Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 2/10

 

 

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 2 KATI YA 10

 


“Sasa fanya iwezekanavyo, ninaihitaji kuondoka na mzee hivi sasa”

“Sawa sawa”

Daktari alizungumza huku akizidi kutetemeka, mwanajeshi mmoja akachomo bastola yake kiunoni na kinipatia.

“Hakikisheni munawazuia”

“Sawa mkuu”

Nikaingia ndani ya chumba, daktari wakamuandaa mzee haraka haraka.

“Mke wangu ninakuomba ujikaze sawa”

Nilizungumza huku nikimshika Yemi mashavu yake huku nikiwa nimekazia macho kwani muda wote huu anatetemeka mwili wake. 

 

“Umeniaelewa?”

“Ndio honey”

Nikaikoku bunduki yangu vizuri, nikafungua mlango na kuchungulia nje, wanajeshi wote nilio waacha nje dakika kadhaa wote nikakuta wamefariki dunia, na kwenye hii kordo hakuna mtu yoyote jambo lililo nifanya nirudi ndani huku nikiwa na wasiwasi mwingi.

“Kuna nini?”   

Yemi aliniuliza huku akitetemeka mwili wake.

“Wanajeshi wote wamekufa”   

“Ohoo Mungu wangu”

“Shiiiiii”

Nilimnyamazisha Yemi baada ya kusikia miguu ya watu wakinyata, kwa haraka nikatazama ndani ya hichi chumba, nikaona mtungi wa gesi. Nikauchukua kwa haraka, kila mtu ndani ya chumba hichi akabaki akinishangaa.

 

“Jificheni”

Nilizungumza huku nikimtazama Yemi usoni mwake. Kwa haraa kila mtu akajibanza kwneye sehemu yake, nikabaki nikiwa nimesimama mlangoni, kwa haraka nikauufiringisha mtingi huu wa gesi chini, kuelekea kwneye kordo. Wavamizi hao wakaanza kushambulia kwa risasi.

“Musipige risasi”

Nilisikia sauti kubwa ya mmoja ya wavamizi hawa, kwa uwazi mdogo wa mlango nilio ucha, unaifanya kuuona mtungi wa gesi, taratibu nikafumba jicho moja huku nikiwa nimeunyooshea bastola yangu, kwa risasi mbili za uhakika zilizo tua juu ya mtingi huu wa gesi, ukaufanya kulipuka, na kusababisha mttemeko mkubwa huku vilio vya wavamizi hawa vikisikika, kwa haraka nikafungua mlango, kila mvamizi aliye hai, nikaahakikisha ninampiga risasi risasi ya kichwa na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake. Wavamizi hawa wapo sita na wamefunika nyuso zao na kubakisha macho yao tu, kwa haraka nikaanza kumvu mvua mmoja baada ya mwengine kinyago alicho jifunika usoni mwake. Kila niliye mfunua ana sura ya kimarekani, hapa ndipo nikaamini kwamba raisi Donald Bush amaeamua kutangaza vita na mimi. 

 

Nikaanza kugagua eneo zima la kutoka nje ya hii hospitali, nilipo hakikisha kwamba usalama upo wa uhakika nikarudi katika chumba walipo Yemi madaktari pamoja na baba yake.

“Tuondokeni”

Nilizungumza huku nikikishika kitanda cha Mzee Okocha, tukaanza kukivuta kuelekea nje, huku nikiwa makini sana. Tukafika sehemu yenye lilipo gari la wagonjwa, tukamuingiza mzee Okocha ndani ya gari.

 

“Mke wangu tangulieni nyumbani, kuna kazi nina imalizia hapa”

“Unasemaje Peter?”

“Umenisikia Yemi tangulieni nyumbani na baba kuna kazi ninaimalizia kukaa kwenu hapa kutahatarisha hali ya baba. Wewe dokta endesha gari”

“Sawa mkuu”

“P…..”

“Tafadhali Yemi nenda nyumbani”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimuingiza Yemi ndani ya gari na kuufunga mlango, daktari akawasha gari na kuondoka eneo hili. Nikato simu yangu mfukoni na kurudi nayo ndani huku nikiwa makini sana. Nikaanza kuchukua video ya maiti za Wamarekani hawa pamoja na wanajeshi wa mzee Okocha kisha nikajirekodi na mimi.

 

“Najua sina hatia katika hili, ila muheshimiwa raisi umenisukuma katika hili. Sikutarajia kwamba unaweza kutembea na mke wangu Hawa, kisha ukanitumia wanajeshi wako waje kuniangamiza, ila waliweza kuwaua wanajeshi hawa, wakiamini kwamba hata mimi wataweza kuniua kirahisi. Muheshimiwa raisi, usihitaji kuirudisha nchi yako katika dhama za Osama Bin Laden kwa maana kwa ujinga wako utapelekea melfu ya watu wako kuweza kuangamia kisa mwanamke, kama unajipenda ni bora kuachana na hii vita. Ulinituma kufanya kazi ya upelelezi, ila kuanzia sasa hivi muheshimiwa raisi, sinto weza kufanya hiyo kazi, nitaishi maisha yangu ya kawaida, na sinto hitaji kabisa kujihusisha na maisha ya kulipiza visasi, yaliyo pita acha yapite. Niawatakie maisha mema wewe na Hawa”

 

Baada ya kumaliza kuzungumza hivi, video hii nikamtumia raisi Donald Bush kupitia mtandao wa WhatsApp.  Nikatoka nje na kuingia kwenye moja ya gari na kuanza kufukuzia gari la wagonjwa huku akilini mwangu nikiwa na mawazo mengi sana ya kufikiria kitu alicho kifanya raisi Donald Bush.

‘Sinto mlipizia kisasi’

Nilijikuta nikizungumza hivyo, huku nikizidi kuendesha gari langu kwa kasi sana. Nikafanikiwa kuwafikia, nilicho kifanya ni kulipita kwa kasi na kuongoza msafara huu mfupi, uzuri wa kichwa changu huwa nikipita sehemu mara moja ni ngumu kunitoka kichwani mwangu. Tukafika katika jumba la mzee Okocha na kukuta wanajeshi wake wakiimarisha ulinzi mkali, wanajeshi wakisaidiana na madaktari hawa wawili tulio kuja nao, wakamshusha mzee na kumpeleka ndani, huku Yemi akifwata kwa nyuma.

“Muheshimiwa”

Mwanajeshi mmoja aliniita huku akisimama mbele yangu, akanipigia saluti kwa ukakamava.

“Ndio kaka unahitaji nini?”

“Kuanzia hivi sasa wewe ndio mkuu wa jeshi letu”

“Nani kasema hivyo?”

Mwanajeshi huyu akanikabidhi simu ndano yenye video inayo muonyesha mzee Okocha akizungumza.

 

“Watu wangu wa Boko haramu, ninaimani kwamba nimetengeneza hichi kikosi kwa miaka zaidi ya kumi na tano sasa. Nimekuwa nikiliongoza kuhakikisha ninapambana na rusha zote zinzo endelea ndani ya nchi hii. Kwa sasa hali yangu ni mbaya, muda wowote na siku yoyote ninaweza kufa. Baada ya kifo changu, nitahitaji Peter mkwe wangu achukue nafasi yangu. Ninaimani kupitia yeye malengo ya boko haramu yatasonga mbele na atapigania haki kama nilivyo kuwa ninapigania mimi. Ninawaomba muweze kufwata amri yake na kila kitu atakacho waeleza muweze kufwata. Niwatakie mafanikio mema”

Nikajikuta nikishusha pumzi nyingi huku nikimalizia kuitazama video hii.

“Mkuu turuhusu tuweze kuvamia kwenye kambi ya jeshi la nchi hii”

“Bado mapema, tuangalie afya ya mzee”

Nilizungumza huku nikimkabidhi jamaa huyu simu yake, nikaanza kutembea kwa kujiamini kuelekea ndani, nikamkuta Yemi akiwa amesimama sebleni huku uso wake ukiwa umelowana kwa machozi. Nikamsogelea na kumkumbatia taratibu.

“Mungu atasaidia baba atapona”

“Kweli Peter?”

“Ndio niamini mke wangu, baba atapona”

Tukaendelea kukumbatiana na Yemi huku kila mmoja akiwa katika hisia za majozi. Tukaachiana taratibu na kukaa kwenye sofa huku sote tukiwa tunashauku ya kuhitaji kufahamu hali ya mgonjwa inaendeleaje.

 

“Peter”   

“Naam”

“Ndani ya hospitali ulirudi kufanya nini?”

“Tutazungumza badaye mke wangu, kwa sasa tumuombee baba sawa mke wangu”

“Sawa mume wangu, ila nilikuwa ninahitaji niweze kufahamu tu, kwa maana kwa sasa nina ogopa, kwani sijajua ni kwa nini tulivam……..”

Tukajikuta tukikaa kimya huku tukinyanyuka kwenye sofa, macho yetu yote tukawa tumeyatupia usoni mwa daktari huyu aliye toka katika chumba alicho lazwa baba.

“Dokta baba yangu anaendeleaje?”

Daktari uso wake unaonekana kujawa na huzuni kubwa, taratibu akavua miwani yake na kujifuta machozi yanayo mlenga lenga. Kwa upande wangu nikawa nimegundua kwamba tayari mzee ameiaga dunia.

 

“Dokta niambie baba yangu anaendeleaje?”

Yemi alizungumza kwa sauti kubwa huku akimshika daktari, koti lake na kuanza kumtingisha kwa nguvu.

“Muheshimiwa hatupo naye tena duniani”

Yemi akamtazama daktari huyu kwa sekunde kadhaa, gadla akalegea na kuanza kwenda chini, kabla hjafika chini nikamuwahi kumdaka asianguke. Nikamnyanyua kwa haraka na kuamlaza kwenye sofa,  nikamfungua kifungo cha suruali yake.

“Amepoteza tu fahamu, la atakuwa sawa”

Daktari alizungumza huku akimtazama Yemi usoni mwake. Sikuweza kuzungumza kitu chochote kwani siku ya leo kwangu imekuwa ni ndefu sana tangu jana usiku, nikajikuta nikikaa kwenye sofa huku nikimtazama Yemi aliye lala tuli.

“Samahani tulijitahidi kadri ya uwezo wetu ila imeshindikana kabisa, ninakuomba unisamehe katika hilo”

Daktari aliendelea kuzungumza kwa sauti ya upole na unyeyekevu. Nikasimama wima na kutoka nje, nikamuita mwanajeshi mmoja.

 

“Ninaomba unikusanyie wanajeshi wote sehemu husika, nina mazungumzo nao”

“Sawa mkuu”

Nikarudi ndani, kwa haraka na kueleka katika chumba ilipo maiti ya mzee Okocha. Nikamkuta daktari akiwa amesimama pembeni huku amejawa na huzuni kubwa.

“Alizungumza neno gani kabla ya kufa kwake?”

Daktari akatingisha kichwa akiniashiria kwamba mzee hakuzungumza kitu chochote kabla ya kufa kwake. Nikampima mzee Okocha kwa vidole vyangu pambenizoni mwa shingo yake, na nikadhibitisha kwamba mzee Okocha amefariki dunia.

“Muandaeni mzee”

“Sawa mkuu”

Nikatoka nje ya hichi chumba, nikawakuta wanajeshi wawili wakiwa wamesimama wakinisubiria.

“Mkuu tayari tumesha kusanyika”

“Wewe baki hapa mlinde mke wangu, wewe tuongozane”

“Sawa mkuu”

Tukatoka nje na mwanajeshi huyu, tukaelekea kwenye kiwanja kimoja na kuwakuta wanajeshi zaidi ya elfu moja wakiwa wamesimama kwenye mistari iliyo nyooka. Nikasimama sehemu ya juu ambayo wanajeshi waote wanaweza kutuona.

 

“Hivi hapa ndio makao makuu ya hili jeshi?”

“Hapana makao makuu yapo nje ya mji huu”

“Kuna wanajeshi wangapi?”

“Zaidi ya laki mbili na nusu”

“Safi”

“Hapa utachukuliwa video moja kwa moja na itarushwa kwenye makao makuu na wanajeshi wote huko pia watakuwa wanakuona muheshimiwa”

“Sawa”

Baada ya kumaliza kuzungumza na huyu mwanajeshi niliyte kuja naye hili eneo. Nikawatazama kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari ni nini ninaaweza kuzungumza.

“Wanajeshi wezangu, ninaimani hili ninalo kwenda kulizungumza litakwenda kuumiza moyo wa kila mmoja ila hakuna budi zaidi ya kulizungumza.”

Nikameza mate kidogo huku nikiwa nimesimama kikamavu.

“Mzee wetu, mkuu wetu amefariki dunia dakika kumi zilizo pita, kufariki kwake dunia kumesababishwa na ugonjwa wa saratani ya damu aliyo kuwa anaishi nayo kwa mwaka mmoja sasa”

 

Nikaona baadhi ya wanajeshi wakidondokwa na machozi, ila hawakutingishika wala kulaza vichwa vyao chini na wamesimama kwa ukakamavu ule ule nilio wakuta nao.

“Mzee ameniachia kiti chake, si kwasababu mimi ni bora zaidi yenu au kwasababu ni mkwe wake. Ila ni Mungu mwenyewe ndio amenilete hapa. Nitahakikisha kwamba ninaongoza jeshi la Boko haramu kuwaangusha viongozi wote mafisadi, wala rushwa na ving’ang’anizi wa madaraka. Na vifo vya wanajeshi walio kufa hospitalini ni lazima wamarekani waweze kulipa hilo”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwatzama wanajeshi hawa.

“BOKO HARAMUUUUUUUUUU”   

Nilizungumza huku nikinyoosha mkono wangu wa kulia juu, wanajeshi wote wakaitikia kwa sauti ya pamoja iliyo nipa matumaini na kujiamini kwamba nina uwezo wa kuongoza wanajeshi hawa katika kutimiza ndoto alizo kuwa nazo mzee Okocha na zikatimia.


     

Mwanajeshi mmoja akanifwata na kuninong’oneza sikioni.

“Mke wako mkuu amezinduka, yupo katika chumba cha maiti”

 

“Ninakuja”

Nilizungumza kwa sauti ya chini na mwanajeshi huyu, kisha nikageuka na kuwatazama wanajeshi hawa.

“Ninaimani kwa pamoja tutasaidia katika kuhakikisha kwamba tunashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba kila lililo pangwa linakwenda sawa kama lilivyo pangwa, na uzuri ni kwamba nitaongoza opareheni hizo kwani bado damu yangu inachemka, ninacho waomba tuendelee na majukumu ya ulinzi huku tukifanya taratibu za mazishi ya wetu”

Baada ya kumaliza kuzungumza hivyo nikashuka katika jukwaa hili, kwa haraka nikaanza kutembea kuelekea ndani, moja kwa moja nikangoza hadi kwenye chumba chenye mwili wa mzee Okocha, nikamkuta Yemi akiwa amelaza kichwa juu ya kifua cha baba yake huku akilia kwa uchungu sana.

 

    Sikutaka kumnyanyua zaidi ya kubaki nikiwa nimesimama huku nikimtazama tu. Jinsi Yemi anavyo lalamika kwa uchungu kunanifsanya nijisikie vibaya sana kwa maana. Taratibu nikatoka nje huku nikijifuta machozi yaliyo anza kunilenga lenga. Nikatoa simu yangu mfukoni, nikaitafuta namba ya meja kisha nikampigia, simu yake ikaita kwa sekunde kadha kisha ikapokelewa.

“Ndio meja”

“Dany video uliyo ituma kwa raisi, imeweza kukabidhiwa kwa FBI, na wamepewa jukumu la kukutafuta”

“Wananitafuta kisa nini?”

“Dany unatambua kwamba umewaua makomandoo, wa Kimarekani jambo ambalo nchi ya Marekani haito kusamehe katika hili”

 

“Meja natambua kwamba unaelewa kitu ambacho kinaendelea, jambo nilio lifanya ni kujilinda mimi na watu wanao nizunguka, na mbona nilisha kubali matokeo mbele ya raisi ila yeye akahataji kuniua sasa anacho hitaji ni kutengeneza uasama”

“Natambua hilo Dany, ila kwa mimi sina la kufanya zaidi ya kuweza kukutaarifu nyendo zao. Unacho takiwa ni kuhakisha kwamba simu unayo itumia mawasiliano yake yanakuwa hayawezi kunyakwa na mtandao wowote wa kipelelezi kwa maana kufanya hivyo inaweza kuwa ni kosa kubwa sana na usalama wako utakuwa ni mdogo”

“Na walifahamu vipi kwamba upo hospitalini?”

“Sijafahamu ila kuwa makini sana Dany”

“Nashukuru meja, ila kama raisi anahitaji kuingia katika matatizo na mimi, sinto baki chini na mimi atanilazimisha kuunyanyua mkono wangu katika kumshuhulikia”

 

“Sawa Dany”

“Nashukuru Meja”

“Peter?”

Niliisikia sauti ya Yemi nyuma yangu, kwa haraka nikageuka huku nikiingiza simu yangu mfukoni mwangu.

“Unauzungumza na nani?”   

Yemi aliniuliza huku macho yake yakiwa yamejaa uwekundu kutokana na kulia sana.

“Njoo”   

Nilizungumza huku nikimshika mkono Yemi, tukaingia kwenye moja ya chumba, ambacho baada ya kutazama kwenye kuta zake, nikakuta kikiwa na shelfu nyingi za kuhifadhia vitabu.

“Mke wangu, kuna kazi kubwa ambayo nitahitaji kuifanya baada ya msiba wa baba”

 

“Kazi gani?”

“Nitahitaji kumuangamiza raisi wa Marekani?”

“Nini…..unaakili kweli Peter?”

“Yemi, ninacho kizungumza nina maanisha. Marekani imekuwa ni nchi ambayo kila siku inajitahidi kujitanua katika kuhakikisha kwamba ina ishikilia dunia, na kuingilia uhuru wa baadhi ya nchi zikiwezo za bara la Afrika pamoja na bara la Asia.”

“Nikiwa kama kiongozi wa jeshi la baba yako kwa sasa, siwezi kuendelea kukaa na kuona kwamba kuna watu wangu wamefariki pale hospitalini na kama nisinge tumia akili mimi na wewe pia tungefariki. Je kwa yule aliye tuua angeshuhulikiwa na nani, angeshikiliwa na nani, ni nani ambaye angedhubutu hata kuigusa Marekani kwa ajili ya vifo vyeu?”

 

Nilizungumza kwa uchungu huku nikimtazama Yemi usoni mwake, akaka kimya kwa maana hana kitu cha kufanya.

“Wamarekani wanahitaji malaki ya wanajeshi wa baba yako wasambaratike, wafe. Je hawa wanajeshi wana hawana famili, hawana wake, hawana wazazi, hawana watoto. Je ni nani atakaye simamia familia zao. Je kuna ajira gani ya kiserikali ambayo itaweza kuwaajiri hawa wanajeshi?”

“Yemi nakuomba uniache niifanye hii kazi, baba yako aliniamini na kunifanya niwez kiongozi wa hili jeshi. Ninakupenda na nitakulinda sinto hitaji mtu yo……..”

 

Sikumalizia kuzungumza sentensi yangu, Yemi akanikumbatia kwa nguvu huku akininyonya lipsi zangu. Taratibu tukaanza kunyonyana huku sote machozi yakitumwagika usoni mwetu.

“Ninakupenda sana mume wangu”

Yemi alizungumza baada ya kuniachia mdomo wangu.

“Ninakupenda pia mke wangu. Ninaomba kwa sasa nikashuhulikie na mipango ya kumzika baba”

“Sawa mume wangu, nakuomba uwe makini kwa maana umepewa majukumu ambayo hakunamtu aliye weza kuyatarajia kama yatakukuta wewe”

 

“Nashukuru mke wangu, ukaribu wako kwangu kwa sasa nina uhitaji kuliko kitu chochote “

“Sawa mume wangu nipo kwa ajili yako”

“Sawa”

Nikatoka ndani ya chumba hichi, nikamuita mmoja wa wanajeshi ambaye nimemkuta akiwa amesimama sebleni.

“Ni nani ambaye ni makamu wa mueshimiwa”

“Ni meja Otomu, na yupo makao makuu kwa sasa”

“Kuna njia gani ambayo ninaweza kuwasiliana naye?”

“Kuna chumba cha mawasiliano, munaweza kuwasilina moja kwa moja kwa kuonana”

“Naomba mundae kikao hicho ninahitaji kuonana naye”

“Sawa mkuu”

Nikaongozana moja kwa moja hadi kwenye chumba maalumu cha mawasiliano, Tv kubwa iliyomo humu ndani ikawashwa na nikaka kwenye kiti kilichopo mbele ya Tv hii.

“Ndani ya sekunde kumi atakuwa hewani”    

 

“Sawa”

Ndani ya sekunde kumi hizo meja Otomu, akaonekana kwenye Tv hii kubwa.

“Habari yako jenero Peter”

“Salama tu meja Otumu. Ninahitaji kusikai maoni yenu kuhusiana na mazishi yam zee wetu”

“Tulikuwa tunasubiria kauli yako, ila kama utakubalina nasi basi tutakuja kumzika mzee huku kwenye makao makuu ya jeshi”

“Siwezi kulikataa hilo kwa maana nyinyi ndio wenyeji wangu, ila kabla ya sisi kufanya maamuzi yoyote ya kijeshi inabidi kumshirikisha mke wangu kwa maana yeye pia katika hili anahusika kwa asilimia mia moja”

“Kwa hilo halina shida”

“Ninda kamuite mke wangu”

“Sawa jenerali”

 

Japo ni kazi ambayo ninaimudu, ila sikuwahi kuwaza kwenye maisha yangu kwamba ipo siku nitakuja kuwa kiongozi wa kijeshi tena jeshi la kigaidi linalo windwa na serikali yake ya nchi ambayo ni Nigeria na dunia nzima. Maisha yangu siku zote yapo katika wakati mgumu sana wa kuwindwa, na chanzo kikubwa ambacho kinaniingiza katika matatizo haya ni mapenzi ambayo yalianza kwa bosi wangu K2, mlango ukafungulia na kujikuta nikistuka kutoka kwenye msongamano huu wa mawazo, Yemi akaka kwenye kiti cha pembeni yangu huku macho yake akitazama kwenye Tv hii kubwa.

“Mke wangu hapa tunajadilisi kuhisina na sehemu gani ambayo tunaweza kumzika baba, na meja amependekeza baba azikwe kwenye makao makuu ya kambi”

Yemi akaka kimya kwa muda huku akinitazama usoni mwangu, taratibu akatingisha kichwaakikubaliana kwa kile ambacho nimemuambia.

“Mke wangu amekubaliana na hilo swala”   

“Sawa jenero, basi nitatuma helicopter mbili, ndani ya dakika arobaini na tano zitakuwa zimefika hapo”

“Nitashukuru meja”

 

Tukamaliza mazungumzo haya na kutoka ndani ya chumba hichi huku nikiwa nimemshika Yemi mkono wake. Mwili wa mzee Okocha ukaandaliwa na madaktari na akavalishwa nguo zake za ujenerali wa hili jeshi.

“Mkuu helicopter zimesha fika, tunahatajia kuondoka sasa”

Nikatoka katika chumba hichi cha kuuandaa mwili wa mzee Okocha. Nikamkuta Yemi akiwa amesimama sebleni.

“Mke wangu tuondoke”

“Na baba?”

“Wanakuja naye”

“Sawa”

Tukaongozana na mwanajeshi huyu hadi kwenye helicopter zilio tua kwenye moja ya kiwanja kilichopo hili eneo, tukaoneshwa helicopter ya kuingia. Tukaingia na taratibu helicopter  hii ikaanzza kuacha ardhi.

“Umeshawahi kufika makao makuu ya kambi ya jeshi la baba yako?”

“Ndipo nilipo kulia, kabla sijaondoka kuelekea Uingereza kusoma”

 

“Sawa sawa”

“Ila baada ya huu msiba kuisha nitaomba nikulezee ukweli kuhusiana na maisha yangyu pamoja na baba yangu”

“Sawa mke wangu”

“Ila ninakuomba usije ukaniacha”

“Kwa nini nikuache mke wangu?”

“Kwa sababu mimi na baba yangu hatukupata muda wa kukueleza ukweli wa maisha yetu”

“Usijali mke wangu, kila jambo linatokea kwa sababu”

Niliendelea kumfariji Yemi ili asizidi kuwa mnyonge. Tukafanikiwa kufika katika makao makuu ya boko Haramu, kwa akili yangu ya kawaida nilihisi kwamba inaweza kuwa ni sehemu ya maficho ila kusema kweli ni eneo lililo jengwa vizuri, mzee huyu aliweza kuwekeza pesa nyingi katika kuwekeza katika hili jeshi, japo ni porini na miimani, ilakumejengeka sana.

 

Tukapokelewa na meja Otumu, moja kwa amoja tukapelekwa kwenye eneo la kupumzi huku ikiwa imesha timu saa kumi na moja alfajiri.

“Tumepanga mazishi ya fanyike saa kumu alasiri”

“Kwa nini ratiba mumeipeleka mbele kiasi hicho?”

“Kwa maana kuna wageni wengine ambo walikuwa ni marafiki wa jenerali tumeweza kuwataarifu na wengi wameahidi kuweza kufika katika mazishi haya”

“Sawa hilo ninawaachia nyinyi ila usalama si upo wa kutosha?”

 

“Ndio upo wa kutosha”

“Basi ninaomba tupumzike kwa maana siku hii imekuwa ni ndefu sana kwetu”

“Hakuna tabu jenerali”

Meja akatoka katika chumba tulichopo mimi na Yemi. Nikaka kwenye sofa huku nikiwa na mawazo mengi sana.

“Mume wangu kweli utaweza kuongoza hili jeshi?”

“Kwa nini unaniuliza hivyo?”

“Nimekuuliza tu mume wangu, ninakuona una mawazo mengi sana”

“Usijali mke wangu nitaweza. Vipi sijasikia swala la mwanao kuweza kuhudhuria mazishi ya babu yake?”

“Yupo mbali na Nigeria hatoweza kuwahi mazishi?”

“Kwani yupo wapi?”

“Yupo Canada kwa sasa”

“Sawa mke wangu”

Kwa uchovu nilio kuwa nao, nikajikuta usingizi ukinipitia na kulala fofofo. 

 

“Baby amka”

Niliisikia sauti ya Yemi akizungumza akizungumza na mimi. Nikafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nimefunikwa na shuka.

“Nimekufunika na shuka mume wangu, baridi ilikuwa kali?”

“Wewe hujalala?”

“Nimekosa usingizi kabisa mume wangu”

“Sawa, ni saa ngapi sasa hivi?”

“Ni saa nne asubuhi, wageni wamesha anza kufika, ila Meja anawapokea itabidi twende nasisi kuwapokea”

“Sawa mke wangu”

Kwa haraka nikajifunuashuka, nikasimama huku nikipiga miyayo ya uchovu mkubwa nilio nao.

“Ila inabidi kubadilisha mavazi kwa sasa wewe ndio jenerali wa jeshi”

“Zipo wapi nguo za kuvaa?”

Yemi akapiga hatua hadi kwneye moja ya kabati, akanitolea nguo za jeshi. Nikaanza kuvaa nguo hizi taratibu. Yemi akaanza kunivisha vyeo ninavyo stahili kwenye shati langu, nikavaa na kofia ya cheo changu ambayo ina rangi nyekundu. Nikavaa na buti za jeshi, kwa utani Yemi akanipigia saluti na kujikuta nikicheka sana.

“Umependeza sana mume wangu”   

“Nashukuru mke wangu”

 

“Twende sasa mume wangu”

Tukatoka ndani ya chumba hichi, kila mwanajeshi niliye kutana naye akanipigia saluti ya kuniheshimu. Tukafika katika kiwanja cha helicoptwer, tukakuta helicopter moja ikiwa ndio inajiandaa kushuka. Taratibu helicopter hii ikasimama sehemu husika, wakashuka wasichana wawili walio valia suyo nyeusi huku kwenye nyuso zao wakiwa wamevaa miwani nyeusi. Sikuamini macho yangu baada ya kumuona K2 akishuka huku akiwa amevalia nguo za jeshi jambo lililo nifanya nibaki nikiwa nimemkodolea macho ya hasira iliyo changanyikana na matukio mabaya aliyo ifanyia familia yangu miaka kadhaa iliyo pita nyuma.



K2 akaanza kutembea kwa kujiamini huku walinzi wake wakiwa wamenzunguka, mmoja akiwa upande wa kulia na mwengine akiwa upande wa kushoto. K2 akaanza kusalimiana na meja, huku wakipeana mikono na kuzungumza maneno mawili matatu na wanaonekana kufahamiana sana. Akasalimiana Yemi, kisha akanifwata mimi, macho yetu yalipo kutana akabaki akinishangaa kwa sekunde kadhaa, ili kuepusha watu kuona tofauti zilizopo kati yetu, nikampa mkono wa kulia huku nikimtazama usoni mwake, taratibu na yeye akanipa mkono wake kiwoga.

“Muheshimiwa raisi huyu ni mume wangu anaitwa Peter, kwa sasa ndio mkuu wa jeshi”

Yemi alizungumza baada ya kugundua kwamba sisi hatufahamiani.

“Nashukuru kwa kukufahamu jenerali Peter”

“Peter huyu ni raisi wa Tanzan, mtu wa karibu kabisa na baba na anaitwa K2”

“Nashukuru kukufahamu muheshimiwa raisi K2”

“Nawe pia”

 

Nikauminya kidogo mkono wa K2 kumuashiria kwamba bado bifu kati yetu lipo, kisha nikamuachia mkono wake, akaongozwa na wanajeshi wenye kazi hiyo ya kuwaongoza wageni rasmi kwenye sehemu husika wanayo takiwa kufikia.

“Wageni leo watafika wangapi?”

Nilimuuliza Yemi kwa sauti ya chini.

“Sijajua labda meja anafahamu ni wageni wangapi wanaweza kufika”

“Muite”

Kwa ishara Yemi akamuita meja, akatembea kwa mwendo wa ukakamavu hadi katika sehemu niliyo simama.

“Wamesalia wageni wangapi kuweza kufika?”

“Wamesalia wageni kumi na moja kufika na wote wapo njiani”

“Sawa kuna mgeni wa karibu munaye taratiji kuweza kufika hapa baada ya dakika kadhaa?”

 

“Mgeni tunaye mtaratajia kufika kwa sasa, atafika hapa baada ya robo saa”

“Sawa meja”

Meja akanipigia saluti kisha akarudi katika sehemu husika.

“Mke wangu naomba niende msalani, haja ndogo imenikamata”

“Sawa mume wangu, vipi tupate chai?”

“Hapana tutapata baada ya muda huyo mgeni anaye kuja kufika”

“Sawa”

Nikaondoka kwa mwendo  wa haraka katika eno hili, sikuwa na haja ya kwenda msalanani ila haja yangu ni kwenda kuonana na K2.

“Raisi wa Tanzania yupo jengo gani?”

“Lile pale mkuu”

 

Nikaelekea katika jengo alilipo K2 nikakuta walinzi wake wakiwa wamesimama nje ya chumba hichi.

“Nahitaji kuonana na raisi wenu”   

Mlinzi mmoja akaiingia ndani, baada ya dakika moja akatoka na kuniruhusu kuingia ndani. Nikaingia, na kuufunga mlango kwa ndani, nikamkuta K2 akiwa ameshika bastola yake huku amekaa kwenye sofa lililomo humu ndani na kuikunja miguu yake katika mfumo wa nne. Mkono wake wa kushoto ameshika sigara kubwa akivuta taratibu. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa kisha nikaka kwenye sofa lililopo mbele ya sofa hili, huku kati yetu tukiwa tumetengenishwa na meza ya kioo.

“Naona una jeshi kubwa sana”

K2 alizungumza huku akitoa moshi mwingi wa sigara mdomoni mwake.

“Sijakuja kujadiliana na wewe, wala kujua nina jeshi au sina. Nimekuja kukuonya kwa kile ambacho utajaribu kukizungumza”

 

“Hahahaaa, Dany oohooo samahani. Jeneral Peter, mbona unajistukia sana? Mimi nimekuja kumzika rafiki yangu na kuondoka au unahisi kwamba nitazungumza ukweli kwamba wewe ni gaidi ninaye kutafuta kwenye nchi yangu na pia ni mpelelezi wa Marekani?”

“Ni nani aliye kuambia mimi ni mpelelezi?”

“Dany tambua kwamba mimi ni mkubwa kwako, kuanzia umri hadi akili. Ninatambua nyendo zako zote ambazo huwa unazifanya, na kama unahitaji kunipa vitisho, nitakwenda kuzungumza kila kitu mbele ya hawa wanejeshi na utaona ni kitu gani watakacho kufanya. Alafu wewe mjanja kweli umetumia uzuri wako kumt** mtoto wa watu hadi baba yake amekupa ujeneral ambao wapo watu ndani ya hili jeshi walistahili kuupata”

 

K2 alizungumza kwa kujiamini, huku taratibu akiendelea kuvuta sigara yake, nikaitazama bastola yake aliyo ishika.

“Bado nitakuwinda hata kama ukihitaji kuniharibia katika hili jeshi kwa manaa si chochote kwangu”

“Hahahaa Dany acha kupiga biti za kitoto, kumbuka hii ni Nigeria na sio Tanz kwamba utaweza kujificha kwenye vichochoro unavyo vijua. Sasa kama umenihitaji bifu lizidi kuendelea humu ndani ya hii ngome eti unayo imiliki, ninakupa masaa ishirini na nne ujivue madaraka ya ujenerali na upotelee unapo pajua, la sivyo utakufa ndani ya hii ngome”

“Siwezi kufa na siogopi kufa, kama ulishindwa kunikamata tangu ukiwa NSS, na umekuwa raisi na nikaka meza moja ya wewe tena ikulu pasipo kunifahamu, basi tambua huwezi kunipiga. Nakujua K2 udhaifu wako na nitaweza kuutumia kuhakikisha kwamba nina kuangusha chini”

 

Nilizungumza kwa kujiamini, kisha nikasimama na kuanza kupiga hatua kuelekea mlangoni. K2 akaanza kucheka kicheko cha dharau na kunifanya nisimame, nikageuka na kumtazama kwa macho makali sana huku nikikunja ngumi ya mkono wangu wa kulia, kitu kinacho nifanya nishindwe kumfwata K2 karibu ni bastola aliyo ishika mkononi mwake.

“Dany siku nyingine uwe makini unapo zungumza”

K2 akatoa simu yake mfukoni, na kunisikilizisha mazungumzo yote tulio kuwa tunatazungumza, kumbe kwa muda wote tulio kuwa pamoja alikuwa anayarekodi.

“Sasa kupitia hii utaniacha mimi niweze kuishi kwa amani ya bwana, na pia utafwata nilicho kuambia kwamba ndani ya msaa ishirini na nne ambayo nitaamua kukaa hapa, hakikisha kwamba ujivua ujenerali na usiwe hata kuruta ndani ya hii kambi. Bye”

 

K2 akanipungia mkono, kwa hasiri nikatoka ndani ya hichi chumba na kuubamiza mlango kwa nguvu hadi walinzi wake wakahawi kuingia ndani kumtazama mkuu wao. Moja kwa moja nikaelekea chumbani kwetu, nikapitiliza hadi chooni, nikasimama mbele ya kioo na kujitazama. Macho yangu yote yametawaliwa na uwekundu ulio  sababishwa na harisa kali pamoja na kejeli za K2.

‘Lazima nimuue’

Nilizungumza kwa hasira na kujiikuta nikipiga ngumi kwenye hichi kioo hadi kikavunjika.

“Peter”   

Nilisikia sauti ya Yemi nyuma yangu, nikageuka nikamkuta akiwa amesimama huku ameduwaa, kwa maana kioo chote kimavunjika vipande vipande.

“Mume wangu una tatizo gani?”

Yemi aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, akautazama mkono wangu wa kulia, kwa haraka akanisogelea na kuushika. 

 

“Mume wangu tazama unatokwa na damu jamani”

Yemi alizungumza huku akiuweka mkono wangu kwenye sinki la kunawia, akanichomoa kipande kidogo cha kioo kilicho nikita katika kidole changu. Kwa haraka Yemi akaanza kuiosha damu zinazo mwagika, akatoka bafuni humu kwa haraka, baada ya dakika akarudi na boksi dogo la kuhifahidhi vitu vya huduma ya kwanza, akaanza kuniosha na dawa ambayo ni ina maumivu makali sana, ila sikuyajali zaidi ya roho yanu kutawaliwa na roho ya mauaji.

“Peter mume wangu ninakuomba uniambie ni kitu gani ambacho kimekupata jamani”

Yemi alizungumza huku akinifunga bandeji yeupe.

“Nahitaji……..”

Nikaka kimya huku nikitafakari nizungumzae kitu kilichopo moyoni mwangu, ila nikaka nikaona Yemi hastahili kufahamu chochote kwani hii vita haimuhusu kabisa.

 

“Unahitaji nini mume wangu”

Yemi alizungumza huku akinishika mashavu yangu kwa viganja vya mikono yake miwili. Nikamtazama usoni mwake kwa sekunde kadhaa, kisha kwa haraka nikaanza kunyonya midomo yake.

“Nahitaji kukut**……..”

Nilizungumza huku nikimshika Yemi makalio yake na kuyaminya kwa nguvu, hakuwa na ubishi kwa maana mimi ni mwanaume ninaye mmiliki. Nikambeba na kutoka naye humu bafuni, nikamlaza kitandani, na kuanza kumvua nguo zake, huku na yeye akiwa na kazi ya kufungua vifungo vya shati langu.

 

“Ila mume wagu kuna wageni wata…….”

“Shiiiii……”

Nilizungumza huku nikimziba Yemi mdomo wake kwa kutumia lipsi zetu, tukaendelea kunyonyana lipsi zetu kwa nguvu. Nikaanza kuchezea ,

    Tukamaliza mzunguko wa kwanza, taratibu tukajikuta tukikumbatiana kwa nguvu huku hasira ikiwa imenipungua kwa kiasi fulani. Tukashuka na kuingia bafuni, tukaoga haraka haraka na kurudi chumbani, tukavaa nguo zetu na kutoka chumbani humu.

 

“Inabidi mume wangu kwa sasa uwe na mlinzi wako”

“Kwa nini?”

“Ahaa wewe ni jenerali kuwa na mlinzi ni lazima na si mmoja bali hata wawili au watatu”

“Nahitaji wewe ndio uwe na walinzi sawa mke wangu”

“Sawa mume wangu”

Tukafika katika kiwanja cha helicopter, wageni kutoka mataifa mbali mbali wakazidi kufika, hadi inafika saa nane mchana tukawa tumemaliza kupokea wageni tulio kusudia kuweza kufika katika msiba wa mzee Okocha. 

 

Tukaelekea kwenye sehemu ya kupata chakula na wageni husika, nikatambulishwa kwa wageni woge walio weza kufika katika eneo hili. Il kila ninavyo mtazama K2 ninahisi moyo wangu kuniuma kwani bado nina kinyongo naye.

Tukaendelea kupata chakula mchana huku sehemu husika ya mazishi ikiwa inaandaliwa na wanajeshi. Baada ya chakula cha mchana hatukuwa na muda wa kupoteza. Moja kwa moja tukaelekea katika kiwanja cha mazishi. Tukakuta wanajeshi wengi wakiwa wamejipanga, huku wote wakiwa wamefunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao ya kushoto.

“Jeneral kuna risala unatakiwa kusoma”

Meja alizungumza kwa kuninong’oneza huku akiweka katarasi kadhaa mezani mwangu.

 

“Risala, mbona hamkunijulisha mapema?”

“Ni kosa tu limejitokea, ila nitakuomba uipitie kwa dakika kadhaa kisha ukifika muda wa risasa nitakuomba uweze kuisoma”

Nikashusha pumzi yangu, nikaizipitia karatasi hizi nne, kisha nikatingisha kichwa kumkubalia Meja kwamba nitazisoma. Meja akarudi kwenye kiti chake na kunifanya nianze sasa kuisoma risasa hii, hatua hadi hatua.

“Wameiandaa vizuri?”

Yemi aliniuliza huku akininong’oneza

“Ndio ninaipitia hapa”

“Hembu niione kwa mana niliwapa maelezo na jinsi ya kuiandika”

“Sawa”

Nikamsogezea Yemi karatasi hizi, akaanza kuzipitia moja baada ya nyingine.

“Kuna vitu hawajaviweka, kama huto jali ninakuomba nikaisome hii risala”

 

“Sawa mke wangu, ila kuna vitu gani ambavyo hawajaviweka?”

“Historia ya baba wameikosea, upiganaji wake katika kuunda hili jeshi wameandika rasha rasha, sasa sijui ni nani aliye andika”

Kwa ishara nikamuita meja, akafika katika eneo tulipo, akanima chini taratibu.

“Meja hii risala mumeiandika tofauti mbona. Hichi sio kile nilicho waeleza watu wako asubuhi”

“Samahani mkuu, kama inawezekana ninaweza kuandaa nyingine”

“Hapana nitatoa kichwani mwangu, sawa”

“Sawa mkuu”

 

Yemi alizungumza kwa ukali kidogo, nikamruhusu Meja kuandoka na kubaki nikimtazama Yemi jinsi anavyo endelea kusoma risasala hii. Muda wa kusoma risasa ukafika, yemi akasimama na kusogela jukwa maalumu, akaanza kusoma risala ya baba yake huku akito historia ya baba yake. Hadi anamaliza machozi yakawa yanashuka kwenye uso wake nikasimama na kumsogelea hadi sehemu simama nikamkumbatia taratibu huku macho yangu yakiwaangalia wageni waalikwa. Macho yangu yakafika kwa K2 ambaye naye ananitazama, kwa ishara ya mkono akanionyeshaea ishara ya kunikata shingo yangu, jambo lililo nifanya nizidi kumchukia hadi nikahisi moyo wangu ukitaka kupasuka kwa maumivu haya ninao yasikia.

       

Muda wa kusoma risasa ukafika, yemi akasimama na kusogela jukwa maalumu, akaanza kusoma risala ya baba yake huku akito historia ya baba yake. Hadi anamaliza machozi yakawa yanashuka kwenye uso wake nikasimama na kumsogelea hadi sehemu simama nikamkumbatia taratibu huku macho yangu yakiwaangalia wageni waalikwa. Macho yangu yakafika kwa K2 ambaye naye ananitazama, kwa ishara ya mkono akanionyeshaea ishara ya kunikata shingo yangu, jambo lililo nifanya nizidi kumchukia hadi nikahisi moyo wangu ukitaka kupasuka kwa maumivu haya ninao yasikia.

   

ENDELEA           

Taratibu nikamrudisha Yemi kwenye kiti alichokuwa amekaa, nami nikaka kwenye kiti changu huku nikiifikiria ishara ambayo K2 ameweza kunifanyia. Ratiba ya mazishi ikaendelea, ikaanza kupigwa mizinga kama kanunu ya kijeshi inavyo kuwa, endapo anakufa kiongozi wa jeshi au kiongozi wa juu katika serikali, basi mizinga kadhaa hupigwa hewani ikiwa ni heshima ya kijeshi. Muda wa kumzika mzee Okocha ukawadia, sote tulipo katika hili eneo tukasimama, na tukawashuhudia wanajeshi wanavyo shusha mwili wa mzee huyu kwenye kaburi, jambo lililo mfanya Yemi kushindwa kujiazuia na kuangua kilio kikali sana. 


Nikamkumbatia kwa nguvu kifuani mwangu huku nikimuomba atulie, sikuhitaji kushuhudia jinsi mzee huyu anavyo fukiwa kwani Yemi analia kiasi kwamba anashindwa hata kusimama. Taratibu nikamnyanyua na kuandoka naye katika hili eneo na kurudi katika jengo lenye chumba chetu.

“Peter nitaishi vipi bila baba yanguu…..”

Yemi alizungumza huku akizidi kulia kwa uchungu sana.

“Nipo mke wangu, nipo usilie tafadhali kwa maana hii yote ni kazi ya Mungu ukilia sana utamkufuru Mungu”

 

Yemi akaendelea kulia, huku kichwa chake akiwa amekiegemeza kifuani mwangu. Zaidi ya lisaa moja nikawa na kazi ya kumbeleza Yemi hadi akapitiwa na usingizi, nikamlaza vizuri kwenye sofa hili tulilo kalia, nikachukua shuka na kumfunika mwili mzima na kumuacha kichwa tu.

Nikatoka nje, huku akili yangu kwa sasa ikianza kuwaza ni jinsi gani ninaweza kumzuia K2.

“Generali”

Mwanajeshi mmoja aliniita huku akinipigia saluti, nikasimama na kumtazama.

“Ndio”   

“Kuna kikao katika chumba kikuu, wageni rasmi wanakusubiria”

“Kikao kaitisha nani?”   

“Meja”

 

Nikamtazama mwanajeshi huyu, kisha nikaanza kuongozana naye. Tukafika katika ofisi inayo fanyikia kikao, kabla ya kuingia, nikawatazama wanajeshi pamoja na walinzi mbali mbali walio jipanga nje ya hii ofisi, wakiwasubiria mabosi wao waliomo ndani ya hichi kikao, kisha nikamruhusu mwanajeshi huyu kunifungulia mlango. Nikaingia nda na kuwakuta wageni waalikwa wakiwa wamekaa kwenye viti, walipo niona wote wakasimama kwa ishara ya kuniheshimu. Ni kiti kimoja tu ambacho hakina mtu, na ndio kiti ambacho ninastahioli kukalia kwani kwenye meza kuna kibao chenye jina langu la uongo ambalo ni Peter.

Nikafika kwenye kiti changu, nikawatazama wageni walikwa wote, kisha kwa ishara nikawaruhusu kuweza kukaa chini nami nikaa. Meja katika sehemu aliyo kaa, akasimama kikakamavu huku akinitazama usoni mwangu.

“Kwanza ninaomba radhi jenerali kwa kuitisha kikao kabla sijakutaarifu ila niche ni kikao cha dharura na ningeomba uweze kusikiliza kile washirika wanao unda kundi la boko haramu wanahitaji kuzungumza na wewe. Nina imani ni mgeni kwenye jeshi hili, ila ninaimani kwa kuzidi kuelekezana utaweza kuelewa ajenda zote za kundi hili.”

 

Nikatingisha kichwa huku nikimkubalia meja msamaha hawake, watu wengi waliomo kwenye hii ofisi ni wazee walio nipita umri na wengine ni kama baba zangu.

“Kwa sasa wewe ndio  kiongozi wa boko haramu, je ni kipi unacho weza kuufanyia huu umoja ili ufanikiwe kufika malengo yake”

Mzee mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama usoni mwake.

“Nitasimama katika malengo aliyokuwa nayo mzee Okocha na nitahakikisha kwamba Boko haramu inazidi kusonge mbele na kuwa ni kundi lenye nguvu kubwa duniani kama ilivyo kwa makundi kama Alquida”

 

“Muheshimiwa jenero, imejipanga vipi kukabiliana na nchi kubwa kama Marekani, Uingereza na Ufaransa ambazo kila siku zinajaribu kuongeza wataalumu wa kijeshi katika kufundisha wazawa hususani wanajeshi wa kiserikali, il badae waje kuangusha hili kundi na kulifuta kabisa kwneye ramani ya dunia?”

“Nitaanzisha mkakati wa kupandikiza watu watu katika kila jeshi la nchi hususani hapa Nigeria, Marekani na sehemu nyingine. Watu hao nitahakikisha wanafanya kazi nasi kufahamu ni kitu gani majeshi hayo yanapanga, hiyo ni moja. Mbili nitaanzisha kikosi cha mauji kwa wasaliti wote ambao watajaribu kuuza siri ya umoja huu, sinto jali ni kiongozi ndani ya kundi hili au upo nje ya kundi hili, nitakacho hakikisha ni kwamba ninakuteketeza wewe na familia yako. Swali jengine”

 

Nilizungumza kwa kujiamini na msisitizo na kuwafanya watu hawa kutazamana, hadi K2 mwenyewe, akabaki akinikodolea macho tu.

“Sisi tumewekeza pesa zetu kuhakikisha kwamba jeshi hili linaitumia pesa hiyo katika kuchukua sehemu tofauti za kibiashara na kuziweka chini ya ungalizi  na kuendesha biashara ya eneo hilo na pesa zetu ziweze kurudi, sasa wewe una mpango gani katika hilo?”

Mzee huyu alizungumza na kunifanya nimtazame kwa sekunde kadhaa kwenye macho yake hadi akatazama chini.

“Unaweza kuitoa pesa yako”

Nilizungumza kwa msisitizo na kuwafanya viongozi hawa kuanza kunong’ona nong’ona.

 

“Mimi nikijana, ninauwezo wa kuchukua silaha na kwenda kupigana na vijana wangu. Nitajitolea maisha yangu kwa ajili ya hilo. Wewe huwezi kukaa huko ulipo na familia yako na ukategemea sisi kupambana au vijana wangu wapambane kwa ajili yako na wewe upate faida na uendelee kuishi maisha ya furaha na amani ikiwa damu za wanajeshi wangu zinamwagika. Kumbukeni hawa ni watu na si kuku au ng’ombe. Na nitoe angalizo katika hilo endapo unategemea kujitoa katika huu umoja, nitahakikisha kwamba ninaipiga nchi yako na kuichukua, hususani katika vitega uchumi unavyo vitegemea”

Wazee wote wakaka kimya huku wakinitumbulia macho, kwani utaratibu nilio  kuja nao hapa ninaimani kwamb ni mpya na kila mmoja utakuwa umemuudhi kwa namna moja ama nyingine.

“Swali jengine?”   

K2 akanyanyua mkono kidogo ili kuomba nafasi ya kuzungumza, nikajikuta tumbo likinicheza kidogo kwa woga kwani sijui anataka kuzungumza kitu gani.

“Zungumza”

 

“Je tukiamua kuzitoa pesa zetu kwenye huu umoja wanajeshi wako si watakufa kwa njaa?”

Swali la K2 likanifanya nishushe pumzi taratibu huku nikiuzuia woga wangu ambao tayari ulisha nitawala mwili wangu wote.

“Kama ulisha ingia kwenye hichi chama, sinto kuruhusu utoke na hilo ninaomba liweze kujulikana kwenu nyote”

“Ila jenero hiyo sio haki na hilo sio alilo kuwa akilifanya jenero aliye pita, kwa maana hichi chama alikiendesha kwa umoja  na upendo ndio maana leo hii tumekuja kumzika?”

“Huu pia ni umoja na upendo ambao nyote mutaupenda. Malengo hayawezi kufika kwa kuchekeana au kuogopana kwa kuwekeza pesa zenu. Malengo yatafika kwa kuhakikisha kwamba heshima inatawala ndani ya hili kundi.”

Msisitizo wangu ukawafanya viongozi hawa kuonekana wakiwa wamejawa na mawazo mengi vichwani mwao nina imani nitakuwa nimependekeza hali ya kuogopwa kwa kila kiongozi.

 

“Sioni cha maana ninaondoka zangu hapa”

Mzee mmoja alizungumza huku akirudisha kiti chake nyuma, kwa haraka nikasimama na kutembea hadi sehemu aliyo simama. Watu wote ndani ya hii ofisi wakabaki wakitutazama.

“Unahitaji kufa?”

Nilimuuliza kwa sauti ya upole huku nikiwa nimemkazia macho.

“Utaongozaje jeshi kwa namna hii?”

“Unahitaji kufa?”

Nikaongeza ukali wa sauti yangu, mzee huyu akabaki akiwa amenikodolea macho, kitu ambacho kinawaogopesha viongozi hawa humu ndani  wote hawanijui uhalisia wangu kwamba mimi ni mtu wa aina gani, ila K2 pekee ndio anaye nifahamu na yeye ananijua akili yangu jinsi ilivyo.

“Kaa chini kikao bado hakijaisha”

 

Taratibu mzee huyu akaka kwenye kiti cheka, nikamsaidia kukisukuma mbele kidogo kwa mana ni kiti cha matairi.

“Ninaimani nyinyi nyote hamunitambu, na kupewa nafasi hii ya kuongoza hili kundi sijapewa kwa bahati mbaya au makusudi. Nina uwezo wa kuongoza, ninajua cha kufanya ndio maana mzee Okocha aliweza kunipatia nafasi hii. Mzee Okocha anaujua ukweli wa maisha yangu”

Ilinibidi kudanganya kidogo ili kumtoa K2 kwenye mawazo ya mpango wa kuhitaji kuelezea ukweli kuhusiana na mimi mbele ya viongozi hawa ambao tayari sasa akili na mioyo yao inachemka kwa kuwazia uongozi wangu.

“K2 naye anajua ukweli wa maisha yangu”

Nilizungumza huku nikiwa nimesimama nyuma ya kiti cha K2, viongozi wote wakanitazama, nikaona jinsi kifua cha K2 kinavyo shusha pumzi nyingi kwani tayari nimesha muingiza kwenye mikono yangu tofauti na alivyo kuwa akifikiria.

“Raisi Donald Bush anajua ukweli wa maisha yangu. Je wewe, wewe, wewe, wewe, wewe na wewe munaufahamu ukweli wa maisha yangu?”

 

Niliwauliza viongozi baadhi kwa kuwanyooshea kidole changu, wote wakatingisha kichwa kukiri kwamba hakuna anaye nifahamu mimi.

“K2 unaweza kuwaleza wezako mimi ni nani?”

Nilizungumza huku huku nikikaa kwenye kiti changu, nikamuona jinsi K2 anavyo pata kigugumizi cha kuzungumza, moyoni mwangu nikajikuta nikianza kushangilia kwa kumuu K2 kiakili na sasa nitahitaji kumuu kimwili.

“Haloooo K2, mbona kimya?”

“Ahaa….ahaa…….”

Meja akabaki akinitazama huku amenitolea macho ya mshangao, mshangao wake ukaendelea kwa kumtazama K2.

“Ameshindwa kuzungumza. Basi kati yenu musihitaji kunijua vizuri kwa maana nitahakikisha ninawapiga hadi vyumbani kwenye kama nilivyo fanya kwenye kundi la Al-Shabab”

Nikawaona viongozi hawa wakistuka kwa maana ninatambua kwamba wameweza kusikia habari ya kufutika kwa kundi la Al-Shabab na wengi wao ninaimani wanahisi kwamba Marekani ndio limeifuta Al-Shabab kwenye ramani ya dunia.

“Meja hakikisha kwamba hakuna kiongozi hata mmoja anaye ondoka leo, nyote nitawahitaki katika chakula cha leo usiku”

“Sawa mkuu”

 

“Swali, maoni, ushauri?”

Hapakuwa na kiongozi aliye fungua kinywa chake, wote wakaka kimya.

“Tutaonana usiku, niwatakie jioni njema”

Nikasimama na kuanza kutembea kwenye chumba hichi kwa kujiamini, viongozi wote wakabaki wakinisindikiza kwa macho, nikafungua mlango na kutoka, nikaanza kusikia minong’ono, ikanibidi kufungua mlango na kuwafanya viongozi wote walio kuwa wamesimama kukaa kwenye viti vyao kwa woga.

“K2 ninakuomba”

Taratibu K2 akanyanyuka na kunifwata mlangoni, nikamfungulia mlango na kuanza kutoka naye nje.

 

“Dany wewe ni mshenzi, mbwa mkubwa wewe”

K2 alizungumza kwa hasira japo kwa sauti ya chini isiyo sikika na mtu yoyote, sikuruhusua mlinzi yoyote kutufwata nyuma yetu, hawa walinzi wa K2 wanao pokea amri kutoka kwake, wakafwata amri yangu.

“Nikuue kwa sumu, risasi, au kukuchinja?”

Nilimuliza K2 huku tukiendelea kutembea taratibu, kwa mtu ambaye anaweza kutuona, atahisi tunazungumza mazungumzo mazuri ya amani. Tukasimama kwenye moja ya bustani ya maua.

“Nimekuuliza nikuue kwa staili gani kwa maana leo hapa kwangu huwezi kuondoka, ulihisi kwamba nitaogopa mazungumzo yako uliyo yarekodi, au ukweli ambao utakwenda kuzungumza kwa watu hawa ambao kwa sasa wanafwata amri yangu?”

“Ukiniua mimi haito kusaidia kitu”

“Hahahaa, unajidanganya, una uhakika haita nisaidia kitu?

“Ndio kwa mana mimi ndio ninajua ukweli wote”

“Ukweli gani wakati umeshindwa kwendwa kuzungumza mbele ya viongozi wezako, eti mumewekeza pesa”

 

“Ukweli kuhusiana na familia yako”

Nikakaka kimya huku nikimtazama K2 usoni mwake. Nikatamani kumzaba kibao, ila wanajeshi wanao linda hii sehemu wakanifanya nishindwe kabisa kumdhalilisha K2 mbele yao.

“Malaya mkubwa wewe unataka kuzungumza nini mbele ya familia yangu?”

“Familia yako ipo hai, hakuna hata mmoja ambaye nimemuua kama unavyo zungumz…….”

Nijikuta nikishindwa kujizuia na kumtandika kofi zito K2 hadi akapepesuka, ila akajikaza na kusimama sawa huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Peter”

Niliisikia sauti ya Yemi akiniita nikatazama pembeni na kumuona Yemi akija katika eneo nililo simama na K2.

“Ohoo samahani mama K2, mume wangu leo hayupo sawa”

Yemi alizungumza kwa sauti ya upole kwa mana hatambui ni kutu gani kinacho endelea kati yangu mimi na K2 anacho hisi yeye ni kwamba ni leo tu ndio tumekutana.

“Bila samahani mwanangu, nilikuwa ninamuelekeza jinsi ya kuongoza hili jeshi ila nikateleza baadhi ya maneno ndio maana akanidhibu kama hivi”

 

“Oohoo samahani sana mama. Peter mume wangu nakuomba utilize hasira yako”

Yemi alizungumza huku akinishika mashavu yangu,  taratibu akaanza k.. midomo yangu na kumfanya K2 kuanza kuondoka hili eneo.

“Tulia ehee mume wangu”

Yemi aliendelea kunibembeleza huku akinishika mashavu yangu. Yemi akanishika mkono na kuondoka katika eneo hili.

“Peter natambua kila mmoja anaweza kukuletea ushauri wake, ila jaribu kuzuia hasira zako kwa maana hakuna ambaye anaweza kukuletea ushauri mzuri mume wangu”

“Yemi”

“Beee”

Sikuzungumza kitu chochote baada ya kumuona meja akija mbele yangu. Akanipigia saluti, akamtazama Yemi kidogo nikampa ishara ya kuzungumza.

“Mkuu tumehakikisha kwamba hakuna kiongozi anaye ondoka”

“Helicopter zao walizo kuja nazo mume ziwekea ulinzi mzuri?”

“Ndio, nina imani kwamba hakuna itakayo urka na atakaye jaribu kufanya hivyo basi tutamuangusha”

Ehee ngojeni kwanza nyinyi wanaume. Ni kitu gani kinacho endelea hadi wageni wa watu wasiondoke katika hili eneo?”

“Ninahitaji kula nao chakula cha usiku”

 

“Kula nao chakula cha usiku ndio kifanye wasiondoke?”

“Yemi huelewi ni kitu gani kinacho endelea”

“Ndio maana ninahitaji nielekezwe mume wangu, nitaelewa vipi wakati sijaeleweshwa?”

“Kati ya hawa viongozi kuna wasaliti ambao ni lazima niwahushulikie ili jeshi lisonge mbele”

“Basi kama hakuna wasaliti waache wengine waondoke”

“Siwezi kufanya hivyo”

“Fanya hivyo”

Yemi alizungumza kwa ukali hadi meja akabaki akiwa ameshangaaa. Nikamgeukia Yemi na kumtazama usoni mwake kwa macho makali.

“Kama huitaji kusikiliza kile ninacho kifwata, nijajiudhuru cheo changu na utaongoza jeshi la baba yako peke yako”

Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, nikaanza kuvua kofia niliyo ivaa huku nikifwatia vyeo ambavyo vipo kwenye shati langu jambo lililo mfanya meja kwa haraka kupiga magoti chini na kunishika miguu yangu huku akilia akiniomba nisitishe maamuzi yangu ninayo yafanya.



“Jenero, bado tunakuhitaji tunahitaji muongozo wako”   

Meja alizungumza huku akiwa ameendelea kunishikilia miguu yangu. Taratibu nikamuona Yemi machozi yakimwagika usoni mwake.

“Nisamehe mume wangu”   

“Meja unaweza kusimama”

Nilizungumza huku nikimtazama Yemi usoni mwake, nikaanza kurudisha vyeo vyangu nilivyo anza kuvivua kwenye shati langu.

“Hakikiasha mpango nilio waelesza unaendelea kama nilivyo zungumza”

“Sawa mkuu”

Meja akaondoka zake, sikutaka kumjibu Yemi kitu cha aina yoyote zaidi ya kuanze kutembea kwa haraka kuelekea kilipo chumba chetu.

“Peter, Peter”

Yemi aliniita huku akinikimbilia, akaniwahi kunishika mkono wa kushoto.

“Twende tukazungumzie ndani”   

Nilizungumza huku nikiuachanisha mkono wangu na mkono wa Yemi. Tukaingia ndani huku nikiwa nimekasiria, si kwasababu ya ukali wa Yemi alio uonyesha mbele yangu na Meja, ila ni kutokana na kitu alicho kizungumza K2. Taratibu Yemi akapiga magoti chini huku akiendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake.

“Peter ninakuomba unisamehe mume wangu, sikutarajia kama ninaweza kukufokea mbele za watu, natambua utakuwa umefedheheka, ila ninakuomba sana unisamehe mume wangu”

 

Nikabaki nikimtazama Yemi usoni mwake, moyo wangu unatamani sana kumueleza ukweli wa maisha yangu ila akili yangu inakataa kabisa.

“Peter tambua wewe ndio mwanaume wa ndoto zangu, tambua wewe ndio kila kitu kwenye maisha yangu, tafadhali ninakuomba usije ukanichukia kwa kile nilicho kifanya”

“Mke wangu usijipe tabu ya kuniomba msamaha, sio wewe uliye nikosea”

Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimnyanyua Yemi, taratibu nikakaa naye kwenye sofa, nikaanza kumfuta machozi yake, kisha nikampiga busu katika paji la uso wake.

“Nahitaji kubadilisha mfumo wa hili jeshi”

“Kivipi mume wangu?”

“Hivi unatambua kuna watu wamewekeza pesa zao, na wao wanajipatia faida kutoka kwenye hili jeshi, ikiwa kuna wanajeshi wengi wanapoteza maisha yao pasipo kufaidika kwa kitu chochote”

“Mmmmmm. Ni kina nani hao mume wangu?”

“Wageni wote walio kuja leo. Mke wangu nishauri ni nini cha kufanya, nahisi kichwa changu kinapata moto”

Yemi akashusha pumzi nyingi sana huku akiwa kimya akinitazama usoni mwangu.

 

“Mume wangu, baba yangu amekuamini hadi kukuachia cheo hichi, naamini kila unacho kifanya ni sahihi. Hakikisha kwamba unaleta mabadiliko yatakayo mjali kila mwanajeshi ili hata akiamua kufanya kazi basi anafanya kazi kwa juhudu zote”

“Nashukuru mke wangu”

Nilizungumza huku nikimvuta Yemi karibu yangu, akakilaza kichwa chake kwenye bega langu la upande wa kulia.

“Sinto rudia tena mume wangu kukuingilia katika uongozi wako. Nimeamini kwamba una nguvu ya kuongoza kwa maana sikutegemea kama meja anaweza kukupigia magoti”

“Naamini kwamba wamesha anza kunielewa, leo usiku nitahitaji uwepo nami kwenye chakula cha usiku”

“Ni jukumu langu mume wangu siwezi kukuacha uwe mbali nami”

“Nashukuru mke wangu”

Taratibu Yemi akanigeukia na kuanza kuniny mdomo wangu, mlango wa chumba chetu ukagongwa ikanilazimu kumuachia Yemi. Nikaanza kutembea kwa kujiamini hadi mlango, nikaufungua mlango wa chumba chetu, nikakutana na meja akiwa anahema.

“Vipi  meja?”

“Raisi K2 ametoroka yeye na walinzi wake, ameua walinzi wetu kumi”

“Shitiiiii”

Yemi kwa haraka akakimbilia sehemu tuliyo simama.

“Meja unasema mama K2 ameua walinzi kumi?”

“Ndio”

“Mke wangu, K2 ni gaidi, na amejidhihirisha kwamba ni gaidi. Meja nahitaji vijana watakao mlinda mke wangu, au mpelekeni katika chumba maalu cha ulinzi kwa maana simuamini mtu mwengine zaidi yako wewe”

“Sawa mkuu”

 

“Peter wewe unakwenda wapi mume wangu”

“Nilazima nimkamate K2 na kumuangamiza mbele ya wanajeshi wangu”

“Peter tuma tu vijana waweze kwenda kumfwatilia?”

“Hakuna anaye mjua K2 zaidi yangu mimi na hakuna ambaye ataweza kumkamata K2 zaidi yangu”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimekazia macho Yemi.

“Unamfahamu?”   

“Ndio, ila huu sio muda wa maelezo juu ya hilo. Meja hakikisha viongozi wengine wote munawawaka chini ya uangalizi mkali, na hakikisheni hakuna anaye weza kutoroka tena”

“Sawa jenero”

Kwa haraka Yemi akanishika mashavu yangu, akanipiga busu mdomoni mwangu, kisha akaniachia huku akinitaza.

“Mkuu vikosi vipo katika jengo la kujiandaa wanahitaji amri yako. Wewe ongozana na jenero”

 

Meja alizungumza na kunikabidhi mwanajeshi mmoja, tukaanza kukimbia na mwanajeshi huyu na kufanikiwa kufika katika uwanja, nikakuta wanajeshi wakiwa tayari wapo kweye magari na silaha zao.

“Naomba bastola mbili, magazine za kutosha pamoja na jaketi la kuzuia risasi”

“Sawa jenero”

“Ila samahani jenero, mimi ningeona kwamba uturuuhusu sisi kumfwata huyu msaliti na wewe uendelee kulinda hii ngome isije ikakosa muangalizi”

Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hamuwezi kumkamata K2, na musipo angalia munaweza kujikuta nyote munakufa kama alivyo waua wezenu, sawa”

“Sawa jenero”

Nikakabidhiwa jaketi la kuzui risasi, nilalivaa kwa haraka kisha nikapoea bastola zangu mbili pamoja na magazine za kutosha. Nikaruhusu magari kuondoka, huku gari niliyo panda ikiwa imetangulia mbele.

 

“Walielekea wapi?”

Nilimuuliza dereva huku nikimtazama usoni mwake.

“Walieelekea kaskazini mwetu?”

“Wana gari au miguu?”

“Wana miguu”

“Hakuna haja ya kutumia magari, simamisha magari na wanajeshi weote waelekee upande huo”

“Sawa jenero”

Dereva wangu akawasiliana na madereva wote kwa kutumia simu ya upepo. Gari zote sita zikasimama huku mawili yakiwa nia malori mawili na yote yamejaa wanajeshi.

“Hakikisheni tunamkata K2 akiwa hai. Ila ikapo lazimika kumjeruhi vibaya, itabidi kufanya hivyo kwa maana sinto hitaji kuona damu hata ya mmoja wenu ikimwagika nikiwa kiongozi wa hichi kikosi”

 

“Ndio muheshimiwa”

Wanajeshi hawa walizungumza kwa pamoja, nikagawa vikosi vya wanajeshi kumi kumi, tukaanza kuingia msituni huku tunakimbia kwa kasi, ila kila mmoja yupo katika umakini mkubwa. Kadri tulivyo zidi kwenda mbele hatukuweza kuona dalili yoyote hata ya yazo za miguu.

“Mkuu tunazidi kwenda mbele bila mafanikio ya aina yoyote, tunafanyaje na ukitegemea giza ndio hivi linaanzakutawala anga”

Mwanajeshi ambaye muda wote tupo pamoja aliniambia huku akinitazama, hata mimi mwenyewe nimejichokea kutafuta watu wasio onekana.

“Wasiliana na vikondi vingine waulize wameona chote”

“Sawa jenero”

Kwa kutumia simu ya upepo, akawasiliana na wanajeshi nilio wagawa kwenye makundi tofauto tofauti. Ripoti aliyo toa kila mkuu wa kikundi hichi, akadai hajaona chochote.

“Waambie wengine waendele na oparesheni kisha nahitaji wanajeshi watano kurudi kambini”

 

“Sawa mkuu. Oparesheni inaendelea, tunatudi na jenerali kambini”

Wanajeshi watano wakaungana na mimi na kuanza kurudi kwenye kambi yetu. Tukatumia zaidi ya dakika arobaina na tano kufika kambini. Ulinzi mkali hapa kambini ukaendelea kuimarishwa.

“Nipelekea sehemu zilipo maiti za wanajeshi”

Nikaongozana na mwanajeshi huyu hadi kwenye chumba maalumu cha kuhifadhia maiti, nikakuta miili ya wanajeshi hawa ikiwa tayari imesha safishwa na kuweka kwenye mafriji maalumu ya kuhifadhia maiti. Kitu kilicho nishanganza ni miili ya maiti hawa kutokuwa na majeraha ya aina yoyote, ila nilicho kugundua ni shingo zao kuvunjwa.

“Alio kuja nao sio walinzi wa serikali”   

Nilijikuta nikizungumza mwenyewe huku nikimgeuza mwanajeshi mmoja shingo yake.

“Mkuu unasema?”    

 

“Walinzi wa K2 ndio wamefanya hii kazi, na wote wanatoka katika kikosi chake cha wasichana tupu ambacho kazi yao ndio hii”

Nilimuambia mwanajeshi huyu huku nikiendelea kuigeuza shingo ya ya mwanajeshi huyu.

“Unaitwa nani?”

“Martin”

“Unaipenda hii kazi?”

“Ndio mkuu”

“Upo tayari kufa kwa ajili ya mtu mwingine?”

“Ndio mkuu”

“Ninaweza kukuamini?”

“Ndio mkuu”

“Utakuwa mlinzi wangu sawa”

“Nashukuru mkuu”

Martin akanipigia saluti huku akiwa amesimama kikakamavu.

“Una muda gani kwenye hii kambi?”

“Miaka mitano mkuu”

“Basi badae nitahitaji unieleze mambo mengii juu ya hii kambi”

“Ndio mkuu”

Tukatoka katika chumba hichi cha kuhifadhia maiti, moja kwa moja nikaelekea jengo walilo hifadhiwa wageni waalikwa.

“Mke wangu yupo wapi?”

Nilimuuliza meja baada  ya kunikaribia.

“Yupo katika chumba salama”

“Mumeandaa chakula cha usiku?”

“Ndio  kipo kwenye holi la chakula”

“Kamlete mke wangu nahitaji kuzungumza na hawa watu”

“Sawa”

 

“Kuna zile maiti kule chumba cha maiti, nitahitaji ukarekodi, hakikisha kwamba kila maiti unaigeuza shingo yake kwa maana wote wamevunjwa shingo zao. Pia hakikisha huo mkanda unafika nao kwenye ukumbi wa chakula”

“Sawa jenero”

Nikafungua mlango na kuingia katika chumba hichi kikubwa, nikawakuta wageni walio hudhuria kwenye kikao hichi wengine wakiwa wamekaa kwenye masofa huku wengine wakiwa wamesimama wakijadiliana.

“Mutaendelea kutufungia humu ndani kama mateka hadi saa ngapi huu ndio uongozi ulio achiwa na mzee Okocha”

Mzee mmoja alizungumza kwa jazba hadi mate mdomoni yakawa yanamtoka. Nikamtazama kwa macho makali hadi akajistukia na kutazama pembeni.

“Tukielewana hapatokuwa na hata mmoja wenu ambaye ataumia katika hili, ila endapo mutakuwa tofauti na mimi, nina waahidi kila mmoja ninampiga risasi ya kichwa na sinto ogopa nchi zenu kuja kunivamia mimi na jeshi langu, kwa maana nyinyi nyote ni wasaliti”

 

“Wa….sa…a….aliti vi…..pi baba ye….tu?”

Mzee mmoja alizungumza huku amitetemeka mwili mzima.

“Tuna dakika kumi za kujiandaa kwenda kula, mutaongozana na wanajeshi wangu hadi kwenye eneo la tukio, narudia tena na hili lieleweke na mulindane, endapo mmoja wenu atajaribu kukimbia ninawahakikishia kwamba nitawaua nyinyi nyote, sasa kama mulipanga mbinu ya kutorika ninawaeleza mapema kwamba mbinu hiyo ife na muifute kwenye akili zenu. Mmoja atayagharimu maisha yenu wote”

Baada ya kumaliza kuzungumza maneno haya nikatoka ndani humu, nikamkuta Yemi akiwa amesimama mlangoni, akanikumbatia taratibu.

“Pole mume wangu”

“Asante”

“Vipi umefanikiwa kumpata?”

“Hapana wanajeshi wanaendelea na kuwasaka, ila nimeamua kurudi kwa ajili ya hawa wageni wengine”

“Sawa mume wangu”

“Umejiandaa kwa ajili ya chakula?”

“Yaa hapa mimi nipo poa”

 

“Sawa. Meja zoezi limekamilika?”

“Ndi mkuu”

“Si kuna tv kule?”

“Ndio mkuu”

“Basi hakikisha unaiweka mipango sawa”

“Ndio mkuu”

“Meja huyu kijana ni mlinzi wangu kuanzia hivi sasa, ninaimani kwamba unamfahamu vizuri?”

“Ndio mkuu ninamfahamu na hata tatizo lolote katika tabia yake na hata upambanaji wa kutumia silaha pamoja miguu na mikono yupo vizuri”

“Nashukuru kwa maelezo yako meja, andaa wanajeshi watakao wasindikiza hawa viongozi hadi kwenye eneo la chakula mimi ninatangulia na mke wangu”

“Sawa”

    Tukaanza kutembea na Yemi huku akiwa amenishika mkono wangu. Kila muda Yemi ananitazama, anaonekana anahitaji kuniuliza swali ila anashindwa.

“Mume wangu unateseka na hii kazi ehee?”

“Hapana, kwa nini umezungumza hivyo?”

“Unaona jinsi ulivyo vaa haya madude ya kuzuia risasi, lakini kama ungekuwa ni mwana mitindo sasa hivi ungekuwa umetulia bichi tu”

“Ahahaaa usijali mke wangu, yote ni maisha”

Tukafika katika holi la chakula, nikakuta meza ndefu iliyo pangwa vyakula. Nikaitazama kwa umakini, nikamuagiza Martin kuanza kukagua kiti kimoja baada ya kingine na chini ya meza, kwa maana tukio la kutegwa bomu chini ya kiti cha raisi jijini Tanga, nilipo kuwa mlinzi wake bado linajirudia kichwani mwangu.

“Kupo sawa mkuu”

“Shukrani?”

Tukaka katika viti vyetu mimi na Yemi, baada ya muda viongozi wote wakaingia ndani ya eneo hili, wengi wao walio nitazama nyuso zao zimejikunja na kama ingekuwa ni amri zao basi wangesha niua. 

 

“Karibuni”

Nilizungumza huku nikiwa nimesimama, hapakuwa na mtu alite itikia ukaribisho wangu, sikulijali hilo zaidi ya kukaa na wao wakaka. Nikamkonyeza meja, akawasha tv iliyopo humu ndani, ikaanza kuonekana video ya jinsi walinzi wa K2 walivyokuwa wakipambana na wanajeshi wangu hadi ikafika hatu ya kuwavunja shingo na kuwaua na kipande hichi cha video kimerekodiwa na kamera zilizo kuwa katika eneo la tukio. Video hiyo ikaendelea kuonyesha jinsi wanajeshi maiti za wanajeshi hao zikiwa katika mafriji ya kuhifadhia maiti. Wageni wote wakaanza kutetemeka.

“Niliwaambia mmoja wenu akienda kinyume nami basi nitahakikisha kwamba ninawaua kwa mkono wangu mimi wenyewe, je kuna anaye weza kujitetea juu ya hilo”

Nilizungumza huku nikitoa bastola yangu kutoka sehemu nilipo ichomeka, na kumfanya mzee aliye nifokea baada ya kuingia ndani ya chumba walicho kuwepo, kuangua kilio kikali na kuzidi kuwatisha wezake ambao nao wote sura zao zimetawaliwa na woga kwani hakuna hata mmoja anaye jua hatima ya maisha yake kutoka kwangu.



“Ni kitu gani munaweza kunishauri nikawaelewa kwamba kati yenu hakuna msaliti?”

Niliwauliza wageni hawa, mzee akazidi kuendelea kulia kwa uchungu.

“Tuleni chakula”   

Nilizungumza huku nikiirudisha bastola yangu kiunoni nilipo itoa.

 

“Mume wangu nikuombe kitu”       

Yemi alizungumza huku akininong’oneza sikioni mwangu.

“Niambie tu mke wangu”   

“Waonee huruma, hembu tazama huyu mzee wa watu anavyo lia”

“Hahahaa, mke wangu huyo mzee mnafki unakumbuka kwenye msiba, uliweza kumuona hata mmoja wako akiangusha chozi?”

“Mmmm”

“Sasa inakuwaje hapa alie wakati wote hawa ni wanafki”

“Sasa unataka kuwaua kweli mume wangu?”

“Hapana nina watisha, nahitaji kuingia nao mikataba”

“Mikataba ya nini?”

“Ya kuhakikisha kwamba wanalete pesa nitakayo ihitaji kila mwezi, kwa maana kuna familia za hawa wanajeshi wanao kufa, je tunaziangalia vipi, nataka kulibadilisha hili jeshi, lisiwe ni jeshi la kigaidi tena, nahitaji liwe jeshi la amani na kuheshimiwa na watu duniani”

 

“Mmmm sawa mume wangu”

Mazungumzo yetu hapakuwa na mtu hata mmoja aliye weza kuyasikia kwa maana tunazungumza kwa sauti ya chini sana.

“Mzee jinsi unavyo endelea kulia ndivyo utakavyo wafanya wezako nao wafe”

Watu wote wakastuka huku wakinikodolea macho. Nikatabasamu kidogo ili kuwafanya waweze kupata hata uwezo wa kula hichi chakula. Tukaanza kula taratibu huku sauti za vijiko na uma ndio vinavyo sikika katika eneo hili.

“Nitahitaji kuingia mikataba na nyinyi. Mkataba huo utakufanya wewe kuondoka kwenye hili eneo salama salimi pasipo kuudhurika, ila ukikataa basi huto ondoka katika hili eneo na utachukua hukumu ambayo ameifanya K2 kwa watu wangu”

 

Watu wote wakaacha kula hata aliye karibia kukiingiza kijiko chenye chakula mdomoni alijikuta akikishusha na kukirudisha kwenye sahani na kunisikiliza kwa umakini.

“Kila momoja wenu ninahitaji ahakikishe kila mwisho wa mwenzi anaingiza kiasi cha dola milioni tano kwenye akaunti ya jeshi hili, naamini mulivuna pesa nyingi kwenye hili jeshi, sasa ni wakati wa nyinti kurudisha kile mulicho kivuna. Angalizo atakaye kwenda kinyume na makubaliano hayo, nitahakikisha ninaigeukia nchi yako na nitakacho kifahanya sihitaji kuzungumza kwa maana munaelewa hilo sawa”

 

Karibia wageni wote wakatingisha vichwa vyao, nikuita meja, akanisogelea, nikaanza kumpa maelekezo ya kutengeneza mikataba hiyo haraka iwezekanavyo.

“Sawa mkuu”

Meja akaondoka.

“Mume wangu jambo ulilo lifanya ni sahihi sana”

“Yaa ninahitaji wanajeshi wangu waishi maisha mazuri tofauti na hapo awali”

Hazikupita hata dakika kumi na tano meja akarudi akiwa ameshika karatasi, akanikabidhi nikazipitia kwa haraka haraka zote zipo sawa kama vile niliyo muagiza kufanya. Nikanyanyuka kwenye kiti changu na kuanza kumpitishia mgeni mmoja badaada ya mwengine.

 

“Usome mkataba vizuri na uelewe maelezo yake, chagua kufa ama kutuma pesa. Muna dakika tano”

Nikarudi na kukaa kwenye kiti changu, hapakuwa na mgeni yoyote aliye bisha mkataba wangu kwa maana wote wanapenda kuishia. Kila mmoja akasaini mkataba huu unao garimu mwaka mmoja tu na baada ya hapo mimi na wao tunaachana. Baada ya wageni kukabidhi mikataba niliyo wapa, sikuwa na jambo jengine zaidi ya kuwaruhusu kuondoka katika kambi hii.

*Mkuu”   

Martin alizungumza huku akinitazama usoni mwangu

“Ndio”

“Kuna kitu inabidi uone”

“Wapi?”

 

“Kwenye televishion”

Nikaongozana na Martin hadi kwenye ofisi yangu, nikaona taarifa inayo husiana na nchi ya Marekani kutuma vikosi vyake vya anga na ardhi kuja kusaidiana na nchi ya Nigeria katika kuhakikisha kwamba inafutilia mbali kundi la Boko Haramu. Nikaka kimya kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari nini cha kufanya.

“Walitangaza kuhusiana na kiongozi wa hili kundi?”

“Hapana nina imani kifo cha mzee bado hakijafika masikioni mwa watu wengi”

“Sawa niitie makamanda wote wa vikosi, nahitaji kufanya nao kikao cha dharura”

“Sawa”

Japo nimechoka sana na muda umekwenda ila sina jinsi inaniladhimu kuhakikisha kwamba ninalinda jeshi langu na sifikirii hata kumpoteza mwanajeshi haya mmoja. Simu ya mezani ikaita kwa haraka nikaipokea.

“Genero Peter?”

“Mkuu tuna tatizo?”

“Tatizo gani?”

“Tupo huku porini ninaona kuna  majeshi yanajiandaa kutuvamia”

 

“Shiitiiii wapo mbali kiasi gani?”

“Kama mili moja hivi, kuna vijana wangu wamewaona”

“Muna silaha za kutosha?”

“Zipo ila ytutahitaji msaada wako mkuu, kwa maana wanaweza kutumia hata ndege kutumaliza”

“Usijali”

Nikakata simu na kushusha pumzi nyingi sana, ikiwa ni siku ya pili katika uongozi wa hili jeshi ila ninakutana na changamoto moja ambayo kusema kweli ni ngumu kuweza kuihimili kwa haraka. Wakaingia wanajeshi watano huku wakiwa wameongozana na meja.

“Naamini mumesikia au bado hajasikia, nchi ya Marekani imetuma jeshi lake hapa Nigeria na wanasaidiana na jeshi la Nigeria, na hadi ninavyo zungumza hivi sasa nimepata taarifa kwa wanajeshi walipo poroni, vikosi vya ardhi vinakuja sasa sijajua vikosi vya anga navyo vitafika hapa saa ngapi?”

Meja na wezake wakaonekana kushangaa sana, 

 

“Mkuu tumeanini kwamba ni lazima kutakuwa na msaliti kati ya wale wageni kwa maana kambi hii ni ngumu sana kuweza kujulikana”

“Ni kweli na hiyo imesha tokea na kwa sasa hatuna njia nyingine zaidi ya kujipanga na kuhakikisha kwamba tunawazuia hata kabla hawajaweza kufika huku”

“Mkuu tuna ndege za kivita kumi na tano ambazo kumi ni jeti zenye uwezo wa kufanya mashambulizi ya anga kwa anga, na tano ni ndege kubwa zenye uwezo wa kubebe mabomu makubwa yenye uwezo wa kulipua zaidi ya ita elfu kumi kwa bomu moja.”

 ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

BLOG