DAPHINE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 3 KATI YA 10
“Mamaaa!Mamaaaaaa!”
Mtoto mdogo wa kike mwenye umri kati ya miaka 12-17 aliingia ndani mbio mbio huku akimuita Mama yake,jambo aliloliona lilimtisha mno.Alimuona mtu amedondoka nje ya geti lao ametapakaa damu mwili mzima.
Mwanamke wa makamo mfupi kiasi maji ya kunde akatoka ndani mbio kama mtu aliyekuwa anaunguliwa na nyumba.
“Wewe Lulu,kuna nini?”
“Njoo uone”
Mama mtu akatoka nje ya geti,jambo aliloliona lilimshtua nayeye pia.Akawa kama amechanganyikiwa hakuelewa ni kitu gani akifanye,kazi yake ilikuwa ni kutembea huku na kule.Kitu kilichomjia kichwani ni polisi,alijuwa angehitajika kujibu mashtaka sababu mwili ungekutwa nje ya geti lake.
Hakutaka kufanya kitu chochote zaidi ya kukimbia ndani ili achukuwe simu yake ampigie mjumbe wa nyumba kumi aripoti jambo hilo,bahati mbaya simu yake haikuwa na salio.
Alivyorudi na kulifikia geti lake alipigwa na butwaa zaidi baada ya kuona mwili huo ulojaa damu unajitingisha,moyo wake ulikuwa ukipiga kwa nguvu pembeni alisimama binti yake mdogo aliyeitwa Lulu.
“Nenda ndani”
Mtoto akakimbia ndani,picha aliyoiona ilimtisha sababu hata yeye alitandwa na hofu.
“Nisaa….idi…eee”
Ngesa alisema kwa tabu na mateso akiwa chini amelala huku akijaribu kusimama lakini alishindwa kutokana na kuishiwa nguvu.
Mwanamke huyu akashindwa cha kufanya, hakuelewa ni msaada gani autoe alitandwa na hofu.Moyo wake ulimwambia atoe msaada lakini upande wa pili alisita kidogo, nafsi yake ilimwambia kwamba wenda mtu huyo ni jambazi na mwisho wa siku angemsababishia matatizo makubwa.Ndani ya nyumba hiyo walikuwa wakiishi wawili tu,yeye na mtoto wake mdogo, Lulu.
“Naa…kuf..a nisaidie”
Ngesa akazidi kuomba msaada baada ya kumuona mwanamke huyo bado anajishauri,hakuwa mwenye nguvu hata kidogo,kila alipojaribu kusimama akashindwa.Mwanamke huyu akajawa na huruma moyo wake ukamsukuma atoe msaada akainama taratibu na kumuinua ambapo aliuchukuwa mkono wa Ngesa wa kulia na kuuviringisha begani mwake,wakatembea mpaka ndani.
Damu zilizokuwa zinamtoka Ngesa zilimtisha,akamuweka ndani sakafuni na kuingia ndani ambapo alichukuwa kitambaa kisafi akatoa kipande cha shati kilichokuwa kimelowa damu na kumfunga kingine kwenye jeraha la mkono ili damu isiendelee kutoka.
“Lulu,wewe Luluuuu”
“Abee Mamaaaa”
Mtoto akasogea karibu na Mama yake.
“Nenda pale duka la dawa kaniletee spirit”
Mtoto akapewa pesa,kwa elimu ndogo aliyokuwa nayo alielewa kazi ya spirit ni kuuwa bacteria kwenye kidonda.Hiyo ndiyo huduma ya kwanza aliyotaka kumpa Ngesa.Baada ya dakika tano chupa ya spirit ikaletwa.Ngesa akaanza kupakwa dawa na pamba,kelele alizopiga zilikuwa kubwa,dawa ilikuwa inaingia kwenye kidonda alihisi kama anachanwa chanwa na viwembe.
“Pole”
Ngesa akapewa pole,nguo nyingine safi ikaletwa kidonda kikafungwa upya baada ya kusafishwa.Baadaye akakorogewa uji na kuanza kunywa taratibu.
Ilivyofika saa mbili ya usiku akapelekewa chakula ili ale.Mpaka inafika saa nne ya usiku Ngesa alianza kupata ahueni kidogo japo sio sana.
“Ahsante kwa msaada wako”
“Usijali,Mimi naitwa Jaqlin Mfinanga au Mama Lulu.Wewe je?”
“Derick Ng..esa”
“Nani?”
“Derick”
“Nini kilikukuta?”
“Ni hadithi ndefu kidogo lakini nitakwambia,ninachokuomba asijuwe mtu yoyote kuwa nipo hapa”
“Kwanini?”
Ngesa alimuangalia mwanamke huyu aliyekuwa mbele yake anayejaribu kumsaili lakini alishindwa ampe jibu gani,hakuelewa amwambie ukweli ama ampige porojo.
“Hapa unaishi na nani?”
Ngesa nayeye akauliza swali badala ya kujibu swali,likawa swali juu ya swali.
“Naishi mimi ni mwanangu”
“Baba yake yupo wapi?”
“Alifariki muda sana”
“Pole sana”
Ngesa alihifadhiwa ndani ya nyumba anayoishi mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Jaqlin Mfinanga akipatiwa matibabu na chakula,mpaka siku mbili zinapita hali ya Ngesa ilionesha matumaini makubwa sababu aliweza kutembea na kufanya kazi ndogondogo kama kusaidia kuosha vyombo na wakati mwingine kuingia jikoni kupika.
Hakuwa na sababu ya kuendelea kuuficha ukweli uliojificha nyuma ya pazia kila kitu alikiweka wazi kwa mwanamke huyu aliyemsitiri na alimuhadithia tangu akiwa Mkoani Morogoro akatupwa msitu wa Mabira nchini Uganda,akakizungumzia kifo cha Mh.Tony Benjamin jinsi kilivyotokea na kuhitimisha kwamba serikalini kuna watu wabaya sana hivyo alitaka kuuweka ukweli wazi,bila kufanya hivyo angeendelea kutafutwa mpaka kihama.
Ilikuwa ni simulizi ya kusisimua na wakati mwingine Jaqlin Mfinanga alidhani ni uwongo tu,isingewezakana kwa binadamu kupitia matatizo kama hayo.
“Mh!pole sana.Mimi kama unavyoniona nina fanya biashara zangu ndogondogo za kuuza samaki na kupika maandazi kila siku,Mume wangu alifariki miaka mingi iliyopita”
Jaqlin Mfinanga nayeye akaanza kutoa historia yake kiufupi,ambapo Ngesa aliisikiliza kwa masikitiko makubwa sana,hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Mama Lulu ama Jaqlin Mfinanga aliendelea kufanya siri kubwa ingawa aliona picha ya Ngesa sehemu mbalimbali ikiwa imebandikwa na chini kulikuwa na pesa nyingi endapo mtu yoyote atapiga simu polisi na kutaja wapi mtu huyo alipo.
Hakutaka kuingiwa na tamaa hata kidogo,sababu aliamini kwamba tamaa ilimponza fisi hata hivyo aliridhika na anachokipata.
***
“Nimekuandalia maji nenda kaoge”
Ilikuwa ni sauti ya Jaqlin Mfinanga,amesimama mlangoni kwa Ngesa anamtaka akaoge usiku.Waliishi nyumba moja lakini vyumba tofauti,Ngesa akasimama na kuweka taulo dogo begani.Hakuwa na shati juu yake.Akampita Jaqlin Mfinanga na kuuendea mlango wa bafuni huku nyuma akimuacha Mwanamke huyo akimuangalia kwa macho yasiyo ya kawaida,Ngesa akaingia bafuni ili ajimwagie maji lakini kabla hajaufunga mlango ukazuiwa,alikuwa ni Jaqlin Mfinanga.Bila kuuliza chochote mwanamke huyo akazama bafuni na kufunga mlango kwa ndani,akamvuta Ngesa na kupeleka mdomo midomoni kwa Ngesa,damu yake ilikuwa inaenda mbio kutokana na hivyo hakuweza kuvumilia.Alikuwa ana hamu na tendo hilo sababu hakulifanya siku nyingi kutokana na kufiwa na mume wake,kila Ngesa alipotaka kujitoa akashindwa,Jaqlin alimparamia mdomoni,hatimaye Ngesa akafungua mdomo wake.Ndimi zao zikakutana wakaanza kubadilishana mate huku wakishikana huku na kule.
Mapenzi kati ya Ngesa na Jaqlin Mfinanga yalianza kuchipua kuanzia siku hiyo sababu walianza kulala chumba kimoja kama wanandoa na kushiriki tendo la wanandoa,mwanamke huyu alifurahi sana baada ya kutoka katika hali ya upweke,bado jambo la Ngesa kuwa ndani ya nyumba yake lilikuwa siri kubwa mno, kuonekana kwake kulimaanisha kwenda kuozea jela ama kunyongwa na Jaqlin hakutaka swala hilo litokee ndiyo maana akamficha ndani.Ngesa alikuwa anafanya kila kitu ndani kwa ndani na matibabu yaliendelea kama kawaida,baada ya wiki mbili hali yake ilikuwa shwari kabisa.
Kupitia televisheni aliona ni jinsi gani wanavyomsaka kwa wudi na uvumba, dau likaongezwa tena,watu wakazidi kupagawa pesa zilikuwa ni nyingi kupita kiasi.Haikuwezekana hata kidogo Ngesa kutoroka popote pale maana ulinzi uliongezwa mara mia yake na mipaka ya nchi walimwagwa wanajeshi kama utitiri,picha ya Ngesa ilikuwa kila mahali maana kwamba jina lake ndio lilikuwa kichwa cha habari.
***
“Ngesa yuko wapi?”
“Miii…mi sii…jui,alivyo…ondoka hakuaa…niambia anapo…enda”
“Unataka tukuamini?”
“Huo ndio ukweli”
“Muheshimiwa,tueleze ukweli.Tutaendelea kufanya hivi mpaka utakaposema ukweli”
Mh.Frank Man’sai alikuwa ndani ya kambi ya jeshi Mabibo Makubuli anakula mateso yaliyozidi kipimo chake baada ya kutolewa kituo cha polisi bila kusema chochote kile.Uso wake ulikuwa umepasuliwa vibaya sana na ulikuwa umelowa damu sio mchezo,alishateswa vya kutosha lakini hakuwa tayari kufungua kinywa chake na kutaja ni wapi Ngesa alipo, kufanya hivyo aliamini kwamba angeharibu operesheni nzima ya Ngesa ya kuusaka ukweli.Kupitia Martha Msoso aliamini ungejulikana ukweli wote juu ya kifo cha Tonny Bejamin.
“Ulikuwa na Ngesa ofisini kwako,alikuwa anataka nini?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Luteni Sajo,huyu ndiye aliyeteuliwa kumsulubu Mh.Frank Man’sai kutoka kwa mkuu wake wa kazi na amri hiyo ilitoka moja kwa moja kwa amiri mkuu wa majeshi Rais Leslie Benjamin kwamba Mh.Frank Man’sai afanywe kitu chochote kile ili aseme ukweli,kauli hiyo iliwafanya wanajeshi wampige vibaya sana bila kujali.
“Nakuuliza tena kwa mara nyingine,siku ile ulivyokuwa na Ngesa alikuwa anataka nini ofisini kwako?”
“Sijui”
Mh.Frank Man’sai alivyojibu alipokea kifuti cha tumbo akadondoka na kiti alichokuwa amefungwa nacho,Luteni Sajo hakuishia hapo.Alimfuata na kuanza kumpiga mabuti kichwani.Mh.Frank Man’sai aliumia vibaya sana,kilichokuwa chini kwa wakati huo ni damu tupu.
“Sema ukweli…Captain”
Luteni Sajo akamuita mwenzake.
“Yes”
“Niletee plies”
Mwanajeshi aliyekuwa pembeni akatoka nje na alivyorejea alikuwa na plies, kifaa kinachotumika kukata nyaya ngumu,kiti alichokuwa amekalia Mh.Man’sai kikawekwa vizuri.Akafunguliwa mikono yake iliyokuwa na kamba,mkono wake wa kushoto ukawekwa mezani.Kidole kilichokuwa na pete ya ndoa kikawekwa vizuri plies ikapitishwa katikati ya kidole ili kikatwe.Hapo ndipo Mh.Frank Man’sai alilia kwa uchungu sana,kidole kilichokuwa na pete ya ndoa kilikuwa kinatolewa endapo asingesema chochote.
“Una sekunde tatu,hiki kidole ninakitoa na baada ya sekunde moja nakutoa kidole kingine.Mpaka vidole vyote viishe”
Luteni hakuwa mwenye sura ya mzaha hata kidogo,kile alichokuwa anakisema alikikusudia.
“Moja…”
Luteni alianza kuhesabu huku taratibu akikaza mikono yake,kwa mbali Mh.Man’sai alianza kuhisi maumivu kidoleni na alijuwa ingefika namba tatu kidole chake kingedondoka chini.
“Mbili…Ngesa yuko wapi?”
“Si..sijui”
“Ta…”
“Alikuja ofisini kwangu,sasa hivi atakuwa kwa Martha”
“Martha,ndiyo nani?”
“Sekretari wangu”
“Alienda kufanya nini?”
“Kutafuta ukweli”
“Ukweli upi?”
“Kwamba sio mimi niliyefanya mauaji,ukweli upo kwenye kompyuta yangu ofisini kwangu”
“Huyo Martha ni nani na anapatikana wapi?”
“Ni sekretari wangu,anaishi Kinondoni block 41”
“Nyumba namba ngapi?”
Mh.Frank Man’sai hakuwa na tatizo lolote lile,ilibidi aongee ukweli,hakuweza kuyakabili mateso yaliyokuwa yanazidi kuendelea kwa maana hiyo kuzungumza ukweli kulimaanisha kuachiliwa ingawa hakuwa na uhakika kama atakuwa huru baada ya hapo.
Baada ya uchunguzi kufanyika wakishirikiana na wanajeshi ikagundulika kuwa Martha Msoso alipigwa risasi na kufa,taarifa hizo alivyopelekewa Mh.Frank Man’sai alisikitika sana na zilimuogopesha.
“Martha amekufa na inasemekana kwamba Ngesa ndiyo kamuuwa.Bado una maswali unatakiwa kujibu”
Sio wanajeshi peke yao hata jeshi la polisi lilichukulia moja kwa moja kwamba Ngesa ndiye aliyefanya mauaji ya Martha Msoso lakini hawakuelewa kwanini,hiyo ilifanya wazidi kumtafuta kila pembe ya jiji wakiamini kwamba hatoweza kutoroka kutoka nje ya Tanzania.Ngesa alitafutwa kuliko pesa na dau lilipandishwa, picha zake zikabandikwa kila kona ya jiji na mikoa jirani.
***
Ulikuwa ni usiku wa saa tano kasoro saba,giza lilikuwa totoro kutokana na wingu kuwa zito angani na baada ya dakika thelathini mvua ilianza kunyesha,radi zikaanza kupiga mtindo mmoja.Wakati watu wanajiandaa kulala yeye alikuwa anajiandaa kwenda Oysterbay ndani ya nyumba ya Mzee Vital Kamere,alikuwa ana hasira naye kuliko maelezo yaliyojitosheleza hasa alivyomkumbuka Marehemu Tonny Benjamin rafiki yake kipenzi aliyeuwawa kwa kupigwa risasi.
“Jaqlin”
Alimuita Mpenzi wake siku hiyo akiwa seblen amevimba kama chura.
“Abee”
“Ubaki salama,mimi ndiyo naenda”
“Kwanini usiendelee kubaki hapa,mimi nitakufichia siri”
“Hapana,inabidi nimalize kitu nilichokianza”
“Ngesa”
Jaqlin aliongea huku machozi yakimlenga akamsogelea Ngesa na kumkumbatia huku akimsihi kwamba asiondoke kwani kufanya hivyo ilikuwa ni sawa na kujikamatisha mwenyewe.
“Hapana,nitaishi hivi mpaka lini?Naomba niruhusu niende”
Kama mwanaume ilibidi achukuwe maamuzi magumu hakujali machozi ya Jaqlin Mfinanga mwanamke aliyetokea kumpenda sana,alichofanya ni kujitoa kwake na kuanza kutembea kuelekea mlangoni.
“Kwaheri”
Kabla ya kutoka nje aliaga ndipo akafungua mlango ambapo alikumbana na mvua kubwa,hilo hakujali alichofanya ni kupita pori kwa pori.Alivyotaka kutokeza barabara ya lami akajificha nyuma ya mti mkubwa.
“Funga ndio,weka na pilipili nyingi mishkaki mitatu.Fanya haraka kaka gari nimepaki vibaya”
Ilikuwa ni kosa kubwa kuacha gari likiwa linaunguruma kandokando ya barabara isitoshe funguo zipo ndani.
“Unafunga?”
“Ndio,fanya fasta basi”
Alikuwa katika kibanda cha chips,alivyogeuza shingo yake nyuma aliona gari lake linaondoka kwa kasi,akaachana na chips akaaanza kulikimbiza lakini alikumbana na utelezi akapiga mueleka mkali akadondoka kwenye matope,akabaki kuziangalia taa nyekundu zinaishia kwa mbali.
Ngesa alikuwa tayari amepata gari la kuiba aina ya Prado,mwendo alioutumia ulitishia amani,kutokana na gari hiyo kuwa juu aliweza kuyafukia mashimo bila wasiwasi,akaingia barabara kubwa.Akaweka usukani sawa na kuzidi kusonga mbele.
Alikuwa ana usongo na Vital Kamere sio masihara,alikimbiza gari kama mwendawazimu.Hakuwa na silaha lakini alijiamini kupita kiasi,akazidi kusonga mbele, ndani ya dakika kumi na saba tayari alikuwa oystarbay polisi akalala na kona mzimamzima,akazidi kunyoosha mguu.
Zilikuwa zimebaki kama mita kumi na mbili ili alifikie geti la Mzee huyu tajiri Vital Kamere,akazidi kukanyaga mafuta gari likazidi kusonga mbele alivyolifikia geti akazungusha usukani gari likagonga geti,Puuu! zilitokea kelele kubwa mno lakini kutokana na mvua kubwa, kuvunjika kwa geti hakukusikika vizuri.
Nyumba ya Vital Kamere ililindwa na walinzi wanne kutoka katika kampuni ya KK security na wote walikuwa wana mitutu.Mlinzi aliyekuwa getini alivyoona geti limevunjwa akakoki mtutu na kuanza kulisogelea gari kwa tahadhari,hakuelewa kuwa Ngesa yupo nyuma ya gari anamuona.Alivyolifikia gari,alikatwa mtama akadondoka chali kama gunia,hakukaa sawa akatulizwa na ngumi ya shingo.Ngesa akachukuwa mtutu.Akatizama mbele yake,ambapo alikumbana na gorofa kubwa na chini kulikuwa na magari mengine ya kifahari.
***
“Yes Brigedia,nadhani Rais atalia na kusaga meno.Upo na mwanaye?Unataka kumfanya nini?Kumkata kichwa?Itakuwa vizuri sana.Alafu mabomu yale yamekaa sana ndio ndio..Moja umesema wapi?uwanja wa taifa.Wiki ijayo nadhani kuna mechi kubwa tu,nadhani tutaliweka moja pale, okay ahsante”Simu ikakatwa.
Yalikuwa ni maongezi ya Vital Kamere akiwa chumbani kwake ndani ya jumba lake kubwa,hakuwa na wasiwasi wowote wala hakuelewa kwamba tayari amevamiwa na walinzi wake wote wapo chini,kutokana na mvua kubwa na radi kupiga hata geti lilivyovunjika hakusikia.
“Ngoja nikapate whisky”
Vital Kamere akajisemea mwenyewe akasimama na kuvaa taulo.Akatembea mpaka seblen akafungua friji,Kabla ya kumimina pombe kwenye glasi akahisi kichuma kimemgusa mgongoni.
“Tulia hivyo hivyo”
Ilikuwa ni sauti iliyomshtua,hapohapo akapigwa na kitako cha mtutu kichwani.Ngesa alijawa na hasira kupita kiasi,akachukuwa chupa ya wisky akampasulia nayo kichwani.
Akamvuta na kumtwanga ngumi ya pua,kibano kiliendelea.
“Nani kamuuwa Tony?”
Ngesa aliuliza kwa gadhabu huku akitetemeka kwa hasira.
“Ki..jana sura yako sio ngeni,nina..taka kukusaidia m…”
Vital Kamere akanyamazishwa na kichwa cha mdomo.
“Nani kamuuwa Tonny?Nani anahusika?”
Ngesa aliuliza swali huku akitoa kipigo cha hali ya juu,pembeni kulikua na taa ndogo ya mezani akaivuta na kumpiga nayo kichwani.Vital Kamere akadondoka chali,taulo pembeni.
“Naniiiii?”
Waya mwembamba wa umeme ulikuwa shingoni mwa Vital Kamere,Ngesa alikuwa kauzungusha anamnyonga nao.
“Da…phi…ne”
“Nani?”
“Da…phine ndiyo alimuuwa”
“Ndio nani na kwanini?Aliwakosea nini?”
Ngesa akazidi kukaza waya uliokuwa shingoni,Macho ya Vital Kamere yalitumbuka mbele kama mjusi,akawa anashindwa kupumua vizuri.Kutokana na hasira mbaya alizokuwa nazo hakutaka kusubiri kitu kingine zaidi,akachukua kipande cha chupa iliyokuwa nusu,akaitumbukiza shingoni mwa Vital Kamere.
“Hii ni kwa ajili ya Tonny”
Damu zilikuwa zinaruka kama chemchem kutoka shingoni mwa Vital Kamere na alikuwa akishika shingo yake, taratibu akadondoka chini na kuanza kukoroma kama kondoo anayechinjwa.
“Kacha kacha,Paa paaaa”
Ngesa akammalizia na risasi mbili za kichwa.
“Griii griiii,griiii”
Kilichomshtua Ngesa ni simu ya mezani iliyokuwa inaita,akatafakari akatembea na kuinua mkonga.
“Kamere nimekupigia kwenye simu yako ya mkononi naona hupokei,mabomu tunatega Jumamosi wiki ijayo uwanja wa taifa, mtoto wa Raisi Leslie kesho tunamtoa kichwa chake,njoo nyumbani kwangu kesho.Halloo Kamere,unanisikia”
Ilikuwa ni sauti nzito ya kukwaruza kutokea upande wa pili wa simu,Ngesa alikuwa hewani akisikiliza kila kitu bila kusema chochote!
Ngesa hakutaka kujibu kitu chochote kile akaweka mkonga wa simu chini.Akaruka maiti ya Vital Kamere iliyokuwa chini ina damu,akaanza kutembea chumba kwa chumba.Hatimaye akaingia chumba alichokuwa analala Vital Kamere,alivyopiga jicho mezani akaona simu na ilikuwa inaanza kuita,alivyosogea na kuangalia juu ya kioo akaona jina KARANJE,akasubiri mpaka ikate.Akaingia kwenye uwanja wa meseji na kuanza kukagua kila kitu,mambo aliyoyaona yalimshtua kupita kiasi na kitu kilichomchanganya akili ni kugundua kwamba mtoto wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Ritha Leslie ametekwa nyara na angechelewa basi kichwa chake kingekatwa kesho yake,jambo hilo lilimchanganya akili zaidi.
Akaingia kwenye majina ya simu na kuanza kutafuta kitu anachokijua yeye,alivyofika jina la RAIS LESLIE akasita.Alijifikiria mara mbilimbili kwa jambo analotaka kulifanya lakini akaweka mawazo yake kando kwanza.
“Siwezi kumwambia Rais kwanza”
Alisita kusema jambo hilo mapema sababu aliamini kwamba hakuna mtu anayemuamini kwa wakati huo,haraka akapita bafuni na kuanza kunawa ili kutoa damu alizokuwa nazo mwilini,akarudi chumbani kubadili nguo,akavaa mavazi ya marehemu.Alivyoangalia pembeni juu ya meza akaona bastola ndogo akaichukuwa na kuchomoa‘magazine’ ili kukagua kama ina risasi,alivyohakikisha zipo akairudisha na kuiweka kiunoni,akaangalia huku na kule na kubeba funguo za gari.
Alishindwa kuelewa kabeba funguo za gari gani sababu nje alikumbana na magari zaidi ya kumi,alichofanya ni kubonyeza rimoti.
“Chwii chwiiii”
Hapo hapo akageuka nyuma na kuona gari aina ya Jaquar linawaka taa na kutoa mlio kumaanisha kuwa ndiyo funguo zake,hakutaka kupoteza wakati.Akaingia na kulitia moto.
Kwenye geti kulikuwa na uwazi kidogo,akapenyeza gari kwa taadhari na kuondoka zake,hakuelewa ni wapi aanzie lakini aliendesha gari mpaka alipofika Msasani,Macho. Hapo alizidi kunyoosha barabara inayopanda Coco Beach akashuka kilima na kukunja kona,akaipita hospitali ya macho CCBRT na kukunja tena kulia,alivyofika bahari ya Hindi eneo la koko beach akaweka mguu kati, gari likasimama.Akatoa simu ya Marehemu Vital Kamere na kuanza kuikagua vizuri.Akili yake ilifanya kazi kwa kasi ya mwewe akachukuwa namba za Karanje na kujaribu kama anataka kumtumia pesa ili kujuwa jina lake kamili,ni kweli wazo lake lilizaa matunda AMIR KARANJE hilo ndilo lilikuwa jina halisi la Brigedia Karanje,akashusha pumzi na kuanza kutafakari.
Akaingia katika mtandao wa ‘Google’ akaandika neno FABBYCOM,kila kitu kikaja kuanzia mkurugenzi wa kampuni hiyo ya simu na kila kitu chake,hapohapo akawasha gari,jinsi alivyozungusha usukani iliogopesha mchanga wa bahari ukaruka juu,tairi zikazunguka akaingiza gari barabarani kwa safari ya kuelekea Maili moja, nje kidogo ya mji wa Dar es salaam,huko ndipo alijuwa atafanikiwa kumpata Mr.Hafidh J Ikram mkurugenzi wa kampuni ya mtandao wa simu, Fabbycom.
***
Ni kweli Kichwa cha mtoto wa Rais kilitakiwa kikatwe na kifungwe ndani ya boxi kama zawadi apelekewe baba yake mzazi ambaye alikuwa Rais wa Tanzania,Brigedia Karanje aliamini kwamba swala hilo lingemuumiza sana na lingemchanganya rais wake,hakupanga hayo tu ilikuwa ni lazima atege bomu la Nuclear uwanja wa taifa na auwe maelfu ya watu.Kitendo cha Ritha kuingia katika himaya yake ilikuwa ni furaha kubwa sana,akawapongeza Zaitun na Daphine kwa kazi nzuri waliofanya.
“Kesho kutwa mje hapa kuna tafrija kidogo,kazi nzuri”
Brigedia Karanje alitoa pongezi za dhati akiwa juu ya sofa, pembeni analindwa na wanajeshi wenye silaha nzito,tena wenye ukakamavu.
“Ahsante”
“Mnaweza mkaendelea na shughuli zenu”
“Ahsante mkuu”
Zaitun na Daphine waliondoka huku nyuma wakimuacha Brigedia Karanje anatafakari,hilo lilikuwa wazi kabisa kwamba anamchukia Rais Leslie kuliko maelezo yaliyojitosheleza.
“Mpelekeni juu gorofani”
Kauli hiyo ilivyotolewa Ritha akawekwa begani kama kitoto cha mbuzi,alikuwa bado hana fahamu.
****
Kilichomchanganya Brigedia Karanje siku hiyo ni kutompata Vital Kamere hewani,mara ya mwisho alivyompigia kwenye simu yake ya mkononi ilipokelewa lakini hakuna mtu aliyezungumza asubuhi yake ikawa hivyohivyo,kuna kitu alianza kukihisi.
Akazidi kupiga tena simu lakini wapi.
“Luteni,mlete Ritha hapa tumalize kazi,naona Kamere hapokei simu”
Hata kama Kamere asingetokea ilikuwa ni lazima siku hiyo kichwa cha mtoto mdogo Ritha kitolewe tena na panga lililokuwa na makali kotekote.
“Dad yuko wapi?nyie ni akina nani?”
Ritha aliuliza baada ya mlango wake kufunguliwa,akapelekwa mpaka seblen ambapo alikumbana na lundo la wanajeshi.
“Mleteni huku”
Brigedia Karanje akaongea kwa hasira za waziwazi,Ritha akabebwa juu juu mpaka uwani,ndani ya chumba kidogo kilichomtisha sababu alikumbana na vitu kama mapanga na sime.
Japokuwa alikuwa ana umri mdogo lakini alielewa nini maana ya kazi ya vitu hivyo,bila kupoteza muda akafungwa juu ya kitanda chali,shingo yake ikawekwa vizuri.Brigedia Karanje akashika sime na ilikuwa yenye makali sio mchezo.
****
Ulikuwa ni usiku wa saa saba ndipo Ngesa alipoingia Maili Moja,akachukuwa tena simu na kuangalia vizuri nyumba ya Mkurugenzi Hafidh J Ikram,akaanza kuisaka.Alikuwa amebakiwa na masaa machache ili kuyaokoa maisha ya Ritha Leslie Benjamin, kwa maana hiyo ilibidi mkurugenzi wa kampuni ya mtandao wa simu ya Fabbycom apatikane ili aweze kujuwa ni wapi Brigedia Karanje alipo kwa njia ya ku’trace’ namba zake za simu.
Hicho ndicho kilimfanya afike Maili moja.Bahati nzuri akaona geti jeusi na namba za nyumba,akapitisha gari na kwenda kuliegesha mbele umbali wa mita kumi hivi,akashuka na kuanza kuistadi nyumba.Alivyoangalia ukuta aliona una nyaya za umeme zenye shoti,kuruka ukuta kwake lilikuwa ni jambo la hatari sana angerushwa na shoti,alichofanya ni kufika getini na kuligonga.
“Wewe nani?”
Mlinzi wa getini aliuliza akichungulia kupitia kidirisha kidogo cha getini.
“Nahitaji kuonana na Mr.Hafidh tafadhali fungua geti”
“Usiku wote huu?”
Mlinzi akauliza swali,hakujuwa kwamba anapoteza mda yeye alichojali ni kazi yake.Na halikuwa kosa lake moja ya kazi yake ilikuwa ni kuhoji watu wanaoingia isitoshe alimuwekea mashaka Ngesa sababu ilikuwa usiku.
“Nina shida naye,ni muhimu”
“Hapana siwezi”
“Subiri nimpigie simu alafu uone kitakachofuata,nadhani hunifahamu”
Ngesa kama kawaida yake alijaribu kupiga mkwara lakini mlinzi hakutingishika akaweka ngumu.
“Ndio wewe njoo kesho au labda nipate ruksa yake”
Mlinzi akahitimisha hiyo ilimfanya Ngesa achukuwe maamuzi mengine magumu.
“Paa paa paaaa”
Akafyatua risasi tatu kwenye kitasa cha geti,kikaachia akalipiga teke kwa nguvu,akazama ndani kama komando.
“Weka silahaa chini,kaa chini”
Ngesa akatoa amri kwa mlinzi huyu wa getini ambaye tayari alikuwa amemwaga mkojo kwa uwoga,Ngesa hakuwa mtu wa mchezo mchezo alikuwa ana masaa machache yaliyosalia.
“Simama,ongoza mbele”Akatoa kauli nyingine kwa hasira.
Mlinzi mbele Ngesa nyuma.
“Kijana weka silaha chini”
Sauti iliyotokea juu ya gorofa ndiyo ilimshtua,tena iliambatana na mtutu mkubwa, alikuwa ni mkuregenzi Hafidh J Ikram.Hiyo ilimfanya Ngesa asiwe na ujanja sababu siku zote aliyekuwa juu na silaha ndiye mshindi.
“Mr.Ikram,nahitaji tuongee.Sikuja kwa nia mbaya”
Ngesa akajaribu kujitetea ingawa bado bastola alikuwa amemuwekea mlinzi kwenye kisogo chake.
“Weka silaha chini…kachakacha”
Mr.Ikram alikuwa juu ya gorofa,ameshika mtutu na sura ya Ngesa ilikuwa inamjia na kumtoka. Ghafla akaikumbuka,alikuwa ni mtu anayesakwa Tanzania nzima tena kwa wudi na uvumba.
“Weka silaha chini”Mr.Ikram akasema tena.
Ngesa taratibu akashusha bastola chini na kunyoosha mikono hewani,Mlinzi wa getini kwa mbwembwe akaiokota bastola.
“Piga magoti”Mlinzi akatoa amri.
Ngesa akageuziwa kibano,akawa amewekwa chini ya ulinzi yeye, akapiga magoti mikono ikiwa hewani.
“Mr.Ikram kuna jambo nataka kuzungumza nawewe”
“Ngoja nipigie simu polisi”
“Usifanye hivyo,kabla hujapiga simu polisi naomba unisikilize”
“Nini?Siwezi kukusikiliza jambazi wewe”
Ni kweli Mr.Ikram hakutania akaingia ndani na kuchukuwa simu ya mkononi,akaweka namba za polisi ili kuripoti swala la kumuona jambazi anayetafutwa.
***
Kwa kasi ya Umeme Ngesa akasimama ,mlinzi akapigwa kichwa cha kidevu,akayumba na kusindikizwa na teke lingine la tumbo akadondoka chali,Ngesa akachukuwa bastola na kuingia ndani ya jumba la Mr.Ikram,alielewa kupigiwa simu polisi ilimaanisha operesheni yake kukwama,akashika bastola vizuri na kupandisha ngazi mpaka juu gorofani.
“Ndio naongea na kituo cha polisi Maili moja…kupuuuuu”
Alihisi maumivu makali kichwani,baada ya kupigwa na kitako cha bastola kichwani,Mr.Ikram akadondoka kama gunia,Ngesa akamsogelea mpaka karibu yake na kumuwekea bastola kichwani.
“Simama juu”
Aliongea kwa hasira huku akiyabana meno yake.
Mlango wa bastola ulikuwa kichwani kwake tena umemgusa,hiyo ilimaanisha kwamba angefanya jambo lingine la kijinga ubongo wake ukasambaratishwa vibaya sana kwa kupigwa risasi,alihofia kifo hicho sababu alishawahi kuona maiti ya mtu aliyepigwa risasi,kilikuwa ni kifo kibaya sana.Ndiyo maana akahisi tumbo linamuuma hakuelewa ni la kuharisha ama uwoga,mwanaume aliyesimama mbele yake alimtisha na alivyoangalia vizuri aligundua kwamba kidole cha Ngesa kipo kwenye kifyatulio yaani triga,kitendo cha kidole hicho kurudi nyuma kilimaanisha risasi kuchomoka ndani ya chemba,Mzee Ikram alikuwa amekaa chini kitako.
“Nimekwambia simama”
Siyo kwamba Mzee Ikram hakutaka kusimama,hakuwa na nguvu za miguu.Ilibidi ajishike na kiti ndipo akapata nguvu.
“Usiniue”
“Ningetaka kukuuwa ningeshakuuwa muda mrefu sana,kompyuta yako iko wapi?”
“Iko iko chumbani kwangu,kile kule mwisho chumba changu”
“Twende”
Mzee Ikram mbele,Ngesa nyuma yake wakatembea mpaka chumba cha mwisho,wakaingia.
“Ile pale”
Akasonta kidole.
“Iwashe”
Jambo hilo ndilo lilifanyika,akasogelea kompyuta yake na kuiwasha.Baada ya sekunde arobaini kila kitu kikafunguka.
“Chukuwa hii namba nataka kujuwa huyu mtu alipo”
“Hapa siwezi mpaka kompyuta za ofisini”
Kauli hiyo ilimfanya Ngesa amsogelee karibu na kumgeuza, akamuwekea bastola kichwani.
“Usinijaribu”
“Sawa,sawa..Nipatie namba”
Mapigo ya mzee Ikram yalikuwa yanakita sio kitoto,alikiogopa kifo,alishindwa kuelewa mtu anayetafutwa Tanzania nzima alikuwa amefuata nini nyumbani kwake,akaingiza namba za simu ndani ya kompyuta.Akasimama na kutembea mpaka kabatini akachukuwa laptop akaiwasha pia,akawa mara abonyeze kompyuta mara Laptop.
“Ti tiiii”
Laptop ikatoa mlio.
“Nini hiko?”
Ngesa akauliza.
“Nimeingiza namba kwenye hii application kwenye kompyuta itakuwa vigumu na itachukuwa muda”
“Kwahiyo baada ya muda gani,nitapata jibu?”
“Dakika tatu”
“Okay”
Ni kweli baada ya dakika tatu juu ya kioo cha Laptop kulitokea ramani kubwa ya jiji la Dar es saalam,ikaanza kujivuta taratibu na kujichambua mpaka kilipotokea kidoti chekundu.mzee Ikram akabonyeza keyboard,akafanya utaalam wake.
“Mtu mwenye namba hii yupo Mabibo Makuburi Jeshini nyumba namba 10”
Hapohapo Ngesa akachukuwa simu na kutafuta majina,alivyofika jina LESLIE BENJAMIN akapiga.
“Vital Kamere”
Ilikuwa ni sauti ya upande wa pili ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupokea.
“Hallo Muheshimiwa Rais unaongea na Derick Ngesa naomba nikwambie kuwa Mh. Frank Man’sai hakufanya mauaji ya mdogo wako,hata mimi pia sihusik..”
“Ngesa Una…”
“Muheshimiwa Rais naomba nikwambie kwanini nimepiga simu hii,Mwanao Ritha ametekwa nyara yupo nyumba namba 10 Mabibo Makuburi na ukichelewa atakatwa kichwa”
“Ngesa jisalimishe mwenyewe”
“Muheshimiwa Rais mimi ninajisalimisha,nipo Maili moja”
“Naomba niongee na mwenye simu”
“Amefariki”
“Unasemaje?kivipi?”
“Mimi ndiyo nimemuua sababu alishiriki kufanya mauaji ya marehemu Tonny mdogo wako,Muheshimiwa Rais tafadhali naipenda nchi yangu na nitakuwa bega kwa bega nawewe kupambana mpaka dakika ya mwisho ya uhai wangu,Kwa sasa hivi fanya nilichokwambia”
“Wewe uko wapi?”
Ngesa akatoa maelekezo yote na sehemu aliyokuwepo.
“Sawa,ninatuma watu waje kukuchuwa usiondoke”
Simu ikakatwa na kumuacha Rais wa Jamhuri ya Muungano akiwa amechanganyikiwa,pembeni alikuwepo mke wake,kila alichokuwa anazungumza alikisikia.
“Vipi?”
“Derick Ngesa amenipigia simu”
“Ngesa?”
Mkewe akashtuka akatoka ndani ya shuka na kukaa kitako.
“Anasemaje?”
“Amesema kwamba Ritha ametekwa”
“Whaaat”(Niniii)
“Sasa usipaniki nishajuwa njama zake,kuna kitu anataka kukifanya.Ritha yupo shule sasa hivi,ningepigiwa simu na walimu.Subiri kanitajia alipo.Nisubiri kitandani”
Rais Leslie akatoka kitandani akavaa suruali haraka haraka na kutoka nje ambapo alikutana na mlinzi wake, wote wakatembea mpaka ofisini kwake,alikuwa yupo ndani ya ikulu na ilikuwa ina kila kitu.Akainua mkonga wa simu na kumtafuta IGP Lucas Marwa hewani.
“Hallo unaongea na Rais Leslie”
“Ndiyo Muheshimiwa Rais habari za majukumu ya ujenzi wa taifa?”
“Salama,naomba utume askari wako Maili moja”
“Eneo gani Muheshimiwa Rais?”
Haikuwa kazi ngumu kusema kila kitu na kutoa ramani ya sehemu Ngesa alipokuwepo,hakutaka kuyaamini maneno ya Ngesa kirahisi namna hiyo ndiyo maana akashirikisha jeshi la polisi ili wamtie mbaroni,bado alikuwa ana hasira na muuaji huyo.
“Sawa ngoja nipige simu maili moja niongee na Sajenti Nasri Mutukuzi”
“Sasa hivi,naomba nipate taarifa zake baada ya dakika kumi kuwa yuko mikononi mwenu!”
“Sawa Muheshimiwa rais”
Rais Leslie Benjamin akaweka mkonga chini akashusha pumzi ndefu za kuchoka,akarudi chumbani kwake.Macho yake yakagongana na mkewe, alikuwa akilia machozi yupo kitandani simu ipo pembeni.
“Nini tena?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Mh.Rais akimuuliza mkewe.
“Rithaaaa mwananguuu”
“Ritha kafanya nini?”
“Ha…yup..o Shu…leni”Akasema kwa kwikwi.
“Embu nieleze vizuri”
“Ritha hayupo shule,alichukuliwa na watu waliosema wametoka ikulu”
“Wakina nani?”
“Sijui,Mwanangu Rithaaa uwiiii”
Kilio kikazidi chumbani,hiyo ilimchanganya sana Rais.Akavuta simu na kuanza kusaka namba za uongozi wa shule akapata namba za mwalimu mkuu,Abdallah Henku kile alichoambiwa kilimchosha akili,hapohapo akamkumbuka Ngesa,bila kupoteza wakati akapiga simu tena makao makuu ya jeshi la polisi.
****
Kama kungekuwa na ndoo ya maji basi siku hiyo Ritha Leslie Benjamin angeijaza kwa machozi,alilia mpaka machozi yakamkauka.Mbele yake kulikuwa na wanajeshi watano,mmoja mwenye sura mbaya ameshika sime yenye makali na isitoshe mikono na miguu yake vyote vilikuwa vimefungwa juu ya kitanda,kichwa chake kimewekwa vizuri.Alikuwa keshajuwa tayari aina ya kifo anachoenda kupambana nacho mbeleni,kilikuwa ni kifo kibaya cha kuchinjwa kama kuku,akapiga picha jinsi kuku anavyotingisha miguu yake kabla ya kukata roho!
‘TOKENI HARAKA KIMENUKA,HAMISHENI KAMBI MNA DAKIKA KUMI,PITIENI NJIA YA EXTERNAL SISI TUNATOKEA HUKU MWANANCHI,MWAMBIE BRIGEDIA KARANJE,MIMI KOPLO BONIFAS’
Ulikuwa ni ujumbe uliosomeka juu ya kioo cha M.P Lewis Mwaipopo nayeye alikuwa ndani ya chumba kidogo ambacho yupo Mtoto wa Rais,ili akatwe kichwa.
Haraka akatembea na kumshika bega Brigedia Karanje ambaye alikuwa ameinua sime juu ili ashushe akitoe kichwa cha mtoto Ritha.
“Mkuu,tizama”
Akanong’ona kwa sauti ya chini masikioni mwa Brigredia Karanje!
“Imetoka wapi?”
Brigedia Karanje akauliza sura ilikuwa imejikunja kama shati lililotemwa kutoka mdomoni mwa Ng’ombe.
“Kwa Koplo Bonifasi”
“Shit,pakieni vitu haraka.Tuhame kambi,Mwambie Luteni Munisi atoke haraka sana na mabomu ya Nuclear pakieni kwenye gari twende Mbagala,fanya upesi”
“Mkuu”
“Nadhani nimeelew….”
“Na huyu mtoto?”
Hiyo ilimaanisha wamfanye nini Ritha,Brigedia Karanje akamtizama kwa kitambo na kuchomoa bastola kutoka kiunoni kwa nia ya kumfyatua.
“Huyu tunamuuwa hapahapa,kachakacha”
Bastola ikakokiwa,Ritha akawekewa bastola kifuani kwa nia ya kupigwa risasi.
“No,mfungue twende naye.Bado nina kazi naye”
Hapohapo akabadili mawazo yake,Ritha akafunguliwa haraka wakampakia ndani ya gari.
“Leta leta leta,ingiza hayo mabomu kwenye Hammer mpigie simu Daphine na mwenzake waje Mbagala,mtafute na Vital Kamere hewani”
Brigedia Karanje alizidi kutoa maagizo hayo huku akifunguliwa mlango wa gari la jeshi aina ya Hammer,akaingia ndani,gari ikawashwa,wakaondoka huku nyuma msululu mwingine wa magari ukifuata.
****
“Ova ova afande Mkude umenipata ndiyo tunapanda usesi ova”
“Kiish kiish ova ova nakupata sisi tushafika tayari”
“Kuna nini ova?”
“Bado hatujaingia ndani ova”
“Tusubirini ova”Yalikuwa mawasiliano kwa njia ya redio upepo.
Difenda kumi za Jeshi la polisi zilikuwa zinapanda kilima Mabibo,Usesi.
Ulikuwa ni usiku wa saa nane.Kauli kutoka kwa Rais Leslie ndiyo iliwapa mori kwamba waingie ndani ya nyumba waliyopewa ramani na kuiweka kati,kila kitu kikawekwa sawa jeshi la polisi likaingia kazini.Siku zote kwenye msafara wa mamba kenge hakosi sababu katika kikosi hicho askari mmoja wapo alikuwa amelitonya jeshi la Karanje na kuwaambia jinsi operesheni inavyokwenda ndiyo maana akatoa kauli kwamba waingilie njia ya usesi ili Brigedia Karanje na Jeshi lake watokee njia ya External.
‘TAYARI TUMETOKA,SHUKRANI’
Ujumbe aliotuma ulirudi,hiyo ilimfanya Koplo Bonifasi arudishe simu mfukoni.
“Tukifika hakuna kupoteza muda,Prosper na Afande baruti mtaingia kwa nyuma.Jombo na wenzako tutaingia getini wengine washafika.Kuweni makini”
“Sawa mkuu”
“Sawa Mkuu”Wote wakaitikia kwa pamoja.
Koplo Bonifasi ndiye alikuwa anaendesha operesheni hiyo ya kuwasaka watu waliomteka mtoto wa Rais, naye ndiye aliwatonya wakimbie.
Diffenda zikafatana spidi mia moja ishirini,huku zikiacha vumbi sio mchezo,zikapiga msele nje ya nyumba kubwa yenye geti zito lenye rangi ya kaki.Askari wakatua ardhini wengine wakazunguka nje ya nyumba,hawakutaka kupoteza wakati wengine wakapiga geti wakiwa na mitutu mikononi mwao,wakazama ndani.
Wakakagua kila mahali lakini hawakuambulia kitu chochote kile.
****
“Ngesa tunajua upo ndani na kwa usalama wako ujisalimishe,huwezi kwenda popote nyumba nzima imezungukwa na jeshi la polisi,jisalimishe mwenyewe”
Sauti ilipenya mpaka ndani sababu askari walitumia kipaza sauti maalum,lilikuwa ni jeshi kubwa la askari wasiopungua themanini na mbili.
Jinsi Ngesa alivyokuwa anafanya matukio ya kutisha walimuogopa ndiyo maana kila askari alishika mtutu na walikuwa nje,ni kweli nyumba nzima ilikuwa imezungukwa na jeshi la polisi,hakukuwa na namna ya Ngesa kutoroka na sauti hiyo aliisikia kutokea nje.
Hakuwa ana ujanja mwingine wowote.Alitamani kutoroka lakini alishindwa ilibidi asalim amri.Akamtizama Mzee Ikram,kisha kuanza kutembea ambapo alishuka ngazi taratibu na kutoka nje.Akakumbana na maaskari thelathini kidogo,hapohapo akapiga magoti na kuweka bastola chini,akalala kifudifudi,akaitandaza mikono yake huku na kule kumaanisha kwamba hatoweza kufanya lolote.
Askari watano wakamsogelea.
“Piga magoti”Askari mmoja akasema,Ngesa hakuwa mkaidi,akatii amri,akapiga magoti.Akawatizama askari wote,hapohapo akapigwa pingu kwa nyuma.
“UPO CHINI YA ULINZI”
Ngesa alikuwa chini ya ulinzi mkali,hakukuwa na njia yoyote ya kujinasua na kundi la jeshi la polisi sababu kila kona kulikuwa na mitutu ameelekezewa yeye.Akaingizwa ndani ya diffenda kwa nyuma, askari saba wakapanda.Kazi ya Ngesa ilikuwa ni kuangalia huku na kule mikono yake ilikuwa nyuma imefungwa pingu.
“Usijaribu kufanya kitu chochote kile cha kipumbavu”
Askari mmoja akapiga mkwara baada ya kumuona Ngesa anatizama huku na kule habari za mtu huyo hatari alizisikia,hapohapo akakoki mtutu wake na kumuwekea Ngesa kichwani ambaye alikuwa kimnya.Diffenda zikageuzwa kwa mkwara mzito tena na ving’ora juu,Ngesa akawa tayari yupo mikononi mwa sheria,moyo wake ulimuuma alivyomkumbuka mpenzi wake Jaqlin Mfinanga,alijionea huruma pia sababu alijuwa ni lazima angeenda kuchomwa sindano ya sumu ama kufungwa kifungo cha maisha tena kabla ya kufanikisha jambo lake, alijuwa kati ya vitu hivyo viwili moja lilikuwa lazima lifanyike,kichwa chake kiliwaza vitu vingi mno.
Diffenda za polisi zilizidi kuchanja mbunga,baadaye walifika kituo cha polisi Maili moja,Ngesa akashushwa na kuwekwa rumande, hata alivyotupwa maabusu ulinzi uliwekwa mara mbili yake.
“Afande Mkude,utakaa hapo Chacha utakaa nje na wengine watatu mkae hapa reception hakikisheni bastola zenu zina risasi za kutosha”
Yalikuwa ni maagizo kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi Maili moja baada ya Ngesa kuswekwa nyuma ya nondo!
***
“Ndio,sawa ahsante kwa taarifa”
Luteni Ibengwe alikuwa simuni,mbele yake alikuwa amesimama Daphine,Zaitun pamoja na Brigedia Karanje.Sura yake ilikuwa imebadilika baada tu ya kukata simu,alimtizama Daphine kwa macho ya huruma kisha kumgeukia Brigedia Karanje.
“Ibengwe kuna nini?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Brigedia Karanje sura ya Luteni ilikuwa ina ujumbe ambao haukuwa mzuri.
“Naweza kuongea nawewe kidogo nje”
Luteni akasema.
“Hapana ongea tu”
Luteni Ibengwe akamtizama Daphine aliyekuwa karibu naye anaangalia televisheni hana habari.
“Ni kuhusu Vital Kamere”
“Kafanya nini?”
“Amekutwa nyumbani kwake amekufa”
Kitendo cha kuongea hivyo kilimfanya Daphine ageuze shingo yake,mapigo yake ya moyo yakapiga paa! Kwa mshtuko, hakuelewa kwamba amesikia vibaya ama masikio yake yana uchafu.
“Anco Ibengwe,umesema kuwa?”
Daphine akauliza huku akimuangalia Luteni Ibengwe kwa umakini.
“Vital Kamere amefariki,amekutwa ndani kwake ameuwawa na inasemekana ni Ngesa”
Daphine aliganda kama barafu,mapigo yake yalimwenda mbio kifua chake kikawa kinapanda juu na kushuka pua zake zikawa zinamcheza akawa anatetemeka kwa hasira kama mtu mwenye kifafa,Vital Kamere alikuwa ni kama nguzo katika maisha yake,Mzee huyo ndiyo aliyemsaidia katika maisha yake mbali na hapo alikuwa ni zaidi ya ndugu kwake.
“No.. Da…d”
Akamwaga machozi.
“Daphine”
Brigedia Karanje akasimama,akamuendea na kumshika bega.
“Pole sana Daphine,nakuhakikishia kuwa mtu aliyefanya hivi tutamshika”
Daphine aliendelea kumwaga machozi tu yaliyochanganyika na hasira.
“Nani kam.u.uwa?”
Akauliza kwa kwikwi.
“Derick Ngesa”
Luteni akajibu.
“Yuko wapi?”
Akauliza swali lingine akiwa mwenye hasira za waziwazi,alitamani amtafute Ngesa wakati huohuo amtie mikononi mwake amfanye kitu kibaya lakini hakuelewa atampata vipi.
“Hap..ana ,lazima mimi nimtafute Ngesa kabla hajatiwa mikononi mwa Polisi”
Daphine aliapia kwa hasira na alimjuwa Ngesa kupitia vyombo vya habari.
“Daphine inabidi tumalize kwanza tulichokianza,tunaenda kutega bomu kesho pale mbagala rangi tatu”
Brigedia akasema na kutoka nje ambapo huko aliwapa maelekezo walinzi wake juu ya namna watakavyolitega bomu la kwanza la ‘Nuclear’ Mbagala rangi tatu,maelfu ya watu walikuwa ni lazima wafe baada ya masaa machache yajayo, hiyo ilikuwa ni kama kumpa ujumbe Mh.Leslie Benjamin.
***
“Imekuwaje mmewakosa na mwanangu je?kivipi?huo ni uzembe inspector.Namtaka Ngesa Ikulu sasa hivi.Ndio sasa hivi,yupo maili moja”
Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Leslie Benjamin alikuwa amechanganyikiwa kwa kiasi cha kutosha asubuhi hiyo akiwa kwenye mkonga wa simu,wahalifu waliomteka mtoto wake Ritha, hawakupatikana na mbaya zaidi mtoto wake pia hakuwepo hiyo ilimaanisha kwamba ni lazima wangemfanyia kitu kibaya hata hivyo hakuelewa kama mwanaye yupo hai ama mfu,hasira zake zote akazihamishia kwa Ngesa akili yake ilimwambia moja kwa moja kwamba Ngesa anashirikiana na watu hao ndiyo maana alimuhitaji Ikulu siku hiyo.
“Darling,vipi?Ritha amepatikana?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa mke wake baada ya kutokeza ofisini kwake.
“Bado wanamtafuta”
“Eh Mungu”
Mke wa Raisi alitokwa na machozi kwani alimpenda sana Ritha na ndiye alikuwa mtoto wake wa mwisho kumzaa,hilo ndilo lilimfanya aumie zaidi.
Siku hiyo Rais hakufanya kazi kabisa akili yake haikuwa sawa,alibaki na mkewe ofisini kwake ndani ya ikulu wakilia kwa uchungu huku wakimuombea Ritha awe salama huko alipo.
“Mheshimiwa Rais”
Mmoja wa walinzi akaingia ofisini,Mh.Leslie Benjamin akafuta machozi harakaharaka.
“Kuna nini Christian?”
“Ngesa anakaribia kufika,unahitaji tukuandalie chumba gani ili uzungumze naye?”
