Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

SIN SEASON 2 SEHEMU YA 9/10

   


SIN SEASON 2

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 9 KATI YA 10


Magreth na Evans wakafika nyumbani na wakaoga kwa pamoja.

“Kuna mahali nina hitaji kwenda kuna mtu nina hitaji kukutana naye”

Evans alizungumza huku akiwa ana vaa nguo zake.

“Ila mpenzi hizo nguo si chafu”

“Yaa nita kwenda kubalisha”

Magreth akatamani kumuomba avae nguo za Evans ila akasita.

“Sawa, ila usije ukaenda kuonana na huyo mtu ukiwa ume vaa hivyo”

“Usijali”

“Ehee uta rudi leo nikuandalie chakula?”

“Tuta zungumza kwenye simu”

“Sawa sawa”

Evns akampigia dereva taski na akafika nyumbani hapo kwa Magreth na wakaondoka kuelekea Hotelini alipo fikizia Evans.

“Kaka wife nimesha mpanga nilikuwa nina subiria simu yako tu”

“Basi twende unipishe hotelini, nibadili nguo kisha baada ya hapo nikaonane na mke wako”

“Sawa kaka”

Evans akafika hotelini na akabadilisha nguo huku akivalia suti ya rangi nyeusi ambayo ime mkaa vizuri mwilini mwake. Kwa muonekano huo ana imani kwa asilimia kubwa ana mshawishi nabii Sanga kuona ni mtu na biashara zake. Akatoka hotelini na kuingia kwenye gari na moja kwa moja wakaelekea hadi nyumbani kwa dereva taski na kumkuta mke wake akiwa amesha jianda kwa ajili ya kuelekea kanisani. Dereva taksi akamtambulia Evans kwa mkewe na kumueleza jinsi anavyo paswa kufanya na kuzungumza pale atakapo mkutanisha na nabii Sanga.

“Akisema ni ndugu yangu kivipi nita mjibuje?”

“Mke wangu kwani nabii Sanga ana fahamu ndugu zako wote. Wewe muambie ni mtoto wa mama mdogo alikuwa nje ya nchi ndio ame rudi na ana mpango wa kufanya biashara hapa Tanzania. Au una semaje kaka”

“Yaa ni kweli”

“Simple tuna kuwa tumesha maliza mchezo”

“Ila yule ni mtu wa Mungu akidanganywa ana fahamu?”

“Ila huu sio uongo mbaya ni uongo mzuri mke wangu. Kaka hapa yeye ana hitaji kufanya biashara hapa Tanzania, kama unavyo jua mtumishi wetu ana miradi mingi sana hapa nchini. Hivyo nina imani kwamba ana weza kumkubali sana kaka hapa na wakafanya biashara pamoja”

“Ni kweli, shemeji usiwe na shaka katika hili”

Evans naye aliendelea kumshawishi mke wa dereva taksi huyo ambaye naye kidogo ana onyesha kujawa na wasiwasi.

“Ume sema una itwa George nani?”

“Geogre Sanga”

“Una ona tena wameendana na majina yao ya ukoo. Muna weza kuwa ndugu aise?”

Dereva taksi alizungumza kwa furaha.

“Hapana, ila nina imani ni koo tu zina fanana”

Wakakubaliana na wakaondoka nyumbani hapo na moja kwa moja wakaeleka kanisani na dereva taksi huyo. Wakakuta ibada ikiwa imeanza. Evans akaka benchi la nyuma kabisa kwa maana sio mpenzi sana na mambo ya kanisa. Ibada ikamalizika majira ya saa moja na robo usiku na mke wa dereva taksi akamfwata nabii Sanga na kumuomba aweze kumkutanisha na ndugu yake ambaye ana hitaji muongozo wa kufanya biashara.

“Mlete ofisini”

“Asanye nabii wa bwana”

Mke wa dereva taksi akamfwata mume wake na Evans walipo simama na kumueleza jambo hilo.

“Muta nisubiri hadi nitakapo toka tuondoke wote”

“Usijali kaka”

Mke wa dereva taksi na Evans wakaingia ofisini kwa nabii Sanga na kumkuta akiwa na mke wake. Wakakaribishwa vizuri na kukaa kwenye masofa mazuri yaliyopo ndani hapo. Evans kila anapo mtazama nabii Sanga ana likumbuka tulio la kupunyuka punyuka kumuua siku aliyo mkuta akiwa na Magreth.

‘Ni muda wa kuwa karibu na maadui zangu’

Evans alizungumza kimoyo moyo huku usoni mwake akiwa ameweka tabasamu pana sana usoni mwake.

“Ehee Rose niambie sasa”

“Huyu ni ndugu yangu. Mtoto wa mama mdogo, ni mtanzania kama sisi ila alikaa nje ya nchi kwa kipindi kirefu sana. Hivyo alikuwa ana omba kupata muongozo wa kibiashara. Nikaona sio mbaya kukukutanisha naye mtumishi wa Mungu, nina imani una fahamu mambo kadhaa kwenye biashara”

“Yaa nina fahamu na ume mleta kwa mtu sahihi”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama kwa umakini sana Evans. Mrs Sanga naye aliye kaa pembezoni mwa mume wake ana mtazama Evans kwa macho yaliyo jaa matamanio kwani katika vijana wazuri wa sura alio wahi kuwaona basi huyu ana ongoza.

“Ehee kijana labda tuanzie kwenye jina lako. Una itwa nani?”

“Nina itwa Geogre.”

“George nani?”

“George Sanga”

“Waoo una jina langu la ukoo. Au sisi ni ukoo mmoja?”

“Hapana mzee wangu. Nina imani majina ya ukoo yame ingiliana”

“Sawa sawa, ehee niambie ni biashara gani ambayo wewe ulipanga kuja kuifungua hapa nchini Tanzania na ulipanga kuwekeza kiasi gani cha fedha katika hiyo biashara?”

“Ahaa kwanza nina hitaji kuwekeza kama dola bilioni mbili na nusu hivi. Hivyo nina hitaji kufahamu ni biashara gania mbayo nikiweka hiyo pesa ina weza kurudi kwa uharaka.”

Nabii Sanga na mke wake wakastuka sana kwa maana kiasi cha pesa alicho kitaja Geogre ni kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho kwa kijana mdogo kama yeye ni nadra sana kukimiliki. Mstuko huo wa nabii Sanga na mke wake hakika ukawa ni pointi ya Evans kutambua kwamba wazee hao wana penda sana pesa na kupitia nafasi hiyo watakayo mpatia ndio uta kuwa ni muda way eye kuwafilisi pesa zao zote kabla hajawaua.




“Waoo ni pesa nyingi sana hizo kijana. Kabla hatuja endelea tunge penda kufahamu back groud yako ya kimaisha pamoja na kibiashara”

Evans akakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akijaribu kutafakari uongoa ambao uta endana na ukweli.

“Dada una weza kutupisha”

Evans alimuambia mke wa dereva taksi na akanyanyuka na kutoka ofisini hapo.

“Mara baada ya baba yangu kuaga dunia nikiwa nina miaka mitano. Mama yangu aliweza kuolewa na tajiri mmoja nchini Marekani, ambaye aliweza kumzaa mdogo wangu wa kike. Nilipo kuwa na miaka kumi na mbili, baba yangu mlezi alianza kuniingiza kwenye biashara zake, moja wapo ikiwemo ni ya software na maswala ya elacronics. Baba yangu aliweza kuingia ubia na kampuni ya South Korea na ndipo walipo anza kutengeneza simu ziitwazo Samsung”

“Wooo kumbe hizi Samsung ni za kwenu?”

“Yes baba ana hisa za asilimia stini na moja kwenye kampuni hiyo, inayo sambaza simu zake kwenye mabara yote duniani.”

Uongo wa Evans uka mfanya nabii Sanga kutingisha kichwa huku akikubaliana na changa la macho hilo analo pigwa.

“Pia kampuni ya baba yangu miaka ya hivi karibuni ilizidi kujitanua katika kutengeneza vifaa vya majumbani kama AC, Tv, Laptop na bidhaa nyingine zenye brand ya Samsung.”

“Nilipo fikisha miaka ishirini na nne nikawa C.E.O wa makampuni yote ya baba, ikiwemo visima vyake vya mafuta vilivyopo nchi mbalimbali hapa duniani. Miaka miwili nyuma baba yangu alifariki na nikawa ndio mrithi wa kila kitu huku mdogo wangu akiwa ni msaidizi wangu katika baadhi ya makampuni. Nime kuja Tanzania kisiri siri ili kuhakikisha kwamba nina pata mtu ambaye nina weza kushirikiana naye katika kuwekeza miradi mikubwa.”

“Ume pata kijana. Ondoa shaka kabisa”

Nabii Sanga alizungumza kwa furaha sana.

“Kweli!?”

Evans alijikuta akiuliza kwa mshangao.

“Ndio, tuta kupa full support ikiwemo serikalini na uzuri ni kwamba watu wote wa serikalini sisi tuna wamuda.”

“Nashukuru sana”

“Usijali kijana, wewe tuambie ni nini una hitaji kufanya nchini Tanzania”

“Kutokana sifahamu fursa zilizopo nchini hapa. Ninge penda muweze kuniambia ni maeneo gani ambayo nikiweka pesa ita weza kurudi kwa asilimia mia moja”

“Kijana wangu George, ninge penda sana utupatia nafasi mimi na mke wangua. Tukajadili hili swala kisha kesho majira ya saa tano uta nipigia simu na kunieleza ni hoteli gani ambayo upo ili dereva wangu aweze kukufwata na kukuleta nyumbani kwetu. Nina imani kesho tuta itenga kwa ajili yako na kufanikiwa katika hilo jambo”

“Asanteni sana na Mungu awabariki”

“Amen nawe pia Mungu akutangulie”

“Ame”

Wakasimama na nabii Sanga akamkabidhi Evans kadi yenye namba zake za simu kisha, wakaagana na Ethana akatoka nje, akaingia kwenye gari ya dereva taksi na kuondoka eneo hilo.

“Nina washukuru sana ndugu zangu”

“Mambo yame kwenda vizuri shemeji?”

“Sana, ni watu wakarimu”

“Basi pale upo sehemu sahihi shemeji. Uta fanya nao biashara vizuri sana”

“Nashukuru”

Evans akatoa milioni moja na nusu kwenye koti leke iliyo fungwa vizuri na kumkabidhi dereva taksi. Akamkabidhi mke wake na kuihesabu na wote nyuso zao zikatawaliwa na furaha kubwa sana.

“Kaka sasa hivi una elekea wapi?”

“Nipitisheni Samaki Samaki hapo Mlimani City”

“Hakuna shaka”

Wakafika mlimani City na Evans akashuka ndani ya gari na dereva taksi na mke wake wakaondoka.

“Vipi upo ofisini?”

Evans alimuuliza Leila kwa kupitia njia ya simu.

“Yes baby ndio nina nina chukua kamisheni yangu ya siku kisha nina toka”

“Sawa nina kusubiria hapa nje”

“Hakuna shaka”

Evans mara baada ya kukata simu akampigia video call mpenzi wake aliye muacha nchini Russia. Akamuadithia mpango wake wote wa kuwa karibu sana na nabii Sanga na akamuomba aweze kutengeneza profile inayo onyesha uongo wake wote alio muambia nabii Sanga.

“Usijali lime kishwa hilo mume wangu”

“Jambo jengine nahitaji hicho kiwango cha pesa kiwe tayari”

“Ume pata mume wangu. Kitu kingine?”

“Hakuna mama yangu. Nina taka nika hakikishe nina wafanya wana kuwa ni masikini kupindukia”

“Una akili sana Evans wangu ndio maana nina kuaminia. Nita kuunga mkono kwa kila kitu”

“Nakupenda sana mke wangu”

“Nina kupenda pia mume wangu.”

“Tuta wasiliana”

Evans alizungumza huku akimtazama Leila anaye kuja eneo hilo

“Hakuna shaka”

Evans akakata simu kabla ya Leila kumfikia. Alipo mfikia wakakumbatiana kisha wakatoondoka eneo hilo kwa usafiri wa bajaji hadi nyumbani kwa Leila. Evans akamueleza Leila kila jambo alilo zumgumza na nabii Sanga ila hakumueleza kwamba alicho kizungumza ni uongo na kumfanya Leila naye kujawa na furaha kwa maana ana amini kwamba George(Evans) ana pesa nyinngi sana.

“Kesho nita hitaji twende nyumbani kwa nabii Sanga. Ila nita kutambulisha kama mke wangu wa ndoa”

“Waoo asante sana mume wangu”

“Usijali. Ila jambo la msingi ni wewe kuwa karibu sana na nabii Sanga na mpango wetu nina hitaji uweze kwenda kama vile tulivyo panga. Ume nisoma mke wangu”

“Asilimia mia mia moja nime kuelelewa”

Ili kuondoa usumbufu wa kupigiwa simu na Magreth. Evans akazima simu yake na usiku huo akautenga kwa ajili ya kumshuhulikia Leila ambaye hadi sasa hivi amesha kufa na kuoza mbele ya macho yake.

***

“Usiniambie muli fanya mapenzi!!?”

Josephine alimuuliza Magreth huku akimtazama usoni mwake.

“Kwa nini nikufiche sasa, yaani G amenipa kitu ambacho ni Evans pekee ndio alikuwa ana nipatia. Yaani haki ya Mungu ni mtamu sana yule mwanaume”

“Kuwa makini sana rafiki yangu. Asije akakuumiza moyo wako”

“Usijali nipo makini. Ila kuna jambo moja ame lifanya leo hadi nime shangaa”

“Jambo gani?”

“Tulikuwa tuna zungumzia maswala ya Evans pia tukawa tuna zungumzia jinsi na namna ambayo nilivyo kutana naye hadi kuachana naye. Huwezi amini tuikwenda kwenye ule mtaa nilio kuwa nina ishi, tukatafuta vibaja wote kisha akaanza kuwatembezea kichapo”

“Weee”

“Haki ya Mungu, yaani aliwavunja vunja vibaya hadi akafanikiwa kupata vyeti vya Evans”

Magreth akamuonyesha Josephine video ya vijana wa panya Road walio pigwa na Evans.

“So kwa nini alikwenda kulipiza kisasi kwa ajili ya mwanaume mwenzake?”

“Hata mimi sielewi, labda alimuonea huruma”

“Kwani Evans alikuwa ana jua kupigana?”

“Kidogo sana, si una jua ngumi za mtaani. Ila huyu ana pigana ki professional kabisa”

“Mmm kweli?”

“Ndio”

“Je alama ya kisu tumboni mwake anayo?”

Josephine aliendelea kuhoji huku akianza kujawa na mashaka mengi juu ya Geogre ambaye ndio Evans.

“Hana alama yoyote na huyu George mwili wake uma jengeka na misuli tofauti na Evans”

“Hiyo mwanaume yoyote awe bonge au mwemamba ana weza kutengeneza misuli mwilini mwake. Hana kitu kingine ambacho ana fanana na Evans?”

Magreth akaka kimya huku akijaribu kuvuta kumbukumbu za matukio aliyo yafanya na Evans kwa sili ya leo.

“Macho yake akikasirika ni sawa na macho ya Evans kabisa.”

“Nina hisi jamho”

“Jambo gani?”

“Asije akawa ni Evans huyu?”

“Mmmm haiwezekani akawa Evans”

“Ngoja picha yake yoyote unayo?”

“Ndio, nakumbuka tulipiga picha kadhaa tulivyo rudi kutoka kule kwa Tumbo”

“Ngoja mara moja. Tusije tukawa tume karibisha adui kwenye maisha yetu alafu baade akatudhuru”

Josephine alizungumza huku akiichukua simu yake mezani. Akamtafuta Samson na kumpigia simu.

“Dogo vipi ume lala?”

“Hapana vipi sister?”

“Salama, upo wapi?”

“Nipo nyumbani”

“Tuna kuja sasa hivi”

“Vipo kwema?”

“Kwema, ila kuna jambo nahitaji utupatie uvumbuzi”

“Sawa”

Josephine akakata simu na kumtazama Magreth ambaye muda wote amekaa kimya akimtazama.

“Kwa hiyo una taka kudhibitisha jambo gani?”

Magreth alihoji.

“Mage wewe ni rafiki yangu. Endapo uta kuwa na mtu mgeni ambaye hatumjui na wala kujua chimboko lake ni wapi ni lazima tufanye jambo na pia angalia nafasi tulizo kuwa nazo hapa serikali. Mimi ni chief staff. Siri zote za raisi zipo mikononi mwangu hata wewe una zijua. Ana weza akawa ni adui ambaye ana tumia udhaifu wa kimapenzi kuhakikisha ana jiweka karibu na kujua mambo mengi kupitia siis pasipo sisi kustuka”

“Hivyo ndivyo Mungu alivyo kuonyesha au?”

“Hapana sio Mungu ila nikiwa kama binadamu ni lazima kuhakikisha kwamba nina weza kuingeza akili yangu kwenye mambo mengine mengine. Najua una mpenda Geogre na una mthamini sana, nakuomba sana twende kwa Samson tuka jiridhishe kwamba upo na mtu wa aina gani. Tafadhali mpenzi wangu nina kuomba uni kubalie”

Josephine alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyenyekevu. Magreth akashusha pumzi nyingi kisha akakubaliana na rafiki yake. Wakaingia kwenye gari na kuondoka nyumbani hapo. Wakafika nyumbani kwa Samsoni majira ya saa tano usiku na akawakaribisa ndani.

“Vipi mbona mupo juu juu, kama kuna tatizo?”

“Samson una mkumbuka yule kijana uliye muomba namba ya simu?”

“Yes namkumbuka vizuri”

“Tuna kuomba ututafutia background yake kabla hatuja mdhibitisha kuwa shemeji yetu”

Josepehine alizungumza huku akimkazia macho Samson.

“Mmmm sawa, kwani dada Mage mumesha kubaliana na jamaa?”

“Ndio”

“Ana itwa nani?”

“George Sanga”

“Una picha yake”

“Ndio”

Magreth akamkabidhi Samson picha inayo waonyesha wakikwa na George Shika. Evans akaingia chumbani kwake na baada ya dakika akatoka akiwa na laptop yake. Akachomeka waya wa USB kutoka kwenye simu ya Magreth na kuingia kwenye laptop hiyo.

“Una mtafuta kipivipi?”

Magreth alihoji.

“Nina scan sura yake nina imani ina weza kutupatia full details zake”

“Sawa”

“Ila kabla hatuja endelea kwani kuna kitu gani ambacho mume kihisi kwake hadi muna hitaji niweze kufanya mambo haya yote?”

“Hakuna tulicho kihisi ila wewe ifanye tu kazi yako”

Josephine alijibu na Samsoni akawatazama kwa sekunde kadha ana kuhisi kuna jambo ambalo ana fichwa na dada zake hao. Samson akaanza kuifanya kazi hiyo ya kutafita historia ya Samson. Hazikupita dakika hata tano akawa amesha pata taarifa nzima ya George Sanga. Macho yakamtoka huku akiwa amejawa na mstuko mkubwa sana.

“Ohoo Mungu wangu!!”

Samson alihamaki huku macho yakiwa yame mtoka.

“Nini?”

Magreth aliuliza kwa mstuko na kumfanya Samson kuwageuzia laptop yake.

“Jamaa ni tajiri wa dola bilioni arobaini na tano za Kimarekani na ndio tajiri mwenye umri mdogo duniani”

Samson alizungumza na kumfanya Magreth na Josephine kunaza kuitazama habari hiyo ambayo hata Josephine na Magreth walibaki midomo wazi kwa maana kwa jinsi anavyo ishi George(Evans) ni tofauti kabisa na utajiri wake.

“Haya mama ume dhibitisha. Hata hiyo Samsung yako unayo itumia ime toka kwenye kampuni yake. Una jengine”

Magreth alimuuliza Josephine aliye baki mdomo wazi na kushindwa kujibu swali hilo kwani ina onyesha Evans ni raisi wa Tanzania kwa kuzaliwa ila ana urai wa Marekani kwani ndipo sehemu aliyo kulia na kuishi na wazazi wako.

“Samahani rafiki yangu nilifanya hivi ili kuweza kumjua shemeji yangu ni mtu wa aina gani?”

Josephine alizungumza kwa unyonge huku akimtazama Magreth usoni mwake kwa aibu kubwa aliyo ipata. Pasipo kujua kwamba hicho wanacho kisoma hapo ni uongo mtupu.

***

“Mke wangu njoouone”

Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amekaa kitandani huku ameipaka laptop mapajani mwake. Mrs Sanga akafunga kabati la nguo na kumsogelea mume wake.

“Huyu George Sanga ana utajiri wa dola bilioni arobaini na tano”

“Mmm alafu bado ni mdogo sana”

“Yaani, wee acha”

“Mume wangu kama ame tufwata wenyewe hii ni golden chance ambayo haito jirudia mara mbili”

“Una taka kusema nini?”

“Ina tupasa kuhakikisha kwamba katika hayo mabilioni yake ya dola tuna mfilisi kiakili hadi yana ingia kwenye akauti zetu na kwa kuanza tuta anza na hizo bilioni mbili zake na nusu anazo taka kuzitoa kwa ajili ya miradi hapa nchini. Nina amini mume wangu una akili ya kumfanya atoa pesa pasipo yeye mwenyewe kujua kama ana liwa au una semaje mume wangu”

Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya ushawishi iliyo mfanya nabiiS anga kufkiria kwa sekunde kadhaa kisha akatabasamu,

“Ndio maana nilikuoa mke wangu. Una akili ya kufikiria nje ya boksi. George Sanga ata kuwa ni mnofu mdogo mdogo kwetu kabla ya kwenda kwenye mnofu mkubwa wa hadhina ambayo nikilala, nikifumba macho nina iyona hiyo. Nina hitaji hao matajiri wakubwa duniani, waje kunisujudia siku moja. Hahaaa”

Nabii Sanga alizugumza kwa kujiamini huku akicheka kwa kicheko cha kebehi pasipo kufikiria wanayo yafikiria wao, Evans naye ana yafikiria hayo hayo.



“Na tukimfilisi, ata potea kwenye macho ya watu na kwenda sehemu kusipo julikana”

Mrs Sanga alizungumza huku akiishika laptop ya mume wake na kuiweka mezani. Akalifunua shuka na taratibu akaanza kumchezea jogoo wa mume wake, mrs Sanga akaongeza utundu na kuanza kumnyonya na kumfanya nabii Sanga kuanza kutoa miguno ya kimahaba. Nabii Sanga naye akaanza kumuandaa mke wake kwa kumnyona kila mahala ya mwili wake ambayo ana fahamu ina leta hisia za kimahaba na baada ya muda wakaanza mtanange wa kukatana shoka.

***

Asubuhi na mapema Evans na Leila wakaelekea hotelini alipo panga Evans.

“Bee hili gauni lita nifaa kweli kwenda kuonana na nabii Sanga pamoja na mkewe?”

Leila aliuliza huku akiwa amesimama mbele ya Evans aliye anza kumtazama kuanzia juu hadi chini.

“Maduka asubuhi hii yatakuwa wazi?”

“Mmmm mengi yana funguliwa kuanzi saa mbili asubihi”

“Sawa, tuta kwenda uka nunue gauni zuri. By saa tano ina bidi nimpigie nabii Sanga”

“Sawa mume wangu”

Ilipo timu saa mbili na nusu wakaelekea maduka yaliyopo eneo la karibu na hoteli hiyo. Kila mtu aka nunua nguo alizo amini kwamba zita mfaa kwa kikao hicho ambacho wana amini kwa asilimia mia moja ni cha ushindi. Wakarudi hotelini na majira ya saa tano kamili Evan akawasha simu yake na kumpigia nabii Sanga na kumueleza hoteli aliyopo.

“Dereva wangu ata fika hapo hotelini na ata kupigia”

“Nashukuru. Ila nipo na mke wangu nita fika naye”

“Hakuna shaka kijana”

Nabii Sanga akakata simu. Baada ya dakika arobaini, simu ya Evans ikaita na akaingia namba ngeni.

“Nimesha fika”

Sauti ya kiume ilisikika.

“Sawa nina shuka”

Evans akakata simu na kumsogelea Leila aliye simama kwenye dreasing table akijiweka vizuri nywele zake.

“Ume penda sana mke wangu”

“Kweli?”

“Haki ya Mungu upo vizuri.”

“Twende sasa tuka pange mipango yetu”

“Sawa”

Wakashuka gorofani na kutoka nje ya hoteli. Wakamkuta dereva akiwa amesimama nje ya gari aya ya Range Rover. Wakasalimiana naye na kuingia ndani ya gari kisha wakaelekea nyumbani kwa nabii Sanga. Wakakaribishwa kwa heshima zote na nabii Sanga pamoja na mke wake. Uzuri wa Leila ukampumbaza sana nabi Sanga na kujikuta akiwa akimtamani sana Leila.

“Karibuni sana”

Mrs Sanga alizungumza huku usoni mwake akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Naye moyoni mwake ametawaliwa na matamanio ya kimapenzi juu ya Evans.

“Tuna shukuru. Kuta neni na mke wangu ana itwa Leila Sanga. Leila hawa ni watumishi wa Mungu, huyu ana itwa nabii Sanga na huyu ni mke wake”

“Nina shukuru sana kwa kuwafahamu”

“Karibuni sana Tanzania”

Nabii Sanga alizungumza kwa kuchachawa pasipo kuelewa kwamba Leila ndio silaha ya maangamizi kwake kwa maana Evans alisha weza kusoma saikolojia ya nabii Sanga na mke wake kwamba ni watu ambao wana penda sana mapenzi.

“Tuna shukuru sana. Wazee wangu au nipende kuwaita wazazi wangu.”

“Tunge penda uwe mtoto wetu wa hiyari”

Nabii Sanga alizungumza huku uso wake ukiwa ume tawaliwa na furaha.

‘Aisee dogo ana kula demu mkali sana’

Nabii Sang alizungumza kimoyo moyo huku akimtazama Leila kwa macho ya kuiba iba.

“Tuna shukuru kwa hilo. Nime kuja rasmi sasa ili niweze kufahamu ni namna gani ambavyo tuna weza kuanzisha biashara Tanzania”

“Jana tuli kaa na mama yenu hapa. Tukaona kwamba biashara ya mtandao wa simu ita kuwa ni nzuri sana kwa maana wewe una kampuni yako ya simu za mikononi so endapo uta fungua mtandao wako wa mawasiliano nina imani ita kuwa ni biashara nzuri na ita kuingizia pesa nyingi sana. Watanzania wengi huwa wana penda sana ofa za vifurushi. Endapo uta wawekea vifurushi vizuri vya kupiga na kuingia kwenye internet nina imani uta pata soko kubwa sana”

Nabii Sang alizungumza alizungumza kwa sauti ya upole kiasi.

“Ahaa ila kwa Tanzania kuna ushindani mkubwa sana na isitoshe kuna makampuni mengi kutoka nje yana fanya biashara hiyo na yapo hapa nchini kwa miaka mingi sana na ina wateja wengi”

“Ni kweli unacho zungumza mwanangu. Ila jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba una kuwa mbunifuu kwenye hiyo biashara. Nina kuapia mwanangu, katika mwaka wa pili wabiashara yako uta kuwa mbali sana kichumi na hata hiyo pesa unayo amua kuwekeza nina uhakika wa asilimia kubwa sana ita kuwa imesha rudi”

“Mke wangu hapo una semaje?”

Evans alimuuliza Leila huku akiwa amemshika mkono wake.

“Mmmm hivi hiyo biashara haina process nyingi za kufwata. Kuanzia usajili, kufunga mitambo na mambo mengine?”

“Kila jambo lina hatua binti yangu na katika biashara hivyo vitu ni vya kawaida gani. Ila uzuri ni kwamba serikali nzimma ipo mikononi mwetu. Kuanzia raisi ambaye kijana wake wa kiume ame muoa binti yangu na uzuri ni kwamba binti yangu hivi sasa ni mmoja wa washauri wa raisi”

“Ahaa hongereni sana”

“Tuna shukuru. Hivyo hayo mambo ya kupata eneo la kufungulia biashara na usajli nina weza kuyashuhulikia”

Nabii Sanga alizungumza kwa kujiamini. Simu ya Evana ikaita, akaitoa mfukoni na kuona ni namba ya Magreth.

“Samahani jamani dakik kadhaa”

Evans alizungumza huku akinyanyuka na kutoka nje. Akaipoke simu na kuiweka sikioni.

“Hei baby mambo vipi?”

Magreth alisalimia kwa furaha sana.

“Salama mke wangu. Nipo kwenye kikao kama huto jali nina kuomba tuzungumze mara baada ya kumaliza”

“Sawa mume wangu. Ila nina swali kama huto jali?”

“Uliza tu”

“Mbona jna usiku siku yako ilikuwa haipatikani?”

“Ilikwisha chaji na nilisahau kuiweka chaji”

“Aha…pole mume wangu”

“Nina shukuru. Nita kutafuta niki toka kwenye kikao”

“Sawa. Mwaaa”

Magreth akambusu Evans.

“Nina shukuru baby”

Evans akakata simu na kurudi ndani na kuwakuta wakicheka kwa furaha sana.

“Aisee mke wangu ni mchehi sana”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama jinsi Evans anavyo kaa.

“Kweli ehe?”

“Yaa yaani dakika mbili hizi tume mzoea sana kana kwamba tume kutana kwa kipindi kirefu”

“Wazee wangu nina shukuru sana kwa ushauri wenu. Kuna simu muhimu sana ime ingia na kuna mahali nina hitajika kama hamuto jali niende kisha nita rudi kumpitia mke wangu”

“Ahaa kama ina wezekana uka enda na gari yetu”

Nabii Sang alizungumza

“Nita shukuru sana muta kuwa mume nisaidia”

“Sawa”

“Baby nina kuomba mara moja”

Evans alizungumza na wakatoka nje na Leila.

“Ndio mume wangu”

“Una lisaa moja la kuhakikisha una mtesa nabii Sanga kihisia. Hakikisha hatoki mikononi mwako”

“Usijali mume wangu nina elewa nini cha kufanya”

Wakarudi ndani na nabii Sanga akamkabidhi funguo ya gari jengine aina ya Toyota V8.

“Ipo full tank hivyo una weza kuzunguka mjini bila wasiwasi”

“Nashukuru”

Evans akaondoka nyumbani hapo kwa nabii Sanga huku akiwa amejawa na furaha kwa maana kama wame weza kutoa gari la garama kiasi hicho hivyo ni rahisi sana kwa yeye kuendelea kuwa karibu na nabii Sanga.

***

Simu ya Julieth ikaanza kuita taratibu. Akaitazama namba hiyo ngeni inayo ingia katika simu yake. Akajifikiria kwa sekunde kadhaa huku akijiuliza ni nani ambaye ana mpigia kwenye namba hiyo ambayo ni watu wachache sana ambao wana mpigia. Akanyanyuka na kufunga mlango wa ofisini kwake na kuipokea namba hiyo.

“Habari yako Mrs Jery Mtenzi”

Sauti ya kike ilisikika vizuri katika simu yake.

“Salama nani wewe?”

“Mimi nina itwa Ms Tramp ni balozi mpya wa Marekani hapa nchini Tanzania”

“Ahaa okay. Una hitaji nini?”

“Nina omba mchana wa leo kama ita wezekana tuweze kukutana Serena hoteli tuweze kuzungumza mambo mawili matatu?”

“Kiofisi au binafsi”

“Ni binafsi kama hutojali”

“Kwanza una fahamu una zungumza na nani?”

“Yes nina zungumza na Julieth Sanga mmiliki wa kundi la majasusi ukisaidiana na baba yako. Muna dili na biashara haramu na moja wapo ikiwa ni kuhusika na kifo cha mmoja wa wapelelezi wa ngazi za juu sana kwa kutegewa bomu ndani ya gari”

Maneno hayo yaka mstua sana Julieth hadi akahisi mikono yake ikimuishia nguvu.

“Nina hisi ume wrong number?”

Julieth alijikaza kuzungumza maneno hayo.

“Hapana miss Julieth, nina full details zako, baba yako pamoja na mama yako. Na familia yako ina husika kwa asilimia mia moja kwa kuchonganisha Tanzania na kundi la Al-Shabab lililo lipiza kwa kulipua jiji la Dar es Salaama. Kama una nibishia hizi data zote uta zikuta ofisini kwa baba yako mkwe. Saa nane kamili uwe peke yako nina kuhitaji Serena Hoteli ukifika hapo nipigie simu nami nita kuelekeza ni wapi nilipo”

Simu ikakata na kumfanya Julieth kuiangusha chini simu yake huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi. Akajaribu kutafakari ni nani ambaye ame toa siri hizo ila akakosa jibu sahihi. Kwa haraka akaikoka simu yake na kuitafuta namba ya baba yake na kumpigia simu.

“Baba mbona una chelewa kupokea simu?”

Julieth alizungumza kwa wasiwasi mkubwa sana huku akitetemeka kwa woga.

“Vipi kwema?”

“Sio kwema baba?”

“Kwa nini?”

“Kila kitu tulicho kifanya kime kaa wazi”

“Kime kaa wazi kivipi?”

“Kipo wazi baba nielewe basi”

“Upo wapi?”

“Nipo ofisini”

“Njoo nyumbani”

“Hapana muda wangu hauniruhusu kuja nyumbani, Tukutane njiani tuzungumze”

“Mmmm”

“Ndio baba fanya hivyo”

“Sawa”

Julieth akakata simu, akachukua pochi yake na kueleka ofisini kwa raisi Mtenzi.

“Muheshimiwa nina omba ruhusa ya kwenda kuonana na baba”

Julieth alizungumza kwa wasiwasi hadi raisi Mtenzi akagundua wasiwasi huo.

“Vipi mwanangu, kwema huko?”

“Ndio baba ni kwema, ila kuna jambo muhimu sana nina bidi kwenda kuzungumza naye”

“Sawa, uta kwenda na walinzi”

“Kama ina wezekana muheshimiwa nina kuomba niende peke yangu muheshimiwa”

“Ila una tambua sio salama kutembea peke yako?”

“Ndio baba ila nina kuomba san asana niweze kwenda peke yangu”

Raisi Mtenzi akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akamkaruhusu. Julieth akatoka ofisini hapo na kuelekea lilipogari analo litumia kwa safari zake binafsi. Akaingia ndani ya gari na kuondoka ikulu. Akampigia baba yake na kumuomba waweze kukutana sehemu ambayo ni karibu sana na hoteli ya Serena. Julieth akawa wa kwanza kufika eneo hilo. Baada ya dakika kumi nabii Sanga akasimamisha gari lake pembeni ya gari la Julieth. Juliethakashuka kwenye gari na kuingia katika gari la baba yake.

“Ume nistua Julieth kuna nini?”

“Baba hapa nilipo sielewi nime changanyikiwa sana”

“Kwa nini?”

“Kuna hii namba ime nipiga. Huyu aliye piga ana jiita ms sijui Trump gani. Ana sema kwamba yeye ni balozi mpya wa Marekani hapa nchini Tanzania. Ameweza kuzungumza siri za kikosi chetu tunacho kimiliki, biashara za madawa ya kulevya tunazo ziendesha. Mfarakano kati ya nchi yetu na Al-Shabab yaani kiufupi wana jua kila kitu kuhusiana na mimi, wewe mama na familia yote kwa ujumla”

“Nabii Sanga akashusha pumzi nyingi sana huku akihisi moyo una kwenda kumchomoka kwa wasiwasi.

“Kwa hiyo ana taka nini?”

“Ameniambia saa nane kamili juu ya alame niwe pale Serena. Nikileta mchezo ana weza kumueleza baba mkwe siri zote. Hembu piga picha kama akimueleza baba mkwe ita kuwaje?”

Nabii Sanga akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akijaribu kutafakari ni nani ame vujisha siri.

“Huku wahi kumuambia mtu yoyote juu ya siri hizi?”

“Hapana baba. Mimi sio mjinga hata mume wangu mwenyewe sija mueleza chochote kuhusiana na hii hali”

“Duuu sasa fanya hivi.Nenda kamsikilize na udhibitishe kabisa ni balozi wa nchini Marekani hapa Tanzania. Kama akiwa ni mjinga mjinga, siku ya leo hato imaliza”

“Baba na ana jua kwamba wewe ulimua yule mpelelezi kwa kutuma vijana na kumuwekea bomu ndani ya gari lake”

“Nabii Sanga akayatumbua macho yake huku akiwa haamini anacho kisikia kwa mwanaye huyo”

“Una sema kweli?”

“Ndio maana nika kuambia kwamba ana full details zangu, zako, za mama na familia yetu kwa ujumla”

“Ohoo Mungu wangu. Kamsikilize na atakacho kihitaji sisi tuta fanya ila kwa sharti moja”

“Sharti gani”

“Ahakikishe ana zika kila kitu anacho kijua endapo hato fanya hivyo haijalishi yeye ni balozi au hizi data zipo ndani ya nchi yao, tuta hakikisha kwamba tuna rudisha mapambano kadri ya uwezo wetu. Ume nielewa?”

“Ndio nime kuelewa baba”

Maneno ya nabii Sanga yakampa ujasiri mkubwa sana Julieth na kujikuta akijiwa na nguvu mpya huku wasiwasi na mashaka ambayo yalimtawala yakimuisha moyoni mwake na yupo tayari kukutana na balozi huyo wa nchi ya Marekani.



“Uta nijulisha ukitoka huko”

“Sawa baba”

Nabii Sanga akamshika Julieth kiganja cha mkono wake wa kulia na kukiminya kidogo ikiwa ni ishara ya kumpa ujasiri wa kwenda kuonana na balozi huyo. Julieth akashuka kwenye gari lake. Akaelekea moja kwa moja katika hoteli ya Serena. Akaelekezwa na mlinzi ni wapi asimamishe gari lake na akafanya hivyo. Akatazama saa yake ya mkononi na ina onyesha zime salia sakika kumi na nne kabla ya kufika saa nane kamili mchana. Akaa ndani ya gari hadi ilipo timu saa nane kamili akashuka na kuelekea mapokezi. Akapiga namba iliyo mpigia na ika pokelewa.

“Nime fika”

“Waoo ni jambo zuri. Ata kuja mwanaume mweupe ana upara kichwani mwake na amevalia suti nyeusi na katika upande wa kushoto wa koti lake la suti kuna kibendera kidogo. Ata kuleta sehemu nilipo”

“Sawa”

Julieth akakata simu na baada ya dakika tatu akamuona mwanaume huyo ambaye akampa ishara ya kuongozana naye kueleka alipo balozi huyo. Wakaingia kwenye lifti na kupandisha hadi gorofa ya saba. Wakatembea kwenye kordo hiyo yenye walinzi sita walio valia suti nyeusi. Mwanaume huyo akamnyooshea Julieth mkono wa kulia kamaishara ana omba kitu.

“Nini?”

Julieth aliuliza huku akimkazia macho.

“Simu yako”

Julieth akamkabidhi mwanaume huyo simu yake. Mlango uka gongwa wa chumba kilichopo mbele yao uka gongwa mara mbili na akatoka mlinzi wa kike.

“Nyoosha mikono”

Julieth akatii hivyo na akanyosha mikono yake upande wa kulia na kushoto. Akakaguliwa na msichana huyo alipo onekana hana silaha ya kumdhuru kiongozi huyo akaingia ndani ya chumba hicho kikubwa sana.

“Kaa hapo”

Mlinzi huyo wa kike alizungumza huku akimuonyesha Julieth sofa zilizopo eneo hilo. Julieth akaketi kwenye moja ya sofa na balozi huyo akatoka chooni huku akiwa ana jifuta futa mikono yake na kitaulo cheupe.

“Karibu sana Julieth Sanga”

“Nashukuru”

Julieth alijibu huku akimtazama mwana mama huyo aliye jawa na tabasamu pana usoni mwake. Mwana mama huyo akaka kwenye sofa linalo tazamana na Julieth. Akampa ishara mlinzi wake huyo wa kike na akaleta faili lenye rangi nyeusi na kumkabidhi balozi Trump.

“Nchi yangu ime weza kujitosheleza kwenye kila aina ya nyanja, ukianzia kiuchumi, kisiasa, kipesa na kijasusi pia. Ume weza kuchukua nafasi katika white house ya Tanzania ila mikono yako na familia yako ikiwa ni michafu sana tena sana.”

Balozi huyo alizungumza huku akiwa ame lifunua faili hilo.

“Ila nina imani kwamba tuna uwezo wa kuwachukulia hatua za kisheria wewe, mama yako na baba yako na kila aina ya pesa haramu muliyo ipata basi tuna weza kuzizuia katika mabeki yote duniani mulipo zificha.”

Balozi Trump aliendela kuzungumza kwa vitisho ila kwa sauti ya upole sana na kana kwamba maneno anayo yazungumza hapo ni mazuri kwa Julieth.

“Nime jaribu kushangaa ni kwa nini nchi ya Tanzania hadi sasa hivi haijui upande wa giza wa baba yako pamoja na familia yake. Isitoshe nina shangaa raisi wa nchi hajui chochote kuhusiana na nyinyi. Una kula naye una shinda naye ila hajui”

“Tukiachana na baba yako. Mama yako pia ni muuaji, alimuua kimada wake baada kwa sumu kali, ila nchi yenu haijui, ila sisi tuliopo mbali kwa maelfu ya miles tuna jua. Hii inaonyesha dhahiri nchi yenu ina ongozwa kwa maono pasipo kufanya upelelezi wa kina”

Julieth akaendelea kukaa kimya huku akimkazia macho mwana mama huyo. Balozi Tramp akamkabidhi faili hilo na akaanza kulipitia taratibu na kuona picha zake, za familia yake. Akastuka sana kuiona meli ambayo ndipo kilipo kikosi chao. Akaona biashara zote haramu, wanazo zifanya huku picha zake kwa baadhi ya mikutano anayo ifanya na kikundi chake nacho ikiwemo hapo.

“Tuna kujua vizuri sana. Baba yako ni mtenda dhambi mkubwa anaye tumia jina la Mungu kuficha dhambi zake.”

“Muna hitaji nini kwetu”

Julieth aliona ni heri ajue nia na lengo la nchi hiyo.

“Muna vitu viwili tunavyo hitaji kutoka kwenu”

“Vitu gani?”

“Mkataba wa makubaliano ya nchi yetu na kundi la Bokoharamu na endapo mkataba huo tukiupata ni lazima uhakikishe kwamba una mua baba yako mkwe, raisi Mtenzi”

“Jambo la pili tuna hitaji uhakikishe kwamba tuna ipata hadhina ya dhahabu kupitia watu wako. Ukikamilisha hayo, kila unacho kiona hapo na tunacho kijua sisi tuta kwenda kukisahau.”

Julieth akaka kimya kwa dakika mbili huku akimkazia macho mwana mama huyo.

“Ni hivyo tu?”

“Yes Julieth ni hivyo tu ndio tunavyo vihitaji”

Taratibu Julieth akasimama, mlinzi akatoka kusogea karibu ila balozi Trump akampa ishara ya kumzuia.

“Nisikilize vizuri sana na uni elewe. Mume kosea mtu wa kublack mail. Labda nikupe siri moja ambayo wewe na watu wako hamuijui. Nipo tayari kufa kwa ajili ya nchi yangu na si familia yangu na sinto kuwa kibaraka wa nchi yako kwa sasabu hata nikifa mimi basi hadhina iliyopo katika nchi yangu ita kwenda kuupita uchumi wa nchi yako na muta kuwa chini ya nyayo zetu na nina iona Tanzania yenye nguvu mara mbili ya Marekani.”

Julieth alizungumza kwa ujasiri hadi balozi Trump akastuka kidogo kwa maana aliamini kwa kutumia vielelezo alivyo kuwa navyo basi wana weza kumtumia Julieth kutekeleza mipango yao.

“Waoo ume jiamini vizuri sana Julieth”

“Mimi ni mtoto wa Simba, kamwe siwezi kuja kuwa fisi au paka”

Julueth mara baada ya kuzungumza hivyo akaanza kutembea kuelekea mlangoni.

“Ume sahau jambo moja Julieth”

Kauli hiyo ikamfanya Julieth kusimama, akashusha pumzi kisha akamgeukia balozi Trump.

“Una weza kwenda na hili faili uka muonyeshe baba yako. Nina imani kwamba wewe bado una akili za kitoto na wala hujui mambo yana kwenda vipi. Ila baba yako na mama yako wakiona hivi basi wata elewa nini tuna maanisha. Mchana mwema”

Balozi Trump akamkabidhi Julieth faili hilo lenye rangi nyeusi huku juu likiwa limeandikwa kwa maandishi mekundu TOP SECRETY. Julieth akalitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatoka ndani hapo. Akakabidhiwa simu yake na moja kwa moja akaelekea kwenye gari lake. Machozi yakaanza kumtoka huku woga mwingi ukiwa ume mtawala. Hakika masharti aliyo pewa ni magumu sana, hapo ndipo akaanza kuyakumbuka maono ya Josephine alipo muambia raisi Mtenzi kwamba ana paswa kuwa makini sana kwani Wamarekani wana uwinda mkataba ambao waliingia na kundi la Bokoharamu na endapo mkataba huo uta toka au kufichuliwa na nchi ya Tanzania, basi una weza kusababisha nchi ya Marekani kuongeza maadui ambao hajui wata kuwa ni nani na nani. Julieth akampigia baba yake.

“Baba upo wapi?”

“Nipo nyumbani mwanangu, vipi mbona una lia”

“Nina kja baba”

“Kwa hali hiyo una weza kuendesha gari?”

“Ndio”

“Sawa nakusubiria”

Julieth akakta simu na kuwasha gari na kuondoka hotelini hapo kwa mwendo wa taratibu.

***

“Baba Julieth vipi?”

Mrs Sanga aliuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi.

“Mtoto ana kuja”

“Ehee Mungu huyo balozi ata kuwa ame mueleza nini?”

Mrs Sanga aliuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana. Chumbani hapo hakukulika hata mgeni waliye muacha sebleni hakika wame msahau kwani tukio hilo liliweza kuvuruga amani yao.

‘Baby njoo unichukue bwana, watu wenyewe wame niacha sebleni, sijui kuna tatizo gani lime wapata’

Leila alituma meseji hiyo kwa Evans.

‘Ume shindwa kumpagawisha huyo mzee?’

‘Hawaeleweki kwa kweli, sijui wame kumbwa na nini. Njoo bwana tuondoke zetu’

‘Poa nina kuja’

Macho ya Leila yakatazamana na Juieth anaye ingia mlangoni hapo. Kwa kumtazama tu una weza kugundua kwamba hayupo sawa kwani macho yake yame tawaliwa na uwekundu mithili ya mvuta bangi anaye jifunza.

“Habari yako”

Leila alimsalimia Julieth ila hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kuanza kupandisha ngazi kuelekea gorofani huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika faili lenye rangi nyeusi.

‘Mmmm ana nini huyu?’

Leila alijiuliza na wala hakushangaa sana kwa maana sura ya Julieth sio ngeni kwake kwani alisha wahi kuiona kwenye tv kwa mara kadhaa. Julieth akagonga mlango wa chumba cha wazazi wake na nabii Sanga akafungua mlango. Julieth akapitiliza hadi ndani pasipo kuzungumza chochote, akajitupa kitandani huku akiwa na mawazo mengi sana.

“Julieth kime tokea nini?”

Mrs Sanga aliuliza huku akimtazama mwanaye.

“Yaani sijio ita kuwaje baba”

“Ita kuwaje nini?”

Taratibu Julieth akakaa kitako na kumkabidhi baba yake faili hilo. Nabii Sanga kaanza kulifungua na kuanza kutazama kilicho ndani. Mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa woga mwingi sana. Mrs Sanga akamsogela mume wake naye macho yakamtoka.

“Wamejuaje?”

Nabii Sanga aliuliza huku akiwa ametawaliwa na woga mkubwa sana.

“Hata sijui baba”

Julieth alijibu kwa sauti ya unyonge mkubwa sana. Katika siku ambazo familia ya nabii Sanga ime tawaliwa na hofu kubwa ni siku hii. Kila mmoja akahisi kama mwisho wao ume wadia. Mlio wa gari ukamfanya nabaii Sanga kutembea kwa kasi hadi dirishani na kuchungulia na kuona gari lake likiingia na George(Evans) akashuka kwenye gari.

“Amerudi”

Nabii Sanga alizungumza huku akifunika dirisha hilo.

“Nani?”

Julieth aliuliza huku akimkazia macho baba yake.

“Kuna kijana mmoja ni bilionea wa kimarekani. Ametufwata na kutuomba tuweze kumpatia idea ya biashara hapa Tanzania kwa maana ana hitaji kuwekeza dola bilioni mbili na nusu za Kimarekani katika mradi wowote hapa nchini”

“Mmmmm!!”

Julieth akaguna tu kwa maana akili yake kwa sasa haiwazii kabisa maswala ya biashara.

“Mume wangu ngoja kwanza. Hili swala tuna limaliza vipi?”

“Hilo sio jambo la kuzungumza juu juu. Tutulize kwanza vichwa, kwa sasa twende tuka zungumze na wageni”

Nabii Sanga na mke wake wakatoka ndani hapo na kuelekea sebleni.

“Nime rudi jamani, nina shukuru sana kwa kila jambo”

“Usijali kijana wetu, nina imani tuta zidi kuwasiliana. Ukiwa tayari wewe nipigie tu simu tuta panga”

“Usijali mzee wangu. Ila mbona kama sura zenu zina wasiwasi?”

“Aha….hakuna kitu George kila jambo lipo vizuri”

Macho ya Evans yakaanza kumtazama Julieth anaye shuka kwenye ngazi huku akionekana kuchoka sana.

“Ahaa Julieth njoo ukutane na George Sanga”

Nabii Sanga alizungumza huku akijitahidi kutengeneza furaha usoni mwake. Julieth akatembea kwa hatua za kinyonge hadi sehemu walipo kaa wazazi wake na kujibwaga kwenye sofa. Kitendo cha Julieth kumtazama Evans usoni mwake akajikuta akistuka sana hadi kila mtu akagundua kwamba ame stusha na jambo hilo lika mfanya Evans kuanza kuhisi kwamba Julieth atakuwa amemgundua.

***

“Baba una muda tuzungumze?”

Jery alizungumza huku akiwa amekaa kwenye kiti kilichopo mbele ya meza ya baba yake.

“Kuna nini tena kwa maana mke wako ameondoka hapa masaa mawili yaliyo pita na ana onekana ana wasiwasi mwingi sana. Vipi tayari umesha muudhi?”

“Hapana, sija gombana naye. Ame kwenda wapi?”

“Ameniambia ana kwenda kuonana na baba yake. Sasa kama kuna jambo ambalo ume muudhi mtoto wa watu ni heri ukazungumza mapema Jery.

“Hapana baba, sija mkera. Ila nina hitaji tuzungumze kama watu wazima”

Raisi Mtenzi akatabasamu kwa maana hakuwahi kumsikia mwanaye huyo akizungumza kauli kama hiyo.

“Watu wazima?”

“Ndio baba nina hitaji tuzungumze kikubwa”

“Ehee nina kusikiliza mtu mzima”

Jery akaka kimya kwa sekunde kadhaa kisha akashusha pumzi nyingi.

“Baba una jua sisi ni wanaume”

“Ndio nina litambua hilo”

“Hivyo tukiwa kama wanaume, kuna mambo mambo huwa tuna yafanya ili mradi kukidhi haja za miili yetu”

“Usitake kuniambia kwamba bado una mahusiano na yule mfagiaji?”

“Baba najua hichi kitu ninacho kizungumza ni kwa ajili ya mstakabali wa familia yetu.”

“Nenda kwenye pointi yako acha kuzunguka sana”

“Baba Shani ni mjaumzito na ana mimba yangu”

Raisi Mtenzi macho yakamtoka na uso wake ukajaa ndiza zilizo mfanya Jery atambua kabisa amesha likoroga kwa baba yake. Ukimya wa dakika mbili uka pita huku raisi Mtenzi akiwa katika hali hiyo ya kukasirika.

“Hichi ndio ulicho kuwa una kitafuta si ndio?”

“Hapana baba, ime tokea tu akapata ujauzito”

“Kwani huwezi kutumia Condomu wewe?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka huku akimtazama Jery.

“Baba nime fanya hivi kwa ajili ya mke wangu wa ndani hataki kuzaa kwa kipindi hichi ambacho mimi nina hitaji mtoto. Nilimvumilia sana tena sana kiasi kwamba nikashindwa kwa maana jukumu la mwanamke ndani ya familia yake ni kuzaa na kulea familia. Yeye anakazi ya kuhangaika huku ofisini akidhani kwamba hii ofisi ndio ime muoa. Nime angali what best for my future famili. Sina kaka, sina dada sina ndugu ambaye hata siku wewe ukifa ata weza kuwa karibu yangu. Ila mtoto aliyopo tumboni mwa Shani ndio rafiki yangu mimi”

Jery naye alizungumza kwa kufoka huku akimkazia macho baba yake. Raisi Jery akasimama huku macho ya hasira yakimtawala.

“Nime ishi na mama yako na wala sikuwahi kumleta mtoto wa haramu. So na wewe usiniletee wajukuu haramu ndani ya ukoo wangu wa Mtenzi. Umenielewa wewe?”

Raisi Mtenzi alizungumza huku akipiga piga ngumi mezani na kuwafanya walinzi wake wawili walio simama nje ya mlango wake kuingia ndani, ila akawanyooshea ishara ya mkono kuwaomba watoke ndani hapo na wakatii agizo hilo.

“Ohoo kwa hiyo mwanangu atakapo zaliwa ata kuwa ni haramu?”

“Ndio ni mjukuu haramu na unazaaje na wafagiaji wa ikulu wewe. Tume kuoezesha kwa binti ambaye wazazi wake ni wacha Mungu na yeye ni mcha Mungu, ana heshima ana pesa ana kila aina ya sifa ya uzuri isitoshe alikutunzia bikra hadi ukampata. Alafu wewe una una kwenda kutembea na wafagiaji kweli Jery?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka.

“Mapenzi sio pesa sio uzuri na kama umemuoana mkwe wako ni mzuri sana kuliko wanawake wote nenda kamuoea wewe”

“Una semaje wewe”

Raisi Mtenzi kwa haraka akapanda juu ya meza yake na kumrukia Jery, akamuanguka chini na kuanza kumtandika ngumi mvululizo ambazo zilizo mfanya Jery kukikinga na mikono yake ili asiumizwe moyo wake.

“Nita kuua wewe, sijawahi kuzaa mtoto haramu na mpumbavu kama weweee”

Raisi Mtenzi alizunguma kwa hasira huku akiendelea kumshushia kipigo Jery. Uvumilivu ukawashinda walinzi wake na wakaingia ndani, hali hiyo ikawaogopesha sana na kuwalazimu kuamua ugomvi huo.

“Niacheni niweze kumuaa mwana haramu mkubwa huyu”

“Hapana muheshimiwa upo ofisini na tena ni ikulu hapa. Hupaswi kufanya hivyo”

Mlinzi wake mkuu alizungumza kwa sauti ya ustarabu huku akimzuia raisi Mtenzi kumendelea na mapambano hayo. Jery akanyanyuka huku chini ya jicho la kushoto akiwa ana mwagikwa na damu kwa maana kuna ngumi ilimpata eneo hilo.

“Nina uwezo wa kukupiga wewe mzee ila siwezi kunyanyua mkono wangu na kukupiga kwa maana wewe ni baba yangu. Ila nilioa mwanamke mwenye bikra feki hakuwa na bikra halisi na ndio maana niliamua kwenda kuzaa nje ya ndoa yangu na kama amenidanganya kuhusiana na bikra yake. Je kuna mambo mangapi ambayo ana nidanganya. So nina mchukua mfagiaji wangu na kutoweka naye pasipo julikana na usijaribu kunitafuta na kuanzia hivi sasa nina hesabia sina baba wala mama”

Jery mara baada ya kuzungumza maneno hayo akajitoa mikononi mwa mlinzi aliye mshika na kutoka ofisini hapo na kumfanya sekretari kushangaa kwa maana Jery aliingiaa kiwa na tabasamu pasana usoni mwake, ila ana toka ofisini humo akiwa ana mwagikwa na damu kwenye shavu lake na inavyo onyesha ndani ya ofisi ya baba yake hakna usalama kabisa.


“Hakikisheni hatoki hapa ikulu. Mume nielewa?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa hasira huku akiwatazama walinzi wake.

“Sawa mkuu”

Mlinzi mkuu wa ikulu alijibu na kuanza kutoa taarifa kwa walinzi wote wa ikulu, kuhakikisha kwamba Jery hatoki eneo la ikulu.

“Niitieni Dev mlinzi wa Jery”

“Sawa mkuu”

Raisi Mtenzi akavua koti lake na kulitupia juu ya sofa. Akavua tai yake na kuitupia lilipo koti lake na akaanza kukunja mikono ya shati lake huku akizunguka zunguka ndani ya ofisi yake kubwa. Hakuamini kama kijana wake tena wa mwisho ana weza kudiriki kumtuka kwa tusi la kulala na mke wake wa ndoa. Devi akaingia ofisini hapo huku akiwa na wasiwasi kwa maana mlinzi aliye kwenda kumuita tayari alisha mgusia ni nini kimetokea ndani ya ofisi hiyo.

“Wewe ndio una msindikiza huyo mshenzi kwenda kufanya mambo yake ya kipumbavu si ndio?”

“Sija kuelewa muheshimiwa”

Devi alizungumz ahuku akiwa amesimama wima.

“Una semaje?”

“Sija kuelewa una zungumza nini muheshimiwa”

“Nina hitaji unipelekea anapo ishi Shani, hawara wa Jery na usipo fanya hivyo cha moto uta kiona”

Raisi Mtenzi aliendelea kufoka na umfanya Dev kusimama kwa muda huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake, akatambua kabisa kwamba kwa ukali huo wa raisi Mtenzi basi Shani ana weza kwenda kuuwawa kikatili sana.

“Samahani muheshimiwa raisi siwezi kukupeleka”

Walinzi wote wakashangaa hadi raisi Mtenzi mwenyewe akamshangaa Devi kwa maana hakutaraji kama ana weza kumjibu kitu kama hicho. Raisi Mtenzi akamsogelea Devi na kumkunja shati lake eneo la kifuani mwake humsogeza karibu yake.

“Una hamu ya kufa”

“Nipo tayari kufa muda wowote kwenye maisha yangu. Moja ya kanunu na sheria ya kazi yangu ni kuhakikisha kwamba nina linda siri ya bosi wangu ninaye mlinda. Haijalishi ni kuutoa uhai wangu au laa, ila nita linda siri hiyo samahani muheshimiwa raisi sinto weza kukupeleka”

“Kuanzia hivi sasa nina kuvua mamlaka yote na kamuweke chini ya kizui hadi pale nitakapo amua mimi atoke”

“Sawa mkuu”

Devi akanyosha mikono yake mbele na akafungwa pingu ya kamba ngumu iliyo tengenezwa kwa plastiki na akatolewa ofisini hapo huku kitambulisho chake na bastola yake vikichukuliwa. Akawekwa kwenye mahabusu iliyopo chichi ya ardhi eneo la ikuku.

“Nina hitaji kuanzia hivi sasa mumtafute yule binti anaye itwa Shani na mukimpata muniambie ni wapi alipo Sawa”

“Hakuna shaka muheshimiwa”

Walinzi hao wakatoka ndani hapo, raisi Mtenzi akaminya kitufe mimoja katika simu yake ya mezani na mawasiliano yakaenda moja kwa moja kwa sekretari wake.

“Niletee wisky yangu”

“Sawa mkuu”

Sekretari akaingia ofisini akiwa ameshika chupa ya wisky aina ya Hennessy pamoja na glasi ngumu na kumuwekea mezani.

“Nikumiminie?”

“Hapana, sihitaji mgeni wa aina yoyote sasa hivi. Sawa”

“Sawa mkuu”

Sekretari taratibu akachuchumaa na kuoko baadhi ya mafaili yaliyo anguka eneo hilo na kuyaweka vizuri mezani hapo na kutoka ofisini. Raisi Mtenzi akamimina wisky hiyo na kuanza kupiga mafumba mfululizo huku akijaribu kusikilizia hasira yake jinsi inavyo uchemsha moyo wake.

Kitu cha kwanza Jery kufanya mara baada ya kuingia ndani kwake, akampigia simu Shani.

“Upo wapi?”

“Nipo nyumbani”

“Nisikilize kwa umakini sana. Vaa baibui lake na uondoke hapo nyumbani kwako na nenda sehemu ambayo haito kuwa rahisi kwa wewe kuonekana”

“Ngoja kwanza Jery, kwa nini nifanye hivyo?”

“Huu sio muda wa kuniuliza maswali ni muda wa wewe kufanya nilivyo kueleza. Nina kuingizia milioni mbili kwenye simu yako hapo nina kuhitaji uondoke sawa?”

“Sawa mume wangu”

“Hakikisha mwanangu ana kuwa salama”

“Ila mume wangu sija kuelewa kwa nini una fanya hivyo”

“Nime mueleza mzee na amekasiri fanya kama nilivyo kueleza”

“Sawa nina fanya hivyo”

Jery akakata simu na kumuingizia Shani milioni mbili na nusu kwenye simu yake.

“Ume ipata?”

Jery alizungumza mara baada ya kumpigia.

“Ndio mume wangu na nimesha jiandaa.”

“Poa ondoka sasa hivi hapo nyumbani”

“Sawa”

Jery akakata simu, akasimama mbele ya kioo kilichopo chumbani hapo na kuangalia jeraha hilo na halikuwa kubwa sana. Akajifuta damu, akafungua kiboksi cha huduma ya kwanza ambacho ndani kina kila aina ya dawa ambayo ina weza kutumika katika kutoa huduma ya kwanza. Akajitibu jeraha hilo kisha akajibandika bandeji. Akabadilisha nguo zake na kuitafuta namba ya Devi ila kabla haja mpigia machale yakamcheza. Akatoka chumbani hapo ila akakutana na walinzi wanne sebleni. Hakuta kuwasemesha chochote zaidi ya kutembea kuelekea mlangoni ila walinzi wawili wakamzui.

“Nini?”

“Huwezi kutoka humu ndani na muheshimiwa raisi ameagiza hivyo”

Mlinzi mmoja alizungumza huku akimkazia macho Jery.

“Ndivyo alivyo waagiza?”

“Ndio”

Jery akarudi chumbani kwake na kujitupa kitandani huku akisubiria majibu kutokwa kwa Shani mwanamke anaye ingia matatizoni kutokana na mimba yake.

***

Shani akajifunga kitambaa cheusi cha baibui hilo na kuyaacha macho yake tu. Akajifunika kitambaa kingine chepesi kinacho muwezesha kuona mbele. Akachukua pochi yake kubwa aliyo weka nguo chache pamoja na vipodiozi pamoja n apes kiasi alizo nazo ndani hapo. Akafunga nyumba yake na kuondoka akasimamisha bajaji moja na kupanda. Kabla bajaji hiyo haijaondoka, gari nne nyeusi ambazo anazitambua vizuri ni gari za ikulu, zikapita pembeni ya bajaji hiyo na kusimama mbele ya geti lake. Hapo ndipo Shani akatambua kwamba mambo yameharibika na walinzi hao wa raisi wamekuja nyumbani kwake kumsaka yeye.

“Kaka tuondoke”

Shani alimuhimiza dereva bajaji huyo na wakaondoka eneo hilo.

“Dada wapi?”

“Wewe twende nita kuambia twende wapi?”

Wakatokemea kwenye mtaa huo pasipo walinzi hao wa raisi kutambua chochote.

“Nyumba yenyewe ndio hii”

Mmoja wao alizungumza huku wakiingia ndani. Kwa bahati mbaya wakakutana na kufuli mlangoni mwa chumba cha Shati.

“Shiti hayupo”

“Nina imani hato kuwa ame toka ndani ya jiji la Dar es Salaam. Tuhakikishe kwamba ana patika mume nielewa”

Mkuu wa kikosi hicho alizungumza kwa msisitizo.

“Sawa mkuu”

Wakaingia kwenye magari yao na kuondoka eneo hilo na kuwaacha baadhi ya majirani wakiwa wana shangaa shangaa pasipo kujua ni kitu gani kinacho endelea.

Shani akaitoa simu yake inayo ita ndani ya pochi na kuitazama na kukuta ni Jery ndio anaye mpigia.

“Vipi?”

“Mume wangu nina ogopa, gari nne za secrety service zime kuja nyumbani kana kwamba sijui wana kuja kumakata muhalifu gani. Hembu niambie mume wangu ni kitu gani kinacho endelea?”

Shani alizungumza kwa wasiwasi mkubwa sana.

“Baba hataki kuuona huo ujauzito wako, hapa alipo amenipiga vibaya sana na hapa nilipo nipo kifungo cha chumbani kwangu. Sasa hakikisha kwamba una kuwa salama wewe na mwanangu. Ume nielewa”

Shani machozi yakaanza kumwagika usoni mwake, kwani jambo kama hili alisha wahi kuliwazia akilini mwake kabla hata hajamkubalia Jery kuzaa naye.

“Kwa hiyo baba ana taka kuniua kisa mimba yangu jamani?”

Shani alizungumza huku akiangua kilio, dereva bajaji akashindwa kuelewa kabisa.

“Ndio, ila nita hakikisha hawezi kufanya hivyo”

“Hawezi kufanya hivyo vipi Jery ikiwa wewe mwenyewe upo mbali na mimi upo kifungoni alafu una niambia kwamba hawezi seriously Jery”

“Nisikilize mimi, hawezi kufanya hivyo. Nina kutumia namba ya mama yangu mmoja hivi ni mama yangu wa hiyari ata kutunza”

“No Jery siwezi kwenda kwa ndugu yangu. Una taka nije nikamatwe na kutolewa mimba yangu si ndio?”

“Sio hivyo”

“Ila?”

Shani aliuliza kwa ukali kidogo kwa maana tayari hofu ya kifo imesha mtawala.

“Nisikilize ukileta ujinga una kufa. Nina mjua baba yangu vizuri sana kama aliweza kumuua kaka yangu wa kwanza una hisi wewe ata kufanya nini?”

Jery alizungumza kwa ukali hadi Shani akaanza kutetemeka kwa maana hakuwahi kuisikia sauti ya ukali ya Jery na ikambidi awe mpole tu kwa maana akifanya ujinga ana kufa kweli.

“Nina kutumia namba ya mama yangu mlenzi. Ata kulea yupo Masaki na nina mpigia hivi sasa sawa”

“Sawa”

Jery akakata simu na meseji ikaingia katika simu ya Shani. Baada ya dakika tano Jery akapiga simu na Shani akapokea.

“Nime zungumza naye na ata kupigia sasa hivi”

“Sawa”

Kitendo cha Jery kukata simu, ikaingia namba ngeni katika simu ya Shani.

“Haloo”

“Nina imani nina zungumza na Shani?”

Sauti ya mwana mama mtu mzima ilisikika.

“Ndio mama”

“Okay upo na usafiri gani mkwe wangu?”

“Bajaji mama”

“Basi mpatie simu”

Shani akampatia dereva bajaji simu na akaanza kuelekezwa ni wapi anapo paswa kumpeleka Shani. Dereva bajaji akamrudishia simu Shani na kuiweka sikioni mwake.

“Nimesha muelekeza, usiwe na hofu ata kuleta hadi kwangu sawa mkwe?”

“Sawa mama, asante sana”

“Usijali”

Kwa ujanja wa dereva huyo wa kupenya penya kwenye foleni. Wakafanikiwa kufika Masaki katika jumba moja kubwa la kifahari. Shani akapiga simu na mwana mama huyo akatoka nje na kumpokea, mwana mama huyo akamlipa dereva bajaji huyo na kabla hajaondoka akampa onyo kali sana la kuto kufungua kinywa chake kwa mtu yoyote kama ame mleta msichana huyo nyumbani kwake na endapo ata fanya hivyo basi ata hakikisha ana msaka na kumuua kwa mikono yake mwenyewe. Dereva bajajai akaondoka huku akiwa na woga mwingi sana kwa maana katika kipindi cha miaka yake mitano ya kazi hiyo hajawahi kukutana na onyo kali kama hilo. Wakaingia ndani na Shani akavua kitambaa cha usoni na kumfanya mwana mama huyo kutabasamu.

“Haki ya Mungu mwanangu amechagua chuma kuliko hata yule mlokole”

Mwana mama huyo alimsimia sana Shani kwa maana ni mzuri wa hasili.

“Hapa nina ishi mimi peke yangu. Nina watoto wawili wa kike, wote wapo nchini Marekani wame olewa huko na Jery alikuwa ni mdogo wao kipindi ana soma Marekani”

“Nashukuru sana mama yangu”

“Nina shanga kwa nini baba yake ana hitaji kukuua ikiwa mjukuu ni kitu cha baraka”

“Sijui ni kwa nini mama”

Shani alijibu huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Pole sana, hapa upo salama, hakuna cha nani wala nani ambaye ana weza kuingia humu ndani. Umenielewa mwanangu”

“Sawa mama”

“Twende nikakuonyeshe chumba chako. Alafu nime sahau kukuambia jina langu. Mimi nina itwa madam Mbwambo au mama Mbwambo”

“Urewedi”(Habari yako)

Shani alisalimia kwa kipare na kumfanya madam Mbwambo kustuka kidogo.

“Sirewedi kaicha we?”(Salama, hujambo?)

“Nchedi”(Sijambo)

“Kumbe na wewe ni mpare”

“Ndio mama”

“Waoo mwanangu ame pata bahati nzuri sana. Wapere sisi ni wazuri wa kila kitu”

Madam Mbwambo alizungumza kwa furaha. Akafungua moja ya chumba kikubwa na kizuri na kumkaribisha Shani ndani.

“Uta kaa hapa hadi pale mume wako atakapo toa maamuzi mengine. Sawa mwanangu”

“Nashukuru sana mama”

Shani akamkumbatia madam Mbwambo na matumaini yake mapya ya kuishi yaka mtawala moyoni mwake na wasiwasi ulio changanyika na woga wote uka muondoka.

***

“Ahaa Julieth mbona ume stuka?”

Nabii Sanga alimuuliza mwanaye huku akimtazama usoni mwake.

“Hakuna kitu baba”

“Au ulisha wahi kumuona huyu kijana?”

“Hapana”

Julieth alijibu kwa kinyonge sana huku akimtazama baba yake.

“George huyu ni binti yangu wa mwisho ana itwa Julieth Sanga. Julieth huyu ni George Sanga na yule ni mke wake ana itwa Leila Sanga”

“Nashukuru kuwafahamu”

Julieth alizungumza huku akijaribu kutengeneza tabasamu usoni mwake, moyo wa Julieth uka jikuta ukijawa na maumivu ya gafla na wivu ambao hakujua hata umesababishwa na nini.

“Hata sisi tuna shukuru kukufahamu. Nina omba tuweze kuondoka kuna sehemu tuna kwenda ila ndani ya siku mbili hizi tuta wasiliana kwa maana nina hitaji kuwasiliana na injinia wangu walipo nchini Marekani, waweze kuunda ramani ya mfumo mzima wa kampuni inavyo paswa kuwa na baada ya hapo nita kuja na mfumo huo kisha tuta jua ni wapi ambapo tuna weza kwenda kuweka makao makuu yetu”

“Sawa sawa George sisi ni wako. Piga simu muda wowote nasi tta kuwa tayari kukupatia msaada”

“Hakuna shaka baba. Acha sisi tuondoke.”

“Dereva wangu ata warudisha hotelini”

“Nashukuru sana”

Nabii Sanga na mke wake wakawasindikiza Evans na Leila nje huku nabii Sanga kwa macho ya kuiba akiangalia msambwanda wa Leila.

‘Haki ya Mungu huyu binti lazima nimle’

Nabii Sanga alijipiza kimoyo moyo. Mrs Sanga naye macho yake ya kuiba iba yapo kwa Jery anaye mtamani hata leo aweze kumpata. Evans na Leila wakaingia ndani ya gari na wakaondoka nyumbani hapo kwa nabii Sanga.

“Baba na mama”

Julieth aliita mara baada ya baba yake na mama yake kuingia ndani sebleni.

“Bee”

Mrs Sanga aliitikia.

“Yule kijana ni mzuri sana, yaani hadi nime stuka”

Nabii Sanga na mke wake wakatazamana huku wakiwa wamejawa na mshangao.

“Yaa pia ni tajiri na ndio ni mmiliki wa kampuni ya Samsung ulimwenguni mwote”

“Weeee?”

“Ndio maana yake.”

“Muna onaje nika vunja ndoa yangu na Jery nika olewa na yeye kwa maana moyo wangu ume tokea kumpenda sana.”

Kauli ya Julieth ika mchukiza sana mrs Sanga kwa maana hata yeye mwenyewe moyo wake umesha kufa na kuoza kwa George(Evans) na hataki kumpoteza na hapo alipo kichwani mwake ana panga mikakati kuhakikisha kwamba ana muondola Leila kwenye nafasi yake na kushika uskani yeye na yupo tayari kumtelekeza nabii Sanga kwa ajili ya furaha ya moyo wake.



“Una wendawazimu nini kichwani mwako wewe?”

Mrs Sanga aliuliza kwa hasira huku akimkazia macho Julieth.

“Nimetania bwana mama. Yaani hadi ume kasirika.”

“Hata kama una tania. Tupo kwenye kipindi kigumu na tuna hitaji kujinasua na wewe una lete masihara”

“Hei mama Jilieth yame kwisha. Hivi sasa ina tubidi kuangalia ni nini tuna fanya, wapi tuna ingia ili kuhakikisha kwamba hili sekeseke lina tupita”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake pamoja na mwenaye. Ukimya wa dakika mbili ukatawala ndani ya seble, huku kila mmoja wao akionekana akitafakari ni kitu gani ana weza kuzungumza.

“Hembu mke wangu kalilete lile faili”

Mrs Sanga akanyanyuka na kuelekea gorofani, baada ya dakika akarudi akiwa na faili alilo kuja nalo Julieth. Nabii Sang akaanza kulisoma taratibu. Ilipo fika kwenye kesi ya mke wake kumuua Tom, akamtazama mkewe kisha akakohoa kidogo.

“Hili swala la Tom mbona hukuniambia?”

Mrs Sanga akastuka kidogo ila akajizuia kuonyesha mstuko wake mbele ya Julieth.

“Yamesha pita hayo mume wangu”

Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya unyonge kwa maana sekeseke la Toms katika nyumba hiyo ilileta mgogoro mkubwa sana.

“Ime kuwaje wajue kila kutu chetu. Ina maana wana tufwatilia kwa kipindi kirefu?”

Nabii Sanga alihoji ila hapakuwa na aliye weza kujibu swali hilo.

“Hili jambo ni gumu sana.”

“Mume wangu muna onaje tukafanya kama wanavyo hitaji wao ili tuepukane na jambo hili”

“Mama, yaani mimi nika muue baba yangu mkwe?”

“Ndio, kwa maana hatuna jinsi”

“Hapana mama, siwezi kufanya hivyo”

“Nina hitaji kukutana na huyo balozi nipatie namba yake”

Julieth kwa haraka akatajia baba yake namba ya balozi huyo na na nabii Sanga akampigia.

“Habari yako Sanga”

Balozi Trump alizungumza kwa sauti ya furaha na kuufanya moyo wa nabii Sanga kuanza kudunda kwa kasi sana.

“Namba yangu ume itoa wapi?”

“Sanga hilo sio swali la kuniuliza mtu mzima kama wewe. Nina imani ume weza kupata ujumbe wangu”

“Ndio, nina hitaji kuonana na wewe”

“Waooo ni maamuzi mazuri. Usiku wa saa nne njoo Serena Hotel. Uta nikuta”

“Nitafanya hivyo”

“Kwa kukumbusha tu. Njoo peke yako kwa maana binti yako niliweza kumpatia nafasi ya kukutana na mimi ila akanijibu majibu ya kejeli”

“Nina kuomba msamehe binti yangu nina imani kwamba alikasiridhwa na jambo kama hilo”

“Nina elewa”

“Nina shukuru sana kwa muda wako”

“Asante Sanga”

Nabii Sanga akakata simu huku akishusha pumzi taratibu.

“Amesemaje?”

Mrs Sanga aliuliza kwa shahuku kubwa sana.

“Ana hitaji kuonana na mimi saa nne usiku. Serena”

“Ila hao watu kwa nini wana cheza na akili zetu?”

Mrs Sanga aliuliza kwa hasira.

“Usijali mke wangu, nita dilia na hili jambo. Julieth mpigie simu mume wako muambie leo utalala hapa nyumbani. Ukirudi ikulu na hiyo hali yako nina uhakika wa asilimia mia moja wata kustukia”

“Sawa baba”

Nabii Sanga akanyanyuka na kuondoka sebleni hapo na kuelekea chumbani kwake. Mke wake naye akamfwata kwa nyuma. Julieth akaitafuta namba ya Jery na akampigia simu.

“Nini”

Sauti ya Jery na jinsi alivyo anza mazungumzo hayo ikamtisha sana Julieth na akahisi labla tayari mambo yamesha julikana.

“Baby mbona una zungumza kwa hasira hivyo?”

Julieth akasikia jinsi mume wake anavyo hema kwa nguvu na dhahiri ana onekana hayupo sawa.

“Sipo poa niache tuzungumze baadae”

“Sawa mume wangu. Ila nina omba nilale kwa baba”

“Hakuna shaka lala”

“Asante”

Julieth akakata simu huku akitafakari majubu ya Jery yaliyo jaa hasira ndani yake. Moyo wake hakuweza kupata amani kabisa. Akatafakari ni mtu gani amabaye ame zoeana na Jery. Akampigia mlinzi wa Jery simu yake ila kwa bahati mbaya akakuta simu hiyo haipatikani hewani.

“Mmmmm!!”

Julieth aliguna huku akiwa na mshangao. Akapiga tena kwa mara mbili za mwisho ila mlinzi huyo hakuweza kupatikana hewani. Hapo ndipo machale yakaanza kumcheza kichwani mwake. Akaitafuta namba ya baba yake mkwe, akaitazama kwa sekunde ishirini kisha akaipiga. Simu ya raisi Mtenzi ikaanza kuita kisha ikapokelewa.

“Sekretari wa raisi hapa nina zungumza”

“Mzee yupo wapi. Mimi ni Julieth”

“Ohoo samahani madam, kuna matatizo kidogo yame tokea hapa ikulu”

“Matatizo!!?”

Julieth aliuliza kwa mshangao huku kasi ya mapigo yake ya moyo ikizidi kumuenda kasi.

“Ndio, muheshimiwa na mume wako waliweza kugombana ofisini”

“Wa….wa…me…gomb…ana?”

Magreth alishikwa na kigugumizi kilicho mshinda kabisa kuzungumza vizuri.

“Ndio”

“Chanzo cha ugomvi ni nini?”

“Sifahamu ila kwa sasa muheshimiwa ana hasira sana na haitaji kuzungumza na mtu yoyote”

Julieth akashusha pumzi nyingi sana huku akiamini kwamba ugomvi huo hausihani kabisa na maswala ya usaliti wa familia yake.

“Sawa nita wasiliana nao baadae”

“Hakuna shaka”

Julieth akata simu, taratibu akajilaza kwenye sofa hilo huku akilini mwake akijaribu kutafakari ni kwa namna gani yeye na familia yake wana weza kutoka kwenye janga lililopo mbele yao.

“Uta kwenda kuzungumza nao nini mume wangu?”

Mrs Sanga aliuliza kwa sauti ya upole huku akimtazama mume wake aliye kaa kwenye moja ya sofa huku amejiinamia chini.

“Hata sijui mke wangu.”

“Una onaje hili jambo uka zungumza na mkuu wako na akakusaidia katika hili”

“Una jua nini mke wangu”

“Ehee?”

“Mkuu wangu aliniambai kwamba endapo nina hitaji hadhina yote ile. Ita nibidi kumuua baba Jery. Huku napo hawa Wamarekani nao wana hitaji baba Jery auliwe. Yaani nashindwa hata kuelewa kwa nini haya mambo yana ingiliana. Huyu mzee ana kitu gani ambacho kina wafanya watu watamani kuona uhai wake una toweka”

“Mmmm hapo kuna mtihani mume wangu”

“Yaani ndio hivyo. Kuna mtihani mkubwa sana na laiti hawa Wamarekani wangekuwa hawajui chochote haki ya Mungu tunge hama hii nchi ila ubaya ni kwamba, popote tutakapo kwenda, wao ni lazima wata fahamu tu kwa maana nina imani sasa hivi macho yao na nguvu kazi yao yote juu ya haya mambo wameiweka kwetu”

“EheeMungu atusaidie kwa maana hizi siri zikivuja tu. Basi kila kitu kina kwenda chini”

“Ndio hivyo mke wangu”

Nabii Sanga alizungumza kwa unyonge sana, kwani hadi sasa hajui nini afanye.

***

“Baby kuna jambo lina endelea katika ile familia”

Leila alizungumza mara baada ya kufika hotelini anapo ishi Evans.

“Jambo gani?”

“Sijajua ila inaonyesha kuna siria mbayo ina watafuna sana wale watu. Unajua katika ule muda ambao nilikuwa nime kaa pale ndani, nabii Sanga alipigiwa simu na sijui yule mbinti wake na akatimua mbioo. Baada ya muda nabii Sanga akarudi huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi sana. Yaani furaha ilimuisha kabisa usoni mwake yeye na mke wake.”

Leila alizungumza na kumfanya Evans kukaa kimya na kumsikiliza Leila kwa umakini mkubwa sana.

“Kitu kilicho nifanya nijuwe kuna hali ya utofauti pale ndani.Ni vile binti yao alivyo kuja akiwa mnyonge na mkoni mwake alikuwa ameshika faili jeusi na lina maandishi yaliyo andikwa TOP SECRETY. Alikuwa ana onekana kama mtu aliyekata tamaa ya jambo fulani ambalo sifahamu ni jambo gani”

“Ngoja kwanza ume sem ni faili jeusi na lime andikwa Top secret?”

“Ndio baby”

“Ina bidi hilo faili nilipate na itabidi usiku wa leo niweze kurudi nyumbani kwa nabii Sanga ila kwa njia ya wizi na sio njia yakuheshimika kama hii”

“Mume wangu endapo ita kamatwa ita kuaje?”

“Siwezi kukamatwa kwa maana endapo nita lipata faili hilo basi tuta weza kupata kile tunacho kihitaji kwa nabii Sanga kwa njia rahisi kulipo hii plan tuliyo ipanga. Ume nielewa mke wangu”

Leila akatabasamu kwa maana akili yake kwa sasa ni kuwa tajiri na kuwa na maisha bora kuliko rafiki yake Caro ambaye kumpata nabii Sanga kumempandisha sana kimaisha kiasi cha kumuonea wivu.

***

“Muite Josephine”

Raisi Mtenzi alimuambia mlinzi wake mmoja na akatoka ofisini hapo. Baada ya dakika tano akarudi akiwa ameongozana na Josephine. Uso wa hasira alio nao raisi Mtenzi kwa namna moja ama nyingine una ashiria kwamba hali ya hewa sio nzuri ndani hapo.

“Tupisheni”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo na walinzi wake hao wawili wakatoka ndani hapo kwa maana waa muamini Josephine.

“Muheshimiwa vipi mbona una hasira kiasi hicho?”

“Kuna binti mmoja amechafua familia yangu. Ana hitaji kuvunja ndoa ya mwanangu. Mimi kama baba sitaki kuingia na aibu za kujinga namba hiyo. Ndoa haina hata mwaka alafu ina vunjika kwa mjinga mmoja tena alikuwa ni mfagiaji hapa ikulu”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa hasira huku akipiga piga mezani na kumfanya Josephine kujawa na wasiwasi kwani toka aanze kumfahamu raisi Mtenzi hajawahi kumuona akiwa katika hali kama hiyo.

“Ahaa samahani muheshimiwa. Huyu binti ana hitaji kuvunja ndoa ya nani?”

“Ndoa ya Jery na isitoshe ame mbebea mimba. Sasa ninacho kihitaji sasa hivi, Sali na utambue ni location gani ambayo huyo msichana yupo kwa maana nime tuma vijana kwenda kumtafuta wana nipa ripoti za kijinga kwamba hawajamuona”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka sana kiasi cha kumfanya Josephine kuanza kutetemeka mwili mzima.

“Sasa hivi sali”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa ukali na kumfanya Josephine kufumba macho yake pasipo kupenda. Josephien akaanza kusali na kuonyesha eneo alipo msichana huyo, akaonyeshwa jinsi na namna binti huyo atakavyo chomwa visu vingi vya tumbo na raisi Mtenzi na kabla ya kufa kwake ana pigwa na mijeledi akiwa uchi kabisa.

‘Ehee Mungu ni kwa nini raisi ana kuwa katili kiasi hicho na ana muua msichana asiye na hatia?’

Josephine aliumuuliza Mungu kimoyo moyo huku machozi yakimwagika usoni mwake. Josephine akaanza kuonyeshwa jinsi raisi Mtenzi alivyo kuwa akimtongoza Shani ambaye alionyesha kuwa na msimamo wake. Akaonyeshwa jinsi raisi Mtenzi alivyo muua mpenzi wa Shani kisa wivu wa mapenzi. Kifo cha kijana huyo kilikuwa ni cha ajali ya kugongwa na lori huku akiwa yeye ndio bodaboda.

‘Ehee Mungu kwa nini una nionyesha haya yote sasa hivi. Kumbe huyu mtu ni mbaya kiasi hichi’

Josephine aliendelea kuzungumza kimoyo moyo huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana. Mtukio ya raisi Mtenzi kwa Shani yakaendelea kupita kwenye macho ya Josephine mithili ya mkanda wa tv. Akaonyeshwa siku moja ambayo mke wa raisi Mtenzi alipo kuwa ame safiri nje ya mkoa wa Dar es Salaama. Akaonyeshwa jinsi raisi Mtenzi alivyo fanya jaribio la kumbaka Shani kwa nguvu, ila jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba Shani aliweza kumzidi nguvu.

‘Ukitoa siri hii nita kuua sasa ole wako ujaribu kutoka nje ya hii ikulu’

Raisi Mtenzi alilalama mara baada ya kupigwa teke la siri na Shani na akakimbilia chumbani kwake na kujifungia kwa ndani. Moyo wa Josephine ukazidi kuumia kuona matukio ya kiongozi huyo ambaye hapo awali alimuamini kupita maelezo. Tukio lililo mfanya Josephine atamani kuzimia ni pale alipo onyeshwa jinsi raisi Mtenzi alivyo mshikia bastola Shani na kumlazimisha kumnyosha uume wake hadi aka mkolea binti wa watu mdomoni na kumfanya atapike sana na kulia kilio cha uchungu sana huku hofu ya kufa ikiwa ime mtawala sana Shani.

Taratibu Josephine akayafumbua macho yake huku machozi yakimbubujika. Akamtazama raisi Mtenzi aliye kunja sura yake huku akisubiria kujua ni wapi alipo Shani.

“Umeonyeshwa yupo wapi?”

“Sija onyeshwa muheshimiwa”

Josephine alijibu kwa kujikaza.

“Nini?”

“Sijaonyeshwa muheshimiwa. Mungu amenionyesha mambo mengine tofauti na hayo”

“Mambo gani na kwa nini un alia?”

“Amenionyesha chanzo cha ajali ya wazazi wangu. Nina kuomba sana muheshimiwa unipatie muda nitakapo fahamu ni wapi alipo tu nita kuambia”

“Sawa fanya hivyo. Umenenielewa?”

“Ndio”

Josephine akasimama huku akitazama glasi yenye wisky iliyopo pembeni mwa raisi Mtenzi. Josephine akatoka ofisini hapo huku akijipangusa machozi yake na kumfanya sekretari kumshangaa huku akitamani kumsemesha ila akachelewa kwani tayari Josephine alisha funga mlango wa ofisi ya sekretari na kutoka. Josephine akatoa simu yake katika mfuko wa koti la suti alilo vaa na akampigia Magreth.

“Mage upo wapi?”

“Ahaa nipo nyumbani nina pika”

“Nina kuja”

“Upo sawa?”

“Sipo sawa nina kuja”

“Sawa”

Josephine moja kwa moja akatoka nje. Dereva wake akamfungulia mlango akaingia na mlinzi mwengine na wakaondoka eneo la ikulu.

“Madam wapi tuna kwenda”

“Nyumbani”

“Sawa”

Josephine njia nzima machozi yakazidi kumwagika. Kila akijaribu kuikumbuka sura ya raisi Mtenzi alivyo kuwa ana shirikiana naye bega kwa bega katika kumsaidia katika kumshauri mambo mazuri ya kuiongoza nchi, kumbe ni chui tena mkali na mwenye hasira kali sana. Wakafika getini na Josespine akashuka.

“Madam tukusubirie”

“Hapana muna weza kurudi ikulu”

“Sawa”

Magreth akafungua geti na Josephine akaingia ndani. Akapitiliza moja kwa moja hadi sebleni na kujibwaga kwenye moja ya sofa huku machozi yakimwagika. Magreth akaingia huku akimshangaa rafiki yake.

“Jose kwa nini una lia?”

“Huyu raisi haki ya Mungu ni mnyama ni katili na hafai kabisa kuwa kiongozi wa nchi kama hii. Ndio maana nchi ina shambuliwa na watu wa kujinga jinga na watu wana kufa kwa ajili ya ushetani wake”

Magreth macho yakamtoka huku akimtazama Josephine ambaye ana onekana kuvurugwa.

“Sikuelewi rafiki yangu. Hembu niambie ni nini ambacho kime kupata na kwa nini una mshutumu raisi kwa nana hiyo?”

Josephine akaanza kumuhadithia Magreth kuanzia mwanzo aliyo onyeshwa hadi mwisho. Magreth akajikuta akishika mdomo wake kwa mshangao sana, kwani hayo anayo yasikia haamini kama kweli raisi Mtenzi ambaye walimpigania maisha yake asiuwawe hadi akawa hai ndio ana weza kufanya mambo mabaya kama hayo.




“Ohooo Mungu wangu. Hayo ndio uliyo kweli Josephine?”

Magreth aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Sijawahi kukosea kwenye maono yangu Mage na kila nilicho kuambia ni kitu cha kweli. Huyu mzee ana roho mbaya ni katili.”

Josephine alizungumza huku akiwa amejawa na huzuni kubwa sana.

“Sasa una shauri tufanye nini?”

“Sijui Mage ila binti wa watu ana kwenda kufa kifo kibaya sana. Ohoo Mungu msaidiwe katika hili kwa maana hana makosa”

Josephine alizungumza kwa unyonge hadi Magreth akamuonea huruma sana.

“Una hitaji tumsaidie kwa kumuokoa?”

“Ikiwezekana Mage”

“Okay una namba ya Jery?”

“Hapana”

“Ngoja”

Magreth akampigia simu Samnson.

“Dogo ni mimi, una namba ya Jery?”

“Jery gani sister?”

“Kwani hapo ikulu una kuna Jery wangapi?”

“Wapo watatu, wawili ni walinzi wa raisi na mmoja ni mtoto wa raisi”

“Okaya nahitaji namba ya Jery Mtenzi”

“Mmmm okay dakika moja”

“Poa”

Magreth akakata simu, haikuisha dakika moja ujumbe wa meseji kutoka kwa Samson ukaingia kwenye simu yake. Akaifungua na kuikremisha kichwani namba hiyo.

“Nina namba ya Jery je tuta anza vipi kumshawishi juu ya jambo hili?”

Josephine akaka kimya kwa dakika mbili kisha akamtazama Magreth.

“Mpigie alafu nizungumze naye mimi”

Magreth akafanya hivyo. Simu ya Jery ikapokelewa na Magreth akampatia Josephine simu hiyo.

“Jery ni mimi”

“Wewe nani?”

“Josephine”

“Kama ni huyo jini ndio amekutuma basi achana na mimi”

“Hapana Jery nisikilize kwa umakini. Nina amini kwamba una fahamu kuwa nina maono ya kuweza kuoa mambo yajayo si ndio?”

“Nisikilize. Mimi siamini katika upuuzi kama huo. Sipo vizuri niache”

Jery alizungumza kwa ukali na dhaihiri ana hasira kali sana ambayo ime mjaa moyoni mwake.

“Jery Shani ana kwenda kuuwawa”

Ilimbidi Josephine kuwahi kuzungumza kabla ya Jery hajakata simu.

“Nini?”

“Shani ana kwenda kuuwawa kwa kuchomwa visu tumboni mwake. Yote ni kutokana na mimba yako. Hivyo kama una hitaji kumuokoa Shani na akuzalie mwanao ina kubidi unisikilize kwa umakini sana”

Jery akashusha pumzi nyingi hadi zikasikika upande wa pili wa simu. Josephine akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku macho yake akiwa ameyafumba. Akaanza kuonyeshwa jinsi raisi Mtenzi anavyo toa maagizo kwa mmoja wa vijana wa IT. Kudukua mazungumzo kila aina ya simu na jumbe za meseji zinazo ingia katika simu ya Jery.

“Nitakupigia Jery.”

Magreth akakata simu na kwa haraka akaifunga(block) namba ya Jery katika simu ya Magreth.

“Vipi mbona una katisha mazungumzo”

“Mungu wangu wana hack simu ya Jery. Hivyo hatuto weza kuzungumza naye kwa sasa”

“Ohoo sasa inakuwaje?”

“Ngoja”

Josephine akampigia simu Samson.

“Sam ni mimi”

“Niambie dada ake”

“Sikia upo sehemu nzuri ambayo tuna weza kuzungumza?”

“Ahaa ngoja dakika moja usikate”

“Sawa”

Baada ya dakika moja Sauti ya Samson ika sikika.

“Niambie”

“Simu ya Jery kuna mtu ana hack kila kitu kinacho ingia. Yupo hapo ndani ya ikulu na amepatiwa maagizo na raisi Mtenzi. Je una wezza kulizuia hilo lisifanyike”

“Duuu sister una juaa kama ni ishu ya mkulu, ina kuwa ni jambo jengine hilo au una hitaji niwe kibarua changu kiote nyasi nini?”

“Hapana Samson ila msaada wako huo uta saidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao hawana hatia”

“Ngoja kwanza. Umesema nita okoa maisha ya mama na mtoto?”

“Ndio”

“Yupi?”

Magreth akaka kimya kwa sekudne kumi kisha akendelea kuzungumza.

“Sam. Jery amempachika dada mmoja mimba hapo ikuku ana itwa Shani, una mfahamu?”

“Yes yes kipindi nilipo kuwa nina ishi Kimara alikuwa ni jirani yangu”

“Okay sasa kama alikuwa ni jirani yako, basi tambua ana ujauzito wa Jery na hadi sasa hivi ana tafutwa na muheshimiwa na akipatikana basi ata uwawa kwa kuchomwa visu. Hayo ndio maono yangu niliyo yaona. Hivyo sisi watu watatu tuna weza kusaidia binti wa watu akawa hai pamoja na mwanaye tumboni”

”Duu ndio maana nsielewi elewi ndani ya ikulu, nina ona magari yana toka, mlinzi wa Jery amekamatwa. Kumbe sababu ndio hiyo?”

“Yes hembu nina kuomba sana mdogo wangu unisaidie. Tafadhali”

“Mmm nime bakisha nusu saa kabla ya kutoka hapa ikulu. So hii kazi nita kuja kuifanyia kwenu. Endapo nita ifanya humu ndani, ita kuwa ni rahisi sana kukamatwa. Umenielewa dada yangu”

“Nime kuelewa, nita shukuru sana”

“Poa badae”

“Poa”

Josephine akakata simu huku akijaribu kutafakari.

“Hapa ina bidi huyo msichana asiweze kutuma meseji kwa Jery kw amaana akituma tu kila kitu kitakuwa kime kwisha”

Magreth alizungumza kwa sauti ya upole huku akimuwazia Shani binti ambaye hajawahi kumuona ila endapo Shani ata fanya kosa tu la kutuma meseji kwenye namba ya Jery basi itakuwa ni rahisi kwa kijana wa IT kuweza kufahamu ni wapi meseji hiyo imetokea na itakuwa ni jambo rahisi sana kwa wao kumkamata Shani.

***

“Muheshimiwa raisi, kazi tayari”

Kijana aliye pewa jukumu la kuhack simu ya Jery alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.

“Una weza kuangalia rekodi za simu zilizo ingia na meseji za nyuma?”

“Hapanamuheshimiwa. Ila tunacho weza kukipata ni kuanzia sasa hivi, simu na meseji zote zitakazo ingia kwenye simu yake tuta zipata”

“Sasa uta kaa hapa ofisini, kila aina ya simu itakapo pigwa, kuingia hakikisha una nifahamisha”

“Sawa mkuu”

Raisi Mtenzi akanyanyua simu na kumpigia mlinzi wake mkuu.

“Ndio muheshimiwa”

“Hamjampata huyo msichana?”

“Ndio mkuu”

“Hakikisha hii siku haiishi uwe ume mpata huyo binti. Tume elewana?”

“Ndio mkuu”

Raisi Mtenzi akakata simu na kumpigia Josephine. Simu ya Josephine ikapokelewa.

“Njoo ofisni sasa hivi”

“Ahaa….samahani muheshimiwa. Ili nibidi niweze kurudi nyumbani ili kusali sana kwa ajili ya kujua ni wapi msichana huyo ni wapi alipo”

“Ehee Mungu wako amekuonyesha nini?”

Josephine akastuka sana kusikia kauli ya kuambiwa Mungu wako kwa maana Mungu ni wa watu wote.

“Bado nina endelea kumuomba muheshimiwa raisi na kila nitakacho kipata nita kuambia”

“Hakikisha hii siku haiishi huyo Mungu wako awe amesha kujibu?”

Raisi Mtenzi alizungumza kwa hasira kiasi.

“Sawa muheshimiwa”

Raisi Mtenzi akakata simu huku macho yakimtoka.

‘Jery nime kuzaa mwenyewe, alafu una chukua utamu wangu, utamu ambao nime uleta mimi mwenyewe hapa ikulu’

Raisi Jery alijisema kimoyo moyo huku akihisi maumivu makali sana ya moyo wake kwa maana kila anapo kumbuka ni wapi alipo mtoa Shani moyo wake una zidi kujawa na chuki na hasira ya kutamani kuua

Jery akaitazama simu yake, akatamani kumpigia Shani, ila roho yake ikasita. Akafungua begi lake la kusafiria na kutoa simu yake ambayo haitumii na katika simu hiyo kuna laini ambayo ina uwezo wa kutimika dunia nzima kwa kupiga simu na kupokea simu na uzuri wa laini hiyo ina someka kwa namba za Kimarekenia. Laini kama hizo ni watu wachache sana duniani ambao wanazo. Sifa nyingine ya laini hiyo ni kwamba hakuna mtu ambaye ana weza kurekodi au kuyanasa mazungumzo yanayo fanywa na laini hiyo. Jery akaiwasha simu hiyo, akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akaandika namba iliyo mpigia.

“Haloo”

“Josephine si ndio”

“Hapana mimi ni Mage ila zungumza na Josephine”

“Nipatie simu niongee naye”

Magreth akampatia simu Josphine.

“Haaloo Jose nina zungumza”

“Okay musishangae nimewapigia kwa nambaya Marekani ingali nipo nchini Tanzania.”

“Usijali hii laini ipo salama kwa ajili ya Mazungumzo?”

“Ndio”

“Ila kabla ya kufanya kuendelea kuzungumza nina kuomba umpigie kwanza Shani kisha umueleze asikutumie meseji kwenye ile namba yako ya kawaida kwa maana hadi nianvyo zungumza sasa hivi imesha kuwa hacked na endapo ata kupigia meseji au kukupigia basi tambua baba yako atafahamu ni wapi alipo”

“Sawa”

Jery akakata simu na kumpigia Shani na kumueleza kwamba asimpige wala kustuma meseji kwenye namba yake kisiha akakata simu na kumpigia Magreth.

“Ehee niambie ume onyeshwa nini?”

“Baba yako ana hitaji kumua Shani na ana mtafuta si ndio?”

“Ndio”

“Sasa tuna hitaji kumsaidia mwanamke wako. Hapo alipo la sivyo baba yako ata mkamata kabla ya hii siku kuisha na endapo ata mkamata basi ata muua kwa kumchoma choma visu. Hivyo uta mpoteza yeye na mwanao”

Jery akastuka kiasi,

“So muambie yule mama wa Kipare amabaye uma mkabidhi mkeo wako aweze kutukabidhi ili sisi tumlinde hadi atakapo jifungua”

“Josephine hayo yote ume yajuaje kama nime mkabidhi kwa mama wa kipare?”

“Nime jua kwa sababu nime kuambia nina uwezo wa kuona maono ya mambo yajayo na hapa ninavyo zungumza ni kwamba baba yako ana subiria niweze kumpatia haya maono ambayo wew enina kuambia sasa hivi. Ila nimeshindwa kumuambia kwa maana mimi ni mwanamke ambaye kesho na kesho kuta nita pata ujauzito na nikiwa kama mama nita hakikisha kwamba nina mlinda mwanangu kwa kila aina ya uwezo kuhakikisha kwamba ana kuwa salama.”

“Sawa kabla sijakupatia hayo yote niambie ni kwa nini baba yangu ana mchukia sana Shani na kufikia hatua ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kuhitaji kumdhuru?”

Josephine akashusha pumzi nyingi na kuanza kuzifikiria dhambi alizo zitenda raisi Mtenzi kwa Shani.

“Haloo”

“Nina kusikiliza, niambie ni kwa nini baba ana hitaji kumuua Shani ikiwa ame baba damu ya hii familia yangu”

“Jery”

“Naam”

“Ninacho kwenda kukuambia ni kitu cha kweli na kama utakuwa hukiamini muulize Shani ata kudhibitishia kila jambo”

“Niambie”

Josephine akaanza kumsimulia Jery kuanzi siku ya kwanza ambayo Shani alikutana na raisi Mtenzi, akamuelezea jinsi raisi Mtenzi alivyo panga ajali ya kumdhuru mpenzi wa Shani hadi akafariki, Shani akamueleza kila kitu Jery na hakumficha kitu hata kimoja. Hadi anamaliza kuzungumza mashavu ya Jery yamejawa na machozi ya uchungu pamoja na hasira kali sana.

“Kama huniamini, muulize Shani hayo mambo”

“Poa”

Jery akakata simu, akampigia Shani simu na kuanza kumuhoji jambo moja baada ya jengine hadi Shani akajukuta akishangaa kwani baadhi ya mambo yalitokea wakiwa yeye na raisi Mtenzi. Kila alicho ulizwa Shani akakiri kwmaba ni ukweli kitendo kilicho mfanya Jery kujawa na nguvu za ajabu. Ujasiri ukamuingia ndani yake. Akatoka chumabi kwake na walinzi walipo.

“Samahani muheshimiwa hupaswi kutoka”

Mlinzi mmoja alizungumza huku akimshika Jery mkono wa kushoto. Macho makali ya Jery yakamfanya mlinzi huyo kuutoa mkono wake.

“Kama kuna mtu ana hitaji damu yake kumwagika humu ndani, athubutu kunishika huu mkono. Nina kwenda ofisini kwa baba yangu kama hamuamini ongozaneni nami, ila kama hamuamini, nita mvunja mmoja baada ya mwengine viongo vyenu. Tumeelewana”

Walinzi wakatazamana kwa maana Jery amezungumza kwa sauti nzito na iliyo jaa kumaanisha. Walinzi wakampisha na kutoka naye ndani hapo. Wakafika ofisi ya raisi mtenzi na walinzi wawili walio simama mlangoni wakafunguamlango na wakaingia ndani hapo na Jery. Raisi Mtenzi akasimama huku akimtazama Jery kwa macho yaliyo jaa hasira. Jery akamtazama kijana aliyopo ndani hapo, kisha akawatazama walinzi hao waliomo ndani hapo.

“Mpango wako wa kumuua Shani sinto ushangaa kwa maana ulimuua kaka yangu wa tumbo moja kisa ni jambazi. Mikono yako iliyo jaa damu na laaana sidhani ni kwa nini hadi leo hii una endelea kukalia hicho kiti cha uraisi.”

Jery alizungumza kwa kujiamini huku akiwa amejianda akwa kila jambo. Raisi Mtenzi akamtazama kijana wa IT pamoja na walinzi wawili kwa maana kuna baadhi ya siri hususani za kumuua mwanaye hapendi watu kuzifahamu. Akatoa ishara kwa kijana huyo kutoka na wakabaki walinzi.

“Haitoshi uliamua kumuua mpenzi wa Shani ili kukizi matamanio yako ya kingono, alafu unakuja kuniambia kwamba ohoo sijui sijawahi kutoka nje ya ndoa. Yaani nyinyi ndio wazazi wapumbavu ambao muna waambia watoto wenu kwamba mulikuwa muna faulu darasani kumbe vichwani ni mabuyu. Ulimshikia Shani bastola ili akunyonye mbo** yako kwani mama yangu alikuwa akutoshelezi eheee?”

Jery alizidi kuzungumza kwa hasiri na kumfanya raisi Mtenzi ahisi kifua chake kina banjika kwa hasira kali. Macho ya walinzi ikawa ni kutazama jinsi vita hiyo ya baba na mwana inavyo kwenda. Raisi Jery akaingiza mkono wake chini ya meza na kuchoma bastola yake ya dharura, kitendo cha kuikoki tu, Jery akakunjua teke moja kali liliyo ipiga mikono ya baba yake na bastola hiyo ikaangukia pembeni. Walinzi wakamsogelea Jery ili wamzuie wasimshambulie raisi kwa maana jukumu lao ni kumlinda raisi. Ila kwa kasi ya ajabu Jery akawashambulia walinzi wote wawili na ndani ya dakika moja walinzi wote wakazimia jambo lililo mfanya raisi Mtenzi kutokwa na macho ya mshangao kwa maana siku zote anatambua kwamba Jery hajimudu kwenye maswala ya kupigana na alimchukulia ni mtoto wa mama.


“Usinifikishe sehemu ambayo sihitaji kufika mzee. Endapo uta dhubutu kumgusa Shani na kuirudhu mimba yake iliyopo tumboni mwake. Nina kuapia kwa Mungu wangu, nita toa siri zako zote kwa waandishi wa habari alafu uta ona kama wale walio kuwa wana kuamini na kukusudia kama wata endelea kufanya hivyo”

Jeru alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama raisi Mtenzi ambaye bado yupo na mshangao mkubwa kwani hadi sasa haamini kama huyo anaye ongea mbele yake ni Jery. Jery akatoka ndani hapo na moja kw amoja akaeleka chumbani kwake huku akiongozana na walinzi wake. Taratibu raisi Mtenzi akaka kwenye kiti chake huku akiwatazama walinzi wake wanao nyanyuka taratibu.

“Muheshimiwa upo salama”

Mlinzi mmoja alizungumza huku akiwa na maumivu makali sana.

“Kapumzikeni niacheni peke yangu”

“Muheshimiwa”

“Nimesema kapumzikeni”

Raisi Mtenzi ikambidi kuzungumza kwa ukali na walinzi wake hao wakaondoka huku kila mmoja akiwa na wasiwasi wa kazi yake kwa maana wameshindwa kumzuia Jery.

‘Ameyajulia wapi huyu chizi?’

Raisi Mtenzi aliwaza akilini mwake na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa moja kwamba ni nani ambaye amatoa siri ya yeye kumua kijana ambaye alikuwa ni mpenzi wa Shani.

***

Majira ya nne usiku nabii Sanga akafika katika hoteli ya Serena. Akashuka kwenye gari lake na kutembea hadia mapokezi. Kabla hajaitoa simu yake mfukoni kumpigia balozi Trump simu yake ikaanza kuita, akaitoa kwa haraka mfukoni na kukuta ni namba ya balozi Trump.

“Nakuona umefika”

Sauti ya kike ilisikika vizuri katika sikio la nabii Sanga. Akatazama moja ya kamera iliyopo eneo hilo la mapokezi.

“Ndio”

“Walinzi wangu wata kuja kukufwata hapo. Wamevaa suti nyeusi”

“Sawa”

Simu ikakatwa, hazikuisha hata dakika mbili walinzi wawili wakafika mbele ya nabii Sanga. Wakampa ishara ya kumfwata. Kabla ya kuingia kwenye lifti waka mkagua na kumkuta hana silaha yoyote. Wakaingia ndani ya lifti na kuelekea juu. Mlango ukafunguna na wakatoka katika lifti hiyo. Nabii Sanga akawatazama walinzi walipo katika kordo hiyo. Wakaingia katika chumba cha balozi Trump.

“Karibu nabii Sanga ni furaha yangu sana kukutana na wewe”

Balozi Trump alizungumza huku usoni mwake akiwa amejawa na tabasamu pana sana.

“Nina shukuru”

“Una weza kukaa”

Taratibu nabii Sanga akaka kwenye moja ya kiti huku macho yake yakimtazama mwana mama huyo ambaye ana urembo fulani ambao una mvutia kila mwanaume. Balozi Trump akawapa ishara walinzi wake kutoka ndani happ na akabaki na nabii Sanga peke yake.

“Leo nilikuwa na binti yako ila nina ona hatukuelewana”

“Nime ona ulicho mtuma kukileta kwangu. Ila kwa namna moja ama nyingine nina hitaji kukuuliza swali, kwa nini familia yangu”

“Una maanisha nini unapo sema kwa nini familia yako?”

“Kwa nini mufwatilie familia yangu”

“Nabii Sanga, tambua kwamba sisi tume iweka dunia nzima mikononi mwetu. Hilo usilisahau kabisa, ndio maana una weza kujiuliza kwa nini tulikwenda kumsaka Osama Bin Laden”

“Mulimsaka yeye kwa manaa aliwaua raisi wenu. Ila mimi sijafanya jambo lolote katika nchi yenu. Kwa nini muitwatikea familia yangu na kuipa vitisho”

Naibii Sanga alizungumza kwa msisitizo huku akimkazia macho mwana mama huyo.

“Sanga sio vitisho. Jukumu letu sisi ni kuhakikisha kwamba dunia ina ishi salama na ina kuwa salama. Ila wewe ni chui uliye jivisha ngozi ya kondoo. Una tumia dini kuficha dhambi zako, una miliki kundi la majasusi na wauza madawa ya kulevya. Una waua vijana wangapi kwa madawa ya kulevya yanayo ingizwa ndani ya Afrika, America na Asia”

Balozi Trump alizungumza kwa ukali sana huku akimkazia macho nabii Sanga.

“Mbaya ume mrithisha mwanao. Do you think kama nchi yako imeshindwa kukujua unahisi sisi wengine wa nje ambao tuna nguvu na uwezo wa kuingia mahala popote tuna shindwa. Tena shukuru Mungu tume kufanyia wema kukupa faili lako lenye siri zako. Ila serikali yangu ilikuwa ime panga kuleta vikosi vya FBI hapa kukukamata kwa maana kama ni ushahidi wote tunao”

Balozi Trump alizungumza kwa ukali huku macho yakimtoka. Nabii Sanga hakuingiwa na hofu yoyote kwani anacho kihitaji yeye kwa wakati huo ni kufahamu udhaifu wa mwana mama huyo na nchi yake.

“lla kwa nini hamkuwatuma kunikamata kama kweli mulikuwa muna nihitaji”

Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mwana mama huyo.

“Ohoo”

“Yaa muna jua ni nini. Muna makosa mengi sana ambayo mume yafanya katika nchi yangu. Moja ya kosa kubwa ni kufanya jaribio la kumuu raisi wa hii nchi, na walio fanya hivyo wapo mikonini mwa nchi hii. Muliwaajiri Boko Haramu ili kumteka chief secretary wa nchi hii na ushahidi wa mkataba upo na nina imani kwamba mkataba huo ukitoka hadharani raisi wako ana kwenda kunyongwa. Una lifahamu hilo?”

Balozi Trump akashusha pumzi nyingi huku akimtazama nabii Sanga.

“Isitoshe nami nina hizi”

Nabii Sanga akaweka moja ya video kwenye simu yake na kuiweka mezani. Balozi Trump taratibu akaichukua simi hiyo na kuanza kutazama video za wanajeshi wa Marekani ambao wana fanya mauaji ya kikatili ya watoto wadogo huku wengine wakiwabaki wasichana wadogo.

“Hayo ni matukio yaliyo tokea Siria, Somalia, Pakistani, na Iraq. Ukipeleka mbele una weza kuona tukio la raisi wako kipindi ni mkuu wa jeshi la Navy alivyo fanya shambulizi la bomu la gesi na kuua thousand of people Kashimir. Nina siri za nchi yako nyingi sana hususani na serikali iliyopo hapa madarakani. So kama muliweza kunijua mimi basi hata mimi nina wajua nyinyi”

Balozi Trump akaishiwa na pozi na kujikuta akikaa kimya huku akitazama video hiyo. Hadi ana maliza kutazama video hiyo akamtazama nabii Sanga.

“Una weza kumtumia raisi wako alafu uka muambia kwamba endapo akijaribu kumake any step katika familia yangu nami nita hakikisha kwamba nina distory nchi yake na ata poteza kila kitu alicho nacho. Una nielewa”

Nabii Sanga akazungumza kwa msisitizo.

“Isitoshe nina watu wangu hadi ndani ya ikulu yenu ya Marekani, kama nilivyo na watu wangu katika ikulu ya Tanzania hivyo endapo mukifanya chochote basi raisi wako naye……”

Nabii Sanga akaonyesha ishara ya kupitisha kiganja chake shingoni mwake ikiwa ni ishara ya kwamba raisi huyo ata uwawa.

Ukimya ukatawala ndani ya chumba hicho huku balozi Trump akionekana kutafakari ni kitu gani afanye.

“Hei madam ume nielewa?”

“Ndio Sanga nime kuelewa. Ila lengo letu halikuwa baya”

"Ila likukuwa ni kunitisha mukihisi kwamba munaye mtisha ni mjinga. Nipo very smart kwenye maisha yangu ndio maana nime kuwa bilionea mkubwa ila nisiye julikana kama ni bilioea.”

Balozi Trump alasimama, akatemba hadi katika friji. Akafungua na kuchukua wyne pamoja glasi mbili na kurudi nazo sehemu alipo nabii Sanga.

“Wyne?”

Balozi Trump alizungumza huku akimtazama nabii Sanga.

“Weka”

Akamina katika glasi hizo mbili kisha akamkabidhi nabii Sanga glasi moja.

“Tuzungumze sasa biashara”

Balozi Trump alizngumza huku akiwa na tabasamu.

“Hatuwezi kuzungumza biashara hadi tuwe na raisi wako kwa pamoja ndio tuta zungumza biashara”

“Raisi wangu?”

“Ndio una masa sabini na mbili nina muhitaji raisi wako ndani ya nchi yangu. Kama ata kuja kwa njia ya siri aje kama ata kuja kwa njia ya kujulikana aje. Ila nikiwa naye ndio tuta zungumza biashara. Nina imani mimi ni mtu mmoja tu ndani ya hii nchi ambaye sitegemewi kwa mambo makubwa. Ila raisi wako ana tegemewa na watu wake hivyo kuwa makini sanaa kwenye huu mchezo kwa maana tusipo kuwa makini tuna poteza wote”

Balozi Trump akashusha pumzi nyingi sana huku akimtazama nabii Sanga kwa maana kile alicho kuwa ana kitarajia sicho alicho kutana nacho. Nabii Sanga akapiga mafumba mawili ya wyne hiyo na ikaisha kwenye glasi hiyo kisha akasimama.

“I hope kwamba tumeelewana”

“Ndio Sanga nime kuelewa. Ila kuna kitu kimoja ume sahau?”

“Kitu gani?”

Balozi Trump akaweka glasi yake mezani kisha akasimama, akaanza kufungua vifungo vya hsti lake jeupe, akalivua na kulitupa pembeni na akabakiwa na siridia. Akamsogelea nabii Sanga na kumshika kidevu chake kwa vidole laini. Akazisogeza lipsi zake karibu na nabii Sanga, ambaye kwa sekunde kadhaa akamtazama kisha akaanza kumnyonya. Hisia za kimapenzi zikapanda kati yao na kila mmoja akamvua mwenzake nguo. Nabii Sanga akambeba mwana mama huyo na kumlaza kitandani na taratibu wakaanza kupeana burudani huku balozi Trump akiamini kwamba kutoa penzi kwa naabii Sanga ita kuwa ni njia rahisi ya kumpata nabii Sanga ili kuitekeleza kazi ambayo serikali yake ina ihitaji, huku akilini mwake nabii Sanga akiamini kwamba penzi la mwanamke huyo ni kama penzi la wanawake wengine halina thamani yoyote kwake.

***

Evans akiwa amevalia nguo nyeusi, gloves nyeusi na mkononi mwake huku usoni mwake akiwa amevalia bushori yeusi lililo funika kichwa chake kizima na ni sehemu ndogo tu ya macho ndio ime salia. Evans akaitazama saa yake ya mkononi na ina muonyesha ni saa sita kasoro usiku. Akatembea kwa umamini kwenye ukuta wa jumba la nabii Sanga kisha akauparamia kwa umakini sana huku akiitazama kamera iliyo mpa mgongo. Haikuwa tabu sana kwa Evans kuruka nyanya za umeme zilizo fungwa juu ya ukuta huo na kuingia ndani. Akanyata kwa umakini huku akizikwepa kamera hizo hadi kwenye dirisha la sebleni. Akachungulia ndani na kuona hakuna kitu chochote. Akaendelea kunyata kwa ukakini hadi kwenye mlango wa kuingilia ndani hapo.

‘Litakuwa wapi?’

Evans alizungumza kimoyo moyo huku akitazama eneo la sebleni na hakuweza kuliona faili hilo. Akapandisha ngazi za gorofani kwa kunyata. Katika eneo la juu kuna vyumba zaidi ya sita jambo lililo mfanya Evans kufikiria kwa dakika kadhaa. Kisha akaanza kufungua chumba kimoja baada ya kingine. Kwa bahati chumba cha pili kufungua akamshuhudia Julieth akiwa amelala kitandani huku akiwa kama amezaliwa Katika kuangaza katika chumba hicho akaona faili alilo ambiwa na Leila likiwa katika meza. Taratibu akaingia chumbani hapo kwa mwendo wa kunyata. Leila aliye jichokea kwa uchovu wa majanga ya siku hiyo hakuweza kisikia chochote kabisa. Evans akachukua faili hilo na kulifungua ndani, kilicho andikwa kikamduwaza sana. Akatoka ndani hapo na faili hilo na kutoka katika njia aliyo ingilia pasipo walinzi getini kuweza kufahamu chochote. Evans akavua kofia hilo, akafika eneo la waendesha pikipiki. Akapanda moja ya pikipiki na kurudi hotelini.

Akaanza kulipitia taratibu na kila ukurasa ana ufungua na kusoma matukio yaliyo andikwa ndani ya faili hilo akajikuta mdogo wake ukiwa wazi.

“What the fuc**?”

Evans alishangaa ila moyoni mwake akaanza kujawa na furaha kwa maana ana amini kwamba sasa ni wakati wake kujipatia pesa nyingi kutoka kwa nabii Sanga kwani sasa ana zifahamu siri zake zote. Akaichukua simu yake na kuitafuta namba ya Magreth na kumpigia.

“Haloo”

Sauti iliyo jaa usingizi ilisikika masikioni mwa Evans.

“Vipi ume lala mke wangu”

“Yaaa nilipitiwa na usingizi. Vipi upo wapi?”

“Nahitaji kuja kwako usiku huu”

“Sawa baby wewe njoo”

Evans akaoga na kuvaa nguo nyingine. Akalitazmaa faili hilo la nabii Sanga na familia yake.

‘Sijui nimpelekee?’

Evans alijiuliza maswali yasiyo na jibu.

‘Kuliacha hapa hotelini sio jambo zuri wapi niliweke?’

Evans aliendelea kuwaza kwa maana hamuamini mtu yoyote. Akalibebe faili hilo na kuondoka hotelini hapo kwa usafiri wa taksi. Akafika nyumbani kwa Magreth na kukaribishwa hadi ndani na Magreth na kumkuta Josephine akiwa sebleni.

“Karibu sana shemeji”

“Nashukuru, vipi nimewasumbua?”

“Hapana huja tusumbua karibu sana.”

Josephine alizungumza huku akilitazama faili lililopo mkononi mwa Evans.

“Leo mpenzi wangu ulikuwa bize nini?”

“Yaa kuna mambo ya kibiashara nilikwua nina yaweka sawa”

“Vipi nikuandalie chakula?”

“Hapana nipo vizuri”

“Hilo faili ni la nini, kwanza ni jeusi pili lime andikwa top secret. Kuna siri gani ndani ya hilo faili”

“Hakuna cha maana mke wangu. Nina imani kwamba nyinyi muna fanya kazi nzuri sana na raisi Mtenzi”

Josephine na Magreth waka tazamana.

“Ahaa hatuna imani naye tena”

Josephine alijibu kwa sauti ya unyonge

“Muna maanisha nini?”

“Leo nime onyeshwa kwenye maono yangu ni mtu mbaya sana ambaye ame ua watu wasio na hatia kwa ajili ya maslahi yake binafsi. Hapa alipo yupo katika mpango wa kumua mke wa mwanaye”

“Mke wa mwanaye ambaye ni Julieth”

“Sio mke ni kimada wa Jery”

Magreth alimsahihisha Josephine sentensi yake.

“Kwa nini sasa ana taka kumuua”

“Yule binti ana ujauzito wa Jery ambaye yupo kwenye ndoa. Ila sababu kuu ya kumuua ni kwamba mzee ana muhitaji kimapenzi yule binti. Kiufupi ana mpenda, yaani toka nifahamu hayo mambo hapa nina fikiria jinsi na namna ya kuweza kumtoa raisi Mtenzi madarakani kwa maana ana igarimu nchi. Ile milipuko ya mabomu iliyo tokea yote ni kwa sababu yake.”

Josephine alizungumza kwa msisitozo na dhahiri ana onyesha kwamba ameuchoka utawala wa raisi Mtenzi.

“Ila si una jua kumtoa raisi madarakani kwa njia za kinyemela ni moja ya makosa ambayo ukijulikana una hitaji kufanya hivyo una uwawa kwa kunyongwa au kuchomwa sindano ya sumu?”

“Shemeji nina lifahamu hilo. Ila ni heri kufa kuliko kuacha akatumia madaraka yake mabaya”

“Mmmm ila hii mada ni nzito jamani”

Evans alizungumza huku akishusha pumzi.

“Ndio mume wangu. Ila tuna kuomba utusamehe tuna imani wewe ni mfanya biashara hivyo mambo ya kisiasa hususani ya nchini kwetu”

“No usijali mke wangu, mimi pia ni Mtanzania na ninapo ona nchi yangu ina teketea kwa vitu au kwa watu kama hawa ni lazima nijisikie vibaya.”

“Hembu shemeji toa maoni yako. Nifanye jambo gani kwa maana hadi una ona hii nchi ipo hivi ina tulia ni kutokana na uwezo wa maono yangu aliyo nipa Mungu.”

Evans akajifikiria kwa sekunde kadhaa, akamfirikia nabii Sanga na matatizo yake, akapiga mahesabu ya haraka haraka na akapata jibu kichwani mwake ambalo ana amiini kwamba atakapo muambia Josephine na Magreth basi wata fwata kile alicho washauri.



“Musimtoe raisi madakarani”

Kauli ya Evans ikawashangaza Magreth na Josephine.

“Kwa nini shemeji?”

“Hadi kuwa raisi ina maana kwamba aliweza kuchaguliwa na watu pamoja na Mungu pia. Tumuache katika nafasi yake n a isitoshe hilo linalo endelea hivi sasa ni matatizo yao ya kifamilia ambayo endpo nyinyi muta yaingilia na siku wakija kupatana baba na mwanaye. Nyinyi ndio muta aibika”

Evans alizungumza huku akiamini kwamba Jery na baba yake wakigombana basi ita kuwa ni rahisi sana kwake kulipiza kisasi kwa Jery.

“Ila anacho kisema George ni kweli. Unajua wale ni mtu na mwanaye, tukiingilia sisi, siku wakipata itakuwa shida kwetu”

“Kwa hiyo Magreth una hitaji sisi tumuache yule binti wa watu afe pasipo kuwa na kosa lolote?”

“Sija maanisha hivyo Jose, ila hii ni vita ya kifamilia. Sisi kama ni kumsaidia, tumsaidie tu yule msichana, ila swala hilo la raisi kutoka madarakani tuachane nalo rafiki yangu. Wewe nenda kazini kama kawaida na wala usimunyeshe kwamba ume weza kufahamu mambo yake. Fanya kazi kama kawaida”

“Akiniuliza kwamba nimeweza kufahamu yule msichana yupo wapi?”

“Wewe muambie bado Mungu haja kujibu na hato weza kukulzamihsha kwa manaa hicho ulicho nacho wewe ni kipawa na Mungu ana kujibu pale anapo hitaji yeye na sio tunavyo taka sisi binadamu”

“Ni kweli shemeji, fanya hivyo kama alivyo kushauri Mage”

“Poa nitafanya hivyo. Jamani ngoja niwaache, usiku mwema”

“Nawe pia”

Josephine akaingia chumbani kwake na akabaki Evans na Magreth sebleni. Taratibu Magreth akamkalia Evans mapajani mwake na kuanza kumnyonya lipsi.

“Hei Mage nikuamini?”

Evans alizungumza huku akimtazama Magreth usoni mwake.

“Yes baby, kwa nini usiniamini”

“Nina maana yangu ya kuzungumza hivyo”

“Niamini mpenzi wangu”

“Twende chumbani”

Wakanyanyuka na kuingia chumbani huku Evans akiwa ameshika faili hilo mikononi mwake. Magreth akafunga mlango kwa ndani na wakaka kitandani.

“Una hisi nabii Sanga ni mtu wa aina gani?”

Swali la Evans likamfanya Magreth kukaa kimya kidogo.

“Kwa nini ume niuliza mume wangu?”

“Kwa sababu, ulinieleza juu ya maisha yako na nabii Sanga. Nina hisi kwamba nina weza kufahamu japo mambo machache juu yake”

“Nabii Sanga sio mtu mwema”

“Una maanisha nini?”

“Ni mwanaume ambaye ana tumia muamvuli wake wa kinabii kufanya mambo yaliyo machafu sana kwenye hii jamii. Nina jaribu kuyatafuya mambo yake ili niweze kulipa kisasi cha kuniharibia maisha yangu, kunitoa usichana wangu na kumfukuza mwanaume niliye mpenda kwenye maisha yangu. Ila samahani kwa kuweza kuzungumzia swala la mwanaume wangu niliye mpenda”

Magreth alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge mwingi.

“Usijali Mage nina elewa. So ukipewa nafasi ya kulipiza kisasi kwa nabii Sanga uta mfanyia nini ili nafsi yako iweze kuridhika?”

“Nahitaji kumuacha uchi kabla hajakufa kifo cha mateso na aibu kubwa yeye na familia yake”

“Kivipi?”

“Endapo nita fahamu udhaufu wa familia yake kwa ujumla na nikawa na ushahidi kamili. Nita kwenda kuyatangaza hadharani ili wale watu wanao msujudia kila siku na kumiamini waweze kuwa wa kwanza kumpinga na ikiwezekana wampige mithili ya kibaka aliye kwapua pochi ya mwana mama. Ila George kwa nini una niuliza hayo yote?”

Evans akaka kimya kisha akaliweka faili hili pembeni na kuvishika viganja vya Magreth.

“Mage”

“Bee”

“Nina kupenda sana”

Evans alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Magreth akajawa na furaha sana, kwani neno hilo la Evans lime usisimua mwili wake wote.

“Asante mume wangu. Haki ya Mungu ume lete furaha kubwa sana kwenye maisha yangu”

“Uta zidi kupata furaha. Muda na wakati ukifika nita kueleza kila kitu”

“Kitu gani?”

“Usijali nita kueleza kila aina ya jambo. Kwa sasa muda bado haujafika”

“Sawa, je nina weza kuona kilichomo ndani ya hilo faili?”

“Hapana”

“Kwa nini?”

“Muda wake haujafika. Ukifika uta ona kila kitu”

“Sawa mume wangu, je nina weza kukujua wewe vizuri kwa maana siku ile tulipo pambana na wale vibaka nime ona una mapigo ambayo ni ya mtu aliye pata mafunzo makali”

“Yaa, katika kipindi changu cha mapumziko baada ya kufanya biashara kwa kipindi kirefu, huwa nina jiunga na mafunzo ya kujilinda binafsi. Kama unavyo tambua ukiwa tajiri hususani kwa nchi kama Marekani, ina bidi uwe una uwezo wa kujilinda mwenyewe. Ndio maana nipo hapa nchini Tanzania na sina hata mlinzi wangu mmoja kwa maana nina jiamini sana”

“Ila ni hatari, kama maadui zako wakifahamu kama upo Tanzania wana weza kuja kukuuliza huku huku”

“Hakuna amabye ata weza kufanya hivyo”

Magreth akaanza uchokozi wa kumpapasa Evans mwili wake, Evans akafungua moja ya droo iliyopo pembeni ya kitanda. Akaingiaza faili hilo na taratibu wakaanza kuchezeana viongo vya miili yao na ndani ya muda mchache wakajikuta wakizama katika dimbwi zima la mapenzi.

***

Sauti ya mlango kugongwa ikamfanya Julieth kufumbua macho yake taratibu huku akiwa amejawa na uchovu mwingi sana.

“Bado ume lala?”

Mrs Sanga alizungumza huku akiingia ndani hapo.

“Nimechoka sana mama kwani sasa hivi ni saa ngapi?”

“Saa nne kasoro”

“Ohoo!!”

Julieth aligamami kidogo huku akiitafuta simu yake, akaiona pembeni ya mto wake, akaichukua na kutazama kama kuna mtu aliye mpigia ila hakukuta missed call hata moja.

“Nime chelewa kurudi ikulu”

“Usijali kwani si uliaga na upo kwenu”

“Ndio, ehee vipi baba amefanikiwa?”

“Baba yako ame rudi asubihi hii. Ana hitaji lile faili”

“Lipo hapo mezani”

Julieth alizungumza huku alipiga miyayo ya uchovu wa usingizi.

“Mezani wapi?”

Mrs Sanga alizungumza huku akitazama katika meza ya kioo iliyopo ndani hapo na hakuona kitu chochote.

“Si hap…..”

Julith macho yakamtoka mara baada ya kuona faili hilo alipo. Akashuka kitandani kwake akiwa uchi, akainama na kuangalia chini ya meza na hakuweza kuona chochote.

“Faili nililiweka hapa”

Julieth alizungumza huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.

“Sasa mbona halipo?”

“Hata sijui mama, ime kuwaje kwani?”

“Ime kuwaje maana yake nini?”

“Mama faili jana usiku nililiweka hapa juu ya meza. Nikapanda kitandani na nika lala, sasa ime kuwaje asubuhi lisionekane”

“Weee mtoto acha masihara”

“Sio masihara mama, nililiweka hapa”

“Ohoo Mungu wangu. Sasa una taka kusema lime potea?”

“Hata sijui mama”

Wakaanza kusaidiana kukitafuta ndani ya chumba kizima ila halikuwepo kabisa jambo lililo sababisha wajawe na hofu kubwa sana.

“Vaa uje sebleni”

Mrs Sanga alizungumza kwa unyonge huku akitoka ndani hapo. Mwili mzima wa Julieth ume jawa na jasho litokanalo kwa woga, japo ndani ya chumba chake kuna AC ila ukweli ni kwamba ana jihisi vibaya sana. Kila akijaribu kuvuta kumbukumbu zake ana kumbuka eneo la mwisho alipo weka faili hilo ni juu ya meza hiyo.

“Lipo wapi?”


ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

BLOG