Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

SIN SEASON 1 SEHEMU YA 10 MWISHO

  


SIN SEASON 1

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 10 KATI YA 10


“Baby”

“Stop calling me baby. Me and you it’s OVER”

“Hapana hapa mke wangu usinifanyie hivyo?”

“No mimi sio mke wako. Hujanivisha pete, huja jitambulisha kwetu na wala hakuna hata ndugu yangu mmoja anaye kufahamu wewe. Kitu kimoja ambacho nina hitaji kukusaidia tu, baki na hiyo sura yako ya bandia. Kapande ndege na urudi Afrika kusini leo. La sivyo nita fichua siri yako na mipango yako yote ya kumuua nabii Sanga na uta ona kama huto ozea gerezani”

Tomas taratibu akanyanyuka huku akimtazama Magreth kwa macho ya hasira sana.

“Magreth uta lipa kwa hili”

“Naamini wewe leo ndio una jua faida ya kulipa. Ulipanga kuniua wewe na mrs Sanga, so haya ndio malipo yake.”

Tomas akamfwata kwa hasira Magreth sehemu alipo simama. Akamkaba koo lake kwa hasira sana.

“Nakuua malaya wewe una niharibia maisha yangu.”

Magreth kwa kasi ya ajabua akaitoa mikono ya Tomas shingoni mwake, akapiga kigoti cha tumboni na kumfanya Tomas kujikunja kwa maumivu.

“Huwezi kuniua Tomas, kumbuka uliyajeruhi maisha yangu kwa kushindwa kufunga kwako mdomo mtoto wa kiume. Sasa leo hii yame rudi kwako.”

“Tomas sihitaji fujo ndani ya nyumba yangu. Umeshindwa kufanya nilicho kuambia ufanye acha nifanye mimi”

Levina akaingia ndani kwa haraka na kuwaacha Tomas na Magreth.

“Kwa nini ume fanya hivi Mage”

“Ni moja ya njia ya kumjua adui yako. Hivyo hata wewe pia nia adui yangu na kama ninge hitaji kukuua basi siku nyingi sana ninge kuua. Shukuru Mungu nina hofu ya Mungu ndani yangu la sivyo inge kula kwako”

“Hahahaaa….una hisi kunigombanisha na mwanake huyu. Mipango yangu haito endelea au?”

“Najua ita endelea hivyo simama wewe kama wewe na usimtegemee mwana mke”

Levina akarudi sebleni hapo akiwa na begi kubwa la nguo. Akamsukumia Tomas bagi hilo.

“Ondoka ndani ya nyumba yangu”

“Sawa usijali nina ondoka. Ila tambua kwamba nina weza kufanya kazi hii mimi peke yangu”

Tomas mara baada ya kufanya hivyo akaondoka ndani hapo huku akiwa amejawa na hasira kali sana.

“Nina ondoka”

“Magreth baki kwanza”

Levina alizungumza kwa upole huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Nakuomba uketi”

Magreth akaka kwenye moja ya sofa.

“Nakuomba sana hiyo video ya Tomas uifute”

“Kwa nini?”

“Ni udhalilishaji. Nakuomba kama mwanamke mwenzako”

“Ohoo sawa kwa ajili yako nina ifuta”

Magreth akaifuta video hiyo mbele ya Levina na yeye akaridhika na ufutaji huo.

“Naweza kuondoka?”

“Ndio japo roho yangu ina niuma”

“Hayo ni mambo yenu nyinyi wewenyewe mimi simo.”

Magreth akaaga na kuondoka nyumbani hapo huku akimuacha Levina akiwa katika wakati mgumu sana, kila alicho kiona ana hisi kama ni ndoto. Magreth moja kwa moja akaelekea Posta. Akapokea mzigo wake wa nguo kisha akaelekea hadi kwenye nyuma anayo hifadhia viafaa vyake. Akazijaribisha nguo hizo na hakika zipo vizuri sana. Magreth akachukua kisu chenye ncha kali na kujaribu kujichoma kwenye paja lake la kulia ila kisu hicho hakikuweza kutoboa nguo hiyo.

“Waoooo”

Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana kwani kama kisu hicho chenye ncha kali hakijaweza kupenye kwenye nguo hiyo basi hata riasi basi haito weza kuingia ndani ya nguo hiyo iliyo kaa mithili ya spider mam japo yake ina rangi nyeusi tupu.

***

“Umeamkaje?”

Mzee Mbogo alizungumza huku akimtazama Evans ambaye bado amejilaza.

“Salama mzee”

“Nina imani kwamba ume weza kujifikia na sasa una weza kunipatia jibu langu”

“Jibu lako lipo wazi mzee. Mimi na mambo usalama ni sawa na mbingu na ardhi.”

Mzee Mbogo akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Evans.

“Endapo unge fahamu faida ambayo uta ipata endapo unge kubali kujiunga nami. Basi nina uhakika kwamba usinge ishi maisha ya kuruka ruka kama ngedere. Kutokana niliweza kukusaidia, basi vijana wangu wata kurudisha pale pale darajani uka endele na mkutano wako na nabii Sanga. Jiandae vijana wangu wakarudishe”

Mzee Mbogo alizungumza huku akianza kutembea, kuelekea mlangoni.

“Nina weza kuuliza swali?”

Mzee Mbogo akageuka na kumtazama Evans.

“Nina weza kupata walinzi wawili ambao wata kuwa wana nilinda na nita walipa kiasi wakitakacho?”

“Huna pesa ya kuwalipa”

“Ninayo pesa hata ya kukulipa wewe mzee. Ninacho hitaji mimi ni walinzi tu wawili”

“Hahaaa una pesa ya kunilipa mimi?”

“Ndio, na jana tu nime toka kulipia eneo ambalo nina mpango wa kujenga kanisa langu. Tafadhali nina kuomba inisaidie katika hilo”

“Na wewe una taka kuwa mtumishi kama baba yako mwe mzee Sanga?”

“Sio mkwe wangu kwa maana mwanaye ana mume wake sasa ambaye ndio ana kwenda kumuoa”

“Mwenye kisu kikali ndio anaye kula nyama. Sasa wewe rafiki yangu kisu chako ni butu hakina uwezo wa kula watoto wa waheshimiwa.”

“Nime kuelewa, ila kama ina wezekana naomba unifanikishie lengo langu. Nipo tayari kuwalipa kiasi chochote”

“Huna kazi mjini, isitoshe wewe umemaliza chuo hivi juzi juzi. Leo hii una taka kuniambia kwamba una uwezo wa kunilipa hata mimi. Hembu acha maigizo bwana”

“Najua wewe ni mpelelezi, ingia kwenye benki ya Bacrays nilipo hifafhia pesa kisha angalia ni kiasi gania mbacho nina miliki, baada ya hapo uta weza kuni jaji kama nina weza kuwalipa walinzi wako au laa”

Evans alizungumza kwa msisitizo.

“Nitajie namba ya akauti yako na jina lake”

Evans akataja namba ya akaunti yake na jina alilo jisajilia kisha akatoka chumbani hapo.

“John niangalizie hii akaunti”

Mzee Mbogo alizungumza na kumtajia msaidizi wake huyo akaunti namba ya Evans. Ndani ya muda mchache tu wakaletewa ripoti ya akauti hiyo. Mzee Mbogo akashangaa sana kuona kiasi kikubwa cha pesa

“Ametolea wapi hii pesa huyu kijana”

“Sifahamu mkuu ita bidi umuulize wewe mwenyewe”

“Hembu angalia kiasi kilicho tolewa kime elekea wapi?”

John akaomba taarifa hizo.

“Zime kwenda kwenye akaunti ya wilaya ya Kigamboni na amelipia ardhi”

“Nashukuru”

Mzee Mbogo akaondoka na kuingia katika chumba alichopo Evans. Mzee Mbogoa kachomoa bastola yake kiunoni mwake na kumyooshea Evans ya usoni mwake.

“Niambie ni wapi ulipo toa pesa nyingi ikiwa hauna rekodi yoyote ya biashara wala kuajiriwa?”

Kitendo hicho kikamfanya Evans kuanza kutetemeka mwili mzima kwa maana hajui hata atamjibu nini mzee Mbogo.

***

Simu ya nabii Sanga ikanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa namba hiyo ngeni kisha akaipokea.

“Haloo”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake, aliye kaa kiti cha mbele huku wakipata kifungua kinywa.

“Habari yako baba”

Sauti ya Tomas ika mstua sana nabii Sanga. Akakirudisha chini kikombe cha chai ambacho alikuwa amekishika. Mstuko huo wa mumewe, mrs Sanga naye aliweza kuutambua.

“Nani wewe?”

“Ohoo naamini kwamab ume nisahau. Mimi ni Tomas kijana wako mtiifu na mwizi wa mke wako”

Tomas alizungumza kwa sauti ya dharau na iliyo jaa kejeli kubwa sana. Nabii Sanga akamtazama mke wake kwa sekunde kadhaa kisha akanyanyuka na kutoka nje.

“Wewe mwana haramu upo Tanzania eheee?”

“Siku nyingi nipo Tanzania na jana nime kukosa kosa kukuua pale darajani na leo nina imani kwamba siwezi kukukosa”

Maneno hayo yakazidi kumstua nabii Sanga na kujikuta akiangaza angaza kwenye magorofa ya majirani zake ila hakuweza kuona dalili yoyote ya mtu.

“Hahahaaa!!! Ila siwezi kukuua kabla sija kufir*** nabiii”

Maneno hayo yakamfanya nabii Sanga kuanza kumwagikwa na jasho la wasiwasi. Mrs Sanga naye akafika eneo hilo na kumtazama mume wake.

“Una zungumza na nani mume wangu?”

“Naisikia sauti ya mahabuba wangu hapo. Mpe simu nizungumze naye”

Nabii Sanga akaiweka simu yake loud speaker.

“Mpe basi mpenzi wangu nizungumze naye”

Mrs Sanga akastuka sana, mapigo yake ya moyo yakaaanza kumuende kasi kwa maana hakutarajia kama Tomas ana weza kupiga simu kwa mume wake.



“Nisikilize wewe mshenzi. Nilicho kufanya mara ya kwanza hakija kutosha, ila nitakacho kwenda kukufanya sasa hivi nina hakikisha uta jutia maisha yako yote. Pumbavu wewe”

Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akakata simu huku akiwa amevimba kwa hasira. Mrs Sanga akashindwa hata kuzungumza chochote kwa maana maneno hayo ya kejeli aliyo yatoa Tomas yame mkera sana mume wake. Nabii Sanga akaingia ndani na moja kwa moja akalekea chumbani kwake. Akafungu droo yake na kutoa simu yake ambayo huwa ana itumia kuwasiliana na vijana wake ambao kazi yako ni kulinda meli yake kubwa ya kifahari na maswasiliano ya simu hayo hayanaswi na mtando wowote wa Tanzania.

“Muheshimiwa”

“Kuna watu nina hitaji wafe leo”

“Nani muheshimiwa”

“Nina watumia namba zao. Hakikisheni muna watafuta na siku ya leo hii hii wana kufa”

“Sawa muheshimiwa”

Nabii Sanga akakata simu yake na kumtumia kijana huyo namba za simu za Tomas pamoja na Evans.

“Baby”

“Nini?”

Nabii Sanga alizungumza kwa hasira hadi mrs Sanga akatetemeka kwa woga.

“Mume wangu natambua kwamba ume kasirika”

“Huyu mpuuzi namba yangu ameipatia wapi?”

“Sifahamu mume wangu”

“Una jua?”

“Kweli mume wangu sijuia, tambua kwamba nime badilika na huyo mtu sina mahusiano naye kabisa. Nina kupenda wewe tu mume wangu”

Mrs Sanga alizungumza hukua kimkumbatia mume wake kwa nyuma.

“Na nina waua leo hawa”

“Kina nani?”

“Kwani ni nani na nani ambao wana paswa kufa. Ehee?”

“Nime kuelewa mume wangu”

Nabii Sanga akajitoa mikononi mwa mke wake. Akaiweka simu yake mezani na kuingia bafuni. Mrs Sanga kwa haraka akaingia kwenye simu ya mume wake, akaikremisha akilini namba ya Tomas, kisha akairudisha simu ya mume wake sehemu ilipo kuwa. Nabii Sanga akatoka huku akijifuta mikono yake na taulo.

“Niandalie ile suti ya rangi ya kaki nina hitaji kuelekea mahali”

“Wapi mume wangu”

“Mbona una maswali mengi sana. Wewe niandalie tu sehemu ya kwenda.”

Nabii Sanga alizungumza kwa hasira na kumfanya mke wake kuandaa kile anacho kihitaji. Nabii Sanga akajiandaa haraka haraka na kuondoka nyumbani kwake hapo huku akiwa na hasira kali sana. Mrs Sanga mara baada ya kuhakikisha mume wake ameondoka. Akaitafuta pochi yake ambayo ina hifadhi laini ambayo alikuwa ana wasiliana na Tomas kwa kipindi kirefu. Akaiweka katika simu ndogo kisha akampigia kwa namba hiyo mpya. Simu hiyo ya Tomas ikapokelewa.

“Nilijua kwamba uta piga”

“Una taka nini kwa mume wangu Tomas”

“Nina taka kumla mkun** kama vile alivyo kula wangu”

Mrs Sanga akaachia msunyo mkali na ulio jaa hasira na chuki ndani yake.

“Hivi ume changanyikiwa wewe?”

“Sijachanganyikiwa kwa maana lazima na mimi niionje ladha yake. Ila ngoja kwanza, nime miss penzi lako”

“Eti ehee?”

“Ndio nime miss penzi lako, hapo mara baada ya kusikia sauti yako ub** wangu ume simama kisawa sawa”

“Upo wapi?”

“Mmmm nipo hoteli moja, vipi una hitaji kuja?”

“Ndio nina hitaji kuja kwa maana hata mimi nime miss kukunwa na wewe”

Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya upole huku akizidi kupanga jambo baya juu ya Tomas.

“Nipo Kigamboni, hoteli moja inaitwa E HOTEL”

“Room namba ngapi?”

“Namba mia moja na ishirini”

“Nina kuja hapo”

Mrs Sanga akakata simu, akajiandaa na kuondoka nyumbani hapo. Moja kwa moja akaelekea hadi duka lake la dawa za mifugo na mimea.

“Karibu sana bosi”

“Salama, hivi muna ile dawa ya kuua wadudu katika zao la kabichi?”

“Ndio boss ipo”

“Hivi ni kali sana?”

“Ndio ni kali na hata bina damu ina weza kukuua ndani ya dakika kumi tu na uka kauka kau kau. Inabidi uwe makini sana boss”

“Sawa nipatie”

Muuzaji wa duka hilo akampatia mrs Sanga kichupa kidogo chenye dawa hiyo ambayo ni sumu kali sana.

“Boss hakikisha una weka tone moja kwenye ndoo ya maji ya lita moja, kisha baada ya hapo una nyweshea mime”

“Sawa nime kuelewa asante”

Mrs Sanga akatoa noti tano za elfu kumi kisha akaondoka. Akaingia ndani ya gari lake na kuelekea Sinza kwenye dula moja kubwa la nguo za kike. Akanunua baibui lenye kitambaa cha kufunika uso wake. Akanunua na bomba la sindano kisha akaelekea hadi kwenye hoteli yake iliyopo eneo hilo hilo la Kigamboni. Akaegesha gari lake kwenye maegesho. Akashuka na kutoka nje kabisa ya hoteli yake, akatembea hatua kadhaa na kulivaa baibu hilo, uzuri ni kwamba eneo ilipo hoteli yake hakuna watu wana katiza mara kwa mara. Akajifunga kitambaa hicho usoni mwake na kubakisha macho yake tu. Akakodisha bajaji na moja kwa moja akaelekea hadi katika hoteli aliyopo Tomas. Akaelekea katika gorofa yenye chumba hicho, akafika mlangoni na kuminya kitufe cha kengele. Mlango ukafunguliwa na akastuka sana kuona sura tofauti na Tomas anaye mjua.

“Heloo mrs Sanga”

Sauti ya Tomas ikamstua sana mrs Sanga na akavuta kumbukumbu ya haraka na akafanikiwa kukumbuka kwamba mwanaume huyo alishwa wahi kupeana naye mkono kanisani na alisha mtekenya kiganja cha mkono wake wa kulia.

***

“Ninarudia pesa ume toa wapi?”

Mzee Mbogo aliendelea kuzungumza kwa hasira huku akiendelea kumnyooshea bastola Evans.

“Pesa nime pewa na roho mtakatifu”

“What the fuc**”

Mzee Mbogo alijikuta akitukana kwa maana jibu hilo la Evans hakulitegemea.

“Kweli mzee wangu ndio maana hiyo pesa nina mpango wa kujengea kanisa.”

Mzee Mbogo taratibu akairudisha bastola hiyo kiuonini mwake.

“Nina miaka stini na mbili sasa.Ila sijawahi kuona malaika wala roho huyo mtakatatifu ambaye ana gawa pesa kwa watu. Hembu nieleze ukweli ni nani ambaye ana kupatia pesa hizo zote?”

“Ni hivyo nilivyo kueleza mzee wangu. Wewe si mpelelezi, nipeleleze nawe uta jua na hicho kiasi ulicho kiona kwenye hiyo akaunti yangu ni kidogo sana. Ila kuna pesa nyingi sana ina kuja. Maisha yangu nime yatoa kwa ajili ya kumtumikia Mungu hivyo nina kuomba unikubalie ombi langu”

Taratibu mzee Mbogo akaka kwenye moja ya sofa huku akimtazama Evans usoni mwake. Kwa uwezowake wa kuyasoma macho ya Evans akagundua kwamba ni kweli anacho kizungumza kijana huyo.

“Huyo roho mtakatifu umekutana naye wapi?”

“Sio ni mtu kwamba uta onana naye. Yeye ni roho ambayo haonekani”

“Sasa kama ni roho, je hizo pesa wewe ana kuleteaje?”

“Ana nipa maelekezo na nina jua ni wapia mbapo nina weza kuzipata pesa hizo”

“Una jua unacho kizungumza mimi sikielewi. Kama huyo roho wako ana weza kukupatia pesa nyingi basi akupatie na walinzi. Muda wako wa kuondoka hapa kwangu ume fika na hii ni simu yako. Tafadhali ondoka”

“Nashukuru mzee wangu”

“Ila huwezi kuondoka hivi hivi”

“Una maanisha nini?”

Mzee Mbogo akapiga mluzi kidogo, wakaingia vijana wawili. Mmoja akamfunga Evans kitambaa chausi usoni mwake kisha wakatoka ndani hapo na wakaingia kwenye gari jeusi na lenye vioo vyeusi. Wakaondoka eneo hilo na moja kwa moja wakampeleka hadi katika daraja la Kigamboni na waka mshusha katika eneo alipo liacha gari lake na wakaondoka zao. Evans akafungua kitambaa cha usoni mwake na kutazama eneo hilo ambalo sio geni kabisa. Akaliona gari lake, akatembea hadi lilipo, akalikagua kwa kulitazama huku akilizunguka. Alipo hakikisha lipo vizuri akaingia ndani na kuondoka eneo hilo na kuelekea hotelini.

***

“Vipi mume fanikiwa?”

Nabii Sanga alizungumza mara baada ya vijana hao wawili alio wapa kazi ya kuwatafuta Evans na Tomas kuingia ndani ya gari lake.

“Tume fanikiwa kupata maeneo ambayo vijana wako”

“Wote ni watu wepesi. Hivyo ina wapasa kutawanyika, kila mtu amchukue wa kwake, nina taka leo hii hii wawe wamesha kufa”

“Sawa mkuu ila picha zao tuna omba utusaidie”

Nabii Sanga akamtumia kila kijana mmoja picha ya Evans na Tomas. Wakashuka ndani ya gari hilo na kuondoka eneo hilo la ufukweni. Nabii Sanga akaitoa simu yake na kumpigia Julieth.

“Ndio baba”

“Upo wapi?”

“Nipo hapa kwa sonara nina tafuta mkufu pamoja na saa ambayo nita mkabidhi mume wangu kwenye sendoff”

“Walinzi si upo nao?””

“Ndio baba nipo na walinzi. Vipi mbona una uliza sana?”

“Ni muhimu kufahamu kwamba upo salama”

“Nashukuru baba nina kupenda”

“Nina kupenda”

“Nina kupenda pia mwanangu”

Nabii Sanga akakata simu na moja kwa moja akaelekea hadi ulipo mgahawa wa Magreth. Akashuka kwenye gari na kutembea hadi kwenye moja ya kiti na kukaa.

“Karibu sana nabii”

Muhudumu wa kike alizungumza kwa furaha sana.

“Nina shukuru sana”

“Una hitaji tukuhudumie nini?”

“Nahiyaji kupata kahawa alisi, sijui hapa ipo?”

“Ndio ipo muheshimiwa”

“Naomba uniletee”

Muhudumu huyo akaondoka. Nabii Sanga akaendelea kutazama jinsi mgahawa huo jinsi ulivyo changamka. Nabii Sanga akaletea kahawa hiyo na kuanza kuinywa taratibu. Akamshuhudia jinsi Magreth akishuka kwenye gari lake. Magreth akatembea kwa hatua za haraka huku akielekea kwenye ofisi yake, ila alivyo muona nabii Sanga akiwa eneo hilo la mgahawa wake, akapunguza mwendo kidogo. Akamtazama nabii Sanga ambaye naye ana mtazama kwa hatua za taratibu akamfwata hadi sehemu alipo.

“Ume kuja kufanya nini kwenye mgahawa wangu?”

Magreth alizungumza kwa sauti ya chini ila iliyo jawa na hasira snaa.

“Mimi nami pia ni mteja. Muna jitahidi sana kwa kahawa yenu”

“Tafadhali nina kuomba unanyuke na kuondoka eneo hilo. Umenielewa”

“Hahaaa, Mage Mage, kumbuka kwamba mimi ndio muasisi wa huu Mgahawa, pesa gari na kila kitu unacho kimiliki ni kutokana na pesa yangu”

“Kwa hiyo?”

“Niache nifanye kile ninacho jisikia. Isitoshe nita lipa kila kitu ninacho kitumia hapa”

Magreth akatamani hata kumzaba makofi nabii Sanga, ila ana shindwa hii ni kutokana na wingi wa watu waliopo katika eneo hilo. Magreth akaka taratibu huku akimtazama nabii Sanga, akamtumia video na sauti ya kijana wake ambaye ali muagiza katika kumuua Evans.

“Kuna meseji nime kutumia fungu”

Nabii Sanga akatoa simu yake na kuifungua video hiyo. Moyo wake uka mstuka sana kwa maana hakutarajia Magreth kama ana weza kuipata video hiyo. Akaifungua sauti hiyo na kumfanya azidi kustuka sana.

“Ume vipata wapi hivi vitu?”

Nabii Sanga alizungumza huku macho yakimtoka. Magreth hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kumpigia Levina.

“Ndio Mage”

“Una jipya lolote?”

“Ndio”

“Nitumie”

Magreth mara baada ya kukata simu. Zikaingia audio mbili. Akachomeka earphone na kusikiliza audio ya kwanza ina husiana na mazungumzo ya nabii Sanga na mwanaye. Akafungua audio ya pili na akayasikia mazungumzo yake na Tomas. Magreth akatabasamu na kumtumia nabii Sanga mazungumzo hayo. Nabii Sanga akafungua audio hiyo. Akamtazama Magreth kwa macho makali sana huku hasira ikianza kumpanda.

“Nina kufwatilia kwa kila hatua. Ume panga kumuua Evans ushahidi huo hapo na leo mbaya wako wame rudi. Ana hitaji kukula kiboga mzee baba. Hahaaa mchezo huu hauitaji hasira, sasa ole wako Evans apate madhara nita rusha uchafu wako wote siku ya harusi ya mwanao. Asubuhi njema nabii Sanga”

Magreth alizungumza kwa dharau huku akisimama na usoni mwake ametawaliwa na tabasamu lililo zidi kumfanya nabii Sanga kukasirika kiasi cha kutamani kumvamia Magreth ila ana shindwa kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo.


Nabii Sanga kwa hasira akatoa noti ya elfu kumi na kuiweka mezani hapo kisha akandoka eneo hilo pasipo hata kumalizia kawaha yake. Nabii Sanga mara baada ya kuingia ndani ya gari lake, akatoa simu yake nyingine ambayo ni maalumu kwa kuwasiliana na vijana wake tu.

“Ndio mkuu”

“Kuna mtu ame hack simu yangu. Mawasiliano yangu yote ninayo yafanya ndani ya simu yangu ile nyingine yana rekodiwa. Nina hitaji munitafutiee huyo mjinga aliye fanya huo upuuzi.”

“Sawa mkuu”

“Nahitaji muda huu”

“Nime elewa mkuu nina fanya”

Nabii Sanga akakata simu yake huku akimtazama Magreth anaye zungumza na wafanyakzi wake, kisha akaondoka eneo hilo. Magreth kwa haraka akampigia simu Levina.

“Hei kuwa makini?”

“Kwa nini?”

“Nabii Sanga ame toka hapa mgahawani kwangu na ameweza kugundua kwamba simu yake ina rekodiwa hivyo fanya nina imani kwamba ata fanya kila linalo wezekana kuhakikisha kwamba ana mtafuta aliye hack simu yake hivyo kubwa makini”

“Usijali hakuna ambaye ana weza kuingia kwenye data base zangu. Tena ngoja hii ishu niihamishie kwa mke wake”

“Kivipi una weza kuihamisha”

“Wewe uta ona nitakacho kifanya baadae”

Levina akakata simu, akafungua laptop yake kwa haraka na kuanza kuhamishi data zake za kuhack kwa mrs Sanga na hata endapo kuna mtu atajaribu kutafuta ni nani ambaye ame hack simu ya nabii Sanga ni lazima itaonyesha muhusika mkuu ni mrs Sanga.

***

“Ahaa samahani, nina ona nime kosea chumba”

“Umekosea vipi chumba mpenzi wangu. Mimi ni Tomas.”

Mrs Sanga akazidi kushangaa kwa maana sura si ya Tomas yule anaye mfahamu.

“Samahani naona sura tofauti na yule niliye panga kuonana naye”

“Hahahaaa Mama Julieth mbona una pagawa hivyo. Tazama kovu la mkononi mwangu, mimi ni Tomas”

Tomas alizungumza huku akiomunyesha Mrs Sanga kovu la mkono wake wa kushoto. Kwakupitia kovu hilo, mrs Sanga akamuamini, taratibu mrs Sanga akaingia ndani ya chumba hicho huku akiangaza angaza kila sehemu. Leongo kubwa lililo mleta ni kuhakikisha ana muua Tomas kwa mikono yake yeye mwenyewe.

“Niambie mke wangu”

Tomas alizungumza huku akimkumbatia Mrs Sanga kwa nyuma.

“Hembu niambie kwa nini sura yako ume ibadilisha?”

“Ni kutokana na kutafutwa na mume wako. Una hisi nita ishije miaka yangu yote”

Tomas alizungumza huku hamu ya ngono ikiwa imemtawala. Tomas akaendelea kuyatomasa Tomasa makalio ya mrs Sanga ambayo ni malaini sana.

“Ahaa kwa hiyo ume ogopa kuishi na sura yako halisi?”

“Ndio”

Tomas alizidi kujibaragua pasipo kujua kwamba ana waziwa mabaya na mwana mama huyo. Taratibu Mrs Sanga akageuka na kulishika taulo la Frank, akalivua na akabaki kama alivyo zaliwa.

“Waoo mashine yako iko vile vile”

“Ndio ulihisi ita pungua”

“Ita puguaje kwa mfano?”

Mrs Sanga alizungumza huku akimshika shika jogoo wa Tomas. Alipo hakikisha amesimama vizuri, taratibu akapiga magoti na akaanza kumnyonya. Udhaifu mkubwa wa Tomas ni kunyonywa jogoo wake. Akiwa katika hali kama hiyo ana hisi kuchanganyikiwa kabisa. Kwa utamu anao upata Tomas akajikuta akifumba macho huku akikishika kichwa cha mr Sanga na kuendelea kukikandamiza kwenye jogoo wake. Taratibu mrs Sanga akafungua pochi yake, akatoa bomba hilo la sindano pamoja na kichupa chenye dawa hiyo na kuulia wadudu wanao shambuliza zao la kabichi. Mrs Sanga akaendelea kuvuta dawa hiyo iliyopo kwenye kichupa pasipo Tomas mwenyewe kufahamu chochochote. Baada ya kuhakikisha kwamba bomba hilo limejaa kisawa sawa, akavirudisha vitu hivyo kwenye pochi yake.

“Baby lala kitandani”

Tomas hakujishauri hata mara mbili akajilaza kitandani huku miguu yake ikinin’inia chini. Mrs Sanga akapiga magoti chini na kuendelea kumnyonya. Tomas akazidi kutoa kelele za raha hadi akajikuta akijifunika na mto usoni mwake. Kitendo hicho kikawa ni kosa kubwa sana kwa Tomas. Mrs Sanga akatoa bomba hicho la sindano, akamkita kwa nguvu zake zote Tomas sindano hiyo maeneo ya tumboni mwake. Tomas akakurupuka, huku akisikilizia maumivu makali sana, ila tayari mrs Sanga alisha sukuma kiasi cha kutosha cha sindano hiyo.

“Malaya mkubwa wewe una niua…..”

Tomas alizungumza huku akisimama. Akajaribu kumshika mrs Sanga, ila mwili ukazidi kumuishia nguvu.

“Kufa mpumbavu wewe. Unahisi una weza kumf*** mume wangu wewe”

Tomas macho yakaaanza kumvuja damu. Pua nazo zikaanza kutokwa na damu, hakika dawa hiyo ina sumu kali sana. Tomas akaanza kuanguka chini huku akigara gara. Mrs Sanga akampigia mume wake, na baada ya kuita kwa sekunde kadhaa ikapokelewa.

“Baby upo wapi?”

Mrs Sanga alizungumza kwa wasiwasi.

“Nina rudi nyumbani, vipi mbona una wasiwasi?”

“Nimesha mmaliza”

“Nani?”

“Tomas”

“Nini?”

“Ndio, nime sha muaa.”

“Wa…api upo?”

“Kwenye hoteli niliyo aliyo fikizia”

“Ohoo Mungu wangu. Kwanini ume taka kuitia damu mikono yako?”

“Nime fanya hivyo mume wangu kwa ajili yako. Unahisi alicho kuambia mimi ninge pendezewa nacho. Nime fanya nilicho kifanya. Hapa nina hitaji msaada wako tu”

“Sikia kuna kijana ata fika hapo ndani ya dakika kadhaa. Ata kupa msaada”

“Sawa”

Mrs Sanga akakata simu huko mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana. Akamtazama jinsi Tomas mwili wake uliamvyo kakamaa. Sauti ya kengele ya mlangoni ikamstua, akatembea kwa hatahadhari hadi mlangoni. Akajifunika kitambaa cha baibui hilo usoni mwake. Akafunua mlango huo na kukutana na kijana ambaye ana mfahamu, kwani ni mmoja wa wafanyakazi wao wa kusambaza madawa ya kulevya duniani.

“Hei madam nime agizwa”

“Ingia”

Kijana huyo akaingia ndani ya chumba hicho na akashangaa kumuona Tomas akiwa amekauka kama mkaa.

“Huyu ni nani?”

“Ndio huyo ambaye mulipaswa kumuua. Hakikisha kwamba hii maiti ina potea na hakuna mtu hata mmoja anaye fahamu kwamba tulimuua”

“Sawa, ila mbona sura yake ni tofauti?”

“Hiyo ya juu ni sura ya bandia, ndio maana una ona amekauka mwili mzima pasipo sura yake tu”

Kijana huyo akausogelea mwili wa Tomas, akaishika ngozi ya sura yake na kweli ina ulaini. Taratibu akaanza kuitoa sura hiyo na Tomas akabakiwa na sura yake halisi.

“Sawa wewe ondoka hapa nita shuhulika naye”

“Poa”

Mrs Sanga akaondoka eneo hilo na kumuacha kijana huyo akitafakari ni jinsi gani anavyo weza kumtoa Tomas katika hoteli hiyo. Mrs Sanga akavua baibui hilo, akafika hotelini kwake, akaingia kwenye gari na kuondoka eneo hilo.

***

Nabii Sanga akaanza kutazama picha alizo tumiwa na kijana wake zikiuonyesha mwili wa Tomas ambaye ameuliwa na mke wake. Picha hizo zikaipa furaha nafsi ya nabii Sanga kwa maana jambo hilo alilitamani litimie siku hiyo hiyo na kweli, lime weza kutimia. Zikaingia picha za binti ambaye hajawahi kumuona kwenye maisha yake, kabla hajamaliza kuzitazama picha hizo, simu yake ikaanza kuita.

“Mkuu za muda kidogo”

“Salama, ehee nipe ripoti”

“Hizo picha ni za msichana ambaye ndio ame hack simu yako. Tunashukuru Mungu tuliweza kuyawahi mazungumzo ya mke wako kabla ya yeye kuyapata na tumeyafuta”

“Ohooo kwa hiyo hii ishu ya kumuu Tomas kumbe ilikuwa ina paswa kumfikia na yeye?”

“Ndio mkuu, ila tume muwahi”

“Safi sana. Nahitaji binti huyo munitafutie na mumkamate”

“Sawa mkuu”

Nabii Sanga akakata simu kisha akashuka kwenye gari. Kabla hajaingia ndani akaliona gari la mke wake likiingia getini. Mrs Sanga akashuka kwenye gari huku akiwa amejawa na wasiwasi, akamkumbatia mume wake kwa nguvu.

“Kazi nzuri mke wangu”

“Naogopa mume wangu”

“Usiogope, nipo pamoja nawe na lelo ume nidhihirishia kwamba wewe upo nami kwenye kila jambo”

“Nakupenda sana Sanga”

“Nakupenda pia mke wangu”

Nabii Sanga akaingia ndani na mke wake. Wakaelekea hadi chumbani kwao.

“Nasikia jamaa alijiweka sura bandia?”

“Ndio, alijiweka sura bandia, na kuna siku alisha wahi kuja kanisani”

“Wee”

“Ndio, nina imani kwamba alikuwa ana tafuta jinsi ya kulipiza kisasi”

“Ila ndio hivyo ameshindwa. Mke wangu kuna mtu ame hack simu yangu na mazungumzo yote yaliyo kuwa yana ingia kwenye simu yangu ana yapata”

Mrs Sanga akastuka sana, macho yakamtoka huku akikumbuka mazungumzo ya mwisho kuzungumza kwenye simu na mume wake sio mazuri sana na endapo yata fika kwenye vyombo vya usalama basi wana weza kumchukulia hatua kali sana na za kisheria.

“Ila usiwe na mashaka, vijana wangu wamesha zuia huo mchezo na wame nitumia picha zake”

“Hembu nimuone”

Nabii Sanga akamkabidhi mke wake, simu inayo onyesha picha za Levina.

“Huyu nina mjua huyu binti”

Mrs Sanga alizungumza huku akimtazama Levina vizuri.

“Ume mjuaje?”

“Ni rafikia wa Julieth.”

“Rafiki yake?”

“Ndio”

“Ime kuwaje sasa ame hack simu yangu?”

“Sijajua, kwani Julieth yupo wapi?”

“Ametoka”

“Basi huyu ni rafiki yake.So una kwenda kumfanya nini?”

“Ngoja siku ya leo iishe alafu nita jua nini cha kufanya”

Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama mke wake kwa maana kama ni kumuua Levina basi ita kuw a ni jambo raisi sana na halito msumbua.

***

Wasiwasi mwingi sana ukazidi kumtawala Levina. Kila jinsia navyo jaribu kuhack simu ya nabii Sanga, anajikuta akishindwa.

‘Mungu wangu huyu mzee amesha fahamu’

Levina alizungumza huku akimwagikwa na jasho mwili mzima. Akakumbuka mameno ya Magreth kwamba ni lazima nabii Sanga ata tumia kila njia ya kuhakikishaa na mtafuta. Levina akanyayuka sebebleni hapona kuingia chumbani kwake. Akachukua nguo zake muhimu, kiasi cha pesa, anacho kaa nacho ndani kwake kisha akampigia Magreth.

“Dada upo wapi?”

“Nipo kwenye mgahawa wangu”

“Nina kuja”

“Vipi mbona una zungumza kwa wasiwasi”

“Nina kuja dada yangu”

Levina akakata simu, akabebe na laptop yake, akaifunga nyyumba yake kisa akaondoka enyumbani kwake. Dakika ishirini na sita zika tosha kabisa kwa yeye kufika kwenye mgahawa wa Magreth. Akashuka kwenye gari na akapokelewa.

“Levina una nini?”

“Naomba uni hifadhi, watu wa nabii Sanga wame weza kuingia kwenye database zangu na wame fanikiwa kuzuia kila nilicho kifanya kwenye simu ya nabii Sanga.”

“Ohooo Mungu wangu nilijua tu”

“Ndio hivyo Mage nina kuomba uni saidie kwa maana maisha yangu kwa sasa yapo hatarini. Wana weza kuniua”

“Ndio wata kuua, nabii Sanga sio mtu wa kawaida. Joho la utumishi wa Mungu alilo livaa ni sawa sawa na ngozi ya kondoo tu ila uhalisia wake ni chui mkali sana”

Maneno ya Magreth yakazidi kumuogopesha Levina.

“Je wana weza kujua location ya wapi ulipo?”

“Hapana”

“Basi uta kaa na mimi na tuta saidiana kuhakikisha kwamba tuna muua nabii Sanga na familia yake. Ume nielewa?”

Levina akajibu kwa kutingisha kichwa, akimaanisha kwamba ame elewa kwa maana kwa sasa hana namna ya kufanya zaidi ya kumsikiliza Magreth kila anacho muambia.



“Twende kwangu”

“Sawa”

Magreth akamuaga Juma kisha akaingia kwenye gari lake na Levina naye akaingia kwenye gari lake na wakaondoka eneo hilo la Mgahawa. Wakafika nyumbani kwa Magreth na akamtambulisha kwa Josephine ambaye naye ana ishi hapo.

“Karibu sana na ujisikie nyumbani”

“Nashukuru sana.”

“Mimi jamani ngoja nirudi kwenye mgahawa nikaendelee na majukumu”

“Sawa, alafu Mage usisahau kuja na yale maziwa mtindi kwa maana humu kwenye friji nina ona yamebaki machache.”

“Sawa best”

Magreth akaondoka nyumbani kwake hapo na kuwaacha rafiki zake hao wawili.

***

Kijana wa nabii Sanga akaondoka hotelini hapo huku akiifunga mlango wa chumba hicho alipo uwawa Tomas. Baada ya nusu saa akarudi akiwa na begi la wastani ambalo kwa ndani ame babe chumpa mbili za lita mbili na nusu ambazo kwa ndani zina tingikali. Akaingia chumbani, akaunyanyua mwili wa Tomas na kuuingiza kwenye sinki la kuogea. Akatoa chupa hizo ndani ya begi na kuanza kuzimwagia tindikali hiyo, kadri jinsi anavyo zidi kuumwagia mwili huo ndivyo jinsi unavyo zidi kuyayuka mithili ya plastiki ndani ya moto. Zoezi hilo la kikatili likadumu ndani ya dakika ishirini. Alipo hakikisha kwamba mwili mzima wa Tomas ume yayushwa na tindikali hiyo ambayo ni kali sana. Akasafisha chumba kizima, akamwaga unga ambao hutumiwa na wapelelezi katika kutafuta alama za vidole katika eneo la tukio la mauaji au mwili wa mtu aliye uwawa. Alipo hakikisha alama hizo zime jitokeza katika maeneo baadhi ya chumba icho, akazifuta kiutaalamu sana.

Alipo hakikisha kwamba ame maliza kuifanya kazi hiyo, akasafisha na sinki la maji na hata akiingia mtu mwengine hato hisi kama ndani ya chumba hicho kuna mtu ameuwawa.

“Bossi”

“Ndio vipi ume mtoa?”

“Ndio, kila kitu kipo vizuri”

“Safi sana nina imani kwamba una fahamu ni jinsi gani ya kufuta ushahidi wa kamera”

“Ndio, pia simu yake nina ondoka nayo”

“Sawa kuwa makini”

“Usijali boss”

Kijana huyo akakata simu, akakikagua chumba hicho kwa umakini sana kisha akaondoka huku akiliacha begi la nguo la Tomas.

“Hei muna weza kuziachia kamera sasa”

“Poa”

Kijana huyo akawasiliana na wezake ambao wapo kwenye meli na kazi yao walikuwa ni kuhakikisha wana daka rekodi zote za kamera za hoteli hiyo. Wakafuta kila kitu ikiwemo jinsi mrs Sanga alivyo kuja kwenye hoteli hiyo na kuondoka.

***

“Usishuke kwenye gari”

Evans akastuka sana na akageuka nyuma.

“Ahaa mbona ume nistua”

“Hilo la kukustua halina msingi wowote kwako, ila ninacho kuomba kwa sasa usishuke kwenye gari”

Jini huyo alizungumza kwa msisitizo sana.

“Kwani kuna nini?”

“Unaiona ile gari nyueusi pale”

Jini huyo alizungumza hukua kimuonyesha Evans garia ina ya Toyota Rav 4.

“Ndio”

“Mule ndani kuna muuaji aliye agizwa kukuua wewe na endapo utashuka basi a=hali yako ina weza kuwa mbaya.

“Ame….ame tumwa na nina huyo muuaji?”

“Nabii Sanga pia kuna watekaji wengine ambao wame tumwa na raisi Mtenzi na wao pia wapo katika eneo hili”

Evans akahisi mwili wake ukiishiwa nguvu.

“Sasa ita kuwaje?”

“Nakuletea vitu vyako vilivyopo ndani ya hoteli na sasa hivi ina kupasa uanze safari ya kuelekea kwennu. Ume nielewa?”

“Ndio”

Jini huyo akafungua mlango wa gari hiyo ya Evans na kushuka. Kijana wa nabii Sanga akajawa an mashangao kidogo kwa maana alihisi kwamba ndani y gari hilo yupo Evans pike yake.

‘Huyu naye ni nani?’

Kijana huyo alijiuliza huku akimtazama mwana dada huyo mrembo jinsi anavyo katiza karibi kabisa na gari lake. Mwana dada huyo alipo pita, kijana huyo akashuka kwenye gari lake na kuangaza eneo hilo zima la maegesho ya magari. Akatoa simu yake mfukoni na kutazama alama ya gprs ni wapi inapo elekea. Alama hiyo ina onyesha eneo anapo kwenda mwana dada huyo.

‘Ina maana huyu ndio Evans au?”

Kijana huyo alijiuliza huku akiwa amejawa na mshangao. Akampigia simu nabii Sanga na baada ya muda mchache simu yake ikapokelewa.

“Mkuu huyu Evans uliye nitumia picha yake, ndio yeye mwenyewe au ume kosea?”

“Kwa nini nikosee?”

“Kwa maana ninaye muona hapa ni mwanamke na sio mwanaume”

“Ume muona wapi?”

“Nipo hotelini n anime jaribu kumfwatilia kama jinsi gprs ilivyo niongoza na kweli nime weza kufanikiwa kumuon ila ni mwanamke”

“Jiongeze wewe, ina weza kuwa simu ya kijana huyo anayo huyo mwanamke. Wewe nenda kambane huyo mwanamke na ata kueleza ni wapi alipo Evans.”

“Sawa mkuu”

Kijana huyo akaondoka eneo hilo na kuanza kueleeka alipo elekeea mwana dada huo. Akaingi akwenye lifti na taratibu akapandisha hadi gorofa ambayo alama hiyo ya gprs ime simama. Kijana huyo akatembea hadi mlangoni na kugonga mlango wa chumba cha Evans. Mlango ukafunguliwa na akakutana na mwana dada huyo.

“Ahaa samahani”

Kijana huyo alizungumza huku akiingia ndani ya chumba hicho pasipo kukaribishwa.

“Una mtafuta Evans?”

“Ndio, una weza kuniambia yupo wapi?”

“Huyu hapa”

Mwana dada huyo kwa haraka akamkaba kijana huyo shingo yake kwa mkono wa kulia. Akaanza kumnyanyua juu na kumfanya kijana huyo kuanza kutapa tapa kwa ajili ya kuyaokoa maisha yeka kwa maana hakutarajia kama mwa na dada huyo ana weza kuwa na nguvu kubwa kama hivyo.

“Usije ukadhubutu siku nyingine kumfwatilia Evans. Rudisha ujumbe kwa mbosi wako kwamba ume ifanikisha kazi yake ume nielewa”

“Nd….io”

Kijana huyo alijibu kwa shida sana.

“Ondoka hapa”

Kijana huyo kwa kasi ya ajabu akatoka hotelini hapo huku akiwa haamini kabisa alicho kiona. Jini Maimuna akachukua kila kitu cha Evans na kurudi kwenye gari.

“Yule mtu nime muona akiondoka hapa kwa kasi, ime kuwaje?”

“Nime mpa meseji akamsimulie mkuu wake. Jambo la kufanya hivi sasa ni wewe kuelekea nyumbani kwa mama na nitakuambi ni lini una paswa kurudi Dar es Salaam”

“Sawa, ila wale jamaa nilio wapa oda ya kujenga kanisa ina kuwaje?”

“Usijali hauto kaa muda mrefu, nahitaji mambo yaweze kutulia kidogo. Sawa”

“Sawa”

Jini Maimuna akatoka ndani ya gari hilo na Evans akaondoka. Jini maimuna akasogelea gari la walinzi wa raisi, akaligusa kodogo pasipo wao kufahamu chochote.

“Ana ondoka ana ondoka”

Mmoja wa walinzi wa raisi alianza kuzungumza huku akijaribu kuwasha gari ila jambo la kushangaza kila anavyo jaribu kuwasha, gari haliwaki.

“Ni nini kinacho endelea?”

“Sijui mwanangu. Naliwasha haliwaki”

Derevawa gari hili aliendelea kufanya kila anacho kiweza ila gari halikuwaka kabisa.

***

“Ume sema?”

Nabii Sanga alimuuliza kijana wake huyo kwa mshangao.

“Nime kutana na binadamu ambaye sio wa kawaida kabisa bosi. Amenikaba koo na ameninyanyua kwa mkono mmoja na isitoshe ni mwamamke.”

Nabii Sanga akashusha pumzi huku akimtazama kijana wake kwa maana hicho anacho kizungumza ana ona ni jambo la ajabu sana.

“Ina maana ni mwanamke ame kupiga wewe?”

“Bosi una nijua, kama nina weza kupigana na wanaume wenye uwezo wao hata sita. Ita kuwaje mwanmke mmoja, huyo sio bina damu wa kawaida.”

“Okay rudi kwenye meli alafu tuta jua ni kitu gani cha kufanya”

“Sawa mkuu”

Nabii Sanga akashuka kwenye gari la kijana huyo na akaondoka nje ya jumba hilo la nabii Sanga.

“Vipi kime tokea nini?”

“Ana dai kwamba ame shindwa kumuua sijui ame kutana msichana ambaye sio wa kawaida, amemkaba koo, ame mnyanyua juu kwa mkono mmoja. Nnashindwa kumuelewa kabisa”

“Mmm sasa ina kuwaje mume wangu”

“Tuta tafuta nafasi yingine, tuta muua”

“Jitahidi mume wangu, sinto hitaji harusi ya mwanangu ivurugike kwa aina yoyote ile ume nielewa?”

“Nime kuelewa mke wangu”

Julieth akarudi akiwa na walinzi wake, akawasialimia wazazi wake kwa furaha sana.

“Siku yako ime kwendaje?”

“Siku yangu ime kwenda poa sana, nime kamilisha kununua kila kitu.”

“Dada nawe ume nunua nini leo kwenye matembezi yenu?”

Mrs Sangaa alimuuliza mfanyakazi wao wa ndani ambaye wame ishi naye hapo kwa kipindi kirefu sana.

“Nime nunua vitu vingi mama, nina imani harusi ita kuwa bomba sana kwetu”

“Nina imani mimi na baba yenu tumesha kamilisha kila kitu”

“Alafu baba kina kaka wana kuja lini?”

“Kesho kutwa”

“Waooo waje tu kwa maana nina nime wa miss sana”

Julieth alizungumza huku fura ikiwa ime mtawala sana.

***

Magreth akarudi nyumbani kwake majira ya saa nne usiku, akawakuta rafiki zake wakiwa bado wakiwa wana zungumza mambo mengi. Wakasalimiana kwa furaha na Magreth akamkabidhi Josephine kidungu cha maziwa.

“Mage mpango wako ni upi kwenye hili swala?”

Levina alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Muna mpango gani?”

Josephine alizungumza huku akirudi sebleni hapo, akitokea jikoni. Magreth akajikuta akipata kigugumizi kwa maana haja mshirikisha Josephine juu ya mpango wake wa kumuua nabii Sanga.

“Mage lini ume anza kunificha mipango yako?”

“Sija kuficha rafiki yangu”

“Ila, najua nini una taka kufanya ila nina kuomba uni ambie kwa kinywa chako”

Magreth akashusha pumzi huku akimtazama Josephine usoni mwake.

“Naamini una tambua juu ya sakala la shemeji yako kupote?”

“Ndio na fahamu na tulikuwa sisi wote siku ile Morogoro.”

“Mtu aliye husika na swala la kumteka Evans ni nabii Sanga nilijaribu kumueleza mara kadhaa kuhusiana na kwa nini ana mteka mume wangu ila alinijibu kwa dharau”

“Mbona nabii Sanga haja husika na kumteka Evans”

“Kwa nini?”

“Najua aliye husika ni mtoto wa raisi Mtenzi huyu anaye muoa Julieth Sanga. Jamaa ana itwa Jerry Mtenzi”

Levina akamtazama Magreth kwa sekunde kadhaa.

“Samahani kwa kuingilia mazungumzo yenu. Dada Josephine ume fahamu vipi kwamba Jery ndio ana husika?”

“Levina mimi huwa nina uwezo wa kuomba na kuonyeshwa kila aina ya jambo ambalo lina fanyika au lina kwenda kufanyika”

Levina macho yakamtoka kwa mshangao mkubwa sana kwa maana haja wahi kukutana na my mwenye uwezo kama huo maishani mwake.

“Kwa hiyo kwa sasa una jua ni kitu gani ambacho kina kwenda kutokea?”

“Ndio nina fahamu kwamba mpango wenu ni kuhakikisha kwamba muna lipiza kisasikwa nabii Sanga kwa kuhusika kwa kupoea kwa Evans pia na kufa kwa Tomas”

Levina akastuka sana macho yakamtoka, kwa maana habari ya kufa kwa Tomas haitambui kabisa.

“U..na…tak…a kuni…ni…ambia kwamba Tomas wangu ame kufa?”

“Ndio ame uwawa leo na Mrs Sanga kwa kuchomwa sindano ya sumu”

Levina na Magreth wote wakajawa na mshangao huku Levina nguvu za mwili zikianza kumuishia huku mapigo ya moyo yakizidi kumuenda kasi huku joto kali la mwili likizidi kumpanda hadi akahisi roho yake ina kwenda kumtoka.



ENDELEA

“Josephine acha utani, una taka kuniambia Tomas ame kufa?”

Magreth aliuliza kwa msisitizo huku akiwa haamini hicho anacho kisikia.

“Haki ya Mungu, nina maono na wewe nina imani kwamba una tambua kwamba sijawahi kukosea kwenye maono yangu:

Magreth akashusha pumzi nyingi huku akitamani hata kumkamata mrs Sanga mbele yake na kumvunja vunja vipande vidogo vidogo.

“Ame muulia wapi mume wangu?”

Levina alizungumza huku machozi yakimwagika.

“Hotelini, ila sijaonyeshwa ni hoteli gani”

“Nina muua mrs Sanga, haki ya Mungu nita muua kwa mikono yangu mimi mwenyewe”

Levina alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Magreth akanyanyuka na kuingia chumbani kwake, akaichukua simu yake na kuiatazama namba ya nabii Sanga kwa zaidi ya dakika kumi. Akaminya kitufe cha kijani na taratibu simu hiyo ikaanza kuita.

“Una hitaji nini tena kwangu?”

“Ulisi kwamba dunia haito jua au kuna siri yoyote”

“Una zungumza nini wewe mwenda wazimu?”

“Mke wako amemuua Tomas kwa kumchoma sindano ya sumu. Ameamini kama ame maliza kila kitu, ila nina hitaji kukuambia kitu kimoja SANGA. Sinto kubali kuona una zidi kuwaonea wanyonge kisa wewe tu ni mtu mwenye pesa na mwenye kujuana na kiongozi wa hii nchi. Nina kuambia ukweli, nita dili na wewe pamoja na familia yako nzima. Mmoja baada ya mwengine ata kwenda kuionja joto ya jiwe”

“Hahaaaa Mage nimesha yazoea maneno yako hivyo ni fanya unacho taka kukifanya. Umenielewa?”

Nabii Sanga alizungumza kwa dharua na kumfanya Magreth kukata simu huku hasiri ikikifanya kifua chake kitanuke mithili ya mbeba vyuma.

***

“Huyu panya jike ana endelea kutufwatilia mke wangu”

Nabii Sanga alizungumza kwa hasira huku mwili mzima ukimtetemeka.

“Ina bidi ushuhulike naye kabla ya harusi mume wangu. Miimi Tomas nimesha dili naye ni zimu yako kushuhulika naye”

Mrs Sanga alizungumza huku akimtazama mume wake usoni.

“Sawa”

“Usiseme sawa, ikiwa mtu ana hack simu yake, pili ana kupigia simu za vitisho. Tatu sijui ame juaje kama mimi nime muua Tomas tena kwa sumu”

“Kuna jambo ambaloa na lifanya. Ila nita lijua tu. Nina kuja”

Nabii Sanga akatoka chumbani kwake hapo na kuelekea katika chumba chake cha siri kilichopo chini ya ardhi ambapo ndipo anapo fanyia sala zake za kishetani. Nabii Sanga akaufunga mlango wa chumba hicho kwa ndani, kisha akavua nguo zake zote. Akawasha mishumaa iliyo zunguka duara ambali ndipo ana abudu kwa mkuu wake wa anaye mpatia nguvu. Nabii Sanga akaanza kuzungumza maneno ya kumuita mkuu wake huyo. Ndani ya muda mchache, moshi mwingi ukaanza kutawala ndani ya chumba hicho.

“Sanga”

“Ndio mkuu”

Nabii Sanga aliitikia na kwa haraka akapiga magoti yake na kusujudia mwana dada huyo.

“Nime kuja”

“Mkuu nina shida kubwa sana”

“Shida gani?”

“Yule Magreth uliye niambie nimtoe sadaka, leo hii ana nisumbua sana. Ana nikosesha amani kwenye mambo yangu, ana taka kuisulubisha familia yangu”

Nabii Sanga alizungumza kwa unyenyekevu mkubwa sana.

“Magreth ana lindwa”

“Na nani?”

“Kuna msichana mmoja ana itwa Josephine, pia ni muumini kwenye kanisa lako. Josephine ana uwezo wa kuona mambo ya yajayo au yaliyo tokea. Ame simama vizuri mbele za Mungu, hivyo una paswa kujiangalia mara kwa mara pale unapo taka kuanzisha vita na huyo Magreth kwa maana ata kuwa ana fahamu mbinu zako na itakuwa ni rahisi kukupiga”

“Nime kuelewa mkuu. Nita fanya nini kumzuia huyo msichana?”

“Hashikiki na pia usijaribu kumuwinda kwa maana ata kuvurugia kila kitu chako kwani malaika wa Mungu wao ndio wana mlinda”

“Yupo wapi kwa sasa huyo Josephine?”

“Nyumbani kwa Magreth”

“Mkuu nisaidie ni fanye nini kuwaangamiza hao watu”

“Ni lazima damu nyingi imwagike ndio uta weza kuwapata”

“Imwagike kwa kina nani?”

“Uta jua, sio kila jambo nina paswa kukuambia. Una kitu kingine cha kuomba?”

“Ndio. Kuna kijana ana itwa Evans nina sikia ana lindwa na mtu ambaye sio binadamu wa kaiwada?”

“Huyo kijana simuoni kwenye ulimwengu wangu. Hivyo sina maoni yoyote kwa ajili yake. Siku mwema”

Mkuu wake huyo akapotea ndani ya chumba hicho na kusababisha moshi wote kuisha. Mishumaa aliyo iwasha yote ikajizima, taratibu akanyanyuka na kuwasha taa. Akavaa nguo zake huku akiwa ameshoshwa na habari hizo. Akarudi chumbani kwake na kumkuta mke wake akitazama televishion.

“Vipi mbona ume choka hivyo”

“Nafikiria jinsi ya kumuua Magreth”

“Leo ina weza ikawa ni siku nzuri ya kumuangamiza. Una vijana tana wenye uwezo, waelekeze ni wapi anapo ishi Magreth kisha wakafanye mambo usiku huu huu”

“Etii ehee?”

“Ndio mume wangu. Hakuna namna ni lazima uhakikishe maadui zetu wote tuna waua”

Nabii Sanga akambusu mke wake shavuni huku akiwa ame furahia ushauri huo. Akampigia kiongozi wa vijana wake.

“Ndio mkuu”

“Kuna kazi nahitaji ifanyike usiku huu”

“Kazi gani mkuu”

“Una vijana wangapi walipo Dar?”

“Sita”

“Nahitaji walekee Kigamboni, nina kutumia ramani ya eneo hilo la nyumba ya huyo msichana. Nawatumia na picha yake nahitaji usiku wa leo hii awe amekufa. Tume elewana?”

“Ndio muheshimiwa. Kazi ita fanyika kifahasa”

Nabii Sanga akakata simu, akatuma picha ya Magreth kwa kijana wake huyo na maelekezo ya wapi ilipo nyumba yake hiyo na amri ni moja tu. Magreth ana paswa kuwawa na kila atakaye kutwa ndani hapo ni lazima auwawe.

***

Dharau na kejeli aliyo onyeshwa na nabii Sanga ikamfanya Magreth kuanza kufanya mazoezi kwa juhudi zake zote. Josephine na Levina kazi yao kubwa ni kushuhudia jinsi Magreth anavyo ruka sarakani na kurusha mateka. Hapakuwa na hata mmoja kati yao aliye hisi kwamba Magreth ni mwepesi kiasi hicho.

“Mage pumzika, ni masaa matatu sasa una fanya mazoezi”

Josephine alizungumza huku akimtazama Magreth aliye simama kwa kutumia mikono yake huku kichwa chake kikiwa chini na miguu juu. Taraibu Magreth akajigeuza na akasimama.

“Lazima nimuue Sanga”

Magreth alizungumza hukua kijifuta jasho kwa kitaulo kidogo.

“Huto weza Mage”

Josephine aliendelea kusisitiza.

“Kwa nini asiweze, ikiwa yeye na mke wake wama wadhuru wapenzi wetu”

“Sanga ana watu wengi sana wanao walinda. Hivyo hilo munali liwazia, ina wabidi mulifikiria kwa mara ya pili tena. Nyinyi sasa hivi mume kuwa zaidi ya ndugu zako hivyo sinto penda mupotee.”

“Jose saa ngapi sasa hivi?”

Magreth alizungumza huku akimtazama Josephine usoni mwake

“Ni saa nane usiku”

“Levina tuna weza kutoka?”

“Sasa hivi?”

“Ndio”

“Na mimi nita ambatana nanyi”

Josephine alizungumza huku akimtazama Magreth aliye panga safari hiyo.

“Sawa, ngoja nichukue funguo ya gari”

Magreth akaingia chumbani kwake, hakuhitaji hata kubadilisha nguo hizo za mazoezi. Akaichukua funguo yake ya gari na wakaondoka nyumbani hapo.

“Tuna kwenda wapi Mage”

Levina aliuliza huku akiwa na wasiwasi kidogo.

“Nyinyi tulieni”

Wakafika katika nyumba aliyo hifadhia pikipiki na silaha zake. Magreth akafungua geti la nyumba hiyo, akaingiza gari kisha akalifunga geti.

“Hii nyumba mbona ime tulia sana. Kuna watu wanao ishi hapa?”

Josephine aliuza uku akitazama tazama kila pande ya nyumba hii iliyopo pembezoni mwa bahari.

“Ni nyumba yangu, niliirithi kwa babu yangu mmoja ambaye alikuwa ni raia wa Japan”

“Ahaa pazuri, kwa nini sasa tusikae huku, kuna upepo mzuri”

Josephine alizungumza hukua akiwa amejawa na furaha. Wakaingia ndani na Magreth akawasha taa za nyumba nzima.

“Tume kuja hapa kwa kazi moja. Eneo hilo ndio eneo la pekee ambalo tuta kuwa tuna fanyia kazi zetu za kupanga mipango yote ya kuhakikisha tuna lipizaje kisasi. Josephine, nina kuomba uwe pamoja nasi ume nielewa?”

“Mimi mbona nipo pamoja nanyi”

Simu ya Magreth ikaanza kutingishika(vibrate) mfukoni mwake. Akaitoa mfukoni mwake kwa haraka, akaingia upande wa kamera alizo zifunga nyumbani kwake. Akashuhudia gari moja aina ya BMW X5 ikisimama nje ya geti lake.

“Njooni muone”

Josephine na Levina wakasimama alipo Magreth na wakaanza kushudia jinsi wanaume sita wenye bunduki huku wakiwa wame ziziba nyuso zao wakishuka kwenye gari hilo na wakaanza kuruka ukuta.

“Hawa ni kina nani?”

Josephine aliuliza huku akitetemeka kwa woga.

“Sanga ame tuma watu wake kwa ajili ya kutuua. Endapo tunge kuwa ndani humo basi leo hii ndio inge kuwa mwisho wa maisha yetu”

Magreth alizungumza huku akikunja ngumi mkono wake wa kulia kwa manaa kama ni vita sasa ni ya uso kwa uso.

***

Vijana wawili walio ruka ukuta, wakafungua geti dogo la nyumba ya Magreth na wezao wakaingia ndani huku nje akibakia mmoja kuhakikisha ana imarisha ulinzi. Vijana hao wakatawanyika na kuizunguka nyumba huku wawili wakiingia ndani. Wakaanza kunyata kwa umakini huku wakikagua chumba kimoja baada ya kingine. Kila chumba walicho ingia hawakumkuta mtu yoyote.

“Hakuna mtu mkuu”

Mmoja wa vijana hao alizungumza huku akitoka nje.

“Wata kuwa wame kwenda wapi?”

“Hatujajua, ila dalili ina onyesha kuna watu wanao ishi humu ndani”

“Ngoja nimpigie mkuu”

Kijana huyo akampigia simu nabii Sanga.

“Muheshimiwa tume fika hapa nyumbani ila hatujamkuta mtu wa ina yoyote”

“Kwa nini?”

“Hatujui, ila hatujakuta mtu”

“Shenzi sana huyo panya. Sasa nyinyi ondokeni na murudi kwenye meli usiku huu huu”

“Sawa muheshimiwa”

Jamaa huyo akakata simu.

“Tuondokeni”

Wakatoka nje, wakaingia kwenye gari lao na kuondoka kwa mwendo wa kasi sana.

***

Josephine akashusha pumzi mara baada ya kuwaona watu hao wakiondoka.

“Mage maisha yetu yapo hatarini tuta fanya nini jamani?”

Josephine alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Mage una onaje uka wasiliana na askari watu hao waka kamatwa?”

“Levina hiyo ina wezekana ila ita kuwa ni kazi bure”

“Kwa nini?”

“Hata wakikamatwa basi wataachiwa huru. Hawa watu ni wa nabii Sanga. Mwanaye ana kwenda kuwa mkwe wa raisi, hivyo nina imani umoja wa kuungana kwa familia hizo uta palekea nabii Sanga kuzidi kuwa na nguvu.”

“Tuna fanyaje?”

“Laptop yako ipo wapi?”

“Nime iacha nyumbani”

“Basi kuna mtu mmoja ndani ya serikali nina weza kushirikiana naye na tuka muangusha nabii Sanga kwa maana yeye na nabii Sanga picha haziendi kabisa?”

“Ni nani huyo?”

Levina aliuliza huku akiwa amejawa na shahuku kubwa ya kuhitaji kumfamu ni nani ambaye ana weza kusaidiana naye katika kumuangamiza nabii Sanga na kikundi chake chote.



Magreth akaipata namba ya RPC na akampigia, kwa bahati nzuri simu hiyo ikaanza kuita.

“Magreth”

“Ndio muheshimiwa samahani sana kwa kukusumbua usiku huu”

“Hakuna shaka kwa maana nipo doria sasa hivi”

“Nyumbani kwangu nime vamiwa”

“Na nani na saa ngapi?”

Bwana Karata alizungumza huku akiwa amejawa na mstuko sana.

“Sijajua ila nina omba msaada wako muheshimiwa”

“Niambie upo wapi kwa sasa ili nikusaidie’

“Ngoja nikutumie video ya uvuamizi wa watu hao kwanza”

“Sawa nitumie sasa hivi”

Magreth akakata simu na kuanza kumtumia RPC Karata video hiyo.

“Ni nani huyo Mage?”

“Ni RPC Karata, ni mtu wangu wa karibu”

“Hapo ni sawa kwa maana yule baba ana ifanya kazi yake kwa haki sana”

Josephine alizungumza huku akimtazama Magreth.

“Sasa sinto hitaji polisi waje hapa. Itawabidi nyinyi mubaki hapa na mimi niende kuonana nao”

“Hapa ni salama kweli Mage tusije tuka vamiwa?”

“Hakuna anaye weza kuja hapa, niaminini katika hilo”

Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama rafiki zake.

“Sawa kuwa muangalifu”

“Sawa”

Magreth akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo. Akafika maeneo ya Mwenge na kusimama kwenye sheli iliyopo eneo hilo. Akampigia simu RPC Karata na akahidi ata fika eneo hilo baada ya muda mfupi tu. Defender ya polisi, ikafika eneo hilo la sheli, wakashuka askari sita wenye bunduki kisha RPC naye akashuka.

“Magreth pole sana”

RPC Karata alizungumza huku wakipena mkono na Magreth.

”Nashukuru, sana yaani nime poteza amani na nimeshindwa kabisa kukaa nyumbani kwangu”

“Tuzungumzie ndani ya gari lako”

Wakiangia ndani ya gari.

“Hizi sura ni ngeni sana machoni mwangu. Pia hatunazo kwenye database zetu za waalifu”

“Ni kweli muheshimiwa, ila hao ni watu wa nabii Sanga”

“Sanga huyu huyu au mwengine?”

“Huyo huyo mkuu. Yeye ndio aliye watuma kwa ajili ya kunia”

“Hivi lile bifu lenu hadi sasa hivi lipo?”

“Tena lime ongezeka na kukua kabisa. Yaani muheshimiwa nina kuomba unisaidie sana”

“Uwezo wa kukusaidia upo, ila jambo gumu sana ni kwamba huyu mzee kwa sasa ana lindwa na walinzi wa raisi. Hapo nina pata ugumu sana wa kumfwatilia na walisha nieleza kwamba nikiendelea kuwasumbua basi kuna mambo mawili, kushushwa cheo au kuhamishiwa mkoani huko”

“Sasa tuna fanyaje mkuu wangu. Ikiwa ni leo tu mrs Sanga ame toka kufanya tukio la mauaji”

“Mauaji? Nani ame muua tena?”

“Tomas”

“Tomas gani?”

“Yule aliye kuwa boyfriend wake”

“Yule mtu si tulimtafuta hadi ikafikia kipindi akataka kunifukuzisha kazi. Alikuwa wapi kipindi chote hicho?”

“Alikuwa ana ishi kwa sura ya bandia.”

“Wee!!?”

“Ndio hivyo leo hii ame uwawa na mrs Sanga kwa kuchomwa sindano ya sumu”

“Mungu wangu, yule mama kumbe ni katili kiasi hicho?”

“Ni zaidi ya katili. Ana hitaji kunia mimi na Evans ambaye juzi alitekwa pale daraja la Kigamboni”

“Hiyo niliipata na kuna habazi za chini ya kapeti kwamba ana swaka na muheshimiwa mwenyewe”

“Raisi?”

“Ndio, sijajua ni kitu gania mbacho amekifanya, ila sijui kama akipatikana ana weza kuachwa akiwa hai”

Magreth akashusha pumzi huku akimtazama RPC Karata.

“Hii nchi sasa ime haribika. Uwezo wa raisi kuongoza sasa ume yumba. Amekuwa ni mtu wa kufukuzisha watu kazi. Mkuu wa kitengo cha NSA amefukuzwa kazi, mshauri wake namba moja pia ame mfukuza kazi hivyo hatujui nani ata fwata. Ndio maana una niona nina jihusisha mambo ya uhalifu wa mkoa wangu tu ila mambo ya kufwatilia wakuu nime kaa kimya mdogo wangu”

“Ehee Mungu sijui nita ishije, sijui ni nani ambaye ata niua. Nashindwa hata kesho kwenda kazini kwangu”

“Ni kweli, ila Mage kuna uwezo fulani niliuona kwako, kwa nini usiitumie?”

“Uwezo gani?”

“Siku ulipo watandika mrs Sanga na mume wake. Kwa nini usiutumie ule uwezo kupambana na maadui zako”

“Nikiutumia wewe ndiye utakaye kuja kunikamata.”

“Ni kweli, ila ina kupasa kutumia akili kupambana na hawa watu. Yaani sasa hivi wewe nina kufananisha na Daud na Sanga ni Gholiath. Ukisema utumie njia za kieshiria my dear una kwenda kupotea. Tumia uwezo wako hakikisha Sanga ana anguka”

“Nashukuru kwa maneno yako, nita yafanyia kazi”

“Nina imani kwamba ume nilewa?”

“Nimekueleawa vizuri sana”

“Utakapo kuwa na uhitaji wa information zozote za ndani ya serikali ambazo una hisi kwamba zita kusaidia, basi nita kupatia ili mradi ninacho hitaji ni kumuona nabii Sanga utawala wake una kwisha”

“Nashukuru sana RPC na nime furahi kwa ushirikiano wako”

“Wala usijali katika hilo. Uta ishi wapi kwa sasa?”

“Nipo kwa rafiki yangu Mbezi beach hapo.”

“Ahaa sawa, ila ushauri mwengine usipende kutumia sana hili gari lako. Ikiwezekana nunua hata gari ndogo ambayo itakuwezesha katika mizunguko yako ya hapa mjini si una jua hili gari alikununulia yeye”

“Ndio”

“Basi fanya hivyo”

“Nashukuru sana kaka yangu”

“Karibu sana”

RPC Karata akashuka kwenye gari la Magreth, akaingia kwenye gari lake na vijana wake na wakaondoka eneo hilo huku naye Magreth akirudi alipo waacha rafiki zake.

***

Evans akafikia kijijini kwao majira ya saa kumi na moja alfajiri. Akasimamisha gari lake nje ya nyumba yao ambayo kwa kweli hajabadilika kwa chochote. Umasikini na ufukara alio nao mama yake hakika uka mfanya kuanza kulengwa lengwa na machozi.

“Ume fika salama sasa”

Sauti ya jini Maimuna ikamstua kidogo.

“Yaa nina imani kwamba mama ata kuwa bado haja aamka?”

“Ni kweli bado haja aamka”

“Nahitaji kubadilisha haya mazingira ya hapa kijijini, nahitaji kujenga nyumba kubwa eneo hilo”

“Ina wezekana kujenga, unajua wewe ni binadamu na una paswa kuishi mahala pazuri.”

“Ita kuwaje tukiamua kurudi Dar es Salaama kama vile ulivyo niambia”

“Hakuna mashaka, jambo zuri ni kwamba uta kuwa ume acha mazingira mazuri nyumbani kwenu”

Evans akashuhudia pazia la chumba cha mama yake likifunguliwa kwa tahadhari huku akichungulia nje.

“Mama yangu ame amka”

“Nenda kamsalimie”

Evans akafungua mlango wa gari na akashuka huku akiwa na furaha.

“Mama ni mimi mwanao”

Evans alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Ngolo ni wewe?”

“Ndio mama ni mimi, nime rudi mwanao”

Mama Evans akafungua mlango, akatoka kwa furaha na wakakumbatiana na mwanaye. Miaka karibia minne Evans hakuwa amerudi nyumbani kwao, hii ni kutokana na kukosa nauli za kurudi kila likizo.

“Tazama mwanangu ume kuwa mkubwa. “

“Ndio mama una endeleaje?”

“Kama ulivyo tuacha mwanangu. Hii gari ni ya kwako Ngolo”

“Ndio mama”

Mama Evans akamuachia mwanaye na kulisogelea gari hilo, akaanza kulizunguka, hakika hakuwa na ndoto hata siku moja kwamba mwanaye ana weza kuwa na hata gari. Japo Maimuna yupo ndani ya gari ila mama Evans hakuweza kumuona.

“Una funguaje mlango Ngolo”

“Hapa”

Evans alizungumza huku akifungua mlango wa upande wa dereva. Mama yake akaingia huku akiwa na furaha sana.

“Jamani Ngolo, Mungu ni mkubwa jamani, hadi ume nunua gari Mungu akubariki mwanangu zaidi ya hapa”

“Nashukuru sana mama. Evelin yupo wapi?”

“Bado ame lala, si unajua leo ni jumamosi haendi shule”

“Amekuwa mkubwa ehee?”

“Ndio,ame kuwa ni mdada sasa. Yupo kidato cha tatu”

Mama Evans alizungumza huku akishuka kwenye gari hilo. Akamshika mkono Evans na wakaanza kuelekea ndani. Maimuna akamkonyeza Evans na akamuga. Mama Evans akaingia chumbani kwa Evelin na kuamuasha.

“Nini mama”

“Kaka yako ame kuja, vaa vizuri”

“Mama una ota au?”

“Sioti wewe, amka kaka yako ame kuja”

Evelin kwa haraka akajifunga kanga na kutoka chumbani hapo. Akasita kidogo alipo muona Evans akiwa ame kaa sebleni. Akamkimbilia na waka kumbatiana kwa furaha sana huku machozi yakiwamwagika.

“Mama maisha yetu yana kwenda kubadilika. Nahitaji kukujengea gorofa hapa”

“Kaka acha zako”

“Haki ya Mungu nahitaji kijijini hapa niwe mtu wa kwanza kujenga gorofa”

“Anayo yasema kaka yako ni kweli, hapo nje ame kuja na gari”

Evelin akamuachia kaka yake na kutimkia nje. Hakuamini kuona gari la kaka yake, kwa jinsi ufukara ulivyo itawala familia hiyo, ni jambo la ajabu sana kwa kaka yake kumiliki gari kama hilo.

“Mama jiandaeni, twendeni mjini tukafanye kwanza manunuzi ya nguo na vitu muhimu vya ndani baada ya hapo tuta jua tuna fanya nini ili turekebishe hili eneo”

“Sawa mwanangu. Wewe Eve sasa zubaa zubaa, tuna kuacha peke yako”

Mama Ngolo au Evans alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Evans akaelekea kwenye karuburi la baba yake lililopo pembezoni mwa nyumba hiyo. Taratibu akachuchumaa na kuanza kung’oa ng’oa vimajani vilivyopo eneo hilo.

‘Baba uli shindwa kutulea kwenye mazingira mazuri. Ila nisamehe kwa kuwahi kukuondoa duniani, ila sikuwa na jinsi siku ile kwa maana mama yangu ni muhimu sana kuliko wewe”

Evans alizungumza maneno hayo huku akilini mwake akikumbuka siku aliyo muua baba yake.

***

Simu ya Magreth ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaipokea.

“Ndio Levina”

“Naomba kama ina wezekana, unichukulie laptop yangu nyumbani kwako”

“Sawa”

Magreth akakata simu,akageuza gari lake na kuelekea nyumbani kwake eneo la Kigamboni. Akasimamisha gari lake mita chache kutoka ilipo nyumba yake. Akatambea kwa haraka hadi getini kwake, akatazama eneo zima kama lina usalama, akaingia ndani kwake, akachukua laptop yake, kisha akaingia chumbani kwa Levina na kuchukua laptop hiyo kisha akandoka nyumbani hapo. Akafika alipo waacha Levina na Josephine.

“Vipi huko ni salama?”

Josephine aliuliza huku akiwa na wasiwasi. Levina akamkabidhi laptop yake na wakaingia ndani.

“Nimezungumza na RPC Karata na ameweza kuelewa hali halisi ambayo tuna pitia na ukweli ni kamba hana msaada wa kutusaidia kwa maana kama ni hilo kundi lipo chini ya nabii Sanga, yeye hana uwezo wa kufanya chochote”

“Mungu wangu sasa tuta fanyaje Magreth?”

Josephine aliuliza kwa unyonge.

“Hatuna namba ya kufanya zaidi ya kujilinda sisi wenyewe.”

Levina akashusha pumzi huku akionekana kukata tamaa kabisa.

“Tukijituma tuta ishi, ila tukizembea tuta kufa. Je ni nani kati yenu ana hamu ya kufa na ujana huu?”

Levina na Josephine wakatazamana.

“Mimi hapana”

Levina alijibu kwa msisitozo.

“Hata mimi?”

“Sawa, tupo watatu ila tuta kuwa ni kama jeshi la watu elfu tatu. Hapa ninacho kifanya ni kuanza kugawa majukumu. Jose una uwezo wa kuona maono, nini kina kuja au nini kina fanyika. Levina una utaalamu wa mambo ya teknolojia. Mimi nina uwezo wa kupigana na ina mafunzo maalumu ambayo nime fuzwa toka nikiwa mtoto mdogo. Mbele yetu tuna maadui wakuu wawili SANGA FAMILY na JERY MTENZI. Tunacho paswa kufanya hivi sasa ni kuhakikisha tuna wawinda wote wawili na tukiwapata hakuna msamaha. Tuna waua mmoja baada ya mwengine tume elewana?”

“Ndio”

Levina na Josephine wakajikuta wakijibu kwa pamoja huku wote mioyoni mwao wakiwa wame kubaliana na wazo hilo kwani pasipo wao kufanya juhudi zozote za kumsaidia Magreth basi wata angamia.



Hadi asubuhi kuna pambazuka hapakuwa na hata mmoja wao aliye pata hata lepe la usingizi. Magreth akaingia kwenye chumba cha siri, akachukua sanduku lenye vifaa vya mapigano pamoja na nguo zake maalumu ambazo ata zitumia katika kazi yake yote ya mauaji.

“Hilo sanduku lina nini?”

Josephine aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao. Magreth akafungua sanduku hilo.

“Waoooo”

Levina alihamaki huku akitazama vifaa hivyo ambavyo mara nyingi ame kuwa akiviona kwenye filamu za wa Japani na wachini.

“Hii niliona kwenye ile movie ya Ninja Assasination”

Levina alizungumza huku akiwa ameshika kishu kilicho jikunja alafu kina cheni ngumu na ndefu.

“Yaa hichi kisu kwa pigo moja la ukakika endapo, kikipita shingoni mwa mtu, kina ondoka na shingo yake.”

“Weee”

“Ndio kina ondoka na shingo yake, ni kikali na nina weza kumpiga mtu wa mbali pasipo ya yeye kunisogelea hata kidogo”

“Hivi ni nini?”

Josepgine aliuliza huku akiwa ameshika nyota yenye ncha nne na kali sana.

“Hiyo ina itwa Star, lete nikuonyeshe utendaji wake wa kazi”

Magreth akaichukua kifaa hicho kilicho kaa mithili ya nyota na akakirusha ukutani na kika nasa.

“Hiyo endapo ita ingia kwenye mwili wa bina damu ana kufa ndani ya dakika tano kwa maana ina sumu kali sana ambayo ina muua mwana damu.”

“Heee zipo nyingi”

“Ndio”

“Umezitolea wapi hizi?”

“Hii nyumba kipindi mimi nipo mdogo kuna mzee mmoja wa kijapani alikuwa ana ishi hapa. Mzee yule alikuwa ana penda sana maandazi ya mama yangu alivyo kuwa ana yapika. Basi yule mzee alimuomba mama awe ana kuja kumpikia kila asubuhi na kumfanyia usafi. Mimi nami nilikuwa nina ambatana na mama. Yule mzee alitoka kunipenda sana hivyo akaanza kunifundisha mafunzo taratibu ya kijapani. Hata lugha ya kijapani akaanza kunifundisha. Baada ya miaka kadhaa, muda wa yeye kuishi Tanzania ukawa umesha kwisha, ika mlazimu kuondoka”

“Sasa kama alikufundisha kwa nini hukujiunga na polisi?”

“Nilishindwa mambo mengi kwani mama yangu alianza kusumbuliwa na ungonjwa wa moyo. Ilinichukua kipindi kirefu sana kumuuguza na baada ya kumuuguza kwa kipindi huku tukiwa mara nyingi nina mpeleka kanisani kusali, basi nami nili okoka na nikwa na Mungu ndani yangu. Hadi mama ana fariki sikuwa na jinsi zaidi ya kuendeleza biashara ya mama ambayo kipindi ana umwa mimi ndio nilikuwa nina ifanya, nika achana kabisa na mambo haya hadi pale mambo yalipo badilika, nami ime ilazimu kuwa hivi”

“Waoo pole kwa mama kufa”

Levina alizungumza kwa sauti ya upole kidogo.

“Nina shukuru, nimesha poa. Kipindi kile mama alinisisitizia sana niwe mple na nisiwe mtu maugomvi gomvi namshukuru Mungu niliishia kwenye msingi huo.”

“Sawa tuachane na hayo Mage. Je una mpango gani?”

Magreth akakunjua karatasi kubwa aliyo chora ramani ya ukumbi mzima wa send off ya Julieth.

“Hizi ni ramani ya ukumbi utakapo fanyika send off ya Julieth. Ulinzi uta kuwa ni mkubwa sana. Nina hiyaji kuhakikisha kwamba bi harusi tuna mchukua akiwa ukumbini?”

“Kwani una mpango wa kumteka Julieth na si nabii Sanga?”

Levina aliuliza huku akiwa na msnag

“Nina mpango wa kumteka yeye?”

“Kwa nini bi harusi, unajua uki mteka yeye tuta swaka Tanzania nzima mimi nina shauri mpango wetu uendelee vile vile. Tudili na nabii Sanga”

Levina alishauri huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Sawa tuangalie shabaha yetu ita tua wapi. Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba hatu feli kwenye jambo lolote lile”

“Mmmm nime pata wazo”

Levina alizungumza.

“Wazo gani?”

“Ile video ya nabii Sanga na Tomas unayo?”

“Ndio bado ninayo?”

“Video gani?”

Josephine aliuliza huku akiwa na shahuku kubwa ya kujua ni video gani.

“Nionyesheni na mimi nina taka kuona”

Josephine alizidi kung’ang’ani kuonyeshwa video hiyo. Magreth hakuwa na jambo la kuficha, akaiweka video hiyo kwenye simu yake na kumuonyesha Josephine.

“Ohoo Mungu wangu!! Huyu si mrs Sanga?”

“Ndio mama yenu wa kanisa”

“Jamani hapa si ana ingiliwa kinyume na maumbile?”

“Ndio”

“Heee kumbe huyu mama ni mchafu kiasi hichi?”

“Ndio maana yake”

Josephine akajikuta akishusha pumzi huku akiendelea kuitazama video hiyo.

“Mage hatuna haja ya kutumia nguvu, akili pia ni moja ya jambo muhimu. Wewe niachie alafu tuta jua ni kitu gani cha kufanya”

Levina alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana.

***

Siku zikazidi kusonga mbele na siku ya send off ya Julieth ika fika. Mamia ya wageni kutoka nchi mbalimbali wamefika nchini Tanzania kwa kushangulia send off na harusi ya mtoto wa raisi. Mahoteli yote yenye hathi kubwa jijini Dar es Salaam yame jaa na ulinzi ume imarishwa mara dufu. Vyombo vya habari vyote nchini na nje ya Tanzania vina tangaza juu sherehe hiyo ambayo ni kubwa sana kuwahi kutokea nchini Tanzania. Ukumbi wa sherehe ya send off ulinzi ume imarishwa kisawa sawa, hakuna mtu ambaye aliruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi pasipo kibali muhimu.

“Vipi ume fanikiwa?”

Magreth alizungumza huku wakiwa awamekaa kwenye chumba kimoja cha gorofa ambacho kipo upande wa barabara kutoka lilipo gorofa hilo.

“Najaribu ku hack kameza zao ila una onekana una badilishwa kila muda”

Levina alizungumza huku akiendelea kuminya batani za laptop yake.

“Kwa hiyo hiyo video hatuwezi kuionyesha ukumbi mzima?”

“Najaribu, tusikate tamaa”

“Mimi nina wazo?”

Josephine alizungumza huku akiwa amekaa kitandani.

“Wazo gani?”

“Muna onaje tuka subiria siku ya harusi ndio tuonyeshe hiyo video na ukitegemea harusi ni kesho kutwa. Hivyo tuna kesho na kesho kutwa?”

“Wazo lako ni zuri best?”

Magreth alizungumza huku mtazama Josephine ambaye kwa sasa mguu wake umesha pona.

“Nipeni dakika thelathini nina endelea kuhushulika na hilo”

“Hivi haiwezekani kuituma kwenye mitandao ya kijamii?”

“Hiyo ina wezekana, ila ndani ya muda mchache wana weza kuifuta. Hivyo haito noga”

“Sawa kazi ni kwako”

Levina akaendelea na kazi yake hiyo huku Magreth akiwa amesimama pembeni ya dirisha akitazama jinsi askri wanavyo linda ukumbi huo wa send off.

***

“Ume pendeza sana mwanangu”

Mrs Sanga alizungumza huku akimtazama Julieth aliye pambwa vizuri.

“Asante mama”

“Mdogo wetu hivi una jua wewe ni mzuri sana”

Mtoto wa kwanza wa nabii Sanga alizungumza huku wakimtazama Julieth wakiwa ndani ya gari la kifahari lenye milango sita.

“Nashukuru”

“Ila mdogo wangu una bahati sana. Kuolewa na mtoto wa raisi sio jambo la mchezo mchezo”

“Hahaa mbona ni kitu cha kawaida”

“Mmmm sisi tunaishi Marekani ila hata mtoto wa raisi hatuja bumiana naye”

“Alafu na nyinyi muoe na sio kushangaa shangaa magofora huko Marekani”

“Mama tuta oat u si una jua kwamba wanaume sisi ni lazima uangalie ni mwanamke gani mzuri, sio kukurupuka tu na kuoa”

“Ila umri una kwenda nahitaji mjukuu mimi”

“Sawa mama usijali”

Furaha ikazidi kutawala kwa familiaya mrs Sanga, huku wakiwa wana subiria muda wa kuingia ukumbini.

“Karibuni sana”

Nabii Sanga alizidi kuwakaribisha wageni wanao ingia ukukumbini hapo

“Tuna shukuru nabii wa Mungu”

Watu walizidi kumiminika na kuingia ndani hapo.

“Muheshimiwa una itwa na raisi”

Mlinzi mmoja alimnong’oneza nabii Sanga. Wakaondoka na mlinzi huyo na wakaingia ndani gari ya raisi.

“Naona mambo yame fika”

“Ndio ndugu yangu.”

“Tume imarisha ulinzi kila mahala hivyo usiwe na shaka ndugu yetu. Lazima watu wafurahie vijana wetu”

“Ni kweli, Jery yupo wapi?”

“Jery yupo gari moja na mama yeke. Lile pale”

“Sawa ndugu yangu”

“Una weza kuwaona”

“Nashukuru”

Nabii Sanga akashuak kwenye gari hilo na kuingia kwenye gari alipo Jery na mama yake.

“Baba mkwe heshima yako”

“Nashukuru sana. Umependeza kwa kweli”

“Kidogo baba”

“Hapana ume pendeza sana aisee.”

“Asante”

“Mkwe wangu karibuni sana mujisikie huru na mujisikie mupo sehemu salama kabisa”

“Tuna shukuru”

Mrs Mtenzi alijibu kwa utaratibu huku akimtazama nabii Sanga. Nabii Sanga akashuka kwenye gari na kuelekea kwenye gari walipo familia yake.

“Waooo mume pendeza sana wanangu”

“Asante baba”

“Ehee niambieni mume jiandaa vizuri na kucheza kwa maana musije muka tia aibu kwa kuingia ukumbini pale”

“Usijali baba tuna bonge moja la suprize kwenye kuingia ukumbini”

“Haya kazi ni kwenu”

Muda wa kuingia ukumbini ukawadia. Wakaanza kuingia wazazi wa bi harusi kisha wakafwatia wazazi wa Jery. Muda wa Julieth na kaka zake kuingia ukumbini ukawadia. Ukumbi mzima ukazizima kwa ukimya. Ukaanza kupigwa mlio kinanda, Julieth akaweka katikati ya kaka zake ambao wakaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu mithili ya gwaride la jeshi jinsi wanvyo tembea kwa mwendo wa taratibu mbele ya raisi. Kwa jinsi kaka zake wanavyo fanana na utembeaji huo hakika uka wavutia watu wengi. Julieth kazi yake ikawa ni kutembea kwa mwendo wa kawaida huku akipunga mkono kwa wageni waalikwa wa eneo hilo. Kila mwenye simu ambayo ina uwezo wa kurekodi video hakusita kuchukua video ya tukio hilo.

***

Magreth na Josephine macho yao yote yapo kwenye tv iliyopo chumbani hapo wakishuhudia sherehe hiyo ya send off inayo rushwa hewani mubasha.

“Ila amependeza bi harusi”

Josephine alizungumza na akajikuta akitazamwa kwa jicho kali sana na Magreth.

“Ohoo samahani ame tisha”

“Hapana una ogopa nini, ni kweli ame pendeza.”

“Sasa mbona ume nitazama kwa jicho kali?”

“Nime kutazama tu kwa ni vibaya jamani”

“Mmm haya.

“Levina kama ume shindwa dada yangu. Achana nalo tu hilo swala tuta dili nalo kwenye harusi”

“Sijawahi kushindwa na kitu chochote”

Levina alizungumza huku akizidi kuumiza kichwa kuhakikisha ana ipenyeza video ya ngono ya mrs Sanga kwenye tv zilizo fungwa ndani ya ukukumbi huo.

“Mmmm haya mama”

Levina akafumba macho yake kwa sekunde thelathini kisha akayafumbua na kuwatazama Magreth na Josephine.

“Vipi mbona ume tukazia macho?”

Magreth alizungumza huku akimtazama Levina anaye onekana kukata tamaa. Baada ya sekunde kadhaa Levina akatabasamu kwa furaha.

“Kazi ime kamilika je naweza kuituma sasa”

Kauli hiyo ikawafanya Magreth na Josephine kukurupuka na kushuka kitandani kwa haraka na kumfwata kwenye meza aliyo kaa huku akiwa amesha andaa kidole chake kimoja kuminya batani ya kuiruhusu video hiyo ya ngono ya mrs Sanga na Tomas kuonekana kwenye tv za ukumbi wa send off



“No usiitume”

Josephine alizungumza huku macho yakiwa yame mtoka.

“Kwa nini?”

Levina aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Huu sio muda wake. Ukifanya hivyo ni lazima wata jua ni wapi tulipo na kumbuka hao nao wana watu wenye ujuzi kama wako”

Josephine alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama Levina na Magreth.

“Hilo ndio nililo onyeshwa sasa hivi, niaminini katika hilo”

Levina akatoa kidole chake kwenye batani ambayo kama ange iminya, video hiyo inge onekana kwenye tv zote za ukumbi huo.

“Laiti kama unge jua jinsi nilivyo umiza kichwa wala usinge zungumza hivyo”

Levina alizungumza hukua akinyanyuka na kuingia bafuni.

***

“Tuna siku mbili za kujiandaa katika mpango wetu. Jiji la Dar es Salaam kwa sasa lina ulinzi mkali sana, ina tupasa kuwa makini sana”

Omary kiongozi wa kundi hio la watoto la Al-Shabab alizungumza huku akiwatazama wezake.

“Muda wa kujitoa muhanga ni saaa tisaa kamili alasiri. Maeneo ya kujitoa Muhanga yataongezeka, badala ya kuwa matatatu sasa yataongezeka na kuwa saba. Kariakoo, Stendi ya mbezi mwisho, Kimara mwisho kwenye stendi ya mabasi ya mwendo kasi. Stendi kuu ya mabasi Ubungo. Tazara, Central polisi na ndnai ya kanisa litakalo fungisha ibada. Tuna kwenda kufa, ila tuna kufa kwa faida, majina yetu yataandikwa mbinguni na mwneyezi Mungu ata tuandikia haki ya hichi tunacho kwenda kukifanya.”

Meneno ya Omary yakazidi kuongeza munkari kwa wezake ambao siku zote wame kuwa wakifundishwa na kuamini kwamba, unapo jitoa muhanga basi hiyo ina kuwa ni zawadi kubwa sana kwa mwenyezi Mungu.

“Kila mmoja ata kuwa na simu yake ya smart phone, simu hizi ni bomu kubwa ambalo lina weza kulipua eneo kubwa sana. Hakuna amabaye ana weza kufahamu kwamba simu hizi ni mabomu kwa maana hata mtu wa kawaida atakapo zitazama ana weza kupiga na kuongea na mtu mwengine kama kawaida”

“Naimani kila mmoja ana fahamu juu ya matumizi ya simu hizi, code zake ni 6616”

“Ndio”

“Tume kija Tanzani si kwa ajili ya kushangaa uzuri na magorofa yake. Tume kuja kulipiza kisasi kama vile walivyo fanya mauaji kwa ndugu zetu wapendwa. Watakao salia basi kazi yenu ni kuhakikisha kwamba muna shambulia watu kwa kutumia risasi. Tumelewana?”

“Ndio”

“Hapo kesho nita gawa majukumu kuhakikisha kwamba kila mtu ana tambu ni eneo gani ambalo ata fania kazi”

“Sawa sawa”

***

“Hii serikali bwana ina nichekesha?”

Mzee Mbogo alizungumza huku akiwatazama vijana wake wanao endelea kuhakikisha kwamba ulinzi una kuwa imara kwenye nchi nzima.

“Kwa nini mkuu?”

“Hadi sasa hivi kitengo cha NSA, hakijarudi hewani, yaani hapa nchi ulinzi wake ni imara huko mipakani ila ndani hakuna kitu”

“Ndio muheshimiwa, ila sisi si tupo?”

“Ndio tupo ila hakuna ambaye ana weza kuheshimu uwepo wetu”

“Wata heshimu uwepo wetu pale kutapo tokea tukio”

“Sawa ila hatuja ona dalili yoyote ya Al-Shabab?”

“Sidhani kama wana weza kufanya lolote, kama leo hii wame shindwa kufanya chochote kwenye hii send off iliyo jaza maelfu ya watu basi hawato weza kufanya chochote hata kwenye harusi”

“Sawa ila tusijiaminishe sana. Tuna paswa kuwa makini”

“Usijali muheshimiwa, timu yetu ime jipanga vizuri sana”

“Sawa nafurahi kusikia hivyo”

Mzee Mbogo akaondoka chumbani hapo na kuingia katika chumba chake cha kulala. Akawasha tv na kuendelea kuitazama send off ya mtoto wa nabii Sanga.

‘Binti ume mletea kijana wa watu matatizo ambayo hakuyatarajia kabisa’

Mzee Mbogo alizungumza huku akiendelea kumtazama Julieth ambaye amependeza kisawa sawa.

***

Watu wengi ndani ya ukumbi hususani wadada, wana hamu kubwa ya kumuona bwana harusi ambaye ana anza kutafutwa na Julieth. Julieth akiwa ameongozana na kaka zake, wakaanza kuzunguka ndani ya ukumbi huo kumtafuta Jery. Wakafanikuwa kumuona Jery akiwa amekaa kwenye moja ya meza iliyo zungukwa rafiki zake. Taratibu Julieth akamkumbatia Jery na kumpa busu moto moto. Akamvalisha saa iliyo tengenezwa kwa garama kubwa sana. Kila msichana aliye hudhuria ukumbini hapo, alihisi moyo wake kupata mstuko, uzuri wa Jery hakika uliweza kuwapagawisha wengi. Julieth na Jery wakarudi hadi eneo la mbele la ukumbi huo, waandishi wa habari na wapiga picha kila mmoja alihakikisha ana pata picha nzuri ya wawili hao.

Baada ya utambulisho wa pande zote mbili ulio fanywa na Jilieth na Jery, muda wa kupata chakula uka wadia kwa watu wote.

“Shemeji”

“Ndio”

“Dada yetu si una muoa alivyo mzuri?”

“Ndio shemeji”

Jery alijibu huku wakiwa wamekaa kwenye meza yao maalumu wakijipatia chakula.

“Tuna hitaji dada yetu awe mzuri zaidi ya hapa.”

“Musijali shemeji zenu. Nita mlinda, nita muheshimu, nita zidi kumpenda na nita hakikisha dada yenu ana kuwa na furaha kwenye kipindi chote cha maisha yake”

“Sawa yetu ni hayo tu. Isije uka tumia kigezo cha kusema mimi ni mtoto wa raisi hivyo nina uwezo wa kufanya chochote dada yetu, aisee tuta rudi Tanzania kwa ajili yako endapo ata tupatia mashtaka ya aina yoyote”

Kaka mkubwa wa Julieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Jery usoni mwake.

“Musijali, ila kwa nini musije kuwekeza Tanzania biashara zenu?”

“Hakuna pesa.Una jua Marekani kulu, kufanya biashara ni rahisi sana kuikuza kuliko Tanzania. Tanzania apa kwanza ukitazama sera za uwekezaji kidogo zime bada. Makodi ni mengi yaani yana katisha tamaa sana kwa wafanya biashara”

“Nita jaribu kuzungumza na baba ili alegeze kidogo kwenye hilo”

“Zungumza naye mambo yakiwa mazuri basi tuta kuja kuwekeza.”

“Nashukuru sana”

“Ila shemeji usisahau tuliyo kuambia. Dada yetu ndio mboni ya familia yetu, yupo peke yake na hatuna dada mwengine”

“Nime waelewa mashemeji zangu”

Wakamaliza kupata chakula hicho na wakarudi kujwaani. Sherehe ikaendeshwa hadi majira ya saa tano na nusu usiku ika malizika. Ulinzi uka zidi kuimarishwa, baada ya bibi harusi mtarajiwa kutoka ukumbini, uka wadia muda wa wazazi kutoka.

“Hakika nime ipenda sana sherehe ime kuwa nzuri na ime pendeza”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa furaha huku akipeana mkono na nabii Sanga.

“Nashukuru sana ndugu yangu”

“Nina imani muta tutunzia bibi harusi hadi siku yake ya ndoa”

“Ndio ndugu yangu”

“Basi acha sisi tuwahi ikulu. Muda ume kwenda”

“Tuna shukuru kwa kujitoa kwako muheshimiwa”

“Wala usijali muheshimiwa”

Raisi Mtenzi na mke wake, wakapeana mikono na nabii Sanga pamoja na mkewe, kisha wakaondoka eneo hilo. Nabii Sanga akaingia kwenye gari walilo panda wana familia yake.

“Baba hongera sana, sherehe ilikuwa bombastiki”

“Nashukuru sana wanangu, ehee nanyinyi lini kwa maana kama ni mdogo wenu ndio amesha anza hivyo?”

“Hata mimi nil wauliza ila naona hawajanipatia jibu la kueleweka”

“Baba tuta oa tu?”

“Llini kwa maana umri una kwenda. Wewe una miaka thelathini na mbili, mwenzio miaka ishirini na nane. Lini muna oa?”

Nabii Sanga alizidi kusisitizoia huku wakisubiria msafara wa raisi kondoka ukumbini hapo. Baada ya masafara kuondoka na waoa wakaanza kuondoka huku nao msafara wao ukisindikizwa na gari za askari, kuhakikisha bi harusi na familia nzima wana kuwa salama.

***

“Yaani hiyo kesho kutwa sijui kama tuta fanikiwa”

Levina alizungumza huku akiwa na hasira kidogo, juhudi zote alizo zifanya kwa siku nzima ya leo zime kuwa bure kabisa kwake.

“Levina ina bidi muda mwengine tumsikilize Josephine, huwezi jua kama tunge fanya vile ni jambo gani ambalo linge tokea. Hapa jambo la kufahanya ni kuhakikisha sote tuna kuwa salama na si kufanya ili mradi wa kufanya”

“Sawa nime walewa. Sherehe ndio hiyo ime isha na hakuna hata mende aliye leta shida kwenye eneo hilo”

Levina aliendelea kulalama huku akijifunika shuka,

“Muna onaje nika mtesa mrs Sanga kisaikolojia?”

“Kivipi?”

“Nikampigia simu na kumueleza juu ya mambo aliyo yafanya na nita mueleza kwamba nita ipost video hiyo kwenye mtandao”

“Magreth hilo sio wazo zuri kabisa kwa maana kwa sasa wata kusaka na wata kuua live live”

Levina alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Anacho kizungumza Levina ni kweli. Tusubirieni siku ya harusi nina imani kazi yetu ita kwenda vizuri”

“Haya”

Wakalala katika hoteli hiyo na siku iliyo fwata asubuhi na mapema wakaelekea katika nyumba wanayo ishi kwa muda.W

“Mpango wetu wa jumamosi kwenye harusi una kuwaje?”

Levina aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Nipeni siku ya leo nikilala nikiamka kisha nita wapatia jibu”

Josephine aliwashauri wezake na wakakubalian ana wazo hilo, Siku hiyo nzima wakaitumia katika kutazama filamu ambazo wana zipenda.

“Juma upo wapi?”

“Kwenye mgahawa bosi”

“Tuletee chakula kama kawaida”

“Sawa bosi”

Magreth akakata simu na baada ya muda lisaa Juma akafika katika nyumba hiyo.

“Biashara zina kwendaje?”

“Ina kwenda poa bosi si una jua sisi ndio wauzaji bora wa chakula hapa mjini”

“Sawa Juma pesa uta ziingiza benki?”

“Tayari nimesha ziingiza za leo”

“Sawa nita angalia baadae”

“Haya bosi acha mimi nirudi ofisini”

Juma akapanda pikipiki yake na kuondoka eneo hilo.

“Huyu kaka ni mzuri jamani”

Josephine alizungumza na kuwafanya wezake wamtazame.

“Si nimeongea ukweli mbona muna nishangaa jamani”

“Mmmmmm umempenda hivyo”

“Jamani kwani kumsifia mtu ni kumpenda?”

“Mbona Levina hajamsifia?”

“Yaishe jamani kwa maana na nyinyi muki ng’ang’ania jambo basi hamuliachi”

“Ila sema kama ume mpenda nikuunganishe naye. Huyo ndio mtu ninaye muamini kupita watu wotte pale kazini kwangu”

“Hivi ana itwa Juma eheee?”

“Ndio una taka namba yake ya simu?”

Magreth alimuuliza Josephine swali la mtego.

“Muda bado, ukifika nita kuambia”

“Wewe chelewa chelewa uta kuta mwana sio wako”

Wakapata chakula cha usiku kisha kila mtu akaingia kwenye chumba chake cha kulala. Magreth hakupata usingizi kabisa kwa maana mtu anaye muwazia ni nabii Sanga. Josephine akaanza kusali huku akimuomba Mungu amuonyeshe ni mambo gani ambayo yana kwenda kutokea kwenye siku ya jumamosi. Josephine akajikuta akistuka sana huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana. Akaa akanyanyuka na kukaa kitandani huku akijaribu kutafakari kitu alicho kiona.

‘Ehee Mungu hichi ulicho nionyesha ni kweli?’

Josephine alizungumza huku akitetemeka kwa woga sana. Akaanza kuomba tena na akazidi kuonyeshwa zaidi mambo ambayo kwenye maisha yake hakuwahi hata siku moja kuonyeshwa. Josephine akanyanyuka kitandani hapo na kutoka chumbani kwake. Akawagongea Levina na Magreth na wakatoka kwenye vyumba vyao.

“Kuna nini mbona ume tustua?”

“Nimeona?”

Josephine alizungumza kwa wasiwasi huku jasho likimwagika usoni mwake.

“Umeona nini?”

Magreth aliuliza huku akianza kujawa na wasi wasi kwani toka amfahamu Josephine hakuwahi kumuona katika hali hiyo.



Josephine akazidi kutetemeka huku akiwa amejawa na kigugumizi kikubwa sana.

“Jose tuambie ume ona nini?”

“Nimeona siku…hiiyoo kabla ya harusi mji mzima wa Dar ukiwa ni jehanamu ya moto. Wadada, watoto, wazee watu wa kila aina wakiteketea kwa moto. Siku hiyo Dar es Salaam haito kuwa salama kwa mtu hata mmoja. Ninacho washauri rafiki zangu tuondokeni Dar es Salaam. Sijawahi kuona kitu kama hicho kwenye maisha yangu yote ya kuomba”

Levina na Magreth wakatazamana.

“Tuwaambie watu tunao wapenda, hawatakiwi kuwa ndani ya mji kwa siku hiyo”

“Jose ulicho kiona ni kweli au?”

Levina aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.

“Haki ya Mungu ni kweli, niaminini, tena nime fanya kuota mara mbili mbili. Laiti kama mungekuwa munaona kile ninacho ona mimi au nina weza kuki rekodi na kukiweka kwenye flash basi ninge waonyesha”

“Huo moto una tokea wapi?”

“Sijajua una tokea wapi, ila hiyo siku hali ya Dar es Salaama haito kuwa nzuri kabisa”

“Ehee Mungu watngu”

“Mage muambie Juma hiyo siku asifungue mgahawa na watu wote wafanyakazi wote watoke nje ya jiji la Dar es Salaam”

“Sasa nina anzia wapi kumuambia?”

“Wewe ndio bosi, muambie ni amri na sio ombi. Levina kama una wafanyakazi wako waambie wote waachane na siku hiyo. Tafadhali niaminini”

“Sawa tuta fanya hivyo”

“Nawaomba sana mufanya hivyo”

Usiku huo huo wakaanza kusambaza habari kwa watu wanao wapenda na kila waliye mpigia simu wali msisitizia siku hiyo waweze kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam na walipo uliza ni kwa nini hawakuwaeleza ni kwa nini ila waliwasisitizia waondoke.

***

“Japo haito kuwa ni kisasi kile tunacho kihitaji ila siku hiyo ita kuwa ni siku ya kulia na kusaga meno kwa watu wote wenye mapenzi kwa familia ya nabii Sanga na raisi Mtenzi”

Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans aliye jilaza kitandani kwenye nyumba mpya yao mpya wanao endelea kuijenga.

“Ni kisasi gani hicho?”

“Siku hiyo kuta fanyika shambulizi moja kubwa sana na baya ambalo Tanzania halikuwahi kutokea”

“Shambulizi gani?”

“Siku kadhaa zilizo pita, raisi Mtenzi alishambulia kundi la Al-Shabab kima kosa. Vijana wa kundi hilo wame amua kulipiza kisasi. Hivyo siku hiyo wata ilipua Dar es Salaama kwenye maeneo yake muhimu sana na itakuwa ni siku ya kukumbukwa”

“Ehee Mungu wangu. Sasa hilo si lina weza likazuiliwa?”

“Hakuna ambaye ana weza kulizuia”

“Kwa nini ikiwa umesha nieleza?”

“Huo ni mpango ambao ume tolewa ili kuwa pigo kwa raisi Mtenzi. Kuna watu ambao ni muhimu sana kwenye serikali yake na hakupaswa kuwafukuza, ila yeye aliwafukuza, basi hayo yanayo kwenda kutokea ndio malipo yake ya kukosa ustamilizvu katika mipango yake.”

“Ila kuan raia ambao wana kwenda kufa pasipo sababu ya msingi”

“Ni lazima wafe”

“Ohoo Mungu wangu. Sasa ita kuwaje?”

“Jiji la Dar es Salaam lina kwenda kuwa moto.”

“Nina mpigia simu Mbogo na kumueleza juu ya hili jambo?”

“Hata ukimueleza hato weza kulizuia. Jambo ambalo una paswa kulifanya kwa sasa ni kumuambia ana paswa yeye na timu yake kuondoka katika jiji la Dar es Salaam tu. Akiwa mkaidi atakufa na watu wake, kwani mabomu ambayo yana kwenda kulipuliwa ni ya nyukilia na yametengenezwa kwenye ubora wa hali ya juu na hakuna ambaye ata jua mabomu hayo sehemu yalipo.”

“Ohoo Mungu wangu.

Evans alijikuta akikaa kitandani huku akihisi mwili wake kuishiwa na nguvu.

“Waambie watu unao wapenda kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam”

“Mage…..Magreth ndio wa kwanza”

Evans alizungumza huku akibabaika. Akaiwasha simu yake na kuiandika namba ya Magreth ambayo ana ifahamu kwa kichwa kuliko hata namba yake mpya.

“Shitiii namba yake ina tumika”

Evans alizungumza huku akizunguka zukunga ndani ya chumba hicho. Akapiga simu kwa mara nyingine na bahati nzuri ikaanza kuita.

“Halooo”

“Mage Mage”

“Evasn!!?”

Magreth alizungumza kwa mshangao.

“Ndio ni mimi sina muda wa kupoteza nisikilize kwa umakini”

“Ngoja kwanza upo wapi?”

“Sina muda wa kukueleza kwamba nipo wapi. Nahitaji kukueleza jambo moja na uliweke akilini. ONDOKA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM, usijaribu kuhudhuria harusi ya Jery na Julieth. Sawa?”

Magreth akashangaa sana kwa maana taarifa hiyo hiyo ambayo wao wana ishambaza kwa watu, ime mfikia Evans”

“Kumbe hata wewe ume ipata taarifa yangu?”

“Nimeipata kivipi?”

“Mimi, nipo na rafiki zangu hapa wawili, Josephine na Levina, tuna wasisitizia watu kuondoka kwenye jiji la Dar es Salaam”

“Nyinyi mume muaje ikiwa wewe ndio mtu wa kwaza kukupa habari?”

“Mimi nina rafiki yangu ambaye ana uwezo wa kuona mambo yajayo na ndio ame niambia. Niambie upo wapi nikufwate mpenzi wangu.”

Magreth alizungumza huku akiwa na furaha. Kitendo cha kuambiwa na Evans kwamba yeye ndio mtu wa kwanza kumueleza habari hiyo, ana amini bado upendo wake una ishi moyoni mwa Magreth.

“Ame ona nini yeye?”

“Ameona jiji zima la Dar es Salaam likilipuliwa siku hiyo kabla ya harusi”

“Duuu sasa tuna fanyaje kuwaokoa watu zaidi ya hawa?”

“Sijajua, ndio hivyo tuna wapigia simu na kuwaambia waondoke jijini Dar es Salaam”

“Nimepata wazo. Kwanini musifungue page ya Facebook, Instargram na Twitter, muwahimize watu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam.”

“Wazo hilo ni zuri, je tuna iitaje kwa maana tukifanya kazi hiyo serikali ina weza kutukamata na kutuambia kwamba tuna wapa hofu wananchi wake?”

Evans akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akitafakari majina ya page hizo yaitwaje.

“Nimepata jina”

“Jina gani?”

“Page zote ziiteni HARUSI YA JERY NA JULIETH NI HARAMU. MUSIHUDHURIE NA MUONDOKE JIJINI DAR ES SALAAM”

“Mmmmm jina ni refu sana ila lina weza kuleta matokea chanya”

“Ndio fanyeni hivyo”

“Hii ni namba yako?”

“Ndio”

“Sawa nita kupigia ngoja kwanza nifanye kazi hiyo”

Evans akakata simu huku akimtazama jini Maimuna aliye simama mbele yake. Akaingiza namba ya mzee Mbogo na kumpigia. Simu ya mzee huyo ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.

“Habari mzee”

“Salama, vipi Evans, mbona ume piga simu usiku huu saa tisa sasa”

“Ni kweli mzee ila nina maono ambayo nina hitaji kukueleza”

“Maono kutoka kwa wale malaika wako walio kupatia pesa zisizo na chanzo?”

“Ndio, ila nina kuomba unisikilize na wala usiyapuuzie”

“Haya una sekunde stini za kunishawishi juu ya maono yako”

Mzee Mbogo alizungumza kwa dharua kidogo kwa maana yeye ni mtu ambaye haamini sana kwenye mambo ya dini na siku zote ame kuwa akiamini akili yake na uhalisia wa maisha ana endana nao kwa kipindi alichopo.

“Al-Shabab wapo nchini Tanzania”

Mzee Mbogo akakurupuka kwa haraka na kukaa kitako kitandani.

“Una sema?”

“Kundi kubwa la Al-Shabab lipo nchini Tanzania na siku ya jumamosi ina kwenda kuilipua Dar es Salaam, katika muda mmoja na jiji lote lita geuka na kuwa moyo”

Mzee Mbogo akaka kimya huku akijaribu kuiamini maneno hayo ambayoa na yapa asilimia ishirini tu kwenye ufahamu wake wa akili kwamba ni ya kweli.

“Evans mimi na wewe tuna utani?”

“Sijawahi kukutania mzee wangu na hili ninalo kueleza ni ukweli kabisa na wala sio utani. Nime onyeshwa raisi Mtenzi alifanya shambulizi kwenye bandari ya Al-Shabab kimakosa pasipo kudhibitisha juu ya muhusika wa mauaji ya askari wake baharini. Ni kweli au uongo?”

“Hizo habari ni nani aliye kueleza?”

“Mungu”

Mzee Mbogo akatamani kuzungumza neno kali, ila akashindwa na kukizuia kinywa chake kisizungumze jambo baya lolote.

“Alikufukuza wewe na mshauri wake wa karibu, ikiwa nyinyi ndio watu muhimu sana kwenye serikali yake. Nina imani kwamba una jua hiyo hali na mimi wala sina mtu ninaye mjua ndani ya serikali zaidi yako. Al-Shabab wamekuja kulipiza kisasi kwa kufanya shambulizi ambalo toka kuumbwa mwa nchi ya Tanzania halijawahi kutokea. Mashambulizi hayo wata yafanya kwa mabomu ya nyuklia ambayo yana uwezo wa kulipua eneo kubwa sana na watu wengi sana wata kufa. Ninacho kushauri, usijaribu kuzuia hayo mashambulizi kwa maana wewe na timu yako muta kufa.”

Evans alizungumza kwa kujiamini sana. Jini Maimuna akamnyooshea dole gumba akimaanisha kwamba anacho kizungumza ni jambo sahihi.

“Timu yako ina kupenda ndio maana waliamua kufukuzwa na wewe. Waonyeshe upendo kwa kuondoka nao ndani ya jiji la Dar es Salaam na kama ni oparesheni zenu muta kwenda kuzifanyia nje ya jiji hilo. Huo ndio ujumbe wangu nilio ambiwa nikuambie wewe. Ukiuchukua na kuufanyia kazi ni heri kwako, ila ukiupuuzia na kuuacha, basi ita kuwa ni maumivu na kilio kwa watu wako. Asante na usiku mwema”

Evans akakata simu na jini Maimuna akajikuta akimkumbatia kwa nguvu na kumnyanyua kwa furaha.

“Ndio maana nilikuchagua wewe”

“Kweli?”

“Ndio, sija fanya makosa kukuchagua wewe”

Jiji Maimuna alizungumza kwa sauti ya furaha. Jinsi walivyo kumbatiana kwa nguvu, taratibu kukaanza kuamsha hisia za kimapenzi za Evans. Akausogeza mdomo wake karibu na limpsi za jini Maimuna, wakazikutanisha lipsi zao, kitendo cha Evans kunyonya lipsi za jini Maimuna, zikamfanya jini Maimuna kumuachia kwa haraka Evans na kurudi nyuma hatua chache.

“Vipi?”

“Siwezi kufanya mapenzi na binadamu na nikifanya naye basi nita poteza kila kitu ikiwemo nguvu zangu. Hivyo usijaribu kufanya kitu kama hicho siku nyingine. Sawa”

Jini Maimuna alizungumza kwa ukali kidogo huku akimtazama Evans usoni mwake.

“Nime kuelewa na nina omba unisamehe”

“Sawa”

***

Mzee Mbogo akaitazama simu yake kwa muda. Habari aliyo ambiwa na Evans kidogo ime mstua sana kwani kuna baadhi ya mambo ya siri ambayo kijana huyo hayafahamu, ime kuwaje ame yafahamu na ameyaelezea kwa usahihi kabisa pasipo kukosae jambo hata moja.

‘Hawa si ndio manabii wa Uongo hawa?’

Mzee Mbogo alijipa matumaini, ila nafsi yake moja ina endelea kumsisitizia kwamba alicho kizungumza Evans ni kitu cha ukweli kabisa. Mzee Mbogo akavaa suti yake nyeusi kisha akatoka ndani hapo, akaelekea kwenye ukumbi wa vijana wake na kuwakuta wakiendelea kufanya kazi.

“Mkuu kuna page zime funguliwa kwenye mitandao ya kijamii usiku huu, tuna ona zina kua kwa haraka sana na kupata wafuasi wengi kiasi cha kutuogopesha”

John alizungumza huku akimuonyesha mzee Mbogo page hizo tatu zilizo andikwa HARUSI YA JERY NA JULIETH NI HARAMU. MUSIHUDHURIE NA MUONDOKE JIJINI DAR ES SALAAM.

“Ni kina nani hao walio fungua page hizo?”

“Hatufahamu mkuu, tume jaribu kumtafuta muhusika wa hizo page ila hatuja mpata na inavyo onyesha kwamba mtu huyo ana high skill sana kwenye maswala ya mtandao”

Mzee Mbogo akashangaa sana kuona jinsi like za page hizo zinavyo panda kwa kasi. Katika dakika tano alizo ingia ndani ya chumba hicho, watu zaidi ya laki moja na nusu wama like page hiyo. Akaitazama saa yake na kukuta ina eleke saa kumi usiku.

“Muda huu watu wengi si wame lala?”

“Ndio muheshimiwa, ila ina imani kwambe wengi wame shinda macho kwa maana wametoka kwenye send off hivyo sidhani kama wata kuwa wame lala”

John alizungumza huku akimtazama mzee Mbogo usoni mwake.

“Tuna fanyaje mkuu”

“Mmmm”

“Tuna fanayaje ikiwa kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi watu wanavyo zidi kupande page hizo za Facebook, Twitter na Instergram?”

“Tusikilizane. Fungeni kila kitu chetu humu ndani. Kama una ndugu, jamaa rafiki una mpenda mupatie habari hiyo ya kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa maana sio salama kwetu sote”

John na wafanyakazi wengine wote wakajawa na mshangao wa bosi wao kutoa kaulio hiyo kila mtu ndani ya chumba hicho akatamani kufahamu ni kwa nini wana ambiwa waondoke jiji la Dar es Salaam ikiwa ulinzi ni mkali sana na wao wana ifanya kazi hiyo kuwalinda watu.



“Kwa nini mkuu?”

John aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Baada ya jumamosi ndio nita waeleza ni kwa nini tume ondoka Dar. Mwenye ndugu yake, jamaa rafiki, mpenzi, watoto. Nina wapa masaa sita hadi ina timia saa mbili kamili asubuhi tuwe tumesha ondoka jijini Dar es Salaam. Magari ya usafiri yapo lori zangu mbili zenye kontena mbili mbili zita beba hivi vifaa. Sasa muna weza kutawanyika”

Baada ya mzee Mbogo kuzungumza maneno hayo akaondoka ndani hapo na kuwaacha vijana wake wakiwa katika majadiliano ya kwa nini mkuu wao ame waambia hivi. John akamfwata mzee Mbogo ndani kwake.

“Mkuu samahani. Bado ume tuacha njia panda tueleze ni kitu gani ambacho kina kufanya uwaamini watu wa mitandao na wanao himiza watu kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam.”

“John una niamini?”

“Ndio mkuu”

“Basi fanya hivyo.”

John akashindwa kuuliza swali jengine na akatoka ndani hapo. Mzee Mbogo akakusanya baadhi ya nguo zake pamoja na vitu vya muhimu na kuviingiza kwenye begi lake kubwa. John akawahimiza wafanyakazi wezake kutekeleza agizo la mkuu wao na kila mmoja akaelekea kwake huku wakiwajulisha watu wao wa karibu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaa.

***

Mli wa simu inayo ita kwa mbali, ukaanza kusikika masikioni mwa Julieth aliye lala fofofo huku akiwa amechoka sana. Akaanza kupapasa pembeni ya mto wa wake na akaishika simu yake, akaitazama kwa sekunde kadhaa na kukuta ni namba ya rafiki yake anaye itwa Rebeca.

“Haloo”

“Julieth bado ume lala?”

“Ndio, vipi mbona asubuhi asubuhi hivi?”

“Amka shosti yangu na uingie kwenye facebook kumechafuka huko”

“Una maanisha nini?”

“Wewe ingia shosti yangu”

Julieth akakata simu na kuiweka pembeni. Akajilaza kidogo, ila nafsi yake ikamshawishi kuangalia ni nini hicho ambacho kimemfanya rafiki yake huko kupiga simu asubuhi hiyo. Akajilaza chali, na kuingia kwenye mtandao wa Facebook. Akastuka sana mara baada ya kukuta ukurasa unao hizimiza watu kutoka nje ya jiji la Dar es Salaam huku wakidai kwamba harusi yake na Jery ni haramu.

“Watu milioni kumi wame like?”

Julieth alizungumza huku mapigo ya moyo yakianza kumuenda spidi. Akajaribu kutafuta nani ni muhusika wa page hiyo ila akashindwa. Akashuka kitandani na kujifunga tenge na akatoka ndani hapo, akaelekea chumbani kwa wazazi wake, akagonga na baada ya muda mlango uka funguliwa na mama yake.

“Mama kuna tatizo”

“Tatizo gani?”

“Ona kilicho andikwa mtandaoni”

Julieth alizungumza huku akimuonyesha mama yake. Mrs Sanga akasoma jina la page hiyo.

“Sasa kinacho kuogopesha ni nini?”

“Mama watu wana seme kwamba ndoa yangu na Jery ni haramu watu waondoke Dar es Salaam alafu wewe una sema ni nini kinaniogopesha?”

“Ahaa hayo mambo ya mtandao mwanangu. Hembu achana nayo, kwenye kipindi kama hichi vitu hivi vita jitokeza vingi tu. Wewe una paswa kuangalia ndoa yako, sawa”

“Mama”

“Wewe achana na wapuuzi tu hao”

“Kuna nini?”

Nabii Sanga aliuliza huku naye akisimama mlangoni hapo.

“Eti ameona hii page facebook huko ndio ina mtatiza mwanao. Nabii Sanga akasoma jina la page hiyo, akaangalia idadi ya watu walio like.

“Mmmm kuna jambo hapa”

“Umeona baba ehee?”

“Ndio, watu milioni kumi, na page ime funguliwa usiku wa kuamki leo. Lazima kuna kamchezo ambako kana fanyika. Hembu ngoja niwasiliane na raisi?”

“Bora baba na wewe ufanye hivyo, mimi ngoja nimpigie Jery”

“Sawa’

Julieth akaitafuta namba ya Jery na kumpigia.

***

Jery akaitazama simu yake kwa sekunde kadhaa na kuipokea namba ya mke wake mtarajiwa.

“Umeamkaje mke wangu?”

“Vibaya baby, ume ona kwenye facebook jinsi watu wanavyo tuchafua kuhusiana na ndoa yetu?”

“Ndio nime ona mke wangu na sio facebook pekee, ila kuna Instergram pamoja na Twitter”

“Sasa tuna fanayaje mume wangu?”

“Watu wa I.T wa baba wana endelea kuhakikisha kwamba tuna mpata muhusika alite fanya huu ujinga”

“Mume wangu fanya hivyo basi kwa maana hili jambo lina niogopesha”

“Usiogope mke wangu. Hivi una weza uka hisi kwamba ni nani ambaye ana weza kuhusika na hili jambo?”

“Sina idea yoyote ya nani ambaye ana husika na hili swala”

“Sawa, jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba una tulia na usipokee pokee simu za watu wasio na maana hadi hili jambo litakapo wekwa chini ya uangalizi.”

“Sawa mume wangu”

“Nakupenda mke wangu na nipo kwa ajili yako na wala usijali katika hilo”

“Sawa mume wangu nina kupenda pia”

Jery akakata simu huku akimtazama baba yake.

“Sija mpokelea simu baba yake nina imani naye ata kuwa ana ulizia kuhusiana na jambo hilo hilo?”

“Ndio baba, wana wasiwasi sana”

“Ni kweli, ila sijui ni kwa nini hao watu wana wameanza kuiandama ndoa yetu”

“Nita muagiza mkuu wa mkoa kuzungumza na wananchi wake”

“Afanye hivyo basi baba kwa maana nina weza kukosa mke”

“Huwezi, hayo ni mambo ya kimtandao tu na hatuna budi katika kuyapuuzia.”

“Sawa, ngoja nika pumzike, kwa maana hili swala lime nifanya nikose usingizi”

Jery akatoka ofisini hapo na kuelekea chumbani kwake. Raisi Mtenzi, akampigia simu mkuu wa mkoa na kumuagiza ahakikishe ana toa angalizo kwa wachafuaji wa harusi ya mwanaye.

***

Magreth akapunguza mwendo wa gari lake na kulivuka tuta lililopo barabarani hapo. Akilini mwake mwote ana muwaza Evans wake.

“Jamani oneni”

Levina alizungumza huku akiwaonyesha wezake hao mahojiano ya mkuu wa mkoa yanayo ruka moja kwa moja kwenye vyombo vya habari.

“Ndugu zangu wana Dar es Salaam. Wengi wenu nina imani kwamba mume weza kuona uvumi ambao una zidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Istergram na Twitter. Habari zina dai kwamba ndoa ya mtoto wa raisi wetu kipendi muheshimiwa mtenzi, kwamba ni harumu na watu waondoke ndani ya jiji la Dar es Salaam.”

“Kwa mtazamo wa haraka haraka, una weza kugundua huyu mtu aliuye fungua huu ukurasa ana tatizo la kiakili. Haiwezekani harusi ikufanye wewe mwananchi kuacha shuhuli zako au makazi yako na ukaondoka ndani ya jiji letu pendwa Dar es Salaam”

Mkuu wa mkoa alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake.

“Labd mimi nitoe angalizo kwa mtu aliye fungua page hizi. Mara moja nina hitaji azifute au wataalamu wetu wa mambo ya mtandao, wana endelea kumtafuta na endapo ata kamatwa basi tuta hakikisha kwamba ana shitakiwa kwa sheria za kimitandao, kama zinavyo elekeza.”

“Ulinzi wa jiji letu ni himara, kama ilivyo kuwa jana siku ya send off. Hapakuwa na tukio hata la kibaka kumwapua mtu simu. Hivyo ndugu zangu wana Dar es Salaam, nina waomba mukae majumbani mwenu na siku ya sherehe basi mujitokeze kwa wingi kanisani na barabarani kuwapungia mikono maharusi wetu wakiwa wame toka kanisani.”

“Nirudie tena, nina wahakikishia ulinzi kila raisin a hakuna haja ya nyinyi kujawa na wasiwasi. Nina wapenda sana wananchi wangu na asubuhi njema”

Mazungumzo hayo ya mkuu wa mkoa na waandishi wa habari yakaishia hapo.

“Huyu baba ata waponza wezake”

Josephine alizungumza huku akiwa amekaa siti ya nyuma ya gari hilo.

“Ni kweli, ila hatuna namna, watakao tusikia watusikie na wasio tusikia acha wajitokeze waka punge mikono barabarani”

Magreth alizungumza huku akiwa nyuma ya basi liendalo mkoani Dododma.

“Au tuwawekee sababu ya kitu kinacho kwenda kutokea Jumamosi?”

Josephine alishauri.

“Hakuna haja na hata tukiwawekea sababu hawato tuamini”

“Hivi Levina hawato weza kuhack na kujua ni wapi ulipo?”

“Hakuna anaye weza. Hii wata sumbuka na ime kula kwao”

Levina alizungumza huku akiifunga laptop yake. Safari ikazidi kuendelea huku wakizungumza mambo mbalimbali. Wakafika mkoani Morogoro majira ya saa tatu asubuhi. Wakakodisha chumba kimoja kwenye hoteli ya kifahari kwa ajili ya kusubiria matokeo ya nini kinacho kwenda kutokea Jumamosi.

***

Omary na wezake, wakaanza kujiuliza ni kina nani wanao himiza watu kuondoka jijini Dar es Salaam.

“Ila mkuu usiwe na wasiwasi. Mkuu wa mkoa alisha toa matumaini kwa wana nchi wake. Tuta kufa na wengi”

“Nahitaji leo hii, tusambaze simu hizi maeneo tofauti na jiji hili. Nahitaji tuhakikishe, tuna ichoma Dar es Salaama kama walivyo ichoma bandari yetu”

“Ila mkuu hapo nina ushauri”

“Ushauri gani?”

“Tunapo kwenda kuzisambaza hizi simu, tuna wapa watu au tuna zisambaza kwa mfumo gani?”

“Nilihitaji kwenda kuzidumbukiza kwenye maeneo mbalimbali kama mitaro mashino ya maji machafu na tuhakikishe ziwe on na pia tuhakikishe kwamba tume ziweka kwenye kirambo ili zisiharibike na maji”

“Sawa mkuu”

Omary akaanza kugawa simu hizo ambazo jina lake maarufu ni Nokia Obama au Nokia tochi. Simu hizo zime fungwa mabomu ambayo kwa muonekano wa macho ni madogo sana, ila kwa jinsi walivyo yaunda yana uwezo wa kusambaratisha eneo kubwa sana. Vijana hao wa kundi la Al-Shabab mara baada ya kugawana simu hizo wakatoka kila mmtu kwa wakati wake na wakaanza kusambaa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Wakafanikiwa kuzisambaza simu hizo katika maeneo muhimu ya jiji la Dar es Salaam kisha wakarudi kwenye handaki lao eneo hilo la Kariakoo kwa kusubiria siku ya kesho kufanya shambulizi moja litakalo kumbukwa na kila Mtazania kwenye maisha ya mbeleni.

***

Mzee Mbogo akaendelea kuongoza msafara wa magari ya wafanyakazi wake pamoja na familia zao. Wakafika Turiani Morogoro, kwenye mashamba makubwa ya mzee Mbogo, eneo analo lima zao la mpunga. Katikati ya mashamba hayo makubwa, ame jenga jumba kubwa la kifahari ambalo alikuwa ana ishi yeye na marehemu mke wake katika siku zao za mapumziko.

Akawakaribisha wafanyakazi wake ambao wame andamana na familia zao na wakaanza kufunga mitambo yao kwenye moja ya holi kubwa.

“Nawashukuru sana kwa kunisikiliza na kuja. Tuta kaa hapa hadi pale tutakapo jua hali halisi inayo endelea Dar es Salaam”

“Ila mkuu tume msikia mkuu wa mkoa kisisitiza kwamba hali ni shwari?”

“Ndio ila kumbukeni kwamba NSA hadi sasa hivi haijarudi hewani. Leo ni ijumaa na kesho ni Juma mosi, tuangalie ni nini kitakacho tokea kisha mambo yatakapo kuwa shwari basi tuta rudi Dar es Salaam. Najua wengi wenu mume zoea kuona magorofa, ila huku ni shamba muta ona mpunga na ndege wengi”

Mzee Mbogo aliwatania wafanyakazi hao na wakaanza kucheka. John akaanza kugawa majukumu yake kwa wezake huku akitenga wapishi ambao wata kuwa wana pokezana kupika.

***

“Mage mbona una onekana una mawazo sana?”

Josephine alimuuliza Magreth huku akimtazama usoni mwake.

“Nina muwazia sana Evans”

“Ila si ume pata namba yake ya simu?”

“Ndio ninayo”

“Mpigie na umuombe msamaha”

“Kwa niliyo mfanyia kweli ata nielewa?”

“Evans ni binadamu ana jua kuna makosa. Ata kusamehe tu rafiki yangu”

Magreth akamtazama Josephine kwa muda kisha akampigia Evans. Simu ya Evans ikaanza kuita na kuyafanya mapigo ya moyo kuanza kunda kasi sana. Simu ikakatika, akashusha pumzi na akapiga tena, simu hiyo ikaanza kuita tena.

“Haloo”

Magreth alianza kuzungumza mara baada ya simu hiyo kupokelewa.

“Nani wewe?”

Sauti nyororo ya kike kidogo ika mstua sana Magreth.

“Aha…mimi nina itwa Magreth naweza kuzungumza na mwenye simu?”

“Mimi ni mke wake hivyo una weza kuniachia maagizo yote nikampatia mume wangu kipenzi Evans”

Maneno ya mwanamke huyo yaka mnyong’onyeza sana Magreth na kujikuta akikata simu huku akiwa amekata tamaa kabisa ya kumpigia Evans. Haikuisha hata dakika mbili, meseji ikaingia kwenye simu yake, akaifungua mseji hiyo kutoka kwa namba ya Evans ambayo ilizidi kumnyong’onyeza Magreth kwa maana hakutaraji kama Evans ana weza kuwa na mke.



“Mage mbona ume nyong’onyea?”

Levina alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake. Magreth hakujibu kitu chochote zaidi ya kuwa katika hali ya unyonge. Levina akaichukua simu ya Magreth na kuisoma meseji hiyo aliyo tumiwa.

‘Wewe malaya, achana na mume wangu. Kama alikujulisha uondoke Dar sio kwamba ana kupenda, tambua sasa hivi nina mimba ya Evans na nikisha jifungua nina funga naye ndoa hivyo kaa mbali na mume wangu’

“Huyu demu fala kweli”

Levina alizungumza kwa ukali huku akiachia msunyo ambao uka mstua Josephine ambaye ana endelea kuperuzi peruzi kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna nini?”

“Si kuna malaya wa Evan ana mtishia rafiki yetu”

“Ana mtishiaje?”

“Eti ana dai kwamba aache kumsumbua mume wake, hembu soma huo ujinga”

Levina akamrushia Josephine simu hiyo na akainyaka. Akasoma meseji hiyo kisha akamtazama Magreth ambaye ame tulia tuli, mithili ya mtu anaye sikilizia jambo fulani asilo lielewa kwa umakini sana.

“Jose lete hiyo simu”

Josephine akamrushia Levina simu ya Magreth. Levina akapiga tena namba ya Evans na ikapokelewa.

“Wewe malaya si nime kuambia usi mpigie mume wangu. Au una taka nikutafute nikuonyeshee ehee?”

“Sikiliza wewe mseng** uliye poteza muelekeo. Usijaribu kudili na watu usio wajua umeelewa wewe mwehu. Kama una taka tukutafute basi, mimi ndio nitakaye kutafuta na nita shuhulika na wewe. Sasa ole wako utume meseji zako za kijinga nita kuonyesha. Una hisi sisi wakijijini eheee, tumezaliwa Dar es Salaam na tume kulia Dar mbwa wewe”

Levina alizungumza bila hata ya kuwa na kituo. Simu ikakatwa, Levina akapiga tena, ikakata, akarudi kupiga tena na ikakatwa.

“Hii ndio dawa ya kushuhulika na machizi kama hawa”

Levina alizungumza na kumfata Magreth kumtazama tu.

“Lev kumbe una zungumza ehee?”

“Tena hap anime mstai tu kutokana upo wewe mtu wa Mungu, laiti ninge kuwa peke yangu, ninge mchamba huyu hadi ange ona dunia nzima ni chungu. Watu tume vurugwa, tuna mastress yetu na yeye ana tuleteea ujinga, na wewe Mage ujifunzage kujibu, sio kuambiwa hivyo kidogo una pooza kama ume chomwa ganzi bwana”

“Levina hujui ni jinsi hani ninavyo mpenda Evans, hujui ni jinsi gani nilivyo umia”

“Utaumia zaidi na zaidi, kutokana na ujinga wako. Pigania penzi lako acha ujinga wewe, ukikaa na kujifanya una jihisi mnyonge ndivyo utakavyo jikuta mwanaume aunaye mpenda akichukuliwa na uta baki uking’aa ng’aa macho”

Maneno ya Levina kidogo yakampa nguvu Magreth.

“Eti”

“Nyoo eti nini, pigania penzi lako. Isitoshe ana dai kwamba yeye ni mjaumzito na hawajafunga ndoa, ni rahisi sana kumchukua mume wake. Fanya juhudi katika hilo”

“Sawa nisaidie kuitafuta namba ni wapi ilipo”

“Poa”

Levina akaanza kuitafuta namba ya Evans ni wapi ilipo kwa kutumia satelate ila jambo la kushangaza hakuweza kujua ni wapi ilipo na ina onyesha kwamba haijasajiliwa katika mtandao anao utumia.

***

“Wata jaribu kukutafuta, ila sinto hitaji uchanganye mapenzi na mipango yetu tuliyo kuwa nayo hivi sasa”

Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.

“Sawa ila maneno uliyo wajubu nina imani yata muumiza sana”

“Ni heri aumie sasa kuliko kupoteza mipango yako.”

Jini Maimuna alizungumza huku akitazama gorofa linalo jengwa nyumbani hapo kwa kina Evans. Uwepo wa Maimuna katika eneo hakuna mtu mwengine anaye muona zaidi ya Evans yeye mwenyewe.

“Maimuna?”

“Bee”

“Hivi hatuwezi kuwasaidia watu wa Dar es Salama kesho waka ondokana na janga lililopo mbele yao”

“Hatuwezi”

“Kwa nini?”

“Una jua kuna mambo duniani yakitokea, mengina yana kuwa ni mpango wa Mungu na mengine yana kuwa ni mpango wa shetani”

“Kwa hiyo hilo la kesho ni mpango wa Mungu?”

“Hamsini kwa hamsini”

“Una maanisha nini?”

“Raisi wenu aliwatoa watu muhimu ambao walikuwa ni muhimili katika kukiongoza kichwa chake hususani kwenye maamuzi. Hilo linalo kwenda kutokea nia adhabu yake kwa kuwasaliti wezake na kufaya maamuzi ambayo hapo awali alipaswa kuwa mstamilivu”

“Ila kuna msamaha?”

“Msamaha uta patikana baada ya kupata adhabu anayo kwenda kuipata”

“Daa ina niuma sana kwa maana kuna watu ambao wata kufa bila ya hatia?”

“Ni kweli, ila kuna kipindi nchi ina takiwa kutoa kafara, ili mambo mengine yaende na iji jenge vizuri. Hilo linalo kwenda kutokea ni kafara na kuanzia hapo uta pata nguvu”

“Nani?”

“Wewe, uta pata nguvu na uta kuwa na ushawishi ambao hata wala walio kuwa wana kuchukulia poa basi wata kusujudia”

Jini Maimuna alizungumza maneno ambayo yakamfanya Evans kujisikia vizuri moyoni mwake kwani tamaa ya mafanikio ime sha mtawala moyoni mwake na sasa tayari amesha yaonja maisha ya utajiri na hataki kurudi tena kwenye umasikini.

***

“Muheshimiwa bado hatuja fanikiwa kumpata muanzilishi wa page hizo”

Kijana anaye shuhulika na mambo ya kimtandao alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.

“Mume jaribu kuzi ripoti kwenye kampuni husika hizo page?”

“Ndio, tume jaribu kuwatumia maombi Facebook, Instergram na Twitter ili wazifunge page hizo ila hadi sasa hivi hatuja pokea majibu yoyote na kila dakika wafusi wana zidi kungezeka”

“Sawa, mukijibiwa uta kuja kuniambia. Sawa”

“Sawa muheshimiwa”

Kijana huyo akatoka ofisini hapo. Raisi Mtenzia akampia simu sekretari wake na akaingia ndani hapo.

“Niandalie kikao na mkuu wa mkoa. Meya wa jiji, mkuu wa majeshi pamoja na waziri wa mambo ya ndani. Nina hitaji kuzungumza nao baada ya lisaa moja wawe hapa”

“Sawa muheshimiwa raisi. Alafu mama yupo hapo nje ana hitaji kuonana na wewe”

“Mruhusu aingie”

“Sawa”

Sekretari huyo akatoka, akaingia mrs Mtenzi ambaye uso wake una onyesha kuto kuwa na furaha.

“Mume wangu nina pata simu za usumbufu. Watu wana niuliza kwa habari hizi za kuondoka jijini Dar hadi nina pata hofu”

“Mke wangu usimjibu mtu yoyote juu ya mambo hayo. Tambua kwamba nchi ipo kwenye hali ya usalama na hili ndio jiji letu na ulinzi ni mkali sana”

“Sawa mume wangu. Je hawa wananchi wanao hoji na kuulizana maswali huko kwenye mitandao ya kijamii tuna watuliza vipi?”

“Nchi yetu ni ya kidemokrasia. Kila mtu ana uhuru wa kuzungumza anacho jisikia, ili mradi asienende kinyume sheria za nchi. Jambo la msingi ni wewe kuhakikisha kwamba una tuliza akili na kesho harusi ipo kama kawaida, hakuto kuwa na hata panya wa kukatiza mtaani. Umenielewa mke wangu”

“Sawa mume wangu”

“Njoo”

Mrs Mtenzi akasimama kutoka kwenye kiti alicho kalia na kuzunguka meza ya mume wake na kusimama pembeni yake. Taratibu raisi Mtenzi akasimama na kumshika kiuno mke wake.

“Tambua kwamba mimi ndio raisi. Nina jukumu la kuilinda nchi yangu na watu wake, huwa una jua nikizungumza nina maanisha. Hivyo maneo ya kimtandao yasikuumize kichwa, sawa mama watoto”

“Sawa mume wangu”

Raisi Mtenzi akambusu mke wake mdomoni kisha akamuachia.

“Wewe nenda kazungumze na wageni wetu, nikitoka ofisini nita jumuika nanyi”

“Sawa mume wangu”

“Nina kupenda”

“Nina kupenda pia”

Mrs Mtenzi akambusu mumewe shamvuni kisha akatoka ndani hapo. Akapisha na sekretari mlangoni.

“Muheshimiwa, nimesha wajulisha na wana kuja”

“Sawa wakifika wote waambie nikutane nao kwenye ukumbi namba moja”

“Sawa muheshimiwa”

Raisi Mtenzi akashusha pumzi taratibu, akaichukua simu yake na kuanza kutazama kutazama kurasa ya Intergram ambayo ina wahimiza watu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam na ndoa ya Jery na Julieth ni haramu. Simu ya mezani ya raisi Jery ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akachukua mkonga wa simu na kuiweka sikioni mwake.

“Halooo”

“Habari muheshimiwa raisi”

“Una hitaji nini The Brain?”

“Natambua kwamba ume nitoa nje ya nafasi ya ushauri. Ila nina imani kwamba una weza kuona ni mambo gani ambayo yana endelea kunywe mtandao si ndio”

“Ndio”

“Hapa nilipo nami nipo kwenye harakati za kuondoka jiji la Dar es Salaam. Ukiachilia mbali kwamba wewe ni raisi au bosi wangu, ila wewe ni rafiki yangu na pia ni mdogo wangu. Nitakueleza ukweli, uwe una penda ua hupendi,ila huu ni ukweli. Hili ambalo una ona lina endelea kwenye mitando ya kijamii, sio jambo la kulipuuzia hata kidogo. Fukua fukua ili uone ni kipi kipo nyuma ya pazia, nina imani kwamba uta kuwa una watafuta waanzilishi wa kurasi hizi kwa ajili ya kuwakamata. Ila jambo moja Chinas, una paswa kuwa na busara, waulize ni kitu gani ambacho kina wafanya wahimize watu kuondoka jiji la Dar es Salaam na endapo uta pata sababu uta jua ni njia gani utatue, ila ukiendelea kuwa mbabe mdogo wangu. Hata mimi sijui ni nini kita tokea, ndio maana nina hamasika na mimi kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam. Nikutakie ndoa njema ya vijana wako”

Simu ikakatwa na kumfanya raisi Mtenzi kuishusha simu hiyo chini taratibu. Jambo hili ambalo hapo awali alilichukulia kama mzaha sasa lina anza kumkaa akilini mwake vizuri. Raisi Mtenzi akampigia simu mr THE Brain.

“Ndio muheshimiwa”

“Nahitaji uje ikulu sasa hivi?”

“Muheshimiwa uta nisamehe kwa maana na mimi nina ondoka Dar es Salaam”

“Tafadhali nina kuomba sana ugahiri hiyo safari nina kuomba uje ikulu sasa hivi”

Mr the Brain akaka kimya kwa sekunde kama thelathini.

“Sawa nina kuja ila nita kaa lisaa moja, kisha nita endelea na safari yangu”

“Nashukuru kwa kuitikia wito wangu”

Raisi Mtenzi akakata simu yake kisha akampigia simu makamu wa raisi ambaye yupo nchini China kwa ziara ya kikazi.

“Habari muheshimiwa”

“Salama, kuna jambo linalo endelea kwenye mitandao ya kijamii. Je ume fanikiwa kuliona?”

“Ndio muheshimiwa, nime jaribu kuomba msaada kwa serikali hii kujaribu kutusaidia kuwapata waanzilishi wa page hizo”

“Wame semaje?”

“Wana lishuhulikia muheshimiwa, ila sija taka kuwaambia kwamba kitengo chetu cha NSA, kina tatizo”

“Kazi nzuri ndugu yangu”

“Watakapo fikia basi nita kujulisha muheshimiwa”

“Sawa sawa”

Sekretari akagonga na raisi Mtenzi akamruhusu kuingia ndani kwa ishara.

“Muheshimiwa wageni wote wamesha fika”

“Sawa twende ila wasiliana na mr the Brain na umuambie aje kwenye ukumbi namba moja”

“Mr the Brain ame rudi kazini?”

“No nime muita kwa ajili ya hili jambo”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Raisi Mtenzi akaingia ndani ya ukumbi huo na kuwafanya viongozi alio waita hapo kusimama kwa heshima. Alipo kaa kwenye kiti chake na yeye akakaa.

“Nime waita hapa wa ajili ya hili swala linalo endelea kwenye mitandao ya kikamii. Wana nchi bado wana hofu kwenye hili, je kuna hata mmoja wenu ambaye ana weza kuwaza au kufikiria ni kitu gani ambacho kita kwenda kutokea?”

“Muheshimiwa kwa upande wangu najaribu kutafuta sababu ya hawa watu au mtu kufungua hizo kurasa, ila nina shindwa kupata jibu la uhakika katika hili.”

Mkuu wa mkoa alizungumza, mlango ukafunguliwa na akaingia mr the brain akawasalimia watu wote, kisha akatafuta kiti na kukaa.

“Nashukuru kwa kuja ndugu yangu”

“Usijali muheshimiwa”

“The Brain swala tunalo jadili ni kuhusiana na hili jambo la wananchi kuhimiza kuondoka jiji la Dar es Salaam nawe ni mmoja wapo ya watu walio kuwa wana ondoka jijini. Tuambie una maoni gani juu ya jambo hili?”

“Muheshimiwa nchi ipo kwenye shambulizi na eneo ambalo lime pangwa kutoka kwa mashambulizi hayo ni jiji la Dar es Salaam”

Mr the Brain alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya viongozi wote kustuka.

“Shambulizi gani na nani ambaye ana kwenda kuishambulia nchi?”

“Dakika tano kabla sija ingia hapa ndani, nilikuwa nina zungumza na mr Mbogo uliye mfukuza kwenye kitengo cha NSA. Yeye na timu yake wamesha ondoka jijini Dar es Salaam na ameniambia kwamba kesho kwenye harusi ya mwanao. Kundi la Al-Shabab ambalo uli lishambulia kima kosa wata fanya shambulizi, hivyo muheshimiwa, haijulikani ni wapi na wapi wata shambuli na wala kati yetu hakuna anaye fahamu ni saa ngapi wanavyo shambulia. Kiufupi muheshimiwa, kesho haito kuwa siku nzuri kwako na taifa kwa ujumla”

Maneno ya mr the Brain yaka wafanya viongozi wote macho kuwatoka, huku raisi Mtenzi mapigo ya moyo yakianza kumuenda kasi sana kwani wamebakisha muda mchache sana kabla ya harusi ya kijana wake kufanyika.



MWISHO WA MSIMU WA KWANZA, ENDELEA KUFUATILIA (SEASON) MSIMU WA PILI


MWISHO




0 comments:

Post a Comment

BLOG