“Conference room namba mbili”
“Okay”
Rais Leslie bado hakupata jibu la kitu gani amfanye Ngesa endapo atakutana naye uso kwa uso.
“Christian”
Akamuita mlinzi wake kabla hajafika mlangoni.
“Naam Muheshimiwa”
“Nipe bastola yako”
“Hapana mtukufu siwezi”
“Mimi ni rais wako nimekwambia nipatie bastola yako”
“Hapana siwezi kufanya hivyo,kwa heshima ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Baada ya Christian kutamka hivyo akageuka na kuondoka zake huku nyuma akimuacha Mh.Leslie amekasirika vibaya sana na kama angepewa bastola siku hiyo angemfyatua Ngesa.
“Darling unataka kufanya nini?”
Mkewe akauliza.
“Sijui”Akajibu huku akiyabana meno yake.
Dakika thelathini baadaye walinzi wakaingia na kumuambia kwamba Ngesa yupo ndani ikulu,chumba alichotaka awekwe.
Akasimama kwa hasira na kusukuma mlango,akatembea mpaka chumba cha mkutano namba mbili.Alivyoingia, akakumbana na Ngesa akiwa amekaa amefungwa pingu kwa nyuma.Kwa adabu zote Ngesa akasimama na kumpa heshima yake Rais huku mikono ikiwa nyuma.
“Derick Ngesa,wenzako wako wapi?”
Lilikuwa ni swali la kwanza kulitupa Rais Leslie,akimtizama Ngesa kama chui mwenye njaa kali.
“Nakuuliza wenzako wako wapi?Mwanangu Ritha yuko wapi?”
Ngesa alimtizama Rais wake kwa umakini.
“Maili moja”Akajibu
“Shut up!Hawapo,nitajie walipo”
Rais akapiga meza kwa hasira mpaka mkewe aliyekuwa pembeni akaogopa mno.
“Mheshimiwa Rais,bado hujachelewa,Brigedia Karanje ndio kahusika na haya yote na ana mabomu ya nuclear is…”
Ngesa akatulizwa na kibao kikali kutoka kwa Rais,alivyotaka kumvaa tena ili ampige walinzi wakamshika.
“Muheshiwa Rais tafadhali punguza jazba”
“Christian niachie”
“Hiyo kazi tuachie sisi”
“Hapana nina sema hivi,nataka apelekwe gereza la Quantanamo,akafungwe huko.Christian naomba niunganishe na General sasa hivi.Kama tutapata ndege aende Cuba leo leo.Nitachapa barua sasa hiv..”
“Lakini..”
“Lakini nini Christian? fanya nilivyokwambia”
Hakukuwa na utani hata kidogo,kauli ilitoka kwa amiri mkuu wa Majeshi, Rais Leslie Benjamin na hicho ndicho kilikuwa kinaenda kufanyika.
Utaratibu ukafanyika,Rais akaandika barua na kutia sahihi kwamba Derick Ngesa asafirishwe nchini Cuba kwenye visiwa vya Quantanamo na huko ndipo gereza hilo lilikuwa na wafungwa sugu pamoja na mateso ya kila aina yalikuwepo.
***
“Naomba nipatie simu kama utaweza”
Alikuwa ni Ngesa anaomba simu afanye mazungumzo,machozi yalikuwa yakimlenga alitamani kulia,taratibu zilikuwa zipo tayari na ndege ya jioni ya saa kumi ilikuwa imepatikana,waandishi wa habari walikuwa nje ya geti wanapiga picha za mnato,siku hiyo vyombo vya habari mbalimbali kama magazeti,televisheni na redio topiki ilikuwa ni Ngesa.
“Tunaomba njia tafadhali”
Mmoja wa walinzi alisema baada ya kutoka nje.
“Naweza nikapata simu”
Ngesa akaomba tena baada ya kuhisi kama hajasikiwa,hakukuwa na kipingamizi akapewa simu ya mkononi ili aongee,hapohapo akamtafuta Jaqlin Mfinanga hewani.Kutokana na uzuni iliyokuwepo hawakuweza kuongea wakaelewana,Jaqlin alikuwa akilia machozi.
“Muda umekwisha,nipatie simu”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa simu ikachukuliwa,Diffenda zikaanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege mwalimu Nyerere ili Ngesa asafirishwe na taarifa kuhusu Ngesa zilikuwa zishatumwa nchini Cuba.
Dakika Arobaini baadaye diffenda za polisi zikapiga misele uwanja wa ndege.
“Nifuateni”
Ni askari mwingine ndiye aliyewapokea,Ngesa akashushwa ndani ya Diffenda mikono yake ikiwa na pingu kwa mbele nyuma anasindikizwa na maaskari wanne wakiwa na mitutu,wakaingia mpaka chumba maalum kwa ajili ya ukaguzi.Kila kitu kilivyoenda sawa,wakaingia ndani ya chumba kingine kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho.
****
“Buuuuuuu buuuuuuu”
Ulikuwa ni mlipuko mkubwa sana mpaka ikafanya ardhi itingishike,moshi mkubwa ulitanda hewani na milio kama ya mizinga ilizidi kusikika,ilikuwa ni Mbagala rangi tatu,mamia na maelfu ya watu walipoteza maisha kwenye mlipuko huo,wakazi wa maeneo jirani walianza kukimbia huku na kule sababu mabomu yaliendelea kufumuka,hali ilitisha sio kawaida ilikuwa ni saa kumi ya jioni.
Mbagala iligeuka ikawa kama siku ya kihama.Lilikuwa ni Bomu la ‘Nuclear’ lililotegwa na jeshi la Brigedia Karanje na tayari lilifumuka.
“Nitafutie Leslie Benjamin hewani”
Brigedia Karanje aliongea akiwaambia walinzi wake baada ya bomu hilo kufumuka,hapohapo akatafutwa Rais Leslie.
“Huyu Hapa mkuu”
Akapewa simu.
“Rais Leslie,ongea na binti yako”
Ritha akawekewa simu masikioni.
“Daaaad…….sasa sikiliza kwa umakini”
Brigedia Karanje akaingilia maongezi.
“Huo ni mwanzo tu,nadhani umesikia nini kimetokea Mbagala.Nina mabomu mengine ya Nuclear”
“Wewe ni Mwanaharamu gani?”
“Utanijua”
“Ala…tititi”
Brigedia Karanje akakata simu.
***
Rais Leslie alikuwa ni kama amerukwa na akili zake,alichanganyikiwa sio kawaida.Mlipuko uliotokea ulimuogopesha mno na simu aliyopokea ikamtisha zaidi hasa alivyosikia sauti ya binti yake,Ritha.
“Ngesa amefika wapi?”
Akamuuliza mlinzi wake.
“Ndio wapo uwanja wa ndege muheshimiwa”
“Sitisha zoezi ninamuhitaji hapa ikulu”
“Mheshimiwa umesema?”
“Nina muhitaji Ikulu sasa hivi”
Mlinzi akatoka nje ya ofisi na alivyorudi sura yake ilionesha kwamba hakukuwa na majibu mazuri.
“Vipi?”
“Geti limefungwa tayari”
“Hapana,fanya juu chini hiyo ndege isiondoke na Ngesa, ongea na Aviation Manager.Hiyo ndege isiruke.Muunganishe namimi”
Rais akasema.
****
Ngesa alikuwa dirishani ndani ya ndege siti namba 12E, hakutaka kuamini kwamba anaiacha ardhi ya Tanzania anaenda kufungwa nchini Cuba,hakuelewa kosa lake lakini aliamini kwamba Mungu yupo na ipo siku ukweli utakuwa wazi,alimuhurumia sana Mh.Frank Man’sai ambaye alifungwa gereza la Keko bila hatia.Vitu vingi sana alivikumbuka,pembeni yake kulikuwa na askari ambaye alichaguliwa kumsindikiza Ngesa.
“….Abiria wa shirika la ndege QATAR airways namba 1278L mnashauriwa kufunga mikanda kwani ndege inakaribia kuondoka, kwa niaba ya captain Leonard Mackdonald mnakaribishwa sana”
Sauti kutokea kwenye spika ilisikika kutoka katika spika, msichana mrembo alikuwa ameshika kipaza sauti lakini kabla ya kumalizia maelekezo mengine,akatokea msichana mwingine mrembo akaonekana kama anamnong’oneza masikioni.
“Saa ngapi?Sasa hivi? Sawa”Msichana mwenye kipaza sauti akajibu.
Yote yaliyokuwa yanaendelea Ngesa aliyaona na alivyochungulia dirishani aliona magari yenye ngazi yapo mlangoni tayari,wanaume watano waliovalia suti nyeusi wakawa wanapanda harakaharaka wakaingia mpaka ndani ya ndege,moja kwa moja mpaka kwenye siti aliyokuwa amekaa Ngesa.
“Derick Ngesa,sisi ni wapelelezi kutoka usalama wa taifa tufuate tafadhali”
“Vipi?”
Askari aliyekuwa pembeni ya Ngesa akahoji.
“Tumetumwa na Mheshimiwa Rais hatuna muda wa kupoteza,mfungue Ngesa pingu”
Ngesa akafunguliwa pingu mikono yake ikawa huru,haraka wakashuka kutoka ndani ya ndege wakatembea na kutoka nje mpaka kwenye maegesho ya magari,wakaingia.
Gari zikaondoka kwa kasi ya ajabu kuelekea ikulu ya rais.
Marcedez benz tatu zilikuwa katika mwendo usio wa kawaida,yalikuwa ni magari ya wapelelezi kutokea usalama wa taifa baada ya kutoka kumchukuwa Ngesa uwanja wa ndege na wangechelewa kidogo wangemkosa sababu ilikuwa ni lazima asafirishwe na kupelekwa nchini Cuba katika magereza ya Quantamano,lakini mambo yalibadilika ghafla.
Ndani ya kichwa cha Ngesa vitu vingi vilipita hakuelewa ni kwanini kitu hicho kimetokea,kilichomchanganya zaidi alivyoangalia nje,akaona kwa mbali kuna moshi mweusi angani,kuna kitu alianza kuhisi lakini hakuwa ana uhakika.Akabaki kimnya,kasi ya magari ilimtisha na yalikuwa yakiongozana,wakaipita barabara ya Mandera wakanyooka moja kwa moja,safari haikuishia hapo,gari zikapita njia za panya ili kufupisha urefu hatimaye wakaibuka Kigogo Mburahati,wakaanyooka moja kwa moja na kutokea Jangwani,wakati huo hakuna mtu yoyote yule aliyemsemesha mwenzake,ukimnya ndiyo uliokuwepo.Dakika ishirini baadaye magari yakasimama Ikulu,Magogoni.
Walinzi wakatokea na kuanza kukagua magari kwa kupitisha chuma chenye kioo chini.
“Kokoko”
Kioo cha gari kikagongwa na mmoja wa walinzi wa ikulu.
“Naenda kuonana na Rais,C.I.D”
Mmoja wa wapelelezi aliyeitwa Tesha alitoa kitambulisho na kumkabidhi mlinzi,hivyo ndivyo wote walivyofanya kabla ya kuingia,wote wakaruhusiwa na kuingiza magari ndani.
“Ngesa shuka tafadhali”
Ngesa akashuka,bado katika akili yake hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kinaendelea.
“Nifuate”
Watu wote walikuwa wamevaa suti nyeusi wamenyonga tai kohoni kama wakurugenzi fulani.Ngesa akafuata nyuma kama mkia ambapo kabla ya kuingia ndani walipita tena kwenye kimlango kidogo,wakavua vitu vyote vya chuma kama Saa,mikanda na bastola zao wakaviweka kwenye vikapu kisha wakapita katika mashine hiyo.
Wakaingia mpaka ndani ya chumba kilichoandikwa ‘Conference room’yaani chumba cha mkutano kwa Kiswahili.Dakika moja baadaye mlango ukafunguliwa,Rais Leslie Benjamin akaingia, wote wakasimama kumpa salam kwa heshima.
“Naomba niongee na Ngesa”
Rais Leslie alisema akimaanisha kwamba anahitaji faragha.
“Christian usijali,hata wewe pia”
Christian ndiye alikuwa mlinzi wa karibu wa Rais hata yeye hakutakiwa kwa wakati huo,wote wakatoka wakabaki Ngesa na Rais Leslie peke yao.
“Ngesa”
“Muheshimiwa Rais”
“Kuna bomu limetegwa na limelipuka tayari,nina amini maelfu ya watu wamekufa Ngesa.Ningejua ningekusikiliza,nina amini kuna kitu unakifahamu.Nilipigiwa simu na watu waliotega hilo bomu na hao ndio wana mtoto wangu Ritha,Ngesa nahitaji msaada wako”
“Msaada gani?”
Ngesa akauliza sura yake ilikuwa makini kidogo, akimuangalia Rais wake usoni aliyekuwa ana hofu kuliko kawaida.
“Kuna bomu lilitegwa Mbagala,limelipuka na limeua mamia na maelfu ya watu.Nina amini kuna kitu unakijuwa.Leo nimepigiwa simu,nikaongea na Ritha.Hao watu ndiyo hao wenye hayo mabomu”Mh Rais akarudia tena.
“Naomba nikwambie kitu kimoja Muheshiwa Rais,watu wanaofanya hivi wana nguvu sana na kiongozi wao mimi nawewe tunamfahamu”
“Ni nani?”
“Brigedia Amir Karanje”
Mapigo ya moyo ya Mh.Rais yaliongezeka kwa kasi,alihisi joto kali.Jina hilo halikuwa ngeni kwake na isitoshe alikuwa ni mtu hatari kuliko maelezo licha ya yote miaka ya nyuma walikuwa marafiki wakubwa sana.
“Lakini hujachelewa Muheshimiwa,bado tuna muda”
“Tunafanyaje Ngesa?Nakuomba uingilie kati.Unahitaji msaada gani?”
Kwanza Ngesa alivyosikia hivyo hakujibu kitu,ilionekana kuna vitu alikuwa anavichambua kichwani kwake,akamtizama Rais Leslie kwa kitambo kidogo.
“Nipo tayari,nina hitaji silaha ndogo,na magazine za kutosha,gari ndogo na kitu kimoja Muheshimwa Rais”
“Kitu gani?”
“Naomba Mheshimiwa Frank Man’sai awe huru,hana hatia na sitaki jeshi la polisi lijuwe hii operesheni naomba niifanye mwenyewe”
Ni kweli Ngesa alikuwa ana usongo wa kumuweka Brigedia Karanje mikononi mwake,mateso aliyopewa miaka mingi iliyopita bado aliyakumbuka.
Rais Leslie hakuwa ana kipingamizi chochote kile akatoka nje na baadaye alivyotokeza alikuwa ana mlinzi wake Christian ameshika begi,akaliweka mezani.
Ngesa akalichukuwa na kulifungua,ndani alikumbana na silaha za moto akachukuwa bastola.
“Kacha kacha”
Akaikoki na kuangalia ndani ya begi ambapo alikumbana na risasi za kutosha,visu vidogo kifupi lilikuwa ni begi lililojaa vifaa vyote vya kijasusi.
“Nahitaji na simu”
Kila alichokitaka alipatiwa na hivyo ndivyo ilivyokuwa,akakabidhiwa funguo za gari na kuanza kuelekea mlangoni kwa hasira huku akiyabana meno yake.
“Ngesa”
Kabla ya kufika mlangoni,akasikia sauti ya Rais Leslie akasimama na kugeuka.
“Nashukuru sana,kila la kheri”
Ngesa alimtizama Rais Leslie lakini hakujibu chochote, alitingisha kichwa kumaanisha kwamba kila kitu kipo sawa,akasukuma mlango na kutoka nje,mlinzi akamfikisha mpaka kwenye gari aina ya BMW X5 nyeusi na hata vioo vyake vilikuwa vyeusi yaani tinted!Akaweka begi ndani pembeni ya kiti na kuingia.
Akawasha gari na kulitoa nje ya ikulu, akili yake ilimpeleka moja kwa moja kwa Hafidh J. Ikram,mkurugenzi wa mtandao wa simu wa Fabbycom,alielewa kwa kufanya hivyo ndiyo ataweza kujuwa ni wapi Brigedia Karanje alipo.
****
Ulikuwa ni msiba uliotingisha jiji la Dar es salaam na mikoa jirani kwa ujumla,kifo cha Vital Kamere kiliwafanya watu wengi wadondoshe machozi.Hakuna mtu aliyejuwa nini hasa kilichofanya majambazi wamvamie na kumuuwa nyumbani kwake,kila mtu alikuwa katika kitendawili.Katika watu waliobanwa na uchungu wa kulipa kisasi ni Daphine akiwa pembeni ya wazazi wake,Hans na Beatrice.Wote walikuwa wakilia na kusaga meno,siku iliyofuata ikawa hivyohivyo.
“Aliyemuuwa Dad ninamfahamu ni lazima nitalipa kisasi”
Daphine aliapia akimwambia, Hans.
“Ni akina nani?”
“Ni Ngesa”
Siyo kwamba Hans hakumfahamu Ngesa na hakumsikia kwenye vyombo vya habari kwamba anatafutwa kwa wudi na uvumba lakini hakuwa ana uhakika kama ndiyo huyo Ngesa anayemfahamu yeye wakiwa mkoani Morogoro akamkabidhi mtoto mchanga ambaye ndiye Daphine,sura aliyokuwa anaiona kwenye vyombo vya habari ndiyo ilikuwa hiyohiyo.
“Umesema Ngesa!Huyu anaetafutwa?”
“Ndiyo Baba”
Katika watu waliokuwa wanajua historia nzima ya Daphine ni Ngesa peke yake na huyu leo hii anafanya mauaji ya kutisha,hivyo ndivyo wote walivyodhani kwamba ni jambazi sugu.
“Polisi wanajuwa?”
“Ndiyo wanajuwa”
“Basi ni lazima atashikiliwa tu”
“Lakini nitahakikisha nitampata mimi kwanza kabla ya polisi”
****
“Sawa ndiyo natoka kazini sasa hivi,ninakuja kwenye kikao.Kumetulia lakini nina wasiwasi,labda kuna mabomu mengine.Sawa ninakuja”
Alikuwa ni Hafidhi J.Ikram,ametoka ofisini yupo ndani ya gari.Hata yeye alikuwa ana wasiwasi mno,mabomu yaliyofumuka dakika thelathini zilizopita yalimtia hofu sana.Akawasha gari,kabla ya kuweka gia akahisi kichuma kimemgusa nyuma ya utosi,akashtuka na kuangalia kioo cha katikati sura aliyoina nyuma ilimuogopesha.
“Tulia hivyo hivyo”
“Ng..esa Ngesa”
“Nataka kujuwa Karanje alipo”
“La la la lakini si nilishakwambia”
“Fungua laptop yako unitajie sasa hivi,fanya upesi”
Ikram kwa hofu ya kifo alivuta laptop yake iliyokuwa pembeni ya kiti,hakutaka kujiuliza mtu huyo kaingia vipi ndani ya gari lake,akafata maagizo yote kwa kuwa namba hiyo ilikuwepo kwenye laptop ilikuwa rahisi, ndani ya dakika tano akawa tayari keshajuwa ni wapi Brigedia Karanje alipo.
“Yupo Kawe,Mwisho.Pale msikitini kwa nyuma”
Ngesa akamtizama Ikram na kuvuta ‘Laptop’akashuka nayo mpaka upande wa pili ambapo ndipo alipoliacha gari,akawasha na kulitoa kwa kasi!
Akilini mwake aliwaza vitu vingi sana,kwanza amkomboe mtoto wa Rais kisha ajuwe mabomu mengine ya ‘Nuclear’ wapi yalipo kisha baada ya hapo apambane na Brigedia Karanje kiume,alikanyaga mafuta mpaka alivyofika Mwenge mwisho akanyoosha mguu na kuvuka mataa,akaipita Lugalo, baada ya mita chache akakunja kulia,hazikupita hata dakika tatu akawa amefika Kawe mwisho,akavuta Laptop na kuitizama.Upande wake wa kushoto ndipo kulipokuwa msikitini,akazungusha usukani na kuingia katikati ya mitaa ya uswahilini akizidi kuifuata ramani.Akaangalia vizuri,kulikuwa kuna nyumba ndogo hapo ndipo alama ilipodondokea,hakuwa ana uhakika sana lakini hakuwa na jinsi.Akaweka bastola vizuri kiunoni na kushuka,akatizama huku na kule na kuanza kutembea kuelekea ndani ya nyumba hiyo,ambayo ilikuwa imechoka.
***
“Kesho kuna mechi ya Simba na Yanga wanacheza uwanja wa Taifa,Salim hakikisha hufanyi makosa.Familia yako itaishi vizuri ninakuhakikishia hilo”
Yalikuwa ni maneno mazito kutoka kwa Brigedia Karanje,mbele yake alisimama kijana mweupe mwenye asili ya kiarabu anapewa maelekezo, ilikuwa ni lazima ajitoe muhanga ili maelfu ya watu wafe katika uwanja wa Taifa,hilo lingekuwa ni pigo lingine la nchi ya Tanzania kama swala hilo lingefanikiwa,tayari walishatega bomu moja Mbagala na liliuwa watu wengi,ilikuwa ni lazima Brigedia Karanje amfunze adabu Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kulivyopambazuka kazi ilikuwa ni moja tu,kuandaa mabomu na kuweka kila kitu sawa.Hivyo ndivyo ilivyokuwa.Ilivyofika saa kumi na moja jioni Salim akawa amefika ili abebeshwe mabomu ya Nucler,kila kitu kilipangwa na mlinzi aliyekuwa analinda siku hiyo geti la uwanja wa Taifa alipewa taarifa hizo,jambo hilo lilipangwa kiu taalam zaidi na kila kitu kilisukwa ipasavyo,Brigedia Karanje alikuwa ana mtandao mkubwa kupita kiasi.
“Hili hapa begi.Najuwa una hofu lakini tambua kwamba kifo chako kitakuwa cha tofauti sana,utakufa kishujaa”
Brigedia Karanje alikuwa anampa maneno ya mwisho Salim,akamwambia kwamba mwisho wa siku kila mtu atauonja umauti.Maneno hayo kidogo yakamfariji lakini sio sana,kifo alichokuwa anaenda kukumbana nacho kilikuwa cha kutisha.
“Sawa”
Alijibu kwa hofu huku majasho yakimtoka.
Wakati hayo yanazungumzwa Ritha alikuwa pembeni amefungwa mikono na miguu yupo juu ya kiti,mdomoni amewekewa kitambaa,hawezi kuongea chochote lakini alikuwa anasikia kila kitu.Alivyoangalia pembeni yake aliona paji la uso wa mtu,akichungulia.
Alikuwa ni Ngesa tayari ameshafika ndani ya nyumba hiyo,akaweka kidole chake kimoja mdomoni kumaanisha kuwa Ritha anyamaze kimnya sababu ndiye yeye peke yake aliyemuona.
“Zai”
Brigedia Karanje akaita,akatokeza binti mwingine wa makamo mbele yake.
“Hakikisha unakaa hapa,mimi natoka naenda kwenye msiba”
“Sawa Mkuu”
“Salim.Kazi njema”
Brigedia Karanje akachukuwa bastola yake kisha kuanza kutembea,Ngesa alivyoona hivyo akarudi nyuma na kujificha nyuma ya mlango akatulia.Alitamani amvae lakini hakuweza sababu angeharibu kila kitu,ilibidi afanye jambo moja baada ya jingine.Brigedia akatoka nje akifuatiwa na Salim.Hapo ndipo Ngesa akachomoza akashika bastola yake vizuri mkononi.
“Tulia hivyohivyo”
Zainab alisikia sauti hiyo akashtuka, alivyogeuka nyuma akakumbana na mdomo wa bastola.
“Kaa chini”
Ngesa akatoa kauli kwa sauti ya hasira.
“Tata..fadhali usiniue,usiniu.. e ta..tafadha..li”
Sio kwamba Zainab alikuwa anatetemeka kwa hofu bali alikuwa akifanya maigizo,ulikuwa kama mtego anautega ili Ngesa azubae kwani nayeye katika maswala ya ndundi alikuwa mzima.Ngesa alikuwa ameishika bastola anamtizama msichana huyu mdogo mwenye hofu sana,alielewa kwamba hakuwa ana hatia,taratibu akaanza kushusha mkono chini.
“Kaa pale”
Ngesa akatoa amri hiyo na kuweka bastola kiunoni hakuelewa kwamba anafanya kosa kubwa la jinai, akamsogelea Ritha na kumfungulia kamba za miguu na mikono,kitendo cha kugeuka alikutana na teke la shingo akayumba na kudondoka chini chali.
Akachomoa bastola lakini kabla ya kufanya chochote ikapigwa teke ikadondoka kando,Zainab akakunja ngumi tayari kwa mpambano,Ngesa akasimama kwa kasi ya umeme na kukaa sawa,akaona ngumi inakuja kulia akahepa kushoto ngumi ya Zainab ikapita hewani,alivyorudi sawa akatulizwa na teke aina ya ‘round kick’ akadondoka juu ya stuli,kama mzigo.
Ngesa akajuwa tayari mtu anayepambana naye sio wa mchezomchezo kwahiyo alitakiwa awe makini kupita kiasi,akasimama tena na kumuangalia Zainab machoni,akamuangalia jinsi alivyokaa akajuwa ni aina gani ya mchezo wa ngumi anaoutumia,ulikuwa ni mchezo hatari wa Judo.Ilibidi nayeye ajiongeze,Ngesa akatisha kama anarusha ngumi ya kushoto,Zainab akayumbisha kichwa chake alivyorudi alipigwa ngumi kali ya pua,Ngesa hakufanya makosa.Hapohapo akamvuta karibu na kum-mtwanga kichwa cha pua tena,damu zikaruka.Tayari pua ya Zainab ilikuwa imepasuka,akamvuta tena karibu akampiga kifuti cha tumbo kwa hasira.Akamzungusha na kumtandika ngumi nyingine za uso,kufumba na kufumbua uso wa Zainab ulikuwa umelowa damu,Ngesa hakuishia hapo.Akamvuta karibu na kuanza kumkaba shingoni ili amuuwe,lakini alivyomtizama Ritha alisita kufanya hivyo sababu alikuwa bado mtoto mdogo kuona tukio kama hilo.
Hata hivyo alikuwa anatakiwa kuwahi uwanja wa taifa ili kuokoa maelfu ya watu,bila kufanya hivyo bomu lingetegwa na usiku huo watu wangekufa.
Zainab akatupwa pembeni,Ngesa akaokota bastola yake,akamchukuwa Ritha harakaharaka wakatoka nje,wakaingia ndani ya gari,akachukuwa simu na kumtafuta Mh.Rais hewani.
“Mheshimiwa Rais,nipo na mwanao Ritha yupo salama.Lakini sina muda wa kupoteza kuna bomu linaenda kutegwa uwanja wa taifa,nitakuwa hapo ndani ya dakika kumi”
“Nitatuma watu uwanja wa Taifa.Naomba nizungumze na Ritha”
“Sawa”
Ritha akapewa simu.
“Daaaad!”
“Are you okay my lovely Daughter?”(Upo salama mwanangu kipenzi)
“Yes Dad,I’m okay but I’m scared”(Ndio baba nipo salama lakini ninaogopa)
“It’s okay,you don’t have to be scared.You are safe now”(Usiwe na wasiwasi kwa sasa,upo salama)
“Okay Dad”
“See you soon”
“Okay”
Simu ikakatwa!
“Ritha funga mkanda”
Ilikuwa ni kauli kutoka kwa Ngesa kumaanisha kwamba mwendo atakao toka nao hapo hautokuwa wa kawaida,Ritha akatii amri,Ngesa nayeye akafunga mkanda akaweka gia.Ni kweli jinsi alivyolitoa gari ilifanya vumbi litimke na kufanya watu wasionane.Akaingiza gari barabara ya lami bila kupunguza mwendo,ilikuwa ni lazima awahi uwanja wa taifa.
****
“Leo mnakula hiiizoooooo,tatuuu. Kum**** make...Sisi ndiyo wa kimataifa.Wase*** nyie”
“Wa Kimataifa wapi,hamna lolote.Subiri tuone”
“Tatizo nyie Simba hamna kitu chochote juzi mmefungwa tano na wale watoto wadogo.Tena leo kuna Simon Msuva,kuna huyu Hamis Tambwe.Hamuwezi kutoka”
“Wacha maneno mengi Samofi”
Siku zote mechi hiyo ikichezwa ilikuwa ni lazima itokee vuta n’kuvute,barabarani watu walipuliza mavuvuzela,bodaboda zilikuwa zinapiga kelele usiseme.Ingawa mechi hiyo ilikuwa inachezwa usiku wa saa mbili kwenye uwanja mpya lakini watu walitaka kushuhudia,kila kona ya jiji vichwa vya habari vilikuwa Simba na Yanga.Hawakujuwa kwamba siku hiyo kulikuwa kuna bomu kubwa linategwa na watu wangekufa,kifupi walikuwa wanakifuata kifo!
****
Saa kumi na mbili na nusu Jioni BMW X5 ilipiga msele nje ya Uwanja mkubwa wa Taifa,Ngesa akashuka.Kulikuwa kuna umati wa watu sio mchezo,mashabiki walikuwa wakipigania tiketi kuliko kawaida,haikuwa kazi rahisi kwa Ngesa kumuona Mwarabu aliyekuwa ameshika bomu,akaangalia huku na kule lakini wapi!
“Grii griii”
Simu yake iliita na aliyekuwa anapiga ni Rais Leslie,vijana wake walikuwa tayari wamefika.Alichofanya ni kusema alipo,watu watatu wakamfuata akamkabidhi Ritha mikononi mwao.
Kazi yake ikaendelea,watu walizidi kuingia ndani ya uwanja.Macho yake yakatua kwa kijana mweupe mwenye asili ya kiarabu mkononi alikuwa ana begi,sura hiyo aliikumbuka vizuri sana na alikuwa getini tayari anaingia ndani ya uwanja.Ngesa akaanza kutembea harakaharaka ili amzuie asiingie lakini alipigwa kikumbo kikali na baadhi ya mashabiki waliokuwa wanakata tiketi,kuja kutahamaki tayari Salim alikuwa ameingia ndani ya uwanja wa taifa ambao ulikuwa una watu sio chini ya elfu moja,hakuelewa angempata vipi na kuokoa roho za watu wasiokuwa na hatia!
Ukweli ulikuwa ni kwamba juhudi zake ndizo zingeokoa maisha ya maelfu ya watu waliokuwa ndani ya uwanja wa taifa wanaangalia mechi ya Simba na Yanga,maisha ya watanzania waliokuwa ndani ya uwanja huo yalikuwa mikononi mwa Salim aliyekuwa tayari yupo ndani na bomu kubwa ambalo lingefumuka watu wangegeuka na kuwa vipisivipisi,hata Ngesa mwenyewe alianza kuogopa,alidhamiria kufa na watanzania wenzake endapo bomu hilo lingelipuka.
Kilichomtisha zaidi watu walikuwa wanazidi kuingia ndani ya lango la uwanja wa taifa,hakuwa ana tiketi mfukoni wala pesa ya kununua ilikuwa ni lazima atumie akili ya kuzaliwa,akatembea karibu na mkusanyiko wa watu,akamuona kijana mmoja mdogo anaweka tiketi yake mfukoni,akamvuta na kumpiga mtama mkali,kabla ya kijana huyo kuinuka akamzaba kofi la uso,akawa anaona nyotanyota.Alivyofumbua macho yake hakumuona mtu yoyote yule.Ngesa alikuwa tayari amejichanganya katikati ya umati wa watu waliokuwa getini wanaonesha tiketi zao.
“Wewe onyesha tiketi,tumieni ustaarabu basi.Embu rudini nyuma”
Mlinzi wa getini alikuwa ana kibarua cha kuongoza watu,staili ya kupita ilikuwa ni kupanga mstari kisha kuonesha tiketi,Ngesa nayeye alijipachika kwenye mstari,akatoa tiketi na kuingia ndani.Cha kwanza alichofanya ni kupiga jicho juu ya uwanja.
“Mungu wangu”Alishangaa.
Watu walikuwa ni wengi kupita kiasi endapo bomu hilo lingelipuliwa basi Tanzania nzima kila nyumba ingepatwa na msiba mzito,akazidi kupepesa macho yake huku na kule,akimtafuta Salim mwarabu aliyekuwa ameshikilia begi lenye bomu,haikuwa kazi rahisi hata kidogo.Kulikuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu.
***
Alihisi maumivu makali puani na mgongoni kipigo alichokopea kutoka kwa Ngesa kilitisha,hakutegemea kama mtu huyo alikuwa shupavu tena ngangari kuzidi yeye,akili yake ilivyokaa sawa akasimama na kwenda kwenye kiti kisha kuketi,akaanza kutafakari ni kitu gani atamweleza Brigedia Karanje amuelewe,alijuwa nini kingetokea endapo angemwambia kwamba alivamiwa na Ritha akachukuliwa tena kirahisi,akafikiria bila kupata jibu.Katika kutafakari akapata jibu la njia gani atumie,ilikuwa ni lazima kwanza amshirikishe rafiki yake Kipenzi, Daphine!Akachukuwa simu na kuanza kumtafuta hewani.
“Daphine upo wapi?”
Simu ilivyopokelewa bila salamu akauliza.
“Nipo msibani,vipi Zaitun?Upo sawa?”
Kuna kitu Daphine alihisi,sauti ya Zaitun haikuwa sawa ndiyo maana akahoji.
“Ndio….hapana”
“Kuna nini?”
“Ngesa alikuja hapa”
Kitendo cha Zaitun kuongea hivyo ukimnya ukatokea wa kama sekunde kumi nzima,Daphine alikuwa kimnya.
“Hallo,Daphine”
“Halloo”
“Zaitun,ulisema Ngesa alifika hapo?”
Hakutaka kuongea jambo hilo hadharani,alihitaji faragha ndiyo maana akatoka nje ya geti ili aongee vizuri na Zaitun,jina la Ngesa liliibua hasira zake,alivyokumbuka kifo cha Vital Kamere, akapandisha mori zaidi.
“Ndio”
“Amekufanya nini?”
“Daphine njoo kawe tafadhali,nakuomba”
“Sawa nakuja”
Simu ikakatwa na kumuacha Daphine anashusha pumzi ndefu za kuchoka,akabana meno kwa hasira na kurudi ndani ambapo aliaga kwamba anaenda kuwapokea wageni wanaokuja msibani.Kwa mwendo aliotoka nao haukuwa wa kawaida,alitembea kwa hatua tatu tatu mpaka ndani ya gari lake,akaliwasha na safari ya kwenda Kawe kuanza mara moja.
Safari nzima alikuwa akimuwaza Ngesa alitamani kukutana naye am-malize tena kabla ya maaskari kumtia mikononi mwake.Dakika arobaini na tano baadaye akawa amefika akaweka gari kando na kushuka,akaingia ndani ya nyumba ndogo ambapo humo ndipo alikuwa amehifadhiwa Ritha,mtoto wa Rais Leslie.Picha aliyoikuta ndani ilimuogopesha vitu vilikuwa shaghala baghala,Meza imetupwa pembeni,viti vimebinuliwa na chini kuna michirizi ya damu,Zaitun alikuwa pembeni anavuja damu puani.Akamsogelea kwa haraka.
“Zaitun”
Akamkumbatia.
“Ngesa alikuja hapa”
“Ritha yuko wapi?”
“Hayupo”
“Ngesa ndiyo kaondoka naye?”
“Ndio”
“Shiiit”
“Lakini ninajuwa alipoenda”
“Wapi?”
“Uwanja wa taifa,ameenda kumfuata Salim”
“Niniiiiiii?”
“Ndio Daphine,tafadhali naomba usimwambie mkuu”
Kitendo Cha Ritha kukosekana hata Daphine kilimtisha alijuwa nini kingemkuta Zaitun kwa uzembe kama huo ambao ulikuwa mwiko kwa Brigedia Karanje,japokuwa alisikitika lakini hakutaka kulionesha swala hilo waziwazi,alitaka kumfariji Zaitun.
“Usijali,twende uwanja wa taifa.Mimi ninamuhitaji Ngesa kwanza”
Chuki yake ilikuwa kwa Ngesa na aliamini kwamba atamuweka mikononi mwake hapo ndipo atajuwa cha kumfanya,akatembea mpaka kwenye kabati na kuchukuwa bastola, akaichomeka kiunoni na kuifunika na fulana aliyovaa.
“Twende”
Wote wakatoka na kuingia ndani ya gari,safari ya kwenda uwanja wa taifa ikaanza mara moja,barabara haikuwa na msongamano wa magari siku hiyo ndiyo iliwafanya wapete barabarani na ndani ya dakika thelathini na mbili waliweka gari kando ya uwanja wa taifa,bado watu walikuwa wengi kupita kiasi na mechi ilikuwa tayari imeanza kuchezwa,wakakata tiketi na wao wakaingia ndani,kumsaka Ngesa!
***
Ngesa bado aliendelea kumtafuta Salim,macho yake ilibidi ayapitishe kwa kila mmoja wao ndani ya uwanja,haikuwa kazi rahisi hata kidogo.Mechi ilikuwa imeanza tayari,siku hiyo hata yeye alikuwa akiyapigania maisha yake kitendo cha bomu kulipuka hata yeye angekuwa majivu.Macho yake yakatua kwa mwarabu mweupe lakini alikuwa mbali sana upande wa mbili,kibarua cha kuzunguka upande wa pili kilikuwa kizito na jambo hilo lingemchukuwa muda mrefu sana mpaka kumfikia,ni kweli mtu aliyemuona alikuwa ameshika begi mkononi mwake.
“Samahani naomba kupita”
Ngesa akaomba njia na kuanza kuwapangua watu,macho yake yote yalikuwa kwa Salim.
“Naomba njia naomba njia,naomba kupita”
“Kaka unanikanyaga bwana,mbona hutulii?”
Mtu mmoja alilalamika lakini Ngesa hakumjali,akaendelea kusonga mbele kwa staili ya kuwasukuma watu,hatimaye akafika upande wa pili.Mita kama tatu zilibaki ili amfikie,akatembea taratibu mpaka pembeni yake na kuanza kumuangalia vizuri.
“Mkubwa”
Ngesa akamgusa begani.Salim aligeuka lakini hakujibu chochote, usoni alikuwa ana majasho yanamtoka.
“Mambo vipi?”
“Poa”Akajibu kwa mkato.
Ngesa alitafakari kwa muda kidogo ni kitu gani akifanye,ilikuwa ni lazima jambo hilo alifanye kimnyakimnya bila ya watu kujuwa chochote.Mkononi mwa Salim kulikuwa na rimoti ndogo yenye kitufe chekundu,kitendo cha kubonyeza kitufe hiko bomu lingelipuka hapohapo.Ngesa akamuangalia vizuri,akauangalia mkono wake.Akasogea karibu yake zaidi!
“Kaka”
“Nini?”
Kitendo cha Salim kugeuka Ngesa aliudaka mkono na kumpiga kichwa cha pua cha nguvu,rimoti ikadondoka chini.Ngesa akaiwahi na kuishika alivyotaka kujaribu kukaa sawa alipigwa teke na Salim, akadondoka juu ya mgongo wa shabiki aliyekuwa anaangalia mechi.Salim akajuwa tayari mambo yameharibika alitaka kukimbia lakini Ngesa akasimama haraka na kuanza kumfuata,kabla hajafika mbali akamkata mtama,Salim akadondoka chini.
“Simama haraka”
“Kaka vipi?”
“Simama”
Akaongea kwa ukali,hakuna mtu yoyote aliyekuwa anajuwa kwanini watu hao walikuwa wanakimbizana na kupigana,kutokana na mechi hiyo kunoga waliwaacha kama walivyo.
Wakati Ngesa na Salim wanakimbizana Daphine na Zaitun walikuwa tayari wameingia ndani ya uwanja wa taifa,wao walikuwa wakimsaka Ngesa kwa wudi na uvumba walikuwa wapo radhi kumtoa mtu mmoja mmoja nje mpaka Ngesa apatikane.Daphine alivyoangalia upande wa viti vya juu aliona watu wameshikana mashati,akaangalia vizuri.Alikuwa ni Ngesa tayari alimuona bila chenga,hapohapo akaanza kuwapangua watu niya yake ilikuwa ni kumfuata na kuanzisha fujo,hasira alizokuwa nazo hazikuwa na kipimo.Alivyofika alipomuona Ngesa alisimama na kuanza kumsaka tena,akaangalia huku na kule na kumuona anatoka nje ya lango akiwa na Salim,bila kupoteza muda nayeye akaanza kufuata lango la kutokea.
Salim alikuwa amekunjwa shati na kitendo cha kutoka nje ya geti alitulizwa na kichwa kizito cha pua Ngesa alikuwa hodari wa kupiga vichwa watu,akavutwa mpaka upande yalipokuwa yamepaki magari.
“Paaaa paaaaa”
Ulikuwa ni mlio wa risasi,hizo zilipita na kumkosakosa Ngesa zikapasua kioo cha gari,alivyogeuka akamuona Daphine akiwa na Zaitun wote wameshika bastola.
“Ingia ndani ya gari”
Ngesa akamuingiza Salim ndani ya gari,akazunguka haraka upande wa pili.
“Paaaaa”
Risasi nyingine ikachomoka,watu waliokuwa pembeni kila mtu alitafuta usawa wa maisha yake,wauza ice crim kwenye madeli waliacha baiskeli zao na kuanza kukimbia, wauza tiketi walitimua mbio sio kawaida.Risasi zilianza kurindima.Kitendo cha Ngesa kuingia ndani ya gari,alilirudisha nyuma kama kichaa.Hiyo haikufanya Daphine asitishe kurusha risasi.
“Paa paa paaaaa”
Vioo vilikuwa vinapasuka Ngesa alikuwa amelaza kichwa chake chini lakini anarudisha gari kinyumenyume.
“Puuuu”
Akagonga gari la nyuma yake,akaweka gia na kuligeuza gari harakaharaka.Daphine na Zaitun hawakuishia hapo,walikimbia na wao kwenye gari na kuanza safari ya kumfukuza Ngesa.Ilikuwa ni kama sinema ya kuigiza lakini ndiyo ukweli.
“Mabomu mengine yako wapi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ngesa akimuuliza Salim aliyekuwa pembeni yake,mikono ipo juu ya usukani.Tayari alikuwa ameokoa roho za watu ilikuwa ni lazima ajuwe mabomu mengine yalipo sababu yalikuwa yana uwezo wa kuteketeza mamilioni ya watanzania.
“Sijuiii sijuiii”
Kama umeme Ngesa akachomoa bastola kiunoni.
“Paaaaa”
Risasi ilipenya mguuni kwa Salim,hiyo ilimaanisha kwamba hakukuwa na muda wa kupoteza.Salim alipiga kelele nyingi za maumivu na damu zilimtoka.
“Nyingine nafumua kichwa chako,Mabomu mengine yako wapi?”
Bastola ilikuwa tayari kichwani kwake.
“Mi..mi sij…iu.Sijui”
“Mabomu mengine yako wapi?”
Ngesa alivyoangalia kioo cha nje aliona gari nyuma yake linakuja kwa kasi ya umeme,alijuwa hao ni wakina Daphine, kabla hajafanya lolote,alisikia milio ya risasi.Akakanyaga mafuta mengi,akaona kona inayoenda Kipawa,akazungusha usukani,Daphine nayeye alikuwa fundi na mtundu kwenye magari nayeye akazungusha usukani,kutokana na mwendokasi wa gari hiyo ilifanya gari iserereke.
Mkononi alikuwa ameshika bastola ana usongo wa kufa mtu,ilikuwa ni lazima amuweke Ngesa mkononi.Gari la Ngesa lilikuwa mita kama kumi mbele yake,akatoa mkono nje uliokuwa na bastola, akaanza kurusha risasi.
Ngesa alizidi kutembeza gari kwa kasi,akaivuka kipawa na kuingia barabara ya kwenda Ukonga,bado gari lilizidi kumfukuza nyuma yake huku wakirushiwa risasi,ulikuwa ni usiku mnene na barabaraa ilikuwa nyeupe,taa za gari za nyuma alizokuwa anaendesha Ngesa zilikuwa zimepasuliwa na risasi.Daphine alizidi kuendesha gari kwa kasi.
“Shika usukani”
Daphinne akamwambia Zaitun aliyekuwa pembeni yake,Zaitun akashika usukani kisha yeye akatoa kichwa nje akaanza kupiga risasi gari la Ngesa, alivyoona hapati saiti nzuri,akapiga matairi ya nyuma.Ngesa akashindwa kuendelea mbele zaidi kwanza gari lilimshinda usukani ukamvuta,gari likapoteza uelekeo likaacha barabara na kuingia pembeni kwenye nyasi,hapo hapo likasimama.Daphine akaweka mguu kati gari yake ikapiga msele na kabla halijasimama akateremka na bastola mkononi mwake.Akatembea mpaka kandokando ya barabara,Ngesa alikuwa bado ndani ya gari ana hangaika kufungua mlango ambao tayari ulikuwa ume ‘jam’ilibidi atumie nguvu,akaupiga kwa nguvu kabla ya kutoka nje akarudishwa na ngumi ya uso kutoka kwa Daphine kabla hajakaa sawa,akavutwa nje na kupigwa ngumi nyingine ya uso.Daphine akamuwekea bastola kichwani,tayari kwa kumfyatua risasi.
Hasira na usongo aliokuwa nao vilitosha kabisa kumfyatua risasi Ngesa aliyekuwa mbele yake,kifo cha Vital Kamere ndicho kilihamsha kisasi.Ngesa hakuwa na jinsi sababu alielewa nini maana ya bastola, picha aliyoiona ilimuogopesha na mwanamke aliyekuwa mbele yake alikuwa amefura kwa hasira kumaanisha kwamba muda wowote angeondoshwa duniani.
“Karakacha karakacha”
Daphine ndiye aliyevuta kifyatulio cha risasi kilichoitwa triga lakini bahati mbaya ilikuwa kwake na nzuri kwa Ngesa sababu bastola haikuwa na risasi ndani.Hiyo ndiyo ilimpa nguvu mpya Ngesa, kwa kasi ya umeme akamvuta Daphine na kumtwanga kichwa cha uso,akarusha ngumi mbili hizo zilizaa matunda sababu zilimfikia Daphine usoni akayumba kidogo na kurudi nyuma,hakuishia hapo akaruka mateke mawili ambayo yalimfanya Daphine adondoke chini chali,Ngesa alikuwa mwenye hasira ajabu na hiyo ilimfanya mpaka macho yake yawe mekundu akawa anatetemeka kwa hasira,akamsogelea Daphine na kumuinua.
“Wewe kahaba,leo nakuuwa”
Kilichofuata hapo ni Ngesa kurusha ngumi nyingi zisizokuwa na idadi kamili.Sio siri tangu aanze kupigana ama kupambana Daphine hakuwahi kukutana na mtu nunda kama Ngesa aliyekuwa anapiga ngumi za uso na ilikuwa ikitoka hii inaingia ile,sio kwamba alikuwa hazioni.Jinsi alivyokabwa koo lake ilimfanya aishiwe nguvu kabisa,maumivu aliyokuwa anahisi hakuweza kuyafananisha na kitu chochote kile, damu zilikuwa tayari zinamtoka puani na mdomoni,akajikakamua na kurusha ngumi lakini Ngesa alipangua na kumzaba kofi kali,akazidi kukandamiza zaidi koo lake hapo ndipo Daphine alipohisi kinyesi kinataka kumtoka.Alijaribu kuutoa mkono wa Ngesa lakini alishindwa,alizidiwa nguvu.
“Paaa paaaaa”
Ulikuwa ni mlio wa risasi,sio Ngesa wala Daphine wote walishtuka.Ngesa alivyogeuka nyuma alimuona mwanamke mwingine ameshika bastola anamlenga yeye,hakuwa mwingine bali ni Zaitun kafyatua risasi hewani.
Kwa kasi ya mwewe Ngesa akamvuta Daphine na kumuweka mbele yake,kivyovyote vile Zaitun asingeweza kufyatua risasi kumlenga Ngesa sababu hakuwa na saiti nzuri,alikuwa nyuma ya Daphine.
“Za..ituni muu.we”
Daphine alitamka maneno hayo kwa shida na tabu,Ngesa alikuwa amempiga roba,alishindwa kuhema vizuri ukichangia na kipondo alichoshushiwa ndiyo usiseme!
Zaitun alisikia lakini kila alipojaribu kuchungulia ili afyatue risasi hakuweza.Akashika bastola vizuri na kubana jicho moja lakini wapi,alitaka kumlenga Ngesa kichwani lakini hakuweza sababu hata kichwa kilikuwa nyuma ya Daphine.Michezo yote ya kimafia Ngesa aliijuwa na alielewa vizuri sana kitendo cha kutoa kichwa ama mwili wake kwa nje angepigwa risasi,hilo alilijuwa wazi ndiyo maana aliendelea kujificha nyuma ya Daphine lakini hakuelewa nini kingefuata mbele.
“Nafyatua risasi,Moja”
Zaitun akapiga mkwara lakini hiyo haikumtingisha Ngesa hata kidogo.
“Mbili”
Hata angefikisha tatu asingeweza kupiga risasi hata kidogo,hiyo ilimfanya aanze kusogea taratibu akiwa na bastola mkononi ameishika vizuri.Ngesa akasogeza kichwa chake kidogo na kuchungulia akamwona Zaitun anavyosogea,akili yake ilifanya kazi kwa kasi ya risasi akawa anamsubiri mpaka mwanamke huyo asogee karibu zaidi,ilielekea alikuwa ana mikakati kabambe ndani ya ubongo wake.Zaitun akazidi kuwasogelea hakuelewa anafanya kosa kubwa kiasi gani,Ngesa akaendelea kupiga hesabu zake kichwani.
Jambo alilokuwa anataka kulifanya Ngesa alilifananisha na kamali,kupuna ama kukosa kama mipango yake ingeenda mrama basi maisha yake angeyapoteza hapohapo ndiyo maana alikuwa akifikiria mara mbili kabla hajatenda.Zilikuwa zimebaki mita kama saba hivi ili Zaitun awafikie,akazidi kumsubiri asogee zaidi.Kitendo cha Zaitun kusogea karibu akamsukuma Daphine mbele wakagongana na Zaitun,hapohapo Ngesa akaruka kama chui na kumvaa Zaitun cha kwanza alikamata mkono wake ulioshika bastola wakawa wanashindana nguvu.
“Paaaaaa”
Risasi ikachomoka bahati mbaya kutoka ndani ya bastola na kupasua kioo cha gari,wakazidi kuvutana huku na kule.Zaitun alivyojaribu kurusha kifuti Ngesa akakizuia.Ikawa vuta n’kuvute.
“Paaaaa”
Risasi nyingine ikachomoka,Ngesa akamvuta kwa nguvu Zaitun akawa nyuma yake akawa anashughulika na mkono wenye silaha, ilikuwa ni lazima aidhibiti silaha ndiyo mambo mengine yafuate.Mkono wa Zaitun ukawa umezungushwa,akautingisha kwa nguvu bastola ikadondoka,hiyo ilimfanya akae vizuri na kukunja ngumi ili mpambano uanze.Aliliona teke la Zaitun linakuja akainama chini kidogo likapita hewani alivyoibuka akamchimbua ngumi mbili za tumbo.Kitu alichokuwa anafanya Zaitun ni kupigana kwa hasira ndiyo maana alikuwa anarusha ngumi na mateke kwa pupa,Ngesa alikuwa akivikwepa vyote na alisubiri mpaka Zaitun achoke kiasi.
Ngumi ya Zaitun ilipita hewani akiwa chini alimpiga ngumi tatu za mbavu,akarudi juu na kumpiga ngumi ya pua nzito,hiyo ilimfanya Zaitun ayumbe hapo ndipo Ngesa akaruka teke lililoitwa ‘round kick’,Zaitun akadondoka chini chali,alichofanya Ngesa ni kuokota bastola iliyokuwa chini.Akaingia ndani ya gari ili kumtafuta Salim niya na madhumuni yake ilikuwa ajuwe ni wapi mabomu mengine yalipo.Alivyoingia ndani ya gari alishtuka kupita kiasi,ubongo wa Salim ulikuwa nje,damu zinamvuja mwili mzima.Kumbe risasi zilimfikia na kuumuwa,hiyo ilimfanya abanwe na hasira ajabu,akatembea mpaka kwa Zaitun na kumuinua.
“Mabomu mengine yako wapi?Nahesabu mpaka tatu”
Bastola ilikuwa kichwani kwa Zaitun anaambiwa aseme mabomu yalipo,japokuwa kulikuwa na giza aliweza kuiona sura ya Ngesa ilivyokuwa imekunjamana kwa hasira.
“Sijui!”
Akajibu kwa kiburi.
“Usinijaribu,mabomu mengine yako wapi,mbili….”
Ngesa akauliza tena huku akizidi kukandamiza bastola zaidi kichwani kwa Zaitun.Hakuwa na punje ya masihara hata kidogo,ilikuwa ni lazima avute triga endapo Zaitun atakuwa mkaidi.
“Go to hell”
Zaitun akajibu kwa nyodo,hakuelewa anamjibu mtu hatari kiasi gani.
“Paaaa paaaaa”
Zilikuwa ni risasi mbili zilizofyatuliwa na Ngesa,damu zikamrukia! Bega la Zaitun lilikuwa linavuja damu kama maji,anaugulia maumivu.
“Mabomu mengine yako wapi?”
“Si..ijui siiijui”
Zaitun akaburuzwa mpaka ndani ya gari walilokuja nalo yeye na Daphine,Ngesa akaondoka naye akawa amemuweka mateka tayari!
*************
Bado hakuelewa mpaka dakika hiyo ni kwanini bomu halikulipuka,akajaribu kusubiri tena lakini wapi.Brigedia Karanje alikuwa msibani lakini akili yake ilikuwa uwanja wa taifa.Aliamini kwamba baada ya dakika chache mamia na maelfu ya watu wangeteketea lakini haikuwa hivyo,kwani dakika arobaini na tano za mpira ziliisha bila kitu chochote kile kutokea.
“Leo Simba wamejitahidi sana,mpaka sasa hivi half time bado hawajatiwa goli”
Sentensi hiyo kutoka kwa vijana wawili waliokuwa pembeni yake ilimfanya Brigedia Karanje apate uhakika kwamba mlipuko bado haujatokea,alitamani kuuliza lakini akasita!Alivyojaribu kumuangalia Daphine hakumuona,sekunde zilisogea harakaharaka hatimaye dakika tisini ikafika mpira ukaisha,Simba na Yanga walitoa suluu.Hakuelewa ni kwa namna gani mpaka mwarabu aliyemtuma ameshindwa kufyatua bomu,hapohapo akatoka kandokando na kuanza kumtafuta hewani,matokeo yake simu iliita lakini haikupokelewa hiyo ikamfanya aingiwe na wasiwasi zaidi.
Akamtafuta Daphine hali ikawa hivyohivyo akajaribu kumpigia Zaitun pia simu haikupokelewa.Wasiwasi ukaanza kumuingia,hakutaka kulifumbia swala hilo macho,akawatuma vijana wake Kawe ili aweze kuzungumza na Zaitun lakini dakika arobaini baadaye alipokea taarifa zilizomfanya ashindwe kuamini.
“Unasemajeee?”
Brigedia Karanje akauliza kwa hamaki.
“Ndio mkuu,Zai hayupo wala mtoto hayupo”
“Shiiiiiit,embu mwangalie vizuri huko uwani”
“Tayari mkuu ni..”
“Nimekwambia muangalie”
Uhakika kwamba Zaitun wala Ritha hawapo alikuwa nao sababu aliangalia kila mahali,hakuna siku M.P Kiboko aliyosumbuliwa kama siku hiyo,alitafuta kila sehemu lakini wapi.
“Mkuu hawapo”
Akatoa jibu lingine lakini upande wa pili wa simu ulibaki kimnya,Brigedia Karanje hakujibu chochote.
“Mkuu ha…”
“Nimekusikia”
Brigedia Karanje alihisi kuchanganyikiwa kupita kiasi,akajaribu tena kumtafuta Zaitun hewani.Simu iliita,kilichomshtua zaidi ikapokelewa.
“Ha..llooo mk..uuu”
Ilikuwa ni sauti ya Zaitun lakini ilionekana alikuwa katika hali ya mateso kupita kiasi.
“Zaitun,uko wapi?Una tatizo gani?”
“Mk..uuu nin…paaaaa paaaaaaa”
Brigedia Karanje alishtuka kwa kiasi cha kutosha,mlio wa risasi upande wa pili wa simu ulimshtua.
“Halloo,halloo Zai..Halloooo”
“Karanje,Unaongea na Ngesa”
Moyo wa Brigedia Karanje ukapiga paaaa!
Sio siri Ngesa alikuwa mwenye hasira kupita kiasi chake na jazba zake hazikuwa na kipimo chake,alikuwa simuni anaongea na Brigedia Karanje huku akiwa ameyabana meno yake ni dhahiri kwamba alitamani hata siku hiyo hiyo wakutane na waanze kupambana,alivyokumbuka mateso kipindi yupo Morogoro ndiyo ilimpa usongo mara mia yake.
“Ha ha ha haaaa Ngesa,Mwanaume jasiri”
Brigedia Karanje alijichekesha akijifanya haogopi na wala hajashtuka.
“Nimeanza na huyu kahaba wako,unafuata wewe.Naomba nikuhakikishie kwamba nitakitoa kichwa chako”
“Ngesa,bwana mdogo embu nachokuomba achana na mambo unayofanya.Utajiingiza kwenye matatizo makubwa sana”
“Wacha tuone”
Hapohapo Ngesa alikata simu sababu hakutaka kusikiliza upuuzi wa Brigedia Karanje,kazi yake ilikuwa ni kum-bana Zaitun ataje kila kitu anachojua,na kwa wakati huo alitaka kujuwa ni wapi mabomu mengine yalipo.
“Risasi nyingine nakuuwa.Mabomu yako wapi?”
Bastola ilikuwa kichwani kwa Zaitun amefungwa na kamba juu ya kiti anavuja damu begani,risasi alizovyatua Ngesa alikuwa akipiga pembeni na alifanya hivyo ili kumtisha Brigedia Karanje.
“Mabomu mengine yako wapi?”
“Sii…jui”
“Okay”
Mwanaume huyu muda wa kupoteza kwake hakuwa nao,kwa nguvu sana akatumbukiza mdomo wa bastola ndani ya kidonda cha Zaitun alichopigwa risasi,akawa anaizungusha bastola.Kelele alizopiga Zaitun zilitisha na alihisi maumivu makali yasiyokuwa na mfano wake.
“Mabomu yako wapiiiiii?”
Ngesa alizidi kuuliza huku akizidi kumtonesha kidonda,akazidi kukandamiza bastola ndani ya kidonda damu zikaanza kumtoka Zaitun lakini mbali na kupokea mateso kama hayo hakuwa tayari kuongea chochote kile.
“Unajifanya unajuwa kuhusu maumivu sio?Haujui.Subiri nikuoneshe”
Mateso hayo yalifanyika ndani ya jumba kubwa ambalo halikumaliziwa vizuri,Ngesa akatoka nje kuna kitu ilielekea alikuwa anakitafuta.Ni kweli aliona mfuko mkubwa wa rambo kisha kurudi nao ndani,akazungusha kamba vizuri mikononi mwa Zaitun na kuzikaza vizuri.
“Nakuuliza mara ya mwisho,mabomu yako wapi?”
Badala ya Zaitun kujibu akamtemea mate usoni yaliyochanganyika na damu, ilielekea mwanamke huyu alikuwa kiburi sana lakini hakuelewa kwamba alikutana na mwanaume jeuri ama chuma cha reli.
“Puuuuuuu”
Ilikuwa ni ngumi kali kutoka kwa Ngesa iliyofanya Zaitun aende upande wa pili,bila kupoteza wakati akamfunika na mfuko wa nailoni usoni.Kumaanisha kwamba baada ya sekunde arobaini ilikuwa ni lazima aanze kutafuta hewa ya oksijeni,na hicho ndicho kilichotokea kwani Zaitun alianza kutupa miguu yake huku na kule ni dhahiri kwamba hewa ya oksijeni iliisha,Ngesa alilijuwa hilo akazidi kuushika mfuko wa nailoni vizuri ambao haukuwa na tundu hata moja lililokuwa linapitisha hewa,akasubiri mpaka dakika mbili nzima zikapita akautoa.
“Puuuuuuuuuuuuuu haaaa haaaa haaaa haaaaa”
Zaitun ndiye alikuwa anaparamia hewa kwa pupa baada ya mfuko kutolewa usoni kwake,isingekuwa hivyo angekufa hapohapo.
“Mabomu yako wapi?Nitafanya hivi mpaka utakufa.Then you will die for nothing,because I’m going to find them on one way or another”
Ngesa alijaribu kuchanganya na kiingereza akimaanisha Zaitun atakufa pasipo kuwa na sababu ya msingi sababu mabomu atayapata hivyo ni heri aseme kuliko kubaki kimnya.
“Mabomuuu..Mabooomu anayo Mkuuu”
“Mkuu gani?”
“Brigediaaaa Karaanje”
“Yuko wapi?”
“Kwa sasaaaa hivi sijuiii alipo”
“Unanitania”
“Huo ndio ukweliiiiiii”
Zaitun alisema kwa tabu mno na Ngesa alikuwa mbele yake anamtizama kwa macho makali kama simba mwenye njaa kali anahema kwa hasira kifua chake kinapanda juu na kushuka, bastola mkononi mwake.
“Una uhakika?”
“Ndiooooo”
*********
Ritha alifikishwa ikulu salama Salmin na hiyo yote ni kwa sababu ya Ngesa,bila jitihada zake wenda siku hiyo Rais Leslie Benjamin angekuwa katika msiba mzito na ni wazi kwamba Brigedia Karanje alikuwa mtu hatari na angemuuwa binti yake.Kwa jinsi mambo yalivyoenda harakaharaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa ana kila sababu ya Kumshukru Ngesa.Yeye na mke wake pamoja na binti yao Ritha walikuwa chumbani.Ritha alikuwa anahadithia kila kitu mpaka alivyokombolewa na Ngesa kijasusi, japokuwa alikuwa mdogo lakini aliweza kuelezea kila kitu mpaka alivyotekwa na baadaye Ngesa akavamia kama Komandoo.Hiyo ilifanya Rais Leslie aweke ulinzi mwingine zaidi na alitaka azungumze na Ngesa ana kwa ana ampongeze kwa jambo alilolifanya na ushauri wa kufanya hivyo alipewa na mkewe.
“Sawa Mke wangu,nitafanya hivyo ngoja kukuche”
“Nashukuru sana,naenda kuoga”
“Okay”
Hayo ndiyo mambo yaliyokuwa yanaendelea ikulu.Na kulivyopambazuka kesho yake na mapema Rais baada ya kupata kifungua kinywa alimtafuta Ngesa hewani, hapohapo simu ikaanza kuita.
“Ngesa,unaongea na Rais Leslie Benjamin.Habari za asubuhi?”
“Salama Mheshimiwa Rais nafurahi kupokea simu yako asubuhi ya leo”
“Ningependa uje ikulu mara moja”
“Sasa hivi?”
“Ndio,kwani upo wapi?”
“Mheshimiwa Rais kuna mambo unatakiwa ujue”
“Mambo gani?”
“Karanje ana mabomu ya Nuclear na mamia na maelfu watakufa kama hatutomthibiti.Na ninavyoongea nawewe tayari keshajuwa mimi sipo Cuba”
“Mungu wangu,nishauri Ngesa nifanye nini?”
“Ngoja nitakupigia baada ya dakika thelathini”
“Sawa”
Ngesa alikuwa anapaki gari nje ya nyumba aliyokuwa anaishi mpenzi wake Jaqlin Mfinanga baada ya kuongea na Rais Leslie,pembeni yake alikuwa ameketi Zaitun anavuja damu.Alivyoteremka akazunguka upande wa pili na kufungua mlango.
“Shuka wewe kahaba”
Nywele za Zaitun zilishikwa akavutwa mpaka chini,akawa anapelekwa mpaka walipofika nje ya geti la bati,Ngesa akagonga.
Geti likafunguliwa.Jacqlin Mfinanga hakuamini mtu anayemuona mbele yake,haikuwezekana hata kidogo kuwepo mahali hapo.Siku zote aliamini kwamba hatomuona tena sababu mara ya mwisho aliongea naye kwenye simu na kumwambia kwamba anapelekwa nchini Cubba kwa ajili ya kifungo chake kutokana na mambo yalivyoenda hakuelewa hata kidogo kinachoendelea,hakujuwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ngesa sasa wamekuwa kama chanda na Pete!
“Jaqlin…”
Ngesa akaita hata yeye alikuwa kama mtu asiyeamini.
“Ngesa”
Hapohapo wakakumbatiana.
“Jacqline sina muda wa kupoteza,naomba tuingie ndani”
“Huyu ni nani?”
“Nitakwambia,ninachokuomba iwe siri yako ili zoezi lifanyike kwa haraka”
“Sawa”
Zaitun aliingizwa ndani na kufungiwa ndani ya stoo,Ngesa akatoka nje na kuonekana anabonyeza bonyeza namba Fulani.
***************
Daphine alikuwa amepiga magoti anaomba msamaha kwa uzembe alioufanya,mbele yake alisimama Brigedia Karanje akiwa amekunja sura kuliko maelezo yaliyojitosheleza,hakuelewa amfanye nini msichana huyu aliyekuwa kapiga magoti,bado alikuwa anamtizama kwa hasira, kitu uzembe kwake kilikuwa mwiko.
“Nisamehee Mk…”
Kabla ya kumalizia sentensi yake alipigwa teke la kifua akadondoka chali chini.
“Stupid,are you insane?Huo ni uzembe,unapigwaje?Tena na mtu mmoja mdogo kama yule.Simama”
Brigedia Karanje aliongea kwa kufoka,hasira zake alizichanganya na jazba akawa anatetemeka.Alimuinua Daphine na kumzaba kibao cha nguvu,Daphine aliyumba na kudondoka chini lakini kutokana na hofu alisimama tena wima.
“Namuhitaji Ngesa,nakupa masaa ishirini na nne”
“Sawa Mkuu”
“Lisaa limoja tayari limekatika,Una maasaa ishirini na tatu.Usipompata,NAKUUWA”
Sio siri Daphine aliogopa na hiyo ilimfanya apate usongo wa kumsaka Ngesa kwa wudi na uvumba.Lakini kitu kilichokuwa kinamchanganya hakuelewa ni wapi angempata,alihaha.
Akaingia ndani ya gari na kugeuza huku akiwa mwenye mawazo chungu mzima kichwani kwake.
*******************
Kilikuwa ni chumba kidogo chenye dirisha moja kwa juu chini kulikuwa na vumbi,hapo ndipo Jacqlin Mfinanga alitumia kama stoo yake.Badala yake siku hiyo Zaitun aliwekwa kama mateka,alivyopata nguvu kidogo alifumbua macho yake,alivyotaka kusimama alishindwa sababu mikono na miguu yake vilifungwa kamba!Akajiangalia vizuri na kujiburuza na matako mpaka alivyofika pembeni ya kichuma chenye ncha kali na kuiweka kamba vizuri,bila kupoteza muda akaanza kuisugua.Kwakuwa ilikuwa na ncha kali hapohapo ikaachia,mikono yake ikawa huru akaanza kuzifungua kamba za miguu yake.Akachukuwa chuma kilichokuwa pembeni yake kama silaha na kulishika vizuri mkononi.
Bahati mbaya ilikuwa kwa Ngesa na nzuri kwake sababu mlango haikufungwa na funguo,alivyovuta ulifunguka akatokeza nje kwa tahadhari,akaanza kunyata taratibu.Akapiga hatua ya kwanza ya pili,akaona jiko akaingia na kushika kisu kwa lolote litakalo tokea ajitetee! Akaangalia huku na kule,hakukuwa na dalili yoyote ya mtu kutoka hiyo ilimfanya atembee mpaka nje kabisa ya mlango na kuanza kuelekea barabarani,hakuamini kama alikuwa huru na amepona.
Mbaya zaidi hakuelewa kila alichofanya haukuwa ujanja bali mambo yote yalitegeshwa na Ngesa na aliacha mlango wazi kwa makusudi yake sababu alitaka Zaitun atoroke ili aanze kumfuatilia hapo ndipo wenda angejuwa ni wapi Mabomu yapo ama Brigedia Karanje alipo,ndio maana alikuwa ndani ya gari amejifungia macho yake yakiwa kodo nje ya geti,akamuona Zaitun anatoka nje anaangalia huku na kulee.Akamshuhudia anaingia barabara kubwa na kukodi pikipiki,hapohapo nayeye akawasha gari na kuanza kumfuatilia nyuma nyuma.
Zaituni alikuwa akifuatiliwa bila yeye mwenyewe kujijua.pikipiki aliyoikodi ilifuatiliwa na Ngesa nyuma yao akiwa na gari anaendesha taratibu.Umbali ulikuwa ni kama mita 100 hivi.Alichotaka kujuwa Ngesa ni wapi anaishi Zaitun na hapo angejuwa pa kuanzia ndiyo maana alifanya ujanja wa kumfuatilia nyumanyuma.Akazidi kuiona pikipiki inasonga mbele mpaka ilipofika Magomeni,Usalama.Kilichomchanganya akili ni baada ya pikipiki kwenda mbele kabisa na kumuacha nyuma kwenye mataa ambapo magari yalikuwa yamesimama baada ya taa nyekundu kuwaka.
“Shit”
Ngesa alikema baada ya pikipiki kuchomoka,akaiona inazidi kusonga mbele. Kuiacha iondoke na kuipoteza ilikuwa ni sawa na kuwaacha watanzania zaidi ya elfu moja walipuke kwenye bomu,hapohapo akageuza shingo nyuma na kupiga gia,gari likarudi nyuma, alivyopata upenyo akatanua pembeni na kupita katikati ya barabara.
“Pipi piiiiiiiii”
Mark II iliyokuwa inatoka Kaskazini ilimkosakosa na kupiga honi lakini Ngesa hakujali,alikanyaga mafuta mengi ili kuwahi pikipiki ambayo ilikuwa tayari imempotea mbele ya macho yake.Akazidi kusonga mbele huku macho yake yakiwa huku na kule anaangalia pembe zote za barabara.Ghafla akaweka mguu kati baada ya kuiona pikipiki kwenye moja ya kichocholo, hapohapo akazungusha usukani na kuingia barabara ya vumbi,akapunguza mwendo taratibu na kukunja kona ambapo alimuona Zaitun anaingia ndani ya geti la rangi nyekundu,akazima taa na kuweka gari kando sababu alitaka kujua kama ni kweli Zaitun aliishi hapo.
********
“Zaitun!Embu ingia ndani”
Alikuwa ni Daphine akiwa na kitambaa mkononi cheupe lakini kina damu ilionekana alikuwa anajikanda nacho.
“Umefanya nini?”
Zaitun akahoji.
“Mkuu,amekasirishwa na uzembe.Ndio alinipa adhabu lakini usijali.Ilikuwaje?Na ulikuwa wapi?”
Daphine akaanza kumuhoji rafiki yake,ilionekana alimshangaa jinsi alivyojeruhiwa vibaya sana usoni na pia begani alikuwa ana jeraha la risasi.
“Nimetoroka kwa Ngesa”
“Kivipi?”
Daphine akataka kujua ndipo hapo Zaitun akaanza kumuhadithia jinsi ilivyokuwa mpaka akajikomboa kutoka kwenye mikono ya mtu hatari, Ngesa!Jambo hilo lilimshangaza sana Daphine lakini hakutaka kulionesha waziwazi.Alichofanya ni kubandika maji ya moto jikoni na kuingia chumbani ambapo huko kulikuwa na kiboxi cha madawa ya huduma ya kwanza,akamsogelea Zaitun na kumvua nguo ya juu,akampangusa majeraha na spirit kisha kupaka kidonda dawa,Zaitun alihisi maumivu makali lakini alijikaza sana.
“Pole sana.Unapakumbuka anapoishi?”
Daphine akauliza akiwa ameshikilia mkono wa Zaituni anaupaka dawa.
“Nani?”
“Ngesa”
“Ndio,napafahamu”
“Ni wapi?”
“Kule Interchick”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Sawa ngoja nikutafutie dokta,nitajuwa cha kufanya”
Ilielekea Daphine alipata wazo jipya kabambe,tumaini la kumpata Ngesa lilirudi tena upya, ilikuwa ni lazima amtie mikononi mwake na amfanye kitu kibaya sana.
“Anaishi na nani?”
“Na mkewe pamoja na mtoto wake nadhani”
“Kweli?”
“Sina sababu ya kukudanganya Daphine”
“Nitaenda kwa mkewe nimuuwe mwenyewe”
Daphine alizungumza kwa kumaanisha na katika sentensi yake hakuwa ana masihara hata kidogo,akainuka na kuingia chumbani ambapo alitoka na bastola,akachomoa magazine ili kukagua kama ina risasi za kutosha,alivyoridhika akairudisha na kuweka bastola kiunoni.
“Unataka kwenda wapi?”
“Interchick,twende ndani ya gari”
“Kwanini tusisubiri kidogo?”
“No,nipeleke sasa hivi.Siwezi kuruhusu Ngesa aendelee kuvuta pumzi”
“Lak…”
“Lakini nini?Unanipeleka au?”
Daphine akauliza kwa ukali kidogo sababu alikuwa ana usongo na Ngesa mbali na hapo alipewa masaa machache na Brigedia Karanje kuwa Ngesa apatikane lasivyo angepewa adhabu nyingine kali sana,kutokana na hilo aliogopa ndiyo maana hakutaka kusubiri,alimshukuru sana Zaitun kwa kumpa mwanga mwingine wa kujuwa ni wapi Ngesa anaishi.
“Ninakupeleka”
“Sawa badilisha nguo”
Hakuwa anaongea tena bali ilikuwa ni amri,Zaituni akaingia chumbani na kubadili nguo akavaa nguo safi na wote wakaongozana mpaka nje ambapo walitoka nje na kuingia ndani ya gari safari ya kwenda Interchick ikaanza dakika hiyohiyo.
*********
Hakuna siku ambayo Brigedia Karanje aliyokasirika kama hiyo,alichukia kwa kiasi cha kutosha.Kukombolewa kwa Ritha mtoto wa Rais kulimfanya apate wazo lingine la kutisha, alikuwa bado anataka kumkomoa Rais Leslie Benjamin.Siku hiyo akiwa kambini alimuita mmoja wa watu wa kazi,ili watete mambo yao kidogo.
“Nahitaji bomu”
“Nuclear?”
“Hapana,bomu la kawaida”
“Sawa mkuu”
“Nataka ukalipue Hospitali ya Muhimbili,leo usiku”
“Leo usiku?”
“Sitaki kurudia mara mbili,fanya nilichokwambia leo saa tano nataka nisikie kwenye habari watu wakiilia na kusaga meno”
“Sawa mkuu”
Lilikuwa ni jambo la kutisha na Brigedia Karanje aliongea kwa hasira za waziwazi.Mikakati ilianza kupangwa saa kumi ya jioni siku hiyohiyo na ilitakiwa kila kitu kifanywe kwa akili sana bila kushtukiwa.Ilibidi atafutwe daktari mmoja kutoka Muhimbili, pia apigiwe simu mlinzi aliyekuwa zamu getini siku hiyo ili iwe rahisi kwa wao kupenyeza mabomu, ilikuwa ni lazima siku hiyo watu wafe na bomu ili Rais Leslie aumie sana na hicho ndicho kitu kilichokuwa kinaenda kutokea.
“Hallo naongea na Dokta Jongo?”
Ni simu iliyotoka kwa Kanali Kitalu,alikuwa ni mwanajeshi mweusi ti na katili kuliko kawaida.
“Ndio nani mwenzangu?”
“Unaongea na Kanali Kitalu,tusipoteze muda daktari.Nimepewa namba zako na Brigedia Karanje.Nadhani amekwambia kila kitu kuhusu leo saa nne”
“Ndio lakini ameniambia kuna mzigo utanipa”
“Mpaka kazi yetu iende sawa”
“Hata nusu sipati?”
“Hupati hata robo mpaka kazi yetu iende vizuri”
“Sawa mtakuja saa ngapi?”
“Saa nne na nusu tutakuwa hapo,pia kitu kimoja?”
“Kitu gani Kanali?”
“Tunahitaji Ambulance”
“Sawa”
“Ahsante kwa ushirikiano”
Hata simu ilivyokatwa na kuongea na Dokta Bakari Jongo aliendelea kuwapigia watu wengine kama walinzi pamoja na mapokezi,jambo hilo lilipangwa kiakili sana na ili kuwaziba midomo ilikuwa ni lazima watembeze pesa nyingi kwa madaktari na walinzi.
“Tayari mkuu,kila kitu kimeenda sawa.Tuna subiri Ambulance saa nne”
Kanali alitoa ripoti kwa mkuu wake wa kazi kuwa kila kitu kipo sawa,Kwa mara ya kwanza Brigedia Karanje alitabasamu lakini meno hayakuonekana.
“Andaa mabomu”
“Sawa mkuu”
Kama ilivyopangwa na ndivyo mambo yalivyoenda,bomu kubwa la kusetiwa likawekwa sawa na ilivyofika saa nne ya usiku gari la wagonjwa likaingia ndani ya jumba la Brigedia Karanje ambapo huko hakuna mtu yoyote aliyekuwa anajuwa siri hiyo na jinsi walivyoenda kumpokea dereva barabarani ilibidi wamuwekee kitambaa cheusi usoni na kuwekwa kando ambapo gari liliendeshwa na mwanajeshi mwingine mpaka wanafika kwenye nyumba hiyo iliyokuwa porini kidogo.Hakukuwa na muda wa kupoteza,bomu likawekwa ndani ya gari na safari ikaanza mara moja.
“Wiiiiiiu wiiiiiiiiu”
Dereva baada ya kufika barabarabni aliwasha king’ola hiyo ilimaanisha kuwa ana mgonjwa ndani ya gari analoendesha kumbe haikuwa hivyo kwani alipakia wanajeshi sita pamoja na bomu hatari.Kwa kasi ya umeme gari ilizidi kuteleza barabarani,hiyo ilifanya magari mengine yakae kando.
Hakuna mtu yoyote yule aliyeelewa kuwa siku hiyo kuna mamia ya watu watakufa kwenye mlipuko wa bomu hilo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Ilikuwa ni lazima wagonjwa waliokuwepo ama waliopelekwa siku hiyo wafe,kifupi hospitali ya Muhimbili angegeuka na kuwa gofu baada ya lisaa limoja baadaye.Dakika arobaini zilikuwa nyingi gari la wagonjwa likawa lipo geti la hospitali,Kwakuwa Mlinzi alipangwa alitoa ruksa gari likapita mpaka mlango wa nyuma huko walitokeza madaktari wengine harakaharaka na kutoa tranka kubwa la chuma lenye bomu ndani,wakalipakia na kulipitisha mpaka ndani stoo,Kuanzia hapo mpango wao ukawa tayari umekamilika,mambo yalikuwa maraisi mno kuliko walivyotegemea.
“Sawa,sisi tunaenda.Muondoke hapa baada ya dakika thelathini,mimi nina rimoti nitabonyeza.Lakini msimwambie mtu yoyote yule kama mngependa mlipwe pesa zenu”
Maagizo yalitolewa kisha watu wa Brigedia Karanje wakaondoka zao.Ilikuwa ni lazima ikifika saa tano kamili juu ya alama bomu lifumuke na hivyo ndivyo walivyolitega bomu hilo na zilikuwa zimesalia dakika kumi na mbili tu.
“Tii tiii tiiii tiii”
Lilikuwa ni bomu linatoa mlio huo mdogo na dakika zake zilikuwa zinarudi nyuma taratibu mpaka zikafika tatu.Kwa harakahakra siku hiyo wagonjwa zaidi ya elfu moja wangekufa na wafanyakazi zaidi ya mia moja wangeteketea ndani ya moto huo hatari.
“Tii ..tiii… tiiitititititit. buuuuuuuuuuuuuuum”
Ulikuwa ni mlio mkubwa wa bomu lililolipuka na kufanya mpaka ardhi itingishike!
Ulikuwa ni Moshi mkubwa unapanda angani tena mweusi sana,hiyo ilitokana na bomu kubwa kulikupa na kusababisha mpaka ardhi itingishike, hakukuwa na mjadala wowote ule sababu wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali ya Muhimbili waliokuwa ndani siku hiyo waliungua moto.Kutokana na jambo hilo kutokea ghafla usiku ilipelekea mpaka wakazi wa maeneo ya karibu kama Upanga,Jangwani na daraja la salenda kuanza kukimbia huku na kule wenye magari yao walishuka na kutimua mbio hakuna hata mtu mmoja kati yao aliyejuwa nini kilisababisha tetemeko hilo zito pamoja na moshi mkubwa angani,walichojua ni hatari tu! Hiyo ikafanya mpaka watu waanze kukimbia hovyo bila uelekeo.Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Brigedia Karanje na hiyo ilitokana na kuuona moshi mkubwa angani,akajua tayari mambo aliyopanga yameenda vizuri.
“Nahitaji kuongea na Rais Leslie”
Brigedia Karanje akamwambia mlinzi wake,hapohapo simu ikapigwa akapewa.
“Huo ni mwanzo tu.Muheshimiwa Raisi,ni kama mfano”
Brigedia Karanje alizungumza kwa dharau zote,hiyo ilifanya Mh.Rais abaki kimnya hakueleewa ni jibu gani alitoe.Ni kweli Raisi Leslie alionekana kuchanganyikiwa kupita kiasi sababu aliusikia mlipuko wa bomu hivyo ikapelekea walinzi wote wajazane ili kumlinda sababu hakukuwa na Amani tena.Ndiyo maana hata alivyopigiwa simu alishindwa kujibu chochote kile.
“Ha..tititi”
Simu ilikatwa,Rais Leslie akakaa chini bila kupenda,ni wazi kuwa kiti cha uraisi alichokikalia tayari kilikuwa kinawaka moto.Na akili yake ilishindwa kufanya kazi kwa wakati huo.
“Muheshimiwa Rais tutafanya nini?”
“Karanje ndio anafanya haya yote nahitaji akamatwe”
“Lakini inabidi tutumie akili sana sababu tunaweza kusababisha vita vya tatu vya dunia”
“Nishauri,nifanye nini?”
“Tufanye mambo taratibu,tuwashirikishe CID”
“C.I.D?”
“Ndio mheshimiwa Rais”
“Sawa”
Lilikuwa ni wazo jipya lililomfungua akili Rais Leslie Benjamin na ushauri huo ulitoka kwa mshauri wake aliyeitwa Benny Josephat Msanya,alikuwa ni kijana mdogo lakini mwenye maarifa mengi kichwani.Hapohapo bila kupoteza wakati akaanza kupiga simu makao makuu usalama wa Taifa ili mchakato uanze na simu ilipokelewa na mkuu wa kitengo cha upelelezi Mr.Dustan Kyoba,hakukuwa na maongezi mengine zaidi ya kuitwa ikulu muda huohuo ili wafanye kikao kidogo.Na dakika kumi baadaye Dustan Kyoba aliingia ndani ya ikulu akapokelewa ingawa ilikuwa ni usiku lakini ilikuwa ni lazima kazi hiyo ianze mara moja.
“Mr.Dustan Kyoba”
Mh.Rais akampa mkono CID Kyoba kisha kuketi kwenye kiti.Kikao hiko kilifanywa na watu watano na kila mtu alichangia hoja yake.
“Upelelezi wangu utaanzia pale hospitali.Ulisema Karanje ndio anahusika na kila kitu?Inabidi kwanza tuwe na ushahidi wa kutosha.Nipe siku mbili nitakuwa nimekamilisha ripoti yangu”
Hiyo ndiyo ilikuwa mipango ya Dustan Kyoba na aliongea kwa kujiamini ilionekana alikuwa ni mzoefu na kitu anachokizungumza,wakapeana mikono na kutoka nje akimuhakikishia Mh.Rais kuwa kila kitu kingeenda sawa kabisa na asiwe na shaka!
*********
Ngesa alikuwa ndani ya gari,mbele yake aliliona geti ambalo Zaitun ameingia muda mfupi,alikuwa akimsubiri ili akamilishe mipango yake,akashuhudia geti linafunguliwa na kumuona Mwanamke ambaye alishawahi kuonana naye tena zaidi ya mara moja,alikuwa ni Daphine na nyuma yake alitokea Zaitun,akashusha kichwa chini kidogo.Akawashuhudia wanaingia ndani ya gari na kuondoka zao!Akili ya Ngesa ilishindwa kuamua ni kitu gani akifanye,bado alikuwa njiapanda.Gari walilopanda Daphine na Zaitun lilimpita pembeni yake lakini aliweka kichwa chini,lilivyopita na kutokomea gizani Ngesa akafungua mlango wa gari na kushuka,kuna kitu kilimsukuma na kumwambia aingie ndani ya nyumba.Akatembea kwa tahadhari sana mpaka getini ambapo alichomoa bastola yake na kuishika kwa mikono miwili ili kwa lolote litakalo tokea ajiteteee,akasukuma geti bastola ikiwa mbele akaingia kwa tahadhari kama paka anayetaka kuiba nyama,akatizama huku na kule.Kulikuwa kuna ukimnya wa hali ya juu,alivyolifikia geti akasukuma taratibu kidole akakiingiza ndani ya triga akazama ndani ya kuona uwazi wa ukumbi,alivyoangalia chini aliona damu nyingi.Akaziruka na kuanza kukagua huku na kule.Akaingia chumba baada ya chumba ambapo huko alikumbana na risasi pamoja na silaha zingine kali,akainama chini ya uvungu.
Wakati Ngesa anapekua nyumba ya Daphine na kukagua kila kilichopo yeye Daphine alikuwa nyuma ya usukani anaendesha gari kwa kasi kubwa anaenda nyumbani kwa Ngesa akafanye jambo la kinyama, ilikuwa ni lazima amuuwe mke wa Ngesa hicho ndicho kitu alichoapia kukifanya,jinsi Daphine alivyokimbiza gari iliogopesha hiyo ilifanya mpaka Zaitun aliyekuwa pembeni ajishike vizuri.Kutokana na mwendokasi wa gari hilo wakawa wamefika Interchick muda mfupi tu,hapo kazi ya Zaituin ikawa ni kumuelekeza Daphine nyumba anayoishi Ngesa ilipo.
“Paki hapo mbele”
Zaitun baada ya kusema hivyo Daphine akaweka mguu kati,gari ikapiga msele na kufanya vumbi litimke.
“Kacha kacha”
Daphine alikoki bastola tayari kwa kumfyatua mtu yoyote yule atakayemkuta ndani hata ingekuwa Ngesa mwenyewe.
“Nyumba iko wapi?”
“Ile pale yenye geti la bati”
Hapohapo Daphine akashuka na kuanza kutembea,alivyofika getini alipiga teke bati likadondoka chini akazama ndani kwa hasira,mlango wa uwani ulikuwa wazi hiyo ilifanya aingie kitemi huku akifunga bastola yake kiwambo cha kuzuia kelele zisitoke.
Kelele za bati kulia zilimshtua Jaqlin Mfinanga hiyo ilimfanya atake kutoka nje.Kitendo cha kufungua mlango alipigwa risasi mbili za miguu hapohapo akadondoka chini,Daphine alikuwa amekasirika na ndiye yeye aliyefyatua risasi bila huruma.
“Pyuuuuu”
Akafyatua nyingine ambayo ilimfikia Jaqlin mkono wa kulia.
“Pyuuuuu”
Ilikuwa ni risasi ya nne hiyo iliyomfikia mkono wa kushoto,Jaqlin alilala chini huku akiugulia maumivu makali,damu zilikuwa zinamvuja nyingi sana hawezi kuongea lolote na mwanamke aliyesimama mbele yake hakuelewa ni kwanini amefanya hivyo.
“Ta.fadh..ali usini..ue”
Jaqlin alizungumza kwa shida sana huku damu nyingi zikiwa zinamtoka mwilini zikalowanisha sakafu nzima hiyo ilifanya Daphine nayeye achuchumae.
“Unamfahamu Ngesa?”
Daphine aliuliza huku akiwa anapalaza bastola juu ya matiti ya Jaqlin Mfinanga akaishusha mpaka chini sehemu za siri.
“Unamfahamu Ngesa,mwanaume anayekutia?”
Alivyosema hivyo akaikandamiza bastola sehemu za siri za Jaqlin Mfinanga.
“Na..omba usi..niue”
“Unapenda kuishi.Sio?Siku yako ya mwisho leo imefika”
“Pyuuuuu”
Ilikuwa ni risasi nyingine ya mguuni mwa Jacqlin baada ya Daphine kuvuta triga hio ilifanya Jaqlin atulie na kuhema kwa tabu sana.
“Baasha ako yuko wapi?Nitajie alipo nakuacha uishi”
Hakuwa ana nguvu za kuongea chochote kile zaidi ya kukoroma kama kondoo aliyekuwa amechinjwa, ilionekana dhahiri kuwa alikuwa anatafuta pumzi kwa tabu sana.
“Mpe salamu zangu,mwambie Daphine niilifika.Pyuuuuu”
Risasi nyingine ikatoka ikamfikia Jaqlin tumboni.Hapo ndipo Jacqlin alipotulia na kukaa kimnya huku damu nyingi zikimtoka yupo chini,kwa mbali aliona macho yake yanafumba.
“Tuuuuuuuuuu”
Daphine alikusanya mate na kumtemea Jaqlin kisha kugeuza na kuondoka zake,alielewa kwa kufanya hivyo ilikuwa ni lazima Ngesa alie na kusaga meno na kwake hilo lingekuwa bonge moja la pigo.
********
Yaani bora angewasha gari na kurudi nyumbani wakati huohuo lakini badala yake aliendelea kupiga msako nyumbani kwa Daphine, hakuelewea kuwa mpenzi wake amevamiwa na anapigwa risasi wenda angewafuatilia wakina Daphine yasingetokea,alivyomaliza kupekua na kukosa anachokitafuta alitoka nje na kurudi ndani ya gari akawasha na kuondoka zake.Siku hiyo aliendesha gari kwa mwendo wa taratibu sana na wa kawaida mno kutokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao kichwani,alivyofika Interchick alikunja kona na kuegesha gari.Alivyoshuka akatembea mpaka getini,alisita kidogo baada ya kuona geti lipo wazi,kwa kasi ya umeme akachomoa bastola kiunoni na kuiweka vizuri mikononi mwake,akatembea taratibu mpaka ndani ambapo alikuta mlango upo wazi.Alivyoingiza kichwa chake ndani moyo wake ukapiga paa!Jaqlin Mfinanga alikuwa amelala chini damu zinamvuja,akatembea kwa haraka mpaka juu ya mwili wa mpenzi wake.
“Jaqlin Jaqliin”
Alimtingisha na kumuinua lakini Jaqlin hakutingishika hata kidogo!
Damu zilikuwa zimetapakaa chini,Jaqlin Mfinanga alikuwa amejeruhiwa na risasi karibia mwili wake mzima.Ngesa alikuwa pembeni yake anamtingisha,hakutofautishwa na mtu aliyechanganyikiwa.Hakuwa na kitu cha kufanya kingine zaidi ya kuweka bastola yake kiunoni haraka kisha kumbeba Mpenzi wake mikononi,akaanza kutoka naye mpaka nje ambapo alimuingiza ndani ya gari siti za nyuma.Kwa kasi ya risasi akazama ndani na kukaa nyuma ya usukani,hapohapo akapiga gia, jinsi tairi zilivyozunguka mpaka mchanga ukaruka ilitisha,Ngesa akauzungusha usukani kama kichaa, gari ikaanza kutembea kwa kasi kubwa sana!Akaingia barabara ya lami na kuanza kuyapita magari mengine.
“Ng….es…a Na..ku..faaaa”
Ilikuwa ni sauti ya Jaqlin akiwa nyuma hiyo ilimfanya Ngesa ageuze shingo yake.Hali ya Jaqlin ilikuwa mbaya sana na kupona ilikuwa ni asilimia thelathini kati ya mia moja, hata hivyo Ngesa hakuonekana kukata tamaa ilikuwa ni lazima amuwahishe hospitalini kwa ajili ya matibabu.
“Jaqlin usiongee tafadhali”
Ngesa alisema huku mikono yake ikiwa juu ya usukani,kitendo cha kufika hospitali aliweka mguu kati gari ikapiga msele,akatoka ndani ya gari huku akiwa anapiga kelele za kuomba msaada.Wauguzi wakatoka mbiombio hata wao walionekana kushtuka.
“Kafanya nini huyu?”
Muuguzi mmoja aliuliza huku wakimuweka Jaqlin juu ya machela.
“Kavamiwa”
“Una PF3?”
“Sina”
“Hatuwezi kumtibu”
“Naomba niongee na Daktari.Nisaidieni,amevamiwa na majambazi ni mke wangu”
“Sisi tutaamini vipi?”
“Nitaweletea PF3 ndani ya dakika tano”
Maongezi hayo yalifanyika huku machela ikiwa inasukumwa mbio mbio ambapo iliingizwa mpaka ndani ya chumba kingine maalum,hapo Ngesa hakuruhusiwa kuingia.
“Atapona?”
Ngesa akauliza sababu alikosa matumaini.
“Tuombe Mungu”
Nguo zake zilikuwa zimelowa damu.Bado hakuelewa ni nani aliyefanya tukio la kinyama lakini alivyotulia na kutuliza akili picha ya Daphine na Zaitun ikamjia,akayabana meno yake kwa hasira hiyo ilimfanya mpaka atetemeke, hakuelewa amfanye nini Daphine endapo akikutana naye uso kwa uso.
Bila kujali kuwa ni usiku kiasi gani alitoka nje na kuingia ndani ya gari.Hiyo ilikuwa ni safari ya kwenda Magomeni nyumbani kwa Daphine akamuuwe,shinikizo la damu lilimpanda na kumfanya azidi kupandisha mori zaidi na zaidi,Picha ya Jaqlin akiwa na damu mwili mzima ilimpitia kichwani kwake,hiyo ilimfanya azidi kukanyaga mafuta mengi zaidi, gari ikazidi kusonga mbele mpaka alivyofika Magomeni mapipa na kukunja kona ya kushoto kuingia nyumba aliyoona anaingia Zaitun,akapiga breki na kuchomoa bastola kiunoni,mbele yake kulikuwa na gari ambalo muda mfupi alitoka nalo Daphine kumaanisha kuwa tayari wamerudi.Kutokana na hasira alizokuwa nazo aliingia getini na kulipiga teke likafunguka akazama ndani na kuingia huku akitembea harakaharaka kama mkuki,akapiga mlango wa seblen teke.
“Paaaa paaaaaa”
Ngesa aliachia risasi baada ya kumuona Daphine yupo mbele yake lakini zilimkosa baada ya kuruka pembeni.
“Paaaaa”
Ngesa akafyatua risasi nyingine Daphine akaruka nyuma ya sofa, tayari mambo yalikuwa yameharibika na bastola yake ilikuwa chini ya kochi lililokuwa mbali kidogo,kwenda kuifata na kujitokeza ilikuwa ni hatari kubwa sana kwake.
“Paaaa paaaaa”
Ngesa aliendelea kufyatua risasi juu ya sofa!Daphine alivyoona hivyo akalala kifudifudi na kuanza kujiburuza kama nyoka,alishaelewa yupo kwenye hatari kubwa kiasi gani,alihofia!
“Paaa”
Ngesa akazidi kusogea karibu kwa tahadhari sababu alimuona Daphine yupo nyuma ya kochi hiyo ilimfanya asogee taratibu mpaka alipomfikia.
“Simama juu”
Ilikuwa ni kauli moja aliyotoa Ngesa tena kwa hasira nyingi sana,kidole kimoja kipo kwenye triga.Kwa jinsi picha ilivyoonekana ilikuwa ni lazima Daphine apigwe risasi.
“Weka silaha chini”
Ngesa akahisi kama kuna kitu cha chuma kimemgusa kwenye kisogo.Ilikuwa ni bastola aliyoshika Zaitun kumaanisha kuwa asalimu amri vinginevyo atapigwa risasi ya kichwa.
“Weka silaha chini Ngesa”
Zaitun akapiga tena mkwara lakini Ngesa bado alikuwa mkaidi alizidi kumuangalia Daphine kwa hasira,kukataa kuweka bastola chini ilimaanisha kupigwa risasi.Kwa tahadhari akaanza kushusha mkono wake wenye bastola chini tena taratibu huku akiwa anapiga mahesabu makali sana kichwani,kitendo cha kuiweka chini aligeuka na ngumi iliyompeleka Zaitun chini mzimamzima,akakanyaga kochi na kuruka ‘round kick’ ili teke limfikie Daphine lakini bahati mbaya lilimkosa kwani Daphine alihepa kulia teke likapita hewani,Daphine akakunja ngumi kwa ajili ya mpambano.Ngesa nayeye akakunja ngumi kwa ajili ya kupambana na mwanamke huyu ambaye siku zote alikuwa ana usongo naye.Waliokutana walikuwa wanajua kucheza michezo ya ndundi.Ngesa alirusha ngumi Daphine akarudi nyuma kidogo ikapita hewani alivyojaribu kurusha teke Ngesa akainama na kumkata mtama Daphine akadondoka chini kama mzigo,hapohapo Ngesa akamuinua na kumpiga kichwa cha pua.Akamvuta kwa nguvu na kuuzungusha mkono wake na kumtupa kando,hakuishia hapo.
Ngesa alikuwa kama mbogo ana hasira chafu,akamfuata tena Dahine na kumshika nywele akamvuta kwa juu,akapigiza kichwa chake juu ya meza ya kioo,Daphine akachanwa vibaya sana usoni na vioo vya meza.
Zaitun alikuwa chini anatizama kila kitu,akajiburuza taratibu mpaka pembeni ambapo aliona chuma kikubwa akakishika vizuri mikononi mwake na kusimama,akatembea mpaka nyuma ya Ngesa na kumpiga na chuma kichwani hapohapo Ngesa akadondoka chini, ilielekea alipigwa sehemu mbaya ndiyo maana hakuweza kuinuka tena!
Daphine alikuwa chini anavuja damu usoni na puani,isingekuwa Zaitun kumkomboa wenda huo ndio ungekuwa mwisho wake.
“Amepa..juaje hapaaa?”
Daphine aliuliza huku akijipangusa damu puani na mdomoni akitumia viganja vyake.
“Tumuuwe?”
“Hapana,subiri.Nipatie simu”
Hakuna kitu alichokifanya Daphine zaidi ya kumpigia simu Brigedia Karanje,bila kupoteza wakati akampasha habari kuwa yupo na Ngesa mikononi mwake.Zilikuwa ni habari nzuri sana!
“Mlete makabe huku”
“Sawa mkuu”
Usiku huohuo Ngesa alipakiwa ndani ya gari kama mateka na safari ya kwenda Makabe kuanza mara moja!Sio siri Daphine alikuwa mwenye furaha mno ndiyo maana kila wakati alikuwa akitizama nyuma kama Ngesa yupo.
“Umemfunga vizuri na hizo kamba?”
Daphine akauliza bado alikuwa mwenye wasiwasi,kutokukazwa kamba kwa Ngesa ilikuwa ni hatari kubwa sana kwao na walijuwa fika balaa la Ngesa endapo atazinduka ndiyo maana walitamani kufika mapema ili wamkabidhi kwa Brigedia Karanje.
“Ndio,hawezi kutoka”
Zaitun akajibu.
Kumbe tangu wanampakia Ngesa ndani ya gari alikuwa ana fahamu zake lakini alijifanya kufumba macho,bado alitaka kujua ni wapi mabomu yalipo!Ndiyo maana akataka kujuwa ni wapi anapelekwa,alijuwa fika kwamba anapelekwa kwa Brigedia Karanje na kivyovyote vile aliamini kuwa huko ndipo yatakuwa yamehifadhiwa mabomu.Gari lilizidi kutembea wakidhani kuwa Ngesa hana fahamu na amezirai kumbe walikuwa wanajidanganya wenyewe.Walifika Mbezi mwisho na kumpigia Brigedia Karanje simu ambapo walipewa maelekezo, Ngesa alikuwa akisikia kila kitu kilichozungumzwa,akaendelea kujikausha!
“Unadhani Mkuu atamfanya nini?”
Zaitun alimuuliza Daphine.
“Ni lazima atamuuwa tu”
Ingawa ilikuwa ni hatari kwake lakini siku zote alitaka kufa kishujaa kupigania nchi yake,gari ikapanda kilima cha kuingia makabe ambapo walipita Msakuzi wakazidi kusonga mbele zaidi.Kwa kuwa walielekezwa ni wapi pa kufika kazi ya Daphine ilikuwa ni kukunja kona,kupanda milima na kushusha mabonde na alikuwa akipita katikati ya miti mirefu sana kama vichaka,mpaka wanafika nje ya geti na kupiga honi walitumia takribani dakika hamsini.Ngesa akafumbua jicho moja na kupiga jicho dirishani ambapo aliona wanaingia ndani ya geti kubwa la kijivu.Gari likazama mpaka ndani,Brigedia Karanje alikuwa katikati ya uwanja,analitizama gari.Lilivyosimama Daphine akashuka,Zaitun akafuata,wakafungua mlango wa nyuma.
“Mkuu,huyu hapa”
Brigedia Karanje akasogea mpaka mlangoni akapiga jicho ndani.
“Amekufa?”
“Hapana,kapoteza fahamu”
“Kazi nzuri,mpelekeni stoo”
Jambo hilo lilifanyika wakati huohuo,Ngesa akatupwa ndani ya stoo,akanyanyuliwa mikono yake ikafungwa kwa juu akawa ananing’inia kama nyama buchani ingawa alihisi maumivu lakini hakutaka kujifanya ana fahamu.
“Mwacheni mpaka asubuhi”
Kauli hiyo ilivyotoka lango likafungwa!
Mpaka kunakucha Ngesa alikuwa ndani ya chumba kilichofanana na Stoo,mikono yake ilikuwa juu imefungwa na kamba.Kwa mbali alihisi vishindo vya watu vinasogea chumba alichohifadhiwa,lango likafunguliwa,akamwagiwa maji ya baridi.Akakurupuka na kufumbua macho yake,mbele yake walisimama wanaume watatu na mmoja wapo alikuwa ni Brigedia Karanje!
“Ngesaaa.Una roho ya paka!Nafurahi kukutana nawewe kwa mara nyingine inapendeza sana.Una deni langu?Mtoto yuko wapi?Unamkumbuka?Alikuwa mdogo sana.Tuachane na hayo nataka kabla ya kukuuwa ushuhudie kitu kimoja”
Brigedia Karanje aliongea kwa kiburi na dharau nyingi,Kwa mara ya kwanza Ngesa hakujuwa Karanje anataka kufanya nini mpaka ilivyofika jioni na kuoneshwa bomu kubwa.
“Muhimbili leo Rais wako ataokota vipisi vipisi vya nyama”
Jambo hilo halikuwa utani kwani usiku ulivyoingia alisikia king’ora cha gari la wagonjwa kisha bomu kupakiwa,alisikitika sana lakini hakuwa na jinsi ya kujinasua.
“Saa tano leo kutakuwa na sherehe Muhimbili,upuuzi wa Rais wako!Kumuokoa Ritha haikusaidia chochote,Kwa kuwa nina mabomu mengine ya Nuclear”
Ngesa alikuwa kimnya ametulia anamsikiliza kila anachoongea Brigedia Karanje.
“Kwanini umeamua kufanya hivyo?Unamsaliti Rais wako.Unauwa watanzania wenzako wasiokuwa na hatia”
“Nyamaza”
“Jisalimishe mapema.Sababu utakufa kifo kibaya sana,jeshi la Tanzania litakutafuta na utapatikana”
Ngesa aliongea akimtizama Brigedia Karanje na ilielekea hakuogopa kitu chochote kile,ndiyo maana alizungumza ingawa alikuwa mateka!Brigedia Karanje hakuwa ana tania sababu alipokea simu na kupewa taarifa kwamba jengo la Muhimbili limelipuka.Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Brigedia Karanje!
“Kata kamba hizo.Mlete thietha kule”
Ilikuwa ni agizo kutoka kwa Brigedia Karanje na kamba ya Ngesa ikakatwa hapohapo,akadondoka kama embe mtini puu,akaburuzwa mpaka chumba kingine.Ndani kulikuwa na vitu vilivyotisha mno kama Mikasi,Sindano,visu na mapanga.
“Nataka kukuuwa kiuungwana!”
Hiyo ilimaanisha kabla ya kifo chake ilikuwa ni lazima aonje mateso makali.Hivyo ndivyo ilivyokuwa sababu alifungwa juu ya kiti akazungushiwa na kamba,Brigedia Karanje akachukua kisu kirefu na kuanza kumkata Ngesa kifuani,akawa kama mtu anayekata kipande cha embe, hakujali maumivu anayohisi Ngesa,damu nyingi zilikuwa zinamtoka na alipiga kelele mno lakini hiyo haikusaidia.
“Captain,leta hiyo ndoo ya spirit”
Ndoo iliyojaa dawa ya spirit ikasogezwa bila kuuliza chochote Brigedia Karanje akammwagia Ngesa mwilini,kelele alizopiga Ngesa zilitisha sababu alihisi maumivu yasiyoweza kuelezeka.
Mateso yalikuwa ni zaidi ya Jehanam kwake,Ngesa alikuwa akisulubishwa vibaya sana na alihisi maumivu makali mwilini mwake baada ya kumwagiwa dawa ya spirit,mbaya zaidi alikuwa ana vidonda vikubwa sana hiyo ilikuwa kinyume kwa Brigedia Karanje ambaye alikuwa ana furaha kufanya hivyo.Baada ya kumwagiwa ndoo ya Spirit aliendelea kupewa kibano na ndani ya dakika moja sura yake ilibadilika na kuwa kama nyama buchani,alivimba uso na macho yake yalivulia damu,hakutofautishwa na mtu aliyejeruhiwa na gari kubwa la mchanga.
“Leta ile grili mashine na biti nchi saba”
Ngesa alijuwa tayari amekwisha,kazi ya grili mashine ilikuwa ni kutobolea ukuta lakini siku hiyo ilikuwa inaenda kutoboa mwili wa Ngesa.
“Leta ile mashine nyingine ya mapigo ya moyo.Nataka akifa hapa juu ya kiti nijue”
Kila alichoagiza Brigedia Karanje kilifikishwa mara moja,Ngesa akavalishwa waya kifuani na mikononi na pembeni ikawekwa mashine ya mapigo ya moyo ambayo ilikuwa inatoa sauti kuashiria kuwa uhai bado upo.
“Vuuuuuuuuuuuuuuuuu”
Grill mashine ilipiga kelele baada ya kuwashwa,mbele ilikuwa na chuma kilichochongoka kirefu sana kilichoitwa biti na kilikuwa kinazunguka kwa kasi kubwa sana kumaanisha kuwa kingeingia mwilini mwa Ngesa kingemchimba na kutokea upande wa pili.
“Chagua,nikutoboe macho au utumbo”
Brigedia Karanje akauliza na Ngesa alikuwa juu ya kiti amechoka, anasubiri kifo chake kibaya damu zinamtoka mwili mzima,ni wazi kuwa alikuwa mdomoni mwa mamba na alikata tamaa kwani hakukuwa na mtu yoyote anayejuwa ni wapi alipo licha ya yote alisikitika sababu hakujuwa hali ya mpenzi wake Jaqlin Mfinanga inaendeleaje.Grill ilikuwa inasogea karibu na jicho lake la kushoto kumaanisha kuwa ingemfikia ingetokea nyuma ya kichwa chake.
“Mkuu.Kuna simu yako hapa”
Zoezi hilo lilisitishwa baada ya Brigredia Karanje kuitwa kwa nyuma,ilikuwa ni simu na ya muhimu sana.
“Nani anapiga?”
“General Kipingu”
“Anataka nini?”
“Anauliza kuwa kama mabomu yapo hapa yote”
“Yapo ndio”
“Pia anataka kuzungumza nawewe.Ni muhimu”
Kila kilichozungumzwa na watu hao Ngesa alikisikia vizuri sana.Alisikitika sana sababu watu wangeendelea kufa kwenye mlipuko wa mabomu kwa maana hiyo ilikuwa ni lazima awaokoe kwa njia moja ama nyingine.
“Ndio nakusikia General”
Brigedia Karanje aliweka simu sikioni na kutoka nje ili kufanya mazungumzo, ndani alimuacha mwanajeshi mwingine.Akili ya Ngesa ikafanya kazi kwa kasi ya risasi,alijivuta karibu na nyaya zilizokuwa kifuani kwake,akatumia meno kuzitoa.
“Tiiiiiiiiiiiiiii”
Mashine ikapiga kelele kuashiria kuwa mapigo yake ya moyo yamesimama na Ngesa alijifanya amekufa.Hakuna kitu alichojichanganya Mwanajeshi huyu kama kumsogelea akijaribu kuweka mikono yake juu ya kifua cha Ngesa akitaka kuhakikisha kama kweli ana uhai.Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya Ngesa kujinasua,hapohapo kwa umakini wa hali ya juu akitumia miguu yake alimkata ngwala na mbaya zaidi akamdondokea,hapo Ngesa alipanua mdomo wake na kung’ata sikio la mwanajeshi huyu kwa nguvu za ajabu mpaka alivyohisi meno yake yamegusana akang’ofoa sikio kisha kulitema na kuivuta miguu yake kwa juu,akaizungusha shingoni mwake na kuiviringisha, jinsi alivyoizungusha miguu yake shingoni alikuwa mwenye uhakika kuwa huo ndiyo ungekuwa mwisho wa uhai wa Mwanajeshi huyo akiwa hapohapo chini na alifanya haraka sababu angetokea Brigedia Karanje angeingia kwenye matatizo makubwa sana.
“Arrggg aaargg”
Mwanajeshi alijitahidi kuutoa mguu wa Ngesa lakini ilishindikana na aliishiwa nguvu kabisa,hapohapo Ngesa akajivuta kwa nguvu akavunja shingo yake.Nafasi hiyo kwake ilikuwa kama dhahabu akajivuta na kiti mpaka alipofikia mikasi,akatumia mikono ya nyuma na kuuvuta na kuanza kusugua kamba,zikaachia.Mikono yake ikawa huru,akasimama.Akatembea mpaka mlangoni na kutoa kichwa nje ambapo hakukuwa na mtu,akaanza kuambaa na ukuta huku akiingiza mikono mfukoni,ilikuwa ni lazima apige simu ikulu na kumueleza Rais kila kitu.Hicho ndicho kitu alichokifanya,alitembea mpaka nyuma ya tenki kubwa na kusimama sababu mbele yake aliona jopo la wanajeshi wenye silaha kali.
“Griii griiii”
Simu ilianza kuita.
“Halloo Mh.Rais unaongea na Ngesa.Trace hii simu”
“Ngesa upo wapi?”
“Sijui nilipo nachokuomba trace hii namba”
Ulikuwa ni usiku mkubwa na simu kutoka kwa Ngesa ilimtisha Mh Rais, hapohapo akachomoka kutoka kitandani mpaka ofisini kwake akiwa ana simu mkononi mwake!Ilibidi awaambie walinzi wake kila kitu na namba zikatumwa usalama wa taifa.
“DK unasikia?”
Rais Leslie alimuuliza Dustan simuni.
“Ndio nimekuelewa,ndiyo nasubiri jibu hapa”
“Ukipata jibu nipigie simu”
“Sawa mheshimiwa”
Zoezi la kusaka namba kwa kutumia GPRS ili kujua ni wapi Ngesa alipo lilianza mara baada ya taarifa hizo kufika kwa C.I.D DK na ndani ya dakika kumi majibu yalikuwa tayari mezani,hakukuwa na muda wa kupoteza Raisi Leslie akapigiwa na kupashwa habari hiyo.Amri ikatoka ikulu kuwa jeshi la polisi liende.
“Mheshimwa Rais,hiyo itakuwa ni vita.Wanahitajika askari kama themanini”
“Sawa,naomba wewe uongoze hilo zoezi”
“Ahsante”
“Kuwa makini”
Operesheni ilianza mara moja,simu zilianza kupigwa usiku huo huo maaskari walikurupushwa kutoka usingizini.Kwa kuwa jambo hilo lilikuwa zito mno ilibidi wafanye kikao kilichojumuisha askari sabini na moja na kiongozi wao alikuwa ni DK.
“Eneo ni Mbezi Beach Makabe,katikati ya huu msitu.Tutaingia kimnyakimnya bila kelele,muwe makini hii nyumba ina wanajeshi na wana silaha za moto.Cha kufanya hii nyumba mtaizunguka.Mimi na wenzangu tutaingia ndani mtasubiri amri yangu.Mmenielewa?”
“Ndio mkuu”
“Ndio mkuu”
Askari wote waliitikia na hakukuwa na yoyote yule mwenye swali.Wote wakaingia kwenye difenda na safari ya kwenda kufanya ambush kuanza mara moja.
“Jenipher upo tayari?”
DK alimuuliza mpelelezi mwenzake baada ya kumuona mwanamke huyo kama ana wasiwasi.
“Nipo tayari”
“Una uhakika?”
“Ndio bosi”
“Sawa”
Msafara uliongozwa na Dustan akitumia marcedez benzi nyeusi ambapo ndani kulikuwa na C.I.D wengine, nyuma difenda tano,zimejaza maaskari wenye silaha za moto.Waliingia mbezi mwisho,hapo wakaanza kupunguza mwendo kisha kuipitia msakuzi.Hawakutaka kuendelea mbele zaidi wakaegesha magari yao katikati ya kipori chenye miti mingi!
“Kuna kama kilomita mbili mbele,hatuwezi kusogea zaidi.Cha kufanya.Ni kuizunguka nyumba kimnya kimnya.Msiingie bila go ahead yangu”
“Sawa mkuu”
Kabla ya kufanya lolote ilibidi wapewe tena maelekezo na baada ya hapo Dustan pamoja na wenzake wakaanza kukatiza pori kwa pori,ulikuwa ni mwendo mrefu kiasi lakini walifanikiwa kufika na kuiona nyumba kubwa iliyozungushiwa ukuta mrefu,nje kulikuwa na wanajeshi wenye mitutu wanalinda.Dustan akatoa Darubani yenye lensi na kuanza kuangalia huku na kule.
“Kuna watu watatu juu.Hapo getini mmoja.Jenipha anza na wa getini”
“Okay”
Huyu alikuwa ni mwanamke mrembo lakini shupavu haswa linapokuja katika swala la kazi yake na ilionekana hakumuhofia mtu yoyote yule ndiyo maana akaanza kutembea taratibu mpaka nyuma ya mti ambapo mita chache kulikuwa na mwanajeshi kasimama ameshika mtutu,akapiga hesabu za harakaharaka.Akaokota kipande cha mti na kukirusha kushoto,kosa la jinai alilofanya mlinzi huyu ni kugeuza shingo ambapo Jenipher alitokea upande wa kushoto na kumpiga roba ya nguvu mpaka pembeni huko alimtuliza na kifuti na chembe,mlinzi akatulia kimnya.
Wakati nje ambush inaendelea ndani Ngesa alikuwa anatafuta njia ya kutoka,Karanje alikasirishwa sana baada ya kuingia na kumkosa Ngesa juu ya kiti.
“Hawezi kutoka ndani humu,msakeni mumuuwe mara moja”
“Sawa mkuu”
Wanajeshi wakaanza kukimbia huku na kule hakuna hata mmoja aliyeelewa kuwa Ngesa yupo nyuma ya Tenki anawaona.
Ngesa alisakwa kila pembe ya nyumba na hakutafutwa akamatwe bali auwawe mara moja!Hiyo ilikuwa amri kutoka kwa Karanje.Jumba lilikuwa kubwa mno na waliamini kivyovyote vile Ngesa hakutoka nje,msako walioufanya haukuwa wa kitoto.Kila chumba kilipekuliwa, wanajeshi wote walimsaka Ngesa kwa wudi na uvumba.
“Huyuuu hukuuuu”
Mwanajeshi mmoja alisikika akipiga kelele baada ya kumuona Ngesa yupo nyuma ya tenki,akamuinua na wanajeshi wote wakamsogelea.
Akapigwa na kitako cha mtutu akadondoka chali.Wakati hayo yanafanyika nje kulikuwa na askari thelathini na nane na waliiweka nyumba katikati wakisubiri amri ya Dustan ama DK ili waanze ambush,ilikuwa ni operesheni ambayo waliamini ingetingisha jiji zima la Dar es salaama na Tanzania kwa ujumla.Ilikuwa ni vita kubwa baina ya polisi na wanajeshi.DK kwa tahadhari aliruka ukuta na kuzama ndani baada ya kuona kila kitu kipo sawa,alisonga mbele mpaka dirishani ambapo aliwaona wanajeshi wamesimama, wamemuweka Ngesa katikati wakiwa na mitutu.Akachomoa bastola yake na kuweka kiwamba cha kuzuia sauti isitoke.
“Namuona Ngesa,narudia namuona Ngesa lakini bado sijapata saiti nzuri.Anzeni kuingia kutokea Kaskazini sasa hivi”
DK alizungumza na askari kupitia kifaa maalumu kilichokuwa ndani ya sikio lake,hiyo ilifanya kila askari asikie kupitia redio upepo.
“Tulia hivyohivyo.Weka silaha chini”
DK aliwekewa bastola kwenye kisogo chake,kumaanisha kuwa yupo chini ya ulinzi.Tayari alikuwa ameonekana na mmoja wa wanajeshi.
“Weka silahaa chini”
Mwanajeshi aliyekuwa nyuma yake alifoka!
DK ama kwa jina lingine ni Dustan,tayari amewekwa chini ya ulinzi akiwa ametekwa nyara katika operesheni yake ya kutaka kumkomboa Ngesa,nje ana jeshi kubwa ambalo aliamini muda wowote ule lingeingia na kufanya ambushi kubwa sana,pengine ingezuka vita vya tatu vya dunia,hivyo ndivyo vitu vilivyokuwa vinapita kichwani kwa mwanaume huyu jasiri baada ya kuona wanajeshi wengi mno wakiwa na mitutu na silaha za moto hiyo ilitosha kabisa kulipitisha wazo lake kuwa vita itakayotokea siyo ya kitoto na ingeingizwa kwenye vitabu vya historia sababu damu nyingi zimemwagika na watu wangepoteza uhai.Nyuma yake alikuwa amewekewa mtutu mikono yake ipo hewani na aliamriwa asonge mbele mpaka walipofika sehemu yenye uwazi mkubwa,hapo alikumbana na lundo lingine la wanajeshi wamevaa kombati.Katikati yao alimuona Ngesa anavuja damu nyingi sana,ni wazi kwamba watu hao aliowaona hawakuwa na roho za kibinadamu,walitisha kuliko ukoma.
“Wewe ni nani?”
Hiyo ilikuwa sauti ya kukwaruza kutoka kwa Brigredia Karanje,akimuuliza Dustan.
“Nakuuliza wewe ni nani?”
Sio Kwamba Dustan hakusikia swali,hakuelewa ajibu nini.
“Kacha kacha”
Ni mlio wa sauti ya bastola kukokiwa,Brigedia Karanje ndiye aliyefanya kitendo hiko akamsogelea Karibu Dustan na kumuwekea bastola kichwani.
“Wewe ni nani?Msachini”
Amri hiyo ilivyotoka makamanda wakaingia mifukoni mwa Dustan na kuanza kumsaula,wakakuta vitambulisho vya usalama wa taifa pamoja na risasi.Hapo ndipo walipoanza kushtuka kuwa kuna kitu kibaya kitatokea na kivyovyote vile wamejulikana walipo.Wakati wanamuuliza Dustan maswali yote hayo C.I.D aliyeitwa Jenipha alisikia kila kitu sababu Dustan alikuwa ana kifaa maalum sikioni cha kuzungumza,hivyo akawapa taarifa askari kwamba wasiingie kwanza mpaka wapate muafaka.
“Narudia msiingie kwanza,narudia tena msiingie kwanza.Dustan najua unanisikia vizuri.Kama upo na Brigedia Karanje,kohoa”
Huyu alikuwa ni mwanamke machachali na makini sana katika swala kama hilo la ujasusi,hivyo aliweza kuwasiliana na Dustan kitaalam bila Brigedia Karanje kujua.
“Koho koho”
Dustan akakohoa,hakuna mtu yoyote kati ya wanajeshi waliokuwa ndani aliyeelewa kwamba Dustan anafanya mawasiliano na kukohoa kwake lilikuwa ni jibu kuwa Brigedia Karanje yupo ndani.
“Nice Dustan,Ngesa yupo pia?Kohoa tena kama yupo”
Hivyo ndivyo ilivyokuwa Dustan akakohoa,hapohapo Jenipha kwa tahadhari kubwa akatembea mpaka ukutani na kuweka bastola yake kiunoni.
“Cover me”(Nilinde)
Kufuatia hapo askari wote wakashikla bastola zao sawasawia wakimlinda Jenipha ili aruke ukuta,bahati nzuri akafanikiwa kuingia ndani ya ngome.Kitendo cha kutua akachomoa bastola yake na kuangalia pembe zote kama komando vitani.
“Dustan,nakuja ndani.Kila kitu kipo sawa”
Jenipha akaongea taratibu huku akizidi kusonga mbele,mbele yake kulikuwa na ukuta mdogo,akatoa darubini yenye lensi kali na kuiweka machoni.Akawa anakagua huku na kule!
“Mungu wangu”
Kitu alichokiona kilimshtua kupita kiasi,Dustan alikuwa amewekewa kisu shingoni na angechelewa dakika nyingine mbili zingekuwa habari nyingine.
“Dustan,nahesabu mpaka tatu.Hakikisha unaruka upande wa dirisha alipokuwa Ngesa,nitarusha Grenade.Askari wote mnanisikia?Mkisia mlipuko wa bomu wote ingieni ndani msipoteze muda,operesheni ianze”
Taarifa alizokuwa anatoa kila afande alizisikia kupitia redio upepo na hapohapo wakaanza kukoki bastola na mitutu yao tayari kwa vita kali dhidi ya wanajeshi waliokuwa wengi.
“Leo nakuuwa.Umetumwa kuja kumkomboa Ngesa?Kabla ya kumkomboa nakata kichwa chako”
Brigedia Karanje alisema maneno hayo ya kutisha na kisu kilikuwa shingoni kwa Dustan.Kwa jinsi mambo yalivyoenda ilikuwa ni lazima shingo ya Dustan inyofolewe kwa kisu,hilo halikuwa na mjadala Ngesa alisikitika na kumuonea huruma Dustan sababu angeenda kufa kifo kibaya hata hivyo alijionea huruma mwenyewe vilevile.
Sikio moja la Dustan lilifanya kazi ya ajabu na alikuwa makini kusikiliza maelezo ya Jenipha aliyekuwa nje anataka kuingia na kutupa bomu,ilikuwa ni lazima wamalize walichokianza.Akawaangalia wanajeshi wote na kumtizama Ngesa kwa umakini hapo alikuwa akipiga hesabu kali mno,kwa kasi ya mwewe akampiga kikumbo mwanajeshi aliyekuwa nyuma yake na kumrukia Ngesa,wote wakadondoka chini.Kabla ya wanajeshi kuinua mitutu yao,kitu kama kimpira cha chuma kilidondoka kwa mbele.
“Grenadeeeee”
Brigedia Karanje akaachia ukelele na kuruka kando,hapohapo ukatokea mlipuko mkubwa.Na kuanzia hapo zikasikika risasi kila kona.
“Griiii gegegeege paa paa paaaaa”
Jeshi la polisi la Tanzania likaanza kuingia ndani huku wakiachia risasi,nyumba ilikuwa tayari imezungukwa na polisi hawa waliokuwa na mafunzo ya kupambana na wahalifu.Ngesa alikuwa chini,akajitahidi ili kuona mbele.Akamuona Brigedia Karanje anasimama na kutaka kukimbia,akajitahidi kusimama na kumvaa na bega wote wakadondoka chini,alikuwa ana usongo naye sio kawaida.Hakuchelewa hapohapo akaanza kumpiga ngumi za mbavu wakiwa chini lakini alizidiwa sababu Brigedia Karanje alimzidi nguvu,akamsukumiza kando kisha kusimama na kukunja ngumi,Ngesa bado alikuwa dhaifu na kabla ya kusimama akapigwa teke la tumbo akadondoka upande wa pili.
“paaa paaaaa paaaa”
Risasi zilizidi kurindima kila kona,Wanajeshi nao walikuwa ngangali.Ilikuwa ni kama sinema ya kuigiza kumbe ni kweli.Wakati Polisi na wanajeshi wanarushiana risasi yeye Ngesa alikuwa anapambana na Brigedia Karanje kiume ingawa alionekana kuchoka lakini alijaribu kadri awezavyo ili kumzidi nguvu.
Kilichokuwa kinamshinda ni baada ya kuwekwa ukutani akiwa amekabwa sana,hakuweza kujitoa tena kwenye mikono ya mwanajeshi huyu aliyekomaa mikono.
“Paaaaaa”
Risasi moja ilichomoka kutoka kwa DK na kumfikia Brigedia Karanje begani,hapo ndipo alipomuachia Ngesa.Walivyotaka kumsogelea walirushiwa risasi na wanajeshi wengine waliotokea mbele yao lakini waliwahi kubiringika na kujificha nyuma ya machuma.
“Mkuu huku”
Brigedia Karanje akainuliwa wakamtoa kwa nje ambapo waliingia chumba cha pili.Huko walisukuma kitanda na chini kulikuwa na tobo kubwa sana yaani andaki,wakaingia ndani ili kukimbia.Wakati hayo yote yanaendelea nyuma uwani Jenipha alikuwa anakula sahani moja na Daphine,bastola yake ilikuwa chini na walikuwa wakipigana misumbwi,sio siri wanawake hawa walikuwa fiti.Daphine alirusha ngumi kali lakini hakufanikiwa sababu Jenipa alihepa kushoto ngumi ikapita hewani,alivyokaa sawa alimvuta Daphine na kumpiga kifuti cha pua,hapohapo kama umeme akamvaa na kumtandika ngumi takatifu ya shingo,Daphine akayumba akahisi kama Israeli mtoa roho za watu yupo mita chache kushoto kwake,Jenipha hakuwa mwanamke wa mchezomchezo na alitumia staili ya judo kupambana na Daphine,akamvuta kwa nguvu na kumpiga pingu mikononi.
“Upo chini ya ulinzi”
Daphine tayari alikuwa chini ya ulinzi hakuwa na ujanja mwingine wa kukimbia.
Mirindimo ya risasi iliendelea kudumu na kila baada ya dakika kumi jeshi la polisi liliongezwa hiyo ilifanya mpaka wanajeshi wasalimu amri na wengine waliingia kwenye andaki alilokimbilia Brigedia Karanje,wengine walipoteza maisha yao.Kwa harakaharaka askari hamsini walikufa na wengine thelathini walikuwa mahututi hata hivyo kazi ilikuwa nzito sana,mpaka kunakucha polisi walifanikiwa kushinda vita hiyo kali.
“Dustan niachie,hawezi kuwa hai”
“Ngesa.Tunaenda kisheria”
“No,kuna asiyejuwa kuwa huyu mwanamke ni jambazi sugu.Niachie nimuuwe”
“Ngesa,tulia”
“Dustan,tuheshimiane.Naomba niachie”
Uliibuka mzozo mkubwa sana kati ya Dustan na Ngesa baada ya Daphine kuwekwa juu ya kiti na Jenipha, akiwa amefungwa pingu,Ngesa hakutaka kumuona mbele yake hasa alivyoikumbuka hali ya mpenzi wake Jaqlin Mfinanga,mwanamke huyo hakustahili kuwa hai hata kidogo ndiyo maana alitaka kusimama amvae na amuuwe hapohapo juu ya kiti.Akamvuta Dustan na kumsukuma kando,kabla ya kumfikia Daphine alipigwa teke na Dustan,hapohapo wakaanza kushikana mashati!Dustan akatupwa mbali na hapo ndipo ugomvi wa ngumi ulipoanzia,Dustan akarusha ngumi lakini Ngesa aliidaka na kumtwanga kichwa kikali cha pua kilichomfanya aone nyota mbele.
“Paaaa paaaaa”
Ni risasi mbili ndizo zilizosikika wote wakatulia,alikuwa ni Jenipha ndiye kafanya hivyo baada ya kupiga risasi hewani.
“Tulieni”
Akasema kwa hasira.
“Mweke Ngesa chini ya ulinzi,mpige pingu”
Dustan nayeye akaibuka kutoka chini akiwa ameshika pua yake inavuja damu.
“Afande, Ngesa yupo chini ya ulinzi,mfunge pingu.Mimi ndio Incharge”
Askari hapohapo wakasogea, tena sio mmoja na wao walimuhofia Ngesa ndiyo maana wakasogea askari watano na bastola mikononi,Ngesa akapigwa pingu kwa nyuma.
“Upo chini ya ulinzi”
Dustan akasema kwa hasira na kumtandika kibao cha uso!
“Naomba niongee na Muheshimiwa Rais”
“Upo chini ya ulinzi,mpakieni kwenye gari”
Dustan akasisitiza na Ngesa akaanza kubuluzwa na maaskari kutolewa nje!
Lilikuwa ni tukio kubwa lililochukuwa hisia za watu wengi mno majirani na watu kutokea sehemu mbalimbali walikusanyika eneo hilo kama kawaida ya wabongo,nje walijaa askari wengi na walizidi kumiminika, waandishi wa habari ndio usiseme!Habari hiyo ilirushwa moja kwa moja katika televisheni ya taifa TBC Na waandishi wa habari walionekana kutoogopa tukio hilo ndio maana walisogea karibu kabisa.Magari ya wagonjwa yalipiga misele na kupakia majeruhi na maiti za wanajeshi na polisi waliouwawa katika operesheni hiyo ya kumsaka Brigedia Karanje!
“Habari zilizotufikia hivi punde hapa maeneo ya Mbezi Makabe, askari walikuwa katika operesheni ya kusaka wahalifu na hapa nilipo nipo eneo la tukio.Kuna majeruhi wengi kama mnavyoona na magari ya polisi yamekusanyika nje ya eneo, bado hatutajua chanzo kamili cha mirindimo ya risasi kutokea TBC taifa mimi ni Neema Mawazo”
Alikuwa ni mmoja wa waandishi wa habari akiwa makini na kipaza sauti na kufanya habari hiyo ionekane kwenye televisheni ndiyo maana ikafanya kila raia wa jiji la Dar es salaam na nchi ya Tanzania kwa ujumla watulie na kutizama nini kilichojiri.Askari walivyotoka nje na kuhojiwa hawakuwa tayari kuongea chochote kile.
“Jenipha helkopta inakuja,Ngesa na huyo Daphine wataingia kwenye Helkopta pamoja na mimi na wewe.Tutaenda ofisini”
“Sawa”
Yalikuwa ni maagizo kutoka kwa Dustan akiwa tayari ameshika bastola huku ameshika pua yake ambayo bado ilikuwa na maumivu ya kupigwa kichwa na Ngesa.Askari waliendelea na kazi ya kupakia maiti na majeruhi bila kuchoka na hapohapo Helkopta kutoka usalama wa taifa ikasikika nje.Dustan akiwa na Ngesa kapigwa pingu kwa mbele, nyuma Mpelelezi Jenipha katikati Daphine ambaye hata yeye alikula pingu kwa nyuma walianza kuongoza kutoka nje.Kitendo cha kutoka nje waandishi wa habari waliwavaa na kuwahoji huku wakipiga picha za mnato.
“Sipo tayari kuongea kwa sasa hivi,tafadhali naomba njia”
Dustan alijibu huku akiwapangua waandishi wa habari.
“Tuambie hata kwa kifupi ilikuwaje?”
“Nimesema siwezi kuongea chochote naomba kupita tafadhali”
Dustan akafoka kidogo lakini waandishi wa habari waliendelea kumganda kama nzi juu ya kokwa la embe,moja kwa moja wakapita mpaka ilipokuwa imeegeshwa helkopta wakaingia ndani.
Rubani wa helkopta akabonyeza bonyeza mitambo hapohapo ikaanza kutoa mlio kisha mapanga boi yakaanza kuzunguka taratibu kisha kuchanganya kasi,ikaanza kuinuka na kuelekea juu.Kichwa cha Ngesa siku zote kilikuwa kinafikiria vitu vingi sana na alitafakari vitu chungu mzima,uchungu ulimbana hasa alipokumbuka risasi alizopigwa kipenzi chake Jaqlin Mfinanga!
Akamuangalia Daphine kwa jicho kali la hasira alitamani hapohapo amvae na kumtupa nje ya helkopta lakini akaupiga moyo konde.Helkopta ilizidi kutoboa mawingu na ndani ya dakika chache ikatua Posta juu ya gorofa kubwa,hapo wote walishuka na kuingia ndani ya jengo kubwa!
Ofisi za C.I.D zilikuwa gorofa namba 14, hivyo iliwalazimu waingie ndani ya lifti na kubonyeza nambari za gorofa waliyotakiwa kufika,baada ya kufanya hivyo ikafunguka na kutoka nje hapo walivyoingia tu wafanyakazi wote wakasimama wima.
“Hongera Dustan”
“Hongera Dustan”
“Hongera Bosi”
Dustan alipewa pongezi na wafanyakazi wote na wengine kwa heshima wakampigia makofi kwa kazi nzito aliyofanya,Ngesa na Daphine wote walikuwa chini ya ulinzi na wote waliwekwa ndani ya vyumba maalum ambavyo vilikuwa tofauti.
Wakati hayo yote yanaendelea Ikulu Mheshimiwa Rais alikuwa bize simuni anapokea simu mbalimbali za viongozi kutoka nchi mbalimbali wakimpa pole na pongezi kwa mambo yaliyotokea na baadhi yao walitaka kujuwa nini kilichojiri lakini hakuwa tayari kufunguka na kuongea ukweli,baada ya kuongea na maraisi kutoka nchi za Malawi,Msumbiji,Kenya pamoja na Afrika ya Kusini akapokea simu nyingine kutoka nchini Uganda kwa Rais Yowel Museven huyu alitaka kuingilia kati sababu siku zote alikuwa mshali.
“Nikutumie jeshi?”
Yowel Museven aliuliza simuni.
“Hapana mzee wangu,mambo yapo sawa sasa hivi”
“Ukiwa na tatizo lolote usisite kunieleza,nina jeshi ngangali kabisa na ndege za kisasa za vita!”
“Ahsante sana,nitakutaarifu nikihitaji msaada”
“Majukumu Mema”
“Ahsante”
Ilimchukuwa Rais Leslie Masaa matano kuongea na simu zote mpaka akamaliza na juu ya kioo chake cha televisheni bado kulikuwa na habari na kwa muda mfupi zilienea karibia nchi zote za Afrika,alishtuka zaidi baada ya habari hiyo kuruka mpaka CNN London,hiyo ilimaanisha ambush hiyo ilijulikana kitaifa.
“Mugolozi”
Akamuita mlinzi wake.
“Naam mh.”
“Niwekee Dustan kwenye laini namba mbili,alafu naomba niongee na watanzania leo jioni saa kumi.Niandalie speech”
“Sawa mtukufu”
Ndani ya dakika moja Dustan alisikika simuni anazungumza na Rais, kwanza alipewa hongera na cha pili alitaka kujuwa kama Brigedia Karanje tayari yupo mikononi mwa Sheria.
“Hapana Mheshimiwa Rais”
“Whaaaaaat?”(Niniiiii)
“Alitoroka”
“Kivipi Dustan?”
“Bado sijajua lakini tumemkamata mmoja wa wafuasi wake”
“Sitaki kusikia hayo maelezo nataka Karanje awe mikononi mwa sheria,Ngesa yupo wapi?”
“Yupo chini ya ulinzi”
“Kwanini?”
“Ameenda kinyume na sheria tulipokuwa field”
“Naomba nizungumze naye sasa hivi”
“Sawa Mheshimiwa”
Hazikupita dakika tano Ngesa akawa kwenye laini na mheshimiwa Rais.
“Ngesa una habari kuwa Brigedia Karanje ametoroka?”
“Mheshimiwa Rais,Karanje alikuwa mikononi mwangu tayari lakini ilishindikana sababu ya hawa watu uliowatuma kuharibu kila kitu”
“Ngesa,naomba Karanje awekwe chini ya ulinzi”
“Siwezi”
“Kwanini?”
“Nipo chini ya ulinzi”
“Mimi ndio amiri jeshi mkuu,upo huru.Naomba wakupe ushirikiano”
“Sawa Mheshimiwa.Lakini Mheshimiwa raisi nakuomba kitu kimoja”
“Kitu gani Ngesa?”
“Mke wangu amejeruhiwa vibaya sana,amepigwa risasi yupo Mwananyamala sasa hivi.Naomba apatiwe matibabu,nakuomba sana!Anaitwa Jaqline Mfinanga”
“Pole sana Ngesa,hilo nitalifanyia kazi.Atatibiwa hapa Ikulu”
“Ahsante sana”
Simu ikakatwa na hakukuwa na kipingamizi kingine chochote kile,Ngesa akawa huru akafunguliwa pingu.
“Daphine yuko wapi?”
Hilo ndilo swali la kwanza kuuliza Ngesa huku akiyabana meno yake kwa hasira.
“Yupo Interrogation room anahojiwa”
“Nipeleke”
“Ngesa hili swala liachie usalama wa taifa”
“Unanipeleka au niende mwenyewe?”
Ngesa akauliza kwa hasira za wazi wazi alikuwa ana usongo na Daphine kwa kiasi cha kutosha.Dustan hakuweza kupinga akatembea mbele Ngesa akamfuata nyuma mpaka kwenye kioo kikubwa ambacho kilikuwa cheusi,kupitia kioo Ngesa alimuona Daphine anahojiwa huku akiwa amefungwa pingu.Jinsi Daphine alivyokuwa anajibu maswali kwa kiburi ilimfanya Ngesa apandwe na hasira zaidi.
“Daphine Hans,hilo ndio jina lako.Hii ni picha yako hapa ulikuwa na Karanje.Mna uhusiano gani?Na yuko wapi sasa hivi?”
Lilikuwa ni swali kutoka kwa C.I.D Yassin Kabwe akimuhoji Daphine na kumuuliza maswali.
“Karanje ni bwana angu,hivi mfano ungekuwa wewe ndiyo mimi ungemtaja bwana ako alipo?Usipoteze muda.Siwezi kumtaja sababu ananipa utamu,anajua mapenzi kitandani”
“Daphine usifanye mchezo,utafungwa sema ukweli ili sheria ikufikirie”
“Unapoteza muda kaka angu,siwezi kutaja alipo”
Hayo ndiyo maswali aliyokuwa anaulizwa Daphine tena kwa kubembelezwa kama mtoto anavyopewa uji na kila swali lilioulizwa Ngesa alilisikia ndiyo maana akawa ana usongo wa kuingia ndani.
“Dustan,nifungulie mlango niingie kumuhoji mimi”
“Hapa sio kituo cha polisi sisi tuna fuata haki za binadamu haturuhusiwi kumtesa mtuhumiwa.Ndio Protocol za usalama wa taifa”
“Kwa staili ile hawezi kujibu chochote,mtapoteza muda”
“Hapana Ngesa siwezi kukuruhusu”
“Rais anahitaji Karanje awe amekamatwa.Nataka nimpigie simu sasa hivi nimwambie kuwa umenikataza,nipe simuuuuu”
Ngesa akafoka kwa hasira,mwili wake ulijaa jasho akawa kama simba mwenye njaa alafu kaona swala mbele yake,hiyo ilimfanya Dustan apate uwoga,akagonga kioo.C.I.D Yassin akasimama na kufungua mlango!
“Umefikia wapi?”
“Hana dalili ya kutaja”
“Naomba Ngesa aingie kumuhoji”
“Okay”
Ngesa akatizama kioo ambapo ndani alikuwa Daphine amekaa, hajui kuwa Ngesa yupo huru na ndiye atakayeingia ndani muda mfupi tu.Ngesa akapiga hatua na kutembea mpaka mlangoni!
“Ngesa”
Dustan akaita,Ngesa akageuka.
“Usivuke mipaka na kuvunja sheria.Kumbuka upo usalama wa taifa”
“Rais wako anahitaji kujua ukweli”
Ngesa akajibu kifupi na kuingia ndani,ambapo kabla ya yote alijifungia kwa ndani na funguo ili mtu yoyote yule asiingie kumtoa.Daphine alivyogeuza shingo yake na kumuona Ngesa alishtuka mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu mkojo ukataka kumtoka,sababu yeye na Ngesa walikuwa na historia mbaya sana huko nyuma na waliwindana kama paka na panya!
“Daphine……..Tushajua tayari kuwa wewe umehusika na mabomu ya Nuclear na unashirikiana na Karanje,kwa taarifa yako mabomu yote tayari tumeyashikilia na sasa hivi nachotaka kujuwa.Alipo Karanje,sitaki kupoteza muda nawewe sababu unanijua”
Ngesa alianza kuongea huku akitembea huku na kule akizunguka akimpasha Daphine kila kitu kilichotokea!
“Unapoteza muda wako bure Ngesa,kukamata mabomu sio solution!Karanje ana kitu kikubwa sana anakifanya huko alipo nina amini watu wataendelea kufa kama kuku wenye videri”
“Karanje yuko wapi?”
“Sijui”
“Karanje yuko wapi moja”
“Sijui alipo,usipoteze muda wako”
“Karanje yuko wapi mbili”
“Kamuulize Mama yako mzazi na…”
Hapohapo Daphine alipokea kibao kikali sana cha shavu,hakuishia hapo alimzaba tena kibao kingine cha nguvu akamvuta na kumbamiza ukutani.
“Jaqlin hakuwa na kosa lolote lile,kwanini ulimfanyia vile?”
Ngesa alibanwa na hasira ajabu na alimtandika Daphine ngumi na makofi na chuki yake ikabadilika na kuwa kisasi cha mpenzi wake kuvamiwa.
“Jaqlin hakuhusika,kwanini uliamua kumpiga risasi?”
“Kwaniniiiiiiii?”
Kipondo kiliendelea na kufanya Dustan aliyekuwa nje avamie mlango na kutaka kuingia lakini ilishindikana sababu ulipigwa ‘lock’ kwa ndani.
“Jenipha,leta spea za funguo fanya haraka Ngesa anamuuwa mtuhumiwa wetu”
C.I.D wakaanza kupishana huku na kule wakijaribu kufungua mlango ili wamtoe Ngesa lakini wapi.
“Paaaa paaaaaa”
Ni Jenipha ndiye aliyefyatua risasi kwenye kitasa na kuupiga mlango teke ukafunguka wote wakaingia ndani wakiwa na bastola mikononi lakini hiyo haikumfanya Ngesa amuachie Daphine,alizidi kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mpaka Daphine akaanza kuvuja damu mwili mzima.
“Ngesaaaa”
Jenipha akasogea karibu na kumvuta lakini alirushiwa ngumi ambayo aliiona akainama ikapita hewani,akampiga Ngesa ngumi ya mbavu ambapo hapohapo akaruka teke likamfikia Ngesa mgongoni akadondoka pembeni akiwa anahema huku anatetemeka kwa hasira.
“Mtoeni haraka sana”
**********
Kukamatwa kwa mabomu ya Nuclear na jeshi la polisi haikufanya Brigedia Karanje ashindwe kutumia njia nyingine mbadala sababu alijipanga vilivyo na alikuwa yupo tayari kuuwa watu wengine zaidi.Baada ya kulitoroka jeshi la polisi Makabe akakimbilia kwenye maficho yake mengine,Mlandizi.
“Zile sumu ziko wapi?”
Karanje akauliza wanajeshi wengine.
“Zipo Vingunguti kule”
“Chukuwa lita mia moja.Nenda kiwanda cha Coca cola,mimina nenda na Brerewies kiwanda cha bia TBL mimina sumu,lazima watu kesho wafe tena”
Karanje alitamka mambo ya kigaidi na ilitakiwa jambo hilo lifanyike masaa machache yajayo ndiyo maana simu zilianza kupigwa usiku huo huo ili mpango huo wa kinyama ufanyike.
“Sawa mkuu,nitafanya hivyo”
“Hakikisha hufanyi uzembe”
“Ndio mkuu”
*******
“Sisi ni wanafunzi tumekuja kufanya field hapa”
“Mna barua?”
“Hapana lakini tuna coursework.Inabidi tutoe ripoti”
“Hatuwezi kuwaruhusu bila barua kutoka chuoni kwenu.Mmetoka chuo gani kwanza?”
“UDSM pale Mlimani”
Yalikuwa ni maelezo kutoka kwa binti mdogo wa makamo,mrembo kwelikweli mwenye nywele za singasinga akijieleza ofisi za Coca Cola huko Mikocheni kiwanda cha soda,nyuma yake kulikuwa na wenzake saba wakiwemo wanaume watatu na ilikuwa ni asubuhi sana.
“Hapa inabidi tufuate utaratibu”
“Tuoneeni huruma”
“Hapana”
“Michael waruhusu tu wanafunzi”
Mwenzake wa pembeni alijisikia kuguswa.
“Sasa mkurugenzi akisikia?”
“Hayupo”
Wafanyakazi wa Coca Cola hawakuelewa kuwa wanafanyiwa mchezo na watu waliokuwa wanazungumza nao hawakuwa wanafunzi bali ni wanyama wakali sana,lilikuwa ni kosa kubwa sana kuwaruhusu waingie ndani ya geti kwani wote waliwekwa chini ya ulinzi na wafanyakazi watatu wakapigwa risasi za kichwa ili kuwatia hofu zaidi.
“Unataka kufa kama wenzako,Tenki liko wapi?”
“Li li li liko kule”
“Twende”
Kiwanda cha soda za Coca cola kilikuwa kimevamiwa tayari na ilikuwa ni lazima sumu hiyo kali ambayo inatoa uhai wa kiumbe hai ndani ya sekunde tano iwekwe kwa maana nyingine watu watakaokunywa soda hizo ilikuwa ni lazima waende na maji,wafe kwa sekunde sio chini ya tano.Bila kupoteza wakati sumu ikamiminwa ndani ya tenki la madini ya Tedje.Mchanganyiko ukaendelea na Soda zilizozalishwa siku hiyo zilikuwa na sumu hiyo kali sana!
“Twende huku”
Kreti za soda zote zikapakiwa ndani ya scania kumi zilizofika ili kwenda kusambaza mikoa mbalimbali, hawakujulikana sababu nao pia walivaa sare za Coca cola wakasaidia kuingiza makreti ndani ya magari makubwa.Na hivyo ndivyo walivyofanya kiwanda cha Bia TBL walivamia na kumimina sumu ndani ya kimea na Bia zikaanza kusambazwa nchini kote.
Masaa matano baadaye watu walianza kudondoka na kupoteza maisha yao na sumu hiyo iliua vibaya sana sababu ilikausha mwili mzima hapohapo.Ndani ya masaa ishirini na tano watu elfu nane na mia tano walidondoka na kufa,hiyo ilizidi kumchanganya sana akili Rais Leslie Benjamin!
Watanzania walitandwa na hofu na kugubikwa na hali ya sintofahamu,watu kudondoka vibaya na kutingishika kama wagonjwa wa vifafa, hiyo iliwafanya raia waogope kwani kwa mara ya kwanza hawakujua ni kitu gani kinafanya mambo hayo yatokee.Hali hiyo iliendelea kwa siku mbili mfululizo,Walevi walidondoka na wanywa soda alikadhalika.
“Dada naomba Coca cola na Biscuit”
Ni kijana mmoja alikuwa dukani ananunua soda bila kujuwa kuwa hiyo ndiyo ingekuwa siku yake ya mwisho baada ya kunywa soda,muuza duka hakuwa na tatizo lolote.
“Chenji?”
“Kaaa nayo kwanza,nipe dume”
“Sawa”
Niya ya kijana huyo ilikuwa ni kwenda kufanya tendo la ndoa ndiyo maana alitaka pia Condom na baada ya hapo akakodi chumba.Kilikuwa ni kitendo cha sekunde tano baada ya kunywa soda na kudondoka,hapohapo akaanza kutingishika kama mgonjwa wa kifafa na kuanza kutoa mapovu mdomoni,wakazi wa eneo hilo walimzunguka kijana huyo na kumuonea huruma kwani hapohapo alikakamaa na kukauka, mwili wake wote ukabadilika rangi,ilikuwa ni picha ya kutisha kupita kiasi hakuna hata mmoja wao aliyejuwa nini chanzo cha watu kufa vifo vibaya namna hiyo,Maimamu,mashekh pamoja na wachungaji walianza kukesha kwenye nyumba za ibada na kumuomba Mungu awapunguzie dhambi zao kwani waliamini siku za Mwisho zimekaribia hakuna hata mmoja kati yao aliyejuwa kwamba kwenye soda za Coca cola na ‘beer’ kuna sumu kali iliyomiminwa na gaidi Brigedia Karanje isipokuwa madaktari waliojifungia ndani ya maabara na kugundua watu waliokufa walikunywa sumu kali aina ya ‘Ricin’.
“Dokta Lugemo,hii sumu imetoka wapi?”
Ndani ya chumba cha maabara madaktari nane walikuwa ndani ya mkutano mdogo lakini mzito.
“Sijajua lakini ni sumu kali sana,kuna mchanganyiko wa Mustard,Sulfur,Ricin na Pottasium Cyaride.Ni sumu kali”
“Mungu wangu”
Dokta Mwingine akadakia.
“Kuna uwezekano wowote wa kuzuia hili?”
“Ni vigumu, bado hatujapata chanzo kamili”
“Ni vimiminika,ni soda pamoja na Bia.Nilishafanya utafiti tayari”
Hata madaktari walionekana kunawa mikono kwa jambo lililotokea na ndiyo maana kikao chao hakikuwa na mwisho wake!
Wakati Watanzania wanahaha na kuwa na hofu yeye Brigedia Karanje kwake ilikuwa sherehe kubwa sana,habari za watu kufa baada ya kunywa sumu zilitapakaa kwenye vyombo vya habari kama Televisheni,redio na Magazeti.Hiyo ikafanya amtafute Rais Leslie hewani na kumwambia kuwa huo ni mwanzo tu,kwani kuna mabalaa mengine yatafuata.
“Ndio nakwambia huo ni mwanzo tu.Leslie wewe ni mpumbavu sana na huwezi kunizuia ninachokifanya”
“Kara…”
“Nyamaza nimalize,kenge wewe”
“Nambie unachotaka?”
“Nataka umuachie Ali Baya kutoka gerezani,full stop”
“Whaaat?”(Nini)
“Umenisikia namtaka Ali Baya awe huru,nakupa masaa arobaini na nane”
“Itawezekana vipi?Hilo ni swala gumu Baya ni muuaji,ni muasi”
“Masaa Arobaini na nane”
“Ha…titi”
Huo ndio ulikuwa msimamo wa Brigedia Karanje na alikuwa hatanii hata punje.Ilikuwa ni lazima Ali Baya Mkemia wa maabara atoke na awe huru siku chache zijazo ili atengeneze sumu nyingine kali sana ambayo angeichanganya kwenye mfumo wa hewa,atakayevuta ni lazima imuuwe hapohapo.Kweli Brigedia Karanje alijisikia kuuwa watanzania wote kwa ujumla,asingeweza kufanya hivyo bila daktari huyu aliyesomea masomo ya Kemia kuwa huru.
Na wazo hilo lilimjia ghafla hapohapo akiwa juu ya sofa mkono wake unatolewa risasi aliyopigwa kipindi cha ambushi huko Mbezi Makabe,sio siri moyo wake ulibadilika na kuwa wa kinyama.
“Daphine amekamatwa sio?”
Akamuuliza Zaitun aliyekuwa pembeni amekaa.
“Ndio mkuu”
“Ataweza kutoa siri,nina wasiwasi”
“Sidhani kama ataweza”
“Una uhakika?”
“Ndio yupo tayari kufa,Ninamjua Daphine”
“Kama ikiwezekana tufanye tukamtoe,yupo kituo gani?”
“Yupo usalama wa Taifa,Posta”
“Sawa,nakupa kazi.Nataka kujua nani mkuu wa kile kituo”
“Sawa mkuu”
Hapohapo Zaitun akasimama kutoka juu ya kiti,akaingia chumbani na kujimwagia maji kisha kuvaa nguo safi zinazovutia,akaomba funguo za gari na kuanza safari ya kuelekea Posta akajue nani mkuu wa kituo hiko,akitokea Mlandizi maeneo ya Disunyara hivyo ilimchukua lisaa limoja na nusu mpaka kutokeza Maeneo ya Lumumba Kariakoo,kutokana na msongamano wa magari ikamchukuwa tena dakika arobaini na tano na tayari ilikuwa imetimu saa kumi ya jioni,akafika nje ya gorofa la usalama wa taifa na kuegesha gari pembeni,hakutaka kushuka kwani alitaka kuchunguza kwanza mbali na hapo vioo vilikuwa vyeusi sana yaani ‘tinted’ kwa maana nyingine isingekuwa rahisi kwa mtu yoyote aliyekuwa nje kumuona.
********
Bado Ngesa alikuwa mwenye hasira kuliko hata Simba aliyejeruhiwa na mkuki mbavuni,hiyo ilitokana na Daphine.Dustan na timu nzima ya usalama wa taifa hawakuwa tayari kumuacha Ngesa aendelee kumtesa Daphine kwani alikuwa anaenda kinyume na sheria ndiyo maana walimtoa na kumuingiza ndani ya chumba kingine ili wao waendelee kumuhoji Daphine.
“Daphine zungumza Ukweli”
Dustan aliingia na kumuhoji Daphine.
“Mnajisumbua nilishawaambia kuwa siwezi kuongea chochote kile.Na anachokifanya Karanje huko nina Imani Raisi Leslie atajuta nina uhakika huo”
“Anataka kufanya nini?”
“Sijui,lakini mtajuta”
“Daphine wewe ni msichana mrembo sana,ulipaswa kuwekwa ndani na kuolewa.Tafadhali naomba nitajie ni wapi tunaweza kumpata Karanje”
“Siwezi kutaja alipo”
Alichofanya Dustan ni kusimama na kufungua mlango akimuacha Daphine juu ya kiti ana pingu mikononi,alivyorudi alikuwa ameshika baasha ya kaki.Akafungua na kutoa picha kumi na moja.
“Hizi ni maiti za watoto,walikufa bila hatia kisa Karanje,hawa ni wakina Mama wajawazito Hospitali ya Muhimbili.Daphine nani aliyekubadilisha?Unakumbuka ulichofanya Kenya,Wastegate?Kumbuka ulivyoitwa na Rais Leslie Ikulu kipindi ulivyofaulu.Tizama hii picha mlivyopeana mkono na Rais Leslie Benjamin hapa ulikuwa ikulu,ulikuwa kichwa uliongoza nchi nzima”
Dustan Kyoba ama D.K alikuwa akitoa historia iliyomuhusu Daphine na kila alichomwambia kilikuwa ni kweli mtupu,historia yake aliipekua kwenye stakabadhi, akaipata!Na alizidi kuongea mpaka alivyofumaniwa baada ya kugonganisha wanaume wawili kisha baadaye Marehemu Vital Kamere akamkingia kifua na kununua kesi hiyo, akamkomboa.
“Usimtaje my Dad tafadhali”
“Vital Kamere hakuwa mtu mzuri,alikuchukuwa kwa niya ya kukutumia na alikuwa rafiki mkubwa wa Karanje.Akakupeleka Cuba.Daphine bado una uwezo wa kuokoa mamilioni ya roho zisizokuwa na hatia”
Siku hiyo Dustan aliongea kiupole akitumia diplomasia ili amshawishi Daphine aseme ni wapi Karanje alipo lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa kwani Daphine aligoma kuongea chochote.
“Mmemuua Baba yangu mlezi,Vital Kamere hakuwa na kosa lolote lile.Alikuwa ni kipenzi cha watu,hata raisi wako anajuwa”
“Sio kweli”
“Hata kama sio kweli,siwezi kutaja ni wapi Karanje alipo”
Huo ndio ulikuwa msimamo wa Mwanamke huyu Comando Daphine na aliongea kwa kujiamini kuliko kawaida.
Wakati mahojiano yanaendelea huku Ngesa alikuwa akitafakari mambo mengi sana ndani ya kichwa chake,ghafla mlango ukafunguliwa na aliyeingia hakuwa mwingine bali ni Jenipha ameshika vikombe viwili,akafunga mlango akatembea mpaka mezani kwa Ngesa.
“Karibu Kahawa”
“Ahsante”
Jenipha,akavuta kiti na kuweka kikombe cha kahawa mezani.
“Niwie radhi Ngesa kwa kitendo kilichotokea,naamini unataka kujuwa ukweli ni wapi Karanje alipo.Lakini hata sisi pia tunahitaji kuujuwa ukweli,naomba utambue kuwa tupo pamoja”
“Wewe ni Jenipha Saki?”
Ngesa akauliza huku akiweka kikombe cha kahawa mdomoni,akavuta kidogo na kurudisha juu ya meza.
“Ndio”
“Marehemu baba yako alikuwa mkarimu sana kipindi anafariki alikuacha ukiwa una miaka kumi nadhani.Alilitumikia jeshi la Tanzania mpaka dakika ya mwisho”
“Umejuaje?”
“Alikuwa kama baba yangu nilivyokuona kule Makabe nikakufananisha lakini baadaye nilivyojua unaitwa Jenipha Saki nikapata jibu”
“Ahsante sana”
“Hata wewe pia ni mchapakazi hodari”
“Ahsante Ngesa”
Siku hiyo Jenipha na Ngesa walizungumza wakiwa chumba kimoja na ilivyofika usiku Jenipha alitoka nje na baadaye akarudi na msosi wote wakaanza kula.Ngesa alikuwa ndani ya chumba maalum kama mfungwa lakini haikuwa hivyo kwani alikula vizuri na kunywa,alichonyimwa yeye ni uhuru wa kutoka nje.Ilikuwa hivyo siku nzima,siku moja usiku wa saa saba aliingia Jenipha akiwa ameshika simu mkononi mwake.Simu hiyo ilitokea makao makuu ya Jeshi la polisi kuhusiana na vifo vya watu vinavyotokea vya kudondoka kama kuku wenye videri,hiyo ilimshtua sana Ngesa.
“Karanje huyo.Daphine alisema”
“Mungu wangu”
Ukweli ndio ulikuwa huo kwani kulivyokucha njia nzima zilitapakaa maiti za watu waliokufa vibaya sana,mbaya zaidi walikufa vifo vya kuteseka kwani kabla ya umauti kumkumba mtu aliyekunywa sumu ni lazima atoe mapovu mdomoni na kukakamaa!
Hali ilikuwa ni mbaya ya kutisha,siku iliyofuata simu ilipigwa moja kwa moja usalama wa taifa ikitokea ikulu kwa Rais Leslie akionekana akiwa amechoka na kukata tamaa kabisa.
“Ndio Mheshimiwa Rais tunaendelea kumuhoji lakini atasema tu”
Dustan ndiye alikuwa simuni anazungumza na Rais Leslie.
“Bado hajasema mpaka sasa hivi?Unafanya kazi au mnatania Dustan?”
“Tunafanya kazi Mheshimiwa Rais”
“Ngesa yuko wapi?”
“Yupo lakini yupo chini ya ulinzi tena kutokana na…”
“Dustan,mbona sikuelewi?”
“Hapana Mheshimiwa”
“Nahitaji Karanje akamatwe leo kabla Jua halijazama nina Imani nina jeshi la kutosha kama huwezi niambie nitafute mwingine atakayeweza,nimemaliza”
Hapohapo simu ikakatwa na ilionekana Rais Leslie amechanganyikiwa kupita kiasi kwani aliambiwa amuachie mfungwa aliyeitwa Ali Baya jambo ambalo hakutaka kulifanya ndiyo maana alitaka Brigedia Karanje akamatwe haraka iwezekanavyo!Dustan alikuwa njia panda na ilionekana amechanganyikiwa kwa kiasi cha kutosha,alivyotoka akatembea mpaka chumba alichofungiwa Ngesa, akaingia ndani.
“Ngesa,njoo nje tafadhali.Naomba unisaidie kitu kimoja.Fanya unavyojuwa ili Brigedia Karanje apatikane”
Hiyo ndiyo kauli aliyotoa Dustan akimuangalia Ngesa usoni kwa maana nyingine ilimaanisha amsulubu Daphine vya kutosha.
“Ngesa,Mamia na maelfu ya watu wamekufa.Fanya unachojua”
Ngesa hakujibu chochote akanyoosha na kukata kona ambapo kushoto kulikuwa na chumba chenye mlango wa chuma,akanyonga kitasa na kuingia.
Uso kwa Uso akakumbana na Daphine na sura yake ilikuwa imejikunja kama mtu aliyelamba ndimu,hiyo ilitokana na hasira kali iliyochanganyika na kisasi!
********
“Ndio Mkuu,anayeongoza operesheni hii anaitwa Dustan Kyoba”
“Dustan Kyoba.D.K?”
“Nadhani ndiyo huyo”
“Ninamfahamu vizuri sana,hanipi shida.Ngoja nikupe kazi nyingine!Nenda kota za usalama wa taifa pale posta, Block C floor ya nne chumba namba 112.Ukifika hapo niambie”
“Sawa mkuu”Simu ikakatwa!
Zaitun alifanya kama alivyoagizwa,akawasha gari na kuligeuza ambapo hapo safari ya kwenda Posta kwenye kota za polisi za wafanyakazi wa usalama wa taifa ilianza mara moja na dakika arobaini na saba baadaye alikuwa tayari amefika,akashuka na kuanza kutafuta huku na kule akaona Block C,akatembea na kuingia ndani ya gorofa na kuanza kupanda ngazi mpaka chumba namba 112,baada ya kufika akampigia simu Brigredia Karanje.
“Kuna mwanamke anaitwa Jesca Kyoba na watoto wawili James na Caroline.Fanya unavyoweza uje nao huku nilipo”
“Sawa mkuu”
Simu ilivyokatwa Zaitun akagonga mlango,haikuchukuwa muda mrefu mlango ukafunguliwa na mwanamke mrembo maji ya kunde mwenye macho ya duara na mwenye tumbo kubwa la mimba.
“Habari dada”
“Nzuri tu karibu”
“Ahsante,samahani hapa ndio kwa Jesca?”
“Ndio hapa,mimi ndio Jesca”
“Nina mzigo wako,naweza kuingia ndani?”
“Karibu”
Zaitun akazama ndani.
******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment