho toka moyoni.

“Ulinikuta nikiwa katika amani yangu. Uistake kutumia cheo cha baba yako kunisanyanyasa ume nielewa. Nilikuja kwako kufwata mapenzi na si kufwata cheo wala pesa kwa maana kama ni pesa mimi nina pesa nyingi kuliko hata wewe”

Julieth mara baadaya kuzungumz ahivyo akanyanyuka na kuingia ndani kwake. Jery akajifikiria kwa sekunde kadhaakisha akamfwata ndani humu.

“Kwa hiyo ukiwa na pesa ndio una kuwa jeuri?”

Jery aliuliza kwa sauti yenye kejeli kidogo.

“Sio nina kuwa na kejeli. Sikiliza mimi sio kam wale wanawake ambao wapo tayari kunyanyasika kisa mapenzi. Hapana aisee ume kosea Jery, mimi ninamisimamo yangu kama mwanamke na nina jielewakama umeshindwa kuishi na mimi, tafadhali nina kuomba sana uniache Jery”

Julieth aliendelea kulalama kiasicha kuanza kumfanya Jery kuanza kuwa mpole.

“Nina ondoka na kurudi kwetu, sikufukuzwa na kama una hitaji kunifwata uta kuja kunichukua kwetu na kuwaeleza mume wa ndo akikasirika ana kwenda kulala nje ya ndoa yake”

Maneno ya Julieth yakaanza kuufanya moyo wa Jery kuanza kumuenda kasi huku akiwa haaminikama mke wake ana ujasiri wa kuzungumza maneno kama hayo. Julieth akachukua begi lake la nguo nakuanza kutoa nguo zilizopo kabatini na kuanza kuziweka katika begi lake hilo.

“Hei Julie ngoja kwanza”

Jery alizungumz ahuku akimshika Julieth mkono wake

“Niacheee”

Julieth akautoa mkono wake kwa nguvu huku akimkazia macho Jery ambaye bado haamini kama mke wake ni mkali kiasi hicho.

“Mimi sio mke wako tena. Mwanaume gani una shindwa kutumia akili.Tupo katikati ya matatizo, tuna hitaji kuupumzisha mwili wa mama yako, alafu wewe una fikiria kuzaa tu, si ujinga huo. Huoni huruma juu ya kupotea kwa ndugu zangu, nime baki mimi peke yangu, wewe hufikiria hayo. Unacho wazia ni bikra feki feki, basi unge kuwani Mungu unge nitengenezea bikra yenye jina lako hivyo palae unapo itoa unge ona jina lako basi”

Julieth aliendelea kuchachamaa kiasi cha kuanza kumchanganya Jery.

“Baba yangu ni mtu wa Mungu, mama yangu ni msaidizi wake. Wamenilea kwneye mazingira ya kumcha Mungu, nime jitunza hadi kwenye ndoa yangu. Alafu una kuja kuropoka tu ohoo bikra feki sijui nini, basi usinge nioa. Nime tambua kwamba Jery hunipendi, ume nipenda kwa ajili ya bikra tu.Okay nashukuru ume weza kufanikiwa kuitoa asante kwa udanganyifu wako”

“Hapana mke wangu, nina kuomba unisamehe?”

Jery alizungumza kwa sauti ya upolesana.

“Nilisha kusamehe toka ulipo anza kunikashifu”

Julieth alizungumza huku akiendelea kukusanya nguo zake na kuzipanga kwenye begi hilo.

“Mke wangu nina kuomba basi tuweze kuzungumza juu ya hili”

“Lipi?”

“Usiondoke, natambua ni wivu wangu tu ndio ume nifanya nizungumze hayo”

“Mwanaume gani ambaye humuamini mke wako. Au ulihisi kwamba mimi ni malaya wa kufuniliwa nguo na kila mwanaume, si ndio?”

“Hapana”

“Ila?”

“Hata sijielewi”

“Kweli hujielewi ndio maana manukato unayo nukia humu ndani hayapo. Jery kaam ume nichoka acha niondoke kwetu, ni heri ndoa hii ikafa kuliko ikaendelea na nikateseka kwa maaneno yaliyo jaa kejeli, dharau, vitisho na masimango. Nimechoka”

Jery alistuka sana mara baada ya kujistukia akinukia manukato ya Shani.

“Jery sijio kwa nini nilifanya haraka kuingia kwenye hii ndoa pasipo kukusoma mapema. Kumbe wewe ni malaya si ndio”

“Hapana mke wangu”

Jery alijibu kwa upole, sasa kibao kikawa kime mgeukia na mambo yame anza kuwa mabaya kwake. Julieth akafunga begi lake hilo na kulishusha kutoka kitandani na kulisimamisha chini.

“Hatujamaliza hata mwezi kwenye hii ndoa ila leo hii ume nifanyia hivi, kwa nini lakini, kwa nini wanaume wa Kitanzania muna shindwa kuwa wa kweli kwa wanawake wanao jitolea mioyo yao kwa ajili ya upendo eheee?”

“Hapana mke wangu nina kupenda sana, usinifikirie hivyo?”

“Ahaa una nipenda ehee?”

“Ndio nina kupenda sana mke wangu”

“Okay ndio maana ukaamua kwenda kunitafutia LOVE BITE hapo kwenye shingo yako ili uje kunidhihirishia kwamba wewe ni mwnaume unaye jua kutomb** sana. Nashukuru, baki na maisha yako kwa heri”

Julieth mara baada ya kuzungumza maneno hayo akaanza kuondoka ndani hapo na kumfanya Jery kukimbilia kwenye kioo, macho yakamtoka huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana kwa maana amejaa alama za kung’atwa ng’atwa shingoni mwake na tukio analo likumbuka lililo msababishia hayo yote ni pale Shani anapo fika kileleni basi alikuwa akimng’ata shingo yake huku akiamini kwamba ni furaha ya kumridhisha mwanamke huyo kimapenzi.



“Ohoo fuc** me”

Jery alijikuta akijitukana kwa maana kama ni ushahidi wa tukio hilo upo shingoni mwake. Akatoka ndani kwake na kwa haraka akakimbilia nje na kumkuta Julieth akiingia kwenye gari lake, akajaribu kumzuia ila Julieth hakuweza kukubali, wanajeshi wanao linda geti hilo la ikulu, wakamsimamisha ikiwa ni utaratibu wa gari zote zinazi ingia na kutoka ikulu ni lazima zikaguliwe kabla na baada ya kuingia. Julieth akashusha kioo chake kidogo, wanajeshi hao walipo mshuhudia ni yeye geti likafunguliwa na akaondoka. Jery akashusha pumzi huku akiwa haamini kama mzaa mzaa ume tumbua usaa. Jery akatoa simu yake mfukonina akatamani kumpigia baba yake ila akashindwa, akataka kumpigia Shani na kumtukana ni kwa nini ame mng’ata kiasi hicho, ila akatambua sio kosa la binti huyo. Mtu wa pekee aliye mkumbuka ni Devi, kabla hajampigia akastukia akiguswa bega kwa nyuma na kujikuta akistuka sana. Akageuka na kukutana na mlinzi mmoja wa baba yake.

“Mzee ameniagiza uweze kujiandaa wewe na mke wako muelekee uwanja wa ndege kwa ajili ya kuendelea kuwapoke wageni waalikiwa?”

Jery akahisi kama tumbo likimuma.

“Sasa hivi?”

“Ndio, tupo kwa ajuli ya kuwapeleka”

“Sasa fanyeni kitu kimoja, wasilianeni na askari waizuie gari ya mke wangu kwa maana tume korofishana kidogo. Peke yangu sinto weza kwenda kwa kweli ni aibu.”

“Ame elekea wapi?”

“Nina hisi kwao, ila atakuwa hajafika mbali. Fanyeni hivyo”

Simu zikapigwa kwa askari usalama barabarani wote na wakaelezewa sifa za gari wanalo paswa kulisimamisha na atakaye lisimamisha ahakikishe wana lirudisha gari hilo ikulu chini ya ulinzi mkali.

***

Moyo wa Julieth uliendelea kufukuta kwa hasira, japo na yeye ni mkosaji ila ame umia mara ya kumuona mume wake akiwa na lovebite nyingi sana shingoni mwake.

“Kwa nini ananisaliti?”

Julieth alizungumza huku machozi yakiendelea kumtiririka machoni mwake. Foleni iliyopo maeneo hayo ya posta kwa kweli inazidi kumchefua na kutamani kushuka kwenye gair hilo. Gafla kioo cha upande wake kikagongwa kidogo, akamuona askari wa usalama barabarani. Akajifuta machozi kisha akashusha kioo hicho.

“Samahani dada nina kuomba ushuke kwenye gari?”

“Nishuke kwa nini, kwani si muna leseni si hii hapa?”

Julieth alizungumza kwa ukali kidogo huku akimkazia macho askari huyo.

“Dada ni kwa ajili ya usalama wako. Shuka kwenye gari tafadhali”

Askari huyo alizungumza kwa sauti ya upole. Julieth akashangaa mara baada ya kuona askari sita wa kikiso cha FFU wakilizunguka gari lake, kitendo hicho kikamfanya kuelewa ni kwa nini askari huyo ana msisitiza kushuka kwenye gari.

“Nani ame watuma?”

Julieth aliuliza huku mapigo yake yakianza kumuenda kasi.

“Ni amri kutoka ikulu, una weza kuhamia siti ya nyuma. Sio ombi ni amri”

Askari mwengine wa kikosi cha FFU, alizungumza huku akimkazia macho Julieth.

“Dada usitushangae sana tupo kazini, tuna fanya hii kwa ajili yako. Hamia siti ya nyuma”

Taratibu Julieth akafungua mkanda wa siti yake na kuhamia kiti cha nyuma huku akiwa na mashaka mengi. Askari huyo mwenye kofia nyekundu, yenye ndembo ya jeshi la polisi, akaingia ndani ya gari, akafunga mkanda huku akipandisha kioo cha gari hilo. Gari zilizopo kwenye foleni upande lilipo gari la Julieth zikaruhusiwa, huku defender ya polisi ikianza kutangulia mbele huku ikiwa ime wajaza askari hao walio kuwa wamelizingira gari lake.

“Dada una fanya michezo ya hatari sana”

Askari huyo alilalama.

“Michezo gani?”

“Tambua kwamba wewe status yako ya kimaisha ime badilika. Huwezi kujiamulia kutoka na kwenda sehemu unayo jitakia pasipo kuwa na walinzi. Jana tu kulitokea mlipuko wa bomu na kumuua mkuu wa kitengo cha upelelezi wa NSA. Sasa hivi una toka mwenyewe, sio jambo zuri”

Askari huyo aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.

“Bomu lilipuka wapi?”

“Hapa hapa Dar es Salaam. Nchi ulinzi wake bado hujakakaa sawa, hivyo una paswa kuwa makini sister. Nina zungumza kama mshari”

Gari hiyo ya ikazidi kuendeshwa kwa kasi na wakafika ikulu. Wakamkabidhisha Julieth kwa walinzi wa ikulu, kisha askari hao wakaondoka nakurudi kwenye majukumu yao. Julieth akalitazama jengo hilo la ikulu ambalo hakika aliapia kuto kurudi tena. Akamuona Jery akiwa amesimama eneo la kuingilia ndani huku uso wake ukiwa ume jaa hasira. Taratibu Julieth akashusha kwenye gari na kuanza kutembea kuelekea ndani. Jery akamshika mkono na wakaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, hadi baadhi ya watu wakaanza kuhisi huenda wanandoa hao hawapo sawa kiamani.

“Ulihisi una weza kwenda kila sehemu unapo jisikia mwenyewe si ndio?”

Jery alizungumza huku akimsukumia Julieth kitandani hadi akaanguka. Kitendo hicho kikazidi kumuogopesha Julieth na kujikuta akianza kutetemeka. Jery akaufunga mlango huo kwa ndani na kusimama pembeni ya kitanda hicho huku mwili wake ukivimba kwa hasira kali snaa. Julieth kwa haraka akajibanza kwenye kona ya kitanda kwa maana kwa staili aliyo simama nayo Jery ina ashiria kabisa kwamba kinacho kwenda kufwata hapo ni kipigo na mbaya zaidi kwenye maisha yake amepigwa kipindi akiwa shuleni tu, ila kwenye kipindi chote cha kulelewa na wazazi wake hajawahi kupigwa. Jery akamnyooshea kidole huku mkono huo wa kulia ukimtetemeka.

“Wewe”

Jery alizungumza kwa sauti ya mikwaruzo ya hasira na kuzidi kumuweka Julieth kwenye kipindi kigumu. Jery moja kwa moja akaelekea bafuni na hasira zake hizo akazimalizia kupiga ngumu kwenye kioo kulichopo bafuni humo. Sauti ya kuanguka kwa vioo ikamfanya Julieth kuzidi kutawaliwa nawoga, ila akajikaza na kushuka kitandani hapo. Akatembea kwa kunyata hadi bafuni na kumkuta Jery akiwa analia kwa uchungu huku akiwa amelishikilia sinki la kunawia mikono. Machozi yakaanza kumbubujika Julieth kwa namna moja ama nyingine yeye ndio aliye sababisha matatizo hayo yote. Naratibu akapiga magoti chini huku akiwa mlangoni mwa bafu hilo.

“Nina kuomba uni samehe mume wangu”

Julieth alizungumza kwa sauti ya upole huku mikono yake akiwa ameifumbata kwa pamoja.

“Sinto rudia tenaa kuondoka hapa nyumbani na kuzungumza maneno yale. Nina tambua nime fanya makosa mume wangu nina kuomba unisamehe”

Julieth aliendelea kuzungumza kwa unyenyekevu wote kwa maana katika siku mbili hizi ameweza kuishuhudia hasira ya mume wake na wala hatamani siku itokeaa, akaingia mikononi mwa mwanaume huyo kwa maana ana weza akapigwa hadi kupoteza fahamu.

“Bikra yako aliitoa nani?”

