Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

SIN SEASON 1 SEHEMU YA 9/10

  


SIN SEASON 1

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 9 KATI YA 10


“Ndio muheshimiwa”

“Muna uhakika eneo hilo ni eneo sahihi la ngome ya Al-Shabab?”

“Ndio muheshimiwa”

“Hembu fanyeni upelelezi wa kutosha ili tufahamu kina biashara gani zinazo endelea eneo hilo”

“Sawa meheshimiwa”

Upelezi wa angani ukaendelea kufanyika huku wakishuhudia wana jeshi wa kikundi hicho cha Al-Shabab wakishusha wakishusha maboksi kwenye moja ya meli kubwa iliyo simamishwa eneo hilo.

“El del clasico?”

Raisi Mtenzi alisoma meli hiyo jinsi ilivyo andikwa.

“Hii meli ime tokea nchi gani?”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwatazama vijana wake.

“Ngoja niitafute”

Kijana mmoja alizungumza, akaitafuta meli hiyo na ndani ya muda mfupi akafanikiwa kufahamu imetokewa wapi.

“Meli hii imetokea ufarasa, ina milikiwa na tajiri mmoja De Rose Jr. Tajiri huyo ana shuhulika na maswala ya uuzaji wa madawa ya kulevya pamoja na silaha”

Kijana huyo alizungumza kwa kujiamini na kumfanya raisi Boaz kushusha pumzi.

“Kwa nini hajakamatwa kipindi chote hicho?”

“Ana tafutwa na nchi kubwa kama Marekani, Ufaransa wenyewe pamoja na Uingereza. Amekuwa akisaidia sana vikundi vya kigaidi kama Al-Shabab, Al-quida na Islamic state”

Kijana huyo alidi kutoa maelezo huku picha ya mmiliki wa boti hiyo ikionekana katika tv kubwa iliyomo hapo ndani.

“Ni wakati wa kuvuruga kila kitu”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama Emmy anaye onekana kwenye tv.

“Sawa muheshimiwa raisi”

Amri hiyo ya raisi Boaz, ikafanya Emmy kutoa maagizo kwa vijana wake anaye endesha drone hiyo, ambayo ina beba mabomu yenye uwezo wa kulipua eneo kubwa. Ndani ya muda mchache eneo hilo la bandari likaanza kulipuka huku likiteketeza meli hiyo pamoja na bandari nzima. Kila mtu ndani ya chumba hicho alishangilia kwa maana ni kazi iliyo leta mafanikio ndani ya muda mchache sana.

“Hongera sana muheshimiwa raisi”

Kila mmoja alimpongeza raisi Mtenzi.

”Nina imani mume fanya kazi kubwa sana. Muna weza kwenda kupumzika sasa”

Raisi Mtenzi alitoa ruhusa hiyo kwa vijana wake ambao ni zaidi ya masaa thelathini wapo ndani ya chumba hicho. Raisi Mtenzi akatoka ndani hapo na kurudi ndani kwake.

“Vipi kazi ime kwisha?”

Jery alimuuliza baba yake huku akimtazama jinsi anayo kaa kwenye moja ya sofa.

“Yaa tume fanya shambulizi la anga”

“Kwa hiyo mume waua?”

“Ndio tume waangamiza wote. Unajua nchi yangu huwa haipendi maswala hayo ya kigaidi, ila endapo mtu ata tushambulia, hakika hatuwezi kukaa kimya ni lazima tulipize”

“Daa ila baba kazi yako kweli ni ngumu, hivi ilikuwaje ukaacha uaskari na kuamua kuingia kwenye siasa?”

“Ni wito mwanangu. Hata wewe huko mbeeni una weza kuacha udaktari na ukaingia kwenye siasa. Marehemu babu yenu alikuwa ni mmoja wa wana siasa wazuri sana, hivyo ile damu yake ya uongozi bado ipo ndani yangu.”

“Ila baba kazi hii ni ngumu sana?”

“Ndio ni ngumu kwa maana unaongoza watu wanao jitambua na wasio jitambua hivyo kila mmtu ana mapungufu yake. Jambo la msingi ni kuhakikisha mtu una kuwa makini kwenye kila kitu unacho kifanya”

“Sawa baba, ila endapo Al-Shabab wakaamua kurudisha mashambulizi ita kuwaje?”

“Ndio ita kuwa ndio mwisho wao kwa maana tuta wafutilia mbali kwenye ramani ya dunia”

“Sawa vipi huyo mwenzako ana endeleaje?”

“Yupo safi tuna subiri tu siku yetu ya harusi”

“Safi sana, ila mwanangu pale ume weza kuchagua chombo”

“Kweli baba?”

“Yaa yule binti ni mzuri kila idara, jambo la msingi hakikisha una muheshimu na kumjali. Endapo uta poteza hivyo vigezo, ata tokea mjinga mjinga mmoja ata mchukua”

“Weee baba endapo atatokea mtu kufanya huo uzembe lazima afe”

“Mmm mimi nime kupa tu tahadhari. Usiku mwema”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akinyanyuka, akatoka ndani hapo na kumucha Jery sebleni akiendelea kutazama filamu yake.

***

Vilio na maumivu ya vikazidi kutanda kwenye bandari ndogo hiyo iliyopo kunisi mashariki mwa nchi ya Somalia. Mabomu yaliyo shambulia eneo hilo dakika ishirini zilizo pita, yame sababisha hasara kubwa sana kwenye eneo hilo huku idadi kubwa ya wana mgambo hao wa kikundi cha Al-Shabab wakipoteza maisha yao. Baadhi ya walio salia ni wale wachache walio wahi kujiursha kwenye maji.

“Mkuu tume shambuliwa”

Mmoja wa anamgambo walio salimika alizungumza kwa kutumia simu ya upepe huku akiwa ana elea elea ndani ya maji hayo.

“Imekuwaje?”

Mkuu wa kikosi hicho alizungumza kwa ukali sana.

“Hatujui, ni mashambulizi ya anga”

“Shiti”

Simu hiyo ikakatwa. Mkuu wa kikosi hicho aliyopo katika mji wa Mogadishu pamoja na mmiliki wa meli hiyo bwana De Rose Jr.

“Kuna nini kilicho tokea?”

De Rose Jr aliuliza huku akimtazama bwana Abuu Mohamed Mohamed aliye fura kwa hasira.

“Bandari yangu ya Rassini ime shambuliwa kwa anga”

“Nini? ina maana na meli yangu pia ime shabuliwa?”

“Sijapata habari acha niulize”

Abuu Mohamed Mohamed, akawasha redio yake ya upepo.

“Nahitaji kujua meli ya tajiri ipo salama. Over”

“Mkuu kila kitu kime shambuliwa. Over”

“Ina maana hakuna kilicho salia. Over”

“Ndio mkuu hakuna, yaani idadi kubwa ya watu wame kufa. Over”

Bwana De Rose Jr, mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa hasira kwa maana meli yake hiyo ime beba itu vingi sana tena vyenye thamani kubwa. Mwili mzima ukabadilika rangi na kutawaliwa na uwekundu, hata vinywaji walivyo kuwa wana kunywa havikuwa na thamani tena kwao.

Upande wa Bwana Abuu Mohamed Mohamed naye akazidi kujawa na hasira, ndevu nyingi zilizo mjaa usoni mwake zikazidi kuifanya sura yake kuwa mbaya akiwa katika hali ya hasira.

“Nahitaji kwenda Rassini sasa hivi nikaone meli yangu?”

De Rose Jr alizungumza kwa ukali sana.

“Unahisi ukienda sasa hivi una weza kuwa salama. Ehee?”

Abuu Mohamed Mohamed alifoka kwa hasira sana.

“Sijali, unajua ndani ya meli kuna nini kule?”

“Sijui ila kumbuka sasa hivi tupo kwenye wakati mgumu wa kushambuliwa. Wewe una maadui na mimi nina maadui una hisi ita kuwaje endapo tukajitoa sura zetu, si tuta uwawa?”

Abuu naye alizungumza kwa kufoka na ujasiri wa hali ya juu na kumfanya bwana De Rose Jr kutulia huku akitafakari ni jambo gani la kufanya kwa maana na yeye ana tafutwa karibia dunia nzima.

“Ina tupasa kutambua aliye fanya shambulizi hili ni nani”

Bwana De Rose Jr alizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo ya hasira.

“Wewe una wataalamu wengi, jaribu kuangalia ni nani ambaye ana husika na kuharibu bandari na meli yako”

Bwana De Rose Jr akamtazama Abuu Mohamed Mohamed kwa sekunde kadhaa kisha akatoa simu yake mfukoni na kumpigia kijana wake mmoja.

“Ingia ndani na laptop yako”

Akakata simu na kijana huyo akaingia ndani hapo.

“Meli yetu na bandari vime shambuliwa nahitaji kufahamu ni nani alite tushambulia.

“Sawa mkuu”

Kijana huyo kwa haraka akaitoa laptop yake kwenye begi lake la mgongoni, akakivaa miwani yake kubwa kidogo kisha akaianza kazi hiyo ya kutafuta mashambulizi hayo ya anga yametokea nchi gani. Haikuwa kazi rahisi sana kwake, ila kazidi kujitahidi kuhakikisha kwamba ana pata jibu sahihi la shambulizi hilo.

“Bado”

Bwana De Rose Jr aliuliza.

“Bado kidogo mkuu”

Kijana huyo alizungumza huku akizidi kujitahidi kuhakikisha ana pata jibu. Baada ya lisa moja la kuhangaika, kijana huyo akafanikiwa kupata jibu la ni wapi bomu hilo limetokea na akajikuta akistuka sana.

“Vipi umpata?”

“Ndio mkuu”

Bwana De Rose Jr na Abuu Mohamed Mohamed, wote kwa pamoja wakamsogelea kijana huyo na macho yao yote wakayapeleka katika kioo cha laptop hiyo.

“Drone iliyo shambulia eneo la bandari pamoja na meli yetu, imetokea nchini Tanzania na oparesheni hii imeendeshwa na serikali ya Tanzania”

Bwana De Rose Jr pamoja na bwana Abuu Mohamed Mohamed, wote wakajawa na mshangao kwa maana wote wawili hawana ugomvi wowote na serikali ya nchi ya Tanzania.



“Una uhakika ni Tanzania!!?”

Bwana De Rose Jr aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio mkuu nina uhakika wa asilimia mia moja na zaidi”

“Abuu una bifu lolote na Tanzania?”

“Hapana sina sijawahi kufanya shambulizi lolote kwenye nchi hiyo. Sasa nina shindwa kujua kwa nni imekuwa hivyo”

“Ila raisi wa Marekani si alikuwepo kule miezi ulio pita?”

“Ndio”

“Kuna mkono wa Mmarekani kwenye hili tukioa”

“Kama kuna kumkono wa Mmarekani ni lazima tulipieze kiasi?”

“Wakuu hapa Wamarekani hawahusiki, hili jambo limefanywa na serikali ya Tanzania wao peke yao na hawajashirikiana na hata nchi yoyote”

“Ni lazima tulipize kisasi na kisasi tutakacho kifanya wata juta kwa nini wameivuruga bandari yangu.”

“Ni kweli Abuu ila kama wame weza kutushambulia kwa anga ina bidi kuwa mkini sana kwa maana nina imani kwamba wata kuwa wame jikua vizuri kwenye maswala ya ulinzi kwa kutumia tecnolojia”

Bwana De Rose Jr alizungumza huku akimtazama Abuu Mohamed Mohamed usoni mwake.

“Ni kweli. Kijana hembu fwatilia Tanzania kuna tukio gani ambalo lina kwenda kutokea katika siku hizi za karibuni?”

“Dakika moja”

Kijana huyo mwenye asili ya kihidi alizungumza huku akiendela kuminya minya batani za laptop yake.

“Mwezi ujao tarehe tisa kuna harusi ya mtoto wa raisi Chinas Mtenzi, ana muoa mtoto wa nabii Sanga, mmoja wa watumishi wa Mungu wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki”

“Harusi ya nini tuna taka tukio kibwa ambalo tukipiga, tuna piga kweli”

Bwana De Rose Jr alizungumza huku akimtazama kijana wake.

“Hapana hilo hilo tulio la harusi ndio la kuonyesha kwamba sisi hatupendi kochokozwa. Hilo jambo la shambulizi ni lazima liwe lime idhinishwa na raisi. Hakuna kitengo cha ulinzi kinacho weza kufanya kazi pasipo kupata idhini ya raisi.”

“Eti ehee?”

“Ndio, kama ni raisi ame idhinisha basi ni lazima ata lipa kwa hili. Nita hakikisha kwamba wana lipa kwa hili jambo”

Abuu Mohamed Mohamed alizungumza kwa sauti ya msisitizo na wakakubaliana na bwana De Rose Jr kuhakikisha wana fanya tukio kubwa kwenye harusi ya mtoto wa raisi Mtenz.

***

“Hei amka”

Evans akakurupuka kitandani. Akamtazama jini ambaye ni mwana dada ambaye kwa sasa ndio mtu wake wa karibu.

“Begi hilo hapo lina pesa dola milioni moja. Nenda benki kaweke na kufungua akaunti, Weka hiyo pesa kisha lipia ile ardhi”

“Sawa, ila nikiulizwa hizi pesa nime toa wapi?”

“Hakuna mtu wa kukuuliza ikiwa benki wao wanacho hitaji ni pesa na sio kuuliza maswali watu”

“Ila dola milioni moja kwetu ni bilioni of shilingis”

“Evans tamuba kwamba upo na nani na hiyo pesa imetoka wapi. Fanya kama niliyo kuambia. Umenielewa?”

“Nimekuelewa. Ila nahitaji kufahamu jina lako?”

“Halito kusaidia kitu ila kitakacho kusaidia ni wewe kufwata utaratibu na kile nilicho kueleza sawa”

“Sawa mkuu”

“Badae”

Jini huyo akapotea ndani hapo. Evans akafungua begi hilo na hakuamini kuona pesa hizo nyingi za kimarekani ambazo kwenye maisha yake yote hajawahi kuzimiliki. Akatoka nje ya hoteli hiyo, akakodisha taksi na kuelekea moja kwa moja kwenye benk Bacrays. Akafungua akaunti na kuweka kiasi hicho chote cha pesa. Baada ya kukamilisha hatua hizo za kibenki akalipia kiasi hicho cha kuinunua ardhi, akampigia dalali na akafika benki hapo na moja kwa moja wakaelekea katika ofisi za mkuu wa wilaya. Evans akajaza fomu za umiliki wa eneo hilo na akakabidhiwa hati yake kuonyesha yeye ndio mmiliki.

“Nashukuru sana”

“Tunashukuru sana na wewe kwa maana tuna penda wawekezaji wa ndani kama wewe”

Mkuu wa Wilaya alizungumza kwa furaha. Dalali akaingiziwa kiasi chake kama kazi yake aliyo ifanya. Evans akaelekea kwenye moja ya show room za magari, akanunua gari ndogo aina ya Toyota ist.

“Kata nisaidia kwenye mizunguko yangu”

Evans alizungumza na muuzaji huyo huku wakikabidhiana pesa za malipo. Evans akarudi hotelini na kuanza kuperuzi kwenye mitandao huku akitafuta kampuni ya utengenezaji wa majengo makubwa. Akafanikiwa kupata kampuni mbili, moja ikiwa ina tokea nchini China na nyingine ikiwa ina tokea nchini Ujerumani.

Akaendelea kupitia sifa za makampuni hayo makubwa ambao yana fanya kazi nzuri za kujenga majengo makubwa na imara duniani.

“Kampuni hiyo ya kijerumani ndio nzuri”

Sauti ya dada huyo ambaye ni jini ika mstua sana Evans.

“Mbona una kuwa una stuka stuka sana au bado huja zoea?”

“Kuzoea nime zoea, ila sio kwa kunistusha hivyo”

“Ahaa sawa. Wasiliana nao na uwatumie picha za huo mchoro mukubaliane bei kisha watakuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuanza kazi”

“Je nina paswa kuwalipa kwanza?”

“Hapana hakuna hajaya kuwalipa kwanza. Waje waone eneo kisha ndio maswala ya kulipana yata anza”

“Sawa”

“Kesho nahitaji ununue nyumba uilete familia yako hapa Dar es Salaam”

“Nita fanya hivyo mkuu”

“Siku nje”

Jini huyo akaondoka na kumfanya Evans ajifikirie kwa muda kisha akanakili namba za mawasiliano za kampuni hiyo kisha akaanza kuwasiliana nao.

***

“Magreth acha kuwa mnyonge. Huja kula chochote toka asubuhi. Nakuomba rafiki yangu, kunywa hata huu uji wa maziwa basi”

Josephine alizungumza kwa sauti ya kumbembeleza huku akimtazama Magreth aliye kaa kitandani kwake huku akionekana kujawa na mawazo mengi sana.

“Mage”

“Mmmm”

“Kula kidogo rafiki yangu”

“Jose sijisikii kula chochote”

“Najua hujisikii kula ila kunywa huu uji nilio kuandalia. Uta pata vidonda vya tumbo rafiki yangu”

Josephine aliendelea kuzungumza kwa unyonge wa hali ya juu. Taratibu Magreth akachukua bakuli hilo la uji, akaanza kunywa taratibu huku akimtazama Josephine aliye anza kutabasamu.

“Usiku uliiomba?”

“Ndio”

“Ume pata nini?”

“Sijapewa jibu la aina yoyote, laiti kama ninge pata jibu basi ninge kueleza”

“Mmmmm sawa”

“Leo huto kwenda kazini?”

“Hapana, nahiaji kufikiria baadhi ya mambo”

“Mambo gani rafiki yangu”

“Nita kuambia rafiki yangu kichwa changu kikikaa sawa”

“Haya ngoja nikiache”

Josephine akashika gongo lake linalo msaidia katika kutembea, akatoka ndani hapo. Magreth akaweka bakuli hilo la uji mezani kisha akashuka kitandani. Akaitafuta namba ya Tomas kwenye simu yake kisha akampigia, simu ya Tomas ikaanza kuita kisha ikapokelewa.

“Upo wapi?”

“Nyumbani vipi ume badilisha mawazo yako?”

“Hapana, sinto weza kuifanya kazi hiyo”

“Sawa”

Magreth akata simu, akaoga haraka haraka, akajiandaa na kutoka ndani hapo.

“Wapi una kwenda”

“Kuna sehemu nina elekea”

Magreth akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana. Akafika kwenye nyumba yenye vifaa ambavyo ana amini ata vitumia katika kazi yake. Akavua shatu alilo kivaa na akabaki na siridi pamoja na suruali. Akachukua upanga mrefu na taratibu akaanza kufanya mazoezi ya kuutumia upanga huo. Hasira na roho ya kisasi kiliyo jaa moyoni mwake, ikamfanya Magreth kuzidi kufanya mazoezi hayo kwa nguvu zake zote. Magreth akaendelea kufanya mazoezi ya vifaa tofauti tofauti, huku kila anavyo zidi kujifua ndivyo jinsi anayo iona sura ya nabii Sanga mbele yake.

“Lazima nikuue”

Magreth alizungumza huku akicheza na cheni ndefu ambayo kwa mbele ina kisu kikali sana ambacho kime jikunja kidogo. Mazoezi yake yakachukua masaa mawili na nusu, alipo hakikisha ame tosheka, akafungia vifaa hivyo kwenye sanduku lake kisha akaondoka eneo hilo.

***

“Aisee jana baba kawachakaza Al-Shabab”

Jery alizungumza kwa furaha huku akiwa na Julieth kwenye moja ya bustuni katika jumba la nabii Sanga.

“Kivipi?”

“Juzi si nilikuambia kuna askari wame vamiwa na kuuwawa?”

“Ndio?”

“Jana usiku baba ame amelipiza kisasi kwa kuwashambulia, yaani hapa nina amani aisee”

Jery alizidi kumsifia baba yake pasipo kujua kwamba wamecheza pata potea.

“Duuu mpe hongera sana baba”

“Usijali zime fika mke wangu”

“Ila Jery mume wangu, una jua hupaswi kuniona hadi siku ya harusi”

“Ahaa wapi, tambua siwezi kukaa pasipo kukuona wewe mke wangu”

“Nallijua hili, tume bakisha wiki mbili tu mume wangu. Kuanzia hapo nita kuwa ni wa kwako daima”

“Nalitambua hilo, vipi baba na mama wapo ndani?”

“Wame toka mara moja, si una jua siku zime baki chache hivyo wana kuwa wapo bize bize sana”

“Ahaa tuna weza tuka toka leo”

“Hapana Jery, sipaswi kutembea tembea mume wangu”

“No baby kuna sehemu nahitaji kukupeleka?”

“Wapi?”

“Wewe twende”

Julieth akajifikiria kisha akakubaliana na ombi hilo. Wakaondoka eneo hilo huku walinzi wakiendelea kuhakikisha wana kuwa salama.

“Niambie mume wangu tuna kwenda wapi?”

“Wewe twende”

Julieth ika mbidi kuwa mpole tu. Simu ya Jery ikaanza kuita, akaitoa mfukoni mwake na kukuta ni simu ya mama yake.

“Mom”

“Upo wapi?”

“Nina kwenda Kigamboni mara moja mama yangu”

“Kufanya nini tena Jery”

“Mama nipo na Julieth tuna kwenda kupata chakula cha mchana”

“Sawa kuwa makini”

“Usijali mama yangu”

“Kumbe tuna kwenda kupata lunch”

“Yes kuna chakula maalumu nime kianda kwa ajili yako”

“Mmmm sasa kwa nini hukunieleza?”

“Nime ona nikufanyie suprize mke wangu”

Wakafika katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano. KX Royal. Walinzi kumi wakashuka kwenye gari zoa mbili na wakaimarisha ulinzi, walipo hakikisha eneo hilo lipo salama mmoja, wao akafungua mlango wa gari alilo panda Jery na Julieth. Wakashuka kwenye gari hilo, wakaingia ndani ya hoteli hiyo na moja kwa moja wakaelekea katika eneo walipo andaliwa chakula hicho.

“Waoo ume juaje nina kipenda hichi chakula”

Julieth alishangaa sana mara baada ya chakula hicho kilicho kiitwacho kishumba kuwekwa hapo mezani.

“Yaa nilijua tu utakuwa ume kimiss hichi chakula”

“Ni kweli mume wangu, nina miaka mingi sana sija kila”

Julieth alizungumza huku akiwa amejawa na uchu wa kula chakula hicho.

“Samahani huruhusiwi kuingia eneo hili”

Mmoja wa walinzi alimuambia Evans ambaye ana hitaji kuingia katika eneo la mgahawa wa hoteli hiyo.

“Ahaa samahani kwani kuna nini?”

Evans aliuliza huku akitazama tazama eneo la ndani, akashangaa sana kuona eneo zima la mgahawa huo kukiwa na watu wawili tu, mwanaume na msichana huko watu wengine wote wakiwa hawapo. Evans akamkazia macho msichana huyo aliye mpa mgongo. Mlio wa simu ya Evans uka mfanya Julieth kugeuka nyuma kwa maana hata simu yake ina mlio wa aina hiyo. Macho ya Evans yakagongana na macho ya Julieth na kumfanya astuke kidogo kwa maana Julieth anavyo tambua kwamba Evans amepoteza kumbukumbu zake mara baada ya mateso makali aliyo patiwa na watu ambao hadi sasa hajaweza kuwafahamu.



ENDELEA

Evans akamtazama Julieth kwa sekunde kadhaa kisha akaondoka eneo hilo huku akiitoa simu yake mfukoni. Akaitazama namba ngeni inayo ingia kwenye simu yake.

‘Ni nani mwenye namba yangu?’

Evans alijiuliza hukua akiendelea kuitazama namba hiyo. Akaipokea na kuweka simu sikioni mwake.

“Halooo, Halooo”

Evans alijaribu kuzungumza ila hapakuwa na mtu yoyote aliye zungumza. Evans akata simu hukua kiamini kwamba huyo mtu ame kosea namba. Kukutana na Julieth kukaanza kuzua maswali mengi sana kichwani mwa Evans, akakumbuka siku alipo kutana na bwana Mbogo na akampatia picha za yeye na Julieth. Akakumbuka jinsi alivyo elezwa kwamba asijaribu kuwa na mahusiano na watoto wa vigogo.

‘Huyu ndio mume wake. Kama ndio mume wake basi yeye ndio aliye niteka mimi?’

Evans aliendelea kuwaza akilini mwake huku akiingia chumbani kwake.

“Baby mbona ume poteza furaha gafla vipi?”

Jery aliuliza huku akimtazama Julieth usoni mwake.

“Najihisi kichwa kuniuma baby”

“Kime anza saa ngapi?”

“Muda huu mume wangu”

“Ohoo pole basi acha tuondoke nikupelekea hospitalia”

“No baby, wewe nipelekea nyumani nikampumzike kidogo”

“Kweli”

“Ndio mume wangu”

“Vipi kishumba huto kula tena”

“Naomba uwambie wanifungie kwenye take way”

“Sawa mke wangu”

Kumuona Evans hakika kume mpotezea hata hamu ya kukaa hotelini hapo, jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba Jery hakumuona Evans. Wahudumu wakakifunga chakula cha Juliethe kwenye vyombo maalumu vya kubebea chakula. Wakaondoka hotelini hapo, wakamfikisha Julieth nyumbani kwako.

“Nashukuru mume wangu. Naomba nipumzike”

“Sawa mke wangu. Hakikisha una nieleza kila jambo linalo endelea. Sawa mama”

“Nime kuelewa mume wangu”

Jery akambusu Julieth mdomoni mwake kisha akaondoka nyumbani hapo kwa nabii Sanga. Julieth akaingia chumbani kwake huku akiwa amejawa na hsira sana kwa maana kumuona Evans ni hatari sana kwa ndoa yake.

“Baba upo wapi?”

“Nipo njiani nina rudi”

“Nakuomba uwahi”

“Vipi kwema?”

“Sio kwema”

Julieth akakata simu na kuirushia kitandani. Hazikupita hata dakika thelathini nabii Sanga na mke wake wakafika nyumbani hapo. Moja kwa moja wakaeleka chumbani kwa Julieth na wakamkuta Julieth akiwa amekaa kwenye moja ya sofa huku uso wake ukionekana dhairi kwamba amekasirika.

“Kuna nini mwanangu?”

Mrs Sanga aliuliza hukua kikaa pembeni ya Julieth.

“Nime muona Evans leo”

“Wapi?”

“Nilikwenda hoteli kupata lunch na Jery, kwenye hiyo hoteli tulikutana na Evans”

“Ila Evans hana kumbukumbu mwanangu?”

“Baba anazo, amenitazama kabisa na amenikazia macho, kama ni mtu ambaye hana kumbukumbu basi asinge nitazama kwa zaidi ya dakika moja”

“Mume wangu kama huyo Evans ana mkosesha amani mtoto kwa nini usimfanye apotee hapa dunianii. Hembu kumbuka ndio mwanaume aliye mtoa usichana mtoto wetu na endapo ata kwenda kufunguka mbele ya raisi au Jery una hisi sura zetu tuta ziweka wapi ikiwa mtoto wetu ana julikana kwamba ana bikra yake”

Mrs Sanga alizungumza kwa msisitizo.

“Umesema hoteli gani?”

“KX Royol”

“Ile ya Kigamboni?”

“Ndio”

Nabii Sanga akatoa simu yake na kumpigia meneja wa hoteli hiyo kwa maana ana fahamiana naye.

“Ndugu habari”

“Salama kaka yangu. Habari za masiku”

“Nina mshukuru Mungu. Nina kuomba uni saidie jambo”

“Jambo gani?”

“Nakuomba unitafutie jina la Evans kwenye listi ya wageni wako alafu uniambie yupo chumba gani”

“Sawa kaka, ila kwema?”

“Kwema tu ndugu yangu”

“Sawa nita kujulisha baada dakika tano”

“Nashukuru sana”

Nabii Sanga akakata simu huku akimtazama Julieth.

“Hivi ana itwa Evans nani?”

“Shika”

Kabla ya hata dakika tano hazijasha simu ya nabii Sanga ikaanza kuita. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio kaka”

“Ndugu yangu nime jaribu kutafuta majina ya wageni wote walio fika hotelini kwangu, ila kwa bahati mbaya sijalipata jina la aina hiyo”

“Ana itwa Evans Shika”

“Ngoja kidogo”

Simu ikaa hewani kwa sekunde kadhaa.

“Sijalipata jina kama hilo ndugu yangu”

“Sawa nina shukuru sana”

Nabii Sanga akakata simu huku akishusha pumzi taratibu.

“Vipi ame semaje?”

“Hakuna mtu kama huyo kwenye hiyo hoteli. Mwanangu wewe usiwe na shaka wala wasiwasi. Nitahakikisha nina mtafuta Evans popote alipo na nikimpata nita hakikisha ana lipa kwa jambo hili. Umenielewa”

“Sawa baba”

Nabii Sanga akamkumbatia Julieth kwa sekunde kadhaa ikiwa ni ishara ya kumfanya ajiamini na wala asihofie kwa jambo la aina yoyote ile.

***

“Mkuu serikali ime fanya shambulizi katika moja ya bandari zilizopo chini ya Al-Shabab”

John alizungumza huku akimtazama mzee Mbogo usoni mwake.

“Ime idhinishwa na serikali?”

“Ndio ni raisi ndio ameidhinisha na hadi ninavyo zungumza hivi sasa tulio lilisha fanyika”

Mzee Mbogo akashusha pumzi taratibu huku akimtazama msaidizi wake huyo. Akawatazama wafanyakazi wengine walipo ndani ya chumba kikubwa kilichopo nyumbani kwake hapo. Wafanyakazi wake hao watiifu kwake wote wapo kwa ajili ya kufanya naye kazi.

“Naombeni munisikilize”

Mzee Mbongo alizungumza na kuwafanya wafanyakazi wote kukaa kimya na kumsikiliza.

“Tupo wachache sana ila tuna uwezo wa kuilinda nchi. Kuondolewa ndani ya ofisi yetu ambayo tume izoea isiwe mwisho wa kuacha kuwa watumishi waamini wa nchi yetu. Oparesheni ambayo nilikuwa nime ipinga ya kuwashambulia Al-Shabab, hadi ninavyo zungumza nanyi ime kamilika”

Wafanyakazi hao wakaanza kutazamana kwa maana wana tambua sababu za mzee Mbogo kukataa juu ya jambo hilo.

“Nina wajua Al-Shabab kuliko hata raisi Mtenzi, yeye alikuwa ni askari wa kulinda wananchi ila mimi nilikuwa nina linda nchi, hivyo nina tambua Wasomalia jinsi walivyo. Anaye kupiga na kukuua humjui kwa maana wote wame valia nguo za kawaida, hata mtoto mdogo wa miaka nane ana weza kutumia bunduki na ana weza kukushambulia. Hili lililo fanyika leo ni lazima watalipa kisasi.”

“Si mimi wala wewe ambaye ata jua wata tushambulia nchi yetu kwa staili gani. Jambo kubwa linalo tupasa kufanya ni kuhakikisha tuna kuwa macho kuhakikisha hakuna shambulizi ambalo lina fanyanyika ndani ya nchi hii.”

“Watakao umia sio raisi na familia yake. Ni familia zetu, ndugu zetu, mama zetu, wanetu na kadhalika. Nina zungumza kwa uchungu kwa maana nina jua ni yapi yaliyo tokea kwenye nchi ya Somalia. Nina hakikisha kila mmoja wenu nina mlipa mara mbili ya kile kiasi ulicho kuwa unalipwa na serikali.”

Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya upole ila yenye msisitizo mkubwa sana huku akiwatazama wafanyakazi wake hao Maandalizi ya utendaji wa kazi katika chumba hicho ume fanyika na hakuna tatizo ambalo lita wazui kwa wao kufanya kazi.

“Ni muda wetu sasa kuwa tegemezi la taifa. Nina wategemea wote”

Wafanyakazi wote wakapiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza mzee Mbogo kwa ujasiri wake. Kila mfanyakazi akaanza kufanya kazi yake ambayo alikuwa ana ifanya katika kitengo cha NSA ili mradi ni kuhakikisha kwamba wana kwenda sambana na wafanyakazi walipo katika kitengo cha NSA.

***

“Tomas nime pata idea amayo ina weza kusaidia katika kulipiza kisasi chako”

Levina alizungumza huku akimtazama Tomas usoni mwake.

“Wazo gani?”

“Nime engeneza glasi ambayo ni bomu”

“Glasi ambayo ni bomu?”

“Ndio, kwenye ukumbi nina imani kuta kuwa na watu wengi na glasi ambazo zita fanyika. Jambo ambalo nina hitaji kulifanya ni kuipenyeza glasi hiyo na kuwa miongoni mwa glasi ambazo zia kuwa ndani ya ukumbi huo. Glasi hiyo tuta ilipua pale tu nabii Sanga na mke wake wata kuwa karibu”

“Ila mke wangu, kwenye ukumbi si kuta kuwa na watu wengine. Itakuwaje wakifa?”

“Wewe una taka kulipiza kisasi au una taka kuangalia watu wengine wata nusurika nini?”

“Japo nina roho ya kikatili sana, ila ukweli ni kwamba nina hitaji nabii Sanga, mwanaye na yeye waweze kufa”

“Hilo ni gumu mume wangu. Ulinzi ambao uta kuwepo katika eneo hilo hatuto weza kufanya jambo lolote”

Levina alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Tomas.

“Jaribu kufikiria idea nyingine mke wangu”

“Yule uliye zungumza naye jana ni nani?”

“Nani huyo?”

“Yule aliye kupigia”

“Magreth?”

“Ndio alikuwa amesemaje?”

“Amekataa kuhisiana na ofa niliyo mpatia ya kushirikiana naye”

“Naomba namba zake”

“Za nini?”

“Nahitaji kuonana naye ili nizumngumze naye hili swala la makini”

“Ata kuamini kweli?”

“Ishu sio kuniamini. Ishu ni kunipatia detail za kuhakikisha una lipiza vipi kisazi chako”

Tomas akajifikiria kwa muda kisha akampatia Levina namba ya Magreth. Levina akaipiga namba hiyo na kwa bahati nzuri ikaanza kuita, kisha ikapokelewa.

“Habari za asuhuhi dada Magreth”

“Salama nani wewe?”

“Mimi nina itwa Levina ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayo jihusisha sana kwa maswala ya tecnolojia. Nina omba kama tuna weza kukutana asubuhi hii?”

“Una weza kuja kwenye mgahawa wangu”

“Basi kama nusu saa nita kuwa hapo”

“Karibu sana”

Levina akakata simu, akaiweka kwenye pochi yake.

“Una kwenda wapi?”

“Ofisini kwake baadae”

Levina akambusu Tomas mdomoni kisha akatoka ndani hapo. Akaingia kwenye gari lake na kuiza safari ya kuelekea ofisini kwa Magreth. Akafika eneo la mgajawa, akasalimiana na Magreth kisha akamuomba waweza kuuzungumza ndani ya gari.

“Ndi ya gari lako?”

“Ndio kama huto jali”

Magreth akamtazama Levina kuanzia juu hadi chini. Kitu alicho weza kukigundua haraka haraka ni kwamba Levina hakuja eneo hilo kwa ubaya. Wakaingia kwenye gari na kukaa siti za mbele, Magreth akatazama nyuma ya gari hilo ili kama kuna mtu basi aweze kutambua. Alipo hakikisha kwamba kuan usalama, akamtazama Levina.

“Magreth mimi ni mke wa Tomas”

“Tomas huyu ninaye mjua mimi?”

“Ndio, nina imani kwamba alikuja hapa akiwa na sura bandia, mimi ndio niliye mtengeneza na wewe pekee ndio ume weza kugundua sura yake. Kufahamu hilo tu nime weza kuhisi kwamba una uwezo wa kipekee sana kama huto jali nina kiomba nikushirikishe jambo letu”

“Kama ni jambo la kumuu nabii Sanga kwa ajili ya kulipiza kisasi chake kwa kweli mimi sipo tayari. Una weza kuondoka kwenye mgahawa wangu”

Magreth alizungumza huku akifungua mlango wa gari hilo, kabla hajashuka Levina akawahi kumshika mkono wa kushoto na kumfanya Magreth kuutazama mkono wa Levina kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama usoni mwake kwa macho makali sana na yaliyo jaa ukali hadi Levina akaanza kuogopa



“Aha…samaahani”

Levina alizungumza huku akiuachia mkono wa Magreth.

“Muna hitaji nini kwangu”

Magreth alizungumza huku akimtazama Levina usoni mwake.

“Nina hitaji kufahamu ni vitu gani ambavyo nabii Sanga huwa ana penda na sehemu gania mbazo anazitembelea. Natambua kwamba una mahusiano naye ya kimapenzi kwa maana kuna siku mwanaye huyu anaye olewa pamoja na mama yake walikuja kazini kwangu waka hitaji niweze ku-hack namba ya mume wake na kweli niliweza kufanikiwa katika hilo na tuliweza kufahamu kwamba wewe na nabii Sanga mupo kwenye moja ya hoteli Bagamoyo”

Maelezo ya Levina yakamfanya Magreth kuikumbuka siku hiyo ambayo alikwenda hotelini na nabii Sanga.

“Hivyo usishangae kwa nini nina tambua kwamba wewe na nabii Sanga muna mahusiano”

“Yalikuwa zamani ila sio sasa”

“Sawa ila nina omba unisaidie katika hivyo vitu?”

“Sikumbuki ana penda nini wala ana tembelea maeneo gani kwa maana mimi na yeye tuliweza kuachana kwa ubaya hivyo sina kumbuku zozote na gata kama zitakuwepo basi ni lazima kwa yeye atakuwa amebadilisha code zake za sehemuambazo alikuwa ana pendelea kwenda”

“Sawa nime kuelewa Magreth je una weza kuniambia ni kwa nini uliachana naye?”

“Ohoo sasa hizi ni ishu ambazo hupaswi kufahamu”

“Hapana naamini zita nisaidia kidogo kwenye kazi yangu”

“Alihitaji kumuu boyfriend wangu, alimteka wakamtesa na akapoteza kumbuku zake”

“Masikini pole sana”

“Nashukuru”

“Je huyo boyfriend wako yupo wapi?”

“Sijui”

“Je huhitaji kufanya jambo kwa ajili ya hilo swala”

“Nimesamehe. Mimi ni mtu mwenye hofo na Mungu wangu hivyo sina haja ya kulipiza kisasi. Mungu mwenyewe ata lipa”

“Mmmmm sawa Mage nashukuru kwa muda wako”

“Nawe pia, ila ume sema kwamba uli hack namba yake?”

“Ndio”

“Sasa kwa nini usiendelee ku hack namba hiyo?”

“Haipo hewani tena”

Magreth akajifikiria kwa muda kidogo kisha akamtajia Levina namba ya nabii Sanga anayo itumia kwa sasa.

“Kupitia hiyo namba uta weza kumpata”

“Nashukuru sana Magreth”

Levina alizungumza kwa furaha kwa manaa kama namba hiyo ita kuwa ime mrahisishia sana kazi yake. Magreth akashuka kwenye gari hilo na kurudi kwenye mgahawa wake huku Levina naye akiondoka eneo hilo.

***

“Roho yako ime anza kuwindwa upya”

Evans akastuka usingizi, akamkuta mwadada ambaye ni jini akiwa amekaa kwenye moja ya sofa lililopo hapo chumbani.

“Una seama?”

“Roho yako ina windwa. Julieth na baba yake nabii Sanga wana taka kukuua”

“Kuniua kwa kosa gani ambalo nime wafanyia?

“Wanahisi kwamba uta toa siri”

“Siri gania mbayo mimi nina ifahamu?”

“Wamefeki bikra ya binti yao”

“Wame feki kivipi ikiwa mimi ndio niliye mvunja bikra yake?”

“Ndio hapo sasa, walimpeleka binti yao kwenye hospitali moja ya kichinana wakampandikiza bikra ya bandia na ndio hiyo walio mdanganya raisin a familia yake kwamba Julieth ni bikra”

“Sasa nifanye nini?”

“Mpigie nabii Sanga”

“Nimpigie alafu?”

“Umueleze kwa upole akikubali kukusikia basi itakuwani jambo jema ila asipo kubali yatakuwa ni mambo mengine”

“Sasa nina mpigiaje ikiwa sina namba yake”

“Inadike na umpigie sasa hivi”

Evans akachukua simu yake kuiandika namba hiyo anayo tajiwa.

“Mpigie”

Evans taratibu akampigia nabii Sanga na kuweka loudspeaker na simu hiyo ikaanza kuita.

“Haloo”

Evans akaisikia sauti ya nabii Sanga na kujikuta akimeza fumba zito la mate kwani ana wasiwasi mkubwa sana.

“Haloo”

“Habari yako nabii Sanga”

“Nani wewe?”

“Nina imani una nitafuta hivyo nime ona nikutute kabla ya wewe kunipata”

“Nani wewe”

“Una zungumza na Evans”

“Pumbavu wewe mwana haramu?”

Nabii Sanga alizungumza kwa kufoka.

“Mzee usinifokee, nimekupigia kwa wema. Nahitaji kuonana nawe”

“Wapi na saa ngapi?”

“Njoo Kigamboni darajani utanikuta nikikusubiri”

Evans alizungumza kwa kujiamini.

“Saa ngapi?”

“Saa mbili usiku”

Evans mara baada ya kuzungumza hivyo akakata simu.

“Saa mbili hiyo usiku nita kuwa nawe”

“Sawa”

Jini huyo akatoweka ndani hapo na kumuacha Evans peke yake akitafakari ni jinsi gani ambavyo ana weza kuonana na nabii Sanga.

***

Vijana ishirini wenye umri wa miaka kumi na sita hadi kumi na nane, wenye mafunzo ya kijeshi kutoka kwenye kikundi cha Al-Shabab wakaingia nchini Tanzania kwa njia tofauti tofauti. Udogo wao wa umri ukaondoa hofo kabisa kwa vyombo vingi vya usalama. Vijana hao wote kwa pamoja wakakutana Kariakoo katika mtaa wa Wasomali, wakakiribishwa na mzee Omary ambaye ana miliki duka la kuuza dawa za asili pamoja na mchele. Mzee huyo ambaye ni miongoni mwa washirika wa kuu wa kikundi hicho cha Al-Shabab aliwahifadhi vijana hao kwenye handaki lililopo chini ya gorofa hilo lenye duka lake.

“Karibuni sana Tanzania”

Mzee huyo alizungumza huku akiwatazama vijana hao.

“Tuna shukuru”

“Bunduki na mabomu vyote vipo tayari. Muna wiki moja ya kuhakikisha kwamba muna jiandaa vizuri kwa ajili ya shambulizi, nina imani kwamba muna elewa nini nina maanisha”

“Ndio mkuu”

“Chakula na vinywaji vyote muta kula. Sihitaji mtu yoyote kutoka huku chini wala kufanya maswaliano yoyote. Nilazima tulipe kisasi kwa ajili ya wezetu walio poteza maisha. Tuna enaelewana”

“Ndio mkuu”

Mzee Omary akatoka ndani humo na kurudi dukani kwake na kuendelea na biashara zake ikiwa hakuna hata mtu mmoja anaye fahamu kwamba chini ya duka lake lipo handaki lililo kusanya vijana wenye mpango wa kufanya shambulizi baya sana kwenye nchini ya Tanzania.

***

“Waoo hii ni nzuri”

Levina alizungumza mara baada ya kuyapata mazungumzo yaliyo ingia kwenye simu ya nabii Sanga.

“Nzuri nini?”

Tomas aliuliza huku akimtazama Levinaa liye vaa headphone masikoni mwake. Levina achomoa pini ya headphone hiyo aliyo ichomeka kwenye laptop yake na kufanya mazungumzo ya Evans na nabii Sanga kusikika.

“Wana kutana kwenye daraja la Kigamboni ehee?”

Tomas alizungumza huku akiwa na shahuku kubwa sana.

“Ndio, huo ni wakati wako sasa kuanza kulipa kisasi”

“Saa mbili usiku leo nabii Sanga una kwenda kuoionja kuzimu”

Tomas alizungumza kwa msisitozo huku akimtazama Levina aliye fanya kazi ya kunasa mawasiliano hayo ambayo kwa upande wao ni muhimu sana.

***

“Evans ana hitaji nionanae naye usiku wa saa mbili”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama Julieth usoni mwake.

“Wapi?”

“Katika daraja la Kigamboni”

“Baba huo ndio muda wa kumua”

“Ngoja tuangalie na yeye ame jipangaje, tusije tuka fanya kosa lolote katika hilo”

“Sawa baba, ila nina hitaji tumuue Evans. Ata haribu kila kitu chetu. Kumbuka ni mambo mangapi tuna yafanya kwa muamvuli wa ndoa yangu”

“Ni kweli mwanangu nina litambua hilo usiwe na shaka. Nahitaji kutoka sasa hivi”

“Una kwenda wapi baba?”

“Kuna kijana nina hitaji kumpatia kazi hii”

“Sawa”

Nabii Sanga akaondoka nyumbani kwake na moja kwa moja akaelekea hadi katika nyumba ya Tyson, mdunguaji aliye acha kazi katika kitengo cha NSA, miaka mitatu iliyo pita.

“Sikutarajia kukuona hapa mzee wangu”

Tyson alizungumza huku akimpa mkono nabii Sanga mara baada ya kushuka kwenye gari lake.

“Nina kazi ya muhimu sana leo usiku nina hitaji uweze kunisaidia”

“Hakuna shaka. Karibu ndani”

Wakaingia ndani na kukaa sebleni.

“Bado una ishi peke yako?”

“Ndio mzee si una jua maisha yangu ni ya kujificha ficha hivyo siwezi kuwa na mwana mke mmoja wa kuweka ndani”

“Ni kweli. Lililo nileta hapa kuna kijana nina hitaji kwenda kukutana naye leo,ila nina hitaji uweze kumuua”

“Kwa nini?”

“Ana mfwatilia sana mbinti yangu na jambo baya zaidi ni kwamba binti yangu ana olewa na kijana wa raisi”

“Ni kweli, nina litambua hilo”

“Yaa sasa huu usumbufu wake una weza kupelekea mapingamizi yasiyo na kichwa wala miguu kwenye ndoa ya binti yangu na mimi wala sihitaji kulisikia hilo”

“Sawa nipatie picha yake”

“Mmmm kwa picha, ngoja kwaza”

Nabii Sanga akampigia simu Julieth akamuomba amtumie picha ya Evans. Mara baada ya picha hiyo kutumwa nabii Sanga akamuonyesha Tyson picha hiyo.

“Kweli mzee huyu perege ndio ana kuumiza kichwa?”

“Sana na ana jiamini hadi nina shindwa kutambua ni kwa nini ana jiamini kiasi hicho”

“So una taka nimteke au nimuue eneo la tukio?”

“Kipi ni kizuri?”

“Kumteka na kumuua eneo jengine. Endapo tuta muua katika eneo hilo basi kutakuwa na maswali mengi sana kwako”

“Basi fanya hivyo. Nina kwenda kuonana naye mida ya saa mbili usiku, katika daraja la Kigamboni. Hivyo nita hitaji uwepo eneo la tukio.”

“Usijali bosi”

“Ukifanikisha hili kikamilifu, una bingo yako”

“Nakuaminia mkuu”

Nabii Sanga akaagana na Tyson kisha akaondoka nyumbani hapo.

***

Majira ya saa moja usiku Evans akaingia kwenye gari lake na taratibu akaanza safari ya kuelekea kwenye daraja hili ambalo halipo mbali sana na eneo la hoteli hiyo. Akafika eneo la kabirbu kabisa daraja hilo, akalisimamisha gari lake pembezoni mwa barabara. Akashuka kwenye gari lake na kuanza kutembea kwa miguu huku akiangaza angaza kila sehemu ya daraja hilo. Wingi wa magari pamoja na taa kubwa zilizo fungwa kwenye daraja hilo vikamfanya Evans kujiamini sana. Akatoa simu yake mfukoni na kumpigia nabii Sanga.

“Nimefika”

“Nipo njiani nina kuja na hakikisha una onana na mimi”

Simu ya nabii Sanga ikakatwa na kumfanya Evans kujiuliza maswala lakadhaa ya kwa nini mzee huyo ame kata simu mapema sana. Evans akafika eneo la katikati ya daraja hilo, akasogea eneo la pembeni ya daraja hilo na kuchungulia eneo la chini ambapo kuna bahari. Akiwa hapo simu yake ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kukuta ni namba ya nabii Sanga.

“Upo wapi?”

“Wewe upo wapi?”

“Nipo darajani nahitaji kujua upo wapi?”

Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo, gafla gari moja likafunga freki pembeni ya Evans wakashuka watu wawili walio valia suti nyeusi huku mikononi mwao wakiwa na bastola na wakamfanya Evans kustuka sana kwa maana uvaaji wao ni sawa na watu ambao walimteka mkoani Morogoro.



“Evans Shika ingia ndani ya gari”

“Nyinyi ni kina nani?”

“Ingia ndani ya gari haraka sana.”

“Nyinyi ni kina nani?”

“Sisi ni walinzi wa mzee Mbogo, nina imani kwamba una mfahamu. Tupo hapa kwa ajili ya kukusaidia, ingia ndani ya gari”

Evans akashusha pumzi hukua akiwatazama vijana hao. Wakaona gari moja ndogo likija kwa kasi sana, dereva wa gari hili akatoa mkono mmoja nje na kuanza kushambulia eneo walilo simama Evans na vijana hao kwa kutumia bastola yake. Hapakuwa na maulizo mengine zaidi ya Evans kuingia ndani ya gari hilo huku vijana hao nao wakiingia ndani ya gari hilo na kuondoka eneo hilo kwa kasi sana.

Tayson akazidi kuendesha gari lake huku akijitahidi sana kuwashambuli Evans na vijana wa mzee Mbogo.

“Hao ni kina nani wanao tushambulia?”

Evans aliuliza kwa mshangao huku akiwa ameinama chini, vijana hao hawakuweza kumjibu chochote zaidi kujitahidi kuhakikisha kwamba wana mzuia Tyson anaye endelea kuwashambulia. Gafla risasi moja ikapiga kwenye tairi la mbele la gari la Tyson na kusababisha gari hilo kukosa muelekeo huku likiyumba yumba na mwishowe likatoka kabisa nje ya barabara na kumfanya Tyson kujirisha na kuliacha gari lake likigonga mti mkubwa na likalipuka. Tyson taratibu akasimama huku akitazama jinsi gari la walio mchukua Evans likitokomea gizani. Tyson akatoa simu yake na kumpigia nabii Sanga.

“Kazi haijafanikiwa”

Tyson mara baada ya kuzungumza hivyo akakata simu na kuivunja vunja, akachomoa laini yake na kuondoka eneo hilo la tukio kabla ya raisi watoa msaada kufika. Vijana wa mzee Mbogo moja kwa moja wakafika katika moja ya fukwe, wakashuka na kuingia kwenye boti na kurudi upande wa pili wa jiji la Dar es Salaam. Wakawakuta wezao wawili kwenye ufukwe wa bahari wakaingia kwenye gari na kuelekea katika nyumba ya mzee Mbogo ambapo kwa sasa ndipo wanapo fanyia kazi.

***

“Madam kuna situation tume iona”

Kijana wa Emmy alizungumza na kumfanya Emmy kutoka ofisini kwake na kuelekea katika chumba cha mawasiliano. Emmy akaona video iliyo rekodiwa na cctv kamera zilizo fungwa kwenye daraja la Kigamboni, jinsi gari nyeusi aina ya Toyota Prado TX inavyo shambuliwa.

“Hao ni kina nani?”

Emmy aliuliza hukua kitazama sura za vijana wawili.

“Madam hawa ni wafanyakazi wazamani wa kitengo cha NSA”

“Majina yao?”

“Mmoja ana itwa Laurent na mwengine ana itwa Criss. Walianza kazi miaka miwili iliyo pita”

“Ina kuwaje wana mfwata huyo kijana?”

“Hatutajua muheshimiwa”

“Huyo kijana ni nani?”

“Ana itwa Evans Shika, ni mwana chuo aliye maliza mwaka jana”

“Hakikisheni kwamba muna ifwatilia hilo tukio”

“Sawa mkuu”

“Madam, raisi yupo kwenye laini namba tatu”

Madam Emmy akanyanyua mkongo wa simu ya mezani, akaminya batani yenye namba tatu na kuiweka simu yake sikioni.

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Kuna tukio gani linalo endelea Kigamboni kwa maana nime pata taarifa kuna tukio la kijambazi limetokea darajani”

“Ni kweli muheshimiwa raisi, ila tuna lifwatilia”

“Ni nani ambaye ana husika?”

“Hadi sasa hivi muheshimiwa tumeweza pata watu watatu, wawili ni wafanyakazi wa zamani wa kitengo cha NSA na mmoja waoa na itwa Evans Shika”

“Evans Shika !!!?”

“Ndio muheshimiwa”

“Hakikisheni muna mtafuta huyo kijana na muna nileta kwangua akiwa hai sawa”

“Sawa muheshimiwa je hawa vijana hujawatuma wewe?”

“Siwajui na wala sio mimi niliye watuma pia nitumie hiyo video ya CCTV”

“Nimekuelewa muheshimiwa raisi”

Emmy akakata simu huku akiwatazama vijana wake wanao endelea kufanya kazi kwa juhudi.

“Hakikisheni kwamba muna fahamu huyo Evans Shika ana pelekwa wapi na Aisha itume hiyo video ikulu”

“Sawa muheshimiwa”

Madam Emmy alizungumza huku akirudi ofisini kwake.

***

“Njoo ofisini kwangu”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa amejawa na hasira kidogo. Baada ya dakika tano Jery akaingia ofisini kwa baba yake huku akiwa na wasiwasi kidogo kwa maana sauti ambayoa aliizungumza baba yake kidogo ime mtisha.

“Kaa hapo”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akimnyooshea Jery kidole. Raisi Mtenzi akamgeuzia Jery laptop yake na kumuonyesha video ya tukio la Evans kuchukuliwa na gari. Jery akastuka kidogo kwa maana ana tambua kwamba Evans alisha uwawa na vijana wake.

“U…u…meiitolea wapi?”

“Huyo mpumbavu bado yupo hai. Garama kubwa ulizo zitumia, kupoteza maisha ya watu ila bado huyo kijana yupo tu?”

Raisi Mtenzia alizungumza kwa kufoka sana.

“Hata mimi baba nina shangaa”

“Una shangaa nini ikiwa ume muona hapo akiwa hai?”

“Sa….asa”

“Nahitaji afe kabla ya hili jua halijakwisha. Fanya ufanyavyo ila nina taka kuona maiti yake hapa mbele yangu. Umenielewa”

“Nimekuelewa baba”

Raisi Mtenzi akashusha pumzi huku akijaribu kuizuia sauti yake.

“Acha”

“Ehee”

“Acha kulifanya hilo tukio”

“Kwa nini baba?”

“Nita hitaji kumpata mimi mwenyewe na nita hitaji kuzungumza naye”

“Una hitaji kuzungumza naye nini baba?”

“Nina jua ni nini cha kuzungumza naye. Wewe endelea kufikiria mambo yako ya ndoa”

“Sawa baba”

Raisi Mtenzi akatoa ishara ya Jery kutoka ofisini kwake. Jery mara baada ya kutoka, akachukua simu yake na kumpigia Julieth.

“Upo wapi baby?”

“Nipo nyumbani”

“Evans ameonekana kwenye daraja la Kigamboni na kuna watu ambao wame mchukua ila baba ana mtafuta nina imani ata mkamata na ana hitaji kuzungumza naye”

“Evans!!?”

Julieth alizungumza kwa mshangao kwa maana kama Evans ata kamatwa na raisi Mtenzi basi ita kuwa ni jambo hatari sana kwa upande

“Ndio, ila kesho tuta lizungumza vizuri. Umenielewa?”

“Sawa mume wangu”

Jery akaka simu na kuingia chumbani kwake huku akiwaza ni jinsi gani anavyo weza kutumia watu wake kuweza kufahamu ni wapi alipo Evans.

***

“Shitii nime chelewa”

Tomas alizungumza huku akikaa kwenye sofa. Levina akamtazama kwa sekunde kadhaa huku akitabasamu.

“Kuchelewa kwako, ila kume tuwezesha kupata jambo”

“Jambo gani?”

Levina akawasha iliyopo sebleni hapo. Wakaona jinsi vijana wawili wakimchukua Evans na kuondoka naye darajani hapo huku wakishambuliwa na dereva aliyopo kwenye gari ndogo.

“Video hiyo ime naswa na kamera za CCTV zilizopo pale darajani. Kwa kutumia video hiyo basi tuta weza kumshawishi Magreth na akatusaidia katika hili”

“Magreth?”

“Ndio”

“Ila si amesha kataa?”

“Amekataa ila kuna ushidi wa mzungumzo”

Levina alizungumza huku akiweka mazungumzo ya mwisho yaliyo ingia kwenye simu ya nabii Sanga.”

“Huyo aliye sema kazi ime shindikana ni nani?”

“Ana itwa Tyson alikuwa yupo kitengo cha NSA ila aliacha kazi kipindi cha nyuma. Amekuwa ni mfanya kazi za uuaji na inavyo onyesha ana fanya kazi na nabii Sanga”

“Kwa hiyo tuki mpata Tyson tuna mpata nabii Sanga?”

“Kumpata Tyson ni jambo gumu kwa maana hata simu yake kwa sasa haionyeshi kwmaba yupo wapi. Amekuwa ni mtu ambaye ni hatari sana na ana ishi kwa kuzunguka zunguka kama kunguru”

“Sasa nabii Sanga”

“Ngoja kwanza”

Levina akaitafuta namba ya Magreth kwenye simu yake na kumpigia. Simu hiyo ikaanza kuita kwa muda kisha ikapokelewa.

“Mage ni mimi Levina”

“Una hitaji nini?”

“Samahani nina weza kufahamu kwamba upo wapi?”

“Sema una hitaji nini?”

“Kuna video na audio nina kutumia kwenye simu yako. Ukisha maliza kuvitazama na kusikiliza, basi nina kuomba unitafute”

Levina akakata simu na kumtumia Magreth video hiyo pamoja na sauti ya Tyson ambayo alimpigia nabii Sanga.

***

Magreth akapunguza sauti ya gari lake huku akisibiria askari walio zuia gari kupita katika daraja hilo la Kigamboni, kuziruhusu. Magreth akafungua video hiyo na akaanza kuitazama. Mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda kasi mara baada ya kumuona Evans akiwa ameshikwa bastola na watu wawili, video hiyo ikaendelea kuonyesha jinsi Evans na watu hao walivyo ingia ndani ya gari kwa uharaka huku gari nyingine ndogo ikiwashambulia kwa nyuma.

Magreth kwa woga na hasira akahisi mwili mzima ukimtetemeka kwa woga. Akatazama jinsi gari hizo zinavyo fukuzana na zilivyo toka kwenye daraja hilo na video hiyo ikakata kwa maana katika barabara za mitaani hakujafungwa kamera za aina yoyote. Hapo ndipo Magreth akatambua sababu ya gari zao kuziwa kupita darajani hapo kwa muda.

“Ohoo Mungu wangu Evans wangu”

Magreth alizungumza huku machozi yakimlenga lenga na isitoshe watu walio ondoka na Evans wamevaa sawa sawa na wale watu walio mteka kule mkoani Morogoro. Magreth akasikiliza audio hiyo ambao ni fupi tu.

‘Kazi haijafanikiwa’

Magreth kwa haraka akampigia Levina ili kufahamu ni kitu gani kinacho endelea.

“Ni nani aliye mteka Evans”

“Tulia Magreth hili jambo halihitaji hasira hara kidogo.”

“Niambie ni nani ambaye amehusika kwenye jambo hilo”

“Nina weza kukueleza ila nita hitaji unisaidie na mimi kama jinsi nitakavyo kusaidia”

Levina alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Magreth kuzidi kupandwa na hasira.

“Una taka nikusaidie nini?”

“Nahitaji uungane nasi katika kumuangamiza nabii Sanga”

“Una taka kuniambia nabii Sanga ndio ana husika na jambo hili?”

“Siwezi kuwa na uhakika wa moja kwa moja ila nina hitaji kushirikiana na wewe. Tukae chini kwa pamoja kisha tujue ni nani ame husika”

Magreth akajifikiria kwa muda huku, kutokana bado ana mpenda Evans na ana muhitaji kwenye maisha yake hakuona haja ya kumkatalia Levina katika kushirikiana katika jambo hilo.

***

Julieth akahisi tumbo lake lina mpasuka kwa maumivu yatokanayo na woga. Hakuweza kabisa kukaa eneo moja na mbaya zaidi kila anavyo mpigia simu baba yake, hapokei. Mrs Sanga naye hakuweza kutulia eneo moja kwa wasiwasi. Wakasikia mgurumo wa gari la nabii Sanga, wote wakachungulia dirishani, wakamuona nabii Sanga akishuka, Julieth akataka kutoka nje ila mama yake akamzuia.

“Nje kuna walinzi na hili jambo lina paswa kuzungumzwa humu ndani”

Julieth aliweza kumuelewa mama yake. Nabii Sanga akaingia ndani hapo, moja kwa moja akapandisha gorofani pasipo kuzungumza jambo lolote na kuwafanya Julieth na mama yake kumfwata. Nabii Sanga akavunja chungu chenye uwa la urembo kwa hasira. Mrs Sanga na mwanaye hawakumsemesha chochote zaidi ya kumtazama jinsi anavyo tweta kwa hasira.

“Baba”

Julieth aliita kwa sauti ya upole. Nabii Sanga akamtazama Julieth kwa macho makali pasipo kumsemesha jambo lolote.

“Imekuwaje?”

“Kuna watu wame tokea na kumchukua Evans, hivyo Tyson hajafanikiwa kumpata”

“Ohoo Mungu wangu”

Mrs Sanga alihamaki huku naye wasiwasi ukizidi kumtawala.

“Baba ina bidi tuwahi kumpata Evans kwa maana hivi ninavyo zungumza raisi Mtenzi ame tuma timu yake kumtafuta na amedai akimpata ana hitaji kuzungumza naye uso kwa uso”

Maneno hayo yakamstua sana nabii Sanga, akahisi kama nguvu zina muishia miguuni mwake kwa maana endapo raisi Mtenzi ata fanikiwa kumpata tu kijana huyo basi siri ya bikra ya msichana wake ita kuwa hadharani.



“Mume wangu tuta fanyaje?”

Mrs Sanga aliuliza huku machozi ya wasiwasi yakimlenga lenga usoni mwake. Nabii Sanga akakosa hata jambo la kumueleza mwanamke huyo.

“Naombeni nipumzike”

“Baba una taka kupumzika ikiwa bado hatujapata muafaka wa hili jambo”

“Nipeni muda wa kutafakari kwa maana mtu niliye kuwa nina mtegemea ndio kama hivyo amemkosa Evans, sasa munataka mimi nifanye nini?”

Nabii Sanga alizugumza kw aukali sana huku akimtazama mke wake na Julieth ambao wote wana onekana kukatishwa tamaa na kauli hiyo ya nabii Sanga. Wakatoka chumbani hapo na kuelekea katika chumba cha Julieth.

“Mama nina waagiza wale vijana wetu wamtafute”

“Hapana hakuna haja ya kuwaagiza”

“Kwa nini mama ikiwa hali halisi ya mambo una iona?”

“Ndio ina iona ila kumbuka wale wapo kwa ajili ya kazi gani. Endapo tutawaingiza kwenye jambo hili binafsi ina weza kutugarimu. Wewe ngoja kwanza tutajua ni nini cha kufanya”

Mrs Sanga alizungumza kwa kumfariji tu mwanaye ila kwa upande mwengine na yeye hana amani kabisa ya moyo wake.

***

Gari waliyo panda Evans na vijana wa mzee Mbogo ikaingia katika maegesho maalumu yaliyo tengenezwa chini ya nyumba hiyo ambayo kwa eneo la juu ina onekana ni nyumba ya kawaida tu. Ila kwa chini ina ukumbi mkubwa sana ambao ndio hao ambao vijana wa NSA walio acha kazi, wana fanya kazi.

“Hapa ni wapi?”

Evans aliuliza, ila vijana hao wakashuka kwenye magari na kumfanya na yeye kushuka. Wakamuingiza Evans katika chumba ambacho kina sofa mbili tu kisha wakatoka.

“Kazi nzuri”

Mzee Mbogo alizungumza huku akimwatazama vijana wake hao.

“Tuna shukuru sana mkuu”

“Muna weza kuendelea na majukumu mengine”

“Hato kudhuru huyo kijana?”

“Hato weza kunidhuru hivyo kuweni na amani”

Mzee Mbogo alizungumza huku akiwatazama vijana wake hao. Mzee Mbogo akaingia ndani ya chumba hicho na kumfanya Evans kustuka kidogo.

“Wewe?”

Evans alizungumza kwa mshangao, mzee Mbogo akakaa kwenye soma lililopo mbele ya sofa alilo kalia Evans.

“Kwa nini ume niteka”

“Ulihitaji nikuache ufa kwa kushambuliwa kwa risasi?”

Mzee Mbogo alizugumza kwa upole sana hukua kimtazama Evans.

“Ulijuaje kwamba nipo pale?”

“Huwa nina tambua kila kitu kinacho endelea kwa sasa katika hii nchi. Tuliweza kukuona pale darajani, hivyo vijana wangu walio kuwa karibu na eneo lile waliweza kukuwahi haraka sana”

“Mulinionaje onaje?”

“Darajani pale kuna CCTV kamera. Tuachane na hayo, una weza kuniambia pale ulikwenda kukutana na nani?”

Evans akaka kimya huku akimtazama mzee Mbogo.

“Ehee”

“Ulikuwa ume panga kukutana na nani?”

“Nabii Sanga”

“Sanga huyu mchungaji?”

“Ndio”

“Bado ana kufwatilia?”

“Ndio na nilikuwa na lengo la kwenda kusawazisha tofauti zetu. Ila kabla ya kuonana kuna yale yaliyo tokea pale”

Mlango wa chumba hicho ukafunguliwa, akaingia msichana mrefu, aliye valia suti nyeusi.

“Mkuu kuna kitu naomba uje kukisikia”

“Sawa. Kuwa na amani kaa kwa amani upo sehemu salama”

Mzee Mbogo alizungumza na kuondoka ndani hapo.

“Kumbe una wasiwasi”

Sauti ya dada ambaye ni jini ika mstua sana Evans.

“Ulikuwa wapi hadi nika chukuliwa na watu nisio wajua”

“Nilikuwa pamoja nawe ndio maana hakuna aliye kudburu. Huyo mzee ni mtu mzuri kwako hivyo usiwe na shaka wala wasiwasi wowote”

“Una uhakika?”

“Kuna siku nilisha wahi kukudanganya?”

“Hapana”

“Baadaye”

Dada huyo akapotea ndani hapo. Mzee Mbogo akakabidhiwa headphone na kuzivaa masikioni mwake. Akaanza kusikiliza mazungumzo ya siri yaliyo naswa ndani ya ofisi ya raisi Mtenzi, akizungumza na mwanaye Jery. Mzee Mbogo akastuka sana kwa maana Evans wa watu ana windwa na mkuu wa nchi akishirikiana na mwanaye.

“Hayo mazungumzo ni ya lini?”

“Dakika kumi na tano zilizo pita na raisi ametoa agizo kwa Emmy kuhakikisha kwamba wana mtafuta Evans popote alipo pale alipo”

“Sawa niingizie hiyo sauti kwenye simu yangu. Pia hakikisheni kwamba muna wafwatilia wao hatua kwa hatu ili kutambua ni kitu gani ambacho wana kifanya”

“Sawa mkuu”

Mzee Mbogo akarudi katika chumba alicho muacha Evans.

“Una hitaji chochote cha kula?”

“Hapana nipo vizuri”

Mzee Mbogo akaiweka mazungumzo hayo aliyo tumiwa kwenye simu yake. Evans akastuka mara ya kusikia yeye ndio anaye zungumziwa hapo.

“Ni kina nani hao?”

“Huyo ni raisi Mtenzi pamoja na mwanaye Jery. Haya mazungumzo yana kulenga wewe na hapa ninavyo zungumza, una tafutwa nchi nzima. Sasa una nafasi ya kuzungumza na mimi, nieleze ni kitu gania mbacho kina endelea ulichukua kitu gania ambacho kina wafanya wakuu wa nchi wakose usingizi kwa ajili yako?”

“Mimi sijui jambo lolote na wanacho kifanya wao ni chuki dhidi yangu”

“Una taka kuniambia haya yote yana tokea kutokana na wewe kuwa na mahusiano na mtoto wa nabii Sanga?”

“Nina hisi hivyo mzee”

Mzee Mbogo akamtazama Evans kwa sekunde kadhaa na kweli anacho kizungumza kina ukweli wa asilimia mia moja.

“Nina kuletea shuka,uta lala humu ndani hadi kesho ume nielewa”

“Sawa ila nikirudi uraiani si wata niua kama walivyo kosa kosa kuniua mara ya kwanza”

“Mara ya kwanza walitaka kukuua?”

Mzee Mbogo akamtazama kwa sekunde kadhaa Evans kwa maana ana tambua kila jambo ambalo alikumbana nalo Morogoro akiwa hotelini na raisi ndio alimpatia amri ya kumzuia kijana wake kuto kuendelea na kazi ya kumlinda Evans huku akimini ilikuwa ni kutokana na usalama wa nchi. Mzee Mbogo akatoka chumbani hapa na baada ya dakika tano akarudi akiwa na mto pamoja na shuka.

“Hilo sofa lina matumizi mawili”

“Ehee!!”

“Usishangae”

Mzee Mbogo akamuomba Evans kusimama, mzee Mbogo akalikunjua sofa hilo na likawa kitanda.

“Usiku mwema. Kama una simu hapa nipatie”

Evans akatoa simu yake na kumkabidhi mzee Mbogo kisha akatoka ndani hapo na kumuacha Evans akiwa amejawa na maswali mengi sana.

“Mkuu tuna fanyaje kwa maana hapa Emmy na vijana wake wame zibaini sura za vijana wetu”

“Hilo lisikupe wasiwasi. Ueni data zote katika kitengo cha NSA”

“Muheshimiwa!!”

John alizungumza kwa mshangao huku akimtazama mzee Mbogo usoni mwake.

“Ndio, ueni data zote kwa kufanya hivyo hawato kuwa na hamu ya kuendelea kutufwatilia. Pigo hili hakikisheni kwamba hawato kaa warudishe kitu chochote ambacho kime potea. Sawa”

“Sawa mkuu”

Mzee Mbogo kutokana yeye ndio aliunda mfumo mzima wa kitekonolojia wa kitengo hicho cha NSA, hivyo ana fahamu code muhimu za kufuta mfumo huo mzima. John na vijana wengien wakanza kazi hiyo hadi wakafika hatua ya kuingiza code hiyo.

“Mkuu ni wakati wako”

Mzeee Mbogo akaisogelea computer ya msaidizi wake John. Akaingiza code hiyo ambayo hata vijana wake hao hawaijui. Alipo maliza kuiandika, akawatazama vijana wake ambao wote wana mtazama yeye. Mzee Mbogo akaminya batani ya kuruhusu code hiyo kuanza kufanya kazi. Watu wote wakahamishia macho yao kwenye tv kubwa iliyopo kwenye moja ya ukuta katika chumba hicho. Neno Delete lililo tokea kwenye tv hiyo kubwa likaandamana na mstari inao hesabu kwa asilimia. Kila mmtu aliweza kwenda na asilimia hizo hadi ilipo fika mia, mzee Mbogo akashusha pumzi kwa maana hadi waje kutengeneza mfumo kama huo basi ita wachuka hata miaka miwili.

“Kitengo cha NSA kwa sasa mfumo wao umezima. Sisi ndio tegemezi la taifa na endapo serikali ita tuhitaji kufanya kazi nasi basi nina wahakikishia kwamba nita hitaji kila mtu awe tajiri kwa kulipwa hata mara kumi na mshahara ninao walipa hivi sasa.”

Kila mfanyakazi akajawa na furaha.

“Muna weza kupumzika, ila nina waomba musiweze kutoka na kwenda majumbani. Huko nje sio salama kabisa. Usiku mwema”

Baada ya mzee Mbogo kuzungumza maneno hayo akatoka ndani hapo na kuwaacha wafanyakazi wake wakipiga stori mbili tatu huku wengine wakitafuta sehemu za kulala ndani ya nyumba hiyo.

***

Emmy na vijana wake wakazidi kuchanganyikiwa kwa maana kila kitu walicho kuwa wana kitegemea kime futika. Hakuna mawasiliano yanayo toka kwa simu za mezani. Hakuna kamera hata mmoja ya ulinzi inayo rekodi.

“Muna shangaa nini, fanyani kazi”

Emmy alizungumza kwa kufoka sana. Computer zote zina onyesha logo ya kitengo hicho na hakuna hata moja ambayo ina weza kuendelea zaidi ya hapo. Wanajaribu kuzizima na kuziwasha ila hakuna kitu chochote kinacho eneokana zaidi ya hiyo logo. Wenye laptop wakajaribu kufanya wanacho kiweza, ila hapakuw ana mtu hata mmoja aliye fanikisha chochote. Emmy akaingia ofisini kwake huku akiwa amejawa na hasira kali sana.

“Kharhgaaaaaa”

Emmy alipiga kelele kwa hasira huku akiitupilia mbali simu ya mezani kwake. Akatoa simu yake ya mfukoni, akashusha pumzi taratibu na kumpigia raisi Mtenzi.

“Mume fikia wapi?”

Raisi Mtenzi alianza kwa kuuliza.

“Mkuu system nzima ya kitengo cha NSA ime zima”

“Nini?”

“Mkuu hapa ninavyo zungumza na wewe kila kitu kwenye computer zetu kime futika.”

“Nina kuja”

Simu ikakatwa na kumfanya Emmya kuanza kutetemeka mwili mzima kwa maana ana muogopa sana raisi Mtenzi.

Raisi Mtenzi akaondoka ikulu na walinzi wachache pamoja na gari tatu. Wakafika katika kitengo cha NSA na yeye mwenyewe akashuhudia jinsi mfumo mzima wa utendaji wa kazi ulivyo zima katika ofisi hiyo kubwa ya usalama wa nchi.

“Hili tatizo limetokea saa ngapi?”

“Limetokea muda mchache kabla sijakupigia simu”

“Mkuu”

Mshauri wa raisi Mtenzi alimuita huku akimtazama usoni mwake.

“Ndio”

“Samahani kama nita kuwa nime kuvunjia utaratibu wako”

“Zungumza”

“Mimi nime fanya kazi katika kitengo hichi kwa miaka mingi ya nyuma”

“Nalijua hilo, huna haja ya kunihubiria. Wewe nenda kwenye pointi yako ya msingi.”

“Mfumo mzima wa utendaji wa kazi, ulitengenezwa na mzee Mbogo. Kumfukuza kazi, haya ndio matokeo yake”

Raisi Mtenzi akamtazama mshauri wake huyo kwa macho yaliyo jaa hasira kali.

“Mbogo yeye ni nani kwenye hili. Tatizo la kawaida kama hili una anza kujaji maamuzi yangua au una taka kuniamia kwamba nime kosea mimi kumfukuza yule kazi?”

Raisi Mtenzi alimfokea mshauri wake huyo ambaye ni mzee wa makamu kiasi.

“Muhehimiwa raisi ume nipa nafasi hii ili niwe mshauri wako. Kunapokuwa na haja ya kukueleza ukweli basi nita kueleza ukweli. Mbogo ndio mtu pekee anaye weza kutengeneza mfumo mzima wa kitengo cha NSA. Kama una bishana na mimi nina apa kwa jila la Mungu. Wape hawa vijana siku ya kufanya kazi kurudisha mfumo huo au kutengeneza mfumo kama huo, endapo wata fanikiwa basi nipo tayari kuachia nafasi yangu kama mshauri wako namba moja”

Mzee huyo alizungumza kwa ukali hadi kila mtu akashangaa.Mzee huyo ame fanya kazi na raisi Mtenzi hivyo ana mfahamu pasipo kuwa na majibizano naye kwenye vitu muhimu vya kuhusu taifa basi ana weza kuchukua maamuzi yatokanayo na hasira. Raisi Mtenzi akakasirishwa sana na kufokewa na mfanyakazi wake huyo, akajikuta akitabasamu huku akimtazama mzee huyo.

“Your fired”(Umefukuzwa kazi)

Kauli ya raisi Mtenzi ikazidi kuwa ogopesha watu wote humo ndani, ila mzee huyo hakuogopa chochote. Akamsogelea raisi Mtenzi karibu kabisa, walinzi wakataka kumzuia ila raisi Mtenzi akanyoosha mkono ikiwa ni ishara ya kuwazuia.

“Ipo siku, uta fahamu umuhimu wa Mbogo kwenye hii nchi. MR PRESIDENTTTTTTT…….”

Mzee huyo ambaye kwa jila la utani anaitwa The Brain, alizumgumza kwa msisitizo kisha akaliweka koti lake la suti vizuri na kuanza kuondoka ndani hapo huku akisindikizwa na walinzi wawili wa raisi Mtenzi kuhakikisha kwambaa na toka kwenye jengo hilo na haleti madara ya aina yoyote.



Mr The Brain akapelekwa hadi kwenye maegesho ya kitengo hicho cha NSA. Akaingia kwenye moja ya gari la kitengo hicho.

“Hakikisha una mpeleka nyumbani kwake.”

Mmoja wa walinzi wa raisi Mtenzi alimuambia dereva wa gari hilo.

“Sawa mkuu”

Dereva huyo akapandisha kioo cha gari lake kisha wakaondoka katika makao makuu ya kitengo hicho.

“Wasiliana na balozi wa Marekeni muambie nina hitaji kuzungumza naye”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akiwa amekaa katika ofisi ya Emmy.

“Samahani mkuu simu zote za mezani hazitoi mawasiliano.”

“Kwa nini?”

“Sijajajua mkuu, ila hazitoi maswaliano”

Raisi Mtenzi akatoa simu yake mfukoni na kumpigia balozi huyo wa Marekeni.

“Muheshimiwa raisi”

“Habari za muda huu”

“Salama tu vipi mbona usiku”

“Kuna matatizo kidogo, nina omba unisaidie”

“Nakusikiliza muheshimiwa.”

“Kitengo changu cha NSA, kime poteza data zake zote na hadi ninavyo zungumza hivi sana kipo katika giza hivyo nina omba sana uweze kunisaidia”

“Una taka kuniambia kwmaba kitengo chote mfumo wake wa mawasiliano yme zimika?”

“Ndio”

“Muheshimiwa hilo ni jambo la hatari sana kwa nchi. Niambie una hitaji nini?”

“Nahitaji wataalamu ambao wana weza kutengeneza mfumo mzima”

“Sawa, ngoja niwasiliane na raisi wangu kisha nita kupigia simu”

“Nashukuru”

Raisi Mtenzi akashusha pumzi huku akimtazama Emmy usoni mwake.

“Mkuu nina weza kuzungumza jambo?”

“Zungumza”

“Wamarekenia endaopo wata tutengenezea mfumo mwengine, nina imani kuna baadhi ya siri zetu za serikali watakuwa wana zipata, isitoshe hichi ndio kitengo nyeti kabisa cha usalama katika nchi yako muheshimiwa. Hilo ume litazamaje?”

Raisi Mtenzi akashusha pumzi na kukumbuka skendo waliyo ipata Marekeni miaka kadhaa, wakishutumiwa na mmoja wa wafanyakazi wake aliye toa siri kwamba Wamarekeni wana iba baadhi ya siri za mataifa mengine pasipo mataifa hayo makubwa kufahamu.

“Hilo jambo ni kweli, sasa tuna fanya nini?”

“Mkuu unge tupa mwenzi mmoja. Nina waamini sana vijana wangu, tuta rudi hewani”

“Mwenzi mmoja?”

“Ndio mwenzi mmoja tu tuta rudi hewani, ila kwa Wamarekeni kwa kweli sikushauri tufanye nao kazi tena kwenye kitengo kama hichi”

“Nimekuelewa sana Emmy, una mwenzi mmoja wewe na vijana wako kuhajikisha muna tengeneza mfumo mwengine ambao utakuwa imara na wenye nguvu na hakuna hakers hata mmoja ambaye ata weza kuuvamia”

“Sawa muheshimiwa raisi, nina shukuru sana kwa kutuelewa”

“Usiku mwema”

“Nawe pia muheshimiwa”

Raisi Mtenzi akatoka makao makuu ya ofisi hiyo na kurudi ikulu.

***

Mzee Mbogo akaitazama simu yake jinsi inavyo ita. Namba ya Mr the Brain kidogo ikamfanya kusita kuipokea kwa maana ana tambua ni lazima kwa sasa serikali ita mtafuta hiyo ni kutokana na yeye kuzima mfumo mzima wa kitengo nyeti cha usalama cha NSA.

‘Ana hitaji nini huyu?’

Mzee Mbogo aliendelea kuzungumza huku akiitazama simu yake. Taratibu akaipokea na kuiweka sikioni mwake.

“Habari Mbogo”

“Salama muheshimiwa habari yako?”

“Sio salama.”

“Kuna nini?”

“Nime fukuzwa kazi kwa ajili yako”

“Kwa ajili yangu. Kivipi?”

“Mfumo mzima wa utendaji kazi wa NSA, ume futika na hapa ninapo zungumza na wewe hakuna mawasiliano yanayo ingia kwenye kitengo hicho wala wao hawana uweze wa kutumia hata CCTV kamera za jengo lao. Nilimshauri raisi Mtenzi kukurudisha wewe katika nafasi yako kwa maana wewe ndio mtengenezaji wa ule mfumo ila alikataa na ikapelekea mimi kufukuzwa kazi”

“Pole sana Mr The brain.”

“Nimesha poa. Ila nina mashaka makubwa saa kwa ajili ya hili. Nchi kwa sasa ipo gizani, hatuwezi kuona ni nani ana tushambulia na nini kitakacho kutokea na wewe mwenyewe una weza kugundua kwamba mfumo wa satelaiti ya ikulu hauwezi kunasa kila jambo kama mfumo wa NSA”

“Sasa yeye amechukua maamuzi gani?”

“Sijajua ndugu yangu. Hapa nipo nyumbani kwangu nime jipumzisha”

“Basi wewe jipumzishe na mimi nina endelea kuchukua mapumziko yangu kwa maana sihitaji tena kujihusisha na maswala ya usalama. Litakalo tokea lolote lita kuwa ni mikononi mwa raisi”

“Ni kweli Mbogo, ila akili yangu ina ona mbali”

“Kivipi?”

“Lile shambulizi tulilo lifanya kwa Al-Shabab nina uhakika ipo siku wata lipiza kisasi, je ita kuwa ni lini, wapi na saa ngapi. Yaani nina omba Mungu hilo jambo lisitokee katika kipindi hichi ambacho NSA ipo gizani”

“Ni kweli ndugu yangu. Tumuombe Mungu katika hilo”

“Nashukuru bwana. Nikutakie usiku mwema”

“Nawe pia”

Mzee Mbogo akakata simu yake huku akiwa amejawa na mashaka kwa maana kama mr the Brain amabaye ndio alikuwa injini kubwa ya kumfanya raisi Mtenzi kuonekana raisi bora Tanzania na bara zima la Afrika, basi nchi kwa sasa ita kuwa katika wakati mgumu sana. Mzee Mbogo akatoka chumbani kwake na moja kwa moja akaeleka katika chumba cha Evans.

“Hei kijana”

Mzee Mbogo alizungumza huku akimgusa Evans aliye lala begani mwake. Taratibu Evans akafumbua macho yake na mzee Mbogo akaka kwenye sofa jengi.

“Vipi mzee kume pambazuka?”

“Bado, ila ina hitaji kuzungumza na wewe”

“Sawa”

“Nina hitaji ujiunge na kitengo cha usalama wa taifa”

“Heeee!!”

Evans ali hamaki sana.

“Ndio nina hitaji ujiunge kwenye kitengo cha NSA”

“Siwezi mzee”

“Kwa nini?”

“Maisha yangu yote nina mtumikia Mungu. Hivyo nina hitaji kuwa na Mungu wangu, nipo kwenye arakati za kufungua kanisa hivyo kuifanya hiyo kazi ita kuwa ni ngumu kwa kweli”

Mzee Mbogo akashusha pumzi huku akimtazama Evans usoni mwake.

“Hakuna kanisa kama hakuna amani. Hakuna usingizi wala kizazi bora kama hakuna amani. Hakuna kulima kama hakuna amania. Hakuna biashara sehemu ambayo haina amani. Hakuna mahusiano wala kujipiga selfie sehemu ambayo hakuna amani. Tafakari kisha uta nipa jibu, usiku mwema”

Baada ya mzee Mbogo kuzungumza maneno hayo akatoka ndani hapo na kumucha Evans akiwa ana jishangaa sana.

“Una hisi ni kwa nini wana taka uwe mwana usalama”

Sauti ya mwana dada ambaye ni jini ikamstua sana Evans akamtazama mwana dada huyo aliye simama dirishani huku akitazama enei la nje la chumba hicho.

“Sijajua”

“Usikubali kushawishika”

“Ndio siwezi kushawishika kwa maana moyo wangu ulisha jiandaa kuwa nabii”

“Sawa, jina langu nina itwa Maimuna”

“Maimuna?”

“Ndio. Usiku mwema”

Maimuna akapotea ndani hapo huku akimuacha Evans akiwa katika hali kuchanganua kauli za mzee Mbogo.

***

“Hii ni ramani ya jiji la Dar es Salaam”

Kijana mmoja aitwaye Juma alizungumza huku akiwaonyesha wezake mchoro mkubwa uliopo kwenye karatasi waliyo ibandika ukutani ndani ya chumba hicho kilichopo chini ya gorofa katika mtaa wa Wasomali, Kariakoo.

“Siku ya harusi ya mtoto wa raisi Mtenzi, tuta shambulia maeneo makuu matatu ya kibiashara. Moja ni stendi ya mabasi Ubungo. Mbili ni katika uwanja wa Taifa wa mpira, kwa maana siku hiyo kuta kuwa na mechi kubwa ambayo watu elfu stini wata kuwepo katika kiwanja hicho. Tatu tuta shambulia katika kanisa ambalo ndipo harusi itakapo fanyika”

Juma alizungumza akiwa ndio kiongozi wa vijana hao kutoka katika kundi la Al-Shabab.

“Mashambulizi haya yote yata kuwa ni ya kujitoa muhanga.”

Vijana hao wakatazamana, huku kila mmoja akiwa hatambui ni nani ata jitoa muhanga”

“Tuna paswa kufanya shambulizi litakalo andika historia katika nchi ya Tanzania. Tume elewana?”

“Ndio”

“Haya tuendelee na kazi”

Vijana hao wakaendelea na kazi ya kuunda mabomu pamoja na kuzifunga silaha ambazo waliingia nazo Tanzania zikwa zime funguliwa vipande vipande.

***

Magreth akafika nyumbani kwake akiwa amechoka sana. Akamkuta Josephine akiwa amejilaza sebleni. Akamuamsha naa kaondoka sebleni hapo na kuelekea chumbani kwake. Magreth akaitazama video hiyo kw amara nyingine jinsi Evans akiingia ndai ya gari na kushambuliwa na watu hao. Akaingia chumbani ni na kuchukua laptop yake. Akakuta ujumbe mfupi wa barua pepe, akaufungua na kukuta maelezo yaliyo mfanya kujawa na tabasamu pana sana usoni mwake. Kutumwa kwa nguo zake hizo ambazo aliagiza zishonwe katika kiwanda hicho, kuka zidi kumuongeza morali wa kuhakikisha ana lipiza kisasi kwa nabii Sanga. Magreth usiku kucha akautumia katika kuperuzi kwenye baadhi ya tovuti zinazo fundisha namna ambayo una weza kuiba(hack) mawasiliano ya mtu mwengine kwenye simu yake pasipo ya yeye mwenyewe kufahamu. Asubuhi na mapema akaingia bafuni, akaoga haraka haraka. Akajiandaa, akamuaga Josephine na kuelekea nyumbani kwa Levina. Akafika katika nyumba hiyo, akafunguliwa geti na mwana dada huyo.

“Nina shukuru kwa kuja kwako”

“Asante”

Walizungumza huku wakipena mikono. Wakaingia ndani na kumkuta Tomas akiwa ameketi sebleni.

“Karibu sana Magreth”

“Nina shukuru. Nina omba munieleze mpango wenu kwa maana kidogo muda wangu ni mdogo sana.”

Tomas na Levina wakatazamana kwa sekunde kadhaa.

“Tuna imai kwamba wewe una muhitaji Evans wako si ndio?”

“Ndio”

“Ila una adui mpya ambaye ameongezeka katika kuisaka roho ya Evans wako”

Levina alizungumza huku akimtazama Magreth machoni mwake.

“Ni nani huyo”

Levina akwasha tv na ikaonekana sura ya raisi Mtenzi.

“Nina imani una mfahamu?”

“Ndio nina mfahamu. Raisi ana husikaje na kumteka mume wangu”

Levina akajibu kauli hiyo ya Magreth kwa kuweka mazungumzo ya raisi Mtenzi pamoja na Jery waliyo kuwa wana zungumza ndani ya ofisi yao. Mazungumzo hayo ya raisi Jery anayo mfokea mwanaye kwa kushindwa kumuua Evans yaka mstua sana Magreth. Hadi yanafikia mwisho, Magreth alihisi kama moyo wake una taka kupasuka kwa hasira

“Hili swala kwa sasa lime kaa kifamilia zaidi. Jery ndio mtu ambaye aliweza kuwatuma vijana wake katika kumuua Evans mkoani Morogoro. Sijajua kama una lifahamu hilo?”

“Ndio nina lifahamu”

“Ulifahamu kama Jery ndio mtu aliye husika nyuma ya lile tukio?”

“Hapana nilifahamu kwamba Evans ame tekwa na nilijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu katika kumzuia mume wangu asitekwe ila nikashindwa kabisa.”

“Uli mzuia kivipi?”

Magreth akaka kimya huku akiwatazama Tomas na Levina kwa maana hadi sasa hivi haja waeleza kwamba yeye ana mpango gani katika ishu nzima ambayo wana iongelea hapo.

“Magreth ulijuaje?”

Levina aliuliza kwa msisitizo huku akimtazama Magreth ambaye bado ana jishauri katika kuwaamini wawili hao ambao bado hajatambua kama ni watu wema kwake au laa.



“Nina rafiki yangu ambaye ana uwezo wa kuonyeshwa ni wapi mtu alipo”

“Ana uwezo wa kuonyeshwa sehemu mtu alipo……!!?”

Tomas aliuliza huku akiwa amejwa na amshangao mkubwa sana.

“Ndio, ni kipawa kutoka kwa Mungu”

“Mmmm hiyo nia isikia leo”

Tomas alizungumza huku akitabasamu.

“Hao watu wapo usishange mume wangu. Huyo rafiki yako ana itwa nani?”

“Jamani sipo kituo cha polisi na kuanza kuhojiana maswali. So nyinyi muna mpango gani katika kumpata nabii Sanga”

“Jana usiku nilijaribu kuwahi darajani kwa ajili ya kumnyaka nabii Sanga ila kwa bahati mbaya sikuweza kumkuta kwa maana tayari Evans alisha chukuliwa”

“Kwa hiyo muna weza kunyaka mawasiliano yake yote yanayo ingia kwenye simu yake?”

“Ndio, kila anacho zungumza au kuingia kwenye simu basi sisi tuna kipata”

“Hivi muna fahamu hatari ya hilo jambo au muna fanya tu?”

“Ndio nina jua ila kwa ujuzi wangu hakuna ambaye ana weza kufahamu kama tume hack simu yake”

“Ujuzi wako ni mdogo Levina. Nyote hapa muna danganyana kwa maana niliweza kumjua Tomas kwamba ana sura bandia kutokana tu na jinsi alivyo itengeneza. Kufikiria za kuhack mawasiliano ya mtu, ina weza kuwapaleka kwenye mtego ambao hamto utegemea. Tazama kuna mambo mengi sana ambayo muna paswa kuyafahamu kabla ya kumkabili adui yake. Moja ina bidi umjue kwa undani sana na si kumjua kwa nje kama jinsi nyinyi munavyo mtazama nabii Sanga”

Maneno ya Magreth yakawafanya Levina na Tomas kukaa midomo wazi.

“Nikiaza kwa Tomas, ulikuwa kariu sana na nabii Sanga, ila kosa kubwa ulilo lifanya ni kutembea na mke wake na mukapanga kumteka kwa pamoja. Mulitumia mbinu za kitoto hadi polisi wakakukamata kirahisi sana.”

Kauli hiyo ikamstua sana Levina kwa maana hatambui kabisa juu ya swala hilo.

“Ulihisi ukimteka nabii Sanga muta zuia mafanikio yangu si ndio?”

“Magreth hilo sio tulilo kuitia hapa”

Tomas alizungumza huku akianza kupandwa na hasira.

“Acha azungumze. Magreth zungumza nahitaji kufahamu ukweli?”

“Kwani hukuweza kutambua mambo aliyo yafanya mume wako?”

“Magreth acha kunichonganisha mimi na mke wangu, sawa. Kama ume tumwa toka nyumbani kwangu”

“Hapa sio kwangu ni kwangu. Magreth zungumza kila kitu”

Levina alizungumza kwa kujiamini na hasira sana. Magreth akatoa simu yake mfukoni, akaipa

kua video ya mrs Sanga na Tomas wakifanya mapenzi ofisini kwa nabii Sanga, kutoka kwenye google drive alipo ihifadhi.

“Angalia”

Magreth alizungumza huku akimkabidhi Levina simu hiyo. Levina macho yakamtoka, akasimama kwa jazba huku akimtazama Tomas.

“What’s fuc**”

Levina alitukana huku akimuonyesha Tomas video hiyo. Tomas nguvu zikamuishia kabisa, akajuta ni kwa nini aliamua kumuingiza Magreth kwenye mpango wake.

“Nijibu swali langu malaya wewe”

Levina alizungumza kwa kufoka huku akijawa na maumivu makubwa.

“Nina poteza muda wangu nina taka kujiingiza kwenye mambo mabaya kwa ajili ya wewe. Kumbe umetembea na yule malaya mzeee. Eheee?”

Levina alizungumza kwa uchungu sana.

“Ilikuwa ni azamani”

“Zamani what…….!! You fuc** this bi** now unaniambia ni zamani”

Levina alizidi kufoka huku akiwa amesimama mbele ya Tomas aliye ishiwa nguvu.

“Naomba nikuonyeshe kitu kingine”

“Nionyeshe nionyeshe”

Levina alizunumza huku akihema kwa hasira sana. Magreth aka ipakua video inayo muonyesha Frank akiingiliwa kinyume na maumbilie na nabii Sanga.

“Hii ndio sababu ya mume wako kuhitaji kulipiza kisasi kwa nabii Sanga”

Levina akahisi nguvu za miguu zikumuishia. Taratibu akakaa kwenye sofa huku akiitazama video hiyo.

“This big dic** ime zama in your as**!!”

Levina alizungumza kwa sauti ya upole hukua akimuonyesha Frank video hiyo.

“Una hitaji mimi kupambana na upuuzi wako kama huu. Ohoo Mungu wangu sijukua Tomas wewe ni mwaanaume wa aina hiyo. Sikujua kama una niingiza kwenye matatizo makubwa ambayo baadae ninge jutia sana.”


ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

BLOG