Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MY LIFE SEHEMU YA 8/10

 

 


 MY LIFE

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 8 KATI YA 10

 


“Jojo?”

“Ehee?”

Wifi akanifungulia geti dogo, akachungulia nje na alipo ona nimekuja na gari, kwa haraka akaanza kufungua geti kubwa, nikarudi kwenye gari na taratibu nikaliigiza ndani kisha akafunga geti. Wifi akanikumbatia kwa nguvu huku machozi yakimlenga lenga.

“Poleni sana”

“Asante wifi”

“Shikamoo wifi”

“Marahab, heee masikini usoni umefanyaje jamani?”

Wifi alizungumza huku akimsogelea Judy na kuanza kumtazama usoni mwake.

“Njooni ndani”

Wifi alizungumza huku tukiingia ndani, tukawakuta walinzi wale wa wili wa mama mkwe wakiwa wamekaa sebleni.

“Wifi mumekuja saa ngapi huku?”

“Huku tumefika kama saa tisa usiku hivi”

“Habari zenu”

“Salama vipi dogo?”

“Safi”

Wifi akamchukua Judy na kuelekea naye chumbani na mimi nikabaki hapa sebleni na hawa walinzi wawili wa mama.

“Jamani mama amekamatwa, si munalifahamu hilo?”

Walinzi hawa wakatazamana kisha wakatingisha vichwa vyao wakimaanisha kwamba hawafahamu kukamatwa kwa mama.

“Jojo njoo”

Wifi aliniita, nikanyanyuka na kumfwata. Tukaini tukaingia chumbani na kuwakuta watoto wakiwa kitandani huku Judy akiwa amekaa pembeni.

“Najaribu kumpigia mama simu, hapatikani?”

Nikaa kimya kwa muda huku nikimtazama wifi usoni mwake, taratibu nikakaa kitandani.

“Mama alikamatwa na askari”

“Alikamatwa na askari kwa nini?”

“Tulipo kuwa tunakwenda kumtafuta Judy, kuna mzee mmoja ni muuza madawa ya kulevya, sasa kuna mambo aliyafanya ikapelekea mama mkwe kusimamishwa kazi na raisi na ninahisi kuna amri ambayo imetolewa na raisi ya yeye kukamatwa”

Wifi akashusha pumzi nyingi, taratibu na yeye akaka kitandani.

“Alafu pale nyumbani tulikuta polisi wakikagua kagua nyumba, waliwakuta?”

“Hapana, sisi waliopo fika Jackson na John, wakaniambia kwamba mama amesema tunatakiwa kuondoka eneo hili na tukaja huku Tanga na sikujua kama kuna polisi wamekuja mule ndani?”

“Judy kuna kitu chochote cha ushahidi ambacho unahisi kinaweza kumuingiza mtu yoyote kwenye hati?”

“Kama nini sasa dada?”

“Chochote tu?”

“Kwa upande wangu hakuna kitu”

“Wifi je?”

Wifi akaka kimya kisha akatingisha kichwa akimaanisha kwamba hakuna.

“Inabidi tuweze kumuokoa mama mkwe kutoka mikononi mwa serikali”

“Judy waangalie hao, Jojo njoo”

Tukatoka chumbani humu na wifi, kisha tukaingia katika chumba kingine ambacho kinatumika kama kamtaba ya kujisomea vitabu.

“Ehee hembu nieleze ni kitu gani ambacho kimemkuta mama yangu?”

Wifi alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.

“Tulipokuwa hotelini, sehemu ambayo Judy alihifadhiwa, mama mkwe aliniomba niweze kuondoka na Judy na akaniambia kwamba atakamatwa na polisi kwa hiyo sio vizuri tukaendelea kuwa pale”

“Sasa imekuwaje raisi akamtengua kwenye nafasi aliyo kuwa amemteu?”

“Ni huyo jamaa anaye itwa Kibopa, yeye ndio chanzo wa mambo yote hayo. Kwa hiyo mama alitenguliwa kwenye nafasi yake, ila alimuahidi raisi kwamba ana ushahidi wa mambo yake mauovu aliyo yafanya ambayo anaweza kwenda kumshitaki ICC”

“Alikueleza ni wapi ulipo huo ushahidi?”

Nikakaa kimya, nikakumbuka maneno ya mama mkwe kwamba mwanaye huyu pia ni mpelelezi ila si wa serikali hii ya Tanzania, ni kutoka Marekani.

“Ndio”

“Ni wapi?”

“Humu humu ndani”

“Sehemu gani?”

“Twende”

Tukatoka chumbani humu, tukakutana na mlinzi mmoja wa mama kwenye kordo.

“Love tunafanyaje kuhusiana na mama”

“Naomba munisubirie nitawaambia ni nini cha kufanya”

“Sawa”

Tukaingia chumbani kwa mama mkwe, tukasaidia kuvuta kitanda hichi kizoto kiasi ila tukakimudu. Sehemu ya chini ya kitanda haionyeshi kama kuna mlango wowote ambao unaweza kuingia chini ya ardhi.

“Mbona hakuna kitu?”

Nilimuuliza wifi huku nikimtazama usoni mwake. Wifi akaanza kukayanga kugonga gonga eneo hili la chini ya kitanda kwa kutumia kidogino cha mguu wake wa kulia.

“Hapa”

Alizungumza huku akioninyesha eneo hili ambalo hakuna sehemu yoyote ya kufungulia.

“Tutaingiaje?”

Wifi akasimama humu chumbani na kuanza kuangalia kisa sehemu ya chumba hichi. Akaifwata picha ya familia waliyo piga wao watatu kipindi walipo kuwa watoto wadogo huku mama naye akiwa pembeni yao. Akaitoa ukutani ila hatukuona kitu chochote. Akaifwata saa ya ukutani nayo akaitoa ila napo hakuna kitu chochote ambacho kipo nyuma ya saa hiyo.

“Mama ameficha wapi naye khaaa?”

Wifi alizungumza huku jasho jingi likimwagika usoni mwake kwa kuchoka.

“Nisaidie kutafuta”

“Sawa”

Tukaanza kujaribu kila kitu ili tuweze kuona japo batani za siri ambazo zinaweza kutusaidia kufungua katika eneo hilo ila tukashindwa kuona kabisa batani hizo.

“Anti, Anti”

Tuliisikia sauti ya Gody mtoto wa kwanza wa shemeji yangu akiita, akaingia ndani humu na akashikwa na bumbuwazi mara baada ya kukuta vitu vimevurugika kabisa.

“Munatafuta nini ndani kwa bibi yangu?”

Gody aliuliza huku akiweka begi lake madaftari chini kwani nahisi ndio ametoka shule wakati huu.

“Na wewe acha maswali ya kipuuzi bwana”

Wifi alizungumza kwa ukali sana hadi Gody akaogopa kidogo, ila nikamfwata Gody huku nikiwa nimetabasamu

“Shikamoo ma mdogo”

Gody alinisalimia kwa unyonge mkubwa sana.

“Marahaba, eti Gody unajua jinsi ya kufungua pale chini?”

“Unamuuliza, hawezi kujua huyo”

Wifi alizungumza.

“Najua, kwanza rudisheni kila kitu sehemu yake mulipo kitoa”

Gody alizungumza kwa kujiamini, tukatazamana na wifi kisha tukatazama jinsi tulivyo changua changua vitu humu ndani nikajikuta nikijihisi kufa kufa kutokana na kuchoka sana.



“Gody kama unatudanganya nitakubamiza mabao hadi ujikojolee”

Wifi alizungumza kwa ukali, ila Gody hakuonekana kuwa na wasiwasi wa aina yoyote.

“Wifi turudishe tu”

Nilijikuta nikizungumza kwa unyonge huku nikianza kunyanyua kitu kimoja baada ya kingine na kupanga chumba hichi taratibu. Ikatuchukua zaidi ya lisaa moja kurudisha kili kitu tulipo kuwa tumekitoa. Hadi tunamaliza viongo vyangu vyote vya mwili ninahisi kama vinavunjika.

“Kwani mulikuwa munatafuta nini?”

Swali la Gody likamfanya wifi kumfwata kwa harisa na kutaka kumpiga kofi, ila nikawahi kumdaka mkono wake.

“Hivi unajua huyu mtoto ni chini?”

Wifi alizungumza kwa ukali kiasi cha hadi Gody akaanza kulengwa lengwa na machozi.

“Hapana wifi, hutakiwi kumkasirikia mtoto kiasi hicho, mbona swali lake linaeleweka”

“Nilijua huyu mtoto ana mawenge sana”

“Hapana bwana. Eti Gody kuna sehemu yoyote chini ya ardhi?”

Gody akaanza kujipangusa machozi na kukisogelea kitanda, akainama chini na kuingiza mkono wa kulia chini ya kitanda cha mama mkwe. Taratibu tukashangaa kuona kitanda kikigawanyika katikati huku ardhi ya eneo la chini ya kitanda hicho nayo ikifunguka. Nikamtazama wifi ambaye mikunjo ya hasira iliyo kuwa imetawala usoni mwake ikaanza kutoweka.

“Ukisogeza kitu kikmoja tu kwenye hichi chumba, bibi aliniambia kwamba huwezi kufungua na kuingia humo ndani”

Gody alizungumza, japo ni mdogo ila ana uelewa mkubwa, kusema kweli laiti ingekuwa si huyu mtoto tungetafuta sehemu ya kufungulia hadi tungegairi.

“Njooni”

Gody alizungumza huku akianza kushuka ngazi za kueeka eneo la chini ya sehemu ambayo mama mkwe anahifadhi vitu vyake vya siri. Baada ya kumaliza kushuka ngazi hizi tukakutana na mlango ambao pembeni yake kuna batani. Gody akaminya baadhi ya batani kisha mlango huo ukafunguka. Akatangulia kuigia na kuwashasha taa. Wifi akataka kutangulia ila akamzuia.

“Ngoja utakufa”

Gody alizungumza na kumfanya wifi kutulia kwa muda huku akimtazama usoni mwake. Akachomoa miwani tatu zilizopo nyuma ya huu mlango na kutukabidhi kila mtu yake na yeye akafaa. Tukaanza mishale mingi myekundu ikiwa imekatiza katika katika ardhi ya hichi chumba.

“Hiyo mionzi ni ya umeme, bibi ameniambia kwamba ukikanyaga tu hapo inakukata”

“Sasa tunaitoaje hii mionzi”

Gody akaka kimya huku akitazama chini, akatugeukia.

“Sasa hapa bibi mwenyewe alikuwa sijui anafanyaje, ngoja”

Gody akatoka chumbani na kutuacha sisi humu ndani pake yetu.

“Yaani huyu mwanamke kweli mafia, unajua siku zote za kukaa hapa kwake sijawahi kugundua kama kuna eneo la siri lililopo chini ya ardhi?”

“Weee”

“Haki ya Mungu, yaani leo ndio naona haya mambo na hichi chumba nacho ndio ninakiona”

“Inaonyesha mama ni msiri sana?”

“Sana, tena sana. Kwa maana sisi wanae hajatuambia, anaye jua ni mjukuu, ambaye wala sio rahisi kudhania kwamba ana weza kufahamu hili jambo”

“Sipati picha kama Gody asinge kuja”

“Yaani, tena nilifanya kumpigia simu mwalimu wao amruhusu leo kuja nyumbani kwa maana tumemuamishia shule ya bwani”

“Ahaa”

Gody akarudi akiwa ameshika kioo kisogo. Taratibu akainama huku akiwa amevaa miwani ambayo inatuwezesha kuona mionzi hii mikali, ambayo kwa macho ya kawaida haionekani. Akakiweka taratibu kioo hicho katikata ya sehemu ambayo mionzi hiyo imekutania kwa pamoja na kuisababisha yote kuzima.

“Hapa nikiondoa tu hichi kioo mionzi yote inarudi kwenye eneo lake”

“Sasa utaendelea kukishika hivyo hivyo?”

“Hapana”

Taratibu Gody akakisimamisha kioo hichi, kisha akakiachia jambo lililo nifanya niongope sana.

“Sasa munwaweza kuchukua munacho kihitaji”

Tukaanza kutazama makabati haya yaluyomo ndani ya chumba hichi.

“Angalizo, mukidondosha kitu chochote kwenye sakafu, kuna miyonzi ya dharura itawaka sasa kuweni makini”

“Mmmmm, hembu tuonyeshe ni wapi bibi yako alipo weka nyaraka muhimiu ambazo ni za siri”

“Kabati lile pale, namba zake za siri nalo ni moja, kumi, kumi kisha sita”

Wifi akaeleka katika kabati hilo, akaiminya batani zilizopo pembeni ya kabati hilo na likafunguka. Tukaona mafaili mengi sana.

“Jojo tunatazama faili la nani?”

“La raisi”

“Litakuwa eneo gani hapa?”

Nikasogea eneo hilo na tukaanza kutoa faili moja baada ya jengine.

“Munaweza kuvua tu hizo miwani”

“Mmmmm ya nini kupigwa mionzi”

Wifi alizungumza huku akirudisha faili ambalo sio la mtu muhusika. Katika faili langu la sika katika kukagua, nikafanikiwa kulipata faili la muheshimiwa raisi.

“Hili hapa”

Nilizungumza huku nikiwa nimelifungua vizuri.

“Gody haya makabati mengine yana nini?”

“Lipi?”

“Lile pale?”

“Lile pale lina vipande vya gold vile vikubwa kubwa”

“Hembu lifungue”

Wifi alimshawishi Gody ambaye hakusita kulifungua kabati hilo. Macho yakatutoka kwani kabati hili kubwa na refu, limejaa vipande vya Gody.

“Hivi bibi amesema ni vya kwangu, nikiwa mkubwa, haya kama atakuwa hayupo basi nitatumia hivi katika kujiendeleza kumaisha”

“Mmmmm”

Wifi aliguna huku akiendelea kutaza vipande hivi, akajaribu kunyanyua kimoja.

“Aisee ni vizito”

Wifi alizungumza huku akinikabidhi kipande hicho, kusema kweli ni kipande kizito.

“Kila kipande ameniambia kwamba kina thamani ya dola laki moja na nusu”

“Huyu mwamamke kazitolea wapi hizi mali?”

Gody akanyanyua mabega yake akimaanisha kwamba hajui chochote.

“Na lile jengine pale?”

“Lipi?”

“Huoni au?”

Gody akafunga kabati hili na kuisogelea kabati jengine, akaingiza namba za siri ana kufungua. Nikashusha pumzi taratibu kwani kabati hili lina pesa aina za dola za kimarekani zikiwa zimefungwa fungwa kwenye vibunda na kupangiliwa vizuri.

“Hizi pesa bibi amesema ni za ba mdogo”

“Za baba yako mdogo zote hizi?”

“Ndio”

“Wewe na bibi yako naona muna utani?”

“Haya ya Mungu vile anti, amesema hizi pesa ni za ba mdogo. Hapa kila mtu ana kabati lake, wewe ni lile pale”

“Kafungue”

Wifi ameanzisha kazi nyingine ambayo haituhusu, ila kutokana ndio mkubwa wetu ndani ya hichi chumba, hatuna budi kuwa wapole. Gody akaingiza namba za siri, wifi kwa haraka akafungua kabati hili na tukakuta halina kitu chochote, jambo lililo mfanya kumtazama Gody kwa macho makali sana.

“Mbona halina kitu?”

“Hujatazama huku chini?”

Gody aliinama na kutoa bahasha, wifi kwa haraka haraka akaanza kuifungua, akatoa karatasi zilizomo ndani ya bahasha hizo. Taratibu akaanza kuzisoma na kujikuta akishusha pumzi taratibu huku akiwa amejawa na tabasamu na sijui ameandikiwa kitu gani.

“Muna bahati”

“Bahati gani wifi?”

“Hii ni power of attorney, mimi ndio msimamizi wa kila kitu cha mama”

“Ahaaa”

Wifi akarudisha karatasi hizo ndani ya bahasha, kisha akamkabidhi Gody, naye akairudisha bahasha hiyo katika sehemu aliyo itoa.

“Baba yako naye kabati lake ni lipi?”

“Lile pale”

“Hembu fungua”

“Wifi tukumbuke kilicho tuleta humu”

“Alfu kweli, tutoke mwanya tusije tukapigwa mashoti ya miguu bure”

Wifi alizungumza na tukatoka chumbani humu, Gody akachukua kioo chake na kufunga mlango. Tukarudi chumbani kwa mama na Gody akakirudisha kitanda hicho sehemu alipo kitoa.

“Shule umekunywa chai?”

“Hapana”

“Nenda kule jikono nimesha pika chai na kuna miogo ya kukaanga kwenye pot”

“Sawa”

Gody akatoka chumbani humu na tukaanza kukagua faili hili ambalo kila tulicho kisoma tukabaki midomo ikiwa wazi, picha za mauaji na ajali kubwa zilizo wahi kutokea miaka ya nyuma tukuamini ni ajali tu kumbe ni mipango ya raisi.

“Mungu wangu, sasa wifi huu ushahidi tunaweza kuupeleka wapi?”

“Najua ni wapi kwa kuupeleka ila kabla ya kuupeleka sehemu yoyote ninahitaji kuwasiliana na raisi kwanza”

“Namba yake unayo?”

“Ndio”

“Jaribu kumpigia”

Wifi akaoka chumbani huku, kisha baada ya dakika kadhaa akaja akiwa na simu kubwa yenye mkonga kidogo, simu ambazo ni za zamani sana.

“Hilo lisimu umelitoa wapi?”

“Hahaa, hizi hazipatikani”

Wifi alizungumza huku akitoa laini kwenye simu yake ndogo na kuiingiza kwenye simu hii kubwa.

“Ukitumia simu hii sauti kwanza inabadilka, kule anaweza kusikia sauti ya kiume au sati mbaya mbaya, inategemea na jinsi ambavyo nitahitaji iwe. Kingine hato weza kuona namba yako kule itamletea private namba na hata wakijaribu kuitafuta hawato weza kuiona”

“Mmmmm”

“Yaa”

“Umeitoa wapi hii simu?”

“Undercovers wengi hususani wa kimataifa huwa tunazitumia hizi simu….shiii usiongee kitu”

Wifi alizungumza huku simu hii akiwa ameiweka mbee yake.

“Raisi Edward”

“Najua hunijui, ila naamini kwamba utataka kunijua.”

“Ni nani wewe na kwa nini unampigia raisi kwa namba private?”

“Nahiyaji kufanua mabadilishano nawe la sivyo, kuna siri zako nyingi niytakwenda kuziachia kwenye mtandao”

“U…una…sema siri?”

Raisi alizungumza kwa kigugumizi. Ujasiri wote alio kuwa nao ukamuishia.

“Ndio, nahitaji bi Joyce, naamini kwamba unamfahamu. Polisi walikamaya jana usiku. Ninakupa lisaa mja hakikisha kwamba umemuachia huru”

“Kwa bahati mbaya huwa sitishiwi na vinyamkera, japo umebadilisha sauti ila nitahakikisha kwamba ninakutafuta na nitakukamata na nitakuchukulia sheri”

“Etie heee?”

“Ndio”

“Kabla ya hujakata simu, ninakwenda kuiachia habari ya njama yako ya kuilipua ndege ya Air China, na kusababisha waziri mkuu wao kufariki paamoja na watu wake wote waliokuwemo ndani ya ndege hiyo mara tu walipo toka kufanya ziara nchini Tanzania. Naamini kwamba siri hii nikiituma kwenye serikali ya nchini China, watakwenda kukushuhulikia ipasavyo”

Ukimya ukatawala ikonyesha kwamba raisi habari hii imemstua sana.

“Ukiachana na hiyo, kuna kifo cha makamu wa raisi wa Russia, naamini kwamba huyo naye unafahamu vizuri habari zake, sasa ninakwenda kutuma ushahidi kwa viongozi wa hizo nchi, utakap……”

“Ngoja goja kwanza”

“Zungumza?”

“Nitamuachia ila nitahitaji uniletee ushahidi huo wote ili niweze kumuachia mtu wako unaye muhitaji?”

“Hahaa, unahisi kwamba mimi ni mjinga sana au?”

“Sio mjinga, ila fanya hivyo utampata mtu wako unaye muhitaji”

“Nitakupigia usiku na kukuambia ni wapi, tuonane na hakikisha kwamba unakuja na mtu wangu na muwe nyinyi wawili tu na ukishindwa basi nitahakikisha kwamba nina kuangamiza”

“Nimekuelewa”

Wifi akakata simu kisha akakashusha pumzi taratibu.

“Usiku huo utakwenda?”

Nilimuuliza wifi kwa sauti ya upole huku nikimtazama usoni mwake.

“Yaani hapa hata sifahamu itakuwaje kwa maana nimezungumza kitu ambacho sidhani kama peke yangu ninaweza kukikamilisha”

“Twende wote?”

“Kwenye hili sihitaji uhusike kabisa, kwa sababu utaongeza matatizo mengi zaidi , uliyo nayo sasa hivi yanakutosha.”

Wifi alizungumza kwa msisitizo huku akifunika faili hili, akatoka chumbani humu na kuniacha nikiwa na mawazo mengi sana, kwa maana mama mkwe aliniambia kwamba mimi ndio tegemezi lake la pekee kwenye hili swala la kumkomboa yeye endao tu akiwa amekamatwa mikononi mwa askari.


Nikatoka chumbani humu kwa mama mkwe haraka haraka na kuingia katika chumba cha wifi, nikawakuta akiwa na Judy ambaye tayari amesha oga mwili wake na kujifunga tenge.

“Wifi naomba tuzungumze”

Wifi akanitazama kwa muda kisha tukatoka nje.

“Vipi tena?”

“Wifi hili jambo unalo liendea kulifanya sio salama, ni hatari sana. Mama mkwe aliniomba niweze kufanya hili swala katika hali ya usalama na si kama hali unayo ifikiria wewe wifi”

“Jojo bado hujawajua watu. Watu sio wa kuwaamini na kumbuka kwamba mtu ambaye tunashuhulika naye hapa, ameshikilai kila kitu katika hii nchi, so unahisi kwamba hata ukipeleka huu ushahidi mahakamani, kuna jaji gani ambaye atasimama kifua mbele na kumfungulia mastaka raisi?”

Wifi alizungumza kwa msisitozo na kunifanya nishushe pumzi taratibu.

“Hii ni vita, vita ambayo itaamuliwa na maisha, nani afe nani abaki ili awe mshindi. Umri wako bado ni mdogo sana. Mdogo wangu Eddy anakupenda tena anakupenda sana, munatakiwa kukaa na kumuangalia mtoto wenu anakua vipi, acha kujihusisha kwenye mambo haya utakufa ukiwa bado mdogo sana. Umenielewa Jojo?”

“Nimekuelewa wifi, ila kumbuka hata wewe una mtoto, kumbuka pia una mume wako. Anakupenda na kukihitaji kwenye maisha yako so unataka kufa na kumuacha akiwa peke yake na mwanaye, je unataka kufa ili mwanao alelelewe na mwanamke mwengine ambaye ataolewa na mume wako?”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenga usoni mwangu. Wifi akashusha pumzi kidogo kisha akajishika paji lake la uso kwa kutumia kiganja cha mkono wa kushoto.

“Jojo”

“Beee”

“Kuna mambo mengi ambayo hujajui juu ya maswala mazima ya visasi”

“Wifi natambua, nimesha wahi kuua watu kwa kutumia mikono yangu mi mwe……..”

Mlio wa kikombe cha dongo kupasuka ukatushuta sote na kujikuta tukitazama eneo ambalo tumesikia mlio huo. Tukamkuta Gody akitutazama huku mwili ukimtetemeka, nikapiga hatua moja ya kumfwata ila akapiga hatua mbili nyuma za kuonyesha kwamba tayari amesha anza kuniogopa.

“Gody mwanangu sijazu……”

Gody akakimbia na kutoka nje kabisa, nikaanza kumkimbiza cha kumshukuru Mungu nikamkuta getikia akihangaika na kufungua geti, nikamkumbatia ila kaanza kujitoa mikononi mwangu.

“Niache, niache. Wewe ni muuaji, umeua watu”

Gody alizungumza huku akilia kwa hasira. Ni mtoto mdogo ila ni muelewa, naamini malezi aliyo lelewa yanadhihirisha kwamba jambo kuua kwake ni jambo la hatari na la kutisha sana.

“Hapana Gody, nilikuwa ninamsimulia wifi kwamba nimeota nimeua watu”

“Umeota wapi?”

“Usingizini, hembu niangali mwangu kweli ma mdogo wako mi naweza kuua. Hata kuku siwezi kumuua”

Gody akanitazama machoni kwa muda kisha akatingisha kichwa cha kukataa.

“Macho yako hayamaanishi kile unacho kizungumza”

Nikajikuta nikipigwa na bumbuazi kubwa.

“Bibi ameniambia mtu muongo ukimtazama machoni unamjua. Wewe unanidanganya”

“Wewe hembu toa upuuzi wako na huyo bibi yako. Nenda kafute chai yako pale ulipo mwaga tena ole wako ukate na vipande vya hicho kikombe nitakubamiza na hospitalini hote kwenda”

Wifi aliungumza kwa hasira na kumfanya Gody kujitoa mikononi mwangu taratibu na kuanza kutembea kwa unyonge sana kuelekea ndani.

“Wifi ila jambo la kumfokea mtoto sio vizuri”

“Humjui huyu, atakusumbua akili na sisi wenyewe hapa akili zetu zimesha choka”

“Mmmm”

“Ndio hivyo. Sasa na ninapitisha mamuzi yangu kwako. Sitaki ujiingize kwenye hili swala. Nitalimaliza mimi mwenyewe”

“Wifi”

“Nimemaliza, nenda ndani na wewe. Vua nguo zako, oga na ulale”

Wifi mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akatoka nje ya geti kabisa. Taratibu kwa unyonge kama alivyo ondoka Gody ndivyo jinsi nami nilivyo anza kutembea kuingia ndani.

“Hei dogo, kuna habari hizi sijui unazifahamu”

Mlinzi mmoja wa mama alizungumza huku akinikabidhi simu yake. Nikasoma habari hii iliyo wekwa kwenye mtandao mmoja wa habari katika internet unao someka. ‘MAUAJI MAKUBWA YATOKEA DAR, WATU TISA WAUWAWA, MMOJA HAJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI NA MKURUGENI DK CKALA ANYONGWA AKIWA OFISI KWAKE NA KILA ALIYE UWAWA AMEKUTWA NA ALAMA YA Z’

Nikahisi utumbo ukinyongorota tumboni mwangu, miguu ikapteza muhimili wake hadi nikajikuta nikikaa kwenye sofa pasipo kupenda. Picha na akili yangu vyote vikarudi kwa mwanaume ambaye ametusaidia mimi na Judy. Mwanaume aliye ificha sura yake kabisa na kutohitaji kuonekana kabisa.

“Ni nani yule”

Nilijikuta nikizungumza huku nikitazama picha ya dokta Clara ambayo shingoni mwake amevisha herufi hiyo Z inayo fana kabisa na herufi ambayo nimepewa.

“Unamfahamu?”

Sauti ya mlimzi mmoja ikanistua sana hadi nikamtolea macho ya mshangao.

“Umamfahamu?”

Nikatamani kumjibu kwamba nina mfahamu ila nikashindwa kabisa kufungua kinywa changu, nikasimama kwenye sofa na nikaanza kujikaza kutembea hadi nikaingia chumbani alipo Judy.

“Judy ona, ona”

Nilizungumza huku nikimkabidhi Judy simu hii niliyo pewa kuangalia taarifa hii. Judy akaitazama kidogo na nikamuona akiuziba mdomo wake kwa mshangao huku macho yametoka..

“Huyu aliye ua si ndio yule aliye kupa ile herufi?”

“Ndio yeye?”

“Sasa ni nani jamani?”

“Hata mimi sifahamu Judy na sijui kwa nini amemuua Clara?”

“Amemuaa kwa sababu na yeye si aliyaka kukuua. Yaani Clara na hawa watu wake wamepata kile walicho kistahii kukipata”

“Ila nitatamani kumfahamu huyo mtu”

“Utamfahamu vipi sasa ikiwa mtu mwenyewe huna namba yake ya simu, huna chochote chake zaidi ya hiyo herefi”

“Hembu isome hiyo taarifa?”

“Wanasema kwamba jeshi la polisi wataendelea kufanya uchunguzi ili kumbaidi muuaji”

Yule mtu anavyo onyesha ni professional killer na si mtu wa kawaida kabisa”

“Mimi alivyo kuwa anau sikumuona niliinama chini nikijisalia zangu. Ila tuache utani Jojo, haya maisha mimi nimesha yachoka. Yaani nahitaji amani, kama ni mali dada yangu kama kuna mtu ulimdhulumu chake, hembu tafadhali hakikisha kwamba unamrudishia mali zake bwana ni bora tukarudi kule uswahilini kuliko tuna magari, tuna pesa tuna nyumba, ila mwishowe tunajikuta tunaishi kama mwemwe”

“Acha ujinga hujui nilivyo hangaika kutafuta. Tafuta zako uone jinsi ugumu wa kurudisha hizo mali jinsi ulivyo”

Nilizungumza kwa hasira na kumpokonya Judy simu ya watu na kurudi sebleni na kuwakuta walinzi hawa wa mama wakiitazama taarifa hii tuliyo toka kuisoma.

“Wamempa jina la Mr Z”

“Mr Z!!?”

Niliuliza kwa mshangao.

“Ndio, naona mkuu wa polisi amesha anza kuchachawa.”

“Ila jamani huyo mtu jana sisi ndio alite tusaidia kutoroka mikononi mwa hao watu ambao wameuwawa na suti suti zao”

“Weee”

“Ndio na aliendesha hiyo gari hapo nje hadi meneo ya ile barabara kama utatoka mkoa wa Pwani, na kuingia hivi kama unakuja huku”

“Unataka kusema jamaa mulikuwa naye kabisa ndani ya gari?”

“Ndio na nimtu ambaye ameificha sura yake kabisa. Yaani hata macho yake ukiyatazama hivi ni ngumu kuweza kuyaona”

“Mmmmm”

Nikazidi kubaki mdomo wazi mara baada ya kuona taarifa nyingine ya habari inayo husisha watu tuliwa waua katika hoteli tukiwa na mama mkwe nao wote kila mmoja amewekewa alama ya Z.

“Huyu ni mtu ambaye anatufahamu”

Nilizungumza huku nikisimama na kuanza kuisogelea hii tv kubwa iliyo hapa sebleni kana kwamba sioni kinacho onyeshwa. Video inayo onyeshwa hivi sasa ni video ambayo imerekodiwa na kamera za CCTV. Badala ya kunionyesha mimi nikiwa nina pambana na watu wa Juma, ila nimauonyesha Mr Z jinsi anayo waaua watu hao kwa kuwapiga risasi.

“Mmmmm huu ni ongo”

“Uongo gani?”

“Mimi ndio nimewaua hao watu wa hapo hoteli, inakuwaje anaonekana yeye?”

Walinzi hawa wa mama mkwe wakabaki kimya huku nao wakionekana kuwa na mshangao.

“Hembu itafute hiyo video kwenye mtanda”

“Huku bado hajarushwa”

“Jamani hapana, huyu mtu siojui ni nani na inakuwaje anaonekena yeye”

“Vipi mbona mumesimama kama vibendera vya mwenyekiti wa kishumundu?”

Wifi aliuliz ahuku akifunga mlango wa kuingilia humu ndani, huku mkononi mwake akiwa ameshika mfuko mweusi.

“Wifi kuna muuaji mpya ameingia Tanzania anaitwa Mr Z”

“Mr Z?”

“Kamuua nani hadi awe maafuru hivyo?”

Jamaa akamakbidhi wifi simu hiyo, wifi akasoma habari niliyo isoma mimi.

“Mmmm yupo vizuri, alafu Jojo huyu si meneja wako?”

“Ndio”

“Mungu wangu, huyu mtu atakugeukia wewe sasa”

“Wifi huyo jana alituasiaida kutoka mikononi mwa hao watu walio uwawa na suti zao”

“Kakusaidia?”

“Ndio na hakuishia hapa akaendesha hilo gari tulilo kuja nalo”

“Hadi hapa nyumbani?”

“Hapana alituacha katika njia ile ya kuelekea Pwaani ambayo ukipita short cut unatokea Tegeta kule”

“Mmmm, ngoja nikapike zangu sabaki mie wasije wakanichachia. Ehee, chukua simu yako”

Wifi alizungumza huku akirudisha simu ya muhusika kisha akaondoka na wala hajaonyesha kushangazwa sana na swala hili la huyu Mr Z, kitu kilicho anza kunifanya ninze kuhisi jambo kwake. Nikaondoka sebleni hapa na kumfwata jikoni na kumkuta akiwa amesha waweka samaki hao ndani ya sufuri.

“Nilikuambia ukaoge, hembu jiangalie jinsi ulivyo chafuka na unanuka jasho”

Wifi alizungumza kimasiraha japo ndio ukweli wenyewe, ia sikuujali kabisa.

“Sawa nitaenda, ila nina swali nahitaji kukuuliza?”

“Uliza”

“Unamfahamu huyu Mr Z?”

“Namjulia wapi mimi, mwenyewe ndio leo ninamuona hapo”

“Una uhakika wifi?”

“Sasa nikudanganye umekuwa Gody wewe?”

“Ila kwa nini ametusaidia sisi?”

“Sasa unakuja kuniuliza mimi ikiwa kwenye hilo tukio sikuwepo jamani, si unanionea Jojo”

“Ila wifi hujaonekana kustushwa kabisa na mtu huyu”

“Sasa nistuke amekuwa jini huyo au amekuwa kiumbe cha ajabu. Mbaya hata sura yake sijaiona”

Wifi alizungumza kawaida kabisa.

“Wifi isije akawa ni mume wangu?”

“Nani, Eddy!!?”

“Ndio”

“Hahaahaa, mumeo amekuwa kichaa, na hana uwezo wa kufanya hayo mambo”

“Ila kwa nini makosa ambayo nimeyafanya mimi ameamua kuyachukua kama ni yeye?”

“Sijui, ila kwa Eddy, tena leo analetwa hapa nyumbani, sikutaka tu kukuambia, ila analetwa”

Nikahisi mwili mzima ukinisisimka, kwani ninapokea taarifa ambayo sikutarajia kuipokea kabisa.

“Analetwa na nani?”

“Na madaktari wake, yaani unaambiwa uzombi ndio umemzidi”

Wifi alizungumza huku akitabasamu.

“Wifi jamani mume wangu sio zombie, hata kama ana hali mbaya ila sio zombie”

Nilizungumza kwa sauti iliyo jaa unyonge mwingi sana huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.

“Sasa ni mtu gani huyo anapenda kula nyama mbichi tu, tena akija humu watoto tuwaweke mbali, asije akavila bure ohoo”

“Wifi bwana usizungumze hivyo?”

Nilizungumza huku nikishundwa kabisa kuyahimili machozi yangu yanayo nimwagika usoni mwangu.

“Tatizo hupendi kuambiwa ukweli, si atakuja wewe muache ache hivyo huyo mwanenu, macho, masikio, viguu, nikono yote itauwa ni halali yake”

Kwa hasira nikatoka ndani humu na kumuacha wifi akicheka kicheko kilicho zidi kunifanya nipate uchungu mwingi, nikaingia chumbani na kumkuta Judy akiwa amembeba mwanangu, nikamtazama mtoto kwa muda kisha nikaingilia baufuni. Nikavua nguo zangu, nikafungua maji ya bomba la mvua, taratibu yakaanza kumwagika. Nongo za mwilini mwangu zikapeleka hadi maji yanayo mwagika chini yakitokea kwenye mwili wangu yakabadilika rangi. Ikanichukua nusu saa kumaliza kusafisha kila kona ya mwili wangu hadi nikajizisha kwa kutakata kabisa. Nikatoka bafuni humu na kukuta Judy akiwa amesha niandalia tenge la kuvaa. Nikalichukua na kijifunga mwilini mwangu.

“Jojo”

“Bee”

“Ile kauli yako ya mwisho uliyo niambia kusema kweli sijaipenda. Imeniumiza sana moyo wangu”

“Samahani”

Nilijibu kwa ufupi huku nikisimama kwenye kioo kikubwa cha dreasing table. Judy akaendelea kunitazama kwa macho ya masikitiko kitu kilicho nifanya nianze kujisikia vibaya kwani siku zote sipendi mdogo wangu ajihisi vibaya kwa ajili yangu. Ila kabla sijazungumza chochote, mlango wa

chumbani hichi ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia Gody huku akimwagikwa na jasho.

“Kuna nini wewe?”

Nilimuuliza kwa ukali kidogo kwa maana ameingia bila kubisha hodi na sipati picha kama angenikuta nipo uchi kabisa.

“Ba mdogo, ba mdogo ameletwa”

Sijui hata nimetokaje humu ndani, nikajikuta nimesimama kwenye mlango wa kuingilia sebleni, macho yakanitoka kwani minyororo mikubwa aliyo fungwa mume wangu kuanzia miguuni, mikononi, ikanifanya mapigo yangu yaniende mbio. Madakari wawili wenye miili mikubwa wamemshikilia kikamilifu kwani anarika ruka akionyesha anataka kutoka mikoni mwao. Kishindo kizito nyuma yangu kikanifanya nigeuke kwa haraka, nikamkuta Gody akiwa ameanguka na kupoteza fahamu kwani hali ya baba yake mdogo inatisha na kusikitisha kwani manywele mengi na ndevu nyingi zilio mjaa zimemfanya aonekane kama msukule aliye chukuliwa mika mingi sana na wachawi.

ITAENDELEA

‘Haya sasa, Jojo alikuwa akimuhisi mume wake ndio Mr Z, ila ameletwa mbele yake, hali aliyo nayo tu imemfanya Gody kuzimia, ni nini kitakacho endelea? Usikose sehemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimu kutoka kwa muandishi Genius Eddazaria G.Msulwa.

Karibu ujiunge na Group zangu za Whatsapp kupitia simu namba 0657072588. Ada ya mwezi ni sh 3000 Tu. Usikose sehemu ya 122.

MY LIFE 121


WRITER………………………………………..EDDAZARIA G.MSULWA(Genius Author)

CONTACT………………………………………0657071588(WhatsApp)/0768516188

IMEDHAMINI NA……………………………GSW(Genius Story Writers)

AGE………………………………………………..18+


ILIPOISHIA

“Usiku huo utakwenda?”

Nilimuuliza wifi kwa sauti ya upole huku nikimtazama usoni mwake.

“Yaani hapa hata sifahamu itakuwaje kwa maana nimezungumza kitu ambacho sidhani kama peke yangu ninaweza kukikamilisha”

“Twende wote?”

“Kwenye hili sihitaji uhusike kabisa, kwa sababu utaongeza matatizo mengi zaidi , uliyo nayo sasa hivi yanakutosha.”

Wifi alizungumza kwa msisitizo huku akifunika faili hili, akatoka chumbani humu na kuniacha nikiwa na mawazo mengi sana, kwa maana mama mkwe aliniambia kwamba mimi ndio tegemezi lake la pekee kwenye hili swala la kumkomboa yeye endao tu akiwa amekamatwa mikononi mwa askari.


ENDELEA

Nikatoka chumbani humu kwa mama mkwe haraka haraka na kuingia katika chumba cha wifi, nikawakuta akiwa na Judy ambaye tayari amesha oga mwili wake na kujifunga tenge.

“Wifi naomba tuzungumze”

Wifi akanitazama kwa muda kisha tukatoka nje.

“Vipi tena?”

“Wifi hili jambo unalo liendea kulifanya sio salama, ni hatari sana. Mama mkwe aliniomba niweze kufanya hili swala katika hali ya usalama na si kama hali unayo ifikiria wewe wifi”

“Jojo bado hujawajua watu. Watu sio wa kuwaamini na kumbuka kwamba mtu ambaye tunashuhulika naye hapa, ameshikilai kila kitu katika hii nchi, so unahisi kwamba hata ukipeleka huu ushahidi mahakamani, kuna jaji gani ambaye atasimama kifua mbele na kumfungulia mastaka raisi?”

Wifi alizungumza kwa msisitozo na kunifanya nishushe pumzi taratibu.

“Hii ni vita, vita ambayo itaamuliwa na maisha, nani afe nani abaki ili awe mshindi. Umri wako bado ni mdogo sana. Mdogo wangu Eddy anakupenda tena anakupenda sana, munatakiwa kukaa na kumuangalia mtoto wenu anakua vipi, acha kujihusisha kwenye mambo haya utakufa ukiwa bado mdogo sana. Umenielewa Jojo?”

“Nimekuelewa wifi, ila kumbuka hata wewe una mtoto, kumbuka pia una mume wako. Anakupenda na kukihitaji kwenye maisha yako so unataka kufa na kumuacha akiwa peke yake na mwanaye, je unataka kufa ili mwanao alelelewe na mwanamke mwengine ambaye ataolewa na mume wako?”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenga usoni mwangu. Wifi akashusha pumzi kidogo kisha akajishika paji lake la uso kwa kutumia kiganja cha mkono wa kushoto.

“Jojo”

“Beee”

“Kuna mambo mengi ambayo hujajui juu ya maswala mazima ya visasi”

“Wifi natambua, nimesha wahi kuua watu kwa kutumia mikono yangu mi mwe……..”

Mlio wa kikombe cha dongo kupasuka ukatushuta sote na kujikuta tukitazama eneo ambalo tumesikia mlio huo. Tukamkuta Gody akitutazama huku mwili ukimtetemeka, nikapiga hatua moja ya kumfwata ila akapiga hatua mbili nyuma za kuonyesha kwamba tayari amesha anza kuniogopa.

“Gody mwanangu sijazu……”

Gody akakimbia na kutoka nje kabisa, nikaanza kumkimbiza cha kumshukuru Mungu nikamkuta getikia akihangaika na kufungua geti, nikamkumbatia ila kaanza kujitoa mikononi mwangu.

“Niache, niache. Wewe ni muuaji, umeua watu”

Gody alizungumza huku akilia kwa hasira. Ni mtoto mdogo ila ni muelewa, naamini malezi aliyo lelewa yanadhihirisha kwamba jambo kuua kwake ni jambo la hatari na la kutisha sana.

“Hapana Gody, nilikuwa ninamsimulia wifi kwamba nimeota nimeua watu”

“Umeota wapi?”

“Usingizini, hembu niangali mwangu kweli ma mdogo wako mi naweza kuua. Hata kuku siwezi kumuua”

Gody akanitazama machoni kwa muda kisha akatingisha kichwa cha kukataa.

“Macho yako hayamaanishi kile unacho kizungumza”

Nikajikuta nikipigwa na bumbuazi kubwa.

“Bibi ameniambia mtu muongo ukimtazama machoni unamjua. Wewe unanidanganya”

“Wewe hembu toa upuuzi wako na huyo bibi yako. Nenda kafute chai yako pale ulipo mwaga tena ole wako ukate na vipande vya hicho kikombe nitakubamiza na hospitalini hote kwenda”

Wifi aliungumza kwa hasira na kumfanya Gody kujitoa mikononi mwangu taratibu na kuanza kutembea kwa unyonge sana kuelekea ndani.

“Wifi ila jambo la kumfokea mtoto sio vizuri”

“Humjui huyu, atakusumbua akili na sisi wenyewe hapa akili zetu zimesha choka”

“Mmmm”

“Ndio hivyo. Sasa na ninapitisha mamuzi yangu kwako. Sitaki ujiingize kwenye hili swala. Nitalimaliza mimi mwenyewe”

“Wifi”

“Nimemaliza, nenda ndani na wewe. Vua nguo zako, oga na ulale”

Wifi mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akatoka nje ya geti kabisa. Taratibu kwa unyonge kama alivyo ondoka Gody ndivyo jinsi nami nilivyo anza kutembea kuingia ndani.

“Hei dogo, kuna habari hizi sijui unazifahamu”

Mlinzi mmoja wa mama alizungumza huku akinikabidhi simu yake. Nikasoma habari hii iliyo wekwa kwenye mtandao mmoja wa habari katika internet unao someka. ‘MAUAJI MAKUBWA YATOKEA DAR, WATU TISA WAUWAWA, MMOJA HAJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI NA MKURUGENI DK CKALA ANYONGWA AKIWA OFISI KWAKE NA KILA ALIYE UWAWA AMEKUTWA NA ALAMA YA Z’

Nikahisi utumbo ukinyongorota tumboni mwangu, miguu ikapteza muhimili wake hadi nikajikuta nikikaa kwenye sofa pasipo kupenda. Picha na akili yangu vyote vikarudi kwa mwanaume ambaye ametusaidia mimi na Judy. Mwanaume aliye ificha sura yake kabisa na kutohitaji kuonekana kabisa.

“Ni nani yule”

Nilijikuta nikizungumza huku nikitazama picha ya dokta Clara ambayo shingoni mwake amevisha herufi hiyo Z inayo fana kabisa na herufi ambayo nimepewa.

“Unamfahamu?”

Sauti ya mlimzi mmoja ikanistua sana hadi nikamtolea macho ya mshangao.

“Umamfahamu?”

Nikatamani kumjibu kwamba nina mfahamu ila nikashindwa kabisa kufungua kinywa changu, nikasimama kwenye sofa na nikaanza kujikaza kutembea hadi nikaingia chumbani alipo Judy.

“Judy ona, ona”

Nilizungumza huku nikimkabidhi Judy simu hii niliyo pewa kuangalia taarifa hii. Judy akaitazama kidogo na nikamuona akiuziba mdomo wake kwa mshangao huku macho yametoka..

“Huyu aliye ua si ndio yule aliye kupa ile herufi?”

“Ndio yeye?”

“Sasa ni nani jamani?”

“Hata mimi sifahamu Judy na sijui kwa nini amemuua Clara?”

“Amemuaa kwa sababu na yeye si aliyaka kukuua. Yaani Clara na hawa watu wake wamepata kile walicho kistahii kukipata”

“Ila nitatamani kumfahamu huyo mtu”

“Utamfahamu vipi sasa ikiwa mtu mwenyewe huna namba yake ya simu, huna chochote chake zaidi ya hiyo herefi”

“Hembu isome hiyo taarifa?”

“Wanasema kwamba jeshi la polisi wataendelea kufanya uchunguzi ili kumbaidi muuaji”

Yule mtu anavyo onyesha ni professional killer na si mtu wa kawaida kabisa”

“Mimi alivyo kuwa anau sikumuona niliinama chini nikijisalia zangu. Ila tuache utani Jojo, haya maisha mimi nimesha yachoka. Yaani nahitaji amani, kama ni mali dada yangu kama kuna mtu ulimdhulumu chake, hembu tafadhali hakikisha kwamba unamrudishia mali zake bwana ni bora tukarudi kule uswahilini kuliko tuna magari, tuna pesa tuna nyumba, ila mwishowe tunajikuta tunaishi kama mwemwe”

“Acha ujinga hujui nilivyo hangaika kutafuta. Tafuta zako uone jinsi ugumu wa kurudisha hizo mali jinsi ulivyo”

Nilizungumza kwa hasira na kumpokonya Judy simu ya watu na kurudi sebleni na kuwakuta walinzi hawa wa mama wakiitazama taarifa hii tuliyo toka kuisoma.

“Wamempa jina la Mr Z”

“Mr Z!!?”

Niliuliza kwa mshangao.

“Ndio, naona mkuu wa polisi amesha anza kuchachawa.”

“Ila jamani huyo mtu jana sisi ndio alite tusaidia kutoroka mikononi mwa hao watu ambao wameuwawa na suti suti zao”

“Weee”

“Ndio na aliendesha hiyo gari hapo nje hadi meneo ya ile barabara kama utatoka mkoa wa Pwani, na kuingia hivi kama unakuja huku”

“Unataka kusema jamaa mulikuwa naye kabisa ndani ya gari?”

“Ndio na nimtu ambaye ameificha sura yake kabisa. Yaani hata macho yake ukiyatazama hivi ni ngumu kuweza kuyaona”

“Mmmmm”

Nikazidi kubaki mdomo wazi mara baada ya kuona taarifa nyingine ya habari inayo husisha watu tuliwa waua katika hoteli tukiwa na mama mkwe nao wote kila mmoja amewekewa alama ya Z.

“Huyu ni mtu ambaye anatufahamu”

Nilizungumza huku nikisimama na kuanza kuisogelea hii tv kubwa iliyo hapa sebleni kana kwamba sioni kinacho onyeshwa. Video inayo onyeshwa hivi sasa ni video ambayo imerekodiwa na kamera za CCTV. Badala ya kunionyesha mimi nikiwa nina pambana na watu wa Juma, ila nimauonyesha Mr Z jinsi anayo waaua watu hao kwa kuwapiga risasi.

“Mmmmm huu ni ongo”

“Uongo gani?”

“Mimi ndio nimewaua hao watu wa hapo hoteli, inakuwaje anaonekana yeye?”

Walinzi hawa wa mama mkwe wakabaki kimya huku nao wakionekana kuwa na mshangao.

“Hembu itafute hiyo video kwenye mtanda”

“Huku bado hajarushwa”

“Jamani hapana, huyu mtu siojui ni nani na inakuwaje anaonekena yeye”

“Vipi mbona mumesimama kama vibendera vya mwenyekiti wa kishumundu?”

Wifi aliuliz ahuku akifunga mlango wa kuingilia humu ndani, huku mkononi mwake akiwa ameshika mfuko mweusi.

“Wifi kuna muuaji mpya ameingia Tanzania anaitwa Mr Z”

“Mr Z?”

“Kamuua nani hadi awe maafuru hivyo?”

Jamaa akamakbidhi wifi simu hiyo, wifi akasoma habari niliyo isoma mimi.

“Mmmm yupo vizuri, alafu Jojo huyu si meneja wako?”

“Ndio”

“Mungu wangu, huyu mtu atakugeukia wewe sasa”

“Wifi huyo jana alituasiaida kutoka mikononi mwa hao watu walio uwawa na suti zao”

“Kakusaidia?”

“Ndio na hakuishia hapa akaendesha hilo gari tulilo kuja nalo”

“Hadi hapa nyumbani?”

“Hapana alituacha katika njia ile ya kuelekea Pwaani ambayo ukipita short cut unatokea Tegeta kule”

“Mmmm, ngoja nikapike zangu sabaki mie wasije wakanichachia. Ehee, chukua simu yako”

Wifi alizungumza huku akirudisha simu ya muhusika kisha akaondoka na wala hajaonyesha kushangazwa sana na swala hili la huyu Mr Z, kitu kilicho anza kunifanya ninze kuhisi jambo kwake. Nikaondoka sebleni hapa na kumfwata jikoni na kumkuta akiwa amesha waweka samaki hao ndani ya sufuri.

“Nilikuambia ukaoge, hembu jiangalie jinsi ulivyo chafuka na unanuka jasho”

Wifi alizungumza kimasiraha japo ndio ukweli wenyewe, ia sikuujali kabisa.

“Sawa nitaenda, ila nina swali nahitaji kukuuliza?”

“Uliza”

“Unamfahamu huyu Mr Z?”

“Namjulia wapi mimi, mwenyewe ndio leo ninamuona hapo”

“Una uhakika wifi?”

“Sasa nikudanganye umekuwa Gody wewe?”

“Ila kwa nini ametusaidia sisi?”

“Sasa unakuja kuniuliza mimi ikiwa kwenye hilo tukio sikuwepo jamani, si unanionea Jojo”

“Ila wifi hujaonekana kustushwa kabisa na mtu huyu”

“Sasa nistuke amekuwa jini huyo au amekuwa kiumbe cha ajabu. Mbaya hata sura yake sijaiona”

Wifi alizungumza kawaida kabisa.

“Wifi isije akawa ni mume wangu?”

“Nani, Eddy!!?”

“Ndio”

“Hahaahaa, mumeo amekuwa kichaa, na hana uwezo wa kufanya hayo mambo”

“Ila kwa nini makosa ambayo nimeyafanya mimi ameamua kuyachukua kama ni yeye?”

“Sijui, ila kwa Eddy, tena leo analetwa hapa nyumbani, sikutaka tu kukuambia, ila analetwa”

Nikahisi mwili mzima ukinisisimka, kwani ninapokea taarifa ambayo sikutarajia kuipokea kabisa.

“Analetwa na nani?”

“Na madaktari wake, yaani unaambiwa uzombi ndio umemzidi”

Wifi alizungumza huku akitabasamu.

“Wifi jamani mume wangu sio zombie, hata kama ana hali mbaya ila sio zombie”

Nilizungumza kwa sauti iliyo jaa unyonge mwingi sana huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.

“Sasa ni mtu gani huyo anapenda kula nyama mbichi tu, tena akija humu watoto tuwaweke mbali, asije akavila bure ohoo”

“Wifi bwana usizungumze hivyo?”

Nilizungumza huku nikishundwa kabisa kuyahimili machozi yangu yanayo nimwagika usoni mwangu.

“Tatizo hupendi kuambiwa ukweli, si atakuja wewe muache ache hivyo huyo mwanenu, macho, masikio, viguu, nikono yote itauwa ni halali yake”

Kwa hasira nikatoka ndani humu na kumuacha wifi akicheka kicheko kilicho zidi kunifanya nipate uchungu mwingi, nikaingia chumbani na kumkuta Judy akiwa amembeba mwanangu, nikamtazama mtoto kwa muda kisha nikaingilia baufuni. Nikavua nguo zangu, nikafungua maji ya bomba la mvua, taratibu yakaanza kumwagika. Nongo za mwilini mwangu zikapeleka hadi maji yanayo mwagika chini yakitokea kwenye mwili wangu yakabadilika rangi. Ikanichukua nusu saa kumaliza kusafisha kila kona ya mwili wangu hadi nikajizisha kwa kutakata kabisa. Nikatoka bafuni humu na kukuta Judy akiwa amesha niandalia tenge la kuvaa. Nikalichukua na kijifunga mwilini mwangu.

“Jojo”

“Bee”

“Ile kauli yako ya mwisho uliyo niambia kusema kweli sijaipenda. Imeniumiza sana moyo wangu”

“Samahani”

Nilijibu kwa ufupi huku nikisimama kwenye kioo kikubwa cha dreasing table. Judy akaendelea kunitazama kwa macho ya masikitiko kitu kilicho nifanya nianze kujisikia vibaya kwani siku zote sipendi mdogo wangu ajihisi vibaya kwa ajili yangu. Ila kabla sijazungumza chochote, mlango wa

chumbani hichi ukafunguliwa kwa nguvu, akaingia Gody huku akimwagikwa na jasho.

“Kuna nini wewe?”

Nilimuuliza kwa ukali kidogo kwa maana ameingia bila kubisha hodi na sipati picha kama angenikuta nipo uchi kabisa.

“Ba mdogo, ba mdogo ameletwa”

Sijui hata nimetokaje humu ndani, nikajikuta nimesimama kwenye mlango wa kuingilia sebleni, macho yakanitoka kwani minyororo mikubwa aliyo fungwa mume wangu kuanzia miguuni, mikononi, ikanifanya mapigo yangu yaniende mbio. Madakari wawili wenye miili mikubwa wamemshikilia kikamilifu kwani anarika ruka akionyesha anataka kutoka mikoni mwao. Kishindo kizito nyuma yangu kikanifanya nigeuke kwa haraka, nikamkuta Gody akiwa ameanguka na kupoteza fahamu kwani hali ya baba yake mdogo inatisha na kusikitisha kwani manywele mengi na ndevu nyingi zilio mjaa zimemfanya aonekane kama msukule aliye chukuliwa mika mingi sana na wachawi.



Ikatubidi tumnyanyue Gody mimi na wifi na kumuingiza chumbani na kuanza kumpepea, ila zoezi hili la kumpepea Gody kwangu halina hata nguvu, kwani akili yangu yote inamuwazia mume wangu ambaye nimemuona akiletwa. Tukasikia kurupushani kwenye kordo, nikanyanyuka na kuanza kutembea kueleka mlangoni. Nikafungua mlango na kukutana na madakatri hawa wawili wakijitahidi kuhakikisha kwamba wanamuingiza Eddazari kwenye chumba ambacho tangu niingie kwenye nyumba hii sijawahi kuingia ndani. Madaktari wakafanikiwa kumuingiza Eddazaria ndani ya chumba hicho, nikaanza kunyata huku nikiwa na hofu kubwa hadi mlangoni. Nikachungulia na nikawashuhudia wakimfunga kwenye kianda cha chuma. Machozi yakaendelea yakaanza kunimwagika usoni mwangu. Madaktari walipo maliza kumfunga katika chumba hichi, taratibu wakatembea hadi mlangoni nilipo simama huku jasho likiwa wamwagika usoni mwao.

“Huruhusiwi kuingia kwa mud huu hadi tumchome sindano ya usingizi”

Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Namuangalia tu mara moja”

“Huwezi, anaweza kukudhuru japo tumemfunga hiyo minyororo ila kuna muda mwengine huzikata kabisa”

Daktari mmoja akaondoka katika eneo hili na kuniacha nikiwa nimesimama na daktari huyu mwengine.

“Ni kitu gani ambacho kinamsumbua sana mume wangu?”

“Hasira”

“Hasira kivipi?”

“Amekuwa ni mtu mwenye hasira kali sana, jambo ambalo anaweza kujipiga ukutani hadi akapoteza fahamu”

Daktari huyu mwengine akarudi akiwa ameshika kijibegi kidogo cheusi, akaingia ndani ya chumba hichi na kutoa sindano pamoja na kichupa cha dawa, akavuta dawa ya kutosha kisha akamchoma sindano Eddazaria sindano ya shingoni mwake, na baada ya muda mchache Eddazaria akapitiwa na usingizi na akalala fofofo.

“Unaweza kuja kumtazama”

Taratibu nikaanza kutembea kwa hatua za woga hadi kitandani mwake. Kusema kweli mume wangu mwili wake umechakaa kwa makovu mengi sana. Ngovi yake imefubaa, uzuri wake wote alio kuwa nao umekwisha, kiasa kwamba amekuwa mbaya. Machozi yakaendelea kunimwagika usoni mwangu. Taratibu nikaanza kamshika Eddazaria ndevu zake hizi nyingi zenye urefu wa mithili ya waarabu wapendao kufuga nywele zao.

‘Ehee Mungu ni nini kinacho endelea kwa mume wangu, ni kwa nini hampi nafasi ya kurudi kwenye maisha yake ya kawaida. Kwa nini unataka kumuangamiza akiwa bado mdogo eheee?’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimkumbatia mume wangu, japo ana kiharufu kikali cha nongo na vidonda baadhi vilivyomo mwilini mwake, ila sikujali hilo zaidi ya kumkumbatia kwa nguvu na kuangua kilia kikali.

‘Yote ni makosa yangu Mungu, yote mimi ndio msababishaji. Kwa nini nisinge kuwa mimi, kwa nini hali hii usinge nipa mimi jamani Mungu wangu ehee?’

Niliendelea kulia na kuzidi kumlaumu Mungu wangu, kwnai pasipo mimi kumkua Eddazaria basi leo hii asinge kuwa katika hali ya matatizo kama haya.

“Eddy nisamehe mume wangu, naomba unisamehe mume wangu”

Nilizungumza huku nikitingisha mwilini mwake.

“Hawezi kukusikia hata ukizungumza”

Niliisikia sauti ya wifi na ikanifanya ninyanyuke kifuani mwa mume wangu na kumtazama.

“Ni zaidi ya mateso ambayo mdogo wangu anapitia. Mimi nimesha lia hadi nimesha choka, kikubwa ni kuzoea hali halisi na kukubaliana hali halisi”

“Wifi kumbuka huyu ni mume wangu?”

“Ni mume wako ila mimi ni mdogo wangu, nimekua wate toka utotoni, nimembeba na kumuogesha so nina uchungu zaidi yako. Hivyo jikaze kikike na hakuna haja ya kulilia lia. Mama anatakiwa kuwa huru sasa”

Maneno ya wifi hayana hata chembe ya huruma, nikamtazama kwa muda kisha taratibu nikambusu mume wangu mdomoni mwake, japo kinywa chake kinatoa harufu isiyo nzuri ila sijali hilo kwani ni mume wangu. Nikanyanyuka na kutoka humu chumbani moja kwa moja nikaelekea jikoni, nikatazama tazama kila eneo, nikaona sufuria kubwa katika kabati la vyombo. Nikaitoa kisha nikaiweka jikoni. Nikaweka maji ya kutosha na kisha nikawasha jiko hili la gesi.

“Maji hayo yote ya nini?”

“Nahitaji kwenda kumuogesha mume wangu”

“Pale kitandani?”

“Ndio”

“Atalala wapi?”

“Wifi najua nini ninafanya sawa”

Nilizungumza kwa ukali kidogo huku nikimtazama wifi usoni mwake kwa macho yangu yaliyo jaa ukungu wa machozi. Maji yalipo chemka vya kutosha, nikachukua moja ya ndoo, nikayamimina kisha nikachanganya na maji ya badidi kiasi na kuyafanya maji haya yawe ya vuguvugu. Nikatoka jikoni humu na kuingia katika chumba cha wifi.

“Naomba taulo”

Nilimuambia Judy huku akiwa anaendelea kumpepea Gody ambaye hadi sasa hivi bado hajazinduka.

“Chukua humo bafuni”

Nikaingia bafuni, nikachukua kijitaulo kidogo na sabuni ya kunikia, nikatoka bafuni humu, nikaibeba ndoo yangu na kuingia katika chumba alicho lazwa Eddazaria na kina kitanda hichi kimoja tu na hakuna vitu vingine.

“Unataka kufanya nini?”

Daktari mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu

“Nahitaji kumsafisha mume wangu, nyinyi munamuona jinsi anavyo nuka, mumethubutu hata kumuogesha?”

Niliendelea kuzungumza kwa ukali.

“Tokeni, sitaki kuwa na mtu ndani”

“Anaweza kuzinduka na kukujerudi.”

“Hata akinijeruhi yeye ni mume wangu, hilo kwangu halina tatizo kabisa”

Niliendelea kuzungumza kwa ukali na kuwafanya madaktari hawa kutoka chumbani humu, nikaufunga mlango kwa ndani, kisha nikarudi kitandani, nikaanza kufungua vifungo vya shati hilo la Eddazaria. Nikastuka sana mara baada ya kuona michoro mingi mwilini mwake, jambo ambalo hapo awali sikuwahi kuliona. Michoro yote hii hakuna hata mchoro mmoja ninao uelewa kwani imechorwa hovyo hovyo. Kutokana na kufungwa minyororo hii, nikashindwa kabisa kumvua shati lake, ila kushindwa kumvua shati haikuwa sababu ya mimi kuanza kumsafisha mwili wake, kwa kuufuta futa kwa kitaulo hichi. Japo mwili una michoro, ila ngozi halisi ya ikaanza kuonekana. Nikaendelea na zoeizi hili kuku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu. Nikaishusha kidogo suruali ya mume wangu hadi maeneo ya magotini. Nikajikuta nikizidi kujisikia uchungu kwani wingi wa nywele za sehemu za siri ninazo ziona ni sawa sawa na ndefu zake.

‘Kwa nini jamani hawamfanyii usafi eheee?’

Nilizungumza huku nikianza kumsugua sugua eneo la jogoo wake. Nilipo hakikisha kwamba eneo zima la jogoo wake pametakata, nikahamia kwenye mapaja yake, nikakuta majeraha kadhaa ya risasi, jambo lililo nifanya nishangae kidogo. Maji yoye niliyo ingia nayo humu ndani yamejaa nongo na hayafai tena kuendelea kumsafisha mume wangu. Nikaipandisha suruali yake taratibu, kisha nikabeba ndoo yangu na kutoka chumbani humu.

“Kwa nini mume wangu hamumuogeshi?”

“Kwa hali hiyo kuna mtu ambaye anathubutu kumsogelea, sisi wenyewe tupo wawili ila tunamuogopa pale hali yake inapo badilika”

“Hata kama, ila mumemfanya amekuwa kama msukule, sasa muna lipwa nini?”

“Jukumu letu ni kumtazama hali yake sister”

Nikawatazama madaktari hawa kisha nikawapita pasipo kuzungumza kitu chochote, nikaingia chumbani na ndoo yangu hii kisha nikapitiliza hadi bafuni, nikayamwagaka na kuanza kukifua kitaulo hichi. Nilipo maliza nikarudi chumbani na kumkuta wifi akimtazama Gody aliye kaa kitandani pamoja na watoto wengine.

“Wifi nahitaji kwenda mjini?”

“Kufanyaje?”

“Kumnunulia mume wangu nguo”

“Sasa huyo mumeo si unaona hali yake ilivyo”

“Na wewe unafurahia kumuona vile?”

Swali langu likamfanya wifi kukaa kimya na kishindwa kunijibu kitu chochote. Nikachukua nguo zangu nilizo kuwa nimezivaa, nikaingia bafuni na kuvua hili tenge nililo jifunnga na kuvaa nguo zangu. Nikazibana nywele zangu ndefu vizuri na kisha nikatoka bafuni humu.

“Hujupulizii hata body spray?”

Wifi alizungumza huku akinitazama, nikachukua moja ya perfume, nikajipulizia mwilini mwangu kisha nikatoka chumbani humu pasipo kuzungumza kitu chochote.

“Naweza kupata ulinzi wako”

Nilimuambia mlinzi mmoja wa mama mkwe.

“Nani, mimi?”

“Ndio”

“Sawa”

Tukatoka ndani, nikaingia ndani ya gari. Vibunda vya pesa nilizo kuwa nimepewa na dokta Clara nikaziweka kwenye droo ndogo ya gari hii. Nikaanza kulirudisha nyuma taratibu hadi nikatoka katoka uzio wa nyumba hii, ,linzi huyu akafunga geti kisha akapanda na kukaa siti ya mbele.

“Nikuendesshe au uniendeshe?”

“Naendesha mwenyewe”

“Tunaelekea wapi?”

“Mjini”

“Sehemu gani?”

“Kwenye maduka ya nguo”

Nilizungumza huku taratibu tuliondoka katika eneo hili. Tukaingia katika barabara kuu na kuendelea na safari hii.

“Jojo”

“Bee”

“Mume wako hali yake inaendeleaje?”

“Sio nzuri”

“Daa pole”

“Asante”

Maswali yote ta mlinzi huyu ninayajibu kwa ufupi fupi, akili yangu yote kwa sasa inamfikiria mume wangu kipenzi tu. Tukafika katika maduka ambayo nakumbuka tulisha wahi kufika na Eddazaria miaka ya nyuma. Sikujali kujulikana kwangu, nilicho kifanya ni kuingia dukani humu. Nikachagua nguo ambazo nahisi zinatamtosha mume wangu, nikaingia kwenye duka jengine na kununua nguo zangu pamojana nguo za Judy. Nilipo hakikisha kwamba nimekamilisha hayo yote nikanua mashine ya kunyolea nywele pamoja na mashie ya kunyolea sehemu za siri.

“Jojo naomba tupige picha”

Dada mmoja alinisemesha, ila kwa jicho nililo muangalia tu, yeye mwenyewe akajua kwamba nimakatalia na mlinzi wangu muda wote yupo nyuma yangu akiimarisha ulizi. Tukarudi kwenye gari na safari hii nikamuachia jukumu la kuendesha gari.

“Tunarudi nyumbani au kuna sehemu unahiyaji kupitia?”

“Kuna hospitali moja nahitaji kwenda”

“Inaitwaje?”

“Ipo barabara sijui ya ngapi?”

“ipoje ipoje?”

“Ni gorofa na ina rangi nyeupe”

“Okay ipo hapo barabara ya nne”

Tukaelekea katika hospitahi hii ambayo kipindi cha mwisho kulitokea varangati kati ya watu wa Nuru na shemeji yangu aliye kuja kutuokoa mara baada ya kupata habari kwamba tumetekwa na Nuru ambaye hasi sasa hivi naye sifahamu yupo wapi. Nikaingia hadi mapokezi, nikamuulizia daktari ambaye ni rafiki wa mume wangu. Kwa bahati nzuri nikiwa hapa kwenye mapokezi nikamuona akitokea kwenye moja ya kordo na kuja eneo tulilo simama huku usoni mwake akiwa amejawa na tabasamu.

“Shemeji mambo”

Nilianza kumsalimia huku nikimpa mkono na yeye taratibu akanipa mkono na kunikumbatia kidogo.

“Safi shem wangu, niambie”

“Safi tu, ndio kwanza nilikuwa ninatoa maelekezo ya jisni ulivyo kwa maana mim nakujua kama dokta tu”

“Hahaaa, usijali, za miaka?”

“Sio salama shemeji yangu?”

“Ohoo vipi mumesha gombana na mumeo?”

“Hapa”

“Ila?”

“Kuna mambo kidogo yameingiliana, kuna tatizo kidogo”

“Ehee taizo gani?”

“Kama hutojali, ninakuomba twende kwa mama kule Kange, naamini utajionea kitu kinacho endelea.”

“Tena una bahati sasa hivi ndio nilikuwa ninatoka hivi kwenda kupata chakula cha mchana”

“Sawa tunaweza kuongozana, nimekuja na gari langu”

“Ahaa…sawa, ila unaonaje ukapanda gari langu, kwa maana nafikiria niende tena Kange, kisha badae unirudishe, itakuwa ni kuchezea mafuta na kama unavyo ona hali halisi ya maisha sasa hivi inakaba hadi kooni”

“Ni kweli dokta sawa, mimi sina neno. Utaendesha gari langu, mimi napanda katika gari la shemeji”

“Poa poa”

Tukatoka nje na tukaingia kwenye gari la dokta na mlinzi niliye ongozana naye taratibu akaanza kutufwata kwa nyuma.

“Umebadilisha gari ehee?”

“Yaa kuna kiji mkopo kidogo tulipewa na wakuu wetu, nikaona nivute hii Prado Tx”

“Ni nzuri”

“Kiasi chake, sio kama zenu hizo, benzi kali nini”

“Ahaa, yaani sasa hivi sijui magari, sijui nini hata sina furaha navyo kabisa”

“Kwa nini?”

“Mume wangu anaumwa”

“Anaumwa na nini?”

“Amekuwa mwendawazimu”

Dokta macho yakamtoka, taratibu akapunguza mwendo kasi wa gari kisha akalisimamisha pembezoni mwa barabara na kumfanya mlinzi wangu naye kusimamisha gari nyuma.

“Shemeji una uhakika?”

“Ndio asilimia mia moja, rafiki yako amekuwa ni mwendawazimu, tena wa kufungwa minyororo ili asijeruhi watu na amekuwa anakula nyama mbichi kabisa”

“Weeeee!!!?”

“Haki ya Mungu vile shem, huo ndio ukweli, hapa yaani nimepoteza furaha yote japo tumejaliwa mtoto wa kike, ila hata sina furaha naye”

Dokta akaka kimya kisha akawasha gari na kugeuza tulipo toka huku akiendesha kwa mwendo wa kasi sana hadi nikajikuta nikiacha kuchanganyikiwa kwa maana siku ya mwisho kuonana mimi na yeye alitumiwa na Nuru kunishawishi kufungua mlango na mwishowe tukajikuta mimi na mume wangu tukiingia kwenye matatizo makubwa yaliyo tutenganisha katika penzi letu hadi leo hii.



“Unakwenda wapi weweeee?”

Nilimuuliza dokta kwa ukali huku nikimtazama usoni mwake.

“Shem tulia najua nini nafanya?”

“Unajua nini unafanya wakati huniambii ni nini unafanya?”

Nilizungumza huku nikigeuka nyuma, nikaona jinsi gari analo liendesha mlinzi wa mama linavyokuja kwa kasi kuhakikisha kwamba anamzuia dokta.

“Dokta nina mlinzi na mlinzi wangu hana masihara niambie ni wapi tunakwenda?”

“Nakupeleka kwa babu yangu, naamini yeye atatusaidia”

“Atausaidia kwenye nini hapo na wewe?”

“Wewe twende”

“Sasa punguza mwendo nizungumze na mlinzi wangu la sivyo atakudhuru”

Dokta akaweza kunisikiliza na taratibu akapunguza mwendo kasi wa gari lake na kulisimamisha pembeni kabisa na kumfanya mlinzi wa mama kutupita na kusimamisha gari kwa mbele. Mlinzi wa mama akashuka huku akiwa ameshika bastola jambo lilolo mfanya dokta kuanza kutetemeka.

“Fungua kioo”

Mlinzi aliamrisha.

“Nipo salama, kaka”

Ilinibidi nijishuku na kuanza kuzungumza.

“Kwa nini umefanya hivi?”

Mlinzi alizungumza huku akifungua kitasa cha mlango wa gari la dokta kwa ndani.

“Nimekuambia kwamba nipo salama”

Japo nimezungumza kwa ukali, halikutosha kwa mlinzi huyu kumshusha dokta kwenye bari na kuanza kumpapasa, alipo hakikisha kwamba hana silaha, akachunguza eneo la karibu kabisa la siti ya doka, alipo ona hakuna silaha yoyote, kwa ishara akamuomba arudi kwenye gari.

“Ila kwa nini unakuwa hivyo?”

“Jukumu langu ni kukuangalia wewe na sifwati amri yako, ila ni amri ya mkuu wangu”

Alizungumza kwa msisitozo na kunifanya nikae kimya.

“Unaelekea wapi?”

“Ninaelekea Pande”

“Kule kwenye eneo la jeshi?”

“Ndio”

“Tangulia mimi ninawafwata nyuma, sasa ole wako ufanye kosa, ninakumwaga ubongo wako sawa”

Dokta akazungumza kwa kutingisha kichwa akimaanisha kwamba ameelewa alicho ambiwa. Tartibu dokta akawasha gari na kuanza kulirudisha nyuma tartibu, kisha akalikwepa gari la mlinzi wangu na kwa mwendo wa kawaida safari yetu ikaendelea, huku mlinzi akitufwata kwa nyuma. Dokta akashusha pumzi nyingi huku akijifungua tai iliyo ifunga vizuri shingoni mwake.

“Maisha ya utajiri bwana khaa”

“Yana nini?”

“Wewe huoni jinsi unavyo lindwa, laiti ingekuwa ni mimi hata mlinzi ningemtolea wapi?”

“Dokta wewe hujui ni maadui wangapi wanavyo tufwatilia”

“Hilo ni lazima kwa maana maadui wenu wote si wanafwata pesa?”

“Sio pesa pekee”

“Kivipi?”

“Tuachane na hayo, ehee kwa bibi yako unanipelekea kufanyanya nini?”

“Sio bibi yangu, ila ni babu yangu ndio tunaelekea”

“Tunakwenda kufanyaje?”

“Tunakwenda kumuangalia kama kuna mdudu ametupiwa na walimwengu aweze kuondolewa”

“Mmmmmm”

“Najua huamini hayo mambo ila walimwengu sio watu wazuri, na si watu wa kuwaamini sana. Wengine wana macho mabaya sana, wakiona mafanikio ya mtu kidogo basi wanaanza kufanya mambo ya kipuuzi ili mradi kurudishana nyuma kimaendeleo.”

Nikamtazama tu dokta usoni mwake jinsi anavyo zungumza, kwani katika maisha yangu japo nimekulia uswahilini, ila kuhusiana na maswala ya Uganda sikuwahi hata siku moja kuweza kuyafikiria na kuyapa nafasi katika maisha yangu. Safari yetu ikatuchukua kama dakika arobaini na tano hivi na tukafanikiwa kufika katika kijiji cha Pande. Tukafika katika nyuma moja iliyopo porini kidogo. Tukasimamisha magari mita kadhaa kutoka ilipo nyumba hiyo.

“Mbona tumesimamisha huku, ikiwa pale nje kuna uwazi?”

“Kila sehemu ina utaratibu wake”

Tukashuka kwenye gari na mlinzi naye tukamkuta akiwa ameshuka kwenye gari.

“Nakuomba umuambia atusubirie hapa”

Dokta alizungumza huku akininong’oneza. Nikamfwata mlinzi hadi sehemu alipo simama.

“Kaka naomba niingie ndani humo wewe nisubiri hapa”

“Una muamini huyo jamaa?”

“Ndio nina muamini ni rafiki wa karibu kabisa wa mume wangu”

“Ninakupa dakika kumi na tano usipo toka utaingia ndani?”

“Bwana hapa ni kwa mganda, sasa ukijifanya mbabe ukageuzwa kukua hilo shauri yako. Wewe acha mimi niingie ndani, tumalize kilicho tuleta humu, kisha tutatoka sawa”

“Siamini uchawi mimi”

“Haya ukiheuzwa kuku mtetea ndipo utakapo amini kwamba mambo sio ya mchezo mchezo”

Nilizungumza kwa msisitizo na kuanza kutembea kumfwata dokta sehemu alipo simama. Tukafika sehe yenye minazi miwili. Dokta akasimama, nikataka kumpita ila akanishika mkono.

“Tuvue viatu”

“Hee!!”

“Ndio”

Tukavua viatu vyetu kisha tukatembea hadi katika mlango, dokta akagonga mara ya kwanza hatukusikia chochote, akagonga kwa mara ya pili mlango ukafunguliwa. Cha kunishangaza sikumuona mtu aliye fungua mlango zaidi ya kuhisi kama upepo mkali ikipita katikati yetu jambo lililo nifanya mwili mzima kusisimka hadi nywele na vinyweleo vya mwili wangu nikahisi vikisimama.

“Babu ni mimi mjukuu wako nimekuja na shemeji yangu ana matatizo”

Dokta alizungumza akiwa amesimama hapa hapa mlangoni huku akiendelea kuung’ang’ania mkono wangu.

“Ingieni”

Dokta akanitazama usoni mwangu na kwa ishara ya macho akaniomba tuingie ndani. Tartaibu tukaingia ndani ya hii nyumba. Tukakuta seble kubwa ila hana kochi wala moja zaidi ya zulia jekundu lililo tandikwa chini pamoja na vitambaa vikubwa viwili kimoja cha rangi nyeusi na kimgine cha rangi nyekundu na vyote vimetandikwa ukutani eneo alipo kaa mzee mmoja mnene.

Kwa ishara mzee huyo akanionyesha sehemu ya mimi kukaa peke yangu, eneo ambalo amenionyesha nikae kwa ishara, chini limechorwa duara kwa rangi nyeusi. Kwa ishara mzee alilinionyesha mara baada ya kukaa katika eneo hilo. Nikabaki nikiwa nimeduwaa, kwa maana ishara hiyo sifahamu vizuri.

“Kunja miguu”

“Ahaa”

Nikaitikia alicho niambia dokta, kwa haraka nikakunja miguu yangu na kutulia tuli. Dokta naye akakaa eneo alilopo kwa kupiga magoti chini na kuikalia miguu yake kwa nyuma.

“Babu huyu ni mke wa yule rafiki yangu Eddy. Sasa leo nimekutana naye wametoka zao huko Dar es Slaam. Sasa shem ameniambia kwamba mume wake amechanganyikiwa na amekuwa ni mtu anaye ishi kwa kufungwa kwa minyororo kutokana na kupiga watu na kula nyama mbichi”

Dokta alizungumza kwa sauti ya upole sana jambo lililo mfanya mzee huyo kuanza kutingisha kuchwa taratibu kana kwamba anasikitika sana.

“Moyo wangu uliumia sana mara baada ya kusikia hili swala hivyo babu ninakuomba uweze kumsaidia ndugu yangu kwa maana nikisema rafiki pia nafsi inanisuta”

“Anatakiwa akaletwe hapa kwangu”

Nikastuka sana kwa maana zaa zaa la mume wangu ni hadi mabaunsa wawili tena wenye nguvu. Sasa tutamletaje letaje.

“Aha…samahani babu”

Nilizungumza kwa kuogopa ogopa, mzee huyu akanitazama kwa kunikazia macho usoni mwangu, ila sikutaka kuonyesha udhaifu wa aina yoyote kwake nikayakaza macho yangu na mimi nikaendelea kumtazama.

“Hali ya mume wangu ni mbaya sana. Hali ya mume wangu kama dokta alivyo zungumza hapo basi huo ndio ukweli, anafungwa minyororo ili mradi tu asiwadhru watu wengine.”

Mzee akatabasamu kidogo.

“Unajua mume wako ndio amekubebea matatizo yako wewe?”

Macho yakanitoka, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio.

“Kama ingekuwa sio nyota ya mumeo kuwa na nguvu ya kukulinda unajua leo hii unegkuwa umesha kufa?”

Dokta akanitazama kwa mshangao, kajasho kembamba kakaanza kunitoka usoni mwangu.

“Nendeni mukamlete na ukichelewa chelewa na nguvu ya nyota yake wakiimaliza kuinyonya basi atakaye fwata ni mwanao wa kike na atakufa”

Nikahisi kama kichwa kimechochewa kwa moto mara baada ya kusikia kwamba watahamia kwa mwangu.

“Angalizo, mutakapo mleta huku hakikisheni kwamba hakuna mtu yoyote anaye weza kufahamu zaidi yenu nyinyi wawili”

“Sawa babu, ila nina swali kidogo”

“Uliza”

“Mume wangu ananguvu za ajabu sasa tutamtoa vipi?”

“Sio nguvu zake hizo, ni nguvu za madudu aliyo wekewa ndani, kwani kwenye akili zake za kwaida ulisha wahi kumuona akifanya hivyo?”

“Mmmmm hapana?”

“Kula nyama mbichi?”

“Hapana”

“Na bado mukawa munaendelea kuwategemea madaktari, mukahisi atapona?”

“Ahaa mama mkwe ndio alikuwa anahitaji iwe hivyo”

“Ifikapo saa nne kamili hakikisheni kwamba munamtoa kule alipo, ndani ya lisaa hilo zima inabidi muwe mumesha mleta hapa mume nielewa, ikizidi saa nne na kuingia saa tano kama mutakuwa naye basi atawadhuru wote na mutakufa, sasa mujitahidi”

“Sawa babu”

Kwa ishara ya mikono mzee huyu akatuomba tunyanyuke na kutoka nje. Tukatoka nje na kuanza kutembea kwa haraka haraka hadi sehemu tulipo vulia viatu vyetu, sikuona hata haja ya kuvivaa, nikavishika mkononi na kuanza kutemeba hadi kwenye gari la dokta na mlinzi akanifwata.

“Vipi kuna nini kinacho endelea?”

“Twende nyumbani”

“Hilio sio jibu?”

“Kaka, twende nyumbani tu, mimi ninapanda huku”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na wasiwasi na mashaka mengi sana, kwenye maisha yangu yote sijawahi kusikia mambo kama haya. Tukaingia kwenye gari, taratibu dokta akageuza gari na safari ya kuelekea nyumbani ikaanza. Mawazo mengi yakaanza kunisonga kichwani mwangu, nikaifkiria jinsi mzee alivyo sema kwamba laiti ingekuwa sio nyota ya mume wangu basi leo hii ningekuwa nimekufa.

‘Heee Mungu wangu, msaidie Eddy wangu’

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.

“Shem usilie ndio walimwengu hivyo”

“Lakini kwa nini wamefanya kwa mume wangu, kwa nini lakini?”

Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu.

“Usijali, babu atamsaidia, babu atafanya jambo juu yake, ndio maana ulivyo nieleza hivyo tu, kwa haraka nikafikiria kumpeleka kwa babu yangu”

Nikakaa kimya huku kumbukumbu za nyuma za furaha kati yangu mimi na mume wangu zikijirudia. Ni mwanaume ambaye katika maisha yangu alinitoa katika mfumo mbaya wa kuwapenda wanawake wezangu hadi kujawa na hisia za kama wanawake wengine katika kuwapenda wanaume. Ni mwanaume ambaye siku zote kwenye maisha yake hakuhitaji kuliona chozi langu linadondoka mbele yake, alijua jinsi ya kunijali na kunilinda kwa ujumla. Nikajikuta nikizidi kulia kwa uchungu sana.

“Dokta”

“Ndio shemeji?”

“Hivi babu anaweze kunieleza ni nani ambaye amemfanyia mume wangu hayo?”

“Inawezekana ila hadi mumeo apone kabisa”

“Kwa sasa hivi hawezi?”

“Una hasira, hato weza kukuambia chochote”

“Haki ya Mungu, nikimfahamu huyo aliye mfanya mume wangu ndondocha nitamuua, haki ya Mungu nitamuua”

Niliapa huku machozi yakiendelea kunimwagika. Dokta hakuzungumza chochote zaidi ya kunitazama kwa huruma sana. Tukafika nyumbani kwa mama mkwe, tukafunguliwa geti na Judy na taratibu tukaingia ndani. Nikashuka kwenye gari huku nikiwa nimejawa na unyonge mwingi sana, sikumzungumza chochote na mtu na kuanza kuelekea ndani, nikapitiliza moja kwa moja hadi kwenye mlango wa chumba alicho lazwa mume wangu.

“Hei umerudi”

Sauti ya wifi ikanistua kidogo na kujikuta nikimtazama kwa macho yaliyo jaa ukungu wa machozi.

“Mmmmm”

Wifi akanifwata hapa mlangoni nilipo simama na kunitazama usoni mwangu.

“Natambua kwamba uma mawazo juu ya mume wako, ila Mungu ni mwema tu atapona. Ila ninacho kuomba ujikaze, nimefikiri sana ombi lako la kwenda kuifanya kazi ya kukomboa mama leo usiku, nimekukubalia jiandae, saa nne usiku nitakuambia ni wapi tunatakiwa kwenda kukutana na raisi”

Nikabaki nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana, kwani muda huo ambao wifi ameniambia tunatakiwa kwenda kumkomboa mama mkwe mikononi mwa raisi ndio muda ambao mimi na dokta tunatakiwa kumpeleka mume wangu Eddy kwa babu ili kutibiwa tatizo lake.



Wifi akaondoka na kuniacha nikiwa ninamsindikiza kwa macho na kuingia chumbani kwake. Judy akanifwata huku akiwa amebeba mifuko ambayo ina nguo zangu na za mume wangu.

“Naomba huo mfuko mweusi”

Judy akanikabidhi mfuko ambao una nguo za mume wangu. Dokta naye akatufwata sehemu tulipo simama.

“Humo kuna nguo zako, jaribisha kama zitakutosha”

“Sawa”

Judy akaondoka na dokta akaanza kumsindikiza kwa macho hadi akaingia ndani.

“Huyu ni nani?”

“Mdogo wangu”

“Ahaa”

“Humu ndani ndipo alipo mume wangu, hivyo basi tunaingia ila sihitaji umshangae”

“Usijali, mimi ni daktari na ninakutana na wagonjwa wa kila aina”

Sikutaka kumjibu chochote dokta, nikafungua kitasa cha mango huu taratibu nikaufungua na tukaingia ndani. Dokta macho yakamtoka huku akionekana dhairi anashangaa kumuona mume wake akiwa katika hali kama hii.

“Masikini jamani, binadamu kweli wana roho mbaya, kwa nini wamemfanya hivi ndugu yangu”

Dokta alizungumza huku akiushika mkono wa kulia wa Eddazaria, akautazama kwa muda, kisha akatingisha kichwa.

“Na anaoupungufu wa damu nyingi, inabidi atundikiwe dripu la damu”

“Ngoja kwanza, tunat……”

Hata kabla sijaimalizia sentensi yangu Eddazaria akfumbua macho yake na tukajikuta tukirudi hatua moja nyuma kutoka sehemu kilipo kitanda. Eddazaria akanitazama kwa macho makali huku akihema kwa nguvu.

“Hei Eddy”

Dokta aliita huku akijaribu kumsogelea, ila galfa, Eddazaria akakata nyororo ya mkono wa kushoto jambo lililo tufanya tutoke kasi chumbani humu huku mimi nikiwa na kazi ya kuwaita madaktari. Madaktari wake wakatupita katika korodo na kuingia ndani ya chumba hicho, tukaanza kusikia vishindo vizito vya kama watu wanao pigana masumbwi.

“Gody rudi ndani”

Wifi alizungumza kwa ukali mara baada ya vishindo hivyo kuzidi. Gody akaanza kuangua kilio, kwani anaye pata mateso hayo ni baba yake mdogo.

“Judy mufunge mlango kwa ndani”

Wifi alizungumza kwa ukali na kumfanya Judy kumchukua Gody na wakaingia ndani na kuufunga mlango kwa ndani. Walinzi wa mama nao wote tumesimama nao kwenye kordo wakisikilizia huku kila mmoja akiwa ameishika bastola yake mkononi. Nikajikaza na kuanza kutembea kuelekea katika chumba hicho.

“Wewe Jojo”

Wifi aliniita kwa sauti ya ukali, ila sikuhitaji kusikia hili nanikahitaji kushuhudia ni nini kinacho tendeka ndani ya chumba hichi. Nikamkuta daktari mmoja akiwa amempiga kabari ya shingo mume wangu huku mwengine akimshindilia mangumi ya tumbo na sehemu nyingine za mwili.

“Kwa nini munampiga?”

Nilizungumza huku machozi yakinitoka usoni mwangu.

“Toka ndani humu”

Daktari anaye mpiga mume wangu alizungumza kwa ukali huku akininyooshe mkono wa kulia. Ila kalba daktari hajaushusha mguu wake, nikastukia akipigwa na miguu ya Eddazaria, kifuani mwake na akaanguka mita kadhaa na inaonyesha ni nguvu za namna gani ambazo mume wangu anazo.

Daktari aliye mpiga kabali akaendelea kumkaba kisasa sawa huku akimujitahidi kumuangusha chini, kwani kuendelea kusimama naye hivi na kuminyana inaweza ikawa ni hatari sana kwake. Eddazaria akatoa mgurumo mzito mithili ya simba jambo lililo nifanya nikae nizidi kutetemeka, yaani katika hali kama hii ambayo anayo mume wangu, ni heri mtu ukasikia tu kuliko kujishuhudia kwa macho.

“Kalete sindano, kuna kibegu kipo pale sebleni kwenye kochi, fanya haraka akanizidi nguvu huyu”

Kwa haraka nikafugua mlango na kutoka nikiwa ninakimbia. Kila aliye simama kwneye kordo naye akaungana nami kukimbia, si wifi, sio dokta wala sio walinzi wa mama kwani hali ina muogopesha kila mtu humu ndani.

Nikaaangaza angaza sebleni hapa na kuchukua kibegi kidogo nilicho agizwa kisha nikakimbilia chumbani, dokta akanipa maelekezo ya haraka. Nikachukua bomba la sindano na kuvuta dawa ya kutosha kwenye kichupa. Kisha dokta akaniagiza nimchome sindano ya shingo.

Kitendo cha kuinama ili nimchome sindano ya shingo mume wangu, nikastukia kikumbo kizito katika miguu yangu na kunifanya niangukie mgungo, nikamshuhudia daktari aliye kuwa amemshika akiwa amesukumiwa pembeni na mume wangu amesimama huku akinguruma.

‘Mungu wangu leo ninakufa’

Nilizungumza mara baada ya kumuona Eddazaria akiwa amekata nyororo zote na kuwa vipande vipande. Mimi na madaktari hawa kila mmoja akawa kimya, macho yamemtoka huku akimtazama Eddy aliye simama huku kifua chake kikipanda na kushuka kwa hasira. Galfa mlango ukafungulia, akaingia Gody na kusimama katikati ya mlango.

“Gody toka”

Nilizungumza kwa sauti ya chini sana huku nikimtazama Gody anaye jipangusa machozi usoni mwake. Mingurumo mithili ya simba muwindaji inayo toke kinywani mwa mume wangu haikumuogopesa Gody.

“Ba mdogo ni mimi”

Gody alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Eddazaria akaanza kumsogelea Gody sehemu alipo simama jambo lililo yafanya mapigo yangu ya moyo kuzidi kunienda mbio. Mtoto huyu sijui ana ujasiri wa kiasi gani kwani hatikisiki wala kuyumba na macho yake yote ametazamana na baba yake mdogo.

“Ni mimi Gody”

Taratibu Eddy akaupeleka mkono wake wa kulia shingoni mwa Gody, nikayafumba macho yangu kwani sihitaji kushuhudia mauaji ya mtoto huyu, kwani maumivu ninayo yahisi mgongoni mwangu hakika yananitosha kwa asilimi zote. Ila kadri ya sekunde ambavyo zinazidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo hisi ukimya ulio nishawishi kufumbua macho. Sikuamini macho yangu mara baada ya kumkuta Eddzaria amepiga magoti mbele Gody huku akimtazama vizuri kama mtu anaye mchunguza.

“Godlisen”

Eddazaria alizungumza kwa sauti yake halisi kabisa jambo lililo mfanya kila mtu ndani ya chumba hichi kushangaa.

“Ndio ba mdogo”

Taratibu Eddazaria akamkumbatia Gody, hadi machozi yakaanza kunilenge lenga usoni mwangu. Daktari mmoja akaichukua sindano niliyo iweka dawa, kisha kwa kunyata, akamsogelea Eddazaria na kumchoma sindano hiyo eneo la shingoni mwake jambo lililo mfanya Eddazaria kumsukuma daktari huyo, ila akajaribu kunyanyuka akajikuta akishindwa na kuanguka chini kwani dawa hiyo inafanya kazi kwa haraka sana mwili mwake. Baada ya sekunde kadhaa Eddazaria akapitiwa na usingizi mzito.

Kwa haraka nikamfwata Gody na kumkumbatia na nikaanza kumbembeleza huku nikitoka naye chumbani humu. Nikawakuta wifi na dokta wakiwa wamesimama katika mlango wa kutokea nje.

“Vipi?”

Wifi aliniuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.

“Ametulia”

“Na huyo naye vipi?”

“Gody ndio aliye mtuliza”

“Weee”

“Haki ya Mungu”

Wifi akakosa cha kuzungumza zaidi ya kuendelea kumtazama Gody usoni mwake. Nikashusha Gody chini na nikajilaza kifudifudi juu ya sofa kwani mgongo wangu unaniuma sana.

“Vipi?”

“Naomba unichue mgongo”

Nilimuomba wifi na taratibu akanisogelea, akaanza kunikanda kadha.

“Kwani umefanyaje?”

“Ohoo nilipigwa mtama huo nikaangukia mgongo mwenzio”

“Jamani huyu mtoto amekuwa mtu wa hatari sasa”

“Yaani bora nyinyo mulio kuwa nje ya chumba, laiti kama mtu angekuwemo ndani ya chumba hicho, basi sijui angefanywa nini, kwa maana hao madaktari na mijisuli suli yao, ila walipigwa mateke wakaangukia huko yaani wee acha tu”

“Mmmmm”

“Hapo hapo katikati paminye minye sana”

Nilimpa maelekezo wifi ya kuniminya katikati ya uti wa mgongo kwa maana ndipo ninapo hisi maumivu makali.

“Gody kalete ile sawa ya kuchua kule chumbani”

“Ipo wapi?”

“Kwenye dreasing table yangu”

Gody akanyanyuka na kuondoka hapa sebleni.

“Wifi”

“Mmmm”

“Hivi Gody amezaliwaje zaliwaje?”

“Kivipi?”

“Yaani amezaliwa namna gani kwa maana ninamuona ni mtoto wapekee sana, huwezi amini kwa ukali wote wa baba yake mdogo, ila amemtuliza na laiti ingekuwa sio yeye na angetoka huku nje, sipati picha sijui mungekimbilia wapi”

“Amezaliwa kama watoto wengine tu”

“Mmmmm, ila huyu mtoto ni special kwa kweli”

Gody akarudi hapa sebleni, nikamtazama kwa umakini sana, akamkabidhi wifi dawa aliyo muagiza na zoezi la kuchuliwa mgongo wangu likaendelea. Baada ya kupata nafuu kidogo nikamuomba wifi asitishe zoezi.

“Jojo tunaweza kuzungumza?”

Dotka alizungumza kwa upole huku akinitazama usoni, nikanyanyuka kwenye sofa na kukatoka sebleni hapa. Tukasimama kwenye moja ya mti mrefu aina ya muashoki ulipo ndani ya eneo hili la nyumba ya mama mkwe.

“Ehee niambie”

“Hivi kwa hali niliyo isikia tu na si kuiona kweli tunaweza kumpeleka kwa babu leo usiku”

“Mmmm, hata mimi mwenyewe nimelifikiria hilo ila nimeshindwa kupata jibu la uhakika kwa kweli. Au unaonaje ukampigia babu simu na ukamuomba aweze kuja huku”

“Kamwe babu hatoi mguu kumfwata mteja, na kama tayari amesha tupa maelekezo inabidi tuyafwate kama atakavyo la sivyo tutakuwa tumevunja masharti”

“Sasa kwa zaa zaa lile nililo liona ndani ya chumba chake kule, akituanzishia ndani ya gari hivi tutatoka salama”

“Usiongee hivyo shemeji yule ni mume wako”

“Sikatai ni mume wangu, yaani ungeshuhudia mtama nilio katwa ndani ya chumba hicho wala usinge kuwa unazungumza mambo hayo, nyinyi wenyewe munakimbia, je kwa mfano sasa hali yake hiyo inaanza akiwa ndani ya gari tunafanyaje na ikiwa babu kule anatutaka tumepeleke sisi wawili tu”

Dokta akashusha pumzi taratibu huku akionekana akitafakari ni nini cha kuzungumza ambacho ndio tunatakiwa kukifanya kama kitakuwa ni kizuri.

“Imekuwaje akatulia?”

“Amechomwa sindano ya usingizi”

“Itakaa kwa muda gani?”

“Sijajua mimi labda uwaulize wale madakari wake.”

“Tukiwauliza wanaweza kustukia ikawa shida kidogo, kwa maana hii familia mama yao anaamini sana kwenye swala la maombi, sasa endapo itatokea wakafahamu, mipango yetu yote inaweza kwenda mrama”

“Hilo mimi nitalisimamia, huyu ni mume wangu, nina umia zaidi ya wao wanavyo nichukulia, ninampenda sana na sipo tayari kumuona akiwa anateseka yote ni kwa ajili yangu”

“Sawa, ila tutamtoa toa vipi, ikiwa muda tunao takiwa kuianza safari ni saa nne usiku”

“Hapo ndipo kwenye mtihani”

Tukaka kimya huku kila mtu akitafakari jambo la kufanya.

“Nina wazo japo sio zuri ni la hatari kidogo”

Dokta alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Zungumza”

“Inabidi uandae juisi, juisi ambazo utaweka dawa ya usingizi, ambayo itawalaza watu kama masaa manne hivi hadi kuzinduka kwao, naamini ndani ya muda huo tutakuwa tumemaliza kukamilisha kazi yetu.”

“Mmmmmm”

“Yaa hiyo ndio njia rahisi ya sisi kufanya, hakuna njia nyingine la sivyo tutashindwa, kwa mfano hao madokta wasipo lala, hao walinzi wasipo lala tutamtoa toa vipi humu ndani”

“Hiyo dawa ya usingizi tutaipatia wapi?”

“Inabidi nirudi hospitali, nikachukue vidonge vya usingizi kisha nirudi huku”

“Sasa fanya jambo moja, ukienda huko mjini, urudi na matunda mengi, ukija hapa unichague mimi kama nitengeneze juisi, hiyo ndio itakuwa ni game ya kumtoa tukifeli ndio basi tena”

“Pao ngoja nikaage huko ndani”

Dokta akaingia ndani na baada ya muda akaoka.

“Hakikisha kwamba hili swala hatumuambii mtu wa aina yoyote”

“Poa”

Dokta akaingia ndani ya gari lake, nikamfungulia geti na akaondoka, baada ya kufunga geti, nikaingia ndani ya gari la Clara, nikaanza kulikagua kwa maana toka nilipo lichukua sikuweza kuligagua. Kwa bahati nzuri nikakuta flash ndogo sana ambayo kwa haraka haraka ukiiazama unaweza kuhisi ni pambo tu la kawaida linalo kaa ndani ya gari. Nikachukua pesa kadhaa nilizo ziacha ndani ya gari hili na kuingiza nazo ndani. Nikaelekea chumbani kwangu na kumkuta Judy na watoto.

“Hivi mara ya mwisho kumshika mwanao ilikuwa ni lini?”

Judy aliniuliza swali lililo nifanya nimtazame kwa muda kidogo kisha nikamsogelea na kukaa kitandani alipo.

“Jojo huyu ni mwanao anahitaji mapenzi yako, sio kuingia toka, toka ingia. Muda mwengine anatamani anyonye ila kwa harakati zako anashindwa”

“Ila mdogo wangu wewe mwenyewe unaona hali halisi ya mambo, laiti kama tusinge kuwa na heka heka si ningekuwa ninamshika vizuri”

“Akiamka mnyonyeshe, kwa maana ana hamu na ziwa lako”

“Sawa”

Taratibu nikanyanyuka kitandani.

“Nguo zimekutosha?”

“Ndio, asante”

“Kuna hii pesa itunze, ukiwana haja ya mahitaji ya hapa na pele utatumia”

“Sawa”

Nikatoka na kuelekea jikoni, nikamkuta wifi akiendelea kupika.

“Wifi una laptop?”

“Ndio”

“Naomba uniazime”

“Ingia chumbani kwa mama, kwenye droo lake ndipo nilipo iweka”

Nikatoka humu jikoni na kuingia chumbani kwa mama mkwe, nikachukua laptop ya wifi, nikaiwasha kishan ikaichomeka flash hii. Nikaanza kukagua faili moja lenye mizikia minne, nikaufungua mziki wa kwanza, nilicho kisikia kikanifanya nikae vizuri ili niweze kusikiliza vizuri kwani sio mziki na yanaonyesha ni mazungumzo ya siri sana kati ya dokta Clara na mwanamke ambaye simfahamu na kitu kinacho nifanya nisikilize vizuri ni baada ya kusikia jina la mume wangu likitajwa.


“Kulipa kisasa kwa Eddy kwa kutumia nguvu za kawaida ni ngumu wifi yangu.”

Niliisikia sauti ya Clara ikizungumza vizuri.

“Najua ni njia gani ambayo ninaweza kumkomesha yeye na yule malaye wake. Hawezi kunichukulia mume wangu na mimi nikaka kimya”

Sauti hii ya mwanamke wa pili ikazidi kunishtua na kujikuta nikijitahidi sana kujaribu kufikiria ni mwanamke gani anaye lalama kwamba nimemchukulia mume wake.

“Ni njia gani?”

“Mimi ni mpare, nitajua njia ya kuwakomesha. Wewe hakikisha kwamba kampuni inakuwa mikononi mwako”

“Itawezekeana kweli?”

“Kwa nini isiwezekane, ila kumbuka ukisha fanikiwa kuichukua kampuni, mwanangu ndio anatakiwa kuwa hisa asilimi sabini”

“Ilo nimekuelewa wifi yangu, ila vipi Gody anaendeleaje?”

“Ahaa anaendelea vizuri tu amesha anasoma vizuri”

“Ila best inaonyesha India pamekupenda ehee?”

“Yaa mapenipenda kiasi fulani, kule ni tofauti na huku. Ila Mungu anawapenda hao mabesti zako”

“Kwa nini?”

“Kuna siku walipo kuwa wapo India, nilituma vijana wawae, ila sikui ikawaje wakafanikiwa kutoroka na kurudi Tanzania yaani ilikuwa imebaki kidogo tu niwaue”

Nikajikuta machozi yakinilenga lenga kwa hasira, kwani lile tukio la uvamizi tulilo tokea tukuta kule nchini India limepangwa na mama Godlove. Kumbe njama ya Clara kutusaliti na kuchukua kampuni aliitoa kutoka kwa mama Godlove. Nikajikuta nikichomo flash hii, nikazima laptop na kuirudisha sehemu nilipo itoa.

Nikatoka chumbani humu huku nikiwa nimejawa na hasira ambayo natamani hata nikutane na mama Godlove ili nimfunze adamu. Kuna mambo mengine akili yangu na mawazo yangu yote yalimsukumia Nuru lawama kwamba yeye ndio chanzo cha matatizo ya tukio lile lililo tokea nchini India, kumbe ni mjinga mmoja.

“Hei mbona umekasirika?”

Mlinzi ambaye nilikwenda naye mjini aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nipo sawa”

“Kwa muda mfupi ambao nimekuwa nawe nimekweza kukufahamu, vizuri”

“Nipo sawa”

Nilizungumza huku nikiingia chumbani kwa wifi. Sikumkuta wifi zaidi ya Judy akiwa amelala na watoto, nikatoka chumbani humu na kuingia jikoni, nikamkuta wifi nikatamani kumueleza juu ya mazungumzo niliyo yasikia, ila nilivyo kumbuka kwamba Clara ameuwawa, ikanibidi ninyamaze na kama kumtafuta mama Godlove nitamtafuta kimya kimya mimi mwenyewe, kumbe alikuwa akinipiga kwa kisirisiri.

“Vipi leo huli chakula?”

“Nitakula”

“Fanya ule basi”

“Sawa wifi”

Dokta akaingia jikoni humu huku akiwa ameshika mfuko mkubwa, ulio jaa matunda mengi sana.

“Shem tengeneza basi juisi”

“Mwenzio hajakula, muache kwanza ale ndio atengeneze”

“Nitatengeneza tu wifi, nikimaliza ndio nitakula”

“Na huo mgongo haukuumi?”

“Usijali wifi”

“Haya”

Dokta akanikonyeza kisiri pasipo wifi kuweza kuona chochote, akatangulia kutoka nje huku kwa ishara akinionyesha kwamba tuonane nje. Sikutaka kutoka muda huu kuepeuka kustukiwa. Nikaiingiza flast hii kwenye kimfuko cha suruali yangu, ambapo sio rahisi kwa flash hii kuweza kupotea, kwani ina mambo ambayo ninaa amini kwamba yananitasidia katika kuhakikisha kwamba ninamkamata.

“Mimi nimesha maliza kupika mida ya saa mbili watengee watu chuakula. Nataka niende mjini mara moja”

“Saa hivi saa ngapi?”

“Saa kumi na mbili”

“Ahaa, sawa”

Wifi akatoka jikoni humu, nikaanza kutengeneza juisi hii ya matunda. Sikuchukua muda mrefu nikamaliza. Nikatenganisha juisi hizi katika makundi mawili, kundi la kwanza ipo kwenye jagi na ndio nimeidhamiria kuiweka dawa za kuwalevya. Kundi la pili ni juisi ambayo nita ihifadhi ndani ndani ya friji na itatumika kwa siku nyingine. Nikatoka nje na kumkuta dokta akiwa ananisubiria.

“Saga hivi vidonge viwili na unga unga uweke ndani ya hiyo juisi, na baada ya dakika kama kumi na tano hivi watapitiwa na usingizi.

“Sawa”

“Mimi ninakwenda kwangu kubadilisha nguo kisha nitakuja hapa mida ya saa mbili usiku”

“Poa”

Dokta akaingia kwenye gari lake na kuondoka, nikarudi jikoni, nikavisaha vidonge hivyo kwa kutumia chupa kisha nikanyunyizia vyote kwenye juisi iliyomo kwenye jagi kisha nikaliweka kwenye friji. Nikapishana na wifi kwenye kordo akiwa amevalia vizuri, akaniaga na kuondoka, na mimi nikaingia chumbani. Nikaoga kwa mara nyingie kisha nikapanda kitandani japo kujipumzisha kidogo. Usingingizi mzito sana ukanipitia na kulala fofofo.

Sauti ya mwanangu kulia ikanistua, taratibu nikafumbua macho yangu na kutazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaka kitako kitandani, nikambeba na nikaanza kumnyonyesha taratibu. Judy akaingia huku akiwa ameshika sahani ya chakula pamoja na glasi ya juisi.

“Umeamka?”

“Yaa hiyo juisi umeichukua kwenye nini?”

“Kidungu”

“Ahaaa, watu wengine je umesha watengea chakula?”

“Yaa kila mtu nimempa na dokta naye yupo hapo sebleni”

“Juisi umewapa?”

“Ndio, si ile ya kwenye jagi”

“Ndio, Gody yupo wapi?”

“Amesha kula na kulala”

“Sawa”

Nikamaliza kumnyonyesha mwanangu, nikafungua kabati na kuchukua suruali moja niliyo inunua pamoja na tisheti, nikavivaa, kisha nikatoka ndani humu. Nikaelekea sebleni na kumkuta dokta akiwatazama walinzi pamoja na madaktari wa mama wakiwa wanasinzia sinzia. Dokata akasimama katika sehemu alipo kaa na kunifwata sehemu nilipo simama.

“Naona dawa imeanza kufanya kazi”

“Yaa, ila wifi ametoka inakuwaje?”

“Amekwenda wapi?”

“Sijajua ila ameniambia kwamba mida ya saa mbili hii ndio atarudi”

“Mmmm sasa hiyo inaweza ikawa tatizo”

“Tunafanyaje sasa?”

Tulizungumza kwa sauti ya chini kabisa ambayo sio rahisi kwa mtu aliye kaa karibu kuweza kusikia.

“Ngoja nimpigie simu”

Dokta alizungumza huku akitoa simu mfukoni mwake. Akaiweka sikioni mwake kwa muda kisha akaanza kuzungumza.

“Ehee dada ake niambie?”

“Upo pande gani?”

“Okay poa”

Dokta akakata simu huku usoni mwake akiwa amejawa na furaha kidogo.

“Anasema atachelewa kurudi, sasa huu ndio muda tunao takiwa kuondoka na Eddy”

“Sawa, sasa ngoja nimpe maagizo mdogo wangu”

“Ina maana mdogo wako hajanywa juisi yenye dawa”

“Wewe huyo ni mdogo wangu na sitaki audhurike na madawa yako”

Nilizungumza maneno hayo kisha nikaingia chumbani na kumkutea Judy akiendelea kula.

“Judy”

“Bee”

“Tunahitaji kutoka hapa na shemeji yako”

“Shemeji yangu, nani?”

“Eddy”

“Eddy…..!!! Unatoka unakwenda naye wapi?”

“Kuna hospitali ninampeleka akapatiwe mataibabu”

“Wee Jojo, hembu acha hatari si unaijua hali halisi ya mumeo wewe?”

“Nalijua hilo, ila nakuomba uweze kuitunza hii siri, sitaki wifi aweze kuifahamu sawa”

“Sasa asiifahamu vipi ikiwa hapo kuna hao walinzi na madaktari wake wamekaa”

“Njoo uone”

Tulatoka na Judy hadi sebleni na akawashuhudia walinzi wa mama pamoja na madaktari wa mume wangu wakiwa wamelala usingizi fofofo.

“Umewafanyaje?”

“Usinywe ile juisi ya kwenye jagi mume ila dawa ya usingizi”

“Weee”

“Ndio hivyo. Sisi tunaondoka na dokta pamoja na Eddy”

“Wifi akija nitamueleza nini?”

“Hili lisikusumbue wewe fanya kama hujui ni kitu gania mbacho kinaendelea”

“Mmmmm”

“Yaa fanya kama hujui kinacho endelea”

“Sawa”

Baada ya makubaliano yangu mimi na Judy, tukaingia katika chumba alicho lazwa Eddazaria mimi na dokta. Kwa pamoja tukasaidiana kumbeba akiwa amelala usingizi fofofo, Judy akatusaidia kufungua mlango wa siti ya nyuma wa gari la dokta. Tukamlaza vizuri, kisha nami nikaa siti ya nyuma ili hata kama kuna tatizo basi niwe wa kwanza kuliona. Judy akazunguka upande ambao nipo, taratibu nikafungua kioo na kumtaza.

“Dada kuwa makini, hapa nilipo mwenzio mapigo yangu yote ya moyo yananienda mbio”

“Usijali kikubwa funga milango, tutawahi kurudi”

“Sasa nani atawafungulia”

“Dokta wakati wa kurudi nani atatufungulia?”

“Una simu?”

“Hapana”

“Chukua haka kasimu kangu kadogo huwa hakapigiwi na watu, so nikirudi nitakupigia utufungulie geti sawa”

“Sawa”

Judy akaichukua simu hiyo ndogo ya dokta, taratibu tukatoka eneo la nyumba hii na tukaianza safari ya kuelekea kwa babu ambaye kwa namna moja ama nyingine nimeyaweka matumaini yangu kwake na nina amani kwamba kupitia yeye ni lazima mume wangu atapona. Njia nzima ninamuomba Mungu mume wangu asiamke hadi tunafika kwa maana akiamka, timbwili timbwili lake sipatii picha itakuwaje.

“Shitiiii”

Dokta alizungumza huku akipiga mskani wake kwa kiganja cha mkono wake wa kulia.

“Vipi?”

“Wifi yako tumepishana naye hapo anarudi nyumbani”

Ikanibidi kugeuka nyuma na kutazama na kweli nikaliona gari la wifi likimalizikia kushuka kilima kidogo.

“Mungu wangu si atakwenda kuona ile hali kule”

“Ndio maana yake”

“Sasa dokta tuna fanyaje”

“Twende tu ndio saa nne hii”

Dokta alizungumza hukua kiongeza mwendo kasi wa gari lake. Tukiwa njiani simu ya dokta ikaanza kuita, akaitazama kwa muda kisha akanionyesha simu hiyo inatoka kwa nani. Nikazidi kujawa na wasiwasi mara baada ya kuona ni simu ambayo inatoka kwa wifi.

“Mpokeleee sasa”

“Nitamuambia nini?”

“Ni bora kumpokelea kuliko kukaa hivyo kimya.”

“Mpokelee wewe basi”

“Ili iweje sasa ikiwa simu ni yako na wewe ndio amekupigia”

Dokta akapokea simu yake hiyo na kuweka loud speaker.

“Ndio dada ake”

“Upo bado nyumbani?”

Dokta akanigeukia na kunitazama kwani swali hilo limekaa kimitego, nikamtingisha kichwa nikimuashiria kwamba ajibu kwamba yupo nyumbani.

“Ndio”

“Naomba niongee na Judy”

“Judy amelala”

“Jojo je?”

“Huyu hapa”

Dokta akanipatia simu yake nikaitoa loud speaker na nikaiweka sikoni.

“Ndio wifi”

“Sasa sikia, leo sinto rudi nyumbani, nipo huku kwa mume wangu. Hakikisha kwamba munamuamsha Gody asubuhi na mapema na anawahi shule kwa maana school bus litampitia hapo”

“Sawa sawa”

“Hao wanaume mutawaonyesha vyumba vya kulala, mimi nitakuja kesho saa nne”

“Sawa wifi”

Simu ikakata jambo lililo nifaya nishagae kwa maana gari lake mwenyewe nimelishuhudia tukipishana nalo, kwamba anarudi nyumbani kwa mama.

“Inaonyesha tuliye pishana naye pale sio wifi”

“Kwa nini?”

“Amenipa maagizi na anadai kwamba hatorudi nyumbani leo”

“Au nimeona vibaya?”

“Sio vibaya ndio gari lake”

“Labada atakuwa mume wake”

Nikaikuta nikistuka galfa mara baada ya Eddazaria kunyanyua kichwa chake kwenye mapaja yangu na kukaa kitako kisha akanigeukia na kunitazama usoni mwangu kwa macho makali sana jambo lililo mstua hata dokta mwenyewe na kumfanya aanzae kuyumbisha gari jambo linalo weza kusababisha gari kupinduka.



“Endesha gari vizuri dokta”

Eddazaria alizungumza kwa sauti ya upole ambayo hakuna kati yetu ambaye aliweza kuamini kwamba anaweza kuzungumza hivyo. Dokta akafunga breki za gafla na kulifanya gari hili kusimama.

“Endelea kuendesha”

Eddazaria alizungumza kisha akajilaza tena kwenye mapaja yangu. Kwa upande wangu mapigo ya moyo yananienda kasi kiasi cha kunifanya nihisi joto kali sana. Dokta akageuka nyuma na kumtazama Eddazaria kwa muda kigo kana kwamba mtu ambaye haamini alicho kiona na kukisikia.

“Hivi ni yeye au?”

“Ndio ni yeye?”

“Amelala?”

Nikamchungulia Eddazaria usoni mwake, nikamjibu dokta kwa kutingisha kichwa kwa maana amelala kweli. Taratibu akawasga gari na tukaendelea na safari, haikuchukua muda mrefu sana tukafanikiwa kufika kwa babu yake. Tukawakuta vijana wawili walio valia kaniki nyeusi wakiwa wanatusubiria, tukataka mushusha Eddazaria kwenye gari ila wakatukataza, wakaniomba nishuke kwenye siti ya nyuma, nikatii amri, wakaanza kumpaka paka Eddazaria mafuta ambayo kwa upande wangu hayanukii vizuri, kwa maana yana harufu ya kuvunda.

“Rudini mulipo toka”

Kijana mmoja alizungumza huku wakiwa tayari wamesha mshusha Eddazaria na mmoja amebeba miguu huku mwengine akiwa ameshika mikono.

“Hatuwezi kumuona babu?”

Dokta aliuliza huku akiwatazama vijana hawa ambao kwa muda wa mchana ambao tulikuja hapa hatukuweza kuwaona.

“Ndio”

“Turudi lini sasa?”

“Babu atakuambia”

Dokta akanitazama usoni mwangu, kwa ishara ya macho akaniomba niingie ndani ya gari. Nikatii, akawasindikiza vijana hao walio mbeba Eddazaria na kuingia naye kwenye nyumba ya babu. Dokta akatembea hadi kwenye usawa wa minazi, akafua viatu kisha akapiga magoti chini, na akainama chini kidogo na paji lake la uso likaigusa ardhi yake. Akaka kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyua uso wake, taratibu akaanza kutembea kuelekea katika nyumba ya baba, kutokana na mwanga wa mbalamwezi, ninamuona dokta vizuri sana. Mlango wa nyumba hiyo ukafunguka na dokta akaingia ndani na eneo hili nikabaki peke yangu. Nilicho kifanya ni kufunga milango kwa ndani ili hata kama kuna tatizo lolote basi lisiweze kunidhuru.

Nikiwa katika hali ya mawazo machanganyiko, juu ya mume wangu na mama Godlove, nikaona mapaka kama kumi na mbili wakisimama kwenye uwanja wa mbele ya nyuma ya babu na wala sikuelewa mapaka hao wametokea wapi. Taratibu mapaka hao wakatengeneza kama duara, mmoja wao akaka katikati ya duara hilo. Hali hii ikazidi kunishangaza sana mara baada ya kuona mapaka hao wakizunguka duara hilo huku wakitoa milio ya ajabu ambayo japo nipo ndani ya gari hili na nimefunga kila kitu, ila ninaishikia vizuri kana kwamba nimekaa nao jirani kabisa.

Moyo ukazidi kunienda kasi mara baada ya kuanza kumuona paka aliye kaa katikati ya duara hilo akibadilika kuwa binadamu kabisa. Haja ndogo ikanikamata, tumbo la haja kubwa nalo likanikamata kisawa sawa, kitu kilicho nifanya nizidi kuchanganyikiwa zaidi ni baada ya pama mmoja baada ya mwengine kubadilika na kuwa binadamu.

‘Ohoo Mungu wangu’

Nilizungumza huku nikiilaza siti yangu taratibu kwani kusema kweli hali inatisha na kunishangaza kwa kweli. Binadamu hao ambao kwa namna mmoja ni wachawi, wakaendelea kumzuguka mzee huyo aliye kaa katikati ya duara huku mzee huyo akiwa na asili ya kihidi. Mzee huo anaye zungukwa ameshika kitu kama filimbi ambazo nakumbuka nilisha wahi kuziona nikiwa mdogo sana, na mama yangu alikuwa akininunulia kwa ajili ya kucheze, japo filimbi alizo kuwa akininunulia zilikuwa za plastiki. Mzee huyo akaendelea kuipiga filimbi hiyo ndefu yenye matundu tofati tofauti. Galfa nyoka mkubwa mwenye vichwa saba akatoka katikati ya kundi hilo, jambo lililo wafanya watu hao kuendelea kumzunguka mzee huyo huku wakipiga makofi kana kwamba kuna wimbo wao mzuri ambao wanauimba ambao haueleweki maneno yake.

Japo ni mambo ya kutisha ambayo kwenye maisha ya kawaida ya kibinadamu ni adimu sana kukumbana nayo, ila nikazidi kujipa ujasiri huku nikiwa nimejificha kwenye gari hili huku nikiendelea kushuhudia mambo ya kidunia ambayo siku zote nilikuwa nikiamini kwamba ni uongo. Joka hilo lilaanza kujikunja kunja huku likielekea kwenye mlango wa nyuma ya babu. Haja ndogo ikanizidi kwani ndani humo yupo mume wangu kipenzi. Gafla nikastukia joka hilo likitawanyika vipande vipande kama vile limelipuliwa na bomu. Wachawi wote wakaonekana kustushwa sana na tukio hilo. Mzee huyo aliye kuwa amekaa katikati yao, akasimama huku akionyesha dhairi kwamba amekasirika. Akapiga hatua kuelekea kwenye mlango huo, ila nikastukia kumuona akipaishwa juu kwa futi kadhaa kisha akapigizwa chini na kudunda mara nne mfululizo mithili ya kitenesi kinavyo pigwa chini. Wachawi wengine walipo ona hali imekuwa mbaya kwa mkuu wao wakajaribu kukimbia ila hapakuwa na hata mmoja wao aliye weza kutoka katika eneo la usawa wa nyumba hiyo.

Nikawaona vijana wale wa badu wakitoka huku kila mmoja akiwa ameshika pembe la ng’ombe, wakawavuta wachawi hao kwa nguvu wanazo zijua wao wenyewe kisha wakapagisha magoti tena kwenye mstari ulio nyooka huku mikono yao wakiwa waminyoosha juu, adhabu kama hiyo kipindi tulipo kuwa shule tulikuwa tukiita ni kuita mvua. Nikamuona dokta akitoka ndani humo, akatembea kwa haraka hadi vilipo viatu vyake akavaa na kurudi kwenye gari. Akaminya rimoti ya gari lake na loki za milago ikafunguka, akafungua mlango na kuingia ndani, akanitazama kwa muda kusema kweli woga wanga sikuweza kusita kuuficha, kwani kwenye maisha yangu sijawahi kuonana na vitu vya ajabu kama hivi. Dokta akawasha gari na tukaondoka katika eneo hili pasipo yeye kuzungumza kitu cha ina yoyote.

“Umeona chochote?”

Dokta aliniuliza huku akizidi kuongeza mwendo kasi wa gari. Nikamjibu ndio kwa kutingisha kichwa.

“Iwe siri yako na usimuambie mtu wa ina yoyote hata mdogo wako hakikisha kwamba hili jambo halifahamu”

“Sawa”

Tukazidi kusonga mbele ila uvumilivu ukanishinda wa kukaa na swali langu moyoni.

“Wale ni kina nani?”

“Watu ambao walikuwa wamekuja kwa mara ya mwisho kumamalizia mume wako”

“Wametoka wapi au wametumwa na nani?”

“Mke mwenzio”

Hapa ndipo nikapata uhakika kwamba ile mipango niliyo isikia waliyo kuwa wakiizungumza mama dokta Clara na mama Godlve kumbe ni kweli.

“Sasa dokta kwa nini ameamua kufanya vile?”

“Kwenye mahusiano yoyote ya wanawake wa Kitanzania baadhi wakigundua kwamba wameacha kwa ajili ya mwanamke mwengine, au waume zao wana unaume wengine basi huu ndio ujinga wanao ufanya na una bahati sana kwa maana mume wako ana nguvu ya asili laiti kama ingekuwa sio hiyo nguvu, siku nyingi tungekuwa tumesha kula ubweche”

“Ila atapona?”

“Ndio atapona”

“Hali yake haijatokana labda na kupigwa au kuchomwa sindano yoyote ambayo inaweza kumfanya kuwa katika hali kama hiyo?”

“Hakuna kitu kama hicho, naamini umejionea wewe mwenyewe”

“Ndio”

“Ndio hivyo nyinyi wanawake muda mwengine akili zenu huwa sijui munafikiria nini, sasa kama angemuua angefaidika na nini, ikiwa hapo awali alisha mtia jamaa hasara kibao ikiwa kumuunguzia nyumba, ila jamaa akasamehe, akaondoka na mtoto, jamaa akasamehe akiamini kwamba mwanaye ni mwanaye na ipo siku tu atarudi kwake. Mtu hajaona havijatosha anataka kumuu”

Dokta alizungumza kwa uchungu sana huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Laiti ningekuwa ni mimi haki ya Mungu, mwanamke huyo ningemgeuza mishikaki ile ya sh mia mia”

Dokta aliendelea kuzungumza kwa kufoka.

“Babu amesemaje?”

“Amesema tukae mwenzi mzima ndio turudi huku”

“Mwezi mzima?”

“Ndio maana yake”

“Mbona mkubwa sana, mama na nduguze si watamtafua”

“Hiyo haijalishi ila kikubwa hivi sasa ukaendelee na maisha mengine na wala usimfikirie kabisa mumeoa hadi huo mwenzi wa matibabu uweze kuisha”

“Hiyo itakuwa nguvu dokta”

“Ngumu nini sasa? Fwata kile ulicho ambiwa na babu alifanya makusudi kukuonyesha upuuzi wa binadamu ulio fanywa kwa mume sasa, wewe kausha hivyo hivyo sijui hisia za kimapenzi, wewe weka kando sawa”

Dokta alizungmza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Sikutaka kufanya ubishi wa aina yoyote zaidi ya kukaaa kimya. Tukafika nyumbani, taratibu dokta akasimamisha gari getini, akatoa simu anayo itumia na kumpigia Judy na kumuomba aje kufungua geti kisha akakata simu.

“Judy akikuuliza wewe muambie kwamba mume wako yupo hospitalini au hata mtu yoyote akikuuliza muambie kwamba Eddy yupo hospitalini, wakihitaji maelezo zaidi basi waelekeze kwangu”

“Sawa sawa”

“Mimi inabidi usiku huu nirudi kwangu, wewe ingia ndani”

Dokta alizungumza mara baada ya kumuona Judy akifungua geti kubwa

“Samahani mara moja dokta”

“Mmmmm”

“Nashukuru kwa msaada wako, sina cha kukulipa, ila ninashukuru sana”

“Usijali, maisha ni kusaidiana na Eddy kwa sasa ni ndugu yangu ni mwaka wa ishiri na kitu tunafahamiana kwa hiyo ni jambo letu sote”

“Asante kwa hilo”

“Sawa, wewe ingia ndani na ulale sasa na wala usiwe na mawazo yoyote”

“Nashukuru”

Nikamtazama dokta kwa muda kidogo kisha nikamkumbatia, nikashuka kwenye gari lake, na kuanza kutembea kuelekea getini.

“Mbona dokta aingii?”

Judy aliniuliza mara baada ya kumuona dokta akigeuza gari lake.

“Anawahi hospitalini tulipo mpeleka Eddazaria”

Dokta akapiga honi ikiwa ishara ya kutuaga kisha akaondoka kwa kasi. Judy akafunga geti na sote tukaingia ndani, sahani zote za chakula za walinzi na madaktari hawa nikakuta zikiwa hazipo.

“Nilizitoa sahani pamoja na juisi zao”

“Ahaa, waliamka?”

“Hapana”

Tukaelekea chumbani.

“Mwenzio ile juisi nimeimwaga na kusafisha kila kitu hadi glasi za hao jamaa ili kufuta ushahidi”

“Kazi nzuri”

Nilizungumza kivivu huku nikivua viatu nilivyo vaa, nikavua na nguo zangu kisha nikaingia bafuni. Kusema kweli mapicha picha ya ajabu ambayo nimetoka kuyaona bado hayajafutika kichwani kwangu na kila ninayo yawaza ninajikuta nikiwa nimejawa na woga mwingi sana hadi mwili wangu wote una nitetemeka. Kwa mawazo mengi sana, nikajikuta nikikaa bafuni humu kwa muda mrefu hadi Judya akafungua mlango na kuchungulia.

“Vipi upo salama dada?”

“Yaa nipo salama”

“Mbona huogi na wala sisikii maji kumwagika?”

“Nitaoga wee nenda tu kalale”

“Hembu niambie huko ulipo toka ni kwema, kwa maana unaonyesha kuna jambo ambalo sio zuri umekumbana nalo”

Judy alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu. Nikayafumba macho yangu kwa sekunde kadhaa, nikashuhudia jinsi hali ya wale wachawi vitu walivyo kuwa akivifanya kutoka hatika hali ya upaka hadi ubinadamu.

“Jojo”

Kitendo cha Judy kuniita huku akinigusa mwilini mwangu, kikanistua sana hadi nikajikuta nikihisi kuanguka.

“Mbona umestuka?”

“Nakuomba uniache peke yangu kwa muda huu, kuna mambo nahitaji kutafakari”

“Jojo, mimi ni mdogo wako, ninakuomba basi unishirikishe”

“Tafadhali mdogo wangu nikikuomba kitu basi ninakuomba uweze kuelewa ni nini ambacho ninahitaji, nenda tu kalale mdogo wangu. Kesho kukipambazuka basi tutazunguma.”

Nilizungumza kwa sauti ya chini sana na iliyo jaa upole wa hali ya juu. Judy akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatoka bafuni humu, nikaanza kuoga taaratibu, nikamaliza na kutoka bafuni humu, nikatafuta taulo na nikajifuta maji taratibu, kisha nikapanda kitandani na nikalala upande wa mwanzo wa kitanda huku Judy akiwa amelala upande wa ukutani na mwanangu tumemlaza katikati ya kianda. Nikamtazama mwanangu jinsi alivyo lala, nikajikuta nikimwagika na machozi usoni mwangu kwani amezaliwa kwenye familia yenye migororo ya kila aina.

“Nisamehe mwanangu, mama anakosa muda wa kukuangalia, mama anakosa muda wa kukulinda kama mwanaye, nisamehe sana mwanangu”

Nilizungumza huku nikiangua kilio cha chini chini, kwani maumivu ninayo sababishiwa na walimwengu kusema kweli yananiumiza sana.

“Ila nakuahidi mwanangu, nitamtamtafuta yule aliye msababishia baba matatizo na nitamchukulia hatua ikiwezekana ni lazima nimuue”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikikunja ngumi katika mkono wangu wa kulia, na taratibu Judy akanigeukia na kunitazama kwa macho yaliyo jaa huruma, kisha kwa kutumia kiganja cha mkono wake wa kulia akaanza kunipangusa machozi usoni mwangu taatibu.



“Jojo dada yangu, ikfike kipindi tusamehe tuwasamehe wale wote walio tukosea kwenye maisha yetu”

Judy alizungumza kwa suati ya upole huku akiendelea kunipangusa machozi usoni mwangu.

“Mmmm, kusamehe, hapana mdogo wangu. Njia ya kulipiza kisasa ndio njia sahihi, ni bora wao au mimi nife hapo nitakuwa nina amani, siwezi kuenedea kuwasamehe watu wasio taka kusamehewa.”

Niliendelea kuzungumza kwa uchugu ulio changanyika na hasira kali sana. Judy hakusita kunipatia maneno ya faraja hadi nikajikuta nikipitiwa na usingizi na kulala fofofo.

***

Asubuhi tafrani ikazuka kwa kila mtu akimtafuta Eddazaria alipo. Walinzi na madaktari kila mmoja akaonekeana kuchanganyikiwa. Ili nisigundulike kwa chochote na mimi nikajifanya kuchanganyikiwa kwa kupotea kwa mume wangu.

“Jamani mume wangu yupo wapiiii?”

Niliuliza huku machozi yakinafki yakinimwagika usoni mwangu. Swai langu likakosa majibu kwa walinzi na madaktari.

“Namtaka mume wangu, nasema namtaka mume wangu”

Nilizungumza huku nikimtingisha mmoja wa madaktari. Walinzi hawa wakatoka nje kwenda kumtafuta huku kila mmoja akiamini kwamba mume wangu ametoka nje yeye mwenyewe. Wifi na mume wake nao wakafika na kukuta tafrani hii.

“Amepote?”

Mume wa wifi aliuliza kwa mshangao mkubwa sana

“Ndio”

Alijibu daktari.

“Ilikuwaje kuwaje?”

“Yani sote hatuelewi”

“Jamani na hali yake ile akionekana huko mtaani si aibu jamani?”

Wifi alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa wasiwasi mwingi sana.

“Ngoja nimpigie Bony waanzishe msako wa kumtafuta”

Shemeji alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni na kusogea pembeni.

“Gody naye yupo wapi?”

Wifi aliniuliza huku akinitazama kwa macho makali.

“Gody alikuja kuchukuliwa na gari la shule asubuhi”

Judy aliwahi kujibu swali hilo na kunifanya nishushe pumzi taratibu.

“Afadhali”

Wifi aliendelea kujibu kwa unyonge mwingi sana. Kila mtu waziwasi mwingi ukazidi kumtawala, pasipo mimi tu na Judy kwa maana ndio titafahamu ukweli wa mambo.

“Ngoja nimpigie dokta, naye asaidie kumtafuta huko mitaani”

Wifi naye alizungumza huku akitoa simu yake kwenye pochi. Akaiminya minya juu ya screan hiyo ya simu kisha akaiweka sikioni mwake.

“Wewe mwenzio amepotea?”

“Ndio watu wameamka asubuhi hatumuni”

“Nisaidie kumtafuta huko na jaribu kuwasiiana na madakari wezako huko kwenye mahospitali yao, laiti wakimuona waweze kutusaidia”

“Sawa”

Wifi akakata simu, sauti ya mwanangu kulia ikanifanya nielekee chumbani. Nikamkuta mwanagu akiwa amejikojolea. Ikanibidi nimbadilishe pampers aliyo ivaa, nikamsafisha vizuri mwili wake, kisha nikamvalisha pampers nyingine pamoja na nguo zake nyepesi kwa maana huku Tanga kuna joto kali sana. Nikamnyonyesha kwa dakika kama kumi na tano hivi kisha nikambeba na kutoka naye chumbani humu.

“Vipi?”

Nilimuuliza Judy mara baada ya kumkuta sebleni peke yake.

“Hakuna aliye fahamu”

Judy alinijibu kwa sauti ya chini na ya kunong’oneza.

“Poa endelea kukausha hivyo hivyo”

“Sawa”

Nikatoka nje waliopo watu wengine.

“Wifi vipi, ripoti isha tolewa polisi?”

“Ndio, hapa nahisi msako wa kumtafuta utaanza hivi karibu, tunataka kumtangaza kwenye mitando ya kijamii”

“Hapana wifi tusimtangaze bwana”

“Kwa nini?”

“Kumbuka ni situation gani ambayo tunaipitia, kumbuka mama yupo mikononi mwa nani. Sasa likija swala la kumtafuta mume wangu tena kwa kuwatangazia watu kwenye mitando ya kijamii inaweza kulete tafrani na inaweza kupelekea maadui zetu kuhakikisha kwamba wanamkamata na watatushinikiza kuutoa ushahidi tulio nao. Unahisi mama tutampata?”

Nilizungumza kwa msisitozo na kumfanya wifi kukaa kimya kwa muda huku akionekana kutafakari jambo hili.

“Kweli”

“Yaa tukumbuke kwamba kuna mama, hadi sasa hivi hatujui tunaanzia kumpatia wapi”

“Ngoja nimuambie Rich kwa maana yeye ndio aliye toa wazo hili”

Wifi akamsogelea mume wake aliye simama na walinzi pamoja na madaktari akizungumza nao. Akamvuta pembeni na wakaanza kuzungumza taratibu. Judy akanifwata na kusimama pembeni yangu.

“Dokta anahitaji kuzungumza na wewe”

Nikamtazama Judy kwa muda.

“Muambie baadae sasa hivi siwezi kuzungmza naye”

“Sawa”

Judy akaingia ndani, wifi akanifwata na kusimama mbele yangu.

“Ameelewa na amasitisha zoezi, cha kufanya hivi sasa ni kuhakikisha kwamba anatafutwa kila sehemu”

“Sawa”

“Sisi ngoja tuelekee mjini kumtafuta, waanzime hawa walinzi gari lako nao wakamsake”

“Sawa wachukue tu”

“Nyinyi mukae hapa nyumbani, hakikisheni kwamba aingii mtu hapa”

“Sawa, je swala la mamam?”

Wifi akaka kimya kwa muda.

“Unaweza kulishuhulikia?”

“Mimi peke yangu?”

“Ndio kwa maana hili swala la mume limesha nichanganya kwa maana ni aibu watu wakamuona mtaani akiwa na manywele yake vile….mmmm jamani”

“Inabidi nirudi Dar”

“Kufanyaje?”

“Siwezi kuifanya kazi hiyo nikiwa hapa Tanga, nilazima nisafiri na huo ushahidi kwa siri sana”

“Inabidi utumie basi”

“Basi nitapata usalama kweli?”

“Ndio, hakuna mtu ambaye anaweza kukudhania kwamba umebeba ushahidi. Ukitumia gari kwanza utachoka, pili unaweza kupata tatizo ukiwa peke yako njiani na ukakosa msaada”

“Sawa ni basi gani ambalo ninaweza kulitumia?”

“Kajiandae hadi ukitoka nitakuwa nimesha jua ni ratiba ya basi gani linalo ondoka hivi sasa”

“Poa”

Nikaingia ndani huku nikiwa nimembeba mwanangu. Nikamkabidhi Judy na nikaanza kutafuta tafuta nguo za kuvaa kwa maana nimevaa dera tu.

“Unatafuta nini?”

“Nataka niende Dar”

“Dar kufanyaje?”

“Kuna kazi ya kumtafuta mama mkwe inabidi niende kuifanya”

“Wewe huoni kama itakuwa ni hatari, Jojo, kwa nini dada yangu unataka kujitia matatizoni?”

“Kujitia matatizoni vipi. Umesahau mama wa watu kwa ajili yako alijitia matatizoni?”

Swali hili likamfanya Judy kutulia kwani ndio ukweli yeye ndio chanzo cha mama mkwe kufutwa kazi na pia kushikiliwa.

“Kuna mambo ukizungumza inabidi ufikiria mara mbili mbili, na hakikisha kwamba mtoto anakuwa katika hali ya usalama, sawa”

“Sawa”

Nilipo hakikisha kwamba nimetoa nguo nitakazo vaa ambazo ni suruali, shati na kofia, nikaingia bafuni, nikasafisha kinywa changu kisha nikaoga. Nikatoka bafuni na nikaanza kuvaa nguo zangu. Wifi akaingia chumbani humu akanitazama jisni ninavyo jiandaa.

“Kuna baibui je utahitaji kuvaa?”

“Labda nivae kwa juu”

“Na hilo joto kweli utaweza?”

Judy aliuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Gari analo safiria lina A/C sio rahisi kwa yeye kuhisi joto”

“Sawa”

Wifi akanitolea baibui, nikalijaribisha, likanikaa vizuri mwilini mwangu. Nikajifunika vizuri kichwani mwangu ushungi wa baibui hili. Nilipo hakikisha kwamba nipo vizuri, nikava na miwani nyeusi.

“Lile fiaili lipo wapi?”

Wifi akafungua kabati na kuoa pochi kubwa, akaifungua na kuutoa faili hilo, nikalifunua na kulikagua, nilipo hakikisha kwamba ndio lenyewe, nikalirudisha ndani ya pochi hiyo.

“Hakuna kiti kingine humu ndani?”

“Ndio”

“Judy naomba zile pesa”

“Chukua kwenye hiyo droo hapo”

Judy akanionyesha droo ya dreasing table, nikaifungua nikatoa kiasi cha pesa, nikaichukua suruali yangu ambayo nilikuwa nimeivaa siku iliyo pita, nikaitoa flash hiyo kisha nikiingia kwenye mfuko wa suruali hii niliyo ivaa pamoja na pesa.

“Wifi naomba usaidiane na Judy kumtazama mtoto”

“Usijali hilo”

“Pia musisite kunijulisha juu ya mume wangu”

“Tena nimekumbuka”

Wifi alizungumza akafungua droo nyingine ya kabati na kutoa simu kubwa ambayo jana tuliwasiliana na raisi. Akanikabidhi kisha akanikabidhi na laini nyingine.

“Simu hii utatitumia kama jana tulivyo fanya, hii laine weka kwenye simu yako. Namba yake ninayo huku”

“Judy hivi simu yangu ipo wapi?”

Judy akatoa simu yangu kwenye droo ya nguo na kunikabidhi”

“Hivi itakuwa na chaji ya kutosha?”

“Kuna power bank kule kwenye gari langu, nitakukabidhi”

Wifi alizungumza. Baad aya maandalizi yote nikaagana na mdogo wangu kisha tukatoka chumbani na kuelekea kwenye gari la wifi. Tukaingia ndani ya gari sisi wawili na kuondoka huku nikiwa nimeibeba pichi hii kubwa. Tukafika stendi ya mabasi hapa hapa Kange, nikakabidhi tiketi ya basi, baada ya muda kidogo basi hili likafika hapa stendi.

“Hakikisha kwamba unanipa kila update ya utakacho fanya”

“Sawa wifi, na wewe hakikisha kwamba munampata mume wangu”

“Hilo ni jukumu langu”

Nikaiweka vizuri miwani yangu na nikaingia ndani ya hili basi, nikaangalia siti ni siti gani ninatakiwa kukaa, nilipo iona ni siti gani nikaka, nikafunga mkanda wa siti hii kama sheria za abiria wote ndani ya basi hili. Kabla gari halijaondoka stendi hapa, wakapanda askari kama sita wakiwa na silaha mmoja wao akaamrisha abiri wote kunyanyua sura zetu juu huku wakidai kwamba kuna muhalifu wa mauaji yaliyo tokea siku mbili Dar es Salaam katika hoteli moja iliyopo Kariakoo yumo ndani ya hili gari, jambo lililo yafanya mapigo ya moyo kuanza kunienda mbio kwani kwenye tukio hilo la mauji mimi ndio niliye niliye yafanya.



Askari hawa wakanza kukagua kuanzia siti ya mbele huku wakiwa wanatazama tazama simu zao. Wifi akaingia ndani ya gari hili na kuzungumza na mmoja wa askari huku akimuonyesha kitambulisho. Askari huyu akakisoma kitambulisho alicho kabidhi na wifi kwa muda kidogo kisha kwa ishara askari huyu akawaomba wezake wote kushuka kwenye gari hili na kuruhusu dereva aondoe gari.

Kitendo cha wifi kuingilia hili swala linadhihirisha kwamba ninaye tafutwa hapa ni mimi, na inanilazimu kuwa makini katika safari hi nzima kwani pasipo kufanya hivyo ninaweza kujikuta nikiingia mikononi mwa askari. Nikamshuhudia wifi akiendelea kuzungumza na askari hawa, basi likaingia barabara kuu ya lami na tukaianza safari yetu rasimi.

“Habari abiria wetu, tunaianza safari yetu ya kutoka Tanga na kuelekea jijini Dar es Salaam. Ninawaomba muweze kufunga mikanda yenu na tumuombe Mungu aweze kutufikisha salama. Dereva wetu leo ni Khalidi Juma na kondakta wenu ni mimi Zuwena Zuberi. Asanteni”

Sati ya dada huyu ambaye ndio kondoka wa basi hili, ilisikika vizuri kabisa kwenye masikio yetu. Safari ikaanza taratibu huku kila abiria akiwa bize na mambo yake. Nikaitoa laini iliyopo kwenye simu yangu na kuiweka laini niliyo pesa na wifi, kisha nikaiwasha simu yangu.

Kwenye siti nilizo kaa nipo peke yangu na pembeni hakuna mtu mwengine, jambo lililo nifanya niweze kuuweka mkoba wangu wenye faili maalumu lenye siri nyingi za raisi, pembeni. Safari ikazidi kupamba moto hadi tukafika katika mji mmoja ambao kondakta wetu alitutaarifu kwamba kunaitwa Muheza.

Nikakumbuka hili jina na eneo kwani kipindi kwa mara ya kwana tulipo kuwa tunakuja Tanga mimi na mume wangu, tuliweza kuwaleta wasichana ambao wezao walipata ajali ya gari katika eneo hili.

Wakaingia baadhi ya abiri na abiria mmoja ambaye ni mtu mzima wa kamamo, akaniomba niusogeze mkoba wangu ili aweze kukaa kwenye siti hiyo.

“Shikamoo”

“Maraba binti”

Mzee huyo aliitikia huku akijipangusa jasho usoni mwake kwa kutumia kitambaa cheke, akafunga mkanda wa siti yake na kujiweka kufunga A/C ili impepee vizuri.

“Huu siku hizi kuna joto jamani”

Alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Yaa joto ni kali siku hizi”

“Hivi na hilo vazi loko hauumii kweli?”

“Hahaa…..mbona kawaida”

“Khaa kawaida, hapana kwa kweli. Yaani mimi nimevaa hili shati tu ila nahisi joto kali sana”

“Ukikaa baada ya muda joto litaisha kwani A/C itakuwa imesha anza kufanya kazi”

Nilizungumza kwa suuti ya upole na iliyo jaa uchangamfu mzuri kwake.

“Kweli. Ninaitwa bwana Mgoma, ni mkuu wa polisi wilaya ya hapa Muheza”

Mapigo ya moyo yakanidunda kwa kasi sana, nikameza mate kidogo ili kuzuia wasiwasi wangu kwa maana watu kama hawa ni rahisi sana kuweza kumgundua mtu akiwa katika hali yoyote ya mashaka.

“Ninaitwa Judy”

Ilinihidi kutumia jina la Judy, Mgoma akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ameelewa nilicho kizungumza.

“Unasoma?”

“Yaa ni nipo chuo”

Niliongopea.

“Chuo gani?”

‘Ohoo huyu mzee vipi’

Nilijesema kimoyo moyo huku nikifikiria ni chuo gani cha kumuambia mzee huyu. Kwa haraka nikakumbuka kuna chuo kimoja kinaitwa Ecenford kipo maeneo ya kule anapo ishi mama mkwe.

“Ecenford”

“Ahaaa, hivi pale wanatoa elimu vizuri ehee?”

“Yaa wanatoa vizuri sana”

Nilizungumza huku moyoni nikiomba kwa Mungu asiniulize ninasomea nini hapo kwani ukweli ni kwamba sijui hata masomo yanayo somwa chuo yapo ya aina gani.

“Kuna binti yangu bwana, naye namtafutia chuo asome some bwana si unajua maisha ya siku hizi ni lazima utafute”

“Ni kweli, nilazima utafute”

“Soma bwana, acheni mambo ya ajabu ajabu. Maisha ya siku hizi ni magumu sana”

“Kweli baba yangu”

Katika muda mfupi huu ambao tumekutana na mzee huyu tukajikuta tumezoeana sana. Tukaendelea kuongea mambo mengi sana huku kwa upande wangu mambo ninayo yazungumza mimi yote ni uongo. Mzee huyu akapitiwa na usingizi, nikapata nafasi nzuri ya kuanza kuperuzi mitandaoni ili kuweza kufahamu ni nani ambaye anatafutwa juu ya mauji yaliyo tokea kwenye hoteli moja Kariakoo jijini Dar es Salaam. Ila kila ninavyo tafuta, muhusika wa mauaji hayo anaonekana ni Mr Z, mwanaume ambaye alsiha wahi kunisaidia kutoka mikononi mwa watu wa dokta Clara.

‘Sasa ni nani ambaye walikuwa wakimtafuta?’

Nilijiuliza swali hili kwa mara kadhaa huku nikijaribu kutazama tazama nyuma na mbele ni mwanaume gani ambaye ninaweza kumuhisi kama Mr Z. Hadi mzee huyu anazinduka kutoka usingizi, sijafanikiwa kumjua mtu yoyote.

“Aisee nimechoka kwa kweli, kazi zetu wengine ni shida kwa kweli”

“Pole sana mzee wangu”

“Aha…asante, jana bwana majira ya saa tisa hivi usku Mr Z alikuwepo Tanga”

Nikastuka kidogo na kujikuta nikikaa vizuri na kumtazama usoni mwake.

“Eheee, tena habari zake ndio nilikuwa nina zipitia kweye mitandaoya kijamii”

“Aisee nimefanya hii kazi huu ni mwaka wa ishiri na tano, ila sijawahi kuona mtu mwenye kasi ya mashambulizi kama huyo Mr Z”

“Kasi ya mashambulizi kivipi?”

“Kwanza ni mtu ambaye anajua kutumia silaha si bunduki, si kisu wala si sime, yupo vizuri. Ana uwezo wa kurusha mateke, ngumi na uzuri ambao nimempendea hagusi polisi”

“Yaani hawapigi polisi?”

“Yaa kwa maana jana kulikuwa na tukio moja la uvamizi wa benki pale mjini, sasa wala majambazo walivamia na kukimbia na pesa, sasa tukiwa katika harakati za kuwafukuzia tukashangaa tu mtu anapikipiki yake kubwa akitupita, akawapita hadi majambazi wenyewe na kuwazuia gari lao. Akawapa kichapo kisawa sawa, kisha akatuachia watu wetu na pesa kisha akaondoka zake”

“Mmm kwa hiyo ni mtu mwema?”

“Kwa mimi ninahisi hivyo japo wakuu wangu wa kazi wanahitaji akamatwe, hapa ndio ninaelekea Dar kutoa maelezo ya kwanini tulimuachia andoke”

“Sasa inakuwaje utoe maelezo kama mtu ni mwema?”

“Kazi yetu haijui hivyo mwanangu. Inatakiwa mtu yoyote anaye fanya kazi na si askari wala hausiani na jeshi, nilazima akamatwe”

“Huyo mutakua muna muonea”

“Kumuonea ni kweli, ila ngoja tukazungumze cha kuzungumza huko tuendapo”

“Poleni sana”

“Asante”

  ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG