Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

POWER SEHEMU YA 4/10

 

 


 POWER

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 4 KATI YA 10

 


Afande Kimaro alizungumza huku akiendelea kutazama majeraha ya Clara mgongoni ambayo kwa namna moja ama nyingine pia yalimshangaza afande Mwanaidi. Tukatoka ofisini humu, askari wakaingai kwenye gari lapo pamoja na mkuu wao nasi tukaingia kwenye gari tulilo jia na walinzi wa kampuni yangu kisha tukaanza safari ya kueleka nyumbani kwa baba mdogo wa Clara huku gari letu likiwa limetangulia mbele. Kutokana na foleni za hapa na pale ikatuchukua lisaa zima kufika katika nyumba moja kubwa ya kifahari ambayo ina gorofa moja kwa juu. Tukashuka kwenye magari, mkuu wa polisi kanda maalumu, akatembea hadi getini, akagonda kwa muda kidogo na mlango ukafunguliwa na mlinzi wa nyumba hiyo.

“Bosi wako tumemkuta?”

“Nd…ioo…o”

Mlinzi alijibu kwa kigugumizi, mkuu wa polisi akaanza kuingia na askari wengien wakimfwatia kwa nyuma akiwemo askari anaye mlinda. Nami nikaingia ndani ya nyumba hii huku tukiwa nimeshika mkono Clara. Akatoka msichana mmoja mweupe kiasi huku akiwa amevalia kijisketi kifupi.

“Kuna nini kinacho endelea?”

Clara akajificha nyuma yangu mara ya msichana huyo kutazamana nasi.

“Huyo ndio ma mdogo”

“Mpigeni pingu huyo kwanza, na mume wako yupo wapi?”

“Jamani kuna nini, munanikamataje nikiwa sina kosa jamani”

Maneno ya msichana huyu hayakuwazuia askari hawa kumpiga pingu mikononi mwake. Akatoka kijana kwa kukadiria ana umri wa miaka kama thelathini hivi.

“Baby nini kinacho endelea?”

Alizungumza kwa sauti ya mapozi, Clara huku machozi yakimwagika usoni mwake, akanyoosha mkono kwa mwanaume huyu.

“Ndio baba mdogo?”

Nilimuuliza Clara huku nikimtazama usoni mwake, Clara akanijibu kwa kutingisha kichwa kwamba ndio huyo baba yake mdogo. Askari wakamkamata kijana huyu naye akapigwa pingu, askari wakawaingiza nani ya nyumba hii nasi tukaingia, hatukuamini macho yetu kukuta pakti kadhaa za madawa ya kulevya zikiwa mezani eneo la hapa sebleni, huku misokoto ya bangi na pombe kali nazo zikiwa juu ya meza hii.

“Washenzi kabisa, kagueni nyumba nzima”

Mkuu wa kituo kanda maalumu alizungumza na askari walianza kutawanyika huku wengine wakipandisha gorofani wakiwa na bunduki zao. Clara akakimbilia moja picha iliyopo pembezoni mwa meza ya tv kubwa. Akaikumbatia picha hiyo huku akiendelea kulia kwa uchungu sana, nikamsogelea na kuitazama picha hiyo na kukuta, akiwa yeye pamoja na wazazi wake baba na mama.

“Mkuu tumekuta begi hili, lina pesa za kigeni”

Askari mmoja alizungumza huku akiwa anashuka kwenye ngazi na kuelekea gorofani. Begi kubwa kiasi la mgoni likawekwa mbele ya mkuu wa polisi. Pesa za kigeni, dola za kimarekani zimejaa katika begi hili.

“Pumbavu hawa ni wauzaji wa madawa ya kulevya. Clara unafahamu juu ya hilo swala?”

Mkuu wa polisi alimuuliza Clara. Clara akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ana fahamu.

“Ohoo Mungu wangu. Pigeni picha vidhibitisho vyote kisha hakikisheni kwamba hawa waalimu wanafika kituoni”

“Sawa mkuu”

“Wewe mtoto wewe mtoto hujakomaa eheee?”

Baba mdogo wa Clara alizungumza huku akimtazama Clara kwa hasira sana. Askari mmoja akamzaba kofi zito la usoni.

“Kaa kimya, washenzi nyinyi”

“Nikitoka Clara nakata shingo yako hiyo, nakuapia haki ya Mungu nakata shingo yako”

“Twende bwana”

Baba mdogo wa Clara alisindikizwa na mateke ya askari walio wakamata. Wakapakizwa kwenye gari la polisi huku sisi tukibaki na mkuu wao pamoja na mlinzi wake.

“Hawa watu ni washenzi sana, kumbe chanzo cha kummpa mateso huyu binti ni kutokana na hii biashara yao”

“Hata mimi nahisi hivyo mkuu”

“Tunashukuru sana Ethan na hawa tunakwenda kuwabana na kuhakikisha kwamba wanatueleza juu ya wasambazaji wezao wa madawa ya kulevya”

“Sawa sawa mkuu nitashukuru sana kama mukilichukulia hatua jambo hili na kama inawezakana wakapolelee kabisa jela, kwa maana kama mulivyo msikia baba mdogo, anakiri kwamba lazima atamuua huyu binti, sasa hiyo ni hali ya kumtishia”

“Kweli, ila nitahakikisha kwamba sheria inafwata mkondo wake”

“Nashukuru, huyu binti mimi ngoja nimpeleke sehemu hivi akafanyie matibabu na usafi wa mwili wake, nitajitahidi kumuwekea wana sheria wenye uwezo mkubwa, kuhakikisha kwamba wanasimamia kesi yake na mali za wazazi wake zinarudi mikononi mwake.”

“Sawa sawa Ethan, laiti kama Tanzania tungekuwa na vijana kumi kama wewe, wenye mioyo kama yako nina imani kwamba nchi hii isinge kuwa na omba omba wengi hivi”

“Nashukuru sana mkuu”

Polisi wengine wakafika katika eneo hili, tukaaga na nikaondoka na Clara, tukiwa njiani ndani ya gari nikampigia simu Biyanka na kumueleza kila jambo lililo tokea, Biyanka akashangazwa sana na akaniomba nimpeleke Clara nyumbani kwake akapatie huduma na msichana wake wa kazi.

“Ngoja kwanza nimpeleke hospitalii, akifanyiwa huduma zote za kiafya ndio aelekee nyumbani”

“Sawa mume wangu, naona nitachelewa kurudi, si unajua mambo ya siasa haya”

“Usijali mpenzi wangu”

“Sawa baadae”

Nikakata simu na kuelekea hospitali. Nikalipa matibabu ya Ckara yoye na madaktari wakanishauri waweze kumpumzishwa kwa siku ya leo kwa maana wanahitaji kumuongezea maji mwilini pamoja na damu kwani afya yake ime dhohofika sana. Nikakubaliana na madaktari hawa huku nikiahidi kwamba nitarudi siku inayo fwata ili nimjulie hali kisha nikaanza safari ya kuelekea hotelini kujipumzisha.

***

Asubuhi na mapema nikaelekea hospitalini na kukuta hali ya Clara ikiendelea vizuri sana.

“Naamini akikaa hapa kwa siku ya leo, kesho basi tunaweza kumruhusu”

Daktari niliye muaachia jukumu la kumtazama alizungumza huku tukiwa tumesimama pembezoni mwa kitanda cha Clara.

“Je vipimo vingine vipo vizuri”

“Ndio, ila ana Malaria pamoja na UTI ila magonjwa yote hayo tumesha anza kumpatia dozi kwa kumchoma sindao na kesho atamalizia sindano hizo”

“Clara unajisikiaje?”

“Safi tu Ethan, nashukuru kwa msaada wako”

Clara alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Ohoo usilie mtoto mzuri, ni jukumu langu kuhakikisha kwamba unakuwa salama, sawa”

“Sawa”

Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni Biyanka ndio anaye nipigia. Nikatoka nje ya chumba hichi ili niweze kuzungumza naye.

“Umeamkaje mume wangu”

“Salama, vipi wewe”

“Safi upo hoteli au?”

“Hapana nipo hospitalini hivi sasa, nimekuja kumtazama mtoto”

“Ohoo anaendeleaje?”

“Yupo vizuri”

“Sawa, ila samahani mume wangu, leo hatuto weza onana kwa sababu, tutatakiwa kwenda Mwanza na mama kuna wanawake wengine anakwenda kuonana nao hivyo tunaweza kurudi usiku na ndege au tukarudi kesho asubuhi.”

“Ohoo sawa, ila kuwa makini”

“Usijali mume wangu, nipo makini sana katika kila hatua ya maisha ninayo ipiga”

“Sawa mimi nitashinda hapa na huyu binti kisha nitakwenda kazini mara moja. Tutawasiliana”

“Sawa mume wangu, nakupenda sana”

“Ninakupenda pia mke wangu”

Biyanka akakata simu na nikairudisha mfukoni mwangu, nikarudi chumbani humu na kujikuta nikiwa nimejawa na mshaongo kwa maana dokta nimemkuta akiwa amelala chini huku damu nyingi zikiwa zinamwagika shingoni mwake na Clara akiwa hayumo ndani ya chumba hichi huku dirisha moja la chumba hichi likiwa lipo wazi jambo lililo nipa ishara kwamba kuna jambo la hatari lililo tokea katika eneo hili.



Nikatoka chumbani humu kwa haraka na kuwaita madaktari wawili waliopo kwenye kordo. Nikaingia nao ndani ya chumba hichi na wakastuka sana kumkuta mwezao akiwa yupo chini katika hali mbaya sana.

“Nini kimetokea?”

“Mimi pia sifahamu ila kuna watu wamefanya hivi na wamamteka mgonjwa wangu”

Nilizungumza huku nikitazama dirisha la chumba hichi lililo achwa wazi, kwa haraka nikaruka dirishani humu na kuanza kukimbia huku nikiangaza macho yangu huku na huku ili niweze kumuona Clara ni wapi alipo pelekwa. Nikawaona wanaume wawili wakiingia kwenye gari ndogo aina ya Toyota Alteza huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi. Nikakimbilia eneo la maegesho ya magari na kuingia kwenye gari langu, nikaliwasha na kuanza kufukuzia gari hii ndogo huku nikiamini moja kwa moja watu hawa ndio walio mteka Clara na ndio watu ambao wamefanya shambulizi kwa daktari. Uwezo wa gari yangu BMW X6 ni mkubwa kuliko hata Toyota Alteza, haikuwa kazi ngumu kwangu kuweza kuwakaribia. Ila nikajikuta nikifunga breki za gafla mara baada ya jama mmoja kujichomoza ndani ya gari hili huku akiwa amekaa siti ya nyuma na akaanza kunishambulia kwa risasi ambazo cha kumshukuru Mungu kioo cha mbele cha gari langu hakiingizi risasi kirahisi.

“Fuc***”

Nilizungumza huku nikianza kuendelea kulifukuzia gari hili pasipo kukata tamaa. Baada ya kutambua ubora wa gari yangu katika kuingiza risasi nikazidi kuongeza mwendo kasi hadi nikaanza kuligonga gari la watekaji hawa kwa nyuma. Kila jinsi nilivyo ligonga gari la watekaji hawa ndivyo jinsi nilivyo zidi kuwayumbisha na kwa mara kadhaa walijikuta wakitoka nje ya barabara. Nikaanza kusikia ving’ora vya gari za polisi vikitufwata kwa nyuma, hapa ndipo nikapata matumaini kwani sina silaha yoyote ambayo ningeweza kupambana na hawa watekaji. Nikaongeza mwendo, kisha nikaligonga gari hili kwa pembeni na kumfanya dereva kupoteza muelekeo wa gari lake na likaanza kuzunguka na kuyumba na mwishowe likaparamia moja ya nguzo za taa za barabarani na kutulia kimya. Ndani ya sekunde kadhaa askari wakafika katika eneo hili huku wakituamrisha watu wote kushuka kwenye gari huku mikono yetu ikiwa juu. Nikatii amri, nikashuka kwenye gari huku mikono yangu ikiwa ipo hewani. Mtekaji mmoja akajifanya anahitaji kuwashambulia askari ila akawahiwa kwa kupigwa risasi nne za kifuani na kufa hapo hapo.

“Wamemteka rafiki yangu, yumo ndani ya gari hilo”

Nilizungumza kwa kujiamini huku nikiwatazama askari hawa wanao nipapasa mwili wangu ili waweze kufahamu kama nina silaha au laa.

“Sina chochote”

Nilimuambia askari huyu mara baada ya kumuona akinipapasa sana pasipo mafanikio ya aina yoyote.

“Kuna binti mdogo ndani ya hilo gari mtoeni bwana”

Askari wawili wakalisogelea gari hilo kwa umakini wa hali ya juu, wakafungua mlango wa sti ya nyuma kama vile nilivyo waeleza ndivyo jisni walivyo mkuta Clara akiwa amelazwa kwenye siti.

“Nahitaji kumuona huyo binti”

“Wewe ni nani yake?”

“Mimi ni kaka yake”

Ilinibidi kuongopea ndipo polisi walipo niruhusu kushusha mikono yangu chini. Wakamtoa Clara kwenye gari hilo, kitu kilocho niogopesha ni ukimya wa Clara, hatikisiki wala hapumui.

”Ohoo Mungu wangu inabidi tumuwahishe hospitalini”

Gari kadhaa za polisi nazo zikafika katika eneo hili, nikamuona mkuu wa polisi kanda maalumu bwana Kimaro naye akishuka kwenye moja ya gari. Moja kwa moja akafika hadi sehemu nilipo simama, hakuamini kumuoana Clara akiwa eneo hili akipatiwa huduma ya kwanza na maaskari hawa.

“Ethan nini tena kimetokea?”

“Walimteka hospitalini, nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba nina mkomboa na kweli Mungu amesaidia tumempata”

“Ohoo Mungu wangu. Afande vipi hali yake?”

“Mapigo yake ya moyo yanadunda vizuri, wamemchoma sindano ya usingizi”

“Muingizeni ndani ya gari na mumpeleke hospitali na ulinzi mkali sana uimarishwe”

“Sawa mkuu”

“Na kule hospitalini wamfanya shambulio la daktari aliye kuwa akimuhudumia Clara”

“Hali yake vipi?”

“Wakimuahi wezake atapona ila wakichelewa basi anaweza kupoteza maisha”

“Mmmm….hapa kuna mtandao mkubwa sana Ethan, nawe ingia kwenye gari tuelekee hospitalini”

“Sawa, hii gari yangu siwezi kutembea nayo, tazama ilivyo pondeka pondeka”

“Nitaagiza askari walichukue na kulipeleka kituoni, kuna maelezo utatoa kisha nitakuelekeza ni gereji gani nzuri hapa jijini Dar es Salaam unaweza kuitumia kwa kulitengeneza gari lako”

“Nashukuru mzee”

Tukaingia kwenye gari la mkuu huyo wa polisi kanda maalumu na kuondoka eneo hili. Tukafika hospitali nyingine niliyo fanikiwa kusoma bango lake lililo andikwa Agakhan Hospital. Clara akawahishwa kwenye chumba cha matibabu, mimi na mkuu huyu wa polisi tukabaki nje ili kusubiria majibu ya madaktari. Baada ya dakika kama ishirini hivi, daktari mwana mama mwenye asili ya kihindi akatoka katika chumba alicho ingizwa Clara, akatusalimia huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.

“Hali ya mgonjwa inaendelea vizuri, sindano aliyo chomwa kidogo haito kuwa na madhara makubwa sana zaidi ya kulala kwa masaa kadhaa”

“Tunashukuru sana daktari ila kule tulipo toka niliambia kwamba ana Malaria pamoja na UTI, na vyoye alisha anzishiwa dozi”

“Hili nimelizingatia pia, usiwe na shaka kila jambo litakwenda sasa sawa na mpango unao hitaji kijana”

“Nashukuru sana daktari. Je anatarajia kuamka baada ya muda gani?”

“Masaa matano au sita kutoka hivi sasa”

“Sawa, nitaacha vijana wangu wawili hapa watamlinda binti huyo. Ninakuomba muweze kuwapatia ushirikiano mkubwa kwa maana huyo binti hadi tumemleta hapa alitekwa kwenye hospitali iliyo pia na binti huyo ni muhimu sana kuweza kuakamata wahalifu ambao tunawatafuta ndio maana wanajitahidi kumteka teka sawa daktari”

“Usijali kamanda, nikuhakikishie mgonjwa wako atakuwa salama hadi pale utakapo rejea”

“Sawa, ila sura hizi mbili, mimi na huyu bwana mdogo hapa ndio watu wa pekee ambao turuhusiwe kuingia ndani ya wodi hiyo, isije akatoke mti mwengine kutoka wasipo eleweka aseme amekuja kumuangalia mgonjwa musimrihusu sawa”

“Nimekuelewa kamanda na nitagakikisha hilo linazingatiwa na mimi nitajitahidi kwamba niwe ni daktari ambaye nitamuhudumia hadi hili jambo litakapo kwisha”

“Nashukuru sana. Ethan tueleke kituoni”

“Sawa”

Tukaondoka eneo hili la hospitali na tukaianza safari ya kuelekea kituo kikuu cha polisi. Tukafika katika eneo hilo na nikaikuta gari yangu ikiwa imeegeshwa kwenye mageesho ya magari yaloyo kamatwa na askari. Tukapitiliza moja kwa moja hadi ofisi kwa mkuu huyu.

“Kesi ya huyu msichana tumeanza kuifanyia uchunguzi. Pale mwanzo tuliitazama kwa macho ya kawaida na tukahisi kwamba ni ndogo, ila ni kesi kubwa sana ambayo imehusisha baadhi ya mabosi wangu, yaani hapa muda wowote na saa yoyote basi naweza kupigiwa simu ya kuwaachia wale watuhumiwa”

Bwana Kimaro alizungumza kwa suati ya upole na iliyo kata tamaa kabisa.

“Imekuwaje kubwa kiasi hicho?”

“Yaani…ila bado tupo kwenye upelelezi, ila ninacho taka kukuambia tu kama kijana wangu kuwa makini, kwa maana sasa umesha anza kuonekana kuwa kikwazo kwao tena kwa jambo hili la leo ni lazima watakuwa wanakuwinda.”

“Nchi hii inaongozwa vipi mkuu?”

“Mwanangu nchi hii wewe ione kwa nje, ila ukifukunua mambo ya ndani unaweza ukalipuka. Ila siwezi kukuambia mambo mengi sana kwa maana mambo mengine ni ya kipolisi. Ila nimekupa tahadhari kuwa makini”

“Usijali nipo makini mkuu”

“Sawa, nitakupa kijana wangu mmoja, atakupeleka kwenye gereji moja ya Wahindi ni wataalamu sana wa kutengeneza hayo magari yenu ya kifahari”

Bwana Kimaro alizungumza huku akinyanyua mkonga wa simu iliyo mezani kwake na kuminya batani kadhaa kisha akaweka mkonga huo sikioni mwake.

“Njoo ofisini kwangu”

Bwana Kimaro baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akaurudisha mkonga huu wa simu sehemu alipo utoa. Akaingia askari mmoja marefu na mweusi sana.

“Afande Nyasesa, huyu ni Ethan. Ethan huyo ni afanye Nyasesa”

“Nashukuru kukufahamu”

Afande Nyasesa alizungumza huku akinikabidhi mkono wake wa kulia. Tukapeana mikono huku akinitazama usoni mwangu.

“Mpeleke Ethan kwenye ile gereji ya Wahindi niliyo peleka ile V8”

“Sawa mkuu

“Ethan kumbuka nilicho kueleza mwanangu.”

“Nitayafanyia kazi, alafu sijapata namba yako ya simu”

“Ohoo lete simu yako nikuandikie”

Tukapeana namba zetu za simu na mkuu huyu wa polisi. Tukatoka nje na kuingia kwenye gari langu na taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili. Afande Nyasesa akanielekeza hadi ilipo gereji hiyo, tukapokelewa na mzee mmoja wa kihindi. Alipo muona afanye Nyasesa akasalimiana naye kwa furaha sana.

“Aisee muna shida sana nyinyi watu”

Mzee huyu wa Kihindi alizungumza huku akitazama gari langu jinsi lilivyo shambuliwa kwa risasi.

“Hiyo ndio maana ya kuwa askari mzee”

“Kweli ehee nawasikiliza”

“Ethna mzee huyu anaitwa Barachuna”

“Nashukuru, mzee nahitaji gari langu lirudi kwenye upya ni kiasi gani na itachukua muda gani?”

“Ahaa……!!! Itagarimu kama milioni kumi na mbili hivi na itagarimu siku tatu”

“Sawa ninaweza kulipia hivi sasa?”

“Ndio hakuna tatizo katika hilo”

Mzee Barachuna akaniingiza ofisini kwake, nikamuhamishia pesa kutoka kwenye benki akaunti yangu na kuingia kwenye akauti yake ya benki.

“Unaitwa Ethan nani?”

Mzee Barachuna aliniuliza huku akiandika risiti ya malipo niliyo yafanya.

“Klopp”

Nilijibu huku nikitazama tazama baadhi ya magari mapya yaliyomo katika jengo hili.

“Hizi gari mpya zinauzwa?”

“Ndio zipo zinazo uzwa na zipo zinazo kodishwa”

“Nahitaji ya kuuzwa kabisa, ila mpya”

“Gari gani?”

“Rang Rover Voge au Sport”

“Umepata kijana”

Mzee huyu alizungumza huku akitabsamu. Tukatoka ofisi kwake na kuzunguka eneo la nyuma la jengo hili, nikakuta magari mengi ya kifahari yakiwa yamewekwa katika eneo moja zuri. Nikatazama magari yote na nikapenda Range Rover moja yenye rangi nyeusi.

“Ile pale ni milioni ngapi?”

“Ni dola laki mbili na hamsini, ila kutokana umekuwa mteja wetu basi tutakupa punguzo kidogo hadi dola laki mbili na ishirini”

“Nahitaji nilikague gari kwanza”

Mzee Barachuna akakubali niweze kuingia ndani ya gari hili, kusema kweli nimelipenda hili gari.

“Pia unaweza kulijaribu”

“Hapana, nitalijaribia barabarani. Malipo nitayafanya kwa nje ile ile”

“Hakuna tatizo”

Nikafanya malipo kwa njia ya kuhamisha kiasi hicho cha pesa kuingia katika akaunti ya bwana Barachuna. Bwana Barachuna alipo pewa ripoti na benki kwamba kiasi hicho kimeingia, akanikabidhi funguo, kadi ya gari, tukaandikishiana kila kitu kinacho takiwa kufanyika katika manunuzi ya magari. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kukuta namba ngeni kidogo, nikajifikria kwa muda kidogo kisha niaipokea.

“Haloo mkurugenzi”

Niliisikia sauti ya kike ambayo moja kwa moja iliweza kunikumbusha wasicha ambao nilipatia kadi yangu ya biasha na niliweka ahadi nao ya kukutana leo.

“Ndio habari”

“Salama naamini umenikumbuka”

“Yaa si wale tulio kutana jana kwenye kordo?”

“Ndio mkurugenzi, mupo wapi?”

“Tupo Mwenge ndio tumetoka saluni, tumesha jiandaa”

“Barachuna mwenge ni wapi?”

Nilimuuliza mzee huyu huku nikiwa nimeizima simu yangu ili wasiweze kunisikia.

“Ukitoka nyoosha barabara hii moja kwa moja hadi utakapo kutana na taa za barabarani basi hapo ndio Mwenge”

“Nashukuru”

Nikaingia ndani ya gari langu mara baada ya kumaliza kufungwa plate namba, nikaagana na bwana Barachuna na nikainza safari ya kuelekea Mwenge huku nikiwa na gari langu jipya kabisa ambalo tayari limesajiliwa kila kitu. Nikafika Mwenge na nikasimama kwenye moja ya sheli, kisha nikawapigia wasichana hawa na kuwaelekeza sehemu nilipo simamisha gari langu. Baada ya dakika tatu hivi nikawaona wakifika katika eneo hili, nikafungua loki za milango ya gari langu na wakaweza kufungua milango na kuingia ndani.

“Mumependeza”

Niliwasifia huku nikiwatazama jinsi walivyo pendaza.

“Asante mkurugenzi”

“Hivi tunavyo kwenda huku kuna benki?”

“Ndio zipo”

“Sawa, sasa mmoja si angekuja kukaa hapa mbele ili anielekeze njia, si munajua kwamba hapa Dar es Salaam mimi ni mgeni.

“Sawa, Queen nenda”

Msichana aliye elezwa na mwenzake, akashuka kwenye gari na kuzunguka upande wa pili wa gari hili, akaifunagua mlango wa siti ya mbele kisha taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili. Tukafika katika moja ya jengo lenye baadhi ya benki na huduma kadhaa za kipesa, nikashuka kwenye gari nikiwa na kadi yangu, ya benki inayo niruhusu kuweza kutoa pesa kwenye benki zaidi ya mia moja duniani. Nikatoa kiasi cha dola elfu ishirini, dola elfu tano nikazibadilisha katika pesa za kitanzani kisha nikarudi kwenye gari. Ujumbe mfupi wa meseji ukaingia kwenye simu yangu na kujikuta nikiziweka hizi bahasha mbili zenye pesa pembeni yangu na kuitoa simu mfukoni. Nikaufungua ujumbe huu uambao umetumwa na namba ngeni.

‘ULIPO PAGUSA SIO SALAMA KABISA ETHAN. NITAHAKIKISHA NINAKUUA KABLA YA SIKU YA LEO HAIJAISHA. PUMBAVU SANA WEWE’

Meseji hii ikanistua sana hadi mwili mzima ukaanza kunitetemeka na jasho taratibu likaanza kunimwagika usoni mwangu hadi Queen na mwenzake wakagundua kwamba kuna tatizo lililo nipata.




“Mkurugenzi kuna tatizo gani?”

Qeen aliniuliza huku akinitazama jinsi mikono inavyo nitetemeka hadi kushika simu yangu nina shindwa.

“Unaweza kuendesha gari?”

“Ndio”

“Njoo uendeshe”

Nilizungumza huku nikiwa nimeishiwa hata ujasiri wa kuendesha gari hili. Nikahamia siti ya pembeni huku Qeen akiingia kwenye siti ya dereva.

“Tunaelekea wapi mkurigenzi”

“Kule kule”

Taratibu tukaanza kuondoka eneo hili huku kichwani mwangu nikiwa na mawazo mengi sana juu ya huu ujumbe nilio tumiwa. Nikaitafuta namba ya afande Kimaro na kumpigia simu, simu yake ikaita kidogo na ikapokelewa.

“Ethan nitakupigia nipo kwenye kikao”

Simu ikakatwa na kunifanya nishushe pumzi nyingi sana. Ukimya ukatawala ndani ya gari huku nikifirikia nimueleze Dany juu ya ujumbe huu, ila nikaona itakuwa sio sahihi, acha nipambane mwenyewe hadi dakika ya mwisho isitoshe yupo Ethan, rafiki yangu anaye nisaidia katika hali zote ngumu ninazo zipitia.

“Mkurugenzi tumesha fika Bagamoyo, sasa unahitaji twende kwenye hoteli gani?”

“Hoteli yenye hadhi kubwa ambayo haina watu wengi na wanao ingia hapo ni matajiri tu”

Qeen akatazamana na mwenzake.

“Unanitazama nini Qeen mimi sijiu hoteli nzuri za huko”

“Ila wewe si viwanja vyako?”

“Bwana Qeen mimi sijui”

“Labda twende pale Ocenic Bay Hotel”

“Haina watu wengi?”

“Hapana watu ni wacheche mkurugenzi”

“Sawa twendeni”

Tukafika katika hoteli hii kubwa, Qeen akasimamisha gari katika maegesho maalumu. Nikatazama eneo hili na kweli lime tulia na watu wengi hapa kidogo ni wazungu wazungu ambao kwa namna moja ama nyingine nina imani kwamba wananitambua.

“Nenda kachukue chumba kimoja chenye hadhi kubwa”

“Kimoja!!?”

Qeen aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.

“Ndio”

“Sawa mkurugenzi”

“Mupende kuniita Ethan nikiwa nje ya ofisi”

“Saw sawa”

Nikamkabidhi Qeen kiasi cha kutosha cha pesa kisha akashuka kwenye gari na kuelekea eneo la mapokezi. Nikabaki na rafiki yake ambaye sio muongeaji sana.

“Hivi unaitwa nani wewe?”

“Latifa”

“Ahaa, mwenzako ni Qeen na wewe ni Latifa?”

“Ehee?”

“Muna muda gani katika kampuni yangu pale?”

“Huu ni mwaka wa pili mkuu”

“Ahaa, kati ya uongozi ulio pita na uongozi huu, upi ni ongozi mzuri?”

“Wa kwako kwa kweli, kwa maana unajua kuwajali wafanyakazi wako. Yule mkurugenzi aliye toka alikuwa anajali wale viongozi wa ngazi za juu hususani ma meneja wale. Ila sisi wa chini huku tulikuwa tunafanya kazi hiyo basi kwa maana hatuna pa kwenda na hapa ni mjini ukiacha kazi ni kazi kupata kazi”

“Poleni sana”

“Tumesha poa, kwa sasa kidogo tunaweza hata kuingia saloon hata mara mbili kwa wiki, ila zamani. Kwa wiki mbili una ingia mara moja, tena sisi tunao hudumia wateja tunatakiwa kuwa safi muda wote ila wala hawakuwa wanatujali, hakuna marupu rupu, yaani tulipitia mtoso mkubwa sana mkurugenzi”

Tukamuona Qeen akija eneo la gari na ikabidi mazungumzo yaishie hapa. Akafungua mlango na kuingia ndani ya gari.

“Nimepata vip room moja ni dola mia moja na hamsini”

“Umechukua?”

“Ndio mkuu”

“Ni gorofa lipi?”

“Lile pale”

Qeen alituonyesha moja ya gorofa, kwa maana katika eneo hili kuna gorofa kadhaa.

“Basi tangulieni nina kuja”

“Sawa”

Qeen na Latifa wakashuka kwenye gari hili,kabla hawajafika mbali nami, simu yangu ikaanza kuita na kukuta ni namba ya Biyanka. Nikaitazama simu yake kwa muda kisha nikaipoke na kuiweka sikioni.

“Mume wangu za muda?”

“Safi vipi?”

“Poa upo wapi?”

“Ahaa nipo sehemu nina pata lunch”

“Ahaa, kuna mtu ameniambia amekuona polisi leo ni kweli kwa maana nilimbishia”

“Hapana sio mimi”

“Amesema pia ameona gari lako polisi”

“Ni nani?”

“Rafiki yangu mmoja hivi?”

“Hapana atakuwa amenifanisha, mimi polisi ninakwenda kufanya nini sasa?”

Ilinibidi niongopee ili kuficha udadisi wa Biyanka.

“Ndio hapo sasa, sawa, sisi tunajianda kuingia kwenye mkutano na mama”

“Sawa”

“Nakupenda mume wangu, nakuomba uwe makini”

“Nashukuru, nakupenda pia”

Nilizungumza hiyo basi ili kumridhisha, akakata simu, kabla sijairudisha mfukoni nikaupitia ujumbe huu nilio tishiwa maisha yangu. Nikafungua kisanduku kidogo cha kuhifadhia vitu ndani ya hili gari nikaiingiza kiasi cha pesa na nikashuka na kiasi cha kutosha cha pesa za kitanzania mbazo zipo kwenye mfuko huu wa kaki, nikafunga mlango wa gari langu kwa funguo na kuelekea walipo elekea Qeen na Latifa. Nikafika katika chumba alicho niambia, nikagonga kidogo na mlango ukafunguliwa na Qeen. Nikapitiliza moja kwa moja hadi kitandani na kijitupa na wote wakabaki wakinitazama.

“Agizeni vyakula na vinywaji”

“Unatumia chakula gani mkuu”

“Chochote mutakacho kula nyinyi. Alafu Latifa usipende kuniita mkuu tunapo kuwa eneo kama hili. Niiteni Ethan tu nitajisikia vizuri”

“Samahani Ethan nilijisahau”

“Je kinywaji unatumia kinywaji gani?”

“Kichwa changu leo hakipo vizuri hivyo nahitaji ninywe wnye hadi nitakapo jisikia vizuri”

Qeen na Latifa wakatazamana.

“Mimi nitakwenda”

Latifa alizungumza, nikamuonyesha bahasha yenye pesa na kumuagiza achukue kiasia nacho kihitaji kwa kwenda kununulia vyakula na vinywaji.

“Ethan unaonekana una mawazo sana boss wangu, hembu niambie ni kitu gania mbacho kina endelea kwako?”

Qeen aliniuliza swali hili mara baada ya Latifa kutoka chumbani humu, nikakaa kimya kwa muda huku nikimtazama usoni mwake.

“Niambie tu unaweza kuniamini”

“Kuna mtu anahitaji kuniua leo”

Qeen akastuka huku akiushika mdomo wake kwa kushangaa sana. Nikamuona naye akianza kujawa na woga fulani.

“Kwa nini?”

“Kwenye maswala ya kibiashara kuna mambo mengi ila potezea naamini kwamba hato weza kufanya jambo hilo ndio maana nime amua kuja kukaa huku Bagamoyo kwa muda kidogo hadi hili jotojoto litakapo pita.

“Jamani, wasije wakatuulia mkurugenzi wetu na maisha yakabadilika kwetu jamani”

“Usijalia hakuna kitu kama hicho. Nikuulize swali?”

“Niulize tu”

“Wewe na Latifa muna urafiki wa muda gani?”

“Mmmm toka tupo chuo IFM hadi mwaka huu tunatimiza mwaka wa tano kama sikosei”

“Na muna ambiana sana mambo yenu ya siri?”

“Ndio, siri yake siri yangu. Hatufichani jambo lolote”

“Sawa”

Latifa akarudi na kukaa kwenye moja ya sofa.

“Ninaweza kuwaamini?”

Latifa na Qeen wakatazamana kwa sekundee kadhaa, kisha latifa akwahi kujibu kabla ya Qeen

“Ndio Ethan kwa maana mimi na Qeen tuna amainiana kwa kipindi kirefu sana, hatujawahi kukorofishana wala kutoleana siri kwenye maisha yetu”

“Ohoo sawa sawa nimewaelewa. Sasa nahitaji muwe ni wapelelezi wangu wakubwa na muweze kufanya kazi moja hatari sana ambayo kwa nama moja ama nyingine inaweza kuhatarisha maisha yenu. Ndio maana nimewaita mazunngumzo haya tuje kuyazugumzie nje ya Dar es Salaam”

Qeen na Latifa wakawa wanyonge kiasi huku kila mmoja akionekana kutafakari juu ya jambo ambalo ninalizungumza.

“Najua nyinyi bado ni mabinti wadogo kama mimi. Bado munatafuta maisha kwa udi na uvumba ila kwa maisha ya Tanzania nina imani kwamba hakuna ambaye anaweza kutusua na kuwa tajiri kwa mshahara wa kupangiwa na bosi wako si ndio”

“Ni kweli Ethan”

Qeen alijibu kwa unyonge sana.

“Kazi ambayo mutaifanya sio ya muda mrefu ila nitawapatia pesa nyingi sana pale ambapo wote kwa pamoja tuta fanikisha kuhakikisha lie ambalo nimelikusudia limekalimilika. Hivyo basi nahitaji kujua mupa tayari au hamupo tayari katika kuifanya hii kazi, na sijawatajia kazi gani kwa maana nina hitaji kuona muitikio wenu, kwa maana usije ukasema nitafanya kazi kutokana kwa kiasi cha pesa ambacho labda nitakitaja au kwa sababu tu unamfanyia Ethan, tahadhari kazi inahitaji usiri, kazi inahatarisha maisha, kazi inahitaji umakini. Sasa kazi ni kwenu”

Qeen akashusha pumzi nyingi sana huku akimtazama Latifa usoni mwake, ambaye naye anaonekana kuwajawa na wasiwasi mwingi sana. Ukimya ukatawala ndani ya chumba hichi huku wote wawili wakiwa wanatafakari sana kwa hichi nilicho waeleza.

“Mimi nipo tayari japo sifhamu ni kazi gani ila nipo tayari Ethan”

Latifa alizungumza kwa ujasiri ambao kwa namna moja ama nyingine ukanifurahisha.

“Nami nipo tayari, nitapambana bega kwa bega hadi kuhakikisha kwamba lile ambalo unatueleza linakwenda kukamilika Ethan”

Maneno ya Qeen nayo yakanipa furaha na hamasa ya kuwaamini japo si kwa asilimia mia moja.

“Nafurahi kusikia hivyo, ila jambo kubwa na la umakini sana ni kutunza siri, kama mutashindwa kutunza siria, hakika mpango mzima unakwenda kuvunjika na ukivunjika. Mimi na nyinyi kila mmoja atakwenda kuuwawa kwa wakati wake”

“Tuamini Ethan hata mama zetu hatuto kwenda kuwaeleza hili jambo”

“Nashukuru. Mimi nipo Tanzania kwa ajili ya kulipiza kisasi kwa adui aliye niulia wazazi wangu kipindi cha miaka mingi sana iliyo pita. Nimenunua ile kampuni ili mradi niwe karibu tu na adui yangu. Hadi kwa sasa hivi nina shukuru Mungu ni kwamba nimesogelea kwa asilimia takribani stini. Asilimia arobaini zilizo salia nina hitaji kumuangamiza kutokea nje kabisa na ninahitaji anguko lake liwe anguko la taifa kwa maana halito mgusa mtu mmoja, litawagusa watu wengi sana”

Nilizungumza kwa mafumbo kidogo ili kuendelea kuwajua Qeen na Latifa kama akili zao zipo vizuri au ni za aabu ajabu.

“Anguko la taifa, una maanisha mtu huyo ni kiongozi au?”

Qeen aliniuliza huku akinikazia macho.

“Si kiongozi ila anatarajiwa kuwa kiongozi”

“Ahaa nahisi hilo swala litakuwa linahusiana na wanao gombani urahisi si ndio bosi”

Latifa aliniuliza, nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba alicho kizungumza yeye ni sahihi kabisa.

“Duu, hilo jambo kweli ni gumu”

“Ndio maana ninazidi kuwa sisitizia kwamba linahitaji kila mmoja wenu kuwa makini na msiri. Ukiropoka hata kwa boyfriend wako basi ujuje unakwenda kufa”

“Sote hapa hatuna wanaume”

“Kweli?”

“Ndio Ethan tuamini”

“Sawa, kwa leo mazungumzo yaishie hapa, ili kila mmoja aweze kujiandaa kisaikolojia kuweza kumpokea huyo mtu ambaye tunakwenda kumshuhulikia. Ninawahakikishia enepo tutafanikiwa basi kila mmoja wenu ninakwenda kumpa kiasi cha dola za Marekani milioni tano na nina uhakika kwamba mutakuwa matajiri wakubwa na nyinyi mutafungua kampuni zenu ndogo ndogo kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi zaidi”

Qeen na Latifa wakwa kama watu walio changanyikiwa wakaanza kuruka ruka huku wakikumbatia kwa furaha sana, jambo lililo nifanya nicheke kidogo.

“Boss tunakuhakikishia kwamba tutafanya lolote utakalo tuamrisha tufanye. Haki ya Mungu ni lazima tumuangamize yule unaye hitaji kumlipizia kisasi”

Qeen alizungumza kwa furaha sana.

“Mimi nipo tayari hata kufa ili mradi huu mpango uweze kukamilika.

“Nafuraha kuweza kusikia hivi. Mbona wanachelewa kutuletea chakula na viywaji”

“Kidogo kulikuwa na foleni ila watatuletea chakula humu ndani”

“Sawa, hivi kila mtu anaishi kwake au?”

“Tumepanga nyumba moja, kila mmoja ana cheke, ila tuna seble moja”

“Basi mpango ukiisha, mutaniambia ni wapi munahitaji kuishi kama ni kuwajengea niwajengee kila mmoja nyumba yake na kama ni kununua basi kila mmoja niwanunulie nyumba yake, hiyo ni nje tu ya kiasi cha pesa ambayo nimewaabia nitakwenda kuwalipa na nilazima tuweze kuandikishana mikataba ya siri ambayo ni sisi watatu tu ndio tutakuwa tunafahamu juu ya mikataba hiyo. Mumenielewa?”

Furaha ikazidi kutawala kwa Qeen na Latifa. Muhudumu akatuletea vijwaji na chakula. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitazama na kukuta ni namba ya Afande Kimaro, nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Ndio Ethan”

“Kuna meseji na namba nitakutumia, nina omba uweze kuniwekea ulinzi mkuu”

“Sawa nitumie”

“Kitu kingine ninaomba umtazame Clara hapo hospitali nitaonana naye kesho”

“Sawa sawa”

Nikakata simu na kumtumia meseji ya vitisho niliyo tumiwa na mtu nisiye mfuamu, nikaituma na namba yake ya simu kisha tukaendelea kupata chakula hichi cha mchana huku tukiendelea kufakamia wyne zilizo letwa hapa.

“Ethan kuna zawadi na kazi ambayo na sisi tuna hitaji utusaidie kuifanya”

Qeen alizungumza kwa sauti nyororo huku macho yakiwa yamemlegea kwa pombe nyingi aliyo kunywa, wakasimama na kunishika mikono yangu, nikatembea nao hatua chache hadi kitandani, kisha wakanisukumia kitandani, wakatazamana kisha wakacheka kidogo. Taratibu wakaanza kunyonyana ndimi zao huku wakianza kuvuana nguo zao jambo lililo nishangaza sana na kunitamanisha sana kihisia na kunifanya nipate msisimko mkali sana wakimahaba hadi nami nikajikuta nikianza kuvua nguo moja baada ya nyingine kwa ajili ya kuwashuhulikia wote wawili.



ENDELEA

Qeen na Latifa wakapanda kitandani huku wakiwa wamebakiwa na nguo zao za ndani. Kila mmoja akaanz akunipapasa mwilini mwangu jambo lililo nifanya nizidi kuchanganyikiwa, mlio wa simu yangu iliyomo kwenye suruali ambayo tayari nimeivua, ukatushtua sote. Latifa akanisogezea suruali yangu na kuitoa simu, nikaitazama kwa sekunde kadhaa namba ya Biyanka kisha nikaimnya kitufe cha kuzima simu hii na kuiweka pembeni.

“Sitaki usufumbufu”

Nilizungumza kwa sauti ya kilevi, nikaitumia simu pembeni na wasichana hawa wakaendelea na kazi walio hitaji wanipatie. Nikaanza kula utamu wa mmoja baada ya mwengine, mazoezi ya uchezaji mpira kwa asilimia kadhaa kusema kweli yamenisaidia, kiasi cha kunifanya niweze kuwahimili wasichana hawa wote wawili huku kila mmoja nikimpa haki sawa na mwenzake.

“Ethan haki ya Mungu upo vizuri”

Qeen alizungumza huku akinichezea chezea kifua changu mara baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.

“Kweli”

“Kweli vile, yaani umenikuna hadi sehemu ambayo sikuwahi kukunwa maishani mwangu.”

“Hahaaaa”

“Yaani mimi hapa nahisi kufa kufa jamani, heeee si kwa kunitomb** hivyo Ethan”

“Mimi mbona naona kawaida”

“Mmmm, sipati picha jinsi unavyo mfanya Biyanka”

Nikastuka kidogo Qeen kulitaja jina la Biyanka.

“Muna fahamu kwamba mimi na Biyanka tuna mahusiano?”

“Ndio ofisi nzima ina fahamu kwamba tuna muna mahusiano kwa maana ana tuchimba biti za chini chini kwamba hakuna mtu anaruhusiwa kukusogelea na kama kuna mtu mwenye shida na wewe basi ipitie kwake kisha yeye ndio anaileta kwako”

Nikazidi kushanga kwa vituko anavyo vifanya Biyanka pasipo kujua nina mtumia kama silaha ya maangamizi kwa baba yake.

“Anacho kifanya sio kitu sahihi kwa maana mimi sifahamu kabisa”

“Ohoo sisi wa chini mkurugenzi ndio tunao jua hilo, hususani sisi wasichana warembo warembo ndio tunakoma kwa kupigwa mikrwa na inafikia hatua ameahidi akigundua kwamba kuna msichana ana mahusiano na wewe basi anamfukuza kazi”

“Heee huko kafika mbali kampuni ni yangu na asinipangie masharti kwa wafanyakazi wangu”

“Qeen unajua tatizo la Biyanka hajiamini, japo ni mzuri ila anaona atazidiwa kete na sisi watoto wa Kiswahili ndio maana kila asubuhi anaitisha vikao vya wasichana wote ofisini na kuwapa onyo”

“Nitamkanya kwa jambo hilo”

“Hapana Ethan, kusema kweli sisi tunaipenda kazi yetu. Najua huko kitandani atakudadisi kujua ni nani aliye kuambia, na utajikuta unatutaja, akatutumbua”

“Hamuniamini?”

Niliwauliza Qeen na Latifa kwa msisitizo.

“Tunakuamini”

“Sasa wasiwasi wa nini, mimi ninao uwezo pia wa kumfukuzisha kazi”

“Hee huko ni mbali sasa Ethan, usije ukafungiwa na baba yake, kumbuka kwamba anakwenda kuwa raisi wa hii nchi na ana washabiki wengi sana na kumbuka na chama chake ndio tawala hapa Tanzania”

Nikaka kimya huku nikiyatafakari maneno ya Qeen.

“Baba yake kuwa raisi anaweza kunifungia ehee?”

“Ndio, wanaweza kukufanyia figisu figisu hadi ukakuta unaitaifisha kampuni. Wanaweza kukufufulia madeni ya nyuma ya kodi hadi wewe mwenyewe ukajikuta unachanganyikiwa.”

“Ahaa….je asipo ingia madarakani itakuwaje?”

“Ni ngumu aisee ujue upinzani bado hawana uwezo wa kuking’oa chama pinzani madarakani”

“Kwa nini?”

“Moja hawana pesa za kutosha kama chama kilicho madarakani.Pili chama pinzani, vina wafuasi wengi mijini tu, ila huko vijijini ni hata havijafika, sasa Tanzania, ina mikoa mingapi, ina vijiji vipapi na kila kijiji kina wananchi wangapi wanao weza kupiga kura, sasa utakuta mwisho chama kilichopo madarakani, kinajichukulia ushindi mkubwa, upinzani wanabaki wana bwela bwela tu, wakidai wanaibiwa kura”

Latifa alizungumza kwa msisitizo.

“Hivi bado wana ibiana kura kweli?”

“Kuibiana ni kwenye kura labda za Ubunge na udiwani, ila kura za raisi ni mara chache kwa maana hapo watu wanapakodolea macho kishenzi”

“Mmmm nyinyi mupo chama gani sass?”

“Mimi sina chama kwa kweli, raisi atakaye patikana ndio huyo huyo.”

“Qeen je na wewe huna chama?”

“Mimi siasa za Afrika wala sizielewagi, unakwenda kupigwa na jua. Unampa mwenzako kura, ila mwisho anakuja kufanya using** serikalini, yaani hapo ndipo ninapo jikuta ninachoka kabisa.”

Maswali yangu ya udadisi yakazidi kunipa njia na mwanya wa kujua ni kitu gani ambacho ninaweza kukifanya. Kutokana baba Camila amesha pata kiti cha uraisi nina imani kwamba kwangu itakuwa ni njia rahisi kuhakikisha kwamba ananipa msaada mkubwa wa kukitoa chama tawala madarakani ambacho kwa sasa kimemsimamisha Poul Mkumbo.

“Muna fahamiana na kiongozi yoyote wa kipinzani?”

“Mmmm mimi sifahamu”

Qeen alizungumza huku akitingisha kichwa chake.

“Mimi nina mjua mmoja wao ila sidhani kama ana nguvu kubwa ndani ya upinzani”

“Ni nini unaye mfahamu?”

“Mbunge wa Arusha mjini, amemuoa dada yangu, mtoto wa mama mkubwa”

“Ahaa unaweza kuwasiliana naye”

“Sasa hivi?”

“Ndio ikiwezekana”

“Alafu nina muambiaje?”

“Utanipa mimi niweze kuzungumza naye”

“Ngoja nitazame”

Latifa akashuka kitandani, akachukua pochi yake kwenye moja ya sofa na kutoa simu yake, akaanza kuiminya minya na kuiweka sikioni mwake.

“Inaita”

Latifa alizungumza huku akirudi kitandani.

“Shem shikamoo”

“Samahani mwaya nitakuwa nimekusumbua”

“Sasa shemeji kuna bosi wangu mmoja hivi anahitaji kuzungumza na wewe, sijui upo tayari kuzungumza naye”

Latifa akanikabidhi simu yake na nikaiweka sikioni mwake.

“Habari yako ndugu”

“Salama tu, naona mazungumzo ya kwenye sio mazuri sana. Sijui tunaweza kuonana”

“Hujanitambulisha jina lako ndugu yangu”

“Ni mmiliki wa kampuni anayo fanyia kazi shemeji yako.”

“Ohoo muheshimiwa Ethan”

“Ndio ni mimi, samahani tunaweza kuonana”

“Ndio niambie mulipo mimi ninaweza kufika”

“Upo Dar?”

“Hapana nipo Bagamoyo, nipo nina mapumziko mafupi”

“Ohhoo asante Mungu, mimi pia nipo Bagamoyo. Sasa huyu binti atakuelekeza sehemu nilipo”

Nikamrudishia Latifa simu yake na akamuelekeza shemeji yake katika hoteli tulipo kisha akakata simu. Nikashuka kitandani na kuwaomba tukaoge pamoja kwa maana tunatakiwa kuwa safi, tunapo kutana na mbunge huyu. Tulipo maliza kuoga kila mmoja akavaa vizuri kisha tukatoka ndani humu na moja kwa moja tukaelekea eneo kupatia vinywaji huku tukiwa tumekaa katika kigiza kidogo ili mradi watu wasiweze kuniona. Baada ya robo saa mbunge huyo akafika katika eneo tulipo huku akiwa ameongozana na mke wake. Tukasalimiana naye na Latifa akatutambulishalisha.

“Munaweza kutupisha tukazungumza kidogo”

Niliwaomba Latifa na wezake, wakatii nilicho waambia na wakasogea meza ya pembeni.

“Niliomba kuweza kukutana na mmoja wa wana chama cha upinzani ili tuweze kujadilia mambo mawili matatu kwenye mbio za uchaguzi munazo zielekea.”

“Sawa sawa”

“Najua upinzani muna kiu ya kukitoa chama tawala madarakani si ndio”

“Ndio ndio”

“Najua kitu kinacho waangusha sana ni pesa za kampeni si ndio?”

“Hujakosea kabisa muheshimiwa”

“Hadi sasa hivi ndani ya chama chako muna bajeti ya kiasi gani?”

“Mmmm baheti kuu ya kampeni ni bilioni mia tatu hamsini, huku chama tawala tunasikia wameandaa bajeti ya trilioni moja kwa ajili ya kampeni zao”

“Trilioni moja na Bilioni mia tatu ni mbali sana, wezenu wamewaacha kwa kiasi cha bilioni mia saba, mutazipata wapi hizo”

“Wao wanategemea pesa kuhonga ili wapate kura ila sisi tutawaua majukwaani kwa maneno na sera zanye nguvu ambazo zitawashawishi wananchi kuhakikisha wana fanya maamuzi sahihi”

“Hilo ndio mulilo litarajia kwa sera za majukwaa mutoe chama kilichopo madarakani?”

“Ndio mkurugenzi”

“Inabidi muweze kuamka sasa, siasa haitaji maneno mengi. Siana ina hiji pesa, bila ya pesa ni kupiga porojo kwa maana wananchi hao munao wapa sera munazo dai ni nzuri, watahamia upande wa pili kusiliza sera huku wakikinga mikono kupata ridhiki ya chote kitu na mwishowe mutajikuta mukiwa munaangushwa kila chaguzi na mutaishi kulalamika weee na hakuna kitakacho tokea kwenu”

Bwana Samweli kama nilivyo tambulishwa na Latifa akaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akionekana kutafakari kile nilicho mueleza.

“Mimi nimeshirikia siasa nchini Ujerumani, wezenu kule upizani hawatumii kelele majukwaani, ni pesa ndio inafanya kazi. Watu wanataka chama chenye pesa kiwaongoze wao, sio chama masikini kama chenu kiwaongoze, kwa mfano tu mdogo muna pewa nchi mukiwa hamuna pesa, mutatumia kiasi gani kukijenga chama kwa pesa ya nchi?”

“Mmmmm hilo nalo neno”

“Ndio hivyo, mutakuta munaacha kuwashuhulikia wananchi shida zao, na munahamia katika kujenga chama ili miaka ijayo musitoke, na mutakuwa ni wezi kwa kuiba pesa za wananchi walala hoi”

“Ni kweli nimekuelewa mkuu, sasa unahitaji sisi tufanye nini?”

“Andaeni mkutano mdogo sana wa siri sana na viongozi wako wa ngazi za juu, kisha nijulisheni nije tukutane. Mukumbuke kwamba mimi ni mkwe mtarajiwa wa mgombea uraisi wa chama tawala. Hivyo muwe makini sana katika kila simu ambayo munanipigia na ikiwezekana musitumie namba zenu. Sitaki siku waje kuhack mazungumzo yangu na ikawa shida kwangu na kwenu. Mume nielewa?”

“Tumekuelewa mkuu nitahakikisha kwamba nina fanya hivyo haraka iwezekanavyo”

“Sawa nashukuru kwa muda wako. Tunaweza kuendelea kujumuika kwa pamoja kupata chakula cha usiku”

“Nashukuru sana ila tunaeleka kwa mama mkwe tuliweka ahadi ya kula nao chakula cha usiku”

“Ohoo vizuri sana, basi hakuna tabu”

Nikaagana na bwana Samweli pamoja na mke wake na wakondoka katika eneo hili kisha mimi nikatangulia chumbani kwetu. Baada ya muda kidogo Qeen na Latifa nao wakaingia chumbani humu. Usiku huu hakika ni usiku war aha kwetu sote watatu, baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku, tukaendelea kupeana burudani ya kitandani hadi majira ya alfajiri ndio tukajipumzisha huku sote tukiwa tumechoka sana.

***

Majira ya saa saba mchana tukaanza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha moyoni mwake kwani kile tulicho kifanya kusema kweli kimetuburudisha na kama ni weekend yetu basi imekwenda poa.

“Narudi jamani haya mahusiano yawe siri, sawa”

“Upo salama Ethan hatuto weza kufungua kinywa chetu kwa mtu yoyote”

“Sawa. Leo usiku nitaandaa mpango mzima wa nyinyi kuweza kufanya katika kazi ambayo nimewajulisha, keso asubuhi ofisini kwangu nikipata muda nita waita niweze kuwaeleza kila mbinu tunayo paswa kuweza kuifanya sawa”

“Sawa mkuu”

Tukafika eneo linalo itwa Mbezi Beach wakaniomba niweze kuwashusha. Nikampa kila mmoja wao milioni mbili za Kitanzania, kisha nikaendelea na safari yangu hadi katika hoteli niliyo pangisha.

“Nahitaji funguo”

Nilimuambia muhudumu wa hoteli hii huku nikimtazama usoni mwake.

“Ohooo samahani Mr Ethan, funguo ameichukua mke wako uliye mtambulisha hapa kwetu na hivi sasa yupo chumbani huko”

Nikastuka kidogo kwa maana jana nilimzimia simu Biyanka na hadi sasa hivi sijaiwasha. Nikaiwasha simu yangu, ndani ya sekunde kadhaa ikaanza kuingia mfululizo wa meseji kutoka kwa Biyanka pamoja na mkuu wapolisi. Nikaanza kupitia meseji moja baada ya nyinngine za Biyanka na zote zinaonyesha malalamiko ya kwa nini sipatikani hewani. Nikaingia kwenye lifti na kupandisha gorofani, nikatembea kwa hatua kadhaa kwenye hii kordo hadi sehemu ulipo mlango wa chumba changu. Nikagonga kidogo na ukafunguliwa. Biyanka akanipokea kwa sura iliyo jaa hasira sana, sikuhitaji kusemeshea kitu cha aina yoyote zaidi ya kuingia ndani. Nikavua koti langu na kulirusha kwenye kiti.

“Umetoka wapi na ulikuwa wapi na ulikuwa na unafanyaje na kwa nini ulinikatia simu kisha ukazima eheeee?”

Biyanka alizungumza kwa ukali sana ambao sikuujali, nikaka kwenye sofa na kuweka nne, nikailegeze vizuri tai yangu kisha nikapitia meseji za afande Kimaro. Nikajikuta nikinyanyuka huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana mara baada ya kusoma meseji ya Afande Kimaro akidai kwamba Clara haonekani hospitalini na askari wake wawili alio kuwa amewaacha waimarishe ulinzi wameuwawa usiku wa kuamkia leo.



Sikutaka kuendelea kujishauri kichwani mwangu kwa muda mrefu, nikaitafuta namba ya afande Kimaro na kumpigia, ikaanza kuita kwa muda kisha ikapokelewa.

“Ndio, afande”

“Nimejaribu kukupigia simu yako kwa muda kidogo nikaona kimya”

“Ni kweli afande nilizima ili watu wale walio panga kuniaua wasiweze kunitafuta kwa kupitia simu yangu”

Biyanka akastuka macho yakamtoka, kwa haraka akanisogelea sehehemu nilipo simama. Uso wa hasira ambao ulikuwa umumtawala nikaushuhudia taratibu ukianza kumuondoka na kuwa mpole huku akinisikiliza kwa umakini kile nilicho kizungumza.

“Ahaa sawa sawa nina imani kwamba meseji zangu umewezeza kuziona?”

“Ndio nimeweza kuzioana kwa sasa mupo wapi?”

“Nipo kituaoni, unaweza kufika”

“Sawa ninakuja sasa hivi”

Nikakata simu na kuirudisha mfukoni.

“Ethan nitakuwa nimesikia vibaya, umesema kwamba kuna watu walihitaji kukuaa?”

“Ndio”

Nikaitafuta meseji ya vitisho niliyo tumiwa na nikamkabidhi Biyanka simu yangu kisha mimi nikaelekea bafuni kuweza kunawa ili niweze kutoa harufu harufu ya pafyumu za Qeen na Latifa. Nikatoka bafuni na kumkuta Biyakna akizungumza na simu.

“Ehee baba wanamtishia mume wangu anahitaji kumuua”

Nikataka kumzuia Biyanka asizungumze na baba yake juu ya hili swala ila nikajikuta nikiwa nimesha chelewa kumzuia.

“Ndio nimekutumia, tayari hiyo namba. Hembu baba nakuomba basi watu wako wa usalama wamtuafute muhisika wa hili tukioa basi”

“Mume wangu anaogopa amekuwa ni mtu wa kuzima zima simu kila mara jamani”

Biyanka alizungumza kwa masikitiko makubwa akionekana ameguswa sana na hili swala.

“Ndio yupo hapa”

“Eheee”

Biyanka akanikabidhi simu yake nikaiweka sikioni.

“Shikamoo baba”

“Marahaba. Ethan una ugomvi na mtu wa aina yoyote?”

“Hapana baba yangu, Tanzania mimi sina hata rafiki kabisa, na nimeshangaa mtu huyo ni wapi ameipatia namba yangu na kwa nini ananitisha ikiwa sijafanya jambo lolote baya”

“Punguza wasiwasi, swala lako nitalihushulikia mwanagu sawa”

“Sawa baba yaani nimejikuta ninanunua gari jipya ili wasiweze kunikremisha kwamba ni mimi”

“Hahaaa, hivi huna mlinzi”

“Ndio kwa sasa sina mlinzi”

“Basi nitaagiza vijana wangu wawili wawe wanakulinda kila unapo kwenda. Nina imani wana ujuzi mkubwa sana wa kukufanya uwe salama kila muda”

“Nashukuru sana baba yangu”

“Sawa sawa, niwatakie mchana mwema na nitawajulisha mara baada ya kuweza kumkamata muhusika wa hili tukio”

“Sawa baba”

Nilijikaza kumuita tu baba, ila laiti kama angefahamu kwamba yeye ndio adui yangu namba moja basi asinge weza kujipendekeza sana kwangu. Simu ikakatwa, Biyanka kwa haraka akanikumbatia huku akilia.

“Jamani pole mume wangu, nilihisi kwamba unanisaliti jamani”

“Siwezi kukusaliti mke wangu, kwa nini nifanye hivyo ikiwa nina kupenda kuliko kitu chochote.”

“Nisamehe kwa kuweza kukufikiria vibaya mpenzi wangu. Nisamehe kwa kweli”

“Usijali mpenzi wangu. Nahitaji kuelekea polisi kwa sasa, tunaweza kuongozana?”

“Ndio”

“Nitolee nguo hapo kabatini”

Biyanka akaniachia na kufanya nilicho muagiza. Nikavaa nguo hizi huku nikijaribu na mimi kuweza kuumiza kichwa juu ya baba mdogo wa Clara tuliye mkamata ana kundi kubwa kiasi gani la kuweza kufanya mauaji ya kiasi hichi kisa kikubwa ni Clara.

“Usiwe na mawazo sana mume wangu, kila jambo litakuwa sawa”

Biyanka alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu. Tulipa maliza kujiandaa tukatoka ndani humu na kuelekea eneo la maegesho. Tukaingia kwenye gari langu hili jipya.

“Gari nzuri”

Biyanka alizungumza huku akilichunguza gari langu kwa ndani.

“Nashukuru, walinzi wako wapo wapi?”

“Gari zao zile pale”

Tukaanza kuondoka eneo hili taratibu huku gari za walinzi wa Biyanka zikitufwata kwa nyuma. Tukafika kituo kikuu cha polisi na moja kwa moja tukaelekea ofisini kwa afande Kimaro. Akatukaribisha kwa furaha kiasi huku wakionekana kufahamiana sana Biyanka.

“Ila baba anaendelea vizuri”

“Ndio anaendelea vizuri na nilisha mdokezea juu ya lile ombi lako la kuwa IGP”

“Akasemaje?”

“Kama kawaida yake, subiri nipate Ikuku mwanangu kila jambo litakwenda sawa”

Biyanka alizungumza huku akiwa ameiigiza sauti ya baba yake jambo lililo tufanya sote tucheke.

“Kumbe muna fahamiana na Ethan?”

“Ndio ni mume wangu mtarajiwa”

“Weee kumbe ningemkoromea mwanzoni nahisi hata hii nafasi ningepokonywa”

“Haaaa ndio”

“Nashukuru Mungu damu zetu mimi na Ethan zimeendana”

“Nanyi mumejuana vipi?”

“Ni swala la binti mdogo aliye muokoata nina imani kwamba atakuwa amekusimulia?”

“Binti gani mume wangu?”

“Yule niliye kuambia kwamba nimemuokota kule kwenye maegesho ya magari pale ofisini”

“Ahaaa…ehee amefikia wapi?”

Afande Kimaro akafungua faili moja na kulisogeza karibu yetu. Tukaona picha za askari walio uwawa katika mlango wa chumba ambacho alilazwa Clara.

“Muuaji ni mwanamke, sura bado hatujaweza kuifahamu na alivalia mavazi ya kidaktari na aliweza kuifumba sura yake kwa kutumia vile vitambaa vyoa wakiwa katika chumba cha upasuaji”

Afande Kimaro alizungumza huku akituonyesha picha za msichana huyo ambazo imerekodiwa na CCTV kamera.

“Baada ya kufanya mauaji ya vijana wetu wawili, akaingia ndani na kumchukua mtoto nahisi alimchoma sindano ya usingizi, alimpakiza kwenye kiti kile cha magurudumu nakuanza kumsukuma kumpeleka nje na aliweza kuzi vunja kamera za nje ambazo hatukuweza kujua aliondoka pale hospitalini kwa gari gani”

“Ila pale hospitalini niliweza kumuona mlinzi naye hakuona jambo lolote?”

“Mlinzi hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo. Ila vijana wangu wanaendelea na msako mkali sana na watahakikisha kwamba wanamtia nguvuni msichana huyo”

Nikashusha pumzi nyingi huku nikionekana kuchoka sana.

“Je muhusika wa namba ambaye amenipa vitisho vipi?”

“Yule muhisika bado tunaendelea kuitafuta namba yake kwenye mitandao ila bado hatujampata”

“Basi utanifahamisha kile ambacho kitaendelea”

“Sawa Ethan”

“Kimaro, jitahidini basi, mume wangu mumemfanya aishi maisha ya woga ikiwa yupo Tanzania nchi yenye amani kuliko nchi zote Afrika bwana”

“Usijali nitahakikisha hili swala linakwenda kuwa sawa hivi karibuni”

“Sawa tunashukuru”

Tukaagana na afande Kimaro na kutoka ofisini humu. Tukaingia kwenye gari letu huku kichwa changu kikiwa na msongamano wa mawazo.

“Utaweza kuendesha kweli mume wangu?”

Nikamjibu Biyanka kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba sinto weza kuendesha gari hili. Nikampisha Biyanka kwenye siti ya dereva na tukaondoka eneo hili la kituo kikuu cha polisi cha kati.

“Kichwa chako mume wangu hakipo sawa, unahitaji tuelekee wapi kupata mapumziko”

“Nahitaji kwenda kulala sasa hivi”

“Huitaji kukaa labda kwenye sehemu ukapunga upepo wa bahari hivi”

“Nahitaji kulala, watu wananiwinda. Unataka wakaniulie huko baharini ehee?”

Nilizungumza kwa ukali kidogo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Biyanka akajawa na unyonge ulio mfanya ajikute akiomba msamaha pasipo kunifanyia jambo lolote baya. Tukafika hotelini na kuingia chumbani kwetu.

“Ethan naona ni vyema nikakuacha peke yako upumzike, ninaelekea nyumbani nitarudi usiku”

“Sawa”

Biyanka akanitazama kwa muda kidogo kisha akanisogelea na kunibusu mdomoni mwangu.

“Ninakupenda sana mume wangu”

“Ninakupenda pia mke wangu”

“Kweli?”

“Ndio au unahisi kwamba nina kudanganya?”

“Hapana mume wangu, nashukuru kwa kunipenda”

“Poa”

Nikajitupa kitandani, Biyanka akanitazama kwa unonge sana kisha akanivua viatu, akaviweka sehemu yake, akataka kunivua suruali ila nikamzuia kwa ishara.

“Nenda tu nyumbani”

“Sawa mume wangu”

Biyanka akanibusu shavuni kisha akatoka ndani humu. Nikanyanyuka kwa haraka hadi mlangoni, nikaufunga vizuri kwa komeo, kisha nikaitoa simu yangu mfukoni na kumtafuta Camila nina imani kwamba atakuwa amenitafuta. Simu ya Camila ikaanza kuita, kisha aikapokelewa.

“Niambie mume wangu”

“Poa baby vipi?”

“Safi, leo nimehitimu mafunzo yanu ya juto, kung fu na taikondo”

“Umeyasomea wapi hayo mafunzo”

“Si Dany amenifundisha, yaani hapa nipo vizuri sana. Mtu anizingui kabisa”

“Hahaa kama ninakuona vile”

“Weee yaani, siku nikikufuamania na mwanamke, yaani nitampiga hadi ajute kuzaliwa”

Tabasamu nililo kuwa nalo usoni mwangu, likapotea gafla kwani hiyo ni si taarifa nzuri kwani huku nilipo nimesha tambulishwa kabisa.

“Sawa mama”

“Mbona unanijibu kwa unyonge”

“Hamna, mwenzangu sasa hivi upo vizuri, mimi bado”

“Nitakufundisha. Uzuri wa mke wako kichwa changu kina shika mambo kwa haraka na ninaweza kumsaidia hata mtu mwengine katika swala zima la kumfundisha”

“Sawa, ehee niambie”

“Kesho ninaanza mazoezi mawili ya mwisho, moja ni kutumia upanga na na jengine kutumia silaha”

“Mmm angalia asije kufundisha ugaidi bure”

“Hahaaa hii ni kwaajili ya kujilinda na familia yetu. Natambua baba wewe una mambo mengi kwa namna moja ama nyingine mimi mama nitasimama kama mlinzi wako”

“Hahaa, haya bwana mama watoto”

“Nikimaliza, tunarudi Ujerumani, ume umemaliza, hujamaliza tunarudi Ujerumani. Mama yangu amenimiss sana”

“Sawa mpenzi wangu, wanaendeleaje lakini?

“Wanaendelea vizuri”

“Nashukuru kusikia hivyo”

“Fanya uwasiliane nao”

“Poa mpenzi wangu”

“Haya baadae, tambua nina kupenda na kukuhitaji. Mtu akijichanganya kwako nami ninamchanganya kisawa sawa”

“Hahaa haya bwana mama”

Nikakata simu, nikaitafuta namba ya mtu ambaye amenitumia meseji ya vitisho, nikampigia ila kwa bahati mbaya nikakuta kwamba hapatikani hewani. Gafla nikamuona Ethan akiwa amekaa kwenye moja ya sofa huku akiwa amevalia suti nyeupe na inayo ng’ara vizuri.

“Naona unaumiza kichwa sana kwa mtu aliye kukoromea?”

“Wewe unahisi nitakuwa na furaha jaaa yangu”

“Hhaaa….hawawezi kukuua”

“Wewe umesha mfahamu mtu ambaye amenitishia?”

“Ninaweza kumfahamu”

“Ni nani”

“Vaa viatu twende”

Nikavaa viatu na tukatoka katika chumba hichi na Ethan, watu ninao kutana nao njiani hawawezi kumuona Ethana zaidi ya mimi pekee, nikakabidhi kadi ya chumba changu mapokezi na tukaingia kwenye gari. Ethan akaanza kunielekeza hadi kwenye moja ya gorofa moja linalo jenge na halijamaliziwa.

“Simamisha gari hapa, tukifika pale mambo yanaweza kuwa mabaya”

“Kwani ni kina nani?”

“Wewe twende”

Nikasimamisha gari kwenye mitimiti kadhaa, tukashuka kwenye gari na Ethan akanisogogelea na kunishika mkono wangu wa kulia na kuniambia kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuniona nikitembea katika eneo hili. Tukapandisha hadi gorofa ya tano, nikaanza kusikia vilio vya mtu akigugumia kulia kwa kipigo anacho kipokea kutoka kwa mtu anaye mpiga. Tukaingia kwenye chumba hicho, sikuamini macho yangu mara baada ya kumkuta baba mke, Biyanka pamoja na walinzi wapatao kumi huku Biyanka akimpiga kijana huyo kwa rungu kubwa.

“Niliwakanya mucheze na kote ila si kucheza na mume wangu. Kama muna fanya kazi chini ya baba yangu mufanye tu ila si kumgusa mume wangu sawa wewe mwana haramu”

Biyanka alizungumza huku akihema, akafuta jasho linalo mtiririka usoni mwake, kisha akaandelea kumshushia marungu kijana huyu huku baba yake akitabasamu kwa binti yake kuifanya kazi hiyo ya kikatili sana.



“Huyu ndio mke na baba mkwe anaye tarajia kuwa raisi wa hii nchi”

Ethan alizungumza kwa sauti ya chini kidogo, hapakuwa na mtu aliye weza kusikia sauti yake wala kuona uwepo wetu ndani ya hichi chumba.

“Yule binti hakikisheni kwamba muna muua mume nielewa?”

Nikastuka tena mara baada ya kuisiki sauti hiyo ya Biyanka akiwaamrisha vijana hawa.

“Sawa madam”

“Endapo yule binti atakuja kutoa ushahidi juu ya baba yangu, vichwa vyemu mimi mwenyewe ndio nitavikata”

“Tumekuelewa Madam”

Biyanka akalitupa gongo alilo lishika chini na kutoa noti kadhaa za shilingi elfu kumi kumi na kumtupia jamaa aliye kuwa anapiga.

“Nenda hospitali na ufunge domo lako”

“Asante sana madam”

Siri ya kumfahamu Biyanka kuwa nii mtu wa hatari, sasa nimeigundua, siri ambayo imezaa chuki na hasira mpya dhini ya yeye na familia yake.

“Wanamzungumzia binti gani?”

Nilimuuliza Ethan huku nikimtazama usoni mwake.

“Clara”

“Nini….!!?”

“Ndio maana yake, ile ni kesi ya bucha ukampelekea fisi.”

“Una maana gani?”

“Afande Kimaro anafahamu mchezo mzima na yeye ndio aliye muagiza binti huyo kwenda kuwaua vijana wake. Hujiulizi ni nani ambaye alikuwa anafahamu kwamba mulimpeleka pale Clara na ndani ya muda mchache wameuwawa?”

Maswali haya mfulilizo ya Ethan yakaanza kujenga picha moja kichwani mwangu ya kuchezewa.

“Umshukuru Mungu kwamba ulipata akili ya kuzima simu yako na laiti usinge izima basi wangekutafute kule ulipo kuwa na unakula bata na watoto wazuri wazuri”

Ethan alizungumza huku akitabasamu. Biyanka, baba yake pamoja na walinzi baadhi wakatupita pembeni yetu pasipo kuweza kutuona.

“Hawa walinzi wa mwisho wawili ndio wataletwa kukulinda , itabidi uwe wakali”

“Nitawakataa?”

“Wala usiwakatae”

“Lazima niwakatae kwa mana kama mke ni bomu unahisi hawa nao watakuwa ni kitu gani kwa maana hapa watakuwa wamenizunguka mimi”

“Usijali katika hilo kumbuka kwmba mimi pekee ndio ninaye kulinda. Hao watakuwa wanafanya kazi bure tu kwako”

“Mmmm na mtoto wa watu je?”

“Clara nitakwenda kumchukua. Nitamtafutia sehememu uweze kumficha bila ya wao kuweza kufahamu, ila siku ya siku mambo yatakapo bunduluka basi atakuwa ni shaidi namba moja kuhakikisha kwamba ana muangusha madarakani adui yako”

“Ushahidi atautoaje?”

“Wewe zubiri uone”

Tukatoka ndani humu na kuwakuta Biyanka na walinzi wake wakiingia kwenye moja ya gari na kuondoka huku baba yao akiingia kwenye gari jengine na walinzi wake na kuondoka eneo hili. Tukaelekea lilipo gari langu na kuanza kurudi hotelini. Nikafika hotelini na kuchukua kadi yangu ya kufungulia mlango, moja kwa moja nikapitiliza hadi chumbani kwangu huku kichwa changu nikihisi kikiwa kimevurugwa kisawa sawa.

“Namuacha huyu mwanamke”

“Unakwenda kuharibu kila kitu. Wakati wako wa sasa si wakumuacha”

“Unataka nikae na jini kweli?”

“Mimi ni nani?”

“Ohoo simahanishi jini kama jini. Namaanisha mwanamke mwenye roho mbaya”

“Kuna msemo wa kuwa muwinda hugeka kuwa muwindaji”

“Una maanisha nini?”

“Wao hadi sasa hivi hawajui kuwe wewe ni adui yao mkubwa. Wanacho jua ni kukuzuia katika kusaidia Clara wakihisi kwamba ndio njia sahihi ya kumtoa mbele ya uso wako”

“Ohoo Mungu wangu”

“Jambo ambalo ninakwenda kukueleza ni juu kuwa makini na wale mabinti wawili. Qeen na Latifa”

“Kwani ni wasaliti?”

“Hakuna ambaye atakwenda kukusaliti?”

“Ila?”

Ethan akazungusha kiganja chake cha mkono wa kulia juu ya tumbo lake.

“Sijaelewa?”

“Angalia usije ukawapa mimba na mbaya zaidi wamekupenda kutoka kwenye mioyo yao na wameridhika kuwa na mwanaume mmoja kimapenzi”

“Heeee!”

“Ndio wewe shangaa ila huo ndio ukweli wa mambo unao endelea kwenye mioyo yao”

“Sawa nimekuelewa, ila tuachane na wao kwa sasa naomba umtafute Clara”

“Usijali, kesho mchana muda wa chakula nitakuchukua ukamuone sehemu nitakapo muhifadhi”

“Nitashukuru, ila kuna muunganiko gani kati ya Clara na muheshimiwa Poul Mkumbo?”

“Muunganiko uliupo ni kwamba baba Clara na Poul walikuwa ni marafiki wakubwa sana. Ila Baba Clara alikuwa ni rafiki mwema kwa rafiki yake, ila Mkumbo hakuwa mwema kwa mwenzake. Clara aliweze kumshuhudia mkumbo akimbaka mama yake na kumpa onyo kwamba endapo atazungumza chochote atamuua”

“Mmmmm”

“Mkumbo hakuishi hapo akapanga mpango mzima wa kumuua rafiki yake pamoja na yule kijana aliye kamatwa, baba mdogo wa Clara, na siku ule mpango unapangwa Clara aliweza kuusikia na aliweza kuurekodi kwenye karedio kake kadogo ka taple, ambacho amekificha sehemu anayo ijua yeye mwenyewe”

Maneno ya Ethan yakanikumbusha kipindi wazazi wangu walivyo kuwa wana uwawa na vijana wa mkumbo huku mimi na mama tukiwa tumejificha kwenye migomba.

“Huyu mzee ni mwana haramu sana”

“Ni zaidi ya mwana haramu, mimi nina ondoka tutaonana kesho”

“Sawa”

“Ila usizungumze kitu cha aina yoyote kwa Biyanka”

“Nimekuelewa”

Ethan akatoweka kwenye upeo wa macho yangu na kuniacha peke yangu humu chumbani. Nikavua nguo zangu zote na kupanda kitandani na kulala.

***

Kengele ya mlangoni ikanistua kutoka usingizini. Nikautazama mlango wa chumba changu kwa sekunde kadhaa kisha nikashuka, nikachungulia kwenye kishimo kidogo na kumuona Biyanka akiwa amevalia vizuri sana. Nikafungua mlango na taratibu akaingia huku akiwa amejawa na tabasamu. Akanikumbatia na kunibusu mdomoni mwangu kama si yeye aliye toka kufanya tukio la ujambazi.

“Umeshindaje mpenzi wangu”

“Salama, vipi”

“Safi, mwili wako mbona ni wa moto?”

Biyanka alizungumza huku akiniwekea kiganja chake kimoja kwenye shingo.

“Nahisi ni uchovu wa kulala ila mwili utakaa sawa”

“Mmmm kama una umwa twende hospitalini mpenzi wangu”

“Nipo sawa”

“Sasa hivi ni saa mbili, una onaje leo tukatoka chakula cha usiku mpenzi wangu”

Nikamtazama Biyanka kwa sekunde kadhaa kisha nikamkubalia kwa kutingisha kichwa. Nikaelekea bafuni na kuanza kuoga, nikarudi huku nikiwa nimeshika taulo la kujifutia maji mkononi mwangu. Biyanka akalichukua taulo hili na kuanza kunifuta, kila nikimtazama usoni mwake nina likumbuka tukio alilo kuwa ana lifanya.

“Ulikuwa wapi?”

Nilimuuliza Biyanka huku nikimtazama usoni mwake kwa macho ya kumdadisi.

“Nilikuwa nyumbani kwa mama”

Nikatamani kumshushia tusi kubwa ila nikajikaza moyo wangu.

“Anaendeleaje mama?”

“Aha…salama ana kusalimia. Pia baba anasehema kwamba analihushulikia swala lako la kutishiwa pia niliweza kumueleza juu ya Clara na akaseme kwamba yote atayafanyia kazi”

‘Jamani mbona umekuwa muongo wewe mwanamke?’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama Biyanka usoni mwake.

“Nitashukuru, nitolee pensi na tisheti ile ya kijivu ndio najisikia kuvaa usiku wa leo”

“Poa mume wangu”

Nikachukua simu yangu na kuanza kuikagua, nikatamani kuwatumia meseji Biyanka na Qeen ila nikajizuia, sihitaji kuwaingiza matatizoni watoto wa watu. Nilipo maliza kuvaa, tukatumia gari la Biyanka kuondoka eneo hili huku walinzi wakitufwata nyuma na gari lao. Tukafika katika moja ya hoteli ambayo sikumbuki hata jina lake lililo andikwa nje.

“Ethan unaonekana una mawazo sana mpenzi wangu”

“Kichwa changu kwa leo hakipo vizuri”

“Tambua baba yangu ana shuhulikia kija jambo mpenzi wangu kuwa na amani na kesho anakwenda kuwaleta wale walinzi alio kuahidi”

Nikafumba macho ili kuzuia hasira yangu, kwani hao watu ninao letewa naamini watakuwa ni wachunguzi kwangu, nikashusha pumzi taratibu na kumtazama Biyanka ambaye taratibu akausogeza mikono yake na kunishika mikono yangu.

“Tambua kwamba familia yetu inakupenda sana Ethna ipo tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha kwamba kila kitu kina kwenda vizuri kwenye maisha yako”

“Nashukuru”

“Tena nina wazo mpenzi wangu. Hivi kodi ya pale hotelini si inaisha mwezi ujao?”

“Ndio”

“Unaonaje ukahamia nyumbani kwangu na tukaishi pamoja”

“Nitalifikiria ila mwishoni mwa mwezi ujao nitakwenda Ujerumani kufwatilia baadhi ya kampuni zangu”

“Unaonaje tukaenda wote?”

“Nani atasimamia kampuni yangu?”

“Si kuna mameneja wengine mume wangu”

“Wewe utasimami”

Nilizungumza kwa jazba kidogo na kumfanya Biyanka kukaa kimya na kukubaliana na kile nilicho kizungumza. Baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku tukarudi chumbani. Biyanka akaanza uchokozi wa kunishika shika mwili wangu. Kusema kweli hata ile hisia ndogo niliyo kuwa nayo kwake imenipotea kabisa. Biyanka akaanza kumnyonya jogoo wangu huku nikiwa nimejilaza chali. Jogoo wangu alipo simama dede, taratibu akamkalia na kuanza kujihudumia.

“Aiisii…ohooo tamu baby”

Biyanka alizungumza huku akiichukua mikono yangu na kishikisha kiuno chake anacho jitahidi kukizungusha kama feni bovu.

“Mume wangu kuwa nami, sijakuzoea kukuona hivi”

“Sawa”

Nikaanza kuvuta hisia za mautundu ambayo nilikuwa nina fanyiwa na Qeen pamoja na Latifa, sikumaliza hata dakika tano nikajikuta nikifika kileleni na mchezo ukaishia hapo, sikujali kama Biyanka amefika kileleni au laa. Taratibu Biyanka akashuka juu yangu huku akiwa mnyonge sana, sikuhitaji kumsemesha kitu chochote zaidi ya kugeukia pembeni na kuulazimisha usingizi.

“Ethan nahitaji tuzungumze kidogo”

“Tutaonge kesho”

“Nakuomba mume wangu”

“Hivi nikisemea kesho hunielewi Biyanka? Akili yangu imechoka nakuomba uniache bwana”

Nilizungumza kwa ukali sana na Biyanka hakuwa na namna zaidi ya kutii. Masaa yakazidi kukatika pasipo sisi wawili kulala kama tulivyo zoeshana, kwani nilizoea kumkumbatia Biyanka kwa nyuma. Sikupata usingizi kabisa hadi kuna pambazuka. Tukaamka na kujiandaa kwa ajili ya kelekea ofisini.

“Kazi njema mume wangu”

Biyanka alizungumza huku akinibusu shavuni mwangu na kuelekea ofisini kwake. Nikaingia ofisini kwangu, kama kawaida, jumatatu huwa kuna ripoti nyingi ambazo kama mkurugenzi ninatakiwa kuzipitia ili niweze kujua ni kitu gani kinacho endelea. Nikawatumia meseji ya Qeen na Latifa, nikiwaomba muda wa mchane nikakutane nao mwenge ili niweze kuongozana nao kuelekea alipo ficha Clara. Kila mmoja akanijibu atakuwa tayari japo sijawaeleza ni wapi tunakwenda. Mlango wa ofisini kwangu ukafunguliwa na Biyanka akaingia, akayatazama mafaili yaliyo jazana ofisini kwangu.

“Mume wangu hujafanya kazi leo?”

“Ndio”

“Ohoo unaonaje ukaenda hotelini ukapumzike na mimi niweze kushuhulika na hii kazi hapa kwani ofisini kwangu nimesha maliza kila jambo”

‘Usiende sehemu yoyote huo ni mtego’

Niliisikia sauti ya Ethan ikinikanya kwa ukali sana, jambo lililo nifanya nibaki nimekodelea macho Biyanka na kushindwa kumjibu kwani sifahamu ni mtego gani ambao mwanamke huyu amekusudia kuniwekea.



“Usijali mke wangu, nitajitahidi kuzifanya kazi zote mwenyewe.”

Nilizungumza huku nikitabasamu.

“Kweli mume wangu?”

“Ndio, nitazifanya taratibu kwa sas anahitaji muda wa kupumzika kidogo kisha nitaendelea na majukumu mpenzi wangu”

“Sawa”

Biyanka akanibusu mdomoni kisha akatoka ofisini kwangu. Nikamuona Ethan akiwa amekaa kwenye moja ya sofa zilizopo hapa ofisini.

“Umesema mtego gani?”

“Tayari amesha anaza kukutilia mashaka”

“Mashaka ya nini?”

“Anahitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa maana jana ulivyo toka hotelini kuna muhudumu alimtumia meseji kwamba umetoka”

“Kwahiyo amewahonga wahudumu ili waweze kunichunguza?”

“Ndio na hapa alihitaji uweze kutoka ili afahamu unaelekea wapi, angekufwata nyuma kwa nyuma na taksi na wewe akili yako ilisha panga kukutana na wale wasichana wako. Ingekuwa ni bonge la tatizo katika siku ya leo”

“Mmmmm kazi kweli kweli, je mtoto yupo wapi?”

“Tayari yupo sehemu salama, ila nahitaji tuelekee sisi wenyewe sasa hivi, hao wasichana wako kwa sasa achana nao. Umenielewa?”

“Sawa”

Ethan akanisogelea na kunishuka kifuani mwangu, nikamshuhudia akiingia mwilini mwangu na mwili wangu wote ukaanza kusisimka na kujawa na nguvu ya ajabu. Sikuweza kulishangaa hili kwani si mara ya kwanza kwa Ethan kuweza kufanya hivi. Kufumba na kufumbua nikajikuta nikielea angani kwa kasi huku magorofa ya jiji hili la Dar es Salaam tukiyaona kwa chini sana. Tukafika kwenye moja ya kisiwa ambacho kina miti mingi sana na katikati kuna nyumba moja tu. Tukashuka ardhini na Ethan akatoka mwilini mwangu.

“Hapa ndipo ulipo muweka Clara?”

“Ndio amelala kwa sasa humo ndani hajaniona”

“Kuna usalama kweli?”

“Ndio kwa maana wale vijana nime waua. Sasa wewe utakuwa ni mtu wa kumshawishi aendelee kuishi hapa na asidhubutu kuinigia jiji la Dar es Salaam kwani itakuwa ni hatari sana.”

“Sawa”

Tukaongozana na Ethan hadi ndani. Japo hii nyumba kwa nje ina onekana ni ya kawaida sana ila kwa ndani ni nyumba moja nzuri. Ina kila kiti kizuri kinacho hitajika katika nyumba nzuri, nikaingia chumbani na kumkuta Clara akiwa bado usingizini. Nikaka taratibu pembeni ya kitanda chake na nikaanza kumuita kwa sauti ya upole sana. Clara akafumbua macho yake, tukatazamana kwa sekunde kadhaa huku akionekana kujaribu kuitathimini sura yangu. Clara akaka kitako na kwa haraka akanikumbatia huku akimwagikwa na mchozi.

“Ethan umekuja kuniokoa tena”

“Ndio mdogo wangu. Nimekueleta sehemu salama”

“Wapi?”

“Hii ni nyumba ambayo nimekununulia, ipo huku porini kisiwani. Nina imani kwamba hapa hakuna adui ambaye anweza kukufikia”

Clara akaanza kuangaza huku na kule ndani ya chumba hichi. Chumba hichi kimejaa midoli mingi ambayo kwa mtoto kama Clara inaweza kumuondolea mawazo pale atakapo amua kuanza kucheza nayo.

“Twende ukaone huku”

Nilizungumza huku nikinyanyuka kitandani, Clara akashuka kitandani na nikamuonyesha bafu lililomo humu ndani ya chumba chake, kisha nikamtoa hadi sebleni, nikampelekea jikoni kisha nikatoka naye nje ambapo nyumba hii imezungukwa na bustani nzuri sana za maua.

“Kila kitu unacho kiona hapa mdogo wangu ni mali yako”

“Kweli kaka Ethan?”

“Ndio mdogo wangu. Kitu ninacho kihitaji ni wewe kuwa salama”

“Nashukuru sana”

Clara alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu na kuanza kulia. Nikamnyanyua na kurudi naye sebeleni, nikamalisha kwenye moja ya sofa kisha nikaka kwenye sola lililopo mbele yake na tukaanza kutazamana.

“Naamini unamfahamu maadui wanao kuwinda si ndio?”

“Ehee”

“Unamfahamu nani na nani?”

“Kwa majina siwafahamu”

“Ohoo ngoja kwanza”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kuanza kumuonyesha Clara picha ya kwanza ya mzee Poul Mkumbo. Clara akastuka sana huku macho yakimtoka.

“Ni huyu?”

“Eheee ni huyu”

Nikamuonyesha Clara picha ya Biyanka. Pia akastuka sana.

“Huyu dada amekufanya nini?”

“Aliniteka”

“Alikuteka?”

“Ndio na alinikabidhi kwa watu ambao siwafahamu na walitaka kuniua na sikujua ni nini kilicho weza kutokea”

Clara alizungumza kwa sauti iliyo jaa mtetemesho. Nikamtazama Ethana aliye kaa sofa jengine na Clara hakuweza kumuona.

“Unamkumbuka aliye kusaidia?”

Clara akatingisha kichwa akimaanisha kwamba hakumbuki.

“Sawa. Unaweza kupika?”

“Ndio”

“Kule jikoni kuna kila kitu, nitakuwa ninakuja kukujulia hali kila baada ya simu moja”

“Sawa sawa”

Nikatazama simu ya mezani.

“Hiyo simu utaitumia kuwasiliana nami kila pale utakapo kuwa na haja nami”

“Sawa kaka Ethan”

Nikatoa kadi yangu ya biashara ambayo ina namba ya simu na kumkabidhi Clara. Nikaagana naye kisha tukoandoka na Ethan. Katika muda mfupi tu tukafika ofisini kwangu huku kidogo nikiwa na furaha.

“Ngoja nikusaidie”

Ethan alizungumza huku akika kwenye kiti changu, akaanza kupitia faili moja baada ya jengine huku akiifanya kazi hiyo kwa kasi kubwa sana. Ndani ya dakika kumi akamaliza kila kitu, kwa ishara akaniomba niweze kukaa kwenye kiti changu.

“Vipi unaonanaje kampuni yangu?”

“Inakwenda vizuri, ila inabidi uwaambie watu wanao shuhulika na maswala ya matangazo wazidishe ubunifu katika matangazo yao. Pia muboreshe vifurushi vya internet, viwe vikubwa ila kwa bei nafuu sana”

“Sawa nimekupata rafiki yangu”

“Kitu kingine kuwa makini na hao wanawake wako. Siku ukiwagonganisha, kutachimbika”

“Hahaaaa”

“Wewe cheke. Camila anakula tizi, sasa siku akija kukupiga mimi sinto kutetea kwa maana huo ni ugomvi wa mke na mume nitakaa pembeni”

“Hivi unahisi kwamba Camila anaweza kufahamu juu ya haya mahusiano yangu mapya”

“Hata sasa hivi akihitaji kufahamu anaweza kufahamu, ila shukuru Mungu nimefunga ufahamu wake wa akili katika maswala ya mahusiano. Wewe mwenyewe nina imani kwamba una fahamu jinsi alivyo na wivu”

“Ndio“

“Haya, namuona mke wako feki anakuja kukuchukua mukale luch baadae”

“Poa”

Kitendo cha Ethan kupotea hapa ofisini, Biyanka akaingia huku akiwa na furaha sana.

“Vipi mke wangu?”

Nilimchangamkia huku nikinyanyuka kwenye kiti changu na kumlaki kwa kumkumbatia.

“Baba amenipigia simu muda mchache ulio pita na kudai kwamba amemkamata yule mtu aliye kutumia meseji za vitisho”

“Weeeee!!”

Niliitikia kinafki tu kwa maana nina elewa kila kitu kinacho endelea.

“Ndio na kwa sasa yupo polisi kwa mahojiano huku wezake ambao walikuwa wamemkamata mtoto, wawili wameuwawa huku yeye akiwa amekamatwa na polisi”

“Na mtoto je?”

“Mtoto sijui wamempeleka wapi hapa ndioa anaendelea kuminywa na askari wapelelezi, kwani afande Kimaro hajakupigia simu?”

“Hapana hajanipigia”

Nikaitoa simu yangu mfukoni na kwa bahati mbaya nikaikuta ikiwa imezima chaji.

“Ohoo imezima chaji”

“Ndio maana nahisi alikupigia sana hajakupata hewani”

“Basi twende huko polisi”

“Mmm sasa hivi ni saa saba, twende tukapate chakula cha mchana kisha ndio tueleke huko polisi”

“Sawa, tukirudi hivi niandalie kikao na watu wanao dili na kitengo cha matangazo”

“Kuna nini tena?”

“Wewe anda kikao mke wangu”

“Sawa, basi ninaomba dakika tano nikawape taarifa”

“Poa”

Biyanka akatoka ofisini humu na kuniacha peke yangu. Nikafungua droo na kutoa chaji yangu na kuichomeka simu yangu huku nikijaribu kuiwasha. Simu ilipo fanikiwa kuwaka, nikawatumia meseji Qeen na Latifa na kuwajulisha kwamba hatuto weza kwenda sehemu niliyo waahidi kwenda mchana wa leo.

“Tayari mume wangu”

Biyanka alizungumza huku akiwa amefungua mlango. Tukatoka humu ofisini na kueeka eneo la magesho. Tukaeleka kwenye moja ya mgahawa, tukapata chakula cha mchana kisha tukaelekea kitua kikuu cha polisi. Tukapokelewa na afande Kimaro ambaye moja kwa moja akatupeleka hadi kwenye chumba cha mahujiano. Nikajikuta nikiachia msonyo mkali sana hadi Biyanka na afande Kimaro wakashangaa.

“Tuliza jazba mume wangu, acha polisi wafanye kazi yao”

Biyanka alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia, akihisi msonyo wangu unahusika na hasira kumbe sivyo kwani mtu waliye mkamata hapa ni tofauti kabisa na yule ambaye Biyanka alikuwa ampiga vizungu.

“Wanampiga kweli atazungumza?”

Nilimuuliza afande Kimaro huku tukiwa tumekaa katika chumba cha pilia na katikati kuna kioo kikubwa ambacho sisi tunaweza kuwaona watu waliopo katika chumba hicho cha mahojiano ila wao hawawezi kutuona sisi tulipo katika chumba hichi cha wasililizaji.

“Ndio kwa kumpiga vile ni lazima atataja ni nani ambaye amemuagiza”

“Ila naona kama haito saidia”

“Hiyo ni adhabu moja tu Ethan, ila kuna adhabu nyingine nyingi sana ambazo zitafwata ni lazima atataja”

Afande Kimaro alizungumza huku akijichekesha chekesha. Laiti watu hawa wangekuwa wanajua kwamba nina fahamu ujinga wao wote wala wasinge kubali hata kukaa karibu na mimi.

“Badilisha adhabu”

Afande Kimaro alizungumza huku akiminya moja ya batani. Askari wawili walio ndani ya chumba hicho nikawaona wakivaa gloves mikononi mwao.

“Samahani, munaweza kunipa dakika hata moja nikazungumza naye?”

Biyanka na afande Kimaro wakanitazama kwa mshangao, kisha wakatazamana na Biyanka akakubali kwa ishara ya macho.

“Sawa ila inabidi askari hao waweze kubaki ndani ya chumba hicho”

“Hapana nahitaji watoke kabisa na vifaa vyao hivyo vya mateso. Nahiji wakalishe kwenye kile chumba wamfunge tu pingu basi”

“Ila huyo tuliye mkamata Ethan ni mtu hatari ni jambazi moja hatari sana”

“Usijali nitakuwa salama”

“Ila mume wangu h…..”

“Hapana mke wangu, niamini, nitakuwa sawa”

Afande Kimaro akawaamuru vijana wake kufanya vile nilivyo hitaji. Nikavua koti langu la suti na kumkabidhi Biyanka, nikavua saa yangu hii ya dhahabu ambayo niliinunua dola elfu ishirini na tano na nikamkabidhi pia Biyanka.

“Kuwa makini mume wangu”

“Usijali”

Nilizungumza huku nikianza kuelekea katika mlango wa kuingia katika chumba hichi. Nikaikunja mikono ya shati langu, nikaburuza kiti kimoja cha chuma na kukiweka mbele yake. Nikatazama kamera nne tatu zilizo weka kwenye kona za hichi chumba.

Jamaa huyu aliye jaa majaraha mwili mzima akanitazama kwa macho yaliyo jaa huzuni kubwa sana. Kwajinsi tu anavyo onekana kwenye macho yake hana hata sifa ya ujambazi. Nikanyanyuka na kuanza kumzunguka jamaa huyu kama mara nne hivi huku nikiendelea kumdadisi huku nikihakikisha kwamba udadisi wangu hauwezi kunaswa na kamera hata moja iliyo kwenye chumba hichi kwani kila kiti kina rekodiwa. Nikajikuta nikitabasamu mimi mwenyewe huku nikikaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia hapo awali.

‘Waseng** hawa wamemleta bubu humu ndani sasa atazungumza nini?’

Nilijikuta nikizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama jamaa wa watu jinsi anavyo chirizika damu, nikashusha mikono yangu chini kidogo usawa wa mweza hii na nikaanza kuzungumza na ishara za vidolea huku nikimuuliza jamaa huyu ni kosa gani ambalo limemfanya hadi kukamatwa na polisi. Nikajikuta nikishtajabu sana mara baada ya jamaa huyu kuniambia kosa la yeye kukamatwa na polisi ni kuiba kuku tena jogoo tena mitaa ya uswahilini, taratibu nikajikuta nikishusha pumzi huku nikitingisha kichwa kwa kumsikitia jamaa huyu mnyonge.



Ili kudhibitisha hilo, nikamuuliza tena kwa ishara jamaa huyu kwamba ni kweli amaeiba kuku. Jamaa akakiri kwa kuapa kabisa huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikanyanyuka kwenye kiti changu na kutoka katika chumba hichi.

“Vipi?”

Biyanka aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu kwa umakini sana.

“Afande mumesema kwamba huyu ndio mtuhumiwa aliye nitumie meseje”

“Ndio”

“Sasa mbona hazungumzi?”

Niliuliza swali la kizushi kwa maana ishara zote ambazo nilikuwa ninazizungumza na jamaa huyu ni tofauti kabisa na ishara ambazo watu wa kawaida wamezizoea kuweza kuzungumza na watu wenye ulemavu wa kuzungumza(Mabubu). Ishara nilizi zitumia mara nyingi tunazitumia katika mchezo wa mpira pale wachezaji wanapo amua kubadilisha mfumo wa kucheza pasipo timu pinzani kufahamu kwamba kuna mkakati unapangwa.

“Nahitaji apelekwe mahakamani”

“Kuna mambo kidogo tunayahitaji kuyapata kutoka kwake, tukiyakamilisha basi tutampeleka mahakamani”

“Ahaa…Itachukua muda gani?”

“Kama siku moja au mbili hivi”

“Sawa afande acha sisi tuende”

Nilizungumza kwa msisitizo hadi Biyanka mwenyewe akashangaa. Tukatoka eneo hili na kuingia kwenye gari tulilo jia.

“Tunaelekea ofisini au nyumbani?”

“Ofisini, nimeiacha simu yangu kwenye chaji”

“Poa”

Tukaondoka eneo hili la polisi huku kichwani mwangu nikijaribu kupanga na kupangua mipango ya kuweza kumsaidia mtu huyu aliye kabambikiwa kosa kubwa toafuti na lile alilo lifanya.

“Nitampata tu”

Nilijikuta nikiropoka hadi Biyanka akanitazama.

“Nani tena mume wangu”

“Hakuna tatizo”

“Niambie tu mume wangu, kama kuna tatizo lolote ninakuomba uweze kuniambia?”

“Hakuna”

Tukafika ofisini, moja kwa moja tukaeleka ofisini kwangu.

“Mkurugenzi kikao tayari”

Sekretari wangu alizungumza mara baada kuingia ofisini hapa. Nikamruhusu atoke ofisini kwangu na akaendelee na kazi zake.

“Unaweza kuingia kwenye kikao na hali hiyo mume wangu?”

“Ndio ninaweza, kwani nipo vipi?”

“Unaonekana kutokuwa sawa. Kama ni adui yako ndio yote tumesha mkamata, askari wakimaliza kufanya upelelezi wao basi watampeleka mahakamani. Au unahitaji polisi wamuulie gerezani ili kusiwe na mlolongo mrefu mume wangu”

Nikamkata jicho kali Biyanka hadi akastuka, toka niwe naye kwenye mahusiano nina imani kwamba hajawahi kukutana na sura yangu ya kuchukizwa kama hii.

“A…ha….a….si..ku….a…w.a na mahaan hiyo mume wnagu”

Nikanyoosha kidole kuelekea mlangoni. Biyanka akautazama mlango kisha akanitazama mimi.

“TOKAAAAAAAAAAA”

Nilizungumza kwa hasira huku nikiibamiza meza kwa nguvu, nikamshuhudia Biyanka akiyumba na kujikuta akiakaa chini pasipo kupenda. Akaanza kuhema kama mtu ambaye amefanikiwa kuwatoroka mbwa walio kuwa wanamkimbizi kwa umbali mrefu sana.

“Nikiwa ninafikiria mambo yangu, sihitaji ushauri wa kipuuzi umenielewa?”

“Eheee”

“Nenda ofisini kwako na muda wa kazi ukiisha nenda nyumbani kwako. Leo ninahitaji kuwa peke yangu sawa”

“Unas…..”

“Hakuna cha ninasema, ni hivi leo nana hitaji kuwa peke yangu. Sihitaji kukupasua kichwa chako hicho Biyanka”

Nilizungumza kwa kujiamini huku nikimtazama kwa hasira, hadi mikoyo yangu ina nitetemeka. Biyanka taratibu akanyanyuka na kujiweka vizuri koti lake la suti hii ya kaki aliyo vaa. Akaanza kutembea kwa unyonge kuelekea nje. Nikaka kwenye kiti changu na kukiburuza hadi karibu kabisa na kioo kikubwa ambacho ni kama ukuta wa kuelekea nje. Nikaanza kutazama madhari ya magorofa ya jiji hili la Dar es Salaam.

Nikaanza kukumbuka kwamba, kipindi nilipo kuwa mdogo, kitu nilicho kuwa nina kihitaji ni nguvu. Nguvu ambayo ni lazima iweze kusimamishwa kwanza na pesa kisha niweze kuwa na watu ambao wanaweza kupigana kwa ajili yangu, iwe kwenye shida au raha.

‘Nahitaji kuwaangusha hawa washenzi’

Niliendelea kuwaza akilini mwangu.

‘Lazima niweze kumtafutia mwana sheria kijana huyu. Hapa ndipo ninaweza kuanza kupata nguvu’

Nikaitazama simu yangu sehemu nilipo iweka, nikaichomoa kwenye chaji. Nikaitafuta namba ya Qeen, nilipo ipata, nikataka kumpigia ila nikaona sio jambo zuri. Nikanyanyua na kueleleka katika ukumbi wa mikutano. Nikawakuta wafanyakazi wote pamoja na meneja wao, ambao wanahusika na maswala ya matangazo.

“Samahani kwa kuchelewa”

“Hakuna mashaka mkurugenzi”

“Sawa, kikao changu hakito kuwa kirefu sana zaidi ya kuhitaji kutoa maagizo machache kwenu nyinyi. Kama munavyo fahamu, nyingi nio watu muhimu sana katika kuhakikisha kwamba wateja wanatumia mtandao wetu wa simu. Ninahitaji kwa mwenzi huu unao kuja, tushushe kiwango cha bei za bando za internet, pia bando za watu kuzungumza. Asilimia ya kushusha iwe ni ishirini kwa kila kifurushi. Lengo ni kuwafikia watu wengi sana ambao wengi wao ni wa hali ya chini. Sijui nimeeleweka?”

“Ndio mkurugenzi una eleweka”

“Mfano mdogo tu, endapo wezetu bando zao zitaanzia buku si ndio munavyo sema”

“Yaa elfu moja”

Meneja alizungumza huku akitabsamu.

“Sisi tukaweka GB 1 kwa sh mia sita tu, nina imani kwamba katika mzunguko wa kibiashara tuatapa wateja wengi sana kuliko wale watakao weka GB moja kwa sh elfu mbili.”

“Wekeni matangazo mazuri, yakuvutia. Wekeni wadada wazuri na wakaka wazuri sana wanao vutia. Walipeni vizuri, sihitaji figisu figisu huko kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na malipo. Kama mtu atafanya kazi ya kutuingizia mabilioni ya pesa, munashindwaje kumlipa milioni mia au mia mbili kwa tangazo. Hilo meneja lifanyie kazi. Munaona tumeshika namba mbili, awamu inayo kuja nahiji tushike namb moja na kama ni moja basi tusing’oke kabisa. Nakaribisha maswali”

Nilizungumza huku nikiwatazama wafanyakazi wangu wote.

“Ahaa mkurugenzi unaonaje tukakuweka kwenye tangazo moja wapo kwa maana una lipa kwa kweli?”

“Haaha, mutanilipa kiasi gani?”

Jibu langu likawafanya watu wote kucheka humu ndani.

“Nilikuwa ninatania jamani. Kwa mimi kuwa katika matangazo ya kampuni yangu mwenyewe, kwanza itakuwa ni roho mbaya, kwani kuna vijana wanajitahidi masikini ya mungu kwenda gym kila siku kutengeneza vifua. Wadada wengine nao ndio hao kila siku kuweka diate kwa ajili ya kutengeneza miili yao. Sasa inabidi juhudi zao siku moja ziweze kuzaa matunda. Nina imani kwmaba nitakuwa nimekujibu kisiasa japo mimi sio mwana siasa”

Watu wakaendelea kucheka, japo moyoni mwangu nimejawa na chuki kubwa sana ila nina hakiksisha kwamba hakuna mfanyakazi wangu hata mmoja ambaye anaweza kutambua ni kitu gani kinacho endelea kwangu.

“Mkurugenzi mimi nikuahidi, hili jambo mimi na timu yangu tutalishuhulikia kwa haraka sana na baada ya mipango yote kuweza kukamilika basi tutakueletea taarifa”

“Sawa. Nina wazo jengine moja muhimu sana. Hivi munaweza kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa timu kubwa kubwa?”

“Ndio inawezekana mkurugenzi”

“Tunaweza kuanzisha kombe letu. Hivi hawa wanao shiriki ligi kuu ya hapa nchini wanagombania milioni ngapi?”

“Sabini au themanini hivi”

“Ni themanini mkuu”

“Ahaa, sasa sisi tuanzishe kombe letu, mshindi wa kwanza ana pata dola laki moja na nusu itakuwa kama kiasi gani?”

“Milioni miatatu na usheee”

“Ushee ndio nini jamani?”

“Hahaaa, mkurugenzi ushee inamaanisha ushenzi. Mara nyingi hutumika kwenye kuongezea vionjo vya pesa nyingi nyingi hivi. Kama milioni kumi na ushenzi hivi”

Meneja bwana George alinielewesha na kujikuta nikiwa na furaha sana ya kufahamu kishwahili cha aina hiyo.

“Sawa hilo anza kulifwatilia kisha utanipa ripoti. Ila hili la matangazo hakikisheni kwamba linafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo”

“Sawa sawa muheshimiwa”

“Kikao kimekwisha”

Baada ya kumaliza hivyo tukanyanyuka kwenye viti vyetu na kutoka ukimbini humu. Nikapita kwenye mlango wa ofisi ya Biyanka, nikapiga hatua mbili mbele kisha nikarufi nyuma. Nikasoma kibao kilichopo juu katika mlango wake huu. Taratibu nikafungua mlango wake na kuingia ndani.

“Nimesema sitaki watu h……..”

Biyanka mara baada ya kunyanyua uso wake alio kuwa ameuinamisha chini ya meza yake na kuniangalia ni mimi akakatisha sentensi yake. Mashvu yake yote yamelowana na machozi, macho yamekuwa mekundu, unyonge mwingi umemtawala hadi nikaanza kumuonea huruma. Taratibu nikatembea hadi alipo kaa, nikamnyoosha mkono wangu wa kulia na taratibu akaupokea, nikamnyanyua na kumshika kiunoni na kumsogeza kifuani mwangu.

“Una lia nini mpenzi wangu?”

Nilizungumza kwa sauti nzito kidogo ila iliyo jaa mahaba mazito hadi nikahisi mwili wangu ukinisisimka.

“We….w…e….si…umenifukuza”

Biyanka alizungumza kwa sauti ya kudeka, nikakiinamisha kichwa chake begani mwangu.

”Nisamehe mke wangu, haikuwa akili yangu. Unajua toka nimekutana na tukio lile la kutishiwa uhai wangu, basi limeniathiri kisaikolojia na nimejikuta ni mtu wa hasira na mtu wa kutamani kukaa peke yangu muda wote”

Nilijitetea kwa hilo ili kuweza kuficha yale ninayo yafahamu juu ya Biyanka na baba yake.

“Ohoo jamani mpenzi wangu. Kama vipi twende kwa mwana saikolojia akakupe japo ushauri mdogo unao weza kuirudisha furaha yako. Hivi leo ndio nimekona na kufahamu kwamba una tisha Ethan”

“Yaa nalitambua hilo mke wangu?”

“Nimeogopa kwa kweli, nimeshindwa kujizuia mwili wangu hadi nimeanguka chini mpenzi wangu. Nakuomba sana mpenzi wangu twende kwa mwana saikolojia tukitoka hapa kazini. Kwa hali ile tukiwa ndani peke yetu siku unaweza kunivunja hata kiuno changu”

“Sinto weza kufanya hivyo mpenzi wangu. Huko kwenda, tutakwenda siku nyingine sawa mama”

“Sawa, nitampigia ili atupangie siku yetu ya pekee na akatushauri juu ya hili swala”

“Poa mke wangu, mimi kuna kazi ninakwenda kuimalizia ofisini kwangu, nitahitaji utulivu wa kuto buguziwa”

“Sawa mpenzi wangu”

Tukanyonyana midomo yetu na Biyanka kwa sekunde kadhaa kisha nikatoka ndani humu. Nikarudi ofisini kwangu na kukaa kwenye kiti. Nikaindika barua pepe kwa wakurugenzi wote wanao simamia kampuni zangu zote duniani na kuwaarifu leo saa nane usiku kwa maasaa ya Afrika mashariki tutakuwa na kikao kwenye mtando wa skype na kila mmoja wao nimemuagiza kufika na ripoti ya mapato ya miezi takribani tisa ambayo sikuwepo katika bara la ulaya. Kila mmoja aliweza kujibu kwamba ameipata email yangu.

“Vipi”

Nilizungumza kwa sauti ya chini chini huku simu yangu nikiwa nimeiweka sikio la upande wangu wa kulia.

“Safi”

“Sasa nahiji namba ya yule shemeji yenu ambaye ni mbunge”

“Sawa mkuu”

“Jambo jengine, kuweni tayari muda wowote na wakati wowote kuna sehemu ninaweza kuwaita”

“Sawa mkuu”

Nikakata simu mara baada ya kuzungumza na Qeen na Latifa ambao simu zao niliweza kuziunganisha kwa pamoja. Muda wa kuondoka ofisini ukawadia. Tukaondoka na Biyanka huku nikimuomba anipeleke eneo ambalo wana uza laptop zenye ubora wa hali ya juu. Baada ya kununua laptop moja tukaelekea hotelini tunapo ishi.

“Laptop hii ya kazi gani?”

“Leo nina hitaji kuzungumza na wakurugenzi wezangu wa kampuni zangu”

“Ahaaa, sasa kwa nini usinge niambia nikupe laptop yangu?”

“Hapana unajua vitu hivi ni kama simu vile. Unaweza ukawa umeweka mambo yako ya siri ambayo mimi sipaswi kufahamu na mwishowe nikajikuta ninaviona na ikawa shida kwenye mapenzi yetu”

“Ni kweli lakini”

Simu ya Biyanka aikaanza kuita, akaipoke ana kuiweka sikioni mwake.

“Sasa ngapi mama?”

“Sawa ngoja nimuage mkwe wako hapa”

Biyanka akaka simu na kunieleza kwamba mama yake ana muomba waweze kuelekea mkono Arusha kwa ziara ya siku mbili, ikiwa ni moja ya mipango ya kutengeneza njia nzuri za baba yake atakapo pita kwenye kampeni aweze kupata wafuasi wengi bila shida na ukitegemea wanawake wengi ndio wanao penda chama tawala.

“Sawa, muunge mkono mama.”

“Acha basi nieeleke nyumbani kwake. Tutawasiliana mume wangu”

“Nashukuru”

Biyanka akanipiga busu na kutoka ndani humu. Majira ya saa sita usiku nikaondoka hotelini hapa na kwenda kwenye hoteli Ramada, nikawatarifu Qeen na Latifa waweze kufika katika hoteli hii na nikawapa maelekezo ya chumba nilichopo. Baada ya kama dakika aruboini hivi wakaweza kufika hotelini hapa.

“Mkurugenzi umetuita usiku sana vipi kuna tatizo?”

“Hakuna tatizo, ila tunakwenda kuianza kuianza kazi ya kumuangusha mgombea wenu munaye mpenda bwana Poul Mkumbo katika uchaguzi huu”

Qeen na Latifa wakabaki wakiwa wameduwaa, kwani wanafahamu uhusiano wangu wa kimapenzi na Biyanka na mtu ninaye hitaji kumfanyia ukatili ni baba yangu mkwe mtarajiwa.



“U..nataka kuniambia kwamba mtu tunaye hitaji kumuangusha katika hii kazi ni muheshimiwa Poul Mkumbo?”

Qeen aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.

“Ndio.”

“Ethan huoni kwamba huu unaweza kuwa ni mtihani mkubwa sana?”

“Kila mtihani una majibu yake na kila mtihani kuna kufaulu na kufeli. Ukiweka asilimia nyingi za kufeli ndivyo utakavyofeli na ukiweka asilimia nyingi za kufaulu ndivyo utakavyo faulu. Mumenielewa warembo?”

“Ndio Ethan”

“Kaaeni pale, nina kikao kidogo na wafanyakazi wangu”

“Kikao?”

“Ndio mbona muna shangaa?”

“Kikao si tupo wachache kiasi hichi?”

“Sio nyinyi mutawaona”

Nikafungua laptop yangu na kufanya mawasiliano na wakurugenzi nilio waachia kampuni zangu ninazo zimiliki. Ndani ya dakika tano wakurugenzi wote tukawa tunaonana kwenye mtandao huu.

“Habari zenu?”

“Salama mkuu”

“Nahitaji uwakilishi wa maendeleo ya kila mmoja katika kampuni yangu. Wakurugenzi hawa ambao nikikutana nao mimi ndio raisi wao wakaanza kuwakilisha ripoti ya maendeleo kama nilivyo waagiza waweze kuwakilisha. Kila ripoti ya kila mmoja ina maendeleao makubwa, na kampuni zimepata faida kubwa toka nilipo anza kuziongoza na ubadhilifu wa mali za kampuni zangu umepungua kwa asilimia kubwa sana.

“Kazi nzuri kwa kila mmoja wenu. Ila kwa sasa tuna kazi ambayo nina hitaji muweze kunisaidia”

“Kazi gani raisi?”

“Nahitaji kuunga mkono juhudi za chama cha upinzani hapa nchini Tanzania. Nahitaji kuangusha chama kilocho madarakani”

“Ahaa muheshimiwa raisi, kumbuka sisi ni wafanya biashara na endapo tukiingilia siasa za nchi fulani itaweza kutuletea matatizo hapo baadae”

“Ninalitambua hilo. Kila kitu kitakwenda kwa siri sana, na endapo raisi wa upinzani ataongoza nchi, hiyo pesa tunayo kwenda kuiwekeza, ndani ya miezi sita itarudi mikononi mwetu kwa maana kuna migodi mingi na mali nyingi ambazo watatupatia”

“Hapo sawa raisi, nini unahitaji tufanye?”

“Kila oda ya nguo za siasa ambazo wahahitaji mkurugenzi Jong utashuhulika katika kiwanda chako cha kutengeneza nguo. Kuna kiasi cha dola za kimarekani bilioni mbili, nitakihitaji kutoka kwenu, kila mmoja atafahamu anatoa kiasi gani sawa”

“Sawa muheshimiwa”

Kikao kikamalizika na nikazima laptop yangu na kuwageukia Qeen na Latifa.

“Hivi hao wazee wote wapo chini yako Ethan?”

“Ndio wote ni wafanyakazi wangu. Kuna wachina humu, waingereza, warusia, wajerumani, waspain, wabrazil na Wamarekani”

“Aisee unajua sisi tulikuwa tunahisi kwamba kampuni unayo imiliki ni hii moja?”

“Mumesahau nili waambia ni kampuni ngapi ambazo nina miliki?”

“Mimi nimesahau.”

“Tuachane na hilo, hembu wasiliana na yule shemeji yako”

“Usiku huu?”

“Ndio, kila kitu kitakuwa kinafanyika usiku usiku tu, hatuna muda wa kupoteza zimebaki wiki mbili kampenzi zianze”

Latifa akawasiliana na shemeji yake, kisha akanipatia simu niweze kuzugumza naye.

“Ndio boss”

“Nahitaji kuonana na viongozi wako. Vipi ulisha lipanga hilo jambo?”

“Ndio nilisha lipanga na nilisha waeleza”

“Basi kesho majira ya saa nane usiku nitawalekeza ni wapi tuweze kuonana.”

“Sawa sawa muheshimiwa”

“Namba yako nitaichukua kwa huyu binti hapa”

“Sawa kiongozi”

Nikakata simu na kumrudishia Latifa simu yake.

“Kesho latifa nahitaji namba ya simu mpya ambayo sio ya kampuni yetu pamoja na simu ndogo sana. Umenielewa?”

“Sawa sawa mkuu”

“Qeen fikiria ni eneo gani la siri ambalo kesho sote tunaweza kuonana na kupanga mpango wa kujua ni jinsi gani tunaweza ninawasiaida”

“Nimekuelewa mkuu”

“Kwa leo ni hayo, sijui muna mpango wa kurudi nyumbani kwenu au kwa maana sasa hivi ni saa kumi kasoro dakika kumi”

Nilizungumza huku nikiitazama saa ya mkononi mwangu.

“Hapana ni hatari kwa mtoto wa kike”

“Sawa nimewaelewa, jambo jengine la msingi. Hakikisheni kwamba muna tunza siri hii. Hii ni vita ambayo mmoja wetu atakapo kuwa na domo la kubwabwaja maneno. Ninawaahakikishia kwamba atakufa, siwatishi ila ninahitaji kuwaleza ukweli juu ya hilo”

“Tumekuelewa mkuu”

Nikajitupa kitandani, Qeen na Latifa wakanifwata huku wakinitazama kwa macho ya matatamanio.

“Nimekumbuka jambo moja muhimu sana”

Nilizungumza huku nikika kitako kwa maana leo sijisikii kufanya mapenzi na wasichana hawa isitoshe tupo katika wiki ya kufanya kazi, ni lazima akili yangu iweze kupata nafasi nzuri ya kuweza kufirikia mipango yangu muhimu ya kuhakikisha nimpiga adui yangu kimya kimya.

“Ninahitaji mwana sheria mmoja aliye soma, mwenye ujuzi mkubwa sana na anaye weza kuzugumza na bubu”

“Bubu!!?”

“Ndio”

“Kuna nini?”

“Kuna kijana mmoja jana mchana tulikwenda kumtazama pale Central Polisi, alikamatwa kwa kosa la kuiba kuku mtaaani huko ila wao wamebambikia kesi ya kunitishia kuniau. Munaweza kukumbuka juzi nilivyo toka kuchukua pesa, nilisoma meseji moja na nikapoteza amani hadi wewe ukaendesha gari”

“Ndio ninakumbuka”

“Sasa sihitaji kijana yule aweze kubeba kesi moja akubwa namna hiyo ikiwa ana hitaji kuwa huru. Yule ambaye amefanya tukio hilo hapo nina mtambua vizuri sana, ila nitahitaji mtu sahihi ambaye anaweza kunifanyia kazi ya kuweza kumtafuta kimya kimya na kumkamata kwa maana ni mtu hatari”

“Boss kama unamfahamu ntu huyo ni kwa nini usitoe ripoti polisi wakamkamata?”

“Siwaamini polisi kwa maana wao wanakula sahani moja kabisa mgombea uraisi. Unahisi kuna nini kitakacho endelea hapo”

“Mmmm na kweli polisi wetu wanapenda rushwa sana. Hawato fanya jambo lolote kwa huyo jamaa”

“Nani muna mjua jua mwenye uwezo wa kupigana pigana”

“Kwa mimi sifahamu”

“Hata mimi kwa kweli sifahamu”

“Basi acheni, nitalishuhulikia mwenyewe”

Mazumzo yalivyo kata, Qeen, akaanza uchokozi wa kunishika shika mapajani, nikatamani kuzungumza jambo fulani ila jogoo wangu tayari alisha anza kunyanyuka na kujikuta nikikubaliana nao tu waweze kufanya kile walicho kikusudia kukifanya. Ndani ya dakika chache tukajikuta tukizama kwenye penzi zito huku nikihakikisha kwamba kila mmoja nina mpatia haki yake sahihi. Tulipo maliza mizunguko mitatu kwa upande wangu, tukaingia bafuni kwa pamoja na kuoga. Tukajiandaa na kuanza kuondoka majira haya ya saa kumi na moja alfajiri. Nikawapitisha hadi kwenye nyumba wanayo ishia kisha nami nikarudi hotelini kwangu. Sikuhiataji kulala, nikabadilisha nguo na kuelekea ofisini ili niwahi foleni ya jiji hili la Dar as Salaam.

“Habari ya asubuhi mkurugenzi”

Wafanyakazi wangu walinisalimia

“Salama”

Niliwajibu huku nikiingia nao kwenye lifti, tukapandisha hadi gorofani ambazo ndipo zilipo ofisi za baadhi ya wafanyakazi wa vingengo mbali mbali pamoja na ofisi yangu.

“Mkurugenzi za kuamka”

Sekretari wangu alinisalimi huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.

“Salama, ehee niambie kuna mpya gani?”

“Ahaa raisi wa TFF, ameomba aweze kukutana na wewe leo saa tatu asubuhi”

“Raisi wa TFF, ndio nani?”

“Ohoo ni raisi wa shirikisho la mpira wa miguu hapa Tanzania. Nahisi jana aliweza kupokea lile pendekezo la kampuni yetu kuanzisha kombe lake”

“Ahaa sawa mkaribishe”

“Sawa mkurugenzi”

Nikaingia ofisini kwangu, nikaikagua ofisi hii nilipo jiridhisha na usafi ulio fanywa na sekretari wangu nikaka kwenye kiti changu.Majira ya saa tatu nikapata ugeni huu wa raisi wa TFF, nikamkaribisha ofisini kwangu kwa mazungumzo zaidi.

“Heshima yako mzee”

“Nashukuru. Nafurahi kukutana na wewe Ethan”

“Nashukuru muheshimiwa.”

“Jana nilipo pokea pendekezo la wewe kuanzisha ligi yako. Kwanza nilistuka kidogo kwa maana ni wawekezaji wachache sana wa Kitanzania wanao penda kuwekeza katika soka, tena nchini Tanzania. Nilipo kuja kujua dau ni dola laki moja na nusu, nikasema ahaa hapa si pakupaachia paende bure bure au wewe ndio utufwate”

Mzee huyu alizungumza huku akijichekesha chekesha.

“Ndio unajua mimi ni mchezaji”

“Mchezaji?”

“Ndio, inabidi uweze kufwatilia baadhi ya mechi zangu. Ila ngoja”

Nikaingia katika mtandao wa YouTube kwa kutumia simu yangu ya mkononi na kutafuta baadhi ya video zangu na nikamuonyesha mzee huyu. Akaanza kuzifwatilia, uso wake ukazidi kunawiri kwa tabasamu pana usoni mwake, kwani vitu nilivyo vifanya kwenye mpira ni vya kustajabisha.

“Aisee ni kama Messi vile”

“Yaaa nina uwezo mkubwa wa kucheza mpira, hapa nina subiri mambo yangu fulani yakikaa sawa, basi nitachagua moja ya klabu kubwa duniani nitaichezea”

“Kwa nini usichezee Simba au Yanga ili uendelee kuborosha vipaji vya wachezaji hapa Tanzania”

“Hahaa, hakuna timu ambayo ina mchezaji mwenye kiwango changu. Njia nzuri ya mimi kuboresha mpira wa miguu hapa Tanzania ni kuanzisha hiyo ligi. Kingine nitahakiksha kwamba nina miliki timi yangu ambayo itaanzia chini kabisa daraja la chini hadi ipande darala la ligi kuu”

“Ohoo utakuwa umefanya la maana”

“Jambo jengine ninalo weza kufanya ni kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania”

“Hivi wewe ni Mtanzania halisi kweli, kwa maana yule jamaa alivyo niletea ripoti yako sikuwa nina amini amnini?”

“Ndio, mimi ni mchaga kabisa”

“Duuu safi sana, niwachaga wachache sana wanao cheza mpira na wengi wao wanapenda biashara biashara”

“Ni kweli. Jambo la kufanya ni wewe kunitengenezea mazingira ya kuanzisha hiyo ligi, na nitafutie eneo moja ambalo nitaweza kujenga kiwanja changu cha mpira”

“Weeee!!!?”

“Mbona una shangaa mzee kwani mimi ndio nitakuwa wa kwanza kujenga kiwanja, si yupo aliye nitangulia mmiliki wa Azam Club”

“Kweli kweli, ila jinsi unavyo zungumza yaani nina piga picha hicho kiwanja jinsi kitakvyo kuwa”

“Hakikisha ligi yangu inafanikiwa kuingia kwenye mzunguko wa nchi hii, na pia nina pata sehemu ya kiwanja changu, baada ya hapo nitakupa fungu lako ambalo hadi unakufa utakuwa unalitafuna hata ukiamua kuto kupokea umshahara wako wa uraisi wa TFF”

“Weee, sawa sawa muheshimiwa nashukuru, tena nashukuru sana”

Mzee huyu alizungumza kwa heshima kubwa sana. Nikaagana naye na akatoka ofisini humu, Latifa akaingia ofisini kwangu na kunikabidhi simu niliyo muagiza.

“Qeen amefahamu ni wapi tukutane?”

“Bado anafikiria”

“Muambie akifahamu aniambie. Humu kuna salio la kiasi gani?”

“Elfu kumi”

“Itatosha kweli?”

“Ndio muheshimiwa na namba ya shemeji yangu ipo humu”

“Poa nashukuru”

Muda wa mchana, Qeen akanieleza ni eneo gani ambalo tunatakiwa kukutana na watanielekeza kwa simu kuweza kufika huko. Nikamjulisha bwana Samweli ni eneo gani tunaweza kuonana saa nane ya usiku ili tuweze kupanga mipango ya kuweza kuonana. Nikiwa ndani ya gari langu nikielekea ofisini kwangu nikitoka kupata chakula cha usiku, Biyanka akanipigia simu, tukasalimiana kwa furaha sana.

“Vipi mipango yenu?”

“Inakwenda vizuri na tunarudi leo by saa nne usiku tutakuwepo Dar es Salaama, baba anatuhitaji mimi na wewe nyumbani anasema kuna kikao muhimu sana cha kuweza kufanya kama wana familia”

Nikajikuta nikiishia na furaha yangu, kwani sikutarajia kumuona Biyanka akirudi leo jijini Dae sa Salaam kwani anaweza kuwa kipingamizi kikubwa sana cha mipango yangu niliyo ipanga kwa siku ya leo.



“Kikao cha usiku hicho cha namna gani mpenzi wangu?”

“Hata sisi hatufahamu mume wangu. Yaani tulipanga kurudi kesho, ila ndio kama unavyo ona mambo yamebadilika”

“Sawa nimekuelewa”

“Nashukuru mume wangu upo wapi?”

“Ninatoka kula chakula cha mchana kwenye huu mgahawa hapa ambao tumezoea kula”

“Jamani pole, leo umekwenda mwenyewe mume wangu?”

“Ndio mke wangu. Ila usijali katika hilo”

“Sawa, tutaonana baadae basi”

Nikakata simu huku nikifikiria ni jambo gani ambalo ninaweza kulifanya ili kikao nilicho kipanga leo kiweze kwenda vizuri. Nikatoa simu yangu ndogo na kumpigia Qeen, simu yake ikaita baada ya muda ikapokelewa.

“Qeen upo wapi?”

“Nipo ofisini mkuu”

“Sasa nisikilize, huyu bibie atarudi usiku wa leo na kuna kikao nyumbani kwao”

“Ohoo itakuwaje bosi wangu?”

“Jambo la kufanya sasa hivi, hembu muambie Latifa aweze kuwasiliana na wale watu kama ikiwezekana tuonane saa kumi na mbili”

“Jioni hii!!!?”

Qeen aliniuliza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio kwa maana tutakosa muda wa kuweza kuoana nao na kama unavyo fahamu kwamba kikao hichi ni muhimu sana kwetu.”

“Sawa mkuu nitawajulisha kwamba muda wa kuonana umebadilika, ila sehemu si ile ile?”

“Ndio”

“Sawa nitafanya hivyo mkuu”

Nikakata simu, nikafika ofisini na moja kwa moja nikapitiliza hadi ofisini kwangu. Ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu kutoka kwa Qeen, nikaufungua na ananifahamisha kwamba kila jambo lipo vizuri. Majira ya saa kumi na moja nikaondoka hapa ofisini kwangu na kuelekea hotelini nilipo pangisha. Simu yangu ndogo ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kuipokea.

“Latifa”

“Mkuu ndio tunaelekea eneo la mkuatano”

“Sawa mimi nipo hotelini, ila nitakodisha taksi na sinto hitaji watu waweze kuniona huko”

“Poa itakuwa ni vizuri pia”

Nikavaa nguo zangu za mazoezi kisha nikachukua begi langu dogo na kuweka laptop kisha nikavaa earphone masikioni mwangu. Nikachukua kiasi cha pesa kidogo cha kutosha, nikavaa raba ili hata wahudumu walio weka kwama wapelelezi watakapo niona basi wasiweze kustukia juu ya kuondoka kwangu katika hii hoteli. Nikatoka nje ya geti la hoteli, nikatazama barabara huku na kule kisha nikaanza kukimbia hadi kwenye kitu kimoja cha waendesha bajaji. Nikaingia kwenye moja ya bajaji na kumuekeleza dereva huyo sehemu ambayo ninahitaji kuelekea.

“Huko bosi nitakuepelekea kwa ishirini”

“Ishirini elfu au ishirini nini?”

“Ndio mkuu”

“Sawa twende”

Kwa mara yangu ya kwanza kupanda bajaji maishani mwangu ni leo. Dereva huyu kwa utaalamu wake kila muda ana jipenyeza penyeza pembezoni mwa barabara ili kuikwepa foleni hii kubwa ya magari majira haya ya jioni. Tukafika eneo la Kunduchi, ambapo ndipo nilipo elekezwa na Qeen. Tukasimama kwenye nyumba moja yenye geti jeusi, nikamlipa dereva huyu elfu thelathini kisha nikaingia ndani ya geti hili na kukuta walinzi takribani ya kumi walio walia suti nyeusi wakiwa wamesimama katika maeneo mbalimbali ya nyumba hii huku kukiwa na magari kadhaa ya kifahari. Nikamkuta Latifa akiwa amesimaa nje ya nyumba hii, tukaingia ndani na nikawakuta wazee watano huku akiwemo na Samweli shemeji wa Latifa, nikawasalimia wazee hawa kisha nikaa kwenye moja ya sofa.

“Nashukuru kwa kuweza kufika kwenu hapa”

Nilizungumza huku nikiwatazama

“Sisi pia tunashukuru”

“Nina imani kwamba bwana Samweli ameweza kuwaeleza lengo na dhumuni la mimi kuwepo hapa. Mimi ni mfanya biashara na si mwana siasa ila ninahitaji nyinyi muweze kufanya mabadiliko ya uongozi wa hii nchi.”

Wazee hawa wakakaa kimya huku wakinitazama sana usoni mwangu.

“Nahitaji kuwawezesha kifedha zaidi ya chama tawala. Ni nani mume mteua kugombania uraisi hapa?”

“Mimi hapa”

Mzee mmoja mwenye mvu kiasi alizungumza huku akinyanyua mkono wake wa kilia juu kidogo.

“Okay, bajeti yenu muliyo ipanga ni kiasi gani?”

“Tumewekeza bilioni mia mbili?”

“Wapinzani wenu je wamewekeza kiasi gani ulisema?”

“Trilioni moja”

“Nikiwekeza trilioni mbili je mutaweza kufanikiwa kukiondoa chama hicho madarakani?”

Wazee wote wakatazamana huku nyuso zao zikiwa na furaha kubwa sana.

“Inawezekana, unajua kitu ambacho kinatuangusha sana katika hizi siasa ni pesa”

“Sawa, mimi Poul Mkumbo ni baba yangu mkwe mtarajiwa, ila sipo kwake kwa ajli ya kuoa ila nipo kwake kwa asili ya kumuangusha chini. Ninacho kihitaji ni kurudisha mgodi wa baba yangu alio uchukua miaka mingi iliyo pita”

“Unataka kusema kwamba mgodi wa Poul Mkumbo ulikuwa ni wa baba yako!?”

Mzee mmoja aliuliza kwa msahangao sana.

“Ndio”

“Aisee huyu jamaa ni mshenzi sana”

“Mzee wangu unaitwa nani?”

“Jonson Malisa”

“Unakwenda kuwa raisi wa hii nchi, ila nina kuomba endapo utachukua hichi kiti, hakikisha kwamba unataifisha mali zake kisha mgodi huo unanipatia, kama ana mali nyingine ambazo amezichukua kwa ubadhilifu basi hakikisheni kwamba muna warudishia wale ambao wameweza kupokonywa mali zao sawa”

“Hilo linawezekana na halina saka kabisa, nilazima niweze kupambana na ufisadi ulio tukuka katika Tanzania hii”

“Nashukuru kusikia hivyo. Kuna mkatababa nimeuandika hapa, ni wa kusaidi kati yanu na mimi kwani kiasi hichi cha pesa ni kikubwa sana na siwezi kufanya kazi ya kanisa ya kujitolea si ndio jamani”

“Ni kweli”

Wazee hawa walizungumza huku wakitabasamu sana. Nikawasha laptop yangu na kuwaonyesha fumo maalumu ambayo wanatakiwa kuijaza kama mkatabasa, kwa uzuri wa laptop yangu unaweza kundika chochote kwa kugusa kioo chake. Kila mmoja akaanza kuusoma mkabata huu kisha nikawakabidhi kalamu ndogo ya kuandikia katike laptop hiyo. Kila mmoja akaandika saini yake sehemu maalumu huku Qeen na Latifa wakitia saini kama mashahidi.

“Kijana tumesaini ila hatujaona hicho kiasi.”

“Ndio tunapo elekea muheshimiwa raisi mtarajiwa”

Nilizungumza huku nikiingia katika mfumo wa benk ya Bacrays ambao ndio nina hifadhia pesa zangu binafsi za kibiashara.

“Naomba namba yenu ya benki”

Wakanitajia namba yao kisha nikaanza hatua za kuamisha pesa hizi ambazo ndani ya dakika kadhaa kila kitu kikwa kimesha idhinishwa na pesa kuingizwa kwenye akaunti yao. Kila mmoja akaonekana kufurahi sana kwa kazi makubaliano haya.

“Kila mmoja ninaomba email yake”

Wakanitajia email address zao na nikawatumia huu mkatabasa na meseji maalumu ambayo benki ina dhibitisha kwamba wametuma kiasi hicho cha pesa kwenye akaunti yao.

“Kila mtu ana mkataba wake kwenye email yake. Kumbukeni kwamba mambo haya ni ya siri. Jambo jengine, kuna kiwanda changu cha utengenezaji wa nguo nchini China, nitahakikisha kwamba sare zenu munaweza kuzitolea kwenye kiwanda hicho. Nina imani kwamba ni sare nzuri sana zitakazo wapendezesha wafuasi wenu”

“Ndio ndio, ila katika siasa za Kitanzania kuna maswala ya kishirikina”

“Kishirikina ndio nini?”

“Maswala ya kurogana. Je katika hilo tutaweza kuwateka kweli wapinzani wetu?”

Nikaka kimya huku nikiawatazama wazee hawa kwa maana kama ni pesa nimesha wapatia ila kwenye maswala ya uchawi sijui nitawashauri vipi.

“Inabidi na sisi tutafute waganga manguli”

“Tutawapatia wapi mwenyekiti?”

“Kwa kuwapatia, humu humu Tanzania”

‘Waambie nitawasaidia, wasitafute Mganga’

Niliisikia sauti ya Ethan masikioni mwangu.

‘Utawasaidia?’

‘Ndio kwani kuna ubaya, kumbuka hawa wanakusaidia kumuangusha adui yako?’

‘Hivi hawato nisaliti kweli?’

‘Siwezi kusema ndio au hapana, ila binadamu wanabadilika kwa kweli?’

‘Tuseme ndio wamebadilika, tunafanyaje?’

‘Nitahakikisha kwamba kila mmoja ana jutia kwa lile ambao amelifanya’

‘Mmmm sawa’

“Kijana”

Sauti ya mwenyekiti wa chama hichi alinistua kutoka kwenye mazungumzo yangu na Ethan ambayo hakuna hata mmoja wao ambaye ana yasikia.

“Ndio”

“Tumeafikiana hapa kwa pamoja kwamba ni lazima tupate waganga kutoka chini nina imani kwamba watatusaidia?”

“Hapan musitafute”

“Kwa nini, kwa maana haya mambo ya kisiasa yana nguvu za ajabu ajabu kijana”

“Kuna rafiki yangu mmoja ata wasaidia, ila ametoa onyo kwa yoyote ambaye atakuwa ni msaliti. Kwangu au kwa chama hichi basi atajutia kwa nini alisaliti, sasa hiyo haijalishi kwamba umesalitije. Mume nielewa?”

Nilizungumza kwa msisitizo na kuwafanya watu hawa wote kukaa kimya huku macho yakiwatoka.

“Nyinyi kwa nyinyi mukisalitiana, nina waambia kwamba hamto fanikiwa. Japo wanasema kwamba siri ni ya mtu mmoja basi inabidi iwe ya mtu mmoja kwenu. Sawa jamani”

“Tumekuelewa ndugu”

“Jambo jengine ninalo lihitaji kwenu nyinyi, nitawapatia siri nyeti sana kutoka kwa wapinzani wenu. Ila hakikisheni kwamba hazivuji kati yenu na zikarudishwa kwa wapinzani mume nielewa”

“Tumekuelewa kijana”

“Na kila siri kama ni ya kufanyiwa kazi, basi ifanyiwe kazi haraka sana. Na sasa hivi si munapiga kura kwa mfumo wa kielectronic si ndio?”

“Ndio”

“Basi nitawatafutia watu makini sana kwenye maswala ya tecknolojia. Kitu kingine ninaomba kwamba vinywa vyenu visinizungumzie popote hata kwa wake zenu. Kwasababu musiwaamini wake zenu katika mipango yenu ya kichama. Umenielewa mgombea urasi”

“Nimekuelewa mkuu”

“Usije ukasema kwamba huyu anakwenda kuwa first lady wa nchi, na yeye akaanza kujigamba kwa wanawake wezake mwisho mukajikuta jahazi linazama kweupe kabisa.”

“Tumekuelewa kabisa muheshimiwa”

“Nashukuru kwa muda wenu. Mungu akawabariki katika harakati zenu”

Nilizungumza huku nikisimama, nikapeana nao mikono kisha wakaondoka katika nyumba hii na nikabaki na Qeen na Latifa.

“Kweli wewe unafaa kuwa kiongozi”

Latifa alizungumza huku akinitazama

“Kwa nini?”

“Unajua saa zote nimekaa pale kwenye sofa, nilikuwa ninakutazamaaa weee unavyo zungumza kwa msisitizo, hadi watu wazima wamejikuta wakikuita mkuu”

“Hahaaaa, kila kitu ni nguvu ya kuzaliwa nayo”

“Kweli”

“Ila hii pesa yangu itarudi jamani?”

“Itarudi tu, kama wakijipanga vizuri itarudi”

“Je wakienda kugawana na kujenga majumba majumba hata kama wakikosa ndio nitolee?”

Qeen alituuliza huku akitutazama.

“Itarudi tu, mkataba utawafunga. Si nimewaambia kwamba sifanyi kazi ya kanisa eheee”

“Mmm haya”

“Qeen mpigie simu yule dereva aje kutuchukua”

Qeen akafanya hivyo na ndani ya muda mfupi dereva taksi akafika nyumbani hapa tukaingai kwenye gari hili na kuondoka. Wakanishusha kwenye moja ya kituo waendesha bajaji na pikipiki, nikangia kwenye moja ya bajaji na kuondoka eneo hili na safari ya kurudi hotelini ikaanza majira haya ya saa tatu kasoro usiku. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitazama na kukuta ni namba kutoka nchini Ujerumani. Nikaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwangu.

“Ethan”

Niliisikia sauti ya Mery akiniita huku akilia lia.

“Naam”

“Mama hali yake mbaya na kama inawezekana rudi Ujerumani, anahitaji kukuambia neno la mwisho kabla ya kukata roho”

Mwili mzima ukahisi kuzizima na viungo vyote vikafa ganzi, nikajikuta mapigo ya moyo yakinienda kasi hadi jasho likaanza kunitiririka mwilini mwangu.



“Ethan unanisikia?”

“Ndio ninakusikiliza dada”

Nilizungumza kwa kujikaza tu.

“Fanya uje, ninaogopa nipo peke yangu huku”

“Sawa ngoja niangalie maswala ya usafiri”

“Sawa”

Simu ikatwa, nikashusha pumzi nyingi sana huku nikifikiria ni kitu gani ninacho weza kukifanya mtu. Mtu wa kwanza kunijia kichwani mwangu ni Camila mwanamke ninaye mpenda kuliko kitu chochote kwenye maisha yangu. Nikaitafuta namba yake kwenye simu yangu kwa haraka na nikaipata, nikaipga na kuiweka sikioni mwangu, simu yake ikaita baada ya sekunde kadha ikapokelewa.

“Ndio mume wangu”

“Upo wapi?”

“Nipo nyumbani baby, tunapata chakula cha usiku”

“Inabidi twende Ujerumani leo hii hii”

“Leo!! Kuna tatizo gani mume wangu?”

“Hali ya mama ni mbaya sana na anahitaji hospitalini. Hivyo pakiza kili kitu chako nina imani usiku huu utaweza kufika Dar, hapa nitashuhulikia maswala ya ndege ya kukodi”

“Sawa mume wangu”

Camila alinijibu kwa sauti ya unyonge kisha nikakata simu. Nikaingia kwenye mtandoa wa google, nikatafuta ni shirika gani ambalo lina ndege za kukodi, kwa habati nzuri nikapata shirika moja liitwalo THRIPPLE P AIR WAYS. Nikaangalia baadhi ya ndege zao ambazo ni private jet. Nikaridhika nazo, nikachukua namba yao ya simu na kuwapigia.

“Karibu Tripple P Air Ways, unazungumza na Liliana, nani mwenzangu”

Niliisikia sauti ya kike nzuri sana ambayo kidogo ikanita hata ujarisi wa kuzungumza kama mweume mwenye pesa zake.

“Mimi ni Ethan, ninahitaji ndege ya kukodi kuelekea nchini Ujerumani”

“Karibu sana, unahitaji kwa lini”

“Nahitaji kwa leo, nimeona ndege moja aina ya Gulfstreem N60983. Nina imani kwamba ipo nchini Tanzania”

“Ndio muheshimiwa inapatikana. Kutoka hadi Tanzania hadi Ujerumani, itakugarimu kiasi cha dola laki sita na nusu”

“Sawa niwekeeni, nafanya malipo ya awali kwenye akaunti yenu sasa hivi na nikifika hapo uwanja wa ndege kwenye ofisi zenu nitafanya malipo mengine ya mwisho”

“Sawa karibu sana na akaunti namba yetu ndio hiyo iliyopo kwenye tovuti yetu”

“Ninashukuru sana”

Nikakata simu na kwa mara kadhaa dereva huyu bajaji macho yake yote anayaelekezea kwangu.

“Kaka wewe ndio yule Ethan, huku tumezoea kukuita Messi?”

“Ndio”

“Aisee tukifika tunapo kwenda ninaomba tuweze kupiga picha japo moja”

“Sawa”

Tukafika hotelini. Dereva akatoa simu yake, akasimama pembeni yangu na kuanza kupiga picha kadhaa huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Nikamkabidhi kiasi cha pesa ambacho hata sikuzihesabu. Nikakimbilia ndani ya hoteli, nikaingi kwenye lifti na kuelekea juu gorofani. Nikaingia chumbani kwangu, kwa haraka nikavua nguo zangu zote nilizo zivaa. Nikafungua laptop yangu na kuingia kwenye akaunti yangu ya benki ya Bacrays na kuhamisha kiasi cha dola laki tatu na nusu kwenye akaunti ya shirika hili la ndege kisha nikaingia bafuni, kwa haraka nikaoga kisha nikarudi chumbani. Nikaweka begi langu juu ya kitanda na kuanza kuweka nguo zangu kadhaa. Nikampigia Camila simu yake, kwa bahati mbaya sikuweza kuipata hewani. Nikaumbuka kwamba kuna watu wa kuwaga. Nikampiagia simu Qeen kisha nikaiunganisha na Latifa.

“Jamani nina habari sio nzuri”

“Habari gani tena mkuu?”

“Hapa ninapo zungumza nipo kwenye harakati za kuelekea nchini Ujerumani, mama yangu ana umwa sana hivyo ninaondoka usiku huu na nimesha kodisha ndege moja ya kutupeleka huko”

“Ya kuwapelekea huko na nani?”

“Mimi na mke wangu”

“Unataka kusema kwamba unakwenda na Biyanka?”

“Nani aliye waambia Biyanka ni mke wangu, ninakwenda na mke wangu halisi”

“Mmm tuyaache na hayo pole sana Ethan”

“Nashukuru Latifa”

“Pole sana boss’

“Asante Qeen. Ila mipango yetu ipo pale pale hakuna jambo lililo haribika mume nielewa?”

“Tumekuelewa mkuu”

“Kitu kingine hakikisheni kwamba hamtoi siri hii kwa mtu yoyote”

“Tumekuelewa mkuu”

“Nashukuru”

Nikakata simu na kumpigia tena simu Camila huku nikimalizia kulifunga begi langu. Simu yake ikaanza kuita, nikaiweka simu yangu loud speaker na kuiweka kitandani na kuendelea kuvaa nguo haraka haraka.

“Mume wangu?”

“Mbona simu nakupigia haipatikani?”

“Tupo njiani na Dany, kuna sehemu nyingine hazina mtandao”

“Mumefikia wapi?”

“Sijajua ni wapi?”

“Hembu mpe simu Dany”

“Ethan”

“Ndio, mume fika wapi?”

“Kwasasa tupo sehemu inaitwa Mkata, ila kama baada ya lisaa moja hivi na nusu tutafika hapo”

“Sasa nakuomba muje moja kwa moja uwanja wa ndege kwa maana mimi huko ndipo ninapo elekea kwa sasa, kuna mambo ninakwenda kuyamalizia kuyakamilisha kwa ajili ya safari”

“Sawa”

Nikakata simu, nikajiweka vizuri suti hii ya rangi ya kaki niliyo ivaa. Nikaangaza huku na huku kwenye hichi chumba, nikaingiza laptop yangu kwenye begi langu la mgongoni kisha nikalivaa. Nikabeba begi langu hili la nguo na nikatoka chumbani humu. Moja kwa moja nikaeleka hadi mapokezi, nikawakabidhi kadi yao ya kufungulia mlango.

“Akija mke wangu muta mkabidhi hii kadi sawa”

“Una safiri?”

“Acha maswali mengi dada. Mkabidhi hii kadi umenielewa”

“Sawa”

Nikatoka nje na kuingiza begi kwenye gari langu hili. NIkawasha gari na kuanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege. Picha ya sura ya mtoto Clara ikanijia kichwani mwangu, wasiwasi wa kuondoka pasipo kuweza kumuaga ikanijaa moyoni mwangu.

‘Nitarudi’

Nilijifariji huku nikiogeza mwendo kasi wa gari langu. Kuna baadhi ya maeneo iliniladhimu kusimama kutokana na foleni za magari. Simu ikaanza kuita na nikaitazama na kuona ni namba ya Biyanka, moyo wangu ukaendelea kujawa na wasiwasi kwa mana sijamueleza juu ya hili swala la mimi kuondoka.

“Ndio mke wangu”

“Samahani mume wangu, tumeshindwa kupata ndege ya kundoka, hivyo tutarudi kesho asubuhi na kikao pia hakuna kwa usiku wa leo”

“Sawa, ila samahni mke wangu. Mama anaumwa nchi Ujerumani amelazwa na yupo mahututi na ana hitaji kuniona haraka iwezekanavyo”

“Ohoo Mungu wangu, ni nini tena kinamsumbua?”

“Madaktari bado hawajananiweka bayana. Hivyo sasa hivi ninaelekea uwanja wa ndege, nimepata moja ya tiketi kwenye shirika la ndege la fly Emirates. Hivyo ninaondoka Tanzania usiku huu”

Nilimuongopea Biyanka.

“Jamani mume wangu nina kuoena huruma. Ningekuwepo tungeondoka na ndege ya baba”

“Usijali, tutawasiliana, yaani kichwa changu hapa kimevurugika sana, hadi nimesahau kukufahamisha”

“Natambua kwa habari kama hiyo ni lazima kichwa kichanganyikiwe mume wangu. Sawa, nitamueleza mama na baba na tunazidi kukuombea uweze kurudi salama”

“Nashukuru. Kampuni, ninakutegemea mpenzi wangu”

“Usijali mume wangu, nitasimama imara na hakuna ambacho kitakwenda vibaya”

“Sawa ninashukuru kusikia hivyo”

“Ukipanda ndege, samahani nina omba uweze kunifahamisha”

“Sawa”

Nikakata simu na kuendelea na safari yangu ya kuelekea uwanja wa ndege. Nikafanikiwa kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nikashuka kwenye gari langu na kuelekea moja kwa moja kwenye shirika la Thipple P Air ways, nikapokelewa vizuri sana na muhudumu niliye zungumza naye.

“Tumeweza kupokea kiasi ulicho kituma. Ndege ipo tayari ni wewe kuweza kufanya malipo ya mwisho ili uweze kuondoka”

“Sawa”

Nikalipia kiasi cha mwisho cha pesa ambacho kimesalia. Tukaandikishana mkataba wa safari hii na endepo kutaotokea tatizo lolote ama ajali ya angani basi kampuni hii italipa familia yangu fidia ya asilimia hamsini ya kile kiasi nilicho lipia.

“Kama unahitaji kwenda kukagua ndege inaweza kuongozana na wataalamu wetu”

Lilian alizungumza mara baada ya kumaliza kulipa kiasi hichi cha pesa.

“Sawa, hili begi langu si ninaweza kuliacha hapa?”

“Ndio unaweza kuliacha tu hapa”

Nikaondoka na mainjinia wawili wa shirika hili, tukafika katika ndege hii, wakaanza kunionyesha sehemu moja baada ya nyingine. Ni ndege nzuri sana.

“Hii spidi mita yake ni kilomita 900 kwa lisaa moja. Sifa yake nyingine inaweza kwenda umbali wa kilomita 8, 000 bila ya kuongezwa mafuta, hivyo boss hapa upo salama”

Injinia huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hivi hizi viwandani zinauzwa kiasi gani?”

“Mmmm inategemea na kile kitu unacho hitaji kutengenezewa na kiwanda husika.”

“Nashukuru nitalifwatilia hilo”

Tukarudi ofisini kwao. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni Camila ndio anaye piga, nikaipoke.

“Tumefika uwanja wa ndege mume wangu njoo unichukue nje”

“Sawa”

Nikatoka hadi nje na kuwakuta Camila na Dany wakiwa wamesimama kwenye maeneo ya maegesho ya magari. Camila akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kuninyonya lipsi zangu, alipo ridhika tukaachiana na nikasalimiana na Dany.

“Nashukuru kwa kumleta mke wangu”

“Usijali, ila poleni sana kwa mama kuumwa”

“Nashukru Dany, kuna gari ile BMW, kidogo ilipata itilfu ipo kwenye gereji moja hapa mjini”

Nikamuelekeza Dany gereji hiyo sehemu ilipo na akanielewa. Nikamkabidhi funguo ya gari langu hili jipya na kumuomba alipeleke kwenye kampuni jengo la kampuni yangu na funguo aikabidhiwe kwa mkurugenzi msaidizi ambaye ni Biyanka. Nikamtumia meseji Biyanka ya kumfahamisha kwamba gari atalikuta ofisini kwetu. Tukaagana na Dany kisa nikabeba mabegi mawili ya Camila na kuelekea kwenye ofisi za Tripple P air ways.

“Tupo tayari kwa safari”

“Sawa na marubani tayari wapo ndani ya ndege”

Lilian alizungumza huku akitutazama.

“Nashukuru”

Tukasaidiwa na vijana wabeba mizigo wa kampuni hii hadi ilipo ndege. Baada ya kuhakikisha kwamba mizogo yote imepakizwa kwenye ndege, tukaingia kwenye ndege hii ya kifahari na safari ikaanza taratubu, baada ya ndege kuwa hewani Camila akafungua mkanda wa siti yake na kunifwata sehemu nilipo kaa, akanikalia mapajani mwangu huku akinitazama usoni mwangu.

“Nina hamu na wewe mume wangu”

“Hata mimi nina hamu na wewe mke wangu, ila tupo angani kwa sasa hatuwezi kufanya chochote”

Nilizungumza kwa unyonge huku nikizichezea chezea nywele nyingi za Camila. Taratibu akakilaza kichwa chake kifuani mwangu na ndani ya muda mchache usingizi ukaanza kumpiti, nami usingizi ukaanza kunipitia, nikajikaza nisilale, ila nikashindwa kujizuia na nikalala usingizi fofofo.Sauti ya rubabi akituomba tuweze kufunga mikanda, ndege ikataka kutua ikatustua kutoka usingizini.

“Tumefika Ujerumani?”

Camila aliniuliza huku akinitazama usoni mwagu”

“Nahisi mke wangu”

Camila akarudi kwenye siti yake na kufunga mkanda, nikafungua kijipazia kidogo cha dirisa na kuchungulia nje, nikaanza kuona baadhi ya majengo marefu ya nchi hii ya Ujerumani, nikashusa pumzi kwani safari hii imetuchukua masaa mengi na sijui ni kwanini tumelala sana. Ndege ikatua uwanja wa ndege, hatukuhitaji kupoteza muda, tukakodi helicopter hadi katika hospitali aliyo lazwa bi Jane Klopp. Da Mery akatupokea, huku akilia kwa uchungu sana, nikakumbatiana naye huku nikihiataji kufahamu ni nini kinacho endelea kwa mama yetu.



“Mama ana endeleaje?”

Nilimuuliza da Mery huku nikiwa na wasiwasi mkubwa sana. Da Mery hakunijibu jambo lolote zaidi ya kuendelea kumwagikwa na machozi, kwa ishara akanionyesa chumba cha mama alicho lazwa, nikamuachia nami nikaingia ndani ya chumba hicho na kumkuta bi Jane akiwa amezungukwa na madaktari huku wakihangaika katuka kutapandisha mapigo yake ya moyo kwa mashine maalumu za umeme. Zoezi hili hata mimi likaufanya mwili wangu kuzizima, hali ya uchungu na majonzi ikaanza kunitawala, nikajikaza huku nikiendelea kutaza zoezi hili. Mashine inayo onyesha asilimia za mapigo ya moyo jinsi yanavyo fanya kazi, taratibu ikaanza kupandisha asilimia hizo kutoka tano hadi kufika asilimia themanini na sita. Madaktari wote wakajawa na furaha kwa maana bi Jane amepunyuka punyuka kwenye kifo.

“Naweza kuzungumza na mama yangu?”

Nilimuuliza mmoja wa madaktari.

”Hapana kwa sasa muache apumzike kidogo, akiwa sawa unaweza kuzungumza naye”

“Sawa sawa ninashukuru dokta, ila hali yake ipo vipi?”

“Kama unavyo muona, yupo hapa ICU”

Madaktari walizungumza huku wakinitazama usoni mwangu. Nikwajibu kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba nime waelewa. Tukatoka nje ya chumba hichi, da Mery pamoja na Camila wakanyanyuka na kunitazama usoni, tabasamu langu nililo liweka kidogo likawafanya wapate matumaini.

“Vipi mama hali yake?”

“Mapigo ya moyo yameweza kupanda na amerudi katika hali yake ya kawaida”

“Ohoo asante Mungu”

Camila alizungumza kwa furaha huku akimkumbatia wifi yake. Tukaendelea kukaa hapa hospitalini na Camila akawasiliana na wazazi wake na kuwajulisha juu ya uwepo wake hapa nchini Ujerumani. Haikupita lisaa moja, walinzi wa raisi walio ambatana na wazazi wa Camila wakafika hospitalini hapa. Furaha ya kuto kuonana nao kwa kipindi cha muda mrefu ikatawala katikati yetu.

“Mume kua”

Mama Camila alizungumza kwa kututania na kutufanya sote tucheke. Kutokana na majukumu ya kiserikiali baba Camila na mke wake wakaondoka hapa hospitalli na kurudi ikulu huku hapa hospitali ikiwa chini ya ulinzi mkali. “Ethan hivi unatambua kwamba waandishi wa habari wameweka kambi huko nje?”

“Weeee?”

“Ndio wanahitaji kutuhoji, sasa tutaongea nini kwa maana baadhi nahisi wana amani kwamba tulitekwa kabla ya uchaguzi?”

“Usijali tutazungumza nao, ila kwa sasa ngoja tuangalie hali ya mama kwanza”

Daktari mmoja ambaye kichwani mwake ana uwalaza, akaingia ndani ya chumba cha mama, baada ya muda akatoka na kwaishara akaniomba niweze kuingia katika chumba cha mama. Nikanyanyuka kwenye kiti ambacho nilikuwa nimekalia. Nikaingia ndani ya chumba hichi ambacho ni mlio wa mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo ndio inasikika kwa sauti ya chini kidogo. Nilipo kisogelea kitanda cha mama, taratibu akatabasamu huku mwili wake ukionekana kudhohofika sana. Nikasimama pemben yake, kwa ishara ya mkono akaniomba niweze kuinama ili anibusu. Nikatii hivyo, taratibu akanibusu mashavuni mwangu, kisha akabalizia busu la upendo kwenye paji la uso wangu.

“Nimerudi mama”

Nilizungumza kwa unyonge sana huku nikimtazama mama usoni mwake. Akatabasamu sana, anaonekana ni mtu anaye hitaji kuzungumza maneno mengi ila anashindwa kutokana na hali yake, akakishika kiganja cha mkono wangu wa kulia na kukiweka kifuani mwake.

“Ni…na..k..upe…nda Etha….n”

Bi Jane alizungumza kwa shida kidogo ila niliweza kumuelewa.

“Ninakupenda pia mama”

Nilizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwangu.

“Mli…nde….M…e….ry. A….sij…e aka…p…a…twa na maba…ya”

“Sawa sawa maam nitafanya hivyo”

“Ca…amm…i….la yu….p…o w..p”

“Yupo hapa nje, ngoja nimuite”

Nikatoka ndani humu na kumuita Camil, tukaingia wote ndani ya chumba hichi na Camila na tukasimama pembeni ya bi Jane. Taratibu akavishika viganja vyetu na kuviweka juu ya kifua chake huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Pen…da…neni”

“Sawa mama”

“Sawa mama”

Kila mtu alijibu kwa muda wake huku tukiwa na huzuni.

“Ny…ny…I nd..io ndug…u wa Mery mulio…oo. Sa..lia”

Bi Jane alizungumza huku akihema kwa shida kidogo, japo anapewa msada wa kuhema kwa mashine.

“Mu…pate wa….to….to”

“Tunashukuru sana mama”

“Me…ry….mu…ite”

Camila kwa haraka akatoka ndani humu na baada ya sekunde kadhaa wakaingia na Mery na moja kwa moja wakatudwata hapa kitandani na wakasimama pembeni yangu.

“Me…ry”

“Ndio mama”

“Pe…nda neni na E….THAN….ata…kul…inda”

“Sawa mama, nina mpenda sana Ethan”

“N…dio….naj…ua. Ha…ta yey…..e ana….kupe…nd…a”

Bi Jane aliendelea kuzungumza kwa tabu sana huku maneno yake yakiwa ni ya kukata kata.

“Nimekuelewa maama”

“Na….m…fwa..ta mu…me wangu sa…sa. Namuona ana….n…ii..ita”

Wote tukabaki na kigugumizi huku macho yakitutoka, tukabaki tukimuangalia bi Jane na kushindwa kuzungumza chochote.

“Nawape…nda. NATAKA KULALA SASA”

Bi Jane mara baada ya kuzungumza hivyo, akatabasamu, kisha akayafumba macho yake taratibu. Mlio wa mashine ya kuhesabu mapigo ya moyo ikaanza kutoa sauti kubwa huku mapigo ya moyo yakianza kushuka chini kwa kasi sana. Kundi la madaktari likaingia ndani humu na wakatuomba tusogee pembeni ya kiitanda hichi. Wakaanza kuhakikisha kwamba wana yapandisha mapigo ya moyo, ila kila wanali lifanya, hali ilizidi kuwa mbaya zaidi, kwani pagigo ya moyo yanaendela kushuka. Nikashuhudia sifuri mbili zenye rangi nyekunduhuku mstari mmoja mrefu wa kijani ukionekana kwenye mashine hii. Da Mery akaanguka kilio kizito na kuwafanya baadhi ya manesi kumdaka kabla hata ya kuanguka chini. Mwili na akili kwa ujamla vikawa kama vimegandishwa, sikuweza kuelewa ni nini kinacho fanywa zaidi ya kuona heka heka ndani ya chumba hichi.

“ETHAN, ETHAN, ETHAN”

Sauti ya Camila ndio ikanistua kutoka katikwa dibwi la bumbuwazi hili. Nikamtazama huku nikiwa nimemtolea macho makali sana.

“Ehhh”

Nilizungumza, Camila akanikumbatia kwa nguvu huku akilia kwa uchungu sana. Nikamshudia daktari akimfunika bi Jane shuka usoni mwake, nikamuachia Camila na kisogea kilipo kitanda, nikataka kumfunua bi Jane shuka hili ila madaktari wakaniwahi kunikamata, kwa maana wana amani kwamba si akili yangu inayo fanya hivyo.

“Nataka kumuoana mama yangu”

Nilizungumza huku nikilia na kujitahidi kujitoa mikononi mwa madaktari hawa. Madaktari wakaongezeka kunishika na kunitoa ndani ya chumba hichi.

“Ethan kazi ya Mungu haina makosa, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu ila tumeshindwa kabisa”

Daktari mmoja alizungumza huku akinitazama, sikumjibu kitu cha aina yoyote kwani akili yangu haina hata uwezo wa kufikiria kwa sasa. Wakaniingiza kwenye chumba cha kupumzikia, nikaka kwenye moja ya kiti huku nikiendelea kushangaa shangaa na kutafakari imekuwaje bi Jane amekufa. Nikamuona Ethan akiwa amesimama mbele yangu huku akiwa amevalia mavazi meupe na usoni mwake akiwa na unyonge mwingi, akakaa pembeni yangu pasipo mtu wa aina yoyote kuweza kumuona.

‘Hei’

Ethan alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

‘Jikaze, mama ndio ameondoka hivyo. Yupo kwenye maisha ya furaha kwa sasa’

“Furaha?”

Nilizungumza kwa sauti kubwa na kuwafanya madaktari waliomo ndani humu kunishangaa. Ethana akawatazama madaktari hawa kisha akanishika kifuani mwangu. Mwili ukazidi kunilegea, giza totoro likanitawala machoni mwangu na mwishowe nikajikuta nikilala usingizi fofofo.

***

Nikafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nipo chumbani kwangu katika jumba la mzee Klopp. Nikaa kitako kitandani huku nikisikilizia mziki mlaini unao tumika katika sehemu za misiba, ukisikika kutokea nje ya chumba changu. Nikashuka kitandani kwangu huku nikiwa na boksa tu mwili mwangu, nikaanza kutembea kuelekea mlangoni kabla sijaufikia mlango, mlango ukafunguliwa na akaingia Camila huku akiwa amevalia gauni kubwa jeusi.

“Umeamkaje mume wangu?”

“Nimefikaje hapa?”

“Ulipoteza fahamu kwenye chumba cha kupumzikia ambacho madaktari walikuingiza. Nikawashauri waweze kukurudisha nyumbani. Hivyo ni jana ndio umerudishwa nyumbani”

“Sasa hivi saa ngapi?”

“Ni saa mbili asubuhi, tayari maandalizi ya msiba yamefanyika na baadhi ya ndugu na marafiki wamesha kusanyika katika eneo hili”

Camila alizungumza huku akifungua kabati, akatoa suti moja nyeusi pamoja na shati jeusi.

“Inabidi uweze kuingia bafuni mume wangu. Oga uvae kisha upendeze”

“Maiti ya mama imesha letwa hapa nyumbani?”

“Hapana bado ipo hospitalini?”

“Yupo wapi Mery?”

“Sebleni, yupo na baadhi ya marafiki zake wana mfariji”

“Sawa”

Nikaingia bafuni, nikauweka sawa mwili wangu ambao bado una uchuvu chovu kidogo. Nikarudi chumbani na kuvaa nguo hizi huku Camila akinisaidia kunifunga vifungo vya shati langu. Tulipo maliza zoezi hili tukatoka chumbani humu na moja kwa moja tukaelekea sebleni, watu wakaanza kunipa pole kwa kufikwa na mama. Nikawashukuru kwa kuja, kisha nikaka eneo alipo kaa da Mery ambaye bado yupo kwenye majonzi mazito sana.

“Hei umepata kifungua kinywa?”

Nilimuuliza da Mary kwa sauti ya chini.

“Hapana”

“Kwa nini?”

“Ethan sijisikii kula chochote”

Da Mery alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Sikuona haja ya kumlazimisha kupata kifungua kinywa kwa maana hata mimi kwa upande wangu sijapata kifungua kinywa. Nikamuona Frenando akiwa amesimama pembezoni ya mlango wa kuingilia ndani humu, nikambusu da Mery kwenye shavu la kushoto kisha nikanyanyuka na kumfwata Frenando rafiki yangu wa muda mrefu sana katuka kusoma kwangu. Frenando akanikumbatia huku akiwa na furaha sana ya kuonana nami.

“Niambie rafiki yangu?”

“Poa kaka, pole sana nilisikia juu ya swala la msiba wa mama nikastuka sana”

“Nashukuru ndugu yangu vipi masomo?”

“Kaka tumesha maliza mbona. Umesahau?”

“Akili yangu haipo sawa”

“Twende huku”

Frenando alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia tukatoka nje na nikakutana na wachezaji wa timu yangu ya shule. Nikasalimiana nao kwa furaha sana huku nikikumbatiana na kila mmoja.

“Nashukuru kwa kuja sana rafiki zangu, hii ni surprise ambayo sikuitarajia kuiona kwa muda kama huu”

“Tupo pamoja ndugu yetu”

“Vipi lile kombe mulilichukua?”

“Ndio tulifanikiwa kupambana hadi dakika ya mwisho na tukafanikiwa kulichukua”

“Hongereni sana”

Mchezaji mmoja akaingia kwenye basi kubwa ambalo wamekuja nalo. Akatoka ndani ya basi na kombe ambalo tulikuwa tunaligombania na kunikabidhi jambo lililo nifanya nizidi kujawa na mshangao.

“Tumekuletea kombe hili kapteni ikiwa kama zawadi kwako kwa maana umetufanya tung’are. Yaani hadi tumavyo zungumza hivi sasa, kila mmoja hapa amepata mkataba katika kabla kubwa za hapa Ujerumani na nje ya Ujerumani”

“Weeee”

“Ndio. Mimi Ethan nasubiria jibu lako ni wapi niweze kujiunga kwa maana nimesha tumia ofa na klabu kubwa tatu. Liverpool, Real Madrid na Man Chester City”

Frenando alizungumza kwa furaha huku akinionyesha email za ofa alizo tumiwa na timu hizo.

“Tutalizungumza hilo maswala ya msiba yakiisha”

“Sawa sawa kaka”

“Ethan samahani”

Jamaa mmoja mwenye asili ya kijerumani alizungumza huku akiwa amesimama pembeni yangu. Nikamkabidhi Frenando kombe hili kisha tukasogea pembeni kidogo na kuzungumza.

“Ndio”

Akanikabidhi simu yake ya kiganjani.

“Ya nini?”

“Zungumza na huyu mtu”

Nikaiweka simu yangu sikioni.

“Nashukuru sana kwa kurudi Ujerumani. Ulihisi unaweza kulikimbia ili. Tunahitaji BOKSI JEUSI haraka iwezekanavyo kabla ya hatujaharibu msiba wa mama yako”

Maneno ya mwanaume huyu yakanistua sana, jamaa huyu aliye simama eneo hili taratibu akafungua koti lake na kunionyesha bastola aliyo ichomeka kiunoni mwake akiashiria kwamba nikifanya jambo lolote la kijinga anaweza kuniua hapa hapa.

ITAENDELEA

 

0 comments:

Post a Comment

BLOG