Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

SIN SEASON 1 SEHEMU YA 7/10

  


SIN SEASON 1

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 7 KATI YA 10


“Ndio mke wangu”

“Ila baba yako ni mkali, sikutarajia kama ana weza kunifokea kiasi kile”

“Usijali alikuwa ana kupima tu kujua ujasiri wako”

“Ila amenionyesha picha za watu wakiwa wame uwawa na ana seme kwamba mimi ndio nina husika”

“Ule mpango wote ulio tokea Morogoro mimi ndio nime husika. Nina muhitaji Evans akiwa hai, bado kuna mambo mengi nahitaji kuyafahamu kwake”

Julieth akastuka kidogo huku akimtazama Jery usoni mwake.

“Wewe ndio una husika”

“Ndio ni mimi na siwezi kumuachia hadi pale nitakapo jiridhisha na maswali yangu nitakayo muuliza”

“Ila baby kwa nini usiachane, ikiwa upo na mimi hapa?”

“Mke wangu hujanijua bado. Mimi nipo hivi, huwa nikianza jambo huwa sipendi liishie katikati, ndio maana nime ishi Marekani maisha yangu, nimekutana na wanawake wa kila aina ila sikuhitaji kuwa nao kwa maana nime anza na wewe na nita hitaji kuyamaliza maisha yangu nikiwa na wewe. Hivyo tambua kwamba sinto weza kumuacha Evans. Maliza kula twende nyumbani”

Jery alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Julieth usoni mwake. Julieth hakuwa na hata hamu ya kuendelea na chakula hicho, akabeba pochi yake, akakabidhiwa simu yake kisha wakaondoka eneo hilo la Ikulu chini ya ulinzi wa walinzi sita wana aminika sana katika kitengo cha NSA.

***

Taratibu Josephine akayafumbua macho yake huku akianza kuangaza angaza ndani ya chumba hicho. Akamuona Magreth akiwa amejilaza kwenye sofa lililopo ndani ya chumba hicho. Akajitazama mguuni mwake na kuukuta ukiwa umefunga bandeji gumu sana(p.o.p.o). Kwa wakati huo hakuweza kuhisi maumivu ya aina yoyote kwa maana bado ganzi ipo mwilini mwake.

“Mage”

Josephine aliita kwa sauti ya uchomvu. Taratibu Magreth akayanyua kichwa chake na kumtazama rafiki yake Akasimama kwa haraka na kusogea sehemu alipo lala Josephine.

“Vipi una jisikiaje?”

“Tupo wapi?”

“Tupo Muhimbilia”

“Tume ondokaje Morogoro?”

“Ni kastori karefu, ila nina shukuru madaktari wa hospitali ya mkowa wa Morogoro walinipatia msaada na nime fanikiwa kukufikisha hapa salama”

“Nashukuru sana rafiki yangu vipi wewe ume umia?”

“Hapana ni michubuko ya hapa na pale, ila hayana madhara”

“Mguu wangu wamesemaje?”

“Wameniambia ume vunjika mara mbili ila wame weza kuuweka sawa na Mungu akibariki uta pona”

“Sawa, je Evans ume pata habari yoyote ya kumuhusu yeye?”

“Hapana sija jua na safari yetu iliishia pale tulipo pata ajali”

“Ila Mungu ata msaidia ata kuwa salama”

“Kweli?”

“Ndio, ila Mage nakuomba umpigie mchumba wangu na umueleze hili sidhani kama ata kuwa ana fahamu kama jana tuliweza kuondoka usiku”

“Usijali una namba zake?”

“Ngoja nikutajie”

Josepheni akataja namba za mpenzi wake kisha Magreth akampigia simu na kumueleza juu ya ajali waliyo ipata.

“Nina kuja hapo sasa hivi”

Kijana huyo alizungumza na simu ikakatwa.

“Magreth nina ogopa, sijui itakuwaje mchumba wangua kija hapa ikia sikumuaga jana usiku”

“Usijali nita zungumza naye mimi”

“Kweli?”

“Ndio nita zungumza naye mimi. Wewe kuwa na amani”

Haikuisha hata lisaa mija, kijana mrefu aliye jazia mwili wake kwa misuli, akaingia ndani ya chumba hicho. Akajawa na mshangao mara baada ya kumuona Josephine akiwa amefungwa bandeji gumu mguuni mwake.

“Kimetokea nini?”

Jamaa huyo alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Tulipata ajali jana usiku”

“Ajali, mulikuwa muna toka wapi?”

Jamaa huyo alizungumza kwa ukali kidogo.

“Joseph, nisamehe mpenzi wangu jana sikuweza kukuaga kwa maana ulikuwa kazini ila rafiki yangu alipata matatizo na alihitaji msaada wangu”

Josephine alijitetea huku akimtazama mpenzi wako huyo.

“Shemeji natambua uta kuwa ume gadhibika kwa hili lililo tokea. Huyu ni rafiki yangu na kama unavyo fahamu ana kipawa maalumu cha kuweza kutambua mambo mengi kwa njia ya maombi. Mume wangu aliweza kutekwa na watu wasio julikana hivyo niliweza kumuomba maada wa kufahamu ni wapi alipo na kwa kupitia kipawa chake tilifahamu kwamba mume wangu yupo mkoa wa Morogoro na kwa bahati mbaya alishikiliwa na watu ambao tuliweza kuwafukuzia na gari na kwa habati mbaya tuliweza kupata ajali”

Joseph akamtazama Magreth kwa macho yaliyo jaa hasira.

“Ume kuwa na mamlaka kwa mke wangu mtarajiwa si ndio?”

“Hapana shemeji”

“Ila”

“Ni jambo la kumuomba msada ila kwa bahati mbaya mambo yame kuwa kama hivi”

“Mulishindwa kutoa taarifa polisi”

“Tuliwakata polisi eneo la tukio ila hawakuweza kufanya jambo lolote”

Magreth aliendelea kuzungumza kwa kujiamini huku akimtazama Joseph aliye fura kwa hasira sana.

“Josephine una tambu kwamba sipendi utoke au kwenda sehemu pasipo idhini yangu kwa nini unisikii. Ona sasa jinsi ulivyo vunjika, je unge kufa wewe malaya ungeniambia nini wewe?”

“Samahani ume niitaje?”

“Malaya, una mchukuaje mke wangu na kutoka naye pasipo idhini yangu?”

“Nina kushehimu ila chunga sana kinywa chako”

“Wewe malaya na una mfundisha mke wangu umalaya”

“Joseph mume wangu usi……”

“Kaa kimya na wewe. Unajifanya mlokole kumbe malaya tu. Umekwenda huko kwa mabawana zenu aoneni sasa mulivyo pata ajali.”

Maneno ya Joseph yakamfanya Josephine kuanza kumwagikwa na machozi ya uchungu kwani katika kipendi chote hicho amekuwa ni mtu wa kuvumilia matusi na manyanyaso kutoka kwa mwanaume huyo ambaye tayari amesha mtambulisha kwa wazazi wake na wapo kwenye hatua za maandalizi ya ndoa.

“Joseph kwa nini hubadiliki, hunionei hata huruma jinsi hali yangu ilivyo. Kwanini una kuwa mwanaume wa aina hiyo.”

“Nikuonee huruma na umalaya wako huo. Jana si ulinieleza kwamba una lala, sasa inakuwaje una niambia oohoo sijui hali yangu ohoo sijui nini. Umalaya tu una kusumbua wewe”

Joseph aliendele kumtusi Josephine na Magreth.

“Nashukuru, ila sidhani Joseph kwa hali kama hii nina weza kuendelea kudumu nayo kwenye maisha yangu yote. Nimechoka kuvumilia manyanyaso yako na mateso hivyo nina kuomba uni ache. Kama nipo tu hivi kitandani una nitusi hivi je nikiwa nina hali mbaya kama hii uta nifanyaje”

“Una semaje wewe mbwa?”

“Nashukuru mimi ni Mbwa ila kuanzia hivi sasa mimi na wewe basi”

Joseph akamsogelea Josephine kwa hasira akataka kumshika mkono wake ila Magreth akauwahi na kumzuia.

“Usione nime kaa kimya ukahisi nina kuogopa tafadhali nina kuomba uweze kutoka ndani hapa”

Joseph akamtazama Magreth kuanzia usoni hadi katika mkono wake ulio mshika.

“Niachie mkono wangu kabla sija kuvuruga sura yako”

“Nitakuachia mkono wangu pale utakapo kubali kutoka ndani hapa”

Joseph kwa nguvu akamashika Magreth shingoni mwake na kuanza kumkaba. Kitendo hicho kika muashiria Magreth kwamba mwanaume huyo hataki amani na analo lihitaji kwa sasa ni fujo. Magreth kwa mikono yake miwili akaupiga kwa nguvu mkono wa Joseph, akampiga kigoti cha tumboni na kumfanya Joseph kuanza kugugumia kwa maumivu makali sana kwa maana hakutegemea kamaa ana weza kupigwa na Magreth ambaye ana mchukulia ni mnyonge kama mpenzi wake Josephine.



“Toka humu ndani na usidhubutu kurudi tena kwa maana ukirudi nita hakikisha nina kufanya kitu amacho hujawahi kufanywa kwenye maisha yako”

Magreth alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasri, Joseph taratibu akaanza kutoka ndani hapo huku akiwa amejikunja kwa maana maamivu anayo yahisi kwenye tombo lake si ya mchezo mchezo.

“Na jambo jengine. Ole wako nione siku una mtukana rafiki yangu au kumdhalilisha kwa aina yoyote ile, nakuapia haki ya Mungu sinto kuacha salama wewe. Umenielewa?”

Joseph akatingisha kichwa, akafungua mlango na kutoka ndani hapo. Taratibu akamsogelea Josephine na kumkumbatia.

“Japo tume umbwa kusikiliza amri ya mwanaume na kufwata yale anayo yahitaji ila haitupasi kuendelea kukaa chini ya manyanyaso yao na kejeli kama hizi. Nimuda wako sasa Josephine kusimama wewe kama wewe na si kumtegemea mwanaume. Sawa”

Magreth alizungumza kwa sauti ya upole huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.

“Nashukuru kusikia hivyo rafiki yangu. Nina kupenda sana”

“Nina kupenda pia Josephine”

Wakakumbatiana huku wote wakimwagikwa na machozi mengi kwenye nyuso zao.

***

Walinzi hao wakazidi kujitahidi kuogelea ila kila aliye jaribu kushika jabali alilo kalia Evans, hakuweza kumruhusua na alicho kifanya ni kuikanyaga mikono yake, kutokana na wingi na nguvu ya maji hayo wakajikuta wakisombwa na kuzidi kupelekwa mbali sana. Evans akaendelea kukaa ju ya jabali hilo kwa muda mrefu huku mwili wake wote ukitetemeka kwa baridi kali pamoja na maumivu ya kujibamiza katika baadhi ya majabali yaliyomo ndani ya mto huo. Masaa yakazidi kusonga mbele na giza likaanza kutawala anga. Baridi kali ikazidi kuutesa mwili wa Evans ambaye hapo alipo ana tisheti na suruali yake tu.

‘Ehhee Mungu kwa nini nina pitia mateso yote haya. Ni nini nilicho kukosea mimi?’

Evans alizungumza huku akiendelea kujikunyata kwa baridi hiyo. Maji ya mto huo hayakuweza kutulia kabisa, matone ya mvua yaliyo anza kumdondokea taratibu yaka zidi kumpa wasiwasi na woga mwingi sana. Hazikuisha hata dakika ishirini mvua kubwa ikaanza kunyesha na kumfanya Evans azidi kuteseka katika eneo hilo. Maji yakazidi kujaa mara dufu, maji hayo sasa yakaanza kufika kimo cha jabali hilo na kuzidi kumfanya Evans kupagawa.

‘Ehee Mungu niokoe’

Evans alizungumza huku akiendelea kung’ang’ania jabali hilo. Wimbi kubwa likamkumba na kujikuta akishindwa kabisa kushikilia jambali hilo. Akasombwa na maji hayo na kujikuta akianza kupiga kelele huku akilia kwa jinsi anayo zungushwa zungushwa na maji hayo yanayo mfanya ashindwe hata kuogelea. Evans naye akaanza kubamizwa kwenye baadhi ya majabali yaliyomo katika mto huo na kumsababishia maumivu makali sana. Maumivu hayo yakazidi kuutesa mwili wake na mwishowe akajikuta akipoteza fahamu.

Sauti za watu wanao zungumza lugha ambayo Evans hakuweza kuitambua kwa uharaka kwa maana ni lugha ya kikabila. Akafumbua macho yake na kujikuta akiwa amelazwa k

wenye kitanda chakavu fulani. Chumba alicho lala kime tengenezwa na matofali ya kuchomwa na juu kime ezekwa na nyasi. Mwanga wa jua unao pitia dirisha dogo, ukamfanya Evans kutambua kwamba kume pambazuka japo hakumbuki ni jinsi gani alivyo weza kufika katika eneo hilo.

Akanyanyuka kitandani taratibu, ila maumivu makali ya mwili mzima yakamfanya aweze kurudi tena kitandani na kulala. Akaingia msichana aliye valia kaniki nyeusi huku kichwani mwake akiwa amenyoa nywele zote. Msischana huyo akamuita baba yake, naye akaingia ndani hapo huku naye akiwa amejifunga kaniki nyekundu huku mkononi mwake akiwa ameshikilia mkia wa Simba. Mzee huyo akazungumza kilugha huku akimtazama Evans usoni mwake.

“Baba yangu ana uliza una jisikiaje?”

Msichana ali tafsiri lugha hiyo ya kiruguru.

“Nasijisikia maumivu mwili mzima. Hapa nipo wapi?”

Msichana huyo akamuambia baba yake huyo ambaye ni mzee sana na wala hafahamu lugha ya kiswahili.

“Baba ana sema uta pona tu”

“Sawa, hapa nilipo nipo wapi?”

“Upo kwenye milima ya Ukaguru”

Binti huyo alijibu na kumfanya Evans kujawa na mshangao mkubwa sana.

“Nimefikaje fikaje hapa?”

“Leo asubuhi tulipo kuwa tuna tafuta samaki kwenye bwawa tuliweza kukuokota wewe ukiwa ume nasa kwenye moja ya jiwe kubwa. Tulipo gundua kwamba upo hai tulikuleta hapa”

Evans akamtazama msichana huyo kisha macho yake akayahamishia kwa mzee huyo na akakutana na tabasamu pana la mzee huyo.

“Nina shukuru kwa kunisaidia”

Msichana huyo akamtafsiria baba yake. Kisha baba yake huyo amampa maagizo ya kuleta dawa walio kuwa ana ichemsha. Baada ya muda msichana huyo ambaye ukimchunguza kwa sana, ana urembo ulio fichika katika dibwi kubwa la umasikini, akaingia ndani hapo huku mkononi mwake akiwa ameshika kikombe cha plastiki ambacho kime jaa dawa.

“Hii ni dawa ya kuponyesha maumivu ya ndani kwa ndani”

Msichana huyo alizungumza huku akimkabidhi Evans kikombe hicho. Taratibu Evans akachukua kikombe hicho, akakitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kunywa. Uchungu wa dawa hiyo ukamfanya Evans kusitisha kwanza kunywa dawa hiyo huku akisikilizia jinsi inavyo mkereketa kwenye kinywa chake.

“Kunywa, ita kusaidia”

“Mbona chungu sana?”

“Ndio dawa kaka”

Msichana huyo aliendelea kumsisitizia Evans, hakuwa na jinsi yoyote zaidi ya kujikaza na kunywa dawa hiyo. Kwani kitendo cha watu hao mkusaidia na kumleta nyumbani hapo basi wana onekana ni watu wema sana hivyo hakuwa na wasiwasi na dawa hiyo.

“Ohooo khragrahaaa!!!”

Evans alilalama huku uso wake ukiwa umejikunja kisawa sawa. Baada ya kumaliza dawa hiyo, binyo huyo akamkabidhi Evans kipande cha sukari guru.

“Ni nini hii?”

“Sukari, lamba ina maliza uchungu wako mdomoni”

Evans akatazama kipande hicho,akakilama kidogo na alipo gundua kweli ni kitambu basi akaanza kukilamba kwa fujo ili mradi kutoa uchungu wote mdomoni.

“Una itwa nani?”

“Mimi?”

“Ndio”

“Naitwa Evans”

“Sawa”

Binti huyo akamtafsiria jinsi alivyo zungumza na Evans.

“Baba ana kuambia ukaribie hapa nyumbani”

Mzee huyo akatoka ndani hapo na kumuacha binti yake huyo na Evans. Taratibu Evans akamtazama binti huo jinsi alivyo jazia maeneo ya kiunoni mwake. Hispi zake kwa kweli zime weza kubeba makalio makubwa kiasi cha kumfanya Evans kuingiwa na tamaa ya ngono. Mbaya zaidi kaniki aliyo ivaa kidogo ina onyesha maumbilie yake ya ndani.

“Mbona una nichunguza sana?”

“Aha….hapana”

“Usinitamani kwa maanaa mwanaume yoyote anaye jaribu kufanya hivyo basi ni lazima afe”

Msichana huyo ambaye haja jitambulisha jina lake alizungumza kisha akatoka ndani hamo na kumuachia Evans maswali ya sinto fahamu ya kwani msichana huyo ame weza kuzisoma hisia zake haraka sana tofauti na alivyo mdhania kwa maana amekaa kishamba shamba.

***

“Ehee jana ilikuwaje?”

Nabii Sanga alimuuliza Julieth mara baada ya kukutana naye sebleni.

“Ahaa katika siku zangu zote za maisha nilizo ishi hapa duniani, jana ilikuwa ni siku yangu ngumu baba”

“Kwa nini ilikuwa ni siku ngumu?”

“Daa wee acha tu. Yaani baba yangu mkwe ni mkali kisawa sawa. Ile nina kutana naye akanionyesha picha za walinzi walio uwawa mkono Morogoro. Weee niliogopa sana, baada ya hapo akaagiza nipelekwe kwa dokta nipimwe kila kitu. Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba nimekutwa nipo salama kila idara”

“Yule mzee ni mkali sana. Ila mwishoni ilikuwaje?”

“Nimepita jaribio hilo na amekubali niolewe na mwanaye”

Nabii Sanga akatabasamu kidogo kisha aka mkumbatia Julieth kwa maana uwepo wake uta leta faidi kubwa sana kwenye familia yake.

“Sasa kuna mambo nina bidi kukueleza kama mwana familia uliye kuwa na una kwenda kuolewa sasa mwanangu”

Nnabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akimtazama Julieth kwa umakini sana usoni mwake.

“Ni nini baba”

“Niandalie kahawa nzuri na uje huku kwenye bustani.”

“Sawa”

Nabii Sanga akaondoka sebleni hapo na Julieth akaandaa kahawa hiyo ambayo yeye na mama yake tu ndio watu wa pekee wanao weza kuandaa kahawa nzuri na inayo mpendeza mzee huyo. Julieth akamuandalia baba yake kikombe hicho cha kawaha kisha akaa kiti cha pembeni katika kijibanda hicho cha kupumzikia, kilichopo katika bustani hiyo yenye majani mazuri sana.

“Ndio baba”

“Kwenye maisha yangu kuna mambo mengi sana sikuweza kukueleza kama mwanangu mpendwa. Japo kuna baadhi ulisha wahi kuyaona na yaka kuumiza ila sasa ni wakati wa wewe kuweza kutambua kila jambo”

Nabii Sanga baada ya kuzungumza hivyo, akapiga fumba moja la kahawa kisha akaendelea kuzungumza.

“Natambua hivi karibuni una kwenda kuwa mkwe wa raisi Mtenzi. Uwepo wake kwenye familia yake si kumzalia wajukuu tu na akafurahi, bali nasi kwa upande wetu ni lazima tuweze kunufaika katika kipindi hichi ambacho yeye ata kuwa ana nufaika na wewe”

“Nahitaji ukiingia kwenye familia yake kuna baadhi ya majukumu uweze kuyafanya”

“Majukumu gani baba?”

“Moja nina hitaji uweze kumshawishi Jery kubaki hapa nchini Tanzania na kama ata rudi nchini Marekani basi akamalizie kusoma tu kisha arudi Tanzania”

“Hilo ni jambo rahisi halina shaka baba”

“Jambo jengine nina hitaji utengeneze uaminifu na uweze kupata nafasi ndani ya ikulu ya raisi Mtenzi, si kama mkwe tu bali uwe kama sekretari au uwe na nafasi yoyote ambayo itakusaidia katika kujua kila jambo linalo endelea ndani ya ikulu ile”

“Kwa nini baba una taka niajiriwe ikiwa una fahamu kabisa kwamba mimi ndoto zangu ni kuwa mfanya biashara mkubwa?”

“Nalielewa hilo mwangu, ila kazi yako utakayo ipata ikulu, ita zitimiza kwa haraka ndoto zako za kuwa mfanya biashara mkubwa sana ndani na nje ya Tanzania. Moja uta weza kuhakikisha kwamba biashara zako zote zina pita bandarini pasipo usubumbu wa aina yoyote na wala huto weza kuchukuliwa kodi ya aina yoyote ila. Nina imani una tambua ni jinsi gani kodi zinavyo waumiza wafanya biashara”

“Yaa ni kweli baba”

“Pili nahitaji tuingie kwenye biashara ya giza”

“Biashara ya giza? Kivipi baba?”

“Biashara ya giza ni biashara ambazo zina tuingizia kipato kikubwa. Mimi na mama yako tulikuwa tuna ifanya biashara hiyo kwa siri sana na wewe ndio uta kuwa mtu wa pekee ambaye una weza kufahamu siri hiyo”

“Ni biashara gani hiyo baba?”

“Tuna uza madawa ya kulevya”

“BABAAAAAAA!!!”

Julieth alishangaa sana huku akimtazama baba yake.

“Usishangae mwanangu. Una hisi kanisa kama kanisa lina weza kutuingizia pesa nyingi kiasi cha nyinyi akaunti zenu kuwa na mabilioni of money? No hii biashara ndio ima wafanya na nyinyi leo mukipangwa kwenye orodha ya vijana matajiri basi na nyinyi wanangu wote watatu muta kuwepo”

Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Julieth kushusha pumzi nyingi.

“Muna muda gani muna ifanya hiyo biashara?”

“Kabla hata wewe hujazaliwa”

“Hee hamjawahi kukamatwa?”

“Hakuna aliye weza kutugusa wala kufahamu au kuhisi. Trust ndio kitu pekee kilicho tufanya tukae zaidi ya miaka ishirini na nane kwenye hiyo biashara. Ni hivi juzi juzi tu ndio tuli simama kama miaka miwili, kuangalia nguvu ya raisi Mtenzi ipo vipi ila kwa sasa tuna yaka kurudi rasmi na tuna hitaji kuingiza kiasi kikubwa sana cha pesa kutokana na mahusiano yetu haya tunayo kwenda kuyajenga”

Julieth akashusha pumzi taratibu huku akimtazama baba yake usoni kwa maana mtihani alio pewa ni mkubwa sana.

“Ila baba ni kazi hatari?”

“Ndio ni hatari ila hakuna ambaye ata fahamu juu ya wahusika wake”

“Ila baba nikiwa ndani ya ikulu, muda wote ita nipasa kuwa karibu sana na raisi. Nina imani kwamba simu zangu zita kuwa zina rekodiwa. Je hapo itakuwaje baba?”

“Kuna mfumo maalumu ambao tuta kuwa tuna utumia kuwasiliana”

“Mfumo gani huo baba?”

“Nita kuamabia ni mfumo gani ila jina lako utakuwa una litumia kwenye uongozi wa biashara hiyo ni BLACK GHOST. Kwa maana mimi baba yako nina kwenda kukurithisha jina hilo”

Nabii Sanga alizungumza huku akitabasamu na kumfanya Julieth naye kutabasamu huku kwa maana mtoto wa nyoka naye ni nyoka.



“Black ghost?”

“Ndio mbona kama una lishangaa?”

“Miaka ya nyuma kama nilisha wahi kulisikia hili jina ila sikuwahi kulifwatili”

“Ulilisikia wapi?”

“Sikumbuki ni wapi nililisikaila nilisha wahi kulisikia”

“Sawa baadae usiku kuna sehemu tutakupeleka sisi na mama yako kukutana na wanachama watakao kuwa chini yako”

“Leo?”

“Ndio leo usiku, kwa maana biashara tuna hitaji kuanza hivi karibuni”

“Sawa baba nipo tayari, ila kuna jambo moja nina hitaji kukuomba”

“Jambo gani?”

“Nahitaji uhidi juu ya usalama wangu”

“Nina kuahidi na kitu cha pekee ni akili, ukitulia basi kila jambo lita kuwa sawa. Umenielewa mwanangu”

“Nimekuelewa baba”

“Sawa”

Nabii Sanga akatabasamu huku akimtazama Julieth usoni mwake kwa maana alicho kipanga kukifanya ni kuhakikisha mwanaye huyo ana kuwa Mungu wa madawa ya kulevya Afrika na duniani kwa uzima.

***

Binti huyo akaingia tena chumbani hapo akiwa amebeba sahani yenye vipande vinne vya maboga. Akakaa pembeni ya kitanda hicho alicho lala Evans.

“Una fahamu haya?”

“Ndio nina fahamu si maboga?”

“Yaa, ndio kifungua kinywa chako kwa leo. Inabidi ule kwa maana hiyo dawa ulio kunywa ina nguvu kubwa sana”

“Nashukuru, ila sijafahamu jina lako una itwa nani?”

“Niite tu dada”

“Dada ndio jina lako?”

“Hapana sio jina langu ila wewe niite hivyo. Kula ukimaliza nitakuja kuchukua sahani kwa sasa kuna wateja nina paswa kwenda kuwashuhulikia”

“Sawa ila nina swali moja kama huto jali?”

“Uliza”

“Una sema kwamba muli niokota kwenye mto je humkuokota mili ya watu wengine?”

“Hapana hatujaiona, ila kwa mto ule huwa ni bahati sana kwa mtu kuweza kupona. Wewe una bahati kwa maana kuna mamba wakubwa sana”

“Wee!!”

“Shangaa ila huo ndio ukweli”

Dada baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka na kutoka ndani hapo. Vijana wote walio agizwa na Jery kumkamata Evans na walijitosa kuhakikisha wana mkamata Evans aiye jirusha kwenye kwenye mto hawakuwa na bahati kwenye maisha yao. Nguvu ya maji ya mto huo hawakuweza kupambana nayo kwa maana wote walijikuta wakiingia kwenye mto ambao una mamba wakubwa sana. Mmoja baada ya mwengine walijikuta wakitafunwa vibaya sana na mambo hao. Mvua kubwa iluyo nyesha iliweza kumsaidia sana Evans kwa maana mamba hao waliweza kwenda mbali na eneo la pembezoni mwa mto huo. Hadi Evans ana pata msaada wa kuokotwa na dada, mamba hao walikuwa bado hawajarudi katika eneo hilo.

Evans taratibu akaanza kula maboga hayo na kujikuta akikumbuka maisha ya nyumbani kwao. Akakumbuka jinsi mama yake alivyo kuwa ana muandalia maboga kabla ya kwenda shule alfajiri. Jitihada zake za kusoma hakika zilimuwezesha kufika mbali kielimu, ila ubaya ni kwamba wa sasa hata hata cheti hata kimoja na kuna watu wana muwinda ili kuyatoa maisha yake.

‘Sinto kuja kumpenda mwanamke yoyote wala kumuamini’

Evans alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Akakumbuka wosia ambao mama yake alikuwa ana mpatia mara baada ya kuchaguliwa kwenda chuo kikuu jijini Dar es Salaam. Mama yake alimsisitizia ajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha ana soma kwa bidii ili kuitoa familia yake kwenye dimbwi kubwa la umasikini. Isitoshe yeye ndio ame husika katika kumuua baba yake ambaye alikuwa ni moja ya chanzo kikubwa cha kuwafanya wame masikini. Evans akajipangusa machozi yake na kuendelea kula maboga hayo. Akamaliza kula, kisha akajitahidi taratibu na kushuka kitandani. Akaanza kujikongoja kuelekea nje huku akiwa ameishika sahani hiyo. Evans akajikuta macho yakimtoka kwa maana eneo hilo ilipo jengwa nyumba hiyo ni mlimani na kumezungukwa na miti mingi pamoja na mawe makubwa makubwa.

“Mbona ume toka, nilikuambia ita kuja kuchukua sahani”

Dada alizungumza huku akimfwata Evans mlangoni hapo.

“Nimeona nisikusumbue’

“Hapana bwana udi ndani usije ukapata maumivu mengine”

Dada alizungumza huku akichukua sahani hiyo na kuontondoka eneo hilo na kuingia katika nyumba ya pembeni ambayo nayo ime tengenezwa kwa matofali ya kuchoma.

***

“Vipi ame kubali?”

Mrs Sanga alizungumza huku akimtazama mumewe usoni.

“Yaa amekubali, na nina imani kwamba Julieth ata kuwa mbaya kuliko hata sisi”

“Hata mimi nina ona. Watoto wetu wa kiume wote wawili naona kila mmoja ana njia yake ila Julieth nina imani ata kuwa nasi pamoja”

“Yaa ndio maana miaka yangu yoye nime kuwa karibu naye ili mradi nije kumrithisha maisha yetu. Nakuambia ata kuja kuwa mkali zaidi ya sisi tunavyo hisi”

Nabii Sanga alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama mke wake. Taratibu mrs Sanga akamsogelea mume wake, akaanza kumfungua vifungo vya shati lake.

“Nahitaji leo uni fuc** hadi nyeg** zangu zote ziniishe”

Mrs Sanga alizungumza huku akimvua mume wake shati hilo. Nabii Sanga akamsukuma mke wake kitandani, akakipandisha kigauni chake alicho kivaa juu, kisha akavua suruali yake na yeye akapanda kitandani. Kabla hajafanya kitu chochote simu yake ikaanza kuita.

“Ohoo sorry mke wanu”

Nabii Sanga alizungumza na kushuka kitandani, akaichukua simu yake mezani na kuitazama kwa sekunde kadhaa.

“Muheshimiwa raisi”

Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kwa maana simu hiyo ni kutoka kwamkwe mwenzake.

“Ndio muheshimiwa”

“Ahaa Sanga ni mara ngapi nilikuleza usiniite muheshimiwa, tukiwa tuna zungumza mimi na wewe”

“Ohoo samahani kwa hilo”

“Sasa saa kumi jioni tuta kuwa na ufunguzi wa kiwanda cha magari. Hivyo kama huto jali nina kuomba uweze kufika hapa ili kufungua kwa maombi, si unajua bila ya maombi ya watu watakatifu kama nyinyi mipango ina weza kwenda vibaya”

“Ni kweli muheshimiwa. Tuta fika hapo na mke wangu”

“Nashukuru sana tena sana”

“Hata sisi tuna shukuru kwa mualiko wako mkubwa ulio tupatia”

“Sawa”

Simu ikakatwa na kumfanya nabii Sanga kuzidi kujawa na furaha kwa maana kama ni mipango yake basi ina zidi kuchanua. Nabii Sanga akapanda kitandani hapo na kuanza kumpa mke wake haki yake ipasavyo.

“I like your dic** baby”

“Really?”

“Yaa I like it”

Mrs Sanga alizungumza huku akizidi kukata mauno huku akiwa amemkalia jogoo wa nabii Sanga. Wakamaliza mzunguko wa kwanza na wakaendelea na mzunguko wa pili. Walipo hakikisha kwamba kila mmoja kiu yake ime katika, wakaingia bafuni kwa pamojana kuoga.

“Muambie Julieth juu ya safari hii”

“Ajumuike nasi?”

“Ndio mke wangu. Kumbuka kwamba Julieth ndio kiunganishi chetu na familia ya mtenzi”

“Sawa mume wangu”

Mrs Sanga akampigia simu Julieth aliyopo chumbani kwake, akamueleza kuhusiana na safari hiyo na Julieth akakubali. Wakajiandaa na saa tisa na nusu wakaianza safari ya kuelekea katika kiwanda hicho.

“Julieth”

“Bee mama”

“Ume tupa heshima kubwa sana mwanangu. Ila nina kuomba usije ukaipoteza heshima hii tuliyo pewa”

“Usijali baba, kuanzia sasa natambua kwamba mimi ni nani na lengo langu la kwenda kwenye familia ile ni nini”

“Ndio maana nina kupenda mwanangu”

Nabii Sanga alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari hilo la kifahari Toyota VX V8. Wakafika eneo hilo la kiwanda lililo jengwa kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo. Nabii Sanga akapokelewa na sekretari wa raisi Mtenzi kisha yeye na vamilia yake wakapelekwa katika jukwaa la V.I.P ambapo viongozi wengine wana zaidi kuongezeka mmoja baada ya mwengine huku wakiwa na hamu ya kumuona raisi wa Marekani pamoja na raisi wao wa Tanzanaia raisi Mtenzi. Haukupita muda mrefu gari za maraisi hao zikafika katika eneo hilo. Watu wengi walio jitokeza katika eneo hilo wakazidi kushangilia maraisi hao. Baada ya maraisi hao kuketi kwenye viti vyao ratiba ikaanza huku shehe mkuu akipewa nafasi ya kuanza kusali kisha akafwatia nabii Sanga kusali.

***

Magreth akaachia msunyo mkali mara baada ya kumuona nabii Sanga akiomba katika ufunguzi wa kiwanda hicho.

“Mbona una sunya. Una muona nabii wetu amealikwa naye?”

Josephine alizungumza huku akimtazama Magreth aliye kasirishwa mara baada ya kumuona nabii Sanga akisali katika tv iliyopo chumbani hapo.

“Hakuna”

“Kweli?”

“Ndio hakuna jambo”

“Magreth kuna jambo moja nahitaji kufahamu”

“Jambo gani?”

“Utajiri wako ume utolewa wapi. Kutoka kuuza maandazi hadi kumiliki mgahawa tena ndani ya muda mchache niambie ime kuwaje?”

Magreth akashusha pumzi huku akimtazama Josphine ambaye ndio mtu wa kwanza kumuuliza swali hilo linalo husiana na utajiri wake. Kabla hajazungumza chochote simu yake ikaita, kwa haraka akaitazama na kukuta ni Juma.

“Juma vipi?”

“Safi vipi mgahawa una kwendaje?”

“Una kwenda vizuri bosi. Tume pata new oder”

“Kutoka wapi?”

“Ubalozi wa Marekani hivyo wana kuhitaji tuweze kuzungumza nao”

“Kwa lini?”

“Leo hii saa moja usiku”

“Duu oder ni ya chakula”

“Ndio bosi una hisi ita kuwa ni oda ya nini tena”

“Nipo Muhimbili, basi acha nije hapo kazini”

“Sawa”

Magreth akakata simu na kumgekia Josephine.

“Jose nina toka rafiki yangu, nina kwenda kwenye ofisi yangu kuna mambo ya kuyaweka sawa. Hilo swali lako nina kuomba sana niweze kukujibu siku nyingine”

“Sawa kuwa makini”

“Usijali, nita kuja kama saa mbili au saa tatu usiku, ila madaktari nitazidi kuwasisitizia wakuangale kwa ukaribu sana ili huyu jamaa yako asije akarudi”

“Usijali rafiki yangu Mungu yu pamoja nami”

“Amen”

Magreth akaondoka hospitalini hapo na kufika kazini kwake. Akasalimiana na wafanyakazi wake ambao toka asubuhi haja onana nao.

“Ehee niambie”

“Jana jioni hadi leo tume pata wateja wengi kutoka nchi ya Marekani na China. Hivyo tume ombwa tuwe tuna tengeneza chakula kwa ajili ya ubalozi huo. Ila wana hitaji chakula hicho kikapikiwe kule kule ubalozini”

“Wamarekani ni wajanja sana”

“Kivipi?”

“Wanatupatia dili hilo ila wanacho kihitaji wao ni kujua ujuzi tunao tumia katika kutengeza chakula chetu kwa maana ni kitamu sana na endapo wakifahamu basi wana weza kumaliza mkataba na sisi na tukarudi katika maisha ya wateja wetu”

“Sasa niwajibu nini bosi”

“Waambie kwamba chakula chetu kina pikwa hapa. Atakaye hitaji kuja kula aje asiye hitaji kuja aondoke ndio maana nime fungua mgahawa. Sawa Juma?”

Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Juma usoni mwake.

“Ndio bosi nime kuelewa”

Juma alijibu kwa unyonge kwa maana kile alicho kuwa ana kitarajia sicho alicho jibiwa na bosi wake.



“Safi kama ume nielewa”

“Ila bosi nina kuomba uweze kufikiria mara mbili hili dili. Una jua wame tuambia wata tulipa kiasi gani kwa wiki?”

“Kiasi gani?”

“Dola milioni moja, hivyo kwa mwenzi tuta kuwa na dola milioni nne sawa na bilioni nane za Kitanzania kwa wakati huu”

Magreth macho yakamtoka kwa maana kiwango hicho cha pesa ni kikubwa sana.

“Bosi haya ni maisha na hii ni bahati. Kuna makampuni mangapi yanayo pika chakula yameachwa na kufwata sisi kwenye mgahawa wetu. Hembu jaribu kulitazama hilo bosi.”

“Juma acha utani?”

“Sikutanii bosi nina kueleza ukweli. Hii ni namba ya mshauri wa balozi wa Marekeni, ameniachia leo baada ya kupata chakula chetu hapa”

Juma alizungumza huku akimuonyesha Magreth kadi ndogo yenye ndani ya mshauri huyo wa balozi wa Marekani nchini hapa Tanzania.Kadi hiyo imeandikwa jina la mshauri huyu, namba zake za simu na ofisi anayo ifanyia kazi na ina dhihirisha kweli ana fanya kazi katika ubalozi huyo wa Marekani.

“Wewe ni bosi wangu, natambua kwenye maisha yako siku zote una wazia kuwa tajiri mkubwa ili uweze kuwa katika orodha ya watu wenye pesa nyingi hapa Tanzania. Sasa huu ndio wakati wako kufanikiwa bosi”

Ushawishi wa Juma ukazidi kumuingia Magreth akilini mwake.

“Hembu niambie ilikuwaje kuwaje?”

“Kama unavyo jua hali halisi iliyopo hapa nchini. Raisi wa Marekani yupo hapa nchini. Wamarekani kwa sasa wapo wengi sana, hivyo walikuja hapa na wakaanza kupata chakula cha jioni. Walivutiwa sana na chakula chetu, wakazungumza biashara na mimi nami nimekuletea ili uwe muamuzi wa mwisho”

“Okay nime kubali, huyo muhisika ana hitaji tuonane naye lini?”

“Hata leo yupo tayari”

“Basi mpigie ili kama ni kuonana naye tuweze kukutana”

“Sawa”

Juma akampigia kiongozi huyo, ila simu yake haikuweza kupokelewa, akarudi kwa zaidi ya mara tatu ila majibu yakwa ni hayo hayo.

“Kama hapokei basi ata pokea baadae kwa maana nahisi wata kuwa kule kiwandani”

“Yaa ni kweli nime kumbuka”

“Alafu acha nikupe namba yangu ya benki pasa ikifikia mchana una kwenda kuzituma benki sawa”

“Sawa bosi”

Magreth akampatia Juma namba ya akaunti yake ya benki kisha akaelekea jikoni kumuandalia Josephine chakula cha jioni.

***

Nabii Sanga mara baada ya kutoka kwenye sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha magari nchini Tanzania. Wakaelekea katika mji wa Bagamoyo, wakapata chakula cha usiku katika hoteli moja ya kitalii ambayo nabii Sanga huwa ana penda sana kwenda kupata chakula akiwa katia mji huo.

“Chakula chao ni kitamu sana”

Julieth alizungumza huku akiendelea kula.

“Umekipenda ehee?”

“Ndio baba nime kipenda”

“Siku ya kwanza tulipo kuja hapa na baba yako nili mshawishi tuwachukue hawa wapishi wakatupike kule kwenye hoteli yetu”

“Ikawaje mama?”

“Walikataa. Wapishi wa hapa wana jali sana utu kulipo pesa”

“Mmmm labda muliwawekea dau dogo”

“Hapana tuliwapa ofa nzuri ila walishindwa kutuelewa, basi hatukuwa na namna”

“Bado muna wahitaji?”

“Ndio, una jua katika biashara yoyote ni lazima mtu uhakikishe kwamba una cheza rafu li mradi mambo yako yaweze kwenda”

“Ni kweli baba, ila nipeni siku kadha, nita washawishi na nita waondoa wote hapa”

Nabi Sanga akatoa simu yake iliyopo mfukoni na kuipokea.

“Ndio”

“Munaweza kuja”

“Haya”

Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza maneno hayo ya mkato mkato akakata simu na kuirudisha mfukoni.

“Baba ni kina nani hao wana kuja?”

“Ni vijana wangu, wana kuja kutuchukua”

“Tuna kwenda wapi kwani?”

“Kwenye eneo ambalo ndio kikao leo kita fanyika kuanzia saa sita usiku. Tambua una kwenda kuwa mrithi wa mtandoa wetu, hivyo akili yako ina kupasa kuwa active zaidi ya hivi sasa”

“Sawa baba”

Majiria ya saa nne usiku, gari moja nyeusi aina ya BMW X5 ikafika katika eneo hilo la hoteli.

“Simu na vitu vyote vya mawasiliano tuviache kwenye gari”

Nabii Sanga alimuambi Julieth na mke wake. Wakaweka simu zao pamoja pochi zao ndani ya gari lao, kisha wakafunguliwa mlango na kijana mrefu aliye valia suti nyeusi na wakaingia katika gari hilo kisha wakaondoka hotelini hapo. Wakafika pembezoni mwa bahari na wakashuka kwenye gari hilo na wakapokelewa na vijana wengine wawili ambao nao wame valia suti nyeusi. Wakapanda kwenye boti ya ndogo na wakaanza safari.

“Mbona una tetemeka?”

Mrs Sanga alimuuliza Julieth aliye jikunyata.

“Baridi”

“Mpatie mwanangu koti”

“Sawa mkuu”

Kijana huyo akavua koti lake na kumkabidhi Julieth na akalivaa. Safari ya boti hiyo inayo kwenda kwa kasi, ikawachukua masaa mawili kufika katikati ya bahari na wakakuta meli moja kubwa ambayo ina lindwa kwa ulinzi mkali sana.

“Hii meli ni mali yetu mwanangu”

“Hii meli?”

“Ndio mwanangu”

Nabii Sanga alizungumza huku akitabasamu. Wakafika eneo la kushukia, wakapokelewa na vijana wengine ambao mikononi mwao wana bunduki. Vijana hao wakamsalimia nabii Sanga kwa kuinamisha kichwa chini. Julieth akazidi kushangaa uzuri wa meli hii kubwa na nzuri.

“Baba acha utani una taka kuniambia kwamba hii ni meli yetu?”

“Ndio mwanangu mbona huamini?”

“Na hawa watu?”

“Hawa ni walinzi wetu ambao ni wa siri sana na wana tulinda kwa siri sana ndio maana na umaarufu wangu wote huja wahi kuniona nikiongozana na walinzi kama watu wengine maarufu”

“Ahaaa…”

“Sisi na baba yako kuna mambo mengi ya siri ambayo taratibu utaanza kuyajua.”

Wakaingia katika chumba kimoja kilicho tengenezwa vizuri.

“Mkuu nguo zenu zipo tayari”

Dada mmoja mwenye asili ya Russian alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.

“Nashukuru Lana”

Dada huyo akainamisha kichwa chake chini kisha akatoka ndani hapo.

“Badilisheni nguo haraka, kikao kina karibia kuanza”

Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akatoka ndani hapo. Julieth na mama yake wakabadilisha nguo zao kwa haraka kisha nabii Sanga naye akaingia ndani ya chumba hicho na kuvaa nguo zoa ambazo ni suti nyeusi tupu. Wakaelekea katika ukumbi mkubwa ambao upo ndani ya meli hiyo. Julieth akashangaa sana kukuta watu wa mataifa mbalimbali, ambao mara baada ya kumuona nabii Sanga waka inamisha vichwa vyao chini ikwia ni ishara ya kumpa heshima. Mrs Sanga na mwanaye nao wakainamisha vichwa vyao chini wakiashiria kumpatia heshima kubwa nabii Sanga. Nabii Sanga mara baada ya kukaa kwenye kiti chake watu wote nao wakakaa. Kikao hicho cha siri ambacho kina wahusisha wauza madawa ya kulevya wakubwa sana kikaanza. Nabii Sanga akawatambulisha Julieth na akatangaza kwamba kuanzia hapo yeye ndio ata kuwa kiongozi wa muunganiko huo. Japo ni jambo la mshangazo kwa wengi, ila wote waka subiria kuona ni jinsi gani Julieth ata zungumza. Julieth akasimama na akapishwa kiti na nabii Sanga.

“Nita kuwa mara tatu na alicho kifanya baba yangu. Nita hakikisha tuna kuwa invisible na dunia nzima tuta itawala. Asanteni”

Julieth alizungumza kwa kujiamini hadi yeye mwenyewe akajishangaa. Watu wote wakaanza kupiga makofi kwa maana ujasiri alio uonyesha Julieth ume zaa imani kubwa kwa watu hao.

***

Siku zikazidi kusonga mbele na hali ya Evans ikazidi kuimarikia. Kwa wiki tatu na siku mbili alizo kaa nyumbani kwa mzee Msese, zika mfanya afahamu mambo mengi sana katika milima hiyo. Siku kadhaa Evans aliweza kuondoka na mzee Msese kwenye milima kutafuta dawa kwa ajili ya wateja mbalimbali wanao fika katika milima hiyo kwa ajili ya kutibiwa.

“Evans”

Kwa mara ya kwanza Evans alishangaa baada ya mzee huyo kumuita jina lake. Siku zote wame kuwa wakizungumza kwa kupitia Dada ambaye ana fahamu lugha ya kiswahili na kiruguru.

“Ndio mzee wangu.”

“Kwenye maisha yako ume kuwa ni mtu wa kudhulumiwa haki zako si ndio?”

“Ndio mzee kumbe una weza kuzungumza kiswahili?”

“Ndio nina tambua tena vizuri sana.”

“Kwa nini kipindi hicho chote ume kuwa ukizungumza kiruguru?”

“Nilihitaji kukujua vizuri na sasa nina kujua vizuri sana”

Mzee Msese alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.

“Ahaa”

“Ndio. Nyota yako ni kubwa sana na ndio inayo kufanya uweze kuwa na ulinzi mkubwa kiasi kwamba hadi mamba walishindwa kukutafuna kwenye ule mto. Nimekaa kwenye hii milima sasa ni mwaka wa stini na sita, sijawahi kuona binadamu wa kawaida anaye ingia kwenye ule mto pale na kushindwa kumtafuna mtu”

“Mmmmm”

“Ni kweli, wewe ndio binadamu wa kwanza kabisa kutoka ukiwa pale salama na tena mamba waliweza kukaa mbali na wewe. Nita kufanyia dawa ambayo nyota yako isiweze kuchukuliwa na watu wabaya”

“Sawa mzee wangu. Na nyota huwa zina chukuliwaje?”

“Ni mambo ya kitaalamu hayo mwanangu. Ila leo twende nika kuonyeshe kitu”

Mzee Msase alizungumza. Wakandoka nyumbani hapo na Evans na wakaelekea kwenye milima mikubwa kabisa iliyopo jirani na wanapo ishi.

“Mzee wangu hivi huku milimani kuna watu wana ishi?”

“Hapana, huku ni sisi tu ndio tuna ishi tena tuna ishi kutokana kukubaliwa na mizimu ya milima hii”

“Kuna mizimu?”

Evans alizungumza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio achilia mizimu peke yake, ila kuna hadi majini wakubwa wana ishi humu. Ndio maana binadamu wa kawaida akiingia humu hawezi kutoka”

“Mmmm mzee wangu una niogopesha.”

“Usiogope kwa maana kuna habari nzuri kwako”

“Habari gani?”

“Mizimu ime weza kukukubali ndio maana una ishi kwa amani na furaha ndani ya msitu huu. Ila inge kuwa sio hivyo unge kuwa umesha potwezwa siku nyingi sana.”

“Mmmm”

Evans alizungumza huku akizidi kumfwata mzee Msese. Wakafika katika moja ya pango kubwa.

“Tuna ingia humu ndani, ila kabla ya kuingia ina bidi ujichane kidogo kwenye mkono wake na umwage damu yako hapa chini”

Maneno ya mzee Msese yaka mstua sana Evans na kujikuta akizidi kujawa na woga.

“Kwa nini?”

“Humu ndani kuna utajiri wako, ila una lindwa na majini na wewe ndio mtu wa pekee unaye weza kuchukua hadihina hiyo.”

Evans macho yakamtoka, akatazama kisu anacho pewa na mzee Msese kisha taratibu akakipokea huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana kwani hakutarajia kama safari hiyo inaweza kufika hapo walipo fika.

“Mzee ume sema kwamba humu ndani kuna majini?”

“Ndio kuna majini na hakuna mtu aliye wahi kuingia humo ndani.”

“Hata wewe hujawahi kuingia ndani humo?”

“Ndio sijawahi kuingia. Ila wewe ndio una pawa kuingia na ukitoka humo hakika wewe ume kuwa tajiri”

Evans akazidi kushangaa huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.

“Evans huu ni utajiri wako ingia ndani humo”

Mzee Msese alizidi kumshawishi Evans. Evans akafikiria maisha aliyo pitia kutoka kwa Magreth hadi Julieth. Katika mahusiano hayo yote hakuweza kuambulia hata biashara ya kuuza machungwa.

‘Liwalo na liwe ni lazima niwe tajiri’

Evans alizungumza kimoyo moyo kisha akajikata kiganja chake cha mkono wa kulia kisha akaanza kumwaga damu eneo alilo onyeshwa na mzee Msese na taratibu akaanza kuingua ndani ya pango hilo ambalo lina giza totoro.



Mwili mzima wa Evans ukaanza kusisimka kutokana na hali ambayo sio kawaida iliyopo ndani ya pango hilo. Giza likazidi kumuogopesha Evans ila akajikuta akijishangaa kwa jinsi miguu yake inavyo zidi kupata ujasiri wa kuzidi kusonga mbele japo haoni kitu cha aina yoyote. Ubaridi mkali taratibu ukaanza kumtawala mwilini mwake. Kadri jinsi anavyo tembea kwa hahadhari ndivyo jinsi baridi hiyo inavyo zidi kuongezeka hadi ikafikia hatua akajikuta akianza kutetemeka.

‘Lazima nizidi kusonga mbele’

Evans alijipa moyo huku akizidi kupiga hatua huku akipapasa papasa ukuta. Gafla Evans akajikuta akianza kuelea hewani na akaanza kupiga kelele kwa maana anapo elekea ni ndani ya shimo tena kwenye shimo refu ambalo hajui itakuwaje pale atakapo fika chini ya shimo hilo.

***

Maandalizi ya ndoa ya Jery na Julieth yanazidi kupamba moto, vikao vya kamati ya watu wachache na wenye pesa nyingi, vikazidi kusonga mbele huku nabii Sanga akipania kufanya shuhuli kubwa sana ambayo Tanzania haijawahi kutokea. Kadri siku zikivyo zidi kwenda ndivyo jinsi michango ilivyo zidi kuongezeka katika familiza za pande zote mbili. Umaarufu wa nabii Sanga uliweza kumsaidia katika kupata michango mingi na kutoka kwa matajiri wengi.

“Nina good new mwanangu”

“Ipi hiyo baba?”

“Shirika la ndege la KLM line tupa ndege yake moja ya kifahari, kukusafirisha wewe na mume wako kuzunguka dunia nzima baada ya harusi yetu”

“Weee tuna walipa kiasi gani?”

“Hatulipi chochote hiyo ni Luxury plane. Hivyo hata mukitaka kutembelea dunia wapo tayari kuwapeka nyinyi wawili tu”

“Weee”

“Ndio, ngoja nikutumie picha za ndege hiyo muta ipenda”

Nabii Sanga akamtumia Julieth picha za ndege hiyo. Julieth akaanza kuitazama moja baada ya nyingine. Hakika ni ndege kubwa ambayo kwa ndani ime tengenezwa kwa mfumo wa nyuma, ina vyumba viwili vya kulala, seble ya kupmzikia, eneo la kulia chakula jiko pamoja na chumba cha baa yenye vinywaji vya kila aina.

“Baba hii ndege yote kweli tuta kuwa watu wawili?”

“Ndio”

“Sasa wao wata nufaiki vipi na sisi?”

“Watakuwa wana watumia kwenye matangazo yao kwa maana hiyo ndege ndio ya kwanza iliyo tengenezwa kwa ajili ya wana ndoa tu. Wewe na Jery ndio mutakao izindua”

“Waoooo”

Julieth akaanza kuruka ruka sebleni hapo hadi mama yake aliye kuwa jikioni akiandaa chakula akatoka.

“Kuna nini?”

“Baba katutafutia ndege ya kututembeza dunia nzima mimi na mume wangu mtarajiwa”

“Weee”

“Ndio mama icheki”

Julieth akamkabidhi mama yake simu hiyo, akazitazama picha hizo za ndege.

“Ni nzuri je sisi tuna weza kupelewa lifti….Hahaaa”

Mrs Sanga alizungumza kwa kutania.

“Yaa na sisi tuna weza kuwasindikiza sindikza kwenye nchi mbili tatu”

Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

***

“Ni lazima nirudi Tanzania hii ndio nafasi yangu kaka”

Tomas alizungumza huku akimtazama Ngosha usoni mwake.

“Tomas yule niliye ondoka nina kimbia kimbia kama kunguru sio wa sasa. Nilazima nirudi Tanzania kulipiza kisasi changu kwa nabii Sanga”

Tomas aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.

“Sawa kaka mimi siwezi kukataa hilo jambo. Je ume zungumza na shemeji na ukakubaliana naye juu ya hilo jambo, kwa maana kuna mambno mawili ndugu yangu. Kufa na kupona, je ukifa ita kuwaje kwa familia yako ikiwa mwanao bado ume muacha ni mdogo sana”

Ngosha alizungumza kwa upole na kumfanya Tomas kushusha pumzi taratibu.

“Nina mtu wa kunisaidia”

“Nani?”

“Yule aliye nifanikisha mimi kufika hapa Afrika Kusini ndio huyo huyo atakaye nisaidia kurudi nchini Tanzania”

“Basi mpigie ili kama ni kufahamu hali halisi inayo endelea kwa sasa nchini Tanzania”

“Sawa”

Tomas akaingiza namba ya Levina kwenye simu yake na kumpigia. Simu ikaita na baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa.

“Ni mimi”

“Tom”

“Yaa”

“Mshenzi kweli wewe. Umekwenda Afrika kusini na ume kaa huko hata kunitafuta”

“No baby ni story ndefu sana na nina hitaji kurudi nyumbani”

“Usitake kuniambia kwamba una rudi kwa ajili ya hii harusi”

“Ndio, huu ndio wakati wangu sasa. Mzee huyo aliniharibia maisha yangu ya amani nami nina hitaji kumuharibia maisha yake”

“Sawa, ehee bado una ile sura au ume rudi kwenye sura yako halisi?”

“Nina sura yangu halisi na sasa nina mshukuru Mungu nina pesa nyingi sana na ya kutosha”

“Okay nitumie nauli nije huko, nifanye kazi kisha turudi pamoja”

“Hapo ndipo ninapo kupendea. Sawa nita fanya hivyo leo. Nitakutumia kupitia western Union”

“Sawa ila nime miss mashine yako”

“Hahaa hata mimi”

Tomas alizungumza huku akitazama tazama eneo hilo walilo kaa kwa maana mke wake ana weza kumsikia ikawa balaa.

“Sawa ngoja nirudi nyumbani nianze kujiandaa fasta. Niingizie nauli ya kutosha”

“Dola elfu kumi si ina tosha?”

“Yaa ina tosha baby”

“Poa naelekea kwa wakala muda si mrefu”

“Sawa mume wangu”

Levina alizungumza kwa furaha kisha akakata simu.

“Usitake kuniambia kwamba msichana huyo ni demu wako?”

“Yaa kaka tena ndio mwanamke wangu wa kwanza kwanza kabisa jijini Dar”

“Sawa, ila asifikizie hapa si una jua heshima kwa shemeji ni lazima iwepo”

“Ni kweli, nita kutana naye hotelini, tuta ifanya kazi yetu tukiimaliza tuna rudi zetu Tanzania”

“Basi mueleze mke wako”

“Sawa”

Tomas akaondoka eneo hilo na kuingia chumbani kwake, akamkuta mke wake akimvalisha nguo mtoto wao.

“Tom mbona kama una jambo una hitaji kunieleza?”

“Ndio mke wangu. Nahitaji kurudi Tanzania kwa kazi moja ya mwisho baada ya hapo nita rudi zangu hapa Afrika Kusini na tuendelee na maisha yetu hadikufa kwetu”

“Mbona gafla?”

“Kweli ni gafla ila ina bidi kuikamilisha kazi hiyo kwa kipindi hichi”

“Sawa mume wangu nakupa baraka zote. Una ondoka lini?”

“Leo, kuna mtu nina paswa kuonana naye kisha nita ondoka saa nane usiku”

“Ume zungumza na rafiki yako?”

“Ndio na muta kaa hapa nina imani mupo mikono salama?”

“Yaa tupo mikono salama. Sawa mume wangu ila kuwa makini”

“Usijali mke wangu”

Tomas akamkumbatia mke wake kisha akambusu mwanaye shavuni. Akaondoka nyumbani hapo, akamtumia Levina kiasi hicho cha pesa na Levina akaahidi siku hiyo hiyo ana kuja nchini Afrika kusini kwa ajili ya kazi ya kumtengenezea Tomas sura ya bandia”

***

Kupoeta kwa Evans kuna zidi kumuumiza Magreth moyo wake. Japo ana dili nono la kufanya kazi ya upishi katika ubalozi wa Marekani na kuingiza kiwango kikibwa cha pesa, ila bado hana furaha kabisa na maisha hayo ya utajiri. Habari za ndoa ya Julieth na Jery zina zidi kumuumiza akili yake.

‘Ina kuwaje wana kula raha ikiwa mimi nina teseka hivi moyoni mwangu’

Magreth alizungumza kimoyo moyo huku akitafakari ni namna gani anavyo weza kutumia nafasi hiyo kuhakikisha ana mpata Evans wake. Akaitafuta namba ya nabii Sanga kwenye simu yake kisha akampigia.

“Una hitaji nini?”

Nabii Sanga aliuliza kwa sauti ya hasira.

“Nahitaji kuonana na wewe”

“Kwa nini una hitaji kuonana na mimi”

“Endapo uta onana nami nita kueleza ni kitu gani ambacho nita kuhitaji”

Ukimya ukatawala kidogo huku nabii Sanga akijaribu kutafakari ni wapi aonane na Magreth.

“Tukutane Koko Beach, baada ya lisaa moja”

“Sawa”

Nabi Sanga akakata simu na kumfanya Magreth kushusha pumzi.

“Juma endeleeni hapa, mimi kuna mahala nina elekea”

“Kwema lakini?”

“Ndio ni kwema. Chochote kitakacho hitajika basi muna nipigia simu”

“Sawa mkuu”

Magreth akaondoka kwenye mgahawa wake huo na kuaza safari ya kuelekea koko beach. Ndani ya dakika arobauni akafanikiwa kufika katika fukwe hizo. Akasimamisha gari lake pembezoni mwa fukwe hizo, hazikupita dakika kumi nabii Sanga akafika katika fukwe, akashuka kwenye gari lake na kuingia kwenye gari la Magreth huku akiwa amevalia kofia ili maradi watu wasiweze kumfahamu.

“Kwa nini ume niita?”

“Nahitaji kufahamu ni wapi alipo mume wangu”

“Baada ya siku zote hizo leo hii ndio una niuliza kwamba yupo wapi mume wako. Kwanza isitoshe mimi sio mlinzi wa kumlinda huyo mume wako sawa binti”

“Sanga Sanga. Usinikere na wala usiwe na kiburi cha kujibu unacho jisikia. Mwanao sasa hivi ana kula bata tu mimi toka siku ile nilipo toka sikuweza kumpata na niliweza kushuhudia usiku ule watu wakiwa wame mteka kule Morogoro na wewe ndio ulisema uta muua. Hivyo nina taka kufahamu ni wapi mume mpeleka mume wangu na kama ni kumuua basi niambieni ili niweze kuona hata kaburi lake”

“Wewe binti nina hisi kwamba uta kuwa ume changanyikiwa. Ukweli ni kwamba, sifahamu ni wapi alipo huyo paka wako na kama ame kufa basi ni jambo la heri kwa maana hato weza kuweka kipingamizi chochote kwenye ndoa ya mwanangu. Na siku nyingine usije ukadhubutu kuniita kwa mambo ya kijinga”

Maneno ya kejeli ya nabii Sanga yakazidi kumuudhi Magreth. Nabii Sanga akafunua shati eneo la kiunoni mwake na kumuonyesha Magreth bastola yake.

“Sasa hivi mimi si yule Sanga niliye pagawa kwa penzi lako. Ila sasa hivi ni mume bora katika familia yangu hivyo usijaribu kuingia kwenye kumi nane zangu nita kumaliza”

Nabii Sanga alijikuta akizidi kujigamba mbele ya Magreth.

“Nashukuru”

Magreth alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Nabii Sanga akamtazama Magreth kwa sekunde kadhaa kisha akashuka kwenye gari hilo na kuingia kwenye gari lake kisha akaondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana. Magreth akajipangusa machozi yake, kisha naye akaondoka eneo hilo huku akiwa na kisasi kikubwa sana moyoni mwake. Akaelekea moja kwa moja katika nyumba ambayo mama yake alikuwa anafanya kazi chini ya mzee wa Kijapani. Nyumba hiyo iliyopo pembezoni mwa bahari, kwa sasa ime jaa majani mengi sana kwa maana haina uangalizi wa mto yoyote kwa kipindi cha miaka sasa. Magreth akashuka kwenye gari lake na kuruka ukuta wa nyumba hiyo na kutua ndani.

Akaanza kutembea kwa umakini huku akichunguza eneo hilo ambalo lime kosa matuzo. Miaka karibia kumi na mbili haja kanyaga katika nyumba hiyo. Akashika kitasa cha mlango huo, akajaribu kuusukuma kwa ndani ila kwa bahati mbaya aka kuta ukiwa ume fungwa. Akarudi nyuma kwa hatua kadhaa kisha akaupiga teke moja la nguvu na mlango uka funguka. Vumbi pamoja na mitando ya baibui imejaa katika seble ya nyumba hiyo ambayo vitu vyake vingi vimetolewa.

Magreth moja kwa moja akaelekea katika chumba alicho kuwa ana lala mzee huyo. Akasogeza kitanda hicho, kisha akalitoa kapeti zito lililopo eneo hilo. Akafungua mlango mdogo wa siri ulipo katika chumba hicho ambao una elekea chini. Magreth hakuogopa kitu chochote kwa maana ana ifahamu nyumba hiyo vizuri na mzee huyo alisha mueleza kila kitu kinacho husiana na wapi anapo tunza vifaa vyake vya siri. Akawasha taa na mwanga ukatawala katika chumba hicho cha siri. Japo kuna vumbi jingi, ila Magreth aliweza kuona sanduku maalimu lilolo tengenezwa kwa mbao ngumu likiwa eneo hilo. Magreth akalisoegelea sanduku hilo, kisha akachuchumaa taratibu, akaanza kuingiza namba za siri ambazo zipo tatu. Sanduku hilo likafunguka. Magreth akatabasamu mara baada ya kukuta kile kilicho mleta kikiwa ndani ya sanduku hilo. Nguo nyeusi ambazo wana vaa maninja, upanga mrefu na wenye sumu kali, nyota ndogo ndoho ambazo ni silaha, visu viwili, kimoja kikiwa kime unganishwa na cheni ndefu huku mbele kikiwa kime jikunja kiasi. Kisu kingine kirefu, mishale ya chuma pamoja na upinde ulio tengenezwa na chuma na una wanya mbili ngumu nao pia umo ndani ya sanguduku hilo.

‘Sasa nina kwenda kuwa vigilante lady nabii Sanga na watu wako ni lazima mulipe, lazima mutalipa tu”

Magreth alizungumza kimoyo moyo huku akitazama vifaa hivyo kwa maana vyote ana jua kuvitumia vizuri sana mithili ya maninja halisi kutoka nchini Japan.



Simu ya Magreth ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kuitazama namba hiyo. Akatabasamu kidogo kisha akaipokea.

“Ndio”

“Madam pikipiki yako tumesha itoa bandarini”

“Nashukuru, nita fika hapo muda si mrefu”

“Sawa”

Magreth akatazama eneo hilo.

“Hakuna haja ya kuondoka na sanduku hili”

Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha. Akatoka ndani hapo, akaingia kwenye gari lake na kuondoka kwa kasi eneo hilo. Akafika Posta kwenye kampuni inayo shuhulika na uingizaji wa magari na pikipiki nchini Tanzania.

“Karibu sana madam”

“Nashukuru ehee niambie yaani njia nzima nina kiwelu welu cha kutaka kuiona pikipiki yangu”

“Hahaa nililifahamu hilo. Kama ulivyo niagiza wiki iliyo pita, nime weza kutafuta pikipiki moja nzuri na ni mpya. Twende ukaione”

Magreth akatoka ofisi hapo huku akiongozana na kijana huyo ambaye ana itwa Sudy na ndio mmiliki wa kamouni hiyo. Wakafika katika holi kubwa linalo hifadhia magari ya kifahari pamoja na pikipiki za kifahari.

“Nimekuchagulia pikipiki nyeusi kama ulivyo nieleza. Hii ina itwa BMW HP4 RACE, ni pikipiki mpya kabisa kwa kampuni hii ya BMW na ina spidi ya hali ya juu ambayo ina kuwezesha kushindana kwa spidi na gari ya aina yoyote”

“Weee”

“Ndio madam”

“Ina spidi mita ngapi?”

“Madam hii ina speed mita 348 km per hour”

“Weeee una taka iniue ehee?”

“Haikuui madam, ni uendeshaji wako na ubora wako katika kutumia vitu kama hivi”

“Mara ya mwisho kuendesha pikipiki nilikuwa binti mdogo sana”

“Kama uliwahi kuiendesha hii basi una weza kuindesha vizuri tu”

“Ehee niambie ni madola mangapi?”

“Ni dola elfu sabini na nane tu na bei ya kukueletta hadi hata tuta kuchaji dola elfu mbili hivyo itakuwa ni dola elfu themanini”

“Weee Sudy una niaona mimi nina pesa ehee?”

“Hapana madam ndio bei yake. Hii pikipiki hapa Tanzania wewe ni wa tatu kuiingiza. Kuna wahindi wawili na wewe pekee”

“Hii nina weza kwenda nayo wapi na wapi?”

“Popote ndani ya Tanzania hata nje ya Tanzania ina tembea. Ni wewe tu na umakini wako”

“Sawa nitalipa kupitia benki.”

“Hakuna shaka madam. Pipikipi hii ime kuja na nguo zake ambazo ni kwa ajili ya dereva.”

Sudy alizungumza huku akimuonyesha Magreth nguo hizo.

“Kama una kwenda sehemu za mbali, hizi nguo ni nzuri uka zitumia kwa maana zina ugumu ambao hata ukia anguka, huto heza kuchubuka, ila kama ni kuvunjika basi uta vunjia kutokana na kuanguka kwako”

“Ahaaa hii kofia yake haivunjiki kweli?”

“Halment yake ni ngumu sana, yaani hata ipige vipi kwenye lami haivunjiki”

“Kwa kweli nime ipenda”

Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha. Akaipanda pikipi hiyo, akakabidhiwa funguo na kuanza kuiendesha taratibu ndani ya ukumbi huo. Japo ni kwa mwendo wa taratibu ila akaamini ameweza kuiendesha hata kwa umbali mkubwa. Magreth akalipa na kukabidhiwa nyaraka zote za umiliki wa pikipikiki hiyo.

“Naacha gari langu, nataka kuijaribu kwa kuelekea morogoro sasa hivi”

“Sawa na uzuri tume kuwekea mafuta full tanki”

“Shukrani sana”

Magreth akavaa nguo maalumu wanazo vaa madereva wa pikipiki hiyo, akaiwasha na kuondoka eneo hilo. Kadri muda anavyo zidi kuiendesha ndivyo jinsi anavyo anza kuizoea. Ikafikia hatua akaweza kuimudu kwa kila kitu. Safari ya kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze haikumchukua hata masaa mawili.

‘Nina ua na hakuna ambaye ata nikamata’

Magreth alizungumza huku akizidi kuongeza mwendo kasi wa pikipiki hiyo. Ndani ya msaa matatu akafika Morogoro mjini. Akakizunguka kiplefti cha mjini hapo mara nne kisha akaanza safari ya kurudi Dar es Salaam kwa mwendo wa kasi sana.Kila trafki aliyopo barabarani alijikuta akishindwa hata kuisimamisha pikipiki hiyo kwa maana mwendo wake ni wa kasi sana. Magreth akarudi ofisini hapo alipo inunua pikipiki hiyo.

“Sudy ni nomaa, asikuambie mtu. Yaani kuna mabasi niliyapita nikiwa nina kwenda. Narudi nime kutana nayo”

Magreth alizungumza huku akishuka kwenye pikipiki hiyo.

“Weee, umefika hadi wapi?”

“Nimefika Msavu nimeizunguka ile around abauti pale mara nne. Yaani njiani, trafiki wana jitokeza, wanajaribu kunisimamisha, ila spidi ninayo wapiti nina imani kwamba wana simuliana”

“Duu ume tumia masaa natano”

“Yaa tena hapa ni mwanzo ila nikizoea nita kwenda na kurudi hata kwa masaa matatu”

“Duu pia Bongo yetu kuna foleni, ila ungepata bararaba ambayo haina magari, basi unge kuwa mbali sana”

“Ni kweli, nashukuru sana Sudy kwa kunichagulia hii pikipiki”

“Nashukuru, nime ona gari yako ime jaa michubuko, imekuwaje?”

“Nilipata ajali?”

“Pole sana una onaje uka badilisha rangi”

“Hapa muna fanya hee?”

“Ndio kampuni yangu ina fanya hiyo kazi, ila gareji yetu ipo kule Tegera”

“Ahaa utanifanyia kiasi gani?”

“Ita gemegea na rangi unayo ihitaji?”

“Nahitaji dark paple ila inayo ng’aa vizuri. Hiyo si ndio rangi za sisi wanawake?”

“Yaa basi una weza kuileta gari tuka kufanyia kazi hiyo”

“Kwani hiyoni kazi ya muda gani?”

“Siku mbili au tatu ina kuwa ime kwisha?”

“Basi nina liacha hapa likiwa tayari uta nipigia”

“Sawa”

Magreth avaa begi alilo weka nguo zake alizo zibadilisha. Akaondoka eneo hilo na moja kwa mojaa akaelekea kwenye nyumba mzee wa kijapani aliye mpatia mafunzo ya kupigana mithili ya maninja. Akaiingiza pikipiki hiyo ndani, kutokana nyumba hiyo ipo pemezoni mwa bahari na ime jitenga sana hapakuwa na mtu aliye weza kufahamu juu ya uwepo wake katika nyumba hiyo.

‘Hapa ndipi nitakapo panga mipango yangu yote’

Magreth alizungumza huku akivua nguo na kuvaa nguo za mzee huyo. Ngoo hizi kidogo hazikuweza kumtosha kutokana na urefu wake na mzee huyo kidogo alikuwa ni mfupi. Magreth akazipiga picha nguo hizo kisha akaondoka nyumbani hapo na kuanza kutembea hadi kituo cha waendesha pikipiki. Akakodi pikipiki na kuelekea kwa mwana mitindo mmoja, akamuelezea wazo la nguo anazo hitaji kushonewa na mwana mitindo huo.

“Si nina weza kushonewa na kitambaa kigumu ambacho hata nikipigwa na kitu kigumu kama risasi hakuto weza kuingia”

“Mmmm dada kwa utaalamu kama huo hapa Tanzani hakuna labda u google una weza kupata wataalamu wa kutengeneza nguo kama hizo ila kwa hapa Tanzania, sijawahi kuona”

“Baso nashukuru kwa ushauri wako, nina omba mchoro ulio uchora”

“Ina bidi ulpie dada”

“Kiasi gani?”

“Elfu hamsini”

“Kuchora tu huku ni elfu hamsini?”

“Ndio dada”

“Mmmm haya”

Magreth akalipa kiais hicho cha pesa kisha akarudi kwenye Mgahawa wake. Akaingia kwenye mtandao na kuanza kuperuzi ni kiwanda gani kina utaalamu wa kutengeneza nguo anayo hitaji na kw abahatu nzuri akafanikiwa kupata kampuni moja kutoka nchini Thailand ambayo ina uwezo wa kutengeneza nguo hizo, akawasiliana nao na akawatumia michoro na vipimo vya nguo anayo ihitaji na wakamuahidi nguo hiyo ndani ya wiki moja ita kuwa tayari.

‘Sanga sasa nina kuja kwa ajili yako’

Magreth alizungumza kimoyo moyo huku akitazama picha ya nabii Sanga na mwanaye huyo wa kike ambaye ni Julieth.

***

Levina akafika nchini Afika kusini na kupokelewa na Tomas. Moja kw amoja wakaelekea katika hoteli ambayo Tomas ama kodisha chumba.

“Vipi Tanzania?”

“Nime kumiss bwana, hembu nipe haki yangu hayo mambo ya Tanzania tuta ulizana baadae”

Levina alizungumza huku akianza kuvua nguo zake. Akamsukumia Tomas kitandana na kumkalia juu ya kiuno chake. Wakaanza kunyonyana ndimi zao huku kila mmoja akiwa na hamu kubwa ya mwezake. Levina akamvua Tomas nguo zake akageuka kwa haraka na kuanza kumnyonya jogoo wa Tomas huku naye Tomas akianza kunyonya kitumbua chake. Zoezi hilo likazidi kuwafanya wapagawishane, Tomas akamgeuza Levina kisha akamlaza chali.

“Noo nataka nimkalie”

Levina alizungumza huku akirudi tena kumkalia Tomas. Taratibu akamkalia jogoo wa Tomas na kuanza kukizungusha kiuno chake huku akitoa miguno ya kimahaba. Mtanange huo ukawa ni piga ni kupige, kila mmoja akaonyesha ujuzi wake katika mikao ya kimahaba. Hadi wana maliza mzunguko wa kwanza kila mmoja, ana mwagikwa na jasho kana kwamba ndani ya chumba hicho hakuna A/C(Air condition).

“Kidogo nye** zime nipungua”

“Kweli?”

“Ndio kidogo zime pungua kwa maana ulipo niambia tu nije, yaani huku chini nilihisi kama kuna vuja vuja. Hata nilipo kuwa kwenye ndege nilihisi kama vile ina chelewa”

“Hahaa huku chepuka kweli?”

“Sikuchepuka, niliamini ipo siku tu uta rudi na nitakuwa tena nawe. Ila kwa sasa Frank nina uomba usiniache kabisa. Nina omba usika mbali na wewe, nina kuomba sana tuweze kuanzisha maisha. Tana tafuta pesa kwa ajili ya nini sasa ikiwa watu wenyewe hatu hitaji hata kuanzisha maisha?”

“Usijali mpenzi wangu tuta azisha familia na nina imani kwamba familia yetu ita kuwa ni bora sana”

“Kweli?”

“Kweli vile niamini mpenzi wangu”

“Niahidi kama uta nipa mtoto?”

“Usijali nita kupatia mtoto”

“Nashukuru mume wangu. Ehee niambie mipango?”

“Nahitaji kurudi nchini Tanzanai, nina ona harusi ya mtoto wa nabii Sanga na mtoto wa raisi Boaz. Ila kisasi changu mimi nina taka kukipeleka kwa nabii Sanga na familia yake tu”

“Ila familia ya Sanga ina ulinzi wa moja kwa moja kutoka Ikulu ni ngumu sana kuivamia”

“Usijali mke wangu katika kipindi chote hicho ambacho nilikuwa nipo nchini humu, niliweza kupata mafunzo ya kijasusi kama nilivyo kuwa nime kusudia. Now ni wakati wa mimi kuhakikisha kwamba nina lipa kisasi kwa nabii Sanga”

“Sawa, kisasi ina bidi tutumie akili sana kuhakikisha kwamba tuna fanya hii kazi”

“NI kweli”

“Basi nime tengeneza sura ile ile na hati za kusafiria zile ulizo kuja nazo. Kazi iliyooi hivi sasa ni kukupachika hiyo sura ya bandia”

“Sawa mama, kazi ni kwako”

Levina akafungua begi lake kubwa na kutoa vifaa vyake vya kufanyia kazi na taratibu akaanza kuifanya kazi hiyo ya kuipashika sura hiyo ya bandia katika uso wa Tomas.

***

Raizi Mtenzi akaagiza walinzi kumi kuhakikisha wana mlonda nabii Sanga na familia yake. Mfumo mzima wa ulinzi wa nyumba ya nabii Sanga uka badilika kabisa.

“Kwa upande wetu huku sisi tuna karibia kukamilisha”

Nabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama raisi Mtenzi aliye mtembelea hapo nyumbani kwake.

“Nashukuru kusikia hivyo. Sisi kwa upande wetu kila kitu kipo tayari na tuna subiri siku ya kumchukua mkwe wetu”

“Nashukuru sana muheshimiwa”

“Jambo ambalo lime niletea hapa ni kuhitaji kufahamu utayari wa mama pale nitakapo amua kumpatia nafasi ya ubunge wa viti maalumu katika serikali yangu”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama mrs Sanga aliye anza kutabasamu.

“Mimi nipo tayari”

“Kweli, kwa maana nyinyi familia yenu ni ya kichungaji hivyo nina ogopa sana kuwaingiza kwenye hizi siasa zetu za Kitanzania”

“Usijali mkwe nita jitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba nina nina pambana bungeni kwa ajili ya wana nchi”

“Nafurahi kusikia hivyo mkwe. Basi nina waomba niwaache nirudi ikulu. Endapo kutakuwa na chochote basi muna weza kuniambia tu”

“Sawa tuna shukuru sana kwa kuja”

“Nanyi karibuni sana Ikulu”

Raisi Mtenzi akapena mikono na nabii Sanga kisha akaondoka nyumbani hapo na walinzi wake.

“Huu ndio wakati sasa”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake usoni mwake.

“Wakati wa nini?”

“Kuhakikisha Julieth ana inyanyua biashara yetu huku na wewe ukimpa support ya moja kw amoja kwa maana nyote mutakuw andani ya serikali”

Mrs Sanga akatabasamu kwa maana anatambu ni kitu gani ambacho kina kwenda kufwata baada ya kupewa nafasi hiyo adimu sana kwenye maisha yao.



“Jamanimbona mume jawa na furaha sana kuna nini mume ambiwa?”

Julieth aliuliza huku akishusha kwenye ngazi akitokea gorofani.

“Bi harusi utakiwi kutoka chumbani kwako”

Nabii Sanga alizungumza kwa kutania.

“Jomoooniiii baba, si nipondani bado”

“Nakutania mwanangu. Mama yako amepewa nafasi ya kuwa mbunge wa viti maalumu”

“Kweli baba?”

“Ndio mkwe ana zidi kutufanyia mambo makubwa na hii ndio nafasi yako Julieth mwanangu”

“Usijali baba nina tambua ni nini ninacho kifanya nyinyi wenyewe mutanikubali”

***

Evans akatua chini, baada ya ubali mrefu kutoka juu alipo kuwa. Gaffa eneo hilo likaanza kuwaka mishumaa mingi iliyo pangwa katika majabali hayo makubwa.Evans akazidi kuogopa huku akijishangaa kwa maana umbali wote ule alio toka juu hadi chini, ila hajaumia wala kuhisi maumivu yoyote kwenye mwili wake. Mishumaa hiyo mikubwa ikazidi kuwaka na kuzudi kumchanganya kwa maana anaye washa wala haonekani.

‘Heiii’

Evans aliita ili kama kuna mtu basi aweze kumuona. Jipande cha jiwe kilicho kaa kama mlango kika funguka katika mwamba huo mkubwa. Evans akaona mwanga mkali mweupe ukitokae ndani ya eneo hilo.

“Ingia ndani”

Ilisikika sauti nyororo ya kike.Taratibu akaingia emeo hilo na kukutana na msichana mmoja mrefu aliye valia nguo nyeupe na zinazo ghara mithili ya malaiki wa mbinguni. Jambo linalo mshangaza Evans ni jinsi msichana huyo alivyo na mikono minne ambayo yote ina fanya kazi.

“Usiogopeee”

Msichana huyo alizungumza huku akimsogelea Evans. Taratibu akaanza kumpapasa mwilini mwake huku akimshika maeneo mbalimbali. Evans alizidi kujawa na woga kwani kwenye maisha yake hajawahi kukutana na binadamu wa aina kama hiyo. Msichana huyo mwenye asili ya kiarabu na macho yenye mboni ya blue, akasimama mbele ya Evans huku akimtazama.

“Nimekuchagua uwe msaidizi wangu duniani”

“Msaidizi wako kivipi?”

Evans alijikaza kuzungumza huku akiendelea kutetemeka kwa maana mikono yote minne ya mwana dada huyo iliendelea kumchezea mwilini mwake.

“Binadamu wengi sana wana hitaji msaada. Wengi wana shindwa kupata msaada, ila wewe uliweza kupata msaada kwa maana bila ya hivyo basi sasa hivi unge kuwa ni marehemu”

Maneno ya msichana huyo yakazidi kumuweka njia panda Evans.

“Una hitaji utajiri?”

“Nd…io…o”

“Ukiwa tajiri sasa hivi uta fanya nini?”

“Ni…niita….a saidia familia yangu na watu wengine wenye shida”

“Ndio maana nika kuchagua. Natambua kwamba uta hisi ume kuja huku kwa bahati mbaya au nguvu zako zime kufikisha huku kwa bahati mbaya. Ila ukweli ni kwamba mimi ndio nime kusaidia kukuleta huku, nilikuweka chini ya huyo msaidizi wangu mzee Msese, kisha nika mpa maagizo ya kukuleta uonane na mimi”

“Wewe ni nani?”

“Jini”

Evans macho yaka mtoka kwa maana kwenye maisha yake yeye ame kuwa akisikia tu habari za majini kwenye vitabu vya dini na maeneo mbalimbali kama filamu, ila hakuwahi kukutana naye ana kwa ana.

“Jini huwa ana onekana”

Gafla dada huyo akapotea mbele ya Evans na kumfanya ahisi haja ndogo ina kwenda kumtoka.

“Hapo una niona?”

Evans aliisikia sauti tu, ila hamuona.

“Ha..ha…aha..pana”

“Hivi je”

Dada huyo akajitokeza tena mbele ya Evans na akamuona.

“Nakuona”

“Majini tupo wa aina mbili. Kuna majini ambao ni wazuri kwa wanadamu na msaada kwao na kuna majini ambao ni wabaya sana kwa watu na wana wadhuru kwa haraka sana. Mimi ni jini mzuri sana pale tu unapo endana na masharti yangu, ila ukienda kinyume na masharti yangu basi hakika nina kuwa mbaya”

“Sa…a…a wewe una itwa nani?”

“Kwa sasa nitambue tu kama jini ila huko baadae uta weza kunifahamu jina langu. Twende kwenye mada ya msingi ambayo ime kufanya nikuite hapa”

Dada huyo alizungumza huku akisogelea sanduku kubwa lililopo eneo hilo.

“Nahitaji uweze kurudi jijini Dar es Salaam”

“Dar es Salaam!!”

“Ndio mbona una shangaa?”

“Kule kwa kweli siwezi kurudi, kuna watu watu wengi sana wanao niwinda. Simfahamu mzuri au mbaya kwangu”

“Nalitambua hilo ndio maana nahitaji urudi Dar es Salaam”

“Nikafe?”

“Hapana huwezi kufa ila una kwenda kufanya kazi ambayo nina hitaji kukueleza”

“Kazi gani?”

“Nahitaji ukafungue kanisa na uwe muhubiri”

“KANISAAAA!!?”

Evans alishangaa sana hadi dada huyo akaachia kicheko cha kejeli kisha akamtazama akamsogelea karibu Evans.

“Ndio nahitaji ukafungue kanisa”

“Na..nani ambaye atakuwa kiongozi wa hilo kanisa?”

“Nani ambaye ame fungua hilo kanisa?”

Evans akabaki mdomo wazi huku akikosa hata cha kumjibu dada huyo kwa maana hana kabisa kipawa cha kuhubiri.

“Wewe ndio utakaye kuwa muhubiri, natambua kwamba adui yakoni nabii Sanga si ndio?”

“Ndio”

“Yeye ndio alikuponya Magreth na huyo huyo akakupokonya na mwanaye si ndio?”

“Ndio”

“Ulijisikiaje?”

“Vibaya sana”

“Na mtu aliye taka kukuua una mjua?”

“Si nabii Sanga?”

“Hapana Sanga alikupokonya malengo yako ila ali taka kukuua wewe ni mume wa Julieth ambaye ni mtoto wa raisi Mtenzi. Yeye ndio aliye tuma watu wake wakakuteka na kukueleta huku”

Evans akajikuta akishusha pumzi kwa maana hilo jambo hakuwahi kulifikiria.

“Watu wengi kwa sasa wana hali ngumu sana za kimaisha. Nahitaji kupitia wewe waweza kufanikiwa kwenye maisha yao na hakika uta fanikiwa kupata wafuasi wengi sana na kuchukua wafuasi wote ambao wapo chini ya watumishi wa dini nchini Tanzania, akiwemo huyo nabii Sanga.”

“Hili lita wezekana vipi?”

“Nina kupatia utajiri, rudi jijini Dar es Saalam, kanunue eneo kubwa eneo la Kigamboni, kisha jenga kanisa ambalo ni la gorofa na liweze kuingiza watu laki moja kwa awamu moja.

“Watu laki moja, si wengi sana hao?”

“Ndio ni wengi ila ila wezekana waka ingia kwenye kanisa lako na kila atakeye kuwa muumini wako basi ata fanikiwa mara mbili ya kile kipato anacho kimiliki kwa sasa”

“Atafanikiwa vipi ikiwa mimi sio mtumishi wa Mungu na wala sina upako wa aina yoyote?”

Dada huyo akatabasamu.

“Evans tambua kwamba mimi nipo nyuma yako na mimi ndio nitakaye fanya kazi hiyo na wala sio wewe. Utawaponya watu, uta wafufua wale ambao wame chukuliwa misukule. Utafanya miujiza mingi sana ambayo watu wata kufananisha na Yesu”

“Mmm Yesu!!?”

“Ndio ila siri ni kwamba nguvu zote zina tokea kwangu”

“Sawa, je ikitokea siku nika kutana na mtumishi ambaye ana tumia nguvu za Mungu ita kuwaje hapo?”

“Muna kutana vipi kwa mfano?”

“Dunia ni ndogo hii, siku ana kuja mtumishi mwenye nguvu za Mungu za kikweli kweli, si nita ingia aibu mimi?”

“Watu wa aina hiyo Tanzania hawafiki hata kumi”

“Nini?”

“Hawafiki hata watano na wengi wao wapo mikoani na ni kadhaa wapo Dar”

“Mmmm una taka kuniambia kwamba nabii Sanga yeye hatumii nguvu za Mungu?”

“Haahaa hatumii nguvu zozote na huyo ndio ana patia nguvu zake za kichawi nchini Nigeri. Ila tusimuongelee sana kwa maana sijapanga leo kumzungumzia. Njoo hapa”

Evans akasogea ene alipo simama dada huyo. Akafungua sanduku hilo kubwa, Evans akashangaa kuona vibunda vya dola mia mia vikiwa vime pangwa vizuri sana.

“Hizi ni pesa za kimarekani, ni dila milioni mia moja. Dola milioni hamsini, kawekeze kwenye kanisa hilo, kuanzia kununua kiwanja hadi kulijenga. Ume nielewa?”

Evans akashindwa hata kujibu kwa maana kwenye maisha yake hajawahi kukutana na kiwango kikubwa cha pesa kama hicho.

***

“Jiangalie kwenye kioo”

Levina alizungumza na kufanya Tomas kushuka kitandani kwa haraka. Akasimama kwenye koo hicho na kuanza kujitazama. Akashangaa jinsi alivyo rudi katika sura feki aliyo ingia nayo nchini hapo Afrika kusini.

“Wewe mwanamke hichi kipaji alikupatia nani?”

“Kwa nini baby”

“Umenibadilisha tu ndani ya muda mchache”

“Yaa ni professional kwenye kazi yangu, kama vile wewe ulivyo kuwa ni professional kwenye udalali wako wa nyuma”

“Hahaa kazi yangu nime imiss sana”

“Tuna weza kurudi Tanzania leo hii?”

“Ndio leo hii tuta ondoka usiku wa saa nne, niliweka booking”

“Sawa, ila kabla ya kuondoka nahitaji unipe mechi ya mwisho”

Levina alizungumza huku akimvua Toma taulo lake. Taratibu akachuchumaa na kuanza kunyonya jogoo wa Tomas na kumfanya aanze kutoa miguno ya kimahaba.

Wakaanza kupeana burudani huku kila mmoja akihakikisha ana mridhisha mwenzake. Walipo maliza mizunguko hiyo miwili, wakaingia bafuni na kuoga. Wakajianda ana kuondoka hotelini hapo na kuelekea uwanja wa ndege. Wakafika uwanjani, wakakta tiketi mbili, kisha wakaingia kwenye mmoja wa mgahawa na kuanza kupata chakula cha usiku.

“Tomas”

“Naam”

“Baada ya kisasi chako kumalizika una mpango gani?”

“Mmmm mapango wangu ni kuhakikisha nina fanya biashara zangu. Kutokana huku south nime acha pesa za kutosha basi nina endelea na maisha ya aina hiyo”

“Ndoa je?”

“Ndoa ni swala la mimi na wewe kukubaliana. Mimi nipo tayari ila wewe mwenzangu sijui”

“Tom, wewe una jua ni jinsi gani ninavyo kupenda. Wewe una tambua ni jinsi gani ambavyo moyo wangu upo kwako, siwezi kukataa ombi kama hilo tena kutoka kwako”

“Nashukuru kusikia hivyo”

Wakamaliza kupata chakula hicho cha usiku, wakasubiri kwa muda machache kisha wakaingia kwenye ndege na kuianza safari ya kurudi nchini Tanzania huku kukiwa hakuna mtu hata mmoja ambaye aliweza kugundua kwamba Tomas ana sura ya bandia.

***

Viongozi wa vitengo vya kuzia uingizaji wa madawa ya kulevya nchini Tanzania, wakaanza kuchanganyikiwa. Baada ya kijiaminisha ndani ya miaka miwili kwamba wame weza kutokomeza mtando una jiita GHOST ambao ulikuwa una fanya kazi ya kuingiza na kutoa madawa ya kulevya nchini Tanzania.

“Mume fikia wapi?”

Raisi Boaz alizungumza huku akiwa ameingia kwenye ukumbi wa mikutano katika kitengo hicho.

“Muheshimiwa bado vijana wetu wapo kwenye oparesheni”

“Wapo wapi kwa sasa?”

“Boti zipo baharini, na inavyo dakika mzigo huo utaingia saa nane usiku leo”

Raisi Boaz akatazama tv kubwa iliyopo ndani hapo, inayo onyesha jinsi askari wa kitengo hicho wakiwa baharini wakisubiria boti walio pewa habari kwamba ina ingia nchini Tanzania na madawa ya kulevya. “

“Tume iona boti mkuu”

Sauti ilisikika ndani hapo kutoka kwa kiongozi wa askari hao walipo kwenye oparesheni.

“Ivamieni na hakikisheni kwamba muna wakamata watu wote waliopo ndani hapo na wata tueleza ni nani ambaye ni muhusika wa mtandoa wao huo unao itwa Ghost”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Raisi Boaz taratibu akasimama na kusogea mbele zaidi ili kushuhudia jinsi vijana wake anavyo ifanya kazi hiyo kikamilifu, kuhakikisha kwamba madawa ya kulevya hayaingia ndani ya nchi ya Tanzania.



Askari hao wakaizingira meli hiyo huku wakiwa makini sana na silaha zao mikononi. Wakaisimamisha boti hiyo na taratibu ikapunguza mwendo na kusimama. Askari hao wakaanza kuingia mmoja baada ya mwengine. Jambo la kushangaza sana ni mara baada ya kukuta boti hiyo haina mtu wa aina yoyote. Gafla mlipuko mkubwa ukasababisha watu wote ndani ya chumba hicho kustuka huku raisi Mtenzi akiwa haamini anacho kiona kwa maana askari karibia nane walio ingia ndani ya boti hiyo wamelipuka na mlipuko huo huku askari wengine walio kuwa kwenye boti ndogo ndogo zinazo kwenda kwa kasi zipatazo sita wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana kwa maana boti zao zilikuwa karibu sana na boti hiyo kubwa.

“Ohoo Mungu wangu”

Raisi Mtenzi alizungumza huku machozi ya hasira yakimlenga lenga. Wakiawa katika hali ya kushangaa wakashuhudia boti moja ikija kwa mwendo wa kasi sana.

“Hao ni kina nani?”

Raisi Mtenzi aliuliza huku akimtazama mkuu wa oparesheni hiyo.

“Hatufahamu mkuu”

“Hembu zoom”

Kijana anaye shuhulika juu ya swala la kuongoza video zinazo rekodiwa moja kwa moja kwa kupitia satelaiti akaifanya kazi hiyo. Wakashuhudia nyuso za watu hao waliomo kwenye boti hiyo wakiwa wamezifunika nyuso zao. Watu hao wanne na wenye bunduki mikononi mwao wakaanza kuwashambulia askari wote walio salia wakielea elea katika bahari hiyo kisha wanaondoka eneo hilo la tukio na kumfanya kila mtu ndani ya chumba hicho kupatwa na uchungu mkubwa sana.

“Wafwatilie wanapo kwenda”

Raisi Boaz alizungumza huku akiwa amejawa na hasira kali sana. Gafla waka shuhudia boti hiyo ikilipuka na kuwafanya watu wa raisi Mtenzi kuchanganyikiwa sana kwa maana wame poteza kila kitu. Raisi Mtenzi akafumba macho yake taratibu kwa maana toka aingie madarakani leo hii ndio siku ambayo ame poteza vijana wengi sana wapatao ishirini na mbili.

“Wasiliana na mkuu wa Navy atume kikosi sasa hivi na nita taka kufahamu ni kitu gani kinacho endele na nani ambaye ame husika katika tukio hili.

“Sawa muheshimiwa raisi”

Raisi Mtenzi akatoka ndani hapo huku akiendelea kutafakari ni mtu gani ambaye ana jiamini sana hadi kupelekea vijana wake kufa vifo vya kinyama namba hiyo.

***

Mlio wa meseji ulio ingia kwenye simu yake ya siri ambayo Magreth alipewa na baba yake uka mfanya astuke kutoka usingizini. Akaifungua meseji hiyo na kumfanya akurupuke na kukaa kitako huku akiwa amejawa na tabasamu. Akavaa nguo za kulalia na kuelekea chumbani kwa wazazi wake, akagonga mlango na kwa bahati nzuri aka kuta wakiwa bado hawajalala.

“Vipi?”

“Mpango wangu ume kwenda kama vile nilivyo panga”

“Mpango gani huo”

“Baba ilisha wahi kuingiza kilo laki moja za dawa katika siku moja?”

Julieth aliwauliza wazazi wake huku akiwatazama kwenye nyuso zao.

“Hapana, vipi?”

“Leo nime fanikiwa kuingiza kiasi hicho cha pesa na kina thamani ya dola BIlioni mbili na nusu”

“Weee mtoto hembu acha kutupagawisha muda huu”

“Haki ya Mungu baba soma hii meseji”

Nabii Sanga akaichuku simu hiyo na kuona meseji ikiwa ime andikwa neno moja tu ‘DONE’

“Hakuna namba ni meseji tu so ume ingizaje hicho kiasi cha mzigo”

“Akili”

“Akili maana yake ni nini?”

“Uliniambia kwanba niwe BLACK GHOST, basi nime kuwa hivyo.”

“Julieth hembu acha kutuweka roho juu bwana”

Mrs Sanga alizungumza huku akiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua ni jambo gani hilo lifanya mtoto wao hadi kujigamba kwa kiasi hicho.

“Njia moja ya kuingiza mzigo mkubwa ambao uki piga ni lazima utokea kimaisha ni kuwapumbaza ambao macho yao muda wote yapo wazi katika kutaka kujua ni kitu gani ambacho kina endelea katika nchi hii. Nikizungumza hivyo nina imani kwamba muna fahamu vizuri ni nini ninacho maanisha”

“Hapana”

“Serikali na vitengo vyake. Nilipanga mpango katika njia kuu mbili, moja ikiwa ni ya kujitoa sadaka na nyingie ikiwa ni ya kuingiza mzigo huo ambao kwa sasa upo sehemu salama”

“Ume jitoaje sadaka”

“Niliagiza vijana watafuta boti moja nzuri na nika penyeza taarifa ya siri kwamba boti hiyo ime lete mzigo wa madawa ya kulevya ndani ya nchi. Basi macho yote ya serikali yalikuwa juu ya boti hiyo ambayo kwa ndani nili agiza iwekwe mabomu ya siri. Nilitambua kabisa kwamba boti hiyo ni lazima ita fwatiliwa tu, kipindi boti hiyo ina fwatiwa, mita mia moja ndani ya bahari niliweka vijana zaidi ya kumi ambao wana jua kuogelea. Walikuwa na mabegi makubwa ambayo ndani yake yalikuwa na kilo hizo za unga”

Nabii Sanga macho yakamtoka huku akimtazama Julieth anaye zungumza kwa kujiamini sana.

“Japo sikuwepo eneo la tukio, ila mpango wangu ulikuwa ni kwamba endapo boti hiyo ita lipuka basi vijana wangu wata kuwa na mwanya mzuri wa kuingia katika zone ya bahari ya Tanzania kiurahisi sana kwa maana vijana hao walikuwa wana tokea Mombasa.”

“Kabla huja kwenda mbali huo mzigo uliutolea wapi Julieth?”

“Colombia na Mexco”

“Mmmm muda mchache sana ume pata watu hadi huko?”

“Ndio maana baba nika kuambia akili. Nyinyi mukiwa muna fikiria harusi yangu. Mimi nina fikiria hii biashara tena mara baada ya kufahamu kwamba ita tuingizia kiasi kikubwa sana cha pesa akili yangu ime tanuka mara dufu”

“Ehee tuambie imekuwaje?”

“Baada ya boti kulipuka, ilikuwa ni rahisi kwa wale viiaja kupita eneo la chini wakiwa na mzigo wote kwa maana macho ya askari wote yalikuwa kwenye mlipuko huo. Nikaweza vijana wengine wanne ambao baada ya mlipuko huo basi wakasawazishe eneo hili kwa kutengeneza statement nzuri kwa serikali kwamba kwa sasa hali ime badilika na kiongozi ni mpya kabisa”

Nabii Sanga aka shusha pumzi huku akiwa haamini hichi anacho kizungumza binti yake.

“Eheee imekuwaje juu ya hao vijana?”

“Wamepoteza ushahidi kwa kulipua boti huku wao wakijirusha kwenye maji na wote wanne wapo salama”

Julieth alizungumza huku akitabasamu sana na kumfanya mrs Sanga kumkumbatia mwanaye huyo kwa furaha sana kwa maana alilo lifanya sio jambo rahisi japo wame poteza maisha ya watu wasio na hatia.

***

Tomas na Levina wakafika nchini Tanzania majira ya saa nne usiku. Moja kwa moja wakaelekea nyumbani kwa Levina na hapakuwa na mtu hata mmoja katka kiwanja cha ndege aliye fahamu kwamba huyo aliye pita hapo ni Tomas ambaye alikuwa ana tafutwa na jeshi la polisi akisadikika na jambazi mkubwa sana. Levina akawasha laptop yake na kunza kuperuzi kwenye maeneo mbalimbali kwenye vitengo vya usalama ili kufahamu ni jambo gani linalo endelea.

“Tom njoo uone?”

Tomas akamsogelea Levina aliye kaa mezani hapo.

“Kuna kuna nini?”

“Hii video ime rekodiwa dakika arobaini na tano zilizo pita.”

“Hao ni kina nani?”

“Hawa ni askari wa kitengo cha kupambana na rushwa”

“Ahaaa sasa mbona wame lipuliwa?”

“Hata sifahamu ime kuwaje, alafu wame uwawa”

Levina alizidi kushangaa video hiyo huku akiendelea kutazama tukio hilo la kinyama.

“Acha wafe, mimi aliye nirudisha hapa ni nabii Sanga na familia yake tu”

“Mmmmm nita lifwatilia kwa kina. Harusi ya mtoto wa raisi pamoja na Julieth ume bakia mwenzi mmoja na siku nne. Ina tupasa kuhakikisha kwamba tuna panga mpango ambao uta muua nabii Sanga taratibu na hakuna atakaye fahamu kwamba wewe ndio unaye husika”

“Mmmmm yaa nita jaribu kufikiria nini cha kufanya. Ila nita hitaji kwenda kwenye ile nyumba yangu niliyo kuwa nina ishi”

“Kule sio salama Tom”

“Kwa nini?”


ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

BLOG