Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AIISSII U KILL ME LEGACY SEHEMU YA 2/10

 


AIISSII U KILL ME LEGACY

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 2 KATI YA 10

 


“Mmmm”

“Kuwa makini kaka, hao jamaa unao kwenda kuwafwata sio watu wa mchezo mchezo japo tumewazidi”

“Nalitambua hili, naombeni munipatie lisaa moja na nusu hii kazi itakuwa imekamilika”

Mmoja wa wezangu akanikabidhi saa yake, ili kuwa makini na muda ambao wamepanga kunisubiria.

“Kama nikimaliza lisaa moja na nusu sijarudi ninawaomba muondoke na musiendelee kuwepo katika eneo hili”

“Poa poa”

Tukapeana tano, kisha nikaanza kutembea porini humu, kutokana hatujaenda mbali sana na kambi hii, sikuona haja ya mimi kutumia gari.

‘Nenda kawaambie waalimu wako wakufundishe tena kijana na usirudie kuifanya hii kazi tena’

Meneno haya ya Dany yakanifanya nizidi kukimbia kwa kasi huku nikiwa nimejawa na hasira sana.

‘Kwa nini anione mimi mzembe’

Nilizungumza kwa uchungu huku nikizidi kuonga mbele. Nikafika katika eneo la kambi hii. Kutokana nimweza kuingia ndani ya hii kambi na kujua ni wapi anapo kaa mkuu wao basi haikuwa kazi ngumu kwangu kuingia ndani ya kambi hii huku nikimuua mwajeshi mmoja baada ya mwengine, tena kimya kimya. Nikafika katika chumba ambacho tulikuwa tumefungiwa, nikachungulia ndani na sikuweza kumuona nesi Husna.

‘Wamemchukua’

Nilizungumza huku jasho likinimwagika. Nikaendelea kunyata na kujificha hadi katika nyumba anayo ishi mkuu wao, nikasikia sauti ya Husna akilia akionekana kukataa kufanya anacho lazimishwa. Nikachomoa visu vyangu viwili huku nikivaa mkanda wa bunduki yagu hii na kuifanya ining’inie mgongoni mwangu.

Nikaanza kupambana na walinzi walio simama katika mlango wa kuingilia katika nyumba hii. Kwa bahati mbaya mlinzi mmoja akapiga risasi ambayo kwa bahati nzuri ilipita pembeni yangu na haikunipata. Sikua na namna zaidi ya kuanza kutumia silaha, kwa mlio wa bunduki yake ni lazima utakuwa umemstua kila mtu ndani ya kambi hii. Nikafanikiwa kuwaua walinzi wote wa mlangoni na kuingia ndani ya nyumba hii, nikanyata hadi kwenye moja ya chumba ambacho nilimsikia Husna akilia kwa uchungu. Nikaingia ndani na kumkuta mzee huyu akiwa amekaba nesi Husna kwa nyuma huku amemuwekea kisu cha shingo.

“Hee umekuja”

Mzee huyu alizungumza huku akicheka kwa dharua. Nikamtazama nesi Husna jinsi maziwa yake yalivyo wazi na shati lake limekatwa vifungo.

“Muachia nesi aondoke”

“Randy, sijaona mtu mpumbavu kama wewe, unahisi kwamba utatoka hai humu kambini kwangu?”

“Hilo sio jambo ninalo lifikiria kwa sasa”

Nilizungumza huku nikimtazama nesi Husna usoni mwake.

“Weka silaha yaka chini”

Mzee huyu aliniamrisha, taratibu nikaanza kuinama huku nikiiweka bunduki yangu chini, kitendo cha kuiweka bunduki hii kubwa chini, nikachomoa bastola yangu moja kwenye mguu wa kushoto na kumpiga risasi moja mzee huu ya paja na kumfanya aanguke chini. Nikaomkota bunduki yangu kwa haraka, nikasikia miguu ya wanajeshi wakinyata ili wafike katika chumba hichi, nikachomoa bomu moja la kurusha kwa mkono, kisha nilalitupia nje ya chumba hichi kisha nikamrukia nesi Husna na kuanguka naye kitandani. Mlipuko mkubwa ukatokae huku kiambatana na vilio vya wanajeshi hao.

Mzee huyu akajaribu kusimama, nikatandika risasi ya mguu, kisha nikamsimimisha na kumkalisha kwenye moja ya kiti.

“Chukua hii, akileta ujinga mfumua ubongo sawa”

Nilizungumza huku nikimkabidhi nesi Husna moja ya bastoa. Nesi Husna akaishika bastola hiyo huku mikono yake ikimtetemeka. Nikachungulia nje na kuona baadhi ya wanajeshi wakiugulia maumivu, nikaanza kumuua mmoja baada ya mwengine. Nikafika sebleni nikaona jinsi wanajeshi wengi wakiizingira hii nyumba.

“Fuc** me”

Nilizungumza huku nikirudi chumbani.

“Tutatoka sote ole wako mwanajeshi wako mmoja alete ujinga ninakuua”

Nilizungumza huku nikimnyanyua mzee huyu.

“Husna vaa koti lako”

Nesi Husna kwa haraka akachukua koti lake jeusi na kulievaa.

“Upo vizuri?”

“Ndio”

Alizungumza huku akifuta machozi usoni mwake. Nikakumbuka cheki ya pesa aliyo kabidhiwa mzee huyu kwamba ipo kwenye moja ya koti lake hili la jeshi alilo livaa. Nikaanza kumpapasa na nikaikuta cheki na barua za makubaliano ya kubalishana kati yangu na pesa alizo kabidhiwa na kundi langu la Al-quida.

“Muda mwengine usipende pesa kuliko utu”

Nilizungumza huku nikimtanguliza mbele mzee huyu. Tulipo fika sebleni, nikampiga kabali kwa nyuma huku nikimuwekea bastola kichwani mwake, japo anatembea kwa maumivu makali ya risasi nilizo mpiga. Ila hana jinsi zaidi ya kuendelea kutembea.

“Waamuru watu wako waondoke kabisa hapa nje?”

Mzee huyu akawaamrisha watu wake waondoke kabisa.

“Husna kuwa karibu nami”

“Sawa”

Tukaanza kutoka ndani humu, huku nesi Husna naye akiwa makini na bastola mkononi mwake. Tukafika kwenye moja ya gari.

“Husna ingia uendeshe gari”

Nilizungumza huku nikiwatazama wanajeshi wa mzee huyu wakiwa makini sana katika kuninyooshea silaha zao. Husna akawasha gari hili aina ya Mitsubishi Pajero sport.

“Hata risasi moja ya kijana wako ikitushambulia au kutufwata, nitarudi tena na nikirudi basi hii kambi yako tutaisambaratisha na huto kuwa na kikundi tena sawa”

“Sawa kijana”

Mzee huyu alizungumza huku akitetemeka mwili mzima. Nikaingia ndani ya gari huku nikimsukumia pembeni na nikamuhimiza nesi Husna kuondoka kwa haraka katika eneo hili. Risasi mfululizo zikazidi kutuandama kwa nyuma ila nesi Husna akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari hili na kuondoka katika eneo hili la hii kambi.

“Upo salama?”

“Ndio, asante Randy”

“Usijali. Nyoosha na kunja kulia sawa”

“Sawa”

Kwa kupitia kioo cha nyuma nikashuhudia gari nne zikituandama kwa kasi sana.

“Fuc** me”

“Nini?”

“Wanatufwata”

Nilizingumza huku nikihamia siti ya nyuma.

“Wewe tembea usipunguze spidi, mbele kuna gari aina ya Range rover utaiona. Wawashie taa mara tatu na kuzima watajua ni mimi sawa”

“Sawa”

Kitu ninacho mpendea nesi Husna, anajua kuhimili gari vizuri hata likiwa katika mwendo wa kasi sana, anaweza kulihimili. Risasi kutoka kwa wanajeshi hawa wanao tufukuzia zikazidi kutuandama. Nikavuja kioo cha nyuma ambacho tayari kimejaa matobo tobo ya risasi. Nikaanza kujibu mashambulizi yao huku nikihakikisha kwamba ninawalenga maderava wa gari hizo.

“Randy gari lile kule”

Nesi Husna alizungumza na kunifanya nitazame mbele, nikawaona wezangu nao wakiingai kwenye gari lao kwa haraka kisha wakaanza kuondoka katika eneo walilo kuwa wakinisubiria.

“Umewawashia taa”

“Ndio”

“Ongaeza mwendo uwafikie”

“Sawa”

Nikachomoa mabomu wawili ya kurusha kwa mkono kisha nikayatupia barabarani. Milipuko ya mabomu hayo yakazifanya gari mbili za watu hao kupoteza muelekeao na kupinduka. Nikahamia siti ya mbele.

“Tunaweza kubadilishana”

“Siri!!?”

“Ndio”

Nesi Husna akatazama barabara kidogo kisha akaanza kuahimia siti yangu ya pembeni huku nami nikihamia katika siti yake. Hadi hapa gari lipo katika spidi mita mia mbili, na tumebakisha spidi ishirini tu ili kufika kiwango cha mwisho cha spidi ya gari hili. Nikaanza kuapigia honi wezangu, taratibu wakaanza kupunguza mwendo nanikawafikia na tukawa sawa.

“Hei vipi munawaogopa?”

“Kumbe ni wewe?”

“Ndio”

“Wamebagi wangapi hao?”

“Zimebaki gari mbili”

“Tuachie tangulia”

“Poa poa”

Nikalipita gari la wezangu hawa na kuongoza msafara huu. Wezangu wawili wakachomoza kwenye vioo, na kuanza kuwashambulia wanajeshi hao wanao tufwata, ndani ya muda mchache wakafanikiwa kuwadhibiti. Wakanipigia honi, nipunguza mwendo na nikawa sawa sawa nao. Wakanitazama huku wakiwa wamejawa na tabasamu na wakanipigia satuli wakimaanisha wameikubali kazi yangu niliyo ifanya.



Hadi kufika katika kambi yetu, ikatuchukua masaa sita na nusu. Mkuu wangu wa kambi hii ambaye alinipatia ruhusua ya kufanya shambulizi la kumuokoa nesi Husna akanishangaa kuniona nikishuka kwenye gari nikiwa nipo salama salmin. Nikampigia salitu ikiwa ni moja ya sheria, akamtazama nesi Husna ambaye ana shangaa shangaa uwepo wake katika eneo hili.

“Nahitaji kuzungumza nawe”

Mkuu alizungumza huku akielekea katika ofisi yake, kwa ishara nikamuomba nesi Husna kunisubiria ndani ya gari. Tukaingia kwenye ofisi yake na mkuu akazungumza meza yake na kukaa katika kiti chake humu akinitazama kwa macho makali.

“Ilikuwaje?”

Swali la mkuu, likaniweka njia panda kwa maana sifahamu nianzie wapi katika kumjibu kwa maana usiku wa jana hadi asubuhi ya siku ya leo kwa upande wangu ilikuwa ni ndefu sana.

“Samahani mkuu, sikuweza kufanikisha zoezi la kumteka makamu wa raisi”

“Ndio maana nilikuuliza imekuwaje. Nipe maelezo ya kueleweka”

“Kama ulivyo tataadharisha. Dany aliweza kujitokeza na kwa bahati mbaya sikufanikiwa kufanya chochote kwani aliweza kunizidi kila aina ya uwezo, ukiachilia utumiaji wa silaha ila alinizidi hadi upambanaji kwa mana ni mtu mmoja mahisi mt……”

Mwalimu alizungumza huku akinyoosha kiganja chake cha mkono wa kulia akiashiria kwamba ninyamaze.

“Una mpango gani juu ya Dany”

“Mkuu nina hitaji muda wa kujipanga ili kuhakikisha kwamba nina mpata”

“Wapi?”

“Sijajua ila nina imani kwamba tukiendelea kumtafuta basi tunaweza kumpata”

Mkuu akanitazama kwa sekunde kadhaa.

“Yule mwanamke ni nani?”

“Ndio nesi ambaye alinisaidia kutoka katika hoteli ambayo tulikwenda kwa lengo la kumteka makamu wa raisi wa Marekani, ila kwa bahati mbaya yakatokea matatizo”

“Una mfahamu kwa undani?”

“Hapana mkuu?”

“Kwa nini umekubali kumleta ndani ya kambi hii ambayo hairuhusiwa mtu wa kawaida kuweza kuingia humu. Kumbuka kwamba hichi sio kikosi cha serikali Randy. Hili ni kundi la kigaidi, narudia tena hili ni kundi la kigaidi, kazi zetu zipo kinyume na serikali za nchi nyingi sana hapa duniani. Je akiwa mpelelezi na akavaa GPRS ya kumuonyesha ni wapi alipo unahisi ni nini kitakacho kwenda kutokea eheee?”

Mkuu alizungumza kwa kufoka huku akinitolea macho.

“Samahani kwa uzembe huo mkuu”

“Ninahitaji umuue huyo mwanamke, umenielewa”

Kauli hii ya mkuu ikanipa wakati mgumu wa kuitikia kwamba nimekubali, japo aliyo itoa kwa upande wangu ni amri ila kusema kweli sijui nitaanzia wapi. Hadi muda huu, sijaona jambo baya kwa nesi Husna.

“Umenielewa Randy”

“Samahani mkuu ninaomba nijitetee”

“Katika hili Randy hakuna kujitete, pata picha, habari ya mwanamke huyu ikafika makao makuu hivi unahisi itakuwaje kwa wakuu wangu”

“Samahani mkuu nitalishuhulikia”

Nilizungumza huku nikitoa hundi ya pesa, nikamuwekea mezani kwake na kumfanya ashangae kidogo.

“Nimeweza kurudisha mulicho kipeleka kwa wale watu, samahani, nilimjerudi mkuu wao wa kikosi na pia niliweza kuwaua baadhi ya wanajeshi wa kikosi chiho”

“Ohooo Mungu wangu, Randy una akili gani wewe. Hivi huyi sisi na ISS ni wanachama wamoja. Inakuwaje unafanya ujinga kama huo”

“Mkuu ilinilazimu kufanya hivyo, ndio maana nilitanguliza samahani”

“Unafunja uhusiano wetu mzuri na ISS, kutokana na huyo mwanamke si ndio?”

Kabla sijajibu chochote simu ya mezani mwa mkuu ikaanza kuita, macho yetu yote yakaitazama simu hiyo. Taratibu akanyanyua mkonga wa simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Haloo”

“Habari mkuu”

Mkuu wangu alizungumza huku macho yakimtoka.

“Ndio mkuu”

“Sawa mkuu”

Akakata simu kwa nguvu na kunitazama, akasimama huku akihema kwa jazba.

“Umenisababishia matatizo, nimeitwa makao makuu. Sasa ole wako lolote baya linipate kwa ajili yako, nitakwenda kukuvuruga hicho kichwa chako”

Mkuu mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akatoka ndani humu na kuniacha peke yangu, nikashusha pumzi taratibu huku nikifungua jaketi langu la kuzuia risasi na kuanza kutoka nje huku nikiwa nimechoka sana. Nikashuhudia gari mbili anazo tumia mkuu katika safari zake zikitoka katika geti kuu la ngume hii kwa mwendo wa kasi sana. Nikafika katika gari na kumkuta Husna akiwa amejilaza kwenye siti.

“Hei”

“Vipi, mbona umekuwa mnyonge?”

“Uchovu tu Randy vipi wewe?”

“Nimechoka, ila nahisi kuto kuchoka”

“Umechoka, ila una hisi haujachoka. Maana yake ni nini?”

Nikatazama wanajeshi jinsi wanavyo endelea na shuhuli zao, kisha nikamtazama Husna usoni mwake.

“Kuna mambo ya kijeshi yametoka kati yangu na mkuu, hususani swala la kuvami kule. Hilo kidogo ndio limeleta shida na hapo unapo munona anaelekea makao makuu”

“Jamani, samahani laiti ingekuwa si mimi haya yote yasinge tokea”

“Huna cha kujilaumu, laiti ingekuwa si mimi kukuomba msaada wako, yasinge tokea haya”

“Sasa huoni ninaweza kuletewa matatizo, isitoshe mimi sio mwanajeshi, pili hichi kukundi hakuna raia wa kawaida anaye jua mako yake, ila mimi nimefika hapa. Kweli Randy huoni hili ni tatizo?”

Mswali na anayo yafikiria nesi Husna ni sawa sawa na kile alicho kizungumza mkuu wangu kwa ukali wake.

“Usijali nitalishuhulikia hilo”

“Randy kwani hapa una cheo gani?”

“Mtu wa kawaida tu”

“Ona sasa Randy tuta uwawa bwana, naogopa mwenzio”

“Niamini mimi Husna, kama nilirudi kukuokoa, inakuwaje nishindwa kwa ajili yako?”

Husna akanitazama huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Tambua upo mikono salama na mtu salama, hivyo siwezi kukuacha upate shida”

“Nashukuru kusikia hivyo”

Kwa ishara nikamuomba Husna kushuka kwenye gari, tukaanza kutembea kuelekea kwenye jengo la hospitali, lililomo ndani ya kambi hii. Tukiwa katika jengo hili, akaletwa mwajeshi mmoja akiwa amevunjika miguu yote miwili.

“Amefanyaje?”

“Amepata ajali ya gari”

“Ninaweza kutoa msaada, mimi ni daktari wa mifupa”

Husna alizungumza huku akiwatazama madaktari wawili wa jeshi walio mpokea mgonjwa huyu.

“Mpeni nafasi”

Nilizungumza ili kulipa uzito jambo hili, wakamruhusu Husna kuingia katika chumba cha upasuaji na mimi nikabaki nje nikimsubiria kwa maana sihitaji kumuacha peke yake wanaweza kumfanyia jambo baya, kitu ambacho sinto kubaliana nacho.

“Randy unaitwa na mkuu”

Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akiwa amesimama mbele yangu. Nikamtazama kwa muda kidogo huku nikijishauri nini cha kufanya.

“Sawa”

Nilizungumza huku nikinyanyuka, nikachungulia katika kioo cha mlango wa chumba cha upasuaji, nikamuona Husna akiendelea na kazi yake pamoja na baadhi madaktari wa hapa. Nikaondoka eneo hili la hospitalini hadi katika ofisi ya mkuu wa kambi. Nikamkuta akiwa amesimama huku akizunguka zunguka ndani ya ofisi yake na dhairi anaonyesha kwamba amejawa na hasira.

“Ndio mkuu”

Kwa haraka akanishika kifuani na kulikwida shati langu na kunigandamiza ukutani kwa nguvu huku akihema kama simba dume aliye choka kumkimbiza swala alite mshinda kasi.

“Umenisababishia matatizo wewe mtoto wa malayaaa”

Mkuu alizungumza kwa uchungu sana huku akiendelea kunikwida shati langu. Kutokana nilisha jiandaa kisaikolojia, sikuweza kuogopa hasira ya mkuu wangu. Mkuu wangu akaendelea kunitazama usoni mwangu huku akitetemeka mwili mzima na kushindwa kuzungumza kile anacho kihisi ndani ya moyo wake. Mkuu akaniachia shati langu na kukaa kwenye moja ya sofa huku akihema sana.

“Mkuu naomba unisamehe, sinto fanya ujinga mwengine na kukuweka katika matatizo”

“Randy kwa amri iliyo toka makao makuu unatakiwa kumuua huyo mwanamke haraka iwezekanavyo”

Mkuu alizungumza huku akihema sana

“Amri imetolewa na nani?”

“Mzee mwenyewe”

Nikafumba macho yangu taratibu kwa maana mzee aliye toa amri hii ni baba Farida ambaye hanipendi kabisa na amekuwa ni msababishaji mkubwa wa penzi langu mimi na Farida kufia hewani.

“Ila ni daktari mzuri na hivi sasa yupo kwenye chumba cha upasuaji anamfanyia mwanajeshi mmoja upasuaji”

Mkuu akanitole macho ya mshangao. Akasimama na akatoka nje ya ofisi hii, nikaona bahasha ndogo aliyo iangusha mkuu nje ya mlango, nikaikota na kuanza kumfwata kwa nyuma. Barua hii inaonyesha ni kadi ya mualio wa harudi, moyoni mwangu nikajikuta nikipata hamasa kubwa ya kuhitaji kuisoma. Nikaifungua kwa haraka na kuanza kuisoma. Sikuamini macho yangu nilipo kuta ni mualiko wa harusi ya Farida, iliyo pangwa kufanyika usiku huu katika makao makuu ya kambi kundi hili la Al-quida na muaoji wa harusi hii ni mmoja wa watoto wa viongozi wa juu kabisa wa kikundi hichi. Moyoni mwangu nikajihisi maumivu makali sana ambayo kusema kweli hayana mfano wa kuyafananisha. Nikamtazama mkuu wangu nikamuona ana karibi katika jengo la hospitali, kwa hasira aliyo nayo nikagundua ni lazima atafanya jambo baya kwa Husna.

Nami nikafika katika jengo la hospitalini na kumkuta mkuu akiwa amesimama mlango mwa chumba cha upasuaji huku akiwa ameshika bastola na amemuelekezea Husna.

“Mkuu ni nini unataka kukifanya”

Daktari mmoja alizungumza huku akimtazama mkuu wetu.

“Tokeni ndani ya chumba hichi”

“Mkuu tupo katikati ya upasuaji”

“Nimesema tokeani sio ombi ni amri”

Madaktari hawa wawili wakatoka na kumuacha Husna peke yake. Nikaingia ndani ya chumba hichi na kusimama mbele ya Husna.

“Natambua kwamba una wasiwasi na maisha yako. Naomba unipe nafasi ya mwisho mkuu wangu”

“Randy ondoka mbele ya huyo binti”

“Siwezi kufanya hivyo mkuu, ikiwezekana niue mimi”

Kitu ninacho jivunia kwa mkuu huyu wa kambi yetu ametokea kunipenda toka kipindi cha mwanzo nina ingia kwneye kambi hii na nimejikuta nikijua mambo mengi sana juu ya kikundi hichi kupitia yeye na yeye mwenyewe alisha wahi kukiri kwamba anatamani kuniona siku moja nina ishika nafasi yake.

“Ninaomba umchukue mjinga mwenzio na uondoke naye mbali kabisa na nchi hii, hakikisha huonekani kabisa katika bara hili”

“Asante muheshimiwa”

Mkuu akatarudisha bastola yake kiunoni, akatoa kitabu cha hundi pamoja na kalamu, akaandika kiasi cha pesa kisha akanikabidhi. Katka hundi hii mkuu ameniandikia kiasi cha dola laki mbili na nusu za Kimarekani na benk ninayo takiwa kuchukua kiasi hicho ipo hapa hapa Afghanistan.

“Randy kumbuka ninavyo fanya hivi nina vunja sheria ya kundi hili, maisha yangu hayana thamani kwa sasa, ila hakikisha unaishi kama mtu mwema, na usitumie uwezo wako vibaya umenielewa”

“Sawa mkuu, na ninashukuru sana”

“Binti kama hukufikiria kumpenda kijana wangu, hakikisha una mpenda, la sivyo…..haya”

Nesi Husna hakuweza kujibu chochote zaidi ya kuendelea kutetemeka mwili wake wote. Mkuu akatupisha mlangoni na tukatoka ndani humu huku nikiwa nimeshika mkono. Tukafika katika gari ambalo tulikuja nalo mimi na Hunsa, tukaingia na kuanza kundoka katika eneo hili la kambi, getini nikaruhusiwa pasipo wanajeshi wezangu kufahamu kwamba ndio sinto rudi tena katika kambi hii.

Safari ya kurudi mjini, ikatuchukua masaa mawili, nesi Husna akaniomba tuelekea kwa mjomba wake, tupate hifadhi ya usiku wa leo tu kisha kesho yake alfajiri na mapema nielekee benki nikachukue kiasi cha pesa ambacho nimepewa na mkuu wangu kisha tuondoke nchini hapa. Nikamkubalia mawazo yake, tukafika kwa mjomba wake ambaye ni mtu mwenye maisha ya kawaida tu. Akatukaribisha kwa ukarimu sana, nikapewa chumba chagu cha kulala huku nesi Husna naye akilala katika chumba kingine. Usiku kucha sikuweza kupata hata lepe la usingizi kwani moyoni mwangu bado nina chembe chembe za kumpenda Farida na jambo la yeye kuolewa pasipo kuzungumza chochote kwangu ni maumivu makubwa kwa kweli, mida nne usiku nafsi yangu ikakata kabisa kuendelea kukaa katika eneo hili, nikatoka chumbani kwangu na kwa bahati nzuri nikakutana na nesi Husna sebleni akiwa ameshika jagi la maji ya kunywa na kikombe.

“Vipi mbona ume amka”

“Nahitaji kufanya jambo”

“Jambo gani tena”

“Nahitaji tuondoke usiku huu, kuna sehemu twende na tukitoka hapa tunaondoka hapa Afghanistan”

Nesi Husna akanishangaa sana, huku akinitazama usoni mwangu.

“Tuna kwenda wapi?”

“Siwezi kukuambia kwa sasa ila je upo tayari kuondoka nami muda huu au haupo tayari kwa maana nikiondoka hapa sinto weza kurudi tena katika eneo hili”



Husna akanitazama kwa muda usoni mwangu, taratibu akashusha pumzi.

“Tuondoke pamoja, naogopa kukaa mbali na wewe Randy”

“Naomba uwaamshe wenyeji wako na uwaambie kwamba tunaondoka na si vizuri kuondoka pasipo kuwaaga”

“Sawa”

Nesi Husna akarudisha jagi la maji ndani ya friji, kisha moja kwa moja akaelekea katika chumba alicho lala mjomba wake. Akagonga kwa muda kidogo, mlango ukafunguliwa na akatoka mjomba wake.

“Husna mbona usiku, vipi kuna tatizo?”

“Hapana mjomba hakuna tatizo, ila sisi tunaondoka”

“Muda huu?”

“Ndio mjomba”

“Mbona ni usiku sana, hamsubiri kupambazuke?”

“Hapana mjomba wangu”

“Ngoja nina kuja”

Mzee huyoa karudi chumbani kwake na Husna akanifwata hapa nilipo. Mzee huyo akatoka akiwa ameongozana na mke wake. Mzee huyu mkononi mwake ameshika kibego kidogo cheusi.

“Natambua kwamba mupo kwenye harakati za kutoka nchi hii, hichi ni kiasi cha pesa ambacho munaweza kukitumia mukiwa katika kazi yenu”

“Tunashukuru sana mzee wangu”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na uso wenye furaha sana.

“Hii funguo mutachukua hiyo Toyota Hilux yangu. Gari lenu kwa jinsi lilivyo jaa matobo ya risasi. Mukisimamishwa na askari lazima watawaletea shida kidogo na isitoshe, Rany hapo umevaa mavazi ambayo ni ya waasi wa Al-quida hivyo ni tatizo jengine”

“Shukrani sana mzee wangu”

“Ngoja mara moja”

Mzee huyu akaingia ndani na baada ya muda akarudi na koti la polisi pamoja na nyota inayo muonyesha askari huyo ni cheo gani.

“Nakuomba umlinde binti yangu, na pale mutakapo fika katika sehemu ambayo mutakuwa muna amani nina kuomba muweze kunijulisha”

“Sawa sawa mzee wangu”

Husna akakumbatiana na mzee wake pamoja na mke wa mzee huyu, mimi nikawapa mikono kisha tukatoka ndani humu na kuingia katika gari ambalo mzee hutu amenipatia funguo. Nikaanza safari huku njiani sote tukiwa kimya.

“Randy tunakwenda wapi?”

“Makao makuu”

“Makao makuu ya wapi?”

“Al-quida”

“Randy kumbuka kule tumefanywa kupewa tu msamaha, au umedhamiria mimi niuwawe?”

Husna alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Randy kumbuka maisha yangu yote sasa hivi nimekukabidhi wewe, sina mtu wa kunitazama mwengine zaidi yako wewe na mjomba wangu. Wazazi wangu walisha uwawa katika shambulizi la bomu toka mimi nilipo kuwa na umri wa miaka kumi na moja. Tafadhali Randy nakuomba tusiende huko”

Husna alizungumza kwa upole na busara kubwa huku machozi yakimlenga lenge usoni mwake. Taratibu akanishika mkono wangu wa kulia.

“Randy nakuomba tafadhali, sihitaji kufa na kukiniacha hapa peke yangu lazima nitauwawa kwa maana watatambua ninafahamu ni wapi ilipo kambi yao”

Taratibu nikajikuta nikisimamisha gari pembezoni mwa barabara. Nikashusha pumzi taratibu huku moyoni mwangu nikijitahidi kumfuta Farida kwa nguvu zangu zote.

“Nakuombe Randy tafadhali, kama uliweza kurudi na kuyaokoa maisha yangu, basi nakuomba unisaidie katika hili tafadhali Randy”

Nikamtazama Husna usoni mwake kwa muda kisha taratibu nikamvuta karibu yangu, nikaanza kuzinyosha lipsi zake huku sote tukiwa tumeyafumba macho yetu. Taratibu Husna akaupitisha mkono wake wa kulia shinoni mwangu na kuanza tukazidi kunyonyana midomo yetu huku kila mmoja akiwa amezama kwenye dimbwi zito la mapenzi. Mlio wa king’ora cha gari la polisi linalo kuja nyuma yetu kidogo likatustua na kutufanya tuachiane, kwa kupitia kioo cha pembeni nikaona askari wawili wakishuka kwenye gari hilo huku wakiwa na bunduki mikononi mwao.

“Usitetemeke na wala usiwajibu chochote, nitazungumza nao sawa”

Nilimuambia Husna huku nikiiweka bastola yangu tayari pamoja na nyota ambayo ni nembo ya cheo kikubwa cha askari hapa nchini Afghanistani. Askari hao wakafika katika kioo cha upande wangu, nikafungua kioo hichi taratibu na kwa bahati nzuri hawana vyeo vikubwa.

“Habari yako kiongozi”

Walinisalimia mara baada ya kuona koti langu la askari nilio livaa.

“Salama vijana”

“Mkuu tunaomba kitambulisho”

Nikawaonyesha nyota hii niliyo pewa na mjomba wa Husna, kwa haraka wakasimama wima na kunipigia saluti.

“Samahani sana mkuu kwa kukusumbua”

“Musijali, vijana kazi nzuri na endeleeni kufanya kazi kwa umakini”

“Sawa sawa mkuu”

Askari hawa wakarudi kwenye gari lao, wakaanza kuondoka, wakanipigia honi huku mmoja akinipungia mkono na wakaondoka hapa na kumfanya Husna akaangua kicheko huku akinitazama.

“Mbona unacheka?”

“Nawacheka hao ulio waita vijana wako”

“Haahaa, usijali. Hivi una mfahamu mtu yoyote ambaye ata tufojia hati feki za kusafiria pamoja na visa ya kuinga nchini Tanzania”

“Nchini Tanzania ndio wapi!!?”

Husna alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Nikatabasamu taratibu huku nikwasha gari na kuondoka eneo hili.

“Randy nchini Tanzania ndio wapi?”

“Ni nchi ambayo inapatikana katika bara la Afrika”

“Afrika?”

“Ndio”

“Mmmmm yaani leo ndio nina isikia nchi hiyo”

“Hata mimi nimesha wahi kuisikia, ila nina sikia sifa ya nchi hiyo wana amani kubwa sana ndio maana nimependa tuende kuishi huko”

“Sawa, mimi nina kusikiliza wewe”

“Ila hujanijibu swali langu, ni wapi ambapo wanapo tengeneza hati hizo bandia za kusafiria?”

“Kuna mzee mmoja nilisha wahi kumtibu katika hospitali niliyo kuwa nina ifanyia kazi. Anafanya kazi hizo”

“Una pafahamu kwake?”

“Labda twende hospitalini pale naamini kumbukumbu zake ninaweza kuzipata kwenye computer kwa maana sifahamu ni wapi anapo ishi”

“Sawa sawa”

Hunsa akanielekea hadi tukafika katika hospitali anayo ifanyia kazi.

“Naomba unisubiri hapa”

Husna alizungumza huku akishuka kwenye gari, akaingia ndani na mimi nikabaki katika maegesho ya magari. Baada ya dakika kama kumi hivi nesi Husna akarudi huku akiwa ametabasamu. Akaingia ndani ya gari na kunikabidhi kikaratasi kidogo.

“Hiyo ni namba yake na mtaa ana ishi, nimezungumza naye muda huu na nimemuambia ni mimi ninaye hitaji huduma hiyo”

“Ahaa sawa mama”

Tukaondoka hospitalini hapa na majira ya saa kumi na mbili alfajiri tukafika katika mji anao ishi mzee huyu. Kutokana Husna ana uenyeji na eneo hili, hatukuweza kupotea na kufika nyumbani kwake.

“Una uhakika ndio hapo?”

“Ndio Randy ni nyumba namba sifuri, tisa, tisa”

“Sawa inabidi uwe wa kwanza kuingia ndani humu kwa maana pasipo kufanya hivyo anaweza kuhisi umekuja kumkamatisha”

“Ni kweli”

Husna akashuka kwenye gari na kuelekea katika nyumba hii, akagonga geti chakavu kiasi, baada ya muda geti hilo likafunguliwa na Hunsa akaingia ndani. Baada ya dakika kadhaa Husna akatoka kwenye geti hilo, akaniita kwa ishara, nikashuka kwenye gari na kulifunga vizuri huku nikiwa nimebeba kibegi chenye pesa na kuingia ndani.

“Ilibidi niweze kumuelewesha kwamba wewe ni mume wangu na tunahitaji kuondoka nchini hapa”

“Sawa”

Tukaingia ndani ya nyumba hii ambayo mpangilio wake wa vitu haupo vizuri. Tukaingia kwenye moja ya chumba na nikamkuta mzee huyu akiwa amekaa kwenye kiti huku meza yake ikiwa imejaa vitambulisho vya kila aina.

“Asalam alykum”

Mzee huyu alianza kunisalimia.

“Walyakum mslam”

“Mzee wangu kama nilivyo weza kukuambia kwamba huyu ni mume wangu na tunahitaji kuondoka nchini hapa haraka iwezekanavyo”

Mzee huyu akanitazama kuanzia juu hadi chini huku akiiweka miwani yake vizuri usoni mwake.

“Kwa nini umeondoka katika kundi la Al-quida?”

Swali la mzee huyu likanistua sana na kujikuta mapigo ya moyo yakianza kunienda kasi. Husna akanitazama usoni mwangu.

“Nisiwe muongo kwako mzee wangu, sababu ya mimi kuondoka katika kikundi hicho ni kutokana na Husna, ni mwanamke ambaye aliweza kunisaidia kwa mambo mengi hivyo sikuhitaji kuona wana muua ikiwa nina uwezo wa kufanya jambo kwa ajili yake.

“Husna anacho kizungumza Randy ni kweli?”

“Ndio mzee wangu siwezi kukudanganya kwa chochote, na mimi nimeamua kuwa naye na kwenda naye popote ninapo hitaji kwenda”

Mzee huyu akanitazama machoni mwangu, kisha akamtazama Husna machoni mwake, taratibu akashusha pumzi kisha akatuonyesha viti viwili tukae.

“Randy una fahamu ni kitu gani ambacho kina endelea katika kundi lako la Al-quida?”

“Sasa hivi?”

“Ndio”

“Hapana mzee wangu”

Mzee huyu akawasha tv yake ndogo iliyomo ndani humu. Habari niliyo iona kwenye tv hii ikanistua sana na kujikuta nikisimama huku macho yakiwa yamenitoka. Kwani kambi ambayo nilikuwa ninaishi imeshambuliwa kwa ndege za kivita za Marekani na kuepelekea mauaji ya wanajeshi wote katika kambi hiyo.

“Imetokea lini?”

“Jana usiku”

Nikamtazama Husna kwa muda kidogo kisha nikaitazama tv hiyo.

“Al-quida wana kutafuta kwa udi na uvumba wewe na huyo mchumba wako Husna. Nikiwa kama miongoni mwa watoa habari zao za siri, nimeweza kutumiwa ujumbe huu”

Mzee huyo alizungumza huku akinigeuzia laptop yake na kunionyesha ujumbe wa kutoa taarifa zangu na Husna popote tutakapo onekana huku ujumbe huo ukiwa umeambatanishwa na picha zetu.

“Laiti ingekuwa si wema wa huyu binti ningeweza kutoa taarifa kwa wakuu wa Al-quida.

“Sasa kwa nini wana tutafuta sisi?”

“Wanahisi huyo msichana ni mpelelezi kutoka nchini Marekani”

“Husna…..”

“Randy mimi sijawahi kuwa mpelelezi wala askari wa kitengo chochote, kazi yangu mimi ni daktari wa mifupa tu”

Husna alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka.

“Anacho kizungumza Husna ni ukweli, yeye ni daktari kwa maana nimetafuta data zake ili niweze kujua yupo kwenye kikosi gani, ila sijweza kupata zaidi ya kuwa ni daktari”

Mzee huyu alizungungumza ili kuniweka sawa, nisiweze kumuwazia Husna kwamba yeye ni mpepelezi wa nchi ya Marekani.

“Mzee wangu hati zetu zinaweza kuchukua muda gani ili tuweze kuondoka nchini hapa?”

“Saa moja ama saa moja na nusu”

“Sawa nakuomba uweze kutusaidia mzee wangu”

Mzee wangu akatandika kitambaa cha rangi ya bluu ukutani, kisha akaanza kunipiga picha mimi huku nikiwa nimebaki na tisheti nyeusi tu. Akafwatia Husna naye akapigwa picha, kazi ya kuanza kutengeneza hati za kusafiria zikaanza huku mara kwa mara mzee huyu akiminya minya laptop yake.

“Randy”

“Naam”

“Nina ogopa mpenzi wangu”

“Usijali kila kitu kitakwenda sawa”

“Kweli”

“Ndio”

Taa nyekundu uliyopo kwenye moja ya hichi chumba ikaanza kuwaka na kutufanya sote tushangae huku tukimtazama mzee huyu.

“Jificheni haraka sana, Al-quida wamesha fika hapa nyumbani kwangu”

Maneno ya mzee huyu yakanifanya nisimame kwa haraka huku nikimshika Husna mkono wa kulia na mkono wangu wa kulia nao nikiwa nimeshika bastola yangu ili hata nikukutana na hatari ya wanajeshi wezangu wa Al-quida niweze kuwashambulia kwani wakiniwahi wao ni lazima wataniua mimi.



“Ingieni hapa”

Mzee huyu alizungumza huku akifunua zulia alilo litandika kwenye sakafu, akafungua mlano wa chuma ambao una ngazi kuelekea chini, kwa haraka tukaanza kushuka huku kisha mzee huyu akafunika kwa juu. Tukajibanza eneo la chini katika sehemu hii ambalo lina giza nene na hatuwezi kupiga hatua kwenda mbele kwani hatujui ndani ya eneo hili kuna kitu gani. Tukaanza kusikia mazunugmza ambayo kidogo yakanistua kwani mzungumzaji ninaifahamu vizuru sauti yake kwani ni Farida mwanamke niliye achana naye kilazima.

“Unataka kutuambia kwamba Randy hajafika kabisa katika eneo hili?”

“Ndio mkuu sijawahi kuenenda kinyume na mipango yenu wala taratibu zenu. Niamini mkuu wangu”

“Mkuu ona”

Sauti nyingine ya kiume ilisikika.

“Kwa nini umenidanganya, hizi picha ulizo zipiga kwenye kamera yako, zimepigwa kama dakika saba zilizo pita. Unalipi la kuzungumza, kwa maana hawa watu ndio tunao watafuta?”

Tukasikia ukimya wa mzee huyu, nikaamini kabisa atakuwa amebananishwa na maswali na hana uwezo wa kujibu.

“Hakikisheni munawatafuta eneo zima. Akionekana huyo malaya wake mueni na Randy mleteni mikononi mwangu akiwa hai na nitamuua mimi mwenyewe”

Husna akanikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kutetemeka mwili mzima.

“Huna haja ya kuendelea kuwepo duniani mzee”

Tukasikia milio ya risasi mbili kisha kishindo kizoto, nikashusha pumzi yangu taratibu huku nikiwa nimejawa na hasira kali kwani siamini kama Farida amedhamiria kunisaka mimi kama adui yake. Tukaendelea kusikia vishindo vishondo vya watu, baada ya muda kidogo nikamwagikwa na matone kwenye shingo yangu, nikajigusa kidogo.

“Shiti…..”

“Nini?”

“Wanamwaga mafuta, wanataka kuichoma hii nyumba”

“Ohoo Mungu wangu, tutafanya nini Randy”

“Shiii”

Nilizungumza huku nikimziba Farida mdomo wake. Nikatazama juu kidogo ambapo kidogo kuna mwanga mwanga.

“Simama hapa kwenye ngazi”

“Unataka kwenda wapi Randy”

“Nisubirie hapa”

Nilizungumza huku nikimuachia Husna, nikaanza kupapasa ukutani na kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuona swichi ukutani. Nikaiwasha na taa yenye mwanga hafifu ikaawaka, eneo la humu ndani linaytumika kama stoo kwani kuna maboski mengi sana ambayo sifahamu ndani yana kitu gani. Nikalisogelea boksi moja na nikalifungua, macho yangu yakapatwa na mshangao mkubwa sana, kwani boksi hili limejaa vibunda vya dola mia mimi za Kimarekani

“Husna”

“Bee”

“Njoo uone”

Husna kwa haraka akasogea katika eneo hili, naye nikamuona akishangaa sana, nikafunua boksi jengine nalo nikakuta likiwa na pesa nyingi sana. Wazo la kuuwawa likanipotea kabisa na akili yangu yote nikaanza kuielekezea kwenye haya maboksi. Kwa haraka nikaanza kuyafunua maboksi haya mengine nikayakuna na vipande vikubwa vya madini aina ya dhahabu.

“Huyu mzee ni tajiri”

“Kweli Randy”

Gafla taa ya humu ndani ikazima na kunifanya nikimbilie kwenye moja ya meza na humu ndani na kutoa tochi na kuiwasha, fukuto kubwa likaanza kutawala ndani humu, ambalo kwa haraka haraka nikaamini kwamba ni lazima watakuwa wamesha ichoma nyumba hii. Harufu ya moshi ikaanza kuingia humu ndani ya hichi chumba.

“Randy tutatokaje humu mpenzi wangu”

“Ngoja nyumba iungue, jizibe pua moshi usije ukakupalia sana”

“Sawa”

“Njoo hapa”

Husna akanisogelea, nikamkumbatia na kumlaza kifuani mwangu huku mawazo yangu yakianza kufikiria ni jinsi gani ambavyo tunaweza kutoka na hizi pesa humu ndani na nina imani mara baada ya kutoka na hizi pesa na tukafanikiwa kuondoka nchini hapa, basi tutakuwa ni matajiri wakubwa sana na hata mama yangu nina imani nitaanza kushindana naye kwenye swala zima la kibiashara. Fukuto lililo ambatana na moshi mwingi lilendelea kutawala ndani ya chumba hichi na kutufanya tuanze kukosa hewa safi ya oksijeni.

“Randy najisikia vibaya”

Husna alizungumza huku jasho jingi likimwagika usoni mwake. Hata mimi mwenyewe jasho jingi likazidi kunimwagika.

‘Lazima nifanye jambo’

Nilizungumza huku nikianza kumulika mulika ndani ya chumba hichi.

“Naomba ushike hii tochi”

“Unataka kufanya nini?”

“Ishike na unimulikie kila sehemu ninayo kwenda”

Husna akaishika tochi hii na kuanza kumulika kila sehemu ninayo elekea. Nikaanza kuyakusanya maboski haya mazito na makubwa katika sehemu moja. Nilipo hakikisha kwaba nimeyapanga sehemu moja nikaanza kuugonga gonga ukuta hu hatua hadi hatua. Nikafika sehemu na mlio wa kugonga ukuta huu ukabadilika, kwa haraka nikatambua kwamba sehemu nii ina mlango wa kutokea ila umejengwa kama ukuta.

“Husna kuna mlango katika hili eneo”

“Kweli?”

“Ndio njoo usikie”

Husna akanifwata hapa nilipo, nikagonga eneo hilo kwa nguvu huku tukitofautisha sauti inayo toka katika sehemu hii ninayo igonga na sehemu ya pembeni ya huu ukuta ambayo haina mlango.

“Sasa tuna fanyaje?”

“Lazima kutakuwa na jinsi ya kufungua hili eneo”

“Sasa tutafunguaje”

“Naomba tochi”

Nikaichukua tochi na kuisogela meza hii ambayo imejaa makorokoro mengi. Nikachukua kitabu kidogo, na kuanza kukifungua, nikaanza kutabasamu kidogo kwani kitabu hichi kina ramani ya kutoka ndani ya hichi chumba. Nikasoma maelezo ya jinsi ya kutoka humu ndani na nikayaelewa vizuri sana. Kwa haraka nikasogea sehemu ulipo mlango huu.

“Umepata nini?”

“Shiii”

Nikaanza kuugonga mara tatu kwa haraka eneo la katikati na taratibu mlango huu ukaanza kufunguka na kutufanya tujawe na furaha kubwa sana. Husna akanikumbatia kwa nguvu huku akiwa amejawa na shahuku kubwa sana ya kutoka katika eneo hili. Nikaanza kumulika katika eneo ambapo mlango huu umefunguka, nikaona barabara moja ndefu iliyopo chini ya hii ardhi huku kukiwa na gari mbili moja ni Toyota Alteza huku gari nyengine ni Hammer.

“Tunaondoka mpenzi wangu”

Nilijikuta nikizungumza huku nikizinyonya lipsi za Husna kwa furaha sana. Nikalisogelea gari hili aina ya Hummer, nikachungulia ndani, nikakifungua kitabu hichi na kuanza kusoma kwa maana eneo hili lina maelekezo mengi. Nikagundua fungua ya gari hizi zimefichwa kwa chini katika tairi la upande wa kulia. Nikalala chini kwa haraka na kutazama sehemu hiyo ambayo imewekewa maelekezo kwenye hichi kitabu. Nikaiona fungua kwa haraka nikaichukua kisha nikaismama na kuufungua mlango. Gari hili kidogo lina utofauti na magari ambayo nimesha wahi kuyatumia kwenye maisha yangu.

Gari hili ukisha ingiza fungu, tv ndogo iliyopo pembeni mwa siti ya dereva inahitaji mtu uingize namba ya siri ili gari liweze kuwaka.

“Mbona huwashi gari?”

“Linahitaji kuingiza namba za siri ili ngoja kwanza”

Nilizungumza huku nikianza kukisoma kitabu hichi kidogo kwa umakini sana. Kila kitu kilicho andikwa ndani ya hichi kitabu kinahitaji mtu utilize akii yako ili uweze kufahamu ni kitu gani unapaswa kufanya kwani hakuna neno lililo andikwa kwa uwazi.

“TANRUQ”

Neno hili ndio linaonyesha ninatakiwa kuingizi ili gari liweze kuwaka. Ila cha kushangaza katika tv hii ndogo ambayo ni ya kugusa kwa kidole kwenye kioo chake haina sehemu ya kuingiza hefuri na kilichopo ni namba tu.

“Hunsa kuna tatizo”

“Tatizo gani mpenzi?”

“Hili neo ndio linatakiwa kuingizwa hapa, ila sioni kwa kuingiza maneno. Husna akakichukua kitabu hichi na kutazama tv hii ndogo.

“Hahaaa huyu mzee ana akili sana”

“Kwa nini?”

“Hapa kila herufi ya neno moja kwenye mpangilio wa alfabeti si ina namba yake. Kama A ni namba moja, T namba ishirini”

“Ahaa umejuaje?”

“Nimejua kwa maana kama hakuna sehemu ya kuingiza maandishi ujue ni lazima ujue kuzinyambulishia hizi herufi na ndio utapata namba ya siri”

Nikamtazama Husna usoni mwake huku nikitabasamu. Husna akashuka kwenye gari na kuelekea kwenye meza yeneye makoro koro mengi, akachukua kalamu na kuanza kuzipangilia namba herufi hizi na namba zake.

“Ngoja nianze kuingiza haya maboksi kwenye gari”

“Sawa mpenzi wangu”

Nikanza kubeba maboksi haya ambayo yapo kumi na kuyaingiza ndani ya gari, kwa bahati nzuri maboksi yote yakafanikiwa kuingia yote kwani nimeyaweka hadi katika siti ya nyuma.

“Nimeipata”

Husna alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana. Akaingiza namba hizo kwenye gari hili na gari likawaka.

“Tumefanikiwa”

Husna alizungumza huku akinikumbatia kwa furaha. Tukanyanyana midomo yetu kwa furaha, kisha taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili huku nikiwa nimewasha taa za gari hili, ili niweze kuona kule ninapo elekea.

“Kunja kulia”

Husna aliniambia huku akiwa anakisoma kitabu hichi

“Kulia?”

“Ndio, hivi ndivyo ramani inavyo hitaji”

Husna alizungumza huku akinionyesha ramani ilivyo chorwa chorwa kwenye kitabu hichi, sehemu ambayo tumeifikia ina barabara mbili za kupita. Tukazidi kusonga mbele kwani baraba bara hii imechongwa vizuri japo ipo chini ya ardhi.

“Huyu mzee ni nani?”

“Hata mimi sijui mume wangu kwa maana si kwa ubunifu huu ambao ameufanya”

“Ni kweli, unajua kwa akili za kawaida huwezi kufahamu kama chini ya ardhi hii kuna barabara na tena sijui ameichongaje?”

“Unajua katika hii nchi yetu, kutokana na vita za mara kwa mara watu wameamua kutengeneza mahandaki yao na njia zao za siri kama hizi na inavyo onyesha mzee huyu alikuwa ni tajiri mkubwa sana ndio maana mali yake aliamua kuiweka chini ya ardhi na kwa juu ukiitazama nyumba yake unaiona imechakaa wala haitamaniki kwa kweli”

“Ni kweli mke wangu, ila sijui kwa nini watu wanakuwa na roho mbaya, mzee wa watu kwa nini wameumuua?”

“Kuna sauti ya mwanamke niliisikia una mfahamu?”

Nikamtazama Husna usoni mwake, huku nikifikiria ni kitu gani niweze kumjibu.

“Yaa nina mfahamu”

“Ni nani?”

“Nahitaji kuwa muwazi kwako na sihitaji kukuficha siri ya aina yoyote kuanzia hivi sasa na wewe na kuomba uwe hivyo Husna sawa”

“Sawa”

“Anaitwa Farida, ni mjukuu wa Osama Bin Laden na alikuwa ni mpenzi wangu niliye toka naye barania Afrika na kuja naye huku nchini Afghanistan. Baba yake hakunipenda niwe na mwanaye hivyo walinitupa nje ya makao makuu yao na kunipeleka kwenye moja ya kikosi chao kile kilicho vamikwa kule.”

“Katika kile kikosi kuna mambo mengi mabaya na hata mtu akifa hakuna ambaye ana jali. Walinipa kazi moja ambayo kwa uhakika kwa kiwango ambacho nilikuwa nimefikia, sikutakiwa kuifanya. Kazi ambayo iliwaua wezangu wanne na mimi pekee ndio niliye salia”

“Kazi gani?”

“Ya kumteka makamu wa raisi wa nchi ya Marekani, naamini kuanzia pale ndipo mimi na wewe tulikutana. Nimekuingiza katika mfumo ambao sio mzuri kabisa kwa maisha yako. Mfumo ambao maisha yako sasa hivi yana windwa kama vile ulivyo sikia. Samahani sana kwa hilo Husna”

Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimtazama Husna usoni mwake. Husna taratibu akanishika mkono wangu wa kulia na kuanza kuuminya minya taratibu.

“Usijali Randy, mimi ni wako na kwa bahati nzuri umeweza kupata mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa akili kwa lugha nyingine mimi ni Genius”

“Waoooo”

“Ndio maana niliweza kugundua kitu kilicho fichwa kwa maandishi humu ndani ya hichi kitabu”

Taratibu nikajikuta nikipunguza mwendo wa gari hili na kulisimamisha kabisa kwani sehemu ambayo tumeifikia kina korongo moja kubwa sana ambalo kwa mbele ndipo kuna barabara na kwa kutumia gari hili hatuta weza kuipita sehemu hii.


Nikashuka kwenye gari huku nikiichomoa bastola yangu kiunoni. Hunsa naye akashuka huku akionekana kushangazwa sana na hili bonde.

“Tunafanyeje mpenzi wangu?”

“Ngoja niangalie hichi kitabu”

Husna alizungumza huku akiingia ndani ya gari, akawasha taa ya ndani ya gari na kuanza kusoma kwa umakini sana. Husna akashuka kwa haraka kwenye gari na kuanza kutembea kuelekea kwenye ukingo wa bonde hili.

“Umegundua nini?”

“Ngoja”

Husna akachungulia kwenye bonde hili refu kwenda chini.

“Kuna sehemu ina batani, ambayo ukiiminya kuna daraja lipanda kutoka juu hadi chini na deraja hilo hudumu kwa dakika moja na sekunde thelathini, kabla halijaanza kuridi chini”

“Hajaandika ni wapi ilipo batani hiyo?”

“Hajaandika, ila kuna sehemu ina batani, tuitafute”

Tukaanza kazi ya kuitafuta batani hiyo kwa umakini sana. Tukazidi kuitafuta ila hatukuweza kuipata kabisa jambo lililo zidi kutupa wasiwasi mkubwa sana.

“Husna hembu soma vizuri basi ili tuweze kufahamu ni wapi ilipo hiyo batani”

“Maelezo yanaonyesha kwamba kuna batani sehemu”

Nikaegemea gari huku nikiwa nimechoka sana. Husna akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akanisogela na kunishika kiuno changu huku akiwa amesimama mbele yangu.

“Randy, usikate tamaa ni lazima tuondoke hapa mpenzi wangu. Kumbuka kwamba tume beba utajiri mkubwa kwenye hilo gari, itatushangaza tukikata tamaa mpenzi wangu”

Maneno ya Hunsa taratibu yakaanza kuyarudisha matumaini yangu upya.

“Nakutegemea mpenzi wangu”

“Hembu hicho kitabu”

Husna akanikabidhi kitabu hichi nikayasoma melezo yanayo husiana na eneo hili kwa umakini. Taratibu nikatabasamu huku nikitazama juu katika hii njia.

“Umegundua nini”

“Ingia kwenye gari”

“Ehee”

“Ndio”

Nilizungumza huku nikifungua mlango na Husna akaingia mlango wa upande wa pili. Kati rufu ya juu katika hili gari ndipo ilupo batani ya kufungulia hili daraja na sin je ya hili eneo.

“Batani hii hapa”

Nilizungumza huku nikimuonyesha Hunsa batani hiyo, akashusha pumzi huku akitanasamu. Nikaiminya batani hiyo na kweli, tukaanza kusikia mingurumo ya vyuma vikisagana, baada ya dakika moja, daraja hilo likawafiti katika barabara hii. Nikawasha gari na tukapita hadi upende wa pili. Nikasimamisha gari na kushuka kulishuhudia daraja hilo, na kweli lilianza kushuka chini dani ya dakika moja na nusu.

“Huyu mzee ana akili sana”

Nilizungumza huku nikirudi kwenye gari. Tukaendelea na safari yetu huku Husna akinisomea ramani ya wapi nipite.

“Hii barabara itatupeleka hadi katika nchi ya Iran”

“Ni kama kilomita ngapi?”

“Sifahamu, ila kutokana tupo chini ya ardhi wewe twende tu tutakapo fika huko tutajua mbele ya safari”

Nikazidi kuongeza mwendo wa kasi wa hili gari huku nikiwa nimewasha taa zote ili niweze kuona mbele kwani hakuna mwanga wowote katika hii barabara zaidi ya giza tu. Ikatuchukua masaa nane hadi kutoka katika hii barabara ya chini ya ardhi na kutokea kwenye moja ya msitu. Kabla ya kusonga mbele, nikashuka ili kuangalia usalama wa huu msitu, nisije nikasonga mbele kumbe tupo katika kambi ya jeshi. Nikatembea kwa hatua kama ishirini kutoka nilipo liacha gari na Husna. Nilipo hakikisha kuna usalama wa kutosha katika huu msitu, kwa ishara nikamuomba Hunsa kuwasha gari na kuja hapa nilipo simama.

“Umeona nini?”

Husna alizungumza huku akinifungulia mlango akahamia kwenye siti yake na mimi nikaka katika siti ya dereva.

“Hakuna chochote cha kutisha”

“Hapa ni Iran mpenzi wangu”

“Lugha ya hapa si una ifahamu mke wangu?”

“Ndio”

“Poa poa mke wangu”

“Hivi unajua tunaweza kwenda hadi barani Afrika na hili gari?”

“Mmmmm itatuchukua miezi mingi sana kufika?”

“Ndio ila ni bora kutumia njia hiyo kuliko tukatumia ndege kwa maana hizi pesa na vipande vya dhahabu hatufahamu huyu mzee amevipata kwa njia gani. Kama amevipata katika njia ya uharamia, ina maana kuna mikono ya watu wengi sana watakuwa wana utafuta mzigo huu”

“Ila ni kweli ulisemalo mpenzi wnagu”

“Yaa, katika hii nchi tunatakiwa tukae kama siku mbili, huku tukitafuta vibali vyote vya kusafiria na kupita katika mipaka tofauti tofauti na inabidi tuweze kuitengeneza namba za gari hili kwa kila nchi, ili tukiingia kwenye nchi husika basi tusiweze kupata shida”

“Una onaje tukakodisha ndege binafsi”

“Itupeleke wapi?”

“Tanzania”

“Mmmm, hiyo nchi una fahamu usalama wake na ukaguzi wake katika eneo la Airport?”

“Siifahamu, ila sikuhizi dunia imekuwa kubwa mke wangu. Tutakaa tutaisoma nchi hiyo kupitia mitandao na tukifahamu kama ina shida katika swala la ukaguzi basi tunaweza chukua hatu nyingine. Ila kuendesha gari kwa kutoka bara hili la Asia kwanza ni ngumu, kuna nchi hapo mbele kama Iraq. Usalama wake nina amani hata wewe una ufahamu, hatuwezi kuimaliza hiyo nchi pasipo kusikia milio ya risasi”

“Sawa mume wangu, ila ni ushauri ambao nilikupatia”

“Usijali, ngoja tuanze na mpango huu kwangza ukifeli basi tunahamia mpango mwengine”

Tukafanikiwa kuingia kwenye mji mmoja ambao una nyumba chache kidogo. Tukasimama kwenye moja ya sheli, tukaongeza mafuta ya gari kisha tukaendelea na safari. Husna akaanza kupiga miyayo huku akinitazama usoni mwangu.

“Ni njaa au uchovu?”

“Vyote vyote mpenzi wangu.”

“Usijali tukiona mgahawa tutasimama na kupata chakula”

“Yaa ila pole kwa kuendesha kwa maana mmm ni masaa mengi una endesha tu gari”

“Yaani hapa nilipo mikono imechoka na ina uma”

“Pole mpenzi wangu”

“Asante, hivi hii inchi nayo kumbe ni jangwa sana?”

“Ndio, yaani hizi nchi, kuanzia Afghanistan, Iran, Iraq, Pakistani zote ni jangwa”

“Duuu”

Nikaona kibao kinacho onyesha baada ya kilomita mbili mbele kuna Motel upande wa kulia mwa barabara. Baada ya kama dakika ishirini hivi tukafika katika motel hiyo ambayo nje kuna malori makubwa ya mizigo.

“Ngoja nishuke mimi kwenye gari”

“Kwa nini?”

“Jinsi ulivyo vaa, unaweza kusababisha matatizo”

Nikajitazama nguo za jeshi nilizo zivaa na nikajikuta nikimkubalia Husna kushuka kwenye gari, akafungua moja ya boksi na kuchukua kibunda kimoja cha pesa, kisha akaelekea ndani ya mgahawa huu ambao umejengwa kwa vioo na watu walipo ndani una waona vizuri. Nikazitazama hivi pesa na kujikuta nikifarijika sana kwenye maisha yangu kwani umasikini ndio kwa heri na nitahakikisha kwamba ninafanya mashindano ya kibiashara na mama ili aweze kufahamu kwamba mwanaye ni jasiri na nina uwezo wa kufanikiwa kama jinsi yeye alivyo fanikiwa.

‘DANY’

Akili yangu ilivyo likumbuka jina la Dany moyo wangu ukanistuka sana, kwani huyu ni adui yangu mwengine. Adui ambaye ameniuliza baba yangu, ambaye alikuwa raisi wa Marekani.

“Hili swala ni lazima nilifwatilie kwa umakini sana”

Nilizungumza mimi mwenyewe huku nikimtazama Husna jinsi anavyo toke kwenye mgahawa huo huku akiwa ameshika fuko kubwa lililo jaa vyakula na vinywaji. Akaingia ndani ya gari, akatoa chupa mbili za juisi ya maembe akanikabidhi ya kwangu.

“Chakula ulicho nunua kitatutosha kuendelea na safari?”

“Kitatutosha mpenzi wanga na nimeambia ni masaa kama kumi na mbili hadi kufika katika mji wa Yazd”

“Kwani hapa tulipo ni mji gani?”

“Hapa ni Birjand”

“Ahaaa sawa sawa”

“Umapajuaje?”

“Nimeuliza mume wangu”

“Sasa hivi ni jioni, giza litatutukutia njiani, unaonaje tukatafuta sehemu tukalala ili kesho tuendelee na safari, si unajua mimi sio mwenyeji wa hii barabara nisije nikakupindua bure”

“Sawa mpenzi wangu, tusonge mbele, tukipata sehemu ya kupumzika basi tutapumzisha miili yetu”

Tukaondoka eneo hili huku Husna akitumia muda mwingi katika kula huku mara kwa mara akinilisha na mimi. Hadi tunakuta mji mwengine ambao una hoteli hoteli nyingi, imetuchukua masaa mawaili na nusu. Tukaelekea kwenye moja ya hoteli nzuri ambayo kwa haraka haraka ina usalama wa kutosha. Husna akashuka na kwenda kuulizia vyumba, kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata chumba cha gharama.

“Siwezi kushuka kwenye gari nikiwa na nguo hizi”

“Sasa utafanyaje?”

“Muulize muhuduma kama kuna sehemu ina duka la nguo, tuende ukaninunulie nguo ili hata nikishuka kwenye gari hakuna mtu wa kunitilia mashaka”

“Sawa”

Husna akafanya kama nilivyo muagiza, alipo pata jibu kamili akarudi.

“Maduka hayapo mbali kidogo na hapo mbele”

Tukaondoka na kufika katika moja ya duka. Hunsa akashuka na kununua nguo zangu na zake kisha akarudi kwenye gari. Nikabadilisha nguo hizi humu humu ndani ya gari, kisha tukarudi hotelini.

“Samahani gari langu linaweza kupata ulinzi wa kutosha?”

Nilimuuliza mmoja wa walinzi wa hii hoteli.

“Ndio mkuu”

“Naomba basi iwe hivyo”

Uzuri wa hili gari vioo vyake vyake vya pembeni na cha nyuma ni vyeusi na mtu akiwa nje hawezi kuona kilichopo ndani, ila mtu wa ndani anaweza kuona kile kilichopo nje ya gari. Tukaingia kwenye lifti na moja kwa moja tukaelekea kwenye chumba chetu. Nikakikagua chumba hichi kuanzia kitandani hadi bafuni, nilipo hakikisha kwamba usalama upo, ndipo nikaiweka bastola yangu mezani.

Nikamsogelea Husna sehemu alipo, taratibu nikamshika kiuno chake huku tukitazamana usoni. Taratibu tukaanza kunyonyana dimi zetu huki kila mmoja akiwa anahema mihemo mizito ya kimapenzi.

“Naomba nikaoge”

Husana alizungumza huku nikiyasikia kabisa jinsi mapigo yake ya moyo yanavyo kwenda kasi.

“Sawa, ila mbona una wasiwasi mwingi sana”

“Hamna”

“Kweli”

“Ndio Randy”

Nikamuachia na akaanza kutembea kwa haraka hadi bafuni, huku akionekana ni mtu aliye jawa na woga mwingi sana.

‘Ana jambo gani analo lificha huyu?’

Nilijiuliza kimoyo moyo huku nami nikiwa nimesha anza kumtilia mashaka Husna. Nikaanza kusikia maji jinsi yanavyo miminika bafuni, nikanyata hadi mlangoni mwa bafu na kutega sikio ili niweze kusikiliza ni kitu gani kinacho endelea ndani ya bafu. Ila sikuweza kusikia kitu chochote zaidi ya maji hayo kumwagika. Nikavua shati nililo livaa na kubaki kifua wazi. Nami harufu ya kijasho cha kwapani, imenitawala kwani nina siku kama nne hivi sijaoga.

Nikatoa magazine ya bastola yangu na kuiweka ndani ya mfuko wa suruali. Niaitoa risasiambayoipo kwenye chamber tayari kwa kutoka na nikaiweka kwenye mfuko wangu mwengine kisha bastola nikairudisha mezani. Nikavua suruali yangu hii na kubaki kama nilivyo zaliwa, nikatembea kwa mwendo wa taratibu hadi kwenye bafu hili na kugonga kidogo.

“Husna, Husna”

“Bee”

“Ninaweza kuingia?”

“Namaliza mpenzi wangu”

Baada ya dakika mbili Husna akatoka akiwa amejifunga taulo mwilini mwake. Akatabasamu huku akininibusu mdomoni mwangu.

“Nenda kisha uje kitandani mpenzi wangu”

Husna alizungumza kwa sauti nyororo na iliyo jaa mahaba, nikamsindikiza kwa macho jinsi anavyo elekea kitandani, nikaingia bafuni kwa haraka na kuanza kuoga huku jogoo wangu akiwa tayari amesha simama na kunesa nesa kisawa sawa. Nirudia kuoga kama mara tatu ili kumaliza nongo zote zilizomo mwilini mwangu. Nikajitazama kwenye kioo cha humu bafuni, kisha nikatoka huku nikiwa na hamu na bashasha ya kupata penzi la Husna. Galfa nikamuona Husna akiwa amesimama mita chache kutoka mlangoni huku akiwa ameshika bastola yangu na amevalia suruali nyeusi, tisheti nyeusi na koti jeusi, huku mkononi mwake akiwa ameishika fungua ya gari ambayo nilikuwa nimeiweka mezani.

“Simama hapo hapo kabla sijakufumua ubongo wako. Unahisi mimi ni mwanamke wa kuolewa na muafrika na ulihisi nitaikimbia nchi yangu kwa ajili ya penzi lako. Sahau, pesa madini na kila kitu kuanzia hivi sasa ni mali yangu”

Husna alizungumza kwa kujiamini sana huku akiendelea kuninyooshea bastola, nikatazama suruali yangu na nikaiona ikiwa ipo vile vile kama nilivyo iacha na nina uhakika wa asilimia mia moja, hajaichunguza bastola hiyo kabla ya kuitumia.



“Husna kwa nini…….”

Nilimuuliza Husna kwa sauti ya upole sana huku tukitazamana usoni.

“Kaaa kimya mpumbavu wewe”

Husna alizungumza huku akihangaika na kitasa cha mlangoni, nikajaribu kumfwata ila tayari akawafanikiwa kutoka chumbani humu. Kwa haraka nikakimbilia suruali yangu na kuivaa. Nikaingiza mkono mfukoni na kukuta magazine ya bastola yangu pamoja na risasi moja. Nikaanza kukimbia kuelekea sehemu yenye lifti, nikakuta lifti zote mbili za gorofa hili zikitumika kuelekea chini.

Nikaanza kukimbia kuelekea kwenye ngazi na kuanza kushuka kwa kasi huku nikiwa nimepandwa na jazba kubwa sana kwa maana mwanamke huyu kwa wema wote nilio mfanyia ikiwemo kuhatarisha maisha yangu pamoja kuisababishia kambi yangu matatizo makubwa ya kushwambuliwa, haya ndio malipo yake anayo amua kunifanyia.

Nikafanikiwa kufika nchini na kukuta gari tulilo kuja nalo ndio linaondoka getini kwa kasi kubwa sana. Nikajaribu kulikimbiza ila sikuweza kufanikiwa na nikashuhudia jinsi Hunsa anavyo tokemea na pesa pamoja na madini yote ambayo tayari nilisha yapangia mahesabu kwamba yananifanya niwe tajiri mkubwa na mfanya biashara ambaye hakika nileta ushindani wa kibiashara kwa mama yangu.

Kwa hasira niliyo nayo nikayashuhudia machozi yangu yakinimwagika machoni mwangu na kunichirizika kwenye mashavu yangu.

“Hei kuna tatizo lolote?”

Mlinzi wa hapa getini aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio ninawezaje kupata picha za lile gari kwa kupitia CCTV camera zilizopo hapa?”

Nilizungumza huku nikitazama kamera zilizopo kwenye eneo hili la magesho ya mgari pamoja na getini.

“Kwa nini unahitaji?”

“Gari langu limeibiwa na kuna mizigo yangu muhimu sana ndani ya lile gari”

“Inabidi tuwasiliane na polisi ili waweze kulisaka”

Nikajifikiria kwa sekunde tano kisha nikatingisha kichwa ikiwa ni ishara ya kukataa kuwahusisha askari kwenye hili swala kwa maana wakimkamata Husna hivyo pesa na vipande vya dhahabu vyote vitawekwa chini ya uangalizi wa serikali hii na inaweza ikawa ndio mwisho wa kuvipata kwa maana hata sisi wenyewe hatuna hati miliki ya vitu hiyo na hata gari lenyewe.

“Kwa nini sasa?”

“Ni mke wangu ndio amefanya hivyo, ila nisaidie kupata picha za gari hili”

“Sawa, ila inabidi niwasiliane na uongozi wa hoteli hii?”

“Ukiwasiliana nao ndio mwanzo wa kuhusisha polisi na mimi sihitaji mambo yaende hivyo, sawa kiongozi”

“Sawa”

“Najua ni wapi nitampata mke wangu, wewe naomba unitolee hiyo picha ninayo kuomba”

Askari huyu akaka kwenye kiti chake katika kibanda hichi cha hapa getini. Akaanza kuminya minya batani za computer, baada ya dakika moja hivi, picha hiyo ikatoka kwenye mashine maalumu ya printer. Akanikabidhi picha hii huku akinitazama usoni mwangu.

“Naomba iwe siri yako usimueleze mtu juu ya hili tukio”

“Sawa”

Nikarudi chumbani, nikavaa tisheti yangu pamoja na viatu kwa maana nilitoka peku peku pasipi kuwa na hata soksi mguuni mwangu. Nilipo maliza kujiandaa, nikaitazama nguo ya Husna aliyo kuwa ameivaa muda tulipo kuwa tunakuja humu ndani, nikaipapasa na kukuta nusu ya kibunda cha pesa ambacho alikichukua kwa ajili ya kununulia chakula kipindi tulipo kuwa safarini. Nikaaingiza pesa hizo mfukoni mwangu, nikapapasa mifuko mingine na kukuta chichi chenchi za pesa alizo tumia.

Nikakaa kitandani kwa muda huku nikiitazama picha ya gari hili, huku akili yangu ikijiuliza maswali mengi ni wapi ninaweza kumpata Husna na nikaondoka na pesa pamoja na vipande vya madini. Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuona kitabu kilicho andikwa maeleozo mengi yaliyo tusaidia kutoka chini ya ardhi kipindi tulipo kuwa nchini Afghanistan, kikiwa kimanguka pembeni ya kitanda. Nikakiokota taratibu na kukifungua, nikaanza kusoma maelezo yaliyo andikwa ndani ya kitabu hichi. Nikafanikiwa kupata maelezo yanayo onyesha jinsi ya kulitafuta gari hilo enepo litapotea sehemu yoyote kwa kutumia satelaiti. Nikatoka chumbani humu kwa haraka na kushuka hadi mapokezi.

“Habari yako dada”

Nilimsalimia mmoja wa wahudumu hapa mapokezi.

“Salama, nikusaidie nini?”

“Ninaweza kupata huduma ya internet?”

“Ndio unaweza pata”

“Ni wapi?”

Dada huyu akanionyesha moja ya chumba pembeni ya sehemu hii ya mapokezi. Nikamshukuru kwa ishara, kisha nikaingia ndani ya hichi chumba na kukuta kikiwa kimegawanywa kwenye vijivyumba vidogo vidogo huku kukiwa na baadhi ya watu katika vyumba hivi huku kila mmoja akiwa na computer yake akifanya anacho kifahamu yeye mwenyewe. Nikaangaza angaza kwa macho yangu katika hili eneo na kuona moja ya chumba eneo la ukutani kikiwa wazi kabisa. Nikatembea kwa haraka hadi katika kijichumba hichi kidogo, nikavuta kiti na kukaa. Nikaminya batani ya moja ya computer hii, ikawaka, ila kwa bahati mbaya nikakuta ikinihitaji niingize neno la siri.

“Samahani”

Nilizungumza huku nikimuika kijana anaye pita pita ndani ya hichi chumba huku akiwa amevalia sare zinazo fanana na wahudumu wengine. Akanifwata na kuinama kidogo ili niweze kuzungumza naye kwa sauti ya chini kwani hii sehemu ina usikivu mkubwa.

“Sifahamu neno la siri”

Kijana huyu kwa kasi akaminya batani za computer hii na kunifanya nishindwe kujua ni neno gani alilo ingiza hadi akafungua. Kitu kingine kinacho nisumbu ni kwamba sina ujuzi mwingi katika maswala ya mtandao hususani katika swala la kutafuta magari yaliyo potea.

“Samahani unaweza kunisaidia kutafuta namba za hili gari?”

Nilimuonyesha muhudumu huyu maelezo ya katika hichi kijikitabu. Akanitazama usoni mwangu kwa muda kidogo, kisha akatazama wateja wengine walipo humu ndani, kwa ishara akanionyeshea kwamba ana hitaji pesa ili anifantie kazi hii. Nikachomoa noti moja ya dola mia mfikoni mwangu, nikamkabidhi, akaiweka keybord ya hii computer vizuri na kuanza kazi ya kuminya minya batani hizi kwa kasi sana huku akikosa kunipa hata muda wa kuweza kukremisha ni wapi alipo weza kupita hadi akafika hatua ya kunza kutafuta gari hilo. Baada ya dakika kama mbili ikatokea ramani ya nchi hii huku ikionyesha alama nyekundu inayo tembea ikiashiria kwamba gari hilo ndipo sehemu lilipo.

“Una gari na simu ukanisaidia?”

Kijana huyu akatingisha kichwa huku akinitazama usoni mwangu.

“Nitapata wapi?”

Kwa ishara ya mkono kijana huyu akanionyeshea nitulia anakuja sasa hivi.

‘Huyu mbona hazungumzi au ni bubu?’

Nilijiuliza huku nikimshuhudia kijana huyu akitoka ndani humu, baada ya muda kidogo kijana huyu akarudi hadi sehemu nilipo. Akaweka simu mezani aina ya Samsung S8. Akatoa waya wa USB na kuuchomeka nyuma ya computer hii huku waya huo akiwa ameuchomeka kwenye simu hii. Akaanza kuahamisha data ninazo zihitaji kutoka kwenye computer hadi kwenye simu. Ilipo fika asilimia mia moja akachomoa waya huu. Akaandika kwenye computer kwamba anahitaji kiasi cha dola elfu mbili aweze kunikabidhi funguo ya gari na simu hii. Nikatoa kibunda hichi na kuanza kuhesabu pesa hizi nilizo kuwa nazo kwa bahati nzuri ni dila lefu mbili na mia moja.

Nikamkabidhi pesa hizi, akanikabidhi funguo za gari aina ya ferari pamoja na pesa. Nikamtazama usoni mwake huku nikiwa siamini kabisa kwa msaada alio nifanyia, akatabasamu na kwa ishara akaniomba niweze kiondoka huku akinileza kwa ishara kwamba gari lipo kwenye eneo la maegesho. Nikaelekea katika eneo la magesho na kuminya batani ya fungua hii, na kuliona gari hilo likiwaka taa za mbele.

Nikalifwata kwa haraka, nikafungua mlango na kuliwasha gari hii ndogo ambayo ina sifa ya kwenda kwa kasi sana. Nikaanza kuondoka taratibu hadi getini, mlinzi akanifungulia geti huku akiwa amejawa na mshangao. Nikaiweka simu hii kwenye sehemu ya kuwekea simu ndani ya hili gari, nikaitazama ramani hii na kuona ni wapi Husna anaelekea, kwa kasi kubwa, nikaondoka eneo hili huku nikiwa makini sana barabarani.

Kwa uwezo mkubwa sana wa gari hili katika kukimbia, nikajikuta kila kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo zidi kumkaribia Husna. Uzuri ni usiku na hakuna magari mengi barabarani. Nikazidi kuongeza mwendo kasi wa gari hadi nikafanikiwa kuliona gari alilo iba Hunsa likimalizia kushusha moja ya muinuko wa hii barabara.

“Malaya utanitambua leo”

Nilizungumza huku nikizidi kuongeza mwendo kasi wa gari hili, nikafanikiwa kumpita Husna kisha kwa kasi nikafunga breki na kulifanya gari hili kusereka na kuziba barabara. Husna akafunga breki mita chache kutoka lilipo gari langu. Kwa haraka nikashuka kwenye hili gari na kuanza kutembea kuelekea lililo gari hili. Nikagonga kioo cha gari kwa kujiamini kwani bastola aliyo nayo Husna haina risasi na magazine ninayo mfukoni mwangu.

Taratibu kioo kikafunguliwa, macho yakanitoka mara baada ya kukiona kibibi cha kiarabu kikiwa ndio kinaendesha gari hili.

“Fuc***”

Nilizunugmza kwa hasira huku nikimtaza bibi huyu usoni mwake.

“Habari yako”

“Shuka kwenye gari”

Nilizungumza kwa hasira sana, bibi wa watu hakuleta ubishi kabisa, akashuka kwenye gari hili huku akitetemeka sana. Nikachungulia nyuma ya gari hili. Hakuna boksi hata moja la pesa. Katika siku niliyo feli kwenye maisha yangu, ni leo.

“Nani amekukabidhi hili gari?”

“Ni binti mmoja alinipatia pesa nyingi pamoja hili gari, na nikamuuzia kagari kangu?”

“Kapoje?”

Bibi huyu akachukua pochi ndani ya gari, akaifungua na kutoa simu yake na kunionyesha picha ya gari kwa jina baarufu bito au mwendo wa kobe.

“Hahaaa….”

Nilijikuta nikicheka kwa hasira sana kwa maana Husna kwa mchezo huu amenipiga chenga moja ambayo sikuweza kuitarajia kwenye maisha yangu.

“Amekukabidhi wapi?”

“Mjini?”

“Sawa pesa aliyo kukabidhi ipo wapi?”

Bibi huyu akafungua mlango wa nyuma ya dereva na kuona vipande vinne vya dhahabu pamoja na vibunda vya pesa vikiwa vipepangwa vizuri eneo la chini ya siti hii ambapo mtu huweka miguu yake anapo kuwa amekaa katika siti. Nikachukua vipande viwili pamoja na vibunda vinne vya pesa.

“Aliye kupa gari ni mke wangu na ameniibia pesa zangu pamoja na hivi vipande. Endelea na safari yako”

Nilimuambia bibi huyu huku nikimtazama usoni mwake.

“Amekuibia!!?”

“Bibi endelea na safari yako”

Nilizungumza kwa kufoka huku nikimtazama bibi huyu usoni mwake. Akaa kimya huku akinitazama jinsi ninavyo ingia kwenye gari langu. Nikajifikiria kwa muda kisha nikashuka kwenye gari hili.

“Samahani bibi”

“Bila samahani”

“Ninawezaje kutafuta gari lako kwa kupitia simu hii?”

Bibi huyu akaitazama simu hii kwa muda. Kisha akaichukua, akaanza kuiminya minya taratibu huku akionekana kuwa makini sana kwa kile anacho kifanya.

“Chukua”

Bibi huyu akanikabidhi simu yangu, nikaitazama na kuona ramani ikiwa imebadilika na gari hilo alilo kabidhiwa Husna kwa sasa linaelekea katika mji mwengine ambapo hadi niweze kumfikia ni zaidi ya msaa matatu kuanzi hivi sasa.

“Kwa nini amekuibia?”

“Ni maswala ya kindoa tu”

“Sasa una pesa nyingine ya kutumia?”

“Hapana”

Bibi akafungua mlango huo na kutoa vibunda hivyo vya pesa, kabla ya kunikabidhi akasita kidogo na kivirudisha ndani ya gari hili.

“Nipe gari hilo na kila kitu kilichopo ndani ya gari, nikiachie hili kubwa kwa maana naogopa ni gari la wizi hili”

Nikaitazama hii gari ndogo, kisha nikalitazama gari hili kubwa. Tofauti ya hizi gari mbili, Ferrari inakwenda kasi ila si salama pale inapo pata ajali, ila Hummer ni nzito na inapo pata ajali kuna unafuu wa mtu kuweza kutoka akiwa hai.

“Sawa”

Nilizungumza huku nikimkubalia bibi huyu, nikamkabidhi funguo ya Ferrari huku nami akinikabidhi funguo ya gari hili. Nikaagana na bibi huyu huku nikiingia ndani ya gari hili, nikaligeuza taratibu na kwa kufwata ramani ya linapo elekea gari la bibi huyu nikanza safari upya huku nikijitahidi sana kuendesha gari hili kwa kasi. Kama nilivyo kadiria inatanichukua masaa kadhaa kupata matumaini ya kumfikia Husna ndivyo ilivyo kuwa. Uzuri wa gari analo endesha Husna halina mwendo mkubwa.

“Lazima nikuue malaya wewe, si kwa kunihangaisha huku”

Nilizungumza huku nikizidi kuongeza mwendo ili kulifika gari la Husna. Nikiwa nimebakisha kama kona mbili hivi kulifikia, alama nyekundu inayo onyesha gari hilo kwenye simu yangu ikapotea na kunifanya nipunguze mwendo kasi wa gari, kitendo cha kumaliza kona ya mwisho nikajikuta nikifunga breki kali sana kwani kagari hako kamegongana uso kwa uso na lori kubwa na kukisababisha kianze kuteketea kwa moto mwingi sana ulio nimaliza nguvu kwani kila kitu kilichopo ndani ya gari hilo vinateketea kwa moto.



Kwa haraka nikashuka kwenye gari langu na kuanza kutembea kusogelea eneo lenye ajali. Kitu kilicho zidi kunishangaza zaidi ni ndani ya gari hii ndogo, hakuna mtu wa aina yoyote wala kitu cha aina yoyote zaidi ya siti tu.

“Fuc*** me”

Nilizungumza kwa hasira huku nikitazama tazama katika eneo hili. Kwa kweli Husna amenichezea mchezo wa pata potea.

“Nisaidie”

Niliisikia sauti ya dereva wa lori akiomba msaada huku gari lake nalo likianza kuteketea kwa moto. Nikafungua mlango wa gari lake kwa haraka na kuanza kumtoa kwa maana mskani wa gari lake ndio umempaba maeneo ya kiunoni mwake. Nikafanikiwa kumtoa ndani ya gari na kumlaza pembeni mwa barabara kwa usalama zaidi. Nikarudi kwenye gari langu na kuligeuza na kuanza safari ya kurudi mjini huku matumaini yote yakiwa yamenipotea. Kwa kutumia simu yangu nikaanza kuutafuta uwanja wa ndege na nikafanikiwa kuweza kuupata, nikaanza safari ya kuelekea katika uwanja huo huku nikitafakari ni jinsi gani ninaweza kupata hati ya kufoji ya kusafiria ili niweze kuondoka nchini humu.

Majira ya saa kumi usiku nikafika uwanja wa ndege, nikaelekea hadi kwenye moja ofisi za mawakala katika mashirika tofauti tofauti ya ndege yaliyopo hapa uwanjani.

“Habari zenu?”

Niliwasalimia vijana watatu wa kiarabu nilio wakuta ndani ya hii ofisi.

“Salama tu”

“Samahani nina tatizo kidogo ninaomba muweze kunisaidia”

“Zungumza tu”

“Ninahitaji kusafiri na ndege ya alfajiri ambayo inaelekea katika bara la Afrika sijui ninaweza kupata tiketi?”

“Ndio, ipo ndege ya shirika la KLM inaondoka saa kumi na mbili kamili asubuhi leo. Safari yake ya kwanza itatua Cairo Misri, ikitoka hapo itakwenda kutua moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa Kenyata nchini Kenya kisha itamalizia safari yake katika uwanja wa Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania”

Kusika nchi ya Tanzania mwili wangu wote ukanisisimka na kujikuta nikitabasamu sana.

“Ninaweza kuzungumza na mmoja wenu pembeni?”

Vijana hawa wakatazamana kisha mmoja wao akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia tukatoka nje ya ofisi yake.

“Mimi hapa unavyo niona sina hata hati ya kusafiria ila ninakuomba uweze kunisaidia kuweza kupata hati ya kusafiria na visa inayo onyesha kwamba ninatakiwa kuingia nchini Tanzania”

Kijana huyu macho yakamtoka, akatazama saa yake ya mkononi kisha akashusha pumzi nyingi sana.

“Hilo ni kosa la kisheria na ikibainika mtu umefanya hivyo katika hii nchi yetu unanyongwa hadi kufa kaka”

“Sema una hitaji kiasi gani nikupatie?”

“Hee?”

“Nina gari langu aina ya Hummer ipo hapo nje ninaweza kukupatia pia gari hilo likawa mali yako kama ukinisaidia”

“Twende tukalione gari hilo”

Nikaongozana na kijana huyu hadi nilipo simamisha gari langu. Akalitazama kwa muda huku akilizunguka.

“Mbona lina namba za usajili za nchi ya Afghanistan?”

“Hilo lisikusumbue unaweza kubadilisha kabisha na likawa mali yako”

Kijana huyu akajifikiria kwa muda huku akilitazama gari hili ambalo ni gari la kifahari na ni watu wachache sana duniani ambao wana uwezo wa kumiliki magari ya namna hii.

“Una uhakika hili gari ni lako?”

“Lingekuwa sio langu nisinge kubali kukupa kwa makubaliano. Ni gari langu na kila kitu unaweza kukitumia katika kubadilishia hati na nimesafiri nako kutoka Afghanistani hadi hapa na lina uwezo wa kuhimili safari ndefu pasipo shida ya namna yoyote”

“Sawa nisuvbiri hapa ninakuja sasa hivi”

“Poa”

“Ila nakuomba usiwaeleze chochote wezangu”

“Sawa”

Kijana huyu akaondoka huku akionekana kujawa na tamaa ya kumiliki gari hili la kifahari. Nikafungua mlango wa nyuma na kutazama pesa hizi zilizo pangwa vizuri pamoja na vipande hivi vya dhahabu.

‘Nitaziweka wapi?’

Nilijiuliza huku nikitazama mali hii ndogo niliyo baki nayo ambayo nina imani nikiondoka na kwenda nayo nchini Tanzania, basi ninaweza kufanya biashara ambayo itanisaidia kuingia kipato kikubwa sana. Nilipo muona kijana huyu akirudi nilipo simama, nikaufunga mlango wa gari hili.

“Tuingie ndani ya gari”

Kijana huyu alizungumza huku mkononi mwake akiwa ameshika laptop ndogo. Nikafungua milango ya mbele na kuingia ndani, akaifungua laptop yake na kuanza kuminya minya vitu huku akionekana kuwa na utaalamu mkubwa sana.

“Unafanya nini hapo?”

“Ninakutengenezea hati ya kimataifa ambayo unaweza kuingia nchi yoyote katika mabara yote duniani pasipo shida ya namna yoyote”

“Unataka kuniambia kuan hati za kusafiria za namna hiyo?”

“Ndio hati hizo wanazo wafanya biashara wale wakubwa sana duniani, na hata wewe utakuwa ni miongoni mwao na hadi kuipata hati hiyo ya kusafiria ni zaidi ya dola laki mbili na nusu ambazo si rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kuimiliki”

“Sawa nashukuru”

“Majina yako?”

“Randy”

“Jina la baba?”

Nikakaa kimya kidogo huku nikifiria jina la baba yangu.

“Donald Bush”

Akanitazama usoni mwangu huku akionekana kuwa na mshangao kidogo.

“Mbona unashangaa?”

“Ahahaa…hakuna”

Kijana huyu akaendelea kuifanya kazi yake, kisha akatoa simu yake mfukoni aina ya Iphone 7. Akanipiga nusu picha kisha akaituma kwenye laptop yake na kuunganisha na hati hii ya kusafiria ambayo aimesha itengeneza vizuri.

“Kagua hati yako”

Nikaitazama vizuri hati hii.

“Mbona hujajaza Taifa, tarehe ya kuzaliwa na kazi yangu?”

“Hivyo vitu vyote niikuwa niniahitaji wewe ndio uvijaze. Je utaifa wako ni upi?”

Nikajirikiria kwa muda huku nikitafakari juu ya nchi mbili kati ya Nigeria na Marekani.

“Marekani”

“Kazi yako?”

“Mfanyabiashara wa mafuta”

Nikamtajia na tarehe yangu ya kuzaliwa, mwezi pamoja na mwaka.

“Nisubirie hapa, nikurudi baada ya dakika kumi na tano nitakuwa na kila kitu chako”

“Sawa njoo na begi kama hutojali”

“Begi la ina gani?”

“La mgongoni dogo kiasi”

“Sawa sawa”

Kijana huyu akaondoka kwa kasi, nikakaa humu ndani ya gari huku nikiendelea kumfikiria Husna, upuuzi wake alio nifanyia.

‘Na mimi nimekuwa mjinga kwa nini nina amini watu kupita maelezo?’

‘Nisipo ondoka nchini humu ni lazima maisha yangu yatakuwa matatani.’

Nikiwa katika dibwi la mawazo, nikamuona kijana niliye mpa kazi akija kwa mwendo wa haraha huku mkononi mwake akiwa ameshika begi dogo. Akaingia ndani ya gari na kunikabidhi begi.

“Passport ipo wapi?”

“Fungua ndani”

Nikafungua ndani ya begi na kukuta hati yangu ya kusafiria, tiketi na yaraka zote muhimu ambazo zitaniwezesha kuingia nchini Tanzania pasipo kustukiwa kwamba vitu nilivyo navyo ni feki.

“Ndege imebakisha nusu saa kabla ya kuondoka, nimekukatia tiketi ya daraja maalumu la wafanya biashara VIP, kazi ni kwako. Nikabidhi funguo yangu ili nilipeleke hili gari sehemu ninayo ifahamu mimi mwenyewe”

“Nashukuru sana ndugu, ngoja nina mzigo wangu niweka kwenye begi”

Nikahamia siti ya nyuma hapa ndipo nikampa wasa kijana huyu kutazama nyuma. Hakuanini alivyo ona vibunda vya pesa vikiwa vimepangwa chini ya siti hizi. Nikanza kuingiza vibunda hivi vya pesa pamoja vipande vya madini. Begi hili likajaa vizuri na nikabakisha vibunda viwili, nikamrushia kibunda kimoja kisha nami nikabaki na kibunda kimoja cha pesa.

“Hapa si kuna maduka?”

“Eheee!!!”

Kijana huyu akashindwa kunijibu chochote zaidi ya kunitazama kwa mshangao kwa maana hakuamini kama nimepatia kibunda hichi ambacho kwa kukadiria kina zaidi ya dola elfu hamsini.

“Si kuna maduka humu ndani ya hili eneo?”

“Ndio, twende nikuepeleke”

Tukashuka kwenye hili gari, nikazunguka nyuma na kufungua mlango wa nyuma wa gari hili na sikuona kitu cha ina yoyote. Nilipo hakikisha kwamba hili gari halina chochote nikamkabidhi kijana huyu funguo.

“Kuanzia hivi sasa hili gari ni lako”

“Nashukuru sana, nashukuru sana kaka”

Kijana huyu alinishukuru huku machozi yakimlenga lenge usoni mwake. Tukaelekea kwenye moja ya duka la nguo za kiume. Nikanunua suti mija ya rangi ya kaki pamoja na miwani moja nzuri, nikabadilisha nguo zangu kwa hizi kwa haraka kisha kijana huyu akanisindikiza hadi kwenye eneo la kukaguliwa hati za kusafiria. Hati yangu ikakaguliwa na ikaonekana ni sahihi, ikagongwa muhuri na nikarudishiwa. Kijana huyu akanipa mkono wa kulia huku akinitazama usoni mwangu.

“Safari njema”

“Nashukuru na ubaki salama”

“Swali la mwisho hivi Donald Bush ni nani yako?”

“Baba yangu”

“Kweli?”

“Ndio”

Kutokana nipo kwenye foleni, nikalazimika kutembea mbele ili watu wengine nao wazidi kusonga mbele. Nikaingia kwenye ndege na nikakaa katika eneo la mbele ambalo lina siti kumi na mbili ila zilizo jengewa vizuri na wanakaa wafanya biashara wakubwa na wenye pesa zao. Kwa jinsi nilivyo pendeza ni ngumu sana kwa mtu kuweza kunigundua kwamba mimi ni miongoni mwa wanajeshi wa kundi la Al-quida.

“Habari yako kaka”

Muhudumu alisalimia huku akitabasamu vizuri usoni mwake.

“Salama tu dada yangu”

“Kuna huu ujumbe wako hapa”

Muhudumu huyu alizungumza huku akinikabidhi kikaratasi kidogo, jambo lililo nistua sana kwani naamini ndani ya hii ndege hakuna mtu hata mmoja ambaye ananifahamu.

“Umetoka wapi?”

“Pale”

Muhudumu huyu alinionyesha mtu aliye mkabidhi ujumbe huu. Mapigo ya moyo yakanistuka sana kwani mtu alie tuma ujumbe huu ni mama yangu mzazi ambaye huu ni mwaka wa tatu sijaonana naye toka niondoke nchini Nigeria. Nikaupoea ujumbe huu huku nikishusha pumzi taratibu, nikaufungua na kuusoma.

‘HAKIKISHA TUNASHUKA WOTE CAIRO NA TUNARUDI NIGERIA SAWA’

Nikaurudia kuusoma soma huu ujumbe, nikaukunja kunja kwa hasira, kwani bado mama ana maisha ya kuamrisha na si kubembeleza. Nikageuka nyuma na kumtazama mama aliye valia miwani nyeusi na kuziweka vizuri nywele zake na kwa haraka ukimtazama huwezi amini kama ni mwanamke wa miaka zaidi ya arubaini na tano. Mama amekaa siti moja na mlinzi wake wa kike ambaye siku zote huwa simpendi kabisa kwani hufwata kile alicho elekezwa na mama. Taratibu ndege ikaanza kuondoka katika eneo hili huku amani na furaha ya kuelekea nchini Tanzania ikiwa imeniondoka kabisa.

“Samahani”

Nilimuita muhudumu mara baada ya ndege kukaa sawa angani

“Bila samahani”

“Naomba kalamu na karatasi”

“Sawa”

Muhudumu akaondoka na baada ya muda akarudi na kitu nilicho muagiza.

“Naomba usubiri huu ujumbe uupeleke kwa yule mama pale nyuma”

“Hakuna tatizo”

‘SAMAHANI SIJAKUELEWA WEWE NI NANI?’

Niliandika makusudi ili kuweza kucheza na akili ya mama na sihitaji kujirahisisha tena kwake kwa maana kwa sasa mimi sio mtu wa kuishi chini ya amri ya mzazi na ninauwezo wa kuyaongoza maisha yangu mimi mwenyewe pasipo kuongozwa na mtu yoyote. Nikageuka nyuma na kumtazama mama jinsi anavyo soma ujumbe huo, nikamuona ndita zikitawala katika uso wake, nikatabasamu kidogo huku nikiamini kile nilicho kuwa ninakifikiria sasa kimeanza kufanya kazi.

Nikanyanyuka na kuanza kutembea kuelekea katika vyoo, nikapita siti ya mama alipo kaa na mlinzi wake, nikawatazama kwa macho makali huku naye mama akionekana kunishangaa sana. Nikaingia katika vyoo vya wanaume huku nikishusha pumzi. Nikajisaidia haja ndogo kishan ikatoka na kukutana na mlinzi wa mama mlangoni akinisubiria huku akiwa ameshika bastola.

“Vipi kuna tatizo lolote la mimi na wewe?”

Nilimuuliza dada huyu huku nikimtazama usoni mwake.

“Mama yako anahitaji ukakae kwenye siti yake pale, hili sio ombi ni am……..”

Kabla ya dada huyu hajamalizia sentensi yake, nikampiga shingoni mwake kwa kutumia upaba wa kiganja changu cha mkono wa kulia na kumfanya alegee mwili mzima kwani nimempiga katika mshipa wa kupoteza fahamu, nikafungua mlango wa choo cha wanawake na kumkalisha kwenye choo cha kukaa, kisha nikafunga vizuri huku nikiichukua bastola yale. Nikatembea kwa kujiamini hadi katika siti ya mama na kimuwekae bastola ya mlinzi wake mapajani mwake.

‘Nimekuambia umekosea mtu, kachukue mzoga wako chooni’

Nilimuambia mama yangu kwa sauti ya kumnong’oneza jambo lililo mshangaza sana na taratibu nikaanza kutembea kwa kujiamini nikirudi kwenye siti yangu na kukaa.



Nikamuona mama akinyanyuka huku akinikazia macho akaelekea eneo la chooni. Nikatabasamu huku nikiwasha tv ndogo iliyopo pembeni yangu, nikachukua earphone kubwa na kuvaa masikioni mwanga na nikafungulia mziki mkubwa kiasi ili mtu ili nisiweze kusikia kinacho endelea. Usingizi taratibu ukanipitia na nikalala usingizi fofofo. Nikafumbua macho yangu kwa haraka mara baada ya kuhisi kushikwa begani mwangu. Nimtazama aliye nishika na kumkuta ni muhudumu, nikavua earphone zangu ili niweze kumsikiliza vizuri.

“Samahani kwa kukusumbua, hii ni menu yetu ya chakula, chochote utakacho kihitaji tutakupatia”

Muhudumu huyu mwenye asili ya kiafrika alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Nashukuru sana”

“Sawa nitaipitia baada ya dakika tano”

Muhudumu huyu akaondoka, nikatazama nyuma na kukutana na macho ya mlinzi wa mama akinitazama kwa hasira sana, nikamkonyeza kisha nikageuka mbele na kuanza kusoma menu hii yenye vyakula tofauti tofauti. Baada ya dakika tano muhudumu akarudi.

“Naomba nipatie huyu kuku mzima wa kochoma na juisi”

“Sawa, je achanganywe na viungo au viwekwe pembeni”

“Vyote viwekwe pembeni”

Muhudumu mara baada ya kuzungumza hivyo akaondoka eneo hili. Uzuri siti ya pembeni yangu hakuna mtu yoyote na nimeweka begi langu ambalo lina vibunda vya pesa pamoja na vipande vya madini. Nikaichukua simu yangu hii na kuiunganisha na mfumo wa wi-fi. Nikaanza kuperuzi kwenye mitandao ya hususani kwenye akaunti zangu za zamani ambazo nilizitelekeza mara baada ya kuondoka nyumbani kwa mama yangu. Nikafwatilia juu ya maisha ya baba yangu marehemu Donald Bush. Nikagezitazama picha ambazo alipiga na mama yangu kipindi cha ujana wao, nikamtazama mama kwa sekunde chache kisha nikatazama picha hizi. Nikatamani kusimama ili niweze kumuuliza swali ila nikashindwa kutoka hapo awali nilisha nitambulisha kwamba mimi sio anaye nifikiria. Muhudumu akafika hapa na sahani kubwa aliyo iwekea sahani ndogo zenye kuku pamoja kachumbari.

“Karibu”

Muhudumu alinikaribisha huku akikunjua meza ndogo iliyopo mbele yangu

“Nashukuru”

Kaniwekea vitu hivyo, huku macho yetu kwa mara kadhaa yakigongana gonga. Uvumilivu ukanishinda kwani kwa uzuri huyu dada ni mzuri kwa kweli.

“Samahani unaitwa nani?”

“Charity”

“Ohoo una jina zuri”

“Asante”

“Samahani Charity ninaweza kupata namba zako za simu?”

Muhudumu huyu akanionyesha kiganja cha mkono wa kushoto ambacho kimevisha pete ya ndogo pamoja na uchumba.

“Ohoo samahani sana sikulifahamu hilo”

“Usijali”

“Ila ninaweza kukuuliza swali la mwisho?”

“Uliza tu”

“Unaishi wapi?”

“Mimi kwetu ni Tanzania, ila mume wangu anaishi nchini Marekani”

“Nashukuru kusikia hivyo”

“Karibu chakula”

Charity akaondoka na kuniacha nikimsindikiza kwa mcho jinsi makalio yake yanavyo tingishika kiasi cha kuniacha nimejawa na msisimko mkali wa kimapenzi. Kabla sijanza kulala, mama akasimama pambeni yangu na kuniombe niweze kusogea ili akae siti ya dirishani ambapo ndipo nilipo weka begi langu lenye pesa. Taratibu nikampisha na akapita huku akisogeza begi langu hilo pasip kuweza kufahamu kilichomo ndani.

“Unahisi mimi ni mjinga hadi kunifananisha?”

“Samahani sijakuelewa kabisa”

“Randy usihitaji hasira yangu inipande dhidi yako”

“Ohoo samahani, mimi siitwi Randy utakuwa umenifanisha dada yangu”

Nilizungumza huku moyoni mwangu nikiwa nimejawa na maumivu makali sana, kwani hakuna jambo gumu kwenye maisha kama kumkana mama mzazi kwa kujifanya humjui. Mama akanitazama huku machozi yakimlenge lenga usoni mwake.

“Kweli?”

“Ndio dada yangu. Mimi ninaitwa Salim Abdulah ni Mpakistan”

Nikaona kifua cha mama jinsi kinavyo shusha pumzi nyingi, akajipangusa machozi usoni mwake kwa kitambaa alicho kishika.

“Samahani dada, yule mfanyakazi wako alinishikia bastola pamoja kunifahamu sasa sijafahamu kwa nini amefanya vile?”

“Samahani kaka yangu, naomba nipite”

Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa nembo ya askari wa Afghanistan niliyo pewa na mjomba wa Husna.

“Mimi ni askari, kwa lile alilo nifanyia mlinzi wako, hapa ndio najitahidi kufwatilia habari zake ili nikifika Cairo aweze kuwekwa chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi”

Nilizungumza kwa ujiamini huku nikimkabidhi mama simu yangu ambayo katika kuperuzi peruzi kwenye mtando niliweza kuipitia historia ya mlinzi wake. Mama macho yakamtoka huku dhairi akionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.

“Labda unieleze huyo Randy ni nani na kwa nini umenifananisha naye”

“Samahani afisa, kusudia langu halikuwa hilo. Naomba unisamehe”

“Kukusamehe inawezekana, ila nahitaji maelezo ya kina la sivyo nipoge simu Cairo na mlinzi wako aweze kushushwa”

“Ni hivi. Randy ni kijana wangu aliye potea miaka miwili au mitatu iliyo pita. Aliondoka kwenye maisha yangu kutokana mambo ya kifamili na nilisikia kwamba alimuua mmoja wa wanajeshi hivyo msakako ukafanyika kwa nchi ya Nigeria, ila hakuweza kupatikana”

“Kwa hiyo huyo mwanao ni jambazi?”

“Hapana si jambazi, nilimkuza kwenye maisha mazuri ya kuwa mtu mzuri ila sijui ni kitu gani ambacho kiliweza kumuingia kwenye ufahamu wake wa kili na mwisho akajikuta anafanya vitu vya kijinga”

“Pole sana. Nimemsamehe mtu wako na muda mwengine hembu jaribu kutumia mabavu au pesa zako kuhisi unaweza kufanya jambo lolote kwenye maisha ya mtu yoyote utakufa kifo kibaya sana. Sawa dada yangu”

Nilizungumza kwa kujiamini na kumfanya mama kunitazama kwa mshangao sana na nina imini kwamba moyoni mwake atakuwa akijiuliza maswali mengi sana kuhusiana nami. Mama akanyanyuka na kurudi kwenye siti yake huku akiwa amejawa na huzuni kubwa. Machozi yakaanza kunimwa, hamu hata ya kula chakula hichi ikaniishia. Charity akapita huku akinitazama sana usoni mwangu.

Nafsi moja inatamani kumueleza mama ukweli kwamba mimi ndio mwanye huku nafsi yangu nyingine ikitaa maamuzi hayo.

Hadi tunafika nchini Misri, sikuweza kula chakula hichi alicho niandalia Charity. Nikamuomba Charity aweze kukitoa chakua hichi na akaniachia kikaratasi juu ya meza hii ndogo, nikakifungua na kukisoma.

‘Kwa nini unalia Randy?’

Nikashusha pumzi taratibu huku nikimuangalia Chariy anavyo wasaidia abiria wanao shuka kwenye nchi hii huku sisi tukiendelea na safari yetu. Nikamshuhudia mama na mlinzi wake wakitoka katika eneo hili huku mara kwa mara wakinitazama. Wakashuka kwenye ndege hii jambo lililo nifanya nikimbilie upande wa pili na kuwachungulia dirishani. Nikamuona mama akishuka huku akijipangusa machozi usoni mwake.

“Randy”

Niliisikia sauti ya Charity akiniita, taratibu nikamtazama na kumkuta akiwa amesimama na wanaume wawili walio valia kanzu nyeupe wakionekana nao wanahitaji kukaa kwenye hii siti yao. Nikarudi kwenye siti yangu huku nikiwa nimejawa na huzuni kubwa sana.

“Hujanijibu swali langu”

Charity aliniambia kwa sauti ya kunon’oneza.

“Tutazungumza nikiwa sawa”

Charity akaninyooshea dole gumba akiashiria kwamba amekubaliana nanilicho muambia. Safari ikaendelea huku moyoni mwangu nikiwa nimepoteza furaha kabisa, japo mama yangu amekuwa ni mtu mkali sana kwangu, ila kuwema kweli kwa upande wangu ninampenda sana.

“Unaweza kusogea huko”

Charity alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Sawa”

Nikasogea kwenye siyi iliyopo dirishana na akakaa kwenye siti niliyo kuwa nimekalia.

“Mbona hukula chakula au hukukipenda?”

“Hapana nimekipenda”

“Ila?”

“Kuna mambo ambayo yamenichanganya. Vipi kwa kukaa hapa huwezi kupata shida katika kampuni yako?”

“Hapana sasa hivi ni usiku ni muda wa sisi pia kupumzika na tunaweza kukaa na abiria wetu na tukasikiliza maoni yao mawili matatu”

“Ahaa sawa sawa”

“Ehee niambie ni nini kinacho kusumbua hadi ukawa unalia au yule mama niliye kuona umekaa naye alikukera?”

“Naweza kukuuliza swali”

“Uliza tu?”

“Unaweza kumuita mama yako dada?”

“Yaani dada kama dada ua katika hali ya utani au?”

“Katika hali ya kawaida na si utani?”

“Hapana siwezi kabisa kumuita dada”

“Kweli?”

“Yaa kweli, huo ni ukosefu wa heshima kwa mama na ukitegemea mama katika maisha yetu ni muhimu sana kuliko mama au baba”

“Sawa sawa. Wazazi wako wapo hai?”

“Ndio, baba na mama wote wapo mkoani Kilimanjaro Tanzania”

“Sawa”

“Niambie ni nini kinacho kusumbua”

Nikakaa kimya kwa dakika kama mbili hivi, kisha nikaanza kumuadithia Charity historia ya maisha yangu toka nilivyo kuwa mtoto mdogo. Sikuhitaji kumficha jambo lolote kabisa kuhusiana namaisha yangu na mama yangu. Nikamuadithi jinsi nilivyo ondoka nchini Nigeria na kwenda kujitafutia maisha ambayo bado hayakuwa na amani kabisa kwenye maisha yangu, na nikamuadisia jinsi nilivyo mkana leo mama yangu ili kuweza kuendelea kujitenga naye. Hadi ninamaliza Charity macho yake nayo yanalengwa lengwa na machozi.

“Pole sana Randy, ila ulicho kifanya sio jambo sahihi. Mzazi hakanwi kabisa hiyo ni laana Randy”

Charity alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Najua hilo ndio maana nina umia na nina muomba Mungu aweze kunisamehe katika hilo”

“Kweli kabisa. Ehee tuachene na mambo hayo. Tiketi yako inaonyesha kwamba unakwenda nchini Tanzania. Vipi una ndugu huko?”

“Hapana, naisikia hiyo nchi na ninapenda kwenda kuanza maisha yangu ya amani nchini humo”

“Sawa sawa, mimi nitakuwa mwenyeji wako, kwa maana nikifika Tanzania, ninachukua likizo ya wiki moja kisha ninarudi kazini na safari ya kwanza ni kuelekea nchini Marekani alipo mume wangu”

“Ahaa sawa sawa. Vipi umezaa na mume wako?”

“Hapana ndio kwanza ndoa ina miezi nane sasa hivi na ukitegemea hizi kazi zetu, leo upo huku kesho upo kule basi ni tafrani kabisa”

“Nawaombea kwa Mungu muweze kupata familia kubwa”

“Hahaaa. Amen. Randy acha nikatembee abiria wengine huko nyuma”

“Sawa sawa”

Charity akanyanyuka nami nikarudi kwenye siti yangu. Safari ikazidi kusonga mbele na tukafika nchini Kenya. Abiria wengi katika daraja letu hili la VIP, wakashuka na tukabaki na mzee mmoja wa kiarabu.

“Hapa hadi Tanzania itachukua muda gani Charity?”

“Mmmmm masaa kadhaa hivi. Kidogo tupo hapa ndege kuna marekebisho kidogo inafanyiwa kisha tunaendelea na safari”

“Sawa sawa”

“Nikuletee kinywaji?”

“Hapana nipo vizuri”

“Sawa”

Baada ya lisaa moja la matengenezo tukaondoka nchini Kenya na tukaanza safari ya kuelekea nchini Tanzania. Haikutuchukua masaa mengi hewani na tukafika nchini Tanzania huku ikiwa ndio mara yangu ya kwanza kufika katika nchi hii, huku lengo langu kubwa likiwa kufwata ushauri wa gaidi Dany alio niambie nielekee nchini Tanzania na nitaweza kufahamu ukweli wa uhalisia wa baba yangu.

“Ukitoka pale nje nomba unisubirie kama nusu saa hivi, nimalize hatua za kampuni kisha nitatoka”

“Sawa”

Nikapota katika hatua zote za ukaguzi na nikafanikiwa kutoka nje pasipo kuwa na tatizo la aina yoyote. Nikalivaa begi langu mgongoni huku nikielekea nje ya uwanja huu wa ndege. Baadhi ya madereva taksi wengi wakanifwata huku wakihitaji wanisafirishe.

“Kuna mtu nina msubiria samahani”

Nilimjibu ili kupunguza zogo la maswali yao ya wapi nina elekea.

“Pole kwa kukuweka”

Niliisikia sauti ya Charity nyuma yangu huku akiwa amebadilisha mazi yake ya kazi na kuvaa suruli iliyo mbana na kunifanya niweze kushuhudia jinsi umbo lake namba nane jinsi lilivyo mpendezesha mwili wake. Kabla sijamjibu nikamshuhudia Husna akitoka kwenye mlango wa abiria kutoka huku akisukuma mabegi mawili makubwa kwenye moja ya kitorori jambo lililo nifanya nianze kumfwata kwa haraka na kumaucha Charity akijawa na mshangao.



Nikamfikia Husna na kumshika mkono wake wa kulia na kumgeuza kwa nguvu na tukatazamana.

“Wewe kaka vipi?”

Sauti ya mwanamke huyu ni tofauti kabisa na Husna ninaye mfahamu japo sura zinafana kwa asikimia tisini na tisa.

“Pesa na madini yangu vipo wapi?”

“Pesa…! ! Madini? Mbona sikuelewi wewe kaka”

“Fungua mabegi yako”

“Nini?”

“Fungua mabegi yako”

“Wewe kama nani?”

Husna kwa namna moja ama nyingine anaonekana kunichezea akili kama jinsi nilivyo mchezea mama yangu akili tukiwa katika ndege. Nikafungua begi moja kwa nguvu na kukuta nguo nyingi. Husna akanza kuomba msaada wa askari wa hapa uwanjani, nikaendelea kutoa nguo hizi hadi askari walivyo nifikia tayari nilisha toa nusu ya nguo hizi mpya. Askari wawili wakanikamata kwa nguvu.

“Niachieni tafadhali huyu dada ameniibia pesa zangu na madini yangu”

“Hili sio eneo la kudaiana”

Askari mmoja alizungumza huku akinifunga pingu mikononi mwangu. Charity akafika katika eneo hili, akawonyesha askari hawa kitambulisho chake kisha akakirudisha kwenye pochi.

“Hili swala tulitafutieni ufafanuzi na si kwa kumfunga pingu Randy”

Charity alizungumza huku akiwatazama askari hawa.

“Dada tafadhali, kuanzia hivi sasa mizigo yako itakaguliwa kutokana na madai ya huyu mtu”

“Unajua huku ni kunidhalilisha je akanikuta sina hatia na sina hizo pesa zake je ataweze kunilipa?”

“Ndio nitakulipa”

Nilizungmza kwa kujiamini huku nikimtazama Husna usoni mwake.

“Sawa nipo tayari mizigo yangu ikaguliwe”

Askari wawili wakarudisha nguo nilizo kuwa nimezitoa ndani ya begi kisha askari mmoja akaanza kazi ya kusukuma kitorori hicho hadi kwenye ofisi za askari hawa. Nikakalishwa kwenye kiti na kufunguliwa pingu zangu. Husna naye akakakalishwa katika kiti cha pembeni kisha mabegi hayo yakawekwa mbele yetu.

“Naombeni hati zenu za kusafiria”

Askari mmoja alizungumza huku akitotazama, nikafungua begi langu na kutoa hati yangu ya kusafiria na kumkabidhi hata Husna mwenyewe akatoa hati yake ya kusafiria.

“Hajirat Hussein Mudathiri, ndio majina yako halisi si ndio?”

“Ndio”

“Na wewe Randy Donald Bush”

“Ndio”

“Muna mahusiano gani kati yenu?”

“Huyu kaka mimi simfahamu kabisa na ninashangaa anavyo niambia kwamba nimechukulia pesa yake. Ipi kwa maana mimi hapa ninatoka china kukusanyaka mzigo wangu wa nguo na mume wangu yupo nje huko ananisubiria”

“Acha unafki mwanamke wewe, si tulikuwa wote Afghanistan?”

“Jamani jamani, mbona hiyo nchi mimi hata sijawahi kutia mguu wangu jamani”

“Wewe mwanamke usijifanye mjinga. Tumefika Iran na ukakimbia na pesa zangu pamoja na gari langu si ndio”

“Ngoja kwanza kaka, wewe kazi yako ni nini?”

“Kwani hicho passport inaonyesha kazi yangu ni nini au unataka ujifanye hufahamu?”

“Hei tafadhali hii sio Marekani hapa ni Tanzania, huna uhuru wa kuzugumza upuuzi kama unavyo jisikia. Jibu swali langu”

“Mimi ni mfanya biashara?”

“Wa nini?”

“Mafuta na madini?”

“Tanzania umekuja kufanya nini?”

“Ndugu maswali mengi ya nini?”

“Jibu swali?”

“Kuwekeza”

“Dada na wewe?”

“Mimi ni mfanya biashara wa nguo, ninachukua mzigo wa nguo China au Dubai, nina duka langu Sinza pale na Kariakoo, sasa nashangaa huyu kaka anavyo nisingizia maswala ya ajabu na kunidhalilisha mbele za watu”

“Afande hembu fungua hizo begi, kuna pesa zangu nyingi sana huyu mwanamke amaniibia”

“Una uhakika?”

“Asilimia mia moja na kama sinto pata hivyo vitu nitamlipa dola elfu tano hapa hapa”

“Dada umekubaliana na jamaa hapo?”

“Nimakubaliana naye na ninaomba pesa hiyo itolewe kwa maandishi, isije akanikabidhi na ikafika huko nje akanipokonya”

“Sawa”

Askari huyu anaye tuhoji akatoka chumbani humu na kutuacha na askari mmoja malangoni. Sikuhitaji kuleta fujo ya aina yoyote huku macho yangu kila muda yanamtazama Husna kwa umakini.

“Na utanieleza vizuri kwa nini uliniibia pesa zangu?”

“Haki ya Mungu kaka mimi sikuelewi unacho kizungumza”

Husna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Sawa”

Askari akaingia huku akiwa ameshika karatasi nyeupe pamoja na kalamu akaiweka juu ya meza. Akanikabidhi huku akiniamrisha niandike maelezo ya ukaguzi na ahadi ya kiasi cha pesa ambacho nitampatia dada huyu mara baada ya kukuta kwamba kile ninacho kihitaji sicho. Nilipo maliza nikasaidi.

“Mbona huyu hamuuandikishi?”

“Tumuandikishe kwani yeye ndio anaye kudai?”

Swali la askari huyu likanifanya nikae kimya kwa muda kidogo. Askari huyu akaanz akuoa nguo moja baada ya ngine huku akiikung’uta vizuri hili hata kama kuna senti moja ya pesa ndani ya nguo hizo, iweze kutoka. Hadi begi la kwanza linaisha, hakuna hata dola moja iliyo anguka chini. Likafunguliwa begi la pili nalo likaanza kukaguliwa kwa umakini na usahihi wa hali ya juu, huku kila mtu akishuhudia ukaguzi huo.

“Begi linakwisha hili hakuna chochote kaka”

Askari huyu alizungumza huku akiendelea kukagua begi hili. Wasiwasi ukaanza kunitawala taratibu kwani ukisikia mtu kuonekana mwenda wazimu ndio leo. Askari akamaliza nguo zote katika begi la pili na kulikung’uta vizuri begi hilo akisisitizia kwamba hakuna chochote katika begi hilo.

“Ohoo Mungu wangu”

Nilizungumza huku nikishusha pumzi.

“Ahadi ni deni, lipa pesa ya watu. Pia unipe pesa ya kunipotezea muda kwa upuuzi wako na ujinga wako”

Askari huyu alizungumza kwa msisitizo.

“Ngojeni mara moja”

Nilizungumza huku nikitoa simu yangu mfukoni.

“Hapa kuna huduma ya Wi-fi?”

“Ndio”

Nikaunganisha simu yangu na huduma hiyo ya mtandao. Nikatafuta jina la hospitali aliyo kuwa anafanyia kazi nesi Husna nchini Afghanistan, nikaipata, nikaingia kwenye orodha ya majina ya wafanyakazi na kwa bahati nzuri nikafanikiwa kulipata jina la nesi Husnapamoja na picha zake.

“Hembu tazama hizi picha alafu niambie ninacho kizungumza hapa ni uongo”

Nilizungumza huku nikimkabidi askari huyu simu yangu. Askari huyu akazitazama picha hizo, huku kwa mara kadhaa akinyanyua macho yake na kumtazama huyu dada anaye jiita Hajirat. Nikamuona askari akijikuta kichwa chake huku akishusha pumzi nyingi.

“Jamani hembu naombeni msaada”

Askari huyu alizungumza kwa kutumia simu ya upepe huku akitazama kioo kikubwa kilichomo ndani ya hichi chumba ambacho kwa namna moja ama nyingine, mtu wa nje anaweza kuona ndani, ila mtu wa ndani katika chumba hichi hawezi kuona nje.Wakaingia askari watatu, wawili wanaume huku mmoja akiwa ni mwanamke. Nao pia wakaanza kutazama picha za Husna.

“Wanafanana”

Askari wa kike alizungumza huku akimtazama Hajirat.

“Nafanana na nani jamani?”

“Unafanana na wewe?”

Askari mmoja alijikuta akiropoka huku akimkazia macho Hajirat.

“Hembu na mimi niweze kuona hizo ppicha ajamni”

Hajirat alizungumza kwa upole huku machozi yakiendelea kumwagika suoni mwake. Askari mmoja akamsogezea simu yangu karibu kabisa na uso wake hata yeye mwenyewe akaonekana kustuka sana kwa kujiona.

“Jamani huyu ni nani?”

“Sasa wewe unatuuliza huyu ni nani ikiwa hapa unajiona wewe hapo”

“Hapana jamani, sio mimi duniani humu watu tunafanana”

Hajirat alizungumza huku akibubujikwa na machozi. Mlango ukafunguliwa na akaingia mzee aliye valia mavazi yanayo fanana na askari hawa. Wakampigia saluti mzee huyu kwa maana vyeo vinavo onekana kwenye bega lake vimewazidi askari hawa waliomo humu ndani.

“Kuna nini kinacho endelea?”

Askari mmoja akaanza kueleze jinsi sakata zima lilivyo mimi na huyu binti. Mzee akakabidhi simu yangu na kutazama picha ya msichana huyu.

“Zitafanisheni picha zao kwa kutumia computer”

“Sawa mkuu”

Sikuelewa kwa haraka maana ya mzee huyu. Tv kubwa ikawashwa humu ndani na tukaziona picha za nyuso mbili na kwa asiliamia mia moja ninaamini kwamba dada huyu ni Husna. Ufananishaji huo wa sura kwa sura hizi mbili ukaanza huku sura hizo zikiwa zimejawa na vistari vingi ambavyo sielewi kazi yake ni nini.

“Hapo ndio munafanyaje?”

Nilimuuliza askari mmoja, akanitazama pasipo kunijibu chochote kwa maana mkuu wake yupo hapa. Asilimia zikazidi kutembea kutoka moja hadi mimia moja na matokea yakaonyesha kwamba dada huyu Hajirat hafaani na Husna ninaye muongelea jambo lililo nistua sana.

“Hawafanani, muachie dada wa watu na muache kuwasumbua watu”

Husna alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Ana faini yangu anatakiwa kunilipa”

Hajirat alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Lipa”

Nikashusha pumzi taratibu, nikafungua begi langu na kutoa kiasi cha pesa nilicho kiahidi na kumkabidhi Hajirat na kumfanya ajawe na furaha mara dufu.

“Ninaweza kuondoka?”

Niliuliza huku nikiwa nimejawa na unyonge wa hali ya juu. Kwa ishara ya kuchezesha vidole, aksari aliye kuwa akindesha hili swala alinionyeshea akimaanisha kwamba anahitaji pesa na yeye. Nikatoa noti mbili za dola mia na kumkabidhi kisiri pasipo mkuu wake kufahamu.

“Potea”

Alizungumza kwa sauti ya chini chini. Nikavaa begi langu mgongoni na kutoka ndani humu. Nikamkuta Charity nje ya chumba hichi akinisubiria.

“Samahani kwa kukuchelewesha”

“Wala usijali, ndio maisha”

Tukatoka nje, akaita taksi, tukaingia na kuondoka katika eneo hili huku nikiwa nimejawa na mawazo mengi sana.

“Kwa nini alikuibia?”

“Sifahamu?”

“Au ilisha wahi kumdhulumu?”

“Hapana, katika maisha yangu kitu ninacho kiogopa ni kumdhulumu mwanadamu mwenzangu”

“Mmmm pole”

“Niwapeleke wapi?”

“Mbezi Beach”

Hadi tunafika katika eneo ambalo Charity alihitaji tufike, badi kichwa changu kinakataa kuamini kwa kile kilicho tokea.

“Tumefika Randy karibu sana”

Charity alizungumza huku tukishuka kwenye gari hili. Akatoa fungua kwenye pochi yake na kufungua geti la nyumba hii. Tukaingia ndani na nyumba hii imejaa majani mengi ardhini kutokana na kuto kufanyiwa usafi kwa muda mrefu.

“Samahani mwaya nimekueleta nyumbani kwangu na si kusafi sana”

“Usijali rafiki yangu”

Akafungua mlango na tukaingia ndani. Ndani ya hii nyumba hii, imepangiliwa vizuri sana na vitu vingi vilivyomo ndani humu ni vya thamani kubwa sana.

“Donald Bush unaye mzungumzia hapa ni yule raisi wa Marekani aliye uliwa hapa nchi Tanzania?”

Charity alizungumza huku akiweka pochi yake juu ya meza ya kioo hapa sebleni.

“Ndio”

“Unataka kusema yule ni baba yako?”

“Vipi unamfahamu?”

“Historia yake inaifahamu, na hata video yake ya mauaji ninayo”

“Ipo wapi?”

“Ngoja”

Charity akatembea kwa haraka hadi kwenye meza ndogo yenye computer, akaiwasha na kuanza kutafuta tafuta video hiyo kwenye mafaili mengi.

“Hii hapa”

Charity alizungumza huku akiiweka video hii ambayo nilisha wahi kuitafuta kwa kipindi cha nyuma ila sikuweza kufanikiwa kuiona, ile leo nimashuhudia dhairi jinsi Dany alivyo kuwa akimuua baba yangu jambo linalo nifanya nizidi kujawa na hasira dhidi ya gaidi Dany na kama yupo hapa nchini Tanzania basi nitahakikisha kwamba nina msaka hadi ninamkamata na kumpa haki yake ya kifo anayo stahili.



Sikuweza kuimaliza kutazama video hii hadi mwisho. Dany sijui ni binadamu wa aina gani, kwani anaonekana hana hata chembe ya huruma kwenye moyo wake, jinsi alivyo kuwa akimkata kata baba yangu vipande utadhani ni jinsi mama wa jikoni anavyo mkata kata kuku wa kitoweo chake cha siku hiyo. Nikaka kwenye moja ya sofa huku nikiendelea kumwagikwa na machozi. Charity akanifwata hadi sehemu nilipo kaa, akanishika bega langu la upande wa kulia.

“Randy samahani kama nitakuwa nimekuonyesha video hiyo pasipo kufikiria hali kama hii. Nakuomba unisamehe”

Nikamtazama Charity uosni mwake na kidogo nikaweka sura ya tabasamu.

“Usijali”

Nilizungumza kwa unyonge. Charity akanitazama kwa muda kidogo kisha akanyanyuka. Akachukua pochi yake na kuingia kwenye moja ya chumba kilichopo katika eneo hili. Nikanyanyuka na kurudi kwenye meza yenye compiter, taratibu nikaifugua video hii na kuanza kuitazama kwa mara nyingine huku nikijitahidi kujikaza kiume niweze kuitazama hadi mwisho. Nikatoa simu yangu mfukoni na kuihamishia video hii kwenye simu yangu. Nikarudi kwenye kochi na kuendelea kuitazama jinsi Dany alivyo kuwa akimchinja baba yangu pasipo huruma ya aina yoyote.

“Unatazama nini?”

Sauti ya Charity ikanistua kidogo na kujikuta nikiisimamisha video hii na kumtaza.

“Una ufahamu wowote kuhusiana na Dany?”

“DANY huyo wa kwenye video?”

“Ndio”

“Hakuna mtu yoyote ambaye anamfahamu ni wapi alipo. Nchi ya Marekani hadi leo wanaendelea kumtafuta kila kona ya dunia na hakuna ambaye anafahamu ni wapi alipo na leo hii majuma wawili yaliyo pita tu nimesikia amemteka makamu wa raisi wa nchi ya Marekani”

Maneno ya Charity hayakunistua sana moyoni mwangu kwani ninafahamu kila jambo na dakika ya mwisho nilishindwa kumdhibiti kabisa Dany.

“Nahitaji kumkamata huyu mshenzi”

“Ni jambo gumu sana Randy, labda nikuulize swali”

“Uliza?”

“Unahisi una uwezo wa kumkamata gaidi ambvaye aliweze kuitikisa dunia kwa miaka kadhaa ya nyuma?”

“Ndio”

“Huwezi Randy kwa ushauri wangu, ningekuomba uweze kuwa mpole na ungendelea na maisha yako”

“Asante kwa ushauri, ni wapi lilipo bafu, ninahitaji kuoga sasa”

Charity kwa ishara ya mkono akanionyesha chumba cha sehemu ninayo takiwa kuingia. Nikabeba begi langu na kuingia katika chumba hichi ambacho kina kitanda, sofa moja, kioo pamoja bafu lenye choo ndani. Nikaufunga mlango wa kwa ndani kisha nikazimwaga pesa zote kitandani pamoja na vipande vya madini ya dhahabu. Nikaanza kuzihesabu pesa hichi na kila kibunda kimoja kina dola za kimarekani elfu hamsini na kibunda na ninavibunda stini katika begi langu ambavyo ni sawa na dola milioni tatu za Kimarekani. Nikarudisha kila kitu ndani ya begi kisha nikaingia bafuni na kuoga.

Siku nzima ya leo tukashinda ndani huku Charity akipiga chakula ambacho kwenye maisha yangu ndio mara yangu ya kwanza kula.

“Unaitwa ugali, na hii ni bamia”

“Huu ugali unatengenezwa na nini?”

“Mahindi yaliyo kauka, yanapukuliwa na kusagwa kwa mashinde. Hata Nigeria, huwa wanakula sana hichi chakula?”

“Ngoja kwanza kupukuchuliwa ndio nini?”

“Kwa lugha rahisi sijui nisemeje, ila ni vile mahindi yanavyo tolewa kwenye magunzi yake”

“Sawa sawa nimekuelewa”

Tukaendelea kula chakula hichi cha asili, tulipo maliza, tukazungumza mambo mawili matatu huku akiniahidi siku inayo fwata atanitembeza katika jiji hili la Dar es Salaam ili niweze kulizoea kwa haraka sana. Tukaagana na kila mmoja akaingia kwenye chumba chake na kulala. Asubuhi nikawa mtu wa kwanza kuamka, nikakagua kiasi cha pesa zangu kwenye begi na kukuta kama zilivyo, nikatoka nje ya nyumba hii na kuanza kuizunguka kwa ajili ya kuweza kutambua mazingira ya hili eneo ili hata kama linatoke tatizo basi nitajia ni jinsi gani ninaweza kukimbia. Miguno ya kimahaba inayo tokea kwenye dirisha la Charity ikanifanya nisimame kwa muda pembezoni mwa dirisha hilo huku nikisikilizia miguno hiyo.

‘Mumewe amerudi?’

Nilijiuliza swali pasipo kupata majibu ya ainayoyote. Uvumilivu ukanishinda na kujikuta nikinyata hadi dirishani na kufungua dirisha hili la kioo, kwa tahadhari kubwa nikafunua pazia na kwa bahati nzuri kwa mkao alio kaa Charity amenipatia mgongo jambo ambalo si rahisi kwa yeye kuniona. Nikabaki nikiwa nimejawa na mshangao kwa maana anajihudumia yenye mwenyewe kwa kusugua kitumbua chake huku masikioni mwake akiwa amevaa earphones.

“Nakoj…..aaa mume wangu”

Charity alizungumza huku akitemeka mwili mzima. Hapa nikagundua anazungumza na mume wake kwa kupitia simu. Nikameza fumba zito la mate kisha nikarudishia pazia hii na kurudi eneo la mbele la hii nyuma. Ili nizitoe hisia za matamanio kwa Charity nikaanza kufanya mazoezi mepesi mepesi.

“Ohoo kumbe umesha amka?”

Sauti ya Charity ikanistua kidogo, nikageuka na kumtazama mlangoni alipo simama. Amejifunga tenge ambalo limeyaacha mapaja yake wazi kwa asilimia fulani hivi.

“Yaa nimeamka, vipi wewe?”

“Mimi nipo safi, vipi niaandae kifungua kinywa au tuende tukanywe mjini?”

“Vyoyote?”

“Basi ngoja nijiandae kisha twende mjini. Nawe jiandae basi”

“Sawa”

Charity akageuka na kuingia ndani, kwa jinsi anavyo tembea na kutetemeka kwa makalio yake kukanifanya hisia zangu kurudi upya na kushindwa kabisa kumzuia jogoo wangu kusimama kiasi.

‘Kweli wanawake wa Kitanzania wamejawaliwa Mungu wangu’

Nilizungumza huku nikirudi ndani, nikaingia chumbani kwangu. Nikagairi kuoga na kutoka chumbani humu na kusimama mlangoni mwa chumba cha Charity, nikagonga kwa muda na akafungua mlango.

“Vipi?”

“Sina nguo za kubadilisha?”

“Kwani kwenye begi lako hakuna nguo?”

“Yaa hapa ninaweza kupata wapi nguo?”

“Mmmm kuna umbali kidogo, ila ngoja nimpigie simu dereva taksi wangu mmoja aje kukuchukua akupeleke dukani”

“Sawa”

Charity akaurudi ndani, baada ya muda akanijulisha dereva yupo njiani anakuja hapa nyumbani. Baada ya dakika kama nane hivi dereva akafika getini, nikaingia chumbani na kutoa noti kumi za dola mia. Nikalifunga begi langu vizuri na kuliingiza chini ya uvungu wa kitanda huku nikiweka mtego ambao kama Charit ataligusa basi nitaweza kufahamu.

“Musichelewe, nimemueleza akupeleke kwenye maduka ya nguo nzuri za kiume”

“Sawa”

Nikatoka ndani humu na kuingia kwenye taksi hii. Safari ikaanza huku nikijitahidi kumuuliza dereva maswali kwenye kila sehemu ambayo tunapita. Tukaingia kwenye moja ya duka, nikachagua suruali tano, tisheti tano na mashati mawili.

“Ni kiasi gani?”

“Zote zitakuwa ni laki tatu na shirini”

“Ni sawa na dola kiasi gani?”

“Mia mbili”

Muhudumu huyu wa duka alizungumza huku akinitazama usoni mwangu kwa macho ya wasiwasi.

“Mbona hujiamini?”

“Hamna kaka ndio bei zake”

Nikatoa noti mbili za dola mia kisha tukaanza safari ya kurudi nyumbani. Nikaingia ndani na kumkuta Charity akiwa amekaa sebleni akitazama tv. Taarifa niliyo ikuta akiitazama ikanifanya nisite kidogo na kuanza kuifwatilia.

“Dany amemua makamu wa raisi wa Marekani aliyekuwa amemshikilia wiki zilizo pita”

Charity alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Sababu ya kumuu?”

“Ametuma video hiyo ipo kwenye mitandao ya kijamii”

“Hembu nisaidie kuitafuta kisha nitunzie”

“Sawa sawa”

Nikaingia chumbani kwangu na kukuta begi langu likiwa lipo tofauti na vile nilivyo kuwa nimeliweka, nikalitoa na kulifungua ndani na kukuta pesa na vipande vya madini vikiwa kama vilivyo viacha. Nikaoga kisha nikajiandaa kwa matembezi ya siku ya leo huku nikibeba pesa ya kutosha kwa matembezi ya leo. Tukatoka ndani humu na Charity akafunga nyumba na funguo moja akanikabidhi mimi, tukaingia ndani ya taksi ya dereva huyu aliye nipeleka madukani kisha safari ikaanza taratibu.

Tukazunguka katika maeneo mengi sana ndani ya jiji hili huku Charity akinionyesha maeneo muhimu sana ya jiji hili, ikiwemo kumbi za starehe. Muda wa mchana tukapata chakula kwenye hoteli moja kubwa iitwayo Serena.

Baada ya chakula hichi tukaendelea na matembezi yetu na majira ya saa nne usiku tukaingia kwenye ukumbi uitwao Bilcanas.

“Kuwa makini kama unahitaji kuchukua mwanamke nijulishe nikutafutie”

Charity alizungumza kwa kuninong’oneza huku tukijikatiza katikati ya watu.

“Sawa”

Tukatafuta eneo moja, tukaagizia vinywaji na kuanza kunywa. Kwa jinsi wanawake wanavyo serebuka ndani ya huu ukumbi nikakumbuka enzi zangu nipo nchini Nigeria. Pesa ya mama yangu ilinitia juuri kubwa sana kiasi cha kunifanya niweze kumchukua mwanamke wa aina yoyote na hata nikifahamu kwamba huyu ni mwanamke wa mtu basi kwa kutumia pesa na ushawishi wa uzuri wangu nilio urithi kwa asilimi themanini na tano kwa mama yangu basi niliweze kufanya mambo ya ajabu sana.

“Mbona unaonekana kujawa na mawazo au hujapenda kuwepo katika eneo hili?”

“Hapana nipo sawa mpenzi”

“Mmm unaonekana kukosa raha”

“Usijali”

Tukaendelea kunywa bia nyingi sana huku muda mwingi nikiwa makini sana kuhakikisha katika eneo hili tunakuwa salama. Jamaa mmoja aliye valia suti nyeusi huku nyuma yake akiwa ameongozana na walinzi wake wawili wenye miili mikubwa kama walinzi wa hii club wakasimama mbele yetu huku jamaa huyu akijishau kwa kuweka tabasamu pana usoni mwake. Mlinzi wake akamvutia kiti kimoja na jamaa kaka.

“Unataka nikupe kiasi gani dogo, uniachie huyo manzi wako?”

Jamaa huyu alizungumza kwa dharuau huku akinitazama kwa kunikejeli sana.

“Samahani unasema?”

“Nikuachie kiasi gani, unipatie huyo mwanamke, kwa maana unaonekana huna hadhi ya kuwa namwanamke kama huyo”

“Samahani nina waheshimu, huyu ni mke wangu na si malaya. Tazama kule kuna malaya wengi sana wanajiuza, unaweza kwenda kumchukua mmoja wao ukamtumia”

“Hahaaaa….hata maneno yako yanaonyesha dhairi kwamba huna hadthi ya kumuoa mwanamke kama huyo. Nakupa dola elfu tano uniachie huyo mwanamke”

“Unaonaje hizo pesa ukasubiria siku ya ijumaa au jumapili ukaenda kutoa misaada makanisani au misikitini”

Nilizungumza kwa kujiamini huku kwa jicho la kuiba nikimtazama Charity jinsi anavyo tetemeka kwa woga.

“Hiyo ni dharau sasa”

“Wewe ndio mwenye dharau. Na hii ni kauli yangu ya mwisho. Nyanyuka eneo hili nenda kajiokotee wanawake wale pale wanatafuta wateja toka tunaingia hapa sawa”

“Hhaaahaa”

Jamaa alicheka huku kwa ishara akimuamrisha kijana wake mmoja kumsogelea Charity ili amnyanyue, hatakabla hajamshika mkono Charity, nikavishika vidole vyake na kwa nguvu zangu zote nikavipindisha vidole vyake viwili na vikavunjika na kumfanya mtu huyu kupiga ukelele ambao umemezwa na sauti ya mziki mkubwa sana unao endelea kusikika ndani ya club hii. Nikavunja chupa moja ambayo haina bia, mlinzi wake wa pili alivyo jaribu kunivamia kwa kurusha ngumi, nikamchoma nayo katika eneo la mbavuni mwake na kumfanya ajikunje kisasa sawa. Jamaa kwa haraka akatoa bastola na kuninyooshea huku akinitazama kwa kuhema, kwani majitu yake aliyo kuwa anayategemea yote yapo chini yakiugulia maumivu makali sana.

“Charity simama nyuma yangu”

“Ole wako usimame, nitakuua”

Mwanaume huyu alizungumza huku akimkazia macho Charity. Akatoa simu yake mfukoni mwake, akaiminya minya huku akinitazama kwa macho yaliyo jaa hasira.

“Niongezee vijana ishirini humu ndani, kuna mshenzi amenizingua”

Baada ya kumaliza kuzungumza na simu yake akairudisha mfukoni mwake na kuishika bastola yake kwa mikono yake miwili kwa msisitizo ambao siwezi kufanya chochote kwa mita hizi chache tulizo simama kwani nikifanya kosa lolote ninaweza kumsababishia mauti Charity ambaye hadi sasa hivi mwili mzima unamtetemeka huku machoni mwake akimwagikwa na machozi mengi sana.



Msichana mmoja aliye ona hili tukio akapiga kelele huku akilalama kwamba kuna mtu mwenye bastola ndani ya ukumbi huu. Kitendo hicho kikamfanya jamaa huyu kuweweseka sana, nikajirusha hewani kwa juhudi zangu zote, nikamtandika mateke mafili huko moja likiupiga mkono wenye bastola yake na kuifanya ianguke chini. Watu wakazidi kutawanyika, nikamshika Charity mkono na tukachanganyika kwenye kundi kubwa la watu wanao kimbilia nje. Tukafanikiwa kutoa nje, kwa haraka tukaingia kwenye moja ya taksi ya kukodi.

“Tuondoke tuondeke”

Nlimumuambia dereva taksi huyu, akawasha gari na kuondoka eneo hili kwa spidi kali sana.

“Kuna nini kilicho tokea?”

“Vurugu”

Tukiwa njiani tukapishana na gari nne za askari zikielekea eneo la tukio.

“Duu kimenuka FFU hawa”

Dereva alizungumza huku akitazama gari hizi zinavyo pita kwa kasi sana.

“Tupeleke Nemax”

Charity alizungumza huku akishusha pumzi nyingi sana.

“Sawa”

“Ndio wapi?”

“Utapaona”

Tukafika katika moja ya hoteli, Charity akatoa pesa kwenye pochi yake na kumkabidhi dereva taksi huyu. Tukashuka na kuingia kwenye hoteli hii, kazi yangu ikawa ni kutazama nje ya hii hoteli, dereva taksi alivyo ondoka nikatoka nje kuhakikisha kama kuna usalama wa kutosha kwa maana kusema kweli siifahamu hii nchi vizuri na ndio kwanza ni mgeni.

“Twende ndani”

Charity alizungumza huku akinikabidhi kadi ya kufungulia mlango. Tukaingia kwenye lifti na moja kwa moja tukaelekea hadi gorofa namba tano. Tukatoka ndani ya lifti na kuingia kwenye chumba alicho kodisha.

“Kwa nini hatujaelekea nyumbani?”

“Hapa kuna usalama zaidi. Laiti tungeenda na yule dereva nyumbani ingekuwani rahisi kwa yeye kutoa siri ya sisi wapi tulipo kwa maana anaonekana ni kijana wa pale pale”

“Kama vipi tuondoke hotelini hapa kwa maana kama ni kutoa taarifa atawaelekeza hapa”

Charity akanitazama kwa muda kisha akaelekea mlangoni akionekana kukubaliana na ushauri wangu. Akafungu mlango na tukaingia tena kwenye lifti na kuanza kushuka chini.

“Tunakuja”

Charity alizungumza huku akimkabidhi muhudumu kadi hii ya kufungulia mlango. Tukaanza kutembeaa eneo la nje, tukafika sehemu wanayo kodisha taksi, tukaingia kwenye taksi moja na Charity akamuelekeza dereva huyo ni wapi atupeleleke. Saa yangu katika simu inaonyesha ni saa kumi kasoro usiku, pombe zote tulizo kunywa zimetutoka vichwani mwetu, kwani sekeseke la kuponyoka kufa si mchezo kwa kweli.

Tukafika nyumbani kwa Charity tukashuka na akamkabidhi dereva pesa yake kisha tukaingia ndani huku kila mmojaa kiwa kimya. Charity akajitupa kwenye moja ya sofa huku akishusha pumzi sana.

“Wale waseng** wangetua unajua”

Charity alizungumza huku akiipandisha miguu yake juu ya sofa hili.

“Yaa unawafahamu?”

“Niwafahamu wapi best, yaani wee acha wamenikata stimu zangu zote za pombe”

“Pole sana ila siku nyingine acha woga”

“Mmmm ila asante kwa kunitetea si kwakuipiga mibaunsa ile. Kumbe upo vizuri ehee?”

“Kiasi chake”

“Ahaa…wapi. Yaani nilijua leo naenda kubakwa mubashara, ila ulivyo lipiga lile baunsa la kwanza nikajua Yes nina kidume hapa”

“Hahaaa”

“Ngoja”

Camila alisimama na kuingia jikoni, akarudi akiwa ameshika chupa moja ya pombe kali(whiskey) iitwayo Old Fashioned.

“Hii ni whiskey bora sana duniani”

Charity alizungumza huku akiweka chupa na glasi hizo mezani kisha akaondoka baada ya mdu akarudi na bakuli kubwa lililo jaa mabarafu pamoja na vipande kadhaa vya machungwa.

“Ulipo kunywa kule hujatosheka?”

“Wapi nitosheke vipi jamani. Pombe yote imekata kichwani rafiki yangu. Unahisi nitalalaje?”

“Unaonekana una kunywa sana”

“Sana, kazi ninayo ifanya mimi ni ngumu sana. Kusafiri angani tu kwa masiku mengi inachosha sana. Ndio maana nakunywa vitu vikali kama hivi”

“Hivi ukinywa huchanganyikiwi?”

“Hata siku moja, na nimejifunza kunywa pombe kali nilipo kuwa nchini Russia. Kule kuna baridi kali kishenzi, ili kukata baridi kunakunywa glasi zako mbili za whiskey mwili mzima unachemka.”

“Hahaaa haya bwana”

Charity akaniandalia kinywaji hichi huku akiwa amekiweka vipande vipande vya bafafu. Taratibu tukaanza kunywa pombe hii huku tukitazama movies iitwayo Fast and Furiuos 8.

“Hawa wajinga wanaendesha magari sana”

Charity alizungumza huku macho yakiwa yamemlegea. Picha ya asubuhi nilivyo muona akijichezea mwili wake, ikaanza kujirudia akilini mwangu. Hisi za mapenzi zikaanza kunipanda, taratibu nikajikuta nikinyanyua kwenye sofa nililo kalia na kukaa kwenye sofa lake huku miguu yake nikiiweka juu ya mapaja yangu.

“Umechoka kukaa kwako?”

“Yaa nimechoka mama”

“Hahaaa”

Tukaendelea kunywa huku tukizidi kutazama filamu hiyo.

“Randy”

“Mmmmm”

“Rafiki yangu umasikini ni mbaya sana”

“Kwa nini unazungumza hivyo?”

“Nazungumza hivyo kwa maana nimejikuta nikifunga ndoa na mwanaume ambaye kwanza sio umri wangu, pili hanitoshelezi, tatu yaani sioni hata hamu ya kutembea naye”

Maneno ya Charity yakanifanya nimtazame kwa muda huku nikishusha pumzi taratibu kwani kama ni sungura mjanja sasa anaanza kuingia kwenye mtego.

“Kwani yupoje mume wako”

Charity akachukua pochi yake mezani, akatoa simu yake na kuanza kuiminya minya. Akanigeuzia simu yake na nikaona picha ya mzee ambaye kwa haraka haraka ana umri kama miaka themanini hivi.

“Huyo ndio mume wangu, anaitwa Domenick, yaani mzee anapesa chafu Marekani. Ana bonge moja la Cassino katika jiji la Las Vegas. Katika matajiri pale Marekani, huyo mzee ni namba tatu, ana utajiri wa dola bilioni thelathini na tano”

“Mmmmm”

“Weee acha tu. Yaani amenipata kimagumashi kishenzi. Kutokana na shida zangu, mtoto wa Kipare mie ninaye penda pesa kuliko kula, nikakubali. Huwezi amini ndani ya mwaka mmoja tu toka niwe naye, nimewajengea wazazi wangu gorofa la dola milioni moja na nusu sawa na kama shilingi bilioni tatu hivi”

“Duu”

“Sikuishia happ nimewafungulia miradi kibao na hivi ninavyo kuambia namalizia kumjengea mama yangu shule ya msingi kwani yeye ni mwalimu.”

“Hongera sana, ukifanikiwa kumaliza mipango yako kwa huyo mzee hakikisha kwamba una apiga chini?”

“Haa huo ndio mpango wangu. Ya nini kizee kinifie kiunoni. Ila kina wivu balaa, hapa nimefanya kumdanganya kwamba mama anaumwa ndio maana nimekuja Tanzania la sivyo ningeenda Marekani likizo hii fupi”

Charity alizungumza huku akipiga mafumba kadhaa ya pombe hii kali hadi muda mwengine anajikuta akifumba macho akiwa anaimeza pombe hii.

Nikauweka mkono wangu wa kushoto juu ya paja lake, taratibu nikaanza kuliminya, ila Charity akausogeza mkono wangu.

“Mmmmm mimi sio wa kirahisi namna hiyo”

“Samahani”

“Bila samahani, ila usidhubutu kunitamani. Utakufa na utanivurugia mipango yangu kwa mzee”

“Nitakufa kivipi?”

“Wewe jua utakufa tu mambo mengine usitake kujua sana”

Nikajikuta nikikaa kimya, nikaishusha miguu yake juu ya mapaja yangu kisha nikanyanyuka.

“Unakwenda wapi sasa?”

“Kulala”

“Randy mbona una habari za kitoto”

“Kivipi?”

“Kukuambia utakufa ndio umepatwa na usingizi?”

“Sio hivyo”

“Ila”

“Nahitaji muda wa kupumzika, kuna mipango yangu nataka kuipanga kwanza”

Charity akanishika mkono wangu wa kulia na kunikalisha chini kwa nguvu. Akanitazama machoni mwangu kisha akanilaza kwenye hili sofa na kupanda juu yangu.

“Nimekuambia utakufa pale mzee atakapo sikia mimi na wewe tuna mahusiano, atakutafuta popote duniani na kuhakikisha anakuondoka duniani, kwa maana ana nipenda kuliko hata pesa yake anavyo ipenda”

“Hilo ndio linakuogopesha?”

“Ndio, atakuua?”

“Kabla hajaniua mimi, basi mimi ndio nitakuwa wa kwanza kumuua”

Charity akanitazama kwa muda kidogo.

“Kweli?”

“Ndio”

Charity akaanza kuninyonya midomo yangu kwa fujo sana huku akitoa mihemo mizito sana. Nikamvua kishati chake na kuanza kuyatomasa maziwa yake yaliyomo ndani ya sidiria. Charity akaanza kuninyonya shingo yangu, huku akiendelea kuhema sana. Nikafanikiwa kumvua siridia na kuendelea kutomasa maziwa yake. Nikambeba huku miguu yake akiwa ameipitisha kiunoni mwangu. Nikaanza kutembea kuelekea chumbani kwake huku midomo yetu ikiwa na kazi ya kuchezesha ndimi zetu.

Nikambwaga Charity kitandani, nikafungua mkanda wa suruali yake, nikamvua suruali na kumuacha na chupi tu. Nikavua nguo zangu na nikapanda kitandani huku jogoo wangu akiwa amesimama kama namba moja. Charity akamshika jogoo wangu na kuanza kumnyonya kwa fujo. Sikutaka makeke mengi sana kwake na taratibu nikaanza huhuli ya kukila kitumbua chake. Mtanange huu ukaanza kumuelemea Charity kwani kila ninalivyo zidi kumpelekea mashambulizi ndivyo jinsi alivyo zidi kushindwa kuyapokea.

“Randy Pooooo…..aaa…s…..iis…….utaniua….ohoo”

“Ngoja nakaribia”

Nilizungumza huku nikiendelea kuongeza kasi, ukijumlisha pombe nilizo kunywa mchanganyiko, zimenifanya nichelewe kukoj****a kwa haraka.

“Nakufa mwenzio”

Charity alizungumza huku ajijitahidi kujitoa mikononi mwangu, ila nikazidi kumbana kiuno chake kisawa sawa na ukijumlisha jinsi alivyo inama ndio kabisa anashindwa hata kutoka kiunoni mwangu. Waarabu weupe wakatoka mpululizo na taratibu nikamuachia Charity huku nikisikilizia utamu ambao wanaume wote dunia wanaupata wakifikia eneo hilo. Charity akajilaza chali huku akihema sana, nikajilaza pembeni yake huku nikisikilizia mapigo ya moyo yanavyo dunda.

“Toka nizaliwe, sijawahi tomb*** kama hivi Randy”

“Kweli?”

“Haki Mungu vile. Isitoshe nipo nah aka kazee yaani ndio kabisa mbo** yake haifiki hata robo yak um** yangu”

“Hahaa pole sana”

“Mmmmm ila wewe nilihisi unanitoa kizani changu jamani. Ahaaa….si kwa kunitom** huko”

Charity alizungumza huku akimshika jogoo wangu taratibu.

“Tuendelee?”

“Nyooo utaniua hivi nikisema utaniua huelewi”

“Basi acha kumshika, kwa maana atasimama sasa hivi tena”

Charity akautoa mkono wake kwenye jogoo wangu. Akaninyosha lipsi zangu taratibu huku akinitazama usoni mwangu.

“Umenipa kitu ambacho hakika kimenifanya nijihisi mwanamke”

“Nashukuru”

“Yaani siku zote kazi yangu ilikuwa ni kujisokomeza mijidoli, ili maradi nikate kiu yangu. Ila kwa penzi hili hakika kuanzia leo naichoma moto mijidoli yote”

“Hivi itakuwaje mzee wako akifahamu?”

“Atafahamu vipi, ikiwa penzi letu litakuwa ni siri”

“Siri ni mtu mmoja?”

“Najua, ila tukishirikiana kuitunza itakua kubwa”

“Sawa”

Charity akashuka kitandani na kuingia bafuni, kwa kweli Charity ni mtamu. Nimetembea na wanawake wengi sana, ikiwemo Farida, ila utamu wake amemzidi Farida. Nikanyanyuka na mimi nikaingia bafuni humu, tukaoga na kurudi chumbani. Farida akabadilisha mashuka na kuweka mengine. Tukalala huku Charity akikiweka kicha chake kifuani mwangu.

“Una mpango gani na Dany?”

Charity alizungumza kwa sauti ya chini sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Nahitaji kumuu”

“Kweli?”

“Kuna mtu ambaye anaweza kunisaidia kufahamu ni wapi alipo Dany na kukipambazuka nitahakikisha kwamba ninawasiliana naye atueleze ni wapi alipo.”

“Mtu huyo ni nani?”

“Utamjua kukipambazuka”



Shahuku ya kuhitaji kumfahamu ni nania mbaye ataniwezesha kumpata gaidi Dany alipo, ikazidi kupamba moto na kujikuta nikishindwa kupata hata lepe la usingizi. Charity akaendelea kukoroma kifuani mwangu huku mkono wangu mmoja ukiwa na kazi ya kumpapasa papasa katika kila kona ya mwili wake. Majira ya saa kumi na moja alfajiri nikahisi kama hatua za mtu sebleni. Taratibu nikamlaza Charity kichwa chake juu ya mto kisha nikashuka kitandani. Nikavaa suruali yangu na kuanza kunyata hadi mlangoni, nikataka kushika kitasa ila mtu huyo aliyopo nje ya mlango huo akawahi kukiminya kitasa na akafungua mlango jambo lililo nifanya nistuke sana.

Mzee ambaye Charity alinieleza akaingia humu ndani huku akiwa amevalia koti kubwa jeusi, nikatamani kumvamia, ila mwili wote ukaishiwa nguvu kabisa kwani sikutegemea kukumbana na fumanizi kubwa kama hili. Mzee huyu akatazama shati langu lilipo chini, akachomoa bastola huku akigeuka taratibu na kunitazama nyuma ya mlango jinsi nilivyo jibanza huku jasho jingi likiendelea kunimwagika.

“Wewe mtoto wa malaya”

Mzee huyu alizungumza na kupiga risasi moja, kitendo cha kuanguka chini, risasi ikapiga ukutani na kumfanya Charity kukurupuka kitandani huku akihema sana. Wakaingia wanaume wanne wenye bunduki mikononi mwao na wana asili ya Kimarekani. Wakaniweka chini ya ulinzi huku wakinipiga ngumi na mateke mfululizo. Charity hakuweza hata kunyanyuka kitandani alipo keti, mzee huyo akamfwata na kumtandika kofi zito hadi mkojo ukamtoka.

“Nikupe nini wewe malaya”

Mzee huyu aliendelea kufoka huku akimtazama Charity usoni mwake. Charity hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu sana.

“Mtooeni nje huyo nguruwe”

Mzee huyu alizungumza kwa uchungu sana huku mwili mzima ukimtetemeka. Nikabebwa mzima mzima na wanaume hawa wenye nguvu zao. Nikatolewa nje na kuingizwa ndani ya boti ya gari, nikafungwa mikono yangu pamoja na miguu yangu kwa pingu na nikashindwa kufanya chochote. Wakafunga buti hii ya gari na kujikuta nikijutia ni kwa nini nimefanya upuuzi nilio ufanya na Charity. Kwenye maisha yangu nilisha wahi kusikia kwamba mke wa mtu ni tatizo kubwa sana, ila niliweza kuyapuuzia maneno hayo ila hakika leo yamenikumba.

Baada kama ya nusu saa nikasikia gari likiwashwa na likaanza kuondoka katika eneo hili. Sikufahamu ni wapi ninapo pelekekwa na kwa haraka picha niliyo ijenga kichwani mwangu ni kupiga hadi kufa kwangu.

‘Ehee Mungu naomba unisamehe mimi makosa yangu, sikukusudia kufanya niliyo yafanya’

Niliomba kimoyo moyo huku machozi yakinilenga. Gafla nikasikia mtikisiko mmoja mkubwa sana ulio nifanya nibamizike ndani ya hili gara na kusababisha maumivu makali kwenye kichwa changu. Mbamiziko huo ukajirudia tena hapa ndipo nikagundu kwamba kuna tatizo kati hili gari. Milio ya risasi ndio ikazidi kunidhibitishia kwamba hili linalo tokea hivi sasa ni tatizo moja kubwa sana, gafla gari hili likaanza kubingirika, na kunifanya nami nitingishwe kisawa sawa ndani ya hili gari. Gari hili likakaa sawa na kutulia, nikasikia milio ya risasi mbili iliyo nifanya nizidi kujawa na woga. Mlango wa sehemu nilipo hifadhiwa ukafunguliwa, sikuamini macho yangu mara baada ya kumuona Dany akiwa amevalia nguo kama alizo kuwa amezivaa siku anakuja kumteka makamu wa raisi wa nchi ya Marekani. Dany akanishika mkono na kunivuta nje ya gari hili na kunibwaga chini.

Eneo tulilipo ni porini sana na walinzi wote waliomo ndani ya hili gari wameuwawa kwa kupigwa risasi. Dany akanitazama kwa muda huku pembeni yake akiwa amesimama dada mmoja ambaye muda wote amekaa akinitazama huku ametabasamu.

“Muda mwengine uwe makini, hii ni Tanzania na si Nigeria”

Dany alizungungumza huku akizikata pingu nilizo fungwa kwa kuzipiga risasi pasipo kukosea. Nikajawa na kigugumizi kikubwa sana, kwani adui ninaye mtafuta ndio huyu hapa mbele yangu, imekuwaje amenisaidia na kwa nini anisaidie.

“Kwa nini umenisaidia?”

Dany hakunijibu chochote zaidi ya kuendelea kutembea huku akipandisha kilima hichi ambacho kinaonyesha tulitokea juu kwa kubingirika kwa gari hili hadi hapa chini tulipo fika.

“Hei wewe Dany gaidi kwa nini umeniokoa mpumbavu wewe”

Nilizungumza kwa hasira huku nikijaribu kumfwata. Msichana aliye ongozana na Dany akasimama na kugeuka. Akanitazama kwa macho makali, kwa kasi ya ajabu akanifwata akanishika shingoni mwangu kwa mkono wa kulia, akanisukumiza kwa nguvu hadi kwenye moja ya mti, nikajibamiza mgongo wangu na kukaa chini mzima mzima. Akanifwata tena akaninyanyua na kunivuta karibu kabisa na sura yangu.

“Ukirudia tena siku kumuita baba yangu ni mpumbavu, nitaondoka na kichwa chako. Umenisikia wewe mjinga?”

Sikuamini uzuri wamsichana huyu anaweza kuwa ni jasiri na hatari namna hii.

“Nimekuelewa”

“Na ole wako umueleze mtu juu ya hili swala au kumuona DANY, popote ulipo, iwe ardhini, angani au majini nitahakikisha kwamba nina kusaka na nikikupata, nitakuvunja kiungo chako kimoja baada ya kingine sawa”

Nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba nimemuelewa msichana huyu. Akaniachia na kunifanya nivute pumzi nyingi saha huku jicho likiwa limenitoka kwani nimepunyuka punyuka kufa. Nikaanza kusikia ving’ora vya gari za polisi vikija katika eneo hili.

“Shitiii”

Nilizungumza huku nikitafuta sehemu ya kutorokea. Nikanza kukimbia katikati ya msitu huu huku nikijitahidi kuhakikisha kwamba siingii kwenye mikono ya polisi. Nikafika kwenye moja ya shamba la hahidi makubwa, hapa kidogo nikapata unafuu wa kuhema huku nikitazama nyuma nilipo tokea. Nikasikia milio ya mbwa wakibweka kwa mbali jambo lililo nifanya niisikilizie vizuri na kwa umakini wa hali ya juu. Kadri jinsi muda unavyo zidi kwenda ndivyo jisni nilivyo zidi kuisikia milio hiyo inavyo kuja kwa kasi.

“Pumbavu”

Nikaendelea kukimbia huku nikiwa tumbo wazi na miguuni mwangu nikiwa sijavaa chochote. Nikazidi kukatika kwenye mashamba ya watu huku nikijaribu kutafuta msaada ila nikashindwa kabisa kupata msaada wa mtu yoyote. Milio ya mbwa bado inaendelea kuniandama, na inaonyesha kwamba hawa ni mbwa wa polisi, ambao wanafwata arufu yangu kila ninavyo jaribu kukimbia.

“Heii”

Nilimuita dereva pikipiki mmoja aliye katiza katika hii barabara ya vumbi, ila dereva huyu aliishia kunitazama na kuendelea na safari yake tena akaongeza mwendo kasi wa pikipiki yake.

“Ohoo Mungu wangu”

Nilizungumza huku nikianza kukimbia kwenye hii barabara huku nikiwa nimechoka, kiasi cha kuanza kukisikia kifua changu kikitoa harufu ya damu.

“Heii lifti”

Nilizungumza huku nikipungua mikono hewani, dereva wa gari hii ndogo akasimamisha, nikamkimbilia hadi alipo na nikamkuta ni mbibi wa miaka kama stini na tano hivi.

“Una tatizo gani kijana?”

Bibi huyu aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kuna majambazi wana nifukuza”

“Pole sana ingia kwenye gari tuondoke”

Bibi huyu alizungumza huku akinitazama, nikafungua mlango wa gari lake hili na taratibu tukaanza kuondoka.

“Huu msitu una majambazi wengi sana. Pole”

“Asante”

“Kichwnai mwako unavuja damu”

Bibi alizungumza huku akinionyesha sehemu ya nyuma ya kichwa changu, nikajigusa na kukuta nina damu nyingi ikinimwagika.

“Ohoo Mungu wangu”

“Ngoja nikuwahishe hospitalini”

Bibi huyu alizungumza huku akijitahidi kuongeza mwendo kasi wa gari lake. Tukafika kwenye moja Zahanati ndogo, tukashuka kwenye gari na kwa bahati nzuri huyu bibi anafahamika na watu wengin wanamuita nesi nesi.

“Muhudumieni huyu kijana, garama zote niandikieni mimi”

“Sawa mama Ruben”

“Kijana, ninakwenda kijiji kinacho fwata, kuchukau kuku wangu, sawa”

“Sawa mama”

Bibi huyu akaondoka na kuniacha na nesi huyu tuliye mkuta hapa. Nesi akaanza kunihudumia taratibu huku midundo ya mapigo yangu ya moyo ikisikika vizuri tu.

“Mbona mapigo yako ya moyo yakwenda kasi sana kaka?”

“Ni kawaida?”

“Kawaida na mbona huku mngongo una michubuko mingi sana?”

“Ni mikubwa?”

“Hapana sio mikubwa sana, ila umekwaruzika kwaruzika”

“Nilipata tatizo kidogo. Hapa tulipo panaitwaje?”

“Magwepande?”

“Nini?”

“Magwepande vipi, ndio mara yako ya kwanza kufika nini?”

“Yaa”

“Au ulikuwa umetekwa?”

“Eheee?”

“Au ulikuwa umetekwa? Kwa maana huku majambazi huteka watu huko mijini na sehemu mbali mbali kisha wanakuja kuwatupa kwenye msitu huu”

Nesi alizungumza kawaida, sana kana kwamba maenelo anayo nipatia hayashangazi. Simu ya nesi huyu ikaanza kuita akauweka mkasi pembeni alio kuwa akikatia bandeji ya kunifunga, akaipokea.

“Niambie mpenzi wangu?

“Yaa nipo kazini”

“Ndio”

“Ndio nipo naye hapa nampatia matibabu”

Kauli ya nesi huyu ikanistua kwa haraka nikanyanyuka na kuuchukua mkasi huu na kumtishia kwamba nitamchoma kama atapiga kelele au atamonyeshea hatari yoyote tu anaye zungumza naye.

“Shiiii….nipe simu”

Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikimkazia macho nesi huyu. Nesi kwa woga akanipatia simu yake, nikaiweka masikioni mwake.

“Yupo Zahanati twendeni”

Nilisikia sauti ya kiume ikizungumza jambo likilo nifanya niongope sana. Nikakata simu hii na kumtazama nesi uosoni mwake.

“Ni nani?”

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG