Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AIISSII U KILL ME LEGACY SEHEMU YA 4/10

 


AIISSII U KILL ME LEGACY

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 4 KATI YA 10

 


“Imemaliza sasa si ndio”

“Ndio”

Nilijibu huku mwili mzima ukinitetemeka.

“Zamu yangu, je upo tayari”

“Ehee?”

“Upo tayari?”

“Ngoja kwanza baba, unataka kuniambia kwamba unahitaji kuniua?”

“Nikihitaji kukua nitakuua. Je upo tayari”

“Nipe basi mbinu za kufanya kama wewe ulivyo fanya”

“Wacha kwanza nikupige kisha ndio nitakupa mbinu”

Nikajikuta nikijutia ni kwa nini nimeacha kulala usingizi wangu na nimekuja kucheza michezo ya hatari namna hii.

“Jiandae”

Nikasimama wima Dany akaanza kuhesabu kuanzia moja hadi tatu, nikajaribu kuchezesha mwili wangu, ila risasi ikanipiga kifuani mwangu na kujikuta nikianguka chini mzima mzima. Dany akatembea hatua chache hadi sehemu nilipo anguka.

“Risasi zote ni za plastiki au kwa jina jengine unaweza kuziita risasi baridi. “

Maneno ya Dany yakanifanya nipapase kiafuni mwangu na kukuta nikiwa salama japo nina maumivu makali. Akanikabidhi mkono wake wa kulia na kuninyanyua juu.

“Kila kitu kwenye maisha kinahitaji umakini. Ulitakiwa kutajazama jinsi bega langu la mkono ambao umeshika bastola. Mtetemesho wa mkono wangu ndio ungekufanya kujua risasi ninayo ifyatua inakuja upande gani katika mwili wako.”

“Kivipi ikiwa mikono yako imejengeka kwa misuli?”

“Hata kama imejengeka kwa misuli, ila ukihitaji kujua ni wapi risasi inapo kwenda, wewe tazama bega langu. Ni sawa sawa na kipa anaye subiria mchezaji anaye taka kupiga penati. Akimtazam mchezaji usoni ni lazima atafeli na atadanganywa na macho ya mchezaji huyo. Ila silaha nzuri ya kumtazama mchezaji anaye piga penati na kumtazama kiunoni mwake, kiuno ndio kitaongoza, mguu upi upige na wapi mpira uelekee”

“Mmmmm!!”

“Ndio, ila kitu kina hitaji umakini. Kitu kilicho kufanya ufeli kwenye mipango yako mingi sana ni umakini. Hukuwa makini, na kila kitu ulikifanya kama vile kinavo onekana. Leo nitakufundisha mazoezi ya umakini sawa”

“Sawa baba”

“Vua nguo ubaki na boksa”

Nikavua nguo zangu na kubaki na boksa, tukaanza mazoezi ya umakini ambayo miongoni mwa mazoezi hayo ni kuzuia makonde ya ngumi ambayo Dany anayavurumusha kwangu. Japo hanipigi kwa nguvu, ila yanauma kwa namna moja ama nyingine. Hadi inatimu saa tisa usiki mwili wangu wote umejaa majeraha mengi sana.

“Ungekuwa makini usinge kutana na maumivu hayo. Nenda kaoge na upumzike”

Nikaanza kuchechemea kuelekea ndani, nikajilaza kitanda na taratibu usingizi ukaanza kunipitia.

***

Jojo akafika nyumbani hapa akiwa ameongozana na vijana wawili huku kijana wa kike akiwa ni mzungu. Tukapata nao chakula cha usiku, kisha wakaelekea kulala na kuniacha sebleni hapa nikiwa na Dany pamoja na Jojo.

“Kesho kama nilivyo zungumza tutakuwa na mazoezi kisha kesho kutwa Randy utakuwa na kazi yako mjini kuna mtu nitahitaji ukamuondoe duniani”

Nikastuka kidogo.

“Unastuka kwani ndio mara yako ya kwanza kuua?”

“Hapana baba”

“Ndio, umakini ni muhimu kwenye kazi hiyo na sinto hitaji makosa ya aina yoyote yaweze kutokea kwenye kazi hiyo. Umenielewa”

“Sawa”

“Maelezo yote nitakupatia kesho sawa”

“Sawa baba”

“Dada Jojo tunaweza kuzungumza?”

“Ndio”

Tukanyanyuka hapa seblenina kuelekea jikoni.

“Vipi?”

“Kuna lolote jipya huko mjini?”

“Kuhisiana na nini mdogo wangu?”

“Mauaji yoyote mapya yaliyo tokea, au yale mauaji niliyo yafanya kipindi cha nyuma kidogo”

“Sijaona mtu aliyo yazungumzia sana.”

“Sawa”

“Nimemuona lile jimama lako”

“Wapi?”

“Uwanja wa ndege kuna mtu alikwenda kumpokea, ila sikuhitaji nizungumze naye”

“Ni mwanaume au mwanamke?”

“Mwanaume”

Nikahisi hali ya maumivu mooni mwangu.

“Ni mwanaume wa aina gani?”

“Kijana ila amekuzidi wewe, nikama wa miaka ishirini na tisa au thelathini hivi”

“Sawa, ninakwenda kulala”

Nikamuacha Jojo akinitazama, nikaingia chumbani kwangu na kuanza kupapasa kwenye mfuko wa suti yangu na kukuta simu ambayo Profesa alinieleza kwamba itakuwemo ndani humo. Nikaiwasha simu hii na nikaanza kusoma maelezo ya utumiaji wa suti hii Profesa aliyo nitengenezea. Nikayakatisha maelezo hayo na kuiingiza namba ya simu ya Jane. Simu yake ikaanza kuita baada ya muda ikapokelewa na mwanaume jambo lililo fanya moyo wangu uzidi kujawa na maumivu makali sana.

“Halooo”

Sauti hiyo ya mwaume ikazidi kuniumiza moyo wangu. Nikatamani kukata simu ila nikajikaza kukaa kimya huku nikiendelea kusikilizia ukimywa wa mwanaume huyo.

“Honey toka bafuni naona aliye kupigia simu hazungumzi”

Nikakata simu huku mwili mzima ukitetemeka kwa hasir sana. Kusema kweli moyo wangu ulisha anza kujawa na upendo wa Jane, na inakuwaje ameamua kunisaliti katika muda mfupi tu ambao tumeachana. Nikiwa katika dibwai la mawazo na hasira simu ikaanza kuita tena, nikaitazama kwa muda kidogo na kukuta ni namba ya Jane. Nikajifikiria kwa muda kisogo kisha nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Haloo, Haloo”

Niliisikia sauti ya Jane ila kwa hasira nikashindwa kabisa kumjibu chochote hadi akakata simu. Nikaizima simu hii na kurudisha kwenye mfuko wa suti yangu. Nikajilaza kitandani, usingizi ukanipitia taratibu. Alafajiri na mapema nikaamka na tukaanza kufanya mazoezi huku tukiwa tumejumuika na Ethna pamoja na mke wake Camila. Kutokaa na hasira ambayo bado ipo kifuani mwagu, sikuhitaji kuonyesha uso wa furaha kwa mtu yoyote. Hadi tunamaliza mazoezi sikuzungumza na mtu yoyote.

“Mbona upo hivyo leo?”

Dany aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hapana baba nipo vizuri”

“Una uhakika?”

“Ndio”

“Itabidi uondoke usiku huu, ili hawa vijana wasiweze kufahamu chochote kwa maana wanaonekana ni watoto wa maam na wanatakiwa wasifahamu chochote kuhusia na sisi”

“Sawa baba”

“Twende nikakuonyeshe maelezo ya yule mtu ninaye muhitaji”

Tukazunguka nyuma ya nyuma na kuingia kwenye ukumbi mkubwa wa kuhifadhi vitu mbali mbali kiwemo silaha. Dany akawasha moja ya computer na kuanza kunionyesha picha za mzee mmoja aliye valia suti ya garama.

“Huyu ni muuzaji wa madawa ya kulevya. Anaitwa Pacheko, ni Mtanzania, ila mama yake ni Mmexco. Atoa madawa ya kulevya kutoka Colombia, Mexco na kuyaleta Tanzania na Tanzania hapa ndio kitovu cha kusafirisha madawa yote katika bara hili la Afrika. Kuna wasaliti ndani ya idara kadhaa za serikali, kuanzia Airport, jeshi la polisi, na mipakani huko na wamekuwa wakimfanya huyu kama Mungu wao. Sasa wewe ndio mtu wa kumua. Mbinu za kumuua, ni wewe utakaye jua nini cha kufanya.”

“Sawa baba, je hapa Tanzania anaishi wapi?”

“Makao makuu yake ni Arusha, ila kwa sasa yopo Dar es Salaam kuna mzigo wake wa kilo zaidi ya elfu kumi atazipokea kwenye ndege ya mizogo itakayoingia Dar es Salaam saa nane usiku, hakikisha kwamba kabla mzigo haujafika katika nyumba yake ya jiji la Dar es Salaam, basi unavamia. Kuna kitu kimebadilika katika hii kazi unayo kwenda kuifanya”

“Kitu gani?”

“Nitahitaji umchukue akiwa hai na ukisha mchukua basi nitakueleza ni wapi uweze kumpeleka sawa”

“Sawa mkuu”

‘Kabla sijaifanya hii kazi Jane na huyo malaya wako, ninakuja kwa ajili yenu’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikikunja ngumi ya mkono wangu wa kulia huku nikimtazama Dany usoni mwake na kumfanya atabasamu akiamini kwamba mwanaye ninakwenda kufanya kazi kama vile alivyo niagiza.



Baada ya maelezo ya Dany, nikaanza kuchagua baadhi ya silaha ambazo ninaweza kuzitumia katika kazi yangu aliyo niagiza kwenda kuifanya. Nilipo hakikisha kwamba nina bastola zaidi ya nane zilizo jaa risasi za kutosha pamoja na magazine, nikaziweka kwenye begi moja kwani muda wa kuondoka hapa bado.

“Kuna hii tisheti hapa”

Dany alizungumza huku akinikabidhi tisheti moja nyeusi ambayo ina vutika vutika.

“Hizi tisheti alikuwa akitengeneza marehemu bibi yako. Tisheti hizi haziingii risasi, vaa nikujaribu”

“Eheee!!?”

“Yaaa vaa nikujaribu”

Nikamtazama Dany kwa macho ya mshangao, kwa ishara akaniomba tena niweze kuvaa tisheti hii, taratibu nikaivaa tisheti hii huku mwili mzima ukinitetemeka.

“Usiogope”

Dany alizungumza huku akichukua moja ya bastola ambayo ina risasi za moto, tofauti na bastola ambazo tulikuwa tunafanyia mazoezi ya umakini. Nikafumba macho yangu kwani sitaki kushuhudia hili linalo kwenda tokea.

“Unafumba nini macho fumbua tu”

Nikafumbua macho yangu, Dany akafyatua risasi mbili ambazo zote zikanipiga kifuani mwangu na kuanguka chini, nikajikuta nikianza kutabasamu taratibu huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana usoni mwangu.

“Hembu rudia tena”

Dany akanipiga risasi kadhaa kifuani ila tisheti hii niliyo ivaa haikuweza kuingiza hata risasi moja, japo nimapata maumivu kadhaa yatokanayo na mikito ya risasi hizi.

“Ubunifu ambao umetokana na tisheti hiyo ndio ubunifu ambao Professa ameutumia kwenye suti yako. Sasa ukivaa hiyo tisheti kwa ndani, kisha ukafwatia na suti, basi hakuna atakaye weza kukudhuru”

“Nashukuru saba baba”

“Usijali, nipo kwa ajili yako”

Dany alizungumza huku akinipiga piga kwenye bega la mkono wangu wa kulia, kisha taratibu akaondoka katika eneo hili huku akiwa amejawa na tabasamu. Nikaanza kutazama magari nane ya kifahari yaliyopo katika eneo hili. Nikabeba begi langu lenye bastola za kutosha na kuelekea chumbani kwangu, nikaufunga mlango wangu kwa ndani na kuzimwaga bastola zote juu ya kitanda. Nikaanza kuzikagua moja baada ya nyingine, huku kichwani mwangu, picha ya Jane na mwanaume wake mpya zikinijia kila mara. Hisia zangu zikazidi kwenda mbali sana kwa kuwaona jinsi wanavyo peana mapenzi. Miguno ya Jane ikazidi kunipandisha hasira na kijikuta nikizidi kujawa na chuki dhini ya tukio ambalo amelifanya.

Mlango wangu ukagongwa, nikazifunika bastola zangu kwa kutumia shuka, kisha nikaufungua mlango. Nikakutana na Jojo akiwa ameshika funguo ya gari.

“Utatumia ile Benz nyeusi ina mafuta ya kutosha. Pia itahimili mikiki mikiki yote ambayo utakwenda kuipitia kwenye kazi yako”

“Nashukuru, ipo wapi?”

“Tayari nimesha kutolea, ipo hapo nje”

“Asante dad”

“Ila nikikuangalia machoni mwako nina hisi kama kuna kitu kina kusumbua, au hujawa tayari kwa kwenda kuifanya hii kazi?”

“Hakuna tatizo dada, nitakwenda kuifanya kazi hii vizuri sana hadi wewe huto amini”

“Una uhakika?”

“Ndio niamini”

“Sawa mimi nipo chini”

Nikaingia bafuni na kuanza kuoga taratibu huku nikikamia sana kwenda kufanya jambo kwa Jane na mpuuzi wake, nilipo maliza kuoga nikaanza kujiandaa taratibu, nilipo maliza kuvaa tisheti pamoja na suti hii niliyo pewa na Professa, nikasimama kwenye kioo kikubwa kilichopo katika eneo hili. Kusema kweli nimependaza sana, nikaanza kuchomeka bastola moja baada ya nyingine kwenye sehemu mbali mbali za suti hii. Nikachukua funguo ya gari na kutoka ndani humu. Nikakutan ana Dany sebleni pamoja na Jojo.

“Gari ina ramani kwa kutumia PRS itaweza kukuekeza njia ya kupita hadi ufike jijini Dar es Salaam”

“Sawa baba”

“Kitu kingine hakikisha kwamba huendi kasi sana kwa maana kuna kona nyingi sana kwenye barabara ya kuondokea huku sawa”

“Sawa”

“Kuwa makini”

“Nashukuru”

“Silaha zako zipo wapi?”

Nikafungua koti la hii suti na kumuonyesha Jojo jinsi nilivyo zichomeka bastola mbili kwenye mifuko ya ndani ya hili koti, akatingisha kichwa huku akitabasamu.

“Hiki ni kitambulisho chako cha taifa hili la Tanzania, hii ni kadi ya mpiga kura na hii ni leseni ya barabarani. Hata ukikutana na askari wakikusimamisha wakakuomba leseni na kitambulisho basi utakuwa salama”

Jojo alizungumza huku akinikabidhi vitambulisho hivi, nikavisoma kimoja baada ya kingine na kukuta vikiwa na majina yangu mawawili ambayo ni Randy Dany, huku vikiambatana na picha yangu.

“Sawa je pesa za kutumia au hakuna haja ya kuwa na pesa?”

“Mmmmm ngoja”

Jojo akapandisha gorofani baada ya muda kidogo akarudi akiwa ameshika vibunda viwili vya pesa za kitanzania.

“Milioni mbili hii itatosha kwa kazi yako”

“Nashukuru”

Nikaingiza vibunda hivi mfukoni mwa suruali yangu. Nikawaaga kwa kuwakumbatia kisha nikatoka nje, nikaingai kwenye gari hii ndogo ambayo ina milango miwili tu. Nikaiwasha gari hii, tv ndogo iliyopo pembeni yangu ikaanza kunionyesha ramani wa wapi ninapaswa kuelekewa. Nikaanza kuondoka eneo hili huku nikikatiza katikati yam situ huu mkubwa ambao una wanayama wa kila aina.Baada ya lisaa moja na nusu, nikaingia kwenye barabara kubwa ya lami na nikaendelea na safari hii. Nikaitoa simu yangu niliyo pewa na professa, nikakuta missed call zaidi ya tano kutoka kwa Jane. Nikafungua meseji moja iliyo tmwa na Jane, ambayo ina niuliza mimi ni nani, nikataka kuijibu meseji hii ila nikaona nitavuruga mpango wangu. Nikiwa katika moja ya kona katika kilima hichi ninacho shuka kwa mbali kidogo nikaona kizuizi cha polisi kinacho kagua kila gari. Taratibu nikaanza kupunguza mwendo kasi hadi nikafika katika eneo hilo na kukuta gari mbii aina ya Fuso zilizo jaa makabichi zikiwa zinakaguliwa. Askari wawili wakanifwata katika gari langu huku mmoja akiwa na tochi kubwa, taratibu nikafungua kioo cha gari.

“Habari viongozi”

Nilianza kuwasalimia huku nikiwa na tabasamu.

“Salama, unakwenda wapi usiku huu?”

“Ninaelekea kwangu hapo chini”

“Wapi?”

Ubaya ni kwamba sifahamu majina ya hili eneo, kabla sijajibu simu yangu ikaanza kuita.

“Ohoo samahani, ninaweza kupokea simu”

“Ukiwa unapokea, tunaomba leseni yako. Nikatoa leseni yangu na kumkabidhi polisi mmoja. Nikaitazama namba hii ngeni inayo nipigia, nikaipoke na kuiweka sikioni mwangu.

“Halooo”

Niliisikia sauti ya Jane, nikakata simu na kumtazama askari huyu.

“Unaweza kuendelea na safari yako ndugu, ila kuwa makini sana”

“Nashukuru”

Askari akanikabidhi leseni yangu, taratibu nikaanza kuondoka eneo hili na kuacha Fuso hizi mbili. Nilipo maliza kona hizi, nikaanza kuendesha gari hili kwa kasi kwani barabara niliyopo imenyooka vizuri na ina kona chache tu. Majira ya saa sana usiku nikaona kibao kimoja pembezoni mwa barabara kikishiria kwamba sasa nina aga mkoa wa Tanga na ninaingia mkoa wa Pwani.

“Pwani, si ndipo anapo ishi Professa?”

Nilijiuliza huku nikiendelea kuchunguza baadhi ya vibao hivi barabarani. Nikazidi kuendesha gari hili kwa kasi sana hadi nikakutana na kibao kingine kilicho andikwa kwamba sasa ninaingia mkoa wa Dar es Salaam. Nikafika katika barabara ambayo ninaikumbuka vizuri sana kwani nilisha wahi kuipita nikiwa na Jane. Kutokana mimi ni mtu wa kutunza kumbukumbu zangu vizuri kichwani mwangu, nikakumbuka nyumbani kwa Jane ni wapi.

Majira ya saa kumi usiku nikasimamisha gari langu nje ya geti la nyumba ya bi Jane. Nikashuka kwenye gari hili huku nikiwa makini kwa kutazama eneo hili viruzi, kwani hili eneo ndio tulilo shambuliwa siku moja tukiwa na bi Jane katika gari lake.

Nikatazama ukuta huu mrefu, ambao juu umepitishwa nyaya za umeme. Pembeni katika ukuta huu kuna mti mmoja mkubwa wenye matawi mengi. Moja ya tawi lime elekea eneo la ndani katika jumba ya bi Jane. Nikaupanda mti huu kwa haraka, kwa bahati nzuri eneo la ndani lilipo elekea tawi hili kuna bustani yenye majani mengi. Nikajirusha chini kwa umakini sana na sikutoa kishindo cha aina yoyo, ambacho kinaweza kuashiria kwamba kuna mtu ameingia ndani humu.

Eneo la ndani katika jumba hili kuna magari mengi sana ya kifahari. Nikachomoa bastola moja na kuifunga kiwambo cha kuzuia sauti, nikaanza kutembea kwa umakini hadi kwenye mlango wa kuingia ndani, nikausukuma kidogo na kukuta ukiwa umefungwa.

“Shiti”

Nilizungumza huku nikiangaza angaza ni wapi ninaweza kupata nafasi ya kuingia. Nikaanza kuikagua nyumba hii ambayo ni ya gorofa. Vyumba vyote vya chini havina mtu.

‘Au nivamie kwa nguvu na kuingia ndani?’

Nilijiuliza maswali haya huku nikirudi katika mlango wa kuingilia humu ndani, kabla sijafanya chochote, mlango ukafunguliwa, akatoka mwanume mmoja akiwa na boksa tu huku mkononi mwake akiwa ameshika bastola. Akaangaza macho yake huku na kule na hakuweza kuniona sehemu nilipo jibanza. Akageuka na kuanza kuelekea ndani, kabla hajaufikia mlango, nikampiga risasi moja ya mkono ulio shika bastola yake na kumfanya aiangushe chini huku akipiga kelele ya maumivu makali sana, nikaanza kukimbilia sehemu alipo, kabla hajaokota bastola yake nikampiga teke la mbavu, lililo sababisha aanguke chini mzima mzima.

“Baby kuna nini?”

Niliisikia sauti ya bi Jane akizingumza huku akikimbilia eneo hili. Kitendo cha kufungua mlango akakutana na sura yangu iliyo jaa hasira na wivu mwingi sana dhini yake. Bi Jane mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa woga.

“Baby ehee?”

Nilizungmza kwa dharau huku nikimtazama bi Jane. Nikamshika mkono jamaa huyu na kuanza kumburuta hadi ndani, huku bi Jane akiwa anarudi nyuma nyuma.

“Kaa pale”

Nilimuamrisha bi Jane kukaa kwenye moja ya kiti katika meza ya chakula. Nikamyanyua jamaa huyu na kumkalisha kwenye kiti kimoja, nikaanzangaza angaza kwenye kabati hili la vyombo, nikaona kisu kirefu na chenye ncha kali sana, nikakichukua na kuwageukia.

“Kwa nini ulinitumia?”

Nilimuuliza bi Jane huku nikimkazia macho.

“Ra…and…n…..”

“Ra Ra Ra Ra nini zungumza?”

“Sio hivyo Randy”

“Ohoo ila?”

Bi Jane akakosa cha kunijibu, kwa maana kama ni ushahidi wa kuwafumania unaonekana dhahiri. Nikamkita jamaa huyu kisu cha paja na kumfanya alia kwa maumivu makali akajaribu kunipiga ngumi, kwa mkono wake wa kushoto, nikaidaka ngumi yake, nikachomoa kisu hichi, nikakiweka kiganja chake juu ya meza hii na kumchomeka kisu hichi na kumfaya yeye na bi Jane kulia kwa uchungu sana.

“Nilikuambiaje kama ikitokea umenisaliti?”

“U…u…l…i…s….ema uta….niua”

“Ohoo kumbe una kumbuka. Huyu ni nani?”

“Ehee?”

“Nikamuelekezea jamaa bastola katika paja lake jengine ambalo sijalijeruhi.

“Huyu ni nani?”

“Ni….rafi…ki yangu”

Nikampiga risasi ya paja jamaa huyu na kumfanya azidi kulia kwa maumivu. Nikamsukumiza na kiti chake na akaanguka chini.

“Jane hunijui mimi. Kwa nini umenitumia?”

“Randy ninakuomba unisamehe, nisamehe mpenzi wangu. Niljua kwamba huto rudi tena?”

“Sinto rudi tena, eheee. Hata wiki haijapita leo upo na mwanaume eheee?”

Bi Jane akakosa cha kunijibu zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu sana.

“Oya hivi ulijua kwamba huyu ni mpenzi wangu eheee?”

“Usiniue kaka, nisamehee”

“Sina msamaha kwa mtu ambaye anaingilia kitu kinacho itwa mapenzi yangu”

Nikampiga jamaa huyu risasi karibia nane mwilini mwake na akafa hapa hapa chini. bi Jane akalia sana kwa uchungu kwani hakutarajia kuweza kukutana na kitu kama hichi. Nikamnyanyua bi Jane na kuanza kupandisha naye ngazi za kuelekea gorofani.

“Kipi ni chumba chako”

“Kile”

Nikaingia naye chumbani kwake na kumsukumia kitandani kwake kwa nguvu na kumfanya mwili mzima kumtetemeka kwa woga.

“Kwa nini ulinitumia, ulinipa penzi ili nipambane na maadui zako si ndio?”

“Sio hivyo Randy”

“Ila?”

“Naomba unisamehe Randy, ni shetani tuu”

“Ohoo kama ni shetani basi ni hivi, muombe shetani huyo akupokee kuzimu kwani lazima nikuue, au Sali salaka yako ya mwisho malaika mbinguni wakupokee kabla sijafumua ubongo wako kwa risasi sasa hivi.”



Bi Jane taratibu akafumba macho yake huku mikono yake akiifumbata sehemu moja huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Kitendo hichi cha bi Jane kikaufanya moyo wangu kuingiwa na huruma ambayo sikujua inatokea wapi. Taratibu, nikairudisha bastola yangu kiunoni, nikatembea kwa hatua za taratibu hadi kitandani alipo kaa. Nikakaa pembeni yake huku nikimtazama usoni mwake, nikaitazama mifomo yake inayo endelea kucheza cheza kwa woga, nikazisogeza lipsi zangu na kuanza kumnyonya, jambo lililo mfanya ashuke sana.

“Nini, amekunyonya sana?”

Nilimuuliza bi Jane huku nikimtazama usoni mwake.

“Ni wapi ninaweza kupata tindikali?”

Bi Jane akapatwa na mshangao mkubwa sana.

“Unaashangaa nini, nahitaji tindikali”

“Zi…i…ipo stoo”

“Twende ukanionyeshe”

Nilizungumza huku nikimvuta kitandani bi Jane. Tukatoka chumbani humu na kuelekea katika stoo kubwa iliyopo gorofa ya chini. Nikaona chupa ishirini za tindikali zikiwa zimepangwa vizuri.

“Randy”

“Mmmm”

“Kwa nini umemua kijana wa watu jamani”

Nikamatazama bi Jane kwa macho makali sana na kumfanya akae kimya, nikachuku chupa mbili za lita tano tano.

“Endapo utafanya ujinga mwengine kwangu, nitakuua. Umenielewa?”

“Ndio”

“Beba na wewe mbili”

Bi Jane akatii kile nilicho mueleza, tukaanza kutembea sebleni.

“Twende tukachukue tena”

Nilizungumza huku nikiziweka chini chupa hizi za tindikali. Bi Jane machozi yakendelea kumwagika usoni mwake huku akitazama mwili wa mwanaume wake niliye muua. Tukarudi stoo na kubebe chupa nyungine na kurudi sebeleni.

“Utataka kufanya nini Randy?”

“Hakuna mtu ambaye atakwenda kuona huu mwili waka kujua ni wapi alipo potelea huyu fala wako. Umenielewa?”

“Sasa unataka kusema kwamba…..”

“Unahitaji kumzika humu ndani kwako si ndio”

“Mmmm”

“Sasa acha nifanye kazi yangu”

Nikavua koti langu la suti na kuliweka pembeni, nikavu shati langu na nikabaki na tisheti hii niliyo pewa na Dany.

“Hapa chini kuna bafu?”

“Ndio”

“Beba huko”

Nilimuambia bi Jane huku akaishiak miguu ya mwanaume huyu huku nami nikishika mikono ya mwanaume huyu na tukaanza kumbebea hadi kwenye bafu. Nikamuweka kwenye sinki la kuogea kisha nikarudi sebleni, nikachukua chupa za tindikali na kurudi bafuni. Nikamkuta bi Jane akiwa amemshika uso mwanayme huyu huku akilia kwa uchungu sana.

“Unalia nini, nyanyuka tukachukue tindikali nyingine”

Tukatoka ndani humu na kurudi sebleni, tukababe tindikali zote kisha tukarudi bafuni. Nikafungua chuma pmoja na kuanza kumwagia jamaa huyu mwili wake na ukaanza kuyayuka mithili ya plastiki inavyo ungua kwenye moto. Bi Jane macho yakamtoka huku machozi yakiendelea kumtiririka usoni mwake, ila sikuweza kulijali hilo zaidi ya kuendelea kumimina tindikali hii sehemu moja baada ya nyingine ya mwili wa jamaa huyu. Ndani ya nusu saa mwili wa mawanaume huyu ukawa umeyayuka nyama zote na kubaki mifupa tu. Bi Jane akawa kama mtu aliye shikwa na bumbuwazi ambalo hata nilipo jaribu kumsghika mkono wake hakuweza kustuka. Nikamshika bi Jane mkono na kumtoa bafuni humu, nikamkalisha sebleni na nikaanza kuifanya kazi ya kusafaisha eneo zima lenye damu. Nilipo maliza kufanya kazi hii nikarudi bafuni na kuichukua mifupa yote kisha nikarudi nayo sebleni.

“Randy kwa nini wewe ni katili sana ehee?”

Bi Jane aliuliza huku akiwa amejawa na huzuni kubwa snaa usoni mwake.

“Sio roho mbaya tu, ila nina asili ya ushetani ndani ya moyo wangu. Nilikupa onyo, ukahisi ni kawaida, sasa hili litakuwa ni fundisho kwako. Sasa ole wako nikukute siku nyingine umefanya ujinga kama huu.”

Nikatoka nje na mifupa hii, nikaiweka katika jiko la kuchomea taka, nikaichoma mfupa hii hadi ikateketea yote kisha nikarudi ndani.

“Leo nitakuwepo hapa kwako hadi usiku”

Nilizungumza huku nikikaa pembeni ya bi Jane.

“Randy kwa unyama ulio ufanya, unahisi moyoni mwangu utapata msamaha?”

“Sijali kama utanisamehe ai usinisamehe umenielewa?”

“Radny wewe ni mnyama, wewe ni shetani”

Bi Jane alizungunza huku akinipiga piga kifuani mwangu. Nikaishika mikono yake yote miwili na kumsogeza karibu kabisa na kifua changu.

“Unahisi kwamba mimi sio binadamu eheee?”

Nilizungumza kwa kufoka huku niimyazama bi Jane usoni mwake.

“Nina moyo, ninajua kupenda. Toka utotoni mwangu nimekuw ani mtu wa kukosa upendo. Mama yangu ameninyanyasa, na juzi tu ndio nimemuona baba yangu. Ulianza kuzinyanyua hisia zangu, nikakupenda hata kama Dany aliweka kipingamizi juu ya penzi letu ila bado nilisimamia msimamo wangu. Ila wewe ukaona uchukua malaya wako sijui kutoka wapi huko ukamuingiza ndani si ndio?”

Nilizungumza kwa kufoka sana na kumfanya bi Jane kutetemeka mwili mzima.

“Huwa nikipenda nina penda, ila nikichukia nitachukia mazima. Kama uliamua kuwa na mimi hakikisha kwamba unakuwa na mimi, ila kama unahitaji kucheza na hisia zangu, haya ndio malipo ambayo utakuwa unayopoke kwa kila mwanaume ambaye utakuwa naye. Umenielewa?”

“Nd….i…io….o”

Sikuhitaji kumpa nafasi bi Jane ya kufanya jambo lolote la kijinga. Kila sehemu aliyo elekea ndani ya nyumba hii nipo nyuma yake.

“Nahitaji kujisaidia haja kubwa”

Bi Jane alizungumza huku akiwa ameshika mlango wa kuingilia chooni.

“Tunaingia wote”

“Jamani Randy kunifwata fwata kote unahisi nitafanya kitu gani?”

“Nimekuambia sihitaji kuisikia sauti yako, ingia, choo si cha kukaa. Wewe jisaidie kisha tutatoka wote”

Bi Jane akakubali kishingo upande, tukaingia chooni humu, taratibu akavua nguo zake na kukaa katika choo hichi huku akiwa mnyonge sana.

“Randy”

“Naam”

“Kwenye maisha yangu sikutarajia kuona kitu kama hichi ulicho kifanya leo”

“Kata gogo mama tutoke”

“Siwezi nikiwa nimesimamiwa hivi. Niamini sinto weza kwenda sehemu yoyote wala sinto weza kufungua kinywa changu juu ya hili lililo tokea leo”

“Una uhakika?”

“Niamini Randy”

“Hahaa sasa hivi unahitaji nikuamini, sio?”

“Ndio, kwenye haya mawili niliyo yafanya tafadhali ninakuomba sana uniamini”

Nikajishauri kwa sekunde kadhaa kisha nikatoka chooni humu. Nikasimama pembeni ya mlango huu wa choo, baada ya muda kidogo Jane akatoka huku akiwa katika hali yake ya unyonge. Taratibu akapitiliaza hadi kitandani, akachukua shuka kubwa na kujifunia.

“Leo hatuli?”

Niliuliza swali la mtego huku nikiwa ninamtazama bi Jane usoni mwake.

“Sijisikii kula”

“Ahaa kwa sababu ni mimi ndio ujisikii kula si ndio?”

“Jamani Randy, hivi kwa ukatili ulio ufanya mbele ya macho yangu unahisi nitakula. Hivi wewe ni binadamu gani wewe eheee?”

Bi Jane alizungumza huku akikaa kitako kitandnai mwake.

“Mkuki ni mtamu kwa nguruwe, ila binadamu munaona ni mchungu sana”

“Niondolee ujinga wako kama ni kunai ni bora unie bwana”

“Nahitaji chakula”

“Kapike mwenywe”

“Nahitaji unipikie”

“Randy….Randy…..Randy ohooo usinione nimekaa kimya ukanihisi mimi mjinga sana sawa”

Bi Jane alizungumza huku akininyooshera kidole cha mkono wake wa kushoto huku sura yake ikiwa imejikunja sana kwa hasira.

“Hahaaa shuka kitandani basi uniue na kunitafuna”

“Randy nitakufanya kitu ambacho hujawahi kufanywa kwenye maisha yako”

“Nifanye”

Nikakishuhudia kifua cha bi Jane kikipanda na kushuka kwa hasira. Taratibu nikamfwata kitandani alipo kaa, nikajaribu kumshika kidogo ila akautoa mkono wangu kwa hasira.

“Niache”

“Nikuache nini mpenzi wangu”

“Randy niache bwana”

Bi Jane alizungumza huku akiushika mkono wangu wa kulioa ambao nilishika ziwa lake, akaanga kuung’ata kwa nguvu zake zote, nikaumtazama kwa furaha huku nikisikilizia maumivu yake ya kuning’ata mkono wangu, sikuhiataji kutumia hasira kwa maana nahitaji amalize hasira yake yote katika mkono wangu. Baada ya dakika mbili akaniachia mkono wangu huku akiendelea kulia sana. Nikatazama damu zinazo anza kunichurizika kwenye sehemu hii aliyo ning’ata.

“Umeridhika”

Bi Jane akanijibu kwa kutingisha kichwa akimaanisha kwamba ameridhika. Akaushika mkono wangu huku akionekana kushangaa sana, akashuka kitandani kwa haraka, akafungua kabati lake na kutoa kisanduku kidogo, akakifungua na kutoa dawa kusafisha kidonda, akaanza kunihudumia kidonda hichi huku mara kwa mara akinitazama usoni mwangu kwa aibu. Akanifunga bandeji eneo hili.

“Randy”

Bi Jane aliniita kwa sauti ya upole sana.

“Naam”

“Naomba unisamehe mpenzi wangu, natambua ulifanya vile kwa ajili ya penzi lako kwangu”

“Usijali nimekusamehe mpenzi wangu”

“Kweli Randy”

“Ndio”

Taratibu bi Jane akanikumbatia huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake. Tukaanza kunyonyana midomo yetu taratibu, bi Jane alipo upeleka mkono wake katika jogoo wangu nikamzuia mkono wake.

“Vipi huna hamu na mimi”

“Ninanayo”

“Mbona umenizuia?”

“Pumzika kwanza kwa maana jamaa ametoka kukuhudumia”

“Hapana Randy, jamaa amekuja hapa ana tatizo”

“Ana tatizo gani?”

“Jogoo wake hasimami, sasa toka aje jatujafanya jambo lolote japo nilijitahidi kuhakikisha kwamba anasimama ila ameshindwa kabisa, na leo ndio tulipanga kwenda hospitalini akafanyiwe vipimo tujue ana tatizo gani”

“Una uhakika na kile ambacho unakizungumza?”

“Haki ya Mungu, dini yangu mkristo. Tumeishia kupeana mate tu”

“Jamaa kwani umemtoa wapi?”

“Ametoka Afrika kusini, ni Mtanzania anaye ishi kule”

“Mulikutana wapi?”

“Facebook”

“Doo sasa…..hahaa kwa hiyo wewe ukitongozwa Facebook tu una kubali?”

“Hapana Randy huyo mwanaume alinitongoza kabla hata mume wangu hajafariki, aliendelea kusubira ombi lake hadi juzi juzi nilivyo mkubalia na kumuomba aje Tanzania kunitembelea. Sasa kuja kwenyewe ndio yamemkuta haya yaliyo mkuta”

Nikamatazama bi Jane kuanzia juu hadi chini. Hakika mwili wake una mvuto wa kipekee, nikaanza kumuhisi jogoo wangu akifurukuta furukuta ndani ya suruali yangu. Nikamshika mapaja yake kwa haraka na nikayatanua, nikapandisha juu kijisketi chake kifupi alicho kiaa, nikaanza kumnyonya ikulu yake, nilipo hakikisha kwamba tayari amekaa mkao wa kula, nikavua nguo zangu na kuanza kumpa shuhuli pevu ili changanyikana na hasira. Bi Jane akamaliza kuzungumza lugha zote anazo zifahamu huku lugha hizo zikiambatana na vilio tofauti tofauti vya kimahaba. Hadi inatimu lisaa, ndio ninamaliza mzunguko wa awalo. Nikatazama saa ya ukutania na kukuta muda ukiwa umekwenda na wale watu ambao Dany ameniagiza nije kuwashuhuhuliki, muda wao wa kupokea mzigo uwanja wa ndege umefika, nikashuka kitandani kwa haraka na kuingia nafuni hadi bi Jane akanishangaa, nikaoga kwa haraka, kisha nikarudi chumbani na kuanz akuvaa nguo zangu kwa haraka.

“Mbona una haraka mume wangu unakwenda wapi?”

“Eheee?”

“Unakwenda wapi mbona mbio mbio hivyo?”

“Kuna kazi ninakwenda kuifanya usiku huu”

“Kazi! Kazi gani mume wangu?”

Nikamtazama bi Jane kwa muda kidogo, ila kutokana simuamini nikajikuta nikikaa kimya na kuendelea kuvaa nguo zangu hizi tayari kwenda kuifanya kazi ambayo kwa asilimia mia moja ina nihatarishia maisha yangu.



“Hupaswi kuifahamu kwa sasa”

Jibu langu likamfanya bi Jane kujawa na mshangao mkubwa sana.

“Ethan hembu niambie mpenzi wangu, kwa maana naona una silaha nyingi sana tofauti na nilivyo kuzoe”

“Hii ni kazi ya siri hapaswi mtu yoyote kuweza kufahamu. Endapo nitaimaliza nitarudi hapa kwako na nitahakikisha kwamba ninakueleza kila jambo linalo endelea sawa”

“Naweza kukuuliza swali, samahani lakini?”

Bi Jane alizungumza huku akikaa kitandani taratibu huku akitazama kwa umakini usoni mwangu.

“Wewe ni mwana usalama?”

“Kivipi?”

“Yaani ni mpelelezi?”

“Hahaaa….Hapana, mimi ni Randy kama Randy na nilisha kueleza historia ya maisha yangu. Sasa ni nini kingine unahitaji kufahamu.”

“Kwa matukio ya leo Randy, umekuwa ni mtu wa ajabu sana. Umekuwa ni mtu ambaye una unyama ndani yako, sijawahi kukutana na mtu kama wewe kwenye maisha yangu haya”

Nikamtazama bi Jane kwa sekunde kadha akisha nikatoka ndani humu pasipo kumjibu chochote.

“Ethan Ethan”

Bi Jane aliniita ila sikuweza kuitika, nikafika sebleni kwenye mlango wa kutokea, nikasimama na kumtazama.

“Mbona hunijibu mpenzi wangu, au kuna jambo baya nililo kuambia?”

“Hapana, nahitaji akili yangu sasa hivi kuielekezea katika kazi niliyo pewa, nikimaliza nitarudi hapa sawa”

“Sawa”

Bi Jane akanijibu kwa unyonge mkubwa sana, nikatoka ndani humu, nikaingia kwenye gari langu, taratibu nikalirudisha nyuma na kuliweka sawa barabarani na nikaanza safari ya kuelekea katika uwanja wa ndege. Nikiwa ndani ya gari nikasikia mlio wa simu, nikajipapa kwenye suti yangu na kuitoa simu niluyo pewa na professa ila ninakuta sio inayo ita. Nikaanza kuepuka pembeni ya siti yangu na kuikuta simu hii. Nikaitazama kwa muda kidogo kisha nikaipokea.

“Ulikuwa wapi muda wote Randy”

Niliisikia sauti ya Dany ikiniongelesha kwa ukali kidogo.

“Nilikuwa mbali na gari baba vipi?”

“Upo wapi?”

“Nipo njiani kwa sasa baba ninaelekea kwenye uwanaja wa ndege”

“Nimekutumia data za mtu ninaye muhitaji, hakikisha kwamba kazi inakwenda vizuri”

“Sawa baba”

“Tazama kwenye simu yako utaona picha ya Pacheko, hakikish a kwamba unamleta huyo tu”

“Sawa”

Dany akakata simu, nikafanikiwa kufika uwanaja wa ndege wa kimataifa wa mwalimua J.K Nyerere. Nikaanza kuipekua hii simu na kuanza kuoana magari ambayo yatatumika katuka katika kusafirishia mzigo wa madawa ya kulevya. Gari hizi ni lori moja ndago huku kikiwa na gari nyingine tatu za kifahari aina ya Range Rover. Nikaitazama vizuri picha ya Pacheko, pamoja na vijana wake ambao ameambatana nao katika kusafirisha mzigo huu.

Nikaa eneo hili kwa takribani kwa lisaa moja na nusu, nikaanza kuona gari hizi zikikipta katika moja ya barabara hapa uwanja wa ndege. Nikazifananisha gari hizi ili kupata uhakika zaidi na kweli ndio gari zenyewe, taratibu nikawasha gari langu la kuanza kuzifwatilia kwa umbali mkubwa kiasi ambao sio rahisi kwa wao kuweza kustukia kitu kinacho endelea. Simu hii ikaanza kuita, nikaipokea na kuiweka sikioni.

“Ndio baba”

“Tunakufwatilia kwa kila jambo hivi sasa na utakuwa unapokea maelekezo kupitia mimi”

“Kivipi?”

“Ninakufwatilia kupitia satelaite hivi sasa. Ninaona misafara yenu”

“Ahaa..sawa baba”

Nikaiweka loudspeaker simu yangu na nikaiweka pembeni yangu ili niweze kusikiliza ni kitu gani Dany naweza kunielekeza.

“Gari ya pili kutoka mbele ndio yupo Pacheko”

“Nimekupata boss”

“Ongeza mwendo kasi wa gari sasa”

“Alafu?”

“Unajua cha kufanya”

“Ngoja kwanza Dany, hii gari ina uwezo gani?”

“Hadi hivi sasa hujaweza kufahamu kwamba ina uwezo gani?”

“Mimi najua kuendesha ndio maaana nikakuuliza baba”

“Moja, haiingia risasi, si kwenye vioo, wala tairi zake. Kiufupi ni gari salama ukiwa ndani, uwezo wake wa spidi mita nahisi unaufahamu”

“Ndio”

“Haya sasa fanya kazi yako sasa”

Nikachomoa bastola yangu moja na kuiweka katika siti ya pembeni. Taratibu nikaanza kuongeza mwendo kasi wa gari hilina kuanza kuyasogelea magari jambo ambalo nikamini lazima limeanza kuwapa mashaka, nilipo karibia kufika karibu dereva wa gari ya nyuma akaanza kunizibia njia, jambo ambalo linaashiria kwamba tayari wahusika wamesha nistukia. Wakachomoka kidogo watu wawili kwenye vioo na kuanza kunishambulia kwa risasi. Sikulijali hilo kwani hakuna hata risasi hata moja ambayo imeweza kuingia ndani ya gari hili. Sikuhitaji kuwashambulia watu wake kwani sio watu ninao wahitaji. Kitu cha kumshukuru Mungu barabara hi ni kubwa sana jambo ambalo lilinifanya niweza kuzipita gari hizi mbili za nyuma ikiwemo hili lori moja. Dereva wa gari la mbele akapunguza mwendo kidogo na kumpa nafasi gari alilo pamba pacheko kupita mbele huku wengine wakiwa na kazi ya kunizuia na kulishambulia gari langu.

Dereva wa lori naye akaanza kuligonga gari langu kwa nyuma, huku madereva wengine wakihitaji kunibananisha gari langu kwa kuliweka katikati.

“Achana nao, anaye takiwa hapo ni Pacheko”

Niliisikia sauti ya Dany ikinipa maelekezo hayo.

“Poa”

Nikaongeza mwendo kasi wa gari langu, taratibu nikaanza kuwapita watu hawa, huku kila mara nikihihakikisha kwamba ninawaepuka watu hawa. Nikafanikiwa kuziacha gari hili na kulifukuzia gari alilo panda Pacheko. Dereva anaye endesha gari la Pacheko akakunja kona moja kali sana na kulifanya gari hilo kuyumba kidogo kisha wakaendelea na spidi, nikameza fumba zito la mate, kisha nami nikakata kona hii na kuifanya gari yangu kuserereka kwa kiwango kikubwa, nikajitahidi kardi ya uwezo wangu hadi gari likaa sawa. Nikaendelea kulifukuzia gari la Pacheko huku gari moja la watu wa Pacheko likiwa nyuma yangu kwa mwendo kwa kasi sana.

“Dany nitafanya nini bado wananifukuzia nyuma”

“Usijali wewe zidi kusonga mbele”

“Naomba unitumie ramani ya hili jiji, nahitaji kuona ni wapi wanaelekea”

“Sawa tazama kwenye gari lako tayari Jojo ameituma”

Katika tv ndogo ya gari langu nikaona ramani inayo onyesha jiji hili jinsi lilivyo. Pia nikaona gari la Pacheko sehemu linapo elekea. Nikafunga breki za gafla huku nikiligeuza gari langu sehemu ninapo tokea. Watu wa Pacheko wanao nifukuzia wakajikuta wakifunga breki za gari lao na kusimama mita kadhaa huku wakiwa wamejwa na mshangao kwani gari zetu zina tazamani. Nikafungua mkango wa gari hili huku nikiwa nimeishika bastola yangu niliyo kuw animeiweka katika siti yangu ya pembeni.

Nikaanza nza kuwashambulia huku nikzidi kuwafwata uzuri wa gari lao linapitisha risasi. Nikawaua watu wote waliomo ndani ya gari hili. Nikarudi ndani ya gari langu, nikaligeuza huku nikitazama gari la Pacheko ni wapi linapo elekea. Nikaanza kupitia barabara za mitaani huku nikihakikisha kwamba ninawahi kulitokezea kwa mbele gari la bwama Pacheko.

Mahesabu yangu niliyo yafikiria yakawa na uhakika, kwani baada ya muda nikanikiwa kufika katika moja ya barabara huku nikilisubiria gari la Pacheko kupita mbele ya barabara iliyo mbele yangu.

“Randy unahitaji kufanya nini?”

“Tulia baba”

“Usitake kuni……”

Kabla Dany hajamaliza kuzungumza sentensi yake, tayari nilisha liruhusu gari langu kwa kasi kubwa na kuligonga gari la Pacheko katika eneo la uvauni na kuliburuza gari lao hadi kwenye mtaro ulipo pembezoni mwa barabara.

Nikashuka kwenye gari langu huku nikiwa na bastola mkononi mwangu. Nikafungua mlango wa nyuma wa gari hili alipo kaa Pacheko, ambaye amepoteza fahamu kwani ajali hii niliyo isababisha ni kubwa sana kwao na hawakuitegemea kuwapata kwa wakati huu. Nikamtoa nje ya gari Pacheko, nikamvuta hadi lilipo gari langu, nikamuingiza ndani ya gari kisha nikazunguka upande wa pili wa gari hili, nikaingia na kuondoka eneo hili kwa kasi.

“Nimempata muhisika”

“Kazi nzuri, je upo salama?”

“Ndio baba”

“Sasa nenda ukamuweke kwenye nyumba uliyo panga”

“U…unataka kuniambia nimpeleke nyumbani kwa Jane?”

“Pale umepanga wewe, kamuweke hapo hadi pale nitakapo kupa malekezo mengine.”

“Kwa nini sije naye huko baba?”

“Kumbuka niliyo kueleza pale awali. Mtu huyo ana muunganiko mkubwa sana na serikali. Vibaraka wake wengi wanaweza kukusababishia wewe matatizo pale utakapo kuwa njiani. Hivyo hakikisha kwamba hakuna anaye jua wewe ni muhusika wa hili tukiio umeniele?”

“Nimekupata baba”

Nikamtazama Pacheko, huku nikiendelea na safari yangu. Nikachukua simu niliyo pewa na Professa, nikampigia bi Jane.

“Hei”

“Randy upo salama”

“Nipo salama, upo wapi kwa sasa?”

“Nimelala mpenzi wangu”

“Funguo za nyumba unazo?”

“Ndio ninazo vipi?”

“Nazihitaji”

“Sasa hivi?”

“Ndio”

“Mmmmm kwema lakini?”

“Kwema ila nahitaji funguo”

“Sawa njoo uzichukue basi nyumbani?”

“Hapana siwezi kuja huko nahitaji kuzikuta nyumbani kule”

“Sawa”

Nikakata simu na kuirudisha mfukoni.

“Una muamini uliye wasiliana naye”

Niliisikia sauti ya Dany kwenye simu ambayo ipo pembeni yangu.

“Kwa asilimia kadhaa”

“Sawa”

Baada ya dakika kama kumi na tano hivi nikafika nyumbani kwangu. Nikasimamisha gari langu mbele ya geti la nyumba hii, baada ya dakika tano gari la bi Jane likasimama nyuma ya gari langu, nikashuka kwenye gari.

“Randy vipi?”

Bi Jane alizungumza huku akiwa ameshuka kwenye gari.

“Fungua geti”

Nilizungumza huku nikurudi kwenye gari, bi Jane akafungua geti hili, nikaingiza gari langu kisha naye akaingiza gari lake na kulifunga geti.

“Randy huyu ni nani?”

Bi Jane aliniuliza huku akishuhudia jinsi nilivyo mbeba Pacheko begani mwangu huku akiwa bado hajajitambua.

“Acha kelele”

Nilizungumza huku nikiendelea kuelekea ndani, nikamuingiza pacheko kwenye moja ya kiti. Nikamkalisha kwenye kiti kilichopo humu ndani.

“Kaniletee kamba”

“Sawa”

Bi Jane akatoka ndani humu, baada ya muda akarudi akiwa na kamba mkononi mwake. Nikamfunga Pacheko kamab hii, nilipo hakikisha kwamba hawezi kuondoka eneo hili, nikamgeukia bi Jane.

“Mbona unashangaa sana?”

“Randy unajua huyu ni nani!!?”

Bi Jane aliniuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Vipi wewe unamjua?”

“Haki ya Mungu Randy huyu ni mtu hatari sana, maisha yetu hayawezi kuwa salama. Nakuapia vile”

“Kama unaogopa nenda nyumbani ukapumzike”

“Randy kuna vitu vya kuletea ubishi ila huyu namsikia tu na nilisha wahi kuona picha yake mara moja. Mwenyewe anajiita Mungu”

“Mungu……!! Mungu wa nini?”

“Mungu wa madawa ya kulevya hakuna ambaye anaweza kumgusa, sasa wewe umeshikwa na nini hadi ukaingia kwenye kumi na nane zake?”

Nikamtazama bi Jane kwa nuda kidogo. Gafla tukaanza kusikia ving’ora vya gari za polisi, kwa haraka nikakimbilia dirishani na kuchungulia, nikashuhudia gari kama sita za polisi zikiwa getini na mbaya zaidi juu kuna helicopter kama mbili za polisi zikiimulika nyumba hii kwa tochi kubwa zenye mwanga mkali sana, jambo lililo tufanya mimi na bi Jane kujawa na woga mkubwa sana.



Nikaitoa mfukoni simu ambayo ninatumia kuwasiliana na Dany. Nikampigia, simu haikumaliza hata sekunde tano ikapokelewa.

“Baba tumevamiwa na maaskari”

“Ohoo Mungu wangu ni kitu gani kilicho tokea”

“Sijajua baba”

“Hana saa mkononi huyo mtu”

Nikamtazama Pacheko mkononi mwake na kukuta ana saa, nikamvua kwa haraka na nikaona saa hii ikiwa na ina waka alama nyekundu kwa chini jambo lililo nistua sana.

“Ndio saa yake inawaka taa nyekundu na kuzima”

“Ohoo, sasa ivunje hiyo saa na hakikisha kwamba munatoka katika hiyo nyumba kabla hamjakamatwa na hao askari”

“Na huyu Pacheko?”

“Hakikisha kwamba una ondoka naye”

“Baba”

“Nakuami mwanangu hakikisha kwamba una ifanya hiyo kazi niliyo kuaambia sawa”

Nikakata simu kwa maana nimekosa msaada wowote kutoka kwa baba yangu Dany.

“Hakuna sehemu ambayo tunaweza tukatorokea?”

“Kwenye hii nyumba?”

“Ndio”

Bi Jane akafumba macho taratibu huku akionekana kufikiria ni wapi tunaweza kutorokea. Nikakimbialia dirishani na kuona askari walio valia nguo nyeusi wakishuka kutoka kwenye helicopter wakitumia kamba wakidhamiria kuingia ndani ya hii nyumba.

“Nimekumbuka”

Bi Jane alizungumza huku akianza kutoka ndani humu, kwa haraka nikamfungua kamba Pacheko na kumbeba begani mwangu, nikaiweka saa juu ya meza. Nikaanza kumfwata bi Jane kwa nyuma, kabla hatujafika sehemu aliyo kusudia mimi na yeye kuweza kufika, nikasimama katika mlango wa chumba changu, nikalitazama kabati ambalo niliweka begi la pesa zangu. Nikaingia ndani ya chumba hichi nikalipiga risasi mbili kufuli la kabati na likavunjika, nikafungua kabati hili na kukuta begi langu likiwa kama nilivyo liweka, nikalivaa mkanda mmoja na kuanza kutoka ndani humu.

“Huku”

Bi Jane alizungumza huku tukiingia jikoni, akafungua moja ya kabati la vyombo.

“Ni wapi sasa”

“Subiri”

Bi Jane alizungumza huku akisogeza glasi hizi nyingi, nikaona batani nyinyi kwenye eneo hili alilo toa glasi, akaanza kuminya batani kadhaa na kabati hili likaanza kugawanyika katika sehemu mbili na kutufanya tuone mlango wa kupita. Bi Jane akawa mtu wa kwanza kuingia ndani ya eneo hili kisha nikafwatia mimi huku nikiwa nimembeba Pacheko pamoja na begi langu la pesa. Eneo zima hili lenye barabara iliyopo chini ya ardhi ikaanza kuwaka taa zenye mwanga hafifu kidogo.

“Unapaacha wazi?”

Bi Jane akarudi kwa haraka na kuminya moja ya batani na mlango ukajifunga na tukaanza kukimbia katika njia hii huku bi Jane akiwa mbele, tukafika sehemu na kukuta boti ndogo ikiwa imeegeshwa pembeni, tukaingia ndani ya boti hii na kuondoka eneo hili huku bi Jane akiwa ndio dereva wa hii boti hiii.

“Tunaelekea wapi?”

“Zanzibar?”

“Tutafika kweli?”

“Ndio”

“Mmmmm”

“Hatuna sehemu ya kwenda zaidi ya visiwani humu. Huku Tanzania bara hali sio nzuri kiusalama wetu”

“Sawa”

Pacheko akaanza kufumbua macho yake huku akionekana kujawa na mshangao kiasi kuanza kukaa kitako.

“Nipo wapi hapa?”

Pacheko aliuliuliza huku akinitazama usoni mwangu nikampiga na kwa kutumia kitako cha bunduki kichwani mwake na akapoteza fahamu tena. Safari ya kuelekea visiwani Zanzibar ikatuchukua masaa zaidi ya matano. Bi Jane akasimamisha boti hii ndogo pembezoni mwa fukwe ambayo imetulia sana, mwanga wa mbalamwezi ukanifanya niweze kuona eneo hili vizuri.

“Hapa ni wapi?”

“Tunapandishi hichi kilima kidogo hapo juu kuna nyumba yangu, huwa ninaitumia kwa mapumziko”

“Ahaa sawa”

Nikambeba Pacheko begani huku bi Jane akibeba begi langu lenye pesa, tukaanza kutembea katika fukwe hii na kupandisha katika kilima hichi kidogo na nikaona nyumba moja kubwa iliyo jengwa vizuri, tukaingia katika jijigeti kidogo.

“Ina ishi watu humu?”

“Kuna wafanyakazi tu huwa ndio wanaifanyia uangalizi kila mwisho wa wiki”

“Sawa sawa”

Bi Jane akanyanyua moja ya chungu cha maua, akatoa funguo kisha akakirudisha chungu hichi sehemu alipo kituo kisha tukaingia ndani ya nyumba hii.

“Naweza kupata chumba cha kumuhifadhi huyu mtu?”

“Ndio”

“Naomba unionyeshe”

Bi Jane akanionyesha moja ya chumba ambacho hakina kitu kabisa. Nikamuagiza aniletetee kiti pamoja kamba ambayo nitaweza kumdhibiti Pacheko. Bi Jane akafanya kile nilicho muagiza, nikamvua Pacheko nguo zake zote na kumuacha na boksa.

“Akizinduka itakuwaje mume wangu?”

“Nitajua nini cha kufanya akizinduka”

Tukatoka ndani humu na kurudi sebleni. Bi Jane akaniomba anitembeze kwenye hii nyumba ili niweze kuijua vizuri. Tukaitembea nyumba hii usiku huu wote na kuimaliza, tukarudi ndani na kujisafisha miili yetu kwa kuoga.

“Randy”

“Naam”

“Gari langu limekutwa kwenye ile nyumba pale, houni nami nitachanganywa kwenye hili tatizo?”

“Sidhani, wewe si unajulikana kama mmiliki wa ile nyumba?”

“Ndio”

“Sasa ni jambo la kawaida gari lako kuonekana kwenye moja ya nyumba zako. Ngoja kesho tutahakikisha kwamba tunaifwatilia hii habari kwenye tv.

“Je baba yako mbona hujamfahamisha kwamba upo salama?”

“Atanitafuta yeye mwenyewe. Nashukuru Mungu kwamba nipo salama”

“Sawa”

***

Habari ya Pacheko mfanya biashara mkubwa nchini Tanzania kupotea katika mazingira ya kutatanisha ikazidi kupamba moto huku mstukiwa wa tukio hilo la utekaji ikisemekana kwamba bado hajulikani na uchunguzi wa polisi unaendelea.

“Nilikuambia, laiti kama tungekuwepo Dar es Salaam sasa hivi tungekuwa matatani”

“Ni kweli”

“Sasa huyu mtu tutamfanyaje?”

“Tutaendelea kumshikilia humu ndani, na leo nitawasiliana na Dany tujue tunafanya nini?”

“Kwa nini baba yako ameamua kumkamata huyu mtu?”

“Sijajua”

Mlio wa simu yangu ukakatisha mazungumzo yangu na bi Jane, nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Ndio baba”

“Upo Zanzibar?”

“Ndio”

“Nahitaji kuonana na wewe leo hii mchana peke yako”

“Ila baba mimi sio mwenyeji sana katika eneo hili”

“Nitakuelekeza uweze kufika”

“Nije na muhisika?”

“Nitakuja kumchukua usiku”

“Sawa”

Nikakata simu na kumtazama bi Jane.

“Vipi?”

“Dany anahitaji niweze kuonana naye”

“Sawa tutakwenda”

“Anahitaji nionane naye nikiwa peke yangu”

“Mmmm…..”

“Ndio nitatumia moja ya gari lako”

“Sawa”

Bi Jane akaandaa kifungua kinywa cha asubuhi hii. Ilipo fika mida ya mchana, nikajiandaa kwenda kuonana na Dany, sehemu alipo nitajia tukutane.

“Ninahitaji huyu mtu awe salama, sihitaji uingie ndani ya hichi chumba, sihitaji akushawishi ukamfungulia umenielewa sawa?”

“Sawa mume wangu niamini sinto fanya jambo lolote kinyume na wewe”

“Nakuamini”

Bi Jane akanikabidhi funguo ya gari, nikamuachia bastola moja ili hata kama kuna jambo lolote baya litajitokeza basi aweze kukabiliana nalo. Nikaondoka eneo hili na kuanza kufwata maelekezo ambayo Dany ananipatia, nikafika katika hoteli moja ya kitalii na kumkuta akiwa amekaa kwenye moja ya kiti huku akinywa juisi taratibu. Kwa ishara akanionyesha nikae kiti cha pembeni, taratibu nikaka hukun nikimtazama usoni mwake.

“Nimekuja mara moja kukuona, kuna mgeni yupo nyumbani ananisubiria”

“Wale vijana?”

“Ndio yupo yule wa kike ila wa kiume yupo Dar es Salaam na dada yako Jojo”

“Sawa kazi nimeikamilisha na ninahitaji kurudi nyumbani sasa?”

“Bado kazi inaendelea ndio kwanza umeianza?”

“Nimeianza baba?”

“Ndio”

Baba akatoa picha ya mzee mmoja ambaye asili yake ni ya kiarabu.

“Anaitwa Mudathiri Yahaya, ni mfanya biashara mkubwa sana hapa Zanzibar. Anashuhulika na kutoa bidhaa nchini Oman, Dubai na kuleta hapa Zanzibar”

“Sasa nimfanye nini huyu?”

“Nahitaji afe?”

“Afe!!?”

Niliuliza huku nikiwa nimejawa na mstuku kiasi.

“Ndio”

“Kwa nini unahitaji niumuue?”

Danya akatoa picha ya mama na kunikabidhi.

“Unazikumbuka safari za Dubai za mama yako?”

“Ndio ninazikumbuka”

Dany akatoa picha nyingine, inayo muonyesha mfanya biashara huyu akiwa katika pozi la mahaba mazito na mama yangu Yemi.

“Sasa baba sababu ya kumuua mzee huyu ni nini haswa”

Dany akanitazama kwa sekunde kadhaa usoni mwangu huku akionekana kujawa na mawazo kiasi.

“Baba”

“Mmmmmmm”

“Unahitaji kumuua mama kwa ajili gani?”

“Sihitaji mama yako awe na mahusiano na mwanaume wa aina yoyote?”

“Heee sasa baba, wewe na mama si hamuna mahusiano ya aina yoyote si ndio?”

“Hiyo sio poiti ya msingi ninacho kuhitaji ni kuhakikisha kwamba una muua huyu hawara wa mama yako umenielewa?”

Dany alizungumza kwa msisitizo mkubwa sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Baba hii ni vita ya kimapenzi sasa ambayo umeianzisha kati yangu na mama yangu. Bora vibaki vita vingine kati yangu na mama ila si kumuingilia katika muhusiano ya kimapenzi baba”

“Mimi na wewe nani ni baba?”

“Wewe”

“Sasa nahitaji u……..”

Dany akapata kigugumizi huku macho yake yote akitazama nyuma yangu jambo ambalo lilinifanya nami kugeuka nyuma ili kuweza kutazama anacho kiangalia kwa msisitizo. Nikapatwa na mshtuku mkubwa sana mara baada ya kumuona mama akiwa ameongozana na mwanaume ambaye baba aliniagiza nimuue dakika kadhaa tu zilizo pita wakijiandaa kukaa kwenye meza ya karibu yetu. Macho yetu yakagongana na macho ya mama jambo lililo sababisha mstuko mkubwa kwa mama hadi akashindwa kukaa kwenye kiti alicho panga kukikalia na akabaki akitutazama hadi mwanaume wake aliye ongozana naye kwa sasa naye akabaki akitutazama pasipo kuelewa ni kitu gani kinacho endelea kati yetu sisi watatu.



Dany akataka kusimama ila nikamuwahi mkono na kumzuia asimame.

“Nini sasa baba”

“Hii kazi acha niifanye mimi mwenyewe sasa hivi”

“Baba tazama eneo lenyewe hili, kuna watu wa kila aina. Unataka kuingia kwenye rekodi ya kutafutwa kama huko zamani. Achana na mama bwana”

Niliendelea kumuhimiza Dany kwa msisitizo, nikageuka nyuma na kumuona mama na mzee huyo wakiondoka katika eneo hili kwa haraka sana huku mama kwa muda wote akiwa anatazama nyuma nyuma. Dany kwa haraka akanyanyuka na kuanza kutembea kuelekea kule alipo kwenda mama na mwanaume wake, nikanayanyuka nami huku nikianza kutembea kwa haraka huku nikihimiza baba awe mpole na asiweze kufanya jambo lolote baya kwa mama. Tukafika nje na kushuhudia gari la walilo panda mama na mwanaume wake likiondoka kwa kasi. Dany akakimbilia kwenye gari lake na kupanda, nami nikaingia kwenye gari lake ili niweze kwenda kushuhudia ni kitu gani ambacho kinakwenda kutokea katika mtanange huu.

“Baba ila tambua kwamba wewe na mama kwa sasa hamuna mahusiano ya kimapenzi”

“Randy kaa kimya”

Dany alizungumza kwa sauti nzito na kunifanya nikae kimya kabisa. Kwa mwendo kasi anao endesha Dany tukaanza kulikaribia gari alilo panda mama. Dereva anaye endesha gari la mama naye akaanza kuongeza mwendo kasi mara baada ya kustukia kwamba anafwata kwa nyuma.

Dany akatoa bastola yake kiunoni na kuishika mkononi huku nikimuona misuli ya mikononi mwake jinsi inavyo kaza na dhairi ana hasira na uchu wa kuweza kumpata mwaume anaye tembea na mama.

“Baba”

“Nimekuambia kwamba kaa kimya”

Dany alizungumza kwa kufoka sana na kunifanya nikae kimya na kugairi lile nililo kuwa nimepanga kumueleza. Kitu alicho kikosea dereva wa gari la mama ni kuliendesha gari hilo kueleekea katika barabara ambayo haina magari mengi. Dany kwa utaalamu mkubwa akaanza kulipita gari la mama taratibu kisha kwa kasi kubwa akali geuza gari letu na kufunga barabara nzima na kumfanya dereva kusimamisha gari hilo. Dany akashuka kwa haraka kwenye hili gari na kuanza kufyatua risasi kadhaa kwenye tairi za gari la mama na mumewe na kuyafanya matairi yote kuishiwa na upepo.

Nami nikashuka kwenye gari hili huku nikimshuhudia Dany akifungua mlango wa nyuma na kumchomoa mwanaume wa mama, mlinzi wa mama ambaye ndio dereva akashuka huku akiwa ameshika bastola, lengo lake ni kumshambulia Dany.

Nikachomoa bastola yangu kiunoni na kumpiga mlinzi wa mama risasi ya mkono ulio shika bastola yake na kumfanya angushe bastola yake huku akigugumia kwa maumivu makali.

Hadi ninafika katika sehemu ambayo yupo Dany, nikamkuta mwaume wa mama, uso wake ukiwa umechakaa kwa damu. Nikafungua mlango wa mama na kumkuta mama akiwa anatetemeka mwili mzima. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa, nikataka kuufunga mlango ila mama akaniita.

“Na…a…om…ba umsa…idi…e ba…..”

Mama alizungumza kwa kigugumizi, nina imani kwamba hakutarajia kukutana nasi katika siku ya leo na mbaya zaidi ni kwamba alisha alisha nikana siku nilipo kuwa nimekamatwa na kundi la Al-Shabab ambalo alikuwa akilihudumia kwa fedha.

Sikumjibu kitu chochote zaidi ya kuzunguka upande alipo Dany.

“Baba kama ni kuondoka naye ni vyema tukaondoka naye muda huu”

Dany akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kuburuta mwanaume huyu hadi kwenye gari lake, akafungua buti ya gari lake na kumuingiza mwanaume huyu.

“Hili litakuwa ni fundisho kwa mama yako”

Dany alizungumza kwa sauti ya mikwaruzo na kuingia ndani ya gari lake. Nikageuka nyuma na kumkuta mama akiwa amesimama nje ya mlango wa gari lake huku akimtazama mlinzi wake anaye endelea kuugulia kwa maumivu.

“Randy”

Mama kwa mara nyingine aliamua kuniita pale alipo niaona ninashika mlango na kutaka kuingia ndani ya gari la Dany.

“Kwa nini unamfwata baba yako eheee?”

Maneno ya mama kidogo yakanifanya nicheke kichini chini, nikaanza kutemeba huku nikimfwata sehemu nilipo simama.

“Samahani mama, Randy ambaye ulikuwa unamjua, tayari amesha kufa siku nyingi sana. Tafadhali ninakuomba uniache, nakuomba usinifikirie kabisa kwenye maisha yako. Ulisha nikana siku nyingi, sasa mimi sina haja kwako umenielewa mama”

“Randy sikukukuza uwe hivyo. Tazama unyama anao ufanya baba yako, kwa nini lakini?”

“Ulinikuza ili nitembee uchi mbele ya wafanyakazi wako si ndio. Uliendeleza maisha yako ila mimi hukunipenda hata theluthi. Ulisahau kwamba ulinikana mimi mbele ya wale magaidi wako. Sasa mimi wa nini sasa. Tafadhali mama, nina kuheshimu na wewe nina kuomba uniheshimu. Sikufahamu, samahani”

Mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo nikaondoka katika eneo hili na kuingia katika gari la Dany na kuondoka eneo hili.

“Mama yako ni kigeu geu sana”

Dany alizungumza huku akiendelea kuongeza mwendo kasi wa gari hili. Tukafika katika moja ya nyumba, akapiga honi na geti likafunguliwa taratibu akaingiza gari hili kisha tukashuka.

“Ni nani aliye fungua geti?”

Nilimuuliza Dany huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana.

“Limejifungua lenyewe. Hili geti nimelitegesha katika mfumo ambao gari zangu zote ndio zinaweza kuingia ndani humu kwa kupiga honi”

“Mmmm!!!”

“Nani amekutengenezea?”

“Ni Professa”

Dany akamfungua buti ya gari na kumshusha mwanaume huyu wa mama, akaanza kumburuza hadi ndani. Akamsukumia kwenye moja ya chumba.

“Inabidi twende hivi sasa nikamchukue yule mshenzi mwengine kule.”

“Huyu hato weza kutoka humu ndani?”

“Hawezi kabisa”

Tukarudi kwenye gari na tukaianza safari ya kurudi hotelini. Hatukuchukua muda mrefu sana tukafika hotelini, nikaingia kwenye gari langu na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwa Bi Jane. Tukafika nyumbani kwa bi Jane na kumkuta akitusubiria nje.

“Nenda kamlete mimi utanikuta hapa kwenye gari”

Dany alizungumza huku akiwa ndani ya gari lake.

“Sawa”

Nikamfwata bi Jane sehemu alipo simama na nikasalimiana naye.

“Vipi yupo?”

“Ndio, ila nina ogopa mpenzi wangu”

“Unaogopa nini?”

“Baba yako yupo hapa na amenikuta na wewe jamani huoni kama inaweza kuwa tatizo?”

“Hapana usijali nilisha mueleza juu ya swala letu”

“Una uhakika Randy?”

“Niaminini mpenzi wangu”

Nilizungumza huku nikitangulia kuingia ndani, nikapitiliza moja kwa moja hadi katika chumba cha Pacheko na kumbeba begani mwangu na kutoka naye nje. Nikamuingiza katika buti ya gari la Dany kisha nikalifunga.

“Utakaa hapa kwa muda gani?”

Dany aliniuliza huku akiwa ameshusha kioo cha gari lake.

“Nitakaa hapa kwa muda kidogo niipumzishe akili yangu kuna mambo mengi sana nahitaji kuyafikiria kwa sasa”

“Kama?”

“Maisha tu baba”

“Achana na hayo mambo. Tumezaliwa ili kuishi na kufa ni moja ya sehemu katika masiha ya mwana damu. Nikifika nchini Tanzani nitakupatia moja ya kazi uweze kuifanya.”

“Kazi gani?”

“Nitakuambia pale nitakapo fika”

“Huyu Pacheko naye unafanya naye nini?”

“Nitakueleza”

Dany akapandisha kioo cha gari lake na kuondoka eneo la nyumba hii.

“Ohoo asante Mungu huyu mtu ametuondokea humu ndani mume wangu kwa maana sikuwa na amani kabisa”

“Usijali mke wangu kila jambo sasa lipo vizuri.”

“Ila baba yako anakwenda kumfanya nini mtu yule?”

“Sijajua, kwa kuwa yupo mikononi mwake, basi watajua wao wenyewe huko”

“Sawa”

“Haya mwaya”

***

Alfajiri na mapema nikastuliwa kutoka usingizi kwa mlio wa simu yangu niliyo iweka pembezoni mwa kitanda changu. Taratibu nikaichukua huku nikimtazama bi Jane aliye lala pembeni yangu. Nikatazama kioo cha simu yangu hii na kukuta ni namba mpta ndio inayo nipigia. Nikakaa kitandani huku nikiwa nimempa mgongo bi Jane. Nikaitazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Nashukuru sana kwa kile mulicho kifanya wewe na baba yako. Ila Randy ninakuahidi kitu kimoja. Nitahakikisha kwamba wewe na baba yako mutalipa kwa hili mulilo litenda. Haki ya Mungu nina apa lazima mulipe”

Niliisikia sauti ya mama akizungumza huku akionekana dhairi kwamba analia.

“Kati vita yako na Dany mimi musinihusishe tafadhali nakuomba unifute kwenye maisha yako kama nilivyo kueleza”

“Kama ulivyo nieleza si ndio, sasa ikitimu saa nane mchana naamini kwamba utaiupata na wewe meseji yako. Kwaheri”

Simu ya mama ikakata na kunifanya nibaki na mshangao mkubw sana. Bi Jane akanigusa mgongoni mwangu na kujikuta nikistuka kidogo huku nikimtazama.

“Kuna nini mpenzi wangu?”

Bi Jane aliniuliza kwa sauti iliyo jaa uchuvu utokanao na usingizi.

“Hakuna kitu mpenzi tulale”

“Unanificha?”

“Hapana mpenzi”

Nilizungumza huku nikijilaza tena kitandani, nikajifunika shuka, kabla hata sijairudisha simu yangu pembezoni mwa kitanda, ikaita tena, nikaitazama kwa haraka na kukuta namba ya Dany ndio inayo nipigia. Nikaipokea huku nikiwa nimekaa.

“Upo Zanzibar bado?”

“Ndio vipi?”

“Sasa hakikisha kwamba leo hii unaondoka huko Zanzibar”

“Na kuelekea wapi baba?”

“Huku usije, ila utajua ni wapi kwa kwenda?”

“Mmmm kuna nini kinacho endelea?”

“Mama yako tayari amesha wapa habari kundi la Al-quida na sasa hivi amaemua kuanzisha vita na sisi. HIvyo kuwa tayari kwa lolote. Mpenzi wako wa zamani Hawa sasa yupo nchini Tanzania”

Nikajikuta mwili mzima kama ukipigwa shoti, nikatulia kimya huku bi Jane akinitazama usoni mwangu akionekana akihitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kinatatiza.

“Mwanangu sasa vita imeanza”

Simu ikakatika na kujikuta nikiwa nimejawa na upole mkubwa sana.

“Randy kuna kitu gania ambacho kinaendelea?”

“Eheee?”

“Ni nini kinacho endelea mpenzi wangu?”

“Kuna…kuna….kuna…..”

Nikajikuta nikishindwa hata kuzungumza kwani habari hii sio nzuri kabisa masikioni kwa bi Jane.

“Tafadhali Randy nakuomba uweze kunieleza mpenzi wangu. Tambua kwamba matatizo yako ni yangu, natakiwa kuweza kukusaidia kwa kila jambo”

“Nakuomba kwa sasa uweze kurudi nchini Tanzania?”

“Kwa nini?”

“Kuna hali ya hatari ambayo inakwenda kutokea. Unakumbuka nilikueleza juu ya maisha yangu ya zamani si ndio?”

“Ndio”

“Sasa maadui zangu wapo nchini Tanzania, wamekuja kwa ajili yangu na wameungana na mama yangu kuhakikisha kwamba wana niangamiza”

Bi Jane mdomo ukambaki wazi, kwani hili nililo mueleza ni baya kwetu sote.

“Nahitaji uwe salama, sihitaji uweze kuangamia kwa ajili yangu. Sehemu ambayo wewe utakuwa salama ni Tanzania tu, na mimi naomba uniache niweze kuendelea na maisha yangu.”

“Randy…..”

“Hakuna jinsi Jane, mimi nina windwa na mbaya zaidi ni juzi tu baba alifanya jambo baya sana kwa mume mpya wa mama”

“Alifanya jambo gani?”

Bi Jane alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Alimuua”

Bi Jane akazidi kujawa na mshangao, mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa woga.

“Ndio maana ninakuambia kwamba sasa hivi nipo kwenye wakati wa kuwindwa, kabla mama yangu hajakutambua wewe ni vyema ukaondoka na kuniacha kwa maana vita yake naamini ataipiga kwa wale watu ninao wapenda ikiwemo wewe”

Maneno yangu yakazidi kumnyong’onyeza bi Jane na kujikuta akiangua kilio kizito huku akinikumbatia kwa nguvu.

“Randy nina ogopa mpenzi wangu”

“Najua una ogopa ila ni muda wa mimi kuwa mwenyewe, kupambana mwenyewe. Tafadhali nakuomba ukusanye kila kitu unacho hisi utakitumia ukiwa Tanzania na uniache na hii nyumba yako.”



Bi Jane akawa kama mtu aliye shikwa na bumbuwazi, maamuzi yanngu ni magumu sana kwa kila mmoja wetu. Uwepo wa mwana mama huyu kwenye maisha yangu, unanisaidia sana kwenye mambo mengi.

“Randy siwezi kukuacha, sitaki kukuacha mpenzi wangu nahitaji kuendelea kuwa nawe”

Bi Jane alizungumza hukua akimwagikwa na machozi usoni mwake. Nikamshika mashavu yake huku nikiusogeza uso wake karibu sana na uso wangu.

“Tafadhali Jane sihitaji kabisa uhusike katika vita hii, tafadhali ninakuomba uweze kunielewa sawa”

Nilizungumza kwa msisitizo huku machozi yakinimwagika usoni mwangu.

“Nakuomba mpenzi wangu, linda penzi langu na nikimaliza nakuahidi nitakufwata popote pale ulipo”

Bi Jane akaitoa mikono yangu usoni mashavuni mwake na kushuka kitandani. Akatembea hadi kwenye dirisha la hapa chumbani, akafungua pazia na kutazama nje huku akiendelea kulia kwa uchungu. Nikamatazama kwa sekunde kadha akisha nikashuka kitandani na kumfwata. Taratibu nikamkumbatia kwa nyuma huku nikiwa na huzuni kubwa sana.

“Randy najua huto rudi kwa ajili yangu”

“No nina kuapia kwa mwenyezi Mungu, nitahakikisha kwamba nina rudi kwa ajili yako mpenzi wangu. Tambua kwamba wewe ndio kila kitu kwenye maisha yangu. Ninakupenda, nina kujali na nina kuheshimu mpenzi wangu. Tafadhali ninakuomba sana, nipo chini ya miguu yako, rudi Tanzania sawa mpenzi wangu?”

Bi Jane akanitazama, kisha taratibu akatingisha kichwa huku akimaanisha kwambaa menielewa. Taratibu nikamgeuza na tukakumbatia.

Tukaanza kunyonyana midomo yetu taratibu huku kila mmoja akionyesha ni jinsi gani alivyo jawa na huzuni iliyo changanyika na hisia kali sana kati yetu. Nikaushusha mkono wangu mmoja hadi kwenye kitumbua chake na kuanza kukishika taratibu na kusababisha bi Jane kuzidi kutoa miguno ya kimahaba. Tukarudi kitandani na wala hatukuhitaji kupoteza muda, tukaanza kupeana utamu huku kila mmoja akijitahidi kuhakikisha kwamba ana kata kiu ya mapenzi ya mwenzake kwa maana hatufahamu tutakaa mbali kwa muda gani.

“Nakupe….nda sana Randy”

“Nakupenda pia Jane wangu, nakuomba usije ukanisaliti tafadhali. Nitafanya dhambi kama niliyo ifanya kwa mtu wako”

“Usijali sinto weza kukusaliti mpenzi wangu. Nimejifunza kutokana na makosa ambayo tayari nimesha yafanya. Ninakupenda sana mpenzi wangu”

“Ninakupenda pia mpenzi wangu”

Tukapata kifungua kinywa, kisha bi Jane akaanza kujianda kwa safari ya kurudi jijini Dar es Salaam.

“Naomba tuwe tunawasiliana kwa kila muda”

“Hilo jambo litakuwa ni hatari sana kwetu?”

“Kwa nini?”

“Wanaweza wakanasa mawasiliano yetu kisha wakakutafuta wewe, na kupitia wewe lazima watanipata mimi. Nilazima tuweze kujiongeza kwenye kila jambo ambalo tunalifanya kuanzia hivi sasa. Sawa mke wangu”

“Nimekuelewa”

Baada ya maandalizi yote kumalizika kufanyika, bi Jane akaondoka eneo hili kwa kukodi taksi ambayo moja kwa moja anaelekea uwanja wa ndege. Nikatoa laini yangu kwenye simu ambayo niliwasiliana na mama pamoja na Dany. Nikaichukua simu ambayo nimepewa na Professa, nikaitafuta namba ya Profesa na kwa bahati nzuri nikaipata. Simu ya Professa ikaanza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.

“Ndio Profesa za masiku”

“Salama Randy, naona upo kimya”

“Kuna mambo tu yameingiliana Profesa. Samahani nakuomba uweze kuwasiliana na Jane na umlinde kwa maana kuna hali ya hatari inakwenda kutokea kwangu na mimi sihitaji na yeye aweze kupatwa na matatizo hayo”

“Nimesha wasiliana naye na alisha nieleza kila kitu. Nitahakikisha kwamba anakuwa salama. Vipi wewe una hitaji msaada mwengine tofauti na huo?”

“Hapana nikihitaji basi tuta wasiliana”

“Sawa”

Nikakata simu kisha nikaanza kuvaa suti yangu. Nilipo hakikisha kwamba kila kitu kipo salama, nikachukua kiasi ch akutosha cha pesa zangu zilizomo ndani ya begi langu kisha nikaanza kuondoka katika eneo la nyumba hii. Nikafika kwenye moja ya hoteli iliyo tulia sana na nikakodi chumba kimoja, ila kama ni mipango yangu ya kupambana na maadui zangu, niweze kuipanga katika hoteli hii. Nikaziweka bastola zangu nne juu ya kitanda pamjoa na magazine zilizo jaa risasi.

“FARIDA”

Nilijikuta nikiliita jina la Farida, mwanamke ambaye alinisaliti katika swala zima la mahusiano na kuamua kuolewa na mwanaume mwengine, japo nami nilimtoa mikononi mwa mume wake.

‘Nahitaji kukuona’

Niliendelea kuwaza, huku nikivuta taswira ya hali ambayo inakwenda kutokea mbele yangu. Mlango wa chumba changu ukagongwa jambo ambalo limenistua sana kwani sijaagiza jambo lolote kutoka kwa mtu wa aina yoyote. Nikaichukua moja ya bastola yangu na nikanyata hadi mlangoni mwangu, nikasikilizia kwa umakini sana huku nikihitaji kusikia chochote kutoka kwa mtu anaye gonga mlango huu. Kwa sekunde kadhaa sikuweza kusikia kitu cha aina yoyote.

Taratibu nikashika kitasa cha mlango wangu na kuuvuta kwa umakini sana, hata kama kuna mtu ambaye amapenga kunishambulia kwa nje basi hato weza kunidhuru kwa haraka. Kwa upendo mdogo wa mlango nilio uacha nikaona boski moja dogo kiasi likiwa pembeni ya mlango wangu na hakuna mtu yoyote. Nikachungulia nje na sikuweza kumuona mtu yoyote kwenye hii kordo ya chumba changu.

Nikalitazama boksi hili kwa sekunde kadha, nikaligonga kidogo na mguu ili kama ni bomu basi lilipuke nje ya mlango. Hapakuwa na madhara yoyote niliyo yaona katika boksi hili. Nikachuchumaa taatibu kisha nikalinyanyua na kuliingiza ndani ya chumba changu. Nikaliweka juu ya meza kisha nikatoa kisu kisu changu kidogo katika mfumo wa koti langu hili la suti na kukata kamba za hili boksi. Nikalifungua na kukuta chupa moja ya wyne pamoja na karatasi ndogo iliyo kunjwa. Nikaichukua karatasi hii na kusoma maelezo yaliyo andikwa kwa luga ya kingereza ‘FOR YOU’(Kwa ajili yako).

‘Nani?’

Swali nililo jiuliza kichwani mwangu, likakosa jibu kabisa, nikaitazama chumba hii ya wyne kisha nikairudisha ndani ya hili boski. Nikatoka chumbani humu huku nikiwa nimebeba boksi hili, nikafika sehemu ya mapokezi na kuliweka juu ya wahudumu.

“Nimegongewa mlango wangu na nimewekewa hili bosky hapa sijafahamu ni nani aliye liweka hivyo, silihitaji”

Nilizungumza huku nikimtazama binti mmoja.

“Samahani kaka hatujaleta mzigo kama huo mlangoni mwako”

“Nyinyi hamjaleta?”

“Ndio na toka ulipo ingia wewe hakuna muhudumu yoyote aliye panda huko juu”

“Okay basi libaki hapa kwenu”

Mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno haya nikaondoka eneo hili na kurudi kwenye chumba changu. Kabla sijafika kwenye mlango wangu nikauukuta ukiwa wazi kidogo jambo lililo nistua kwani nilipo toka niliacha nikiwa nimeufunga. Nikaitoa bastola yangu na kuanza kunyata, nikausukuma mlango huu na kuingia ndani na kukuta boksi jengine likiwa juu ya meza na linafanania kabisa na boski nililo lipeleka mapokezi. Nikachunguza chumba kizima na sikuweza kumuona mtu wa aina yoyote.

Nikafungua boksi hili kwa hasira, nikakutana na chupa nyingine ya wyne pamoja na katarasi iliyo kunywa, nikaifungua karatasi hii na kuisoma.

‘Majira ya saa mbili usiku njoo Nugwi umuokoe mpenzi wako la sivyo damu yake itazidi kuisha kadri ya muda unavyo zidi kwenda’

Maelezo haya yakanistua sana, kwa haraka nikaitazama chupa hii nyeusi ya wyne. Nikaingia nayo bafuni na kufungua, nikamwaga kiasi kidogo kwenye sinki la kupigia mswaki, sikuamini macho yangu mara baada ya kukuta ni damu na si wyne kama vile nilivyo kusudia. Woga mwingi ukanijaa huku mwili mzima ukinitetemeka.

‘Ohoo Mungu wangu’

Nilizungumza huku mwili mzima nikihisi ukiishiwa na nguvu. Nikarudi chumbani nikachukua bastola zangu zote na kuzichomeka kiunoni mwangu kisha nikavaa vizuri koti langu hili. Nikampigia Professa huku mwili mzima ukiwa na wasiwasi.

“Ndio”

“Profesa umezunguza na Jane?”

“Ndio na amesha fika jijini Dar es Salaam na hivi saa anakuja huku kwangu”

“Una uhakika Professa?”

“Ndio nina uhakika asilimia mia moja na ukifika utawasiliana naye”

“Kuna picha ya karatasi ulio andikwa ujumbe, ninakutumia picha zake sasa hivi usikate simu”

“Sawa”

Nikaipiga picha karatasi hii kisha nikarudi bafuni na kupiga picha chupa hii ya wnye ambayo kwa ndani imewekwa damu. Picha zote nikamtumia Profesa.

“Nimezipata picha ngoja nianze kuzifanyia kazi sasa hivi”

“Sawa professa”

“Kwani kwa sasa upo wapi?”

“Nipokwenye moja ya hoteli na huu mchezo unafanyika hapa hotelini na sifahamu ni nani ambaye ananichezea akili Professa”

“Mmm….huu ujumbe unamaanisha kilicho andikwa”

“Sasa Nungwi ni wapi?”

“Ni sehemu moja huko huko Zanzibar, nina imani kwamba ukizungumza na nahodha yoyote mwenye boti yake basi anaweza kukupeleka”

“Sawa nitazungumza nao”

“Ila Randy hakikisha kwamba unakuwa makini, kama ni maadui zao wanahitaji kukuua kisaikolojia kabla hawajakuvamia”

“Sawa professa”

“Una mwanamke mwengine ambaye upo naye kwenye mahusiano tofauti na Jane?”

Nikaka kimya huku nikifiriria ni nini cha kuzunguza. Akili yangu ikaangukia kwa Marieta, mwanamke niliye muokoa kutoka katika mikono ya watu walio kuwa wamekusudia kumbakan kisha wamuue.

“Marieta”

“Sasa naamini kwamba huyo ndio wamekusudia kumuangamiza”

“Ngoja nikalishuhulikie hili jambo. Ila Professa nani kuomba usimueleze Jane kitu cha aina yoyote”

“Sawa, usijali”

Nikakata simu kisha nikatoka chumbani humu. Nikafika kaunta na kuwakuta wahudumu wakiendelea na shuhuli zao, nikawakabidhi funguo ya chumba changu.

“Ninatoka, sina mgeni yoyote ambaye atakuja kuniulizia”

“Sawa, je hii wyne yako”

Dada huyu alinionyesha chupa hii ya wyne, nikaitazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaichukua. Nikatoka ndani na kuingia kwenye gari langu. Nikaianza safari ya kuelekea katika bandani ya hapa Zanzibar huku saa yangu ya mkononi ikinionyesha kwamba muda huu ni saa kumi na mbili kasoro jioni.

Majira ya saa kumi mbili na robo nikafika katika bandari hii, nikashuka na kuelekea katika boti za kukodishwa.

“Samahani ndugu”

Nilizungumza huku nikimtazama mzee mmoja aliye simama kwenye moja ya boti ndogo kiasi iliyo pembezoni mwa maji ya bahari.

“Bila samahani kijana”

“Kuelekea Nungwi inaweza ikagarimu kiasi gani?”

“Mmmmm….Nungwi?”

“Ndio”

“Hali ya hewa katika bahari kwa sasa sio nzuri. Unaonaje ukasubiri kwa kesho”

“Mimi ninahitaji leo hii mzee wangu, samahani unaweza kunisaidia?”

“Nisiwe muongo kwako kijana, sinto weza kwenda kwenye eneo hilo kwa sasa kwani sehemu yenyewe pia ina hatari sana”

“Okay sawa”

Nilizungumza uhku nikielekea kwa mtu mwengine.

“Kijana”

Mzee huyu aliniita na kunifanya nigeuka na kumtazama. Nikarudi sehemu nilipo kuwa nimesimama.

“Ndio”

“Ni muhumu sana kwa wewe kwenda Nungwi muda kama huu?”

“Ndio mzee”

“Utanilipa mulioni moja kwa maana eneo lenyewe ni hatari sana”

“Sawa, nitakulipa kwa mfumo wa dola za Kimarekani, inawezekana?”

“Hakuna tabu”

Nikatoa noti tano za dola mia moja na kumkabidhi mzee huyu. Nikaingia ndani ya boti yake, akakiwasha na taratibu tukaanza kuondoka eneo hili huku mzee huyu akianza kuvuta sigara yake.

“Eneo hili wewe ni mgeni?”

“Ndio mzee wangu”

“Nugwi unafwata nini?”

“Kuna watu ninakwenda kuonana nao”

Mzee huyu akanigeukia huku akiwa amejawa nashangao.

“Watu!!!?”

“Ndio, mbona umeshangaa”

“Mmmm hapana, twende”

Safari ya kuelekea katika eneo hili la Nungwi ikatugarimu kama lisaa moja na nusu huku hali ya bahari kwa namna moja ama nyingine sio shwari kabisa.

“Hapa ndio Nugwi”

Mzee huyu alizungumza huku tukiwa tumesimama kwenye eneo ambalo halionyeshi kama kuna dalilili ya kuwepo kwa watu wala boti ya aina yoyote. Nikaitazama saa yangu na kukuta zikiwa zimebaki kama dakika mbili kutimu saa mbili kambili. Gafla nikastukia kishindo kizito sana nikamkuta mzee huyu akiwa ameanguka chini ndani ya boti hili huku damu nyingi zikimtoka kichwani mwake jambo lililo nifanya nistuke sana.


Nikiwa katika hali ya kutaharuki, nikashuhudia bonti nzee zikitokea katika pande zote za dunia. Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini mwa eneo hili. Boti hizi zikaizunguka boti niliyo panda huku watu wake wakiwa wamevalia nguo nyeusi tupu huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Wakaniamrisha kunyoosha mikono yangu juu na nikatii amri, watu wawili wakarukia kwenye boti hii na kuanza kunipapasa mwilini mwangu, kila silaha yangu niliyo ivisha katika suti hii niliyo ivaa wakaichomoa. Mmoja wao akanipiga kitako cha bundukia katika mguu wangu wa kulia na nikaanguka chini na kupiga magoti pasipo kupenda.

Boti moja kubwa ikawasili katika eneo hili huku ikiwa inamulika mwanga mkali sana kwenye boti tuliyomo na hawa watu. Nikaamrishwa na kuipandishwa kwenye boti hii kubwa. Nikapokelewa na watu wengine wawili wenye silaha, tukaanza kutembea kwenye boti hii hadi kwenye moja ya chumba, nikakalishwa kwenye moja ya kiti kisha nikafunguliwa pingu na watu hawa wawili wakaka mlangoni kuimarisha ulinzi. Moja ya pazia likafunguliwa na nikamshuhudia mama akiwa amevalia joho jekundu huku katikati likiwa na msalaba mkubwa wenye rangi nyeusi.

Mkono wa kushoto, mama ameshika kisu kikali sana na kinacho meremeta, akatembea hatua chache hadi sehemu nilipo kalishwa, kwa ishara akawaamrisha watu wake kufanya tukio ambalo kwa haraka haraka sikuweza kulielewa, mlango ukafunguliwa na akaingizwa mwanamke ambaye kichwani mwake amefunikwa kitambaa cheusi ambacho kinanifanya nisiweze kuuona uso wake vizuri. Mwanamke huyu akapigishwa magoti mbele ya mama huku watu wake wakiwa wamemshika.

“Kuna mambo mawili Randy nahitaji kukubaliana na wewe la sivyo huyu anakufa”

Mama alizungumza huku akikivua kitambaa hicho kichwani mwa mwanamke huyo. Kama vile nilivyo kuwa nimewazia kwamba waliye mkamata ni Marieta, na ni kweli waliye mshikilia ni Marieta.

“Ehee Mungu wangu”

Nilijikuta maneno hayo yakinitoka pasipo kutarajia. Mikaitazama mikono ya Marieta na kuiona ikiwa inachuruzikiwa na damu nyingi sana, huku mwili wake ukionekana kuishiwa nguvu kabisa, kwani hata macho yake hayafunguki vizuri.

“Huyu binti ni mjauzito na mimba ni yako, mimi sinto jali kuona mjukuu wangu anakufa kwa ajili ya upumbavu wako na baba yako”

Habari hii ikaziidi kunistua sana moyo wangu na kujikuta nikilengwa lengwa na machozi.

“Hivyo basi chagua. Umuokoea mama na mwanaye ajaye tumboni au uniletee kichwa cha DANY hapa niwaachie huru na mukaunde familia yenu. Chaguo ni wewe, nitamuacha afe kwa mateso kwani damu zinataendelea kumtoka mikononi mwake hadi atakufa”

Nikamtazama Marieta, hakika ni mwanamke ambaye hastahili kupitia mateso kama haya. Ila mtu ambaye nina agizwa nikafanye mauaji yake ni mtu ambaye sinto dhubutu hata kumshika hata nywele yake pale ninapo kwenda kwa lengo la kumfanyia ubaya.

“Ninasubiria jibu”

Mama alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Machozi yakazidi kunilenge lenga kwani sina ujanja wa aina yoyote zaidi ya kukubaliana naye ili niweze kumuokoa Marieta. Walinzi wa mama wakanifwata na kunifunga mikono yangu pamoja na kunifunga macho yangu, nikatolewa katika eneo hili na sifahamu ni wapi ninapo elekea. Nikastukia nikiwa nimechomwa na kitu chenye ncha kali kwenye shingo yangu, haikupita hata sekunde ishirini nikajikuta mwili mzima ukinilegea na kulala usingizi fofofo.

***

Minong’ono ya watu, ikaanza kusikika vizuri masikioni mwangu, taratibbu nikafumbua macho yangu taratibu na kuona watu wawili wakiwa wamesimama mbele yangu huku mikononi mwao wakiwa wameshika makapu. Mwanga mkali wa jua unao nipiga machoni mwangu, ukanifanya nijifunike uso wangu kwa kiganja cha mkono wanu wa kushoto huku nikiendelea kutazama eneo hili.

“Hei unajisikiaje kaka?”

Mwanaume mmoja alizungumza huku wakiendelea kunitazama usoni mwangu.

“Nipo sawa”

Nilizungumza huku nikijitahidi kunyanyuka, nikajitazama mwilini mwangu na kukuta shati langu likiwa limefunguliwa vifungo vyote, huku koti langu la suti likiwa pembeni pamoja na chupa ya pombe kali(wisky)

“Kaka kama una hitaji msaada zungumza tukusaidie, kwa maana inaonekana umekunywa sana hadi umekuja kulala huku ufukweni mwa bahari.”

“Hapa nilipo ni wapi”

“Ni Zanzibar”

“Sawa asanteni”

Nilizungumza huku nikiokota koti langu la suti, nikajifunga, nikaanza kutembea huku nikilipapasa koti langu hili katika mifuko yake. Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kukuta pesa zangu zote, nikaendelea kutembea huku nikitoka katika fukwe hizi. Nikakuta waendesha bajaji kadhaa katika eneo hili, nikaingia kwenye moja ya bajaji pasipo hata kumsalimia dereva.

“Tunaelekea wapi?”

“Wewe twende, nitakuelekeza kwa kwenda”

“Sawa”

Nikaanza kumuelekeza dereva huyu hadi nyumbani kwa Bi Jane, nikamlipa dereva doa mia na wala sikusubiria chichi yangu, nikaingia ndani mwa nyumba hii. Nikapitiliza hadi ndani na kujitupa kitandani, huku kichwa changu kikiwa kimejawa na msongamano mkubwa sana wa mawazo.

Gafla nikasikia mlio wa glasi ikivunjika, kwa haraka nikanyanyuka kitandani hapa, nikanyata hadi mlangoni huku nikisikilizia miguu ya watu jinsi inavyo tembea katika eneo la nje ya chumba changu. Ubaya ni kwamba sina silaha hata moja, nikaangaza huku na huku, nikaona kiti kidogo cha kukalia kwenye dreasing table ya bi Jane, nikakishika vizuri huku nikisubiria mtu wa kwanza kuingia ndani ya hii nyumba ndio halali yangu. Kioo cha dirishani kikavunjika na nikashuhudia bomu la machozi likitua chini na kuanza kutoa moshi mwingi sana ambao ulianza kunipalia. Nikakimbilia bafuni na kufungua maji mengi kwenye sinki la kunawia uso, nikaanza kunawa uso wangu ili kuuzuia moshi huu kuendelea kunidhuru.

Watu wawili walio funika nyuso zao na kubakishia macho tu wakaingia humu ndani na wakanza kunishambulia kwa kunipiga. Sikuhitaji kuwa mnyonge wala mnyonge kwao nami nikaanza kupambana nao huku nikihakikisha kwamba nina wazidi. Kwa bahahati mbaya watu hawa wakanizidi uwezo na kunidhibiti kwakunipiga sana. Wakaanza kunikokota na kunitoa ndani humu huku wakiniburuta, sebeleni nikakutana na Farida akiwa na vijana wake sita wote wakiwa wananisubiria mimi kuletwa.

“Haloo Randy za masiku”

Farida alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu kubwa sana. Sikumjibu chochote Farida akanisogelea hadi sehemu nilipo simamishwa, akaanishika kidevu changu, taratibu akaanza kuninyonya midomo yangu, kisha akasogea hatua mbili nyuma, akanipiga teke moja la kifuani na kusababisha watu wake walioni nihikilia kuniachia na nikaanguka chini.

“Mbebeni”

Farida alizungumza kwa hasira sana, watu wake wakaninyanyua na kuanza kunitoa ndani humu huku nikiwa nimelegea mwili mzima na kila sehemu ya mwili wangu ina maumivu makali sana. Wakafungua moja ya buti la gari na kuniingiza na kunifungia.

***

Maumivu makali ninayo anza kuyahisi kwenye mikono yangu, taratibu yakanifanya niyafumbue macho yangu ambayo yametawaliwa na ukungu mwingi sana. Kila nilipojaribu kutazama ni wapi nilipo sikuweza kupata muono halisi kwani bado ukungu huu wa macho umenitawala na kuyafanya macho yangu kutoweza kuona vizuri. Baada ya muda kidogo, nikaanza kuona hali ya eneo hili, ni sehemu yenye maboksi mengi ambayo sifahamu yana nini ndani yake, mikono yangu imefungwa kwa juu na kunifanya nining’inie hewani na kushindwa kukanyaga chini. Katika mwili wangu nimebakiwa na boksa tu, huku suti yangu nikiwa nifahamu ni sehemu gani ilipo. Joto kubwa lililomo ndani ya hichi chumba, husabisha mwili wangu kutokwa na jasho jingi sana mithili ya mtu aliye toka kuoga dakika kadhaa zilizo pita.

‘Ohoo Mungu’

Nilizungumza huku nikijaribu kuzunguka huku na kule ili kuweza kutazama chumba hichi kama kina eneo lolote ambalo ninaweza kutokea, ila kwa bahati mbaya sikuweza kuona hata dirisha la kutokea. Baada ya dakika kama hamsini hivi mlango ukafunguliwa na wakaingia wanaume wawili walio jazia misuli ya miili yao huku mikononi mwao kika mmoja akiwa ameshika bunduki ya AK47.

Wanaume hawa wana asili ya kiarabu, kwa haraka nikagundua kwamba hawa watu ni kutoka katika kundi la kigaidi la Al-quida ambao linamilikiwa na Farida pamoja na baba yake. Wanaume hawa wakakta kamba walio nifunga na kunishusha, huku mwili wangu ukiwa umeishiwa na nguvu kabisa, hata kutembea sikuweza.

Mmoja waoa kaninyanyua na kuniweka begani mwake kisha taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili. Katika uchunguzi wangu wa haraka haraka nikagundua kwamab eneo hili nililopo ni ndani ya meli. Wakaniingiza kwenye moja ya chumba chenye taa nyingi. Wakanilaza kwenye kitanda kidogo kiasi, kilicho tandikwa shuka la kijani.

Katika kitanda hichi pembeni kuna mashine kadhaa kama chumba cha upasuaji jambo lililo nifanya nistuke kidogo. Wanaume hawa wakanifunga mikono yangu kwa kamba ngumu ambayo si rahisi kuweza kuikata. Wakaingia madaktari sita walio valia nguo za kijani huku nyeuso zao wakiwa wamezifunika kwa vitambaa vya rangi hizo za kijani.

“Munataka kunifanya nini?”

Nilizungumza mara baada ya kuwaona madaktari hawa wakinizunguka kitanda hichi na kuanza kuwasha kila mashine iliyomo hapa. Farida akaingia katika chumba hichi huku akinitazama kwa tabasamu pana sana usoni mwake.

“Ni nini unacho hitaji kukifanya Farida”

Nilizungumza huku mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi sana.

“Unaogopa nini, kumbuka kwamba wewe ni mwanajeshi wangu”

“Naomba unisikilize Farida, mimi sio mwanajeshi, tafadhali ninakuomba uniachie maisha yangu. Naomba niishi maisha yangu na amani”

“Hahahaa……Randy, ulihisi kwamba ukiingia katika kundi la Al-quida ni rahisi sana kutoka eheee. Hata ungepotea miaka kumi, tungekusaka na kukupata. Sasa kinacho kwenda kufanyikia ni kitu kizuri sana kuliko ulivyo zania”

Farida baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, akawamrisha madaktari hao mmoja wao kunichoma sindano. Daktari mmoja akanichoma sindano ya mkononi mwangu ambayo taartibu ikaanza kunipa usingizi mkubwa na kupelekea kupoteza kumbukumbu.

***

“Unajisikiaje?”

Niliisikia sauti ya Farida, ikingia katika ngome zangu za masikio mithili ya mwangwi. Nikamatazama Farida usoni mwake pasipo kumjibu kitu chochote.

“Randy unajisikiaje?”

Sauti ya mara ya pili kidogo nikaanza kuisikia vizuri.

“Nipo wapi?”

Nilimuuliza Farida huku nikijishangaa sana kwa uzito wa sauti yangu, kwani si kawaida mimi kuzungumza kwa sauti nzito kama hii.

“Upo sehemu salama”

Farida alizungumza huku akinisaidia kunyanyuka kitandani. Nikaka kitako huku nikimtazama, taratibu Farida akanisogeza karibu kabisa na katabati kubwa lililomo chumbani humu, nikastuka sana kuona uso wangu ukiwa umefungwa bandeji nyingi sana na kilicho bakishwa wazi ni macho tu.

“Mumenifanya nini?”

Nilimuuliza Farida huku nikimtazama usoni mwake.

“Kuna mabadiliko kidogo tumeyafanya katika mwili wako, hii ni kutokana na kazi kubwa sana iliyopo mbele yetu”

Mabadiliko, mabadiliko gani mbona sikuelewi?”

Niliendelea kuzungumza huku sauti yangu ikiwa nzito sana, inayo fanana na mmoja wa wacheza filamu wa Kimarekani, Silvester Stallon(RAMBO).

“Nilikuwa ninafikiria wazo moja la kukuua, ila niliweza kukumbuka mambo mengi sana ambayo mimi na wewe tuliweza kufanya pamoja. Ni mwanaume ambaye nilikupenda kwa gafla sana, hivyo nikaona si vyema kama ninekutowesha duniani”

Farida alizungumza huku sote tukiwa tumekitazama kioo hichi, manguo ya rangi ya bluu mpauko niliyo valishwa mwilini mwangu yannanifanya nishindwe kuona sehemu nyingine za mwili wangu.

“Kwa sasa wewe huitwi Randy tena”

“Nini?”

“Ndio huitwi Randy, umekuwa mpya, wewe sasa ni expendable men.”

Farida alizungumza huku akikunja ngumi kwenye mkono wake wa kulia.

“Wewe ni mwanaume wa wanaume, mpiganaji, hakuna ambaye atasimama mbele yako, si Dany si mtu yoyote”

Maneo ya Farida yakazidi kunichanganya kwa maana ninashindwa kumuelewa kabisa.

“Nieleze kitu kinacho eleweka sikuelewi”

“Okay ngoja kwanza”

Farida akachukua kijimkasi kidogo na kuzunguka nyuma yangu, akaanza kukata bandeji hizi nilizo fungwa usoni mwangu. Taratibu akatoa bandeji hizi jambo lililo nifanya nistuke sana kwani sura yangu imebadilishwa kwa asilimi mia moja. Muonekano wangu huu mpya unanifanya nionekane mtu mpole sana na mwenye sura nzuri sana.

“Kwa nini mumenifanya hivi?”

Niliuliza huku mwili mzima ukinitetemeka kwa hasira, nikamgeuka Farida na kumshika koo lake, nikajishangaa jinsi ninavyo mnyanyua taratibu kuelekea juu tena kwa mkono mmoja kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwenye maisha yangu yote.

Nikamgandamiza ukutani Farida huku akiendelea kutapa tapa, mlango ukafunguliwa kwa nguvu, wakaingia wanaume waame wanye bunduki, wakaanza kunipiga na vitako vyao vya bunduki mgongoni mwangu, nikamuachia Fatida na kuwashika wawili na kuwanyanyua juu na kuwatupa kwenye kitanda kilichomo humu ndani, jambo lililo zidi kunishangaza sana, kwani sijui ni kitu gani walicho kiweka kwenye mwili wangu na kunifanya niwe na nguvu kiasi hichi cha kuwanyanyua wanaume wawili walio jazia miili yao na kuwatuma kana kwamba nimebeba boksi tu.



Madaktari wawili wakaingia ndani ya chumba hichi, wakisaidiana na watu walinzi wengine wa Farida wakanichoma sindano ambayo baada ya muda mfupi mwili mzima ulianza kuishiwa nguvu na nikaanguka chini.

“Unatakiwa kujifunza kuzuia hasira yako.”

Farida alizungumza huku akiniangalia hapa chini nilipo lala.

“Kitu kikubwa na cha msingi ambacho nahitaji kukuambia, mwili wako kwa sasa tumeweza kuuongezea nguvu, na utakuwa unatumia sindano hizi kila baada ya miezi miwili ili kuhakikisha kwamba mwili wako unaendelea kuwa na nguvu”

Farida alizungumza huku akinionyesha sindano zipatazo nne zilizopo kwenye kibegi kidogo cheusi. Zindazo hizi zimejaa dawa yenye rangi nyeupe.

“Kwa…a….nini umenifanya hivi Farida?”

“Kwasababu ninakupenda Randy, bila ya mimi kukufanya hivi ni lazima wewe ungekufa…..”

“Bora ningekufa kuliko huu ujinga ulio nifanyia Farida”

“Hahaaa unahisi kufa ni jambo zuri kwa mwanadamu. Randy upo chini yangu kuanzi hivi sasa na angalizo ni moja tu, endapo usipo tumia sindano hizi ndani ya muda wa miezi miwili, basi utakufa. Na mimi ndio mtu pekee ninaye fahamu dawa hiyo, sasa kuwa makini. Utafanya kila jambo ambalo nitakuambia uweze kufanya umenilewa?”

Macho yangu nikamabaki nikimtazama Farida usoni mwake.

“Mlazeni kitandani”

Farida alizungumza kisha akatoka ndani ya chumba hichi na kuniacha na madaktari wawili.

Siku zikazidi kusonga mbele, nikaendelea kuizoea sura yangu pamoja na hali yangu. Maisha ya hapa Karachi Pakistani, ninazidi kuyazoea huku nikipewa mafunzo ya dini ya kiislam huku jina langu ambalo watu wananiita ni Tarique Hussein. Hata uvaaji wangu wa mavazi umebadilika kwa asilimia kubwa, kwani muda wote nimevalia kanzu na kilemba kikubwa kidogo kichwani mwangu.

“Vipi sala inakwendaje?”

Farida aliniuliza mara baada ya kuingia sebleni katika jumba hili tunalo ishi mimi pamoja na wafuasi wengine wa kundi la Al-quida.

“Imekwenda vizuri”

“Mawaidha umeyaelewa?”

“Ndio ninayaelewa”

“Vizuri sana, sikutarajia kama utaipenda hii dini”

Sikumjibu chochote Farida zaidi ya kumtazama tu usoni mwake, kwani kitu ninacho kipanga moyoni mwangu sihitaji kukionyesha kwa wakati huu.

“Ahh kuna kazi sasa ambayo utakiwa kuifanya”

“Kazi gani”

Kwa ishara Farida akaniomba tuingie kwenye moja ya chumba ambacho hutumika kama ofisi yake. Tukaingia na nikawakuta waarabu wawili walio valia suti.

“Tarique kutana na waziri wa ulinzi hapa Pakistan bwana Abdul Yasin, huyo hapo ni makamu wake anaitwa Hussein Hussein”

Farida alinitambulisha kwa viongozi hawa, nikapeana nao mikono kisha nikakaa pembeni huku nikimtazama usoni mwake.

“Kuna kazi moja wameileta nina imani utaifanya vizuri”

Waziri wa ulinzi akamkabidhi Farida faili lenye rangi ya kaki. Farida akalifungua faili hilo akalisoma kwa muda kisha akanikabidhi, nikalifungua faili hili na kuanza kulisoma taratibu, nikaona picha za mzee mmoja hivi ambaye kwa maelezo yaliyo andikwa hapa chini ni balozi wa Pakistani nchini Syria.

“Syria kwa sasa kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe, nchi kubwa kama Marekani, Uingereza na nyinginezo wanaendelea kuwatoa mabalozi na wananchi wao wanao ishi katika nchi hiyo ya Syria.”

“Balozi wetu bwana Ozizi Awadh yupo nchini humo. Amekamatwa na magaidi wa Islamic State na yupo katika mji uitwao Raqqa ambao unamilikiwa na magaidi hao wa Islamic State na huo mji ndio makao makuu ya kundi hilo la Islamic State”

Waziri wa ulinzi alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nini munacho hitaji mimi kufanya?”

“Ni kwenda kumkomboa kutoka mikononi mwa kundi hilo kwa maana endapo watamuua basi Pakistani itakwenda kuanzisha vita na Syria na nina imani kwamba hali itakuwa mbaya zaidi ya hapa”

Nikamtazama Farida usoni mwake kwa muda kidogo.

“Kuna kiasi cha dola milioni tano hapa, hayo ndio malipo ambayo utalipwa kwa kufanikisha kuifanya kazi hii”

“Samahani, Farida tunaweza kuzungumza kidogo?”

“Ndio”

Nikanyanyuka kwenye kiti changu na kutoka nje, Farida akanifwata. Tukasimama katika eneo ambalo hakuna mtu ambaye ataweza kutusikia mazungumzo yetu.

“Hivi ulishindwa nini kuwatuma vijana wako hadi mimi?”

“Randy kumbuka kwamba sisi tupo hapa kwa ajili ya pesa. Fanya kazi tupate pesa maisha yasonge mbele”

“Hujanijibu swali langu, kuna vijana wangapi katika eneo hili, kwa nini sio wao hadi unitume mimi?”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimkazia macho Farida.

“Wewe una uwezo mkubwa Randy oooh Tarique, nakuomba sana ukaifanye hii kazi”

“Umenifanya hivi kwa ajili ya kunitumia kwa ajili ya maslahi yako binafsi si ndio?”

“Hapana Randy?”

“Ila”

“Ni hivi, kundi letu la Al-quida, halipatani na kundi la Islamic State kwa sasa, kila watu wanaendesha oparesheni zao kivyao. Tulisha fanya mazungumzo na serikali hii ya Paksitani, tukagawana maeneo ya kutawala ndio maana unaona hivi sasa hakuna mashambulizo yoyote tunayo yafanya hapa ndani ya Pakistani. Tunahitaji kuliteketeza kundi la Islamic State, tunahitaji kuhakikisha kwamba kundi la kigaidi hapa duniani linabaki moja ambalo ni sisi”

Nikafumba macho yangu kwa sekunde kadhaa huku nikifirikia kitu cha kufanya. Kiasi hihi cha pesa kama nitakipata basi kinaweza kunisaidia kwenye mipango yangu kadhaa huko mbeleni.

“Sawa nimekuelewa, ila nitahitaji pesa yangu kwanza ndio nifanye kazi”

“Hilo ni swala la kwenda kuzungumza nao”

“Katika kazi hii, kundi kama kundi linanufaikaje?”

“Wanatulipa kiasia cha dola milioni tano nyingine hivyo kazi hii ukiikamilisha ni sawa na dola milioni kumia ambazo tutapatiwa. Randy hizi ni pesa nyingi sana. Maamuzi ni yako katika hili”

“Ni mara ya ngapi unafanya kazi na hii serikali?”

“Hii ni kazi ya tatu sasa”

“Ni waaminifu?”

“Sana, wanatujua tukicharukwa”

“Sawa twende ndani”

Tukarudi ndani na kukaa kwenye viti vyetu.

“Kijana wangu amekubali kuifanya kazi”

“Ohoo asante Mungu, ila hakikisha kwamba kazi hii inakwenda kimya kimya hakuna watu wengine watakao ifahamu kazi hii nje ya hichi chumba”

Waziri wa ulinzi alizungumza huku akiwa na furaha sana usoni mwake.

“Oparesheni yako ipo salama, ila jambo moja nitahitaji kuzungumza kwenu?”

“Zungumza”

“Endapo kutakuwa na udanganyifu wowote ambao utafanyika, vichwa vyenu nitakuwa halali yangu, sijali muna lindwa na walinzi wangapi, ila kila mmoja nitamchinja kwa muda wake, mume nielewa?”

Nilizungumza huku nikiwakazia macho mawaziri hawa.

“Tumekuelewa mkuu”

“Haya”

“Katika hilo faili kuna maelekezo yote hivyo unaweza kuyafanyia kazi”

“Sawa”

“Sasa tunaona tuondoke”

“Haya jamani karibuni sana”

Farida alizungumza huku akinyanyuka, akatoka ofisini hapa na walinzi hawa na kuniacha pake yangu. Nikalipitia faili hili kwa muda kidogo huku nikihakikisha kwamba ninasoma maelezo haya kwa umakini sana. Farida akarudi ofisi hapa huku akiwa na furaha sana.

“Nahitaji kuondoka leo usiku, fanya mipango ya maandalizi ya safari”

“Sawa Tarique nitafanya hivyo”

“Jambo jengine….ila basi”

“Zungumza”

“Nitalizungumza mara baada ya kurudi kutoka Syria”

Nikatoka ofisini humu na kuelekea chumbani kwangu, nikaanda nguo zangu na kuziweka katika begi langu. Nikachukua bastola zangu nne pamoja na magazine nane na kuziweka ndani ya begi hili. Mlango wa chumba changu ukagongwa, nikatembea hadi mlangoni na kuufungua, nikamkuta Farida akiwa amesimama, akaingia ndnai moja kwa moja.

“Chumbachako kina nukia marashi mazuri”

Farida alizungumza huku akikaa katika moja ya kiti.

“Asante”

“Mume wangu ameondoka muda huu unakwenda China kwa biashara”

“Sawa”

Nilimjibu kwa ufupi huku nikifunga zipu ya begi langu.

“Randy”

Nikageuka na kumtazama Farida usoni mwake.

“Natambua kwamba kuna mambo mengi sana nimekufanyia. Moja wapo ni la kuolewa na mwanaume huyu, natambua kwamba uliiumia sana na huna hata hamu nami katika hili. Naomba nitumie muda huu kukuomba msamaha kwa yote yaliyo tokea”

“Ni hilo”

“Ndio”

“Sawa, toka chumbani kwnagu nahitaki kupumzika kidogo”

Farida akasimama na kunitazama kwa macho yaliyo jaa huruma.

“Randy najua unanichukia, samahani mpenzi wangu, tambua kwamba nina kupenda”

Farida alizungumza huku akinishika kiuno changu, nikautoa mkono wake na kumtazama.

“Sikiliza Farida, sina hisia na wewe. Ninakwenda kuifanya hii kazi, itakuwa kazi yangu ya mwanzo na ya mwisho. Sipo tayari kuwa mtumwa wako, sipo tayari kuwa mtu ambaye anapokea oda kutoka kwako. Nitakuwa tayari kufa kwa ajili ya uhuru wangu umenielewa”

Maneno yangu yakamfanya Farida kunitolea macho sana.

“Nina uwezo wa kukuua hata sasa hivi, ila sihitaji kufanya hivyo. Ila pale utakapo jaribu kuingilia uhuru wangu kwa mara nyingine, tambua kwamba nitakuaa, tena kwa mikono yangu mwenyewe. Na hii sura ya bandia muliyo nipandikiza nitakwenda kuitoa, nahitaji kuishi maisha ya amani sawa”

“Rand…..”

“Hakuna cha Randy, huo ndio ukweli wangu. Nilikuamini sana Farida, ila umevunja uaminifu wako kwangu, nami hivi sasa nitaishi maisha yangu. Toka chumbani kwangu”

Nilizungumza kwa msisitizo na kumfanya Farida amwagikwe na machozi usoni mwake. Taratibu akaanza kutembea hadi mlango, akafungua mlango na kutoka, nikaufunga mlango kwa ndani kisha nikajilaza kitandani huku kichwani kwangu nikiwa na mawazo mengi sana. Usingizi taratibu ukanipitia.

Nikastuka kutoka usingiizi majira ya saa moja usiku, nikaingia bafuni nikaoga, nikaoga na kutoka chumbani kwangu, nikamkuta Farida akitoka ofisini kwake huku mkononi mwake akiwa ameshika bahasha ya kaki. Akanikabidhi.

“Hati ya kusafiria, tiketi za ndege zimo humo ndani. Ndege itaondoka saa nne usiku hapa Pakistani”

Farida mara baada ya kumaliza kuzungumza hivyo akaanza kuondoka na kuniacha nikimtazama.

“Pesa ya kutumia”

“Unakwenda kwenye mission pesa ya nini?”

“Hivyo sinto kula, sinto kunywa wala kukodi chumba cha kulala au?”

Farida akanitazama kwa macho yaliyo jaa hasira kisha akanirudia na kunitazama.

“Utajua mwenyewe ni wapi kwa kutua pesa na usiniulize chochote tena”

Nikamkamshika mkono wake wa kulia na kumkabidhi bahasha yake.

“Utakwenda kuifanya hiyo kazi mwenyewe, sina muda wa kujitolea maisha yangu kwa mpumbavu mmoja”

Baada ya kuzungumza maneno hayo nikaanza kutembea kuelekea chumbani kwangu.

“Tarique simama”

Farida alizungumza kwa ukali sana, sikuhitaji kusikiliza kitu chochote, mlio wa risiasi ambayo imepita na kupiga kwenye ukuta uliopoa mbele yangu ukanifanya nisimame na kugeuka nyuma taratibu, nikamkuta Farida akiwa ameshika bastola huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira.

“Nitakuuaa”

Farida alizungumza kwa hasira sana, walinzi wapatao kumi wakaingia sebleni humu na kuninyooshea bundiki zao kama mkuu wao alivyo fanya.

“Wewe ni mbwa wangu, lazima ufwate kile ninacho kihitaji umenielewa mpumbavu wewe”

“Heheee….mbwa si ndio?”

“Ndio wewe ni mbwa wangu”

“Okay niue bwana wangu”

Nilizungumza kwa dharau huku nikimkazia macho Farida. Farida akaanza kutembea kwa hasira hadi sehemu nilipo simama, hakuushusha mkono wake alio nishikia bastola. Akanikabidhi bahasha ambayo nilikabidhi.

“Utaifanya kazi hii na sinto kulipa hata shilingi mia moja umenielewa wewe mwana haramu?”

“Hehee”

Nilicheka kisha nikaanza nikaiangusha bahasha chini, nikaendelea kutembea hadi chumbani kwangu. Hazikupita hata sekunde hamsini, Farida akaingia huku akiwa ameendelea kuishika bastola yake.

“Chagua mambo mawili, ufanye kazi hii au huyu malaya wako auwawe”

Farida alizungumza huku akinionyesha picha ya Marieta kwenye simu yake, jambo lililo nifanya nistuke kidogo na kujikuta nikianza kuwa mnyonge kwani Farida na mama yangu wanashirikiana katika ugaidi wao wanao endelea kuufanya dhini yangu na baba yangu Dany.


“Chaguo ni lako sasa”

Farida mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akatoka chumbani humu huku akiniacha katika hali ya hasira iliyo changanyikana na mawazo mengi sana. Sikua na jinsi zaidi ya kukubaliana na kazi iliyopo mbele yangu. Nikabadilisha nguo na kuvaa suti moja ambayo alinikabidhi Farida siku kadhaa zilizo pita. Nikatoka ndani ya chumba changu na kumkuta Farida pamoja na watu wengine wakiwa sebleni wameketi. Nikaanza kutembea kuelekea katika mlango wa kutokea.

“Pesa hii hapa ya matumizi”

Farida alizungumza na kunifanya nigeuke nyuma nikaona kibunda cha pesa za kimarekani akiwa amekishika mkononi mwake, nikarudi hadi sehemu alipo kaa. Akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akanikabidhi kibunda hichi ambacho sifahamu ni kiasi gani cha pesa.

“Hakikisha kwamba kazi inakwenda kama vile tulivyo kusudia”

“Sawa”

Nilijibu kwa ufupi na kuelekea nje, nikakuta dereva akiwa ananisubiria. Nikaingia ndani ya gari na tukaianza safari kuelekea katika uwanja wa ndege. Nikafungua begi langu na kutoa bastola zote na kuziweka chini ya siti ya gari hili kwa maana uwanja wa ndege ni lazima watatukagua na endapo nikapatikana na silaha basi ni kesi nyingine tena.

Tukafika uwanja wa ndege, nikakaguliwa kama wanavyo kaguliwa abiria wengine, nikasubiri kwa dakika kadhaa ili abiri wa ndege yetu turuhusiwe kuingia ndani ya ndege. Muda wa abiri kuingia ndani ya ndege ikawadia, nikatafuta siti yangu kwa bahati nzuri nikakutana na dada mmoja wa kizungu huku akiwa amevalia kitabulisho kinacho mtambulisha kwamba yeye ni mtangazaji wa shirika moja la Aljazira.

“Habari yako”

Nilimsalimia huku nikikaa siti ya pembeni yake.

“Salama tu, habari ya wewe”

“Salama”

Nikafunga mkanda wa siti yangu. Abiria walipo kamilika kuingia katika ndege hii, tukatangaziwa na muhudumu kwamba tuweze kufunga mikanda kwani ndege yetu inajiandaa kuondoka. Taratibu ndege ikaanza kuondoka katika eneo hili huku kichwani mwangu nikiwa na mawazo mengi sana juu ya Marieta.

‘Mimba yangu’

Niliwaza kichwani mwangu huku nikiyakumbuka maneno ya mama yangu ambaye yeye ndio aliye mshikilia Marieta.

‘Inabidi niweze kufanya jambo katika hili’

Niliendelea kuwaza na kila ninalo lipanga kichwani mwangu ninaona halikai sawa.

“Unaonanekana una mawazo sana?”

Dada huyu wa kizungu aliniongelesha huku akinitazama usoni mwangu.

“Ehee….”

“Unaonekana una mawazo, kuna tatizo lolote linalo kusumbua?”

“Hapana kuna mambo tu ya kibiashara nina yawaza”

“Ohoo sawa, ninaitwa Victoria ni mtangazaji wa shirika la Aljazira.”

“Nashukuru kukufahamu Victoria, mimi ni Tarique”

“Ndio jina lako?”

“Ndio ndio”

“Nashukuru kukufahamu, vipi unaelekea wapi?”

“Syria”

“Ohoo hata sisi tunaelekea huko huko kuweza kufanya matangazo kuna baadhi ya waandishi wezetu walitekwa huko hivyo tumetumwa kuchukua nafasi zao”

“Mmmm huoni kwamba ni hatari kwenu?”

“Kweli ni hatari ila kazi ni kazi na popote ni kazi. Nimekuwepo hapa Pakistani kwa muda sasa na nimeshuhudia mambo mengi ya hatari ila ndio kazi yenyewe”

“Kweli, imekuwaje wamatekwa?”

“Unajua kundi la Islamic State, bado lina mtafaruku na serikali ya Syria, sasa waandishi wale walio kuwa wametumwa ni Wamrekani, nahisi kuwakamata kwao wanahitaji chochote kutoka katika serikali ya Marekani”

“Ahaaa….”

“Yaa ila Mungu atusaidie, nipo na kamera man wangu amekaa siti ya mbele kule”

“Ahaa yeye vipi amependa kwenda huko?”

“Mmmm mimi na yeye hakuna aliye pendelea kwenda huko, ila kutokana ni maagizo kutoka makao makuu tukaona hakuna jinsi zaidi ya kukubaliana na tulilo ambiwa”

‘Hawa watanisaidia?’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama Victoria usoni mwake. Safari ikazidi kusonga mbele huku tukijikuta tukiwa tumezoeana gafla sana na Victoria, tukasimuliana mambo mengi sana juu ya maisha yaliyo pita japo kwa upande wangu sikuihtaji kujiweka wazi juu ya uhalisia wangu. Safari ikatugarimu maasaa zaidi ya thelathini na mbili kwani kuna baadhi ya nchi ilitulazimu ndege kusimama na ilikaa kwa masaa kadhaa.

Tukafika nchini Syria majira ya saa saba mchana.

“Tarique kama huto jali, tunaweza kufikizia katika hoteli ambayo tuliweka booking?”

“Mmmm sawa kama huto jali”

“Nashukuru kwa kunisikiliza”

Tukainia kwenye taksi wote watatu pamoja na kijana mmoja mwenye asili ya Kipakistani. Tukafika kwenye hoteli hii, kutokana sikuwa nimeweka booking ya chumba ilimbidi Victoria kuniomba niweze kukaa naye chumba kimoja.

“Mimi na wewe chumba kimoja?”

“Ndio kwani unaogopa?”

“Hapana siogopi ila kumbuka mimi na wewe ni jinsia mbili tofauti”

“Hilo halina tatizo kwani utashindwa kustahimili kuniona katika hali yoyote”

“Mmm wacha nijaribu”

“Sawa”

Tukaingia katika chumba hichi, tukaweka mabegi yetu kwenye moja ya kabati. Nikaanza kukagua chumba hichi kama kuna kamera yoyote au kinasa sauti niweze kufahamu.

“Vipi mbona una kagua sana chumba, kuna tatizo”

“Ni kawaida ambayo nimejijengea kwenye maisha yangu kila ninapo ingia kwenye hoteli niweze kufanya hivi”

“Ahaa sawa sawa au wewe ni mpelelezi?”

Nikamtazama Victoria kwa sekunde kadhaa kisha nikatabasamu.

“Hapana, mimi ni mfanya biashara na nipo hapa kwa ajili ya kukutana na wafanya biashara baadhi”

Mtikisiko wa mlipuko mmoja mkubwa sana ukatufanya tukimbilie dirishani na kuchungulia nje, kwa mbali tukaona moshi mwingi sana ukitanda hewani.

“Karibi Syria”

Victoria alizungumza huku akitabasahmu na kuanza kuelekea mlangoni.

“Unakwenda wapi?”

“Kutangaza habari hichi ndicho kilicho tuleta huku”

“Tunakwenda wote”

“Unaweza kukaa tu hapa kwenye hoteli”

“Victoria tunakwenda wote”

Nilizungumza kwa msisitizo mkubwa hadi Victoria akapatwa na kigugumizi.

“Sawa twende”

Tukatoka chumbani humu na tukamkuta kijana wake akiwa amesha toka chumbani kwake huku akiwa na mabegi. Tukatoka nje na kukodi bajaji.

“Ongeza mwendo”

Victoria alimuambia dereva huyu wa bajaji na kumuomba tuzidi kuelekea katika eneo lilipo tokea mlipuko huo. Kitu kinacho nishangaza ni kuto kuogapa kwa dereva huyu bajaji, tulipo karibua eneo la tukio tukasikia mlio mingi ya risasi na kumfanya dereva kufunga breki za gafla.

“Vipi?”

Nilimuuliza dereva bajaji huku nikimtazama usoni mwake.

“Hapa ndio mwisho wangu, hilo eneo kundi la magaidi limevamia hivyo nitauwawa”

“Tushukeni”

Victoria alizungumza huku akianza kushuka kwenye bajaji hii. Tukashuka wote, akamlipa dereva huyu na akaondoka, tukajibanza kwenye moja ya duka lililo fungwa. Kijana wa Victoria anaye itwa Omary akafungua begi kubwa alilo libeba, akatoa majaketi mawili ya kuzuia risasi ambayo kwa nyuma yameandikwa Tv kwa herufi kubwa huku chini kukiwa na maandishi madogo yaliyo andikwa Aljazira. Wakatoa kamera pamoja na vinasa sauti, wakawasha vifaa vyao vya wawasiliano.

“Vipi signal inakwenda vizuri?”

“Ndio”

“Tarique utakuwa nyuma ya Omary, hakikisha huendi mbali nasi, usije ukatekwa na kuuwawa?”

“Usijalia””

“Omary upo tayari”

“Ndio boss”

Victoria akasimama mbele ya Omary aliye shika Kamera kubwa na kuanza kumrekodi.

“Nyuma yangu ni moshi mwingi una elekea angani, na kwa masikio yako utaweza kusikia milio kadhaa ya risasi huku nyuma yangu. Sasa jumuika nani Victoria Thomas kutoka hapa Syria, nami nitakueleta kila aina ya tukio ambalo linatokea eneo hili”

Victori alizungumza huku akiwa ameshika maiki mkononi mwake, akaanza kutembea na sisi tukaanza kumfwata kwa nyuma. Kadri jinsi tulivyo zidi kwenda ndivyo jisni tulivyo zidi kusikia mashambulizi hayo yakiendelea. Tukakutana na eneo ambalo polisi wamesimamisha magari yao kama manne huku wakirushiana risasi na mahgaizi wa Islamic State waliopo upande wa pili.

“Kama unavyo jionea mpenzi mtazamaji polisi wanaendelea kupambana na taarifa ni kwamba kundi la Islamic State wanataka kuuchukua mji huu ila polisi nao wanaifanya kazi yako kuhakiksiha kwamba mji huu unabaki mikononi mwa serikali”

Nikawashuhudia askari wawili wakipigwa risasi na mdunguaji aliye kaa eneo la mbali sana.

“Kuna sniper hili eneo”

Nilizungumza huku nikijibanza pembeni ya moja ya nguzo, huku macho yangu yakiwa na kazi ya kutazama ni wapi mdunguaji huyo anapo tokea. Nikamshudia mdunguaji huyo akitokea katika moja ya gorofa ambapo si rahisi kwa askari kuweza kumuona. Kwa ishara nikamuonyesha Victoria kwamba ninaondoka katiak eneo hili. Victoria akampa Omary ishara ya kukatiasha mazungumzo haya.

“Unataka kwenda wapi Tarique?”

“Kuna mdunguaji kwenye lile gorofa kule, hapa askari wataendelea kuteketezwa hawa wanao pambana nao huku chini ni wadogo wadogo.

“Unataka sasa kufanya nini?”

“Kuelekea kuelekea kwenye lile gorofa”

“Huwezi kwenda Tarique huna mafunzo yoyote ya kijeshi”

Victoria alizungumza kwa suati kubwa sana kwani bili kufanya hivyo hatuto sikiana hii ni kutokana nilio ya risasi.

“Kuweni makini”

Nilizungumza huku nikikimbilia upande wa pili wa barabara, nikaingia kwenye moja ya gorofa na kuanza kukimbia kupandisha juu, nilipo fika gorofa ya nne, nikaanza kuruka kutoka gorofa moja kwenye jengine kwani gorofa hizi zimekaribiana sana na si rahisi kwa mtu mwenye mazoezi kama mimi kushindwa kuruka.

Nikazidi kuruka kwa kupitia madirishani kutoka gorofa moja hadi jengine. Nikafanikiwa kufika kwenye gorofa ambalo yupo mdunguaji. Katika chumba nilicho ingia kwa bahati nzuri hakina mtu, nikakimbilia mlangoni na kijibanza huku nikisikilizia nje ya chumba hichi ni nini kinacho endelea.

Nikaufungua mlango huu taratibu na kuchungulia kwenye kordo hii na sikuweza kumuona mtu wa ina yoyote, nikaanza kukimbia kwa umakini huku nikipandisha ngazi kuelekea gorofa ya juu zaidi alipo mdunguaji huu. Nikafika gorofa ya tisha ya hili gorofa, nikaanza kutembea kwa kunyata hadi ilipo chumba alipo mdunguaji. Nikashusha pumzi nyingi sana ili kuyapa mapafu yangu pumzi mpya kwani shuhuli ninayo kwenda kuifanya ndani humo ni kubwa.

Nikarudi hatua kadhaa nyuma na kwa kasi kubwa nikaurukia mlango huu na ukauvunjia na kuzamia ndani, nikabiringira kwa kasi kubwa hadi alipo mdunguaji huyu ambaye alibaki akiwa anaduwaa kwani hakutarajia kuona uwepo wangu humu ndani. Mdunguaji huyu kwa haraka akachomoa kisha na kukishusha kwa kasi katika eneo nililo lala, nikakikwepa na hapa hapa chini nikampiga teke la kifua na kumfanya aangukie chini. Nikasimama kwa haraka na kurukia kwa kumpiga kigoti cha kifua na kuzidi kumlainisha na kuanguka chini. Akajaribu kunyanyua ila sikuhitaji kumpa nafasi hiyo, nikamuwahi mkono wake kwenye kisu, nikavunja kwa kutumia miguu yangu kwani niliubana katikati. Nikachukua kisu chake na kumchoma nacho kifuani, nikakichomoa na nikamchoma tena kwa mara ya pili na kusababisha damu nyingi kumwagika na akapoteza maisha hapo hapo.

Nikaichukua bunduki yake kubwa, na kuchomoa magazine na ambayo inainia risasi tano, nikakuta ina risasi moja tu huku pembeni kukiwa na boksi la risasi. Nikajaza risasi zilizo pungua kwenye magazine hii, kisha nikaichomeka kwa haraka, nikachukua darubini na kutazama ni wapi walipo magaidi wa Islamic State wanao pambana na askari. Nikawaona wakiwa kaika moja ya eneo huku akiendelea kupeleka mashambulizi kwa askari ambao nao wamajitahidi kuupigania mji wao. Nikaikoki bunduki hii kubwa, kisha kwa kutumia lensi ilivyo funga kwenye hii bunduki nikaanza kumuua mpiganaji mmoja baada ya mwengine wa kundi la Islamic State.

“Mother Fuc**”

Nilizungumza huku nikifanya matukio yangu kwa kasi sana ili kuhakikisha kwamba ninawasaidia polisi kadri ninavyo weza. Magaidi wa Islamic State nao wakastuka juu ya mimi kuwashambulia, wakaanza kuleta mashambulizi katika eneo hili nililo jificha. Nikaona bastola kiunoni mwa mdunguaji niliye muua. Nikaichoma, nikaikagua magazine yake na kukuata ina risasi zilizo jaa. Nikaichomeka kiunoni mwangu kisha nikaanza kujaza risasi nne zilizo salia kwenye akiba ya kiboksi kidogo nilicho kukuta pembeni ya bunduki hii. Mashambulizi kwa upande wangu yakazidi kuwa makali, nikapata upenyo wa kuchungulia nje, nikamshuuhudia haidi mmoja akiwa ameweka begani bomo moja aina ya bazooka huku akiwa ameliekekezea kwangu, kabla ya sijafanya maamuzi ya kulenga tayari akawa amelifyatua bomu hilo na likaanza kuja eneo hili nilipo kwa kasi kubwa sana.



Nikaitupa chini bunduki hii kwa maana ni ina uzito kiasi, nikaanza kukimbia kuelekea mlangoni kitendo tu chakutoka mlangoni mwa chumba hichi, nikasikia mlipuko mkubwa sana ukitokea ndani ya chumba nilicho kuwepo na kusababisha baadhi ya kuta za eneo hili kuanza kupasuka huku nyingine zikianguka chini.

Nikazidi kukibia huku nikishuka kwenye ngazi zinazo elekea gorofa ya chini ambayo nayo imechakaa na ina matundu mengi ya risasi.

‘Ohoo Mungu wangu’

Nilizungumza huku nikisimama kwenye kordo huku nikitazama huku na kule. Nikaona mlango mmoja wa chumba ukiwa, kwa haraka nikaingia ndani ya chumba hichi na kukuta kikiwa na kitanda tu cha chuma huku gororo likiwa limetupwa pembeni, nikachomoa bastola yangu na kuchungulia eneo walipo magaidi hawa wa Islamic State. Kwa bastola niliyo nayo siwezi kufanya jambo lolote na inaweza kuwa tatizo kwa upande wangu. Nikiwa katika majadiliano akilini mwangu nikasikia milio ya ndege za kivita aina ya jet, nikashuhudia jet mbili zikipitwa kwa kasi kubwa sana huku zikiachia mabimu eneo walipo wapiganaji hawa wa Islamic State jambo lililo sababisha milipuko mikubwa sana katika eneo hili hadi baadhi ya magarofa yakaanza kumengenyuka kuelekea chini. Jinsi nilivyo ingia kwenye gorofa hili ndivyo jinsi njia niliyo itumia kuondoka katika gorofa hili na kurudi katika gorofa nililo ingilia. Nikachungulia nje na kumuona Victoria na kijana wake wakiwa wamejibanza kwenye moja ya gari huku wakitazama jinsi magorofa yaliyo shambuliwa kwa mabomu ya ndege hizi za kijeshi jinsi yanavyo anguka chini. Nikakimbilia hadi eneo ambalo wapo, wote wakaonekana kunishangaa.

“Vipi?”

Niliwauliza ila Victoria akanipa ishara ya macho kwamba muda huu wapo hewani wanarekodi kila tukio linalo endelea katika eneo hili. Polisi wakaanza kushangilia kwa ushindi huo, Victoria na kijana wake wakakimbilia katika eneo hilo na kuanza kufanya mahojiano na askari wa Syria. Ikanilazimu mimi kuwasubiri hadi walipo maliza mahojiano yao, tukaanza safari ya kurudi hotelini huku ndani ya bajaji hii kila mtu yupo kimya pasipo kumsemesha mwenzake. Tukafika hotelini na moja kwa moja mimi na Victoria tukaeleka chumbani.

“Wewe ni nani?”

Victori aliniuliza huku akiwa amenikazia macho hadi nikastuka kidogo.

“Samahani sijakuelewa?”

“Tarique wewe ni nani, mpelelezi, mwanajeshi au nani eheee?”

Victori alizungumza kwa ukali sana huku akiendelea kunitazama. Taratibu nikaa kwenye moja ya kiti, nikashusha pumzi, nikaitoa bastola niliyo ichomeka kiunoni mwangu na kuiweka juu ya meza na kumfanya Victoria kustuka kidogo.

“Hata nikikueleza haito kuwa na maana yoyote kwako”

“Lazima iwe na maana kwangu, nimesha kueleza mambo mengi kwa maana nimetokea kukuamini kwa nini unashindwa kuniamini na mimi eheee. Ona”

Victoria alizungumza huku akinionyesha video kwenye simu yake aliyo nirekodi jinsi nilivyo kuwa ninaruka kwneye magorofa yale.

“Una uwezo mkubwa namna hii. Wewe sio raia wa kawaida, si ndio”

Nikamtazama Victoria kwa sekunde kadhaa.

“Mimi ni mpelelezi”

“Ohoo unaona sasa, ulikuwa unanificha nini sasa?”

“Unahisi kwamba hii kazi ni ya kumueleza kila mtu ehee?”

“Hata kama ila mimi nimesha kuwa rafiki yako Tarique”

Victoria alizungumza kwa kulalamika huku akinitazama usoni mwangu.

“Sasa ni nini kilicho kuteleta huku Syria?”

Nikanyanyuka kwenye kiti hichi nilicho kikalia na kufungua kabati nikatoa begi langu la nguo na kutoa faili ambalo linamaelezo ya kutekwa kwa balozi wa Pakistani nchini humu Syria, nikamkabidhi Victoria. Akaanza kulipitia faili hili kwa umakini sana.

“Mmmmmm huu mji ambao ameshikiliwa huyu balozi ni ngumu sana kuweza kuingia. Sasa utafanyaje?”

“Sijafahamu cha kufanya hadi hivi sasa ila inabidi niweze kuingia na kumuokoa huyo balozi na kurudi naye nchini Pakistani”

“Ngoja hadi jioni basi nitakuwa nimepata wazo la nini tufanye”

“Sawa”

“Vipi chakula cha usiku tutapata pamoja?”

“Ikiwezekana”

“Sawa”

Victoria akaingia bafuni na kuoga, nikaendelea kulipitia faili hili. Katika hali ya kustajabisha, Victoria akatoka bafuni humu akiwa uchi huku mkononi mwake akiwa ameshika taulo huku akijifuta futa maji. Akasimama mbele ya kioo kilichomo humu ndani na kuendelea kujifuta maji huku kwa mara kadhaa akiinama na kunifanya niweze kukiona kitumbua chake vizuri. Hali ya jogoo wangu ikazidi kufurukuta ndani ya suruali yangu, uvumilivu nahisi utanishinda baada ya muda mchache.

“Nenda kauoge”

Victoria alizungumza huku akinitupia taulo alilo kuwa akijifutia maji. Nikalitazama kwa umakini taulo hili kisha nikanyanyuka sehemu nilipo kaa, nikaanza kutembea kuelekea bafuni huku nikiwazia ni kwa nini binti huyu ameamua kunitega kwa kujiacha maungo yake wazi. Nikaanza kuoga taratibu huku nikitafakari mbinu na jinsi ambazo ninaweza kuzifanya kuhakikisha kwamba ninaifanya vizuri kazi iliyo nilete huku Syria. Nikamaliza kuoga na kutoka bafuni humu huku nikiwa nimejifunga taulo hili kiunoni, nikamkuta Victoria akimalizia kuvaa gauni lake jekundu na refu kuelekea chini.

“Tarique kuna mtu ninahitaji kukutananisha naye”

“Ni nani?”

“Tutatatoka usiku huu na kwenda kwenye moja ya mgahawa, ndipo nilipo ahidi kuonana naye”

“Tunaonana naye kwa madhumuni yapi?”

“Ya kazi yako au huitaji kazi yako iweze kwenda haraka”

Nikamtazama Victoria kisha nikamsogelea sehemu alipo simama na kutazamana naye usoni mwake.

“Kazi yangu sikuhitaji uitangaze kwa watu na sihitaji msaada wa mtu”

Kwa jinsi sauti yangu ilivyo nzito ikamfanya Victoria kutetemeka kidogo huku akitingisha kichwa akimaanisha kwamba amenielewa.

“Il….a..mtu ambaye nitakukutanisha naye atakuwa ni msaada mkubwa sana kwako?”

“Mtu huyo ni nani?”

“Kamanda wa jeshi la Uingereza lililopo nchini hapa Syria. Wapo hapa kwa ajili ya oparesheni ya kuwaokoa baadhi ya raisi wa Uingereza walio tekwa nao wapo ndani ya huyo mji. Hadi sasa hivi wana siku ya tisa katika nchi hii ila hawajafanikiwa kuweza kupata mwanya wa kuingia katika mji huo kwa maana umeimaeishwa vizuri na wapiganaji wa Islamic State. No body in, no body out”

Victoria alizungumza kwa haraka sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Kama wao wameshindwa unahisi watanisaidia nini mimi?”

“Tarique kumbua kwamba wewe una mission yako na wao wana mission yao, ila sehemu ya tukio ni moja. Endapo mutachanganya mawazo yenu kwa pamoja, nina imani munaweza kutengeza kitu. Isitoshe wanaweza kukusaidia hata silaha na mambo mengine ya kijeshi humbug tazama una bastola moja hadi sasa hivi unahisi unaweza kufanya nini mpenzi?”

Nikakaa kimya huku tukiendelea kutazamana na Victoria, kweli jambo analo lizungumza ni la ukweli kabisa, isitoshe nimeweza kushuhudia mziki wa wapiganaji hawa wa Islamic State si watu wa mchezo mchezo.

“Niazime simu yako”

Kwa ishara Victoria akanionyesha simu yake mezani, nikaichukua na kumuomba aweze kutoa neno la siri ili niweze kuitumia, alipo fanya hivyo nikaingiza namba ya Professa na kuipiga, kwa bahati nzuri namba hiyo ilianza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.

“Habari Professa”

“Mmmm nani mwenzangu?”

“Randy”

“Hapana si Randy, nakata simu kwa heri”

Simu ikakatwa na nikajikuta nikishusha pumzi taratibu kwani sauti yangu ya asili imebadilika na hata sura yangu nimefanyiwa upasuaji ambao umenibadilisha kwa kweli muonekano halisi ambao nimezaliwa nao. Nikarudia tena kuipiga namba ya Preofessa, ikaaza kuita kwa muda kisha ikakatwa. Nikarudi kwa mara ya tatu, ikaita kwa muda mrefu kabla hata haijakatika ikapokelewa.

“Haloo”

Nikaisikia sauti ya Jane, jambo lililo ufanya mwili wangu wote kusisimka. Nikatamani kuzungumza kitu ila nikashindwa.

“Halooo”

“Ja…..”

Nikajikututa nikiishia njiani kuliita jina la Jane kwani sauti iliyo toka ni mbaya zaidi na hata sauti ambayo nilizungumza na Professa.

“Randy”

Nikastuka sana Jane kuniita sauti yangu, machoni yakaanza kunilenga lenga huku Victoria akinitazama kwa umakini sana.

“Ndio ni mimi”

“Ohoo asante Mungu, vipi una umwa baba angu?”

“Hapana”

“Nini tatizo kwa maana sauti imebadilika kidogo”

“Nitakujulisha tukionana ila ninaomba nizungumze na Professa”

“Professa huyu ni Randy kweli”

Niliisikia sauti ya Jane akizungumza na Professa.

“Mbona sauti yake inatisha hivi?”

“Mimi ninamfahamu Randy kwa mambo mengi sana, huyu ndio yeye niamini mimi. Wewe zungumza naye”

“Haloo”

“Nashukuru umepokea simu Professa. Kuna jambo moja ninahitaji kukuomba”

“Jambo gani?”

“Nipo nchini Syria kwa sasa, kuna kazi moja nimakuja kuifanya huku kama undercover agent. Ila ninahitaji uweze kunisaidia kuweza kugundua ni eneo gani alipo huyu mtu niliye kuja kufanya kazi ya kumchukua.”

“Ohoo…taratibbu Randy, umekuwa undercover kwa maagizo ya nani?”

“Ninafanya kazi chini ya serikali ya Pakistani kwa sasa”

“Pakistani?”

“Ndio”

“Kwa nini?”

“Ni historia ndefu sana Professa, ila tambua kwamba kwa sasa sina muda wa kutosha kuweza kuendelea kuzungumza ila jambo ninalo kuomba ndio hilo naninakuomba uweze kunisaidia kuhakikisha kwamba nina mpata mtu ambaye nitakutumia detail zake.”

“Sawa nitakusaidia, ila nilazima nimueleze baba yako kwa maana tumejaribu kukutafuta kwa udi na uvumba ila tumegonga mwamba”

“Natambua hilo, ila samahani naomba umuweke Dany nje ya hili jambo kwa maani ni hatari sana kwa ajili ya maisha yake. Nimefanya hivi kwa ajili ya familia nzima. Tafadhali Professa naomba uweze kunisaidia hili swala”

“Nitakusaidia, nitumie detail zake kisha baada ya muda nitakueleza ni wapi alipo”

“Nashukuru”

Nikakata simu na kuanza kupiga picha maelezo yote ambayo yapo kwenye faili hili, kisha nikamtumia Professa kupitia mtandao wa Whatsapp.

“Watu ulio zungumza nao unauhakika watakusaidia?”

“Ndio watu wa pekee ninao waamini kwenye maisha yangu na ninaamini watanisaidi”

“Wapo wapi?”

“Tanzania?”

“Afrika!!?”

“Ndio mbona una shangaa?”

“Ni mbali sana kuweza kuupata huo msaada”

“Wewe tulia kila jambo litakuwa sawa”

Nikamkabidhi Victoria simu yake kisha nikaanza kuvaa suti yangu nyingine nyeusi. Nikajiweka sawa, kabla sijamaliza kufunga tai yangu, simu ya Victoria ikaanza kuita.

“+225 nahisi ni namba yako ndio inapiga kwa maana hizi code ni za mbali sana”

“Ndio”

Victoria akanikabidhi simu yake na nikaanza kuzungumza na Professa, akaanza kunitajia eneo alipo balozi huyu na akanitumia ramani ya mji huo na maeneo yote yenye ulinzi mkali sana na maeneo yasiyo na ulinzi mkali ambao ninaweza kuingia pasipo kugundulika kwani kuna baadhi ya wananchi wanakaa katika mji huo.

“Nashukuru sana Professa”

“Usijali ila kuwa makini kwa maana Jojo dada yako sasa hivi ana hangaika kuweza kukutafuta sehemu ulipo ila hadi sasa hivi sijaweza kupata update yoyote kutoka kwake”

“Naomba usimueleza chochote, kila jambo ninahitaji kulifanya kwa uangalizi na sihitaji mtu yoyote aweze kuumia”

“Sawa ila kwa Jojo ni ngumu kuweza kuumia”

“Kivipi?”

“Kwani hujafahamu uhalisia wa dada yako hadi sasa hivi?”

“Uhalisia gani?”

“Malizia kazi yako kisha nitakueleza. Kwaheri”

Simu ikakatwa, nikapitia ramani hii iliyo pigwa kwa juu kwa mfumu wa Satelait na inanionyesha vizuri majengo katika eneo hilo na maneo yote ambayo tunaweza kuingia. Tukatoka chumbani humu huku nikiwa nimeichomeka batsola yangu kwa kiononi kwa nyuma kwa ajili ya ulinzi binafsi kwa maana hii nchi haina amani hata theluthi, Victoria akamgongea Omary chumbani kwake.

“Ndio boss”

“Tunatoka, hakikisha kwamba una kuwa makinia. Hata malaya unao taka kuwachukua hakikisha kwamba hawakujui wewe ni nani, usije ukauwawa kizembe umenielewa?”

“Sawa boss nimekuelewa”

Omary alizungumza huku akitabasamu. Tukatoka ndani hapa na kuingia kwenye moja ya taksi ya kukodi. Victoria akamuelekeza dereva huyo eneo la mgahawa ambao tunatakiwa kuelekea.

“Una hakika huyo mtu ataweza kusai……”

Kabla sijamalizia sentensi yangu tukastukia gari ikianza kuyumba huku risasi moja ambayo hatujui imetokewa wapi, ikiwa imempiga dereva kichwani mwake na kumfanya apoteze maisha hapo hapo jambo lililo tuchanganya sasa mimi na Victoria.



Gari ikazidi kupoteza muelekeo na kujikuta ikigonga ngozo moja ya umeme iliyopo pembezoni mwa barabara na gari ikasimama.

“Upo salama?”

Nilimuuliza Victori huku tukiwa tumeinama chini.

“Yaa na wewe?”

“Nipo salama, fungua mlango wa upande wako huko na uangukie kwenye mtaro”

Victoria akafanya kile nilicho mueleza, akatoka kwenye gari hili na kuingia kwenye mtaro, nikatoka kwenye mlango alio tokea yeye kisha tukaanza kukimbia ndani ya mtaro huu ili hata wale walio kusudia kutufanyia uvamizi basi wasiweze kutukuta eneo la tukio. Tukazidi kusonge mbele hadi tukafika kwenye moja ya karavati.

“Ohoo Mungu wangu”

Victoria alizungumza huku akihema sana, akatoa simu yake na kuanza kuminya minya.

“Unataka kuwasiliana na nani?”

“Na rafiki yangu, nahitaji nimueleze kilicho tokea waje kutupa msaada wa kijeshi?”

“Hapana acha kwanza”

“Tarique!!?”

Victoria alishangaa huku akinitazama usoni mwangu, nikaichukua simu yake na kuiingiza mfukoni mwake. Tukatokezea upande wa pili wa karavati hili na kusimama barabarani huku tukitazama eneo la ajali kwa mbali sana huku tukiona baadhi ya watu wakiwa wamelizunguka gari tulilo kuwa tumependa.

“Tuondoke”

Nilizungumza huku nikimshika Victoria mikono yake, tukazidi kusonga mbele hadi tukafika eneo ambalo kuna magesho ya waendesha bajaji kadhaa, tukaingia kwenye moja ya bajaji na Victoria akamuomba dereva huyo atupeleke katika mgahawa ambao tumekusudia kukutana na huyo rafiki yake ambaye ndio mkuu wa kikosi cha jeshi la Uingereza nchini hapa Syria. Hatukuchukua muda mrefu sana tukafika katika mgahawa, Victoria akamlipa dereva huyu kisha tukashuka na kuinhia katika mgahawa huu na kumkuta jamaa mmoja mwenye asili ya Uingereza akiwa amekaa katika meza iliyo jitenga huku akiwa amevalia mavazi ya kirai. Victoria akaongoza hadi kwenye meza ya jamaa huyo, tukaa katika viti viwili ambavyo vimeandaliwa kwa ajili yetu. Nikaangaza eneo hili huku nikiwa makini kutazama watu waliomo humu ndani, baadhi ya wateja nikagundua ni wanajeshi kutoka Uingereza japo wamevalia nguo za kiraia na wapo hawa kwa ajili ya kumlinda mkuu wao.

“Vipi mbona mumechelewa?”

Jamaa huyu aliuliza huku akimtazama Victoria usoni mwake.

“Katika taksi ambayo tulipanda, tulishambuliwa na watu tusio wafahamu”

“Wameweza kufahamu ni wapi muna kuja?”

“Hapana hawajafahamu kwa maana tuliwatoroka”

“Ahaaa…..Ehee huyu ni nani?”

“Anaitwa Tarique ni afisa upelelezi kutoka nchini Pakistani, niliongozana naye kwenye ndege niliyo kuwa nimepanda na alisaidiana na askari kuhakikisha mji ule ulio kuwa umevamiwa leo ubaki mikononi mwa serikali. Tarique huyu ni rafiki yangu anaitwa Henderson.”

“Nashukuru kukufahamu”

Nilizungumza kwa sauti yangu nzito hadi Hendarson akashangaa kidogo.

“Sura yako haindeni na sauti yako”

Henderson alizungumza huku akinikazia macho.

“Hivi ndivyo jinsi nilivyo umbwa.”

“Hapana sio jinsi ulivyo umbwa, ila tuendelee”

Nikaanza kujiuliza maswali kadhaa kichwani mwangu, huyu Henderson atakuwa amefahamu kitu nilicho fanyiwa na Farida na watu wake au, ila nikakosa jibu la uhakika.

“Nimekuja na Tarique na nina imani kwamba munaweza kusaidia katika oparesheni ambayo mutakwenda kuifanya kuwaokoa baadhi ya raisi wezetu wa Uingereza na hata Henderso mwenye ana kazi ya kumuokoa balozi wa Pakistani aliye shikiliwa na magaidi wa kundi la Islamic State katika mji wa Raqqa.”

Victoria alizungumza hukua kitutazama. Nikatoka simu yake mfukoni na kuweka ramani ambayo tulitumiwa na Professa kwenye hii simua ya jinsi tunavyo weza kuingia kwenye mji huo wa Raqqa.

“Umeipata wapi hii ramani?”

“Ni ramani niliyo tumiwa na mtaalamu wangu wa maswala ya IT, hivyo kazi ni kwetu, tunahitaji kusonga mbele au mimi mwenyewe nisonge mbele”

“Nitawezaje kukuamini wewe na kuamini ramani yako ikiwa sikufahamu?”

“Mimi pia sikufahamu na siwezi kukuamini, hii ni kazi tunashirikiana na tunafanya kwa pamoja ukihitaji tunafanya usipo hitaji hatufanyi”

Nilizungumz akwa kujiaminni huku nikimtazama Henderson, ambaye bado anaendelea kuitazama ramani hii.

“Tumejaribu kutafuta picha za satelaiti kwa muda mrefu juu ya mji huo ila tumeshindwa, sasa wewe kutujia na hii hapa ni jambo ambalo ninahitaji kukudasisi kidogo kwa maana sihitaji nikawapeleka vijana wangu sehemu ambayo mwisho watauwawa kizembe”

“Swali unaamini unacho kiona au huamini?”

Henderson akakaa kimya kwa muda kidogo kisha akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ana anaamini kile anacho kiona.

“Ila angalizo, ninahitaji kuifanyia uchunguzi hiyo ramani, kama huto jali ninaomba unitumie kwenye simu yangu ili tukiruzi kwenye base yetu tuweze kuifanyia uchunguzi”

Nikaichukua simu ya Victoria kutoka mikononi mwa Henderson.

“Nenda kajadiliane na vijana wako, siku ambayo mutakuwa na haja ya kwenda kuifanya hiyo kazi basi unajua wapi kwa kunipata, ila kwa sasa sio rahisi kwa mimi kuweza kutoa hii ramani. Samahani kwa hilo”

Henderson akanitazama kwa muda kisha akatabasamu.

“Sawa bwana Tarique tumekuelewa, tuhakikisha kwamba tunafanya hivyo”

“Nashukuru”

“Vipi niagize chakula cha usiku?”

“Hapana, tutakwenda kula hotelini, ila kama hamtojali tunaomba msaada wa usafiri”

“Sawa tutawapelekea hadi kwenye hoteli muliyo fikia, nina imani kesho asubuhi tutafika hapo kuwachukua ili tuweze kupanga jinsi gani tunavyo weza kwenda kuifanya hii oparesheni kwa pamoja”

“Nashukru”

Tukaondoka katika mgahawa huu na kuingia kwenye moja ya gari kati ya magari mawili ya wanajeshi hawa wa Uingereza, tukainza safari ya kurudi katika hoteli. Ndani ya gari sikuzungumza chochote zaidi ya kumuacha Victoria na Henderson wakiendelea kuzungumza, tukafika hotelini salama salmini, tukaagana na Henderson kisha tukaingia ndani.

“Tangulia juu mimi ngoja niagize chakula”

Victoria alizungumza hukua akinitazama.

“Hapana twende wote”

“Sawa”

Tukafika katika eneo la kuagizia chakula, tukaagiza chakula tutakacho tumia usiku wa leo kisha tukaelekea chumbani, kabla ya kuingia chumbani kwetu, Victoria akagonga mlango wa chumba cha Omary.

“Nani?”

“Mimi”

Baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa na Omary akiwa amevaa taulo kiuoni mwake.

“Tumerudi, vipi mbona jasho lina kumwagika?”

Victoria alimuuliza Omary ambaye kdogo akafungua mlango na tukawaona wasichana watatu wakiwa uchi kitandani.

“Mmmmm haya usiku mwema”

Tukaingia kwenye chumba chetu.

“Yaani starehe kubwa ya Omary ni ngono aisee”

“Wasichana watatu atawamudu?”

“Heee hata watano anawamudu”

“Mmmm”

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG