MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE)
WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+
SEHEMU YA 4 KATI YA 10
***
Madam Mery baada ya kumaliza kuzungumza na dokta Ranjiti, akakata simu huku akishusha pumzi na kujiuliza ni kwa nini Phidaya ameemua kumsaidia mwanaume ambaye ni adui wa mujme wake. Akatamani kumpigia Eddy simu ila akashijikya akisitisha zoezi hilo akiamini kwamba ina weza kuleta matatizo makubwa katika watu hao ambao anawafahamu kwa miaka mingi hususani haswa Eddy ambaye alikuwa ni mwanafunzi wake na alikuwa ni mwanaume wake wa kwanza kumpa ujauzito.
Madam Mery akaanza kuandika ujumbe ufupi wa meseji, unao muomba mfanyakazi wake aliyopo jijini Dar es Salaam kuhakikisha anaweza kufahamu sababu zinazo endelea katika familia hiyo japo amekubaliana na Phidaya kishingo upande tu.
‘Sawa bosi nitafanya hivyo’
Mfanyakazi huyo akamjibu madam Mery kwa ujumbe mfupi wa meseji.
“Niandalieni helicopter ninahitaji kwenda jijini Dar es Salaam”
Madam Mery alimuambia mfanyakazi wake na mshauri wake wa karibu sana.
“Unahitaji kwenda muda huu bosi?”
“Kwani nimekuambia muda gani, nenda kaniandalieni helicopter”
“Sawa bosi”
Madam Mery akamalizia wyne iliyo salia kwenye glasi yake kisha akanyanyuka na kueleeka chumbani kwake, akavua nguo zake zote na kubaki kama alivyo zaliwa, akajitazama jeraga alilo pigwa risasi na mzee Godwin miaka ya nyuma, akatingisha kichwa huku akitabasamu kwani ni maisha ya tanu sana aliyapitia hadi leo hii amefanikiwa na kuwa mfanya biashara mkubwa jijini Mwanza. Madam Mery akajitazama mwili wake ambao tayari amesha anza kusinyaa kutokana na umri wake kwenda.
‘Eddy hawezi kunitamani tena’
Madam Mery alizungumza huku akijishika shika makalio yake ambayo nayo pia yameanza kusinyaa. Madam Mery alipo jithaminisha kwamba uzuri wa ndani wa mwili wake umeweza kupungua kwa asilimia kubwa sana, akaingia bafuni na kuanza kuoga huku akijifikiria ni jinsi gani anavyo weza kukutana na Eddy Godwin na kumpeleleza kuhusiana na kazi ambayo mke wake amemkabidhi ya kumficha dokta Ranjiti katika nyumba siri hadi pale kusakwa kwake kutakapo isha.
Madam Mery akamaliza kuoga, akarudi chumbani kwake. Akajiandaa haraka haraka na kuianza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaama kwa kutumia helicopter yake binafsi.
***
Baadhi ya abiria ndani ya ndege hiyo wakaanza kusali sala zao za mwisho huku wengine wakiendelea kulia kwa uchungu na kusaga meno. Adrus kitu alicho weza kukifanya ni kumshika mkono mpenzi wake Cookie, kwani watu wote wamesha poteza matumaini ya kuweza kupona katika ajali hiyo. Kwa kasi kubwa ndege hiyo ikazama kwenye bahari hiyo.
“Hatuwezi kufa kirahisi”
Adrus alizungumza huku akiendelea kumshika mkono Cookie ambaye woga mwigi sana umemtawala. Adrus akachukua moja ya kiti na kuanza kupasua kioo cha mbele katika chumba hicho cha rubani, kwani maji bado hayajaanza kuingia ndani ya ndege hiyo.
“Unafanyaje wewe?”
Njing alizungumza kwa wasiwasi huku akimtolea macho Adrus.
“Unataka tufie humu ndani au?”
“Sasa kupasua kioo unaona ndio solution ya sisi kuokoa?”
“Unataka tufe taratibu au, ni bora tupasue kioo tutoke humu ndani”
“Acha ujinga wewe”
Njing alizungumza kwa msisitizo na kumpokonya Adrus kiti alicho kishika. Baadhi ya abiria tayari walisha fariki kutokana na mstuko mkubwa walio upata huku wengine wakiwa wamekanyagana vibaya sana wakati ndege ilipo kuwa ipo katika kuyumba kwani kitendo cha abiria kuarishwa kukaa katika madaraja tofauti tofauti kumepelekea wengi wao kuto kujifunga mikanda yao.
“Sasa tunafanyaje?”
Adrus alizungumz ahuku macho yakiwa yamejaa uwekundu.
“Sio kila mtu anaweza kuogelea na huwezi juua kama hili eneo ni salama kwani kunaweza kuwa na papa wakali na wakamrarua kila ambaye anaweza kutoka nje ya ndege hii, cha kumshukuru Mungu maji hayajaanza kuingia.”
”Ila hujanishauri ni kitu gani tufanye, na ndege inazidi kwenda chini hii”
Adrus alizungumza kwa hasira sana huku akimtazama Jing ambaye amekosa jibu la kuweza kumjibu.
***
Dokta Ranjiti na Anna wakafikishwa katika jumba maalumu linalo milikiwa na Madam Mery lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Jumba hili lina kila aina ya kitu muhimu kinacho patikana ndani ya jumba hili. Dokta Ranjiti na Anna wakashuka katika gari. Jamaa huyu akawaogoza hadi ndani.
“Jisikieni mupo nyumbani, mkuu aliye niagiza atafika eneo hili muda mchache kuanzia hivi sasa”
“Ni nani?”
“Utamtambua, kama yeye mwenye amashindwa kukuambia kwamba yeye ni nani basi hata mimi sinto weza kukuambia. Juu gorofani kuna vymba vya kulala, muna weza kupanda na kwenda kutazama, kama unahitaji huduma zote basi muna weza kujishulikia wenyewe. Sheria namba moja katika hii nyumba, hamutakiwi kufanya mawasiliano ya simu ya aina yoyote kwenda nje ya nchi au ndani ya nje kwa maana hadi ninavyo zungumza sasa hivi sauti zetu ni most wanted kwa mitandao yote ya simu hapa Tanzania, so zikisikiwa basi mutambua kwamba mume kamatwa kwani wataweza kufahamu ni location gani ambayo nyinyi mupo. Mbili hamrusiwi kutoka nje ya huo mlango wa kuingilia hapo ndani kwani kufanya hivyo satelait angani zinaweza kunasa sura zenu na wakafahamu ni wapi mulipo na kumajitafutia tatizo ambalo litakuwa ni kubwa sana.”
“Vyakula vya aina yote, pamoja na vinywaji vya aina yote vipo kwenye friji so munaweza kujihudumia. Walinzi wanawalinda, masaa ishirini na nne, kama kuna muna maswali katika hivyo zitu nilivyo vizungumza munaweza munaweza kuniuliza kabla sijaondoka?”
“Mimi sina”
Anna alizungumza huku akimtazama mwanaume huyu, dokta Ranjiti akajifikira kwa sekunde kadha akisha akatingisha kichwa akimaanisha kwamba hata yeye hana swali la aina yoyote kwa mwanaume huyo, ambaye baada ya kupata majibu hayo akatoka zake nje na kwenda kujiandaa kumpokea madam Mery kwenye moja ya kiwanja cha Helicopter ili kumtembeza katika shuhuli zake zote anazo hitaji kuzifanya hapa jijini Dar es Salaam.
“Baba ninaimba uniambie ni kitu gani ambacho kinaendelea?”
Anna alizungumza kwa msisitizo huku akimtazam dokta Ranjiti usoni mwake.
“Nitakuambia?”
“Lini na saa ngapi, baba nimekatisha masomo yangu ya msingi na nipo kwenye kipindi cha kuingia kwenye mitihani kwa ajili yako. Hembu kuwa muwazi baba wewe ni nani na sijui huyo Eddy ana mpango gani na wewe?”
Anna alizungumza kwa hasira sana huku akivua shati la jeshi alilo livaa. Dokta Ranjiti akamtazama mwanaye huyu ambaye ni kwa miaka mingi hajakutana naye hii yote ni kutokana na mwanye huyu kumchukia tangu alipo kuwa binti mdogo na yote ni kutengena na mama wa mtoto wake.
“Anna, unatambua kwamba baba yako mimi ninakupenda, ninakujali kwa kila kitu ndio mana ninakuwa ninakuhudumia kwa kila jambo kwenye maisha yako”
“Hiyo sio pointi ya msingi na wala usipotezee mada ambayo nimekuuliza, wewe ni nani?”
“My daughter mimi ni doktari, kwa nini unakuwa huniamini….?”
“Acha uongo baba, ninataka kujua wewe ni nani na kwa nini ulitekwa?”
“Nimetekwa yote kwa ajili ya Phidaya?”
“So Phidaya ndio amekufanya utekwe kwa kipi labda huyo Phidaya alicho kufanyia wewe?”
“Anna kumbuka kwamba ninampenda sana mama yako Phidaya?”
“Acha kuzungumza upuuzi wako, Phidaya si mama yangu, mama yangu nilisha mzika mika minne nyuma pasipo wewe kuhudhuria mazishi yake, sina mama duniani na kama nimapenzi yako wewe na Phidaya hilo swala mimi halinihusu”
Anna aliendelea kuzungumza kwa hasira sana.
“Anna?”
“Nini?”
“Ninakuomba unisamehe kwa kila kitu kilicho tokea kwenye maisha yako”
“Nimekueleza kwamba sinto kusamehe kwenye maisha yangu hadi kufa kwangu, na hili lililo tokea tena litazidisha uadui wangu kwako, natamani hata ufe sasa hivi, nijue sina baba”
Anna baada ya kuzungumza maneno hayo akaanza kupandisha gorofani huku akimwagika na machozi mengi sana na kumuacha dokta Ranjiti akiwa na masikitiko makubwa kwani huyo ndio mwanaye wa pekee, ambaye aliamua kuungana na mama yake kipindi walipo kuwa binti wa miaka mimi na tatu na yote hayo yalisababisha na dini, kwani mkewe alihitaji mwanaye kuwa katika dini ya kikristo ila yeye alihitaji mwanye afwate dini ya uislam anayo iabudu.
***
Shamsa akakurupuka kitandani na kukaa kitako na kumsababisha nesi aliyomo ndani ya chumba hicho kustuka sana hadi kitabu kidogo alicho kishika mkononi mwake kikaanguka chini.
“Yupo wapi??”
Shamsa aliuliza huku akitazama tazama mandhari ya chumba hichi cha hapa hospitalini.
“Nani?”
Nesi aliuliza huku akijitahidi sana kurudi katika hali ya kawaida kawaida.
“Yule malaya niliye kuwa ninapigana naye?”
“Aha..samahani dada kwa sasa upo hospitali ya Muhimbili, umeletwa hapa ukiwa umepoteza fahamu”
“Kwa hiyo alinipiga?”
“Ahaa siweziz kusema ndio au hapana ila umeletwa hapa ukiwa katika hali kama hiyo niliyo kuambia”
Shamsa akajitazama sindano aliyo chomwa mkononi mwake ambayo inaingiza maji kwenye mishipa yake, taratibu akaichomoa sindano hiyo na kushuka kitandani.
“Ila haujawa sawa?”
“Nani amekuambia kwamba ninaumwa”
Shamsa alizungumza huku akitazama tazama ni wapi vilipo viatu vyake, kwa bahati nzuri akafanikiwa kuviona viatu vyake na kuvivaa.
“Baba yako na mama yako nao wapo hapa hospitalini”
Meneno ya nesi huyu yakamfanya Shamsa kumtazama kwa muda huku akifiria ni nini cha kufanya.
“Nipeleke sehemu walipo?”
“Sawa”
Wakatoka nje, Shamsa akashangaa wingi wa walinzi waliopo nje ya chumba chake, hakuwasemesha kitu chochote zaidi ya kuendelea kumfwata nesi huyo aliye tangulia mbele yake, walinzi wawafwata kwa nyuma. Wakafika katika chumba allicho lazwa Eddy, walinzi walipo hapa mlangoni wakamruhusu kuingia ndani. Shamsa akamkuta Eddy akiwa anazungumza na dokta Benjamini.
“Dokta naomba utupishe”
Eddy alizungumza huku akimtazama Shamsa aliye simama mbele ya mlango wa kuingilia ndani humo.
“Sawa mkuu”
Dokta Benjamini akatatoka na kuufunga mlango, taratibu Shamsa akatembea hadi kilipo kitanda cha Eddy. Wakatazamana kwa muda kisha taratibu Shamsa akausogeza mdomo wake karibu kabisa na lipsi za Eddy na kunyonyana midomo yao.
“Eddy”
Shamsa aliita kwa sauti ya chini iliyo jaa upole.
“Naam”
“Nafurahi kwa wewe kuwa hai?”
“Hata mimi ninashukuru kukuona, nilihisi labda nitakuwa nimekufa. Nasikia Phidaya naye amepigwa risasi”
“Amepigwa risasi?”
“Ndio ninasikia kwamba na yeye amepigwa risasi ya paja?”
Shamsa akatulia kwa muda huku kwa mbali akijaribu kukumbuka sauti ya Phidaya ambayo ilikuwa ikimuomba mtu kumpiga risasi, baada ya hapo akasikia sauti ya mazungumzo ambayo hakuyaelewa kutokana na kupoteza kwake fahamu.
“Shamsa….Shamsa”
“Mmmmm?”
“Unawaza nini?”
“Aaa….hamna”
“Dokta Ranjiti na mwanye wametoroka?”
“What?”
“Yaa”
“Haiwezekani wakatoroka, mbona kulikuwa na idadi kubwa ya wanajeshi walio weza kufika baada ya wewe kupigwa risasi?”
“Nasikia dokta Ranjiti na mwanaye walihusika kuwaua wanajeshi wanne kisha wakachukua nguo zao na kuondoka pale nyumbani pasipo kustukiwa”
“Kuna mtu amewasaidia kutoroka”
Shamsa alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Eddy usoni mwake.
“Unahisi ni nani atakuwa amewasaidia?”
Shamsa akaka kimya tena huku akiendelea kuyatafakari maeno ya Phiday aliye ombwa kupigwa risasi mguuni mwake.
‘Kwa nini aombwe kupigwa risasi?’
Shamsa aliendelea kujiuliza huku akiendelea kumtazama Eddy usoni mwake.
“Mama yupo wapi?”
“Yupo kwenye chumba cha upasuaji anatolewa risasi”
Shama pasipo kuaga akatoka chumbani hapo kwa haraka na kumfanya Eddy abaki akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana kwani hajui ni wapi Shamsa anapo kwenda. Walinzi wakaanza kumfwata na kumfanya Shamsa kusimama na kuwaangali.
“Ninaomba musinilinde”
“Jukumu letu ni kuimarisha ulinzi wako?”
Shamsa akatazama tazama ni mlinzi ambaye alifanya naye mazozi leo asubuhi ila hakumuona.
“Ninaweza kujilinda mimi mwenyewe”
“Madam tunafwata amri ya makamu wa raisi si amri yako utakapo kwenda ni lazima tukulinde”
Shamsa akageuza na kurudi ndani ya chumba alicho lazwa Eddy.
“Vipi?”
“Baby nakuomba uwazuie walinzi wako, kwa maana kila ninapo kwenda wananifwata, sehemu ninayo hitaji mimi kwenda sihitaji kufwata na mtu wa aina yoyote.
“Unataka kwenda wapi tena Shamsa, ikiwa hali ya kiusalama ya hii nchi bado ni mbaya?”
“Najua nini ninacho kifanya Eddy ninakuomba watu wako wasinifwate?”
“Unakwenda nje ya hospitali hii?”
“Hapana nipo ndani ya hii hii hospitali, nakuomba basi uwazuie wasinifwate”
Eddy alamtazma Shamsa kwa muda.
“Muite kiongozi wao”
Shamsa akafungua mlango na kuwatazama walinzi hawa.
“Kiongozi wenu anaitwa ndani humu”
Mzee mmoja mwenye mvi kadhaa kichwani mwake akaingia ndani ya chumba hichi.
“Nawaomba mumpe nafasi binti yangu, aende anapo pahitaji”
“Ila mkuu hali ya kiusalama sio nzuri?”
“Natambu ila kama hospitali nzima mumeilinda basi mpeni nafasi ya kuwa peke yake”
“Sawa mkuu”
Shamsa akatabasamu, akatoka ndani humu na kuanza kutembea kuelekea katika chumba cha upasuaji. Kitendo cha kufika katika eneo hilo, akakutana na madaktari wakifungua mlango wa chumba hicho na kuanza kukisukuma kitanda alicho lazwa Phidaya huku akiwa tayari amesha maliza kufanyiwa upasuaji ila bado amelala kutokana na sindano ya usingizi ambayo amechomwa.
“Hei dokta mtoto yupo wapi?”
“Yupo katika uangalizi mzuri”
“Je simu ya mama yangu?”
Daktari huyo akamtazama mmoja wa manesi wake, nesi huyo akaitoa simu ya Phidya kwenye mfuko wa koti lake, akamkabidhi Shamsa simu hiyo.
“Atazinduka baada ya muda gani?”
“Kama dakika arobaini na tano”
“Jeraha lake ni kubwa sana?”
“Hapana sio kubwa na halijaleta madhara makubwa sana”
“Nashukuru”
Shamsa akatazama jinsi kitanda hicho kinavyo sukumwa kupelekwa kwenye chumba maalumu. Uzuri wa simu ya Phidaya haina neno la siri ambalo bila kulitambu hilo huwezi kuitumia simu ya muhusika aliye weka neno hilo. Shamsa akaingia upande wa namba zilizo pigwa ila hakukuta mabadiliko yoyote, akaingia upande wa meseji hapo ndipo akakutana na meseji inayo mpa maagizo madam Mery kwamba ahakikishe kwamba anamsaidia dokta Ranjiti na mwanye na awafiche kwenye eneo la siri hadi pale hali ya kutafutwa kwao itakapo tulia.
‘Malaya wewe nimekupata sasa’
Shamsa alizungumza kwa msisitizo huku akianza kufikiria ni jinsi gani anavyo weza kubananisha madam Mery ili aweze kusema ni wapi walipo dokta Ranjiti na mwanaye Anna ili kama ni kuwaua basi awaue kwa mkono wake yeye mwenyewe.
Shamsa akaitazama simu ya Phidaya kwa sekunde kasha kisha akaandika ujumbe mfupi kwa ajili ya kumtumia madam Mery.
‘Wifi upo wapi?’
Hazikupita hata dakika mbili meseji yake ikajibiwa na madam Mery ambaye hafahamu kwamba anafanya mawasiliano na Shamsa.
‘Nipo kwenye helicopter ninakuja huko Dar’
Shamsa akafikria ni kitu gani anaweza kukiandika, ili asiji akachanganya matukio na kustukiwa kama sio yeye.
‘Basi wifi ukifika usisite kunitumia ujumbe sawa’
‘Sawa wifi, ila kuna kitu gani ambacho kinaendelea kwa maana ninashindwa kukuelewa kwa nini umeamua kufanya hivyo?’
‘Usijali tutayazungumza, unafikia eneo gani?’
‘Nitakujulisha wifi yangu nikifika’
‘Sawa ila nitahitaji tuonane eneo la siri’
‘Sawa wifi’
Shamsa akatabasamu kidogo kisha akaanza kutembea kuelekea katika chumba alicho lazwa Eddy.
***
Rahab akafika nyumbani kwa Fetty na kukuta magari kadhaa ambayo anayatambua kwamba wanayatumia wazeke. Akashuka kwenye gari lake na moja kwa moja na kuelekea ndani huku walinzi wake wakibaki nje. Akawakuna Fetty, Anna na Agnes wakiwa wamekaa sebleni, walipo muona kwa pamoja wakasimama na kuanza kusalimiana kwani tangu walipo achana kwenye mazishi ya Halima kila mmoja waliweza kuendelea na maisha yake japo aliweza kuwapa wazara za kusimamia.
“Unatumia kinywaji gani?”
Fetty alimuuliza Rahab huku akimtazama usoni mwake.
“Hapana sihitaji kinywaji chochote”
“Kuna kitu gani kinacho endelea mkuu?”
“Kuna mtu amegusa mboni yangu”
“Kivipi Rahab?”
Anna aliuliza huku akimtazam raisi Ragab ambaye muda wote macho yake yanaonyesha dhairi kwamba yamejaa hasira kali.
“Hadi ninavyo zungumza hivi sasa makamu wa raisi amepigwa risasi na watu wa dokta Ranjiti, hili ni tukio la kigaidi ambalo linaonyesha kwamba watu wa marehemu mzee Godwin bado wanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba wanamuangusha Eddy chini”
Taarifa hiyo ikamshangaza kila mmoja kwanini ni taarifa ambayo haijasambaa kwa viongozi wengi.
“Anaelendeleaje?”
Anna aliuliza huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio kwani hata yeye mwenyewe hapo awali alisha wahi kuwa katika mahusiano na Eddy.
“Sijapata ripoti kwa daktari”
“Kabla hatujasonga mbele Rahab inabidi tuweze kujua hali yake”
“Na je alipigwa risasi eneo gani la mwili wake?”
“Naogopa hata kuuliza hali yake, kwa maana nililishuhudia tukio la yeye kupigwa risasi, kwani ni zaidi ya risasi kumi zimempiga mwilini mwake”
“Ohooo Mungu wangu!!”
Anna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Yupo hospitali gani?”
Fetty aliuliza kwa ujasiri mkubwa sana kwani katika kipindi chote, yeye ndio kiongozi wa hicho kikundi chao na ujasiri wake umemfanya hadi leo kikundi hicho kuwa katika maisha mazuri na kuachana na matukio maomu na kuahimia katika matukio mazuri.
“Muhimbili?”
“Mkuu wao pale ni nani?”
“Benjamini”
Agnes alizungumza huku naye akiwa amejawa na huzuni nyingi. Fetty akaichukua simu yake aliyo iweka katika meza ya kioo. Akaifafuta namba ya dokta Benjamini, akaipata na kumpigia. Simu ya dokta Benjamini ikaanza kuita taratibu.
“Ndio kiongozi”
“Habari yako?”
“Salama kiongozi?”
“Hali ya makamu wa raisi inaendeleaje?”
Dokta Benjamini akaka kimya huku akionekana kutafakari swali hilo, jambo lililo anza kuwapa wasiwasi watu wote kwani Fetty aliweka loudspeaker.
“Dokta Benjamini?”
“Ndio mkuu”
“Nina imani swali langu umelisikia vizuri”
“Ahaa, ndio muheshimiwa nimelisikia swali lako”
“Niambie anaendeleaje?”
“Hii taarifa ningetakiwa kumpa raisi kwanza, kwa hiyo ninakuomba u…..”
“Benjamini ninakusikia”
Rahab ilibidi azungumze huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana, jambo lililo pelekea jasho kuanza kumwagika usoni mwake.
“Madam President”
“Ndio ninakusikia”
“Hali ya makamu wa raisi……ni nzuri, ameamka tunashukuru Mungu kwamba amejeruhiwa tu kwenye mguu wake kwa risasi mbili na hazijaleta madhara ya kuvunja mfupa wa ina yoyote na hata sasa hivi nimetoka kuzungumza naye”
“Oyooooooo”
Anna alisimama na kushangilia kwa furaha sana kwani ni habari ambayo imetuliza moyo wake kwa na,na moja ama nyingine.
‘Ohoo asante Mungu’
Rahab naye alizungumza kimoyo moyo.
“Ninaweza kuisikia sautii yake”
“Ndio muheshimiwa raishi ngoja nielekee chumbani kwake.”
“Usikate simu tunakusubiria”
***
Shamsa akaingia katika chumba cha Eddy huku akiwa na usongo wa kuhitaji kumueleza Eddy kwa kile kitu ambacho amekigundua kwa Phidaya ili hata kama ni kuharibu mahusiano hayo yaharibike kabisa na yeye awe sasa ndio mke halali wa Eddy. Kabla hajazungumza kitu chochote mlango ukafunguliwa, akaingia dokta Benjamini huku akiwa ameishika simu mkononi.
“Muheshimiwa kuna simu yako kutoka kwa kwa madam President”
Eddy akaonyoosha mkono kwa ishara ya kuipokea simu hiyo, akakabidhiwa simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Haloo”
“Eddy upo salama?”
“Yaa Mungu amenisaidia nipo salama, ni mguu tu ndio umepata majeraha ya risasi”
“Pole sana, nipo na Anna, Agnes na Fetty tunalijadili swala la dokta Ranjiti na mwanaye kutoroka. Tunahitaji kulishuhulikia sisi wenyewe”
Sauti ya Rahab alisikika hadi masikioni mwa Shamsa, kwani simu hiyo kidogo ina sauti kubwa ya kumsikia mtu anaye zungumza upande wa pili wa simu.
“Ahaa, ila nyingi kumbukeni ni viongozi, na hili swala linalo endelea ni langu na dokta Ranjiti, tusije tukaipelekea nchi kukosa viongozi ambao wanaweza kuendelea kuipigania nchi katika changamoto zinazo tukabili”
Maneno ya busara ya Eddy yakamfanya Shamsa kushangaa kabisa, kwani alihisi kwamba hiyo ndio ingekuwa nafasi ya pekee kuweza kuungana na Rahaba kuongeza nguvu katika swala hilo.
“Eddy tunalitambua hili, ila huu mzizi wa chama cha D.F.E bado unaendelea, kumbuka watakuzidi kukuandama hadi kuhakikisha kwamba unakufa. Watu wa marehemu baba yako mzee Godwin wanakuhitaji bado”
Meneno hayo ya raisi Rahab yakamfanya Eddy kukaa kimywa kwa muda huku akifirikia.
“Hembu kumbuka jinsi mwanao alivyo achiw pale gorofani, hivi kama unahisi ni watu wenye nia nzuri wangefanya vile, sasa hiyo haitoshi wameamua kumteka kabisa mwanao mwengine kweli bado unataka kuendelea kukaa ukiwaonea huruma?”
Menono hayo yakamgusa hadi Shamsa ambaye anayasikia vizuri, Shamsa akamtazama dokta Benjamini, kwa ishara ya macho aliyo muonyeshea dokta Benjamni, yeye mwenyewe akaelewa kwamba mazungumzo hayo ni muhimu kwa raisi, na ikamlazimu kutoka nje na kuwaacha Shamsa na baba yake ndani ya chumba hicho.
“Eddy unatakiwa kufanya maamuzi sasa, tunatakiwa kung’oa mizizi yote ya D.F.E, hichi kivuli kilicho baki kitaendelea kukitesa kizazi chako, mke wako hadi na wanao. Fanya maamuzi sahihi sasa, nimejitoa mimi na wezangu potelea pote uongozi tulio kabidhiwa ila tunataka kukutengenezea amani ya maisha yako yote”
Sauti ya raisi Rahab iliendelea kuzungumza kwa msisitizo mkali sana hadi ukamfanya Eddy kuanza kulengwa lengwa na machozi ya hasira.
“Baba huu ni muda wa wewe kufanya maamuzi, hatuna jinsi ya kufanya maadui wapo hadi mlangoni kwako baba, amua”
Shamsa naye akaendelea kumchochea Eddy katika jambo hilo.
“Eddy”
“Mumepanga plan gani?”
Eddy aliuliza kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo mingi.
“Plan ambayo yupo nayo hivi sasa ni kuhakikisha kwamba tunaye mkamta hivi sasa, hatuna muda wa kumuacha si dokta Ranjiti wala mwanaye, si John wala watu wake ni lazima tuwaue”
Eddy akashusha pumzi nzito iliyo sikika hadi kwa raisi Rahab.
“Zungumza kitu Eddy”
“Hakikisheni kwamba muna msaka dokta Ranjiti popote alipo, musimuue kabla ya amri yangu?”
“Sawa mkuu”
“Ila angalizo, hii ni vita ya kimya kimya, raisi usionyeshe dalili yoyote ya kukiuka kanunu na taratiba za katiba ya nchi hii, kama ni kuua tunaua kimya kimya”
“Yes boss, ninaimani utafurahia kazi yetu”
“Nashukuru kwa hilo”
Eddy akakata simu na kumtazama Shamsa aliye jawa na hasira sana, kwani mtu aliye sababisha kutoroka kwa dokta Rajiti ni Phidaya na yeye ndio msaliti wa kila kitu.
“Mbona macho yako yamekuwa mekundu?”
“Nani?”
“Kwani humu ndani tupo wangapi?”
“Nikiwa kama mama niliye pata uchungu wa mwanangu, nilazima nichanganyikiwe katika hili”
“Usijali tutampata mtoto wetu sawa”
“Eddy maneno hayawezi kumrudisha Junion Jr wangu, ila vitendo ndi kitu cha pekee kinacho weza kumrudisha nyumbani mwanangu”
“Kama Rahab ameamua kulisimamia hili nina imani kwamba mtoto anaweza kurudi”
Shamsa akamtazama Eddy kwa macho makili, kisha akatoka chumbani humu pasipo kuaga chochote. Akakutana na dokta Benjamini mlangoni ambaye hakumsemesha chochote. Akawatazama walinzi hawa wanao endelea kuimarisha ulinzi katika eneo hili.
“Wewe twende”
Shamsa alimchagua kijana mmoja mrefu na mweupe kidogo. Kijana huyo hakunyanyua mguu wake. Alicho kifanya ni kumtazama mkuu wake ambaye hapo awali Shamsa alikataa kabisa kuweza kuwekewa ulinzi na walinzi hao wa makamu wa raisi.
“Hutaki?”
“Binti hata kama baba yako ni makamu wa raisi, ila unatakiwa kuwa na heshima, hauwezi kuzungumza chochote sisi tukakifanya ikiwa hapo awali ulikataa msaada wetu”
Mkuu wa kikosi hicho alizungumza kwa msisitizo huku akimkazia macho Shamsa. Shamsa akajifikiria kwa muda huku akiwatazama walinzi wengine, taratibu akamsogela mkuu huyu wa kikosi hichi.
“Ninakuomba unisamehe kama nitakuwa nimekuudhi au kuwaudhi, ninaomba kijna wako aweze kunisindikiza eneo ambalo ninahitaji kwenda?”
“Msamaga wako umekubalika, ila kwa sharti moja?”
“Sharti gani?”
“Kila kitu ambacho kinahusiana na ulinzi, kinana wangu atakuambia hakuna kubisha ni lazima umsikilize sawa”
“Usijali katika hilo”
“Chichi hakikisha binti anakuwa salama”
“Sawa mkuu”
“Muniazime na gari?”
“Kama ni nje ya hospitali hii, basi inabidi ulinzi uzidi kuimarishwa kwako na baba yako anaakiwa kulifahamu hilo”
“Ila ninahitaji mlinzi mmoja”
“Haiwezekani, kwa hali halisi ya sasa hauwezi kupewa mlinzi mmoja ukaondoka naye”
Mkuu huyo akaingia katika chumba alicho lazwa Eddy akamuelezea ombi la binti yake, Eddy akakubaliana na ombi hilo ila akaombwa aitiwe Shamsa.
“Unataka kwenda wapi?”
“Kuna swala ninahitaji kulifwatili?”
“Sihitaji matatizo Shamsa, mimi nimelala hapa kitandani, mama yako naye amelazwa huko kitandani, na wewe unataka kuniletea matatizo sihitaji”
“Usijali baba nitakuwa salama
“Sawa”
Shamsa akambusu Eddy kwa mbali, jambo ambalo dokta Benjamini hakuweza kuliona, kisha kwa mwendo wa haraka akatoka chumbani humu huku akiwa amejawa na furaha kwani kumpata madam Mery basi kutamsaidia yeye kumpata dokta Ranjiti sehemu alipo.
***
“Nimekuelewa bosi”
“Usijali nitakuwa makini sana”
“Sawa mkuu”
Nesi huyu aliye jificha katika chumba cha kubadilishia nguo alimaliza kuzungumza na simu yake ya siri anayo ificha kwenye droo yake ya chuma ambayo sio rahisi kwa mtu wa aina yoyote kuwea kuiona na ni simu ambayo ina imeunganishwa na kifaa maalumu ambacho hakuna mtambo wa aina yoyote aunao weza kusana mazungumzo yanayo ingia katika simu hiyo. Nesi huyo akaiificha simu yake kisha akachukua bastola yake maaulu aliyo ihifadhi katika sanduku hilo, akaifunga kiwambo cha kuzuia risasi kisha akatoka ndani humo huku akiwa ameichomeka katika koti lake jeupe lenye mikono myeupe. Moja kwa moja akaanza kutembea kwa mwendo wa umakini sana hadi kwenye chumba maalumu alicho pumzishwa Camila mtoto wa Eddy, akawaonyesha kitambulisho chake cha kazi walinzi wawili walipo nje ya chumba hichi, walipo hakikisha kwamba nesi huyu ni mfanyakazi halali wa hospitali ya muhimbili wakamruhusu kuingia ndani ya chumba hicho ambacho.
“Ehee bora umekuja Nansi kunipokeaa”
Nesi mmoja aliyomo ndani ya chumba hicho alizungumza kwa furaha sana, kwani kazi ya kumbembeleza Camila ilikuwa ni ngumu sana kwake.
“Anasumbua sana?”
“Mmmm watoto wa wakubwa hawa wakiwaona watu kama sisi na mazingira hawayaelewi elewi basi wanaliaje?”
“Hahaaa pole, sawa nenda kaendelee na mambo mengine”
“Sawa”
Nesi huyu akasimama na kumkabishi nesi Nansi, Camila. Nesi hiyo akatoka na kumuacha nesi Nansi akiwa na mtoto. Kwa haraka Nesi Nansi akamuweka mtoto kitandani akafungua dirisha na kukutana na nondo ambazo si rahisi kwa yeye kuweza kutoka. Camila akaanza kulia tena, jambo lililo mfanya nesi Nansi kumtolea macho ya kukasirika , sauti ya Camila ikawafanya walinzi hawa kutazamana, mmoja wao akafungua mlango na kuingia ndani na kumkuta nesi Nansi akiwa katika harakati za kutazama dirisha hili.
“Unafanyeja?”
Sauti ya mlinzi huyu ikamfanya nesi Nansi kusimama kwa sekunde kadhaa huku akiwa amempa mgongo mlinzo huyo. Kwa haraka nesi Nansi akageuka huku akiwa ameitoa bastola yake mfukoni, akampiga mlinzi huyu risasi moja ya kichwa na kumfanya aanguke chini mzima mzima, kishindo kuanguka kwa mlinzi huyo kimamfanya mwenzake kustuka sana nje, akachomoa bastola yake na kuanza kunyata ndani, nesi Nansi kama mtu aliye fahamu kwamba ni lazima mlinzi wa pili ataingia ndani humu, akajitokeza kwenye kabati alilokuwa amejificha na kumtandika risasi ya kichwa mlinzi huyo na kumfanya naye aanguke chini na kufa hapo hapo. Nesi Nansi kwa haeraka akaanza kuwavuta walinzi hao na kuanza kuwaingia ndani ya uvungu hata kabla hajamaliza shuhuli hiyo mlango ukafungulia na kumfanya astuke sana kwani aliamini kwamba amesha hatua ya kwanza ya kazi yake.
ENDELEA
Nesi Nansi akatazamana na nesi mwenzake aliye kuwa amepokezana naye katika kumtazama Camila. Nesi huyo alipo ona maiti hizo na bastola mkononi mwa nesi Nansi, akakajiribu kukimbia ila kwa kasi ya ajabu sana nesi Nansi akamuwahi na kumshika kwa nguvu na kumrisha ndani.
“Am Sorry Mariam, nipo kazini”
Nesi Nansi baada ya kumaliza mazungumzo hayo akamtandika nesi Mariam risasi kadhaa za kifua na akafariki hapo hapo. Kwa haraka akaanza kuzisukuma maiti hizo chini ya kitanda, alipo hakikisha kwamba amemaliza,akamtazama Camila ambaye anaendelea kulia. Kwa haraka akafungua vifungo vya shati lake alilo livaa, akatoa kichupa kidogo chenye unga unga wa dawa ya kulala, akajipaka kwenye maziwa yake kisha akambeba kamila na kumlisha ziwa lake la kulia, Camila akajaribu kunyonya ziwa hilo, ila kama mtoto ambaye amezoea ziwa la mama yake akashindwa kuendelea kunyonya, ila chembechembe za dawa hizo akazimeza na kumfanyanya kasi yake ya kulia kuanza kupungua na baada ya dakika chache sana akajikuta akilala usingizi fofofo.
Akamuweka kindani Camila, kisha akayarudisha maziwa yake ndani ya sidiria yake na kuyaweka sawa, kwa harakaa kajifunga vifungo vya shati lake, akambeba vizuri Camila na kumfunika na nguo maalumu ya kubebea watoto. Bastola yake akaificha kwenye mfuko wa koti lake na kutoka chumbani humu huku akiwa makini. Kwa kutembea kwa kijiamini kabisa akafanikiwa kufika katika maegesho ya magari, akafungua gari mlango wa nyuma ya gari lake aina ya vitz, akamuingiza Camila na kumuweka katika siti maalumu ya kubebea watoto. Akafungua mlango wa mbele na kuingia ndani ya gari hilo na kuondoka katika eneo hilo kwa mwendo wa kawaida. Ukaguzi mkali wa magari yanayo toka hapo geniti unaendelea, nesi Nansi akaonyesha kitambulisho chake, kutokana baadhi ya walinzi wanamfahamu wala hapakuwa na askari aliye weza kulisogelea gari lake na kulitazama ndani. Nesi Nasi akaruhusiwa kuondoka hospitalini hapa huku mbele yake akiwa ameongozana na gari nyeusi, nyenye bendera ndogo ya Tanzania.
***
Ndege za waokoaji, kutoka nchini Marekani, kwa haraka sana zikafika katike eneo ambalo ndege ya shirika la KLM, imezama. Wazamiaji wenye vifaa maalumu vya kupumulia wapatao hamsini wakaanza kuzama kuelekea chini kabisa, huku wakiwa na matochi makubwa ambayo yanaweza kuwawezesha kuona kila kitu kinacho endelea ndani ya bahari hiyo. Meli nyingine za kijeshi nazo zikafika katika eneo hilo ili kuhakikisha kwamba wanaokoa watu wambao wamo ndani ya ndege hiyo kwani uzuri ni kwamba hadi sasa hivi hawajaona mabaki ya aina yoyote yanayo elea angani na wana amanini kwamba kuna uwezekano wa asilimia kubwa sana ya abiria hao hadi sasa hivi kuwa hai.
Adrus na abiria wengine tayari wamesha jikatia tamaa, kwani hawaoni dalili yoyote ya kujiokoa, na wanacho kisubiria hivi sasa ni kufia ndani ya ndege hiyo kwani hewa ya oxygen inazidi kupungua. Adrsu akamtazama Cookie ambaye machozi yamemtoka kwa kulia hadi yamemkauka.
“Adrus?”
“Naam”
“Hatuna bahati, penzi letu ni jipya ila ndio tunakufa hivi”
“Usijali mpenzi wangu, hata tukifa basi Mungu nina imani atatupokea”
“Mungu atakupokea wewe, ila mimi hatoweza kunipokea”
“Kwa nini?”
“Mimi ni mwenye dhambi, nilipanga kukuua, nimesha ua pia watu wengi kwa kuweza kupewa amri na wakuu wangu ambao hivi sasa wapo huko juu wanaishi maisha ya raha na furaha”
Meneno ya Cookie yakamgusa vizuri Jang, ambaye akatamani kujielezea na yeye ila akashindwa kabisa kufanya hivyo.
“Hakuna aliye kamilia mbele ya Allah, hata mimi ni mwenye dhambi, ila kutokana tumesali na kutubu basi atatusamehe”
“Hei heii oneni kule”
Jing alizungumza huku akiwaonyesha Adrus na Cookie, mwanga unao ongekana kupitia kioo cha pembeni katika chumba hicho cha marubani. Mwanga huo mkali ukazidi kuongezeaka huku ikionekana fika ikajuka katika eneo hilo la ndege.
“Ni nini hicho”
Cookie aliuliza huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga.
“Hata mimi sifahamu”
Jing alijibu, Adrus akatazama vizuri mianga hii, taratibu akashusha pumzi huku amani ya moyo wake ikianza kufufuka kwa mara nyingine tena, kwani kwa jinsi mianga hii inavyo kuja dhairi inaonuesha ni watu ndio wanao kuja katika eneo hilo.
“Tumekuja kuekolewa”
Adrus alizungumza kwa furaha sana huku akiendelea kutazama mianga hiyo. Abiria wengine nao ambao tayari walisha anaza kukata tamaa, wakaanza kushangaa mianga hiyo mikali ikiizunguka ndege hiyo.
“Hichi ni nini?”
Bibi mmoja aliye kaa kwenye siti yake huku amejifunga mkanga aliuliza huku akitazama mianga hiyo, hapakuwa aliye weza kumjibu kwani hakuna abiri wa pembeni yake ambaye anafahamu ni nini kinacho endelaea na kila mtu anashangaa mianga hiyo.
Waokoaji hawa wakaanza wakendelea kuikagua ndege hii, cha kumshukuru Mungu kila eneo la ndege hiyo ipo salama na ahaina sehemu ambayo imekatika. Waokoaji wawilili wakaanza kurudi juu ili kutoa taarifa kwamba wameipata ndege hiyo, wakatumia dakika kama kumi kufika juu.
“Ndege ipo salama na abiria wake wapo ndani”
Muokoaji mmoja alizungumza huku akimtazama mkuu wa kikosi hicho.
“Haijaingia maji sehemu yoyote?”
“Ndio mkuu”
“Itabidi ivutwe kutoka chini kuja juu”
***
Madam Mery akafika jijini Dar es Salaam, helicopter yake ikatua katika kiwanja kikubwa cha mpira kilichopo Mbezi kwa Msuguri, akamkuta kijana wake Maliki akiwa anamsubiria.
“Karibu madam”
“Asante, wanaendeleaje?”
“Wanaendelea vizuri”
“Umeweza kuwapatia maelezo yoyote ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao?”
“Ndio madam”
Maliki akamfungulia madam Mery malango wa gari hilo, madam Mery akaingia na wakaondoka katika eneo hilo.
“Kuna nini kinacho endelea hapa jijini?”
“Aaahh ukaguzi upo mwingi katika kila sehemu ndio maana nimemuelekeza rubani kutua huku kwa maana tutapita katika njia ambazo hazina ukaguzi”
“Sawa”
Madam Mery akaitoa simu yake mfukoni na kumtumia meseji Phidaya.
‘Nimefika’
Meseji hiyo kwa haraka meseji hiyo ikajibiwa
‘Tutaonana wapi Wifi kwa maana sihitaji walinzi wangu waweze kufahamu nimekutana na wewe’
“Mmmmm”
Madam Mery liguna huku akiitazaama meseji hiyo, kisha akaijibu.
‘Ila wifi, hembu niambie ni kitu gani kinacho endelea’
‘Wifi vitu vingine si vya kuzungumza kwenye simu, ninahitaji kuonana na wewe uso kwa uso ili tuweze kuzungumza’
‘Sawa mimi kwa sasa ninataka kuelekea hotelini’
‘Hoteli gani?’
‘Kwenye hoteli yangu ya KF International’
‘Sawa tutaonana hapo’
‘Sawa wifi’
Madam Mery akaitafuta namba ya Eddy kwenye orodha ya kumbukumbu za kuhifadhia namba katika simu hiyo. Akaipata namba hiyo na kuitazama kwa muda, kisha akaipiga. Kwa bahati mbaya namba hiyo haikuweza kupatikana, akajaribu kurudia mara kadhaa ila jibu likawa ni hilo hilo. Madam Mery akatafakari kwa muda ila kutokana anafahamiana na Phidaya hakuwa na wasiwasi mwingi sana katika kukutana kwao.
***
Shamsa baada ya kumaliza kuchati na madam Mery akairudisha simu hiyo mfukoni mwake hukuakimtazama mlinzi anaye endesha gari hilo.
“Umesha wahi kukutana na ambushi?”
“Yaa nimesha wahi kukutana nayo”
“Ulishuhudia watu wakifa katika hiyo ambush?”
“Ndio”
“Okay basi leo tunakwenda kwenye ambushi, ambayo sinto hitaji uwe muoga, kuna kufa na kupona”
Shamsa alizungumza kwa kujiamini na kumfanya mlinzi huyu kumtazama tu.
“Ila hiyo itakuwa ni kazi nje ya majukumu yangu?”
“Jukumu lako si kunilinda mimi kwa kila hali?”
“Ndio”
“Basi utanilinda hata kwenye ambushi, nina jiamini katika hilo”
Mlinzi hakujibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kufwata maelezo ya wapi anapaswa kuelekea. Wakafika katika hoteli ya KF International.
“Tusishuke kwenye gari kwanza”
Shamsa alizungumza huku akiitoa simu ya Phidaya mfukoni mwake, akamuandikia Madam Mery ujumbe wa kumuuliza yupo wapi.
‘Ninakaribia kufika baada ya dakika kama mbili nikatuwepo hapo’
‘Sawa’
Shamsa akajilaza vizuri kwenye siti hiyo huku akiwa na hamu na shauku kubwa sana ya kuwea kumsubiria madama Mery.
***
Phidaya taratibu akajikaza na kukaa kitako kitandani mwake, akawatazama manesi wawili walipo katika chumba hichi. Akautazama mguu wake ulio fungwa bandeji.
“Mwanangu yupo wapi?”
“Yupo katika chumba maalumu yupo na manesi”
“Kamleteni”
“Sawa mama”
Nesi mmoja akaanza kutembea kuelekea mlangoni.
“Hei sister, naomba na simu yangu”
“Ahaa, simu tulimkabidhi yule binti yako”
“Nani…Shamsa!!?”
Phidaya aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.
“Ndio mama”
“Ohooo”
Pdhiaya alizungumza huku akijikuna kichwani mwake kwani anaamini lazima Shamsa azionene meseji alizo kuwa anawasiliana na madam Mery, anazo muomba kumsaidia dokta Ranjiti ambaye amemtorosha katika jumba la Eddy kwa kufanya mauaji ya wanajeshi wanne.
“Shamsa mwenyewe yupo wapi?”
“Nilimuona akiondoka na mmoja wa walinzi”
“Shitii naomba simu yako binti”
Phidaya alizungumwa huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Nesi huyo aiye baki ndani ya chumba hicho akamkabidhi Phidaya simu. Phidaya akafumba macho yake kidogo akijaribu kuikumbuka namba ya madam Mery, alipo hakikisha ameikumbuka, kwa haraka akaanza kuiandika katika simu hiyo na kumpigia madam Mery. Simu ya Madam Mery ikaanza kuita baada ya sekunde tano ikapokelewa
“Haloo”
“Mery mimi Phidaya ninazungumza hapa”
“Wifi vipi mbona unazungumza ukiwa na wasiwasi na umenipigia kwa namba nyingine ikiwa tunachati?”
“Wifi nakuomba unisikilize huyo unaye chati naye sio mimi, Shamsa ameiba simu yangu na yeye ndio anaitumia kuwasiliana na wewe?”
Meneno ya Phidaya yakamstua kidogo madam Mery.
“Heee, kumbe hapa nilipo ndio tunasimama kwenye hoteli yangu na nilipanga kuonana naye eneo hili sasa hivi”
“Ohoo Mungu wangu ninakuomba usionane naye, tafadhali ninakuomba usionene naye sawa”
“Sawa wifi ila ni kitu gani kinacho endelea?”
“Mery mimi ndio mtu wa pekee ambaye unaweza kuonana namimi na kukuelezea ni kitu gani kinacho endelea”
“Mmmm, wifi unaniogopesha mwenzio?”
“Usiogope ila ninakuomba ufanye kama nilivyo kueleaza sawa?”
“Sawa wifi nimekuelewa”
“Mimi ndio niyakuwa ninakupigia simu na kuwasilian ana wewe kwa maana hapa nilipo nipo Muhimbili nimejeruhiwa kwenye paja langu kwa risasi”
“Wifi, na Eddy yupo wapi?”
“Mume wangu naye pia ameshambuliwa kwa risasi, kwa hiyo ninakuomba uwe makini sana na Shamsa, sio mtu mzuri hivi sasa”
Meneno hayo yakazidi kumuogopesha madama Mery.
“Sawa wifi”
Phidaya akakata simu huku jasho likimwagika usoni mwake. Mlango ukafunguliwa, akaingia nesi huyu ambaye uso wake umejaa machozi na wasiwasi mwingi sana.
“Nesi Mariam……na….wa….le walinzi pale mlangoni wameuwawa na mtoto hayupo?”
Maeno ya nesi huyu yakazidi kumpa wendawazimu Phidaya aliye tamani kushuka kitandani mwake, ila akashindwa kutokana na maumivu mengi sana.
“Unasema?”
“Wameuwawa na mtoto hayupo”
Mlango ukafunguliwa na walinzi wawili wa kike wakaingia ndani ya chumba hichi.
“Madam tuna habari mbaya”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akimtazama Phidaya usoni mwake.
“Mwanao amepote na walinzi walio kuwa wakimlinda wameuwawa kwa kupigwa risasi”
Meneo ya mlinzi huyo wa kike yakazidi kumnyong’onyeza Phidaya na kujikuta akiwa amekaa kimya huku akikoa hata jambo la kuzungumza na machozi yakaanza kumwagika usoni mwake taratibu.
Mkuu wa kikosi cha ulinzi akaufungua mlango wa chumba alicho lazwa Eddy, akamtazama dokta Benjamini anaye endelea kuzungumza na Eddy, kisha akamtazama Eddy mwenyewe kwani taarifa anayo kwenda kuizungumza ni nzito sana kwa Eddy
“Vipi kuna tatizo?”
Eddy aliulizahuku akiyatazama macho ya mzee huyu.
“Ndio mkuu”
“Li…ii…nauhusiana na nani tena?”
Eddy alizungumza huku akimtazama mlinzi huyo. Dokta Benjamini akatingisha kichwa akimuashiria mlinzi huyo asizungumze kwani tayari Eddy amesha tawaliwa na wasiwasi mwingi sana.
“Niambie ni nani anatatizo?”
Eddy alizungmza kwa ukali sana.
“Muheshimiwa mwanao Camila amepotea katika mazingira ya kutatanisha na walinzi wawili pamoja na nesi walio kuwa wakimlinda wameuwawa”
“What…….?”
Eddy mwili ukaanza kumtetemeka kwa hasira kali sana, japo ana maumivu makali sana mguuni mwake, akaanza kushuka kwenye kitanda. Dokta Benjamini akamuwahi kumzuia ila akamsukumia pembeni. Eddy akasimama wima huku mguu wenye jeraha la risasi, ukimtetemeka sana na taratibu damu zikaanza kumwagika katika jeraha hilo na kusababisha bandeji alilo fungwa kujawa na damu nyingi.
***
Nensi Nansi akasimamisha gari lake katika jumba moja kubwa lililopo porini kidogo maeneo ya Mbezi luis. Walinzi walio valia nguo nyeusi walipo katika eneo hilo wakalisogelea gari hilo. Nesi Nansi akashuka kwenye gari hilo akaitoa bastola yake na kumkabidhi mlinzi mmoja, wakamkagua kila eneo la mwili wake, walipo hakikisha kwamba hana chochote, akaruhusiwa kuigia ndani ya jumba hilo.
“Nina mzigo nilio agizwa”
Nesi Nansi alizungumza huku akifungua mlango wa nyuma wa gari hilo, akamchukua Camila ambaye hadi sasa hajaamka kutoka usingizini. Akambebe na kuuanza kuondoka naye kuelekea ndani akafunguliwa mlango wa kuingilia katika eneo la sebleni humo. Akamkuta bosi wake aliye muagiaza kuifanya hiyo kazi.
“Mkuu nimefika”
Mwanamke huyo mrefu akageuka taratibu huku akitabasamu, mkononi mwake ameshika glasi moja ya mvinyo. Kwa mwendo wa madoido akatembea hadi alipo simama nesi Nansi.
“Waooo mtoto mzuri, anaitwa nani?”
“Anaitwa Camila”
“Ahaa, Camila karibu kwa anti K2”
K2 alizungumza huku taratibu akimchukua Camila mikononi mwa Nansi.
‘Naamini baba yako atanipa nafasi kwa ajili ya hili swala’
K2 alizungumza huku akimbusu Camila mdomoni mwake kwa furaha kubwa sana kwani kupitia mtoto huyo kile anacho kihitaji basi anaweza kukipata haraka iwezekanavyo na malengo yake na kaka yeka basi yatatimia muda si mrefu kuanzia hivi sasa
K2 akamgeukia nesi Nansi na kumtazama msicha huyu kazi nzuri aliyo weza kuifanya.
“Passport yako ya kusafiria na pesa zako dola milioni moja na nusu za kimarekani, vipo tayari. Vijana wangu watakuchukua hadi mpakani mwa Kenya na Tanzania, utapanda ndege na kuelekea nchini Brazili na utaanza maisha yako mapya huko, hakikisha kwamba hurudi nchini Tanzania pasipo mimi kukupigia simu umenielewa?”
“Nimekuelewa mkuu, ninashukuru sana kwa msaada wako”
“Usijali, mimi nikutakie safari njema”
K2 akapeana mkono wa kuana na nesi Nansi, kisha nesi Nansi akatoka ndani humo, akaingia kwenye gari maalumu lililo andaliwa kwa safari yake hiyo, akakbidhia hati yake ya kusafiria yenye jina lake pamoja, huku akipewa kadi ya benki anayo weza kutoa pesa nchi yoyote kwenye akauti yeke yenye kiashi hicho kikubwa cha pesa.
***
Shamsa kwa haraka akaka vizuri kwenye siti yake na kuliangalia gari la kifahari aina ya lililo katika eneo la hoteli hiyo, kwa haraka haraka akatambu kabisa kwamba gari hilo ni gari la madam Mery.
“Naomba bastola yako”
Shamsa alizungumza huku akimnyooshea mkono mlinzi aliye naye ndani ya gari.
“Mmmm”
“Naomba bwana una guna nini, au unahisi kwamba siwezi kuitumia?”
Mlinzi hiyo taratibu akaichomoa bastola yake aliyo ichomeka kiunoni mwake, akamkabidhi Shamsa, aliye anza kuikagua kwa kutoa magazine, alipo hakikisha kwamba amekuta risasi za kutosha akairudisha magazine hiyo, kisha akaikoki vizuri na kuendelea kulitazama gari la madam Mery.
“Mbona hashuki?”
“Sijajua hata mimi, humbu jaribu kumpigia simu”
“Ngoja nimuandikie meseji”
Shamsa akakitoa simu ya Phidaya mfukoni mwake na kuanza kumuandikia madam Mery ujumbe mfupi.
‘Wifi umefika?’
Kitendo cha madam Mery kumaliza kuzungumza na simu na Phidaya aliye mpigia kwa ndamba mpya kukamfanya kutazama eneo la maegesho ya magari katika hoteli yake hiyo. Ujumbe mfupi wa meseji uliyo ingia kwenye simu yake kutoka katika namba ya Phidaya ukamstua sana, akautazama kisha akaendelea kukagua magari, akabahatika kuona gari moja jeusi alilo litilia mashaka sana, alipo tazama namba za usajili wa gari hilo hapo ndipo akadhibitisha kwamba gari hilo ndipo alipo Shamsa.
“Vipi madam”
“Huyu binti mshenzi sana, anacheza na akili yangu”
“Kuna nini kinacho endelea?”
“Ameiba simu ya mama yake, na muda wote anao chati na mimi nilihisi ni Phidaya kumbe ni yeye”
“Kwa nini ameamua kufanya hivyo?”
“Sijajua lengo lake haswa ni nini, geuza gari tuondoke?”
“Ila madam kama ana lengo baya huyo biti lazima atatufwatilia, inabidi na wewe umdanganye”
“Nimadanganye vipi ikwa tumesha fika hapa na gari lake ni lile pale”
Madam Mery alizungumza huku akinyooshea kidole gari analo amimi kwamba Shamsa ndipo alipo, uzuri ni kwamba magari yote mawili yana vioo vyeusi ambavyo sio rahisi kwa mtu wa nje kuweza kuona ndani ya gari hilo.
“Mdanganye kwamba bado upo kwenye foleni ili iwe rahisi kwa sisi kuweza kuondoka hapa”
Madam Mery akafikiria wazo hilo kwa sekunde kadhaa, akaona ni wazo zuri kwa upande wao, kwa haraka akaanza kuandika kile alicho elezwa na kijana wake kisha akaituma katika simu ya Phidaya.
“Tuondoke tayari nimesha tuma”
“Subiria kwanza”
Shamsa kwa haraka akaufungua ujumbe huo wa meseji ulio andikwa kwenye namba yake ya simu. Akaachia msunyo mkali hadi mlinzi wake akamtazama.
“Nini”
“Kuna kitu ambacho ananifisha huyu mpuuzi?”
“Kitu gani?”
“Anasemaa yupo kwenye foleni na mimi nina wasiwasi na gari lile pale”
“Kuna foleni gani hapo barabarani sasa, hajui kudanganya”
“Ninashuka hakikisha kwamba unakuwa makini na mimi sawa”
Shamsa alizungungumza kwa msisitizo huku akifungu amlango, akaichomeka bastola hiyo nyuma ya suruali yake na kuifunika na tisheti yake aliyo ivaa, akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea katika gari hilo aina ya Hammer.
“Tuondoke, tuondoke anakuja”
Madam Mery alizungumza kwa sauti ya misistizo huku akimtazama Shamsa anaye kuja kwa hatua za haraka haraka sana, kijana wa madam Mery akawasha gari na kuandoka kwa kasi katika aneo hilo, jambo lililo mshangaza kila mmoja ambaye aliweza kuona tukio hilo. Mlinzi wa Shamsa kwa haraka na yeye akawasha gari na kumfwata Shamsa sehemu alipo simama. Shamsa hakuhitaji hata kusubiri gari hilo kusimama vizuri, kwa haraka akafungua mlango na kurukia kwenye siti na kuufunga mlango kwa nguvu, mlinzi hiyo akakanyaga mafuta kwa kasi na kuzifanya tairi za nyuma za gari hilo kuserereka kwa sekunde kadhaa, kisha ziklipa gari hilo nguvu ya kuondoka kwa kasi na kuzidi kuwashangaza mashuhuda huku wafanyakazi wa hoteli hiyo wakjiuliza ni kitu gani kinacho endelea kwa bosi wao anaye fukuzwa
***
Walinzi wote macho yakawatoka baada ya kumuona Eddy akiwa amesimama kwenye mlango wa chumba alicho lazwa.
“Ni chumba gani?”
“Huku muheshimiwa”
Mkuu wa kikosi hicho alizungumza huku akianza kuongoza njia , na walinzi wote wakamuweka kati makamu wa raisi, Eddy Godwin anaye tembea kwa kuchechemea. Dokta Benjamini naye hakuhitaji kupitwa na tukio hilo, kwnai jukumu lake kubwa ni kumtazama Eddy kwamba anakuwa salama salmini, wakafika katika chumba kulipo toke mauji na kuwakuta wanajeshi pamoja na walinzi wa ikulu wakiendelea kufanya uchunguzi wa eneo hilo. Eddy akaingia ndani ya chumba hicho na kutazama maiti za walinzi wawili pamoja na nesi mmoja.
“Muuaji ni professional killer kwa maana watu wote amewaua kwa kuwapiga risasi za kichwa”
Mkuu wa upelelezi wa matukio ya mauaji alizungumza huku akimuonyesha makamu wa riais jinsi watu hao walivyo uwawa.
“Hichi chumba hakina CCTV camera?”
Eddy alimuuliza mpelelezi huyo.
“Ndio muheshimiwa, na kwa bahati mbaya hata hapo kwenye kordo hakuna CCVT camera”
“Pumbavu, hakikisheni kwamba mwanangu anapatikana kabla ya siku hii ya leo kuisha sawa”
“Sawa”
“Nipe simu yako”
Eddy alizungumza huku akimnyooshea dokta Benjamini mkono, doka Benjamini akatoa simu yake na kumkabidhi Eddy aliye ipokea na kuanza kutoka nje ya chumba hicho huku akiwa amejawa na hasira kali sana. Akaiandika namba ya Rahab na kumpigia, simu ya Rahab ikaanza kuita na baada ya sekunde sita ikapokelewa.
***
Rahab na wezake wakika waktikati ya kuendelea kupanga mipango yao ya wao kuweza kuanza kusaka wanachama wa chama cha D.F.E, mmoja badaa ya mwengine, simu yake ikaanza kuita, jambo lililo mfanya kusitisha mazungumzo aliyo kuwa anayazungumza. Akaichukua simu yake iliuo juu ya meza na kukuta ni namba ya dokta Benjamini, akaipokea simu hiyo na kuiweka sikoni mwake.
“Ndio dokta”
“Ni mimi”
“Eddy?”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake ambao nao walipo sikia jina la Eddy likitajwa, wakakaa kimya kumsikiliza ni kitu gani ambacho anakizungumza.
“Ndio, kuna tatizo ambalo limetokea”
“Tatizo gani tena?”
“Hadi ninavyo zungumza hivi sasa hivi, Camila inasadikika kwamba ametekwa. Walinzi wawili pamoja na nesi aliye kuwa akimuhudumia wote wameuwawa”
“Ohoo Mungu wangu”
Raisi Rahab alizungumza huku akijaa vizuri kwenye sofa alilo kali, kwani habari hiyo nayo imemuogopesha na kumsikitisha.
“Ndio hivyo, nimewapa siku hii nzima hii, vijawa wamtafute mwanangu hadi pale atakapo patikana”
“Haki ya Mungu, ninakuahidi Eddy nitahakikisha kwamba siku hii haiishi Ranjiti lazima awe amepatikana na akipatikana basi lazima aseme ni wapi alipo mchukua Camila”
“Nashukuru, ila na mimi ninaingia katika msako wa kumtafuta mwanangu”
“Eddy, aa….acha….cha kunitania”
“Ninacho kizungumza nina kimanaisha, siwezi kuendelea kulala kitandani ikwa mwanangu amechukuliwa na wapuuzi, Junioni Jr hayupo, huyu pia wamchukue haiwezekani hata kidogo”
“Eddy, tupo kwa ajili yako, ninakuomba uweze kuuuguza majeraha yako afya yaki ikwa nzuri basi utarudi katika kazi ila kwa sasa habapana baba yangu haujakaa sawa”
“Nilipambana miaka yangu yote ya ujana kwa ajili ya familia yangu, leo hii siwezi kuachia watu wa ajabu ajabu waipoteze furaha ya familia yangu umenielewa”
Eddy alizungumza kwa msisitizo jambo lililo mfanuya Rahab kukaa kimya kwa muda.
“Sawa ninekuelewa, ila ninakuomba uwe makini?”
“Usijali”
Simu ikakatwa na kumfanya Rahab kushusha pumzi yak echini taratibu.
“Kuna nini kinacho endelea?”
Ann aliuliza kwa shauku sana.
“Camila ametekwa”
“Huyu mtoto aliye zaliwa juzi juzi?”
“Ndio”
“Kum***ke zao waseng*** hao, lazima tule nao sahani moja”
Fetty alizungumza kwa hasira sana huku aking’ata meno yake, tukio hilo linazidi kuonyesha kwamba maadui wa serikali ya Rahab, hususani wa makamu wake wa raisi Eddy Godwin, bado wana nguvu kubwa ya kufanya chochote wanacho jisikia na muda wowote wanao utaka wao kufanya hivyo.
***
Mlinzi wa Shamsa, katika upande wa uandeshaji wa magari yupo vizuri sana, kwani kwa jinsi anavyo lipeleka kasi gari hilo hadi Shamsa yeye mwenyewe anashangaa.
“Shiti”
Mlinzi huyo alizungumza huku akikamata breki za gafla baada ya gari lori la mchanga kuingia bararabani humo galfa bila ya dereva wake kufwata sheria za barabara vizuri.
“Mseng*** huyu”
Shamsa alizungumza huku akitazama lori hilo, huku dereva wake akijitahidi kuliweka sawa barabarani. Mlinzi wa huyo akaanza kuopig honi kwa nguvu ili kuhakikisha kwamba gari hilo linawapisha. Vijana wanne walio chafuka sana walio pakizwa nyuma ya lori hilo wakaanza kushangilia huku wakiwazomea Shama na mlinzi wake wanao jaribu kulipita gari hilo ila derava wao analeta masiraha ya kuttanda njia nzima.
“Pumbavu”
Shamsa alizungumza kwa hasira, kwa haraka akafungua kioo cha upande wake, akaikoki bastola yake vizuri, akautoa mkono wake wa kushoto na kuanza kupiga tairi za nyuma za lori hilo risasi, zilizo sababisha tairi zote kupasuka na lori hilo kuserereka vibaya na kuingia kwenye mtaro likiwa na watu wake ambao shangwe zikabadilika na kuwa vilio huku kila mmoja akimuita mama pamoja na Mungu wake anaye muabudu.
“Wapo wapi?”
Madam Mery alizungumza kwa wasiwasi mwingi, huku akitazama nyuma kwani halioni gari la Shamsa lililo kuwa likiwafukuza kutoka hotelini.
“Tumewapoteza madam, kuwa na amani”
Madam Mery akashusha pumzi nyingi huku akiupelekea mkono wake wa kushoto katika batani ya kufungua mkanda, kabla hata ajaiminya batani hiyo, akashtukia kuona gari alilomo Shamsa likimalizia kukunja kona ambayo wameipita.
“Hao wanakuja”
Madam Mery alizungumza huku macho yakimtoka na kumfanya kijana wake naye kuzidi kuongeza mwendo wa gari hilo la kifahari linalo sifika kukimbia sana japo lina uzito mkubwa unao sababishwa na vyumba vilivyo tengenezea gari hilo.
“Nimekuaminia”
Shasma alizungumza hukua kitabasamu, kwani alisha kata tamaa ya kuwakamata madam Mery na kijana wake walio kuwa wamewapoteza kutokana na ujinga wa dereva wa lori la mchanga.
“Tuwapite au?”
Mlinzi huyu alizungumza huku akitazama spidi yake gari lake ambayo inaelekea kwenye mia mbili na ishirini na sita.
“Wapite niwashambulie kwa mbele”
“Hiyo gari ni Hammer, haiingia risasi sehemu yoyote, si kwenye tairi wala tairi lake”
“Duu sasa si tunawakimbiza bure?”
“Kwani unawahitaji kuwaua wau unahitaji kufanyaje?”
“Ninamtaka madam Mery kumuhoji yeye ndio ameuhusika katika kumficha dokta Ranjiti”
“Heee, hili swala ni kubwa basi, tuwasiliane na kitengo changu tujue tunawakamata vipi, pasipo kufanya hivyo tutawakimbiza bure tu”
“Sihitaji kitengo cha aina yoyote kuweza kuingilia hili swala, hili ni tatizo la kufamilia na watu wa nje hawapaswi kufahamu”
“Ila kumbuka huyo dokta amewauwa wetumishi wa serikali?”
“Nalitambua, kuna mtandao mkubwa unao endelea, pasipo kufanya hili swala kimya kimya hatuwezi kufanikiwa, wewe nisikilize mimi ninacho kuambia sawa”
“Sawa mama”
“Wewe, twende nao…ninafikiria nini cha kufanya”
Shamsa alizungumza huku akiitoa simu yake mfukoni inayo ita, akakuta namba ngeni, akaitazama kwa muda kidogo kisha akipokea.
“Haloo”
“Upo wapi wewe?”
Shamsa aliisikia sauti ya ukali ya Eddy akizungumza.
“Eddy”
“Sema upo wapi?”
“Aha…a….a..aa nipo nipo mjini vipi mbona unafoka hivyo?”
“Nataka kurudi sasa hivi hapa hospitalini, umenielewa”
“Kuna nini kwani?”
“Nimekuambia rudi hapa hospitalini, hali ya usalama sio nzuri, hadi ninavyo zungumza hivi sasa Camila ametekwa na watu wasio julikana na walinzi pamona na nesi walio kuwa wakimlinda wameuwawa”
Taarifa hiyo ikamufanya mwili wa Shamsa kuzizima kwa ubaridi kwani sio kitu alicho kitarajia kukisikia kwa muda huu.
“Shamsa”
“Ninakusikia Eddy”
“Nimekuambia rudi sasa hivi hospitalini, hili sio ombi ni amri”
“Siwezi kurudi”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya msisitizo.
“Unasemaje?”
“Siwezi kurudi kwani hadi sasa hivi ninamfwatilia mtu aliye wahifadhi dokta Ranjiti na mwanaye”
“What? Ni nani huyo……?”
Simu ya Shamsa ikazima chaji, akaitazama kwa sekunde kadhaa, na kurudisha mfukoni mwake huku jazba ikiendelea kukitesa kifua chake.
“Wapite hata kama wapo ndani ya Hammer nitahakikisha ninawasimamisha sawa”
“Yes madam”
Mlinzi wa Shamsa akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari hili na taratibu akaanza kuliopita gari la madama Mery jambo lililo washangaza madama Mery na kijana wake.
“Wanataka kufana nini hawa?
Madam Mery alizungumza huku akilitazama gari la Shamsa jinsi linzavyo zidi kuwapita.
“Sijajua madam”
“Hembu funga breki kwanza?”
“Madam”
“Simama, sioni haja ya kukimbizana, tusije tukafa kwa vitu vya kijinga bwana”
Madam Merry alizungumza kwa msisitizo mkali, kijana wake katii amri na kuanza kukanyaga breki na kusababisha gari hili kuanza kuserereka barabarani huku dereva wa Shamsa akijitahidi na yeye kupunguza mwendo kasi wa gari lake analo liendesha. Kwa utaalamu mkubwa huku akiwa amenyanyua hand brake, mlizi wa Shamsa akaligeuza gari hilo na kusababisha ligeukie linapo tokea na kusimama mita chache kutoka lilipo simama gari la madam Mery. Shamsa kwa haraka akafungua mlango huku akiichomo bastola aliyo ichomeka kiunoni mwake. Kitendo cha Shamsa kuwa na bastola mkononi mwake, kikazidi kumchanganya kijana wa madam Mery.
“Madam ana silaha”
“Muache hawezi kuniua”
Madam Mery alizungumza huku akifungu mlango wa gari lake na kushuka, huku akimtazama Shamsa usoni mwake anaye onekana amefura hasira kali sana.
***
Eddy huku jasho likiendelea kumwagika na damu zikiendelea kuchurizika kwenye mguu wake ulio patwa na jeraha, anazidi kumtafuta Shamsa hewani ila hampati, jambo lililo zidi kumchanganya, kwani sentensi ya mwisho aliyo izungumza Shamsa anaonenekana yupo kwenye wakati mgumu sana wa kumfawatilia mtu anaye dai kwamba anajua ni wapi dokta Ranjiti na madam Mery walipo jificha.
“Muheshimiwa pasipo kukuvunjia heshima, utazidi kujingezea matatizo katika jeraha lako, tazama damu zinavyo kumwagika, ninakuomba ukae chini utulie tulishuhulikie jeraha lako”
Dokta Benjamini alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge huku akimtazama Eddy usoni mwake. Eddy akatazama jerala lake linalo mwaga damu, kwa ukakamavu akaanza kutembea kurudi katika chumba alicho kuwa amelawa, si mlinzi wala si dokta Benjamani aliye jaribu hata kumshika mkono wake ili kumsaidia kwani kila mtu anamuogapa kwa hasira kali aliyo nayo.
“Una weza kutrack namba ya mtu na kufahamu ni wapi alipo?”
Eddy alimuuliza mzee, ambaye ndio mkuu wa kikosi kinacho mlinda.
“Ndio muheshimiwa inawezekana”
“Hembu hakikisheni muna itrack namba ya Shamsa na kujua ni wapu alipo sasa hivi na munipatie jibu sawa”
“Sawa mkuu”
“Na kumbukeni mwanangu amatekewa, ninahitaji kila baada ya dakika thelathini muwe munanitapatia ripoti sawa”
“Sawa mkuu”
Mzee huyo akatoka katika chumba hicho na kumuacha dokta Benjamii akianza shuhuli mpya ya kuhudumia jeraha la Eddy linalo zidi kumwaga damu. Kila baada ya dakika kadhaa, Eddy aliachi msunyo mkali ambao ndani ya moyo wake anajilaumu ni kwa nini ameumia na kushindwa kuilinda familia yake ipasavyo.
“Haujamaliza tu?”
Eddy alimuuliza dokta Benjamini anaye endelea kukishuhulikia kidonda hicho.
“Muheshimiwa bado kwa maana nyuzi za kidonda zimeachia kabisa na kusababisa kidonda kuongezeka zaidi na zaidi”
Dokta Benjamini alizungumza kwa sauti ya upole na unyenyekevu mkubwa sana kwa makamu wa raisi bwana Eddy Godwin.
“Fanya unavyo fanya, ukimaliza ninahitaji unichome sindano ya kupunguza maumivu na nitahitaji kuendelea na kazi zangu kama kawaida sawa?”
“Sawa muheshimiwa”
“Ninahitaji mke wangu aitwe ninahitaji kuzungumza naye”
Ikamlazima dokta Benjamini kupiga hatua hadi mlangoni, akafungua na kumnong’oneza mlinzi mmoja juu ya amri hiyo iliyo tolewa na makamu wa raisi kisha akarudi ndani ya chumba hicho na kuendelea na jukumu la kumuhudumia.
Mlinzi huyo akaongoza hadi katika chumba alicho lazwa Phidaya na kuwakuta wezake wengine wakiendelea kuimarisha ulinzi.
“Madam anahitajiwa na mumewe”
Mlinzi wa kike akaingia ndani ya chumba hicho na kumkumta Phidaya akiwa bado yupo katika hali ya kupumbaa huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.
“Ahaa madam muheshimiwa makamu wa raisi anakuhitaji?”
Phidaya akamtazama mlinzi huyo wa kike kwa sekunde kasha, kisha akaendelea kukaa kama alivyo kuwa amekaa. Nesi mmoja akatingisha kichwa akimuashiria mlinzi huyo kwamba hali ya Phidaya sio nzuri na toka apokee taarifa hiyo ya kupotea kwa mwanaye amekuwa ni mtu mwenye mawazo mengi na hata umsemeshe basi hana jibu la kukujibu.
“Naomba tumpe muda”
“Sawa”
Mlinzi huyo akatoka na kurudisha ujumbe kwa mlinzi mwenzake aliye agizwa na dokta Benjamini kwamba Phidaya hali yake sio nzuri na amekataa wito wa mume wake.
***
Anna akamaliza kuoga, akatoka bafuni huku akiwa yupo uchi kabisa, akafungua kabati kubwa la nguo lililopo katike chumba hicho alicho ingia. Akakuta nguo nyingi za kila aina. Akatoa jinzi moja ya kike, akaithaminisha kwa mcho na kunai inamfaa sana, taratibu akaivaa, akatafuta tafuta ndani ya kabati hilo na kuona tisheti nyeusi, akaipenda sana na kuivaa. Akazibana nyele zake ndefu kwa nyuma huku akijitazama kwenye kioo kikubwa kilichopo humu ndani, alipo hakikisha kwamba yupo poa, akarudi sebleni na kumkuta baba yake dokta Ranjiti akiwa amejilaza kwenye sofa.
“Huna njaa?”
Anna alizungumza kwa ufupi huku akielekea jikoni, akafungua friji na kukuta matunda ya kila aina. Akachukua matunda, ma-apple mawili pamoja na juisi mbili za kopo na kurudi sebleni. Akaweka juisi moja na tunda moja juu ya meza na kukaa katika sofa jengine huku akimtazama baba yake anaye onekana kujawa na mawazo mengi sana.
“Sikutegemea siku hata moja ningeweza kufika katika nchi kama hii”
Anna alizungumza huku akimtazama baba yake, taratibu dokta Ranjiti akaka kitako na kumtazama mwanye, kisha akatazama tunda na juisi aliyo wekewa mezani, taratibu akavichukua na kuanza kuling’ata tunda.
“Ila kwa ajili yako nimefika, ni bora ningefika kwa wema ila nimefika kama muhalifu kwa ajili ya madhambi yako, hivi baba kuna kitu gani ambacho umekikosa kwenye maisha yako lakini eheeee?”
“Anna”
“Nini?”
“Natambua kwamba mimi ni miongoni mwa mababa waovu duniani, nafasi ambayo ninakuomba mwanangu, tafadhali ninakuomba uweze kunisamehe katika hili, natambua nimekuingiza katika mikono mibaya ya kiserikali ambayo kusema kweli itakuwia shida kwenye maisha yako ila ninakuomba unisamehe sana mwanangu”
“Siwezi kukusamehe pasipo kuniambia uhalisia wako, siwezi kuwa na baba mwenye matatizo makubwa na ukanishawishi mimi kukufwata wewe”
Dokta Ranjiti akaendelea kufakamia tunda hilo alilo pewa huku na mwanaye, huku akiwa anawaza ni kitu gani anaweza kukizungumza ili mwanye huyo aweze kumuelewa. Anna akachukua rimoti ya Tv na kuwasha, wakakutana na picha za sura zao wakiambiwa kwamba wanatafutwa na jeshi la ulinzi chini Tanzania na wamejihusisha kwenye mauaji ya wanajeshi kadhaa huku wakiwa wamebambikiwa kosa jengine lililo washangaza kila mmoja kwamba wamehusika katika kumteka mtoto wa makamu wa raisi Camila.
“Baba”
Anna aliita huku akimtazama dokta Ranjiti ambaye naye taratibu akasimama huku akiendelea kushangaa, kwani wao sio wahusika wa tukio hilo na wala si wahusika wa mauaji ya wanajeshi hao wanne.
***
John akaka vizuri huku akitazama taarifa hiyo ya habari inayo zidi kuzaagaa duniani kwa kasi kwamba mtoto wa makamu wa raisi Tanzania, Camila aliye jipatia umaafuru mkubwa kipindi alipo kuwa amefanyiwa sherehe kubwa ya kukaribishwa nyumbani, kwamba ametekwa na dokta Ranjiti pamoja na mwanaye ambao pia wanahusika na mauji ya wanajeshi wanne. Muandishi wa kituo hicho cha BBC akaendelea kuzungumza kwamba dokta Ranjiti na mwanaye Anna, wamajeruhi kwa risasi mke wa makamu wa raisi bi Phidaya kisha wakatokomea pasipo julikana. John akachukua rimoti na kupunguza sauti ya Tv hiyo na kumgeukia mlinzi wake aliye simama pembeni ya meza ya ofisi yake hiyo iliyopo katika manuari hii iliyo chini ya bahari ambapo ndio eneo lake ambalo anaweza kujificha kwa sasa kwani hata yeye anatafutwa kwa udi na uvumba na vikosi vya usalama vya nchini Uingereza.
“Hembu mpigie yule rafiki yako, sijui Livna sijui nani ahakikishe kwamba anamuokoa dokta Ranjiti na mwanaye kwani kazi walio ifanya ni kubwa sana na tunamuhitaji huyo Camila sawa”
“Sawa mkuu ila inabidi kumuomba msamaha Livna kwa kauli zako ulizo zungumza dhidi yake”
Mlinzi wa John alizungumza kwa upole huku akimtazama bosi wake huyo.
“Tatizo ni msamaha tu?”
“Ndio mkuu na endapo utasawazisha tofauti zilizopo katia yako na yeye basi tunaweza kuingia kwenye makubaliano ambayo yatakuwa na faidi kwa upande wetu”
“Sawa migie kwa mfumo wa video kwa maana ninahitaji kumuona huyo ninaye zungumza naye”
“Sawa”
***
Msaidizi wa Livna akagonga katika mlango wa chumba cha Livna, taratibu mlango ukafunguliwa na Livna akasimama huku akimtazama msichana huyo.
“Mkuu kuna simu yako hapa”
Msichana huyo alizungumza huku akiwa ameshika simu kubwa aina ya tablate.
“Ni nani?”
“Yule rafiki yako”
Livna akaichukua tablate hiyo na kutazama na rafiki yake hiyo.
“Kuna ulicho kisahau?”
“Livna kwanza ninakuomba nitangulize msamaha kwako kwa maana ninatambua kwamba bosi wangu alikukosea katokana na kauli zake alizo kuwa akizizungumza mbele yako”
“Nenda kwenye pointi?”
“Bosi wangu anahitaji kuzungumza na wewe”
“Mpe simu nimuone”
Livna alizungumza kwa sauti ya msisitozo huku akiwa amemkazia macho rafiki yake huyo. Sura ya John aikaanza kuonekana.
“Livna ninakuomba unisamehe kwa kila kitu ambacho kilitokea, ninakuomba unisamehe sana”
“Nimekuelewa, unahitaji nini?”
“Kuna daktari na mwanaye ambao kwa sasa wapo nchini Tanzania na serikali inajitahidi kuwatafuta kwa udi na uvumba, ninakuomba uweze kuwaokoa na nitakupa malekezo ya wapi uwalete”
“Dola milioni tatu nikufanyie kazi yako?”
“Dola milioni tatu!!?”
John aliuliza huku macho yakimtoka kwani kiasi alicho tajiwa ni kikubwa sana.
“Kama huna hiyo pesa, siwezi kukufanyia kazi yako, siwezi kuweka maisha ya vijana wangu hatarini kwa ajili ya pesa ndogo”
John akaka kumya huku akimtazama Livna.
“Nitakupa dola milioni mbilli na nusu?”
“Kwenye biashara ya kuhatarisha maisha huwa sihitaji kupangiwa bei tofauti na niliyo sema, kama unahitaji kufanya kazi na mimi potezea”
“Nitakupatia hicho kiasi na niahidi kwamba utaweza kuwasaidia dokta Ranjiti na huyo mwanaye na pia amemteka mtoto wa makamu wa raisi anaitwa Camila pia huyo ninamuhitaji”
“Kwa ajili ya mtoto ongeza dola milioni mbili, jumla dola milioni tano, kama umuhitaji mtoto itabaki hiyo dola milioni tatu”
“Mmmm ila ni mtoto mchanga?”
“Ila anatafutwa, unahisi kwamba nchi kwa sasa nguvu yao wataipeleka wapi, so biashara ni biashara, ingiza pesa ufanyiwe kazi unayo hitaji”
John akafumba macho taratibu huku akishusha pumzi nyingi sana, taratibu akayafumbua macho yake na kumtazama Livna.
“Sawa nipatie detail za akaunti yako ya benki nikuingizie hicho kiasi”
“Utatumia na kijana wangu sawa, utanipatia masaa ishirini na nne watu wako watakuwa mikononi mwako sawa”
“Sawa, ninakuamini”
“Poa”
Livna akakata simu hiyo na kumrudishia kijana wake.
“Nahitaji muda wa kupumzika, panga kikosi kitakacho kwenda kulishuhulikia hilo tatizo hakikisha kwamba pesa inaingia na kazi ndio inafanyika, sawa”
“Sawa, ila mkuu upo sawa?”
“Sipo sawa, ndio maana ninahitaji kupumzika kwa sasa”
Livna baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akaufunga mlango wa chumba chake na kurudi kitandani alipo kuwa amejilaza.
***
Madam Mery akaendelea kumatazama Shamsa anaye mfwata kwa haraka huku akiwa amemshikia bastola.
“Shamsa unanishikia silaha, mimi na wewe tuna matatizo kwani?”
Madam Mery alizungumza huku akimtazama Shamsa aliye simama hatua chache sana kutoka sehemu walipo simama.
“Ninahitaji kuzungumza na wewe sasa hivi”
“Hata mimi ninahitaji kuzungumza na wewe”
“Hivi ni kitu gani kinacho endelea kati yako wewe na Phidaya?”
“Niambie ni wapi alipo dokta Ranjiti na mwanaye, ukishindwa kufanya hivyo ninakufumbua ubongo wako na sinto jali kama ninakujua au una ukaribu gani na familia yangu?”
Shamsa alizungumza kwa msisitizo huku akiendelea kumnyooshea madama Mery bastola hiyo aliyo elekea usawa wa kichwa chake.
“Shamsa siwezi kukuambia juu ya hao watu pasipo wewe mwenyewe kuniambia ni kitu gani kinacho endelea”
Shamsa bila ya utani akapiga risasi chini mita chache sana kutoka alipo simama madam Mery na kumfanya atetemeke.
“Huwa sitanii pale ninapo uliza swali langu, niambie wapo wapi, safahi hii ninakumwaga ubongo wako chini”
Madam Mery akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Shamsa, aliye chafukwa hadi roho, na hapo ametawaliwa na hasira inayo weza kumpelekea kufanya kitu chochote.
“Ninao wapo kwenye nyumba yangu ya siri”
“Twende kwenye gari langu na utupelekea katika nyumba hiyo”
“Sawa”
Madam Mery alizungumza huku akinyoosha mikono yake juu, taratibu akaanza kutembea hadi sehemu alipo simama Shamsa, amabaye bado anaendelea kumnyooshea bastola hiyo aliyo ishika kikakamavu sana.
“Tangulia kwenye gari”
Shamsa alizungumza na kumfanya madam Mery kuanza kutangulia na kuelekea lilipo gari la Shamsa, kijana wa madam Mery kwa haraka akashuka kwenye gari hilo ili kumsaidia bosi wake ila alipo kutana na macho ya Shamsa yalliyo mtazama kwa ukali huku akiwa ameelekezewa bastola hiyo.
***
Vijana wanne wa Livna ambao wapi jiji Dar es Salaam kwa pamoja wakakutana, ili kuweza kuifanya kazi iliyopo mbele yao. Kwa haraka wakaingia kwenye gari aina ya Range Rover huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi.
“Location inaonyesha muhusika yupo wapi?”
Dereva aliuliza huku akiwageukia wezake wawili walio kaa nyuma ya gari hilo huku wakiwa na simu maalumu zinazo onyesha ni wapi alipo dokta Ranjiti na mwanaye.
“Wapo nje ya Dar es Salaam, kutoka hapa tulupo tuna kilmita kumi kuweza kufika”
“Poa, kila mmoja ajiweke tayari hatutakiwi kuwakosa hawa watu”
“Sawa mkuu”
Msichana huyo akawasha gari na kuianza safari ya kuelekea katika eneo hilo huku wote kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi. Kwa uwezo wa gari lao linalo kwenda kwa kasi kubwa sana, wakatumia muda mchache sana kuweza kufika eneo ilipo nyumba ya madam Mery, walipo hakikisha kwamba wahusika wapo kwenye nyumba hiyo, kwa haraka wawili wakaruka ukuta wa jumba hilo la kifahari, huku buduki zao wakiwa wamezifunga viwambo vya kuzuia sauti. Walio walio wakuta katika eneo hilo hawakuwa na bahati kabisa, kwani hawakujali kwamba wapo hapo kwa ajili ya kumlinda dokta Ranjiti au laa. Wakawaua walinzi wote wapatao nane walio zunguka jumba hili, kisha mmoja wao akafungua geti na gari hilo likaingia kwa ndani.
“Ni nani?”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akijikaza kunyanyuka kwenye sofa alilo kalia, kwa haraka Anna akakimbilia hadi sidishani na kuchungulia nje, akawaona wasichana wawili wakishuka kwenye gari hilo aina ya Rangerove huku wakiwa wameshika bunduki mikononi mwao.
“Shiitiiii”
Anna alizungumza huku akitazama tazama hapo sebleni, akaiona bunduki ya baba yake kwa haraka akaiwahi na kuichukua akiamini kwamba watu hao watakuwa wapo kinyume na wao.
“Jifiche hapo?”
Anna alizungumza huku akimuonyesha dokta Ranjiti sehemu ambayo anaweza kujificha, wasichana wawili walio weza kutangulia kuingia katika nyumba hiyo, waliweza kufahamu milango kadhaa ya kuingilia ndani kabisa ya jumba hilo, wakaingia kwa mwendo wa kunyata hadi sebleni na kumkuta Anna na baba yake macho yao yote wakiwa wameyaelekezea katika mlango mkubwa wa kuingilia humo ndani.
Kwa hatua za kunyata na za haraka, msichana mmoja akamuwahi Anna aliye shika bunduki hiyo, na kumuwekea bastola nyuma ya kichwa chake, na kumlazimu kuiweka chini bunduki yake hiyo.
“Munaweza kuingia”
Msicha huyo alizungumza kupitia kinasa sauti chake alicho kivaa sikioni mwake. Mlango huo ukafunguliwa na wasichana hao wakaingia ndani. Wakazitazama picha mbili walizo tumiwa kwenye simu kwamba hao wanao wachukua hivi sasa ni wahusika, mkuu wao alipo dhibitisha hilo, akatoa simu yake mfukoni na kumpigia msicha aliyopo makao makuu.
“Tumewapata”
“Ngoja nikuunganishe na mkuu wao”
“Sawa”
“Halooo”
Sauti ya John ilisikika baada ya kuunganishwa simu yake na msichana huyo.
“Tuna watu wako, dhibitisha kwa sauti kama ni wao?”
Msichana huyo alizungumza huku akimsogelea dokta Ranjiti, akamuwekea simu yake sikioni.
“Zungumza”
“Haloo”
“Ranjiti wewe mshenzi, unaniumiza kichwa pumbavu weweee”
John alizungumza kwa ukali sana.
“Mkuu….sa…sa..aaamahani”
“Pumbavu, ila hongera, yupo wapi Camila?”
“Sijui sijamchukua ila taarifa zinadai kwamba nimamchukua”
John akaka kimya kwa sekunde kadhaa.
“Mpe simu huyo binti”
Dokta Ranjiti kwa ishara ya macho akamuonyeshea binti huyo kwamba tayari amemaliza kuzungumza na John, msichana huyo akaiweka simu sikoni mwake.
“Kuna mtoto wa kike, nimekubaliana na bosi wako muweze kuniletea, na huyo fala anadai hajui alipo na mimi ninamuhitaji mtoto huyo”
“Umeeleweka”
Msichana huyo akakata simu, kwa ishara akawaonyeshea wezake na wote wakatoka nje huku wakiwa makini sana, kwa haraka wote wakaingia kwenye gari hilo, huku Anna na baba yake wakiwa wamewaweka siti za katikati, dereva huyo akalirudisha gari hilo kwa kasi, akaliweka sawa barabarani na kuondoka katika eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana huku wakiwa wameliacha geti la nyumba hiyo wazi.
***
Minyororo mikubwa sana ikaanza kushushwa chini ya bahari, wataalamu wa swala zima la uokoaji wakaanza kuizugusha minyororo hiyo kwenye ndege hiyo iliyo zama chini ya bahari. Zoezi hili kikawashukua zaidi ya lisaa moja kwani uzioto wa minyororo hiiyo iliwalazima kubeba zaidi ya watu kumi katuka kuuzungusha katika ndege hiyo.
“Ohoo Mungu amesikia maombi yetu”
Adrus alizungumza huku akimtazama Cookie usoni mwake.
“Kweli mpenzi wangu”
Adurs akaanza kupita katika daraja moja baada ya jengine huku akisaidiwa na Martha kuwasisitizia watu waweze kukaa kwenye siti na wajifunga mikanda. Kila aliye hai akatii ombi hilo la kukaa kwenye siti, kwani matumaini mapya ya kuwa hai yamerudi kwenye maisha yao. Martha na Adrus wakarudi kwenye siti zao na kukaa huku kila mmoja akijifunga mkanda wa siti yake.
“Mungu akinitoa salama humu ndani nilazima nikamuue Livna”
Jing alizungumza maneno yaliyo mstua sana Cookie pamoja na Adrus.
“Ukamuue Livna. Livna ndio nani?”
Adrus aliuliza huku akimtazama Jing usoni mwake.
“Unamfahamu Livna Livba?”
Cookie naye aliuliza huku akiwa amemkazia macho Jing
“Ndio, ni bosi wetu, nilipewa jukumua la kuwaua nyinyi wote wawili ila alipo nisaliti ilinibidi kughairi maamuzi yangu”
“Livna mpumbavu wewee, malay** lazima na mimi nikuangamize”
Cookie alizungumza kwa hasira sana baada ya kugundua ukweli huo.
“Ngojeni kwanza huyo Livna ni nani kwani kwa maana munamtaja taja, mimi siwaelewi?”
Cookie na Jing wakatazamana kisha Cookie akamjibu.
“Ni jasusi mmoja mbaya sana hapa duniani niliye weza wahi kumuona, anamiliki maelfu ya wasichana ambao wanapata mafunzo ya ujasusi, kazi yake ni kupokea oda kutoka kwa matajiri wanao hitaji kufanyiwa kazi za mojawapo ikiwa kama yako ya kukuondoka duniani, kisha hulipwa pesa nyingi sana”
“Mmmmmm”
“Usigune, tunatakiwa kuwa makini kwa asilimia kubwa sana, kwnai pasipo kufanya hivyo mimi, wewe na huyo mpenzi wako Cookie tutakwenda kuuwawa mmoja baada ya mwengine kwa maana wasichana wake si rahisi kuwafahamu na wapo karibia duniani nzima na akiwapa kazi tu basi wao huitekeleza pasipo huruma ya aina yoyote”
Maneno hayo yakaazidi kumshangaza Adrus na kujikuta akiwa na shahuku kubwa sana ya kuweza kumfahamu msichana huyo mwenye nguvu kubwa kiasihi hicho anaonekanaje.
***
Mlango wa chumba alicho lazwa Eddy ukafunguliwa akaingia mlinzi aliye agizwa na dokta Benjamini.
“Vipi?”
“Muheshimiwa madam amekataa kuja huko, ila nesi anadai kwa sasa hayupo sawa”
“Poa nimekuelewa, mkuu wako yupo wapi?”
“Labda niwasiliane naye”
“Muambie kwamba nina muhitaji sasa hivi”
“Sawa”
Mlinzi huyo akatoka nje na kuwasiliana na mkuu wake wa kikosi, ambaye hakumaliza hata dakika tano akafika katika chumba alipo makamu wa raisi Eddy Godwin.
“Mumefikia wapi katika kumpata Shamsa”
“Nimewasiliana na kijana aliye ongozana naye anadai kwa hivi sasa, Shamsa amameshikilia madama Mery, kwa ajili ya upelelezi zaidi ya kuhusu ni wapi alipo dokta Ranjiti”
“Madam Mery, anahusika vipi na kupotea kwa dokta Ranjiti na mwanaye?”
“Hatujafahamu mkuu, ila tunakupa ripoti muda wowote kuanzia hivi sasa, kwa kutumia signal ya kijana wangu, nimetuma timu iweze kuwafwata sehemu walipo”
“Hembu mpigie simu huyo kijana wako”
“Sawa mkuu”
Mzee huyo kwa haraka akatoa simu yake mfukoni na kuitafuta namba ya mlinzi anaye mlinda Shamsa, alipo hakikisha kwamba ameipata, kwa haraka akampigia simu.
“Ndio mkuu”
“Makamu wa raisi anahitaji kuzungumza na wewe”
“Sawa mkuu”
Mzee huyo akakabidhi Eddy simu hiyo.
“Wewe huyo binti yangu umesema amemshikilai nani?”
“Mama mmoja aliye mtaja kwa jina la madam Mery”
“Pumbavu upo naye hapo?”
“Ndio ila wapo nje ya gari amemshikia bastola mama huyo na anamuelekeza kuja naye huku kwenye gari lililpo”
“Ahaaa, amechanganyikiwa au? Hembu shuka umpatie simu”
Eddy alizungumza kwa jazba hadi dokta Benjamini akaacha kwanza kukihudumia kidonda cha Eddy.
“Shamsa baba yako anahitaji kuzungumza nawe”
“Muambie muda bado”
“Mkuu naamini umesikia”
“Hembu weka loud speaker hapo”
“Tayari mkuu”
***
“Wewe Shamsa umechanganyikiwa au?”
Sauti ya ukali ya Eddy ilisikika kutokae katika simu aliyo ishuka mlinzi huyo aliye jaribu kumpa simu ili azungumze na baba yake ila akakataa kufanya hivyo. Madam Mery akamtazam Shamsa anaye itazama simu hiyo.
“Shamsa”
“Eddy nini lakini, nimekuambia kwamba nipo ninamfwatilia mtu ambaye anafahamu ni wapi madam Mery alipo na wewe umekaa kunipigia kelele maana yake nini sasa?”
“Kwa nini umteke madam Mery”
“Yeye ndio muhusika anaye fahamu ni wapi dokta Ranjiti na Anna walipo”
“Yeye anafahamu?”
Eddy aliuliza kwa sauti ya upole sana.
“Ndio anafahamu, so acha nifanye kazi yangu sawa”
Shamsa alizungumza kwa ukali sana.
“Madam Mery yupo hapo?”
“Anakusikia”
“Madam”
“Beee”
“Ni kweli alicho kizungumza Shamsa?”
Madam Mery akashusha pumzi nyingi huku akimtazama Shamsa ambaye bado amenyooshea bastoka hiyo.
“Yaaa”
“Ohoo Mungu wangu, kwa nini sasa Mery umefanya hivi, huyujui huyo mtu amefanya maovu gani kwangu?”
“Eddy bila ya kukuvunjia heshimi mimi kusema kweli sifahamu kitu kinacho endelea”
“Hufahamu vipi ikiwa wewe ndio umawatorosha watu hao”
Eddy alizungumza kwa ukali kidogo.
“Mimi nilipokea amri ya kufanya hivyo na sikufanya kwa ajili ya kukusudia, ila nilifanya kwa ajili ya kumsaidia huyo aliye niomba?”
“Ni nani huyo aliye kuomba?”
Swali la Eddy Godwin likawafanya Madam Mery na Shamsa kutazamana kwani kumtaja muhusika ambaye ni Phidaya kutapekekea mgawanyiko mkubwa sana kwenye familia hiyo anayo itambua kwa kipindi cha miaka mingi sasa.
Shamsa akatingisha kichwa kumkanya madam Mery asizungumze kitu chochote.
“Mery nijibu ni nani huyo?”
“Samahani Eddy ni makubaliano ambayo, sinto weza kukuambia muhusika ila kiu cha kuwasaidia nitawapeleka kwenye katika nyumba yangu alipo dokta Ranjiti na mwanaye”
“Shiiitiiiii, Mery kumbuka mimi ni nani katika hiii nchi, nataka kujua ni nani ambaye amehusika na tukio la kumtorosha dokta Ranjiti, tazama mke wangu amepigwa risasi, tazama mwanangu Camila ametekwa kwa ajili ya huyo mpuuzi hembu niambie ni nani?”
Eddy Godwin alizungumza kwa hasira sana, jambo lililo mfanya madama Mery kukaa kimya huku akimtazama Shamsa. Shamsa akamsogelea mlinzi wake na kuichukua simu hiyo na kutoa mfumo wa loud speaker, kisha akaiweka simu hiyo sikioni.
“Eddy, nimekuambia nitalishuhulikia hili swala kwa hiyo usimpeleke mbio madam Mery”
“Mwanangu ametekwa?”
“Si mwanao pekee aliye tekwa, kumbuka hata mwanangu pia amatekwa. Junion wetu ametekwa pia”
Shamsa alizungumza kwa sauti ya chini huku akijitenga na watu alio simama nao kwani hawatambui ni kitu gani kinacho endelea katika familia hiyo.
“Eddy nitalishuhulikia hili swala mimi mwenyewe na watoto wako nitahakikisha kwamba wanarudi kwenye mikono yetu haraka iwezekanavyo umenielewa?”
“Nimekuelewa, kuna timu maalumu imetumwa hapo kuja kuwasaidia?”
“Sihitaji msaada wa kiserikali, warudishe nikihitaji nitakuambia. Kumbuka leo serikali imepoteza vijana wengi sana, na wote wameuwawa kikatili na ukumbuke kwamba vijana hao nao pia wana familia zao, wake zao. Tusizidi kupeleka misiba kwenye familia zao ikiwa tatizo ni la kufamili zaidi sawa Eddy”
“Sawa nimekuelewa, ila kama unamfahamu muhusika wa hili tukio ninakuomba uniambie”
“Kusema kweli ninamfahamu, ila sihitaji kumtaja kwa sasa, ninakuomba uchukua uangalizi mzuri kwa mama Phidaya, kwa maana maadui wapo wengi na hatujui ni muda gani na saa ngapi wanaweza kutuvamia sawa”
Shamsa alizungumza kiujasiri sana jambo lililo zalisha matumaini kwa Eddy Godwin ambaye anamfahamu binti huyo toka alipo kuwa mdogo na alimtoa katika mikono ya kundi la Al-Shabab.
“Hei Shamsa”
“Bee”
“Nakuomba uwe makini sana”
“Usijali mpenzi wangu, ninakupenda sana”
“Nami pia”
Shams akakata simu hiyo na kumrudishia mlinzi wake.
“Muambie kijana wako aje kuingia katika gari hili, mimi na wewe tutatumia hammer”
Shamsa alizungumza huku akimtazama madam Mery, ambaye pasipo kipingamizi akatii ombi hilo, kijana wake akapanda gari moja na mlinzi wake huku wao wakipanda katika gari hilo la kifahari na yeyey akiwa ndio dereva. Safari ikaanzataratibu huku madam Mery akiwa na jukumu la kuwaelekeza ni sehemu gani wanapaswa kuelekea.
“Kwa nini Phidaya ameamua kufanya hivi?”
Madam Mery aliuliza kwa sauti ya chini na iliyo jaa unyenyekevu, Shamsa akamtazama kwa muda kidogo kisha akamjibu.
“Ni mapenzi”
“Mapenzi, unataka kuniambia kwamba Phidaya na dokta Ranjiti wamerudiana tena kwenye mapenzi?”
“Ndio”
“Jamani, kwa nini sasa anafanya hivi au tayari akili yake imesha haribiwa na daktari huyo?”
“Ninahisi ametambua ukweli?”
“Ametambua ukweli!! Ukweli gani?”
Shamsa akajikoholesha kidogo na kuliweka koo lake sawa kwa kumeza fumba zito la mate.
“Amejua mimi na Eddy tunamtoto wa kiume”
Madam Mery macho yakamtoka, akabaki akiwa ameduwaa kwa kushangaa sana kwani hicho alicho kisikia kimestajabisha sana
***
Wasichana wa Livna wakapiga simu katika makao makuu ya kikosi chao na kuomba msaada wa kuweza kumtafuta Camila ni wapi alipo. Kazi ya kumtafuta Camila kwa kutumia Satelaiti haikuwa ngumu kwao kwani kikosi hicho kina wataalamu wa kutosha na wenye ujuzi wa kuweza kucheza na maswala ya mtandao.
“Tumempata, yupo maeneo ya Mbezi Luisi, Signal itawalekeza ni wapi munaweza kumpata mtoto huyo”
“Sawa shukrani?”
“Ila kuna angalizo hilo eneo lina walinzi zaidi ya ishirini na inaonyesha kwamba eneo hilo linalindwa sana, je mutahitaji msaada wa aina yoyote?”
“Hapana, tunaweza kulishushulikia hilo”
“Sawa kazi njema”
“Tunashukuru, ila hatujamsikia mkuu, kwani yupo wapi?”
“Mkuu leo hajisikii vizuri na majukumu yote amenipa mimi kuweza kuyashuhulikia”
“Sawa, na hawa watu wawili ingekuwa vizuri wakachukuliwa, ili nasi tuweze kulishuhulikia hilo swala itakapo timi saa mbili usiku”
“Sawa, tutatuma boi ije kuwachukua”
“Katika hilo swala mshirikishe mkuu, kwa maana unatambua sheria za hilo eneo na mtu mwenye jinsia ya kiume hapaswi kufika hapo”
“Sawa nimekuelewa, ngoja nimpigie sasa hivi”
“Sawa, niunganishe naye”
***
Livna akaitazama simu yake aliyo iweka pembeni ya mto wake, taratibu akaichukua na kutazama ni nani anaye mpigia na kukuta ni kijana wake. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake kiuvivu.
“Mkuu, Lizzy amempata dokta Ranjiti na mwanaye anahitaji kuzungumza nawe”
Livna baada ya kusikia maneno hayo kwa haraka akaka kitako kitandani huku akiwa amejawa na furaha kidogo kwani siku zote anamuaminia Lizzy huwa ni mtu ambaye akipewa jukumu hulitekeleza kama vile alivyo agizwa.
“Muunganishe naye”
“Lizzy”
“Ndio mkuu”
“Hongera sana kwa kazi ngumu uliyo ifanya”
“Nashukuru madam ila bado hatajamaliza kibarua, kwa maana mtoto mchanga anaye hitajika kuna sehemu yupo na inaonyesha amechukuliwa na mtu hatari sana”
“Ohooo gosh!! Sasa inakuwaje hapo?”
“Tunahitaji kuweza kuwakabidhisha dokta Ranjiti na mwanye, ili tukienda katika hiyo kazi tusiwe na mzigo wa kuutilia maanani zaidi ya mtoto huyo”
“Mupo eneo gani hivi sasa?”
“Tupo kwenye moja yam situ, siufahamu jina lake ila, kama Lidya anaweza kututafuta basi anaweza kutupa kiurahisi”
“Basi tulieni hapo hapo, ninatuma helicopter ambayo itawachukua hao na kuwapeleka katika kisiwa cha Madagasca”
“Sawa mkuu”
“Dakika kumi na tano helicopter hiyo itaweza kufika hapo, na je hali ya ulinzi ipo vipi huko Tanzania?”
“Msako kusema kweli ni mkali, roadblock ni nyingi sana magari yanakaguliwa, yaani hadi sisi kufika huku porini ni kwa neema za mwenyezi Mungu”
“Sawa Lizzy, ninawatumia timu ambayo inaweza kuwapa nguvu zaidi?”
“Hapana mkuu mimi na vijana wangu tunatosha katika kukamilisha hili zoezi ila tunacho kihitaji hivi sasa ni silaha za kutosha kwa maana hao tunao kwenda kupambana nao inaonyesha ni watu ambao wamejipanga sana”
“Sawa, kila kitu umepata, au kuna jengine mama yangu”
“Hakuna jengine”
“Sawa”
Livna akakata simu na kunyanyuka kitandani kwake, akatoka chumbani humo na moja kwa moja akaelekea katika chumba kinacho tumika kwa ajili ya kuendesha mfumo mzima wa mawasiliano ndani ya meli hiyo kubwa. Kwa haraka Lidya na wezake wakawatafuta Lizzy sehemu walipo, wakawapata. Livna akagiza helicopter kwenda kuwachukua madam dokta Ranjiti na wezake huku kukiwa na wasichan wengine ambao watazidi kuimarisha ulinzi katika tukio hilo. Huku wakiwa na sanduku kubwa lililo jaaa silaha za kila aina ambazo ni maalumu kwa Lizzy na wezake.
***
K2 akasimama kwenye sofa alilo kuwa amekaa, kwa haraka akamfwata kaka yeka anaye ingia ndani humo na kumkumbatia kwa furaha kubwa sana.
“Vipi?”
“Mpango umekwenda kama nilivyo upanga”
“Yupo wapi huyo mtoto”
“Yupo huku”
K2 alizungumza huku wakainza kupandisha kuelekea gorofani, wakaingia katika chumba alicho mlaza Camila kwenye kitanda maalumu, vinavyo tumiwa wa watoto wadogo.
“Shiiiii, amelala usipige kelele”
K2 alizungumza kwa suauti ya upole sana huku tabasamu likiendelea kuchanua kwenye uso wake.
“Waoooo, she is very beautiful”
“Yaaa, yaani haoa nina imani lizima Eddy Godwin atachanganyikiwa”
“Kweli huyu mtoto anakwenda kutupa nguvu mdogo wangu, nilazima niwe raisi, nilazima niiongoze hii nchi na lazima niionyooshe, nchi imekuwa ya kipuuzi sana”
“Kaka yangu mimi nitakusupport kwa lolote utakalo niomba niweze kulifanya. Yote hiyo ni kuhakikisha kwamba familia yetu inakuwa na heshima, hata wazazi wetu kule kuzimu walipo lala watakuwa wanafurahia juhudi ambazo tutazifanya”
“Sawa sawa, kwa hili mdogo wangu leo twende tukasherekee, tunyweee tule, naamini kwamba kesho tutakuwa tuna tunaamkia akili nyengine na tutajua ni kitu gani ambacho tunapaswa kufanya.”
K2 na kaka yeka wakatoka katika chumba hicho, wakarudi sebleni, K2 akachukua mzinga mkubwa wa pombe ya kali aina ya wicky. Wakaanza kunywa huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha sana moyoni mwake.
“K2, hivi utaolewa lini?”
“Bado kaka, nitaolewa baada ya kila kitu ambacho tunakihitaji kikamilike”
“Olewa bwana ninahitaji kuona wajomba, kaka yako kama unavyo jua sina uwezo wa kuweza kupata mtoto, so ikitoke kwamba mimi na wewe tumekufa hatutakuwa na kumbukumbu yoyote ambayo tumeiacha hapa duniani”
Maeno hayo yakamfanya K2 kutulai kwa muda huku akitafakari.
“Sawa kaka nimekuelwa, nitajitahidi kumtafuta mwanaume ambaye anaweza kunizalisha, ila nitakacho kihitaji mwanaume huyo asiwe ni mume wa kunipangia maisha yangu, nataka kufanya kile ninacho kihitaji mimi mwenyewe”
“Mmmm sasa mwanaume wa aina hiyo, sidhani kama yupo”
“Wapo na atapatikana na asipo kubaliana nami si tunaachana naye na mwanangu si ninaishi naye mimi mwenyewe”
“Sawa maamuzi ni yako wewe mwenyewe, aisse humu ndani kwako hakuna hata nyama?”
“Ipo kwenye friji”
“Twende tukachome bwana, kunywa mapombe makali kama haya, mwisho wa siku unaweza kujikuta utumbo ukijikunja kunja na mtu ukafa”
“Haaaahhaa, sawa kaka yangu”
K2 na kaka yake wakaondoka eneo la sebleni na kuingia jikoni na kuanza zoezi hilo la kuendelea kuburudisha nafsi zao kwa hatua kubwa ambayo wamepiga kwneye maisha yako kwani uchu mkubwa kwao ni kupata madaraka makubwa katika nchi ya Tanzania.
***
Taratibu Sa Yoo akaanza kushuka kwenye ngazi za ndege aliyo kuja nayo kutoka nchini Uingereza, hali ya hewa ya joto nchini Tanzania, haimshangazi kabisa kwani amesha wahi kuishi hapa kwa muda mrefu kiasi. Akatazama mazingira ya uwanja huu wa ndege na ulinzi mkali umeongezeka.
“Ninatakiwa kukukabidhi katika ubalozi wa Uingereza”
Mlinzi maalumu wa kike aliye ongozana na Sa Yoo alizungumza huku akimtazama Sa Yoo usoni mwake.
“Sawa hakuna tatizo”
“Kuna watu wamekuja kutupokea hapo nje”
Wakaongozana na mlinzi huyo hadi nje ya uwanja, wakakuta gari mbili aina ya Jeep zikiwasubiria, wakaingia kwneye gari moja wapo na kuondoka katika eneo hili. Sa Yoo muda wote macho yake ameyeelekeza katika nje, akitazama jinsi mandhari ya jiji la Dar es Salaam.
“Ninaweza kupata simu nikawasiliana na rafiki yangu?”
“Hapana hadi tukukabidhi, katika ubalozi basi kiongozi yoyote atakaye kuwa ameagizwa na makamu wa raisi basi atakuja kukuchukua kwenye ubalozi.”
“Sawa ila kwa nini siwezi kuzungumza na rafiki yangu kwa maana ninamjulisha tu kwamba nimesha fika nchini Tanzania”
“Rafiki yako ni nani?”
“Shamsa, mtoto wa makamu wa raisi”
Mlinzi wa kiume aliye kaa siti ya mbele akamtazama Sa Yoo kwa sekunde kadhaa kisha akaichomoa simu yake kwneye mfuko wa shati lake na kumkabidhi.
“Asante”
Sa Yoo alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake kwani kuisikia sauti ya Shamsa, itakuwa ni faraja kubwa sana kwake. Akaingiza namba ya Shamsa, akaipiga ila kwa bahati mbaya namba hiyo haipatikani hewani. Akaka kwa muda huku akiifikiria namba ya Phidaya, alipo hakikisha kwamba ameikumbuka, akaiandika na kuipiga. Simu ya Phidaya ikaanza kuita kwa muda kisha ikapokelewa.
***
Mlio wa simu ya Phidaya ukawafanya madam Mery na Shamsa kutazamana machoni. Shamsa akaitoa simu hiyo mfukoni mwake akakutana na namba mpya kabisa. Akataka kuikata ila ila akapata ujasiri wa kuipokea kwani anatambua fika kwamba ni Phidaya ndio anaye endelea kumtafuta.
“Nini?”
Shamsa alizungumza kwa mkato.
“Shamsa”
Sauti ya Sa Yoo ikausisimua mwili wa Shamsa
“Sa Yoo”
“Habari yako”
“Salama, umepiga na namba ya Tanzania ina maana umesha fika nchini Tanzania?”
Shamsa aliuliza kwa furaha sana, kwani anampenda sana rafiki yake huyo.
“Ndio, ninaelekea ubalozi wa Uingereza ili kama ni kuchukuliwa basi niweze kuchukuliwa pale”
“Ohoo karibu sana rafiki yangu, nimekumiss sana kukuona”
“Hata mimi, nimejaribu kukupigia kwenye simu yako nikaona haipatikani?”
“Imezima chaji rafiki yangu”
“Ohoo sawa, upo wapi?”
“Kuna sehemu ninaekea, ngoja nimpigie baba tatume watu waje kukuchukua hapo kwneye ubalozi”
“Sawa”
“Badae”
Shamsa akakata simu mara baada ya kuelekezwa kukunja kona inayo elekea katika jumba la madam Mery. Wakafika getini katika jumba hilo jambo lililo wafanya wote kushangaa baada ya kukuta geti la nyumba hiyo ikiwa wazi kabisa.
“Kuna tatizo hapa”
Madam Mery alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Shamsa akasimamisha gari hilo mita chache kutoka lilipo geti, akafungua mlango na kushuka, mlinzi wake na kijana wa madama Mery nao wakaoshuka kwenye gari lao huku nao wakionekana kushangaa mazingira ya ndani hapo. Shamsa akatoa bastola yake na kuanza kuingia ndani taratibu huku mlinzi wake akimfwata kwa nyuma, maiti ya walinzi wawili walio wakuta pembezoni mwa geti, ikaanza kuwachanganya na kuwafanya wazidi kuwa makini sana, madam Mery na kijana wake nao wakaingia ndani,w alipo ziona maiti hizo mbili, wakatambua kabisa lazima dokta Ranjiti na mwanaye watakuwa wametoroka jambo litakalo wafanya wao wawili waingie katika mtafaruku mkubwa sana na serikali kwani wamehusika kwa asilimia kubwa sana katika kuwatorosha watu hao ambao kwa sasa ndio wameeanza kuamini kwamba ni magaidi, kwani hakuna mlinzi hata mmoja ambaye wamemkuta akiwa hai.
“Madam tutoroke”
Kijana wa madam Mery alizungumza huku wakiwatazama Shamsa na mlinzi wake wakiingia ndani ya jumba hilo kubwa.
“Hapana”
“Madam hii ni kesi ambayo hatutaweza kuiepuka kwa maana hapa inao yesha kwamba watuhumiwa wamekimbia”
“Nimekuambia kwamba hakuna kukimbia, tukikimbia tutaongeza tatizo na kuanzwa kusakwa jambo ambalo sihitaji kulifanya sawa”
Madam Mery alizungumza kwa ukali ulimfanya kijana wake huyo hukaa kimya na kukubaliana na amri aliyo zungumza bosi wake huyo.
Shamsa na mlinzi wakendelea kukagua nyumba hiyo kwa umakini sana ila ndio hivyo kila chumba walicho kiingia hawakuweza kuona chochote, wakarudi sebleni na kuwakuta madama Mery na kijana wake wakiwa wanawatazama. Shamsa akaitazama seble hiyo kwa umakini sana na kugundua kwamba katika seble hiyo kwenye moja ya kona kwa juu kuna kamera ya ulinzi.
“Hiyo kamera hapo si inafanya kazi?”
Shamsa aliuliza huku akiinyooshea mkono kamera hiyo.
“Ndio”
“Naomba niweze kupata rekodi yake”
“Ipo katika chumba cha chini”
“Twende”
Shamsa alizungumza huku akiwa amemnyooshea bastola kijana wa madam Mery. Wakaondoka eneo hilo la sebleni huku kwa ishara Shamsa akimuamrisha mlinzi wake kuweza kumlinda madam Mery na asitoroke. Wakaingia kwenye chumba cha siri kilichopo chini ya ardhi.
“Hiyo computure ndio inarekodi matukio yote”
“Tafuta rekodi za muda ulipo pita”
Kijana huyo akaka kwenye kiti ambacho kipo katika eneo hilo, akaanza kurudisha nyuma matukio ya kile ambacho kilitoke katika nyumba hiyo. Wakaanza kushuhudia matukio yote ambayo yametoke katika nyumba hiyo. Wakaoni ni jinsi gani walinzi hao walivyo kuwa wakiuwawa, kisha wakaona jinsi dokta Ranjiti na mwanye walivyo ingizwa kwenye gari aina ya Range rover na kuondoka katika eneo hilo.
“Unawafahamu hawa mabinti?”
“Hapana”
Shamsa akashusha pumzi nyingi sana kwa maana wasichana hawa wanaonekana ni watu hatari sana ambao kusema kweli wanaujuzi wa hali ya juu.
“Unaweza kutafuta hilo gari na kugundua kwa sasa lipo wapi?”
“Nalitafutaje?”
Shamsa akamtazama jamaa huyo kisha akaachia msunyo mkali. Akatoa simu ya Phidaya, akaitazama kwa muda huku akitafakari ni nini cha kufanya. Kwa haraka akakumbuka kwamba Sa Yoo ni mjuzi katika maswala ya telnolojoa. Kwa haraka akaitafuta namba ya simu aliyo itumia Sa Yoo katika kumpigia dakika kadhaa zizlizo pita.
Namba hiyo ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa na mwanaume.
“Ndio”
“Ninahitaji kuzungumza na Sa Yoo”
“Nani wewe?”
“Shamsa, muambie mimi ndio ninahitaji kuzungumza naye”
“Sawa”
“Kuna simu yako”
Shamsa aliisikia sati hiyo ya kiume akizungunza na Sa Yoo.
“Shamsa”
“Jojo ninahitaji msaada wako”
“Msaada gani?”
“Umefika kwenye ubalozi wa Uingereza?”
“Hapana, ila ndio tunakaribia kufika”
“Kuna msaada wa gari moja ninahitaji uweze kulitafuta kupitia satelaiti unaweza kunisaidia?”
“Hemnbu ngoja niombe laptop kama wanayo”
‘Samahani kuna mtu mwenye laptop?’
“Hapana”
Sa Yoo akaka kimya huku akifiriia ni kitu gani ambacho anaweza kukifanya kwa muda huuu
“Kaa hewani ngoja nijaribu kutumia hii simu”
“Sawa”
***
Sa Yoo hakukata simu zaidi ya kuanza kuingia katika mfuno anao ufahamu yeye mwenyewe kwamba unaweza kumfuta mtu yoyote pale alipo.
“Shamsa nitajie namba ya hilo gari”
Shamsa akamtajia Sa Yoo namba ya usajili wa namba hiyo, ila cha kushanganza kwamba namba hiyo haipo na haijasajiliwa kwa gari la aina yoyote.
“Namba inakataa kupatikana?”
“Huembu angalia vizuri Sa Yoo”
“Kweli hii namba haipo na inaonyesha kwamba wameibuni tu”
Walinzi hawa wa ubalozi wa Uingereza wakabaki wakimtazama Sa Yoo.
“Unatafuta nini?”
Mlinzi mmoja alizungumza.
“Kuna gari ambayo inatafutwa na rafiki yangu”
“Kwa kupitia simu huwezi kulipata. Limeibiwa au kuna nini kimetokea?”
“Eti Shamsa limeibiwa?”
Sa Yoo alizungumza huku akiweka loudspeaker
“Hapana ila ni gari lililo tumiwa na mgairi ambao wamemchgukua dokta Ranjiti na mwanaye walio kuwa wakishikiliwa na serikali ya Tanzania”
Walinzi walipo sikia sentensi hiyo ya Shamsa wakaonekana kustuka, hata Sa Yoo mwenyewe wasiwasi mwingi ukamjaa moyoni mwake.
“Magaidi!!”
Mlinzi mmoja aliuliza kwa mshangao.
“Ndio”
“Unaweza kuitaja namba ya hilo gari”
Mlinzi mmoja alizungumz ahuku akiitoa laptop yake kwenye begi la mgongoni lililopo ndani ya gari hilo. Akafunua kwa haraka na Sa Yoo akamtajia namba hiyo. Hazikupita hata dakika mbili wakafanikiwa kujua ni wapi gari hilo lipo.
“Shamsa simu yako na uwezo wa kupokea signal ya mahali lilipo gari hilo?”
“Yaa tume kwenye simu hii”
“Sawa tunakutumia sasa hivi”
“Munamtumia je amewasiliana na serikali yake, kwa maana kama anasema kwamba hilo gari ni la magaidi ujue si watu wa kawaida”
“Ninyi nitumieni mimi nitajua nini cha kufanya”
“Shamsa usije ukaingia kwenye matatizo rafiki yangu”
“Siwezi kuingia nyinyi nipatieni”
Walinzi hawa wakatazamana na Sa Yoo ambaye akamruhusu mlinzi huyo kwa ishara ya kutingisha kichwa. Mlinzi huyo kwa haraka akamtumia Shamsa signala ambayo inaweza kuwaonyesha magaidi hao ni eneo gani ambalo wapo.
“Nashukuru”
Shamsa akajibu na kukata simu.
***
Helicopter ikatua katika eneo ambalo Lizzy na wezake wapo , Lizzy kwa haraka akeleekea katika gari alipo dokta Ranjiti na Anna. Kwa haraka akafungua mlango huku wezake wakiendelea kuimarisha ulinzi wa eneo hilo.
“Munaweza kushuka”
Lizzy alizungumza huku akimtazama dokta Ranjiti, kwa haraka dokta Ranjiti na Anna wakashuka kwenye gari hilo. Kwa mwendo wa haraka wakatembea hadi ilipo helicopter hiyo. Wakasalimiana na wezao walio waletea silaha pamoja na kuwachukua dokta Ranjiti na Anna.
“Binti ninakushukuru sana”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya juu huku akimpa mkono Lizzy.
“Sawa ingia na uondoke”
“Kazi njema”
“Mzee acha maneno mengi ingia uondoke”
Dokta Ranjiti akaingia kwenye helicopter hiyo huku Anna akimfwata kwa nyuma. Lizzy akaufunga mlango wa helicopter hiyo na taratibu ikaanza kupaa hewani na kutoweka kwenye uwepo wa macho yao. Kwa haraka Lizzy na wezake wakaurudi kwenye gari lao huku wakiwa wamebeba sanduku lenye silaha. Wakaingia ndani ya gari lao na kuanza kuondoka.
“Hei kuna tatizo”
Msichana mmoja alizungumza huku akitazama simu aina ya tablate aliyo ishika.
“Tatizo gani?”
“Kuna walio tu track signal yetu”
“Shiti ni kina nani hao?”
Msihana hiyo akaanza kutafuta ni nani muhusika, baada ya dakika kadhaa akafanikiwa kujua ni kina nani.
“Anaye tutafuta anaitwa Leonard Rooney, ni agent wa Uingereza na anafanyaka kazi katika ubalozi wa Uingereza haapa nchini Tanzania”
“Block asituone”
“Sawa mkuu”
Msichana huyo kwa haraka akaanza kuifanya kazi hiyo aliyo elezwa na mkuu wake ambaye ni Lizzy.
“Tayari mkuu”
“Kazi nzuri”
Lizzy alizungumza huku akiongeza mwendo kuelekea eneo la watu ambao wamamteka mtoto Camila ambaye ndoo kazi ya pekee ambayo wameibakisha.
***
Eddy kila alivyo jaribu kufikiria ni jinsi gani madam Mery amehusika katika swala zima la kumtorosha dokta Ranjiti na Anna hakuweza kupata jibu kabimili kabisa kwa maana madam Mery ni mtu ambaye amefahamiana naey kwa kipindi kirefu ila kama kuna baadhi ya mambo mabaya hapo kipindi cha nyuma walisha wahi kufanyijana ila inakuwaje kwa kipindi hichi.
Edddy akajaribu kuendelea kukumbuka matukio kadhaa ambayo madam Mery alijaribu kumfanyia na moja wapo tukio la kutaka kumkata kata viongo vyake kipindi alipo wateka yeye na Phiadya ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni mjamzito wa mimba ya Junio ambaye amesha fariki dunia.
“Haiwezekani”
Eddy alijikuta akizungumza peke yake hadi dokta Benjamini akabaki akiwa amekodolea macho.
“Nitaftie namba ya madam Mery”
“Ndio nani mkuu?”
“Ahaa…hembu niitie huyo mkuu wa hicho kikosi”
“Sawa”
Dokta Benjamini akatoka ndani humo, akamuita mzee hiyo.
“Ndio muheshimiwa makamu wa raisi”
“Hembu nitafutie namba ya madam Mery”
“Ahaa samaahni mkuu madam Mery ndio nani?”
“Hembu moigie kijana wako”
“Sawa”
Mkuu akapiga kijana wake simu, ambayo ikaanza kuita baada ya sekunde kadha akaipokea.
***
Ukimya uliopo hapo sebleni kati ya madam Mery na mlinzi wa Shamsa ukaatishwa na mlio wa simu ya mlinzi huyo, kwa haraka akaitoa mfukoni mwake na kuipokea.
“Ndio mkuu”
“Makamu wa raisi anahitaji kuzungumza na wewe”
“Sawa mkuu”
“Kijana upo na Shamsa hapo?”
“Hapana mkuu”
“Umemuacha wapi?”
“Yupo katika chumba cha siri kilichopo katika jumba la madam Mery anatazama rekodi ya cctv camera zilizopo katika eneo hili kwa maana kuna tukio la mauaji limetike akatika enei hili”
“Tukio la mauji? Ya kina nani hayo?”
Ni mauaji ya walinzi ambao walikuwa wakilinda hii nyumba na kwabahati mbaya dokta Ranjiti na mwanaye Anna hawapo katika eneo hili”
Maelezo ya kijana huyo yakamfanya Eddy kupandwa na hasira sana.
“Upo na madam Mery hapo?”
“Eddy alizungumza kwa sauti uliyo jaa mikwaruzo ambayo inaonyesha dhairi kwamba amekasirishwa na ripoti hoyo.
“Ndio nipo naye”
“Mpatie simu”
Mlinzi huyo akamkabidhi madam Mery simu.
“Halooo”
“Mery nisikilize, mimi ninaimani unanifahamu vizuri sana, sio mgeni kwako na ninaweza kukufanyia kitu chochote kibaya na mahusiano yetu mema yakapotea hivi hivi ukiwa unajiona sawa”
Eddy alizungumza kwa ukali hadi madam Mery akaanza kujawa na wasiwasi mwingi sana.
“Niambie ni nani ambaye yupo nyuma ya hili tuko na aliye kukabidhi oda ya kumtorosha Ranjiti na Anna?”
“Eddy unaju….”
“Unajua nini, au unataka sasa hivi nikuripoti kwa vijana wangu wakutangaze kama most wanted eheeee? Sema nani ni muhiusika”
Kauli hiyo ya Eddy Godwin ikazidi kumuongopesha madam Mery, akavuta taswira ya jinsi Eddy anavyo kasirika akatambua dhairi kwamba hali kwake imesha anza kuharibika.
“SEMA NANI MUHUSIKAAAAAAAAA”
Eddy alifoka kiasi kwamba madam Mery akahisi haya ndogo ikiaza kumwagika.
“Ni….ni……ni……”
“Nini nini nini NANI”
“Ni PHIDAY MKUU”
Kaluli hiyo ikamstua mlinzi pamoja na Shamsa ambaye ndo kwanza amefika hapo sebleni na kumkuta madam Meryakiwa katika hali ya woga huku machozi yakimwagika usoni mwake.
Shamsa akamtazama Madam Mery aliye ishikilia simu mkono wake wa kushoto, taratibu akaanza kutembea hadi alipo simama madam Mery. Shamsa akaichukua simu aliyo ishika madam Mery na kukuta bado ipo hewani, akaiweka sikoni mwake na kusikia ukimya, akausikilizia ukimywa huo kwa sekunde kadhaa, kisha akakata simu hiyo.
“Ni nani?”
Shamsa alimuuliza madam Mery ambaye kwa hali aliyo nayo akashindwa kumjibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kububujikwa na mchozi, Shamsa akamgeukia mlinzi wake na kumtazama.
“Ni muheshimiwa”
“Eddy”
“Ndio”
Shamsa akaweka kiganja cha mkono wake wa kushoto kwenye paji lake la uso huku akijaribu cha kufikiria ni kitu gani ambacho Eddy atakifanya.
“Kwa nini sasa umtaje Phidaya?”
Shamsa alimuuliza madam Mery kwa sauti ya chini.
“Ningefanyaje wakati Eddy alitaka kunifunga eheee?”
Madam Merry alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi. Shamsa akaka kimya kwa muda akaitazama simu yake na kuona signal ya gari walilio tumia majambazi hao, ikisogea.
“Hei ninempata signal ya majambazi ambao wamefanya tukio hili, twende sasa hivi”
Shamsa alimuambia mlinzi wake huyo.
“Inabidi kuwasiliana na kiongozi wangu, tunatakiwa kupata msaada”
“Hili ni swala la kifamilia”
“Hata kama ni swala la kifamilia ila kumbuka hao walio kufa sio wana familio wako ni walinzi walio ajiriwa kama mimi kwa hiyo inatupasa kuwa makini katika hilo umenielewa Shamsa?”
Mlinzi huyo alizungumza kwa msisitizo, ulio mfanya Shamsa kukubaliana na wazo la mlinzi huyo. Shamaka akiwa katika hatua za kutembea kumfwata mllinzi huyo sehemu alipo simama ili amkabidhi simu yake, simu ya Phidaya anayo onyesha signal ya eneo walipo magaidi hao ikapotea jambo lililo mfanya mapigo ya moyo yaanze kumuenda mbio
“Nini?”
Mlinzi wa Shamsa aliuliza baada ya kugundua hali ya Shamsa imebadilika.
“Signal imepotea”
“Hembu”
Shasma akamkamkabidhi mlinzi wake simu ya Phidaya na yeye akashuhudia alicho elezwa na Shamsa.
***
Eddy mara baadaya kutajiwa kwamba Phidaya ndio amehusika na swala zima la kumtorosha dokta Ranjiti na Anna, hasira yote ikayayuka kama barafu lililo wekwa juani. Hata hamu ya kuzungumza ikamuishia kabisa na kuishusha simu hiyo kutoka sikioni mwake na kuiweka pembeni yake. Mkuu wa kitengo cha ulinzi pamoja na dokta Benjamini wote wakakabaki kimya wakimsubiria Eddy aweze kuwaambia kwamba ni nani muhusika ili wamshuhulikie mara moja.
“Mkuu”
Dokta Benjamini aliita kwa sauti ya upole huku akimtazama Eddy usoni mwake.
“Kuna jambo baya limejitokea?”
Eddy hakujibu chochote zaidi ya kuinyanyua simu hiyo na kumkabidhi mzee huyo. Eddy akajaribu kuapanga na kupangua mawazo yake juu ya mke wake Phidaya jinsi gani amehusika na tukio hilo bado akili yake haikuweza kukubaliana na maneno ya madam Mery.
“Nipelekeni kwa mke wangu”
“Ahaa…”
“Nimesema nipelekeni katika chumba cha mke wangu”
“Sawa muheshimiwa”
Kwa haraka mzee huyo akatoka chumbani humo, baada ya dakika kama tatu akarudi na kiti cha magurudumu, kwa kusaidiana na dokta Benjamini wakammlisha katika kiti hicho.
“Nichome sindano ya kupunguza maumivu”
“Muheshimiwa kuna dawa amba…..”
“Nimekuambia nichome sindano ya kupunguza maumivu kwa muda mfupi?”
Eddy alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama dokta Benjamini kwa macho makali sana. Dokta Benjamini kwa haraka akachukua kichupa chenye dawa ya kupunguza maumivu, akachukua na sindano, akavuta dawa hiyo kwa kiasi cha kustosha, kisha akaushika mkono wa kushoto wa Eddy na kumchoma sindano hiyo na taratibu akaanza kusukuma dawa ndani. Alipo maliza akmpatia pamba ndogo yenye dawa na akaibandika katika sehemu hiyo ambayo ameichoma sindano.
“Twende”
Eddy alimuambia mzee huyo huku akiwa ameigandamiza pamba hiyo kwenye kidole chake. Wakatoka katika chumba hichi na walinzi wengine wakatangulia mbele huku wangine wakiwafwata kwa nyuma. Wakafika katika chumba alicho lazwa Phidaya, mzee huyo akamuingiza ndani na wakamkuta Phidaya akiwa na manesi wawili wanao jaribu kumfariji.
“Tupisheni”
Eddy alizungumza huku wakitazamana na Phidaya, manesi hao pamoja na mlinzi huyo wakatoka chumbani humo na kuwaacha wawili hao.
“Ni kweli?”
Eddy aliuliza swala la kimtego.
“Kweli nini?”
“Kwamba umehusika na kutoroka kwa dokta Ranjiti na Anna?”
“Eddy unawazimu”
Phidaya alizungumza kwa hasira sana huku machozi yakimwagika usoni mwake. Macho yake yamekuwa mekundu kiasi hata cha kumtisha Eddy, midomo yake inatetemeka kiasi cha kuyafanya meno yake kugongana gongana hadi mlio huo ukasikika vizuri masikioni mwa Eddy. Eddy taratibu akashusha pumzi nyingi huku akijaribu kufikiria kitu kingine cha kumuambia Phidaya.
“Nimepigwa risasi na yule mtoto wa yule mbwa, mwanangu ametekwa alafu unakuja kuniambia upuuzi wa aina hiyo. Wewe ni baba wa aina gani, baba gani usiye jua kulinda familia yako, ni baba gani unaye endekeza umalaya wa kipuuzi hadi mtoto anatekwa eheheeeee”
Phidaya alifoka hadi sauti yake ikasikika nje ya chumba hicho. Walinzi waliopo katika eneo hilo kwa ishara mkuu wao akawaomba wasimame mita kadhaa kutoka eneo la mlango ili kuto sikia mazungumzo hayo. Eddy akazidi kupooza ujasiri wake wote ukatoweka mbele ya mke wake.
“Mimi nitakuwa ni mwanamke wa aina gani, ninabeba mimba na kulea kidogo wanawangu wnaakufa. Camila sina naye hata miaka miwili, ila kwa upumbavu wako na umalaya wako. Tanzama sasa mwanangu amepoteaa, taama sasa mwanangu ameondoka nitampata wapi eheeeee?????”
Phidaya akaendelea kuzungumza kwa ukali huku akiwa amekaa kwenye kitako kwenye kitanda hicho.
“Phida…..”
Eddy alijaribu kuzungumza huku akiupeleka mkono wake wa kulia ili amshike Phidaya hata paja lake, ila kibao alicho pigwa kwenye mkono huo, ukamfanya Eddy kuliahirisha zoezi hilo haraka sana.
“Usidhubutu siku hata moja kurudia kunishika wala kuliita jina langu, kama Camila wangu hujamrudisha mikononi mwangu, nimekuvumilia wewe na mpuuzi mwenzako Shamsa na ninajua uchafu wenu wote mulio ufanya jana usiku, sasa hiii ndio adhabu ambayo Mungu anakuumbua mpuuzi wewe”
Phidaya aliendelea kuwa mkali kiasi cha kuzidi kumchangaya Eddy kwani tayari emegusha gundua kwamba mke wake huyo tayari emegundua mapenzi yake ya siri na Shamsa.
Eddy machozi yakaanza kumwagika usoni mwake, taratibu akaupeleka mkono wake hadi kwenye mkono wa kulia wa Phidaya, akaanza kupiga mkono huo wa Eddy, ili autoe ila Eddy hakuhitaji kuutoa mkono wake huko zaidi ya kuendelea kumshikilia mke wake huyo huku akimtazama usoni mwake na wote machozi yakiwamwagika. Phidaya alipo ona Eddy amekuwa mbishi katika swala hilo kwa haraka akaushika mkono wa Eddy na kuanza kuung’ta kwa nguvu ili maradi amuachie.
***
Uokoaji wa ndege iliyo zama ndani ya bahari ukafanikiwa kwa asilimia mia moja, abiria walio hai wakaanza kutokewa ndani ya ndege hiyo na kuingizwa katika meli maalumu iliyo andaliwa kuwapokea watu hao na ndani ya meli hiyo kuna madaktari na wauguzi wa kutosha.
Adrus hakuhitaji kukaa mbali na Cookie pamoja na Jing kwani anaamini kupitia wao kuna kazi kubwa ambayo wanaweza kusaidiana kuifanya ili mradi kuhakikisha kwamba wanamuangamiza msichana anaye itwa Livna ambaye ndio amepelekea matatizo hayo yote ya kuanguka kwa ndege hiyo.
“Habari bwana Adrus Maldin”
Mzee mmoja aliye valia mavazi ya kijeshi ya nchi ya Marekani alizungumza huku akimpa mkono Adrus’
“Salama”
“Tuzungumze”
Mzee huyo baada ya kuzungumza maneno hayo wakasogea pembeni na kuwaacha Cookie na Jing wakiendelea kuhufanyiwa vipimo vya miili yao.
“Tunamshukuru Mungu kwamba upo salama, na shukrani kwa jitihaza zako za kuwasaidia hao maelfu ya watu”
“Ninashukuru”
“Kuna helicopter maalumu ipo tayari kwa kukuchukua na kukupeleka nchini Marekani, unasubiriwa ili uendele na utaratibu wa kama nchi zetu mbili zilivyo ingia makubaliano.”
Adrus akashusha pumzi nyingi sana kwani moyo wake na akili yake tayari vilisha sahau kabisa juu ya kazi ambayo Wamarekani wamepanga kumchukua.
“Ninaomba muda wa kulifikiria hilo swala kwa maana nilimtoka kuokoka katika kifo, nahitaji muda wa kuwa sawa kisaikolojia, sihitaji kukurupuka katika hilo”
“Sawa, ila muda huo wa kujifikria itakuwa ni vizuri sana kwama sote tukielekea muda huu Marekani”
“Mzee wangu ninakuomba unipe muda kwanza. Naomba dakika kumi”
“Sawa ninakusubiria”
Adrus akamtazama mzee huyu kwa sekunde kadhaa kisha, akarudi sehemu alipo waacha Cookie na Jing.
“Vipi baby”
“Nina habari mbaya”
“Habari gani tena?”
“Yule mzee pale ametumwa na Wamarekani, yaani ndani ya dakika tisa kuanzia hivi sasa ninatakiwa kuelekea nchini Marekani kuendelea na majukumu ambayo ndio yamenitoa nchini Tanzania na kunipeleka huko”
“Mmmmm, umekubaliana naye?”
Jing aliuliza huku akimtazama kwa siri mzee hiyo, kitu alicho weza kukigundua Jing ni wingi wa wanajeshi ambao macho yao yote yapo kwa Adrus.
“Sihitaji kuifanya hiyo kazi kwa sasa, nahiyaji kufanya mambo yangu binafsi”
“Kuna wanajeshi zaidi ya kumi na tano wanakuangalia wewe pasipo wewe mwenyewe kujua”
Adrus akatka kugeuka nyuma kutazama hao wanajeshi, ila Jing akamuwahi kumshika mkono.
“Usigeuka wala kutazama pembeni kwa maana watajua kwamba tunawazungumzia wao”
“Sawa”
“Baby kama moyo wako haujaridhika, inabidi uhakikishe tunatoroka katika eneo hili”
“Mlinzi ni mkali sana.”
Adrus alizungumza huku akiwatazama wanajeshi wengine walipo mbele yake.
“Ngoja uone nitakacho kifanya”
Jing alizungumza na kuwafanya Adrus na Cookie wabaki wakimtazama, wakisubiria kuona ni kitu gani ambacho Jing atakifanya.
***
“Kwa nini umekuwa hivi?”
Mlinzi wa Shamsa aliuliza kwa mshangao.
“Hata mimi kusema kweli sitambui kwa nini imekuwa hivi”
“Kwa mara ya kwanza uliwapata pata vipi?”
“Kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Sa Yoo ndio amenitumia hii Link”
“Hembu mpigie”
Shamsa akaichukua simu hiyo ya Phidyaa na kuitafuta namba ya mwanaume ambaye yupo karibu na Sa Yoo.
“Ndio”
“Sa Yoo yupo wapi?”
“Ahaa mimi nimesha toka ofisini na nipo njiani ninaelekea nyumbani.”
“Ohoo samahani kaka yangu kwa kukusumbua, unaweza kunisaidia kupata ile signal ya lile gari kwa maana huku kwangu imepotea”
“Imepotea kivipi?”
“Haipo kabisa, sioni kwenye simu yangu”
“Hembu ngoja usikate simu”
Shamsa akaanza kuzunguka zunguka humu sebleni huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana kwani kumpoteza dokta Ranjiti ni kitu ambacho kitazidisha ugumu wa yeye kuto weza kumpata mwanaye.
“Binti”
“Ndio kaka yangu?”
“Kama nilivyo zungumza awali hao magaidi ni watu hatari sana, hadi ninavyo zungumza hivi sasa hawaonekani hata huku kwangu na wamefunga kila kitu ambacho kinaweza kunisaidia kuweza kuwaona”
“Ooohoo Mungu wangu jamani nitafanyaje jamani”
“Kwani hao magaidi wamefanya tukio gani?”
“Wamewaua walinzi na wamewatorosha dokta Ranjiti na mwanaye”
“Hawa ambao tunawaona wanatangazwa mostwanted kwenye televishion?”
“Ndio”
“Duuu”
“Ngoja nirudi Ubalozini kwa maana kule kuna wataalamu zaidi yangu ambao wanaweza kuifanya hii kazi ila inabidi sasa hili swala lishuhulikiwe kiusalama zaidi, na inabidi tupate ruhusa ya raisi wako”
“Sawa kaka yangu yaani nisaidieni nyinyi kuwatafuta jamani”
“Katika eneo hilo walilo fanya tukio kuna rekodi yoyote ya cctv camera?”
“Ndio ipo”
“Nenda kachukue baadhi ya video zao na unitumie sasa hivi, kwa kupitia sura zao tunaweza kufahamu ni sehemu gani walipo”
“Sawa”
Shams akwa haraka akatoka sebleni hapo hukua kikimbia, akaingia katika chumba cha siri na kumkuta kijana wa madam Mery akimalizia kufuta kumbukumbu ya video hizo za matukio ya mauji yaliyo tokea katika eneo hilo jambo liilo mfanya Shamsa kuchomoa bastola yake kiunoni na kupiga risasi ya mkono kijana huyo na kumfanya aanguke chini na kuanza kuugulia kwa maumivu makali sana.
Kwa haraka Shamsa akalizuia faili ambalo ndio lina video zote za matukio yaliyo tokea katika nyumba hii. Kijana wa madam Mery kwa akajisogeza hadi ilipo swichi ukutani na kuizima swichi hiyo na kupeleka computure hiyo kuzima jambo lililo mkasirisha sana Shamsa.
“Huwezi kupambaba na wasichana hao”
Kijana huyo alizungumza huku akitabasamu jambo lililo zidi kumkasirisha Shamsa amabye mwili mzima unamwagika jasho.
***
Majira ya saa mbili na kasoro dakika kumi na tano usiku, Lizzy na wezake tayari wafika eneo la karibu kabisa na sehemu inayo onyesha Camila alipo, Lizzy akalisimamisha gari hilo kwenye moja ya kichaka na kuzima taa zote.
“Unaweza kuona eneo hilo lina walinzi wanga?”
Lizzy alimuuliza msaidizi wake.
“Ngoja mara moja”
Msichana huyo mwenye utaalamu mkubwa sana kwenye maswala ya teknolijia, akaanza kucheza na batani za laptop ndogo ambayo waliikuta ndani ya sanduku la silaha. Hazikupoita hata dakika tatu akafanikiwa kupata mfumo mzima wa nyumba hiyo.
“Kuna walinzi ishirini na mbili”
“Mmmm, mbona wengi, ni nyumba ya kiongozi?”
Msicha hiyo akajaribu kutafuta rekodi za nyumba hiyo ila hakufanikiwa kabisa kuweza kuona.
“Sio nyumba ya kiongozi na inaonyesha kwamba nyumba hii ni ya siri”
“Ina milango mingapi?
Lizzy aliendelea kuuliza, huku akiwa ndio msikilizwaji wa mwisho kwenye tukio hilo.
“Mbele kuna mlango mmoja, kuna walinzi wanne wamesimama, nyuma kuna mlago wa pili ambapo kuna walinzi wawili, walinzi walio salia wanazunguka zunguka katika eneo hilo”
Msichana huyo alizungumza huku akiendelea kuminya minya batani za laptop hiyo. Lizzy akaitazama simu yake ya mkononi, akaona zimesalia dakika saba.
“Tunadakika sita mbeleni, tunagawana majuku, tunatembea wawili wawili, umakini ni muhimu. Tukumbuke hatuendi kwa wakwe zetu, tunakwenda kuua na kuhakikisha kwamba tunaondoka na kilicho tuleta hapa. Sinto hitaji uzembe wa aina yoyote, sheria ukikamatwa hakikisha unajiiua mwenye kwa vidonge vya simu tulivyo navyo naamini nimeleweka”
“Ndio umeeleweka muheshimiwa”
“Mkuu nimepata chumba ambacho yupo mto mchanga.”
“Hembu”
Msichana huyo akamgeuzia Lizzy laptop hiyo na kuanza kumuonyesha jinsi signal za watu hao zinavyo onekana.
“Hizi alama nyekundu ndio watu?”
“Ndio mkuu, alama zote zinasoege, kasoro alama hii. Ninauhakika wa asilimia mia moja kwamba huyu ndio Camila na amelala katika chumba cha gorofani”
“Okay tagert yetu sasa ni kuhakikisha kwamba tunampata mtoto sawa”
“Sawa mkuu”
“Tutatumia dakika tatu, kila mtu aitege saa yake vizuri mkononi mwake. Zikiisha dakika tatu kabla hatujarudi kwenye kituo chetu ambacho kitakuwa ni hapa kwneye gari basi kila mmoja ahakikishe kwamba anamtafuta mwenzake, sawa”
“Sawa mkuu, ila ninashauri kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Uonaonaje tukavaa vinyago ambavyo vinaweza kuficha sura zetu kwa manaa kitu nilicho weza kugundua, kwenye ile nyumba sura zetu zimebaki, na kuna mtu nimempatia jukumu la kuweza kuzifuta”
“Nani umempatia jukumu hilo!!?”
Lizzy aliuliza kwa mshangao mkubwa sana”
“Kuna kijana nilikuwa ninachati naye anahusika na ile nyumba, alikuwa ni mtu wangu kwa muda mrefu sana, ila bado nina mawasiliano naye”
“Ahaaa hapo nimekuelea, ila hawezi kubwanwa na kukutaja?”
“Hawezi:
“Kuwa naye makini asije akakuingiza matatani”
“Sawa mkuu”
“Poa basi kila mmoja avae azibe sura yake, muda sasa umewadia. Hakikisheni kwamba munakumbuka kwamba ni dakika tatu na bunduki zifungwe kiwambo ya kuzuia sauti”
Kila mtu akaanza kufwata maelekezo ambayo Lizzy ameyatoa. Walipo maliza kujiandaa, wakashuka kwenye gari na kuanza kutembea msituni humo kwa umakini wa hali ya juu. Wakafanikiwa kufika katika eneo ilipo nyumba ya K2. Lizzya kaatoa darubini ndogo iliyopo mfukoni mwake na kuanza kutazama walinzi wote, walipo eneo la mbele la nyumba hiyo na kuwaona wakiwa makini sana katika kuimarisha ulinzi wa eneo hilo.
***
Njing akamsogelea mmoja wa wanajeshi katika eneo hilo, akachomoa sindano yake ndogo sana yenye sumu kali.
“Ahaa, samahani kaka”
Njing alizungumza huku akimpa mkono mwanajeshi huyo ambaye naye yopo makini sana katika kumlinda Adrus kwani ndio mtu wa pekee amabye wanamuhitaji katika eneo hilo. Pasipo kufahamu, mlinzi huyo akajikuta akimkabidhi Jing mkono wake jambo lililo kuwa ni harari kwani Jing akamchoma kisindano hicho ambacho si rahisi sana kwa mtu kuweza kupata maumivi ya haraka.
“Bila samahani”
“Ninaomba unielekeze chooni”
Mwanajeshi huyo akamuelekeza Jing chooni kwa ishara, Jing akaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida, huku akiendelea kutazama wanajeshi wengine. Hazikupita hata dakika mbili, mwanajeshi huyo akaanza kuhisi kizunguzungu kilicho mfanya aanze kutingisha kichwa chake, huku akijaribu kujiweka sawa. Jasho jingi na joto likaanza kumtawala mwilini mwake. Kwa bahati akajikuta akivuta traiga, na kuruhusu risasi mojakutoka na kumpiga mwenzake aliye simama mita kadha akutoka sehemu ambayo amesimama yeye, kitu kilicho msababisha wanajeshi wote pamoja na watu kustuka. Mwanajeshi huyo akaanguka chini na mapovu kuanza kumtoka mdomoni mwake huku damu zikimtoka puani na masikioni mwake. Umakini wa wanajeshi wengine kwa Adrus ukapotea kabisa, na kuanza kuwashuhulikia wanajeshi hao wawili.
“Tuondoke”
Adrus alizungumza huku akimshika Cookie mkono kwani eneo hili tayari hata majeruhi ambao wanajiweza nao wakaanza kutawanyika, jambo lilio zidi kuwapa Adrus nafasi nzuri ya kuweza kutoweka katika eneo. Jing akaungana na Adrus pamoja na Cookie na kuanza kutoweka katika eneo hilo.
“Huku”
Njing alizungumza huku akiongoza kukimbia huku Cookie na Adrus wakimfwata kwa nyuma. Wakaingia kwenye moja ya chumba amacho kina mitambo mingi ikiwemo mashine kadhaa za kuweza kuisaidia meli hiyo kujiendesha. Njing akaanza kutazama tazama ndani ya chumba hicho.
“Unatafuta nini?”
Adrus aliuliza huku akimtazama Jing usoni mwake.
“Ninatafuta sehemu ambayo ninaweza kuzima system ya umeme ya meli nzima…..Hii hapa”
Njing alizungumza huku akisogelea swichi kubwa iliyopo kwenye moja ya nguzo nene ya chumba. Akafungua mlango wa kioo ulipo kwenye swicho hiyo. Akawatazama Cookie na Adrus wanao mtazama.
“Hii ndio njia ya pekee inayo weza kutufanya tuondoke eneo hili”
Njing alizungumza, kisha akaishusha swichi hiyo yenye kishikizio chini. Taa zote katika meli hiyo zikazima na zikabaki taa maalumu ambazo hujitegeme katika kuwaka na hazitumii umeme wa meli hiyo na zina mwanga mdogo sana. Hali ya umeme kukatika katika meli hiyo ikazidisha taharuki kubwa kwa kila mwanajeshi aliyomo ndani ya eneo hili.
“Naohodha ni nini kinacho endelea”
Mkuu wa kikosi cha uakoaji alizungumza huku akimtazama nahodha mkuu wa meli hiyo.
“Umeme umekatika hembu tuma vijana wako kwenye chum ba cha mitambo huko chini”
Mkuu huyo wa jeshi akafanya kama alivyo elekezwa na nahodha hao. Vijana wanne wakaanza kushuka katika chumba ambacho Adrus na wezake wapo. Cookie akafumba macho yake na kusikilizia miguu ya watu wanao kuja katika eneo hilo.
“Kuna watu wanne wanao kuja katika eneo hili”
Cookie alizungumza huku akimtazam Adrus usoni mwake.
“Umejuaje?”
“Hisia, ninatumia hisia zangu kuweza kufahamu nini kinacho weza kuja katika eneo hili”
Cookie alizungumza kwa kujiamini sana. Hazikupita hata dakika moja wakasikia miguu ya watu wakiingizana na katika eneo hilo huku wakiwa na tochi. Jambo hilo likawafanya wote kijibanza katika eneo ambalo hawato weza kuonekana kirahisi.
“Hei”
Jing alizungumza kwa sauti ya chini sana huku akimuonyesha Adrus na Cookie ishara ambayo inamaanisha waashuhikie watu hao. Wanajeshi hao wakaanza kumulika mulika ndani ya chumba hicho huku wakijitahidi kuangalia ni sehemu gani ambayo kuna tatizo. Jing kwa kasi ya ajabu akaanza kumshambulia mwanajeshi mmoja, jambo lilolo wafanya Cookie na Adrus nao kuwashambulia wanajeshi walio salia. Ndani ya dakika tano wanajeshi wote wakawadhibiti,
“Ili tuweze kutoka hapa inabidi tufanane nao”
Jing alizungumza huku akianza kumfungua vifungo vya shati mmoja wa walinzi hao. Adrus na Cookie hawakutana kufafanuliwa zaidi kwani walisha elewa maana ya Njing, kwa haraka kila mmoja akaanza kumvua mwanajeshi mmoja nguo zake
***
Eddy akaendelea kusikilizia na kuvumilia maumivu ya meno ya Phidaya anaye endelea kumng’ata kwa nguvu kwenye mkono wake huku akilia kwa uchungu sana. Phidaya akautoa mdomo wake kwenye mkono wa Eddy na kumuacha akimwagikwa na damu.
“Ninakupenda mke wangu”
Eddy alizungumza huku machozi yakimgika usoni mwake.
“Naomba utoke chumbani kwangu”
Phidaya alizungumza kwa hasira sana.
“Mke wangu tafadhali ninaomba kuzungumza na wewe”
“Eddy sihitaji kuzungumza na wewe, toka chumbani kwanguuuuuu”
Phidya aliendelea kizungumza kwa ukali.
“Wallinziiiiiiiiii”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya juu sana. Walinzi waliopo nje mita chache kutoka katika mlango wa chumba hicho, wakamtazama mkuu wao ambaye naye pia ameweza kusikia sauti ya mke wa makamu wa raisi akiwaita.
Mkuu wao huyo akawapa ishara vijana wake kila mtu kuweza kusimama katika eneo lake kisha yeye akaanza kutembea kueleka katika mlango wa chumba alipo Eddy na mke wake Phidaya.
“Walinzi ananiuaaaaaaaa”
Sauti hiyo ya Phidaya ikamfanya mkuu huyo wa kikosi cha ulinzi hapo hospitalini kuingia ndani humo kwa haraka pasipo hata kubisha hodi, akamkuta makamu wa raisi akiwa amekaa pembeni ya kitanda cha mke wake.
“Mkuu”
Mzee huyo alizungumza hukua kimtazama Eddy na Phidaya.
“Toka nje ninazungumza na mke wangu”
“Sawa mkuu”
“Mtooeni hapa bwanaaa”
Phidaya alizungumza kwa hasira, mkuu huyo wa kikosi cha ulinzi hakusikiliza kauli ya Phidaya zaidi ya kusikiliza kauli ya mkuu wake wa kazi.
“Hawato kusikiliza wewe”
Eddy alizungumza huku akijitahidi kunyanyuka katika kiti cha magurudumu alicho kikalia. Japo paja lake alilo pigwa risasi ilina maumivu makali ila akajika kiume kuto kuonyesha udhaifu wowote mbele ya mke wake. Taratibu Eddy akaka pembeni ya kitanda cha Phidaya, ambaye kwa haraka akajaribu kumsikuma Eddy ili asiweze kukaa katika kitanda hicho, jambo lililo mkasirisha sana Eddy na kujikuta akimtandika kibao kikali cha shavuni Phidya.
“Unataka nini wewe mwanamke eheee?”
Eddy alizungumza kwa kufoka sana huku macho yakimtoka huku jasho likimwagika usoni mwake na shingoni.
“Ninamtaka mwanangu, hata ukinipiga na kuniua mimi ninamyaka mwangu sawa wewe malaya uliye kubuhu”
Phidaya alizungumza kwa jazba kubwa sana.
“Mimi malaya eheee?”
Eddy alizungumza huku akiliwahi koo la Phidaya na kuanza kulikaba kwa nguvu.
“Ndio wewe malaya, mseng*** wewe”
Phidaya aliendelea kuzunguza kwa jazba huku akiutoa mkono wa Eddy ulio mkaba koo lake.
“Phidaya sihitaji ugovi na wewe”
“Kwenda zako, umemtomb** Shamsa ulidhani kamba sito jua eheeee?”
Phidaya aliendelea kuzungumza maneno ya ukali ambayo yakazidi kumuongezea Eddy hasira kali.
“Phidaya nimekuambia sihitaji uzungumze utumbo wako huo”
“Kama ni utombo, uchemshe na uule mseng** wewe”
Eddy kwa macho ya hasira akamtazama Phidaya, mke wake huyo aliye geuka na kuwa kama mbogo jike aliye jehuhiwa kwa risasi. Taratibu Eddy akanyanyuka na kukaa kwenye kiti cha magurudumu.
“Na tambua kwamba nitawaonyesha wewe na malaya wako Shamsa, ngoja nipone”
Phidaya alizungumza huku uso mzima ukiwa umejaa wekundu ambao kusema kweli katika maisha yake yote tangu kuzaliwa hakuwahi kuwa nao. Maeno ya hayo ya Phidaya yakaanza kumpa uhakika Eddy kwamba Phidaya ndio amehusika kwenye tukio zima la dokta Ranjiti na mwanaye Anna kutoraka.
“Etiii ehee?”
Eddy alizungumza huku akitabasamu kwa dharau.
“Ndio lazima niwaonyeshe waseng** nyinyi na tambua hadi kuna pambazuka ninahitaji kumuona Camila wangu hapa”
“Ni wako au wangu”
“Wangu, kama angekuwa ni wako, ungembeba tumboni mwao na kwenda lebour kujifungua”
Phidaya aliendelea kuzungumza kwa kujiamini sana.
“Etii ehee?”
“Ndio”
“Poa. Ila chunga kinywa chako Phidaya, sijapenda”
“Utapenda na wewe chunga mb*** yako kwa maana huoni sehemu za kuiingiza hiyo, si kila k**a ya mwanamke ni ya kuzaaa naye”
Meneno hayo ya Shamsa yakamfanya Eddy taratibu kuyasukuma magurumu ya kiti alicho kikalia, alipo fika mlamgoni akamgeukia Phidaya, ambaye akaachia msunyo mkali ulio mfanya Eddy kugonga mlango wa chumba hicho, mkuu wa kikosi cha ulinzi akafungua mlango huo, akamtazama Eddy usoni, kisha akayahamishia macho yake kwa Phidaya amabye analia kwa hasira sana huku akiwa ameukumbatia mto wake.
***
Lizzy taratibu akaishusha darubini yake aliyo kuwa akiitumia kuwatazama walinzia liopo katika eneo la nyumba ya K2. Akanza kuwapangilia wezake hao, huku akiwapa maeleekezo ya wapi waweze kupita. Kwa kasi ya ajanu Lizzy na wezake wakaanza kuwashuambulia walinzi hao walipo sehemu ya mbele ya jumba hilo. Walipo hakikisha kwamba ulinzi wa nje wa jumba hilo wwamewamaliza, kwa umakini mkubwa sana wakaanza kuingia ndani ya gari huku akihakikisha kwamba wanampata Camila ambaye ndio amewafanya waweze kufika katika eneo hilo.
Wakafanikiwa kuingia ndani ambapo, harufu ya nyama choma imetawala kila upande wa eneo hilo. Kijana mmoja wa Lizzy akapandisha gorofani na kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona Camila kwenye moja ya chumba.
“Nimempata mtoto?”
Msichana huyo alizungumza huku akitumia kifaa chake cha mawasilano alicho kivaa sikionioi mwake.
“Sawa mchukue”
Lizzy akiwa hapo sebleni akiimarisha ulinzi akaanza kusikia makofi yakipgwa kutokea ejeo la jiokoni ambapo hakuelewa ni nani huyo ambaye anapiga hayo makofi. Akatoka dada mrefu akiwa amevalia suruali nyeusi na sidiria tu kifuani mwake. Nywele zake amezifunga kwa nyuma vizuri na kwa muonekano wa haraka haraka basi mwili wake unamuonyesha ni mwana mazoezi.
“Mumepanga sana kumuwezi kutoka eneo hili pasipo kupambana na mimi mawahakikishia kwamba vifo vyenu vitakuwa ndani ya hii nyumba?.
K2 alizungumza kwa kujiamini huku akiwatazama Lizzy na wezake wawili ambao mmoja, amembeba Camila| mikononi mwake na mwengine ameshika bunduki mkononi mwake.
Lizzy akatabasa huku akimtazama K2, ambaye hujui ni kwa nini amejiamini kwa kiasi hicho. Lizzy akamkabidhi msichana wake bunduki ambayo aliyo ishika, akaanza kuvinyoosha vidole vya viganja vyake, ili kujiweka sawa. Akasimama mbele ya K2 ambaye hukuihitaji kumuua kwa kumpiga risasi. Harufu ya pombe inayo toka kinywani mwa K2 ikazidi kumuhuzunisha Lizzy kwani anatambua kwa pigo moja linaweza kumuua kabisa K2.
“Muwekeni mtoto chini kisha muondoke ndani hapa?”
K2 aliendela kuzungumza huku akimtaza Lizzy usoni mwake. Lizzy kwa haraka akafanya shuambulizi la kumpiga K2 kigoti cha tumboni mwake na kumfanya K2, kujiipinda kisawa sawa, kwani kigoti hicho kimempata kisawa sawa, Lizzy hakuishia katika shambulizi hilo tu, alicho kifanya ni kupiga nguvi sita za mbavu zilizo muangusha K2 chini na kuanza kutapika kila alicho kula. Lizzy akachomoa bastola yake, akaikoko vizuri na kutaka kumpiga K2 kichwani mwake ila alivyo muona anatapika damu, akatambu kwamba mapigo hayo aliyo mpatia ni lazima yatakuwa yameharibu baadhi ya vitu vya tumboni mwake.
“Mkuu vipi?”
“Atakufa taratibu, sihitaji kupoteza risasi zangu”
“Sawa”
Lizzy na wezake wakatoka ndani humo, wakaelekea kwenye gari lao ambalo wameliacha mita kadhaa kutoka eneo hilo, wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwa kasi sana.
***
Shamsa akamtazama kijana wa madam Mery, pasipo na huruma yoyote, akamtandika risasi kadhaa zakifuani ambazo milio yake iliweza kusikaka sebleni na kuwafanya madam Mery na mlinzi wa Shamsa kwa haraka wakaondoka katika eneo la seblenin a kukimbilia katika chumba hicho cha siri. Wakaingia ndani na kumkuta Shamsa akichomeka waya wa computure kwenye swichi ya ukutani, huku maiti ya kijana huyo ikiwa pembeni. Madam Mery mwili mzima ukaanza kumtetemeka, akajaribu japo kutoka katika chumba hichi kwa woga ila mlinzi wa Shamsa akamzuia akaimini kwamba madam Mery anahitaji kukimbia.
“Kaa hapa”
Mlinzi huyo alizungumza huku akimpa kiti madam Mery, taratibu akamkalisha. Shamsa hakushuhulika nao kabisa, alicho kifanya ni kutazama computure hii anayo isubiria kuwaka. Haikuchukua hata dakika moja na nusu, computure ikakaasawa. Shamsa akalitafuta faili hilo na kwa bahati nzuri akalipata. Akaanganza angaza katia meza hiyo ya computure, na kuona waya wa USB. Akauchukua na kuuchomeka kwenye sehemu maalumu katika computure hiyo kisha akauchomeka katika simu ya Phidaya. Kwa haraka akaanza kuhamisha faili hilo la video na kuziingiza kwenye simu yake. Alipo maliza, kwa haraka akaitafuta na mwanau usalama kutoka katika ubalozi wa Uingereza. Shamsa akaipiga namba ya kijana huyo, hazikupita dakika hata sekunde mbili simu ikapokewa.
“Ndio”
“Ninaimani kwmaba umeona”
“Ndio numeziona. Nipo ubalozini sasa hivi, tayari balozi wangu hivi sasa anafanya maongezi na raisi wako”
“Sawa shukrani sana”
“Tunakupatia full detail”
“Sawa, na kama ni oparesheni basin a mimi ninaihitaji kuhusika”
“Sawa”
ITAENDELEA
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 1/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 2/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 3/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 4/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 5/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 6/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 7/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 8/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 9/10
- MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 10 MWISHO
0 comments:
Post a Comment