Swali la Jery likayafanya mapigo ya moyo ya Julieth kumuenda kasi sana.

“Nime kuuliza bikra yako aliitoa nani?”

“Evans”

Julieth alijikuta akitoa siri ambayo alipanga yeye na wazazi wake wasiizungumze kwa mtu yoyote. Jery akamtazama kwa macho yaliyo jaa wekundu mithili ya mtu aliye vuta bangi kwa siku ya kwanza. Mishipa ya mwili mwake ilijitokeza juu ya mikono huku mingine kijitokeza vizuri shingoni mwake.

“Ulihisi kwamba ungeniambia kwamba huna bikra nisinge kuoa. Si ndio?”

Jery aliendelea kuhoji maswali yaliyo mfanya Julieth kukaa kimya huku akizidi kulia. Jeuri ya pesa aliyo kuwa ana iringia yote ime mkatika.

“Bado una hisia na Evans sindio?”

“Hapana mume wangu nina hisia na wewe”

“Acha unafki mwanamke. Julieth, toka nilipo kuwa nipo shuleni nilisha kuambia kwamba sipendi kudanganywa. Kwa nini mimi siwezi kudanganya ila wewe una nidanganya. Nina ona jinsi body structrure yako tukifanya mapenzi inavyo kuwa. Natambua una nipenda, ila huna hisia na mimi, huo ndio ukweli wako”

Jery aliendelea kumstumu Julieth ambaye hakufungua kinywa chake kujibu shutuma hiyo kwani anacho kizungumza Jery ni kweli. Ana mpenda sana Jery ila hisia zake zipo kwa Evans ndio maana hata ikitokea amenyonywa kitumbua chake na Jery ana jikuta akimkumbuka Evans Shika ambaye kwa sasa hafahamu yupo wapi.

“Sikuwahi kufikiria kutoka nje ya ndoa yangu.Ila umenifanya nitoke, kwa nini una taka tulete maradhi ndani ya ndoa yetu ikiwa bado sisi ni vijana wadogo na tuna malengo mengi ya kuyatimiza”

Jery alizungumza kila kitu huku akimkazia macho mke wake.

“Okay ni heri basi ungeniambia kwamba Jery. Upendo wangu nilio kuwa nao ni ule wa kishuleshule. Ninge umia ila nisinge fanya maamuzi ya kukuoa au ninge kuoa basi ninge jua nifanye nini ili kuhakikisha nina ziweka sawa hizo isia zao. Ona sasa unayo yafanya”

Jery alizungumza huku machozi ya uchungu yakimwagika. Taratibu akakaa kwenye choo hicho cha kukaa huku akimtazama mke wake usoni mwake. Julieth akamsogelea mume wake na kupiga magoti mbele yake, akaishka mikono yake yote miwili.

“Nina kuomba unisamehe mume wangu. Nina kupenda sana”

“Kama una nipenda, basi hisia zako zirudishe kwangu. Ume nielewa?”

“Ndio mume wangu nime kuelewa”

“Nami nina kuomba unisamehe kwa kukusaliti usiku wa kuamkia leo. Ilikuwa ni hasira ndio maana nilitoka nje ya ndoa”

“Usijali mume wangu, nime kusamehe”

Wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakakumbatia huku kila mmoja akiufungua moyo wake na kuahidi ata kuwa muwazi kwenye kila jambo linalo husiana na hisia zao za kimapenzi. Wakaoga kwa haraka, kisha wakajindaa na kuelekea katika uwanja wa ndege kama vile raisi Mtenzi alivyo agiza.

***

‘Ila hana makosa yule kijana’

Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amejilaza kitandani.

‘Laiti nikimuua nita kuwa nime idhulumu nafasi yake’

Nabii Sanga alizidi kumuwazia Tumaini. Akachukua simu yake kwa haraka na kumpigia kijana wake aliye mkabidhi kazi ya kumteka Tumaini.

“Za asubuhi mkuu”

“Salama, mume fikia wapi?”

“Tumesha fahamu sehemu anapo ishi yule kijana.”

“Waambie vijana wako wasitishe hiyo kazi”

“Kwa nini mkuu?”

“Nime msamehe”

“Sawa mkuu”

Nabii Sanga akakata simu na mke wake akaingia ndani hapo huku akiwa mnyonge sana.

“Mume wangu, kifungua kinywa tayari”

Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya unyonge, akatazamwa kwa jicho kali sana, kisha nabii Sanga akasimama huku akimkazia macho. Akamanza kumfwata hadi sehemu alipo simama na kumfanya mrs Sanga kuanza kurudi rudi nyuma hadi akajigonga ukutani.

“Usaliti wako huu, tambua ipo siku uta kuja kuangukia sehemu ambayo ita kuja kukupa majuto kwenye maisha yako yote. Siwezi kukupiga wala kukufanya jambo lolote baya, nime kusamehe”

Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza maneno hayo akamkumbatia mke wake, kisha akambusu mdomoni mwake.

“Siku nyingine usitembee na vijana wadogo kama wale, ni kujidhalilisha utu wako. Ume nielewa?”

“Nimekuelewa mume wangu”

“Haya twende tukapate hicho kifungua kinywa”

Wakatoka ndani hapo na kuelekea sebleni huku mrs Sanga akiwa haamini kama mume wake ame kuwa mwepesi wa kumsaheme kwenye jambo zito kama hilo.

“Ehee mume wangu niambie lile swala lime fikia wapi?”

“Swala gani mke wangu?”

“La hadhina?”

“Bado ni bila bila”

“Kuna kipingamizi gani?”

“Una mjua yule Josephine?”

“Josephine gani?”

“Yule binti ambaye ana maono na alikuwa ana sali kanisani kwetu?”

“Yaa nina mkumbuka”

“Sasa yule ndio kivuruge wa kila aina ya mpango wetu”

“Ana vuruga vipi mume wangu?”

“Moja sasa hivi ndio mshauri mkuu wa raisi”

“Ohoo na mtoto wetu je?”

“Naye ni mshauri, ila nina hisi hasikilizwi sana kama anavyo sikilizwa Josephine. Sasa binti yule ndio nina shindwa kupambana naye yaani hadi nina hisi kuchanganyikiwa”

“Mume wangu nina wazo moja”

“Wazo gani?”

“Una onaje uka rudi kwa mkuu wako Nigeria na kumshirikisha juu ya hili jambo kwa maana Josephine yeye ana uwezo wa Kimungu, ili na wewe uweze kumshinda ni laizma utumia nguvu tofauti na kuwalipa watu kufanikisha hili swala”

Nabii Sanga akakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akimtazama mke wake. Kisha akatabasamu huku akitingisha kichwa akimaanisha kwamba amekubaliana na mke wake.

“Ndio maana nilikuoa mke wangu. Una akili sana”

“Kweli?”

“Ndio. Ngoja tumalize huu msiba wa kesho kisha nijipange niende Nigeria”

“Sawa mume wangu, kwa maana uta kuwa una maliza pesa zako na mwishowe uta jikuta kila jambo lina bumburuka”

“Ni kweli, yaani sijui ni kwa nini nilishindwa kupata idea kama hizo?”

“Ndio maana una mke, nipo kwa ajili yako mume wangu”

Mrs Sanga alijishebedua mbele ya mume wake, ili maradi tu kupoteze tukio lake alilo samehewa.

***

“Hizi shuhuli zite kwenda vizuri”

Josephine alizungumza huku akiwa amejilaza kwenye sofa huku akitazama tv.

“Shuhuli gani?”

Magreth aliuliza uku akiendelea kucheza game kwenye simu yake.

“Hizi za mazishi, nina ona lile jambo la makamu wa raisi kuuwawa lime futwa”

“Mungu ni mwema. Alafu Josephine kuna jambo nina kuomba unisaidie”

“Jambo gani?”

“Una weza kumuomba Mungu na akanionyesha nita kuja kuwa na watoto wangapi hapo baade. Yaani huwezi kuamini rafiki yangu, nina hamu sana ya kuwa na mtoto”

“Mtoto ni baraka rafiki yangu. Ila hayo maono Mungu alisha niambia hato nionyesha hadi tuweze kuipata hadhina”

“Hivi ita tuchukue muda gani kuipata hiyo hadhina?”

“Sijajua kwa kweli, ila muda ukifika tuta ipata. Kwa sasa hivi ninacho kiona ni suluhisho la amani kati ya Tanzania na Marekani”

“Basi lita kuwa ni jambo zuri”

Josephine akafumba macho kwa sekunde thelathini, kisha akayafumbua na kukaa kitako huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Vipi?”

Magreth aliuliza mara baada ya kumuona Josephine akimtazama kwa muda mwingi.

“Una kalamu na peni uandike hicho ninacho kuambia?”

“Ngoja nikachukue”

Magreth akakimbilia ndani, akachukua notebook yake pamoja na kalamu kisha akarudi sebleni hapo.

“Ehee niambie”

“Wiki ijayo siku ya juma tano, saa sita na nusu mchana, shirika la ndege la Fly Emirates, katika daraja la V.I.P, namba sifuri nne, ata kaa muhusika ambaye, yeye ndio ame husika katika kuniteka, kumuua Sia kamara na yeye, ndio aliye husika na biashara za madawa ya kulevya yote hapa Tanzania na yeye ndio pia ana mpango wa kuipata hadhina tunayo ihitaji. Ndege hiyo ita kuwa ina fanya safari ya kuelekea nchini Nigeria.”

Josephine alizungumza kwa haraka haraka na Magreth akawa na kazi ya kuandika hiyo sentensi kisha akamtazama Josephine aliye jikuta akirudi kwenye hali yake ya kawaida, kwani hayo yote aliyo kuwa ana yazungumza ndio mambo ambayo alikuwa ana onyeshwa kwa wakati huo.

“Ume onyeshwa sura ya huyo mtu?”

“Hapana, ila nime pewa sifa hizo. Mage ina bidi tuweke booking kwenye hiyo ndege ili tuweze kumfahamu muhusika wa haya mambo. Ume nielewa?”

“Nime kuelewa vizuri sana, nina ona mwisho wake sasa ume karibia”

Magreth alizungumza huku akiwa na furaha sana kwa maana wana mtafuta sana huyo mtu bila ya mafanikio, ila kwa wakati huu wana amini wata mpata.



“Ila hii ishu tusimuhusishe mtu yoyote zaidi ya raisi”

“Sawa, itakuwa ni jambo zuri”

Siku nzima hawakutoka nyumbani hapo na kazi yao ni kutazama jinsi wageni mbalimbali wanavyo pokelewa katika kiwanja hicho cha ndege. Ikafika zamu ya makamu wa raisi wa nchi ya Marekani kupokelewa huku akiwa ameandamana na mke wake pamoja na mke wake na wapambe wake pamoja na wafanyakazi wake. Wakapeana mikono na raisi Mtenzi kisha wakakagua ju1kwaa, kisha wakapanda kwenye jukwaa la kawaida na wimbo wa taifa ukapigwa. Baada ya shuhuli kikamilika na makamu huyo wa raisi akaondoka na kumuacha raisi Mtenzi akimsubiria raisi wa nchi ya Russia ambaye naye ana kadiria kufika nchini Tanzania baada ya lisaa moja mbeleni.

“Baba”

Jery alimnong’oneza baba yake.

“Ndio”

“Kuna haja ya mimi na mke wangu kuendelea kukaa hapa?”

“Ndio, tumsubirini raisi wa Rusia kwa maaana yeye ndio wa mwisho kufika hapa”

“Sawa”

Muda wa raisi wa Rusia kufika uwanjani hapo ukawadia, akakaribishwa kama maraisi wengine walivyo pokelewa kisha akaelekea kwenye hoteli ambayo amepangiwa kufikia kisha raisi Mtenzi na familia yake wakarudi ikulu.

***

Siku iliyo fwata wananchi wengi kutoka mikoa mbalimbali ya nchi yaTanzania wakakusanyika katika kiwanja kikuu cha mpira kuuaga mwili wa makamu wa raisi pamoja na mke wa raisi Mtenzi. Viongozi mbalimbali wa kitaifa na wale walio toka nje ya nchi ya Tnazania, nao ni miongoni mwa watu walio udhuria shuhuli hiyo ya kuiaga miili hiyo. Vilio vilitawala kila upande wa uwanja huo huku raisi Jery na mwanaye wa pekee aliye salia, wakiwa katika huzuni kubwa sana. Ibada ikaanza huku taratibu zote za kidini za kusomea mazishi ya wafiwa zikifwata. Baada ya ibada kuisha, ukafata wasaa wa kuiaaga miili hiyo kwa kupita mbele ya majeneza, akaanza raisi Mtenzi, mwanaye pamoja na mkwe wake. Raisi Mtenzi alijikuta machozi yakimwagika mara baada ya kumuona mke wake katika jeneza hilo. Akapiga magoti pembeni ya jeneza hilo, akasali kwa dakika tano kisha akasimama. Jery akamtazama mama yake huku machozi yakimbubujika. Walipo maliza kuaga familia, wakafwata ndugu, kisha wakafwata viongozi wa kimataifa, wakitaifa kisha wakafwata raisi wa kawaida. Hakika ilikuwa nis iku ya majonzi sana hususani kwa kuondokewa kwa makamu wa raisi ambaye alikuwa ni mtu wa watu wengi.

Baada ya shuhuli za kuuaga miili hiyo shuhuli ikahamia makaburini, ambapo,miili hiyo iliweza kuzikwa kwa nyakati tofauti, huku ukianza mwili wa makamu wa raisi kisha yakafwatia mwili wa mke wa raisi Mtenzi. Miili yote ilizikwa kwa heshima za kiserikali kisha watu waondoka makaburini hapo. Raisi Mtenzi siku hiyo hakuhitaji kuzungumza kitu chochote na mtu na alicho kifanya ni kuingia ndani kwake na kujifungia kwa ndani. Akapanda kitandani na kukala.

“Duu ina uma sana”

Magreth alizungumza huku wakiingia ofisini kwa Josephine.

“Yaani wee ach anime muona huruma sana raisi pale alipo kuwa amepiga magoti pembeni ya mwili wa mke wake”

Josephine alizungumza huku akikaa kwenye kiti chake.

“Kwa mtazamo wako muheshimiwa ana weza kuwa sawa juu ya tukio hili?”

“Sijajua ila Mungu amtie nguvu”

“Amen, vipi una kwenda nyumbani?”

“Ndio”

Magreth na Josephine wakaondoka ikulu apo na kurudi nyumbani.

“Mume wako yupo wapi?”

Nabii Sanga alimuuliza Julieth huku akimtazama usoni mwake.

“Nyupo chumbani ame jipumzisha haitaji kuzungumza na mtu yoyote”

“Okay ehee niambie ime kuwaje?”

“Tukaongolee nje”

Nabii Sanga na mwanaye huyo wakatoka na kuingia kwenye gari la nabii Sanga.

“Baba, mume wangu amejua”

“Amejua nini?”

Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na mstuko.

“Kwamba bikra yangu ni feki”

Nabii Sanga macho yakamtoka huku akishikwa na kigugumizi cha kushindwa kuzungumza chochote.

“Yaa alikasirika sana, sikuwahi kumuona mume wangu akiwa amekasirika kwa kiasi hicho”

“Alikupiga?”

“Hapana, ila hasira yake ilikuwa ni zaidi ya kupigwa”

“Sasa alijuaje?”

“Mume wangu ni daktari hivyo halikuwa jambo gumu kwa yeye kuweza kutambua kwamba bikra hiyo ni feki”

“Duu sas mipango yetu ina weza kwenda kama tulivyo panga?”

“Kwenye sekta hiyo hakuna aliye weza kutambua chochote. Ila kwenye maswala ya mahusiano ndio kidogo ime kuwa rahisi kustukiwa”

“Basi ina bidi kuwa makini sana na mume wako. Pia mazungumzo yetu ya kupeana siri mimi na wewe tafadhali usiyazungumzie ndani ya ofisi yako, kwa maana huwezi jua wakawa wana wapeleleza”

“Ni kweli baba. Ehee mpango wako wa hadhina umefikia wapi?”

“Kuna kivuruge”

“Nani huyo?”

“Ni Josephine, hapa nina hitaji kwenda nchini Nigeria”

“Lini?”

“Juma tano ijayo”

“Kufanya kitu gani?”

“Kuzungumza na yule mkuu wangu na baada ya hapo nita rudi nchini nikiwa na nguvu ambazo hazito mfanya Josephine kugundua jambo lolote kuhusiana na mipango yetu kwa maana ime kuwa kila mpango yeye ana ujua na kumwambia mkweo”

“Sasa ana juaje?”

“Si maono yake. Hivi una hisi kwamba ana elimu kubwa ya kumfanya awe chief Staff? Kilicho muweka hapo ni maono yake”

“Una hisi kwamba ukienda huko una weza kupambana naye?”

“Kwa asilimia mia moja”

“Sawa baba. Fanya chochote kiwezekanano kwa maana kama tukitusua kwenye hili jambo nina imani kila kitu kita kwenda vizuri.”

“Sawa, acha nielekee nyumbani kwa maana sasa hivi nina hisi sito weza kuonana na huyo mkwe wako”

“Sawa baba”

Julieth akashuka kwenye gari hilo na nabii Sanga akaondoka ikulu hapo na kurudi nyumbani kwake.

***

Josephine alikurupuka kutoka usingizini mara baada ya kuona maono ambayo yalimstua sana. Akanyanyuka kitandani kwake na moja kwa moja akaelekea hadi chumbani kwa Magreth. Akagonga mlango na baada ya dakika moja Magreth akafungua mlango huo.

“Vipi?”

“Magreth nime ona maono ya kuogopesha sana.”

“Maono gani tena?”

“Nime ona makomandoo wanne wa Kimarekeni, wana mpango wa kuvamia kambi ya jeshi ya kule Kigamboni, wana hitaji kuwatorosha wale watuhumiwa ulio wakamata siku ile”

“Wale walio uvamia msafara wa raisi?”

“Ndio”

“Shitii sasa nyinyi si mume sema kwamba kwesho kuta kuwa na kikao sijui na huyo makamu wa raisi”

“Ndio hivyo, alafu sijui ni kwa nini wame tuma hao makombandoo wakawaokoe”

“Sasa wana kwenda kuwaokoa saa ngapi hao wanajeshi?”

“Kesho muda wa kikao”

“Mungu wangu, sasa ita kuwaje?”

“Hembu wasiliana na RPC”

Magreth akaichukua simu yake pembeni ya kitanda chake na kumpigira RPC Karata.

“Kaka habari ya muda huu”

“Salama, vipi kwema?”

“Sio sana, upo wapi?”

“Nipo kituoni”

“Basi tuna kuja japo”

“Sawa nina wasubiria, wahini kwa maana nilihitaji kutoka na kutembelea vijana kwenye doria zao”

“Sawa”

Magreth akakata simu kisha wakajiandaa haraka haraka huku Josephine akimuomba Magreth kuvaa nguo zake za kazi. Wakaondoka na kufika kituo kikuu cha polisi.

“Ehee vipi?”

“Kaka kuna makomandoo wanne wa Kimarekani wana mpango wa kuivamia kambi ya kijeshi ya Kigamboni na wana mpango wa kuwatorosha wale wanajeshi tulio wakamata walio uvamia msafara wa raisi”

“Weee!!”

RPC Karata alistuka sana”

“Ndio hivyo kaka, tuna shindwa kuwasiliana na raisi kutokana na hali yake”

“Ni kweli, kwa sasa hayupo sawa. Sasa hapa cha kufanya ngoja niwasiliane na mkuu wa kambi hio kisha twendeni huko mukamueleze hilo jambo”

“Sawa”

RPC Karata akawaslinana an mkuu wa kambi hiyo ya kiheshi. Wakakubaliana waende kambini hapo, usiku huo huo wakaondoka na kuelekea kambini hapo na kukutana na mkuu huyo. Josephine akelezea hali halisi itakavyo kuwa. Akawataja na makomandoo wenyewe ambao wata husika kwenye oparesheni hiyo.

“Ni washenzi sana, ina bidi niwapange vijana wangu, na kama kweli wakija nita hakikisha tuna wapiga risasi mmoja baada ya mwengine hadi wafe”

Mkuu wa kambi alizungumza kwa msisitizo.

“Ni jambo zuri na asubuhi nita shiriki kwenye kikao na makamu wao wa raisi”

Josephine alizungumza huku akimtazama mkuu huyo wa kambi.

“Una onaje uka itoa siri yao katika kikao hicho?””

“Etii?”

“Ni kweli Jose ukiitoa siri ya hao makomandoo ita kuwa ni vizuri na kikao hakito kuwa na kazi tena kwa maana watakacho kuwa wana kifanya hapo ni ulaghai tu”

“Sawa nime waelewa, Magreth tuta kuwa tuna wasiliana kwa siri mimi nikiwa kwenye kikao hicho na nyinyi muta subiri amri ya raisi kama tuwashambulie au laa”

“Sawa”

Mipango yote ikapangika na Josephine akawaonyesha eneo ambalo wame panga kuingilia katika kambi hiyo ya kieshi. Kila kitu kilipo kamilika, Josephine akarudishwa nyumbani na RPC Karata, akajianda vizuri na kuelekea ikuku.

***

Saa mbili kamili asubuhi, raisi Mtenzi pamoja na washauri wake wakakutana na makamu wa raisi katika ukumbi wa mikutano ndani ya ikulu. Ajenda kuu mbini ni kwanza kwa nchi ya Marekani kuiomba msamaha kwa kuwatuma wanajeshi wake walio shambulia msafara wa raisi huku ajenda ya pili ni kuomba kujenga jiji la Dar es Salam upya.

“Kilicho fanywa na wanajeshi wetu kwa kweli ni kosa kubwa sana ambalo mimi na serikali yangu, tuta waadhibu vikali sana wanajeshi wote walio husika na tukio hilo”

Makamu wa raisi bwana Henry Godlisen alizungumza huku akiwatazama washauri wa raisi Mtenzi akiwemo Josephine.

“Makamu wa raisi pasipo kukuvunjia heshima, ila kilicho fanywa na wanajeshi wako kwa kweli mimi na nchi yangu hatuwezi kuwasamehe. Huu mpango sio wa bahati mbaya, ni mpango wa kimakusudi kabisa. Moja muliweza kupndikiza ua moja ndani ya ofisi yangu ambalo lilikuwa na kinasa sauti ambayo kiliweza kurekodi kila majadiliano yaliyo fanyika ndani ya ofisi yangu. Ina oneysha kwamba muli kusudia kufanya hivyo. Mbili muliwaua walinzi wangu katika shambulizo hilo, je muna hisi kwamba ni jambo zuri ambalo lina weza kufuta kumbukumbu hiyo mbaya kwenye serikali yangu?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama bwana Henry Godilisen.

“Tuna kiri ni makosa ila kwenye kosa lolote mtu anapo omba msamaha basi ni vyema akasamehewa muheshimiwa raisi”

‘Muheshimiwa nina weza kuzungumza?’

Josephine alimnong’oneza raisi Mtenzi sikionii mwake.

‘Ndio’

“Muheshimiwa makamu wa raisi, nina itwa Josephine ni Chief Staff wa ikulu.”

“Nashukuru kukufahamu Josephine”

“Kwa nini muna mpango wa kuwatorosha wanajeshi tulio wakamata kwa kosa la kuvamia msafara wa raisi?”

Makamu wa raisi na wapambe wake wakastuka sana kwa maana mpango huo ni kweli upo na hata raisi Mtenzi na washauri wake wengine nao walijikuta wakistuka kwa maana hawajui kinacho endelea.

“Ahaa….a….as….asamahani binti una zungumza nini?”

“Nina imani kwamba ume nielewa. Hivi ninavyo zungumza hivi sasa, kuna makomandoo wanne, mume watuma kwa ajili ya kuwatorosha wafungwa hao ambao wapo katika kambi ya kijeshi Kigamboni. Una bisha?”

Makamu raisi akameza fumba zito maji huku akimtazama Josephine usoni mwake, kwa macho yaliyo jaa wasiwasi ambao kwa namna moja ama nyingine unadhihirisha ukweli wa maneno ya Josephine.




“Jose ni kweli?”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama Josephine aliye kaa pembeni yake.

“Ndio muheshimiwa. Kama huamini washa tv yako hapo kwa maana kuna video ambayo tayari Magreth ameituma”

Raisi Mtenzi akachukua rimoti ya tv iliyopo mezani. Akawasha tv hiyo na watu wote wakayaelekezea macho yao kwenye tv hiyo. Akaonekana video ikiwaonyesha makomandoo wanne wa Kimarekani, wakiwa karibu kabisa na kambi ya jeshi iliyopo Kigamboni.

“Makamu wa raisi kwa hiyo tuna fanyana watoto?”

“Ahaa muheshimiwa raisi hatuwajui hao watu sisi na hawahusiani kabisa na nchi yetu”

Makamu wa raisi alijitetea huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.

“Hadi kwa majina nina weza ninakutajia na vyeo vyao pia nina weza nika kutajia na nita kuambia mpango mzima huo muliupangaje”

Josephine alizungumza kwa kujiamini sana na kuwafanya Wamarekani hao kujawa na hofu moja kubwa sana kwani waliamini kwamba kila walicho kifanya ni siri na hakuna atakaye weza kufahamu.

“Muheshimiwa raisi kwa kweli anacho kizungumza mshauri wako hapa, hatukifahamu kabisa”

“Muna kwenda kuwapotea watu wenu, na nina imani muna jua hasara ya kumpoteza komandoo mmoja ni sawa ume poteza askari mia moja”

Josephine aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.

“Ni kweli tuna jua na kama wangekuwa ni watu wetu tunge sema”

Mshari wa makamu wa raisi naye alizungumza kwa msisitizo.

“Sawa kama muna bisha. Muheshimiwa raisi hapo unavyo ona ni video ya moja kwa moja na vijana wako wamesha jipanga toa amri ya kuwashambulia hao wavamizi”

Josephine alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake. Raisi Mtenzi, akamtazama makamu wa raisi pamoja na watu wake walio jikausha kimya.

“Muna uhakika sio watu wenu?”

“Ndio sio watu wetu kabisa na hatuwezi kuja kutafuata amani hapa alafu tutume watu mlango wa pili ili kuwadhuru”

Makamu wa raisi alizungumza kwa kujiamini sana.

“Sawa. Washambuliwe”

Simu ya Josephine ambayo ipo hewani kuanzia mwanzo wa kikao, amri hiyo iliweza kumfika mkuu wa kambi ya jeshi la kigamboni. Makomandoo hao wanao pasipo kujua kwamba wapo kwenye kumi na nane, wakajitokeza ndani ya maji kisha wakaanza kutambaa hadi karibu na fensi kubwa iliyo zunguka kambi hiyo. Wakakata fensi hiyo huku watu wote wakitazama video hiyo inayo rekodiwa kwa drone maalumu ya jeshi iliyopo juu sana na hata wanajeshi hao hawajaweza kujua chochote. Wakafanikiwa kuingia katika fensi hiyo huku wakiwa wamevalia mavazi ya jeshi la Tanzania. Kitendo cha kusogea hatua mbili mbele, mvua ya risasi ikaanza kuwa miminikia. Hakika shambulio hilo liliwaumiza Wamarekani wote walipo ndani ya ukumbi huo, kila wapo wasaidizi wawili wa makamu wa raisi walilengwa lengwa na machozi. Makomandoo hao waligeuzwa kama machojio kwa maana risasi za karibia wanajeshi mia moja ziliwalenga wao.

“Kazi nzuri”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akizima tv.

“Nchi yangu ina nguvu sana kweye maswala ya kujilinda na huwa hatuna adui ambaye tuna mfumbia macho pale tu anapo ingia kwenye ardhi yangu ya Tanzania”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo na kumfanya makamu wa raisi atamani kumvamia kwa hasira, ila kilicho msaidia ni tabasamu lake feki la usoni, ila moyoni kume vurugika kwa kweli huku akianza kujiapia kwamba ni lazima ata lipa kisasi na macho yake yote ana mtazama Josephine ambaye yeye ndio chanzo cha vifo hivyo.

“Ni kweli muheshimiwa raisi”

Makamu wa raisi alizungumza kwa kujikaza tu.

“Kitu kimoja ambacho nina weza kuwahakikishia ni kwamba hatuto weza kuwaachia huru wanajeshi wenu tulio wakamata. Hilo nina omba mulisahau. Wanajeshi ambao tutakao waachia huru ni wale ambao muliwaleta nchini kwa ajili ya kuijenga Dar es Salaam”

“Ila muheshimiwa raisi tume kuja kiamani ili tuzungumze kwa amani?”

“Nalitambua hilo, ila na sisi ni nchi huru. Niwaambie tu ukweli, kama muna mshikilia mpelelezi wa Kitanzania nchini Marekani na ame kuja kwa lengo kuipeleleza nchi yenu, mukimkamata muna haki ya kumuua. Tume elewana?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo.

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Ili nyinyi na sisi twende sawa na huu uhusiano wetu usiyumbe. Nina waachia hao wanajeshi wajenzi wa Dar kisha nita omba muondoke nao la sivyo hili vuguvugu linalo endelea endapo likitoka nje kila kitu kita badilika”

“Muheshimiwa raisi tume kueleawa sana na tuna shukuru kwa maamuzi hayo. Ila tuna waomba wanajeshi hao waweze kuendelea katika ujenzi wa hili jiji?”

“Kwa nini?”

Josephine alizungumza huku akimtazama makamu wa raisi usoni mwake.

“Ni katika hali ya kuborosha mahusiano yetu kwa maana ujenzi wetu tuta ufanya kwa garama zetu sisi wenyewe”

“Hakuna kitu cha bure kwenye hii nchi. Mpango wenu una fahamika kwamba kilicho kuwa kime waleta hao wana jeshi ni kutafuta hadhina ambayo ita wafanya muwe mataji mara dufu”

Josephine alizungumza kauli iliyo zidi kuwaumiza mioyo Wamarekani hao kiasi cha kuwafanya kuzidi kumchukia na kumuona kama mwiba katika kikao hicho.

“Hadhina? Hadhina gani?”

Makamu wa raisi alijifanya kushangaa sana kana kwamba hajui chochote.

“Okay ni hivi siwezi kukubaliana na wanajeshi wenu kuwa ndani ya nchi yangu. Kiukweli, siwamini tutashirikiana kwenye mambo mengine ila sio maswala ya ujenzi wa nchi yangu. Tume elewana makamu wa raisi”

“Ndio muheshimiwa.”

“Kikao kime vunjwa”

Mara baada ya raisi Mtenzi kuzungumza maneno akasimama na watu wote wakasimama. Wakamsindikiza makamu wa raisi hadi nje ya ikulu. Wakaagana mbele ya waandishi wa habari walipo piga picha za hapa na pale kisha makamu wa raisi akaondoka na wapambe wake pamoja na walinzi wake.

“Kazi nzuri Josephine”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akipeena mkono na Josephine.

“Ninashukuru muheshimiwa”

“Kwa nini hukunishirikisha juu ya hilo swala la Makomandoo?”

“Muheshimiwa kwanza samahani, pili ni jambo lililo nijia usiku sana, isitoshe kwa hali iliyo kuwepo jana hivyo nilihisi kwamba haito kuwa jambo zuri na la kupendeza pale ambapo ninge kusumbua usiku wa jana”

“Sawa usijali, ila siku nyingine hata nikiwa katika hali ya namna gani ina bidi unieleze kila jambo unalo onyeshwa na linalo husiana na hii nchi”

“Sawa muheshimiwa”

Kupongezwa Josephine hakika kuka uumiza moyo wa Julieth ambaye ana chuki na Josephine kwa maana uwezo wake una vuruga mipango yao mingi sana.

‘Siku zako zina kuja’

Julieth alizungumza huku akimtazama Josephine na raisi Mtenzi wanao ingia ofisini kwa raisi.

“Alafu muheshimiwa kuna kazi ambayo Juma tano nita omba tuweze kuifanya mimi na Magreth.”

“Kazi gani?”

“Juma tano ya wiki hii inayo anza kesho. Nime onyeshwa yule mtu ambaye ana dili na haya mambo yote ata kuwa katika ndege ya shilila la Fly Emirates. Nimeonyeshwa siti ambayo ata kaa hivyo, muheshimiwa siku hiyo ndio tuta weza kumjua mbaya wetu”

“Safi sana, kwa hiyo tuandae vikosi?”

“Hapana muheshimiwa. Mimi na Magreth tuta ipanda ndege hiyo ambayo ita elekea nchini Nigeria, hivyo nina imani kwamba uwezo wa Magreth uta saidia kumdhibiti tukifika nchini Nigeria”

“Sawa, nita wasiliana na ubalozi wa Nigeria ili muweze kupata visa ya kuwapeleka huko. Umenielwa?”

“Ndio muheshimiwa nina shukuru kwa kutukubalia hilo”

“Ila Josephine nina hisi una paswa kuwa na walinzi wa kutembea nao kwa sasa?”

“Kwa nini muheshimiwa?”

“Nina ona tu huko tunapo elekea ina bidi uwe na walinzi”

“Muheshimiwa, mlimzi wangu mkuu ni Mungu. Nina imani ata niongoza kwenye kila jambo hivyo usiumize kichwa sana”

“Sawa kama ni hivyo”

Josephine akaagana na raisi Mtenzi na akatoka ofisini kwake.

“Jose”

Sauti ya Julieth ikamfanya asimame na kumtazama.

“Ndio”

“Tuna weza kuzungumza?”

“Ndio”

Josephine akamkaribisha Julieth ofisini kwake.

“Naweza kukuuliza maswali”

Julieth alizungumza kwa heshima zote kwa maana Josephine ni bosi wake kicheo.

“Ndio”

“Hivi una wezaje wezaje kuona maono ya mambo yajayo?”

Josephine akatabasamu kwa sekunde kadha huku akimtazama Josephine usoni mwake.

“Ukiwa karibu na Mungu, basi kila jambo uliombalo una weza kulifanikisha. Nina imani baba yako ni nabii hivyo kuna mambo mengi sana ambayo ana weza kukufundisha na uka yaelewa juu ya vipawa ambavyo Mungu ana vitoa kwa watu wake”

“Ahaa sawa. Je una weza kumuomba Mungu akakuonyesha juu ya hatima ya ndoa yangu?”

“Hatima ya ndoa yako?”

“Ndio?”

“Kwa nini una hitaji kujua hatima ya ndoa yako ikiwa hata miezi miwili hamujamaliza?”

“Ni kutokana na mambo yanayo endelea ndani ya ndoa yangu hivi sasa.”

Julieth alizungumza ili kuupima uwezo wa Josephine.

“Ngoja nikuambie kitu kimoja Julieth. Mwanamke mwerevu huijenga ndoa yake ila yule aliye mpumbavu basi huivunja ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe. Sijui ume nielewa hapo?”

“Ndio nime kuelewa kwa hiyo una taka kuniambia mimi nipo kwenye eneo gani hapo?”

“Julieth, ngoja nikuambie kitu kimoja. Nina kujua vizuri kuliko unavyo fikiria, haya yote unayo nihoji ni kuunipima na mimi huwa sipimiko ndio maana hata baba yako hawezi kunipima kwa maswali ya namna hiyo. Ila kuwa makini sana kwa kila unacho kifanya kwa maana ipo siku Mungu ata dhihirisha kila jambo, iwe ni kwenye ndoa yako au humu ofisini kwako”

Josephine alizungumza kwa msisitozo huku akimkazia macho Julieth aliye jikuta mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.

“Nashukuru”

Julieth taratibu akasimama kisha akatoka ofisini hapo. Josephine akamtazama kwa sekunde kadha kisha akatingisha kichwa huku akitabasamu tu.

“Niitie Mzee Mbogo nina mazungumzo naye”

“Sawa sawa”

Sekretari wa raisi Mtenzi akampigia simu mzee Mbogo ambaye naye upo hapo hapo ikulu. Mzee Mbogo akaingia ofisini kwa raisi Mtenzi na kukaa kwenye moja ya kiti.

“Ndugu yangu kama unavyo ona nchi kwa sasa ime mpoteza makamu wa raisi na mambo yana zidi kuwa magumu siku hadi siku”

“Ni kweli, na lile jambo la Makomandoo, aisee sikuweza kulijua kabisa. Hakika yule binti ana uwezo mkubwa sana”

“Ndio hivyo, nina muamini sana Josephine. Ila nahitaji kukuambia jambo moja au nina hitaji kukuomba”

“Jambo gani muheshimiwa”

“Nina hitaji uwe makamu wangu wa raisi. Tafadhali nina kuomba usinikatalie. Hembu tumalizie hichi kipindi changu cha uongozi kilicho salia. Wewe ni mtu ambaye una ijua hii nchi vizuri, kiusalama hadi siasa hivyo tafadhali nina kuomba sana uweze kunikubalia”

Mzee Mbogo akaka kimta huku akiwa ameshikwa na mshangao mwingi sana.

“Mkuu hili jambo ni zito sana kwenye maisha yangu. Isitoshe umri wangu pia una nipasa nipumzike?”

“Nalitambua hilo, ila hii miaka mitatu iliyo baki madaraani, ina tutosha sana kufanya kila linalo wezekana kuhakikisha kwamba tuna ijenga Tanzania mpya, Tanzania yenye nguvi na ita kuwa ni urisi mzuri sana kwa vizazi vijavyo”

Raisi Mtenzi aliendelea kumshawishi mzee Mbogo.

“Nime kuelewa muheshimiwa. Nina kuomba nika litafakari hili jambo, tafadhali nina kuomba unipatie tu siku ya leo. Kesho nita kupatia jibu”

“Nashukuru ila nina tarajia kupata jibu lililo zuri kutoka kwako”

“Hakuna shaka muheshimiwa”

Mzee Mbogo akaaga na kutoka ndani hapo huku akiwa haamini kama raisi Mtenzi ame mteu kuwa makamu wake wa raisi.

***

“Ina uma sana”

Makamu wa raisi bwana Henry Godlisen alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Wakiwa ndani ya gari akielekea hotelini.

“Muheshimiwa ina bidi tufanye jambo juu ya hivi vifo?”

Mshauri wake alimchochea.

“Tutafanya ila tukiwa nje ya hii nchi. Yaani nchi Masikini kama hii ina jifanya kutunisha msuli mbele yetu”

Makamu wa raisi aliendelea kulalama.

“Muheshimiwa, ita kuwaje sasa?”

“Hembu nitafutieni details za yule Chief Staff, alafu tuta jua ni nini tufanye”

“Sawa”

Jina la Josephine likatuma kwa wataalamu wa udukuzi wa data(hackers) walipo nchini Marekani na baada ya dakika tano, taarifa za Josephine zikatumwa kwao.

“Ameishia form six na hana kozi yoyote aliyo somea. Ime kuwaje ame kuwa ni mshauri wa raisi?”

“Ndio muheshimiwa?”

“Hana rekodi yoyote ya kwamba ni jasusi au?”

“Hana muheshimiwa, nime angalia profile yake haina kitu zaidi ya kuwa ni muimba kwaya katika kanisa mmoja lililopo hapa jijini Dar es Salaam na lina milikiwa na mtumishi mmoja ana itwa nabii Sanga ambaye mwanaye ame olewa na mtoto wa raisi Jery”

“Kwa hiyo huyo nabii Snaga ata kuta ana mtambu vizuri huyo binti?”

“Ndio mkuu”

“Nahitaji kuonana na huyo nabii Sanga. Tafuta namba yake ili niweze kuzungumza naye mimi mwenyewe”

“Sawa muheshimiwa, ila kabla hauja wasiliana naye muheshimiwa. Kumbuka huyu nabii Sanga yupo karibu sana na raisi Mtenzi hivyo chochote unacho zungumza naye tambua kwamba kita kuwa na asilimia tisini ya kuvuja”

Mshauri wa makamu wa raisi alizungumza huku akimtazama bosi wake usoni.

”Kwa hiyo una nishaurije?”

“Mkuu kama ni kudili naye yule binti tudili naye sisi kama sisi. Hii ishu tusimshirikishe Mtanzania yote, kwa maana ita vuja tu na ita zidi kututengenezea mazingira mabaya na hii nchi”

“Sawa, nita tuma watu kumpeleleza yule binti na nilazima alipe kwa damu za makomandoo wangu”

Makamu wa raisi Henry Godlisen alizungumza kwa msisistizo pasipo kujua kwamba huyo mtu anaye mzungumzia ana uwezo wa kujua mipagno yake yote pasipo kuambiwa na mtu yoyote.



Makamu wa raisi wa Marekani akafika hotelini hapo ambapo ulinzi ume imarishwa. Kichwani mwake hakika mawazo mengi sana yame mtawala. Kikao akicho kuwa amekikusudia hakija kwenda kama alivyo panga, isitoshe amepoteza makomandoo wake.

“Muheshimiwa, kuna video call kutoka white house”

Sekretari wake alizungumza na moja kwa moja makamu wa raisi bwana Henry Godilise alizungumza huku akimtazama usoni mwake.

Akanyanyuka kwenye sofa alilo kaa, akatembea hatua nne hadi kwenye meza, ambayo ina laptop yake. Akavuta kiti akaka huku, kisha akaminya moja ya batani. Akamuona raisi pamoja na viongoziwengine wa kiserikali wakiwemo wa kijeshi wakiwa wana mtazama. Akawasalimia na kikao hicho cha dharura kikaanza. Makamu wa raisi akaanza kusimulia jinsi kikao kilivyo kwenda kunzia mwanzo hadi mwisho. Akaeleza jinsi mbinu yao ilivy o weza kuvumbuliwa na binti anaye itwa Josephine ambaye ni chife Staff wa raisi Mtenzi.

“UNa fikiria nini juu ya huyo binti makamu wa raisi”

“Hadi sasa sija weza kujua ni nini cha kufanya muheshimiwa”

“Ina bidi huyo msichana tuweze kumteka ili kutambua ni nani na ana uwezo gani hadi ametambua siri nyingi ambazo nina uhakika hazikuweza kutoka”

“Sawa muheshimiwa raisi, illa ita bidi tusiwatumie vijan wetu kwa maana hapa nina anza kupata mashaka mengi sana ndani ya hii nchi”

“Ume panga kutumia vijana gani?”

“Kuna hili kundi la Al-Shabab, munaonaje tuka tumia vijana wake kwenye hii kazi. Kwani waliweza kufanikiwa kulipua jiji la Dar es Salaam na hawakuweza kujua chochote, kwenye hili la kumteka huyu msichana nina imani halito kuwa jambo zito na gumu kwao”

“Ni wazo zuri sana. Ina bidi kuhakikisha kwamba ana anza kufwatiliwa kuanzia hivi sasa na kuendelea na hili swala la Al-Shabab nina kuachia Jeneral Stuwart dili nalo”

“Sawa muheshimiwa”

“Makamu wa raisi kuwa makini na hakikisha una rudi nyumbani na vijana wetu”

“Hakuna shaka”

Kikao kikaishia hapo huku mipango ya kumteka Josephine ikianza kutekelezwa haraka iwezekanavyo.

***

Mkuu wa kundi la Boko Haramu, ambaye kwa sasa ana wafadhili wana mgambo wa Al-Shabab akapokea simu kutoka kwa mmoja wa wanajeshi wa Marekani ambao wana fanya nao kazi kwa ukaribu sana.

“Kuna kazi, ninta hitaji kufika kambini kwako”

“Ni ya kiserikali, au kawaida?”

“Ni ya kiserikali”

“Sawa, njoo majira ya saa mbili usiku. Nina imani kwamba una fahamu ni wapi kwa kukutana nami”

“Natambua ila nina hitaji uje na kiongizi wa kundi la Al-Shabab”

“Kwa nini nije naye?”

“Hii kazi ita wahusu sana wao, ila na nyinyi pia muta pata gawio kubwa sana kwenye hii kazi”

“Isiye ikawa ni mbinu ya kutugeuka?”

“Una jua kwamba mimi sina mambo hayo na kama inge kuwa ni kukugeuka, ninge fanya hivyo siku nyingi sana”

“Sawa, usiku saa mbili njoo kambini”

“Nime kuelewa”

Meja Kane akakata simu huku akimtazama jenerali Stuwart aliye kuwa akifwatilia mazungumzo hayo ya simu kwa kupitia video call kwa maana yeye yupo ikulu nchini Marekani.

“Nita kwenda kuonana nao saa mbili usiku mkuu”

“Nina imani kwamba ile picha na details za huyo msichana?”

“Ndio muheshimiwa, nita kwenda na faili lake”

“Hii ni oparesheni ya kijeshi, waaifanye kwa umakini wa hali ya juu sana. Tuna muhitaji huyo msichana akiwa hai kabisa na tuna muhitaji kwa ajili ya kumfanyia mahojiano ya kina”

“Sawa jeneral nime kuelewa”

“Chochote watakacho kihitaji, serikali ipo tayari kutoa”

“Hakuna shaka”

Mazungumzo hayo kati ya meja Kane pamoja na jeneral Stuwart yakaishia hapo. Meja Kane akaanza kutazama picha za Josephine na kujikuta akiwa na amejawa na maswali mengi sana, ime kuwaje binti mdogo namna hiyo ata tafutwa na serikalili tena kwa kutumia upande wa pili ambao ni wa kigaidi. Majira ya saa moja usiku akaanza safari ya kuelekea katika kambi ya kundi la Bokoharmu lililo katika moja ya msitu mnene na wakutisha ambao sio rahisi kwa vikosi vya serikali ya nchi ya Nigeria kuweza kufika. Kutokana ana julikana na wapiganaji hao hivyo halikuwa ni jambo gumu kwa yeye kuingia ndani ya kambi hiyo. Wakasalimiana na mkuu huyo wa kundi la Bokoharamu pamoja na mkuu wa kundi la Al-Shabab na mazungumzo yakaanza. Taratibu akamsogezea mkuu wa kundi hilo Bokoharamu, faili lenye maelezo ya Josephine na akalifungua na kuanza kulikagua karatasi hizo pamoja na picha moja baada ya nyingine zinazo muonyesha Josephine akiwa katika matukio tofauti tofauti.

“Ni nani na muna muhitaji wa nini?”

“Ni mshauri namba moja wa raisi wa nchi ya Tanzania. Tuna hitaji kumteka na kazi hii tuna hitaji kundi la Al-Shabab kuweza kuifanya”

“Muna hitaji vijana wangu kurudi tena nchini Tanzania?”

“Ikiwezekana, ila kwa safari hii sio kwenda kulipua magorofa na kuwaua watu wengine. Sisi tuna muhitaji huyu msichana tu”

“Hii kazi ni ngumu sana kwamaana nchi ya Tanzania ita kuwa ime jipanga vizuri kwenye maswala ya kiusalama”

“Tuna tambua ila mukihitaji mbinu za kijeshi, silaha tupo tauari kuwapatia ila kitu cha pekee tunacho kitaka ni huyu msichana”

“Malipo kiasi gani muta tupatia?”

“Serikali yangu ipo tayari kuwapatia kitu chochote mutakacho hitaji”

“Moja hatuto hitaji serikali yako iweze kutuma vikosi vyake nchini Somalia wala Nigeria kwa lengo la kututafuta sisi. Pili tuta hitaji kulipwa dola milioni kumi na tatu tuta hitaji kupewa silaha tutakazo zihitaji. Kama muta kubaliana na kile ambacho tume kizungumza basi muna weza kupata huduma ya Al-Shabab”

Meja Kane akashusha pumzi taratibu huku akitingisha kichwa akimaanisha kwamba serikali yake ipo tayari kuhakikisha ina wapatia kila wanacho kihitaji.

“Nita wasiliana na serikali yangu na tuta wapatia jibu la lini muweze kuifanya hii kazi”

“Sawa, ila Kane makubaliano yetu tuna hitaji yawe ya mkataba wa maandishi nay awe na saini ya raisi wenu la sivyo hatuto ifanya hii kazi”

“Nime waelewa”

Meja Kane akaondoka kambini hapo na kurudi katika kambi ya kijeshi. Akatoa ripoti kwa mkuu wake juu ya makubaliano hayo jinsi yalivyo kwenda na ripoti ikarudishwa ikulu kwa raisi ili kutolewa maamuzi kamili.

***

“Ila Jose una jua Wamarekani ni watu wabaya sana, yaani ni sawa na chui aliye vaa ngozi ya kondoo ambayo ndani yake ni chui wakali na wenye njaa kali”

“Ni kweli hilo unalo lizungumza, kwa kuwaaribia mipango yao na kuwafichua hakika hawato kuwa wana cheza mbali na mimi?”

“Kwa nini sasa ume kataa kulindwa?”

“Mage anaye nilinda mimi ni Mungu na si binadamu hawa wa kaiwada. Hata wao wakinilinda, kama Mungu ata kuwa na kusudi la jambo fulani liweze kutokea hakuna ambaye ata weza kulizuia”

“Tume fanya kazi nyingi na tume weza kufwatilia vitu vingi ila ukweli ni kwamba hii ni vita mpya ambayo ina nipa hofu moyoni mwanagu Jose”

Magreth alizungumza kile kitu ambacho kipo moyoni mwake kwa maana ni kweli ana ogopa hali halisi ya mambo yaliyo tokea.

“Isitoshe makomandoo wanne wame uliwa mbele ya macho yangu, kwa kweli, hii vita tuliyo ichagua sasa hivi ni nguvu”

Maneno uya Magreth yakamfanya Josephine kukaa kimya kwa sekunde kadha huku akimtazama rafiki yake huyo.

“Nini tufanye?”

“Sijui rafiki yangu. Ila tumuombe Mungu tuone ni nini kitakcho tokea”

Magreth mara baada ya kuzungumza hivyo akaondoka sebleni hapo na kuelekea, jikoni. Akarudi sebleni hapo akiwa na sofa mbili za kopo, akamrushia Josephine moja kisha akajilaza kwenye sofa.

“Mage”

“Bee”

“Nime kuingiza kwenye matatizo ehee?”

“Hapana, mimi ndio niliye kuingiza kwenye matatizo. Kutoka kipindi kile cha kina Evans, tulivyo pata ajali kule Morogoro. Yaani ni mambo mengi sana nina yakumbuka, laiti ingekuwa sio ule usiku kwa kweli, leo hii tusinge kuwa hapa”

“Ila lile tatizo liliweza kutufungulia njai. Tumeweza kukutana na watu wakubwa na leo tuna weza kukaa nao karibu ni jambo la kumshukuru sana Mungu”

“Ehee tuachane na hayo, ulimueleza raisi juu ya safari ya Juma tano?”

“Yes na tayari visa imesha katwa na tiketi zipo tayari hivyo ina bidi kujiandaa kwa safari ya kwenda nchini Nigeria”

“Ila sijawahi kufika nchini Nigeria siku hata moja. Ila si tuta pokelewa na mwenyeji wetu?”

“Naamini raisi ata anzaa mtu wa kutupokea”

“Sawa”

Usiku huyo Magreth na Josephine wakautumia katika kutazama filamu walizo zihitaji, walipo choka kila mmoja akaingia chumbani kwake kujipumzisha.

***

“Baba bado huja lala?”

Jery alimuuliza baba yake mara baada ya kumkuta akiwa amekaa sebleni huku akisoma moja ya kitabu.

“Yaa nikikaa huko chumbani na kukiona hicho kitanda, nina hisi kama vile mama yako yupo ndani hapo”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya upole sana huku Jery akimtazama usoni mwake baba yake. Kiulweli baba yake japo ana jikaza kupambana na hali halisi ya kuondokewa na mke wake, ila yupo kwenye kipindi cha majonzi makubwa sana. Jery akaitazama saa ya ukutani na kukuta ni saa nane usiku.

“Baba”

“Naam”

“Twende nje kidogo tuka punge upepo”

“Mke wako vipi?”

“Ame lala muda mrefu”

Raisi Mtenzi akajifikiria kwa muda kisha akakubali ombi hilo.Wakatoka nje na kuelekea kwenye eneo la michezo. Jery akapanga kete za pooltabe kwa maana ana tambua ndio mchezo anao upenda baba yake. Raisi Mtenzi akatabasamu huku akichukua moja ya fimbo ya kuchezea.

“Ndoa yako ina maendeleo gani sasa hivi?”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akianzisha mchezo huo.

“Ina endelea vizuri?”

“Una uhakika?”

“Ndio”

“Kilitokea nini hadi uka enda kumzuia kwa hari za polisi na akarudishwa ikulu?”

Swali la raisi Mtenzi likamfanya Jery kukaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akimtazama baba yake usoni.

“Tulipishana kidogo”

“Hapana sio kidogo, niambie ukweli ni jambo gani ambalo lililo tokea. Mimi ni baba yako na mimi ndio mtu niliye salia kwenye hii duni, endapo ukinificha mambo yanaweza kukuenda kombo huko baadae na ukashindwa kunipa taarifa sahihi”

“Nili lala nje ya nyumbani”

“Ina maana ulikuwa na mwanamke mwengine?”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimkazia macho Jery.

“Ndio baba”

“Una mjua huyo msichana uliye lala naye?”

“Ndio baba”

“Ni nani?”

Maswali ya raisi Mtenzi yakazidi kumbana Jery aliye jikuta akizidi kujawa na kigugumizi kikubwa sana.

“Niambie ni nani?”

“Shani”

“Shani gani?”

“Yule house keeper wetu”

Sura ya raisi Mtenzi ikaanza kujawa na mikunjo kiasi cha kumfanya Jery aanze kujawa na wasiwasi na hofu kwa namna moja ama nyingine ame mkera baba yake.

“Una jua chimbuko la yule msichan hadi ukaaamua kutembea naye. Una ndoa haijamaliza mwezi ila una fanya mambo ya ajabu, hivi una akili wewe. Hakuna mwanamke hata mmoja ambaye ana weza kukaa kwenye ndoa ya kipumbavu kama hiyo. Kama ulikuwa una hisi kwamba haujamaliza mambo yako usinge tupa watu hekaheka za kuandaa harusi ambazo zime igarimu familia yangu na kuigarimu nchi yangu”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka kiasi cha kumfanya Jery ajutie ni kwa nini aliamka usiku huo.

“Mtoto wa watu, ameacha mambo yake yote na kuamua kuolewa na mtu ambaye ume kaa hukoMarekani kwa kipindi kirefu na kutembea na wasichana hadi ukachoka, leo hii una kuja kumuumiza binti wa watu. Mbona mimi baba yenu sikuwa malaya. Hiyo tabia ume jifunza wapi wewe?”

Raisi Jery alizidi kufoka kwa msisitizo.

“Ila baba wewe hujui…..”

“Sijui nini? Nimekaa kwenye ndoa na mama yako zaidi ya miaka arobaini alafu una niambia kwamba sijui. Ulitaka nijue nini zaidi ya kwamba ume endeleza kufungua zipu. Una tembea na mfanyakazi wa ndani kweli, una akli sawa sawa wewe eheee?”

“Ila baba nimesha yamaliza?”

“Umeyamaliza wewe na mke wako ila sio kwangu. Jery sinto hitaji unitie aibu mimi na ile familia ya nabii Sanga, usije ukawafanya wajutie ni kwa nini wamekupatia mtoto wao?”

“Baba ila nilikuta ana tazama picha za Evans Facebook kwa siri”

“So picha tu ndio zime kupagawisha, je ungewaona pamoja unge fanyaje?”

Jery akatamani kumueleza baba yake ukweli kwamba bikra ya Julieth ilikuwa ni feki ila akajihisi kwamba atazidi kuchochea hasira ya baba yake.

“Hili nina kupa onyo la mwisho. Nikisikia una mahusiano na yule mfanyakazi wa ndani, na mke wako yupo ndani, mimi ndio nita kuwa wa kwanza kuivunja ndoa yako na mke wako na asubuhi uje ofisini uchukue hati zako za nyumba ukamuonyeshe mke wako na ninahitaji muende kwa mwana sheria ukaandikishe na jina la mke wako. Tumelewana?”

“Ndio baba”

“Na niweke jambo moja vizuri hapa. Siku nyingine usidhubutu kutumia askari wangu kutatua matatizo ya familia yako. Mimi ndio raisi wa hii nchi, ila sio wewe, tume elewana?”

“Ndio baba”

Raisi Mtenzi akaitupa fimbo hiyo ya kuchezea pool table na kuondoka eneo hilo na kumuacha Jery akimsindikiza baba yake kwa macho tu. Jery akarudi chumbani kwake, na taratibu akapanda kitandani huku akimtazama mke wake aliye katika usingizi mzito sana. Taratibu akajilaza pembeni ya Julieth huku akitafakari maneno ya baba yake, ila alipo kumbuka baadhi ya mikao aliyo kuwa ana fanyiwa na Shani, akahisi kuchanganyikiwa kwani toka aanze kukutana kimwili na wanawake hajawahi kupata penzi tamu kama hilo kutoka kwa Shani.



Usiku kucha raisi Mtenzi hakupata usingizi, akili yake ilizidi kufikiria mambo mengi sana yanayo endelea katika taifa na familia yake kwa ujumla. Ilipo gonga saa kumi na moja kamili asubuhi akaamka, kama kawaida yake akafanya mazoezi mepesi mepesi ikiwamo ya kupiga push up mia moja, kisha akaingia bafuni, akaoga na kujianda akwa ajili ya siku hiyo mpya. Akatoka chumbani kwake na kumkuta Shani akiwa akisafisha eneo la sebleni.

“Shikamoo muheshimiwa?”

“Marahaba, tuongozane ofisini kwangu sasa hivi”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akielekea mlangoni, jambo lililo mfanya Shani kujishauri kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kumfwata raisi Mtenzi hadi ofisini kwake.

“Ume kuja kufanya kazi au kuna kitu kingine una kitafuta?”

Swali la raisi Mtenzi likamuacha Shani kwenye alama kubwa ya kujiuliza kwa maana hajui ajibu nini kwa wakati huo.

“Nakuuliza mbona una nitumbulia macho?”

Raisi Mtenzi alizugumza kwa ukali kidogo hadi Shani akaanza kutetemeka mwili mzima.

“Kazi muheshimiwa?”

“Kwa nini una mvulia nguo mwanangu. Huoni kama amefunga ndoa majuzi tu hapa ehee?”

Shani akahisi haja ndogo ina kwenda kumwagika kwa woga huo.

“Una taka kuivunja ndoa ya mwanangu si ndio?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya ukali sana kiasi cha kumfanya Shani kupiga magoti chini huku akimwagikwa na machozi ya woga.

“Simama, na ninapo zungumza na wewe sihitaji kusujudiwa”

Shani akasimama kwa haraka huku miguu yake akiwa ameifumbata mithili ya askari aliyopo kwenye gwaride huku akiwa amesimama mguu sawa.

“Mwanangu ana mpenda sana mke wake, ndio maana ame muoa. Usihisi kukuvua chupi wewe ana weza kumuacha mke wake ume nielewa?”

“Ndi…iooo mkuuu”

“Kwa usalama wa ndoa ya mwanangu. Kuanzia hivi sasa huna kazi”

Kauli hiyo ikawa ime ustua sana moyo wa Shani, macho yakamtoka, mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi sana kiasi cha kumfanya ahisi giza mbele ya usawa wa macho yake. Akajikaza kumtazama raisi Mtenzi, ila hakuweza kuona kitu chochote zaidi ya maruwe ruwe, akapiga hatua moja mbele ila akahisi mguu wake ukikosa uhimili wa mwili wake na taratibu akajikuta akianguka chini na kuzimia.

Kitendo hicho kikamstua sana raisi Mtenzi na kujikuta akisimama wima, akamuwahi kwa haraka na kumnyanyua kichwa chake, akamuwekea vidole viwili katika shingo yake na kugundua kwamba ame zimia.

“Doktaaa”

Raisi Mtenzi aliita na walinzi wake wakaingia ndani hapo. Wakafanya mawasiliano na daktari wa ikulu na kwa haraka daktari akaitwa na Shani akatolewa ndani hapo huku akiwa amebebwa kwenye kitanda cha matairi na kukimbizwa kwenye hospitali ya ndani ya ikulu hiyo. Raisi Mtenzi, akaitafuta namba ya Jery kwenye simu yake na kumpigia.

“Haloo”

“Njoo ofisini kwangu sasa hivi”

Raisi Mtenzi akakata simu hiyo, baada ya dakika kumi Jery akaingia ndani hapo huku akiwa amevalia pensi na tisheti.

“Ofisi yangu sio ya kihuni na kuniingilia hivyo. Rudi ukavae mavazi ya heshimia?”

Kauli hiyo ikamstua sana Jery, akamtazama baba yake kwa sekunde kadhaa kisha akatoka ndnai hapo pasipo kuzungumza chochote.

“Baby mbona una rudi?”

Julieth alimuuliza mume wake mara baada ya kukutana naye kwenye mlango wa kuingilia ndani ya nyumba hiyo.

“Mzee kanirudisha nibadilishe nguo”

Jery alizungumza huku akiwa amenuna sana. Ikamwalazimu kurudi ndani wakiwa wameongozana na mke wake ambaye alikuwa ana toka kuelekea ofisini.

“Ila mbona hivyo ulikuwa ume pendeza tu?”

“Mzee ana kisirani sasa hivi, yaani hata simuelewi kwa maana sio mara ya kwanza kuingia ofisini kwake nikiwa nimevaa pensi, isitoshe mimi sio mfanyakazi wa hapa ikulu”

“Kwa nini sasa eme kuwa mkali, au ni kutokana na msiba wa mama?”

Jery akamtazama mke wake kwa macho ya masikitiko kisha akavua tisheti hiyo.

“Jana usiku aliniuliza kuhusiana na ugumvi wetu”

Julieth akastuka hata hamu ya kufungua kabati hilo la nguo ikamuishia kabisa.

“Ilikuwaje uka mueleza?”

“Hakuna kitu kinacho endelea hapa ikulu baba asijue. Ila tutazungumza baadae nipe suruali”

Julieth akatoa moja ya suti ya mumewake na kumpatia, huku akilini mwake akiwaza ita kuwaje kama baba yake mkwe huyo ame fahamu kama bikra yake ni bikra.

“Ulimueleza baba kila kitu?”

Julieth alizungumza huku akiwa ana wasiwasi mwingi sana.

“Ndio”

“Ohoo Mungu wangu, Jery hadi siri yangu ume mueleza?”

Jery akamtazama Julieth kwa sekunde kadhaa kisha akatoka ndani hapo pasipo kuzungumza chochote. Jery akaingia ofisini kwa baba yake pasipo kubisha hodi.

“Malaya wako ame anguka yupo hospitalini. Ila akizinduka muambie msimamo wangu upo pale pale, hana kazi”

Jery akamtazama baba yake kwa macho ya ukali kisha akakaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza ya baba yake.

“Hivi una nichukia?”

“Sikuchukii ila nina chukia vitendo vyako”

“Baba mimi ni mwanaume na nilijari. Maisha ambayo mulikuwa muna ishi huko kwenye kipindi chenu ni tofauti na sasa kipindi kilicho jaa tenknolojia ya kila namna. Sawa nime chepuka na kumshawishi mtoto wa watu hadi nikampata kimapenzi. Isifikie kipindi ukatumia hisia za mtu kumuumiza mtu mwengine. Ngoja nikuambie kitu kimoja baba, kama ume mfukuza Shani kazini sawa. Nita mfungulia biashara za kumuendeleza maisha yake na familia yake. Ila ukweli sinto muacha”

Jery alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama baba yake kwa macho makali sana.

“Una akili wewe, hapa ninacho kizungumzia ni kutetea ndoa yako?”

“Ni ndoa yangu na sio ndoa yako. Mimi ndio nitajua jinsi gani ya kuishi na hawa wanawake. Baki kwenye mipaka yako na usijaribu kunipangia kufanya mimi na wanawake zangu”

Raisi Mtenzi akatabasamu kiasha akasimama kwenye kiti chake, akamfwata Jery sehemu alipo kaa, akamshika koti lake la suti eneo la kifuani na kumnyanyua na kumsimamisha wima.

“Ume kua si ndio?”

“Siwezi kukua mbele yako ila ifikie kipindi utambua ukweli, baba mimi sikuogopi, ila nina kuheshimu. Ubabe wako usio wa maana ndio ulipelekea uka fanya maamuzi ya kijinga kumuua mwanao kisa tu alikuwa jambazi. Ulishindwa kukaa nay echini na kumpa malezi, ulikuwa na kazi ya kwenda kufanya opareshei zako na kutuacha nyumbani na mama. Una jua ni malezi gani tulipitia. Watu walikufa kwenye harusi yangu akiwepo mama una hisi ni kwa ajili gani? Nikutokana na maamuzi yako ya kijinga ya kushambulia Al-Shabab mwisho wa siku maelfu ya watu wamekufa. Kama humu ndani ya ofisi yako wanashndwa kukueleza ukweli, nina kueleza ukweli mtupu”

Jery alizungumza kwa kujiamini sana na kumfanya raisi Mtenzi kumuachia koti lake taratibu huku akijihisi maumivu makali sana ya moyo wake kwa maana Jery ame weza kuzungumza ukweli mtupu.

“Laiti usinge fanya mamauzi yale uliyo yafanya, mama yangu, ndugu zangu wengine wangekuwa hai. Mungu hakukupa hiyo nafasi kwa ajili ya kuongoza unavyo jisikia. Ila Mungu huyo huyo kumbuka naye ana watu wake wanyonge kama kina Shani ambao wana ishi kwa ajili ya kazi zao. Nipatie hati zanu za nyumba yangu, nita ondoka ikulu leo na nita kuwa nina kuja hapa kukusalimi tu.”

“Huwezi kuondoka kuondoka hapa ikulu?”

“Kwa nini? Baba hadi nime oa una niambia kwamba siwezi kuondoka hapa ikulu, kweli?”

“Ndio, kichwa changu kwa sasa hakipo sawa. Wewe ndio mtu wa pekee ninaye kuamin kwenye maisha yangu. Baki na mimi, hapa ume nielewa?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya upole hadi Jerya kaingiwa na imani na kuanza kumuoena huruma baba yake.

“Mama yako ame kufa, nina hisi kuchanganyikiwa. Yeye ndio mtu wa pekee aliye kuwa akiniwezea mimi, tafadhali, kamuangalie yule binti hospitali, jaribu kumuweka sawa na ata endelea kufanya kazi kama kawaida na kama mukiendelea kufanya mambo yenu ila hakikisha kwamba mke wako hatambui. Ume nielewa?”

“Ndio baba”

Jery akashusha pumzi nyingi kishaa akatoka ndani ya ofisi hiyo. Akaingia hospitalini na kumkuta Shani akiwa amekaa kitandani huku akilia kwa uchungu sana.

“Jery tafadhali nina kuomba utoke humu ndani”

Shani alizungumza kwa uchungu sana hukua kimnyooshea Jery kidole.

“Nesi tupishe”

Nesi akatoka ndani hapo na Jery akaufunga mlango huo kwa ndani na wakabaki wawili.

“Jery ume niharibia maisha yangu. Familia yangu itaishije, ikiwa kazi hii mimi ndio nilikuwa nina itegemea”

Shani alizungumza kwa masikitiko sana. Jery akaka pembeni yake na kumshika mkono wake.

“Niangalie”

Shani akanyanyua uso wake taratibu nakumtazama Jery.

“Nime zungumza na baba na ameweza kuelewa kila kitu kilicho tokea”

“Jery aha kunifariji ikiwa baba yako hakuwahi hata siku moja kunifokea wala kunionyeshea hali aliyo nionyesha”

“Shani sikia kama una hitaji hii kazi niambie na kama huihitaji pia niambie”

“Ninge kua nina umia kama nilivyo umia sasa hivi?”

“Sasa mimi nina hitaji ubadilishe maisha yako”

“Kivipi ikiwa kazi yangu hii ndio nina itegemea”

“Nina hitaji ufanye biashara, ili penzi letu liweze kuwa salama”

“Natolea wapi pesa Jery?”

“Nita kupatia, fikiria ni biashara gani una hitaji kuifanya kisha uta nipatia jibu. Ila acha kulia na hakuna kilicho haribika kati yangu mimi na wewe”

Jery mara baada ya kuzungumza hivyo akaanza kumnyonya Shani lipsi zake kisha akatoka ndani hapo na kumuacha Shani hakiwa ajui amini kipi, kati ya maneno ya Jery au raisi Mtenzi.

***

“Huyo msichana ni muhimu sana kuliko hata hizo pesa na wanacho kiomba. Hivyo wapatiwe kila kitu”

Raisi wa Marekani alizungumza na jenerali Ambros.

”Ila muheshimiwa wana hitaji na mkataba wa maandishi. Huoni kama hiyo siri ikivuja ita tia doa taifa?”

“Hawawezi kutusumbua hao wajinga. Baada ya hili jambo kuishi, tuta ua kundi moja baada jengine”

“Kwa hio muheshimiwa tuwapatie mkataba?”

“Ndio”

“Ukiwa na saini yako”

“Ndio”

Jenejali Ambros akaka kimya kwa sekunde kadha kwa maana hicho kinacho fanyika ni kinyume na sheria ya nchi na mamlaka ya raisi kuweza kudhamini makundi ya kigaidi. Mkataba huo ukaandaliwa kisha raisi akatia saini, Ukatumwa nchini Nigeria kwa kupitia barua pepe. Meja Kane akautoa nakala mbili kisha akaelekea kwenye kambi ya Bokoharamu. Wakasaini mkataba huo kati yao pna nchi ya Marekani, huku kikundi cha Al-Shabab nao wakisaini mkataba huo huo.

“Tuna muhitaji huyu msichana akiwa hai, tume elewana?”

“Ndio”

“Angalizo hatuhitaji kumwaga damu za watu wengine”

“Hata tukishambiwa?”

“Labda itokee mume shambuliwa”

“Sawa”

“Kwa sasa muta ingiziwa dola milioni tano baada ya kazi kukamilika muta pata dola nyingine milioni tano. Solaha nita zileta leo usiku”

“Sawa,tuta watuma vijana wetu wawili nchini Tanzania”

“Angalizo jengine, Tanzania kwa sasa ina ulinzi mkali sana hivyo ina wapasa kuwa makini sana na isitoshe Wasomalia muna sakwa sana”

“Wata kwenda wasichana wangu”

Mkuuw Bokoharamu aliozungumza na kikao hicho kikamalizika na sajenti Kane akarudi kambini. Maandalizi ya wasichana wawiliwa Kinaijeria walio na maumbo mazuri sana wakakata tiketi za haraka haraka pamoja na visa kisha safari ya kuelekea nchini Tanzania ikaanza huku kazi yao ikiwa ni moja tu. Kuhakikisha wana mteja Josephine.

***

Makubaliano ya wanajeshi wa Marekani nchini Tanzania, yakafanyika kwa njia ya maandishi, kisha raisi Mtenzi akamsindikiza makamu wa raisi wa nchi ya Marekani hadi uwanaja wa Taifa. Akapanda ndege yake na wapambe wake wote alio kuja nao nchini Tanzania kisha akaondoka. Raisi Mtenzi mara baada kukamilisha jukumu hilo, akarudi ikulu na kumkaribisha raisi wa nchi ya Rusia kama ratiba yake hiyo ya kazi inavyo mpasa kufanya. Lengo kuu la kikao hicho ni kuendelea kujadiliana kuhusian ana uhusiano wa nchi ya Tanzania na Rusia. Wakaahidia katika kushirikiana katika kuwafundisha wanajeshi wao katika nyanja zima za utengenezaji wa silaha kubwa za kisasa. Mazungumzo hayo yakaenda vizuri kisha akamsindikiza raisi huyo wa Russia uwanaj wa ndege na yeye akaondoka nchini Tanzania.

“Pole muheshimiwa”

Josephine alizungumza kwa maana kuna kikao kingine na raisi wa Ghana Ikulu.

“Nashukuru, leo nin aona siku yangu ina kuwa ngumu sana”

“Ni kweli, ila ina bidi ratiba zote tuzikamilishe”

Wakarudi ikulu na baada ya dakika ishirini, wakampokea raisi wa Ghana na kikao kikaanza mara moja. Kikao hicho kina husiana na maswala ya kiusalama huku raisi wa nchi ya Ghana aki ahidi kwamba atasaidia na nchi ya Tanzania katika kupambana na ugaidi ikiwemo katika kulisaka kundi la kigaidi la Al-Shabab ambalo kwa sasa wana uhakika lipo ndani ya nchi ya Nigeria.’

“Naona kitu”

Josephine alijikuta akizungumza akiwa katikati ya kikao hicho cha maraisi pamoja na washauri wao. Watu wote wakamtazama kwa maana haikuwa ni zamu yake ya kuzungumza.

“Umeona nini?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza.

“Hapo kwenye kundi la Bokoharamu, nime weza kuona eneo walipo”

“Samahani muheshimiwa raisi, chief staff wako ame ona vipi?”

“Ahaa muheshimiwa ni mambo ya kipelelezi, endapo tuta yakamilisha basi tuta zungumza kwa pamoja”

“Sawa, nina shukuru sana kwa muda wenu”

“Nawe pia”

Mara baada ya kikao hicho raisi Mtenzi akamsindikiza raisi huyo wa Ghana na kisha akarudi ikulu kwa ajili ya kuzungumza na washauri wake ili kutathimini yote waliyo weza kuyafanya katika siku hiyo.

“Ehee Jose une ona nini?”

Raisi Mtenzi alimuuliza Josephine mara baada ya kukianzisha kikao hicho.

“Nina ona kambi ya kundi hilo la Bokoharamu ndani yake wakiwepo Al-Shabab na nina ona wana mipango mibaya dhidi yangu”

Raisi Mtenzi, Mr the Brain, Julieth pamoja na mzee Mbogo wakastuka kidogo.

“Mipango gani mibaya dhidi yako?”

Mzee Mbogo aliliza huku akiwa na shahuku kubwa ya kuhitaji kufahamu jambo hilo.

“Nina ona wasichana wawili wa nchi ya Nigeria ambao wana fanya kazi na Bokoharamu, wata ingia chini Tanzania kwa ajili ya kuniteka na kunipeleka katika kundihilo na nina onyeshwa na Mungu kazi hiyo wametumwa na watu ambao wana nihitaji mimi”

Josephine alizungumza kwa sauti ya upole na nyonge kidogo.

“Wasichana wenyewe wataingia na ndege ya saa ngapi?”

MzeeMbogo aliuliza huku akimtazama Josephine usoni mwake.

“Sijaonyeshwa wana ingia Tanzania saa ngapi, ila ni lazima waingie nchini Tanzania”

“Walio watuma je umeonyeshwa?”

Josephine aliliza huku akiwa ana shahuku ya kujua jambo hilo.

“Hapana, bado sija wajua, ila huu ndio wakati wa kuweza kuwajua maadui zetu halisi. Nipo tayari waniteke ila katika kipindi kile cha kumfwatilia muhusika wa mambo yote yaliyo tokea, ikiwemo jambo la kuingiza madawa ya kulevya nchini na aliye niteka hivi majuzi. Nina imani muheshimiwa una fahamu nini ninacho kizungumza?”

Raisi Mtenzi alitingisha kichwa akimaanisha kwamba ana fahamu mpango huo, jambo ambalo likaanza kumfanya Julieth kujawa na wasiwasi kwa maana anaye zungumziwa hapo ni yeye na baba yake mzazi, isitoshe bado ana wasiwasi wa siri yake ya bikra feki, ime mfikia babayake mkwe huyo ambaye ana muogopa sana kwa ukali wake.



“Ila Josephine Bokoharamu na hao Al-Shabab ume ona walicho kifanya kwenye hii nchi?”

Mzee Mbogo alihoji huku akimtazama Josephine usoni mwake.

“Ndio nime ona ila hawawezi kunifanya jambo lolote baya kwangu kwa maana kuna watu nyuma yao wana wadhamini katika hili”

“Ila hiyo ishu ni hatari Jose”

Mzee Mbogo aliendelea kusisitiza.

“Ni kweli mzee wangu ila ina bidi kufanya hivyo kwa ajili ya kuweza kumaliza haya matatizo”

“Sawa hilo tuta lijadili kesho ila kuna jambo moja ambali nilihitaji kulijadili kwa pamoja. Kama munavyo fahamu kwa sasa nchi haina makamu wa raisi”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama mzee Mbogo usoni mwake.

“Nchi haiwezi kwenda pasipo kuwa na makamu wa raisi”

“Ni kweli muheshimiwa”

Mr the Brain alizungumza huku akimtazama raisi Mbogo.

“Nyinyi ndio watu wangu wa karibu sana na nyinyi ndio watu pekee ambao muna fahamu kwa sasa nchi hii ina kwenda vipi. Jana niliweza kumuomba mzee wangu, mr Mbogo kuwa makamu wangu wa raisi, japo hajanipatia jibu bado ila nime weza kumuomba aweze chukua nafasi hiyo”

“Ni mtu sahihi, huja kosea muheshimiwa”

Josephine aliunga mkono jambo hilo na kumfanya mzee Mbogo kumtazama kwa macho ya mshangao kwa maana hadi wakati huo bado hakuwa na jibu sahihi kama yupo tayari kuwa makamu wa raisi.

“Jamani mume lipitisha hili?”

Raisi Mtenzi aliwauliza watu wote na wakaunga mkono.

“Japo tume lipitisha hili ila muheshimiwa ninge omba tusikie upande wa mr Mbogo kama yupo tayari au laa?”

Mr the Brain alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.

“Mbogo tuna kusikiliza”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya upole. Mzee Mbogo akashusha pumzi nyingi sana huku akiwatazama watu wote waliomo ndani ya ofisi ya raisi.

“Muheshimiwa raisi kama unavyo fahamu, mimi sio mwana siasa. Nime ishia kwenye maisha ya ujasusi kwa kipindi kirefu, kifupi ni maisha yangu yote nime ishi kwenye maisha hayo. Leo una nipa jukumu la kuwa makamu wa raisi, hivyo nina hisi kwamba ita nichukua mud asana kuweza kuelewa mfumo wa serikali”

Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya unyonge kidogo.

“Ngoja nikuambie ndugu yangu. Mimi pia nilikuwa askari na una fahamu hilo. Ila niliweza kuingia kwenye siasa na nika fanikiwa kuwa raisi na leo nchi ina kwenda.”

“Ni kweli muheshimiwa. Namuomba Mungu aniongoze katika hilo, nipo tayari”

Mzee Mbogo alikubaliana na ombi hilo na likawafanya watu wote kupiga makofi.

“Nina kushukuru sana ndugu yangu. Nina imani tuta endelea kuombeana kwenye hili jambo”

Raisi Mtenzi na mzee Mbogo wakakumbatiana. Josephine akaomba nafasi ya kuwaombe kisha kikao hicho kikavunjika huku wakipanga kumuapisha mzee Mbogo baada ya siku tisini.

“Julieth naomba ubaki”

Raisi Mtenzi alizungumza na kumfanya Josephine mapigo yake ya moyo kuanza kumuenda kasi sana kwa maana ana tambua ni jambo gani lililo mpelekea mume wake asubuhi ya siku hiyo kurudishwa. Baada ya watu kotoka mazungumzo ya Julieth na baba yake mkwe yakaanza.

“Ni nini kinacho endelea kwneye ndoa yenu?”

Swali la raisi Mtenzi likamfanya Josephine kukaa kimya kwa sekunde kadhaa.

“Aha…baba…tupo saalama tu?”

“Una nidanganya Julieth. Niambie ukweli kwa maana nimesha zungumza na Jery na amenieleza kila kitu”

Mapigo ya moyo ya Josephine yakazidi kwenda kasi sana, wasiwasi mwingi ukazidi kumtawala..

“But it’s okay. Ila kuwa makini sana na Jery. Chochote atakacho kufanya au kukufanyia kibaya hakikisha una nieleza. Umenielewa mwanangu”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa upendo ndani yake. Hali hiyo ikamfanya Julieth kushusha pumzi nyingi huku mapigo yake ya moyo yakianza kutulia taratibu.

“Sawa baba”

“Una weza kwenda kupumzika”

“Asante”

Julieth akasimama na kutoka ofisini hapo huku akimuacha raisi Mtenzi akimtathimini kwa uzuri wake.

‘Hakika sisi wanaume haturidhika. Mwanangu amepata binti mzuri ila ana kwenda kupambana na mikurumbembe’

Raisi Mtenzi alijisema kimoyo moyo huku akianza kufunga mafaili yake kwa ajili ya kutoka ofisini kwake hapo kwa maana tayari muda umesha kwenda.

***

Josephine akafika nyumba na kukuta Magreth akiwa amesha andaa chakula cha usiku. Akamsimulia jinsi vikao na maraisi wa nchi tatu tofautu jinsi vilivyo kwenda. Akamsimulia kuhusiana na kuchaguliwa kwa mzee Mbogo kuwa makamu mpya wa raisi. Ilipo fikia wakati wa kuzungumzia kuhusiana na swala la kutekwa kwake na wasichana wa Bokoharamu, kidogo akaa kimya huku akilitafakari namba atakavyo liwasilisha jambo hilo kwa raifiki yake kipenzi.

“Kuna jambo jengine hatari”

“Jambo gani?”

“Katika safari ya kulekea nchini Nigeria ni lazima nitekwe”

“Nini?”

“Ndio ni lazima nitekwe”

“Na nani?”

Magreth alizungumza hukua akisitisha kabisa zoezi la kula chakula hicho wanacho kula.

“Na kundi la Bokoharamu wakishirikiana na Al-Shabab”

“Mungu wangu, hivi una hisi kwamba ukikamatwa huko una weza kwenda kusalimika ehee?”

“Ila Mage tambua Mungu yu pamoja nami?”

“Hata kama, yaani ni sawa na mtu anaye jiweka mbele ya treni ya umeme, alafu ana sema asigongwe cse Mungu yupo pamoja naye. Muda mwengine ina bidi uweze kumuuliza Mungu wangu ni kwa nini ana fanya hayo mambo, umenielewa?”

Julieth alizungumza huku dhahiri akionekana kupinga jambo hilo.

“Ila Mage hii ni nafasi ya kuwajua ni kina nani maadui zetu?”

“Achana na upumbavu huo. AL-Shabab walio ua maelfu ya watu katika hii nchi alafu sasa hivi una niambia sijui ndio nafasi ya kumjua adui yetu. Yeye kwanza ni adui yetu namba moja ana tosha kabisa kuhukumiwa kwa kile walicho kifanya hapa nchini”

“Huja ielewa maana yangu Mage”

Josephine aliendelea kuzungumza kwa sauti ya upole na unyenyekevu kwa maana tayari Magreth amepandisha hasira.

“Una maana gani tena, au una taka nianze kuingia msituni na kuwasaka hao Bokoharamu na Al-Shabab. Hivi ujiulizi hadi wana kutafuta wao una hisi hapo uta kuwa salam kweli wewe? Najua Mungu ana kuongoza ila muda mwengine ina bidi kumuomba Mungu akuepushie vitu vya ajabu kwa maana hadi kukutoa mikononi mwa hao Al-Shabab ni lazima damu za watu zimwagike. So una furahia kuona damu za watu zina mwagika au?”

Magreth aliendelea kufoka kwa msisitizo na kumfanya Josephine kukaa kimya.

“Raisi hato leta tumbo lake katika oparesheni ya kukutafuta. Nitakaye pata tabu na kuumia ni mimi na wengine, kama yeye kakukubalia badi nina wasiwasi na uwezo wake wa akili”

“Hapana Mage usifike huko?”

“Sio nisifike huko. Ungekuwa wewe ni mtoto wake alafu una ambiwa ukamatwa na Bokoharamu pamoja na Al-Shabab angekubali yeye?”

Josephine akakaa kimya ikiwa ni ishara ya kukosa jibu la swali hilo la Magreth.

“Sasa nina kushauri kama ndugu yangu. Nitapambana hadi dakika ya mwishokama hakuna njia nyingine ya kumjua adui, ni heri tuachane na hiyo kazi. Tuna pesa ya kutosha na tuna weza kusimamisha mgahawa mpya ambao tuta endelea kufnaya kazi kama kawaida. Umenielewa”

Josephine akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Magreth.

“Jose ume nielewa?”

“Nimekuelewa. Ila usikate tamaa mapema katika hili?”

“Nisikate vipi tamaa. Ngoja nikuambie sifa ya hao unao jilengeshwa kwao ili wakukamate. Watakubaka wewe na hawato jali kama ume okoka au laaa, sasa wewe jichanganye tu kwa kuamini kwamba huko una pokwenda ni peponi.”

Magreth mara baada ya kumaliza kuzungumza kauli hiyo akaendelea kula huku akijaribu kuishusha hasira yake iliyo mpanda. Kitendo hicho kilimuuzunisha sana Josephine, mara baada ya kumaliza kula akaelekea chumbani kwake, akapiga magoti pembeni ya kitanda chake na kuanza kusali huku akimuomba Mungu amsaidie katika jambo hilo lililopo mbele yake.

***

Jery akamtazama mke wake huku wakiendelea kupata chakula hicho cha usiku. Akatamani kumuonyesha hati za jumba alilo nunua ila akajikuta akisita kwa maana bado moyo wake una kuwa mzito sana kufunguka mambo mengi mbele ya mwanamke huyo. Simu ya Julieth ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akajifuta mikono yake na kitambaa cha kufutia mikono kisha akaipokea.

“Shikamoo baba”

“Marahabaa, habari ya wewe”

“Sawa za nyinyi?”

“Tuna mshukuru Mungu vipi mama?”

“Mama yako yupo salama. Upo na mumeo hapo?”

“Ndio”

“Mpatie simu”

Julieth akaishusha simu yake hiyo kutoka sikioni mwake na kumtazama mume wake.

“Baba ana hitaji kuzungumza nawe”

“Ohoo”

Jery naye akafunta mikono yake kisha akaipokea simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Baba shikamoo”

“Marahaba muna endeleaje na ndoa yenu”

“Mungu anasaidia baba. Tupo salama”

“Basi ni jambo la kumshukuru Mungu. Mimi na mama yako mkwe tuna waombea kwa Mungu.”

“Nashukuru sana baba”

“Basi niwatakie usiku mwema”

“Nanyi pia baba”

Jery akamrudishia simu Julieth na akaiwaka sikioni mwake.

“Baba”

“Yes, vipi kuna jipya?”

“Ndio”

“Una weza kupata muda wa kuzungumza sasa hivi?”

“Hapana baba labda kwa kesho”

“Sawa hakikisha una nipatia kila taarifa inayo endelea”

“Nashukuru baba”

Julieth alizungumza huku akitabasamu.

“Haya usiku mwema”

“Nawe pia baba. “

Julieth akakata simu na kuirudisha mezani.

“Mke wangu”

“Bee:”

“Nahitaji tujenge nyumba ya pamoja”

“Ni wazo zuri sana mume wangu”

“Hivi wewe huna nyumba hapa mjini?”

“Zipo ila ni za familia. Hivyo siwezi kusema kwamba ni za kwangu moja kwa moja”

“Aahaa wewe una penda kuwa na nyumba ya aina gani?”

“Kubwa na yenye mandhari mazuri ambayo hapo baadae watoto wetu wata pata nafasi nzuri ya kucheza”

“Sawa, nitatafauta injinia wa ujenzi kisha tuta ianza kazi hiyo mara moja kwa maana nina hitaji tuondoke hapa ikulu na pia nina hitaji tuanzishe biashara za kifamilia ambazo mimi na wewe tuta shiriki kwa asilimia mia moja. Baba amebakisha miaka mitatu ya kumaliza muda wake so akimaliza mama huto kuwa na kazi aisee”

“Ni kweli mume wangu. Mimi nipo tayari kufwata kile unacho kizungumza”

“Nashukuru kusikia hivyo”

Wakamaliza kupata chakula hicho cha usiku. Jery akanyanyuka na kutoka nje. Akakutana na Devi mlinzi wake ambaye alimpatia jukumu la kumsindikiza Shani hadi nyumbani kwake.

“Ehee nipe ripoti ime kuwaje?”

“Nime mfikisha kwake na kumpatia maagizo yale uliyo niambia”

“Safi, natamani nika lale naye usiku huu ila daa siwezi kutoka wife ata zingua na mzee vile vile”

“Jery tulia. Nahisi sasa hivi huoni umuhimu wa mke wako, ila siku akiondoka mikononi mwako ndio uta jua umuhimu wake. Huyu Shani mfanye kama wale wanawake wengine ulio kuwa una wachapa kisha una tembea. Nakupa ushauri kama rafiki yako wa kipindi kirefu. Ukiupenda ufanyie kazi ila usipo upende sawa upuuzie, ila usimumize Julieth”

Devi alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Jery usoni mwake.

“Usijali kaka nina jua nini nina fanya”

Jery alijibu kimzaha mzaa, wakaagana na Devi kisha akarudi ndani. Moja kwa moja akapitiliza hadi chumbani kwake na kumkuta mke wake akivua nguo kwa ajili ya kuoga. Taratibu akamsogelea na kumkumbatia kwa nyuma, akakishika kiuno chake na kuanza kukitomasa taraibu. Hali hiyo ikampelekea Julieth kusisimka kwa kiasi kikubwa na taratibu wakajikuta wakiingia kwenye dimbwi zito la mahaba.

***

Majasusi wa kike wa kikosi cha wapiganaji cha Bokoharamu wakafika katika uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere. Wakatazama ramani waliyo pewa ya eneo ambalo ana patikana Josephine. Wakakodisha takisi na kuombwa kupelekwa kwenye mtaa huo. Walipo fika, wakashuka kwenye taksi hiyo na kumlipa dereva ujira wake kisha akaondoka. Kwa kutimia simu ya mmoja wao waliweza kufwata location inayo onyesha eneo ambalo ana ishi Josephine. Mita kadhaa kutoka eneo ambalo nyumba ya Magreth ipo, wakasima huku wakiitazama kwa umakini.

“Pale ndipo anapo ishi”

Mmoja wa wasichana huyo ambaye mkononi ameishika simu yake hiyo, alionyesha nyumba ya Magreth.

“Vipi signal ina onyesha yupo ndani?”

“Ndio”

“Ina bidi hii kazi tuifanye usiku huu huu na kama kurudi nchini Nigeria, ina bidi turudi usiku huu huu au una semaje?”

“Yaa hatuna muda wa kupotea”

Wasichana hao walishauriana huku kila mmoja akifungua pochi yake. Wakatoa vipande vipande vya bastola zilizo gawanyishwa kisha wakaanza kuziunga kwa uharaka na ndani ya muda mchache wakawa wamesha kamilisha zoezi hilo na wapo tayari kwa ajili ya kuielekea katika nyumba ya Magreth.



Mwanga wa taa ya gari linalo kuja kwa mbali kidogo likawafanya kuzirudisha bastola zao kwenye pochi zao, huku wakilisindikiza gari hilo kwa macho ambalo, walijikuta wakistuka sana mara baada ya gari hilo la polisi kusimama kwenye geti la nyumba ya Magreth. Wakashuka askari sita wenye bunduki huku wakiwa wamevalia majaketi ya kuzuia risasi. Wasichana hao wakajibanza kwenye moja ya mti na kuendelea kutazama kinacho endelea.

Kengele ya getini ikamfanya Magreth kuichukua simu yake na moja kwa moja kuitazama upande unao rekodi kamera hizo za getini. Akastuka kidogo kuwaona askari hao wakiwa wamesimama hapo, akaingia chumbani kwake, akachukua bastola kisha akarudi sebleni. Akahesabu idadi hiyo ya askari polisi kisha akatoka nje huku bastola yake akiwa ameichomeka kiunoni mwake kwa nyuma.

“Nani?”

Magreth alizungumza huku akisikilizia jibu atakalo pewa na askari hao.

“Sisi ni jeshi la polisi tume agizwa na RPC Karata”

“Kufanya nini?”

“Kuimarisha ulinzi wenu”

Magreth akajifikiria kwa sekunde kadha akisha akafungua geti hilo. Akatazamana na askari huyo kwa sekunde kadha kisha askari huyo akatabasamu.

“Kwa jina nina itwa Emily ni kiongozi wa hichi kikosi hapa. Tume agizwa na RPC Karata kuimarisha ulinzi wa nyumba yenu”

Afande Emily alizungumza huku akimkabidhi Magreth kitambulisho chake cha kazi. Magreth akakipitia kitambulisho hicho kwa sekunde kadhaa kisha akamkabidhi.

“Okay so muna imarisha kwa usiku huu au?”

“Hapana ni jukumu endelelevu hadi pale tutakapo pangiwa mahala pengine, ila tuta kuwa tuna pokezana na askari wengine kila baada ya masaa kumi na mbili”

“Sawa karibuni ndani, naamini muna jua jinsi ya utendaji wenu wa kazi?”

“Ndio”

“Si muna linda eneo la nje ila si hadi ndani?”

“Yaa ni eneo la kuzunguka nyumba yako”

“Okay usiku mwema”

“Nawe pia dada”

Magreth akaingia ndani na kumuacha Emily akipanga vijana wake. Magreth akafunga mlango wa mbele wa kuingilia sebleni, akaichomoa bastola yake na kuiweka mezani kisha akaichukua simu yake na kutafuta RPC Karata.

“Kaka habari ya muda huu”

“Safi Mage aisee vijana wangu wamesha fika hapo nyumbani kwako?”

“Ndio, ila ni suprize kaka, vipi tena?”

“Nimepewa oder na raisi usiku huu wa kutuma vijana hapo kwenu kwa ajili ya kuwalinda”

“Ahaa…sawa sawa. Asante kwa hilo kaka”

“Nashukuru usiku mwema”

“Nawe pia”

Magreth akakata simu hiyo na kushusha pumzi nyingi. Akatembea hadi mlangoni mwa chumba cha Josephine akashika kitasa akajaribu kuusukuma mlango huo ila akasikia jinsi Josephine anavyo sali, hivyo akaona sio muda sahihi kwa yeye kumsumbua rafiki yake huyo.

***

“Tufanyaje”

Pili alimuuliza mwenzake huku wakitazama jinsi askari wanavyo jipanga katika geti la nyumba ya Magreth.

“Hata sijui tufanye nini rafiki yangu.”

Hawa naye alijibu.

“Au tuwashambulie?”

“Hapana hatujui wezetu wamejipanga nini na hatujui ni kwa nini askari wapo eneo hilo. Jambo la msingi, tutafute hoteli tulale na tujipange kwa ajili ya siku nyingine.”

Pili alijibu kwa suai ya upole kwa maana mpango wao ume vurugika. Wakatembea hadi bararaba ya lami, wakakodisha taksi na kumuomba dereva awapeleke kwenye hoteli yenye hadhi ya juu hapo Kigamboni. Moja kwa moja wakafikishwa kwenye moja ya hoteli, wakamlipa dereva taksi kisha wakalipia chumba kimoja katika hoteli hiyo kisha wakakabidhiwa kadi ya kufungulia mlango. Wakaingia kwenye chumba hicho na kuanza kukikagua vizuri, walipo jiridhisha hakina kamera za siri ambazo mara nyingi huwa zina kaa kwenye taa na kwenye kuta, wakaanza kufanya mazungumzo na viongozi wao walipo nchini Nigeria kwa kutumia mfumo wa video kupitia laptop ambayo yao.

“Kwa hiyo mkuu ita tubidi hii kazi ituchukue muda kidogo kwa maana muhusika nina ona amewekewa ulinzi wa askari polisi”

Hawa alizungumza huku akitazamana na mkuu wake huyo.

“Ina maana ana lindwa?”

“Ndio mkuu”

“Nina tambua kwamba mukia askari muta shindwa kutoka kwenye hiyo nchi. Hivyo hakikisheni kwamba muna tumia akili ya kiwango cha hali ya juu kabisa. Tume elewana”

“Ndio mkuu”

“Usiku mwema”

“Tuna shukuru mkuu”

Hawa akakata simu hiyo na kumgeukia Pili aliye simama pembeni yake.

“Hembu jaribu kuangalia detail za huyu binti kama ana safari yoyote, aliyo kata tiketi kupitia mtandao?”

Pili alizungumza na Hawa akainaza kazi hiyo mara moja. Uzuri ni kwamba wote wapo vizuri kwenye mambo tenkonolija. Wakaanza kupitia kwenye mashirika ya ndege moja baadaya jengine.

“Bingo”


ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

BLOG