DAPHINE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 10 KATI YA 10
Saa 9;47 ya usiku Ngesa aliegesha gari,umbali wa mita tisini kutoka katika nyumba ya Olina Kalumuna!Alichokiona,kilimfanya aogope zaidi karibu na geti aliona gari aina ya Carina na taa za nje za nyumba,hazikuwashwa hiyo ilimaanisha hakukua na mtu ama kama wapo basi walisahau kuziwasha,hakutaka kuumiza kichwa sana,alichokifanya ni kutoka ndani ya gari akiwa makini.
Wasiwasi wake ulikua mkubwa kwani hakua na silaha yoyote ile,alinyata kwa tahadhari mpaka alipoufikia ukuta wa nyumba hiyo ambapo sasa kando kulikua na gari,akatembea taratibu akijihami sababu hakua ana uhakika kama ndani kulikua na watu,alivyoufikia mlango wa gari akachungulia ndani kwa umakini hakukua na mtu yoyote!Alivyoangalia geti,lilikua wazi akatembea taratibu akitizama huku na kule.Milango yake yote ya fahamu,ilikua makini sana kuanzia hisia mpaka masikio!Alichokifanya ni kupitia mlango wa nyuma,ambapo huko alishangazwa na mazingira aliyoyakuta!Sufuria zipo chini na baadhi ya mabakuli yapo mezani,alivyoona kisu akakichukua na kukishika mkononi vizuri ili lolote litakalotokea,aweze kujihami.Taa ya hatari ikawaka kichwani kwake,baada ya kuona damu chini,akachuchumaa kidogo na kuigusa,alivyoinusa akashtuka kwani bado ilikua na harufu kwa harakaharaka aligundua damu hizo,zilitokea sio chini ya lisaa limoja nyuma!Sasa akawa makini zaidi kutembea,akatokezea seblen na kuona jinsi vitu vilivyo vurugika,kichwani alikua na mengi ya kujiuliza kwani upekuzi uliofanyika ulikua wa kitemi na kilichomsaidia kuona ulikua ni mwanga wa mbalamwezi.
Akaingia chumba baada ya chumba,lakini alivyofika cha mwisho alishtuka na moyo wake ukapiga kwa nguvu,juu aliona maiti ya mwanaume inaning’inia,pembeni yake kuna maiti nyingine imechomwa kisu cha shingo,kando kuna nyingine mbili zina matundu ya risasi!Akainama kidogo,harufu ya damu ilimfanya agundue mauaji hayo yalifanyika muda mfupi uliopita lakini hata hivyo hakuelewa nini kilitokea,mpaka maiti hizo zikawa kwa namna hiyo.Ngesa alikua katika kitendawili kikubwa sana ambacho alishindwa kukitegua,alivyojaribu kuunga matukio kunyongwa kwa mwanaume aliyekua juu,maiti mbili kupigwa risasi na moja kuchomwa kisu akashindwa kupata jibu!Kifupi alichanganyikiwa na hakuelewa aanzie wapi,alichokifanya ni kuingia kwenye makabati na kuanza kukagua.
“Griii griiii….Griii griiiii….griiii griiiii”
Mlio wa simu ulimshtua kwa kiasi cha kutosha,akatizama huku na kule kutafuta mlio huo unatokea wapi.Alivyotuliza akili,akaona mwanga wa simu unatokea chini kwenye maiti iliyochomwa kisu cha shingo, ambacho kisu hiko kilitokea upande wa pili,hiyo ilimfanya mpaka Ngesa ameze mate kwani muuaji huyo ilielekea alikua na hasira mno!Alivyoichukua simu,akaona jina ‘BIG’akasita kidogo lakini aliipokea na kuiweka sikioni.
“Mmefanikiwa?”
Upande wa pili,ukauliza.Ngesa akabaki kimya hakuelewa ajibu kitu gani!
“Halloo,Nyoka!Mmefanikiwa?”
“Ndio”
Ngesa akajibu kwa sauti ya chini kidogo ili kupima maji.
“Bosi anauliza huyo Malaya mpo naye?”
Sasa Ngesa akagundua kua upande wa pili wa simu,mtu anayeongea hakushtukia sauti.
“Ndio,tumlete wapi?”
“Subiri,nitakupigia nitakwambia pa kumleta!”
Hapohapo simu ikakatwa,alivyotaka kugeuka akashindwa kwani alipigwa ngumi kali ya shingo iliyomfanya apepesuke kama mlevi aliyelewa mnazi.
Hakukaa sawa,akachimbwa ngumi nyingine ya kidevu iliyomfanya ahisi taya yake ya chini imevunjika!Sasa akaona kuna hatari mbele yake,alivyoshika kisu vizuri ili kumkabili adui yake ambaye hakujua ni nani,mkono ulioshika kisu ukapigwa teke kisu kikadondoka kando!Sasa hapo Ngesa,akaona kuna ugumu mkubwa mbele na adui yake ni mtundu na hatari,alichokifanya ni kurudi nyuma hatua moja,akajifanya kama anarusha ngumi ya kulia lakini alizunguka na teke aina ya ‘round kick’ iliyomfikia adui yake kifuani,likampepesa mpaka ukutani,akili ya Ngesa ikafanya kazi kwa kasi ya kompyuta isiyokua na mafaili.Hapohapo,akajibetua kwa mtindo wa ninja na kumtandika pigo matata adui huyo,tumboni.Kilichomshangaza na kupigwa na butwaa ni baada ya kugundua mpambanaji huyo ni mwanamke,hiyo ni baada ya kushika nywele zake na kumbamiza kwenye kabati,Ngesa alikua mwepesi lakini mwanamke huyo alikua mwepesi mithili ya kambale kwenye tope kwani baada ya Ngesa kurusha ngumi akainama kidogo na kujibu mbili ambazo zilimfikia Ngesa kwenye mbavu,moja kulia moja kushoto.Ngesa akayumba kidogo lakini hakutaka kukubali,akazidi kumsoma mwanamke huyo hatari,ambaye alikua akichanganya mapigo mara kareti mara judo!Na mara kadhaa alichezesha miguu yake yaani alitumia pia mapigo ya kick Boxa,sasa hapo Ngesa alikua makini baada ya kuona teke la mwanamke huyo linakuja kiholela,akamdaka na kumnyanyua juujuu,ambapo alimbwaga kitandani na kumkunja vizuri mikono na miguu jambo lililomfanya mwanamke huyo,akukuruke lakini hakuweza kufua dafu,jinsi alivyoshikwa na Ngesa ilikua ni vigumu kuchomoka.
“DAPHINEEEE!!!!!!”
Ngesa aliita akiwa kama mtu asiyeyaamini macho yake.
“Ngesaaaaaaaa!”
Kumbe alikua ni Daphine,moyo wake ulipiga mkambo na furaha aliyokua nayo haikuweza kuelezeka kiwepesi kwani hakuna hata mmoja kati yao aliyeamini kama wangekutana, tena mbaya zaidi katika mazingira kama hayo.
***
“Griii griiii….Griii griiiiii”
Simu kutoka kitandani,iliwashtua Ngesa na Daphine wakiwa katikati ya mikakati na mipango yao!Kila mtu aliitupia macho lakini kwa Ngesa,swala hilo halikua ngeni alishaelewa mpigaji angekua ni yule aliyemtaka Olina Kalumuna,akamtizama Daphine kwa kitambo na kuiweka simu sikioni.
“Nyoka”
Upande wa pili wa simu ukaita,ilikua ni sauti nzito ya kitetemeshi.
“Sema”
Ngesa akaitikia nayeye huku akijaribu kubadilisha sauti ingawa alishaelewa mtu anayezungumza naye hata yeye aliagizwa vile vile na hakumjua Nyoka kwa sura wala sauti yake,hakuijua pia.
“Unapajua Vingunguti,kyembe Mbuzi?”
“Ndio”
“Fika hapo nipigie simu,huyo Malaya upo naye hapo?”
Ngesa akatafakari kidogo na kuguna huku akimuangalia Daphine,ambaye alimtingishia kichwa kua aseme ndio.
“Yupo”
“Angalia,asionekane kua makini”
Simu ilivyokatwa tu,ikabidi Ngesa aseme kila kitu kilichotokea na ni kwanini yupo mahali hapo,hata hivyo walijikuta wapo kwenye misheni moja ya kumsaka muhusika aliyetega bomu lakini kwa Daphine alichotaka kujua ni wapi Brigedia Karanje alipo kwani alikua na biashara naye nzito sana,alikua mwenye hasira za kumuua kwa mikono yake mwenyewe ndiyo maana muda wote alibana meno!Kuanzia hapo,hakukua na muda wa kupoteza zaidi ya kutoka nje ambapo huko walitembea hatua za miguu kumi na kukunja kushoto,wakakutana na gari aina ya Pickup hardboard,wote wakaingia ndani!Sura alizoziona Ngesa ndani zilimfanya atake kujua nini kimetokea.
“Huyu ni Olina”
Daphine,akatoa utambulisho mfupi.
“Namfahamu”
“Frank Ntagara,nadhani unamjua”
“Ntagara,imekuaje yupo hapa?”
“Ni stori ndefu,Ngesa hatuna muda wa kupoteza inabidi kazi hii iishe kabla hakuja pambazuka”
“Olina,unaweza kukumbuka siku ndege inalipuka jana yake ilikuaje?”Ngesa akaanza kuhoji.Hata,hivyo Olina hakua na sababu tena ya kubaki na kitu chochote kile ndani ya kifua chake,akazungumza kila kitu,wanaume wawili waliingia ofisini kwake wakiwa na bastola wakimtaka azime kamera zote!
“Kwa sura unaweza kuwafahamu?”
“Mmoja nikimuona nitamjua”
“Sawa,usijali”
“Inabidi niende na Olina.Simu hii,itaniongoza”
“Ngesa huo ni mtego watakuua wakikugundua”Daphine,alishikwa na wasiwasi na alihisi kuumia kwani aliona ni jinsi gani mambo yangeenda kuwa magumu endapo wangegundua kua ni Ngesa anawachezea mchezo!
“Nilizaliwa mara moja na nitakufa mara moja”
Ngesa alivyomaliza kauli yake,akateremka ndani ya gari na kuzunguka upande wa usukani ambapo Daphine aliruka upande wa kushoto na safari ikaanza hapohapo,hakukua na maongezi mengine zaidi ya Ngesa kuipeleka akili yake kazini.
“Dustan yuko wapi?”
Ngesa akatupa swali,akimuangalia Daphine kisha kurudisha macho yake mbele akiwa makini anaendesha gari.
“Mpaka sasa hivi sijui alipo,tangu mlivyoondoka siku ile hospitalini”
“Jaqlin?”
“Yupo Bagamoyo,sehemu salama”
“Sawa”
Mbele yake kulikua na gari ndogo aina ya Mark II ikiwa katika mwendo wa taratibu,hakutaka kuremba zaidi ya kupandisha gia na kulipita gari hilo.Alivyofika Buguruni,akanyoosha moja kwa moja ambapo kulikua na utulivu wa hali ya juu isipokua dada poa waliokua wanaranda kuwinda wanaume katika ‘bar’ maarufu inayoitwa Kimboka,hakua na habari nao zaidi ya kupiga honi ili wapishe barabarani na kuzidi kusonga mbele.
Moyo wake haukutulia hata kidogo maneno ya Daphine yalipita kichwani kwake,akaingiwa na hofu na kuanza kuogopa itakuaje endapo wangemgundua kabla operesheni yake haijakamilika,alivyokumbuka mateso aliyopitia aliogopa zaidi,hata hivyo hakutaka kuurudisha moyo wake nyuma ilikua ni lazima amalize alichokianza,gari lilitembea umbali wa kilomita kama tano,wakawasili Kyembe Mbuzi,taa kali za baadhi ya viwanda zilimulika na kufanya eneo hilo liwe kama mchana kweupe kiasi kwamba hata ungedondosha sindano ungeiona.
“Frank,nipe koti lako”
Ngesa akasema na alivyofanya upekuzi ndani ya gari,akafurahi baada ya kuona kofia ya ngozi aina ya kapelo,akaiweka kichwani na kuvuta kioo cha katikati akijaribu kujiangalia kama angegundulika kwa urahisi,akaishusha kidogo machoni na kupewa koti la rangi ya kijivu,lilikua ni koti zito kiasi!Hakutaka kwenda mbali,alivyoona kuna nafasi ya kuweka gari,akapaki kando ambapo mbele kidogo kulikua na ‘bar’ inayowaka waka taa kwa juu,hakutaka kupoteza muda zaidi ya kuchukua simu na kuipiga namba ya mtu ambaye hata yeye hakumjua anafanana vipi.
“Nipo Kyembe Mbuzi”
Ngesa akasema!
“Kyembe mbuzi ni kubwa”
“Hapa hapa kwenye soko la Mbuzi”
“Mbele yako unaona nini?”
“Kuna lori la mafuta”
“Kuna bar hapo,achana nayo izunguke kwa nyuma kuna nguzo ya umeme simama hapohapo, Nyoka”
Ngesa alivyosikia hivyo,akamuangalia Daphine!
“Inabidi mshuke mniache na Olina,kama una bastola nipatie”
Operesheni ilikua mbioni kuanza na Ngesa hakuonesha wasiwasi wowote isipokuwa Olina,ambaye muda wote alitetemeka mithili ya mgonjwa mwenye homa ya usiku,Ngesa aliliona hilo na kumgeukia!
“Olina,nisikilize kwa makini.Nachokuomba usiwe na wasiwasi,hawawezi kukufanya chochote!Cha muhimu wasijue kama tupo pamoja,umenielewa?”
“Nao…ogopa na..gopa”
“Usiogope,unavyotuona hivi wote tupo kulinda usalama wako!”
“Sa….waaaa”
Olina alibubujikwa na machozi ya uchungu,roho yake ilikua katika mzani wa kifo na alielewa kabisa hatari yake endapo mambo yangeenda kinyume,kifupi alianza kusali sala yake ya mwisho!Ilibidi Daphine atoe bastola yake na kumkabidhi Ngesa,ambapo mwanaume huyu bila wasiwasi akachomoa ‘magazine’ na kuridhika kwani ilijaa risasi za kutosha,alichokifanya ni kujiinua kidogo na kuipachika nyuma ya kiuno!
“Ngesa,kua makini.Nipo nyuma yako”
Daphine akasema na kumtizama Ngesa kwa macho fulani ya kumtia moyo!
“Ahsante Daphine,Olina tushuke”
Ngesa alivyoteremka tu,akavuta kofia kwenye macho na kumshika Olina mkono na kuanza kusonga mbele,ambapo mbele kidogo kulikua na kichochoro chenye giza totoro!
Mbele yake,akaona nguzo ya umeme na kuyakumbuka maelezo ya mtu aliyezungumza naye kwenye simu, akatembea na kusimama eneo hilo huku akiwa makini kuangalia huku na kule,dakika moja baadaye akahisi hatua za mtu zinakuja upande wa kushoto akatulia kidogo na kumuona mwanaume mfupi,aliyevaa singlendi hakuweza kumuona vizuri usoni lakini alivyomuangalia kiunoni akaona amechomeka bastola.
“Wewe ndio Nyoka?”
Jamaa huyo akauliza huku akimuangalia Ngesa kwa umakini,kisha macho yake akayapeleka kwa Olina.
“Ndio mimi”
“Twendeni huku”
Jamaa huyo mbele, Ngesa nyuma akiwa na Olina walianza kuongozana mpaka kwenye kona nyingine ya kulia ambapo walitokea kwenye mlango mdogo wa bati,akausukuma na kuingia ndani.
Kwa haraka Ngesa akaanza kukagua eneo zima na alichunguza kila kitu na kuangalia ukuta huo ulivyo,hiyo ndiyo ilikua kanuni yake ya kwanza kukagua eneo endapo ikitokea rabsha yoyote ajue ni wapi ataanzia!Walivyotokezea kwenye uwazi,wakavuka chumba cha kwanza na kuingia cha pili!Ambapo ndani,alikutana na wanaume wanne walioshiba na kujazia miili,bila shaka walikua wanyanyuaji hodari wa vyuma vizito,maana vifua vyao vilituna vikafanana na matako ya nyani.
“Nyoka,safi sana!Kaa hapo”
Alichogundua Ngesa ni kwamba hakuna hata mtu mmoja kati yao alimyemjua huyo mtu anayeitwa Nyoka kwa sura,hiyo ilimpa wasiwasi sababu aliamini mtandao ni mkubwa mno na mtindo wa namna hiyo hupenda sana kuutumia majasusi wa kirashia!Mmoja kati ya mabaunsa hao,akasimama kwa mbwembwe na kumuendea Olina.
“Mrembo,usiogope sana!”
Alivyoongea hivyo,akatoka kando kidogo na kutoa simu yake ambapo alisikika akiongea na upande wa pili,Ngesa hakuweza kusikia lakini alichojua kua anazungumza na mkuu wake wa kazi.
“Nipo hapa na Nyoka,huyo Malaya pia yupo naye hapana yupo Nyoka peke yake!Tumuuwe?Anhaa,wapi?Kunduchi,sawa tunakuja”
Mapigo ya moyo ya Ngesa sasa yalianza kupoteza utulivu,lakini akajaribu kuificha hofu yake isionekane kwa jicho pembe,akamuona yule baunsa aliyetoka kuongea na simu anamuita mwenzake nje.Ni kitendo kilichomfanya aone kuna hatari kubwa mbeleni na si ajabu,alijulikana tayari,hata hivyo alijipa subira kwanza na kutulia huku taratibu mkono wake ukisogea nyuma ya kiuno ili kuikaribia bastola yake.
“Mwenzako yuko wapi?”
Lilikua ni swali lililomlenga moja kwa moja Ngesa.
“Nimemuuua”
Ngesa akapata jibu la haraka ambalo hata yeye hakutegemea kulitoa,alichoelewa yeye alikua katika mtego mkubwa na alijua kivyovyote vile baunsa huyo anamuulizia,mtu aliyekua na Nyoka!
“Kwanini?”
“Alitaka kunizunguka,aniue lakini nikamuwahi mtu mnayemtaka ni huyu hapa,mbona maswali mengi?Hatuaminiani?”
“Sasa wewe utabaki hapa sisi tutaondoka na Olina”
Jasho jembamba lilimtoka Ngesa na jambo hilo halikua utani hata kidogo kwani Olina aliinuliwa kitemi,Ngesa alivyotaka kusimama akatulizwa na kitako cha bunduki cha kichwa,kikamchana na damu kuanza kumvuja!Ni tukio lililomfanya aone mambo yameharibika tayari lakini hakutaka kulianzisha,akatulia kimya.Walichokifanya ni kumsachi na kuitoa bastola yake iliyokua kiunoni.
“Mnataka kuniua?”
“Sisi kazi yetu ni kutekeleza amri ya mkuu”
Olina alipiga kelele na alielewa kifo kipo karibu yake,akamtizama Ngesa aliyekua juu ya kiti kawekwa chini ya ulinzi,matumaini ya uhai wake yakawa asilimia kumi kati ya mia moja!Bila kujali chochote,wakamtoa Olina nje kinguvu ndani wakabaki wanaume wawili waliojazia miili yao,wanamtizama Ngesa kwa uchu huku mikononi wameshika bastola.
****
Safari yake ya kujitoa muhanga isingekua na maana yoyote ile endapo angeruhusu wamchukue Olina Kalumuna,hilo lilikua mbioni kutokea kwani mpaka dakika hiyo aliwekwa chini ya ulinzi na Olina alikua tayari keshatolewa nje,kwa maana hiyo wasingekua na sababu yoyote ile ya kumuacha hai,Ngesa akawa tayari kainusa harufu ya kifo!Hofu ilimtanda ingawa alijipa matumaini kua Daphine yupo nje, hata hivyo katika maisha yake hakutaka kulipa swala la kumuamini binadamu mwenzake asilimia mia moja,ndiyo maana alianza kuisumbua akili yake ni kwa namna gani angeweza kujikomboa dhidi ya watu hao hatari wasiokua na punje ya huruma hata kidogo!
Kifupi Ngesa alijihurumia baada ya kukumbuka kashkash alizopitia tangu anaanza harakati,hakukumbuka alipata muda gani wa kupumzika hilo lilimfanya ajutie kujiingiza kwenye mkasa huo na serikali,ikampelekea mpaka aapie operesheni hiyo ikimalizika atafute sehemu apumzike ama nchi yoyote jirani,kiherehere chake kilimuingiza kwenye matatizo mazito sana!Mbali na misukosuko iliyotokea nyuma hakuacha kumshukuru Mungu kwa kumuepusha na aina nyingi za vifo,ambavyo aliponea chupchup kwenye tundu la sindano.Mkakati wa kuuwawa kwake wakidhani ni Nyoka ulifikia tamati baada ya kufikishwa chini ya mti mkubwa ambapo hapo aliambiwa apige magoti na kugeukia upande wa Mashariki kwa maana hiyo,awape mgongo wampige risasi ya kisogo!
“Kwanini usiniue huku unaniangalia usoni?”
Ngesa akahoji akipima maji na kujaribu kununua muda,hata hivyo hakuna hata mmoja kati yao aliyemuongelesha zaidi ya kumpiga piga mgongoni!
“Piga magoti hatuna muda wa kubembelezana,sisi tunapewa oda tu hata tukitaka kukuua huku unatuangalia, poa”
“Nani kawatuma mniue?”
“Piga magoti”
Watu hao ilionekana hawakutaka mazoea kabisa na Ngesa na walitaka kuyapeleka mambo harakaharaka,wamuue kisha waendelee na taratibu nyingine kwani mara kwa mara walipokea simu.
“Tunamalizia ile kazi,tunakuja sasa hivi”
Mmoja kati yao alimaliza kuongea na simu kisha kukata,moja kwa moja Ngesa akajua kazi wanayotaka kuimalizia niya kumuua kisha waondoke zao,moyoni aliomba Mungu Daphine awahi vinginevyo angeuwawa sababu hakukua na jinsi yoyote ile ya yeye kujikomboa labda tu muujiza ungetokea!Alivyotaka kujikomboa kwa kufanya purukushani akajionya kwani aliamini angefanya mjongeo wowote usio rasmi angeharakisha kifo chake!
“Kacha kacha”
Mlio huo wa bastola kukokiwa ulimfanya ameze mate mazito ya uchungu sasa aliamini wakati wake umefika,akafumba macho akisubiri risasi imfikie na kumuondoa duniani lakini cha ajabu sekunde tatu nzima zilipita bila kusikia chochote kile,hakutaka kufumbua macho yake mpaka aliposikia jina lake linaitwa,akashusha pumzi ndefu baada ya kugundua ni sauti ya Daphine!
“Tuondoke Ngesa”
Alivyosimama akaona maiti iliyochomwa kisu kirefu cha shingo kilichotokezea upande wa pili,mpini ukabaki nje!Ni mauaji yaliyomfanya akumbuke maiti aliyoikuta kwa Olina Kalumuma sasa akajua ni nani aliyefanya mauaji yale,hata hivyo hakutaka kutia neno lolote lile zaidi ya kusimama na kumtizama Daphine.
“Frank yuko wapi?”
“Anamfuatailia Olina,mimi nimekuja kwako”
Baada ya Daphine kusema hivyo,akamkabidhi Ngesa bastola kama silaha ya kujihami,wakaanza kutembea mpaka walivyotokea kwenye mlango mkubwa ambapo hapo walimuona Mwanaume mrefu amekaa kwenye sofa, bastola ipo mezani hana wasiwasi wowote ule!Kufumba na kufumbua,akawa amepigwa na butwaa tayari kwani Daphine na Ngesa walikua mbele yake wakiwa na bastola mikononi.
“Wameenda wapi?”Ngesa akauliza!
Mkono wa jamaa huyo ukaanza kwenda nyuma taratibu huku akijaribu kuwazuga hakuelewa hila yake iligundulika mapema kwani alivyochomoa bastola kwa kasi,hakucheleweshwa risasi nne zilichomoka, mbili zilitoka kwa Daphine na mbili kwa Ngesa wote walimlenga na kuacha matundu makubwa mwilini mwake,akabaki ameacha mdomo wazi huku bastola yake ikiwa mkononi!
Hawakua na muda wa kupoteza zaidi ya kuanza kutoka nje kwa haraka kuhofia kujaza watu eneo hilo, sababu waliamini mirindimo ya risasi ingeibua hali ya sintofahamu!Walivyotokezea kwenye ‘bar’ wakanyoosha moja kwa moja na kukunja kushoto ambapo walitokea kwenye ukuta mrefu,mbele kuna geti.Ilikua kama Mungu yupo upande wao,sababu waliona taa za gari linakunja kuelekea getini,kabla geti halijafunguliwa Ngesa akavuka upande wa pili wa gari na kumtoa mwanamke aliyekua anaendesha gari kitemi.
“Toka ndani ya gari Mama”
Mwanamke huyo kwa kutetemeka akashuka na kulala chini kwenye mchanga,Ngesa akaingia kwenye usukani Daphine akapanda na safari ikaanza hapohapo, ambapo kitu cha kwanza kilikua ni kumsaka Frank Ntagara hewani.
“Morogoro Road,Magomeni Mapipa”
“Poa,tunakuja”
“Upo na Ngesa?”
Frank Ntagara akauliza akitaka kujua kama Daphine alifanikiwa kumkomboa Ngesa.
“Yes,nipo naye”
“Thank God”(Ahsante Mungu)
Ngesa alikua makini kwenye usukani na aliendesha gari kwa kasi mikono yote miwili ikiwa juu ya usukani,hasira zake zilikua waziwazi na alitamani kuwahi sehemu ya tukio ahakikishe kila kitu,alivyoona mbele kuna gari akakunja kushoto na kupanda tuta la katikati,akatokezea upande wa pili ambapo huko aliingia barabara ya vumbi,niya yake ilikua kufupisha njia alivyokaribia kufika Magomeni Mapipa,akapunguza spidi ya gari na kumtaka Daphine ampigie simu Frank Ntagara ili ajue ni wapi,wangepaki!
“Magomeni Mapipa,kunja kushoto kuna barabara ya Vumbi mtaa wa kwanza wa pili…Daphine,Mungu wangu”
“Frank,kuna nini?”
“Kuna gari,imekuja mbele yangu!Wamemuingiza Olina”
“Whaaat?”
“Ndio fanyeni haraka”
“Tunakaribia”
“Jesus,wameniona”
“Frank….Frank….Frank”
Daphine aliita baada ya ukimya wa ghafla jambo lililomfanya Ngesa amtizame kwa makini akitaka kujua nini kimetokea.
“Toka nje ya gari,sasa hivi.Nitakuuua,toka nje ya gari wewe ni nani?…Shuka”
Simu ilikua bado hewani na Daphine alisikia sauti za watu watatu kisha mpasuko mkubwa wa kioo,tukio hilo likamfanya aingiwe na mashaka pamoja na hofu kumtanda,ndani ya sekunde mbili simu ikakata!Kwenye kona ya kushoto Ngesa aliingia nayo akiwa na mwendo uleule mkali,akapiga breki tairi zikapiga msele,bila kupoteza muda akashuka na kuweka bastola yake kiunoni!Daphine hakua mbali,nayeye akawa nyuma!Mbele akaona gari alilokua anaendesha Frank Ntagara,mlango upo wazi kioo kimepasuka!Akatembea kwa tahadhari,na kuona simu ya Frank Ntagara imepasuliwa vipande vipande!Walivyotizama kulia kwao,wakaona taa za gari zinaishia kukata kona hapohapo wakaingia ndani ya gari kwa safari ya kuwafuata.
******
Waziri mkuu Okama,muda wote alikua katika presha kubwa!Asingeweza kuishi kwa amani endapo angemuacha Olina Kalumuna akiwa hai,taarifa zote alipewa na watu aliowatuma kwamba kuna kijana mdogo anayeitwa Frank Ntagara anataka kufukua makaburi,ndiyo maana akawahi kuwatuma vijana wake wamuue Olina Kalumuna,akiamini kwa kufanya hivyo angeishi kwa raha mustarehe bila wasiwasi wowote ule!Jumba lake lilikua kubwa sana na muda wote alikua na simu mkononi akitaka kujua mchakato ulifikia wapi,taarifa za kua Rais Leslie amekufa zilimfanya apate nguvu kwa kiasi cha kutosha mbali na kujutia kwa kutega bomu lakini hakutaka kujilaumu kwa chochote kilichotokea, isipokua angejilaumu sana kama Olina Kalumuna angekua hai.Waziri Okama tangu,afanye ukatili huo miyenendo yake ilibadilika kwanza alitembea na walinzi kila mahali cha pili alimkodi mpiganaji maarufu Zeliytan Humudi kutoka visiwani Zanzibar,alikua ni bondia maarufu na hatari kuliko kitu chochote kile huyo ilisemekana kwamba mafunzo yake alisomea Hongkong ili alinde usalama wa Waziri Okama alimpa kazi ya kumuendesha kila anapoenda!Mbali na kuimarisha ulinzi wake lakini bado alikua na mashaka,akiwa chumbani kwake simu yake ikaita ambayo ilimshtua sababu ilitoka kwa vijana wake.
“Kuna tatizo Mtukufu”
Upande wa pili wa simu ukasikika.
“Tatizo gani tena?”
“Kuna mtu alikua anatufuatailia”
“Ni nani?”
“Tumekagua kitambulisho chake,anatoka idara ya usalama wa taifa.Frank Ntagara”
Hapo Waziri Okama,alikaa kimya kidogo akitafakari.
“Halloo Mtukufu”
“Mleteni hapa kwangu tumuhoji”
“Na huyu Olina?”
“Muuweni”
Ilikua ni oda na kazi ilitakiwa ifanyike kwa wakati huohuo!Hakukua na njia ingine ya kubadilisha maamuzi isipokua ni kumuua Olina Kalumuna na kumpeleka Frank Ntagara akiwa hai.Ndani ya gari,walikua wanaume sita,wanne nyuma wawili mbele akiwemo dereva!Olina na Frank waliwekwa siti ya nyuma wakiwa wamefunikwa na vitambaa vyeusi,mikono na miguu yao imefungwa!Hawakujitofautisha na kuku wanaoenda kuchinjwa kwani hawakujua hatma yao!
“Tuombe Mungu,usijali Olina”
Frank Ntagara akasema kwa namna ya kumtia moyo Olina,gari lilitembea kwa umbali wa Kilomita ishirini na kusimama ghafla!Mlango wa nyuma ukafunguliwa Olina na Frank wakaburuzwa na kutupwa chini.Eneo hilo lilikua na upepo mkali kwa hisia kabisa walielewa ni lazima kungekua ni kandokando ya ufukwe wa bahari.
“Kuna mmoja kati yenu,safari yake itaishia hapa!”
Yalikua ni maneno ya kutisha kwa Olina na Frank,vitambaa walivyofungwa usoni viliwafanya wasione mbele,wote wakaanza kusali sala zao za mwisho!
“Fanya haraka,Kitulo!Tumalize kazi,tuondoke muda umeenda sana”
“Poa,dakika moja”
Kauli hiyo ilimfanya mwanaume huyo amvute Olina na kumburuza kama mzigo mpaka pembeni kabisa tayari kwa kumtoa duniani!
Hawakujua kua gari anayoendesha Ngesa ilikua kando umbali wa mita sabini upande wa Mashariki,kila kilichoendelea walikiona na alichokifanya Daphine ni kuteremka ndani ya gari kimya kimya na kuanza kunyata,umakini wake ulikua mkubwa kwa wanaume wawili,mmoja aliyekua mbele kando ya mti mwingine aliyeshika bastola anataka kumuua Olina!Kwa mwendo wa paka taratibu,akamfuata mwanaume aliyekua kando ya mti na kumtandika pigo moja la Judo shingoni,alivyotaka kutoa bastola mkono wake ukashikwa kwa utaalam na ufundi ukavunjwa!Kutokana na mawimbi ya bahari,ilikua ni vigumu purukushani hizo kusikika.Jamaa huyo alivyotaka kurusha ngumi akashindwa kwani Daphine alimtandika pigo moja la kareti lililomdondosha chini na kulamba mchanga,hakutaka kumkawiza akamshika shingo yake na kuivunja!
Mawimbi ya bahari yaliendelea kupiga na kusababisha mvumo mkubwa wa sauti,hiyo ilimfanya Daphine aendelee kufanya kazi yake kiwepesi zaidi.Bahati nzuri ilikua kwake sababu hakushtukiwa na sasa mbele yake,alisimama jamaa mwenye bastola kamuelekezea Olina anataka kumuua,alichokifanya Daphine ni kuweka bastola yake kiunoni na kutoa kisu kirefu,akanyata taratibu mpaka nyuma yake!Kiutaalam na kwa mtindo wa Ninja akamvuta jamaa huyo nyuma na kumchoma kisu shingoni,kukuruka yake ilifanya afyatue risasi moja hewani.Kelele za bastola hiyo iliwashtua wauaji wengine waliokua ndani ya gari,mmoja alivyotaka kutoka akarudishwa na ngumi takatifu ya Pua kutoka kwa Ngesa aliyekua kando ya gari,alivyoona wengine wanataka kuleta vurugu hakutaka kupoteza muda akawatandika risasi hapohapo!Ki ukweli alichukia sababu alitamani operesheni hiyo iende kimyakimya lakini hakua na jinsi kwani alifanya ukombozi na sasa Olina pamoja na Frank Ntagara walikua hai,kwa mbali akamuona Daphine na Olina wanasogea upande wake,wakafika mpaka alipo!Olina,alilia muda wote hakutaka kuamini kua amekipiga chenga kifo,kwake ulikua ni kama muujiza na shukrani alizotoa hazikua na idadi kamili.
“Tunataka kujua nani kawatuma”
Lilikua ni swali kutoka kwa Ngesa,akimuuliza muuaji aliyemtandika ngumi ya pua!Hakukua na punje ya mzaha hata kidogo ndani ya swali lake na sura yake ilikua ya kinyama,isiyohitaji majibu ya mkato!
“Paaaaaaaaa”
Mlio mkubwa wa bastola ulisikika,Ngesa hakutaka masihara wala kupotezewa muda hiyo ilimaanisha swali linalofuata lijibiwe kwa wakati bila kusua sua,kelele alizotoa jambazi huyo huku akiwa ameshikilia paja lake zilimfanya Olina aangalie pembeni na kuhisi huruma,hata Ngesa alimtisha pia kwa ukatili alioufanya.
“Sipendi kupotezewa muda,risasi inayofuata ya kichwa”
Sasa bastola akawa ameelekezewa kichwani kwa jamaa huyu,hiyo ilimaanisha kucheleweshewa jibu lake angeuliwa.
“Nananana mimi sijui chocho…te”
“Sawa…Paaaaaaaaa”
Risasi nyingine ikapenya mguu unaofuata sasa hiyo ilimfanya jambazi huyo apige yowe na kutaja jina la Mungu wake,damu nyingi zilimvuja miguuni lakini kwa Ngesa kwake ilikua kawaida sana sababu vitu kama hivyo alivizoea na hakutaka kitu kingine isipokua majibu yaliyonyooka!
“Eeeh Mu…ngu baba Yesu wa Nazareth nasemaaa nasemaaa tafa…dhali usiniue”
“Nakusikiliza”
“Waziri Okama,ndiyo alitupigia simu tu…tumpeleke Frank Ntagara na tumuuwe Olina”
“Na ndiyo huyo aliyetega bomu?”
“Ha..po sina uhakika”
“Nataka kukwambia kitu kimoja,uhai wako upo mikononi mwangu.Piga simu,mwambie kazi aliyokutuma umemaliza!Naomba nikuonye kitu,ukithubutu kuzungumza kitu chochote cha kipumbavu.NITAKUUA”
Ilikua ni amri na ni wazi kabisa kifo kilikua mlangoni kwa muuaji huyu ambaye alitambulika kwa jina moja Elias Mufindi,alilia kwa kwikwi na maumivu aliyohisi hayakua na kipimo chake mbaya zaidi alishindwa kusimama,alivyochukua simu akabonyeza namba fulani na kupiga,alivyoweka sikioni Ngesa akamuonya aweke laudispika ili wote wasikie,simu ikaita mara mbili na kupokelewa.
“Kazi imeisha nadhani”
Ngesa alitetemeka kwa hasira na hakutaka kuamini baada ya kusikia sauti ya Waziri Okama simuni,aliumia moyo kwa vitu chungu mzima,Waziri Mkuu alikua mwanaume mkarimu na mwenye moyo wa utoaji!Hata hivyo hakutaka kutia neno lolote zaidi ya kusikiliza maongezi huku akitafakari ni aina gani ya kifo kingekua halali yake.
“Ndio”
“Changudoa yule,mmemuua?”
“Tayari”
“Ntagara,upo naye?”
“Yes,yupo nyuma ya buti”
“Kua makini sana,tukutane Mikocheni Kwa Warioba nyumbani kwangu pale!Aaaah upo na Sele karibu hapo?”
Swali hilo kutoka upande wa pili lilimfanya Elias amuangalie Ngesa!
“Hallooo”
Upande wa pili wa simu ukasikika baada ya Eliasi kusita kutoa jibu.Ngesa akamtingishia kichwa akatae.
“Hapana,sipo naye”
“Yupo wapi?”
“Yupo kwenye gari la nyuma,hapa nipo peke yangu”
“Natangulia Mikocheni,hakikisheni maiti mmeitupa katikati ya bahari”
“Tumefanya hivyo”
“Okay,nawasubiri….titititi”
Simu ikakatwa,hakukua na muda wa kupoteza zaidi ya Ngesa kuingia nyuma ya usukani na kumweka Elias pembeni ili amuongoze njia,kwani nyumba ya Waziri Okama iliyokua Mikocheni hakuijua!Olina na Daphine pamoja na Frank Ntagara waliingia ndani ya gari,Ngesa akapiga gia na mkono wake uleule ulioshika bastola,gari likatoka kwa kasi na kuingia barabarani!Usiku ulikua mkubwa na Ngesa alihisi kuchoka,akitamani zoezi hilo liishe kabla hakujapambazuka hasira zake ghafla zikahamia kwa Waziri Okama,alijiuliza maswali mengi sana ilikuaje atege bomu kwenye ndege ya Rais Leslie!Waziri Okama na Brigedia Karanje wana mahusiano gani?
“Umefanya kazi na Waziri Okama kwa muda gani?”
Lilikua ni swali lililomlenga Eliasi akiwa siti ya pembeni,ameshikilia miguu yake inayovuja damu!Hiyo ilimfanya atetemeke na kuhisi homa kali sana.
“Ndio mara ya kwanza,ndio mara ya kwanza Haki ya Mungu”
Eliasi aliujua mziki wa Ngesa tayari ndiyo maana akaapia ili kupigilia sentensi yake msumari,alijua fika kinachofuata hapo ni risasi.
“Ulijuana naye vipi?”
“Mimi nilipigiwa simu na Kombo”
“Kombo ni nani?”
“Ni mshkaji wangu,ndio bosi wetu pale gereji”
“Gereji ipi?”
“Magomeni”
Mahojiano hayo,yaliwafikisha mpaka Mwenge mataa wakakunja kushoto na kuanza kuitafuta barabara ya Coca Cola,walivyofika Mlalakua Ngesa akachepukia kulia na kuingia barabara ya vumbi ambapo mbele kidogo alikuta lami na kutokea kwa Warioba.
“Wapi?”
“Upande wa pili,nyoosha na huo mtaa”
Maelekezo ya Eliasi yalimfanya Ngesa aanze tena safari na walivyozipita nyumba nne,akaambiwa apunguze mwendo kwani wanakaribia ni kweli haukua utani.Mita chache tu,wakawa wanauona ukuta mrefu wenye rangi nyeupe na juu una nyaya za umeme.
“Ndio pale”
“Mpigie simu mwambie umefika”
“Sawa”
Simu ikapigwa na Waziri Okama akawa kwenye laini anatoa maelekezo kua waingie ndani,mlinzi atawafungulia geti.
“Daphine”
Ngesa akaita mara moja na kugeuza shingo nyuma,kama kamanda wa jeshi au komandoo alishaelewa ni kitu gani,anatakiwa kukifanya!Akachomoa bastola na kuikagua kama ina risasi,baada ya hapo akafungua mlango na kuteremka kwa niya ya kuzunguka nyumba na kupitia mlango wa uwani.
Ulikua ni mtindo unaofanywa mara nyingi na majasusi kabla ya kuvamia eneo lolote, wachache wanashuka kwanza kuizunguka na ndicho alichokifanya Daphine kwani alizunguka nyuma ya nyumba hiyo na kuona geti fupi na dogo hapo akatulia na kuanza kupiga hesabu za kuruka ukuta kwani juu kulikua na nyaya hatari za umeme!Bastola ya Ngesa ilikua tayari kwenye mapaja yake,anaendesha gari taratibu na alivyofika getini akapiga honi mara moja,geti likafunguliwa na gari likaingia ndani.Hakukua na ukaguzi wowote na hilo lilikua afadhali kwa Ngesa ni wazi kabisa ilielekea walinzi walipewa taarifa ya ujio huo!Kupitia kioo cha ubavuni cha nje,aliwaona walinzi watatu wenye mitutu na mmoja kushoto ambaye huyo alianza kutembea kulifuata gari.
“Olina weka kichwa chako chini, Frank upo tayari?”
Baada ya kufanya tathmin ya kutosha,akataka kutoka na kulianzisha hapohapo!Olina alilala chini huku akilia machozi,Frank Ntagara hapohapo akachomoa bastola na kuikoki,kwa kua gari lilikua ‘tinted’ yaani lina vioo vyeusi haikua rahisi wa nje kumuona aliyekua ndani.
Ngesa akawa makini kutizama kioo cha ubavuni na kumuona jinsi mlinzi anavyolisogelea gari huku akiwa amekamata mtutu kikakamavu!Alivyoufikia mlango tu,Ngesa hakufanya makosa shabaha moja ya risasi haikufanya makosa ilipenya katikati ya kichwa,akatupwa hewani na kudondoka kando!Mshtukizo huo uliwafanya walinzi wakamate mitutu yao,hata hivyo Frank Ntagara alijiandaa kwa hilo,akageuka na kuanza kutupa risasi hovyo!Kilichosikika ilikua ni mirindimo ya risasi na Walinzi walilishambulia gari kwa hasira.
Kazi ya mlinzi ama bodigadi Zeliyatan Humudi ilikua ni kumkinga kwenye hatari tajiri yake ndiyo maana baada ya kusikia mirindimo ya risasi nje,akamchukua kwa haraka na kumpeleka ndani ya chumba kilichotumika kama stoo!
“Bosi,usitoke humu ndani!Wiliam,linda hapa”
Baada ya Zelytan Humudi kutoa maagizo akachomoa bastola yake na kuteremsha ngazi kwa kasi akitoka nje ili kusaidia walinzi wa nje!Walinzi wanne walikua chini,wametobolewa vibaya sana na risasi gari alilokua anaendesha Ngesa halikutamanika risasi ziliharibu vibaya sana,pembeni mwili wa Eliasi ulilala baada ya kufumuliwa na risasi sita kutokea nje!Hali ilivyokua shwari Ngesa na Frank wakateremka na kumtoa Olina!
“Cover me”(Nilinde)Ngesa akasema.
Frank Ntagara alikua makini macho yake yapo kila mahali,bastola yake ipo mkononi kulinda ulinzi kwani Ngesa alikua anakatiza upande wa pili akiwa na Olina!
“Paaaaaaaa”
Risasi kutokea juu,ilisikika Ngesa alipigwa na butwaa baada ya kumuona Frank Ntagara yupo hewani akamshuhudia kadondoka chini chali.
“Nooooooo”
Ngesa akapiga yowe na kuachia risasi hovyohovyo bila shabaha akilenga juu huku akimfuata Frank Ntagara aliyekua chini amelala chali.
“Frank…Frank…”
Ngesa akaita huku akimtingisha Frank Ntagara ambaye alikua akivuja damu mkononi,alichoshukuru risasi hiyo ilipenya begani kumaanisha kwamba isingekua na madhara,akamvuta na kumtoa kando huku akimtaka atulie hapohapo!
Kwa wakati huo Ngesa alikua makini mno,alishaelewa kivyovyote vile kuna walinzi wengine ndani,akatembea kwa kuambaa ambaa na ukuta,alivyoona mlango akaufungua taratibu na kuingia ndani.Ukimya alioukuta ndani ulimfanya atulize akili,mbele yake kulikua na ngazi ndefu kwenda juu,kando kulikua na seble kubwa yenye masofa ya gharama,akasita kidogo baada ya kuhisi kuna mtu upande wa pili,kabati lililokua pembeni lilimsaidia kumuona adui anayetokeza mlango wa jikoni hapo aliinua bastola yake taratibu na kubana jicho moja,alivyoona amemjaza kwenye saiti akavuta kilimi cha bastola,risasi moja tu ya kifua ilimtupa adui huyo ukutani,akaguna kidogo na kutulia hapohapo akapoteza uhai!
“Paa paa paaaaa”
Risasi tatu zilimkosa kosa Ngesa zikachana upepo,tukio hili lilimfanya ajitupe pembeni kama golikipa anayedaka penati ya mwisho!Akatambaa kwa kasi mpaka chini ya meza ya mbao,risasi zikamfuata hukohuko alichokifanya ni kubinua meza na kukaa vizuri,sasa akawa ana uhakika risasi zinatokea kushoto kwake!
Alivyochungulia pembeni akamuona mlengaji yupo nyuma ya sofa na hakupata saiti nzuri ya kumtungua,wazo la haraka likamjia baada ya kuona feni juu usawa wa adui huyo,kwa shabaha ya risasi moja akaipiga feni risasi!Ambapo ilidondoka na kumponda adui huyo kichwani,kichwa chake kikatokeza nje hakuchelewa hapohapo akammalizia!Sasa akaanza kuchomoka kwa kujihami,akitizama huku na kule!Akaingia jikoni na kukagua,hakukua na kitu chochote cha maana,akarudi seblen na kuanza kupandisha ngazi kuelekea juu kwa tahadhari kubwa,alivyofika mlango wa kwanza akasita kufungua!Kwa nguvu akaupiga teke lakini hakukua na mtu yoyote yule,hapo aliamini hakuna mtu yoyote licha ya hisia zake kumuonya kuamini hilo lakini aliendelea kusonga mbele na kuingia chumbani.
“Tupa bastola chini”
Ilikua ni sauti nzito,kutokea nyuma yake na kwa wakati huo alihisi kichuma cha baridi kimemgusa shingoni,akaelewa maana yake hivyo kuleta upinzani wowote ule kifo kingemuhusu!Akiwa katikati ya kuisumbua akili yake akaonywa tena aweke bastola yake chini,bila kubisha chochote akaitupa na kuiweka mikono yake hewani kusalimu amri.
“Nahitaji kuzungumza na waziri Okama”
Ngesa akavunja ukimya kwa namna ya kununua muda kwanza ingawa hakua ana uhakika kama jamaa wa nyuma yake angependezwa na jambo hilo.
“Hayupo,sema shida yako”
“Kama hayupo naomba niruhusu niondoke”
Jamaa huyo akaachia tabasamu lililojaa unyama na kuguna kibabe.
“Uende wapi?”
“Nyumbani,kama hayupo nitakuja siku nyingine ni mambo binafsi”
“Ujue,usilete komedi kwanza piga magoti”
Sauti ikawa kali nyuma yake,jambo hilo lilimpa Ngesa matumaini sababu aliamini siku zote mtu mwenye hasira na jazba ni vigumu kuwa makini!
“Piga magoti”
Ngesa taratibu akaanza kwenda chini ili ampumbaze adui yake,lakini kabla ya kufika chini alijibetua kwa mtindo wa kongfuu na kurusha teke la kinyume kama punda au Ng’ombe lakini hilo halikuzaa matunda ilielekea Zeliyatan Humudi alishtukia hila hiyo,ndiyo maana akahepa kushoto alivyotaka kutumia bastola akaukamata mkono huo na kuanza kupimana nguvu!Mvutano mkubwa ukatokea,wakapelekana mpaka ukutani!Ilikua ni hatari kwa Ngesa sababu adui huyo alikua na silaha mkononi hata hivyo alijitahidi kwa kumtandika kichwa kimoja cha pua,kilichomfanya Zelyatan Humud aone nyota hapo Ngesa akaupiga mkono wenye bastola, ikadondoka chini,wote wakakunja ngumi ili kuzichapa kiume!
Kwa mtindo wa Kick Boxa Zelyatan Humud alifanikiwa kurusha ngumi tatu,zilizomfikia Ngesa kwenye mbavu na nyingine usoni,hapohapo kama ngedere akakanyaga meza na kujirusha hewani,teke hilo halikufanya makosa lilimfikia Ngesa kifuani na kumtoa nje ya chumba ambapo alipepesuka mpaka kwenye korido,alivyokaa sawa ili ajibu mashambulizi,akawa amechelewa tayari kwani alipigwa kiwiko cha shingo kilichomfanya abweke kama mbwa,hakika alihisi maumivu makali alivyotaka kujishika na chuma za ngazi akawa amechelewa kwani aliporomoka kwenye ngazi kama mpira na kufika mpaka chini puu!
Ngesa alitamani kupiga kelele na kuomba msaada wa huduma ya kwanza kwani alihisi mgongo wake pamoja na shingo vimevunjika,kutoka ngazi ya juu mpaka chini sakafuni kulimfanya ahisi amepalalaizi mwili mzima!Mapigo hatari aliyochanganyiwa na Zeliyatan Humudi yalimpagawisha kwa kiasi cha kutosha,alivyotaka kuinuka akahisi kiuno kinamuuma, sasa akaona hatari yake mbeleni kwani aliamini Zeliyatan Humudi,angeshuka ingekua rahisi kwake kumshambulia.Alichokifanya ni kuanza kutambaa mithili ya konokono akijivuta akitumia mkono mmoja!Alivyoifikia,stuli kubwa ya kioo akasikia hatua za mtu zinatokea gorofani,hapo akajigeuza na kumuona Zeliyatan Humudi anavyoshuka ngazi kwa mapozi bila wasiwasi mithili ya Miss Tanzania kwenye jukwaa,hiyo ilimaanisha ni dharau tosha kwa tafsiri nyingine Ngesa asingeweza kufanya chochote kile.Ngesa hakua na ujanja,isipokua ni kusubiri nini kingefuata kuanzia hapo!Zeliyatan Humudi,akamsogelea na kuchuchumaa kidogo,akamshika kidevu na kumtizama usoni.
“Una Mungu sana,mpaka sasa hivi unavuta pumzi”
Zeliyatan Humud,alizungumza maneno hayo kwa umakini na kujiamini sana mithili ya Simba msituni,hapo Ngesa aliweza kumuona vizuri usoni!Alikua ni mwanaume mweupe,mwembamba na mrefu wa kimo!Mwili wake mdogo lakini mwenye mambo makubwa yenye hatari.Pembeni,kando kidogo kulikua na maiti moja ya mlinzi ambapo kushoto Zeliyatan aliona bastola akaisogelea na kuichukua,akamtizama Ngesa aliyekua amelala chali amekata tamaa,hapohapo akamuelekezea bastola usawa wa kichwani kumaanisha risasi moja tu,ingemuondoa duniani.
“Paaaaaaaaaa”
Risasi ilifumuka ndani ya chemba na kutoa sauti mbaya ya kutisha!Kufutia hapo,zilionekana damu na kusikika kelele za mguno!Kisu kilipenya mkononi mwa Zeliyatan Humud na kumfanya akose shabaha,risasi ikapiga pembeni hakukaa sawa akapokea mateke mawili ya kifua aina ya ‘round kick’Daphine alikua kama mwehu na alirusha mapigo tofauti tofauti ambapo kwa asilimia sitini yalifanikiwa kumlevya Zeliyatan Humud ambaye kwa wakati huo pia alionekana yupo fiti,ngumi ya Daphine ilivyokuja kulia kwake akainama na kumsomba na bega la kushoto,licha ya kuhisi maumivu makali begani lakini Zeliyatan Humudi alijitahidi kupambana na mwanamke wa shoka Daphine,ambaye alionekana kabisa ana hasira za mkizi.Sijui ilikuwaje,akakosea kurusha ngumi ambapo Daphine aliidaka kwa niya ya kumvunja mkono lakini ikaonekana kama Zeliyatan Humud,alishtukia hila hiyo ndiyo maana akajiwahi kwa kubetuka kwa nyuma na kumtandika ngumi kali Daphine iliyomfikia vizuri shingoni!Ulikua ni mpambano wa kukata na shoka,wote wakawa wanatizamana kama majogoo wawili wakiwa wamekunja ngumi.
Daphine alikua makini kuangalia mkono wa Zeliyatan unaovuja damu tena bado una kisu,shabaha yake ilikua hapo hapo!Ndiyo maana akamtisha kama anarusha ngumi ya kushoto lakini badala yake aliruka ‘flying kick’ hewani iliyomfikia Zeliyatan na kumdondosha chini,hata hivyo aliinuka kwa kasi ya ajabu,sasa Daphine akawa makini zaidi.Zeliyatan Humud alivyotaka kurusha ngumi,akapigwa kikumbo na Ngesa ambaye alionekana kupata nguvu,sasa wakaanza kumchangia.Hiyo ikawa rahisi zaidi kumthibiti.Kipigo alichopokea Zeliyatan Humudi kilimfanya avuje damu nyingi sana,mdomoni na puani,wakamuacha hivyo hivyo akiwa ana hema juu na kupandisha ngazi wakielekea juu wakiamini ni lazima Waziri Okama,atakua mahali fulani amejificha.Mtindo wa kukagua kila chumba na kupekua kila mahali ukaanza.Kilivyobaki kimoja,wakatizamana kwa pamoja na kupeana ishara kua waupige mlango teke kwa nguvu!Kama makomandoo vitani,wakaupiga mlango teke wote wakazama ndani wakiwa na bastola zao mikononi.Walichokiona,kiliwafanya wapigwe na butwaa la waziwazi,dirisha lilikua limevunjwa kumaanisha kua dakika chache kuna mtu alitumia kama njia ya kutoroka,wote wakakimbilia dirisha ili kuangalia chini.
“Shiiiit”
Ngesa akakema kwa hasira baada ya kumuona Waziri Okama anaingia ndani ya gari na kuliwasha,hiyo ilimaanisha wangemkosa hapo wasingempata tena.
****
“Griii griiii griii griiiii”
“Griii griiiii…Pokea simu mwana haramu”
Waziri Okama,alifoka kwa hasira baada ya kupiga simu muda mrefu bila upande wa pili kupokea,akiwa ndani ya gari aliligeuza kwa kasi na kulitoa nje ya geti.Akaendelea kupiga simu,kwa mara nyingine baada ya kukata tamaa.
“Uko wapi,Karanje?Siwezi kufungwa kwa ajili yako”
Waziri Okama,akazungumza kwa haraka baada ya simu kupokelewa!Kila kitu kwake kiliharibika alielewa nini maana yake kama angekamatwa.
“Kuna nini?”
“Kila kitu kipo wazi,sijui nitaweka wapi sura yangu?”
“Ukiwa una maana gani?”
“Nimevamiwa nyumbani kwangu na usalama wa taifa”
“Umezungumza chochote?”
“Hapana,nimefanikiwa kuwatoroka”
“Uko wapi?”
“Mikocheni”
“Unaelekea wapi?”
“Karanje wacha maswali ya kipumbavu ujue,umeniingiza kwenye matatizo usiniulize maswali ya kijinga”
Waziri alipayuka kwa sauti, maswali ya Brigedia Karanje yalimkera kwa kiasi cha kutosha.
“Mimi hua sifokewagi Okama,unapoongea namimi kua na adabu”
“Upo wapi nije ulipo?”
“Sasa hivi nipo Zanzibar,tukutane feli Posta”
“Saa ngapi?”
“Tukutane hapo”
Maongezi hayo yalimuacha Brigedia Karanje akiwa katikati ya maongezi nyeti na Mzee Ngesa pamoja na Komando Iddi Gogo,mwanaume mwingine hatari aliyeongezeka aliitwa Gadafi.Huyu alikua mkakamavu na mrefu kwenda hewani,makamo yake yaliendana na Karanje!
“Gadafi,umeelewa nini?”
Lilikua ni swali kutoka kwa Brigedia Karanje,akitaka kusikiliza mawazo ya Gadafi kwani kuna kitu alihisi hakipo sawa.
“Okama huyo?”
“Ndio”
“Kuna kit…”
“Okama anataka kutufanya sisi wapumbavu,kuna mawili kati ya haya.Moja yupo chini ya ulinzi ama anafuatiliwa na usalama!Hii,hainiingii akailini”
“Yote yanawezekana tuwe makini”
“Tutajua tu,Gogo mwambie rubani awashe helkopta”
Ilibidi wote waingie ndani ya Helkopta na aliyeonesha chuki za waziwazi ni Brigedia Karanje na moyoni alijisikia kuua sababu aliamini kumuacha hai Waziri Okama mambo yote yasingekua na maana yoyote ile,kila kitu kingekua bure kabisa!Helkopta ilianza kuchana mawingu dakika hiyohiyo ikiwa imewabeba wanajeshi hao waliohasi nchi,mikononi walishika mitutu hatari ya kivita na walipanga mikakati mingi ya kuipindua nchi,siku zijazo za usoni wakiamini kua Rais Leslie amekufa tayari.
Haukua mwendo wa masaa mengi isipokua ndani ya dakika hamsini Helkopta ilianza kushuka taratibu na kutibua mchanga wa ufukwe na ilikua ni lazima watue pembezoni kidogo na feli.Ulikua ni usiku mzito na jiji lilikua kimya, wa kwanza kushuka alikua rubani wa helkopta akafungua mlango Brigedia Karanje akashuka kisha Mzee Ngesa akiwa na sigara kubwa mdomoni.Hakukua na muda wa kupoteza zaidi ya kumtafuta Waziri Okama hewani.
“Umefika wapi?”
“Nishafika muda mrefu sana”
“Wapi?”
“Huku feli kwenye samaki”
“Njoo huku kando kando moja kwa moja”
“Karanje us…”
“Nimekwambia njoo”
Giza lilimtisha Waziri Okama,aliogopa kutembea akiwa peke yake eneo lenye vichaka namna hiyo,alishazoea kutembea na walinzi na moyoni mwake kulikua na uwoga,alishaelewa kivyovyote vile angefuatiliwa na usalama wa taifa waliovamia nyumba yake,alivyoikumbua familia yake moyo ukamuuma sana kwani aliamini kuanzia siku hiyo angeishi maisha ya kutanga tanga tu.Mbele yake kidogo aliona miale ya tochi,akazidi kusonga mbele zaidi mpaka alipofika kwenye mitumbwi mingi,hapo alipigwa tochi kali ya macho na kuambiwa apige magoti na avue nguo zote.
“Kwanini?”
“Vua nguo zote,au tukuvue?”
“Mimi ni waziri lakini”
“Uwaziri wako kwa mkeo,toa nguo”
Jeshi la Brigedia Karanje,lilikua makini sana walielewa mtindo wa usalama wa taifa kupachika GPS!Ndiyo maana walimtaka kwanza Waziri Okama avue nguo zote!Walivyoona anataka kuleta ubishi wakamtishia kumuua,hapo alivua nguo zote wakampa shuka la kimasai ajistiri huku akitetemeka na baridi la baharini alianza kutembea!Kilikua ni kitendo cha aibu kwa mtu kama yeye mwenye heshima zake serikalini lakini hakua na jinsi zaidi ya kutetea uhai wake.Safari,ilizidi kusonga mpaka kilomita moja mbele ambapo hapo kando aliona Helkopta,upande wa kulia amesimama Brigedia Karanje,kuna kitu alijifunza kwa mwanaume huyu kua siku hiyo hakukua na uhai kivyovyote vile angeuliwa!Hata hivyo hilo lilikua kweli sababu ilikua ni lazima litokee ndiyo maana Brigedia Karanje aliweka watu wake wa kazi pembe zote za msitu huo,akiamini ni lazima Waziri angekua anafuatiliwa tu,sababu aliwaelewa vizuri sana usalama wa taifa.
“Ova mkuu kishiiii”
Redio upepo ilisikika kutokea kwa Brigedia Karanje,akatuliza akili na kuiweka mdomoni.
“Nakusoma ova kishiiii”
“Naona kuna gari,imepaki watu wawili wameshuka wanakuja upande huo ova kishiiii”
Moyo wa Brigedia Karanje,ukakosa utulivu akamtizama Waziri Okama kwa hasira.
“Upo na nani?”
“Mi..mi mi sipo na mtu”Amri aliyotoa Brigedia Karanje kwa jeshi lake ni kua makini kulinda usalama!Haukua utani,tangu Waziri Okama anatoka kwake nyuma Ngesa aliweza kumuona na alikua akimfuata sambamba akiwa na Daphine!Wakaweza kumfuatilia nyuma nyuma mpaka alivyoegesha gari feli.Kulikua kuna uwezekano mkubwa wakumkamata lakini hawakutaka kufanya hivyo badala yake walipenda kujua anaenda kwa nani.Daphine na Ngesa waliteremka ndani ya gari wakiwa na bastola zao mikononi,bila kujua chochote kua wanaonwa na walitembea umbali wa mita mia,wakifuata nyayo za viatu vya Waziri Okama!Ilikua ni hatari kubwa sababu wanajeshi hao makini walifanya jitihada kubwa za kuwaweka kati huku wakifanya mawasiliano ya chini kwa chini.
“Ile nini?”
Daphine akauliza kwa sauti ya chini.
“Helkopta”
Ngesa akajibu na kusimama nyuma ya mti,akiangalia huku na kule!Kuna kitu alihisi hakipo kawaida.Ukimya wa eneo hilo,ulimfanya ajiulize maswali mengi sana.Haikuwezekana hata kidogo,kuwe na Helkopta alafu kuwe kimya namna hiyo ama isiwe na dalili yoyote ya kuondoka.Kivyovyote vile Helkopta hiyo,ingekua angani.Kengele ya hatari ikaanza kugonga kichwani,akamuangalia Daphine alivyotaka kujitokeza mafichoni,akamuwahi na kumshika mkono.
“Vipi?”
Daphine akauliza.
“Kuna kitu hakipo sawa,subiri”
Hapo Ngesa akaanza kuangalia chini kwa makini kupitia michanga hiyo ya ufukweni akaona nyayo za mabuti ya kijeshi,sasa akawa ana uhakika yupo kwenye hatari kubwa sana endapo asipotumia akili ya ziada.Milango yake yote ya fahamu ilikua makini ingawa upepo mkali ulivuma eneo hilo,alichokifanya ni kulala chini na kumwambia Daphine pia afanye hivyo,wakatambaa mpaka nyuma ya mnazi mrefu.
Mwanga hafifu wa mbalamwezi uliweza kusaidia kuona,umbali wa mita hamsini waliona kivuli cha mtu aliyeshika mtutu.Ngesa akajua tayari kumekucha,akajiandaa mithili ya chui anayevizia lindo msituni,taratibu kwa tahadhari kubwa akachomoa kisu kilichokua nyuma ya kiuno chake!Akaanza kutambaa,alivyoyafikia majani marefu kiasi akasimama kwa staili ya kuchuchumaa,sasa akawa anamuona vizuri adui yake aliyeshika mtutu!Mwili wa mwanaume huyo,ulimfanya ajipime uwezo kwani kwa wakati huo bado alikua mwenye maumivu makali yaliyosababishwa na Zeliyatan Humudi.Shingo yake na mgongo vyote vilimuuma sana lakini hilo halikumfanya asitishe vita yake.Kwa umakini zaidi,akashika kisu na kuanza kusimama,kwa kasi akarudi mafichoni baada ya kusikia redio upepo inazungumza.
“Ovaaa,umefikia wapi kishiiiii?”
“Bado kishiiii”
Kitendo cha mwanajeshi kumaliza na kuweka ‘Redio call’ kiunoni Ngesa akaruka kama swala akiwa na kisu mkononi,akamchoma mgongoni kabla ya mwanajeshi huyo kufanya chochote,akamtandika ngumi mbili za mbavu na kumziba mdomo huku akiwa amempiga kabali ya nguvu,alivyohakikisha amelegea!Akaivunja shingo yake,akamburuza na kumuangalia Daphine aliyekua upande wa pili anahema kwa wasiwasi.Alichokifanya Ngesa ni kumshika mwanajeshi huyo shingoni ili kuhakikisha kama amekufa kweli, sababu alizijua tabia za kijeshi wakiwa vitani,hujifanya wamekufa ili kumzubaisha adui.Alivyohakikisha hana uhai,akachomoa kisu kilichokua mgongoni na kunyata mpaka kwenye mti wa mnazi uliokua kando.
“Shiiiiiii”
Ngesa,alimuonya Daphine na kumzuia asipige kelele yoyote ile sababu alisikia sauti za watu!Alivyotokeza shingo yake,moyo wake ukapiga paa baada ya kuona sura ya baba yake mzazi Mzee Ngesa.Moyo wake ulidunda kwa nguvu jasho jembamba lilimtoka akawa kama amezubaa,mambo mengi alikumbuka hususani jinsi alivyoishi na baba yake kipindi yupo mdogo wakiwa marafiki wakubwa,taswira ikaanza kujijenga kichwani kwake akawa kama anaangalia filamu ya kusisimua.Licha ya yote ilikua ni lazima ayaokoe maisha ya watanzania wengi,akachomoa bastola kutoka kiunoni na kutoka mafichoni akiwa na jazba.
“Babaaa!”
Ngesa akaita akiwa na bastola mkononi ni kitendo kilichomfanya Mzee Ngesa,akageuke na kupigwa na butwaa la waziwazi.
“Derick!”
Baba na mwana walitizamana,lakini aliyeonekana kupigwa na butwaa ni Mzee Ngesa!
“Weka bastola chini Derick,unataka kumuua baba yako?”
“Ndio”
Ngesa alijibu huku kifua chake kikipanda juu na kushuka chini,mapafu yake yalijaa hewa hiyo ilikua ni hasira.Alivyokumbuka jinsi mama yake mzazi alivyouwawa na mzee huyu katili,akaumia zaidi.
“Kwanini ulimuua mama?”
“Mama yako?Kuhusu kumuua mama yako,tutaongea weka bastola chini.Najua huwezi kufanya chochote Derick,weka bastola chini mimi ni baba yako,nimekulea”
Mzee Ngesa,alizungumza kwa kujiamini lakini sio sana kwani alikielewa kichaa cha Ngesa wakati mwingine dishi lake huwa linacheza,ndiyo maana akawa anamsogelea karibu.
“Baba,usinisogelee!Simama hapohapo”
“Okay niue”
Mzee Ngesa akasema,alivyomfikia Derick karibu kwa utaalam wa hali ya juu,akachota mchanga kutumia mguu mmoja ambao ulimfikia Ngesa machoni.Mzee alikua hodari na mjanja, kwa kutumia vidole vyake viwili vilivyokomaa akavichomeka kwenye macho ya Ngesa na kumtandika kifuti cha kifua!Ngesa hakua na ujanja,kwanza hakuweza kuona mbele kutokana na mchanga pamoja na vidole vilivyotumbukizwa machoni mwake,lilikua ni pigo hatari wanaotumia makomandoo wa Cuba lililomfanya apepesuke na kurudi kinyume nyume huku akifikicha macho kutokana na mchanga kua mwingi akapiga mweleka na kudondoka chali puu, hilo ndilo kosa alilofanya Ngesa baba yake tayari alikua mtu hatari kwenye mapambano,hapohapo akainama na kuiokota bastola iliyodondoka chini pembeni ya Ngesa!
“Kacha! Kacha!”
Akaikoki na kumuelekezea usawa wa kifuani kwa niya ya kumuua.
“Usimuue”
Sauti nene ya kitetemeshi iliyojaa unyama,ilisikika upande wa pili,Ngesa alikua chini haoni vizuri kutokana na mchanga uliomwingia machoni!Kauli hiyo ilimfanya Mzee Ngesa asitishe zoezi hilo na kugeuka nyuma ambapo alimuona Brigedia Karanje akiwa na Daphine aliyekua chini ya ulinzi,ulikua ni usiku wa kutisha na kosa la Daphine kuzubaa lilimponza,ndiyo maana Brigedia Karanje alimuwekea bastola utosini na kumuamuru asonge mbele atokeze mafichoni.
“Siku zote kinyago,nilichokichonga hakiwezi kunitisha”
Brigedia Karanje alisema,kila kitu alikumbuka tangu alivyomchukua Daphine akiwa mtoto mdogo na kumpeleka katika mafunzo ya kikomandoo!Alisikitishwa sana kwa kitendo cha kumgeuka kwani ndiye mwanamke aliyekua akimtegemea siku zote katika kazi zake,alichukizwa kwa kiasi cha kutosha lakini alifurahi na roho ya kuua ilimuingia baada ya kumuona Ngesa amelala juu ya mchanga yupo chali,akamsogelea kwa karibu na kumkanyaga kifuani.
“Siku zako,zimeshafika tayari”
Brigedia Karanje,akasema na kumkanyaga tena kichwani jambo lililomfanya Ngesa ahisi maumivu makali mno.Matumaini yake yote yaliegamia kwa Daphine lakini cha kushangaza alimuona mbele yake yupo mateka,tukio hilo lilimpelekea moja kwa moja akate tamaa kabisa,matumaini ya kutoka salama katika himaya ya Brigedia Karanje ilikua ni asilimia kumi kati ya mia moja.Alivunjika moyo sana baada ya kuwaona wanajeshi wengine watatu wamesogea eneo hilo,wakiwa wameshiba na wamejazia miili yao.Sura zao zilionesha chuki za waziwazi kabisa na kati yao mmoja alimtambua vizuri sana, Komando Iddi Gogo,mwanaume hatari ambaye kuua kwake lilikua ni jambo la kawaida mno.Ki ukweli alihisi kuchanganyikiwa na akili yake ikakosa utulivu kabisa,dalili zote za kifo zilikua karibu yake.Akiwa katikati ya mawazo,akashikwa shingoni na mkono uliokomaa mno,akaanza kuburuzwa mpaka chini ya mti wa mnazi,hapo alifungwa vizuri mikono na miguu yake huku akimshuhudia Daphine,anapigwa makofi na kuambiwa maneno fulani na Brigedia Karanje ambayo hakuweza kuyasikia vizuri kutokana na upepo mkali ulioambatana na mawimbi kuvuma baharini.
“Kamanda”
Ngesa akaita akijaribu kupima maji alitaka kutumia tabia yake ya siku zote ili kumpumbaza mwanajeshi huyu,mkakamavu.Lakini badala ya kujibiwa mwanajeshi huyo,alimkata jicho kali la hasira!
“Kwanini umenifunga hivi kama mbuzi ala….?”
Ngesa akajibiwa na kitako cha mtutu,ambacho kilimfikia kichwani ni tukio lililomfanya ahisi kama ubongo wake umecheza na mafaili yametingishika,ilikua ni wazi kabisa mwanajeshi huyo alitumia hasira nyingi na hakutaka mazoea kabisa.
“Kelele”
Ngesa akatulia sababu alijua athari yake endapo angeendelea kuzungumza kwa mara nyingine,hakuna kitu kilichomuuma zaidi baada ya kumuona Frank N’tagara pamoja na Olina Kalumuna,wapo chini ya ulinzi pia.Ni tukio lililomfanya aumie moyoni na kuanza kujuta ni kwanini aliongozana nao katika msafara huu uliojaa misukosuko na damu kumwagika!Kilichomuuma zaidi ni kumuona pia Baba yake mzazi yupo kwenye mkasa huo wa kutisha na aliapia akiwa hapo,endapo angefanikiwa kujikomboa angeanza naye, hata hivyo matumaini hayo yalikufa baada ya kumuona Brigedia Karanje,anatembea mpaka karibu yake chini ya mti wa mnazi,alipofungwa kamba!
“Derrick,nilikuambia nitakuja kukuua mwenyewe kwa mikono yangu!Ulidhani ni ndoto”
“Niue,unasubiri nini sasa?”
“Kufa utakufa tu ni swala la muda,bado najadili ni aina gani ya kifo kinakufaa”
Ilikua ni kauli ya kutisha,iliyomfanya Ngesa ameze fundo la mate, hofu ilitawala na uhakika wakua asingetoka salama ulikua waziwazi baada ya kumuona Daphine,anapigwa ngumi za mbavu na kusukumizwa chini.
Alitamani kumuokoa lakini hakukua na jinsi yoyote wala muujiza wa aina yoyote ile na alivyojipima nguvu akaelewa asingeweza kufanya lolote lile dhidi ya wanajeshi hawa waliojazia miili yao kwa mazoezi ya kutosha,hakika alichoka kabisa.
“Mngeniacha nimuue,hawezi kutukwamisha kila siku,yeye kama nani?”
Kauli hiyo ilipenya kwa Ngesa na sauti hiyo aliitambua vizuri sana ya Baba yake mzazi!Hakua tayari kuamini kama angetaka kumuua,akaendelea kusikiliza mabishano kati yake na Brigedia Karanje ambaye alipanga kumuua kinyama!
“Yaani nataka hata akifika anapoenda,awahadithie Marehemu wote atakaowakuta”
“Lakini tuna muda mchache sana”
Hapo Brigedia Karanje,akaonekana kushtuka kidogo na kutizama saa yake ya mkononi!Alivyogeuka upande wa kulia alimuona Waziri Okama,amesimama wima akamsogelea kwa karibu.
“Kazi yangu,hukuifanya inavyotakiwa.Nadhani unajua nini maana yake”
Baada ya kuzungumza maneno hayo akamtizama Komando Iddi Gogo aliyekua pembeni,ameshika bastola mkono wa kulia,akampa ishara kwa kumtingishia kichwa!
“Paaaaaaaa”
Kilikua ni kitendo cha ghafla na tukio la kutisha kwani Waziri Okama,alitupwa juu na risasi alivyodondoka chini ubongo ulikua umemwagika vibaya sana,risasi imepita katikati ya fuvu la kichwa ilikua ni maiti ya kutisha mno Waziri Okama alikua chini mdomo upo wazi katumbua macho,ilikua ni maiti iliyomfanya hata Ngesa ajawe na huruma.Kwa dharau na madoido Komando Iddi Gogo akaipuliza bastola yake na kuiweka kiunoni kwa mbwembwe na maringo.Waziri Okama,akawa amefariki tayari katika kifo ambacho hata Ngesa alisikitika sana hata hivyo hakuumia kwani alielewa malipo ni hapahapa duniani,kitendo cha Brigedia Karanje kumsogelea Olina Kalumuna kilimfanya aanze kuhema juujuu hizo zilikua ni hasira na alitamani kukata kamba amvae Karanje sababu hakutaka kuona Olina anauliwa hata kidogo!
“Najiuliza kwanini mrembo kama wewe umejiingiza kwenye hii misukosuko”
Brigedia Karanje akaanza mazungumzo huku akimtizama Olina Kalumuna machoni,akashusha macho yake mpaka kwenye kifua cha mwanamke huyo,hapo akachukua bastola na kuindakamiza katikati ya maziwa.
“Kipindi cha nyuma nilikua siui wanawake na watoto,lakini sasa hivi……”
Hapo alishindwa kumalizia sentensi yake na kutingisha kichwa kumaanisha anakataa kitu,akabenua mdomo wake na kumgeukia Daphine aliyekua chini amelala chali,amefungwa kamba za miguu na mikononi,akashusha pumzi ndefu na kumsogelea mzee Karanje karibu na kumpa bastola.
“Naona una haraka sana,muue mwanao tuondoke!Gogo,leta dumu la petroli”
Brigedia Karanje hakutaka kupoteza muda na wazo lililomjia kichwani ni kuwamwagia mafuta hatari ya petroli na kuwachoma moto kisha wao kupanda helkopta na kuondoka zao,hiyo ndio hatua aliyotaka kuichukua kwa wakati huo kwani muda haukua rafiki tena.
****
Giza lilikua totoro lakini waliweza kuona mbele wakitumia usaidizi wa mbalamwezi,mbele yao kulikua na gari lililotelekezwa,wakaamini kabisa ndiyo hapo!Upepo wa bahari uliwafanya wasiweze kusikilizana vizuri hata hivyo walijitahidi kusonga mbele huku mikononi wakiwa na mitutu yenye viwambo vya kuzuia sauti isitoke,sasa wakawa wamefika kando ya fukwe za bahari mbele!Aliyeongoza msafara huo ilielekea alikua makini sana ndiyo maana alitumia ishara ya mkono kuwazuia kwanza wenzake watatu wasisonge mbele!Hakuna kelele iliyofanyika isipokua ishara ya vidole,mmoja akaelekea Magharibi mwingine Kusini na aliyebaki akachukua upande wa Kaskazini.
****
Kilikua ni kifo kibaya sana kwao endapo wangechomwa na moto wa petrol,hilo lilikua wazi kabisa kutokea kwani dumu la petrol lilienda kufuatwa wakimuacha Ngesa yupo chini ya mti amechoka yupo hoi,ana sali sala zake zote za mwisho.Kifo cha kuchomwa na moto kilimuogopesha,akaanza kupata picha jinsi atakavyoteketea mpaka kifo chake na kubaki majivu,alisikitika kiasi kwamba mwili wake ukaanza kusisimka!Katika hali ya kushangaza akahisi kama kuna hatua za mtu,anakuja nyuma yake alivyogeuza shingo akashindwa kutokana na jinsi alivyofungwa na kamba, lakini cha ajabu kamba za mikono yake zilikatwa mwanaume aliyemkata kamba akasogea mbele yake.
“Dustan!”
“Shiii Ngesa”Dustan,akamnyamazisha!
“Dustan ulikua wapi?Umejuaje tupo huku?”
“Ngesa,sio wakati wake huu”
Kwake ilikua kama ndoto ama kiini macho,kumuona Dustan yupo mbele yake tena anafanya ukombozi!Ni tukio lililomfanya agande kama sanamu,akamuona Dustan anamkata kamba za miguuni na kumpa mkono kwa ishara kwamba asimame,wote wakatembea mpaka nyuma ya mti.
“Shika hiii”
Ngesa akapewa bastola lakini badala ya kuipokea akabaki anamtizama Dustan mithili ya mtu anayesoma bango.alivyoipokea akaikoki na kuishika vizuri mkononi.
“Nipo na akina Badi”
“Hapa?!”Ngesa akauliza huku akitoa macho kwa mshangao,kila kitu kwake kilikua kama ndoto!
“Ndio”
Walizungumza kwa sauti ya chini huku Ngesa akionekana mwenye hasira za waziwazi,alivyogeuka alimuona Mwanajeshi mmoja anaranda randa!Hapohapo,hakumkawiza akafyatua risasi moja iliyomtupa kando akadondoka na taswira ya Brigedia Karanje ikamjia kichwani.Na kilichomchanganya zaidi ni kusikia mlio wa Helkopta kumaanisha kwamba muda mfupi kuanzia hapo ingepaa angani,lilikua ni jambo ambalo hakutaka litokee!
“Dustan,Cover me”(Dustan nilinde)
Alichohisi ni kama aliyepata nguvu mpya kwa mara nyingine tena,macho ya Dustan yalikua pande zote mtutu mkononi akijaribu kumlinda Ngesa kwa chochote kitakachotokea!Wakatembea pamoja mpaka walipoufikia uwazi ambapo sasa waliweza kuona Helkopta inazungusha mapanga boi yake tayari kwa ajili ya kupaa angani,Ngesa akabana jicho moja ili amlenge Brigedia Karanje aliyekua upande wa rubani pembeni,aliamini kabisa kwa shabaha hiyo makini risasi isingeweza kufanya makosa yoyote yale!
“Karakacha karakacha”
Mlio huo kutoka kwenye bastola yake ulimfanya apigwe na bumbuazi,hiyo ilimaanisha hakukua na risasi hata moja,ilibidi achukue maamuzi mengine ya kiume kwa kuikimbilia Helkopta hiyo ambayo taratibu ilianza kuinuka,lakini cha kushangaza alisikia milio ya risasi nyuma yake!Jambo hilo likamfanya Brigedia Karanje ageuke na kumuona,Helkopta ilivyoanza kupaa angani Ngesa hakukubali kama swala akaruka na kudaka chuma la Helkopta,haikua kazi rahisi hata kidogo mbali na hofu aliyokua nayo lakini alikazana kujivuta kwa juu.
Mtikisiko wa Helkopta na kuonekana kwa Ngesa anaikimbilia ilikua ni dalili tosha kua amedandia,alichokifanya mwanajeshi aliyekua mlangoni ni kuchomoa bastola ili amfyatue Ngesa,akatoa kichwa na mkono wenye bastola nje!Kilikua ni kitendo cha kufumba na kufumbua,mkono wa mwanajeshi ulishikwa akavutwa nje na kudondoka mzima mzima puu hapohapo akatulia sababu alidondokea shingo bila shaka ilivunjika.Kilikua ni kitendo kilichomshangaza Brigedia Karanje na Mzee Ngesa aliyekua ndani.
“Paaa paaaa paaaaa”
Risasi kutoka chini,zilisikika na Daphine ndiye aliyeshika bastola alichokifanya ni kumimina risasi ubavuni mwa Helkopta,hakuishia hapo akazidi kurusha risasi!Helkopta,haikua juu sana hivyo risasi nyingine zilipenya na baadhi zilichana upepo!Jambo hilo lilimfanya Ngesa ajivute na kushika kingo ya Mlango,kabla hajaingia ndani akapigwa teke la uso,lililomfanya apepesuke na ilikua kidogo adondoke chini.Akajikaza na kuangalia chini,sasa hofu ikaanza kumtanda kwani helkopta ilizidi kwenda juu angani!Maji alikua tayari kayavulia nguo ilikua ni sharti ayaoge,Mzee Ngesa alivyotaka kumpiga teke lingine akahepa kidogo na kumshika shati,hiyo ilimfanya mzee huyu aingiwe na hofu kwani alielewa nini maana yake endapo angedondoka chini,alichokifanya ni kujishika vizuri jambo hilo likamfanya Ngesa apate mwanya wa kujivuta juu huku akiwa amemshika shati baba yake,alivyofika juu akamkwida shingoni.Hapo,akapata nafasi na kuupandisha mguu mmoja juu,hakuelewa stamina hizo alizitoa wapi lakini alivyofika juu,akakutana na ngumi kali ya pua kutoka kwa Brigedia Karanje,maumivu aliyohisi akahisi kama amepigwa na nyundo!Hata hivyo,aliiona ngumi nyingine inakuja,akarudi kidogo na kumtupia Brigedia Karanje teke la tumbo,lililomfanya ayumbe na kuchomoa bastola!
“Paaaaaa”
Isingekua Ngesa kuwa mwepesi wenda risasi ingefumua kichwa chake kwani aliupiga mkono wa Brigedia Karanje kiwiko na kufanya risasi hiyo ipenye mgongoni mwa Rubani ikatokea upande wa mbele tumboni,kufuatia kitendo hiko Helkopta ikaanza kukosa uelekeo!Mara iende vile mara irudi kule,ikawa inazunguka zunguka tu hewani kwani rubani alikua tayari kapoteza maisha!Ndani ya Helkopta kulikua na patashika kubwa,hawakuelewa waongoze Helkopta ama wapambane.
Zaidi na hilo,walikua kama wapo ndani ya gari linaloshuka mlima na kupanda ama linaloendeshwa na mlevi,mara wadondoke huku mara watupwe kule.Kitendo cha Ngesa kukaa upande wa mlango kulimfanya ajishike vizuri,alivyoangalia chini akaona hatari kubwa mbeleni kwani Helkopta ilikua inaenda chini usawa wa bahari.Akamshika Brigedia Karanje vizuri na kumpiga kichwa cha pua,akamsindikiza na ngumi nyingine nzito ya mbavu.Hilo lilimfanya Brigedia Karanje ajikunje lakini hakukubali,akarusha ngumi lakini haikuzaa matunda kwani iligonga chuma sababu Ngesa aliinama chini kidogo,alivyotaka kujishika vizuri akateleza sababu Helkopta ilibadili upande na kuanza kuelekea chini.Waliokua pembezoni mwa bahari Daphine na Dustan,waliona tukio zima walitandwa na hofu kwa wakati huo!Wasingeweza kufanya chochote sababu Helkopta ilikua juu angani na ipo katikati ya bahari!
“Ngesaaaaaaaaaaa”
Daphine aliita kwa sauti ya juu iliyojaa uchungu baada ya kushuhudia Helkopta,inatumbukia ndani ya bahari.Aliumia kwa kiasi cha kutosha na kutamani ajitose ndani ya maji,apige mbizi ili akamkomboe Ngesa!
Ulikuwa ni uchungu uliomfanya Daphine ahisi kuchanganyikiwa na kutamani kujitosa ndani ya maji,ni tukio lililomfanya aanze kukimbia huku na kule kama mwehu na cha ajabu zaidi akanyoosha kuyafuata maji ya bahari ili apige mbizi,lakini maji yalivyomfikia kifuani akasita kuendelea mbele zaidi na kutizama upande wa pili,kuna akili fulani mbaya aliipata ndio maana akaanza kukimbia mithili ya mtu anayevuka mtaro kwani miguu yake aliinua juu na kukanyaga kule,alivyofika kwenye michanga akakimbia kwa kasi akiwa amelowana hivyo hivyo mpaka yalipokua magari.
Alichoshukuru gari moja wapo aliona lina funguo kwenye swichi,hapohapo akalitia moto na kuanza kurudi kinyume nyume kwa kasi ya ajabu na kufanya mpaka michanga iruke juu,alivyopata saiti nzuri.Akaweka gia na kulitoa gari kwa kasi ya mashindano,alifanya hayo yote Dustan na Frank Ntagara wakishuhudia hawakuelewa lengo la Daphine ni nini isipokua ni Badi kijana machahari na mwepesi kuanza kumfukuzia na kuingia ndani ya gari lingine na kumfuata kwa nyuma!Kwa upeo wa Daphine ilikua ni lazima afanye ukombozi ingawa alielewa operesheni hiyo ingekua nzito na ngumu.Alivyofika maeneo ya daraja la Salenda akazungusha usukani upande wa darajani ambapo huko aliingiza gari kweye miti mingi na kabla gari halijasimama vizuri akateremka kwa kasi ya kimondo na kuanza kukimbia,mpaka kwenye vibanda vya makuti akaingia kimoja wapo na kumkuta mwanaume amelala juu ya nyavu ngumu iliyokua hewani yaani kamba zake zimefungwa huku na kule,akawa kama mtu anayebembea!Daphine hakua na muda wa kumuamsha zaidi na kumtandika kibao kikali cha shavu,alivyotaka kukurupuka akamshika na kumdondosha chini.
“Nahitaji boti,fanya haraka”
Daphine akasema kwa ukali,hacheki alijua fika jambo analofanya hakubahatisha hata kidogo ndio maana alifunga safari mpaka kwa watu hao alimaarufu kama ‘beach boys’ na kazi zao zilikua ni kuwavusha watu kuwapeleka visiwani wakitumia mitumbwi ama boti.’Beach boy’ alikua ni kama mtu aliyepigwa na butwaa hakuelewa kama amevamiwa ama amepigwa na mteja anayetaka kwenda kisiwani,swali alilojiuliza sasa hivi ni saa ngapi?Wakati mwingine alidhani ni jini limemvamia usiku,kabla ya kujijibu kitu,akashtuliwa na kibao kingine kikali akavutwa juu juu na kutolewa nje.
“Nahitaji boti sasa hivi”
“Wewe nani?”
Daphine alichukizwa na swali hilo lakini kabla ya kujibu,alishtuliwa na teke kali la mgongo lililomfanya ayumbe na kupepesuka kidogo,alivyogeuka akaona ngumi inakuja upande wa kushoto akahepa kulia ikapita hewani,akatupa pigo maridadi la judo lililomfikia kijana huyo ambaye aliamini alikua ni ‘beach boy’ kwani alikua kifua wazi,ngumi yake moja ilimfikia mbavuni alijua fika isingemfanya ainuke tena kwani alikua ana uhakika kabisa,ametegua mbavu moja!Ni kweli jamaa huyo alivyoenda chini,alipiga yowe kali mithili ya mbwa koko aliyepigwa buti la mdomo,akatulia chini huku ameshika mbavu.
“Nahitaji boti liko wapi?”
Kazi ikaonekana kuwa rahisi baada ya Badi kufika eneo hilo akiwa na bastola mkononi,hofu ikatawala wakaanza kutembea mpaka kandokando ya fukwe hiyo ambapo hapo walichukua mafuta na kutembea mpaka boti ilipokuwepo,waliikuta imetiwa nanga!Walijaza mafuta,Daphine mwenyewe akavuta kamba iliyokua kwenye injini mithili ya mtu anayewasha jenereta,kwa mara ya kwanza boti ikagoma kuwaka.Badi,akamgeukia ‘Beach boy’ na kumuwekea bastola kichwani.
“Washa boti”
Ilikua ni kauli moja ya kutisha iliyomfanya jamaa huyo,mkojo utake kumpenya!Akashuka mpaka kwenye maji ambayo yalimfikia kwenye magoti na kuchomeka swichi ambayo kwa makusudi alielewa anachokifanya,baada ya hapo aliambiwa akimbie mbali na ndani ya boti wakabaki Daphine na Badi.
Upana wa boti hilo haukuwa mkubwa sana na jinsi ilivyotengenezwa kienyeji,iliogopesha sababu ilikua ni lazima ushike chuma lililounganishwa na injini ili isonge mbele na kukata kona ilikua ni lazima utumie chuma hilo hilo,boti ilitoa sauti kali mno huku ikikata maji taratibu na kutokana na mawimbi kuwa makali wakati mwingine ilizima lakini iliwalazimu wawashe,hapo wakaanza kujuta ni kwanini walimuacha ‘Beach boy’ nyuma.Macho ya Daphine yalikua makini mbele ili mahali ambapo Helkopta ilidondoka isimpotee!
“Zungusha huku”
Kelele za Badi zilimfanya Daphine azungushe chuma na boti ilizidi kupiga kelele mithili ya bajaji inayopanda mlima,walitumia takribani dakika arobaini nzima mpaka kufika eneo hilo,ambapo waliishia kuona panga la Helkopta linazama.Daphine aliomba Mungu amkute Ngesa salama sababu aliamini kivyovyote vile asingeweza kupiga mbizi kwa muda mrefu namna hiyo,kutokana na majeraha aliyokua nayo mwilini mwake, baada ya kuteswa na jeshi la Brigedia Karanje.
“Ngesaa….Ngesaaa…Ngesaaaa”
Daphine aliita huku viganja vyake vya mikono akiwa ameviweka mdomoni akiamini sauti itaenda mbali zaidi lakini ukimya bado ulitawala.
“Chubwiiiiiii”
Sauti ya mtu kutumbukia ndani ya bahari ilimshtua Badi,alivyoangalia mbele alipigwa na butwaa la waziwazi,Daphine hakuwepo kwa maana hiyo alijitosa ndani ya maji.Halikua tatizo kwa Daphine kupiga mbizi ndani ya maji kutokana na mafunzo ya ukomandoo aliyojifunza,hivyo macho yake yalikua makini chini ingawa kulikua kuna giza lakini aliweza kusaidiwa na tochi ya majini ambayo aliichukua ndani ya boti,tochi hiyo mara nyingi walitumia wavuvi zilikua na mwanga mkali mno,mkono mmoja ukiwa umeshika tochi mwingine unapiga mbizi huku miguu yake akiichezesha chezesha aliweza kuzidi kuingia chini zaidi huku akipishana na samaki wadogo,alichoomba Mungu asikutane na samaki wakubwa ambao wangemfanya chakula cha usiku.
Matumaini yakaanza kumjia baada ya kuona ubavu wa Helkopta upo chini zaidi,hapohapo akazidi kupiga mbizi na kwenda chini kwa kasi.Ambapo,aliiona ikiwa imenasa kwenye pango kubwa!Akiwa kwenye maji aliomba Mungu asiishiwe pumzi mapema kwani ndio ungekua mwisho wake,sasa akawa tayari kaishika Helkopta akamulika ndani na kumuona Rubani yupo kwenye kiti chake,huyo akaachana naye akijua tayari amekufa.Alivyomulika,akasononeka baada ya kuona hakuna dalili yoyote ile ya Ngesa,kilichomtuma moja kwa moja ilikua ni lazima wenda Brigedia Karanje kamchukua lakini hilo hakutaka kulipa kipaumbele,akaingia ndani ya Helkopta kabisa.Upande wa pili alivyomulika vizuri akashtuka sana baada ya kuuona mwili wa mtu,umekandamizwa na chuma kubwa la ubavuni,hapohapo akapiga mbizi na kuingia chini zaidi ili kuhakikisha ingawa hakuweza kujua ni nani,alichokifanya ni kutoka nje ya Helkopta akiwa na tochi vizuri.
“Mungu wangu!”
Akashtuka kimoyo moyo,asingeweza kusema kwa sauti sababu maji yangemuingia mdomoni.Akamulika vizuri usoni na kuona sura ya Ngesa ametulia,ulikua ni mshtuko uliomfanya achanganyikiwe kiasi kwamba akatamani kuita watu wamsaidie lakini alivyokumbuka yupo ndani ya maji akatuliza akili kabisa na kuanza kuingia ndani,akakanyaga pango na kuanza kumvuta Ngesa mguu,akajitahidi kadri anavyoweza!Alivyoona zoezi linakua gumu na pumzi zinamuishia!
Akazunguka na kumshika begani ambapo hapo alikamata na mkono na kuanza kumvuta,zoezi likaanza kufanya kazi kwani Ngesa alianza kusogea taratibu!Akajitahidi kumsogeza,mpaka akafanikiwa!Mapigo yake ya moyo yalimwenda mbio sababu Ngesa hakuwa na fahamu hata kidogo na aliamini Helkopta ilimkandamiza ndiyo maana alishindwa kujinasua,hakutaka kupoteza wakati alichokifanya ni kumshika vizuri kitaalam na kuanza kupanda naye juu,halikua zoezi rahisi hata kidogo na alichozidi kumuomba Mungu ni samaki wakali ambao aliamini wangekuwepo wangem-meza,akapiga mbizi mpaka juu kabisa na kuibua kichwa chake ambapo alivyotizama huku na kule akaona boti aliyokuwepo Badi ipo mbele yake mita ishirini!Akapiga mbizi huku akiwa na Ngesa mkononi ambapo baada ya kufika Badi akawa tayari kamuona akampa mkono,na kuanza kupanda ndani ya boti wote walivyoingia wakamlaza Ngesa chali.
“Ngesa…Ngesaa Mungu wangu Noo Ngesaaa”
Daphine alilengwa na machozi,kuondokewa na mtu kama Ngesa katika maisha yake ingekua ni vigumu sana kukubali,mwanaume huyo alikua ni mtu wa pekee mno!Ndio maana kwa kasi akaanza kumvua shati tena kwa kulichana na kumkandamiza kifuani kama huduma ya kwanza!
“Ngesa please…Usiondoke nooo Ngesa amkaa”
Ngesa alikua kimya,mdomo wote mweupe na tumbo lake lilijaa maji ndiyo maana Daphine alihangaika kumpa huduma ya kwanza,bila kuogopa chochote akainama kidogo na kuifungua midomo yake,akaanza kumpulizia hewa kupitia mdomo wakawa kama wanapigana madenda,aliendelea na zoezi hilo bila kuchoka.
“Daphine,pole sana ni mipango ya Mungu”
Badi akasema na kumfariji Daphine lakini kwa mwanamke huyu ilikua ni vigumu kuamini hata kidogo,aliendelea kumpulizia Ngesa hewa kupitia mdomo huku akimkandamiza kifuani,hapo akaona maji yanatoka puani na baadhi mdomoni,Daphine akaendelea huku akilia machozi ya kwikwi.
“Ngesa amka…Amka Ngesaaa amkaa nakuomba..Ngesa”
Akazidi kufanya kila jitihada,maji yakaanza kutoka puani kwa Ngesa na mdomoni pia.Akaendelea kumkandamiza bila kuchoka.
“Koho! Kohooo! Kohoo! Kohoooo!”
Ni sauti iliyomfanya Daphine,apigwe na butwaa baada ya kusikia Ngesa anakohoa na kutema maji huku bado akiwa amefumba macho yake,hiyo ilimfanya azidi kumkandamiza kifuani zaidi na zaidi!
“Kohoo kohoo”
Safari hiyo Ngesa alipaliwa na maji na kukohoa mfululizo bila kuchoka huku akihema kwa kasi,Daphine hakuamini akamuinua na kumkalisha akamkumbatia kwa nguvu,kwa furaha aliyokuwa nayo akajikuta anambusu mdomoni na kumnyonya denda ni tukio lililomfanya Badi ashtuke mno lakini kwa Daphine hakujali,aliendelea kumpiga Denda Ngesa huku akimpiga piga mgongoni kwa furaha ya ajabu!
****
Kila alichokifanya Rais Leslie,hakikufaa kabisa katika maisha yake!Mawazo yake yote na macho yake mawili yalikua kwenye simu ya mezani kusubiria simu kutoka kwa Ngesa lakini matokeo yake yalipita masaa na siku kadhaa bila kupata majibu kutoka popote pale,kuishi kwake ikulu kwa siri kubwa kulimfanya ashindwe hata kuzungumza na simu,karibia asilimia themanini ya watu walidhania amekufa kwenye mlipuko wa ndege na ndiyo maana walilia na wengine kuomboleza.Kuna watanzania wengine walifurahi sababu Rais huyo alitawala kwa takribani miaka zaidi ya ishirini.Ni kitu ambacho kilikua ni kinyume na katiba ya nchi,aliwaza vitu vingi sana endapo akiachia ngazi angeishi vipi.Ghafla akapata wazo moja kabambe la kukusanya pesa na kutoroka nchi hiyo aende mbali,akiwaacha watanzania waamini tayari amekufa!Kwake yeye ingekua afadhali kuliko kuishi kama ndege tunduni.Nje ya jengo la Ikulu na katikati ya jiji alimwaga utitiri wa usalama wa taifa pamoja na jeshi la polisi wakilinda amani na usalama wa nchi hiyo,ilikua ni lazima wamlinde Rais Leslie kwa juhudi zao zote!
“Griii griiii…Griii griiii”
Mlio wa simu ya mezani,ulimshtua kutoka katika dimbwi la mawazo usiku huo wa saa tisa!Akashusha pumzi nzito na kusimama kiu vivu uvivu.
“Halloo”
“Mheshimiwa Rais,unaongea na Dustan”
“Dustan…”
“Tayari kazi yako,nimeifanya”
“Mpo wapi?”
Dustan ilibidi aelezee kila kitu kilichotokea na hakuacha kuomba msaada wa Rais Leslie!Taarifa hizo zikaibua matumaini mapya kwa Rais Leslie,hapohapo bila kupoteza wakati akaruka na kupiga simu moja kwa moja katika idara ya jeshi la anga,akawapa maelekezo wapi pa kumpata Ngesa!
****
“Tuku tuku tuku tuku tuku tuku”
Mlio wa Helkopta ukiambatana na taa kali ulimfanya Daphine aliyekua juu ya boti anaendesha kurejea nchi kavu akiwa na Ngesa pamoja na Badi,aangalie juu hofu ilimtanda lakini alitulia baada ya kuona ubavuni kuna nembo kubwa na bendera ya Tanzania,hapo alipunga mkono na kutabasamu kwani alijua kivyovyote vile walifika hapo kufanya ukombozi,kweli haukuwa utani jeshi lililotumwa na Rais Leslie lilifika hapo ili kuwachukua,Helkopta ilikua angani bado na mlangoni walisimama askari wawili wakiwa na mitutu yao wakiangalia huku na kule!Cha ajabu umbali wa mita hamsini waliona kitu kinawaka taa,walivyomulika wakashtuka mno.
“R..P..G..”
Askari mmoja akasema kwa sauti baada ya kuona kombora linaelekea upande wao,kilikua ni kitendo cha kufumba na kufumbua helkopta hiyo ililipuka na kukatika vipande vipande,moto na moshi mkubwa ukatokea!
“Paaa paaa griiii griiiii”
Mirindimo ya risasi ikaanza kusikika kutokea upande wa pili,boti walilopanda Daphine,Ngesa pamoja na Badi lilianza kushambuliwa na risasi nzito za kivita ambapo,wote wakalala chini kwa hofu kubwa sana!
Boti ya mbao yenye injini nyuma aliyopanda Ngesa,Daphine pamoja na Badi.Ilishambuliwa kwa risasi za kivita na zilifanikiwa kupasua pasua boti hiyo vibaya sana!Wote walikua wamelala chini na isingekua Daphine kutumia akili ya ziada wangefia ndani ya boti kwani risasi zilianza kupenya na kuwakosa kosa,alichokifanya ni kupiga teke upande mmoja na kujitupa upande wa kulia,boti ikapinduka chini juu!Wakawa wamefunikwa,ilikua ni hatari sana kwa Ngesa aliyekua dhaifu mwenye majeraha makubwa,hiyo ilifanya aishiwe nguvu kabisa.
“Peleka boti kule”
Ilikua ni amri kutoka kwa mwanaume mrefu mweusi,begani amening’iniza mkanda wa mtutu ambao aliushika vizuri kikakamavu,kwa haraka haraka alionekana ni mwanajeshi aliyefudhu kwenye mafunzo yote kwani alikua makini baada ya kuishambulia boti iliyowapakia wakina Ngesa,mbele yake walisimama wanaume wengine wawili mmoja amevaa vest ya kijeshi huyu kifua chake kilikua kipana na mwenye misuli na alikua nahodha wa chombo hicho aina ya boti!
Alikua makini sana na kiunoni alikua na bastola huku mkononi akiwa na tochi kali,alivyoambiwa hivyo tu akazungusha usukani wa boti ambayo ilianza kuyakata maji taratibu.Kushoto alisimama mwanaume mfupi aliyevaa kofia aina ya kapero.Mkononi ameshika mtutu kwa maana hiyo,ndani ya boti kulikua na wanaume watatu shupavu na makini.Ilikua ni lazima wamalize walichokianza kwani walipotoka kisiwani zilikua ni kama kilomita nne tu!
Muungurumo wa boti kuwafuata,ulimfanya Daphine aishiwe nguvu na kukaa kimya mwanga wa tochi ulimfanya atulie na mikono yake ambayo sasa ilianza kuchoka ilimfanya aogope zaidi kwani juu,alilishikilia boti lililowafunika na kuwaficha wakiwa wanaelea kwenye maji.Tochi yenye mwanga mkali,ikapiga palepale juu ya boti ni tukio lililomfanya ashtuke mara mbili moja,hofu ilimtanda cha pili alivyopiga jicho pembeni hakumuona Ngesa,ilikua ni hatari kubwa zaidi.
“Griiiii….Paaaa paaaaa…”
Mirindimo ya risasi ilimuogopesha mno sababu hakua na silaha yoyote ya kujitetea.
****
Kila kilichoendelea Rais Leslie alifahamishwa na Dustan kwa njia ya simu, mpaka Helkopta ilivyoshambuliwa na risasi.Hiyo ilimfanya Rais Leslie achanganyikiwe,hakujiuliza mara mbili akaamuru Helkopta nyingine tatu za kivita ziruke mpaka Bahari ya Hindi.Kilikua ni kitendo cha kufumba na kufumbua,Helkopta tatu zilikua angani na jeshi la Brigedia Karanje lilisambaratishwa kwa kiasi cha kutosha!Kombora moja,likachomoka kutoka kwenye moja ya Helkopta na kupasua vibaya sana boti waliopanda wanajeshi hao makatili.Ilikua ni kama filamu ya kuigiza.Utulivu baada ya mirindimo ya risasi ilimfanya Daphine,aingiwe na mashaka kwa kiasi cha kutosha.Hata hivyo hakutaka kujiamini sana,akatingisha miguu yake na kusukuma kiboti kwa pembeni ili achungulie,alichokiona kilimshangaza!Boti iliyokua inawashambulia,ilikua vipande vipande lakini kilichomfariji ni kusikia kelele za helkopta.Hapo,aliangalia juu na kupunga mkono!Mwanga ukapigwa chini na kum-mulika,kwa kasi akageuka na kumtizama Badi ambaye kwa wakati huo alikua hoi bin taaban.Ngesa,hakuonekana alichokifanya ni kuzama chini huku akiwa makini kutumbua macho yake mbele,ambapo sasa mwanga wa helkopta ulimsaidia kumulika kweny maji.Akamuona Ngesa anazidi kushuka chini,akaogelea kwa kasi na kumdaka kwa staili ya kumkumbatia!Hapohapo akaanza kupanda naye juu,mpaka wakaibuka.Sasa Helkopta ilikua maeneo ya chini kabisa,ambapo ngazi mithili ya kamba ilishushwa chini na kumfanya Badi,afanye utaratibu wa kumsaidia Daphine.
Askari mmoja,mkakamavu akateremka akitumia ngazi akamshika Ngesa vizuri wote wakaanza kusaidiana kumpandisha juu,haikua kazi rahisi!Mlinzi aliyekua kwenye mlango wa Helkopta,alikua makini sana na mtutu wake,hakutaka kufanya makosa kabisa alitizama huku na kule mpaka walivyohakikisha wote wameingia ndani.
“Hakuna mtu mwingine?”
Askari mmoja,alimuuliza Daphine kwani hakutaka kumuacha mtu yoyote nyuma!Daphine alitingisha kichwa,Magharibi na Mashariki kumaanisha hakuna mtu.Mawazo yake yote yalikua kwa Ngesa ambaye alikua amelala,amezirai.Helkopta ilizidi kuchana mawingu na walivyofika eneo walilolisimama Dustan na Frank Ntagara wakiwemo wanajeshi ambao kwa wakati huo walikua mateka,wakamulika tochi na kuona tayari magari ya Polisi yamefika.
Wakaendelea na safari yao,ambapo kituo cha mwisho kilikua ni Ikulu ya Rais.Kitendo cha kutua tu,madaktari wakasogea kwa kasi wakiwa na kitanda,wakamuweka Ngesa juu yake na kuanza kumkimbiza!Usalama wa taifa waliwazunguka huku wakiwa makini na kujihami kwa lolote lile.Ndani ya ikulu kulikua na hospitali,kitendo cha kufika tu Ngesa aliwekewa mtungi wa Oksijeni,ambapo hapo bila kuchelewa Rais Leslie alifika.
“Anaendeleaje?”
Rais Leslie akauliza huku akiwa amejaa simanzi usoni.
“Anapumua kwa mbali,Mheshimiwa Rais”
“Ataweza kuamka leo?”
“Hatuna uhakika”
Rais Leslie,akainamisha kichwa chini.Moyo ulimuuma kwa kiasi cha kutosha!Alitamani Ngesa azinduke wakati huo huo,lakini alivyomuona Daphine, akamsogelea kwa kasi.
“Shikamoo mheshimiwa Rais”
Daphine alisalimia kwa heshima na adabu zote huku goti moja la kulia,likienda chini kidogo!Moyo wake muda wote ulimuenda mbio na alijua kivyovyote vile angeshtakiwa kwani alikua na kesi ya mauaji.
Hata hivyo alikumbuka vitu chungu mzima kichwani kwake,hususani alivyoingia ikulu kwa mara ya kwanza alivyokua mtoto mdogo baada ya kufaulu mitihani,akiongoza Tanzania nzima.Vitu vingi sana vilipita kichwani mwa Daphine.Walikaa hapo,zaidi ya dakika thelathini wakitaka kujua hali ya Ngesa inaendeleaje.Bado hakuzinduka kutoka kitandani ingawa mapigo yake ya moyo yalidunda.
*****
Ngesa,aliendelea kulala kitandani kwa siku tatu mfululizo, akipatiwa matibabu Ikulu.Alikua katika uangalizi maalum na alilindwa mithili ya mtoto wa Rais,kila kitu kilichotakiwa kilifanyika hapohapo huku wanajeshi waliokua chini ya ulinzi wakihojiwa maswali humo humo ndani ya ikulu.Usalama wa taifa,hawakuambulia chochote kile.Walivyomuhoji Daphine awaambie kila kitu kilivyotokea ndipo wakaanza kuamini ni kwa namna gani Ngesa alivyokua mtu makini na kiungo mzuri katika operesheni hiyo nzito,Frank Ntagara alivyohojiwa alizungumza kila kitu lakini alibanwa na kuwekwa nyuma ya nondo sababu tu alienda kinyume na itfaki za Usalama wa taifa.
“Nani aliyekupa amri ya kufuatilia hii Kesi?”
Hilo ndilo swali aliloulizwa na mkurugenzi wa usalama wa taifa Ramadhan Nurdin Mpelembe!Kitendo cha Frank Ntagra kuingilia faili hilo la Olina,kilimkera kwa kiasi cha kutosha.Chumba kinachofuata,Olina Kalumuna alikua juu ya kiti na alihojiwa jinsi mambo yalivyoenda,mpaka alivyofuatwa akiwa uwanja wa ndege,hata hivyo hakuacha kumshukuru Ngesa pamoja na Frank Ntagara hakumsahau Daphine vile vile.Aliongea huku akilia machozi ya uchungu na kilichomuumiza moyo ni baada ya kupewa taarifa za mume wake,kukutwa amenyongwa na kufariki dunia!
“Eeeh Mungu”
Olina,alilia kwa kwikwi na hasira.
“Usilie dada,pole sana”
Mwana usalama Magreth,alimuonea huruma mwanamke mwenzake akampa kitambaa ili ajifute machozi kisha kutoka nje ambapo huko alionana na Ramadhan Mpelembe!
“Kasema nini?”
Akakumbana na hilo swali.
“Ntagara hana kosa,naomba umuhoji vizuri”
“Hapana,haiwezekani.Yupo chini ya ulinzi na lazima apewe adhabu”
“Kwanini?”
“Haina haja ya kuniuliza,mimi ni bosi wako.Fuata nachokwambia na kitu kimoja..”
Hapo Ramadhan Nurdin akamsogelea karibu Magreth,mpaka sikioni.
“Rais Leslie,asijue chochote!Umenielewa?”
Kufuatia hapo Ramadhan Nurdin akaondoka,bado moyoni alikua na kinyongo na Ngesa na alishangaa sana kusikia Rais Leslie yupo naye karibu kwa kiasi cha kutosha!Alielewa nini maana yake endapo Ngesa angezinduka kutoka kitandani.Alichokifanya ni kunyoosha mpaka mlango wa hospitalini alipolazwa Ngesa,hapo alikutana na maaskari wawili,wakamzuia kuingia.
“Nataka kuonana na Ngesa”
“Hairuhusiwi mtu kuingia”
“Kwanini?Nipo kazini nipisheni nipite”
“Nasisi tupo kazini,tunafata amri tu”
“Mimi ndio incharge”
“Ndio maagizo tuliyopewa na Rais Leslie”
“Mimi ni bosi lakini…”
“Hakuna cha lakini”
“Mnajua mimi ni nani?”
“Hatuongei na mbwa,tunaongea na mwenye mbwa”
Askari huyu,ambaye alikua kauzu kama dagaa,alimpa majibu ya shombo Ramadhan Mpelembe ni jambo lililomfanya achukie kwa kiasi cha kutosha!Aliamini fika Ngesa akipata fahamu nafasi yake itachukuliwa,hilo lilikuwa wazi asilimia zote mia moja!Ndiyo maana kichwa kilimuuma mara ghafla akapata wazo la kumuua Ngesa akiwa kitandani,wakati akitafakari hayo alikua ofisini kwake mikono yake yote miwili kaifumbata chini ya kidevu.
“Griii griiii”
Simu yake ya mezani,ilimshtua kutoka katika dimbwi la mawazo!
“Yes”
“Boss,wamekataa kusema”
“Hawajaongea chochote?”
“Ndio,lakini nina wazo”
“Wazo gani?”
“Tuwakabidhi jeshi la polisi”
“Hell no,hii ni inshu ya kiusalama zaidi.Haitowezekana”
“Siku zinaenda”
“Nitajua cha kufanya Jemima,Ngesa kaamka?”
“Bado”
Nurdin Mpelembe alijibu kwa hasira za waziwazi na kuweka mkonga chini.
***
Ndoto mbalimbali akiwa katika operesheni maalum nchini Sudan,Darfur!Zilimfanya aweweseke kitandani kwani kilichosikika ni mirindimo ya risasi.
“Ngesaaa”
Patashika ilikua kubwa na magorofa yalikua yanaporomoka,risasi zilipigwa kila kona!Ghafla,akakurupuka kutoka usingizini,akatizama huku na kule huku jasho jingi likiwa linamtoka mwilini.Hakuelewa yuko wapi lakini alichokumbuka mara ya mwisho alikua ndani ya helkopta na baada ya hapo sura ya Daphine ikamjia wakiwa ndani ya boti.Alivyojaribu,kuvuta kumbukumbu jinsi alivyofika mahali hapo,akashindwa kabisa kuelewa alifika vipi hospitalini.Pembeni ya mkono wake aliona mrija ambao juu kulikua na dripu ya maji,alivyojiangalia vizuri akaona bandeji,hapo akakumbuka jinsi alivyotekwa na kuteswa!Sasa kila kitu,kikaanza kuingia taratibu kichwani kwake.Kilichomshtua,ulikua ni mlango kufunguliwa,akamuona Daktari mwanamke,aliyevaa koti refu shingoni kaweka kifaa maalum cha kupima mapigo ya moyo.
“Unaendeleaje?”
Dokta akauliza huku akitoa tabasamu la kirafiki.
“Nimefikaje hapa?”Akajibu kwa swali.
“Uliletwa juzi”
“Juzi?!”
“Ndio,mimi naitwa Dokta Anna.Nimefurahi kukuona unafumbua macho”
“Nipo hospitali gani?”
“Upo Ikulu”
“Ikulu?”
“Ndio”
Kuna vitu vilianza kupita kichwani kwa Ngesa,akatizama dripu ya maji iliyokua kwenye mshipa wake na kuinyofoa kitemi,hapohapo akatoka kitandani.
“Ukijaribu kunifata,nitakuua”
Ngesa alisema kwa ukali ni tukio lililomfanya dokta huyu,aone mgonjwa wake amerukwa na akili ama maralia imempanda kichwani,kabla Ngesa kuufikia mlango.Ukawa umefunguliwa,Rais Leslie akawa ameingia huku pembeni akiwa na walinzi wake.
“Derick Ngesa”
“Rais Leslie”
Wasiwasi wa Ngesa ulikua ni juu ya Rais huyu Leslie,kigeugeu ambaye muda wote hubadilika kama kinyonga sio ajabu baada ya hapo angewekwa chini ya ulinzi,ndiyo maana akajihami na kutaka kutoroka.
“Derick,pole sana”
“Ahsante”
Hapo ilibidi Rais Leslie amuelezee kila kitu kinagaubaga jinsi ilivyokua mpaka akaletwa mahali hapo.
“Daphine yuko wapi?”
“Chumba cha mkutano”
“Nahitaji kuonana naye”
“Vaa shati kwanza twende”
Pembeni kulikua na shati jipya lenye rangi ya kijivu.Ngesa akalitia mwilini na kuongozana na Rais Leslie mpaka alipokaa Daphine,walivyoonana wakakumbatiana kwa nguvu.
“Nashukuru Mungu upo salama Ngesa”
“Wako wapi?”
“Wakina nani?”
Swali hilo lilimaanisha wale mateka,ambao mara ya mwisho walikua chini ya ulinzi.Ngesa hakutaka kupoteza muda,usongo aliokua nao dhidi ya baba yake mzazi ulitisha na kupitia wanajeshi waliokua mateka aliamini kivyovyote vile,wangekua msaada mkubwa kutoboa siri hiyo.
“Mheshimiwa Rais,naomba ruksa yako”
“Derick,fanya unavyoweza.Nimekupa madaraka ilimradi wahalifu wote wapatikane sanasana Brigedia Karanje,amekua tishio la nchi”
Ni kitendo kilichomfanya Ngesa,atabasamu ikawa ni sawa na chizi kupewa rungu!Alichokifanya ni moja kwa moja akiwa amebana meno yake kwa hasira,akapitiliza mpaka ofisini kwa Ramadhan Mpelembe ili ampe taratibu zote na namba za mahali walipowekwa wanajeshi mateka,ikiwemo na faili zima.Ngesa akaingia kitemi bila hodi,macho kwa macho wakakutana na Ramadhan Nurdin.Ni tukio lililomfanya mwanausalama huyu,atetemeke na kuogopa kwa wakati mmoja.
“Nipatie faili zote za hao wanajeshi,waliokua chini ya ulinzi pamoja na password”
Bila salamu Ngesa,akaamuru akawa sasa kama yeye ndiye bosi na Ramadhan sekretari.
“Umeingia hujapiga hodi ala..”
“Napata mafaili,sipati mafaili?Nijibu”
Hapo Ngesa alizungumza huku akitembea taratibu akimsogelea Ramadhan Nurdin.
“Wewe kama nani?Nikupe nyaraka hizo kienyeji”Akavimba na kusimama,sasa wakawa wanatizamana kama majogoo!
“Hayo maswali muulize bosi wako sio mimi”
“Hayo mambo unayotaka kufanya yatakutokea puani Derrick,kwanza unajua malaya wako Jaqlin Mfinanga alipo,usiji…”
Kabla ya Mkurugenzi Ramadhan Mpelembe kumalizia sentesni yake!Aliona ngumi moja inakuja kwa Ngesa,akarudi nyuma kidogo na kupita hewani hata hivyo hakuweza kuona kifuti kilichotua katikati ya shingo yake na kumfanya aparamie kabati la mafaili,Ngesa akapanda juu ya meza na kumfuata kule kule kwenye makabati.
“Leo,utanitajia kila kitu nachotaka kujua naanza nawewe”
Ramadhan akawa amevuna alichokipanda kwani alikabwa vizuri kwa mtindo wa Judo ambapo shingo yake,iliwekwa ukutani huku akiwa amekandamizwa na kiwiko,hiyo ilimfanya ahisi maumivu makali sana sehemu za shingo,akashindwa hata kutoa sauti.
****
“Si…jui chochote”
“Nitakuua leo”
“Nge…sa sijui chochote,sina sababu ya kukudanganya”
“Jaqlin yuko wapi?”
“Siju..i unachoongelea”
Roba kali,ama kabali alilopigwa Ramadhan Nurdin Mpelembe lilimfanya ashindwe kutoa sauti vizuri,hata alivyojaribu kujitoa ilishindikana kabisa.Ulikua ni utaalam wa hali ya juu,uliyomfanya mpaka ashindwe kupumua vizuri.Aliumia sana sehemu za shingo na kichwani kwani kiwiko cha Ngesa kilipita katikati ya shingo yake na mkono mmoja ukawa umekandamiza kichwa chake,nyuma yake kulikua na kabati lililomfanya azidi kupata maumivu zaidi.
Picha ya Jaqlin Mfinanga ilimjia Ngesa kichwani,hasira zilimpanda na sasa alitaka kujua ni wapi alipo,kilichomfanya asitishe zoezi hilo ni baada ya kusikia mlango unagongwa kwa nguvu.Ilielekea kulikua na dharura kali na kabla hajafanya kitu chochote,ulisikika mlio wa risasi.Ni jambo lililomfanya Ngesa amtizame Ramadhani Nurdin kwa macho makali,akamuachia na kuruka meza!Niya yake ikiwa ni kuufikia mlango lakini kabla hajafika,ukawa umefunguliwa tayari.
“Kuna nini?”Ngesa akauliza.
“Koplo Chirege anataka kutoroka”
Mwanamke mnene kiasi,alizungumza harakaharaka bila kumeza mate ni tukio lililomfanya Ngesa apigwe na butwaa la waziwazi.Alivyotokeza mlangoni,akaona heka heka za maaskari na usalama wa taifa wakipigana vikumbo wakimtafuta Koplo Chirege,aliyekua na bastola na niya ya kutoroka.Jambo hilo lilimfanya Ngesa achukie,hapohapo akachomoka na kuanza kuwafuata maaskari nyuma nyuma.
“Nipe bastola”
Akasema na hilo halikua na pingamizi,baada ya kupewa akaikoki na kuanza kutembea korido kwa korido akiwa sambamba kufanya msako.Aliamini kabisa Koplo Chirege,asingekua na uwezo wa kutoroka eneo hilo lililokua na ulinzi mkali.Hiyo ilimaanisha alikua humo humo ndani,akili ya Ngesa ikaanza kufanya kazi kwa haraka na kuanza kujiuliza maswali mengi. Na kulikua kuna uwezekano mkubwa sana wa Koplo Chirege kupewa ushirikiano wa kutoroka kwani isingekua rahisi kuchomoka kienyeji namna hiyo.
“Paaaaa”
Ulikua ni mlio mwingine wa risasi uliosikika na kumfanya Ngesa atulie kidogo ili kusikilizia uwelekeo wa maaskari ungeenda wapi.Hekaheka za maaskari wakiwa na bastola zao mikononi walianza kupita kwenye korido,hiyo ilikua ni wazi kabisa wakiongozwa na redio upepo juu ya tukio.
Ndio maana Ngesa akaunga mkia mpaka waliposhuka ngazi na kuingia chumba cha tatu kutoka mwisho.Jambo aliloliona lilimuogopesha,chini kulikua na damu maaskari wamezunguka,alivyowapangua pangua akaona kitu kilichomfanya aumie moyo.Koplo Chirege,alikua chini amelala ubongo wake umefumuliwa vibaya sana na risasi,ambapo mkononi alishika bastola.Koplo Chirege aliamua kujiua hilo lilimfanya Ngesa aumie zaidi na zaidi kwani alikufa na siri nzito kifuani,hata hivyo bado kuna kitu kilimsumbua kichwani.Alitokaje tokaje?Akiwa selo inayolindwa na maaskari.
“Nani alikua zamu?”
Lilikua ni swali kutoka kwa Ngesa akimuuliza askari aliyekua makini anapiga picha maiti ya Koplo Chirege,aliyeamua kuutoa uhai wake.Ngesa,akaitizama maiti hiyo ambayo ilitisha ingawa kwake yeye vitu kama hivyo vilikua vya kawaida mno kuvishuhudia.
“Sirgent Kaiza”
“Yuko wapi?”
“Sijui”
Kuanzia hapo,msako wa Sirgent Kaiza ukaanza, niya ya Ngesa ilikuka ni kumuhoji ili apate picha kamili ingawa ndani ya akili yake alishamuhukumu moja kwa moja,alichokifanya ni kumuulizia kila kona,alivyoambiwa yupo nje!Akamfuata kwa haraka,kilichomshtua ni kumuona Sirgent Kaiza tayari keshabadili nguo kwa maana hiyo anataka kuondoka.
“Sirgent”
Ngesa akaita huku akimtizama machoni bila kupepesa kope.
“Yes”
“Nakuomba mara moja”
“Bila shaka”
Hapo Ngesa alimeza fundo zito la mate,lililochanganyika na hasira!Sirgent Kaiza mbele Ngesa nyuma,wakaongozana mpaka ndani na walivyoingia kwenye korido,Ngesa akatizama huku na kule!Alivyoona kuna usalama,kama ngedere akamrukia Sirgent Kaiza shingoni na kumpiga kifuti kimoja cha mbavu,kilichomfanya Sirgent Kaiza abweke kama mbwa,kwa mtindo wa judo akamtuliza kando ya korido ndefu ambapo mtu yoyote yule angepita isingekua rahisi kuwaona.
“Sirgent,sitaki ufie mikononi mwangu.Nataka kujua jambo moja,nitajie watu waliokutuma umtoroshe Koplo”
Sirgent Kaiza,alitumbua macho mithili ya mjuzi aliyebanwa na mlango!Na swali aliloulizwa na Ngesa lilimfanya ababaike kidogo,hapohapo akageuzwa na kupigwa kichwa kizito cha pua.
“Kacha kacha”
Sasa Ngesa akakoki bastola ambayo aliichomoa kiunoni na kumsogelea mpaka chini alipokua, akamuwekea kwenye paji la uso.
“Nitajie”
“Nili..pigiwa simu na mtu asiyejulikana..Yupo nyumbani kwangu,alikua na familia yangu.Aliniambia nimtoroshe Koplo Chirege na nisipofanya hivyo,atamuua mke wangu na watoto wangu”
“Ulikua na uhakika gani kama alikua na mkeo?”
“Niliongea nao,naip..penda sana familia yangu Ngesa”
“Simama”
Sirgent Kaiza,alisimama kwa kutetemeka na miguu yake ilikosa nguvu kabisa wakaongozana moja kwa moja mpaka kwenye chumba kimoja, ambapo humo alimtaka Daphine awepo ili wajue wangeanzia wapi na kila kilichotokea kuanzia hapo Rais Leslie,alipewa taarifa na kwa hilo alitoa ushirikiano na aliumia sana moyoni huku akimsisitizia Ngesa afanye kila jitihada ili genge hilo hatari la Brigedia Karanje,liwe mikononi mwa sheria.
“Unaishi wapi?”
Daphine akauliza baada ya kusikiliza kila kitu kilichotokea.
“Bom bom kijiwe samli”
“Tupe hiyo namba iliyokupigia simu”
Walivyopatiwa namba ya simu,wakajaribu na kukuta haipo hewani.Ni kitendo kilichowafanya wachukie na kuona giza mbeleni.Hata hivyo hawakukata tamaa walichokifanya ni kutoka nje ambapo hapo waliongozana Ngesa na Daphine huku ndani ya gari,akiwa amepanda Sirgent Kaiza.Kwa safari ya kuelekea Bombom kijiwe samli.Ndani ya gari,Ngesa alikua makini kwenye usukani na Daphine yupo kushoto kwake,nyuma amekaa Sirgent Kaiza,akiwa kama mtu asiyeamini kinachoendelea katika maisha yake.
“Jaqlin,yuko wapi?”
Lilikua ni swali kutoka kwa Ngesa,akimuuliza Daphine.
“Mara ya mwisho,nilimuacha Bagamoyo akiwa na mke wa Dustan”
“Mpigie simu Bonta,muelekeze ni wapi walipo awafuate”
Ngesa,alikua huru maisha yake yalibadilika yakawa tofauti na mara ya kwanza alivyokua anatafutwa jiji zima,sasa hivi alikua mwanaume mwenye madaraka ya kuamrisha askari yoyote na usalama pia Rais Leslie alikua naye bega kwa bega.Ndiyo maana ikawa rahisi kwake kutoa amri na ikafanyika mara moja,kwa kuwa Daphine alikua na simu.Akapiga moja kwa moja na kutoa maelekezo,ambapo hapo waliwasiliana na jeshi la polisi la Bagamoyo ili taratibu na kuwapa ulinzi Jaqlin pamoja na mke wa Dustan zianze mara moja.
“Tunaelekea wapi Sirgent?”
Walivyofika Relini,ikabidi Ngesa aulize.Sirgent Kaiza,akawa ana kazi ya kuelekeza,walivyopita reli,wakanyoosha na kukunja kulia ambapo huko kulikua na barabara ya vumbi,ulikua ni mtaa uliotulia na mara chache walionekana watoto wadogo wakicheza mpira wa kufuma yaani chandimu.Wakanyoosha na kukunja kona kulia,ambapo mbele kidogo kulikua na miti ya minazi.
“Kwenye ile nyumba nyeupe pale”
Sirgent Kaiza,akanyoosha kidole na kumfanya Ngesa aweke gari kando ili kuangalia usalama wa eneo hilo,hapo alichomoa bastola na kuikagua kama ina risasi,alivyoridhika.Akaiweka juu ya kiuno upande wa nyuma,akashuka na kutizama huku na kule!
“Shuka”
Sirgent Kaiza,akawa ameshuka huku akitetemeka hofu ikiwa imemtanda.Daphine,alivyoona hivyo akatizama tena kwa mara nyingine ili kuangalia usalama kisha wakaanza kuongozana kwa tahadhari kubwa,walivyofika mlangoni Daphine akaelekea upande wa nyuma wa nyumba hiyo.Huku Ngesa taratibu akitembea kuusogelea mlango wa mbele.
Milango yake yote ya fahamu ilikua wazi na makini,hisia mbaya zikaanza kumsumbua kichwani hiyo ikampelekea mpaka vinyweleo vyake,visimame!Hiyo ilikua ni dalili mbaya sana kwake,ndiyo maana akanyata kwa tahadhari mpaka dirishani,ambapo alichungulia lakini alishindwa kuona ndani kuna nini kutokana na pazia kufunikwa!Alichokifanya ni kunyata taratibu mpaka mlangoni,ambapo kwa tahadhari kubwa akaanza kushusha kitasa,mlango ukafunguka na kutoa sauti ya kelele iliyosababishwa na kutu za bawaba hilo lilimfanya Ngesa achukie lakini alivyoingia ndani,akachomoa bastola na kuanza kutembea taratibu huku Sirgent Kaiza,akiwa nyuma yake.Alishangazwa sana na mazingira ya nyumbani kwake,namna kulivyotulia na hakuna sauti ya mkewe wala watoto!Mbele ya seble hiyo kulikua na korido fupi yenye vyumba viwili!
“Nisubiri hapo”
Ngesa akasema kwa sauti ya chini akimuonya Sirgent Kaiza,asimfuate nyuma!Mlango wa kwanza,aliufungua na kuingia ambapo huko alikuta kitanda kidogo na nguo juu ya kiti,hakutaka kuendelea kubaki,alivyofungua chumba kinachofuata!
Akasita kidogo,harufu ya damu ikamfanya ajihami na kukamata bastola yake sawasawa,akafungua mlango taratibu na kupigwa na butwaa la waziwazi.Juu ya kitanda,aliona maiti ya mwanamke akiwa uchi wa mnyama,miguu yake imetanuliwa huku na kule!Bila shaka kabla ya kuuwawa alibakwa na mbaya zaidi alikua na majeraha shingoni na tumboni,tundu la risasi ya shingo ilimchakaza vibaya sana na kuchukua uhai wake,unyama huo ulimfanya Ngesa aumie kwa kiasi cha kutosha na kumuonea sana huruma Sirgent Kaiza,aliyefanya kazi bure iliyokua na malipo ya kifo cha mkewe.
Alivyopeleka macho yake kushoto,akaona mlango mwingine akawa ana uhakika kabisa ulikua ni mlango wa bafuni,lakini kilichomshangaza ni kitasa cha mlango kilivyojaa damu iliyoganda.Akafungua mlango kwa tahadhari na kukuta maiti za watoto wawili,zina matundu ya risasi kifuani.Hakika yalikua ni mauaji ya kinyama na aliyefanya hivyo,hakustahili kuitwa binadamu hata kidogo.Watoto wadogo,hawakua na hatia yoyote ile lakini alielewa muuaji alitaka kumuumiza Sirgent Kaiza.Hapo,Ngesa alitoka bafuni na kuanza kukagua chumba,kuanzia kwenye madroo mpaka juu ya kabati.Hakukuta chochote cha maana,alichokifanya ni kutoka na kumfuata Sirgent Kaiza alipo.
“Sirgent”
Ngesa akaita kwa macho yaliyojaa huruma,hakuelewa habari hizo mbaya amfikishie vipi.Lakini ilikua ni kama Sirgent alianza kuhisi kitu kwani kupitia sura ya Ngesa kuna kitu,alijifunza ndiyo maana hakutaka kusubiri aambiwe chochote akanyoosha moja kwa moja mpaka chumbani,alichosikia Ngesa kilikua ni kilio mno.
“Mke wangu Salome..Kwanini hivi?Ehhh Mungu,wanaangu”
Sirgent Kaiza alilia na kusaga meno,ni tukio lililomfanya Ngesa nayeye ajiunge naye chumbani!Alichokifanya ni kuchukua shuka ili kumsitiri marehemu kwa kumfunika huku akimpiga piga Sirgent begani.
“Jikaze Sirgent,kulia kwako hakutobadilisha chochote nachohitaji ni ushirikiano wako”
Ngesa alisema kwa niya ya kumfariji Sirgent kisha akatembea mpaka dirishani,ambapo hapo alifungua pazia na kuangalia nje.Ilikua ni kama Mungu kwani aliona pikipiki imepaki upande wa pili,dereva wa pikipiki amechomoa mtutu hadharani,kabla ya kujihami risasi zikaanza kurushwa upande wa dirishani
!Ilielekea mlengaji alikua mwenye hasira kwani alimimina risasi nyingi kama mvua.Na mtutu huo,ulikua hatari wa kivita kwani ulitoboa toboa ukuta kama mzaha,Ngesa alikua tayari amelala chini kifudifudi lakini anatambaa na tumbo kama mwanajeshi vitani,alivyoufikia mlango akajitupa kwenye kordo na kuanza kutambaa tena mpaka alivyofika usawa wa seblen,hapo akasimama na kuchomoa bastola na kumtizama mlengaji yule aliyekua nje na pikipiki,kuna kitu kilimshangaza na kumfanya ajiulize maswali juu ya mtu huyo kufika eneo hilo kwa haraka.Hata hivyo,aliibuka dirishani kwa shabaha makini akairuhusu risasi ichomoke.
“Paaaaaa”
Risasi ikachomoka na kumkosa kosa dereva wa pikipiki ambaye alikua hatari,hiyo ilimfanya ajihami na kupanda kwenye pikipiki kwa haraka.Hapohapo,akaizungusha kwa kasi na kufanya mchanga uruke.Ni tukio lililomfanya Ngesa aanze kukimbia mpaka lilipokua gari,akaingia kwa kasi ya umeme!Akaliwasha na kuligeuza kitaalam,akaweka mguu kwenye mafuta.Gari,likachomoka kwa kasi ya ajabu lakini cha ajabu na kilichomshangza ni baada ya pikipiki hiyo kupanda jiwe ikawa hewani,dereva wa pikipiki kwa utaalam wa hali ya juu akaanza kurusha risasi zilizofanya kioo cha gari la Ngesa kipasuke vibaya sana,sasa hapo Ngesa akaona hatari ya dereva huyo aliyekua mtundu na mfanisi kwenye michezo ya pikipiki,hazikupita hata dakika mbili wakawa wameingia kwenye lami.
Pikipiki bado ilikua katika mwendo wa kasi kila mtu akijaribu kuchochea Ngesa akitumia mguu jambazi akitumia mkono,lilikua ni tukio lililowafanya wakazi wa bom bom,kushangilia wakidhani ulikua ni utani.Pikipiki,ilimuacha Ngesa umbali wa mita ishirini akiwa na gari,kutokana na dereva huyo kupenya penya katikati ya magari kulimfanya Ngesa apate kikwazo!
Alichokifanya Ngesa baada ya kuona vijana wa bodaboda wamepaki,umbali wa mita tano,hapohapo akapata akili!Alivyowafikia,akaweka mguu kati gari ikapiga msele.Akashuka kwa kasi akiwa na bastola mkononi.Hakutaka kuongea chochote zaidi ya kumshika shati kijana mmoja aliyekaa juu ya pikipiki aina ya boxa na kumsukuma kando.Akapanda na kupiga kiki,pikipiki ikatoa mlio,hapohapo bila kupoteza muda akaitoa kwa kasi ya kimondo.
****
Vijana ama madereva wa pikipiki katika kijiwe hiko maeneo ya Bombom walipigwa na mduawo wakishangazwa na tukio hilo la ghafla lililotokea baada ya kumuona mzee wa makamo akiwa na bastola mkononi na kufanya uvamizi wa pikipiki,tukio hilo liliibua hali ya sintofahamu na kuvuta macho ya watu eneo hilo, kila mtu akitaka kumuuliza maswali dereva huyo aliyeshikwa shati na kusukumwa na Ngesa kwenye mtaro wa maji machafu,kisha boda boda yake ikatimua mbio.
Akiwa katikati ya kuwahadithia wenzake simulizi hiyo ambayo ilimuudhi akiamini hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumsaidia kupatikana kwa chombo chake!Yeye Ngesa alikua akikatiza mataa ya Tazara,mkono wake mara zote ulivuta mafuta na kufanya pikipiki hiyo ichomoke kwa kasi ya Roketi na kufanya wakazi wa eneo hilo washike vichwa.
“Ndio maana wanakufa hovyo hawa mbwa!Pale hana lolote anakimbilia kupaki”
Mwanaume mmoja,aliyeonekana kukerwa aliropoka baada ya kuona pikipiki ya Ngesa imepita kwa kasi ya kuogopeka!
“Sijui anawahi nini?Mwenzake kapita mbele”
Mwingine hakukosa kutoa neno!
Ukweli wa mambo ulibaki pale pale pikipiki aina ya ‘BMW S1000 San Marino’ aliyokua anaendesha jambazi,ilikua na uwezo mkubwa wa kukimbia tofauti na boxa aliyokua nayo Ngesa hiyo ikampa wakati mgumu sana Ngesa kwani umbali alioachwa ulikua mrefu mno!
Dalili za kukata tamaa zikaanza kujijenga kwenye fikra zake na kupata wasiwasi zaidi, baada ya kuangalia kwenye dashbod ya mafuta.Matumaini ya kumpata jambazi huyo hatari yakayeyuka mithili ya mshumaa uliopulizwa na upepo!Alivyofika Buguruni pikipiki hiyo ya boxa ikaanza kutoa muungurumo wa ajabu mithili ya jenereta linaloisha mafuta, hiyo ilikua na maana ya kuwa pikipiki imeisha mafuta tayari,alichokifanya ni kupaki pembeni na kusimama kando alivyoona sheli pembeni yake akajipa matumaini la wazo la kwenda kujaza mafuta lakini akajionya kufanya hivyo kwani angepoteza muda na adui yake angefika mbali sana,wazo lililomjia hapo ni kuanza kukimbia kwa miguu mpaka kwenye kijiwe cha boda boda kilichokuwa eneo hilo,kwa mtindo aliofanya Bom bom ndicho alichokifanya eneo hilo kwa kutoa bastola ili kusiwe na upinzani wowote ule.
Hila yake ilifanikiwa bila kupoteza muda lakini alikasirika baada ya kutoona pikipiki ya jambazi.Akawa ana kazi ya kuangalia kila kichochoro kilichompa mashaka lakini hilo halikumsaidia kitu chochote,hapohapo akakata tamaa na kuamua kurudi Bom bom kijiwe samli,ambapo yalikua makazi ya Sirgent Kaiza!Alivyofika eneo hilo,akakuta tayari taratibu za kiaskari zimeanza kufanyika kama kuweka Warning tep,kupiga picha za maiti na mahojiano kwa majirani wa hapa na pale.Ngesa akatoka nje,ambapo hapo alifanikiwa kuonana na mkuu wa kikosi hiko Kamanda Mwandu,urefu wa mwanaume huyo na mwili wake ulivyokua mkakamavu ulimfanya aogopeke kwa kiasi cha kutosha!Kamanda Mwandu hakupenda mazoea ya ajabu hata kidogo!
“Kamanda mmefikia wapi?”
Ngesa,akatupa swali.Kutokana na kupewa taarifa za Ngesa kutoka kwa wakuu wake wa kazi,ikabidi ampe heshima kwa kuchapa mguu mmoja chini na kutoa salamu ya kikakamavu.
“Bado tunafanya upelelezi”
“Chochote cha maana?”
“Kipo”
“Nipe ripoti”
Kamanda Nyandu,alianza kutoa ripoti kwa juujuu tangu alipofika hapo na kuhitimisha usiku wa jana yake,lilionekana gari la jeshi maeneo hayo kisha kutokomea kusikojulikana!Mbali na hapo,kulikua na mabishano makubwa na vishindo vizito ndani ya nyumba hiyo kabla ya umauti kuwakuta marehemu waliokua ndani.
“Taarifa hizo umetoa wapi?”
Ngesa akauliza kwa udadisi huku akimtizama Kamanda Nyandu kwa makini,urefu wa askari huyo ulimfanya Ngesa ainue kichwa chake juu kidogo ili kumsikiliza kwa makini.
“Kuna Mama mmoja alijitambulisha kwa jina la Fatuma”
“Yuko wapi?”
“Yule pale”
Kamanda Nyandu akatumia kidole chake kumuonesha Mama mtu mzima aliyejifunga kanga mwili mzima,akiwa na baadhi ya maaskari kutoa ushirikiano!
“Za sa hizi mama angu?”
Ngesa alimkatisha kwa kutoa salamu hiyo!Kama ilivyokua kwa maaskari wote,ndivyo alivyomueleza Ngesa licha ya kukerwa kwa kurudia kutoa ushahidi huo akiurudia kwa kila askari lakini alijitahidi kutoa ushirikiano!Bado Ngesa,hakupata picha kamili,hata hivyo kuna wazo moja lilimjia kichwani kurudi Ikulu na kuanza kuwahoji wanajeshi waliokua chini ya ulinzi akiamini hao wangempa mwanga,akaomba gari moja na safari ya kurudi Ikulu ikaanza mara moja.
Akiwa njiani anaendesha gari,alihisi mapigo yake ya moyo yanapoteza utulivu baada ya kusikia Jaqlin Mfinanga na Mke wa Dustan!Hawajaonekana na wala hakuna dalili za mtu yoyote kujua walipo,Ngesa alitamani kupaki gari pembeni lakini alivyokumbuka jukumu zito alilokua nalo mbele,akapiga moyo konde akiamini atakaoenda kuwahoji ndio watampa mwanga wa kujua kila kitu.Baada ya ukaguzi Ikulu,akaingia ndani na kusaini kibali cha kuingia ndani ya chumba kidogo cha maabusu.Kilikua ni chumba kidogo chenye viti viwili na meza katikati,kwenye kiti alikaa mwanaume mrefu na mnene aliyejazia kila mahali,alikua ni mwanaume aliyeonekana mtu wa mazoezi.Ngesa alilitambua hilo baada ya kukaa na kumdadisi bila kusema chochote.
“Luteni Sagasa”
Ngesa,akaita huku akimtizama kwa macho makali yaliyojaa chuki.
“Derrick Ngesa”Luteni Sagasa,nayeye akajibu huku akitoa tabasamu la kinyama!
“Kwanini,umeisaliti nchi yako Luteni?”
“Unajua mwenyewe,hilo ni swali la kitoto sana”
“Sisi wote ni watanzania,hayo unayoyafanya hayatoweza kubadilisha chochote”
“Hujui kitu Ngesa,muulize baba ako”
“Ndio maana niko hapa nawewe,nataka kujua alipo ili nimuulize vizuri”
Sentensi hiyo ilimfanya Luteni Sagasa,acheke kwa dharau!
“Umuulize nini?”
“Kwanini ameisaliti nchi yake,nitajie alipo”
“Hata,nikikutajia alipo.Haitokusaidia chochote Derick Ngesa,kwanza unajisumbua bure pili siwezi kukutajia chochote kile”
“Najua,huwezi.Wewe ni Luteni,una mafunzo yote na sio rahisi kutoa siri.Lakini naomba nikuhakikishie,utasema kila kitu”
Hapo Luteni,aliangua kicheko na kufanya sauti yake iwe kama mwangwi.Kwani chumba hiko kilikua kidogo sana.Ni tukio lililomfanya Ngesa achukie kwa kiasi cha kutosha lakini hakua na jinsi zaidi ya kusimama na kutoka nje ya chumba hiko bila kupata chochote cha maana!
Alivyomkumbuka Jaqlin Mfinanga kipenzi cha roho yake,akakosa raha kabisa.Ghafla akaanza kumchukia Daphine kwa kitendo cha kuwaacha peke yao huko Bagamoyo bila sababu ya msingi wakati mwingine alihisi wenda mwanamke huyo ana ajenda zake binafsi,hata hivyo alilitupa wazo hilo mbali.Alichokifanya Ngesa ni kutembea kwenye chumba maalaum cha mitambo,ambapo huko nyenzo mbalimbali za mawasiliano hutumika!Mwanamme makini ndani ya chumba hiko,kazi yake ilikua ni kudukua mitandao ya simu.Hiyo ilikua siri kubwa ya kiusalama.
“Nahitaji simu ya Luteni,uangalie miezi miwili alizungumza na watu gani”
Hilo lilikua rahisi kwa Lucas Sizya!Mwanaume makini kwenye maswala ya IT namba ya simu ya Luteni ilivyoingizwa namba zote zikaonekana,kwenye namba mbili za mwisho zilimfanya Ngesa atulie kidogo ni mbunge wa viti maalum Sarah Koku Ishengoma na mfanyabiashara mkubwa na maarufu Isaya Msophe!Hakuelewa namba hizo zimefata nini na waliongea nini na Luteni,kengele ya hatari ikaanza kugonga kichwani kwake.
“Huyu Sarah Ishengoma,anaishi wapi?”
Ngesa akauliza kwa makini huku akimtizama Lucas Sizya.
“Mbezi beach,lakini sina uhakika”
“Fuatilia uniambie”
Hiyo ilikua amri,madaraka aliyopewa Ngesa yalitakiwa kutekelezwa hapohapo bila kuhoji!Ndani ya dakika mbili,Lucas Sizya akaja na data zote mpaka namba ya nyumba!
“Msakuzi,Mbezi mwisho!Karibu na nyumba ya balozi”
“Anaishi na nani?”
“Sijui lakini yupo na mumewe na familia yake nadhani”
“Poa”
Ngesa,alisema na muda huohuo!Akatembea mpaka nje ambapo alichukua bastola yake pamoja na ‘magazine’ mbili zilizojaa risasi za kutosha kwa safari ya kwenda Mbezi Beach.
***
Saa tatu ya usiku,Ngesa aliegesha gari aina ya Prado!Kando kando ya ukuta mrefu ambao juu aliona kamera za ulinzi.Hizo hazikumpa tabu sababu ziliangalia upande wa Magharibi.Hivyo alishuka kwa tahadhari,alivyotaka kuingia akitumia geti kubwa alisita sababu aliamini kungeibua maswali mengi kutoka kwa walinzi na pengine asingepewa ushirikiano.Alitaka kuingia ndani ya jumba hilo kwa siri kubwa na kumshtukiza Sarah Ishengoma mwanamke mwenye mashauzi akiwa bungeni.Alikua ni mama muongeaji na mropokaji,uzuri na umbo lake havikufanana kabisa na mdomo uliokua muda wote unataka kuropoka ungemtizama kwa juu juu ungedhani ni Mnyankole!Ngesa aliamini kivyovyote vile mwanamke huyo angekua anajua vitu vingi,hususani genge la Brigedia Karanje,ndiyo maana akamfungia safari akiamini kwa utaalam wake angeweza kupata taarifa anazotaka!
Ukuta wa mbele ulikua mrefu na nyumba ilizungukwa na miti ya kivuli kila pembe.Alichokifanya Ngesa ni kuanza kuizunguka nyumba hiyo,akiangalia upenyo wa kuingia bila kushtukiwa lakini alipata wazo baada ya kuzunguka upande wa nyuma,ukuta wa Mbunge Sarah Ishengoma ulipakana na ukuta mwingine!Ngesa akatizama huku na kule,akaitandaza mikono yake na miguu kisha kuanza kupanda juu kwa tahadhari,alivyofika juu kabisa akapata nafasi nzuri ya kutizama ndani,akaona walinzi wawili wenye mitutu wanaranda huku na kule.
Akawasubiri,mpaka walivyopita upande wa pili,kwa utaalam akaingia upande wa ndani,kashesehe ilikua kwenye kutua.Ngesa alikua mfupi ukuta ulikua mrefu,jasho likaanza kumtoka hofu ya kukutwa ikaanza kumtanda, akatamani apige kelele za kuomba msaada.
Urefu wa ukuta huo ulimfanya miguu yake ining’inie hewani.Wazo la kutua mpaka chini likamtoka na kujuta kwanini alipanda bila kujua ndani kupoje,alivyoangalia kando akaona mti na kuanza kujiburuza akitumia mikono,mpaka alivyoufikia mti.Hapo,aliukumbatia na kushuka nao taratibu kama mkwezi wa nazi.Alivyotua chini,akachomoa bastola!Akatizama huku na kule,ambapo mbele yake aliona Landcrusier V8 ya Mbunge huyo na kando kulikua na magari matatu madogo,macho yake yakampeleka mpaka mlango wa uwani.Ambapo alitembea na kusikia sauti za watu.
“Caren,nenda kalale.Unafanya nini mpaka sasa hivi?Kesho shule”
Sauti hiyo ilitokea jikoni,haikua ya Mheshimiwa Sarah Ishengoma.Akanyata taratibu mpaka mlangoni na kumuona msichana mdogo,aliyesuka mtindo wa mabutu.Akaamini kua alikua dada wa kazi,alimlaani sana dada huyo kwa kitendo cha kufunga mlango na funguo.
Hata hivyo,hilo halikumshtua Ngesa,akakumbuka kwenye begi lake la mkanda mmoja lililokua begani mwake kuna funguo maalum za kutekenya vitasa!Alivyozishika vizuri akashika kitasa,alivyoingiza na kuchokonoa kitasa hakikuleta upinzani,taratibu akiwa na bastola mkononi alianza kunyata!Mbele yake aliona jiko kubwa la oveni,juu makabati yaliyopangiliwa vizuri.Akaurudishia mlango vizuri na kuingia nyuma ya mlango baada ya kuhisi kuna mtu anakuja.Akiwa nyuma ya mlango,alimuona msichana dada wa kazi aliyesuka mabutu,anaweka mboga kwenye friji kisha akazima taa!Hilo lilimfanya Ngesa afurahi sababu aliamini alienda kulala na zoezi lake lingefanyika kwa wepesi.Sasa akatokeza kwenye korido ndefu na pana yenye vyumba vitano,kulia vitatu kushoto viwili.Katika mazingira ya kawaida,alikua ana uhakika kama Chumba cha Mbunge Sarah Ishengoma hakikua miongoni mwa vyumba hivyo vitano,hiyo ni kutokana na ngazi zilizoenda juu gorofani.
Hakutaka kupoteza muda,akaanza kupanda moja baada ya nyingine!Ambapo sasa juu,alikumbana na mlango mkubwa!Alivyonyonga kitasa,ukagoma kufunguka akalazimika kutumia funguo zake za kazi hapo alifanikiwa na kuingia.Alivyozama alikumbana na seble kubwa,kwa kua kulikua na giza totoro.Akatoa kurunzi yake ndogo yenye mwanga mwembamba na kuanza kukagua ndani ya seble hiyo,ambapo ukutani kulikua na picha za viongozi mbalimbali.Televisheni kubwa nchi 75 ya Sony.Redio ya home thieta ya gharama na masofa ya bei mbaya,hapo alijua ni kwa namna gani Mbunge huyo anaishi maisha ya kifahari.Kando yake kulikua na kordo nyingine,hapo akapiga tochi na kuona choo na chumba kimoja kilichojitenga mwisho.Mapigo ya moyo ya Ngesa,yakakosa utulivu akajua tayari kazi imeanza!Akanyata taratibu,kadri alivyozidi kusogea karibu alisikia kelele za sauti.Mwanamme na mwanamke huku tivi ikiwa inawaka na alivyoufikia mlango,aligundua haukufungwa vizuri,kulikua na uwazi kidogo!Ilielekea walijiamini sana kutokana na kufunga kwa mlango mkubwa.
Hilo lilimfanya Ngesa achungulie kwa jicho moja,alichokiona kilimfanya apigwe na mduao.Mbunge Ishengoma alikua uchi wa myama yupo juu ya kiuno cha mwanamme,anazungusha kiuno kama sio yeye vile alikua katika dunia nyingine ya huba.Tukio hilo lilimfanya Ngesa ameze mate kwa kuangalia sinema ya bure ikampelekea aanze kubadilisha mapozi kwani alisisimka mno!Kuna kipindi alitamani aangalie pembeni lakini alijikuta ananogewa namna ambavyo Mbunge huyo,alivyokua mtundu kitandani.Miguno mbalimbali aliitoa katika tendo hilo,hawakuishia hapo!Wakabadilisha mikao mbalimbali ilimradi raha duniani na dakika tano baadaye,wakawa wamelaliana!Kwa Ngesa ndio ulikua wakati muafaka kwani hakupenda kuwakatisha.
“Hivi,ulifunga mlango Mama Caren?”
Sauti nene yenye madaraka,ilisikika kutokea ndani.Ngesa hakuweza kumuona mwanaume huyo anafananaje sababu alikua kwenye kona ya kitanda!
“Ah,wa nini Darling?Mimi nimechoka!Nilifunga mlango wa seblen tu kule”
“Sawa”
“Naenda kuoga”
Ngesa aliona kila kitu,mpaka Sarah anavyovuta kanga yake na kuelekea mlango wa bafuni.Hapo ndipo Ngesa akaingiza mguu mmoja ndani kwa tahadhari.Akamuona mwanaume mzee kiasi,amelala amegeukia ukutani na Sarah Ishengoma anaelekea bafuni huku nyuma akitingishika nusu ya mapaja yake yapo nje kwani alivaa kanga moja iliyoanzia kifuani.Ngesa,akamsogelea kwa kunyata akiwa na bastola yake mkononi!Akamuwekea kichwani kwenye kisogo.
“Ishengoma,tulia kama ulivyo”
Kwa sauti ya chini Ngesa alisema na kumfanya mume wa Sara Ishengoma kushtuka,tukio la kuvamiwa lilimshangaza!Akachomoa bastola chini ya mto kabla ya kufanya lolote,Ngesa akamuwahi na kumuelekezea bastola usawa wa kichwani.
“Tupa bastola chini,sihitaji kuua mtu leo mzee”
Ngesa akasema kwa sauti iliyomaanisha na kumfanya Mzee huyo azidi kutetemeka!
“Nina ela kwenye droo,usimuue mke wangu nakusihi”
“Sina shida na ela”
Wakati Ngesa anazungumza,ilimfanya Sarah Ishengoma apate mwanya wa kugeuka!
“Derrick Ngesa!”
Akaita kwa mshangao!Mduawo aliopigwa ulimfanya aishiwe nguvu,hakuelewa Ngesa ameingia vipi kwenye ngome hiyo inayolindwa,jasho jembamba likaanza kumtoka sababu alimuelewa Ngesa.
“Kaa kwenye kiti,kuna kitu nahitaji kutoka kwako.Ushirikiano wako,ndiyo utakufanya uendelee kuwa hai Sarah Ishengoma”
Ngesa akasema na kumfanya mwanamke huyo mbunge, atembee mpaka kwenye sofa na kukaa!
“Umeingiaje ndani kwangu?”
Sarah akauliza,wasiwasi wake ulikua kwa walinzi wake alikua ana uhakika mkubwa waliuwawa lakini alivyovuta pazia,akawaona wana randa randa bila wasiwasi.Akahisi kuwachukia na kuapia kuwafukuza kazi sababu hakuona wanacholinda.
“Hilo,sio lililonileta hapa”
“Nini kimekuleta Derick?Uliniona nikiwa nafanya mapenzi?”Sarah akauliza, akiona aibu.
“Unamfahamu vipi Luteni Sagasa?”
Lilikua ni swali la kwanza kutoka kwa Ngesa,akiwa katika uso wa mbuzi.Ilikua ni wazi kabisa,hakutaka kupotezewa muda wake!
“Luteni Sagasa?!”
“Ishengoma,hua mara nyingi sipendi kuuliza kitu mara mbili, kwa macho yako nilivyoyaona nadhani unajua nini kimenileta hapa”
“Luteni Sagasa ndio nani?”
Hapo Ngesa akasogea karibu kabisa akiwa na bastola mkononi mwake,akamgusisha nayo kichwani.Ni tukio lililomfanya mwanamke huyo atetemeke kwa hofu,historia ya Ngesa aliifahamu vizuri sana na si ajabu angepigwa risasi na kufa hapohapo.Kupitia kioo cha kabati Ngesa akagundua kitu,hiyo ni baada ya kumuona Mme wa Sarah Ishengoma,anapapasa bastola yake!Hapohapo akamgeukia.
“Mzee,nitakuua.Tupa bastola chini”
Ili Ngesa kurahisisha zoezi lake,akamchukua mzee huyo na kumshusha kitandani akiwa uchi wa mnyama,akamburuza mpaka bafuni.Huko alimfunga kamba na kumuweka chini ya sinki kisha kurudi kwa Sarah.
“Nataka kujua mahusiano yako na Luteni Sagasa”
Ngesa akauliza kwa mara nyingine,badala ya mwanamke huyo kujibu akacheka kwa nyodo huku akirembua macho yake na kulamba lips!Kwa Ngesa alishaelewa nini maana yake.
“Derick,nitakupa kitu chochote unachotaka”
Sarah akazungumza huku akijilegeza!
“Sio kwa sasa hivi”
Muda waliopoteza ulikua tayari umeisha,alichokifanya mwanamme huyu Ngesa ni kuzishika nywele zake akamuinua nazo,akamburuza mpaka bafuni kelele alizopiga Sarah hazikumsaidia.Ndani ya bafu hilo kulikua na choo cha kukaa,akamsukuma na kumshika kichwa chake na kukitumbukiza ndani ya sinki hilo!Akafanya hivyo kwa takribani sekunde hamsini na kumtoa.
“Nataka kujua”
Kitendo cha Sarah kutolewa,kilimfanya aheme kwa pupa.Baadhi ya maji ya chooni yalimuingia mdomoni na puani,akamtumbukiza tena na kumtoa.Zoezi hilo halikukoma mpaka Sarah akaanza kuzungumza kila kitu anachoelewa yeye kuhusu uhusiano wake na Luteni Sagasa!
“Ni bwana angu”
Sarah Ishengoma akaropoka ni tukio lililomfanya mzee aliyekaa chini ambaye ni mumewe,apigwe na mshtuko!Kusikia mkewe anachepuka,lakini hata hivyo Ngesa alikubuhu kwenye masuala hayo ya kuhoji watu,akagundua kwamba jibu la Sarah Ishengoma halikua la kweli hata kidogo,akamtizama machoni na kumtandika kibao kikavu, kilichomyumbisha mpaka akajigonga ukutani.Akamvuta na kumtumbukiza tena kwenye maji ya sinki.Humo alimkandamiza kwa dakika moja nzima na kumfanya mwanamke huyo akukuruke kama kuku kwa kukosa pumzi.
“Nase…ma Na…see..ma Ngesa”
Hatimaye,akazungumza kila kitu kuhusu pesa alizoingiziwa kwenye akaunti yake!Ili amlaghai Waziri wa mambo ya ndani,akamueleza Ngesa jinsi alivyolala na waziri huyo ili atoe ‘password’ ya kompyuta yake.Baada ya hapo,silaha zikachukuliwa na jeshi la Brigedia Karanje.Na siku hiyo usiku walikua na mpango wa kutoroka!Mbaya zaidi walishachonga hati bandia,taarifa hizo zilimsisimua sana Ngesa na hakua ana uhakika kama angeweza kuwawahi.
“Wanaondoka na ndege ya saa tano usiku, KLM”
Ngesa akaangalia saa yake ya mkononi na kuona kua zimebakia dakika hamsini na tano tu ndege iruke, alihisi kuvurugwa kwani alikua na usongo sana na Brigedia Karanje,na alitamani kumtia mikononi baba yake mzazi MZEE NGESA!
Maandalizi ya safari ya Brigedia Karanje akiwa na Mzee Ngesa yalipangwa kikamilifu,ilikua ni lazima siku hiyo waondoke na kuelekea nchini Urusi.Njama na mipango hiyo ilisukwa na watu makini mno.Hata ingekuaje ingekua ni vigumu kuwagundua,Brigedia Karanje alipachika ndevu za bandia zenye sharubu nyingi mdomoni huku kichwani akiwa na kofia ya duara!Miwani meusi machoni ilimfanya mpaka dereva aliyembeba atandwe na hofu lakini hakua na jinsi, ilikua ni lazima ampeleke abiria wake uwanja wa kimataifa wa ndege Mwalimu Nyerere kwa malipo ya shilingi laki moja,wakitokea Mtava!Dereva alishikwa na wasiwasi lakini kwa wakati mmoja,alikenua meno sababu pesa aliyopewa na kazi anayofanya vilikua ni vitu viwili tofauti,hata hivyo hakuacha kuangalia kioo cha katikati akimtizama abiria wake anavyohangaika kwenye siti.
Brigedia Karanje,hakutulia kwenye siti yake mara kadhaa aliangalia nje na mara mbili tatu aligeuka nyuma akihakikisha hakuna gari yoyote inayomfatilia.Dereva taxi kwa mwendo wa kawaida aliingia uwanja wa ndege na kupewa kadi maalum ya wageni,hapo aliendesha gari mpaka kwenye maegesho.Kwa heshima zote,akashuka na kumfungulia abiria wake mlango huku akimsaidia mabegi.
“Usijali kijana”
Brigedia Karanje,akasema akimzuia dereva huyo asimsaidie chochote!Baada ya hapo,akatoa kiasi cha laki moja na kumkabidhi.
“Ahsante,mzee wangu.Safari njema,ufike salama”
Dereva taxi alishukuru huku moyoni akifurahi sana kwani tangu aanze kazi hiyo hakuwahi kupewa pesa kubwa kwa mkupuo namna hiyo,kwa haraka akaanza kutafakari ni kiwanja gani kingekua na warembo siku hiyo ili ikiwezekana aondoke na watatu,akiamini pesa hiyo kwa mtaa anaoishi yeye ni bilionea!Hakupoteza muda,akaingia ndani ya taxi yake na kuondoka kwa haraka eneo hilo.Brigedia Karanje,alitembea kwa mwendo wa kawaida huku pasipoti yake ikiwa mkononi,amebeba begi moja mgongoni! Kubwa analiburuza mpaka alipofika sehemu maalum ya kusubiri ndege na abiria wenzake,hapo akachukua simu na kumtafuta Mzee Ngesa hewani.
“Ndio naingia getini hapa”
“Kama tulivyoongea”
“Sawa”
Brigedia Karanje na Mzee Ngesa,hawakutaka kuongozana kuhofia macho ya watu.Ndiyo maana kila mtu alitoka kivyake!Saa 4;30 usiku Brigedia Karanje alikua kwenye kidirisha kidogo ametoa pasipoti yake ili igongwe muhuri,mwanamke huyo mrembo mwenye sura ya kisomali akamtizama mara mbilimbili.
“Abdulaziz Mohamed”
Mwanamke huyo akaita na kumtizama Brigedia Karanje ni tukio lililomfanya Brigedia Karanje ageuke nyuma, akidhani wa pembeni yake ndiye anaitwa,ghafla akakumbuka hilo ndilo jina feki aliloandika kwenye pasipoti mpya aliyotengenezewa kimagumashi ili asafiri bila kugundulika.
“Naam,binti”
“Vua miwani tafadhali”
Brigedia Karanje,akavua miwani na kuambiwa pia avue na kofia kwani vitu hivyo haviruhusiwi,wasiwasi ulitawala moyoni mwake lakini alijitahidi kuificha hali hiyo kabisa.
“Safari njema”
Mwanamke huyo akatoa tabasamu na kugonga muhuri pasi ya Brigedia Karanje!Hiyo ilikua hatua moja kubwa sana kwa Brigedia Karanje, hata hivyo hakutaka kujipa uhakika asilimia zote mia moja,ndiyo maana aligeuka huku na kule kutizama kama kuna mtu anamtizama kwa mashaka,akagundua kila mtu yupo na hamsini zake!Huko hakukaa sana baada ya dakika kumi nyingine abiria wakaruhusiwa kuingia ndani ya ndege,hapo akamuona Mzee Ngesa pia.Bila kumsemesha akampita na kukaa nyuma ya siti inayofuata!Kutokusalimiwa na Mzee Ngesa kulimfanya aamini sura yake bado haijagundulika.
****
Ngesa alihisi kuishiwa nguvu kabisa,alitamani kuruka kwa kasi na kuchukua usafiri ambao ungemfikisha uwanja wa ndege ndani ya dakika hizo chache zilizobaki lakini hilo lisingeweza kutokea,muda ulikua mchache hapohapo bila kupoteza muda,akataka kupiga simu Ikulu ili amwambie Rais Leslie kila kitu kinachoendelea,alivyofikiria kitu kimoja tu.Kikamfanya asite,Rais Leslie ilijulikana ameuwawa tayari akiwa na ndege yake.Hilo likamfanya aanze kuisaka namba ya IGP Boniface Marwa,simu hiyo ilimkuta kituoni anashughulikia kesi nzito ya mwanamke aliyemuua mumewe kwa kumkatakata na mapanga.
“Unaongea na Derick Ngesa”
IGP Marwa,akatulia kidogo ili kusikiliza maelekezo,baada ya hapo akashusha pumzi ndefu.
“Mheshimiwa Rais,ndio anatakiwa kutoa amri hii.Hatuendi hivyo Ngesa”
“Ni jambo la kiusalama”
“Sawa,naelewa!Nachosema ni kwamba,nataka kupokea simu kutoka Ikulu”
“Kwani huna taarifa?”
Ngesa akahoji.
“Taarifa gani?”
“Za Rais Leslie,kifo chake”
“Derick,nimetoka kuongea na Rais Leslie jana!Najua kila kitu”
Kuna kitu Ngesa alianza kuhisi kichwani kwake,kupoteza kumbukumbu!Hapo ndipo akakumbuka taarifa za uhai wa Rais Leslie,askari wote wa ngazi za juu wanazo akiwepo IGP Marwa!Alivyokata simu,akapiga simu Ikulu ili kuomba msaada wa askari.
“Sawa,Ngesa nimekuelewa”
“Pia jambo moja Mheshimiwa Rais”
“Lipi?”
“Naomba Ishengoma awekwe chini ya ulinzi,asije kuharibu harakati zinazoendelea”
Tekelezo hilo lilifanyika ndani ya dakika tano,difenda tatu zikazingira nyumba ya Mbunge Ishengoma akawekwa chini ya ulinzi mkali.Kwa kua ilikua ni amri kutoka kwa Rais mwenyewe ilibidi Mbunge Ishengoma aanze kuhojiwa humo humo ndani ya nyumba yake.
“Nipatie funguo zako za gari na magazine mbili”
Ngesa aliomba vitu hivyo,vifanyike.Akapewa funguo za gari pamoja na ‘magazine’ zilizojaa risasi.Kitendo cha kupokea akaanza kushuka ngazi mbili mbili.Akatoka getini na kuona maaskari walivyokua makini,akaingia ndani ya gari na kulirudisha nyuma.Hakutaka kupoteza muda,akalitoa gari kwa kasi ya ajabu sana,mpaka maaskari wakashika vichwa.
“Atafika kweli yule?”
Askari mmoja akamuuliza mwenzake,lakini swali lake likaonekana kupuuzwa kwani kila mtu hapo alipo alimfahamu Ngesa kindakindaki.
***
Hakuna diffenda yoyote ile iliyoruhusiwa kuingia ndani ya geti kubwa la uwanja wa ndege wala askari yoyote yule kuingia ndani,hayo ndiyo maagizo aliyotoa Rais Leslie akipewa na Ngesa akimpa sababu kua hiyo ingemshtua Brigedia Karanje na kufanya kazi yao iwe ngumu.Hivyo walioruhusiwa kuingia ni watu wa usalama wa taifa na baadhi ya makachero waliovaa nguo za kiraia.Gari saba zilizoingia kwa muda tofauti zilipaki katika maegesho maalum.Usalama wa taifa walishuka na kila mtu akajigawa upande wake,hakuna abiria yoyote aliyeshtukia chochote hiyo iliwafanya wawe huru.Kuna baadhi ya usalama wa taifa walitumwa kabisa waingie ndani,wakajifanya wabeba mizigo.Lakini dakika kumi nzima hakukua na dalili ya Brigedia Karanje wala Mzee Ngesa kuonekana.
“Bado,hajaonekana?”
“Bado”
“Kule juu,John.Tupe ripoti”
“Hakuna kitu”
‘Headphone’ za masikioni walizovaa ziliwafanya wafanye mawasiliano lakini dakika zilikwenda na hakukua na dalili yoyote ile,hata hivyo mara kwa mara Ngesa alipiga simu akiwa njiani kuuuliza ripoti.Alihisi kuchoka,taarifa za kutokuonekana kwa Brigedia Karanje zilimuumiza mtima,wakati mwingine akaanza kuhisi wenda Sarah Ishengoma kamlisha matango pori.
“Ndege ya KLM,Ishatua?”
Ngesa akauliza simu.
“Muda mrefu sana na inataka kuondoka”
“Shiit,msiruhusu iondoke!Ikiwezekana ombeni list ya abiria wote waliokuwepo ndani ya ndege kuweni makini ana hati bandia ni vigumu kumtambua”
Ngesa alizungumza akiwa ndani ya gari aina ya Mark x,mkono mmoja umeshika simu mmoja kwenye usukani,pedeli za mafuta zimegusa chini kumaanisha kwamba gari linakimbia mithili ya roketi.
Angejilaumu sana kama asingemtia Brigedia karanje na Baba yake mzazi mikononi siku hiyo, hata hivyo angewakosa Mbunge Sarah Ishengoma angekua katika wakati mgumu mno,hiyo ilimfanya abane meno yake kwa hasira.Na badala ya kukunja kona kuingia ndani ya geti kubwa la uwanja wa ndege yeye akanyoosha moja kwa moja!Akitaka kupita denge,ni wazi kabisa alikua anataka kufanya jambo la hatari mno hilo hakujali alichotaka yeye ni kumtia Ngesa mikononi mwake,sio vinginevyo!Alivyohakikisha,amewasili na kuingia uwanja wa ndege mdogo,akatoa bastola yake na kuipachika kiunoni,akaanza kutembea mpaka kwenye ukuta mrefu ambapo huko alitizama huku na kule,na kuuparamia alivyochungulia upande wa pili,akaona miale ya tochi na taa za ndege kwa mbali,hata hivyo moyo wake ulikosa utulivu baada ya kusikia mbwa anabweka kwa sauti upande huo,anaoangalia.Alielewa vizuri baada ya dakika chache angeonekana kutokana na mbwa hao wa polisi walivyokua na mafunzo ya kuhisi harufu tofauti.
Kitendo cha kutua tu,mbwa wa polisi akazidi kubweka.Hapo akasikia parakacha za mtu,zinakuja upande alipo.Akajificha nyuma ya chuma kubwa lakini hilo,halikuweza kumsaidia kutokana na mbwa huyo mkali aliyekua anatoa ulimi nje.Taratibu akaanza kuishika bastola yake vizuri baada ya kuona kivuli cha mtu kimeshika mtutu wa bunduki,kinamfuata alipo ilielekea askari huyo alifuata maelekezo ya mbwa wake.
“Shiiiii,weka mtutu chini”
Ngesa kabla hajawahiwa yeye,akachomoka mafichoni huku akiwa na bastola mkononi.Mbwa alizidi kubweka baada ya kuona tukio hilo,isingekua jamaa huyo askari kuushika mnyororo wa mbwa wenda mbwa huyo,angemjeruhi Ngesa na kumdondosha chini kwani alishiba na alikua mnene mithili ya ndama.
“Naitwa Derrick Ngesa,afsa usalama”Derick Ngesa,akajaribu kutoa utambulisho mfupi ingawa aliweza kumjeruhi ama kumuua.
“Kitambulisho chako”
“Niamini nachokwambia,ningekua mtu mbaya sidhani kama ungekua hai mpaka sasa hivi”
Hilo lilikua kweli,kwani Ngesa alishika bastola na kidole chake kipo kwenye triga tayari kwa kufyatua risasi ni tukio lililomfanya jamaa huyo,taratibu aweke mtutu wa bunduki chini bila kupenda.Jasho jembamba likaanza kumtoka,hakua ana uhakika na maneno ya Ngesa wakati mwingine alitamani aachie mnyonyoro ili apoteze utulivu wa Ngesa kwani mbwa huyo,angemrukia na hapo ingekua rahisi kufanya shambulio la kushtukiza.Lakini baada ya kutafakari sana,akajionya kufanya hivyo!
“Mbona umepitia huku?Unataka nini?”
Jamaa huyo askari akauliza kwa hofu baada ya kufanya jitihada za kumtuliza mbwa wake.
“Ni mambo ya kiusalama endelea na ulinzi,unaitwa nani?”
“Boscow,Boscow Mutashobya”
“Upo kituo gani?”
“Gongo la Mboto”
“Mbele kuna askari wangapi?”
“Niko mimi peke yangu,mwenzangu ametoka kidogo”
“Kua makini”
Kupitia macho ya Boscow Mutashobya,Ngesa akaamini asingeweza kumdhuru hivyo alimpa mgongo na kuendelea na safari ya kusonga mbele huku moyoni akiwa mwenye wasiwasi mkubwa na kujilaumu kwanini alimuamini kwa kiasi kikubwa Boscow Mutashobya!
Lakini hata hivyo alipiga moyo konde,akiamini kwa wakati mwingine inatupasa kuwaamini binadamu lakini sio kwa asilimia zote.Mbele yake,akaona senyenge na kontena kando yake lenye urefu wa futi arobaini.Hilo halikumpa tabu yoyote ile,akaweka bastola kiunoni lakini alivyotaka kuparamia kwa juu,akahisi kitu kilichomfanya akose utulivu.Hofu ikaanza kumtanda,vinyweleo vikamsimama kwa umakini wa hali ya juu akashika bastola yake kisawasawa.
****
Badala ya ndege kuanza hekaheka za kuruka angani ilivyogonga saa tano,ilikua ndiyo kwanza wahudumu wanaranda huku na kule.Wakitembea na kunong’onezana.Jambo hilo lilimfanya Brigedia Karanje aliyekua katika muonekano wa babu mwenye mvi akose utulivu,akaanza kutizama huku na kule.Kupitia dirishani akawaona wanaume wawili wanaongozana na kupanda ngazi kwa kasi.Ni tukio lililomfanya apigwe na butwaa na taa nyekundu ikaanza kuwaka kichwani kwake.Isingekua rahisi hata kidogo kwa abiria yoyote kuruhusiwa kuingia kwani geti lilikua tayari limefungwa.Alichokifanya ni kuchukua simu yake ya mkononi,akaanza kuandika maneno fulani kisha akasimama.
‘USALAMA,KIMENUKA’
Ujumbe huo ulisomeka juu ya kioo cha simu ya Brigedia Karanje,akiwa ameipitisha kwa Mzee Ngesa siti ya nyuma.Kwanza mzee huyo alitaharuki,cha pili alipigwa na butwaa baada ya kumtizama babu huyo ambaye hakumjua ni nani.Lakini alivyotuliza akili vizuri, akagundua kua ni Brigedia Karanje hiyo ni baada ya kumuona mtindo anaotembea,kwa tahadhari nayeye akasimama kuelekea upande wa chooni.
“Sijaelewa”Mzee Ngesa,akahoji kwa sauti ya chini baada ya kumfikia Brigedia Karanje
“Kuna jambo halipo sawa,wamejua tupo humu”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Fungua pazia angalia”
Hapo Mzee Ngesa akapata nafasi ya kufungua pazia la katikati, kupitia korido akawaona wanaume wanne wamesimama wanaanza kukagua pasipoti za wasafiri.
“Unadhani,watatugundua?”
“Sina uhakika lakini kujihami ni muhimu”
“Sawa,tunafanyaje?”
“Nifuate”
Michezo ya kikomandoo na mafunzo ya kijasusi ilimfanya brigedia Karanje,aelewe jinsi ya kutoroka akiwa ndani ya ndege.Kwanza alianza kutafuta sehemu ya mizigo.Akatembea na kuchomoa kisu kidogo ambacho mara nyingi hupenda kukitumia,chini kulikua na kapeti zito jekundu.Akalinyanyua na kulichana.Akakumbana na kitu kama lichuma,lenye skruu!Kwa kutumia kisu hiko cha kijeshi.Akaanza kufungua moja baada ya nyingine.Zilivyoachia,akaliinua kwa juu na chini akaona mabegi na mizigo mingi.Akawa ana uhakika,akampisha mzee Ngesa apite kisha akafuatia kwa nyuma.Akalifunika chuma hilo la bati na kuanza kupanda juu ya mizigo.Sasa,kazi ya kutafuta matairi ya nyuma ya ndege ikaanza mara moja,wakiamini kwa kufanya hivyo ingekua rahisi kuchomoka bila kushtukiwa.
***
“Samahani dada,abiria mwenzako yuko wapi?”
Lilikua ni swali kutoka kwa Detective Maxmilian Bumarwa.Mwanaume mwembamba mrefu,kiunoni ana bastola yenye uchu.Usongo aliokua nao ulizidi kipimo chake,ndiyo maana alianza kumkagua abiria mmoja baada ya mwingine.Ingawa hakuelewa sura ya Brigedia Karanje inafananaje kwa wakati huo hata hivyo,aliamini kubobea katika kazi yake kungemfanya amgundue mapema zaidi,licha na hayo yote kilichomfanya awe ana haha ni kutokana na agizo hilo lililotoka moja kwa moja kwa Mheshimiwa Rais.Kukosekana kwa abiria wa pembeni katika kiti,alichokaa mwanamke mrembo aliyeonekana yupo bize na mambo yake,kulimfanya aibue hoja mpya na kujenga sura ya tofauti.
“Sijui,ameelekea wapi lakini nadhani ameenda chooni”
“Ameenda muda gani?”
“Dakika kumi zilizopita”
Kupitia kordo hiyo,hakuweza kuuona mlango wa chooni kwani ulizibwa na pazia.Hilo likamfanya aombe pazia lifunguliwe,akamuona mwanaume mmoja anatoka chooni.
“Ndio yule?”
Detective Maxmilian akahoji,mwanamke mrembo akageuza shingo nyuma na kutikisa kichwa kuashiria sio yeye.
“Inawezekana vipi?Anafafanaje huyo mtu?”
“Ni mzee mzee,amevaa kofia kubwa na miwani”
“Ni yupi kati ya hawa watu?”
Detective Maxmilian,akatoa picha kubwa iliyojaa abiria wote waliotakiwa kusafiri na ndege hiyo,kisha kumtizama mwanamke huyo mrembo!
“Ni huyu hapa”Mwanamke huyo akasema akiwa mwenye uhakika,nguo pamoja na mavazi aliyovaa abiria mwenzake yalikua yale yale.Na kwa haraka zaidi,picha hizo zilipigwa na CCTV camera zilizokua ndani ya uwanja huo wa ndege.Detective Maxmilian hakukaa sana alivyosogea kiti kinachofuata,akapewa taarifa iliyozidi kumsisimua kwani abiria mwingine pia hakuonekana,hapo ndipo umakini ukaongezeka zaidi.
Wakaingia vyoo vyote bila mafanikio yoyote yale,walivyoingia upande wa jikoni mkono wa kushoto wakaona zulia limechanwa,kwa udadisi wa haraka haraka wakaelewa nini kimeendelea.Taarifa zikatolewa,ndege ikazungukwa na afsa usalama kumi,wakihakikisha mtu yoyote yule atakayetoka ama kuingia wanamuona bila chenga!
****
Kitendo cha Mzee Ngesa,kutua kwenye kontena ndipo maafsa Usalama walifika,kwa maana hiyo.Angechelewa kwa sekunde moja nyuma.Angeonekana,baada ya kutokea kwenye tairi la nyuma ya ndege wakaamua kujigawa kila mtu akashika uelekeo wake.Brigedia Karanje akatokomea kwenye usawa wa matenki ya mafuta ya ndege huku Mzee Ngesa akishika upande wa Mashariki lilipokua kontena kubwa,hapo alipanda na kutua chini.Akiwa mwenye wasiwasi mkubwa.Hiyo ilimfanya Ngesa,aliyekua katika harakati za kuruka kontena hilo atulie kwani kishindo hiko kilimfanya ajihami.Akapisha utulivu kidogo na kuona kivuli cha mtu,akarudi nyuma na kumuona mzee mfupi kiasi.Amevaa kofia ya duara,anatembea kwa kunyata.Kwa muonekano huo akashindwa kumgundua.Alivyotaka kuchukua hamsini zake,aachane naye.Akajionya kufanya hivyo!Taratibu akaanza kumfuatilia nyuma,alivyomkaribia akainua bastola yake vizuri na kumuelekezea!
“Simama hapohapo,usigeuke nyuma”
Mzee Ngesa,kusikia hivyo alitabasamu kwani aliijua sauti hiyo niya mtoto wake wa kumzaa!Hilo likamfanya ageuke nyuma huku akitabasamu, mikono yake ikiwa hewani.
“Derick”Mzee Ngesa akaita huku akimuangalia mwanaye usoni.Ni tukio lililomfanya Derrick Ngesa ababaike kidogo lakini hakutaka kulionesha hilo waziwazi.
“Derick mwanangu,unataka kumuua baba ako?Najua huwezi,weka bastola chini”
Hisia za Ngesa,akiwa ameshika bastola zikamrudisha nyuma kwa kasi ya ajabu!Akakumbuka jinsi alivyoishi na baba ake,akipelekwa shule nzuri.Moyo wake ulimuuma mno kwani kazi aliyokua nayo,ilimfanya atake kumuua baba yake.Ghafla akaanza kuichukia kazi yake.Bila kujua akiwa katika mawazo hayo,Mzee Ngesa alikua taratibu anamsogelea kitaalam.
“Kumbuka nilivyokulea Dericik,leo hii umesahau?Hata Mama yako angekua hai,nadhani asingekubali.Huko alipo,anakuangalia Derick”
Mzee Ngesa,alizungumza huku akisogea taratibu kama chui anayemnyemelea njiwa amrukie!Ngesa alikua hapo kimwili lakini kiroho,hakuwepo kabisa. Aliwaza vitu vingi sana jinsi alivyoishi na baba yake mzazi!Lakini alivyokumbuka kifo cha Mama yake,jinsi baba yake alivyomchoma moto ndani ya nyumba,hasira ikampanda akainua bastola kwa lengo la kumpiga baba yake risasi.
“Paaaaaaaa”
Risasi ilichomoka ndani ya bastola,lakini shabaha haikuwa makini kwani mkono wa Ngesa ulipigwa panchi na mzee Ngesa,hapo hapo Ngesa akapigwa pigo moja la Judo na baba ake.Bastola ikadondoka chini,akiwa katika maumivu makali akapigwa kifuti cha mbavu.
Ngesa alionekana kupagawa,akayumba kidogo!Alivyoona ngumi inakuja akakinga mkono lakini hakuweza kupingana nayo kwani baada ya ngumi ya Mzee Ngesa kumfikia ilimfanya apepesuke kama mlevi,mzee Ngesa hakumchelewesha wala kujali kama mwanaye wa kumzaa,akamrukia teke kali lililomfikia Ngesa kifuani na kumtupa chali puu chini.Maumivu,aliyohisi Ngesa yalikua ya aina yake,sio mgongo,kichwa wala mkono!Akahisi kama amepigwa ganzi.
“Derrick,leo nitakuua kama nilivyomuua mama yako!Kinyango nilichokichonga,hakiwezi kunitisha hata siku moja”
Mzee Ngesa,alizungumza kwa dharau na nyodo akiwa na dhumuni la kumuua Ngesa,hiyo ilimfanya ageuke nyuma na kuitizama bastola kwa niya ya kuiokota na kummaliza Ngesa,hakua ana huruma hata kidogo moyo wake ulijisikia kumuua.Ngesa alikua chini,anaugulia maumivu.Hila za baba yake,alizishtukia sababu alimuona anatembea kuifuata bastola.Akamkamata baba yake mguu na kumvuta,mzee Ngesa alivyotaka kumpiga teke akawa amechelewa kwani Ngesa alijibiringisha kwa mtindo wa Ninja na kumchota baba yake mtama,uliomfanya adondoke chini.Hata hivyo mzee huyu alikua mwepesi kama karatasi,alivyotua chini.Akajibetua na kusimama wima.Akarusha ngumi lakini ilipita hewani,hapo Ngesa hakufanya makosa,akamtisha kama anarusha ngumi ya kushoto lakini alitupa ya kulia na kujizungusha teke aina ya ‘Round kick’,teke hilo ilielekea mzee huyo aliliona kwani alilikwepa hata hivyo aliweza kulikweka teke la kulia la kushoto,likamchapa vibaya sana kwenye kidevu.Na kumfanya mzee huyu abweke kama mbwa.Ngesa hakujali tena,aliamini akiendelea kumuendekeza baba yake,atakuja kufa ndiyo maana akapigana kwa hasira na mara nyingi alichanganya mapigo hatari ya kombati,akampiga baba yake ngumi kavu ya kohoni.Iliyomfanya mzee huyu,ashindwe kuhema vizuri.Ngesa akainama kidogo na kumtandika ngumi tatu za mbavu,zilizomfanya mzee huyo ayumbe.Alivyoinuka,akamkwida na kumpiga kichwa kimoja hodari cha pua kilichomfanya mzee Ngesa,amwage damu kama mchuzi.Ngesa hakuishia hapo,akamvuta kwa nguvu na kuukamata mkono wake,akauweka begani akauvunja kama mua,akakumbuka’Akuanzae mmalize’!Hapohapo,akajitupa chini kwa mtindo kwa Karate,akainuka na bastola na kumuoneshea baba yake aliyekua amekaa chini damu zinamvuja,puani na mdomoni.
“Paaaa!Paaaaa!Paaaaa!Paaaaaaa!”
Zilikua ni risasi nne!Mbili zilitoboa kifua cha Mzee Ngesa,mbili zilifumua kichwa chake ubongo ukawa umemwagika chini!Kifua cha Ngesa kilikua kinapanda juu na kushuka,hakuamini kama amemuua baba yake kwa risasi.Moyo ulimuuma kiasi kwamba machozi yakaanza kumlenga!
“I’m sorry Dad”(Samahani baba)
Ngesa,akasema maneno hayo,bado bastola ikiwa mkononi mwake inatoa moshi kwa mbali,akabana meno yake kwa hasira akiamini bado ana kazi nzito na ngumu mbele ya safari.
****
Yalikua ni maamuzi magumu aliyochukua.Hata yeye alishindwa kuamini baada ya kumuua baba yake,maiti yake ilikua chini ubongo umefumuka kwa risasi kifua kina matundu ya risasi.Macho yake yamemtoka,hilo lilimfanya Ngesa aendelee kuutizama mwili wa baba yake mzazi huku vitu vingi vikianza kumiminika kichwani kwake,malezi ya baba yake akimpeleka shule enzi za uhai wa mama yake vilijenga taswira kichwani chake na kumfanya ahisi huzuni sana,ghafla roho ya kujuta ikamuingia.Akaanza kujitathmin kwa kitendo cha mauaji aliyofanya kisa tu anaitumikia serikali ya Tanzania,ghafla akajikuta anaichukia nchi yake na kumchukia Rais Leslie na serikali yake kwa ujumla.Miguu yake ikakosa utulivu na kukosa nguvu kabisa,alijisikia vibaya na huzuni ulimjaa moyoni.
Machozi yakaanza kumlenga machoni akiamini kwamba baba yake hakustahili kufa kifo cha kinyama namna hiyo tena cha aibu na fedhea,kitu kilichomuuma zaidi yeye ndiye aliyemuua.Akashindwa kujizuia,chozi moja likaanza kutiririka mashavuni huku akiitizama maiti ya baba yake mzazi.
“Ngesa,usijali.Umefanya kitu kikubwa sana kwa ajili ya taifa lako”
Wakati akiwa katika dimbwi la mawazo hakuelewa kabisa kama maaskari wamemzunguka baada ya kusikia mirindimo ya risasi,hilo lilifanya hata wao wapigwe na butwaa na kumuangalia Ngesa ili wajue angefanya nini.Kufuatia hapo,Ngesa hakujibu kitu chochote kile zaidi ya kutupa bastola chini na kutembea mpaka ilipokua maiti ya baba yake,akachuchumaa na kuifumba macho.Hapo,hakuweza kuvumilia tena zaidi ya kulia kama mtoto mdogo.
“Baba,nisamehee sana”
“Najua,nime..kukosea….Nisamehe lakini kwanini umefa..nya hivi?”
Ngesa alilalamika na kuanza kulia kwa sauti kama mtoto mdogo aliyeachwa na mama yake huku akinung’unika na pia kumlaumu kwa kitendo cha kuihasi nchi yake bila sababu ya msingi.Askari,walikua pembeni wengine wanamuonea huruma sana Ngesa!
“Ngesa,simu yako”
Ngesa alikua chini,yupo na marehemu baba yake!Mwanaume mmoja mrefu aliyefahamika kwa jina la Mr.Mbuya,kutokea katika kitengo cha usalama wa taifa,alikua na simu mkononi!Akampa Ngesa.
“Ongea na Rais Leslie”
Ngesa,akaambiwa na kuweka simu sikioni.
“Ngesa….”
Rais Leslie,akaita upande wa pili wa simu.
“Naam,mheshimiwa Rais”
“Pole na kila kitu,najua ulichokifanya.Naelewa jinsi unavyojisikia sasa hivi,lakini amini nakwambia umefanya kitu kikubwa kwa ajili ya taifa lako wewe ni mzalendo.Vizazi na vizazi,vitakukumbuka….”
Wakati Rais Leslie anazungumza maneno hayo,yeye Ngesa alibubujikwa na machozi.Ukomandoo wote ulimwisha na mara kwa mara aliitizama maiti ya baba yake,iliyolala pembeni yake.Hiyo ilifanya mpaka adondoshe simu chini na kumuacha Rais Leslie kwenye laini.Alichokifanya Mr.Mbuya ni kuchukua na kuanza kuongea na Rais Leslie,baada ya hapo gari la wagonjwa lilifika na mwili wa Mzee Ngesa ukaanza kupigwa picha.
Hiyo ilimfanya Ngesa asimame baada ya mwili wa baba yake kubebwa na kupakiwa kwenye machela.Ni kweli alihisi maumivu makali moyoni lakini kwa upande mwingine,alijipongeza kwa hatua ngumu aliyoifanya.Hata hivyo kwa jambo alilolifanya hakutaka tena kuendelea kufanya kazi na serikali, ndiyo maana akasimama wima na kumtizama mmoja wa usalama wa taifa,bila kusema kitu chochote akampangua ili apate njia ya kupita katikati,ki ukweli akili yake ilishindwa kufanya kazi kwa wakati huo.
“Ngesaa….Ngesa…..”
Ingawa alisikia sauti nyuma yake inamuita lakini hakugeuka nyuma,alizidi kusonga mbele akipiga hatua za harakaharaka!
“Ngesa…”
“Mbuya,achana na maisha yangu”
Ngesa aligeuka na kuzungumza maneno hayo kwa ukali wa hali ya juu sana!Jambo hilo lilimfanya Mbuya akae kimya na kumuacha Ngesa akitokomea mbele kwenye giza,akamshuhudia anaruka ukuta mfupi na kuingia kwenye moja ya gari na kulitoa kwa kasi ya ajabu.
Ngesa,hakutaka tena kufanya kazi na serikali alisusa kabisa na aliamini tangu afanye kazi serikalini matatizo nayeye yeye na matatizo zaidi na hilo hakunufaika na chochote kile.Fikra zake zilimtuma wenda angekua raia wa kawaida,kwa wakati huo angekua na familia yenye watoto.Aliumia zaidi mpaka umri aliokua nao hakua na mtoto hata wa kusingiziwa,ghafla aliichukia serikali kwani ilimpotezea muda wake mwingi sana.Akiwa ndani ya gari,alishika kioo cha katikati na kutizama ili kujua kama kuna mtu anamfatilia,alivyojiridhisha akapiga jicho kwenye kioo cha ubavuni.Alivyoona hali ni shwari,akashusha pumzi ndefu na kuzidi kusonga mbele.Aliamini angeingia mjini usiku ingekua rahisi kugundulika na kuonekana alichokifanya ni kukunja kushoto na kuelekea Kyembe Mbuzi,ambapo huko alivuka reli na kupunguza mwendo, baada ya kuona bango kubwa lililoandikwa Elarldo Hotel,akaliingiza gari ndani na kuliweka kando.Hapo,alijisachi mfukoni na kuona amebakiwa na shilingi laki mbili,aliamini kwa kiasi hicho cha pesa angeweza kulala na kula chakula cha usiku.Alichokifanya ni kushuka na kutembea mpaka mapokezi.
“Vyumba vipo?”
Ngesa,akamuuliza mwanamke wa mapokezi ambaye alionekana kuduwaa, kumuangalia Ngesa kuanzia juu mpaka chini jinsi alivyo mchafu.
“Aaaah,ngoja kwanza”
Mwanamke huyo,akaingia kwenye kompyuta na kuanza kubonyeza ‘keyboard’.
“Yes,kimebaki chumba kimoja tu cha elfu sabini”
“Ahsante,naomba”
Ngesa akaingiza mkono mfukoni na kuhesabu kiasi cha pesa,kisha kumkabidhi mwanamke huyo!
“Naweza kupata nguo nyingine mpya?”
“Ndio,mashati yapo”
“Nitafutie mawili na jeans moja”
Ngesa akaacha maagizo huku akipewa daftari aandike majina yake!Hata hivyo hakutaka kuandika majina yake kamili kuhofia kushtukiwa kirahisi.
“Pandisha juu,gorofa ya tatu”
“Ahsante”
Ngesa alishukuru sababu mpaka wakati huo,aliamini hakukua na mtu yoyote anayemfuatilia.Alivyoingia ndani ya lifti akashusha pumzi ndefu.Ilivyofunguka,akaanza kazi ya kuangalia milango mpaka chumba namba 312,akaweka kadi kwenye mlango na kusukuma mlango ndani.Ilikua ni hoteli nzuri yenye hadhi ya kutoa ‘stress’ ya maisha ya mtanzania.Kitanda kikubwa cha sita kwa sita,sofa kubwa na pembeni kulikua na friji dogo,juu ya meza kuna simu ya mezani.Hiyo ilimfanya asogee na kubonyeza namba zilizokua mezani,ambazo ziliandikwa jikoni.
“Niletee kuku wa kuchoma na ugali,weka pili pili nyingi,niletee na Grant kubwa!Na maji ya baridi”
Alivyomaliza akaweka mkonga chini na kuvua nguo zote akanyoosha mpaka bafuni huko alipata wasaa mzuri wa kuoga na kunyoa ndevu zake zilizoota hovyohovyo.Alivyomaliza,akavaa taulo na kurudi mpaka kitandani,akajitupa na kuwasha televisheni.Habari aliyoiona kwenye televisheni,ilimsisimua sana!Aliona maiti ya baba yake pamoja na askari waliokua uwanja wa ndege.
“Sk tivii tupo live hapa uwanja wa ndege,ulipotokea ugaidi lakini jeshi la Tanzania linaendelea kutuliza amani.Kama mnavyoona hili ni eneo ambalo lilitokea shambulio la ghafla na kupelekea jambazi mmoja kuuwawa”
Mtangazaji maarufu wa tivii kutokea katika stesheni ya Sk tv Caroline Ambrose, alikua makini na kipaza sauti ana ripoti habari hiyo,kitu kilichomfanya Ngesa awe makini kufatilia kila hatua.Kilichomtoa katika dimbwi la ubize ni mlango wake ulivyogongwa.
“Naniiii?”
“Room service”
Ngesa akaweka taulo lake vizuri kiunoni na kutembea mpaka mlangoni,ambapo alipokea trei la chakula na kuliweka mezani kwake.
“Kaka samahani,uliagiza mashati mangapi?”
“Mawili”
“Large?”
“Lolote,litakalo nifaa”
Mlango ulivyofungwa ndani ya dakika moja Ngesa akapewa mashati mapya na jeans,hakutaka kujaribisha alichokifanya ni kulipa kwanza na kukisogelea chakula.Hakutaka kuremba,akala kwa kasi.Akashushia na maji na kumimina pombe kali kwenye glasi huku akitafakari vitu vingi sana,vinavyoendelea katika maisha yake.
***
‘Nimemfatilia,ameingia Erlado Hotel’
‘Una uhakika?’
‘Ndio’
‘Fanya kama nilivyowaambia’
‘Hakuna shaka’
‘Kitu kingine,kuweni makini ni mtu hatari na mwenye mafunzo ya kijasusi’
‘Hatuwezi kufanya kosa hata kidogo’
‘Tukutane Block 41’
‘Shega’Meseji hiyo,ilisomeka juu ya kioo cha simu!
Ndani ya gari aina ya Vigo nje ya hoteli ya Erlado aliyoingia Ngesa lisaa limoja lililopita walikaa wanaume watano,waliojazia miili yao mithili ya wacheza mieleka.Kila mtu alishika bastola yenye kiwambo cha kuzuia kelele.Zoezi hilo,lilikua ni lazima likamilike muda huohuo.Kwani tangu uwanja wa Ndege walikua wakimfatilia Ngesa kwa umakini sana,walielewa ni jinsi gani alivyokua mtu hatari na mwenye machale hivyo,fatilia yao ilihitaji umakini wa hali ya juu.Na jinsi walivyofanya ilikua ni vigumu kwa Ngesa kuwagundua,hilo waliamini asilimia mia.
“Nyoka…”
Jamaa mmoja akamuita mwenzake na kugeuka nyuma.
“Yes”
“Zunguka nyuma ya hoteli,Wamboo…Pita upande wa kule.Dusco na mwenzako kaeni humu ndani ya gari.Hakikisha Ngesa hatoki humu”
“Atatokea wapi unadhani?Yaani atakamatwa kama kuku bandani”
Dusco,akazungumza kwa majigambo huku akikoki bastola yake na kutabasamu!Shati jeupe alilovaa Damson na kuchomekea vilimfanya aonekane ni mteja na anahitaji chumba,bastola ikiwa ndani ya begi alilobeba kama gelesha lilimfanya muhudumu wa mapokezi,ampokee kwa tabasamu la biashara.
“Vyumba hamna kaka,vimeisha”
“Kwahiyo siwezi kupata chumba?”
“Ndio,pole kwa usumbufu”
Baada ya jibu hilo mwanamke huyo akaendelea kuangalia kompyuta yake.Alivyoinua uso wake juu,akahisi mkojo unataka kumpenya kwani alikutana na mlango wa bastola yenye uchu inamtizama,mapigo yake ya moyo yakakosa utulivu.
“Ngesa ameingia chumba gani?”
Swali hilo lilimfanya dada huyo,apagawe na kubabaika!
“Nge Ngesa Ngesa yupi kaka angu?”
“Nipe daftari la wageni”
Kwa uwoga mwanamke huyo akatoa daftari hilo na kumfanya jambazi aliyeshika bastola aanze kupekua kwa fujo,akiangalia majina na jina la mwisho lilisoma BENSON MAFUWE.
“Huyu ni nani?”
“Si..jui kaka angu”
“Tizama hii picha,ndio huyu?”
Jamaa huyo,aliyeonekana hatari kwa uhai wa binadamu, aliitoa picha ya Ngesa na kumuonesha mwanamke wa mapokezi.
“Angalia haraka kenge wewe,sijaja kucheza mdako hapa”
Jamaa huyo akafoka na kumfanya mwanamke wa mapokezi awe makini kuangalia picha ya Ngesa,hapo akatingisha kichwa kuashiria kua ndiye mwenyewe huyo BENSON MAFUWE!
“Yupo chumba namba ngapi?”
Hisia za kwamba muda unakwenda na sio ajabu,angekutwa eneo hilo ulimfanya Damson amvute mwanamke huyo na kumsogeza karibu.
“Ukileta ujinga nitakuua,usinipotezee muda”
Hatua za mtu kutokea,zilimfanya Damson achukue tahadhari.Alivyomuona mhudumu mwingine anatokeza kwenye ngazi,akampa ishara ya kumtaarifu asipige kelele,lakini mwanaume huyo alikahidi na kutaka kukimbia.Hata hivyo hakufika mbali,risasi mbili za mgongo zilizotokea upande wa pili tumboni,zilimrusha na kumtuliza chini akabaki anahema na kukoroma.
“Pyuu pyuuu”
Risasi nyingine mbili zisizokua na sauti,zikamnyamazisha na kumfanya atulie hapohapo sakafuni.
“Nipeleke,alipo huyu mzee”
Mbele mwanamke wa mapokezi nyuma jambazi hatari,akiwa na bastola.Wakaingia ndani ya lifti na ilivyofunguka,wakaanza kutembea kwenye korido mpaka chumba namba 312,hapo walisimama kwa muda na mwanamke wa mapokezi akawekewa bastola kichwani na kupewa ishara agonge mlango.
“Ngo ngo ngo…”
“Ngo ngo ngooo…”
Usingizi ulimpitia Ngesa,televisheni ikiwa inawaka.Uchovu ukichanganya na ulevi vilimfanya apitiwe na usingizi mzito wa ajabu.Hata chumba kilivyogongwa haikua rahisi kusikia,alikua mbali kwenye ndoto iliyomfanya asitamani kushtuka hata kidogo.Hata hivyo fujo za mlango kugonga zilimfanya,apekeche macho na kujigeuza upande wa pili.Kero ya mlango,ikamfanya afumbue macho!
“Naniiii?”
Ngesa akauliza kwa sauti ya kukwaruza iliyojaa uchovu na usingizi.
“Room service,samahani kwa usumbufu baba angu”
“Una shida gani?”
“Tunahitaji vyombo”
“Kesho,nimechoka.Siwezi kufungua mlango sasa hivi”
“Ni taratibu za hoteli hii”
“Kesho, kua na heshima na wateja…”
Ngesa alivyojibu hivyo,ukimya kidogo ukatawala!
“Ngo ngo ngoo”
Mlango ukaendelea kugongwa.
“Wee mwanamke,unataka nini usiku huu?Huna mume?”
Ngesa alionekana kukerwa kwa kukatishwa usingizi wake ulioambatana na ndoto nzuri za kupendeza,jambo hilo likamfanya ajibu shombo!Mara ghafla,akaanza kuhisi kitu kisichokua cha kawaida, hatua za viatu kwa mbali,damu yake ikamwenda mbio kwa kasi ya ajabu akatoka kitandani na kuvaa bukta,hapo alitembea mpaka dirishani na kutizama chini.Moyo wake ukapiga paa na kuhisi amepigwa na ubaridi, baada ya kuona gari aina ya Vigo nje ya ukuta wa hoteli,alivyoangalia vizuri akawaona wanaume wawili wanatembea huku na kule akajua tayari kumekucha!Alichokifanya ni kutembea mpaka kwenye meza,akachukua chupa ya Grants,akaishika vizuri mkononi.
“Nakuja”
Akatoa sauti ya juu,alielewa vizuri sana kama kungekua na hatari basi jambazi huyo alimtumia mwanamke wa mapokezi kama chambo,ghafla akaanza kuunga sentensi za mwanamke wa mapokezi.
Tangu aanze kulala hotelini,haikuwahi kutokea akalala usiku na kusumbuliwa kisa vyombo kutolewa.Akagundua kabisa,mwanamke huyo yupo chini ya ulinzi lakini alichokosea jambazi huyo ni kutompanga na kumpa maneno ya kuzungumza!Ngesa,alitembea taratibu mpaka kwenye mlango!Akashika kitasa vizuri na ufunguo,akazungusha ufunguo kwa taratibu mno!Kutokana na sauti ya televisheni alielewa isingekua rahisi mtu wa nje kusikia.Alivyohakikisha mlango umetolewa loki.Kwa kasi ya umeme,akafungua mlango na kumpiga kikumbo kikali mwanamke wa mapokezi,lilikua ni tukio la kushtukiza.Na kumfanya jambazi huyo,apoteze umakini hilo likawa kosa kubwa kwani alipigwa na chupa ya grants kichwani,Ngesa akarusha teke lililomfanya apepesuke kama mlevi aliyelewa togwa,bastola ikadondoka chini.Akamfuata alipo na kumshika shati,kichwa kizito cha pua kilimfikia na kumpasua vibaya sana damu zikaanza kumtoka,hilo halikutosha,Ngesa akamuongeza ngumi nyingine mbili za mbavu na kumfanya jambazi huyo,akae chini bila kupenda.
“Kwanini,mnanifatilia fatilia?Nani kakutuma?”
Ngesa,akahoji kwa ukali huku akimkaba jamaa huyo shingo,ambapo alianza kutoa macho baada ya kukosa hewa!
“Usala..ma wa tai..fa”
“Nani?”
“Ramadhan Nurdin Mp..elembe”
Roba ya Ngesa,ikamfanya ataje kila kitu bila kupenda.
***
Ngesa alikasirishwa kwa kiasi cha kutosha,hakuelewa kwanini anafatiliwa namna hiyo wakati tayari alikua amejitoa serikalini baada ya kumuua baba yake mzazi,alielewa serikali ya Tanzania ndiyo ilikua chanzo cha kila kitu kutokea!Kitendo cha kusikia kwamba Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Nurdin Mpelembe ndio kawatuma kiliamsha hisia nyingine na chuki ndani yake,alivyomkumbuka mpenzi wake Jaqlin Mfinanga,akazidi kupandisha Mori.
“Anataka nini?”
Ngesa akauliza swali,bado mikono yake ilikua kooni mwa mwanaume huyo.
“Ame..sema tukuue”
“Unaitwa nani?”
“Wam..boloo”
Kichwa cha pua kimoja,kilimpasua vibaya sana Wambolo na kumfanya avuje damu nyingi mno.Ngesa akamshindilia na kifuti cha mbavu na kumuacha chini ametulia,hakuelewa kama amekufa ama amezirai.Hilo halikua swala lake,kitu alichokiwaza yeye kwa wakati huo ni kujua alipo Jaqlin Mfinanga kwanza.Ndiyo maana alianza kutembea kwa tahadhari huku bastola ikiwa mkononi,aliamini kabisa majibu ya swali hilo angekua nayo Ramadhan Mpelembe kwani mara ya mwisho kuna sentensi alimwambia kuhusu Jaqlin Mfinanga!
Ukimya wa kordo,ulimfanya Ngesa atembee kwa tahadhari akielekea kwenye lifti.Ambapo kwa bahati nzuri,ilikua inapanda juu.Akaona aingie ili baadaye ashuke nayo.Lakini ilikua ni bahati mbaya sana kwake,mlango ulivyofunguka akakumbana na mwanaume aliyeshika bastola mkononi hata yeye ilionekana alipigwa na butwaa, baada ya kumuona Ngesa.Kabla hajafanya shambulizi lolote Ngesa akamuwahi kwa pigo moja la judo,akashika mkono ulioshika bastola na kumtandika kiwiko cha kifua kilichofanya bastola yake idondoke chini,jamaa huyo alivyojiweka sawa na kurusha ngumi,ikapita hewani hapo Ngesa alimvaa na bega na kumuweka kwenye kona kisha akabonyeza lift,ilivyojifunga tu.Kama kawaida ya Ngesa,akamtuliza na kichwa cha pua kilimchanganya na kumfanya jamaa huyo aone nyota.Akazunguka kwa nyuma na kumkaba kwa nguvu,alivyohisi jamaa huyo ameishiwa nguvu,akaivunja shingo yake na kumuachia adondoke chini kama gunia la viazi.Bahati nzuri kwa Ngesa mpaka lifti inafika juu na kushuka chini hakuna mtu yoyote aliyeingia kwa maana hiyo hakuna taharuki iliyotokea,lifti ilivyofunguka akashtuka baada ya kuona maiti ya muhudumu inavuja damu,akairuka na kutembea mpaka lango la kutokea.
Hapo alitembea mpaka nje kabisa,kwa tahadhari kubwa akajificha nyuma ya ukuta mkubwa na kuliangalia gari lililowaleta watu waliotumwa na Ramadhan Mpelembe,bado kulikua na dereva ndani ya gari hilo.Akiwa makini anatizama huku na kule,alichoshukuru katika hoteli hiyo hakukua na mtu wa aina yoyote yule, akiamini walikua tayari wamelala.Kuhusu mlinzi aliamini aliuwawa na mjambazi hayo!Kabla ya kupiga hatua moja,akamuona mwanaume mrefu anatembea kutokea nyuma ya hoteli,alivyodadisi akagundua ameshika bastola mkononi.Anachungulia madirishani.Ngesa alitamani kuondoka usiku huo huo kabla hakujapambazuka ili amuibukie Ramadhan Mpelembe lakini asingeweza kumuacha jamaa huyo hivyohivyo, akihofia wenda angekua kikwazo,hata hivyo alivyomuona anapanda ngazi za kupandisha kibarazani akamuacha aende zake,roho ya huruma ikamuingia.
Akachomoza mafichoni na kuanza kutembea kuifatisha lami,akaambaa na ukuta ambapo kulikua na giza totoro.Alivyoona kuko shwari,akavuka barabara upande wa ng’ambo na kuingia kwenye miti.Niya yake ilikua ni kufanya uvamizi wa kushtukiza kwa dereva.Alichokifanya ni kuinama chini kwa chini.Mpaka lilipo gari,akaibuka dirishani kwa dereva na kumuwekea bastola kichwani.Ni tukio lililomfanya dereva huyo abanwe na haja ndogo,sura ya Ngesa ilimtisha na wakati mwingine alidhani ni zimwi.
“Sitaki kukuua lakini nitakuua kama utaenda kinyume na jambo nalotaka”
Ngesa alizungumza kwa sauti iliyojaa unyama na uchu wa kuuwa,alikua yupo tayari kuua sababu kidole chake kilikua kwenye triga yaani kitendo cha kuvuta tu nyuma,ubongo wa jamaa huyo ungemwagika mithili ya nyanya iliyopasuliwa.
“Nakusikiliza mkuu”Jamaa huyo akasema,jasho jingi likimtoka mwilini!Alichokifanya Ngesa ni kufungua mlango wa nyuma akaingia ndani ya gari,bastola ikiwa mkononi.
“Hii bastola ina risasi kumi na nane,sitoshindwa kuzimalizia mwilini mwako.Nipeleke kwa Rama Mpelembe”
Dereva,hakubisha wala kuleta upinzani zaidi ya kuwasha gari na kulitoa eneo hilo kwa taratibu huku akipisha ukimya.Mapigo yake ya moyo yalipiga kwa nguvu yakataka kutokeza nje ya kifua.Japokua alikua na bastola kiunoni lakini alihisi mikono yake inatetemeka.Hakua na nguvu ya kuichukua,Ngesa alimuogopesha akamfananisha kama Israeli.Sasa akajua safari yake ya uhai inakaribia kufika ukingoni.
“Mimi ni..metumwa tu Ngesa”
Akajaribu kujitetea.
“Namtaka huyo aliyekutuma”
Safari iliendelea walivyofika kwenye makutano ya njia panda ya Kinyerezi wakapandisha kushoto,huko gari ilienda kwa kama kilomita kumi na kukunja kushoto!Barabara ya vumbi,nyumba ya kwanza kushoto wakaipita na kukata kulia ambapo kulikua na transfoma,moja kwa moja wakanyoosha.
“Amehamia lini huku?”Ngesa,akavunja ukimya!
“Ana wiki ya pili sasa”
“Ni mbali na hapa?”
“Hapana,baada ya hiyo nyumba.Ile pale yenye geti jekundu”
“Ana walinzi wangapi?”
“Mmoja,ana bunduki”
“Simamisha gari”
Ngesa,akamtizama jamaa huyo!Alipendezwa na ukarimu wake na upole lakini alisikitika sababu alihisi kumuua japokua roho yake ilikataa kufanya hivyo,hapohapo akiwa nyuma ya kiti akazungusha mikono yake na kuanza kumkaba kwa nguvu huku akiushika mshipa unaopitisha hewa kwa utaalam wa karate,akauminya na kufanya ashindwe kuhema dakika tatu baadaye akamuachia,baada ya kuhakikisha amezirai.Akamsachi na kumkuta akiwa na bastola pamoja na pesa,zote akazichukua na kuziweka mfukoni.Hapo,alishuka na kuanza kutembea kwa tahadhari huku akinyata na kutizama huku na kule!
Alivyohakikisha kuna usalama akatizama ukuta wa nyumba ya Ramadhan Mpelembe ili aangalie namna ya kuruka,ukuta ulikua mfupi hilo halikumpa shida sana akaweka bastola kiunoni akatizama mbele na nyuma kisha kuushika vizuri ukuta, akachungulia ndani na kumuona mlinzi amelala juu ya kiti,mtutu upo mikononi mwake!Akashuka taratibu na kutua kwa mtindo kwa paka,bila kutoa kishindo chochote kile.Shabaha yake ilikua kwa mlinzi kwanza,akamnyatia taratibu na kumuwekea bastola kichwani.
“Hey”
Ngesa akasema neno hilo,mlinzi akakurupuka mithili ya masai aliyenyang’anywa shuka lakini alitulizwa na kibao cha mdomo kilichomfanya arudi kwenye kiti bila kupenda.
“Tulia”
Mlinzi hakua nala kufanya zaidi ya kupigwa na bumbuazi la waziwazi,hakua nala kufanya zaidi ya kutii amri ambapo aliingizwa ndani ya chumba kidogo Ngesa akafunga mlango kwa nje .Kisha akachukua mtutu wa mlinzi na kuutupa kwenye majani.Sasa akawa tayari,ana uhakika wa kuingia ndani ya nyumba hiyo,mkononi akiwa na bastola akatembea mpaka uwani ambapo huko aliona mlango.
Alivyojaribu kuufungua akitumia utundu ukagoma,jambo hilo lilimfanya azunguke upande wa pili.Akaona dirisha lililokua wazi,kabla ya kufanya maamuzi mengine zaidi akaona chuma kilichofanana na tindo,akaokota na kurudi mlangoni!Ambapo kwa utaalam wa hali ya juu akajaribu kucheza na mlango huo ili ufunguke,akaokota chuma kingine kidogo na kuanza kuuchokonoa!Bahati nzuri ilikua kwake ukafunguka,taratibu akausukuma huku bastola yake ikiwa mkononi kaishikilia vizuri!Sasa akajikuta yupo upande wa jikoni,hakukua na kitu cha maana zaidi ya kunyoosha na kordo,akatokeza seblen!Ambapo huko kulikua na giza totoro kilichomshtua zaidi ni pangaboi la feni ambalo kwa mbali lilikua linazunguka kumaanisha kwamba feni lilizimwa kama sio dakika tano basi mbili zilizopita,uhakika wa kwamba alionekana tangu anaingia ulianza kumsumbua kichwani.Hilo lilimfanya azidi kuweka bastola yake vizuri mkononi na kuangalia upande wa vyumbani,akapiga hatua mbili kusogea.Alivyolivuka kabati tu,moyo wake ukapiga paa!Baada ya kuhisi kichuma cha baridi kimemgusa kisogoni.
“Tupa bastola chini Ngesa”
Ilikua ni sauti ya Ramadhan Mpelembe,imepenya ndani ya masikio ya Ngesa, hiyo ilimfanya Ngesa aweke bastola chini na kupandisha mikono yake yote miwili juu,kusalimu amri!
“Unataka nini nyumbani kwangu?”Ramadhan Mpelembe akahoji kitemi.
“Nimesikia unanitafuta,nimejileta mwenyewe”
“Nani anakutafuta?”
“Wewe hapo”
“Kwahiyo umekuja kufanya nini?”
“Nimejileta kuuliza,unataka nini kutoka kwangu”
Hila ya Ngesa ilikua ni kununua muda na kumpumbaza Ramadhan Nurdin,bila kujua.Kichwa cha Ngesa kilichaji mithili ya kompyuta isiyokua na mafaili.Taa ya nje,iliyofanya miale ipenye dirishani ilichora vivuli vyao,kazi ya Ngesa ilikua ni kuangalia chini na ukutani ili kutathmin umbali wa Ramadhan Mpelembe!Hata hivyo ilikua ngumu kwa namna Ramadhan Mpelembe alivyokaa ilikua ni ngumu kwa Ngesa kufanya anachotaka kukifanya ili ajikomboe,badala yake akazidi kununua muda.
“Nurdin,mmefikia wapi kuhusu Brigedia Karanje?”
“Hilo sio swala lako Ngesa,kwanza piga magoti”
Katika kosa alilofanya Ramadhan Mpelembe ni hilo,kumruhusu Ngesa apige magoti.Kitendo hiko kilimfanya Ngesa afanye mjongeo usio rasmi kwani alikanyaga pembe ya kabati na kujibetua kwa niya ya kumvaa Nurdin Mpelembe na mgongo,lakini hila yake ilikua kama imegundulika kwani Ramadhan alizunguka kitaalam na kumtandika Ngesa ngumi mbili za mbavu.Hata hivyo alitaka kufyatua risasi,akashindwa. Ngesa alimvaa na bega wote wakadondoka chini.Ramadhan alivyotaka kuiwahi bastola,Ngesa akamvuta na kumtandika ngumi ya shingo wakiwa hapohapo chini, wamelala.Ramadhani Nurdin alikua mwepesi na hodari kwenye mpambano,kwa utaalam akajibiringisha kwa mtindo wa ninja mpaka kwenye moja ya pembe ya ukuta hapo alijibetua na kusimama akawasha taa ili waonane.Hakukaa sawa akaona teke la Ngesa lina kuja upande wa kulia akainama kidogo na kumchota na bega juu juu na kumtupa juu ya meza ya kioo iliyomfanya Ngesa aipasue vibaya sana,vioo vingine vilimtoboa mgongoni na kumfanya ahisi maumivu makali mno.Ramadhan hakuishia hapo akatembea mpaka kando kando ya kabati na kuchomoa jamvia.Lilikua ni panga refu lenye makali kote kote.Jambo hilo lilimfanya Ngesa atetemeke kwa kiasi cha kutosha!Mapigo yake yalikosa utulivu sababu alielewa hatari anayoenda kukumbana nayo isitoshe katika mafunzo yake kupigana kwa mtindo wa mapanga alifeli yaani hakuweza kabisa,alivyojaribu kutizama huku na kule akitafuta kitu cha kujihami akaona Ramadhani Mpelembe kainua jamvia juu,kulishusha ilimaanisha kumbalalua Ngesa kati kwa kati.Ni tukio lililomfanya Ngesa ajitupe upande wa pili na kudondoka juu ya kochi,Ramadhan akamuendea kwenye kochi na kumshushia, Ngesa akabiringika kwa mtindo wa ninja mpaka chini ambapo alipiga teke meza kwa nguvu,ikamgonga Ramadhani mguuni,hapohapo akasimama na kumtandika ngumi tatu za haraka mbavuni.
Mategemeo yake ilikua wenda Ramadhani angeangusha panga chini lakini ilikua ni tofauti,Ramadhani alikua na panga mkononi bado,isingekua wepesi wa Ngesa kuinama chini wenda kichwa chake kingetenganishwa na kiwili wili.Ngesa alikoswa koswa na panga la shingo!Kwa kweli siku hiyo Ngesa alitamani kukimbia.Katika kitu ambacho alikosea ni kutaka kurusha teke bila kupiga hesabu,hilo lilikua kosa la jinai kwani panga lilimpitia tumboni na kuchana nguo yake,damu zikaanza kumvuja.Sasa hapo ndipo akaona ni kwa namna gani,hatari ipo mbeleni.Na akifanya mchezo atakufa kifo kibaya cha kukatwa na Jamvia,damu ziliendelea kumtiririka maeneo ya tumboni huku akihisi maumivu makali sana.
Hapo ndipo akaelewa Nurdin Mpelembe dhamira yake kubwa ilikua ni kumuua.Umakini ukawa mkubwa sana,kazi yake ikiwa ni kufanya jitihada kuukamata mkono wa Ramadhan Nurdin Mpelembe ulioshika jamvia,japokua ilikua ni kazi ngumu lakini alijitahidi.Jamvia lingine lilipita mgongoni kwake na kumchana,hapo ndipo alipata nafasi nzuri ya kuzunguka teke aina ya ‘round kick’ baada ya kukanyaga sofa na kubinuka sambasoti.Teke lilimfikia Ramadhan Mpelembe akapepesuka kidogo,hapohapo akadaka mkono uliokua na jamvia,hakumchelewesha alimgeuza na kumpiga vifuti vitatu vya tumboni,akamzungusha tena na kumtandika kichwa kikali cha pua,kwa utaalam wa pigo la ‘Karate’ alicheza na mbavu za Ramadhan Mpelembe mpaka alivyoleweshwa,akamvuta na kulichukua Jamvia.Hapohapo bila kuchelewesha akalichomeka tumboni mwa Ramadhan Mpelembe!Uhakika wa kutoka hai,haukuwepo tena sababu Jamvia lilitokea upande wa mgongoni.
“Jaqlin yuko wapi?”
Ngesa akauliza huku akizidi kulisokomeza panga tumboni kwa hasira.
“Kar..nje Briged..ia Kara..nje”
Ramadhan Mpelembe,alizungumza huku damu nyingi zikimtoka tumboni hakika alikua katika mateso makubwa na zilisalia sekunde chache aage dunia.Damu nyingi ziliendelea kumtoka huku akitetemeka na kukoroma kama kondoo,aliyechinjwa hiyo ilimfanya Ngesa abane meno yake kwa hasira huku akimtizama jinsi anavyokata roho.
“Nge..s…a um..”
Ramadhan Nurdin Mpelembe,hakuweza kumalizia sentensi yake hapohapo akaaga dunia.
****
“No,ni lazima afungwe.Umesahau kuna mauaji alifanya.Alivyoua maelfu ya watu.Tusiwe watu wa kusahau namna hii”
“Sawa,upo sahihi.Lakini kumbuka ameisaidia nchi sana”
“Haijalishi,swala ni ameua.Kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii.Lazima afunguliwe mashtaka, tena ya mauaji”
“Kwani hakuna njia nyingine?”
“Hakuna njia nyingine,afunguliwe mashtaka.We unadhani,wapinzani watatuchukuliaje?”
“Kama tukiwa na misimamo,hawawezi kufanya chochote kile alafu mambo mengine tusiangalie siasa”
“Usijaribu kucheza na nguvu ya uma,hata kidogo.Sheria lazima ifuate mkondo wake DAPHINE afungwe”
Kilikua ni kikao kidogo lakini kizito,kilichofanywa ndani ya Ikulu.Ndani ya chumba hiko kulikua na viti sita,katikati kuna meza kubwa!Siku hiyo waliongelea ajenda nyingi sana lakini kichwa cha habari na topiki kubwa ilikua kuhusu Daphine ambaye mpaka wakati huo bado alikua Ikulu.Anatoa maelezo yake,lakini hiyo haikumsaidia chochote badala yake wakaunda tume ili afungwe gerezani.Kikao hiko kiliendeshwa na wanausalama sita.Mbali na majadiliano ya hapa na pale lakini watu wawili walionekana kubishana,huyu alikua upande wa Daphine na yule alikua upande mwingine.Kabla ya kikao hiko kuisha,mlango ukagongwa akaingia mwanamke mrefu,mweusi aliyevalia fulana nyeusi na ‘jeans’.Akapita moja kwa moja mpaka kwa Mr.Kasera,mpelelezi na mtafiti katika kitengo hiko cha usalama.
“Nakusikiliza Penny”
Mr.Kasera akatega sikio!Penny,akamsogelea karibu na sikio la kulia.
“Nurdin Mpelembe,amekutwa nyumbani kwake!Ameuwawa”
“Whaaat?”(Niniii)
Shtuka hiyo ilifanya wanaume wote,wamtizame yeye, kupitia mshangao huo ilimaanisha hakukua na habari njema hata kidogo!
“Amekutwa ameuwawa nyumbani kwake Kinyerezi,usiku wa kuamkia leo”
Hapohapo Mr.Paul Kasera akavuta kiti nyuma na kusimama wima.Ni jambo lililomshtua kwa kiasi cha kutosha!Moyoni alisikitika sana kumpoteza mtu kama Nurdin Mpelembe,mwanaume mchapakazi.Hasira zake zilipanda kwa kiasi cha kutosha akitaka kujua ni nani aliyefanya mauaji hayo!
“Mheshimiwa Rais anajua?”
“Bado,hajui”
“Fanya utaratibu aambiwe,nani yupo eneo la tukio?”
“Polisi wanafanya uchunguzi,hatua za awali zimeshaanza”
“Ahsante Penny”
Mr.Paul Kasera,aliipokea habari hiyo kwa masikitiko makubwa mno!Akawatizama wanausalama ambao wote walikua wakimwangalia yeye.
“Nasikitika kuwaambia kua Mkurugenzi wa Usalama wa taifa Ramadhan Mpelembe,ameuwawa nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.Na watu wasiojulikana”
Lilikua ni pigo kubwa mno,hakuna mtu yoyote aliyekua tayari kupokea habari hizo za kushtua!Zilikua ni habari nzito zilizomgusa kila mtu ndani ya chumba hiko,hapohapo mikakati na mipango madhubuti ikaanza kupangwa lakini Mr.Paul Kasera aliapia atakula sahani moja na mtu yoyote aliyehusika na kifo cha Nurdin Mpelembe!Kifo cha Nurdin Mpelembe,mkuu wa idara ya usalama wa taifa kilikua ni pigo sana kwa wanausalama hususani kwa waliomfahamu,licha ya msiba huo mkubwa lakini haikuzuia kwa Daphine kupigwa pingu ili taratibu za kumfungulia kesi ianze.
“Nipo tayari,kufungwa usijali”
Daphine alizungumza kwa unyonge na upole huku akiweka mikono yake mbele,avalishwe pingu!Japokua moyo wake ulimuuma kwa kuingia gerezani bila ya kumuua Brigedia Karanje.
“Naomba mnihaidi kitu kimoja”Daphine akasema huku akimtizama askari huyo,aliyemvalisha pingu.
“Kitu gani?”
“Mumuue Karanje,vinginevyo nitakuja kumuua mwenyewe”
“Usijali,serikali inafanya kila namna kumtafuta.Kwa mambo aliyofanya ni lazima anyongwe”
“Ngesa yuko wapi?”
“Hatujui alipo”
“Kwanini?”
“Baada ya kumuua baba yake,akatokomea kusikojulikana”
Daphine,alimeza mate kwa masikitiko makubwa mno!Moyoni alielewa ni kwa jinsi gani Ngesa aliumia kwa kiasi cha kutosha hata hivyo,alianza kuhisi kwanini alitokomea. Hapo hakutaka kutia neno lolote lile zaidi ya kuongoza mbele akitoka nje,ambapo aliamini wakati wake wa kutumikia kifungo cha maisha ama kunyongwa kimewadia tayari.
Vitu vingi sana viliendelea kumiminika ndani ya ubongo wake,picha ya miili ya wazazi wake ikiwa imelala katikati ya mbuga ya mikumi zilitekenya hisia zake na kufanya aingiwe uchungu kwa kumuacha Birigedia Karanje hai kwani ndiye alikua mkandarasi wa vifo vya wazazi wake!Alisikitika mno lakini hakua na jinsi zaidi ya kuingia ndani ya gari la polisi bila kupenda.Ndani ya gari kulikua na askari mmoja mwenye bastola kiunoni.Hapo upande wa kulia akaingia askari mwingine mfupi,mwenye kitambi pia kushoto akafungua mlango askari mwingine.Wakamuweka katikati!
“Ushampigia Malisa?”
Askari mmoja,akamsemesha mwenzake!
“Ndio”
“Sawa,washa gari”
Nyuma kulikua na magari mengine matatu ya polisi huku mbele kukiwa na difenda ya polisi iliyobeba askari wenye mitutu mikononi ili kuimarisha ulinzi.
***
Pekua pekua ya Ngesa ilizaa matunda sababu alikutana na silaha za moto pamoja na mabomu aina ya ‘grenade’ hayo yalifanana na viazi mfiringo.Akaweka ndani ya begi na kuchukua kila kitu muhimu ndani ya nyumba ya Ramadhan Mpelembe ambaye sasa alikua marehemu tayari.Akili ya Ngesa ilikua tayari imevurugika kwa kiasi cha kutosha,hasira zilimpanda kwa kiwango cha mwisho hasa sura ya Brigedia Karanje ilivyompitia.Kifo cha baba yake kilimuhuzunisha na akaituhumu serikali moja kwa moja ndio chanzo cha kila kitu kutokea.Alivyomkumbuka Daphine akabana meno yake kwa hasira.Bado aliisumbua akili yake kujiuliza ni kwanini alimuacha Jaqlin Mfinanga peke yake huko Bagamoyo wakati alijua ni hatari kubwa sana.Ghafla chuki za waziwazi zikaanza kujijenga akiamini baada ya kumpata Daphine angepewa majibu yaliyoonyoka pengine angemtajia ni wapi Jaqlin Mfinanga kipenzi cha moyo wake alipo.Parakacha za mlinzi wa nje,aliyehisi ndani kuna kitu zilimshtua Ngesa na kumfanya akamate bastola yake sawasawa iliyokua na kiwambo cha kuzuia sauti,kupitia ndani alimuona mlinzi huyo akiwa na mtutu anakatiza dirishani.Akainua bastola yake juu!
“Pyuuuu”
Risasi moja ya shingo ilimtupa mbali mlinzi na kumlaza chali,hapohapo akakata kauli.Muda ulizidi kwenda na kumfanya Ngesa atoke nje kwa tahadhari kubwa huku akiwa na begi lenye mkanda mmoja begani.Hakukua na mtu yoyote anayekatiza hivyo,akatembea mpaka nje ambapo aliona gari moja limeegeshwa,akalisogelea kwa karibu zaidi.Kwa kutumia kitako cha bastola akafanikiwa kupasua kioo na kutoa loki.Kwa utundu wa hali ya juu,akaanza kubomoa swichi ambapo alikutana na nyaya mbili,akagusisha gari ikawaka.Hapohapo,wazo la kwenda Ikulu ili amtoe Daphine lilimjia,hata hivyo hakujua angetumia njia gani ili amkomboe!Kutokana na mwendo wa taratibu aliokua anautumia barabarani huku akitafakari ilifanya mtu yoyote asimuwekee mashaka,hata alivyopishana na maaskari walimpuuzia.
Haikumchukua muda mrefu,akawa tayari amefika nje ya Ikulu mita kama ishirini akawa amepaki gari,akachukua darubini na kuiweka machoni.Hakukua na kitu chochote zaidi ya walinzi kuranda huku na kule.Pamoja na yote,alikua makini sana kulitizama geti kubwa la Ikulu ilivyotimu saa kumi na moja ya asubuhi,akajivuta kwa chini kidogo baada ya kuona magari ya polisi yanaingia ndani ya Ikulu,hakutaka kupitwa akachukua darubini na kuiweka machoni.Alichokiona kilimfanya ashtuke kidogo,alikua ni Daphine amefungwa pingu mikononi anaingizwa ndani ya gari la polisi.Tukio hilo lilimfurahisha sababu aliona urahisi wa kazi hiyo mbeleni.Kandokando yake kulikua na lori kubwa lenye kontena,ambapo dereva wake alikua pembeni anaweka mizigo sawa.Akili yake ikafanya kazi kwa kasi ya ajabu,hapohapo akafungua mlango taratibu akaiweka bastola yake kiunoni na kuliweka begi lake lenye zana za kazi vizuri.Hatua chache tu,akawa amelifikia lori!Akaingia chini ya uvungu na kushika vyuma viwili vilivyoungana.Japokua kulikua na joto lakini aliamini baada ya muda mfupi angeingia ndani.Kumteka nyara dereva kungewashtua wapita njia pamoja na askari waliokua Ikulu lakini pia alijilaumu kwa kukurupuka sababu hata angeamua kulifuatilia lori hilo nyuma nyuma kwa gari,angefanikiwa pia.
“Suka,fanya haraka.Ngoma ishatia nanga.Breki ya kwanza Kurasini.Funga tela vizuri”
“Shega,saa ngapi tuna aamsha popo?”
“Kwani mzigo si upo tayari”
“Upo mwake”
Dereva akiwa na utingo wake,walikua katika mazungumzo na Ngesa alisikia mipango yao akiwa uvunguni mwa gari,hakuweza kuona sura zao zaidi ya miguu tu.Aliumia zaidi baada ya kuona magari yaliyokua ikulu yanatoka nje hususani gari la polisi lililombeba Daphine,akatamani kujiachia chini lakini alijionya kufanya hivyo,dakika moja baadaye akatamani kushuka ili atumie utemi lakini alivyoona askari pembeni akasita.
Dakika tatu baadaye,lori likapigwa moto na safari ikaanza ambapo hapo alijaribu kutumia mbinu mbadala kwani mwanga ulianza kuchomoza!Kuambaa ambaa na chuma za difu kulimfanya akoswe koswe kusuguliwa na gurudumu la gari hilo linalozunguka kwa kasi,hata hivyo alijiwahi na kujivuta kwa juu kidogo,sasa akawa ametokea kwenye kichwa cha lori hilo akiwa bado chini upande wa mlangoni.Kilikua ni kitendo cha dakika sifuri akajivuta kwa juu na kushika ‘site mirror’ ilikua kidogo adondoke nayo kwani ‘site mirror’ iling’oka na kudondoka chini.Dereva alipigwa na butwaa ni kitendo kilichotokea ghafla kabla ya kufanya chochote,Ngesa akawahi kabali ya mlango akauvuta ulivyofunguka akamshika dereva shati na kumtandika kichwa cha mdomo,bahati mbaya ilikua kwake kwa dereva kwani hakufunga mkanda ikawa rahisi kwa Ngesa kumvuta nje na kumtupa,sasa kazi ilikua kwa utingo bado alikua ameyatumbua macho yake anashangaa kinachotokea badala ya kutoa msaada.Ngesa akachomoa bastola huku mkono mmoja ukiwa juu ya usukani,ambapo Lori lilianza kuyumba akaliweka sawa barabarani.
“Potea”
Ilkua ni sentesni moja tu,kutoka kwa Ngesa akiwa na bastola mkononi.Utingo bila kupenda,akafungua mlango na kujitupa nje ili kuokoa uhai wake.Mahesabu ya Ngesa yakawa tayari yamekamilika bila kutarajia.Kwa mbali,aliona difenda za polisi zinakata kona kuelekea barabara ya ‘Morogoro Road’hapo Ngesa akashusha gia na kulikunja lori hilo lililokua na kontena kwa nyuma.
Alivyokaa sawa,akapandisha gia na kuchochea mafuta.Shabaha yake ilikua ni gari la katikati ambapo alikua Daphine,akili yake ikaingia kazini,akaingia upande wa kushoto na kuchochea zaidi spidi, sasa akawa sambamba na diffenda moja wapo,akasonga mbele zaidi.Alivyoangalia ‘site mirror’ ili apige hesabu zake,akajikuta anatoa tusi zito kwani haikuwepo, ilidondoka akiwa katika harakati za kuingia ndani ya roli hilo.Hiyo ilimlazimu atoe shingo nje kuangalia nyuma.Akaona tela la nyuma lipo mkabala na Diffenda ya polisi,mbele yake kidogo kuna gari la polisi alilokua Daphine.Bila kujifikiria mara mbili,akazungusha usukani na kufanya kontena la nyuma ligonge difenda mbili za polisi,hapohapo akaligonga gari alilokuwepo Daphine,kwa utaalam wa hali ya juu akakanyaga breki za ghafla na kufanya gari tatu ziiingie uvunguni mwa lori tena nyuma kwani zilikua ni breki za ghafla.Kwa kasi ya ajabu akashika bastola na kutoa bomu la kurusha ndani ya begi,akatoa kipini na kulitupa nyuma likatua juu ya diffenda.Haraka akatoka ndani ya gari.Ndani ya sekunde mbili,kulitokea mlipuko wa ajabu uliofanya askari wote wapigwe na butwaa kuangalia nyuma.Ngesa akapita mbele!
“Paa paaaa”
Askari wawili walitupwa hewani kwa risasi,Ngesa akainama chini ya gari na kuanza kutembea mithili ya mwanajeshi vitani.Mpaka kwenye gari,alilokua Daphine!Askari mmoja aliyekua anashangaa,hakumkawiza risasi moja ya kifua ilimtupa angani na kumfanya adondoke chini.Hapohapo,akaingia ndani ya gari na kumtoa Daphine.
“Ngesaa!”
Daphine,akaita kwa mshtuko!Tukio hilo la ukombozi lilimfurahisha sababu hakutegemea kitu kama hicho kutokea!Ngesa hakua na muda wa kuzungumza zaidi ya kujibu mashambulizi na kuingia kwenye moja ya gari la polisi,akamuingiza Daphine ndani.Akatoa bomu lingine la kurusha,akachomoa kipini na kuwarushia askari waliokua ndani ya gari wameshika bastola wanamlenga,haikuchukua sekunde tatu,ukatokea mlipuko mwingine na moto mkali.
Tukio hilo,lilimfanya Ngesa apige gia na kulitoa gari kwa kasi huku likipiga kelele kutokana na mkwaruzo wa lami na tairi.Ngesa,hakucheka wala kuzungumza chochote, uso wake ulijaa unyama na chuki za waziwazi na hakutaka kumwangalia Daphine usoni tofauti na siku nyingine,ki ukweli Ngesa siku hiyo alibadilika kabisa hilo lilimfanya Daphine aogope kuongea chochote,hata pingu alizokua nazo mkononi hakuomba zifunguliwe.
“Pole Ngesa,nilisikia kuhusu baba yako” Daphine,akavunja ukimya akijaribu kupima maji.
Ngesa hakujibu,alimtizama tu mara moja na kurudisha shingo mbele!Na mara kadhaa alikua makini kuangalia vioo vya ubavuni kama kuna usalama,alivyoridhika akakunja kona ya ‘Mandela Road’akawa tayari amefika Buguruni,bado hakuongea chochote walivyofika Tabata Mwananchi,ilibidi Daphine avunje tena ukimya na kuuliza.
“Tunaenda wapi?”
“Wewe ndio uniambie”
Ngesa,akajibu huku akibana meno!Alitokea kumchukia Daphine kupindukia na si ajabu angeenda kumuua huko mbele ya safari kama angeonesha kiburi,dharau na kejeli hilo lilikuwa wazi kutokea sababu hakua na kitu cha kupoteza duniani,akili ya Ngesa tayari ilivurugika na alijisikia kuua hadi mwenyewe alijishangaa.Na kila alivyojaribu kutaka kupaki gari pembeni ili amuhoji Daphine,msongamano wa watu ulimzuia hiyo ilimfanya baada ya kufika ‘Riverside’ apandishe barabara ya kwenda Ubungo Kibangu.Kwa mwendo wa kasi,akakunja kona nzimanzima na kuingia kwenye moja ya kichochoro,hapohapo ghafla akaweka mguu kati mpaka gari likapiga msele na kumfanya Daphine apigize kichwa chake kwenye dashbodi sababu kilikua ni kitendo cha ghafla mno!Ngesa akafungua mlango na kuzunguka upande wa pili,huko alifungua mlango aliokua Daphine akamteremsha kwa hasira.
“Shuka wewe Malaya”
“Nge…”
“Nyamaza nitakuua”
Ngesa alikua kama mbogo,akamshika Daphine akiwa amemkamata shingoni kwa nyuma,akamuweka ukutani na kumzaba kibao kilichompeleka chini mzimamzima!
“Kacha kacha”Akakoki bastola na kumuwekea kichwani.
“Jaqlin yuko wapi?Daphine nakuua leo hii sasa hivi,niambie Jaqlin alipo”
Macho ya Ngesa yalibadilika rangi,hasira zake hazikuweza kupimika kwa kitu chochote kile.Mikono yake ilimtetemeka.
“Niambie Jaqlin alipo, moja….”
“Sijui Ngesa”
“Niambie Jaqlin alipo mbili…..”
“Nilimuacha Bagamoyo”
“Kwanini ulimuacha?”
“Ilikua ni hatari kuja naye mjini”
Ngesa akasogeza bastola yake mpaka ikagusa kichwa cha Daphine.
“Twende ukanioneshe alipo,asipoonekana.Nitakuuua!Ingia kwenye gari”
Ilikua ni kauli ya kitemi na kumfanya Daphine azidi kutetemeka kwa hofu,alimjua Ngesa na alielewa angeenda kinyume chake angeuwawa kufikia hapo ilibidi awe mpole.Akaingia ndani ya gari safari ikaanza hapohapo,kutokana na hofu ya kukamatwa barabarani, iliwalazimu kubadilisha gari walivyofika Mwenge,walivyomuona muhindi mmoja amepaki ananunua magazeti,Ngesa akamvamia na kumtupa nje.Wakawa wamepata gari nyingine aina ya Pajero!Safari ikaanza kwa mara nyingine na hakuna hata mmoja kati yao,aliyemuongelesha mwenzake!
****
Jeshi la polisi lilikua katika msako mkali mno,barabara zote zilifungwa na haikua rahisi kumkamata Ngesa!Kila gari lilipekuliwa mpaka viti vya ndani,watu walitolewa nje na kuhojiwa maswali.Maeneo kama Ubungo,Mwenge pamoja na Mbagala viliwekwa katika msako wakihofia wenda Ngesa angetoka nje ya mji.
“Shukeni ndani ya gari,dereva weka gari kando”
ASP Kitogo,kamanda wa polisi kanda ya pwani siku hiyo nayeye alikuepo.Alishikwa na usongo kwani vijana wake kumi waliuwawa katika bomu lililotupwa na Ngesa,kwa maana hiyo alipanga kula naye sahani moja mpaka amtie mikononi.Alivyoona coaster,akaliweka kando na kuanza msako huku akiwa na picha ya Ngesa mkononi pamoja na Daphine.Mtindo wa kusachi,ulikua kero kwa abiria sababu mpaka mabegi yao yalipekuliwa.
“Mama fungua mkoba wako”
Askari mmoja akasema,haikueleweka kama wamechanganyikiwa ama Ngesa yupo ndani ya mkoba yaani pochi.
“Mkoba wangu?”
“Ndio
Polisi hawakua wastaarabu hata kidogo hiyo ilitokana na wao kupelekeshwa kama watoto wadogo.Katika kitu ambacho kilimchanganya Ngesa ni baada ya kufika Tegeta,msongamano wa magari ulimfanya apoteze utulivu na kutizama mbele kwa umakini zaidi.Umbali wa mita mia mbili,akaona Diffenda za polisi,moyo wake ukamdunda akamtizama Daphine.
“Kuna askari mbele”
Hapo Daphine,hakujibu chochote zaidi ya kuziangalia pingu zake.Hata angetoa ushauri jinsi ya kutoroka ingekua vigumu kutokana na mikono yake kufungwa pingu.Jambo hilo lilimfanya Ngesa afungue begi lake dogo,akachomoa vichuma viwili na kuchukua mikono ya Daphine,kwa utundu na utaalam akachomeka vichuma hivyo vyembamba kwenye pingili za pingu,akatekenya zikafyatuka sasa mikono ya Daphine ikawa huru.
“Hiyo haimaanishi kwamba upo huru,utafata kile nachotaka”Akatoa onyo!
Magari yaliendelea kusogea kwa mtindo wa kusachiwa na kupekuliwa hiyo ilimfanya Ngesa atizame huku na kule akiisumbua akili yake.Kwa kweli,isingekua rahisi kuwatoroka polisi hao waliokua wengi tena wenye mitutu begani.Magari matano mbele,yalibaki ili gari walilopanda likaguliwe.Upekuzi,haukuwa wa kitoto!Polisi walipekua gari moja baada ya jingine kwa uangalifu mkubwa sana,mpaka walipolifikia gari aina ya Pajero.
“Ko! Ko! Koo! Koo! Koo!”
Askari akagonga kioo cha gari ili kifunguliwe,alivyoona kimya akagonga tena.Cha ajabu kioo hakikushushwa chini,hiyo ilimfanya apeleke mkono wake taratibu kwenye mtutu ili ajihami kwani ukimya wa gari hilo,ulimuogopesha na kumfanya ahisi wenda Ngesa angekua ndani ya gari hilo.
***
Kuuwawa kwa askari kuliibua mtafaruku wa aina yake.Mji wa Dar es saalam uliwekwa katikati wakiamini Ngesa asingeweza kutoroka,safari hiyo waliongeza ulinzi.Haikuwahi kutokea mtu akasakwa namna hiyo katika historia ya jiji la Dar es salaam.Ngesa alisakwa kwa wudi na Uvumba ili awekwe chini ya ulinzi ahojiwe na kufungwa mara moja,mbaya zaidi baada ya upelelezi na uchunguzi wa kina wakagundua kwamba yeye ndiye aliyehusika na kifo cha Mkurugenzi wa usalama wa Taifa Ramadhan Nurdin Mpelembe.Usongo waliokua nao askari uliogopesha mpaka raia,jiji la Dar es salaam lilikua katika hekaheka,pekua-nikupekue hususani kwenye mipaka ya Dar es salaam.Hakuna gari lolote lililoruhusiwa kupita bila kukaguliwa.
“Mmempata ova?”
Redio upepo,ilisikika kutoka Kigamboni ikiuliza kila kitu kinachoendelea.
“Hapana”
“Hakikisha anapatikana,sawa?”
“Sawa mkuu”
Miongoni mwa askari waliokua na usongo wa kumtia Ngesa mikononi ni ASP Kitogo,sura yake ilijikunja muda wote na mara zote alikuwa simuni anazungumza na vijana wake,vifo vya askari wake vilimtia hasira na kutamani Ngesa akamatwe.Historia ya Ngesa ilimfanya atamani kumuona na aliamini kabisa angepandishwa cheo kazini kwake,hilo ndilo lilimfanya afanye kazi kwa uadilifu.Msululu wa magari ulikua mrefu mno kiasi kwamba abiria mbalimbali waliokuwepo kwenye safari zao,waliona kama ni kero na wengine kulaani kitendo hiko.Askari wengi walikua na bunduki mikononi,wakiendeleza msako mkali.Upekuzi uliendelea mpaka walipolifikia gari aina ya Pajero na walivyogonga kioo hakukua na mtu yoyote aliyewafungulia,hapo askari mmoja akasogea kwenye kioo cha mbele,mshtuko aliopigwa ulifanya askari wote wasogee karibu.Hakukua na dereva ndani ya gari hilo,hiyo ikapelekea waanze kuhisi jambo la hatari.Hapohapo wakavunja kioo na kuanza upekuzi,waliambulia damu kwenye kiti zilizofanya watoe jibu moja kwa moja kua wenda angekua ni Ngesa.
“Askari wote,piteni kule”
Mkuu wa kikosi,akatoa amri askari ishirini wakaingia mitaani ambapo kulikua na makazi ya watu.
***
Ngesa na Daphine walizidi kusonga mbele,wakikatiza katikati ya makazi ya watu.Walielewa nini maana ya kukamatwa na jeshi hilo la polisi waliokua na usongo wa kuwatia mikononi na kuwaweka chini ya ulinzi.Isingekua Brigedia Karanje yupo hai wenda Ngesa angekubali kujisalimisha kwa jeshi la polisi,kilichomfanya amkomboe Daphine hakikua kingine bali ni Brigedia Karanje,alipania kumuua mwenyewe kwa mikono yake,ndiyo maana siku zote hakulala akimfikiria mbaya wake huyo.Walizidi kusonga mbele wakikatiza nyumba kwa nyumba,mpaka walivyotokea nje ya nyumba moja iliyokua haina rangi,nje kuna wakina mama wamekaa wanasukana,waliowaona waliwashangaa lakini hawakujali.
“Habari,barabarani ni wapi?”Ngesa akauliza!
“Kule,ukinyoosha moja kwa moja.Mtaa wa tatu”
“Ahsante”
Baada ya kuuliza,wakaendelea na safari wakifuata maelekezo,lakini walivyokunja njia ya pili karibu na nguzo ya umeme walishtuka baada ya kuona kundi la maaskari wakiongozana kama kumbikumbi wakiwa na silaha mkononi,wakazi wa eneo hilo walifunga milango wengine walikimbia wakiogopa silaha za moto.Zoezi la utafutwaji wa Ngesa ukaibua hofu na karaha kwani askari walianza kuingia ndani ya nyumba moja baada ya nyingine,kuwasaka Ngesa na Daphine.
“Hapa hakuna jinsi Ngesa”Daphine akavunja ukimya,hatari aliyoiona ilimtia hofu.
“Kwanini?”
“Hatuwezi kutoka,tutafute njia nyingine”
“Tutapoteza muda”
“Hatuwezi kuingia barabarani,kuna msako mkali”
Daphine akajaribu kutoa ushawishi wa hali ya juu na kumfanya Ngesa amtizame kwa umakini zaidi akipima hoja yake kama ina mashiko,bado moyoni alimchukia mwanamke huyo kwa kitendo alichokifanya cha kumuacha Jaqlin Mfinanga Bagamoyo,bado alikua na dukuduku moyoni.
Alichokifanya Ngesa ni kuingiza mkono ndani ya begi lake na kutoa bastola na kumkabidhi Daphine kama kujilinda,hiyo ilimaanisha wazo lake lilikua mwanga kwenye giza nene.Walichokifanya ni kugeuza na kuanza kurudi walipotoka,mbele yao kulikua na nyumba tatu,kando kuna choo aina ya ‘passpot size’ yaani mtu akioga anaonekana nusu,hapo Ngesa na Daphine wakaingia na kulivuta bati likitumika kama mlango ikawa kama kuna mtu yupo chooni.Msako wa nyumba kwa nyumba,uliendelea na hakuna nyumba isiyopekuliwa,redio upepo zilisikika wakiulizana kama Ngesa ama Daphine amepatikana,jibu walilolipata lilizidi kuwachanganya akili kabisa,hakukua na dalili ya Ngesa wala Daphine kuonekana.
“Atakua wapi?”
“Bado tunafanya msako mkuu”
“Hakikisha hatoki,najua yupo humuhumu Tegeta tena kwenye nyuma hizihizi amejificha.Asitoke,napiga simu kituo kikubwa cha polisi askari wengine waje”
Wakazi wa Tegeta kwa ndevu,walipekuliwa kwa kiasi cha kutosha, Ngesa alitafutwa mpaka kwenye makabati ya nguo,wenye ushungi walivuliwa bado hawakujua ni wapi Ngesa alipo,askari walichanganyikiwa hata hivyo hawakukata tamaa walikua wapo tayari wakeshe eneo hilo kumtafuta Ngesa.
“Nimebanwa,naenda chooni”
Bibi mmoja,alisema akiwa ndani.Huku akihangaika kutafuta maji ya kwenda chooni.Alivyopata ndoo ya maji,akanyoosha mpaka chooni ambapo alikuta mlango wa bati umeegeshwa akatoa,alichokikuta huko kilimfanya aogope na haja yote kuyeyuka.
“Nyamaza,rudishia mlango”Bibi akakutana na mlango wa bastola,ilikua kidogo apige kelele lakini alivutwa ndani na kuwekewa bastola kichwani hiyo ilimaanisha akae kimya asipige kelele na afuate alichoambiwa!
Watu waliokua ndani ya choo chake,walimuogopesha kwa kiasi cha kutosha zile fununu kua kuna majambazi wana tafutwa na wapo Tegeta,sasa walikua ndani ya choo chake wamekaa, mbaya zaidi wana bastola mikononi.Kupiga kwake kelele ilimaanisha kuharakisha kifo chake.Wakiwa ndani ya choo chakavu chenye shimo katikati wakivumilia harufu mbaya wakasikia vishindo vya watu,hiyo ilimfanya Daphine achungulie kwenye kitobo kidogo na kuona lundo la maaskari,kilikua ni kitendo kilichomuogopesha kwa kiasi cha kutosha.
“Askarii”Akanong’ona kwa sauti ya chini akimtaarifu Ngesa!Jambo hilo lilimfanya Ngesa aingize mkono kwenye begi na kutoa ‘Magazine’ iliyojaa risasi akampa Daphine.Ni tukio lililomfanya Daphine ashtuke,akachomoa ‘magazine’ ya bastola aliyopewa na Ngesa wakiwa katika harakati za kukimbia na kugundua haikuwa na risasi.
“Nilikua sikuamini bado:”Ngesa akasema
“Usijali”Baada ya hapo,akaweka Magazine ndani ya bastola kisha kuikoki na kumtizama bibi aliyekua pembeni yao,anatetemeka kwa hofu ya kifo.
Upekuzi ulikua kwa mtindo uleule,askari hawakua na ustaarabu hata kidogo,walimtafuta Ngesa mpaka kabatini na uvunguni mwa kitandani bila mafanikio yoyote yale.
“Chooni kuna mtu?”Askari mmoja,akauliza!Baada ya kuona mlango wa bati umeegeshwa.
“Ndio afande”Dada huyo akajibu.
“Ni nani?”
“Bibi yangu”
“Anafanya nini chooni?”
Lilikua ni swali la kiwaki kwani kazi ya choo ilijulikana.
“Ameenda kujisaidia”
“Mbona hatoki?”
“Sijui afande”
Walikaa hapo,dakika tano nyingine bila mtu yoyote kutoka chooni.Hiyo ilimfanya askari mmoja asogee karibu zaidi.Kila kilichoendelea Daphine alikiona kupitia kitobo kidogo kilichokua kwenye mlango wa bati,askari alivyokaribia Daphine akamuwekea bibi bastola kichwani.
“Wee bibi,unafanya nini chooni huko muda wote?Toka nje tupige sachi katisha haja yako mara moja, kabla hatujaingia”
Askari alisema kwa mkwara akiwa na mtutu mkononi,tayari kwa kumimina risasi kama kungetokea purukushani ya aina yoyote ile,jinsi walivyotumikishwa na kutukanwa kama watoto wadogo iliwafanya wawe kama vichaa, ndiyo maana hawakutumia ustaarabu hata kidogo,heka heka ilikua sio ya kitoto.Ngesa alikua makini kusikiliza kila hatua,kaishika bastola yake mkononi kwa lolote litakalo tokea ingawa aliamini umati wa askari hao isingekua rahisi kupambana nao hivyo aliamini wazi kwamba akili nyingi inahitajika sio nguvu.Daphine alikua karibu kabisa na mlango huo wa bati kashika bastola tena kamuwekea bibi kichwani kumaanisha asijaribu kuwaonya kwa chochote kile.
“Daphinee…”
Ngesa akaita kwa sauti ya chini kisha akatoa ‘Magazine’nyingine iliyojaa risasi iliyokua ndani ya begi lake.Ni tukio lililomfanya Daphine aichomeke nyuma ya kiuno chake.
“Ahsante..”
Daphine akashukuru huku akirudisha shingo yake kwenye tundu ambapo alimuona askari anazidi kuukaribia mlango ili aufungue.
“Jamani kuweni na adabu nyie watoto,sawa?Nyie ni askari najua lakini nitawashtaki kwa jambo mnalotaka kulifanya.Kama,mnataka radhi fungueni”
Bibi akaropoka kwa sauti ya ukali,alizungumza kwa sauti ya juu akilalamika kwa kitendo walichokua wanafanya askari.
“Bibi unafanya nini muda wote huo chooni?”Askari akauliza tena.
“Kwani watu chooni hua wanafanya nini?Nanunua mkate”Jibu hilo lilifanya baadhi ya maaskari wacheke na kuona ni kwa namna gani Bibi alikua amekasirishwa na isingekua rahisi mtu mwingine kuwepo ndani isipokua ni yeye,bila kujua kuwa yupo chini ya ulinzi mkali.
“Tuondokeni,tuingie mtaa wa nyuma bibi anakata gogo,tusije kupata laana bure”
Mkuu wa kikosi hiko alitoa amri,hiyo ilimaanisha itekelezwe mara moja bila kipingamizi cha aina yoyote ile,jambo hilo lilimfanya Ngesa ashushe pumzi ndefu ya uwoga na kimoyo moyo alimshukuru sana bibi huyo.
“Umefanya jambo la maana sana,ahsante bibi”
Daphine akashukuru.
“Piteni njia ya huku nyuma,huko watawaona.Mtaruka ukuta wa nyuma hapo,mtanyoosha mtatokea barabarani”
“Sawa,bibi ahsante”
Kama walivyoambiwa ndivyo walivyofanya kwani walifanikiwa kutokea upande wa pili,kulikokuwa na lami bila mtu yoyote kuwawekea mashaka,hiyo haikuwafanya wasiwe makini.
Mara moja moja waliona difenda za polisi zikipita kwa kasi kuwatafuta.Walizidi kutembea kandokando ya barabara mpaka walipotokea barabara inayoenda ‘Twiga Cement’ hapo walivuka upande wa pili,wakasimama sehemu baada ya kuona ‘Canter’ linapakia nyanya,haikua na haja ya kuambiana wafanye nini baada ya kuangaliana tu,wakajua ni kitu gani wakifanye.Hapohapo,wakakimbia na kulidandia bila mtu yoyote kuwaona,wakaingia katikati ya nyanya na kutulia ambapo utingo baada ya kupakia magunia kadhaa ya nyanya na vitunguu wakafunga na kufuli kisha dereva akaingia kwenye usukani, safari ikaanza hapohapo.Kupitia njia ya Bunju,walifanikiwa kufika Boko hapo gari lilitembea umbali wa kilomita ishirini likasimama.Ni tukio lililomfanya Ngesa asimame kidogo na kuchungulia kwenye moja ya uwazi ili ajue kuna nini,moyo wake ukakosa utulivu baada ya kuona kizuizi cha maaskari hiyo ilimaanisha mwisho wa safari yao ingekua hapo.
“Naomba leseni na kadi ya gari dereva”Askari wa usalama barabarani,wakiongozana na polisi aliyevaa nguo za kaki walikua sambamba.Hakuna siku dereva aliyotetemeka kama hiyo,gari hiyo aina ya ‘Canter’ haikua na kibali hata kimoja na ilitembea barabarani kimagumashi.Hiyo ilimfanya Dereva achomoe noti tatu za shilingi elfu kumi akaifinya nyuma ya leseni na kumpa askari.
“Tunawahi poti,najua mnafanya kazi usiku na mchana”
Dereva huyo alizungumza.Na askari alivyomtizama mwenzake na kuona hajaona tukio hilo,akaichukua leseni,kwa utaalam wa hali ya juu akaiingiza pesa mfukoni.
“Nawewe unaongea sana Chinga,mwambie utingo wako afunge mkanda.Aya,ondokeni”
Dereva akapiga gia akimuacha askari akikenua meno yake, baada ya kupokea mlungula.Hakuelewa kwa kufanya hivyo aliwaokoa Daphine na Ngesa ambao walikua ndani ya gari lake,gari lilizidi kwenda lilivyofika katikati ya msitu dereva akasikia kuna kitu kinagonga kwenye bodi.
Kiliendelea kugonga kikiwa ndani ya magunia ya nyanya na vitunguu,mpaka alivyopaki pembeni na kuteremka na panga ili kujihami,alivyofungua mlango wa nyuma akakutana na mdomo wa bastola.Daphine akashuka na kumuwahi utingo ambapo alimshusha na kumfunga kamba kisha kumtupa porini,hivyohivyo kwa dereva wote wakatupwa porini.Ngesa akaingia kwenye usukani safari ikaanza hapohapo.
“Pale mbele,utakata kona kwenye lile kontena”Daphine alitoa maelekezo baada ya kukaribia.Walivyokunja kona tu,wakapunguza mwendo na kuliegesha gari kando ya mti mkubwa.Hapo Ngesa alishuka akiwa na Daphine wote wakaanza kuongozana wakikatiza pori kwa pori.
“Ulipajuaje huku?”Ngesa akavunja ukimya kwani eneo hilo,hakukua na dalili yoyote ya binadamu kuishi.
“Zamani,tulikua tunafanya mafunzo huku.Tulikua tukificha silaha maeneo haya”
“Kuna umbali gani?”
“Pale karibu na ule mnara”
Mategemeo ya kumpata Jaqlin Mfinanga katika pori kama hilo la kutisha yalikua ni asilimia kumi kati ya mia moja,hata hivyo alijipa moyo na kujifarji wenda angepata muongozo wowote ule.Bado aliendelea kumtupia lawama zote Daphine kwa kitendo cha kuwatelekeza Jaqlin Mfinanga na mke wa Dustan,ulikua sio uungwana.Ngesa,alilalamika njia nzima akiwa na masikitiko makubwa mno,hata hivyo Daphine aliomba msamahaa na kukiri kosa lake akidai kuwa asingeweza kuingia nao mjini,kutokana na hatari iliyokuwepo kwa kipindi hiko.
Mbele yao,kulikua na nyumba ya udongo iliyochoka kwa kiasi cha kutosha,juu ina nyasi na kufanana na zile nyumba za zamani za makumbusho.Hapo wakatoa bastola na kuziweka sawa kwa tahadhari kubwa na kujihami,wa kwanza kuingia alikua ni Ngesa akiwa makini.Akasukuma mlango ambao ulitoa sauti,kutokana na bawaba kuingia kutu.Nyumba ilikua ya udongo lakini mlango wa mbao,utulivu wa ndani ulimfanya Ngesa atege masikio yake kwa makini na milango yote ya fahamu kua wazi.Pembeni ya nyumba hiyo kulikua na kiti,kilichobinuka ukutani kuna michirizi ya damu.Alivyochunguza vizuri akaona matundu mawili ya risasi kwenye ukuta huo wa udongo!Nywele zikamsimama.
“Kulikua na nani mwingine humu?”Ngesa akahoji.
“Jaqlin na mke wa Dustan”
“Kuna matundu ya risasi haya,umeona na damu hizi”
Ni wazi kabisa kulikua na hekaheka ndani ya nyumba hiyo na uvamizi ulitokea ndiyo maana kulikua na damu pamoja na matundu ya risasi.Ngesa aliomba Mungu anachofikiria kisiwe cha kweli hata kidogo,ndiyo maana akanyata mpaka mlango mwingine wa nyuma ambao aliukuta,umevunjwa kwa risasi.
Michirizi ya damu chini,ilimfanya aogope zaidi na kuanza kuifata akielekea katikati ya majani huku nyuma akiwepo Daphine makini akitizama huku na kule.Alihisi nywele zake zimemsimama baada ya kupiga hatua tano mbele,hisia za kwamba kuna hatari mbele zilimfanya hata vinyweleo vimcheze.Hali hiyo aliifahamu sana haikumdanganya,akatulia na kusimama akimpa ishara Daphine asimame.Katika hali ya kushangaza,alipigwa teke kali la kifua na kumtupa hewani kabla ya kutua chini,akapigwa kifuti kikali cha mbavu.Daphine alivyotaka kutumia bastola,mkono wake ukashikwa na kupigwa kofi kali ya shavu,mkono wake ukafutwa akapigwa kifuti cha tumbo.Hakuna mtu aliyeweza kujitetea kwani wapiganaji hao walikua hodari,mbaya zaidi walivaa Ninja usoni.Walikua wafupi na wepesi kuruka sambasoti.Ngesa alivyotaka kusimama akapigwa teke la mgongoni,alivyogeuka ili kujua ni nani akamuona Ninja mwingine,kashika kamba anabembea hewani na kutua juu ya mti wa mwembe kama ngedere.Ngesa akaelewa anapambana na watu hatari kiasi gani,NINJA waliogopewa na Ngesa alielewa jinsi gani walivyokua hatari na hodari kwenye mapambano hasa katika mapigano hatari ya Kong-fu na Tai-chi,hapo alisimama na kukunja ngumi huku akimuangalia Daphine aliyeonekana hata yeye kupagawa,asijue nini cha kufanya.
Ilikua ni hatari na hofu kubwa sana kwao,hususani kwa Ngesa ambaye alielewa hatari ya maninja hao.Ki ukweli alihisi jasho kumtoka na hakuelewa kama vita hiyo angeshinda ama la. Kwani hakujua idadi ya maninja hao wapo wangapi,isitoshe walikua ni hatari mno wenye mafunzo ya aina yake.Ninja mmoja alikuja nyuma ya Ngesa akaruka hewani na kumtandika teke lililomfanya apepesuke kama mlevi kabla ya kutulia akachotwa mtama kimo cha mbuzi na kufikia mgongo mpaka chini,alivyotaka kuinuka akakanyagwa na teke kifuani.Mchezo wote Daphine aliuona lakini alikua makini akiamini kua kufanya uzembe kidogo wasingetoka salama,kwake ilikua rahisi kidogo kwani katika mafunzo ya ukomandoo alifundishwa mbinu mbalimbali za kukabiliana na maadui wa namna hiyo.
Kwanza alielewa tabia za maninja kutumia aina ya mapigo ya Kongfu na karate, kingine alijua jinsi ya kuwathibiti.Ninja mmoja aliruka hewani na teke ili ampige Daphine.Lakini mwanamke huyu alikua makini kwani nayeye aliruka teke aina ya ‘round kick’,Ninja akiwa huko huko hewani akapigwa teke na kudondoka chini kama mzigo.Daphine akamsogelea kwa haraka na kumtandika teke,alivyotaka kumpiga lingine akawa amechelewa sababu alipigwa ngumi tatu za haraka za mbavu na ninja mwingine aliyekua nyuma yake.Ki ukweli,aliona kazi ngumu mbeleni lakini alijitahidi kupambana nao akitumia mapigo ya Judo.Ambapo ninja mmoja,alirusha ngumi Daphine akainama kidogo na kumpiga ambakati ya kidevu,bila kumkawiza akamvuta na kumtwanga kichwa kikali cha mdomo ninja akaonekana kupagawa na hapo Daphine hakufanya makosa,akamvuta na kumshika shingo akaivunja kwa kuizungusha.Ninja,mmoja akawa tayari amepoteza maisha.Ngesa alikua tayari amezidiwa kila alipojaribu kurusha ngumi hazikuzaa matunda,haikueleweka kama alichoka sana ama mapigo ya maninja hao ambapo walikua watatu wanamshambulia walimzidi nguvu.Kupepesuka kwake na kurudi nyuma kulimfanya atulie nyuma ya mti hapo aliona teke la Ninja likakuja hewani,akalidaka akamvuta karibu na kuliweka begani kwake,kwa hasira na bila kuchelewa akaushika mguu vizuri na kuuvunja kama mua.Makeleke aliyopiga Ninja,yalitisha na Ngesa alishaelewa kwamba tayari kamvunja mguu.Ninja mwingine akaingilia kati Ngesa akarusha ngumi iliyozaa matunda kwani ilimfikia kwenye koromeo na kumtupa mbali akabaki chini anahangaika kama mtoto mdogo aliyemeza ugali wa moto.Sura ya Jaqlin ilivyomjia kichwani akagundua kua kuendelea kubaki hapo ni kupoteza muda,alichokifanya ni kutuliza akili yake na kukunja ngumi.Mbwembwe za maninja na madoido ya kuruka huku na kule mitini kama ngedere sasa zilienda kuisha sababu Ngesa na Daphine waliwa shughulikia ipasavyo mpaka wakabaki wawili wakiwa hoi bin taaban.Wote wakavuliwa kofia zao za juu,kilichomshtua Ngesa watu hao hawakua watanzania.Walikua ni watu waliochanganyika mmoja alikua ana asili ya kiarabu mwingine mchina.Lakini wote walizungumza Kiswahili fasaha.
“Karanje yuko wapi?”
Ngesa akauliza huku akiokota bastola yake iliyokua chini,akachomoa ‘magazine’.Alivyoridhika baada ya kuona ina risasi za kutosha,akamuangalia Ninja huyo wa kiarabu aliyekua anavuja damu puani na mdomoni, kutokana na kipondo alichochezea.
“Sij..uiii Paaaaaa”
Risasi moja tu,ilimfumua vibaya sana ninja aliyekua pembeni ya mwarabu anayehojiwa.Ubongo wote ukawa umemwagika chini,ilikua ni maiti ya kutisha kwani risasi ilipita mbele kwenye komwe na kutokea kisogoni.
“Sitorudia tena swali”Ngesa akamrudia tena Ninja huyo mchina,ambaye aliona mambo yameshabadilika tayari.Hofu ilimtanda mno baada ya kuona mwenzake yupo chini ameaga dunia,hakua na sababu ya kukaa kimya zaidi ya kuonesha ushirikiano.
“Twende utupeleke”
Bila kipingamizi chochote,ninja huyo ambaye sasa alikua mateka akasimama wima na kuongoza mbele ambapo nyuma alisimama Daphine na Ngesa mwenyewe wakiwa makini na bastola zao mikononi.Ki ukweli hawakua na masihara hata kidogo,kila mtu alikua mwenye usongo wa kumtia Brigedia Karanje mikononi mwake kwa matendo ya kinyama aliyofanya waliamini kifo chake kisingekua cha kawaida hata kidogo.Waliendelea kusonga mbele,wakipanda milima na mabonde na kupita katikati ya miti mingi ambapo mara chache walisikia sauti za mbwa mwitu,bado hawakuelewa walipo lakini walichotaka wao ni kumtia Brigedia Karanje mikononi mwao.
“Tunakaribia kufika,mbele kidogo kwenye ule mti tuwe makini.Kuna mabomu ya chini”Ninja,aliamua kutoa ushirikiano,hawakuelewa ni kwanini ameamua kua upande wao kwani uwezo wa kukaa kimya na kuwaacha walipuke ulikuwepo lakini hakutaka kufanya hivyo,hata hivyo.Walizidi kusonga mbele mpaka walipofikia chini ya mti mkubwa wa mbuyu,hapo walichuchumaa kidogo.Ngesa akawa makini kutizama mbele,ambapo kulikua na nyumba yenye geti jeusi.Ukuta wake ulikua mrefu,umezungukwa na miti.Nje kuna magari matatu,ambapo kulikua na wanaume shupavu waliojazia misuli wameshika mitutu.
“Mlijuaje kama tutafika huku?”
Daphine akauliza,kuvamiwa na maninja kulimfanya atake kudadisi kitu.
“Tulikaa pale kwa muda mrefu sana,karibia mwezi mzima.Tunawasubiri”
“Mlijuaje kama ningeenda pale?”
“Karanje alituambia,ndiyo sehemu mliyokua mnaficha silaha kama sio hapo Bagamoyo ni lazima ungeenda Kibaha”
Ninja,akafunguka kila kitu cha kushangaza alizungumza Kiswahili kilichonyooka.
“Jaqlin yuko wapi?”
Ngesa,akadandia maongezi.Akaibuka na swali.
“Jaqlin yupi?”
“Mke wangu”
“Wako wanawake wawili,wote wapo ndani ya hii nyumba.Mmoja ana mimba,ndiyo huyo Karanje alisema atamuua ili kulipiza kisasi kwa Ngesa”
Ngesa alishtuka baada ya kusikia Jaqlin ana mimba cha pili alitetemeka kwa hasira,alivyosikia habari hizo mpaka akahisi vinyweleo na nywele zote zimemsimama.
Alitamani kusimama na kuivamia nyumba hiyo lakini alijionya kufanya hivyo sababu angeishia kubaya.Kilichotakiwa hapo ni akili nyingi kutumika.Kwa kumuangalia tu machoni ninja huyo akagundua kwamba kila anachosema kina ukweli ndani yake na kilichobakia hapo ni kufanya ukombozi na kumuua Brigedia Karanje, aliyekua ndani.Usongo ulimpanda lakini asingeweza kukurupuka kama nyumbu wenye kiu mtoni.Alichokifanya ni kuitizama nyumba hiyo jinsi ilivyokua na kumuangalia Ninja.
“Kuna mlango gani mwingine?”
“Kule nyuma upande wa pili”
“Unatumika?”
“Hapana”
“Unaweza kwenda kutufungulia?”
Ngesa akauliza. Ni swali lililomfanya Daphine,apigwe na mshtuko.Hakuelewa kama Ngesa amechanganyikiwa ama ‘stress’ za mapenzi zinamfanya asifikirie mara mbili,haikuwezekana hata kidogo amuamini mtu kama huyo hatari kirahisi namna hiyo.
“Ngesa,hiyo ni hatari kubwa”Ilibidi Daphine atoe dukuduku lake.
“Hatuna chaguo lingine”
“Unahisi hilo ni chaguo sahihi?”
“Ndio”
“Kwanini umemuamini namna hiyo?”
“Hawezi kusema uongo,yuko upande wetu”
Hapo Daphine alishusha pumzi nzito ya kuchoka,hakua na chochote cha kuongeza zaidi ya kumsikiliza Ngesa anachotaka.Maamuzi yaliyotoka ni kwamba Ninja huyo ambaye yupo mateka aingie ndani atumie mbinu yoyote ile ili akafungue mlango wa uwani.Lilikua ni jambo la hatari lakini Ngesa alielewa ni kitu gani anakifanya.Baada ya Ninja huyo kuanza kutembea na kufika mbali,akamtizama Daphine.
“Nina maana yangu kumtuma”
“Ipi?”
“Nataka kujua ndani kuna walinzi wangapi”
“Kivipi?”
“Akienda kuwaambia kwa niya ya kutugeuka wote watatoka,itakua rahisi sisi kuingia.Twende twende upande wa kule”
Hoja hiyo ilimfanya Daphine atabasamu na kuona ni jinsi gani Ngesa alikua mwenye akili nyingi,zilikua ni akili ambazo hata yeye hakuwa nazo.Aliunga mkono hoja yake na wote wakaanza kupita chini kwa chini mpaka walivyotokea upande wa pili wa nyumba hiyo,ambapo mbele yao walilitizama gari aina ya ‘Pickup hard board’Ngesa akalisogelea akiwa makini na bastola yake mkononi,akatembea huku ameinama mpaka kwenye gari hilo.
Taratibu,akaweka bastola yake kiunoni na kuchomoa kisu chake cha kukunja kilichokua na makali kotekote.Mwanajeshi aliyekua mbele yake,mrefu kwenda hewani ndiye huyo aliyetakiwa aanze naye ili wapate mwanya wa kusonga mbele.Umakini mkubwa kama simba akiwa kwenye lindo,alikamata kisu vizuri,alivyotaka kuibuka ili amkabe na kumchoma kisu,akasikia muungurumo wa gari.Ikabidi arudi tena mafichoni na kutulia.Gari hilo lenye mabaka ya jeshi,likapita kando yake na kusimama.Hakuweza kuwaona watu waliokua ndani vizuri,isipokua geti lilifunguliwa na gari kuingia ndani.Alichokiona ndani kilimfanya apigwe na butwaa.Yule ninja aliyemtuma alikua amepigishwa magoti,amewekewa bastola kichwani tayari kwa kuuliwa,hakusikia nini anahojiwa lakini alishushudia akipigwa teke kali la kifuani na kudondoka chali,alitamani kuinuka lakini akajionya kufanya hivyo,geti likafungwa na hakuweza kuona kilichokua kinaendelea ndani tena.Isipokua aliona wanajeshi wanne wanatembea nje ya nyumba hiyo.Akamtizama Daphine,aliyekua nyuma ya mti na kumpa ishara ya mkono kua,atamuua mwanajeshi aliyekua mbele yake hivyo akae mkao wa kula.Hali ilivyokua shwari,Ngesa akaibuka kutoka mafichoni na kumkaba kooni mwanajeshi huyo,ambapo alikukuruka akitaka kushindana na Ngesa,hata hivyo alishindwa kwani alichomwa kisu cha shingo,akashikwa mdomo na kuvutwa nyuma ya gari.Hapo Ngesa alimshindilia kipepsi kimoja cha utosi na kumfanya mwanajeshi huyo,atulie.Ngesa akachomoa kisu kilichokua kimebaki mpini kwa nje,akakifuta akitumia nguo za maiti huyo mwanajeshi kisha kukirudisha kwenye kiatu chake,akamuangalia Daphine na kumpa ishara apite sasa kupo salama.
“Tulia hivyo hivyo Ngesa,ukijitingisha naweka risasi kwenye ubongo wako”
Mapigo ya moyo wa Ngesa,yalikosa utulivu.Kichuma cha baridi kilimgusa kisogoni ikiambatana na sauti nene ya kukwaruza,kwa taaluma yake alielewa fika sauti hiyo haikua na mzaha hata kidogo ndiyo maana alimeza mate ya hofu.Aliamini kabisa,kufanya mjongeo wa ghafla kungehatarisha maisha yake na pengine kufumuliwa na risasi.Hakutaka hilo litokee ndiyo maana akakubali kua mateka.
“Simama taratibu”
Kitendo cha kuaza kusimama,akasikia kishindo kikali nyuma yake na mkoromo kama kondoo anayechinjwa,kwa mara ya kwanza hakuelewa lakini alivyogeuka nyuma,akapigwa na butwaa baada ya kuona mpini wa kisu umezama shingoni mwa mwanajeshi huyo,alivyoangalia upande wa kulia akamuona Daphine ambaye alimpa ishara ya dole gumba huku akitabasamu.Ilikua ni shabaha makini kwani Kisu kilirushwa na Daphine aliyekua mbali na kugota shingoni mwa Mwanajeshi huyo,hapo Ngesa alimkubali Daphine na kumpungia mkono kama ishara ya kushukuru.Alichokifanya ni kuiburuza maiti hiyo na kuiweka pembeni ya tairi,akatizama mbele na kuona kuna mwanajeshi mmoja aliyesalia,akiwa anavuta sigara.Anaranda randa huku na kule,kashika mtutu begani kikakamavu kuimarisha ulinzi.Jambo hilo likamfanya Ngesa awe makini zaidi na kumuangalia Daphine kwa mara nyingine aliyekua umbali wa mita ishirini,nyuma ya mti.Kama kawaida Ngesa,akiwa makini,akachomoa kisu na kuiweka bastola nyuma ya kiuno akanyata taratibu kwa mwendo wa paka,mpaka nyuma ya mwanajeshi huyo,ambapo alimkaba kwa nyuma lakini alivyotaka kumchoma kisu mwanajeshi huyo akawa ameshtukia hila hiyo,akaupangua mkono wa Ngesa na kurudi nyuma kwa kasi ambapo nyuma kulikua na ukuta,Ngesa akagota kwenye ukuta.Mwanajeshi huyu ilielekea alikua hodari na mtundu kwani kwa mtindo wa ajabu,akarudisha kichwa chake nyuma na kumfikia Ngesa puani,hivyo hivyo akajaribu kutupa kipepsi lakini Ngesa akawa makini kwani alikipangua na kumtandika ngumi tatu za haraka mbavuni,kosa la Mwanajeshi huyo lilikua ni kuinama kusikilizia maumivu kwani alijibinua kwa mtindo wa Pweza,miguu yake ikawa imejiviringisha shingoni mwa mwanajeshi huyo ambaye alionekana kupagawa hapohapo akachomoa kisu na kumchoma nacho kifuani,upande wa kushoto shabaha yake ilikua ni kulenga moyo.Ilikua ni shabaha nzuri iliyozaa matunda kwani Mwanajeshi huyo alidondoka chini bila kuomba maji ya kunywa.Sasa nje,kukawa salama kabisa hakukua na kipingamizi cha walinzi,Ngesa akazidi kusonga mbele.Wakajigawa Daphine akazunguka upande wa nyuma,Ngesa akaingilia mlango wa mbele bastola yake ikiwa mkononi.Akatembea taratibu mpaka kwenye kibanda cha mlinzi,huyo hakumpa tabu yoyote,kisu kimoja cha shingo kilimpeleka moja kwa moja chini akabaki anakukuruka kama kuku aliyechinjwa.Mbele yao,sasa kulikua na nyumba akiamini humo ni lazima Brigedia Karanje atakuwepo,alichokifanya ni kutembea mpaka kando ya tenki la maji hapo alitulia.Lakini alishtuka baada ya kusikia mkoromo wa mtu,akageuka nyuma na kumuona yule Ninja akiwa katika dakika za mwisho za kutetea uhai wake,kifuani alikua na tobo la risasi.Ngesa akaingiwa na huruma akamsogelea karibu.
“Ng…esa kamuokoe Mke..o sasa hivi”
“Unasemajee?Sikusikii”
“Sikutaka kuwaambia ulipo Ndi..o maana ika..wa hi…”
Ninja,alizungumza roho yake ikiwa inakaribia kutoka.Alikua katika mateso makubwa mno,damu nyingi zilimtoka kwenye jeraha hilo lililomfanya Ngesa achane kipande cha shati lake na kulifunika jeraha lakini ilikua ndio kama anammalizia kumuua.Kwani hapohapo,alikata kauli macho yakiwa yamemtoka ameacha kinywa wazi,alichokifanya Ngesa ni kumfunika macho na kushusha pumzi ndefu ya kuchoka moyo ulimuuma mno kwani Ninja huyo alionesha ukarimu sana kwao.Hata hivyo hakua na namna ya kufanya zaidi ya kusimama na kushika bastola kwa umakini na kusonga mbele, akielekea kwenye nyumba hiyo,alitembea kwa kunyata ambapo baada ya kufika mbele.Akahisi kuna mtu anakuja kwenye kona ya ukuta,hapo akatulia na kushika bastola yake vizuri kwa umakini.Hatua za mtu huyo zilikua zinakaribia,akawa tayari kwa shambulio.Mtu huyo alivyotokeza tu akamuwekea bastola kichwani lakini akajikuta,anatulia baada ya kugundua ni Daphine.
“Pole”Ngesa,akasema kwa sauti ya chini.
“Ahsante,kule kupo vizuri”
“Pita,upande wa nyuma”
Mikakati waliyopanga ilikua ni kabambe,Ngesa akatembea kwa taratibu na kusimama karibu na dirisha ambapo hapo alichungulia ndani na kuwaona wanajeshi wawili,mbele yupo Brigedia Karanje.Alishukuru Mungu kumuona Brigedia Karanje ndani,akaapia siku hiyo ni lazima ale naye sahani moja kifupi siku ya arobaini kwa Brigedia Karanje ilikua ndio hiyo.Akageuka nyuma na kumuangalia Daphine ambapo alimpa ishara akionesha vidole vitatu kumaanisha ndani wapo watatu hivyo,apite chini ya dirisha kwa staili ya kuinama.Daphine,akapita na kutokea upande wa pili wa dirisha.Akazidi kusonga mbele ambapo huko,kulikua na dirisha lingine alivyochungulia akapigwa na butwaa moyo wake ukakosa utulivu baada ya kumuona Jaqlin Mfinanga na Mke wa Dustan,wakiwa wamefungwa kamba mikononi.
Akamuangalia Ngesa na kumpa ishara asogee karibu.Ngesa alivyofika tu na kuchungulia moyo ukamuuma ajabu,akabana meno yake kwa hasira.Mtihani mkubwa ulikua ni kuingia ndani,kwa utaalam wa hali ya juu Daphine akanyata taratibu mpaka mlangoni,ambapo hapo Ngesa alikua pembeni hakukua na jinsi zaidi ya kutumia njia mbadala kwani kimya kimya isingewezekana tena.Hiyo ilimfanya Ngesa aingize mkono ndani ya begi dogo lenye mkanda mmoja akatoa bomu aina ya ‘Granade’ la kutupa kwa mkono,akampa ishara Daphine afungue mlango.Ulikua ni uvamizi wa ghafla kwani Daphine aliupiga mlango teke kwa nguvu,ulivyofunguka Ngesa akarusha bomu ndani.
“Grenadeeee!”
Mwanajeshi mmoja alipiga kelele lakini alikua amechelewa tayari,ukatokea mlipuko mkubwa sana ndani.Kila kitu kikasambaratika vibaya sana.
“Paaa paaaaa”
Ngesa aliachia risasi mbili,zilizowarusha wanajeshi wawili ukutani zilikua ni shabaha makini sana.Mwanajeshi mmoja alivyotaka kutoa bastola Daphine akamuwahi kwa risasi moja tu ya kichwa.Umakini wa Ngesa ulikua kwa Brigedia Karanje hapo hakumuona tena,wazo likamjia aingie chumbani alipomuona Jaqlin Mfinanga na Mke wa Dustan.Alivyoingia tu,alijikuta amepigwa na mshtuko wa waziwazi.Alikua ni Brigedia Karanje,yupo nyuma ya Jaqlin kumuwekea bastola kichwani akimtumia kama ngao yake.Hiyo ilimaanisha mjongeo mmoja wa Ngesa,ungepelekea kifo cha Jaqlin hapohapo.Ni tukio lililomfanya Ngesa ashindwe kutoa maamuzi sahihi na kubaki njiapanda.
“Uhai wake,upo mikononi mwako Ngesa.Cha kufanya,weka bastola chini rudi nyuma taratibu.Sitanii”
Ni amri iliyomfanya Ngesa atetemeke kwa hofu huku akimuangalia Jaqlin anavyolia kwa kwikwi,ilikua ni wazi kabisa Brigedia Karanje hakua katika mzaha hata kidogo.Jambo hilo lilimfanya Ngesa ateremshe mkono chini taratibu na kuweka bastola chini.
“Ipige teke ije kwangu,fanya haraka”Brigedia Karanje,akatoa amri hiyo.Ngesa akaipiga teke bastola ambapo iliteleza mpaka karibu na Brigedia Karanje.
“Taratibu rudi nyuma,usijaribu kufanya kitu chochote cha kipumbavu Ngesa.Nitamuua huyu kahaba”
“Kwanini usimuachie,udili na mimi?”
“Haupo katika nafasi yoyote ya kutoa amri,rudi nyuma nimekwambia”
Kinyume nyume kama gari Ngesa alirudi huku akiangalia kila hatua anayofanya Brigedia Karanje.Akili yake ilikua kazini,aliamini kabisa kama siku hiyo Brigedia Karanje angetoroka angejilaumu ndiyo maana aliwaza vitu chungumzima,kila hesabu aliyokua anapiga ilikataa.Akawaza kisu alichokua nacho kwenye kiatu,akichomoe lakini ingekua hatari zaidi kuliko iliyopo.Alivyokua anarudi nyuma kupitia jicho pembe,akamuona Daphine ametulia kando ya ukuta,bastola yake ipo makini kabisa.Akashukuru Mungu,kilichobaki hapo ilikua ni kumjaza Brigedia Karanje kwenye mtego huo.
“Nisharudi,unataka nini kingine?”Ngesa akauliza ili kununua muda.
“Rudi tena…”
“Mpaka wapi?”
“Mpaka nitakapokuambia basi”
Brigedia Karanje,asingeweza kumuona Daphine kwani alikua nje ya chumba hiko kwenye korido kaweka bastola yake kwa umakini akimsubiri atokeze,amm-alize.Brigedia Karanje hakuelewa lolote zaidi ya kusogea mbele kwa niya ya kutoroka.Mawazo ya Jaqlin Mfinanga yalikua mbali sana,akawaza vitu chungu mzima alielewa kabisa ni lazima Brigedia Karanje angeondoka naye kitu ambacho hakutaka kitokee,mimba yake ilikua kubwa na ilianza kuonekana tayari.Kilikua ni kitendo cha kufumba na kufumbua,Jaqlin Mfinanga akaung’ata mkono wa Brigedia Karanje kisha akamsukuma nyuma.
“Paaaaa”
Risasi ikachomoka kutoka kwenye bastola aliyoshika Brigedia Karanje,ulikua ni mlio mkubwa uliomfanya Jaqlin Mfinanga adondoke chini chali.Brigedia Karanje alivyotaka kujiweka sawa ili amlenge Ngesa alikua tayari amechelewa kwani mke wa Dustan alikua makini na shapu,chuma kilichokua chini alikiokota akiwa amefungwa kamba hivyo hivyo na kumpiga nacho kichwani.Kwa kasi ya Mwewe Ngesa akajipindua sambasoti na kumrukia mateke mawili ya kifua.Brigedia Karanje,akayumba mkono wake ulioshika bastola ukapigwa teke,bastola ikadondoka chini.Ngesa alivyotaka kurusha ngumi, Karanje akawa ameshtukia hila hiyo.Kwa utaalam akarudi nyuma na kumchapa Ngesa ngumi nzito ya chembe kwa mtindo wa boxa kwani alinesa nesa kidogo na kumsindikiza na teke aina ya ‘Flying kick’ ni jambo lililomfanya Ngesa apepesuke kama mlevi wa togwa na kurudi kinyume nyume mpaka akampiga kikumbo Daphine aliyekua mlangoni na bastola, wote wakadondoka chini chali.
Lilikua ni shambulio la ghafla sana na hakuna yoyote kati yao aliyetegemea kwani walidondokeana chini na kulaliana.Daphine alivyotaka kunyanyua bastola ikashindikana kwani Brigedia Karanje alimuwahi na kumtandika shuti kali la mkono, bastola ikaruka mbali.Brigedia Karanje akawa tayari kawathibiti lakini alivyotaka kutembea kurudi nyuma mguu wake ukashikwa na Ngesa, akavutwa lakini alijitahidi kujitoa,ilivyoshindikana akarusha teke. Hilo Ngesa aliliona akainama kidogo likapita hewani na kumpiga Daphine la pua ikampelekea mpaka ahisi kizunguzungu kikali!Maumivu aliyohisi yalimfanya aone nyota nyingi, taratibu akajishika na ukuta ili asimame kitendo cha kukaa sawa,akaona ngumi inakuja upande wa kushoto akainama kidogo ikakata upepo,alivyoangalia pembeni akamuona Ngesa anaelea hewani na kutua chini kama embe juu ya mti.
Lilikua ni pigo kali la tai Kwando alilopigwa Ngesa na hapohapo Brigedia Karanje akajibetua kwa mtindo wa paranawe akamchota Daphine vibaya sana na kumfanya adondokee bega chini, maumivu aliyohisi hakika yalikua makali.Ndani ya chumba hiko kulikua na hekaheka na Brigedia Karanje alionekana kuwamudu vizuri Ngesa na Daphine,alichokifanya ni kumfuata Daphine na kumuinua,akampigiza kwa nguvu ukutani.
“Siku zote kinyago nilichokichonga hakiwezi kunitisha”
Brigedia Karanje akasema na kumpiga ngumi nzito ya tumbo,akamchukua na kumpiga kifuti cha mbavu.Tayari alichakaa na damu zilimvuja puani na mdomoni,Ngesa alivyoona hivyo akasimama taratibu akiwa mwenye maumivu akamfuata Brigedia Karanje na kurusha ngumi lakini haikuleta madhara yoyote yale sababu Brigedia Karanje aliiona akahepa pembeni.Ngesa akavutwa na kutulizwa na kifuti cha mbavu,akapigwa teke kali aina ya ‘Round kick’.Bado Brigedia Karanje alionekana kutawala katika mchezo huo hatari kwani aliendelea kuwachakaza Ngesa na Daphine kama watoto wadogo!Hata hivyo hakuna hata mmoja kati yao aliyekata tamaa,ngumi kali iliyokua inakuja upande wa kushoto wa Daphine aliiona jambo hili lilimfanya Daphine ainame kidogo na kutupa ngumi tatu za mbavu zilizomfanya Brigedia Karanje agune kidogo,alivyotaka kurusha teke likazuiwa na Ngesa kwa mtindo wa Karate.Ngesa akawa tayari kaelewa udhaifu wa Brigedia Karanje wa kuchanganya mapigo,jambo hilo lilionekana kumsaidia sababu alifanikiwa kukanyaga meza akaruka kama ngedere hewani na kurusha teke lililomfikia shingoni,hiyo ilimfanya Brigedia Karanje apepesuke kidogo lakini alijizuia na stuli iliyokuwa pembeni iliyomfanya apate muhimili wa kukaa sawa.
Sasa akaona tayari mambo yamekua magumu,akaangalia chini na kuona bastola kabla hajaiwahi Daphine akawa ameruka tayari na kumpiga teke la kifua lililompepesua na kumfanya arudi kinyumenyume bila kupenda,alivyotaka kurusha teke hila yake ikawa imeshtukiwa na Ngesa aliyekua pembeni na kumchota na bega wote wakadondoka msobe msobe mpaka chini,Ngesa yupo juu Brigedia Karanje yupo chini.Kwa utaalam miguu ya Ngesa ikawa imejikunja kwenye shingo ya Brigedia Karanje,ni tukio lililomfanya Brigedia Karanje ashindwe kuelewa ni kitu gani akifanye,alivyojitahidi ajivute ikawa kama anajiongezea maumivu hata hivyo tumaini alilopata ni baada ya kuona chuma pembeni yake,akakivuta na kukishika mkononi.Bila kujiuliza mara mbili akampiga nacho Ngesa kichwani,hiyo ilimfanya Ngesa atulie hapohapo bila kusema kitu chochote kile yalikua ni maumivu makali ya kichwa yaliyosambaa mwili mzima na mbele aliona giza nene hapohapo akapoteza fahamu.
Karanje alihakikisha juu chini,anapambana mpaka tone la mwisho kuwathibiti Daphine na Ngesa.Hata hivyo ilionekana kama anazidiwa nguvu na Daphine kwani kila alivyorusha ngumi Daphine aliziona na kujibu kwa mapigo ya Kick boxa,yaani alikua akidunda huku na kule huku akiwa amekunja ngumi.Purukushani ilikua nzito na kubwa,Daphine alikumbuka mafunzo mengi aliyofundishwa nchini Urusi na ndiyo hayo Brigedia Karanje alikua akitumia hivyo ilimlazimu achanganye mapigo.Katika kitu alichojichanganya Daphine ni kurudi nyuma,hakujua kama kuna stuli iliyomfanya ajikwae, hapo ndipo Karanje alipopata mwanya wa kurusha teke lilimrusha Daphine hewani,kabla hajatua akadakwa shingo na kusukumizwa ukutani.Lilikua ni roba kali lililomfanya Daphine aanze kukosa pumzi.
***
“Mkuu,nimepigiwa simu kutoka Bagamoyo”
“Inasema nini?”
“Daphine na Ngesa wameonekana huko”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Bagamoyo sehemu gani?”
“Chiliwe,msitu wa Chiliwe”
“Ushaongea na OCD wa Bagamoyo?”
“Anazo taarifa ndio, kashapiga simu kwa OCS,wanaleta Difenda”
“Sawa,operesheni iende vizuri Ngesa na Daphine ni watu hatari kuliko mnavyodhani”
Simu pamoja na redio upepo zilipigwa karibia Bagamoyo nzima,taarifa za Ngesa na Daphine kuwepo Bagamoyo ziliwafanya maaskari wamwagwe kama kumbikumbi.Wakazi na wananchi wa maeneo hayo walitandwa na hofu kiasi kwamba wakashindwa kuelewa ni kitu gani kinaendelea.Mbali na hayo walipewa taarifa za watu hatari wanaotafutwa.Msitu mzito wa Chiliwe uliwekwa katikati na maaskari wenye mitutu na silaha aina ya SMG,baadhi yao walikua na usongo kiasi kwamba walitamani Ngesa na Daphine wajitokeze wawamiminie risasi.Walizidi kusonga mbele wakiwa makini mpaka walivyofika kwenye nyumba ndogo ya udongo, walitulia na kuingia ndani kitemi,walichokiona waliamini kabisa Ngesa na Daphine walikua maeneo hayo.
“Redio two ova”
“Nakupata poti ova”
“Njoo huku nyuma ova”
Askari watano wenye mitutu walitoka nje na kusimama wakishangaa maiti za maninja zilizokua chini,wote walitizamana na kushindwa kuelewa mkasa huo wa aina yake.Hali ya sintofahamu iliwatanda polisi na kushindwa kuelewa maiti hizo zimetokea wapi lakini jibu lilikuwa wazi kwamba ni Ngesa na Daphine.
“Kamanda,tizama”
Damu zilizokua chini juu ya majani zilimfanya mmoja wa makamanda wa polisi achuchumae na kutizama,kwa udadisi na taaluma ya kazi yake alielewa kabisa kwamba haikuwa muda mrefu kabla ya mtu huyo kuvuja damu kupita mahali hapo,hakutaka kuacha hivihivi akazigusa.Kuna kitu aligundua!
“Wapo karibu”
Baada ya kauli hiyo amri ikatoka,wafatilie michirizi ya damu mpaka wajue mwisho wake.Kila askari alikua mwenye usongo na silaha zilikua begani kwa ajili ya shambulizi la aina yoyote ile mbeleni.
***
“Lazima wote wafe au wafungwe”
“Lakini walijitoa muhanga kwa ajili ya nchi hii ya Tanzania,umesahau?”
“Hata kama,ukitaka kua salama inabidi wafe”
“Hilo litakua gumu”
“Litakua gumu?Hujui kua Ngesa anajua kila kitu”
“Nitaongea naye mimi”
“Sio rahisi kama unavyodhani Leslie,tambua itakuweka pabaya lazima unyongwe”
Rais Leslie alikua ofisini kwake,Ikulu.Sikio la kushoto ameweka simu anazungumza na mtu wa upande wa pili, ambaye kivyovyote vile ilionekana alimuhofia na kumuogopa kwa wakati mmoja.Ilikua ni simu iliyomtoa mudi yote.Ni wazi kwamba angekua katika wakati mgumu sana endapo Ngesa na Daphine wangeendelea kua hai,kichwa kilizidi kumuuma na aliona kabisa ugumu wa mambo siku zijazo.Ilikua ni lazima serikali imshtaki na kumnyonga mpaka kufa kutokana na maovu yote aliyofanya alivyomkumbuka Brigedia Karanje akahisi kuchanganyikiwa kabisa,maisha kwake yalibadilika alihisi kujuta kua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Leslie,kusuka au kunyoa kazi kwako”
Baada ya sentensi hiyo kusikika kutoka upande wa pili wa simu,ikakatika ikimuacha akiwa katika dimbwi la mawazo mazito.Mikono yake akaifumbata kifuani mithili ya mtu anayesali!Alikua katika mawazo mazito kiasi kwamba hata mtu aliyekua anagonga mlangoni,hakuweza kumsikia.
“Mheshimiwa Rais…Hodi”
Mwanaume mmoja mrefu kutoka idara ya usalama wa taifa aliingia ndani na kumuangalia Rais Leslie machoni,alionekana mwenye hofu kidogo baada ya kumuona Rais Leslie hayuko sawa.
“James,karibu kiti”
“Ahsante mheshimiwa Rais”
“Kuna mpya?”
“Ndio”
“Nakusikiliza”
Japokua alijitahidi kupachika sura yake halisi lakini bado alionekana hayupo sawa kabisa.
“Wamefanikiwa,kuingia Bagamoyo”
“Akina nani?”
“Jeshi la Mukulu,askari walidai walisikia Ngesa na Daphine wapo huko”
“Walisikia au wamewaona?”
“Wamesikia”
“Nashindwa kuelewa,mnamtafuta Karanje au Ngesa na Daphine”
“Wote kwa pamoja”
“Karanje atafutwe, Ngesa na Daphine nitadili nao mimi”
Rais Leslie akasema huku akiwa amekunja sura kiasi,bado hakuelewa awafanye nini watu hao wawili.
“Nitafutie Dustan”
“Nani DK?”
“Ndio James,namuhitaji sasa hivi ofisini kwangu”
Mchakato wa kumsaka Dustan,ukaanza mara moja!
****
Kabali kali kwenye ukuta ilimfanya Daphine aanze kuishiwa nguvu kabisa alihisi kulegea.Nguvu zilimuisha na alielewa tayari mwisho wake umefika Brigedia Karanje,alidhamiria kumuua Daphine akiwa mikononi mwake hapohapo.Lakini ilishindikana sababu alipigwa teke kali la mgongo na Ngesa ambaye tayari alizinduka,kabla ya Karanje kufanya chochote alitulizwa na kifuti cha shingo.Ngesa alikua kama mwenye nguvu mpya,akakanyaga kiti kilichokua pembeni na kumrukia mateke dabo ya kifua,kabla ya Karanje hajatulia chini.Miguu ya Ngesa ikawa tayari kwenye shingo wote wakadondoka chini Ngesa akawa amekaza miguu yake kwa nguvu akiikaba shingo ya Karanje.Kabali ya mguu ilikua kali na ilimfanya Karanje akukuruke lakini alishindwa kujitoa.Daphine aliyekua pembeni hana nguvu akaanza kujiburuza kukifata kisu kilichokua pembeni kirefu cha kijeshi,akakishika vizuri kwa nguvu za ajabu akakiinua juu na kumchoma nacho Karanje shingoni.Damu nyingi zikaruka na kutapakaa eneo hilo,Brigedia Karanje alikua chini anatapatapa!Haikua rahisi kuamini kama tayari wameshinda na kivyovyote vile haikua rahisi kwa Karanje kupona kwani Kisu kilitokea upande wa pili kikimuacha Karanje ameshika shingo yake,ametumbua macho tayari amekufa baada ya kukoroma kama kondoo kwa muda mrefu.Jaqlin na Mke wa Dustan walikua chumbani,hakuna hata mmoja kati yao aliyeamini.Ngesa alikua hoi chini Daphine usiseme,alihisi maumivu mwili mzima.Akamuangalia Ngesa kwa macho fulani yaliyojaa ushindi baada ya kumuua Karanje.Taratibu wakaanza kusimama Jaqlin Mfinanga na tumbo kubwa la mimba,akakimbia mpaka kwa Ngesa na kumrukia kwa furaha,wakakumbatiana kwa nguvu.Kila mtu alikua mwenye furaha baada ya ushindi huo,kilichobaki ilikua ni kuondoka lakini hawakujua ni wapi waelekee.Wote wakaanza kutembea kutoka nje,kitendo cha kufungua mlango wakashtuka.Kila mtu alipigwa na bumbuazi baada ya kuona Diffenda saba na askari zaidi ya hamsini wamejipanga na mitutu yao, tayari kwa kuachia risasi.
“Chini ya ulinzi pigeni magoti”
Mmoja wa maaskari akasema hiyo ilifanya Daphine,Ngesa Mke wa Dustan pamoja na Jaqlin wote wapige magoti kusalimu amri.Hakukua na chaguo lingine zaidi ya hilo kwani askari waliwazingira kila pembe wakiwa na mitutu iliyojaa risasi za kutosha.Askari watano wakasogea karibu na kuwainua Daphine na Ngesa na kuwafunga pingu kwa nyuma,haraka wakakokotwa mpaka kwenye Diffenda.Hakukua na maongezi zaidi ya askari kuingia ndani ambapo humo waliikuta maiti ya Brigedia Karanje.Harakati za kuipakia ikaanza mara moja,redio upepo pamoja na simu zikapigwa ikulu wakitoa taarifa ya Ngesa pamoja na Brigedia Karanje.Daphine na Ngesa walikua chini ya ulinzi mkali sana,hakukua na upenyo wowote wa wao kutoroka,Diffenda zikatoka kwa mikwara na kuondoka kwa kasi ya ajabu.Ulikua ni ushindi mkubwa kwa polisi na walijisifu kwa hilo.Mawazo mengi yalipita kwa Ngesa lakini sasa alikua huru baada ya Karanje kufa,hata hivyo alijisikia uchungu sana kumuacha Jaqlin Mfinanga akiwa katika hali hiyo ya ujauzito alielewa ni jinsi gani angekua mpweke.Akiwa katika mawazo makubwa ghafla,kikasikika kishindo kikubwa cha mlipuko.Diffenda ya mbele ilirushwa hewani lilikua ni kombora aina ya RPG.Ni tukio lililofanya askari na mitutu yao waanze kurusha risasi hovyo,hawakukaa sawa.Likapigwa kombora lingine gari la nyuma likasambaratishwa.Upande wa kushoto likatokea gari aina ya Noah,mlangoni wamesimama wanaume warefu waliojazia na mkononi wameshika silaha hatari aina ya AK47,kitendo cha kuachia risasi askari wote walikua wanatupwa mbali na kudondoka kama kuku wenye mdondo kutokana na uzito wa silaha.Hali ilivyokua shwari kidogo wanaume sita wakashuka wakiwa na vitambaa usoni kuziba sura zao.Wakaingia mpaka ndani ya gari alilokuwepo Ngesa na Daphine,wakafunikwa vitambaa vyeusi na kuanza kuwaburuza mpaka kwenye Noah.Jinsi Noah ilivyogeuzwa ilitishia amani,ilitimua vumbi na kutoka kwa kasi ya kimondo.
Sio Daphine wala Ngesa kila mtu alikua katika hali ya sintofahamu,hofu iliwatanda na kujua tayari wanaenda kufa kwani watu hao walikua hatari sana.Hakuna mtu yoyote aliyezungumza isipokua gari ilitembea zaidi ya masaa sita barabarani waliamini kabisa kwa masaa waliyotembea ni lazima wangekua nje ya mji tu!Lisaa limoja lingine ndipo taratibu gari likaanza kusimama na kupaki kando.Mlango wa NOAH ukafunguliwa.
“Wafungueni pingu na vitambaa usoni”
Sauti hiyo ikasikika jamaa huyo akasema akiwa na kitambaa cheusi,Ngesa na Daphine wakafunguliwa pingu na vitambaa vyeusi usoni vilivyokua maalum ili wasione ni wapi wanaenda.Mbele yao kulikua na wanaume wanne walioshiba na kujazia miili yao.Walivyoangalia nje,wakaona gari aina ya Toyota Mark Mark II grande inakuja kwa kasi kisha kupiga breki mbele ya NOAH,mtu waliyemuona anashuka aliwashangaza sana.Sio Ngesa wala Daphine kila mtu alipigwa na bumbuazi.
“Dustan”Ngesa,akaita kwa sauti ya mshangao!
“Ngesa hatuna muda wa kupoteza,nimetumwa na Rais Leslie”
“Umetumwa nini?”
“Anataka muende London,passpoti zenu hizi hapa.Helkopta itawachukua na kuwapeleka mpaka Kisumu nchini Kenya huko mtachukua Ndege”
Dustan alizungumza akiwa makini huku akiwa na hati mbili feki za kusafiria,akamkabidhi Daphine na Ngesa.
“Na familia yangu?”
“Ngesa kwa sasa hivi,inabidi uondoke mengine baadaye mambo yakitulia.Haitakiwi mtu yoyote kujua mlipo”
“Dustan,asante sana.Hakikisha Jaqlin anakua salama”
“I promise you…Ongea na Rais Leslie”
Simu ikapigwa hapohapo,Rais Leslie akapokea simu na kuzungumza na Ngesa pamoja na Daphine.Zilikua ni shukrani za aina yake!
“Ngesa,nakutakia kila la kheri”
“Ahsante Mheshimiwa Rais”
“Ukifika London mtafute mtu mmoja anaitwa Carlos Vendaz,atakupokea kuna baasha amekupa Dutan itakuelekeza mji utakaofikia.Maagizo mengine nishampa Carlos Vendaz”
Simu ikakatwa.Dakika tano baadaye,mlio wa helkopta ukasikika.Taratibu Helkopta ikaanza kutua mpaka ardhini huku vumbi kali likitimka. Daphine na Ngesa wakapanda.Taratibu ikaanza kuinuka juu huku Ngesa akiangalia chini na kumpungia Dustan kwa ishara ya kumuaga,Dustan akabaki chini mpaka alivyohakikisha Helkopta imepotea kwenye upeo wa macho yake!
***MWISHO****
0 comments:
Post a Comment