Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AIISSII U KILL ME LEGACY SEHEMU YA 3/10

 


AIISSII U KILL ME LEGACY

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 3 KATI YA 10

 


“Ni mpe….nzi wangu”

“Kwa nini umemuambia kwamba nipo Zahanati?”

“Ni askari na ameniuli….iliiza ka…..”

Nikampiga ngumi nzito ya shingo nesi huyu na akaanguka chini na kupoteza fahamu. Nimamvua raba zake alizo zivaa, nikazijaribisha kwa bahati nzuri mguu wangu unaingia. Nikazivaa, kisha nikatungua koti jeupe lilipo kwenye moja ya msumari hapa mlangoni. Nikalivaa na kuchungulia kwenye kordo na kuwaona wagonjwa wengine wakiendelea kusubiria huduma ya matibu. Nikaanza kutembea kwenye kordo hii kw akujiamini, nikafika nje nikatazama pande zote za hili eneo. Nikamuona mzee mmoja akimshusha mke wake mjamzito kwenye pikipiki huku akiicha ikiwa inawaka. Kitendo cha kuingia ndani mzee huyu nikapanda pikipiki hii, nikaigeuza kwa nguvu na kuondoka eneo hili na kuifwatisha barabara ambayo kwa kweli sifahamu ni wapi inapo elekea.

“Ehee Mungu wangu, kweli hii ndio Tanzania ya amani jamani?”

Nilizungumza huku nikiongeza mwendo kasi wa pikipiki hii ya wizi. Nikafika katika barabara ya lami. Nikasimamisha pikipi pembeni na kuitoa simu hii mfukoni, nikaanza kufikiria ni mtu gani ambaye ninaweza kumpigia akanipatia msaada ila nikashindwa. Simu hii ikaingia meseji iliyo nifanya nitamani kuifungua ila nikashindwa na kuirudisha simu mfukoni.

Nikaendelea kuendesha pikipiki hii, huku nikinyoosha hii barabara ya lami. Nikafika kwenye moja ya mji ambao umechangamka changamka kidogo.

“Ninakwenda wapi Mungu wangu”

Nilizungumza huku nikisimama pembeni mwa moja ya kibanda cha chakula. Nikaitoa simi hii mfukoni na kukuta meseji zikiwa zimeongezeka na kufika nne. Nikapata ujarisi wa kuzifungua.

‘KIMBIA JINSI UNAVYO KIMBIA ILA TUTAKUKAMATA TU’

Meseji zote zimeandikwa maneno yanayo fanana kiasi cha kunifanya nitishike sana. Nikatazama watu walio kaa kwenye kibanda hichi ambacho kuna mama anauza chakula. Nikajitazama jinsi nilivyo vaa, kwa asilimia kadhaa nikimdanganya mtu anaweza akakubali. Nikashuka kwenye pikipiki na kutoa funguo.

“Habari zenu”

“Salama”

Nikaa kwenye moja ya kiti na mama huyu muuza chakula akanifwata.

“Tuna wali maharege, nyama, kisamvu, bamia, mchicha na samaki. Ugali pia upo. Unataka nini?”

Mama huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, nikashusha pumzi taratibu.

“Samahani tunaweza kuzungumza dada?”

“Zungumza tu”

“Mimi ni daktari Zahanati moja hapo kijiji cha Nyuma, nahitaji kuiuza hii simu yangu ninataka kwenda mjini sasa hivi kuna matatizo kidogo yamemkuta mke wangu. Nataka nikayashuhulikie”

Mama huyu akanitazama usoni mwangu, nikajikaza kuto kuonyesha wasiwasi wa aina yoyote.

“Mmmm simu yenyewe hiyo smartphone ukiniambia milioni mimi nitainyea wapi, usawa huu wenyewe wa Magufuli”

“Wewe leta kiasi chochote ulicho nacho?”

“Chochote?”

“Ndio”

“Hata buku kumi”

“Ndio”

Mama huyu akafungua fundo tenge elilo vaa na kutoa noti moja nyekundu nyenye masifuri manne na kunikabidhi. Nikamuachia simu hii na kuanza kuondoka kwa kasi na kumuacha mama huyu akiwa amejawa na furaha. Kabla sijafika mbali, nikashuhudia gari sita za polisi zikizingiria kibanda hicho cha chakula na moja kwa moja nikajua namna ya wao kunitafuta mimi ilikuwa ni kutumia simu niliyo kuwa nimeiuza na hivi sasa haipo tena mikononi mwangu.



Nikamshuhudia askari mmoja akimpokonya mama huyo simu, kutokana nipo mbali na nipo sehemu niliyo jibanza sikuweza kusikia wanazungumza kitu gani. Nikatuliza macho yangu vizuri na kuanza kumtazama askari huyo mdomoni mwake, kutoka nina mafuzo ya kijeshi ambayo yananiwezesha kujua ni kitu gani mtu anakizungumza kutokana na lispi zake zinavyo cheza. Ikawa ni rahisi kujua ni kitu gani askari huyo anakizungumza.

‘Wapi?’

Nilimuona askari huyo akiuliza swali hilo, mama muuza chakula akaonyesha sehemu nilipo elekea, nikamuona askari huyo akitazama eneo nilipo, na kwa bahati mbaya macho yetu yakagongana. Askari huyo akawaamrisha wezake kuanza kunikimbiza. Sikuhitaji kukamatwa kwama kuku, moja sijui ninafukuziwa nini, pili sifahamu mfumo wa kipolisi wa hii nchi.

Nikazidi kukatiza kwenye vichochoroa katika mji huu, ila kuto kuwa mzoefu kukaanza kunipoteza matumaini ya kutoka katika mji huu kwani kuna baadhi ya vichochoro nilivyo katiza nilijikuta nikiishia kwenye kuta za nyumba kwa nyumba.

“Nyoosha mikono juu kabla hatujakumwaga ubongo”

Nilisikia sauti yenye ukali nyuma yangu. Nikasimama huku taratibu nikinyoosha mikono yangu juu, nikageuka na kuwaona askari wawili wakinisogelea huku wakiwa wamezishika bunduki zao vizuri sana kwa kujiahami kwa lolote ambalo linakwenda kitokea. Ushikaji wa bundiki wa askari hawa dhairi unaonyesha kwamba hawana mafunzo mazito kama niliyo pitia mimi. Nikajaribu kuishu mikono yangu chini, ila mmoja wao akaniamrisha kwa ukali sana kwamba nisithubutu kufanya hivyo, wakanisogelea ili wanifunge pingu, sikukubali upuuzi huo kwani, kitendo cha mmoja wao kunishika mkono wangu wa kulia ili afunge pingu, nikajizungusha hewani na kumtandika mwenzake aliye shika bunduki, teke zito la kichwa na kumpafanya ajibamieze kichwa ukutani na kuanguka chini. Huyu aliye nishika, kwa kuchachawa alijikuta akihitaji kunishambulia kwa kufyatua bunduki aliyo ining’iniza mgongoni mwake kutokana na kuvaa mkanda wa bunduki hiyo, ila akachelewa kufanya hivyo kwani kichwa kizito nilicho mpiga usoni mwake, kikamzuzua, nikamsindikiza na teka zito pamoja na gumi ya kifua na akaanguka chini na kupoteza fahamu. Nikakikimbilia hadi sehemu ya mwanzo wa uchochoro huu nilio ingia na kukuta ukiwa hauna sehemu ya kutokea zaidi ya ukuta ulio ziba njia. Sikuona dalili ya polisi wala mtu kukatika katika eneo hili. Nikawarudia askari hawa, kwa haraka, nikamvua askari mmoja nguo zake, kisha nikavua za kwangu na nikavaa zake. Nilipo hakikisha nimevaa kila kitu, nikavaa kofia yake ambayo ni nyekundu na ina nembo ya taifa hili la Tanzania.

Nikatazama bundiki zao, ila sikuhitakji kuzichukua kwani kukimbia na silaha ya askari tena polisi, inaweza kusababisha matatizo makubwa sana kwangu.Nikatoka katika kichochoro hichi, nikatazama ni wapi pa kuelekea, nilipo ona sehemu ambayo ni kimya kidogo nikaanza kukimbia ila nikiwa makini sana. Nikaanza kuzunguka katika mji huu huku nikiwa sina pa kukimbilia.

‘Ehee Mungu nisaidie mie’

Nilizungumza huku nikiwa nimesimama kwenye moja ya kituo cha daladala huku nikiwatazama watu wanao panda na kushuka kwenye kila daladala inayo simama katika eneo hili. Gari nyeusi aina ya BWM ikasimama katika hili eneo, akashuka mwanadada aliye valia mavazi mazuri sana. Wanaume karibia wote tuliopo hapa tukabaki tukimtazama mwanadada huyu. Kitu lilicho nishangaza zaidi ni mwanadada huyu kunifwata hapa nilipo simama na akasimama pembeni yangu.

“Muda mchache kuanzia hivi sasa utakuwa mikononi mwa jeshi la polisi. Una kama dakika mbili za kufanya maamuzi yako Randy. Ondoka na mimi au ukamatwe”

Dada huyu alizungumza huku akitazama saa yake ya dhahabu aliyo ivaa katika mkono wake wa kushoto.

“Wewe ni nani na umenijuaje?”

“Huna haja ya kunijua, na ninavyo kuambia picha yako imezagaa maeneo mbalimbali hapa nchini na mtu ambaye atakukamata amehakikishiwa kukabidhiwa kiasi cha milioni mia moja za Kitanzania, je unahisi watu hawa wote hapa kituoni hakuna hata mmoja wao amabaye amekustukia?”

Maneno ya msichana huyu yalizidi kunishangaza na kuniogopesha.

“Kika jambo ni maamuzi yako”

Dada huyu mara baada ya kuzungumza hivyo akaanza kuondoka katika eneo hili na kuniacha peke yangu. Nikageuza macho yangu katika pande zote katika eneo hili, nikashuhudia watu baadhi ya watu wakiwa wananitazama kwa umakini sana huku wengine wakionekana na wakiendelea na mambo yao. Nikaanza kumfwata dada huyu na tukaingia kwenye gari hili na dereva akaondoka gari katika eneo hili.

“Nahitaji kukufahamu wewe ni nani na umenijuaje mimi?”

Nilimuuliza dada huyu huku nikiwa na msisitizo mkubwa sana. Dada huyu hakunijibu zaidi ya kunitazama usoni mwangu huku akiwa amejawa na tabasamu.

“Unatakiwa kutulia usijali katika hili”

“Nitatulia nini ikiwa sifahamu wewe ni nani na sifahamu ni wapi unapo nipeleka”

Dada huyu akatoa simu yake mfukoni aina ya Iphone 7. Akanionyesha tangazo langu lililo tolewa na jeshi la polisi kwamba mmi ni gaidi niliye vamia nchi hii ya Tanzania na ninatafutwa kwa hudi na uvumba.

“Ila mimi sijafanya kosa la aina yoyote”

“Natambua, Dany ameweze kukupatia kesi hii ya maaujia ndio maana imekuwa hivyo”

“DANY!!?’

Niliuliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio Dany”

“Mbona yeye ndio mtu ambaye amenisaidia kunitoa katika mikono ya watu ambao waliniteka?”

“Ilikuwa kwa sababu”

“Ip?”

“Mimi na wewe hatuifahamu, ila unacho takiwa ni kuwa mpole. Nisikikize mimi kisha nitakupatia maelekezo ya nini cha kufanya sawa”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama msichana huyu usoni mwake. Gari taratibu likasimama katika foleni ya magari mengi sana.

“Natambua kwamba Dar es Salaam huna sehemu ya kwenda si ndio?”

“Ndio”

Dada huyu akachomoa faili moja lililo kuwa limechomekwa nyuma ya siti ya dereva. Akatoa picha mbili za kijana mmoja mwenye asili ya kiafrika.

“Ainaitwa Ethan Klopp, anaishi nchini Ujerumani. Kijana huyu ana boksi maalumu ambalo sisi tunalihitaji kulipata kutoka kwake”

Msichana huyu akaendelea kuniongezea picha za kijana huyu ambaye anaonekana ni kijana wa umri kama miaka kumi na saba hivi.

“Ni mchezaji mpira maarufu na hapa ninavyo zungumza yupo kwenye michuano ya kugombania kombe la bara la ulaya kwa shule za sekondari.”

Msichana huyu akaniwekea video kwenye simu yake. Video hii inaonyesha kukamatwa kwa wanafunzi wa kike ambao sifahamu ni wa shule gani.

“Hawa ni wanafunzi kutoka nchini Ujerumani, kwa sasa wapo katika nchi ya Somalia na wameshikiliwa katika kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab. Jukumu lako la kwanza ni kuhakikisha kwamba unakwenda kuwakomboa. Natambua kwamba ulikuwa katika kikosi cha Al-quida una mafunzo ya kudili na magaidi, hivyo safari yetu ya kwanza ni kueleekea nchini Somalia sasa hivi”

“Ngoja kwanza, nahitaji kufahamu wewe ni nani na una lengo gani kwangu?”

“Kufahamu jina langu sio jambo muhimu sana. Ila hapa kuna mambo mawili ya kufanya. Unahitaji kuwa huru, au shuka kwenye gari langu nikukabidhi kwa askari hao hapo pembeni”

Msichana huyu alizungumza huku akinionyesha gari la polisi lililo simama pembeni yetu kwenye hii foleni. Nikawatazama askari hawa kwa dakika moja, uzuri wa gari hili vioo vyake ni vyeusi, ni ngumu sana kwa mtu wa nje kuweza kumuona mtu wa ndani.

“Chaguo ni lako, uhuru au jela?”

“Utanilipa kiasi gani kwa hii kazi?”

“Hivi una elewa kitu ninacho kizungumza kweli wewe. Nimesema uhuru wako ndio kitu muhimu kwenye maisha yangu, unahitaji au auhitaji?”

Dada huyu akamgusa dereva kwenye bega lake, taratibu kioo cha upande wangu kikaanza kufunguka. Askari hawa wote macho yao wakayatupia kwangu.

“Sawa sawa, nimekuelewa, nitaifanya”

Kioo taratibu kikapandishwa, gari zikaruhusiwa kuondoka katika eneo hili, sisi tukaelekea katika eneo jengine huku gari la polisi likielekea katika eneo jengine.

“Ili kuweza kupata ukaribu na usalama kwa kuishi nchini Ujerumani na kuifanya kazi ambayo tunakwenda kuagiza kuifanya, ni lazima kuhakikisha kwamba una wakoamboa hawa wasichana haraka iwezekanavyo”

“Wamekamatwa kwa sababu gani hawa wasichana?”

“Hakuna hata mmoja ambaye anafahamu sababu ya kukamatwa kwao, ila lengo la hichi kikundi ilikuwa ni kuhakikisha wanamkamata mtoto wa mgombea Uraisi wa nchi ya Ujerumani, ila kwa bahati mbaya au nzuri hakuwemo kwenye msafara huo. Sasa walio salia ndio kama hawa. Hadi sasa hivi wamesha uwawa waalimu wao kikatili kama unavyo jionea.”

Dada huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikaitazama video hii kwa kweli ikanipa hamasa ya kuifanya hii kazi kwani ukatili unao fwanya na hawa wapiganaji wa Al-Shabab umepitiliza.

“Kampuni yangu imeweza kufahamu ni wapi walipo shikiliwa hawa wanafunzi ndani ya Somalia hivi basi ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unawakomboa na kuwarudisha nchini Ujerumani”

“Nikuulizwa ninafanya kazi chini ya kitengo gani nitawajibu vipi?”

“Hilo jambo naomba uniachie mimi, wewe kwanza hakikisha unafwatilia hawa watoto kisha mambo mengine yanafwata”

“Sawa”

Gari likaingia katika geti kubwa linalo lindwa sana. Katika eneo hili kuna majengo mawili ya gorofa nne nne. Tukashuka na kuanza kutembea kuelelekea ndani. Nikaingizwa kwenye moja ya chumba chenye kiti pamoja na meza tu.

“Watakuja madaktari sasa hivi, naomba uwape ushirikiano muhimu”

“Sawa”

Msichana huyu akatoka ndani humu na nikabaki peke yangu huku nikiendelea kukichunguza hichi chumba ambacho kinafanania na vyumba vya mahojiano vinavyo tengenezwa katika taasisi mbalimbali za usalama wa nchi au raia. Wakaingia madaktari wawili wanaume wenye asili ya Kihindi. Mmoja wao akaweka brufcase kubwa mezani. Akaifungua na nikaona kifaa kilicho kaa muundo wa bastola. Mmoja waoa akanichoma bamba la sindano katika mkono wangu wa kulia, akatoa damu kiasi kisha akaiweka katika kipimo chao kingine na wakaanza kuminya minya batani za laptop yake ambayo sifahamu ni kitu gani anacho kitazama.

”Yupo salama”

Alizungumza daktari mmoja kwa kutumia kifaa kidogo cha mawasiliano alicho kifunga mkononi mwake. Daktari mmoja akachukua hii mashinde yenye muundo wa bastola na kutaka kunichoma shingoni mwangu, ila nikamshika mkono.

“Ni nini hii?”

Daktari hakunijibu chochote zaidi ya kunitazama. Akaingia dada huyu niliye kuja naye katika eneo hilo.

“Hiyo ni GPRS device, kkila utakapo kuwa unakwenda duninai basi tutaweza kukufwatilia na kukuona. Sehemu salama zaidi ya wewe kuhifadhiwa hicho kifaa ni shingoni mwako”

Dada huyu alizungumza huku akinitazama usonim wangu.

“Hakiwezi kuniletea madhara yoyote?”

“Hakiwezi kukuletea madhara yoyote, niamini mimi”

Dada huyu alizungumza kwa upole huku akitusogelea karibu katika sehemu hii tulipo. Daktari kwa kutumia kifaa hichi kilicho kaa muundo wa bastola akaniingiza kifaa kidogo ndani ya shingo yangu, japo ninahisi maumivu, ila si makakali sana. Wakanigeuzia laptop yao, wakanionyesha ni sehemu gani kifaa hicho kilipo karibu kabisa na mshipa wangu damu.

“Ukijaribu kukitoa, basi unakata mshipa wako wa damu na mwishowe utajikuta ukifa.”

“Kitadumu mwilini mwangu kwa siku ngapi?”

“Hadi pale utakapo maliza kazi”

“Hadi nitakapo maliza kazi hata ikichukua wiki moja?”

“Ndio na nitahakikisha kwamba ninalisafisha jina lako kwa polisi na utaishi huru”

“Sawa naomba uwe muwazi na mkweli katika hilo na endapo ikatokae ukaenenda kinyume na mpango wangu basi nitahakikisha kwamba ninakua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”

Msichana huyu akatabasamu kisha akanisogelea sehemu nilipo kaa na kuniinamia. Akausogeza mdomo wake hadi sentimita chache sana kutoka ulipo mdomo wangu.

“Hakikisha kwamba unafanya kazi unayo ifanya la sivyo nitakuwa wa kwanza kukuua kwa kuminya batani hii”

Dada huyu alizungumza hukua akinionyesha moja ya batani ndogo aliyo itoa mfukoni mwake. Kwa ishara akamuelekeza daktari kitu cha kuweka kwenye hii laptop, nikamuona mtu mmoja akiwa anawekewa kifaa kama hichi nilicho wekewa mimi shingoni mwangu. Video hii ikamuonyesha mtu huyo akijaribu kukimbia, ila kwa kuminya batani aliyo nayo dada huyu mtu huyo alichanguka changuka mwilini wake na kufa hapo hapo, jambo lililo nifanya nipate wasiwasi mkubwa sana.

“Hii ni game Randy, kosa moja goli moja. Maisha yako kwa sasa yapo mikononi mwangu. Hakikisha kwamba hunikatishi tama kwa maamuzi yoyote ya kijinga umenielewa?”

“Ndio nimekuelewa”

“Jiandae kwa safari”

Dada huyu alizungumza huku akisimama wima. Akatembea hadi mlangoni kisha akanigeukia na kunitazama.

“Ninaitwa LAURA LIVNA LIVBA”

Dada huyu mara ya kuzungumza hivyo akatoka ndani humu na kuniacha nikiwa ninafikiria jinsi nilivyo ingia kwenye mtego wa kufa pasipo mimi kujijua.



‘Laura Livna Livba’

Nilirudia jina la dada huyu kulitaja kimoyo moyo. Daktari walivyo maliza kunifanyia wanacho nifanyia wakaniruhusu kutoka ndani ya chumba hichi. Nikakutana na Laura na akanionyesha video nyingine ambayo watekaji hao wanamtaja Ethan Klopp kuwa ndio mmiliki wa boksi hilo jeupe.

“Amepokea simu na kukatisha mauaji yake, inaonyesha dhairi kuna mtu yupo nyuma ya kikundi hichi cha kigaidi”

Laura alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Unahisi ni nani ambaye atakuwa yupo nyuma ya hili swala?”

“Sifahamu, ila unacho takiwa wew eni kuelekea katika nchi hiyo. Utahakikisha kwamba watoto wote wa kike wanakuwa salama sawa”

“Sawa”

Kwa kutumia kadi laura akafungua mlango wa chumba kimoja. Kitendo cha kukanyaga ardhi ya chumba hichi. Taa zote zikawaka, chumba hichi kimejaa silaha za kila aina jambo lililo nifanya nijawe na mshangoa mkubwa sana huku moyoni mwangu nikihisi furaha kubwa san aya kukuatan na silaha za namna hii.

“Chagua silana yoyoyote unayo ihitaji, na nguo zako zipo katika hatua ya mwisho kuandaliwa. Kumbuka endapo utakwenda kinyume nami basi utakufa”

“Nimekuelewa Laura na sinto penda kila muda uwe una nihusia katika hilo, natambua jukumu langu”

“Nafurahi kusikia hivyo”

Nikaendelea kuzunguka zunguka katika chumba hichi huku kila bunduki ninayo ihitaji ninaichukua kwa ajili ya kazi yangu ninayo kwenda kuifanya. Nilipo hakikisha nimachagua bunduki mbili pamoja na bastola mbili ninazo zipenda, nikamfwata Laura sehemu alipo simama.

“Tayari”

Laura akanikabidhi simu pamoja na kifaa cha mawasiliano ambacho mtu unakiingiza ndani ya sikio na baadhi ya watu wengine hawawezi kufahamu kama una mawasiliano.

“Hichi kikundi kimekuja miaka ya hivi karibuni. Kilisambaratishwa miaka kadhaa ya nyuma na kupelekea kiongozi wao kuweza kufariki dunia. Hivyo unatakiwa kuma makini sana kwenye hii kazi ambayo unaiendea, kwani kwa sasa wamejipanga kwa kila aina ya upambanaji.”

“Simu hiyo itakuwa inakupa muongozo wa ramani ni wapi unatakiwa kwenda na nini unapaswa kwenda kufanya. Hakikisha kwamba haipotezi”

Akaingia msichana mmoja akiwa ameshika mavazi meuzi, akawayawe juu ya meza kisha akaindoka.

“Nguo zako zipo tayari unaweza kuvua hizo nguo zako za kipolisi na kuvaa hizi”

“Ngoja kwanza”

Nilizungumza huku nikimuangalia Laura.

“Kabla sijakwenda kuifanya kazi hii nina ombi”

“Ombi gani?”

“Ninahitaji kumkamata Dany. Dany ni mtu ambaye ameniulia baba yangu kikatili. Kama utashindwa kufnaya hivyo naomba nikurudi uniambie hata ni eneo gani basi ninaweza kumpata ili niweze kumshuhulikia”

“Sawa ombi lako limepita. Vaa nguo zako safari inaanza sasa hivi”

Laura akatoka chumbani humu na kuniacha mimi peke yangu. Nikavua nguo zangu zote na kubaki kama nilivyo zaliwa. Nikaanza kuchambua nguo moja baada ya nyingine, nilipo zikagua vizuri, nikaanza kuvaa suruali, nikafwatia tisheti kisha shati zito kiasi. Nikavaa jaketi maalumu la kuzuia risasi(bullet proof). Nikavaa buti hizi, kisha bastola zangu nilizo zichagua pamoja na magazine, nikaanza kuzichomeka katika kiuno huku bastola nyingine nikiichomeka katika mguu wangu wa kulia.

Nikaitazama simu hii jinsi inavyo nipatia maelekezo ya wapi nielekee. Nikatoka humu chumbani na kukutana na Laura mlangoni.

“Umependeza”

“Asante”

“Watoto hao ukisha maliza kuwaokoa, hakikisha unawasiliana nasi na tutakueleza ni wapi kwa kuwapelekea. Watoto wapo kwenye bandari bubu katika fukwe za Mogadishu Somalia. Bandari hiyo inamilikiwa na magaidi wa kikosi hicho cha Somali. Rubani wetu atakuacha mita elfu mbili kutoka katika sehemu ya bandari hiyo”

“Samahani kwanza. Umesema mita elfu mbili nchi kavu au ndani ya bahari?”

“Ndani ya bahari”

“Mmmmm”

“Usigune, hatuwezi kuruhusu helicopter yetu kuingia katika usawa wa bahari hiyo kwa maana wataidungua na mwisho usalama wa watoto wale wa kike utakuwa ni mdogo sana.”

“Nimekuelewa”

“Utapewa vifaa vya kukusaidia ukiwa baharini, kazi ni kwako. Hakikisha hakuna mtoto hata mmoja ambaye ana udhurika katika hiyo kazi. Tunakutegemea Randy”

“Sawa”

Nikaongozana na Laura hadi kwenye uwanja wa helicopter na kukuta helicopter moja ikiwa inatusubiria.

“Hii kampuni yako inaitwaje?”

Niliuliza kwa sauti ya juu sana huku nikimtazama Laura usoni mwake, kwani kelele za mlio huu wa helicopter ndio zimenilazimu kuzungumza kwa sauti ya juu sana.

“Nitakuambia ukirudi”

Laura naye alizungumza kwa sauti ya juu huku akinitazama, nikaingia ndani ya helicopter hii nikamkuta mwanaume mmoja mweye asili ya kizungu, huku rubani wa hii helicopter akiwa naye ni mzungu. Taratibu milango ikafungwa, na helicopter hii ikaanza kuondoka katika eneo hili.

“Tuna masaa mnne kufika katika fukwe za Somalia”

Mzungu huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu

“Sawa sawa, kwani mimi na wewe tupo kwenye kazi hii?”

“Hapana, kazi yangu ni kuhakikisha kwamba umefika katika sehemu husika”

Mzungu huyu akanitolea begi la parachute.

“Utaruka ukiwa hewani”

“Sawa”

Safari ikazidi kusonge mbele huku masaa nayo yakizidi kuyoyoma. Hadi inatimia majira ya saa tatu usiku, tukafika katika ukanda wa bahari katika nchi hii ya Somalia. Nikavaa mtungi wa gesi kisha nikavaa begi la parachute.

“Ni muda wa kuruka sasa, tumia saa hii”

Mzungu huyu aliye jitambulisha kwa jina la Potter alinipatia saa ya mkononi, nikaivaa kisha akafungua mlango wa helicopter hii.

“Miwani hii utaitumia chini ya bahari”

“Sawa sawa”

Katika eneo hili lote la bahari kuna giza kubwa sana hadi woga ukanitawala kama binadamu wa kawaida. Potter akaanza kunihesabia kuanzia moja hadi tatu, nikajirusha na kuanza kuelea angani, nikiwa muta kadhaa kutokea chini nikafungua begi hili la parachute na kuanza kuelea elea angani. Taratibu nikatanguliza miguu yangu kuingia baharini. Nikavua begi hili la parachute, nikaitoa simu yangu mfukoni kwa bahati nzuri simu hii haiingia maji.

‘Ehee Mungu wangu ninaomba unisaidie’

Nilizunngumza kimoyo moyo, huku nikiangaza kila sehemu katika eneo hili la bahari. Nikaitazama dira inayo nionyesha kwenye simu hii, nikaiweka miwani hii taratibu, kisha nikauweka mtungi huu wa gesi vizuri mgongoni mwangu, na kuvaa kifaa maalumu cha kupumulia.

Nikazama chini ya maji kwa mita mia moja kisha nikaanza kusonga mbele kuelekea ilipo bandari hii ya maharamia. Dira hii iliyopo kwenye simu ikazidi kunipeleka mbele hadi nikafika eneo la karibu kasisa katika kambi hii. Saa yangu ya mkononi inanionyesha hivi sasa ni saa tano kasoro usiku. Nikairudisha mfukoni simu mfukoni kwani tayari nimesha ona eneo la bandari ilipo.

Nikaogelea kwa umakini mkubwa hadi ilipo bandari hii, nikajitokeza taratibu na kuanza kuchunguza eneo la bandari hii.

Shuhuli zinazo endelea hapa zionaonyesha hivi hivi ni za magendo. Ulinzi ni mkali sana, nikiwa katika eneo hili nikaona gari nne aina ya Range Rover zikisimama, wakashuka watu karibia nane walio valia suti nyeusi kisha watu hao wakasimama kwenye Range Rover moja nyeusi na mlango ukafunguliwa.

Macho yakanitoka na kujawa na mshangao mkubwa sana mara baada ya kumuona mama yangu mzazi akishuka kwenye gari hilo. Akaongozana na walinzi hao huku akiwa ameambatana na mlinzi wak ewa kika amabaye kwenye maisha yangu simpendi kabisa.

“Mama amakuja kufanya nini huku?”

Nilijiuliza swali ambalo kwa namna moja ama nyingine nimejikuta nikikosa jibu. Mama akangia kwenye moja ya jumba bovu bovu lililopa hapa bandarini. Kwa umakini mkubwa sana nikatoka kwenye maji haya, nikanyanta hadi kwenye moja ya matairi mengi makubwa yaliyo pangwa kando kando ya fukwe hii. Nikavua mtungi wa gesi mgongoni mwangu na kuuficha kwenye moja ya tairi kubwa. Nikatoa bastola yangu pamoja na kiwambo cha kuzia sauti ya risasi pale inapo toka.

“Hei?”

Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikiwa nimeweka kidole changu cha kiganja cha kulia kwenye sikoo langu nikijaribu kuwasiliana na Laura, sikuweza kusikia kitu chochote kwani kifaa hicho kimeingia maji mengi na kuharibika.

“Shiti, nikaitoa simu yangu mfukoni na kutazama rafami ya eneo hili ninayo iona kwa juu kwa kutumia satelaite. Jengo ambalo watoto hawa wamefungiwa ninaliona na lipo mita chache sana kutoka hapa nilipo, ila kwa namna moja ama nyingine nimejawa na shahuku kubwa sana ya kufahamu ni kwa nini mama yangu amefika katika eneo hili.

Nikaanza kutembea kwa tahadhari hadi kwenye jemgo hilo, ambalo katika mlango wake kuna walinzi wanne wenye bunduki. Nikachungulia kwenye moja ya dirisha lenye nondo, nikawaona watoto hao wa kike wakiwa wamelala sakafuni huku wengine wakilia chini chichi.

“Nitawarudia”

Nilizungumza huku nikianza kutembea kwa kunyanta nikielekea katika jengo ambalo ameingia mama yangu mzazi kwa maana ninahitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kimemfanya aje katika eneo hili.

“Hei”

Nilisikia sauti ya mwanaume nyuma yangu. Nikasimama kidogo huku nikijaribu kusikilizia ni kitu gani atakizungumza.

“Wewe ni nani?”

Aliniuliza kwa lafudhi ya Kisomali.

“Nipo na bosi wangu madam Yemi”

Ilibidi kuongopea kwa maana walinzi wote wa mama yangu ninafahamu maneno yao wanayo yatumia hususani wakiwa katika ziara nje ya nchi ya Nigeria.

“Huku umefwata nini?”

Nimekuja kuimarisha ulinzi kufahamu kama boso wangu yupo salama.”

Nilizungumza huku nikiwa nimempa mgongo mtu huyu. Nikaona nikiendelea kuojiana naye nita nitapoteza muda wangu, kwa haraka nikageuka nyuma kwa kasi na kufyatua risasi mbili ambazo zote zikampata mpiganaji huyu wa kundi la Al-Shabab.

Nikausogelea mwili wake, nikaanza kumvuta hadi sehemu yenye giza kidogo kisha nikaendelea na upelelezi wangu. Nikafanikiwa kufika katika jengo alipo mama yangu, japo kuna ulinzi mkali, ila kwa mbinu za kijeshi nilizo funzwa, zimeniwezesha kuingia katika jengo hili pasipo watu kuweza kunistukia.

Nikanyanta hadi kwenye moja ya ukuta na kuanza kusikiliza mazungumzo yanayo endelea huku sauti ya mama yangu nikiwa ninaisikia vizuri sana.

“Hii ni biashara ni kwaajili ya nchi yangu”

“Tunatambua, ila hivi karibuni tuna imani kwamba boksi tutakuletea Madam”

“FanytUMEKUELEWA MKUU”

eni munavyo fanya, ila ndani ya siku mbili hizi nahitaji hilo boksi na endapo mutakwenda kinyume na biashara yangu, nitahakikisha kwamba ninawaua. Mumenielewa?”

“Tumekuelewa madam”

“Na kitu kingine kabla sijasahau. Endapo hawa hawato toa boksi jeusi ndani ya siku mbili hizi. Waueni watoto wote na hakikisheni kwamba dunia inafahamu hilo sawa”

“Sawa mkuu”

Nikiwa katika hali ya kusikiliza mahojiano haya. Gafla kitu kigumu chanye muundo wa bastola ukasogoni mwangu, jambo lililo nistua sana. Nikajaribu kushusha mikono yangu kiunoni ila nikawahiwa, kuchomolewa bastola zangu zote. Watu wanne wenye bundiki mikonomni mwao wakaniamrisha kutembea kueleeka katik eneo wanalo hitaji wao.

“Kuna mvamizi”

Mmoja wao alizungumza huku akiwa ametembea. Nikafikishwa kwneye kwenye ofisi ambayo mazungumzo yanafanyika. Mama akastuka sana kuniona nikiwa nimetekwa nyara, sikuhitaji kuonyesha moyo wa kustuka sana kwa maana nilisha tambua uwepo wa mama katika eneo hili.

“Mkuu huyu tumemkuta katika eneo la pili la chumba hichi akifwatilia mazungumzo yenu”

Mwanaume aliye valia kanzu akasimama kwenye kiti alicho kikalia na tararibu akaanza kunifwata eneo hili nilipo pigishwa magoti huku mitutu ya bunduki zaidi ya mitano ikiwa imeelekezewa kwangu. Mama na mlinzi wake wa kike wote macho yao yapo kwangu.

“Ni nani aliye kuagiza kuingia katika ngome hii?”

Mwanaume huyu alizungumza huku akikabidhiwa kisu kikali na mmoja wapo wa watu wake. Mama akanikazia macho huku akinitazama kwa umakini. Ubaya sura yangu inafanana sana na sura ya mama yangu, na mara nyingi watu wengi wana dai nimefanan na mama yangu. Mwanaume huyu akanitazama mimi kisha akanitazama na mimi.

“Mkuu unamfahamu huyu mtu?”

Mama akaitazama kwa umakini sana, taratibu akasimama na kutembea kwa utaratibu hadi sehemu nilipo pigishwa magoti.

“Simfahamu, hakikisheni kwamba munamuua na imarisheni ulinzi katika bandari nzima. Kama huyu ameweza kuingia humu ndani na kusikiliza tulicho kiongea basi kuna wengine watakuja sawa.”

Mama baada ya kuzungumza maneno hayo akatoka chumbani humu na taratibu mwanaume huyu akakiweka kisu chake shingoni mwangu, tayari kwa kunichinja kama kuku.



Akili yangu ikafanya kazi kwa haraka sana kama computer, sikujali kuelekezewa mitutu hii ya bunduki kwani kama ni kifo basi tayari kipo usoni mwangu.Nikampiga kisukusuku huyu mkuu wao, akayumba kidogo, nikapata upenyo wa kuukamata mkono wenye kisu chake. Nikampiga mtama na kwa haraka nikamuhi shingo yake na kuipiga kabari moja kali sana ambayo nina imani hawezi kuitoa kabisa. Kitendo cha kumuweka mwanaume huyu katika mikono yangu hakikumaliza hata dakika moja, jambo lililo sababisha walinzi wake kubaki wakiwa wamebabaika sana. Njee nilisikia milio ya magari ikiondoka eneo hili na nikatambua kabisa mama yangu ameondoka eneo hili.

“Yoyote atakaye fyatua hata risasi moja kwangu, kiongozi wenu nitamuu”

Nilizungumza huku nikinyanyuka hapa chini na mwanaume huyu huku nikiwa nimemkaba kisawa sawa shingo yake huku nikiwa nyuma yake. Kutokana ni mkuu wao hapakuwa na mtu hata mmoja aliye weza kufyatua risaisi. Kutoka nje ya chumba hichi hichi ni hatari kwa upande wangu kwani wanaweza kunivamia na kuniua kiurahisi sana.

“Nirudishieni bastola zangu”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwatazama kwenye nyuso zao. Nikamkaba kwa nguvu mkuu wao shingo yake jambo lililo wafanya wanikabithi bastola zangu.

“Wekeni sailaha zenu chini?”

Nilitoa amri hiyo na wakaweka bunduki zao chini. Kwa ishara nikawaamrisha waweze kutoka ndani humu, pasipo kupinga wakaanza kutoka mmoja baada ya mwengine.

“Hahaaa huwezi kutoka humu ndani na kambi hii imezingirwa kila eneo”

Mwanaume huyu alizungumza kwa kejeli huku akinitazama usoni mwangu.

“Eti eheee?”

“Ndio”

Nikampiga na kitako cha bastola nyuma ya kichwa chake, akaanguka chini na kupoteza fahamu. Nikaufunga mlango wa chumba hichi kwa ndani, bunduki za watu wake zote nikazikushanya sehemu, nikasogea hadi kwenye moja ya dirisha, nikachungulia nje na kweli jengo hili limezingirwa kila pande na kwa kweli siwezi kutoka nje ya eneo hili nikiwa hai. Nikaanza kuchomoa magazine moja baada ya nyingine ya kila bunduki hizi aina ya SMG huku nyingine zikiwa ni AK47. Baadhi ya bunduki zina risasi nusu nusu. Nikaibinua meza hii na kuiweka katika dirisa hili la nondo. Nikachukua moja bunduki, nikaikoki vizuri, nikajibanza nyuma ya meza hii na kuanza kuwashambulia wanajeshi wote walio simaam usawa wa dirisha hili. Shambulizi langu hili la kustukiza, likazidi kuwapagawisha wapiganaji wa kundi hili la Al-Shabab.

Kitu kinacho wafanya washindwe kunishambulia ni kutokana na bosi wao kuwemo ndani humu. Udhaifu wao ukazidi kunipa ujasiri wa kuwasambulia. Bunduki hii ikaisha risasi, nikachukua bunduki nyingine na kuendelea kuwashambulia.

Uvumilivu kwa upande wao nao ukaanza kuwashinda. Wakaanza kushambulia risasi nyingi sana hadi mwenyewe nikaamua kutulia huku nikiwa nimejibanza kwenye ukuta wa dirisha hili. Mlango nao ukaanza kujaa matundu ya risasi, ikionyesha kwamba wamedhamiria kuingia humu ndani.

“Ehee Mungu wangu”

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama mkuu wao aliye lala chini kifudi fudi. Nikatambaa hadi sehemu alipo mkuu wao na nikaanza kumvuta hadi kwenye moja ya kona ya chumba hichi, sehemu ambayo sio rahisi kwa risasi kutupata. Nikamkalisha na kuanza kumzaba vibao vya usoni ili aweze kuzinduka.

“EHHHEEEEEE”

Alizinduka huku akiweweseka sana. Nikamtuliza kwa kumpiga kichwa cha puani mwake na kumsababisha atoe ukelele mkali sana wa maumivu. Ukelele huo ukasababisha kasi ya kushambuliwa.

“Ninakuweka hapo mlangoni watu wako wakuue”

Nilizungumza huku nikianza kumburuza.

“Usiniburuzee, usiniburuzee”

Alizungumza kwa kulalama. Nikamkaba shati lake na kumnyanyua juu huku nikimkazia macho yake.

“Waambie wat……”

Kabla sijamalizia sentensi yangu, nikasikia mlipuko mkubwa sana nje ya jengo hili. Milipuko hiyo ya mabomu ikazidi kuongezeka na kunifanya nimpige mtamza mwanaume huyu na kumuangusha chini, nikachungulia dirisani na nikashuhudia helicopter za kijeshi zikiendelea kufanya mashambulizi dhidi ya watu wapiganaji hawa. Mashambulizi yakazidi kupamba moto jambo ambalo, likanifanya nipate matumaini ya kuweza kutoka katika eneo ili salama.

Jukumu langu nililo nalo hivi sasa ni kuhakikisha kwamba nina muweka chini ya ulinzi mwanaume huyu ambaye ndio mkuu wao. Mashumbulizi huko nje yakazidi kupamba moto, milio ya risasi ikazidi kurindika kila mahala katika eneo hilo.

“Nyanyuka”

Nilimuamrisha mwanaume huyu na akatii amri yangu pasipo kupinga chochoe, niakfungua mlango wa chumba hichi, nikamtanguliza huku akwia amenyoosha mikono yake juu. Nikakutana na wanajeshi wa Kimarekani wakiwa na nguo zao. Wakatuamrisha wote kunyoosha mikono juu huu na nikatii amri huku bundiki zangu nikiitupa pembeni. Wakatuamrisha kulala chini, bila ya kipingamizi nikatii, wakatufunga pingu mikono yetu kwa nyuma na wakenda kutukusanya na kundi kubwa la wapiganaji walio kamatwa.

Nikawashuhudia watoto wa kike wakiwa wanapatiwa huduma ya kwanza na wanajeshi hawa mchanganyiko ambao nina imani kwamba wameungana kuhakikisha kwamba wana wakomboa watoto hawa wa kike. Wapiganaji hawa wote nilio wekwa nao chini ya ulinzi wakanikazia macho huku wakionekana kujawa na hasira na mimi.

“Lazima tutukuua”

Mkuu wao aliye kaa karibu nami aliniambia kwa sauti ya chini, jambo lililo nifanya nimpige kichwa cha sikioni mwake na akaanguka chini huku akilia kwa uchungu sana. Wanajeshi wawili wa Kijerumani wakanisogelea na kunitoa katika eneo hili na kunitenga na watu wapiganaji hawa.

“Mimi sio miongoni mwao, nilikuja hapa kuwaokoa hawa watoto”

Nilizungumza kwa kujiamini ila hapakuwa na mwanajeshi hata mmoja ambaye aliweza kunisikiliza. Baada ya kama nusu saa hivi meli kubwa ya kijeshi ikapaki pembezoni mwa bandari hii. Wapiganaji hawa wa Al-Shabab wakaanza kumarishwa mmoja baada ya mwengine kuelekea katika meli hiyo kubwa. Walipo kwisha waingiza wote nami pia nikaingizwa katika meli hii kubwa na nikafungiwa katika chumba kimoja chenye giza ambacho kipo chini kabisa kabisa ya meli hii.

Nikaanza kuhisi mtetemesho kwenye mkono wangu wa kushoto ambao nimevaa saa. Nikaitazama saa yangu na kuona kuna simu inayo ingia. Nikaitazama saa yangu ambayo hapo awali sikuweza kufahamu kwamba ina mfumo wa simu. Nikaipoke simu hii na nikamuona Laura.

“Randy unanipata?”

“Ndio ninakupata”

“Mimi sikuoni, ila niambie ni kitu gani ambacho kinaendelea”

“Jesi la Wamarekani na wajerumani wamevamia katika ili eneo na ninavyo kuambia hivi sasa nipo katika chumba

kidogo sana chini ya meli hii”

“Mungu wangu, unataka kuniambia kwama umekamatwa?”

“Ndio na sio mimi peke yangu, ila nimekamatwa pamoja na kundi la wa hawa magaidi wa Al-Shabab”

“Meli hiyo imekaaje?”

“Kivipi?”

“Yaani kwa nje?”

“Ni meli kubwa snaa na bado ipo kwenye fukwe hii”

“Ahaa sawa”

“Sawa nini. Inabidi muweze kuniokoa mikononi mwao”

“Hatuwezi kufanya hivyo, samahani sana Randy makubaliano yetu hayakuwa hayo.”

“Laura, Laura”

Simu ikakata, na saa ya mkononi taratibu ikaanza kutoa moshi ambao ukanifanya niivue na kuitupa pembeni. Matumaini ya msaada kutoka kwa Laura na watu wake yakanipotea, nikajishika katika shemeu ambayo walinichomeka kifaa kidogo cha GPRS, kwa namna moja ama nyingine siwezi kukitoa. Masaa yakazidi kusonga mbele, sikuweza kufahamu muda huu ni saa ngapi ila jinsi masaa yanavyo zidi kuwemo ndani humu ndivyo jinsi nilivyo gundua kwamba nimekaa muda mrefu humu ndani.

Kidirisha kidogo kilichopo hapa mlangoni kikafunguliwa, nikaingizwa sahani yenye maandazi na kidirisha hicho kikafungwa. Taa yenye mwanga hafifu sana ikawashwa ndani humu na ikaniwezesha kuweza kuona kilichopo kwenye sahani hiii. Taratibu nikaanza kula maandazi haya manne kwa kufujo sana, kwani njaa niliyo nayo ni kali sana. Nikamaliza maandazi haya na kiu ikaanza kunisumbua kooni mwangu. Baada ya masaa kama matatu hivi mlango huu ukafunguliwa, wanajeshi watatu wakaniamrisha niweze kutoka nje ya chumba hichi.

Nikatii amri waliyo niambia na taratibu nikatoka ndani ya chumba hichi na mmoja wao akaanza kuongoza mbele. Tukapandisha juu kabisa katika meli hii, nikakuta wapiganaji saba wa Al-Shabab wakiwa wamepangwa mstari mmoja huku vichwani mwao wakiwa wamevalishwa vigunia vyeusi.

Wanajeshi saba wa Kimarekani wakajipanga mstari mmoja, mkuu wao akawaruhusu wanajeshi wake wote na wakapigwa risasi wote saba na wakaanguka chini jambo lililo nifanya nijawe na woga mwingi sana.

“Ni nani aliye kuagiza”

Mkuu huyu wa jeshi hili la Wamarekania lizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama usoni mwake. Kosa kubwa nililo lifanya ni kuto kufahamu kampuni ya Laura linaitwaje.

“Mvalisheni”

“Ngoja ngoja”

Nilizungumza ili kuepeuka kuvalishwa kigunia hicho cheusi kwani hatua ambayo itafwatia ni kupigwa risasi hadi kufa.

“Niliagizwa kuja kuwakomboa hawa watoto. Nimetokea nchini Tanzania.”

“Wewe ni mpelelezi?”

“Hapana”

“Sasa utautumwaje kuja kuwakomboa ikiwa si mpelelezi au upo kwenye kitengo gani cha ulinzi ndani ya nchi ya Tanzania?”

“Sipo katika kitengo chochote, ila mkuu wangu anaitwa Laura Livna Livba”

Kulitaja jina hilo likawastua sana wanajeshi hawa. Mmoja wao akanisogelea na kwa haraka akaanza kunipishia kifaa maalumu ambayo kama mtu ana kifaa chochote cha ndani ya mwili wake basi lazima kitaoneonekana. Alipo kifikisha eneo la shingoni mwangu, kweli kifaa hicho kikaanza kutoa mlio wa ishara ya hatari. Kwa haraka nikapigishwa magoti chini. Mwanajeshi mmojaa kaja na sindano yenye dawa, akanichoma shingoni mwangu sindano hiyo. Mmoja wao akanichana kidogo kwa kutumia kisu chenye ncha kali sana katika eneo la shingoni mwangu. Akanitoa kifaa hicho kinacho waka taa nyekundu, kitendo cha kukirusha kifaa hicho baharini kikalipuka na kutufanya sote tujawe na mshangao. Wakanipa huduma ya kwanza, nikaondolea katika eneo hili na kuingizwa kwenye chumba cha mahojiano. Baada ya muda kidogo akaingia mkuu ambaye alikuwa akinihoji maswali kadhaa.

“Unaitwa nani?”

“Randy”

“Randy nani?”

“Randy Donald Bush”

Nilijitambulisha kwa kutumia jina la baba yangu halisi. Mwanajeshi huyu akanitazama usoni mwangu huku akikaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu.

“Donald Bush?”

“Ndio”

“Unamfahamu huyo Laura sehemu alipo?”

“Ndio yupo nchini Tanzania”

“Tanzania sehemu gani?”

“Kwenye jiji moja linaitwa Dar es Salaam.”

“Umejipatia wapi mafunzo yako ya kijeshi?”

Swali hili likanifanya nikae kimya huku nikimtazama mkuu huyu wa jeshi la Marekani.

“Nimekuuliza?”

“Mimi sina mafunzo ya kijeshi, nilikuwa ninapenda kuwa mwanajeshi tena mpelekezi. Nilijifunza mafunzo ya kupambana katika baadhi ya majudo.”

“Macho yako yanadanganya unacho kizungumza. Ni wapi ulipo jifunza mafunzo yako ya kijeshi?”

Mkuu huyu alizungumza kwa kufoka sana hadi nikapata wasiwasi. Nikakumbuka jinsi nilivyo ingia kwenye kundi la Al-quida. Nikakumbuka jinsi nilivyo weza kupata mafunzo ambayo kwa namna moja ama nyingine yanakuimarisha mtu kuwa msiri na mkakamavu. Mkuu huyu akachomoa bastola kiunoni mwake na kuniwekea kichwani mwangu.

“Nilcho kueleza ndio kitu cha ukweli, siwezi kuzungumza zaidi ya hilo jambo”

Mkuu huyu akanipiga ngumi ya tumbo na kujikuta nikijikunja sana huku nikisikilizia maumivu hayo makali sana.

“Niambie ni wapi ulipo jifunza?”

Nikatamani kusema ni kundi la Al-quida ila wanaweza kunitumia mimi kwa ajili ya kulipata kundi hilo ambalo kwa sasa wana nisaka sana na endapo watakamata basi wataniua. Mkuu huyu akaniongeza kunipiga ngumi nyingine ya tumbo hadi nikaanguka chini. Gafla mtikisiko mkubwa ukatokea kwenye hii meli jambo lililo mfanya mkuu wao huyu kuanguka chini, nikaiwahi bastola yake na kumpiga risasi mbili za miguuni. Hali ya meli hii ikaazidi kuyumba huku mtikisiko huu wa pili ukiambatana na mlipuko mkubwa sana.

Milio ya risasi ikaanza kusikika kila kona ya eneo hili jambo lililo nifa nafasi ya kaunza kuelekea kwenye mlango wa kutoka katika chumba hichi, ila kabla sijaufikia mlango huo, mtikisiko mwengine mkubwa ukatokea na kusababisha kurushwa vibaya na kinajibamiza kichwa changu kwenye moja ya meza ya chuma iliyomo humu ndani na kujikuta macho yangu yakitawaliwa na giza kubwa sana na sikuweza kufahamu ni kitu gani kinacho endelea ndani ya meli hii.



Kukosa kwangu pumzi kukaanza kunifanya nianze kuhangaika ndani ya maji haya. Nikajaribu kufumbua macho yangu ila hali ya mwanga hafifu ulio ambatana na giza, ukazifanya fahamu zangu kufanya kazi haraka sana. Nikatambua kwamba nipo ndani ya maji mengi tane ndani ya chumba nilicho kuwa nipo na mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa Marekani. Nikaanza kuangaza angaza kila sehemu ya chumba hichi na nikafanikiwa kuona mlango wa kutoka. Taratibu nikaanzaaka kuogelea hadi mlangoni apa, nikatoka na kuanza kutafuta sehemu ya kutokea, japo niweze kupata pumzi tu. Nikiwa katika harakati za kuokoa maisha yangu, nikashustuka sana kukutana na maiti nyingi za wanajeshi wa Kimarekani zikiwa zimejeruhiwa vibaya sana.

‘Imevamiwa nini?’

Nilijiuliza swali ambalo kwa sasa siwezi kupata jibu. Nikaendelea kujikaza na kutafuta sehemu ya kutokea, kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuona sehemu ya kutoka katika meli hii. Nikaogelea na kujitokeza katika usawa wa bahari huku nikihema sana, kwnai kukaa ndani ya maji kwa muda kidogo ni shuhuli pevu sana. Ukubwa wa meli hii nilio kuwa ninauona kwa sasa hipo hivyo. Vilivyopo hivi sasa ni vipande vipande vya meli hii ambayo baadhi vinaelea kwenye maji uku vingine vikiwa vinawaka moto.

Miili mingine ya watu bado inaelea elea juu ya maji, huku ni watu wachache sana wanao jitahidi kuogelea ili kuokoa maisha yao.

“Ohoo Mungu wangu, nini kilicho tokea?”

Nilijiuliza maswali mengi huku nikiendelea kutazama eneo hili. Ubaya tupo katikati ya bahari na sijui ni wapi ninaweza kuelekea ili kujiokoa ndani ya maji haya. Nikafanikiwa kupata boya moja linalo elea elea juu ya maji. Taratibu nikalivaa na likanipa uwezo wa kuelea juu ya maji pasipo kuzama.

“Ni…s…a…i…di…e”

Nilisikia sauti ya kike inayo katika katika. Nikageuka nyuma yangu na kumuona dada mmoja wa Kimarekani akiwa katika hali mbaya ya kupoteza maisha. Kutokana yupo mita kadhaa kutoka hapa nilipo, sikuona haja ya kumuacha ateketee. Nikaanza kuogelea kwa kasi hadi sehemu alipo. Mwili wake umelegea sana na amekunywa maji mengi sana. Nilicho kifanya ni kimvalisha boya nililo kuwa nimelivaa. Kisha nikaanza kumpa huduma ya kwanza ya kumpulizia pumzi mdomoni mwake. Dada huyu akatapika maji mengi aliyo kunywa na kidogo sura yake ikaanza kuchangamka.

“Asante”

Dada huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Karibu”

Nilizungumza huku nikiendelea kutazama ni kitu gani ninaweza kufanya ili niweze kuondoka katika eneo hili.

“Wewe si mwanajeshi?”

Nilimuuliza dada huyu?”

“Ndio, ila ni daktari wa kijeshi”

“Sawa, unakumbuka ni kitu gani kilicho tokea katika meli hii?”

“Tumesambuliwa kwa mabomu?”

“Na nani?”

“Sifahamu, ila yanaonekana yametoka masafa marefu sana”

“Katika meli yenu hakuna boti za dharura?”

“Zipo ila sidhani kama utaziona kwa maana meli imesha zama kwa kina kirefu sasa”

Nikatazama katika hili eneo, ninacho kiona ni miili ya watu walio fariki dunia kuelea elea juu ya maji.

“Nahiji tufanye kitu”

“Kitu gani?”

“Nahitaji kutafuta boti ya kuondoka katika hili eneo”

“Sidhani kama utapata hilo boti kaka yangu”

“Nitapata, meli ilitembea kwa umbali gani kutika Mogadishu hadi hapa?”

“Masaa arobaini na nane?”

“Siku mbili?”

“Ndio”

Nikashusha pumzi huku nikivumilia baridi kali inayo endelea kututesa miguu yetu. Nikisema kwamba niingie chini ya bahari ili nikatazame ni wapi ninaweza kupata bozi za dharura, sinto weza kufanikiwa kwani sasa hivi ni usiku sana na giza litachangia katika kushindwa kwangu.

“Nitaingia asubuhi kukipambazuka”

“Sawa”

“Ninaitwa Randy”

“Nashukuru kwa kukufahamu ninaitwa dokta Sara”

“Nashukuru kukufahamu dokta Sara”

“Hata mimi, nashukuru kwa kuniokoa maisha yangu kwani nilikuwa nipo kwenye hatua za mwisho za maisha yangu”

“Ni jukumu langu”

Tukatazamana kwa sekunde kadhaa na Sara kisha akatabasamu na kuangalia sehemu nyingine. Tukaendelea kuelea katika eneo hili na hapakuwa na msaada wa aina yoyote ile hadi kunapambazuka. Mwanga wa jua ukatupa matumaini mengine mapya ya kuokoa maisha yetu. Kusema kweli shambulizi hili limeharibu vitu vingi sana. Maisha ya watu wengi sana yamepotea.

“Naomba unisubirie hapa”

Nilimuambia nesi Sara huku nikimtazama usoni mwake.

“Nahitaji kuja na wewe”

“Hapana huna nguvu za kutosha”

“Ninazo Randy, tafadhali ninakuomba nikusaidie”

Nesi Sara alizungumza huku akivua boya nililo kuwa nimemkabidhi, akavua shati lake la kijeshi na akabakiwa na siridia pekee kifuani mwake.

“Utaweza kweli?”

“Ndio nitaweza Randy na ninafahamu muundo wa meli yetu, nikiona mabaki yake basi ninaweza kuelewa ni wapi zilipo boti”

“Sawa”

Tukavuta pumzi ya kutosha, kisha taratibu tukaanza kusama ndani ya maji, kutokana kuna mwanga wa jua kali, tunaweza kuona kila kitu ndani ya maji haya. Dokta Sara kwa ishara ya mkono akaanza kunionyesha sehemu ambayo unatakiwa kwenda. Japo ni chini sana ila ndipo ilipo boti. Tukazidi kuzama hadi kwenye upande mmoja wa meli ambo nao umevunjika. Tukafungua kamba za boti ndogo iliyo fungwa pembeni. Taratibu tukaanza kupanda nayo juu. Uzuri wa boti hii ni nyepesi kwani ni boti za kujazwa upepo na mara nyingi hutumiwa na wanajeshi wa majini. Tukafanikiwa kufika nalo juu ya maji, tukaliweka sawa boti hili na dokta Sara akawa wa kwanza kupanda, kisha nami nikapanda. Nikamuona jinsi dokta Sara anavyo tetemeka, taratibu nikavua jaketi langu la kuzuia risasi ambalo sikulivua toka awali, nilipo kamatwa. Nikavua shati langu hili zito nililo livaa nikamkabidhi dokta Sara naminikabakiwa na tisheti nyepesi niliyo ivaa.

“Randy nakuonea huruma utapigwa na baridi kali”

“Usijali, vaa wewe. Unajua wanawake miili yenu ni daifu kuliko sisi wanaume”

“Ni kweli ila tupo katika hali ya hatari”

“Usijali, ikiwa tumefanikiwa kupata hii boti ndogo, nina imani kwamba tunaweza kuondoka eneo hili”

“Ila boti hizi kama ulivyo iona haina mashine kabisa”

“Usijali”

“Ile mifuko ni ya vyakula”

Dokta Sara alizungumza huku akiinyooshea mifuko kadhaa inayo elea elea juu ya maji. Taratibu kwa kutumia mikono tukaanza kuiendesha boto hii ndogo kuelekea ilipo mifuko hiyo. Kardri tulivyo jitahidi kuyakata maji kwa mikono yetu ndivyo jinsi boti hii ilivyo zidi kuongeza kasi hadi tukaifikia mifuko hiyo. Tukaokota mifuko sita na kuiweka katikati yetu. Sara akaanza kutoa vikopo vya vyakula hivi vya kujeshi, akanikabidhi viwili na yeye akachukua viwili na taratibu tukavifungua na kuanza kula.

“Mmmm ni nyama hii ehee?”

Nilimuuliza dokta Sara huku nikiendelea kutafuna nyama hii.

“Ndio ni nyama ya kusaga imechanganywa na viazi”

“Ohoo sawa sawa”

Ndani ya muda mchache nikawa nimemaliza kula vikopo vyote viwili, dokta Sara akaniongeza kikopo kimoja nacho nikakila na kukimaliza na kidogo nikajihisi uafadhali tumboni mwangu. Nikashusha pumzi taratibu huku nikiangaza kila kona ya eneo hili.

“Tuelekee huku”

Nilimuambia dokta Sara huku nikimuonyesha ni wapi tunatakiwa kwenda.

“Kwa nini?”

“Unaona jinsi mfumo wa wawingu unavyo kwenda?”

“Ndio”

“Ukiona maji mengi yanakimbilia katika mfumo mmoja, utambue kika lile eneo, karibu kuna ardi kavu, inaweza kuwa ni kisiwa au pembezoni mwa fukwe yoyote”

“Ahaa sawa”

Tukaokota mifiko mingine ya vyakula, kisha tukaanza safari hii ambayo kwa kweli ni ngumu sana. Tukaendesha boti hii kwa masaa mengi sana, na kila muda tulijikuta tukipumzika kwani mikono yetu inachoka sana. Hadi inafika usiku hatukuweza kuona dalili yoyote ya kukoka kutoka ndani ya bahari hii.

“Tusiendelee na safari yetu. Tupumzike”

Nilimuambie dokta Sara huku nikimtazama usoni mwake. Dokta Sara hakunijibu chochote zaidi ya machozi kuanza kumwagika usoni mwake huku mwili mzima ukimtetemeka kwa baridi, nikahama sehemu yangu niliyo kaa na kumsogelea karibu yake. Nikajilaza pembeni kidogo kisha nikamuegemesha mwili wake kifuani mwangu.

“Najua umekata tamaa Sara, ila Mungu atatusaidia na tutaweza kuondoka katika eneo hili”

“Hatuwezi Randy. Tutafia hapa baharini, ona mikono yangu ilivyo myekundu. Nashindwa kuendelea na safari hii”

“Usijali tutafanikiwa tu Sara, ni bora tusonge mbele kuliko kuendelea kufia hapa”

Nilizungumza kwa sauti ya upole ila iliyo jaa utetemeshi. Dokta Sara hakunijibu chochote zaidi ya kuendelea kulia kwa uchungu sana. Nikafungua kikopo kimoja cha chakula na taratibu nikaanza kumlisha dokta Sara huku nami nikila taratibu taratibu.

“Ngoja”

Nilizungumza huku nikimsogeza dokta Sara pembeni, nikasimama ili niweze kuona eneo la mbali katika bahari hii. Kwa mbali sana nikaona taa nyingi zikiwa zinawaka, jambo lililo nipa matumaini na nguvu mpya kabisa.

“Sara, Sara kule kuna taa”

Nilizungumza huku nikitazama eneo hilo ambalo hapo awali nilimuomba Sara tueleke. Sara naye kwa haraka akasimama na kutazama eneo hilo, kwa haraka tukaa na kuanza kukiongoza kiboti hichi kwa mikono yetu huku tikijitahidi kuyarudisha maji nyuma ili chenyewe kisonge mbele. Tukazidi kukipeleka kwa kasi kadri tunavyo wezaha hadi tukaanza kuziona taa hizo karibu kabisa.

Tukafanikiwa kufika kwenye ufukwe wa mji huu ambao maeneo haya yamechangamka na watu wanaendelea na shuhuli zao kuvua na mambo mengi.

“Ohoo Mungu wangu hapa ni wapi?”

Dokta Sara aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu. Watu hawa ni waafrika kama mimi, ila tatizo hatujui ni wapi tulipo. Nikamuona mzee mmoja akichambua chambua nyavu yake, taratibu nikamfwata, nikamsalimia kwa heshima zote naye akaniitikia kwa upole.

“Samahani, ninaomba kuuliza hapa ni wapi?”

“Hapa ni Unguja, Zanzibar”

“Unguja Zanzinbar?”

“Ndio, kwani wewe ni mgeni hapa?”

“Ndio mzee wangu, mimi ni mgeni”

“Karibu sana Tanzania”

Moyo wangu ukanistuka sana, kwani sehemu ambayo hapo awali nilibambikiwa kesi na nikafanikiwa kuondoka, ndio sehemu ambayo nimerudi tena.

“Vipi mbona uonaonekana kustuka kidogo?”

“Hapana mzee wangu, nashukuru sana”

“Karibu sana”

“Asante na sasa hivi ni saa ngapi?”

“Ni saa nne usiku mwanangu”

“Nashukuru”

Nikarudi sehemu alipo simama dokta Sara.

“Amesemaje?”

“Hapa ni Zanzibar”

“Zanzibar?”

“Ndio, tena ipo Tanzania”

“Ohooo asante Mungu, kama tupo Tanzania ni rahisi kwa sisi kuweza kupata msaada wa kijeshi na tukarudi Marekani”

Dokta Sara alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa ambayo kwa upande wangu, ni tatizo. Kama Laura alishindwa kunisaidia na akahitaji kuniua kwa kulipua kifaa walichokuwa wamekiweka shingoni mwangu, ni lazima wataniua wakigundua kwamba nipo hai.

“Mbona unaonekana kama huna raha?”

“Siwezi kuwa na raha”

“Kwa nini, ikiwa hapa tunaweza kupata msaada wa karibu”

Sikuhitaji kumueleza chochote dokta Sara.

“Randy naomba uniambie kama kuna tatizo lolote mimi nitakusaidia, isitoshe, siwezi kurudi tena kazini. Tunaweza kuwasiliana na baba yangu Marekani, akanitumia pesa ya kutosha, kisha tukajua nini tunafanya”

“Hapa Tanzania?”

“Inaweza ikawa hata nje ya hii nchi. Tafadhali nakuomba twende tukatafute japo simu, tuwasiliane na baba yangu na tumuelezee nini kinacho endelea. Atatusaidia wala usijali”

“Sawa”

Nilikubali kishongo upande kwa maana sina pa kueleeka. Tukaanza kutembea kwenye fukwe hii na tukaona eneo ambalo lina watu wengi sana, huku kukiwa kunapikwa vyakula vya kila aina ambavyo kwa kweli vinanukia vizuri na kutia hamasa ya kumeza mate kwa kuvitamani. Tukasimama kwenye moja ya eneo na macho yangu yakamkodolea dada mmoja ambaye amekaa peke yake kwenye meza huku akila miskaki kadhaa na juisi. Macho ya dada huyu yakagongana na macho yangu, kutokana na hamu ya kula viti hivi nikajikuta nikikaa kwenye kiti cha pembeni yake hadi dokta Sara akashangaa.

“Samahani naweza kupata mmoja?”

Nilizungumza kwa sauti ya upole huku nikimtazama dada huyu.

“Ngoja nikuagize ya kwako”

“Nipo na mwenzangu pale”

Nilizungumza huku nikimuonyesha Sara. Dada huyu akamtazama Sara, kisha akamuita kwa ishara. Dokta Sara akajikataza na kuja eneo hili, akaka katika kiti cha pembeni yangu, dada huyu akamuita muhudumu na akatuagizia tunacho hitaji.

“Samahani unaweza kunisaidia simu yako nikawasiliana na baba yangu”

Dokta Sara alizungumza huku akimtazama dada huyu usoni mwake. Dada huyu akajishauri kwa muda kisha akamkabishi dokta Sara simu yake aina ya Samsung Edge 7.

“Mumetoka wapi?”

Dada huyu alituuliza huku akitukazia macho.

“Kuna meli yetu imeshambuliwa na magaidi, mimi ni dokta katika jeshi la Marekani na huyu ni Randy”

“Mimi ni mwanajeshi pia”

Niliongopea kidogo ili kuficha uhalisia wangu na kuepuka kuulizwa maswali mengi sana.

“Nashukuru, dada hujanijulisha jina lako”

“Naitwa dokta Sara”

“Sawa mimi ninaitwa Mariam. Karibuni sana Zanzibar”

“Tunashukuru”

“Ndio baba”

Tulimtazama Sara usoni mara baada ya kuzungumza hivyo.

“Nipo Zanzibar nchini Tanzania”

“Hata wewe upo Zanzibar, ohoo asante Mungu”

Sara alizungumza kwa furaha na kunifanya nijawe nami na furaha kama ni kuondoka katika nchi hii, basi tutaondoka mapema sana kabla ya maadui wangu hawajakupata.

“Eti hapa ni wapi?”

“Panaitwa Forozani”

“Nipo Forozani”

“Sawa baba, nitakueleza kila kitu”

Dokta Sara akakata simu huku akiwa amejawa na furaha sana.

“Baba anakuja kunichukua baada ya robo saa”

“Sawa, nahisi baba yako atakuwa amekuja mapumzikoni, si unaona eneo hili kuna wazungu wengi”

“Kweli”

Muhudumu akatuletea chakula, tukaanza kula taratibu. Baada ya robo saa, simu ya dada huyu ikaita.

“Nahisi ni namba yako”

Dada huyu alizungumza huku akimkabidhi Sara simu hiyo. Sara akaipokea simu.

“Ndio baba”

“Umeniona ehee?”

“Sawa”

Dokta Sara akakata simu huku akiwa amejawa na furaha sana. Baada ya sekunde kadhaa, Sara akasimama na kumkimbilia baba yake. Macho yangu yakagongana na macho ya mzee huyu.Moyo ukanistuka, mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi snaa, kwani mzee ambaye ni baba yake Sara ndio mume wa Charity na alinifumania na mke wake na agizo alilo litoa kwa walinzi wake siku ile ninalikumbuka vizuri kwani alihiyaji niuliwe na kwenda kutupwa mbali sana na walinzi wake hao.



Nikaanza kurudi nyuma nyuma huku mzee huyo akinikazia macho, walinzi wake. Sikuhitaji kupoteza muda kwa maana kuendelea kukaa hapa ndivyo jinsi ninavyo weza kujiingiza matatizoni. Nikaanza kujichanganya na watu huku nikitazama nyuma kwa macho ya kuiba iba. Nikawaona walinzi wawili wakinifwata kwa mwendo wa haraka. Nikaanza kukimbia huku nao wakinkimbiza kwa kasi, nina imani nitakuwa nimewaachia maswali dokta Sara pamoja Mariam.

Nikakatika mitaani na kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuwapoteza walinzi wa mzee huyu. Mitaa niliyo tokea, ina nyumba nyingi zilizo jipnga katika mistari mizuri. Kila mtu katika eneo hili anaendelea na mambo yake.

‘Nitakwenda wapi Mungu wangu?’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiwa sijui nina anzia wapi nitaanzia. Hadi majira ya susiku sana sikuweza kupaata sehemu ya kulala. Nikapanda kwenye moja ya mti, kati ya miti mingi iliyopo katika kijimsitu hichi, ili niweze kujiegesha na asubuhi nitaweza kujua nini cha kufanya.

Sikuweza kulala usingizi fofofo kutokana na mazingira yenyewe si salama. Nikiwa katika mti huu, gafla nikaona gari nyeusi ikisimama pembezoni mwa miti miti hii mingi. Wakashuka wanaume wawili walio valia makoti makubwa meusi. Mmoja wao akafungua buti ya nyuma ya gari hili na wakamtoa mwana dada mmoja aliye valia kigauni kifupi, huku mikononi mwake wakiwa wamemfunga kamba na mdomoni wamemfunga kitambaa ili asiweze kupiga kelele.

“Ninaanza mimi”

Mwanaume mmoja alizungumza huku akimlaza msichana huyo chini.

“Ahaa mskaji, kumbuka kazi tuliyo pewa bwana”

“Acha kwanza tumle, kisha ndio tunamuua. Wewe mtoto mzuri kama hivi unataka tumuue tu”

“Poa fanya fasta fasta unipishe”

“Haina nona”

Mwanaume huyo alizunguma huku akifungua mkanda wa suruali yake. Nikamtazama dada huyo kusema kweli ni mzuri na ana vutia sana, ila sitambu ni jambo gani ambalo limepelekea hadi kufikia hatua hii ya kutaka kuuwawa. Roho ya huruma ikanitawala, kwani jamaa tayari amesha anza kumvua chupi dada huyo. Nikashusha pumzi, kidogo, kisha kwa haraka nikashuka kwenye mti huu, kishindo changu kikawashua sana wanaume hawa na wakabaki wakiwa wamepatwa na bumbuwazi. Kwa kasi nikawakimbilia katika eneo ambalo wamesimama, wakajaribu kuchomoa visu vyao ili kunishambulia, ila tayari nilsiha anza kuwapa mapigo mazito mazito ambayo yaliwafanya wachanganyikiwe. Kutokana wapo kwa ajili ya kumuua huyu dada, sikuona haja ya kuwaacha wakiwa hai. Nikawavunja shingo zao wote wawili na wakafa. Dada huyu akanitazama huku mwili mzima ukiwa una mtetemeka sana.

“Upo salama”

Nilizungumza huku nikiokota moja ya kisu, nikazikata kamba za mikononi za mwana dada huyu kisha nikamfungua kitamba cha usoni mwake.

“Mimi ni mtu salama kwako sawa”

Dada huyu akatingisha kichwa huku akinitazama usoni mwangu.

“Unaitwa nani?”

“Marieta”

Nikalitazama gari hili walilo jia, aina ya Toyota Alteza. Taratibu nikamnyanyua dada huyu na kukuingiza ndani ya hili gari, nikatazama eneo hili na kukuta fungua ikiwa haipo. Nikashuka na kurudi kwenye miili hii, nikaanza kumpapasa mmoja baada ya mwengine. Wapili kumpapasa, nikafanikiwa kukuta funguo za gari, nikaichukua na kufunga buti ya gari hili. Nikaingia ndani ya gari, ili niweze kumuona vizuri dada huyu nikawasha taa ndogo iliyomo humu ndani.

“Nakuomba tuondoke kaka yangu, hili eneo sio salama”

Dada huyu alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Nikawasha gari na tukaanza kuondoka eneo hili huku nikiwa sifahamu ni wapi tunaelekea. Tulipo fika eneo la mbali kidogo na msitu, nikasimamisha gari pembezoni mwa barabara.

“Mbona usimesimisha gari?”

“Sifahamu ni wapi tuna elekea. Nahitaji kufahamu vizuri, ni kwanini watu wale walitaka kukuua?”

Swali langu likamfanya dada huyu kukaa kimya kwa muda huku akinitazama usoni mwangu.

“Nahitaji jibu?”

“Bosi wangu aliagiza niweze kuuwawa?”

“Bosi wako, kwa nini?”

Dada huyu akashusha pumzi taratibu huku akijifunika vizuri mapaja yake ambayo yapo wazi.

“Niliweza kufahamu siri yake”

“Siri gani?”

“Anauza madawa ya kulevya, hivyo alipo gundua kwamba ninajua, akaona ni vyema aniuae ili nisitoe siri yake kwa polisi”

“Mbona kuvaa kwako, hakuendani na unacho kizugumza?”

Nilizungumza huku nikianza kumtazama Marieta kuanzia juu hadi chini.

“Kaka yangu, mimi ni sekretari wa hoteli hiyo, hapa nilikuwa ninatoka zangu kazini usiku huu, ndio waliniteka nikiwa njiani kabla ya kufika kwangu na wakanileta huku kwa ajili ya kuniua”

Marieta alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Kwako ni wapi?”

“Ni mbali na hapa ila ninaogopa kurudi kwangu, nina imani wakitambua uwepo wangu, wataniua tena kaka yangu”

“Usijali nitakulinda”

Kabla ya kuzima taa hii ya gari nikageuka siti ya nyuma. Nikakuta bahasha kubwa ya kaki, nikaitazama kwa muda, kisha nikaichukua, nikaifungua na kuchungulia ndani. Sikuamini macho yangu mara baada ya kukuta vibunda vya dola mia moja mia moja vikiwa vimepangwa vizuri.

“Hizo ni pesa ambazo wamelipwa kwa kazi yangu hii. Tafadhali kaka yangu naomba unisaidie. Sisi kwetu sio huku Zanzibar, nilikuja kikazi tu”

“Kwenu ni wapi?”

“Tanzania bara, mkoni Kilimanjaro, mimi ni Mpare”

Marieta alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Nikazima taa ya humu ndani kisha nikaendele na safari.

“Umesema kwamba kwenu ni Tanzania bara”

“Ndio”

“Na huku ni Tanzania wapi?”

“Visiwani, kwani wewe ni mgeni?”

Marieta alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio mimi ni mgeni Tanzania”

“Umetokea nchi gani?”

“Marekani”

Niliongopea kwa maana Marekani ninakumbuka nilienda nikiwa mdogo sana.

“Ahaa karibu sana Tanzania. Sasa mbona ulikuwa kule porini, wewe ni askari?”

“Hapana”

“Ila?”

“Tukikaa vizuri tutazungumza, nahitaji tuelekee bandarini, tuondoke hapa kisiwani”

“Hakuna tatizo, nakushukuru sana kwa msaada wako”

Marieta akanielekea hadi bandarini, tukakata tiketi ya boti ya saa kumi na moja alfajiri. Ilipo timu saa kumi na moja tukaingia kwenye boti hiyo na tukainza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam.

“Unaitwa nani kaka?”

“Randy”

“Una jina zuri”

“Ninashukuru, hata wewe jina lako ni zuri”

“Asante.”

Tukaa kimya huku kila mmoja akionekana kichwani mwake akiwa amejawa na msongamano wa mawazo.

“Kwa nini Wataliano huwa wana roho mbaya?”

“Inategemea”

“Mmmmm wana roho mbaya kiasi cha kuchukiza kwa kweli. Huwezi amini yule mzee nilimfanyia kazi zaidi ya miaka sita, ila sikuwahi kufahamu kama ana uza madawa ya kulevya, sasa jana asubuhi ndio nilifahamu kwamba ana uza tena ndio msambazaji mkubwa sana wa madawa”

“Unajua hizo biashara, sio za kwaida sana. Ndio maana walihitaji kukua. Jambo la msingi la kufanya kabla ya kuelekea kwenu, inabidi ukae Dar es Salaam kwa muda kidogo ili kama hata kama watagundua kwamba watu wao wameuwawa, basi nini imani wataanzisha msako wa kukuua, na sehemu ya kwanza kwenda kukutafuta itakuwa ni kwenu. Umenielewa?”

“Ndio nimekuelewa”

“Yaa, tufike Dar es Salaam. Mimi nitakukabidhi kiasi cha pesa. Utachukua chumba hotelini, au utafanya vile utakavyo kisha utasikilizia kile kitakacho endelea”

“Na wewe je unaelekea wapi?”

“Matatizo yangu ni makubwa sana kuliko yako. Hivyo hutakiwa kuambatana nami. Watamuua mapema”

“Kina nani?”

“Maadui zangu”

Marieta akanitazama usoni mwangu kwa sekunde kadhaa, kisha taratibu akaushika mkono wangu wa kulia na kuanza kuuminya minya.

“Tanzania wewe ni mgeni. Unatakiwa kupata mtu ambaye atakupa msaada, msaada japo wa kujificha. Nakuomba nikupatie msaada huo”

“Hapana Marieta, lile nililo lifanya kwa vijana wa bosi wako, tambua ni bomu. Bomu ambalo likilipuka na likatukuta tupo pamoja basi umekwisha kabisa”

“Randy, nilisha kata tamaa ya kuishia pale nilipo kuwa nimefungiwa kwenye buti lile la gari. Niliwaza vitu vingi, nillia sana na nikaamini kwamba sinto weza kuwaona wale watu wangu wa karibu tena kwenye haya maisha. Ila wewe ukanirudishia maisha, wewe ukanifanya niweze kuona tena maisha. Wewe leo hii umenifanya niweze kuiona hii barari, kwa nini nikuache peke yako Randy mmmmm?”

Marieta alizungumza huku machozi yakimagika usoni mwake.

“Siwezi kukuacha peke yako, nipo tayari twende wote kijijini kwetu. Tukaishi huko, tuna pesa ya kutosha. Tunaweza kuanzisha maisha mapya Randy na tukaishi kwa amani sana”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama Marieta.

“Maritea, hunijui, hujuia ni wangapi wanao niwinda. Ninakwenda Dar es Salaam, ila ninatambua kwamba ninawindwa sana, tena maadui zangu wapo tayari kunitoa roho pale tu watakapo niona. Hivyo sipaswi kuwa nawe”

“Hapana Randy unapaswa kuwa nami. Kama uliyahatarisha maisha yako kwa ajili yangu, basi nami nipo tayari kuyahatarisha maisha yangu kwa ajili yako. Ninakupenda Ranyd”

Marieta alishindwa kuzizuia hisia zake na kujikuta akinipiga busu la mdomo. Kutokana daraja tulilo panda halina watu wengi, sikusita kulipokea busu hilo.

“Randy, sijawahi kumfanyia mwanaume hivi, sijawahi kabisa. Nimefanya kazi kwenye mazingira hatarishi ya kutongozwa ila nilikuwa na msimamo mkali sana, tafadhali nakuomba unipokee kwenye hizi shida tulizo nazo”

Marieta alizungumza huku machozi yakiendelea kumbubujika usoni mwake. Upande mmoja moyo wangu unamuonea huru, kiasi kwamba ninatamani kumkataa. Ila upande mwengine wa moyo unatamani sana kuweza kuwa naye.

“Tufike Dar es Salaam kwanza”

Nilizungumza kwa kujiamini. Taratibu Marieta akalaza kichwa chake kwenye bega langu la upande wa kushoto na taratibu akalala.

Tukafika katika bandari ya jiji la Dar es Salaam. Tukashuka kwenye boti na kwa mara nyingine ninakanyaga jiji hili ambalo hapo awali liliniadamisha sana. Tukatoka bandarini humu na kukodisha taksi. Marieta akaomba taksi hiyo itupeleke hadi kwenye hoteli aliyo ihitaki yeye.

“Dereva naomba upite katika duka la kubadilishia pesa”

“Sawa sawa dada”

Tukafika katika moja ya dula. Marieta akaomba noti kumi za dola mia moja. Nikamtolea noti hizo, akashuka kwenye gari na kuingia kwenye duka hilo. Baaada ya dakika tano akatoka huku akiwa na bahasha ndogo na kuingia ndani ya gari.

“Noti hizo ndio zimezalisha pesa zote hizo?”

“Yaani wee acha tu pesa yetu ya Tanzania haina thamani kivile”

“Hapo ni sawa na kiasi gani umepata”

“Kwa rate ya leo dola moja ni sawa sa shillingi elfu mbili na mia moja, hivyo dola elfu moja ni sawa na milioni mbili na machechi yake”

“Sawa sawa. Dereva unaweza kutupeleka Mbezi beach”

“Unapafahamu Mbezi beach!!!?”

Marieta alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa kiasi.

“Ndio napafahamu”

“Kuna nini huko?”

“Kuna mzigo wangu ninakwenda kuuchukua”

“Mzigo gani?”

“Unafahamu tukifika hiyo sehemu”



Kutokana nina uwezo mkubwa wa kukumbuka maeneo ninayo pia nikamuelekeza dereva hadi nyumbani kwa Charity.

“Naomba munisubirie hapa” “Unakwenda wapi Randy?” “Ninakuja” Nikashuka ndani ya gari, nikatembea taratibu hadi kwenye geti, nikajaribu kulisukuma geti hili ila halikufunguka, nikajaribu kuchungulia kwenye uwazi mdogo wa geti hili na nikaona walinzi kama wanne wakiwa wanazunguka zunguka ndani ya nyumba hii. Nikarudi kwenye gari na tukamuomba dereva atupeleke hotelini aliyo hitaji Marieta tupelekwe. Tukafika hotelini hapa, nikawa mtu wa kwana kushuka ndani ya gari. Nikatazama mazingira ya eneo hili, nilipo ridhika nayo. Marieta naye akashuka na akaanza kutembea kuelekea ndani. Sasa ikawa ni nafasi yangu kuweza kumuona Marieta vizuri mwili wake. Kwa kweli ni mwanamke aliye umbika, amajaliwa hipsi pana na zilizo shirikiana na kubeba kalio linalo eleweka na kubwa kiasi. Kiuno chake ni chembabamba kama nyigu na Mungu amemjalia kuto kuwa na tumbo kubwa kama baadhi ya wanawake. Kiafuani amejawali chuchu zilizo jaa kiasi,huku sura yake ikiwa imejaliwa umbwaji ambao nina amani kwamba Mungu alitumia muda mwingi sana katika kumuua, na si siku moja, labda ilimgarimu wiki kumuumba binti huyu. “Randy….Randy” Sauti ya Marieta ilinistua kidogo na kujikuta nikimtazama usoni mwake.

“Ehee?” “Mbona unanishangaa?” Marieta alizungumza huku akiwa ameshika kadi ndogo mkononi mwake. Kweli ninamshangaa, kwani hata kitendo cha yeye kulipia chumba na kupewa maelezo yote sikuweza kusikia wala kuona. “Hamna kitu” Nilizungumza huku nikitabasamua kidogo. Marieta akanishika mkono na tukatembea hadi kwenye eneo la lifti, tukaingia na kupandisha kuelekea juu. Tukafika gorofa ya tisa na kuelekea chumbani kwetu, kitendo cha kwanza tu kuingia ndani, nikamshika Marieta kiuno chake na kumbananisha kifuani mwangu hadi yeye mwenyewe akajawa na mshangao.

Akataka kuzungumza neno, ila nikamuwahi mdomo wake na kuanza kumnyonya kwa fujo. Mikono ya Marieta nayo haikuhitaji kufanya kosa katika mwili wangu, kwani taratibu ilianza kunipapasa kifuani mwangu na hatua ya mwisho mkono wake ukaishia katika jogoo wangu na kuanza kumshika kidogo. Nikamnyanyua Marieta na kumlaza Marieta kindani, kwa haraka nikamvua sketi yake huku naye akishiriki kwa asilimia zote kunivua suruali yangu.

Tukaanza kupeana shuhuli pevu, shuhulia mbayo hakika kila mmoja anaonyesha uhodari wake katika sita kwa sita. Mzunguko wa kwanza tukaumaliza huku kila mmoja akiwa na haja ya kuendelea na mtanange huu. “Tuendelee?” Nilimuuliza Marieta huku nikimtazama usoni mwake.

“Ndio” Tukapumzika kwa dakika mbili kisha tukaendelea na mtanange wetu, mzunguko wa pili ambao ulitugarimu zaidi ya lisaa moja hadi kufikia tamati. Tukaingia bafuni kwa pamoja, tukaoga kisha tukarudi chumbani hapa. “Randy” “Naaam” “Una mpango gani na maisha yangu?” “Kivipi?”

“Nahitaki kufahamu kama wewe ndio utakuwa mume wnagu au laa?” Nikamtazama Marieta kwa muda kidogo kisha nikamsogelea, nikamkumbatia kwa nyuma huku tukitazama kioo kikubwa cha kabati lililomo humu chumbani.

“Kuwa nami, niendelee kuwa nawe” “Una maana gani Randy” “Ukiniacha unahisi nitakuwa nawe, sinto weza kuwa nawe. Ikiwa umeamua maisha yako yoye kuishi nami basi naomba iwe hivyo. Huwa ninamchukia mwanamke kigeu geu” “Siwezi kuwa kigeu geu, nitakupenda na kujujali kwa maisha yangu yote hadi kufa kwangu” “Nashukuru sana”

Siku nzima tukashinda ndani humu bila ya kwenda sehemu yoyote huku, kazi yangu ikiwa ni kubadilisha chaneli za televishion iliyomo humu ndani, lengo kubwa ni kuweza kufahamu ni kitu gania mbacho kinaendelea juu ya wale majambazi wawili nilio waua.

“Randy niwapigie simu watuletee chakula?” “Yaa unaweza kufanya hivyo” Taariafa ya habari ya saa mbili usiku, ikatangaza kuokotwa kwa miili hiyo ya watu wawili wanao sakikika kuwa ni majambazi, na mkuu wa polisi aliahidi watafanya uchunguzi ili kugundua ni kitu gani ambacho kilitokea hadi majambazi hao wakauwawa.

“Unahisi kwamba watafahamu kama ni wewe ndio umewau?” “Sidhani kama watafahamu ila ninatakiwa kupata silaha kwa sasa” “Silaha ya aina gani?” “Bastola” “Mmmm ya nini sasa?” “Maisha yetu lazima yatakuwa yanawindwa na watu wengi sana. Moja kuna kundi moja lilinipa kazi ya kuwaokoa watoto fulani was hule kutoka nchini Ujerumani. Walikuwa wameshikiliwa mateka nchini Somalia, ila nilishindwa kukamilisha kazi na waliamua kuniua. Pili kuna kundi moja duniani linaitwa Al-quida, ni kundi la magaidi, nilikuwa ninafanya kazi kwenye kundi hilo na kwa bahati mbaya kulitoka matatizo na wananiwinda ili kuniua. Ndio maana hapo awali Marieta nilikuambia uweze kwenda kwenu, kuendelea kuwa nami ninakuweka wewe matatizoni”

Nilizungumza kwa upole na kwa umakini wa hali ya juu. “Matatizo nikiyapata nikiwa nawe, sinto jutia. Uzuri umeweza kunieleza ukweli kwamba wewe ni nani” “Sawa” Kengele ya mlangoni kwetu ikagongwa, nikajifunga taulo kwa haraka na kusimama pembezoni mwa mlango huu. Kwa ishara nikamuoma Marieta aulize ni nani aliyopo mlangoni. “Muhudumu, nimeleta chakula” Marieta akafungua mlango na kupokea shani ya chukula pamoja na vinywaji. Akamkabidhi muhudumu huyu pesa anayo idai kisha akafunga mlango.

Tukaanza kula huku tukizungumza mambo mengi sana kuhusiana na maisha yetu ya nyuma. Marieta akanielezea historia yake toka alipo kuwa mtoto na hadi hapa alipo fika. Hata mimi nikamueleza historia ya maisha yangu, ila nikaficha kumueleza tofauti iliyopo katik yangu na mama yangu. “Huoni kuwa mbali na mama yako kunaweza kumfanya awe na majonzi mengi snaa?” “Hapana, nina imani atakuwa na amani moyoni mwake kwa jisni ninavyo endelea kuvuta hii pumzi ya bure ya mwenyezi Mungu” “Inabidi twende kwa mama tukamsalimie japo anifahamu” “Usijali tutaenda” Baada ya kupata chakula hichi cha usiku, tukaingia bafuni na kuoga. Tukapeana raha kwa awamu nyingine kisha tukalala. Majira ya saa saba usiku, nikanyanyua kitandani na kuvaa nguo zangu. Nikachukua kadi ya kufungulia mlango huu, nikachukua kiasi kidogo cha pesa, kisha nikatoka kwa kunyata pasipo Marieta kugundua chochote. Nikaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini, nikatoka nje hoteli hii na kwa bahati nzuri nikawakuna madereva taski wakiwemo katika hili eneo wakiendelea na shuhuli zao. Nikamuomba dereva taksi anipeleke mbezi beach, nikamuelekaza nyumbani kwa Charity. Safari ikaanza huku akilini mwangu nikiwa ninatafakari ni jinsi gani ninaweza kuingia ndani ya nyumba hiyo, nikachuku begi langu la pesa na kuondoka. Nafsi moja inanishauri kwamba begi hilo halito kuwepo, huku nafsi ya pili inanishawishi kwamba begi langu lipo.

Tulipo fika katika mtaa wenye nyumba ya Charity nikamuomba dereva taksi aniache hatua kadhaa kabla ya kufika katika nyumba hiyo. Nikamkabidhi kiasi chake anacho kihitaji kisha akaondoka na kuniacha peke yangu. Usiku huu mtaa huu umetulia sana na katika hii barabara hakuna hata gari moja linalo pita.

Nikatembea kwa umakini sana hadi katika geti la nyumba hii ya Charity, nikachungulia ndani na kuwaona walinzi wakiwa wapo bado. Nikatazama ukuta huu nan ikaona kuna sehemu ninayo weza kupanda na nikaingia ndani.

Kutokana mimi ni mrefu, nikajirusha kidogo na nikafanikiwa kushika sehemu hii ya juu ya huu ukuta,.Taratibu nikapanda kisha nikajirusha kwa ndani kwa umakini sana pasipo kutoa kishindo cha aina yoyote.

Eneo nililo shukia ni eneo la nyuma ya nyumba hii. Uzuri ni kwamba nina ifahamu hii nyumba na kwa kipindi ambacho nilikaa hapa niliweza kuichunguza kila sehemu. Nikatembea hadi kwenye dirisha la chumba cha Charity, nikasikia miguno ya kimahaba ikiendelea. Taratibu nikafungua pazia kwa umakini sana, nikamuona mume wa Charity ambaye mara ya mwisho nilimuaona Zanzibar.

Mzee huyu nikamuona jinsi anavyo faidi tuna la Charity. Nikanyata hadi dirishani mwa chumba nilicho kuwa nina lala, nikamuona dokta Sara akiwa amelala kitandani, huku begi langu la pesa likiwa kwenye moja ya kona katika chumba hichi huku likiwa limefungwa vizuri sana.

“Fuc***” Nilizungumza kwa sauti ya chini kwani eneo la mbele lenye mlango wa kuingilia hapa ndani ndipo walipo walinzi wa mzee huyu. Nikajikiria kwa muda kisha nikamuita doka Sara kwa sauti ya chini sana. Dokta Sara akawa kama ni mtu anaye hisi kama anaitwa, ila kutokana yupo usingizini aliendelea kujigeuza geuza kitandani mwake.

“Hei Sara ni mimi Randy” Ilibidi nijitambulishe jina langu. “Randy, Randy yupi?”

Dokta Sara alizungumza huku akikaa kitandani na kutazama huku dirishani. “Rafiki yako uliye pata naye ajali baharini” “Mbona hupo hapa, umepajuaje hapa?” “Nitazungumza nawe nikipata muda, nakuomba uweze kuniingiza ndani humu basipo baba yako na walinzi wake kuweza kufahamu” “Kwa nini?” “Nakuomba unisaidie hivyo Sara, samahani sana kama nitakuwa nimekuudhi.

“Bila samahani, ngoja” Uzuri wa Sahara hama maswali mengi, akanyanyuka kitandani kwake na kufungua mlango. Nikanyata hadi sehemu ya mbele katika nyumba hii, nikachungulia kidogo na kumuona Sara akizungumza na walinzi hawa huku akiwaomba wakapumzike. Walinzi hawa wakamuewa Sara na wakaingia kwenye moja ya gari kubwa lililo kaa muundo wa costa. Dokta Sara akakazunguka nyuma sehemu nilipo, kwa haraka akanikumbatia kwa nguvu sana huku akiwa na furaha kubwa ya kuniona.

“Umejuaje kama nipo hapa” Dokta Sara alizungumza kwa sauti ya chini huku akiwa amenikumbatia.

“Vipi tunapo pita hapo walinzi hawawezi kutuona?” “Hawawei kutuona, twende ndani” Tukaingia ndani humu na moja kwa moja nikapitiliza hadi chumbani. Sara akaingia ndani humu na kunikumbatia kwa mara nyingine.

“Nilijisikia vibaya ulipo kimbia Randy” “Usijali” “Kwani wewe na baba yangu muna fahamiana?” “Nitakueleza Sara ngoja mara moja” Nilizungumza huku nikimuachia Sara, nikatembea hadi lilipo begi langu, nikaligonga kidogo na mguu na kukuta likiwa na ujazo wake. Taratibu nikachuchumaa huku nikishusha pumzi taratibu, nikafungua begi langu na kukuta likiwa na pesa zangu huku simu niliuyo kuwa nikiitumia ikiwa juu ya pesa hizi.

“Asante Mungu” Nilizungumza kwa sauti ya chini chini na kumfanya dokta Sara kuchungulia ndani ya begi hili.

“Heee kumbe lina pesa” “Yaa lina pesa. Hili ni begi langu” “Nitaamini vipi kwamba hili ni behi lako” “Hii simu ina neno la siri, ninaweza kukutajia na ukaifungu” “Hembu naiomba” Nikamkabithi dokta Sara simu yangu, nikamtajia neno la siri la simu hiyo na akaifungua simu hiyo na kunikabidhi huku akiwa amejawa na tabasamu.

“Nimekuamni” “Ndio hivyo nahitaji kuondoka na begi langu” “Unakwenda wapi Randy na kwa nini unamkimbia baba yangu ikiwa ni mtu mwema sana” Nikamtazama Sara usoni mwake, taratibu nikamsogelea dokta Sara na kumshika mashavuni mwake.

“Nilimkosea baba yako, kutoka na ushawishi alio nifanyia mwanamke wake” “Ushawishi gani?” “Baba yako alinifumania nikiwa na mwanamke wake. Alipanga kuniua, ila kuna msaada niliupata kabla ya adhimio la mimi kuuwawa kukamilika.” Nilizunumza kwa upole sana huku nikimtazama dokta Sara usoni mwake.

“Randy utamkimbia baba yangu hadi lini?” “Sifahamu, ila ninahitaji hizi pesa ili niweze kutoweka katika nchi hii. Nahitaji kwenda kutafuta sehemu yenye amani niaze maisha yangu mapya” “Naomba twende sote” Maneno ya dokta Sara yakanishangaza sana.

“Naomba twende wote popote duniani. Randy ninakupenda na nilijiapiza moyoni mwangu kukupenda hadi mwisho wa maisha yangu. Nijijiapiza kukutafuta popote ili uwe mwanaume wa maisha yangu. Nakupenda sana Randy” Dokta Sara alizungumza huku akinikumbatia. Nikamkumbuka Mariata wangu niliye muacha hotelini akiwa amelala.

“Nakuomba uniachie email yako, nitakutafuta nikipata sehemu iliyo salama, ili uje mani. Ukitokoka naamini kwamba baba yako nitazidi kumchukiza sana. Tafadhali nakuomba uniamini” “Sawa” Dokta Sara akaniomba simu yangu, akaandika emil yake, kisha akanirudishia simu yangu. Akaninyonya lipsi zangu kwa sekunde kadhaa, kisha akachungulia nje na kuniomba niweze kutoka. Tukaongozana hadi nje, kitendo cha kuvaa begi hili mgongoni, nikahisi kitu kigumu kikinigusa kwa nyuma yangu huku mbele yangu, nikiwaona walinzi wa mzee huyo wakiwa wameshika bastola zao huku wakiwa wamezielekezea kwangu.

“Ulihisi sinto kukamata tena” Niliisikia sauti ya baba Sara an kunifanya nistuke sana huku nikigeuka nyuma. Nikamona mzee huyu akiwa amenishikia bastola huku akiwa amekasirika sana usoni mwake



Nikamuona Charity akitoka chumbani kwake huku akiwa na nguo ya kulalia. Macho yakamtoka sana na hakuamini kunikuta hapa. “Baba” “Sara acha kuingilia hili” Mzee huyu alizungumza kwa ukali sana huku akinikazia macho. “Sihitaji matatizo na wewe mzee, mke wako ndio alinitamani na nikiwa kama mwanaume mwenye hisia zilizo kamilika nisinge muacha. Naomba niondoke na mzigo wangu na tuachane kwa wema” Nilizungumza kwa upole sana huku nikimtazama mzee huyu usoni mwake.

“Baba naomba msamehe kijana huyu. Kumbuka yeye ndio aliye niokoa maisha yangu. Amenisaidia kwa hali na mali na hata koti nililo kuwa nimelivaa siku ile tunaonana ni lake. Aliamua kukaa na kanguo kepesi ili maradi tu mimi nisi udhurike. Tafadhali baba nakuomba umruhusu kijana wa watu aondoke” Dokta Sara alizungumza kwa upole huku akimshika baba yake mkono wenye bastola. Mzee huyu akanitazama kwa mdua kidogo kisha akaushusha mkono wake.

“Ni nani aliwaua walinzi wangu?” Nikaka kimya huku nikikumbuka siku ya tukio. Dany alinisaidia, ila sikufahamu kwamba ana lengo gani kwangu.

“Sifahamu, nilifungiwa ndani ya buti ya gari na sikuweza kuona ni kitu gani kinaendelea. Nilishutukia gari likibingiria baada ya hapo buti ilfunguka, nikapata fursa ya mimi kutoka, sikuhitaji kujua kinacho endelea kwa walinzi wako kutokana nilikuwa chini ya ulinzi wao na nikiwa kama mtuhumiwa nikaona ni bora nikimbie na kuondoka eneo hilo” Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nikiuficha ukweli kuhusiana na Dany ambaye yeye ndio aliye nisaidia. Mzee huyu akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha kwa ishara ya mkono akaniomba niondoke.

“Nashukuru” Nikawatazama dokta Sara na Charity, kisha nikaanza kuondoka eneo hili huku walinzi wake wakinipisha nikafika getini na kufungua geti na kutoka. Nikaanza kukimbia kwenye barabara hii iliyo tulia sana. Nikafika katika kituo cha madereva, nikawakuta waendesha pikipiki watatu, nikamuomba mmoja anipeleke kwenye hoteli niliyo muacha Marieta. Tukaianza safari huku nikiwa na furaha sana kwa kupata pesa yangu. Mipango ya kujiimarisha kiuchumi, ikaanza kunitawala kichwani kmwangu. Hadi tunafika hotelini, sikuwa na mpango madhubutu wa kufanya na hizi pesa nilizo zipata kwa shida sana. Nikamlipa dereva pikipiki mara mbili na kiasi alicho kihitaji kisha nikaingia ndani ya hoteli hii, moja kwa moja nikaingia kwenye lifti. Taratibu ikaanza kunipandisha juu hadi kwenye gorofa yenye chumba tulicho pangisha. Nikatembea kwa mwendo wa haraka hadi kwenye chumba chetu. Kwa kutumia kadi hii nikafungua mlango taratibu na kuingia ndani. Nikamkuta Marieta akijigeuzia upande wa ukutani mwa kitanda hichi na akaendelea na usingizi. Nikaingia bafuni, nikavua nguo zangu zote kisha nikafungua begi hili na kuanza kutoa kibunda kimoja baada ya kingine cha pesa. Nikavikuta vipande vyangu vya dhabu vikiwa vipengwa chini ya pesa kitu ambacho zikuziweka hivyo.

Nikanyanyua kipande kimoja cha dhahabu, sikuamini macho yangu mara baada ya kukuta bomu la kutegwa linaolo onyesha zimesalia sekunde thelathini hadi lilipuke.

“Mungu wangu” Nilizungumza huku nikiangaza angaza kila sehemu ya bafu hili. Tararibu nikalitoa bomu hili ambali si kubwa sana. Nikafungua dirisha hili dogo la bafu na kuchungulia nje, nikaona nyumba ya kawaida ikiwa imepakana na gorofa hili. Nikalipitisha kwa umakini sana kwenye nondo hizi, nikalirusha huku nikitazama sekunde zake na kuona zikiwa zimesalia sekunde kumi na mbili, nikarudi chumbani kwa haraka na kumrukia Marieta hadi akastuka. Akiwa katika hali ya kustuka, tukasikia mlipuko mkubwa sana wa bomu ulio ambatana na mtemeko wa ardhi

“Ni nini chihoooo?”

Marieta alizungumza huku akitetemeka sana.

“Ni bomu, vaa nguo zako” Nilimuambia Marieta huku nikishuka kitandani, nikaingia bafuni humu, nikaanza kuingiza vipande vya madini napesa zangu kwenye begi. Nikavaa nguo zangu kwa haraka kisha nikatoka chumbani humu na kumkuta Marieta akimalizia kuvaa nguo.

“Tuondoke” “Pesa” Marieta alizungumza huku akichukua bahasha yenye pesa. Nikalivaa begi hili na kufungu malango, nikachungulia nje na kuona watu wakikimbia kwenye kordo hii huku wengine wakiwa uchi kabisa, huku kila mtu akihitaji kuyaokoa maisha yake.

“Twende” Nilizungumza huku nikimshika Marieta mkono. Tukaanza kukimbia kwenye kirdo hii. Tukakuta watu wengi wakiwa wanasubiria lifti ifunguke.

“Huku” Nilizungumza huku nikaelekea katika eneo la ngazi. Tukaanza kushuka kwenye ngazi hizi kwa kasi huku tukiwakuta watu wengine ambao nao wameamua kutumia ngazi kushuka wakishuka kwa kasi. Mtetemeko wa gorofa hili ukazidi kiongezeka jambo lililo pandisha hofo kwa watu wengi sana. “Nisaidieni” Nilimuona dada mmoja akiwa amenguka kwenye ngazi huku watu wengine wakija na kumkanyaga juuu yake.

“Nishikilie vizuri” Nilimuambia Marieta na akaung’ang’ania vizuri mkono wangu huku mkono wake mwengine akiwa ameshikilia bahasha ya pesa. Nikanyanyua dada huyu kwa nguvu na kumsimamisha ukutani.

“Asate” Dada huyu alizungumza hukua kihema, sikuhitaji kumitika asante yake. Tukaendelea kushuka kwenye ngazi hizi huku baadhi ya vipande vya maeneo ya gorofa hili vikianza kumeguka taratibu taratibu jambo ambalo linazidi kuhatarisha maaisha ya kila mtu aliyomo ndnai ya hoteli hiii. Tukafanikiwa kufika nje ya hoteli huku tukiwa tumeambata na kundi kubwa la watu ambao wameokoa maisha yao huku wengine nao wakiendelea kutoka. Nikashuhudia gorofa hili kwa upande nilio rushia bomu, ukiangukia kwenye nyumba ya jirani ambayo nayo imechanguka changuka.

“Tuondoke” Nilimuambia Marieta huku nikimshika mkono, kwani wingi wa watu nao unazidi kuongezeka na muda huu inaelekea majira ya sakumi na moja alfajiri. “Ohoo Mungu wangu Randy nina ogopa” Marieta alizungumza huku akilia kwa uchungu sana.

“Usiogope, jikaze” Nilizungumza kwa hasira huku taswira ya baba Sara na kundi lake la watu ikinijia kichwani mwangu. Tukafika katika hoteli nyingine, tukaulizia vyumba na kwa bahati nzuri tukafanikiwa kupata chumba kimoja kilicho kuwa kimesali. Marieta akalipia na tukaingia katika chumba hichi.

“Ni kitu gani kilicho tokea Randy?” “Sifahamu na mimi. Nahitaji ufanye jambo moja kwa ajili yangu” “Jambo gani?” “Maadui zangu wanakaribia kunisogelea. Wanakaribia kunikamata na mimi sihitaji kukamatwa kijinga ni lazima na mimi niwashambulie. Hivyo ninakuomba uweze kwenda kwenu ukanisubirie huko. Hapa Dar es Salaam sio salama kabisa” “Randy ila tambua ninakupenda na…..” “Marieta huu sio muda wa mapenzi, lile bomu lililo tegwa pale lilikuw ani kwa ajili yangu wewe mwanamke nieleweee basi” Nilizungumza kwa kufoka sana hadi nikahisi kifua changu kinahitaji kupasuka kwa hii hasira kali sana niliyo nayo. Marieta mwili mzima ukamtetemeka kwa woga.

“Nataka uende nyumbani kwenu. Kakae na familia yenu huko. Nisubirie nitakuja huko umenielewa?” Marieta akanijibu huku akitingisha kichwa akimaanisha kwamba amanielewa

“Safi, gari za kwenu zinapatikana wapi?” “Ubungo” “Ndio wapi?” “Stendi kuu ya mabasi hapa jijini Dar es Salaam” “Sawa, tunaondoka sasa hivi. Ingia bafuni upige mswaki, oga tunakwenda Ubungo” Taratibu Marieta aakanisogele, mkono wake mmoja akaupisha kiunoni mwangu na mkono mmoja akauweka kifuani mwangu.

“Nakuomba uwe hai kwa ajili yangu Randy, nitajitunza, nitajilinda hadi pale utakapo kuja” Marieta alizungumza kwa sauti ya mahaba huku akinitazama.

“Nashukuru, sasa ingia bafuni oga. Tuinze safari” Marieta akanitazama kwa muda kidogo, kisha akaniachia na kuingia bafuni. Nikaka kitandani huku nikiwa na mawazo juu ya mume wa Charity au kwa jina jengine baba Sara. Wazo la mwisho lililo gota kichwani mwangu ni kuhakikisha kwamba nina muua mzee huyu yeye na kundi lake. Kwa ajili yake amesababisha watu wengi watakuwa wamekufa kwneye ile ajali ya gorofa kuangua.

“Wewe huogi?” Marieta alizungumza huku akiwa amesimama mlangoni, uchi kama alivyo zaliwa. Umbo lake zuri kidogo likaishusha hasira yake, nikapata kigugumizi cha kumjibu, taratibu akatembea na kusimama mbele yangu, akanipa mkono.

“Natambua kwamba una hasira snaa, ila nakuomba tukaoge” Nikajifikiria kwa sekunde kadha, kisha nikavua begi hili na kuliweka kitandani. Nikarudi mlangoni na nikahakikisha kwamba mlango tumeufunga vizuri. Nilipo hakikisha nikarudi dirishani, nikachungulia vizuri, kwa jinsi dirisha hili lilivyo tengenezwa, ni ngumu sana kwa mtu kuweza kulifungua. Kabla ya kuingia bafuni, Marieta akanivua tisheti yanu, akanivua viatu kisha akamalizia kunivua suruali yangu nami nikabaki kama nilivyo zaliwa. Tukaingia bafuni, huku Marieta akiwa amenishika mkono wangu wa kulia. Taratibu Marita akafungulia bomba la maji ya mvua kisha akanikumbatia na tukaanza kunyonyana midomo yetu huku maji yakiendelea kutumwagikia mwilini mwetu.

Hisia zaungu hazikuzubaa katika kumsimamisha jogoo wangu. Taratibu nikajikuta nikianza kula kitumbua cha Marieta. Shuhuli ikazidi kuwa pevu kwani kila ninapo jikuta ninakumbuka baba Sara, hasira inanipanda na kuongeza mikiki mizito kwa Marieta hadi akaanza kulia kama mtoto mdogo. Nikamaliza mzungukoa huu huku nikiwa nimechoka sana, kwani shuhuli nimeifanya kihasira. Marieta taratibu akaka chini huku akilshika tumbo lake na kujikunja kidogo. “Vipi?” Nilimuuliza Marieta huku nikishusha pumzi nyingi sana.

“Eheee?” “Unajisikiaje?” “Tumbo langu, linauma sijui umetengua kizazi changu” Marieta alizungumza huku akionyesha dhairi ana maumivu makali sana tumboni mwake. Nikachuchumaa, taratibu nikamnyanyua.

“Jikaze kusimama, nishikilie, inabidi twende hospitalini”

“Hapana Randy acha niande nyumbani tu” “Napenda kuwa karibu na wewe, ila nakogopa kukukatishia maisha yangu. Kama unaweza kunisaidia niambie jina la bosi wako na kama unaweza kuikumbuka sura yake basi wewe niambie, ili niweze kukulinda nikiwa nipo mbali na wewe” “Unanilinda vipi mpenzi wangu” “Nitajua jinsi ya kukulinda” Marieta akanitazama kwa macho yake mazuri, kisha akanikumbatia.

“Randy” “Mmmmmm” “Sinto mpa mwanaume yoyote penzi lako. Tambua kwamba nina kupenda mpenzi wangu” “Ninakupenda pia mke wangu” “Nahisi kuna kitu kimeingia kwenye via vyangu vya uzazi, ila sitaki kuamini, ila kama ni kweli basi utakikuta kile ulicho kiingiza” “Unataka kuniambia kwamba upo kwenye siku zako za hatari?” “Ndio, ila sitaki kuamini haraka kwamba umenipatia ujauzito. Kama sinto kuona basi namuomba Mungu, mtoto wako awe ndio kumbukumbu yangu kwako. Ninakupenda sana Randy” “Ninakupenda pia Marieta” Tukaendelea kuoga huku Marieta, akijikaza kuyasikiliza maumivu ya tumbo lake. Tukatoka bafuni humu na kuvaa nguo hizi.

“Inabidi tupate nguo nyingine. Kama maadui zako wamekutambua nguo hizo nyeusi. Basi ni rahisi kwa wewe kukamatwa mpenzi wnagu” “Nimekuelewa mama tutanunu” Tukavaa nguo zetu. Majaira ya saa kumi na mbili na nusu, tukatoka katika hoteli hii na moja kwa moja tukaelekea hadi kwenye kitua cha waendesha taksi. Tukamuomba atupitishe eneo lenye maduka ya nguo.

“Kaka umeendana na mpenzi wako” Dareva taski huyu alizungumza huku akitutazama kupitia kioo kidogo alicho kiweka mbele yake.

“Nashukuru” “Ninaitwa Benzi, ukija kijiweni kwetu pale unaweza kuniulizia tu kwa watu au chukua hii kadi yangu, ina namba za simu na unaweza kuwasiliana nami muda wowote” “Nashukuru sana” Nilizungumza huku nikipokea kadi hii ya yenye namba zake za simu. Tukafika duka la nguo za kiume, tukashuka mimi na Marieta huku dereva taksi huyu tukimuacha kwenye gari.

“Hili begi lina nini mume wangu kwa maana nina kuona unalibeba tu” “Usijali” Nikachagua suruali mbili, pamoja na tisheti mbili. Viatu pea moja.

“Kuna chumba cha kujaribishia?” “Ndio kile pale” Tukaingia na Marieta katika chumba hichi kidogo kiasi. Nikafungua begi hili na kumuonyesha pesa zilizomo ndani ya hili begi.

“Hizi ni pesa mpenzi wangu. Huu ndio mzigo wangu nilio kueleza kwamba upo mbezi Bech, jana usiku ulipo kuwa umelala niliufwata na kurudi nao” “Wewe mwanauem hata kuniambia?” “Ningekupa presha” Nikajaribisha nguo zote, zilizo nipendeza sana, nikazivaa muda huu huu. Tukatoka chumbani humu. Nikanunua sweta lenye kofia kubwa na kulivaa, nikanunua miwani pamoja kofia na vyote nikavivaa kwa pamoja. Nikalipa kiasi ninacho takiwa kulipa kisha tukatoka nje ya duka hili. Benzi akatoka katika taski yake huku akiwa amejawa na furaha, akataka kufungua mlango wa siti yetu ya nyuma, ila kitendo cha yeye kutembea hatua mbili mbele tukashuhudia akianguka chini huku risasi ambayo hatujui imetokea wapi ikiwa imepasua kichwa chake jambo lililo sababisha yujawe na wasiwasi mwingi sana.


Kila mtu aliye shuhudia tukio hili nje ya duka hili, akanza kukimbia, nikamshika mkobo Mariata na kuanza kukimbia huku macho yangu yakiwa makini sana kutazama upande wa pili wa barabara ambapo kuna gorofa moja refu, nikamshuhudia mtu mmoja akiimalizikia kuondoka katika eneo hilo jambo lililo nipa udhibitisho kwamba muuaji alikuwa juu ya gorofa na alitumia bunduki maalumu za kuulia watu hata akiwa mbali na eneo ambalo anahitaji kumuua mtu. Nikakimbia hatua chache kisha nikasimama, nikamtazama Marieta huku namfsi moja ikiniagiza niweze kurudi kwenye eneo alipo muuaji huku nafsi nyingine ikinishauri niendelee na safari yangu.

“Twende”

Nilizungumza huku tukiendelea kukimbia. Tukafika kwenye eneo ambalo kuna usafiri wa kila aina.

“Unajisikiaje?”

Nilimuuliza Marieta mara baada ya kuona sura yake ikiwa imejikunja.

“Tumbo linaniuma sana”

Marieta alizungumza huku mkono wake kmmoja akiwa ameshika tumbo lake.

“Inabidi nikupeleke hospitalini?”

“Hapana Randy”

“Kwa nini hapana”

“Nahisi ni woga nao pia umechangia”

“Taksi”

Nilimuita dereva mmoja huku nikimtazama usoni mwake. Dereva huyo akaingia kwenye taski yake aliyo kuwa ameigemea, akatufwata hadi hapa tulipo. Tukaingia ndani ya taksi hii.

“Unaweza kutupeleka kwenye hospitali yoyote?”

“Hapana dereva, naomba utupeleke kwenye duka la dawa lolote, baada ya hapo tupitishe kwenye yale maduka ya nguo za kike pale kwa Ramy”

“Sawa”

Nikamatazama Marieta usoni mwake na sikuzungumza chochote. Dereva taski akatufikisha kwenye moja ya duka kubwa la nguo

“Subiri ninakuja”

Marieta alizugumza na akashuka kwenye gari. Akaingia kwenye duka hilo kisha baada ya muda akatoka. Akaingia ndani ya taksi hii, akafungua kichupa cha maji ya kunywa, akachukua vidonge viwili na kunywa, kisha akavisindikiza kwa kunywa maji.

“Hivyo vidonge vitakusaidia kweli?”

“Ndio. Ndani ya dakika tano nitakuwa nimepona.”

“Sawa”

Tukaendelea na safari yetu hadi kwenye moja ya duka la nguo. Tukaingia ndani kwa pamoja. Marieta akachagua nguo zipatazo ishirini, kwa ununuzi huo hadi mwenye duka akaamua kumpa begi moja la nguo bure. Nikalipa garama za nguo zote.

“Kuna mikoba mikubwa ya kike?”

Nilimuuliza muuza duka huyu

“Ndio ile kule”

Nikausogelea mkoba mmoja mzuri, nikauchukua na kurudi nao hapa. Nikaulipia.

“Randy hapo je?”

Marieta alizungumza juhu akitoka kwenye chumba kidogo cha kubadilishia nguo.

“Hapo poa mpenzi”

“Hilo wigi limekupendeza dada”

“Etii ehee. Asante”

“Nami naweza kuingia kwenye chumba hicho?”

“Hakuna tatizo”

Tukaingia na Marieta ndani ya chumba hicho kwa pamoja. Nikalishusha begi langu la mgongoni lenye pesa. Nikatoa vibunda viwili vya pesa vitano vya pesa na kumuwekea kwenye mkoba wake.

“Hii ni dola milioni moja, sawa na dola bilioni ngapi za hapa Tanzania. Jitunze, jilinde na nisubirie mimi nije na kama utakuw ana kiumbe changu. Kipe jina la Brina Randy sawa”

Marieta macho yakamtoka, kigugumizi kizito kikampata hata uwezo wa kunijibu ukamuishia. Machozi yakendelea kumwagika usoni mwake. Taratibu akanikumbatia huku akilia sana.

“Nakupenda Randy”

“Nakupenda pia. Jitunze kwa ajili yangu tafadhali”

“Nitajitunza hadi siku utakapo kuja”

“Naomba unitajie jina la bosi wako”

“Jina la hoteli yake inaitwa BOH maana yake. Black Ocean Hotel ukiingia hapo utaona uongozi mzima. Yeye ndio wa kwanza ni mzee mwenye makamu kama niaka stini hivi ni mgiriki”

“Sawa mke wangu, nitaitafuta”

Tukatoka katika chumba hichi. Tukaagana na muuza duka huyu kisha safari ya kuelekea stendi ya mabasi Ubungo ikaanza. Tukafika katika stendi hii kubwa ya mabasi, nimalipa dereva taksi huyu na kumuomba anisubirie. Tukaongozana hadi kwenye ofisi ya magari yaendayo kwao katika mkoa wa Kilimanjaro. Akakata tiketi na kwa bahati nzuri akapata gari ambalo linaondoka ndani ya dakika kumi na tano zijazo. Tukaongozana na mmoja wa wakilishi wa kampuni hii ya mbasi hadi kwenye basi lao. Tukaingia ndani ya basi hili. Marieta akaka kwenye siti yake huku akiwa amejawa na majonzi mengi usoni mwake. Nikatoa simu yangu mfukoni na tukapiga picha kadhaa za ukumbusho.

“Nakuomba uwe makini Randy”

“Usijali mpenzi wangu”

Nikampiga busu la mdomo Marieta kisha nikashuka kwenye basi hili.Nikaasubiri kwa dakika kadha ahadi basi hili lilivyo anza kuondoka ndipo nami nikaanza kuondoka kuelekea kwenye eneo nilipo iacha taksi. Nikaingia kwenye taski hii huku nikishusha pumzi.

“Nikupeleke wapi mkuu?”

“Nahitaji tutafute nyumba iliyo tulia sana ya kupangisha.”

“Kwa maeneo gani unahitaji mkuu?”

“Maeneo yaliyo tulia hapa Dar es Salaama ni yapi?”

“Masaki, Mbezi baech na kwengineko”

“Unafahamu ni dalali gani ambaye anaweza kutupatia huduma hiyo?”

“Wapo wengi sana, ngoja kuna jamaa yangu mmoja nimpigie simu”

Dereva huyu akawasiliana na rafiki yake huyo. Rafiki yake akatuelekeza sehemu alipo kisha tukaanza kazi ya kutafuta ni wapi tunapo weza kupata nyumba nzuri. Hadi inafika saa tisa alasiri tukafanikiwa kupata nyumba moja iliyo tulia eneo la masaki na ipo pembezoni mwa bahari.

“Nyumba hii ina kila kitu ndani ila ni garama sana”

Dadali alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ni kiasi gani?”

“Dola elfu tano kwa mwenzi. Hii huwa wanakodisha wazungu tu ndio wenye uwezo wa kuhimili hicho kiasi”

“Wasiliana na mwenye, nahitaji kuingia hapa”

“Sawa mkuu”

Dalali akawasiliana na mwenye nyumba na baada ya nusu saa mama huyu mwenye hii nyumba akafika katika eneo hili. Akatufungulia geti na kuingia ndani humu, akaanza kututembeza kila sehemu ya hii nyumba ambayo ni ya kisasa na imejengwa katika hadthi ya kimataifa kwani ina kila kitu ndani na ina vyumba viwili vikubwa vya kulala.

“Nimepapenda kwa kweli”

“Sawa unaweza kufanya malipo”

Mama huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nahitaji kulipia mwaka”

Watu wote wakatazamana kwa maana kiasi hicho cha kulipia ni kikubwa sana kwa watu wa nchi wa nchi hii.

“Mwaka mmoja!!?”

Mama huyu mwenye asili ya kiafrikasti aliniuliza kwa mshangao

“Ndio, au siruhusiwi kufanya hivyo?”

“Unaruhusiwa”

“Yaa nahitaji iwe hivyo mama yangu”

“Kutokana malipo ni makubwa, siwezi kuyafanyia hapa. Tunaweza kuongozana hadi ofisini kwangu, wewe utamlipa huyu dalali kisha tutaelekea huko”

“Sawa”

Nikafungua begi langu na kutoa dola elfu sita na kumkabidhi dalali na kumfanya azidi kujawa na furaha kwani ni dili ambalo hakulitegemea kabisa. Nikamlipa dereva taksi dola elfu moja kama malipo ya kuzunguka naye siku mzima hii.

“Kaka chukua namba yangu wewe ukiwa na haja ya mimi utanijulisha”

Dereva taksi huyu alizungumza, nikaiandika namba yake kwenye simu yangu kisha wakaondoka na dalali. Mama huyu akafunga geti kisha nikaingia kwenye gari lake aina ya Toyote VX V8.

“Toka niiijenge hiyo nyumba sikuwahi kupata mteja wa kulipia mwaka mzima kama wewe”

“Usijali, nipo Tanzania kwa kazi maalumu”

“Kazi gani baba yangu?”

Mama huyu alizungumza huku akiwa amejawa na furaha usoni mwake.

“Mimi ni mfanya biashara, nimekuja kuwekeza nchini hapa, sasa nahitaji kutazama fursa nyingi nyingi. Kama nitapendezewa basi nitafungua kampuni yangu kubwa tu”

“Aisee ni vijana wachache sana wadogo wenye aliki kama zako. Mimi nina kampuni nne ninazo zimiliki. Mume wangu alifariki mwaka ulio pita hivyo akanichia hizo kampuni. Moja inshuhulika na maswala ya ujenzi wa nyumba, magorofa na barabaraba. Nyingine inashuhulika na mswala ya utalii, huwa ninapokea oda za watalii wanao hitaji kuja Tanzania, kisha mimi kazi yangu ni kuwaandalia makazi. Kampuni nyingine inashuhulika na uchimbaji wa damini hii alikuwa anaisimamia mume wangu na kampuni ya mwisho inashuhulika na mswala ya usafirishaji, wa anga, barabani na majini.”

“Duuu hongera sana, uneonekana ni mfanya biashara uliye bobea kwenye mambo ya kibishara?”

“Sana, huu ni mwaka wa thelathini sasa, nipo kwenye bisha. Nilianza kufanya bisahara nikiwa na umri wa miaka ishirini hapo nilikuwa ndio nilikuwa ninamaliza kidato cha sita, saxa katika kile kipindi cha kusubiria majibu, ndio nilianzisha biashara ya kuuza ubuyu. Huwezi amani, hapo awali watu walikuwa wananiona kama chizi, ila ubuyu ulivyo anza kunilipa. Kila mmoja akajidai kuanza kuuza na yeye jambo lililo wapelekea wengi wao kushindwa kufikia malengo”

Mama huyu alizungumza kwa furaha sana huku akiendesha gari lake hili la kifahari kwa umakini sana.

“Hongera sana mama”

“Nashukuru. Lengo la kukuambia hivyo. Ninahitaji na wewe uhamasikie. Natambua ni mgeni, sasa usije ukakutana na changamoto hususasi na serikali hizi zetu za kiafrika, ukaona mambo ni magumu ukaamua kukimbia na kuachana na biashara. Hakika utakuwa umepoteza pesa, muda na pia malengo yako yatayumba na mwishowe utarudi nyuma”

“Kweli, ila siwezi kurudi nyumba. Nina degree ya biashara na nimezaliwa kwenye famili ya kibiashara. Hivyo toka nina miaka tisa, mama yangu alikuwa akiniachia kampuni yake na nilikuwa ninaiongoza vile vile alivyo kuwa akihitaji. Hadi nimefika hapa nimekomaa”

“Aisee safi sana kijana, alafu nimesahau kukuuliza jina unaitwa nani?”

“Randy Donald”

“Waooo vizuri sana. Mimi ninaitwa Jane. Kwa bahati mbaya sijafanikiwa kupata mtoto hadi kwenye umri huu. Ila natambua kwamba Mungu awezi kukupa vyote. Amenipa pesa, amaninyima mtoto na hapa nina kituo kikubwa cha watoto yatima hivyo nimekuwa kama mama kwao na ninawapa mapenzi yote wanayo stahili”

“Ni jambo zuri sana, ila pole kwa kukosa mtoto”

“Usijali Randy. Una mri gani?”

“Miaka ishirini na sita”

“Ohoo bado mdogo kumbe”

“Yaaa”

“Basi nitakuwa mama yako wa hiyari kwa hapa Tanzania. Ukipata tatizo, au ukihitaji ushauri basi wewe nifahamishe tu, nitakusaidia”

“Nashukuru sana”

Tukafika katika jengo moja la gorofa mama huyu akaingiza gari ndani ya gorofa hili na kulisimamisha katika maegesho ya magari yaliyomo chini ya ardhi. Tukashuka na kuingia kwenye lifti, moja kwa moja tukaelekea gorofa ya nane.

“Hapa ndipo zilipo ofisi zangu, sasa hivi wafanyakazi wamesha ondoka hivyo usiogope kuona kuna ukimya”

“Usijali”

“Karibu Randy”

Mama huyu alizungumza hukua kifungu mlango wa ofisi yake. Akanikaribisha na nikaa kwenye moja ya kiti katika ofisi yake hii. Akatoa mikataba inayo husiana na nyumba yake. Nikaisoma na nilipo ridhia, nikatoa kiasi cha pesa na kumkabihi.

“Miezi miwili nitakupa ofa, wewe lipia miezi kumi”

“Nashukuru sana mama”

Nikafanya malipo yanayo takiwa ambayo ni dola elfu hamsini. Mama huyu akanihesbu pesa kwenye mashine maalumu ya kuhesabia pesa. Zilivyo kamilika tukaandikishana mkataba huu kisha akanikabidhi funguo za nyumba.

“Naamini vitu vya ndani vitakuwa salama, kwani nimepangisha mtu salama”

“Usijali mama, sina mtoto ambaye unaweza sema anaweza kuharibu vitu vile”

“Sawa. Ngoja nikupitishe Mlimani City, nina imani kwamba kuna vitu utakuwa unahitaji kununua kwa ajili ya ndani kwako”

“Sawa mama”

Tukaondoka na mwana mama huyu. Japo kuna foleni barabarani, ila tukafanikiwa kufika katika jengo hili lenye maduka mengi sana. Mwanamama huyu akaanza kunitembeza kwenye maduka haya, nikanunua baadhi ya vitu vya kupika. Tulipo maliza manunuzi, tukarudi kwenye nyumba aliyo nipangisha. Tukasaidiana kushusha vitu ndani ya gari na kuviingiza ndani ya nyumba hii.

“Naomba sasa mimi niondoke kwa maana, nimechelewa kurudi nyumbani kwangu na unavyo jua ukiwa mfanya biashara basi kuna mambo ya kutekwa au kuvamiwa na majambazi”

“Kwenye hii nchi mambo hayo yapo?”

“Sana tu na hapa nilipo nina bifu na mfanya biashara mmoja, yaani tunafikia hatua ya kuwindana kuuana”

“Mmmmm”

“Yaaa, kwa hiyo ndio maana nahitaji kurudi nyumbani kwangu mapema sana”

“Unaonaje ukatafuta walinzi?”

“Walinzi mimi sitaki. Unajua ukiwa na mlinzi, adui yako anaweza kumshawishi mlinzi wako na kupitia mlinzi wako akakuua kirahisi sana, ndio maana nilifukuza walinzi wangu wote, nimebaki mimi kama mimi napambana kama mwanamke jasiri”

Mama huyu alizungumza kwa msisitozo na kweli anaonekana ni mwanamke jasiri na anaye jiamini na maamuzi yake.

“Kama kuna mambo kama hayo, basi nakuomba nikusindikize kwako. Tafadhali nitarudi mimi mwenyewe”

“Hapana Randy nisikusumbue?”

“Kama vile ulivyo nisaidia, basi acha na mimi nikusaidie. Siwezi kumuacha mama yangu audhurike ikiwa mwanaye wa kiume nipo hapa”

Nilizungumza kwa utani kidogo na kumfanya mama huyu kutabasamu. Nikaingiza begi langu la pesa ndani ya chumba changu. Nikalifungia kwenye kabati moja kubwa la chumba, kisha nikatoka nje. Tukaanza safari na mama huyu huku saa iliyomo ndani ya gari hili ikionyesha sasa hivi ni saa nne kasoro usiku. Tukafika katika jumba moja kubwa na mama huyu akasimamisha gari lake mbele ya geti hili. Gafla gari moja kubwa jeusi likasimama nyuma ya gari letu.

“Randy tumevamiwa”

Mama huyu alizungumza huku akichomoa bastola yak echini ya siti ya gari lake. Nikampokonya bastola hiyo nikajirusha siti yamba ambapo kioo chake tayari kimeshaanza kutobolewa kwa kupigwa risasi, nani nikajiandaa tayari kwa kujibu mashambulizi ya watu hawa walio tuvamia na huyu mama.

***************


Hahaaa Randy mume mwangu acha dharau bwana” Tukashuka kwenye gari hili tukasimama mlangoni, nikatazama eneo la juu la mlango huu kuna kamera ndogo. Bi Jane akaminya kitufe cha kengelea, mlango ukafunguka na hatukuona mtu yoyote aliye tufungulia. “Mbona hakuna mtu?” “Twende bwana” Tukaingia kwenye seble hii liyo pangwa vizuri. Tukaingia kwenye kordo yenye vyumba kadhaa, tukatembea hadi kwenye moja ya chumba. Bi Jane akaingiza namba za siri katika batani maalumu zilizopo hapa mlangoni kisha mlango ukafunguka. Tukaingia ndani ya chumba hichi na kukutana na mzee mmoja wa makamo kidogo. Amevalia miwani kubwa na koti kubwa jeusi. “Jane habari” “Salama mzee wangu, Randy huyu ni rafiki yangu wa muda mrefu ni Profesa. Profesa huyu ni Randy, ni yule kijana niliye kueleza mchana” “Sawa sawa karibuni sana” Profesa alizungumza huku akifunua moja ya pazia humu ndani. Nikaona lifti, tukaingia wote watatu na lifti hii ikaanza kushuka chini taartibu. Tukafika kwenye moja ya ukumbi mkubwa sana ambao umejaa vitu vingi sana ikiwemo magari jambo ambalo lilinifanya nishangae sana. Bi Jane akanikonyeza huku akitabasamu, kwani kile nilicho kuwa nimefikiria kwenye kijumba hichi kidogo kumbe sicho. “Karibu Randy, naomba mkono wako wa kulia” Nikamakabidhi profesa, akanichoma sindano ndogo kwenye moja ya kidole, akatoa kichupa kidogo kwenye mfuko wa koti lake na kukamulia kidogo damu yangu. “Pole” Profesa alizungumza huku akiondoka katika eneo hili, nikabaki na mshangao sana kwani sijatambua ni kwa nini Profesa ameamua kuchukua damu yangu



“Maana ya kufanya hivyo ni nini?”

“Ninahitaji kufahamu wewe ni nani”

Profesa alizungumza huku akiweka kichupa hicho kwenye moja ya kifaa kinacho zunguka kwa haraka. Akakaa kwenye computer yake kubwa na kuanza kuminya minya batani. Nikashuhudia picha yangu ikitokea kwenye computer yake kitu kilicho nifanya nishangae. Profesa akaiweka vizuri miwani yake huku akitazama compture yake baada ya dakika kadhaa akatugeukia mimi na Bi Jane.

“Unaitwa Randy nani?”

“Randy Donald Bush?”

“Uongo”

Profesa alizuungumza kwa ukali kidogo hadi nikapatwa na mshangao.

“Baba yako halisi ndio nina muhitaji?”

“Ndio huyo na ninambua yeye ndio amezaa na mama yangu Yemi”

“Tazama kule”

Profesa alinionyesha tv kubwa sana iliyopo kwenye moja ya ukuta wa hichi chumba. Sikuamini macho yanngu mara baada ya kuona vipomo vya DNA yangu vinafanana sawa sawa na DANY gaidi ambaye ninaamini kwamba yeye ndio aliye niulia baba yangu.

“DNA zenu ni sawa na Dany, ndio maana nilihitaji kukujua wewe ni nani, kwani nilipo kuona tu nilihisi hilo jambo”

Preofesa alizungumza huku akinisoge, akanishika bega langu la mkono wa kulia na kusimama pembeni yangu huku sote tukiwa tunatazama tv hii kubwa. Mwili wangu wote ukazizima, uwezo wa kuzungumza ukaniisha kabisa, mawazo mengi ambayo niliyapanga juu ya Dany yote yakaanza kububujika moyoni mwangu.

“Sikuzote Dany alihitaji kuona mwanaye una uwezo gani”

“Ki….v..p profess”

Niliuliza huku nikiwa nimeshikwa na kigugumizi.

“Dany anafahamu uwepo wako hapa Tanzania na bado upo kwenye vipimo vyake, na ukifanikiwa utakuwa karibu yake”

“Professa kwa kweli sielewi kitu unacho kizungumza”

“Siku moja utaelewa nini nazungumza. Ehee Jane mumekuja kufanya nini?”

“Ahaa professa, unataka kusema kwamba umesahau?”

“Sawa silaha zipo sasa sijajua mtumiaji anahitaji silaha za aina gani?”

“Nahitaji bastol ambili, magazine kumi na ziwe zimejaa risasi?”

Nilimjibu Professa huku nikimtazama usoni mwake.

“Kuna bastola inaitwa Beretta M9-22 uwezo wa magazine yake moja ni mizunguko kumi na tano ya risasi kwa magazine moja”

“Ina uwezo mzuri?”

“Ndio uwezo wake ni mzuri na ina nguvu”

Profesa alizungumza huku akiondoka karibu yangu, akafungua mlango wa moja ya kabati akatoa bastola hiyo na magazine zake tano. Akanikabidhi na nikaanza kuichunguza bastola hii na kweli ipo vizuri.

“Kwa leo ningeomba kazi unayo hitaji kwenda kuifanya ukaihairisha”

“Kwa nini?”

“Nahitaji kuchukua vipimo vya nguo unazo zivaa. Nahitaji kukushonea suti, suti ambazo kwanza, haiingii risasi, mbili itakupa uwezo mzuri wa kufanya kazi yako unayo taka kwenda kuifanya”

Nikamtazama Bi Jane kwa sekunde kadha, akanikonyeza akimaanisha kwamba nikubaliane na kile anacho kizungumza Professa.

“Sawa”

“Kitu kingine, huwezi kuvamia maadui zako kama vile unakwenda kuvamia banda la kuku. Moja unatakiwa kufahamu mfumo mzima wa hii nchi, jambo ambalo wewe hujalifahamu. Mfumo wa hii nchi, endapo utakamatwa kama jambazi, adhabu yake ni moja tu. Unapigwa risasi kichwa na unakufa hapo hapo”

Professa alizungumza, huku akinitazama usoni mwangu.

“Japo sheria hiyo kwa watu wa kawaida hawawezi kuifahamu, ila kwa sisi watu tunao ijua serikali tunalifahamu hilo. Jambo jengine huwezi kuipelekea sura yako hadharani, kumbuka wiki kadhaa zilizo pita vyombo vya habari vilitangaza kutafutwa kwako, japo ile habari ilipotelea hewani, ila kumbuka kwamba umesha ingia kwenye listi ya wanao sakwa”

“Sasa nitafanya nini Professa?”

“Kwa kazi yoyote unayo taka kuifanya ni lazima surayako iweze kufanyiwa marekebisho ya hali ya juu, yote ni kuhakikisha kwamba unaificha sura yako halisi”

“Analo lizungumza Professa ni jambo muhimu msikilize kwa umakini Randy”

“Sawa nimewaelewa”

“Leo utalala hapa, utafanya yale nitakayo kueleza na kazi yako utaiana kesho, muda ambao nitakupangia”

“Sawa, je Jane naye?”

“Ataondoka”

“Jane utaweza kurudi peke yako?”

“Ndio usijali katika hilo. Gari hili la laeo tulilo kuja nalo alilfanyia marekebisho Professa na halina uwezo wa kuingiza risasi ndani, hivyo hata nikivamiwa na maadui zangu bado nitakuwa nipo salama”

“Ni kweli Professa?”

“Ndio hakuna tatizo juu ya hilo”

“Sawa”

Bi Jane akanisogelea, akanishika kiuno changu taratibu na kunibusu mdomoni mwangu.

“Nitakuja kesho kukutazama mpenzi wangu”

“Sawa hakikisha kwamba unakuwa salama sawa”

“Usijali mpenzi wangu”

Bi Jane akaniachia, akamuaga Professa na wakaondoka katika eneo hili.

“Baba na mwana tabia zenu ni moja”

Professa alizungumza huku wakiwa wamejawa na furaha sana usoni mwake.

“Kivipi mzee?”

“Utajua ni kivip, siku itakapo fika”

Nikabaki nikiwa na maswali mengi sana, ambayo sikuweza kuatapatia majibu yoyote na kitu kibaytya zaidi sifahamu imekuwaje kuwaje Dany na mama yangu walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi. Usiku mzima huu Profesa akautumia katika kuniandalia suti mbili ambazo katika mashono yake ameyashonea na kitambaa maalumu ambacho hakiingizi risasi yoyote. Professa akaanza kunionyesha maadui wote wa Jane ambao ninatakiwa kuwaua kiakili na si kama vile nilivyo kuwa nimepanga katika kuifanya kazi hii.

“Nahitaji uwe professional killer na si muuaji wa kawaida kawaida”

“Sawa Professa”

“Pumzika kesho mchana nitakupa maelekezo”

“Sawa, ila nina swali nahitaji kuuliza”

“Uliza”

“Unamfahamu mama yangu?”

“Ndio nina mfahamu?”

“Pia baba yangu unamfahamu?”

“Ndio ninamfahamu na nimtu amabye anapokea msaada mkuwa sana kutoka kwangu”

“Unaweza kunisaidia kufahamu ni kitu gani ambacho kilitokea kati ya wazazi wangu hadi leo hii hawapo pamoja?”

Professa akanitazama kwa muda kisha akatabasamu.

“Ni historia ndefu sana, ila siku nitakukutanisha na baba yako. Yeye nahisi ana historia yote iliyo tokea wewe na mama yako. Nenda kapumzike ujiandae na kazi ya kesho”

Professa alizungumza huku akinishika bega la mkono wangu wa kulia na akakaa kwenye moja ya kiti chake. Nikaondoka ukumbini hapa na kuruidi katika eneo la juu ilipo nyumba hii ndogo. Nikaaa kwenye moja ya sofa hapa sebleni na kujilaza, nikajitahidi kutazama vipindi vinavyo endelea kwenye televishion, ila kutokana na uchovu nilio nao nikajikuta nikipitiwa na usingizi na kulala usingizi fofofo.

***

Muda wa kwenda kuifanya kazi yangu ikawadia. Nikaivaa suti ambayo Profesa amenishonea.

“Hii suti kwenye eneo la kifuani ina kamera ndogo sana. Ukiwa katika kazi yako. Mimi huku nitakuwa nina shuhudia kila kitu ambacho kitakuwa kianaendelea, Umenielewa?”

“Ndio”

“Hii ni gari ambayo utaitumia. Ni BMW i8. Gari hii ina mwendo mkali sana, nimeinyanyua kidogo kwa ajili ya barabara zetu za hapa Tanzania. Haiingii risasi, hata tairi zake haziingii risasi.”

Professa alizungumza huku akinionyesha gari hii ndogo nzuri na ya kifahari.

“Gari hii kama upo mita mia tano, kwa kutumia hii simu, unaweza kuliendesha kwa kutumia hii simu hadi sehemu ulipo na ukaingia na kuondoka zako”

“Ngoja kwanza Professa unataka kuniambia ninaweza kuindesha kwa simu?”

“Ndio, kama vile unavyo endesha magari kwenye playstation ndivyo jinsi unavyo weza kuliendesha hili gari”

“Duuu!!”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na mshangao sana. Nikafungua mlango mmoja wa gari hili ambao unafunguka kwa juu. Nikaingia ndani huku nikiwa na furaha moyoni mwangu.

“Kwenye gari hili kuna simu ambayo imeunganishwa simu hiyo niliyo kupatia sawa”

“Sawa Professa”

“Kwa kupitia ramani iliyopo katika gari lako kwenye hiyo tv ndogo. Inaonyesha kila sehemu ambayo yupo adui yako na sura zao zote zipo kwenye hiyo tv ambayo ina mfumo wa kuhifadhi vitu kama simu”

“Sawa sawa”

“Chukua hizi ni ndevu za bandia, zivae usoni mwako. Ni ngumu sana mtu kuifahamu sura yako ukiwa aumevaa hizo ndefu”

“Nashukuru”

Nikafanya kila kitu alicho nielekeza Professa. Nikaagana na bi Jane kisha Professa akaminya moja ya batani kweye ukuta. Taratibu eneo la moja ya ukuta ikafunguka na nikaona sehemu ya kupitisha hii gari. Nikalitoa hili gari na kutokea eneo la nyuma ya hii nyumba. Ambayo ina geti jengine kubwa. Geti hili likafunguka na nikaondoka katika eneo hili. Ramani iliyopo katika gari hili inanionyesha kati ya maadui walio tuvamia wiki kadhaa zilizo pita. Ramani hii ikanipeleka hadi kwenye moja ya ukumbi wa starehe. Nikasimamisha gari langue neo maalimu la maegesho na kuwafanya watu wengi kulishangaa kwani ni miongoni mwa magari ya kisasa zaidi katika eneo hili. Nikaziweka vizuri batsola zangu mbili kiunoni, kisha nikajifunika koti langu vizuri la suti, nikatoka ndani ya gari hili. Wadada wawili wakanisogelea huku wakionekana wakiwa wamejawa na furaha.

“Unahitaji huduma yetu kaka?”

“Hapana”

Niliwajibu kwa ufupi kisha nikawapita na kuwaacha wakiwa na mshangao mkubwa. Nikakaa kwenye moja ya kiti, nikatoa simu yangu na kutazama ni eneo gani alipo adui namba moja ambaye nimemfwata hapa kwenye huu ukumbi wa starehe. Nikamuona akiwa amekaa na kundi la wasichana wapatao sita huku juu ya meza wakiwa wameweka vinywaji vingi sana. Nikasoge akatika meza ya karibu yake, nikaaa huku nikitazama watu wa karibu na meza yangu, kila mtu nikamuona akiendelea na shuhuli yake. Nikachomoa bastola yangu taratibu kwenye kiuno changu, nikauweka mkono wnagu chini ya meza huku bastola nikiwa nimeielekezea kwa jamaa huyu. Nikatoka kiwambo cha kuzuia sauti, kisha taratibu nikakifunga kwenye bastola yangu. Kitu kinacho nifanya nishindwe kumuua jamaa huyu kutoka hapa nilipo ni msichana aliye mkalia mapajani mwake kwani ameziba sehemu kubwa ya kifuani mwake. Nikiwa katika mawazo ya kutafuta ni jinsi gani ninaweza kumuua, jama akanyanyuka huku akiyumba nyumba. Akaanza kushikwa mkono na msichana huyo na wakaanza kuelekea eneo la vyoo vya kiume. Nikairudisha bastola yangu kiunoni mwangu, nikaanza kuwafwata kwa nyuma hadi chooni. NIkamkuta msichaba huyu akiwa amechuchumaa huku akinyonya jogoo wa mwanaume huyu. Hawakujali hata kuniona eneo hili. Nikasimama katika sinki la kunawia mikono, nikatoa bastola na kwa umbali niliopo nikampiga risasi ya kichwani na kumfanya anguke chini na mwanamke huyo akabaki akiwa amejawa namshangao mkubwa sana. Kutokana bastola yangu haijatoa mlio wa risasi ikawa ni ngumu kwa mtu kutambua kwamba nimehusika na kifo hicho. Nikatoka chooni humu na kurudi kwenye gari, nikaondoka eneo hili huku nikielekea kwa adui mwengine ambaye hayupo mbali na eneo hili.

Ramani ikanielekeza hadi kwenye kituo kikubwa cha polisi na adui inaoneakana yupo ndani ya kitua hicho. Nikatazama saa yangu ya mkononi na sasa inanionuyesha ni saa sita kasoro usiku. Nikatazama kituo hichi na kinaonekana kuimarishwa vizuri ulinzi wake. Kioo cha gari langu kikagongwa kidogo na polisi aliye shika silaha mkononi mwake, nikajiweka vizuri koti langu na kuficha bastola zangu.

“Habri yako ndugu”

Askari huyu alizungumz ahuku akinitazama usoni mwangu.

“Salama tu kiongozi”

“Samahani hauruhusiwi kusimamisha gari katika eneo hili, naona kuna kibao umekiona pale mbele”

Asakri huyu alizungumza huku akinionyesha kibao kidogo kilichopo mbele yangu.

“Ohoo samahani sana”

“Bila samahani”

Nikawasha gari na kuanza kuondoka eneo hili. Nikiwa mita chache kutoka kilipo kituo cha polisi, kwenye ramani yangu, iliyomo ndani ya hili gari nikaanza kumuona adui yangu akiondoka taratibu katika eneo la kituo cha polisi, kwa kupitia kioo changu cha pembeni nikashuhudia gari ikiondoka katika eneo la mbele la kituo hichi cha polisi, kwa bahati nzuri gari hili linakuja eneo nililopo. Gari hili kikapita pembeni yangu, taratibu nikaanza kuwafwatilia huku nikiwa makini sana kuhakikisha kwamba hawastukii kuona nina fwatiliwa. Gari hili likasimama kwenye duka moja dogo la dawa. Akashuka mwanaume mmoja mrefu kiasi huku akiwa ameongozana na mtoto mdogo wa kike, jambo lililo nipa kigugumizi cha kwenda kumuua jamaa huyu mbele ya mtoto wake.

“Randy vipi muue”

Niliisikia sauti ya bi Jane kwenye simu maalumu ya gari hili.

“Hapana siwezi kumuua sasa hivi”

“Kwa nini?”

“Ni baba, kwa leo ninahitaji tumsamehe ila nitampa fundisho leo tu”

Mara baada ya kuzungumza hivyo nikashuka kwenye gari na nikaanza kutembea kwa kujiamini huku nikimfwata jamaa huyu ndani ya duka hili alilo ingia.



Nikaingia ndani ya duka huli ambalo lina bidhaa za kila aina na kila mteja anapita katika eneo lenye bidhaa yake, anachukua anacho kihitaji kihitaji. Nikamfwata kwa nyuma jamaa huyu huku akiwa emeshika mtoto wake mkono.

“Hei habari”

Nilizungumza huku nikitabasamu, jamaa huyu akageuka na kunitazama. Nikampa mkono wangu wa kulia na taratibu akaupokea, nikaanza kumbana mkono wake kwa nguvu huku nikimkazia macho, jambo ambalo mtoto wake hakulifahamu.

“Ahaa unanikumbuka”

Nilimuuliza huku nikizidisha maumivu ya kumbana mkono wake. Jamaa akajitahidi kuubana mkono wangu, ila kutokana mimi ndio nimemuwahi kumbana mkono akashindwa kabisa kunibana.

“Saa sita usiku katia geti moja la mmoja wa matajiri, umekumbuka”

Jamaa macho yakamtoka sana huku jasho likimwagika usoni mwake.

“Candy kachukue pipi pale ninakuja”

“Sawa baba”

Mtoto huyu akaondoka na kuniacha na baba yake.

“Wewe ni nani?”

“Hupaswi kunijua, ila nina kujua. Sasa onyo nimekusamehe leo, endapo utarudi tena kufwatilia maisha ya Bi Jane, nitaanza kumuua mwanao umenielewa?”

“Nd….nd…i….ooo”

Janaa alijibu kwa kigugumizi huku mwili mzima ukimteteme.

“Wewe tu kwenye hii list ndio utapona kwa sababu una mtoto wako na nimempenda, ila ukirudia. Nitahakikisha kwamba humalizi siku utakuwa umesha wafwata wezako walio tangulia kufa”

Nilizungumza huku nikitabasamu. Kamera nyingi zilizopo ndani ya duka hili zimenifanya nisitoe bastola yangu.

“Kwaheri”

Baada ya kumaliza kuzungumza hivyo nikaondoka, nikaingia kwenye gari langu na nikaondoka eneo hili kwa kasi sana. Nikatazama kwenye ramani yangu ni nani ambaye anafwatia kufa.

“James”

Nilizungumza huku nikimtazama picha ya James mwenyewe kwenye simu yangu. Umbali uliopo kutoka hapa hadi alipo James ni kama kilomita moja hivi. Kutokana ni usiku, hakuna foleni ya magari mengi barabarani. Nikafika nyumbani kwa James. Ni nyumba nzuri ya kisasa, iliyo zungushiwa geti. Nisimamisha gari pembezoni mwa geti hili, nikashuka huku nikijiweka sawa koti langu la suti. Nikajaribu kusukuma kigeti kidogo kwa bahati nzuri kikafunguka, mziki mkubwa unao endelea ndani ya nyuma hii ukaniashiria kabisa hivi sasa hivi kuna sherehe inayo endelea ndani. Nikatazama eneo la nje ya nyumba hii na kukuta gari zipatazo nne, huku katika mlango wa kuingilia ndani kukiwa na viatu kadhaa vya wadada.

Nikatembea kwa kunyata hadi kwenye moja ya dirisha, huku nikiwa nimeichomoa bastola tangu niliyo ifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Nikawaona wadada karibia kumi wakiwa uchi, huku wakicheza mziki na James mwenyewe naye akiwa uchi na kazi yake ni kuyapiga piga makalio ya wasichana hao.

‘Masikini ukiaambiwa nitakuua mbwa wewe’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikitazama jinsi anavyo lama makalio ya msichana mmoja huku mkooni mwake akiwa ameshika chupa ya pombe kali. Simu moja mezani ikaita, James akaitazama simu hiyo, kisha akanza kutembea kuelekea mlango wa kutokea huku nje, nikajibanza kwenye moja ya kona ambayo sio rahisi kwa yeye kuniona.

“Vipi Deve?”

Niliisikia sauti ya James.

“Nani?”

“Ahaa kaka acha woga, hakuna wa kutugusa sisi bwana si unajua serikali ipo mikononi mwetu na unatishwa tishwa na wahuni tena super makert rafiki yangu na wewe una tishika. Hahaaa”

James alizungumza kwa kujiamini na nikatambua moja kwa moja kwamba anaye zungumziwa hapa ni mimi.

“Yupoje?”

Nikajitokeza kwenye sehemu niliyo kuwa nimejificha huku nikimnyooshea bastola usoni mwake.

“Yupo hapa kaka”

Nikasogelea James na kumpokonya simu yake huku mwili mzima naye ukimtetemeka kwa woga.

“Nilikusamehe ili uwe salama ila bado unaendelea kutoa taarifa za msamaha wako si ndio?”

Niliendelea kuzungumza kwa kujiamini. Nikakata simu na kumpiga James risasi ya kichwa na akaanguka chini mzima mzima. Kutoka na risasi niliyo ifyatua haitoi mlio wa aina yoyote, ikawa ni ngumu sana kwa wasichana walimo ndani kusikia chochote na isitoshe wanacheza mziki mkubwa sana. Nikampiga risasi tatu za kifuani kisha kwa haraka nikatoka ndani humu huku nikiwa na simu yake. Nikaingia ndani ya gari na kuanza kuondoka.

“Professa, nimefanikiwa kumuua mtu wa pili”

“Nimeona sasa cha kufanya wewe rudi huku, kwa hatua hiyo uliyo ifanya ni lazima wataweweseka na wakihitaji kukutafuta wewe ndio itakuwa ni kazi rahisi ya wewe kutekeleza matukio yako”

“Sawa Professa”

Nikanza safari ya kurudi nyumbani kwa Professa ambapo ni mkoa wa Pwani. Ikanigarimu lisaa kufika nyumbani kwake, kama nilivyo toka ndivyo jinsi nilivyo ingia katika nyumba hii. Nikashuka kwenye gari huku nikiwatazama Professa na Bi Jane wanao nisubiria.

“Hii simu ya James, aliyo kuwa akizungumza na jamaa niliye muacha hai”

Nilizungumza huku nikimkabidhi Professa simu hiyo.

“Kazi nzuri, kwa kupitia hii simu tutapata vitu vingi na uzuri ni kwamba James ndio mkuu wao”

“Ahaaa sawa sawa”

Bi Jane akanivua koti langu la suti na kulikunja kidogo kwenye mkono wake wa kushoto na kulifanya lining’inie.

“Inabidi upumzike kwa kwazi nyingine”

“Sawa”

“Twende mpenzi wangu”

Bi Jane alizungumza kwa sauti ya upole huku tukiondoka eneo hili. Tukaingia kwenye lifti na taratibu tukaanza kupandisha juu. Tukaingia kwenye moja ya chumba kilicho andaliwa vizuri.

“Unajua mpenzi wangu nilikuwa nimejawa na woga mwingi sana nilipo nje ya hapa?”

Bi Jane alizungumza huku akinishika kiuno changu kwa nyuma.

“Hahaa, kwa nini?”

“Mmmm watu ambao umewafwata ni hatari, ni watu ambao hapa Dar es Salaam wao ndio madon. Hakuna polisi ambaye anazungumza juu yao. Wewe mwenyewe ulisikia kwamba wameishika Dar es Salaam”

“Usijali mpenzi wangu, siwezi kufa kirahisi namna hii”

“Mmmm kweli?”

“Ndio, niamini”

Nilizungumza huku nikimvuta Bi Jane mbele yangu, taratibu nikaanza kumnyonya midomo yake. Akaliweka koti hili kitandani huku akinifungua vifungo vya shati lamgu taratibu. Nikamkalisa kitandani, huku mikono yangu ikiwa na kazi ya kupita kila kona ya mwili wake. Ndaya ya sekunde stini, kila mtu akajikuta akiwa hana nguo hata moja kabisa. Tukaanza mtanange huu wa kukata kwa shoka, mtanange ulio jaa kila aina ya mapigo. Mapigo ambayo nina uhakika wa asilimi mia moja kwamba Bi Jane hakuwahi kukutana nayo kwenye maisha yake yote.

“Nakupenda sana Randy”

Bi Jane alizungumza mara baada ya mtanange huu kuisha, huku akiwa amenikumbatia kwa nguvu na machozi ya furaha yakimwagika usoni mwake.

“Ninakupenda pia”

“Kweli Randy?”

“Niamini mimi”

“Nashukuru kusikia hivyo Randy wangu”

Nikajilaza pembeni yake, kisha na yeye akakilza kichwa chake pembeni yangu, usingizi taratibu ukaanza kunipitia na kujikuta nikilala usingizi fofofo.

***

“Randy”

Niliisikia sauti ya Bi Jane ikiniita.

“Mmmmm”

Niliitikia huku nikifumbua macho yangu, nikamkuta akiwa amekaa pembeni ya kitanda.

“Kumepambazuka, twende ukapate kifungua kinywa”

“Saa ngapi sasa hivi?”

“Saa nne asubuhi”

“Duuu pamewahi kupambazuka ehee?”

“Hapana, sema jana usiku ulichelewa kulala”

“Ahaa, sawa mpenzi wangu, ninakuja”

“Amka sasa hivi bwana”

Bi Jane alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia, nikaamka huku nikiwa na wenge kubwa la usingizia. Nikaingia bafuni kuoga, nikatoka chumbani humu na kukuta akiwa amesha niandalia nguo za kuzivaa alizo ziweka juu ya kitanda.

“Nimekununulia hizo nguo, sijajua kama zitakutosha?”

Nikaanza kutazama nguo moja baada ya nyingine, nikavaa na kwa bahati nzuri zinanitosha mwilini mwangu. Tukatoka ndani humu na kumkuta Professa sehemu akiwa amekaa katika moja ya kiti kilichopo pembeni mwa mwez aya chakula.

“Habari Professa”

“Salama, sana naona umeamka na furaha sana”

“Kiasi Professa, sio sana”

“Vipi lakini, unaendeleaje?”

“Safi”

Bi Jane akatuandalia kifungua kinywa kishaa katukaribisha. Kabla hatujaanza kunywa mlango wa nyuma hii ukangongwa kwa nje na kujikuta nikistuka sana. Profesa akatoa rimoti ndogo kwenye mfuko wa shati lale alilo livaa kisha akaminya moja ya batani na mlango ukafunguka.

“Professa unajua ni nani anaye gonga?”

Professa akatabasamu huku akinitazama usoni mwangu, nikayaelekeza macho yangu mlangoni, akaingia binti aliye nikoromea siku walipo niokoa kwenye ajali. Akaingia DANY na kujikuta nikisimama huku mapigo yangu ya moyo yakizidi kuienda kasi. Mwili mzima ukasisimka huku ukiishiwa nguvu kabisa.

“Professa nimekuja muda sahihi ehee?”

Kadada haka kalizungumza huku kakikaa kwenye moja ya kiti.

“Ndio karibu Jojo”

“Nashukuru Professa”

Tukatazamaa na Danya kwa sekunde kadhaa. Akatabasamu huku akitufwata hapa mezani.

“Dogo hujambo?”

Nikashindwa hata kumjibu Dany zaidi ya kumkodolea macho, akanipa mkono wake wa kulia, nikautazama kwa sekunde kama arobaini hivi, kisha nikampa mkono wangu, akanibana kama nilivo kuwa nimembana jamaa wa jana dukani. Akaniachia huku akitabasamu akazunuka na kukaa kiti cha mbele yangu na tukawa tunatazamana. Taratibu Bi Jane akanishika mkono na kunikalisha chini. Ukimya ukatawala ndani humu huku akilini yangu ikishindwa kabisa kujua ninazungumza kitu gani kwa huyu Dany ninaye muona hapa.

“Inaonekana umestuka sana kuniona hapa?”

“Sikumueleza kama chai ya asubuhi hii utajumuika nasi”

“Ndio maana”

“Mdogo wangu kumbe ni mzuri”

Jojo alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Mazungumzo yao nina yasikia vizuri, ila ujasiri wa kuwajubu ninashindwa kabisa.

“Kama wewe, na Jojo nilikuambia nahitaji kukuoa.”

“Hahaaa…….Professa umesha zeeka bwana”

“Hahaaa…..ng’ombe mzee hazeheki maini”

“Wapi, goli moja chali”

“Hahaaaaaa”

Professa na Jojo wakaendelea kucheka.

“Dogo kula, acha kuduwaa sana”

“Baby jikaze ule”

Bi Jane alizungumza kwa sauti ya upole na kumfanya Jojo na Dany kumtazama kwa mshangao.

“Baby!!?”

Jojo aliuliza kwa mshangao mkubwa sana. Nikanyanyuka kwenye kiti changu na kuanza kutembea kuelekea chumbani.

“Randy…..Randy”

Bi Jane aliniita ila sikugeuka, nikaingia ndani, baada ya mud kidogo bi Jane naye akaingia ndani ya chumba hichi huku naye akiwa amejaa na wasiwasi.

“Unalifahamu juu Dany kuja hapa?”

“Hapana, ni Professa yeye mwenyewe mpenzi wangu. Mimi sifahamu kitu chochote”

“Kwa nini analeta watu ambao……..”

Nikashindwa kuimalizia sentensi yangu baada ya kumuona Dany akiwa amesimama mlangoni mwa chumba.

“Toka nahitaji kuzungumza na dogo”

Dany alizungumza huku akitutazama, bi Jane taratibu akanyanyuka kabla hajapiga hatua yoyote nikamshika mkono wake.

“Kama unahitaji kuzungumza na mimi, atakaa humu ndani na kusikiliza kila unacho kihitaji kukizungumza”

Dany kwa haraka akachomoa bastola yake kwa nyuma na kumuelekezea bi Jane usoni mwake.

“Huwa sina huruma na mtu yoyote, naamini ulisha wahi kunisikia na kama si kunisikia basi ulisha wahi kusoma historia yangu. Toka mara moja kabla sijafumua ubongo wako kama nilivyo mfanya K2”

Dany alizungumza kwa msisitizo, taratibu bi Jane akauachanisha mkono wake na wangu kisha akatoka ndani humu na kutuacha wawili mimi na Dany tu.


 Dany akaufunga mlango kwa ndani kisha bastola yake akaichomeka kiunoni mwake kwa nyuma. Taratibu akavuta moja ya kiti cha mbao humu ndani na kukaa. Kwaishara akanionyesha nikae kwenye kitanda, sikuwa na pingamizi zaidi ya kukaa. “Unakumbuka siku tuliyo kutana kwenye hoteli mulivyo panga kumteka makamu wa raisi wa Marekani” “Ndio” “Unakumbuka nilikuambiaje?” “Ndio ninakumbuka” “Nifanye kwa ufupi haya maelezo yangu. Kataa, ukubali, ila tambua kwamba mimi ndio baba yako. Mimba ambayo Yemi aliibeba nilimpa mimi na amekuzaa wewe na siku zote aliamua kukuficha ili nisiweze kufahamu ni wapi ulipo sasa upo mikononi mwangu, huto kwenda kwake tena umenielewa” “Heeee?” “Hakuna cha heeee wala haahaa…Mimi ni baba yako na nimesha zungumza, kinacho fwata ni utekelezaji” “Nina mamuzi yangu kumbuka hilo na tambua kwamba umenikuta kwenye ukubwa wangu na si utoto sawa. Nina maamuzi ya kupanga ni nani nimfwate na nani nisimfwate. Nimeachagua njia yangu ya kuishi kama mwanaume hivyo musinipangie, si wewe wala mama. Hivi nyinyi ni watu wa aina gani eheeee, mama anaishi kwa amri amri za kipumbavu. Wewe unaishi kwa amri za kijinga siwaelewi munajua” Nilizungumza kwa ukali huku machozi yakinitoka usoni mwangu. Dany akacheka kwa dharaua na kunifanya nizidi kupangwa kwa hasira sana. “Mama yako ndio mpumbavu, mama yako hahaaa kweli ni mpumbavu tena zombie kabisa” “Koma kumtukana mama yangu unanisikia” Nilizungumza kwa hasira huku nikisimama na kumsogelea. “Unataka kunipiga au?” Dany alizungumza kwa dharau huku akisimama na kunitazama usoni mwangu. “Unahisi kwamba siwezi kukupiga si ndio” Nilizungumza huku kifua changu kikituna kwa hasira. “Hahaahaaaa haki ya Mungu watoto wa wapi nyinyi, munao wapandishia wazazi wenu vifua,wewe” 


Nikamuga Professa kwa kumpa mkono na nikaanza kitembea kuelekea nje. Tukatoka nje ya nyumba hii na kumkuta Jojo akiwa ndani ya gari aina ya Range Rover. “Unashangaa nini, unataka nikufungulie mlango kama raisi” “Ninaingia bwana, ikiwezekana pia nitakataa kuongozana na wewe. Uhisi kufanya ubabe wako mbele yangu ni kunipenda, huko ni kunipoteza katika upendo wa kukupenda wewe” Dany akanitazama, kisha akanigusa pua yangu, kitendo kilicho nikera sana. “Niache bwana” Nilizungumza huku nikiutoa mkono wake. Tukaingia ndani ya gari na Jojo akaanza kuendesha gari hili taratibu. “Tunaelekea wapi?” “Nyumbani?” “Ni wapi?” “Mbona una maswali mengi, umekuwa mkuu wa kitua cha polisi au?” Nikakaa kimya huku nikimtazama Dany usoni mwake kwa hasira.Safari hii ikazidi kusonge mbele huku tukiwa tunapita mkatika msitu jambo lililo nipa mashaka kidogo. “Huku ni wapi?” “Nyumbani” “Nyumba ndio iwe msituni kiasi hichi, munaishije?” “Tunaishi kama tunavyo ishi” “Kwa nini wewe na mama majibu yenu ni ya karaha sana eheee?” “Usinifananishe mimi na mama yako siku hata moja” “Muna fanana, kataa, kubali ila wewe na mama mupo sawa tu” Dany akanitazama kwa macho ya hasira ambayo sikuweza kuyahofia kwa chochote kwa maana tabia ya kuwa na mahasira wote wanayo



“Unaona huu msitu?”

“Ndio”

“Una Simba, una kila aina ya wanayama wakali. Mimi na Jojo hata tukishuka hapa hawawezi kutudhuru, ila wewe ukishusha pua yako tu watakutafuna na hawato kuacha hata mifupa yako. Sasa funga bakuli lako kwa maana nitakushusha hapa na uwe chakula chao cha leo. Umenielewa?”

Maneno ya Dany yakanifanya nitazama nje ya gari, kile alicho kizungumza ni kweli, ninawaona Simba wakubwa sana ambao kwenye maisha yangu sikuwahi kuwashuhudia zaidi ya leo hii.

“Huu msitu kuna nyumba moja tu ambayo alinirithisha Marehemu bibi yenu, sasa weka akili yako vizuri na achana na mambo ya kitoto. Nahitaji hivi sasa uwe mwanaume, tena mwaume wa shoka umenielewa?”



“Nimekuelewa”

Nilimjibu Dany kwa ufupi huku tukiendelea kusonga katika msitu huu ambao sifahamu upo kwa wapi hapa Tanzania. Tukafika katika moja ya jumba kubwa ambayo ni ya gorofa moja. Tukashuka kwenye gari na kuingia ndani ya jumba hili.

“Karibu”

Jojo alizungumza huku akipandisha ngazi za kuelekea gorofani. Nikaanza kutazama picha kubwa kubwa zilizo bandikwa kwenye moja ya ukuta katika seble hii. Picha hizi ni za mwana mama mmoja, mzee mmoja, mtoto mmoja, pamoja na binti mmoja.

“Hiyo ndio ilikuwa familia yangu”

Dany alizungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu.

“Wapo wapi kwa sasa?”

“Wote wamekufa”

Nikamtazama Dany usoni mwake kwa mshangao mkubwa sana. Kitu kinacho nishangaza kwa Dany ni juu ya mwili wake, kwani bado anaonekana ni kijana mdogo sana wa miaka kama arobaini hivi ila picha zilizopo hapa zinaonyesha ni za watu wa zamani kidogo.

“Walikufa na nini?”

“Mama, Diana na mwanangu huyo wa kike ambaye ndio dada yenu wa kwanza kabisa waliuwawa na mwana mama mmoja anaitwa K2, ila baba yangu aliuwawa kwenye maswala ya kibiashara ila muonganiko wa wauji unatokea kwa K2.

“K2 si alikuwa ni raisi wa hii nchi ya Tanzania?”

“Ndio, ila si kila mtu ambaye anakuwa raisi, eti ni malaika. Wengine ni majini na nimashetani”

“Mmmmm”

“Ndio hivyo uweze kutambua kwamba katika dunia hii kuna matatizo mengi sana na kuna watu wengi sana ambao wanaweza kukuwinda pasipo wewe kukufahamu”

Dany alizungumza huku akinishika begani mwangu.

“Nilisikia kwamba ulimuua K2?”

“Ndio nilimuu, kwa mtu yoyote ambaye anathubutu kukuumizia watu wa karibu yako. Basi kuna haki ya wewe pia kuhakikisha kwamba una mkabili kuhakikisha kwamba unakomesha ujinga wake”

“Pandisha gorofani dada yako aka kuhudumie uso wako”

Dany alizungumza huku akiondoka kwenye eneo hili zilipo pangwa vizuri ukutani kisha akaelekea kwenye sofa kuwa zilizopo hapa sebleni na kukaa. Nikamtazama kwa sekunde kadhaa, kisha nikatazama ngazi hizi zinazo elekea juu goforani, nikaanza kupanda taratibu huku nikiitazama nyumba hii ambayo kwa nje ina onekana ya kawaida, ila kwa ndani imepangiliwa vizuri. Nikakutana na Jojo kwenye kordo.

“Twende huku”

Jojo alizungumza huku akigeuka na kuanza kurudi kule alipo tokea. Tukaingia kwenye moja ya chumba kikubwa ambacho kina vitu vya kizamani.

“Kaa hapo”

Jojo aliniambia nikae kwenye kiti kimoja cha miti. Nikaa taratibu huku nikiendelea kutazama chumba hichi. Jojo akachukua moja ya kibegi cheusi, akakifungua na kutoa vichupa vya dawa.

“Dany ni mtu wa aina gani?”

Nilimuuliza Jojo huku nikimtazama usoni mwake.

“Swali lako lina maanisha nini?”

“Nahitaji kufahamu tu, kwa maana kama ni baba yangu basi ukweli hauwezi kubadilika”

“Hahaaa….utamuliza mwenyewe, ila kuna tabia moja ambayo mume fanana”

“Tabia gani?”

“Wote munapenda chini”

“Tunapenda chini?”

“Ndio”

“Sijakuelewa?”

“Munapenda kutomb**. Hivi kama lile jimama kweli uliweza kulihimili?”

Nikajikuta nikicheka sana huku nikimtazama Jojo usoni mwake.

“Kwani nina mbeba?”

“Chizi wewe, jimama lote lile. Hembu achana nalo. Tazama wewe bado ni mdogo sana, una jimudu, ni mzuri. Unalipa na una kila aina ya sifa tulia na mwanamke wa aina yako bwana”

“Nikuulize kitu”

“Najua unataka kuniuliza kwamba nina mchumba si ndio”

“Umejuaje?”

“Ninajua kila unacho kiwaza kichwani”

“Mmmmm”

“Ndio”

Jojo akaendelea kunitibu majeraha yangu. Alipo maliza akaniomba tutoke ndani ya chumba hichi na akaanza kunionyesha kila chumba kimoja hadi kingine, tukatoka katika jumba hili na kuzunguka upande wa pili na kukuta ukumbi mmoja mkubwa sana ambao una sihala nyingi na ukumbi huu hautofautiani sana na ukumbi wa ukumbi wa Professa.

“Bibi yetu huu ndio ulikuwa ni ukumbi wake wa kufanyia mambo kadhaa ikiwemo kutengeneza hizi silaha”

“Unataka kuniambia bibi yetu alikuwa ni mwanajeshi?”

“Hapana hakuwa mwajeshi, ila baba ndio alikuwa kitengo kimoja cha usalama wa Taifa”

“Taifa hili la Tanzania?”

“Ndio”

“Ila kuna usaliti walimfanyia ikiwemo kumuulia familia na ndio maana akaamua na yeye kuwa kinyume nao akawaua ndio mambo yalivyo kwenda miaka hiyo zaidi ya ishini na na sita iliyo pita. Kipindi hicho mama yako alikuwa ni mjamzito”

“Wewe ulikuwa na umri gani kipindi hicho?”

“Nilikuwa kama hivi”

“Kama hivyo kivipi?”

“Kwani wewe una nionaje. Ukipona tunaanza mazozezi ya kukufanya uwe poa. Tuna vita nyingine ambayo ipo mbele yetu”

“Vita gani?”

“Ume wasahau Al-quida?”

Nikaa kimya kimnya kwani kundi hilo ni kundi la watu ambao nilikuwa nimejiunga nao na hata kuondoka kwangu kwenye kundi hilo ni matatizo”

“Najua hujui ni kitu tulikifanya kuhakikisha kwamba tunakutoa nje ya kikundi kile”

“Kitu gani?”

“Kwanza ulindanganywa kwamba Dany si baba yako si kweli?”

“Ndio”

“Na wewe ukaamini?”

“Ndio niliamini, ikiwa simfahamu baba yangu, wewe ulihisi kwamba sinto amini”

“Okay, wangekutumia wewe kumuangamiza Dany”

“Kivipi?”

“Siku ambayo tulikuja kumteka makamu wa raisi wa Marekani, tulifahamu uwepo wenu pale na ndio maana tuliweza kuwaua wezako wote na wewe tukakuacha hai”

“Wewe ulikuwa wapi?”

“Mimi ndio niliye kuwa nikiwaua walinzi kwa kupitia dirishani, nilikuwa na bunduki hii”

Jojo alizungumza huku akinionyesha bunduki hiyo ambayo ni ndefu na ina uwezo wa kumua mtu akia katika eneo la mbali kidogo.

“Tulimuhitaji yule makamu wa raisi kisha tukakuharibia wewe kwa kutuma taarifa ya wapi ilipo kambi yenu kwenye jeshi la Marekani”

“Sijakuelewa Jojo”

“Tuliamua kukuchonganisha wewe na kundi lako la Al-quida kwa maana siku ambayo tunakwenda kulisambaratisha kundi hilo na nchi nzima ya Marekani, basi wewe ungekuwemo ndani yake hivyo vita yetu tusinge ifanya vizuri”

“Unataka kuniambia kwamba muna uwezo wa kusambaratisha Al-quida?”

“Ndio na mwanzo tulisambaratisha kundi la Al-Shabab ambalo juzi juzi ulijitia kimbelele mbele kwenda kukomboa wanafunzi wa Kijerumani. Pia baba yako ndio mtu pekee aliye weza kumua Osama Bin Laden.”

“Ahaa….sasa hapa ndio ninaanza kupanta picha”

“Ndio utambue kwamba uliingizwa kwenye mzunguko wa kuangamiza familia yako. Yule mwanamke wako sijui nani”

“Farida?”

“Ehee huyo huyo. Alikuwa anacheza sana na akili yako. Sasa ishu inakuja kwamba hii vita mama yako amejiingiza”

“Kivipi?”

“Mama yako anajiunga na kundi la Al-Shabab na ameunda kundi la Boko haramu, japo kwa sasa haliiti boko Haramu. Kundi ambalo hapo awali baba yake alikuwa ndio muanzilishi na kundi hilo, akamrisisha baba yako Dany ila Dany akaboronga, vita yake na Marekani pamoja na K2 akaileta kwenye kundi la watu na mwisho kundi likafa na mambo yakawa kama yalivyo”

Nikakumbuka siku nilipo mkuta mama kwenye kambi ya Al-Shabab na akizungumzia juu ya boksi jeusi”

“Jojo hivi boksi jeusi ndio nini?”

“Boksi jeusi?”

“Ndio, kwa maana nilimkuta mama akiwa na mkuu wa kundi la Al-Shabab, wakizungumzia juu ya boksi hilo na silaha ya pekee ambayo walikuwa wanaitagemea ili waipate hilo boksi jesui ni wale wanafunzi ila mipango ya imefeli.”

“Kwa nini wanalihitaji boksi hilo jeusi?”

“Mama yako anahitaji kulipiza kisasi kwa Dany. Anataka awe na nguvu kubwa sana hapa dunia. Ndio maana anahitaji hilo boksi jeusi”

“Kwani kilitokea kitu gani kati yake na Dany?”

Swali langu likamfanya Jojo kuvuta pumzi nyingi na taratibu akaanza kuitoa huku akimtazama usoni mwangu.



“Mapenzi ndio chanzo cha baba yako na mama yako kugombana na kuwa maadui wakubwa”

“Mapenzi tu?”

“Ndio, hujui tu ni jinsi gani baba yako alivyo pambana kuhakikisha ana mrudisha mama yako mikononi mwako na hata pale alipo mrudisha hali haikuwa ya amani kabisa.”

“Mmmmm”

“Ndio hivyo, unajua baba yako alikuwa na wanawake karibia wanne ambao aliwabebesha mimba kwa wakati unao endana”

“Hahaaa….Baba alikuwa kiboko”

“Ndio maana nikakuambia wewe na baba yako nyayo zenu zinaendana na baba yetu alifeli kwenye vitu vingi sana kutokana na kupenda kugongana”

Nikazidi kucheka sana maneno anayo niambia dada yangu Jojo.

“Wewe cheka, kipindi mama yako akiwa na mimba yako, kuna mwanake alikuwa anaitwa Livna Livba naye alimtundika mimba, ukiachilia Livna kuna mwanamke mwengine anaitwa…….”

Kabla Jojo hajamalizia kuzungumza jambo lolote, simu yake ikaanza kuita taratibu, akaitoa mfukoni mwake na kuitazama kwa muda.

“Mmmmm”

“Mbona una guna?”

“Huyu anaye nipigia simu ni siku nyingi sana sijawasiliana naye sasa sijajua leo amekubwa na jambo gani”

“Mpokelee tu”

Jojo akapokea simu yake na kuiweka sikioni, akatoka chumbani humu ili aweze kuzungumza na simu hiyo vizuri kwa faragha pasipo mimi kuweza kuisikia. Maelezo madogo ambayo Jojo amenipatia nikajikuta nikianza kuipenda hii familia yangu upande wa baba ambayo kwa miaka mingi sana nilikuwa ninamuuliza mama yangu anieleze japo ukweli ila alishindwa kufanya hivyo. Jojo akarudi chumbani humu huku sura yake ikiwa na tabasamu pana usoni mwake.

“Ehee tuendelee”

“Ohoo hapana tutaendelea siku nikipata muda. Kuna wageni wawili nimeombwa kwenda kuwapokea, wanatokea nchini Ujerumani hivyo nahitaji kujiandaa kuelekea Dar es Salaam”

“Ahaa sawa dada yangu. Hivi hapa ni wapi?”

“Huu msitu upo kwenye mkoa mmoja unaitwa Tanga, ndipo alipo zaliwa baba yako”

“Sawa”

“Twende sebleni ukakae na baba”

Tukatoka chumbani humu na kuelekea sebleni, tukamkuta Dany akiwa anatazama taarifa ya habari.

“Jojo umeisikia hii”

“Ipi?”

“Mtoto wa mgombea uraisi wa Ujeruamani ametekwa na hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo na ametekwa na mpenzi wake”

“Ahaa sasa ninaanza kupata jibu”

Jojo alizungumza huku akiongeza sauti ya tv hii.

“Jibu gani?”

“Ethan amenipigia simu, akaniomba niwapokee hao vijana wawili. Mmoja anaitwa Ethan na mwengine anaitwa Camila si ndio”

“Yaa picha zao ndio hizo zinazo onekena kwenye tv”

Dany alizungumza huku tukizitazama picha za vijana hawa. Nilipo ona jina la Ethan Klopp kwa namna moja ama nyingine sio geni kwangu. Nilisha lisikia sehemu na huyu kijana ndio niliye ambiwa kwamba ana miliki boksi jeusi, boksi ambalo nami nilipewa kazi ya kulifwatilia kwa kijana huyu.

“Nani na nani wanafahamu ujio wao hapa Tanzania?”

“Ni sisi watatu hapa, ila hakuna mwengine ambaye ana fahamu”

“Huyu kijana ni madini makubwa sana”

“Madini makubwa kivipi baba?”

Nilijikuta nikiuliza huku nikimuita Dany baba, jambo lililo wafanya waduwae kwa sekunde kadhaa. Dany akatabasamu usoni mwake, kwani nina imani kila mzazi anapenda kupewa cheo chake, kuliko kuitwa jina lake halisi.

“Kijana huyu ana boksi moja lenye mbinu za kutengeneza bomu moja zito la nyuklia ambalo endapo wana sayansi wakifahamu hiyo mbinu basi dunia inaweza kwenda kuchanguliwa changuliwa pale bomu hilo litakapo pigwa duniani”

Dany alizungumza kwa upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Mmmmm”

“Kila mtu ana muhitaji huyo kijana, ukiwa na hiyo mbinu, dunia nzima itakuogopa”

“Inabidi niwahi uwanja wa ndege, nikawapokee kwa siri sana pasipo mtu yoyote kuweza kugundua kama wapo Tanzania, baba si unafahamu huyu kijana ni maarufu kwenye maswala ya mpira”

“Ndio, tena tuongozane”

“Hapana baba kumbuka na wewe unajulikana sana, sihitaji tuwape mashaka katika hili. Nahitaji wanione peke yangu pale uwanaja wa ndege na nitarudi nao hapa”

“Ila mdogo wako Ethan anaendeleaje?”

“Yupo vizuri”

“Sawa hakikisha unarudi nao hapa wakiwa salama salmini”

“Usijali baba. Dogo mimi nasepa, maelezo mengine ukihitaji utayapata hapo kwa baba yako”

“Poa dada”

Jojo akachukua koti lake kubwa na zito kiasi. Akatoka ndani humu na kutuacha mimi na Dany.

“Ahh….samahani baba kwa kila kitu ambacho kilitokea kati yetu na…..”

“Usijali natambua, ulijazwa chuki na kila mtu hata mama yako hakuhitaji ufahamu upendo ambao ninao juu yako. Ila kikubwa ilikuwa ni muda. Muda umefika na nimekuchukua”

“Nafurahi kusikia hivyo baba, ila ninaweza kukuuliza swali”

“Uliza”

“Kwa nini wewe na mama picha haziendi?”

“Hahaaa, mama yako ana wivu wa kijinga”

“Wivu gani?”

“Nilimuulia mabasha wake, na nikajidai ninampenda kisha nami nikampiga kibuti na kumuacha ili apate maumivu kama yale ambayo mimi nilikuwa nikiyapata kipindi alipo kuwa na hao watu wake”

“Watu gani?”

“Duuu ni historia ndefu mwanangu ambayo inahitaji muda kidogo kukuadisia. Ila kwa ufupi mama yako nilimpata nchini Nigeria, kipindi hicho alikuwa ni mrembo kweli kweli tena mwana mitindo maarufu. Baba yake alikuwa ni kiongozi wa kundi la Boko Haramu. Nilimkuta mama yako na mwanaume mmoja ambaye alikuwa akimtesa sana na alikuwa na walikuwa na mtoto mmoja wa kiume. Kipindi hicho baba yako nilikuwa nalipa kishenzi na ukichukulia mapigo niliyo kuwa nikiwapa kitandani, basi walipagawa sana, hususani mama yako ndio alichanganyikiwa hadi akaamua kumpiga chini mwanaume wake”

“Basi babu yako aliamua kunipima kwa kunipambanisha na kijana wake aliye kuwa akimuamini kupita vijana wengine wote katika kundi lake hilo la Boko haramu. Kijana wake nilimpiga vibaya tena nilimvunja vunja mbele yake jambo lililo mfanya babu yako kunikubali na kunipa uongozi wa kundi hilo huku nikimuoa mama yako”

Nikakaa vizuri kwenye sofa ili niendelee kuipata historia ya baba yangu na mama yangu.

“Ehhee”

“Babu yako alifariki dunia. Kipindi nilikuwa ninakwenda Nigeria, nilikuwa ni mpelelezi kutoka Marekani”

“Kwa hiyo baba ulikuwa mpelelezi?”

“Ndio, kwa uwezo wangu mkubwa kwenye Nyanja za usalama nilikuwa ni zaidi ya komandoo. Nchi kubwa kama Marekani, Uingereza, zilitamani sana kufanya kazi na mimi, ila toka Wamarekani walipo amua kunisaliti hapo ndipo nilipo badilika maziwa na kuwa jeshi la mtu mmoja|”

“Kwa nini Wamarekani walikugeuka?”

“Chazo alikuwa ni mama yako. Raisi wa kipindi hicho bwana Donald Bush alimuiba mama yako na akawa mpenzi wake, sasa ili wafurahie penzi lao vizuri, waliamua kutuma makomandoo kama siti hivi kuniangamiza”

“Duuu uliwaua?”

“Yaa nilifanikiwa kuwaua kwa kutumia akili nyingi sana. Unajua kitu kizuri ambacho mimi baba yako nilibarikiwa ni kuwa na uwezo mkubwa wa akili na kujua kupambana. Kuanzi siku hiyo niliamua kufanya jambo juu ya mama yako. Kipindi hicho ambacho alianza mahusiano na raisi huyo, mimi huku tayari nilisha muachia mbegu tumboni mwake ambazo ni wewe”

“Ahaa…..”

“Yaa, basi nikafanya kile ninacho kiweza mimi, nikahakikisha kwamba mama yako ninamrudisha mikononi mwangu, kisha nina muua raisi Donald Bush”

“Niliona video ya jinsi ulivyo kuw auna mchinja”

“Yaa ipo video tu tena kwa watu wachache sana inayo onyesha tukio hilo. Nimefanya mambo mengi ya kipuuzi hapa nyuma ambayo kwa sasa siwezi kuyafanya kwa maana nimekua sasa”

“Baba kwani una umri gani?”

“Naelekea miaka stini sasa”

“Stini?”

Niliuliza kwa kushangaa sana kwani baba bado ni kijana sana.

“Ndio au unashangaa mwili wangu kwamba bado ni kijana?”

“Ndio nashangaa, mimi nikijua una miaka kama arobaini na kitu hivi”

“Hahaa, ninakwenda miaka stini. Mama yako pale mwenyewe ana miaka hamsini na kitu ila una muona anavyo onekana, bado binti binti”

“Kweli lakini, ila pesa ndio ina msaidia?”

“Yaa hata mimi nina pesa nyingi sana, ila sihitaji kujionyesha kwamba nina pesa. “

“Duuu”

“Tuachane na mambo hayo, kuanzia kesho nahitaji uanze mazoezi rasmi, sihitaji mtu mzembe mzembe sawa’

“Sawa baba ila mimi sio mtu mzembe kwa maana nina uwezo mkubwa wa kupambana”

“Huna, mafunzo liyo yapata kwenye kundi hilo la Al-quida sio mafunzo kabisa. Nahitaji kukupa mimi mafunzo ambayo hata siku ninakwenda kuondoka hapa dunia, basi nijue nyuma yangu ninacha jembe, tena jembe la kueleweka sawa”

“Sawa baba”

Siku hii nzima ikapita huku Dany akinifundisha kupika vyakula vya kitanzania ikiwemo Ugali.

“Kipindi upo na mama yako ulisha wahi kula hiki chakula?”

“Hapana, mara ya mwisho mama kunipikia chakula ni siku ya kutumiza miaka kumi na nane. Hapo ndio ilikuwa ni mara yangu ya mwisho kula chakule chake”

“Duuu siku nyingine ilikuwaje?”

“Mama yupo bize na pesa, maam yupo bize na maisha ya kutengeneza uchumi wake, ndio maana hadi leo amekuwa mwanamke wa kwanza tairi barani Afrika”

“Hahahaa nakumbuka maam yako aliniahidi jambo kwamba akikuzaa atakuu kwa maana amebeba damu ya mwana haramu”

“Mmmm”

“Yaa, mama yako alianza kukuchukia toka ulipo kuwa tumboni na kwa bahatii mbaya hawezi kubeba tena ujauzito mwengine ndio maana akaamua kukulea, laiti kama angepata uwezo wa kubeba ujauzito wa mwanaume mwengine basi wewe angakuua”

“Mmmmm, unataka kuniambia mama hanipendi?”

“Mara ya mwisho kuondoka kwenye ofisi yake uliondokaje?”

Kumbukumbu zikanikumbusha siku ya mwisho kuondoka kwenye kampuni ya mama yangu. Niliondoka nikiwa sina hata nguo moja mwilini mwangu na niliweza kukubalia aibu hiyo.

“Umekumbuka ehee?”

“Ndio”

“Je anakupenda mtu wa aina hiyo?”

“Ila baba nilisha yazoea mateso ya mama”

“Kama ungekuwa umeyazoea usinge ondoka ofisini kwake ukiwa uchi.”

“Ila baba najua wewe na mama muna chukiana, ila ninakuomba muweze kupata”

“Hilo jambo halipo. Mama yako ameamua kupita njia nyingine, njia ya kujaribu kuniangusha jambo ambalo ni gumu ndio maana amehusika hata kwenye mpango wa kuwateka wale wanafunzi wa Kijerumani. Unajua ni kwa nini amefanya hivyo?”

“Hapana”

Nilijibu hivyo japo nina fahamu sababu ndogo.

“Mama yako amerudisha kundi la baba yake japo halipo Nigeria kwa sasa lipo Niger ndio maana uliingia kwenye kundi hilo pasipo kufahamu kama ni kundi la maam yako”

“Unataka kuniambia mama anahusika na lile kundi?”

“Ndio na nilifanya makusudi kuhakikisha nina muua mkuu wako ambaye uliambatana naye siku ambayo ulitoka kwenye mjini. Unakumbuka siku hiyo ulivyo kuwa Niger?”

“Ndio nina kumbuka baba”

“Yaa nilifanya hivyo ili nikutoe kwenye kundi hilo na kwa bahati mbaya sasa ukaangukia mikononi mwa mwanamke ambaye alikuingiza kwenye maisha ya kigaidi ambapo huko pia nilikutoa kuhakikisha kwamba una rudi kwenye mstari. Hadi ninavyo zungumza hivi sasa yule mwanamke sijui nani…..”

“Farida?”

“Ndio huyo Farida. Hadi ninavyo zungumza hivi sasa bado anakutafuta bado wanakuhitaji kukuangamiza na mimi nikiwa kama baba yako siwezi kukuacha kama uangamie. Nahitaji mimi, wewe na Jojo, tuungane kwa pamoja, tushikamane kwa pamoja, kuhakikisha kwamba tunawaangamiza maadui zetu wote kuanzia kundi la Al-quida hadi mama yako mzazi.”



“Mama yangu mzazi?”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana.

“Ndio una shangaa nini, mama yako kama angekuwa na mapenzi na wewe asinge kuacha ukiwa umeshikiliwa katika kundi la Al-Shabab, si alikukana na kudai kwamba wewe si mwanaye?”

“Ndio”

“Usipo kuwa makini naya atakuua umenielewa”

“Ndio nimekuelewa baba”

“Nenda kapumzike sasa nonia imani kwamba dada yako atafika kesho na wageni”

“Umezungumza naye?”

“Hapana, ila nitazungumza naye kesho”

Nikamuaga Danya na kuelekea chumbani kwangu kwa ajili ya kujipumzisha kwa maana tumesha maliza kupata chakula cha usiku. Usiku huu sikuweza kupata usingizi kutokana mawazo mengi yanayo endelea kutafuna ubongo wangu na mbaya zaidi hayana majibu kabisa.

‘Kivipi tunaweza kuliangusha kundi la Al-quida?’

‘Itakuwaje nimwage damu ya mama yangu ambaye ameniweka tumboni mwake kwa miezi tisa? Ila mama hanipendi. Nimfwate baba au mama?’

‘Kipindi chote baba alikuwa wapi hadi akashindwa kunilinda?’

Maswali haya mfululizo ninayo jiuliza kichwani mwangu yakanifanya ninyanyuke kitandani, taratibu nikasimama dirishani na kuanza kutazama msitu huu ambao kwa kweli una tisha. Nikiwa hapa dirishani, nikamuona Dany akiwa ametoka nje huku akiwa tumbo wazi pamoja na boksa tu. Hapa ndipo nikapata muda mzuri wa kuweza kuliona umbo la baba yangu jinsi lilivyo gawanyika kwa mazoezi. Dany akaanza kuruka sarakasi kadhaa huku akiwa katika kasi ambayo hakika sijawahi kumuona binadamu anaye ruka kama hivyo. Dany akaendelea kufanya mazoezi kadha ambayo kwa namna moja ama nyingine yakanivutiia kwa kweli. Nikatoka chumbani kwangu na kueleke nje kwenye uwanja mdogo ambao Dany anafanyia mazoezi.

“Vipi hujalala?”

Dany aliniuliza huku jasho likiwa limelowanisha mwili wake mzima na kuwa kama mithili ya mtu ambaye ametoka kuoga bafuni.

“Hapana baba, mazoezi yako yamenivitia”

“Unapenda kuwa kama mimi?”

“Hapana, ila inapenda kuwa zaidi yako wewe”

“Hahahaa, kuwa zaidi yangu inahitaji ujitume sana, unatakiwa usiyasikilizie maumivu utakayo yapata. Zaidi unatakiwa kupenda maumivu hayo”

“Kivipi?”

“Ingia pale sebleni, utaona bastola mbili juu ya meza, njoo nazo”

Nikaingia ndani kwa haraka, nikachukua bastola hizo mbili na kurudi nazo uwanjani. Nikamkabidhi Dany bastola hizo mbili.

“Chukua bastola hii”

Dany aliniambia na nikaipokea vizuri.

“Toa magazine”

Nikatoa magazine ya bastola hiyo.

“Ina risasi ngapi?”

“Imejaa”

“Sawa hitaji risasi zote hizo unishambulie”

“Ehee!!?”

“Ndio nipige risasi hizo zote hadi ziishe, ukishindwa kunipiga risasi hata moja basi nami nitakupiga risasi moja tu, so kuna mawili kufa na kupona”

Mwili mzima ukazizima, woga ukanitawala macho yakanitoka huku mkono wangu ulio shika bastola ukaanza kutetemeka taratibu.

“Jiamini, nakufundisha ujasiri na umahiri. Nipige”

Dany alizungumza huku akirudi hatua mbili nyuma na kutufanya tuwe na umbali wa hatua kama nne hivi. Nikashusha pumzi taratibu huku nikishika vizuri bastola hii. Taratibu mapigo ya moyo yakarudi katika mfumo wake wa kawaida.

“Unauhakika baba?”

“Ndio nina uhakika nipige”

Dany alizungumza huku akiwa amesimama wima. Nikamtazama kuanzia juu hadi chini kisha mikono yangu iliyo ishika hii bastola vizuri nikaielekeza kifuani mwake. Nikaanza kufyatua risasi mfululizo, ila jambo la kushangaza ni jinsi Dany anavyo zikwepa risasi hizo. Nikatumia uwezo wangu wote wa kumuweka kwenye tageti ya kumshambulia, ila hadi risasi zinakwisha sikuweza kufanikiwa kumpiga hata moja.

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG