Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 4/10

 

 

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 4 KATI YA 10

 


“Hilo wazo nimepewa ni mke wa raisi mama Donald Bush, mimi ndio mtu wa pekee ambaye aliweza kuniamini na kuniomba niweze  kumpindua mume wake kwa njia ya ina yoyote na nihakikishe kwamba ninaichukua nchi”

“Ila kumbuka kwamba nchi yako ni kubwa na utampindua kwa namna gani?”

“Hakuna njia nyingine zaidi ya kumuu”

“Na baada ya kumuua inchi itachukuliwa na makamu wa raisi ambaye ataongoza nchi hadi kwenye uchaguzi mkuu?”

“Ndio kwa sasa tumebakisha miaka miwili hadi kuufikia uchaguzi mkuu, miaka hiyo inanitosha sana kujitengenezea jina katika chama cha siasa na nafasi ya kuiongoza nchi ninayo kwa maana jeshi zima linanipenda na kuniheshimu na uzuri kwamba wanatambua mchango wangu katika kupambana na maswala makubwa ya kigaidi duniani. “

“Kama ni hivyo nitakusaidia katika hilo”

“Kwa nini na wewe usiiongoze Tanzaian?”

“Ahahaaa hapana sijafikiria kabisa kuwa mwanasiana, hivi unahisi hii sura ni nani anaye weza kuipenda na kuniona nikiwa ni raisi wa Tania”

“Mbona Godwin aliongoza Tania na alikuwa ni gaidi?”

“Tazama mwisho wake ulivyo kuwa mbaya, nikifanikiwa kumuua K2 basi nitaachana na kila jambo na nitakwenda kuishi mbali sana Afrika nikiwa na familia yangu”

“Sawa niwazo tu nilikupa”

“Nashukuru, ila muda unaweza kuamua  sijui”

Tukajikuta tukifurahi sana na Meja huyu. Safari ikachukua masaa kadhaa tukafanikiwa kufika nchini Madagascar, kitendo cha kushuka kwenye ndege hii, nikaingia kwenye gari ya kifahari pamoja na meja, kisha vijana wake wakiingia katika gari nyingine mbili ambazo zimeliweka gari letu katikati.

“Hii nchi ninaipenda sana ndio maana nikaamua kuja kujenga huku”

“Marekani una nyumba?”

“Ndio ninazo nyingine, Dany mimi ni bilioner japo huwa sipendi sana watu kuweza kufahamu wala nchi yangu kufahamu, ila utajiri wangu unaweza kufika hata dola bilioni kumi”

“Mmmmmm upo mbali sana”

“Yaa nina vijana wachache wa ulinzi binafsi na ninawalipa pesa nzuri sana”

“Utajiri huo uliupata wapi?”

“Kwa marehemu baba yangu na mama yangu, wao walikuwa mabilioner wa enzi hizo, na mimi nilikuwa mtoto wa pekee kwenye famili yao, ila kwa kipindi kile sikuweza kupenda kabisa maswala ya biashara na ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuja kuwa mwanajeshi na ndicho nilicho kifanya hadi kufikisha uzee wangu huu”

Tuliendelea kuzunugumza mambo mengi hadi tukafanikiwa kufika katika jumba kubwa la kifahari, hari zote zikakaguliwa getini na kuruhusiwa kuingia ndani.

“Karibu Dany hapa ndio nyumbani kwangu”

“Shukrani mzee umejitahidi sana?”

“Kidogo kidogo tu”

Tukashuka kwenye magari na kuanza kuingia ndani huku nikiwa nimeongozana na meja. Tukaingia sebleni na kumkuta Yemi na Martin wakiwa wamekaa. Yemi kwa haraka akasimama na kunikimbilia tukakumbatia kwa furaha huku tukinyonyana midogo yetu.

“Mmmmmm”

Meja alikohoa kidogo tukajikuta tukiachiana na Yemi na kumtazama.

“Karibuni sana hapa ni kwangu na mujisikie kama mupo nyumbani”

“Tunashukuru sana meja. Yemi kutana na meja huyu ni rafiki yangu ambaye yeye ndio ametupa msaada wote huu”

“Shukrani sana meja kwa msaada wako”

“Usijali, shemeji yangu”

“Meja huyu ni…..”

“Aahaa Dany unataka kunitambulisha shemeji yangu wakati ninamfahamu”

Meja alizungumza kwa utani na tukajikuta tukicheka sana. Ikanibidi kumtambulisha Martin kwa meja.

“Martin nimepata taarifa zako kwamba upo vizuri, uliwasumbua sana vijana wangu hadi kuweza kukuweka sawa”

“Hapana mkuu, nilikuwa ninafanya kazi yangu kumlinda mke wa mkuu”

“Kweli natambua huwa najua walinzi binafsi ni ngumu sana kuweza kumuelewa mtu tofauti na bosi wako. Ila Dany hapo umepata mtu muaminifu sana laiti ingekuwa ni mwengine basi mke na yeye sasa hivi wangekuwa wamesha kufa”

“Ni kweli”

“Jamani tupate chakula kwanza na mambo mengine yataendelea”

Meja alizungumza, tukakaribishwa mezani na wafanyakazi wake wa ndati, tukala chakula taratibu huku meja akiendelea kutusimulia mambo mengi ya maisha yake ya nyuma.

“Kweli ninawashauri Dany na Yemi kabla ya kufanya chochote kesho fungeni ndoa, tule tusherekee maisha yanasonga. Na yamebaki masaa machache sana kwa kijana wenu kuweza kufika nchini hapa”

“Ohoo sijui niseme nini shemeji, mimi nipo tayari kufunga ndoa hata sasa hivi?”

“Mchungaji tutampata wapi?”

“Dany wewe tatizo lako ni mchungaji au ndo, kama ni mchungaji hata kesho tunaweza kumleta hapa na ndoa ikafungwa, yaani ndoa yeni haitaji mashabiki, ni sisi sisi hapa tunahudhuria baada ya hapo ratiba nyingine zinafwata”

“Sawa hakuna tabu”

Baada ya kupata chakula, tukaonyeshwa chumba chetu huku Martin na yeye akikabidhiwa chumba chake. Kitendo cha kuingia ndani humu, tukajikuta tukivua nguo zetu haraka haraka na kubakiwa kama tulivyo zaliwa.

Nikaanza...

“Nipe mume wangu”   

..... taratibu nikamshusha Yemi huku sote tukimwagikwa na jasho jingi.

“Ninakupenda sana mume wangu, yaani kwao nimefika kwa raha hisi sidhani kama kuna mwanaume anaweza kunishawishi ili niwe naye”

“Wewe ndio mwanamke wa mwisho kwenye maisha yangu, nakupenda sana Yemi wangu”

“Nakupenda pia mume wangu”

Nikamnyanyua Yemi kwa nguvu na kuanza kumbeba na taratibu tukaingia bafuni, na kuanza kuoga, hatkuchukua muda mrefu sana tukamaliza na kutoka, huku tukuwa tumevaa mavazi maalumu tuliyo yakuta humu bafuni.

“Yaani kesho natamani haya ifike sasa hivi, yaani nitafurahi sana mwanangu akiwepo kwenye harusi yetu”

“Nina imani matatizo sasa yataisha, japo nina kazi ndogo ya kuikamilisha ila ikiisha hiyo nataka sisi na mtoto wetu tukaishi maisha mbali kabisa na Afrika”

“Wapi unataka twende tuishi?”

“Popote ili mradi tuondoke kwenye ardhi ya bara la Afrika kwa maana watu wake wame……”

Mlango ukagongwa taratibu, nikakatisha sentensi yangu, nikaanza kutembea hadi mlangoni, nikafungua na kumkuta meja akiwa amesimama, kwa ishara ikaniita.

“Mke wangu ninakuja”

Nilizungumza huku nikitoka na kuufunga mlango huu, tukatembea hatua kadhaa kutoka mlangoni.

“Dany kuna tatizo limejitokeza”

“Tatizo gani meja”

“Mtoto wenu amefariki kwa kuuwawa”

Mwili mzima nikahisi ukizizima kwa kupoteza nguvu, macho yakanitoka kwani taarifa hii kwangu ni nzito ila ninaweza kuihimili, ila sijuia Yemi mke wangu kama anaweza kuihimili taarifa isitoshe nimemuacha akiwa katika furaha kubwa sana ya kuifikiria ndoa yetu tuliyo panga kuifunga kesho.          


        

Ukimya ukatawala kati yetu mimi na Meja, nikajikuta nikiwa nimeshika na kigugumizi kizito kabisa, sijui hata nizungumze kitu gani.

“Walipo kuwa wanakuja huku wamevamiwa na watu wasio julikana njiani, yeye na watu wangu wawili walio kuwa wakimleta haku wameuwawa”

Nikahisi jasho likinimwagika mgongoni.

“Nimeagiza vijana wangu kuweza kufwatilia na kujua ni nani ambaye ameweza kuhusina na mauaji haya”

 

“Hapo meja unahisi atakuwa ni nani kama sio raisi Donald Bush, kwa maana huyu mtoto ndio alikuwa ni shabaha yake ya kuweza kunipata mimi na ameshindwa kunipata na amaemua kulipiza kwa mtoto”

“Majibu kamili Dany tutapata vijana wangu watakapo niletea taarifa?”

“Meja samahani ninakuomba hili niweze kulishuhulikia na liwe ni jambo la siri kati yangu mimi na wewe sihitaji Yemi kwa sasa aweze  kujua hili swala”

“Sawa itakuwa ni siri kwa sasa ila kulishuhulikia hili Dany, kwa sasa ni hatari tulia kwanza upumzike na mke wako hili swala     vijana wangu watalishuhulikia”

 

“Hapana meja hii ni vita yangu, vita inayo garimu maisha hadi ya vijana wako kwa ajili yangu, ninakuomba niimalizie hii vita ilipo fikia sasa hivi hata nikifa basi najua nitakufa kwa ajili ya kuitafuta haki ya moyo wangu. Tafadhali meja ninakuomba”

Nilizungumza kwa msisitizo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Meja akanitazama kwa sekunde kadhaa, mlio wa simu ukamstua na akaitoa simu yake mfukoni na kuipokea.

“Ndio”

“Ipelekeni hospitali”

“Sawa”

Meja akaka simu na kunitazama.

“Miili ya marehemu wanaiepeleka hospitali sasa hivi, ikiwemo mwili wa mtoto wenu”

“Nahitaji kwenda kuiona tafadhali ninakuomba uniruhusu katika hilo”

 

“Sawa jiandea, ndani ya chumba chenu ndani ya kabati kuna suti ninaimani utazipenda”

“Shukrani meja”

Nikarudi chumbani na kumkuta Yemi akiwa amesimama mbele ya kioo huku akiweka mapozi kadhaa huku akiwa ameshika kiuno chake.

“Mume wangu kesho yaani nitatembea kimadoido kama hivi”

Yemi alizungumza na kuanza kutembea kama wanavyo tembea mamisi wakiwa majukwaani. Nikajitahidi kutabasamu kwani sihitaji Yemi kugundua ukweli unao endelea.

“Mke wangu umependeza ukitembea hivyo?”

“Asante sana mume wangu sasa na wewe inabidi nikufundishe mwendo wa kutembea kwenye harusi yetu sawa mume wangu”

 

Furaha aliyo nayo Yemi kusema kweli laiti akigundua kwamba mwanae amefariki sijui atakuwa katika hali gani kusema kweli.

“Njoo njoo mume wangu tuanze kutembea”

Yemi alizungumza hukua kinishika mkono, nikakubali kufanya hivyo, maumivu ninayo yapata moyoni mwangu kusema kweli hayana kipimo. Yemi akaanza kunifundisha kutembea taratibu, lengo langu ni kumfurahisha kwa muda kidogo ili niweze kumuaga kuondoka katike eneo hili.

“Mke wangu kuna sehemu nahitaji kwenda na meja mara moja”

Nilizungumza huku nikitabasamu nikihakikisha kwamba Yemi hawezi kuona utofauti wowote ambao nipo nao kwenye moyo wangu.

“Unakwenda wapi mume wangu?”

“Kuna baadhi ya vitu vya arusi anahitaji kwenda kunionyesha, mke wangu vitu vingine inabidi kukufanyia suprize usinifanye nivizungumzee”

“Mmmm jamani mume wangu wala hatujakaa sana”

“Mke wangu kuna zawadi nzuri sana ninakwenda kuitafuta”

“Zawadi gani?”

“Mmmmm mke wangu itakuwa ni suprize sawa”

“Haya mume wangu naamini ukija utamkuta mtoto wetu amesha fika”

 

Maeno ya Yemi bado kidogo yanimwage machozi ila nikaikuta nikitabasamu tu.

“Ndio, meja ameniambia kwenyeh hili kabati hapa kuna suti ngoja niangalie kwa maana ana nisubiria”

“Sawa mume wangu”

Nikatoa suti nyeusi ambayo ina kila kitu kuanzia tai hadi shati, nikaanza kuvaa kwa haraka, Yemi akanisaidia kunifunga tai hii. Nikamshika kidole cha shahada cha mkono wake wa kushoto nikakitazama kwa umakini.

“Nini mume wangu”

“Naangalia ni pete gani ambayo inaweza kukupendeza mke wangu”

“Yoyote mume wangu kikubwa ni upendo wangu mkubwa nilio kuwa nao kwako”

 

“Nashukuru kwa kunipenda mke wangu”

Nilizungumza kisha taartibu nikamkumbatia Yemi huku bado nikizidi kupata maumivu mengi moyoni mwangu.

“Haya nenda sasa mume wangu usije ukachelewa”

“Sawa mke wangu”

Nikarudia tena kumbusu Yemi kisha nikatoka chumbani humu, nikakutana na meja akinisubiria kwenye kordo. Moja kwa moja tukaelekea kwenye gari ambazo zimendaliwa tayari. Msafara wa gari mbili hizi ukaanza huku kwenye gari nikiwa nimejawa na mawazo mengi kichwnai mwake. Hatukuchukua muda mrefu tukafika kwenye moja ya hospitali kubwa, tukashuka na kupokelewa na mtu mmoja ambaye yupo chini ya meja.

“Wamejeruhiwa vibaya sana kwa risasi”

“Gari je?”

 

“Gari zipo sehemu ya tukio lilipo tokea polisi wanaendelea na uchunguzi”

“Kipindi munafika katika eneo la tukio waandishi wa habari walikuwa wamefika?”

“Hapana meja ila watu kadhaa ndio walikuwa wameanza kufika eneo la tukio”

“Wahusika mumeweza kuwajua?”

“Tunaongeza juhudi katika kuwafwatilia na ninaimani kwamba tukiwafahamu tutawashuhulikia”

Tukafika katika chumba cha kuhifadhia maiti, maiti ya kwanza kuonyeshwa ni mtoto wa Yemi ambaye nilimuona picha yake kwenye simu ya mama yake. Ni mtoto mzuri sana kisura japo ni wa kiume ila ni mzuri sana na amebarikiwa kuchukua sura ya mama yake.

“Ni kijana mdogo sana”   

Meja alizungumza huku akimtazama mtoto wa Yemi.

“Yaaa, kifo chake kipo mikononi mwangu”

 

“Hapana Dany, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu ila waliweza kutuwahi?”

“Najua meja, ila ukweli ni kwamba huyu mtoto hakustahili kufa, ni lazima nifanye jambo kabla ya kumzika huyu mtoto”

“Vijana wangu wanaendelea kufwatilia wakipata muhusika basi tutajua ni kitu gani cha kufanya”

“Na Yemi nyumbani anasubiria kumuona mwanaye tutafanyeje katika hili?”

Meja akashusha pumzi nyingi huku akinitazama usoni mwangu.

“Tutatakiwa kutumia akili kubwa sana katika hili”

“Akili gani?”

“Mimi nitajua cha kumueleza nina imani ananiamini sana”

“Tujartibu katika hilo, ila sidhani kama harusi itafungwa kabla ya kumuona mwanaye”

 

“Kila jambo niachie mimi Dany”

“Mkuu tumepata sehemu ya wahusika ambao wamesababisha mauji ya watu wetu”

“Mume weza kuwafahamu ni watu wan chi gani?”

“Hapana mkuu ila tumeweza kufahamu ni wapi gari lao lilipo”

Kijana huyu wa kimarekani alizungumza na meja.

“Twende tukawavamie sasa hivi”

Nilizungumza huku nikimtazama meja usoni mwake.

“Dany……”

“Meja usinichukulie kama mgeni wa heshima ninaimani unaijua. Suti hii niliyo ivaa isinifanye nibadilike uahalisia wangu. Mimi nimefuzu mafunzo mengi ya kijeshi unajua niliweza kuiangusha kambi ya Al-Shabab na wewe ulishuhudia juhudi zangu nilizo zifaya. Tafadhali meja ninakuomba uniruhusu katika hili”

 

Nilizugumza huku machozi ya hasira yakinimwagika usoni mwangu, japo ni aibu mwanaume kulia mbele ya mwanaume mwenzake, ila kwangu sikuhitaji kulitilia maanani.

 

“Sawa Dany mpatie bastola”

Meja alimuambia kijana wake, akanikabidhi bastola nikaichomeka kiunoni mwake kisha tukatoka hapa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Safari ya kuelekea katika sehemu walipo jificha watu walio husika na kifo cha mototo wa Yemi ikaanza. Tukafanikiwa kufika katika jengo moja, tukawakuta vijana wengine wa meja wakiwa wamesha imarisha ulinzi wa kuingia katika eneo hili. Vijana wa meja wakaanza kutuonyesha ramani ya jengo hili kupitia laptop.

“Ndani ya jengo kuna watu sita na hao ndio walio weza kufanya mauaji mkuu”

“Hakikisheni kwamba tunawakamata wakiwa hai”

“Sawa mkuu”

 

Vijana wa meja wakaanza kusonga mbele huku mimi na meja pamoja na mlinzi wake mmoja tukibaki kwenye gari.

“Nahitaji kuingia ndani meje”

“Dany tulia nina waamini vijana wangu, nina uhakika watakwenda kukamilisha hii kazi kiumakini sana.”

“Sawa meja”

Vijana hawakuchukua muda sana wakatupa ishara ya sisi kuweza kuingia ndani, kwa haraka tukakimbilia ndani na kukuta kundi la vijana likiwa limewekwa chini ya ulinzi.

“Muna uhakika kwamba hawa ndio wamefanya mauaji?”

Meja alizungumza huku akiwatazama vijana hawa wa kiafrika, nyuso zao zinaonyesha kwamba hawana uwezo kabisa wa kufanya tukio ambalo wamelifanya.

 

“Ndio mkuu hawa ndio wa husika. Wana silaha za kutosha sana”

Nikachomoa bastola na kuvututa mmoja wa hawa kijana.

“Ni nani aliye waagiza?”

Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikimtazama kijana huyu usoni mwake.

“Sijui unacho zungumza”

Kijana huyu alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Kwa taaluma yangu ya kuwafahamu watu nikajua kabisa kwamba huyu kijana ananidanganya. Nikampiga kwa kitako cha bastola hii kwenye sikio lake na kumfanya jamaa huyu akianguka chini na kulia kwa uchungu.

“Dany huyo hana la kuzungumza, vijana wenyewe hawa ninawaona kama wavuta bangi”

 

“Hapana meja wanatutania hawa. NINIANI ALIYE KUAGIZAAAA”

“Sijui mimi maisha yangu ya shida sifahamu ni kitu gani unacho kizungumza”

“Sioni sababu ya nyinyi kuishi”

Nikampiga risasi ya kichwa kina huyu nikamgeukia kijana wa pili naye nikampiga risasi ya kichwa pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote. Nikampiga risasi kijana wa tatu, kabla sijampiga risasi kijana wa nne akaniomba nimsamehe kwani anakwenda kuzungumza ukweli.

“Nazungumza nazungumza ukweli”

“Ni nani aliye watuma”

“Ni madam”

“Madam madam gani?”

“Madam Hawa, mke wa raisi wa Marekani”

Meja akanitazama kwa macho ya mshangao, kwani sote hapa tunamfahamu vizuri Hawa kwani alikuwa ni msichana mwema sana kipindi nipo naye.



“Hawa, Hawa ndio alio waagiza?”   

Niliendelea kuwauliza kwa sauti ya ukali huku nikimtazama kijana huyu aliye toboa siri ambayo tayari imesha wagarimu wezake watatu uhai wao.

“Ndio, alitumbia kwamba tumue mtoto mara baada ya kufika hapa Madagascar”

“Alijuaje kama mtoto anakuja hapa Madagascar?”

“Sijui, sisi tulipewa kazi na tumeikamilisha mkuu”

Kijana huyu alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

 

“Meja nina imani kuna mtu anatoboa siri katika hili”

“Nitalifanyia upelelezi wakimya kimya kuhakikisha kwamba ninamfahamu ni nani ambaye alitoboa siri katika hili”

“Nina ombi jengine meja”

“Ombi gani?”

“Ninaihitaji kwenda Mosscow Urusi”

“Mossow?”

“Ndio meje, sina muda wa kupoteza katika hili kwa maana raisi wa Marekanai hadi sasa ninavyo zungumza yupo inchini Urusi na nina imani kwamba hiyo ndio nafasi yangu ya pekee kwa mimi kuweza kumuaa Donald Bush pamoja na Hawa kwani siwezi kumsamehe katika hili alilo lifanya”

 

“Dany kumbuka ulinzi ambao umeimarishwa katika eneo hilo unalo taka kwenda ni mkubwa sana na kuna watu makini sana. Huto toka kabisa endapo utakwenda”

“Hilo kwangu sijalishi meja, hii ndio kazi yangu ya mwisho. Ninakuomba unipe baraka zako za mwisho”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama meja usoni mwake. Akaanza kutoka katika hichi chumba ambacho tayari tumeweza kugundua ukweli wa wahusika walio sababisha tukio la mauaji la mtoto wa Yemi.

“Meja najua hili  ambalo  ninakwenda kulifanya hata kwako litakuwa na nafasi kubwa, ninakuomba niweze kwenda kuifanya hii kazi sinto weza kukaa hapa na kuendelea kuyaona machozi ya Yemi yakimwagika mbele yangu na nikiwa sina msaada wowote kwake ikiwa mimi ndio nimepelekea matatizo haya yote kwa mwanae”

“Unahisi ni kwa nini Hawa amemua kufanya mauaji ya mtoto wa Yemi?”

 

“Meja ukiniuliza hivyo utakuwa unakosea kwa maana mimi na wewe sote tupo hapa na isitoshe walifahamu vipi kama mtoto anakuja Madagascar na hadi akauwawa hapa?”

Meja akakaa kimya kwa muda kisha akanishika bega la mkono wangu wa kushoto.

“Ninakuruhusu Dany katika hili ninajua ni mangapi ambayo yaliweza kukupata katika maisha yako na yote hayo yametokea kwa dhuluma na husda za watu walio kuzunguka. Ninakuomba hakikisha kwamba unakuwa hai kwa manaa bado hujamalizana na K2”

“Shukrani meja kwa kuligundua hilo”

“Yaa ninajua ni kitu gani ambacho kipo ndani ya moyo wako”

“Ninakuomba niondoke pasipo mke wangu kuweza kufahamu”

 

“Hapana Dany hilo linaweza kuwa kosa kubwa sana litakalo kugarimu kwenye maisha yako yote”

“Kivipi meja, kwa maana hii ni kazi ambayo ninatakiwa kuifanya kikamilifu”

“Ngoja kwanza nifwatilie leo kwamba raisi wa Marekani atakaa kwa muda gani Urusi kisha tutapanga mapango mzima wa mauaji yake na wewe ndio utayakamilisha kwa mkono wako wewe mwenyewe”

“Sawa meja”

“Maandalizi ya harusi yaendelee kama kawaida, jikaze kiume na mke wako asifahamu kitu chochote hii itabaku kuwa siri kati yangu mimi na wewe”

 

“Nimekuelewa”

“Mkuu”

Mmoja wa vijana wa meja alizungumza huku akifika katika eneo hili tulilo  simama.

“Ndio”

“Kuna hichi kitu unatakiwa kukiona hapa”

Jamaa huyu akamkabidhi meja simu aina ya iphone six, akatazama kwa muda kisha uso wake kidogo ukaonekana kujawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Dany kazi yako nina imani itakuwa raisi sana”

“Kwa nini?”

“Baada ya siku mbili raisi Donald na mke wake wanaelekea nchini Tanania kwa ziara yasiku mbili na mwenyeji wao atakuwa ni raisi K2 na hii ni taarifa kutoka ikulu ya Marekani”

Meja akanikabidhi simu aliyo ishika, nikasoma maelezo haya yanayo onyesha ziara hii ya raisi Donald Bush pamoja na Mke wake.

 

Furaha ikaanza kutawala moyoni mwangu kwani kazi hii inakwenda kuwa raisi kwangu kwani ninaifahamu Tanzania vizuri sana kuliko hata nchi yoyote ambayo nimeweza kwenda.

“Tuelekee madukani sasa kutafuta pete ya mke wangu”

Nilizungumza kwa sauti iliyo jaa msisitizo, meja akakubaliana nami. Tukaondoka eneo hili, siku nzima hii tukaitumia katika kufanya manunuzi ya harusi ambayo itahudhuriwa na watu wachache sana ila ni harusi ya kifahari sana. Nikamnunulia Yemi pete ya dhahabu yenye garama kubwa sana, pamoja pia nikamnunulia na mkufu wenye thamani kubwa sana.

“Dany”

 

“Ndio meja”

“Nimeweza kukutana na vijana wengi, na nimefundisha vijana wengi ila sijawahi kuona kijana mwenye kipaji kama wewe”

“Kipaji cha nini meja?”

“Laiti ingekuwa ni mtu mwengine wa kawaida kawaida tu ambaye aliamua kuingia jeshi kwa ugumu wake wa maisha basi hadi sasa hivi sidhani kama angekuwa hai hapa duniani”

“Una maanisha nini kuzungumza hivyo meja?”

“Nina maanisha kwamba umepitia maisha magumu ambayo hata mimi na uzee huu sikuweza kuyaptia. Umeweza kuimili mikiki mikiki mingi sana kwenye haya maisha, ninakuomba sasa hakikisha kwamba unaimaliza hii kazi, hakikisha hawa watu watatu wanafia kwenye mikono yako. Chochote kitakacho tikea nipo nyuma yako nitakusaidia, iwe kifedha, kimali au hata kuyagarimu maisha yangu basi ninaweza kufanyaa hivyo”

 

Meja alizungumza kwa msisitizo huku tukiwa ndani ya gari tunarudi katika jumba la meja.

“Ninashukuru sana meja, natambua baada ya hii kazi dunia nzima itakuwa inanitafuta mimi”

“Hilo nitalifanyia uangalizi kikubwa ni kumuoa Yemi na kunza maisha yenu mapya mbali sana na Afrika”

“Sawa meja.”   

Tukafanikiwa kufika nyumbani salama salim, nikamkuta Yemi akiwa amekaa sebeleni pamoja na Martin anatazama filamu. Yemi akanifwata na kunikumbatia kwa furaha sana, akanipokea begi kubwa kiasi ambalo lina gauni lake la harusi pamoja na vitu kadhaa. Tukaelekea chumbani kwetu na akanza kufungua begi hili huku furaha ikiwa imemtawala sana.

 

“Waooooo mume wangu umejuaje kama ninapenda magauni ya aina hii”

Yemi alizungumza kwa furaha sana huku akililaza gauni hili kitanani.

“Yaani mume wangu umejuaje ninapenda magauni ya aina hii”

“Kweli?”

“Yaa kweli yaani hata kwenye mitindo yangu ninayo buni huwa ninajisikia furaha kuunda magauni ya aina hii, ngoja kwanza mbona kama lina chata ya kampuni yangu”

Yemi alizungumza huku akichukua kikaratasi kidogo na kukisoma

“Mume wangu ni kampuni yangu kumbe bidhaa zangu zinafika hadi huku”

“Yaaa, alafu wala sikujua nilipo kuwa ninanunua”

Furaha ya Yemi ikazidi kutawala baada ya kutoa pete mbili za ndoa ambazo tutavishana wakati wa kuoana siku ya kesho.

“Yaani mume wangu natamani hata ndoa yetu tufinge hata sasa hivi ili tuwe mume na mke”

 

“Usijali mke wangu, Mungu ni mwema kesho itafika kikubwa ni ulinzi wake”

“Amen, vipi umemuuliza shemeji juu ya safari ya mwanangu?”

“Yaa nilimuuliza ila kidogo ndege yake ilipata itilafu ikawabidi kutua nchini Senegal, kwa matengenezo zaidi”

Nilizungumza uongo huku nikifahamu kila kitu kinacho endelea

“Ahaaa, kwa nini sasa wasipande ndege nyigine ili mwanangu awahi”

“Kwa ajili ya usalama, si vizuri kwa mtoto kupanda ndege nyingine, kwa maana nina imani watakuwa wanafwatiliwa si unajua kwamba ametolewa mikononimwa Wamarekani ambao hawahitaji kushindwa na lolote”

“Kweli, ila akiwahi sawa asipo wahi pia sawa, kikubwa yupo salama”

 

“Ni kweli mke wangu. Jaribu basi gaini nione kama nimepatia kununua au laa”

Nilizungumza huku nikijaribu kujenga tabasamu  usoni mwangu, Yemi akaanza kuvua nguo alizo vaa kisha akavaa gauni hili, nikamsaidia kufunga kamba ndefu  zilizopo nyuma ya hili gauni. Kusema kweli sijakosea katika kuchagua gauni hili kwa maana limependeza sana Yemi.

“Yaani kama ulinijaribisha mume wangu, hujakosea kabisa”

“Yaa ila ni mali ya kampuni yako nina imani kwamba watakuwa wametengeneza mahususi kwa ajili yako”

“Ni kweli yaani natamani hata kualika marafiki zangu kuja kusherekea hii harusi yangu ila ndio hivyo ni ngumu, umehitaji iwe harusi ya watu wachache”

 

“Ni kweli mke wangu ila ulihitaji kuwaalia kina nani?”

“Ahaa hata tukisema tuwaalike, hawawezi kufika muda umesha kwenda. Ila kuna rafiki yangu mmoja ningetamani sana awepo kwenye harusi yangu sema nimepoteza mawasiliano naye”

“Anaitwa nani?”

“Hawa yaani huyo kipindi tunasoma tulipanga kualikana kwenye harusi zetu sema ndio hivyo maisha yameingiliana”

‘Laiti ungejua alicho kifanya Hawa wala usinge zungumza hivyo mke wangu’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama Yemi usoni mwake. Nikamvalisha mkufu  nilio mnunulia na kumfanya azidi kujawa na furaha.

“Mke wangu nina kuja mara moja”

“Unaenda wapi?”

“Kuzungumza na meja”

“Njoo unisaidie kufungua hivi vijikamba huku mgongoni”

Nikafanya kama alivyo niagiza Yemi, nikamfungua vimikanda vya hili gauni kisha nikatoka humu chumbani, nikamkuta meja akiwa amekaa sebleni na Martin wakiendelea kuzungumza  mambo mawili matatu.

 

“Meja ninakuomba”

Taratibu meja akasimama na kunifwata sehemu nilipo simama.

“Nimezungumzana na mke wangu, na nimemueleza kwamba ndege walio yapanda watu wako imeharibika na imetua nchini Segegal, ili kutia msisitizo zaidi katika hili ninakuomba umueleze hivyo na uwaambie kwamba ndege inaendelea kufanyiwa marekebisho na hawawezi kupanda ndege nyingine kwa ajili ya usalama na msako wanao ufanya Wamarekani”

“Hilo halina shida, ila anaonekana kuhisi chochote?”

“Hapana, ana furaha tu ya kujiandaa na harusi yetu”

 

“Sawa nimekuelewa, hapa nimekodisha hoteli moja ipo kwenye kisiwa cha pembeni na hapo ndipo ndipo itakapo fanyika harusi yenu”

“Meja mbona umeingia garama kubwa sana katika hili?”

“Dany ukiachilia mbali kwamba wewe ni rafiki yangu wa karibu, ila ni sawa na mwanangu, sina mtoto wa kuweza kumfanyia haya yote na isitoshe nina miliki kiasi kikubwa sana cha pesa, kwa hiyo hilo wala lisikumize kichwa”

“Ila meja kuna mambo mengine unanifanyia hadi najihisi aibu kwa manaa naona sina uwezo wa kufanya na mimi mwenyewe”

“Uwezo unao na ninajua kwamba una utajiri mkubwa sana wa baba yako ila bado hujauweka mikononi mwako”

“Unafahamu chochote kuhusiana na baba yangu?”

“Ndio nina fahamu mengi sana kuhusiana na familia yako, niliamua kufwatilia familia yako baada ya kuweza kukufahamu”

 

“Umegundua kitu gani kwa maana hadi dakika ya mwisho K2 aliniambia kwamba familia yangu ipo hai na yeye ndio mtu wa pekee ambaye anafahamu ni wapi familia yangu ilipo?”

“Hapana amekudanganya na yeye ndio muhusika mkuu wa mauaji ya famili yako na kikosi chake cha wasichana anacho kimiliki, ninakuhakikishia kwamba nitakwenda kukivunja siku si nyingi”

“Shukrani sana meja”

“Karibu tutazame filamu”

Meja alizungumza hukua kielekea kwenye sofa, nikaitazama filamu hiyo, ila kutokana si mpenzi sana wa kutazama filamu ikanibidi kuwaaga na kurudi chumbani. 

 

“Dany kusema kweli ninakupenda, ninakupenda kutoka moyoni mwangu. Sijui ni kwa nini nilishindwa kukufahamu siku zote za maisha yangu”

Yemi alizungumza huku akinifwata sehemu nilipo simama, akanikumbatia huku mikono yake akiiweka begani mwangu.

“Ninakupenda pia mke wangu, kila jambo linakuja na wakati wake. Kuna wakati wa furaha na wakati wa kulia, wakati wa kupata na wakati wa kupoteza, kwa hiyo kila kitu mke wangu kinakuja kwa mpango wa Mungu”

“Amen mume wangu, ila leo naona neo la Mungu lipo moyoni mwako au ndio harusi?”

Yemi alizungumza katika hali ya utani, nikajikuta nikicheka tu, nikamnyanyua taratibu na kuanza kumzungusha ili mradi nitengeneze furaha ambayo hato weza kunistukia au kustuka kama kuna jambo lolote baya ambalo linaendelea.

“Utaniangusha bwanaaaa Danyyyyy nishusheeee nahisi kizunguzunguuuu mwenziooo”

“Badooo”

Niliendelea kuzungumza huku nikiendelea kumzungusha Yemi, kisha tukajirusha kitandani huku sote tukiwa tumetawaliwa na furaha kubwa sana.

 

“Sijawahi kufurahi na mwanamke kwa namna hii, nina imani kwamba wewe ndio mke wangu sahihi”

“Kweli mume wangu?”

“Ndio mke wangu, yaani ninajisikia furaha sana kuwa nawe”

“Hata mimi mume wangu, ila ninaomba nikuulize swali?”

“Ni ulize tu mke wangu?”

“Mimi ni mwanake wa ngapi kwako?”

Swali la Yemi likanifanya nigune kimoyo moyo kwa maana nina mlolongo wa wasichana wengi ambao nilitembea nao, na laiti nikimjibu idadi kamili ya wasichana nilio tembea nao kimwili nina unakika kwamba ni lazima Yemi atapata wasiwasi na mimi.

 

“Mbona kimya mume wangu, wewe nijibu tu, kama mimi ni wa pili au watatu?”

‘Hata kwenye thelathini bora haupo’

Nilijibu kimoyo moyo huku nikimtazama Yemi usoni mwake.

“Wewe ni wa tatu?”

“Kweli mume wangu?”

Nilijikaza kujibu uongo kwa Yemi

“Ndio”

“Nakupenda, nakupenda, nakupenda sana mume wangu. Wewe ni mwanaume wa pili na utakuwa ni mwanamke wa mwisho kwenye maisha yangu”

 

“Asante mke wangu”

Siku hii ikatawaliwa na furaha, hadi tunaingia kitandani kulala furaha imetawala. Asubuhi na mapema, wasichana maalumu wanao shuhulika na maswala ya urembo wakafika katika jumba hili la meja na wakaanza kumshuhulikia Yemi. Na mimi nikaletewa kinyozi mmoja ambaye meja ameniambia yupo vizuri katika unyooaji nywele kwa wanaume.

Shamra shamra za harusi hii hazikumuacha nyuma Martin kijana wangu aliye bahatika kutoka mikononi mwa jeshi la Marekani ambao wameteketeza kambi nzima ya boko haramu. Martin ndio msimamizi wa harausi kwa upande wangu huku Yemi naye akiwa na msimamizi wa kike ambaye aliletwa na meja.

 

Tukatumie helicopter kuelekea katika kisiwa kidogo ambacho kina hoteli moja tu ya kufahari, tukafanikiwa kufika salama katika hoteli hii ambayo tumekuta umeandaliwa vizuri sana na ulinzi mkali wa vijana wa meja unaendelea kuimarishwa kila kona.

Wahuzuriaji wa harusi hii ni watu wachache sana ambao hawazidi hata kumi na wote wanaonekana ni matajiri wakubwa sana kwani ni marafiki wa meja. Mchungaji hakuwa na mahubiri marefu juu yetu alicho kifanya ni kuingia katika ibada ya kufungisha ndoa hii. Tukavishana pete na Yemi na kuwafanya watu wote kufurahia. Tukakumbatia kwa nguvu na Yemi huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Gafla kipande kimoja cha goroa la hoteli hii kikalipuka kwa bomu jambo lililo wafanya walinzi wote wa meja kukimbilia katika eneo tulipo na kuanza kututoa katika eneo hili kwa haraka sana kwani hatujui ni nani ambaye amefanya shumbulizi hili.


 

Heka heka za kututoa katika hili  eneo zikaanza huku walinzi hawa wakiwa makini sana. Kazi yangu ni kuhakikisha kwamba mke wangu anakuwa salama hata kama kutatokea jambo baya zaidi ila ni lazima kumuokoa Yemi.

“Huku huku”  

  

Mlinzi mmoja  alizungumza, na tukaanza kukimbilia ndani ya hoteli hii, huku meja na Martin wakiwa ni miongoni mwetu. Tukaingia kwenye moja ya chumba, tukakuta ngazi za kwenda chini, tukazidi kushuka chini huku tukiwa kasi. Tukakuta boti maalumu iliyopo katia eneo hili la chini ya hii hoteli ambayo inatumika kwa ajii ya dharura ya kutorokea, endapo kunatokea uvamizi kama huu.

“Ingieni kwenye hii boti itawapeleka moja kwa moja hadi nyumbani”

Mlinzi mmoja alizungumza, anaonekana yeye ndio mkuu wa hichi kikosi maalumu cha meja.

“Sawa hakikisheni munaniletea ripoti ya nani aliye sababisha hili shambulizi”

Meja alizungumza huku uso wake ukiwa umefura hasira hadi amekuwa mwekundu kiasi kwenye uso wake.

“Sawa mkuu”    

 

Wakaingia walinzi wawili na wengine wakabaki na kuondoka katika hili eneo. Mlinzi mmoja akawasha hii boti ya mwendo wa kasi na kuanza kuondoka katika hili eneo la hii hoteli ambalo lina maji ya bahari tukatoke katika usawa wa bahari. Meja ndani ya boti hii hakutulia kabisa, mara asimamae mara akae, mara asunye hii yote ni kuonyesha ni jinsi gani amekasirika. Muda wote Yemi usoni mwake machozi yanamtiririka, jambo lililo nifanya nimkumbatie pasipo  kuzungumza kitu chochote kwa maana ni jambo ambalo hakuna hata mmoja wetu ameweza kulitegemea.

 

Tukafika katika ukingo wa bahari lilipo jumba la meja, tukashuka sote na kupokewa na walinzi wengine, tukaingia kwenye gari lililo tufikisha moja kwa moja hadi kwenye jumba hili kwani kuna umbali kiasi. Yemi hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kukimbilia chumbani na kunifanya na mimi kuelekea chumbani huko. Nikamkuta Yemi akiwa amelala kwenye kitanda huku akiendelea kulia kwa uchungu sana.

“Kwa nini, kwa nini sisi kila siku, hadi leo siku ya harusi badooo wanatundama jamaniii akhaaaa”

 

Yemi alilia kwa uchungu huku akikipi piga kitanda. Nikamnyua na kumkalisha kitako, nikaka pembeni yake na kumshika mikono yake yote miwili huku kigugumizi cha kuzungumza kikiwa kimenitawala mdomoni mwangu.

Dany mume wangu ni lini tunakuwa na furah, lini tunakuwa na amani jamanii”

“Ye….yemi”

Nilizungumza huku machozi ya hasira yakianza kunichuruzika kwenye mashavu yangu.

“Ndio mume wangu…….”

“Nitaitengeneza furaha ya familia yangu, nitahakikisha kwamba kila jambo kwenye maisha yetu linafikia mwisho sasa”

 

“Kwa nini jamani mume wangu, hawatuachi hata tukashangilia siku moja. Moja hii ya harusi akhahaaa”

Yemi aliendelea kulalamika kwa uchungu sana. Nikikipeleka kiganja changu cha mkono wa kulia kwenye shingo yake, taratibu nikakaanza kumnyonya mdomo wake, japo ana hasira na uchungu ndani yake ila Yemi hakuwa na hiyana kwangu, akanipa usihirikiano mzuri wa kunyonyana midomo yetu huku sote tukiwa katika hali ya huzuni na hasira ndani yake.

“Nitaua watu wote wanao niandama katika maisha yangu. Ninakuomba mke wangu ukubaline nami katika hili”

Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikimtazama Yemi usoni mwake, Yemi machozi yakaendelea kumtiririka mashavuni mwake.

 

“Nipo tayari mume wangu waue woteee”

Baada ya Yemi kuzungumza maneno hayo nikamvutua tana kichwa chake na tukaanza kum midomo yake, safari hii  ukajawa na hisia kali za mapenzi,........Tukajikuta tukimaliza mzunguko wa kwanza huku wote tukiwa tumechoka sana. Nikashuka kitandani huku nikipepesuka na koo langu likiwa limekabwa na kiu  kikali cha maji.

 

“Ahahaa….Yemi leo umekula nini mke wangu”

Nilizungumza huku nikielekea bafuni, nikafungua maji ya bomba na kuanza kuyanywa taratibu kuhakikisha kwamaba nina kata kiu cha maji kilicho nitawala kooni mwangu.

“Hasira mume wangu, yaani hata mimi mwenyewe ninajishangaa”

 

Yemi alizungumza huku akinikumbatia nyuma yangu, tukajitazama kwenye kioo kilichopo mbele yetu.

“Namshukuru Mungu kwa kuweza kunipatia mwanamke kama wewe”

“Hata mimi mume wangu, ninakupenda sana Dany, japo ninakutana na mambo mengi ya kuniumiza kichwa changu, ila kusema kweli  una nifurahisha na kunifanya nijihisi mimi ndio mwanamke bora kuliko wote ulimwenguni. Umenipa dunia yangu peke yangu, ninakuomba sana Dany wangu uhakikishe kwamba dunia yangu hakuna mtu anaye weza kunipokonya”

Taratibu nikageuka, na kumtazama Yemi huku mikono yangu nikiipitisha kiunoni mwake.

 

“Nakuahidi mke wangu, nitahakikisha kwamba ninakulinda hadi mwisho wa maisha yangu”

“Asante mume wangu”

“Na kitu kingine ninahitaji kueleka Tanzania katika siku mbili hizi”

“Tanzania!!?”

“Ndio mke wangu, huko ndipo nyumbani kwetu sasa, hatuwezi kuendelea kuishia kwenye nchi hii wala kuishi kwa mtu ikiwa kwetu kupo”

“Nipo tayari kukufwata popote utakapo kwenda Dany wangu, utajiri wangu wote bila ya wewe si kitu kwangu, nina kupenda sana Dany wangu”

“Ninakupenda pia mke wangu kipenzi, ninakuomba usiniache peke yangu”

“Siwezi mume wangu, na hicho kitu wala usije ukakifikiria hata siku moja kama kinaweza kutokea kwneye maisha yangu”

 

Tukakumbatia na Yemi, kisha taratibu akayafungulia maji ya bomba la mvua yaliyo anza kutitirika kwenye miili yetu. Tukasimama kwa dakika zaidi ya tano huku tukiwa tumekumbatiana kisha taratibu tukaanza kuoga. Tukatoka bafuni huku huku tukiwa tumeshikana mikono               

“Yaani simaini kama sherehe yetu imeisha naamna hii”

Yemi alizungumza huku akijitupa kitandani.

“Kikubwa Mungu ametulinda na mpango mbaya ambao waliupanga juu yetu”

“Kweli mume wangu”

“Ngoja nikafwatilie tujua kwamba ni kina nani walipanga kutuangamiza?”

 

“Sawa hapa miguu yangu yote imechoka, leo umejua kunikoj...** hadi sina hamu kabisa”

“Huo mzunguko wa kwanza wa pili tutaendelea usiku muda wa kulala”

“Mmmmm utaniua mwenzio”

“Hufi”

“Ila chamoto nitakiona eheee”

“Yaa”

“Sawa mume wangu”

Nikavaa nguo zangu na kutoka chumbani kwangu, nikafika sebleni na kumkuta meja akiendelea kunywa mzinga wa pombe kali.

“DANNYYYYYYYYYYYYY…………”

Meja alizungumza huku akinyanyua mtungi huo juu.

“Karibu rafiki yangu”

Meja aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ulevi huku akinitazama usonimwangu. Nikaka kwenye moja ya sofa huku nikimtazama.

 

“Kinywaji Dany”

“Hapana meja nipo vizuri”

“Samahani bwana rafiki yangu, hawa washenzi wamevuruga harusi yetuu bwana”

“Usijali meja natambua mambo kamaa hayo kwenye maisha yangu ni jambo la kawaida.”

“Kweli, ila hawa wana haramu kama ni wao hata mimi nitashiriki katika kuwaangamiza, potelea pote na mimi nikiwa gaidi”

“Meja aliendelea kuzungumza kwa sauti ya ulevi.

“Hapana meja, acha nishuhulike nao mimi mwenyewe”

“Njoo njoo”

 

Meja alizungumza huku akinyanyuuka kwenye sofa, akayumba kidogo ila akajihimili huku akiwa ameendelea kushika chupa yake.

“Kuna vitu vingi ninahitaji kukuonyesha rafiki yangu”

Meja alizungumza huku tukielekea nje, tukatoka na kuendelea kutembea kwenye jumba hili la kifahari.

“Kwenye maisha yangu siku zote niliishia kwa ajili ya kutafuta amani, niliishia kwa ajili ya kuwa mtu mwema, ila siku zote kwenye maisha maadui nao hujitokeza kama ilivyo kwenye maisha yako”

 

Nikaka kimya huku nikimsikiliza meja anacho kizungumza. Tukaingia katika moja ya chumba ambacho kipo katika jengo la nje, chumba hichi kimetawaliwa na michoro mikubwa iliyo jengewa kwa fremu za dhahabu.

“Kipindi nilipo kuw amdogo wazazi wangu waliipenda sana hii michoro na waliweza kuiweka kwneye jumba letu Calfoni nchini Marekani, na michoro hii unavyo iona kila mmoja una maana yake”

Meja akapiga fumba jingine la pombe kali kisha akainyooshea kidole picha moja. Kabla hajazungumza chochote simu yake ikaita, akaitoa mfukoni na kuipokea.

“Halooo”

“Wapo wangapi?”

“Waleteni hapa nyumbani”

Meja akakata simu na kunigeukia.

“Tumewakamata walio sababisha mlipuko wa pale hotelini, na wanaletwa hapa nyumbani”

“Wapo wangapi?”

“Wapo watatu”

 

Meja alizungumza huku akitoka chumbani humu, hata hamu ya kuendelea kunisimulia michoro hii aliyo nionyesha ikaishia hapo. Moja kwa moja tukaeleka katuka kiwanja cha helicopter ambapo ndipo meja alisema kwamba watu hao wanaletwa hapa.

“Watanitambu”

Meja alizungumza huku akiendelea kusunya sunya tu, haukupita muda mrefu helicopter ikatua katika hili eneo. Wakashushwa watu watu watatu ambao wamefunikwa nyuso zao na vigunia vidogo vyeusi. Meja akawatazama watu hawa, kisha akatoa amri kwamba wapelekwe kwenye chumna cha mateso. Watu hawa wakanza kupelekwa haraka haraka huku mikono yao ikiwa imfungwa na kamba ngumu ambazo sio rahisi kwa wao kuweza kuzifungua.

 

“Dany”

Nilimuona Yemi akija eneo letu huku akiwa anakimbia huku akionekana kuonekana ana wasiwasi mwingi sana usoni mwangu.

“Ni kitu gani kinacho endelea mume wangu”

Yemi alizungumza baada ya kutukaribia.

“Shemaji hakuna tataizo, ila tumewapata wale walio sababisha mlipuko kwenye harusi yenu na ndio wale wanao pelekwa kule”

Meja alinisaidia kujibu swali la Yemi alilo nikuliza. Yemi akawatazama watu hao, kisha akaachia msunyo mkali huku akionekana kukasirishwa sana.

“Nini?”

Nilizungumza huku nikimshika mkono Yemi.

“Wamenistua na mlio huu wa helicopter nikadhani tumevamiwa tena”

 

“Hapa kwangu shemeji hakuna ambaye anaweza kuingia, ila ulinzi kila sehemu”

“Naombeni na mimi niwaone hawa watu walio vuruga harusi yangu”

“Mke wangu……”

“Dany mimi pia ni muathirika katika hili, umeona ni uchungu gani ambao nimeupata kwa tukio lile”

Yemi alizungumza kwa msisitizo na kutufanya mimi na meja kumtazama kwa sekunde kadhaa, meja akatingisha kichwa akishiria kukubaliana naye ashiriki nasi kwenda kuwaona hawa watu.

“Sawa”

Niliitikia kinyonge kwani sina sababu ya msingi ambayo ninaweza kumzuia Yemi. Tukaanza kutembea kuelekea katika chumba walicho ingizwa watu hawa. Hatukuchukua muda mwingi kufika katika hichi chumba, tukaingia ndani na tukawakuta watu hawa wakiwa wamefungwa mikono yao huku wakiwa wamening’inizwa juu juu.

 

“Wavueni hivyo vitatambaa”

Meja alizungumza huku sote tukiwa tunawatazama watu hawa, akafunuliwa mtu wa kwanza, kwangu sura yake yake ni ngine, akafunuliwa mtu wa pili naye sura yake ni ngeni, ila nilipo yageuza macho yangu kwa Yemi akaonekana kama anawatambua kwani sura na macho yake yanaonyesha vizuri kwamba anawafahamu watu hawa. Mtu wa tatu kufuniliwa sasa hata mimi nikastuka kwa manaa huyu aliye funuliwa ni mume wa Yemi ambaye mara ya mwisho waliachana kwa ugomvi mkubwa sana ambao hata mimi nilishiriki katika kumpiga vibaya sana na kumpokonya mke wake ambaye nipo naye hivi sasa.              




“Wee mwehu…..kk…umbe ndio umekuja kuvuruga harusi yangu”

Yemi alizungumza kwa kigugumizia huku akimsogelea mume wake huyu wa zamanai. Yemi akaongeza kasi na kumfikia, Yemi kwa harisa akaanza kumpiga vibao vya mashavuni huku akimtukana matusi mfululizo jambo lililo nifanya kwa haraka nimsogelee Yemi na kumtoa.

 

“Acha anipige hivi unahisi sijui kinacho endelea”

Jamaa huyu alizungumza kwa ukali huku akimtazama Yemi usoni mwake.

“Hata kama umejua kwamba ninaolewa, kwa nini uje kuvuruga harusi yangu, mimi na wewe mapenzi yalisha isha, nimepata mwanaume anaye niridhisha kuliko wewe”

Yemi aliendela kuzungumza kwa sauti hadi machozi yakaanza kumwagika mashavuni mwake.

“Acha ujinaga Yemi wanacheza na akili yako, unafurahi vipi ikiwa mtoto wetu yopo Mochari na amekufa kwa ajili ya huyo mwanaume?”

 

Macho yakatutika na tukabaki tumepatwa na mshangao mkubwa sana. Yemi akajitoa mikononi mwangu na kututazama mimi na meja kwenye nyuso zetu, nikatamani kuzungumza ila sijui hata nianzie wapi.

“Sijakuelewa unasema kwamba……..?”

“Mtoto wetu amekufa, na yupo mochwari hadi hivi sasa hivi ninazungumza. Unakuwaje na mwanaume ambaye amepelekea kifo cha mtoto wetu kwa mazambi yake?”

Mume wazamani wa Yemi alizidi kuzungumza maneno ambayo yalizidi kuniumiza ngumu. Nikastukia meja akimpita jamaa huyu chupa ya uso jambo lililo mfanya Yemi kupiga kelele za uchungu. Nikajaribu kumshika, Yemi akaitoa mikono yangu kwa nguvu huku akinitazama kwa jicho kali  sana usoni mwangu.

 

“Dany umenidanganyaa eheee”

Yemi alizungumgumza huku akinishika shati langu, na kulinyongorota maeneo ya kifuani.

“Ehehee Dany kwa nini unidanganyeeeee?”

Yemi akanisukumia hadi kwenye ukuta huku akiendelea kunikaba shiti langu, kusema kweli nguvu  zote zimenishia mwili mwangu, sijui hata nizungumze kitu gani kwa Yemi ambaye amekuwa na hasira kali kama samba jike aliye jeruhiwa katika zoezi la kuwakomboa watoto wake.

 

Yemi akanitandika ngumi ya tumbo iliyonifanya nijikuje huku nikisikilizia maumivu yake, akaninyanyua na kuniweka sawa.

“Nimeyatoa maisha yangu kwa ajili yako, nimetoa watu zaidi ya laki mbili kwa ajili yako na wamekufa kwa ajili yako nikijua nitakuwa na familia  bora na wewe leo hii umeamua kunisaliti, mwaanangu anakufa, unakaa kimya na kunifungisha ndoa nikirufahi nikujua mwanangu yupo sehemu salama kumbe unaniletea maswala ya kiku** na wewe”

Yemi aliendelea kuzungumza kwa hasira, kila ninapo jaribu kufikiria ni jambo gani ninaweza kuzungumza litakalo muweka Yemi katika mstari wa kueleweka na kuituliza hasira yake ila sina kabisa.

 

“Nimbie Dany mwanangu amekufaa eheeee”

Yemi alizungumza huku akinitingisha kifua changu.

“NIAMBIEEE WEWEEEEEEE”   

“NDIOOOOOO AMEKUFAA”

Nilizungumza kwa ukali huku akiniachia shati langu, akanitazama usoni mwangu kama mtu ambaye haamini kwa kile ambacho anakisikia. Akamgeukia mume wake wa zamani, kwa haraka akaanza kutembea hadi sehemu alipo fungwa, huku damu zikimwagika usoni mwake.

“Mfungueniiii”   

Yemi alizungumza kwa ukali, hapakuwa na mfanyakazi wa meja aliye weza kupokea amri ya Yemi.

“Nimesemamfungueni”       

“Hawawezi kukusikia pasipo amri yangu”

Meja alizungumza kwa sauti nzito hata ile sauti ya ulevi imemuaondoka sasa.

“Waambie hawa mende wako wamfungulie mume wangu la sivyo nitaua mtu”

 

Yemi alizungumza huku akiokota kipande cha chupa na kukishika mkono wake wa kulia. Meja akanitazama usoni mwangu, kwa ishara ya macho akaniuliza niwafungulie au laa. Nikamtazama Yemi usoni mwake,

“Wewe gaidi toa jibu, nanitaji mwanaume wangu afunguliwe, sio wewe mwanaume unayte taka familia yangu iishe kwa ajili ya matatizo yako”

“Yem…..”

Hata sikumalizia kuzungumza sentensi  yangu nikajikuta nikikwepa kipande cha chupa alicho kirusha Yemi na kikapiga ukutani. Nikamshuhudia Yemi akivua pete yangu ya ndoa niliyo mvisha masaa machache yaliyo pita na kunirushia miguuni mwangu jambo lililo mshangaza kila mtu humu ndani.

 

“Mimi na wewe basi, sikutaki Dany, wewe si mwanaume wa maisha yangu. Wewe ni gaidi, wewe ni muuaajiiii hufaiiii kuishi na mwanamke yoyoteee pumbavuuuuuu weweeeeee”

Taratibu nikachuchumaa na kuikota pete yangu huku machozi yakinitiririka usoni mwangu. Nikasimama na kumtazama Yemi usoni mwake. Taratibu nikaanza kusogelea huku nikiwa nimekazia macho, Yemi akabaki amesimama huku akinisubiria kufika sehemu alipo. 

 

Kitendo cha kumkaribia Yemi, akarusha kofi kwa mkono wake wa kulia, ila nikamdaka na kumshusha mkono wake chini.

“Huwezi kuvua peta yangu ya ndoa, ikiwa nilijaribu kwa uwezo wangu wote kuhakikisha kwamba wewe na mwanao munakuwa salama, nilijisalimisha mikononi mwa Wamarekani kwa ajili yako wewe na mwanao leo hii unaona kwamba msaada wangu hauna maana kwenye maisha yako eheee?”

 

Niliuliza kwa ukali huku nikimtazama Yemi usoni mwake.

“Nitolee sera zako za kisen** kujitoa kwako mimi kuna nihusu nini mimi eheeee?”

Yemi aliendelea kuzungumza kwa ukali. Nikamtazama mume wake huyu anaye enedeleka kuugulia maumivu ya uso wake ulio chanwa na mpasuko wa chupa iliyo tua usoni mwake.

“Siogopi kuua, na wala sihofii kuua na kama huyu msen** hapa ndio amekufa uvue pete yangu sasa nina muua”

Nilizungumza huku nikimuomba mlinzi mmoja wa meja bastola yake. Jamaa akachomoa bastola yake kiunoni na kunikabidhi, Yemi akanitolea macho huku akihema kwa hasira.

 

“Sikumuomba baba yako kuwa kiongozi wa kundi lake, sikukuomba wewe uwe mwanamke wake ila ni kwa ajili ya kufanya maamuzi yako ya kijinga ndani ya muda mchache baada ya kumfumania mume wako, nilitumwa kuwaua wewe na baba yako na huo uwezo nilikuwa nao na ningefanya ndani ya masaa machache tu. Ila nimakuacha leo  hii unavua pete yangu, unajua ni jisni gani ninavyo kupenda na nimeyatoa maisha yangu kwa ajili ya kusaidia mkund** wa baba yako na wako eheee. Hivi unahisi kwamba mimi ninawea kupigana na Marekanini, mimi nani? Osama Bin Laden, Gadafi eheeeeee?”

Nilzungumza kwa hasria huku nikiwa nimeishika bastola yangu, hasira niliyo nayo nina imani kwamba Yemi alisha wahi kuniona nayo siku ambayo alifahamu ukweli wa jina langu.

 

“Dany Dany”

Niliisikia sauti ya meja ikiniita nyuma yangu, nikageuka na kumtazama meja usoni mwake. Akatingisha kichwa akiniomba nisifanye kile ambacho ninahitaji kukifanya kwani yeye mwenyewe hajawahi kuniona katika hali kama hii.

“Maishani mwangu nimepoteza mtoto wangu, mama wa mtoto wangu, mama yangu mzanzi, baba yangu mzazi na mdogo wangu  wa kike na wote wamechinjwa leo hii unaona kifo cha mwanao kina thamani kubwa sana, kulilko damu za watu walio jitahidi kunifanya niwe Dany eheeee?”

 

Niliendelea kuzungumza kwa ukali hadi kukamfanya Yemi kutetemeka. Nikaishika pete aliyo ivua na kumnyooshea.

“Najua leo hii imevua pete mbele ya watu walio shuhudia jinsi nina kuoa, na niajua kwamba ipo siku utanisaliti mbele ya watu kwa ajili ya maamuzi yako ya kijinga. Chagua pete na mume wako mimi nitakuwa tayari kwa lolote”

“Dany Dany usifanye hivyo rafiki yangu?”

“Meja hapa hakuna mwanamke, acha afanye chaguo nipo tayari amesha niita gaidi unahisi kuna nini hapa?”

Yemi akanitazama usoni mwangu huku machozi yakimwagika, taratibu akamsogelea mume wake na kumkumbatia jambo lilio nistua hadi mimi moyoni mwangu, kwani ni maamuzi magumu aliyo yachuku Yemi.

 

“Ni bora niishi na mwanaume ambaye ni malaya kuliko kuliko kuishi na mwanaume gaidi na anaye hatarisha maisha ya familia yangu, kama kifo cha familia yako hakikuwa na thamani kwako ila kifo cha mwanangu kina thamani kubwa kwani si wewe uliye ibeba mimba yake na wala hujui uchungu wake”

Yemi alizungumza kwa sauti ya msisitizo huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Nikamrudisha kijana wa Meja bastola yake nikakunja vidole vya kiganja kilicho shika pete ya Yemi kwa nguvu huku nikitingisha kichwa kwani nina hisi maumivu makali moyoni mwangu hadi ninahisi kwamba moyo wangu unaweza kupasuka muda wowote

 

“Meja ninakuomba uwasamehe na uwafungulie warudi Nigeria salama na wamchukue mtoto wao”

“Dany…”

“Meja nina kuomba kama rafiki yako, ninakuomba usiwashuhulikie kwa lolote”

Nilizunguza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, meja akanitazama kwa sura ya unyonge na iliyo jaa masikitiko. Nikamgeukia Yemi na kumtazama usoni mwake.

“Ninakuomba unisamehe Yemi kwani nilishindwa kukuambia ukweli kwa ajili ya kulinda furaha yako, ya kujiandaa kwa ajili ya harusi. Niwatakie maisha mema huko muendapo”

 

Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, hata uwe ni jasiri kiasi gani ila maumivu ya mapenzi kusema kweli yanaumiza na yanaweza kukuambisha kwa kumwaga machozi mbele za watu.

“Jamaa nisamehe kwa yale yote yaliyo jitokea, nisamehe kwa kushindwa kuyalinda miasha ya mwanao najua kama baba kweli ulistahili kufanya hivyo, ninakuomba unisamehe jamaa yangu”

Baada ya kamaliza kuzungumza maneno haya nikatoka katika hichi chumba na kumuacha Yemi akiangua kilio kwa sauti ya juu. Kila ninacho kiona mbele yangu ninakiona katika mtazamo wa ajabu ajabu jambo lililo nifanya nianze kupiga kelele huku nikihisi dunia kama ina vitu vya ajabu.

“Dany Dany Dany”

 

Niliisikia suti ya meja kama ya jitu fulani hivi baya ambayo ikanifanya nipike kelele huku nikijaribu kukimbia ila nikajikuta nikikamatwa na watu ambao nao nikiwatazama usoni mwao ninahisi kama ni majini fulani yaliyo kuja kunikamata.

“Mpelekeni ndani amechanganyikiwa”

Nilizidi kuisikia sauti nzito ya meja, iliyo nifanya nijiziba masikio yangu, nikanyanyuliwa juu, kila ninapo tazama angani na kuziona nyota ninahisi kama zipo usoni mwangu, jambo lililo zidi kunipagawisha.

“Mchomeni sindano ya usingizi”

“Sawa mkuu”

Nikahisi kitu chenye ncha kali kikiingia kwenye mkono wangu wa kulia, sikumaliza hata dakika mbili nikajikuta usingizi mzito sana ukinipitia na kulala fofofo.

  ***               

“Mkuu”

Niliisikia sauti ya Martin, taratibu nikageuza kichwa changu na kumtazama.

“Vipi?”

Nilimuuliza huku  nikijaribu kunyanyuka ila Martina akanizuia na kuniomba nilale.

“Mkuu bado afya yako haijawa sawa, tulia kidogo nina imani kwamba utakuwa unahisi kizunguzungu”

 

“Umejuaje?”

“Nimefahamu”

Nikayafumba macho yangu kwani ni kweli nina hisi kizungu zungu, nikayafumbua yena na kumuona Martina akinyanyuka na kufungua friji iliyopo humu ndani akatoa mfuko wenye barafu kubwa kisha akarudi sehemu nilipo lala.

“Naomba tu”

Nilizungumza mara baada ya muonoa Martin akihitaji kuniwekea mfuko huo wa barafu kichwani mwangu, nikauchukua mfuko huu na kujiweka upende wa kichwa ninapo hisi maumivu.

“Meja yupo wapi?”

“Ameelekea uwanja wa ndege”

“Kufanya nini?”

“Amemsindikiza Yemi na watu wake, wamaetokea hospitali kuchukua maiti ya mtoto”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama Martin usoni mwake.

 

“Siwezi kumlaumu Yemi, yote ni kwa ajili yangu”

“Hapana Dany huwezi kujilaumu siku hata moja ikiwa wewe mwenyewe ulikuwa mikononi mwa wanajeshi wa Kimarekani na uliamua kujisalimsha wewe mwenyewe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo”

“Nisingekuwa gaidi wala yasinge mkuta mtoto wa watu, isitoshe bado ni mdogo sana”

“Wewe sio gaidi Dany”

“Kwa nini unasema kwamba mimi sio gaidi, ikiwa hata mwanamke ninaye mpenda ameniita gaidi?”

“Yemi ninajua huko aendapo atakuwa anajutia kwa maamuzi yake na kinywa chake kwa kukuita gaidi, nina imani hatambui ni kutu gani kimetokea kwenye maish yako”

“Wewe una amini kwamba mimi si gaidi?”

“Asilimia mia moja mkuu nina kuamini kwamba wewe sio gaidi”

 

“Martin kwa nini huitaji kunisaliti mimi, ikiwa dunia nzima kwa sasa nina imani wananitafuta mimi?”

“Nilikuahidi kwamba tutakufa pamoja na pia tutaishi pamoja, na siwezi kukusaliti ni bora nife wa kwanza kuliko kukuona wewe unakufa wa kwanza”

Martin alizungumza kwa msitizo mkubwa sana, jambo lililo nipa matumaini makubwa sana. Taratibu nikaka kitako kitandani huku nikindelea kuugandamiza mfuko huu wenye barafu  kwneye kichwa changu na kidogo maumivu  na kizungu zungu kinacho nikabili vinatoweka.

“Dany sasa ni wakati wa kuimalizia kazi iliyopo mbele yetu, nina uchungu mkubwa sana kwa kuwapoteza rafiki zangu katika mashambulizi walio yafaya Wamarekani, pale ilikuwa ni nyumbani kwangu, pale palikuwa ni kwetu, nina imani kwa pamoja tunaweza kumungusha yule aliye pelekea vifo vya wapendwa wetu”

Martin alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu.

 

“Upo tayari katika hili?”

“Hata kama ni sasa hivi nipo tayari kuua, mapenzi kwa sasa mkuu wangu yaweke pembeni. Yatatufelisha kwenye mengi”

“Siwezi kupenda mwanamke yoyote kwenye maisha yangu, Yemi amesha nirudisha kwenye maisha ambayo kusema kweli damu ndio itakuwa kinywaji changu. Nitahakikisha kwamba wale wote walio niumiza na kuyapeleka kwenye maisha haya ni lazima niwaue tena kwa mkono wangu mimi mwenyewe”

“Hayo ndio maneno kaka yangu. Ninasubiria amri kutoka kwako mimi nitafanya”

Martin alizungumza kwa furaha huku akitabasamu, taratibu akanisaidia kushuka kitandani. Nikasimama wima huku nikitazama hichi chumba ambacho usiku wa siku mbili nililala na Yemi katika kitanda hichi.

“Maisha yanabadilika mdogo wangu”

 

“Kwa nini?”

“Jana tu nilitoka kumt** Yemi kwenye hichi kitanda leo ameondoka”

Martin akacheka chihi chini nina imani kwamba hakutarajia kwamba ninaweza kuzungumza maneno kama hayo. Tukatoka humu chumbani, tukakuta wahudumu wakiwa tayari wamesha andaa kifungua kinywa.

“Meja amesema anarudi saa ngapi?”

“Hajaniambia ila nina imani atarudi muda si mrefu”

Martin akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa pete ya Yemi na kuniwekea karibu na sehemu nilipo kaa. Nikaitazama kwa sekunde kadhaa hii pete kisha nikaichukua hapa juu ya meza na kuiingiza mfukoni.

 

“Jana uliiangusha, nikakutunzia”

“Asante, nitaiweka kama ukumbusho kwa maana kwenye maisha yangu sikuwahi kuoa mwanamke kwa ndoa”

“Haito kuumiza hiyo pete utakapo iona?”

“Sijajua kwa kweli, nitajaribu kukaa nayo nikishindwa nitaitupa”

“Na hiyo ya kwako huko kidoleni?”

Kabla sijamjibu Martin malango ukafunguliwa, akaingia meja moja kwa moja akatufwata hadi tulipo kaa, akavuta kiti taratibu na kukaa.

 

“Vipi Dany?”

“Safi nimesikia umewasindikiza Yemi na mume wake?”

“Ndio ila ninahitaji kusikia neno la mwisho kutoka kwako, kwani ninahitaji kufanya kitu kwa ajili ya yule mpumbavu kwani amebadilisha hali ya hewa?”

“Kitu gani gani unacho hitaji kumfanyia?”

“Nimewapakiza ndege mbili tofauti na Yemi. Yemi amependa katika ndege yangu binafsi na mwili  wa mwanaye, jamaa na watu wake nao wamepanda kwenye ndege nyingine na wale wajinga wake watatu. Kwenye ndege waliyo panda, kuna bomu liliko tegwa, na nitahitaji maamuzi yako kwamba tuwalipue wafie hewani au tuwaache waendelea na maisha yao?”

 

Swali la meja likanifanya nitazamane na Martin, taratibu nikamtazama meja usoni mwake, huku nikikumbuka uwenda wazimu ulio nipata jana usiku kutokana na ukweli walio uzungumza mume mwenzangu kwa Yemi na kujikuta nikisikia sauti moyoni mwangu ikihitaji niweze kumuangamizaa jamaa huyu kwani amenipotezea mwanamke aliye nipa furaha maishani mwangu.



Taratibu nikajiku nikiyang’ata meno yangu kwa hasira huku sauti ninayo isikia moyoni mwangu ikiendelea kunipa uchochezi wa kufanya mauaji haya.

“Dany nasubiria jibu lako?” “Samahani meja kama ninawaingilia, ila ninaomba nishauri katika hilo” Sote tukamtazama Martin aliye zungumza kwa sauti ya upole.

“Kwa jinsi nilivyo agana na Yemi leo asubuhi, aliniomba nimlinde Dany hadi mwisho wa maisha yangu. Sikuhitaji kulizungumza hapo awali kwako mkuu, ila ukweli ni kwamba Yemi bado anakupenda. Tukimuua mume wake huyu ni lazima atajawa na chuki ambayo itapaelekea yeye kulipiza kisasi kwako jambo ambalo litakuzidishia maadui hapa duniani ikiwa hawa maadui waliopo mbele yetu hatujawamaliza” Martina alizunguzma kwa upole na usikivu mkubwa sana, taratibu nikajikuta moyo wangu ukianza kutulia.

“Sasa hivi tunatakiwa kuwaangalia maadui hawa watatu walipo mbele yetu, inabidi kuwazuia kwa manaa hao wana nguvu ya kiserikali, wana nguvu ya kuendelea kukutangaza Dany wewe kama gaidi, hembu tuangalie hili sasa” “Kwa hiyo Martin unapendekeza bosi wako amuachilie mbali mwanaume aliye mpokonya mke?” “Mimi ndio nilimpokonya mke wake” Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimtazama meja usoni mwake na kumfanya anishangae.

“Nilimpokonya jamaa mke wake kwa kumpiga na pia nimepelekea mtoto wao kufa, yote ni kwa ajili yangu. Nina hisi hata nikimuua jamaa damu yake itenililia maishani mwangu na pia inaweza kupeleka kuto kukamilisha hili zoezi la kulipiza kisasi” Nilizidi kuzungumza kwa upole huku n ikijitahidi hasira na sauti ya uchochozi inayo endelea moyoni kuipinga ili kutoa maamuzi mazuri kwa ajili ya maisha yangu ya baadaye kwa maana Yemi hajanifanyia jambo lolote bada.

“Sawa kama umeridhia rafiki yangu siwezi kuendana kinyume na makubaliano yako, ngoja nimpigie simu rubabi niliye mpa jukumu la kujitoa muhanga kwa ajili hili” “Kumbe ulikuwa umemtoa mtu muhanga?” “Ndio nimemkabidhi kiasi kikubwa cha pesa kitakacho isaidia familia yake kwa miaka mingi tu baada ya kifo chake” “Mmmmmmm” Nilijikuta nikihema kwani maamuzi aliyo kuwa ameyachukua meja katika kunisaidia ni magumu sana. Meja akatoa simu yake mfukoni akaminya minya juu ya kioo kisha akaiweka sikioni.

“Zoezi nimelisitisha” “Sawa” Meja akakata simu huku akitabasamu.

“Jaamaa ameshusha pumzi sana, masikini wee” “Nani?” “Rubani, emeshusha pumzi nina imani hapo alikuwa anaomba zoezi lisikamilike” “Hivi kumbe kuna watu wanaweza kujitoa muhanga kwa ajili ya pesa?” “Ohoo rafiki yanu umasikini mbaya sana, kwa maana nimemlipa jamaa pesa ya mshahara wake kwa mawaka mara mbili nikazidisha kwa miaka kumi mbele” “Ni sawa na kiasi gani?” “Dola milioni tano, ni utajiri mkubwa sana” “Pesa yote hio utamuacha ande nayo?” “Yaa ni dili, wewe ndio umemuakoa, itabidi nije kumuambia kwamba wewe ndio umeweza kuyaokoa maosha iyake atajua ni jinsi gani atakushukuru”

“Usimuambie bwana kwa maana sijafahamu anaweza kunichukulia vipi, isitoshe nina imani atakuwa amesikia habari zangu” “Sidhani, unajua huku Madagasca watu sio wafwatiliaji sana wa mambo, ndio maana juzi tuliweza kutembea barabani kwa kujiamini na wala hakuna hata polisi aliye weza kukutilia mashaka” “Kweli. Sasa ni muda wa kujua tunaanzai katika hii kazi iliyo bakia mbale yetu”

Nilizungumza huku nikimtazama meja usoni mwake.

“Jambo la kwanza ambalo tunatakiwa kufanya ni kuhakikisha kwamba unaingia nchini Tanzania pasipo mtu yoyote kuweza kukufahamu, kwani nina imani kwa sasa ulinzi nchini Tanzania utakuwa ni mkali sana kutokana na ujio wa raisi Donald Bush” “Tutatumia ndege au?” “Hatuwezi kutumia ndege kwa maana kila ndege inayo ingia katika angala la Tanzania ni lazima ikaguliwe na wewe nina imani picha yako itakuwa imesambazwa kwenye vituo vyote vya usifiri.

Meja aliendelea kusisitiza huku akitutazama.

“Njia ya usalama itakayo kuwezesha wewe kufika nchini Tanzania ni kutumia bahari?” “Unahitaji tutumie meli?” “Hapana nina boti za mwendo kasi ambazo zinaweza kuwafikisha Tanzania katika masaa machache sana ila itabidi kuwaacha japo maili moja kabla ya kuingia Tanzania, na mutazamia majini hadi kufika Tanzania.” Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi huku nikimtazama meja usoni mwake.

“Hapo ni lazima kuogela rafiki yangu, pasipo kufanya hivyo unakwenda kuingia mikononi mwa Wamarekani na wakikukamata ndugu yangu kwa sasa hawato kuacha na watakuua haya kwa kukuchoma sindano ya sumu” “Hilo halita weza kutokea” Martin alizungumza kwa kujiamini. “Yaa mukiwa makini nina imani kwamba hilo halito weza kutokea” “Mukiwa makini basi halito weza kutokea. Tanzania mutakwenda kukutana na kijana wangu anaotwa Godlove, atawapokea katika fukwe ambayo mutatokea” “Kwa Dar es Salaam ni fukwe gani ambayo haina ulinzi sana?” Nilizungumza huku nikikmtazama meja. “Wewe ndio mwenyeji mwenzetu unatuuliza na sisi tena?” “Nimeondoka muda sana Tanzania kwa hiyo siwezi kuelewa kama mambo yamebadilika au laa”

“Ngona nimpigie Godlov” Meja akampigia kijana wake baada ya sekunde kadhaa akaiweka simu mezani huku akiwa ameweka loudspeaker.

“Mkuu habari yako?” “Salama meja” “Hii laini yako ina usalama wa kuweza kuzungumza?” “Ndio mkuu hakuna anaye weza kupata mawasiliano yetu” “Sawa ni bichi gani kwa jijini Dar es Salaam hapo mulipo ina ulinzi dhaifu?” “Koko bichi ipo dhaifu, japo kwa wiki hii umeimarishwa ulinzi kwa ajili ya ujio wa raisi wetu ila bado ulinzi wake ni wa kusua sua” “Sasa Dany na mwenzake watakuja Tanzania nina imani watakuwepo huko majira ya saa tisa usiku nina imani kwamba ume waandalia mazingira mazuri?” “Hilo usijali mkuu nimeanda kila kitu kipo sawa, na nitawasubiria katika ufukwe huo hadi wafike” “Itakuwa vizuri, nina imani utawapa ratiba nzima ya shereha na ziara za Donald pamoja na K2” “Ndio mkuu” “Basi nikutakie asubuhi njema” “Nashukuru mkuu” Meja akakata simu na kututazama usoni mwangu.

“Kazi ni raisi sana kilicho baki ni nyinyi kuanza safari muda wowote mukiwa tayari” “Shukrani sana meja sijajua hata nikulipe kitu gani kwani kwa msaada wako ulio nipatia sijawahi kuupata kutoka kwa mtu yoyote duniani” “Usijali Dany haya ni maisha na pesa inatafutwa, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hilli” “Kitu kingine ninakuomba umlinde Yemi, ninajua baada ya haya matukio ambayo nitakwenda kuyafanya nina imani kwamba kuna watu watakao mfwatilia na kumuua” “Unampenda?” Meja aliniuliza kwa sauti ya upole huku akinikazia macho. “Ndio nina mpenda, upendo hauwezi kufutika kwa siku moja na…..” “Usijali Dany huna jaya ya kujieleza sana katika hilo ikiwa hata mii ninazielewa hisia zako” “Shurkani meja kwa kuweza kinielewa” “Sawa ngoja niwaache muzungumze mawili matatu, niandae mpango mzima wa safari” “Sawa meja” Meja akasimama na kuondoka katika eneo hili na kuniacha na Martin.

“Mkuu isije ikatokea siku ukamkosea huyu mzee” “Kwa nini?” “Amekusaidia kwa asilimia kubwa sana na pasipo yeye nina imani kwamba tungekuwa tumesha kufa ile siku tuliyo tekwa na Wamarekani” “Yaa ni mtu mwenye thamani kubwa kwangu nina mthamini sana. Sasa jiandae kama kuna cha kuchukua chukua safari itaanza asubuhi hii” “Sawa mkuu” Nikanayuka na kuelekea chumbani kwangu kwangu, nikaingia bafuni na kuaoga, japo ninayakumbuka matukio machache niliyo yafanya humu bafuni na Yemi ila sina jinsi zaidi ya kuvumilia na kuweka hisia za mapenzi pembeni na kuimalizia kazi iliyopo mbele yangu.

Nikava jinsi, tisheti na raba, nilipo hakikisha kwamba nimekamilika, nikachukua pete ya Yemi na kuivaa katika kidole changu cha mwisho cha mkono wangu wa kushoto kisha nikatoka humu chumbani. Nikamkita Martin akiwa amesimama sebleni na meja.

“Boti ipo tayari kwa ajili ya safari” “Sawa meja” Tukaanza kutoka na kuelekea katika kingo za fukwe ya bahari iliyopo pembezoni mwa jumba la meja.

“Hakikisheni kazi munaifanya kikamilifu na safari hii Dany usifanye makosa yoyote ambayo yatakugarimu” “Usijali meja, nikishindwa kufanya sasa hivi nina imani kwamba sinto weza kufanya tena hii kazi” “Sawa sawa nakuamini katika hili” “Pia meja nina shukuru sana kwa kila kitu ulicho nifanyia na unacho endele kunisaidia” “Usijali rafiki yangu, niwatakie safari njema” “Asante” Tukaingia kwneye boti moja kubwa ya kifahari.

“Mukifika Tanzania, Godlove atawaeleza jinsi ya kuwasiliana nami” “Sawa meja” Taratibu boti hii ikaanza kuondoka eneo hili huku tukiwa tumekabidhiwa vijana wawili wa meja pamoja na nahodha wa hii boti. Safari ikazidi kusonga mbele huku boti hii ikienda kwa mwendo kasi sana.

“Mkuu unahitaji tuwaue vipi maadui zako?”

“Hilo tutalijua tukifika nchini Tanzania kwa sasa ni vigumu kulizungumzia kwani bado hatujajua wamejipanga vipi katika hilli swala” “Sawa” Nahodha wahii boti kusema kweli ni mtaalamu kwania kasi anayo kwenda nayo ni kibwa na muda mwengine tunakutana na mawimbi makubwa ya maji ila tunafanikiwa kupita. Masaa yakazidi kwenda hadi giza likaingia.

“Tuna masaa kadhaa mbele, kuna maelezo tunatakiwa kuwapatia” Kijana mmoja wa meja alizungumza huku akitutazama kwenye siti tulizo kaa. Nikanyanyuka na kumsogelea.

“Sawa” “Kuna nguo maalumu za kuzamia kwenye maji pamoja na mitungi maalumu nina imani kwamba munaweza kuitumia?” “Kwa mimi ninaweza, Martin unaweza?” “Ndio ninaweza mkuu” “Basi hii mitungi inagesi itakayo wawezesha kukaa chini ya maji kwa masaa zaidi ya kumi. Pia kuna hii simu haiingii maji na inatumika hata ukiwa ndani ya bahari. Itawasaidia katika swala zima la kutazama muelekeo wa wapi munakwenda, kwani tumeambiwa kuwaacha maili moja kutoka Tanzania ilipo” “Sawa”

Kijana huyu akanikabidhi simu hii nikaitazama vizuri, kisha nikamkabidhi Martin.

“Kuna swali munahitaji kuniuliza?” “Hapana” “Basi niwatakie kazi njema na karibuni Madagascar” “Asante” “Tukiwa tunakaribi kufika basi tutawaambia muweze kuvaa mavazi hayo?” “Tunaweza kuvaa juu ya hizi nguo zetu?” “Hapana labda muziweke kwenye begi maalumu ambalo lipo hapa na haliingii maji?” “Sawa sawa na sehemu ambayo munatuacha haina samaki wakali?” “Hapana samaki wake ni wa kawaida. Na kuna tochi maalimu mutazitumia mikiwa chini ya maji ila munatakiwa kuwa makini sana” “Shukrani kaka” “Niite Michael” “Sawa asante sana Michael” Nikarudi kwenye siti yangu baada ya kupata maelekezo hayo, huku kichwani mwangu nikifikiria jinsi nilivyo poteza uhuru katika nchi yangu na nina rudi kama mvamizi ambaye endapo nitaonekana basi ninaweza kupoteza maisha yangu.

‘Mungu nisaidie katika hili’

Nilijikuta nikizungumza maneno hayo huku nikiwa nimeyafumba macho yangu. Baada ya masaa mawili, Michael akaingia tena kwenye hichi chumba tulipo kaa huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana.

“Vipi?” “Tumepata tatizo” “Tatizo gani?” Boti yetu inafukuziwa na boti za jeshi la majini na wanamlazimisha nahodha kusimamisha boti la sivyo wanakwenda kutulipua na hadi sasa wametupa onyo la pili tunasubiria amri yako tusimamishe boti au tusonge mbele ili tulipuliwe” Michael alizungumza haraka haraka na kunifanya ninyanyuke kwa haraka hukun ikiwa nimejawa na wasiwasi mwingi, kwani hili ni tatizo jengine ambalo sikulitarajia litokee kwenye safari yangu hii.

 

0 comments:

Post a Comment

BLOG