Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

DAPHINE SEHEMU YA 9/10

 

 


DAPHINE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 9 KATI YA 10

 

 


Upepo wa bahari na mawimbi makubwa,yalikuwa yakichapa kingo fupi za ukuta katika fukwe hiyo ambayo mara nyingi usiku,hakai mtu yoyote yule!Baridi lilikuwa kali lakini hilo halikumfanya Ngesa asitishe operesheni yake, iliyotokea kumsumbua siku nyingi sana!Swala la kumtia Karanje mikononi mwake lilikuwa ni ndoto sasa aliitimiza tayari kwani gaidi huyo alikuwa kando yake,kamfunga kamba za miguu na mikono,pembeni amesimama Daphine ana usongo ajabu anahema kwa hasira hasa alivyokumbuka wazazi wake walivyouwawa kikatili na Karanje,kando yupo Dustan ametulia na bastola yake mkononi, ambapo nyuma kidogo aliketi Jaqlin Mfinanga pamoja na mke wa Dustan,kila kitu katika maisha yao kilikuwa kama sinema fulani ya kusisimua!

“Najua wewe ni komandoo,naelewa mnapitia mafunzo mazito sana!Sio rahisi kutoboa siri lakini naomba nikuhakikishie,utaniambia ninachokitaka leoleo, tena sasa hivi”

Ngesa,alisema akiwa amesimama wima anamtizama Brigedia Karanje aliyekuwa chini amekaa ametulia, alikuwa mwenye hofu lakini jambo hilo hakutaka kulionesha waziwazi kwani ilikuwa ni mwiko,komandoo kama yeye alitakiwa asioneshe udhaifu hata kidogo kwa adui yake ndio maana alikuwa tayari kwa kila kitu mbeleni!

“Nataka kujua,mabomu yalipo pamoja na kaseti inayoonesha unyama wa Rais Leslie”

“Sijui unazungumzia nini Ngesa na usijisumbue”

“Wacha tuone”

Kujibu majibu ya kebehi na kujifanya hajui kitu,kulimfanya Ngesa achukulie ni upotevu wa muda ndio maana akaiweka bastola yake kiunoni na kuchukua begi lake dogo, ambapo humo alitoa plaizi ya kukatia nyaya ngumu,alivyotaka kumsogelea Brigedia Karanje akasita na kumgeukia Daphine!

“Wapeleke kule pembeni”

Ngesa hakutaka Jaqlin Mfinanga na mke wa Dustan,washuhudie unyama unaotaka kwenda kufanyika,wakatolewa kando kabisa hapo ndipo Ngesa akasogea karibu na Brigedia Karanje,akauchukua mkono wake wa kushoto akakishika kidole chake kidogo cha mwisho na kutumbukiza plaizi!

“Nitajiee”

“Siju…….iiii”

Maumivu aliyohisi Brigedia Karanje,hayakua na mfano wake kwani kidole chake cha mwisho,kilikatwa na plaizi kikadondoka chini na kufanya damu nyingi zimwagike.Ngesa,hakuishia hapo akahamishia plaizi kwenye kidole kingine!

“Nitafanya hivi mpaka vidole vyote viishe,baada ya hapo nahamia vya miguu”

Haukua utani,ulikuwa ni unyama wa hali ya juu sana!Akakamata kidole kinachofuata na kukikata,damu zikazidi kutoka kwa wingi,hiyo ilimfanya Brigedia Karanje apige yowe la maumivu vidole vyake viwili vilikuwa chini,hakutaka kuamini kimasihara masihara vidole vyake vinaondoka,kelele za Bridegia Karanje hazikumzuia Ngesa, akahamishia kidole kingine cha tatu ili akitoe!Kuendelea kukaa kimya aliamini kabisa kwamba vidole vyote vya mikono angevikosa ndiyo maana akawa tayari kusema kila kitu!

“Kila kitu na mipango yote ana….jua Mzee Ngesa..aaaa!Mabomu alipoyatega”

Ngesa alivyosikia jina la Baba yake linatajwa,alishtuka lakini haikumfanya amuamini Brigedia Karanje, asilimia zote mia moja!

“Sio kweli”

Akasema na kutaka kuanza kukata kidole kingine kinachofuata!

“Ni ukw…eli Baba yako ndio anajua kuhusu mabomu na na na na na na moja limebaki siku chache lilipuke”

“Liiiini?”

“Sijuiii”

“Mkanda wa kasetiii?”

“Huo upooo…o”

“Waaapi?”

“Mtwaraa…Sinaaa uhakika ni Tandahimba ama Wilaya ya Maaasaassiiii”

“Nani anao?”

“Kuna seheemuu upooo ni mimi peke yanguu ndio najuaaa ulipoooo”

Mahojiano yalizidi kuendelea kwa njia ya mateso kwani Ngesa aliukandamiza kwa nguvu mkono wenye majeraha ya kukatwa vidole,hiyo ikapelekea Karanje ataje kila kitu kwa tabu na maumivu,kiapo chake cha kukaa na siri hiyo kifuani kikagonga mwamba akajikuta anaropoka kila kitu,mpaka mambo yaliyokuwepo ndani ya mkanda huo!Hiyo ilimfanya Ngesa apigwe na butwaa na kuzidi kutetemeka kwa hasira hata hivyo jambo la kwanza alitaka amsake baba yake alipo akamkomboe kutoka mahabusu kisha amuhoji vizuri hakua ana uhakika kama angeweza kwani alikuwa ni baba yake mzazi,akashusha pumzi ndefu na kubana meno yake kwa hasira kwani aliamini kwamba mapambano ndio kwanza yanaanza!




Maumivu aliyohisi Brigedia Karanje hayakuwa na kipimo chake,chuki na hasira dhidi ya Ngesa zilipanda mara dufu hasa alivyoona vipande viwili vya vidole vyake vipo chini,kuna mateso ya watu wenye roho mbaya ambao alishawahi kukutana nao katika harakati zake lakini siku hiyo alikiri Ngesa ana roho ya kinyama na kwa jinsi mambo yalivyoenda, asingeshindwa kumkata vidole vyote vya miguu na mikononi akavikaanga na kuvila!

“Mzee Ngesa anahitajika hapa”

Ngesa alitoka pembeni na kumwambia Dustan,ilionekana alitaka kupewa ushauri!

“Tutampataje sasa?”

Daphine akadakia,alitaka kujua mchakato mzima utakavyoenda!

“Yupo maabusu,staki shari”

“Noo,yupo Ukonga”

“Ukonga?”

“Yes”

“Tunaweza kumtoa leo?”

“Silaha tunazo,tunaweza”

“Tusubiri kupambazuke”

“Hapana,hatuna huo muda!Kinachotakiwa ni sasa hivi”

Daphine alivyomtizama Brigedia Karanje,hasira zilimpanda ajabu akakumbuka matukio mengi sana ya nyuma hasa wazazi wake walivyouliwa kinyama katika mbuga ya Mikumi,mbaya zaidi Brigedia Karanje alijifanya kumsaidia akamchukua na kumsomesha kumbe alikuwa ni adui yake mkubwa!Alichokifanya ni kuchukua bastola na kumsogelea karibu,akamuwekea kichwani!

“Nitakuua mwenyewe kwa mikono yangu,baada ya hapa”

Daphine akasema kwa hasira huku akibana meno yake,alikuwa ana kila sababu ya kutamka maneno hayo kutoka ndani ya moyo wake na alidhamiria kumuua Brigedia Karanje, endapo operesheni yao ikikamilika,hilo Brigedia Karanje alilijua ndio maana alinyamaza na kumeza fundo zito la mate!


***

Kukamatwa na jeshi la polisi,haikumaanisha kusitisha mipango yao ya kutisha na kuendelea kuisumbua serikali ya Rais Leslie,jeshi la Brigedoa Karanje lilizidi kuongezeka na safari hii walipanga mpango kabambe wa kumuua Rais Leslie,wakiamini ingetokea siku moja Brigedia Karanje angekua huru wangeungana tena na kusherekea ushindi huo!Ndio maana katika mkakati huo walimshirikisha Comando Iddi Gogo,alikuwa ni mwanajeshi mrefu wa kimo,amejazia misuli,mweusi wa kutisha!Comando Iddi Gogo hakutisha sura peke yake bali ni kila kitu na habari za Ngesa alizisikia vizuri,akatamani siku moja wakutane uso kwa uso,wazichape na amuuwe mara moja aliamini jambo hilo lilikuwa rahisi kama kuua mbu ndani ya neti, sababu alimfananisha mwanaume huyo na kidudu mtu anayeharibu mipango yake yote!

“Mmefikia wapi?”

Comando Iddi Gogo siku hiyo aliuliza wakiwa mafichoni,chumba alichokuepo kilikuwa kikubwa kiasi na mezani kulikuwa na vipisi vya sigara vilivyotumika!

“Tumefanikiwa kwa kiasi chake”

Mmoja wa wanajeshi akajibu,akiwa kando kando amesimama kikakamavu mbele ya mkuu wake wa kazi!

“Kesho kutwa,watakuwa tayari wamemaliza mkuu”

“Una uhakika?”

“Hua sibahatishi”

Mwanajeshi huyo akajigamba kishujaa hiyo ilimfanya Comando Iddi Gogo,aaachie tabasamu kwani jibu hilo lilimfurahisha,hapohapo akainua mkonga wa simu na kuuweka sikioni!

“Kesho kutwa,kila kitu kitakuwa sawa!Rais Leslie atakua amekufa tayari!”

Baada ya kutoa maelekezo hayo,akaweka mkonga chini!Akachukua kipisi cha sigara na kukiweka mdomoni,mwanajeshi wa pembeni yake akainua kiberiti cha gesi na kumuwashia sigara mkuu wake wa kazi!

***

Saa tisa ya usiku Derick Ngesa pamoja na Daphine,walikuwa magereza ya Ukonga upande wa pili wa barabara wameweka gari,wanatafakari jinsi ya kuingia ndani ya geti hilo kubwa!Haikuwa kazi rahisi kama walivyofikiria,kulihitajika akili ya ziada na umakini mkubwa sana kwani wangeenda kichwa kichwa,wangeuwawa siku hiyohiyo bila mpango wao kutimia,jambo ambalo hawakutaka litokee katika hatua hiyo ya awali.

“Hakuna geti lingine?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ngesa akimuuliza Daphine!

“Liko moja jingine kule nyuma,ndio hilo hapo!Naona polisi watatu pale,wengine siwaoni vizuri”

“Una visu?”

“Vipo”

“Nipatie na silencer”

Ngesa akakabidhiwa kisu kirefu na kiwambo maalumu cha kuzuia mlio wa bastola usitoke,alivyomaliza kufunga akalitizama geti na kuanza kulipekua gari,katika pekuapekua yake akakutana na kamba aina ya manira,akaiweka ndani ya begi lake dogo lenye mkanda mmoja,kisha akakoki bastola na kuiweka kiuoni!

“Nikifika getini,uanze kuja”

Hapo Daphine hakuitikia alitingisha kichwa kwa namna ya kukubali,Ngesa akateremka na kuvuka barabara!

Kulikuwa na giza lakini taa zilizowekwa nje ya geti la gereza la Ukonga zilikuwa kali mno,hiyo ilifanya kuonekana kama mchana ilikuwa ni hatari sana kwa Ngesa kuingia kichwa kichwa ndiyo maana wakati anatembea alikua makini kutizama majani ya mchongoma yaliyochongwa vizuri, na kufanana na fensi,huko ndio kulikuwa na giza totoro,akatembea mpaka pembeni na kujibanza!Akatoa mkono na kupunga hiyo ilimfanya Daphine ateremke ndani ya gari,akashusha fulana yake vizuri ili kuficha bastola iliyokuwa nyuma ya kiuno chake!

Akatizama huku na kule kisha kuvuka barabara,alivyomuangalia Ngesa akampa ishara asonge getini,hiyo ikamfanya Daphine aunganishe moja kwa moja,mpaka getini!Ambapo kitendo cha kufika tu,askari watatu wakasimama na kumsogelea kwa haraka!

“Haturuhusu mtu yoyote sasa hivi”

Askari mmoja akasema huku akimkagua Daphine kuanzia juu mpaka chini,maswali mengi alijiuliza kichwani mrembo kama huyo anatafuta nini usiku huo!

“Hapa ndio Magereza ya Ukonga?”

Daphine akajifanya kuuliza huku akichungulia ndani akitumia jicho pembe,niya yake kubwa ilikuwa kujua ndani kuna askari wangapi.

“Ndio hapa,lakini njoo kesho”

Kwa ishara ya chini kwa chini akitumia vidole aliweza kuzungumza na Ngesa akiwa pembeni,ambapo alimwambia kuna askari watano ndani wanalinda!Hiyo ilimfanya Ngesa achomoke mafichoni kwa haraka na kutoa bastola yake kiunoni!

“Pyuu pyuuu pyuu pyuuu”

Kila risasi moja,ilimfikia askari anayelinda na kumtupa mbali na mlio wake ulikuwa mithili ya mtoto mchanga akijamba,hakuna mtu yoyote aliyesikia!Kwa tahadhari wakaanza kuziburuza maiti mbili za askari mpaka ndani na kuzificha!

“Twende kule,nifuate”

Operesheni ilitakiwa kufanyika muda mfupi tu,kabla purukushani hazijaanza!Ngesa akawa mbele, nyuma Daphine yupo na bastola mkononi anatizama usalama pande zote!Kwa umakini zaidi wakafanikiwa kuvuka jengo la kwanza ambapo zilikuwa ni ofisi za utawala,wakanyoosha na kukunja kushoto hapo walisimama na kuwaona askari wawili wanapita,walivyohakikisha usalama upo wakasonga mbele mpaka walipofika jengo kubwa la maabusu,nje kulikuwa na askari watatu wenye mitutu!Mmoja kashika redio upepo anasikiliza ripoti za hapa na pale!

“Namalizana na hawa wawili,wewe Yule pale”

Ngesa akazungumza kwa sauti ya chini!Akimpanga Daphine,ambapo alitoa kisu kirefu sana akaanza kunyata taratibu mithili ya paka shume,alivyomfikia askari aliyeshika redio upepo kwa nyuma yake,akamziba mdomo na kumchoma kisu shingoni!

Askari akakukuruka mithili ya kuku aliyechinjwa,akakichomoa kisu na kukitumbukiza tena shingoni,damu ziliruka nyingi mno,ndani ya dakika mbili roho ya askari ikawa imeacha mwili!Ngesa,hakutaka kutumia nguvu nyingi na kupoteza muda wake,bastola yake iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti isitoke ilitosha kabisa kuwafyatua askari wawili,wakadondoka chini hapohapo na kutulia!Wakaingia ndani ambapo kulikuwa na utulivu wa hali ya juu,alichokifanya Ngesa ni kumtandika risasi moja askari aliyekuwa mapokezi,ambapo ilimtupa ukutani,damu zikaruka!Akatembea mpaka kwenye meza,akachukua daftari na kuanza kuangalia orodha ya majina!

“Yupo selo namba kumi,twende”

Wakazidi kusonga mbele huku wakitafuta,selo namba kumi ilipo!Wakakunja kulia na kuifikia,risasi moja tu ilitosha kusambaratisha kufuli kubwa lililokuwa nyuma ya nondo,Ngesa akaingia na kumkuta baba yake amekaa chini kwenye moja ya pembe!

“Baba…”

Ngesa akaita na kusogea huku akibana meno yake,jambo lililomfanya Mzee Ngesa ashtuke kwani hakutegemea kumuona mwanaye sehemu kama hiyo,alichojua yeye kwa wakati huo yupo magereza ya Quantanamo!

“Derick”

Mzee Ngesa akaita na kusimama!Wakati jambo hilo linatokea Daphine alikuwa nje ya mlango,anatizama huku na kule alichokiona kilimshtua mno!Diffenda tatu za polisi,zikiwa na askari wengi kwa nyuma wameshika mitutu!Na waliteremka kwa haraka wakilizunguka jengo hilo!


*****

“DK nipatie simu yako”

“Dk,au Dustan naomba simu!Si unataka kufahamu mabomu yalipo?”

Brigedia Karanje,alikuwa chini ya ulinzi amefungwa kamba miguuni na mikononi pembeni yupo Dustan ameshika bastola,anamlinda akiwa na hamu kubwa sana ya kumuona Ngesa na Daphine ambao waliaga wanaenda kumkomboa Mzee Ngesa ili misheni yao izidi kusonga mbele!

“Siwezi kukupa”

“Muda unakwenda,una masaa machache!Haitakuwa na maana yoyote kunifunga hapa”

“Subiri kifo chako”

“Najisikia hatia sana,nahitaji kuwaokoa mamia na maelfu ya watu kabla sijafa!Naelewa baada ya hapa,mtaniua kwahiyo sina jinsi”

Ushawishi wa Brigedia Karanje,uliendelea na alizungumza maneno hayo akionekana kujuta kwa kila kitu alichokifanya,hakuelewa ni aina gani ya moto angeenda kukutana nao siku akifa,ndiyo maana alijisikia kusema kila kitu kilichotokea!Akazidi kumsisitiza Dustan,ampatie simu!

“Unataka kuongea na nani?”

“Vijana wangu,wategue mabomu”

“Kwanini usiniambie yalipo”

“Sio rahisi kama unavyofikiria,sitaki kufa nikiwa na dhambi nyingi!Bora nipunguze madhambi”

“Taja namba”

Dustan akasema na alichokifanya Brigedia Karanje ni kutaja namba za simu, Dustan akaziandika na kuiweka simu laudispika akaiweka karibu na mdomo wake!Simu,ikaita kwa muda mfupi kisha kupokelewa.

“Brigedia Karanje”

Alivyozungumza hivyo,ukimya kidogo ukasikika!Na baadaye mtu wa upande wa pili alivyorudi kwenye laini akaanza kuzungumza lugha zisizoeleweka lakini Brigedia Karanje alikuwa makini kusikiliza,akajibu kidogo na kutaja jina Comando Idd Gogo kisha kuendelea kuzungumza kwa kilugha,kilichomfanya Dustan abaki njiapanda, alivyoona haelewi akakata simu!

“Ulikua unaongea nini?”

“Nilikua namwambia ayategue mabomu”


****

Lugha iliyokuwa inatumika niya kijeshi,hususani wakiwa katika hatari na wanataka kuzungumza kwa siri maadui wasijue!Hicho ndicho alichokifanya Brigedia Karanje,akimuelekeza Komando Iddi Gogo wapi alipo!Jambo liilomfanya Comando huyo,atoe taarifa ya haraka gari tatu za kijeshi zikafika kwa nje,Comando Iddi Gogo akapanda ndani ya Hammer ya kijeshi na safari ya kwenda kwenye ufukwe wa Kibo kuanza mara moja,kwa jinsi alivyokuwa ana hasira aliapia kuua, mbaya zaidi alimpania sana Ngesa!


****

Swala la kutaka kukutwa na jeshi la polisi,ungekua tena mchakato mwingine mgumu wa ziada ndiyo maana akamchukua Mzee Ngesa na kuanza kufanya utaratibu wa kutoka nje ya eneo hilo kwanza, bila kupoteza muda,alichokifanya Ngesa ni kuchomoa magazini ili ahakikishe kama ina risasi za kutosha,alivyoridhika akatembea kwa kunyata mpaka mlangoni,ambapo alivyochungulia aliona kundi la polisi wakazidi kushuka kwenye magari,ilikuwa ni wazi kabisa walipewa taarifa juu ya uvamizi huo!

“Tumia geti la kule chini mimi nipite huku”

Ngesa alitoa maelekezo hayo,alishaelewa hatari yake endapo wangetumia wote geti moja!Pembeni kulikuwa na dirisha dogo la kioo,alichokifanya ni kulisogelea na kulivunja akitumia kitako cha bastola,kupitia mlangoni ilikuwa ni hatari zaidi,kwa kujipinda akafanikiwa kulishika dirisha na kupenya nje,ambapo huko kulikuwa na kichochoro chembamba sana,kando kuna ukuta mrefu!Akatizama huku na kule na kutanua miguu yake huku akipanda juu,akapanda zaidi kiutaalam,hatimaye akafika juu kabisa na kuchungulia nje,akagundua kwamba angetokea upande wa nyuma!Hakutaka kupoteza muda,akajivuta upande wa pili na kuserereka, bahati mbaya akadondoka vibaya,lakini hiyo haikumfanya atulie na kuugulia maumivu,alichokifanya ni kuanza kukimbia upande wa pili wa geti,akimsubiri Daphine ambapo aliweza kumuona akiwa amejibanza nyuma ya tenki kubwa la maji,anamsubiri polisi atoke,kwa Ngesa ilikuwa ni sawa na upotevu wa muda ndiyo maana akachomoa bastola yake na kumtungua polisi huyo,hiyo ilimfanya Daphine achomoke wote wakatoka nje na kuvuka barabara kwa tahadhari kubwa kwa safari moja tu,kurudi alipokuwa Dustan na Brigedia Karanje,wakiamini kwamba siku hiyo wangejua ni wapi mabomu yalipo!Kitendo cha Ngesa kuingia ndani ya gari,alipiga gia na kulitoa kwa kasi kisha kumgeukia Baba yake mzazi na kumtizama kwa hasira za waziwazi,hiyo ilitosha kuelezea kuwa hakuwa katika mzaha hata kidogo!




Magari ya kijeshi nane,yaliyobeba wanajeshi sio chini ya thelathini shupavu, walikuwa tayari wamefika Mwenge na walikuwa na usongo kuliko kitu kingine chochote kile,Komando Iddi Gogo akiwa katika Hammer ya kijeshi alishikwa na hasira za waziwazi amepandisha mori ya kumkamata Ngesa kuliko kitu chochote kile,haikuwahi kutokea katika kazi yake ya kikomandoo kusumbuliwa na mtu mmoja,ndiyo maana alimuhimiza dereva azidi kukanyaga mafuta wazidi kusonga mbele zaidi.

“Itachukua muda gani kufika?”

Aliuliza Komando Iddi Gongo,akachomoa bastola yake na kukagua kama ina risasi za kutosha!

“Dakika ishirini mkuu”

“Ni nyingi sana”

“Dakika kumi”

Hiyo ilimaanisha spidi ya gari ilikuwa ni ndogo, alichofanya dereva huyo ni kukanyaga mafuta mengi zaidi akaweka gari katikati,mwendokasi wa gari ulitishia uhai kabisa mpaka mmoja wa wanajeshi akajishika vizuri.


****

Swala la kumpata baba yake,lilikuwa tayari limekamilika na kilichofuatia hapo ilikuwa ni kumpeleka kwa Brigedia Karanje kisha mambo mengine yafuatie,Derick Ngesa alimtizama baba yake kwa macho makali sana!

“Kwanini unafanya hivi baba?”

Lilikuwa ni swali lililomshukia Mzee Ngesa!

“Haki inatakiwa”

“Haki gani?”

“Ipo siku moja utanielewa na kunisapoti”

“Sitoweza kufanya hivyo”

“Shauri lako”

Lilikuwa ni jibu la Mzee Ngesa,alijiamini mno!Kiasi kwamba alimtizama Ngesa kana kwamba hakuna kitu chochote kile kinachoendelea.

“Tutajua tu”

Wakati huo Daphine alikuwa kimya hazungumzi chochote,mambo mengi sana yalikuwa yanapita kichwani kwake,hususani maisha yake kwa ujumla!

“Kuna shida yoyote?”

Ngesa akamtupia swali,jinsi Daphine alivyokua mbali kifikra ilimfanya adadisi!

“Hapana”

“Upo sawa?”

“Yeah, nipo sawa”

“Unawaza nini?”

“Maisha,nawaza mambo mengi sana hapa Derick!”

“Yapi hayo?”

“Hivi siku moja namimi nitakuja kutulia,kua na familia yangu na watoto labda”

Lilikuwa ni wazo lililomfanya Ngesa,atabasamu kwa mbali sana, akamtizama Daphine na kumkagua kuanzia usoni jinsi alivyokuwa mrembo wa kuvutia,isipokua tu makovu machache ya michubuko!Lakini angejiremba kidogo tu,angekua ni moto wa kuotea mbali.

“Wewe ni mzuri sana Daphine,ushawahi kuwa na Boyfriend?”

“Kipindi cha nyuma,nilishawahi kufumaniwa!Mwanaume wangu mmoja akafa”

“Ilikuwaje?”

“Ni story ndefu kidogo,pumzika kwa amani Moris,nilimpenda sana huyo mwanaume”

Kidogo ilikuwa ni simanzi kwa Daphine baada ya kukumbuka miaka iliyopita alivyokua na mpenzi wake,hapo ndipo akakutana na Marehemu Vital Kamere na baada ya hapo akampeleka kwa Brigedia Karanje,mambo mengi yalitiririka kichwani kwake akawa kama anatizama filamu ya kusisimua!

“Ngesa….”

Daphine aliita kwa staili ya kushtuka jambo hilo likamfanya Ngesa atupe macho yake mbele,alichokiona kilimfanya ashtuke mno!Magari ya kijeshi yalikuwa yametanda ufukweni na bahati mbaya ilikuwa kwao kwani tayari walionwa kilichosikika hapo zilikua ni kelele za risasi tu,jambo lililomfanya Ngesa apige breki na kuruka nje!Daphine hakuchelewa,akapiga mlango teke na kujitupa kwa mtindo wa Ninja,akatulia chini ya mti na kuangalia upande waliokuwa wanajeshi.

“Paaa paaa paaaaa”

Ngesa alichopa upande wa pili,baada ya kuona risasi zinaelekea kwake na mbaya zaidi wanajeshi walikuwa wanamfuata alipo mikononi wakiwa na silaha kali za kivita,jambo lililomfanya aogope zaidi.

Kwa staili ya kubiringika alifanikiwa kulifikia pango kubwa na kujificha hapo,akiamini ndio ingekua salama yake!Hata hivyo hakua mwenye uhakika kama vita hiyo angeshinda kwani wanajeshi walikua wengi mno!Ni kweli katika mafunzo yake shuleni,alifundishwa namna ya kupambana na wingi wa maadui namna hiyo lakini waliokuwa eneo hilo waliogopesha sababu hata hao aliamini wana mafunzo ya kijeshi vilevile,kuingia kichwa kichwa uhai wake ungekua matatani!

Katika hesabu zake akachomoa ‘magazine’ ili aangalie kama kuna risasi za kutosha lakini alipigwa na butwaa baada ya kukutana na risasi tatu peke yake!Akarudi nyuma kidogo na kuchungulia kwenye kona ya pango lililokuwa kando ya ufukwe huo,akawaona wanajeshi wamelifikia gari lake na kumshusha mzee Ngesa akapigwa na bumbuazi zaidi baada ya kumuona Brigedia Karanje yupo huru jambo lililomfanya ajiulize maswali mengi kuhusu Dustan na Jaqlin walipo,hisia kali za kuuwawa kwa kupigwa risasi zilimfanya jasho jembamba limtoke,akakosa utulivu kabisa!Kutaka kutoka mafichoni alipenda lakini nafsi nyingine ilimuonya asifanye hivyo sababu angepigwa risasi na kufa hapohapo kwani alielewa ni kwa namna gani wanajeshi hao, wangekua na usongo naye!

“Ninamtaka Ngesa akiwa hai,nina amini yupo humu humu!Imran na kundi lako piteni kule,Kiko pita huku na Sam zunguka kule”

Kwa namna wanajeshi walivyojigawa ingekuwa ngumu kwa Ngesa kutoka salama kwani kila mtu alielekea upande wake akiwa na mtutu begani,ilikuwa ni kauli kutoka kwa Komando Iddi Gogo!

“Na hawa je?”

Mwanajeshi mmoja akauliza baada ya kutembea mpaka kwenye gari.

“Dk,nilikuonya miaka mingi sana uachane na hii vita hukutaka kunielewa”

Komando Iddi Gogo,alimtizama Dustan kwa macho makali ya kinyama,hakukua na punje ya masihara hata kidogo machoni mwake,kuharibiwa mipango yake kulimchukiza kwa kiasi cha kutosha mbaya zaidi alivyouona mkono wa swaiba wake Brigedia Karanje una majeraha yaani hauna vidole viwili.

“Huyu ni nani?”

Komando Iddi gogo,akauliza swali huku akimtizama Jaqlin Mfinanga!

“Malaya wake Ngesa”

Mmoja wa wanajeshi akajibu,jambo lililomfanya Komando Iddi Gogo atoe tabasamu fulani la kinyama,akamtizama Jaqlin Mfinanga na kuzishika nywele zake zilizokuwa ndefu,akamnyanyua nazo hivyo hivyo,maumivu aliyohisi mwanamke huyo yalimfanya apige kelele lakini alinyamazishwa na kibao kikali kilichompeleka chini mzima mzima,hakika lilikuwa ni jambo la kikatili mno alichokifanya ni kuchuchumaa kidogo na kumtizama Jaqlin Mfinanga akiwa chini ametandwa na hofu,anatetemeka!

“Baasha ako,amekuponza nitakuua mbele yake anaona leo hii sasa hivi!”

Ilikuwa ni kauli ya kutisha,isitoshe bastola ya Idd Gogo ilikuwa katikati ya matiti ya Jaqlin Mfinanga anaikandamiza,anazungumza kwa hasira tena macho yake yalikua mekundu. Baada ya kuzungumza hayo akasimama na kutizama huku na kule akisubiri kwa hamu sana kumuona Ngesa amekamatwa, hata hivyo mpaka zinapita dakika kumi hakukua na dalili ya Ngesa kuonekana!


*****

Mawazo yake yalikuwa juu ya kipenzi chake Jaqlin Mfinanga pamoja na Dustan,jambo lililomfanya atulie nyuma ya pango hilo akitizama huku na kule.Kilichomshtua ni kuwaona wanajeshi wamezagaa huku na kule,wengine wameshika tochi. Akatulia kidogo na kutambaa kwa mtindo wa nyoka mpaka chini ya pango lingine,hapo alimuona mwanajeshi mmoja ana mtutu analikaribia pango alilokuwepo,akatulia kidogo na kumpigia hesabu mithili ya simba anayenyemelea windo lake,kabla ya hapo akajipima nguvu na kulinganisha urefu wa mwanajeshi huyo aliyekuwa na misuli mikononi!Akabiringika kidogo na kupanda juu ya pango,akachuchumaa na kumtizama mwanajeshi huyo ambaye sasa alikuwa amempa mgongo,bila kuchelewa akamrukia shingoni,miguu yake akawa ameiviringisha shingoni kwake!Kwa utaalam wa judo,akamshushia kiwiko cha paji la uso,jambo lililomfanya mwanajeshi huyo apate kizunguzungu,akajibetua kwa nguvu,wote wakadondoka chini hapo ndipo akatumia mguu wake kuuviringisha vizuri,kila mwanajeshi huyo alipojaribu kufanya hila za kujinasua alishindwa,akawa anakukuruka kama kuku aliyenaswa na kicheche!Ngesa akajivuta kwa nguvu na kuvunja shingo!Hapohapo,mwanajeshi akatulia.Alichokifanya ni kuanza kumkagua kwa haraka,akachukua visu viwili na mtutu,akaushika vizuri na kuelekea upande walipopaki magari yao ya jeshi huku akiwa mwenye tahadhari kubwa sana, akitizama huku na kule.

Alivyoona tochi inakuja upande wa mbele,akarudi nyuma na kujificha nyuma ya mti mkubwa wenye matawi mengi kwa juu,akaweka mtutu chini na kuchomoa kisu kirefu chenye makali kote kote,akawa anapiga hesabu za mwanajeshi huyo kufika,alivyokaribia akampiga ‘Cross’ jebu ya mbavu kabla ya kufanya chochote,akatumbukiza kisu shingoni mwake,damu ziliruka lakini hilo hakujali hata kidogo,akamvuta kando huku akimshuhudia anarusha rusha miguu yake mithili ya kuku aliyetoka kuchinjwa,mwanajeshi wa pili akawa amepoteza maisha yake tayari,hiyo haikumfanya ajipongeze alitambua kwamba ana kazi kubwa sana mbele kama ‘movie’ ndio kwanza ni trela!Alivyoangalia huku na kule na kuhakikisha kuna usalama kidogo,akaokota mtutu lakini alivyotaka kutembea akahisi kuna kichuma cha baridi kimemgusa kichogoni,hofu ikamtanda sababu alielewa maana yake endapo angepiga hatua moja nyingine mbele.

“Tupa silaha chini”

Ilikuwa ni sauti ya kukwaruza,kutokea nyuma yake iliyomfanya aanze kuhisi baridi kali.

“Sitorudia tena”

Sauti hiyo ilizidi kumchimba mkwara!Taratibu akaanza kuweka mtutu chini huku akitafakari na kupiga hesabu ya namna ya kujinasua kutoka kwenye mtego huo hatari ambao asingetumia akili ungekua ndio mwisho wake.

“Wewe ni nani?”

Ngesa akauliza kwa namna ya kununua muda!

“Weka bastola chini fisi maji”

“Naomba tufahamian…..”

Kabla ya kumalizia sentensi yake,akapigwa na kitako cha mtutu shingoni na hilo ndilo jambo alilokuwa analitaka,kuiona sura ya mtu aliyekuwa nyuma yake alichokifanya ni kujidondosha chali puu kama mzigo huku akiugulia maumivu makali shingoni,hakika aliyempiga na mtutu alikuwa mwenye mafunzo na alivyomtizama vizuri akagundua ameiva kutokana na alivyoshika mtutu kwa uhodari na kujihami.

“Piga magoti”

“Kwanini nipige magot….”

Kabla ya kumalizia sentensi yake,alipigwa teke kali la mbavu.Hapo sasa akajiandaa vizuri,akijua kwamba mwanajeshi huyo angempiga teke lingine ili audake mguu lakini ilionekana kama hila yake iligundulika kwani jamaa huyo hakurusha teke kwa mara nyingine.

“Nimekwambia piga magoti nitakuuaa”

Huyo alikua ni mwanajeshi wa pili kama sio wa tatu kumpiga mkwara bila kumpiga risasi jambo lililomfanya aanze kuhisi kitu fulani,lakini hata hivyo alitaka kuhakikisha!

“Sitorudia tena,piga magoti mikono juu”

Hesabu za Ngesa zilikua kali, kwanza alikua ana uhakika asilimia mia moja asingeweza kupigwa risasi sababu ingekua hivyo,angeshauliwa muda mrefu na wanajeshi waliopita!

Alielewa kabisa nyuma ya operesheni hiyo kuna mkuu wao aliyemtaka akiwa hai jambo ambalo hakutaka litokee sababu alielewa atakavyoenda kuteswa mpaka kifo chake,akiwa chini anatafakari akamuona mwanajeshi huyo anamsogelea akipiga hatua chache,hapohapo akasimama kwa kasi na kumrushia michanga machoni,akamvaa na bega hata hivyo bahati mbaya ilikuwa kwake,ilielekea mwanajeshi huyo alikuwa fiti kwani alijibinua kwa mtindo wa ajabu sana akampiga Ngesa kiwiko cha mdomo kilichomfanya akose muelekeo,hakukaa sawa akaruka hewani na kumchapa teke kavu la shingo,hapo Ngesa akajua mpambanaji huyo hakua wa mchezo mchezo na alimchanganyia mapigo!Alivyoona anazidiwa na kupotezewa muda,ilibidi achomoe kisu kiunoni ili ammalize lakini cha ajabu mwanajeshi nayeye akachomoa kisu kirefu,wote wakawa wameshika visu!

Hiyo ilimfanya Ngesa aogope kiasi kwani alielewa hatari ya mchezo huo endapo ungefanya makosa kidogo!Sasa jamaa akaanza kumfuata,akataka kumkata lakini Ngesa akaruka kidogo kwa niya ya kukikwepa lakini alivyorudi akawa amechelewa kwani kisu kilikata nyama yake mkononi,damu zikaanza kumtoka!Kazi ya kuanza kubadilishana upande ikaanza,Ngesa akawa anazunguka vile mwanajeshi anarudi hivi ilimradi kila mtu anatafuta saiti nzuri,Ngesa akatishia kisu jamaa akajaa hapo ndipo hakufanya makosa,akamchoma cha mbavu lakini cha ajabu jamaa akajikaza na kujishika vizuri akachomoa kisu kidogo kutoka kiunoni na kukirusha, isingekua Ngesa kujibetua kama ngedere kisu kingetua kifuani kwake!Kitendo cha kukaa sawa,akajipindua kwa sarakasi na kumtandika jamaa mateke mawili dabo yaliyomfanya ayumbe,hakuchelewa akamsindikiza na ngumi moja takatifu ya chembe iliyomfanya jamaa abweke kama mbwa,ki ukweli Ngesa alielewa shambulio hilo asingeweza kutoka salama,hapohapo akamfuata kwa nyuma na kumpiga kabali kali,iliyomfanya jamaa apaparike kutafuta hewa akijaribu kuutoa mkono wa Ngesa lakini wapi,baada ya dakika nne nzima za kujinasua na kushindwa Ngesa akavunja shingo yake,hapohapo rohoo yake ikatangulia mbele za haki akashusha pumzi ndefu ya kuchoka!

Lakini alivyosimama tu,alishtukia kupigwa mateke makali ya mgongo hakukaa sawa,akapigwa ngumi tatu za haraka za mbavu alivyotaka kugeuka akatulizwa na ngumi nzito ya shingo iliyomfanya ahisi kichefu chefu cha kutapika.Hakika aliyekua anampiga safari hiyo,alikua yupo vizuri mno, bado hakuweza kumuona vizuri,anayemkabili hakika alikuwa katika wakati mgumu sana na nguvu zilianza kumuishia,kuna teke aliliona linakuja kushoto akalipangua lakini ilionekana kumzidi nguvu sababu alipepesuka, akahisi mikono inamuuma kutokana na buti la jeshi lililokua na chuma mbele,alivyokaa sawa aliweza kuuona mwili wa mwanajeshi huyo,aliyekua mrefu futi nyingi kwenda hewani mkono wake mnene mithili ya mguu wa mtoto,kifua chake kimeenda mbele kama sokwe mzee!Hakika mtu huyo alikuwa na nguvu,sura hiyo alikuwa anaifananisha lakini hakua ana uhakika kama ni Komando Idd Gogo.

“Derick Ngesa”

Hapo ndipo Ngesa akawa ana uhakika mwanaume huyo ni Komando Idd Gogo,Komando hatari mno historia yake aliifahamu sababu miaka ya nyuma walishawahi kufanya kazi pamoja.

“Gogo”

“Ndio mimi,nimekuja kukuua mwenyewe kwa mikono yangu”

Komando Idd Gogo aliongea huku akinesa nesa kama wapiganaji wa boxa,akatisha kama anarusha ngumi lakini aliruka ‘round kick’ iliyomfikia Ngesa kifuani na kumtupa kando kama mzigo,alivyotaka kusimama akawa amechelewa tayari kwani Komando Idd Gogo,alimfikia na kumkanyaga kifuani,akapiga kimluzi fulani cha ishara.

Hapohapo kundi la wanajeshi sita likatokea wakiwa na mitutu mkononi,wakamnyanyua msobe msobe na kumpeleka kwenye gari ambapo hapo alipandwa na hasira mno baada ya kumuona Jaqlin Mfinanga anavuja damu puani na mdomoni hakika aliumia mno.Na alivyomuangalia Komando Idd Gogo,akamuona anacheka kwa dharau! Hapo hakuweza kuzuia hasira zake bila kujali akasimama kwa kasi ili amvae lakini akashindwa kumfikia baada ya kupigwa kwa nguvu na mwanajeshi mwingine pembeni na kitako cha mtutu kichwani,akahisi kizunguzungu kikali na giza nene,akadondoka chini na kupoteza fahamu jambo lililomfanya Jaqlin Mfinanga apige yowe la nguvu,hakika kwa mwanamke huyu ilikuwa ni picha mbaya mbele ya upeo wa macho yake.




Ngesa tayari ametekwa nyara na jeshi la Karanje wakishirikiana na komando Iddi Gogo,mwanaume hatari aliyetokea kuitingisha nchi ya Tanzania miaka ya themanini,usongo wa kumtia Ngesa ulitisha ndiyo maana muda wote alimtizama akiwa chini amezirai kwa macho ya kinyama,hiyo haikutosha alitaka kumuua kabisa kwani alitokea kumsumbua kwa kiasi cha kutosha,bado wanajeshi wengine waliokua pembeni walichukulia kitendo hiko kama kiini macho,haikua rahisi kumkamata Ngesa kama kuku bandani.

“Nipe bastola”

Komando Idd Gogo alisema,hakukua na muda wa kupoteza akakabidhiwa bastola mkononi na kumuangalia Ngesa aliyekua chini amelala chali,hana fahamu kabisa!

“Kacha kacha”

Ni sauti iliyosikika baada ya bastola kukokiwa kumaanisha chemba zimefunguka, kitendo cha kuvuta triga risasi ingechomoka!Bastola akaelekezewa Ngesa aliyekua chini tena kwenye saiti ya kichwani,Komando Idd Gogo hakutaka kupoteza muda alitaka risasi moja tu imuondoe Ngesa duniani,pembeni alikaa Dustan na mkewe,hofu nyingi imetawala mioyoni mwao hawakuacha kumuomba Mungu atende miujiza lakini hata hivyo waliamini hakuna namna ya ukombozi isipokua baada ya Ngesa kuuwawa wao wangefuata,Jaqlin Mfinanga alikuwa akilia mpaka machozi yakamkauka kabisa, alielewa nini maana ya risasi kuingia ndani ya kichwa cha Ngesa,alilia akiomba wasemehewe lakini kelele zake zilikuwa ni sawa na chura kumzuia tembo kunywa maji.

“Karakacha karakacha”

Komando Idd Gogo,alipigwa na butwaa la waziwazi baada ya kuvuta kilimi cha bastola ili amuue Ngesa lakini sauti ya bastola kuashiria hakuna risasi ilimshtua na kumgeukia mmoja wa Wanajeshi mwenye cheo cha Mp,akamtandika kibao cha nguvu kilimchofanya aende chini mzima mzima!

“Nitakuuua”

Kufuatia hapo kuna kitu alikiwaza ambacho aliamini kingemsaidia mbeleni,ilikua ni kama amebadili mawazo na kumtaka Ngesa awe hai kwanza,amri ikatoka dakika hiyohiyo kua ainuliwe na kupakiwa ndani ya gari pamoja na Dustan na Mkewe.

“Kuna mtu mmoja simuoni”

Mzee Ngesa akavunja ukimya,walivyokua wanaelekea kwenye magari yao ili waanze safari.

“Nani?”

Komando Gogo akauliza na kusimama hapohapo,wakatizamana!

“Daphine”

“Ndio nani?”

“Alikuja na Ngesa”

Kwa kujihami zaidi jeshi likaamuliwa wamsake Daphine kwa wudi na uvumba mpaka wampate lakini mpaka linapita nusu saa lizima,hakukua na dalili yoyote ya Daphine kuonekana,hawakuelewa kwamba muda wote alikua nyuma ya gogo kubwa lililokuwa chini amelala chali,kila kilichoendelea alikishuhudia, alielewa fika kwamba vita hiyo ingekua kali ndiyo maana alijificha eneo hilo mwanzo mwisho ili kusoma mazingira.Lakini wasiwasi mkubwa ulimuingia baada ya kuona wanajeshi wawili walioenda futi nyingi hewani wanasogea karibu na gogo alilokuepo,akajivuta taratibu na kujibana vizuri pembezoni,alishaelewa nini maana yake endapo wanajeshi hao magaidi wangemuona,wakazidi kusogea sasa walikua mbele yake kumaanisha wangegeuza shingo zao tu,Daphine angeonekana!

“Heeeeey”

Sauti nene na nzito kutoka upande wa pili iliwashtua wanajeshi,wakageuka kushoto na kumuona mwenzao anawapungia mkono kama ishara ya kuwaambia ‘Tuondokeni’Hapo hawakutaka kusimama tena wakaanza kukimbia kwa hatua chache,jambo lililomfanya Daphine ashushe pumzi ndefu,akachomoka kidogo na kuchungulia ambapo aliona magari ya kijeshi yanageuza na kuingia barabarani,hakutaka kukaa hapohapo kwa tahadhari kubwa,akaanza kuambaa ambaa na miti akajitupa chini na kuanza kutambaa kwa mtindo wa nyoka,mpaka karibu na gari la Jeshi ambalo lilikuwa linasumbua kuwaka!

“Umecheki temino?”

Dereva wa gari la kijeshi aina ya Landrover,alimuuliza mwenzake baada ya kujaribu kuliwasha na kugoma.

“Ebu piga tena”

Gari ikagoma kuwaka,ilibidi mmoja ashuke na kufungua boneti la mbele hapo ndipo Daphine alipopata mwanya wa kubiringika mpaka chini ya uvungu,akatizama kwa umakini kwa juu,akaona sehemu ya kujishika ingawa hakuwa ana uhakika kama ingekua salama kwake,alivyoangalia kulia akaona buti kubwa la kijeshi,kamanda mwingine akawa ameteremka ili kusaidia!

“Kuna nini?”

“Maji kwenye rejeta hakuna”

“Kuna dumu nyuma,lina maji”

Mazungumzo yao yote yalisikika na Daphine akiwa chini ya uvungu,jasho linamtoka kutokana na joto,alijikaza kisabuni mpaka walipomaliza kuweka maji kwenye rejeta na kufunga boneti alivyoangalia upande wa pili akaona kuna gari lingine la jeshi,ilielekea wanawasubiri wenzao!

“Ingia tuondoke”

Dereva akasema kwani kwa wakati huo tayari gari liliwashwa,boneti likafungwa vizuri mmoja akazunguka upande wa kushoto lakini jambo lililomshtua Daphine ni baada ya kuona pochi yaani ‘wallet’ imedondoka,hiyo ilimaanisha kitendo cha mwanajeshi huyo kuinama angeonekana na huo ndio ungekua mwisho wake.

Ilikua ni wazi kabisa,Mp akainama kidogo lakini Mungu alikua upande wa Daphine,dereva alipiga gia gari likaanza kuondoka alichokifaya mwanajeshi huyo baada ya kuokota ‘Wallet’ akaanza kukimbia na kufungua mlango,akajitupa ndani kitaalam na kufunga mlango, kwa kua alikua ana mafunzo ya Kijeshi,kwake aliona ni kawaida sana!


****

Rais Leslie,alikua katika wakati mgumu mno!Mambo mengi sana aliyafikiria kichwani kwake,kiti cha uraisi kiliwaka moto na alijua nini maana yake endapo siri nzito aliyokua nayo ingevuja na kuingia katika mikono ya watu hatari ama wananchi,kutoroshwa kwa Brigedia Karanje kulimfanya ahisi kujiua hapohapo sababu hiyo ilikua na maana siri kusambaa kwa kasi,jinsi mambo yalivyokwenda ilikua ni lazima auwawe kifo kibaya cha mateso,kilichomchanganya zaidi ni kutokua hewani kwa Mkurugenzi wa usalama wa taifa,Ramadhan Nurdin Mpelembe!Huyo ndiye aliyemtegemea lakini matokeo yake,hakua na mawasiliano naye tena!

“Una taarifa zozote za Rama?”

Raisi Leslie,akamuuliza mmoja wa wasaidizi wake siku hiyo ofisini!

“Hapana Mheshimiwa Rais”

“Alikua na nani?”

“Sina uhakika,tangu juzi sijamuona”

“Ukipata taarifa zake,niambie”

Wafanyakazi Ikulu,walielewa siku hiyo Rais Leslie hakua sawa hata kidogo kwani muda wote majasho yalimtoka na alionekana kama mtu mwenye wasiwasi sana!Hakutaka kufanya chochote zaidi ya kunyoosha mpaka chumbani kwake,huko alijitupa kitandani akiwa na suti yake!

“Mme wangu,mbona umelala sasa hivi?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa mkewe,kwa wakati huo alijua kila kitu kwa asilimia sitini ingawa hakua ana uhakika kama ndilo jambo hilo linamsumbua mumewe,akataka kudadisi zaidi.

“Nimechoka tu”

“Unaumwa?”

“Hapana nimechoka”

“Mme wangu al….”

“Nimekwambia nimechokaaaa,niache nipumzikee”

Rais Leslie,akaropoka kwa nguvu na sauti yake ilichanganyika na ukali jambo lililomshtua zaidi mkewe,hata hivyo hakutaka kukaa tena chumbani kusikiliza kero za mkewe akatembea mpaka seblen,akachukua chupa ya ‘whisky’ akanywa kwa pupa na kutulia kwenye kochi,hakukaa sana simu yake ya mkononi ikaita,moyo wake ukapiga kwa nguvu baada ya kuona ni ‘private no’ akajua ni lazima litakua jeshi la Brigedia Karanje,hakutaka kupuuzia akaweka simu sikioni huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa nguvu!

“Leslie,sitaki kujitambulisha sana!Kifupi,Ngesa ninaye na mkanda ninao!Nitakupigia baada ya dakika kumi,nikwambie cha kufanya Ha!Haaa!Haaaaa!Haaaa!Haaaa!Haaaa!Haaaaa!”

Ilikua ni sauti kavu kutoka kwa Brigedia Karanje,katika maneno yote hakuonesha mzaha hata kidogo jambo lililomfanya Rais Leslie ahisi kinyesi kinataka kumtoka!


****

Walitembea zaidi ya Kilomita arobaini,usiku huo!Daphine alihisi kuchoka na aliumia mikono joto la gari lilimfanya ahisi kama ameiva,hata hivyo hakutaka kuachia licha ya mara kadhaa kutaka kujitupa lakini alijionya na kujipa subira,alivyoona gari linakata kona kuingia barabara ya vumbi alishukuru sababu alielewa kivyovyote vile wamekaribia kufika,kumbe haikuwa hivyo walizidi kusonga mbele zaidi katikati ya msitu,wakati mwingine alipaliwa na kukohoa!Kilichomtia wasiwasi mwingi,hakuelewa ni wapi alipo!Pembeni ya barabara kulikua na miti mingi kama pori na mara chache walipishana na magari pamoja na pikipiki za kuhesabika,alikua ana uhakika kabisa wapo nje ya mji wa Dar es salaam,nusu saa baadaye gari likasimama alivyobinua kichwa mbele akaona magari mengine pia ya jeshi waliyoongozana nayo yamesimama pia!

Mbele kulikua na geti kubwa lenye ukuta mrefu sana kwenda hewani,nje kulikua na wanajeshi zaidi ya watano na mbwa wawili wakubwa wenye meno makali na muda wote ndimi zao zilikua nje,walikua ni mbwa walioshiba mithili ya kindama cha Ng’ombe!Gari moja moja likaanza kupita kuingia ndani.

“Wuuuw! Wuuuw! Wuuuw! Wuuuuuw!”

Kelele za mbwa kubweka zilisikika baada ya gari la mwisho kupita,hiyo ilimaanisha kulikua kuna hatari sababu siku zote waliamini mbwa ndiye mlinzi wa kuaminika,mbwa walipiga kelele huku wakitumia nguvu nyingi kutaka kulifuata gari la mwisho ambalo Daphine alikua uvunguni.

“Wuuw! wuuw! wuuuw!”

Sasa kelele za mbwa zilizidi na walibweka huku wakitingisha mikia,wakiliangalia gari!Wanajeshi wakaachia minyororo hapo mbwa walichomoka kwa kasi mpaka uvunguni kwenye gari na kuanza kubweka huku wakilifuata wakiangalia chini na kutingisha mikia yao,bila kuchelewa wanajeshi wawili wenye misuli wakashika mitutu yao vizuri na kuwafuata mbwa wakiamuru gari lisimamishwe ili walikague,walikua wana kila sababu ya kuamini kua kuna hatari, hivyo walijihami na kukoki mitutu yao.




Chini ya uvungu wa gari ambapo mara ya kwanza alijificha ili wanajeshi hao magaidi wasimuone sasa hakukua salama tena kwake,mbwa walibweka mno na mbaya zaidi aliona mabuti ya wanajeshi wanasogea alipo,kumaanisha kwamba endapo wangeinama chini wangemuona na huo ndio ungekua mwisho wake kwani alielewa ni kwa kiasi gani alivyokua anasakwa mithili ya Osama Bin Laden.Gari la kijeshi la nyuma ilivyosimama ilimlazimu Bridegia Karanje aamuru magari yote yasimamishwe,kitendo cha mbwa kubweka kiliwafanya wahisi wenda magari yao yana mabomu hivyo kuingia nayo ndani kungekaribisha hatari zaidi.

Komando Idd Gogo,wasiwasi ukamuingia akachomoa bastola na kuishika mkononi akateremka kutoka ndani ya gari na kukaa kando akiwatizama wanajeshi walioshika mitutu, akulifuata gari ambalo mbwa walikua wakibweka sana!

“Pita kule”

Mmoja wa wanajeshi akaamuru,akimaanisha waliweke gari katikati kwanza alichokifanya mmoja wapo ni kuchukua kifaa maalum chenye kioo kikubwa na kupitisha chini kabla hajafikisha uvunguni.Kifaa hiko kikavutwa kwa nguvu hapohapo wanajeshi wakakoki silaha zao wakijua kuna mtu chini.Daphine hakua na ujanja mwingine zaidi ya kubiringika na kutokea upande wa pili,akajisalimisha sababu alielewa kivyovyote asingeweza kuendelea kujificha mpaka mwisho!

“Daphine!”

Dustan,alipigwa na butwaa la waziwazi baada ya kumuona Daphine katoka chini ya gari!Kitendo hiko kilimfanya adhani wenda ni mazingaombwe lakini ukweli ni kuwa Daphine tayari aliwekwa chini ya ulinzi,akashuhudia anapigwa na kitako cha mtutu kichwani,akadondoka chali!Komando Iddi Gogo akasogea karibu na kumkanyaga kifuani.

“Hukupaswa kuja huku”

Komando Iddi Gogo,akazungumza na kuchuchumaa chini akimtizama Daphine kwa karibu.

“Inabidi uwe mke wangu,utanifaa kwa matu…..”

Komando Iddi Gogo hakuweza kumalizia sentensi kwani alitemewa mate ya uso na Daphine,aliyekua chini ambapo kwa wakati huo alikerwa sana na kitendo cha Komando Iddi Gogo kumtomasa kifua chake,kitendo hiko hakutaka kukifumbia macho ndio maana akamtemea mate bila kujali.Sura ya kinyama,ilianza kuonekana waziwazi, dharau aliyooneshwa na Daphine ilizidi kiwango chake,akawatizama wanajeshi waliokua wanamuangalia haikuwezekana hata kidogo mtu mzito kama yeye atemewe mate na mwanamke kama Daphine, tena mbele ya vijakazi wake!Ili kuonesha yeye ni nani,akamvuta Daphine kwa nguvu na kuanza kumburuza kwenye michanga baada ya hapo akamuinua na kumbeba juu juu,akambwaga chini kama gunia!Jambo lililomfanya Daphine ahisi maumivu makali mgongoni,hakuishia hapo akamsogelea na kumpiga teke la tumbo akamuinua kwa mara nyingine,safari hii mkono wake ulikua shingoni mwake!Komando Idd Gogo alikua mrefu mwenye misuli na mkakamavu sana, jinsi alivyomuinua Daphine iliogopesha,kwa mkono mmoja akawa amemkaba shingoni akawa amemuinua juu,miguu ya Daphine ikawa inaning’inia kama nyama buchani!Shingo ya Daphine iliumia kwa kiasi cha kutosha,alivyojaribu kujinasua akashindwa mkono wa Komando Iddi Gogo ukawa umebana koo lake la hewa,pumzi zikawa zinamuishia taratibu akajaribu kurusha rusha miguuu ili ajinasue lakini ikawa kazi bure,alichokifanya Iddi Gogo ni kumrusha juu ya gari,kichwa cha Daphine kikajipiga juu ya boneti,akadondoka chini kama mzigo!Akatoa maagizo kwamba akafungiwe kama wenzake,jambo hilo likafanyika akaingizwa ndani ya gari na safari ikaendelea mpaka walipofika nje ya jumba kubwa wote wakateremka,nje kulikua na magari mengi ya kijeshi na vifaru vitatu vya kivita!

“Lazima Rais Leslie,afe”

“Analindwa sana lakini”

“Hilo niachie mimi,ana masaa machache sana ya kuvuta pumzi”

“Tutaanzia wapi?”

Swali kutoka kwa Brigedia Karanje lilimfanya Komando Iddi Gogo asimame na kumtizama wakawa wanatizamana,akamshika bega na kumpiga piga kwa ishara ya kumtoa wasiwasi.

“Karanje,lazima Leslie afe!Amini nachokwambia”

Maneno hayo tu,yalitosha kusisitizia,wote wakaingia ndani na kupitiliza mpaka seblen!


***

Hali ya ubaridi ilifanya kumbukumbu zake zianze kurudi taratibu,bado hakufumbua macho lakini mara ya mwisho alikua katikati ya mapambano makali sana,alivyotaka kujigeuza akashindwa shingo ilimuuma sana,kichwa kilikuwa kizito mithili ya ndoo iliyokua na zege,alivyofumbua macho akagundua yupo sakafuni amefungwa kamba miguu na mikononi,yupo uchi wa mnyama!Mbele yake kuna wanajeshi wawili warefu,wenye miili ya mazoezi,vifuani wamejazia!Alivyokichunguza chumba hiko,akagundua kuna madirisha mawili,mlango upo kushoto maswali aliyojiuliza ni wapi Dustan alipo pamoja na mpenzi wake Jaqlin,hisia mbaya zikaanza kujijenga ndani ya kichwa chake kwamba wapo katika hatari kubwa zaidi.

“Nina kiu”

Ngesa,akasema kwa makusudi ili kutingisha kiberiti!Matokeo yake,wanajeshi hao walimtizama bila kumjibu.

“Nina kiu,naombeni maji ninywe najua baada ya hapa nitakufa tu”

Hakuna mtu yoyote aliyejibu isipokua mmoja wapo,akasimama na kuweka mtutu pembeni akamtizama Ngesa aliyekua chini,akafungua zipu na kuanza kumkojolea mdomoni jambo lililomfanya Ngesa ageuze shingo yake,mwanajeshi huyo nayeye akasogea kwa nyuma na kuzidi kumkojolea,alivyomaliza akafunga zipu!

“Kiu imekata?”

Jamaa huyo,akauliza kwa sauti iliyojaa unyama wa hali ya juu tena yenye dharau!Ngesa hakujibu chochote,alichokifanya ni kujaribu kujisugua chini ili afute mikojo iliyokua mdomoni,hata hivyo alishindwa sababu jamaa huyo alimfuata na kumgeuza!

“Una masaa machache sana ya kuishi”

“Kwanini usiniue sasa hivi?”

“Tunataka kukupa muda mzuri wa kuongea na Mungu wako,utubu dhambi zako zote,sisi ni watu wema sana”

Hapo Ngesa akatulia,akaanza kutafakari jinsi kifo chake cha mateso kitakavyokua alielewa kabisa asingeweza kutoka salama tena,tayari alishakata tamaa ya kuishi akainamisha kichwa chini na kufumba macho!


****

Kichwa chini miguu juu,ndivyo walivyomuweka!Miguu yake kwa juu ilifungwa vizuri kamba ikapitishwa juu ya chuma,mikono yake ikakazwa vizuri na kamba ya katani.Hakua na ujanja tena,alibaki ananing’inia hewani anahisi kizunguzungu kikali,hakika alikua katika mateso makali mno!Juu alibaki na sidiria peke yake huku chini alikua na suruali ya ‘jeans’,baada ya dakika mbili kupita akasikia hatua za mtu zinakuja!Akatulia na kuangalia mlango,ulivyofunguliwa akamuona Brigedia Karanje ameingia,ilikua tabu kwake kumuangalia vizuri sababu alikua juu-chini.

“Karibu kuzimu”

Brigedia Karanje akasema na kumtizama Daphine kisha akatoka nje,ambapo huko alimfuata Iddi Gogo akitaka kujua mchakato mzima unaendeleaje.

“Leslie lazima afe,ndio nafanya mawasiliano hapa”

“Kabla ya kufanya hayo nataka aaibike sana,nina mkanda wake upo Mtwara,ufike hapa niusambaze”

“Anao nani?”

“Mzee Malosha”

“Ndio nani?”

“Naweza kusema ni babu yangu”

“Unautaka lini?”

“Hata leo”

“Uletwe,nataka kuzungumza na Waziri Okama”

“Waziri Okama?”

“Ndio”

“Atakupa ushirikiano?”

“Niachie mimi,huyohuyo atatusaidia kutega mabomu kwenye ndege ya Rais,shughulikia huo mkanda uje leo”

“Sawa,alafu hawa tunawafanya nini?”

“Nani?”

“Ngesa na wenzake”

Iddi Gogo baada ya kusikia swali hilo,akatabasamu na kuwasha sigara!Akapuliza fundo moja hewani na kuutizama mkono wa Karanje ambao hauna vidole.

“Watakufa kifo kibaya sana”


*****

“Tiiii tiiiii tiiii tiiiii tiiii”

Ilikua ni mashine inayotoa sauti mithili ya bomu la kutegeshwa,hiyo ilimaanisha mapigo ya moyo bado yanadunda na uhai upo!Juu ya kitanda alilala Jenifa, hali yake ilikua mbaya ndani ya wodi la wagonjwa mahututi,madaktari walijitahidi sana kupambana na uhai wake,walipofikia walijipongeza kwani walifanikiwa kutoa risasi tatu kwenye mbavu,mbili tumboni. Ulikua ni muujiza ambao kila daktari aliyepewa mkasa huo alishangaa,hata hivyo kutokana na cheo chake serikalini na jinsi mambo ya kiintelijensia ililazimika apewe ulinzi mkali wa kutosha,siku hiyo msafara wa magari ulifika mpaka hospitalini hapo!Hakuna mtu aliyejua ni nani anafika,mpaka Waziri wa ulinzi na usalama Mheshimiwa Frank Okama aliposhuka!Manesi na madaktari walipigana vikumbo,akatoa salamu za hapa na pale na kunyoosha mpaka alipolazwa Jenifa!

“Anaendeleaje?”

Ni swali la kwanza kutoka kwa Mheshimiwa Frank Okama!

“Anaendelea vizuri tu Mheshimiwa,lakini mfumo wa upumuaji ndio una shida kidogo risasi ilichimba sana kwenye mapafu ”

“Atapona lakini?”

“Ndio”

Dokta ilibidi aondoke na kumuacha Mheshimiwa ndani,ambapo aliendelea kumtizama Jenifa aliyekua haelewi lolote,mashine zinapiga kelele!Kilichomshtua ilikua ni simu,alivyotoa ilikua ni namba ngeni,akaipokea na kuiweka sikioni!

“Okama,unaongea na Iddi Gogo.Naelewa sana,mkeo yupo Nairobi St.Theresa anasubiri kujifungua,kama unataka ajifungue salama fuata ninayokwambia vinginevyo,utapoteza wote wawili mtoto na Mama”

Waziri,alihisi kuishiwa nguvu za miguu jasho jembamba likaanza kumtoka, ulikua ni mkwara wa kutisha!

“Unanijua vizuri mimi?”

“Wacha tuone nitakachomfanya Mkeo Josephine”

Swala la mkewe kutajwa mpaka jina,kilimuogopesha akajua kweli mtu huyo yupo Siriazi!

“Unataka nini?”

“Ukatege bomu,kwenye ndege ya Rais”

“Unajua kabisa,hilo haliwekan…”

“Basi sawa,wacha tuone”

“Halloo halloo,subiri kwanza!”

“Nakusikia”

Hofu iliyomtanda hakua na jinsi zaidi ya kukubali kufanya kila kitu kwani kwa wakati huo mke wake na familia yake,ilikua ni jambo la kwanza katika maisha yake,mbaya zaidi akaambiwa kwamba Ngesa wapo naye, hivyo muda wowote atatumiwa kichwa cha mtu huyo msumbufu!

“Ngesa mpo naye wapi?”

Waziri akauliza.

“Mbali sana,nje ya mji kwenye kambi yetu karibu na Mlandizi”

“Mnataka kazi yenu niifanye lini?”

“Hata leo,itakua vizuri”

Waziri Okama,alikua katika presha kubwa mno!Alipata kitete cha ajabu,akaanza kutafakari mambo mengi sana!

“Yaani nimuue Rais Leslie?Nisipofanya hivyo wataua familia yangu,Eeh Mungu”

Hakua na chaguo lingine zaidi ya kumpigia simu mtu anayefahamika kwa jina la Madebe,akamwambia kila kitu kinavyotakiwa kwenda.

“Sawa,tuonane leo saa mbili nyumbani kwangu”

Waziri,akakata simu na kutoka nje bila kujua kipindi anazungumza hayo yote Jenifa alikua tayari amerudiwa na fahamu zake!Akaanza kufumbua macho yake taratibu,akamtizama Waziri Okama anavyopotelea kwenye kona ya hospitali,alivyotaka kuinua mkono akahisi maumivu makali sana sehemu za mbavu.


****

Yalikua ni zaidi ya mateso,Komando Iddi alipania mno!Ngesa alifungwa kwenye senyenge za kuchoma ambazo nyuma yake kulikua na vichuma pia vilivyochongoka!Amefungwa mikono huku na kule kama Yesu msalabani,hana nguo hata moja!Mbele yake kulikua na meza kubwa,juu kuna vifaa vya kutisha kama visu,misumari na mapanga!Hata hivyo kilichomtisha kilikua ni kitu kilichofanana na manati,muonekano wake ulikua kama wa chuma,nyaya ndefu ilifika mpaka kwenye mashine ndogo mithili ya jenereta.Katika mafunzo yake ya kijasusi alielewa ni aina gani ya mateso angeenda kukumbana nayo.Aliogopa na aliyajua,akakata tamaa kabisa ya kuishi,mbele yake alisimama Iddi Gogo kushoto yupo Brigedia Karanje!

“Nisingependa kukuua ghafla,nataka ufie taratibu hapohapo”

Iddi Gogo,akachukua bastola na kuikoki.

“Paaaaaa”

Akafyatua risasi ikapita na kupunyua sikio la Ngesa jambo lililofanya hofu izidi kumtanda,licha ya kuelewa aina hiyo ya kitisho lakini alijua ana masaa machache ya kuishi.

“Ningetaka kukuua na risasi moja,nisingeshindwa lakini nataka kifo chako ukione na ukisikilizie”

Iddi Gogo baada ya kusema hayo,akachukua vichuma viwili vilivyokua juu ya meza,akavigusisha vikatoa cheche,akamtizama mwanajeshi na kumpa ishara!

Kilichofuata hapo ni Ngesa kumwagiwa maji mwili mzima,hapohapo Iddi Gogo akasogeza na kuvigusisha vichuma hivyo mwilini mwa Ngesa,kimoja kichwani na kingine kifuani,ilikua ni shoti kubwa ambayo ilipenya mwilini mwa Ngesa na kumtetemesha,maumivu aliyohisi yalimfanya apige kelele mno,hilo halikusaidia wakaendelea kumpiga shoti!Mwili wake wote ukafa ganzi,maumivu aliyosikia kichwani yalizidi kiasi kwamba akahisi kichwa kinataka kupasuka,hata hivyo aliomba sana Mungu amchukue dakika hiyohiyo kuliko mateso hayo makali anayopitia,zoezi hilo liliendelea mpaka alivyopoteza fahamu akiwa hapohapo kwenye senyenge!

“Akiamka,zoezi liendelee”

Kauli hiyo ilitoka kwa Iddi Gogo huku akichukua simu ili amtafute Waziri Okama,alitaka kujua mpango mzima umefikia wapi.




Mwili wake wote ukafa ganzi,maumivu aliyosikia kichwani yalizidi kiasi kwamba akahisi kichwa kinataka kupasuka,hata hivyo aliomba sana Mungu amchukue dakika hiyohiyo kuliko mateso hayo makali anayopitia,zoezi hilo liliendelea mpaka alivyopoteza fahamu akiwa hapohapo kwenye senyenge!

“Akiamka,zoezi liendelee”

Kauli hiyo ilitoka kwa Iddi Gogo huku akichukua simu ili amtafute Waziri Okama,alitaka kujua mpango mzima umefikia wapi.

SONGA NAYO.

“Okama,umefikia wapi?”

“Kazi inaenda vizuri,alafu tafadhali usinipigie pigie simu kila wakati unanikera.Naelewa nachokifanya Gogo”

Waziri Okama,alichukizwa na simu za Iddi Gogo kila wakati akimpiga mikwara na kumtisha,hata hivyo hakua na ujanja kwani kwenda kinyume kulimaanisha familia yake kuingia kwenye matatizo!Akiwa ndani ya ndege ya Rais mkononi ameshika begi dogo ambalo ndani lina bomu,alisita kwanza kulitegesha kuna kitu alianza kuhisi,hapohapo akachukua simu na kupiga moja kwa moja nchini Kenya,hospitali aliyolazwa mke wake!Alitaka kujua kama ni kweli Iddi Gogo,anachokiongea ama alikua anamtingisha!Alichokisikia kilimuogopesha mno.

“Kuna watu wawili,wamekuja!Wanasema,umewatuma”

Mkewe alizungumza simuni,hakua mwenye wasiwasi hata kidogo kwani hakuelewa chochote kinachoendelea nyuma ya pazia!

“Naomba niongee na mmoja wao”

Simu,ikawa hewani ndani ya sekunde tatu sauti nzito ikasikika kutokea upande wa pili.

“Fuata tulichokuambia,vinginevyo unaelewa kitakachotokea Okama”

“Nimekuelewa”

“Ahsante,kua makini ukikosea hatua moja tu!Tunakata kichwa cha mkeo”

Mwanaume mrefu,alikua na simu pembeni karibu na mlango kando kuna kitanda ambacho mke wa Waziri Okama alilala juu yake,alivyokata akamsogelea karibu!

“Mmeo ni mkarimu sana,anakupenda katutuma tukulinde!Utajifungua salama usijali”

Jamaa huyu akasema ili kumtoa wasiwasi mke wa Waziri Okama!


***

“Naona umeshtuka,zoezi letu litaendelea”

Sauti aliyosikia Ngesa ilikua kama inajirudia rudia,masikio yake yalikua kama yameziba!Kipigo na mateso vilikua ni sehemu ya maisha yake na kwa wakati huo alisubiri kifo tu na wala sio kitu kingine!

“Niu…eni sa..sa mnangoja nini?”

“Kufa utakufa,lakini utachelewa kidogo tu usiwe na haraka!Tutakuua taratibu taratibu yaani ado ado”

Kamanda wa jeshi,aliyekua kando ya Ngesa akasema kwa nyodo huku akivuta sigara yake,mkononi ana mtutu ambao ulikua na mkanda aliovaa begani!Alikua na majigambo sababu alielewa hapo alipo Ngesa hawezi kujinasua!

“Saa nga..pi nitakufa?”

“Wenda baadaye,ama kesho asubuhi!Unataka kufa kwani?”

“Ndi…o”

Kwa upande mwingine Ngesa,alijaribu kununua muda kwa kuongea na kudadisi huku mara kadhaa akitumia jicho pembe kuangalia huku na kule kama kungekua na kitu ambacho kingekua msaada kwake na kujikomboa,umbali wa mita tano aliona kamba ya katani na kisu juu ya meza,alivyopiga hesabu za haraka zikakataaa kabisa!Nyuma kulikua na waya wenye shoti ya umeme,ambao uliunganishwa na umeme,hakika alikua katika wakati mgumu sana!Katikati ya kuumiza kichwa chake,Komando Idd Gogo akatokeza akiwa katika tabasamu!

“Tunahesabu masaa sita,Rais Leslie auwawe”

“Umefanikiwa?”

“Tayari bomu lipo kwenye ndege yake”

Maongezo hayo yalimfikia Ngesa,akasikitika sana sababu sura ya Iddi Gogo, ilikua ya kinyama na kila kitu,alichoongea alikimaanisha!Hapohapo,akamgeukia Ngesa na kumsogelea!

“Kifo chako,lazima kiandikwe kwenye vitabu vya kihistoria baada ya Rais wako kufa!”

“Kwanini,usiniue sasa hivi mpaka umsubiri Rais Leslie afe,hiyo itabadilisha nini unadhani?”

“Kabla hujafa,nataka ushuhudie kifo chake”

Hapo Ngesa akameza mate kwa tabu sana,hofu ilimtanda na alielewa nini maana ya kauli hiyo mateso makali kabla ya kifo chake ndio kitu pekee kilichobakia!


***

Lilikua ni kosa kubwa sana kwa mlinzi kutoka nje na kupokea simu akimuacha Daphine peke yake ndani ya chumba hiko,kichwa chini miguu juu!Alichokifanya Daphine ni kuinua kichwa chake kwa nguvu,mikono ikawa imegusa miguu kwa nguvu akajitutumua na kuanza kufungua kamba,alihisi mgongo wake unamuuma lakini hakua na jinsi zaidi ya kuendelea mpaka kamba za miguu zilivyoanza kulegea, hapo akatulia kidogo na kurudi vilevile baada ya kusikia mlinzi anarudi!

“Yes kipenzi,kesho nakuja!Usijali kuhusu mke wangu,hajuui kitu kitandani kama gogo…”

Mazungumzo hayo alifanya mlinzi akiwa na simu sikioni kwa haraka Daphine akajua tayari amekolea na alikua akizungumza na awara wake,alichokifanya mlinzi ni kumuangalia Daphine kwa namna ya kuhakikisha kama yupo kisha akatoka nje,jambo ambalo kwa Daphine ilikua kama nafasi ya kipekee,hapohapo akitumia meno akaanza kung’ata kamba za mikononi,zilivyoachia akarudi tena juu na kufungua huku akiwa makini na milango yake ya fahamu kama masikio na macho,kama zilivyolegea akajidondosha chini kwa mtindo wa paka,bila kutoa kishindo!Akanyata taratibu mpaka mlangoni,ambapo sasa alimsikia mlinzi anaaga kwenye simu akajiandaa!

Kitendo cha mlinzi kutokeza,alipigwa ngumi kavu ya shingo alivyotaka kujigusa tena,akawa amechelewa kwani alipokea kifuto cha tumbo na ambakati ya kidevu iliyomfanya adondoke chini kama mlevi,mtutu ukaenda kando!Daphine akamsogelea lakini akachotwa mtama,hata hivyo Daphine alikua mtundu na mwepesi kwenye michezo hiyo,sababu alijibetua kwa nyuma na kusimama wima ambapo aliona ngumi inakuja akainama kidogo,ikapita hewani akiwa ameinama hakutaka kumuacha salama mwanajeshi huyo ambaye hakua saizi yake kwani aliamini kiuwezo bado mdogo,akamchapa pigo la judo katikati ya mbavu zake,jambo lililomfanya mwanajeshi huyo,ashindwe kuhema akawa kama amepigwa shoti!Daphine,hakutaka kumruhusu aombe maji,amtandika pigo moja la kareti shingoni,akajizungusha na kumshika shingo,hakutaka kupoteza muda akavunja shingo yake!Kijasho jembamba kilimtoka sababu ilikua kazi nzito, isitioshe alitoka katika mateso makali,alichokifanya ni kubeba mtutu uliokua chini,akaukagua na kuushika vizuri tayari kwa ajili ya kwenda kufanya ukombozi!Ndani ya jumba hilo,kulikua na giza totoro,jambo lililomfanya asiweze kuona mbele vizuri,hata hivyo kilichomchanganya hakukariri njia!Kilichomfanya arudi alipotoka ni baada ya kusikia sauti za watu kwenye kordo!

“Kipumbu….Kipumbu…Kipumbu….”

Mmoja akaanza kuita akiwa karibu na mlango,iliekea walikua wakimuita mwenzao ambaye sasa alikua chini amekufa,Daphine alielewa nini maana yake endapo wangeona maiti hiyo akawa tayari kwa lolote ndio maana akaweka mtutu vizuri.

Kabla ya wanajeshi kufika mlangoni,redio upepo ikawashtua wakasikika wanazungumza kitu kisha kugeuza kwa haraka,jambo lililomfanya Daphine atoke kabla mambo hayajaharibika!Mbele yake kulikua na kona na korido ndefu yenye kuta pana,milango ilikua mingi na kila alipojaribu kufungua ilikua imefungwa,akasonga mbele na kujikuta ametokezea seblen kwenye masofa na tv,hakukua na kitu cha maana zaidi ya kuchungulia dirishani,ambapo aliona magari ya jeshi na kando kuna kijumba kidogo,ambacho nje kina wanajeshi wameshika mitutu!

Hapo alikumbuka ndipo Ngesa,aliwekwa alichokifanya ni kutuliza akili na kuangalia usalama,akarudi kwenye korido na kufungua mlango wa nje!Hapo,alikua makini mtutu kautanguliza,alivyoona kuna utulivu,akanyata na kuvuka upande wa pili,kwa staili ya kujificha kwenye magari mpaka alipotokea kwenye nyumba ya pili,akachungulia dirishani na kuogopa baada ya kumuona Ngesa hana nguo hata moja,hasira zilimpanda akatamani avamie lakini alijionya kwa kufanya hivyo kwani ingekua hatari zaidi.Alichokifanya ni kuzunguka kwa nyuma na kusimama nyuma ya tenki la maji,hapo alitafakari lakini kabla ya kufanya lolote akamuona mwanajeshi mrefu na mweusi ana mtutu mkononi!Alichokifanya Daphine ni kuzunguka kwa nyuma,akampiga na kitako cha mtutu kwenye utosi,mwanajeshi ambaye sasa alishtuka na tukio hilo alivyotaka kujibu ikawa kama Daphine ameshtukia hila yake,akakanyaga ukuta na kujibetua sambasoti ambalo teke lake lilimfikia kifuani,akadondoka chini kizembe na kuchomoa kisu kirefu,bila kuchelewa akarusha kwa kasi ilikua kidogo kimfikie Daphine shingoni,kama asingekua mwepesi kama ngedere kingemtoboa na kumuuwa,hakutaka kuchelewa akamrukia shingoni na kumkaba!

Jamaa huyo mwanajeshi,ilielekea bado alikua na nguvu, akamuinua Daphine juu juu kama karatasi jambo ambalo lingekua hatari kwa Daphine endapo angezembea,ampiga pigo moja la judo katikati ya utosi akawa ana uhakika kabisa sehemu aliyompiga ni mbaya sana,hakubahatisha sababu mwanajeshi huyo mwenye miguvu,alianza kudondoka chini taratibu hapohapo Daphine akamuwahi shingoni na kumkaba kwa nguvu,akaivunja shingo yake!Kuanzia hapo,akaanza kuhema kwa pupa na kukaa chini kwa uchovu,hata hivyo alivyokumbuka ana safari ndefu akasimama na kuchomoa kisu ambacho kiligota kwenye tenki la maji,akakichomeka kwenye kiatu,akabeba mtutu na kuanza kumsachi mwanajeshi,ambapo alikuta bastola ndogo iliyojaa risasi,akaiweka nyuma ya kiuno na kusonga mbele!Alichokifanya ni kuingia ndani,taratibu sana huku milango yake yote ya fahamu ikiwa makini kusikilizia mjongeo wowote wa kiumbe kinachokuja!

“Utaenda kuwasalimia marehemu wote,huko kuzimu hususani Bob Marley!Wape salamu zangu,Ngesa!”

“Poooo….a”

Ngesa alikua tayari,amekata tamaa kabisa ya kuishi hana tegemeo tena,hana nguvu ya kujikomboa mateso aliyokua anapitia yalizidi kipimo chake na alikua katika himaya ya watu hatari,wenye uchu wa kuua mtu!

“Mwisho wako umeshafika,hesabu masaa”

Akiwa nyuma ya mlango,mita saba alimsikia kamanda huyo wa jeshi akimwambia Ngesa maneno hayo!Akawa makini kutizama mazingira,kulikua na wanajeshi watatu lakini kati yao hakukua na Brigedia Karanje wala Komando Iddi Gogo,jambo lililomfanya ajiulize maswali mengi sana bila kupata majibu.Alivyotaka kuchomoka mafichoni,akaona mlango unafunguliwa, akatabasamu baada ya kumuona Brigedia Karanje anaingia,huyo ndiye alikua na usongo naye kuliko mtu yoyote yule duniani!Mtutu ulikua mkononi,taratibu kidole chake kinavuta kilimi ili amfyatue Brigedia Karanje!

“Tupa silaha chini”

Ni sauti iliyotokea nyuma yake,kavu haina mzaha hata kidogo!Asilimia za kujikomboa kwa wakati huo zikaanza kuyayuka!Akiwa bado ameganda,anajishauri akamuona Brigedia Karanje pamoja na Komando Iddi Gogo,wanajadiliana na kutoka nje!

“Tupa silaha chini,piga magoti”

Kichuma cha baridi tayari kilimgusa kisogoni,hiyo ilimaanisha kufanya mjongeo wowote wa ghafla ndio ungekua mwisho wa maisha yake,hata hivyo ilikua ni bora afe akiwa katika harakati za kujikomboa kuliko kufa kikondoo kapiga magoti kwani alielewa ni lazima baada ya hapo,angeuwawa tu!

Taratibu akaanza kushusha silaha chini,huku akijaribu kupima utulivu wa adui yake aliyekua nyuma,kitendo cha kuweka mtutu chini akageuka na teke aina ya ‘Round kick’ lakini halikufua dafu,ilielekea adui yake aliitambua hila hiyo ndiyo maana aliinama teke likapita hewani na kuchana upepo,hata hivyo alichelewa Daphine alikua mwepesi,kwa pigo la shaulin lililomfikia vizuri shingoni lilimfanya adui ayumbe na kudondosha bastola chini,hapo Daphine hakutaka kumkawiza kwa kufanya hivyo aliamini ingeleta patashika na kuvuta watu wengine,alichokifanya ni kujizungusha mateke mawili ya hewani,moja lilikata upepo lingine lilimfikia kifuani,adui akadondoka chini alivyotaka kuinuka akawa amechelewa Daphine akawa tayari,amewahi shingo kamkaba kwa nguvu zote,alivyohakikisha ameishiwa pumzi akavunja shingo yake kisha kumsukuma kando,alichokifanya ni kuokota bastola na kuishika mkononi,alichoshukuru Mungu ni baada ya upekuzi akakuta kiwambo cha kuzuia bastola isitoe mlio,akaivalisha bastola kwa mbele.

“Pyuu pyuuu”

Ilikua ni sauti ya chini,mithili ya kikohozi cha mtoto mdogo anayesumbuliwa na kifua!Risasi hizo mbili hazikufanya makosa,moja ilipenya katikati ya moyo wa Mwanajeshi mnene,ikaacha tundu kubwa kifuani. Ya pili ilipenya kichwani kwa mwingine, wote wakawa chini tayari roho zao hazipo tena!Alichokifanya Daphine bila kupoteza muda,akaanza kuzikata kamba alizofungwa Ngesa!

“Dap….hineeee”

Ni sauti ya Ngesa,iliyotoka kwa mbali sana mithili ya redio inayokaribia kuisha betri,amefungua jicho moja anamtizama kwa shida,alivyomfungua mkono wa kwanza!

Hakuweza kuendelea tena kwani alipigwa kikumbo kikali,kilichomfanya ayumbe alivyokaa sawa,akapigwa mateke mawili ya mbavu na kumfanya ahisi maumivu makali mno,sasa akaelewa hatari yake kwani mtu aliyekua anapambana naye alikua makini,mbaya zaidi anatumia mtindo hatari wa Kombati,mwanajeshi huyo kwa mbwembwe akawa anatingisha miguu kwa chini,akarusha teke lakini Daphine aliliona akaweka mkono ili alipangue hata hivyo, hakujua uzito wa teke hilo,kwani alijikuta anayumba na kupepesuka kama mlevi aliyelewa Ulanzi,akaanza kuwa makini sana na kukunja ngumi huku akimsoma mwanajeshi huyu ambaye sasa alijua namna ya kumthibiti, alichokifanya ni kumtisha kama anampiga ngumi,lakini kwa uwepesi akazunguka na kurusha mateke ya mtindo wa ‘paranawe’mateke yote yakamfikia adui huyo akahisi kulewa,hakumchelewesha akampiga ambakati ya chembe,iliyofanya arudi kinyume nyume na kujikuta amemuangukia Ngesa hapo ndipo,akajikuta amejaa kwenye kabali kali ya shingo,mkono mmoja wa Ngesa uliokua huru,ukafanya kazi yake hata hivyo kwa Daphine,ulikua kama upotevu wa muda akaokota bastola na kumfyatua ya kichwa!Kwa wakati huo Ngesa aliamini yupo nje ya muda kwani masaa yalienda na Rais Leslie,alitegewa bomu alichotakiwa kukifanya ni kumuokoa,alivyofunguliwa tu akamvua nguo mwanajeshi mmoja wapo na kuvaa yeye,akachukua bastola na kuiweka kiunoni!

“Rais Leslie,ana masaa machache ya kuishi,wakina Dustan wako wapi?”

Ngesa akauliza huku akikagua bastola kama ina risasi za kutosha,akasogea mpaka dirishani ili kuangalia namna watakavyotoroka!Haikua rahisi walipokua ilikua kama ngome anayoishi malkia kwani walinzi waliovaa sare za jeshi walikua wakiranda kila kona!

“Sijajua,lakini nahisi chumba kile pale”

“Kwanini?”

“Nilisikia Dustan,akihojiwa maswali baada ya hapo mkewe akaanza kupigwa sana na kuteswa”

“Walikua wanataka kujua nini?”

“Sikusikia vizuri”

“Jaqlin?”

Ngesa akauliza swali hilo kwa msisitizo.

“Watakua wote hu…”

Bila kumalizia sentensi yake,Ngesa akaanza kuongoza mbele huku akiwa makini kutizama huku na kule,alivyofika kwenye mlango!Anamtizama Daphine na kumpa ishara,taratibu wakaanza kufungua mlango,sauti zilizokua ndani ziliwafanya wawe makini zaidi,mahojiano yalizidi kuendelea na mateso ya kila aina,chumba kizima kilinuka damu,alichokua anakifanya Daphine ni taratibu kuchomoa kisu kilichokua kwenye kiatu chake,akashika vizuri,sasa wakawa tayari wameingia ndani!

Mbele yao kulikua na wanajeshi watatu,wote wamewapa mgongo,Dustan yupo kwenye kiti kafungwa kamba mkewe amekabwa ukutani na mwanajeshi ambaye mkononi ana bastola,chini pembeni alilala Jaqlin Mfinanga amefungwa kamba mikononi na miguuni,Daphine na Ngesa wakatizamana na kupeana ishara kua kila mtu ashughulike na mwanajeshi wake,alichokifanya Daphine ni kurusha kisu ambacho hakikufanya makosa,kikaingia mgongoni mwa mwanajeshi mmoja,alivyotaka kupiga yowe risasi moja ya kichwa ikamtuliza, mwingine alivyotaka kujihami,risasi moja ya kifua ikamrusha ukutani akajigonga na kutulia,mwingine alivyotaka kuleta ujuaji,akatulizwa na risasi moja ya mkono na kufanya bastola aliyoshika idondoke chini,akacharazwa tena risasi ya paja!Iliyofanya damu nyingi imvuje hiyo ilimfanya atukane matusi ,Ngesa akamsogelea karibu na kumkanyaga pajani kwenye jeraha la risasi!

“Kwa sasa hivi naomba utambue kitu kimoja,maisha yako yapo mikononi mwangu!Natokaje humu ndani?”

“Getini”

Mwanajeshi aliyekua chini,anaugulia maumivu damu zinamvuja akajibu kwa nyodo huku akitabasamu, kwa Ngesa alishaelewa kua alikua tayari kufa lakini sio kusema lolote.

“Okoa maisha yako,nakupa nafasi ya mwisho”

“Huwezi kunipa nafasi ya mwisho wewe sio Mungu…Siwezi kukutajia Ngesa,niue na nachokwambia huwezi kutoka humu ndani,unajisumbua Rais Leslie ana masaa machache an….pyuuu pyuuuu”

Risasi mbili tu za kifua,zikamnyamazisha hapohapo tayari akawa amekufa huku ametumbua macho yake kama dagaa, mdomo wazi!Kwa uzoefu wa Ngesa alielewa angejisumbua tu kumuhoji,alichokifanya ni kumpekua na kutoa simu mfukoni mwake,hapohapo akabonyeza bonyeza na kuiweka sikioni!

“Unampigia nani?”

Dustan,akauliza akiwa na Jaqlin Mfinanga pembeni wote wanamtizama yeye Daphine yeye yupo mlangoni,mkononi ana bastola kaishika vizuri anaangalia usalama!

“Magogoni,Rais Leslie”

“Unataka kumwambia nini?Utaharibu…..”

Kabla ya kumalizia neno,upande wa pili wa simu ukapokelewa simu ikawa kwenye laini na aliyepokea alikua ni sekretari hilo Ngesa alianza kulijua kabla!

“Naomba niongee na Rais Leslie ni dharura”

“Kwa sasa huwezi kumpata”

“Nimekwambia ni dharura”

“Wewe nani?”

“Mwambie Ngesa,anataka kuongea naye”

Kufuatia hapo,ukimya ulitawala ilielekea Sekretari huyu kuna kitu alikiwaza na Ngesa aliamini kwa kutaja hivyo,simu hiyo ingetiliwa maanani sababu alielewa ni kwa jinsi gani wanamsaka kwa wudi na uvumba!

“Halloo”

“Subiri kidogo nikuunganishe naye”

Msichana mrembo aliyefahamika kwa jina la Cecilia Njige,akasukuma kiti nyuma kidogo akachomekea shati lake vizuri na kushusha sketi chini,iliyombana na kufanya umbo lake matata lijichore vizuri akafunga shati vizuri ili kifua chake kisionekane!Kwa mikogo akatembea mpaka kwenye mlango mkubwa wa kioo na kugonga,bila kukaribishwa akausukuma na kumkuta Rais Leslie,ameweka kichwa juu ya meza!

“Mheshimwa Rais ku….”

“Sesi baadaye! Sasa hivi sipo sawa kamwambie Kusa,aweke mambo vizuri nikajiandae kwa ajili ya safari make sure ndege ipo tayari”Alizungumza huku kichwa chake kikiwa vile vile!

“Ngesa yupo kwenye laini namba mbili”

Mshtuko wa Rais Leslie ulikua wa waziwazi kwani aliinua kichwa chake kwa kasi na kumtizama Cecilia kana kwamba alipewa habari za kifo!

“Whaaaat!”(Niniii)

“Ngesa yupo laiini namba mbili,anahitaji kuongea nawewe”

Kwa kasi akanyanyua mkonga wa simu na kuiweka sikioni!

“Unaongea na Rais Leslie”

“Mheshimiwa Rais unaongea na Derick Ngesa,pole na majuk…”

“We mwanaharamu,upo wapi?Jisalimishe sasa hivi kabla sijatuma jeshi langu uko ulipo Ngesa,sema ulipo sasa hivi?”

Rais Leslie alizungumza kwa hasira na chuki,iliyochanganyika na jazba bila kujua simu kutoka kwa Ngesa, ingeokoa maisha yake!




“Mheshimiwa Rais u….”

“Upo wapi?Ngesa,upo wapi?Usicheze na akili yangu al….titititi”

Kila Ngesa alipojaribu kumuelewesha Rais Leslie kuhusu bomu lililotegwa kwenye ndege yake,alikatishwa mwisho wa siku akaamua kukata simu na kuipigiza ukutani kwa hasira simu ikapasuka pasuka vipande,kila mtu akamshangaa kwani alihema juu juu kama bata aliyekula pumba kavu.

“Derick kuna nini?”

Dustan akawa wa kwanza kuuliza,alitaka kujua ni kitu gani kimetokea, Rais Leslie kamjibu nini!

“Kinachotakiwa ni kuzuia ndege ya Rais isiondoke”

“Sio rahisi kama unavyodhani Ngesa”

“Siamini katika kushindwa Dustan,tufanye tuondoke humu ndani”

Kwa wakati huo Ngesa,alikua kama kamanda wa msafara alichokifanya ni kutembea mpaka dirishani na kuona wanajeshi wengi mno nje,haikuwa kazi rahisi kutoroka zilihitajika akili nyingi pamoja na nguvu kabambe,kila wakati Ngesa akili yake ilikua kazini na ndiyo maana akatembea mpaka kwenye moja ya chumba ambapo huko alikuta mabomu ya kutegwa na kutupa kwa mkono,akayakusanya na kuanza kuyatega!Moja,alilipachika kwenye tenki la petroli akategesha dakika arobaini na tano,jingine akaliweka mlangoni na kulitegesha pia dakika arobaini tano,kipindi anafanya hivyo kila mtu alimshangaa!

“Nisubirini”

Akili za Ngesa zilikua vitani na asingekubali kutoka hivi hivi bila kuitia hasara kambi hiyo iliyomtesa kwa kiasi cha kutosha,hata hivyo kuhusu kutoroka hakuelewa angetumia mbinu gani,lakini alijipa moyo kua asingeshindwa,hiyo ndiyo ilikuwa desturi yake katika maisha yake,aliamini kila kitu kinawezekana chini ya jua!

Bastola yake ikiwa mkononi vizuri huku mkono mwingine akiwa na mabomu ya kutega,akanyata huku akiinama inama na kulipachika juu ya gari kubwa la kijeshi,baada ya hapo akaliendea lingine na kufanya hivyo hivyo,akapata akili mpya ya kutoboa matairi yote ya gari isipokua gari moja aina ya ‘Land rover’ akiamini hilo ndilo wangetumia kutoroka nalo!Alivyohakikisha kila kitu,kimekua sawa akaanza safari ya kurudi ndani!Akiwa katika mwendo wa taratibu ananyata huku milango yake ya fahamu ikiwa makini sana,akahisi kuna kitu nyuma yake!Hisia zake hazikumdanganya kwani alishtukia kapigwa kumbo la bega bastola ikadondoka chini,akapepesuka kama mlevi wa chang’aa na kukaa sawa,hata hivyo hakuweza kufanya chochote akachapwa ngumi mbili za mbavu zilizomfanya ajinyonge nyonge!Ngumi nyingine ilikuja hiyo aliiona na kuipangua,hakuchelewa akamtandika kichwa kikali mwanajeshi huyu kilichomfikia puani na kupasua mshipa mmoja damu zikaanza kumtoka,mwanajeshi alivyotaka kupiga yowe Ngesa akamuwahi na kumchoma kisu cha shingo huku akimziba mdomo,akamvunja shingo na kumvuta kando!

“Pumzika hapa captain”

Baada ya hapo,akavuta pumzi ndefu akiwa makini mno akaokota bastola yake,alichoshukuru zoezi hilo lilienda kimya kimya,bila kutoa aina yoyote ile ya kishindo!Akaendelea kusonga mbele mpaka alivyoingia kwenye nyumba aliyowaacha wakina Dustan!

“Mpo tayari?”

Ngesa akauliza huku akimuangalia kila mmoja,akitaka kupata jibu kamili!Sura za watu wawili zilimfanya ajue kua wana uwoga.Mkewe Dustan na Jaqlin Mfinanga akajaribu kuwatoa wasiwasi kua wasiogope kila kitu kitakua sawa!

“Tutatumia mlango huu,Daphine utatangulia mbele!Jaqlin,kaa nyuma yangu mpo tayari?”

Ngesa akauliza kijasiri kana kwamba kutoka nje ilikua ni sawa na kuingia chumbani kulala,kila kitu kilikua hatari lakini yeye hakuonesha hofu yoyote!Dustan,akiwa pembeni na mke wake!Daphine katikati Ngesa kando ya Mlango waliungana na sasa walikua tayari kutoka nje ili wajikomboe,wa kwanza kutoka alikua ni Daphine!

Akiwa na bastola mkononi kidole kipo kwenye triga tayari kwa ambushi,hapo ndipo Ngesa akabonyeza rimoti kuruhusu bomu lianze kujihesabu kwa maana hiyo ndani ya dakika arobaini na tano wawe tayari wametoka la sivyo wangekufa wakiwa ndani.Kwa dakika za kurudi nyuma mabomu yote yalisoma 44;42 yaani bado dakika arobaini na nne na sekunde arobaini na mbili!Wakiwa katika ukuta mmoja mpana Ngesa akatoa ishara wasimame kwani sasa alikua mbele,hatua za mtu zilikua zinakuja zilimfanya atulie na taratibu alianza kuweka bastola yake kiunoni na kuchomoa kisu kirefu mithili ya sime,akajiweka sawa na kukusanya nguvu kitendo cha mwanajeshi kutokeza,akavutwa kwa kasi bila kufanya chochote kisu cha tumbo kilitumbukia na kutulizwa na kifuti cha utosi,lilikua ni pigo hatari lililomfanya mwanajeshi huyo aage dunia bila kutoa sauti,Ngesa akachomoa kisu na kufuta damu akitumia nguo za huyo huyo mwanajeshi ambaye sasa alikua maiti!Alivyogeuka nyuma akaona jinsi gani wakina Jaqlin walivyokua na hofu,akatoa ishara ya mkono kua waanze safari ya kuondoka tena,wakafanikiwa kupita kwenye mapipa ya petroli,hapo wakatulia kidogo kwani walinzi wawili walipita,baada ya hapo wakaendelea na msafara wao kimya kimya!Kwa mwendo wa paka mwizi bila kugundulika wakafanikiwa kufika kwenye moja ya Karakana ambapo hapo,kulikua na skrepa nyingi pamoja na magari mabovu,Ngesa akatulia na kumtizama Daphine!

“Inabidi twende upande wa kule”

Ngesa akatoa wazo jambo lililowafanya wote watizame upande wa pili,ambapo juu kulikua na mlinzi anaangalia chini,isingekua rahisi kukatiza bila kuonekana, Daphine akatizama juu na kuona ngazi za kupanda akamuangalia Ngesa na kumshauri kua wamshughulikie kwanza maana angekua ni kikwazo kikubwa sana kwao,alichokifanya Daphine ni kuwaacha Ngesa na wengine kisha yeye akaweka bastola kiunoni na kuanza safari na kuelekea kwa mlinzi ambaye kwa wakati huo alimpa mgongo,kwa tahadhari kubwa na mwendo wa kujihami akafanikiwa kuzifikia ngazi bila kashkash lakini alivyotaka kukanyaga akahisi hatua za mtu,akatulia na kurudi nyuma ambapo alimuona Mwanajeshi mmoja mfupi wa kimo mkononi ana mtutu,alivyofika kwenye ngazi akaweka kituo na kutizama huku na kule,ilielekea kuna kitu alihisi!Kitendo cha kuendelea kubaki hapo aliamini ulikua ni upotevu wa muda ukizingatia kuna mabomu walitega alichokifanya Daphine ni kuchomoa kisu,akamtizama kwa makini kwa shabaha nzuri akakirusha, kisu kikapenya kifuani upande wa moyo,ilikua ni shabaha iliyoleta matunda kwani mpini wa kisu ulibaki nje na ncha ilizama ndani,mwanajeshi akaanza kudondoka taratibu huku akijishika kifua akijaribu kuchomoa kisu,Daphine akamuwahi kwa kumshika ili asije kutoa kishindo atakapo dondoka,baada ya kumtuliza vizuri akamvuta chini ya ngazi na kuanza kuzipanda kwa tahadhari kubwa,alivyokua juu alikuwa makini zaidi kwani aliweza kuona kila kitu kwa chini,akamuona Ngesa yupo chini wakaangaliana na kupeana ishara kua kila kitu kipo shwari!Mlinzi aliyekua juu,alikua amezubaa huyo hakumpa shida,kisu kimoja cha mgongo kilichoharibu utumbo kilimfanya atulie,mbaya zaidi Daphine alikizungusha ndani kwa ndani mithili ya mtu anayezibua chemba ya choo!Baada ya hapo,akamuoneshea Ngesa ishara ya dole gumba kuashiria kua kila kitu kipo sawa kwahiyo wanaweza kusonga mbele!

“Paaaaaaa!”

Risasi iliyogonga mlingoti wa chuma na kutoa sauti mbaya sana,ilimfanya Daphine ayumbe kidogo na kutaka kudondoka chini!

“Paaaaa”

Ilikua ni risasi nyingine,iliyotoa mlio hiyo ilimkosa kosa begani na kuchana upepo ikapita hewani ni wazi kwamba tayari alionekana na mdunguaji ambaye hakua na shabaha, tena alikua chini jambo hilo lilimtia hofu sana Daphine ndiyo maana akainama,hata hivyo Ngesa nayeye alikua makini mno akatizama pembeni na kumuona mdunguaji,amesimama kando ya mti!Risasi moja tu,aliyoachia Ngesa ilimfikia kifuani mdunguaji huyo na kumtupa hewani,kuanzia hapo kilichosikika ilikua ni mirindimo ya risasi kwani wanajeshi walikua tayari wameshtuka!

Mashambulizi yalikua makali mno,ilikua ni hatari na hakukua na jinsi zaidi ya Ngesa kuchukua bomu la mkono,akatoa kipini na kulirusha upande wa pili ambapo aliona wanajeshi wengi wanatoka!Kilichosikika zilikua ni yowe baada ya mlipuko wa bomu hilo,baadhi walitoka wakiwa wanaungua na moto lakini wote walitulizwa na risasi za Dustan!Daphine hakuweza kutumia tena ngazi kushuka alivyofika katikati akajitupa na kudondoka juu ya kontena,akabiringika na kutua chini kikomandoo na kuchomoa bastola ambapo alianza kurusha risasi mpaka alipowafikia wakina Ngesa!Risasi nyingi zilitokea upande wao wa kushoto huko napo Ngesa alirusha bomu mithili ya kiazi,wakasonga mbele huku risasi zikiwa kosakosa!

“Paaa paaa paaaaa”

Mashambulizi yalizidi kuendelea,wanajeshi walikua na mafunzo ya kivita hivyo walirusha risasi mno lakini nyingi hazikuzaa matuda sababu walizitumia bila hesabu!

“Dustan,pita kule!Daphine zunguka huku Jaqlin nisikilize,kamata hii narudi sasa hivi msitoke hapa”

Yalikua ni maagizo na hayakuhitaji maswali isipokua ni kutii tu,Ngesa akamkabidhi bastola Mpenzi wake Jaqlin Mfinanga,akimpa kila mtu majukumu yake ilikua ni lazima watoke eneo hilo kabla ya mlipuko wa bomu kutokea jambo lililozidi kuwafanya watandwe na hofu,alichokifanya Ngesa ni kuruka upande wa pili ambapo alitambaa kama nyoka na kuibuka upande wa magari,hapo alimuona mwanajeshi mmoja na kumtandika risasi moja ya kichwa iliyomtupa chini,akaingia ndani ya Landrover na kuanza kubomoa swichi ya funguo akitumia kitako cha bastola,akachomoa waya mbili na kugusisha gari ikawaka!

“Weka bastola chini Ngesa,huendi popote”

Ilikua ni sauti kavu katika kugeuka akaona mlango wa bastola wenye uchu unamtizama,alikua ni mwanajeshi mrefu mwenye misuli na mkakamavu kweli kweli,isingekua rahisi kumvaa kiholela,yalihitajika mahesabu makali mno!Ndiyo maana Ngesa akameza mate mengi ya uwoga, akatupa bastola chini.

“Shuka ndani ya gari,mikono juu Ngesa!Usije kufanya kitu chochote cha kipumbavu maana nitakuua hapahapa, shuka haraka”

“Sawa,natoka Mkuu!Haina haja ya kutumia nguvu”

Kosa kubwa alilolifanya mwanajeshi huyo ni kurudi nyuma kumpisha Ngesa afungue mlango,alichokifanya Ngesa ni kusukuma mlango kwa nguvu,ulivyomgonga tu! Kwa kasi ya umeme akarukia mkono wenye bastola na kuuvuta ndani ya gari,pigo moja takatifu la judo lilimfanya mwanajeshi huyo abweke kama mbwa mwizi,hakumkawiza akamvunja mkono na kumtandika ngumi moja ya pua iliyompasua vibaya sana,akachukua bastola iliyokua pembeni yake na kumuwekea tumboni,akamfyatua kwa kua aliikandamizia tumboni kwake haikutoa mlio mkubwa wa kutisha!Hakukua na muda wa kupoteza zaidi ya kupiga gari gia na kuchomoka kwa kasi,mashambulizi ya risasi hayakumtisha sababu kitu kama hiko alikitegemea, akainama chini risasi zikapasua vioo na taa za mbele,alivyowafikia Jaqlin Mfinanga na Mke wa Dustan,akapiga msele na kuwapungia mkono waingie ndani ya gari!Bila tahadhari na kuangalia popote wakachomoka mithili ya nyumbu kutoka mafichoni,wakaanza kusindikizwa na risasi zilizochimba ardhi na moja ilimpata mke wa Dustan na kumtupa pembeni,hiyo ilimfanya Ngesa ageuke na kujibu mashambulizi huku akishuka ndani ya gari!Akamvuta mke wa Dustan ambaye alikua anavuja damu mguuni,akambeba begani na kumuingiza ndani ya gari akachana shati lake.

“Kandamiza hapo,damu zisitoke”Ngesa akatoa huduma ya kwanza!

Jaqlin Mfinanga muda wote alikua akipiga kelele,tayari yupo ndani ya gari kainama mirindimo ya risasi inamtisha sana!Jinsi gari lilivyogeuzwa iliogopesha, mbele kidogo wakampakiza Dustan safari ikaendelea, walivyokaribia getini wakamuona Daphine,kajificha nyuma ya msingi mkubwa wanajeshi watatu wapo nyuma yake wanamrushia risasi,hao kwa Ngesa aliwatungua kama utani wote wakadondoka!

“Ngesaaa…”

Dustan akaita na kumuonesha Ngesa saa,jambo lililomfanya Ngesa atoe macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango kwani zilisalia dakika tisa tu ili mabomu aliyotega yalipuke tafsiri yake ingekua kifo!

“Paa paaaaa”

Risasi ziliendelea kurushwa hapo ilibidi Ngesa apunge mkono amuharakishe Daphine waingine ndani ya gari waondoke,dakika zilizidi kurudi nyuma hatimaye zikabaki dakika nne tu!Ilikua wazi kabisa,wangefanya masihara wangefia ndani ndiyo maana Ngesa akajitosa na kusimama juu ya gari huku mkononi akiwa na mtutu alijitahidi sana kuwasambaratisha wanajeshi na mtutu aina ya AK 47, ambao ulikua na mkanda mrefu,makasha ya risasi yalidondoka chini hovyo mithili ya mbuzi anavyokunya!

“Daphineeee”

Ndani ya gari Dustan alipiga yowe,akimpungia mkono Daphine aanze kukimbia!Isingekua rahisi lakini akajitosa na kuanza kulikimbilia gari,ambapo sasa dakika zilisalia mbili na sekunde nne tu!Risasi nyingi zilimkosa kosa Daphine na kuchana upepo!Dakika moja ilisalia sasa,ndipo Daphine akarukia gari kama ngedere mtini,bila kupoteza muda Ngesa aliingia kwenye usukani na kulipiga moto,namna tairi zilivyozunguka na kutimua mchanga, iliogopesha spidi 120 alimanusura lipinduke sababu alikata kona kali yenye mwendo wa hatari,kitendo cha kufika karibu na geti mlipuko mkubwa ukasikika nyuma moto ukatanda hiyo ikafanya mpaka gari litingishike kidogo na majengo yakaendelea kulipuka kwa mfululizo,jambo lililowafanya wanajeshi waanze kupata kitete na kutawanyika huku na kule hawakuelewa wawashambulie wakina Ngesa wazime moto ama waokoe uhai wao!Ngesa,alikua makini mbele yake mita kumi kulikua na geti limefungwa akapandisha gia na kukanyaga mafuta mengi akalisomba,likavunjika na kudondoka kando,akazidi kusonga mbele huku akibana meno yake kwa usongo na hasira juu!



*****

Simu kutoka kwa Ngesa,ilimfanya akurupuke kutoka kwenye kiti chake akawa kama amepagawa kwani alimsaka mtu huyo kwa wudi na uvumba,kutokupatikana kwa Ngesa ilionesha dhahiri kua jeshi lake nicha mtoto kwa mwanaume huyo, ambaye alikua anasumbua Tanzania nzima kwa ujumla,kitendo cha kusimama tu akanyoosha mpaka kwenye mlango wa Sekretari, Cecilia Njige.

“Ngesa,alikwambia nini?”

Lilikua ni swali la moja kwa moja na lililohitaji jibu la hapohapo,jambo hilo likamfanya Cecilia Njige akohoe kidogo ili kuweka koho sawa kwani hakulitegemea.

“Alihitaji kuongea nawewe Mheshimiwa Rais”

“Ulimrekodi?”

“Ndio Mheshimiwa Rais”

“Nitumie sauti yake kwenye email yangu,sasa hivi!Alafu kitu kingine mpigie Ramadhani Nurdin,mwambie namuhitaji sasa hivi”

Kazi ya Cecilia Njige,ilikua ni kumtafuta Mkurugenzi wa Usalama wa taifa hewani alivyompata tu akamwambia kitu kilichotokea!

“Nitakua hapo,baada ya muda mfupi”

Upande wa pili wa simu ukasikika,Cecilia Njige msichana makini na mtulivu akaweka mkonga wa simu mezani na kushusha pumzi ndefu,hata yeye alijaribu kumtafakari Derick Ngesa na kushindwa kuelewa ni binadamu wa namna gani,ambaye Tanzania nzima inamtafuta zaidi na hilo kwa ujasiri akampigia simu Rais Leslie,kuna kitu alitaka kujifunza na kukifatilia lakini alivyofikiria hatari yake moyo wake ukampiga ‘stop’ hakukaa sana simu yake ya mkononi,ikaita alivyoangalia akashangaa kuona inatoka kwa Mke wa Rais!

“Sesi”

Kitendo cha kupokea simu upande wa pili wa simu ukaita jina lake.

“Abee Mama”

Alizoea kumuita Mama sababu kwa asilimia sitini za maisha yake, alilelewa na mama huyo mpaka akamtafutia kazi Ikulu,ndiyo maana akampa heshima hiyo.

“Nimekupigia kwenye simu yako ya mkononi nina maana yangu,cha kufanya jibu ndio au hapana”

“Sawa Mama”

“Mme wangu yupo ofisini?”

“Ndio”

“Nahitaji kujua Ngesa alipo,nitumie sauti yake kwenye simu yangu nimesikia kila kitu!Naomba mtu yoyote asijue hili”

Mapigo ya moyo ya Cecilia Njige,yalipiga kwa nguvu ilikua ni hatari kubwa sana kuvujisha mambo hayo ambayo yalikua ya kiusalama zaidi.

“Lakini Mam…”

“Hakuna cha lakini,nitumie sauti na ninahitaji kujua yupo wapi..Kaa karibu na Rais Leslie”

“Sawa Mama,nitakutumia lakini kuhusu kujua Ngesa alipo itakua ngumu kidogo”

“Kwanini iwe ngumu mwanangu?”

“Sijasikia fununu zozote na alivyopiga simu hakusema alipo”

“Fuatilia,nani kapewa kazi hiyo?”

“Ni ni ni…okay sawa Nipael Mshunga,nitakupigia baadaye ndio tutaonana ahsante jioni”

Msichana Cecilia Njige alikua mjanja na makini,haraka akabadili mazungumzo baada ya Rais Leslie kuingia ofisini kwake ghafla,kitendo cha kukata simu akaiweka ndani ya mkoba wake!

“Ulimpata?”

“Nani Mhesimiwa Rais?Aaah ndio Ramadhan Nurdin nilimpata atakua njiani anakuja”

“Mwambie Aziz Sume,aandae msafara nakaribia kusafiri!”

Rais Leslie alikua bado yupo ofisini hata hajaoga lakini alitaka barabara isafishwe ili msafara uandaliwe kwa ajili ya safari yake,ilikua ni lazima apande ndege yake baada ya masaa machache na kusafiri, hilo lilifanyika kwa haraka sababu dakika thelathini baadae kuanzia Magogoni mpaka Uwanja wa ndege barabara ilikua nyeupe,hakuna hata nzi yoyote aliyekatiza kilichosikika ilikua ni milio ya ving’ora na pikipiki ili kuhakikisha Rais hatopata bugudha yoyote endapo msafara wake ukianza!


*****

Swala la kuweka nguo sawa kama kupasi na kuchagua suti gani Rais Leslie avae lilikua ni jukumu la mkewe,siku hiyo mkewe alikua bize kupekua makabatini ili mumewe asafiri!Kila kitu kilivyokua sawa kuanzia viatu na soksi,akaenda sebleni kumtaarifu.

“Tayari”

“Ahsante,nakuja”

Rais Leslie,alisimama kinyonge akaingia mpaka chumbani ambapo huko alikuta nguo zake zipo kitandani,akavua kila kitu na kuchukua taulo na kunyoosha bafuni.

Siku hiyo mawazo yalikua mazito sana hususani nchi yake ya Tanzania,ambaye yeye alibeba dhamana ya wananchi.Ilikua ni picha mbaya sana na mauaji yaliyotokea aliamini kabisa kwa asilimia mia moja yametia doa serikali yake kwa ujumla,mpaka wakati huo hakuelewa sura yake ataiweka wapi endapo wakati wake wa utawala ukifika tamati,wazo la kukimbia nchi likamjia dakika hiyohiyo lakini hilo akaliona halifai sababu tu alielewa ni kwa jinsi gani atakavyosakwa na kuishi bila amani duniani,kifupi alijuta sana na kiti cha uraisi kwake kilikua cha moto!Kila kitu kilikua wazi kwamba baada ya hapo,ni lazima ashtakiwe kwa makosa yaliyotokea!Mawazo yalikua mengi kiasi kwamba maji yaliyokua yanamdondokea juu ya bomba mithili ya mvua yakuyasikia,hata mkewe alivyoingia bafuni hakumuona!

“Mme wangu”

Mkewe akamuita huku akimkwaruza mgongoni na kucha na kumsugua kimahaba akiwa hana nguo hata moja mwilini!

“Naam”

“Pole na kila kitu nakuona una mawazo sana,punguza”

“Siwezi,nahisi kuchanganyikiwa”

“Usiseme hivyo,watanzania wote wanakuangalia wewe kama baba yao!Usiwaangushe”

Mwanamke huyu,alizungumza kimahaba huku mkono mmoja ukishuka taratibu kwenye tumbo la Rais Leslie,ukateremka mpaka kwenye kitovu,akazidi kuushusha chini alichokipata anachokitafuta akatulia na kufanya njonjo zilizomfanya aolewe,mwili wa Rais Leslie ukaanza kusisimka mawazo yote yakatoka kwa muda,akafumba macho yake wakazidi kutomasana mpaka walivyoingia kwenye tendo la ndoa!


****

Kioo cha mbele cha katikati kilimfanya Ngesa awe makini kukitizama ili ajue kama kuna gari lolote linawafatilia,hali yote ilikua shwari tangu walivyoacha kambi ya jeshi imelipuka,walivyofika Kisaki hali ya Mke wa Dustan ilizidi kua mbaya zaidi alipoteza lita nyingi za damu mwilini,hapo ilimbidi Ngesa azungushe usukani na kuacha barabara ya lami,akaaingiza porini kidogo!Kwake ilikua kama upotevu wa muda kwani yalibaki masaa machache Rais Leslie alipuke na bomu lililokua ndani ya ndege yake hata hivyo aliingiwa na roho ya huruma!Kitendo cha kupaki gari,akateremka na kufungua mlango wa nyuma!

“Damu zinavuja nyingi sana kandamiza hapo”

Ngesa,akasema na kuangalia jeraha la risasi,lililokua na tobo kubwa linalotoa damu nyingi iliyopelekea mpaka Mke wa Dustan aishiwe nguvu kabisa na kuhisi kizunguzungu kikali.

“Tumpeleke hospitali”

Lilikua ni wazo la Dustan!

“Hapana,hatuwezi hiyo ni hatari nadhani unajua nini maana yake,watahitaji PF3 kutoka polisi, utatoa wapi?Ala…”

“Ngesa no,she is my wife!Siwezi kubaki,namuangalia anafia mikononi mwangu”

Dustan akafoka,tayari alipaniki na aliongea akimaanisha jambo hilo likamfanya Ngesa amtizame Daphine aliyekua pembeni yao.

“Sawa,ingieni ndani ya gari.Hospitali gani ipo karibu?”

“Ni kilomita tano kutoka hapa”

Daphine,akajibu!Hapohapo Ngesa akapiga gia na jinsi alivyolitoa gari ulikua ni mtindo ule ule,kwa kasi ya kimondo bila kujua hesabu za Ngesa,waliingia ndani ya hospitali hiyo kwa mikwara mizito sana gari likapiga msele!

Hata manesi walivyoona hivyo,walilisogelea kwa haraka hilo lilitokana na gari hilo kua na mabaka ya kijeshi,wa kwanza alikua ni Ngesa kuteremka akafuata Daphine!Wauguzi wakafika na kiti chenye matairi na kumpakia mke wa Dustan juu yake,kwa haraka wakaanza kumburuza mpaka ndani ambapo hapo!Baada ya nesi kufika mlango wa upasuaji akamzuia Ngesa asiingie.

“Humu hamruhusiwi kuingia,subiri hapo nje”

Badala ya Ngesa kujibu,akachomoa bastola na kumuwekea nesi tumboni!Hakuna mtu yoyote aliyeona tukio hilo,isipokua Daphine na Dustan tu kwani ndio waliokua karibu.Ni kitendo kilichomfanya Nesi,atetemeke na kuanza kujuta kuwapokea,wema wake ukawa umemponza!

“Fungua mlango”

Hakuweza tena kupinga,bastola ilimtisha Nesi!Akafungua mlango,ambapo ndani kulikua na madaktari watatu na manesi sita wakiwa katikati ya operesheni.

“Jamani hakuna mtu ku…..”

Kabla ya daktari kumalizia sentensi yake,akanyamazishwa na bastola ambayo ilikua inamtizama,akanyamaza kimya na kubaki ameganda!

“Kuna mgonjwa hapa,fanya haraka anahitaji matibabu”

Ngesa,akasema Daphine akafunga mlango na funguo ili mtu yoyote asiingie ndani.

“Tupo katikati ya operesheni lakini”

“Hilo sio swala langu dokta, nachohitaji huyu mgonjwa apone kama huwezi niambie”

Shinikizo la Ngesa na mkwara mzito,akiwa na bastola mkononi lilimfanya Dokta Msuya achukue maamuzi mengine magumu, alichokifanya ni kumsogelea mke wa Dustan na kuanza kumpatia matibabu,baada ya jambo hilo kuanza Ngesa akamfuata Dustan karibu na sikio lake na kuzungumza kwa sauti ya chini.

“Inabidi tumuwahi Rais Leslie”

“Na mke wangu?”

“Atabaki na Daphine”

“Hapana Ngesa,siwezi kumuacha al….”

Ngesa,hakutaka kubishana kwa hasira akamuwekea Dustan bastola kichwani ikawa imemgusa juu ya paji la uso.

“Tunaenda au hatuendi?Sina muda wa kukubembeleza”Ngesa,akauliza kwa sauti kubwa iliyojaa hasira jambo lililofanya kila mtu aliyekua ndani,awatizame!

“Derick…”

Jaqlin Mfinanga,mpenzi wake na Ngesa akaita tukio hilo lilimshangaza sana kuona Ngesa anambadilikia Dustan na kutumia nguvu nyingi,hapohapo Ngesa akashusha bastola chini vinginevyo Dustan angeuwawa kwani Ngesa alikua mwenye hasira mbaya sana!

“Dustan,nisikilize ningekua najua ulinzi wa Rais Leslie upoje ningeenda mwenyewe tafadhali nakuomba tuongozane,kwenye hili mwenyewe sitoweza!Sijui Rais Leslie,analindwa na usalama wa taifa wangapi siwezi kukurupuka”

Maneno ya Ngesa kwa sauti ya chini akiwa katuliza jazba, akitumia ushawishi mkubwa na kumuhakikishia Mkewe angekua salama yalimfanya Dustan,ashushe pumzi ndefu na kumuangalia Ngesa usoni.Moyo,wake ulimuuma akiamini kumuacha mkewe lingekua kosa kubwa sana na wenda asingeweza kumkuta akiwa hai,akamtizama Daphine aliyekua makini mlangoni kashika bastola na kurudisha shingo yake kwa Ngesa.

“Twende Ngesa”

Dustan akasema huku akibana meno yake.Walichokifanya ni kuagana kwa kukumbatiana,Ngesa alivyomkumbatia Daphine akamshukuru kwa kila kitu kilichotokea.

“Kua makini Daphine,tutawasiliana ukiona kimya ujue nimeshakufa tayari usimwambie Jaqlin kuhusu kifo changu”

“Usiseme hivyo Ngesa”

“Kwaheri Daphine”

Ilikua ni kama Ngesa anajitabiria kifo chake kwani alielewa kivyovyote vile asingerudi salama,vita aliyokua anaenda kupambana haikua ya kitoto,kuzuia msafara wa Rais halikua jambo la kawaida hata kidogo!

Baada ya kutoka nje na kuficha bastola zao,walitafuta gari moja aina ya Nissan Safari,wakavunja kioo na kubomoa swichi ya funguo!Ngesa,akagusisha nyaya mbili,gari ikawaka wakaanza safari ya kuondoka hapohapo kwa niya ya kuuzuia msafara wa Rais Leslie!Walivyofika Kimara,baruti. Ngesa akaweka gari pembeni hayo yalikua ni maagizo kutoka kwa Dustan,akatoa peni na karatasi akaanza kumuelekeza namna Rais Leslie anavyolindwa!

“Rais Leslie analindwa na walinzi thelathini na mbili kwa ujumla,leo ana safari hivyo basi kumi wapo Mwalimu Nyerere tayari, hawa ni usalama ni watu hatari sana huwezi kuwajua kirahisi,sita wana sniper wanakaa digrii tisini kwenye kona nina maanisha magorofa yaliyo karibu wapo juu kabisa!Rais Leslie anatembea na magari sita kwenye msafara wake,wengine wapo ndani ya magari”

Ngesa alikua makini kusikiliza na kuangalia mchoro,anaochora Dustan kama kwenye somo la ‘Geography’ kwani alikua anachora magorofa kwa umakini kabisa na kumuelekeza jinsi Rais anavyolindwa,hapo Ngesa alijifunza kitu.

“Hawa,sniper ndio waku deal nao kwanza”Hatimaye Ngesa,akatoa wazo na kunyamaza akimsikiliza Dustan nayeye atoe hoja yake!

“Hawa ukiwathibiti,huku chini rahisi sana niachie mimi!Ngesa,samahani kwa kila kitu.Naelewa,unaipambania nchi yetu hapo awali,sikujua kama una uchungu!Nisamehe sana”

“Sio muda wake huu Dustan”

Ngesa akahitimisha,akawasha gari na safari ikaanza mara moja!

Walichoshukuru njiani,hawakukuta kizuizi chochote na hakuna mtu yoyote aliyewaletea mashaka ya aina yoyote yale,isipokua walivyofika Buguruni,wakakumbana na msongamano mrefu sana wa magari!Walivyodadisi wakagundua kuna msafara wa Rais unapita ndiyo maana magari yote yakasimamishwa,Ngesa akamtizama Dustan kwa macho fulani yanayosema ‘Tuanze kazi’ hilo ndilo lililofanyika Dustan akakoki bastola yake vizuri na kuiweka kiunoni,akashuka na kuweka shati vizuri ili bastola isionekane!Kwa Ngesa,ilikua ni vigumu kutoka ndani ya gari sababu alikua bado na gwanda la kijeshi hata hivyo alielewa ni kwa namna gani,sura yake ilivyokua maarufu kwani ingekua hatari kwake sababu alielewa ni kwa namna gani watu hatari wenye silaha aina ya Sniper walivyokua makini,ndiyo maana swala hilo akamuachia Dustan!Ambapo kwa wakati huo,alimuona upande wa pili anatembea kwa hatua za haraka haraka,mpaka alivyopotelea katikati ya majengo!

Dustan,alikua makini nyendo na mbinu zote za usalama wa taifa alikua nazo kwahiyo kwake haikua ngumu sana,kuelewa namna wanavyojipanga sababu yeye alitoka katika idara hiyo,ndiyo maana kwa macho tu aliwatambua,wawili alipishana nao pembeni wakijifanya watembea kwa miguu,mmoja akamuona amekaa anakula mahindi ya kuchoma!Mwingine,akamuona anaendesha baiskeli ya kuuza ‘ice crim’ hao wote aliwagundua,akazidi kusonga mbele akipiga hatua za harakaharaka mpaka alivyoifikia reli,akatizama huku na kule na kujipenyeza kwenye kontena kubwa,hapo aliruka mtaro na kusimama nyuma ya gorofa hilo,ambalo aliamini ni lazima lilikua na ulinzi kutoka usalama wa taifa,alichokifanya ni kulizunguka kwa nyuma!Utulivu,ulikua mkubwa akanyata na kuchomoa bastola!

Mbele yake kulikua na dirisha la kioo,akatizama ndani kwa umakini,hakuona mtu yoyote alichokifanya ni kukipasua akitumia kitako cha bastola,alivyopima na kuona upenyo utakaomfaa akajikunja na kuingia ndani,ambapo kulikua na giza totoro!Masikio yake,yalikua makini sana kusikiliza kama kuna mjongeo wowote ule, hata hivyo kulikua kimya lakini hilo halikumpa uhakika wa asilimia zote mia moja kwani alijua tekiniki za watu hatari wa usalama wa taifa,sio ajabu hapo wanamtizama wakimchora na kumsubiri ajae ili wamkamate kama kuku bandani.

Bastola yake akiwa nayo makini mkononi,akaanza kupandisha ngazi kuelekea juu kwa staili ya kunyata bila kutoa kishindo.Sasa akawa amefika kwenye korido ndefu,yenye milango sita huku mitatu upande mwingine mitatu!Asingeweza kupita hivihivi,ilikua ni lazima afanye upekuzi na kujiridhisha.Alivyoufikia mlango wa kwanza,akaufungua lakini haukufunguka kuashiria ulifungwa kwa ndani, akaachana nao akapitiliza wa pili,nao ilikua hivyo hivyo wa tatu ulifunguka!Jambo lililomfanya asite kidogo kwani jinsi ulivyofunguka ulitoa kelele kuashiria bawaba zake zina kutu,akarudi nyuma kidogo ili kupisha utulivu mlango ulivyofunguka wote, mpaka mwisho kukatokea ukimya,tukio hilo lilizua maswali kichwani kwake!

Kivyovyote kama kulikua na adui yupo ndani,itakua ni lazima amejipanga kumsubiri hakutaka kuingia kizembe, ilikua ni lazima aingie kwa mshtukizo ili amshangaze adui,kwa kasi ya umeme akazama ndani kwa mtindo wa kujibiringisha kama tairi,ilikua ni kama ametabiri kwani alikoswa koswa na teke lililompitia hewani na kuchana upepo,alivyokaa sawa alipigwa mateke mawili ya dabodabo kifuani,alivyotaka kuiweka bastola yake vizuri ikapigwa teke na kudondoka kando,akachapwa ngumi kavu ya shingo iliyomfanya ahisi imevunjika,adui aliyekua mbele yake alikua ni mtu hatari na mbaya zaidi alimchanganyia mapigo!Dustan akawa makini,alivyogundua hatari iliyokua mbeleni.

Mwanaume aliyekua mbele yake mrefu kwenda hewani,amejazia misuli alikua hodari kwenye kurusha mateke na mwepesi kama karatasi,sababu alishangazwa na namna alivyojibetua baada ya kukanyaga meza,hata hivyo Dustan alishaelewa niya ya adui huyo,akamkwepa kidogo na kumtuliza na kifuti cha kidevu.

“Mmmmh”

Adui,akaguna!Pigo lilimuingia kisawasawa hapo kwa mara nyingine Dustan akarusha ngumi lakini haikuzaa matunda jamaa aliikwepa kimadoido na kutupa ‘round kick’ iliyomfanya Dustan,apepesuke kwani mateke hayo yote yalimfikia usoni na kumdondosha chini.Alichokosea adui huyo ni kumsogelea,hapo hapo Dustan kwa utaalam wa hali ya juu,alimchota mtama wa kimo cha Ng’ombe lakini cha kushangaza jamaa alivyodondoka alitua kwa mtindo wa paka na kusimama wima,hakika Dustan aliishiwa nguvu kwani jamaa huyo alimuogopesha mno,akasimama kwa kasi na kukwepa ngumi tatu za haraka zilizokua zinakuja usoni kwake,hakika adui huyo alikua ni moto wa kuotea mbali.

Jambo,lililomfanya awe makini zaidi.Baada ya purukushani za hapa na pale,Dustan akawa tayari amegundua adui yake nguvu zake nyingi zipo kwenye miguu,akawa makini na kilichotakiwa kufanyika ni kupigana mtindo wa ‘boxer’ yaani awe naye karibu kwani angekaa mbali ingekua rahisi kwa adui kurusha mateke,pigo moja la judo likamfikia adui shingoni akaambatanisha na kifuti cha tumbo!Akarusha ngumi tano za haraka mithili ya mvua,kitendo cha adui huyo kuweka mikono usoni Dustan akaanza kucheza na mbavu akirusha Cross jebu,akamtandika ngumi nne za mbavu,mpaka adui akajipinda alivyojaribu kujibu kwa mateke, Dustan akagundua hila hiyo teke moja lilivyokua hewani yeye akatumia mwanya huo,kuinama kidogo na kumchota mtama!Adui,akakosa muhimili wa kusimama akadondoka kizembe mithili ya mlevi aliyelewa ulanzi,hapo Dustan hakufanya makosa meza iliyokua pembeni akaivuta na kuidodosha,lakini hilo halikusaidia adui yake aliona na kubiringika meza ikagonga chini.Dustan alitambua kua anapambana na mtu hatari kutoka idara ya usalama wa taifa,alihema juu juu na alihisi kuchoka!Mateke,yaliyokua yanakuja akayaona na kuinama kidogo hapohapo bila kuchelewa,akambeba adui yake juujuu na kumbwaga chini kwa nguvu,kilichosikika kilikua ni kilio kama cha mbwa kubweka shingo ya adui huyo iliteguka,hapohapo Dustan hakuchelewa pembeni sakafuni kulikua na bastola yake iliyodondoka, alivyotaka kupiga hatua kuifuata,mguu wake ukavutwa na mkono wa jamaa aliyekua chini,Dustan akapiga mueleka na kudondoka chini puu!

Patashika ikatokea,kila mtu akataka bastola Dustan akasogezwa mbali jamaa alivyotaka kuiwahi,akawa amechelewa Dustan nayeye akawa amemvuta mguu,ukawa kama mchezo wa kitoto wa vuta n’kuvute!Bahati mbaya ikawa kwa Dustan na nzuri kwa jamaa huyo kutoka usalama wa taifa kwani alifanikiwa kuikamata bastola,akageuka nayo kabla ya kumgeuzia Dustan, ikashindikana akarukiwa!Kila mtu akawa anatumia nguvu,kumuelekezea mwezake mdomo wa bastola akiwa anajaribu kutetea uhai wake.

“Paaaaaaaaaaa!”

Kilichosikika ulikua ni mlio wa bastola,damu zikaanza kutapakaa chini sakafuni.Mwili,wa Dustan ukajitoa juu ya adui yake na kudondoka kando huku damu nyingi, zikiwa maeneo ya tumboni kwake.



***

Ilikua ni furaha kubwa kwa Komando Iddi Gogo pamoja na Brigedia Karanje,kando yao alisimama Mzee Ngesa baba yake mzazi na Derick,wote walionesha tabasamu na kushoto kwao kulikua na helikopta!Kwa mujibu wa masaa na mikakati waliyopanga ilikua ni lazima baada ya lisaa limoja na dakika thelathini Rais Leslie afe kwa kulipuka na bomu ambalo walisuka mipango na Waziri Okama,kwao ingekua shangwe kumuua binadamu mwenzao na waliamini kufuatia hapo wangekula kuku kwa mrija na ingekua rahisi kupindua nchi.

Katikati ya shamba hilo kubwa ambalo kulikua na kambi ya siri, ndipo waliamua kuweka makazi yao kwa muda, wakisikilizia kila ripoti inayoendelea!Juu ya kiti kulikua na redio upepo,taarifa zote zinazoendelea walisikia mpaka mikakati ya safari ya Rais Leslie kupangwa!

“Kishiii kisshiii redio two,unanipata ovaaa”

“Kishiiiii nakupata kamanda,barabara ipo sawa tayari kishiiiii unaweza ukaruhusu msafara ovaa”

Redio upepo,ilikua ikisikika na waliamini Rais Leslie atafia angani kutokana na bomu hilo kulipuka,furaha yao ilikua ni kwamba hawatopata mabaki ya aina yoyote ile.

“Mpaka tuhakikishe,ndege yake imelipuka!Hapo tutaanza safari ya kuelekea Zanzibar kisha Mombasa”

Lilikua ni wazo kutoka kwa Brigedia Karanje,macho yake yalionesha chuki za waziwazi dhidi ya Rais Leslie.

"Hilo ondoa shaka”

Komando Iddi Gogo,akajazia na kuweka kipisi cha sigara mdomoni akachukua kibiriti cha gesi na kukiwasha,akatoa moshi puani na mdomoni.

“Lazima tufanye sherehe kubwa,tunastahili kujipongeza”

Mzee Ngesa,hakukosa neno!Na kila mtu,alikua na kihoro cha kusikia ndege ya Rais Leslie imelipuka!


*****

Kila alipotokeza askari walichapa miguu chini na kuinuka kidogo kumpigia saluti Rais Leslie,tafsiri yake ilikua ni heshima kwa mkuu wao wa kazi,tangu anatoka Ikulu alipigiwa saluti na mlinzi ama polisi atakayekutana naye!Nyuma ya Rais Leslie,kulikua na wanaume wanne mbele wawili,hao wote walilinda usalama wake,suti zao nyeusi na makoti vilifanya waonekane nadhifu na kupendezesha msafara huo!Rais Leslie alivyotoka nje,akanyoosha mpaka kwenye gari ambapo hapo kabla ya kufunguliwa mlango,alipigiwa saluti na kuingia ndani.

“Za asubuhi Mheshimiwa Rais”

Dereva aliyefahamika kwa jina la Habibu,alimsabahi bosi wake akahakikisha amefunga mkanda,hapo ndipo akawasha gari.

“Habibu,naomba gazeti la leo”

Rais Leslie akasema na mara nyingi hupenda kusoma magazeti,hapo ndipo alijua kero za wananchi wake na jinsi dunia inavyokweda kwa ujumla!

Licha ya kupewa gazeti na kusoma lakini akili yake haikuwa hapo hata kidogo,vitu chungu mzima vilipita kichwani kwake hususani sakata la Ngesa kumpigia simu,kuna jambo alilikumbuka hapohapo akatoa simu yake mfukoni na kumtafuta Mkurugenzi wa Usalama wa taifa,Ramadhan Nurdin akitaka kujua mchakato ulipofikia.

“Umefikia wapi?”

Rais Leslie,hakutaka kuleta hadithi nyingi akauliza swali moja kwa moja.

“Bado mhe….”

“Bado nini Rama?”

“Nitakupa majibu baada ya masaa mawili al..”

“Ndani ya dakika thelathini nataka kujua Ngesa alipo,kama huwezi namtafuta mtu mwingine wa kufanya hiyo kazi”

“Nitakupa majibu mhe… tititi”

Raisi Leslie,alichukizwa kwa kiasi cha kutosha!Majibu aliyopewa na Ramadhan Nurdin Mpelembe yalimchefua na alitamani amfute kazi hapohapo,kitendo cha Derick Ngesa kupiga simu ikulu yeye alikitafsiri kama dharau kwa mtu anayetafutwa kama yeye!

Hata hivyo alishangazwa sana na Ngesa kua huru sababu siku chache zilizopita alipigiwa simu na watu wasiojulikana wakidai kwamba wamemteka Ngesa na muda mfupi wangemuua,kitu hiko kilizidi kumchanganya kabisa!

Hakuelewa bila kumsikiliza Ngesa wenda angefaidika na angekipiga chenga kifo ambacho kwa wakati huo alikua akikifuata uwanja wa ndege!Akiwa siti ya nyuma,alipata muda mfupi wa kuangalia nje na kuona wananchi wamejipanga kando ya barabara wakipunga mikono huku magari mengine yakiwa yamesimama ili kupisha msafara wake,moyoni alikua na machungu na alitamani hata angejivua uraisi.

Walivyofika Tazara,wakanyoosha moja kwa moja, na kasi ilikua ni ileile na sasa walikua wanakaribia Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere,msafara wote ukakunja kona kwa kasi ya ajabu na kunyoosha moja kwa moja ambapo huko ndipo kuna kitengo maalum na ndege ya Rais inapopaki yaani VIP,magari yalivyosimama walinzi wakatangulia kushuka Rais akafunguliwa mlango na kupigiwa saluti kwa heshima,kabla ya kupiga hatua tatu kwenda mbele, simu yake kutoka mfukoni ikamshtua hiyo ikamfanya asite kidogo!Akaiangalia na kuiweka sikioni baada ya kugundua mpigaji ni Cecilia Njige,sekretari wake.

“Mheshimiwa Rais,samahani kwa usumbufu”

“Nakusikiliza Sesi”

“Kuna simu yako,ni muhimu”

“Imetoka kwa nani?”

“Imetoka hospitali,Jenifa Harrison”

“Ameshapata fahamu?”

Taarifa za Jenifa,Rais Leslie alikua nazo ndiyo maana alishtuka baada ya kusikia amepata fahamu.

“Ndio”

“Sawa,muunganishe”

Dakika moja baadaye Jenifa Harrison akawa kwenye laini anazungumza na Mheshimiwa Rais,sauti yake ilikua ya chini mno,hakusikika vizuri kwani aliongea kwa tabu.

“Mheshi…wa Rais..ku..na watu wab..aya wanata..ka kuku…a usi..”

“Jenifa,sikusikii vizuri”

“Usi..safiri kuna bo....mu waziri Oka….”

“Jenifa naomba upumzike kidogo,nipo safarini nikirudi tu.Nitakuja kukujulia hali,ugua pole Mama”

Rais Leslie,akakata simu!Laiti kama angejitahidi kumsikiliza na kumpa nafasi angeokoa maisha yake.

Hatua zake zilikua za taratibu na kila sehemu alipigwa picha za mnato na waandishi wa habari,televisheni nyingine zilirusha mubashara safari yake ambapo kwa wakati huo aliingia kwenye lango kubwa,akatokezea katika uwanja wa ndege!Uwanja huo ulikua na ndege nne,moja wapo ilikua ya Rais!Walinzi kutoka kitengo cha usalama wa taifa wakatangulia kisha yeye akaanza kupanda ngazi taratibu,alivyofika juu mlangoni akapunga mkono kwa ishara ya kuwaaga bila kujua huo ndio ungekua mkono wa mwisho na yalibaki masaa machache ili alipuke na bomu afe,alivyofika kwenye kiti akakaa kitako na kufunga mkanda!Mbele kidogo alikaa mlinzi wake kwa maana hiyo ndani ya chumba hiko cha Rais,walikaa watu wawili tu yeye mwenyewe pamoja na mlinzi wake makini aliyefahamika kwa jina la Arafat Musoke,muda wote alikua makini anatizama huku na kule akihakikisha usalama wa Rais upo na mipango yote inaenda sawa,hata yeye mwenyewe hakua anaelewa kua ndani kuna bomu hatari ambalo sasa zilibaki dakika chache,lilipuke!


*****

Damu zilikua chini,zimetapakaa sakafuni!Dustan,yupo hoi anahema juu juu risasi iliyochomoka iliacha tundu kubwa sana kwenye mwili wa adui huyu,ambaye sasa Dustan alimfahamu kwa jina la Seleman Abdul Bonzo,hiyo ni kutokana na upekuzi na kuona vitambulisho vyake!Macho ya Selemani Bonzo,yalikua wazi mdomo kaupanua kumaanisha kuwa kifo chake alikiona.Baada ya upekuzi akafanikiwa kupata redio upepo pamoja na kisu kidogo,alivyomaliza!Akaachana naye na kutoka nje ya mlango ambapo sasa alikua makini sana,akapanda gorofa ya tatu,huko kulikua kimya mno!Hakukua na kitu cha maana,alivyofika gorofa ya nne hapo ndipo alituliza akili yake kwani alisikia sauti za watu,akanyata taratibu!Kupitia tundu dogo la mlango,alifanikiwa kuwaona wanaume watatu,mmoja ameshika silaha aina ya Sniper,yupo makini jicho lake kwenye darubini yenye lenzi kali,wawili walikua kando wanapiga stori.Hapo Dustan,akatulia kidogo akapisha utulivu ili atafakari namna ya kuwaingia kwani alishaelewa angefanya uzembe kidogo operesheni hiyo ingefeli na angekamatwa ama kuuliwa.

“Psiiiiii”

Alichokifanya ni kupiga mluzi laini,akachungulia na kuona watu wawili wa usalama!Wanaangalia mlango,wakaanza kusakiziana na kutupiana mpira,nani aende.

Alichokifanya mmoja wapo ni kuchomoa bastola kutoka kiunoni na kuanza kuusogelea,hayo ndiyo yalikua mahesabu ya Dustan alivyoona jamaa kaufikia mlango na kutaka kuufungua,akaupiga teke kwa nguvu.Lilikua ni tukio la kushtukiza sana,llilomfanya jamaa apagawe,kutokana na mlango kumgonga kwa nguvu,akayumba na kudondoka chini chali,mwingine alivyotaka kuchomoa bastola,akawa tayari amechelewa,teke moja la shingo lilimvuruga na kumdondosha,aliyeshika ‘Sniper’ alivyogeuka akarudishwa na kifuti cha tumbo akashikwa shingo vizuri na kujaa kwenye kabali ya Dustan,hakutaka kumuachia akaendelea kumkaba shingo kisawasawa!Alivyomuona usalama aliyegongwa na mlango anasimama,akazunguka teke aina ya ‘Round kick’,ambalo lilimpata kichwani akajigonga kwenye ukuta na kutulia na alifanya hivyo huku bado akiwa amemkaba kabali,mdunguaji wa Sniper alivyohakikisha kalegea,akamvunja shingo!Teke lililokuja kushoto kwake,aliliona akainama kidogo na kutupa ambakati ya kidevu,iliyomfanya usalama huyo abweke kama mbwa kwani alihisi taya zake zimevunjika!Mwingine aliokota bastola yake lakini Dustan akamuwahi kwa kumpiga kikumbo kikali,wote wakadondoka chini kama mizigo!


****

Kukaa na kumsubiri Dustan,amalizane na wadunguaji watano waliokua na silaha hatari za ‘Sniper’ ingemgharimu na operesheni yake ingekufa kwani aliamini yalibaki masaa machache mno ndege ya Rais Leslie ilipuke!Msafara wa Rais,kupita ulimshtua alikua nje ya muda, alichokifanya ni kutoka nje ya gari,kichwa kikiwa chini.Aliamini ni lazima wadunguaji wangekua makini kwa kila mtu,aliyekua ana randa randa eneo hilo!Maelezo ya Dustan kwamba wadunguaji wanakaa juu ya magorofa hilo lilimfanya awe makini mpaka alipofika kwenye ukuta wa gorofa la kushoto,akatizama kwa makini upande wa pili na kuona watembea kwa miguu akajichanganya nao na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka!Mwendo wake,haukuwa wa kawaida hata kidogo alitembea kwa haraka akiogopa zaidi, baada ya msafara kumpita kwa kasi ya ajabu!Hapo,nyuma zilifuata pikipiki sita zikipiga vingo’ra!Baada ya kupita,magari mengine yakaruhusiwa kuendelea na shughuli zingine,hakutaka kuchelewa akakodi pikipiki alivyopiga hatua saba mbele.

“Wapi unaenda?”

“Twende nitakwambia”

Ngesa,akapanda nyuma lakini dereva huyo alikua na wasiwasi mkubwa kutokana na Ngesa kuvaa kombati za jeshi.Kwenye njia ya kuelekea Gongo la mboto Ngesa akamuamuru dereva asimamishe pikipiki!

“Hapa,inakua efu tano mkuu”

Dereva wa pikipiki akasema,Ngesa akapeleka mkono nyuma badala ya kutoa pesa akachomoa bastola!

“Mara mojamoja,jifunze kutoa sadaka!POTEA”

Dereva wa bodaboda,jicho lilimtoka sura ya Ngesa ilimuogopesha bila kujibu chochote akawasha pikipiki na kuitoa kwa kasi ya ajabu,alichokifanya Ngesa ni kuanza kutembea kwa tahadhari bastola kaificha kiunoni,kichwa chake kipo chini.Akatembea huku akikimbia mpaka alivyofika getini,alishangaa hakuna mtu yoyote aliyemuuliza,lakini akagundua kombati aliyovaa ya jeshi ilimkingia kifua,alivyofika getini akasimamishwa.

“Habari”

“Salama”

“Unaelekea wapi?”

“Ndani,kuna dharura imetokea”

Ngesa alizungumza kichwa kikiwa chini bado,picha yake ipo ukutani kwa chini imeandikwa ‘WANTED’

“Tunaomba kitambulisho chako”

Mwanamama mmoja wapo aliyetaka sifa ili aonekane anafanya kazi alianza kuleta unoko,akasema jambo lililomfanya Ngesa achukie na kuliona swala hilo ni upotevu wa muda.

“Okay”

Alivyojibu,akaingiza mkono mfukoni akijifanya anajipekua pekua alivyowasogelea karibu akachomoa bastola.

“Sitaki kujitambulisha mimi ni nani?Nadhani mnanijua vizuri mimi ni yule pale kwenye picha,wote laleli chini”

Kilikua ni kitendo kilichowafanya wapigwe na mduao,kwa hofu wote wakalala chini kifudifudi alichokifanya Ngesa ni kuwafunga kamba za miguu na mikono!

“Nataka kuingia ndani,kupitia mlango wa dharura!Napita wapi?”

Ngesa akauliza bastola ikiwa mkononi,hana mzaha hata kidogo, yupo tayari kuua mtu yoyote atakayeenda kinyume naye!

“Kwa nyuma kule,kuna ukuta lakini mlango wake hautumiki”

“Sawa”

Pembeni kulikua na gundi kubwa ya kufungia mizigo,alichokifanya Ngesa ni kuichukua akawaziba nayo midomoni,akaanza safari ya kutembea kwa miguu!

Kuna gari,akaliona linakuja mbele yake, hiyo ilimfanya ainame na kuchuchumaa kando ya mti uliokua karibu,lilivyopita akaendelea na safari!Mlango wa tatu kutoka mwisho mbele yake,aliona wabeba mizigo watatu waliokua katika sare maalum,kuna wazo lilimjia la kuingia ndani kirahisi!Mlango waliotokea akaingia na kumkuta jamaa mmoja kainama anabeba mizigo,akamvuta na kumtuliza na kichwa cha pua kilichomuingia vizuri na kufanya mshipa upasuke,damu zikaanza kumchuruzika,hakutaka kumuongeza dozi ingine sababu alijua ataua, alichokifanya ni kumburuza mpaka kwenye chumba kingine akamvua nguo zake zote na kuzivaa yeye!

Ngesa,akawa amefanana na wabeba mizigo,kitambulisho kinachoonesha namba kilikua shingoni kwake isingekua rahisi kwa mtu yoyote kumtilia mashaka,ndiyo maana alijiamini na kupita mlangoni bila kuulizwa chochote,sasa akawa ametokea upande wa uwanja ndege zilizokua zimepaki nje!Kushoto aliona ndege ya Rais,mlango unajifunga ikiwa katika harakati za kuanza safari,akatizama huku na kule akiwa na begi kubwa mkononi,akizuga na kujifanya mbeba mizigo, akiifuata.

“Hey”

Sauti kutoka nyuma ikamshtua,moyo wake ukapiga kwa nguvu akajua tayari hila yake imegundulika!Hata,hivyo alisimama bila kugeuka nyuma.

“Unaelekea wapi?”

Sauti hiyo ilimkaribia,akiwa amesimama aliweza kuona kivuli cha mtu, anayekuja nyuma yake,wazo la kumtandika kifuti likamjia lakini alijionya kuhofia watu wangemuona na operesheni yake kuharibika.

“Kuna spea,zinatakiwa kwenye ndege ya Rais”

“Ndege inataka kuondoka lakini”

“Ni Emergence”

“Fanya haraka”

Kwa hatua za haraka haraka,akatembea mpaka kwenye ndege ambayo ilitaka kuondoka!Ilikua nafuu kwake kwani ndege hiyo ilikua na mlango wa nyuma,akaingia na begi na kutulia,ambapo baada ya muda mfupi mlango ukaanza kufunga!Alivyohakikisha hilo,akashusha pumzi ndefu sasa akawa ana kazi ya kutafuta bomu lilipotegwa,katika kupekua pekua ndege ikaanza kutembea!Jasho jembamba likaanza kumtoka sababu hakuelewa kwa wakati huo,zilisalia dakika ngapi!Katika upekuzi wake,ghafla mlango wa chumba hiko ukafunguliwa.

“Wewe ni nani?Unafanya nini humu?”

Sauti yenye madaraka kutoka nyuma yake ikamuuliza kwa utemi.

“Mbeba mizigo tu”

Ngesa akajibu bila kugeuka.

“Unaiba, sio?”

“Hapana”

Alichoharibu jamaa huyo ni kumsogelea Ngesa karibu,bila kutarajia alipigwa ngumi kavu ya mbavu,akajikunja kusikilizia maumivu Ngesa hakumchelewesha akamsindikiza na cross jebu tatu za shingo,jamaa kutoka usalama wa taifa akakakamaa na kudondoka chini.

“Huwa sipendi kuulizwa ulizwa maswali”

Ngesa akasema,akaanza upya na upekuzi wake ambapo humo ndani hakuona chochote!Alichokifanya ni kuchomoa bastola yake,akaanza kutembea kwa makini!Akasukuma mlango,kabla ya kwenda zaidi akayumba sababu ndege ilikua inaanza kupaa,akajishika vizuri ilivyokaa sawa angani akazidi kusonga mbele.

“Mjunii… mjuniii…mjuniiiii”

Sauti ilimshtua,Ngesa akajua kabisa anayetafutwa ni mwenzake ambaye sasa hakuelewa kama alikufa ama kazirai,Ngesa alikua katikati ya Kordo ndiyo maana hakua ana uhakika kama sauti inatokea nyuma ama mbele,kwa tahadhari akarudi na kujificha nyuma ya mlango!

Akimsubiri jamaa apite,alivyomvuka tu akamvuta na kumtia kabali,ngumi moja ya pua na pigo moja la kareti,lilimnyamazisha na kumkata kauli!Ngesa akazidi kusonga mbele,sasa alikua makini sana sababu hakuelewa ndani kuna watu wangapi!Mbele yake,aliona mlango ambao alielewa humo ndimo Rais Leslie,atakuepo hata hivyo kuna nafsi ilimwambia afungue chumba cha kushoto kwake,siku zote aliamini nafsi yake akafanya hivyo!Ndani,alikumbana na utulivu mkubwa ambapo kulikua na makochi pamoja na tv,hilo halikumshangaza sababu alielewa ndege ya Rais ina kila kitu kuanzia,ofisi,chumba na seble.Upekuzi wake,ukaanza upya kila sehemu alipita!Macho yake yakatulia nyuma ya kochi,ambapo kulikua na begi kubwa!Mapigo yake ya moyo yakaanza kumpiga kwa nguvu!Akaanza kulifungua taratibu,moyo wake ukapiga paa!Baada ya kuona juu kuna dakika zimeandikwa 10;23 yaani zilisalia dakika kumi tu na sekunde ishirini na tatu ili bomu lilipuke,jambo hilo lilimfanya akose amani.

Lilikua ni bomu hatari mno na isingekua rahisi kulitegua ndani ya muda uliobaki,hata hivyo akataka kujaribu na kuanza kulichezea!Katika masomo ya kutegua mabomu hapo akamkumbuka mwalimu wake,alivyolifungua vizuri akaona nyaya sita zenye rangi tofauti,alivyotaka kukaa sawa akaingiwa na hofu kwani zilibaki dakika tisa tu.

“Shiiit”

Akasema kwa hasira na kuweka bastola yake sawa mkononi ili akafanye ukombozi, ilikua ni lazima achukue maamuzi magumu yenye faida!Kwa kasi na hasira akiwa mwenye haraka akafungua mlango na kutokeza kwenye korido,alivyoufikia mlango ambao aliamini Rais Leslie yupo akaupiga teke kwa nguvu.

“Paaaaaa”

Ngesa akampiga risasi ya bega mlinzi mmoja aliyetaka, kuchomoa bastola.

“Ngesaaa!”

Rais Leslie,akashtuka hakuelewa anaona mzimu ama ni macho yake kwani hakutegemea kumuona binadamu kama huyo ndani ya ndege yake.

“Rais Leslie,sina muda wa kupoteza hii ndege ina bomu!Tuna dakika nane tu”

Ngesa alizungumza kwa ukali akimuoneshea Rais Leslie bastola,hakua na muda wa kubembeleza kwa wakati huo!

Alichokifanya ni kuchukua begi aina ya parachuti na kulivaa mgongoni,kabla ya kufanya chochote,akapigwa kikumbo cha bega kikali kilichofanya adondoke juu ya kiti bastola ikadondoka chini,hakukaa sawa akachapwa ngumi mbili za uso,zilizomfanya aone nyota na maluweluwe!Huyo alikua mlinzi mwingine kutoka usalama wa taifa,alivyotaka kumrukia teke Ngesa akaona,akajibetua lakini bahati mbaya akateleza jambo lililomfanya adui yake amvae na kumpiga kifuti cha mbavu.Dakika,zilibaki tano tu ili ndege ilipuke jambo lililomfanya Ngesa atulize akili sababu aliamini angepaniki na kujitetea bila kutumia akili angefia ndani ya ndege na kila kitu kingekua bure kabisa.

Ngumi,iliyokua inakuja usawa wa usoni ilimfanya arudi nyuma kidogo,ikapita na kuchana upepo!Mikono yake,akaitanua kidogo akashika kiti hiki na kile,akaruka sambasoti ambapo teke lilimfikia adui yake kwenye kidevu,akamvuta hapohapo na kumtandika pigo moja la judo la kufungia kazi,akamsindikiza na teke aina ya ‘flying kick’ akiamini adui huyo asingeweza kusimama tena!Dakika tatu,zilisoma juu ya bomu zikizidi kurudi nyuma.

“Ngesa weka mikono juu”

Rais Leslie,alishika bastola akiwa amemuelekezea Ngesa akimtaka asalimu amri lakini kwa Ngesa ingekua ni kosa kubwa la jinai,kusalimu amri na hiyo ilimaanisha wote kufia ndani ya ndege!Hakujali kama ni Rais wake wala nini,akakanyaga kiti na kuruka kama ngedere pigo moja la ‘kongfu’ lilimfanya Rais Leslie,adondoke chini kama embe mtini, hapohapo Ngesa akaokota bastola kwa haraka!

“Paaa! Paaa! Paaa! Paaaaa!”

Risasi nne,zilipasua kioo cha ndege na bodi na kusababisha upepo mkali kuingia ndani na kupeperusha vitu nje!Hapohapo,Ngesa hakutaka kupoteza wakati,akamchukua Rais Leslie na kumshika vizuri,wakajitosa nje!Kitendo cha kutoka tu nje ulitokea mlipuko mkubwa sana, uliotoa sauti kubwa na kumfanya Rais Leslie asiamini anachokiona,ingawa alikua angani anaelea aliweza kuona jinsi ndege yake ilivyopasuka vipande vipande, ikiwaka na moto mkali!



****

CCG Abdallah Matochi mkurugenzi mkuu katika idara nzima ya usafiri wa anga hususani ndege ya Rais,alikua makini sana juu ya kiti chake anawasiliana na rubani wa ndege!Katika hali ya kushangaza,mawasiliano yakakatika jambo ambalo halikua la kawaida kabisa kutokea.

“Ruben Ruben Ruben”

Alimuita mara tatu rubani,kupitia mawasiliano hayo maalum lakini kulikua na ukimya wa hali ya juu na kuanzia hapo,rada haikusoma tena!Hakutaka kubaki kimya,akachukua mkonga wa simu kwa haraka na kuwasiliana na idara nzima ya mawasiliano akitaka kujua ni wapi shida ilipo.Lakini matokeo yake akaambiwa data zipo vizuri hivyo hakuna tatizo lolote.

“Nimepoteza mawasiliano na Ruben”

“Rubeni?!”

“Ndio Captain”

“Pilot wa Rais Leslie?!”

“Ndio”

“Oh My God,jaribu kumtafuta tena”

“Najaribu simpati”

Kuanzia hapo,ndege ya Rais Leslie haikuonekana tena kwenye rada wala hakukuwa na mawasiliano jambo lililomfanya CCG Abdallah Matochi apate kitete,akalegeza tai na kusukuma mlango wake na kushuka ngazi mbilimbili kama mtu aliyeambiwa nyumba yake inaungua.

“Attention”Matochi,akaombwa asikilizwe!

Yeye ndiye alikua mkurugenzi ama bosi wao,kitendo cha kusema hivyo kila mtu akaacha kompyuta yake na kumuangalia kwani ilielekea ana dharura.

“Nina habari nzito kidogo,naomba masikio yenu na ushirikiano!Hapa ninavyoongea na ninyi nadhani kila mtu anajua machafuko ya hii nchi.Ngoja niwe short and brief,tumepoteza mawasiliano na ndege ya Rais Leslie mpaka sasa hatujui ilipo!Naomba wote kwa pamoja tufokasi kwenye hilo”

CCG Matochi,alizungumza kwa utulivu na upole na kitu cha kwanza baada ya kupanda ngazi na kuingia ofisini kwake ni kumtafuta mkurugenzi wa usalama wa taifa Ramadhan Nurdin Mpelembe,hata yeye habari hizo zilimchanganya akili yake na kumshtua kwa wakati mmoja.

“Ilikuaje?”

“Kama nilivyokwambia Mkuu”

“Nitakupigia baada ya muda mfupi lakini kwa sasa hivi habari hii iwe low profile”Ramadhan Nurdin,akashauri.

Hakuna mtu yoyote ndani ya dakika hiyo aliyejua ni wapi ndege ya rais ilipo,mambo yalienda chini chini mpaka masaa manne baadaye walivyopokea simu kutoka nchini Uganda kua kuna ndege imelipuka ikiwa angani!Wa kwanza kupata habari hizo alikua ni Makamu wa Rais Dokta Jonathan Mlawa,alipokea simu hiyo akiwa chumbani kwake, kitandani na mkewe anajiandaa kulala.

“Mungu wangu,Rais Leslie yeye alikua ndani ya ndege?”

“Ndio,alikua ana safari leo”

“Itisha press ya waandishi wote,Ikulu waambie kuna dharura usimueleze mtu yoyote.Lakini una uhakika Raisi Leslie,alikua ndani ya ndege?”

Simuni Makamu wa Rais Dokta Jonathan Mlawa,ambaye uteuzi wake haukuwa na mwaka hata mmoja aliuliza mara mbilimbili,jibu likawa ni lilelile kua Rais Leslie alipanda ndani ya ndege,kifo cha Rais Leslie kilimaanisha yeye ndiye angekua Rais wa nchi,jambo hilo lilimfanya atabasamu na kukata simu.Akamtizama mkewe,aliyekua kitandani.

“Mke wangu,unaenda kua fisrt lady”

Dokta Jonathan Mlawa aliongea hayo,meno yote thelathini na mbili yakiwa nje!Akatembea mpaka kwenye friji na kuchukua glasi ya mvinyo akamimina na kufungulia mziki mkubwa wa redio.

“Mbona sikuelewi wewe mwanaume?”

“Rais Leslie,amekufa”

“Niniiiiiii?”

Mkewe alishtuka na kutoa shuka mwilini,hakuelewa kama alisikia vibaya ama ni kweli,hakutaka kuamini kua Rais Leslie amefariki dunia,ndiyo maana akamsogelea mumewe karibu zaidi,machozi yanamlenga akitamani habari hiyo iwe ndoto.

“Jona,unasema niniii wewee?”

“Nakwambia hivii,tuserebuke naenda kuwa Rais nawewe Mke wa Rais..Cheers mke wangu…”

Mwanamke huyu aliachia kilio kikubwa,akimlaumu mumewe kwa kunywa pombe!Moyo wake uliumia sababu alielewa ni kwa jinsi gani,Raisi Leslie alivyompa msaada wa hali ya juu!

“Yaani unafurahi..a kifo cha rafiki yako Yona?”

“Ndio,nawewe inabidi ufurahi sasa”

Dokta Yona alizungumza na kumfanya mkewe asiamini kile anachokisikia wakati mwingine alidhani wenda mumewe,amelewa alichokifanya ni kuchukua simu na kumtafuta mke wa Rais hewani.

“Unataka kufanya nini?”

“Kumpigia Mama Witness kumuuliza”

“Achana na hiyo biashara”

Makamu wa Rais akatoa amri,tayari alishajiona yeye ni Rais wa nchi akazidi kunywa pombe huku akicheza mziki.


****

Sherehe ilikua kubwa na shangwe,Brigedia Karanje na Komando Iddi Gogo pamoja na rafiki yao Mzee Ngesa walichekelea wakifurahi kwa kifo cha Rais Leslie!Sasa wakawa na uhakika Rais Leslie amelipuka na ndege yake,hiyo ilimaanisha hakutokua na ushahidi wa aina yoyote ile na kilichobaki kwa wakati huo ni kupindua nchi kibabe kwani dhumuni lao lilikamilika.

“Hakika ilikua ni vita,ngumu”

“Hatimaye tumeshinda”

Hapohapo,wakapanda Helkopta na kuiwasha ikapaa angani na safari ya kwenda visiwa vya Zanzibar kujipongeza,ikaanza!


*****

Upepo ulikua mkali angani,katika mazoezi ya kijasusi kwa Ngesa hilo lilikua kawaida kucheza na upepo wa angani,mafunzo aliyopitia aliyakumbuka ndiyo maana akabana mikono yake na kunyoosha miguu kichwa chake kikiwa chini,sasa akawa anaelekea chini kwa kasi ya ajabu!Akamuangalia Rais Leslie jinsi anavyoweweseka angani mara huku mara kule,bila uelekeo na alikua ana uhakika kabisa tayari alipoteza fahamu akiwa angani.Kila alivyotaka kumshika,alishindwa!Akatuliza akili akatanua mikono na kumshika sehemu ya kiuno,alivyohakikisha kamshika vizuri!Akarudia staili ileile ya kuangalia kichwa chini.Kwa mbali aliona maji,sasa akaanza kuogopa na kuona hatari endapo angetua katikati ya bahari au ziwa akiwa na Rais Leslie lakini kabla ya kufika chini kabisa,akavuta kamba maalum.

Puto kubwa likafumuka na kumrudisha juu kidogo,hilo lilikua parashuti sasa akawa anaelea hewani.Kwa taaluma aliyokua nayo,ilikua ni rahisi kwake kucheza na kamba,akaivuta kulia kwani huko kulikua ni pembezoni mwa bahari.Hata hivyo,bahati mbaya ilikua kwake sababu alitua ndani ya maji!Kwa kasi,akalivua begi na kumshika Rais Leslie vizuri akaanza kupiga mbizi kwa tabu,mpaka alipofika nchi kavu ambapo alishukuru alitokezea sehemu ambayo hayakua makazi ya watu.

Miti mingi ya pembezoni,ilimfanya apate dakika kumi za kuvuta pumzi!Baada ya hapo,akamsogelea Rais Leslie na kumlaza chali.Akamvua koti la suti na kumfungua vifungo vya shati na kumuacha kwa dakika tano nzima!Ngesa hakutaka kuganda sehemu hiyohiyo alichokifanya ni kulichunguza eneo hilo,akitembea kila kona,akaingia katikati ya msitu mzito na kuangalia kama angepata sehemu salama ya kujificha kwanza yeye na Rais Leslie kuliko kujianika ufukweni,alichokifanya ni kumbeba Rais Leslie begani,mpaka kwenye kichaka hiko kisha kumuweka juu ya gogo kubwa,akatembea mpaka kwenye moja ya mti na kukaa hapo, akachomoa bastola iliyokua kiunoni na kuishika vizuri mkononi,upepo ulikua mkali wenye kubembeleza kutokana na uchovu wa safari na pilika nyingi usingizi ukamchukua hapohapo bila kutegemea!


****

Ukubwa wa chumba hiko ulifananishwa na ukumbi wenye mita za mraba mia moja na mbili,viti vilikua kumi na tisa na katikati kulikua na meza ndefu!Kulikua na kikao nyeti kilichowashirikisha usalama wa taifa kumi na tisa!Kikao kilikua kifupi lakini kizito na ajenda ilikua ni kifo cha Rais Leslie aliyelipuka na ndege yake kwani kila mtu alidhani amekufa tayari,kilichofanyika ni uchunguzi mkali na jibu walilolipata ni kua Ngesa ndiye aliyehusika kwenye kila kitu.Hawakuongea kwa kubahatisha kwani mbele yao kulikua na kioo kikubwa kinachoonesha video ya Ngesa,alivyokua anaingia Uwanja wa ndege mpaka ndani ya ndege ya Rais,hata hivyo kuna mmoja wao akasimama.

“Huu uchunguzi,hautoshi.Ngesa hakua na kitu chochte mkononi,hilo bomu kaingia nalo vipi?”

Frank Ntagara,mwanaume makini na mwenye misimamo akasimama na kuhoji,kuna kitu alikua na mashaka nacho na hakua ana uhakika sana kama Ngesa amehusika kwa asilimia zote mia moja!Na swali hilo liliwafanya wanausalama wote,wamgeukie.

“Ntagara,Ngesa ni mtu hatari.Hilo wote tunalifahamu,kama aliweza kuingia airport atashindwaje kuingiza bomu?”

“Mimi binafsi nakataa,nani anajua kwamba kabla ya ndege kuruka Ngesa alipiga simu ikulu na kuongea na Rais Leslie,kuna jambo alitaka kumwambia lakini simu ikakatika!Naomba niulize swali”

“Uliza”

“Kwanini usiku ule kabla ndege ya Rais kusafiri,CCTV zilizimwa?Kuna kitu kilifichwa na ndiyo hapo nina uhakika hundrend percent bomu liliingizwa,nani alikua zamu siku hiyo?”

Frank Ntagara aliibua hoja nzito na alizungumza kwa kujiamini bila kujua anaingia kwenye matatizo mazito sababu kila kitu kilitengenezwa na Waziri Okama,mpaka kamera zote kuzimwa kisha yeye kuingiza bomu ndani ya ndege!

Ramadhan Mpelembe Mkurugenzi wa usalama wa taifa,akashindwa kujibu hoja hiyo nzito akabaki kimya na kuhaidi kwamba siku inayofuata angekuja na majibu.Kwa Frank Ntagara,hilo halikutosha,baada ya kufunga kikao akanyoosha moja kwa moja uwanja wa ndege ili kujua siku hiyo ni nani alikua zamu,kuna kitu kilichokua nyuma ya pazia alitaka kukijua!

“Zamu siku hiyo alikua…Ebu ngoja”

Mwanamke,aliyekua katika idara hiyo ndani ya ofisi alibonyeza bonyeza kompyuta yake na kutulia kisha kumtizama Frank Ntagara, aliyekua wima amesimama anamtizama anasubiri majibu.

“Olina Kalumuna”

“Anaishi wapi?”

“Kurasini,high way”

“Naomba address yake”

Frank Ntagara alifanikiwa kupata data zote anazohitaji kwa wakati,ilikua ni lazima ajue ni kwanini kamera zilizimwa siku hiyo bila sababu ya msingi,alikua yupo tayari kwa kila kitu ndiyo maana hakutaka kuliacha jambo hilo lipite juujuu!

Kuanzia hapo,hakutaka kupoteza wakati akawasha gari na kuanza safari ya kuelekea Kurasini.Kutoka alipokua hakukua na umbali sana,ndiyo maana ndani ya dakika ishirini alikua tayari yupo Kurasini,sehemu inayoitwa Highway!Hapo,aliegesha gari nyuma ya lori kubwa kwa niya ya kulificha sababu magari yao ya usalama wa taifa,yalijulikana!

Kitendo cha kushuka akatizama huku na kule na kuanza kupiga hatua zake huku akiwa makini kukagua nyumba aliyoelekezwa na mwanamke wa uwanja wa ndege,akakata kona na kuingia mtaa mpana wenye vumbi,mbele kidogo akaona ukuta wa rangi nyeupe wenye geti jekundu.Kwa mujibu wa maelekezo, hapo ndipo Olina Kalumuna aliishi.

Alikua ana kila sababu ya kumtafuta na kumuhoji maswali,akiamini kua msichana huyo mdogo angemfafanulia kila kitu.Baada ya kufika getini akagonga,lakini hakukua na mtu yoyote aliyefungua!Akajaribu tena lakini kimya,akafanya kama kujaribu kulisukuma geti.Likafunguka,kumaanisha kuwa lilikua wazi,mbele yake alikumbana na magari mawili madogo,moja ‘Starlet’ na jingine ‘Mark II’.Akaendelea kukagua huku akitembea,alivyoufikia mlango akagonga lakini ukimya ulikua upo vilevile.Hapo,akatulia kidogo na kugonga kwa mara nyingine.

“Hodi jamaanii,hodiii”

Bado,kulikua kuna ukimya sasa akawa ana uhakika kua ndani hakukua na mtu yoyote yule ingawa jambo hilo hakutaka kulipa kipaumbele sana,alivyonyonga kitasa ili kufungua,mlango ukagoma!Kumaanisha kua ulifungwa kwa ndani,jambo lililomfanya azunguke uwani akiamini huko kuna mlango mwingine,alivyofika alishangazwa na kukuta mlango upo wazi.

“Hodiiii”

Ukimya ukaendelea kua vile vile,sasa akaanza kupiga hatua za taratibu mpaka alivyotokezea jikoni!

Juu ya jiko la gesi aliona sufuria,lenye maharage pembeni kuna nyanya na kisu,akawa ana uhakika wenyewe wapo ndani,alivyotokeza upande wa pili alikumbana na korido yenye vyumba vitatu.Cha ajabu bado kulikua na ukimya,akatembea mpaka seblen ambapo huko kulimfanya apigwe na butwaa la waziwazi.Hali ya sebleni,ilimshtua na kumfanya agande kidogo.Masofa yalisogezwa huku na kule,tv ilikua chini imepasuka,meza ya kioo imepasuka pasuka vitu vya kwenye kabati vimetolewa nje vipo chini,ilielekea kulikua na upekuzi usio na ustaarabu hata kidogo.

Hata hivyo,hakuishia hapo sasa akaanza kukagua vizuri,ambapo aliingia chumba cha kwanza na kukuta magodoro yote yametupwa chini jambo hilo lilizidi kumchanganya akili yake,chumba kinachofuata hali ilikua ileile!Chumba cha tatu,ambacho aliamini kilikua ndio ‘master’ kilimfanya asite kuingia,hata hivyo alitafakari kwa muda kabla ya kuchomoa bastola yake.

“Kacha kacha”

Akaikoki,akiwa tayari kukumbana na jambo lolote lile,sasa akawa ana uhakika mtu aliyepekua pekua hakua mtu wa kawaida hata kidogo!Kuna kitu kilikua kinatafutwa,akanyata taratibu mpaka kwenye mlango akausogeza taratibu huku bastola yake ikiwa mkononi kidole kipo kwenye triga,kaitanguliza mbele.

Picha,aliyoiona ilimtisha kwa kiasi cha kutosha,juu ya paa aliona mwili wa mtu unaning’inia umetoa macho,alikua ni mwanaume wa makamo!Ambaye sasa kivyovyote vile alijua ni mume wa Olina Kalumuna,maskini alikua juu amenyongwa na kwa harakaharaka alipitia mateso makali kabla ya kifo chake kumkuta na kifo chake kilikua cha kibabe sana kwani kifuani,alitobolewa tobolewa na vitu vyenye ncha kali.

Frank Ntagara alibana meno yake kwa hasira na kumeza fundo zito la mate,akapiga ishara ya msalaba na kushusha pumzi ndefu!Yalikua ni mauaji ya kinyama mno na aliamini mwanaume huyo,hausiki hata kidogo kwa haraka haraka alijua ni lazima tu,alikua anahojiwa ni wapi mkewe alipo akagoma kusema ndiyo maana umauti ukamkuta!Frank Ntagara hakutaka kuondoka hivi hivi,nayeye akaanza kufanya upekuzi wa hapa na pale,alivyofika kwenye kabati ili aendelee na upelelezi wake usio rasmi.Mapigo yake ya moyo yakapiga kwa nguvu baada ya kuhisi kichuma cha baridi kimemgusa kisogoni,hakutaka kuuliza alishaelewa nini maana yake.

“Frank Ntagara,tupa bastola chini.Sikupenda ufe lakini shobo zako,zinakuaa!Kwanini usingekaa kimya tu?”

Lilikua ni swali,kutoka nyuma yake na mtu huyo aliuliza kwa sauti ya utemi yenye kumaanisha kile anachosema,hiyo ilimfanya Frank Ntagara ameze mate na kuukumbuka mwili alioukuta juu ya paa umenyongwa,akaamini watu waliofanya hivyo hawana mzaha hata kidogo na ana sekunde chache za kuishi duniani.

“Kosa langu ni nini?”

Frank akajitutumua na kuuliza.

“Hujui?Unafanya nini hapa?”

“Nimekuja kusalimia tu”

“Una undugu na Olina?”

“Ni rafiki yangu sana”

“Usijifanye mjanja Frank Ntagara! Kudanganya kwako hakutokusaidia chochote,tupa silaha chini,piga magoti”

Labda ungetokea muujiza lakini Frank Ntagara hakua na ujanja zaidi ya kusali sala ya ‘baba yetu’ kama ishara ya kuzungumza na Mungu,akatupa bastola chini na kupiga magoti akisubiri kifo chake!Akapata muda mfupi wa kukitafakari kifo kinavyofanana,akashindwa kupata jibu akafumba macho yake.

“Paaaaaaaaaa”

Mlio mkubwa wa bastola ukasikika risasi ikapenya kichwani,damu zikaruka ubongo ukamwagika chini!Frank Ntagara,alishangazwa sana baada ya kusikia mlio huo wa bastola lakini bado alikua mzima,jasho linamtoka!Bado,alishindwa kuelewa kama tayari amekufa ama yupo hai.

“Frank,simama tuondoke.Hapa sio salama tena”

Sauti hiyo ilimshtua mno akageuka,hakuamini macho yake baada ya kumuona mwanamke mrefu kiasi mwenye shepu iliyojichora namba nane,kabana nywele zake kwa nyuma kavaa tisheti ya kijani na Jeans,kashika bastola mkononi!

“Daphineeee!”

Frank Ntagara akaita kwa mshangao,hakuamini kinachotokea, kwake ilikua kama mazingaombwe!Mwanamke jasiri DAPHINE, kuwepo mbele yake!



***

Isingekua utemi wa Ngesa kuingia hospitalini na bastola na kuwaweka madaktari wote chini ya ulinzi ili Mke wa Dustan atibiwe kwa haraka,wenda kwa wakati huo wangekua wanazungumza habari za msiba,hiyo ilifanya madaktari waache kazi zao zote na kumpatia matibabu!Ndani ya masaa matatu walikua bize kukarabati kidonda cha Mke wa Dustan,ambapo walitoa risasi na kulisafisha jeraha vizuri.Wakakifunga na kumchoma sindano ya kutoa sumu pamoja na dawa za kupunguza maumivu,swala hilo lote lilisimamiwa na Daphine,akiwa na bastola yake mkononi!Baada ya hapo,waliingia ndani ya gari na safari ikaanza mara moja!Nyuma ya usukani alikaa Daphine,kushoto yupo Jaqlin na nyuma yupo mke wa Ngesa amelala kwani sindano alizochomwa zilimfanya ahisi kuchoka na nguvu kumuishia.

Safari yao ilikomea Bagamoyo ambapo hapo Daphine alikunja kushoto na kuingia kwenye barabara ya vumbi,pembeni kulikua na miti mingi.Wakazidi kusonga mbele mpaka walipopandisha kilima kidogo na kukunja kulia,hakuna mtu yoyote aliyejua ni wapi Daphine anawapeleka,hata hivyo walikaa kimya.Mawazo ya Daphine hayakua hapo hata kidogo,alimfikiria sana Ngesa huko alipo na kumuombea afanikiwe,hata hivyo mambo yote alimuachia Mungu na kutokana na mambo yalivyoenda aliamini kabisa Ngesa asingeweza kurudi salama.

Mbali na kuamini hivyo,bado kisasi chake kilikua kwa Brigedia Karanje na ilikua ni lazima ajue ni wapi alipo kwa njia moja ama nyingine,mbele kidogo kulikua na barabara nyembamba,ambayo ilitosha kupita gari moja tu,majani yalikua mengi kuashiria kwamba hakukua na makazi ya mtu yoyote yule.Umbali wa mita kumi,waliona kibanda kidogo cha nyasi,hapohapo Daphine akasimamisha gari na kushuka.

“Tumefika”

Daphine akasema na kuteremka,akafungua mlango wa nyuma ambapo huko alimshusha mke wa Dustan na kumpeleka mpaka ndani ya kijumba hiko chenye nyasi kwa juu,mfano wa nyumba hiyo ilikua ni kama zile za makumbusho,juu zina nyasi na zimetengenezwa kwa udongo!Mlango wa mbao,hapo Daphine aliusukuma bila wasiwasi hilo lilimshtua Jaqlin Mfinanga lakini hakutaka kuhoji chochote.Walivyoingia ndani,wakakumbana na stuli tatu,kioo kikubwa na kando kuna begi kubwa la chuma mithili ya Tranka!Ilionekana wazi kwamba Daphine alikuwa mwenyeji wa nyumba hiyo,ndiyo maana hakuonesha wasiwasi wa aina yoyote ile.

“Unaendeleaje?”

Lilikua ni swali kutoka kwa Daphine akimuuliza mke wa Dustan,aliyekua chini amelala chali.Kwa wakati huo,alifumbua macho yake na kuyapepesa huku na kule.

“Ha..pa ni waaapi?”

Akauliza kwa sauti ya chini.

“Bagamoyo”

“Dustan,yuko wapi?”

“Atakuja,kuna kazi anamalizia”

“Saa ngapi?”

Maswali yalikua mengi,alichokifanya Daphine bila kujibu ni kutembea mpaka karibu na tranka ambapo hapo,alichukua chuma kilichofanana na tindo na kupiga kufuli,likavunjika!Jaqlin Mfinanga,alishtuka baada ya kuchungulia ndani, moyo wake ulianza kumwenda mbio na kuogopa kwani alianza kuhisi hakuna usalama tena!

Kwa Daphine nyumba hiyo,miaka iliyopita ndio aliitumia kama maficho yake,hakuna mtu yoyote aliyejua chimbo hilo,ndani ya tranka kulikua na kila aina ya silaha, kuanzia bastola, visu na mabomu.Mitutu mitatu,bastola nne na risasi zaidi ya mia moja zilikua ndani ya tranka,jambo lililomfanya Daphine achukue bastola moja na kuiweka kiunoni na kisu pia.Akabeba boxi,lililojaa risasi na kuliweka mfukoni,alivyohakikisha kila kitu kipo sawa akawatizama mke wa Dustan na Jaqlin Mfinanga.

“Nitarudi,msiondoke hapa!”

“Tuondoke wote”

“Hapana hatuwezi”

Daphine,akazungumza na kutoka nje ambapo huko aliingia ndani ya gari na kuegemea usukani akitafakari ni wapi aanzie ili ampate Brigedia Karanje,amuuwe kwa mikono yake kwani alikua mwenye usongo naye kuliko kitu chochote kile.Akili ikaingia kazini na hapohapo,akagundua njia ya kumpata Brigedia Karanje kwani maongezi yake aliyasikia wakiwa wanataka kutega bomu ndani ya ndege ya Rais Leslie,hakutaka kuchelewa akalitia gari moto na kurudi kinyume nyume huku shingo yake akiwa ameigeuza nyuma,alivyokaa sawa akapiga gia na kukanyaga mafuta kwa safari ya kuelekea uwanja wa ndege!Akiwa makini anaendesha gari,alimfikiria sana Ngesa huko alipo kwani hakua na ripoti yoyote ile kuhusiana na ndege ya rais, licha na hayo yote aliamini kuwa usalama wa taifa ni lazima wangeliweka jambo hilo kua siri kwanza mpaka wafanye uchunguzi wa kina.

*****

Saa tisa ya Alasiri Daphine alikua nje ya uwanja wa ndege,amepaki gari.Ungemuangalia ungedhani wenda anamsubiri mgeni wake kutoka nje ya nchi kwani alipendeza na nywele zake alizibana vizuri kwa nyuma!Macho yake yote yalikua kwa Mzee mmoja mwenye kitambi,amechomekea shati jeupe shingoni kanyonga tai iliyombana vizuri kooni.Kupitia huyo aliamini kwamba angepata taarifa anazotaka siku hiyo,ndiyo maana akamuacha mpaka alivyoingia ndani ya gari nayeye akaanza kumfuata kwa nyuma!

Daphine alikua makini mpaka wanafika kituo kinachoitwa Banana,barabara ya kuelekea Gongo la Mboto akaona gari hilo,linachepukia kushoto nayeye akawa makini kabisa,lilivyofika nje ya geti jeusi Daphine akasimamisha gari.Akabaki,analitizama gari hilo linaingia ndani na geti likafungwa,hapohapo hakutaka kupoteza muda akachukua bastola yake akaikoki,akaiweka nyuma ya kiuno na kushuka ndani ya gari huku akitembea na kuikagua nyumba hiyo kwa staili ya kuzunguka ukuta,mpaka alipofika kwenye geti dogo la uani,ambapo hapo alitulia kidogo!Akatizama huku na kule na kusukuma geti,likagoma ikabidi atembee kwa upande wa pili ambapo alikutana na ukuta wenye vitobo vitobo,hiyo ilikua nafuu kwake sababu alianza kupanda kwa tahadhari!

Akafanikiwa kufika juu,alivyoona kuna usalama akatua chini kwa mtindo wa paka bila kutoa kishindo sasa akawa ameingia ndani,hapo alichomoa bastola na kuuendea mlango,akausukuma na kuingia ndani ambapo alikumbana na ukimya wa hali ya juu sana!Akapita kwenye korido na kufika seblen,ambapo pia kulikua na ukimya,sasa akajua ni lazima mzee huyo angekua chumbani kwake,akanyata taratibu sababu alisikia kuna sauti inatokea kwenye mlango wa mbele yake kushoto,akatembea mpaka karibu kabisa na mlango!Akainama kidogo na kuchungulia kupitia kitundu cha funguo,alichokiona kilimfanya atulie kidogo kwani mzee huyo alikua katikati ya tendo la ndoa na alikua kamuweka mkewe chini,yeye yupo juu!Daphine hakutaka kuwaharibia starehe yao,akasubiri mpaka wamalize,alivyotaka kuingia akamuona mzee huyo mwenye kitambi anachukua taulo na kuusogelea mlango kwa niya ya kutoka nje,hapo Daphine alirudi nyuma kidogo na kumsubiri atoke.

“Rudi ndani”

Sauti hiyo ilimshtua mzee huyo na kufanya mpaka taulo lake lidondoke chini bastola iligusa pua yake,ambapo huko hata mkewe alipigwa na butwaa la waziwazi.

“Wewe ni nani?Na unataka nini?”

Mzee akauliza,bastola ilimtisha kwa kiasi cha kutosha ikapelekea mpaka amsogelee mkewe na kumkumbatia.

“Nahitaji kujua nani aliyekua zamu,juzi tarehe tisa ofisini kwako”

“Mimi sijui chochote”

Alichokifanya Daphine ni kumuelekezea bastola mkewe na kumuangalia mzee huyo kuashiria kwamba angeendelea kusema hajui,mkewe angepigwa risasi.

“Bado hujui?”

“Najua,tafadhali naomba usimuue mke wangu usituue”

“Maisha yake yapo mikononi mwako”

Mzee huyo hakua na jinsi zaidi ya kukubali,alichokifanya ni kusimama na kumbusu mkewe kama ishara ya kumuaga endapo angekufa,akatembea mpaka kwenye kabati ambapo huko alitoa ‘Laptop’ na kuanza kutafuta majina.

“Anaitwa Olina Kalumuna,ndio alikua zamu”

“Anaishi wapi?”

“Kurasini”

Kila kitu kikawa wazi mzee akasema mpaka nyumba anayoishi Olina Kalumuna akapewa na picha yake, ili kurahisisha kazi.

Wakafungwa kamba za miguu na mikono kisha kuchukua simu zote na kuwafungia mlango kwa nje,Daphine hakutaka kuwaua aliamini hawana hatia hata kidogo, alichokifanya baada ya kutoka ni kuingia ndani ya gari na safari ya kwenda Kurasini kuanza mara moja!Safari yake,haikumchukua masaa mengi alivyofika tu,aliweka gari kando na kujaribu kupima utulivu wa eneo hilo.Ukimya ulimfanya,asijipe asilimia mia moja!


***

Hakua mweupe sana wala mweusi,rangi yake ilikua ya katikati.Olina Kalumuna,muda wote alikua mwenye mashaka na alitamani kuhama nyumbani kwake kabisa,kuna jambo lilimsumbua ndani ya akili yake,hilo lilionekana mpaka kwa mumewe ambaye muda mwingi alimuuliza kinachomsibu.Kutokana na mkwara aliopigwa na waziri Okama kwamba angeuwawa endapo angesema siri hiyo,ilimfanya aogope!

“Upo sawa baby?”

Mumewe akamuuliza kwa mara nyingine tena,alimfuata mpaka jikoni na kumuona jinsi alivyokua mnyonge anakata nyanya na vitunguu kwa ajili ya kupika chakula cha usiku.

“Niko sawa,Mme wangu!Leo,nakupikia kuku wale wa rangi,unaowapenda”

“Sekela?”

“Yes honey”

Olina,alijitahidi kuficha mawazo aliyokua nayo akapachika tabasamu la plastiki na kumuacha mumewe aingie chumbani huku akitoka nje baada ya kugundua chumvi imeisha.

Akaacha jikoni kama kulivyo na kutoka nje!Daphine,alikua makini anatizama usalama wa eneo hilo lakini akashtuka na kukilaza kiti baada ya kumuona mwanamke anatoka nje ya geti,akachukua picha aliyopewa na mzee mwenye kitambi ambaye mpaka wakati huo hakumjua jina lake.Alivyojiridhisha ndiye yeye,akafungua mlango taratibu na kumuendea kwa haraka.

“Usipige kelele”

Ndani ya dakika sifuri,Olina alikua mateka na hakuna mtu yoyote aliyeona tukio hilo sababu aliwekewa bastola kwenye mbavu,wakaongozana mpaka kwenye gari la Daphine.Olina,alitetemeka kwa kiasi cha kutosha,moyo wake ulimwenda mbio sababu alijua huo ndio mwisho wake.

“Sikumwambia mtu yoyote yule,hakuna mtu yoyote anayejua haki ya Mungu”

Olina,akaropoka na kujiongelesha mwenyewe akidhani Daphine alitumwa na Waziri Okama.

“Karanje yuko wapi?”

“Mimi simjui”

“Humjui?”

Bastola ikawa kichwani kwa Olina,Daphine hakuonesha mzaha hata kidogo!Kuna kitu Daphine,alikiona ambacho hakikuwa cha kawaida,gari aina ya ‘pickup hardboard’ kusimama kando ya geti alilotoka Olina,mwanaume mmoja mrefu akashuka na kuweka bastola kiunoni.Jambo hilo,lilimfanya atulie na kumtizama.

“Nyumbani kwako yupo nani?”

Daphine,akauliza.

“Mme wangu”

“Hakuna mtu mwingine?”

“Ndio”

Hakutaka kuzungumza kitu chochote zaidi ya kutulia kama nusu saa lizima,ndipo alipomuona mwanamme mwingine anaingia ndani ya geti hilohilo,huyo alimtambua ni Frank Ntagara kutokea idara ya usalama wa taifa,hakuelewa ameingiaje kwenye mkasa huo hatari!

Alichohisi ni lazima Frank Ntagara anafahamu mchakato mzima,alivyosubiri kwa dakika kumi nzima,ilibidi ajiridhishe alichokifanya ni kumfunga kamba vizuri Olina Kalumuna kisha yeye kushuka!Umakini ulikua mkubwa sana,akaingia chumba hadi chumba,alivyoingia chumba cha mwisho akamuona Frank Ntagara kapiga magoti, nyuma yake amesimama jambazi kashika bastola ili amuuwe,bila kuuliza akafyatua risasi hapohapo.


****

Kilichomshtua Ngesa zilikua ni njozi mbaya alizokua anaota,alikurupuka kama mtu aliyepigwa kofi lindoni na mkuu wake wa kazi,akachomoa bastola yake kwa kasi akitizama huku na kule,anahema juu juu.Butwaa alilopigwa halikua la kawaida baada ya kutizama mbele alipomlaza Rais Leslie,hakumuona!Ni kitu kilichomfanya achanganyikiwe na kuona kuna ugumu wa kazi mbeleni,hofu ya kwamba Rais Leslie ametekwa ilianza kujijenga ndani ya kichwa chake!Akasimama taratibu huku bastola yake ikiwa mkononi yupo makini,alichokifanya ni kutembea kwa mwendo wa kunyata mpaka alipomlaza,hapo akaona alama za viatu kwenye mchanga,akaamua kuzifuata taratibu mpaka zilipoingia kichakani.

“Mheshimiwa Rais”

Ngesa akaita baada ya kumuoa Rais Leslie,amekaa chini ya mti anatafakari tena ameshika tama.

“Hapa ni wapi?”

“Sijajua bado”

“Ngesa,nini kimetokea?”

Rais Leslie aliuliza swali,ilikua ni wazi kabisa akili yake haikutulia hata kidogo!Taswira ya ndege yake kulipuka ilimfanya aone kila kitu kilichotokea ni muujiza,akaamini kwamba isingekuwa Ngesa wenda kwa wakati huo angekuwa majivu na hata mwili wake usingejulikana ulipo.

“Bomu lilitegwa kwenye ndege yako”

“Na nani?”

“Inabidi tujue,bado sifahamu”

“Nataka kuzungumza na mke wangu”

“Hapana Mheshimiwa Rais,kwa sasa hivi ni hatari sana kuongea na mtu yoyote yule”

“Hata mke wangu?”

“Ndio,hata yeye! Tuondoke mahali hapa”

Ngesa na Rais Leslie walianza safari wakitembea kwa miguu bila kujua ni wapi walipo,walikatiza njia kwa njia pori kwa pori bila kuchoka,wingu angani lilikua zito hiyo iliashiria muda mfupi mvua ingeanza kunyesha!

Hazikupita dakika mbili,mvua kubwa ikaanza kushuka na radi kupiga hapo wakaanza kukimbia na kusimama kwenye nyumba moja iliyokua kuukuu,madirisha ya mbao!Mlango wa bati na ilikua imejengwa kwa matofali ya kuchoma,hapo Ngesa aliichunguza nyumba hiyo kwa umakini na kusukuma mlango,ambapo ulifunguka!Akaanza kufanya udadisi,baada ya kuingia ndani!Mvua ilichachamaa na kuzidi kunyesha na milio rangi kupiga.

“Tupumzike hapa,mpaka mvua iishe”

Ngesa akasema kwa sauti akijaribu kushindana na kelele za mvua zilizokua zinapiga bati kwa fujo,ndani ya nyumba hiyo Ngesa akaanza kufanya upekuzi na kugundua hakukua na mtu anaishi ama kama wapo basi walihama miezi mitatu kabla.Rais Leslie,alimuangalia Ngesa mara mbilimbili,akashindwa kumuelewa ni binadamu wa aina gani,kwa mabaya yote aliyomfanyia lakini bado aliweza kumuokoa katika kifo,hakutaka kuliweka jambo hilo kifuani akamsogelea karibu.

“Ngesa,naomba tusahau yaliyopita”

Rais Leslie,hakutaka kuomba msamahaa moja kwa moja!Akajifanya kuingizia methali ili asionekane kwamba amejishusha!

“Naomba nikuhaidi nikirudi Tanzania salama,sitokusahau”

Rais Leslie akaendelea,hapo akatoa mkono na kumpa Ngesa kama pongezi nzito na kubwa!Ni tukio lililomfanya Ngesa amuangalie Rais Leslie kwa makini na kugundua alimaanisha kutoka moyoni lakini hata hivyo hakutaka kumuamini moja kwa moja kwani alizifahamu tabia za Rais huyu Leslie kigeugeu,si ajabu baada ya kurudi Tanzania akatoa amri Ngesa afungwe gerezani,ndiyo maana hakuitikia alichokifanya ni kutingisha kichwa kumaanisha kua amekubali.

Katika hali ya kushangaza Ngesa,akawa makini sana kuna kitu alikiona dirishani kisichokua cha kawaida,ghafla kikapotea!Akatizama kwa makini dirisha la pili,akawa ana uhakika na fikra zake!Nje kulikua na kivuli cha mtu,mrefu kwenda hewani na isingekua msaada wa mbalamwezi ama mwanga wa radi uliomulika,asingeweza kuona kivuli hiko!Alichokifanya ni taratibu kumsogeza Rais Leslie kando,nayeye kutembea mpaka nyuma ya mlango!Ambapo,aliona mlango unafunguliwa bastola imetangulia mbele,akajua tayari kasheshe nyingine imeanza!Ngesa hakutaka kumkawiza,akamvuta na kumpiga kiwiko cha mbavu na kifuti cha shingo,bastola yake ikadondoka kando!

Ngesa akarusha teke lakini jitu hilo lililovaa koti refu la mvua lilikua makini,akawa ameshtukia hila ya Ngesa kwani alirudi nyuma teke likapita hewani na kuchana upepo,akarusha mateke mawili ya dabodabo moja likamfikia Ngesa shingoni na jingine usawa wa sikio,akapepesuka kabla ya kutulia akapigwa ngumi kavu ya taya maumivu aliyohisi yalikua ni kama mtu aliyetoka kung’oa jino!Ngesa,akawa amepagawa tayari, akaelewa hatari yake na katika kupepesuka akaona ngumi ya mtu huyo aliyevaa koti la mvua inakuja usawa wa usoni,akainama kidogo na kumchapa ngumi tatu za haraka mbavuni,jambazi huyo akaguna kuashiria ngumi zimemuingia.Hata hivyo ilionekana mpambanaji huyo,alikua mtaalam na mzoefu katika michezo hiyo,sababu alikanyaga pembe ya meza na kujibetua kama ngedere.Ngesa akashindwa kulizuia pigo hilo la Shaulin,akadondoka chini mzima mzima chali, hapohapo jamaa huyo akasogea na kumkanyaga kifuani na buti lake kubwa la ngozi,lililojaa matope!




Mwanga mkali ulimpiga machoni,ukapelekea mpaka kushindwa kuona sura ya mtu aliyemkanyaga kifuani.Maumivu makali aliyahisi kwenye kifua chake pamoja na shingoni kwenye mshipa wa nyuma,kutokana na kuchoka sana pamoja na njaa aliyokua nayo aliamini asingeweza kufanya purukushani yoyote ile,akili yake ikarudi kazini kwa mara nyingine baada ya kukumbuka yupo na Rais Leslie na alitakiwa kurudi naye nchini Tanzania salama salmin.

“Ngesaaaa!”

Sauti hiyo nzito ya kukwaruza ilimshtua,mwanaume aliyemkanyaga na buti na ndiye aliyeita jina lake ingawa hakua mwenye uhakika kama ndiye yeye ama mtu mwingine,jambo hilo likamfanya akae kimya.

“Derrick Ngesa”

Sasa akawa ana uhakika baada ya jamaa huyo kuinama kidogo na kumpa mkono,kuashiria kwamba ainuke!Sura ya mwanaume huyo haikua ngeni kwake ingawa hakukumba walikutana wapi,jambo hilo lilimfanya atulize akilli yake.

“Derrick mimi ni Rudolf Kuboko,umenisahau?”

Baada ya utambulisho huo Ngesa akatulia,akaonekana kama mtu anayetafakari kitu,akaachia tabasamu na kumpa mkono Rudolf Kuboko!

“Rudooolf”

“Deriiiick”

Kwa furaha wakakumbatiana na kupigana migongoni,Ngesa akakumbuka vitu vingi sana kipindi yupo na Rudolf wanasoma kozi moja nchini Cuba,hata hivyo yeye aliwahi kumaliza na kumuacha Rudolf nchini humo kumalizia mafunzo ya ukomandoo.Ki ukweli,ulikua ni muujiza ambao haukuwa na mfano wake,kitu cha kwanza alichotaka kufahamu ni kitu gani kilimfanya Rudolf awe mahali hapo.

“Nipo kwenye operesheni maalum,by the way mimi sio mtanzania tena nilipata uraia wa kule baada ya kuoa!”

“Kumbe ulipata mwanamke kulekule?”

“Kwakua nilimtia tu mimba,vinginevyo!Nisingemuoa,kuna mambo ya kiusalama yalinifanya nije hapa nchini Uganda”

Hapo ndipo Ngesa akajua kwamba yupo nchini Uganda,hata hivyo hakutaka kushtuka sana na kufunguka kila kitu kilichotokea,katika maisha yake hakumuamini mtu yoyote yule hapohapo akatunga uwongo ili operesheni yake ikamilike na Rudolf alivyomuona Rais Leslie,akashtuka mno.

“Poleni sana”

“Ndiyo hivyo,ilibidi tutoroke!Rudolf sina muda mwingi wa kupoteza,nahitaji kurudi Tanzania kuna kazi natakiwa kuimaliza”

Kwa Rudolf haikuwa tatizo sana,alionesha furaha ya waziwazi na wote wakaanza kutoka kwenye kijumba hiko na kuingia katikati ya mashamba ya migomba,ambapo huko walivuka mto unaopitisha maji na kutokea upande wa pili,mbele yao kulikua na kijumba kingine kidogo hapo wakaingia na kukuta kuna moto katikati,pembeni kuna mawe matatu na juu kuna nyama iliyochomekwa kwenye chuma chembamba,hawakukaa sana akaingia mwanaume mwengine mweusi mrefu kwenda hewani,begani kavaa mtutu!

Wakasalimiana kwa lugha ambazo sio Rais Leslie wala Ngesa kuhifahamu lakini Ngesa alisikia jina ‘Tanzania’ jamaa huyo akaangalia na kuwasabahai.

“Jambo,mimi siongei sana Swahili lakini najua mudogomudogo!Jinya yangu ni Mugisha”

Mugisha alivyotambulisha kwa Kiswahili kibovu!Wote wakakaa chini na kugeuza nyama!Rais Leslie alishangazwa sana na mazingira hayo,hata siku moja hakuwahi kuwaza kama angekuja kula nyama kwenye eneo kama hilo kwani alizoea pembeni yupo na walinzi huku mkononi akiwa na uma na kijiko,hiyo ilikua tofauti mbali na hapo hakuongea kitu chochote mpaka walipomaliza kula nyama hiyo ya digidigi,sasa tumbo la Ngesa angalau likawa shwari.

“Rudolf,nahitaji kurudi Tanzania”

Ngesa akavunja ukimya.

“Usijali Derrick”

Rudolf hakutaka kuzungumza maneno mengi,alichokifanya ni kuwatoa nje upande wa nyuma,ambapo kulikua na Helkopta .

“Nitawapeleka”

Ngesa hakutaka kuamini kua mambo yangeenda kua mepesi namna hiyo,hakuacha kumshukuru Rudolf kwa moyo wake wa kipekee,akamuahidi ipo siku wangekaa na kuongea mengi!Kabla ya kuondoka wakamuaga Mugisha,mwanaume mkakamavu ambaye muda wote alikua siriazi na mdadisi.Wote,wakaingia ndani ya Helkopta.

“Mheshimiwa Rais”

Ngesa akaita na kumuangalia.

“Derrick,nakusikiliza”

“Naomba mtu yoyote asijue,nilipo”

“Una maana gani Ngesa?”

Hapo Ngesa hakutaka kujibu chochote,akaingia ndani ya Helkopta na kufunga mlango,Helkopta ikawashwa na kuanza kuchanganya taratibu.

“Tuku tuku tuku tuku tuku”

Mlio wa Helkopta huku mapangaboi yakizunguka kwa kasi,yalifanya ianze kunyanyuka taratibu kuelekea juu angani,chini walimuacha Mugisha anaangalia usalama wa eneo hilo!Ulikua ni usiku wa saa saba na kila mtu alivaa mtambo maalum masikioni wakafanana kama ma ‘dj’ ilikua ni kwa ajili ya mawasiliano.

“Ngesa,tukifika Tanzania salama nitakupa cheo kikubwa sana Serikalini”

Rais Leslie akavunja ukimya,Ngesa akamtizama bila kumjibu chochote ilielekea kuna kitu kichwani alikua akikifikiria.

“Nasikitika kukwambia kwamba hatutoongozana wote Mheshimiwa Rais”

“Kwanini?”

“Inabidi nimalize nilichokianza”

“Nakuomba twende wote ikulu”

“Mheshimiwa Rais,bado vita haijaisha mpaka niimalize”

Ngesa hakutaka kuongeza neno lolote zaidi ya kuangalia chini ambapo aliona taa za nyumba,hapo ndipo akagundua helkopta haikua umbali wa juu sana.

“Tupo wapi Rudolf?”

Ngesa akauliza!

“Tunakaribia bahari ya Hindi,niwashushe wapi?”

“Rais Leslie,utampeleka Ikulu”

“Nawewe je?”

“Popote pale”

Walikua wakiongea kwa sauti ya juu kiasi wakishindana na kelele za radi na mvua,helkopta ilizidi kukata mawingu na Rudolf alikua makini kuiongoza.

“Mheshimiwa Rais,nakuomba tena usiwaambie chochote kuhusu mimi nawewe”

Alichokifanya Ngesa ni kuanza kuvua kifaa maalum cha mawasiliano kuashiria kwamba anakaribia kufika safari yake,akamtizama Rais kwa mara nyingine tena na kumpa mkono wa kumuaga,akimsisitiza kua asiseme kitu chochote kile!

“Tunakaribia Ikulu Ngesa”

Rudolf akasema huku akizungusha kitu kilichofanana na rungu hapo helkopta ikahama uelekeo na taratibu kuanza kushuka chini karibu na bahari ya Hindi,pembezoni kidogo mwa nchi kavu.

“Rudolf ahsante sana,mfikishe Raisi Leslie salama!Mimi nawewe tutaonana”

Upepo ukawa mkali sana baada ya Ngesa kufungua mlango,akakanyaga machuma ya helkopta na kutizama chini ambapo alionekana kupepesuka kutokana na upepo mkali,kumpuliza!Bila kupoteza muda,akabana mikono yake na kujiachia ambapo baada ya sekunde ishirini,akawa ametumbukia kwenye bahari!Akaanza kupiga mbizi chini kwa chini,akiamini anakaribia kufika ufukweni, alivyoibuka nchi kavu akatizama Helkopta ambayo aliiona inatua,akashusha pumzi ndefu na kuanza kukimbia kuelekea upande wa Kivukoni kwani alishaelewa ni wapi alipo!


***

Kelele za Helkopta,ziliwa kurupua wana usalama pamoja na polisi waliokua makini kulinda Ikulu!Ulinzi uliokuwa hapo,haukuwahi kutokea hata kidogo.Kifo cha rais Leslie kiliibua hisia kali na kilipelekea vyombo vyote vya usalama kutolea macho jengo hilo na kulilinda huku wakifanya uchunguzi wa kina!Baadhi ya wafanyakazi waliwekwa chini ya ulinzi kwa uchunguzi zadi,wakihojiwa lakini helkopta ilivyotua askari kumi na saba waliizunguka wakiwa na mitutu yao mkononi tayari kwa kufyatua risasi kwani walielewa fika wamevamiwa na jeshi hatari la Brigedia Karanje,hivyo walijihami kwa kujipanga na kuizunguka!Mlango wa Helkopta ukafunguka,askari watano wakakoki bastola zao tayari kwa ambush.

“Mr.President”(Mheshimiwa Rais)

Mmoja wa wanausalama akaropoka,bado hakuamini mtu anayemuona mbele yake ni Rais Leslie,kila mtu alipigwa na butwaa hapo ndipo mlango wa rubani ukafunguliwa Rudolf akateremka lakini matokeo yake,aliwekwa chini ya ulinzi mitutu yote ilimgeukia yeye.

“Muonesheni heshima huyo kijana,shusheni silaha zenu chini nipo naye”

Hiyo ilikua ni amri kutoka kwa Rais Leslie,hakuna hata mmoja kati yao aliyepinga kitu hiko,wote wakashusha silaha zao chini na kumshangaa Rais Leslie!

“Rudolf,karibu ikulu”

Rais Leslie akasema!


****

Ingekua ni vigumu sana kwa Daphine kuondoka eneo hilo bila kujua watu hao wametumwa na nani,alielewa fika ulikua ni mtandao mkubwa sana tena kutoka serikalini hiyo ni baada ya kukagua maiti moja aliyoipiga risasi,kwa maana hiyo ukimya wa watu hao bila kurudisha ripoti ingekua ni lazima watumwe wengine wafatilie,ndiyo maana alibaki eneo hilo mpaka saa saba ya usiku na kuona gari aina ya Carina,limezima taa umbali wa mita ishirini!Wanaume wawili wakashuka.

“Shusheni vichwa vyenu chini”

Frank Ntagara pamoja na Olina Kalumuna,wakatii amri na kulaza vichwa vyao chini kwani wanaume hao walianza kutembea kuelekea upande wa gari lao lilipo,kupitia kioo cha ubavuni Daphine akawaona wanavyotoa bastola zao na kuweka viwambo vya kuzuia sauti isitoke!Akaendelea kuwa mdadisi,akatulia na kujivuta chini hapo,aliikamata bastola yake vizuri ili lolote litakalotokea aweze kujitetea.

“Una uhakika nyumba ndio ile?”

Sauti kavu kutokea nje,ilimuuliza mwenzake ilielekea ni kama watu ambao hawana uhakika.

“Ndio yenyewe,hua sibahatishi katika kazi zangu”

“Sasa kwanini asipokee simu?”

“Ndio tutajua”

Wanaume hao wawili,wakasonga mbele mpaka walipoifikia nyumba ya Olina,hapo walisita kidogo!Mmoja akaizunguka nyumba kwa uwani,mwingine akapitia kwa mbele!Sasa Daphine,akawa makini.

“Frank”

“Yes”

“Mimi nitaingia ndani,wewe utakua nje!Usimuue,tunawataka wakiwa hai”

“Kwanini?”

“Fanya nilichokwambia Frank”

Daphine,akateremka kutoka ndani ya gari huku bastola ikiwa mkononi nyuma akimuacha Olina Kalumuna anatetemeka kwa kiasi cha kutosha,sasa alishaelewa ni kwa jinsi gani anatafutwa ili auliwe.

Mwendo wa Daphine ulikua wa kunyata na alivyofika getini akageuka na kumtizama Frank Ntagara,ambaye kwa wakati huo alikua anateremka kutoka ndani ya gari,akamsubiri mpaka alivyoanza kuizunguka nyumba kisha yeye akasonga mbele!Milango yote ya fahamu ya Daphine ilikua makini kabisa kuanzia masikio mpaka macho,alivyoingia kupitia mlango wa nyuma akasita kidogo baada ya kusikia hatua za mtu upande wa korido,akatulia nyuma ya mlango!

“Haule….Haule….Haulee…”

Sauti hiyo ilisikika ikimuita mwenzake,kwa utaalamu wa Daphine alijua fika sauti hiyo imeambatana na uwoga ndani yake,alivyohisi kuna ukimya akachomoka na kuanza kuifuata kwa nyuma!Ingawa kulikua na giza lakini Daphine aliweza kuona kivuli cha mwanaume huyo mrefu kiasi,mkononi ana bastola!

“Tupa bastola chini,sitorudia tena”

Ilikua ni sauti ya Daphine ikiwa mbali na mzaha,amemuwekea jamaa huyo bastola kisogoni.

“Tupa bastola chini. Moja……”

Bila upinzani,akatupa bastola chini na kuamriwa asonge mbele ambapo huko waliingia ndani ya chumba,kilichokua na maiti iliyoning’inizwa juu yaani mume wa Olina na nyingine chini,jamaa huyo alivyomuona mwenzake yupo chini amekufa,akameza mate kwa uwoga!

“Kaa hapo”

Daphine,akatembea mpaka dirishani kwa tahadhari,alivyofungua pazia akamuona Frank Ntagara ameshika bastola na jambazi yupo chini anavuja damu,alivyoangalia vizuri akamuona ana jeraha la kisu mguuni.

“Good,mlete huku”Daphine akasema!

Ubabe ukatumika jambazi huyo akaamrishwa asimame,akatii amri na kuanza kuchechemea!Alichotaka kujua Daphine ni nani aliwaagiza bomu litegwe na angemfahamu mtu huyo,ndipo angejua ni wapi Brigedia Karanje alipo.

“Unafanya nini hapa Tobias?”

Daphine akauliza,kwa jazba na hasira baada ya kugundua jina la jamaa huyo anaitwa Tobias Machau.

“Mimi nimetumwa tu yaani nimetumwa tuu”

“Na nani?”

“Na na na simjui,nilipigiwa simu nije huku”

“Kufanya nini?”

“Kumuangalia Haule,kama kamaliza kazi”

“Kazi gani?”

“Hata sielewi kazi gani”

Kupitia macho yake, Daphine alijifunza kitu kwamba hakuna ukweli ndani yake hata kidogo na katika kutafakari kabla ya kuchukua maamuzi,Frank Ntagara akawa ameingia na jamaa mwingine aliyechomwa kisu cha mguu,akiwa anachechemea.

Alichokifanya Daphine,bila kupoteza muda akachomoa kisu kilichokua kiunoni kwake,akamsogelea na kumchoma nacho shingoni, damu zikaruka nyingi mno!Mpini wa kisu ukawa upande wa kushoto huku ncha ya kisu ikiwa imetokea upande wa pili wa shingo,ilikua ni picha mbaya iliyomtisha mpaka Frank Ntagara,ambapo alishuhudia jamaa huyo akitapatapa.

“Arhgsss aaarrrrrhhh”

Ilikua ni sauti mithili ya kondoo aliyechinjwa huku akiwa ameshika shingo,anakukuruka chini na kutupatupa miguu,damu nyingi zikatapakaa eneo hilo dakika mbili baadaye,akawa ametulia ametumbua macho mithili ya mjuzi aliyebanwa na mlango, ulimi kaubana na meno,tayari alikua amekufa!Hapohapo Daphine akamgeukia,Tobias Machau aliyekua anatokwa na jasho mwili mzima baada ya kushuhudia tukio hilo la kinyama.

“Bado hujui?”

Daphine,akauliza huku akimsogelea kwa karibu zaidi,mikono yake imelowana damu.

“Na..na..na…najua kila kitu,nakutajia mkuu usiniue”

Tobias Machau,hakua na sababu ya kubaki kimya kifo cha mwenzake kilimtisha na hilo ndilo lilikua kusudi la Daphine,kumuonya Frank Ntagara asimuuwe mtu yoyote kwanza!Hesabu zake,zikawa tayari zimefanikwa.



*****

Ngesa alifanikiwa kuibukia katika kivuko cha feli,akiwa amelowa chapachapa na maji!Amechoka hoi bin taaban,giza lilikua totoro na mvua ilikua inaishia kwani kulikua na manyunyu tu!Pilika za watu hazikua nyingi,zaidi tu wavuvi wachache walioshika matenga ya samaki.Hilo halikumpa shida kwani alielewa alipo kusingekua na mtu yoyote ambaye angemuwekea mashaka kwani kila mtu alikua na hamsini zake,taratibu akatembea na kukutana na makutano ya barabara,hapo alivuka upande wa pili na kusimama nje ya duka kubwa la Sonara,akitafakari ni wapi aende!Alitulia kwa muda mfupi na kupata wazo baada ya kumkumbuka Khalfan Sigwa anaishi mitaa ya Kariakoo na aliamini kuna jambo angeweza kumsaidia lakini moyo wake ghafla ulikosa utulivu baada ya kuona askari wawili wapo karibu yake, tena wanamfuata alipo,alichokifanya kabla mambo hayajaharibika ni kuanza kutembea huku kichwa chake kikiwa chini,aliogopa kugundulika mapema kwani operesheni ingefeli katika hatua za awali,aliamini kabisa ni jinsi gani alivyokua maarufu sababu ya picha zake kubandikwa mara kwa mara,Ngesa alitishia jiji na hakuna mtu asiyelifahamu hilo kwani kuna kipindi alisakwa Tanzania nzima, ndiyo maana jina lake lilikua midomoni mwa watu akawa maarufu.Alivyopiga hatua tano,akaingia mtaa wa tatu,ambapo kulikua na kichochoro chembamba alifanya hivyo kusikilizia kama askari aliwaacha ama bado wanamfuatilia,alivyoona kimya akanyoosha kuifuata barabara ya Ohio,ambapo alitokea mtaa wa Samora,mkabala na sanamu la askari aliyeshika mtutu!

Sehemu aliyopo mpaka Kariakoo,aliamini isingemchukua muda mrefu kwani alitembea kwa haraka na kutokezea Mnazi mmoja!Sasa kukawa tayari kumepambazuka,hilo lingekua hatari sababu aliamini angeonekana!Alijitahidi kuamba ambaa pembezoni mwa nyumba na kutumia vichochoro visivyo rasmi mpaka akatokea mtaa wa Muheza,huo aliachana nao alichotaka yeye apitie mtaa wa Mafia kisha baadaye Masasi,hilo lilifanyika bila kushtukiwa na mtu yoyote yule.Akasimama nje ya benki moja na kuhisi wenda amepotea sababu tu ya mazingira ya eneo hilo,akatizama huku na kule. Kilichomfanya atabasamu ni baada ya kuona gorofa la rangi ya kijivu,hilo ndilo lilikua alama yake akajua kabisa kando ndimo Khalfan Sigwa anaishi,akaanza kutembea na alivyofika eneo hilo,akawavuka wazee waliokua wanacheza bao,moja kwa moja mpaka kwenye mlango wa kwanza kushoto.

“Ngo! Ngoo! Ngooo!”

Ngesa akagonga na kupisha utulivu,alikua makini sana kukagua huku na kule na hakua ana uhakika kama bastola yake ina risasi ni kitu alichoanza kujilaumu kwa kutoikagua, ingekuaje kama ingetokea purukushani yoyote ile!Kwake kuwa na bastola ambayo haina risasi ilikua ni sawa na nyoka wa kibisa,hang’ati.

“Ngo! Ngoo!Ngooo!”

Akagonga tena kwa mara nyingine,aliamini fika kwamba ni lazima atakua amelala kwani ilikua ni asubuhi,katika kusikiliza akasikia hatua za mtu anakuja kisha kitasa kikalia,mlango ukafunguka!Mbele yake,alisimama mwanamke mrembo akiwa kwenye vazi la kanga,anafikicha macho ilionekana kabisa alitoka usingizini.

“Samahani,namuulizia Khalfan”

Ngesa,akauliza bila kutoa salamu.

“Khalfan, gani?”

Mwanamke huyu akauliza huku akimtizama Ngesa kuanzia juu mpaka chini kwa madoido, Ngesa akatamani kumzaba kibao kwani hakua na muda wa kupoteza hata hivyo alivuta subira.

“Khalfan Sengwa”

“Khalfani Sengwa,ni mme wangu una shida naye gani?”

“Ni rafiki yangu sana,nina mazungumzo naye”

“Unaweza ukaniambia hapahapa,amepumzika hua hapendi usumbufu!Kwahiyo unaweza ukasema ama urudi baadaye”

“Tafadhali,nahitaji kumuona ni muhimu”

“Bwana eeh,nishakwambia. Njoo baadae”

Mwanamke huyo,ambaye mdomo wake ulikua mkubwa na mwingi wa maneno akaropoka kwa sauti na kumfanya Ngesa achukie kwa kiasi cha kutosha,isingekua heshima ya Khalfan Sengwa wenda angeshapigwa kichwa cha pua muda mrefu.Zaidi na hilo,hakujali baada ya kuongea hayo akarudishia mlango kwa niya ya kuufunga lakini kabla haujafika mwisho,Ngesa akaingiza mkono ndani kwa niya ya kuuzuia,akasukuma kwa nguvu na kuingia ndani.

“Wee mze….”

Hapohapo Ngesa akachomoa bastola,ilikua ni lazima afanye hivyo ili kuepusha kelele na mwisho wa siku alijua ni lazima angejaziwa watu.

“Nyamaza,usiongee!Funga mlango,namuhitaji Mumeo”

Hapo ikabidi mwanamke huyo anyamaze,alitetemeka na kufunga mlango ambapo walipitiliza mpaka chumbani,Ngesa akasubiri nje.

“Khalfan,mimi Derick Ngesa”

Ngesa akasema kwa sauti ya chini kidogo aliyoamini kua aliyekua chumbani ni lazima asikie.Ukimya,ukawa umetawala akasikia sauti ya mwanamke aliyemfungulia mlango akisema ‘kuna jambazi’lakini Khalfan hakutaka kubaki chumbani,alichokifanya ni kusimama na kujitokeza baada ya kusikia kua ni Ngesa.

“Derrick Ngesa,Laa haulaaa!”

Mshtuko wa Khalfan Sengwa,ulikua wa aina yake ikapelekea mpaka kuacha kinywa wazi.Mwanaume aliyesimama mbele yake,alimshtua kwa kiasi cha kutosha!

“Ni siku nyingi sana,ndio maana unashangaa”

“Pole kwa matatizo Ngesa”

“Nishapoa”

“Karibu nyumbani,ulipakumbuka vipi hapa?”

“Naachaje kusahau eneo hili Khalfan”

“Karibu sana,karibu kiti”

Ngesa na Khalfan walikaa seblen na maongezi yao yalianza rasmi dakika hiyo hiyo,shida ya Ngesa ilikua ni moja tu.Kutaka kujua ni nani aliyekua zamu,siku ambayo bomu lilitegwa kwenye ndege ya Rais Leslie!Aliamini kabisa,Khalfan angemsaidia kwani kwenye mambo ya IT alikua ni mtundu kwa kiasi cha kutosha.

“Ngesa naogopa,unataka kuniingiza kwenye matatizo unajua,unataka nifungwe tena?”

“Naelewa lakini lazima tufanye hivi,ni muhimu sana nisaidie”

“Mpaka niwe na laptop yangu, ni hack system zao”

“Iko wapi?”

“Iko pale mezani,sidhani kama nitakua na wale wadudu wa virus”

“Kwanini unasema hivyo?”

“Lazima nisend kwenye system yao,ndio nitaweza kuingia kiurahisi”

“Fanya hivyo,itachukua muda gani?”

“Kama mtandao upo vizuri nusu saa litanitosha”

Khalfan,kijana mjanja na makini ambaye pia aliajiriwa katika kampuni tatu katika maswala ya IT aliingia mitamboni,Ngesa akiwa nyuma yake macho ameyakodoa juu ya kompyuta haelewi chochote lakini alikua makini katika kila hatua.

“Ngo! Ngoo! Ngoo! Ngooo!”

Mlio wa mlango kugongwa uliwashtua wote wakageuka nyuma,kuutizama!

“Naniiii?”

Khalafn akauliza kwa sauti kubwa.

“Fungua mlango”

Sauti ya kibabe,kutokea nje ilimfanya Ngesa atulie kidogo na kumshika Khalfan mkono asisimame kwanza,alichokifanya ni kunyata mpaka nyuma ya kabati na kujificha!Khalfan akasimama na kufungua mlango,alichokiona kilimshtua na kumfanya apigwe na bumbuazi.

“Tunaomba kusachi nyumba yako”

Askari mmoja mrefu,mwenye mwili mkubwa na kitambi akapiga mkwara kwa kujiamini.

“Mna kibali cha kusachi?”

Khalfan akavimba,alizijua sheria zote kwamba polisi haruhusiwi kusachi mpaka awe na kibali maalum.

“Pisha mlangoni,acha maswali”

“Tumepigiwa simu kuna jambazi ameingia humu,huyo Mama aliyepiga simu yuko wapi?”

Askari mwingine,akadakia huyu alikua mfupi na alionekana ana kiherehere kuliko wengine saba walioingia ndani.

“Labda sio nyumba hii”Khalfan akasema.

“Sisi sio wapumbavu,tulia kama unaogeshwa”

Mke wa Khalfan ndiye alipiga simu polisi,kitendo cha kuoneshwa bastola kilimuogopesha kwa kiasi cha kutosha ndiyo maana akapiga simu kituo cha polisi, Msimbazi.

“Khalfan,ongea ukweli Mume wangu.Yule uliyekua naye seblen yuko wapi?”

Ngesa aliyasikia malumbano hayo akiwa nyuma ya kabati na kupitia kwenye uwazi mdogo, aliweza kuwaona askari wote,waliosimama na kuanzia hapo walianza kupekenyua nyumba nzima chumba baada ya chumba,wengine wakabinua mpaka viti.

“Mwenzako,yuko wapi?La sivyo,tunaondoka nawewe”

Hakukua na utani,ilikua ni lazima waondoke na Khalfan kama wasingempata mtuhumiwa wao,walichokifanya askari hao ni kumuweka chini ya ulinzi.Ngesa alishuhudia hayo yote na asingekua muungwana kama angeacha hilo litokee kwanza angeumia kwa mambo mawili,la kwanza asingeweza kupata taarifa anazozitaka sababu ni lazima wangeondoka na Khalfan kingine angejiona ni mwenye dhambi kama wangemchukua kwani yeye ndiye angekua chanzo!

Alichokifanya ni kujivuta kwa nguvu na kusukuma kabati!Polisi wanne waliokua nyuma,wakafunikwa nalo!Kwa kasi Ngesa akapanda juu na kuruka teke lililomfikia askari mwingine,wa kando alivyotaka kutoa kirungu akavutwa na kupigwa kifuti cha kifua,akazungushwa na kutandikwa pigo moja la shingo,puu chini.Sasa askari watano wakawa makini,ndani kuligeuka na kua na purukushani za kufa mtu,mmoja wa askari akarusha kirungu Ngesa akainama kikamfikia polisi mwingine kichwani,akabweka kama mbwa!Hapo hapo Ngesa,akazungusha teke aina ya ‘Round kick’ teke la shingo askari aliyekua upande wa kabati,likamtupa kwenye meza ya chakula,akabaki anaugulia.

Ki ukweli,mapigano hayo yalimshangaza mke wa Khalfan,hakutaka kuamini kama mtu mmoja angeweza kupambana na askari kwani vitu kama hivyo alizoea kuviona kwenye sinema za ‘Rambo’Kivumbi,kilitimka ndani.Vitu vilivunjika vunjika na katika kosa alilofanya Ngesa ni kuikwepa ngumi ya askari mmoja bila kuangalia vizuri ambapo nyuma,alipigwa kirungu cha mgongo,maumivu aliyohisi hayakua na mfano wake!Alivyotaka kujiweka sawa,akapigwa kirungu kingine cha mbavu,hakika yalikua ni maumivu makali mno na aliona dalili zote za kuzidiwa nguvu na askari hawa waliokua wanamshambulia kama mpira wa kona!

Nyuma yake,kulika na meza ndogo,akaishika vizuri na kumrushia mmoja wapo ikampiga ya kifua,alivyoona kirungu kinakuja upande wa kulia akarudi nyuma kikapita na kumpunyua puani,kwa hasira akakunja ngumi na kuituma,moja tu ya pua haikufanya makosa ilimpasua askari na kumfanya avuje damu nyingi sana.

Sasa akawa amebaki polisi mmoja mrefu kwenda hewani,huyu hakumkawiza ngumi tatu za mbavu na pigo moja la kareti lilimfanya aone nyota,akampiga ngumi moja ya shingo, hiyo ilikua funga kazi akaamini kabisa askari huyo akiinuka basi yeye kidume.

Sasa askari wote walikua chini,kila mtu anaugulia maumivu yake!Katika hali ya kushangaza,akapigwa na kitu kizito kwenye utosi akahisi kizunguzungu kikali sana alivyotaka kupiga hatua,akashindwa mbele akaona giza nene,hapohapo Ngesa akadondoka kama mzigo puu!Na kupoteza fahamu,ni tukio lililomfanya Khalfan akasirike kwani mkewe ndiye aliyeshika chuma na kumpiga nacho Ngesa kichwani.

“Ndio umefanya nini sasa wee mwanamke?”

Khalfan akauliza kwa hasira huku akimuangalia Ngesa aliyekuwa chini,kazirai.




*****

Siku zote jogoo hafi kwa utitiri,nusu saa baadaye Ngesa alirudiwa na fahamu lakini hakutaka kufumbua macho isipokuwa ni milango yake mingine ya fahamu ilikua makini,masikio yake aliyatega vizuri ili asikie kwanza kuna sauti ngapi,hata hivyo hisia zake pia zilikua kazini alichohisi ni yupo mahali fulani chini amelazwa,alichoshukuru hakufungwa mikono wala miguu!Ukimya wa sehemu hiyo ulimfanya aingiwe na mashaka makubwa sana,hiyo ikampelekea mpaka afumbue jicho moja kwanza ili ajue ni wapi alipo.Alichokiona kilimshangaza sana,vitu kama masufuria na mabakuli pamoja na ndoo za maji vilimfanya agundue kua yupo stoo ya jikoni,akatega sikio vizuri akiendelea kuusikilizia ukimya uliotawala ndani ya stoo hiyo.

Kwa tahadhari kubwa baada ya kumbukumbu kurudi,zilimwambia wenda maaskari bado wapo ndani ya nyumba hiyo na uhakika huo alikua nao asilimia mia moja sababu muda mfupi uliopita aliwatembezea mkong’oto wa kufa mtu,hio ilimaanisha ni lazima wangeita wenzao na mambo yangekua makubwa,baada ya kusimama alitembea kwa kunyata mpaka kwenye mlango ambapo alichungulia kupitia kitundu cha funguo!Moyo wake ukapiga mkambo baada ya kumuona Khalfan,amefungwa pingu na mbele yake kuna askari watatu!Ni kitu ambacho alikitarajia kabisa ndiyo maana akaanza kujihami,alivyojigusa kiunoni akazidi kupoteza utulivu,bastola yake haikuwepo alivyoangalia pembezoni,hakukua na kitu chochote ambacho angeweza kukitumia kama silaha ya kujihami.

“Wamefika wapi?Waambie wafanye upesi,ndio yupo chini ya ulinzi mkali…Hawezi kutoka,tumemfungia stoo”

Sauti ya Kamanda,kutoka nje ilisikika akizungumza simuni!Alivyofungua kitasa ili kuhakikisha maneno anayozumgumza Kamanda huyo wa polisi, akakuta ni kweli kwani mlango ulifungwa kwa funguo na asingeweza kutoka na kuendelea kubaki ndani ya chumba hiko ilimaanisha kukamatwa kama kuku bandani na alielewa nini maana yake,hakutaka operesheni yake ifeli wakati ndio kwanza ilikua inaanza,baada ya kuangalia juu akapata wazo kabambe,silingi bodi kwa pembeni lilikua wazi na alivyoona jiko bila kujiuliza akalikanyaga na kuingiza mikono kwa juu,hapo alijivuta na kufika juu ambapo huko alikumbana na nyaya kadhaa za umeme,ilibidi awe makini sababu alielewa silingibodi zilivyokua nyepesi isitoshe baadhi ya kenchi zilianza kuliwa na mchwa.

Hakutaka kupitia juu ya silingibodi akawa anatambaa na kingo za ukuta mpaka alivyohisi amefika upande wa seblen,akiwa juu sasa aliweza kuona wote waliokua chini akiwepo mke wa Khalfan ambaye alikua amesimama pembeni anatoa unoko.Huyo ndiye alikua mwenye hasira naye kwani ndiye aliyefanya yote yakatokea!Kushoto alisimama polisi mmoja,mwenye kitambi kashika kirungu anachukua maelezo ya Khalfan kwenye mlango alikaa mwingine huyu haikueleweka kazi yake ni kitu gani, lakini kwa haraka haraka alikua akilinda usalama wa mlangoni!Alichokifanya Ngesa ni kupapasa silingibodi vizuri ili aridhike na uimara wake,kuna kitu alitaka kukifanya na hakutaka kupoteza muda kwenye hilo sababu alisikia simu kua kuna askari wengine wanakuja.Usawa wa chini,sasa alisimama Kamanda aliyemuweka Khalfan chini ya ulinzi,kwa hesabu zake huyo ndiye alitakiwa kuwa wa kwanza!Alichokifanya Ngesa ni kutumia nguvu nyingi akajikita kwenye silingibodi,ilikua ni kama ametabiri kwani Silingbodi halikua na nguvu kabisa,akashuka nalo zimazima na kumdondokea askari kichwani puuu!Kilikua ni kishindo kikubwa na picha ya kutisha kwa wakati mmoja, askari wawili waligongana vikumbo,kwa kuhofia wenda ni mzimu.

Hiyo ikamfanya Ngesa apate mwanya wa kuwachakaza,mmoja aliyekuja na kirungu,akataka kumpiga nacho Ngesa kichwani!Kikapita hewani na kuchana upepo,kifuti kimoja cha mbavu na teke aina ya ‘flying kick’ akatupwa mbali,mmoja akarusha ngumi Ngesa akainama kidogo na kumvuta kwake,huyo hakumchelewesha kwa utaalam wa hali ya juu,akauweka mkono huo begani na kuuvunja ukatoa sauti kama muwa ukivunjwa,kelele za maumivu alizopiga askari huyo zilinyamazishwa na kipepsi cha shingo,akatulia na kukakamaa hakuweza kutoa tena sauti.Ngesa,akamtizama mke wa Khalfan,akamvuta karibu na kumtwanga kichwa kizito cha pua,hakujali kama ni mwanamke, dozi hiyo kali ilimfanya mwanamke huyo adondoke chini na kupoteza fahamu hapohapo!

“Khalfan,beba laptop tuondoke”

Ngesa akasema kwani hali,ilishakua mbaya akachukua funguo za pingu na kumfungua.

“Na mke wangu?”

Lilikua ni swali lililomfanya Ngesa amgeukie Khalfan na kumkata jicho baya la hasira,jambo hilo likamfanya Khalfan ajishtukie bila kuambiwa chochote akabeba laptop wote wakaanza kutoka nje,kwa kupitia mlango wa uwani wakafanikiwa kutokea kwenye kichochoro chembamba,ambapo huko waliona magari matatu!Ngesa hakutaka kupoteza muda,akaokota chuma kilichokua chini na kuvunja kioo cha gari,akazama ndani na kubomoa swichi ya funguo,hapo alitoa nyaya mbili na kuzigusisha,gari ikawaka!

“Tuondoke”

Khalfan,akaingia ndani ya gari na safari ikaanza hapohapo!Walivyokunja kona tu,wakapishana na difenda mbili za polisi hapo waliamini kabisa,wangechelewa kidogo tu!Wangekutwa.Safari yao ilikomea,Buguruni kwa mnyamani,wakaegesha gari kando ya ‘bar’ moja ambayo,haikua na watu wengi sana.

“Tuendelee”

Ngesa akasema,jambo lililomfanya Khalfan afungue laptop yake na kuanza kufanya kazi aliyoambiwa,dakika arobaini na tano zilikua nyingi Khalfan alikua kwenye ‘system’ ya idara nzima ya uwanja wa ndege,akadukua mitandao yao na kuona kila kitu kinachoendelea.

“Ilikua lini umesema?”

“Wiki iliyopita,Jumatano”

“Okay okay okay, hapaa hapaa haapaaa alikua zamu ni Olina Kalumuna!Huyu hapa”

Picha ya Olina Kalumuna ikajaa kwenye kioo cha Laptop,Ngesa akamtizama binti huyo mdogo kwa umakini na kumkariri vizuri.

“Anaishi wapi?”

“Sijajua”

“Pitia Cv yake,lazima utapata data nyingine”

Khalfan akaingia tena mitamboni,kijana huyo aliijua kompyuta kama aliitengeneza yeye na baada ya muda mfupi,akawa tayari amepata majibu ya kila kitu kuanzia anapoishi Olina mpaka muda anaotoka kazini,kwa Ngesa aliamini kupitia msichana huyo angeweza kupata majibu ya maswali yake!

“Samahani,nimekuingiza kwenye matatizo makubwa.Usirudi nyumbani,kwa sasa hivi sio salama kwako watakuua,ahsante sana Khalfan”

Ngesa alishukuru kwa kila kitu na kuagana na Khaflan,akimwambia ukweli halisi na hatari yote ilivyo,baada ya hapo akapiga gia na kulitoa gari kwa kasi sababu kila muda kwake ulikua ni mali.


****

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG