Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MY LIFE SEHEMU YA 4/10

 

 


 MY LIFE

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 4 KATI YA 10

 


Eddazaria aliwasalimia kwa pamoja.

“Safi kaka Eddy”

Mlio wa simu yangu ukanifanya nitoke kwa haraka katika wodi hii yenye wangojwa wengine. Nikaitoa simu yangu mfukoni na kukuta ni namba ngeni ambayo ndio inapiga. Nikaipokea simu na kuiweka sikioni huku nikitafuta eneo zuri ambalo ninaweza kuzungumza.

“Bari yako Jojo”

Niliisikia sauti ya kiume yenye lafudhi ya kihidi.

“Salama tu”

“Mimi Kanjubai, yule taka fanya tangazo hapa katika gahawa yangu”

“Ndio ndio mzee nimekupata”

“Pata habari, maliza shoot filamu yako, mimi taka wewe weza fanya sasa lile tanagazo ambia weza fanya”

“Ohoo sawa sawa muheshimiwa ila kwa sasa nipo safarini, baada ya wiki moja nitakuwepo Dar es Saalam, hivyo basi tutawasiliana”

“Sawa sawa Jojo, takia wewe safari njema”

“Asante mzee”

Nikakata simu na kuirudisha mfukoni mwangu, nikaanza kupiga hatua kuelelea katika wodi niliyo waacha wezangu. Kabla sijafika simu yangu ikaita tena, nikaitoa mfukoni na kukuta namba kutoka nchini China, mapigo ya moyo yakaanza kunianda kasi, kwani moja kwa moja inaonyesha anaye nipigia ni Nuru, nikarudi katika sehemu niliyo kuwa nimesimama, nikaipokea simu hii.

“Hongera sana kwa hatua uliyo fikia”

Niliisikia sauti ya Nuru ilio nifanya niweze kuamini kwamba hisia zangu zilikuwa sawa kwa asilimia mia moja.

“Hongera ya nini?”

“Ya kwenda kutambulishwa ukweni”

Moyo ukanipasuka sana, kwani habari hii ya kwenda kutambulishwa nyumbani kwa kina Eddy ni sisi wawili tu ndio tunaijua, hata kuijua kwangu nimeweza kuifahamu asubihi ya kuamkia leo.

“Nania amekuambia ujinga kama huo”

“Hahaaa, kutambulishwa ni ujinga, Jojo umesahau kwamba ulikuwa kapuku wewe, tena mbeba madawa ya kulevya. Ulikuwa ufungwe na kuozea jela, ila kwa pesa yangu nikakufanya uonekane mtu, na uepuke na kifunguo hicho”

“Si bishi, kwa maana hata nia yangu ya kuja China, nilikuja kutafuta pesa ila niwe tajiri siku moja, sishangai kwa hilo unalo niamabi”

“Hahaaaa…….narudia umeniharibia biashara yangu niliyo kuwa ninaingiaza mabilioni ya pesa, sasa ninakuambia kwamba ni lazima itakugarimu sana maishani mwako, umenielewa?”

“Kutokana na dhambi ambayo uninishurutisha niweze kuifanya, naamini hata Mungu yeye mwenyewe atanisimamia na hakuna kitu kibaya ambacho unaweza kunifanya sawa Nuru. Kumbuka hata mimi niliweza kuyaokoa maisha yako, laiti ingekuwa sio mimi Sosiono angekuwa amesha kuchinjilia mbali”

“Hahaaa…….leo hii una Mungu wewe, umesahau ulivyo kuwa unaninyonya kum** na mkund** eheee?”

“Shida ndio zilinifanya niwe hivyo, ila kumbuka mimi ni binti mdogo, ninahitaji kuwa mama siku moja, wewe kum** yako inaweza kunipatia shahaw** mimi ehee. Nimepata mwanaume ninaye mpenda na ananipenda, sasa ngoja nikuambie kitu kimoja, sikuogopi Nuru, na kama unaanzisha vita ili kunikabili mimi, ninakuambia ukweli hapa kwangu umedunda, nitakufanya kitu ambacho hukuwahi kufanywa kwenye maisha yako umenielewa?”

“Hahaahaha……wacha weee”

“Sema niache tu, ila siku nitakuja kusambarataisha hicho kichwa chako, naamini ulishuhudia matukio yangu, sinaga huruma”

“Ahaaa…kwa hiyo unataka tuianzishe vita”

“Anzisha vita, laiti ungekuwa unanitia mbo** na kuniridhisha hapo sawa, kumbe tunasuguana suguana kum** zetu, huwezi kunifanya chochote. Kwanza wewe ni bibi mtu mzima tafuta bibi mwenzio akuridhishe”

Nilizungumza kwa hasira na kwa msisitizo mkali sana hadi machozi yakaanza kunilenga lenga usoni mwangu.

“Umedhamiria ehee?”

“Nimedhamiria na achana na maisha yangu, kenge, malaya mkubwa wewe. Kazi kueneza usagaji ikiwa dunia inapinga, jiweke mbo** bandia basi ujulikane na wewe unamilikia mwanamke”

Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, nikakata simu yangu na kuizima kabisa, nikajipangusa machozi yaliyo nimwagika usoni mwangu. Nikashusha pumzi taratibu na kujiweka vizuri mavazi yangu. Nikarudi wodini na kuwakuta wezangu wakiendelea kupiga story na wagonjwa, walio jaa uchangamfu. Eddazaria akanitazama kwa macho yaliyo jaa uchunguzi, japo ninajitahidi kuonyesha furaha ila kusema kweli nimekasirika, na moyo wangu umejawa na chuki kubwa sana dhidi ya Nuru.

“Hei vipi upo poa?”

Eddazaria aliniuliza huku akinigonga kidogo kwa bega lake, kwani nimesimama karibu naye.

“Yaa nipo safi”

“Kabisa?”

“Ndio baby”

“Sawa.”

Tukaendelea kuzungumza zungumza na wagonjwa hadi kumi nambili jioni, tukaingia kwenye gari na kuendelea na safari huku tumiwaacha wagonjwa na mwenzao mmoja aliye jitolea kuwahudumia. Tukiwa katikakati, Eddazaria alinionyesha vijiji kadhaa, na kunitajia sifa na shuhuli wanazo jishuhulisha watu katika vijiji hivyo.

“Hapa panaitwa Kange, ndipo anapo ishi mama yako Mkwe, ila ibaidi twende hadi mjini, ukarekebishe hizo nywele zako kisha ndio tutarudi huku”

“Sio mbali sana na hapa?”

“Dakika tatu au tano hivi”

“Basi sio mbali”

“Best zangu munafikia hoteli gani?”

“Tuchukue Nyinda au Mtendele?”

“Nyinda ipo barabarani sana, Mtendele kidogo mapejificha”

Pamela alizungumza, tukawapeleka hadi kwenye hoteli hii yenye gorofa kadhaa kwenda juu. Kisha tukaondoka, huku tukiwaahidi kwamba tutawafwata kesho asubuhi. Tukafika kwenye saluni kubwa ya kike. Nilipo ingia tu ndani ya saluni hii nikakutana na picha yangu kubwa ikiwa imebandikwa ukutani, jambo lililo nifanya niitazame kwa sekunde kadhaa huku nikishindwa kuamini kwamba kweli ni nini au ni mtu mwengine. Wadada na wamama kadhaa nilio wakuta humu ndani kila mmoja akanichangamkia sana.

“Karibu sana kwenye saloon yangu Jojo”

Dada mmoja mnene kiasi alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Asante sana”

Akanionyesha kiti cha kukaa, nikaa na kumuelekza ni kitu gani ambacho anatakiwa kunifanyia kichwani mwangu. Kwa haraka akaanza kunihudumia, huku kwa mara kadhaa, wadada wakinipiga picha, kazi yangu ikawa ni kutabamu tu. Ndani ya robo saa wakwa wamemaliza, nikamlipa dada huyu kiasi alicho nitajia kisha nikatoka ndani humu. Tukaingia kwenye gari na kuelekea ukweli, kiwaga na wasiwasi kikanishika baada ya kufika nyumbani kwa kina Eddazaria.

“Hapa ndio nyumbani, tumefika sasa”

“Eddy mwenzio ninaogopa”

“Hembu shuka unaogopa nini kwani kuna wala nyama za watu nyumbani kwetu?”

“Hapana jamani baby maana yangu sio hiyo”

“Ni ipi sasa?”

“Kufika ukweni kwa mara ya kwanza lazima niogope mume wangu”

Tukashuka kwenye gari, mwadada mrwefu na mweupe akatufwata kwa shangwe na kutukumbatia kwa nguvu.

“Waooo karibu mke mwenzangu”

“Asante”

Tukaingia ndani na kumkuta mama Eddy pamoja na dada yake wakiwa sebleni. Wakanikaribisha kwa shangwe sana, ikanibidi kusalimia kwa heshima ya kupiga goti chini, japo ndio mara yangu ya kwanza ila salamu hii kwa asilimia tisini nimefanikiwa kuiweza. Makaribisho haya kusema kweli sikuyategemea hata siku moja kwenye maisha yangu. Mama mkwe akatukaribisha chakula cha usiku, tukajumuika wote mezani, wifi yangua anakongoza sala ya chakula hichi. Tukaanza kupata chakula cha usiku huku haidthi za hapa na pale zikitawala katika eneo hili, simu ya wifi yangu ikaingia ujumbe, akaufungua na kuanza kuusoma taratibu. Nikaona sura yake ikibadilika kidogo, akampatia Eddy simu hiyo. Eddy akautazama ujumbe huo, kwa haraka akanyanyuka kwenye kiti.

“Unakwenda wapi wewe hujamaliza kula”

Mama mkwe aliuliza.

“Nakuja, Jojo njoo mara moja”

Nikamtazama mama mkwe, kwa ishara akaniruhusu nimfwata Eddazaria sehemu alipo elekea. Eddazaria akanitazama usoni mwangu, kwa macho yaliyo jaa wasiwasi.

“Kuna nini baby”

“Ona”

Eddazaria akaniwekea simu ya dada yake mbele yangu, nikatamani ardhi ipasuke nidumbukie na inimeze, kwani video hii aliyo tumiwa wifi yangu inanionyesha mimi na Nuru tukinyonyana ndimi zetu huku tukiwa kwenye hisia kali za kimapenzi jambo lililo nifanya haja ndogo nihisi ikinitoka, ni ujumbe wa maandishi uliandikwa. ‘Musipo mkataa huyo malaya kwenye familia yenu. Video hii ninamtumia mama yako’



Eddazaria akanitazama jinsin inavyo tetemeka mwili wangu mzima.

“Jojo”

Nikaitaka kwa kumtazama tu Eddazaria, kwani hata kinywa changu hakina uwezo kabisa wa kufunguka kwa woga na aibu kubwa ambayo imenipata.

“Nitazungumza na mama kabla ya huu mchezo anau ufanya Nuru haujakua mkubwa”

“Mama…”

“Ndio, ni bora nikazungumza naye mapema kuliko yeye akaja akajua, unahisi ni kipi kitatokea hapo”

Nikaka kimya na kusoka cha kujibu, furaha yangu yote imemezwa na woga ulio nitawala, yaani ni mara kumi hili video ingeingia kwenye simu ya Eddazaria ila ubaya imengia kwenye simu ya wifi yangu ambaye sina mazoea naye sana.

“Nenda kale, ila jitahidi kuondoa huo woga”

“Eddy sina ujasiri wowote mpenzi wangu, hapa nilipo ninaogopa, hapa nilipo ninatamani hata kufa”

“Usijali haya ni maswala yanayo weza kuzungumzika mpenzi wangu. Ukionyesha hali ya wasiwasi na woga, itapelekea mama yako mkwe kuweza kugundua hili na atahitaji kufahamu, sasa hili jambo linahitaji muda mzuri la kumueleza sawa”

“Sawa baby, ila wifi utazungumza naye?”

“Yaa yeye hana shida, nitazungumza naye”

Nikaivuta pumzi nyingi kisha nikiishusha taratibu, tukarudi kwenye meza ya chukula huku tukiwa na tabasamu pana kwenye nyuso zetu. Kila mtu akaka kwenye kiti chake.

“Jojo wewe ni kabila gani?”

Mama mkwe aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Mama mimi ni Mrangi”

“Waooo, safi sana. Unajua kuna makabila niliweza kuwakataza vijana wangu wasiweze kuoa huko”

“Kwa nini mama?”

“Anaa unatazama na nature ya kabila husika, kila kabila huwa lina sifa yake. Kama mimi ni mpare, ila nimemuambia mwanangu, asioe mpare, kutokana na sifa zao za ugumzi, gubu gubu. Hivyo hiyo hata kwa wachanga, wadigo, wasambaa.”

“Mamaaa”

Eddazaria alizungumza huku akimtazama mama yeka.

“Yaa, nimemuambia kwa maana hayupo kwenye hayo makabila. Sio kama yule mpare uliye zaa naye. Ona amekutia hasara ya kukuchomea hadi nyumba, mtoto kakimbia naye umebaki wewe kama wewe”

Kitu kinacho zidi kuniongopesha kwa mama mkwe, anaonyesha ni mtu asiye penda masihara kabisa na vijana wake wa kiume.

“Mama jamani hayo si yalisha pita”

Wifi naye alizungumza na kunifanya nimtazame, macho yetu yakagongana, ila kwa haraka nikayakwepesha, kwani bado swala la video halijazungumziwa.

“Ehee mumemaliza kutengeneza hiyo filamu yenu?”

“Ndio mama”

“Mimi inawaombea kwa Mungu muwe na maisha mazuri, na kitu kikubwa cha kuwasisitizia ni amani na upendo, mukiweza kuvihimili hiyo basi hakuna ambaye anaweza kutoka nje na kuja kuwavurugia amani yenu”

“Sawa mama”

Tukamaliza kupata chakula cha usiku, tukahamia sebleni, ambapo mama mkwe akaongoza sala ya usiku kisha akatuaga na kuelekea chumbani kwake kulala.

“Shem chumba chenu kipo tayari”

Mama Gody mkubwa alizungumza huku akimtazama Eddazaria.

“Sawa shem. Oya tunaweza kuzungumza”

Eddazaria alimuambia dada yake.

“Poa”

“Shem, mpeleke mke mwenzio chumbani”

“Sawa Jojo twende”

Nikanyanyuka kwenye sofa nililo kalia. Tukaongozana na mke mwenzangu hadi chumbani tulicho andaliwa.

“Karibu, jisikie huru kabisa”

“Asante mwaya”

“Ila mbona kama umepoteza amani, tofauti na pele ulipo kuja?”

“Hapana, nipo sawa”

“Hapana zungumza bwana, umepoteza amani. Mimi ni mwanasaikolojia, ninaweza kukusoma na kukufahamu vizuri, wee, niambie ukweli. Eddy amekuudhi?”

“Hapana”

Nilizungumza huku nikijitahidi kuweka tabasamu pana usoni mwangu.

“Mmmm Jojo unanificha, au umemuogopa maama alivyo kuambia?”

“Aha…kwa asilimia kadhaa hivi”

“Mzeoee, mama yetu kwa haraka haraka ukimumuona unaweza ukahisi ni mkali, ila siku za mbeleni huko utamzoea kabisa. Pale alikuwa anakupima kwa maana hata mimi kwa mara ya kwanza aliniuliza kama wewe alivyo kuuliza”

“Sawa mwaya”

“Ngoja nikuache upumzike, mimi ngoja niende nikamnyonyeshe mtoto”

“Waoo,kumbe wapo huku?”

“Yaa Gody wangu na mdogo wake wamelala chumbani huko”

“Sawa tutazungumza kesho”

Mke mwenzangu, akatoka chumbani humu na kuniacha mimi mwenyewe. Nikaitoa simu yangu katika pochi yangu ndogo, nikaiwasha. Nikaingia katika bafu lililomo ndani ya chumba hichi. Nikaitafuta namba ya Nuru ambayo alitoka kunipigia muda wa mchana nilipo kuwa njiani. Simu yake ikaanza kuita, ikapokelewa.

“Hahaaaa….hahaaaa umenitafutia nini tena?”

“Nuru ukinipotezea bahati yangu ya kukubalika hapa ukweni, nakuahidi kwamba nitahakikisha kwamba ninakuua, tena nitakuua kikatili sana”

“Hahaa…..Jojo, unahisi kwamba utaweza kunipata mimi au?”

“Wewe sema kwamba siwezi kukuapata, ninakujua”

“Wewe si ulihitaji vita na mimi, basi vita umeipata”

“Sawa nimeipata, ila na wewe utaisoma namba”

“Poa jiandae kwa kufukuzwa ukweni”

Nuru akakata simu na kunifanya niyang’ate meno yangu kwa hasira kali sana. Nikatoka bafuni humu na kukutana na Eddazaria akiingia chumbani humu.

“Vipi?”

“Nimezungumza na Nuru hapa anasema nijiandae kufukuzwa ukweni”

“Asihisi kwamba familia yangu ina wenda wazimu. Mama ni muelewa na hata sister ameniahidi kwamba atazungumza na mama kesho asubuhi”

“Ila yeye mwenyewe amesemaje?”

“Hana tatizo katika hilo”

“Kweli mpenzi wangu”

“Ndio”

“Na Nuru amepataje namba yake?”

“Hata yeye mwenyewe hajui imekuwaje, hadi Nuru ameipata namba yake, ila ninanhisi itakuwa ni mambo ya kimtandao”

“Mmm sawa”

Eddazaria akaupitisha mkono wake wa kulia kiunoni mwangu, akanivuta hadi karibu kabisa ya kifua chake.

“Jojo ninakupenda sana, nipo tayari kwa chochote kwenye maisha yangu. Nitahakikisha kwamba ninakulinda na kukutunza katika kila hali, sawa mke wangu”

Eddazaria alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama, taratibu nikausogeza mdomo wangu kwenye mdomo wake, hakuwa na hiyana zaidi ya kuupokea mdomo wangu. Tukaanza kunyonyana midomo yetu. Hisia za mapenzi zikaanza kututawala, taartibu Eddzaria akanilaza kitandani huku ndimi zetu zikiendelea kufanya kazi ya kupigana, mapigo ambayo hayana maumivu.

“Shikamoo ba mdogo”

Sauti ya mtoto mdogo wa kiume ikatustua na kujikuta tukiachiana, tukakaa kitandani na kumtazama mtoto wa kiume aliye simama mlangoni.

“Marahaba Gody, ingia”

Gody akatufwata hadi kitandani tulipo kaa.

“Muamkie mama mdogo”

“Shikamoo ma mdogo”

“Marahaba mtoto mzuri, hujambo”

“Sijambo”

“Vipi ndio unatoka kuamka?”

“Eehhee”

“Sawa, nenda kwa mama, zawadi zako tutakupatia asubuhi”

“Sawa”

Gody akatoka chumbani humu na Eddazaria akanyanyuka na kuufunga mlango kwa ndani.

“Unamdanganya mtoto utampa zawadi kesho, ikiwa hujanunu hata pipi njiani”

“Nitamnunulia kesho, itabidi twende mjini kununua baadhi ya zawadi”

“Ila nimestuka, hamu yote imeniiisha”

“Hahaaa…..muoga, hana tatizo hapa wote tunatabia za kizungu”

“Mmmmm Eddy”

“Yaa ndivyo jinsi tulivyo lelewa na mama yetu”

“So unaweza kunila denda mbele ya mama”

“Yaa naweza bila wasiwasi wa aiana yoyote”

“Mmmm mimi nimezaliwa uswahilini na nimekulia uswahilini, hayo mambo sijawahi yafanya”

“Unatakiwa uyafanye sasa, ndio umesha ingia kwenye famili isiyo na itikadi hizo”

“Sawa bwana”

Eddazaira kaanza kunivua guani langu, huku kwa mara kadha akainitekenya tekenya na kujikuta nikiangua kicheko.

“Eddy kumbuka hatupo kwetu, tupo kwa mama bwana, atasikia”

“Unaogopa”

“Ndio mume wangu?”

Nilizungumza huku nikimvua Eddazaria nguo zake, tukaingia bafuni kuoga. Uzalendo ukatushinda na kujikuta Eddazaria akiniinamisha, taratibu nikshika ukuta, na tukaanza kuburudisha. Shuhuli ikatuchukua kama dakika thelathini hivi tukamaliza. Tukaoga na kurudi chumbani kwetu, kama kawaida yangu nikajilaza kifuani mwake, sikuchukua hata dakika nyingi, usizingizi mzito ukanichukuana kulala fofofo.

***

Asubuhi na mapema nikawa wa kwanza kuamka, nikamtazama Eddazaria aliye lala fofofo. Nikashuka kitandani na kuingia bafuni, nikajisaidia haja ndogo kisha nikaoga. Nikarudi chumbani, nikachukua gauni la kushindia na kutoka chumbani humu. Nikatembea kwa mwendo wa taartibu hadi sebleni na kumkuta mama mkwe akifanya mazoezi ya viungo.

“Shikamoo mama”

“Marahaba mwanangu, umelalaje?”

“Ahaa namshukuru Mungu nimelala vizuri, sijui wewe”

“Mimi nimeamka poa, nyinyi hamfanyagi mazoezi ehee?”

“Tunafanya mama”

“Nenda kavae nguo za mazoezi uje tufanye hapa”

“Sawa mama”

Nilikubali tu, ila kusema kweli bado nina woga na mama mkwe, video aliyo ituma Nuru kusema kweli bado inaniweka njia panda. Nikaingia chumbani kwetu.

“Eddy, Eddy, Eddy”

“Mmmmm”

“Mama anataka nikafanye naye mazoezi na mimi sina nguo za mazoezi”

“Nilikiwekea traksuit humo ndani ya begi”

“Sawa”

Nikatoa tracksuit yangu yenye rangi nyeupe, nikaivaa, nikachukua raba nyeusi na kuvaa. Nikatoka sebleni na kumkuta mama mkwe akijiweka vizuri viungo vyake.

“Tunakimbia nje huko”

“Sawa mama”

Tukato nje ya geti na kuanza kukimbia kwenye barabara iliyo tulia sana, utulivu wa eneo hili umesababishwa na majumba makubwa ya kifahari. Japo ni mama ambaye ana umri mkubwa kiasi ila yupo vizuri hata kimbia yake inaonyesha ni mwana mama wa mazoezi. Tukazidi kukimbia hadi tukaucha mji na kuingia eneo lenye mashamba makubwa sana. Tukafika katika moja shamba lenye bonde kubwa mama mke akasimama na ikanilazimu na mimi kusimama huku jasho likitumwagika kwenye miili yetu. Mama mkwe akajipapasa nyuma ya kiuno chake, nikastuka sana baada ya kumuona amechomoa bastola, akaikoki na kunielekezea usoni mwangu, jambo lililo nifanya kitu cha kwanza niwaze juu ya yeye kutumia video na mshenzi Nuru.



Mama mke akaendelea kuninyooshea bastola yake pasipo kuzungumza kitu chochote, nikajikuta nikifumba macho yangu kwa woga ulio nitawala.

“Unampenda mwanangu?”

Swali la mama mkwe likanifanya nifumbue macho yangu na kumtazama.

“Nd…..iooo ndio mama ninampenda”

“Una uhakika?”

“Ndio mama”

Ilinibidi kujikaza kajibu maswali hayo. Taratibu mama mkwe akashusha bastola yake chini.

“Unajua kwenye maisha ya mahusiano huwa sihitaji vijana wangu waweze kuharibikiwa, ndio maana ninakuwa mkali sana. Sipendi na sihitaji wapiti maisha kama niliyo wahi kupitia mimi kipindi cha ujana wangu”

Mama mke alizungumza huku akitazama tazama eneo hili lenye bonde kubwa sana.

“Eddy ndio my last born wangu. Nilimzaa kwa shida sana, nilikutana na vipingamizi vikubwa sana hususani kwenye ulimwengu wa kiroho. Kuna watu walihitaji wamuue tangu akiwa tumboni mwangu, ila ni Mungu pekee ndio aliye weza kunisimamia kwa kipindi hicho hadi leo hii umemuona amekuwa mvulana ambaye unampenda”

Mama mke walizungumza kwa suati ya upole sana, ila iliyo jaa umakini fulani ndani yake.

“Mara nyingi huwa sipendi kumuona mwanangu huyo akilalamika, au akiumia kwa namna yoyote kwa maana ninaamini ni zawadi kubwa sana kutoka kwa Mungu, nilimuweka tumboni mwangu miezi saba na si tisa kama wengine wanavyo kuwa wamekaa, kwa hiyo utaweza kuona ni jinsi gani mwenyezi Mungu alivyo mlinda kijana wangu.”

“Nakuomba umpende, yale maisha ya kudanganyana, yale maisha ya kuchezeana nakuomba uyafute kwenye mawazo yako, kama unahisi humpendi ni vyema ukajitenga naye mapema. Sihitaji muingie kwenye ndoa ambayo siku moja itakuja kuwa ni ndoa yenye matatizo makubwa. Sijui unanielewa kile ninacho kizungumza?”

“Nimekuelewa mama yangu”

“Jana wifi yako alinionyesha video aliyo tumiwa”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio. Nikajikuta hata nikishindwa kuitikia.

“Kwa upande mmoja ni jambo baya kwenye jamii yetu, ila kwa mimi nimeelewa kutokana na sababu ambayo nimeelezwa na wifi yako. Pole kwa kumpoteza mama pia na pole sana kwa maisha magumu ambayo umepitia”

“Asante mama”

“Unaweza kutumia hii?”

Mama mke alizungumza huku akionyesha bastola yake, nikaka kimya kwa sekunde kadhaa nikifiria cha kujibu japo ninafahamu jinsi ya kutumia ila sijui nikisema ndio anaweza kunifikiria mimi ni mtu wa ajabu.

“Aha…aahh”

“Shika”

Nikaichukua bastola hii.

“Kipindi nilipo kuwa jeshini nilikuwa ninasifika kwa kuwa mlenga shabaha mzuri sana, sniper”

“Mama kumbe ulisha wahi kuwa mwanajeshi?”

“Yaa nilikuwa mwanajeshi, japo baba yangu hakupenda mimi nilipenda kuwa hivyo. Wanangu hawa wote nimewafundisha mbinu za kijeshi, tangu walipo kuwa watoto wadogo”

“Ahaaa…..”

“Yaa wote wanajua kutumia bastola, kama utakuwa umekawa umekaa vizuri na Eddy, atakuwa amekufundisha”

“Mara moja moja”

“Unawaona wale ndege juu ya ule mti pale?”

Mama mkwe alinionyesha ndege wengi walio jaa juu ya mti mmoja mkubwa ulipo katika ng’ambo ya mbili ya bonde.

“Ndio”

“Niangushie mmoja”

Mama mke walizungumza huku akitoa kiwambo cha kuzia sauti, akanikabidhi huku akinitazama, nikakifunga taratibu na kumfanya mama mkwe kutabasamu.

“Unajua kutumia bastola, kwa mtu wa kawaida, angeniuliza hichi ni nini ila wewe moja kwa moja umekifunga”

“Aa..a…mama mara moja moja huwa Eddy ananifundisha hususani kwenye hii filamua mbayo tumeigiza ni sehemu nyingi sana ambapo tumeweza kutumia silaha”

“Ahaaa, sawa sawa, haya niangushie ndege mmoja”

Nikaishuka vizuri bastola hii, nikafumba jicho moja na kumlenga ndege mmoja. Nikafyatua risasi na ndege huyo akaanguka chini. Mama mkwe akaanza kunipigia makofi huku akinipongeza kwa kazi nzuri ambayo nimeifanya.

“Twende tukamchukue”

Tukakatiza katikati ya bonde hili lenye mazoa madogo madogo, nikamuokota ndege wangu niliye muua.

“Mama huyu ndege anaitwaje?”

“Jina lake kidogo limenitoka ila nikimkumbuka jina nitakuambia”

Mama mke wakaanza kunitembea katika eneo hili la mashamba huku akinionyesha ni wapi anapo miliki, tulipo maliza tukaanza safari ya kurudi nyumbani taratibu huku tukitembea. Tukafika nyumbani saa moja na nusu na kumkuta mke mwenzangu akiwa amesha amka.

“Hee, umekuwa muwindaji na wewe”

“Yaani wee acha tu shikamooo”

“Marahaba, lete nikupokee huyo ndege”

Mama Gody mkubwa akanipokea ndege niliye mbeba, tukaingia ndani.

“Huyo Eddy hajaamka?”

“Bado mama”

“Amechoka sana, jana barabarani tulipata maswaibu mengi sana, ila tunashukuru Mungu tumeweza kufka salama?”

“Maswaibu gani tena?”

“Kuna gari ambayo tuliongozana nayo ilipata ajali nyuma yetu ikatubidi tugeuze na kuwasaidia”

“Masikini weee, walikufa?”

Mama Gody aliniuliza huku akiwa amejawa na sura ya huzuni usoni mwake.

“Hapana, hawakufa ila walijeruhiwa watatu, tena ni mabinti tulikutana nao pale Lugoba na wengine wawili alipanda gari yetu kutokana katika gari lao walikuwa wamejaa sana”

“Mmmm pole yao”

Mama mkwe alizungumza huku akiondoka sebleni hapa.

“Walikuwa wamelewa au?”

“Hapana, yaani hiyo sehemu ambayo wamepata ajali wala hakuna ambaye anaweza kuhisi kama ni eneo ambalo mtu anaweza kupata ajali kwa maana ni la kawaida sana”

“Na wote walikuwa wanawake?”

“Ndio”

“Mungu awasaidie wapone. Best mimi ngoja niandae chai”

“Ngoja nikusaidie”

“Hapana wee acha tu”

“Mmm jamani mama Gody ngoja nikusaidie”

“Utanisaidia kupijka jioni sawa”

“Jamani”

“Yaaa, utanisaidia kupika jioni. Sasa hivi wewe nenda kaoge usubiri kunywa chai sasa”

“Sawa bwana Gody bado hajaamka?”

“Bado hajaamka”

“Sawa”

Nikaelekea chumbani, nikamkuta Eddazaria bado akikoroma. Nikavua nguo zangu zilizo lowana kwa jasho, nikaingia bafuni na kuanza kuoga taratibu. Nikaanza kufikiria maneno ya mama mkwe, furaha na amani vikaanza kuchukua nafasi taratibu kwenye moyo wangu.

‘Asante Mungu’

Nilizungumza huku nikisisimama mbele ya kioo kilichopo katika bafu letu, nikajitazama vizuri sura yangu. Eddazaria akaingia bafuni humu huku akiwa anapiga miyayo mingi sana.

“Umeamkaje?”

“Nipo poa baby wangu”

“Ninausingizi ile mbaya”

“Si ulale jamani kwa maaana muda bado upo”

“Saa ngapi sasa hivi?”

“Nahisi ni saa mbili”

“Inabidi asubuhi hii twende mjini, tukanunue baadhi ya vitu”

“Sawa mume wangu”

“Ngoja nikanunue miswaki?”

“Kwani hukubeba?”

“Ahaa…tutatembeajea na miswaki kwani tumekuwa wanafunzi sisi?”

Eddazari alizungumza huku akitoka ndani humu. Nikaendelea kuoga taratibu, kisha nikatoka chumbani humu, nikiwa ninajiandaa kuvaa nguo, Eddazaria akaingia akiwa na miswaki miwili na dawa ya meno. Akanikabidhi mswaki wangu kisha akajitupa kitandani.

“Heee unalala tena?”

“Nalala kidunchuuu utaniamsha”

“Mmmm si ulisema tunakwenda mjini asubihi hii?”

“Wachaga bado hawajafungua maduka yao, ikifika saa tatu utaniamsha”

“Heee haya bwana”

Eddazaria akageukia upande wa pili wa kitanda na kuendelea kulala. Nikaingia bafuni na kusafisha kinywa changu. Nikarudi chumbani baada ya kumaliza zoezi hilo, nikavaa nguo zangu na kutoka chumbani humu. Nikakutana na wifi kwenye kordo akiwa amembeba mwanaye.

“Shikamoo wifi”

“Marababa”

“Waooo naona katotoo kamekuwa sasa”

“Yaaa, leo ameamka mapema”

Nikamchukua mtoto huyu kutoka kwa wifi.

“Anaitwa nani vile”

“Heavenlight”

“Waooo nice name”

Tulizungumza huku tukielekea sebleni, tukaka kwenye moja ya sofa.

“Wifi”

“Beee”

“Asante kwa msaada wako”

“Usijali nia mambo ya kawaida mbona”

“Mmmm nilijawa na woga mwingi sana”

“Jamani chai ipo tayari karibuni mezani”

“Nenda tu kanywa, mlete nimnyonyeshe kwanza huyo bibie”

Nikamkabidhi shem yangu, mtoto. Nikaelekea mezani, sikukaa hata dakika moja mama mkwe naya akfika mezani hapa. Nikaanza kumtengea chai, kisha nikajitengea na mimi.

“Ombea chakula”

Mama mkwe aliniambia kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu. Katika maisha yangu yote kusema kweli sifahamu hata sala ya chakula inaongozwa vipi, nikajikuta nikishikwa na kingugumizi kizito kilicho mfanya mama mkwe kunikodolea macho akinishangaa.



“Vipi hau huko kwenu hamsaligi na huyo mumeo?”

“A…aha.. hapana mama”

“Haya ongoza sala”

Taratibu nikafumba macho yangu, nikajifikiria cha kungummza kwa muda kidogo.

“Mungu bariki chakula hicho kitokacho mikononi mwako. Amen.”

Nikamfumbya macho yangu na kumkukuta mama mkwe akitabasamu.

“Jumapili inabidi twende kanisani, sawa”

“Sawa mama”

“Mara ya mwisho kwende kanisani na huyo mumeo ilikuwa ni lini kwa maana yeye kama yeye ni mvivu sana wa kwenda kanisani”

“Mmmmm….”

“Hamjaenda”

Sikuwa na la kujibu zaidi ya kutabasamu tu. Tukaendelea kupata kifungua kinywa, mama mkwe akawahi kumaliza, akaniaga na kuondoka. Nikaendelea kunywa chai taratibu hadin nikamaliza.

“Shikamoo ma mdogo”

“Marahaba, umeamkaje Gody”

“Safi tu”

“Gody nimekuambiaje, njoo upige mswaki bwana”

Nilisikia sauti ya mke mwenzagu. Gody akaelekea sehemu alipo mama yake. Nikaingia chumbani kwetu na kumkuta Eddazaria bado akiwa anendelea kuutandika usingizi.

“Hembu amka bwana, muda umekwenda”

“Saa ngapi sasa hivi?”

“Inaenda saa nne, yaani hapo kwenye kordo nimekutana na Gody nimeshindwa hata kumtazama usoni, kwa maana sina hata zawadi ya kumpa”

“Mmmmm”

“Amka basi, twende huko madukani, najisiki aibu, hata mama mkwe sijampa kitenge hata kimoja”

Eddazaria akanitazama kwa sekunde kadhaa, akashuka kitandani na kuingia bafuni. Baada ya kumaliza kuoga akarudi chumbani.

“Nitolee ile pensi yangu ya kaki”

“Unataka kuvaa pensi hadi huku”

“Khaa, sasa huku si nyumbani”

“Hata kama baby”

“Nitolee bwana”

Nikafanya kama anavyo hitaji mwenyewe. Eddazaria akajiandaa, tukatoka chumbani humu.

“Umechukua kadi za benki?”

Nilimuuliza Eddazaria huku nikimtazama usoni mwake.

“Yaaa zipo kwene wallet”

Eddazaria akasalimia na shemeji yake, akaelekea hadi kwenye meza ya chakula.

“Mama Gody, mtoto mdogo yupo wapi?”

“Yupo ndani, kumbe hukuuona?”

“Yaa sijamuacha”

Tukaingia ndani ya chumba cha mama Gody na kumkuta mtoto wake wa kike akiwa kitandani anacheza cheza.

“Waoooo, jamani mumezaa watoto wazuri jamani”

“Etii eeeheee?”

“Yaa yupo vizuri jaamani”

Nilizungumza huku nikimnyanyua mtoto huyu.

“Inabidi na nyinyi mujitahidi mutuletee mtoto mwengine”

“Yaani natamani sana kuzaa, ila kuna mambo ngoja kwanza tuyaweke sawa”

“Sawa”

“Ila anafanana na bibi yake eheee?”

“Sana”

“Baba Gody atakuja lini huku?”

“Mmmm sijajua kwa maana bado hajapata likizo kazini kwake”

Eddazaria akaingai chumbani humu.

“Tayari umesha maliza kunywa chai”

“Yaa. Godliver”

Eddazaria alizugumza huku akimshika shika mashavu mtoto huyu. Nikamkabidhi Eddazaria mtoto huyu.

“Jojo ukinizalia mtoto wa kike nakuhonga gari”

“Hhahaa jamani unanihonga au unanipa jamani”

“Nakuhonga”

“Yaani shemeji yangu hiyo anapenda sana mtoto wa kike sijui kwa nini?”

“Napenda mtoto wa kike, kwa sababu kuu mbili”

“Ehee moja?”

“Kwanza mahari itakuwa kubwa, mtu akitaka kumuona namuambia alete ndege moja”

“Hahaaa chizi kweli wewe, kwani mimi umenipata kwa kutoa mahari ya ndege”

Nilizungumza huku sote tukicheka.

“Ndio hivyo utaona tu”

“Shem usisema hivyo, unaweza ukakuta mtoto wako amemapata kijana choka mbaya na akampenda hadi wewe mwenyewe ukashindwa hata kuzuia mahusiano yao”

“Alafu kweli”

“Ahaa, kama atakuwa ni choka mbaya basi awe mzuri, sio ananijia na mwanaume hana mbele wala nyuma”

“Haaa Eddy jamani”

“Ndio, kwani wewe kama mama utataka mwanao awe mwanaume ambaye hata wasichana wezake washinde kumtamani shemeji yao”

“Hahaaaa, ehee sababu ya pili?”

“Sababu ya pili, nataka aje kuwa raisi wa kwanza wa kike Tanzania”

“Heeeee?”

“Ndio, yaani tangu akiwa chini, nitampa roho ya ujasiri, roho ya kujiamini. Roho ya kumshinda hata mwanaume”

“Mmmm makubwa”

“Ndio hivyo, mtu inabidi una na malengo juu ya mwanao kwa maana kuna wazazi wanacho jua ni kuzaa, kumpeleka mtoto shule ila malengo hawana na mtoto, hadi mtoto ije kufikia maisha yampige ndio awe na malengo yake”

“Haya baba”

“Shem sisi ngoja tukimbie mjini mara moja”

“Sawa jamani, tena inabidi mutoroke, kwa maana Gody akiwaona hapa hato kunywa hata uji ataanza kuwalilia”

“Si tumsubirie muoendoke naye”

“Hapana Jojo, Gody ni mkorofi huko atawasumbua hadi wenyewe mushindwe kufanya mambo yenu vizuri”

“Hapana jamani mama Gody acha tu twende naye”

“Mmmm labda kesho, leo muacheni kwanza atulie nyumbani”

“Haya mwaya”

Tukatoka chumbani humu, nikaingia chumbani kwa wifi na kumuaga kisha, nikatoka nje na kumkuta Eddazaria akiwa tayari amesha toa gari nje ya uzio wa nyumba hii. Tukaanza safari taratibu.

“Mama amekwenda wapi?”

“Hakuniaga, alimaliza kunywa chai na kuondoka”

“Wale rafiki zao kuna haja ya kuwapitia hotelini?”

“Kwa muda huu?”

“Ndio”

“Sidhani, kwa maana si tuna mizunguko binafsi na sifahamu kama wao wanaweza kuwa na haja ya kuzunguka na sisi”

“Sawa”

Tukaendelea na safari.

“Kile kiwanda ni cha nini?”

“Kiwanda cha maziwa, kinaitwa Tanga fresh”

“Ahaa kipo barabarani kabisa”

“Yaa, vipo vingi, ambavyo vipo barabarani”

“Huu mji nasikia hapa kipindi cha nyuma ulikuwa ni mji wa viwanda eheee?”

“Yaa ila vilikufa kufa, sijui kulikuwa na kitu gani kilicho sababisha majanga hayo”

“Labda vilifilisika”

“Ufisadi, kuna wapiga madili, walipiga madili hadi vimekufa”

Tukafika katika maduka mengi ya wachafa.

“Unajua sifa moja ya Tanga ni nini?”

“Ni nini?”

“Hizi barabara, kuna barabara ya kwanza hadi ya ishirini na moja, zimepanga vizuri sana”

“Mmm, kwa hiyo kuna barabara ya kwanza, ya pili hadi ishirini na moja”

“Yaa”

“Hapa tulipo ni barabara ya ngapi?”

“Ya kumi na tano”

“Kumbe”

“Ndio. Sasa na umaarufu wako, hapa tutapata shida sana, so kuwa makini na simu. Usije ukaibiwa”

“Sawa”

Tukashuka kwenye gari na kuingia kwenye duka kubwa la nguo za wanawake. Tukaanza kuchagua nguo zinazo weza kuwatosha mama mkwe, wifi na mke mwenzangu.

“Samahani dada aiseeee”

Kijana muuza duka hapa alizungumza kwa lafudhi ya kichaga.

“Bila samahani”

“Wewe ndio yule ninaye mfikiria au nimekosea aiseee?”

Nikabaki na kigugumizi, huku nikimtazama kijana huyu, akaito simu yake mfukoni na kunionyesha picha aliyo iweka katika wallpaper ya simu yake. Nikajikuta nikitabasamu kwani ni picha yangu, hapa ndipo nikaanza kufahamu nguvu niliyo nayo kwa mashabiki wangu.

“Ndio mimi”

“Kiruuuu, leo Jojo umekuja kwenye duka langu aisseeee, naomba hata selifiiii”

Kijana huyu alizungumza kwa furaha sana, nikamtazama Eddazaria akaniruhusu kwa ishara nipige naye picha. Kijana huyu akapiga picha kadhaa.

“Jojo chukua hata gauni moja hapo aisee, nikupige picha kwenye mtandao nitupie kwenye mtandao”

“Usifanye hivyo”

Sauti ya Eddazaria ikapoteza furaha ya kijana huyu.

“Eddy”

“Yaa usifanye hivyo. Ndugu hii ni biashara, kumpiga picha mke wangu akiwa kama anafanya manunuzi kwenye duka, it’s mean tunakutangazia wewe biashara na sisi je tutanufaika na nini?

“Eddy just one picture baby”

“Picha moja tu broo”

“Hapana, hizo mulizo piga zinawatosha. Vitu vyote vinagarimu kiasi gani?”

Eddazaria alizungumza kwa msisitizo huku akikazia kijana huyu macho.

“Ahaa, ni laki mbili na elfu saba”

Eddazaria akatoa kibunda cha pesa mfukoni mwake, akahesa kiasi alicho ambiwa na muuza duka huyu. Eddazaria akabeba mfuko mkubwa ulio jaa nguo hizi na tukaanza kutoka humu ndani huku amenishika mkono. Tukaingia ndani ha gari, akaweka mfuko wa nguo nyuma ya siti ya gari.

“Eddy umemkatili kijana wa watu”

“Nimemkatili na nini?”

“Hata picha moja”

“Jojo, unajua umesha kuwa super star sasa hivi, yeye mbona amekataa kutupunguzia. Pale akiweka picha moja kwenye instergram au Facebook, atawapiga bao wachaga wezake haap wote, atatumia jina lako kujipatia wateja, tena kwa gauni moja la bure”

“Mmmmm”

“Ndio hivyo jiweke kibiashara, maisha yenyewe mafupi sasa hivi. Tunatengeneza pesa nyingi kwa maisha ya badae”

“Sawa meneja wangu”

“Tena yule muhindi wako, muambie kabisa ajupange atakapo hitaji kufanya kazi na wewe”

“Alafu unajua kwamba jana niliongea naye?”

“Muda gani?”

“Pale tulipokuwa hospitali, si nilitoka nje, ndio nilikuwa ninazugumza naye”

“Amekubali kufanya kazi nawe?”

“Ndio, ila nimemuaombia kwamba tupo mkoani”

“Sawa”

Tukaelekea katika duka jengine la nguo za watoto, tukanunua nguo za kutosha pamoja na vifaa vya watoto kuchezea. Tukanunua na sisi baadhi ya nguo zetu, kisha tukaelekea katika hoteli ambayo tuliwaacha Pamela na wezake, kwa bahati nzuri tukawakua wakiwa wapo eneo la kupumzikia. Tukasalimiana nao kisha na sisi tukakaa kwenye viti vya pembeni yao.

“Vipi kuna habari yoyote juu ya wale wezenu?”

“Ndio, tumezungumza nao muda huu. Mmoja ataruhusiwa asubihi hii ila wengine wataendelea kulazwa hadi hali zao zitakapo kuwa sawa”

Pamela alizungumza kwa sauti ya upole.

“Mbona kama huna raha una umwa?”

“Hamna, unajua usiku wa leo sijalala kabisa, kila nikilala ninawaza ile ajali, hadi muda mwengine huwa ninajikuta nikipiga makelele”

“Mmmmm”

“Pole jaamani, ila unatakiwa kufanya vitu unavyo vipenda ili kuiweka akili yako sawa”

“Soma stori zangu, akili yako inaweza kukaa sawa. Ukiwasoma kina Dany na K2 unaweza kuwa sawa”

“Kusema kweli, sitamani hata kufanya kitu chochote jamani”

“Tumemshauri kwamba anywe japo pombe kali akili yake iweze kukaa vizuri”

“Huo sio ushauri mzuri kwa mwezenu. Kwa sasa anatakiwa kukutana na mwana saikolojia ambaye anaweza kumshauri nini cha kufanya ili akili yake iweze kukaa vizuri.”

Nilizungumza huku nikimtazama Pamela usoni mwake.

“Mwanasaikolojia nitampata wapi jamani?”

“Eddy huku ndio kwetu, atampata wapi?”

“Wifi yako ni mwanasaikolojia, anaweza kuzungumza naye na ukamueleza tatizo lake”

“Jamani……hii video vipi?”

Msichana mmoja alizungumza huku akitoa macho kwenye simu yake. Akanipa simu yake, kwa mara nyingine nikakutana na video yangu inayo nionyesha ninanyonyana midomo yetu na Nuru na mbaya zaidi imepostiwa kwenye mtandao wa Instergram. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi tena, Eddazaria akaitazama video hii, nikamshuhudia akikunja ngumi mkono wake wa kushoto hadi mkono huo ukimtetemeka kwa hasira kali.



“Twende zetu”

Eddazaria alizungumza huku akisismama na kuiweka simu mezani. Sikuzungumza chochote zaidi ya kufwata amri ya kumfwata Eddazari kwa nyuma. Kwa kuchanganyikiwa sijakumbuka hata kuaga, tukaingia ndani ya gari. Eddazaria akaachia msunyo mmoja mkali sana huku akiwasha gari. Akalirudisha nyuma kwa haraka, akakanyaga breki, akakunja kona na kuondoka eneo hili kwa kasi.

“Nitamuua huyo mtu wako sawa”

Eddazaria alizungumza kwa hasira, huku akipunguza mwendo, akisubiria gari jengine liweze kupita katika barabara ambayo tunahitaji kuingia. Eddazaria akaminya honi kwa nguvu baada ya dereva huyo kuonekana kuto kujielewa.

“Huyu mseng** naye vipi atoe kijigari chake”

Eddazaria akashusha kioo cha upande wake.

“Oya wewe demu niaje, hujui sheria za barabara au, toa kijigari chako bwana”

Cha kushangaza badala ya dada huyo kuondoa gari lake, akasimamisha kabisa na kutuzuia. Mlango wa nyuma ukafunguliwa, wakashuka wanaume wawili walio valia vinyago usoni mwao huku kila mmoja akiwa ameshika bunduki yake.

“Fu**k Eddy tumevamiwa”

Niluzungumza kwa kupiga kelele, kwa kasi Eddazaria akaanza kulirudisha gari letu nyuma, wanaume hao wakaanza kutushambulia kwa risasi, cha kumshukuru Mungu gari letu lina uimara ambao hauwezi kuruhusu risasi kuingia ndani. Kwa utaalamu wa hali ya juu, Eddazaria akaligeuza gari na tukageuka kule tulipo tokea. Kwa kasi tukaondoka eneo hili, huku nikitazama nyuma, nikawaona wakiingia kwenye gari lao, na kuanza kutufukuzia.

“Eddy ni kina nani wale?”

Nilizungumza huku mwili mzima ukinitetemeka kwa woga

“Sifahamu, sijioni kina nani”

Kioo cha mbele cha gari letu kimejaa alama alaza za risasi ambazo zilikuwa zinapigwa.

“Ingiaza mkono chini ya siti yako, kwa pembeni”

“Wapi?”

“Hapo”

Eddazaria alinionyesha sehemu ya upande wa kulia nilipo kaa. Nikakapasa papasa na kufanikiwa kushika kitu kigumu gumu. Nikakishika vizuri na kugundua kwamba ni bastola. Nikaitoa na kuitazama vizuri, katika siku zangu zote ninalitumia hili gari ila sijawahi kufahamu kwamba kuna bastola.

“Angalia magazine yake ina risasi za kutosha?”

Nikachomoa magazine na kukuta ikiwa na risasi za kutosha. Nikairudisha na kuikoki bastola hii.

“Hawa ninakwenda kuwaulia, huku”

Eddazaria alizumgumza huku akizidi kuongeza mwendo kasi wa gari.

“Eddy hawa ni kinana nani lakini?”

Eddazaria akanitazama kwa macho makali ila hakunijibu chochote zaidi ya kujitahidi kuyapita magari kadhaa ambayo yaliyopo mbele yetu.

“Baby”

“Jojo sifahamu na mimi, ningekijibu”

“Mmmmmmm”

“Huku tunaelekea wapi?”

“Hili eneo linaitwa Chumvini, tunaelekea Amboni, huko mbele ndipo yalipo mapango ya ambani”

“Ahaa sawa”

Nikatazama nyuma nikaliona gari la watu wanao tufwatilia lizidi kuja kwa mwendo wa kasi sana. Eddazaria akaanza kupunguza mwendo wa gari.

“Mbona unapunguza mwendo”

“Subiri, naomba hiyo bastola”

Nikamkabidhi Eddazaria, bastola. Akanaitazama huku nikona jinsi koo lake linavyo mweza mafumba ya mate. Akashusha kioo cha upande wake, akanyanyua brake ya mkono(hand brake huku akizungusha mskani wa hili gari, kwa bahati nzuri gari likageuka na kuziba barabara. Akautoa mkono ulio shika bastola na kuanza kufyatua risasi kuelekea katika gari la watu wanao tufukuzia.

Tukalishuhudia gari hilo likianza kuyumba na mwishowe likatoka kabisa barabarani na kuanza kuvaa vichaka vilivyopo pembezoni mwa barabara na mwisho likapinduka.

“Liweke sawa gari”

Eddazaria alizungumza huku akimfungua mkanda wa siti, akashuka kwenye gari, kwa haraka na mimi nikafungua mkanda wa siti, nikahamia kwenye siti nikafunga mlango na kuligeuza gari vizuri na kulisimamisha pembezoni mwa barabara huku nikimshuhudia Eddazaria akisimama pembeni ya gari hilo.

Kwa haraaka na mim inikashuska na kukimbilia hadi eneo walipo, wale wanaume walio kuawa wakitushambulia kwa raisasi nikawashuhudia wakiwa wameumia vibaya sana. Eddazaria akafungua mlango wa mbele wa gari hili, akamvuta dada huyu ambaye anagugumia kwa maumivu.

Akamlaza chali, kwa haraka akamfungua mkanda wa suruali yake aina ya jinzi pamoja na kifungo. Eddazaria akachukua kijimto kidogo cha siti kilichopo ndani ya gari hili, akakiweka mbele ya bastola yake na kuwapiga risasi wanaume hawa mmoja baada ya mwengine na hakuna mlio wowote wa risasi ambao uliweza kusikika.

“Shikaa”

Eddazaria alizungumzahuku akinikabidhi bastola hii. Akamnyanyua dada huyu na kumuweka begani mwake, tukaanza kuokaa eneo hili huku nikiangaza macho yagu kila mahali, cha kumshukuru Muguu sijamuona mtu wa aina yoyote. Eddazaria akamlaza dada huyu kwenye siti ya nyuma, kisha akaingia upande wa dereva.

“Mbona unashangaa ingia kwenye gari”

Nikaingia katika upande amabo nilikuwa nipo kuwa nimekaa. Safari ya kurudi tulipo toka ikaanza huku kwa mara kadhaa nikimtazama dada huyu anaye endelea kugugumia kwa maumivu akionekana kuumia sana. Eddazaria akatoa simu yake mfukoni, akatafuta tafuta namba kadha akisha akampigia mtu ambaye sifahamu ni nani.

“Oya mwana niaje?”

“Safi, upo hospital au home?”

“Poa ninakuja sasa hivi kuna mgonjwa ninahitaji uweze kumshuhulikia”

“Poa kama dakika kumi na kitu nikakuwepo hapo”

Eddazaria akakata simu.

“Tunaelekea wapi?”

“Kuna jamaa yangu mmoja ni daktari yupo meneo fulani hivi tunakwenda kwake akamshuhulikei huyo mpuuzi”

“Sawa”

“Maji, maji”

Dada huyu alizungumza kwa sauti ya chini na kunifanya macho yanitoke.

“Ukimpa maji anakufa huyo”

“Anakufaje?”

“Kwani mtu akifa anakufaje”

“Ila Eddy tunatakiwa kumuuliza kwamba ametumwa na nani”

“Hawezi kujibu chochote hapo”

Tukafika katika mtaa mmoja wenye nyumba zilizo tulia, akasimamisha gari kwenye moja ya geti, akapiga honi, baada ya muda kidogo gari likafunguliwa. Taratibu Eddazaria akaingiza gari letu hadi kwenye maegesho yaliyopo katika eneo hili.

“Mambo vipi kaka”

“Salama za masiku”

Eddazaria alizungumza huku akikumbatiana na rafiki yake huyu.

“Ahaa….huyu ndio shem wetu nini?”

“Yaaa, ndio shemeji yetu bwana, aisee kuna mzigo huku nyuma nahitaji umshuhulikie”

“Mambo”

“Safi niambie shemeji”

“Safi tuu, za wewe”

“Salama, karibu sana bwana hapa ndio home”

“Asante”

Eddazaria akamtoa dada huyu na kumbeba mikononi.

“Huyo naye vipi?”

“Aahha, kaka weee acha tuu, nahitaji azungumze mambo fulani hivi, sasa sijui unaweza kumfanya aweze kuzungumza?”

“Bila shaka, mlete huku”

Tukamfwata dakari huyu hadi kwenye kijuba kidogo kilichopo pembezoni mwa nyumba hii anayo ishi, ndani ya kijumba hichi kuna maabara ndogo pamoja na kitanda kinacho tumika hospitalini. Doktari huyu akaanza kuvaa gloves nyeupe mikononi mwake, akaanza kumkagua mgonjwa huyu.

“Amevunjika mbavu huyu”

“Za upande gani?”

“Upande huu wa kulia”

“Zote au?”

“No ni mbili”

“Ila si anaweza kupona”

“Yaa anaweza kupona, vipi mumemtolea wapi?”

“Si umeona gari langu likiwa lina alama alama kwenye kioo cha mbele”

“Yaa nimeona, nikataka kukuuliza huko utokapo kwema ila nikajikuta nikisaua kwa kumshangaaa shemeji, umeibua kifaa mshikaji wangu”

“Hahaa, hembu acha hizo. Sasa huyu fala na wezake walikuwa wataka kutuua, sasa nahitaji kufahamu ni nani aliye watuma”

“Sasa si nimchome sindano ya maumivu, ili aweze kuzungumza, kwa maana anaweza kutufia humu ndani na kujikuta tukikosa bara na pwani”

“Poa fanya hivyo”

“Baby mkague uone kama anaweza kuwa na simu au laa”

Eddazaria akafanya kama alivyo nilivyo muagiza. Kwa bahati nzuri akakuta simu, aina tecno H5.

“Hivi vimeo hadi leo bado vipo”

“Hahahaaa”

“Yaa na kumbuka ndio simu yangu ya kwanza kuitumia, tangu nilipo anza kuishika pesa yangu”

Eddazaria alizungumza huku akiikagua kagua simu hii.

“Angalia watu alio fanya nao mawasiliao”

Niliendelea kumshauri Eddazaria ili tuweze kufahamu ni mpango gani msichana huyu aliweza kuupanga hadi kuja kutuvamia sisi.

“Simu yake ina namba ya siri”

“Ngoja nimchome sindano kwanza”

Daktari alizungumza huku akivuta dawa kwenye kichupa kidogo kwa kutumia sindano. Alipo hakikisha kwamba amejaza sindano hiyo akamchoma dada huyu kwenye mkono, kitendo cha kuanz akuisukuma dawa, dada huyu akaanza kupiga kelele za maumivu makali.

“Nitajia namba ya siri ya simu yako”

Eddazaria laizungumza huku akiwa amemsogelea dada huyu karibu kabisa na uso wake.

“Ni…..n….”

Kwa ishara Eddazaria akamuomba rafiki yake huyu kuminya dawa ndani zaidi.

“Ni mbili, mbili, sita, nane moja”

Eddazaria akamzuia rafki yake huyu kuendelea kuongeza kuiminya dawa hiup ambayo kwa mtazamo inaonyesha dhairi kwamba ina mpa mtu maimivu makali sana. Eddazaria akaingiza namba hizo alizo elezwa.

“Imefunguka”

Eddazaroa taratibu akaanz akuikagua simu hiyo, nikaiona sura yake ikianza kutawaliwa na mikonjo kadhaa kwneye paji lake la uso. Akamtazama dada huyu kwa macho ya hasira sana, kwa haraka akautoa mkono wa rafiki yake kwenye sindano aliyo ishika, akaanza kuiminya dawa hiyo kwa nguvu na kumfanya dada huyu kuzidi kupiga kelele za maumivu makali sana, huku alilia kwa uchungu

“Kaka utamuua”

Rafiki yake alizungumza huku macho yakimtoka.

“Una uhakika huyu ndio aliye kuagiza eheeee?”

Eddazaria alizungumza huku akimuonyesha dada huyu simu aliyo ishika karibu kabisa ya uso wake huku akiendendelea kuiminya dawa iliyo katika sindano aliyo ishika mkononi mwake na kuzidi kumliza dada huyu kwa maumivu makali sana.



“Kaka utamuua”

Dokta alizungumza huku akiutoa mkono wa Eddazaria kwenye sindano aliyo ishika. Kwa mara nyingine nikabahatika kumuona Eddazaria akikasirika katika kiwango cha hadi mwili wake kutetemeka.

“Dokta mpeleke Jojo kwa mama, sasa”

“Sawa”

“Edd….ila…..”

“Fanya kama nilivyo kuambia”

Kwa sauti ya ukali aliyo niongelesha Eddazaria nikashindwa hata kuzungumza neno la pili. Dokta akanitazama na kutingisha kichwa chake akinisihi kwamba nisizungumze chochote. Kwa ishara dokta akaniomba tutoke nje ya nyuma hii, nikamtazama Eddazaria ila bado anaonekana kujawa na hasira kali sana.

“Hamisheni mizigo kwenye gari lako, mutaniachia gari hilo kubwa”

“Poa kaka”

Dokta akaingia ndani kwake, baada ya muda kidogo akatoka akiwa amebadilisha nguo. Akawasha gari lake aina ya Grand Mark X. Akaliwasha ana taratibu akalisimamisha karibu na gari letu, akashuka kwa kusaidiana tukaanza kuingiza mizigo tuliyo inunua kwenye hili gari. Moyo na nasfi yangu vikasita kabisa kuondoka katika eneo hili pasipo kuweza kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa Eddazaria. Nikaanza kutembea kuelekea katika nyumba ndogo niliyo muacha Eddazaria na mwanamke huyo aliye mpatia mateso makali sana.

“Shem”

Dokta aliniita kwa haraka huku akinikimbili hapa nilipo simama.

“Shema ninakuomba usiingie ndani, jamaa yupo kazini sasa”

“Kazini!! Kazini kivipi?”

“Nitakuambia mbele ya safari, ila kwa sasa ninakuomba uweze kumuacha animalize hiyo kazi”

“Shem, sikuelewi. Eddy ni mume wangu, ninahitaji kufahamu kila kitu kinacho endelea kwake, so ninakuomba katika hili usiliingilie”

Nilizungumza kwa msisitizo, dokta akaniruhusu kwa ishara kuingia katika chumba hicho. Kitendo cha kuingia ndani ya chumba hicho, nikamkuta Eddazaria akimkita kisu cha kifua msichana huyo. Macho yakanitoka, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio, maswali mfululizo yakaanza kukatiza kwa kasi katika kichwa changu. Swali ambalo linajirudia rudia mara nyingi katika akili yangu, ni kwamba Eddazaria ni nani, kwa nini amemuua msichana huyu.

“Nimekuambia uende nyumbani, hujanielewa?”

Eddazaria alizungumza kwa ukali sana.

“Ni…m..e…kue…..lewa”

Nilizungumza kwa sauti ya kukata kata huku nikitetemeka, nikatoka chumbani humu nikapokelewa na sura ya tabasamu ya dokta. Kwa ishara ya mkono akaniombe niingie ndani ya gari. Nikashusha pumzi nyingi sana, kisha nikapiga hatua za kawaida hadi ndani ya gari hili. Dokta akazunguka upande wa pili na kuingia ndani ya gari.

Taratibu tukaelekea hadi getini, akashuka, akafungua geti na kuingia ndani ya gari, akalitoa gari ndani ya geti hili, kisha akashuka, akalifunga geti na tukaondoka katika eneo kwa mwendo wa kawaida.

“Shem”

“Naam”

“Naomba uniembie ni kitu gani kinacho endelea kwa Eddy”

“Mmmm”

“Please naomba uniembie ukweli”

“Hilo swali shem, ninakuomba uweze kumuuliza yeye mwenyewe, kwa maana nikizungumza mimi, inaweza kunileteleta tabu hapo badaye”

“Tabu gani?”

“Nyinyi ni wapenzi, na munashare kila kitu, so ninaweza kukuambia na ukaenda kumuambia kwamba mimi ndio nilizungumza”

“Haki ya Mungu shem, siwezi kuzungumza chochote, siwezi kuizungumza siri ambayo tunaweza kuizungumza mimi na wewe”

“Hapana shem, siwezi kukuamini katika hilo”

Nikaka kimya kwa muda mara baada ya kumuona dokta akiwa amekataa kabisa kunieleza ni nini kinacho endelea. Safari ikazidi kwenda mbele, kuna alama za maeneo ambazo niliziweka, ili hata nikipita kwa mara ya pili nisiweze kuzisahau kirahisi, hapa ndipo nikagundua kwamba tupo karibu katika na kufika nyumbani kwa mama mkwe.

“Shem naomba usimamishe gari”

“Vipi?”

“Ninaomba tu usimamishe gari”

Dokta pasipo kujiuliza mara ya pili, akasimamisha gari pembezoni mwa barabara. Nikafungua mkanda wa siti yangu niliyo kalia, nikashuka ndani ya gari na kuanza kutembea kwa miguu nikiifwata barabara hii ya lami. Dokta kwa haraka akashuka kwenye gari na kuanza kunikimbilia huku akiniita jina langu. Nikazidi kuongeza mwendo wa kutembea na kumfanya akizidi kunimbilia, alipo nifikia akaniwahi kunishika mkono na kunifanya nigeuke kwa hasira huku nikimtazama usoni mwake.

“Niache”

“Sasa shem unakwenda wapi jamani”

“Ninakwenda ninapo pajua mimi, ninaweza kiomba hata lifti kwenye basi lolote hapa nikarudi zangu Dar sawa”

“Shem usinifanyie hivyo bwana, jukumu lango mimi ni kukurudisha nyumbani”

“Utanirudishaje nyumbani ikiwa na wewe ni mnafki, ikiwa hutaki kuniambia ni kitu gani kinacho endelea kwa rafiki yako eheee?”

Nikamuona dokta jinsi anavyo shusha pumzi nyingi sana, akionekana kutamani kuzungumza ukweli ila anashindwa kwa ajili ya kumlindia rafiki yake siri. Nikaona basi moja likija upande wetu, nikaanza kupunga mkono huku nikijitokeza barabarani, dereva wa basi hilo akaanza kuniwashia taa huku akizima, kwa haraka shem akanishika mkono na kinivuta upande wake na basi hilo likapita kwa kasi sana.

“Shem mbona unakuwa hivyo lakini?”

“Niambie ni nini kinacho endelea, ulihisi kwamba ninakutania kwamba nina uwezo wa kwenda Dar sasa hivi”

“Okay okya ninakuambia ukweli, ila ninakuomba urudi kwenye gari ili tuweze kuzungumza basi”

“Niambie sasa hivi”

Dokta akaanza kunitingisha tingisha kichwa chake akama mtu aliye kabwa na tonge la moto kooni mwake, kulitema anashindwa na kulimeza pia anashindwa. Gari aina ya NADIA, ikasimama mbele yetu kidogo.

“Ohoo asante Mungu”

Dokta alizungumza na kunifanya nitazame gari hili, nikamuona wifi akishuka, hapo ndipo nikajukuta nikuishiwa nguvu kabisa.

“Jojo vipi, mbona hapa barabarani. Dokta gari lako limeharibika?”

“Yaa sister, shikamoo”

“Marahaba”

“Shikomoo wifi”

“Marahaba twende ukapende kule kwa maana hata mimi ninaeleka nyumbani”

“Sawa wifi”

“Shem hivi vitu ndani ya gari si nivihamishie huko?”

“Hapana, utavileta nyumbani?”

Nilizungumza hivyo makusudi kuhakikisha kwmaba ninamkomesha dokta ili ajue kwamab kuniponyoka hapa sio mwisho wa mimi kuendelea kuhitaji kufahamu ni siri gani inayo endelea. Tukaingia na wifi ndani ya hari lake na umkuta akiwa amemuweka mwanaye siti ya nyuma katika siti maalumu za watoto.

“Mumetoka wapi?”

“Tumetoka clinic, tumepitia nyumbani kwangu, hapa tunakwenda kwa mama”

Wifi alizungumza huku taratibu tukiondoka katika eneo hili, niktazama kwenye kioo cha pembeni yangu, nikamuona dokta akiwa ameshika kichwa.

“Mwenzio yupo wapi?”

“Kuna sehemu amepitia”

“Aaa na yeye naye, akija Tanga hatulii kazi kupunyanga tu”

“Labda ame wamiss marafiki zake”

Nilijitahidi kudanganya na kuto kuonyesha utofauti wowote kwa wifi yangu huyu, ambaye sijamzoea kabisa.

“Anahela za kucheza, na mgari wake unavyo kula mafuta, nashangaa, anavyo safiri nalo kutoka Dar hadi Tanga”

“Hahaa….mbona kawaida shem”

“Mmmmm kawaida, mimi mwenyewe haka kanadai kangu, niktoka mjini hadi huku kwa mama roho inaniuma, pasipo baba Heveanlight kuniwekea mafuta, sitembee nacho”

“Haaaahaa wifi wewe mbaiili eheee?”

“Ahaa….kwa maisha haya mtu usipo kuwa mbaili utaramba sumu gani, raisi mwenyewe ndio hivyo amebana kila kona”

“Kweli lakini”

“Ehee niambie filamu yenu inatoka lini?”

“Siku kwa kweli bado sijaifahamu, kwa maana bwana mkubwa ndio mfwatiliaji wa kila kitu”

“Na itoke tuone kwa maana anavyo jisifia, mmmmmmm hadi muda mwengine huwa nina mponda namuambia movie itakuwa kama Bongo movie, basi huwa hapendi kabisa hata kusikia”

“Hahaa yeye anatakaje?”

“Anataka nimuambie movie ni kama Hollywood, basi hapo roho yake ndio inamridhika”

“Hahaaa Eddy huwa anavituko sana”

“Sasa hivi ndio amechangamka kipindi alipokuwa mtoto, alikuwa ni mpole sana, alikuwa si mzungumzaji kabisa na watu. Hadi nikawa ninamtania domo zege”

“Hahaahaaaa wifi jamani”

“Eheee, yaani alikuwa kazubaaa huyo, ila akili yake ilikuwa nzima darasani, alikuwa anawaburuza sana wezake kwenye masomo. Ila uchangamfu na wezake ndio ulikuwa unamfanya aonekane goi goi”

“Jamaani, hajawahi kuniadisia hivyo?”

“Kuna mwanaume atakuadisia uboya wake wa utoto. Kuna kipindi nilikuwa ninamchonganisha hadi kwa wezake wababe wababe, wakimpiga vile basi mimi nafurahi kama nini”

“Hahaahahaaa……jamani wifi…..wifi…utaniua mbavu zangu”

Nilijikuta nikicheka sana hata mawazo juu ya Eddazaria na matukio yake yakaanza kuniondoka.

“Yaani alikuwa anapigwa huyo, mama alikuwa hapendi, alikuwa anafokaa akimkuta mwanaye na manundu”

“Hahaa alikuwa anapigwa hadi anatoka nundu?”

Heee, sasa hawezi kupigana unadhani ni nini kitatokea”

“Jamani kama namuona hivyo”

“Nakumbuka bwana kuna mvulana mmoja hivi nilimchonganisha naye, sasa sijui hiyo siku alikuwa na hasira zake za wapi. Ebwana weee, achaa ambumunde mtoto wa watu, alimbumunda, kila nikimuamua nilikuwa ninashindwa kabisa, alikuwa na nguvu. Ule ugoi goi wake wa siku zote hiyo siku bwana ulipotea”

“Jamaniii wifii”

“Ooohoo nilijuta kwa nini nilimchonganisha kijana wa watu, na tena alikuwa ni mkubwa kumzidi hata yeye, ila mmmm alipiga hata akazimia”

“Mungu wangu!!!”

“Ohoo hapo ndipo tukajua kwamba ana hasira. Ile siku mama alinichapajeee”

“Hata wewe ulikuwa unachapwa?”

“Ohoo mama yetu alikuwa ni mkali, mumemkuta kipindi hichi amesha anza kuitwa bibi. Ila enzi hiyo, anakutandika na fimbo ya mti mmoja hivi unaitwa muwanzi, na jinsi ulivyo mgumu, anakuchapa anahakikisha hadi unatakatika vipande vipande”

“Mmmmm pole”

“Asante bwana, ndio yamesha pita hayo. Enzi hizo zilikuwa za utoto, sasa hivi na sisi tuna watoto ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli”

“Ni kweli wifi”

Hapa ndipo nikagundua kwamba wifi ni mtu mmoja ambaye ukimtazama unaweza kuhisi ni mtu ambaye hana muda na mtu ila ukiwa naye karibu ni mtu ambaye anajali na mchangamfu sana. Tukafika nyumbani na kumsaidia kumshusha mtoto kwenye gari, tukaingia ndani na kumkuta mama Gody mkubwa akiwa anatazama tv.

“Mama bado hajarudi?”

Wifi aliuliza huku akikaa kwenye sofa.

“Bado hajaridi, Jojo umerudi mwenyewe?”

“Eheee”

“Nilikutana nao hapo njiani na dokta, gari limewaharibikia”

“Ahaaa….umemuachia huyo dokta nilitaka aja hapa ninamdai zawadi yangu”

“Atakuja, kuna mizigo nimeiacha ndani ya gari lake nina uhakika ataileta hapa”

“Safi, shem naye yupo wapi?”

“Kuna sehemu ameelekea”

“Ahaa…sawa, chakula cha mchana tayari nimesha kipika”

“Jojo nenda kale”

“Nitakula badae kidogo, kuna sehemu tulipitia na Eddy tukapata chakula kidogo”

“Najua hapo shem amekupitisha kwenye vikuku”

“hahaahaa hamna”

“Namjua shem, anapenda vikuku vya kukaanga”

Tukasikia honi ya gari geti.

“Eheee dokta huyo anakuja”

Mama Gody alizungumza huku akinyanyuka, akakimbilia gatini, ikanilazimu na mimi kutoka nje, kwa maana wazo lakuhitaji kufahamu kujua ni nini kinacho endelea bado lipo pale pale. Mama Gody akafungua geti, dokta alipo niona mimi akaonyesha dhairi kustuka sana. Taratibu akasimamisha gari lake pembeni ya gari la wifi, mama Gody, akafunga geti.

“Dokta nakuambia hapa hutoki hadi unipe zawadi yangu, eheee funguo hii hapa ya geti”

Mama Gody mkubwa alizungumza huku akimyooshea dokta funguo. Dokta akajaribu kutengeneza tabasamu usoni mwake, ila woga ukalizidi tabasamu lake hilo na mtu akimtazama lazima atagundua juu ya woga.

“Dokta mbona unamuangalia Jojo na unatetemeka?”

Sawali la mama Gody mkubwa likamfanya dokta kuzidi kutetemeka, hadi fungua ya gari aliyo ishika mkononimwake ikamuanguka chini.



“Ha…ah…hapana”

Doctar alijibu kwa kutetemeka, taratibu nikaifwata funguo yake sehemu ilipo anguka kisha nikaiokota na kukaa nayo.

“Karibu ndani shem”

Mama Gody alizungumza kwa furaha, huku akijaribu kupotezea swali alilo liuliza.

“Ah..aa kuna mizigo kwenye gari”

“Tutashusha shem”

Ilinibidi niwahi kuzungumza. Dokta akaingia ndani na kutuacha nje mimi na mama Gody mkubwa.

“Mbona dokta amekuangalia na kutetemeka hadi amenagusha fungupo, vipi kuna kitu kinacho endelea?”

Nikaka kimya huku nikilifikiria swali la mke mwenzangu, nikaona hakuna haja ya kumficha zaidi ya kumuuliza na yeye swali ili kama anaweza kufahamu kitu kidogo juu ya mume wangu Eddazaria.

“Hivi unafahamu kazi nyingine ya Eddazaria?”

“Mmmm kivipi?”

“Yaani hana kazi nyingine zaidi ya hii anayo ifanya”

“Mmmm shem wangu yule ana kazi nyingi, ila yeye amekuambia kwamba ana kazi gani anayo ifanya?”

“Hajanieleza mengi, ila kuna tukio moja ambalo leo limetokea kipindi tunarudi huku, ndio hili linalo niumiza kichwa hadi sasa hivi nikimuuliza dokta aka kazi ya kuingia huku na kutokea huku”

“Tukio gani?”

“Kipindi tunakuja huku, tunatoka sijui hoteli gani pale mjini, tukiwa njia tukavamiwa na majambazi wenye silaha kabisa, wakaanza kutupiga risasi za kutsha, yaani laiti ingekuwa si lile gari kuto kuwa linaingia risasi, kirahisi hivi sasa hivi tungekuwa tunazungumza mambo mengine kabisa”

Mama Gody mkubwa akaka kimya huku akionyesha na yeye ana kitu anacho kifahamu ila ana shindwa kukiungumza.

“Unajua chochote?”

“Mmmmm….hapana”

“Kweli?”

“Ndio, ningekuwa nina faamu chochote basi ningekuwambia, kwa maana mmmmm hilo tukio limenistua sana”

“Kweli hufahamu chochote mama Gody?”

“Kweli ningekuwa ninafahamu chochote ningekuambia, nisinge kuficha, hembu muulize huyo huyo rafiki yake si ujaua kwamba wanaume wana kazi ya kufichiana siri”

“Sawa au wifi anafahamu chochote?”

“Hapana, ila usimuambia kwanza hilo tukio kwa maana ninamfahamu wifi ni mtu wa kupanic so anaweza kumuambia mama alafu mambo yakawa mabaya zaidi”

“Sawa”

Tukaanza kushusha mizigo ya nguo tulizo zinunua, tukaingiza ndani na kumkita dokta akiwa amekaa kwenye moja ya sofa huku ametulia sana, nikaanza kuzigawa zawadi hizi.

“Asante wifi”

Wifi yangu alizungumza huku akitazama moja ya gauni nililo mnunulia.

“Usijali wifi. Dokta nakuomba”

Nilizungumza huku nikitangulia kutoka nje, dokta akanitazama kwa macho ya woga kidogo, akashusha pumzi kisha akanyanyuka, nikatembea hadi lilipo gari lake. Nikaliegemea huku nikimtazama anavyo nifwata kwa woga.

“Ndio shem”

“Swali langu ni lile lile tu, ninaomba uniambie ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa rafiki yako”

“Kusema kweli hata mimi siwezi kufahamu kitu chochote”

“Acha unafki dokta unafahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea”

“Sifahamu kweli, ila wewe ndio unaye takiwa kufahamu ni kitu gania mbacho kinaendelea kwa mume wako. Wewe kama umeshindwa kujua unahisi kwamba mimi ninaweza kweli kufahamu?”

Dokta alizungumza kwa kujiamini, woga wote ambao alikuwa akinionyesha wote ukaisha.

“Eddy ni rafiki yangu toka tukiwa darasa la tano, ila kusema kweli siwezi kufahamu kwa kila kitu chake kinacho endelea kwa maana hapa katikati tumetawanyika, yeye yupo Dar na mimi nipo Tanga kwa hiyo siwezi kufahamu ni kitu gani kinacho endelea.”

“Ila shem, mbona yule dada nimemkuta akimuua?”

“Mimi na wewe sote tulikuwa nje, wewe ndio ulirudi ndani ukakutana na hilo tukio hivi hapo mimi nitakuwa ninafahamu kitu gani jamani?”

“Sawa bwama”

“Aa….aaa usiseme hivyo, kikubwa kaa nay echini na umuulize ni kitu gani ambacho kuimemsibu, na ninaimani kwamba ataweza kukuelezea A to Z, nikikuambia mimi nitaonekana mchonganishi au mnafki na kama unavyo mjua mumeo ni mtu mwenye hasira hususani mambo yake yanayo elezwa pasipo idhini yake”

“Mmmmm”

“Yaa hata kama ninafahamu ukweli wa kitu kinacho endelea sinto weza kukuambia, kwa maana siwezi kuharibu uradiki wetu wenye miaka zaidi ya kumi na tano kwa ajili yako”

“Kwa hiyo unafahamu?”

“Ndio ninafahamu, ila sinto kuambia ukweli, ukitaka kujua ukweli, muulize yeye mwenyewe au mama yake”

“Mama anafahamu?”

“Nimekupa machaguo mawili, yeye au mama yake hapo utaweza kupata ukweli”

Dokta alizungumza huku akininyooshea mkono, nikamkabidhi funguo ya gari lake na kuiweka kwenye mfuko wa suruali yake.

“Kwa ushauri tu mdogo, kuwa makini na jamaa”

Dokta baada ya kuzungumza maneno hayo akaondoka na kuingia ndani. Nikashusha pumzi nyingi huku nikiwa nimejawa na maswali ambayo kusema kweli hayana majibu sahihi. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia Eddazaria, simu yake ikaanza kuita hadi ikakata. Nikarudi tena kumpigia, simu ikaita kidogo kisha ikapokelewa.

“Baby upo wapi?”

“Hahahaa….hahaa…..baby eheeee?”

Nilisikia sauti ya kike ikicheka kicheho cha dharaua, mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi, joto kali likanitawala mwilini mwangu.

“Wewe ni nini na kwa nini upokee simu ya mume wangu?”

“Hahaaaa, mume wako. Ngoja”

Simu ikakatwa, nikajikuta hasira ikizidi kukibana kifua changu hadi nikasikia moyo wangu kama unataka kuchomoka kwa maumivu makali sana. Kabla hata sijafanya maamuzi ya kumpigia simu tena, picha ikaingia whatsapp, ikitokea kwa Eddazaria, kwa haraka nikaifungua. Macho yakanitoka, nikaanza kutetemeka hadi nikatamani kukaa chini. Kwani picha hii inamuonyesha Eddazaria akiwa amepigika, amevimba uso karibia mzima na eneo ambalo amekaa amefungwa kwenye kiti huku nyuma yake kukiwa na mambomba makubwa kama ya gesi.

‘Ohoo Mungu wangu’

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, tisheti yake aliyo ivaa, imechanika chanika, huku ikiaonyesha dhairi kwamba amepigwa tena amepigwa sana.

“Jojo”

Sauti ya wifi ikanistua sana, nikamtazama nikamuona akinifwata huku usoni mwake akionekana kama ananishangaa.

“Vipi mbona unalia?”

Aliniuliza mara baada ya kunifikia karibu.

“Kuna tatizo?”

“Eheee”

“Tatizo gani tena?”

Hata kuzungumza nikajikuta nikishindwa kabisa, nikamkabidhi wifi simu yangu huku ikiwa na picha ya mdogo wake. Naye nikamuona akitokwa na macho.

“Hii….hii..picha imetumwa na nani?”

“N…ni..limpigia kwenye simu yake, akapokea msichana mmoja, baada ya muda akapokea hii picha”

“Oooohoo Mungu wangu”

Wifi naye akaonekana kuchanganyikiwa kwa hili. Kwa haraka akaanza kuelekea ndani, na mimi nikaanza kumfwata kwa nyuma. Akaanza kuangaza angaza sebleni.

“Unatafuta nini?”

Mama Gody aliuliza huku akimtazama wifi usoni.

“Simu yangu ipo wapi?”

“Ile pela kwenye kochi”

Mama Gody mkubw alijibu huku akimtazama wifi. Kwa haraka akaichukua simu yake na kuanza kuiminya minya.

“Jojo kuna nini kinacho endelea?”

Mama Gody aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kuna picha”

“Picha, picha ya nini?”

“Yaa Eddy”

“Akifanyaje?”

“Chukua simu kwa wifi”

Mama Gody mkubwa akamfwata wifi, akamuomba simu yangu, wifi ambaye tayari simu yake alisha iweka sikioni mwake, akampa mama Gody mkubwa simu yangu, akaitazama picha hiyo, nikamshuhudia akishika mdomo wake huku akikaa kwenye sofa.

“Ohoo Mungu wangu, kuna nini kinacho endelea jamani?”

Mama Gody mkubwa alizungumza ila sikuweza kumjibu chochote zaidi ya kumtazama dokta kwa macho makali sana.

“Kuna nini kinacho endelea?”

Dokta aliuliza huku akimtazama mama Gody.

“Unauliza ni nini kinacho endelea ikiwa wewe unafahamu ukweli eheee?”

Niliuliza kwa ukali sana hadi dokta akashangaa.

“Ehee Rich upo wapi?”

“Sasa Eddy ametekwa”

“Eheee kuna picha hapa tumetumiwa na watekaji”

Dokta naye macho yakamtoka baada ya kusikia mazungumzo hayo ya wifi.

“Eheee, yaani hapa nimechanganyikiwa”

“Nipo kwa mama tayari”

“Ngoja nikutumie”

Wifi akakata simu, akaichukua simu yangu kutoka mikononi mwa mama Gody, ambaye tayari machozi yamesha anaza kumtoka.

“Sema mume wangu yupo wapi?”

Nilizungumza kwa ukali, sikujali kama nipo ukweli au laa, kwani tayari mambo yamesha haribika kabisa na sasa hivi sina muda wa kumbembeleza dokta.

“A…H….a….aa…ssi…sijui……jamani”

“Acha unafiki mwanaume”

Nizungumza huku nikimfwata dokta kwa hasira, nikamshika shati lake nikamnyanyua juu, nikamsogeza karibu kabisa na uso wangu.

“Niambie mume wangu yupo wapi?”

“Jojo, jojo, jojo”

Mama Gody aliniita huku akinifwata na kunitoa mikono yangu kwenye shati la dokta.

“Huyu anajua ni wapi mume wangu alipo”

“Dokta kama unajua si uzungumze jamani”

Mama Gody alizungumza huku akilia.

“Jamani mimi sifahamu, zaidi ya kujua ni kazi ambayo anaifanya”

“Kazi gani tena”

Dokta akaka kimya kidogo, mlango wa hapa sebleni ukafunguliwa, na kutufanya sote tuangalie mlangoni, akaingia mama mke huku akiwa amebeba mfuko mweusi, ikatubidi sote tukaushe kimya.

“Shikamoo mama”

Mama Gody aliwahi kusalimia huku akifuta machozi usoni mwake.

“Marahabaaa, mbona mume simama kama kuna ugomvi?”

“Shikamoo mama”

Nilisalimia na mimi huku nikijaribu kuhakikisha kwamba ninaificha hasira yangu kwa dokta.

“Bwana mama hapa kuna tatizo”

“Wifi alizungumza na kutufanya sote tumgeukie na kumtazama.”

Nikamuona mama Gody akitingisha kichwa akiomuomba wifi asizungumza chochote.

“Tatizo gani?”

“Ahaa…mama hakuna tatizo mwaya”

Mama Gody aliwahi kuzungumza huku akiendelea kumsisitizia wifi asiongee chochote.

“Au mumesha anza kuombana na nyinyi?”

“Hapana mama hakuna tatizo lolote mwaya”

“Mmmmm haya, kuna ndizi hizi na nyama mupike, mimi najiandaa niende kanisani”

“Sawa mama”

Mama mkwe akaondoka sebleni hapa huku mfuko alio ingia nao akiwa amemkabidhi mama Gody mkuubwa.

“Wifi hili swala ni mapema sana kumuambia mama, ninakuomba kwanza tutulie tumesikilizie Rich ataweza kufikia wapi”

“Wifi hili swala ni kubwa, hivi unahisi mama akilifahamu huko anapo kwenda itakuwaje, tunatakiwa tumuweke chini na tumueleze kila kitu kinacho endelea”

“Dokta una nafasi ya kunieleza ni wapi alipo mume wangu, la sivyo hili jambo wewe ndio utakaye libeba.”

“Mimi kusema ukweli nafahamu jamaa anaf……”

“Jojo huyo mwenzako yupo wapi anipeleke kanisani kwa maana ninampigia simu ila naona hapokei simu”

Sauti ya mama mkwe ikatustua sote tulipo humu ndani. Kigugumizi kikali kikanitawala, jibu la kumjibu mama mkwe likanishinda kujibu kabisa. Simu ya mama mkwe ikaanza kuita, akaitazama kwa muda.

“Anapiga sijui alikuwa ameiweka wapi simu”

Mama mkwe alizungumza, sote tukajawa na umakini wa kumtazama na kusikilizia ni kitu gani ambacho mama mke atakizungumza na Eddy.

“Weee upo wapi?”

Mama mkwe alianza kuzungumza, ila baada ya sekunde mbili sura yake ikabadilika kidogo na kujawa na mikonjo.

“Wewe ni nani?”

Swali la mama mkwe likatushua sote hapa sebleni, hususani mimi kwani tayari nimesha fahamu mwanamke huyo aliye nipokelea simu yangu ndio huyo huyo aliye mpokelea mama mkwe simu yake.




“Mumemteka!!?”

Mama mke alizungumza huku suru yake ikibadilika kabisa na kujawa na mshangao mkubwa ulio tufanya sote tuzidi kukaa kimya.

“Haloo haloooo”

Mama mkwe aliita ila inavyo onyesha kwamba simu imekatwa kabisa. Akaitoa sikuoni mwake na kuminya minya kioo cha simu hiyo kisha akairudisha sikioni mwake. Akaitoa tena hapo ndipo wifi akamsogelea mama mkwe ambaye anaonekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.

“Mama kaaa kwanza”

Wifi alizungumza huku akimkalisha mama mkwe kwenye sofa.

“Ametekwaje tekwaje?”

“Hata sisi hatujui, ndio nimeongea na Rich na kumtumia picha zake, nimemuambia azungumze na polisi tuone tunamtafuta vipi”

“Wewe si ulitoka na mwenzako?”

Mama mkwe aliniuliza huku akinikazia macho.

“Ndio mama…ila ila alihitaji mimi nirudi nyumbani, alinikabidhi kwa dokta akanirudisha nyumbani, ila tukiwa njiani tukakautana na wifi akanipakiza kwenye gari lake”

“Na wewe mwenzako yupo wapi?”

“Ehee.e…..”

Dokta alipatwa na kigugumizi kizito cha kushindwa hata kulijibu swala la mama mkwe, nikatamani kuzungumza kitu ila nikajukuta nikishindwa kuzungumza kabisa.

“Unajua ni kina nani walio mteka?”

“Hapana mama, ila yeye aliniomba nimlete shem nyumbani na nikafanya hivyo”

“Maelezo yenu hayajitoshelezi”

“Ila mama ngoja tumsikilizie Rich ni kitu gani ambachgo anaweza kukifanya kwa sasa kwa maana wametuma picha yake”

“Picha ya nani?”

“Ya Eddy”

“Hembu niione”

Nikamkabidhi mama mkwe simu yangu baada ya kupewa maelezo na wifi. Akaitazama picha ya Eddazaria kwa muda kisha akanirudishia simu yangu pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote. Gafla simu yangu ikaanza kuita, nikaitazama na kukuta ni namba ya Eddazaria, kwa haraka nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Haloo”

“Tusikilizeni kwa umakini, tena umakini unao eleweka…”

Nikaiweka simu yangu loud speaker ili tuweze kusikia kila kitu kinacho endelea.

“Tunawapa masaa ishirini na nne kuanzia hivi sasa tunahitaji mutupatie milioni mia moja na hamsini ili tuweze kumuachia huru huyu nguruwe wenu, la sivyo mutakuja kushuhudia kichwa chake kikiwa kimetenganishwa na mwili wake, munatuelewa?”

Sauti ya kike iliendelea kusikika ikuzungumza kwa msisitizo mkubwa sana.

“Milioni mia jamani…..!!!?”

Wifi alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Hakujibiwa jibu lake zaidi ya simu kukatika

“Mmmm milioni mia na hamsini saa hivi tutazitolea wapi?”

Mama mkwe alizungumza kwa sauti ya unyonge iliyo jaa masikitiko makubwa sana.

“Nitazitoa mimi”

Nilizungumza kwa kujiamini, watu wote wakanitazama huku wakionekana kushangaa maamuzi yangu.

“Wifi hizo pesa unazo kweli au?”

Wifi alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio wifi ninazo, nipo tayari kuzitoa hata sasa hivi”

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga. Mama mkwe naye akanitazama usoni pasipo kuzungumza kitu chochote.

“Hili swala sio la kukurupuka”

Mama mkwe alizungumza na kutufanya sote tumtazame, akaondoka sebleni hapa. Tukabaki kimya huku kila mtu akiwa akimtazama mama mkwe akimalizia kuingia ndani.

“Wifi naomba tuzungumze”

Nilizungumza huku nikitoka nje, wifi akanifwata kwa nyuma. Tukasimama nje sehemu yenye bustani ya maua.

“Wifi hili swala nahitaji tuweze kulishuhulikia mapema”

“Kivipi?”

“Kama watu wanavyo hitaji hizo milioni mia na hamsini ni bora nikatoe kwenye akaunti yangu, kisha tuwapatie hao watu”

“Ngoja kwanza mama alishuhulikie hili swala”

“Analishuhulikia kivipi?”

“Sifahamu ila ngoja tuone ni jinsi gani ambavyo anaweza kufanya”

“Mmmm sawa”

Sikuwa na kitu cha kuzungumza zaidi ya kukubaliana na maamuzi ya mama mkwe. Tukaingia ndani, furaha sote ikatupotea kila mtu akajawa na mawazo mengi sana. Kwa msongo wa mawazo nikajikuta nikiondoka sebleni, nikaingia ndani kwangu na kujitupa kitandani, nikaitoa simu yangu mfukoni mwangu, nikaanza kutafuta majina ya mtu ambaye ninahisi anaweza kunisaidia katika hili swala la kumuokoa mume wangu. Nikaiona namba ya simu ya dokta Clara nikaitazama kwa muda kisha nikampigia. Simu ya Clara ikaanza kuita kwa muda, kisha ikapokelewa.

“Clara”

“Ehee habari yako”

“Salama vipi mbona unazungumza kama una wasiwasi”

“Eddy umetekwa”

“Ametekwa kwenye nini, labda”

“Ametekwa kwenye nini ndio swali gani hilo eheee?”

Niliuzungumza kwa kufoka kwa maana hapa nilipo akili yangu haipo sawa kabisa.

“Jojo tulia hembu kaa uniambie ni kitu gani kinacho endelea”

“Nimekuambia kwamba Eddy ametekwa, hadi sasa hivi watekaji wanahitaji milioni mia moja na hamsini ili waweze kumuachia huru”

“Ooohoo Mungu wangu”

“Ndio hivyo”

“Sasa kwa nini wamekuteka?”

“Hilo sio swala la kulijadili kwa muda huu, ninacho kuambia ninaomba unitafutie watu ambao wanao weza kunisaidia katika hili”

“Watu wa aina gani?”

“Hata majambazi wanao weza kufanya hili jambo haraka kama ninavyo hitaji mimi sawa”

“Mmmm”

“Fanya hivyo kama ninavyo kuambia”

“Sawa”

“Ndani ya nusu saa naomba hili swala liwe limesha pata muafaka”

“Sawa Jojo”

Nikakata simu huku nikishusha pumzi nyingi sana. Nikajifikiria kwa muda kisha nikatoka chumbani humu, nikakutana na mama mkwe kwenye kordo akiwa amevalia nguo za mazoezi.

“Twende huku”

Mama mkwe alizungumza, ikanilazimu kuanza kumfwata kwa nyuma. Tukafika sebleni na kumkuta dokta na wifi.

“Dokta tupeleke sehemu”

“Sawa mama”

Dokta akanyantuka, tukatoka nje na kuingia kwenye gari lake. Mama mkwe amekaa siti ya mbele huku mimi nikiwa nimekaa kwenye siti ya nyuma.

“Mume siku mbili tatu hizi ana ugomvi na mtu wa aina yoyote?”

“Hapana”

“Una uhakika?”

“Ndio mama”

“Tukio lile la juzi kati mulivyo kuwa mupo kambini ilikiwaje?”

“Ahaa….liliisha tu”

“Halikuisha hapo”

“Kivipi?”

“Watu ambao walihusika kwenye tukio lile ndio hao hao ambao wamemteka mwanangu leo”

Nikajikuta nikikaa kimya huku nikianza kumfikiria Nuru ambaye yeye ndio amehusika kabisa katika yukio lililo tokea katika msitu wa kandekamaha ulipo katika wilaya ya Lushoto. Nikiwa katika mawazo hayo, nikaona mkono wa mama mkwe akinielekezea mimi, nikautazama na kuona akinikabidhi bastola. Taratibu nikaichukua huku macho yakiwa yamenitoka, si mimi tu hata dokta naye macho yamemtoka.

“Tunakwenda kumuokoa mwanangu sasa kuna mawili kufa na kupona sasa kila mmoja awe makini kwa kile ambacho tunakiendea mumenielewa?”

Mama mkwe alizungumza huku akimkabidhi dokta na yeye bastola yake, kwa woga akashindwa hata kuipokea na kijikuta akipunguza mwendo kasi wa gari na mwishowe akalisimamisha kabisa.


“Mbona umesimamisha gari?”

Mama mkwe aliuliza huku akimtazama dokta usoni mwake.

“Mama mimi taaluma yangu ni udaktari, vitu kama hivi sijawahi kufanya siku hata moja mama”

Dokta alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka.

“Mimi kwani taaluma yangu ni nini, si nimekufundisha wewe primary?”

“Ndio mama”

“Haya washa gari tuondoke”

Dokta hakuwa na jinsi zaidi ya kuwasha gari na kuendelea na safari huku tukifwata maelekezo ya mama mkwe. Tukazidi kusonga mbele hadi tukaufikia msitu wenye miti mingi sana iliyo fungamana kwa ukaribu sana. Mama mkwe akamuonyesha dokta sehemu ya kusimamisha gari lake katika kichaka ambacho si rahisi kwa mtu kuweza kuliona kwa ukaribu. Tukashuka kwenye gari.

“Kama kuna mtu mwenye simu yake yenye mlio aweke vibration au silence isije ikatugarimu huko mbele”

“Sawa mama”

Nilijibu huku nikiitoa simu yangu mfukoni, nikaiweka nikapunguza sauti ya muito wake hadi mwisho kabisa. Kabla sijairudisha mfukoni, simu ya dokta Clara ikaanza kuita, nikamtazama mama mkwe kwa muda kidogo kisha nikasogea pembeni kidogo na kuipokea.

“Ndio”

“Nimewapata wauaji maalumu wapo wanne wanahitaji maelekezo ya wapi ulipo na kazi ifanyike muda gani”

“Sikia nitakupigia baada ya muda kidogo, ila waambie wake tayari”

“Sawa”

Nikakata simu na kurudi sehemu alipo simama dokta na mama mkwe. Mama mkwe akanitazama kidogo kisha akaanza kutembea kuelekea mbele kabla hatujafika mballi kidogo, akasimama.

“Wewe rudi kaangalie gari lako, usije ukatuaharibia”

Mama mkwe alimuambia dokta, aliye tingisha kichwa huku akitabasamu. Dokta akaanza kutembea kwa haraka kuelekea tulipo toka.

“Vijana wengine wa kitanga ni lege lege sana, sijui wazazi wao wamewakuza vipi”

Mama mkwe alizungumza huku akimtazama dokta jinsi anavyo ongeza mwendo kasi wa kuondoka. Mama mkwe akatoa simu yake, kwenye mfuko wa suruali yake ya mazoezi aliyo ivaa.

“Mupo wapi?”

“Kaeni tayari kwenye position”

Mama mkwe akakata simu na kurudisha mfukoni mwake.

“Kuna watu ambao umesha waandaa”

“Yaa kuna vijana wangu watatu tayari wapo katika nyumba ambayo amekamatwa mume wako, wanasubiria, tuweze kufika”

“Sawa mama”

Tukazidi kusonga mbele, huku kwa mara kadhaa mama mkwe aliweza kutazama kila eneo la msitu huu, kwa umakini mkubwa sana.

“Mama ninaweza kukuuliza kitu?”

“Unaweza kuniuliza?”

“Unajishuhulisha na nini?”

“Kivipi?”

“Unajishuhulisha na nini haswa kwenye maswala haya ya kiusalama”

Mama mkwe akaka kimya kwa muda huku tukiendelea kutembea.

“Nakumbuka kipindi nilipokuwa binti wa umri wako, kipindi hicho ukimaliza form four ulikuwa unapelekwa jeshini, yaani ilikuwa ni amri na wala sio ombi. Nilipo kuwa jeshini niliweza kuwa the best sniper, nikizungumza hivyo si unanielewa”

“Yaa si mduguaji?”

“Yaaa, sifa ya kipaji chagu hicho iliweza kutawala kwenye kambi, na serikali ikaamua kuniongeza zaidi, kipindi hicho ilikuwa ni sereikali ya awamu ya kwanza kabisa. Nilipelekwa Marekani, nikajiunga kwenye kikosi kimoja cha kijasusi, na nikwa ndio mduguaji wao wa kazi ngumu ngumu. Niliifanya kazi hiyo kwa miaka minne, nikarudi Tanzania, kitu kikubwa ambacho niliaweza kupewa nafasi ya kuchagua ni kazi gani ambayo ninatakiwa kujiunga kwa kipindi hicho, serikali ilikuwa na watumishi wachache sana kwenye sekta ya elimu”

“Basi nilikaa na baba yangu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na cheo cheo serikalini, kanishauri niwe mwalimu, aliweza kunieleza faida nyingi sana za kuwa mwalimu, moja ni kuwa na famili. Na kutokana na mimi nilihitaji kuitwa mama, basi ilinibidi kukubali kuwa mama, kwa maan aniliweza kuona ni mambo mengi ya hatari ambayo nilikuwa ninakutana nayo kipindi nilipo kuwa katika vikosi vya kiusalama. Ila serikali ikiwa inakazi ngumu au inahitaji mafunzo ya vijana wapya katika tathinia, ya udunguaji huwa wananiita, ninakuwa mkufunzi”

“Kwa hiyo hadi sasa hivi hujaiacha hiyo kazi?”

“Yaa kazi hiyo kuiacha ni hadi mimi nife ndio mwisho wa kazi. Ila mambo haya niliyo kueleza hakikisha kwmaba haumuambii mtu wa aina yoyote”

“Siwezi kufanya hilo mama, sasa Eddy naye uliweza kumuingiza huko?”

“Hapana, mume wako ni mbishi, na pia hakupenda kabisa maswala ya kuajiriwa, ila wanangu wote hakuna mzembe niliwafundisha toka wakiwa watoto, hivyo kila mmoja ameamua kuchagua maisha yake, siwezi kuwalazimisha wawe kama mimi nilivyo pitia”

“Sawa mama”

Sikuwa na swali la kuuliza zaidi, tukatembea kwama dakika kumi hivi, tukaona nyumba iliyo tengenzwa na mbao. Vijana wa mama mkwe wakatufwata sehemu tulipo simama.

“Vipi?”

“Tumechunguza na ndani wapo watu sita, na huku nje kuna walinzi kama kumi na mbili hivi”

“Munaweza kuwachukua wangapi katika hao?”

“Tunaweza kuwaangusha wote”

Tukiwa hapa tukaona gari mbili nyeusi zikisimama nje ya nyumba hii.

“Kila mtu achukue position yake. Jojo, njoo na mimi”

Kijana mmoja akampkabidhi mama mwe bunduki kubwa, kisha bastola yake hiyo akaichomeka kiunoni mwake. Nikamfwata mama mkwe hadi kwenye moja ya mti, tukalala chini, kwenye gogo moja kubwa, mama mkwe akaisimamisha bunduki hiyo yenye vijichuma viwili vya kusimamia. Akaiweka lensi vizuri ya kutazama mbali, kwa ishara akaniomba nitazame na mimi kwenye lenzi hiyo. Nikachungulia na kuwaona walinzi wawili kwa ukaribu sana.

“Unaweza kuwaua kwa pamoja?”

“Kivipi mama?”

“Risasi moja inaweza kuwau kwa pamoja”

“Mmmm unawauaje mama?”

“Wewe waangalie”

Mama mkwe akashika vizuri bundiki hii huku akitumia lensi hii kuwatazama walinzi hao. Macho yangu yote nikayaelekeza kwa walinzi hao ambao wapo karibu sana wakionekana kuzungumza zungumza kitu. Kitendo cha walinzi hao kusogeleana karibu, na kukaa sawa, nikawashushudia wakianguka chini kimya kimya huku kila mmoja akiwa ameishika shingo yake.

“Nimewapiga risasi ya shingo, kila mmoja anakufa kwa sekunde zake”

“Mmmmm kumbe hii bunduki ina nguvu?”

“Ukiachilia nguvu tu, ukiwa katika mapigano kama haya unatakiwa kuangalia ni sehemu gani ambayo unaweza kumpigia adui yako na kuhakikisha kwamba anakufa haraka pasipo wewe kupoteza risasi zako”

“Sawa mama”

Tukamuona Edazaria akitolewa nje na wanaume wawili walio jazia misuli yao. Kabla hata hawajamfikisha kwenye gari walizo kuja nazo, mama mkwe akaanza kuwashusha mmoja baada ya mwengine na kuwafanya walinzi wengine kuchanganyikiwa. Nilipo muona Eddazaria yupo huru kwa haraka nikanyanyuka pasipo kujali kama kuna watu wenye silaa au laa. Eddazaria akajibaza kwenye gari la watu hao. Nikafanikiwa kumfikia Eddazaria sehemu alipo, kwa haraka nikamkumbatia huku nikimbusu mashavuni mwake.

“Umeku…jaa….na nani huku?”

Eddazaria aliniuliza kwa sauti ya kukata kata huku mdomo wake ukiwa umevimba sana kutokana na kipigo hicho alicho kipata kutoka kwa watu hawa.

“Mama, nimekuja na mama”

“Nyma yakoooo”

Nikageuka nyuma, nikamkuta mwanaume mmoja akihitaji kutupiga risasi, ila hata kabla hajanyanyua mkono wake, tukashangaa akianguka chini huku kichwa chake kikipasuka vibaya. Nikautazama upande nilio muacha mama mkwe, nikamuona akija akiwa wameibeba bunduki yake hiyo kubwa, kabla hatajatufikia akaitupa chini na kuchomoa bastola yake, na kuendelea kuwashambulia baadhi ya walinzi walio salia.

“Ingieni kwenye gari”

Mama mkwe alizugumza mara baada ya kutufikia karibu. Nikafungua mlango wa gari lililopo karibu yetu, nikamuingiza Eddazaria siti ya nyuma, kisha sisi nasi tukapanda siti ya mbele, huku mimi nikiwa ndio dereva. Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuikuta fungua kwenye gari hili, nikaliwasha, nikalirudisha nyuma kwa kasi kisha tukaanza kuondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi sana huku tukiacha ukimya kwani watu wote wameuwawa. Mama mkwe akatoa simu yake na kuiminya minya kidogo kisha akaiweka sikoni mwake.

“Vipi umesha ondoka”

“Hapana mkuu tunawamalizia na kuchukua ushahidi”

“Sawa hakikisheni munafahamu mkuu wapo alipo”

“Sawa mkuu”

Niliweza kuyasikia mazungumzo hayo kutokana ukimya ulio tawala ndani ya gari.

“Kunja kulia”

Mama mkwe alizungumza, nikakunja barabara inayo elekea kulia, baada ya muda kidogo tukafika katika gari tulipo muacha dokta. Mama mkwe akawa wa kwanza kushuka kwenye gari, akamfwata dokta aliye jificha kwenye gari lake.

“Baby, baby”

“Mmmmm”

“Pole mume wangu, tunakupelekea hospitali, sawa mume wangu”

“Mmmmm”

Eddazaria aliitikia kidogo huku macho yake akiwa ameyafumba.

“Unajisikiaje?”

“Mmmm….mmm…”

Eddazaria alitika kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo mingi sana huku damu zikimtoka puani na masikioni, nikachanyikiwa na kujikuta nikihamia siti ya nyuma.

“Eddy, Eddy”

Niliita kwa suati huku nikimtingisha Eddazaria kifuani mwake, ila Eddazaria hakuitika kabisa zaidi ya kutoa sauti iliyo jaa mikwaruzo. Mama mkwe akafungu mlango wa siti ya nyuma, alipo muona Eddazaria katika hali kama hii naye pia akanonekana kustuka sana.

“Weee dokta njoo unashangaa shangaa nini?”

Dokta kwa haraka akafika katika eneo hili, kwa kusaidiana wote watatu tukamshusha ndani ya gari na tukamlaza chini. Dokta akaamkagua kagua kila eneo la mwili wake ulio jaa mikwaruzo mingi sana na damu zilizo mtiririka. Dokta akaweka viganja vyake vyote viwili juu ya kifua cha Eddazaria na kuanza kukiminya kwa nguvu. Eddazaria hakuonyesha dalili yoyote ya kuzinduka, dokta akaendelea na zoezi hilo, ila baada ya muda akaweka sikioo lake la upande wa kulia juu ya kifua cha Eddazaria kusikilizia mapigo ya moyo. Dokta akajaribu kufanya vipimo vyote vyote ambayo anavifahamu yeye. Baada ya muda akanyanyua uso wake na kututazama kwenye nyuso zetu huku macho yake yakiwa yamelengwa lengwa na machozi.

“Eddy……EDDY AMEKUFA”

Maneno ya dokta yakanifanya niiishiwe nguvu, miguu ikaanza kunyong’onyea, nikakaa chini mzima mzima huku machozi yakianza kunimwagika usoni mwangu. Nikamuona mama mkwe akifyatua risasi hewani huku akiwa amejawa na hasira kali sana huku machozi yakimwagika usoni mwake na akapiga ukelele ulio nifanya nizidi kuumia moyoni mwangu kwa kumpoteza mume wangu kipenzi.



“Muingizeni kwenye gari”

Mama mkwe alizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi yanayo tokana na kulia. Nikajikaza kusimama ila nikajikuta nikishundwa kabisa. Dokta taratibu kwa kujikaza kama mwanaume, akaanza kuunyanyua mwili wa Eddazaria na kumuingiza ndnai ya gari. Mama mkwe akawa mtu wa kwanza kupanda kwenye gari hilo, dokta akanifwata na kunisaidia, akanishika mkono na kuninyanyua chini nilipo kaa huku nikilia. Akaniingiza siti ya nyuma alipo ulaza mwili wa Eddazaria. Machozi yakazidi kunitiririka kila ninapo muangalia Eddazaria usoni mwake. Nikamnyanyua kichwa chake na kukilaza kwenye mapaja yangu.

“Ongeza mwendo”

Mama mkwe alizungumza huku akimpiga piga dokta katika bega lake. Dokta akazidi kujitahidi kuendesha gari lake kwa mwendo wa kasi sana huku mwili mzima ukimtetemeka.

“Hawezi kufaa mwanangu, hawezi kufa kabisa mwanangu”

Mama mkwe alizungumza huku akipiga piga ngumi kwenye dashbody ya gari hili.

“Tunaelekea wapi mama?”

“Hospitalini kwako, ongeza mwendo”

“Sawa mama”

Tukazidi kusonga mbele, tukafika katika jengi kubwa la gorofa, sikutazama hata lina gorofa ngapi au lina kibao kilicho andikwaje, kwa haraka tukashuka kwenye gari, dokta akakimbilia ndani, baada ya dakika moja na sekunde zake akatoka akiwa ameongozana na manesi wawili wakiwa wanasukuka kitanda, wakamanza kumtoa Eddazaria ambaye kusema kweli katika kipindi chote ambacho nimekilaza kifua changu juu ya mapaja yangu sukuweza kuona hata dalili yoyote ya kifua chake kuonyesha kama kina mapigo ya moyo. Kwa haraka tukaongozana na manesi hawa hadi kwenye moja ya chumba. Dokta akaingia, ila nilipo taka kuingia mama mkwe akanishika mkono.

“Waache wafanye kazi yao”

Mama mkwe alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikatafuta kiti kilichopo pembeni ya mlango wa kuingilia katika chumba hichi, nikakaa huku nikiinamisha kichwa changu chini.

“Mupo nyumbani?”

Niliisikia sauti ya mama mkwe, ikanifanya ninyanyue kichwa changu na kumtazama, nikamuona akizungumza na simu huku akiwa anatembea tembea kwenye kordo hii, kwenda na kurudi.

“Hakikisheni kwamba hamtoki ovyo hivyo na munafunga geti mapema”

Mama mkwe akakata simu na kunifwata hapa nilipo, akaka pembeni yangu huku akinitazama usoni mwangu.

“Usimuembie mtu yoyote kitu chochote hadi pale tutakapo jua mbivu na mbichi sawa”

“Sawa mama”

Taratibu mama mkwe akanishika kichwa changu na kukilaza kwenye bega lake.

“Moyo wangu hauamini mwanangu kwamba amekufa, naamini Mungu yu pamoja naye hawezi kumchukua akiwa katika umri mdogo kama huu”

“Kweli mama?”

Niliuliza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Masaa yakazidi kusonga mbele, watu baadhi kwenye kordo hii kila wakipita wananitazama wakionekana kunishangaa.

“Mama mbona hawatoki”

“Hii ni dalili njema”

“Jema kivipi mama?”

“Inaonyesha dhairi kwamba mwanangu hajafariki dunia”

“Kweli mama”

“Ndio amini hilo. Hivi tutampata wapi Nuru”

Nikastuka kidohgo baada ya kumsikia mama mkwe akilitaja jina la Nuru.

“Eheee?”

“Tutapata wapi Nuru, nahitaji hili swala nilishuhulikie mimi mwenyewe, nahitaji kuhakikisha kwamba analipa kwa ajili ya kitu alicho kifanya kwa mwanangu”

Nikashusha pumzi kidogo huku nikimtazama mama mkwe

“Niambie anapatikana wapi?”

“China, China ndipo yalipo makazi yake”

“Nyumbani kwake una pafahamu?”

“Ndio mama”

“Inabidi twende, ngoja Eddy apate nafuu sawa”

“Sawa mama”

Mlango wa chumba cha daktari ukafunguliwa akatoka dokta huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake. Mimi na mama mkwe kwa pamoja tukasimama huku tukimtazama dokta.

“Vipi?”

“Kwanza nitangulize samahani mama kwako na kwa shemeji hapo kwa kuweza kutoa taarifa ambayo hapo awali ilitoka kutokana na wasiwasi ulio changanyikana na woga. Aha….Eddy yupo hai, hakufa kama nilivyo sema…..”

Nikashusha pumzi nzito iliyo mfanya hata dokta yeye mwenyee kukatisha sentensi yake na kutabasamu.

“Asante Mungu eheee ameumia sana?”

“Yaa ameumia kwa ndani, maeneo ya kwenye mbavu cha kumshukuru Mungu bavu hazikuvunjika”

“Labda kuna haja ya kumuhamisha hospitali na tukampeleka hospitali nyingine?”

“Hapana mama, uzuri hapa hospitalini tumejitosheleza kwa kila kitu, kutokana mimi ndugu yake wa karibu nipo hapa nitahakikisha kwamba anaendelea vizuri”

“Sawa dokta”

“Dokta naweza kumuona mume wangu”

“Hapana kwa sasa tumuache apumzike, baada ya kama lisaa hivi na nusu basi tunaweza kumuona kwa pamoja”

“Sawa sawa”

“Niwagizie chakula kantini kwa maana muda umekwenda?”

“Tutakwenda tu kununua wala usijali”

“Sawa”

Dokta akarudi ndani ya chumba hicho, kwa furaha nikajikuta nikimkumbatia mama mkwe.

“Sasa akipona mwenzio inabidi muhakikishe kwamba munakodisha walinzi wenye uwezo wa kuwalinda, sawa?”

“Sawa mama tutafanya hivyo”

“Hilo ni jambo zuri, mumesha fanikiwa kimaisha, mumesha kuwa na maendeleo makubwa ya kimaisha, walinzi ni lazima. Nyinyi kama nyinyi hamuwezi kujilinda wenyewe na ninahisi mwezio ubishi wake umemponza, sidhani kama akipoana kama atakuwa mbishi”

“Hahaaa sawa mama”

“Mpigie love muambie kwambie kwamba ampigie mumewe aje hapa hospitalini”

“Sawa, kumbe wifi anaitwa love”

“Yaa anaitwa Loveness”

“Sikulijua jina lake zaidi ya kuzoea kumuita wifi wifi”

“Ahaa, hilo ndio jina lake”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia wifi, simu yake ikaita baada ya sekunde kadhaa ikapokelwa.

“Wifi”

“Beee”

“Mama anasema mpigie shem aje hapa hospitalini”

“Mupo hospitali gani?”

“Ngoja nimuulize mama. Eti mama tupo hospitali gani?”

“Muambie barabara ya nne”

“Anasema barabara ya nne”

“Ahaa, ila hali ya mgonjwa vipi?”

“Dokta amesema anaendelea vizuri”

“Sawa ngoja niwasiliane naye”

“Sawa wifi, sijui unaweza kumuagiza na chakula”

“Poa, awaletee chakula gani?”

“Chochote”

“Sawa”

Nikakata simu na kuirudisha mfukoni. Baada ya kama nusu saa hivi kijana mmoja mweupe akafika, akamsalimia mama mkwe hapa ndipo nikajua ni mume wa wifi yangu, na mimi nikamsalimia huku nikiupokea mfuko wake.

“Mgojwa anaendeleaje lakini?”

“Anaendelea vizuri tunasubiri aweze kuzinduka”

“Nimezungumza na jamaa fulani hivi ni askari wameniuliza kama aliyetekwa amepatikana, ila sikuwapatia jibu, nikawaambia waenddelea kumtafuta tu”

“Yaaa waambie waendelea kumtafuta tu”

Mama mkwe alijibu kwa msisitizo. Mida ya saa tatu usiku hivi dokta akaturuhusu kuingia katika chumba alicho lazwa Eddazaria. Tukaingia sote watatu, tukamkuta Eddazaria akiwa ametundikiwa dripu la maji pamoja na dripu la damu.

“Unaendeleaje mwangungu”

“Kidogo po…oa mama”

Dokta akafunua shuka kidogo lililo mfunika Eddazaria tukaona bandeji nyingi walizo ziweka katika vidonda vyake.

“Hayo ni majeraha ya nje nje kidogo, kuna opasheni ndogo tumemfanyia katika mbavu za upande wa kuli ili kuto adamu ambayo imevilia ndani”

“Ahaaa….sawa sawa”

Mama mkwe aliitikia huku akitingisha kichwa.

“Tunahitaji kumuahimisha katika chumba hichi na kumpeleka chumba cha usalama zaidi ya hichi”

“Sasa hivi”

“Ndio mama”

“Sawa hakuna tatizo”

“Baby”

“Mmmm”

“Unajisikiaje?”

“Mmmm”

“Unajisikiaje?”

“Safi”

Eddazaria alinijibu huku akitabasamu. Tukawapisha manesi hao walio anza kukisukuma kitanda hichi kuelekea katika chumba wanacho kijua wao wenyewe. Tukawafatwa hadi katika vyumba ambavyo vimejengwa chini ya ardhi.

“Vyumba hivi huwa wanalala wale wagonjwa ambao kidogo hali zao si za kuhihitaji kelele na ni salama sana hata likitokea tatizo la uvamizi basi si rahisi kwa wavamizi kuweza kufahamu kama chini ya ardhi huku kuna vyumba vya wagonjwa”

“Ahaa sawa sawa, ni jambo zuri”

Eddazaria akaingizwa kwenye moja ya chumba, tukasubiri kwa muda manesi waweze kukiandaa chumba hicho kisha wakaturuhusu kuingia ndani.

“Shem pole bwana”

“Asante shem”

“Daaa ila watu ni wabaya sana”

“Yaa!!”

“Ila nahisi watahushulikiwa, ikiwa taarifa ipo tayari polisi naamini kila kitu kitakwenda sawa”

“Shukrqani sana shem”

“Mimi nakwenda nyumbani, kina Gody kule watakuwa wapo peke yao. Jojo baki hapa na mwenzio. Chakula hichi naamini mutaweza kula usiku huu”

“Yaa nimeleta chakula kingi naamini mgonjwa utaweza kula”

“Sawa shukrani shem”

“Dokta kwani kuna dawa yoyote anatakiwa kunywa sasa hivi?”

Mama mkwe aliuliza

“Hapana mama, kuna sindano atachomwa alfajiri na mapema sana”

“Ahaa basi sawa. Tutakuja kukuona kesho”

“Sawa mama”

“Jojo njoo”

Mama mkwe alizungumza huku akitoka nje, nikatoka nje na kumfwata sehemu alipo simama. Akatchomoa magazine mfukoni mwake na kunikabidhi.

“Utatumia hii endapo kuna tatizo litajitokea, na hakikisha kwamba munakuwa salama. Usipate muda wa kulala kizembe sawa”

“Sawa mama nimekuelewa”

“Hakikisha kwamba ana kula”

“Sawa mama”

Shem akatoka nje akiwa ameongozana na dokta. Wakaniaga na wote wakaondoka, nikarudi chumbani na kumkuta nesi akimalizia kuweka weka mitambo ya humu ndani vizuri.

“Usiku mwema”

“Nawe pia, hivi toilet ni wapi?”

“Mlango ule pale”

“Asante”

Nesi akatoka chumbani humu na kutuacha sisi wawili, nikamsogelea Eddazaria kabribu, nikabusu katika mdomo wake ambao kidogo lipsi zake zimevimba hii ni kutokana na kipigo alicho kipata.

“Pole mume wangu”

“Asante baby”

Nikatoa simu yangu mfukoni baada ya kuhisi kama inaita, kwani nakumbuka niliipunguza suati. Nikakuta namba ya Clara ndio inayo nipigia, nikaipokea taratibu.

“Jojo, mbona nakupigia hupokei jamani?”

“Sorry nilikuwa bize kidogo”

“Vipi Eddy amepatikana?”

“Yaa amepatikana tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri”

“Ahoooooo asanye Mungu”

“Ngoja nitakupigia muda si mrefu”

Nilizungumza mara baara ya kuona meseji ikiwa imeingia. Nikakata simu na kuifungua meseji hii ilyo tumwa kwa namba ngeni.

‘UNA MASAA MAWILI YA KUAMUA, URUDISHE KILE KITU CHANGU NILICHO KUPATIA KWENYE MAISHA YAKO AU NIMUANGAMIZE HUYO KUNGUNI WAKO AMBAYE UPO NAYE HAPO HOSPITALINI”

Meseji hii ikanitetemesha mikono yangu na kujikuta nikimtazama Eddazaria kwa woga mwingi sana kwani anaye zungumziwa katika kuuwawa hapa ni yeye.



“Baby vipi?”

Eddazaria aliuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hakuna kitu mume wangu”

“Mbona unatetemeka?”

“Hakuna wala usijali. Ngoja niandae chakula tuweze kula sawa baby”

Nilizungumza huku nikijaribu kutabasamu ila ukweli ni kwamba sina furaha ya aina yoyote, woga umenitawala kwa kweli. Nikaufunga mlangowa chumba hichi kwa ndani, kisha nikaingia chooni ambapo ndipo lilipo bafu. Nikafungua kiasi kidogo cha maji ya bomba lililopo chumbani hapa, nikachuku sabuni na kujipaka vizuri mikononi mwangu, nikaisugua vizuru mikono yangu kisha nikanawa kwa maji huku nongo nyingi zikinimwagika. Nilkarudi chumbani na kuufungua mfuko ambao shem aliweza kutuletea, nikafungua kifuko cha kwanza na kukuta kuku wa kukaanga huku akiwa amekatwa vipande vipande vingi. Nikafungua kifuko cha pili nacho na kukuta chipis mayai zilizo kaushwa huku zikitoa harufu nzuri inayo nipa hamasa kubwa ya kutamani kuzila kwa haraka haraka kwani njaa niliyo nayo si ya mchezo mchazo.

Nikakata kipande kidogo cha chipsi na kuila, huku nikimtazamana na Eddazaria usoni mwake.

“Mmmm tamu hizo?”

“Tamu eheee?”

“Eeheee”

“Mimi hapa sidhani kama ninaweza kula mdomo wangu una niuma sana”

“Baby jaribu kula hata kidogo please”

“Ningepeta uji mke wangu ningejisikia vizuri”

“Mmmm baby uji nitaupatia wapi usiku wote huu”

“Wana kantini yao hapa, naamini haifungwi masaa yote”

“Na sina pesa hapa mfukoni”

“Utawaambia dokta Abdalah atalipa”

“Dokta Abdalah ndio nani?”

“Dokta rafiki yangu”

“Sawa mume wangu, ila jaribu hata kuonja kipande cha kuku?”

“Baby mdomo wangu umevimba hivi wee, mwenyewe unaona jinsi maumivu yalivyo makali, sidhani hata kama ninaweza kufanya hivyo unavyo hitaji mimi nifanye”

Eddazaria alilalamika na ni kweli hata mimi mwenyewe nikiktazama ni dhairi kwamba hawezi kula chakula kigumu cha kutafuna hata kwa sekunde chache.

“Wanitengenezee uji wa ulezi na wauweke blue band”

“Sawa mume wangu”

Nikaichomoa bastola yangu niliyo ichomeka kiunoni mwangu, nikamkabidhi Eddazaria.

“Baby kaa nayo hii hadi nitakapo rudi”

Eddazaria akanitazama kwa muda kisha akatingisha kichwa kwa kukubaliana nami. Taratibu nikainama na kumbusu mdomoni mwake. Nikavifunga vifuko vya chips hizi kisha nikatoka chumbani humu, nikasimama kwenye kordo hii iliyo tulia na yenye mwangu wenye taa hafifu kidogo. Nikaitoa simu yangu mfukoni na kuirudia meseji vya vitisho niliyo tumiwa, kwa mwendo wa haraka nikaanza kukimbia kupandisha juu. Nikakutana na nesi akiwa amebeba vichupa viwili vya dawa.

“Samahani nesi kantini ni wapi?”

“Fwata hii kordo, kunja kushoto utaona mlango umeandikwa kantini hapo hapo uingia ndani na utakuta wahudumu”

“Asante sana dada”

Nilijibu huku nikianza kukimbia kwa mwendo wa haraka, nikaukuta mlango huo na kuusukuma. Nikakuta ni ukumbi mkubwa kiasi wenye viti vingi pamoja na meza kadhaa, nikatembea hadi mapokezi.

“Habari?”

Nilisalimia huku nikishusha pumzi nyingi, kwani nimekimbia kwa kasi.

“Salama za wewe dada?”

Mwanaume huyu alinijibu huku akifuta futa meza yake kwa kutumia kitambaa.

“Salama, nahitaji uji wa ulezi, dokta Abdalah asubuhi atalipa”

“Ohoo uji wa ulezi ndio tumemaliza sasa hivi, kuna mgonjwa amepelekewa chupa ya uji”

“Jamani, sasa mutanisaidiaje?”

“Aha…..hapa kitu kilichopo ni chai na maandazi”

Nikajikuta nikishika kiuno, huku nikijifikiria kwa muda. Mwanaume huyu akanitazama kwa macho ya kunichunguza.

“Wewe ni Jojo?”

“Ndio ni mimi”

“Ohooo safi, sasa skia. Nitakupa uji wangu, ila ni chupa ndogo, sasa sijajua kama mgonjwa wako atapenda au laa”

“Nashukuru, atapenda tu”

“Sawa.”

Mwanaume huyu alizungumza huku akigeuka na kufungua kabati kubwa la vyombo lililopo nyuma yake. Akato kijichupa kidogo, akanitolea na vikombe viwili vya plastiki.

“Mgonjwa wako ni nani Jojo?”

“Ni mume wangu”

“Nani….Eddy”

“Eehheee”

“Amepatwa na nini tena?”

“Ni story ndefu kaka yangu, ila naomba kama una sukari na blue band uweze kunipatia”

“Sawa…..ila daaa umpe pole sana mskaji, ndio maana siku hizi stori zake facebook hatuzipati kwa muda”

“Yaa….yaaaa”

“Daaa mumelazwa wodi gani?”

Nikamtazama jamaa huyu, kwa maana swala la kuzungumza ni wapi alipo mume wangu, kwa nama moja ama nyingine inaweza kuwa ni shida kwa upande wetu hapo baadae.

“Wodi ya wanaume”

Nilijibu kwa kubuni tu, kwa maana sifahamu kama humu ndani ya hii shospitali na kuna wodi ya wanaume au laaa.

“Ahaaa, basi nitakuja kuwacheki kukipambazuka.”

“Asante”

Nilizungumza huku nikiupokea mfuko alio wekwa chupa na vitu nilivyo muomba.

“Karibu tena Jojo”

“Asante sana”

Nikatoka kantini hapa, nikaanza kukimbia tena kuelekea kule nilipo muacha mume wangu. Nikafungua mlango na kuanza kushuka kwenye ngazi kwa haraka sana. Kabla sijafika katika mlango wa chumba cha Eddazaria uso kwa uso nikakutana na nesi ambaye alinielekeza ni wapi ilipo kantini. Nikamtazama mikononi mwake na kukuta akiwa ameshika sindano, yenye dawa chache sana.

‘Mungu wangu amesha muua mume wangu’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiuachia mfuko wenye chupa ya chai. Kwa kasi ya ajabu nikamvamia nesi huyu na kumbamiza ukutani, nikaupiga mkono wake kidogo na kuifanya sindano aliyo ishika kuanguka chini.

“Da….da…..a….d….uta….ni…ii….uaaaa…..a”

Nesi huyu alizungumza kwa shida mara baada ya mimi kumkaba koo lake.

“Umetoka kufanya nini ndani ya chumba cha mume wangu?”

“Ni……ni…..me……nime…..toka ku…ku…..ku”

Ikanibidi kumuachia koo lake kidogo ili aweze kuzungumza, akaanza kukohoa kwani mkabo nilipo kuwa nimemkaba, ningeendelea ndani ya sekunde hata hamsini basi angepoteza maisha yake.

“Nimekuja kumchoma sindano ya kupunguza maumivu, kama dokta alivyo niachia maagizo”

Nikarudi hatua chache nyuma na kumtazama Eddazaria, kwnai mlango wa chumba chake upo wazi, nikamkuta akiwa amekaa kitandani kidogo huku akijaribu kung’ata kipande cha kuku. Nikashusha pumzi huku nikimtazama nesi huyu na kijikuta nikimuoena huruma sana kwani nime muadhibu kwa kosa ambalo sio lake.

“Naomba unisamehe dada yangu”

Nilizungumza huku nikiufwata mfuko wenye chupa ya uji. Nikaunyanyua na kuukagua ndani, kwa bahati nzuri hakuna kitu kilicho pasuka. Nesi huyu akaondoka eneo hili huku akiwa amejishika eneo ya koo lake. Nikaiokota sindano hii na kuingia nayo ndani.

“Huyu nesi amekuchoma sindano?”

“Eheee…..maumivu sasa nahisi yanaanza kupungua”

“Pole mume wangu”

“Nashukuru, vipi mbona jasho linakumwagika?”

“Hamna, ni kukimbia tu”

“Nimeona kama umamparamia nesi wa watu, au macho yangu yalikuwa vibaya?”

“Aha….amekuja huku pasipo idhini yangu, kidogo ndio nimemfanya hivyo”

“Huku nilipo kuja sidhani kama wanaweza kunifwata”

“Unawajua wanao weza kukufwata?”

“Ndio ni Nuru na watu wake, walihitaji kuniua wakihitaji kwamba nikuache wewe, ila sikuweza kukubaliana nao, kwa maana nina kupenda mke wangu. Nilikuwa nipo tayari kabisa kufa kwa ajili yako”

Nikamtazama Eddazaria kwa macho ya mshangao sana, taratibu nikanyanyuka na kumbusu shavuni mwake huku machozi yakinilenge lenga usoni mwangu. Kwa dunia ya sasa hivi kusema kweli ni habati sana kumpata mwanume ambaye anaweza kukubali mateso ya mwili wake na hata kupoteza maisha yake kwa ajili ya mpenzi wake.

“Ninakupenda sana Eddy na nitakufa kwa ajili yako pia”

“Asante mke wangu, ila kifo si haki yako kwa sasa”

“Hata wewe sio haki yako.”

Nikanyanyuka na kuufunga mlango huu kwa ndani, kisha nikarudi kitandani.

“Nimepata uji mume wangu”

Nilizungumza huku nikiitoa chupa hii ndogo, nikaanza kuifungu nikamimina uji huu kwenye kikombe kikubwa kiasi nilicho pewa.

“Ngoja niuonje wasije wakawa wameuweka sumu bure”

“Hahaaaa……”

“lla Eddy siku nyingine kwenye matatizo kama haya nakuomba sana usiende mwenyewe nakuomba sana tena sana mpenzi wangu”

“Sihitaji wewe uumie hata kidole chako cha mguu, mimi ni mwanaume. Nikipambana basi tambua kwamba nina pambana kwa ajili ya familia yangu. Jojo, ninaipenda famili yangu kuliko kitu chochote unacho kifikiria akilini mwako. Wewe ni familia yangu, wewe na wengine wote ni familia yangu. Duniani hakuna kitu kizuri kama kuwana familia nzuri”

Maneno ya Eddazaria yakanifanya nikae kimya huku machozi yakinibubujika usoni mwangu.

“Jojo histori yako umeweza kunieleza, umeyatoa sadaka maisha yako kwa asilimia kubwa sana. Yote ulikuwa unapambana kwa ajili ya familia, mdogo wako, wewe na hata yule ambaye ulikuwa humjui kama atakuja kuwa mume wako. Majukumu hayo sasa hayapo kwako, yapo kwangu. Acha nipambane kwa ajili yenu”

“Ila Eddy we…….”

Eddazaria hakuhitaji nimalizie kuzungumza nilicho kikusudia, akanivuta kichwa changu karibu kabisa na lipsi zake, japo zimevimba ila hakujali hilo, akaanza kuninyonya taratibu.

“Baba bora ni yule ambaye, anapambana kwa ajili ya watu wanao mzunguka, familia yake. Mama bora ni yule anaye angalia malezi ya familia yake kuanzia mume hadi wato wake”

Taratibu nikamkumbatia Eddazaria huku nikiendelea kulia. Baada ya dakika kama tano hivi nikamuachia huku nikimtazama usoni mwake.

“Muda wa kunywa uji sasa”

“Sawa mke wangu”

Nikaweka blue band kwenye uji huu, nikaanza kuukoroga taratibu, nilipo hakikisha imekaa vizuri, nikaweka na sukari nikaonja kwa mara kdhaa kiwango ambacho ninakitaka mimi kisha taratibu nikaanza kumnywesha Eddazaria.

“Ilikuwaje hadi wakakuteka?”

Eddazaria akanitazama kwa sekunde kadhaa huku akionekana kama anavuta kumbukumbu ya matukio fulani kichwani mwake.

“Nilipo toka nyumbani kwa dokta nikiwa na ile maiti ya yule dada, moja kwa moja nikaanza kufwata signal ya wapi alipo Nuru”

“Ngoja kwanza…..Nuru ina maana yupo hapa Tanga?”

“Ndio yupo hapa Tanga”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwa wasiwasi. Nikaitoa simu yangu mfukoni na kukagua kama kuna meseji yoyote ila sikuweza kuona meseji yoyote. Nikaongeza suuti ya simu yangu, hata kama kutakuwa na tatizo basi niweze kulifahamu.

“Eheee?”

“Nilifika katika msitu ule, gari nililisimamisha mbali kidogo kwa maana hapakuwa na njia ya kueleka huko, sasa nilipo kuwa katika harakati za kuzidi kumsogelea, nikajikuta nikiingia kwenye mtego, walikuwa ni watu wengi wenye silaha, nilishindwa kutumia hata risasi moja ya bastola yangu.”

Nikachukua kipande kidogo cha kuku na mimi nikaanza kula ili kupoza makali ya njaa yangu inayo zidi kulisumbua tumbo langu.

“Basi walinipiga na kitak cha bunduki kichwani. Nilipoteza fahamu kwa muda ule na wala sikuweza kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea, nilizinduliwa kwa maji baridi waliyo nimwagia kichwani na usoni mwangu”

“Basi wakaanza kunipiga, huku Nuru na kundi lake la wasichana wakinilazimisha kukiri kwamba ninaachana na wewe na nitajitenga mbali nawe. Nilikuwa mbishi sana, wakaendelea kunipiga hadi unapiga simu wanazungumza na wewe, wanapiga picha na kukutumia vyote nilikuwa ninashuhudia. Muda wanazungumza na mama pia niliweza kusikia kila kitu. Baada ya matukio hayo, Nuru aliondoka na wasichana wake hao, na kuniacha na majaa, huku akiniahidi kwamba pesa walizo zitaja kama hazito tolewa basi atatuma watu watakuja kunichukua na kwenda kuniua”

“Sasa Nuru atatakaje milioni mia na hamsini ikiwa ana mamilioni ya mapesa?”

“Anasema lazima akufilisi taratibu, na atahakikisha kwamba mimi na wewe tunarudi chini, chini kabisa, na kutufanya tuwe omba omba mitaani kwa kukosa pesa”

“Pumbavu zake huyu Nuru”

Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama Eddazaria usoni mwake. Nikaichukau simu yangu na kuitafuta meseji ya vitisho ambayo nilitumia. Nikairudia kuisoma, kisha nikampigia dokta Clara.

“Ndio Jojo”

“Sikia hao wauaji wapo wapi?”

“Wapo huku Dar es Slaaam”

“Wana vigezo gani?”

“Ahaaa, kwanza walikuwa ni majasusi wa kiserikali na wameiacha hiyo kazi kwa sababu kadha wa kadha ambazo hawakuhitaji kuniorodheshea. Pili wamesha fanya mauaji ya watu wengi, hapa Tanzania na nje ya Tanzani na walisha weza kunionyesha picha ya viongozi kama thelathini walio weza kuwaua, hiyo ukiachilia wafanya biashara na watu mbalimbali. Tatu ni watu ambao wapo makini na kazi yao, wanacho taka wao, ni kufanya kazi wanza, ikiisha basi malipo yao yatafwata”

“Chukua gari la kampuni lolote, kesho hakikisha kwamba unakuja nao Tanga sawa”

“Sawa nitafanya hivyo”

Nikakata simu na kumgeukia Eddazaria, kwani nilimpa mgongo nilipo kuwa ninazungumza na simu hii.

“Ni kina nani ambao unataka waje Tanga?”

“Dokta Clara na watu fulani hivi nahitaji kuwapa hii kazi ya kumsaka Nuru hadi wampate”

Kabla hata Eddazaria hajazungumza chochote, mlango wa chumba chetu ukagongwa, kwa haraka nikaichukua bastola niliyo mpa Eddazaria, nikaikoki vizuri na taartibu nikaanza kutembea kwa kunyata na kueleka mlangoni.

“Nani?”

“Mimi shem”

Niliisikia sauti ya dokta, taratibu nikafungua mlango huu, akaingia ndani hata kabla sijaurudishia wanaume wawili wenye misuli mkubwa, mmoja wao akanisukumiza chini na mwengine akaninyooshea bunduki yake.

“Tulieni kama munakuny****”

Mwanaume huyo alizungmza kwa ukali sana na sauti nzito sana. Sikuamini macho yangu mara baada ya kumuona Nuru akiingia ndani humu huku akiwa ameongozana na wasichana wawili ambao nao pia wameshika bastola mikononi mwao.


“Habari yako Jojo?”

Nuru alizungumza huku akitabasamu. Mwanaume mmojaa kaninyanyua juu kwa nguvu, akanikalisha kitandani, kusema kweli sina ujanja wa kufanya jambo lolote zaidi ya kutulia tuli kwani bastola zao zote wametuelekezea mimi na Eddazaria.

“Nilikupa masaa mawili ya kurudisha kila kilicho changu, ila hukuweza kufanya maamuzi, sasa nimekuja mimi mwenyewe. Nahitaji ufanye maamuzi yaliyo sahihi kabla na mimi sijafanya maamuzi yaliyo sahihi kwangu kama vile nilivyo kueleza katika ujumbe wangu wa meseji”

Nuru alizungumza huku akikaa kwenye kiti kilichopo karibu kabisa na kitanda. Nikamtazama Eddazaria usoni mwake kwa macho ya kuiba, nikakosa jibu la kuzungumza kabisa.

“Jojo fanya maamuzi, Eddy wako huyo au pesa zangu. Una dakika tano za kujifikiria kabla masaa mawili hayajakamilika”

“Ishu ni pesa zako si ndio?”

“Ndio?”

“Nipo tayari nikupatie”

“Jojo huwezi kufanya hivyo?”

Eddazaria alizungumza huku macho yamemtoka.

“Eddy pesa kitu gani, kama Mungu amepanga amepanga tu tufanikiwa kwa namna nyingine ila si kwa pesa za namna hii”

“Hapamna kwani kufa ni kitu gani, pesa hizo hakikisha zinakusaidia wewe katika maisha yako”

“Hahahaaa…..kwenye maisha yangu yote sijawahi kukutana na mtu mbishi na mwneye ubishi wa kijinga kama mume wako, anaonekana anakupenda eheee?”

Taratibu nikaingia mkono wangu kwenye mfuko wa suruali ambao una simu. Nikaanza kuminya minya namba kadhaa za mama mkwe kisha nikaipiga na simu nikaiacha hewani.

“Eddy acha tu nimpatie”

“Hapana hakuna kumpatia”

Nuru akachomoa bastola yake iliyo tengenezwa kwa dhahabu, taratibu akaanza kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti, ili hata akipiga risasi basi mlio wake usiweze kusikika sehemu yoyote.

“Una dakika moja?”

Nuru alizungumza huku akitazama saa yake ya mkononi. Kazi ya Eddazaria ni kutingisha kichwa akionyesha kwamba hakubaliani kwa maamuzi ambayo ninakwenda kuyachukua.

“Una sekunde ishirini?”

Nuru aliendelea kuzungumza kwa msisitizo huku vijana wake wakiwa wamenikodolea macho. Galfa mlango ukafunguliwa, kwa nguvu, kitu kama kitenesi ikiatupwa kwa ndani, moshi mkali ukaanza kutawala ndani ya chumba hichi, na kutufanya sote kuanza kukohoa kwani kilicho tupwa ni bomu la machozi.

Nikaanza kusikia miguno ya watu wakitoa milio ya maumivu huku vishindo vya wao kuanguka chini ikisikika.

Gafla mkono wangu ukashikwa na kujikuta nikivutwa na kutolewa nje, machozi yanayo nimwagika usoni mwangu yakanifanya nishindwe hata kumuona mtu huyu vizuri. Nikakajipangusa machozi yangu, nikaona kitanda cha Eddazaria nacho kikitolewa nje, na mtu huyu, ambaye kwa haraka akuchomoa sindano ya dripu iliyo chomwa Eddazaria mkononi mwake. Akanyanyua na kumuweka begani mwake, begani mwake. Akanishika mkono na mimi na tukaanza kukimbia huku tukipandisha juu kwenye ngazi. Mtu huyu nimeweza kumtambua kwamba ni mwanaume kwani ana nguvu za kutosha, ameificha sura yake kwa kuvaa kivaa maalumu cha kuzuia bomu la machozi kumdhuru na yeye. Tukatoka nje ya hospitali hii na akafungua mlango wa gari aiana ya Range Rover Sport, tuliyo ikuta, akamuingiza Eddazaria katika siti ya nyuma na kwa haraka akaniingiza na mimi kwenye siti hiyo hiyo aliyo ingia Eddazaria. Akazunguka upande wa pili wa dereva akafungua mlango na kuingia ndani. Safari ya kuondoka eneo hili ikaanza kwa mwendo wa kasi sana.

“Chukua maji unawe uso”

Mwanaume huyu alizungumza huku akinikabidhi chupa kubwa ya maji ya Kilimanjaro. Nikaichukua na kuhitaji kufungua kioo cha gari hili ila kwa ishara akanikataza na kuniamuru ninawie uso wangu ndani ya gari hili hili.

Nikaanza kunawa uso wangu, huku nikihakikisha kwamba macho yangu yamepata maji ya kutosha. Nikaanza kumnawisha Eddazaria na yeye uso wake kwani bomu hilo la machozi limeweza kumuathiri na yeye.

“Asante bro”

Eddazaria alizungumza kwa sauti ya chini huku akijaribu kukaa kitako katika siti hii.

“Yaani una bahati sana, yaani mama ananipa taarifa ndio nilikuwa ninaingia Kange ikanilazimu kupitiliza moja kwa moja na kuja huku”

Mwanaume huyu alizungumza huku akivua kifaa hichi hapa ndipo nikatambua kwamba mwanaume huyu ni kaka yake Eddazaria.

“Umemuua yule mjinga?”

Eddazaria aliuuliza huku akimtazama kaka yake.

“Kwa jinsi nilivyo washambulia sidhni kama kuna mtu atakuwa hai mule ndani”

“Umewaua wote!!?”

Niliuliza kwa mshangao.

“Ndio shem”

“Kuna dokta?”

“Namfahamu niliweza kumgusa gusa na yeye amezimia”

“Shikamoo lakini shem”

“Marahaba, imekuwa bahati kuonana leo, japo tumekutana kwenye matatizo kama haya ila nina imani yatakwisha tu”

“Nashukuru shem”

“Oya dogo, ninawapeleka uwanja wa ndege sasa hivi na munaelekea Zanzibar, huko mutakaa hadi pake hali yako itakapo kuwa poa sawa”

“Sawa broo”

“Kitu kingine, badilisheni namba zenu za simu, hakikisheni kwamba hampigii watu hovyo hovyo na kama ni watu wa kuwapigia muwe muna waamini, huku mimi na bi mkubwa tutaendelea kuiweka hali ya usalama wenu sawa”

“Poa poa”

Tukafika katika kiwanja cha ndege kilochopo eneo la Kange, tukakuta ndege ndogo ikiwa na rubabi wake. Tukashuka kwenye gari, Eddazaria akabebwa na kaka yake na kuingizwa ndani ya ndege hii ndogo. Kisha shem akarudi kwenye gari na kunikabidhi brufcase yenye uzito kidogo.

“Humo ndani kuna pesa za kutosha, melezo ya wapi munatakiwa kwenda kuishi, picha ya nani atakaye wapokea, simu mpya za kutumia, laini mutatafuta sawa”

“Sawa shem tunashukuru sana”

“Hakikisha kwamba unamuangalia mdogo wangu, hakikisha sasa hivi hamushuhuliki na maswala ya kupiga piga picha na kuweka kwenye mtandao, bado hatujajua mtandao wa Nuru anahusika watu gani, so kuweni makini sana”

“Nakuhakikishia shem nitakuwa makini sana na halite jitokeza swali kama hili tena”

“Sawa niwatakie mapumziko mema”

Shem alizungumza huku akinikumbatia, akaniachia taratibu.

“Nashukuru shemeji”

“Usijali”

Nikaanza kutembea taratibu huku nikigeuka geuka nyuma. Nikaingia ndani ya ndege hii na kufunga mlango. Taratibu rubani wa ndege hii akaiwasha na tukaanza kuondoka, baada ya muda mchache ndege ikaacha ardhi hii ya Tanga na kunza kutafuta muelekeo wa Zanzibar.

“Eddy”

“Mmmmmm”

“Mama yako amepata watoto wazuri sana, wanao jitambua na kujimudu kwa kila jambo”

“Sikia, Nuru ameniharibia mfumo wa amani ya moyo wangu, kama hajabatika kuuwawa, basi endapo nitapona hakika nitamchinja, haki ya Mungu ninaapa nitamuua”

“Eddy mume wangu samahani sana kwa kila kitu, natambua kwamba mimi ndio niliye leta matatizo haya kwenye familia yako, laiti ingekuwa si mimi kukujua yasinge tokea haya”

“Matatizo yapo kwa kila binadamu na hakuna mtu ambaye anaweza kufahamu ni nini kinacho fwata kwenye maisha yake ya mbeleni, iwe ni furaha au matatizo”

“Sawa mume wangu, ila hadi ninajisikia aibu”

“Aibu ya nini?”

“Kuwasumbua familia yako”

“Acha hizo”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kukuta ikiwa imekata, nikaizima. Nikafungua brufcase hii na kukuta ikiwa na vibunda vitano vya dola mia mia zilizo fungwa vizuri. Nikakuta na simu mbili aina ya Samsung galax S7. Nikakuta picha ya mwanadada mmoja aliye valia ushungi.

“Unamfahamu?”

Nilimuuliza Eddazaria huku nikimuonyesha picha ya msichana huyo.

“Yaa”

“Ni nani?”

“Alikuwa X girl wa broo”

“Ahaa, sawa”

Tukafika Zanzibar majira ya saa kumi na moja kasoro, tukashuka kwenye ndege. Kwa bahati nzuri tukakutana na dada huyo akitusubiria.

“Karibuni Zanzibar”

“Tunashukuru”

“Eddy umekuwa mkubwa aissee”

“Hata wewe umekua”

“Hahaaa, acha utani”

“Kweli, umesha olewa?”

“Haaaa…bado nipo nipo”

“Utazeeka wewe endelea kuwepo wepo”

“Wanaume wenyewe wapo wapi mdogo wangu”

“Huku hujaona hata mpemba wa kukuoa”

“Hahaa, nani anataka kuolewa na mpemba na kuzaliwa watoto wengi kama paka”

Eddazaria na dada huyu walizungumza huku tukielekea kwenye maegesho ya magari. Tukaingia kwenye gari aina ya Rav 4L.

“Sijakutambulia, huyu ni mke wangu anaitwa Jojo?”

“Nashukuru kumfahamu, japo nimjua kupitia mitandao ya kijamii tu”

“Sawa, Jojo huyu anaitwa Mwanamvua, kipindi hicho nipo shule ya msingi ndio alikuwa akitoka na kaka yangu”

“Ahaaa nashukuru kukufahamu Mwanamvua”

“Asante jamani, ngoja niwapelekea kwenye nyumba ambayo kaka yako ameniagiza niwapeleke”

“Poa”

“Inabidi nikakushuhukikie hayo majeraha yako kwa maana mmmmm…..”

“Hivi umekuwa dokta kweli?”

“Yaa nimekuwa dokta best”

“Hongera bwana”

“Asante”

Tukafika kwenye nyumba moja iliyopo pembezoni mwa bahari, nyumba hii imezungushiwa ukuta mrefu na si kubwa sana ila ina gorofa moja juu. Mwanamvua akatukaribisha, akatuonyesha mazingira ya nyumba hii.

“Mumepapenda?”

“Yaa tumepanda”

Nilizungumza kwani hii nyumba ina kila kitu kinacho hitajika ndani ya nyumba.

“Eddy inabidi hii alfajiri nielekee hospitali kwanza nika saini, kisha nitakujia na dawa za kukuhudumia”

“Sawa, ila unajua nina mshono hapa”

Eddazaria alizungumza huku akifunua shati la hospitalini tuliyo toka. Mwanamvua akautazama mshono huu kwa muda.

“Haujapata itilafu, unajisikia maumivu?”

“Kwa sasa sio sana, ila nahisi kwa hapo badaye maumivu yatakuwa makali sana”

“Bye saa mbili nitakuwa hapa”

“Sawa”

“Wifi niambie ni kitu gani mutakula ili niwanunulie kabisa”

“Vitu vyote vta kupigwa ndani ya nyumba”

“Sawa”

Mwanamvua akatuaga na kuondoka eneo hili la nyumba, nikafunga geti, nikarudi ndani.

“Wasiliana na mdogo wako, tuweze kufahamu yupo wapi, ila hata kama ni kuja aweze kuja huku Zanzibar”

“Nitawasiliana naye kukipambazuka mume wangu, muda huu nina usingizi sana”

“Sawa lala mpenzi wangu”

Nikajilaza kwenye sofa kubwa lililopo hapa sebleni. Kwa msongamano wa mawazo yanayo nitawala kichwani mwangu, nikajikuta nikikosa usingizi kabisa, nikakaa huku nikipiga miyayo.

“Vipi usingizi hauji?”

“Hauji mume wangu”

“Tuangalie angalie movie”

Eddazari alizungumza huku tukitaza filamu iitwayo What Now, iliyo chezwa na msanii wa vichekesho nchini Marekani Kevin Hart. Kengele ya mlangoni ikaanza kugonga na kutufanya mimi na Eddazaria kutazamana usoni kwani ni muda mchache sana tumehamia ndani ya nyumba hii, na mtu wa pekee ambaye ametuleta hapa ni Mwanamvua na tunaamini kwamba yeye ndio anaye fahamu juu ya uwepo wetu hapa. Swali linalo tuumiza kichwa ni nani ambaye anagonga kengele hiyo alfajiri hii na nini anacho kihitaji kwetu.



Nikafungua brufcase hii niliyo pewa na shemeji, nikatoa bastola ninili ikuta humu ndani, niakatoa magazine na kukuta ikiwa na ujazo wa risasi. Nikairudisha na kuikoki kuiweka tayari kabisa kwa kushambuli risasi muda wowote. Nikamtazama Eddazaria, ambaye hata yeye mwenyewe anaonekana kuwa na wasiwasi.

“Kuwa makini?”

Eddazaria alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikamnyooshea kidole gumba nikiashiria kwamba nipo makini sana, nikatoka nje huku nikinyata. Kengele badi inaendelea kusikika masikioni mwangu, ubaya wa geti hili haina hata uwazi mdogo wa kuweza kuchungulia nje. Taratibu nikafungua geti hili, nikausukuma mlango huu mdogo wa geti kidogo, kisha nikajibanza pembeni. Akaingia kijana aliye valia kanzu, kwa haraka nikamuwekea bastola ya usogoni, huku nikimuonya kwa sauti nzito asigeuke nyuma. Nikamtazama mkononi mwake na kumuona ameshika magazeti mengi sana, pamoja na kifoko chenye mkate mkubwa.

“M…mm….mi…..”

Kijana huyu alijibwabwaja bwaja, hata kinywa chake hakikuweza kufunguka kabisa na kuzungumza jambo la msingi. Japo nimeikaza sauti yangu na nilazima itasikika ni ya kike, ila kwa woga wa bwana huyu ninaimani hata hawezi kuitilia maanani kabisa, kwani nimeigandmiza batsola niliyo ishika kisawa sawa kichwani mwake.

“Umefwata nini?”

“Ma..ma….mwa…..mwana…..mvu……aa…..ameniagiza nile….te magazeti na huu mkate”

“Weka vitu hivyo chini?”

Kijana huyu akaweka mzigo wake wa magazeti pamoja na mfuko wenye mkate.

“Hivyo hivyo geuka na utoke. Kijana huyu kwa jinsi alivyo jivaa vaaa na kujikwaa juu, nikashudia akipiga mzinga mzito chini, akanyanyuka huku kanzu yake nyeupe ikiwa imejaa vumbi jingi, akaacha kobazi lake moja na kuondoka na kobazi jengine jambo lililo nifanya nianze kuanguka kicheko cha kimya kimya. Nikafunga geti hili, sasa hapa ndipo nikapata wasaa mzuri wa kucheka huku nikianza kuokota mfuko huuu wenye mkate, kisha nikaokota magazeti haya mengi ambayo sijui ameagizwa ayakate yote au ni woga ndio umemfanya ayasahau.

Kicheko changu, kikaanza kupotea taratibu huku nikisoma maandishi yaliyo pambwa kwa maandishi meusi na makubwa yanayo someka. ‘JOJO, MKE WA EDDY NI MSAGAJI’

Chini ya maandishi haya kuna picha yangu inayo nionyesha mimi na Nuru tukinyonyana ndimi zetu japo kuna kipicha cheusi kilicho ficha midomo yetu, ila kwa namna moja ama nyingine kusema kweli ni udhalilishaji ambao sikuutarajia kuuona kwa asubuhi ya leo. Nikafunua gazeti jengine nikaona maandishi makubwa yaliyo andikwa. USAGAJI SAS ANI JANGA LA TAIFA, huku maneno haya nayo yakiandamana na picha yangu pamoja na Nuru japo picha ya Nuru imefichwa sura, ila yangu ndio imeachwa wazi na watu wote ambao wataitazama lazima waweze kunifahamu.

Nikaanza kurudi ndani kwa kasi huku jazba ikiwa imenipanda, nikamkuta Eddazaria akifunga pazia la hapa sebleni, na muda wote nahisi alikuwa akinitazama kupitia dirishani.

“Yule ni nani?”

“Mpuuzi tu mmoja ameleta magazeti na amekuja kunichafulia siku?”

“Kukuchafulia siku kivipi?”

Nikachomoa gazeti moja na kumkabidhi Eddazaria, kitendo cha kutulia sekunde chache za kusoma kichwa cha habari kilicho andikwa kuhusiana na mimi, akaachia msunyo mkali sana, akatembea kwa mwendo wa kuchechemea hadi kwenye sofa alilo kuwa amekalia. Ukimya ukatawala kati yetu kwani hii sasa ni skendo chafu, tena ni mbaya kwa kipindi hichi ambacho tupo mbioni katika kuachia filamu yetu ya kwanza.

“Tunakwenda kufanyaje mume wangu?”

“Mpigie Clara”

“Sasa hivi?”

Eddazaria akanijibu swali langu kwa kunitazama kwa macho makali sana. Nikajipapasa na kuitoa simu yangu mfukoni, nikaiwasha, mfululizo wa notification za instergra, zikaanza kuingia jambo lililo nifanya nikae kimya kwa muda, huku nikitamani kuzitazama.

“Vipi umempata?”

“Hapana simu ipo hewani”

Ikanibidi kuushuhulikia uongo wangu, kwa haraka nikaitafuta namba ya dokta Clara, nikampigia kwa bahati nzuri simu yake haikuita sana ikapokelewa.

“Clara”

“Ohoo asante Mungu nimekupata jamani, kwa maana ninapata usumbufu mwingi Jojo kutoka kwa waandishi wa habari wanahitaji kuzungumza nawe ili kujibu tuhuma za usagaji”

“Lete simu”

Eddazaria alizuungumza huku akiniyooshea mkono. Nikamkabidhi simu yangu huku nikimtazama usoni mwake.

“Clara”

“Hembu hakikisha kwamba unanitafutia hao wajinga wote walio andika habari juu ya mke wangu”

“Clara ahakuna cha lakini, sawa. Fanya kama nilivyo kuagiza tena ikiwezekana watekwe wote na ninahitaji kuzungumza nao uso kwa uso”

“Hadi inafika saa kumi na mbili jioni uwe umesha watia nguvuni”

“Wawe wa kampini, gani sijui kampuni gani tuna pesa ya kufanya chochote na hakuna mtu atakaye uliza. Walipo fikia inatosha sawa”

“Unipe jibu Clara usitake hili swala nilishuhulikie mimi mwenyewe unanielewa”

Eddazaria akakata simu na kuanza kukohoa, kadri sekunde zinavyo zidi kusonga mbele, ndivyo jinsi hali yake ilivyo zidi kuwa mbaya, kwani akaanza kutokwa na damu mdomoni mwake.

“Baby, baby”

Niliita huku nikiwa nimechanganyikiwa kiasi cha kushindwa hata kujua nifanye nini. Nikatamani kumpigia mama mkwe ila kusema kweli ninashindwa kabisa, ukiachilia umbali alipo, ila sidhani kama anaweza kunipa msaada wa kidaktari. Mtu wa mwisho kumfikiria ni Clara, nikaichukau simu yangu na kumpigia.

“Clara”

“Ndio”

“Eddy anatena damu”

“Anatema damu!!!?”

“Ndio, ametoka kuzungumza na wewe sasa hivi na hali yake imebadilika, si unamsikia jinsi anavyo kohoa?”

“Ndio….Ohoo Mungu wangu kwani mupo wapi?”

“Tupo Zanzibar”

“Sasa hemhu msikilizie baada ya dakika tano, kama bado hali yake inaendelea kuwa kama hivyo basi hakikisha unanipigia na kuna namba ya rafiki yangu ni daktari huko Zanzibar nitakupatia ili uweze kumpigia ili aje eneo mulipo”

“Sawa”

“Ni…ni….nipo poa”

Eddazaria alizungumza huku akijitahidi kunyanyuka.

“Unakwenda wapi?”

Eddazaria hakumaliza hata hatua nne, akaanguka chini mzima mzima, hapa ndipo nikazidi kuchangunyikiwa. Nikamlaza chali, nikayasikilizia mapigo yake ya moyo kwa kuinamisha uapnde wangu wa siko la kulia juu ya kifua chake na nikaya hisi mapigi take ya moyo jinsi yanavyo kwenda kwa utaratibu. Japo sijasomea maswala yoyote ya udaktari ila kwa mapigo ya namna hii , kusema kweli si ya kawaida, kwa moyo wa binadamu unavyo paswa kwenda.

“Eddy, Eddy, Eddy nyanyuka jamani, nyanyuka mume wangu”

Niliita huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, wazo la kumpigia dokta Clara wala sikuwa bias nalo kabisa kichwani mwangu.

Kengele ya getini ikaanza kuita, macho yakanitoka huku nikiwa nimejawa na wasiwasi, nikatambaa hadi kwenye sofa, nikaichukua bastola yangu na kwa haraka nikaanz akukimbilia nje nikaufungunga mlango kwa hasira huku nikiwa nimeitanguliza bastola yangu mbele.

“Woo wooo woooo…..ni mimi wifi”

Mwanamvua alizungumza huku akinitazama usoni. Nikamshika mkono na kumvutia ndani. Kwa haraka tukakimbia ndani, alipo mkuta Eddazaria amelala sakafuni, kwa haraka kaanza kufungua vifungo vya shati alilo vaa.

“Nenda nje kwenye gari langu utakuta kuna kibegi cheusi, njoo nacho”

Nikatoka nje na kukimbilia hadi nje ya geti, nikajaribu kufungua mlango wa gari lake, ila nikaikuta ikiwa imefungwa, ikanilazimu kurudi ndani, Mwanamvua alipo niona tu, akanikabidhi fungu za gari.

“Kibegi kipo siti ya nyuma ya dereva”

Sikumjibu chochote zaidi ya kuchanganya miguu yangu kwa kasi hadi kwenye gari hilo, nikafungua mlango na kutoa kibegi hicho cheusi. Nikaubamiza mlamgo wa gari hilo na kurudi ndani kwa kasi, nikampa dokta Mwanamvua kibegi chake, akakifungua kwa haraka, akatoa makoro koro mengi ya udaktari na kuanza kumshulikia Eddazaria ambaye hadi hapa sasa hivi hajitambui kabisa.

“Ana nini dokta?”

“Tulia”

Dokta Mwanamvua alizungumza huku akimchoma sindano Eddazaria katika mkono wake wa kulia. Baada ya dakika kama mbili hivi Eddazaria akafumbua macho yake, akatutazama kwenye nyuso zetu, akajaribu kukaa kitako ila Mwanamvua akamzuia.

“Tulia kwanza dogo, unajisikiaje?”

“Mmmmmm……?”

“Bado hali yake haijakaa sawa, fungua friji pale na mletee maji ya baridi”

Nikafwata maamuzi ya Mwanamvua, nikarudi na chupa ya maji ya baridi, akaanza kumnawisha Eddazaria uso wake kwa kutumia maji haya ya baridi, alipo hakikisha kwamba yupo vizuri, kwa ishara akanifomba tukasaidiana kumnyanyua na kumlaza juu ya sofa.

“Imekuwaje?”

“Aha…kuna dokta tumezungumza naye hapa kidogo, akawa anfoka foka, akaanguka na hali yake ikawa kama hivyo ilivyo kuwa.”

“Kwa hali kama hiyo aliyo kuwa nayo yeye, hatakiwi kutumia nguvu kwenye kitu chochote, yaani kuanzia kutembea, kuzungumza wala kuwaza.”

“Sawa sawa dokta”

“Au hiyo habari hapo ameiona?”

“Yaa ameiona na ndio imesababisha mambo yote hayo”

“Mmmmmm”

“Hao waseng** lazima hili liwagarimu”

Eddazaria alizungumza huku akitutazama, jambo lililo tufanya mimi na Mwanamvua kukaa kimya huku tukiwa tumekodolea macho.

“Na msisitizie Clara kwamba wanawateka wote?”

“Dogo umeanza kucngananyikiwa au?”

Mwanamvua alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Ningechanganyikiwa ningekuwa mirembe sasa hivi”

Jibu la msisitizo la Eddazaria likanifanya ninyanyuke na kuelekea jikoni na kumuacha na Mwanamvua. Nikaanza kuandaa kifungua kinywa huku saa ya ukutani humu jikoni ikinionyesha kwamba sasa hivi ni saa mbili kasoro asubuhi. Dokta Mwanamvua akaingia jikoni humu huku akionekana kuwa ni kama my mwenye wasi wasi fulani hivi.

“Vipi?”

“Mmmmm mwenzio simuelewi mume wako. Wewe unamuelewa kwa kweli?”

“Yaa nina muelewa”

“Unataka kuniambia kile anacho kizungumza juu ya hao waandishi ni kweli kabisa?”

“Amezungumza nini?”

Niliuliza huku nikidumbukiza mayai sita mabichi kwenye sufuria yenye maji.

“Amesema kwamba atawaua wandishi wote walio andika mabaya kuhusiana na wewe”

“Huwa mume wangu akizungumza humaanisha, na hana masihara kabisa, hivi unajua ni nini kilichotokea hadi sisi kuwa hapa kwa muda huu?”

“Ahaaa…..Pray alinielezea juu juu tu na akaniambia niwaangalie?”

“Basi endelea kutuangalia na usihitaji kujua mengi juu tetu?”

“Tafadhali Jojo nidokeze japo hata kidogo nami niweze kufahamu”

Nikamtazama dokta Mwanamvua, nikarudi hatua chache hadi mlangoni nikachungulia kama Eddazaria anaweza kwua karibu ya eneo hili. Nikamsogelea dokta Mwanamvua, kwa kasi nikamvuta karibu yangu, nikaupitisha mkono wangu wa kulia nyuma ya shingo yake na kuanza kumnyonya midomo yake kinguvu, japo anajaribu kujitoa mikononimwangu, ila nikazidi kujitahidi kuhakikisha ninamnyonya denda hadi nitakapo ridhika mimi.



Nikamuachia dokta Mwanamvua, kwa hasira akajipangusa mdomo wake, akajaribu kunipika kibao ila nikaudaka mkono wake na kumsogeza karibu tena.

“Naamini umejua mimi ni nani”

“Fedhuli, baradhuli wewe. Mwanamke msagaji kumbe”

Mwanamvua alizungumza kwa hasira sana. Nikamsukumiza hadi ukutani na kumtazama kwa macho makali sana.

“Maana ya kumtuma mtu mwenye magazeti, ilikuwa ni nini, si ili ujua kama ni kweli au uongo. Sasa nikuambie kitu kimoja, usidhubutu kuniletea ujinga nitakugeuza mke sawa”

Nilizungumza kwa msisitizo na kuzidi kumkasirisha dokta Mwanamvua, kila alivyo jaribu kujitoa mikononi mwangu, akajikuta akishindwa kabisa.

“Kumbe nimakaribisha mashatani hapa kwangu, na nitamuambia Pray niwaondoe, mukakae hotelini?”

“Hahaaa….ukizungumza utanijua mimi ni nani, ni bora uwe mpole hivyo hivyo sawa”

Nilizungumza kwa ubabe sana huku nikiendelea kumtishia dokta Mwamvua.

“Umenielewa?”

Akatingisha kichwa akikiri kwamba amenielewa, kwani biti langu kwake limekuwa zito na kumshinda kulihimili.

Taratibu nikamuachia dokta Mwanamvua na kurudi sehemu lilipo jiko, nikazima na kuichukua birika hii niliyo kuwa nikitumia kuchemshia chai, taratibu nikaanza kumimina chai ndani ya chupa. Nikapeleka vitu sebleni, eneo lenye meza ya chakula, nikamkuta Eddazaria akiwa anakoroma kwenye sofa, akionyesha dhairi amelala fofofo.

“Usimsumbue, ameniomba nimchome sindano ya kutuliza maumivu na kumpatia usingizi”

“Itamchukua muda gani hadi yeye kuamka?”

“Masaa kama mawili na nusu hivi”

Nikatazama saa ya ukutani na kukuta ni saa tatu na dakika tano.

“Umekunywa chai na wewe?”

“Hapana, ngoja niombe ruhusa kazini”

Dokta Mwanamvua alizungumza huku akiifwata pochi yake ndogo, akatoa simu yake na kuanza kuminya minya, kisha akaiweka sikioni.

“Asalam Allyakum dokta?”

“Nimepata dharura, mara moja naomba kama inawezekana naomba leo kidogo niwe off, kesho naamini nitafika”

“Mama yangu kidogo nampelekea kwenye yale maombi ya shehe niliyo kuambia akafanyiwe kisomo”

“Asante sana”

“Haya”

Dokta Mwanamvua akakata simu, nikarudi jikoni na kuchukua sahani yenye vitafunwa, na kurudi nayo mezani. Nikajiandali kifungua kinywa, kisha taratibu nikaanza kunywa, dokta Mwanmvua naye akaja na kukaa kiti cha pembeni yangu. Akajiandalia na yeye kifungua kinywa kisha taratibu na yeye akaanza kunywa, chai hii.

“Chai yako nzuri, inanikumbusha bara”

“Ina tofauti gani?”

“Aha…chai za huku huwa zinaweka maviungo mengi sana kiasi kwamba mtu unashindwa kuifurahia”

“Si upike ya kwako kama hii, majani tu na sukari”

“Ahaa yaani nimesha athiriwa na mifumo ya huku”

Tukaemaliza kunywa chai, nikamfwata Eddazaria kwenye sofa alilo lalia, nikamuweka vizuri kichwa chake.

“Inaonekana unampenda sana mume wako?”

“Ninampenda kuliko ninavyo jipenda mimi mwenyewe”

“Mmmmm”

“Guna, ila huo ndio ukweli, sijawahi kupata mwanaume anaye jua kujitoa kama huyu, ninampenda kwa kweli na mimi nipo tayari kujitoa kwa ajili yake”

“Ila ni vizuri kwa kweli mukawa munapenda kama hivyo, ila nina ombi”

“Ombi gani?”

“Hamjaja na nguo, ningekushauri katika muda huu ambao Eddy amelala, tungeenda madukani huko kununua nguo japo za kushindia siku mbili tatu hapa.”

“Hivi sura yangu nitaiweka wapi ikiwa asubuhi tu ya leo ninaonekana kwenye magazeti hayo”

“Kuna baibui kwenye gari langu pamoja na mshungi na miwani, unaweza kuvivaa na mtu asikufahamu”

Nikamtazama dokta Mwamvua, mwili wake kidogo ni mnene, ila ninahisin ninaweza kuvaa naye nguo.

“Sawa, inabidi nikaoge kwanza, najihisi kunuka jasho”

“Hilo halina shida”

Nikelekea katika chumba chetu cha kulala, nikavua nguo zangu zote na kuingia bafuni. Nikafungua bomba la maji ya mvua, kabla hata sijapaka sabuni nikahisi mlango wa chumba hichi ukifunguliwa, nikaoka bafuni na kumkuta doka Mwamamvua akiwa amesimama mlangoni huku amelishika baibui alilo nielezea.

“Nilihisi sijui nimevamiwa”

“Hapana niliona nikalichukue kabisa kwenye gari”

“Shukrani”

Nikayashuhudia macho ya dokta Mwanamvua jinsi yanavyo shuka taratibu hadi kwenye mapaja yangu yaliyo jijenga vizuri kwa kuibeba shepu yangu ambayo huwa inawapagawisha wanaume wengi. Bumbuwazi likazidi kumtawala na kushindwa hata kuliweka baibui hilo kitandani, nikaanza kumsogelea huku maji yakiendelea kunichuruzika mwilini mwangu. Hadi ninamshika kiono chake ndio akastuka.

“Ehee…..”

Dokta Mwanamvua aliitikia huku akipepesa macho yake.

“Sijakuita mimi”

“Ahaa…ngoja nikaweke maji bafuni”

“Ukaweka maji bafuni…..!!! Hahaa bafuni wapi?”

Dokta Mwamvua dhairi anaonekana amechanganyikiwa, nikaanza kukitomasa kiuno chake taratibu, akaanza kujikunja kunya kimahaba, safari hii hatumii mikono yake kunisukuma kama vile alivyo kuwa anafanya jikoni. Nikaanza kufungua vifungo vya shati lake la rangi ya blue bahari alilo livaa. Nikakaribishwa na chuchu zilizo nona kifuani mwake, huku zikiwa zimebanwa vizuri na sidiria yenye rangi nyeupe.

“Jo…o…jo tutakamatwa bwana”

“Na nani?”

“Mume wako”

“Si umemchoma sindano ya usingizi?”

“Ndio”

“Sasa atatukamataje?”

Dokta Mwamavua akashindwa la kijitetea kwani maswali yangu yamemkamata kisasa sawa. Nikaufunga mlango kwa ndani, kisha nikaendelea na zoezi la kumvua shati lake hili. Japo kwa namna mmoja anaonekana hataki, ila asilimia za kuhitaji ninacho kifanya ni kubwa sana. Nikaanza kuyatomasa maziwa yeka taratibu huku nikiwa nimekazia macho, dokta Mwamavua akaanza kutoa miguno ya uhamsishaji wa mimi kuendelea kuonyesha mautundu ambayo nilimfanyia Nuru na leo yamempagawisha hadi anaamua kuniwinda na kuhitaji kunirudisha mimikono mwake kinguvu.

“Ohoo…..a….ooo…aaii.s…ii”

Dokta Mwamavua alizungumza maneo ambayo hayaeleweki. Nikaanfungua kifungo cha suruali yake ya kitambaa aliyo ivaa, nikaishusha zipu yake, nikakutana na chipi iliyo mkaa vizuri mwilini mwake. Akamshika mkno wake mmoja wa kulia na kushikisha makalio yangu, huku na mimi nikiwa na jukumu la kuhakikisha kwamba nikasaka kitumbua chake kwa vidole vyangu vya kiganja vya kulia, ili nianze kukiburudisha kwa kukishika vizuri.

“Jojo stop it”

Dokta Mwanamvua alizungumza kwa misistizo huku akitoa mikononi mwangu. Akaanza kufunga kifungo cha suruali yake.

“Nini sasa?”

“Ahaa….nina mpenzi wangu, ninampenda, na sihitaji niingie kwenye mchezo huo”

“Mimi mbona ninaye ninaye mpenda”

“Kama unampenda kweli usiendelee kufanya hivi, utamuumiza akijia kama alivyo umia baada ya kuona habari hiyo”

“Anajua, si yeye tu hadi mama yake”

Dokta Mwamvua macho yakamtoka, akaka kimya huku akionekana kushangaa kwa kile ninacho kuzungumza.

“Ina maana hata mama anajua?”

“Ndio, kwa hiyo hiyo sio taarifa ya kuwashangaza wao”

“Sawa, ni wao ila mimi kwetu wakijua nitatengwa. Na kumbuka mimi ni muislamu niliye kamilika na huu mchezo kwenye dini yangu pia hairuhusu, sasa naomba tuishie hapa sawa”

Dokta Mwamvua alizungumza kwa msisitizo huku akijifunga vifungo vya shati lake, nikamtazama kwa macho ya kumdadisi, nikafahamu anacho kizungumza kinatoka kweli moyoni mwake. Akafungua mlnago na kutoka chumbani humu, nikarudi bafuni, nikaoga taratibu. Nikamaliza na kurudi chumbani, nikajikausha mwili wangu kwa taulo kisha nikalivaa hili baibui pasipo chupi wala siridia, kwani nguo hizo zimechafuka na sina nyingine.

Nikashuka gorofani na kumkuta dokta Mwanamvua akiwa amekaa kwenye sofa lililopo pembeni ya Eddazaria huku akisoma moja ya gazeti.

“Upo tayari?”

“Ndio, ila ndani mwenzio sina chupi wala siridiria”

“Tutapitia kwenye maduka hayo kwanza, utanunua”

Nikafungua brufacase na kutoa kibunda kimoja cha pesa, nikakihesabu na kukuta kikiwa na dola za kimarekani, dola elfu kumi, nikatoa dola elfu mbili na nyingine nikazirudisha kwenye brufcase hii. Nikaiweka simu yangu pembeni ya Eddazaria, kisha nikachukua simu moja mpya ambayo haina laini.

“Mbona unaacha simu?”

“Akiamka anaweza kututafuta alafua akashindwa kufahamu ni wapi alipo, nataka tukifika huko mjini ninunue line nyingine ambayo nitampigia na kumuambia ni wapi tulipo”

“Ahaa, hapo nimekuelewa”

Nikachuchumaa karibu na Eddazaria, nikambusu shavuni mwake, kisha nikasimama na kuanze kueleka nje. Dokta Mwamvua akaingia kwenye na kulitoa nje, nikafunga geti kisha na mimi nikaingia ndani ya gari hilo.

“Zanzibar ina majengo mengi ya zamani”

“Yaa ni mji wa Zamani sana, kipindi hicho wakoloni, Waingereza na Waarabu walitawala ndio walijenga majengo haya”

“Ahaaa…..ila kuna pendaza”

“Kwani hujawahi kuja huku Zanzibar?”

“Hii ndio mara yangu ya kwanza kufika huku”

“Mmmm”

“Ndio, japo nimezaliwa Dar es Slaam, nimeenda China, ila hapa kwa kupanda boti sijawahi kufika kwa kweli”

“Usijali leo nitakutembeza maeneo mengi mengi sana”

“Kumbuka kwamba mume wangu yupo nyumbani peke yake na ana umwa”

“Sindano niliyo mchoma sidhani kama kwa muda anaweza kuamka muda huu”

“Haya bwana”

Tukafika katika doka la nguo za kike za ndani, ikanilazimu kabla ya kushuka kwenye gari, nikavaa miwani na kujifunga mtandio kiuoni mwangu. Tukaingia ndani ya duka hili linalo uzwa na mama wa kihindi. Tukaanza kuchagua nguo za ndani, nikanunu nyingi sana, nikalipa, kisha tukaendelea kwenye maduka mengie ya nguo ambayo yapo mtaa huu huu. Manunuzi ya nguo zangu hayakuchukua muda sana, tukahamia katika maduka ya wanaume hapa, ndipo nilipo anza kupata kazi ya kumchagulia mume wangu nguo ya kuvaa.

“Kwa nini serikali isitunge sheria kwa watu wa aina hii?”

Mwanaume mmojaa aliye valia kanzo pamoja na barakashia, alizungumza huku akisoma gazeti.

“Watu gani?”

“Tazama kama huyu mtoto eti ni msagaji, yaani angekuwa Pakistani huko angesha chomwa moto, kwa tabia za usagaji. Nachukia sana wasagaji na mashoga”

Maneno ya mwanaume huyu yakatufanya mimi na dokta Mwamvua kutazamana.

“Ahaa ndio utandawazi ndugu yangu”

“Utandawazi gani na ni upuuzi huu, alafu huyu binti si anafilamu yake anataka kuitoa?”

“Ndio”

“Yaani nitakuwa mtu wa kwanza kutangaza isinunuliwe kwa maana itakuwa imejaa laana tu humo ndani”

“Hahahahaa. Huwezi jua ndani kumeigizwa kitu gani”

“Akhaa….upuuzi mtu, laiti kama ninepata tafasi ya kumuona uso kwa uso basi hii bakora yangu ingemuishia mwilini mwake”

“Hahaaa”

“Haki ya Mungu vile, anatuletea ushenzi tu, unahisi vijana watoto wetu wa kike tutawaficha wapi?”

Maneno ya mwanaume huyu, yakaanza kuumiza moyo wangu, dokta Mwanamvua akanitazama na kuligundua hilo, taratibu akanishika bega huku akiliminya minya akioniomba nisifanye chochoye kIbaya.

“Shehe wangu, unayo yazungumza ni ya kweli kabisa, ila inabidi sasa watu waweze kufahamu kwamba hii dunia imejaa mauovu mengi, watoto wetu inabidi tuwalinde kwa heshima”

“Kweli ila huyu Jojo namchukia sasa, simpendi kabisa. Toka nijue hizi tabia zake za usagaji sinto mpenda kabisa, na hiyo siku ya uzinduzi sijui wa filamu yake nipo hata tayari kuwapika Al-Shabab wakajilipue naye akafilie mbalia”

Maneno ya mwanaume huyu yakaanza kunitoa machozi, nikajikuta nikikambidhi kiasi cha pesa dokta Mwamvua, kisha nikatoka dukani humu nikimuachia nguo nilizo zichagua, nikaingia ndani ya gari na kuvua miwani, machozi yakaanza kunimwagika kwa wingi sana. Baada ya dakika kama mbili dokta Mwamvua akaja akiwa amebeba mfuko mkubwa wenye nguo za Eddazaria, akanitazama kwa sekunde kadhaa.

“Tuendele kun…”

“Turudi nyumbani”

Nilizungumza huku nikipangusa machozi usoni mwangu. Kusema kweli nikaanza kujikuta nikuchukia eneo hili. Dokta Mwanamvua hakuwa na kipingamizi zaidi ya kufwata matakwa yangu kwani tayari siku yangu imesha haribika. Safari yetu ya kurudi nyumbani ikachukua kama dakika ishirini na sita hivi, macho yakaanza kututoka mara baada ya kuona mkusanyiko mkubwa wa watu nje ya nyumba yetu, mashi mwingi wa moto azidi kututisha na nikajikuta nikfungua mlango wa gari hili bila hata halijasimama. Nikaanza kukimbilia katika eneo la nyumba hii ambayo ndani tumemuacha Eddazaria, wanaume wenye nguvu zao wakanizuia, kuingia ndani kwani nyumba yote inateketea kwa moto mwingi sana, na sijui kama Eddazaria kama yupo hai au emeteketea na moto ndani kwani tulimuacha akiwa amelala fofofo.


“Niachieni”

Nilizungumza huku nikijitahidi kujitoa mikono mwa wamaume hawa, machozi yakazidi kuendelea kunitoka machoni mwangu.

“Ni kitu gani kimetokea?”

Dokta Mwanamvua alizungumza huku hakihema sana.

“Ni mlipuko kama wa bomu”

“Mlipuko kama wa bomu?”

“Ndio, yaani daaa ni bora hata mumetoka yaani”

Kijana huyu alizungumza pembeni yetu jambo lililo nifanya nizidi kuchanganyikiwa kwa kweli.

“Hamjaona mtu akitoka humu ndani?”

Dokta Mwanamvua alizungumza huku macho yakuendelea kumtoka.

“Kwa mlipuko ule dada sidhani kama kuna mtu anaweza kutoka hai”

Maneno ya mwanaume huyu yakazidi kunichanganya, kusema kweli nikahidi kama kuna kitu kina urarua moyo wangu, na kunifanya nishindwe kabisa kusimama na kujikuta nikianguka chini pasipo kutarajia. Mwanga wa juu taratibu ukaanza kutoweka machoni mwangu, baada ya muda giza nene likanitawala na kuanzia hapa sijafahamu ni nini kinacho endelea.

***

Sauti za watu wanao zungumza kwa sauti ya chini, wakanifanya niweze kufumbua macho yangu taratibu. Nikakaa kwa sekunde kadhaa huku nikijitahidi kuziingiza sauti hizi kwenye kumbukumbu zangu, ili nijue ni nani anazungumza. Kumbu kumbu zangu za sauti zikaweza kufahamu anaye zungumza kwa sauti hiyo ya chini ni mama yangu mkwe. Nikageuza shingo yangu na kumtazama na kumkuta wakiwa wamekaa kwenye sofa na Judy mdogo wangu. Nikafumba macho tena ili niweze kujaribu kukumbuka kama Judy na mama yangu mkwe wamefikaje fikaje hapa Dar es Salaam.

“Dada”

Niliisikia sauti ya Judy ikiniita, nikafumbua macho zaidi na kumkuta akiwa amesimama karibu kabisa na kitanda hichi nilicho kilalia.

“Shikamoo”

“Marahaba”

Niliitikia kiunyonge huku nikitazama mandhari ya hili eneo, sio geni machoni mwangu kwani ni ndani kwangu katika jumba langu nililo linunua.

“Umeamka?”

“Eheee. Mama”

“Beee”

Mama mkwe aliitikia huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kalia humu ndani kwangu, akakaa pembeni ya kitanda changu.

“Eddy yupo wapi mama?”

Mama mkwe akaka kimya, sura yake ikazidi kujawa na unyonge, nikajaribu kunyanyuka ila mama mkwe akanizuia nisinyanyuke.

“Mama Eddy yupo wapi?”

“Usijali mwanangu, ngoja nimpigie dokta aje kukuangalia, hali yako sawa mwanangu?”

Mama mkwe alizungumza kwa haraka haraka huku akinyanyuka, akatoka chumbani humu na kutuacha mimi na Judy tukimtazama.

“Eddy yupo wapi?”

“Shem?”

“Ndio shemeji yako?”

Judy naye akaonekana kupatwa na kigugumizi. Macho yakamtoka akatamani kufungua kinywa chake ila inaonyesha dhahiri anashindwa kuniambie kile ambacho anakifahamu.

“Naiambi……”

Mlango ukafunguliwa, akaingia mama mkwe pamoja na dokta wa kiume ambaye ndio mara yangu ya kwanza kumuona katika maisha yangu. Dokta huyu akanitazama huku akitabasamu, akanisogelea na kunishika mkono wangu wa kulia, akautazama tazama kwa muda, akachukua kijitochi kidogo na kunifunua macho yangu na kuanza kunimulika mulika.

“Unajisikiaje?”

“Eheee?”

“Unajisikiaje?”

Nikakosa cha kumuambia kabisa na kjikuta nikimtaza kwa muda, akanishika maeneo ya tumboni kwa muda kidogo kisha akamgeukia mama.

“Mwili wake umerudi katika hali yake ya kawaida”

“Ahaaa sawa sawa asante sana dokta”

“Nashukuru sana, ila kukiwa na mabadiliko ya aina yoyote mumaweza kuniambia”

“Sawa, je mimba yake ipo vizuri?”

“Ndio mama haijatoka”

“Ohoo asante Mungu”

Mama mkwe alizungumza kwa hisia sana, hapo ndipo na mimi nikastuka na kuanza kujishika shika tamboni kwangu. Tumbo langu kwa kiasi fulani nikajikuta likiwa limenyanyuka kidogo na halipo flat kama siku zote ninavyo lijua.

“Mama nina mimba?”

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga.

“Ndio mwanangu una mimba”

“Ya muda gani?”

“Mwezi na wiki tatu na siku nne, inakaribia mwezi wa pili”

Nikawa kama mtu niliye shikwa na bumbuwazi. Kufurahi ninataka, kucheka ninataka, kulia ninataka, yaani hali zote zikajikamata kwa wakati mmoja.

“Dada familia yetu inakwenda kuongezeka”

“Kweli”

“Eheee, familia inakwenda kuongeka”

“Mama imekuwaje kuwaje nipo Dar?”

“Tutazungumza baadaye mwanangu, kwa sasa pumzika kwanza kisha baada ya hapo tutazunguma sawa mwanangu”

“Sawa mama”

“Mgonjwa, jitahidi sana kunywa maji na kula matunda mengi sana”

Dokta alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Sawa”

“Haya kwa heri”

“Sawa”

Daktari na mama mkwe wakatoka chumbani hapa, nikabaki mimi na Judy taratibu nikaka kitako kitandani.

“Vipi imekuwaje kuwaje mbona sielewi?”

“Mmmm dada ni muda sasa umekuwa umelala kutandani, tangu nije nimekukuta ukiwa umelala hapa kitandani”

“Ni muda gani?”

“Kama wiki tatu sasa toka mimi nije?”

“Wiki tatu?”

“Eheee. Yaani tulikuwa tunaomba, wanakuja wana maombi humu ndani wanakuombea ili fahamu zako ziweze kukurejea”

“Ina maana….”

Mama mkwe akaingia humu ndani na kunifanya nisizungumze kile nilicho kuwa nimekikusudia kukizungumza.

“Jojo usikae hivyo ulivyo kaa, jaribu kidogo kulipa tumbo nafasi usilikunje sana”

Mama mkwe alizungumza huku akinifwata, akauchukua mito miwili ya kitandani na kuiweka nyuma yangu. Alipo maliza kuiweka akanilaza kidogo.

“Hapo sasa sawa, Judy nenda kule jikoni kuna ule mtori nimeuwweka kwenye ile chupa kubwa ya chai naomba unaniletee. Leta na bakuli, na kijiko”

“Sawa mama”

Judy akanyanyuka kitandani na kutoka humu chumbani na kuniacha mimi na mama mkwe.

“Mama naomba uniambie ukweli yupo wapi mume wangu?”

“Sikia Jojo, utanakiwa kwanza kula na ushibe, si unaona jinsi mwili wako ulivyo poteza nguvu, umekonda konda mwanangu, dokta alikuwa akikuwekea dripu za vitamin, ili kuupa mwili nguvu”

“Kwani hapa kitandani mama nina muda gani?”

“Una mwezi na wiki mbili sasa”

“Mmmm”

“Yaa mstuko ulio kuwa umeupata kwenye tukio la kuagua kwa nyumba mulio kuwa munaishi ulikuwa ni mkubwa sana, ulikuwa una amka na kuzimia, unaamka na kuzimia. Yaani kulikuwa kama umetupiwa kitu fulani hivi ambacho kusema kweli pasipo kufanyiwa maombi wala usinge weza kuamka tena”

“Na mume wangu je?”

Swali langu likabaki pale pale kwa mama mkwe.

“Eddy…..”

Nikajiweka vizuri kitandani huku nikimsikiliza mama mkwe kwa umakini sana.

“Eddy katika ile ajali ya kuugua kwa moto ame…..”

“Amefanyaje mama yangu?”

Niliuliza huku mapigo ya moyo yakianza kunienda kasi, yale maumivu makali ambayo niliyo yapata kwa dakika za mwisho kabla sijapoteza fahamu zangu.

“Hakuwemo ndani ya nyumba ile”

Nikashusha pumzi zangu, ubaridi mkali ukanitawala katika mwili wangu, maumivu niliyo kuwa ninayahisi moyoni mwangu yakapotea kabisa.

“Ila hadi sasa hivi hatujafahamu ni wapi alipo, ila ndani ya nyumba hapakuwa na mtu kabisa”

“Sasa mama hamjajua hata ni wapi alipo?”

“Bado kaka yake na vikosi vingine vya usalama vinaendelea kumtafuta, ila tunaamini kwamba yupo hai kwa maana kama ndani ya nymba hakuweza kuwepo, na hatujaweza kusikia fununu za maiti iliyo tupwa sehemu yoyote basi tuna imani ya asilimia mia moja kwamba bado yupo hai”

“Ohoo Mungu amsidie huko alipo, na hii mimba kweli nitailea peke yangu?”

“Usijali mwanangu, upo kwenye uangalizi wangu mimi mwenyewe, ndio maana nimeamua kuacha kila kazi yangu kuhakikisha kwamba ninakulinda na kuhakikisha kwamba afya yako na mjukuu wangu zinakuwa salama”

“Asante mama”

Nilizungumza kwa sauti ya unyonge huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Kwa upande ni taarifa iliyo nipa matumaini, akaingia Judy akiwa na vitu ambavyo mama mkwe ameweza kumuagiza. Mama mkwe akaandaa mtori huu na kuanza kuninywesha taratibu, nikanywa chupa nzima ya mtori huu ambao ni mtamu sana. Mama mkwe akanisaidia kushuka kitandani, huku akiwa anasukuma bomba refu la chuma lenye vitairi vidogo chini ambalo limening’iniziwa dripu linalo ingiza maji mwilini mwangu. Mama mkwe akanisindikiza hadi bafuni, akanivua nguo zangu taratibu, hapa ndipo nikagundua kwamba nimepungua mwili wangu tena sana.

“Mama nimekuonda ehee?”

“Yaa ila sio sana, kidogo tu”

“Mmmmm”

Mama mkwe akafungua bomba la maji ya mvua na kuanza kuniogesha taratibu, kwa upando wa mama huyu kusema kweli nikajikuta machozi yakinitoka usoni mwangu.

“Jojo usipende kulia sana, utajikondesha mwanangu?”

“Hapana mama silii kwa sababu hizo, nalia kwa furaha mama yagu ambayo ninayo, yaani unanijali, sijawahi kupata upendo kama huu, sijui kama leo ningekuwa peke yangu kama ningeweza kufanya haya yote”

Usijali hili ndio jukumu lango kwa kila mtoto anye ongezeka kwenye familia yangu. Nina watoto watatu, ila sasa ninao sita, na wajukuu ndio kama hivi muna zidi kunipatia, hata mimi huwa nina ona furaha kuona kwamba sipo peke yangu, na uzao wangu umezaa matunda yaliyo mema”

Maeno ya mama mkwe yakezidi kunipa hisia zilizo nifanya nizidi kumwagikwa na machozi kwa kweli.Mama mkwe akamaliza kuniogesha na nikarudi chumbani, nikamkuta Judy akiwa amesha niandalia dera.

“Jamani mumesha niandalia hadi madera?”

“Ohoo mwenzio nilisha kwenda kununua hadi nguo za mtoto”

Judy alizungumza huku akiwa amejawa na furaha.

“Hahaaa nguo za mtoto. Umenunua za jinsia gani?”

“Zote mbili, akiwa wa kiume sawa, akiwa wa kike pia sawa”

“Judy mdogo wnagu unavituko sana””

“Vituko gani ikiwa na mimi nitaitwa ma mdogo”

“Hahaaa”

“Jojo njoo uchungulie dirishani”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amefunua pazia kidogo, taratibu nikanza kutembea huku nikiwa ninasukuma bomba hili lililo ning’inizwa dripu. Nje nikakuta watu wengi sana wakiwa wameshika maua pamojana mabango yanayo niombea kwa Mungu ni nipone haraka niendelee na majukumu ya kila siku, jambo lililo nishangaza kwa kweli kwa maana matukio kama hili nilisha wahi kuliona kwa raisi wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela pale alipo kuwa amelazwa hospitalini. Nikiwa katika tafakari na furaha kuona mashabiki wangu wananipenda na kunijali, gafla tukastukia mlio wa risasi uliowafanya watu hao kuanza kuchanguka huku wakitupa mabango na maua walio kuwa wameyashika.



Mama mkwe kwa haraka akanirudisha hadi kitandani na kunilaza taratibu.

“Asitoke mtu nje sawa”

“Ma…..”

Judy alitaka kuita ila tayari mama mkwe alisha toka nje.

“Mama anakwenda mwenyewe nje si hatari”

“Usijali mama yupo vizuri”

“Kivipi?”

“Wewe tulia tu hapa ndani”

Nilizungumza kwa sauti ya upole, Judy akakimbilia dirishani na kuanza kuchungulia nje.

“Bado wanakimbia?”

“Ehee, naona kuna polisi kuna mtu wamemshikilia”

“Mwanaume au mwanamke?”

“Mwanaume, ila anaonekana kama muhuni muhuni hivi”

“Mama amefika getini?”

“Yaaa ila hajafungua geti bado”

“Judy namba simu yako”

“Simu yangu nijmeiweka chaji, jana usiku nilisahau kuiweka chaji, ila ngoja nikuchukulie simu yako”

“Simu yangu ipi?”

“Hii nasikia ulikutwa nayo kipindi ulivyo anguka na kuzimia”

Judy alizungumza huku akielekea kwenye dreasing table iliyomo humu chumbani, akafungua droo na kutoa simu na kuniletea kitandani.

“Sema haina laini”

“Nitafutie basi laini”

“Mmmm kuna laine jana niliinunua ngoja nikupatie uwe unaitumia kwa muda kwa maana nimeipenda, ina namba nzuri sana”

“Sawa naomba”

Judy akatkka chumbani humu, baada ya muda akarudi akiwa ameshika simu yake, akaifungua na kunitolea laini moja kati ya mbili zilizo kuwa katika simu yake. Nikaiweka laini hiyo kwenye simu yangu hii na kuiwasha.

“Ina salio la kutosha”

“Kiasi gani?”

“Elfu kumi na tano”

Baada ya simu hii kuwaka, nikaitazama kwa muda, nikaiandika namba ya simu ambayo nilimuachia Eddazaria. Nikaipiga namba yangu na kuiweka simu sikioni mwangu. Sauti ya kike ikasikika ikinitaarifu kwamba mteja ninaye mpigia kwa sasa hapatikani hivyo basi nijaribu tena baadaye.

“Vipi?”

“Haipatikani”

“Kwa nini unampigia nani?”

“Hii ni namba yangu ya zamani, nilimuachia shemeji yako simu yangu kabla ya ajali ya moto”

Mama mkwe akaingia humu ndani, akaka kitandani.

“Vipi mama?”

“Kuna kijana mmoja alijaribu kuwasambaratisha watu kwa kutumia bastola ila amesha kamatwa na askari”

“Ahaaa”

“Hivi unajua hao watu wapo hap oleo tangu asubihi, kwa maana nilianzisha kampenzi ya watu kukuombea kupitia vyombo vya habari na ninashukuru Mungu ameweza kujibu majibu yangu na sasa umeamka”

“Asante sana mama”

“Kikubwa kwa sasa unatakiwa kufwata taratibu za kula, ili mwili wako uweze kurudi katika hali yake ya kawaida”

“Sawa mama”

“Kuhusiana na usalama kwa sasa usalama upo wa kutosha, kuna walinzi zaidi ya kumi na nane, wanne ni wanawake, niwewaajiri kwa ajili ya kukulinda, wewe na mjukuu wangu ajaye”

“Mmmm….mama mbona walinzi ni wengi sana?”

“Lazima uweze kupata ulinzi mkubwa na wa kutosha, sihitaji huyo mshenzi Nuru aweze kukughusa tena"

“Kwani mama Nuru bado hajakamatwa?”

“Ndio bado hajakamatwa, na inavyo sadikika kwamba yeye ndio amehusika katika kuilipua ile nyumba na vijana wake, kwa maana waliweza kuitrack down namba yako ya simu na wakafahamu ni wapi mulipo”

Hapa sasa ndipo nikaanza kupata picha ya kwa nini ile nyumba iliweza kulipuliwa, kwa maana ni watu wachache sana ambao waliweza kufahamu ni wapi tulipo, na kosa kubwa ambalo nililifanya ni kuicha simu ikiwa nimeiwasha.

“Ila mama kama Nuru ndio atakuwa amemshikilia mume wangu, si anaweza kuwa amemuua?”

“Hawezi kumua kwa sasa, laiti angemuua moyo wangu ungehisi kitu. Ila naamini kwamba bado hajamuu"

“Kweli mama?”

“Ndio. Kitu kingine hakikisha kwamba hauweki post yoyote kwenye mtandao wa kijamii kwa sasa. Nahitaji urudi katika afya yako mwanangu sawa”

“Sawa mama”

“Hivyo hiyo Judy, isije na wewe ukajisahau siku ukamuweka dada yako huko kwenye Facebook, sijui instergram, halitokuwa jambo zuri sawa”

“Sawa mama nimekuelewa”

***

Siku zikazidi kusonga mbele, huku afya yangu kila siku ikizidi kuimarika, malezi na matunzo ninayo yapata kutoka kwa mama yangu mkwe, nina imani kwamba kila mwanamke ambaye angeolewa kwenye familia hii, ninaimani kwamba angeyapenda. Ujauzito wangu ukazidi kukua na nikazidi kunawiri, umbo langu la mazoezi taratibu likaanza kuondoka.

“Mama leo natamani kuelekea ofisini kuangalia ni kitu gani ambacho kinaendelea”

Nilizungumza huku nikimtazama mama mkwe anaye niandalia uji wa ulezi.

“Sawa, utandoka na walinzi, ila usiende ukafanya kazi nyingi uangalie afya yako”

“Usijali mama”

“Kunywa kwanza uji kisha ndio uende”

“Sawa mama”

Nikafwata taratibu ya chakula kama mama mkwe alivyo nipangia, nikapiga kombe moja la uji wa ulenzi, kish a nikaingia chumbani kwangu na kujiandaa.

“Wapi leo mbona unajipodoa?”

Judy aliniuliza mara baada ya kuingia chumbani kwangu.

“Naelekea kwenye kampuni yangu”

“Twende wote basi”

“Kajiandae fasta, ukichelewa ninakuacha”

“Mimi hapa ni kuchana nywele zangu tu”

“Sawa”

Nikamaliza kujiandaa, nikachukua pochi yangu kubwa, nikatoka chumbani humu na kumkuta Judy naye akitoka chumbani kwake. Tukamuaga mama na tukaingia kwenye gari aina ya Benzi Compresa na tukaka kwenye siti ya nyuma. Walinzi wangu wawili wa kike wakakaa siti za mbele huku mmoja akiwa ni dereva. Mbale ikatangulia gari nyingine aina ya Range Rover, na nyuma napo kuna gari nyingine aina ya Range Rover na zinafanana na gari la mbele.

“Haya magari yote ya nani?”

“Yote kayanunua mama, yaani kuna mabadiliko ya vitu vingi sana amefanya kwenye maisha yetu”

“Tunabahati kwa kweli, yaani sijui tungekuwa sisi wenyewe sijui ingekuwaje”

“Yaani wee acha tu”

Tukaendelea kuzugumza mambo mengi ambayo mama mkwe ameweza kutufanyia. Tukafika katika ofisi zangu, nikajikuta nikijshana sana mara baada ya kukuta sanamu yangu ikiwa imewekwa eneo la nje ya gorofa hili. Nikajikuta nikitabasamu huku machozi yakinilenge lenga. Mlinzi wangu mmoja akanifungulia mlango kisha nikashuka kwenye gari, nikatazama eneo zima la hili eneo la hilo gorofa, kisha tukaanza kuelekea ndani ya ofisi hizi, kila nilipo pita watu walitutazama. Tukaingia kwenye lifti na kuelekea juu zilipo ofisi zangu. Nikaingia kwenye ofisi zangu na kuwakuta wafanyakazi wakiwa bize sana wakiwajibika na majukumu ya humu ndani. Wafanyakazi wangu walipo niona kila mmoja akaacha alicho kifanya na kunifwata sehemu nilipo simama.

Wakanisalimia kwa shangwe sana, huku kila mmoja akionyesha hisia zake za kuwa na hamu nami.

“Jamani Jojo”

Dokta Clara alizungumza huku akinikumbatia. Machozi ya furaha yakaanza kunilenga lenge kusema kweli, ni wakati mwengine kwenye maisha yangu ninao weza kuona jinsi nguvu ya watu wangu wa karibu wanavyo nipenda.

“Mambo zenu jamani?”

“Salama”

“Na……”

Nikajikuta nikishikwa na kigugumizi kizito, nikakosa hata la kuzungumza, machozi yakanizidi na kujikuta nikilia kabisa, dokta Clara na Judy wakanishika mkono na kuniondoka katika eneo hili, wakaniingiza katika ofisi yangu ambayo nayo nimekuta ina mabadikiliko kiasi.

“Usilie dada”

“Silii kwa mabaya, nalia kwa furaha, nalia kwa jinsi upendo wa watu ulivyo juu yangu”

“Ni kweli Jojo japo kampuni inajiendesha ila kusema kweli kuto kuwepo wewe na na Eddazaria kusema kweli imekuwa ni kitu ambacho kimetuweka katika wakati mgumu sana.”

“Kweli hilo nalitambua rafiki yangu, kuna kitu gani ambacho kinaendelea kwa sasa?”

“Aah…kuna zaidi ya filama kama tano hivi tumezitengeneza ila bado hatujaziachia, tuliona kuka bila ya kufanya kazi itakuwa sio jambo zuri la kupendeza ikiwa hii ni kampuni hata mama alivyo kuja hapa kufanya mkutano nasi, kusema kweli alitupa nguvu sana. Ya kuendelea kufanya kazi kwa juhudi sana”

Dokta Clara alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge huku akinitazama usoni mwangu.

“Nawashukuru sana”

“Usijali, na uongozi umebadilika, mama alikuja kubadili uongozi kuanzi kwenye swala zima la usimamizi wa uzalishaji wa filamu, nafasi ambazo aliziacha wazi ni yako ya mume wako”

“Ahaaa…..”

“Kwa hiyo hapa kila kitu sasa hivi kina kwenda vizuri, kuanzia uzalishwaji wa filamu hadi kusambaza"

“Yale makampuni ambayo tuliingia nayo mkataba vipi yana kipi cha kuzungumza?”

“Ahaa…wao wanasubiri tu ile filamu iweze kutoka, kwa maana waliingia mkataba kwenye filamu ile ila kuna makampuni mengine nayo yamejitokeza katika udhamini”

“Sawa sawa, nahitaji uniandalie kikoa cha dharura nizungumze na wafanyakazi wote”

“Sawa bosi, ila na huyo kijacho kweli utaweza kusimama kwa muda mrefu?”

“Si cha kusimama, waingia kwenye ule ukumbi wa mkutano”

“Sawa”

Dokta Clara akatoka ofisini humu.

“Unataka kuzungumza nao nini?”

Judy alizungumza hukua kinitazama usoni mwangu.

“Mambo mengi mengi tu, ikiwemo kuwaeleza juu ya maendelea ya afya yangu”

“Hivi unajua mama aliwaambia kwamba unaumwa ndio maana hapakuwa na tetesi wala skendo mbaya mbaya”

“Ahaaa….je juu ya swala la Eddazaria?”

“Yeye aliwaambia kwamba yupo nje ya nchi kwa masoma maalumu, japo ndio hivyo hatufahamu ni wapi alipo.”

“Sawa”

Dokta Clara akaingia ofisini kwangu na kuniambia kwamba tayari amesha wakusanya wafanyakazi wote katika ukimbi wa mkutano. Tukanyanyuka mimi na Judy na tukaelekea katika ukumbi huo, nikakutana na sura ngeni za wafanyakazi wapya. Nikakaribishwa kwa makofi mengi ndani ya hii ofisi, nikaka kwenye kiti changu nilicho andaliwa na Judy akakaa kwenye kiti cha pembeni yangu. Nikasimama taratibu huku nikimtazama mfanyakazi mmoja baada ya mwengine.

“Habari zenu jamani?”

“Salama”

“Kwanza ninamshukuru Mungu kwa kuweza kutuongoza hadi muda huu, kusema kweli ninamshukuru sana Mungu ninaendelea vizuri na hali yangu kama hivi ninavyo niona kusema ni kwa neema ya mwenyezi Mungu”

Nilizingumza kwa sauti ya upole huku nikiwatazama wafanyakazi wangu.

“Natambua wengi wenu mumeweza kuniombea, ninawashukuru kwa hilo. Lengo la kuwaita hapa ni kuweza sasa kuandaa mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaisambaza trela ya filamu ya kwanza iliyo chezwa, nina imani kwamba itakuwa imepo tayari?”

Dokta Clara akatingisha kichwa akishiria kwamba ipo tayari. Simu ikaanza kuita na kutufana sote tumtazame Judy aliye shika pochi yangu. Akaitoa simu ndani ya picha na kunionyesha kwa ishara kwamba ni simu yangu. Akanyanyuka kwenye kiti chake na kunikabidhi simu hiyo, nikaichukua na kukuta namba ngeni kabisa ambayo sijui hata imetokea nchi gani kwani ndio mara yangu ya kwanza kuiona namba kama hii.

 

0 comments:

Post a Comment

BLOG