Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 5/10

 

 

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 5 KATI YA 10

 



“Boti zipo ngapi za hao wanajeshi?” “Zipo boti nne” “Muambie nadhodha asimamishe boti” “Sawa mkuu” Michael akatoka katika chumba hichi, na kutuacha mimi na Martin tukiwa tumesimama huku wasiwasi mwingi ukiwa umetutawala.

“Tutafanyaje mkuu wakitukuta humu ndani?” “Ni lazima tufanye jambo” Nilizungumza huku nikitoka ndani ya hichi chumba, nikawakutua Michael na wezake wakiwa wamesimama wakitazama jinsi boti hizi za jeshi zikiizunguka boti hii tuliyo panda.

“Michael njoo” Michael akanifwata sehemu nilipo jibanza.

“Kuna silaha humu ndani ya hili boti” “Ndio mkuu” “Zipo wapi?” Tukarudi kwenye chumba tulichopo, Michael akafungua moja ya kabati lililomo humu ndani akasogeza nguo zilizopo kwenye hili eneo, akaanza kutoa bunduki moja baada ya nyingine na kutukabidhi. Nikachukua bunduki moja iliyo jaa risasi za kutosha.

“Wanajeshi wakileta shida tutawashambulia” “Sawa mkuu” Michael akatoka ndani humu na kutuacha mimi na Martin kila mmoja akiwa na bunduki yake na tumejibanza kwenye sehemu ambayo si rahisi kwa mtu wa nje kuwea kutuona ila sisi ni rahisi kuweza kumuona mtu wa nje hii ni kutokana na vioo vigumu viliyomo kwenye kuta za hichi chumba.

Tukawashuhudia wanajeshi watatu wakiingia kwenye boti hii huku wakiwa wameshika bunduki zao, ila katika kuwatazama sare zao sio za wanajeshi wa jeshi la maji Tanzania.

“Hawa wanajeshi ni wa wapi?” Nilimuuliza Martin huku nikiendela kuwatazama wanajeshi hawa.

“Ni wanajeshi wa Msumbiji” “Ina maana bado hatujaingia Tanzania?” “Yaa” Tukaendelea kuwatazama wanajeshi hawa walio anza kugaua vibali vya hii boti huku wakiwatazama Michael na mwenzake, wakazungumza nao kwa dakika kadhaa, Michael akatoa kibunda cha dola za kimarekani na kumkabidhi mwanajeshi mmoja aliye anza kuhesabu pesahii haraka haraka kisha akamtazama Michael huku akitingisha kichwa. Taratibu nikawaona wakishuka kwenye boti kisha wakaruhusu boti yetu kuondoka. Nikajikuta nikishusha pumzi nyijngi kisha nikarudi kukaa kwenye siti yangu. Michael akaingia kwenye chumba chetu. “Walihitaji nini hao wanajeshi?” “Walikuwa wanafoka foka tu kwa nini tumepita kweney ukanda wa nchi yao, pasipo kuw ana kibali” “Wana vichaa kweli” “Nimewapa dola elfu tano, ndio maana wametuachia” “Sawa tumebakisha muda gani hadi kufika nchini Tanzania?” “Tumesha ingia kwenye ukanda wa nchi ya Tanzania, hapa tutatumia muda mchache kufika usawa wa Dar es Salaam” “Sawa sawa” Michael akaanza kurudisha silaha ndani ya kabati hili huku akisaidia na Martin. Baada ya muda wa kama dakika aroboini na tano Michael akatuommba tuweze kuvaa nguo maalumu za kuogelea kwani muda kuzama baharini umefika.

Tukaanza kujiandaa mimi na Martina hatukuchukau muda mrefu tukawa tumefanikiwa kuvaa nguo hizi pamoja na mitungi maalimu ya gesi ya oksijeni tuliyo ivaa mgononi. Tukavaa miwani maalimu, kisha Michaela katukabidhi tochi.

“Niwatakie kazi njema” “Shukrani na murudi salama. Martin mbona umemeba begi?” “Nimeweka nguo zetu na vifaa vichache” “Sawa” Nikampa mkono wa shukrani Michael na mwenzake kisha taratibu tukajitosha kwenye maji. Tukaanza kushuka chini huku tukiwa tumewasha tochi zetu. Tulipo fika katika usawa ambao tunaamini hata mmtu awe kwa juu hatoweza kuona mwanga wa tochi tulizo ziwasha, tukaanza kuogelea kwenda mbele huku Martin akiongoza kwa kufwata malekezo kwenye simu aliyo ishika, tukazidi kusonga mbele huku tukiwa makini sana hadi tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyavu kubwa ya chuma. Martin akanikabidhi simu aliyo ishika kisha akavua begi na kutoa koleo kubwa la kukatia njavu hii. Taratibu akaanza kukata njavu hii huku mimi nikiwa makini kutazama tunapo toka na tuendapo.

Alipo maliza kukata taratibu tukaanza kuingia kwenye uwazi alio kata na tukaendelea na safari yetu. Hadi inatimu saa tisa usiku tukafanikiwa kufika katika ufukwe wa koko bichi huku tukiwa tumechoka sana. Tukatoka ndani ya maji na kukaa chini ya mwamba mmoja ulipo hapa pembezoni.

“Ohooo kukaa kwenye maji ni kazi kweli kweli” Nilizungumza huku nikihema sana.

“Yaani wee acha tu” “Huyu jamaa sijui atakuwa amesha fika” “Ngoja nikamtazame” Martib alizungumza huku akinyyanyuka, akavua viatu maalumu vya kuvulia, akaivua na tochi na kuizima, akatoka kwenye mwamba huu ambao umeingia ndani, hata hazikupita dakika mbili nikiaiskia milio ya risasi iliyo nistua sana, kwa haraka nikachungulia kwenye mwamba huu, nikamuona Martin akiwa amezungukwa na watu walio valia nguo nyeusi.

Nikatamani kujitokea ila sina silaha amabayo itawezesha kushambuliana na watu hawa. Nikamuona Martin akipigishwa magoti chini huku mikono yake akiweka nyuma na kufungwa pingu. Akanyanyuliwa kwa haraka na watu hawa wakaondoka naye katika hili eneo.

“Shitiii” Nilizungumza huku nikiwa nimekasirika sana kwani sijajua mpango huu umevurugwa na nani na mtu ambaye tumeambia kwamba atakuja katika hili eneo ni Godlove ambaye hata sura yake siifahamu. Nikafungua begi lenye nguo, kwa haraka nikaanza kubadilisha nguo nilizo zivaa na kuvaa nguo za kawaida, nilizo kuwa nimezivaa nilipo toka katika kisiwa cha Madagasca.

Nikachunguza hili eneo kwa umakini na nikaanza kutoka katika huu mwamba sikuelekea katika usawa alio kuwa amekwenda Martin. Nikaanza kutembea huku nikiwa makini sana katika kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaye weza kunifwatilia au kuniona. Nikiwa katika moja ya barabara iliyo tulia nikaona gari aina ya Toyota Mark X ikiwa imefunuliwa boneti ya mbele huku ikitoa moshi mwingi na mlango wa dereva nao umefunguliwa.

Nikataza hili eneo nikagundua kwamba hakuna sehemua mbayo askari wanaweza kujificha na ikawa ni mtego kwangu. Nikaanza kulisogelea hili gari hadi nikanikiwa kufika, nikamkuta msichachan mmoja akiwa amejilaza kwenye siti yake akionekana kuchoka sana na kwenye zake zimefunika sehemu ya uso wake. Mkononi ameshika chupa ya wyne na inaonyesha amelewa sana.

“Hei” Nilimuita huku nikiendeleak kutazama eneo hili kwa umakini sana. Binti huyu akakurupuka na kunitazama huku akiziweka nywele zake sawa. Sote tukabaki tukishangaana kwani huyu binti ninamfahamu sana.

“Dany!!” “Lucy!!” Nilimuita huku sote tukishangaana. Lucy akatoka kwenye siti aliyo kaa na kusimama, akanikumbatia kwa haraka, tukajikuta tukiwa tumejawa na furaha.

“Oohoo Dany ni miaka mimi sasa hatujaonana, upo wapi wewe?” Lucy alizungumza huku akiwa ametanasamu.

“Maisha tu, gari lako lina tatizo gani?” “Sijui ninaona limenizimia tu hapa” Nikamuachia Lucy huku nikitembea hadi mbele ya hili gari, nikaanza kutazama tazama tatizo la hili gari, mwanga mkali wa gari inayo kuja nyuma yetu ukanifanya nisigeuke na kujifanya nipo bize ninaendela kutengeneza hili gari. Gari hili likasimama karibu kabisa na gari hili, taa za gari hilo zikazimwa na kunipa nafasi ya kugeka kidogo, nikajikuta nikistuka baada ya kuona platenamba za hili gari inaonyesha ni gari ya polisi.

‘Nitawaua’

Nilijikuta nikiapia huku nikiendelea kuinama kugusa gusa baadhi ya vitu viluyopo kwenye hii bonet.

“Mbona mumechelewa?”

Nilisikia sauti ya Lucy akizungumza na polisi hawa, jambo lililo nifanya moyo wangu kunistuka sana na kuhisi kwamba Lucy ameniuza kwa askari hawa. Nikataka kugeka ila nikajikuta nikiwa mvumilivu nikisikilizia kauli ya askari yoyote atakaye jibu swalli la Lucy mtoto wa Mzee Jogoo, niliye wahi kumsaidia mikaa mingi katika ajali ya moto kipindi nilipo kuwa ninaishi Sinza.

“Kidogo tulikuwa kwenye patroo Ubungo ndio maana tumechelewa samahani” “Ahaa gari limenibumia hapa” “Huyo anaye kusaidia ni nani?” Kwa jicho la kona nikamuona Lucy akigeuka na kunitazama, akatabasamu na kunisogela nilipo simama na kuendelea kujifanya nina tengeneza gari hili.

“Ni mpenzi wangu” Nikashusha pumzi kidogo kwani tayari nilisha anza kujiandaa kiakili jinsi ya kupambana na askari hawa wanne.

“Ingia ndani ya gari ujaribu kuwasha” Nilizungumza huku nikaza moja ya nati ambayo nimeikuta imelegea. Lucy akatembea kwa madoido hadi ndani ya gari akajaribu kuwasha na gari ikawaka.

“Waooooooooooo” Lucy alishangilia huku akishuka kwenye gari.

“Asante mpenzi wangu” Lucy alizungumza huku akinifwata na kunikumbatia, sikutaka kabisa kuigeuza sura yangu kuwatazama hawa askari kwani nina imani wataingia kwenye msiba ambao sihitaji niwe chanzo cha vifo vyao.

“Ngoda mumaweza kuondoka tu gari langu tayari” “Mkuu ametuagiza tukusindikize hadi nyumbani” “Mumbieni baba kwamba mimi ninaendelea kula bata weekend ndio imeanza hivi” “Ila ni kwa ajili ya usalama wako” “Nipo salama si munamuona shemeji yenu hapa” “Mbona shemeji haitaji kututazama” “Eheee kwani ni lazima jamani. Ngoda ondoka na watu wako bwana” “Sawa”

Askari hawa wakarudi kwenye gari lao, wakapanda na kuondoka eneo hili na kutuacha tukiwa tumesimama tukisindikza gari lao kwa macho.

“Asante” Nilizungumza huku nikielekea katika mlango wa pili wa hili gari, Lucy akazunguka hadi katika mlango wa dereva na sote tukaingia ndani, tukafunga milango na kuanza kuondoka eneo hili.

“Dany ni kwa nini wewe?” Lucy alizungumza kwa sauti ya chini huku akinitazama. “Tunaelekea wapi kwanza?” “Jibu swali langu kwanza” “Unahisi ni kweli ni mimi?” “Ndio maana nina hitaji kujua ukweli kuhusu wewe kwa kipindi chote ambacho unatafutwa na kutangazwa kama Gaidi tena wa kimataifa?” “Mimi sio gaidi ila hao wanao watangazia wao ndio magaidi” “Nitakuamini vipi ikiwa nimesikia umeua watu wengi sana na hapa Tanzania unatafutwa kama shahabu na endapo mtu atafanikishwa kukamatwa kwako basi yeye na umaiskini ndio kwaheri” “Lucy” “Beee” “Una niamini?” “Ndio ninakuamini, ndio maana sikuhitaji kukuchomesha kwa wale askari pale kwani bado sijakaa na wewe kufahamu ukweli ulio pelekea kuitwa gaidi na kuwindwa sana” “Nashukuru, baba yako yupo wapi?” “Baba ni waziri mkuu” “Ananizungumziaje mimi katika hili swala” “Baba yangu nina imani amejazwa chuki kubwa na anakuchukia sana na anatamani hata leo akukamate na kukuadhibu kwa makosa yako yote uliyo yafanya” “Asijaribu kufanya hivyo kwani na yeye nitamua” Gafla nikastukia Lucy akifunga breki za gari lake huku akinitazama kwa macho makali akionekana kushangaa kauli yangu niliyo itoa kwani ni kauli ambayo nina amini kwamba ni mbaya sana kwake ila ndio ukweli kutoka moyoni mwangu.



“Dany unacho kizungumza una kimaanisha kweli au?”

“Nina kimaanisha ndio kwa maana kwani baba yako hatambu ni kitu gani kinacho endelea ndio maana ananichukia pasipo kufahamu ukweli wa mambo”

 

Nilizungumza huku nikimtazama Lucy usoni mwake.

“Nina imani kwamba hukuwepo Tanzania, umekuja kufanya nini Tanzania?”

“Siwezi kukuambia sasa hivi kilicho nilete ila utakiona kilicho nileta”

“Dany unatakiwa kuniamini?”

“Si kirahisi namna hiyo ikiwa mtu wangu amekamatwa”

“Nani aliye kamatwa?”

“Huwezi kumfahamu”

“Niambie ninaweza kukusaidia kwa maana nina fahamu mfumo mzima wa hili jeshi la Tanzania”

Nikamtazama Lucy usoni mwake huku nikiendelea kujiuliza maswali moyoni mwangu kama ninaweza kumuamini msichana huyu ambaye alisha wahi kunitamkia kwamba sina hadhi ya kuwa na mahusiano naye.

 

“Shukrani kwa msaada wako”

Nilizungumza huku nikifunga mlango wa gari na kushuka, Lucy kwa haraka na yeye akashuka kwenye gari na kuanza kunifwata ninapo elekea huku akiniita jina langu. Alipo ona sigeuki akanishika mkono.

“Dany umekuwaje jamani, kukuomba kukusaidia unahisi kwamba ninaweza kuwa msaliti kwako”

“Nitakuamini vipi ikiwa baba yako mwenyewe amejazwa chuki dhidi yangu, je wewe utakuwa fungu gani?”

“Dany hivi utambua kwamba nilijitunza miaka yote hiyo nikikusubiria wewe. Hivi unajua usichana wangu bado upo na hakuna mwanaume yoyote anaye ijua kum** yangu?”

Lucy alizungumza huku machozi yakimlenga lenga  usoni mwake. Nikabaki nikimtazama tu kwani ninamshangaa na siamini kwa hichi anacho kizungumza. 

 

“Dany natambua huniamini, kama huamini twende kwangu sasa hivi ukanivunje hii bikra, nimekuwa nimwanke wa kujipa matumaini kwamba wewe ndio mtu sahihi uliye jitolea maisha yako kwa ajili yangu na ukaungua mgongo, mikono yote kwa ajili yangu. Ni wanaume wangapi walikuwepo ile siku ila hakuna aliye thubutu hata mmoja kuja kujitolea maisha yake kwa ajili yangu eheee, kwa nini ulikuwa ni wewe?”

 

Lucy aliendelea kuzungumza kwa sauti iliyo jaa kilio ndani yake. Kusema kweli nikabaki nikiwa na kigugumizi na moyoni mwangu nilisha apia kwamba sinto mpenda mwanake yoyote na ninahitaji kuifanya kazi iliyo nilete Tanzania na hata nikiondoka Tanzania basi niondoke kabisa na maisha yangu yote yaliyo salia duniani yatamalizikia huko nitakapo elekea. Radi kali iliyo piga na kuandamana na mgurumo wake ikamfanya Lucy kunikumbatia kwa nguvu huku akilia.

 

“Dany nisamehee kwa maneno yangu ya kukukatisha tamaa kwa kipindi kile, sikuwa ninajua thamni ya mwanume, sikuwa ninajua kupenda ni nini. Nisamehee Dany wangu, leo imekuwa kama bahati kuonana na wewe tafadhali Dany”

Lucy alizungumza huku akiendelea kulia na kunikumbatia kwa nguvu. Matone ya mvua yakaanza kutumwagikia taratibu, kadri jinsi sekunde zinavyo zidi kwenda mbele ndivyo jinsi matone haya yaliyo zidi kuongezekana kulowanisha miili yetu.

‘Martin amekamatwa, atakuwa yupo wapi?’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiwa ninatazama eneo hili kwa umakini ili kuangalia kama kuna mtu yoyo anakuja katika hili eneo.

‘Siwezi kumpenda Lucy, sio mwamke anaye stahili kufa kwenye dhambi zangu’

Niliendelea kuzungumza kimoyo moyo, taribu nikamtoa Lucy mwilini mwangu.

 

“Lucy nitakuamini vipi?”

“Niamini Dany chochote utakacho niambia mimi nitafanya mume wangu”

Lucy alizungumza huku akiwa katika majonzi makibwa.

“Twende kwako”

“Kweli Dany?”

“Ndio twende”

Lucy akaniachia na kwa furaha tukaanza kurudi tulipo liacha gari. Tukingia ndani ya gari na moja kwa moja tukaelekea hadi maeneo ya Mbezi mwisho, sehemu inayo itwa Makabe. Tukaingia kwenye moja ya jumba kubwa la kifahari.

“Kuna walinzi wangapi  kwenye hii nyumba yako?”

“Wapo sita”

 

“Ni polisi au  walinzi wa kawaida?

“Ni walinzi wa kawaida wa kampuni moja inaitwa Group four”

“Ahaaa sawa”

Tukashuka kwenye gari huku nikiwa makini kuwatazama askari wawili walio simama eneo la kuingilia ndani ya hili jumba.

“Waondoe walinzi wako hapo mlangoni”

Nilizungumza huku nikirudi ndani ya gari cha kumshukuru Mungu sehemu niliyo kuwa nimesimama ina giza kidogo. Lucy akatembea hadi kwenye mlango akazungumza na walinzi wake huku akionekana kuwaelekeza. Walinzi walipo ondoka, Lucy akageuka na kunitazama, nikashuka kwenye gari na kuanza kutembea na kuingia naye ndani.

“Kuna mfanyakazi wa ndani?”

“Hapana huwa wanakija asubuhi kufanya fanya usafi”

Tukaanza kupandisha kuelekea gorofani huku Lucy akiwa amenishika mkono wangu wa kushoto. Tukaingia katika chumba chake cha kulala amacho kimepambwa na mapambo mazuri.

 

“Dany umeoa?”

Lucy alizunngumza huku akivua shati lake lililo lowanishwa na maji. Nikaitazama pete yanug kidoleni, ambayo nilivishwa na Yemi siku mbili zilizo pita.

“Mbona hujibu”

“Kwani kuna tatizo lolote katika hilo?”

“Nimekuuliza tu”

“Tutazungumza baadaye”

Lucy akanisogelea na kusimama mbele yangu.

“Dany hata kama umeoa, hata kama utakuwa na watoto ila ninakuapia kwamba nitakupenda kwa maisha yangu yote”

“Utampendaje mwanaume anaye chukiwa na watanzania wote?”

“Siamini kwa kile wanacho kizungumza na kama ungekuwa ni gaidi basi ungea watu wa kawaida, ila ni kwa nini unaua watu fulani na wenye nafasi fulani za juu”

“Umejuaje kama ninaua watu wa nafasi za juu?”

“Mbona kila siku ndivyo vyombo vya habari vinavyo tangaza. Vinasema umemuua waziri mkuu wa Somali”

 

“Waziri mkuu wa Somali!!. Nimemuua lini?”

“Wiki kama mbili zilizo pita na ipo listi kubwa tu ya watu ambao inasaidikika kwamba una waua wewe”

“Ni uongo vifo vya watu hao sijahusika kabisa”

“Mimi nina amani hilo. Pia kuna ulinzi mkali sana ambao umeimarishwa kwa ajili ya kukukamata wewe”

“Hawawezi kunikamata sasa ni lazima niweze kujua ni nani ambaye anahusika na vifo vya hao viongozi ambao unaniambia”

“Nitakusaidia”

“Sawa nitakuomba unisaidie katika kupata taarifa ya kuweza kufahamu mtu wangu amekamatwa na nani na yupo wapi”

“Sawa nitafanya mpenzi wangu, mimi kwa sasa ni mtumwa wako”

Kwa haraka haraka unaweza kufikiria kwamba anayo yazungumza Lucy ni kutokana na pombe alizo kunywa, ila kwa upande mmoja ninaamini kwa kile alicho kizungumza. Nikamshika kiuno chake na kumsogeza karibu yangu kabisa, nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaanza kumsogeza mdomo wangu. Lucy akafumba macho yake huku midomo yake ikimtemeka, hapa ndipo nikagundua kwamba woga alio kuwa nao kipindi kile bado hadi leo anao.

“Unaogopa nini?”

Nilimuuliza Lucy na kumfanya ayafumbue macho yake huku akinitazama usoni mwangu.

 

“Eheee”   

“Mbona una ogopa?”

“Kusema kweli Dany sijawahi kufanya hivi”

“Kweli?”

“Ndio”

Kwa haraka nikamsogeza Lucy mdomo wake na kuanza kumnyonya kwa nguvu, jambo lililo mfanya kaunza kulegea taratibu. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo lizidi kumuhimili Lucy na kumfanya alegee sana.  Mlio wa simu ya Lucy ukatufanya tuachiane, akazama simu yake aliyo iweka juu ya meza.

“Samahani”

Lucy alizungumza huku akiniacha moja kwa moja akaielekea ilipo meza na kiichukua simu yake, akaipokea na kuiweka sikioni mwake.

“Baba”

Lucy akanifanya nimtazame kwa macho makali.

“Nimsha rudi nyumbani baba yangu”

“Waogo bwana sina mwanaume yoyoye, baba yangu wewe mwenyewe unanijua, ni wanaume wangapi huwa nina wakataa mbele yako, sembuse leo ndio nilale na mwanaume”

 

“Hapana baba, niamini mwanao”

“Sawa baba”

“Nakupenda sana baba yangu”

“Nawe pia baba usiku mwema”

“Haya”

Lucy akakata simu na kusogelea nilipo simama, akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kuninyonya midomo yangu.

“Baba yako anahitaji nini?”

“Alikuwa ana nihofia usalama wangu, wale askari wamempelekea umbea”

“Haito leta tatizo hii?”

“Haito weza kwa maana baba yangu ana niamini sana katika maswala ya mahusiano na yule askari aliyekuwa anazungumza zungumza alisha wahi kuleta posa kwa baba ila nikamkataa kabisa”

Nikamtazama Lucy kwa macho ya kumchunguza usoni mwake, kisha taratibu tukaendelea kunyonyana huku akilini mwangu nikiwa ninawaza ni jinsi gani ninaweza kumtumia Lucy katika kuhakikisha kwamba mipango yangu inazidi kuwa rahisi katika kuitekeleza.

 

Lucy akaanza kutoa miguno ya maumivu huku akibana bana mapaja yake.

“Na….naumia baby”

“Unaenda wapi baby”




Baada ya dakika kama arobaini, nikamaliza mzunguko wa kwanza ulio mfanya Lucy kulia kwa machozi ya furaha huku akiongea maneno mengi ambayo hata mengine hayana faidi yoyote kwa mimi kuweza kuyasikia.


 

“Mmmmm siamini kam…..”

Lucy akajaribu kusimama ila akashindwa kabisa na kujikuta akikaa tena kitandani huku akinitazama usoni mwangu huku akionekana kujawa na wasiwasi mwingi.

“Nini?”

“Miguu inakataa kabisa kusimama”

“Ndio maana nikakuuliza”

“Hembu nisaidie”

Lucy alizungumza huku akinipa mkono wake wa kuliaa, taratibu nikamvuta na kumnyanyua. Akasimama kwa sekunde kadhaa.

“Mmmmm hapana jamani si kwa maumivu haya”

“Pole ukikaa baada ya muda utaweza kunyanyuka”

“Nilikuwa nina sikia sikia tu kwamba kuvunjwa bikra msichana lazima achechemee kumbe ni kweli?”

“Yaaa”

“Mmmmm kazi kweli kweli”

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtingisha tingisha jogoo wangu. Nikaanza kuoga huku nikifikiria jinsi ya kumpanga Lucy katika kufanikisha kazi yangu. Nilipo maliza nikatoka bafuni na kumkuta Lucy akijjitahidi kutembea kueleka kwenye kabati lake la nguo.

 

“Najikaza nitoe taulo siwezi kuaa na hii michiri ya damu”

“Sawa”

Lucy akafanikiwa kufika kabatini, akafungua na kutoa mataulo mawili, akanirushia taulo moja kunwa lililo tawaliwa na rangi nyeupe kisha na yeye akabakiwa na kitaulo kidogo cha rangi nyeupe kabisa.

“Kitambaa hichi na hilo shuka nitaviweka ukumbusho”

“Ukumbusho wa nini?”

“Wa siku niliyo tolewa bikra na mwanaume niliye msubiri kwa kipindi kirefu sana.”

“Je tusinge onana leo ungeendelea kuishi na bikra yako”

“Ndio ningeendelea kujitunza hadi kufa kwangu”

“Mmmmmm”

“Mbona unaguna sasa?”

“Hakuna kitu”

“Ngoja na mimi nioge”

Lucy alizungumza huku akianza kujikokota kuelekea bafuni. Nikamtazama umbo lake kusema kweli  ameumbika vizuri. Nikachukua rimoti iliyopo juu ya meza na kuwasha tv kubwa iliyopo humu chumbani. Kila chaneli ya Tanzania ninayo ifungua inaonyesha matangozo ya ujio wa raisi Donald Bush wa marekani huku ikiwa ndio mara yake ya kwanza kujia nchini Tanzania.

 

‘Huondoki Tanzania wewe’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiitazama video ya raisi Donald Bush akiwa amesimama kwenye ngazi za ndege yake ijulikanayo Air Force One.

“Watanzania wanamsubirije huyo raisi”

Lucy alizungumza huku akiwa amesimama kwenye mlano wa bafu lililopo hapa chumbani.

“Anafika Tanzania saa ngapi?”

“Anatarajiwa kufika saa moja usiku”

“Aahhaaa”

“Yaani ujio wa huyu raisi umemfanya baba kuwa katika heka heka hadi ninamuonea huruma”

“Heka heka za nini?”

“Kuhakikisha kwamba ulinzi unaimarishwa na hakutokea tukio lolote la ugaidi”

“Kwani kuna ukio ambalo wanataraji litokee?”

“Hof yao wote wanakuhofia wewe huo ndio ukweli na ulinzi wote anao lindwa huyu raisi pamoja na raisi K2 yote ni kwa ajili yako”

 

“Sawa, tuachane na hayo, kuna kijana wangu amekamatwa utanisaidiaje kumpata kwa maana yeye ndio kila kitu kwangu?”

“Amekamatwa lini?”

“Usiku huu wa leo”

“Ngoja nimpigie simu baba”

Lucy alizungumz ahuku akiichukua simu yake iliyopo juu ya meza. Akampigia baba yake na baada ya muda kidogo akaanza kuzungumza huku simu akiwa ameiweka loudspeker.

“Baba”

“Vipi kuna tatizo?”

“Hapana baba yangu”

“Haya mbona umepiga simu usiku huu?”

“Nasikia mumemkamata Dany?”

“Nani amekuambia?”

“Nimesikia tetesi tu”

“Haana ni mwanajeshi mmoja kutoka katika kundi la Boko Haramu alikuwa pembezoni mwa bahari huko”

 

Tukatazamana na Lucy huku macho yakiwa yamenitoka.

“Boko haramu kwa hiyo wapo Tanzania?”

“Hapana huyu yupo peke yake, ila hapa ndio anaendelea kuhojiwa katika makao makuu ya polisi huku”

“Mumemkamataje?”

“Lucy mbona una maswali mengi vipi?”

“Baba mwanao si muandishi wa habari, ninahitaji kufahamu tu kwani hujayazoea maswali yangu?”

“Ahaa. Huo uandshi wa habari wako sio kwenye maswala haya ya kiusalama wewe andaa habari za kuja kwa raisi Donald Bush basi”

“Sawa baba yangu kwa hiyo mupo makao makuu ya NSS ?”

“Ndio”

“Sawa baba yangu ninakupenda ehee?”

“Ninakupenda pia binti yangu. Hakikisha kwamba unalala muda umekwenda sasa”

“Sawa baba yangu”

Lucy akakata simu huku akishusha pumzi nyingi.

“Ninahitaji kwenda sasa hivi?”

“Wapi?”

 

“Alipo mtu wangu”

“Dany wewe mbona una hatari?”

“Hatari ni jambo la kawaida kwenye maisha yangu.”

“Sasa Dany hapo ulinzi lazima utakuwa ni mkali sana, yaani hadi baba yupo hapo ujue ulinzi ni mkali sana na huyo mtu wako anahojiwa vikali sana”

“Usijali nitakuwa salama, je una bastola yoyote”

Lucya akanitazama kwa sekunde kadhaa usoni mwangu huku akionekana kujishauri juu ya hili nililo mueleza.

“Eheee”

“Ninaomba unipatie”

Lucy akasimama na kuanza kutembea hadi kwenye droo iliyopo pembezoni mwa kitanda chake, akaifungua na kutoa bastola moja ndogo sana ambayo inaingia risasi tano.

“Hiyo ndio uliyo kuwa nayo?”

“Ndio  ina uaa hiii”

“Yaaa najua inaua ila kwenye hii kazi hainitoshelezi”

“Kwani unakwenda kuua mtu!!?”

“Ikitokea hivyo inabidi nisiwe na jinsi, ila kwa usalama zaidi  inabidi nisiende na silaha yako kwa maana wakigundua ni silaha yako imetumika basi inaweza kukuletea tabu wewe”

“Dany”

 

Lucy aliniita kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio”

“Nakuomba usiue, na kama baba yangu atajiingiza katika hili nakuomba usimuue kama ulivyo niambia”

“Sawa sito fanya hivyo kwa baba yako”

Nilizungumza huku nikisimama, taratibu Lucy akanisogelea na kunikumbatia.

“Dany ninakupenda sana, natambua kwamba umekuja kwa ajili ya kazi unayo ijua wewe mwenyewe ninakuomba usipata tatizo kumbuka nimekusubiria kwa muda wote huo ili niweze kuishi nawe kwa amani na upando”

Sijui hata nimfariji vipi Lucy kwa maana moyoni mwangu hayupo kabisa.

“Usijali nitakuwa salama tu”

“Kweli Dany?”

“Ndio”

“Nakupenda sana Dany wangu”

 

Lucy akazidi kunikumbatia kwa nguvu huku akiwa amejawa na furaha. Taratibu nikamuachia, nikambusu kwenye paji la uso wake kisha nikaanza kuokota nguo zangu na kuanza kuzivaa moja baada ya nyingine.

“Baba yako amezeeka sana?”

“Hapana yupo bado kwenye ubora wake”

“Kweli?”

“Ndio anafanya mazoezi sana”

“Sawa inapendeza, je unaweza kunipatia gari lako?”

“Ngoja nikupe gari jengine ambalo silitumii mara kwa mara”

“Kama una kofia pia nisaidie”

“Tena ninazo nyingi tu humu kabatnini”

Lucy akanitolea kofia moja na kkinikabidhi, nikaivaa, nikajitazama kwenye kioo nilipo ona sura yangu sio rahisi kuweza kuonekana nikamgeukia Lucy.

“Hapo upo poa”

Lucy akajifunga matenge mawili kisha tukatoka chumbani humu na kueleka kwenye maegesho ya magari yake, akanikabidhi funguo ya gari moja aina ya Toyota Brevis.

“Kuwa makini”

“Poa nitarudi hapa”

“Saa ngapi utarudi?”

“Kabla ya saa moja asubihi”

“Sawa”

 

Lucy akanibusu mdomoni mwangu, hakuwajali walinzi wake, nikaingia ndani ya gari na kutoka katika hili eneo. Safari ya kuelekea posta ikaanza, cha kumshukuru Mungu usiku huu barabarani hakuna foleni ya magari, ikanichukua muda mchache sana kufika karibu kabisa na makao makuu ya  NSS, kitengo ambacho nilikitumikia kwa zaidi ya mikaa mitano na ninalitambua vizuri hili jengo kwani limejaa kamera nyingi za ulinzi(CCTV CAMERA).

‘Lazima niiingie humu ndani’   

Nilizungumza huku nikilitazama jengo hili lililo refu kwenda juu, kisha taratibu nikashuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa kujiamini nikielekea katika geti la kuingia gorofa hili ambapo kuna askari wa NSS wasio pungua watano na wana bunduki za moto pamoja na mbwa wakubwa wakali wenye uwezo wa kumrarua binadamu dakika chache pale watakapo pewa amri ya kufanya hivyo.



Nikaiweka kofia yangu vizuri huku nikiishusha usawa ambao sio rahisi kwa mtu kuweza kuiona sura yangu vizuri. Taratibu nikajikuta nikipunguza mwendo wa hatu zangu baada ya kuuona mlinzi mmoja akinifwata huku ameshika bundiki yake mkononi.

“Habari yako kiongozi”   

Nilimsalimia mlinzi huyu anaye onekana kuwa makini sana katika kunitazama usoni mwangu.

“Unahitaji nini usiku wote huu?”

“Gari yangu kidogo imepata itilafu sasa nikaona niombe msaada wenu hapa kwenu”

“Unahisi hapa ni kwa fundi magari”

“Hapana kiongozi, nimeona niombe msaada”

“Anataka nini huyo?”

Mlinzi mmoja aliuliza huku akitutizama.

“Eti anahitaji msaada gari lake limeharibika”

“Anazingua hembu mpeleke mahala husika huyo”

“Twende huku”

Jamaa alizungumza huku akianza kuongoza mbele.

“Ahaa gari langu lipo kule!!” 

   

Nilizungumza huku  nikijifanya ninashangaa.

“Wewe twende huku”

Mlinzi huyu alizungumza, sikuwa na ujanja zaidi ya kumfwata kwa nyuma.

“Ingia hapo”

Mlimzi huyu alifungua mlango wa moja ya chumba ambacho kwa kukichungulia ndani kina maboksi mengi.

“Samahani mkuu, ila huku sipo nilipo kuwa nina pahitaji kwenda”

“Ingia bwana”

Jamaa huyu alifoka, kwa macho ya haraka nikatazama kamera za hili eneo nikaziona zimeelekea upande mwengine.

“Tena uvu……”

Sikumpa nafasi mlizi huyu ya kumalizia maneno yake. Nikamtandika ngumi kadhaa za shingo kisha nikamvutia ndani ya chumba hichi na kuufunga mlango. Nikamvunja mlinzi huyu shingo yake, nilipo hakikisha roho yake imeacha mwili, nikaanza kumvua nguo zake na kumuacha na nguo zake za ndani.

 

Nikavua nguo zangu nilizo ziva ana kwa haraka nikaanza kuvaa nguo zake, nikachukua maboksi kadhaa ambayo yana uzito kiasi na sikujua yana vitu gani ndani, nikayaweka juu ya mwili wa huyu  jamaa na kumficha na hata kama kuna mtu ataingia ndani ya hichi chumba basi hatoweza kumuona kirahisi.

Nikaivaa kofia yake vizuri kisha nikavaa na kitambulisho chake pamoja na bunduki yake, nikatoka humu chumbani, kisha nikaanza kuelekea getini walipo wezake huku kofia nikiiweka sawa usoni mwangu.

“Vipi umemuweka?”

Jamaa aliye zungumza mara ya kwanza alionge huku akinitazama.

 

“Ndio ndio”

Nilijitahidi kuiingia sauti ya jamaa niliye muua kwani kitu ambacho katika kikosi hichi cha NSS, ni udhaifu mkubwa ni juu ya askari wake kujuana kisura.

“Pombe zake zikimuishia asubuhi tutamuachia”

“Sawa”

Nikapita getini humu na kuanza kuelekea ndani na kuwaacha askari hawa wakiendelea kusimulia story wanazo zijua wao wenyewe. Nikaingia kwenye lifti na taratibu nikaanza kwenda juu, nilipo hakikisha nimefika katika gorofa husika nikatoka kwenye hii lifti na kwa kutumi kitambulisho cha jamaa niliye muua nikafanikiwa kufungua mlango wa kioo ulipo mbele yangu na kuingia kwenye ofisi hii yenye wafanya kazi wengi sana. Kitu ambacho hadi sasa hivi kinanishangaza ni kwa hawa watu kuto weza kunitambua kabisa, japo kofia imeficha sura yangu kiasi ila wameshindwa kabisa kufanya hivyo.

 

Nikatazama mandhari ya eneo hili nikaona chumba cha mahojiano, nikatembea kwa kijiamini hadi katika chumba hichi, nikafungua mlango na kuingia ndani.

“Habari”

Nilimsalimia mlinzi niliye mkuta mlangoni”

“Salama”

Nikamuona waziri mkuu pamoja na askari wengine wa hapa NSS wakiwa wamesimama katika moja ya kioo kikubwa huku Babyanka akiwa ameikunja mikono yake akifwatilia mazungumzo hayo kwa umakini mkubwa sana.

 

‘Hawa wameshindwa kunifahamu, ila Babyanka sidhani kama atashindwa kunifahamu’

Nilizungumza kimoyo huku nikianza kusonga mbele, nikafanikiwa kusimama nyuma ya moja ya askari, nikamuona Samweli jinsi anavyo endelea kupatiwa mateso makali na askari wawili walio shika vifaa maalumu vya mateso huku wakizidi kumlazimisha Erick kuzungumza ukweli wa kwa nini yupo nchini Tanzania.

“Zungumza ukweli ni nani aliye kuagizaa la sivyo tunakuua?”

Sauti ya ilisikika kutoka kwenye spika ndogo zilizopo katika hili eneo.

“Hahaahahaaaa………!! Kufaaa ni jambo la kawaida kwa kila binadamu ukiniua mimi leo kesho nawe pia utakufa”

Martin alizungumza kwa dharaua na kumfanya jamaa huyo aliye muuliza swali kumpiga ngumi ya shavu.

 

“Hakuna njia nyingine ya kumuhoji huyu mtu?”

Waziri mkuu alizungumza huku akimtazama Babyanka.

“Kusema kweli mkuu kila njia tumejaribu ila kusema kweli imeshindikana”

Babyanka alizungumza huku akiishusha mikono yake chini.

“Mchomeni sindano ya sumu afe anatupotezea muda”

“Mkuu”

“Nimesema mchomeni sindano ya sumu kwani kuna serikali itakuja kudai kifo chake na kama itajitokeza serikali itakayo dai kifo cha huyu gaidi basi hiyo ndio  itakuwa imemfuga gaidi Dany”

Waziri mkuu alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Babyanka usoni mwake.

“Sawa mkuu nimekuelewa”   

“Sasa hivi mchomeni sindano ya sumu ninahitaji kuona jinsi anayo kufa”

 

“Munamtaka Dany?”

Martin alizungumza na kuwafanya watu wote hum ndani kustuka na kumfanya hata waziri mkuu kumtazama Martin.

“Ndio seme yupo wapi?”

“Nitawaambia ni wapi alipo ila ni kwa masharti yafwatayo”

“Zungumza hayo masharti yako?”

“Kwanza ninahitaji miniachie huru, pili nahitaji raisi wenu afe”

“Shenzi shenzi kabisa, raisi wetu afe yeye ni nani?”

Waziri kuu alifoka huku akiingia ndani ya chumba cha mahojiano na mateso.

“Choma choma sindano ya sumu kabisa, anacheza na maisha ya raisi wetu”

Babyanka kwa haraka kapita mbele yangu, alipo fika kwenye mlango wa kuingilia katika chumba hicho akasita na kunigeukia na kunitazama kwa sekunde kadhaa.

 

“Nipe sindano nimchome mwenyewe”

Kelele za waziri mkuu zikamfanya Babyanka kugairi kunitazama, na kuingia ndani kumzuia waziri mkuu kuto kumuua Martin.

“Mkuu huyu anafahamu ni wapi Dany alipo na tukimtumia huyu tunaweza kumpata Dany kirahisi.”

“Sasa swala la raisi wetu kufa, anajua raisi wetu ni nani, anajua ana heshima gani kwetu ehee”

“Tunajua hilo muheshimiwa ila ombi lake la pili hatuto weza kulishushulikia”

“Munaraisi au muna gaidi, munahisi Dany ni gaidi ila si gaidi. Nani katika hichi chumba anajua kwamba raisi wenu aliiua familia ya Dany kwa kuwachinja hadi mtoto wake mchanga eheeee?”

Martin alizungumza huku machozi yakimtoka, waziri mkuu na Babyanka wote wakajikuta wakisitisha mazungumzo yao na kumtazama Martin.

 

“Nitakufa kwa ajili ya Dany, musipo niua leo basi siku nyingine zinazo kuja nitakufa na raisi wenu”

“Unazungumza nini wewe mshenzi?”

“Umenisikia muheshimiwa waziri mkuu na usijiingize kwenye vita hii kwa maana utakuf…….”

Waziri mkuu akampiga ngumi ya shavu Martina na kuwafanya jamaa walio kuwa wakimuhoji Martin kumshikilia wakimzuia.

“Njooeni mumtoe muheshimiwa”

Babyanka alizungumza kwa haraka nikaingia huku nikiwa nimeongozana na askari wengine tulio kuwa nje ya chuma hichi. Nikamtazama Martin kwa bahati nzuri macho yetu yakakutana, taratibu Martin akatabasamu kwa maana yeye ndio anaye nijua vizuri hata niwe katika muonekano wa namna gani.

“Wewe hembu vua kofia yako?”

Babyanka alizungumza huku akinitazama kwa macho makali. Kwa haraka sana, kwa kutumia kitako cha bunduki hii nikaanza kuwapiga askari nikio ongozana nao kuingia katika chumba hichi, jambo lilo mshangaza waziri mkuu na Babyanka. 

 

Babyanka akahitaji kutoa bastola yake kiunoni ila akajikuta akishindwa kufanya chochote kwani bunduki yangu tayari nimesha ielekeza kichwani mwa waziri mkuu. Jamaa hawa walio kuwa wanamuhoji Martin wote nao wakajikuta wakishindwa kufanya chochote, huku askari nilio wapiga kwa kitako cha bunduli wapo chini wamepoteza fahamu. Taratibu nikavua kofia yangu na kuwafanya wote mimacho yakiwatoka kwa kunishangaa, ni sawa mtu akakutana na yule asiye mpenda katika wakati ambao hajategemea kabisa kukutana naye.

“Mfungueni”

Nilitoa kali moja iliyo mfanya jamaa kutoa fungoa ya pingu mfukoni mwake na kumfungua Martina haraka sana kwani nina imani kwamba wote wanaijua historia yangu, na huwa nikizungumza mara moja sirudii mara ya pili. Martin akasimama taratibu huku akijinyoosha viungo vya mwili wake.

“Dany huyo hapo mkamateni sasa”

Martin alizungumza huku akiichomoa bastola ya Babyanka kiunoni mwake.

 

“Dogo vaa nguo za mmoja wapo hiyo ndio njia rahisi ya kutoka hapa”

“Sawa mkuu”

Kwa haraka Martin akaanza kuvua nguo zake kisha akamvuaa askari mmoja aliye lala chini akiugulia maumivu. Akazivaa nguo za askari huyo na watu wote ndani ya hichi chumba wanatazama kila kitu kinacho endelea kwani maisha ya mkuu wao yapo mikononi mwao kwani kosa moja kifo cha waziri mkuu kitakacho pelekea hata ugeni wa raisi Donald Bush kusitishwa.

“Wewe kum** umenipiga sana”

Martin alizungumza huku akimpiga jamaa mmoja aliye kuwa akimhoji, teke la tumbo na kumfanya jamaa huyo kuanguka chini hiku akigumia kwa maumivi. Akamtandika mateke mfululizo ya tumbo hadi jamaa akaanza kutapia damu mdomoni mwake.

“Kumbe  vinaume eheee”

“Oya dogo muda wa kuondoka sasa”

“Sasa hawa tunawaacha hai?”

“Usiwaue”

 

“Sawa mkuu”

“Sasa sikieni, sihitaji kuwaua wala sihitaji kua mtu wenu. Mzee utaniongoza kutoka humu ndani, na wewe Babyanka utaniongoza pia. Martin naomba kofia yangu”

Martin akaiokota kofia yangu na kunikabidhi.

“Martin”

“Naam”

“Walaze”

Kwa haraka Martina akaanza kuwashambulia walinzi walio ndani ya hichi chumba na wote akawazimisha. Nikaishusha bunduki yangu taratibu huku nikimtazama waziri mkuu jinsi anvyo tetemeka kwa woga mwingi.

“Twendeni”

Martina akawatazama askari hawa alio washambuli, wote wamezimia hata watu walio kuwa wanamuhoji nao wamezimia. Tukatoka katika chumba hichi huku waziri mkuu na Babyanka wakiwa wametangulia mbele kwa jinsi tunavyo tembea hakuna hata mfanyakazi ambaye anaweza kustuka kwa kwamba tumewatekea viongozi wao.

 

“Madam madam”

Dada mmoja alizungumza huku akimfwata Babyanka na mkononi mwake ameshika karatasi.

“Simama”

Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya Babyanka na waziri mkuu kusimama huku wakimtazama msichana huyu anaye tembea kwa haraka kufika hapa tulipo simama.

“Kuna simu kutoka kwa raisi”

“Niunganishe naye kwenye simu yangu ya mkononi”

“Sawa”

Tukaendelea kutembea kueleke kwenye lifti, taratibu tukaingia kwenye lifti na kuanza kushuka chini.

“Dany kwa nini unafanya hivi?”

“Kimya pokea simu ya raisi wako na weka loud speker”

Babyanka akatoa simu yake mfukoni na kuipokea na kufanya kama nilicho muambia.

“Ndio madam raisi”

“Mumefanikiwa kufahamu ni wapi Dany alipo?”

“Hapana madam ila tunaendelea kulishuhulikia”

“Si upo na waziri mkuu?”

 

“Ndio?”

“Mpatie simu”

Babyanka akampatia waziri mkuu simu akabaki akiwa ameishika huku mwili ukimtetemeka.

“Muheshimiwa raisi”

“Waziri mkuu nimepata picha inaonyesha Dany ameingia katika nyumba ya mwanao na kwa sasa walinzi wangu wamemshikilia binti yako kwa mahojiano zaidi kwa maana inaonyesha ana mahusiano mazuri na Dany, labda tunaweza kumtumia binti yako kumkamata Dany sawa waziri mkuu?”

Waziri mkuu akaka kimya huku mwili ukiendelea kumtetemeka kwa woga sana.

“Waziri mkuu”

“Nd……iiiiooo muheshimiwa raisi”

“Umenielewa nilicho kizungumza?”

“Ndi…oo madam raisi”

“Mbona unazungumza kwa wasiwasi mwingi vipi?”

Nikamkazia jicho kali waziri mkuu na kujikuta akiirudisha simu kwa Babyanka pasipo kujibu chochote kwani kuropoka kwake kunaweza kukawa mwisho wa maisha yake hapa duniani.


“Haloo”   

Niliisikia sauti ya K2 akizungumza kwenye hii simu hii ni baada ya kuona swali alilo muuliza waziri mkuu limekosa jibu.

“Samahani muheshimiwa raisi naona waziri mkuu amestuka kwa kusikia taarifa hiyo ya mwanaye kuwa kuhisika na kumuhifadhi Dany”

“Sawa basi akiwa sawa nitaomba kuzungumza naye”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Na mutakuwa munatakiwa kunijulisha kila kitu  kinacho endelea baada ya nusu saa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Babyanka akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake huku akihema, taratibu lifti ikafunguka na tukaanza kutoka ndani ya lifti hii, iliyo fika chini kabisa ya ardhi ambapo kuna maegesho maalimu ya magari. Tukaingia kwenye moja ya gari huku Babyanka akiwa ndio dereva.

 

“Tunaelekea wapi?”

“Toka kwanza kwenye hili jengo”

“Ila Dany hili jambo unalo lifanya ni hatari sana kumteka waziri mkuu pamoja na mimi mkuu wa NSS”

“Hatari eheee?”

Nilizungumza huku nikiwa nimekaa siti ya pembeni huku  waziri mkuu akiwa amekaa siti ya nyuma pamoja na Martin. Babyanka hakuzungumza kitu chochote kwani tayari tumefika katika geti la kutoka katika jengo hili taratibu akafungua dirisha, mlinzi wa geti alipo muona ni bosi wake, akarusu geti kufungulia na tuokaondoka.

“Dany tunaelekea wapi?”

“Sehemu salama ni kwako”

“Kwangu unahisi kwamba utashindwa kukamatwa”

“Najua kuna kamera nyingi ila jambo la muhumu ni kuhakikisha kwamba kila kamera iliyo tegwa nyumbani kwako unaizima”

 

“Yaani siamini kama Dany umebadilika kiasi hichi, kwa nini lakini umekuwa muuaji, gaidi?”

Babyanka alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Sikumjibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya ukweli wa kila kitu kilicho tokea kwenye maisha yangu anakijua kwa asilimia kadhaa.

“Unaelekea wapi huku?”

Nilimuuliza Babyanka baada ya kumuona anaelekea sehemu nyingine ambayo ni tofauti na sehemu ninayo ifahamu ilipokuwa nyumba yake ambaye alipewa zawadi na raisi aloye pita madarakani.

“Ninaelekea nyumbani kwangu”

“Kwako?”

“Ndio ulihisi nitakuwa ninaishi kwenye nyumba ile ile?”

“Ukifanya makosa yoyote Babyanka nitakuu wewe na huyu mzee hapa”

“Sawa”

 

Tukaelekea tegeta na gari likasimama kwenye moja ya nyumba yenye uzio wa ukuta na geti kubwa, hatukumaliza hata sekunde mbili geti hili likafunguka, tukaingia kwenye eneo la hili nyumba ambayo ni ndogo kiasi, baada ya gari kusimama nikawa mtu wa kwanza kushuka ndani ya gari hili, niksihika bunduki yangu vizuri huku nikitazama eneo la hii nyumba, sikuona dalili  yoyote ya mtu, nikazunguka upande wa dereva na kwa ishara nikamruhusu Babyanka kushuka huku nikiwa nimenyooshea bunduki hii, taratibu Babyanka akashuka akashuka huku mikono yake ikiwa juu. Martin naye akashuka huku akiwa amemnyooshea waziri mkuu bunduki.

Nikiwa ninashangaa kuangalia kitendo cha Martin kuhakikisha kwamba waziri mkuu hafanyi jambo lolote nikastukia teke kali kwenye mikono yangu na bunduki niliyo ishika ikaangukia pembeni. Babyanka akanipiga teke la kifua lililo nirudisha nyuma kidogo ila nikajiweka sawa, Martin akahitaji kuingilia ili swala ila kwa ishara ya mkono nikamuzuia asiingilie hili swala.

Nikajiweka sawa huku nikimtazama Babyanka aliye kunja ngumi za mikono yake huku akiivuta juu kidogo suruali yake ya jinzi ambayo imembana kidogo.

 

Babyanka akaanza kunifwata kwa kasi huku akirusha ngumi ambazo nikaanza kuzizuia kwa mikono yangu, kwani hata mimi mwenyewe kwenye swala la kupigana nipo vizuri sana. Nilipo  ona mashambulizi ya Babyanka yamekuwa makali sana na nimechoka kuyazuia, ikanilazimu na mimi kuanza kujibu mashambulizi hayo kwa haraka kadri nilivyo weza. Uzuri ni kwamba ninamfahamu vizuri Babyanka na tulisha wahi kuwa walinzi wa raisi aliye pita madarakani na tulisha yatoa maisha yetu kwa ajili ya kumlinda raisi huyo ambaye mwisho wa siku alinisaliti kwa kufwata amri ya dada yake K2.

Nikajirusha hewani na kuvurumisha teke langu kwa kumguu wa kulia lililo mpiga Babyanka mabegani mwake na kumuangusha chini.

“Sihitaji kukua ila ukihitaji kukua, nitafanya hivyo”

Nilizungumza huku nikimtazama Babyanka akisimama huku akijiweka sawa mikono yake. Babyanka akajaribu kurusha teke ila nikalizuia hewani kwa teke lililo mfanya ayumbe kwani matarajio yaliyo yatarajia kwa teke lake yameenda tofauti kabisa. Nikamtazama mguu wake wa kulia ambao nimemzuia teka lake nikaona akiutingisha tingisha kuuweka sawa kwani nina imani ameumia kwa kiasi fulani.

 

“Babyanka acha hichi unacho taka kukifanya”

“Siwezi kuwa msaliti kwa ajili ya nchi yangu”

“Unahisi mimi ni msaliti wa hii nchi?”

“Wewe ni msaliti na nilazima nikuue”

“Usiingilie matatizo ambayo hayakuhusu wewe kuingilia”

“Kazi yangu ni kulinda viongozi wa nchi hii”

“Kulinda viongozi ambao hawahitaji kulindwa, viongozi  ambao wameweza kuitekeza familia yangu. Hembu funguka Babyanka utakufa bure, kufa kwa ajili ya vitu vya maana na si kufa kwa ajili ya watu wasio na maana yoyote”

“Siwezi kufwata maneno yako”

Babyanaka baada ya kumaliza kuzungumza maneno yake, akaanza kunishambulia tena. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuanza kupigana naye kana kwamba ninapigana na mwanaume mwenzangu. Kila Babyanka alipo jaribu kunishambuli akajikuta akishindwa kabisa kunihimili kwani nimecharukwa na nina uwezo mkubwa sana kuliko yeye. Nikahakikisha  kwamba ninampiga Babyaka hadi mwili ukamlegea kabisa na kulala chini. 

 

“Mmmmmm”

Martin aliguna huku akimtazama Babyanka jinsi anavyo mwagikwa na damu mdomoni mwake.

“Wakistukia hili ni lazima wata itafuta simu ya huyu malaya”

Nilizungumza huku nikihema kwani shuhuli ya kumdhibiti Babyanka nayo sio ndogo.

“Ngoja nichukue simu yake”

“Hapana muangalie huyo mzee”

Nilizungumza huku nikimsogelea Babyanka, nikachuchumaa na kuanza kumpapasa mifukoni mwake, nikaitoa simu yake hata kabla sijasimama simu ya Babyanka ikaita na kuona namba inayo andikwa imeandikwa ‘Madam President’. Nikaitazama simu hii kwa umakini mkubwa kisha nikikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Nusu saa limepita Babyanka mumefikia wapi?”

“Mbona unawasiwasi muheshimiwa raisi?”

Nilizungumza kwa sauti yangu ya asilia ambayo nina imani kwamba K2 anaifahamu vizuri sana.

 

“DANYYYY…….!!!!”

“Ninaimani utakuwa umeshangazwa na uwepo wangu karibu na vibaraka wako ulio wajaza sumu ya kunichukia mimi si ndio?”

“Mwanaharamu wewe ni nani aliye kupa ujasiri wa ku…kkuuu..uuu”

“Kufanyeje……? Unapatwa na kigugumizi ikiwa una mamia ya walinzi walio kulinda hapo ikulu. K2, ohooo samahani. Muheshimiwa raisi hili swala ukishirikisha walinzi wako nitahakikisha kwamba Babyanka na waziri mkuu wako wote maisha yao ninayaondoa kwa kuwaua kinyama sana na vifo vyao vitakuwa mikononi mwako”

Nilizungumza kwa msisitizo jambo ambalo nina imani kwamba linampa wasiwasi mkubwa K2, nikaweka simu hii loudspeaker ila sote tulipo hapa tuweze kumsikia muheshimiwa raisi K2.

“Dany unahisi kumua waziri mkuu na Babyanka vifo vyao vitakuwa na hasara kwangu, umekosea baba na nitahakikisha kwamba ninakuwinda hadi mwisho wa pumzi yangu”

 

“Unaniwinda ila tambua ya kwamba mimi ndio nitakuwa mtu wa mwisho kuweza kuikatisha pumzi yako na hapo ndipo nami nitakuwa radhi kuingia katika mikono ya hii serikali”

“Hahahahaaaaaaa…..ohoo Mungu wangu Dany unahisi wewe peke yako unaweza kupambana na maelfu ya wanajeshi nilio nao eheee?”

K2 alizungumza kwa dharau kubwa sana hadi waziri mkuu akashangaa. Taratibu nikasimama huku nikiendelea kumtazama Babyanka jinsi alivyo lala chini akiugulia muamivu kwani kipigo nilicho mpiga ni kipigo cha kumnyong’onyeza na si kumuua.

“Unatumia jeshi kulinda mauvo yako ya kumchinja mama yangu, kumchinja dada yangu, kumchinja mwanangu, kumchinja mama wa mwanangu eheee?”

“Yaaa niliwaua kuhakikisha kwamba unaijisikia maumivu ya ujinga wako ulio jaribu kuifanya mbele yangu. Kumbuka kwamba nilikuambia kwamba sisi ndio wenye nchi na nilikuahidi kukuonyesha na ndio nimekuonyesha sasa wewe waue tu huyu waziri mkuu na Babyanka na wala usihisi kwa kuwatumia hao nitasitisha uovu wangu kwako”

 

Simu ikakatwa taratibu nikamuona waziri mkuu akikaa chini huku akionekana haonekani kushangaa sana kwa kile alicho kisikia.

“Mwenye masikio haambiwi sikia mwenye macho haambiwi ona.”

Nilizungumza huku nikimnyanyua Babyanka chini alipo lala na nina imani kwamba amesikia kila kitu kinacho endelea.

“K2, K2, K2 mshenzi mkubwa weweee”

Waziri mkuu alizungumza huku akilia kwa uchungu. Nikafungua mlango wa gari siti ya nyuma na kumkalisha Babyanka.

“Huyu mzee vipi!!?”

Martin aliuliza huku akimtazama mzee huyu jinsi anavyo lalamika chini alipo kaa.

“Muache amesha elewa nchi yake inaenda vipi”

Nilizungumza huku nikiiokota bunduki yangu.

“Dany”

Babyanka aliniita kwa sauti ya upole. Nikamsogelea karibu alipo kaa kwa ajili ya kumsikiliza kitu anacho hitaji kukizungumza.

 

“Samahani”

“Kwa kipi?”

“Kwa hili lililo jitokeza”

“Ulikuwa unafanya kazi yako, sikulaumu katika hilo”

“Siamini kama K2 anahusika na kifo cha mama yako, alikuwa mwalimu wangu mzuri sana”

“Nashukuru kwa kuweza kusikia kwa masikio yako wewe mwenyewe. Je upo tayari kuungana nami?”

“Nipo tayari”

Babyanka alizungumza kisha akatema damu kidogo, nikamtazama waziri mkuu. Taratibu akanyanyuka huku Martin akiendelea kuwa makini naye.

“Mzee upo tayari kwa hili, kwa maana raisi wako haioni thamani yako. Je nikuue kama alivyo sema raisi wako kwamba kifo chako kwake hakina thamani”

Taratibu nikamuona waziri akipiga magoti chini huku akilia kwa uchungu. Taratibu akanishika miguu yangu huku akiniomba msamaha”

 

“Nisameheeeee”

Alizungumza huku akiendelea kulia.

Nikamnyanyua waziri mkuu huku nikimtazama usoni mwake.

“Nina imani mwanao Lucy yupo mikononi mwa K2 na ninakuambia kwamba hayupo salama, anaweza kumfanya chochote ili mradi mimi nijisalimishe, ili hayo yote yanaweza kwenda tofauti pale tu utakapo amua kuungana nami”

 

“Nipo tayari, nipo tayari”

Waziri mkuu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu kwa macho yalio jaa uwekundu wa machozi yanayo endelea kumwagika usoni mwake.

“Dany eneo hili sio salama tena na nina imani kwamba NSS, wamepewa kazi ya kunitafuta na wakija kunipata hapa basi hata wewe utakuwa umekamatwa”

“Twendeni shambani kwangu”

Waziri mkuu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ni wapi?”

“Bagamoyo ndani ndani, sidhani kama huko kuna mtu anaweza kuja au kufahamu kwamba tupo huko”

“Hatuwezi kutumia gari hili tena”

Babyanka alizungumza kwa sauti ya upole huku akiwa ameinama.

“Tunaweza kupata gari lolote?”

“Lipo gari langu moja ni jipya kabisa nimelinini wiki  iliyo pita nina imani linaweza kutupeleka huko”

 

“Twende tukachukue funguo”

Nilizungumza huku nikimpa mkono Babyanka akaushika na taratibu tukaanza kutembea kuelekea ndani kwenye nyumba yake hii, akaniomba nitoe funguo chini ya kapeti, na nikafanya hivyo na kumkabidhi funguo. Moja kwa moja tukaelekea hadi chumbani kwake, Babyanka akachukau funguo kwenye droo ya dressing table yake.

“Unajisikiaje?”

Nilizungumza huku nikimtazama Babyanka usoni mwake.

“Najisikia maumivu kwenye mbavu na tumboni”

“Utakuwa umepata itilafu kidogo, ila utakaa sawa”

“Yaaa, hembu fungua hilo kabati la nguo”

“Kuna nini?”

“Kuna begi lina silaha”

Nikafungua kabati hili na kukuta begi kubwa jeusi, nikalitoa na kulibeba mkononi tukatoka humu ndani na kuifunga nyumba yake. Moja kwa moja tukaelekea nyuma ya nyumba hii ambapo kuna maegesho ya magari. Babyanka akanionyesha gari husika tukaingia ndani, ya hili gari na taratibu nikaliwasha gari hili na kuliweka sawa na kuanza kuelekea getini. 

 

“Magari yangu yote yana kifaa maalumu nilicho funga kwa chini, hayawezi kunadwa na rada wala satelaiti popote niendapo”

“Kwa nini umefunga kifaa hicho?”

“Niliamua tu kufunga kwa usalama wangu binafsi”

Waziri mkuu na Martin wakaingia ndani ya gari hili aina ya Toyota TX. Taratibu geti likafunguka nikaanza kutoa gari hili taratibu. Kabla hata sijakunja kona ya kuingia barabarani gari zipatazao nne kutoka katika kitengo cha NSS, nikaziona zikija kwa kasi jambo lililo nifanya nianze kufikiria kwa haraka ni kitu gani ninaweza kukifanya ili kuhakikisha kwamba ninawakimbia askari hawa wa kikosi cha NSS, mabao tayari wamesha gundua kwamba mkuu wao pamoja na waziri mkuu wapo mikononi mwangu jambo ambalo nina imani wanaamini kwamba ni hatari kwao.


“Wewe twende”   

Babyanka alizungumza huku naye akitazama gari hizi zinavyo kuja kwa kasi katika eneo hili, kwa taratibu nikaanza kuingia barabarani gari hizi nazo zikakatiza katika njia ambayo tumetokea, njia inayo elekea nyumbani kwa Babyanka.

 

“Mzee ni wapi tunapo elekea?”   

“Elekea hii njia ya Bagamoyo tukifika mbele huko nitakuambia ni wapi pa kuelekea”

Nikaanza kuongeza mwendo kasi wa hili gari huku nikikimbizana na muda ambao tupo nao kwani tayari hali ya hatari imesha tangazwa kwenye vyombo vya usalama na ninatambua ni lazima hadi  kuna pambazuka ni lazima kutakuwa na vizuizi vingi barabarani.

“Hembu simu yangu”

Babyanka alizungumza kwa haraka nikatoa simu yake mfukoni na kumkabidhi.

 

“Unataka kufanya nini?”   

“Nahitaji kufunga kila kitu wasinione kwenye satelaiti”

“Sawa”

Babyanka akaanza kuminya minya kioo cha simu yake, mimi kazi yangu ni kuhakikisha kwamba ninafika Bagamoyo mapema sana.

“Hawawezi kutufwatilia”

“Umezima?”

“Hapana nimeonyesha muelekeo tofauti na ninapo kwenda”

“Kivipi yaani?”

“Kwa sasa wanaona tunaelekea Mbagala”

“Haiwezi kulete hatari wakastukia?”

“Hapana hakuna mwenye ujuzi  huo ofisi nzima”

“Sawa”

 

Hadi inatimu saa kumi na mbili alfajiri tayari tukawa tumefanikiwa kufika mji Bagamoyo. Waziri mkuu akaanza kunielekeza kuelekea kuelekea katika shamba lake. Japo barabara sio nzuri ila gari hili kidogo linaweza kuhimili mashimo mashimo yaliyopo barabani.

“Kunja sasa kulia nenda moja kwa moja kwenye huo msitu”

“Sawa mzee”

Kusema kweli hii sehemu tunayo elekea kweli ni porini na wala sidhani kama kuna mtu yoyote ambaye anaweza kutupata kirahisi kwani kuna pori kubwa lililo jaa misitu  mingi sana.

 

“Waziri mkuu hivi huku kweli kuna dalili ya watu kiishi?”

Babyanka alimuliza waziri mkuu huku akigeuka na kumtazama siti ya nyuma.

“Wee acha huku nimepapata siku nyingi sana, hata kabla ya kuwa waziri mkuu”

“Mmmmm kazi kweli kweli yaani na hivi ninavyo jisikia ninajihisi kunyong’onyea kabisa”

“Tumebakisha kama kilomita moja hivi?”

“Mmmmmm, kilomota moja!!?”

Martin naye aliuliza kwa kushangaa, kwani hata mimi mwenyewe dereva ninahisi mikono yangu kuniuma.

“Ndio tuvumilie tu kidogo tutafika”

“Huku pia ni Tanzania?”

“Ndio ni Tanzania”

“Mmmmmm kweli Tanzania ni kubwa”

“Yaa”

 

“Ila Martin hata Nigeria ni kubwa”

“Sio kubwa snaa kama Tanzania mkuu”

Mazungumzo ya hapa na pale ndani ya gari, tukajikuta hata mawazo ya uchovu wa hii safari ya kipotea na watu wakazidi kuzoeana sana hususani kwa Martin. Hadi inatimu saa mbili na nusu asubuhi tukafanikiwa kufika eneo la shamba kubwa la huyu mzee, ambapo tumekuta nyumba moja ndogo iliyo tengenezwa kuta zake kwa mbao.

“Karibuni jamani”

Waziri mkuu alizungumza huku tukishuka kwenye gari. Taratibu nikaanza kujinyoosha viungo vyangu vya mwili.

“Karibuni ndani”

Waziri mkuu  alizungumza huku akianza kutangulia mbele, Babayanka akaanza kumfwata kwa nyuma.

“Mkuuu”

“Ndio”

 ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

BLOG