Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

POWER SEHEMU YA 5/10

 

 


 POWER

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 5 KATI YA 10

 


Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama jamaa huyu usoni mwake. Kwa ishara ya macho akaanza kunionyesha wingi wa vijana alio ambatana nao kwenye nyumba hii. Wingi wa vijana hawa wanaweza kumua mtu yoyote humu ndani. Nikamuona Camila akija eneo nililo simama kwa kasi, jamaa huyu akaliweka sawa koti lake ili bastola yake isiweze kunekana.

“Nimekuelewa, nitajitahidi kukupatia. Nipeni muda”

“Sawa sawa bwana Ethan. Tunamuona mrembo wako anakuja hapo. Angalia usije ukampoteza”

Mwnaaume huyo aliendelea kuzungumza jambo lilio nifanye nizidi kupatwa na wasiwasi.

“Sawa sawa usijali katika hilo”

Simu ikakatwa na nikamkabidhi kijana huyu na akaondoka.

“Ulikuwa unazungumza na nani mume wangu?”

“Ahaa, kuna mfanya biashara mmoja alikuwa akinipa pole sasa ametuma wawakilishi wake hapa nyumbani”

Nilizungumza huku nikiwa na wasiwasi mkubwa sana.

“Mbona kama una wasiwasi mume wangu?”

“Hakuna”

“Kuna hii video mume wangu. Huwezi amini kumbe yule Dany ni gaidi yule ambaye nilisha wahi kumsikia sikia kwenye historia ya magaidi wa dunia”

Camila alizungumza huku akinionyesha video hii inayo muonyesha Dany tulite muacha nchini Tanzania na alikuwa ni msaada mkubwa sana kwetu hadi baadhi ya mazoezi amemfundisha mke wangu. Maneno ya vitisho anayo yazungumza Dany juu ya nchi ya Marekani yakaniacha mdomo wazi.

“Mbona hata haonekani kama ni gaidi?”

“Hata mimi mume wangu sielewi. Yaani huwezi kuamini kama ni gaidi, kuishi nasi vizuri kutusaidia kumbe ndio yule Dany halisi”

“Oooh Mungu wangu hali ya dunia inakwenda kuwa mbaya mke wangu”

“Ni kweli, sijui hili tatizo tunaweza kulitatua vipi kwa maana hii ni vita mume wangu”

Nikajikuta nikiguna huku nikimtazama Camila usoni mwake. Nikatamani kujizuia kumuambia Camila kuhusiana na vitisho ambayo nilipewa na mtu nisiye mfahamu ila nikajikuta nikizungumza tu.

“Mke wangu tuta tatizo?”

“Tatizo gani?”

“Eneo zima hili la hapa nyumbani. Limezungukwa na watu ambao wanahitaji kutuangamiza, usiangalie nyuma kwa maana wana tufwatilia”

Nilimzuia Camila kugeuza shingo yake ili kuweza kutazama watu hao walipo.

“Kutuangamiza kwa nini?”

“Wanahitaji boksi jeusi. Hili sekeseka la Dany na Marekani nina imani kwamba linaweza kuwasukuma watu hawa kuzidi kutushinikiza kuhakikisha kwamba tunalitoa boksi hilo jeusi”

“Ohoo Mungu wangu. Kwani boksi hilo jeusi wewe unalifahamu?”

“Sijawahi kuliona kwenye maisha yangu, ila mwanasheria alisha wahi kuniambia kwamba baba ameliacha sehemu na kuna maelekezo ambayo yapo kwenye mwili wangu na unakumbuka ulisha wahi kunichana ila ukakosa?”

“Ndio”

Camila alinijibu kwa unyonge kwani tukio hilo alilifanya kwa uadui mkubwa kati yangu mimi na yeye.

“Mambo ndivyo jinsi yalivyo mpenzi wangu, mimi wewe, Mery ndani huko sote hatupo salama”

“Hiyo kazi naomba uweze kuniachia mimi”

“Kazi gani?”

“Kazi ya kushuhulika na hao watu.”

“Utawafahamu vipi?”

“Dany alinifundisha uwezo mkubwa sana wa kuweza kuwafahamu maadui zangu. Nina imani kwamba nitawafahamu mmoja baada ya mwengine taratibu. Jambo la kufanya hakikisha kwamba huonyeshi wasiwasi wowote kwa mtu wa aina yoyote kwamab kuna jambo baya limepangwa kufanywa hapa nyumbani”

“Sawa mke wangu”

“Ngoja nijaribu basi kumtafuta Dany kama nitaweza kuzungumza naye nitamuomba aweze kusitisha mpango wake wa kwenda kuishambulia Marekani”

“Sawa mke wangu”

Camila akanibusu mdomoni kisha akaondoka eneo hili, nikarudi eneo walipo kina Frenando na nikaendelea kuzungumza nao mambo mawili matatu kisha nikachukua kombe walilo niletea na kuelekea ndani. Nikiwa ninapandisha ngazi za kuelekea gorofani, Camila akanifwata kwa nyuma na tukaingia kwa pamoja ndani huku akionekana ana habari anayo hitaji kunieleza.

“Tumewapata maadui wote”

“Wapo wangapi?”

“Hapa nyumbani wapo ishini na mbili”

Camila alizungumza huku akianza kunionyesha picha za watu hao. Nilamuamini sana juu ya upelelezi wake mara ya kumuona kijana ambaye amenikabidhi simu nizungumze na bosi wake.

“Eeehe tunafanyaje juu ya hawa watu?”

“Tunamuangamiza mmoja baada ya mwengine tena kimya kimya. Kisha yule kijana ndio atakuwa wamwisho yeye atatupeleka walipo wezake”

“Hili swala inabidi uwe makini sana mpenzi wangu”

“Usijali, nina jiamini na nina uwezo mkubwa zaidi ya unavyo fikiria. Ila sijajua kwa upende wangu wewe mwenzangu”

“Unapnaje tukamueleza baba yako?”

“Ethan hili ni jambo la sisi wawili. Hakuna kumuambia mtu. Hapa ninasimama kama mke wako, baab yeye naye anamajukumu yake bwana”

“Nimekuelewa mke wangu”

Camila akanisogelea taratibu na kunibusu mdomoni mwanngu. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa huku kila mmoja akisikilizia msisimko wa mwenzake. Tukaanza kunyonyana midomo yetu huku taratubu nikirudi nyuma nyuma na tukaingia bafuni kwani kufanya mapenzi katika chumba chetu kunaweza kuwafanya watu watakao pita nje ya mlango wetu kuweza kusikia kelele zetu za mahaba.

Camila kwa haraka akapandisha sketi yake juu na kushusha chupi yake, nikafungua suruali yangu na kumtoa jogoo wangua ambaye tayari alisha simama kwa ajili ya mashambulizi. Camila taratibu akainama kidogo na kumpokea jogoo wangu kwa mguno mlaini wa kimahaba. Nikaanza kumshuhulikia taratibu na kadri dakika zinavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo zidi kushambulia kitumbua chake.

“Aii…sii..aiii….baby”

Camila alilalama huku akiwa ameyafumba macho yake.

“Ume ni miss mke wangu”

“Yes baby….yea..hhhh…ohooo fuc** my pu**”

Camila aliendelea kuzungumza maneno yaliyo zidisa muamko mkubwa wa mashambulizi kwake.

“Am coming baby”

Camila alizungumza huku akikizungusha kiuno chake, unaweza kuhisi si mtoto wa Kijerumani vile na ni mswahili halisi aliye zaliwa katika kabila la wadigo ama wazaramo.

“Kweli”

“Yess baby….ohooo”

“Aa….ahaa…aiissi…nako….nako…j……o……”

Nami nilizungumza maneno yatokanayo na utamu wa waarabu wangu wanao hitaji kuvamia kitumbua cha Camila. Tukajikuta kwa pamoja tukiimaliza safari yetu ya mapenzi, huku kila mmoja akisikilizia utamu wa viungo vyake.

“Ahaa…nilikuwa na hamu na wewe mume wangu”

“Hata mimi mke wangu”

“Sasa hapa kiu kidogo imepungua, nina imani kwamba ninaweza kwenda kufanya jambo sasa juu ya hawa washenzi”

Camila alizungumza huku akijichomoa taratibu kwenye jogoo wangu. Akakaa kwenye choo hichi cha kukaa, akachukua toilet paper na kuanza kujifuta taratibu kitumbua chake.

“Yaani Ethan shahaw** zako ni za moto. Yaani ninazisikilizia hadi kwenye ubongo”

“Kweli?”

“Ndio, yaani hapana kwa kweli. Wewe mwanaume sijapata ona”

“Nashukuru mke wangu.”

Tulipo hakikisha kwamba viongo vyetu vipo salama. Kila mmoja akajiweka sawa nguo yake, tukatoka bafuni humu, tukajipulizia perfume kisha tukaendelea na mipango ya mazishi ya bi Jane Klopp. Wachezaji wa zamani ambao walicheza na mzee Klopp nao wakazidi kufika katika msiba huu kutoa pole ya kuondokewa na mama yetu.

Majira ya saa moja kasoro usiku, Camila akaniomba tuelekea kwenye moja ya chumba cha chini ya ardhi katika hii nyumba yetu. Nikaongozana naye na kuingia kwenye chumba hicho, sikuamini macho yangu mara ya kuwakuta watu wote ambao alinionyesha wakiwa wamelala chini.

“Umewaua hawa?”

“Hapana hakuna niliye muua. Ila kuna sumu fulani ya kisindano Dany alinifundisha nimeweza kuwashoma mmoja baada y mwengine na nimeweza kuwaleta hapa”

“Ehee huyu ndio kijana ambaye ameniletea simu yake nizungumza na bosi wake.”

“Simu yake hii hapa ninayo na nimeweza kuangalia muda ule ni nani aliweza kumpigia nimeweza kupata ni nani uliye zungumza naye”

“Ni nani?”

Camila akanionyesha picha ya mwanaume mmoja ambaye kwa haraka sana niliweza kumfahamu kwani ni miongoni mwa watu nilio kutana nao kikao cha siri nilicho fanya na viongozi wa chama cha upinzani nchini Tanzania.



“Vipi mbona unashangaa mume wangu?”

“Huyu , huyu mtu nina mfahamu”

“Huyu mzee una mfahamu?”

“Ndio”

“Anapatikana wapi?”

“Tumemuacha nchini Tanzania, katika ule mpango wangu wa kulipiza kisasi kwa mzee Poul Mkumbo huyu mzee, nimeamua kudhamini moja ya chama cha siasa ili kiweze kumuondoa madarakani. Sasa huyu mzee ni muhisika”

“Ohoo basi kutakuwa na jambo linalo endelea hapo katikati?”

“Yaa”

“Basi kama ni hivyo, muhusika mkuu yupo Tanzania, itabidi hawa tuwaweke chini ya ulinzi wa serikali?”

“Alafu?”

“Tunamfwatilia huyo mwengine?”

“Huoni kwamba hiyo inaweza kuvujisha siri na kumbuka kule Tanzania tumewekeza kwenye kampuni kubwa na kama adui nimeweza kumuweka karibu yangu jambo ambalo ni hatari sana”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Camila usoni mwake.

“Basi tuwaue?”

“Hilo nalo ni kosa jengine ambalo tutalifanya mume wangu na kumguka kwamba hapa ni Ujerumani na upelelezi ukianza kufanyika haijalishi mimi ni mtoto wa nani, mwishowe nitaishia jela na nitamchafua baba yangu”

“Nimekuelewa mke wangu”

“Nampigia baba na ninamueleza juu ya swala hili na akikubaliana tuwashikilie chini ya ulinzi wake basi tunaweza kufanya hivyo”

“Sawa”

Camila akafanya kazi hiyo kama nilivyo mueleza. Baada ya lisaa kikiso maalumu cha makachero ambacgo kina fanya kazi chini ya raisi kikafika nyumbani hapa. Wakawabeba wahalifu hawa kimya kimya pasipo watu wengine walipo kwenye msiba huu kuweza kufahamu ni kitu gani kinacho endelea.

Siku iliyo fwata taratibu zamazishi zikakamilika , na maiti ya bi Jane ikapelekwa katika kanisa la Lutheran kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho, wingi wa watu na umaarufu wa familia hii ukafurika hapa kanisani, watu wengi wakazidi kutoa pole zao kwa mimi na dada Mery. Tulipo maliza ibada tukaelekea katika eneo alilo zikwa mzee Klopp miaka kadhaa ya nyuma iliyo pita. Tukauaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho kisha akazikwa. Kusema kweli kama ni kubaki yatima basi sasa ni yatima mkubwa, hata ukiwa na pesa nyingi sana duniani, ila umuhimu wa wazazi ni mkubwa na ni wa muhimu kuiko hata pesa. Mazishi yalipo malizika tukarudi nyumbani huku muda wote Camila akiwa pembeni yetu mimi na Mery kwani yeye ndio mtu wa pekee anaye weza kutufariji.

Baada ya wiki mbili tukaendelea na shuhuli zetu za kawaida. Nikanza kufanya ziara za kustukiza katika kampuni zangu zote za hapa nchini Ujerumani. Nilipo hakikisha kwamba ziara yangu ya siku tano imekwenda kama nilivyo hitaji, nikanunua ndege yangu binafsi aina ya The Boeing 747-8 VIP private jet ambayo imenigarimu kiasi cha dola za kimarekani milioni mia tatu na sabini. Jet yangu hii ina sifa zote nilizo kuwa nina zihitaji, kwanza ina uwezo wa kusafiri kwa umbali mkubwa sana, pili ina seble kubwa, chumba cha kulala chenye bafu na choo. Pia ina ofisi kubwa ambayo ninaweza kufanya vikao na wafanyakazi wangu baadhi.

“Ohoo Mungu wangu”

Camila alizungumza kwa furaha mara baada ya kumfungua kitambaa nilicho kuwa nimemfunga usoni mwake, mara tu ya kuingia kwenye ndege hii kubwa. Kwani katika mipango yangu ya ununuzi ndege hii sikuweza kumshirikisha mtu wa aina yoyote na Ethan pekee ndio aliye fahamu na uzuri yeye si binadamu.

“Ethan unataka kuniambia kuanzi hivi sasa hii ni ndege yetu?”

“Yaa ni ndege yetu, popote ambapo tutahitaji kwenda basi tunaweza kwenda”

“Ohoo Mungu wangu nakupenda sana mume wangu”

“Ninakupenda pia mke wangu”

Nikaanza kumtembeza Camila ndani ya ndege hii, kila sehemu aliyo ingia hakuamini macho yake, kwani imetengenezwa katika mtindo mzuri sana ambao umeendana na kiasi cha pesa ambacho nimenunulia.

“Camila fumba macho yako”

“Kwa nini?”

“Wewe funga tu mpenzi wangu”

Camila akanitii na kufumba macho yake. Taratibu nikatoa kisanduku kidogo cha kuhifadhia pete, nikapiga goti moja chini kisha nikamuomba aweze kufumbua macho yake.

“Je upo tayari kuwa mke wangu?”

Camila akapatwa na mshangao mkubwa ulio ambatana na furaha kubwa pamoja na machozi mengi sana.

“N…dioo Ethan”

Taratibu nikamvisha pete hii iliyo nigarimu kiasi kikubwa cha pesa. Camila akaninyanyua na kunikumbatia kwa nguvu huku akiendelea kulia. Taratibu tukaanza kunyonyana midomo yetu na kutokana tupo ndani ya chumba chetu cha kulala hatukuona haja ya kunyimana haki inayo stahili katika penzi letu

Usiku wa siku ya leo tukalala katika ndege yetu siku iliyo fwata tukaelekea ikulu ya Ujerumani ambapo sasa ndipo familia ya Camila inapo ishi. Tukawaleza wazazi wake juu ya swala zima la mimi kuhitaji kumuao mtoto wao pale nitakapo maliza kufanya kazi yangu ambacho itanirudisha nchini Tanzania.

Wazazi wa Camila hawakuana kipingamizi chochote na mimi, kila mmoja akaonekana kujawa na furaha kubwa sana kwa pendekezo langu kwa mtoto wao.

Tukamueleza Mery juu ya mpango wetu wa sisi kufunga ndoa. Mery kwa upande wake hakuwa na pingamizi la aina yoyote kwani naye mapenzi yake na rafiki yangu Ethan yamekoaa na wanapenda sana. Nikaka Ujerumani kwa siku mbili kisha nikaanza safari ya kurudi nchini Tanzania na safari hii nikiwa peke yangu katika ndege yangu hii ya kifahari. Nikiwa angani nikawasiliana kwa njia ya skype na Qeen pamoja na Latifa na nikawaomba waweze kuniandalia hoteli ambayo nitafikizia kwa siri sana.

“Tunafurahi sana mkuu kwa kurudi kwako kwa maana katika kipindi hichi cha wiki tatu tumekuwa tunapelekeswaha sana na huyu mwanamke wako”

“Musijali, kila jambo litakwenda sawa na hii ndio safari yake ya mwisho ya yeye kuweza kuumia”

“Sawa mkuu, tunafurahi kuendelea kusikia hivyo”

“Lile swala la yule mzee katika kikundi cha kile chama mume lishuhulikia?”

“Ndio mkuu tunakusubiria wewe ufike ili kama ni kumteka aweze kutekwa na kuweka chini ya uangalizu maalumu si unajua tayari watu wamesha anza kampeni?”

“Ndio natambu hilo. Clara je munakwenda kumtembelea?”

“Ndio hata leo tumetoka huko na ameweza kutuulizia”

“Sawa, nahitaji muje kunichukua uwanja wandege”

“Saa ngapi?”

“Sijajua marubani wangu wanaweza kutumia muda gani kufika nchini Tanzania, ila nina ndege ambayo ipo vizuri sana”

“Kuna taratibu za kutua nchini Tanzania kwa ndege binafsi je umezikamilisha?”

“Ndio nimezikamilisha, na nimepewa ruhusa ya kutua nchi karibia ya ishirni barani Afrika”

“Sawa mkuu tukutakie safari njema”

“Nanyi pia”

Tumaliza mazungumzo haya, nikaingia kwenye upande wa barua pepe katika simu yangu na nikaanza kupitia ofa kadhaa za timu kubwa barani Ulaya ambazo zinahitaji niweze kucheza mpira. Sikuhitaji kujibu ujumbe hata mmoja kwa maana nina hitaji kuikamilisha ndoto yangu ya kumfilisi bwana Poul Mkumbo na nina imani kwamba hapo akili yangu inaweza kuwa tayari katuka kucheza mpira na kuendelea kuishia katika kipaji changu ambacho siku zote mzee Klopp alinihusia niweze kukifanyia kazi. Nikawauliza marubani wangu ni muda gani ambao ninaweza kufika nchini Tanzania, walipo nipa muda husika, niwatumia meseji Qeen na Latifa na kuwajulisha kwamba nitaingia nchini Tanzania majira ya saa kumi usiku.

‘Tutakuwepo hapo mkuu’

Niliipokea meseji hii kutoka kwa Latifa. Majira ya saa kumi usiku kwa mara ya kwanza ndege yangu toka nianze kuitumia ikatua katika ardhi ya nchini Tanzania. Nikashauriana na wa marubabi wangu waweze kurudi Ujerumani na ndege yangu baada ya siku mbili kwani sinto weza kuiacha ikae katika uwanaja wa ndege wa hapa Tanzania, moja inaweza kutumia na maadui wangu kama moja ya sehemu ya kujipatia kipato kwani endapo wataamua kuiteka na kudai pesa nyingi basi itanilazimu kutoa kiasi kikubwa cha pesa.

Kwajinsi nilivyo vaa kofia pamoja na jinzi na tisheti ni ngumu sana kwa watu wa kawaida kuweza kunifahamu. Baada ya kukaguliwa begi langu la nguo nikatoka nje ya uwanja huu na kukutana na Latifa pamoja na Qeen. Tukaingai kwenye gari walilo kuja nalo ambapo siku kadhaa za nyuma niliwatumia pesa za kutosha kwa ajili ya kununua gari maalumu kwa kazi ambazo zimetuleta huku.

“Kuna update yoyote kwa masaa haya kadhaa ambayo hatujawasiliana nanyi?”

“Hapana mkuu”

“Huyo kijana muliye sema kwamba atakuwa ni mlinzi wangu wa siri je anajiweza katika kila idara ya kunilinda au mumemchukua mbeba vyuma ambaye akipigwa ngumi moja tu anaanguka?”

“Hahaaa hapana ni kijana mmoja smart na hata ukimona huto weza kutegema kama anaweza kuwa ni mpambanaji mzuri sana”

“Nahitaji kuonana naye usiku huu huu”

“Sawa”

Latifa akampigia simu kijana huyo na kumueleza aweze kufika katika hoteli ambayo tunaiendea hivi sasa. Tukafika katika hoteli moja iliyo nje ya jiji la Dar es Salaam. Moja kwa moja tukaeleka hadi katika chumba walicho nikodishia, baada ya muda kidogo kijaan huyo akafika. Ni mwembaba, ana sura nzuri na ya upolea sana na kwa haraka kwa kweli huwezi kufahamu kama ana uwezo wa kuweza kufanya mambo makubwa sana.

“Ethan huyu anaitwa Raman kwa kifupi tunamuita Roma. Roma huyu ndio bosi wetu ambaye yeye ndio anatufanya tuweze kuishi hapa mjini naa kupendeza”

“Nashukuru sana bosi kwa kukufahamu”

Sauti ya Roma ni ya upole sana.

“Nashukuru pia. Unaweza kunipa sifa ya kazi yako?”

“Ndio. Niliishi South Korea kwa miaka zaidi ya kumi na mbili. NIliweza kuiingia katika vikosi vyao ya kijasusi na nimefanya kazi katika vikosi hivyo kwa miaka zaidi ya saba. Nimerudi nchini Tanzania baada ya mikataba yangu kuisha katka vikosi hivyo”

Roma alizungumza huku akinionyesha picha zake za zamania kiwa katika vikosi hiyo kwa kupitia simu yake ya mkononi mwake.

“Wewe ni Mtanzania?”

“Ndio ni Mtanzania, mama yangu ni mkorea, ila baba yangu ni mtanzania”

“Sawa ndio maana unaonekana kuwa mpole mpole”

“Ndio mkuu”

“Nina imani kwamba unajua jinsi ya kulinda siri za mkuu wako na nina amani kwamba unajua jinsi ya kufanya mission zote nzito na kali?”

“Ndio”

“Nashukuru. Tusipoteze muda sana, tuna kazi moja nina imani kwamba mabinti hapa wamekupa maelezo ya juu ya mzee huyo?”

“Ndio nimesha andaa mazingira ninasubiria amri yako”

“Nimekuruhusu, inaweza kufanyika leo hiyo kazi?”

“Kwaleo hapana mkuu ila kabla ya siku ya kesho kuisha nitakuwa nimeikamilisha hiyo kazi”

“Basi fanya hivyo”

“Nashukuru mkuu”

“Basi nikutakie usiku mwema”

“Asante”

Roma akatoka ndani hapa na kuniacha na Qeen na Latifa.

“Ehee kampenzi zao zinakwenda vipi?”

“Huwezi kuamini mkuu, yaani ni mafuriko”

“Mafuriko ndio nini?”

“Yaani watu wanajaa, kampenzi ni za nguvu na sasa zinaingia hadi vijijini huko ndani ndani yaani ni raha sana.”

“Tuna video hapa tunaweza kukuonyesha jinsi pesa yako inavyo leta nguvu kwa wananchi. Pia shemeji yangu yaani ananiambia kwa miaka yake yote aliyo fanya siasa hajawahi kuona jinsi mikutano na chama chao kinavyo pendwa kama msimu huu”

“Kwahiyo inatia matumaini?”

“Asilimia mia moja matumaini yanaonekana katika kampenzi hizi”

“Watawala nao vipi?”

“Yaani wao wana henya henya. Mkuu wao hana sera yaani huyo mke anavyo tukazania tuweze kumuunga mkono baba yek na hapa kesho huwezi amini ametuambia watu wote tuelekee jangwani kwenda kusikiliza kampeni za baba yake hapa Dar es Salaam”

“Yaani wafanyakazi wote, kesho wanao weza kubaki ofisini ni mainjinia tu”

“Munakwenda saa ngapi?”

“Kuanzia saa kumi ndio tunakwenda hivyo kuanzia saa nane mchana hivi magari yote ya kampuni yatatumika katika kuwapeleka wafanyakazi katika kampeni”

Nikatoa simu yangu na kuweka laini ninayo itumia nchini Tanzania kwa siri, nikampigia mkuu wa ulinzi wa katika kampuni yangu hii ya simu na kumpa onyo la kuto kuruhusu gari yoyote ya kampuni kutoka nje ya viwanja vya kampuni yangu ikiwa na wafanyakazi. Onyo langu likaeleweka, majira ya saa kumi na mbili alfariji Qeen na Latifa wakaondoka hotelini hapa na nikawahisi kwamba nitafika ofisini muda wowote. Nikajipumzisha hotelini hapa hadi majira ya saa sita mchana, nikajiandaa na kuanza safari ya kueleka ofisini kwangu tena kwa kutumia usafiri wa bajaji. Majira ya saa nen kasoro hikafika katika geti kuu na kuwakuta walinzi wa kampuni niliyo wapa dhamana ya kulinda ofisi yangu wakiwa wametanda katika geti hilo huku Biyanka akionekana kufoka sana na kuwaamrisha walinzi hao waweze kuondoka la sivyo atawafukuza kazi. Kutokana hakutarajia kuweza kuniona kwa wakati huu, taratibu nikashuka kwenye bajaji hii huku nikiishusha kofia yangu chini kidogo na kufika nusu uso. Watu wa pekee walio weza kunigundua na Qeen na Latifa ambao wapo mbele ya moja ya gari aina ya Costa wakisubiria kuelekea kwenye kampeni za mzee mkumbo.



ENDELEA

Nikasimama karibu na geti hili,mlinzi mmoja akaniambia kwamba siruhusiwi kuingia kwa sasa na ofisi zimefungwa.

“Nisaidie kuniitia mkuu wenu”

Nilizungumza kwa sauti ya upole na ya chini kidogo, kutokana sifahamiki sana na walinzi, ikawa ni ngumu sana kwa mlinzi huyu kuweza kunitambua. Kiongozi akaja usawa wa eneo nilipo.

“Ni mimi fungua”

Mkuu wao akanifahamu, taratibu akawaamuru vijana wake kufungua geti dogo ambalo hutumika kupitia watu. Nikaingia ndani ya eneo hili huku nikivua kofia yangu na kuwafanya wafanyakazi wote katika eneo hili washangae hadi Biyanka mwenyewe akabaki akiwa na bumbuwazi.

“Watu wote murudi kwenye majukumu yenu ya kazi. Madereva rudisheni magari kwenye maeneo yake”

Baada ya kuzungumza hivyo wafanyakazi wakaanza kutawanyika.

“Ethan”

Biyanka aliniita huku akiwa katika hali ya upole na unyonge kwani lile ambalo amekusudia kulifanya limeshindikana na mbaya sikuweza kumueleza juu ya kuja kwangu nchini Tanzania.

“Twende ofisini”

Nilizungumza kwa msisitozo na kuelekea ndani, kila sehemu ninayo pita wafanyakazi wangu wananisalimia kwa furaha kubwa sana. Tukaingia kwenye lifti na taratibu ikatupeleka hadi gorofa ya juu kabisa, moja kwa moja nikaelekea ofisini kwnagu huku Biyanka akanifwata kwa nyuma.

“Oohoo jamani mume wangu ni suprize gani hii jamani!”

Biyanka alizungumza huku akijitahidi kujenga furaha usoni mwake. Kwajicho nililo mtazama ni ishara kwamba nimekasirika. Akataka kunikumbatia ila nikamzuia.

“Hivi ndivyo unavyo ongoza kampuni yangu?”

Nilizungumza kwa ukali na kumfanya Biyanka kukaa kimya kwa muda huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndiyo unavyo ongoza kampuni yangu?”

“Ha…aaha.ahapana Ethan?”

“Ila, uhisi kila mmoja humu ndani ni mwanachama wa chama cha baba yako ehee?”

“Ethan umenifikiria vibaya?”

“Ujinga na upumbavu wako wote unao ufanya nimeuelewa na ninaufahamu. Usihisi kwamba nimekwenda kumzika mama yangu ndio sinto rudi nimerudi. Kama unahitaji kwenda kwenye mikutano ya kisiasa ya baba yako toka sasa hivi”

Nilifoka huku jasho likinimwagika usoni mwangu kwa hasira na kitu cha pekee ninacho jizuia kinywani mwangu ni kuropoka kwamba mimi ni mpizani wa baba yake na nipo kwa ajili ya kuiharibu familia ya baba yake.

Biyanka akakaa kimya huku akinitazama kwa wasiwasi mwingi sana.

“Hii ni kampuni yangu na hawa watu humu ni watu wangu. Mimi ndio mwenye maamuzi ya mwisho kwenye kila jamgo hivyo jitazame mara mbili Biyanka sitaki kampuni yangu ijihusishe na chama cha aina yoyote hapa Tanznaia. Itabaki kama kampuni ya kujitegemea kwa maana inatoa huduma kwa watu wa pende zote wawe chama tawala au wapinzani ila kinatoa huduma. Umenielewa?”

“Nimekuelewa”

“Nenda kwenye mkutano wa baba yako”

“Ethan mbona umekuwa ni mtu wa hasira sana?”

“Unanifanya niwe na hasira. Mama yangu amefariki, ni nani kati yenu ambaye ametoa japo hata pole ikiwa ni taarifa ambayo imesambaa kwenye mitando yote ya kijamii. Ehee au nyinyi hamkujua hilo?”

Biyanka akatazama chini akiashiria kwamba kile ninacho kizungumza ni kitu cha ukweli kabisa.

“Nimewajua nyinyi ni watu wa aina gani. Umenichukua niingie kwenye familia yako ili uweze kunitumia si ndio?”

“No no no no Ethan usingumze hivyo.”

“Ila unataka niendelee kuwakumbatia, kuwajali ikiwa nyinyi hata pole hamjafanya. Una account ya Twitter, Instergram na Facebook. Ila hakuna hata sehemu uliyo andika pole. Huku ukidai kwamba wewe ni mke wangu, mwanamke wa maisha yangu. KIVIPI……..EHEEEE?”

“Ethan akili zetu tumechanganyikiwa, kampeni zinatuendea mrama. Watu wamekuwa ni wasaliti, hawaonekani kabisa kwenye mikutano ya baba yangu. Nakuomba sana mpenzi wangu unisamehe. Tambua mkeo na familia yangu kwa ujumla tupo kwenye mapambano makubwa sana. Ninakuomba sana Ethan unielewe”

“Okay nenda kwenye kampeni. Tutazungumza baadae”

“Ethan!!!”

“Elewa kitu ninacho kizungumza Biyanka alaa!! Nahitaji kuwa peke yangu sasa”

Biyanka akanitazama kwa macho ya upole kisha akageuka na kutoka ndani humu, akaubamiza mlango wa ofisi yangu kwa nguvu na kunifanya niachie msunyo mkali sana. Nikanyanyua simu yangu ya mezani na kumpigia sekretari wangu, baada ya muda kidogo akaingia.

“Ndio mkuu”

“Itisha kikao cha wafanyakazi wote kwenye ukumbi wa mikutano gorofa ya tano”

“Sawa mkuu”

Sekretari akaondoka na kuniacha peke yangu. Mawazo mengi sana juu ya kuhakikisha kwamba ninawapokonya kila kitu wanacho kihitaji hii familia ya bwana Mkumbo, bado yanaendelea kunijaa kichwani mwangu, huku kila ninacho kipanga ninakiona hakiki sawa. Nikapata wazo moja kubwa sana ambalo kwa namna moja limtamchafua bwana mkumbo yeye na chama chake.

“Mkuu kikao tayari”

Sauti ya sekretari wangu ikanitoa kwenye dibwi hili la mawazo. Nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kalia na kuongozana naye. Tukaingia kwenye ukumbi huu mkubwa ulio jaa wafanyakazi wote wa kampuni yagu. Nikasimama kwenye jukwaa na kuwatazama wafanyakazi wote kwa muda wa kama dakika tano, kisha taratibu nikashusha pumzi.

“Habari yenu”

“Salama mkurugenzi”

Nikasogeza karibu kipaza sauti na kuendelea kuzungumza.

“Kwajambo lililo jitokeza leo. Sinto hitaji lijitokeze tena kwenye kampuni hii pasipo idhini yangu mimi. Kapuni yangu si kampuni ya siasa, wala si kampuni ya kumpigia kura mtu gani. Hata ikitokea mimi nina gombea uraisi, sito mlazimisha hata mmoja wenu aje kwenye kampeni zangu eti kisa mimi ni mkurugenzi wako. Hapana hicho kitu hakita jitokeza”

Nikanyamaza kidogo huku nikisikilizia makofi yanayo pigwa na wafanyakazi wangu ambao wnaaonekana kururahishwa na hichi nilicho kizungumza.

“Nimepitia account zenu kipindi nipo nyumbani nchini Ujerumani. Asanteni kwa kunipa pole kwa kile ambacho kimetokea kwenye familia yangu. Nina imani kwamba wengi wenu mulishangaa kwa kuondoka kwangu gafla pasipo taarifa yoyote kwenu. Nimerudi na nitaongoza kampuni yangu katika mstari ambao siku zote huwa ninauamini. Upendo, uchapakazi na hekima. Ndio vitu vinavyo niongoza toka nilipo kuwa mtoto mdogo”

“Kama kuna malalamiko yoyote ambayo yametokea kwa kipindi hichi cha wiki tatu ambazo sikuwepo hapa nchini. Ninawaomba muweze kuniandikia malalamiko hayo kwa siri sana, kisha mutamkabidhi sekretari wangu na atayawasilisha ofisini kwangu. Naweka siri kwa manaa wengi wenu natambua kwamba muna muogopa meneja Biyanka. Hivyo fanyeni katika utaratibu nilio waagiza sawa”

“Sawa”

Mfanyakazi mmoja akanyoosha mkono juu, nikamruhusu aweze kuzungumza.

“Kwanza kwa niaba ya wafanyakazi wote. Tunapenda kukupa pole kwa mara nyingine mkurugenzi, tulitamani kutuma japo wawakilishi wawili kwenye msiba ila kwa jibu alilo tupa meneja nina imani kwamba kila mmoja wetu hapa ana lifahamu”

“Jibu gani lizungumze usilifumbe fumbe?”

“Ahaa si jibu la kiungwana mkurugenzi ni jibu ambalo linaweza kupelekea mtafaruku kidogo kwenye mahusiano yenu”

“Wewe kuwa na amani, zungumza ni jibu gani?”

“Ngoja nimsaidie muheshimiwa”

“Sawa mama zungumza”

“Meneja alisema kwamba yeye ndio mwana familia wako hivyo msiba hautuhusu wawakilishi watulize mishono yao na waendelee na majukumu ya kazi kama kawaida”

“Mishono ndio nini?”

“Kwa lugha nyepesi mkuu niseme ni kihere here”

“Nashukuru sana mama yangu. Endelea kaka”

“Ndio hivyo muheshimiwa, tulishindwa na tukaona tuji organize kimya kimya. Tukachanga kijimchango kidogo naona mtuza pesa wetu tuliye mchagua hapo anaweza kuzungumza”

“Nani mtunza pesa?”

Akasimama msichana mmoja mpole kwa kumtazama.

“Ndio zungumza”

“Tumeweza kukusanya kiasi cha shilingi milioni kumi na tano mkuu na pesa yote hiyo ipo benki”

“Nawashukuru sana. Zawadi muliyo nipatia hakika ni kubwa sana kwangu ninawashukuru sana”

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu kwani sikutarajia kama wafanyakazi wangu wana umoja kiasi hichi na hii ni ishara moja nzuri inayo onyesha kwamba hata siku nikipata tatizo basi wanaweza kuungana kwa pamoja na kunisaidia.

“Mama yangu alifariki kwa saratani pia kwa baba ndio hivyo hivyo. Pesa iliyo patikana nitaongezea na kiasi kingine na kwa pamamoja tunatembelea hospitali inayo shuhulika na magonjwa hayo na kutoa kiasi hicho ili wagonjwa waendelee kufanyiwa matibabu na kama Mungu anaweza kuwajalia basi waweze kupona”

Nilizungumza kwa upole na wazo langu likaonekana kupokelewa na wafanyakazi wangu wote.

“Nawashukuru kwa muda wenu na moyo wenu wa kujitoa na Mungu awabariki”

“Nawe pia mkurugenzi”

Nikatoka ukumbini humu na kuacha minong’ono mingi kwa wafanyakazi. Nikarudi ofisini kwangu, nikapokea ujumbe wa simu kutoka kwa Qeen akinitaarifu kwamba Roman amesha kamilisha kazi niliyo mkabidi.

‘YUPO WAPI’

Nilimjibu kwa ujumbe mfupi wa meseji.

‘KAMA HUTO JALI TUKUPELEKE’

‘SAWA BAADAE TUTAKWENDA’

‘SAWA MKUU’

Nikafuta meseji zote. Baada ya muda sekretari akaingia akiwa ameshika karatasi nyingi.

“Yote hayo ni maoni?”

“Ndio mkuu”

“Mmmmmm kazi kweli kweli. Inaonekana kuna madudu yalitokea mengi sana kipindi mimi sipo?”

“Yapo mengi ila ndio hivyo mkuu wetu alikuwa anafanya vile anavyo jisikia yeye.”

“Hembu niambie kwa ufupi, alikuwa anafanya nini?”

“Ukiachilia na swala hili la leo la kulazimiswa kuelekea kwenye mikutano wa baba yake. Mwezi ulio isha juzi, kila mtu amekatwa elfu hamsini hamsini kwenye mshahara wake, kilazima ili kuweza kuchangia kampeni za baba yake”

“Fuc** Huyu mwanamke anahitaji nini kwangu.?”

Nilizungumza kwa jazba kidogo kwa maana upuuzi alio ufanya Biyanka ni wa kushangaza kwa kwlei.

“Jambo jengine, kuna wafanyakazi kumi wamefutwa kazi”

“Wamefutwa kazi kwa kosa gani?”

“Walikuta wakijadili maswala ya chama pinzani kwenye group la whatsapp ambalo tumejiunga wafanyakazi wote. Ila Meneja mkuu hayupo kwenye hilo group ila kuna vibaraka wake wamempelekea ushahidi wa wafanyakazi hao jinsi walivyo kuwa wakimuunga mkono mpinzani wa baba yake. Na ndio hivyo wamefukuzwa kazi”

“Hao walio fukuzwa kazi ni nani na nani?”

“Kwamajina kwa haraka haraka siwafahamu. Ila wapo kwenye takwimu zangu ofisini”

“Sasa wapigie simu wote. Waambie mkurugenzi kesho asubuhi, saa mbili ana wahitaji warudi kazini nakabla ya hawajaanza kazi wakutane na mimi tuzungumze kwanza. Sawa?”

“Sawa mkuu”

“Unaweza kuendelea na majukumu yako”

Sekretari wangu alipo toka, nikaanza kupitia maoni ya wafanyakazi wangu na wengi wanalalamika kwa swala la wao kukatwa mishahara. Nikampigia muhasimu wa kampuni na kumuita ofisini kwangu.

“Karibu ukae Mr Merema”

“Nashukuru mkuu”

“Mauzo kwa wiki tatu yamepanda au yameshuka?”

“Yameongezeka kwa asilimia mbili mkuu. Tofauti na uwepo wako kazini”

“Sawa, kuna swala nimelisikia la watu kukatwa elfu hamsini hamsini kwenye mishahara yao hilo limekaaje?”

“Ni kweli, mimi nililetewa oda na meneja mkuu nami sikuwa na pingamizi na nikafanya kama alivyo niamrisha japo nilijaribu kumshauri ajaribu kuzungumza na wafanyakazi ila ila akakataa na kunipa vitisho vya kunifukuza kazi muhesimiwa”

“Sasa kila mfanyakazi arudisiwe pesa yake leo hii na ujinga huo sihitaji ujitokeze tena kwenye kampuni hii. Nimekupa dhamana ya pesa zangu simamia. Mtu anaye weza kukufukuza kazi ni mimi. Umenielewa?”

“Nimekuelewa mkuu”

“Nashukuru”

Muhasibu akanyanyuka na kuondoka eneo hilo la hapa ofisini. Muda wa kutoka ofisini ulipo wadia, nikaondoka ofisini hapa huku nikikodi bajaji kurudi hotelini nilipo fikia. Majira ya saa nne usiku Roman akaja kunichukua hotelini hapa na moja kwa moja akanipeleka hadi katika godauni moja lililopo katika mji wa Bagamoyo. Tukaingia kwenye godauni hili lenye ukimya huku kofia yangu nyeusi nikiwa naimeivaa vizuri kichwani mwangu na kuficha kabisa sura yangu. Kwa mavazi haya meusi niliyo yavaa si rahisi kwa mtu kuweza kunitambua kwamba ni mimi. Tukaingia katika chumba ambacho amemning’iniza mzee huyu kichwa chini miguu juu huku akiwa amemvua nguo zote na kumbakisha na boksa tu na usoni mwake amemfunga kitambaa cheusi ambacho si rahisi kwa mzee huyu kuweza kuniona. Nikamtazama mzee huyu na wazo la kuweza kumchafua mzee Poul Mkumbo taratibu likaanza kunijaa kichwani mwangu na nikaona muda huu ndio mzuri wa kuweza kutekeleza kile nilicho kikusudia kukifanya.



ENDELEA

“Simu yako ina rekodi vizuri?”

Nilizungumza kwa kumnong’oneza Roman.

“Ndio mkuu”

“Nipatie”

Roman akatoa simu yake, nikamuomaba aniwekee upende wa kamera na akafanya hivyo.

“Ulinimpiga?”

“Kiasi kidogo ila kwa sasa amepoteza fahamu ila kama unahitaji nimuamshe basi ninaweza kufanya hivyo.”

“Fanya hivyo”

Roman akachukau wanya mrefu wa umeme ambao umekatwa kwa mbele. Akachukua ndoo ya maji ya baridi.

“Kabla ya kumuasha, hakikisha kwamba anajibu maswali haya”

Nikayaandika maswali hayo kwenye simu yangu na kumkabidi Roman. Taratibu akaanza kusoma swali moja baada ya jengine. Akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ameelewa. Alipo hakikisha kwamba kila kitu alicho kihitaji kipo vizuri akafunika uso wake na ni ngumu sana kwa mtu kuweza kumtambua. Akamwagia maji mzee huyu na kumfanya aanze kujitishisha tingine. Akamfungua kitambaa chake usoni.

“Ohoo nipo wapi, eheee?”

Mzee huyu alizungumza kwa kukoroma. Roman akachukua waya huu wa umeme, akamgusisha mzee huyu eneo la kifuani na kumfanya atetemeshwe sana huku akipiga kelele za maumivu.

“Kwa nini unahitaji boksi jeusi?”

“Pumbavu wewe uanahisi nitazungumza”

Roman akamgandamiza kwa nguvu mzee huyu waya huo wa umeme na kumfanya azidi kupiga kelele kwa maumivu makali sana.

“Nani kakutuma?”

Roman alizungumza kwa sauti nzito na iliyo jaa mikwaruzo mingi, tofauti kabisa na sauti anayo itumia katika kuzungumza. Kazi yangu kubwa ni kuendelea kurekodi kila tukio. Roman alio ona mzee huyu ni mbisha sana akamvua boksa yake na kichana na akabaki kama alivyo zaliwa. Roman akabadika waya huu wa umeme kwenye uume wa huyu mzee na kumfanya alie kama mtoto mdogo kwani shoti anayo ipata hapo sio ndogo kwa kweli.

“Nas…em…a”

Mzee huyu uzalendo ulimshinda kwani huku ni kwenda kupoteza uwanaume wake.

“Ni nai?”

“Ni….ni.ni…mimi mwenyewe. Nilihitaji kulipata hilo boksi kwa manufaa yangu mimi.”

Roman akanitazama, nikampa ishara yakuendelea kumuuliza maswali.

“Kwahiyo wewe ni msaliti?”

“Hahaaaa….haa…haa…hahaa….pana”

Nikampa ishara Roman ya kupiga shoti nyingine mzee huyu. Akatii amri yangu na kuendelea kumpiga shoti mzee huyu aliye endelea kulia kwa uchungu sana ila hakuna mtu wa kuweza kumsaidia.

“Ni mipango gani ya chama chako”

“Najua wewe ni mtu wa Mkumbo, ila sinto kwenda kukueleza kitu cha aina yoyote kwangu juu ya chama changu ninacho kipigania usiku na mchana”

Hapa ndipo nilipo kuwa nina pahitaji. Roman akaendelea kumpa mateso makali mzee huyu, ila kila mateso yanavyo zidi kuendelea ndivyo jinsi anavyo mtaja bwana Mkumbo kwamba hata akimuua basi hato weza kushinda kiti cha uraisi. Hali iliyo kuwa mbaya zaidi kwa mzee huyu, nikamuamuru Roman ampige risasi mzee huyu na kummalizia kabisa.

Romani akampiga risasi za kichwa, kisha akamfungua katika eneo alilo mfunga. Akachukua dungu la mafuta ya petroli na kuumwagika mwili huu kisha akaanza kumwaga mafuta yaka katika chumba hichi kisha tukatoka nje. Akatupia njiti ya kiberiti ndani ya chumba hicho na kukifanya kianze kuwaka moto huku mwili wa mzee huyo ukiwemo ndani. Tukatoka ndani ya godauni hili tukaingia ndani ya gari la kuianza safari ya kuondoka eneo hili kwa kasi pasipo mtu yoyote kutuona.

“Bosi video umeipata vizuri?”

“Yaaa”

Nilizungumza huku nikiifungua video hiyo, nikaanza kuitazama na kila jambo limekwenda kama vile nilivyo kuwa nimepanga.

“Kuna ushahidi mzuri mwengine ambao unaweza kumuweka Mkumbo katika hali mbaya”

“Ushahidi gani?”

Roman akatoa simu nyingine na kuniwekea mazungumzo ambayo kwa kuyasikiliza vizuri ni mazungumzo ya mzee huyu tuliye muua na mzee Poul Mkumbo.

“Wewe mwana haramu unasambaza chuki juu ya wafuasi wangu si ndio”

Nilisiikia sauti ya baba yangu mkwe, mzee Poul Mkumbo akifoka sana.

“Huna jipya mzee wewe. Wewe na chama chako jiandaeni kuangukia pua uchaguzi huu”

“Hahaaa….hata kwa kuiba kura ni lazima nishinde uchaguzi huo”

“Tanzania ya miaka ileee sio Tanzania ya sasa. Sasa wewe jidanganye tu na utaona cha mtema kuni mukifanya ujinga wenu”

“Eti eheee?”

“Ndio maana yake. Dalili ya mvua ni mawingu Mkumbo”

“Pumbavu wewe nitaakikisha nina muua mmoja baada ya mwengine shenzi nyinyi. Tena wewe uanjidai afisa mwenezi wa chama chako. Nitakwenda kukuchoma moto huo mwili wako”

“Hahaaa jaribu uone. Nimejipanga mzee, na tena usinitishe kwa maana wewe bado kwangu ni mtoto mdogo sana.”

“Leo huimalizi”

“Hahaaa, utaona”

Mazungumzo hayo yakaishia hapa na kujikuta nikumtazama Roman usoni mwake ambaye analiendesha gari hili kwa mwendo wa kasi sana.

“Umeyapatia wapi?”

“Niliweza ku hack system za simu zote za mzee Poul Mkumbo ili niweze kujua mpango wake. Bahati nzuri alicho kizungumza ndicho nilicho kifanya. Nilianda kila kitu alicho kizungumza na nilimteka mzee huyu kabla ya watu wake kuweza kufanikisha mpango wao kwa maana leo alikuwa anatekwa kweli na kwenda kuuwawa”

“Kazi nzuri sana Roman. Sasa hii video inabidi tuiachie kwenye mitandao ya kijamii?”

“Kwa sasa bado mapema mkuu na ni watu wengi sana wanaweza kuitafuta hiyo accont na kidogo italeta msako makali sana na kumbuka kwamba mataifa makubwa duniani yana tazama huu uchaguzi hivyo wanaweza kuleta wapelelezi wao na itapelekea kukamatawa kwetu”

“Unashaurije sasa kwa maana mimi kwenye mambo hayo ya kiusalama. Sina ninalo lijua sana”

“Nitakuonyesha nini cha kufanya mkuu”

“Sawa”

Tukafika hotelini na Roman akaniacha kisha yeye akendelea na safari yake huku akiwa na simu yake niliyo rekodia tukio hilo. Nikaingia chumbani kwangu huku nikiwa na mawazo mengi sana kichwani mwangu kwani hili tukio la leo ni la kikatili sana kwa mimi kuweza kulishuhudia kwenye maisha yangu. Sikupata usingizi hadi kuna pambazuka. Nikajiandaa na kuelekea kazini kwangu guku nikikodi bajaji, nikashuka kwenye bajaji na kumlipa dereva huyu na kila mfanyakazi aliye niona nimo kwenye bajaji hii hakusita kunishangaa na wengine walitamani hata kuniuliza.

“Mbona unshangaa sana”

“Mgurugenzi imekuwaje umepanda bajaji?”

Kijana mmoja mchangamfu aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Foleni kubwa barabarani, ndio maana nimepanda bajaji”

“Ahaa sawa mkurugenzi, sisi tukahisi labda kuna tatizo”

“Hakuna, kazi njea”

“Nawe pia mkurugenzi”

Nikaelekea ofisini kwangu. Baada ya kama dakika kumi hivi Biyanka akaingia ofisini kwangu huku akiwa amevaa na kupenda sana. Japo mimi na Biyanka tuna matatizo binafsi ila kusema kweli ni mwanamke mmoja mzuri sana na aliye jaliwa uzuri wa aina yake. Kwa takribani dakika tano nikabaki nikiwa nimeduwaa nikimtazama.

“Ethan, Ethan”

“Na..anaaammm”

“Mbona nina kuita dakika zote hizo. Hunisikii mpenzi wangu”

“No umependeza”

Nilijikuta nikiropoka maneno hayo na kumfanya Biyanka atabasamu kidogo huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu akanisogelea na kuniinamia hapa kwenye kiti changu nilicho kikalia, kwa macho yaliyo mlegea, akazikutanisha lipsi zake na zangu na taratibu akaanza kuninyonya midomo yangu na kuufanya mwili wangu kusisimka sana.

Nikapitisha mkono wangu wa kulia kiunoni mwake, kiganja changu taratibu kikaanza kukitomasa tomasa kiuno chake na nilipo ona haitoshi zaidi, nikashusha mkono wangu wangu hadi kwenye makalio yake malaini na kuanza kuyatomasa. Uzalendo ukaendelea kunishinda na kujikuta nikianza kufungua zipu ya sketi hii fupi aliyo ivua.

“Mmmmmm Ethan tupo ofisini mume wangu”

“Nina hamu na wewe mke wangu”

“Najua hilo mume wangu ila muda huu ni wa kazi”

“Sitaki”

Nilizungumza huku nikisimama, nikamkalisa Biyanka mezani na kuangusha baadhi ya mafaili. Nikaivua skin tait yake pamoja na chupi. Biyanka hakuwa na kipingamizi zaidi ya kukubaliana na kile ambacho kinakwenda kutokea. Taratibu nikafungua zipu yangu na kumuingiza jogoo wangu ndani ya kitumbua chake ambacho tayari kilisa lainika kwa kusubiria utamu wa jogoo wangu. Tukaanza kupeana raha hii huku ubosi tukiuweka pembeni. Utamu ulipo zidi kuongezeka, nikamshusha Biyanka kwenye meza na kumuinamisha huku kifua chake akikilaza kwenye meza hii.

“Oho….Ethan u…t…a…ani…ua”

“Eh….eeh!!!”

“Utaniua uuuuwwiiii mamaaa weee”

Niliendelea kuhakikisha kwamba nina mshuhulikia Biyanka mikiki ya kutosha na kila ninapo kumbuka tukio la mauaji ya jana usiku ndivyo jinsi ninavyo jikuta nikikikitafuna kitumbua cha Biyanka kwa hasira sana. Hadi tunamaliza mtanange huu kila mmoja ana mwagikwa na jasho na mbaya zaidi hatujavua nguo zote.

“Ohooo asante mume wangu”

Biyanka alizu gumza huku akinigeukia na kakanikumbatia kwa nguvu.

“Asante nawe pi”

Nilizungumza huku nikihema. Taratibu tukaachinaa na Biyanka huku kila mtu akivaa nguo zake.

“Vipi mkutao wa jana?”

Nilimuuliza Biyanka huku nikiufunga mkanda wa suruali yangu vizuri.

“Umekwenda poa sana. Watu walijitokeza wengi sana”

“Ohoo safi”

Nimemueleza baba na mama kwamba umerudi. Wamefurahi kusikia kwamba umerudi na wameniomba nikuambia kwenye mkutano mwengine wa kesho wanaomba tuongozane wote Dodoma.

“Dodoma!!?”

“Ndio mume wangu. Kidogo nawe ukatembee tembee nchini ukaione nchi”

“Mmmm sawa na wewe si unakwenda?”

“Ndio nitakwenda”

“Poa utaniandalia mazingira”

“Usijali mume wangu ninakupenda sana na kama huto jali twende ukulele kwangu leo kwa maana tutaondoka asubuhi sana”

“Sawa”

Biyanka akanibusu kwa furaha, kisha akajiweka sawa shati lake alilo livaa na kutoka ndani humu na kuniacha peke yangu. Nikaokota mafaili yaliyo anguka na nikaendelea na majukumu yanug ya kiofisi. Nikawajulisha Qeen, Latifa na Roman juu ya safari yangu ya kesho wote wakakubaliana na jambo hilo.

“Mkuu utahitaji ulinzi wangu?”

“Ndio ila uwe wa pembeni sana. Isitokee mtu akafahamu juu ya uwepo wako”

“Sawa mkuu”

Muda wa mchana tukaondoka ofisini hapa na Biyana na kuelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kijiandaa na safari ya kesho. Biyanka akaniomba msamaha kwa yale yote yaliyo jitokeza.

“Nimekusamehe mke wangu”

“Nashukuru sana mume wangu. Nakuapia na kukuhakikishia kwamba sinto rudia tena kuenenda kinyume na wewe mume wangu”

“Nimekuelewa”

Siku iliyo fwata alfajiri na mapema tukaanza safari ya kuelekea katika mkoa wa Dodoma huku gari letu nalo likiwa miongoni mwa magari ya msafara wa mgombea uraisi wa chama tawala. Sikuona ajabu ya mimi kuvaa tisheti ya sare ya chama hichi cha baba mkwe pasipo wao kujua kwamba mimi ndio adui yao namba moja ninaye wapiga kimya kimya. Tukafika kwenye moja ya mji na wananchi wakasimamisha msafara huu.

“Hapa ni wapi baby?”

“Chalinze”

Mzee Poul Mkumbo akahutubia watu wa haba walio kusanyika kumsikiliza na baada ya hapo tukaendelea na msafara huu. Kuna baadhi ya miji miwili wananchi nao walijitokeza kumzuia mzee Poul Mkumbo na walipo ridhika kwa sera za mgombea huyu tukaendelea na safari. Majira ya saa sita mchana tukafika katika mji wa Dodoma na kupokelewa kwa shangwe kubwa sana huku mabango mengi barabarani yakiwa yamebandikwa sura ya mzee Poul Mkumbo.

“Baba mkwe ana wafuasi ehee?

Nilimuambia Biyanka huku nikiwatazama wamama walio valia sare za chama hichi jinsi walivyo kusanyika barabarani.

“Ndio mume wangu”

Tukafika katika moja ya hoteli tukapata chakula cha mchana na baada ya hapo tukaelekea katika uwanja mkubwa wa mpira ambapo nikakuta watu wengi sana wakiwa wamekusanyika hadi wakaanza kunitisha kwani sidhani kama wapinzani wana watu wengi kiasi hichi. Burudani mbalimbali zikaanza kutolewa kisha wakaongea viongozi baadhi wa chama hichi huku wakimnadi mgombea huyu. Ukafika muda na wakati wa bwana mkumbo kuzungumza. Taratibu Biyanka akanishika mkono wangu wa kulia huku tukiwa tumekaa kwenye viti vya hili jukwaa kuaa.

“Dodomaaa Hoyeeeeeeeeeeeeee”

Watu wote wakaitikia kwa shangwe sana. Gafla spika za eneo hili zikaanza kusikika mazungumzo ya bwana mkumbo na mzee tuliye muua jana usiku jambo lililo tufanya sisi sote kushangaa kwani sikutarajia kama Roman anaweza kumwaga mchele kwenye kuku wengi namna hii.



Watu wote uwanja mzima ukatulia huku wakisikiliza mazungumzo haya yaliyo jaa vitisho. Walinzi wakamzunguka mzee mkumbo ili kama kuna tatizo lolote linalo weza kujitokeza basi iwe rahisi kwa wao kumuondoa uwanjani humu.

“Ethan mume wangu nini nini hicho?”

Biyanka aliniuliza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Wapambe wa mzee Mkumbo nao nyuso zao zimejawa na wasiwasi mwingi sana. Mazungumzo hayo nayo yakazidi kujirudia rudia na kuwafanya wananchi waanze kuzua minong’ono na fujo ambazo zikawafanya warushe chochote walicho. Walinzi wakaanza kututoa mkuku mkuku huku wakisaidiana na jeshi la polisi. Tukaingizwa kwenye gari zetu na zikaanza kuondoka uwanjani humu huku vurugu zikiwa zimetawala. Nikamtazama Biyanka usoni mwake na kumuona akiwa analia kwa hasira kwani ii iliyo tokea ni aibu ya chama na familia kwaujumla.

‘Safi sana Roman’

Nilizungumza kwa furaha kubwa sana moyoni mwangu huku usoni mwangu nikiwa nimetengeneza sura ya mawazo iliyo andana na mawazo mengi sana.

“Lazima huyu mshenzi aliye fanya huu ujinga afeee”

Biyanka alizungumza kwa hasira huku mwili wake wote ukitetemeka. Kwajinsi gari hizi zinavyo endesha kwa kasi hakika endapo gari moja likipata ajali basi mzinga wake utakuwa ni wa historia. Nikashusha pumzi taratibu huku nikimshika Biyanka kiganja chake cha mkono wa kulia.

“Nina amini vyombo vya ulinzi vinaweza kufanya kazi yao mke wangu”

“Hapana ni lazima tumshuhulikie mume wangu. Hawawezi kumchezea baba yangu na kumdhalilisha vile”

“Oooooohoo lala haba mke wangu. Punguza jazba”

Nilizungumza kwa upole huku nikimlaza Biyanka kichwa chake katika bega langu la upande wa kulia. Tukafika katika mji wa Morogoro majira ya saa mbili usiku. Msafara ukasimama kwa sekunde kadhaa kwenye moja ya hoteli na sikuweza kujua ni kitu gani kinacho endelea kwa maana tulikatazwa kabisa kushuka kwenye gari. Baada ya kama dakika kumi msafara ukaendelea kurudi jijini Dar es Salaam na kwa jinsi ulinzi ulivyo imarishwa gari zote zilipisha msafara huu ambao mbele zimetangulia gari za polisi zinazo piga ving’ora kuashiria kupishwa kwa msafara huu.

“Mom”

Biyanka alizungumza huku simu yake ikiwa sikioni mwake. Nikamzama kwa macho ya kuiba na kuendelea kuishuhudia huzuni yake jinsi inavyo mtawala.

“Mom ni aib…..u”

Biyanka akashindwa kujizuia na kuangua kilio kizito sana hadi mlinzi aliye kaa siti ya mbele akageuka nyuma kutuangalia. Nikaichukua simu yake na kuiweka sikioni mwangu.

“Mama”

“Ndio mwanangu, naomba mujikaze hiyo ni siasa”

“Naelewa hivyo mama. Nina imani kwamba kila jambo litakuwa sawa hivi karibuni”

“Ndio mwanangu. Tunaendelea kulishuhulikia”

“Sawa mama”

“Tunawasubiri nyumbani”

Simu ikakatwa. Majira ya saa tano usiku tukafika makao makuu ya chama hichi hapa mkoani.

“Nahitaji kwenda kuzungumza na baba”

Biyanka alizungumza huku huku akishuka kwenye gari. Ikanilazimu na mimi kushuka kwenye gari hili. Tukaanza kutembea kuelekea gorofani, tukaingia kwenye ofisi moja ya kuwakuta wazee wenye heshima zao wakiwa ndani ya hii ofisi huku baba mkwe akizunguka zunguka kila sehemu ya chumba hichi.

“Baba”

Mzee Mkumbo akakumbatiana kwa nguvu na binti yake.

“Nahitaji kabla hapajapambazuka nimfahamu huyu mshenzi aliye weka ile sauti kwenye vipataza sauti”

“Sawa mkuu na hiyo kazi inafanyika vizuri hivi sasa”

Mlango ukafunguliwa na akaingia kijana aliye valia suti nyeusi na katika kumuangalia dhairi ni mwana usalama.

“Mkuu kuna habari mbaya”

Watu wote tukastuka na kumtazama yeye.

“Habari gani?”

Kijana huyu akachukua rimoti ya tv kubwa iliyomo humu ndani na kuiwasha. Tukashuhudia habari ya dharura ikionyesha jinsi ofisi za chama hizo kwa mkoa wa Dodoma jinsi zinavyo teketezwa kwa moto na wanachama wa chama hicho.

“Hawa ni mamluki. Sikia waambieni askari watumie silaha za moto sawa”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa jazba kubwa sana.

“Hapana”

Mzee mmoja alizungumza kwa kujiamini sana na kutufanya sote tumtazame.

“Polisi wazuie gasi tu na wasitumie risasi za moto kabisa katika hilo jambo”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Kijana huyu akatoka na kutuacha humu ndani.

“Mkumbo kaa pale”

Raisi alizungumza huku akimuonyesha bwana Poul Mkumbo sehemu ya kuka. Bwana Mkumbo akaitazama sehemu hiyo kwa sekunde kadhaa kisha akakaa kwenye kiti hicho.

“Kila mmoja anatakiwa kukaa ila kijaan tunakuomba utupishe”

Raisi alizungumza huku akininyooshea mkono mimi.

“Huyo ni mkwe wangu, hawezi kwenda mahala popote”

“Kumbuka mimi ndio mwenyekiti wa chama na pia ni raisi wa hii nchi. Kijana toka sio ombi ni amri”

Sikutaka kuzua mfarakano. Nikamtazama Biyanka usoni mwake kisha nikatoka katika chumba hichi huku nikiwa na wasiwasi mwingi sana na maswali ambayo kusema kweli nitapata majibu mara tu ya kumuona Raman. Nikarudi kwenye gar letu na kumtumia meseji Raoman ya kumuomba tuonane sehemu yoyote. Raman akanijibu amenielewa. Ulinzi katika makao makuu ya chama hichi yameimarishwa kisawa sawa. Idadi ya askari polisi na wanajeshi nayo imeongezeka jambo ambalo kwa raisi wa kawaida ni lazima atajawa na wasiwasi.

Kikao hicho kikagarimu kama masaa mawili ndipo Biyanka akatoka na kuingia kwenye gari hili.

“Vipi baba haondoki?”

“Anabaki hapa, kuna swala anahitaji kulishuhulikia”

“Sawa, ni nini kilicho zungumzwa”

“Tutazungumza nyumbani”

Kwa majibu ya Biyanka nikaanza kuhisi kuna jambo linaweza kuendelea. Tukaondoka eneo la ofisi hizi nakuelekea nyumbani kwa baba yake. Tukapokelewa na mama na eneo la nyumba hii napo ulinzi upo imara. Tukaingia ndani huku mama huyu akijikaza ili kutuweka sisi katika hali ya amani.

“Chakula vipi niwatengee”

“Hapana mama, tutakula kesho”

Biyanka alizungumza huku akinipa ishara ya tuondoke sebleni hapa na tuelekea kwenye moja ya chumba.

“Ethan”

Mama mkwe aliniita na kujikuta nikisimama na kumuacha Biyanka atangulie ndani.

“Ndio mama”

“Nashukuru sana kwa kumjali mwanangu na ninaomba utusamehe kwa kila jambo lililo tokea. Kuanzia msiba wa maama yako hadi haya yaliyo tokea leo”

“Usijali mama yangu naelewa hilo”

“Sawa, niwatakie usiku mwema na ninaomba ujaribu kuzishusha hasira za huyo bibie kwa maana nina muelewa vizuri snaa”

“Nitajitahidi kadri ya uwezo wangu”

“Sawa asante mwangu”

Nikaachana na mama huyu na kuingia kwenye chumba alicho ingia Biyanka. Nikamkuta akiwa amekaa kwenye kiti maalumu cha dreasing table yake huku akijitazama kwenye koo hicho cha meza yake hiyo ya kuirembea. Nikavua shati hili na kulitupia kwenye moja ya sofa, taratibu nikamfuata Biyanka sehemu alipo, nikamkumbatia kwa nyuma huku nikikishika kiuno chake taraibu. Biyanka hakuonyesha kujawa na msisimuko wa aina yoyote.

“Unahitaji nini mke wangu?”

“Huyu aliye fanya jambo hili afe”

“Afe kwa njia gani?”

“Yakikatili sana. Yaani ikiwezekana nimkate kate mimi mwenyewe kwa mapanga”

Nikajifanya kustuka kwa hili analo lizungumza Biyanka, ili nizidi kuipoteza ngozi yangu ya chui ambayo kwa juu nimejivisha ngozi ya kondoo mmoja tena mzuri na mtakatifu.

“Kama ni kufa basi atakufa tu mke wangu. Ila mikono yako naomba isijae damu?”

“Hapana mume wangu. Mimi bado hujanijua vizuri. Mimi nina roho mbaya, nina hasira yoyote ninaweza kumua kwani, kumuua yeye haito kuwa mara yangu ya kwanza mimi kuua”

“Samahani umesema!!!?”

“Hato kuwa mtu wa kwanza kuuwawa na mimi”

Maneno ya safari hii ya Biyanka yakaustua kweli moyo waangu kwani anacho kizungumza dhairi uso wake unaonyesha kwamba ana kimaanisha.

“Chama pinzani wanatuchezea mchezo huu wa kijinga. Yule mzee lazima afe”

“Mzee gani?”

“Yule aliye rekodi mazungumzo na baba yangu”

Hapa ndipo nikapata picha kwamba hawana habari kwamba yule mzee wa chama pinzani amefariki dunia.

‘Roman atakuwa amempeleka wapi?’

Nilijiuliza swali ambalo kwa namna moja ama nyingine nimekosa jawabu la moja kwa moja.

“Unahisi kwamba hiyo ndio njia nzuri ya kurudisha imani kwa wanachama wenu”

“Ndio. Wanachama wetu ni wanyenyekevu, watulivu na wanajua nini wanafanya. Pale uwanjani kuna mamluki walio pandikizwa na chama pinzani na ndio wao alionzisha kumrushia baba mawe na mayai viza”

“Hili swala mke wangu lina hitaji kutimia akili na si nguvu”

“Hapan mume wangu. HIi ni Afrika na si ulaya, hapa bila nguvu hakuna ambacho kinaweza kwenda vizuri”

“Naona kwa sasa una hasira naweza kukuacha upumzike mwenyewe”

“Poa”

Nikamtazama Biyanka kwa sekunde kadhaa kisha nikapanda kitandani na kuendelea kumtazama. Sikuweza kupata usingizi huku nikijaribu kupanga mbinu gani mpya ambayo inaweza kuwatuliza wananchiw a chama hichi tawala ila kama ni panya basi niwe nina ng’ata na kupuliza.

Majira ya saa kumi na mbili na dakika kama tano hivi, Biyanka akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na kuingia bafuni pasipo kunisemesha jambo lolote. Nikashuka na kuingia bafuni na kumkuta akiwa amefungualia bomba la maji huku yakimlowanisha mwili na nguo zake ambazo hajazivua bado.

“Unaweza kuzungumza na wewe?”

“Zungumza”

“Nina wazo moja endelevu juu ya hili swala”

“Wazo gani?”

“Ukiacha kujawa na hasira zako. Tutazungumza ila kwa sasa, vua nguo uoge”

Biyanka akanitazama kwa macho makali ambayo katika udadisi wangu nina hisi ana jambo ambalo anahitaji kulizungumza ila anashindwa.

“Ethan”

“Ndio”

“Unanipenda?”

“Yaa”

“Kwanini una niongopea?”

Swali la Biyanka yakaufanya moyo wangu kuhisi kama ubaridi mkali sana ila nikajikaza kutoa kuutoa wasiwasi wangu huo usoni mwangu.

“Kivipi?”

“Kumbe una mwanamke, tena ni mtoto wa raisi wa Ujerumani, alafu unakuja hapa na kunitania tania mimi si ndio?”

Biyanka akazungumza kwa hasira huku akinikazia macho. Nikatabasamu huku nikimtazama usoni mwake.

“Nilikuwa naye ila sipo naye. Kuna la ziada?”

“Kuna picha zinazo endelea kwenye mtandao na zimekuonyesha kwamba upo naye kwenye msiba wa mama yako”

“Hilo ndio linalo kutatiza. Kwani msiba ni sherehe eheee, au unahisi kuna gadi za mziba zilitolewa waalikwa nani na nani au nani asije. Wewe ni mwaneamke mwenye akili, mwanamke mwenye kujitambua inakuwaje unatekenywa tekenywa na picha tu”

Nilizungumza kwa kufona na nikaanza kumuona Biyanka akiaanza kuwa mpole.

“Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba baba anatokaje kwenye hili zahama. Wewe ukakazi ya kutekenyeka tu na mambo ya kijinga”

“Ila Ethan yote nafanya ni moyo tu”

“Acha upuuzi. Oga na tujue tunamsaidia vipi baba sawa”

“Sawa”

Kumkoromea kwangu Biyanka kukazaa matunda. Tukavua nguo zetu na kuoga kwa pamoja. Tukarudi chumbani humu na kujiandaa na hadi inafika majira ya saa moja asubuhi tukatoka chumbani humu. Tukamkuta baba mkwe na baadhi ya wazee wengine nilio wanoa kwenye kikao cha jana usiku wakiwa sebleni hapa wakitazama taarifa ya habari. Tukawasalimia wazee wote, baba mkwe akanyanyuka na kwa ishara akaniomba nimfwate. Tukaingia kwenye ofisi yake iliyomo hapa nyumbani kwake.

“Mkwe natambua hili ninalo kwenda kukueleza ni jambo zito kwa wewe kulisikia ila ninaomba uwe jasiri na hadi kuwa na mwanangu nina amani kwamba nimekuamini kwa uhai wangu. Upo tajayari kulisikia hili jambo?”

Nikaka kimya huku nikimtazama mzee Poul Mkumbo kwa macho ya ujasiri huku moyoni mwangu nikijawa na furaha kwani aduia yangu anazidi kuingia kwenye kumi na nane zangu pasipo yeye mwenyewe kujitambua.



“Asilimia mia moja baba nipo tayari”

“Sawa. Naamini wewe ni tajiri na umetembea nchi nyingi na una juana na watu wengi ikiwemo majasusi wenye uwezo mkubwa sana wa kimaangamizi si ndio?”

Nikajifikiria kwa sekunde kadhaa, kisha nikamjibu baba mkwe kwa kutingisha kichwa huku nikimkazia macho.

“Nahitaji wauaji wawili. Professional, wenye uwezo wa kufanya tukio ambalo hakuna mtu ambaye anaweza kufahamu kama kuna tukio limenyika katika sehemu fulani”

“Hao watu wapo. Ila huwa hawafanyi kazi kwa mtu ila wanapokea kazi ya mtu. Sijui umenielewa nini ninacho kizungumza?”

“Ndio nimekuelewa”

“Hivyo wanahitaji kazi maalumu na kiasi chao wanacho hitaji. Panga matukio yako unayo hitaji kufanyiwa kisha mimi nitakutafutia hao watu”

“Nashukuru ila hili jambo ninahitaji liwe kati yangu mimi na wewe. Usimueleze hata Biyanka”

“Nimekupata baba”

“Nashukuru kwa kunielewa”

“Unaweza kunidokezea moja ya hiyo kazi unayo hitaji kufanyiwa. Ili hata nikiwatafuta basi nijue ni wapi ninaanzia?”

“Muda ukifika basi utatambua”

“Sawa”

Nikatoka ofisini humu na kujumuika na wazee hawa sebleni huku wakiendelea kupanga mikakati ya kuhitaji kurudisha imani kwa wanachama wao ambao tayari wamesha ingiwa na moyo wa kinyongo kwa kile walicho kisikia.

‘HABARI ZA HIVI PUNDE’

Sauti ya mtangazaji huyu wa kike ikatufanya watu wote tuyatupie macho yetu kwenye televishion.

‘Mwili wa aliye kuwa asifa mwenezi wa chama pinzani hapa nchini Tanzania. Bwana Tomas Lukindo. Umekutwa umeteketezwa kwa moto katika moja ya godauni huko mjini Bagamoyo. Tuungane na ripota wetu kwa taarifa kamili’

Macho karibia ya watu wote humu ndani tukamtazama mzee Poul Mkumbo.

“Sijafanya chochote mimi”

Bwana Poul Mkumbo akaanza kujishuku huku, huku watu wote tukiendelea kumtazama.

‘Hili ni godauni ambalo kwenye moja ya chumba ndipo ulipo kutwa mwili wa bwana Thomas Lukindo. Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi ili kuhakikisha kwamba wauaji wa tukio hili wanafikishwa mahakamani haraka iwezeka…..”

Mama Biyanka akazima tv hii na kutufanya watu wote nihamishie macho kwake.

“Mume wangu sio muuaji. Nina mjua mume wangu ni mtu wa kusimamia haki. Ni mtu anaye ipenda nchi yake na katika hili naomba akili zetu zisichanganyikiwe kabisa ndugu wajumbe”

“Mkumbo umefanya nini sasa. Jana tuliongea nini na leo kinatangaza nini. Huu ni upuuzi mtu na ushenzi. Kuanzia hivi sasa mimi sio kampeni meneja wako. Ninaachia ngazi yangu”

Mzee huyu baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka kwenye sofa alilo likalia na kutoka nje.

“Hili ni lako mkumbo”

Mzee mmoja alizungumza huku naye akisimama na kuondoka eneo hili na wakabaki wazee watatu. Gafla mzee Poul Mkumbo akapiga glasi aliyo ishika ukutani na kuondoka sebleni hapa kwa hasira na kuelekea chumbani kwake. Mama Biyanka akamfwata mume wake kwa nyuma na kutuachia utata mkubwa sisi tulio baki hapa sebleni.

“Kwaherini”

Wazee hawa wakaaga na kuondoka na kutiacha mimi na Biyanka, ambaye taratibu akatafuta sofa la peke yake na kukaa huku akionekana dhairi kwamba ana mawazo lukuki kichwani mwake.

“Fuc**”

Nilizungumza huku nikijiinamia na moyoni mwangu furaha ya kuhakikisha kwamba nina muharibu bwana Poul Mkumbo inazidi kujaa.

“Ina maana baba ameua kweli. Eti Ethan?”

Biyanka alizungumza kwa unyonge huku akiwa amejawa na bumbuwazi kubwa.

“Sidhani baba mkwe anaweza kufanya hilo jambo”

“Ethan kila mtu amesikia yale majibizano. Ona sasa leo hii ametangazwa yule mzee kwamba ame uwawa. Kweli jamani eheee?”

Biyanka alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Nikanyanyuka kwenye sofa langu na kuhamia kwenye sofa lake. Taratibu nikamlza Biyanka kifuani mwangu na kuanza kumbembeleza.

“Mke wangu ninaweza kumsaidia baba kutoka katika hili?”

Biyanka akanyanyuka kwa haraka na kukaa kitako kwani kama ni hali ya kisiasa kwa baba yake inamuendea mrama na muda wowote basi anaweza kupoteza muelekeo.

“Niambie….niambie mume wangu”

“Kama wazee hawa wameamua kumuacha baba kwenye hili peke yake basi mimi nitasimama kama kampeni meneja wake. Kikubwa ninacho kihitaji kutoka kwako ni kuhakikisha kwamba unakuwa mkakamavu zaidi ya ukakamavu ambao ulisha wahi kuwa nao kipindi cha nyume. Umenielewa mke wangu?”

“Ndio nimekuelewa baba watoto”

Nikamshika Biyanka mashavu yake na kuzinyonya lipsi zake kidogo kisha nikasimama.

“Unaenda wapi?”

“Ninakwenda kuzungumza na baba”

“Yupo na mama chumbani kwao.”

“Nalitambua hilo mke wangu ila sina muda wa kupoteza hivi sasa.”

Nikaelekea katika chumba cha mzee Poul Mkumbo. Nikagonga kwa sekunde kadhaa na mlango ukafunguliwa na mama. Macho ya mama Biyanka yamejawa uwekundu ambao dhairi unamuashiria kwamba ni mtu aliye lia kwa muda mrefu.

“Mama ninahitaji kuzungumza na baba”

“Ohoo samahani Ethan mwanangu. Baba ha….”

“Muache aingie”

Sauti ya mzee Poul Mkumbo ilisikika kutokea ndani ya chumba hichi. Mama hakuwa na budi zaidi ya kunifungulia mlango na nikaingia ndani. Japo mimi nina pesa nyingi sana ila sijawahi kufanya kufurau kama hii, kwani hichi chumba kuta zake zimetengenezwa kwa gold halisi na si rangi. Kitanda chao, milango, dreasin table, kwa ufupi asilimia tisini na nane ya chumba hichi kimetengenezwa kwa dhababu.

“Ndio Ethan una mpango gani hivi sasa?”

“Natambua muda ulio baki katika kampeni ni mchache sana. Nina imani kwamba bado watu wana imani na wewe na kama uchunguzi ukifwanywa vizuri basi hili sakata utakuwa umelitoka”

Nilizugumza kwa kujiamini na kumfanya mzee Mkumbo kunitazama huku na kutingisha kichwa chake.

“Nipo tayari kusimama kama kampeni meneja. Nina ushawishi mkubwa sana kwenye jamii, watu wana nipenda, wana nijua na kuniheshimu. Ngoja nitengeneze kwanza timu ya watu wachache ambao ninaweza kufanya nao hili jambo kwa pamoja na nina uhakika kwamba linakwenda kufanikiwa hivi karibu”

Mzee Mkumbo akanitazama kwa macho ya huruma kisha akasimama na kunipa mkono.

“Ninashukuru sana Ethan nilisha kata tamaa, nilisha amini kwamba inakwenda kushindwa kwenye hili jambo ila ninakushukuru sana mkwe wangu”

“Usijali baba”

Nilizungumza huku nikimpa mkono mzee Mkumbo. Nikatoka ndani humu na kurudi sebeleni.

“Ninatoka mke wangu”

“Wapi unakwenda?”

“Kuna kazi ninakwenda kuifanya. Kaa hapa nyumbani na hakikisha munabaki salama”

“Sawa mpenzi wangu. Kuna haja ya kupewa walinzi?”

“Hapa, ninahitaji gari lolote”

“Kuna Benzi moja hapo nje. Unaweza kuitumia”

“Funguo”

Biyanka akaondoka hapa sebleni na baada ya muda kidogo akarudi akiwa ameshika fungua.

“Nina imani kwamba hii ndio funguo yake”

Sawa”

Nikatoka nje, nikaingia kwenye gari hili na kuondoka. Moja kwa moja nikaelekea hadi makao makuu ya kampuni yangu. Sikuhitaji kufanya mawasiliano ya aina yoyote ndani ya gari hilo kwani wanaweza kutega hata vinasa sauti. Nikachukua simu yangu ya siri ambayo ninatumia kuwasiliana na viongozi wa upinzani. Nikatafuta namba ya mgombea uraisi wao na kumpigia.

“Ndio mzee”

“Ni muda sasa hatujasikia chochochote kutoka kwako”

“Ndio, kuna sababu za msingi za mimi kuweza kufanya hivyo. Ila nina imani kwamba hili ninalo kwenda kukuambia ni jambo zuri sana.”

“Ehee niambie ndugu yangu”

“Upon a nani?”

“Nipo peke yangu”

“Upo Dar au mkoani?”

“Nipo mkoani Arusha, leo jioni nina kampeni kubwa eneo hili”

“Sawa. Hakikisha utakapo maliza kampeni zako. Nahitaji timu nzima tulio kutana siku ile muje jijini Dar es Salaam nina mazungumzo muhimu sana na wewe”

“Ila mkuu Dar kwa sasa sio salama kwa sisi viongozi kwa maana kama mwezetu mmoja mumeona tukio lililo fanyika na sisi hapa tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunawatuliza wafuasi wetu wasifanye fujo huku tukihitaji kujua ni kitu gani serikali inaweza kufanya juu ya mauaji haya”

“Nimewaelewa, ila kwa sasa nipo ndani”

“Upo ndani wapi sijakuelewa mkuu?”

“Hakikisheni kwamba siku ya leo haiishi muwe mume onana na mimi kwani tupo karibu sana kuweza kushinda na kukichangua chama tawala vipande vipande ambavyo itawachukkua miaka zaidi ya mia moja kuweza kukirudisha madarakani.”



Mgombea uraisi kwa chama pinzani akakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akionekana kutafakari jambo.

“Sawa tumekuelewa mkuu. Tujulishe ni wapi na saa ngapi tuweze kuonana”

“Sawa baada ya muda mfupi nitawatumia location ya wapi tunaweza kukutana”

“Sawa mkuu”

Nikakata simu huku moyo wangu ukiwa umejawa na furaha kubwa sana pamoja na amani kwani dalili za ushindi zinakaribia hivi karibuni. Nikawapigia simu Qeen na Latifa na kuwaita ofisini kwangu.

“Kuna jambo la muhimu sana nahitaji liweze kufanyika kuanzia hivi sasa”

“Jambo gani”

“Nina imani kwamba munaelewa kila kitu kinacho endelea kwenye familia ya baba yangu mkwe pamoja na chama chake tawala muna kifahamu?”

“Ndio mkurugenzi”

“Nimeamua kumsaidia kikamilifu”

Qeen na Latifa wote wakanitazama kwa mshangao kwani ninacho waeleza sicho kile ambacho nimekipanga kwenye mapambano haya.

“Nahitaji wasanii wenye uwashawishi ambao kwa kipindi hichi kifupi kilicho baki wanaweza kurudisha imani kwa baba yangu mkwe”

“Samahani Ethan. Kuna kitu gani kilicho kupata?”

Nikatabasamu kwa maana hawaelewi nini maana yangu. Kutokana ofisi yangu siiamini sana kwa mazungumzo ya siri, kwani kunaweza kuwa na kamera au kinasa sauti kilicho tegeshwa. Nikaona sio jambo jema na la muhimu kwa mimi kufafanua maana yangu ya mimi kuwa hivi."

“Ninaomba muweze kufanya kama nilivyo waagiza. Wasanii tutawalipa kiasi chochote cha pesa ambacho watakihitaji. Lifanyeni hilo na usiku nahitaji kuonana na wasanii hao hapa ofisini”

Qeen na Latifa wote wawili wakaonekana kuto kuwa na furaha na maamuzi yangu. Nikawaruhusu kwa ishara ya mkono ili waweze kunyanyuka na kuondoka. Japo ni maamuzi ya kuwaumiza Qeen na Latifa ila kwa sasa nina takiwa kuwa makini sana kuhakikisha kwamba mpango wangu nilio kusudia unakwenda kama vile nilivyo panga. Qeen wakanifahamisha kwamba wamewapata wasanii kumi, sita wakiwa wa muziki na sita wakiwa wa kuigiza. Majira ya saa moja usiku nikakutana nao ofisi hapa huku wakiwa na mameja wao. Nikaanza kuwaeleza mpango madhubuti wa kufanya kazi kubwa sana katika siku chache ili niweze kuhakikisha kwamba mzee Poul Mkumbo anarudi kwenye mfumo mzuri.

“Mkurugenzi ila hili swala linaweza kutufukuzia mashabiki wetu kwa maana hivi sasa mashabiki wengi sana wapo kwenye upande wa chama cha upinzani”

“Hilo nalifahamu, ila kwa mwaka unaingiza kiasi gani?”

“Nani….Mimi?”

Nikatabasamu kwa jinsi msanii huyu anavyo jistukizia.

“Ndio”

“Si chini ya milioni themanini”

“Je tukikupatia milioni mia na stini utalifanikisha hilo?”

Wasanii hawa wakaanza kutazamana na kitu nilicho kifahamu kwa haraka haraka, uchu wa pesa ndio ulio wafanya waanze kutazamana tazamana.

“Zungumza musiogope kuweni huru?”

“Mimi nitafanya”

“Wote mupo kumi, kila mmoja nitamlipa milioni mia mbili. Tuna wiki moja na siku tatu, kabla ya watu hawajaanza kupiga kura. Je mutalifanikisha hilo?”

“Ndio tutalifanikisha”

Wasanii hawa walijibu kwa pamoja huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Sharti namba moja. Muna account zenu za Instergram, Facebook, Snapchat na Twitter. Hizo ndio ninazo hitaji muweze kuzitumia kuanzia muda huu na kuwapa watu taarifa. Kama ulikuwa chama pinzani, futa picha za chama hicho kwenye accout yako kish ingiza picha ambazo ni za chama chako”

“Namba mbili. Kuna mikoa kadhaa ambayo muheshimiwa anakwenda kufanya kampeni zake. Mutazunguka nasi na nina imani kwamba mutapiga shoo za kufa mtu si ndio”

“Hilo halina tatizo mkuu”

“Tatu, sinto penda usnich wenyewe munaita umbea. Ukiwa huna kifua cha kuweka siri. Mlango upo wazi, nyanyuka na toka sasa hivi ofisini kwangu hata kabla sijafanya malipo kwenye accont zenu.”

Wasanii wakatazamana kwa sekunde kadhaa na sikumuona hata mmoja aliye jaribu kusogeza hata kiti chake ili anyanyuke.

“Ukimya nao pia ni jibu kwamba kati yetu hakuna mmbea si ndio”

“Ndio mkurugenzi”

“Qeen niitie muhasibu ila ngoja…..”

Nikanyanyua simu ya mezani kwangu na kumpigia muhasibu wa kampuni yangu, nikamuhitaji afike ofisini kwangu na ndani ya muda mfupi akafika. Nikamuagiza sekretari kuchapisha mikataba ya makubaliano yangu na wasanii hawa juu ya kuzunguka nao katika kuhakikisha kwamba wanakipigia kampeni baba yangu mkwe. Ndani ya muda mfupi mikataba yote ikawa imeisha na kila msanii aliye taja accont namba yake kabla ya kuingiziwa pesa kwenye accont yake, anatia saini karatasi mbili, moja nina baki nayo mimi na nyingine anaondoka naye yeye. Baada ya makubaliano hayo na kila mmoja kudhibitisha kwamba milioni mia mbili zimesoma kwenye simu zake tukasimama kwenye viti vyetu na kuanza kupeana mikono huku wote wakiniomba tuweze kupiga picha za pamoja.

“Jambo moja la mwisho jamani. Nina amni kwenye vipaji vyenu, tufanye hili jambo kwa pamoja na nyote kumi nina imani kwamba mutakuwa ni mabalozi wa kampuni yangu hii ya simu. Endapo tutafanya matangazo basi nyinyi mutakuwa ni wa kwanza kabisa na mutakula shavu kubwa sana kwangu”

“Tunashukuru sana mkurugenzi”

Kikao hichi kikaisha na nikabaki na Qeen pamoja na Latifa ofisini hapa.

“Unajua hadi sasa hivi mkurugenzi sijaelewa ni kitu gani kinacho endelea kwenye Ubongo wako wa akili”

“Ni wapi ninapo weza kumpata Roman?”

Sikulijibu swali la Latifa zaidi ya kuuliza swali langu.

“Roman anapatikana”

“Wasiliani naye, nahitaji kuonana naye leo pamoja na nyinyi. Kisha muniambie ni wapi mupo niwafwate”

“Ila Ethan”

“Shiiiiii Qeen nina waelewa nini munahitaji kuzungumza ila mimi ni Genius. Musiondoe imani kwangu mimi kila jambo lipo katika uangalizi mzuri sawa”

“Sawa baadae”

“Poa”

Nikaanza kuipitia mikataba hii ya wasanii mmoja baada ya mwengine. Nikaanza kupitia account zao na nikaanza kuwaona jinsi wanavyo niweke kwenye accont zao na wengine wakitangaza hadharani kahama cha cha upinzani. Nikampigia mgombea uraisi chama pinzani na kumfahamisha ni wapi tuweze kuonana. Nikatoka ofisini hapa na moja kwa moja nikarudi nyumbani kwa mzee Poul Mkumbo. Nikawakuta baadhi ya viongozi wa chama tawala wakiwa sebleni wakijadili mambo mengi mmoja wapo ni raisi. Nikawasalimia kwa heshima kubwa sana na mzee Mkumbo akanikaribisha kwenye kikao hichi.

“Nilishindwa kukupigia nina imani kwamba kuna idea mpya uliyo kuja nayo”

“Ndio baba mkwe”

Nikaka kwenye moja ya sofa na kutoa kwenye bahasha mikataba niliyo ingia na wasanii hawa. Nikaanza kutandaza mitaba hiyo wa viongozi hawa nane na wakaanza kuipitia.

“Hii ni nini kijana?”

“Hiyo ni mikataba niliyo ingia na wasanini wenye ushahiwishi mkubwa sana kwneye hii nchi. Nimetazama watu wengi katika kampeni zenu ni vijana na wamama. Ili kuweza kuwaweka pamoja hawa watu na wakakiamini tena chama ni vyema nikahakikisha kwamba wasanii wale walio kuwa chama pinzani tunawarudisha kwenye chama tawala na kutokana wana mashabiki wengi nina imani kwamba wale mashabiki lazima watawafwata wasanii wao wanao wapenda”

“Aiissee hili ni bonge la idea. Unajua hawa wasanii ambao tupo nao huku, naona wanakula tu pesa zetu”

Raisi alizungumza huku akitazama mkataba huo.

“Ndio na isitoshe ni kwamba kila msani hapo nimemlipa milioni mia mbili. Baba mkwe hembu ingia kwenye accont yako ya instergram uangalia watu kama wameongezeka.

“Weee Biyanka”

Mzee Poul Mkumbo aliita.”

“Biyanka”

“Yes Dany”

“Ingia hapo chumbani nichomolee simu yangu kwenye chaji”

Baada ya muda kidogo Biyanka akafika hapa sebleni na simu ya baba yake. Akamkabidhi mzee Poul Mkumbo simu hiyo.

“Ebwana wameongezeka”

Mzee mwengine alizungumza huku akiwa ameishika simu yake mkononi.

“Unajua jana baada ya ile sauti watu walishuka kutoka milioni mbili hadi milioni moja nuka mbili.

“Eheee aisee wamefika milioni nane!!”

Mzee Mkumbo alizungumza huku uso wake ukiwa umejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Hao sasa ni watu waliomo mitandaoni tu. Ila tuna kazi moja, kwa kupitia hawa wasanii, kwenye kila kampeni ambazo tutatembea popote pale ndani ya Tanzania. Basi tutakwenda nao na watatumika kuvuta watu. Hawa wasanii ambao tayari mulish kuwa nao, hakuna haja ya kuwaacha ibabidi nao wawemo kwenye hili swala. Sawa jamani”

“Sawa sawa kijana. Aissee wewe ni Genius”

Mzee mwengine alizungumza huku akitingisha kichwa.

“Ndio maana sikuhitaji mwanangu aje kueloewa na mtu boya boya. Safi sana Ethan”

Mzee Mkumbo alizungumza huku akitabasamu jambo lililo nifanya nitabasamu huku moyoni mwangu nikiiwazia siku ambayo atalia kilio cha kusaga meno.

“Huu mpango wa wasanii kweli una nguvu”

“Hee milioni tisa”

Mzee mkumbo alizungumza huku akiendelea kuishika simu take na meno yote thelathini na mbili yapo nje.

“Jambo jengine ambalo nina lihitaji. Kuongeza nguvu ya matangazo kwenye vyombo vya habrai. Redio, tv, blogs, website za watu. Yaani tuchafue kila sehemu yaani hata mpinzani akifungua simu yake kwenye mtandao wa whatsapp basi anaona sura yako mzee”

Maneno yangu yakawafanya watu wote kucheka saha huku kila mmoja nikiona sura yake jinsi inavyo tawaliwa na furaha pamoja na shangwe kubwa sana.

‘Jamani mutalia na huyu mbwa mwezenu siku’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nami uso wangu ukiwa umejawa na kicheko kizuri sana.

“Hiyo kweli. Ethan mkwe wangu hakika mchango wako, sikutarajia kama unaweza kuwa na nguvu. Yaani hapana unajua watu wazima tulikaa hapa zaidi ya lisaa. Vicha vinauma, dhairi tunaona jinsi chama kinavyo kufa ila kwa hili hapana jamani ni lazima tuchukue nchi tena kwa kishindo kikubwa. Ile wasiwasi sijui nini ni lazima iishe yote”

“Nashukuru sana baba yangu mkwe. Kwenye maswala ya matangazo ya vyombo vya bahari mimi na Biyanka tutayasimamia. Na kitu kingine, ninatahitji tutengeneze video ya historia yako iwe kama dakika moja au sekunde arobaini na tano hivi. Nina imani kwamba itafaa sana kwenye matangazo yetu.”

“Hilo halina shida. Yaani hivi sasa ni nyinyi tu vijana wangu. Fanyeni kazi yanani sijui niseme nini Mungu wangu”

“Usijali baba, nimejitolea kupambana, yaani hizi siku sijui kumi na mbili sijui ngapi”

“Kumi na tatu”

Biyanka alizungumza huku akinitazama.

“Yale mafuriko ya wapinzani, yatahamia kwenye chama chako. Niaminini”

“Kwahili mimi sina wasiwasi na wewe. Au kuna mtu mwenye wasiwasi na kijana wangu?”

Wazee wote wakajibu kwamba wana niamini. Nikatingisha kichwa nikiamini sasa nina zidi kuwaelekezea kibla mbuzi wangu na ukifika muda wa kuwachinja basi sinto kuwa na huruma na hata mmoja wao.

“Basi ya kuanza kutembelea vyombo vya habari niianze sasa hivi. Usiku huu. Biyanka tugawane wewe utakwenda kwenye vituo kadhaa nami ninakwenda kwenye vitua kadhaa. Hadi inafika asubuhi kila kiitu kiwe kimekwisha na mkutano wako mzee kesho kama kawaida utaendelee na matangazo yatakuwa ya kumwaga”

“Sawa sawa”

Nikaondoka sebleni hapa na Biyanka akaniomba niweze kipata chakula cha usiku kisha ndio tuianze kazi hii. Tukala kwa pamoja kisha nikabadilisha nguo alizo ninunulia, tukawaaga wazee hawa, huku Biyanka akiwa ameniandikia vitua vya habari ambayo ninatakiwa kuvitembelea usiku huu kisha naye akaniandikia vitua vyake anavyo kwenda kufanya mazunguzo na wamiliki wake.

“Walinzi”

“Hapana, hii kazi tambua tunatakiwa kuifanya kisiri pasipo kuvuja. Tukiambatana na walinzi mama kesho tutakuwa na skendo mpya za kuzitolea majibu, sasa hapo mimi nitashindwa”

“Nimekuelewa mume wangu”

Nikaingia kwenye gari langu aina ya Range rover, huku Biyanka naya akaingia kwenye gari lake la kila mtu akaende sehemu yake anayo ona kwake ni karibu. Nikawapigia simu Qeen na Latifa na kuwaomba sote tukakutane kwenye kisiwa anacho ishi mtoto Clara ambaye ana siri kubwa sana juu ya mzee Poul Mkumbo. Nikaliacha gari langu kwenye moja ya kitua cha habari, sikuingia ndani nikatoka na kukidi pikipiki hadi karibu na fukwe za bahari, nikamlipa mwenye pikipiki. Kabla sijapanda boti ndogo ya siri tuliyo ificha kwenye fukwe hizi. Qeen, Latifa na Roman wakafika eneo hili. Tukapanda kwa pamoja kwenye hii boti na moja kwa moja tukaelekea hadi kwenye kisiwa hichi. Tukafika katika nyumba anayo ishi Clara peke yake, alipo niaona kwa haraka akanikumbatia huku akilia kwa furaha sana. Ndani ya robo saa, helicopter iliyo wabeba viongozi wa upinzani ikafika. Tukawakaribisha ndani kisha nikamuomba Clara aende kwenye chumba chake ili tuweze kufanya mkutano huu wa siri.

“Kila mmoja simu yake aweke mezani”

Niliwaambia viongozi hawa kwa maana siwaamini toka mwenzao alipo hitaji kuniua. Wakatii amri yangu na nikamuomba Roman aiunganishe simu yake kwa kupitia USB waya na Tv na kuiweka video ya mauaji ya mzee yule. Roman akafanya hivyo na baada ya muda mchache sana video hiyo ya mateso na ya kutisha ikaanza kuonekana jambo lililo wafanya watu wote kushangaa unyama na ukatili huu ambao alifanyiwa mwenzao.



Hadi video hii inakwisha nyuso za watu wote humu ndani zimejawa na huzuni kubwa sana huku wote wakionekana kutingisha vichwa vyao kusikitishwa na tukio hilo la kinyama. Nikamshuhudia mgombea uraisi akimwagikwa na machozi usoni mwake.

“Huyo ni mwenzenu alifanyiwa hilo jambo la kikati. Kesho au kesho kutwa inaweza kuwa ni mmoja wetu humu ndani na hatujui je naye anaweza kurekodiwa kama hivi au hato weza kurodiwa na kuuwawa kimya kimya na kutupiliwa mbali au porini na akaliwa na wanyama wakali”

Nilizungumza kwa kujiamini huku nikiwatazama watu wote humu ndani.

“Hii ndio siasa yenu muna ipigania hivi sasa. Unyama na ukatili umetawala. Je nini tufanye?”

“Mkuu hiyo video ni lazima tuipelekea kwenye mahakama za kimataifa ila sheria husika iweze kuchukua mkono wake. Haiwezakni kabisa”

“Hata mimi pia nina shauri jambo hilo. Haiwezekani kabisa mtu afe kwa meteso kiasi hicho na sisi tukae kimya”

Wazee hawa walizungumza kwa jazba kubwa sana.

“Katika mchozo wowote lazima kuwe na plan B. Si ndio?”

“Ndio mkuu”

“Hii video kwa sasa hatuwezi kuitoa hewani kwani inaweza kuwa karata ya muhimu sana kwa ushindi wako mzee. Hivi sasa nimechaguliwa kuwa kampeni meneja wa Mkumbo. Hivi ninavyo zungumza sasa hivi nimeweka wasanii muhimu kuhakikisha kwamba wanamuingizia wanachama wengi zaidi katika kuhakikisha wana mpa kura”

“Nini….Sa…sa..hiyo si itatufanya sisi tushindwe?”

Mgombea uraisi alizungumza huku akiwa amejawa na kigugumizi kizito sana.

“Hapana”

“Ila nini sasa hapo kijana unacho kifanya”

“Nahitaji waniamini”

“Alafu?”

“Nina waangusha chini. Kikubwa nyinyi ni kusimama kwenye nafasi zenu. Endeleeni na kampeni zenu kama kawaida mume nielewa”

“Mmmmm”

“Mkurugenzi samahani”

Qeen alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio”

“Huo mpango wako kwa mfano ukishindwa kufaulu itakuwaje, na endapo watashinda kiti cha uraisi itakuwaje pia?”

“Hakuna jambo la kushindwa katika hili. Moja, nitahakikisha kwamba hata kura moja hato pigiwa?”

“Nini?”

“Ndio nita hakikisha hata kura yake yeye mwenyewe hajipigi”

“Hiyo itawezekana vipi?”

“Kila kiti ninahitaji muhiachie mimi. Kitu kingine usaliti ni mbaya sana kati yenu, endapo mtu atarudi tena kunisaliti sina msamaha naye”

“Akirudia kukusaliti, nani tena mkuu alikusaliti?”

“Hilo ni jambo langu binafasi. Kitu nilicho kihitaji kukizungumza kwenu ni hicho. Niwatakie usiku mwema na upambanaji mwema”

“Tunashukuru sana”

Kila mzee akachukua simu yake. Tukawasindikiza hadi nje, wakapanda helicopter yao na kuondoka eneo hili. Tukarudi sebleni na Roman akazima tv hii. Nikaingia chumbani kwa Clara na kumkuta akiwa amesha pitiwa na usingizi. Nikampiga busu la shavuni mwake kisha nikatoka chumbani humu.

“Tuondokeni”

“Ila Ethan, sisi watatu ni watu ambao una tuamini sana. Hembu naomba uweze kutupa siri ya mpango wako ambao unahitaji kuufanya juu ya hii video?”

Latifa alizungumza kwa upole na kwa unyonge. Roman akanikonyeza pasipo wao kuona, ikiwa ni ishara kwamba nisiweze kuzungumza jambo la aina yoyote.

“Musijali, zimebaki siku chache tu kila jambo litakwenda kuwa poa”

“Jamani Ethan”

“Musijali, lengo letu ni ushinda. Hivyo ushindi hivi karibuni utapatikana. Mumenielewa?”

“Sawa bwana, ila sisi mbona hatukufichi mambo yetu”

“Hapo mumevaa chupi za rangi gani?”

Utani wangu ukawafanya watu wote kucheka. Tukaanza safari ya kurudi upende wa pili ambao ni Dar es Salaam. Tukaingia kwenye gari lao, wakanipeleka karibu na jengo la kituo cha utangazaji nilipo acha gari langu. Nikaiwasha simu yangu ambayo niliizima kwa sababu maalumu za wao kuweka kunitafuta kwa kutumia GPRS. Mlinzi akanipeleka hadi kwa mkurugenzi wa vipindi katika kituo hichi. Nikazungumza naye juu ya wao kuungana nasi katika kufanya matangazo.

“Milioni mia nina imani kwamba itasaidia kuhakikisha kwamba tunawapigia kampeni kubwa na nyinyi wenyewe mutafurahi”

“Sawa haina tatizo kuna hivi vituo je unaweza kunikutanisha na wawiliki wake usiku huu huu?”

“Ndio”

Mkurugenzi huyu akaanza kuwasiliana na wamiliki wa vitua vinne vilivyo salia. Nikazungumza nao kwa kupitia simu na tukakubaliana wote kwa pamoja ni kiasi gani ambacho ninawezza kuwalipa.Nikapanga kuonana nao kesho majira ya saa nne asubuhi ofisini kwangu ili kuingia mkataba huo wa matangazo. Nikaondoka kituoni hapa na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwa mzee Mkumbo. Nikiwa njiani, Latifa akanitumia wimbo ulio imbwa na wasanii tulio wapa kazi ya kutufanyia kampeni.

Nikaanza kuusikiliza wimbo huu na kuwafahamisha kwamba wimbo huu ni mzuri sana na wasiutoe hewani hadi pale nitapo msikilizisha mzee Mkumbo. Nikafika nyumbani na kuwakuta mzee Mkumbo na mke wake wakiwa wameka sebleni.

“Biyanka hajarudi?”

“Naye yupo njia anarudi. Tulijaribu kukupigia na haukuwa hewani”

“Ni kweli, nilikuwa na kikao na wakuu wa vituo na tumesha kubaliana juu ya kufanya kampeni hizo kwa nguvu kubwa”

“Wamesemaje?”

Kesho saa nne ninafanya nao kikoa cha kuwapa pesa za kuifanya kazi hiyo”

“Wamehitaji kiasi gani?”

“Kila kitua milioni mia moja mia moja”

“Duu mkwe wangu unajitolea vya kutosha jamani”

Mama Biyanka alizungumza kwa upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Usijali mama”

“Hiyo pesa mwanangu usiwe na shaka. Ndani ya mwezi mmoja tu imerudi. Yaani nikiingia serikalini kwanza nitahakkikisha kwamba ninarudisha garama zangu zote nilizo poteza. Yaani lazima wananchi waisome namba”

Mzee Mkumbo alizungumza kwa majigambo jambo lililo nifanya nitabasamu. Ila moyoni mwangu sidhani kama hiyo ndoto anayo izungumza kama inaweza kwenda kukamilika.

“Jamani hamjalala”

“Ndio tulikuwa tunakusubiria wewe. Vipi huko umefanikiwa”

“Asilimia mia moja, yaani baba lazima ushinde”

Biyanka alizungumza kwa furaha kubwa sana. Akatuelezea juu ya mafanikio ya kazi yake aliyo kwenda kuifanya na kwa bahati nzuri kiwango ambacho nilipanga kuwapatia wamiliki wa vitua hivyo vya habari ndio kiwango ambacho hata yeye amepanga kuwalipa wamiliki hao.

“Jamani kuna mziki hapa. Wale wasanii wameweza kuimba kwa ajili ya kampenzi naomba tuusikilize”

Nikauweka mziki huu kwenye simu yangu na kuiweka mezana. Kila jinsi mziki unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi ninavyo muona mzee Poul Mkumbo anavyo tingisha kichwa chake kwa furaha kubwa sana.

“Ngoma kali asieee”

“Kweli baba?”

“Ndio, Ethan wewe kichwa”

“Hivyo mume ipitisha itumike kwenye kampeni”

“Mimi asilimia mia moja”

“Mama je?”

“Kwangu imepita?”

“Baby?”

“Umepita, tena nirushie na mimi ili niwatumie hawa wamiliki na kuanzia kesho waanze kuupiga kwenye vyombo vyao vya habari”

Nikawaruhusu wimbo huo waanze kuusambaza, kisha nimatumia Biyanka kwenye namba yake pamoja na baba yake. Kazi ya kuusambaza wimbo huu haikuwa ngumu kwani mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa sana kwa upande wetu. Siki iliyo fwata nikaingia mikataba na wakurugenzi wote wa vituo nilivyo kubaliana nao kuweza kuifanya hii kazi ya kempeni. Tukawatafuta wamiliki wa website, blogs na chanel za Youtube ambao kwenye jamii ya Kitanzania wana nguvu kubwa katika kuwashawishi watu, tukawalipa pesa ya kutosha na wakaanza kazi ya kupiga kampeni.

Ndani ya ya siku tatu, hali ya wapinzani kwa upande wao ikazidi kuwa mbaya. Mikutano yao ikaanza kukosa watu jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine likazidi kuwastua wapinzani wezangu ambao tupo kwenye mpamgo mmoja. Kila mkoa ambao mzee Poul Mkumbo ana pita akakutana na wingi mkubwa sana wa watu jambo ambalo linamfanya kila akimaliza kampeni zake anishukuru sana kwa juhudi zangu ninazo zifanya.

Zikabaki siku mbili kabla ya siku ya kupiga kura kuwadia. Watu wakazidi kurudisha kadi za chama pinzani na kuhamia chama tawala.

Ikabaki siku moja, siku ambayo wana siasa wote wanamwaga sera zao kwa wakati wa mwisho kuhakikisha kwamba wanapata kura kutoka kwa wananchi wao. Si Latifa wala Q een wote wamekata tamaa kwa kuona mzee Poul Mkumbo akizidi kupeta tu mtaani kwani siku inayo fwata ndio siku ya wananchi kupiga kura. Nikampigia Roman simu kwa namba yangu ambayo siitumii mara kwa mara na ni namba ambayo ni Roman pekee tu ndio anaye ifahamu na namba hii hakuna mtu ambaye anaweza ku hack mawasiliano yake pale ninapo zungumza na Roman.

“Unajua nini cha kufanya?”

“Ndio boss”

“Muda wake umefika sasa”

Nilizungumza huku nikimtazama mzee Poul Mkumbo anaye serebuka jukwaani na wasanii hawa ambao hakika wameifanya kazi kubwa kuhakikisha wanamuingiza ikulu mzee Poul Mkumbo.



Nikakata simu na kuingia ndani ya gari langu ili kusubiri msafara awa kuondoka katika kiwanja hichi kuwadia. Safari ya kurudi nyumba ikaanza huku wanachama wa chama tawala pamoja na viongozi wao wakiwa na matumaini makubwa sana mioyoni mwao. Tukafika nyumbani kwa mzee Poul Mkumbo majira ya saa mbili usiku, tukamkuta mama Biyanka akiwa na huzuni kubwa huku simu yake ikiwa mkononi.

“Mke wangu tumerudi tutarajie ushindi mkubwa sana”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa furaha kubwa sana. Mama Biyanka akamtazama mume wake tu kwa macho ya unyonge.

“Hivi umetashika simu yako?”

“Hapana niliizima nilikuwa jukwaani”

“Hembu iwashe”

“Kuna nini mke wangu”

“Wewe iwashe”

Mzee Poul Mkumbo akaitoa mfukoni simu yake na kuiwasha. Mlio wa meseji kwa njia ya whatsapp ukasikika. Mzee mkumbo akafungua meseji hiyo, baada ya sekunde kama sita hivi nikaanza kumuona akitoa macho akatafutata sofa na kukaa chini huku akionekana kuwa na wasiwasi mkubwa sana.

“Mama ni nini kinacho endelea?”

Nilimuliza mama Biyanka huku nikimtazama usoni mwake. Mama mkwe hakujinibu chochote zaidi ya kumwagikwa na machozi usoni mwake. Biyanka akaingia ndani hapa huku akiwa na furaha kubwa sana, ila hali aliyo tukuta nayo kidogo ikaifanya furaha yake kuanza kutoweka.

“Kuna nini kinacho endelea?”

Biyanka alituuliza huku akionekana kuwa na shahuku ya kuhitaji kujua ni kitu gani ambacho kinaendelea.

“Sijajua, tumerudi na kumkuta mama akiwa katika hali ya huzuni, baba amewasha simu yake hapo ila siju ni nini kinacho endelea”

“Eti mama kuna nini?”

Mama mkwe akamkabidhi Biyanka simu yake. Biyanka akaanza kutazama video ambayo nina imani kwamba Roman ameituma katika muda sahihi.

“Ohoo Mungu wangu. Baba ni nini hichi umefanya!!?”

Biyanka naye alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikaichukua simu hiyo ya mama mkwe ili nami nijishuhudie hichi ninacho kiona. Uso wangu nikauweka katika hali ya mshangao huku moyoni mwangu nikishangilia kwa furaha kubwa sana.

“Baba hii ni kesi itakayo kupoteza baba yangu. Kwanini unafanya vitu vyako bila ya kufikiria jamani eheee?”

Biyanka alilamika huku akionekana matumaini ya kile kitu alicho kifanya baba yake yanakwenda kufifia. Simu ya mezani ikatustua sisi sote na kuitazama. Mtu pekee ambaye ninaweza kuipokea ni mimi mwenyewe. Nikaisogelea simu hii na kuipokea.

“Halo unazungumza na Ethan kutoka nyumbani kwa muheshimiwa Poul Mkumbo”

“Kijana nahitaji kuzungumza na Mkumbo mimi ni raisi”

Raisi alizungumza kwa sauti ya kufoka, nikamtazama mzee Poul Mkumbo kisha nikamsogezea simu hii, akaichukua kwa hali ya unyonge na kuiweka sikioni mwake.

“Sio hivyo mkuu”

Nikamshuhudia mzee Mkumbo akifumba macho yake nina imani kwamba hayo anayo yapokea huko ni michambo ya haja.

“Mkuu mimi sija……”

Mzee Poul Mkumbo baada ya muda akakata simu na kuiweka mezani. Akashusha pumzi nyingi huku akionekana kuchoka sana. Simu ikaanza kuita tena, kwa ishara mzee mkumbo akaniomba niipokee. Nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Halooo”

Sauti nzito na mbaya inayo tisha nikaisikia na kunifanya nikunje sura yangu kidogo. Nikaiweka simu hii katika mfumo wa sauti kubwa na kila ili kila mtu aweze kuisikia.

“Nina imani kwamba muna nisikia.”

Sauti hiyo ya mbaya ilizungumza na kuwastua Biyanka na mama yake.

“Mzee Mkumbo. Video yoko hadi sasa ipo kwa watu sita. Sasa hivi ni saa mbili dakika hamsini na mbili. Ikifika saa nne kamili usiku hakikisha kwamba unajizuru nafasi ya ugombea uraisi na unaitwangaza kwenye vyombo vya habari na wananchi wote waweze kuisikia. La sivyo, video hii tunakwenda kuiachia kwenye mitandao ya kijamii na kuituma katika mataifa makubwa duniani ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yako ikiwemo ya kunyongwa”

Mwanaume huyo alisisitiza na kumfanya mzee Poul Mkumbo kushika kichwa chake.

“Kila baada ya dakika kumi na tano nitakuwa ninakupigia kujua umefikia wapi katika maamuzi yako.”

Simu ikakatwa. Nikajishika kichwa kuonyesha kwamba nimechanganyikiwa kwa taarifa hii. Mama Biyanka akajaribu kunyanyuka kwenye sofa alilo kalia ila hata kabla hajapiga hatua moja mbele akaanguka chini na kupoteza fahamu, jambo lililo tufanya watu wote tuchanganyikiwe.

“Muite dokta”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa sauti ya juu huku akimkimbilia mke wake sehemu alipo lala. Nikatoka nje na kumuomba mlinzi mmoja aweze kuwasiliana na daktari wa hii familia kisha tukaingia ndani na walinzi kadhaa.

“Mama amkaaa”

Biyanka alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu sana. Walinzi wakasaidiana na mzee Mkumbo kumbebe mama Biyanka na kumuingiza katika chumba chake cha kulala. Mimi na Biyanka tukaingia ndani ya chumba hichi na kumkuta mzee Poul Mkumbo akimpatia mke wake dumua ya kwanza.

“Huyo daktari hajafika bwanaaa?”

Mzee Mkumbo alizungumza kwa hasira.

“Yupo njiani mkuu”

Mlinzi mmoja alijibu.

“Ohoo mama jamani”

Biyanka alilia huku akijaribu kumtingisha mama yake ila mama huyo hakuweza kuamka. Daktari akafika na moja kwa moja akaanza kumpima mama Biyanka.

“Amepoteza fahamu, ila sukari yake pia imeshuka kwa kiwango kikubwa sana. Nitamchoma sindano na nitaomba aweze kuachwa apumzike kwa masaa kadhaa.”

“Sawa daktari hakikisha kwamba unafanya kila liwezekanalo mke wangu apone umenielewa”

“Nimekuelewa muheshimiwa raisi mtarajiwa”

Matamshi hayo yakamfanya mzee Poul Mkumbo kumtazama kwa muda daktari huyo kisha akatoka humu chumbani pasipo kuzungumza kitu chochote. Nikatoka sebleni na kumuacha Biyanka ndani humu, nikamkuta mzee Poul Mkumbo sebleni akiwa ameshika simu yake, kisha akaiweka sikioni.

“Nyinyi ni ujinga gani mulio ufanya?”

“Munanigarimu sana wajinga nyinyi. Mumeniweka matatizoni, sasa ninawapa masaa mawili tu muwe muoneodoka nchini Tanzania na endapo mutabaki hapa nchini nitahakikisha nina WAUAA NGURUWE NYINYI”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa kufoka sana. Mlango ukafungulia, raisi akaingia huku akiwa ameongozana na walinzi wake pamoja na wazee wengine ambao sio mara yangu ya kwanza kuweza kuwaona.

“Unataka kuua mtu mwengine eheee?”

Raisi alizungumza huku akimtazama mzee Poul Mkumbo. Wazee hawa wakaka huku wote nyuso zao zikiwa zimejawa na huzuni iliyo changanyikana na gadhabu kubwa sana.

“Kaa hapo usitutolee macho”

Raisi alizungumza kwa hasira na kumfanya mzee Mkumbo kujishauri kwa sekunde kadhaa kisha akaka kwenye sofa alilo kuwa amelikalia hapo awali.

“Kujipendekeza kwako kwangu hadi nikaamua kukupitisha kwenye nafasi ya kugombania uraisi katika chamba changu pendwa. Haya ndio malipo yake si ndio?”

Raisi alizungumza kwa kujiamini huku walinzi wake wakiwa wameimarisha ulinzi sebleni hapa jambo ambalo si kawaida na siku zote kwani raisi akia hapa nyumbani walinzi wake wanabaki nje. Leo wanaonekana wamekuja kishari.

“Hilo ndio lililo waleta”

“Wewe Mkumbo acha jeuri. Hili ulilo lifanya likisambaa unahisi sura ya chama tutaiweka wapi?”

Mzee mwengine alizungumza kwa kufoka sana.

“Wewe mzee acha ujinga bwana. Ni watu wangapi tumewaondoa duniani. Huyu ndio awe wa ajabu sana au kwa sababu amerekodiwa?”

Mzee Poul Mkumbo naye alijibu kwa hasira kubwa sana na dhairi anaonekana kuchanganyikiwa.

“Ndio amerekodiwa eheee. Sasa hatuhitaji kuona sura ya chama inachafuliwa na mjinga mmoja. Huwezi kuua chama mtu mmoja. Ulikuja ukakikuta chama na utaondoka na utakiacha chama umeelewa?”

Mzee huyo naye alimpandishia kibesi mzee Poul Mkumbo. Nikamuona Biyanka akiwa amesimaa kwenye moja ya pembe huku machozi yakimwagika usoni mwake.

‘Samahani sana Biyanka sikuwa na jinsi mpenzi wangu. Nilikuwa ni lazima niweze kufanya hivi, ili baba yako aonje msoto wa mateso ya dhuluma aliyo ifanya kwa wazazi wangu’

Nilizungmza kimoyo moyo huku nikimtazama Biyanka kwa macho ya huruma sana.

“Ohoo kwa hiyo hii dakika ya mwisho ndio munaniona mimi sifai kwenye chama chenu”

“Ndio hufai. Kumbe tupo na jambazi, katili. Muuaji….HUTUFAI”

Mzee huyo alizidi kukoroma na kwa kumtazama tu huyu mzee ni Mkuria kwa maana ana hasira hadi anatamani kunyanyua meza hii ya kioo amshushie bwana Poul Mkumbo kichwani mwake.

“Sasa munabidi murudishe mabilioni ya pesa zangu nilizo wapatia?”

“Tulikuomba….TULIKUOMBA”

“Alafu wewe mzee acha ukum**”

Mzee Poul Mkumbo alisimama kwa jazba huku akifungua vifungo vya shati lake kwa ajili ya kuzichapa na mzee huyu aliye panda hewani na kujazia mwili wake. Mzee huyo naye akasimama kwa kuhakikisha kwamba ana kabiliana na mzee Poul Mkumbo. Wazee wezake wakamzuia, mzee Mkumbo akajaribu kuizunguka meza iliyo watengenisha na mzee huyo. Ila mlinzi mmoja wa raisi Poul Mkumbo akatoa bastola yake mfukoni na kumnyooshea mzee Poul Mkumbo usoni mwake na kumfanya atulie. Walinzi wa mzee Poul Mkumbo nao wakatoa bastola zao na kuwanyooshea walinzi hao wa raisi.

“Ooohoo Boy!!”

Nilizungumza kwa mshangao mara baada ya kuona watu wamenyoosheana silaha jambo ambalo linaweza kupelekea damu kumwagika katika eneo hili.

“Wote wekeni silaha zenu chini”

Raisi alizungumza kwa ukali sana na kuwafanya walinzi wake kuanza kuweka silaha zao chini na walinzi wa mzee Poul Mkumbo nao wakaweka silaha chini. Simu ya mezani ikaanza kuita na kuwafanya watu wote tuitazame.

“Pokea si simu ya nyumbani kwako”

Raisi alimuambia mzee Poul Mkumbo huku akimkazia macho. Mzee Mkumbo akaipokea simu hiyo na kuweka loud speaker.

“Ndio”

“Maamuzi yako yamefikia wapi mzee?”

Sauti ya mwanaume huyo ilizungumza na kuwafanya watu wote kukaa kimya na kutazmaana. Bwana Poul Mkumbo akaonekana kujawa na kigugumizi.

“Ninakupa robo saa jengine. Usipo toa maamuzi ya kujiuzuru nafasi ya kugombania uraisi. Video hii itasambaa dunia nzma.”

Simu ikakatwa na kumfanya mzee Poul Mkumbo kukata simu yake.

“Hakuna namna jamaa jiudhuru”

Raisi alizungumza huku akimtazama mzee Poul Mkumbo usoni mwake.

“Haya ndio maamuzi yenu?”

“Sio ya kwetu. Tunakuraisishia mzee, achia ngazi na makamu wako wa raisi asimame kama mgombea uraisi. Sihitaji damu ya wananchi wangu imwagike kisa wewe mpuuzi mmoja”

“Mimi sio mpuuzi. Tuheshimieane”

“Hakuna la kukushehimu hapo na kumbuka mimi bado ni raisi wa hii nchi. Nina jeshi nina nguvu na nina uwezo wa kuhakikisha kwamba unakwenda jela kwa maovu yako yote uliyo yafanya. Usione kwamba ninakuwekea wekea kivuli cha urafiki ukahisi kwamba nimesahau na makosa yako mengine ya nyuma, ikiwemo ya kujipatia mali kwa njia zisizo za halali ikiwemo ule mgodi wako. Umenielewa?”

Raisi alizungumza kwa msisitizo na kumfanya mzee Poul Mkumbo kuwa mpole sana. Swala la mgodi likanifanya kutambua kwamba huyu mzee ubaya wake haukuazia kwangu tu, nina imani kwa kupitia mimi basi nitakuwa nimelipa visasi vya wanyonge wengi sana ambao hadi leo wamekosa nguvu ya kumuangusha mzee Poul Mkumbo.

“Mzee Chacha wapigie waandishi wa habari wafike hapa nyumbani kwa Mkumbo”

“Sawa muheshimiwa”

Moyo wangu ukazi kujawa na furaha kwa maana mpango wangu nilio upanga juu ya mzee Poul Mkumbo unatimia taratibu. Ndani ya nusu saa waandishi wa habari wapatao kumi wakafika nyumbani hapa huku wakiwa na makamera yao ya kila aina.

“Baba kweli unakwenda kufanya hivyo?”

Biyanka alizungumza huku akimwagikwa na machozi. Mzee Poul Mkumbo akamtazama Biyanka kwa sura ya huruma sana huku machozi yakimlenga lenga. Waandishi wa habari wakafunga mitambo yao huku saa ya ukutani ikionyesha zimesalia dakika tano kabla ya kutimia saa nne usiku. Mzee Mkumbo akaka kwenye sofa la mtu mmoja. Raisi pamoja na viongozi wengine wote wakaka nyuma ya waandishi hawa wa bahari ili kushudia tangazo hili ambalo nina imani wananchi wengi wa chama tawala wataumia sana mioyoni mwao. Ubaya zaidi ni kwamba habari hii inaruka hewani msubashara na dunia nzima itashuhudia kinacho tokea nchini Tanzania leo



Ukimya mkubwa ukatawala ndani ya seble hii. Macho ya kila mtu yapo kwa mzee Poul Mkumbo.

“Ndugu Watanzania. Ninaimani kwamba muwazima wa afya. Nina imani taarifa hii ya jioni hii inaweza kuletea mshtuko kwenu wengi ila inabidi tuweze kukubaliana na ukweli nitakao kwenda kuuzungumza”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa sauti ya unyonge na iliyo jaa upole. Waandishi hawa wa habari ambao hawajui ni kitu gani kinacho endelea wakaanza kutazamana tazama. Nikamtazama Biyanka na kumuona jinsi anavyo endelea kulia kimya kimya.

“Majira ya usiku huu niliweza kupoteza fahamu. Nilivyo zinduka daktari wangu amethibitisha kwamba nina Saratani ya ubongo. Japo ipo kwa kiwango cha chini sana nikaona si vyema nikaendelea na upambanaji wa kugombania kitu cha uraisi.”

Waandishi wa habari baadhi wakaanza kutingisha vichwa vyao huku wakionekana kusikitishwa na ujumbe huu.

“Haya ni maamuzi yangu, sijashauriwa na mtu wala sijashinikiwa na mtu. Ila nimefanya maamuzi haya yote kwa ajili ya taifa nchi yangu na chama changu tawala. Sinto hitaji nichukue taifa, kisha baada ya siku chache niwe nina fanya mambo yasiyo eleweka. Mambo ambayo hakika yanaweza kupelekea nchi yangu pabaya. Hivyo natangaza rasmi kwamba mimi sio MGOMBEA URAISI TENA.”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Shangwe inayo endelea moyoni mwangu hakika si ya kuelekeza, japo usoni nami machozi yananichuruzika kumshuhudia baba yangu mkwe anakwenda kuiachia nafasi ambayo nina imani nilihakikisha kwamba ninamtengenezea sumu tamu inayo ua haraka kuliko anavyo fikiria.

“Hivyo nina waomba mueze kuendelea kupiga kura kwa amani na utulivu kwa maana Tanzania ni ya kwetu sote. Tunatakiwa tuijenge kwa pamoja na kwamshikamamo kama jinsi tulivyo achiwa na wazee wetu walio tutangulia. Mungu ibariki Tanzani, Mungu ibariki Afrika asanteni kwa kunisikiliza”

Mzee Poul Mkumbo mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akanyanyuka na kuondoka sebleni hapa na kuwaacha waandishi wa habari wakiwa na maswali mengi sana ambayo kwa namna moja ama nyingine yameosa makosa.

“Haya waandishi wa habari tunawashukuru. Kma kuna chochoyte kitakacho endelea basi tutawajulisha muweze kufika. Tunashukuru sana”

Mzee huyu wa Kikurya alizungumza na kuwafanya waandishi wa habari waanze kufunga funga kila kilicho chao.

“Muheshimiwa raisi unalizungumziaje hili swala?”

Muandishi mmoja alimuuliza raisi, ila walinzi wa Raisi wakamzuia muandishi wa habari huyo asizungumze jambo la aina yoyote. Waandishi wa habari wakaoka ndani humu, nikatazama eneo alilo kuwa amesimama Biyanka ila sikumuona. Nikaeleka chumbani na kumkuta akiwa amelala kitandani huku akiendelea kuia kwa uchungu sana. Nikalala tembeni yake na taratibu nikamkumbatia kwa nyuma.

“Inauma, inauma kwa nini wamfanyie baba vile jamani?”

Biyanka alilia kwa uchungu sana. Sikuwa na jinsi zaidi ya kumbembeleza taratibu huku nikihakikisha ninampa maneno ya kumfariji sana. Baada ya muda kidogo Biyanka akapitiwa na usingizi na kulala fofofo. Nikanyanyuka kitandani hapa na kutoka chumbani humu, sebleni sikukuata mtu wa aina yoyote. Nikatamani sana kuwapigia simuw apinzani ila sikuipata nafasi hiyo. Nikiwa katika hali ya mawazo mengi sana, nikamshuhudia mzee Poul Mkumbo akisimama sebleni hapa huku akiwa na kaptura pasipo shati lolote.

“Mkwe bado hujalala tu?”

“Ndio baba, nina mawazo mengi sana”

Mzee Mkumbo akachukua chupa ya wisky pamoja na glasi mbili fupi. Akaka kwenye moja ya sofa na kunimiminia kiasi kidogo cha pombe hii kisha na yeye akajimiminia na kupiga fumba moja zito hadi akatingisha kichwa kidogo kwani pombe hiyo ni kali mithili ya pombe ya Kitanzania iitwayo gongo grade one.

“Aha…duniani kuna watu ni wanafki sana. Nimeamini”

“Kwa nini baba?”

“Unaona kama hawa wazee. Yaani wamenitoa dakika za mwisho kisa chama. Yaani nina jaribu kutafuta mpango mmoja madhubuti wa kukiua chama chao ambacho nilikijenga kwa pesa yangu leo hii wananiletea mambo ya kiseng** seng**.

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa hasira iliyo changanyika na uchungu mkumbwa.

“Ila kukiharibu chama sidhani kama itaweza kuwa njia mbadala sana ya kulipiza kisasi. Tumepoteza pesa mzee, billions of shilingis, tumeziteketeza. Ni vipi tunazirudisha kwa haraka ili biashara zetu zisitetereke?”

Swali langu likamfanya mzee Poul Mkumbo kuinamisha kichwa chake chini.

“Kwasasa baba tunatakiwa kufikiria nje ya boksi”

“Kivipi Ethan mwanangu, kwa maana baba yako kichwa changu kimesha scrachi?”

“Watu ulio wapa pesa wamekufukuza kama mbwa tena kwa kukudhalilisha mbele yetu. Imeniuma sana baba, nimeumia sana, juhudi zote za usiku kucha, sijui huko kesho mtaani nitaamkaje mimi na mke wangu na kutembea. Fanya jambo mzee”

Nilizungumza huku machozi ya kinafki yakinimwagika usoni mwangu. Kwani kufanya hivi ndivyo jinsi ninavyo zidi kujaribu kumuweka mzee Mkumbo katika sehemu ambayo nikimfumua basi nina mfumua mazima na kumuacha mweupe bila mali yoyote. Mzee Mkumbo akaka kimya kwa sekunde kadhaa kisha akaivuta simu yake ya mezani. Akaanza kuminya minya batani za simu hiyo kisha mkonga wa simu hiyo akauweka pembeni huku akiminya kitufe cha loudspeaker. Simu hiyo ikaanza kuita taratibu.

“Haloo”

Niliisikia sauti ya mgombea uraisi wa chama cha upinzani.

“Ni mimi”

“Ooho nimeona kwenye televishion video yako. Hivi ni kweli au bado ninaota?”

“Ni kweli ndugu yangu”

“Ni nini sasa kilicho pelekea kujitoa kwenye mbio kirahisi hivi kwa maana nilijua tunakwenda bampa to bampa hadi dakika ya mwisho?”

“Nililazimishwa tu kuachia madaraka.”

“Ohoo nilijua tu ndugu. Pole sana”

“Pole haina haja kwa sasa. Ila nahitaji msaada wako”

“Msaada wangu mimi tena usiku huu. Nikusaidie nini?”

“Nahitaji ulinzi wa biashara zangu ila kwa sharti moja tu”

Nikaka kimya huku nikimtazama mzee Poul Mkumbo jinsi anavyo zungumza na mgombea uraisi wa chama pinzani ambaye kwa mazungumzo yao tu. Wanaonekana ni watu wanao fahamiana kwa muda mrefu ila inavyo onekana kila mmoja ana urafiki wa kimaslahi ambao anasubiria mwenzake aweze kuteleza ili yeye apate nafasi ya kumtawala mwengine.

“Nipo tayari kuwashawishi wapinzani wangu wakupigie kura usiku huu ili uchukua nchi”

“Mmmmmm….alafu?”

“Ukichukua nchi unanilinda kimali na ikiwezekana pesa ambayo nimewekeza na kukopeshwa na watu mbalimbali, inarudi mikononi mwangu ili niweze kurudi kwenye biashara zangu”

“Mmmm labda tukubaliane hivi kwa maana nisiwe mnafki, nikichukua nchi hii mtu wa kwanza kumfwatilia juu ya mali zake ni wewe.”

“Mimi?”

“Ndio ni wewe kwa maana najua hata wewe ungechukua nchi wa kwanza kunifwatilia kwenye biashara zangu ni mimi na ungenifilisi hadi chupi yangu ya ndani. Mkumbo mimi na wewe niwafanya biashara wa muda mrefu katika hii nchi na tumekuwa na vita ya kibiashara toka kipindi cha wazee wetu ambao kwa sasa wametangulia mbele za haki si ndio?”

“Nalijua hilo”

“Hivyo nahitaji mgoni wako wa madini. Kisha kuanzia hapo nitakuacha salama na huto ona hata afisa mmoja wa TRA akikujia nyumbani kwako kukuomba hata hati ya biashara yako moja”

Nikamshuhudia mzee Poul Mkumbo akikunja ngumi ya mkono wake wa kulia huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira sana.

“Halooo upo hewani”

“Nipo nina kusikia”

“Fanya hivyo la sivyo. Nitakuhamisha nchi ukiwa huna hata kijiko Mkumbo. Hahahaaaaaaa”

Mzee huyo akacheka kwa dharau.

“Tutazungumza asubuhi?”

“Ni wewe tu. Iwe asubui, mchana au usiku. Nipo tayari kuipokea ofa yako mzee mwenzangu la sivyo. Bye bye Poul Mkumbo”

Mzee Poul Mkumbo akarudisha kwa nguvu mkonga huo wa simu, huku mwili mzima akitetemeka kwa hasira.

“Huyu mwana haramu ni lazima nimue”

Macho yakanitoka huku nikimtazama mzee Poul Mkumbo kwani maamuzi haya anayo hitaji kuyachukua ni makubwa sana.

“Mzee hapo unakwenda mbali aisee”

“Hapana, anataka kuchukua mgodi wangu. Hajui nimeupataje pataje ule mgodi”

Mzee Poul Mkumbo alizungumza kwa kufoka. Akanyanyuka kwenye sofa alilo kalia na kuondoka sebleni hapa. Baada ya muda kidogo akarudi akiwa na simu yake, akaanza kuminya minya kioo cha simu hiyo kisha akaiweka sikioni.

“Washenzi hawapatikani”

Mzee Mkumbo alizungumza huku akirudia kuminya minya tena simu yake na kuirudisha sikioni mwake.

“Wapumbavu hawa wapo wapi?”

“Kina nani mzee?”

“Kuna vijana wangu ni majasusi. Wametokea nchini Kenya sasa niliwaambia warudi kwao mara baada ya kuifanya kazi ya kumua yule fala”

Nikashangaa sana kwani kama ni swala la mauaji ya mzee yule wa chama pinzani ni Roman ndio ameyafanya na si vijana wake kama anavyo dai.

“Baba mkwe kwenye hili inabidi tutumie akili”

“Akili gani?”

“Lazima tufanye jambo ambalo halito tuumiza. Kama waliweza kurubuniwa na kurekodi mauaji ya mpinzani wako. Huoni hili unalo taka kupanga kwa kuwatumia wao nalo linaweza kukupeleka jela moja kwa moja kama wakilikamilisa na kutoboa siri hiyo”

“Eti eeeehee?”

“Ndio”

“Hawa Wakenya ni washenzi sana. Nitawapandia ndege kwenda kuwasaka nchini mwano na nitahakikisha kwamba nina waangamiza kwa mkono wangu mimi mwenyewe”

‘Mzee tuliza akili yako utakuwa kichaa’

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikimtazama mzee Poul Mkumbo usoni mwake jinsi anavyo hangaika kupiga piga simu.

“Mzee acha nikatafute sehemu ya kulala. Tukiona kukiwa kumepambazuka ninaimani nitakuwa na wazo jipya. Naomba nafasi hiyo mzee wangu”

“Sawa nina kuamini genius wangu”

“Nashukuru”

Nikasimama, nikarudi chumbani na kuchukua funguo ya gari langu. Nikatoka nje na kuingia kweye gari ili na kuondoka eneo hili huku njia nizima nikiimba nyingo za ushindi kwa lugha ya Kijerumani. Nikaelekea katika mji wa Bagamoyo hadi ninafika katika mji huu imetimu saa kumi na moja alfajiri. Nikachukua chumba katika hoteli ambayo nilisha wahi kulala pamoja na Qeen na Latifa. Nikaingia bafuni huku nikiendelea kuimba kwa furaha sana, kwani kama ni usindi basi nimeupata mkubwa sana.

“Ehee Mungu nikurudishie nini sasa”

Nilizungumza huku nikichukua simu yangu kutoka kwenye mfuko wa suruali yangu. Nikampigia Qeen na Latifa na kuwaomba waweze kufika katika hoteli hii huku wakiambatana na Roman. Nikampigia mgombe uraisi wa chama cha upinzani.

“Mkuu nimekukubali aiseee”

Mzee huyu alizungumza huku akiwa na furaha kubwa sana.

“Umeona ehee?”

“Ndio asiee. Yaani huwezi amini ninachukua uraisi kiulaini kabisa. Hapa ninajiandaa na familia yangu twende tukapige kura”

“Sawa sawa, nina imani matokea yatatangazwa mapema sana kuliko kama vile ulivyo tarajia”

“Kweli kwa maana hakuna wizi tena. Miaka ya nyuma yalikuwa yakichelewa chelewa kutokana na watu walikuwa wanapenda kuchakachua”

“Ahaa sawa sawa. Vipi hujapata ofa yoyote kutoka kwa chama tawala?”

“Hapana mkuu sijapata chochote. Hakuna wakunitafuta ni lazima watulie tuli kwanza wasome upepo”

Nikastuka kidogo, kwani mzee huyu ananidanganya sasa.

“Ahaa kweli ehee?”

“Ndio ndio mkuu”

“Swala la kumfilisi huyo mtu lipo vipi?”

“Lipo pale pale. Nitaakikisha kwamba ninamuacha na chupi tu”

“Hahaaa…nashukuru. Nikutakie asubuhi njema na upigaji mzuri wa kura.”

“Nashukuru sana muheshimiwa”

Nikakata simu na kuitupia kitandani. Huku machale ya kusalitiwa na mzee huyu yakianza kunisumbua kichwani mwangu. Gafla nikamuona Ethna akiwa amekaa kwenye moja ya sofa.

“Ukiwa unakuja basi uje kwa ishara utaniua kwa presha”

“Hahaaa…umesha anza kuaptwa na presha na udogo huo?”

“Ndio kwa maana huyu mzee mimi simuelewi kabisa. Yaani ameanza kunichanganya kwa maana mimi nina hitaji mgodi wa baba yangu. Najana usiku niliyasililiza mazungumzo yake na Mkumbo inakuwaje sasa ana nisaliti.

“Ethan rafiki yangu hili ndio bara la watu weusi. Sifa moja wapo ya viongozi wao wanapenda sana pesa, kujilimbikizia mali zisizo halali, rushwa na mambo mengine mengi.”

Maneno ya Ethan yakanifanya nishushe pumzi taratibu huku mawazo yakinijaa.

“Nini tunafanya sasa rafiki yangu?”

“Kitu ulicho kifanya wewe ni sawa sawa umetupa jiwe gizani. Sasa hujui, litatua wapi, litampata nani na litakuletea faida gani.”

“Ndio nimekuelewa Ethan niambie nini tunafanya?”

“Kwenye mpira huwa munabadilisha mfumo wa uchezaji si ndio?”

“Ndio”

“Basi mfumo wa sasa inabidi ubadilike na ubaidlike kwa kukaba. Na mpira lazima uucheze upande wako?”

“Sijakuelewa kivipi?”

“Mpira lazima uurudishe kwa Mkumbo. Lazima umfanye bwana Pou; Mkumbo kuwa raisi”

Nikabaki mdomo wazi huku nikimshangaa Ethan na mbaya hakuhitaji nimuulize swali lolote kwani akapotea mbele ya macho yangu na kujikuta nikiishiwa nguvu na kukaa chini bila kupenda.



“Hapana siwezi”

Nilizungumza huku nikinyanyuka hapa chini kwani juhudi na mitego yote niliyo ifanya hadi nimefanikiwa siwezi kurudisha ushindi kwa adui yangu. Baada ya nusu saa Qeen, Latifa na Roman wakafika hotelini hapa.

“Mkurugenzi sikutarajia kama ulilo kuwa unalifikiria ndio hili lililo kwenda kujitokea kwa kweli”

Qeen alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Nashukuru. Roman nashukuru kwa kazi nzuri uliyo ifanya”

“Nashukuru nawe pia boss”

Tukaka kwenye sofa zilizomo ndani ya hichi chumba. Kichwa changu muda wote kinafikiria jambo alilo niambia Ethan, kila ninapo fikiria kuzungumza kwa watu hawa juu ya pendekezo hilo ninajikuta moyo wangu ukisita kabisa.

“Mkurugenzi mbona kama unaonekana huna furaha. Kuna jambo linalo kusumbua?”

“Hapana, ninasikilizia matokeo ya leo. Hivi huyu mgombea uraisi kwa chama cha wapinzani. Kuna mtu anafahamu historia yake?”

“Kwa nini unaulizia historia yake?”

“Unajua nimempa nguvu mtu ambaye hapo awali sikuwahi kuifwatilia historia yake. Hii yote ni kutokana na kuhitaji kumuangusha adui yangu. Hivyo naogopa nisije nikawa nimecheza pata potea”

“Ilo nalo ni neno mkurugenzi. Kwamimi kwa kweli simfahamu undani wa huyo mgombea uraisi”

Latifa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Qeen naye akadhibitisha kwamba hamfahamu mtu hoyo.

“Ngoja nilifwatilie hili swala muheshimiwa. Kama huto jali naomba uniruhusu nielekee Dar es Saalam nyumbani kwangu. Baada ya muda nitakupatia historia yake na matukio yake”

“Sawa Roman.”

Roman akanyanyuka na tukabaki sisi wenyewe. Qeen akawasha tv na tukaanza kufwatilia matikio yanayo rushwa moja kwa moja kutoka kwenye vituo vingi vya kupigia kura. Wananchi wengi sana wamejitokeza katika kupiga kura huku wananchi walio kuwa wakikiunga chama tawala wakionekana kukatishwa tamaa kutokana na kiongozi wao kujitoa katika kinyang’ranyiro cha kugombania uraisi.

“Masikini hadi wanaonea huruma”

Nilizungumza huku nikiwatazama wapigaji kura wa chama tawala ambao nyuso zao zimejawa na huzuni.

“Hao kama ni kupiga kura leo watawapigia madiwani, na wabunge wao. Kwamaana jana usiku nasikia fomo zote za kupigia kura zimebadilishwa na Mkumbo na mpinzani wake wamekatwa kwenye sehemu ya wagombea uraisi”

Latifa alizungumza huku akiwa amejawa na furaha. Baada ya masaa mawili Roman akarudi akiwa amebeba Laptop yake pamoja na faili moja.

“Mkuu tuna tatizo”

Roman alizungumza huku akinikabidhi faili hilo. Nikaanza kulifungua faili hili, nikastuka sana mara baada ya kukutana na picha ya mauaji ya kutisha na maiti hizi zikionekana kumwagiwa tindikali.

“Hawa ni kina nani?”

Nilizungumza huku mwili ukitetemeka kwani nimeuliza swali ambalo sitamani hata jibu lake jinsi litakavyo kuwa.

“Hao ni watu walio uwawa na huyu mgombe uraisi wa chama cha upinzani”

Qeen na Latifa kwa haraka wakasimama na kunifata sehemu nilipo kaa. Wakaungana nami kutazama picha hizi. Nikafungua ukurasa wa pili napo nikaona baadhi ya picha za majengo yaliyo ungua kwa moto. Nikaendelea kusonga mbele na kuona baadhi ya picha zinazo muonyesha mgombe uraisi wa chana pinzani akiwabaka vijana wawili wa kiume tena wadogo wenye umri kama wa miaka sita au saba. Jambo hili likatufanya sote midomo yetu iwe wazi kwani mtu tuliye amua kuungana naye kusema kweli hafai hata kidogo kuwa raisi wa nchi hii.

“Ohoo Mungu wangu! Jamani huyu mzee mbona katili hivi?”

Qeen alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Inabidi tumzuie kabla ya matokeo kutoka”

Nilizungumza huku mwili mzima ukinitetemeka kwa woga.

“Huyo mzee moja baba yake si mtu wa nchi hii. Aliingia nchini Tanzania mwaka 1969 akitokea nchini Rwanda. Alibadilisha urai na kuwa Mtanzani wa nchi hii na alikuwa na kijana wake huyo”

“Ina maana huyu mzee sio Mtanzania?”

“Ndio alizaliwa nchini Randwa na ameingia nchini Tanzania kiwa na mika mitano”

“Nchi haiwezi kuongozwa na Mrwanda”

“Ni kweli Mkurugenzi. Sasa tunafanyaje?”

“Inabidi tuweze kufanya jambo hapa. Japo Mkumbo ni adui yangu ila ninanibidi kuweza kufanya jambo la msingi kuhakikisha kwamba huyu Mrwanda hawezi kuichukua nchi”

Watu wote wakaka kimya huku wakionekana kufikiria wazo hili nililo lizungumza.

“Ila Mkuu tumetumia nguvu nyingi kuhakikisha kwamba Mkumbo haingii madarakani. Sasa inakuwaje tunamrudisha kiraisi namna hii?”

“Nalitambua hilo Roman, ila natambu ni jinsi gani ambayo tunaweza kuifanya. Lazima tuhakikishe kwamba naye tunambana sehemu ambayo hato weza kukurupuka. Unajua jana usiku niliwasikia Mkumbo na huyu mzee wakizungumza jinsi ya kuweza kulindana katika mali zao enendapo mzee huyu atachukua nchi. Ubaya ni kwamba huyu mzee aliomba aweze kupatiwa mgodi wa Poul Mkumbo. Leo nilizungumza na huyu Mrwanda, nikamgusia juu ya swala la mgodi ila akaonekana kukana kabisa kwamba hajazungumzia swala hilo na Mkumbo sasa hapo ndipo nilipo anza kupatwa na mashaka juu yake”

“Mmmm hilo nalo sasa ni tatizo”

“Kwenye nafasi hizo za wagombea uraisi hivi hakuna mtu gani ambaye kidogo anaonekana kuwakimbiza hawa wagombea uraisi”

“Kuna mwana mama huyu ambaye anaitwa Tasiana Ramadhan. Naye ni mgombea uraisi”

Nikatazama saa yangu ya mkononi na kukuta ni saa tano asubuhi. Vituo vya kupiga kura vinafungwa saa kumi jioni.

“Tutampatia wapi huyu mwana mama”

“Kwanini mkurugenzi?”

Latifa aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Huyu mwana mama inabidi ikiwezekana tufanye juu chini ili aweze kuwa raisi”

“Ooohoo Boy”

“Ndio hatuna jinsi. Ila ili awe raisi inabidi tuweze kuwasiliana naye na akubaline na makubaliano yetu”

“Sasa huyu yupo Moshi kwao, ndipo anapo pigia kura”

“Sawa”

“Sasa Ethan sawa tunaonana na huyu mwana mama je itakuwaje juu ya hizo kura”

“Kura kwa sasa zi zinapigwa kwa mfumo wa kielectronic basi. Roman unaweza kuhack system ya tume ya taifa ya uchaguzi kisha kura hizo zitaingia kwa huyo mwana mama”

“Nitafanya hivyo mkuu”

“Sasa Ethan wananchi je si watalalamika?”

“Hapana si wanajua chama tawala hawapigi kuru. Hivyo lazima watajua kwamba ule wingi wa watu wa chama tawala wamehamia kwa mwana mama huyo kutoka nawakubali chama cha upinzani”

“Ehee hilo nalo ni wazo ruzi”

Qeen mimi na wewe tunakwenda Moshi. Latifa na Roman hakikisheni kwamba munadili na hilo swala la ku hack system ya tume ya kupigia kura”

“Sawa muheshimwa”

Tukatoka ndani humu na kuingia kwenye magari yetu huku nikiwa nimepanda gari moja na Qeen aliye anza kazi ya kutafuta usafiri wa ndege ya kukodi. Kwabahati nzuri akafanikiwa kupata ndege moja ambayo itatupeleka hadi uwanaja wa KIA(Kilimanjaro)

“Nimepata namba ya mwana mama huyo”

“Mpigie”

“Alafu?”

“Muombe sana kwamba tunahitaji kuonana naye”

“Sawa”

Qeen akaanza kuifanya kazi hiyo ya kuwasiliana na mwana mama huyo kwa bahati nzuri akafanikiwa kumpata hewani na akapokea.

“Ndio mama yangu. Ninaitwa Qeen Jonson ni miongoni mwa watu ambao tunafwatilia siasa zako toka ulipo zianaza. Kama inawezakana mama yangu ninaomba tuweze kuoanana. Hapa nipo uwanja wa ndege jijini Dar es Saalam ninakodi ndege na kuja huko Moshi kuonana na wewe”

“Sawa karibuni mimi ndio nimetoka kupiga kura kwenye kituo changu nilicho jiandikisha”

“Ninashukuru mama yangu kwa kunikubalia”

Tukafika uwanja wa ndege na kupanda ndege ndogo ambayo kwa jinsi rubabi alivyo tuleza, itatuchukua dakika arobaini na tano hadi kufika mkoani Kilimanjaro. Ndani ya lisaa moja tukafika uwanja wa Kia. Tukakodi taksi na dereva wa taksi hiyo akatupeleka hadi nyumbani kwa mana mama huyo ambapo ulinzi wake ni mdogo na dhairi anaonekana kwamba amejaribu tu bahati yake katika kugombania uraisi ila hana matumaini kama ana weza kushindwa uraisi huo. Mwana mama huyu anaye itwa Tasiana Ramadhani akatukaribisha kwa furaha pasipo kufahamu lengo letu la sisi kuweza kuwepo hapa nyumbani kwake.

“Tunahitaji uwe raisi?”

“Mmmmm….ni ndoto wanangu. Kwa maana mimi nimejaribu tu bahati yangu na mbaya zaidi sikua na fedha nyingi za kuzunguka nchi nzima ili nipige kampeni”

“Tunalitambua hili mama. Mim ninaitwa Ethan Klopp nahisi utakuwa umeniona kwenye kampeni za mzee Mkumbo?”

“Yaa sura yako si ngeni kwangu. Imekuwaje mzee akaamua ku stap down katika kinyanganyiro hichi?”

“Kuna sababu imepelekea iwe hivyo ila hilo sio lililo tuleta hapa.”

Nikamkabidhi mwana mama huyu hili faili lenye siri za mgombe uraisi wa chama pinzani ambacho kwa sasa nina imani kwamba mioyo yao wana amini kwa asilimia mia moja lazima waichukue nchi”

“Ohoo Mungu wangu ni nini hichi tena?”

“Huyo ndio raisi ambaye watu wengi wana mtazamia kwenda kuichukua nchi”

“Alafu si Mtazania kwa kuzaliwa?”

“Ndio mama. Hadi kufika hapa kwako tumeaandaa mfumo mzuri wa kukuingiza wewe madarakani ila kwa sharti moja muhimu”

“Sharti gani wanangu?”

“Tunahitaji unahikikishe kwamba Poul Mkumbo na huyu Mrwanda unawafilisi mali zao zote na wanaishia gerezana na ikiwezekana wote wanafia gerezani. Umenielewa mama?”

Ma Tasiana akanitazama usoni mwangu huku akijawa na tabasamu linalo onyesha dhairi kwamba amekubaliana na ombi langu nililo muomba.


“Nimekuelewa kijana your so smart?”

“Nashukuru mama. Ila kuna jambo nahitaji tuweze kufanya hivi sasa hivi”

“Jambo gani Ethan”

“Ninakupa nguvu ya kutawala hii nchi na wewe unanipa kile ninacho kihitaji au kile ninacho kuambia kufanya”

“Huoni kama utakuwa unaniingiza majaribuni katika uongozi wangu?”

“Sikuuingizi majaribuni. Katika mataifa yote makubwa dunia, raisi akiingia madarakani si kama anaingia yeye kama yeye ila kuna watu nyuma yake huwa wana muunga mkono na watu hao pia wanakuwa na nguvu kwenye maamuzi yake katika kuongoza nchi. Hivyo ndivyo inavyo kuwa je unahitaji uraisi au auhitaji uraisi?”

Bi Tasiana Ramadhani akaka kimya kwa sekunde kadha huku akitazama faili hili lenye madhambi ya mgombea uraisi wa chama pinzani.

“Nauhitaji, ili niweze kushuhulika na watu wenye dhambi kama hawa”

“Sawa. Mimi na wewe tunatakiwa kuwa kitu kimoja hivi sasa. Tuingie mkataba wa makubaliano hayo”

“Sawa mimi nipo tayari. Bahati nzuri mwanangu ni mwanasheria hivyo ngoja nimuite ili tuweze kuingia makubaliano”

“Sawa mama”

Bi Tasiana akasimama na kuondoka sebleni hapa. Baada ya dakika kama tano akarudi akiwa ameongozana na msichana mmoja mrefu na mzuri. Shepu yake hakika imenifanya mdomo wangu kuwa wazi, bumbuwazi halikuacha kunishika kwa kumshangaa msichana huyu. Nikajistukia mara baada ya Qeen kunigonga begani mwangu.

“Bwana Ethan huyu ni mwanangu wa pili na wa mwisho anaitwa Hawa. Ukiachilia kwamba ni mwanangu pia ni mwanasheria wangu”

“Ohoo nashukuru kukufahamu Hawa”

“Nawe pia ninashukuru kukufahamu Ethan.”

Tukapeana mikono na Hawa kisha akakaa pembeni ya mama yake. Bi Tasiana akamuelezea mwanaye kwa ufupi adhima ya sisi kuwepo hapa. Hawa akatutazama kwa umakini sana.

“Ila sijajua ni njia gani ambazo munaweza kuzitumia kuweza kumuingiza mama yangu madaraka ikiwa hivi sasa watu wapo kwenye vitua vya kupiga kura.

“Kuhusiana na njia ambayo sisi tunaweza kuzitumia kumuingiza mama yako madarakani tunazifahamu sisi. Kikubwa ni makubaliano madogo tu ambayo ninahitaji kutoka kwa mama yako”

Nilimjibu Hawa huku nikimtazama usoni mwake. Kusema kweli Hawa ana uzuri kupita karibia wanawake wote nilio wahi kuwoana kwenye maisha yangu.

“Unahitaji kuwa na kauli kwa mama yangu pale anapo ingia madarakani?”

“Sio kuwa na kauli. Ila ninahitaji aweze kufanyia kazi kwa yale ambayo nitayahitaji moja wapo likiwepo la kuwashuhudikia mafisadi wote ndani ya nchi hii”

Hawa akayazungusha macho yake makubwa kiasi na kunifanya nijawe na msisimko mkali wa kimahaba ambao sifahamu ni kwa nini umenitawala kwa haraka namna hii.

“Nina imani kwamba huto muingiza mama yangu katika wakati mgumu kipindi cha uongozi wake?”

“Asilimia mia moja. Kila kitu atakacho kuwa anakifanya kitakuwa ndani ya uwezo wake namamlaka yake kama raisi”

“Sawa mama hili ni dili zuri.”

“Basi andaa mkataba”

“Utasaidiana na msaidizi wangu hapa Qeen”

“Sawa, Qeen twende ofisini”

Qeen na Hawa wakanyanyuka na kuondoka eneo hili.

“Mama samahani kwa hili swali maana ni nje ya topic iliyo tuleta hapa”

“Uliza tu”

“Hawa ameolewa?”

“Hahaa hapana ila ndio amemaliza masomo yake last year nchini Marekani”

“Ahaa yupo very smart”

“Yaa ninajivunia yeye. Mwanangu wa kwanza yeye yupo nchini Dubai ameolewa kule”

“Ahaa kumbe ni wakike wote?”

“Yaa wote ni watoto wa kike. Baba yao alifariki miaka mingi ya nyuma kipindi bado wapo O level, ila nashukuru Mungu alituachia mali hivyo sikupata shida sana katika kuwakuza hawa watoto”

“Sawa sawa”

“Ila nawe unaonekana ni mdogo sana. Una umri gani?”

“Miaka ishiri na moja”

“Waoooo…!! Ni mdogo sana na idea unazo kuna nazo hakika ni kubwa sana. Unawezaje wezaje kufanya mambo hayo?”

“Nilizaliwa Moshi”

“Moshi hapa hapa?”

“Yaa na mimi ni mchaga”

“Shimboni shafoo mbee?”

Nikabaki nikitabasamu huku nikimtazama bi Tasiana kwa maana sijamuelewa kitu alicho kizungumza.

“Wewe ni mchaga gani hujui hata salamu jamani”

“Hapana mama, kidogo historia ya maisha yangu ni ndefu na toka nipo mdogo nilikulia nchini Ujerumani hadi nimekuwa hivi mtu mzima”

“Weee basi hapo sawa. Karibu ukae nami hapa nikufundishe fundishe kichaga”

“Hahaa usijali mama yangu”

Qeen na Hawa wakafika sebleni hapa. Wakatukabidhi mikataba hii, tukaisoma, tulipo kubaliana tukatia saini huku Qeen na Latifa wakiwa kama mashahidi kwa kila upande. Tukaagana na mwanamama huyu kisha tukarudi uwanja wa ndege wa Kia na kuianza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam.

”Ethan leo umeniudhi”

Qeen alizungumza huku akitazama dirishani jinsi ndege hii inavyo endelea kukata mawingu.

“Nimekuudhi na nini?”

“Jinsi ulivyo kuwa unamtazama yule dada. Ina maana umempenda au?”

Nikajikuta nikitabasamu kwa maana hii ongea ya Qeen inadhihirisha kwamba kwamba ana wivu moyoni mwake.

“Kumtazama mtu tu ndio kumekukasirisha?”

“Ndio, umenishusha thamani kama vile uliye kwenda naye pale sina maana yoyote mbele yako”

“Mmmmm!!”

“Sio mmmm wewe hujui tu jinsi ninavyo jisikia moyoni mwangu”

“Unajisikiaje?”

“Ninakupenda Ethan, sema ndio hivyo sina uwezo wa kuwa na wewe”

Qeen alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Hapa ndipo nikaaza kufahamu udhaifu katika kikosi changu. Udhaifu huu nisipo kuwa nao makini unaweza kuharibu kila kitu nilicho kifanya kwa mzee Poul Mkumbo.

“Mimi ni mwanamke, nina hisia nina moyo wa nyama wala si moyo wa chuma. Kukuona hivi karibu tu huwa nina jawa na furaha. Sasa wewe unavyo onyesha hisia zako kwa mwanamke mwengine haki ya Mungu nina umia. Najua utanifikiria vibaya ila huo ndio ukweli Ethan”

Qeen alizungumza huku akiachia kilio, taratibu nikamlasogeza karibu yangu na kukilaza kichwa chake begani mwangu.

“Nakuomba uwe mvumilivu sawa”

“Sio mvumilivu Ethan. Ninavumilia ila ninashindwa, kama utanifikiria vibaya wewe nifikirie ukweli ndio huo na ubaya umesha nionjesha penzi lako na si mara moja”

Ikabidi nikae kimya tu kwa ni kosa ambali nililo lifanya kwenye hichi kikosi changu ni kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Qeen pamoja na Latifa japo hapo kwa mara ya kwanza niliyachukulia kama utani ila wezangu wamemaanisha. Tukafika katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Tukashuka kwenye ndege hii na kuingia kwenye gari na kuiza safari ya kuelekea nyumbani kwa Roman.

Tukafika nyumbani kwa Roman na kuwakuta wa Latifa wakiendelea na kazi ya kuchakachua matokeao.

“Muna kura ngapi hadi sasa?”

“Milioni kumi na tano ambazo ukitupa ruhusu ya kuzihamisha sehemu unayo ihitaji tunaweza kufanya hivyo”

“Sawa zihamishieni kwa mama Tasiana Ramadhani, ila zihamisheni kwa awamu ili kusiwe na utata wa aina yoyote”

“Sawa mkuu”

“Mimi ngoja nieleke nyumbani kwa mzee”

“Poa”

Qeen hakuhitaji hata kunisemesha zaidi ya kunitazama kwa macho makali jambo ambalo likamshangaza hata Latifa ambaye muda wote amezoea kutuona tukiwa katika hali ya furaha. Nikafungua mlango na kutoka ndani humu, kabla sijaingia kwenye gari langu Latifa akaniwahi.

“Vipi mkurugenzi mbona kama pacha wangu amenunua. Kwema huko mulipo toka?”

“Kwema na kuna ushindi mkubwa kwetu. Ila kuna jambo ambalo rafiki yako kwa namna moja halijampendeza”

“Jambo gani?”

“Kuna binti wa mwana mama huyo Tasiana nilimtazama kwa macho ya matamanio sasa hilo ndio lililo muudhi na anadai kwamba ana nipenda”

“Mtoto huyu ameanza using** ehee. Hajui kwamba sisi na wewe ni mtu na wafakazi wake.”

“Siwezi kumlaumu kwa maana najua kosa ni la kwangu. Kama tusinge kuwa tumefanya chochote kitandani basi isinge fikia huku”

“Hata kama, mimi mbona umenitomb** ila sina hata mshipa wa kukupenda kimapenzi. Ngoja nikaongee naye aache useng** wake”

“Poa tutawasiliana zoezi likiwa linaendelea”

Nikaingia kwenye gari langu, Latifa akanifungulia geti na kutoka ndani humu. Nikiwa njiani nikalitazama faili hili la mgombea uraisi wa chama pinzani. Gafla Ethan akaka siti ya pembeni.

“Fuc** umenistua bwana”

“Haa.Uluhitaji nikupigie simu. Nimependa wazo lako umejiongeza vizuri sana”

Nikamtazama Ethan kisha nikatabasamu.

“Ila kuna jambo jengine”

“Jambo gani?”

“Huyo mwana mama hato kuwa na maisha marefu ya uongozi wake”

“Mmmmm!!”

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG