SIN SEASON 2
WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+
SEHEMU YA 10 KATI YA 10
Nabii Sanga alimuuliza mke wake mara baada ya kumuona akiwa mikono mitupu.
“Baba Julieth hata sijui niseme nini?”
“Useme nini nini?”
“Mwanao ana dai kwamba faili aliliweka mezani chumbani kwake, ila hatulioni”
Nabii Sanga akastuka sana huku macho yake akimtazama mke wake.
“Tumejaribu kutafuta kila sehemu, ila kwa bahati mbaya hatujaweza kuliona”
Nabii Sanga akamtazama Julieth anaye shuka kwenye ngazi taratibu huku akionekana kujawa na wasiwasi. Akakaa pembeni ya mama yake.
“Shikamoo baba”
Nabii Sanga wala hakuitikia salamu hiyo kwa maana tayari kichwa chake kimesha vurugika. Akasimama huku akiwa amevimba kwa jazba, kitu ambacho kina mzui kumzaba makofi Julieth ni kwamba ana mpenda sana mwanaye huyo wa kike.
“Baba haki ya Mungu vile nililiweka juu ya meza lile faili, ila sijaliona na sijui lime kwenda wapi”
Julieth alizungumza kwa sauti ya woga huku machozi yakimwagika usoni mwake. Ukweli ni kwamba ana muogopa sana baba yake akiwa katika hali hiyo ya kukasirika.
“Muna taka kuniambia jana usiku muliingiza mtu humu ndani?”
“Mtu kivipi baba Julieth”
“Kivipi nini, ina maana nyinyi kwa nyinyi muna weza kuibiana au?”
Nabii Sanga alifoka hadi Julieth na mama yake wakaanza kutetemeka.
“Muna jua ni jinsi gani tuna weza kuanguka kama lile faili likiingia mikononi mwa watu wengine eheee?”
Nabii Sanga alizidi kufoka hadi mishipa ya shingoni mwake ikajitokeza vizuri.
“Ila baba Julieth, unavyo tufokea sio vizuri. Sisi hatujaingiza mtu humu ndani. Kama huamini angalia hizo cctv Kamera si zina rekodi kila kitu”
Mrs Sanga alijikaza kuzugumza kwa maana hakuna jinsi nyingine zaidi ya kufanya hivyo. Nabii Sanga akachukua rimoti ya Tv na kuwasha tv kubwa iliyopo sebleni hapo. Akaingia upande wa kamera za ulinzi na kuanza kurudisha matukio nyuma kuanzia muda alio toka yeye kuelekea Serena hotelini. Kila mtu macho yake yakwa katika tv hiyo huku kila mmoja wao mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana. Wakstuka sana mara baada ya kuona kamera ya siri iliyopo hapo sebleni ikionyesha mtu aliye valia nguo nyeusi pamoja na bushori jeusi akiingia ndani hapo na kuelekea gorofani. Wakatazamana huku wakiendelea kufwatilia jinsi mtu huyo alivyo rekodiwa na kamera nyingine za siri zilizopo katika ngazi na kordo ya gorofani.
“Huyu ni mtu maalumu aliye tumwa”
Nabii Sanga alizungumza kwa maana kama ni mwizi basi angeiba vitu vya thamani vilivyopo sebleni hapo kama baadhi ya mapambo yaliyo tengenezwa na dhahabu tupu.
“Sasa ame tumwa na nani?”
Mrs Sanga aliuliza kwa mshangao.
“Sifahamu, ila anaonekana ni mtu ambaye ana mafunzo ya kijasusi kwa maana ameweza kuzikwepa kamera za nje ila kamera za hapa ndani zime weza kumnasa. Wakamuona mtu huyo akiingia chumba cha kwanza kisha akatoka na kuingia chumba cha pili ambacho ni cha Julieth. Wakamuona akitoka na faili hilo na nabii Sanga akaisimamisha video hiyo hapo na akajishika mdomo wake kwa mshangao mkubwa sana.
“Mume wangu tume kwisha”
Mrs Sanga alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Hapana, hatuwezi kwisha kirahisi. Kama ni Wamarekani ndio waliye mtuma huyu panya wao. Haki ya Mungu nita shuka nao jumla jumla”
Nabii Sanga alizungumza huku akihema kwa hasira. Moyo wake una hisi kama una chanwa chanwa kwa viwembe kwani hasira yake ime pitiliza kiwango sasa. Akaiingiza video hiyo kwenye simu yake na kuwatumia vijana wake walipo kwenye meli kisha akampigia mkuu wao.
“Kuna video hiyo mume iona?”
“Ndio mkuu”
“Nina hitaji kufahamu ni nani aliyopo nyuma ya hilo hushori kwa maana ameingia ndani kwangu na kuiba kitu kilicho muhimu sana kwangu”
“Sawa mkuu, dakika kadhaa kila kitu kitakuwa tayari”
Nabii Sanga akakata simu huku akizunguka zunguka sebleni hapo.
“Baba?”
“Nini?”
Nabii Sanga aliitikia kwa jabza badi Julieth akastuka.
“Ehee niambie”
Nabii Sanga ikabidi ajishushe na kuzungumza kwa sauti ya kawaida kwa maana ana tambua kwamba ame mtisha sana mwanaye.
“Jana kikao chako kime kwendaje?”
“Nime wapa machaguzi wale wajinga. Walihisi na mimi nita kwenda kinyonge. Wana fahamu siri zangu nami nina fahamu siri zao hivyo ngoma droo. Nime waambia nina hitaji raisi wao aje hapa Tanzania na tuzungumze biashara la sivyo nina kwenda kutoa siri za raisi wao. Tuone kama mimi na yeye ni nania mbaye ata pata hasara kubwa”
“Kwa hiyo wame kubaliana na wewe?”
“Ni machaguzi yao, kama wata kubali sawa, kama wata kataa tuta pamanana nao uso kwa uso.”
Nabii Sang alizungumza kwa kujiamini na kurudisha amani iliyo weza kutokea nyumbani kwa nabii Sanga. Simu ya nabii Sanga ikaita na kwa haraka akipokea na kuiweka sikoni mwake.
“Muheshimiwa kila kitu tayari nakutumia sasa hivi”
“Sawa na hakikisheni muna kuwa macho na hili eneo”
“Hakuna shaka mkuu”
Nabii Sanga akakata simu huku mayo waka, macho yake vikiwa na hamu kubwa sana ya kuona ni nani aliye ingia nyumbani kwake usiku huo. Nabii Sanga taratibu akaifungua picha hivyo ilivyo weza kufanyiwa scanig na vijana wake.
“WHAT’S FUC**”
Nabii Sanga alijikuta akitoa tusi zito huku macho yakimtoka kwani sura ya mtu anaye onekana hapo ameifahamu vizuri sana na si mwengine bali ni George Sanga aliye jitambulisha kama mfanya biashara mkubwa na mtu aliye hitaji kufanya uwekezaji wa pesa nyingi sana ndani ya nchi ya Tanzania.
“Kuna nini mume wangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akinyanyuka na kumsogelea mume wake. Akayatupia macho kwenye simu, naye akajikuta akiwa amejawa na bumbuwazi kubwa sana.
“Hu…yu….mshenzi, nita muua”
Nabii Sanga alizidi kujawa na hasira.
“Nani huyo baba?”
“George Sanga”
Julieth kusika jina hilo kwa haraka akasimama na kuichukua simu ya baba yake na akatazama picha hiyo. Akahisi mwili wake ukiishiwa na nguvu kwani mwanaume aliye jikuta akitokea kumtamani, amekuwa ni mpelelezi kwenye familia yake.
“Mume wangu hapa kuna mchezo kwa maana. Baada ya huyu kijana kuja uja juzi, jana Julieth akapigiwa simu na huyo sijui Balozi sijui nani, akapewa hilo faili. Hapo hapo jana huyo kijana amekuja kuchukua hilo faili. Huoni kama hawa Wamarekani wamekuchezea pata potea na isitoshe ametoka nchini kwao. Una weza kukuta ni mpelelezi wao”
“Shenzi sana hawa ngoja kwanza”
Nabii Sanga akampokonya Julieth simu, akaitafuta namba ya balozi Trup na akampigia.
“Ndio Sanga”
“Kwa hiyo mume amua kucheza mchezo mchafu”
Nabii Sanga alizungumza kwa kufoka.
“Una maanisha nini Sanga”
“Mume tuma mpelelezi wenu kuja kuiba lile faili”
“Mpelelezi wetu. Hell no kwa nini tufanye hivyo Sanga ikiwa tupo kwenye wakati wa mazungumzo.”
“Kwa hiyo hamjamtuma George Sanga”
“Hahaa nabii Sanga, hilo jina mbona halipo hata kwenye list ya wapelelezi wa nchi yetu. Isitoshe mbona ni kama ndugu yako kwa maana muna ukoo mmoja”
“Trump sipo wakati wa masihara”
“Okay Okay Sanga, nitumie hiyo picha ya huyo mpelelezi pamoja na details zake”
“Poa sasa ole wako ni kute ni mpelezi wetu haki ya Mungu, mambo yataishia leo hii. Bora wote tupoteze”
“Nitumie Sanga acha hasira”
Nabi Sanga akakata simu na kutuma picha hizo kisha akaandoka na taarifa zinazo muhusu George Sanga kama mmiliki wa kampuni ya Samsung. Baada ya dakika kumi simu ya nabii Sanga ikaita. “
“Ndio”
Nabii Sanga aliitikia mara baada ya kuipokea simu hiyo.
“Kwanza hakuna tajiri Marekani anaye itwa George Sanga. Mbili hakuna mtu mwenyesi anaye miliki kampuni ya Samsung kwa maana chimbuko lake ni North Korea hivyo una weza kutambua ni nani wamiliki. Tatu hatuna mpelelezi kama hiyo kwenye kitengo chcohote nchini Marekani. Hivyo kama ni mpelelezi basi atakuwa na ana kufwatilia wewe.”
“Trump una uhakika na unacho kizungumza?”
“Asilimia mia moja, nchi yangu haihusiki kabisa na huyo mtu na tumejaribu kufwatilia rekodi za nyuma za mtu huyo, tume gundua kwamba hazipo sehemu yoyote. Hana familia, hana mke na kilicho andikwa kwenye huo mtandoa kwamba ni tajiri ni habari feki na yakutengezwa”
Nabii Sanga akahisi tymbo la haja likimkamata, nguvu zza mwili zika muishia hata hamu ya kuzungumza ikamkatika kabisa.
“Tume elewana Sanga?”
“Sawa”
Nabii Sanga akakata simu huku akiwa haamini alicho kisikia.
“Baba ume jua ni nani?”
Nabii Sanga akawaeleza alicho elezwa na balozi Trump na kila mmoja akajikuta akiishiwa pozi kwa maana walimuamini sana George Sanga na kuubali kumuingiza kwenye maisha yao pasopo kujua ni mtu wa aina gani.
***
“Hei baby chai tayari”
Magreth alizungumza huku akiwa amuinamia Evans ambaye bado yupo usingizini.
“Saa ngapi sasa hivi?”
Evans alizungumza huku akikaa kitako kitandani.
“Ni saa nne na dakika zake”
“Ohoo shit”
Evans alizungumza huku akifungua droo na kuchukua faili la nabii Sanga.
“Ume lifungua hili?”
“Hapana mume wangu siwezi kuenenda kinyume na matakwa yako”
Magreth alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Kwani hili faili lina nini?”
“Usijali lina mambo muhimu”
“Mambo yanayo husiana na nini?”
“Ni baadhi ya biashara zangu tu”
“Sawa mume wangu. Una weza kwenda kuoga kisha tuka jumuika pamoja mezani.”
“Twende tukaoge pamoja”
“Sawa”
Wakaingia bafuni na kuoga kwa pamoja, hiyo ikiwa moja ya njia ya Evans kulinda faili hilo. Wakarudi chumbani.
“Vipi shemeji yupo?”
“Yaa hajakwenda kazini.”
Wakatoka na kumkuta Josephine akiwa sebleni, wakasalimiana kwa furaha na Evans kisha kwa pamoja wakaketi kwenye viti vilivyo zunguka meza ya chakula. Magreth akaandaa kifungua kinywa hicho kisha wakaanza kunywa taratibu. Josephine akafumba macho yake kwa dakika tano na kumfanya Evans kujawa na mshangao.
“Shemeji una umwa?”
Evans aliuliza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Hapana ila kwa nini George una tudanganya?”
“Nawadanganya?”
Evans aliuliza huku akiwa amejawa na mstuku mkubwa sana.
“Ndio, una tudanganya.”
“Jose tafadhali shemeji yako ana tudanganya nini?”
Magreth aliingilia kati mazungumzo hayo.
“Mungu amenipatia maono juu yako. Ukweli wako ndio utakao kuweka huru George kwa maana nime onyeshwa kila kitu”
“Sikuelewi shemeji una maanisha nini?”
“Mage nina imani kwamba una mtafuta Evans kwenye maisha yako?”
“Stori hizo zina kujaje hapa Josephine”
“Samahani ila huyu ndio Evans Shika na sio George Sanga. Hapo ulipo shemeji umefanyiwa upasiaji na ume weka sura ya bandia. Kama nina bisha seme nina bisha”
Magreth akastuka sana huku mapigo ya moyo yakimnda kasi. Ikambidi sasa kumtazama George vizuri kwa umakini sana. Mshangao wa Evans ukamfanya Magreth kuamini kitu alicho zungumza Josephine.
“Shemeji kuwa muwazi kwa maan kuna vita kubwa ipo mbele yako na vita hiyo ita muondoa kila aliyo kuwa karibu nawe kuanzia yule msichana wa pale Samaki samaki, mama yako, mdogo wako wa kike pamoja na sisi”
“George jibu hichi anacho kizungumza Josephine ni kweli au?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Evans kuendelea kukaa kimya.
“Sema bwana”
“NDIOO, mimi ni Evans”
Evans ikamabidi kuzungumza kwa sauti yake halisi jambo lililo mfanya Magreth kujawa na mshangao mkubwa sana.
“Nimerudi Tanzania kwa sura hii kwa ajili ya kulipa kisasi. Nilipanga kulipiza kisasi kwako ila nilipo gundua kwamba huna makosa yoyote na chanzo kikubwa cha matatizo yangu kuongezeka kwenye maisha yangu ni nabii Sanga na familia yake”
Evans alizungumza huku machozi yakimwagika.
“Nime amini kwamba una nipenda na kunijali. Kama ni uwezo wa kuwaua nilikuwa ninao ila sikuhitaji kufanya hivyo.”
Magreth akachukua glasi ya juisi na kumwagia Evans usoni mwake.
“Toka nyumbani kwangu muuaji mkubwa wewe”
Magreth alifoka hadi Josephine akashangaa.
“Magreth tafadhali, usimfukuze. Ana kitu muhimu ambacho sisi tuna kihitaji”
Josephine alimtetea Evans.
“Potelea pote sitaki kumuona nyumbani kwangu. Tokaaaaaaaa”
Evans taratibu akasimama na kutembea kuelekea chumbani kwa Magreth.
“Una kwenda wapi?”
Magreth aliuliza kwa kufoka.
“Nina chukua kilicho changu.”
“Mage tafadhali, huu sio wakati wa kugombana. Tukaeni chini tujue tana pambana vipi na maadui zetu kwa maana jana Evans aliiba faili kutoka nyumbani kwa nabii Sanga na faili hilo ni muhimu sana kwetu”
Magreth na Evans wakastuka huku Evans akujiuliza ime kuwaje Josephine ame fahamu juu ya faili hilo.
“Faili?”
Magreth aliuliza kwa mshangao. Evans hakuhitaji kupoteza muda, akaingia chumbani kwa Magreth na kuchukua faili lake na kutoka.
“Hasira zako zikikuisha muta nitafuta”
“Hapana shemeji usiondoke. Sisi watatu tuna weza kufanya kitu juu ya kila jambo. Siku zote Mungu alikuwa ana nificha juu ya jambo hilo na alinieleza ata mleta mtu ambaye ata nipatia ushahidi wa kila kitu ambacho nilikuwa nina tamani kufahamu juu ya nabii Sanga na familia yake. Tafadhali shemeji tuwe pamoja katika hili”
Josephine ilimbidi kutumia busara nyingi sana kuzuia hasira za Magreth dhidi ya Evans ambaye kwa sasa wamesha tambua ukweli kwamba sio George Sanga bali ni Evans Shika. Wakakaa katika masofa tofauti huku Magreth akiendelea kumtazama Evans kwa macho ya hasira.
“Shemeji natambua malengo yetu na yako yana weza kutofautiana kidogo, tafadhali tuambie ni kitu gani kilichopo kwenye faili hilo”
Evans akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akimtazama Magreth.
“Siwezi kuwaambia kwa mana njia zenu na zangu ni tofauti”
“Shemeji tafadhali tuambie tu”
“Evans”
Kwa mara ya kwanza Magreth akamuita Evans kwa jina lake halisi.
“Ndio”
“Natambua nili kumiza na niliyaweka maisha yako kwenye wakati mgumu. Nilikutafuta ili niweze kukuomba msamaha ila sikuweza, Josephine hapa ni shahidi”
“Ulisha niambia juu ya jambo hilo. Okay mpango wenu nyinyi ni upi kwa nabii Sanga”
“Tuna hitaji aweze kuhukumiwa kwa makosa yake yote”
Josephine alijibu huku uso wake ukiwa na tabasamu pana sana.
“Kwa makosa yapi?”
“Hayo ambayo uta tuonyesha”
“Nisikilizeni na muni elewe kwa umakini sana. Nabii Sanga ana nguvu kuliko raisi Mtenzi, si ndani ya hii nchi ila duniani kwa ujumla. Nabii Sanga sio mtu wa kawaida kama akili zenu zinavyo mfikiria, ana nguvu ya kubadilisha sheria ikawa pesa na pesa ikawa sheria. Nyinyi ni watu wadogo sana kwake na mukisema kwamba ahukumiewe kwa sheria, kuanzia raisi na watu wote wa chini hakuna anaye weza kumuhukumu nabii Sanga”
“Mmmm hata kama kuwe na ushahidi?”
Magreth aliuliza huku macho yakimtoka.
“Ni wangapi wapo uraiani walifanya makosa makubwa sana na ambayo yalikuwa na ushahidi wa kuwafanya waweze kufungwa ila waliweza kuinunua sheria na leo hii wana endelea na maisha yako ya kawaida”
Evans alizungumza kwa msisitizo.
“Mmmm”
“Musigune hichi ndio kitu cha ukweli, nabii Sanga ana mtandao wake ni mkubwa sana hivyo mawazo hayo munayo muwazia futeni kwa sasa”
“Sasa shemeji tuta fanya nini?”
“Natambua tamaa ya nabii Sanga na tamaa ya nchi ya Marekani ni kuweza kupata hadhina ambayo wewe Josephine pekee ndio una fahamu ni wapi ilipo hiyo hadhina.”
“Hilo ni kweli unalo seme shemeji.”
“Hawa ni mabepari wawili ambao kukaa zizi moja hawawezi. Ninacho kihitaji kutoka kwenye ni kumpata kiongozi wa serikali wa ngazi za juu ambaye muta weza kumuamini”
“Yupo mmoja”
Magreth alizungumza na kumfanya Josephine kushangaa kidogo.
“Nani?”
Josephine aliuliza kwa mshangao kwa maana imani yake imesha ondoka kwa viongozi wa kiserikali.
“Mzee Mbogo, isitoshe amesha teuliwa kuwa makamu wa raisi”
Magreth alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Nina muamini, ni kwa mara kadhaa nilisha kutana naye mzee Mbogo kipindi kile katika harakazi ya yale mabomu aliweza kunisikiliza. Kama tuna muamini basi hiyo kazi ya kuzitafuta hadhina ita baki mikononi mwake kwa maana hapo awali nilikuwa na hamu ya kuweza kuipata hadhina hiyo ila siwezi kuwa mbinafsi nita hakikisha nina wasaidia katika kuitafuta”
“Kweli moyo wako umebadilika shemeji. Hivi yule jini aliyekuwa ana kupa maelekezo aliishia wapi?”
“Alinipa kazi ya kuwau, wewe, Magreth, nabii Sanga, Jery na Julieth, ili niweze kuipata hiyo hadhina. Il anime kuja kugundua jambo kwamba mimi ni binadamu na nyinyi pia ni binadamu. Siwezi kuwa mnyama na kuongozwa na jini ambaye sifahamu chimbuko lake ni lipi. Hivyo nilifutulia mbali mpango huo”
“Ume fanya jambo jema shemeji. Katika kipindi ulicho potea ulikuwa wapi?”
“Russia. Niliamua kujiunga na kikundi cha kijasusi na nilipatia mafunzo ya hali ya juu. Niliyafanya kwa bidii na juhudi kubwaa kuhakikisha kwamba nina fanikiwa katika kazi yangu ya kulipiza kisasi”
“Woo sasa nina anza kuina timu mpya. Timu yako wewe na Magreth au una semejae Mage?”
Magreth akatabasamu tu huku akiendelea kumsikiliza kwa umakini wa hali ya juu Evans.
“Turudi kwenye mada yetu shemeji. Je tuna fanya nini kupambana na nabii Sanga?”
“Ili tuweze kupamaban na nabii Sanga ina bidi tumpokonye kila kitu anacho kipenda yeye na familia yake”
“Kitu anacho kipenda yeye na familia yake kivipi?”
“Kitu gani?”
Magreth auliuliza.
“Utajiri wake ndio nguvu yake. Endapo tuta uchukua na kuumiliki, itakuwa ni rahisi kupambana naye”
“Kwa kipindi kifupi nilicho kaa na Sanga nime weza kutambua ni mtu msiri sana na ni mtu ambaye yupo tayari kufanya chochote kwa ajili ya kulinda mali zake ambazo chanzo chake sisi hatujui”
“Ni kweli, ila kwa njia hii hatotoka”
Evans alizungumza huku akiweka faili lenye siri zote za nabii Sanga, mezani. Magreth akawa wa kwanza kulichukua na kulifunua, mshangao alio upata hakika hakuwahi kuupata toka kuzaliwa kwake. Josephine akashindwa kujizuia na kumsogelea Magreth na wakalitazama faili hilo kwa pamoja na kila ukurasa wanao ufungua kila mtu alihisi kuishiwa na nguvu kwa maana ni matukio machafu na ya kustajabisha yaliyo fanywa na nabii Sanga na familia yake.
***
Nabii Sanga na familia yake, wakaingia kwenye boti iliyo wapeleka moja kwa moja hadi katika meli kubwa ambayo ndipo kikosi chake cha majasusi kina ishi. Wakaingia ndani ya meli hiyo na kukutana na kikao cha dharura cha majasusi hao wapatao elfu moja na mia mbili hamsini. Nabii Sanga akasimama mbele ya moja ya jukwaa lililopo ndani ya ukumbi mkubwa sana. Akawatazama kikosi chake hicho kilicho valia makombati ya kijeshi. Wanaume wote walio simama katika eneo hili wamajazia miili yao yenye misuli itokanayo na mazoezi makali sana, ambayo yana wawezesha kupambana na mtu au kikosi chochote kile.
“Kuna kiumbe ndani hapa ana tupeleleza. Siri nyingi za humu ndani zipo mikononi mwa serikali ya Marekani. Hivyo tuta mjua ni nani hivi karibuni na muna fahamu ukijulikana huna bahati ya kuendelea kuishi hapa duniani. Kitu kingine kuna mjinga mmoja amekanyaga mstari wangu mwekundu. Picha yake ni hiyo hapo”
Picha ya Evans ikaonekana kwenye mwanga wa projecta(sinema) iliyopo ukumbini hapo.
“Ana kitu muhimu ninacho kihitaji hivyo muna msaa ishirini na nne ya kumsaka ndani ya jiji la Dar es Salaama tume elewana?”
Ndio mkuu”
Majasusi hao wakaitikia kwa pamoja huku wakiwa na uchu mkubwa sana kwani ni mara chache sana huwa wana pata kazi za kutoka nje ya meli na isitoshe ni watu ambao ni hatari sana kwani swala la kuua kwao ni sawa na kumuua sisimizi kwa kumkandamiza kwa kidole gumba.
“Timu ya watu mia moja ita tosha kukamilisha hili jambo. Kuna mke wake anaye itwa Leila katika kufwatilia, nime weza kugundua ana fanya kazi Samaki Samaki. Tukimpata huyo mwanamke itakuwa ni rahisi kumpata na yeye”
Nabii Sanga akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akimtazama mke wake pamoja na mwanaye.
“Kuanzi lei hii nina hitaji ulinzi wa siri mimi na familia yangu. Ninahitaji munilinde pasipo watu kufahamu kama muna tulinda. Yoyote ambaye muta muona ana hitaji kutudhuru nina imani kwamba muna fahamu nini cha kufanya”
“Ndio””
“Leo mimi na familia yangu tuta kuwa hapa, hakikisheni kwamba muna rudi na huyo kijana”
Baada ya kikao hicho nabii Sanga akaelekea kwenye ofisi yake ambayo huitumia akiwa katika meli hiyo ambayo ukubwa wake una izidi meli ya Titanic kwa mita kadhaa. Katika meli hiyo kuna huduma zote za kijamii, ikiwemo hospitali, maduka yenye kila kitu pamoja na viwanja vya michezo. Majasusi hao wote wanao fanya kazi chini ya nabii Sanga wamekuwa ni watiifu kwake na wapo tayari kufa kwa ajili yake.
“Baba ita kuwaje kurudi ikulu, na mume wangu hatambui kama nipo huku?”
“Hapaswi kutambua na jambo la muhimu sasa hivi ni sisi hii familia. Nipo tayari kumuua yoyote yule atakaye ingia igusa familia yangu. Nime wapoteza kaka zako sihitaji kukupoteza na wewe pia”
“Julieth mwanangu nina imani kwamba kwa sasa siri zetu zimesha fahamika na maadui zetu. Wata jaribu kutukabili. Sasa hivi ndoa na mambo mengine hembu jaribu kuyaftulia kichwani sawa mama”
Mrs Sanga alizungumza huku akimtazama mwananye usoni.
“Sawa mama”
‘Endapo lile faili lita patikana na tuka mpata adui yetu basi kila jambo lita kuwa salama na tuta rudi nyumbani”
Mrs Sanga aliendelea kumshawishi Julieth hadi akaelewa hali iliyopo kwa wakati huo. Mkuu wa majasusi hao, akaingia ndani hapo, akasimama wima huku mikono yake akiwa ameirudisha kwa nyuma.
“Mkuu kikosi kipo tayari. Je una haya ya kukiona?”
“Kipo tayari kwa kuondoka?”
“Ndio mkuu”
“Waruhusu sasa wakaifanye kazi”
“Sawa mkuu”
Mkuu huyo akatoka na kumuacha nabii Sanga na familia yake wakiwa wamejawa na hamu kubwa sana ya kuona George Sanga ana kamatwa.
***
“Habari ya mchana muheshimiwa makamu wa raisi?”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole na unyenyekevu mkubwa sana.
“Salama Jose habari ya wewe?
“Salama muheshimiwa. Samahani nina omba kuona na na wewe kama huto jali”
“Sawa una weza kuja ofisini kwangu”
“Hapana muheshimiwa nje ya ofisini. Kama huto jali muheshimiwa nia kuomba nikualike chakula cha mchana nyumbani kwangu, nina mazungumzo muhimu sana muheshimiwa”
“Mmmmm leo huja kwenda ikulu?”
“Hapana niliomba udhuru kwa muheshimiwa raisi asubuhi. Hali yangu ya kiafya kidogo haipo sawa”
“Ohoo pole sanabasi saa nane na nusu nita kuja hapo nina imani baadhi ya walinzi wana pafahamu”
“Ndio muheshimiwa ila kama huto jali nina kuomba uje peke yako au na dereva tu. Usiongozane na msafara wowote”
“Ni kwema kweli?”
“Ndio muheshimiwa ni kwema ila nia kuomba sana”
“Kwema?”
“Ni kwema muheshimiwa, ila nina kuomba sana”
“Sawa nita fika hapo na mlinzi wangu mmoja tu. Je kuna haja ya kumueleza raisi Mtenzi”
“Hapana muheshimiwa”
“Sawa nita fika”
“Nashukuru sana muheshimiwa”
Josephine akakata simu na kuwatazama Magreth na Evans ambao walikubaliana kumshirikisha makamu wa raisi katika jambo la kukabiliana na nabii Sanga. Magreth na Josephine wakaanza kuandaa chakula cha mchana. Saa nane na nusu, kengele ya getini ikasikika. Magreth akatazama kwenye simu yake na kuona gari la mzee Mbogo.
“Amefika nenda kamfungulie”
Josephine akaeleke getina na kufungua geti na taratibu dereva akalisimamisha gari eneo la maegesho ya magari na mzee Mbogo akashuka na akasilimuana naye.
“Waoo mtaani kwenu kume tulia sana”
“Nashukuru mkuu, karibu sana ndani”
“Asante”
Wakaingia ndani na Evans akanyanyuka na kumsalimia mzee Mbogo.
“Sauti yako sio ngeni kwangu ila sura yako ni ngeni kwangu”
“Ni kweli muheshimiwa. Mimi ni yule kijana wa kipindi kile, Evans Shika”
“Ohoo nami nilihisi hivyo. Nina ona ume weka sura bandia?”
Ilikuwa ni rahisi kwa mzee Mbogo kufahamu juu ya sura ya Evans kwamba ni bandia kwa maana ana fahamu vizuri mtindohuo na kwa mara kadhaa hata yeye alisha wahi kubadilisha sura yake kutokana na kazi zake za kipelelezi.
“Ndio muheshimiwa ni sura bandia.”
“Nina hisi kuna sababu nyuma ya wewe kufanya hivyo?”
“Ndio mkuu”
“Sawa uta nieleza”
Magreth naye akafika sebleni hapo na kumsalimia mzee Mbogo, kisha akarudi jikoni kumalizia kuandaa chakula.
“Ehee nina imani una mazungumzo makubwa sana na mimi Josephine”
“Ndio muheshimiwa. Kuna mambo yame jtokeza hivyo nime ona nikuambie kabla hayaja haribika”
“Mambo gani?”
“Ni kuhusiana na raisi Mtenzi”
“Ohoo amesha fanya nini tena?”
Josephine akamueleza kila kitu alicho kifanya raisi Mtenzi kwa Shani, akamuelez amipango mibaya aliyo kuwa nayo kwa Shani.
“Toka nilipo gundia hayo mkuu, nime jikuta nime poteza uaminifu wangu kwake”
“Una haki ya kupoteza uaminifu, hiyo ni kutokana hukumjua mapema. Huu ni mwaka wa arobaini toka nimfahamu Mtenzi. Nilifanya naye kazi kadhaa kipindi yeye ni IGP na mimi ni mkuu wa kitengo cha NSS. Ni mtu mbishi, mwenye roho mbaya, mbinafsi na asiye penda kushauriwa pale anapo amuaga jambo lake. Ubishi wake ulipelekea kumpoteza mke wake katika siku ya harusi ya kijana wake, nina imani kijana hapa aliweza kunitahadharisha juu ya mabomu hayo na kweli niliondoka jijini Dar, japo nilimuhasa sana mwenzangua ondoke, na asitishe harusi ila alikataa katu katu, hivyo kilicho tokea, alistahili kukipata. Hivyo usimuamini mtu kwenye maisha yako kwa maana siku ukimjua ukweli wake ata kuumiza vibaya sana”
“Sawa muheshimiwa. Je una onaje wewe ukawa raisi?”
Mzee Mbogo akatabasamu huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Jose”
“Bee”
“Kuwa raisi sio jambo dogo au kumtoa raisi madarakani sio jambo dogo kama hivyo unavyo hisi wewe. Nafasi nilio kuwa nayo hii ina nitosha na kitu kingine katika kipindi changu chote cha maisha yangu nime kuwa ni mwana usalama. Hivyo sijui siasa, hivyo hata kwenye hii nafasi nina iendesha kutokana na njia anayo iongoza Mtenzi, ila ni njia nzuti tu ndio nina fwata, kwenye njia mbaya nina mshauri abadilike”
“Nime kuelewa muheshimiwa. Tulikuwa na kikao asubuhi ya leo na wezangu hapa kwenye ile hadhina ambayo mimi ndio nina fahamu ni wapi ilipo. Tuna kuhitaji wewe ndio uwe msimamizi mkuu”
“Mmmm hilo ni jambo gumu sana kwa maana muna tambua kwamba raisi amesha fahamu na yeye ndio aliukataa mkataba walio ingia makamu wa raisi aliye pita na raisi wa Marekani juu ya kujenga jiji la Dar es Salaam ila ulivyo tufungua macho juu ya hilo ndio maamuzi yakatokea ya kutokea. Ila tukisema kwamba tufanye sisi kama sisi. Mtenzi ata kwenda kutupiga risasi sisi sote”
“Mmmm”
“Ndio na hashindwi, kama alitoa agizo mwanye tena damu yake kuuwawa kwa kupigwa risasi kisa ni jambazi je una hisi sisi wasaliti tena wa mali kubwa kama hiyo tuta fanywa nini”
Josephine akashusha pumzi nyinngi sana. Magreth akawakaribisha mezana na wote wakaelekea. Mara baada ya kuandaa chakula na kuanza kula, mazungumzo yakaendelea.
“Muheshimiwa”
Magreth alizungumza huku akimtazama mzee Mbogo.
“Naam”
“Una mchukuliaje mkwe wa raisi Mtenzi?”
“Julieth?
“Ndio”
“Ahaa ni binti sahihi, eme tokea familia ya kidini. Sijaona shida yoyote kwake”
“Je familia yake”
“Familia ya nabii Sanga. Nime ifahamu miaka mingi sana ya nyuma, kuna vimakosa vidogo vidogo walivyo kuwa wana vifanya ila sio vya kuchuliwa very serious sana”
“Vikosa gani muheshimiwa?”
“Kuna kipindi walikamatwa kwa kutoa kulia kodi serikali. Hilo ndio kosa ambalo nililifahamu kwenye ile familia na kutoea kipindi kile wame kuwa wakiishi kwa amani na furaha. Japo kuingia kwa Jery katika familia yao kulisababusha kuwapoteza vijana wawili wa ile familia”
“Hapo hapo muheshimiwa. Yaani Jery alisababisha nini?”
Evans aliuliza.
“Kulitokea tukio la kuuwawa kwa askari wetu kwa mlipuko wa bomu katika moja boti baharini. Raisi Mtenzi alinipa nafasi ya kulichunguza lile jambo ila kabla sijakamiisha uchunguzi wangu akachukua jukumu la kuwashambulia Al-Shabab ambao ndio walikuja kulipiza kisasi na kugarimu maisha ya maelefu ya Watanzania”
“Katika uchunguzi wako uliweza kugundua ni nani muhusika?”
Magreth aliuliza.
“Sikuweza kugundua kwa sasabu lile tukio watekelezaji walitumia akili kubwa sana na kama munavyo jua kwenye bahari kuweza kupata ushahidi wa moja kwa moja ni ngmu sana hivyo ilitufanya hadi leo tubaki kuwa vipofu katika tukio hilo. Ila mpishi chakula ni kitamu sana hichi”
“Asante muheshimiwa. Ila tume weza kufahamu ni nani ambaye amehusika na tukio lililo pelekea tukapoteza ndugu zetu, watoto zetu, kaka, dada, mama, bibi na babu zetu”
Magreth alizungumza kwa sauti ya upole sana.
“Ni nani huyo?”
Evans akanyanyuka na kuingia ndani, akachukua faili hilo alilo liweka kwenye droo. Akalifungua na kulipitia kwa mara kadhaa kwani ana hitaji kuhakikisha kwa mara ya mwisho kile kilicho kiona ndicho kilichopo, alipo jiridhisha akapiga hatua kuelekea mlangoni, kitendo cha kushika kitasa simu yake ikaanza kuita. Akaitoa mfukoni mwake na kuitazama na kukuta ni private number. Akilini mwake kwa haraka haraka akaamini ni Baby Al ndio anye mpigia hivyo ikamlazimu kughairi kufungua mlango na kuingia chooni ili aweza kuzungumza na simu hiyo kwani endapo Magreth ata sikia ana zungumza na mwanamke mwengine basi kila kitu kita tibuka ndani hapo.
***
Majasusi wawili walio valia nguo za kawaida, wakashuka ndani ya gari lao na kuanza kutembea hadi katika mgahawa wa Samaki Samaki, Mlimani City. Wakakaribishwa na mmoja wa wasichana ambaye ni muhudumu wa mgahawa huo.
“Niwasaidie nini waheshimiwa?”
“Juisi ya parachihi”
“Niletee juisi ya tikiti maji”
“Sawa”
Msichana huyo akaondoka na macho ya majasusi hao, yakaendelea kuangaza angaza kwa baadhi ya wahudumu wanao huhumiwa watu wengine. Juisi zao zika letwa na wakatamani kumuuliza muhudumu huyo ila wakavuta subira.
“Tukimpata tuta mfanya nini?”
“Tuta subiri maagizi ya mkuu”
Kwa bahati nzuri kwa upande wao ila kwa bahati mbaya kwa upande wa Leila. Wakamuona akitoka katika eneo la wahudumu huku wakiwa wasichana wawili wambao kwa muoneonekano wa nguo zao ina onyesha kwamba wamesha maliza muda wa kuondoka kwao.
“Leila nina hamu ya kumuona huyo mwanamume wako kwa mana aunavyo msifia mmmm”
“Yaani wee acha. Hivi una jua kuna wanaume na vijiwanaume. Sasa hivi nime pata mwanaume ambaye nina amini kwamba ana kwenda kunitoa kwenye huu umasikini wa kuwahudumia watu hadi kuwa tajiri”
“Nakuombea shosti yangu mambo yako yafanikiwe kwa maana najua na mimi nita nukia nukia utajiri si una jua ukika karibu na uwa ridi ni lazima unukie”
“Ndio maana yake mpenzi. Hapa nataka niandae chakula cha mchana, kisha nimpie aje kula”
“Sawa”
Walinzungumza huku wakielekea nje ya eneo la Mlimani City. Jasusi mmoja akanyoosha mkono mmoja juu na kumuita muhudumu aliye wahudumia. Akatoa noti ya dola mia na wakanyanyuka pasipo kudai hata chenchi. Wakaingia kwenye gari lao huku wakiwa makini sana kutazama muelekeo wanapo elekea Leila na rafiki yake. Wakatoka katika geti la Ubungo na kuwaona wakiwa wame simama kwenye kituo cha bajaji wakishauriana kukodisha bajaji au kupanda daladala.
“Hei warembo muna kwenda wapi?”
Jasusi mmoja ambaye huwa ana jiamini kwambaa na mvuto mzuri kwa wanawake alizungumza huku akiwatazama Leila na rafiki yake.
“Safi”
Rafiki wa Leila aliitikia huku akiwa amajewa na furaha.
“Wapi muna kwenda tuwapatie lifti?”
“Asanteni kaka zangu”
Leila alizungumza huku akimtaza kijana huyo.
“Hapana jamani. Warembo kama nyinyi ina bidi mupate usafiri”
Jasusi huyo alizungumza huku akishuka kwenye gari hiyo aina ya Benz jambo lililo mfanya rafikiwa Leila kushawishika kirahisi sana naye akaanza kushawishi rafiki yake wapande gari hilo. Ushawishi wa jasusi huyo na rafiki yake uka mshinda Leila na kujikuta akiingia ndani ya gari hilo huku moyoni mwake akiwa ametawaliwa na wasiwasi.
“Muna elekea wapi warembo”
Leila akawa wa kwanza kujibu na kuwaambia eneo analo ishi. Jasusi huyo akaminya moja ya batani, ambayo ina toa gesi maalumu inayo kufanya upitiwe na usingizi wa haraka. Kutokana wana elewa ni nini wanacho kifanya, wakajiziba pua zao kwa vitambaa vyenye unyevu nyevu wa maji na gasi hiyo haikuwadhuru hata kidogo. Ndani ya sekunde thelathini, Leila na rafiki yake wakakoroma usingizi fofofo na jasusi huyo akazima gesi hiyo kisha wakafungua vioo na gesi hiyo ikaisha kisha na wakaelekea eneo walipo wezao.
“Huyu nani tena?”
Mkuu wa kikosi hicho aliwauliza.
“Huyu tume mkuta na huyu msichana”
Mkuu huyo akatoa bastola yake, akaikoki. Akakata kumpiga risasi za kichwa msichana huyo ila roho yake ikatisa.
“Mlazeni hapo kwenye majani kwa maana tunaye muhitaji ni huyu”
Wakatii agizo hilo na kuondoka eneo hilo na moja kwa moja wakaeleka kwenye moja ya godauni la siri la nabii Sanga lililopo maeneo ya Kawe. Wakawasiliana na nabii Sanga na kumueleza wame mpata Leila.
“Safi niunganisheni na private namba nimpigie huyu chizi. Nitumieni na picha za msichana wake”
“Sawa mkuu”
Vijana hao wakafanya kama alivyo agiza nabii Sanga ambaye yupo kwenye meli yake. Nabii Sanga akapiga simu kwa Evans(George Sanga) huku mke wake pamoja na familia yake wakiwa wana sikiliza mazungumzo hayo kwa maana simu yake ameiweka loud speaker.
***
Evans akafungua bomba la maji ya kunawia ili kama Magreth ataingia kwa galfa ndani hapo asiweze kusikia mazungumzo yake ndani ya bafu hilo. Akaipokea simu hiyo na kuweka sikioni mwake.
“George George George Sanga kwa nini una cheza na mimi”
“Nani wewe?”
“Mtu uliye chukua kitu muhimu sana kwenye maisha yangu.”
Evans akatambua kwa haraka kwamba huyo anaye zungumza na niabii Sanga. Kitu alicho kifanya ni kuminya kitufe cha kurekodi mazungumzo hayo yote ili abaki kuwa na ushahidi.
“Sijui una zungumzia nini na sikujui wewe ni nani kwa mana aume piga kwa private namba”
“Mimi ni Sanga ama Nabii Sanga. Ume chukua faili langu kwa njia ya wivi, ulikuja kwangu ukijifanya mfanya biashara na mtu mzuri sana na nikakuamini sana. Ila ume vunja uaminifu wangu kwako Sasa una masaa matano nina hitaji faili langu ili nimrudishe mke wako mrembo. Endapo huto fanyah ivyo ndani ya masaa hayo matano, basi jiandae kupokea zawadi ya kichwa chake kikiwa kimetengenishwa na mwili wake. Kama huamini hilo nina kutumia picha zake na endapo uta jaribu kumjulisha mtu yoyote juu ya hilo faili, basi nita hakikisha, una poteza kila kitu ambacho una kipenda kwenye maisha yako. Nita kupigia baada ya lisaa moja nipate jibu lako. Machana mwema”
Simu ikakatwa na Evans akajikuta akisema Haloo zisizo na idadi huku aksihisi kuchanganyikiwa. Haikuisha hata dakika moja, zikaingia picha kwenye simu yake zikimuonyesha Leila jinsi alivyo wekewa bastola kichwani mwake kitu kilicho mfanya ahisi kuishiwa nguvu hadi akajikuta akikaa kwenye chuoo cha kukaa kilichomo ndani hapo huku mkono ulio shika fili hilo ukitetemeka kwa hasira iliyo changanyikana na woga mkubwa sana.
Frank akaliweka faili hilo pembeni na kusimama taratibu na kunza kunawa uso wake.
“Baby”
Sauti ya Magreth ika mstua sana na kumfanya atazame mlango huo huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi.
“Ethan”
“Naam”
“Vipi tuna kusubiria. Kuna tatizo?”
Magreth alijaribu kuufungua mlango ila akakuta ukiwa ume fungwa kitu ambacho sio cha kwaida. Ethana akaufungua mlango kwa ndani na Magreth akaingia ndani hapo. Hali aliyo miona nayo Ethan ikawa ni rahisi sana kwa Magreth kuweza kutambua kwamba kuna jambo lililo tokea.
“Vipi mume wangu kuna nini?”
“Nabii Sanga amepiga simu”
“Simu?”
“Ndio na amemteka yule msichana ambaye uliniona naye siku ile Samaki Samakai”
“Ohoooo sasa amesemaje?”
“Ana hitaji hili faili. Sijui alijuaje kwamba mimi ndio nime lichukua ikiwa nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kukwepa baadhi ya kamera siku ile kwake”
“Nyumba ya nabii Sanga ina kamera nyingi sana ambazo nyingine zina onekana kwa macho na nyingine hazionekani kwa macho. Huo ni utaratibuwake kwa maana hata kwangu hapa aliweka kamera ambazo zina onekana kwa macho na nyingine hazionekani kwa macho na nina mshukuru Mungu niliweza kubalidisha system nzima ya ulinzi hivyo hawezi ku access chochote katika kamera za hapa nyumbani kwangu”
Evans akamuonyesha Magreth picha za Leila akiwa ametekwa.
“Ngoja mara moja”
“Una taka kufanya nini?”
“Nataka nimshikirishe Josephine juu ya hili swala”
“Hapana nabii Sanga ame sema kwamba hili faili nikitoa siri kwa mtu mwengine ni lazima ata muua”
“Hapana. Nisikilize mimi, ni lazima tumshirikishe makamu wa raisi. Mbili ni lazima sasa hivi tujue kwamba tupa vitani. Tatu kupoteza maisha ya mtu mmoja ila kwa kuvuruga mipango na mtu bedui kama huyu ni jambo la muhimu sana Evans kwetu na vizazi vijavyo. Una nielewa mume wangu”
Magreth alizungumza kwa sauti ya ushawishi na kumfanya Evans kufumba macho yake huku akijaribu kutafakari.
“Una nielewa mume wangu?”
“Ndio”
“Niamini mimi hili jambo lina kwenda kuisha hivi karibuni. Ni lazima nabii Sanga aweze kuadabishwa kwa dhambi zake zote alizo zifanya. Sawa baba yangu”
“Ndio”
Maneno ya Magreth yakanyanyua munkari na hamasa ndani ya Evans. Maggreth akamnyonya Evans lipsi zake kisha wakaotoka ndani hapo na kurudi sebleni na kumkuta makamuwa raisi na Josephine wakizungumza mambo mengi sana.
“Muheshimiwa kuna hili faili lina siri nyingi sana ambazo hukuweza kuzitambua katika utendaji wako wa kazi na nina imani kwamba nabii Sanga ni mtu wako wa karibu na kama ulivyo zungumza kwamba ni mtu mwema ila hayo ndio mambo yote mabaya aliyo yafanya”
Evans alizungumza huku akimsogezea taratibu faili hilo mzee Mbogo. Kabla hajalichukua Evans akalibana.
“Utakayo yaona hapo usiulize ni wapi tume weza kuyapata kwa maana hatupo kwa ajili ya kumuonea mtu au kumtengeneze mtu kesi. Ila kazi iliyo fanyika hapo ni utaalamu ambao, vikosi vyako vya kipelelezi visinge weza kutambua jambo lolote lililomo hapo ndani”
“Sawa”
Macho ya watu wote watatu yakawa kwa mzee Mbogo ambaye taratibu akalinyanyua faili hilo na kuyasoma manadishi yaliyo andikwa TOP SECRETY. Akafungua ndani na kuanza kusoma, kadri jinsi anavyo endelea kusoma ndivyo jinsi macho yake yalivyo zidi kujawa na mshangao ulio wafanya watu wote kujua ni kitu gani ambacho ana kishangaa. Uso wake ukatawaliwa na mikonjo mara baada ya kukutana na upelelezi na mipango yote yaliyo sababisha kuuwawa kwa mpelelezi wake ambaye alihusika katika kumteka Josphine kanisani kwake. Mikono ya mzee Mbogo ikaanza kutetemeka kwa hasira kali sana ambayo mtu huyo aliye kuwa ana muheshimu na kumuona ni msaada mkubwa kwenye nchi ya Tanzania kumbe ni gaidi wa siri ambaye alimpenyeza mwanaye Julieth ndani ya ikulu ili siri zote za raisi na mipango yote ana ifahamu. Mzee Mbogo akatumia dakika ishirini kupitia neno moja baada ya jengine lililo andikwa pamoja na ushahidiwa picha. Taratibu akalifunga faili hilo na kuliweka juu ya meza huku macho yake yakiwa ni mekundu sana.
“Naomba maji ya kunywa”
Magreth akamina maji katika glasi na kumkabidhi mzee Mbogo. Akainywa maji hayo pasipo kupumzika kisha kwa ishara akaomba kuongezwa glasi ya pili ya maji ambayo nayo akainywa kwa mfufulizo kisha akaiweka glasi hiyo mezani huku mikono yake ikimtetemeka kwa hasira kali sana.
“Sanga, Sanga ume cheza namimi sana”
Mzee Mbogo alilalama huku akiwa amekunja ngumi mikononi mwake.
“Mzee, nabii Sanga ametoka kunipigia simu muda si mrefu na ameweza kumteka mwanamke mmoja ambaye ni mtu wangu wakaribu. Ana hitaji hilo faili na hapa ninavyo zungumza na wewe ni kwamba nipo katika kipindi cha muda wa kuweza kutafakari kama nita rudisha hilo faili au huyo msichana aweze kufa”
Evans alizungumza huku akimuonyesha nabii Sanga picha zilizo tumwa kwenye simu yake.
“Hilo faili muheshimiwa hatujaweza kumuonyesha kiongozi mwengine zaidi yako. Kwa maana raisi Mtenzi kwa sasa mimi simuamini zaidi yako”
Josephine alizungumza.
“Nina washukuru sana kwa kunionyesha mimi, nina imani kwmaba lingefika kwa raisi Mtenzi angeweza kulimezea kwa maana yule ni mkwe mwenzake”
“Ndio na ukiona hadi raisi Mtenzi ana gombana na mwanaye kisa yule mkwe wake basi ujue ame mpenda sana yule mkwewe.”
Magreth naye alichangia jambo hilo.
“Nina imamni nipo na watu wa kazi. Je tuna fanya nini katika hilo”
“Mkuu mimi na Magreth tuna iweza kuifanya hii kazi ila tunge pata mtu wa IT wa kuaminika nina imani kazi yetu inge kuwa ni raisi sana”
“Samson yupo nina weza kumpigia simu akaja hapa nyumbani”
Josephine alizungumza.
“Sawa fanya hivyo”
Mzee Mbogo alimuambia Josephine huku akijaribu kutafakari kichwani mwake ni kitu gani aweze kukifanya ili kupambana hii vita kubwa na nabii Sanga ambaye alikuwa ni rafiki yake waliye saidiana kwenye mambo mengi ambayo hapo awali hakujua kwamba rafiki yake huyo ni bonge moja la gaidi ambalo halipaswi kuwa hata duniani.
***
Nabii Sanga akatafakari kwa dakika kadhaa kisha akamtazama Julie
“Jiandae twende ikulu”
“Mume wangu huoni kama hilo jambo lina weza kuwa hatari kwenu nyote wawili”
“Nina jua nini nina fanya. Julieth jiandae”
“Sawa baba”
“Mimi je?”
“Utabaki kukaa na kutazama utaratibu wa mambo yote jinsi yanavyo kwenda. Sawa”
“Sawa”
Nabii Sanga akampigia simu raisi Mtenzi. Simu ya raisi Mtenzi ikaanza kuita na ikapokelewa.
“Habari mzazi mwenzangu?”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Salam asana ndugu yangu. Nina hitaji kufika ikulu kwako. Nina mazungumzo muhimu sana na wewe?”
“Ya kifamilia au kiserikali?”
Raisi Mtenzi aliuliza kwa wasiwasi huku akihisi kwamba siri ya Jery imesha bumbulika.
“Kiserikali ndugu yangu”
“Ahaa karibu sana ndugu yangu”
“Kutokana nipo nje ya mji. Je uta niruhusu kufika hapo na helicopter yangu”
“Karibu sana tena sana”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa furaha.
“Asante mzazi mwenzangu”
Nabii Sanga akawasiliana na walinzi wake na helicopter ikaandaliwa. Nabii Sanga na Julieth wakaingia ndani ya helicopter na kuondoka eneo hilo huku wakiwa na rubani peke yake. Ndani ya dakika kumi na tano wakafika ikulu na wakapokelewa na raisi Mtenzi.
“Karibuni sana”
“Tuna shukuru sana ndugu yangu”
“Shikamoo baba”
Julieth alisalimia kwa heshima kubwa,
“Salama mwanangu”
Moja kwa moja wakaelekea ofisini kwa raisi Mtenzi.
“Jery yupo kweli kwa maana ni siku nyingi sija muona?”
“Yupo kijana. Mke wake nina imani hata leo ume zungumza naye”
“Ndio baba”
Julieth alidanganya ila ukweli ni kwamba toka kupambazuke mambo yalikuwa varu varu na wala hakupata muda wa kumpigia Jery simu.
“Ndio ndugu yangu, ni mazungumzo gania muhimu ambayo ume yaleta.”
“Kwanza nitangulize samahani kwa maana kuna vitu ambavyo mwanangu hapaswi kuniambia kama mshauri wa raisi. Ila kuna kitu kimoja aliweza kuniambia.”
Julieth macho yakamtoka kwa maana hajui baba yake ame panga kuzungumza kitu gani.
“Julieth aliniambia kwamba nchi ya Marekani ime weza kuingilia katika mambo kadhaa katika nchi yetu moja wapo ikiwa ni kuitaka hadhina ambayo hatujui ni wapi ilipo. Natambua hizo ni siri za kofisi ila nami nime weza kuona nina weza kuisaidia nchi yangu katika kuhakikisha kwamba hakuna mtu yoyote anaye chukua mali ambazo ni kwa ajili ya nchi yetu na si kwa ajili ya nchi yao”
Nabii Sanga alizungumza kwa ushawishi mkubwa na kumfanya raisi Metenzi kutingisha kichwa akionyesha kwamba ana kubaliana naye.
“NI kweli huo ni uzalendo ulio tukuka”
“Ndio ndugu yangu. Nina siri muhimu sana ambazo zina ina mgusa raisi wa Marekani pamoja na nchi yake kwa ujumla.”
“Hembu nizione siri hizo?”
Raisi Mtenzi alichachawa. Nabii Sanga akatoa simu yake mfukoni na kumuonyesha raisi Mtenzi siri ambazo nchi ya Marekani wana zilinda kuhakikisha hakuna ambaye ana zitambu ana endapo zita fichuliwa ita dhohofisha uongozi wa raisi aliyopo madarakani.
“Waooo Sanga ume tolea wapi haya mambo?”
“Mimi ni mtu ambaye nina washirika wengi sana duniani. Wengine wakiwa ni wafanyakazi ndani ya ikulu ya Marekani na wengine wakiwa vitengo vya juu katika nchi hiyo kama FIB, CIA na vinginevyo. Wamarekani wana hitaji kukuua”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo na kumfanya raisi Mtenzi kulegeza tai yake vizuri kwa maana hata uwe nani ila linapo kuja swala la kufa ni ishu inayo muogopesa kila bina damu.
“Nahitaji kukulinda mzazi mwenangu. Watu wako ndani ya ikuku yako wana weza kulipwa pesa na waka kuua”
Raisi Mtenzi akaanza kujawa na hofu.
“Hili jambo Josephine alisha litabiri”
“Ndio ndugu yangu. Umejipangaje au una hitaji kufa?”
“Hata sielewi nina hisi kuchanganyikiwa. Kama una mpango wowote niambie”
“Kwa nguvu niliyo nayo nime weza kumuita raisi wa Marekani na ameahidi kuweza kuja nchini Tanzania kati ya leo usiku au kesho asubuhi ata kuwa hapa”
“Mb….o…na hiyo taarifa mimi sina?”
Raisi Mtenzi alishikwa na kigugumizi.
“Hakuna mtu yoyote ambaye ana tambua kwamba raisi wa Marekani ana kuja hapa zaidi ya Balozi wake aliyopo hapa nchini Tanzania na pia ata ingia nchini kwa siri sana. Sasa ni wakati wa mimi kukupa wewe nguvu. Kukufanya kuwa mtu wa koogopewa na mtu unaye heshimika”
“Samani ndugu yangu. Ila Sanga wewe ni nani?”
Raisi Mtenzi ilimbidi kuuliza nabii Sanga kwa maana jinsi anavyo zungumza si jinsi alivyo kuwa naa mchukulia. Nabii Sanga akatabasamu.
“Mimi ni nabii wa bwana na nina nguvu kubwa kuliko nguvu uliyo kuwa nayo wewe. Kuna mambo mengi huyafahamu katika nchi unayo iongoza pamoja na watu wake. Kama hoto jali nina hitaji nikuonyeshe nguvu yangu”
Raisi Mtenzi akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamrudishia nabii Sanga simu yake.
“Sawa nina hitaji kukujua nguvu yako”
“Una fahamu ni nani alihusika na milipuko katika jiji la Dar es Salaam na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu ikiwemo vijana wangu wawili na mke wako?”
“Ha..pana na hadi kesho nina mtafuta huyo mtu?”
“Nahitaji kukuonyesha kama huto jali nina kuomba uweze kuongozana nami nika kuonyeshe”
“Wapi?”
“Hapa hapa nchini. Ila nita hitaji tuondoke sisi wawili na Julieth ata baki hapa na Jery”
“Mmmm sawa, sisi wawili?”
“Ndio kama ina wezekana”
“Ila si una tambua kwamba mimi ni raisi hivyo sipaswi kutembea mimi peke yangu”
“Nina lijua hilio ndugu yangu ila ni sehemu salama na ni sehemu ambayo uta rudi salama kabisa hapa ikulu”
“Sawa”
Raisi Mtenzi akamuita mlinzi wake mkuu na kumueleza juu ya safari hiyo ya watu wawili. Kutokana raisi ndio mwenye maamuzi ya mwisho mkuu huyo hakujibu. Raisi Mtenzi na nabii Sanga wakaingia kwenye helicopter ya nabii Sanga na moja kwa moja wakaeleka katika meli ya nabii Sanga.
“Karibu sana”
Nabii Sanga alizungumza mara baada ya kushuka kwenye meli hiyo. Kila mtu ndani ya meli hiyo akashangaa sana kumuona raisi Mtenzi na raisi Mtenzi naye akashangaa sana kuona ukubwa wa meli hiyo na jinsi iliyo na wanajeshi walio jaiza miili yao. Moja kwa moja wakaingia ofisini kwa nabii Sanga na raisi Mtenzi akasalimia na mrs Sanga.
“Aiisee huku ni mafichoni ehee?”
“Ndio ndugu yangu. Hapa Wamarekani hawawezi kukuua wala kukuuangamiza. Karibu sana”
“Nashukuru”
Wakaka kwenye sofa zilizopo ndnai hapo. Nabii Sanga akamuita mkuu wa kikosi hicho na kumtambulisha kwa raisi Mtenzi.
“Nina hitaji mumuonyeshe raisi nini aliye husika katika ile milipuko ya jiji la Dar es Salaam”
“Sawa mkuu”
Tv kubwa ya ndani hapo ikawashwa na yakaanza kuonekana maelezo yanayo muhusisha mzee Mbogo kwamba yeye ndio aliye kula njama na kundi la Al-Shabab kulipiza kisasi juu ya kushambuliwa kwao. Maelezo hayo yakamstua sana raisi Mtenzi na kujikuta akianza kuvuta kumbukumbu ya jinsi mzee Mbogo alivyo kuwa ana msisitizia kuondoka jijini Dar es Salaama na mzee Mbogo aliondoka na hakuudhuria harusi ya Jery.
“Sasa nina anza kupata picha”
“Ndio na jambo jengine ni hili hapa”
Nabii Sanga akaweka video nyingine ambayo ina sikika sauti za Josephine, Magreth na msichana mwengine jinsi walivyo kuwa wame panga mpango wa kuvuruga send off ya Julieth.
“Hawa mabinti kumbe ni washenzi ehee?”
“Tena sana na wao ndio walihusika katika kutoa matangazo kwenye mtandao kwamba watu wakimbie jiji la Dar es Salaam kwamba siku ya harusi kuta kuwa na milipuko. Walisaidiana na kijana huyu amnaye kama una mkumbuka ana itwa Evans Shika.”
“Nina mkumbuka huyo mshenzi. Aisee kumbe walinizunguka na wana nifanya maboya ehee?”
“Ndio. Nilihitaji kukueleza hili jambo awali ila nikashindwa kufanya hivyo kwa maana nilihofia na kuhisi kwamba nita kuwa nina ingilia maamuzi yako ya serikali yako”
Raisi Mtenzi hasira ikaanza kumtawala, kichwani mwake akaanza kuziona sura za Josephine, mzee Mbogo na Magreth. Akakumbuka ushauri wao ambao walimpatia na kuona kumbe ni wanafki wakubwa sana.
“Sanga nina hitaji kuwaua hawa wajinga kwa mikono yangu mimi mwenyewe. Nina taka kuwateketeza, kuanzia hivi sasa wewe ndio mtu pekee nitakaye kuamini katika hii dunia na nina hitaji vijana wako wanikamatie huyu Mbogo nianze naye kisha hawa panya wawili walio toka kusipo julikana niwaangamize mimi mwenyewe. Tume elewana?”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa amevimba kwa hsira kiasi cha kumfanya nabii Sanga kujawa na tabasamu pana usoni mwake kwani maheshabu ya kete zake sasa yanaanza kufanya kazi taratibu na kama amesha mshawishi raisi Mtenzi na akaaminika basi hakuna mtu yoyote atakaye mtisha juu ya siri zake kuwa hadharani.
“Nime kuelewa mzazi mwengu, ila una hisi kwamba kumuu yeye ndio ita kuwa solution?”
“Ana paswa kufa. Kwa maana yeye ni gaidi na msaliti wa hii nchi ana takiwa kufa”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa jazba kubwa sana.
“Sawa sawa. Je una hitaji hiyo kazi ifanyike lini?”
“Leo, kama ina wezekana ngoja niwapatie code namba ambazo zita weza kuwaonyesha ni wapi alipo makamu wa raisi kwa maana mimi na makamu wangu huwa tuna kifaa ndani ya milii yetu ambacho kita tufanya, endapo tukitekwa au kupotea ni lazima kionyeshe ni wapi tulipo”
“Aisee huo ni utaratibu mpya?”
“Ndio mara baada ya ile milipuko ili bidi tubuni hicho kifaa ambacho hata Josephine ambaye ni chief staff wangu anacho na yeye pia ana takiwa kukamatatwa kwa makosa hayo”
Nabii Sanga akatabasamu kinafki kwa maana game anayo icheza sio ya kitoto. Raisi Mtenzi akawatajia code hiyo na kijana wa maswala ya IT kaiandika katika laptop yake. Haikuwa kazi ngumu kwake kufahamu eneo gani ambalo yupo mzee Mbongo.
“Kwa sasa yupo Kigamboni”
Nabii Sanga akaisogelea laptop ya kijana huyo na kulitazama vizuri eneo hilo na kwa haraka akatambua kwamba eneo hili ni nyumbani kwa Magreth.
“Hapa ni nyumbani kwa Magreth ina maana kwamba mzee Mbogo ana uhusiano mzuri na Magreth?”
Nabii Sanga aliuliza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.
“Sijajua, ila ngoja kama ni muwazi ata weza kuniambia ni sehemu alipo ila kama kuna njama wana ipanga nita fahamu tu”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni na kumpigia mzee Mbogo. Simu ya mzee Mbogo ikaanza kuita, kisha ikapokelewa.
“Habari muheshimiwa raisi”
“Salama. Upo wapi?”
“Nipo nyumbani nime jipumzisha”
“Vipi una umwa?”
“Kidogo uchovu ndugu yangu. Vipi una nihitaji?”
“Hapananilikuwa nina kujulia hali kwa maana hatuja wasiiana leo siku nzima”
“Nashukuru kwa kunikumbuka”
“Sawa”
Raisi Mtenzia akakata simu huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira.
“Unaona una ona anavyo danganya. Ana sema yupo nyumbani kwake ana daganganya”
“Usijali ndugu yangu katika ile nyumba kuna kamera nime zime fugwa hivyo tuna weza kufahamu kama ni kweli yupo ndani au hayupo ndani”
“Etii ehee?”
“Ndio”
Nabii Sanga akamtajia neno la siri linalo weza kuingia katika mfumo wa kamare hizi alizo zifunga nyumbani kwa Magreth ila kwa bahati mbaya akakuta kamera hizi zikiwa zimebadilishwa mfumo wake mzima. Nabii Sanga akawapigia ofisi ambayo alinunua kamera hizo na kuwaomba msaada kama ina wezekana waweza kufungua kamera hizo kwa namna wanavyo weza kwao kwani ana dai amesahau neno la siri.
“Sawa mkuu hakuna shaka tuta fanya hivyo”
Mkurugenzi wa kampuni hiyo alijibu huku akiwa hana wasiwasi kabisa kwani ana tambua fika kwamba nabii Sanga ndio mmiliki wa nyumba hiyo na isitoshe ni mteja wao mzuri kwani hata kamera za siri walizo zifunga nyumbani kwake woa ndio wame husika. Hazikupita dakika mbili nabii Sanga akatumia neno la siri ambalo ndio analo litumia Magreth.
“Ime kubali mkuu”
Kijana wa IT alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Hembu ziweke kwenye tv kubwa”
Kijana huyo akahamishia video hizo zinazo rekodiwa na kamera zilizopo nyumbani kwa Magreth katika tv iliyopo ndani hapo. Wote wakatazmaa jinsi kikao hicho cha siri kinavyo endelea nyumbani kwa Magreth huku kikiwa kime muhusisha mzee Mbogo, Magreth, Josephine na kijana ambaye nabii Sanga na mke wake wana mfahamu vizuri sana.
“Huyo kijana mwengine ni nani?”
Raisi Mtenzi auliuliza.
“Hiyo kijana ni mwizi ambaye alihitaji kunitapeli mimi na familia yangu. Sasa hapa nina anza kupata picha”
Nabii Sanga akamuadisia raisi Mtenzi kila kitu walicho kizungumza na George Sanga. Akamuonyesha video ya wizi wa siri alio ufanya nyumbani kwake.
“Tuna weza kusikia kinacho endelea?”
Raisi Mtenzi alizungumza.
“Ndio”
Kijana huyo akaongeza suati ambayo moja ya kamera iliyopo sebleni hapo ina rekodi na sauti.
“Muheshimiwa. Wewe una kwenda kuapishwa na kuwa makamu wa raisi. Ili tuweze kupambana na hili kundi ni lazima wewe uwe madarakani. Ni lazima raisi Mtenzi umtoe madarakani”
Maneno ya Josephine yalisikika vizuri kwa kila mtu aliyopo ofisini hapo. Raisi Mtenzi akahisi kama moyo wake una kwenda kupasuka kwa hasira. Msuguano wa meno yake anayo yang’ata kwa hasira hakika. Mtu aliye muamini na kumthamini kuliko wafanyakazi wake wote ndio huyo ambaye ana hitaji leo hi yeye atolewe madarakani. Nabii Sanga na mke wake wakatazamana kisha wakaonyezana pasipo raisi Mtenzi kuona chochote kwani umakini wake wote upo katika tv hiyo.
“Tukimpata ita kuwa ni rahisi kwa mimi kumpata Jery ni lazima alipe kwa yale yote aliyo nifanyia yeye na mwanamke wake alafu nabii Sanga na familia yake wata furahi na roho zao.”
Sauti ya George ikamstua sana nabii Sanga na hapo ndipo akatambua kwamba kijana huyo sio Geogre kama wanavyo mfahamu ila ni Evans.
“Shenzi huyu kijana ni yule Evans Shika”
Nabii Sanga naye alizungumza kwa msisitizo na kumfanya raisi Mtenzi na mrs Sanga nao wastukie jambo hilo.
“Sanga tuma jeshi lako kwenda kuwakamata”
“Sawa nina vijana wangu jijini Dar es Salama wana kwenda sasa hivi”
Nabii Sanga akampigia simu mkuu wa kikosi kilichopo jijini Dar es Salaam na kumueleza ahakikishe kwamba ana wana vamia nyumba hiyo na kumchukua kila aliyopo ndani hapo na wana wahitaji wakiwa hai.
***
Kengele ya getini ikamfanya Magreth kutoa simu yake na kuingia upande wa kamera na akamuona ni Samson ndio yupo eneo hilo. Akatoka na kumfungilia mlango, Samson akashangaa kuona gari binafsi la makamu wa raisi pamoja na mlinzi wake namba moja.
“Vipi kwema?”
Samson alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza.
“Tuna kikao kizito ndani huko. Makamu wa raisi yupo”
“Mmmm kwema?”
“Yaa twende”
Wakaingia ndani na Samson akajikuta akistuka mara baada ya kumuona mwanaume aliye muomba namba ya simu na akamdanganya kwamba yeye mwana mitindo. Akasalimiana na watu wote ndani hapo.
“Muna muamini?”
Mzee Mbogo aliuliza.
“Ndio”
Simu ya mzee Mbogo ikaanza kuita kwa mara nyingine. Akaitoa mfukoni mwake na kukuta ni namba ngeni.
“Haloo”
“Baba upo wapi jamani”
“Ceopatra”
“Yes baba, nimesha tua na ndege ya jioni hii nakusubiria hapa Airport mboja huji kunichukua au umesha sahau kama nina kuja”
“Hapana mwanangu siwezi kusahau. Nina kuja sasa hivi”
“Sawa baba”
Mzee Mbogo akakata simu huku uso wake ukiwa na furaha sana.
“Jamani nina toka mara moja nina kwenda Airport. Hakikisheni muna panga mipango yote vizuri tuna elewana”
“Ndio mkuu”
“Nita rudi saa sita usiku”
“Sawa mkuu”
Wakajibu watu wote na mzee Mbogo akatoka ndani hapo. Magreth akawafungulia geti na wakaondoka.
“Muda ambao alinipatia nabii Sanga sasa umebakisha dakika chache kuisha. Ita kuwaje?”
Evans alizungumza mara baada ya kukutana na Magreth nje.
“Una taka kwenda?”
“Ina bidi yule msichana wa watu tuweze kumuokoa Mage”
“Samson ana weza kuwa track na kujua ni wapi alipo. Sasa tufanye jambo moja. Mimi nina jiandaa na wewe jiandae. Tuna ondoka wote, mimi nita endesha pikikipi au wewe uta endesha pikipiki. Josephine na Samson wata tufwatilia sisi”
“Sawa”
Wakaingia ndani na wakuwashirikisha Samson na Josephine juu ya wazo hilo kisha Magreth akaingia ndani na faili hilo na kulihifadhi ndani ya shelf yake ya kuhifadhia pesa. Magreth akavaa makavazi yake ya kazi kisha kwa juu akavaa suruali na tisheti hivyo sio rahisi kwa watu kumtambua alicho kivaa ndani. Mara baada ya kumaliza maandalizi hayo. Magreth na Evans wakapanda pikipiki na kuondoka huku nyuma wakifwata na Samson pamoja na Magreth ambao wapo ndani ya gari la Magreth.
Vijana wa nabii Sanga wakafika nyumbani hapo baada ya dakika kumi na kuingia kwa umakini.
“Mkuu hakuna mtu”
Mkuu wa kikosi hicho alizungumza.
“Ingia ndani kwake tafuteni moja ya faili lililo andikwa top secrety”
Vijana hao wakaendelea kutafuta na kuina shelf hiyo. Wakajaribu kuifungua ila wakashindwa.
“Ibebeni”
Mkuu wao alizungumza na wakaibeba jamaa wawili wenye nguvu zao kwa maana ni kubwa kiasi na ni nzito. Wakaingiza kwenye gari Shelf hiyo na wakatawanyika, katika makundi makuu mawili. Wapo walio elekea Airport kwa maan kupitia simu zao wana ona muelekea anao kwenda makamu wa raisi. Huku wengine wakielekea katika godauni lililopo Tegeta huku wakiwa na shelf hiyo ambayo wamepanga kuifungua ili kutambu ani kitu gani kilichopo ndani.
***
Magreth na wezake wakafika katika nyumba ya siri ambayo Magreth huifadhia silaha zake. Magreth kitu cha kwanza kufanya ni kuingia katika simu yake kwa maana kuna notification aliyo ipata kutokana na camera zake alizo zifunga nyumani kwake. Magreth akaangalia video za kamera zilizo rekodiwa dakika kumi zilizo pita zikionyesha mara baada ya wao kuondoka kundi la wanaume wapata kumi nane waliingia nyumbani kwake huku wakiwa na bunduki. Magreth akastuka sana na kuwaonyesha wezake.
“Hawa ni kina nani?”
Samson aliuliza huku akiwa na wasiwasi.
“Ni watu wa Sanga. Wame fahamu vipi kama sisi tupo pale?”
Josephine aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mwingi sana.
“Hata sifahamu wame tambua vipi”
Magreth alizungumza, kitendo cha Shelf yake kutolewa ndani hapo moja kwa moja ikamfanya kutambua kwamba watu hao wametumwa na nabii Sanga.
“Samson katika shelf yangu kwa ndani kuna trake device ndogo. Passowrd yake ni 126570797569. Ingia sasa hivi tujue ni wapi wanapo elekea.”
Samson akaianza kazi hiyo na hazikupita dakika chache wakatambua ni wapi shelf hiyo inapo pelekwa.
“Ina pelekwa Tegeta”
Magreth akachukua silaha zake huku Evans naye akichukua bastola nne, mbili akazichomeka kiunoni mwake, huku mbili akizichomeka kwenye soksi zake. Wakapanda pikipiki na kuondoka eneo hilo kwa kasi huku wakifwata alama nyekundu inayo onyesha ni wapi shelf hiyo inapo pelekwa.
“Jose naweza kukuuliza”
Samson alizungumza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Ndio niulize”
“Kuna kitu gani kinacho endelea?”
“Nita kuambia baadae mpenzi”
Josephine alizungumza huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana.
***
Gari tatu aina ya Range Rover nyeusi za wanajeshi wa nabii Sanga yakafika katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu J.K Nyerere.
“Ina bidi kuwa makini”
Mkuu wa kikosi hicho aliwaatadharisha vijana wake kwa maana wana tambua uwanjani hapo kuna ulinzi mkubwa tu. Mzee Mbogo akakumbatiana na mwanaye huku akiwa na furaha kubwa sana.
“Baba yangu una zidi kuwa kijana”
“Hahahaa ni mazoezi ndio yana nifanya niwe safi”
Wakasaidina na binti yake kubeba mabegi hayo na kuyaingiza ndani ya gari.
“Peter huyu ni binti yangu ana itwa Cleopatra ana ishi Calfonia Marekani”
“Nashukuru kukufahamu Cleopatra”
“Asante”
“Huyu ni mlinzi wangu namba moja ambae sehemu yoyote ninapo kwenda basi nina kuwa naye”
“Ahaa sawa ila ni very handsome”
Maneno ya Cleopatra yakamfanya Peter kutabasamu. Peter akawasha gari na taratibu wakaanza kuondoka uwanjani hapo.
“Ehee baba, uniambia kwamba ume chaguliwa kuwa makamu wa raisi. Sasa mbona sikuoni ukitembea na walinzi wengi?”
“Hahaa bado sija apishwa. Zime baki siku kama nne niapishwe. So baada ya hapo nita kabidhiwa ofisi pamoa na walinzi wengine”
“Nina hamu sana hiyo siku ikfike ni kuone baba yangu ukiwa makamu wa raisi. Naamini nami nita kuwa na jambo la kujivunia nikiwa Marekani”
Kwa mara kadhaa Peter macho yake ana yatupia katika kioo cha pembeni cha gari hilo kuangalia gari tatu nyeusi aina ya Range Rover zinazo wafwatilia kwa mwendo wa taratibu.
“Mkuu tuna mkia”
Peter alizungumza lugha ambayo mzee Mbogo ana ielewa ila Cleopatra hakuweza kuielewa kwa uharaka. Mzee Mbogo akatazama nyuma na hakuweza kuzitambua gari hizo. Mzee Mbogo akatoa bastola yake huku Peter naye akitoa bastola yake kujianda tayari kwa lolote.
“Baba ni nini kinacho endelea?”
“Tulia mwanangu usijali. Peter una jua nini cha kufanya?”
“Ndio”
Peter akashika kirungu cha gia ya gari hiyo na kuhama kutoa gia namba tano na kuingia namba sita huku mguu wake wa kulia ukikanyaga pedeli iliyo ifanya gari hilo aina ya Toyota VX V8, kuzidi kuongeza mwendo na kuwafanya madereva wa gari hizo tatu za nabii Sanga nao kuanza kuongeza mwendo kuhakikisha kwamba wana lifukuzia gari hilo la mzee Mbogo hadi wana lipata.
**********************************************
“Baba nina ogopa”
Cleopatra alilalama huku machozi yakimlenga mlenga machoni mwake. Mzee Mbogo akatazama gari hizo jinsi zinavyo wafukuzia na moja kwa moja akapata picha ni ishu gani itakayo kuwa ina endelea.
“Chochote kitakacho tokea. Hakikisha una mtafuta binti mmoja ana itwa Magreth na mwengine ana itwa Josephine tume elewana”
“Ndio baba”
Mzee Mbogo akaukaza mkanda wa siti ya binti yake vizuri. Gafla lori lililo tokea barabara ya kushoto likaigonga gari ya mzee Mbogo aneo la ubavuni na kusababisha gari hiyo kuanza kubingirika mara saba mfululizo na ikatulia huku matairi yakiwa juu. Wanajeshi wa nabii Sanga wakasimama karibu na eneo hilo la ajali ambalio tayari watu walisha anza kukusanyika. Wakapiga risasi hewani na kusababisha mashuhuda hao kutawanyika kila mtu akiokoa maisha yake. Wakalisogelea gari la mzee Mbogo na kufungua mlango wa upande wake ulio potendeka pondeka. Wakamchomoa mzee Mbogo anaye vujwa na damu katika paji lake la uso. Wakawatazama dereva na msichana aliyomo ndani ya gari hilo na kuwaona wakiwa wapo kimya na kwa akili za haraka haraka wakatambua kwamba wame kufa na pia hawakuwa na haja nao zaidi ya mzee Mbogo. Wakamuingiza mzee Mbogo ndani ya gari na moja wapo na kuondoka naye kwa mwendo wa kasi eneo hilo. Vijana wa bodaboda walipo katika eneo hilo walipo ona gari hizo zime ondoka kwa haraka wakakimbilia kwenye gari lililo pinduka na kwa kusaidianza wakaanza kumtoa dereva na msichana huyo, jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba Cleopatra alizimia tu kutokana na mstuko na kilicho muumiza ni baadhi ya vioo vilivyo mchana mchana katika mkono wake wa kulia. Hali ya Peter nayo sio nzuri kwani mguu wake wa kushoto ume vunjika mara mbili na kumfanya alie kwa maumivu makali sana. Gari mbili za polisi zika fika eneo hilo na kutoa huduma ya kwanza kuwawahisha hospitalini wagonjwa hao.
***
“Ohoooo Josephine ona”
Samson alizungumza huku akimuonyesha video ya cctv kamera iliyo fungwa kwenye moja ya nguzo za taa za barabarani ikionyesha jinsi gari la mzee Mbogo likigongwa na lori kwa bahati mbaya.
“Mungu wangu!!”
Josephine alihsi kuchanganyikiwa mara baada ya kuona jinsi gari hilli linavyo pinduka kwa mara kadhaa. Kisha wakashuka wanajeshi walio piga risasi hewani na kumtoa mzee Mbogo kwenye gari hilo na kuondoka naye.
“Hao si watu ambao wame walitoka nyumbani?”
“Ndio wenyewe”
Josephine kwa haraka akampigia simu Magreth na Evans wanao elekea eneo la kawe.
“Jamani makamu wa raisi ame tekwa na wanajeshi wa nabii Sanga”
Josephine alizungumza huku akiwa ametawaliwa na wasiwasi ulio changanyikana na woga mwingi sana.
“Ume sema?”
“Makamu wa raisi ametekwa”
“Wapi na nani?”
Ethan aliuliza kwa msisitizo.
“Maeneo ya kutokea Airport ila ametekwa na watu wa nabii Sanga. Jamani fanyeni jambo basi”
Pumzi nzito aliyo ishusha Magreth ilisikika vizuri masikoni mwa Josephine.
“Makamu wa raisi kwa sasa ndio mtu muhimu na anaye paswa kuokolewa.”
“Sasa Josephine muna fahamu ni wapi anapo pelekwa?”
“Samson una tusikia?”
“Ndio nina wasikia vizuri dada Mage”
“Una weza kuzi tracke hizo gari na kujua ni wapi zinapo elekea”
“Ngoja ngoja dakika moja”
Samson alizungumza huku videle vyake vikiminya batani ya laptop yake kwa kasi ya ajabu sana huku akihakikisha kwamba ana hack kamera zote za barabara za jiji la Dar es Salaam.
“Zime potea hizi gari”
Samson alizungumza huku macho yakiwa yame mtoka kwa maana kila akijaribu kufwatilia ni wapi gari hizo zina elekea, anashindwa.
“So tuna fanyaje Samson?”
Josephine aliuliza huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana.
“Ila Magreth wewe si una maono. Muombe basi Mungu akusaidie”
Magreth alishauri kwa njia ya simu hapo ndipo Magreth akapata wazo hilo. Akafumba macho yake na kuanza kumuomba Mungu. Samson akaanza kumtazama jinsi Josephine anavyo tetemeka mikono yake hadi mwili mzima ukaanza kutetemeka na gafla akaanguka chini na kuzimia.
“Josephine Josephine”
Samson aliita huku akiacha kufanya kazi yake na kuanza kumtingisha Josephine amabye ame tulia kimya.
“Samson kuna nini?”
“Jose amezimia”
“Ohoooo”
Ethan alistuka kwa maana hajawahi kusikia jambo kama hilo kwa Josephine.
“Sasa nisikilize Samson, achana na Magreth kwa sasa hakikisha kwamba una tafuta hizo gari tujue ni wapi alipo makamu wa raisi”
“Sawa”
“Ndani ya gari alikuwa na nani?”
“Alikuwa na dereva na binti yake”
“Wamepona?”
“Nime ona gari za mbili za polisi zikiwaondoka eneo la tukio. Sasa sifahamu ni wapi walipo pelekwa”
“Mpigie simu RPC Karata”
“Alafu nina muambia nini?”
“Kwani huoni lililo tokea Samson, mbona una maswali ya ajabu”
Magreth alizungumza kwa kufoka kwa maana hapo alipo amesha changanyikiwa kwani hajui ni wapi aende kwani kwenda Kawe ana hitaji na kumtafuta makamu wa raisi pia ana hitaji.
“Habari muheshimiwa. Mimi nina itwa Samson ni IT Meneja wa Ikulu, hadi ninavyo zungumza sasa hivi makamu wa raisi ameweza kutekwa na watu wasio julikana na vijana wako wame weza kumchukua dereva wa gari ya makamu wa raisi pamoja na binti yake. Hivyo nina hitaji kufahamu ni hospitali gani wame pelekwa”
“Ohoo Mugu wagu ngoja nina kupigia”
“Nina kuomba taarifa hiyo umpatie Magreth kwa maana hivi sasa yupo sehemu ana hitaji kufwatilia ni wapi alipo pelekewa makamu wa raisi”
“Sawa nita mpigia baada ya dakika chache”
“Asante”
Samson akakata simu huku akimtazam Josephine ambaye bado hajazinduka. Samson angaangaza angaza sebleni hapo na moja kwa moja akaelekea jikoni. Akamimina maji ya baridi kwenye glasi na kurudi sebleni na kumwagia Josephine usoni mwake na kumfanya azinduke huku akikurupuka mithili ya mtu anaye ogopa jambo fulani.
“Hei hei hei ni mimi”
Samson alizungumza huku akimshika Josephine mikono yake. Wakatazamana na Samson usoni mwake, kisha kwa haraka Josephine akamkumbatia Samson na kuanza kuangua kilio kizito sana.
“Jose una lia nini?”
“Makamu wa raisi ana uwawa”
“Nini?”
“Ndio ana uwawa na wapigie Magreth na Ethan warudi kwa maana kuna vita kubwa ina kuja juu yetu sisi wanne”
Samson hakuhitaji kupoteza muda akwapigia Magreth na Ethan na kuwapa habari hiyo ambayo nao walitishika. Samson akawasisitizia kwamba warudi kwani mambo yamesha haribika.
“Poa tuna rudi”
Magreth alizungumza na wakageuza pikipiki na kurudi katika nyumba hiyo ya siri.
***
Gari hizo za wanajeshi wa nabii Sanga zikasimama katika maegesho ya magari yaliyopo chini ya ardhi katika moja ya gorofa la nabii Sanga, ambalo lina gorofa thelathini na ame likodisha kwa makampuni mbalimbali. Wakapanda na makamu wa raisi hadi juu kabisa ya gorofa hilo. Wakaingia kwenye helicopter na kuianza safari ya kuelekea katika meli ya nabii Sanga iliyopo katikati ya bahari mashariki mwa bara la Afrika. Wakafika eneo hilo na kupokelewa na nabii Sanga aliye waelekeza wampeleke mzee Mbogo moja kwa moja kwenye chumba cha kupumzikia ambacho ndani yake kina kitanda na kina ukuta mmoja ambao ni wa kioo. Kwa mtu aliyopo nje ana weza kuona kilichopo ndani ila aliyopo ndani ya chumba hicho hawezi kuona kinacho endelea nje.
“Kazi ime kamilika ndugu yangu nini tufanye”
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.
“Nina hitaji kumuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.
“Ila bado haja zinduka, inge kuwa vizuri akaaona kwamba ana kufa kwa ajili ya kitu gani”
“Mchomeni sindano ya kumzindua”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo na agizo hilo likatimika. Mzee Mbogo akachomwa sindano ya kuzinduka na kweli, akazinduka katoka katika hali ya kuzimia.
“Nipo wapi hapa?”
Mzee Mbogo alimuuliza mwanajeshi aliye mchoma sindano hiyo.
“Upo kuzimu”
“Wewe ni nani na ume tolea wapi jeuri ya kunijibu mimi hivyo?”
Mzee Mbogo alizungumza kwa ukali ika akashindwa kufanya chochote kwa maana mkono wake wa kulia ume fungwa pingu iliyo unganishwa na kitanda hicho cha chuma. Mwanajeshi huyo akatoka na kumpa taarifa nabii Sanga kwamba tayari amesha zinduka.
“Niwekeeni hayo mazungumzo yao ya usaliti na nina omba bastola iliyo jaa risasi”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa kujiamini na vijana wa nabii Sanga wakateleza agizo hilo. Nabii Sanga, mke wake pamoja na raisi Mtenzi wakaelekea katika chumba hicho ila akaingia raisi Mtenzi peke yake na kumfanya bwana Mbogo kustuka sana.
Nabii Sanga akawaanda vijana wake wawili waweze kurekodi kila kitu kinacho tokea ndani ya chumba hicho pasipo raisi Mtenzi mwenyewe kujijua.
“Mtenzi nipo wapi hapa na kwa nini ume nishikilia”
“Pumbauvu wewe. Msaliti mkubwa sana. Yaani una taka kunitoa madarakani mimi”
“Mbona sijui una zungumza nini ndugu yangu”
“Ogoo hujui nini nana zungumza ikiwa ulikaa na wale malaya zako na kupanga kunitoa madarakani mimi kweli. Yaani bado sijakutangaza wala kukuapisha alafu una niletea ujinga”
Raisi Mtenzi alifoka, akawasha ipad na kumuonyesha mzee Mbogo mazungumzo yaliyo rekodiwa nyumbani kwa Magreth. Mzee Mbogo akastuka sana na kushindwa kutambua kwamba mazungumzo hayo yame rekodiwa vipi.
“Huyu si wewe, huyu si chief staff, huyu si Ethan na huyu si Magreth. Kumbe mulikuwa ni wema kwangu alafu muna nizunguka na huyu fala ana taka kumuua mwanangu. Sasa nisikilize wasaliti siku zote hawana nafasi kwenye maisha yangu au serikali yangu”
Raisi Mtenzi alifoka huku akiikoko bastola yake.
“Mtenzi usinuue kwanza. Acha nikueleze ukweli”
“Ukweli gani mbwa wewe. Nilikupigia simu uka sema kwamba upo kwako ume pumzika. Hapo ni kwako eheee. Sasa uta anza kufa wewe alafu hao watu watatu nita wasaka hadi niweze kuwapata nao pia wata kufwata huko ulipo. Shenzi wewe”
“Ndugu yangu tume toka mbali usi……….”
Mzee Mbogo hakupata nafasi ya kumalizia sentensi yake hiyo kwani tayari raisi Mtenzi alisha fyatua risasi moja iliyo penya kifuani mwa mzee Mbogo na kumfanya macho yamtoke. Akamtazama Mtenzi, rafiki yake wa kipindi kirefu, aliye msaidia kwenye mambo mengi sana hususasni nafasi ya kuingia madarakani na kuwa raisi wa nchi ya Tanzania.
“Chinas Mtenzi kweli una niua ndugu yangu”
Mzee Mbogo alijikaza kuzungumza kwa uchungu huku damu zikimtoka mdomoni mwake na machozi yakimwagika machoni mwake.
“Msaliti siku zote ana paswa kufa. Kama mwanangu alikufa kwa ajili ya usaliti wake basi hata wewe ni lazima ufee”
Raisi Mtenzi akaachia risasi nyingine sita mfululizo na kikampiga mzee Mbogo maeneo mbalimbali ya mwilini mwake na kumfanya apoteza maisha kitandani hapo huku damu nyingi zikitapakaa katika shuka la kitanda hicho. Nabii Sanga akawaonyesha ishara vijana wake kuondoka eneo hilo kwa maada muda wowote raisi Mtenzi ata toka ndani hapo. Raisi Mtenzi akausogelea mwili wa mzee Mbogo akakusanya mate mengi na akamtemea usoni mwake kisha akatoka ndani hapo huku akitetemeka kwa hasira. Nabii Sanga wakatazama na mke wake kisha wakatabasamu sana. Wakarudi ofisini kwa nabii Sanga na raisi Mtenzi akaa kwenye moja ya sofa huku akivua tai yake.
“Nahitaji mwili wake ufungwe chuma kizito na utupwe baharini nikishuhudia”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo.
“Sawa ndugu yangu”
Vijana wa nabii Sanga waka wakatoa mwili wa mzee Mbogo, wakamvua nguo zake zote na akabakiwa na boksa. Kisha wakamfunga chuma chenye uzito wa kilo themanini, wakaikaza vizuri minyoro katika mwili wa mzee Mbogo kisha nabii Sanga, mke wake pamoja na raisi Mtenzi wakatoka hadi eneo ulipo mwili huo na raisi Mtenzi akatoa ishara ya mwili huo kutupwa ndani ya maji na wanajeshi hao wakatii agizo hilo.
“Sasa ni panya watatu ndio walio salia. Kama huyu panya buku amesha kufa, basi hao panya watatu ni rahisi sana kuwapata”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
“Ni kweli ndugu yangu ila kuna yule binti Josephine ana maono makali sana.?”
“Maono yake ni kwa mambo yajayo. Ila hawawezi kupambana na dola. Sasa nirudisheni ikulu, nika dili na hao panya watatu. Ila nina shukuru sana Sanga. Mungu azidi kukuongezea miaka mingi sana ya kuishi kwa maana inge kuwa sio wewe, mimi ninge endelea kula nao meza moja hawa wajinga kumbe wange endelea kunisomea ramani na mwisho wa siku wangenitoa madarakani
“Ndio hivyo ndugu yangu ndio maana binti yangu alipo ona mambo yana fikia pabaya akaona ni heri aniambie kwa maana yeye ana ogopa kuzungumza ukweli”
“Yaani kuanzia sasa hivi wewe, mke wako na familia yako ndio watu nitakao kuwa nina waamini”
“Nashukuru sana kwa hilo”
Raisi Mtenzi akamtazama mrs Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama nabii Sanga.
“Nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Nanahitaji nikirudi ikulu muda huu niwatangazie wananchi kuwa mke wako ni makamu wa raisi. Hiyo nafasi shemeji si una iweza?”
Mrs Sanga na mumewe wakapatwa na mshangao wa karne. Mrs Sanga akabaki akitabasamu pasipo kujibu swali hilo.
“Au shemeji una onaje. Kwa maana muna jeshi muna watu wenye nguvu. Nyinyi ndio mutakao kuwa muna nilinda mimi na mwanangu Jery. Watu nilio wapa nafasi na moyo wangu ndio hawa kina Mbogo wameishia kuniumiza tu”
“Nina imani mke wangu ni mkakamavu ana uwezo na ata weza kukusaidia nami nita kuwa nanyi bega kwa bega katika jambo hilo”
“Jiandae kesho nita kuapiasha uwe makamu wa raisi wa Tanzania. Ndio maana nilikuwa nina pata wakati mgumu kumuapisha Mbogo kumbe ni msaliti wa nchi. Pumbavu sana”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa furaha. Wakaagana na nabii Sanga na mke wake kisha raisi Mtenzi akaingia kwenye helicopter na kurudi ikulu. Nabii Sanga na mke wake wakakumbatiana kwa furaha kubwa sana kwani yeye na familia yake wana zidi kupata nguvu katika serkali ya nchi ya Tanzania.
“Mkuu kazi ime kamilika”
Kijana mmoja wa nabii Sanga alizungumza huku akimkabidhi faili lenye siri zake na familia yake ambazo ni chafu kupindukia. Nabii Sanga akalitazama faili hilo kisha akalipokea.
“Mume lipataje?”
“Tulichukua shelf yake yule binti. Tuka ifungua na kutoa hilo fail na kwa bahati mbaya tulikuta track device hivyo tuliivunja na ika tulazimu tuje na yule mwanamke tuliye mkamata na yupo ndani ya hii meli”
Nabii Sanga kusikia uwepo wa Leila kuwepo ndani ya meli hiyo, akajawa na furaha ndani ya moyo wake kwani alimtamani mwanamke huyo aweze kumpata kimapenzi na sasa ame kuja kiulaini na isitoshe siku ambazo mke wake ata kuwa ana fanya kazi ikulu kama makamu wa raisi basi Leila ata kuwa ndio mwanamke atakaye rithi nafasi ya mrs Sanga.
“Huyo mwanamke ni bora muka muua”
Kauli ya mrs Sanga ikamstua kila mtu akiwemo nabii Sanga mwenyewe.
“Ndio ina paswa auwawe sihitaji kumuona ndani ya hii meli”
Mrs Sanga alizungumza kwa msisitizo huku wivu ukiwa ume mtawala ndani ya moyo wake.
“Mke wangu sasa hivi ni muda wa wewe kujiandaa kuwa makamu wa raisi mambo ya huyo mwanamke achana nayo. Ume nielewa”
Nabii Sanga alizungumza huku akimshika mkono mke wake na wakarudi ofisini.
“Uta fanya nini mara baada ya kutangazwa kuwa makamu wa raisi?”
Nabii Sanga aliingiza mada ambayo anafahamu ita mtoa mke wake kwenye swala zima la kumuwazia Leila.
“Mmmm una jua ime kuja kama suprize. Yaani sijui hata nita fanya nini?”
“Hadi sasa hivi tuna ufahamu udhaifu wa Mtenzi. Kwa tukio zima la kumuua mzee Mbogo. Hivyo ni muda wa wewe kuipa familia yetu nguvu. Una paswa kuhakikisha kwamba katika miaka mitatu iliyo salia ya raisi Mtenzi una unda mamlaka kuhakikisha kwamba tuna fikia malengo yetu.”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama mke wake.
“Sawa mume wangu nime kuelewa”
“Kumbuka, tuna hitaji ile hadhina ambayo tuna isikia. Mshawishi raisi kuhakikisha kwamba tuna ipata”
“Raisi wa Marekani ana kuja kuonana na wewe. Uta kubaliana naye nini?”
Nabii Sanga akashusha pumzi taratibu huku akimtazama mke wake.
“Nchi ipo mikononi mwetu sasa hivi. Nita jua amekujaje kujaje, akija kwa kiburi basi nina malizana naye kwa kiburi na akija kwa amani basi nina malizana naye kwa amani”
Nabii Sanga alizungumza kwa furaha kwani ana amini sana mambo yana kwenda kumnyookea.
***
Raisi Mtenzi kitu cha kwanza kufanya mara baada ya kurudi ikulu, akakutana na Julieth pamoja na Jery. Raisi Mtenzi akawatazama mkwe wake na mwanaye na akahisi hakuna amani iliyopo kati yao.
“Baba tuna kusikiliza”
Julieth alizungumza mara baada ya ukimya wa kama dakika tatu kutawala katika seble hiyo. Raisi Mtenzi akatoa flash na kumkabidhi Jery.
“Ichomeke kwenye tv”
Jery akaipokea flash hiyo na kuichomeka nyuma ya tv huku akionyesha akiwa ame nuna. Julieth na Jery wakastuka sana mazungumzo ya mzee Mbogo, Josephine, Magreth na George Sanga. Sauti halisi ya George Sanga ikamstua kidogo Jery.
“Huyu ana taka kuniua mimi?”
Jery aliuliza kwa ukali kidogo.
“Ndio”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama Jery kw amacho makali sana.Julieth akaka kimya kwa maana sauti hiyo ana ifahamu vizuri sana.
“Huyo kijana ni Ethan Shika, uliye mteka kwa ajili ya mke wako na amerudi katika sura ya tofauti na ana hitaji kukuua. Watu wote nilio kuwa nime wawekea imani na mapenzi mengi. Wame nisaliti”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa upole huku akimtazama Jery na Julieth.
“Nyinyi watu wawili muliopo hapo ndio watu ninao waamini. Tukilegea sote tuna anguka, maadui zetu tuliwapa nafasi ya kuwa nasi. Wametupeleleza vya kutosha na sasa wana panga kutuangusha”
“Sasa baba nini tuta fanuya?”
Jery aliuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana kwani kwa kipindi kirefu sasa hakutarajia kuona kama Ethan ata rudi.
“Sisi ni familia moja. Shukrani sana kwa baba yako mkwe kwa kusweza kutusaidia kufahamu siri kama hizi kwa maana tunge jikuta siku tuna tolewa hapa ikulu kabla ya muda kufika.”
“Baba hawa watu wana paswa kufa”
Jery alizungumza kwa ukali sana.
“Julieth una maoni gani katika hili?”
“Baba kutokana wame amua kutusaliti ina bidi tuwa wahi kabla ya wao kutu wahi”
“Nime mchagua mama yenu kuwa makamu wa raisi na kesho nita Mtangaza katika vyombo vya habari”
Julieth na Jery wakastuka kwa maana hiyo habari hawakuwa nayo kabisa.
“Mama yangu?”
Julieth aliuliza kwa mshangao.
“Ndio kwa maana nina imani ata kuwa ni msaada mkubwa sana kwangu kupambana na maadui zangu. Nlimuambini mzee Mbogo kwa miaka zaidi ta thelathini na tisa sasa. Ila mwisho wa siku ana panga kunitoa madarakani. Nini kibaya nime kifanya kwenye hii nchi.”
Raisi Mtenzi alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Jery na Julieth wakatazamana huku kila mmoja akimuonea huruma raisi Mtenzi.
“Kipindi changu chote cha maisha yangu nime kuwa ni mtu wa kuipigania hii nchi. Nimejitoa hadi mke wangu mwanangu wakafariki kwa ajili ya hii nchi. Alafu leo mtu mmoja mpumbavu mpumbavu ana ungana na watu wapumbavu wapumbavu ambao niliwatoa huko vichakani hadi kuingia ikulu alafu wana hitaji kuniondoa mimi ikulu, wana taka kumuua mwanangu. Siwezi kuliruhusu hili kutokea kwenye maisha yangu”
“Baba”
Jery aliita kwa sauti ya upole huku akimtazama baba yake usoni.
“Ndio”
“Samahani sana kwa kila jambo lililo tokea. Sasa nina elewa ni kwa nini ume kuwa ni mkali kwenye kila jambo baya ninalo lifanya”
Jery alizungumza kwa upole sana na unyenyekevu mkubwa sana kiasi cha kumfanya raisi Mtenzi kujihisi amani moyoni mwake.
“Nita kuwa nawe bega kwa bega kwenye kila hili jambo kwa maana wewe ndio ndugu wa pekee uliye salia katika maisha yangu”
Maneno ya Jery yakamsisimua sana raisi Mtenzi na kumfanya anyanyuke na wakakumbatiana na mwanaye huku machozi yakiwamwagika usoni mwake. Taratibu Julieth akasimama na kuwakumbatia kwa pamoja baada ya dakika mbili wakaachiana.
“Baba nini una hitaji kufanya kwa ajili ya hawa wasaliti?”
“Nina hitaji wote waweze kukamatwa na kuanzia hivi sasa hivi wata kuwa ni wasaliti wa hii nchi. Tume elewana?”
“Ndio baba”
“Julieth mpigie simu mr the Brain nahitaji kukutana na wakuu wote wa majeshi pamoja wakuu wa usalama usiku huu”
“Sawa baba”
Julieth akaanza kushuhulikia hilo, kutokana ni mshauri wa raisi hivyo ana namba zote za wakuu wa vitengo vya usalama. Mtu wa kwanza kufika ikulu ni mr the Brain ambaye moja kwa moja wakakutana na raisi Mtenzi ofisini kwake.
“Ndugu yangu kuna nini mbona mkutano wa galfa”
Raisi Mtenzi akamjibu mr the Brain kwa kuwasha tv yake na kumuwekea mazungumzo ya siri ambayo yalikuwa yakipangwa na mzee Mbogo, Josephine, Magreth na Ethan. Mr the Brain akajikuta akistuka sana kwa maana mipango inayo zungumziwa hapo ni ya kumpindua raisi Mtenzi.
“Ohoo Mbogo ana fanya kitu gani aisee?”
Mr the Brain alizungumza huku akiwa ana shangaa sana.
“Ndio hali ya mtu ambaye nilimchagua kuwa makamu wangu wa raisi ila akaamua kuingiwa na tamaa kabla hata ya kuapishwa ana mawazo ya kunipindua”
“Hili ni kosa kubwa sana Mbogo ana fanya”
“Una jua adhabu ya msaliti wa nchi”
“Ndio ila ina bidi tumtafute kwanza Mbogo na kumuuliza ni kwa nini ana fanya hivi”
“Msaliti una hisi ana weza kuja na kutueleza ni kwa nini anahitaji kutusaliti. Hawa ni watu wa kuwakamata na kuwa funga na hawa ndio nina imani wana vujisha siri za nchi”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka na kumfanya mr the Brain kukaa kimya.
“So una hitaji wakamatwe”
“Ni wasaliti wa nchi na wana paswa kushuhulikiwa kikamilifu”
“Sawa tume kuelewa mkuu.”
Julieth akaingia ofisini hapo na akamsalimia mr the Brain.
“Muheshimiwa wakuu wote wamesha fika”
“Sawa”
Wakatoka ofisini hapo na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano. Wakuu wote wa vitengo vya usalama wakasimama huku kikao hicho kikifwatiliwa na wakuu wa mikoa wote kwa njia ya video call.
“Kaeni”
Raisi Mtenzi alizungumza na watu wote wakakaa na kikao hicho cha dharura kikaanza.
“Nchi ina wasaliti”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwatazama viongozi hao.
“Wasaliti ni wale watu ambao niliwapa nafasi ya kuwaamini na kuwa karibu yangu huku wengine wakutumia nafasi ya kidini kwa kuona maono ila mwisho wa siku wana hitaji kuichukua hii nafasi”
Watu wote wakaka kimya huku wakimtazama raisi Mtenzi kwa maana hakuna anaye jua ni nani msaliti.
“Haijalishi wewe ni nani, uwe ni mtu wangu wa karibu, uwe ni ndugu yangu au uwe ni nani, ila utakapo isaliti nchi hii ni lazima ufe. Hakuna mtu aliyopo juu ya sheria”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo na kuwafanya watu kuanza kujistukia na kutazamana kwenye nyuso zao kwa manaa hakuna hata siku moja ambayo raisi Mtenzi aliitisha kikoa kama hicho. Raisi Mtenzi akampa ishara Julieth ya kuchomeka flash kwenye tv kubwa iliyopo ofosini hapo. Baada ya kuichomeka raisi Mtenzi akawasha tv hiyo na wakaanza kufwatilia kikao hicho cha siri kilicho ongozwa na mzee Mbogo. Kila mtu aliye yasikia maneno hayo alistuka snaa na hata RPC Karata naye alijihisi kuchanganyikiwa kw amaana watu hao watatu ana wafahamu vizuri sana kasoro huyo mmoja ambaye hawajui ni nani.
“Huyo wa pili hapo ana itwa Ethana Sanga na ni miongoni mwa watu tunao watafuta. Sasa nina hitaji kuanzia hivi sasa upelelezi wa umakini sana uweze kufanyika. Nina hitaji wakamatwe mmoja baada ya mwnegine. Mzee Mbogo naye pia akamatwe”
Raisi Mtenzi hakutaka kuweka bayana kwamba tayari amesha muua mzee Mbogo kwa maana japo ni raisi wa nchi ila hana mamlaka ya kumuua mtu na akifanya jambo hilo ni lazima na yeye ata chukuliwa hatua za kijesheria.
“Nina hitaji picha za hao wasaliti wa nchi baada ya hichi kikao zitangazwe nchi nzima kuhakikisha kwamba wana patikana”
“Ahaa samahani muheshimiwa”
Jenerali wa jeshi alizungumza.
“Ndio”
“Nina ona sio jambo la busara sana kuwaweka kwenye vyombo vya habari. Kutokana tumesha wajua, basi hizi picha zita samba katika vyombo vyetu vya uslama ana tuta wakamata wote. Tukumbuke adui akisha jua kwamba ana fwatilia ni lazima naye ata kuwa na mipango yake ya kujiepusha na mikono ya vyombo vya usalama.”
Jenerali wa jeshia alizungumza na kumfanya raisi Mtenzi kukubaliana na pointi yake hiyo.
“Kesho nina kwenda kumtangaza makamu wangu mpya wa raisi kwa maana nchi sasa ina hitaji nguvu kuhakikisha tuna pambana na hawa maadui ambao kwa asilimia mia moja nina waamini. Tume elewana”
“Ndio muheshimiwa”
“Samahanii muheshimiwa tuna weza kumfahamu makamu mpya wa raisi”
“Muta mfahamu kesho nitakapo mtagaza na haraka iwezekanavyo nita muapisha. Kikao kime isha na kazi ya kuwasaka hao mabedui ianze haraka iwezekanavyo”
Mara baada ya kuzungumza hivyo raisi Mtenzi akatoka na picha hizo zikaingizwa kwa wakuu wote hao walio udhuria kikao hicho. RPC Karata akaondoka ikulu huku akiwa na mawazo mengi sana. Akafikiria jinsi Magreth na Julieth walivyo jitahidi kumuokoa raisi Mtenzi kipindi alipo taka kuuwawa akiwa yupo kitandani na makamu wa raisi aliye pita bwana Madenge Jr. Akashindwa kupata jibu la uhakika.
“Mkuu mbona una mawazo sana”
Mlinzi wake alimuuliza huku akiendesha gari hilo.
“Yaani hii nchi ina mamo mengi sana”
“Mambo gani mkuu”
“Una mkumbuka yule binti aliye tusisitiza kipindi kile tuondoke hapa Dar es Salaam na kuziahamisha familia zetu na kutuambia kuna mabomu yata lipuka?”
“Ndio nina mkumbuk avizuri na siwezi kuacha kumsahau na pia nina mshukuru kwa maana laiti ingekuwa sio hivyo familia yangu inge teketea”
Mlinzi huyo alizungumza.
“Sasa wana tuhumiwa kwa kupanga njama za kumpindua raisi Mtenzi madarakani”
Mlinzi huyo akastuka sana.
“Nini?”
“Ndio na video ninayo hii hapa. Simamisha gari uitazame”
RPC Karata kutokana ana muamini sana kijana wake na ndio msiri wake namba moja, akaona hakuna haja ya kumficha na alicho kifanya ni kusimamisha gari pembeni na akaipoke simu hiyo na kutazama mazungumzo hayo ambayo naye pia akajikuta akistuka sana.
“Kama walimuokoa raisi kipindi kile ni kwa nini wana hitaji kumpindua?”
“Hata sielewi. Sasa nina hitaji kuonana nao kwa siri sana kwa maana nina muamini sana Magreth.”
“Ila mkuu ni hatari”
“Nalitambua ila nina hitaji kukutana naye. Tena ngoja nimpigie simu kwa namba yangu private”
RPC Karaka akatoa simu yake ya ziada na kumpigia simu Magreth na kwa bahati nzuri simu hiyo ya Magreth ikaanza kuita.
***
Mlio wa simu ya Magreth ukawastua watu wote walipo sebleni huku kila mmoja akionekana akiwa amejawa na mawazo mengi sana kwani kitu alicho waeleza Josephine hakika kime wastua. Magreth akaitazama namba yake na kukuta ni namba iliyo andikwa privete.
“Vipi mbona hupokei?”
Ethena aliuliza.
“Ni private namba”
“Pokea ujue ni nani”
Magreth akawatazama Samson na Julieth ambao wote nao wana mtazama yeye. Akaipokea simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Ni mimi”
Sauti ya RPC Karata kidogo ikamfanya aishiwe na wasiwasi kwa maana ana mfahamu askari huyo kwani alimsaidia kwenye mambo mengi sana kipindi cha nyuma.
“Ndio kaka”
“Nina hitaji kukutana na wewe upo wapi?”
Magreth akajifikiria kwa dakika kadhaa kujibu swali hilo kwa maana kama jinsi Josephine alivyo waambia kwamba wa sasa wapo kwenye kipindi kigumu hivyo ni lazima awe makini sana.
“Mbona una uliza hivyo kaka na kwa nini ume nipigia kwa private namba na hujapiga kwa namba yako ya kawaida”
“Magreth mupo matatizoni. Nina jua una niamini niambie ni wapi ulipo nije kuonana na wewe kwa maana nahitaji kujua kwa hili linalo endelea”
“Jambo gani kaka?”
“Sio la kuzungumzia kwenye simu niambie upo wapi nije?”
Josephine akampa ishara ya kumruhusu kwa maana ukimya ulipo ndani hapo waliweza kuyasikia mazungumzo hayo japo Magreth ame iweka simu yake sikioni mwake. Magreth akamuelekea sehemu alipo na RPC Karata akaahidi baada ya dakika ishirini ata kwua eneo hilo.
Kama jinsi alivyo ahidi RPC Karata, akafika nyumbani hapo na kijana wake ila wakitumia gari ya siri ambayo ni mali ya RPC Karata. Wakasalimiana naye pamoja na kijana wake huyo. RPC Karata akazitazama nyoso za watu wote walimo ndani hapo na ni Samson pekee tu ndio hayupo kwenye video hiyo.
“Kaka ni nini kime kufanya uonena na mimi muda huu”
“Nina hitaji kufahamu ukweli”
“Ukweli gani?”
Magreth aliuliza kwa sauti ya upole sana.
“Je muna njama ya kumpindua raisi Mtenzi madarakani?”
Josephine, Magreth, Ethana na Samson waka stuka sana hususani Samson ndio akastuka kwa maana hajashirikishwa mazungumzo ya nyuma na alifika mwishoni kabisa wa mazungumzo hayo.
“Nani ame kuambie hilo japo kaka?”
Josephine aliuliza kwa mshangao. RPC Karata akatoa simu yake na kuiweka video hiyo na kuwaonyesha watu wote mazungumzo walio kuwa wana yafanya nyumbani kwa Magreth. Hapo ndipo hofu kubwa ikawatawala kwa maana waliamini kwamba mazungumzo hayo wanayafanya kwa siri sana huku Magreth akiamini kwamba ni yeye wa pekee tu ndio anaye fahamu neno la siri la kamera za nyumbani kwake hapo. Baada ya video hiyo kuisha RPC Karata akashukua simu yake na kuirudisha mfukoni mwake, akakunja nne huku akitazama nyuso zao zilizo jaa hofu na mashaka makubwa sana.
“Hii video ipo mikononi mwa raisi Mtenzi na ime tolewa oder nchi nzima ya nyinyi kutafutwa na kukamatwa na mzee Mbogo ambaye hadi sasa hivi sijui yupo wapi. Magreth nilikuamini sana tena sana kuliko hata ninavyo muamini mke wangu. Nina taka kufahamu ni kwa nini muna mpango wa kumtoa madarakani raisi Mtenzi?”
RPC Karata alizungumza kwa ukali ulio mfanya Magreth kutetemeka sana huku akihisi haja ndogo ina kwenda kumwagika kwani masihara masihara sasa yame kuwa ni jambo linalo weza kuwapelekea wakauwawa kikatili sana.
Magreth akatamani kuzungumza jambo ila kutokana na hofu na woga ulio mkamata akajikuta akishindwa kabisa kuzungumza ukali.
“Raisi hastahili kukaa katika sehemu ambayo ame kaa kwa sasa”
Josephine alijitahidi kujibu.
“Ohoo una hisi wewe ndio ume muingiza madarakani na kuamua ni muda gani ambapo raisi ana paswa kutoka madarakani si ndio?”
RPC Karata alizungumza kwa msisitizo huku akimkazia macho Josephine.
“Raisi ame fanya matukio mengi mabaya. Matukio ya mauaji, ana tumia madaraka yake vibaya. Watu wengi wame weza kupoteza maisha kwa ajili yake na familia ya Sanga”
Josephine aliendelea kujitetea.
“Hivi unacho kizungumza una kielewa wewe binti. Hii ni nchi na sio mtaaa na huyo munaye mzungumzia hapo sio mwenyekiti wa nyumba kumi. Huyu ni raisi wa nchi ya Tanzania na ana watu zaidi ya milioni hamsini. Muna jua nini juu ya kuongoza nchi. Muna hisi bila kuua nchi ina weza kuwa na amani. Wewe unaye ongozwa na Mungu, omba na muulize Mungu wako ni kwa nini wafalme wake wa za maani walikuwa wana ua maelfu ya watu kwa ajili ya nchi zao. Ila nchi iende na iwe katika usalama wa nyinyi kukaa na kujadili mambo ya kipumbavu kama haya ni lazima watu wafe.”
RPC Karata alizidi kuzungumza kwa kufoka kiasi cha kuwatia hofu watu wote waliomo ndani hapo.
“Ona sasa upuuzi munao uletea ndani ya nchi. Hembu zungumzeni kitu ambacho kina weza kunishawishi na kuwaelewa kama ni poiti zenu hizi za kipumbavu kama hafai au muna visa binafsi kama wewe mpumbavu hapo unaye taka kumuua Jery, musiingize nchi katika hili kwa maana hamjui nini maana ya nchi”
Maneno ya RPC Karata dhahiri yana onyesha ni jinsi gani alivyo kasirishwa na jambo hilo.
“Mkuu nina kuomba nizungumze jambo”
“Ndio nina wasilikiliza na sio muna omba tu”
Samson taratibu aka play video ya jinsi gari la mzee Mbogo lilivyo gongwa na lori na kupinduka mara kadhaa. RPC Karata na kijana wake wakaitazama video hiyo.
“Nina imani uliweza kupatia taarifa kwamba mzee Mbogo ametekwa na hao walio mteka kwa ujuzi wake je una hisi kwamba ni wana jeshi wa nchi hii ya Tanzania?”
RPC Karata wakatazamana na kijana wake.
“Hapana”
“Hao ni wanajeshi wanao milikiwa na nabii Sanga pamoja na familia yake.”
Samson akaanza kuelezea jinsi ushahidi wa matukio aliyo weza kuyaona kwenye faili ambalo walikuwa wakilijadili. Hadi ana maliza kumuelezea RPC Karata hasira yake ikwa ime mtulia na kuamini japo sio kwa asilimia mia moja.
“Hilo faili lipo wapi?”
Samson akaonyesha video nyingine jinsi watu hao walivyo kwua wana vamia nyumbani kwa Magreth na kuondoka na shelf ambayo ndio ilihifadhia faili hilo.
“Hatuna ushahidi wa faili kwa sasa ila kila mmoja wetu aliweza kuona kila kitu kilichopo ndani ya faili hilo na kama unavyo ona kwenye hiyo video katika simu yako. Hilo faili jeusi hapo mezani ndio faili ambalo nina lizungumzia.”
“Muna taka kuniambia kwamba nabii Sanga ana fahamu ni wapi alipo mzee Mbogo?”
“Ndo ana fahamu na amesha kufa”
Josephine alijibu kwa unyonge huku akimtazama RPC Karata usoni mwake.
“Ame uwawa?”
“Ndio na hizo ni njama za nabii Sanga za kuweza kupata nguvu na kukaa karibu na raisi Mtenzi na endapo nchi ita shikiliwa na familia ya Sanga basi tuta kwenda kujuta. Sio sisi tu bali hata nyinyi viongozi wa kijeshi kwa maana Sanga ana miliki jeshi lake ana nguvu ambayo hakuna mtu hapa Tanzania anayo. Wanajeshiwa wana msujudia na wapo tayari kufa kwa ajili ya nabii Sanga na familia yake”
“Hilo halito wezekana”
“Kaka kama ime wezekana kumuua mzee Mbogo itashindikanaje kuiendesha hii nchi kama watakavyo wao wenyewe”
“Nini muna hitaji niwasaidie?”
“Moja tuna hitaji kulipata faili hilo japo ni ngumu sana ila ina bidi tulipate. Mbili tuna hitaji raisi Mtenzi a step down.”
Josephine alizungumza kwa msisitizo.
“Nani ambaye ana kwenda kuwa raisi mara baada ya raisi Mtenzi ku stape down?”
“Utafanyika uchaguzi kwa maana ata step down for good. Ila akitolewa kwa nguvu ina bidi yule aliye mtoka ndio ashikilie nchi. Kwa maana kwa sasa nchi haina makamu wa raisi”
“Magreth una hisi hilo lina wezekana?”
“Ndio lina wezekana ila ni jambo gumu sana. Kikubwa ni kuhakikisha kwamba tuna pata udhaifu wa nabii Sanga pia udhaifu wa raisi Mtenzi ambao uta mfanya aachie madaraka kwa usalama wake”
RPC Karata akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Nita lifikiria hilo. Ila kwa sasa nina hitaji musiweze kutoka hadi pale nitakapo waeleza. Hii nyumba ni nani na nani ambaye ana fahamu ilipo?”
“Ni sisi na wewe tu”
“Sawa nita wapatia ushirikiano kwa kila mutakacho kihitaji, kwa sasa ngoja niaondoke”
RPC Karata na kijana wake wakaondoka eneo hilo.
“Mkuu una waamini walicho kizungumza?”
“Kwa asilimia stini nina waamini. Una jua hii familia ya Sanga ina mambo mengi sana waliyo kuwa wana yafanya nchini ya kapeti. Hivyo jinsi walivyo nieleza kwa namba moja ama nyingine nina weza kuwaamini”
“Ila mkuu hatuwezi kuwaachanisha Sanga na familia ya raisi Mtenzi kwa maana ndoa ndio ime waunganisha”
“Nalitambua hilo. Ila hadi sasa hivi nchi haipo salama”
“Una maanisha nini?”
“Wale wanajeshi wame ingiaje, wana fanya matukio katikati ya mji. Polisi tupo, jeshi la nchi lipo ila hakuna ambaye amedhubutu kuwashika au kuwafwatuli”
“Ngoja kwanza ina bidi niweze kukutana na yule mlinzi wa mzee Mbogo”
“Kwa hiyo tuelekee Muhimbili?”
“Ndio”
Wakaelekea katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na wakaelekezwa wodi aliyo lazwa mlinzi wa mzee Mbogo na kwa bahati nzuri wakamkuta akiwa hajalala ila mguu wake mmoja ukiwa ume fungwa bandeji ngumu(P.O.P.O) huku ukiwa ume ning’inizwa juu kidogo.
“Mkuu habari yako”
Peter alisalimia kwa heshima zote kwa maana ana mfahamu vizuri RPC Karata.
“Salama Peter pole sana”
“Nashukuru mzee”
“Ilikuwaje?”
Peter akaelezea kuanzia walipo kuwa wana toka nyumbani kwa Magreth na kuelekea uwanja wa ndege. Akamueleza mambo ambayo mzee Mbogo alimueleza wakiwa ndani ya gari na vitu alivyo mueleza ni sambaba na vitu ambavyo alitoka kuelezwa na Magreth na wezake. Akamueleza jinsi walivyo kuwa wana fukuziwa na magari hadi ikafika hatua ya kupata ajali iliyo polekea kuzimia.
“Binti yake yupo wapi?”
“Yupo katika wodi za wanawake. Ila alikuja kuniona mida ya saa mbili usiku. Nina hisi asubuhi ana weza kuruhusiwa kwa manaa kwenye ajali hiyo haja udhurika sana”
“Nahitaji kuonana naye”
Peter akamtajia RPC Karata wodi ambayo amelezwa mtoto wa mzee Mbogo. RPC Karata akelekea eneo hilo huku akimuacha mlinzi wake chumbani hapo na Peter.
“Nesi kuna mgonjwa nina hitaji kumuona ndani ya hii wodi”
“Sawa”
Wakaingia chumbani hapo na nesi.
“Habari yako binti”
“Salama shikamoo”
“Marahaba, nesi una weza kutupisha”
“Sawa”
Nesi akatoka chumbani hapo na kuwaacha wakiwa wawili.
“Nina imani wewe ndio Cleopatra Mbogo”
“Ndio ni mimi.”
“Mimi nina itwa RPC Karata”
“Nina kufahamu”
“Pole kwa ajali iliyo tokea”
“Nina shukuru sana. Vipi mume fahamu ni wapi alipo baba yangu?”
“Hapana, ila tuna endelea kumtafuta”
“Magreth ndio nani?”
“Kwa nini una uliza?”
“Baba yangu aliniambia kwamba chochote kitakacho tokea nikutane na huyo msichana. Hivyo kama una mfahamu nina kuomba unikutanishe naye”
“Sawa asubihi nita kupeleka uka onanae naye”
“Nita shukuru sana”
“Basi pumzika asubuhi saa mbili nita kuwa hapa twende nyumbani kwa Magreth”
“Sawa”
RPC Karata akarudi katika chumba alicho lazwa Peter akamuelezea hali halisi aliyo elezwa na Magreth pamoja na Josephine.
“Hivyo ina sadikika hadi sasa hivi mzee wetu atunaye tena”
Peter akajisikia maumivu makali sana kiasi cha kujikuta akimwagikwa na machozi kwani mzee Mbogo alimleya kama mwanaye wa kiume na amlimfundisha mambo mengi sana.
“Cleopatra mulimueleza juu ya jambo hili?”
“Hapana sija mueleza chochote”
“Basi nina kuomba usimueleze”
“Ila kesho nita mkutanisha na Magreth kama alivyo omba”
“Sawa ila Sanga ni lazima afe”
Peter alizungumza kwa uchungu sana huku akijiapiza akipona ni lazima tu adili na nabii Sanga haijalishi ita kuwaje ila ni lazima ata dili na Sanga. RPC Karata akaondoka aneo hilo huku akidili kurudi majira ya saa mbili asubuhi.
***
Majira ya saa moja kamilia nabii Sanga na mke wake wakatua katika kiwa cha helicopter ikulu, wakapokeleza na raisi Mtenzi pamoja na familia yake. Wakakaribishwa ndani kwanis iku hiyo ni siku maalimu sana kwa mrs Sanga kwa maana ana kwenda kutangazwa na kuwa makamu wa raisi.
“Ehee shemeji vipi ume weza kufikiria juu ya ombi langu?”
“Ndio shemeji yangu na nipo tayari”
“Mama uta weza kweli?”
Julieth aliuliza huku uso wake ukiwa ume jawa na tabasamu.
“Asilimia mia moja nita weza uzuri shemeji pia ana weza kunielekeza baadhi ya mambo”
“Ni kweli, isitoshe nime bakisha miaka mitatu tu ya kukaa madarakani. Nina imani ita tosha kupata ujuzi wa kutosha ambao nina imani kwa asilimia moja uta kuwa kiongozi mzuri hata siku nikitoka madarakani una weza kurithi kiti changu”
“Kweli?”
“Ndio na nita kupa support yoyote unayo ihitaji”
Wakaendelea na mazungumzo huku wakipata kifungua kiywa.
“Jery”
“Naam mama”
“Vipi ndoa yenu ina endeleaje?”
Mrs Sanga aliuliza kwa swali la mtego huku akikumbuka mtanange walio piga na mkwe wake wiki kadhaa zilizo pita.
“Mungu ana saidia tupo vizuri mimi na mke wangu hapa”
“Ina bidi mutuletee mjukuu sasa, si muna fahamu familia zetu zime kosa mjukuu”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo.
“Mungu ni mwema baba tuta pata”
Sekretari wa raisi Mtenzi akaingia sebleni hapo.
“Muheshimiwa kila kitu kipo tayari”
“Sawa nina maliza mazungumza nina kuja”
“Haya”
Sekretari akatoka na wakaendelea na mazungumzo ya kifamilia huku nabii Sanga akiwa na hamu kubwa sana ya kumuona mke wake ana tangazwa kuwa ndio makamu mpya wa raisi na kuapishwa.
***
Saa mbili kamili RPC Karata na mlinzi wake wakafika katika hospitali ya Muhimbili na kukuta Cleopatra akiwa amesha ruhusiwa na dakrari. Wakamasalimia Peter na kuondoka na kuelekea nyumbani kwa Magreth. Wakiwa njiani RPC Karata akampigia simu Magreth na akamueleza juu ya ugani huo na akawakaribisha.
“Je muna mahitaji gani ninunue niwaletee”
“Ngoja nikuandikie meseji na nita shukuru sana”
Meseji ikaingia katika simu ya RPC Karata. Wakapita Mlimani City na kununua mahitaji hayo yote aliyo elezwa na Magreth na wakaendelea na safari yao.
“Nina weza kuuliza”
“Uliza tu Cleopatra”
“Huyo Magreth ninaye kwenda kuonana naye ndio nani?”
RPC Karata akaanza kumuelezea kwa ufupi Magreth kuanzia jitihada zake za kuuza maandazi hadi sasa alipo sasa hivi. Wakafika nyumbani kwa Magreth na wakapokelewa vizuri sana.
“Nini?”
Watu wote ika bidi wamsikilize Samson ambaye ame ameweka simu yake sikioni.
“Poa ngoja nawasha”
Samson akachukua rimoti na kuwasha tv iliyopo sebleni hapo na watu wote macho yao wakayaelekezea katika tv hiyo huku wakitazama habari hiyo kutoka ikulu kwa maana raisi Mtenzi ana hutubia taifa. Ika bidi kila mtu macho na masiko yake wayaelekezee katika tv hiyo.
“Habari ndugu wananchi. Ni matumaini yangu mu wazima wa afya na muna endelea vizuri.”
Samson akaongeza sauti kidogo ya tv ili kila mtu asikie.
“Nchi kwa kipindi kirefu ime kuwa haina makamu wa raisi hivyo leo nina hitaji kuwatangazia makamu mpya wa raisi ambaye nita kuwa naye na kushirikiana naye katika kipindi hicho cha miaka mitatu iliyo salia”
Cleopatra akajiweka sawa huku akiongojea kusikia jina la baba yake likitajwa.
“Makamu wa raisi niliye mchagua ni Beatrice Sanga mke wa nabii namba moja Afrika na duniani nabii Sanga. Sheree za kuapishwa kwa makamu wa raisi zita fanyika leo hii hapa ikulu. Asanteni na Mungu awabariki amen”
Kila mtu ndani akastushwa na habari hiyo hususani Cleopatra pamoja na RPC Karata kwa maana mwana mama huyo ana mtambua vizuri na madhambi yake aliyo yafanya kwa miaka ya nyuma.
“MR SANGA ni makamu wa raisi?”
Magreth alihiji huku akiwa kama haamini alicho kisikia.
“Ndio hivyo amechaguliwa kuwa makamu wa raisi na leo ana apishwa”
“Jamani tuna bidi kulizuia hili jambo. Nchi ina kwenda mikononi mwa wauaji na nchi haito kuwa salama”
Josephine alizungumza huku machozi yakimlenge lenga usoni mwake. Hakika habari ya kuchaguliwa mrs Sanga kuwa makamu wa raisi ime mnyong’onyeza kisawa sawa.
RPC Karata akajikuta akishusha pumzi kwa maana hali anayo ishisi mbele juu ya Taifa la Tanzania kwa kweli ni hali ya hatari.
“Hii ni vita kubwa sana ambayo kwa sisi kama sisi kupambana na hawa watu ni ngumu sana. Ni sawa kwamba tupo ndani ya bahari alafu wezetu ni mapapa alafu sisi ni wale vidagaa vidogo”
RPC Karata alizungumza huku dhairi akonyesha kukatishwa tamaa na jambo hilo.
“No kwa udogo wetu wa maumbo endapo tuka shikana kwa pamoja na kupambana na nabii Sanga na familia yake tuna weza”
Magreth alizungumza kwa msisitizo.
“Jamani samahani, nina omba niwatoe kwenye mada hiyo. Tafadhali nina omba kutambua baba yangu yupo wapi?”
Swali la Cleopatra likaleta ukimya wa dakika mbili huku kila mtu akikaa kimya akijaribu kutafakari ni nani ata kuwa wa kwanza kumueleza ukweli Cleopatra kwamba baba yake ame kufa japo hawana ushahidi ila kwa asilimia mia moja ina onyesha kwamba baba yake hayupo duniani kwa sasa.
“Dada”
Samson aliita huku akimtazama Cleopatra.
“Beee”
“Mimi nina itwa Samson ni mfanyakazi wa ikulu katika kitengo cha IT. Jana kuna tukio lilitokea wakati mulipo pata ajali. Sidhani kama uliweza kuliona na kama uliliona tuna imani kwamba uliliona ukiwa ndani ya gari. Ila hichi ndicho kilicho tokea”
Samson akamuonyesha Cleopatra video hiyo katika laptop hiyo. Akaziona gari ambazo zilikuwa zikiwafukuzia wakitokea uwanja wa ndege zikisimama karibu na eneo la ajali na wakashuka wanajeshi walio piga risasi hewani na watu kutawanyika.
“Hao ni wanajeshi wa kitengo gani hapa nchini?”
Cleopatra aliuliza.
“Hao sio wanajeshi wa nchi hii. Ila kuna mtu ana itwa nabii Sanga ndio anaye miliki hao wanajeshi wake. Mke wake ndio huyo uliye msikia akitangazwa kwamba ana kwenda kuapishwa na kuwa makamu wa raisi wa nchi hii. Hivyo inavyo onyesha ni kwamba nabii Sanga na mke wake wamejaribu kumpindua baba yako kwenye nafasi ambayo alipaswa yeye kama yeye kuwa ndio anaye apishwa”
“Kwa hiyo una taka kuniambia kwamba baba yangu ame uwawa kwa ajili ya mtu mwengine kupata madaraka?”
Swali la Cleopatra likawafanya watu kukaa kimya.
“Niambieni baba yangu ame uwawa?”
Cleopatra aliuliza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake, kiasi cha kumfanya kila mtu kumuonea huruma.
“Wewe ni RPC wa polisi kwa nini hili jambo huja fanya kitu chochote?”
Cleopatra alilalama huku akilia mithili ya mtoto mdogo kwa maana kitu kilicho mrudisha nchini Tanzania ilikuwa ni kushuhudia baba yake ana apishwa kuwa makamu wa raisi na mbaya zaidi ni kwamba yeye ndio mtoto wa pekee kwa mzee Mbogo.
“Ahaa Cleopatra kusema kweli hadi sas hivi hatujaweza kutambua kwama ni kweli ame uwawa au ame shikiliwa mahali. Ila tuna endelea kufanya uchunguzi”
RPC ilibidi kumpa matumaini ambayo kwa kweli kwa upande wa jeshi la polisi hadi sasa hivi hawajafanya jambo la ina yoyote na kume tolewa amri maalumu ya kuhakikisha kwamba mzee Mbogo ana tafutwa pamoja na wezake.
“Tatizo la yeye kukumbana na hayo yote ni nini?”
Cleopatra alihoji. RPC Karata akatoa simu yake na kumuweka video inayo waonyesha baba yake pamoja na mzee Mbogo wakipanga kumtoa raisi Jery madarakani.
“Ngoja kwanza ina maana baba yangu alikuwa ana ongoza kumpindua raisi?”
“Kwa sababu raisi kuna mambo ana yafanya ya ukandamizaji wa watu. Milipuko ya mabomu hivyo ana garimu vifo vyo watu wengi na hadi sasa hivi nchi haipo katika hali ya kuwa na amani japo watu wana ishi ndani yake”
Magreth alizungumza huku akimtazama Cleopatra usoni mwake.
“Baba yako ndio mtu sahihi ambaye ana alikuwa ana weza kuongoza hii nchi. Burasa, hekima, na maarifa aliyo kuwa ame mpatia Mungu ndivyo vitu vilivyo kuwa vina hitajika kwa kiongozi wa nchi”
Cleopatra akayafumba macho yake kwa dakika mzina kisha akayafungua huku akiyapangusa machozi yake.
“Mume sema hawa wanajeshi ni watu wa nabii Sanga?”
“Ndio, pia huyo nabii Sanga ni chui aliye jivisha ngozi ya kondoo. Ila kuna mambo mengi sana ambayo ameyafanya.”
Magreth alizungumza na ika mbidi kuanza kumsilimulia visa vyote alivyo vifanya nabii Sanga kwenye maisha yake. Akasimulia matukio mabaya aliyo yafanya yeye pamoja na mke wake. Hawakumficha chochote Cleopatra kwa maana wana hitaji washirikiane naye kwenye kuhakikisha kwamba wana zuia zoezi la mrs Sanga kuapishwa na kuwa makamu wa raisi.
“Video ya ngono uliyo irekodi je unayo?”
Cleopatra alimuuliza Magreth.
“Nina hisi nili ihifadhi kwenye google drive japo hapo katikati nilipotteza poteza simu nyingi sana ila nina imani kwamba ipo”
“Basi tuitumie hiyo. Hakuna kitu kizuri kama kutambua udhaifu wa adui yako. Endapo tuta isambaza au kumtumia mwana mama huyo na kumuambia aachane na kuapishwa kuwa makamu wa raisi ita tupa hatua ya kufanya kazi”
“Haito saidia”
Josephine alizungumza na kuwafanya watu kumtazama.
“Hadi hapa tulipo fikia sio wakati wa kum blackmail mtu. Kilito baki sasa hivi ni kupigana kwa nyama kwa nyama. Bila ya damu kumwagika hatuwezi kuwatoa raisi Mtenzi madarakani na familia ya Sanga, ipo hivi hata ikisambaa video hiyo watu wata itazama na endapo wata jaribu kutumiana kwenye mitandao ya kijamii ni watu wengi sana wata kamatwa na kuuwawa vibaya sana. Hivyo hatupo tayari kuwaingiza watu wengine kwenye shida kwa ajili ya mipango yetu”
Josephine alishauri.
“Wata kamatwa vipi ikiwa watu wata kuwa wana tumiana private?”
Cleopatra aliuliza.
“Samson nina imani kwamba una fahamu nini nina maanisha”
“Yaa anacho kizungumza sister Jose ni sawa. Kuna mfumo ambao tuna weza kutracke mtu ambaye ana sambaza video hiyo na akak kamatwa kirahisi sana”
“Sasa tufanye nini jamani?”
Ethan aliuliza huku akiwatazama wezake.
“Mrs Sanga ina bidi atekwe”
Kauli ya Josephine ikawastua watu wote.
“Ana tekwaje ikiwa yame baki masaa machache sana na mbaya yupo katika jengo ambalo lina lindwa kuliko majengo yote hapa nchini, ikulu”
RPC Karata naye alihoji.
“Magreth una weza kuitekeleza hiyo kazi. RPC Karata wewe uta kwenda ikulu kutazama sherehe hizo. Basi uta msaidia Magreth kuingia ikulu kwa kutumia gari lako. Akiingia ndani sisi ita kuwa ni rahisi kuhakisha kwamba ana ingia kwenye chumba ambacho mrs Sanga ana jiandaaa kwa ajili ya kwenda kuapishwa na ata mtoa kwa njia ya kuingia baharini ambapo sisi tuta mpokea tukiwa katika boti na kumleta hadi huku”
“Ume zungumza kitu ila sija kuelewa hata kidogo Josephine. Una hitaji mimi nijulikane kwamba nina shirikiana na nyingi. Kumbuka pale ikulu kila anaye ingia ana kaguliwa. Haijalishi wewe ni RPC au ni waziri, ila walinzi wana kukagua. Wewe ume kuwa ni chief Staff pale nina imani kwamba una tambua hilo”
“Kumteka mrs Sanga pia una weza kuzidisha nguvu ya serikali katika kuwatafuta”
Mlinzi wa RPC Karata naye alishauri.
“Mimi Josephine nime muelewa”
Ethan alimuunga mkono Josephine.
“Aisee hembua acheni plan za kitoto. Kumbekeni hapa tuna kwenda kudili na papa sio kidagaa na mbaya zaidi yupo Ikulu jamani. Au wewe Josephine huijui ile ikulu?”
“Nina ijua vizuri tena na nina ielewa vizuri sana na ramani nzima ipo kichwani mwangu.”
Josephine alizungumza kitu anacho kielewa kwa maana kwa kipindi cha yeye kuwa Chief Staff kuna mambo mengi sana aliweza kujifunza ya kuyafahamu ndani ya ikulu na ikiwemo njia zote za siri za kuingia na kutokea ndani ya ikulu ambazo ni watu wa chache tu ndio wanazo zifahamu akiwamo raisi pamoja na mkuu wa walinzi wa raisi.
“Mage alicho kizungumza mwenzako umekielewa?”
RPC Karata aliuliza.
“Ngojeni kwanza”
Josephine alizungumza huku akiyafumba macho yake na akaanza kusali ili Mungu amsiaide kuhakikisha kwamba ana fanikisha mpango huo.
“Ana fanya nini?”
Cleopatra aliuliza kwa sauti ya chini kidogo.
“Ana sali”
Magreth alijibu kwa sauti ya chini kiasi.
“Ahaa sawa”
Baada ya dakika tano akafumbua macho.
“Nina ombeni kalamu na karatasi”
Magreth akanyanyuka na kuiongia kwenye moja ya chumba na akatoka akiwa na karatasi na kalamu. Josephine akaanza kuchora ramani nzima ya ikulu. Akaweka idadi ya walinziw atakao kuwepo ni eneo gani ambalo ulinzi uta kuwa mkali sana na eneo gani ambalo ulinzi hauto kuwa ni mkali. Jinsi na namna watakavyo mteka mrs Sanga mbele ya hadhira ya watu.
“Muda wa kuapishwa ndio muna mteka?”
RPC Karata aliuliza hukua akiwa na mshangao mkubwa sana.
“Ndio kwa maana ndio nafasi ya pekee iliyo salia kwa sisi kukamilisha mpango wetu na hii kazi tuta ifanya sisi sote.”
“Sisi wangapi?”
RPC karata alihoji huku akimtazama Josephine.
“Sisi wote tulimo ndani ya hii nyumba. Tunacho kiomba kwako tuna kuomba utupatie mabomu yaliyo katika mfumo wa baruti zinazo weza kuata ukuta kwa namna jinsi tunavyo hitaji. Hapo kazi yako ita kuwa ime isha”
RPC Karata wakaazamana na kijana wake kisha wakatingisha kichwa wakimaanisha kwamba wana weza kufanya hivyo. Josephine akaanza kugawa majukumu ya kufanya ambayo kila aliye patiwa jukumu lake japo ndio mara ya kwanza kulifanya ila aliamini kwamba ata ifanya.
“Ana apishwa saa ngapi?”
Josephine alimuuliza Samson.
“Habari za kuaminika ana apishwa saa kumi kamili”
“Sawa, sasa hivi ni saa sita dakika thelathini na tano. Tuna masaa manne ya kujiandaa kaka tunakuomba msada wa hayo mabomu”
“Sawa ngoja tuondoke tukawaletee. Je silaha zozote muna hitaji?”
“Hapana”
RPC Karata na kijana wake wakaondoka na kuwaacha watu wakiendele kujianda kwa kazi hiyo ambayo ita kuwa ni hatari sana. Baada ya lisa moja RPC Karata na kijana wake wakarudi na kuwakabizi mabomu hayo ya kupasulia ukuta.
“Ila kuweni makini sana kwa maana ulinzi na msakako wa kuwasaka nyinyi haufanywi na polisi peke ila jeshi na usalama wa taifa wapo kazini. Tume elewana”
“Ndio”
RPC Karata baada ya kuwatahadharisha akaondoka na kijana wake. Baada ya maandalizi kukamilia, Magreth, Cleopatra, Ethan na Josephine wakaondoka kwa kutumia njia ya baharini huku wakiwa wamevalia mitungi ya gesi inayo wasaidia kugelea wakiwa ndani ya maji. Samson kazi yake ni kuhakikisha kwamba ana jua kila kitu kinacho endelea ndani ya ikulu kwa kuhack mfumo mzima wa kamera. Wakaogelea kwa umakini sana hadi wakafika eneo la karibu kabisa na ikulu ambalo lina njia inayo elekea katika maeneo manne ya ikulu. Eneo la kwanza ni katika viwanja vya ikulu, enep la pili ni katika ukumbi wa ikulu. Eneo la tatu ni katika nyumba ya raisi na eneo la nne ni katika chumba maalumu cha ulinzi wa raisi ambapo chumba hicho kime tengenezwa kwa chumba tu endapo ikulu ina vamiwa au kupata tatizo lolote la kuhatarisha maisha ya raisi basi akiingia ndani ya chumba hicho ana kuwa salama na kuna mfuniko maalumu ambao una mshusha chini na kutoke katika njia hiyo inayo weza kumsaidia kutoroka ndani ya ikulu.
Wakafika katika njia inayo wafikisha katika ukumbi ambao ndipo itakapo fantika sherehe ya kumuapisha mrs Sanga.
“Eneo hilo hapo la juu ndio atakalo simama”
Josephine alizungumza hukua kiwaonyesha wezake aneo ambao ndipo mrs Sanga atakapo simama kwa ajili ya kula kuiapo. Ethan akakunjua ngazi walio kuja nayo na kuisimamisha vizuri kisha akapanda eneo hilo na kulizungushia duara kubwa. Wakazungushia mabomu hayo kwenye eneo hilo ambapo endapo wata lipua wakati mrs Sanga ame panda basi ata shuka na kipande hicho cha ukuta na wakatengeneza chuma kingine ambacho endapo tukio hilo lina tokea basi chuma hicho kina funika kwa haraka eneo hilo na wata shindwa kuingia katika shimo hilo. Haikuwa kazi rahisi kuamilisha mambo yote kwa wakati mfupi ila kutokana na kushirikiana na jitihada zao waka fanikiwa kuimaliza dakika thelathini kabla ya sherehe hizo kuanza.
“Samson una tupata?”
Magreth alizungumza huku akiwa na earphone ndogo na maalumu sikoni mwake, inayo muwezesha kuwasiliana na Samson na wezake hao muda wowote.
“Nina wapata loud cleare”
“Tutumie video za CCTV Kamera”
“Poa”
Samson akatuma video zinazo onyesha kila kinacho endelea ndani ya ikulu na tayari wageni wengi sana walisha fika kwa ajili ya shuhuli hiyo.
“Mbona una mawazo mke wangu?”
Evans alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Nina hofu”
“Usijali kila jambo lita kwenda vizuri”
Samson alizungumza huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika rimoti maalumu ya kulipulia mabnomu hayo muda na wakati utakapo fika.
***
“Ume pendeza mama yangu”
Julieth alimsifia mama yake huku wakijitazama kwenye kioo kilichopo ndani hapo.
“Kweli?”
“Ndio yaani leo kweli una kuwa makamu wa raisi, hahaa yaani nina ona kama ni ndoto”
“Ndio hivyo mwanangu. Una jua Mungu akiamua kukufunulia basi kila kitu kina kaa kwenye mstari.”
“Ni kweli mama”
Mlango ukagongwa na Julieth akamruhusu anaye gonga. Nabii Sanga akaingia huku naye akiwa amevalia suti ya garama sana iliyo mpendezesha.
“Jamani mambo tayari ni muda wa kuelekea ukumbini”
Nabii Sanga na familia yake wakatoka ndani hapo na kuelekea ukumbini huku walinzi wa raisi Mtenzi wakiwalinda. Wakaingia ukumbini hapo na wageni waalikwa wakiwemo viongozi mbalimbali wa sekta za serikali, wakawapigia makofi japo wengine hawajaridhishwa na uteuzi huo kwa maana wana hisi kwamba raisi Mtenzi ana wapendelea wakwe zake. Wakaka eneo walilo andaliwa, Jery naye akaka kiti cha pembeni ya mke wake. Baada ya dakika tano raisi Mtenzi akaingia ukumbini na watu wote wakasimama, baada ya raisi Mtenzi kukaa na watu wote wakaka na shuhuli zikaanza.
“Mume wangu nina hisi hofu”
“Usijali mke wangu jikaze nchi ndio imesha kuwa ya kwetu huyo”
Nabii Sanga alimnong’oneza mke wake. Wakati wa mrs Sanga kuelekea mbele ya ukumbi ukafika. Akakabidhiwa bibilia pamoja na kitabu chenye kiapo ambacho ata kisimoa kumfwatisha anaye muapisha.
‘Leo muta lia mbwa nyinyi’
RPC Karata alizungumza kimoyo moyo huku akimtazama mrs Sanga ambaye ameanzakusoma kiapo hicho.
“Time to goo baby”
Sauti ya Samson ilsikika vizuri masikioni mwa Josephine, Cleopatra, Magreth na Ethan. Magreth akatazama simu yake na kuona jinsi mrs Sanga alivyo simama katika eneo walilo lizungushia duara kwa chini.
“Moja, mbili tatu”
Magreth alihesabu na ilipo timia tatu Evans akamisha rimoti ya kulipulia mabomu hayo na eneo walilo lizungushia duara likaanza kuwaka moto unao kata aradhi hiyo ngumu.
“Ehee mwenyezi Mungu uni saa……..”
Mrs Sanga hakumalizia sentensi yake galfa akajikuta akidumbukia kuelekea chini na kuwafanya watu wote ndani ya ukumbi huo kuchanganyikiwa hususani nabii Sanga aliye jikuta akikimbilia eneo hilo alipo dumbukia mke wake na akakutana na mfuniko wa chuma ulio mfanya ashindwe kuona ni wapi mke wake alipo angukia.
Taharuki hiyo hakika iliwaacha watu katika alama za kuuliza. Si watu waliopo ndani ya ukumbi huo,hata watu walio kuwa wakifwatilia tukio hilo kwa njia za luninga kila mmoja alistajabu kupotea kwa mrs Sanga. Josephine akamchoma mrs Sanga sindano ya usingizi shingoni mwake, wakamvalisha kifaa cha kumsaidia kupumua ndani ya maji na Evans akambeba begani mwana mama huyo na kuelekea katika njia ya kutokea baharini. Wakaanza kuogelea ndani ya maji hayo huku Evans akiwa amemshika mrs Sanga kwa ukaribu sana kwa maana hana uwezo wa kufanya chochote. Cleopatra alivyo ona shuhuhuli hiyo ina mpa uzito Evans, akamsaidia Evans kwa kumshika mrs Sanga mkono wa kulia huku Evans akiwa ameshika mkono wa kushoto na wakaendelea kupiga mbizi ndani ya maji huku wakijitahidi kwenda kasi kadri ya uwezo wao. Walinzi walivyo jitahidi kufungua milango ya siri inayo wapelekea eneo la chini ya ikulu ila wakashindwa kwani kila wanavyo jaribu kuingiza namba za siri zina kataa.
“Wooo muta pata tabu sana”
Samson alizungumza kwa maana yeye ndio amebadilisha mfumo wa mifuniko hiyo na kuweka namba zake za siri ambazo baada ya dakika ishirini ndipo zitakapo funguka. Hakika si tukio la kawaida na hata nabii raisi Mtenzi mwenyewe alijikuta akiwa na hofu kubwa sana. Ndani ya dakika hizo ishirini ziliweza kuwatosha Magreth na wezake kufika eneo la nyumba walio jificha ambayo ipo pembezoni mwa bahari. Wakamuingiza mrs Sanga kwenye moja ya chumba na kumkalisha kwenye kiti cha chuma, wakamfunga mikono yake kwa pingu pamoja na miguu yake kwa minyororo.
“Hana gprs mwilini mwake?”
Ethan halihoji.
“Hana”
Samson alizungumza huku akiwa na kifaa ambacho kina weza kugundua kama mtu ana kifaa ambacho kina muwezesha kila anapo kwenda aweze kujulika. Baada ya dakika ishirini milfuniko hiyo ikafunguka na walinzi wa ikulu wakaanza kuingia eneo ambalo wana amini mrs Sanga ame dumbukia. Walipo fika eneo alipo anguka, wakakutana na vipande vipande vya sakafu hiyo iliyo pasuka pasuka ila mrs Sanga hayupo. Wakatafuta eneo zima la chini ya ikulu hiyo na hawakuweza kumuona mrs Sanga.
“Ripoti”
Raisi Mtenzi alimuuliza mlinzi wake mkuu mara baada ya kuingia ofisini hapo. Nabii Sanga, Julieth, Jery na mr the Brain macho yao yote yapo kwa mlinzi huyo.
“Hatujaweza kumpata zaidi ya kiatu chake kimoja. Inavyo onyesha ni kwamba ame tekwa”
“Mke wangu ana tekwaje?”
Nabii Sanga aliuliza kwa ukali.
“Ndio hivyo mkuu na watu walio mteka wana onyesha ni professional sana katika kazi hiyo kwa maana tukio jinsi walivyo lifanya ni ndani ya muda mchache na waliweza ku hack mfumo wa mifuniko mizima ya ikulu na ilishindwa kufunguka ndani ya dakika ishirini”
“Niitie jenerali”
“Sawa mkuu”
Baada ya dakika tano jenerali wa jeshi akaingia ofisini hapo na kupiga saluti.
“Nina hitaji wanajeshi wako wa majini, wanajeshi wa nchi kavu, anga na kadhalika waweze kufanya oparesheni kubwa ambayo Tanzania nzima haijawahi kutokea. Yoyote ambaye muta muhisi ana husika katika hili, mkamateni na kumsweka ndani”
“Sawa muheshimiwa”
“Kumbuka aliye tekwa hapa ni makamu wa raisi”
“Nime kuelewa muheshimiwa raisi”
Jenerali akapiga saluti na kutoka ndani hapo na kuwaacha watu wakiwa wamejawa na huzuni isiyo ya kawaida.
***
Simu ya Magreth ikaanza kuita kwa haraka akaichukua na kukuta ni namba private ya RPC Karata.
“Ndio kaka”
“Mission ime kwendaje?”
“Tuna mshukuru Mungu tume ifanikisha salama. Vipi ni kitu gani kinacho endelea huko nje?”
“Kuna msako mkali sana. Kuweni makini ikiwezekana jaribuni kuzima vitu ambavyo muna hisi wana weza kuvi tracke kama simu na kadhalika musije muka kamatwa”
“Usijali kaka, tupo na Samson hapa tuna imani kwamba kila jambo lita kwenda vizuri”
“Sawa ila kazi nzuri sana”
“Asante kaka”
Magreth akakata simu na kuwageukia wezake.
“Nahitaji kumuhoji mrs Sanga sasa hivi”
Evans alizungumza huku akivuta dawa kwenye kichupa kidogo kwa kutumia bomba la sindano.
“Hata mimi nina taka kufahamu ni kwa nini ame muua baba yangu”
Cleopatra naye alizungumza kwa msisitizo. Wakaingia kwenye chumba walicho mfunga mrs Sanga. Evans akamchoma sindano ya kumzindua mrs Sanga na hazikupita dakika mbili akarudi katika hali yake ya kawaida na kuanza kushangaa eneo alilopo.
“Nipo wapi hapa?”
“Kuzimu”
Evans alimjibu mrs Sanga huku akiwa amechuchumaa mbele yake.
“We…we…..!!”
Mrs Sanga alizungumza kwa kigugumizi.
“Yaa ni mimi nina imani ume shangaa sana kuona nime zikatisha ndoto zako na ndoto za mume wako. Cleo rekodi kila kitu”
“Sawa”
Cleopatra akatoa simu mfukoni mwa suruali yake na kuanza kurekodi tukio hilo.
“Najua mume wako ame weza kumteka Leila. Maumivu ambayo niliyapata basi hata yeye kwa sasa ana yapitia. Ukinijibu vzuri basi sinto kuumiza, ila ukishindwa kunijibu basi mume wako ata ona video ya kifo chake kwa maana sinto jali wewe kufa”
Mrs Sanga akaanza kutetemeka mwili mzima.
“Leila na mzee Mbogo wapo wapi?”
“Mi…mi…mi sijui”
“Nina rudi tena Leila na mzee Mbogo ambaye wanajeshi wa mume wako waliweza kumteka wapo wapi?”
“Nimesema sijui na sijui una zungumzia nini”
Evans akachomoa kisu kidogo alicgo kochomeka katika kiatu cha mguu wake wa kulia. Akalichana gauni la mrs Sanga na mapaja yake yakawa wazi.
“Mama nina kuuliza kwa mara ya tatu na ya mwisho. Yupo wapi Leila na mzee Mbogo”
“Nina sema sifahamu”
Mrs Sanga alijibu kwa ujasiri. Evans akakikika kisu hicho katika paja la mguu wa kulia wa mrs Sanga na kumfanya apige yowe lililo wastua hadi watu walipo sebleni na kujikuta wakikimbilia ndani ya chumba hicho.
“Nimesema yupo wapi mzee Mbogo na Leila”
Mamumivu makali makali yakamfanya mrs Sanga kuzimi kwa maana katika kipindi chake chote cha maisha hajawahi kukutana na wakati mgumu kama huo.
“Usimchome sindano”
Josephine alizungumza na kumzuia Evans asimchome mrs Sanga sindano ya kumzindua.
“Tumpeni wakati wa kutosha. Hiyo video Samson itengeneze vizui na umtumie nabii Sanga ila asifahamu ni wapi ilipo tokea”
Josephine akatoa maagizo hayo na Samson akaitengeneza vizuri video hiyo kwenye laptop yake na wakaipitia vizuri huku sauti ya Evans kwenye video hiyo ikisikika kwa uzito ambao sio rahisi sana kwa watu kuitambua sauti hiyo. Walipo ridhiana wakaituma video hiyo kwenye namba ya nabii Sanga huku ikiandamana na maleo ambayo wana amini nabii Sanga ni lazima ata yatakeleza kwa uharaka sana.
***
Mlio wa meseji iliyo ingia kwenye simu ya nabii Sanga, ukamfanya aitoa simu hiyo kwenye mfuko wa koti lake kwa uharaka sana.
‘Private namba’
Nabii Sanga alizungumza kimoyo moyo na kufungau meseji hiyo. Akasoma malezo hayo yaliyo mstua sana na kujikuta akiifungua video hiyo kwa uharaka sana. Sauti hiyo ya kilio cha mke wake ika wafanya watu wote ofisini hapo kwa raisi kumtazama nabii Sanga aliye anza kutetemeka.
“Hembu nione”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akiichukua simu hiyo ya nabii Sanga na kuitazama video hiyo iliyo mpa wakati mgumu. Jery na mke wake naye wakaitazama video hiyo huku mr the Brain akiwa wa mwisho kuitazama video hiyo na akasoma maelezo hayo.
‘Ukimuhitaji mke wako asipitie mateso makubwa zaidi ya haya. Mrudisheni Leila pamoja na mzee Mbogo wakiwa hai una masaa mawili la sivyo kisu hichi kitaingia katika uke wa mke wako na kuuchana chana vibaya sana’
Mr the Brain akawatazama nabii Sanga na raisi Mtenzi.
‘Ina maana Mbogo wame mteka?’
Mr the Brain aliwaza kichwani mwake.
“Tuna masaa mawili. Kama mume muna fahamu chochote kusiana na hili ina bidi tutekeleze ili maisha ya makamu wa raisi yaweze kuwa hai”
“Jery mchukue mke wako nendeni nyumbani”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama Julieth anaye lia kwa uchungu sana mara baada ya kuina video ya maam yake akikitwa kisu katika paja lake. Taratibu Jery na mke wake wakatoka ofisini hapo.
“Jamani muna fahamu chochote juu ya hilo?”
Mr the Brain ili bidi aulize tena kwa msisitizo.
“Brain ukweli ni kwamba Mbogo hayupo tena duniani”
Raisi Mtenzi ili mbidi kuwa wazi.
“Jesus Christ! Sasa tuna fanyajae na ime kuwaje akafa”
“Jamani hili jambo nita jua jinsi gani ya kudili nalo kwa maana huyu mtekelezaji wa hili jambo nimesha mfahamu”
“Ni nani?”
Mr the Brain aliuliza.
“Ni kijana mmoja ana itwa Evans Shika”
“Evans Shika ndio yule wa kipindi kile muheshimiwa raisi?”
“Ndio”
“Duu na huyu Leila anaye zungumziwa hapa ndio nani?”
“Huyo ni mwanamke wake”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upole.
“Ila huyo msichana si yupo hai?”
“Ndio nime mshikilia”
“Sasa tuna fanyaje kwa huyu Mbogo na ime kuwaje akafariki?”
Maswali ya mr the Brain yakawapa wakati mgumu sana nabii Sanga na raisi Mtenzi kayajibu kwa maana jambo la kumuu mzee Mbogo ni siri kwao. Mlango uka funguliwa na akaingia mlinzi wa raisi Mtenzi.
“Muheshimiwa raisi una hitajika commanding room”
Raisi Mtenzi akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na wakatoka ofisini hapo wakiwa wameongozana na mr the Brain na kumuacha nabii Sanga akiwa ofisini kwake. Nabii Sanga akatoa simu yake kwa haraka na kumpigia kiongozi wa wanajeshi wake.
“Mumeshuhudia mke wangu akipotea?”
“Ndio mkuu”
“Nina hitaji utume vijana kuhakikisha wana msaka. Nina kutumia video ya mateso aliyo yapatia”
“Sawa”
Nabii Sanga akakata simu na akatoka ofisini hapo na kuelekea walipo Julieth na mume wake. Raisi Metenzi akaingia kwenye ukumbi huo na kumkuta waziri wa ulinzi, pamoja na jenerali wa jeshi.
“Muheshimi raisi tume weza kugundua ndani ya nchi wame ingia wanajeshi ambao hadi sasa hivi hatutambui ni wapi walipo tokea. Wanajeshi hao wame weza kuvamia nyumbani kwa chief staff wa happ ikulu na wanajeshi hao hao waliweza kumteka mzee Mbogo”
Jenerali wa jeshi alizungumza huku video hizo mbili zilizo tumwa na Samson zikoonyesha wanajeshi wa nabii Sanga wakiwa nyumbani kwa Magreth huku video nyingine wakimteka mzee Mbogo.
“Muheshimiwa ina onyesha ulinzi wa nchi una lega lega hadi wana jeshi wana ingia wana fanya matukio na hatujui wana toka nchi gani basi ni hatari sana kwa taifa na raia”
Mr the Brain alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.
“Muheshimiwa raisi ina bidi kuwaondoka haraka iwezekanavyo ndani ya ardhi ya Tanzania. Tupatie ruhusa yako”
Jenerali alizungunza huku akimatazama raisi Mtenzi usoni mwake ambaye ana onekana kushikwa na kiguumizi cha kufanya maamuzi na watu wanao mfahamu vizuri hiyo sio kawaida yake.
“Muheshimiwa raisi hadi sasa hivi hatambui mzee Mbogo yupo wapi, ushahidi wa video una onyesha walimteka kutoka eneo la ajali na wakaondoka naye. Vijana wangu wana subiria amri yako kuwaondoka wavamizi hao ndani ya nchi na wata tueleza ni wapi alipo mzee Mbogo.”
Jenerali wa jeshi alizungumza kwa msisitizo na kumfanya raisi Mtenzi kushusha pumzi nyingi.
“Muheshimiwa raisi tuna subiria maamuzi yako”
“Waacheni”
Karibia watu wote walipo ndani ya chumba hicho wakamtazama raisi Mtenzi kwa mshangao.
“Una sema?”
Jenerali wa jeshi alizungumza kwa mshanagao
“Wametokea wapi?”
Raisi Mtenzi aliuliza kana kwamba hapo awali hajasikia alicho kizungumza.
“Hatufahamu muheshimiwa raisi”
Jenerali alijibu kwa msisitizo.
“Mkuu is your call”
Mr the Brain alizungumza huku akimkazia macho raisi Mtenzi ambaye ana fikiria endapo wana jeshi hao wakishambuliwa na kuuwawa, basi mahusiano yake na nabii Sanga yana weza kuvunjika.
“Nina omba nifikirie”
“Samahani muheshimiwa una sema?”
Jenerali ilibidi amkazie macho raisi Mtenzi.
“Nime sema nina omba nifikikire”
Raisi Mtenzi alijibu kwa ukali kiasi cha kuwafanya watu wazidi kumshangaa. Raisi Mtenzi akanyanyuka na kuingia kwenye moja ya ofisi iliyopo katika ukumbi huo.
“Muheshimiwa vipi una wafahamu hao wana jeshi?”
Mr the Brain alizungumza mara baada ya yeye kuingia ofisini hapo.
“Nina omba nipumzishe kichwa changu kwa sasa. Mambo yana tokea mfululizo nina shindwa kuelewa”
“Mkuu nchi kwa sasa ipo kwenye wakati wa hatari. Hawa wanajeshi wana endelea kuzagaa hatujui lengo lao ni nini na wana mpango gani?”
“Ndio nina lijua hilo ila nina hitaji muda wa kumpumzika na kufikiria nini cha kufanya”
Jenerali wa jeshi akaingia ndani hapo huku akiwa na vijana wake wawili.
“Samahani muheshimiwa raisi kwa hichi ninacho kwenda kukizungumza. Nikiwa kama jenerali wa jeshi nina kwenda kukuvua madaraka yako yote kwa muda na kuanzia hivi sasa nchi ita ongozwa na jeshi kwa maana ume kosa maamuzi ikiwa adui amekanyaga ardhi ya Tanzania. Na uta kuwa chini ya uangalizi wa vijana wangu hadi pale tutakapo fanikiwa kumtoa adui ndani ya ardhi ya nchi hii. Hatuhitaji kosa la milipuko liweze kutoea tena. Tuta pambana kufa na kupona kwa ajili ya nchi. Mpokonyeni raisi simu yake na mumueke chini ya uangalizi na asiwasiliane na mtu wa ina yoyote”
Jenerali wa jeshi alizungumza kwa msisitozo huku akimkazia macho raisi Mtenzi na wakajikuta wakijawa na mshangao yeye na mr the Brain.
“Sawa mkuu. Muheshimiwa tuna kuomba utukabidhi simu yako na uongozane nasi kwa utaratibu tu”
“We…e.ww…eee ni nani hadi una nivua madaraka?”
“Mkuu sio mimi ila katiba ina nielekeza kama raisi ata shindwa kutoa amri katika kipindi ambacho jeshi lina hitaji kuingia vitani basi huna sifa ya kuongoza kwa kipindi hicho. Tafadhali kuna watu na wageni wengi waliopo hapa ikulu hivyo nina kuomba ujiheshimu katika hilo la sivyo vijana wangu wata tumia nguvu.”
Raisi Mtenzi akamtazama jenerali wa jeshi kwa macho makali na yaliyo jaa hasira. Akanyanyuka taratibu na akatoa simu yake mfukoni na kumkabidhi jenerali wa jeshi na taratibu akatoka ofisini hapo huku wanajeshi hao wawili wakihakikisha hazungumzi na mtu yoyote wala kuingia sehemu yoyote hadi katika chumba maalumu ambacho ata kaa humo hadi pale oparesheni ya kuwaondoa wanajeshi wasio julikana itakapo kishwa ndani ya nchi.
Jenerali wa jeshi akamtazama mr the Brain kwa sekunde kadhaa kisha akatoka ofisini hapo na kurudi katika ukumbi huo.
“Tusikilizane”
Jenerali wa jeshi alizungumza na watu wote wakaa kimya kumsikiliza. Kijana wake mmoja akachukua bibilia pamoja na bibilia kwa ajili ya kumuapisha kuchukua nafasi ya muda kuongoza nchi. Watu wote waka simama huku wafanyakazi wengine wakiwa wana jiuliza kimoyo moyo ni wapi alipo raisi Mtenzi. Jenerali wa jeshi akala kiapo hicho na akawa raisi wa muda. Baada ya zoezi hili kuisha jenerali akakakwenye kiti ambacho ana kaa raisi peke yake wakiwa ndani ya chumba hicho.
“Nchi kwa sasa ime weza kuvamiwa na maadui. Hatuwezi kufumbia macho hawa maadui wanao endelea kuivamia hii nchi na jeshi likiwepo. Niwahakikishie jambo moja tu. Tuta wapiga tena tuna wapiga kipigo cha mbwa Koko.”
Jenerali alizungumza huku wakuu wa majeshi wa kambi zote nchini Tanzania wakiwa wana fwalilia kikao hicho kwa kupitia mfumo wa video call.
“Muna jua ni nini cha kufanya. Wanajeshi wote ambao wame ingia nchini Tanzania waanze ushambuliwa sasa hivi”
“Sawa mkuu”
Wakuu wa kambi zote za jeshi wakajibu kwa pamoja na shuhuli ya kuwasaka wanajeshi ambao hadi sasa hawajajuliakana kama ni wa nabii Sanga ikaanza.
***
“Raisi Mtenzi amepigwa chini”
Samson alizungumza huku uso wake ukiwa ume tawaliwa na tabasamu pana sana.
“Una maanisha nini?”
Josephine aliuliza huku macho yame mtoka.
“Niliweza kumtumia rafiki yangu ninaye fanya naye kazi pale ikulu video zile za wale wanajeshi wa nabii Sanga na aliweza kuziweka hadharani na ameniambia kwamba jenerali wa jeshi alihitaji kuanza kufanya mashabulizi kwa wanajeshi hao ila raisi Mtenzi akwa hatoa amri. Hivyo jenerali wa jensi ame weza kuongoza nchi kwa muda hadi pale watakapp waua wanajeshi wote walio vamia nchi”
“Ime wezekana vipi kwa raisi kutolewa madarakani?”
Magreth alihoji.
“Ina wezekana na katiba ina mruhusu jenerali wa jeshi kuchukua madaraka kwa muda pale tu raisi anapo onyesha ana lege lega kutoa maamuzi hususani pale nchi inapo kuwa katika wakati wa kuvamiwa. Hivyo adui yetu sasa tuna weza kumpiga mbele na nyuma”
Samson alizungumza kwa kujiamini.
“Aisee Mungu ni mwema. Ata sikiliakilio chetu”
“Ndio hivyo sister Josephine”
“Jenerali wa jeshi ni rafiki wa baba mzuri tu. Je nina weza kuonana naye?”
Cleopatra alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Una taka kuonana naye umuambie nini?”
“Nimpe picha halisi kwamba wanajeshi hao ni wa nabii Sanga na pia nina hitaji kuwafutia nyinyi makosa na muweze kutoka nje tena na kufanya kazi kama kawaida”
“Hilo ni wazo zuri. Cleopatra ana weza kusafisha majina yetu na adui yetu akakamatwa na kusekwa ndani”
Ethan naye alishauri.
Josephine akatafakari kwa muda kisha akamtazama Cleopatra usoni mwake.
“Una weza kwenda ila ina bidi kuzungumza na RPC Karata kwanza. Mage mpigie RPC”
“Sawa”
Magreth akampigia RPC Karata na kumueleza mpango wake na RPC Karata akamtuma mlinzi wake kwa ajili ya kumchukua Cleopatra.
“Cleopatra nina kuomba ukawe very smart utakapo kutana na jenerali wa jeshi. Tuna hitaji kuwa hurukwa maana hatuna makosa ambayo yana weza kutufanya kuwa katika hali kama hii”
“Musijali nina elewa kila kitu”
“Jamani nime weza kupata location ya meli ya nabii Sanga ilipo”
Samson alizungumza huku akiendelea kuminya minya laptop yake na watu waote wakatazama laptop hiyo.
“Vizuri niingizie hiyo location kwenye simu yangu na nikifika ikulu nita muonyesha jenerali.”
Samson akafanya hivyo na kumuingizia Cleopatra ramani inayo onyesha ni wapi ilipo location ya meli ya nabii Sanga. Hazikupita dakika tano dereva wa RPC Karata akafika nyumbani hapo na wakaondoka na Cleopatra.
“Ina bidi twende kuvamia meli hiyo”
Ethan alizungumza wa kujiamini na kuwafanya watu wote kumtazama.
“Shemeji hatuwezi kupambana na watu wengi kama hao tuta kufa. Tumuombee Cleopatra aweze kuaminika huko anapo kwenda”
Josephine alizungumza kwa upole huku kila mmoja akiwa ameyaweka matumaini yake kwa Cleopatra
***
Wanajeshi wa nchi ya Tanzania wakasambaa katika jiji la Dar es Salaama huku shuhuli za usafiri na shuhuli nyingine zikisimama kwa muda. Hapakuwa na mwananchi aliye ruhusikwa kutembea wala magari yanayo toka mkoani kuingia katika jiji la Dar es Salaam. Kwa ufupi jiji zima lime zibitiwa na wanajeshi. Wanajeshi wa nabii Sanga ambao wameingia jiji Dar es Salaama kwa lengo la kumsaka mrs Sanga wakaanza kupatwa na machale ya kuona hali ya utulivu inayo endelea ndani ya jiji hilo.
“Mkuu tuna ona jiji limetulia hakuna raisi wana otembea wala magari?”
Kiongozi wa kikosi hicho alizungumza na nabii Sanga kwa kutumia simu.
“Una maanisha nini?”
“Yaani jiji lipo kimya hatuoni magari wala watu. Au ndio hiyo shuhuli ya kumtafuta mke wako?”
“Ndio si muna jua kwamba amesha kuwa makamu wa raisi hivyo musiogopo. Hakikisheni na nyinyi muna ifanya kazi niliyo waagiza”
“Sawa mkuu”
Nabii Sanga akakata simu na mkuu huyo wa jeshi la nabii Sanga akaamrisha vijana wake kuingiza magari yao yapatayo thelathini huku yakiwa yamejaa wanejeshi katika jiji la Dar es Saalam.
“Wame ingia kwenye mtego wetu”
Mwanajeshi mmoja wa Tanzania aliye kaa gorofa ya tano alizungumza kwa kutumia simu ya upepo huku akitazama gari hizo kwa kutumia darubini. Wanajeshi wa Tanzania walio samba maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam waliweza kusikia sauti hiyo ya mwenzao.
“T Zero wapo wangapi?”
“Zipo gari thelathini na tano mkuu na tume ziweka katikati”
“T Tena una nisikia?”
Jenerali alizungumza na vijana wake wote wakamsikia.
“Ndio mkuu nina kusikia”
“Troops yako ina watu wangapi?”
“Watu ishini mkuu”
“Hakikisheni kwamba hatoki mtu”
“Sawa jenerali”
Wanajeshi wa Tanzania walio jificha katika magorofa eneo la Morroco. Wakaziweka silaga zao tayari kw amashambulizi. Mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa nabii Sanga akatoa ishara ya gari hizo zikasimama.
“Moyo wangu una poteza amani kabisa?”
“Kwa nini mkuu”
Kijana wake alimuuliza.
“Huu ukimya sio wa kawaida katika jiji la Dar es Salaam. Yaani hadi sasa hivi hatuoni hata daladala moja?”
“Hata mimi nina shangaa mkuu”
“Na kama mrs Sanga angekuwa ana tafutwa, basi tungeona polisi wakiwa wame zagaa kila mahala. Ila ni kimya na sio kawaida”
“So mkuu turudi au?”
“Ngoja kwanza”
Mkuu huyo akafungua mlango wa gari lake aina ya JEEP, akachukua darubini yake na kuanza kutazama kwenye magorofa yaliyopo eneo hilo la Morocco mataa.
“Fuckk ambushhhhhh!!”
Alizungumza mara baada ya kumuona mwanajeshi mmoja akiwa amemuelekezea bundiki. Kitendo cha kujaribu kuingia ndani ya gari, akatandikwa risasi ya bega na akaanguka chini. Mvua ya risasi ikaanza kuwanyeshea. Hakika hapakuwa na aliye tarajia kukutana na kipigo kama hicho. Wanajeshi wa Tanzania wakazidi kuwashambulia wanajeshi wa nabii Sanga ambao walijikuta wakitawanyika kwa kukimbia huku kila mmoja akijitahidi kuhakiki ana okoa maisha yake kwani ambushi hiyo hawakuitegemea.
***
“Mbona mitaa ipo kimya sana?”
Cleopatra alimuuliza mlinzi wa RPC Karata huku wakiwa katika gari hilo la RPC.
“Kun oparesheni inayo endelea ya wanajeshi hivyo hakuna gari wala mtu anaye ruhusia kukota nje kwa msaa zaidi ya sita.”
“Duuu”
“Ndio”
“Mbona wewe una endesha?”
“Hii gairi ni ya RPC hivyo ina julika”
“RPC mwenyewe yupo wapi?”
“Ikulu”
“Sawa sawa”
Wakafika ikulu na kijana huyo akaeleza kwamba Cleopatra ni mgeni wa RPC hivyo akaruhusiwa kuingia.
“Uta pumzika hapo hadi RPC atakapo toa commanding room”
“Sawa je jenerali yupo?”
“Ndio naye yupo kwenye chumba hicho. Wakitoka ndio uta kutana nao”
“Sawa”
Cleopatra akaa kwenye chumba maalumu cha wageni kupumzika. Mlinzi wa raisi Mtenzi akaingia sebleni na kumuita Jery pembeni ili wazungumze. Wakatoka nje ya seble hiyo kwa ajili ya mazungumzo.
“Vipi?”
“Sio shwari”
“Una maanisha nini?”
“Mzee kwa sasa yupo kizuizini na nchi ina ongozwa na jeshi na jenerali sasa hivi ndio raisi wa muda”
Jery akastuka sana huku akimtazama mlinzi huyo.
“Acha kunitania?”
“Huo ndio ukweli. Raisi kwa sasa yupo kizuizini na haruhusiwi kuonana na mtu yoyote na hadi hapa ninavyo zungumza ni kwamba wana jeshhi wame funga mitaa yote na watu wote wapo ndani, huko barabarani hakuna gari linalo ruhusiwa kutembea”
“Hembu hayo melezo njoo uyazungumzie huku ndani kwa maana nina hisi una nichanganya”
Wakarudi sebleni na kuka kwenye sofa zilizop hapo sebleni.
“Baba kuna tatizo lime tokea”
Jery alianza kuzungumza na kumfanya nabii Sanga kukaa vizuri.
“Kuna nini mwanangu”
“Ahaa baba ame wekwa kizuizini na sasa hivi jeshi ndio lina ongoza nchi”
“NINI?”
Nabii Sanga alihamaki huku akihisi kama tumbo likimkata kwa maumivu makali.
“Ndio mzee. Sasa hivi jenerali wa jeshi ndio raisi wamuda. Amemtoa madarakani raisi Mtenzi na kumuweka kizuizini mara baada ya kugundua kwamba kuna wanajeshi ambao wame vamia jiji hili na hawajulikani ni wapi walipo tokea. Raisi alipaswa kutoa amri kwa jeshi ila akashindwa. Hivyo ilimlazimu jenerali kuchukua mamlaka na inavyo sadikika kwamba wanajeshi hao ndio walio mteka makamu wa raisi’
Nabii Sanga akahisi kama nguvu za mwili zikimuishia. Taratibu akakaa chini huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana.
“Baba upo salama?”
Jery aliuliza huku akimsogelea baba yake mkwe.
“Yaa nipo salama. Vipi ime kuwaje?”
“Hapa ninavyo zungumza wanajeshi hao wame pewa ambushi ya maana na sidhani kama wata weza kutika ndani ya hili jiji wakiwa hai”
Maneno ya mlinzi huyo yakazidi kumfanya nabii Sanga kuhisi mapigo yake ya moyo yanayo kwenda kwa kasi kubwa yata toboa kifua chake.
“Baba hii presha”
Jery alizungumza huku akikimbilia chumbani kwake. Akamkuta Julieth akiwa ame lala fofofo kitandani.Jery kwa haraka akachukua kisanduku chake cha kuhifadhia vifaa vya huduma ya kwanza. Akatoka chumbani hapo na kurudi sebleni na kumkuta nabii Sanga akiwa ameiweka simu yake sikioni mwake. Simu ya kijana wake aliye toka kuongea naye muda mchache ulii pita, ina endelea kuita pasipo kupokelewa. Jasho jingi lina mwagika nabii Sanga usoni mwake, hakika katika siku aliyo pata mapigo ya kutisha ni leo.
“Baba kaa vizuri nikupime presha?”
“Hapana Jery. Nina hitaji kuondoka hapa ikulu, muamshe Julieth tuna ondoka sasa hivi”
“Samahani mze hilo halito wezekana kwa maana sisi walinzi wote wa raisi tume pokonywa silaha zetu. Ime tolewa hakuna mtu hata mmoja kutoka nje ya ikulu hii.”
“Nahiaji kuonana na huyo jenerali wa jeshi?”
“Haiwezekani mzee wangu. Yaani hapa ninavyo kuambia ni kwamba kuanzia getini hadi ndani ya ikulu, wanao linda ni wanajeshi na sio sisi walinzi wa raisi”
“Sawa ila nina hitaji kuondoka now. Jery muamshe Julieth tuna ondoka sasa hivi nina kwenda kuonana na huyo jenerali wa Jeshi”
Nabii Sanga alizungumza na kutoka sebleni hapo na kuwaacha Jery na mlinzi huyo kushangaa. Nabii Sanga akamuomba mwanajeshi mmoja kuitiwa jenerali wa jeshi.
“Mkuu kwa sasa yupo bize”
“Muambie ni dharura nina hitaji kuondoka”
Nabii Sanga alisisitizia, kutokana nabii Sanga ana sifa nzuri na watu wengi wana mfahamu kwamba ni mtu wa Mungu basi mwanajeshi huyo akamuelewa na akalekea katika commanding room na akamnong’oneza jenerali wa jeshi.
“Ana taka nini?”
“Sijajua mkuu ila na sehema ni muhimu sana”
Jenerali wa jeshi akatazama jinsi wanajeshi wake wanavyo endelea kupambana na wanajeshi wa nabii Sanga. Akanyanyuka na kutoka nje kwa maana hata yeye ana muheshimu sana nabii Sanga na isitoshe ni mara kadhaa ame kuwa akihudhuria katika kanisa la nabii Sanga kwa ajili ya kusali.
“Habari yako Jenerali”
“Salama heshimiwa yako mtumishi”
“Nashukuru ndugu yangu. Nina omba nafasi ya kuweza kuondoka hapa ikulu na kuelekea nyumbani kusali”
“Ahaa samahani mtumishi wa Mungu hivi sasa nchi ipo katika hali ya hatari hususani hapa Dar es Salaama hivyo huto weza kutembea kwa gari huko barabarani ni hatari sana”
“Nime kuja na helicopter yangu na nina imani nita ondoka nayo. Nina kuomba niondoke na mkwe wangu pamoja na binti yangu. Kukaa hapa ikulu na mke wangu alitekwa mbele ya macho ya watu wengi hivyo nina kosa amani sana ndugu yangu nina kuomba sana uweze kuniruhusu’”
Jenerali wa jeshi akamtazama nabii Sanga anaye omba kwa unyenyekevu. Kutokana ni mtu anaye muamini na kumuheshimimu sana, akamruhusu aweze kuondoka na helicopter yake.
“Mungu akubariki katika kila ulifanyalo”
“Nina shukuru sana mtumishi”
Nabii Sanga akarudi sebleni na kumkuta Jery na Julieth wakiwa salama. Wakaondoka na kuelekea kiwanja cha helicopter. Wakaingia kwenye helicopter hio na taratibu ikaanza kupaa kuelekea hewani.
“Tuelekee nchini Kenya”
Nabii Sanga alimueleza rubani wake na akatii.
“Baba vipi mama?”
“Ata patikana na kila jambo lita kwenda vizuri. Jery nina kuamini na nina imani kwamba uta mlinda mwanangu”
“Ndio baba nipo tayari kufa kwa ajili ya mke wangu”
Jery alizungumza kwa msisitizo huku akimshika mkono wa kulia Julieth ambaye naye amejawa na wasiwasi kwa maana Jery alimueleza kinacho endelea huko mtaani na Jery pekee ndio hajui baba yake mkwe na mke wake ni watu wa aina gani.
***
“Jenerali pia kuna binti ana hitaji kukuona”
Mlinzi wa jenerali wa jeshi alizungumza kabla ya jenerali hajarudi kwenye chumba cha kuongozea oparesheni hizo.
“Ni nani?”
“Mtoto wa mzee Mbogo”
“Yupo hapa nchini?”
“Ndio na yupo hapa ikulu. Yupo katika chumba cha mapumziko”
“Twende nikamuone”
Jenerali akaanza kuongoza kwa mwendo wa haraka hadi katika chumba hicho. Alipo ingia tu, Cleopatra akanyanyuka kwa haraka na kamkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu huku akiangua kilio cha uchungu sana. Jenerali akamkumbatia kwa dakika kadhaa Cleopatra kisha akamuachia.
“Cleopatra mbona una lia mwaangu?”
“Ba mdogo, baba ame uwawa?”
Jenerali akastuka sana huku akimtazama Cleopatra usoni mwake kwa maana anacho jua yeye ni kutekwa kwa mzee Mbogo ila swala la kuuwawa kwake halitambui kabisa.
“Na nani aliye muua?”
“NABII SANGA NA WANAJESHI WAKE”
Jenerali macho ya mshangao yakamtoka kiasi cha kuhisi kupagawa. Akamtazama Cleopatra machoni mwake na kugundua kwamba anacho kizungumza ni kitu cha ukweli kwani ana mfahamu Cleopatra toka utotoni mwake na ana muelewa vizuri sana.
.
MWISHO
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 1/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 2/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 3/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 4/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 5/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 6/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 7/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 8/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 9/10
- SIN SEASON 2 SEHEMU YA 10 MWISHO
Ndio nn xaxa mwendelezo je,
ReplyDeleteInaumiza sana nyakati tulizo nazo ni za hatari sana tuwe making sana ukimwona mtumishi utadhani kondoo kumbe ni mbwa mwitu katika kundi la kondoo
ReplyDelete