AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2
WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+
SEHEMU YA 9 KATI YA 10
“Asallam Alghaikum?” “Salama, nina imani umepata sehemu sahii ya kujificha?” “Ninashukuru sana Dany kwa maana kuna mmoja wa watu wangu ndio alikuwa anavujisha signal ndio maana wamarekani waliweza kufanikiwa kuyanasa mawasiliano yetu” “Sawa ninaimani hilo umelishuhulikia?” “Ndio nimelishuhulikia kabisa kabisa. Ila sijasikia mashambulizi yoyote kutoka sehemu ambayo ilikuwa maficho yangu?” “Niliweza kuziteketeza ndege zote hewani, kwa hiyo hapakuwa na ndege moja iliyo weza kufika nchini Pakistani” “Ohoo Allah akuzidishie” “Shukrani” “Sasa tunaweza kuonana, kwa maana kuna mengi sana ninahitaji kuzungumza nawe” “Hilo halina kipingamiza, ila kuna jambo moja ninahitaji unisaide” “Zungumza” “Wamarekani wamamkamata mke wangu ambaye ni mjamzito kwa sasa, wanamtumia yeye kuhitaji nijisalimishe mikononi mwao, ninakuomba sana uweze kuniasidia katika kumuokoa kutoka mikoni mwao, na siku tukionana basi itakuwa ni siku nzuri ya urafiki wetu” “Usijali katika hilo, nitahakikisha kwamba wapelelezi wangu wanafanya kazi usiku na mchana kufahamu ni wapi alipo mke wako kisha tutamchukua tu. Nipatie picha yake ili iwe raisi kuweza kumpata” “Utatumia muda wowote kuanzia hivi sasa” “Tayari” Ester aliziungumza
“Nimeipata, ninakuahidi rafiki yangu nilazima mke wako tumpate” “Ninashukuru” “Basi nikimpata nitakuambia ni wapi tuonane ili tuweze kukabidhiana” “Sawa sawa” Mazungumzo kati yangu na Osma yakaishia hapa na kunifanya niwageukie Livna na Sara walio simama pembeni yangu.
“Sara nina imani kwamba umeamini” “Jamani huyu baba tuliambiwa ni marehemu kabisa” “Yupo hai na taafira zilikuwa ni za uongo” “Mmmm makubwa basi” “Martin pole sana mdogo wangu” “Usijali mkuu ni jukumu langu” “Usiku huu ninahitaji tufanye sherehe na wasichana wangu wote, kwa maana leo nimepata nafasi nyingine ya kuishi. Ninakuomba Ester ulisimamie hilo, pia tutamkaribisha Sara nyumbani sasa” “Sawa mkuu”
“Jamani ninaomba nikapumzike kidogo” Martin alizungumza kwa sauti ya upole kidogo nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikatingisha kichwa kumkubalia kwamba aende akapumzike.
“Unaonaje ukawasiliana na K2 sasa hivi ili kumpa presha?” “Hapana ngoja siku ya leo ipite, tunahitaji kupumzika, kwani tumefanya kazi kubwa sana” “Sawa ni wewe tu Dany” Maandalizi ya sherehe yakaanza kufanyika, Livna akaanza kunitembeza katika meneo ambayo sikuwahi kuingia ndani ya hii meli kubwa sana.
“Dany” “Naam” “Ninakupenda” Livna alizungumza huku tukiendelea kutembea taartibu tukielekea katika eneo jengine ambalo ameniambia linatatumika kwa kuzalishia mazoa mbali mbali yanayo tumika ndani ya hii meli.
“Ninakupenda pia” “Kweli Dany, yaani leo nilipo zimia pale, picha ambayo inijia akilini mwangu ni yako, nilihisi ninakwenda kufa kusema kweli nilimuomba Mungu kwa mara yangu ya kwanza kunipa nafasi ya kiishi ili nije kuishi kama mama sasa” “Unahitaji kuzaa na wewe?” “Ndio, Dany umri wangu unakwenda sasa, na mimi siku nahitaji kuwa mama ninahitaji kuwa mama. Wewe ndio mwanaume sahihi wa kunipatia ujauzito sihitaji kufa nikiwa sina mtoto japo kwa mara ya kwanza niliapa kutokuwa na mtoto ila sasa ninahitaji” Tukaingia katika eneo hili ambalo ni kubwa kama hekari kumi, limejaa udogo mwishi pamoja na mazoa ya kila aina, nikajikuta nikiwa ninashangaa kwani utaalamu huu sijajua wameutolea wapi.
“Mumefanyaje fanyaje hadi kuwa hivi?” “Mimi mwenyewe kusema kweli nimekuta hili shamba kutoka kwa waanzilishi, na mimi nikaliendeleza kulilima na vijana wanaendelea kupata matunda ya kila aina” “Kusema kweli sijapata ona kitu kama hichi” Tukaanza kutembea ndani ya hili eneo ambalo kwa pembeni limezingushiwa vioo.
“Haya mazao yanakua kwa mionzi ya jua inayo ingia, seme sasa hivi ni jioni kama tungefika mchana basi tungeweza kuona jinsi mionzi ya juu jinsi inavyo ingia ndani ya hili eneo” “Inashangaza kusema kweli daaaa” Niliendelea kuzungumza huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa kwani hili eneo unaweza kusmea ni shamba ambalo lipo nchi kavu kumbe ni ndani ya meli hii kubwa ambayo imeundwa kwa utaalamu mkubwa ambao unaweza kuwafanya watu kuishi miaka kwa miaka. Simu ya Livna ikaita, akaitoa mfukoni mwake na kuipokea. Akasikiliza kwa sekunde kadhaa akionekana anakabidhiwa maeleo fulani.
“Tunakuja sasa hivi” Livna akakata simu na kuiridisha mfukoni mwake.
“Kuna nini?” “Martin” Livna alijibu huku akianza kukimbia, tukazidi kukimbia kuelekea ndani. Tukafika katika chumba cha Martin na kukuta madaktari wawili wa kike wakiwa wamemvua shati lake huku pembeni ya tumbo lake upande wa kulia kukiwa na damu nyingi.
“Amefanyaje?” “Amepigwa risasi iliyo zama ndani na imeharibu sehemu kubwa sana ya vitu vya ndani, jambo linalo weza kupelekea kufa muda wowote kuanzia hivi sasa” Maneno ya msichan huyu ambaye ni daktari yakanifanya nibaki na mshangaoo huku machozi yakinilenge lenga, hapa ndio nikakumbuka jinsi nilivyo mtazama Martin usoni mwake kipindi alipo aga anakwenda kupumzika, alikuwa ni mnyonge sana kupita siku zote nilizo wahi kumfahamu na kufanya naye kazi.
“Apegiwa risasi saa ngapi jamani?” Livna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Hili jeraha alikuja nalo na mimi ndio mtu wa kwanza kumuona” Daktari alizungumza huku wakiendelea kujaribu kuitoa risasi iliyopo tumboni mwa Martin.
“Martin, Martin, Martin?” Niliita huku niwa nimechumaa pembeni yake. Martina hakuitika wala kuyafumbua macho yake zaidi ya kukaa chini.
“Tunahitaji damu ya mtu mwenye group A plus” Nesi alizungumza huku akiweka kifaa maalumu cha kupumulia pauni mwa Martin.
“Nitoeni mimi” “Inagidi kukupima kwanza, tufahamu kwamba ni group O plus kwa maana Martin kundi lake la damu ndio hilo” “Nipimeni tu” Nilizungumza huku nikikunja mikono ya shati hili la jeshi nililo vaa, nikatoka chumbani humu na daktari mmoja na kuelekea hadi maabara. Akatoa damu yangu kiasi na kuipima.
“Damu yako ipo safi, na ni group A plus, inabidi utoe japo chupa mbili za damu” “Sawa dokta fanya haraka haraka basi” “Sawa” Dokta akaufunga mkono wangu na mpira unao vutika kisha akanichoma sindano iliyo anza kupeleka damu kwenye dripu. “Itachukua muda kidogo hadi kujaza chupa moja” “Sawa, hivi ulimuonea wapi Martin kama amepigwa risasi?” “Nilimkuta karibu na mlango wake akiwa ameegemea ukutani huku ameshika tumbo lake, nilipo mchunguza nikaona kiganja chake kimelowana damu, ikanibidi kumdadisi sana japo alikuwa anaficha mtu asione, katika kuminyana minya ili nione, akaanguka chini na kupoteza fahamu. Nikamuingiza chumbani kwake na tukaanza kumshuhulikia, na katika semehu ya jeraha tuliona amejifunga kitambaa kikubwa ambacho kilizuia kuonekana kwa damu yake” “Daaa” Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na majonzo mengi sana. Ikamalizika chupa moja, dokta akaitoa na kuweka chupa nyingine, kisha akatoka na chipa hii na kuniacha mimi nikiendelea kutoa damu hii.
‘Mungu ni mwema kwa kweli, kugongana kote huku sijapata Ukimwi mmmmmm’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kutazama damu hii jinsi inavyo ingia kwenye dripu. Nesi akaingia ndani ya chumba hichi huku akiwa ameshika dripu alilo toka nalo.
“Vipi?” Nilimuuliza huku macho yakiwa yamenitoka sana.
“Martin amekufaa” Nikahisi kama nipo ndotoni, nikajaribu kuyafumbua macho yangu zaidi na zaidi ila hakuna kilicho badilika mbele yangu kwani, daktari ninaye muona na mandhari ninayo yaona ni yale yake. Kwa haraka nikachomo sindani niliyo chomwa kwenye mkono wangu, nikafungua mpira huu na kutoka chumbani humu nikikimbia kuelekea katika chumba cha Martin. Nikiwa ninakaribia mlangoni nikaisikia sauti ya Winy akilia kwa uchungu, nikaingia ndani na kumkuta Winy akiwa amelaza kichwa chake kifuani mwa Martin, Livna amesimama pembeni yake huku naye machozi yakiwa yanabubujika usoni mwake. Daktari amesimama pembeni Livna akiwa ametulia kimya.
“Hapana Martin huwezi kufa kizembe hivi” Nilizungumza huku nikisegelea kitanda cha Martin, nikakaka pembeni ya kitanda hichi na kumtazama usoni mwake.
“Martin acha ujinga basi kuigiza vipi hivi rafiki yangu eheeee” Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Hawa na Babyanka nao wakafika ndani ya hichi chumba kila mtu aliye muona Martina akiwa amelala hapa kitandani na ameyafumba macho yake kusema kweli roho yake iliweza kumuua kwa staili yake.
“Martin si umetoka kuniaga kwamba unakwenda kumchukau mtoto wa K2 jamani mbona umeondoka mapema jamani, ikiwa penzi letu ndio kwanza limeanza jamaniii Martinnnnnnn” Winy aliendelea kuzungumza machozi yakizidi kumwagika. Nikanyanyuka kiitandani humu na kumshika mkono Livna na kutoka naye.
“Dany tunaelekea wapi jamaani” Livna alizungumza huku akijaribu kusimama ila nikamshika kwa nguvu na kuendelea kumvuta. “Mtoto wa K2 na Wamarekani ni lazima walipe kwa hili walilo lifanya, siwezi kumpoteza mtu ninaye mpenda. Martin ni sawa na mdogo wangu” Niliendelea kuzungumza kwa jazba kubwa. Tukaingia katika chumba cha mawasiliano na kukuta kukiwa hakuna mtu.
“Niitie Ester na Logate, waje na huyo kibonge” Livna akabaki akabaki na bumbuwazi, nikamgeukia na kumtazama kwa macho makali sana, akatoka chumbani humu yeye mwenyewe. Baada ya dakika mbili akarudi akiwa ameongozana na Ester pamoja na Logate.
“Yupo wapi kibonge?” “Amelala” “Kamlete, analala hapa kwao. Fanya fasta sawa” Nilizungumza kwa ukali, Logate akatoka kwa haraka humu ndani kwani kila mmoja nina imani leo hii ndio ananiona nikiwa nimekasirika kwa kiwango hichi.
“Wasiliana na LIVNA” “Livna!!?” “K2” Ester akati kufanya kile nilicho muagiaza, haikuisha hata dakika moja nikamuona K2 mbele ya hii video. “Mbona macho mekundu hivyo unavuta bangi siku hizi?” Swali la kejeli la K2 likanifanya nizidi kupangwa na hasira, mtuto wake akaingizwa humu ndani, alipo muona mama yake kwenye hii tv akakibilia sehemu nilipo simama.
“Mamaaaa” K2 akastuka sana kumuoan mtoto wake mikononi mwake.
“U…..uu….umefikaje huk…..” K2 alizungumza kwa kigugumizi kikali sana, nikamuona jinsi jasho likimwagika usoni mwake.
“Nipatie bastola” Niliungumza huku nikimshika mtoto wa K2 na kumuweka mbele yangu.
Livna akanirushia bastola yake, nikaidaka vizuri, nikaikokoki na kuiweka kichwani mwa mtoto wa K2 aliye anza kutetemeka mwili mzima.
“Mtu wangu mmoja amekufa. Martin amekufa kwa ajili yako wewe malaya, pamoja na huyu nguruwe wako. Umemua Lucy sasa shuhudia ninavyo mfumua ubongo sawa” Nilizungumza kwa ukali sana.
“Mamamaaaaaaa” “Dany, Dany ninakuomba, ninakuomba sana nipo chini ya mguu yako, nipo tayari kufanya chochote unacho niagiza hivi sasa” K2 alizungumza huku machozi uakiendelea kumwagika usoni mwake.
“Dany vita yako ni mimi na wewe, mwanangu hana hatia yoyote katika hii vita…ha……” “Hana nini mpuuzi wewe, ulivyo muua malaika wangu ambaye hata raha ya dunia hakuwahi kuiona. Hadi leo sitambuu ni wapi walipo zikwa, alafu unaniambia kwamba hana hatia” “Dady nimekosa, shetani shetani alini……” Nikampiga risasi ya bega mtoto wa K2 na kumfanya aanguke chini na kuangua kiliok ikali sana. Nikamnyanuyua huku nikimtazama K2.
“Ulihisi nitakushindwa, ulihisi kumuweka mwanao mbali na Afrika, nitashindwa kumuangamiza eheeee” Niliendelea kufoka, K2 machozi yaliyo ambatana na makamasi yakazidi kutiririka usonimwa K2.
“Dany nipo tayari kufa, nipo tayari uniue na mkono wako” Kilio cha mamuvu cha mtoto wa K2 pamoja na mama yake vikaendelea kutawala hapa. Nikamtazama K2 kwa muda wa dakika moja, kisha nikamsukumia mtoto wake pembeni.
“Unamasaa kumi na mbili hakikisha unajisalimisha kwa mtu nitakaye kuambia” “Niambie tu Dany, niambie mimi nipo tayari kujisalimisha” “Kwanza kiri dhambi zako kupitia vyombo vya habari, nitakatishe na useme kwamba mimi sina hatia na ugaidi wote huo. Wewe ndio gaidi japo itakuwa ni ngumu kwa watu kunielewa, ila hakikisha kwamba unanisafisha mimi sawa” “Nitafanya hilo” “Pili ukimaliza jisalimishe mikononi mwa OSAMA Bin Ladane” “Osama!!?” “Fanya hivyo, sihitaji maswali mengi na sihitaji kuwasiliana nawe, nikiwasiliana nawe masaa kumi na mbili yajayo uwe mikononi mwa Osama sawa” “Sawa nimekuelewa, nimekuelewa Dany” Nikazima Tv na kumtazama mtoto wa K2 anye endelea kulia hapa chini huku bega lake likiendelea kuvujika damu.
“Mtoeni hapa nisije nikamuua” Logate kwa haraka akamnyanyua mtoto huyo na kuondoka naye.
“Dany” Livna aliniita huku akinisogelea pembeni yangu, akanishika mkono wangu wa kulia na kuichukua bastola yake na kuichomeka kiunoni mwake. Taratibu akanikumbatia huku machozi yakiendelea kumwagika.
“Naogopa Dany, Martin amechukua kifo changu. Yote ni makosa yangu Dany” “Shiiii…..sio makosa yako, usijilaumu katika hili” “Kwa nini jamani nisinge mzuia, kwanini eheeeee?” Nikazidi kumkumbatia Livna. Baada ya dakika kama kumi nikamuachia na kumkalisha kwenye kiti.
“Ester sherehe zote zikatishe, watu wote wavae nguo nyeusi. Tupo kwenye msiba” Livna alizungumza kwa sauti ya ungonge huku akimtazama Ester usoni mwake.
“Sawa mkuu”
“Muje kusafisha hii damu hapa sawa” “Sawa mkuu”
Masaa yakazidi kusonga mbele huku nikiwa siamini kabisa kwamba Martina amekufa, kwa mara kadhaa nikajikuta nikienda kwenye sehemu maalumu alipo hifadhiwa, kumuangalia kama atanyanyuka kutoka katika usingizi ila ndio hiyo hata kufumbua macho yake hawezi. Uhodari wake na kujitoa kwake kote kumeishia hapa. “Samahani kwa kukusumbua” Daktari aliye muhudumia alizungumza huku akiingia akirudishia mlango wa chumba hichi maalumu cha kuhidadhia maiti.
“Kwenye nguo za Martin tumeikuta hii karatasi, nina imani kwamba ni ujumbe wako” Daktari akanikabidhi karatasi hii iliyo kunjwa vizuri, kisha akatoka chumbani humu. Taratibu nikaifungua na kuanza kuisoma humu ndani.
{Dany kaka, ninajua utaumia sana kuona siku moja nikiwa nimeondoka duniani. Ninautambua upendo wako mkubwa unao zidi kuuonyesha kwangu mimi. Leo hii roho yangu imekuwa ni nzito sana, sijui kama siku ya leo kama nitaimaliza. Ninawaona rafiki zangu wa boko haramu wakiniita niwafwate kule walipo, natamani kubaki na wewe, ila muito wao ni mkubwa sana……}
Nikajikuta nikimwagikwa na machozi yaliyo anza kuidondokea karatasi hii, nikajifuta kisha nikaendelea kuisoma.
{……Sina jinsi kaka itabidi niondoke nikuache peke yako. Sijui ni kwa nini ninajikuta ninaandika maneno haya ila moyo na hisia zangu zinanisukuma kuandika hivi. Sijawahi kufanya kazi na mtu cheshi kama wewe, japo watu wa nje wanakuchukualia wewe vibaya, ila kusema kweli nimefurahi sana kufanya kazi kwako. Umenifanya niwe mahiri, japo ilikuwa ni hatari ila hukusita kunitetea na kunielekeza nini cha kufanya pale nilipo hitajika kufanya hivyo. Bro walinde watu wako, hakikisha maadui zako unawamaliza wote na baada ya hapo kaka mrudie Mungu wako, kwani yeye ndio atakuwa muamuzi wa mwisho pale siku ya mwisho itakapo wadia. Ninakuependa sana kaka Dany na Mungu azidi kukulinda. Amen}
Kijikatuni kidogo alicho kichora Martin hapa chini ya barua yake kinachomuonyesha amenipigia saluti kikanifanya nizidi kulia kwa uchungi tena kwa sauti ya juu sana. Kusema kweli kutoka moyoni mwangu, kifo cha Martin kinaniuma sana.
Hadi kunapambazuka sijapata hata lepe la usingiza zaidi ya kukaa pembeni ya mwili wa Martin ambao umechomwa sindao maalimu ya zuia kuto kuoza. Nikasimama wima, kisha nikapiga saluti huku machozi yakiendelea kunitiririka usoni mwangu. Nikatoka katika chumba hichi, kila msichana ninaye muona amevaa nguo nyeusi ikiashiria kwamba msiba huu umewagusa wote japo wengine. Nikaelekea chumbani mwa Livna na kumkuta akiwa amekaa kitandani, machozi uyamemjaa mwilini mwake na mkononi mwake ameshika pete ya ndoa.
“Japo nilichukulia ni jambo la kupita, ila pete hii inanikumbusha tabasamu lake. Kusema kweli Martin alikuwa ni mcheshi sana. Alijitoa kwa ajili yangu, japo nilimuumiza moyo wake na nikashindwa kujali hisia zake, ila bado aliona umuhimu wangu kwake.” Livna alizungumza kwa sauti ya upole sana huku macho yake yote ameyaelekezea kwenye pete hii ya dahabu anayo endelea kuizungusha zungusha taratibu.
“Martin kusema kweli sipati mfano wake, jana aliweza kunilinda kwa kila namna kwa maana yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kuzinduka baada kuzima. Kusema kweli alijikaza, kupigwa risasi na kutembea nayo pasipo kuonyesha dalili yoyote ya maumivu, kusema kweli amejikaza” Livna aliendelea kuzungumza, mlango ukagongwa.
“Nimesema sihitaji kusumbuliwa leo nahitaji kichwa changu kutulia” Mlango ukafunguliwa akaingia Ester na kusimama mbele yetu.
“Kuna nini tena Ester, hujasikia nilicho kuambia?” “Samahani mkuu ila hili swala ni muhimu sana. Ninawaomba mukaone” “Ni nini?” Nilimuuliza Ester huku nikinyanyuka kitandani na kusimama.
“Ni vyema tukaenda kujionea” Hatukuwa na namna zaidi ya kutoka humu ndani, moja kwa moja tukaeleka hadi chumba cha mawasiliano. Tukamkuta K2 akiwa amesimama kwenye Tv hii, usoni mwake amejawa na tabasamu pana sana.
“Nashukuru kwa kuja pole kwa msiba Dany wa huyu nguruwe wako. Ninahitaji tufanye biashara ya amani, niachie mwanangu nikupatie huyu” K2 akamsogeza Yemi mbele yake, akamkaba kabali ya shingo na kumuweka bastola begani mwake.
“Ninawashukuru Wamarekani kwa kuniletea hii zawadi nono. Sasa ni kidonda kwa kidonda” K2 akafyatua risasi iliyo toboa bega la Yemi na kumfanya alie kwa uchungu sana hadi nikabaki nikitetemeka mwili mzima kwa hasira kali sana.
Kilio cha Yemi kikaendelea kutawala humu ndani, hazikupita hata dakika tano akaanguka chini na kupoteza fahamu.
“Nipatie mwanangu, nikupatie huyu malaya wako la sivyo ninamuua huyu malaya. Sharti nilazima uje wewe katika mabadilishano akija mtu tofauti na wewe nilazima nitamuua” Nikaichukau rimoti iliyopo mezani na kuzima hii Tv, nikashusha pumzi nyingi huku nikikosa kitu cha kuzungumza.
“Dany” “Namm” “Tunafanyaje?” “Sijui kwa kweli” “Samahani wakuu ila ninaomba nishauri kitu” “Zungumza tu Ester” “Mimi ningeona tufanye kwanza mazishi ya Martin baada ya hapo tutajua ni kitu gani tunaweza kukifanya juu ya K2” “Wazo zuri, Dany tufanye kwanza mazishi ya Martin” “Tutamzika wapi?” “Utaratibu uliopo hapa, huwa mtu akifariki tunamchoma moto kisha majivu yake tunayamwaga baharini” Nikakaa kimywa kwa muda huku nikimtazama Livna usoni mwake, kisha nikatingisha kichwa kwa kukubaliana na utaratibu wao wa mazishi. Taratibu za mazishi zikaanza, baada ya masaa mawili, sote tukakusanyika katika ukumbi mkubwa. Msichana mmoja akaongoza sala iliyo fanyika kwa imani ya kikristo. Baada ya hapo mwili wa Martin ukaingizwa kwenye chumba maalumu cha kuchomea miili, sikuhitaji kukaa karibu kabisa na chumba hicho kwani sihitaji kusikia mzinga wa kichwa cha Martin kikipasuka katika moto.
“Dany” Hawa aliniita na kunifanya nimgeukie na kumtazama usoni mwake.
“Ninaweza kuzungumza nawe?” “Ndio” Tukaka kwenye viti vilivyopo katika mgahawa uliopo humu ndani ya hii meli.
“Ninaimani kwamba bado una chuki na mimi ila….” “Kwa sasa sihitaji kuzungumzia mazungumzo hayo, zungumza jambo la muhimu unalo hitaji kuzungumza na mimi” “Samahani kama nimekuudhi, ila pole kwa yaliyo mkuta rafiki yako” “Ni hilo ndio ulihitaji kuzungumza?” Kabla Hawa hajanijibu kitu chochote, nikamuona Ester akija huku kwa kasi akasimama pembeni yangu na kininong’oneza.
“Osama anahitaji kuzungumza na wewe, ameweza kufahamu ni wapi alipo Yemi” “Ni wapi?” “Tanzania” Kwa haraka nikasimama pasipo kumuaga hawa nikaondoka eneo hili na moja kwa moja tukaelekea katika chumba cha mawasiliano na kumkuta Osama akizungumza na Livna.
“Dany nina habari njema” “Ndio” “Yemi kwa sasa yupo Tanzania na vijana wangu tayari wamesha ingia nchini hapo” “Mumefahamu anashikiliwa na nani?” “Ndio, anashikiliwa na raisi wa nchi hiyo je tumlete raisi huyo akiwa hai au amekufa” “Ninamuhitaji akiwa hai, mukimkatama sehemu yoyote niambieni mimi nitafika sawa” “Sawa baada ya masaa kumi nitakufahamisha ni wapi tukutane nina imani vijana wangu watakuwa wamesha ikamilisha kazi hiyo” “Sawa nitashukuru sana” “Sawa ila pole kwa msiba wa rafiki yako Martin” “Asante” Tv ikazimwa na Livna.
“Unatakiwa ukayamwage majivu ya rafiki yako baharini” “Muda huu?” “Ndio” Tukatoka chumbani humu na kuelekea juu kabisa ya meli hii, nikakabidhiwa chungu kilicho jaa majivu ya mwili wa Martin. Taratibu nikachoa majivu haya na kuanza kuya mwaga baharini, zoezi hili nikasaidiana na Livna, Winy pamoja na Babyanka.
“Mwezetu ametutoka, kifo chake tuchukulie kama changamoto. Tutambue tupo kwenye changamoto kubwa, tupo katika vita. Tupo katika hali ya kupambana, sasa inakwenda kuisha, sasa nilazima kuwaagusha maadui walio baki mbele yetu. Si K2 wala Marekani” Nilizungumza kwa msisitizo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
“Baada ya masaa kumi, kila kitu kitaelekeweka, ninajua sasa hivi Wamarekani wameungana na K2, na sasa watakuwa wanashirikiana kwa kila jambo, sasa ninacho hitaji ni kunzisha vita. Acha dunia ilie kwa uzumbe wa viongozi wao” Niliendelea kuzungumza huku nikiwatazama wezangu hawa walio simama mbele yangu.
“Ninahitaji kila mmoja wenu kuhakikisha kwamba masaa kumi yanayo kuja dunia nzima imesha badilika, niwakati wa vita niwakati watu kuweza kunifahamu mimi kama wanavyo mfahamu Adolf Hitler” Watu wote wakaka kimya wakinitazama usoni mwangu.
“Dany natambua kwamba hupendi huruma yangu wala hupendi jinsi ninavyokuwa ninakushauri. Wewe sio gaidi, wewe ni mtu mwema, kwa nini wengine walie kwa ajili ya watu wachache. Kuna wamama, kuna watoto ambao hawana hatia ya vita ambayo unakwenda kuianzisha. Tafadhali Dany nipo chini ya miguu yako” Babyanka alizungumza na kupiga magoti chini huku akimwagikwa na machozi chini. Taratibu Winy naye kapiga magoti chini akiwa ni mnyonge sana. Kilicho zidi kunishangaza zaidi ni Livna naye kupiga magoti chini, wasicha walipo katika eneo hili nao wote wakapiga magoti chini kuniomba nigairi kwa maamuzi yangu niliyo yapanga. Nikawatazama kwa muda kisha nikaondoka eneo hili, nikaelekea chumbani kwangu na kujitupa kitandani. Hazikupita hata dakika kumi akaingia Livna huku akiwa mnyonge sana
“Dany” Livna alizungumza huku akinisogea akaka pembeni yangu huku akinitazama usoni mwangu.
“Samahani kwa kuweza kukutatisha tamaa katika lile ambalo umekusidia kulifanya. Jana nilitoka kukuambia kwamba ninahitaji kuzaa na wewe, alicho kizungumza Babyanka kusema kweli ni kitu cha muhimu hakuna haja ya watu wengine kuingia kwenye vita kwa ajili y….” “Nimekuelewa” Ilinibidi kumkatisha Livna sentensi yake kwani anahitaji kuzungumza kitu kule kile ambacho tayari walisha kizungumza.
“Ninakuomba nipumzike, ninahitaji kulala. Osama akihitaji kuwasiliana nami ndio muniamshe” “Dany sijamaliza kuzungumza mpenzi wangu”
“Kuna kitu gani hapo cha kuzungumza Livna?” Livna akakaa kimya baada ya kuniona nimekasirikia sana. Taratibu akanyanyuka na kuanza kutembea kueleka mlangoni, nikamtazama jinsi alivyo mnyonge kwa haraka nikasimama na kupiga hatu za haraka sana hadi mlangoni na nikauegemea.
Nikamvuta Livna kifuani mwangu na kuanza kumnyonya mdomoni, nikamnyanyua juu juu, nikamlaza kittandani huku nikiendelea kumnyonya midomo yake, Tukaanza kuvuana nguo, nikayashika maziwa ya Livna kwa pamoja na kuyakutanisha semu moja, nikaanza kuyanyonya kwa fujo na kumfanya Livna kutoa kilio cha mhaba.
Shuhuli ya kuburudishana ikaanza, kila mmoja safari hii anajitahidi kuhakikisha kwamba anamburudisha mwenzake, Livna hakuihitaji kuwa mnyonge sana kama mara ya kwanza, kili nilivyo jaribu kumgeuza akawa makini sana kuhakikisha simzidi maarifa.
“Dany ninakupenda mume wangu, ninakupenda mume wangu, nipe nipe mume wangu ooohoooo” Livna aliendelea kulalamika huku akijaribu kuzungusha kiuno chake. Mzunguko wa kwanza ukamalizika na kila mmoja akiwa anahema sana na kumwagikwa na jasho mwilini mwake. “Kwa shuhuli hii lazima tupate mtoto wa mwendo kasi jamani ahaaa” Livna alizungumza na kunifanya nicheke kidogo.
“Yaani mmmmm wewe mwanaume unanitomb** hadi hadi ninajisikia nipo kwenye dunia yangu mimi peke yangu. Kipindi kile nili’shindwa kukufaidi kutokana na yule Mariana ila kwa sasa nizamu yangu” “Faidi tu sasa hivi, ila muda wangu wa kuondoka duniani ukifika, itabaki historia” “Usizungumze hivyo Dany unanitisha mwenzio” “Ninakutisha na nini hapo ikiwa watu wengi wananiwinda kuitoa roho yangu. Vita ya dunia kwangu ndio kupona kwangu, na nyinyi mumekataa kunisikiliza ujue kwamba siwezi kutoroka katika mitego yote ambayo dunia nzima wanaipanga kunikamata. Ila wakipigana wao kwa wao basi nitaishi maisha marefu duniani”
“Mmmmm kusema kweli Dany hayo ni maamuzi magumu kwa kweli” “Kwa mfano Osama na watu wakefeli kumkamata K2 ni kitu gani kinacho kwenda kutokea hapo, nilazima Yemi afe. Kifo chake kitaniuma ila kitaniuma zaidi kwa ajili ya mtoto wangu aliyekuwa tumboni mwake.” “Una uhakika gani kwamba ni mwanao aliyopo tumboni, ikiwa Martin alinisimulia kwamba Yemi alichukuliwa na aliyekuwa mume wake” “Mimi ndio ninaye fahamu kitu gani ambacho kimetokea kati yangu mimi na Yemi. Japo aliondoka akiwa ananichukia ila hawezi kuzaa na mwanume yule” “Sawa Dany swala hilo sihitaji kuliingilia sana” “Poa” Baada ya muda mchache tukajikuta tukingia katika mzunguko wa pili ambao kusema kweli ukatufanya tufurahie penzi letu. Baada ya mechi hii kuisha nikajikuta nikipitiwa na usingizi mzito sana.
“Dany, Dany” “Mmmmm” “Amka muda umekwenda limebaki lisaa moja tu yatimie masaa kumi, ninaimani kwamba Osama ndani ya muda huo atawasiliana nawe” Nikamtazama Livna kwa macho yaliyo jaa usingizi, taratibu nikajivuta kitandani na kukaa kitako.
“Bado nina usingizi nina siku nyingi sijalala vizuri” “Amka bwana, nenda ukaoge upande nguvu” Livna akaendelea kunishawishi hadi nikajikuta nikiamka taratibu kitandani, nikaingia bafuni na kuoga, nirudi chumbani na kukuta Livna akiwa ameniandalia nguo nyingine za kuvaa tofauti na nguo za jeshi nilizo kuwa nimevaa. Tatatibu nikaanza kuvaa nguo hizi ambazo zote ni nyeusi kuanzia suruali hadi tisheti.
“Umependeza mpenzi wangu” “Asante, saa ngapi hivi sasa?” “Ni saa tato usiku” “Mmmmmm” “Yaaa, ndio maana nimekuamsha mpenzi wangu” Tukatoka chumbani humu na kueleka katika chumba cha mawasiliano. Tukawakuta Logate na Ester wakiendelea na kazi.
“Hamulaji jamani?” Niliwauliza huku nikikaa kwenye kiti ambacho nimezoea kukaa nikiwa ofisini humu.
“Tukilala sisi mkuu hakuna kitu kinacho weza kwenda” “Sawa sawa, ninashukuru kwa kujitoa kwenu” “Usijali ni jukumu letu” “Vipi kuna mpya yoyote hadi sasa?” “Hapana” “Hembu fwatilieni kuna mpya yoyote kutoka Tanzania” “Sawa” Ester na Logate wakaendelea kufanya kile nilicho waagiza, baada ya dakika tano, Ester akanitazama usoni mwangu huku akiwa na tabasamu kubwa.
“Kuna website moja imeandika kwamba raisi wa Tanzania amepotea katika mazingira ya kutatanisha” Taarifa hii ikanifanya nianze kupata matumaini makubwa ya kuamini kwamba Osama Bin ladanen na way wake wameifanya kazi ambayo waliniahidi kwamba wataifanya.
“Website hiyo munaweza kuiamini kweli je ikiwa imezusha story za uongo?” Livna alizungumza huku akitutazama usoni.
“Mkuu hii website ni ya uhakika hata taarifa zake ni za uhakika” “Serikali ina mamlaka ya kuambia website, blog ziandike chochote wakitakacho wewe na mukumbuke kwamba K2 ni mtu mmoja mjanja sana, mukumbuke kwamba ana uwezo wa kubadilisha moja ikawa mbili na mbili ikawa moja kama alivyo yafanya maisha ya Dany hapa” Maneno ya Livna kidogo yakakata matumaini yangu yote niliyokuwa nayo juu ya hii taarifa.
“Tusubirini tuone kitakacho si limebaki saa moja?” “No zimebaki dakika kama arobaini na tano hivi” “Sawa” Tukajaribu kufwatilia ya kutekwa kwa K2 kwenye vyombo vya habari vya Tanzania, ila hakuna kituo chochote cha Tv kilicho tanganza kutekwa kwa raisi. Hadi lisaa moja linakwisha hapakuwa na taarifa yoyote kutoka kwa Osama Bin Laden.
“Umeona, niliwaambia hiyo website imefanya kitu walicho elezwa na K2”
Livna alizungumza na kunifanya nikae kimya pasipo kuzungumza kitu chochote.
“Hembu jaribu kumpigia Osama video call” Ester akaanza kazi ya kumtafuta Osama Bin Laden hewnai.
“Hapatikani” Ester alizungumza kwa sauti ya upole.
“Shitiii…..” “Ninahisi kuna mpango ambao unaendelea” Livna alizidi kuzungumza na kunifanya nifikirie ni kitu gani ninaweza kuzungumza.
“Osama anaweza kuwa msaliti kwetu” Livna aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
“Tumpe muda?” “Muda gani tena hapo?” “Jamani kuna hichi munatakiwa kukiona” Logate alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka. Tukaona video ambayo inaonyesha nje ya ikulu ya Tanzania, gari mbili aina za Range rover nyeusi zilisimama, wakashuka waarabu wawili walio valia kanzu huku wakiwa na bunduki, akashuka Osama, tukamuona K2 akitoka ndani ya ikulu hiyo akisalimiana na Osama huku wakipeana mokono wakioneakana ni watu wanao juana kwa muda mrefu sana. Vidoe hiyo ikawaonyesha watu hao wakiingia ndani, hazikupita hata dakika tano zikaja gari nyingine mbili zikiwa na bendera za Marekani ikiasiria kwamba anaye fika hapo ni kiongozi wa Marekani.Wakashuka walinzi wenne kisha akashuka mwanamama mrefu na mweusi .
“Ni nani huyo?” Livn akanyanyuka kwenye kiti kikalia akasogelea karibu kabisa na Tv hii akionekana kuwa na wasiwasi. “Ni balozi wa Marekani anaitwa Bi Efracia Godwin” “Haiti Efracia hilo ni jina feki” Livna alizungumza kwa msisitizo huku akiendelea kumtaza mwanamama huyo.
“Jina lake ni Livna Tomsond miaka ishirini iliyo pita nilikuwa naye kwenye chuo kitengo cha FBI, ila mimi nilikwenda kama undercover kwenye kitengo hicho. Kama sasa hivi ni balozi basi tupo katika hali ya hatari” “Kwa nini?” “Ana roho mbaya ya Osama ni ndogo, nina imani kwamba yeye ndio mshawishi mkubwa kwenye nchi yake hadi wameamua kukaa meza moja na Osama. Tagert ya kwanza watakayokuwa wanaijadili hapo ikulu ni juu yetu sisi” Livna aliendelea kuzungumza kwa msisitizo mkubwa sana.
“Tukumbuke kwamba tunapigana na vita na watu watatu, wote wana uwezo, sisi tupo peke yetu.” “Ningependa kupata majina yote yenye uhasama mkubwa na Marekani, tunatakiwa kuzishawishi hizo nchi ili kutengeneza kikosi ambacho wakituanza tu, basi nasi tutapata msaada” “Ni nchi gani ambayo kwa sasa inaweza kutoa jeshi pamoja na silaha zake kutusaidia sisi ambao si nchi na tunahesabiwa kama kikundi cha kigaidi?” “Naomba hiyo listi ya nchi japo tano tu, mimi nitajua ni kitu gani cha kuzungumza” “Sawa, mimi ninanza ya Korea ya Kaskazini, Russia. Nyingine Ester zitafuteni” “Sawa mkuu” “Kabla hamjazitafuta hizo nyingine tatu ninaomba nizungumze na raisi wa Russia” “Raisi wa Russia!!!!?” “Ndio mbona unashangaa?” “Mmmmm Dany sidhani kama hilo ni wazo zuri kuwasiliana na raisi huyo ni mkali sana” “Ukali wake ni katika kuiongoza nchi yake na kuilinda nchi yake ila ninacho kihitakuzungumza naye ni kitu muhimu” Wakatekeleza kile nilicho waomba, baada ya dakika kumi ikulu ya Russia ikakubaliana na ombi la mimi kuzungumza na raisi wao. Nikavaa earphone inayoweza kubadilisha lugha yoyote na kuwa katika lugha ya kiswahili.
“Habari yako muheshimiwa raisi” “Wewe ni nani?” Raisi huyu mwenye sauti nzito aliniuliza huku akinikazia macho.
“DANY” “Ndio nani?” “Kifupi mimi ni gaidi, vita yangu ninajitahidi kupambana na Marekani, katika siku mbili hizi nimeweza kuifanya Marekani kukaa katika hali ngumu ya wasiwasi mkubwa, je umenifahamu” “Zungumza nini unahitaji kwangu” “Ninahitaji kuiangusha Marekani. Mimi sio raisi wala sina nchi ya kuipigania, ila wewe ni raisi na una nchi ya kuipigania. Unapenda nchi yako kupitwa kiuwezo wa kiuchumi kijeshi na Marekani?” Swali langu likamfanya raisi huyu kukaa kimya kwa dakika kadhaa huku akionekana kuwa mdadisi mkubwa sana kwangu.
“Nikisiema sipendi unahisi utafanya nini?” “Ninahitaji kuungana na wewe, ninahitaji kuanza kuishambulia Marekani, tazama jinsi alivyo kuwekea vikwazo katika kutengeneza silaha za nyuklia na yeye anatengeza je unahisi nini. Ni ubabe au amekufanya uwe mnyonge?” “Nchi yangu kwa sasa haipo tayari kupambana na nchi ya aina yoyote ninahitaji nchi yangu iwe na amani” “Ni amani gani uliyo nayo ikiwa Ukrain inakusumbua. Hii ndio nafasi ya wewe kuiongoza dunia, ukishindwa sasa hivi hadi mwisho wa dunia huto weza kushika namba moja kama aliyo nayo Mmarekani. Haya mazungumzo laiti kizazi kinacho fwata kwenye nchi yako kikija kuyaona au kuyasikia watakulaumu kwani umeshindwa kutengeneza future nzuri kwao na watabaki kuwa mbwa wa Marekani ha…..” “Tulia” Raisi huyu alizungumza kwa sauti nzito huku akiunyanyua mkono wake mmoja, nikanyamaza huku nikiendelea kumkazia macho.
“Unazungumza sana, nipe muda nitakujibu” “Kuwa makini, kwa maana vita ninayo kwenda kuianzisha duniani, usipo jipanga na wewe taifa lako linakwenda kufitika duniani. Kama nimemuweza Mmarekani, basi kukuweza wewe pia ninaweza” “Kijana uinajiamini nini?” “Unahisi kwamba ninajiamini na nini?” “Nionyeshe unajiamini na nini?” Nikavua earphone moja kisha nikamgeukia Ester aliyekaa pembeni ya Logate.
“Kuna kitu gani ambacho tunaweza kukifanya kwa huyu mtu?” “Tuelekeze mabomu yake ya nyuklia kwenye mji wake wa Mossow?”
“Itachukua muda gani kwa yeye kuweza kugundua?” “Ndio tunamalizia kuyaelekezea kwenye mji wake mwenyewe?” “Itamchukua muda gani?” “Sekunde hamsini hazifiki” Taratibu nikavaa eaphone hii na kumgeukia raisi huyu.
“Muheshimiwa unahakika na kitu ambacho umekizungumza kwamba ninajiamini kwa kitu gani?” “Ndio” Hata kabla sijanyanyua kinywa changu, msichana aliye valia nguo za jeshi akaonekana kwenye video, akamnong’oneza raisi wake. Raisi akaonekana kustuka, akanitazama kwa macho makali yaliyo jaa wasiwasi mkubwa.
“Je unahitaji nikuaminishe kwa vitendo?” “Hapana sihitaji vitendo, nipe lisaa nijikirie na ninahitaji kujadiliana na kamati yangu” “Muda ni wako” “Shukrani kwa kunisikiliza muheshimiwa raisi” Nikazima Tv hii huku nikimgeukia Livna nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu.
“Mmmm si kwa biti hilo, yaani kauli yangu haijaanguka” “Kauli gani?” “Ile niliyokuambia kwamba ninahitaji kukufanya uwe gaidi, ni kweli umekuwa gaidi tishio hadi kwangu sasa” “Hahahaaa, eheee raisi wa Kaskazini mwa Korea naye vipi?” “Tunasubiria majibu yetu kujibiwa, kwani tayari tumesha pelekea maombi” “Ila si munaficha sehemu ambayo tupo?” “Ndio nilazima tufiche, na jinsi wanavyo ona wao sehemu uliyo ona ni kwenye sayari nyingine ambayo ninaimani kwamba wanapata wasiwasi.” “Sayari nyingine?” “Ndio winaonyesha sisi tupo sayari ya Mars na si duniani” “Duu kweli hilo lazima wachanganyikiwe” “Ombi limekubaliwa, wanaomba dakika tano raisi wanajiandaa”
Logate alizungumza huku akiwa amejawa na furaha.
“Kazi nzuri Logate, je kikao chao hakijaisha?” “Bado nahisi wana mipango mikubwa wakitoka nitawajulisha” “Raisi yupo online sasa unaweza kuwasha Tv” Ester alizungumza, nikajiweka vizuri nguo yangu niliyo vaa, nikawasha Tv hii na kukutana na raisi wa Korea Kaskazini ambaye siku zote ninamuona kwenye Tv na anashria zake kali sana na ana maamuzi ya kipeke yake peke yake.
“Muheshimiwa raisi”
“Habari yako Dany” Aliuzungumza huku akiwa amejawa na tabasamu tofauti na raisi wa Russia.
“Salama muheshimiwa raisi?” “Nimefwatilia harakati zako kusema kweli ni harakati ambazo zimenivutia sana ila nikawa ninajaribu kukutafuta tangu jana ila nikawa ninashindwa kwani sikujua ni wapi unapo patikana” “Basi Mungu ameamua kutukutanisha muheshimiwa raisi, nimekuja kwako na ombi moja” “Ombi gani?” “Ninaimani umeweza kukiona nilicho kifanya kwa Marekani, nina imani kwamba hakuna mtu aliye weza kukifanya hicho kitu. Nanitaji nchi yako iwe namba moja duniani. Mimi sio raisi wala sina nchi ila wewe unayo inchi na raisi je unakubali kuwa chini ya Marekani miaka yote hiyo?” Ilibidi nitumie ujanja huo ili kuwaroga maraisi hawa, ambao watashirikiana nami katika kupambana ila mwisho wa siku watajua wao wenyewe nani atakuwa namba moja.
“Nipo tayari kukupa msaada wangu kwa asilimia mia moja, wewe niambie ni lini na saa ngapi tuanze kufanya mambo kwa maana ninaona ninafanya tu majaribio ya makombora yangu ila nashindwa kujua ni nani nimtupie japo mawili matatu, akijinyanyua tu kurudisha majibu basi mimi ninaye” Raisi huyu alizungumza kwa furaha sana.
“Ninashukuru sana muheshimiwa raisi, ninakuomba usubiri simu yangu. Kabla ya siku ya kesho kuishi nitamjaribu tena Mmarekani, akiona hivyo ninakuomba na wewe ujaribu makombora yako mawili matatu yaliyo shiba, akitujibu, basi ninaimani kesho haiisi atakuwa amebaki magofo kama ilivyo Iraq” “Wewe ndio watu ninao wahitaji hapa duniani, sio kuwa na maamuzi ya ajabu ajabu. Ninahitaji nguvu basi nguvu yanu umeipata mdogo wangu” “Shukrani muhshimiwa raisi” “Ninakukaribisha” “Shurkani” Tukaagana na raisi huyu w Korea Kaskazini, nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kali huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana kwani mpango wangu niliokuwa nimeupanga umekwenda sawia.
“Tumepata nchi nyingine ambazo zina chuki na Marekani, ila hazina nguvu kubwa ya kuweza kutusaidia katika mpango wetu” “Ziacheni, tusije tukazisababishia matatizo makubwa ikiwa wenyewe wana matatizo yao” “Sawa” “Naona kikao chao cha siri kimekwisha, je tuwafanyaje?” “Unamaanisha nini Logate?” “Kana ni kuwashambulia hapa sasa hivi tunaweza kuwashambulia?” “Tusiwashambulie sasa hivi”
“Kwa nini?” “Ninahitaji kukutana na Livna, kuna mambo mengi sana ninahitaji kumuhojia” “Mambo gani hayo?” “Utafahamu siku tukionana naye” “Sawa” “Ester andaa kikosi ambacho kitakwenda kumkomboa Yemi na kumrudisha hapa, watu wote wakiwa ndani ya hii meli nina ikani kwamba hakina mwengine ambaye ataweza kutuumiza kichwa huko nje, tukishambulia tumewashambulia” Livn alizungumza kwa msisitizo.
“Livna huoni kwamba inaweza kuwasababishia matatizo hao wanakwenda huko?” “Wanakwenda wasichana wawili tu, hao wanauwezo mkubwa wa kufanya chochote kinachokuja mbele yao, na wakishindwa hao basi ujue hakuna yoyote atakaye weza kufanya oparesheni hiyo” “Ninahitaji kuwaona wasichana hao kabla ya kwenda” “Sawa” Tuakanyanyka kwenye viti tulivyo vikalia na kutoka ndani humu, tukashuka chini kabisa ya meli hii ambapo kuna ndege kadhaa za kivita, na eneo zima limetawaliwa na rangi nyekundu.
“Mbona kuna taa nyekundu?” “Huku huwa hashuki mtu wa aina yoyote zaidi yangu mimi, na aliyeweza kuja huku ni Logate tu, ila wasichan wengine hawakuwahi kuja huku” “Sasa wasichana hao wapo huku chini?”
“Ndio wanaishi huku chini, wapo nane tu, wasichana hawa ni hatari kuliko unavyo fikiria, na akili zao yaani zipo kama zimechanganyikiwa fulani hivi, wanaye msikiliza ni mimi sasa chochote watakacho kuambia ninakiomba uwe mpole, ukileta ujinga watakua, na mimi nitashindwa hata kukutetea sawa” Livna alizungumza huku tukiwa tumesimama nje ya mlango huu wa chuma. Akaweka kiganja chake cha kulia katika sehemu ya kufungulia mlango huu, ukakaguliwa na mionzi ya rangi nyekundu, baada ya sekunde kadhaa ikabadilika na kuwa na rangi ya kijana. Mlango ukafunguka, tukakaribishwa na mwanga mweupe, eneo hili limejengeka vizuri na lina kila kitu cha ndani, akatoka msicha mmoja mzuri kwenye moja ya chumba, akamtazama Livna akatabasamu, alipo geuza macho yake kwangu akakasiria akaanza kutembea kwa kasi na kunifwata sehemu nilipo simama, nikaanza kuridi nyuma nyuma kwa bahati mbaya nikagota mlangoni na tayari mlango umesha funga. Msichana huyu akasimama mbele yangu, akanikaba koo langu kwa mkono wa kulia, sikuwa na jinsi zaidi kujitahidi kuutoa mkono wake, cha kushangaza Livna akatingisha kichwa akiniomba niitoe mikono yangu kwenye mkono wa msichana huyu ambaye nikimuachia basi habari yangu ya kuishi duniani itaisha kizembe kwani hapa nilipo nimesha anza kuhisi pumzi kuniisha na haja kubwa nanisi ina dalili ya kunitoka muda wowote kwa maana kukabwa koo sio mchezo.
Msichana huyu akanitazama kwa muda kisha akaniachia na kujikuta nikikaa chini huku nikikohoa sana kwani pumzi zimeniishia kabisa.
“Mkuu huyu ni nani?” Msichana huyu aliuliza kwa sauti ya upole sana hadi nikajikuta nikishangaa.
“Anaitwa Dany ni rafiki yetu mpya tutakuwa naye hapa” “Mzuri, naweza kumgusa tena”
“Ahaaa sio kihivyo bwana” Nilizungumza huku nikijizoa zoa chini nilipo kaa na nikanyanyuka.
“Kivipi Dany?” Msichana huyu aliendelea kuzungumza kwa upole sana. Sihitaji hata kumuamini, kwani alicho nifanyia ni nusu ya kufa Wakatoka wasichana wengine, alipo niona wakaonekana kunishangaa sana. Wakamsalimia Livna ila mimi hawakunisalimi wote wana kazi ya kunitazama kwa dharau huku wakinishusha na kunipandisha kwa macho yao. Mbaya zaidi hawa wasichana wote ni wazuri, hakuna hata mmoja ambaye ana ubaya wa sura wala mwili, ila roho zao ndio hivyo ni mbaya na kuua mtu kwao ni swala la kawaida sana.
“Warembo huyu anaitwa Dany, ni mwezetu yupo nasi hapa kwa kipindi chote cha maisha yetu hapa duniani” “Ngoja kwanza mkuu, huyo yupo nasi kwa kipindi cha maisha yetu yote. Ila yeye ni mwanaume inakuwaje aishi na sisi?” Msicha mmoja alizungumza huku akinitazama kwa macho makali sana
“Kuwa mwanaume hilo kwetu sisi halina shida sana” “Ila mkuu utakuwa unavunja utaratibu tulio uzoea” “Ninaelewa ila kwa sasa mambo yamebadilika, huyu kwa sasa ni tegemezi letu kwa asilimia kubwa” “Samahani mkuu, unasema ni tegemezi. Ana kitu gani cha maana ambacho kinakufanya wewe useme kwamba nitegemezi letu?” Livna akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akawatazama wasichana hawa huku akishusha pumzi nyingi kwani maswali ya wasichana hawa kwa upande mmoja ama mwengine ni magumu sana.
“Sipendi kuwaamrisha na kuwapa amri kama wezenu huko juu. Dany kwa sasa ndio kiongozi msaidizi. Ninahiji heshima ifwate mkondo wake sawa” Ilibidi Livna azungumza kwa ukali wasichana wote wakabaki kukaa kimya huku wakionekana hawajaridhishwa kwa kitendo cha mimi kuwa humu ndani.
“Mkuu tunakuheshimu na tunaishi huku chini tunakosa raha za kujiachia huo juu huko. Kusema kweli hatujaridhika na majibu yako. Hembu tupe ufafanuzi wa kueleweka huyo jamaa anafanyaje humu ndani ya meli yetu.” Wasichana hawa wanaonyesha hawana nidhamu ya woga kabisa. Livna akabaki kimya kwa muda huku akionekana kutafakari ni kitu gani atawajibu wasichana hawa.
“Nitaondoka kama hamunihitaji kwenye hii meli. Livna umenisaidia sana na ninashukuru kwa kunifikisha hapa, kwa hareni” Nilizungumza huku nikijiweka sawa shingo yangu.
“Hembu ngoja wewe unaga aga nini?” Msicha mmoja alizungumza kibabe huku akinitazama usoni mwangu, akaanza kunisogelea taratibu huku akionekana kuhitaji kufanya jambo fulani kwangu.
“Tutakukubali endapo utapambana na mmoja wetu hapa, ukimshinda utakuwa kiongozi wetu kama anavyo hitaji mkuu hapa, ukishindwa utafanya kile tutakacho kuambia kukifanya” Livna akanitazama na kutingisha kichwa kwamba nikubaliane na pambabo hilo analo lihitaji msichana huyu.
“Poa” “Chagua ni nani hapa upigane naye?” Nikawatazama wasicha wote hawa, kila mmoja anaonekana ana uwezo wake.
“Ninakuhitaji wewe” “Mimi hahaaaaaa” Msichana huyu akaanguka kicheko cha dharau kubwa sana.
“Atakaye shindwa lazima apige mkono chini kuashiria kushindwa sawa” “Poa” Nilizungumza kw akijiamini huku nikimtazama msichana huyu. Wote wakarudi nyuma na kutuachia duara kubwa, msichan huyu akaruka hewani huku akirusha teka lililo nifanya niiname chini, kabka hata sijanyuka nikastukia teke jengine likitua kifuani mwangu na kunipeleka chini.
“Kumbe mzembe hivyo, nyanyuka mwanaume, kwa maana hatuwezi kuongozwa na mwanaume ambaye hata kupambana na mwanamke hawezi” Msicha huyu aliendelea kizungumza kwa dharau kubwa sana. Nikanyanyuka na kusimama wima, kama kawaida yangu ya kumsoma ninaye pambana naye ikaanza. Msichana huyu akaanza kurusha mateke mfululizo pamoja na ngumi kadhaa. Ambazo zote nilizidi kujitahidi kuhakikisha kwamba ninayazuia kwa kadri niwezavyo, huku nikiendelea kumsoma mapigo yake ya kasi. Nikakumbuka siku nilipokuwa ninapambana na mtu wa baba Yemi, ambaye aliamini kwamba mtu hiyo ana uwezo mkubwa sana kuliko mwanajeshi wake yoyote ila nilifanikiwa kumumpiga.
‘Umekwisha’
Nilizungumza mara baada ya kuweza kugundua siri zote za msicha huyu japo amenipiga kwa kiasi fulani ila sasa ni muda wangu wa kuhakikisha kwamba ninamdhibiti. Hali ikabadilika kwa msichana huyu kwani mateke ambayo ninayatuma kwake ni mfulilizo na yana guvu kiasi kwamba akikwepa mawili nikimpata moja basi ni lazima apepesuke na akishindwa kupepesuka basi nilazima aanguke chini. Sikuwa na huruma hata kidogo kwa msicha huyu kwani ninahitaji kuwaonyesha uwezo kwamba japo Livna anawasifu wana uwezo mkubwa wa kupambana ila hata wao wenyewe wanabaki wakiwa wamenikodolea macho.
Masichana huyu akajifanya kujikaza ili kuto waingiza wezake katika ahadi ambayo ameiweka, ila sikuhitaji kumpa nafasi hiyo, akaanza kunifwata huku akipiga kelele, nikaruka hewani na kumtandika teke moja la kichwa lililo mfanya anguke china na hakunyanyuka tena.
Nikajifuta damu za mdomo zinazo nitaoka huku nikimtazama msichana aliye nikaba koo. Nikawatazama wasichana wengine wote wakaonekana kuingiwa na hofu nami.
“Huyu ndio mkuu wenu?” Niliwauliza huku nikimnyooshea kidole msicha huyu aliye lala chini akiwa amepoteza fahamu.
“Musipende kujaribu kurusha mawe kwenye mzinga wa nyuki, mutakufa” Nilizungumza huku nikielekea mlangoni na kuacha ukimya mwingi ukiwa umeyawala humu ndania.
“Njoo unifungulie” Nilizungumza kwa sauti nzito inayo kwaruza kwaruza.
“Dany” Livna alizungumza na kunifanya nigeuke nyuma, nikawaona wasichana wote wakiwa wamepiga magoti chini.
“Tunakuomba utusamehe” Mmoja wao alizungumza, nikaka kimya kwa sekunde kadhaa. Taratibu nikarudi sehemua lipo simama Livna.
“Simameni” Wakasimamammoja baada ya mwengine.
“Kiongozi wenu ni Livna, mimi hapa sio mkaaji wa kuduma kama alivyo sema mkuu wenu. Muwe na amani juu yangu, sijakuka kumdhuru yoyote kati yenu kwa maana vita yangu si kwa ajili yenu, ni kwa ajili ya Marekani na K2. Ninahitaji msaada wenu” “Msaada gani?” Msicha aliye nikaba koo langu alizungumza kwa haraka hukua akinitazama usoni mwangu.
“Kuna msicha ninihtaji mukamlete hapa kama inawezekana” “Msaidieni huyu, nitawahitaji wanne muweze kuiteleza hiyo kazi, Livna anawalete katika chumba cha mawasiliao” “Sawa mkuu” Nikatembea hadi mlango, Livna akanifungulia mlango kwa kuweka mkono wake sehemu maalumu ambayo pasipo kuweka mkono wake mlango hauwezi kufunguka. Moja kwa moja nikaelekea chumbani kwangu, nikapitiliza hadi bafuni na kusimama mbele ya kioo kimoja. Nikatazama jinsi nilivyo umia sehemu ya juu ya jicho langu la upande wa kulia. Nikaanza kujisafisha damu zilizo nitawala usoni mwangu, japo msichana yule nimemuhimili ila na yeye amenipa kipondo kila sehemu ya mwili wangu inaniuma.
Mlango wa bafuni ukafungukiwa, akaingia Livna, akasimama pembeni yangu.
“Upo vizuri mpenzi” “Ulihisi nitapigwa?” “Ndio nilihisi utapigwa kwa maana wasichana wale wapo vizuri” “Wapi, unatambua kwamba ni jinsi gani nilivyo mbishi. Siwezi kupigwa na msichana ambaye hana hata presha ya kutafutwa na majeshi makubwa duniani”
“Sawa, nikuletee nguo nyingine” “Kama ikiwezekana” Livna akajaribu kunishika mbavu zangu ila kwa haraka nikamtoa mkono wake.
“Vipi?” “Mwili mzima unaniuma, hapa sitamani hata kushikwa” “Kumbe na wewe umebumundwa”
Livna alizungumza huku akicheka sana. Nikavua tisheti yangu, baadhi ya sehemu zimejaa alama nyeusi nyeusi zinazo onyesha jinsi gani ambayo alama za mateke na ngumi zilivyo jichora.
“Mungu wangu, Dany huyu msichana amekufanya vibaya, inabidi upate huduma ya dokta” “Hapana nipo poa” “Dany kwa hali hii kila unapo guswa mwili unakuuma unasema kwamba upo sawa” “Livna ninakuomba unielewe nipo sawa, ninakuomba ukaniletee hizo nguo” “Sawa baba” Livna akatoka bafuni humu, baada ya dakika tano akarudi akiwa ameshika nguo nyingine zinazo fanana na nguo hizi, nilizo zivaa.
“Wasichana wapo tayari wanakusubiria katika chumba cha mawasiliano” “Ninakuja” “Sawa” Livna akatoka humu ndani, nikaanza kuoga taratibu kutokana na maumivu makali ya mwili wangu. Nikavaa nguo hizi safi na kutoka humu chumbani huku nikiendelea kuyavumilia maumivu yaliyopo humu chumbani. Nikaingia ndani ya chumba cha mawasiliano na kuwakuta wasichana wanne wakiwa wamesimama wakinisubiria mimi. Ester na Logate wakaonekana wakinishangaa.
“Vipi mkuu umepata ajali?” Logate alizungumza huku akitabasamu.
“Jamani si umetoka humu ndani mzima?”
Ester naye alizungumza akiwa amejawa namshangao. Sikujibu chochote zaidi ya kukaa kwenye kiti changu. Sikuweza hata kuegemea kwani mgongo mzima unaniuma.
“Kuna jipya gani?” “Hakuna jipya hapa kitu kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunampata Yemi” “Mumewapa maelezo japo kidogo?” “Hapana” “Livna wape maelezo” Livna akaanza kuwapatia maelezo wasichana wake hawa. Maelezo yakaenda sawa kama ninavyo hitaji.
“Mutaweza kuifanya hiyo kazi” “Ndio mkuu” “Itawachukau muda gani?” “Masaa kumi, kwa maana si Tanzania” “Ndio” “Masaa kumi yatatosha sisi kuweza kuifanya hiyo kazi kikamilifu” “Niwatakie kazi njema” “Sawa” Wasichana hawa wakatoka hapa humu ofisini na kuelekea kujiandaa. “Osama anapiga video call je tuwasiliane naye?” Ester alizungumza huku akinitazama usonimwangu.
“Mpokelee” Livna akanisaidia kuiwasha video. Nikamuona Osama akiwa amecaa mavazi niliyo muona nayo masaa machache alipokuwa anaonana na Livna. Nikavaa earphone sikionim wangu huku nikimtazama Osma kwa macho ya kumdadisi huku nikiwa nina hamu ya kusikia ni nini atazungumza kwangu kwani tayari ninamuhesabu ni msaliti kwangu.
“Habari yako Dany” “Salama, umefanikisha kupatikana kwa Yemi?” “Bado vijana wangu wanaendelea kuifanya oparesheni ya kuwatafuta” “Uliniambia masaa kumi, na sasa ni masaa zaidi ya kuni na tano kama sijakosea” “Ndio, ila ninaendelea kujitahidi kumtafuta. Ila unaweza kukutana nami baada ya kupambazuka” “Unahisi kwamba mimi ni mpumbavu. Nilikusaidia Wamarekani wasikuue kwa mara ya pili, sasa sijajua ni kwa nini umeamua kuungana nao tena umeungana na mtu ambaye nilikuagiza ukamkombea mke wangu ila umekwenda kushirikiana nao.” Osma akabaki macho yamemtoka na jinsi ndevu zake zilivyo nyingi na uzee ulio mtawala akazidi kunifanya nimuone kituko hadi nikatamani kuchekea.
“Mimi na wewe sasa sio marafiki, ninakuomba ukae mbali na mimi. Usiingie kwenye kumi na nane zangu, kwa maana nitakupiga zaidi ya Marekani alivyo kupiga umenielewa mzee, kama muda wako ulisha kwisha katika kuwa mbabe wa dunia tulizana na kundi lako” “Siawa kutishwa maisha mwangu, na wewe unajaribu kunitisha unajiamini nini kijana mdogo ambaye hata maziwa ya mama hayajaisha kukunuka mwilini mwako?” ‘Mungu wangu wazee wengine hawa wanatokea wapi wanapi mbona wanatafuta bifu za kijinga hivi?’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama mzee huyu. Nikamgeukia Ester ambaye anajua nini cha kufanya kwa watu wabishi kama hawa ambao wameshoboka na ngoma waliyo ikutia katikati na wanataka kuicheza pasipo kufahamu ngoma hiyo ni ya kabila gani.
“Unamfahamu mama yangu mzee?”
“Sina haja ya kimfahamu mama yako”
“Sasa utamfahamu kilazima”
Nilizumgumza kwa msisitizo kisha nikaizima Tb hiii, nikamge Ester anaye subiria amri yangu.
“Tumshambulie?”
“Hapana, yupo wapi?”
“Yupo bado Dar es Salaam”
“Ninahitaji kwenda kumakamata mimi mwenyewe”
“Dany huwezi kufanya hivyo hali yako haipo sawa”
“Niitie daktari”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Livna.
“Dany huwezi kwenda kumkamata Osama, ni mtu hatari ana jeshi kubwa na amesha ungana na K2 pamoja na Marekani, kwa nini unahitaji kujitoa sadaki ikiwa bado lengo halijamilika?”
Livna eliendelea kuzungumza huku akinibembeleza niitengue maamuzi yangu niliyo yaamua. Kwa macho makali niliyo mtazama Livna akajikuta akitulia, akanyanyua mkonga wa simu ya mezani na kumpigia daktari na kumuagiza aweze kufika katika chumba hichi haraka iwezekanavyo. Hazikupita hata dakika tano daktari akaingia huku akiwa na kibegi kidogo. Nikapandisha tisheti yangu juu kidogo na kuwafanya watu kuona alama za mateke na ngumi nilizo pigwa mwalini mwangu.
“Oooohooo my God, ni nini kimekupata?”
Daktari alizungumza huku akinifwata nilipo kaa. Akaanza kunichunguza mwili mzima huku a kionekana kuzidi kushangaa hizi alama.
“Nichome sindano ya kutoa maumivu mwilini”
“Ila inabidi tukufanyie chake up ya ndani, kama nje kuna alama kama hizi basi ujue ndani ni lazima kutakkuwa na tatizo kubwa”
“Nimekuambia nichome sindano ya kuzuia maumivu”
“Sawa sawa”
Daktari alizungumza huku akimtazama Livna usoni mwake, kwa haraka akafungua kibegi chake, akatoa kichupa kidgo pamoja na bomba la sindano. Akafunga sindano na kuifunga kwenye bomba hilo kisha akaichomeka kwenye mfuniko wa kichupa hichi ambao umetengenezwa na mpira mlaini. Akavuta kiasi cha dawa, kisha akaniomba ninyooshe mkono wangu wa kushoto huku nikiwa nimekunja ngumi.
Hakuwa na haja ya kunifunga kitu chochote kwani mishipa inaonekana vizuri. Akanichoma sindano hii na kuisukuma dawa taratibu hadi ikaisha ndani ya bomba hili.
“Munaweza kutengenza sura bandia?”
Swali langu likamfanya daktari kumtazama Livna, aliye kaa kimya kwa muda huku akionekana kujawa na wasiwasi mweingi sana.
“Ndio”
Livna alinijibu kwa unyonge sana.
“Ninahitaji kufanyiwa hiyo oparesheni sasa hivi”
“Dany mpenzi wangu ninakuomba usifanye hivyo”
Livna alishindwa kuzuia hisia zake mbele ya wasichana wake anao waongoza ambao nina imani kwamba hawajawahi kufahamu upendo ni kitu gani.
“Kuna kitu muhimu sana ninahitaji kukifanya juu ya dunia. Tafadhali Livna ninakuomba unielewe, ninakuomba uridhike juu ya hilo sawa mama”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama mbele ya Livna. Ukimya ukatawala ndani ya chumba hichi huku sote tukisubiria jibu la Livna.
“Tafadhali ninakuomba ukubali, Osama ndio atakuwa ufunguo wa kila kitu kilicho fungwa kwangu”
“Una maana gani?”
“Nikubalie kisha utaweza kufahami ni kitu gani nina maanisha”
Livna akashusha pumzi nyingi, akamtazama daktari ambaye naye anasubiria jibu.
“Mtengeneezeeni sura ya bandia”
“Nahitaji kufanyiwa oparesheni kabisa ya sura ya bandia, itachukua muda gani dokta?”
“Ahaa…. Itachukua masaa kama sita hivi au saba”
“Niandalieni”
“Je unahitaji sura gani?”
“Nichagulie”
“Sasa Dany mimi nitajua ni sura gani itakufaa jamani”
“Dokta hakikisha unanitengeneezea sura ambayo sio rahisi mtu kuweza kunigundua hata ikitokea wanajaribu ku scan kwenye mtandao wasiweze kuiona siura yangu halisi. Sijui umenielewa?”
“NImekuelewa nimekuelewa vizuri sana. Itanichukua kama dakika ishirini kuunda sura kama hiyo”
“Sawa fanya hivyo”
“Sawa”
Daktari akafunga kibegi chake na kutoka chumbani humu.
“Ester hakikisheni kwamba Osama hapoteni kwenye mitandao yenu, hakikisheni munamfwatilia kila anapo elekea, kama atapiga simu yoyote ninaomba mazungumzo yake muweze kuyarekodi”
“Sawa mkuu”
Nikatoka chumbani humu huku Livna akainifwata kwa nyuma.
“Dany sipendi maamuzi ya kwako peke yako?”
“Kama yapi?”
“Kwa nini unaamua kwenda kupambana na Osama ikiwa unajua unatafutwa kila kona ya dunia”
“Livna umejitolea sana juu yangu, umewatoa watu wako wengi na woye wananipigania mimi. So nilazima na mimi niweze kufanya jambo, si kukaa mule ofisini na kutazama mambo jinsi yanavyo fanywa kwenye Tv, sasa unapo nipeleka ni kuwa gaidi boksi. Nahitaji kufanya kitu katika hili, nanitaji kuionyesha dunia kwamba ninauwezo wa kudanya jambo”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiendelea kumtazama Livna usoni mwake.
“Nahitaji kwenda kuzungumza na Hawa”
“Sawa”
Nikamuacha Livna akiwa amesimama kwenye hii kordo huku akinitaazama. Nikaingia kwenye chumba anacho kaa Hawa, nikamkuta akiwa amelala kitanda kimoja na Livna huku wamekumbatia. Nikafunua shuka lililo wafunika na kuwakuta wote wapo uchi. Nikawatazama kwa muda jinsi maumbo yao yalivyo, nikaushusha mkono wangu karibu na alipo Hawa, ila nikasita, taratibu nikawafunika kama nilivyo wakuta na nikatoka humu ndani.
“Mbona umewahi kutoka?”
“Wamelala”
“Ila muda umekwenda kwa kweli”
“Ndio, ninahitaji hii oparesheni niifanye na msichana mmoja”
“Nitakwenda na wewe?”
“Ni hatari hatuwezi kwenda sisi wawili, ni juzi tu umetoka kwenye hatari na tumempoteza Martin, sihitaji uende kwenye matatizo hembu angalia kwanza afya yako itakavyo kwenda”
“Afya yangu ipo poa mbona”
“Simaanishi afya ya mwili, hapa”
Nikamshika tumbo Livna na kumfanya atulie kwa muda, akatabasamu nikatambua amenielewa.
“Niwakati wa kumuangalia mwanangu, na mama utakaa ndani na mimi baba ninakwenda kuifanya kazi hii sawa”
“Sawa mume wangu”
Livna akanibusu kwenye lipsi zangu. Tukaelekea katika chumba cha oparesheni na kuwakuta madaktari wanne wakike wakiwa tayari wamesha fanya maandalizi ya kufanya opareshi hii ya kuniweka sura ya bandia.
“Mkuu inabidi kukuchoma sindano ya usingizi kwa maana hii kazi haitaji usumbufu”
“Hakuna tabu, nipo tayari”
“Ngoja kwanza nimbusu mume wangu”
Livna alizungumza kwa furaha, akanikumbatia kwa muda kisha tukanyonyana midomo yetu kwa muda kidogo kisha tukaachiana.
“Ninakupenda sana Dany”
“Ninakupenda pia”
Nikamuachia Livna kisha nikaka kitandani, taratibu nikalala, daktari akanichoma sindano ambayo hata dakika mbili hazikuisha nikajikuta nikilala fofofo.
***
Nikayafumbua macho yangu taratibu, nikamuona Livna akiwa amekaa pembeni ya kitanda huku anasinzia sinzia.
“Hei”
Nilimuita huku nikijitahidi kukaa kitako.
“Mume wangu umeamka”
‘Yaaa, niambie”
“Safi, umependaza, hembu jitazame kwenye kioo”
Nikashuka kitandani taratibu, nikajinyoosha viungo vyangu huku nikipiga miyayo mingi. Nikaanza kutembea kwa hatua za kivivu hadi kwenye kioo. Sikuamini muonekano ninao onekana kwa maana ninaonekana tofauti sana, sura waliyo niweka inanifanya nizidi kuonekana mzuri.
“Hapo hakuna mtu ambaye anaweza kukugundua hata iweje”
“Kweli?”
“Ndio yaani hapo hata mimi mwenyewe nikikutana na wewe barabarani na nikiwa sifahamu kama umebadilishwa sura basi sinto weza kukufahamu”
“Duuuu, sasa mauaji yote yaliyo baki mke wangu ninakwenda kuyafanya mimi mwenyewe”
“Ahahaaa, wewe unakwenda kumuua Osama, ninakuomba hii sura ya sasa hivi usiichafu, usiwape watu wazo kwamba unaweza kutumia sura ya bandia”
“Sawa nimekuelewa mpenzi”
“Hakikisha kwamba kazi unaifanya kisha unarudi hapa salama”
“Ninahitaji kurudi na Osama ndio maana ninameomba msaada wa kupata msichana mmoja ambaye anaweza kushirikiana nami”
“Sawa, nitakuchagulia msichana mmoja katu ya wale kule chini”
“Sawa. Hivi sasa ni saa ngapi?”
“Ni saa moja kasoro”
“Asubuhi?”
“Ndio”
“Poa, nahitaji suti nyeusi, bastola mbili, magazine kumi na mbili”
“Bastola mbili zinatosha kweli?”
“Ndio zinatosha, kikubwa ni kuhakikisha kwamba ninashabaha nzuri”
“Sawa mume wangu, ninakuandalia wewe. Pia kuna zawadi moja ninahitaji kukupatia”
“Zawadi gani?”
“Mmmmmm zawadi haisemwi hadi utakapo iona”
“Sawa”
Tukatoka katika chumba hichi na nikaelekea chumbani kwangu na kumuacha Livna akielekea sehemu ambayo anaweza kupata vitu ambavyo nimemuagiza. Nikavua nguo zangu na kuingia bafuni, nikaanza kuoga huku nikiwa na shauku kubwa ya kwenda kuifanya hii kazi iliyopo mbele yangu.
“Ni lazima nimfundishe kazi huyu mzee”
Nilizungumza huku nikizidi kuoga kwa furaha kubwa kana kwamba ninaelekea katika sherehe fulani hivi ambayo mimi ndio mgeni mualikwa, nikaanza kucheza huku nikijitazama kwenye kioo cha humu bafuni kwanini nimebadilika sana. Mlango wa bafuni ukafunguliwa, na nikamuona Livna akiwa anashangaa.
“Unashangaa nini?”
“Nashangaa jinsi unavyo cheza, unafuraha kubwa eheee?”
“Yaa nina furaha, yaani takacho mfanya Osama, lazima akafurahi na roho yake”
“Hahaaaaa haya mwanya”
Livna naye akavua nguo zake na kubaki kama alivyo zaliwa, akanisogelea huku akinitazama usoni mwangu. Akanikumbatia kwa nguvu.
“Dany unanipa raha sana, unanifanya nionekane mtu kati ya watu. Unajua muda mwengine nyege zinaweza kumfanya mtu afaye vitu vya ajabu ajabu, unalitambua hilo?”
“Yaa ninalitambua”
Livna akaanza kumchua chua jogoo wangu aliye anza kusimama.
“Hujisikii maumivu huku ulipo pigwa?”
“Hapana ile sindano imenisaidia”
Liva taratibu akachuchumaa, akamshika jogoo wangu ana kuanza kumnyonya taratibu.
“Mmmgmmm….mgg…….”
Nikatoa miguno ya kimahaba na kumfanya Livna azidi kuongeza ujuzi wa kumnyonya jogoo wangu. Nikamsimamisha, kisha nikamuinamisha na kuanza kumnyonya kitumbua chake huku nikiuchezesha ulimi wangu jinsi ninavyo weza mwenyewe.
“Fuc** me baby”
Livna alizungumza huku akiwa ameshika bomba la maji lililomo humu bafuni. Nikasimama na kumshika jogoo wangu vizuri, taratibu nikamzamisha kwenye kitumbua chake na kumfanya Livna kuuacha mdomo wake wazi pasipo kutoa mlio wowote.
Nikaanza shuhuli ya kula kitumbua chake huku nikiwa nimezishika nywele zake ndefu, Livna akaanza kutoa miguno ya raha inayo endana na maji yanayo tumwagikia kwenye miili yetu. Tukaendelea kubadilisha mikao ya kupeana raha hadi tukamaliza. Tukaoga vizuri sasa na kutoa bafuni humu, nikakuta nguo zikiwa zimewekwa juu ya kitanda. Livna kaanyanyua koti la suti na kunionyesha tisheti moja nyeusi ambayo kwa haraka haraka nikaikumbuka. Tisheti kama hii nilisha wahi kukabidhiwa na mama yangu kipindi cha ujana wake, sifa yake ni moja, ni kwamba haiingii risasi.
“Umeipata wapi hiyo tisheti?”
“Hii tisheti alinikabidhi baba yako kipindi cha nyuma, aliniambia sifa yake ni kwamba haiingii risasi na ni kweli niliweza kuifanyia majaribio mengi sana na kweli haiingi risasi”
“Marehemu mama ndio alikuwa anazitengeneza hizo tisheti”
“Ni kweli hata baba yako aliniambia kwamba mke wake ndio alimtengenezea hizi tisheti. Sasa leo ninakukabidhi wewe, nina imani kwamba itakusaidia sana”
“Shukrani mpenzi wangu”
Nikabusu Livna mdomoni mwake, nikaichukau tisheti hii na kuivaa, na kunibana vizuri mwilini mwangu. Nikachukua shati jeupe na kuvaa, kisha nikafwatia, bosa pamona na suruali na nikamalizia koti. Livna akanivisha mkanda wa suruali vizuri. Akachuchumaa na kunivisha soksi kila mguu pamoja na viatu vizuri.
“Hapo unaonekana ni bonge moja la bilionea”
“Wapi”
“Kweli mume wangu na hiyo sura, ninapata mashaka wanawake jinsi watakavyokuwa wanakushobokea”
“Yaaa, ila ninakwenda kikazi na ninahitaji kurudi hapa nikiwa na kichwa cha Osama Bin Laden”
“Usirudi na kichwa chake, ninahitaji urudi naye hapa akiwa hai, nahitaji na mimi niweze kumuona”
“Etiee eheee?”
“Ndio”
Livna akanikabidhi bastola mbili, nikaanza kuikagua moja baada ya nyingine na kuzikuta zikiwa salama, akanikabidhi magazine za bastola hizi ambazo nikaanza kuzichomeka kila moja sehemua mbayo ninaona itakuwa ni rahisi kwangu pale nitakapo amua kuichomoa.
“Hii ni saa ambayo popote utakapo kwenda huku tutaweza kukuona, hakikisha kwamba unaitunza mume wangu, endapo itapotea utaniweka mimi katika wakati mgumu sawa mume wangu”
“Usijali mke wangu”
Livna akavaa nguo zake, tukatoka ndani humu na kwenda moja kwa moja katika chumba cha mawasiliano, Ester na Logate wakabaki wakiwa wananishangaa kwani nimebadilika sana.
“Mupo poa?”
Niliwasalimia, hapakuwa na aliye weza kuitikia salamu yangu kwa mshangao ambao bado unaendelea kuwatesa.
“Wanakushangaa wamekupenda”
Akaingia msichana mrefu, mweupe amevalia gauni jeusi lenye mpasuo mkubwa hadi karibi kabisa na kiuno chake, paja lote la mguu wa kulia lipo wazi. Nywele zake ni ndefu zinaning’inia mgongoni mwake na baadhi zimeficha jicho lake la kushoto kidogo. Umbo lake ni namba nane yenyewe, kwani ana hispi ambazo kusema kweli zinanitamanisha.
“Dany huyu anaiwa Magreti, ndio utakuwa naye kwenye kazi unayo kwenda kuifanya ya kumkamata Osama Bin Laden”
‘Mmmmm kweli lazi itafanyika hapa?’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama binti huyu aliye jaribu kunipa mkono wake wa kulia ila nikabaki nikimazama kwani ni mzuri kupindukia hata Livna mwenyewe hamfikii msicha huyu hata nusu yake.
“Dany si unapewa mkono?” Livna alizungumza huku akinigonga kidogo kwenye bega kangu an kujukuta nitoka kwenye dibwi la mawazo la kumfikiria msichana huyu.
“Ndio habari yako” Nilizungumza huku nikimabidhi mkono msichana huyu, akatabasamu na kunifanya nizidi kujawa na bumbuwazi kwani kwenye maisha yangu sijawahi kukutana na msichana mzuri kama huyu, japo nilio wahi kukutana nao ni waziru ila huyu amewazidi wezake kwa asilimi zote mia moja.
“Salama” Nikashindwa hata kuijibu salamu yake kwani msisimko ninao upata hapa ukaanza kumuamsha jogoo wangu taratibu. Nikameza funda zito la mate kisha nikauachia mkono wa huyu msichana.
“Bado Osama yupo Tanzania?” Niliuliza ili kuipoteza hali ya uchu wa mapenzi nilio nao juu ya huyu msichana ambaye kusema kweli ni kibarua kikubwa cha kupambana na hisia zangu.
“Bado hajaondoka Tanzania na leo usiku kutakuwa na sherea ya mtoto wa shemeji yake anaoa. Na harusi hiyo ndio iliyo mfanya kubaki nchini Tanzania” “Amejiingiza machinjioni”
”Hatari moja ni kwamba katika hiyo ulinzi ni mkali sana, ukiachilia mbali tu watu wake basi kuna NSS ya Tanzania na wana FBI kutoka Marekani” “Wote wanafanya nini?” Niliuliza huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana. “Wanamlinda Osama, sasa itakuwa ni ngumu sana kuweza kumteka katika hiyo harusi” Ester aliendelea kunipatia maelekezo huku akinitazama usoni mwangu.
“Na hapo Dany humuwezi kutumia bunduki ni lazima itakuwa ni hatari kwenu” Livna naye alisisitizia katika hilo.
“Ila kuna njia ambayo munaweza kuitumia” Logate alizungumza huku akinikabidhi simu aina ya iphone 7.
“Kupitia hiyo simu tutakusaidia kukutumia video za kamera zote ambazo zipo ndani ya huo ukumbi. Mbili kuna hivi viji layer vya macho ya bandia, unatakiwa kuyavaa, ili hata kukitoke kukafanyika ukaguzi wa macho basi hakuna anaye weza kukugundua kwamba wewe ndio Dany” Logate alizungumza huku akitoa viji leyer vya macho na kunivisha katika macho yangu. Akanikabidhi kioo, macho yangu yangu yamebadilika mboni yake na kuwa mboni ya kijani kwa mbali jambo lililo zidi kunipendezesha.
“Ingia upande wa wa picha katika hiyo simu” Logate alinipatia maelekezo na nikafanya hivyo.
“Jicho lako la upande wa kushoto utaweza kuona jinsi muonekano wa watu kwa ndani, it’s mean unaweza kutuona sote hapa nguo zetu za ndani” “Kweli bwana” Nikata kumgeuzia Logate simu hii ila Livna akaniwahi.
“Hembu acha utoto Dady, sikiliza maelekezo” “Unataka nikuone wewe tu ehee?” “Ndio” “Sawa mama, mwalimu wangu ehee endelea”
“Lengo la kuweza kuitumia program hiyo ni nini haswa, ni kuhakikisha kwamba unaweza kumuona kila mlinzi mwenye silaha ndani ya ukumbi mzima, pili utaweza kuiona sura ya Osama vizuri kwani kuna watu watakuwa wamejifunga vilemba usoni mwao na kubakisha macho ilimradi kutoweza kumtambua Osama ni yupi” “Sawa sawa” “Magreti si unanielewa vizuri?” “Ninakuelewa Logate”
“Na wewe Magreti simu yako hiyo hapo, na ina uwezo kama huu wa Dany hapo. Na wewe itakulazimu kuvaa hivi viji leyers vya macho kwa maana kupitia macho yako nawe rekodi zako wakizidaka basi utatiliwa mashaka. Hapa tumewatengenezea vitambulisho vya uraisi nchini Tanzania, ambavyo kwa Dady utatumia jina la Mpoki Samweli na Magreti utatumia jina la Nagenjwa Petro” “Wewe Logate majina ya wapi haya jamani?” Niliuliza huku nikitazama kitambulisho changu.
“Wewe ni Muhaya na Magreti weweni Mpare sawa?” “Sawa ila hili jina la Mpoki ahaaa sio haki jamani” “Dany be serious” Livna alizungumza huku akinikazia macho.
“Tuendelee, nina imani kwamba kila mmoja ana silaha zake, ila katika ukumbi ambao mutaingia nilazima gari zetu zitakaguliwa, sio kukaguliwa kwa kutazamwa kwa macho. Ila computer ndio itakuwa na kazi ya kukagua gari lenu. Sasa kuna gari aina Aud A7, ambayo ipo huko chini ya meli, mutaondoka nayo sasa hivi” “Usiniambie kwamba ina uwezo wa kutembea juu ya maji?” “Hapana, munaondoka na boti kubwa, mutapelekwa hadi katika fukwe za Kigamboni, kisha mutapita katika daraja na kuitokea katikati ya jiji. Sasa maana yangu ni kwamba mutaacha silaha zenu ndani ya gari, mukiwa munaingia ukumbini, na hakuna program yoyote ya kukagulia magari itakayo weza kuona silaha zenu, japo itawaonyesha nyinyi katika mfumo wa mafuvu ya watu pale munapo kaguliwa” “Kwa hiyo watauona nguo za ndani?” “Hapana, watawaona nyinyi katika mfumo wa mafumfu tu kwa ndani” “Sisi nasi tutajiona?” “Hapana, mtaalamu atakaye kaa kwenye computer hiyo ndii atakaye weza kuona kila kitu, si nyinyi tu bali wageni wote watakao ingia kwa miguu, magari wataonekana hivyo” “Hapo nimekupata” “Kuna hii kadi, hapa. Ukiitazama unaweza kusema kwamba ni kadi ya benki, ila hii ndio kadi ya harusi sasa. Ukifika mlangoni utawakabidhi hii kadi wakaguzi nao wataweza kuipitisha kwenye mashine ya ukaguzi na majina yenu yataokea. Kumbuka kwamba Dany unaitwa Mpoki Samweli na Mage” “Nagwenjwa” Magreti alimuwahi kumjibu Logate na kunifanya nimtazame kisha nikatabasamu.
“Picha zenu zitatokea katika kadi hiyo” “Picha mulinipiga saa ngapi?” “Sasa hivi ulivyo simama hapo” Nikamtazama Ester nikamuona akininyooshea dole gumba ikionyesha kwamba yeye ndio aliye nipiga picha anayo izungumzia Logate.
“Kuna hivi vinasa sauti kila mmoja avae kwenye sikio lake, mutaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja” “Nimevimisije hivi vidumwana, nakumbuka nilivivaa kipindi nilipokuwa nina oparesheni ya kuliangamizi kundi la Al-Shabab” “Dany mbona unaongea sana leo, unafuraha. Hembu tilia maanani kwa kazi unayokwenda kuifanya basi” Livna alizungumza kwa kulalamika kidogo, nikamkonyeza huku nikitabasamu na kumfanya akenue midomo yake akionyesha kupuuzia mkonyezo wangu.
“Kuna hii sindano ndogo, Magreti unaweza kuficha kwenye nywele zako, hiyo sindano utamchoma nayo Osama na italewesha, na atakusikiliza kila utakacho muambia. Hakikisha kwamba unautumia uzuri wako kumteka mzee huyo” “Sawa”
Magreti akapokea kisindano kidoho na kichomeka katika nywele zake na si rahisi kwa mtu kuweza kufahamu kwamba ana sindano ndogo.
“Baada ya hapo nina imani kwamba kila kitu kitakuwa kimekamilika kwa upande wenu. Sisi kazi yetu itakuwa ni kuwapa maelekezo kuhakikisha kwamba munakwenda salama na kurudi salama kama tulivyo kubaliana” “Tunashukuru” “Ninawatakia kazi njema” “Asante Ester” “Twende tukawaonyeshe gari mutakayo tumia” Ester alizungumza, tukatoka katika chumba hichi huku Livna akitufwata.
“Dany mpenzi wangu ninakuomba uwe serious katika hii kazi, kumbuka tayari umesha pandikiza kitu kwangu, sinto kubali kukuona unaingia kwenye matatizo” “Mungu nisaidie, nitakuwa serious nitahakikisha kwamba ninarudi salama sawa” “Sawa mpenzi wangu mimi ninakuombea kwa Mungu. Magreti hakikisha kwamba unamlinda huyu” “Sawa mkuu” Tukafika katika sehemu maalumu ambayo boti maalumu huwa ndipi zinapo tokea, tukakuta boti moja ikiwa tayari imesha andaliwa huku kukiwa na gari nzuri yenye rangi nyekundu.
“Dany hembu shika kioo cha upande wa dereva”
Nikauweka mkono wangu. Logate akaanza kuminya minya tablate yake kubwa, mlango ukafunguka.
“Utaweza kuifungua hiyo gari kwa mkono wako wa kulia. Mage na wewe weka mkono wako kwenye mlango upande wa dereva. Dady wewe funga mlango” Nikaufunga mlango, kusema kweli dunia inazidi kukua na tecknologia inazidi kuchukua nafasi kwenye maisha ya watu.
“Tayari, sasa nyinyi kupitia mikono yetu ya kulia munaweza kufungua mlango wa hilo gari, hakuna mtu mwengine atakaye weza kufungua. Gari unawasha kwa hiyo batani iliyo andikwa start engine. Itawaka na utaweza kuendesha” “Halina funguo?” “Hakuna funguo. Ingieni ndani ya gari” Tukaingia ndani ya gari huku nikikaa upande wa dereva.
“Angalizo, ambaye hatofunga mkanda wa siti aliyo kalia awe dereva ama abiria wa siti ya mbele wala nyuma, gari haliwaki sasa muwe waangalifu katika hilo” “Mmmmmm kazi kweli kweli” “Yaa ndio magari ya kisasa. Kitu kingine, hii gari haiingii sirasi, pia ina uwezo wa kubadilisha mfumo wa rangi yake ya nje, hapo kuna rangi tatu. Hii nyekundu, nyeupe na nyeusi. Kila rangi ina namba zake za usajili sasa inaweza kuwa rahisi kwenu kubadilisha muonekano wa gari lenu pale endapo kutakuwa na hatari itakayo wafanya mufanye hivyo.” “Tunabadilishia wapi hiyo rangi?” “Mimi ninafahamu” “Magreti anafahamu, so vitu vya ndani ya gari atakuelekeza kama wewe ndio utakuwa dereva?” “Mfuno wake ni manuel au automatics?” “Ina mifumo yote miwili chaguo ni lako wewe mwenyewe” “Ohoooo sawa sawa” “Kwa mimi nimemaliza, nami nitawakie safari njema” “Tunashukuru” Livna akainama kwenye dirisha langu, akanitazama kwa muda huku akitabasamu kinyonge.
“Dany fanya hii kazi ila kumbuka kwamba huku nyuma umeacha watu wawili wenye viumbe vyako, watatu ni Yemi ambaye amekwenda kuchukuliwa, hakikisha kwamab hii kazi unaifanya kiumakini mpenzi wangu sawa” “Usijali mama” “Mungu awatangulie” Livna bila kujali wasichana wake hawa wawili waliopo katika hili eneo, akaninyonya midomo yangu taratibu huku akinitazama usoni mwangu kwa macho malagevu.
“Mage, mlinde huyu” “Sawa mkuu, atarudi salama” “Jamani kushuka je, kuna haja ya kuweka mkono kwenye kioo?” “Hapana, unafungua mlango kama kawaida” “Ahaaaa hapo sawa” Livna na Logate wakatoka katika boti hii ambayo ni kubwa kiasi yenye uwezo wa kubeba gari hili la kifahari ikaanza safari huku ikiendeshwa na msichana mmoja.
“Tutachukua masaa mangapi kufika Tanzania?” “Masaa kama manne au matano” “Duu kumbe kuna umbali ehee?” “Ndio” Nikabaki kumtazama Magreti kwa macho ya matamanio. Hakulijali hilo, kwani anatambua kwamba mimi ni mume wa bosi wake. Ili hali ya matamanio isiendelee humu ndani, nikafungua mlango na kutoka, nikaanza kutazama mandhari ya hii bahari kwani tangu siku nifike hapa sijawahi kutoka kabisa. Magreti naye baada ya muda kidogo akashuka kwenye gari na kunifwata sehemu nilipo simama.
“Kwa mavazi yako utaweza kupambana kweli?” “Yaa tena yananipa uhuru mzuri sana wa kufanya chochote ninacho jisikia” “Upo vizuri” “Kwenye nini?” Nikatamani kumsifia ila ninashindwa kwani mazungumzo yetu yote Livna na watu wake wanayasikia.
“Kupambana na nguo hizo” “Kawaida, ukiwa unaifanya hii kazi inabidi uwe unaweza kupamba kwa kila vazi, liwe ni shele, suruali, baibui. Chochote unatakiwa kuweza kupambana” “Kweli, nina imani kwamba mke wangu amenichagulia mtu sahihi” “Hajakosea kabisa.” Meli ikazidi kusonga mbele, huku tukipata kifungua kinywa. Baada ya masaa kadhaa tukafanikiwa kufika katika fukwe za mji wa Kigamboni. Tukaagana na msichana alite tulete kisha tukaingia kwenye gari hili, nikafwata maelekezo kama jinsi alivyo nieleza Logate, nikawasha gari hili. Taratibu nikaanza kulitoa ndani ya boti hii, nikaanza kuondoka taratibu kwenye eneo hili, japo kuna mchanga mwigi wa bahari ila gari hii haititii chini wala kuyumbishwa na mchanga huu. Tukafanikwia kuingia barabarani na kuianza safari ya kuelekea katikati ya jiji.
Tukafanikiwa kufika darajani na kukuta mlolongo mrefu wa magari yanayo elekea Dar es Salaam. Ikatulazimu na sisi kupanga foleni. Tataratibu gari ikaanza kusogea mbele hadi tukafika katika sehemu ya ukaguzi, mwanajeshi mmoja akaniomba nishushe kioo cha gari langu, nikafanya hivi, akachungulia ndani na kututazama.
“Habari yako kiongozi” Nilimsalimia mara baada ya kutuona anatutazama sana, hakunijibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kunikazia macho mimi na Magreti jambo lililo anza kunipa mashaka, akaiwasha simu yake ya upepo iliyo anza kukoroma kwa sauti ya juu. Kwa kupitia kioo changu cha pembeni nikaanza kuona wanajeshi wengine wawili wakilisogela gari letu huku wakiwa wamezishika bunduki kwa umakini wakionekana wakiwa na mashaka nasi jambo lililo nifanya nianze kuupeleka mkono wangu katika sehemu nilipo ichomeka bastola yangu kujiandaa na lolote litakalo jitokeza mbele yetu.
Magret taratibu akanishika mkono wangu na kwa ishara ya macho akaniomba nisifanye kitu chochote.
“Tunaomba vitambulisho vyenu” Mwanajeshi huyu alizungumza, taratibu nikachia tabasamu. Nikaingiza mkono wangu mfukoni na kutoa kitambulisbo changu. Magreti naye akanipatia kitambulisho chake na kwapamoja nikamkabidhi huyu mwanajeshi. Wanajeshi wawili waliokuwa wanakuja nyuma yetu wakachungulia chungulia ndani ya gari.
“Habari zenu” “Salama tu, munaelekea wapi?” “Posta hapo” “Ohooo, aisee dada Mungu amekujalia. Kama ni manzi wako kusema kweli umepata mwanamke” “Shukrani kiongozi” “Munaweza kwenda” Askari tuliye mpatia vitambulisho vyetu alizungumza huku akinirudishia. Taratibu nikafunga kioo cha upande wangu na kuondoka eneo hili.
“Huwa una maamuzi ya haraka eheehee” “Yaa nilidhani wanahitaji kutuzingua” “Siku nyingine usijaribu kufanya hivyo. Inaweza kuharibi mipango yote tuliyo nayo” “Sawa bosi, au uliwapagawisha kwa uzuri wako” “Shauri yao ila kikubwa ni kufanya kazi iliyo tuleta huku” “Poa, sasa harusi si inafanyika usiku na muda huu, tutafanyaje?” “Tutafute hoteli ambayo tunaweza kupumzika” “Mimi sina pesa yoyote” “Usijali” “Unazo wewe?” “Wewe twende”
“Sawa.”
Tukafika katika hoteli moja ya kitalii, iliyopo maeneo ya hapa Posta.
“Silaha zetu tunatakiwa kuziacha ndani ya gari tukifika kwenye hiyo hoteli unayo kwenda” Magreti alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Poa poa”
Nikasimamisha gari sehemu ya maegesho na kushuka. Nikajiweka vizuri koti langu la suti na kuanza kutembea kuelekea ndani, Magreti taratibu akaingiza mkono wake wa kulia katikati ya nafasi iliyo achwa na mkono wangu wa kushoto, nikamtazama kwa macho ya mshangao.
“Tunatakiwa kutembea kama mume na mke” “Una uhakika?” “Ndio upo huru kwangu kwa muda huu” “Weeeee” Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na tabasamu. Kila tunapo pita watu hawakusita kututazama hususani Magret kwani anavutia kwa kila macho ya kila mwanaume. Tukachagua sehemu iliyo tulia na iliyo jificha kidogo, tukakaa huku sote macho yetu yakiwa na kazi ya kutazama tazama eneo hili kwa umakini.
“Habari zenu” Dada mmoja muhudumu alizungumza huku amesimama pembeni yetu kwa heshima kubwa sana.
“Salama tu dada, tunaomba menu ya chakula” “Sawa” Dada huyu akaondoka, baada ya dakika mbili akarudi akiwa ameshika vitabu viliwi. Akatukabidhi kila mtu cha kwake, nikaanza kutazama orodha ya vyakula hivi, vilivyo orodheshwa na bei zake.
“Niletee chipsi na miskaki na juisi ya embe” “Na mimi niletee hicho alicho kiagiza mume wangu” “Sawa karibuni” Dada huyu akaondoka.
“Unapenda sana nionekane kama kama mume wako” “Ni kama, na hii nikazi na ninacho kizungumza sikimaanishi” “Sawa mwaya” “Ila umependeza na wewe, ninaona wadada wakikushangaa shangaa”
Tukaendelea kuzungumza mambo mengi hadi chakula kikaletwa pamoja na vinywaji. Tukaanza kula tartaibu huku kkwa mara kadhaa nikiwa na kazi ya kumtazama Magret usoni mwake.
“Hivi tunakula tutalipa na nini?” “Mbona una wasiwasi, tukishindwa kulipa si tutaosha vyombo vya hii hoteli” “Hahahaaa wewe acha masihara” “Eheee tunaosha, tunasogeza sogeza muda mbele” “Oya kama huna pesa seme nianze kufikiria njia ya kuondoka hapa” “Usiwe na wasiwasi” Magreti alizungumza huku akifungua kipochi yake kidogo, akanionyesha jinsi noti za dola mia mia zikiwa zimejipanga vizuri kwenye hii pochi.
“Tuna uwezo wa kula chochote na kunywa chochote” “Daaa hapo nina amani, inabidi tule kwa maana kazi tunayo kwenda kuifanya ni kubwa sana” “Ukila ukishiba utashindwa kufanya kazi, kula wastani” Kusema kweli Magreti ni mchangamfu sana na endapo anatokea mtu ambeye hatufahamu katika huu moango anaweza kusema kwamba sisi ni wapenzi wa muda mrefu sana.
“Unajua katika haya mahusiano yetu feki kilicho kosekana ni pete. Hapa hata tukimuambia mtu sisi ni mke na mume inaweza kula kwetu, atakapo hiji kuhusiana na pete” Magreti alizungumza alizungumza huku akinitazama kwa macho malegevu kiasi, japo tupo kazini ila kuna kitu ambacho tayari nimesha kihisi kwa Magreti, ninaimani kwamba kuna chembechembe za hisia za penzi langu vimeingia moyoni mwake. Nikaitazama saa yangu ya mkononi mwa sekunde kadhaa.
“Hivi sasa ni saa kumi kasoro, tunaweza kutafuta pete za kofoji” “Sawa” Magreti akamuita muhudumu aliye tuhudumia.
“Dada naomba bili” “Sawa” Dada huyu akaondoka na kurudi akiwa na kijitabu kidogo akamuwekea Magreti pembeni yake. Akakifunua na kutoa kararasi ndogo.
“Elfu thelathini na mbili eheee?” “Ndio”
Magreti akafungua pochi yake na kutoa noti ya dola mia.
“Si ninaweza kulipa hata kwa dola?” “Ndio dada unaweza kulipia” Magreti akaiweka noti hiyo kwenye kijitabu hichi tulicho letewa.
“Chechi itakayo baki chukua mdogo wangu” “Asante sana dada yangu” Binti huyu aliondoka huku akiwa amejawa na tabasamu pana. Tukasimama na kutoka nje huku tukiwa tumeshikana mikono.
“Unajua umemuachia pesa nyingi sana” “Ahahaa hembu acha ubaili kama mpare bwana” “Ohoo pesa ni nyingi ile” “Muache bwana” “Hembu nipe kiasi kidogo cha pesa, maswala ya wewe kutoa pesa ninaonekana mimi ni boya bwana” Magreti akaanza kucheka hadi tunaingia ndani ya gari bado anacheka.
“Wewe mwanaume sijui mwanamke utakaye muoa atapataje tabu” Magreti alizungumza huku akifungua kipichi chake akachomoa noti kumi za dola mia mia na kunikabidhi, nikazikunja vizuri na kuziweka kwenye mfuko wa suti.
“Hapo sawa, ngoja tumtafute sonara kwanza” “Hakia ya Mungu, Dany unanipa raha una vituko hadi basi” Tukafika katika duka moja kubwa la sonara, tukashuka kwenye gari na kuingia ndani. Tukachagua ni pete gani ambazo tunahitaji kuchongeshewa kisha nikafanya malipo na kila pete moja ina thamani ya milioni moja na nusu na ikamlazimu Magreti kuongeza kiasi cha pesa kwani alichonipatia kimekwisha.
“Ndugu zitachukua muda gani?” “Nusu saa muheshimiwa” “Sawa, fanyeni fanyeni kwa maana tuna haraka” Simu yangu ikata nikaitoa mfukoni na kukuta namba isiyo na jina, nikamuonyesha Magreti kwa sauti ya chini akaniambia kwamba ni Livna. Nikaipokea na kuiweka sikioni
“Mume wangu?” “Niambie” “Munaendeleaje?” “Tunaendelea vizuri tu, vipi” “Nimekumiss tu ndio maana nikakupigia” “Kwani husikii tunacho kizungumza?” “Mimi sipo chumba cha mawasiliano, kidogo ninajisikia sikia joto mwilini. Nipo chumbani nimepumzila” “Umepata sawa?” “Yaa dokta ndio amenitazama muda huu, ameniambia ni mabadiliko ya hali ya hewa” “Pole mama” “Nashukuru. Ninakuomba uwe makini” “Usijaki nitakuwa makini sana” “Ninakupenda Dany wangu” Nikawatazama waty walipo karibu nasi ambao nao wamekaa kwenye viti wakisubiri huduma zao.
“Na mimi pia” Nikakata simu na kuirudisha hewani.
“Mr na Mrs Mpoki ninawaomba munifwate” Dada mmoja wa kiarabu alizungumza, tukaingia kwenye moja ya chumba na kukutana na muarabu mmoja menene akiwa amekaa kwenye kiti kikubwa cha kuzunguka.
“Habari zenu” “Salama tu” “Pete zenu zipo tayari, nina imani kwamba zitawapendeza” Muhindi huyu alizungumza huku akitukabidhi pete zetu za dhahabu na zimechonga vile tulivyo hitaji. Nikaichukua pete ya Magreti, nikamtazama muhindi huyu, kisha nikauchukua mkono wa kushoto wa Magretu na nikamvisha pete hii kwenye kidole husika cha pete ya ndoa.
“Mulikuwa bado hamjavishana pete?” “Hapana, pete zetu za ndoa, kuna sehemu kidogo tuliziacha” “Ahaaaa, ila mumependezana. Dada na wewe mvishe mwenzio” Magreti kwa tabasamu pana, akaichukau pete yangu ambayo nilipanga kujivisha mimi mwenyewe, akanivisha kidole changu cha pete. Taratibu nikamsogelea na kumbusu mdomoni jambo lililo nifanya nipate msisimko mkali sana. Magreti hakuonekana kuchukizwa na lolote zaidi ya kufurahi kwa kile nilicho kifanya kwake.
“Tunashukuru ndugu” “Karibuni sana” Tukatoka katika ofisi hii na kuridi ndani ya gari letu. Magreti akanitazama kwa macho ya matamanio, taratibu nikamshika mkono wake wa kulia, nikamsogeza kichwa chake karibu yangu, tukatazama kwa sekunde kadhaa huku nikizilamba lamba lipsi zangu tararibu. Nikausogeza mdomo wangu hadi sehemu ulipo mdomo wake.
“Mmmmmm” Magreti alizungumza huku akikaa sawa kwenye siti yake akafunga mkanda wa siti.
“Tuondoke, tuna kazi ya kufanya” Safari ya kuelekea ukumbini ikaanza huku nikihakikisha kwamba ninafuta mawazo yote ya kijinga ninayo muwazia Magreti na ninahitaji kukakikisha kwamba ninawaza kazi iliyopo nbele yetu. Kutokana na foleni kubwa ya barabarani. Tukafika ukumbi muda husika,, gari letu likakaguliwa mlangoni kisha tukaruhusiwa kuingia ndani.
“Tupo kazini sasa, tuwe makini, kila kilicho tokea muda ulio pita tupotezee, hakikisha kwamba unajilengesha kwa Osama Bin Laden ninahitaji akiwa hai” “Nimekuelewa” “Sawa” Sote tukashuka kwenye gari huku kadi ya mualiko nikiwa nayo mimi. Nikamshika kiuono Magrerti hadi mlangoni. Walinzi kusema kweli wapo wengi sana katika huu ukumbi huu, nikatoa kadi hii na kumkabidbi jamaa ambaye ndio mkabidi, akaipitisha katika mashine ya ugaguzi na macho yake akayatupia kwenye computer iliyopo pembeni yake. Akanirudishia kadi yangu huku akiwa ametabasamu.
“Karibuni sana” “Shukrani ndugu” Tukaingia ndani humu ambapo kumejaa watu wengi sana wakiwa na wamependeza sana. “Hakikisha kwamba hugusi sikio lako sawa” Magreti alizungumza kwa sauti ya kunining’oneza.
“Usijali katika hilo ninaelewa kila kitu” Tukatafuta viti ambavyo tunaweza kuliona jukwaa vizuri na tukaa.
“Mungu wangu tunamuonaje hapa” Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikiwa nimesogelea karibu sana Magreti.
“Tutamuona, Logate unatusikia?” “Ndio ninawaiskia tangu mulipo ondoka hapa” “Basi tunakuomba utusaidie katika hili” “Nipo kwa ajili yenu” Sherehe ikaanza huku tukiendelea kuwatazama watu waliomo humu ndani. Wakaingia watu wapatao nane wakiwa wamevalia kanzu na wamejifunika nyuso zao na kubakisha macho tu
‘Osama ameingia ukumbini’
Tuliisikia sauti ya Logate akitupatia maelekezo.
“Ni yupi sasa kati ya hawa watu tisa?” ‘Tumieni simu zenu kifanyeni kama munapiga picha’
Tulaemdelea kutazama walinzi walipo katika eneo hili. Bibi harusi na bwana harusi walipo anza kuingia ukumbini hapa, watu wote wakanyanyuka huku wenye simu zao wakijitahidi kuchukua video kwa kile kinacho endelea katika eneo hili. Na sisi tukatoa simu zetu mifukoni na kuanza kuchupiga picha maharusi hawa wanao ingia kwa mbembe kubwa za kucheza.
Nikaweka upande wa video na kuigeuza simu yangu sehemu alipo Osam Bin Laden na kundi lake, nikajikuta macho yakiwa yamenitoka kwani watu wote walio zifunika sura zao kwa vitambaa ni sura ya Osama Bin Laden.
“Mage umeona hichi kinacho tokea hapa?” “Mbona wamefanana jamani?” “Logate hii inakuwaje?” “Hata sisi tunashangaa huku hatujui Osama ni nani kati yao kwa maana wote wanafanana” Hatukujua ni nini cha kufanya hadi watu wote tulipo ruhusiwa na muongoza sherehe(MC) tukae kwenye viti vyetu
Tukaendelea kuifwatilia sherehe hii huku tukijitahidi kuhakikisha kwamba waarabu hawa walio jifunga vitambaa kwenye sura zao tuna wafwatilia nyendo zao hadi katika ukaaji wao.
“Tunatakiwa kuwa makini, ninaona jinsi walinzi wanavyo tutazama tazama”
Magreti alizungumza huku akiwa ameniegemea kwenye bega langu.
“Yaaa ninawaona. Logate vipi umefanikiwa kumjua ni yupi Osama?”
“Hapana bado tunaendelea kumtafuta ila tunaomba muda kidogo”
“Sawa”
Tukaendelea kupata vinywaji taratibu. Huku muongozaji wa hii sherehe akijitaidi kuhakikisha kwamba tunafurahia sherehe hii kwa kuzungumza maneno yaliyo wachekesha watu wengi humu ndani.
“Ila tutaangalia muda muda wa chakula ni lazima watasimama sasa kwenye kula hapo ndio tutaweza kuwaona”
“Ngoja tusubiri tuangalie”
Muda ukazidi kusonga mbele, ukafika muda ambao mimi na Magreti tunausubiria kwa hamu. Kama kawaida maharusi wakaanza kutangulia kwenda kuchukua chakula, wakafwata wazazi wa pande zote mbili pamoja na ndugu, ila katika meza waliyo kaa hawa waarabu hapakuwa na hata mmoja aliye nyanyuka.
“Hawali au?”
Magreti alizungumza huku akiwatazama kwa macho ya kuiba iba.
“Wala sifahamu.”
Ikafika zamu yetu kunyanyuliwa kakika meza yetu pamoja na wezetu walio kaa humu. Tukapanga foleni huku Magreti akitangulia mbele na mimi nikiwa nyuma yake huku mkono wangu wa kushoto nikiwa nimemshika kiunoni. Akachukua sahani mbili na tukaanza kupita kwa kila muhudumu na akatupakulia chakula kisha tukarudi katika viti vyetu.
“Logate sisi tunagonga msosi ila hatuelewi hawa jamaa kama wanakula ua hawali kwa maana hawajakunywa kinywaji wala kula chakula”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikindikiza na paja la kuku lililo kaangwa vizuri na kunona sana.
“Wakinyanyuka nitaweza kumfahamu ni nani Osama kwa kutembea kwao”
“Sawa”
“Ila jamani hatukaribishani”
“Ester karibu”
“Mmmmm hadi niwaambie”
“Livna yupo?”
“Yupo hapa anawaona jinsi munavyo kandamiza hiyo minyama”
“Ila Dany mpenzi wangu upo vizuri katika kugonga msosi, mmmm chakula chote hicho”
“Ahaaa jamani nipo kazini”
“Alafu mkuu, mumeo alikuwa ananilazimisha kuongeza msosi hadi nikajisikia aibu”
“Hahahaaaaaa”
Mazungumzo yetu tunayazungumz a kwa sauti ya chini sana na ningumu sana kwa mtu kuweza kustuka kama tunazungumza na watu ambao hawapo ndani ya ukumbi huu.
“Angalieni musije mukavimbiwa”
“Ndugu waalikwa tukiwa tunaendelea kupata chakula kilicho andaliwa kwa ubora wa hali ya juu. Tunawakaribisha muweze kutoa zawadi kwa maharusi wetu, na wazazi watafwatia nyuma”
Muongoza sherehe alizungumza, tukawaona waarabu hawa wakinyanyuka kwa pamoja na kuanza kuelekea walipo simama maharusi.
“Mtu wa tatu kutoka mbele ndio Osama Bin Laden, kumbea kwake na hawa wezake ni tofati. Mguu wake mmoja wa kulia anachechema kiasi, japo si rahisi kumuona”
Tuliisikia sauti ya Logate katika vinasa sauti vyetu tulivyo vivaa masikioni mwetu. Sote tukamtazama mtu wa tatu kutoke mbele. Kweli tukaweza kuona udhaifu katika kumbea kwake.
“Hakikisheni sasa hawatoke kwenye targrt yenu”
“Tumekusoma tuachieni hilo jukumu”
Wakampa mkono wa shukrani bwana harusi pamoja na bibi harusi, hawakuwapa mikono wasimamizi wa harusi hii, hatukulijali sana hilo, wala hawakurudi kwenye viti vyao na moja kwa moja wakaanza kueleleka nje. Walinzi kadhaa walimo humu ndani wakanza kutangulia nje.
“Ngoja watoke”
Nilizungumza huku niikiendelea kumalizia vipande vya vyama katika sahani yangu. Wakatoka watu wawili watatu ambao si walinzi kabisa. Nikachukua tishu na kujifuta mikononi mwangu, nikasimama na Magreti naye akasimama na tukaanza kutembea kwa pamoja huku nikiwa nimemshika kiuno. Watu wengi ndani humu wakabaki wakiwa wametukodolea macho, wengi wao wanamtazama Magreti. Tukafika nje na kuwaona walinzi walivyo wazunguka watu hawa walio valia kanzu, wote wanaelekea katika maegesho ya magari yaliyopo mbali kidogo na hii sehemu ya ukumbi.
“Samahani wapendwa hamuruhusiwi kueleke huku kwa sasa”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akisimama mbele yetu.
“Kwa nnini kamanda?”
“Kuna viongozi wanaondoka, wakiondoka basi ndio tutawaruhusu”
“Sawa kaka asante, baby tusubiri kwanza”
Magret alizungumza huku akinishika kifua changu, tukatafuta sehemu na kusimama huku macho yetu tukihakikisha kwamba gari wanazo ondoka nazo tunaweza kuziona vizuri”
“Logate umesikia tulicho ambiwa?”
“Ndio, ninawatumia picha ya gari aliyo panda Osama”
“Pao, amepanda peke yake?”
“Yupo na mlinzi wake ambaye naye anafanana naye”
“Poa”
Kijimlio kidogo cha simu yangu ikanifanya niitoe mfukoni, kabla ya kuangalia hii picha nikatazama eneo hili tulilo simama kwa juu kuna camera yoyote ambayo inaweza kuchukua kile niitakacho kitazama kwenye simu yangu. Kwa bahati nzuri hakuna kamera yoyote, nikaifungua picha hii na kuona BMW X6 yenye namba za usajili I86GSW.
“Hii namba ya ni ya nchi gani?”
“Iraque, walikuja na gari zao na zipo gari nne zinazo fanana sasa munatakiwa kuwa makini sana”
“Poa.”
Tukaziona gari hizo zikiondoka katika eneo hili, zikatoka getini na kupotelea kwenye upeo wa macho yetu.
“Kiongozi tunaweza kuondoka sasa?”
“Ndio munaweza kuondoka”
Mlinzi huyu alizungumza mara baada ya kuwasiliana na mwenzake.
“Poa poa kaka. Hivi ni kiongozo gani huyo aliye ondoka hapa?”
“Hampaswi kufahamu, kama munaondoka munaweza kuondoka”
“Samahani mwaya kaka, mume wangu amelewa ana maswali ya ajabu ajabu”
“Hakuna tabu dada”
Tukaanza kutembea kwa hatua za kwaida kuelekea lilipo gari letu, tukaingia ndani, nikaliwasha na kuliweka sawa. Taratibu nikaanza kueleka getini, tukafanyiwa ukaguzi kama tulivyo ingia humu ukumbini, kisha gari zikaruhusiwa kutoka.
“Logate tumewapoteza sijui wameelekea wapi tutumieni ramani ya wanapo elekea”
“Tayari nimesha tuma kwenye simu ya Mage”
“Mage hembu angali”
Mage akaitoa simu yake kwenye kipochi chake.
“Nimeipata”
“Wanaelekea wapi?”
“Wanaelekea……kunja kushoto hapo mbele”
Nikapunguza mwendo wa gari na kukunja kushoto kisha nikaanza kuongeza mwendo wa gari uzuri ni kwamab ni usiku na hakuna foleni ya magari barabarani.
“Kunja kushoto tena. Gari zao zipo kasi sana ongeza mwendo baba”
“Kaa vizuri kwenye siti”
“Mimi nipo vizuri, kazi ni kwako”
Nikazidi kuongeza mwendo hadi nikafika spidi mia mbili na kuanza kuelekea spidi mia mbili na kumi.
“Kuli, kulia”
Kutokana nipo kwenye mwendo kasi na kona aliyo niambia Magreti ipo mita chache kutoka nilipo, ikanilazimu kunyanyua handbrek huku nikikunja kona hii, jambo lililo pelekea gari kuserereka sana, nikajitahidi kuhakikisha kwamba ninahimili mserereko huu, nilipo kaa sawa. Nikaendelea na kasi zangu jambo lililo mfanya Magret kunitazama mara mbili mbili.
“Tutakufa?”
“Hatufi niambie wanalekea wapi”
“Nyoosha, kwa sasa wanakaribia Mwenge”
“Watakuwa wanaelekea wapi?”
“Wakinyoosha mazima watakuwa wanaelekea Mbezi Beach”
“Poa poa”
Sikufwata sheria za mataa ya humu barabarani, nilipo pata nafasi ya kupita nikahakikisha kwamba ninapita pasipo kusubiri kuruhusiwa kupita.
“Wanaeleka Mbezi Beachi”
“Hawa tunatakiwa kuhakikisha kwamba tunawafikia kabla hawajafika katika sehemu wanapo kusudia”
Maneno ya Magreti ayakanihimiza kuongeza kasi yagri hili hadi ikafika hatua nikaanza kuogopa na kuamini kwamba ikitokea bahati mbaya tumepata ajali basi sijui itakuwaje.
Kwa mbali nikaanza kuziona gari hizi zikienda kwa kasi sana, nikazidi kuongeza kasi hadi nikazifika karibu. Gari za mbili za nyuma zikaanza kuzuia nisipite huku nazo zikienda kasi.
“Hii mijamaa mijinga kweli kweli”
Nilizungumza huku nikitazama jinsi gari hizi zinavyo tamba barabarani na kuicha gari aliyo panda Osma ikiwa mbele kabisa. Magreti akaanza kutoa bastola zake mbili akazikoki vizuri, akanitazama kisha taratibu akafungua kioo cha upande wake. Akatoa mkono mmoja wa kushoto na kuanza kushambulia gari hizi zinazo tuzuia.
“Funga kioo”
Nilimuambia Magreti na kumfanya atii nilicho mueleza. Nikapunguza mwendo huku nikitazama kijinjia cha pembeni upande wa kulia wa barabara, nikaanza kuingia kwenye barabara hii ambayo ninaifahamu na inatokea kwa mbele.
“Unakwenda wapi?”
“Tulia”
Nikazidi kuongeza mwendo kwenye njia hii ndogo ambayo imetenganishwa na msitu ambao unatufanya tusizione gari za barabarani wala gari zinazo pita narabarani zisituone.
“Upo tayari?”
“Eheheeee”
Nikaongeza mwendo hadi gari ikaanza kutoa mlio wa tahadhari, tukaingia barabarani na gari nikaanza kuizungusha kwa mfumo wa dura. Gari hizi za msafara wa Osama Bin Laden zikaanza kutoka barabarani wakihakikisha kwamba wananikwepa mimi kwani kitu walicho kutana nacho ni cha gafla sana. Gari zote zikaendelea kuelekea maporini, nikalisimamisha gari, kizunguzungu tunacho kihisia, sikukipa nafasi ya kunipoteza muda wa kumpoteza Osama Bin Laden. Niachomoa bastola zangu sehemu nilipokuwa nimeziweka.
“Hei upo poa?”
Nilimuuliza Magreti huku nikimtazama tu usoni mwake, hakunijibu nikatamba bado anasikilizia kizunguzungu kwani gari imezunguka zaidi ya mara kumi na tano. Nikafungua mlango na kushuka, walizni wa Osama wakaanza kushambulia huku wakijitahidi kuhakikisha wanamlinda bosi wao.
Cha kumshukuru Mungu huku nikiwa nina bastola zenye risasi za kutosha huwa sifanyi makosa kabisa ya kuhakikisha kwamba ninawashambulia maadui zangu. Nikaanza kumuangusha mlimzi mmoja baada ya mwengine kwa maana baadhi ya ndio kwanza wanatoka kwenye magari yao ambayo yamebondeka bondeka kwa kugongana wao wenyewe, wengine kwa kugonga miti mikubwa iliyopo pembezoni mwa hii barabara.
Nikafika lilipo gari alipo Osama, nikakuta mlango upo wazi na ndani hakuna mtu.
“Dany wanakimbilia mbele”
Niliisikia sauti ya Logate masikioni mwangu.
“Mage hakikisha kwamba hushuki kwenye gari, endesha hadi kwenye kona inayo fwata sawa”
“Poa”
ITAENDELEA
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 1/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 2/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 3/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 4/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 5/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 6/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 7/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 8/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 9/10
- AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 10 MWISHO
0 comments:
Post a Comment