Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

DAPHINE SEHEMU YA 7/10

 

 


DAPHINE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 7 KATI YA 10

 


Ngesa hakuwa mpumbavu,alijua ni namna gani Wanausalama wanavyofanya mambo yao kusaka wahalifu hivyo asingekuwa makini angekamatwa kizembe,hakutaka hilo litokee hata kidogo!Alichokifanya ni kutembeza gari mpaka Mwenge Bamaga,hapo aliingia vichochoroni,akatoa simu yake akaandika namba za Rais Leslie na kuipasua simu chini,akamtizama Jenipha kwa huruma.Kuna kitu alitaka kumfanya lakini akamuacha kama alivyo bila fahamu,akateremka ndani ya gari na kuanza kutafuta pikipiki.

“Nipeleke Ubungo,uwanja wa Ufi”

“Poa”

Ngesa akapanda juu ya pikipiki kwa nyuma na safari ya kwenda Ubungo kuanza mara moja,alivyofika anapoenda hakuwa nacha kufanya zaidi ya kutafuta kibanda cha simu ili ampigie Rais Leslie,matokeo yake simu iliita bila kupokelewa,akapiga tena na tena ndipo ikapokelewa.

“Halloo Mheshimiwa Rais!Ni mimi Ngesa”

“Yes,nakupigia sasa hivi”

Kwa kuwa jambo hilo lilikuwa ni siri kubwa sana, ilibidi Rais Leslie awaombe walinzi wake wakae mbali kidogo kwani simu hiyo kwake ilikuwa ya siri kubwa,hakutakiwa mtu yoyote yule kusikia mazungumzo yake na Ngesa.Alivyoona walinzi wote wapo mbali,akarudisha simu sikioni.

“Ngesa,upo wapi?”

“Nipo sehemu salama”

“Umefanikiwa kutoka?”

“Ndio”

“Hilo nililijua,nisikilize kwa makini.Kuna wanafunzi zaidi ya mia tano wametekwa nyara nchini Uganda ni watanzania,wanamtaka Brigedia Karanje nawewe”

“Ni nani amefanya hivyo?”

“Sijajua ni nani,Ngesa nakuomba.They are innocent,please save them”

“Umesema walikuwa wananihitaji mimi na Karanje?”

“Ndio”

“Wametoa masaa mangapi?”

Ngesa alitaka kudadisi kwani alikuwa ni mwanamme makini.

“Chini ya masaa ishirini na nne”

“Madogo sana”

“Ngesa,una maana gani?”

“Jaribu kuzungumza nao,wakupe masaa mengine zaidi.Waambie mshanipata na mtawapa Karanje pia.Baada ya hapo,mimi na wewe tutakuwa tunawasiliana kuwa karibu na simu”

“Sawa,ahsante sana Derrick”

“Kitu kingine Mheshimiwa Rais”

“Kipi?”

“Siwezi kwenda mwenyewe”

“Unataka kwenda na nani?”

“DAPHINE”

“Yupo wapi?”

“Usalama wa taifa”

“Hilo litakuwa gumu kumtoa al..”

“Niachie mimi”

Huo ungekuwa mtihani mwingine mgumu sana,kumtoa Daphine nje ya jengo hilo la usalama wa taifa sababu alikuwa katika mahojiano mazito,akiandika maelezo yake! Hakuwa anaelewa hili wala lile.

Licha ya yote,ilikuwa ni lazima aandike kwa njia ya maandishi namna walivyomkamata Brigedia Karanje na historia nzima kwa ujumla,haikuwa kazi rahisi, ilihitaji utulivu ndiyo maana akawekwa ndani ya chumba maalum ili aandike kila kitu,akiwa ameshika kalamu anaandika yaliyojiri, ghafla mlango wake ukasukumizwa akaingia mwanamke mrefu mwenye rangi ya maji ya kunde.

“Daphine njoo,kuna simu yako”

Hiyo ilimfanya Daphine asimame na kutoka nje ya chumba hiko,akatembea mpaka kwenye moja ya ofisi,akapewa mkonga wa simu.

“Daphine mwanangu,Mimi mama yako Beatrice”

Sauti ya mwanamke huyo ilimfanya ashikwe na uchungu ajabu,katika wanawake aliowaheshimu ni Mama huyo aliyemlea tangu akiwa mtoto mdogo, baada ya wazazi wake kuuwawa kinyama na Brigedia Karanje,hakujibu kitu badala yake alishusha pumzi ndefu.

“Mom,shikamoo”

“Marahaba,mzima?”

“Ndio,Mimi mzima”

“Pole na kila kitu”

“Ahsante Mom”

“Nisikilize Daphine,tunaweza kuongea kitu.Upo peke yako?”

Alichokifanya Daphine ni kuwatizama wanausalama,ambapo kila mmoja alikuwa bize na mambo yake.

“Ndio,ongea Mom”

“Ongea na Ngesa huyu hapa,nipo naye”

“Ngeeeesa!?”

“Ndioo”

Baada ya sekunde sita,Ngesa akawa kwenye laini.

“Daphine nisikilize kwa makini,siwezi kuelezea kila kitu kwenye simu.Naomba tukutane Gongo la Mboto Ulongoni”

“Ngesa,uko wapi?”

“Tukutane Gongo la Mboto,Ulongoni.Ukifika hapo,nipigie simu!Chukuwa peni na karatasi”

Hapohapo Daphine,akachukua peni na karatasi na kuanza kuandika namba za simu,akaziweka mfukoni na kukata,akashusha pumzi na kutafakari namna ya kutoka eneo hilo.


****

Hasira za Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Bwana Ramadhani Mpelembe zilifika mwisho,muda wote aliuma meno yake.Kitendo cha Ngesa kumtoka mchana kweupe tena akiwa na vijana wake ilikuwa ni aibu kubwa kwake na ilimshushia heshima,mwanamme huyu hakuwahi kuchafua Cv yake hata siku moja,aliamini katika kila jambo analolifanya ni lazima litimie kwa gharama yoyote ile,hiyo ikafanya mpaka shati lake lichore alama ya baka kubwa la jasho,akatafakari na kuwaza vitu vingi sana.

Kazi ikabaki moja tu,kuanza kufuatilia GPRS ya Jenipha ambayo mara ya mwisho ilimpeleka mpaka sheli ya kujazia mafuta,hapo akashindwa kuendelea zaidi mpaka walipochukua namba za Ngesa na kuingiza kwenye mitambo yao,ramani ikaja na kuonesha mara ya mwisho simu yake ilikuwa Mwenge Bamaga,hawakutaka kupoteza wakati.

Wakawasha magari yao mpaka Bamaga huku Mkurugenzi akiongoza msafara huo,hakutaka tena kufanya makosa ndiyo maana akajitanguliza mbele huku bastola yake ikiwa pembeni ya gia ina risasi kumi na nane tayari kaikoki kwa kumfyatua Ngesa kama akileta ukahidi,alikimbiza gari kwa kasi ya ajabu na alivyowasili Bamaga,akaliona gari la Jenipha lipo pembeni,mlango mmoja wa dereva upo wazi.

Hapohapo akachukua bastola yake na kuiweka mkononi,akashuka na kutizama huku na kule!Akatembea kwa tahadhari kubwa sana,alivyolifikia akamkuta Jenipha amelala kwenye kiti cha kushoto hajitambui,moyo wake ukapiga kwa nguvu.Kwa haraka akaingia ndani ya gari na kugusa shingo ya Jenipha ili ajuwe kama bado mwanamke huyo yupo hai,hapo hakuridhika akaweka kidole chake kimoja chini ya pua za mwanamke huyo ili ajuwe kama kweli anapumua.

“Thomas,njoo na first aid kit.Fanya haraka”

Haikuchukuwa muda sana,Thomas akawa amefika na boxi dogo la huduma ya kwanza ambalo lilikuwa na dawa kadhaa,hapo akatoa kichupa kidogo akamuwekea Jenipha puani,haikuchukuwa sekunde tano Jenipha akakohoa akawa kama amepaliwa na kitu,alivyofumbua macho yake akakumbana na sura ya Mkuu wake wa kazi huku shingo ikiwa inamuuma sana,akavuta kumbukumbu zake kwa kasi.

“Upo sawa?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa mkuu wake wa kazi.

“Nd..io”

“Nini kimetokea?”

“Ngesaa”

“Kafanya nini?”

Hapohapo,ilibidi aeleze kilichotokea mpaka alivyopigwa kabali ndani ya gari,alikuwa mwenye kila sababu ya kuamini kwamba ni lazima Ngesa ameshtukia mchezo.

“Haiwezekani,itakuwa ulimwambia”

“Siwezi kufanya hivyo mkuu”

“Sasa niseme nini,wakati ulikuwa naye ndani ya gari?”

“Hata mimi nashindwa kuelewa,nina uhakika kuna mtu kamwambia.Namfahamu Ngesa,nimekaa naye kwa muda mfupi lakini sio mtu wa kufanya vile bila kuwa na uhakika na jambo analofanya”

“Unataka kusema nini Jenipha?”

“Kuna simu aliipokea”

“Una uhakika?”

“Ndio”

Mambo hayakuishia hapo,namba ya Ngesa ikaanza kusakwa na ilitakiwa ijulikane ni nani alizungumza naye simuni,swala hilo kwa wanausalama lilikuwa ni sawa na kumsukuma mlevi adondoke.Haikuchukuwa dakika nyingi,namba za simu alizokuwa anawasiliana nazo Ngesa zikaingia kwenye kompyuta ndogo.

“Ilikuwa saa ngapi?”

Mkuu wao wa kazi akauliza,kuna jambo alitaka kulijua.

“Kama lisaa limoja na nusu lililopita”

“Hapa mbona mara mwisho imeonesha kawasiliana siku mbili nyuma, leo hakuongea na mtu”

“Haiwezekani”

“Angalia kompyuta hii hapa”

Kila mtu alihisi kuchanganyikiwa,walichokitarajia kilikuwa tofauti, hiyo ilimfanya Jenipha azidi kutetemeka.

“Nina wazo”

Jenipha,akazungumza kila mtu akamuangalia.

“Kitu gani?”

“Daphine yuko wapi?”

“Usalama,ofisini”

“I’m sure.Ni lazima amfuate Daphine”

“Una maana gani?”

“Namjua Ngesa,nimekaa naye kwa muda mfupi lakini nishamuelewa ni mtu wa aina gani.Nina uhakika kuna jambo anataka kulifanya,tumuwahi”

Wazo la Jenipha,hawakutaka kulifumbia macho haraka wakaingia ndani ya magari,wakaanza kurudi usalama wa taifa walivyowasili tu.Macho yao yote yalikuwa kwa Daphine, lisaa limoja baadaye,simu ya mezani ikaita mwanamke aliyejitambulisha simuni, akataka kuzungumza na Daphine hapo ndipo wakaweka umakini zaidi,walichokifanya ni kuweka mtambo maalum ili wasikie anachozungumza Daphine,walivyosikia sauti ya Ngesa kila mtu akamtizama mwenzake,hiyo ilimaanisha ni lazima wamfuatilie Daphine ili wamuweke Ngesa chini ya ulinzi.


****

Alichokiwaza ni kutoka ndani ya jengo hilo bila kugundulika,akatafakari mara mbilimbili,ilikuwa ni vigumu sababu hakuwa mwenye silaha yoyote ile isitoshe jengo hilo lililindwa na kamera kila kona.Hilo halikumvunja moyo,akatafakari zaidi na zaidi!Akarudi ndani ya chumba alichokuwa anaandika ripoti juu ya kilichotokea na kumalizia,akachukuwa peni na kuiweka mfukoni,akatoka nje ya ofisi hiyo.

“Tayari,nishamaliza karatasi hii hapa”

“Okay,subiri hapo!Tukupe utaratibu mwingine”

Simu ikapigwa moja kwa moja mpaka kwa mkurugenzi wa Usalama wa taifa,ambapo alitoa ruksa kwamba Daphine aachiwe sababu hakuwa ana sababu ya kuendelea kubaki eneo hilo,hiyo ilimshangaza sana Daphine,lakini hakuhoji chochote alichokifanya ni kushukuru na kuanza kuteremsha ngazi akitafakari.Nje kulikuwa na Pikipiki upande wa pili,hapo alisogea karibu.

“Nipeleke Kariakoo”

“Karikoo,sehemu gani Sista?”

“Mtaa wa Kipata”

“Poa”

Daphine,alivyojibiwa hivyo akatizama Mlango wa ofisi za usalama wa taifa akamuona mwanamme mmoja,anamtizama alafu baada ya macho yao kugongana mwanaume huyo akaangalia chini,hapo kuna kitu alijifunza kwamba kuna kitu kisichokuwa cha kawaida,akapanda nyuma ya pikipiki na safari ikaanza.Hapakuwa mbali na Posta,walivyowasili tu, Daphine akateremka!

“Nakuja,nisubiri naingia hapo nyuma”

Mitaa hiyo kwa Daphine ilikuwa ni kama Simba aliyekuwa msituni,Kariakoo ilimkumbusha miaka ya nyuma alivyokuwa gaidi la kutisha,hiyo ilimaanisha ni lazima siku hiyo awafanyie michezo ya kimafia wana usalama hao,ambao aliamini ni lazima wanamfuatilia,hilo alikuwa ana uhakika nalo,sababu mbele yake kwa juu katikati ya kichochoro alichopita kulikuwa na kioo kikubwa,alivyoangalia akawaona wanaume wawili wapo nyuma yake,akatembea mwendo wa kawaida na kuingia ndani ya uchochoro mwingine mwembamba sana,hapo akatulia na kujiandaa kwa lolote lile.

Wanausalama hao wawili,hawakuwa wanajua kwamba wameshtukiwa na walitembea kichwakichwa kama wanaenda kununua nazi gengeni wakimfuatilia Daphine, mmoja alivyoingia ndani ya kichochoro hiko,alitoa ukelele mkali hiyo ni baada ya kupigwa ngumi moja ya chembe ambapo alitulizwa na kifuti cha mbavu,akajikunja na kulala sakafuni,alivyoingia mwingine alivutwa na kupigwa kichwa puani,hakukaa sawa Daphine akashika chuma cha juu akaning’inia nacho na kumrukia teke takatifu la kifua, lililomfanya mwanamme huyo akipige kichwa chake ukutani hapohapo akalala chali,alichokifanya Daphine ni kuwasachi na kuchukuwa silaha zao pamoja na pesa, bastola moja akaiweka kiunoni pembeni na nyingine kwa nyuma,akafunika tisheti lake vizuri kisha kuanza kutembea,akatokeza mtaa wa pili!Ambapo huko,alimuona Jenipha kwa mbali,akakunja mtaa mwingine!Akatokeza mtaa wa Swahili ambapo huko,alikumbana na bodaboda nyingine!

“Mambo,nipeleke Mtaa wa Agrey”

“Hapo nyuma?”

“Ndio”

Dereva huyo ilibidi ashangae,sababu mtaa huo haukuwa mbali na hapo.Hakuwa na jinsi zaidi ya kutii amri ya abiria wake,niya ya Daphine ilikuwa kwanza,awachanganye wana usalama hao na kuwatia adabu ili siku nyingine waelewe wanacheza na mwanamke hatari kuliko MAFIA.




Pikipiki ilianza safari mara moja,hawakuchukua hata sekunde tatu wakawa tayari wamewasili mtaa wa Agrey,kama alivyofanya kwa dereva wa mara ya kwanza,ndivyo alivyomwambia pia na huyo kwamba anarejea dakika hiyohiyo.

Jenipha hakuwa mbali naye,alikula naye sahani moja sababu nayeye alikodi pikipiki ili amfuatilie nyuma yake.Niya ya mwanausalama huyu alitaka kujua ni wapi Ngesa alipo ili amtie kwenye mikono ya Sheria akiamini kwa kufanya hivyo angepata ujiko mkubwa sana,ndiyo maana swala hilo akalivalia njuga.

Daphine alikua mbele yake umbali wa kama mita mbili hivi,akiamini kwamba mwanamke huyo hajagundua kumbe alikuwa akijidanganya, kifupi ni kwamba yeye ndiye alikuwa anajazwa ndani ya kumi na nane,Daphine akapita mtaa wa kwanza akatokea mtaa wa Masasi akanyoosha moja kwa moja, mpaka kwenye kanisa la KKKT,akatembea taratibu na kuingia kwenye kichochoro chembamba.Jenipha bila kufikiria nayeye akaingia kichwa kichwa.Akavutwa kwa nguvu na kutulizwa na kifuti cha tumbo,hakukaa sawa akapigwa ngumi ya shingo,alivyotaka kutoa bastola kutoka kiunoni,mkono wake ukashikwa bastola ikadondoka chini,Daphine akaipiga teke ikaserereka na kutumbukia kwenye mtaro wa maji machafu.

Hapohapo wakakunja ngumi,Jenipha akarusha konde, Daphine akainama kidogo ambapo alivyorudi juu, akamchota na ngumi ya taya,mpambano ulikuwa mkali kati ya wanawake hawa wawili kwani wote walikuwa fiti na walijua kupambana,lakini aliyeonekana kuzidiwa zaidi alikuwa ni Jenipha sababu alikuwa akipigwa ngumi nyingi za usoni,alivojaribu kuweka mkono usoni ili zisimpate Daphine akawa anamshindilia ngumi za mbavu,hiyo ilimfanya awe anarudi nyuma.Daphine hakuremba akaruka teke aina ya ‘round kick’ lililomfikia Jenipha Kifuani,akadondoka puu kama embe mtini.

Haikuwa kawaida kwa Jenipha kupokea kipigo kikali namna hiyo kiasi kwamba akawa haoni mbele vizuri,akamuona kwa mbali Daphine, anaondoka zake,alivyotaka kusimama akahisi maumivu makali kwenye nyonga zake na kifua.

Akatulia,akibaki kumuangalia bila kufanya chochote!

Ilikuwa ni habari mbaya sana kwa Mkurugenzi wa Usalama wa taifa, Ramadhan Nurdin,alichoka na akakasirika akimtaka Jenipha afike ofisini kwake, mara moja.

“Nakuja”

“Sasa hivi,nakuhitaji ofisini.Na timu yako nzima”

“Sawa”

Koti lake jeusi alilovaa akahisi linambana,akafungua vifungo likabaki wazi,hiyo ikawa haitoshi.Akalegeza tai ambayo ilionekana kama inamkaba,zoezi la kumsaka Ngesa alitegemea lingekuwa rahisi kumbe ilikuwa kinyume chake,kitu alichokifanya ni kutembea tembea ndani ya ofisi huku na kule akizidi kutafakari mbinu ya kumnasa Ngesa,atumie mitego gani ili amuweke chini ya ulinzi mkali,kifupi alimchukia sana Ngesa kuliko kawaida na ndiyo maana alitaka kufanya juu chini amtie nguvuni.Mlango uliokuwa unagongwa ukamfanya atulie kidogo.

“Ingia”

Akasema kisha mlango ukafunguliwa,akaingia mwanamme mmoja mrefu,amevalia shati jeupe kachomekea.

“Daff,vipi?”Akauliza.

“Vijana wote wamepigwa”

“Vijana gani?”

“Wakina Timoth,timu nzima”

“Whaat?How?Nani kawapiga?”

“Daphine”

Ramadhan Nurdin,akaganda kidogo habari hizo zilionekana kumshtua, ndiyo maana akakosa jibu la harakaharaka,hakukaa sawa Jenipha akafika kwa kumuangalia tu alionekana amepokea kipigo kikali sana kwani usoni alivimba na mdomoni alikuwa ana damu.

“Imekuaje?”

Mkurugenzi akataka maelezo kutoka kwa Jenipha,akaachana na Daff aliyekuwa mlangoni.

“Amegundua”

“Amegundua nini?”

“Kwamba,tunamfuatilia”

“Kwahiyo?”

“Nilijitahidi,kupambana naye.Lakini bahati mbaya ni..”

“Shut up,hakuna cha bahati mbaya…”

Hapo meza ilipigwa kwa hasira,kuonesha kwamba maelezo ya Jenipha hayakumuingia akilini hata kidogo yaani timu nzima ipigwe na mwanamke mmoja.

“Huo ni uzembe,tunafanyaje kazi namna hii.Jenipha,yote ni kwasababu yako.Inaelekea umekula njama na Ngesa,umemtorosha”

“Siwezi kufanya hivyo”

“Usinidanganye,najua historia yako na Ngesa.Ni marafiki,nimesoma faili lako.Kwahiyo basi,naomba uniambie Ngesa yuko wapi?”

“Boss,sijui chochote”

“Nitakuamini vipi?”

“Naomba nafasi nyingine nimtafute”

“Count me out no way.Siwezi kubeba lawama nyingine”

“Tufanye kitu kimoja,naandika barua ya kuacha kazi.Nitafanya mimi kama mimi”

Swala hilo lilimfanya Ramadhan Nurdin amtizame kwa umakini akaonekana kama anatafakari kitu.

“Jeni…”

“Naomba niruhusu,nitakuwa comfortable bosi please nakuomba”

“Sababu gani utatumia kuacha kazi?”

“Niachie mimi”


*****

“Griiii griiiii”

“Griii griiiii”

“Uko wapi?”

Lilikuwa ni swali la kwanza kutoka kwa Daphine, baada ya Ngesa kupokea simu

“Gongo la Mboto,Ulongoni”

“Nakuja”

Ngesa alikuwa tayari Gongo la Mboto,maeneo ya Ulongoni yupo katikati ya miti mingi amejificha.Alijihami sababu alijua fika,kivyovyote vile ni lazima Wanausalama watakuwa nyuma ya Daphine,ndiyo maana alipiga simu makusudi akiamini ni lazima simu ya Daphine ingesikilizwa na alikuwa hapo kwa lengo la kupambana nao,ndiyo maana akatulia kwenye kichaka hiko ili aangalie namna ya kupambana nao.

Usalama wa taifa walikuwa ni watu hatari sana na wakiamua kukukamata kwao ni jambo la sekunde sifuri,hiyo ilimfanya asifanye kosa hata punje.Dakika mbili baadaye akapokea simu kutoka kwa Daphine,akitaka kuelekezwa ni wapi alipo.

“Unaona hiyo pikipiki”

Ngesa akasema simuni.

“Ndio”

“Ifuate”

Ngesa hakuwa kwenye pikipiki,niya yake ilikuwa ni Daphine avuke mbele aangalie nyuma yake yupo nani na nani,akamuona Daphine anavuka akaangalia nyuma yake na kuona gari dogo limepita, akaliwekea mashaka lakini baada ya kutulia sana,akagundua kwamba gari hilo halikuwa la wanausalama.Hata hivyo,hakutaka kujionesha,akampigia simu Daphine na kumwambia azunguke nyuma ya kibanda cha simu.

“Ndio upo huko?”

Daphine akauliza.

“Ndio,usikate simu”

Daphine,akawa ametulia anashangaa huku na kule.Kitendo cha kufumba na kufumbua akavutwa kwa nguvu kwa nyuma, mpaka kwenye miti mingi na kuzibwa mdomo,alivyotaka kurusha kifuti kikazuiwa,akageuzwa kwa kasi.Hapohapo akashusha pumzi baada ya kugundua ni mwanaume wa shoka,NGESA!

“Subiri”

Ngesa akasema huku akitizama pembeni ili kuangalia kama kuna watu walikuwa nyuma ya Daphine,wanamfuatilia.

“Vipi?”

“Naangalia usalama”

“Nishamalizana nao”

“Kivipi?”

“Hakuna anayenifuatailia”

“Una uhakia?”

“Niamini Ngesa,kwanini umeniita?”

“Twende”

Ngesa,hakutaka kujibu maswali mengi sana.Wakaingia katikati ya miti wakazidi kutembea, ambapo huko kulikuwa na barabara kubwa ya vumbi,wakasogea mbele kidogo wakakutana na gari.

Wote wakaingia,safari ikaanza mara moja, bila Daphine kujua ni wapi wanaenda,lakini alihisi ni lazima kuna jambo zito walitakiwa kulifanya.

Alichokifanya Ngesa ni kupiga simu na kuiweka sikioni.

“Tayari nipo naye….Wapi?Majumba sita?Napafahamu,makaburi yapi?Pale darajani.Sawa,nimekuelewa,nitakujulisha”

Hayo ndiyo maneno aliyokuwa anayasikia Daphine kipindi Ngesa anazungumza na simu,hakuelewa upande wa pili ni nani anazungumza,lakini baadaye alivyohoji akashangaa kwamba simu hiyo ilikuwa ya Raisi Leslie.

“Rais Leslie?!”

Daphine akauliza kwa mshangao wa waziwazi.

“Ndio,Rais Leslie”

“Kuna nini Ngesa?Mbona sielewi”

“Tunatakiwa kwenda Uganda,mimi nawewe”

Taratibu Ngesa,akaanza kumuhadithia kila kilichotokea mpaka alivyopigiwa simu na Rais Leslie,kwamba anatakiwa kuuwawa.Hivyo maelezo aliyopewa ni kwamba aende nchini Uganda kufanya ukombozi.

“Nisingeweza kwenda mwenyewe,nikakuchangua wewe”

“Kwanini mimi?”

“Ninakuamini sana”

Hapo Daphine alitabasamu kidogo na kumtizama Ngesa aliyekua makini kashika usukani,anaangalia mbele.

Safari yao ilikomea,maeneo ya Majumba sita,wakaacha barabara ya lami na kukunja kwenye vumbi, hapo walivuka kwenye daraja na mbele kuanzia hapo,yalionekana makaburi.Hapo ndipo Ngesa alipoanza kuangalia kwa makini huku akipunguza mwendo,akasimamisha gari kabisa.

“Natafuta msalaba ulioandikwa Mack Tarimo,pita kwa kule tafuta”

Bado Daphine hakuelewa ni kwanini wanatafuta jina hilo kwenye kaburi,wa kwanza kuliona jina hilo alikuwa ni Ngesa mwenyewe,akasogea karibu kabisa.

“Kuna nini kwenye jina hilo?”

Ngesa hakujibu badala yake,akawa anatizama huku na kule.Akainama kidogo na kugusa udongo!

“Inatakiwa tuchimbe hapa”

“Kuna nini?”

Bila kujibu chochote,Ngesa akaanza kutafuta huku na kule ambapo pembeni yake kulikuwa na mti mzito,akaanza kuchimba kaburi hilo, ambalo kwa juu lilikuwa na udongo.Baada ya kuchimba sana wakakumbana na kitu kizito, mithili ya ubao,wakafungua.Kila mtu alipigwa na butwaa baada ya kuona kuna ngazi kwa chini.

“Ngesa….”

“Nifuate”

Wakatizama huku na kule na kuanza kushuka ngazi taratibu ndani ya andaki,chini pembeni kulikuwa na swichi wakawasha.Kitendo cha mwanga kumulika walichokiona,kiliwafanya washangae zaidi.

Kulikuwa na kila aina ya silaha eneo hilo zima.

“Rais Leslie,amenituma nije huku kuchukua silaha”

“Kwanini azifiche huku?”

“Mimi sielewi”

Kilichotokea baada ya hapo ni kila mtu kuchukua begi lake na kuanza kupakia silaha inayomfaa,wakijua kwamba wanapoenda kulikuwa na vita kali sana!

“Shika hii”

Daphine akapewa kisu kirefu akakipachika kwenye kiatu,akachukuwa bastola ndogo akaiweka kiunoni.Akawa anapakia silaha nyingine kwenye begi kama mtu anayepanga nguo mpya, ndani ya begi!

“Tunatakiwa kuondoka,inabidi tufike Uganda leo usiku”

“Tutaondoka na usafiri gani?”

“Helkopta”

“Tutatoa wapi?”

“Ipo maeneo ya karibu na hapa”

Kila kitu kwa Daphine kilikuwa kipya lakini kwa Ngesa yeye alikuwa mwenye maelekezo yote kwamba baada ya hapo,wataingia katikati ya msitu kuna helkopta imefichwa,licha ya hayo yote aliwaza sana ni kwanini Rais Leslie ameficha nyaraka hizo za serikali,walivyomaliza kila kitu wakafunga na kuanza kutembea kuelekea katikati ya miti,ambapo huko waliingia kwenye kinyumba kidogo ambacho nyuma yake kilikuwa na kitu kama kichuguu,kumbe ndani kuna helkopta imefichwa na majani,wakatoa majani hayo na kuingia ndani ya Helkopta,kwa Ngesa kuendesha Helkopta haikuwa kazi ngumu sana!


****

Bado haikumuingia akilini hata kidogo kwamba Ngesa simu yake ilivyochunguzwa mara ya mwisho ilionesha alizungumza na mtu,siku tatu nyuma.Wakati akiwa naye ndani ya gari kuna mtu alisikia anaongea naye akisema kwamba amekosea namba baada ya hapo,akakabwa na kupoteza fahamu.Akaunganisha tukio la simu na kukabwa ghafla, akajua ni lazima kuna kitu kisichokuwa cha kawaida

“Haiwezekani”

Jenipha alijisemea mwenyewe na kuchukua simu yake ili kuangalia namba ya Ngesa,akagundua kwamba niya mtandao wa Emmacom,inayomilikiwa na wahindi ambapo makao makuu yake yapo Kinondoni Moroco,hapohapo bila kupoteza muda akageuza gari na kutaka kuelekea huko.

Akiamini ni lazima kuna mchezo umechezwa,hilo alikuwa mwenye uhakika nalo kwa asilimia zote mia moja!Alichokifanya baada ya kufika hapo ni kumuulizia mkuu wa idara nzima ya mawasiliano.

“Ametoka kidogo”

“Naweza nikamsubiri?”

“Ndio”

“Ahsante”

Jenipha,akakaa kwenye moja ya viti vya wageni,dakika kumi na tano baadaye akaitwa na kuambiwa apite ofisini.Ambapo huko alikutana na mwanamama mnene kiasi,mwenye rangi ya maji ya kunde yupo nyuma ya kiti cha kuzunguka.

“Naitwa Jenipha”

“Karibu”

Mwanamama huyo alisema huku akitizama kompyuta yake.

“Nimetokea usalama wa taifa,kuna mambo nahitaji kufahamu”

“Mambo gani?Pia naomba kitambulisho chako”

Hapo Jenipha,akababaika kidogo.Ukaibuka mgogoro mkubwa mwanamama huyo,akagoma kutoa ushirikiano na siri za mteja,Jenipha akasimama na kuondoka zake bila kubishana naye.


*****

Elizabeth Mrosso kama jina lake lilivyo,alikuwa ndani ya gari lake siku hiyo anarudi nyumbani kwake Madale , baada ya kutoka kazini,alikuwa ni mwanamke mtaratibu na mchaMungu ndiyo maana kwenye gari lake aliweka nyimbo ya Boni Mwaitege unaoitwa Mama ni Mama,alivyofika maeneo ya Tegeta ili akunje kona, akasimama baada ya kuona kuna gari,linamuwashia taa kwa nyuma,akatizama kupitia vioo vya nje.

Alivyoona limempita,akaendelea na safari yake,alivyoingia barabara nyingine ndogo,gari moja aina ya Vitara.Ikampita na kusimama mbele yake ghafla,hiyo ikamlazimu afunge breki kali,kitendo cha kufumba na kufumbua,kioo chake kikawa kimepasuliwa.

“Kaa pembeni,fanya haraka”

Sura ya mwanamke huyo haikuwa ngeni kwake,alitoka kuiona mchana wa siku hiyo ofisini kwake.Kwa uwoga na hofu,akasogea kiti cha pembeni Jenipha akaingia na kulitoa gari kwa kasi,sio kwamba watu hawakuona mchezo huo lakini waliogopa.

“Kaaa kimya,usiponipa ushirikiano.Nitakuuwa”

Jenipha alizungumza kwa mkwara mzito,japokuwa hakuwa na silaha yoyote ile isipokuwa kisu kirefu chenye makali kotekote!Gari,likazidi kwenda kwa kasi mpaka walivyofika Intachiki hapo walikunja kushoto na kunyoosha barabara ya vumbi,gari likasimama nje ya nyumba ndogo iliyojengwa na matofali ya kuchoma,ilielekea kwa Jenipha hakuwa mgeni na eneo hilo.

“Teremka na laptop yako,fanya haraka”

Elizabeth Mrosso,akiwa anasali sala ya Baba yetu, akateremka na kusukumizwa mpaka ndani,ambapo huko alikumbana na kiti kidogo ambapo juu kulikuwa na taa moja,pembeni kulikuwa na karai kubwa lenye maji.

“Sina muda wa kupoteza,nachotaka kujua hii namba ilizungumza na nani mara ya mwisho”

Jenipha alisema huku akitoa namba za simu,ambapo mwanamke huyo alitingisha kichwa kumaanisha hajui.

“Hujui?”

“Siwezi kujua labda ofisini,naapa katika Jina la Yesu”

“Usinitanie,piga simu ofisini kwako.Fanya haraka!”

Haikua lazima sana kupiga simu ofisini lakini alisema hivyo ili apoteze muda,alivyoanza kubabaika Jenipha akamvuta na kukishika kichwa chake vizuri, akakitumbukiza ndani ya maji kwa sekunde tano nzima kisha kumuibua.

“Usinipotzee muda”

“Mimi sijui Eh Yesu ni…”

Kabla ya kumaliza sentensi yake,kichwa chake kikaingizwa tena ndani ya maji,akaanza kukosa hewa na kutapatapa.Akaibuliwa kwa mara nyingine akiwa anahema juu juu.Kuendelea kubaki kimya, ilimaanisha zoezi hilo lisingekoma,ndiyo maana akaichukua namba hiyo na kuiingiza kwenye laptop yake,akiwa mwenye hofu sana akimtizama Jenipha.

“Nili..pigiwa simu kutoka iku..lu”

“Na nani?”

“Rais Leslie,akaniambia nifute mazungumzo yake na Ngesa”

“Unanidanganya”

“Sina sababu ya kukudanganya,mimi ni mtumishi wa Mungu”

“Ulifuta?”

“Ndio lakini nilichukuwa nikahifadhi kwenye email”

Elizabeth Mrosso,hakuwa na kingine zaidi ya kuongea ukweli licha ya kwamba alikuwa na wasiwasi kwani Rais Leslie,alimtishia maisha endapo angevujisha siri hiyo nzito.

Sauti ikawekwa na maongezi yote ya Ngesa pamoja Rais Leslie, yakaanza kusikilizwa na Jenipha.

“Yes”

“Wanaenda kukuteka ili wakupeleke Uganda wakuuwe,fanya juu chini utoroke.Nenda popote pale salama kisha nipigie simu.Usimwambie mtu kama tuliwasiliana”

“Mzee naona kama umekosea namba,mimi sio Juma…”

Sauti hizo zilimfanya Jenipha ashushe pumzi ya kuchoka,akazidi kusikiliza mipango mingine waliyopanga, mpaka mikakati ya kuondoka na helkopta.

“Nisikilize,usimwambie Rais Leslie kama umeniambia chochote kwa usalama wako”

“Ndio nimekuelewa”

Hapohapo Jenipha,akachomoka ili awahi makaburini,aizuie safari ya Ngesa akiwa na Daphine.

Kitendo cha kuingia ndani ya gari na kukaa nyuma ya usukani,kilimfanya apate wazo la kumtafuta ,Mkurugenzi wa Usalama wa taifa ampe habari hizo,lakini matokeo yake simu iliita bila kupokelewa,hapohapo akapiga gia na kulitoa gari kwa kasi ya risasi,huko nyuma akiacha vumbi jingi.Hakuwa ana uhakika kama angemuwahi Ngesa ama angekuwa tayari ameruka na Helkopta.Spidi ya gari la Jenipha ilitisha,hiyo ilimlazimu atanue na kupita pembeni,akiwa katika mwendo kasi wa ajabu.

“Piii piiiiiii”

Mara kadhaa alipiga honi mfululizo ili watu wampishe,kila aliyeliona gari hilo alishtuka.


*****

“Vipi?”

“Sielewi kwanini haichanganyi”

“Ebu ngoja nishuke,nicheki kwenye mota”

Alikuwa kila akijaribu kubonyeza na kuweka mambo sawa ili Helkopta iruke,iligoma hiyo ikamfanya Daphine ashuke ili kuangalia tatizo,kukaa sana nchini Urusi kulimfanya awe mtundu kidogo.Ndiyo maana akashuka na kusogea mpaka kwenye mtambo wa kuzungusha pangaboi na kuanza kuangalia vizuri.Ngesa alikuwa ndani,anazidi kujaribu lakini ghafla katika hali asioitarajia mlango wa helkopta ukafunguliwa,mbele yake akamuona Jenipha ameshika bastola.

“Ngesa shuka,fanya haraka”

Bumbuazi alilopigwa Ngesa,halikuwa na kipimo chake.Kwanza hakuelewa Jenipha alipajuaje hapo,ghafla akapata jibu wenda alimfuatilia Daphine.

“Ngesa,shuka teremka.Nitakupiga risasi”

Akili ya Ngesa,ikafanya kazi kwa kasi ya umeme,ikawa ipo kazini anajaribu kutoa na kujumlisha ili ajinasue.

“Na usijaribu kufanya kitu chochote cha kipumbavu,shuka haraka weka mikono juu..Kacha kacha”

Jenipha akakoki bastola na kumuonya Ngesa kwani aliuelewa mziki wa mwanamme huyo akiachiwa nafasi vurugu zake,ndiyo maana akarudi nyuma huku akiwa makini naye.Ngesa hakuwa na ujanja,akateremka kutoka kwenye Helkopta mikono yake ikiwa hewani kumaanisha kasalimu amri,jambo la Jenipha kufanya hivyo lilimkera kwani ilikuwa ni kama upotevu wa muda kwake na muda mfupi, alitakiwa kuwa nchini Uganda.

“Daphine yuko wapi?”

“Sijui”

Hakuelewa kwamba Daphine,alikuwa yupo nyuma ya Helkopta.Anavuta mtungi wa kuzimia moto uliokuwa pembeni ya Helkopta, yaani ‘fire extinguisher’ akaushika vizuri.Sio kwamba alishindwa kutumia bastola lakini hakutaka kufanya hivyo sababu ingetoa mlio mkubwa na kuleta taharuki eneo hilo,kwahiyo alitaka kufanya jambo hilo kimyakimya,akasogea taratibu akiwa na mtungi huo mkononi.Akajiweka sawa,akaunyanyua juu na kumpiga nao Jennipha kichwani,hapohapo adandoka puu kama mzigo na kupoteza fahamu.Kwa haraka,akamsogelea na kuokota bastola yake.

“Huyu kahaba,kajuaje tupo hapa?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ngesa.

“Sijui,acha nimmalize kwa risasi”

Daphine akajibu huku akimuelekezea bastola,Jenipha aliyekuwa chini amezirai.




Ni masaa machache ndiyo yalibaki ili wasafiri na kuwasili nchini Uganda,kuwaokoa wanafunzi wa vyuo vikuu waliowekwa mateka chini ya operesheni ya kigaidi, inayoongozwa na Aron Karanje,mtoto wa gaidi huyu hakutaka kitu kingine zaidi ya baba yake aachiwe huru na jeshi la Tanzania akiwepo na Ngesa,usongo aliokuwa nao juu ya Ngesa, ulikuwa hauna kipimo kwani kifo alichopanga kumuua alitaka kizungumziwe na ulimwengu mzima.

Masaa hayo machache yanatumiwa vizuri na Ngesa akishirikiana na mwanamke jasiri Daphine, wanapanga kuondoka na Helkopta lakini wakiwa katikati ya harakati za kuondoka kidudu mtu Jenipha, anaingilia operesheni hiyo lakini anathibitiwa vilivyo,Daphine alikuwa mwenye hasira kashika bastola yake mkononi Jenipha yupo chini kapoteza fahamu kabisa,niya na lengo lake lilikuwa ni kumpiga risasi amuuwe lakini Ngesa anamzuia.

“Atatusaidia baadaye,twende naye”

“Ngesa kwanini?”

“Nina maana yangu”

“Okay”

Hakukuwa na kipingamizi,alichokifanya Daphine ni kutizama pande zote kama kuna mtu mwingine anakuja,akaiweka bastola yake kiunoni,wakasaidiana na Ngesa kumbeba Jenipha na kumpakia ndani ya Helkopta,hapo walimfunga kamba mikononi,wakaingia ndani ya helkopta na kuvaa ‘headphone’ kubwa,wakafanana na ma dj wa club. Hiyo ilikuwa ni maalum kwa ajili ya kusikilizana.Alichokifanya Ngesa ni kubonyeza bonyeza mitambo,taa za kwenye kioo zikatoa mwanga kuashiria kwamba helkopta imewaka,akavuta kitu kama ‘switch’ ikaanza kuunguruma na mapanga boi yakaanza kuzunguka,ilivyochanganya akashika kitu kama kirungu na kuanza kukizungusha.Taratibu helkopta ikaanza kupaa angani,wakaanza kuiacha ardhi,wakazidi kupaaa juu zaidi.

“Tunatakiwa kuingia,usiku huuhuu”

Ngesa akavunja ukimya na kilichokuwa kinasikika hapo, ulikuwa ni muungurumo wa injini ya Helkopta,chini kulikuwa na mataa ya jiji, yamewaka kumaanisha kwamba jioni tayari imeshafika.

“Tutatua wapi?”

“Mtukula,pale tutachukuwa gari”

“Kwanini tusitue Kampala kabisa?”

“Kule ni karibu,watajua.Inabidi tuingie kimyakimya”

Kilichowasaidia kusikilizana ilikuwa ni mitambo maalum waliyoweka masikioni,ndani ya masaa matatu Ngesa akatizama chini na kuangalia kwenye kioo maalum,alivyoangalia ramani akagundua kwamba wamefika tayari mpaka unaotenganisha Tanzania na Uganda,kupitia Bukoba yaani Mtukula.Ngesa aliwaza vitu chungu mzima ndani ya kichwa chake,hususani vita aliyokuwa anaenda kupambana nayo!Hakutaka kumuangusha Rais Leslie,ambaye alitokea kumuamini hata hivyo mapigo yake ya moyo yalimdunda sababu hakuwa ana uhakika kama angeshinda vita hiyo,machozi ya hasira yakamlenga baada ya kumkumbuka Brigedia Karanje na unyama wote aliofanya.

“Tunatua hapa”

Akasema na kumuangalia Daphine ambaye baada ya kusikia hivyo akageuka nyuma na kubeba begi lililokuwa na silaha za kazi,akaliweka vizuri mgongoni na Helkopta ikaanza kutua taratibu.Kwa kuwa Helkopta ilikuwa inatua sehemu yenye mchanga hiyo ikafanya vumbi jingi litimke.

“Tuku tuku tuku tuku tuku”

Mapanga boi yaliyokuwa yanazunguka yalifanya majani yaruke juu na vumbi litimke,mpaka machuma yalivyotua aradhini.Wa kwanza kushuka alikuwa Ngesa akainama kidogo na kumfungulia mlango Daphine, wote wakashuka.

“Nisubiri”

Giza lilikuwa totoro,lililosababishwa na miti mingi sababu walitua katikati ya msitu,hiyo ikamfanya Ngesa atembee taratibu mpaka kwenye barabara ya vumbi iliyochongwa,ambapo hapo ilionekana magari hupita.Akatizama huku na kule,kwa mbali akaanza kusikia muungurumo wa gari,akarudi nyuma na kujificha kando ya mti mkubwa wa mbuyu,taa za gari zikawa zinamulika baada ya kufika alipo,akajitokeza mbele na kutoa bastola.

“Toka nje ya gari sasa hivi”

Ngesa alizungumza kwa ukali,mzee wa makamo mweusi aliyekuwa nyuma ya usukani, aliogopa! Taratibu akafungua mlango.

“Don’t kill me”(Usiniue)

Mzee hakuelewa Ngesa anazungumza nini,japokuwa alielewa lugha hiyo niya Kiswahili,mikono akaiweka hewani,anatetemeka!Alichokifanya Ngesa ni kumvuta akachukua begi lake dogo kutoka mgongoni na kutoa kamba ya Manila,akamfunga mikono na miguu kisha kumuweka katikati ya msitu huo,akapita mbele ya gari ambayo ilikuwa bado inawaka taa inaunguruma,akavuka upande wa pili na kuanza kukimbia,huko akamueleza Daphine kila kitu,wakamchukua Jenipha pia ambaye tayari alikuwa amezinduka.

“Tupo wapi?”

Jenipha,akauliza mikono yake ikiwa imefungwa kwa mbele,hakukuwa na mtu wa kumjibu.Wakamsukuma mpaka walipotokea, lilipokuwa gari.

“Ingia Daphine,fanya haraka”

Hata kabla Daphine hajafunga mlango,tayari Ngesa alipiga gia na kulirudisha nyuma kwa kasi,akaliweka sawa na kukanyaga mafuta mengi hiyo ikafanya tairi zizunguke na kutifua mchanga,hapo Ngesa alishikilia usukani kwa mikono miwili, akiwa makini macho yake yapo mbele,anafikiria kuingia jijini Kampala usiku huohuo,hakuwa ana uhakika kama angefanikiwa sababu kulikuwa na umbali mrefu sana.Mbaya zaidi gari aliyokuwa anatumia hakuwa ana uhakika nayo kama ingefua dafu,kutoka msitu waliokuwepo mpaka kuikamata lami iliwachukuwa masaa mawili,ndipo wakakumbana na Lami,hapo Ngesa alikunja kushoto na kuingia kwenye barabara kubwa,mwendo kasi ulikuwa ni uleule.

Nchi ya Uganda,haikuwa ngeni kwake ndiyo maana kutokea Mtukula mpaka Jijini Kampala,aliamini angefika.

“Ushawahi kufika Uganda?”

Daphine alivunja ukimya,akiwa kushoto baada ya kumuona Ngesa yupo bize na usukani alifanya hivyo makusudi ili wapige stori mbalimbali na Ngesa asiboreke.

“Yes,nishawahi kufika.Wewe hapo,ulinifanya nifike huku”

Ngesa akajibu na kumtizama Daphine,akarudisha macho yake mbele.

“Mimi?Kivipi?”

Swali hilo lilihitaji majibu marefu,hiyo ikamfanya Ngesa ashushe pumzi ndefu za kuchoka!Akamuangalia Daphine na kuanza kumsimulia tangia akiwa mtoto mchanga,kundi la brigedia Karanje lilivyouwa wazazi wake,Morogoro mbuga za Mikumi.Hakuishia hapo,akaenda mbali zaidi mpaka alivyomchukua Daphine na kumkabidhi Kwa Hans kuanzia hapo,jeshi la Karanje likamteka kwa miaka mitatu akila mateso ya kila aina kisha wakamtupa Uganda,ndani ya msitu wa mabila ambapo aliokotwa na wanakijiji wakamtibu.

Ilikuwa ni historia ya kusisimua iliyomfanya Daphine alengwe na machozi,akashindwa kuvumilia na kujikuta analia kabisa.

“Hapo ndipo ugomvi wangu na Karanje ulipoanza.Tukaanza kuwindana,alipogundua nipo hai,akaanza kuniwinda upya”

Jenipha alisikia kila kitu,historia hiyo ilimfanya agundue kitu fulani ambacho hakuwahi kukijua katika maisha yake.

“Ilikuwaje ukawa naye?Ulimfahamu vipi Karanje?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ngesa,ikawa zamu ya Daphine kuhadithia kilichotokea mpaka kukutana na Brigedia Karanje,namna alivyochukuliwa na Vital Kamere,akamuunganisha na Brigedia Karanje!Akafafanua jinsi alivyokuwa akiongoza darasani, akashika namba moja kwenye mtihani wa taifa na kutingisha jiji la Dar es salaam,hakusahau kuhadithia alivyokuwa nchini Urusi na kupewa mafunzo ya kijasusi.

“Nilikuwa nakuchukia sana Ngesa,nilitumwa nikuuwe.Naomba unisamehee kwa kumpiga risasi mkeo Jaqlin Mfinanga”

“Sio kosa lako,hukua unajua”

“Nisamehee sana,sikujua kama bila wewe ningeishi”

Jenipha aliyekuwa nyuma amefungwa kamba,alisikia kila kitu.Mambo aliyokuwa anayasikia yalikuwa ni kama hadithi vile kumbe ni kweli,hakutaka kuamini kama watu hao wawili walipitia mikasa ya kusisimua namna hiyo!

“Ukimpata Karanje,utamfanya nini?

Daphine akauliza huku akifuta machozi akitumia kiganja chake.Swali hilo lilimfanya Ngesa, atabasamu kwa hasira.

“Mungu,ndio anajua”

Kasi ya gari aliyokuwa anatumia Ngesa ilikuwa ni kilomita moja kwa dakika,haukuwa mwendo wa kawaida.Mpaka wanaingia Kijiji cha Chotera walikuwa tayari wamekata masaa matano,hiyo ilimaanisha bado masaa mawili waingie jiji la Kampala.Bado walikuwa na safari ndefu!

“Mafuta,yanatosha?”

Daphine akahoji.

“Yes,yapo”

Wakazidi kuchanja mbuga!

“Wangapi,wanajua kama tupo Uganda?”

Ngesa akavunja ukimya,haikueleweka swali hilo limemlenga nani, sababu aliuliza huku macho yake yapo mbele anaendesha gari.

“Jenipha,nani anajua tupo Uganda?Umejuaje?Nani kakwambia?”

Namna alivyouliza ilielekea kabisa alikuwa ni mwenye hasira za mkizi.Swali hilo lilimfanya Jenipha,atafakari kidogo bila kutoa kujibu.

“Sijui”

“Nakuuliza kwa mara nyingine,nani anajua tupo Uganda?Umejuaje?”

“Sijuii”

Kitendo cha kujibu sentensi hiyo,ilimfanya Ngesa apatwe na ghadhabu kwa kasi ya umeme,akapiga breki ya ghafla akakanyaga mafuta na kuingiza gari katikati ya kichochoro kilichokuwa na mitimiti kiasi,akashuka bila kuzima gari, kwa kasi mpaka mlango wa nyuma,akaufungua na kumvuta Jenipha kwa nguvu,bila kusema chochote akamuweka sawa na kumkaba shingoni akitumia mkono mmoja,mgongo wa Jenipha ukawa umeegemea gari,hawezi kufanya chochote kwani mikono yake imefungwa na kamba.

“Nani anajua?”

“Ng..esa sijui kitu”

Alijibu kwa tabu,roba alilopigwa halikuwa la kawaida, hiyo ilimfanya ashindwe kutoa sauti,Ngesa akazidi kumkandamiza!

“Nani anajua?”

“Mimi mwe..nyewe”

“Unanidanganya,umejuaje?”

Roba liliendelea kupigwa,Jenipha akaanza kuishiwa pumzi kwani mishipa yake ya shingo ilishikwa vizuri akawa anaumia,hapo Ngesa akamuachia ili avute pumzi nyingine alivyotaka kumkaba tena!Akakiri kwamba anasema kile anachokijua,hakuwa na sababu ya kuficha chochote kwani mateso yasingefika kikomo, akazungumza kila kitu kilichotokea, tangu alivyomfuata Mwanamke wa mtandao wa simu.

“Unanidanganya,Nurdin hajui?”

Hapo Ngesa alitoa bastola na kumuekea kichwani,namna alivyokunja sura yake kulikuwa kuna kila dalili ya kufyatua risasi na kumuua siku hiyo.

“Kweli Ngesa,sikudanganyi”

“Ingia ndani ya gari”

Halikuwa ombi bali ni amri,akamsukuma na kumpakia ndani ya gari kisha kurudi nyuma ya usukani,hapo hawakusimama tena mpaka walipoingia Mbarara,wakanyoosha moja kwa moja!

Waliwasili Jijini Kampala saa saba ya Usiku,wakapaki gari katikati ya Jiji hilo maeneo ya Bweyogerere.Hapo Ngesa akatoa begi na kuchukua vidude vidogo vilivyofanana na tunda za ubuyu,kimoja akaingiza sikioni kimoja akampa Daphine,nayeye akaweka sikioni.

“Unasikia hapo,testing one two”

Vilikuwa ni vidude maalum kwa ajili ya mawasiliano ambapo mtu yoyote Yule asingeweza kugundua hata kidogo,baada ya kujaribu kila kitu.Ikabaki kazi ya kuchagua silaha.Kila mtu akachukua silaha yake inayomfaa.

“Upo tayari?”

Ngesa akamuhoji Daphine.

“Ndio”

Hapohapo gari likawashwa safari ya kuelekea Galaxy Club ikaanza,kwa tabu na kuulizia ulizia wakafanikiwa kufika lakini walisimama umbali wa mita mia mbili,alichokifanya Ngesa ni kutoa darubini na kuangalia.

“Shiit”

“Nini?”

“Aroon”

“Ni nani?”

Hapo Daphine nayeye akachukua Darubini na kuanza kuangalia,ambapo aliona ndani wanaume wameshika mitutu wengine wapo nje wanalinda haikuwa rahisi kuingia ilikuwa ni lazima waingie kwa mbinu ya kimafia!

“Mtoto wa Karanje”

Haikua kazi ndogo kama walivyofikiria kwani watu hao waliweka walinzi kila mahali,hapo Ngesa akashuka ndani ya gari na kumtaka Daphine apitie upande wa pili.

“Nikikwambia uje,unakuja”

“Sawa”

Ngesa akaanza kutembea taratibu kwa tahadhari kubwa,alivyofika nyuma ya nguzo kubwa akavisha bastola yake kiwambo cha kuzuia bastola isitoe sauti,alivyohakikisha zoezi hilo tayari,akaweka bastola kiunoni na kuchomoa kisu kirefu.Mlinzi mmoja,aliyekuwa anavuta sigara yupo nje ndiye angekuwa wa kwanza kutokana na hesabu zake,akamnyemelea taratibu,akampiga roba kwa nyuma kabla mlinzi huyo hajafanya chochote,akamchoma kisu shingoni.Damu zikaruka kama chemchem ya maji,akamvuta pembeni taratibu na kumuweka kandokando ya jaba la uchafu.

“Njooo,upande wa kushoto.Kupo sawa”

Alivyozungumza hivyo tu,Daphine akaanza kutembea taratibu mpaka alivyomfikia!

“Mimi napita huku,wewe zunguka kule!Tutakutana mlango wa nyuma”

Yalikuwa ni maagizo kutoka kwa Ngesa,akimwambia Daphine kumaanisha kwamba wanatakiwa waingie ndani ili kumaliza operesheni hiyo waliyoagizwa na Rais kuwakomboa Wanafunzi,siku hiyo wakawa kama makomandoo,jinsi walivyojipanga!




Jengo la Galaxy club lilikuwa kubwa lenye gorofa mbili kwenda juu na lenye upana mrefu,hiyo ilimaanisha walitakiwa kuwa makini kuliko kawaida,ndiyo maana Daphine alikuwa makini kabla ya kuingia akitumia mlango wa nyuma, ambao ulikuwa umefungwa,alivyochungulia akamuona Mwanamme mweusi tii kashika mtutu yupo kwa ndani,hiyo ilimaanisha analinda usalama na kuingia kichwakichwa kulimaanisha operesheni hiyo kufeli.

Alichokifanya ni kuvuka mlango na kutizama juu, ambapo aliona ‘pipe’ kubwa akaitizama vizuri na kugundua imekwenda mpaka gorofa ya juu,kwa kuwa alikuwa ameshika bastola mkononi, asingeweza kupanda,alichokifanya ni kutizama huku na kule kisha kuipachika kiunoni,akashika vizuri ‘pipe’ hiyo ya chuma huku miguu yake akiitanuna huku na kule ili akanyage ukuta apate muhimili wa kupanda juu zaidi,hilo likafanikiwa, taratibu akaanza kujivuta kwenda juu,haikuwa kazi rahisi ilihitaji umakini wa hali ya juu sana.

Alivyofika kwa juu akashika kibambazi cha ukuta,usawa wa dirisha na kuchungulia, hapo alimuona jambazi mwingine amesimama amempa mgongo,akajivuta tararibu na kujibanza kwa pembeni,akitafakari aingie vipi kupitia dirisha hilo kubwa la kioo.Waliokuwa wanafanya operesheni hiyo ya kuwakomboa wanafunzi walikuwa makini mno,hata Ngesa akajiongeza na kuzunguka upande wa mbele,ambapo hapo alipata nafasi ya kuwaona wanafunzi wamelala kifudifudi,majambazi walikuwa sita wamewazingira,haikuwa kazi rahisi hata kidogo kumaanisha kwamba akibugi stepu kila kitu kitakuwa bure kwani angeuwawa hivyo ilibidi asifanye uzembe wa aina yoyote ile!

Akiwa anaangalia na kufikiria namna ya kuingia, akaliona geti dogo kwa pembeni hakuwa anaelewa angeingia humo angetokea wapi lakini alijua ni lazima lingempa mwanya wa kuzama ndani kirahisi kifupi alikuwa kama ana bahatisha,hapohapo akashika bastola vizuri na kuanza kutembea kwa tahadhali akiangalia nyuma na mbele!Akafika mpaka kwenye geti fupi la chuma,akapanda taratibu na kuingia kwa ndani ambapo huko alikutana na ukuta mrefu na mgumu,pembeni kuna mlango una kufuli nje kubwa.

“Daphine,ushaingia?”

Ngesa akauliza,kidude maalum kilichokuwa ndani ya sikio lake kwa ajili ya mawasiliano kilifanya Daphine asikie.

“Bado,ndio naingia niko juu wewe uko wapi?”

“Chini huku”

“Okay,take care”

Ngesa hakujibu,akalitizama kufuli na kuvuta begi dogo lililokuwa mgongoni kwake,akatoa kitu kama kibomba cha chuma,hiyo ilikuwa kwa ajili ya kuzuia mlio wa bastola.Akavisha mbele ya bastola yake taratibu!

“Pyuuu”

Kilichosikika hapo kilikuwa ni kama mtoto mchanga kakohoa,risasi moja tu kufuli likadondoka chini.Kwa tahadhali kubwa Ngesa akashika kitasa taratibu akaanza kufungua mlango, ulipiga kelele kiasi lakini alijitahidi sana kuusukuma taratibu.Hatimaye,akafanikiwa kuingia ndani.

“Nipo ndani,Daphine”

“Good,mimi ndio naingia”

Kitendo cha kufunga mlango taratibu mbele yake alimuona mwanamme mrefu,amejazia misuli anavuta sigara.

Bahati nzuri ilikuwa kwake alikuwa anazungumza na simu, hiyo ilimfanya amnyatie taratibu,akaweka bastola kiuoni na kuchomoa kisu kirefu kilichokuwa nyuma ya kiuno chake,akamsogelea karibu zaidi.Akamvuta kwa kasi na kutaka kumchoma shingoni lakini zoezi hilo likaonekana gumu sababu jamaa huyo,alijihami na kurudi nyuma kidogo kisu kikapita pembeni.Alivyokaa sawa akashika bastola kwa niya ya kumfyatua Ngesa lakini hata yeye alishindwa sababu mkono wake ulipigwa teke bastola yake ikadondoka chini,wote wakakunja ngumi yaani ‘Man to Man’Urefu wa futi nyingi wa jamaa huyo ulimfanya Ngesa ashindwe kumsoma vizuri,ndiyo maana alipokea ngumi ya kwanza ya uso iliyokuwa nzito.

Akashikwa shingoni na kubebwa juujuu kama mtoto,akatupwa chini kama mzigo!Alivyotaka kusimama ili apambane alishindwa sababu alipigwa shuti kali la tumbo kama mpira,mpaka akahisi anataka kutapika nyongo, Ngesa akahisi maumivu makali!Alichokosea jamaa huyo ni kuokota simu yake ili awataarifu wenzake,hapo ndipo Ngesa akapata Mwanya wa kutoa bastola yake kwa kasi kiuoni.

“Pyuuu pyuuu pyuuu pyuuu pyuuuuu”

Akam-miminia risasi nyingi,mpaka akadondoka chini na kukata kauli.


*****

Rais Leslie alichanganyikiwa kuliko kawaida,kila kitu kwake kikawa hakifanyiki kabisa!Mambo yaliyokuwa yanatokea ndani ya nchi yake yalimfanya ashindwe kufanya kazi,akili yake ikashindwa kufikiria nje ya boxi.Akatamani hata asingekuwa na madaraka ya kuwatumikia wananchi.Mbaya zaidi alielewa baada ya kuachia kiti hiko angeshtakiwa na pengine kunyongwa kabisa.Aliyekuwa anampa faraja na matumaini ni mkewe tu,akimwambia kwamba atulize akili na kila kitu kitaenda sawa kabisa!

“Mme wangu,pumzika basi.Leo siku ya tatu hujalala”

Mke wake,alimshauri siku hiyo baada ya kuamka usiku na kumkuta Mumewe yupo kwenye sofa amekaa seblen.

“Siwezi,nitalalaje?”

“Ukipumzika,utapata akili mpya”

“Hapana,what if ndiyo watoto wetu wametekwa.Wapo ndani mule kwenye ile Club mmoja baada ya mmoja anauliwa,wewe ungelala?”

Raisi Leslie akamuuliza mkewe,tena mbaya zaidi kwa ukali kumaanisha kwamba amechukia sana.

“Hapana”

“Ndio hivi,mimi sio Rais tu ni mzazi.Nina dhamana ya Watanzania”

“Ushawasiliana na Ngesa?Keshafika?”

“Bado hajanipigia”

“Itakuaje kama nayeye ametekwa na wamemuua?”

“Namuamini”

“Mme wangu,hata kama.Inabidi uwe na plan B,vilevile”

“Una maana gani?”

“Naomba nikushauri,kwanini usiwapigie simu kule.Uwaambie wasogeze muda,maana yamebaki masaa matatu tu”

“Unadhani watakubali?”

“Bora ujaribu,kuliko kukaa kimya”

“Ni watu wenye misimamo sana”

“Tafadhali jaribu Mme wangu”

Mke wa Rais,alikuwa ni mwanamke mwenye busara sana.Hakupenda hata siku moja mumewe akose raha hata kidogo,siku zote huingilia kati wakimsema,hata iwe chama pinzani ama wanasiasa ni lazima atawaibukia na kupandisha mori, ndiyo maana swala hilo ikabidi aungane naye bega kwa bega,alichokifanya ni kutembea mpaka mezani na kuchukuwa simu ya mezani,akamletea mumewe.Alichokifanya Rais Leslie ni kumtafuta Mkurugenzi wa Usalama wa taifa Ramadhan Nurdin hewani, simu ikaita na kupokelewa.

“Habari yako”

“Nzuri Mheshimiwa Rais”

“Nahitaji uniunganishe na wale wanaharamu”

“Sasa hivi?”

“Ndio,sasa hivi”

Hiyo ilikuwa amri kutoka kwa mkuu wake wa kazi,ikimaanisha itekelezwe mara moja.Alichokifanya Mkurugenzi wa usalama wa taifa ni kuanza kutafuta namba,alivyofanikiwa akawapigia.

“Unaongea na Nurdin,Raisi ana mazungumzo nawewe al..”

“Ngesa yuko wapi?Karanje,mshamtoa?”

Kabla ya kumaliza sentensi yake jamaa huyo akauliza.

“Rais anahitaji kuzungumza nawewe”

Hapohapo,akaunganishwa kwenye laini kukawa na watu watatu hewani.

“Unaongea na Rais Leslie nin…”

“Una masaa matatu Leslie,kitakachofuata hapo.Siku nzima mtakesha kuotoka vipisi vya wanafunzi”

“Nimekubali,naomba tuzungumze kitu kimoja”

“Sema”

“Naomba uniongezee masaa mengine mawili,utapata unachokitaka”

“Listen,ile ni amri.We are not debating!Saa tatu kamili namtaka Ngesa na Karanje,Nambole Stadium!Na ukijaribu kufanya kitu chochote cha kipumbavu,sitosita kuuwa wanafunzi wote”

“Laki…”

“Rais Leslie,ngoja nikuoneshe mfano….Wewe mlete huyo,mwambie apige magotii….Paaaa paaaaaa”

Moyo wa Raisi Leslie ulipiga kwa nguvu,alisikia upande wa pli mlio wa risasi kumaanisha kwamba kuna mwanafunzi ameuliwa tayari,hapohapo simu ikakatwa.


Haukuwa utani,Ngesa alikuwa ndani alishuhudia kila kitu kwa macho yake,kupitia wavu mdogo wenye matundu madogo madogo, kabisa!Ngesa alihisi kuchanganyikiwa,roho ilimuuma ajabu.Lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kutulia kwani angekurupuka nayeye angepigwa risasi sababu alishaelewa watu hao hawakuwa na mzaha hata kidogo na kuuwa kwao lilikuwa jambo la kawaida sana,wakati mwingine alitamani kujitoa muhanga ili aokoe maisha ya wanafunzi hao waliokuwa na ndoto kubwa na wadogo kufa.Maiti ya mwanafunzi aliyepigwa risasi mbili za kichwa,aliishuhudia ikiburuzwa na mmoja wa watu, tena akiivuta mguu mmoja.


*****

Jenipha,akiwa ndani ya gari amefungwa kamba alihangaika huku na kule,mikono yake ilikuwa imefungwa kwa nyuma na imekazwa kwa nguvu,hiyo haikumaanisha akate tamaa!Alichokifanya ni kujitahidi kujiburuza na makalio,mpaka upande wa mlango.Akafungua kitasa kwa shida na kujitupa chini ardhini!Hakukuwa na mtu aliyemuona sababu gari lilipaki mafichoni,ukizingatia ulikuwa ni usiku sana!Akazunguka upande wa dereva,na kufungua mlango, hapo alichuchumaa kidogo na kuingiza mikono yake katikati ya mlango,akaanza kusugua kamba kwa nguvu.Zoezi lilikuwa gumu na aliumia na kuanza kuchunika,damu zilimtoka lakini hakujali.Akaendelea kujisugua mpaka kamba zikaachia,mkono wake ukiwa umelowa damu.

Hakutaka kupoteza muda,akaangaza huku na kule!Mbele yake,umbali kidogo akaona jengo refu limeandikwa Galaxy Club,akajua kabisa hapo ndipo Ngesa na Daphine walipo.

Hakutaka kujua kuna hatari namna gani,alichotaka yeye ni kwenda kushuhudia kinachoendelea ikiwezekana awakomboe pia wanafunzi hao,bila kuwa na silaha akatembea kwa tahadhari,kutokana na mafunzo aliyokuwa nayo,akafanikiwa kulifikia jengo hilo ki ujanja ujanja.

Akafika kwenye ukuta,akaambaa nao!Mbele yake,akaona kuna mlango upo wazi,bila kujua kwanini upo wazi.Akaingia kichwa kichwa,hapo ndipo alipokutana na njemba mbili,zimeenda hewani futi nyingi.Akawekewa bastola kichwani na kuwekwa chini ya ulinzi.

“Who the hell are you?”

Jamaa mmoja akauliza,bila kuremba anampiga na kitako cha bastola kichwani.Jenipha,akadondoka chini.

“Kacha kacha”

Bastola ikakokiwa,kwa niya ya kuuliwa.Lakini jamaa mwingine,akamzuia mwenzake asimuue, alichokifanya ni kuanza kumsachi mifukoni,walishtuka sana baada ya kukuta ana kitambulisho cha serikali ya Tanzania.

Majambazi hayo yakaogopa,wakajua ni lazima Jenipha atakuwa na wapelelezi wenzake tena kaja na mapolisi kutoka Tanzania,walichokifanya ni kumuinua haraka na kumpeleka kwa mkuu wao, Aron Karanje.

“Mungu wangu”

Ngesa hakutaka kuamini,baada ya kumuona Jenipha.Amekamatwa mbaya zaidi amepigishwa magoti, tayari kwa kupigwa risasi.

“You gona tell us what you know,Who sent you?”(Utatuambia,unachojua.Nani kakutuma)

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Mkuu msaidizi,aliyekuwa pembeni ya Aron.Huyu alikuwa na sura mbaya ya kutisha na alizungumza kwa hasira mno.Jenipha,akapigwa kelbu moja akadondoka chali na kuanza kuvuja damu puani.

“Talk to me bitch”(Ongea Malaya)

Akainuliwa na kupigishwa magoti,hakuwa tayari kuzungumza chochote lakini alielewa huko mbeleni kuna mateso makubwa,alivyoangalia pembeni na kuziona maiti akaogopa zaidi,akajua kivyovyote vile angeuwawa tu.

Kando yake kulikuwa na wanafunzi wamelala kifudifudi,wametekwa nyara!Akahisi kujuta ni kiranga gani kilimtuma aingilie operesheni hiyo,mbaya zaidi hakumuona Ngesa wala Daphine mahali hapo!Hiyo ikamchanganya zaidi na zaidi lakini alichojua yeye ni lazima wapo ndani ya jengo hilo.

“Tunachotaka kujua,upo na nani?Pengine tunaweza kukuhurumia tukakupa zawadi ya kuendelea kuishi”

Swali hilo likamfanya Jenipha,ashangae kwani Aron alitumia kiswahili fasaha kabisa.

“Upo na nani?”

Aron akauliza,hapo alisimama na kumuendea karibu zaidi.Kila kitu kilishuhudiwa na Ngesa pamoja na Daphine, kila mtu akiwa kwenye kona yake.

“Nakuuliza kwa mara nyingine,upo na nani.Unaona zile maiti?Uhai ni kitu muhimu sana kwako,tuambie tukuache huru”

“Ni kwe..li,sipo mwenyewe”

Kauli hiyo iliwafanya watu hao wamtizame na kumsikiliza kwa umakini zaidi,Ngesa na Daphine wakabaki wameduwaa.

“Upo na nani?”

“Upo na nani nakuuliza?”

“I said, i’m not alone”(Siko mwenyewe)

Jenipha,akajibu kwa hofu sana huku akiwatizama majamaa hao wenye mitutu, damu zinamchuluzika puani.



Kila kitu kilivurugika,operesheni yao iliingia dosari na Jenipha ndiye alikuwa kidudu mtu,Daphine na Ngesa walielewa nini maana ya Jenipha kujibu hayupo mwenyewe.Hiyo ilimaanisha angebinywa kidogo angeropoka kila kitu,isingekuwa na maana yoyote kwao kwani wangekuwa wamepoteza muda, kutokea nchini Tanzania mpaka Uganda,Daphine alikuwa juu nyuma ya chuma kubwa.

Isingekuwa rahisi kuonekana,yeye Ngesa alikuwa upande wa chini kushoto nyuma ya pipa,ambapo mbele yake kulikua na wavu mkubwa.Wote walimuona Jenipha,anavyohojiwa na walimsikia vizuri sana.

“Ngesa”

Daphine akaita kwa sauti ya chini.

“Yes”

“Tufanye nini?”

Daphine akauliza,ilielekea aliishiwa mawazo ndiyo maana alimuuliza Ngesa juu ya nini wafanye siku hiyo alimchukulia kama mkuu wake wa kazi.

“Subiri”

Kupitia vifaa maalum vya mawasiliano waliweza kuwasiliana na kila mtu akamsikia mwenzake,Ngesa akawa makini kabisa kutizama kinachoendelea.

“Upo na nani?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Aron Karanje,kijana mdogo ambaye miaka yake ilikuwa kati ya 28-32!Ilikuwa ni ngumu kuamini mtu kama yeye anajihusisha kwenye maswala ya kigaidi kama hayo.Alivyoona hajibiwi akamtizama mwenzake aliyekuwa pembeni mweusi,akampa ishara ya kichwa kwamba Jenipha ashughulikiwe,hapohapo akapigwa na kitako cha mtutu kichwani,akadondoka chini.

Akaongezewa tena kingine juu ya paji la usoni,damu zikaanza kumvuja sababu alipasuka vibaya sana!

“Umesema haupo mwenyewe,upo na nani?”

“Nipo na Yesu pamoja na malaika wake,wananilinda”

“Stupid”

Hapohapo akapokea kifuti!

“Kacha kacha”

Bastola ikakokiwa kwa niya ya kumuuwa,hilo halikuwa utani sababu waliokuwa mbele yake, jambo la kuuwa lilikuwa ni kawaida mno.Ngesa alihisi kuchanganyikiwa,ilikuwa ni lazima waingilie kati kabla Jenipha hajapigwa risasi, japokuwa walijua ingekuwa ambush kubwa sana.

“Daphine,upo tayari?”

“Ndio”

“Okay”

Ngesa alivyohakikisha hivyo,akatembea taratibu kwa kunyata ili atafute saiti nzuri ya kulenga shabaha,kuendelea kubaki eneo hilo ilikuwa ni sawa na upotevu wa muda,aka ambaa ambaa mpaka nyuma ya mlango hapo akachomoa ‘Magazine’ ili ahakikishe kama ina risasi,alivyoridhika akairudisha na kubana jicho huku akimlenga jamaa aliyeshika bastola, anataka kumuuwa Jenipha.

“Pyuu pyuuuu”

Zilikuwa ni risasi mbili,zilizomfikia jamaa huyo kichwani, akadondoka kama mzigo hapo ndipo Ambush na mirindimo ya risasi ilipoanza kusikika kila pembe.

“Paa paaa griiiiiii”

Milio ya risasi ilisikika ndani ya club hiyo,majambazi walipagawa na kuogopa sababu hawakuelewa ni wapi risasi zinatokea,Jenipha alivyopata mwanya akatambaa mpaka kwa jambazi aliyelala chini, akanyanyua mtutu na kuanza kuwalenga.

“Namuhitaji Aron akiwa hai,Daphine cover me”

Ngesa alizungumza kwa sauti baada ya kumuona Aron Karanje,anakimbia hiyo ilimfanya amuunganishie huku Daphine akirusha risasi,Ngesa akapita na kuingia chumba alichoingia Aron.Kitendo cha kuzama ndani, risasi zilimkosa kosa akarudi nyuma kwa kasi.

“Shit”

Ngesa akasema kwa hasira huku akiikamata bastola yake kwa mikono miwili.Alielewa kwamba angeingia ndani ya chumba hiko angemiminiwa mvua za risasi!Ndio maana akatulia na kupiga hesabu za harakaharaka!Akapata wazo kabambe na kuingiza mkono ndani ya begi, humo alitoa kitu kama kiazi,juu kina kama koki,alivyofungua ukatoka moshi mkali sana, akakirusha ndani.Nayeye akazama kwa kasi na kupitiliza mpaka kwenye kona,kilichofuata hapo ilikuwa ni milio ya risasi.

Kwa kuwa shabaha yake ilikuwa ni kumuweka Aron Karanje chini ya ulinzi,akashika bastola vizuri akabana jicho lake lakini alishindwa sababu jamaa mmoja kushoto, alisimama na mtutu akaanza kumrushia risasi hiyo ilimfanya alale chini na kuanza kutambaa chini kwa chini,alivyopata saiti nzuri,akaibuka na kumpiga risasi ya kichwa.

Jeshi la polisi la Uganda,lilikuwa tayari limefika na kuzama ndani baada ya kupokea kauli kutoka ngazi za juu.Hao ndio walitoa msaada na kuwaongezea nguvu wakina Ngesa!

“Daphine,hakikisha tunaondoka na Aron.Kabla Polisi hawajamchukua”

“Copy that”

Hiyo ilimfanya Daphine atii amri,akaruka upande wa pili kikomandoo!

“Paa paaaa”

Kwake ilikuwa risasi moja mtu chini,alikuwa makini sana!Akakumbuka mafunzo ya kijeshi alivyokuwa nchini Urusi.Akamuona Jenipha kwa mbali,amekabwa kwa nguvu anataka kuchomwa kisu cha tumbo,hakuchelewa akabana jicho lake na kumlenga gaidi huyo kichwani.Jenipha,akaokolewa!Risasi zilirushwa nyingi kiasi kwamba wanafunzi waliokuwa mateka walitandwa na hofu kubwa sana.

Wengine walipigwa risasi kutokana na kukimbia huku na kule.Ngesa alihisi kuzidiwa lakini hakukata tamaa,alichokifanya ni kutulia chini akiwa amelala.

Akahisi watu wanakuja upande wake aliolala amejificha,mbaya zaidi wote walikuwa wameshika mitutu,wawili kushoto watatu kulia.Akasikilizia na kutoa bomu aina ya Grenade,akawarushia kilichofuata hapo baada ya sekunde mbili, ulikuwa ni mlipuko mkubwa.Akatokeza na kuanza kumimina risasi nyingi,kwa kuwa niya yake ilikuwa ampate Aron hiyo ikawa rahisi sababu alimfikia na kumuwekea bastola kichwani.

“Simama”

Ilikuwa ni sentensi moja iliyomfanya Aron atokwe na jasho mwilini,hofu ilikuwa kubwa sana kwake!Alichokifanya Ngesa ni kumkamata shati kwa nyuma, akamuwekea bastola shingoni.

“Nataka tutoke nje,waaapi?”

Lilikuwa ni swali lililomfanya Aron ababaike sana,akanyoosha kidole mlango wa katikati,wakachomoka nje.Ngesa akamvuta Aron kidogo baada ya kuona askari wa kiganda wanapita,walivyoisha akatembea.Bado risasi zilisikika!

“Daphine,natoka nje.Aron ninaye narudia Aron ninaye tuondoke”

“Vipi kuhusu wanafunzi?”

“Askari washafika”

Ngesa alikuwa ana shida kubwa sana na Aron kiasi kwamba alitamani afike nchini Tanzania dakika hiyohiyo, akutane na Brigedia Karanje macho kwa macho!Alivyotoka nje,akatembea taratibu mpaka nyuma ambapo huko kulikuwa na magari,akatumia kitako cha bastola kuvunja kioo.Akapasua switch ya gari na kutoa nyaya,akazigusisha gari likawaka.

“Daphine,tuondoke”

“Nakuuja”

Kila pembe walikuwa magaidi,wanamuwinda Daphine pamoja na Jenipha ilikuwa ni ngumu kutoka nje kirahisi lakini hawakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima wafosi kingi.

Ndiyo maana Daphine akaokota Mtutu mkubwa na kuanza kumimina risasi, hiyo ilimfanya hadi Jenipha apate nguvu,mmoja anamimina risasi upande wa kulia mwingine wa kushoto, wakafanikiwa kutoka nje.Ngesa akawasha gari na kuwasogelea karibu zaidi.

“Ingia ingia ingia ingiaaa paaa paaa paaaa”

Ngesa alizungumza hivyo huku akiwarushia risasi majambazi, waliokuwa nje wanawafuata,hapohapo akapiga gia na kulirudisha gari nyuma baada ya Jenipha na Daphine kuingia kwa haraka.

“Ge gegegeegege”

Mmoja wa magaidi alisimama mbele na kuanza kulimiminia risasi gari la akina Ngesa,mpaka kioo cha mbele kikapasuka.Ngesa akalaza kichwa chini huku akizidi kurudisha gari kinyume nyume kwa mwendo wa kasi,bila kuangalia nyuma akajikuta amegonga gari lingine.

Hapohapo akaweka gia namba moja na kuzungusha usukani,jinsi gari lilivyoteleza iliongopesha ikawa kama filamu ya kijasusi kumbe ni kweli.

“Mpigie Rais Leslie simu mwambie kila kitu kipo sawa”

Ngesa akatoa wazo!

“Nina uhakika atakuwa anajua,huyu tunaenda naye wapi?”

Daphine akauliza,wakimaanisha Aron.

“Huyo nina kazi naye maalum Tanzania”

Kitendo cha kujibu hivyo,akapandisha gia na kuzidi kwenda mwendo wa kasi.

“Daaphineeee”

Sauti ya Jenipha kutoka pembeni ilimshtua,akapigwa na butwaa la waziwazi.

“Mungu wangu!”

Kilikuwa ni kitendo kilichofanya mpaka Daphine aogope,Jenipha alikuwa anavuja damu nyingi sana tumboni!Alivyomshika na kumkagua vizuri,wakaona shimo la risasi.Alichokifanya Daphine ni kuvua shati alilovaa,akabaki na sidiria kisha shati hilo akaliweka tumboni kwa Jenipha ili damu isiendelee kuvuja.

“Ngesa twende hospitali,Jenipha anavuja damu nyingi”

“Hapana,hatuwezi kwenda”

“Kwahiyo tutafanyaje?”

Daphine akauliza kama mtu aliyekata matumaini.Hiyo ilimfanya Ngesa ageuze shingo nyuma.

“Tunarudi Tanzania”

Alivyorudisha shingo mbele akabadili gia,wakazidi kusonga mbele.

Lakini katika hali ya kushangaza walivyofika Mbarara, pembeni ubavuni mwa Ngesa,likatokeza lori kubwa na kuwagonga kwa nguvu sana,gari lao likaburuzika na kupinduka mara tatu matairi yapo juu!Mlango wa lori ukafunguliwa wakashuka wanaume sita wenye mitutu,wanazungumza kisudani!Ngesa alivyojaribu kutoka,akashindwa sababu alibanwa vibaya sana, mbaya zaidi gari yao ilikuwa inavuja mafuta ya petroli kumaanisha tenki la mafuta limepasuka, hivyo muda wowote gari lingelipuka.Daphine akajitahidi kujichomoa lakini ikashindikana, wakawasikia jamaa hao wanazungumza kwa lugha yao huku wakitaja jina, Aron!




Kila kitu kilikuwa kimeharibika,gari walilokuwa wanaendesha lilipinduka chini juu, juu chini.Mbaya zaidi walibanwa na kushindwa kutoka,isitoshe tenki la petroli lilikuwa linavuja.Ngesa akajaribu kila namna kujinasua lakini akashindwa kabisa.Daphine alivyojaribu kujivuta,mguu ukawa umebanwa kwa juu ya paja.Akajishika kwa nguvu zote lakini zoezi hilo likaonekana kuwa gumu mno,damu zilimtoka Jenipha kwa wingi lakini yeye bahati nzuri ilikuwa kwake, hakubanwa na kitu chochote,akageuza shingo yake kwa tabu na kuona miguu ya watu inatembea kuelekea usawa wa gari lao, lililopinduka.Akajivuta kwa nguvu kwa tabu na mateso mpaka kwenye begi,akanyoosha mkono na kufungua zipu ambapo humo alikumbana na mabomu aina ya Grenade,alichokifanya ni kulishika moja na kutoa kipini, kwa nguvu akalirusha nje.Hiyo ikafanya majambazi waliokuwa wanakaribia gari, wakimbie na kuruka mbali,mlipuko mkubwa ukatokea!Sio kwamba walishindwa kurusha risasi,kilichowazuia ni kuona mafuta ya petroli yanatoka kwenye gari,kumaanisha wangerusha risasi,ungetokea mlipuko mkubwa,wangemkosa Aron!Ambaye walitakiwa kumkomboa akiwa hai.

“Daphine,kanyaga hapa.Vuta kwa nguvu”

Sauti ya Ngesa ilisikika,akiwa amebanwa chini akimuambia Daphine atumie mguu wake kukanyaga chuma cha usukani,kwa kuwa mwanya huo alikuwa nao akafanya hivyo wakisaidiana kuchomoka!Hatimaye Ngesa,akawa wa kwanza kutoka ndani ya gari,akachukuwa bastola na kuikoki.Akatizama huku na kule,akainama kidogo ili atoe msaada,akafanikiwa kumtoa Daphine.

“Paaa paaaa”

Alivyoona majambazi wanachomoza,akarusha risasi.

“Jenipha”

Wakasaidiana kumtoa Jenipha,wakamvuta kwa nguvu.Baada ya zoezi hilo kukamilika wakamtoa na Aron ambaye huyo walitakiwa kusafiri naye mpaka nchini Tanzania, kwa madai ya kwamba Ngesa ana shughuli naye pevu na nzito.Mungu akawa upande wao,kitendo cha kuchoropoka tu gari likaanza kushika moto taratibu.

“Paa paaaa”

Niya ya Ngesa kurusha risasi ilikuwa ni kuwapa nafasi Daphine,Jenipha pamoja na Aron wavuke upande wa pili,hilo likafanikiwa na walivyofika umbali wa mita kama kumi hivi,Ngesa akalilenga gari kwa risasi,mlipuko uliotokea haukuwa wa kawaida.

“Twendeni,fanyeni haraka”

Jenipha,alipoteza damu nyingi sana mwilini.Maumivu aliyokuwa anahisi hayakuwa na mfano wake,mbele yake alianza kuona giza lakini hilo halikumfanya akate tamaa wakazidi kusonga mbele huku Ngesa akiwa amemshika Aron!Wakatokeza barabara kubwa ya lami,hapo waliona supamakert kubwa,nje kuna magari mengi yamepaki.

“Nisubiri hapa”

Ngesa akasema baada ya kutizama magari hayo,akaangalia huku na kule.Akayafuata yalipo,kwa kutumia kitako cha bunduki akapasua kioo cha dereva,akafungua mlango na kuingia ndani ambapo humo akavunja switch ya funguo,akachomoa nyaya mbili,akazichonga na meno.Alivyozigusisha gari likawaka,bila kupoteza wakati akapiga gia na kurudi kinyume nyume mpaka walipo wakina Daphine.

“Tuondoke fanya haraka”

Hakukuwa na muda wa kupoteza,gia ikapigwa kasi waliyotoka nayo hapo iliogopesha maisha na niya ya Ngesa, ilikuwa ni kufika mpakani Mtukula,wachukue Helkopta waliyotumia kusafiria kisha warudi nchini Tanzania.Wakiwa katikati ya safari hali ya Jenipha,ilibadilika ghafla!Damu zilimvuja nyingi mbaya zaidi macho yake yakaanza kubadilika rangi.

“Ngesa”

Daphine akaita kwa sauti ya chini kama mtu aliyekata tamaa.

“Tunawahi,tunakaribia kufika”

Ukweli ni kwamba hata Ngesa nayeye alishaelewa kwamba kwa hali aliyokuwa nayo Jenipha,ilikuwa ni mbaya sana hakuwa ana uhakika kama angefika salama labda Mungu afanye miujiza yake,licha ya hayo yote alitoa jibu hilo kumpa faraja.

“Atapona,sio kidonda kikubwa”

Akazidi kutoa matumaini,hiyo ilimfanya Daphine ashushe pumzi nzito!


****

Raisi Leslie,alipandwa na presha!Usingizi kwake ukawa hadimu kupatikana usiku,alifikiria vitu vingi sana kuhusu nchi yake na watanzania kwa ujumla!Hakuelewa ni jambo gani alifanye kwani Brigedia Karanje alimnyima raha ya maisha na kumpa tumbo joto!Kifupi kwa muda mchache alipungua kilo tano nzima,mkewe aliligundua hilo akajaribu kuwa karibu naye lakini ikashindikana.Mbaya zaidi tangu amtume Ngesa akafanye ukombozi hakupokea simu yoyote ile kutoka kwake,hilo ndilo lilimtia mashaka na hofu akidhani wenda Ngesa aliuwawa.Usiku wa siku hiyo,alikuwa bize kuangalia luninga, akifuatilia sakata la mateka waliokuwa nchini Uganda,hiyo ilifanya kila sekunde amtafute balozi wa Tanzania aliyekuwa nchini Uganda,Mh.Joseph Ladislaus Komba!Masaa mawili baadaye, akapewa za chini ya kapeti kwamba wanafunzi wote wameokolewa na jeshi la Uganda,alivyodadisi ili kujua kama Ngesa alikuwepo alikosa jibu la kueleweka.Hapo ndipo akahisi joto kali!Hata hivyo ilikuwa ni furaha kwake sababu majambazi waliokuwa wamefanya jambo hilo la utekaji waliwekwa chini la ulinzi kwa ajili ya kujibu mashtaka.

“Griii griiiii”

Kilichomtoa katika mawazo hayo ni simu yake ya mezani,akaipokea ki uvivu na kuiweka sikioni.

“Mh.Rais,unaongea na Nurdin”

“Kuna tatizo gani?”

“Karanje,anahitaji kuzungumza nawewe”

“Unasemaje?”

“Karanje,anahitaji kuzungumza nawewe.Anadai anataka kukwambia mabomu yalipo”

“Kwanini asiwaambie nyie?”

“Amesisitiza anahitaji kukuona”

“Okay,andaa usafiri na ulinzi. Nitakuja asubuhi”

“Okay,Mh rais”

Maswali mengi alibaki akijiuliza ni kwanini Karanje anataka kumwambia yeye ni wapi mabomu yalipo,hilo lilimfanya azidi kuingiwa na wasiwasi mkubwa sana!


******

Mwendo wa Ngesa haukuwa wa kawaida,hiyo ilimfanya mpaka Daphine ajishike vizuri kwani roho yake ilikuwa mkononi.Mshale wa spidi uligota mwisho kabisa,kumaanisha kwamba gari inakimbia mno!Kwa kuwa ilikuwa usiku sana,ilifanya barabara iwe nyeupe.Saa kumi na moja alfajiri, walifika Mtukula,hapo walisimama na kushuka,wakamshika Jenipha vizuri na kuanza kuelekea walipoacha Helkopta.Hawakuwa na muda wa kupoteza wakaingia na kuiwasha mara moja,mapanga boi yalivyokolea ikaanza kupaa angani wakiiacha nchi ya Uganda.

Masaa mawili na nusu baadaye,wakawa wamefika na hawakutaka kulifanya jambo hilo liwe siri tena,ndiyo maana wakatua makao makuu ya Usalama wa Taifa Posta,Helkopta ikatua juu ya gorofa, hapo wakashuka na kumshusha Jenipha huku wakiomba msaada wa huduma ya kwanza.

“Nini kimetokea na ulikuwa wapi?”

Lillikuwa ni swali la mwana usalama mmoja,akiuliza kinoko na swali hilo lilimlenga Ngesa!

“Unachotakiwa kufanya ni kunielekeza ni wapi Karanje alipo,sasa hivi”

“Wee kama nani?”

Ngesa hakutaka kujibu chochote,alichokifanya ni kumvuta Aron mpaka ndani ya jengo ambapo huko alisachiwa na kunyang’anywa silaha.Taarifa za kufika kwa Ngesa zilimfikia Nurdin, alivyojaribu kumuhoji,akashindwa na Ngesa hakuwa tayari kuweka wazi harakati zilivyoenda.

“Mpigie simu Rais,mwambie nimefika.Nahitaji kuzungumza na Karanje!Sasa hivi”

Kauli hizo zilimfanya Nurdin achukie zaidi sababu alichukulia kama anaendeshwa na kuburuzwa wakati yeye ndiye mkurugenzi,hiyo ilimaanisha muda mfupi Ngesa angechukua cheo chake!Ndiyo maana akachukia zaidi lakini hakuwa nala kufanya,akampigia simu Rais na kumwambia kila kitu kilivyotokea,Ngesa akapewa simu.

“Hongera Ngesa”

“Ahsante Mh.Rais.Aliyekuwa nyuma ya kila kitu ni Aron Karanje,mtoto wake!Nilichokuwa naomba niweze kumuhoji Karanje naomba ruksa yako”

“Hilo halina shaka”

“Kitu kingine Mh.Rais”

“Kitu gani?”

“Jenipha ana hali mbaya sana,nahitaji msaada wako.Atibiwe!”

“Nitalifanyia kazi”

“Ahsante”

Baada ya simu kukatwa Ngesa akaomba,aonyeshwe alipo Karanje.Hakukuwa na kipingamizi chochote kile,mlango ukafunguliwa akaingia ndani.

“Una bahati mbaya sana,kila wanachojaribu kufanya wanashindwa!Hapa una kitu kimoja cha kufanya ama cha kuniambia,ni wapi mabomu mengine yalipo?”

Ngesa,alizungumza kwa kujiamini akimuangalia Karanje kwa macho yaliyojaa hasira na chuki za waziwazi.

“Unapoteza muda na pumzi zako Ngesa,sitokutajia”

Karanje nayeye akajibu kwa kiburi,alichokifanya Ngesa ni kuomba atoke nje ya chumba hiko,akamuendea Mkurugenzi Nurdin aliyekuwa makini pia kusikiliza mazungumzo yao.

“Namuomba Aron na bastola yenye risasi”

“Ngesa unataka kufanya nini?”

“Tunataka kujua ni wapi mabomu yalipo”

“Siwezi kukupa silaha”

“Nampigia Rais,namwambia unakataa kunipa ushirikiano”

Ngesa hakutania,akatoa simu na kupiga hatua mbili ili awasiliane na Rais Leslie.

“Sawa nakupa”

“Nasubiri”

Nurdin,aliogopa kibarua chake kuota nyasi.Hakuwa na jinsi zaidi ya kumkabidhi Ngesa bastola,wakamtoa Aron.

“Bado mdogo sana kufa, lakini nitakuuwa leo kama ulivyofanya Uganda,twende”

Ngesa alizungumza akimwambia Aron,akamshika shingoni kwa nguvu.Mlango ukafunguliwa,kitu cha kwanza alichokifanya Ngesa ni kuvunja kitasa kwa ndani akitumia kitako cha bastola na kuweka meza kubwa nyuma yake ili wa nje isiwe rahisi kuingia ndani,alifanya hivyo makusudi kwani alielewa ni kitu gani anaenda kukifanya.

“Kacha kacha”

Akakoki bastola na kumtizama Karanje,akamuwekea Aron bastola kichwani.

“Najua ni namna gani,unampenda mwanao.Nitamuuwa mbele yako.Mabomu yako wapi?”

Kuonekana kwa Aron mbele yake kulimfanya achanganyikiwe na kuingiwa na hofu kwa wakati mmoja,alivyotaka kusimama akashindwa sababu alikuwa na pingu mikononi na miguuni.

“Mabomu yako wapi?”

Ngesa akauliza kwa sauti ya juu sana,macho yake yamebadilika rangi yakawa mekundu ana hema juujuu, hiyo ilimaanisha tayari hasira zimemshika.Brigedia Karanje,aliogopa hakutaka kumpoteza mwanaye kipenzi, katika kujitafakari afanye nini ukasikika mlio mkubwa wa risasi.

“Paaaaaaaaaaaaaaaa”

Ngesa,akaachia risasi kilichoonekana hapo zilikuwa ni damu, kutapakaa chini.

“Nooooooooo”

Karanje,akapiga kelele kwa sauti iliyojaa uchungu baada ya kumuona Aron, yupo chini.




Saa 12;30 ya asubuhi,kila kitu kilikuwa kimetayarishwa tayari, kuanzia usafiri na barabara atakayopitia Rais Leslie, pikipiki na askari wa usalama barabarani walipewa amri kwamba wasimamishe magari yanayotoka mjini kuelekea Posta kwani kungekuwa na msafara wa Rais asubuhi hiyo.

Japokuwa ilikuwa kero kubwa kwa wakazi wa jiji hilo lakini hakukuwa na jinsi,wanaowahi makazini ilibidi washuke na kutembea kwa miguu sababu walisubirishwa takribani nusu saa nzima.

Wakati barabara zinasafishwa Rais Leslie alikuwa chumbani kwake,anavaa. Kichwani akiwa na mawazo mengi sana hususani kuhusu Brigedia Karanje ni kitu gani alikuwa anahitaji kumueleza,uwezo wa kupuuzia alikuwa nao lakini akaona ni vyema kwenda kumsikiliza wenda angemtajia ni wapi mabomu yalipo!Baada ya kuvaa suruali na kuweka tai yake vizuri,akapita kwa mkewe wakaagana kwa mabusu.Kisha yeye kutoka nje, ambapo huko alipigiwa saluti nyingi zisizokuwa na idadi.Pembeni yake kulikuwa na wanaume wawili warefu,hawa walikuwa walinzi wake maalum.Alivyofika kwenye magari,akafunguliwa mlango na kuingia.

Hakuwa ana haja ya kusema anakwenda wapi sababu kila kitu kilifahamika wazi.

Kuanzia hapo kilichosikika vilikuwa ni ving’ora vya magari ya polisi.

Ingawa alikuwa mwenye mashaka lakini kwa upande mwingine alijiamini pia sababu taarifa za Ngesa alikuwa nazo na aliamini huko anapoenda, angeonana naye na kumpa pongezi kubwa kwa kazi nzito aliyoifanya.Kasi ya magari ilikuwa kubwa sana,yakiongozwa na pikipiki zaidi ya sita barabarani,hiyo ilifanya ndani ya dakika kumi na nane, wawasili makao makuu ya Usalama wa taifa.Gari zikasimama,akafunguliwa mlango na kupigiwa saluti kama kawaida.Akaingia ndani, nyuma yake akisindikizwa na walinzi wake!

“Ahsante kwa kuja Mheshimwa Rais”

Alizungumza Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa,Nurdin Ramadhani huku akitoa mkono wake, ambapo waliongozana mpaka ndani ya chumba maalum.

Kitendo cha Rais kuweka makalio yake juu ya kiti,ulisikika mlio mkubwa wa risasi.Lilikuwa ni jambo la ghafla,walinzi wote wakawa makini na kumtoa Rasi Leslie eneo hilo kwani mlio huo uliwatisha.

Baada ya kufuatilia sana wakagundua Ngesa ndiye aliyefyatua risasi.

“Mabomu yako wapiiiii?”

Aron Karanje alikuwa chini,anavuja damu nyingi mguuni kwani risasi ilipenya katikati ya mguu wake,kelele alizopiga hazikuwa na mfano wake.Hiyo ilimfanya Brigedia Karanje apate uchungu ajabu,akatamani akate pingu lakini ikashindikana, akabaki anabana meno kwa hasira na uchungu mno!

“Mabomu yako wapi?”

Hapo Ngesa alimkanyaga Aron juu ya jeraha la risasi kwa nguvu,kwa mateso hayo aliamini Karanje angesema kila kitu.Ni kweli,jambo hilo lilienda kufua dafu sababu Karanje alihaidi kusema kila kitu lakini wamwachie Aron.

“Siwe..zi kusema!Mpaka mumuachie Aron hana kosa”

“Ngoja nikwambie kitu, kwa sasa hivi haupo kwenye nafasi ya kutoa amri!Nakuuliza tena kwa mara ya mwisho,mabomu mengine yako wapi?”

Macho yake yakawa mekundu ghafla,akamuekea Aron bastola kichwani kumaanisha Brigedia Karanje asingetoa ushirikiano basi ni lazima Aron angeuwawa kwa kupigwa risasi, jambo lililomfanya Karanje azidi kuogopa zaidi sababu alimpenda sana mwanaye.

“Sawa nakutajia ya…”

Alivyotaka kumalizia Sentensi yake,mlango ukapigwa kwa nguvu.

Wana usalama wakitaka kuuvunja ili waingie wamtoe Ngesa sababu alikuwa anaenda kinyume na sheria,alikuwa tayari amefanya kosa la kumpiga Aron risasi hivyo hawakutaka afanye madhara mengine zaidi.Alichokifanya Ngesa ni kuzidi kumsisitiza Karanje ataje.Lakini hilo likashindikana sababu mlango ulivunjwa wakaingia wana usalama sita wakiwa na bastola mikononi,zote zinamuangalia Ngesa.

“Ngesa,Mikono juu”

Alichokifanya Ngesa ni kumuinua Aron kwa kasi akamuweka mbele yake,bastola akaishika vizuri kamuwekea Aron kwenye kisogo.

“Namuuuwa,tokeni nje”

“Ngesa mikonoo juuu,moja”

“Namuuwa”

Ngesa alikuwa nyuma ya Aron na kila alichozungumza alikimaanisha kutokana na hasira mbaya alizokuwa nazo,jambo lolote baya lingeweza kutokea.Lakini alijikuta anakuwa mdogo ghafla, baada ya kumuona Rais Leslie katokea mlangoni.

“Ngesa,kila kitu kitakuwa sawa!Weka silaha chini,shusheni silaha zenu chini”

Ilikuwa ni amri sio ombi kutoka kwa Rais Leslie,hapo walimtoa Ngesa nje.Wakambeba Aron ili kwenda kumpatia huduma ya kwanza!Rais Leslie akaingia ndani ya chumba alichokuwa Brigedia Karanje!

“Unasemaje?Nimefika”

Rais Leslie,bila salamu akamsemesha Brigedia Karanje.

“Waambie watu wako watoke nje”

Jambo hilo likafanyika ndani ya chumba hiko wakabaki Rais Leslie na Brigedia Karanje,wanausalama wote pamoja na Ngesa walisimama nje ya kioo wakawa wanatizama na kusikia mazungumzo yao!Mara ghafla sauti ikapotea,hakuna hata mmoja kati yao aliyesikia nini kinaongelewa ndani.

“Mbona wametoa sauti?”

Ngesa akawa wa kwanza kuhoji,kuna kitu alianza kuhisi.

Mbali na hapo cha ajabu na cha kushangaza,wakaona jinsi Rais Leslie anavyofokewa na Brigedia Karanje hiyo ilizidi kuwashangaza zaidi na zaidi.Kuna kitu kisichokuwa cha kawaida kilikuwa kinaendelea!Dakika kumi baadaye Rais Leslie akatoka,macho yake yakiwa mekundu, akionekana mwenye hasira na hayupo sawa!

“Ngesa nifuate”

Akasema,hiyo ikamfanya Ngesa amfuate nyuma nyuma mpaka kwenye chumba maalum.Ambapo huko walinzi walisimama kando yao!

“Naomba hii kesi,uiache kama ilivyo.Karanje ameshaniambia ni wapi mabomu yalipo.Naomba usiendelee kumuhoji tena”

“Mheshimiwa Rais sijakuelewa”

“Kesi ishafika Usalama,cha msingi kaa nayo mbali.Mambo mengine yatafuata waachie usalama”

“Lakini alikuwa ananiambia ndiy…”

“Ngesa,sijaja kubishana.Hiyo ni amri”

Kitendo cha Rais Leslie kubadilika ghafla kilimfanya Ngesa aingiwe na mashaka sana!Kuna kitu alianza kuhisi,alivyotaka kuhoji akakatwa ndimi.Cha ajabu zaidi Rais Leslie akamkumbushia kesi yake kwamba anahitajika gereza la Quantanamo.

“Leo saa saba mchana,utaondoa na Ndege!Ukaanze kifungo chako”

Kwa Ngesa jambo hilo alilifananisha na ndoto ya kutisha,haikuwezekana hata kidogo Rais Leslie abadilike ghafla namna hiyo,machale yalimcheza ni lazima Brigedia Karanje kamwambia jambo zito, hivyo anataka kumkingia kifua,alichukia lakini hakuwa na jinsi.Alichokifanya Rais Leslie ni kuzungumza na Mkurugenzi wa Usalama wa taifa,aandae kila kitu kuanzia usafiri wa Ngesa na ulinzi wa kutosha.

“I’m sorry Ngesa,sina jinsi”

Rais akaongea lakini Ngesa hakujibu chochote,kilichotokea ni wanausalama kufika eneo hilo na kumtaka waongozane.

“Naomba nikaongee na Mke wangu”

Ngesa akaomba,hilo halikuwa tatizo Jaqlin Mfinanga akaitwa.

Wakaingia ndani ya chumba kidogo,kitendo cha Jaqlin Mfinanga kumuona Ngesa alimrukia kama mtoto mdogo huku akibubujikwa na machozi,ambayo hayakueleweka kama ya furaha ama huzuni.

“Jaqlin,nisikilize kwa makini”

“Ngesa nakuomba,usinia…..che tena Mme wa..ngu”

“Usijali tutaendelea kuwa wote.Lakini nachokuomba sasa hivi Uende Bagamoyo kwa Filbert Makalla,nitakukuta hapo”

“Mbona sikuelewi Nges..”

“Nisikilize Jaqlin…”

Hapo Ngesa akatumia ukali kidogo,akimuangalia usoni.Hakutaka tena kubembeleza mapenzi akaweka pembeni ukarimu,ilikuwa kazi kwanza sababu aliamini vita anayoanza haikuwa lele mama, ilikuwa ni lazima aishinde ndiyo maana akaanza kumpanga Jaqlin.

“Nenda kwa Filbert Makalla na usimwambie mtu yoyote kama unaenda huko,umenielewa?”

“Ndi…o”

Machozi yalizidi kumtiririka Jaqlin Mfinanga huku akilia kwa uchungu,aliumia moyo sababu hata siku moja hakuwahi kupata muda na Ngesa wa kupumzika na kujadili kuhusu mapenzi yao!

Wakakumbatiana kwa nguvu,mlango ukafunguliwa,akaingia Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Nurdin Ramadhan.

“Twende,muda umeisha”

Ngesa akashusha pumzi ndefu,akamtizama Jaqlin kwa macho fulani ya kumwambia,kila kitu ni shwari.Kisha akatoka nje,ambapo huko alikumbana na Daphine,akamsogelea karibu na sikio lake, kabisa!Alivyotaka kumwabia kitu,akashindwa sababu wanausalama walikuwepo karibu yake!Kurudishwa kwa Ngesa katika gereza la Quantanamo haikuwa siri tena kwa wanausalama,wao ndio wakaanza kuratibu safari nzima mpaka tiketi inatoka, ndani ya masaa mawili.

“Namjua Ngesa.He won’t give up, trust me!”

Maneno hayo yalitoka kinywani mwa Dustan akimwambia Nurdin Ramadhan kwamba Ngesa hakati tamaaa ni lazima amalizie jambo alilolianza,ambaye muda wote alifurahishwa na jambo hilo akiamini sasa cheo chake kitakuwa salama.

Ndiyo maana muda wote alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Ngesa anapewa ulinzi mkali kwani walielewa wangefanya kosa lolote lile,Ngesa angewatoka!Ngesa,alipekuliwa na kukaguliwa kila sehemu ya mwili wake kama ana silaha kisha wakamtoa na kumuingiza ndani ya gari maalum,ambapo nyuma kulikuwa na magari mengine sita.Wanamsindikiza kwenda uwanja wa ndege Mwl.Nyerere ambapo huko,wangempakia kwenye ndege!Akiwa ndani ya gari,amefungwa pingu, Ngesa aliwaza vitu chungu mzima,hususani nchi yake ya Tanzania na alishaelewa tayari ametengeneza uadui mkubwa na Rais Leslie,hiyo ilimaanisha anaenda kupambana na Serikali.Hio hakujali,alichotaka yeye amalize vita aliyoanza!


******

Saa 8;12 mchana,magari yalifika uwanja wa ndege,hapo aliteremshwa akiwa katika ulinzi mkali yaani chini ya ulinzi,pingu mkononi.Mbele kidogo wakakutana na wanaume wawili mmoja mtanzania mwingine mrusi.Hao ndio watu waliotakiwa kusafiri na Ngesa!

“Kuweni makini,ni mtu hatari sana!Documents zote hizi hapa,hii atasaini Rudolf.Mkifika Urusi,nipigie simu”

Nurdin Ramadhan aliwaambia wanaume hao,kwa sauti ya chini ili Ngesa asisikie.Kila kitu kilivyokuwa sawa wakasubiri mpaka waliporuhusiwa kuondoka,ambapo walitumia kibali maalum kutoka ubalozi wa Tanzania kwamba wanamsafirisha Mtuhumiwa gerezani,simu ikapigwa ili kuhakikisha.

Lilikuwa ni jambo la haraka lakini hakukuwa na jinsi,Ngesa akaingizwa ndani ya ndege.Kazi yake ilikuwa ni kuangalia na kupiga hesabu jinsi ya kutoroka ndiyo maana alivyoingia tu,akautizama mlango vizuri kwa umakini.

“Kaa hapa”

Mwanausalama mmoja akamwambia,Ngesa akakaa kwenye kiti lakini baada ya dakika moja akaomba kwenda chooni,hiyo ilikuwa ngumu kidogo kumruhusu.

“Kwahiyo,nikojoe hapahapa?”

“Kojoa tu”

Alijibu ki utani lakini Ngesa alimaanisha,hakuwa na mkojo lakini ilibidi achukuwe chupa ya maji na kuanza kunywa kwa wingi.Dakika mbili baadaye,akafanya kusudi kujikojolea kwenye suruali.

“Wee mpumbavuu nini?Ndio nini sasa?”

Jamaa huyo alifoka.

“Umeniambia nikojoe,ndio nachofanya.Nimebanwa pia na haja kubwa,”

“Nenda chooni,ukanye hukohuko.Usije ukajinyea hapa”

Alichokifanya Ngesa ni kusimama,akaonesha mikono yake iliyofungwa pingu ili ifunguliwe,jamaa hakuwa na shida akamfungulia hakuelewa kwamba anafanya kosa kubwa sana tena la jinai!

Ngesa akatembea mpaka chooni ambapo huko aliangalia kama kuna njia ya kutokea,akakagua vizuri akakosa.Ilikuwa ni lazima ashuke ndani ya ndege hiyo kabla haijaruka angani,akatafakari sana kwa kipindi kirefu.

Akatoka na kurudi kwenye kiti chake.

“Na utulie,ole wako ujikojolee tena!Unakuwa kama mtoto mdogo,leta mikono yako”

Jamaa huyo akasema lakini Ngesa akasita kidogo,akaanza kupiga hesabu ni jambo gani alifanye.Kwa kuwa jamaa huyo alikaa dirishani, haikuwa rahisi kwa mtu yoyote aliyekuwa pembeni amuone.

Alichokifanya ni kuinama kidogo,akarudi kwa kasi na kumpiga kifuti cha pua,kwa kasi ya risasi akaiviringisha mikono yake shingoni mwa jamaa huyo na kuanza kumkaba kwa nguvu sana shingo, bila mtu yoyote kuona tukio hilo!





Kumsafirisha Ngesa kwenda gerezani Quantanamo hakupenda lakini hakuwa na jinsi yoyote ile ilikuwa ni lazima ailinde siri yake kubwa ambayo kipindi cha nyuma alishirikiana na Brigedia Karanje wakiwa marafiki wakubwa,kilichokuwa kinatakiwa hapo ilikuwa ni kaseti ndogo iliyokuwa na mazungumzo ya Rais Leslie pamoja na wahasi kutoka nchi za Asia na Kambodia,Brigedia Karanje alimweleza anayo na asingeweza kuitoa mpaka awe huru.

Jambo hilo linakuwa gumu sana kwa Rais Leslie,kufanya uamuzi kama huo ilikuwa ni sawa na kujichimbia kaburi.Hakuwa na jinsi ndio maana akachukua maamuzi ya kumfunga kwanza Ngesa, akifufua kesi yake ambayo alitakiwa afungwe magereza ya visiwa vya Quantanamo!Kabla hajatoka nje ya jengo la Usalama wa taifa, akampigia simu mkurugenzi wa Uslama wa Taifa Ramadhan Nurdin!Akimuuliza kama walifanikiwa kumpandisha Ngesa, ndege.

“Ndio Mheshimiwa Rais,kwa sasa hivi ndege inaondoka”

“Una uhakika?Hakikisha inapaa angani subiri hapo kama nusu saa nzima”

Rais Leslie aliuelewa mziki wa Ngesa,hakutaka kuamini kama Ngesa angekubali kirahisi namna hiyo ndiyo maana akasisitiza ahakikishe kama ni kweli aliingia kwenye ndege.

“Nitafanya hivyo”

“Kitu kingine..”

“Naam”

“Brigedia Karanje,asihojiwe na mtu yoyote Yule mpaka nitakapotoa kauli yangu”

“Sawa Mheshimiwa Rais”

“Ahsante”

Rais Leslie,akahitimisha na kuanza kutembea mpaka kwenye msafara wa magari yake,ambapo alipigiwa saluti na kuingia!Ving’ora vikaanza kulia wakaanza kuondoka zao!


***

Hakuna hata abiria mmoja aliyejuwa kwamba ASP Joseph Peter kapigwa kabali kali kwenye siti anagugumia anataka kuomba msaada,mbaya zaidi mshipa wake wa kutolea hewa ndio ulibinywa sana kumaanisha kwamba asingeweza kutoa hewa wala kuingiza.

Ngesa alikuwa jasusi alijua ni wapi sehemu ya kumdhibiti mtu ndio maana akang’ang’ania shingo kwa nguvu huku akiubinya mshipa huo,Asp aliendelea kutingisha miguu kisha akatulia kumaanisha kwamba amepoteza fahamu tayari.Hiyo ilimfanya Ngesa atizame huku na kule kama kuna mtu anamtizama.Alivyoona zoezi limeenda vizuri,akachukua mto na kumuwekea Asp nyuma ya kichwa,akachukua shuka lililokuwa pembeni akamfunika, kuanzia kwenye miguu mpaka kifuani,akamuweka vizuri.Kwa kumuangalia kwa haraka ungedhani ni mtu aliyechoka sana na amelala fofofo kumbe kazirai!

Zilikuwa zimebaki dakika ishirini ili ndege ipae angani, hiyo ilimfanya Ngesa azidi kutafakari juu ya kitu gani akifanye,akili yake ikafanya kazi kwa kasi ya umeme!Akasimama wima lakini ghafla akashikwa bega kwa nyuma,alivyogeuka akakumbana na msichana mrembo,mrefu mwenye sura nyembamba!Hakutaka kujiuliza,sare alizovaa zilionesha alikuwa ni mhudumu wa ndani ya ndege.

“Kaka samahani,kaa chini na ufunge mkanda.Ndege inakaribia kuondoka”

Ngesa akatafakari kidogo!

“Ikitoka hapa,inatua wapi?”

“Rwanda,Kigali”

“Ahsante,wewe ni mrembo sana!Umeolewa?”

Ngesa akatoa sifa,akijaribu kujenga mazoea kidogo na kisura huyo aliyeonekana kupita kila kiti ili ahakikishe abiria wote wamefunga mikanda!

“Muamshe mwenzako,afunge mkanda”

“Sawa,acha nimfunge amechoka sana huyu ndugu yangu!”

Hivyo ndivyo alivyofanya,akamsogeza ASP Joseph Peter,akavuta mkanda na kumfunga vizuri!Hesabu za Ngesa siku hiyo zilionekana kufeli lakini hakutaka kukubaliana na hilo,alivyotafakari sana akakumbuka kwamba ana ndugu yake yupo Nchini Rwanda jiji la Kigali,akaamini atafikia huko na taratibu za kurudi Tanzania angezipanga kuanzia huko,ndani ya dakika ishirini na mbili ndege ikaanza kutembea kisha kupaa angani,alichokifanya Ngesa ni kuanza kumsachi Asp,akafanikiwa kukuta pesa kwenye koti lake,akachukua akijua ni lazima zingemsaidia mbele ya safari.


*****

Jaqlin Mfinanga,muda wote aliendelea kulia na kububujikwa na machozi tu.Hakuelewa ni jambo gani alifanye na hatma ya maisha yake ingefikia wapi siku ya mwisho.Maisha ya Ngesa ya mashaka aliyachoka na wakati mwingine alianza kujuta ni kwanini kajiingiza kwenye mapenzi na mwanamme huyo,mwenye misukosuko kila kukicha.Hata hivyo aliendelea kumvumilia tu.Alichokifanya baada ya kutoka jengo la usalama wa taifa,alitafuta daladala iliyompeleka mpaka nyumbani kwake Tegeta,ambapo huko hakukaa sana!Alitafuta usafiri mwingine utakaompeleka Bagamoyo kama Ngesa alivyotaka afanye!

*****

Swala la kuhakikisha Ngesa anafika magereza ya Quantanamo lilikuwa chini ya kitengo maalum cha usalama wa taifa,ndiyo maana mpaka ndege inapaa angani walikuwa makini kuhakikisha hakuna vurugu zozote ambazo Ngesa angezifanya!Kupaa kwa ndege angani kulimaanisha ushindi mkubwa sana kwao!Taarifa hizo alivyopelekewa Rais Leslie,akaonesha kufurahi sana!Akashika glasi ya wisky na kuiweka mdomoni akiwa,ikulu!

“Kwanini,umefanya hivyo lakini?”

LiIikuwa ni swali kutoka kwa Mkewe,swala la Ngesa kupelekwa gerezani lilimfanya ajisikie vibaya sana!

“Ni mambo ya kiintelijensia”

“Hapana,una uwezo.Una mamlaka ya kukataa hilo,kumbuka Ngesa ana mchango mkubwa sana.Hastahili kufanyiwa hivyo”

“Tatizo ni sheria”

“Mara ya kwanza mbona ulimwachia?”

“Mke wangu,kulikuwa na kazi maalum”

“Kwani imeisha?Mabomu yamepatikana?”

Mkewe alichukizwa,hata hivyo hakumuelewa kabisa mumewe!Ni mwanamme aliyebadilika ghafla,maamuzi aliyokuwa anayachukua hayakuwa ya kawaida hata kidogo!Mkewe akahisi kwamba ni lazima kuna kitu kisichokuwa cha kawaida kinaendelea!

“Yatapatikana”

“No,kuna nini Leslie?Mimi ni mkeo”

“Naelewa,lakini mambo mengine ya kiusalama zaidi.Kila kitu kipo sawa”

“Tangu lini,umeanza kunificha?”

“Naomba nilale nimechoka sana”

“Leslie ala..”

“Please,niache nilale tutaongea Kesho”

Rais Leslie hakutaka kuweka neno lingine zaidi,alichokuwa anafikiria ni kaseti yenye sauti yake ambayo Brigedia Karanje ndiye mwanamme pekee aliyejua ni wapi ilipo,kumaanisha kwamba amuachie huru ili siri ibaki kuwa palepale.


*****

Haikuchukuwa masaa mengi kwa ndege hiyo kutua jiji la Kigali nchini Rwanda,ambapo hapo ilitakiwa abiria wengine wapande na wengine washuke.Waliotakiwa kuendelea na safari walibaki ndani ya ndege, kwa Ngesa hapo ingekuwa ndio mwisho wa safari yake!Hakuonesha wasiwasi wowote ule,akachukua begi la Asp Joseph Peter pamoja na simu zake,akateremka nazo mpaka nje, ambapo huko alitafuta taxi.

“Hallo my friend”

Dereva taxi mmoja wapo,akamfuata kwa nyuma na kumshika mkono Ngesa!

“Do you speak Swahili?”Ngesa akauliza!

“Yes ndio,naongea Swahili muzuri.Jambo jambo!Hakuna matata mambo ni poa,twende kwa gari”

Dereva aliongea kwa uchangamfu akilazimisha kuzungumza kiswahili, ilimradi apate mkate wake,Ngesa hakuwa na tatizo akavuta kitasa na kuingia mlango wa nyuma,akitafakari jina la sehemu anayoishi ndugu yake!

“Nipeleke Remera”Akalikumbuka!

“Una faranga ama dolla?”

“Dolla”

“Poa,tutaenda”

Dereva akawasha gari na safari ya kuelekea Remera kuanza mara moja,ambapo ilikuwa ni nje kidogo ya mji wa Kigali.

Moyo wa Ngesa ulijaa hasira na chuki za waziwazi na cha kwanza alichofikiria baada ya kurudi nchini Tanzania ni kumteka nyara Rais Leslie ili ajue ukweli,hilo lilimfanya aumize kichwa sana juu ya namna ya kumteka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani ulinzi wake ulikuwa sio wa kawaida.Akabana meno yake kwa hasira na kushusha pumzi nzito!



Hakuwa mgeni sana wa jiji hilo lakini alivifahamu vitongoji vichache kwani alishawahi kufanya kazi ya kipelelezi miaka mingi iliyopita,katika wapelelezi mbalimbali kutoka nchi tofauti waliotumwa kupeleleza kuhusiana na vita ya kikabila ya wahutu na watutsi,Ngesa alikuwa mmoja wapo!

Kipindi hiko anafanya kazi ya kipelelezi,kazi hiyo ilimkutanisha na watu wengi sana na ilifanya iwe nyepesi kwake kutokana na ndugu yake Yowel Buchanan kumsaidia na kumuonesha vichocho vyote vya mji huo!Ndani ya taxi kulikuwa na ukimya na hakuna hata mmoja aliyemuongelesha mwenzake,ingawaje dereva wa taxi hiyo alikuwa mara nyingi akimtizama abiria aliyempakia kupitia kioo cha katikati akitamani kumsemesha ili wazoeane!

“Rafiki,ndio mara moja kufika hapa Kigali?”

Dereva taxi akavunja ukimya,akizungumza Kiswahili kibovu.

“Hapana”

“Mutanzania?”

“Ndio”

“Mimi nilifika Tanzania,Mwanza kule Nyegezi.Nilikula sana fish na…”

“Itachukuwa muda gani kufika Ramera?”

Ngesa akahoji na kumkatisha dereva,hakutaka mazoea na mazungumzo ya dereva kwake aliyafananisha na makelele tu,alichotaka yeye ni utulivu ili atafakari mbinu za kumnasa Rais Leslie ama ikishindikana ameteke nyara Brigedia Karanje!

Zoezi hilo aliamini lisingekuwa rahisi kama anavyofikiria, ilihitajika akili kubwa tena ya ziada.Dereva,alivyomjibu,akashusha pumzi ndefu na kuanza kuchora ramani kichwani kwake namna ya kuingia Ikulu ama sehemu yoyote ile kisha kumchukua Rais Leslie kinguvu,ghafla akakumbuka kama ana familia akafikiria aiteke familia yake!Lakini wazo hilo hakulipa kipaumbele sana,akalipiga chini.Akazidi kutafuta namna nyingine,kilichokuwa kinamuumiza kichwa sana ni jinsi Rais Leslie,alivyobadilika ghafla baada ya kuzungumza na Brigedia Karanje!Akajaribu,kuunga matukio jinsi sauti ilivyozimwa,akaanza kupata picha!Mawazo aliyokuwa nayo,yalimfanya afike mapema.Kitendo cha kushtuka akaona gari imepaki kando,pembeni yake kulikuwa na gorofa moja refu sana kwenda juu,mbele kulikuwa na nyumba zimejengeka vizuri kwa mtindo wa vioo!Baadhi zilikuwa ni ofisi na kwa juu yake,ziliandikwa kwa lugha ya kifaransa kilichochanganywa na Kinyarwanda.

Alivyoteremka,akampatia dereva ujira wake na kuanza kutembea moja kwa moja!Hakuwa anaelewa anapoenda lakini kutembea kungemsaidia zaidi sababu hakutaka kuonekana ni mgeni wa maeneo hayo,baada ya kupiga hatua kumi, mbele yake aliona makutano ya barabara na katikati kulikuwa na saa kubwa,kumbukumbu zikaanza kumiminika kichwani kwake,akaanza kukumbuka akachukua barabara ya kushoto na kunyoosha nayo!Ambapo,hapo kichochoro cha kwanza alikunja kulia!Alichoshukuru siku zote na kujipongeza ni namna kichwa chake kilivyokuwa kigumu kusahau mambo!Mbele yake aliliona geti dogo,japokuwa lilibadilishwa rangi lakini haikuwa vigumu kupakumbuka kwa bwana Yowel Buchanan,alivyowasili nje ya geti,akaligonga!


******

Kitendo cha Asp Jopesph Peter,kukaa kimya bila kufanya mawasiliano yoyote yale kiliashiria kulikuwa na jambo la hatari mbeleni,hisia za kwamba Ngesa ametoroka zilianza kujijenga kichwani mwa Ramadhan Nurdin,alikuwa ana kila sababu ya kufikiria hayo yote sababu alimjua Ngesa ni mwanamme hatari kiasi gani.Akajaribu tena kujipa muda wa lisaa lingine,lakini hakupigiwa simu yoyote ile.Machale yalianza kumcheza na kuanza kufuatilia ndege aliyopanda kama ilishatua jijini Kigali,hapo ndipo akazidi kupigwa na butwaa baada ya kuambiwa ndege hiyo ilishatua na kuondoka nusu saa lililopita,akashindwa kujua ni kitu gani akifanye.Alivyotaka kumtaarifu Rais Leslies, aliogopa sababu alijua kabisa CV yake ingeshuka kwani mpango wote wa Ngesa mpaka operesheni hiyo kukamilika ilikuwa mikononi mwake,ghafla akapata wazo la kumpigia Kamanda mmoja ambaye alikuwa katika kikosi cha usalama nchini Rwanda,akafanya hivyo mara moja na kuomba msaada wake!

“Nurdin,unataka nifanye kitu gani?”

Upande wa pili wa simu,ulisikika.

“Kujua kama huyo mtu alishuka”

“Hapa Kigali?”

“Ndio”

“Nipe dakika tano,nipe na majina yake na ndege aliyopanda”

Haikuwa kazi ngumu kwa mtu kutoka serikalini kutaka ripoti hiyo,kupitia cheo chake wakafanya mawasiliano na marubani wa ndege,taarifa zikafika kwa wahudumu wa ndege!Katika msako wao wakagundua kwamba abiria anayeitwa Derick Ngesa katoweka,wakarudisha taarifa hizo na Ramadhan Nurdin,akapigiwa.

“Shiiit”

“Kuna nini?”

“Ni mtu hatari sana huyo,fanya unavyoweza apatikane”

“Nipe dakika chache”

Kama ilivyokuwa awali,watu wa usalama hawakuwa watu wa kawaida.Mpango wa kuingia vyumba vya CCTV camera ukaanza mara moja,wakaanza kuangalia!Ndani ya chumba kikubwa kilichokuwa na askari kumi na saba walikuwa makini kwenye tv zao kutizama kwa makini kila mtu anayetoka na kuingia.

“Rudisha nyuma”

Yalikuwa ni maagizo kutoka kwa Gael,alikuwa ni mwanamme mrefu mwembamba mwenye mwili mkakamavu,alikuwa amevaa kiraia lakini amependeza sana!

Kutokana na kuyapeleka mambo haraka namna hiyo,ilimaanisha alikuwa mwenye cheo kikubvwa sana serikalini.Sura yake ilikuwa nyembamba ya Kinyarwanda,alikuwa mzuri wa sura na ndevu zake alizichonga mtindo wa O.Macho yake yalikuwa makini kuangalia watu waliokuwa kwenye luninga,alivyomuona Mwanamme mfupi kiasi,amevaa koti akamfananisha na picha aliyotumiwa na Ramadhani Nurdin,ndiyo maana akataka warudishe nyuma ili ahakikishe,tukio hilo likafanyika.

“Stop,mtu anayetafutwa ni huyu hapa.Camera ya nje namba 7,angalieni kama alitoka”

Kauli hiyo baada ya kutamkwa,utekelezaji ulifanyika.

“Ndio,alitoka baada ya dakika kumi nyuma na taxi namba 7AMD 01R”

“Tafuta dereva wa taxi hiyo,haraka sana”

“Okay”

Ilikuwa ni hatua kubwa yenye matumaini,bila kuchelewa akamrudishia majibu Ramadhan Nurdin na kumpa taarifa hizo zilizoonekana kuwa njema kwake.

“Gael,huyo mtu ni hatari.Akileta ukaidi,unajua cha kufanya”

“Una maanisha nini?”

“Muueni na naomba operesheni hiyo iwe kimyakimya,tafuta watu unaowaamini”

“Sawa”

Gael,alipokea taarifa hizo kwa uzito mkubwa sana!Mtu aliyeambiwa amtafute aliamini alikuwa ni hatari mno!Ndio maana akaanza kwanza kuratibu mipango,ndani ya dakika ishirini taxi iliyompeleka Ngesa, maeneo ya Remera.Ikawa imerudi!Gael akamfuata dereva na kumuhoji maswali mawili matatu kisha akatoa picha ya Ngesa!

“Ulimshusha wapi huyu mtu?”

“Remela”

“Sehemu gani?”

Dereva akasema kila kitu,kilichofuata hapo ni Gael na watu wake kuingia ndani ya gari na kuelekea Remera ili kumtia Ngesa chini ya ulinzi,mbaya zaidi wote walikuwa na bastola viunoni tayari kwa mashambulizi endapo Ngesa angeleta ukahidi wowote ule.


*****

Hakukuwa na stori nyingi,zaidi ya Ngesa kumuomba Yowel Buchanan,amsaidie kutoka nje ya mipaka ya Rwanda wakitumia njia za panya!Sio kwamba hakuweza kufanya peke yake lakini alihitaji mwenyeji ambaye angemuongoza katika safari hiyo yenye milima na mabonde,Ngesa alikuwa mpole na muda wote hakuwa sawa kabisa.

“Upo sawa?”

Hiyo ni mara ya nne kwa Buchanan kuuliza swali hilohilo.

“Usijali,niko sawa!Tuondoke sasa hivi,natafutwa sana Tanzania.Wakisikia kwamba nimetorokea Rwanda ni lazima watatuma watu,sitaki nikamatwe kabla sijaianza safari yangu”

“Kuna nini?”

“Nitakuelezea Yowel,nachokuomba usimwambie mtu yoyote kwamba nilifika hapa”

“Usijali,naomba nimuage mke wangu”

Yowel Buchanan,alivyotaka kurudi ndani Ngesa akamshika mkono!

“Usifanye hivyo,hata yeye asijue”

“Sasa nitamwambia nini?Nimwambie naenda wapi sasa hivi”

“Mwambie chochote,hata yeye sitaki ajue nilifika hapa.Ni hatari sana kwa maisha yake”

Hilo halikuwa tatizo,Buchanan akaingia ndani na alivyotoka alikuwa ameshika funguo za gari,wakanyoosha mpaka kwenye maegesho wakawasha gari na kuanza safari.

“Gari yako ina mafuta ya kutosha?”

“Sidhani”

“Shika hii,utaongeza”

Ngesa akatoka dolla mia mbili,akamkabidhi Buchanan,hapo safari ikaanza mara moja!Hakukuwa na mtu yoyote mwenye habari kwamba nyuma yao kuna wapelelezi kutoka Rwanda wanawafuatilia,mpaka pale Ngesa alipoangalia kioo cha ubavuni,kuna gari aina ya Marcedenz benz,muda mrefu ilikuwa nyuma yao!Kwa mara ya kwanza alilidharau lakini walivyozidi kwenda mbele,akaanza kuingiwa na hofu ingawa hakutaka kumfanya Yowel agundue hilo.

“Ebu tujaze mafuta,sheli ya karibu”

“Tutajaza mbele”

“Ni vizuri tujaze mapema”

Ngesa alishauri ili kutaka kujua vitu viwili cha kwanza alitaka kuhakikisha kama gari hilo linawafuata kweli,jambo la pili kama ni kweli iwe rahisi kuwakimbia sababu wangekuwa tayari wamejaza mafuta ya kutosha.

Kilichomtia uwoga,hakuwa na silaha yoyote ile ya kujitetea hata hivyo,akili yake ilianza kufanya kazi kwa kasi ya risasi.Buchanan,hakutaka kupingana na hoja,akaingiza gari sheli ya mafuta.Ngesa akatupa jicho kwenye kioo cha nje,akaona gari hilo limewapita na kwenda kusimama upande wa kushoto hapo akawa ana uhakika,anafuatiliwa lakini hakutaka kuonesha mshtuko wowote ule,safari ikaanza baada ya kujaza mafuta ‘full tank’ macho ya Ngesa yalikuwa kwenye Marcedez benz iliyokuwa mbele yao,imepaki.

Hakutaka kugeuza shingo ilipo walivyopita,akiamini kwa kufanya hivyo wangeshtuka mapema kama wamegundulika.Walivyotembea umbali wa mita mia moja,akaliona gari hilo limewafungia mkia bado.Alichokifanya Ngesa ni kuwa makini sana kuangalia kioo cha ubavu wake,kila walivyokata kona aliliona gari hilo kwa mbali.

“Unaweza kupaki pembeni,nimebanwa kidogo”

“Nini tena?”

Buchanan akauliza,Ngesa akashika tumbo akizuga.

“Tumbo,linakorofisha kidogo”

“Umekula nini ndugu?Ngoja nitafute grocery yoyote ama sehemu yoyote ile yenye huduma ya choo”

“Nitashukuru”

Buchanan,akapunguza mwendo wa gari.Akaanza kutafuta vibao,mpaka alipoona sehemu kuna huduma ya choo.Hapo akasimamisha gari, alivyotaka kushuka Ngesa akamzuia akidai ataenda mwenyewe.

“Narudi sasa hivi”

Alivyoteremka tu,akalitizama gari aina ya Marcedez Benz kwa jicho pembe,akaliona linavyopaki pembeni.

Akajua ni lazima watu hao wanamtizama na kumuangalia,mbele yake kulikuwa na mkusanyiko wa watu,akapita katikati yao na kuvua koti!Alivyompita mtu wa tatu,akajificha nyuma ya jengo la benki!Hapo aliweza kuliona gari hilo vizuri,akajipima vizuri na kuingiza akili yake kazini.Kufuatiliwa mpaka mwisho aliamini mikakati yake isingefika mbali,ndiyo maana akawa makini sana akatembea akiambaa na ukuta na kulikaribia gari hilo,hakuwa ana uhakika kama alichokua anataka kukifanya kingezaa matunda lakini ghafla akabadilisha mawazo,akajipitisha mbele ya gari kuhakikisha wamemuona,alivyoona zoezi lake limefanya kazi, akaanza kutembea kuelekea nyuma huku mara kadhaa akigeuka,akafurahi baada ya kuona mlango wa gari hilo, umefunguliwa akajua tayari mahesabu yake yanaenda kufanya kazi.

Watu wa Gael walikuwa makini kumfuatilia Ngesa,ndiyo maana mmoja akashuka na kumuendea nyuma yake ili asipotee kwenye upeo wa macho yao!Ngesa alikuwa makini sana kwa kila hatua anayopiga.Akakata kushoto na kunyoosha moja kwa moja,akaona kichochoro kidogo kilichokuwa mbele yake kulia na hakukuwa na msongamano wa watu,akaingia hapo na kutulia akijibanza!Akatega masikio vizuri,akisikilizia hatua za mtu aliyekuwa anamfuatilia akija, alivyokaribia akajiandaa vizuri kwa mashambulizi,mtu huyo alivyotokeza akamvuta kwa kasi ya umeme na kumpiga kichwa kizito puani,kwa sekunde moja akainama na kumchapa ngumi mbili kavu za mbavu,zilizomfanya mtu huyo apige yowe kali la maumivu,alivyotaka kuchomoa bastola alikuwa tayari amechelewa kwani Ngesa alimuona na kumuongezea ngumi nyingine nzito ya tumbo,akamvuta na kuichomoa bastola yake iliyokuwa kiunoni.

“Tulia hivyo hivyo,wewe ni nani?”

Ngesa akauliza,bastola ikiwa mkononi mwake hana punje ya utani.

“Nakuuliza wewe ni nani?”

Akauliza tena lakini alivyotaka kumsogelea,akahisi kuna kichuma cha baridi kimemgusa shingoni nyuma yake.Akajua nini maana yake!

“Tupa bastola chini Ngesa”

Kauli hiyo kutoka nyuma yake,iliyomuonya ilimfanya Ngesa atulie kidogo, akaelewa kwa kufanya mjongeo wowote ule wa ghafla tafsiri yake ilikuwa ni kifo kwani alishaelewa mtu huyo mkononi alishika mguu wa kuku, yaani bastola.

“Umelijuaje jina langu?”

Ngesa akahoji kwa niya ya kununua muda ili aendelee kutafakari jinsi ya kujinasua.

“Tupa bastola chini,nimekwambia.Sitorudia”

“Sawa naweka,lakini tufahamiane kidogo ndugu yangu”

“Mimi sio ndugu yako”

Kitendo cha jamaa huyo kumjibu Ngesa kilimfurahisha sana,taratibu akaanza kuweka bastola chini huku akijaribu kuanzisha mazungumzo mengine na jamaa huyo!

“Mnataka nini kutoka kwangu?Mmejuaje nipo hapa?”

Ngesa akahoji baada ya kuweka bastola chini,jamaa huyo akaanza kumsachi sehemu mbali na kumpapasa mifukoni.

“Taratibu basi,utanisachi vipi hivyo?Unakuwa kama shoga!Bwege nini wewe al..”

Kabla ya Ngesa kumalizia sentensi yake,akapokea ngumi kavu ya shingo iliyomuingia kisawasawa na kuhisi kama shingo yake imevunjika,akagugumia kwa maumivu hakukaa vizuri akapokea teke la tumbo lililomfanya adondoke mpaka chini kama embe kutoka mtini,sio siri alihisi maumivu makali na kujuta kwanini aliuliza kwa jeuri.

“Nani shoga?”

Jamaa huyo aliuliza kwa jazba,bastola yake ikiwa mkononi!Jambo hilo Ngesa ndilo alilokuwa analitaka,kumpandisha hasira ili apate kiwewe.

Jamaa huyo akiwa na bastola yake,akarusha teke,hapo ndipo alipofanya makosa kwani Ngesa alilidaka vizuri bila kufanya makosa,akaushika na mguu wake mwingine,akamvuta akadondoka chini mzimamzima bastola yake ikadondoka kando,kwa kasi akasimama na kumuendea akamuinua na kumtandika ngumi moja ya pua,iliyomfanya aone maluweluwe,aliyekuwa pembeni alivyoona mwenzake amepigwa akajaribu kusimama ili kutoa msaada lakini alitulizwa na teke la kifua aina ya fly kick,likamrusha na kumtuliza ukutani.

Wepesi aliokuwa nao Ngesa,ulimfanya ajivute na kubiringika kama mpira,akainuka kitaalam na kumpiga kikumbo na bega wote wakadondoka chini,Ngesa akaokota bastola iliyokuwa chini na kumuwekea usawa wa kichwani.

“Hua,sipendi kuuliza kitu kimoja mara mbili.Nadhani aliyewatuma,kawaambia vizuri mimi nani!Mnataka nini kutoka kwangu?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Ngesa,akimtizama mwanamme huyo aliyekuwa chini anahema,aamini kilichotokea na mambo yalivyogeuka kwa sekunde chache!



Lilikuwa ni tukio la kusisimua mno! Na la kushangaza kwa wakati mmoja,hakuna hata mmoja kati ya wapitanjia waliokuwa pembeni, aliyegundua mambo yaliyotokea ndani ya sekunde chache zilizopita nyuma kwani shughuli ziliendelea kama kawaida,alichokifanya Ngesa ni kuwasogelea watu hao waliotumwa na kuwasachi mifukoni,akachukua pochi zao pamoja na silaha walizobeba!Akaficha nyuma ya shati lake na kulifunika,akawatizama jinsi walivyokuwa wanaugulia maumivu kisha yeye akatokeza barabarani, ambapo huko kulikuwa na purukushani za watu,ilikuwa ni lazima afanye maamuzi mengine ndani ya sekunde sifuri.

Ndio maana baada ya kuliona gari liliowabeba wapelelezi hao wa Rwanda,akalisogelea kwa kasi na kuvuta kitasa,ndani akakumbana na wanaume wawili.Kitendo cha Ngesa kuingia ghafla,kiliwafanya wasiweze kujitetea kwani tukio hilo kwao hawakulitegemea kabisa na mbaya zaidi Ngesa alikua tayari keshatoa bastola,anawatizama.

“Toa bastola yako,weka pembeni.Sitorudia mara mbili”

Ngesa alisema na hiyo ilikuwa ni amri sio ombi,uso wake haukuonesha hata punje kidogo ya mzaha.Kukahidi kauli hiyo tafsiri yake ilikuwa ni kifo!Hakukuwa na mtu yoyote aliyeweza kufanya ujanja wowote ule, kutokana na gari hilo kuwa na vioo vyeusi yaani tinted.Kila mtu akatoa bastola yake,wakamkabidhi Ngesa!

“Chukua hiyo pingu,mfunge mwenzako nawewe jifunge”

Jambo hilo likafanyika bila ukaidi wa aina yoyote ile,ndani ya Dakika moja wakajikuta wamejifunga pingu.

Alichokifanya Ngesa ni kutizama huku na kule,alivyoona nje kuna hali ya usalama akavuta begi dogo lililokuwa ndani ya gari kisha kuweka bastola,akalivaa mgongoni akiamini mbele ya safari lingemkomboa!Jinsi alivyoshuka hakutofautishwa na mtu aliyetoka kupewa lifti maana alitizama huku na kule kisha kuufunga mlango,akavuka barabara kwa umakini mpaka lilipokuwa gari la Buchanan,akafungua mlango!

“Mbona umekawia hivyo?”

Kidogo Buchanan,alikijua kiswahili cha kibongo japokuwa hakuwahi kuishi Tanzania lakini alikaa na watanzania,hivyo lugha hiyo alijua kuongea vizuri.

“Tumbo lilikuwa linakata,tuondoke”

“Sawa,inabidi tukifika mbele upate dawa”

Buchanan,alikuwa nyuma ya kila kitu hakuelewa chochote, hiyo ilimfanya Ngesa ajisikie huru sababu alielewa ni kwa namna gani Buchanan,angepaniki na ingesababisha safari yao wasifike mapema!


****

Ramadhan Nurdin,alitokwa na jasho kila mahali.Hakuelewa ni kitu gani akifanye baada ya kumkosa Gael hewani kwa masaa mawili,wasiwasi ukamuingia akidhani wenda Ngesa amewashtukia na kuwathibiti lakini alivyokumbuka uhodari wa Gael,akajipa moyo na kutembea kifua mbele!Ofisi yake ilikuwa kubwa sana,juu kabisa kuna picha ya Mwalim.Julius Kambarage Nyerere,akaitizama picha hiyo na kujaribu kupiga simu kwa mara nyingine nchini Rwnanda,lakini simu iliita bila kupokelewa,mawazo mengi yalitawala kichwa chake!

Ramadhan Nurdin,alimchukia sana Ngesa akiamini uwepo wake duniani ungemfanya asingeishi kwa raha ndiyo maana alituma watu kimya kimya wamuuwe akiwa huko huko Rwanda lakini matokeo yake ikawa kinyume.Ghafla akaanza kuhisi joto,akavua koti alilovaa na kulegeza tai iliyomshika kohoni!Hiyo akaona haitoshi,akatembea huku na kule akikuna kichwa!Kilichomshtua ilikuwa ni simu yake ya mkononi, iliyokuwa mezani,akatembea kwa kasi na kuipokea baada ya kugundua mpigaji alikuwa ni Gael.

“Vipi?Mmefikia wapi?”

“Usijali,tupo sambamba naye”

“Gael,sikuelewi.Nambie huyo mtu,mshamkamata?”

Ramadhan Nurdin,akafoka kwa sauti huku akipiga meza kwa hasira.

“Bado,amejua tunamfuatilia.Lakini bado tupo naye”

“Kivipi?Sitaki majibu hayo,nachotaka kusikia ni tayari mpo naye”

“Sawa”

Hakuelewa kwamba anadanganywa na Gael,hapo alipo ana maumivu ya shingo pamoja na mgongo anatafuta hospitali akatibiwe!

Kila kitu kwa Ramadhan Nurdin,kiliharibika lakini kuna jambo alilikumbuka na kuliona ni lazima zoezi lake litafanya kazi,alivyokisumbua kichwa akamkumbuka Jaqlin Mfinanga!Akatafakari kwa muda na kuchukua mkonga wa simu ya mezani!

“Kenge,njoo ofisini kwangu”

Baada ya kuzungumza sentensi hizo,akaweka mkonga wa simu na kushusha pumzi ndefu za kuchoka.Hazikupita hata dakika mbili,mlango ukafunguliwa akaingia mwanaume mrefu mwembamba!Amevaa miwani ya macho!

“Funga mlango”

Ramadhan Nurdin,alisema huku akitoa ishara kwa mkono.Mlango ukafungwa,mwanamme aliyefahamika kwa jina la Kenge,akasogea karibu.Hiyo ilimfanya Ramadhan Nurdin, atembee mpaka kwenye kiti chake cha kuzunguka na kukaa!

“Karibu kiti”

“Ahsante boss”

“Nimekuita hapa,nina mambo hayooo…Mawili”

Ramadhan Nurdin aliongea kwa msisitizo na vitendo sababu alionesha vidole viwili,hiyo ilimfanya Bwana Kenge asikilize kwa makini zaidi.

“Ndio boss”

“Kwanza kitu kimoja,nilitaka kusahau.Sitaki mtu yoyote akijue,hususani Mheshimiwa Rais”

Hapo Bwana Kenge hakujibu,akajivuta karibu zaidi.

“Ngesa ametoroka,alivyoshuka Kigali.Mpaka sasa hivi,hatujui alipo.Lakini nina uhakika hundrend percent,yupo njiani anakuja Tanzania!”

“Ametoroka?!”

Jinsi Kenge alivyoyatoa macho yake,iliogopesha taarifa hizo kwake zilimshtua, akatafakari kwa kina Ngesa ni mtu wa aina gani, mpaka aweze kuwapiga chenga namna hiyo!

Hata hivyo habari za Ngesa kufanya matukio makubwa hayakuwa mageni kwake.

“Ndio,nachotaka kukwambia tafuta watu wakakae boda zote za Tanzania!Nina amini ataingilia Bukoba ama Arusha,tafuta watu Mtukula na Namanga”

“Nitafanya hivyo boss”

“Jambo jingine,nahitaji kujua Jaqlin Mfinanga alipo”

“Ndio nani?”

“Malaya wake Ngesa,nina uhakika kuna mambo wameongea”

“Hakuna shaka,kuna la ziada?”

Bwana Kenge aliuliza kwa kujiamini na majivuno yote kana kwamba kazi hiyo ilikuwa ni sawa na kuuwa mbu ndani ya neti!

“Fanya kwanza hilo”

“Nitafanya,sasa itabidi nitafute watu wakunisaidia”

“Tafuta watu unaowaamini,ambao wataweza!Mtafute Rocka,yupo Arusha!Ataiweza hiyo kazi,kitakachoendelea please i need feed back!Ngesa ni mtu hatari na ana mafunzo,kuwa makini”

Sio kwamba hakuulewa mziki wa Ngesa,jeshi la mtu mmoja lakini alijifanya kiburi na alijipa matumaini ya kwamba, siku zake zinahesabika japokuwa hakuwa ana uhakika kama siri hiyo ingebaki,kwani ni lazima Rais Leslie angeulizia amefikia wapi,hiyo ilimaanisha afanye anachojua ili Ngesa apatikane kwa wakati.

“Alafu kitu kimoja…..”

Ramadhan Nuridn,akawa kama ana neno la kujazia,hiyo ilimfanya Kenge agande kwenye mlango na kugeuka ili asikilize!

“Vyovyote itakavyokuwa,mkipata nafasi.Kill him”

Kenge badala ya kujibu akatingisha kichwa kukubali kauli hiyo!


*******

Kilikuwa ni kikao kidogo lakini kizito,kilichowashirikisha wanausalama kumi na moja,ambao waliaminiwa wangekuwa watunza siri,mkutano huo wa dharura uliongozwa na Kenge!Ambaye kwao alionekana kama bosi,kilikuwa ni chumba kidogo cha mkutano lakini kamera zote zilizimwa tofauti na siku zote!Kenge alisimama akawa kama mwalimu wa somo la Hisabati,anaeleza jinsi mambo yalivyo mpaka Ngesa alivyotoroka akiwa nchini Rwanda jijini Kigali.

Hilo liliwashtua wengi lakini hawakutaka kulionesha waziwazi kwani kilichotakiwa ni Ngesa apatikane awe mzima au maiti yake.

Mwisho wa Siku Kenge akahitimisha kwamba kazi hiyo inatakiwa iwe imetimia ndani ya masaa arobaini na nane yaani siku mbili.Ripoti iwe imekamilika na hakuacha kusisitiza kwamba jambo hilo liwe chini ya kapeti,mtu yoyote asijue!

“Nadhani,nimeeleweka!Kila mtu anajua cha kufanya,mna mafunzo ya kutosha!James,make sure unampata Jaqlin Mfingana,muweke chini ya Ulinzi mkali.Nina amini hilo ni jambo dogo kwako!”

“Hilo swala ni dogo pigia mstari mkuu”

James,alijibu hoja kwa kujiamini sababu yeye sekta yake ilikuwa upande wa mawasiliano hivyo alichokijibu alikuwa ana uhakika nacho,jambo alilotakiwa kulifanya ni kuingia TCRA kupekua.

Ambapo huko alijifanya mfanyakazi wa kuajiriwa kumbe ni shushusu,hakuna mtu yoyote aliyejuwa kwamba James ni usalama wa taifa, tangu aanze kufanya kazi mamlaka ya mawasiliano Tanzania,ndiyo maana kazi hiyo kwake ikawa ni sawa na kuweka kibakuli cha supu mdomoni!

Mchakato ulianza mara moja,wenye kusafiri walipewa fungu lao na kuwekewa pesa kwenye akaunti benki,wakapanda ndege na kwenda kutega baadhi ya mipaka ya Tanzania!Na kila mtu aliyefika aliripoti kwa Kenge,alichokifanya Kenge ni kumpa taarifa bosi wake Ramadhan Nurdin.Mbinu hiyo ikaonekana kuwasaidia!

Kitu kilimchofurahisha zaidi Kenge ni kusikia kwamba tayari Jaqlin Mfinanga amepatikana na ni nyumba ipi amefikia.

“Bagamoyo huku,juu kabisa.Sipajui vizuri..Halloo..”

“Naona mtandao,unasumbua”

“Nitakupigia baadaye,lakini nachokwambia tupo nje ya nyumba.Hawezi kutukimbia”

“Kazi nzuri”


****

Ulikuwa ni usiku wa saa tisa,baada ya msoto wa safari ndefu iliyokuwa na milima na mabonde!Ngesa alikuwa hoi bin taaban,mbaya zaidi hakupata mlo kwa muda mrefu sana!Aliamini angefika mpakani Namanga,ingekuwa ahueni kwake sababu uliobaki ni mkia peke yake!Alivyokaribia kufika,akamuomba dereva wa texi, amshushe kandokando wasivuke kwanza kuingia Tanzania kwani alikuwa bado Kenya,ilikuwa ni lazima!Aangalie usalama sababu alishaelewa anatafutwa na taarifa zake zipo kila mahali.

“Umefika my friend?”

Dereva,akauliza kwa rafudhi ya Kenya lakini Ngesa badala ya kumjibu akamdadisi kidogo kisha kutoa pesa za Kenya ambazo alichenji alivyoingia nchini humo!

“Shika”

“Chapa ngapi hii?”

Ngesa,akashika begi lake na kulipuuzia swali la dereva huyo ambaye alikuwa kama kero kwake kutokana na stori nyingi,ambazo kwake hazikuwa na faida yoyote!

Alivyoweka begi lake mgongoni,akatizama huku na kule.Hakuwa mgeni wa eneo hilo,njia zote za Panya alizijua na mbinu zote alizifahamu jinsi watu wanavyopita boda kinyemela,alichokifanya ni kusonga mbele huku akilifuata giza lilipo,akaingia katikati ya miti na kuchomoa bastola yake ili kujihami na kiumbe chochote kile kitakacholeta shida!Bahati nzuri,ikawa kwake akafanikiwa kumaliza msitu wenye miti michache!

Kazi nzito ikawa ni kupita katikati ya maaskari, waliokaa upande wa Tanzania,walikuwa ni wengi sana!Alichokifanya ni kusubiri kwa dakika kadhaa,akaliona basi kubwa la abiria,utaratibu ulikuwa ni lazima abiria wote washuke ili wakagonge passport zao mihuri,baada ya abiria kushuka yeye akaingia kwa tahadhali,akajipachika kwenye siti ya katikati na kujifinya kwa chini kidogo!Hapo alifanikiwa sababu abiria walianza kuingia mmoja baada ya mwingine lakini baaadhi walionekana kumshangaa!

Hilo,halikumuogopesha!

Gari likaanza kutembea taratibu ili livuke boda na kuingia upande wa pili,lakini cha kushangaza likasimama ghafla, jambo hilo likamfanya ashtuke sana!Kitu kilichomshtua zaidi ni baada ya kuwaona askari wawili, wanatokea kwa nyuma ubavuni.

“Samahani ndugu zangu abiria,najua mmechoka na safari lakini kuna ukaguzi unatakiwa kufanywa mara moja”

Kondakta aliwataka radhi abiria,hiyo ilimfanya askari mwenye mtutu, aingie ndani ya gari!Moyo wa Ngesa ukapiga paa!Taratibu akaanza kugusa kiuno chake upande uliokuwa bastola,akawa tayari kwa ambush yoyote ile kwani aliamini kivyovyote vile,wanamsaka yeye ama walimwona kipindi anaingia ndani ya basi,kimagendo!




Wanausalama walimwagwa kila sehemu ya boda,hususani Mtukula na Namanga!Wakiamini kabisa mipaka hiyo ni lazima Ngesa angetumia kuingia kwani ndio njia kubwa wanayotumia watu wanaotokea nchi ya Rwanda!Operesheni hiyo ilikua ni kimya kimya,hakuna askari yoyote aliyejuwa kwamba mpakani Namanga wapo usalama wa taifa kwani wote walivaa kiraia na wengine walishika baiskeli zilizobeba machungwa na biskuti,wakijifanya wamachinga!

“Psii psiii,eyoo majiiii”

Mmoja wa wanausalama aliyefahamika kwa jina la Majala,alibeba boxi lililojaa biscuit na maji mkononi akizuga na kujifanya machinga,macho yake yalikuwa makini na sikioni alivaa kidude maalum cha kufanya mawasiliano,upande wa kushoto alionekana Abdallah ama Dulla,huyu alijifanya chokoraa na ombaomba lakini macho yake yote yalikuwa boda hata hivyo wengine walifanikiwa kuingia ndani ya boda ya Kenya,wakaanza kuranda huku na kule!

“Majala,unanisoma upo upande gani?”

Mmoja wa wanausalama alisikika na wenzake akiuliza!

“Nipo huku juu”

“Nimemuona”

“Ngesa?!”

“Ndioo”

“Una uhakika?”

“Ndio mwenyewe,nimemuona anakuja upande wako huo”

Tangu Ngesa anatembea akiranda huku na kule,alionekana na wanausalama na mara kadhaa waliangaliana lakini ilikuwa vigumu kuwatambua kwani walivyovaa isingekuwa rahisi hata kidogo!Mpaka anaingia ndani ya basi walimuona ingawa hawakuwa na uhakika sana kutokana na giza totoro,hiyo iliwafanya waitane wakiwa watatu ili watete jambo!

“Hapa,hatuna jinsi!Inabidi tutumie akili nyingi”

“Kivipi?”

“Nina wazo”

Mmoja wa wanausalama,akadakia hoja wote wakamtizama yeye!

“Ili kuhakikisha kama kapanda lile basi,inabidi tuwashirikishe polisi!”

“Tutaharibu”

“No,tutawaeleza ukweli.Ilimradi tu,tuwe na uhakika”

“Baada ya hapo?”

“Tutapiga simu mbele kule,wazuie basi.Tumkamate kirahisi”

“Wazo zuri”

Hoja yake ikaonekana kuwa na mashiko,wakamfuata askari mmoja mwenye cheo kikubwa na kumpa mkanda halisi,kila kitu kinavyokwenda na mtu wanayemsaka kwa wudi na uvumba!

Askari alishtuka,akatandwa na hofu lakini hakutaka kukahidi kwani lilikuwa jukumu lake,alichokifanya ni kuchukua picha ya Ngesa na kuwaita askari wenzake,akawaambia kila kitu kilichotokea!Basi,lilivyoanza kuondoka wakalisimamisha na kuingia ndani ili wahakikishe Ngesa ni mwenyewe!

“Abiria poleni na safari”

“Ahsante”

Mmoja wa abiria aliyekuwa nyuma akaropoka kwa sauti na baadhi yao wakamfuatisha kwa kusema ‘Ahsante’

“Nilichotaka kuwaambia ni kwamba karibuni Tanzania.Na hakikisheni mnafunga mikanda kwenye siti zenu kwa usalama wenu”

Askari huyo,alizidi kuyafanya maongezi yawe marefu huku akiwa na mtutu mkononi akaanza kutembea katikati ya kordo ya basi huku akimuangalia abiria mmoja baada ya mwingine,alivyofika kwa Ngesa akamtizama kwa kama sekunde tatu nzima na kugeukia upande wa pili,ambapo alitoa picha na kuangalia kama mtu huyo amefanana na picha aliyoshika!Baada ya kujiridhisha alizuga akizidi kutembea!

“Abiria,mimi naomba niwatakie safari njema!Dereva,endesha gari kwa makini”

Kitendo cha askari kushuka kuna baadhi ya abiria walisonya kwa kupotezewa muda wao,licha ya yote muda wote Ngesa alikuwa makini akili yake ilikuwa kazini.Bado hakutaka kuamini kama askari wameshuka,akiwa katikati ya mawazo konda akamgusa bega!

“Umepandia wapi?”

“Namanga”

“Umepitia wapi?”

“Kuna mwenzako,alikua chini pale alinipandisha”

“Nani?”

“Mimi simfahamu jina lake”

“Unashukia wapi?”

“Mwisho wa basi”

“Mwisho Dar”

“Ndio,nitashuka hapo”

“Kaa siti ya pale,hapo kuna mtu atapandia Arusha”

“Nitampisha”

“Nitakuja kuchukua nauli yangu,anza kujisachi”

Konda,hakujua mtu anayezungumza naye!Alijua tu ni abiria wa kawaida licha ya yote ilikuwa ni usiku, giza likamfanya asiweze kumuona sura vizuri!Baada ya mazungumzo hayo, Ngesa akashusha pumzi ndefu za kuchoka,alijihisi ni dhaifu sana kutokana na kutokula kwa kipindi kirefu!Basi,lilizidi kukimbia kwa kasi mno!Mpaka wanaingia Arusha,ilikuwa saa nne ya asubuhi!


****

Gari aina ya Pajero yenye namba za usajili TZ 6514 lilikuwa nyuma ya basi,ndani lilibeba wanausalama wanne wote walikuwa na bastola zenye risasi kumi na nane,tayari kwa mashambulizi endapo Ngesa angeleta ukahidi wowote ule!Amri iliyowapa kiburi ni kumuuwa kutoka kwa Ramadhan Nurdin,jambo lililowafanya wavimbe!Hata hivyo,walifanya mawasiliano na wenzao, waliokuwa Mkoani Kilimanjaro ili watege Njia panda.

“Kaeni hapo njiapanda,baada ya mizani.Nataka tum surprise Ngesa!Hatoamini”

“Tutakuwa hapo,ndani ya dakika mbili.Basi limefika wapi?”

“Arusha, tunaingia Sakina”

“Tupo kamili gado,kazi kwenu”

Swala hilo,halikuwa utani.Walidhamiria kumchukua Ngesa kimya kimya ndio maana operesheni hiyo iliendeshwa kijasusi,magari matatu yalifika mkoani Kilimanjaro, Njia panda na kutega pembeni kusubiri basi alilopanda Ngesa!Ndani walijaa wanausalama wakiwa na bastola pamoja na mitutu!Mtego walioweka,waliamini Ngesa angetoka angekuwa kidume kwanza waliiweka kati njia panda cha pili walijipanga kivyovyote vile.

“Kama nilivyowaambia Ngesa ni mtu hatari,ana mafunzo yote!Kwa taarifa nilizopata, alafu akileta ukahidi msisite kujitetea”

“Sawa mkuu”

“Sawa mkuu”Wote,wakaitikia!

Kazi ya Usalama wa taifa,haikuwa kuuwa wala kufanya wanachokifanya lakini hiyo ilikuwa ni amri kutoka kwa mkuu wao wa kazi na ilikuwa ni lazima ifanyike kisiri,ndiyo maana kila kitu kilipangwa kikamilifu.


*******

  ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG