Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 5/10

 

 


 MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE)

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 5 KATI YA 10

 


***

Rahab akiwa ndani ya gari kuelekea ikulu simu yake ikaanza kuitwa. Kwa haraka akiatoa mfukoni na kukuta ni namba ya balozi wa Ungereza hapa nchini Tanzania, akaipokea na kuiweka sikioni.

“Habari yako muheshimiwa raisi”

“Salama bwana Balozi”

“Kuna habari za kiusalama nimweze kuzipata kutoka kwa mmoja wa wananchi wako ninaweza kukuambia?”

“Yaa unaweza niambia, zinahusiana na nini?”

“Kuna binti anaitwa Shamsa, ametutumia video ya wasichana magaidi ambao wamehusika katika tukio zima la mauaji ya walinzi katika jumba moja huku akiwatorosha dokta Ranjiti pamoja na mwanaye”

Habari hiyo ikamstusha sana Rahab na kujikuta akikaa vizuri kwenye siti hiyo ya gari.

“Tumeweza kuwa track na kugundua kwamba kwa muda huu wapo Mbezi Luis, na kunatukio jengeni la kigaidi ambalo wamelifanya na kuondoka na mtoto mmoja wa kike ambaye kwa asilimia mia moja tumefahamu ni mtoto wa makamu wa raisi”

“U….me…sema ni ni mtoto wa Eddy?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Kwa sasa yupo wapi?”

“Wanaondoka katika eneo hilo na wapo katika barabara ya Morogoro, wanaelekea Chalinze”

“Muheshimiwa balozi, ninakuomba msaada wa kikosi chako huku na mimi nikitoa taarifa kwa vikosi vyangu ili tuweze kuwaweka kati”

“Sawa muheshimiwa raisi nitatoa helicopter yenye vijana wanne ambao wataweza kuhakikisha kwamba wanawafwatila kwa juu, kila wanapo kwenda na vikosi vya ardhini nina amini muheshimiwa raisi utaweza kulishushulika hilo sasa hivi”

“Ndio, asante kwa taarifa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Rahab kwa haraka kakata simu yake na kumtafuta kamanda mkuu wa jeshi. Simu ya kamanda huyo ambaye hadi sasa hivi hajafanikiwa kumpata dokta Ranjiti na alipewa masaa ishirini na nne ili aweze kuikamilisha kazi hiyo, akaipokea simu ya raisi kwa wasiwasi.

“Muheshimiwa”

“Andaa vijana wako waizunguke barabara ya Morogoro Road tumewapata wahusika ambao wamehusika na tukio la kumtorosha dokta Ranjiti na Anna na hadi sasa hivi wana mtoto wa makamu wa raisi”

“Sawa muheshimiwa, wapo kwa miguu au gari?”

“Wapo na gari, fanya hiyo. Au fanya hivi, piga simu kwenye ubalozi wa Ungereza watakueleza detail mzima za tukio hili”

“Sawa madam President”

Rahab akakata simu kwa haraka kampigia mlinzi mkuu anaye mlinda Eddy eneo la hospitalini alipo lazwa.

***

Kila aliye weza kuiotazama sura ya makamu wa raisi, akatambua dhairi kwamba huko ndani alipo toka hali si shwari, mkono wake unamwagikwa na damu ila hilo wala halijali sana.

“Muheshimiwa una jeraha mkononi mwako”

Mkuu wa kiosi hicho akapata ujasiri wa kuzungumza na Eddy hata kama amekasirika sana. Eddy akalitazama jeraha hilo, akashusha pumzi nyingi pasipo kujibu chochote. Mkuu huyo hakuwa na jinsi zaidi ya kuhakikisha anakisukuma kiti cha makamuwa wa raisi kurudi katika chumba alicho kuwa amelazwa. Akiwa hatua chache kutoka eneo la mlango wa chumba hicho, simu yake ikaanza kuita, ikambidi kwa haraka aitoe mfukoni mwake, alipo kuta ni muheshimiwa raisi, ikamlazimu kwa ishara kumuamrisha mlinzi wake mmoja kumuingiza muheshimiwa makamu wa raisi kuingia ndani ya chumba hicho.

“Ndio muheshishimiwa raisi”

“Upon a makamu wa raisi hapo?”

“Ndio muheshimiwa”

“Mkabidhi simu”

“Sawa dakika moja”

Mzee huyo akainigia kwenye chumba alichopo Eddy, kwa bahati mbaya akakukta Eddy akiwa ameshika moja ya chupa ya jagi la glasi, akalipiga chini na likasambaratika.

“Ni nini hicho kilicho pasuka?”

Rahab aliuliza kwa mshangao.

“Muheshimiwa raisi, makamu wa raisi hayupo sawa kwa sasa, sidhani kama anaweza kuzungumza na wewe”

“Nimsema mupe simu, kwani umeweza kusikia kauli yake ya kukataa kuzungumza nami?”

“Samahani muheshimiwa”

Mzee huyo alizungumza n kumsogelea makamu wa raisi, ambaye uso wake umelowana kwa machozi mengi sana.

“Mkuu kuna simu yako kutoka kwa muheshimiwa raisi”

Jicho la ukali alilo tazamwa nalo mzee huyo, kikamfanya kunywea kwa sekunde kadhaa, kwani ni jicho la ubaya. Taratibu mzee huyo akairudisha simu yake sikioni.

“Muheshimiwa raisi, makamu wa raisi kwa sasa hayupo sawa”

“Weka loud speaker”

Mzee huyo akaweka.

“Eddy nina imani kwamba unanisikia vizuri. Nina habari nzuri. Tumeweza kugundua watu ambao wammteka Camila na hadi sasa hivi tunashirikiana na vikosi vya usalama vya Ungereza kuhakikisha kwamba tunaweza kuwapata wasichana hao”

Eddy akaitazama simu hiyo, taratibu akaichukua na kutoa loud speker kisha akaiweka sikioni mwake.

“Wapo wapi?”

Eddy alizungumza kwa sauto nzito na iliyo jaa mikwaruzo.

“Wapo katoka barabara ya Morogoro Road”

“Una uhakika wana Camila wangu”

“Ndio”

“Hakikisha hawatoki hivi sasa”

“Sawa:”

Eddy akakata simu na kumgeukia mzee huyo.

“Niitie dokta Benjamini”

“Sawa mkuu”

Eddy akamkabidhi mzee huyo simu, kisha akatotoka katika eneo hilo. Baada ya dakika tatu dokta Benjamini akaingia katika chumba hichi.

“Nichome sindano ya kuzuia maumivu”

“Tena muheshimiwa!!?”

“Fanya hivyo”

Dokta Benjamini macho yakamtoka huku akitazama jereha la Eddy lililopo mkononi mwake. Kwa harak akaanza kuhudumia jeraha hilo, alipo hakikisha kwamba amezuia damu kumtika Eddy, akachukua dawa ya kutuliza maumivu, akamchoma tena Eddy kwenye mkono wake. Eddy akayafumba macho yake kwa sekunde kadhaa huku akisikilizia dawa hiyo inavyo fanya kazi mwilini mwake.

Baada ya dakika kama tano Eddy akasimama, akatazama jeraha la mguuni mwake, pamoja na mkononi mwake.

“Nipatie dawa ya kutuliza maumivu, na sindano”

“Muheshimiwa kukuvunjia heshima, siwezi kufanya hivyo, unaweza kujidhuru”

Eddy kwa haraka akamshika dokta Benjamini koti lake na kumsogeza karibu kabisa na uso wake ulio kunjamana kwa hasira huku uso ukiwa unameremeta kwa jasho jingi linalo mtoka japo ndani ya chumba hichi kuna hewa ya A/C.

“Nimesema nipatie dawa, na sindano, la sivyo utanijua mimi ni nani?”

Dokta Benjamini huku akitetemeka, akachukua kichupa kidogo kiasi kilicho jaa dawa ya kujizuia maumivu, akachukua bomba la sindano na kumkabidhi Eddy mkononi mwake.

“Nenda katika chumba cha mke wangu, mchome sindano ya usingizi anayo weza kulala hadi kesho asubuhi nitakapo rejea sawa”

“Sawa muheshimiwa”

Eddy akamsukumia dokta Benjamini pembeni kisha akatoka ndani humo. Walinzi wote walipo muona makamu wa raisi anatembea wakabaki wamejawa na mshangao.

“Hakikisha munalinda katika chumba cha mke wangu na hakikisheni kwamba hatoki nje ya chumba hicho mume nielewa”

“Ndio muheshimiwa makamu wa raisi”

“Wewe na wewe twnedeni”

Eddy alizungumza huku akiwanyooshea vidole vijana wawili.

“Muheshimiwa makamu wa raisi, kama unahitaji kutoka hutakiwi kutoka na vijana wawili?”

Mkuu huyo wa kikosi alizungumza huku akimtazama Eddy usoni mwake.

“Nimekuambia wewe na vijana walio salia hakikisheni kwamba munamlinda mke wangu sawa. Hili sio ombi ni amri”

Mzee huyo akameza mate taratibu kwani makamu wa raisi amekuwa mbabe kupita maelezo na kila anacho kizungumza anahitaji kiweze kutekelezwa.

“Sawa muheshimiwa. Hakikisheni muheshimiwa anakuwa salama”

“Sawa muheshimiwa”

Vijana hao wakaondoka na Eddy ambaye hadi sasa hivi hakuna anaye tambua kwamba usiku huu muheshimiwa huyo anaelekea eneo gani.

***

Adrus na wezake walipo hakikisha kwamba wamezivaa nguo hizo za jeshi na kuwaficha wanajeshi hao walio wapiga, wakatoka nje, huku wakiwa wamevalia kofia zao vizuri, wakaanza kutembea katika karodo ya aneo hilo. Wakapandisha juu kabisa ya meli hiyo ambapo kuna uwanja mkubwa wa helicopter za kijeshi. Wakatembea kwa kujiamini huku Jing akiwa ametangulia mbele, huku Adrus na Cookie wakiwa nyuma wameshililia bunduki zao.

“Hapa tunatakiwa kuondoka na helicopter moja pasipo kustukiwa”

Njing alizungumza huku wakiendelea kutembea.

“Hapa helicopter ile inaweza kutufaa”

Adrus alizungumza huku akionyesha helicopter kubwa ya kijeshi.

“Inatufaa, kwa kweli ila jinsi ya kuondoka nayo, inabidi tusome mazingira”

“Sawa”

Wakasimama kwenye eneo moja, Jing akawageukia Adrus na Cooke na kujifanya anawapatia maelekezo. Wanajeshi wengine hawakuweza kwuastukizia kwa maana wingi wa wanajeshi katika eneo hilo ni kubwa na si wote wanajuana kwa majina wala sura. Wakatumia dakika tano kuweza kuyaelewa mazingira ya eneo hilo, kisha kwa hara wakaanza kuelekea kwenye helicopter hiyo waliyo ihitaji kuichukua.

Wakafanikiwa kuifikia, Jing kwa kujiamini sana, akaufungua mlango wa helicopter hiyo, macho yakawatoka baada

ya kuwakuna marubani wawaili wakiwa ndani ya helicopter hiyo.

***

Mwanga mkali wa gafla unao tokae angani ukamfanya Lizzy kupunguza kidogo mwendo wa gari lake na huchungulia.

“Ni nini?”

“Helicopter mkuu”

“Fuc** wamefahamu”

Lizzy alizungumza kwa hasira, akakanyaga breki za gafla na kusababisha gari hilo kusimama.

“Mbona umesimama mkuu?”

“Hatuwezi kusonga mbele, wala kurudi nyuma”

“Kwa nini?”

“Kuwa na akili ya kufikia haraka, mbele ni lazima watakuwa wamezuia barabara, na nyuma lazima watakuwa wanakuja na helicopter hii ni lazima itatufwatilia kila tunapo kwenda”

“Sasa tutafanyaje mkuu?”

“Nina PLAN B”

Lizzy alizungumza huku akimtazama Camila aliye bebwa na mwenzake aliye kaa siti ya nyuma katika gari hilo.



“Dora njoo uendesha gari”

Lizzy alizungumza huku akimtazama Dora, kwa haraka Dora akahamia siti aliyo kaa Lizzy huku Lizzy akikaa siti ya pembeni yake.

“Namuomba mtoto”

Lizzy alizungumza, akakabidhiwa mtoto.

“Endesha gari”

Dora kwa kasi akaondoka eneo hilo na kusababisha Helicopter hiyo kuzidi kuwafwatila. Lizzy akatoa simu yake mfukoni mwake, kwa haraka akamtafuta Livna na kumpigia. Simu ya Livna ikaanza kuita baada ya sekunde kadhaa ikapokelewa.

“Mkuu tuna tatizo”

Lizzy alizungumza huku kitazama umahiri wa Dora katika kuliendesha gari lao hilo.

***

“Tatizo gani?”

Livna aliuliza huku akivaa shati lake kwa haraka na kuanza kukimbilia katika chumba cha mawasiliano.

“Tunafwataliwa na hapa tupo katika matatizo makubwa sana”

Livna akazidi kuongeza mwendo kasi wa kukimbia hadi baadhi ya vijana wake wake wakabakiwa wakimshangaa. Kwa haraka akfungua mlango wa chumba hicho na kuwakuta vijana wake wakitazama video kupitia satelaiti ikionyesha jinsi gari hilo linvyo kimbizwa na helicopter hiyo.

“Ohoo Mungu wangu”

Livna alizungumza huku akiwa bado ameishikilia simu yake sikioni.

“Mkuu bora punda afe ila mzigo ufike salama”

“Lizzy una maanisha nini Lizzy?”

Livna alizungumza huku wasiwasi mwingi ukizidi kumjaaa. Simu ikakatwa jambo lililo zidi kumpagawisha.

“Waokooeeni wezeeenuuuuu”

Livna alizungumza kwa kufoka sana huku macho yakimtoka, kwani kumpoteza kamanda kama Lizzy ni pengo kubwa sana ambalo litakiyumbisha kikosi chake hicho cha kijasusi.

***

“Tuelekee nyumbani kwangu”

Eddy alizungumza na dereva huyo akafwata maelekezo anayo pewa na bosi wake. Wakafika nyumbani kwa Eddy ambapo bado ulinzi ni mkali sana. Eddy akashuka kwenye gari hilo, moja kwa moja akelekea katika chumba kilichopo chini ya ardhi, akatazama damu zilizo kauka ndani ya chumba hicho, ambapo majira ya asubuhi kulitoka mauaji ya wanajeshi wanne. Hakutaka kuzifwatilia sana, ndani ya chumba hicho kuna mlango wa siri ambao yeye na familia yake ndoo wanaufahamu. Ukitazama mlango huo upo kama ukuta tu na si jambo la rahisi sana kwa mtu kuweza kufahamu. Akaminya moja ya batani ya siri na sehemu maalumu yenye batani za nyingi ikafunguka. Akaingiza namba za siri na mlango huo ukafunguka, akasimama katikati ya mlango huo na kutazama vibunda vya pesa za kimarekani, zilizo pangiliwa vizuri na kufika nusu ya chumba kizima. Akaingia ndani na kufunga mlango wake, akachukua moja ya bastola yake anayo ipenda sana. Akavua nguo hizo za hospitalini alizo zivaa na kuchukua mavazi ya kijeshi, akayavaa taratibu. Alipo hakikisha kwamba yupo tayari kwa kila kitu, akatoka katika chumba hicho huku akiwa amebeba jaketi maalumu za kuzuia risasa. Akakifunga chumba chake hicho, akatoka nje kabisa la eneo hilo na kuwakuta walinzi wakiendelea kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.

“Nipatie simu yako”

Eddy alizungumza huku akimnyooshea mlinzi wake mkono. Mlinzi huyo akachomoa simu yake kumkabidhi Eddy, aliye anaza kundika namba ya Rahab alipo hakikisha kwamba ameipata akampigia. Simu ya Rahaba ikapokelewa.

“Mumefikia wapi?”

“Eddy”

“Nijibu hao magaidi walio mteka mwanangu wamefikia wapi?”

“Bado wapo barabarani”

“Nitumie signal nifahamu ni wapi walipo”

“Eddy si upo hospitali, hii oparesheni inafanywa na wa…..”

“Fanya kama nilivyo kuambia sawa”

Eddy alizungumza kwa ukali sana. Rahab hakuwa na jinsi zaidi ya kuwaamerisha watu wanao shuhulika na swala zima la mtandao kuweza kumtumia Eddy signa ya eneo wanapo elekea Lizzy. Eddy akalitazama eneo hilo, kisha akazunguka nyuma ya nyumba yake ambapo kuna gereji kubwa ya magari ambayo mara nyingu hayatumii. Eddy akapiga hatua hadi kwenye kabati lenye fungoa za magari yote hayo. Akazitazama funguo hizo kwa sekunde kadhaa, akachukua fungua ya gari aina ya Ferrali Spider.

“Mkuu unakwenda mwenyewe”

Mlinzi aliye kuja na Eddy alimuuliza huku akimtazama Eddy anaye fungua mlango wa gari hilo. Jicho kali alilo mtazama mlinzi wake ikawa ni jibu tosha kwake kwamba anaondoka mwenyewe na haitaji kuongozana na mtu. Akawasga gari lake na kutoka eneo hilo taratibu. Akaiweka simu hiyo pembeni yake inayo muonyesha ni eneo gani magaidi hao wapo. Kwa kasi akaondoka katika eneo hili huku moyoni mwake akidhamiria kuhakikisha kwamba anamuokoa mwanaye Camili ili marafi mke wake aweze kupata amani. Uzuri wa gari hilo, lina spidi mita mia nne na hamsini, uwezo ambao ni mkubwa sana kiasi cha kusababisha kila jinsi muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi alivyo zidi kufanikiwa kulifikia gari la Lizzy na vijana wake.

***

“Muheshimiwa?”

Msichana mmoja anaye shuhulika na swala zima la satelait katika chumba hichi cha mawasiliano kilichopo chini ya ardhi eneo hilo la ikulu.

“Nini?”

Rahab alijibu kwa hasira huku akimgeukia msichana huyo. Msichana huyo pasipo kuzungumza kitu chochote, akamgeuzia raisi Rahab laptop aliyo ishika mkononi mwake. Raisi Rahab akashuhudia gari dogo likizidi kusogelea gari la Lizzy na wezake.

“Ni nani?”

“Sijafahamu muheshimiwa ila inavyo onyesha ni mwenzo anaweza kwenda kuwapa msaada”

“Shit, hembu jaribuni kugundua ni nani aliyopo ndani ya gari hilo dogo”

Rahab alizungumza kwa sauti ya juu sana, wahusika wa kitengo hicho wakaanza kazi hiyo ya kutafuta ni nani aliyomo ndani ya gari hilo. Kijana mmoja akastuka sana baada ya kuina ni sura ya makamu wa raisi, akamtazama raisi Rahab anaye zunguka zunguka ndani ya chumba hicho.

“Nimempata”

Kijana huyo alizungumza kwa sauti ya juu huku akinyoosha mkono wake juu.

“Itume kwenye big screean”

Rahab alizungumza huku akiigeukia Tv kubwa sana iliyopo ndani ya chumba hicho. Kila mtu akabaki na kigugumizi hususuani Rahab ambaye anatambua kwamba Eddy anaumwa na kulazwa hospitalini kutokana na majeraha ya risasi alizo pigwa mguuni mwake.

Rahab kwa haraka akatoa simu yake mfukoni na kuipiga namba ya mwisho ambayo alizungumza na Eddy. Simu ikaita hadi ikakata, akapiga tena huku mapigo ya moyo yakizidi kwenda kasi kwani kwa jinsi mwendo kasi wa gari hilo unavyo kwenda, kusema kweli ni hatari sana. Simu ikapokelewa.

“Eddy ni nini unacho kifanya”

Raisi Rahab alizungumza huku machozi yakimlenda lenga usoni mwake.

“Ninafanya hili kwa ajili ya familia yangu”

“Eddy kumbuka kwamba wewe ni kiongozi”

“Uongozi si muhimu kama ilivyo familia yangu na mwanangu”

Simu ikakatwa na watu wote wakashuhudia jinsi raisi anavyo mwagikwa na machozi usoni mwake.

***

“Tunahitaji usafiri”

Jing aliwaabia marubani hao wa kijeshi huku akiwa amechomoa sindano mbili za sumbu. Marubani hao wakajawa na vigugumizi kwani hawajapokea amri yoyote kutoka kwa mkuu wao anaye husika na kitengo cha anga. Jing akapanda ndani ya helicopter hiyo na kuwafanya Adrus na Cookie nao kupanda. Jing kwa kasi akawachoma sindano za shingo marubani hao, ambao hawakumaliza hata dakika mbili hali zao zikawa mbaya na kupoteza maisha. Wakasaidiana na kuwahamisha marubani hao katika eneo la nyuma huku Jing na Adrus Wakikaa kwenye siti za marubani hao. Taratibu Jing akawaisha helicopter hiyo ambayo kwa mwendo wa taratibu ikaanza kutoa mlio ulio wafanya wanajeshi wengine walipo katika eneo hilo kushagaa.

“Kuna helicopter iliyo ruhusiwa kuondoka?”

Mwejeshi mmoja alimuuliza mwenzake huku akimtazama usoni mwake.

“Sidhani, hembu muulize mkuu”

Mwanajeshi huyo kwa kutumia simu ya upepo akawasilinaa na bosi wake.

“Mkuu kuna helicopter yoyote umeiruhusu kutoka muda huu?”

“Sijaruhusu ni kitu gani kinacho endelea?”

“Kuna helicopter moja inaondoka”

“Nini?”

“Ndio mkuu”

“Hakikisha kwamba muna izuia isiondoke”

“Kwa risasi au?”

“Vyovyote ila hakikisheni kwamba haindoki”

“Sawa mkuu”

Mwanyeshi huyo kwa haraka kawasiliana na wezake na kuwapa amri ya kuizuia helicopter hiyo iliyo anza kunyanyuka taratibu.

“Fanyeni haraka haraka”

Cookie alizungumza huku akiwatazama wanajeshi wapatao sita wanao kuja kwa kasi katika eneo hilo huku wakiwa wameshika bunduki mikononi mwao. Jing kwa juhudi zote akajitahidi kuzidi kuinyanyua helicopter hiyo, na kuzidi kwenda juu. Wanajeshi hao wakaanza kushambulia helicopter hiyo wakiamini kabisa kwamba risasi zao zitaweza kuiangusha na kuwakamata watu wanao toroka na helicopter hiyo.

***

Shamsa macho yakamtoka baada ya kuona signal inayo onyesha eneo walipo magaidi walio mtorosha dokta dokta Ranjiti na mwanaye. Kwa haraka akatoka katika chumba hicho na kuwaacha madam Mery na mlinzi wake wakimshangaa, huku maiti ya kijana wa madam Mery ikiendelea kulala chini. Mlinzi huyo akamtazama madam Mery aliye mkalisha kwenye kiti, ila akaona hana sababu ya kuendelea kumshikilia ikiwa yeye jukumu lake ni kumlinda Shamsa aliye toka ndani humo.

“Nisubiri”

Mlinzi huyo alizungumza kwa sauti ya juu mara baada ya kumuona Shamsa akilirudisha gari walio kuja nalo eneo hilo kwa kasi kubwa. Shamsa hakuhitaji kumpakiza mlinzi wake kwani lengo lake ni kuhiji kuwakamata maadui hao ambao kupitia wao ataweza kufahamu ni wapi alipo dokta Ranjiti ambaye atatoa siri ya wapi Junion Jr wake alipo. Simu hiyo ya Phidaya ikaanza kuita, kwa haraka Shamsa akaipokea.

“Shamsa umeiona hiyo signal”

Sauti ya Sa Yoo ilisikika upande wa pili wa simu hiyo.

“Ndio nimeipata asante Sa Yoo”

“Nimekuibia tu ila hawakuhi wewe uweze kulifahamu hilo kwani tayari kuna vikosi vimetumwa barabarani kuhakikisha kwamba wanawapata”

“Sawa, asante”

“Ila Shamsa ninakuomba usiende kwa manaa watu hao wamefwatiliwa ni hatari sana kwa mana hadi ninavyo zungumza hivi sasa kuna tukio moja kubwa la mauji wamelifanya Mbezi Louis”

“Usijali”

Shamsa akakata simu na kuzidi kuongeza mwendo kasi wa gari hilo. Akidharia kuhakikisha kwamba anawapata magaidi hao.

***

“Mkuu wameongezeka”

Dora alizungumza huku akitazama kioo cha pembeni kinacho weza kumsaidia kuona nyuma. Lizzy na wezake wengine wakalazimika kugeuka nyuma na kuona gari aina ya Fellari ikizidi kuja mwa mwendo kasi jambo lililo zidi kuwapa wakati mguu.

“Ishambulieni”

“Sawa mkuu”

Wasichana walio kaa siti za nyuma kwa haraka wakafungua vioo vya na kila mmoja kwa utaalamu wa hali ya juu akaanza kushambulia gari hilo aina ya Ferrali spider linazo wakaribia kwa kasi yaa jabu.

Eddy akatabasamu huku akiichomoa bastola yake aliyo ichomeka kiononi mwake na ina risasi za kutosha. Uzuri wa gari lake hilo haliingii risasi ya aina yoyote, risasi za magaidi hao hazikuweza kumfanya kumzuia kupunguza mwendo kasi wa gari hilo.

“Mkuu gari hilo ni buller proof.”

Msichana mmoja alizungumza huku akimtazama Lizzy aliye jaa waziwasi mwingi sana.

“Ingieni ndani”

Lizzy alizungumza, na vijana wake wakatii amri ya bosi wao huyo. Eddy kwa haraka akalipita gari hili, kisha akakakanyaga breki na kuligeuza gari hilo huko walipo tokea. Hata kabla gari halijatulia na halijafikiwa na gari la Lizzy linao ziku kuja kwa kasi, akaanza kulirudisha nyuma kwa kasi huku akifungua kioo cha gari hili na kuuchomoa mkono wake ulio shika bastola.

Akili ya Lizzy ikafanya kazi haraka sana, afungua mlango pasipo woga wa aina yoyote akajitoa kidogo na kumchomoa Camila huku akiwa amemshika mguu wa kulia na kumuinamisha kichwa chini miguu juu akimuashiria Eddy endapo atajaribu kupiga risasi ya aina yoyote basi atamuachia Camila anaye lia sana na huo ndio utakuwa mwisho wa kifo cha mwanaye huyo anaye mpenda kuliko kitu chochote kwa sasa.



Eddy akamtazama mwanaye jinsi anavyo endelea kulia kwa uchungu sana. Taratibu Eddy akaurudisha mkono wake ndani huku akizidi kurudisha gari lake nyuma. Lizzy akaingia ndani na kuufunga mlango wa garo hilo.

“Mkuu tunafanyaje?”

“Hawawezi kutushambukia kwa maana wanatambua tuna mtoto, hii ndio ngao ya pekee ambayo itatufanya sisi kuweza kuondoka katika eneo hili.”

Lizzy alizungumza huku akimtazama Eddy ni kitu gani atakacho kifanya baada ya kudhihirishiwa kwamba mtoto wake yupo ndani ya gari hilo.

***

Dokta Benjamini akazidi kujiuliza maswali mengi kichwani mwake juu ya amri ambayo amepewa na makamu wa raisi juu ya kumchoma sindano ya usingiza Phidaya.

‘Kuna nini kinacho endelea hapa?’

Dokta Benjamini aliendelea kujiuliza maswali ambayo hakuweza kupata jibu la iana yoyote. Akaingia kwenye chumba alichopo Phidaya na kumkuta akiwa amekaa kitandani na kujikunyata kwenye moja ya kona ya chumba hicho.

“Sihitaji mtu ndani kwangu”

Phidaya alizungumza huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.

“Samahani madma kuna vipimo ninahitaji kukufanyia”

“Nimesemaaa tokaaaaaaaaaaaaaa”

Phidaya alizungumza kwa sauti kali hadi dokta Benjamini akatetemeka. Walinzi wawili wa kike wakaingia ndani ya chumba hicho.

“Mtooeni”

Phidaya alizungumza kwa ukali, dokta Benjamini hakuhitaji kushikwa na walinzi hao, alicho kufanya ni kuanza kutoka nje taratibu huku zoezi la kumchoma sindano ya usingizi Phidaya ikiwa imeshindikana.

***

Dokta Ranjiti na Anna wakafika katika kisiwa cha Madagasca katika mji wa Antananarivo. Wakapelekwa kwenye hoteli kubwa ya kitalii iitwayoColbert-Spa&Casino. Wakapokelewa na katibu mkuu wa chama cha umoja wa siri sana cha D.F.E. Moja kwa moja wakapelekewa katika chumba chao ambapo wakakutana na ulinzi wa vijana wapatao sita wakiwa nje ya chumba hicho.

“Karibu daktari na pole sana kwa kila jambo lililo kupata”

“Asante sana”

“Kuna madaktari wawili watafika hapa baada ya nusu saa na watakuhudumia majeraha yote uliyo nayo mwilini mwako”

“Nashukuru sana”

“Marija ya saa mbili usiku utazungumza na mkuu, anahitaji kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wewe”

“Sawa”

“Pumzikeni sasa”

Katibu huyo akatoka ndani humo na kumuacha dokta Ranjiti na mwanaye Anna.

“Baba kwa nini sasa umechagua maisha kama haya?”

“Anna kwa sasa ninakuomba nipumzike, hayo mambo tutayazungumza wakati mwengine mwili wangu haupo sawa”

“Hata kama baba, nina haja ya kufahamu vizuri ni nini kinacho endelea. Mara tumetekwa, mara tumeokolewa, mara tumeletwa kwenye miji ambayo toka kuzaliwa sikufikiria kufika. Na hapa nasikia habari ya mkuu. Kumbuka mimi ni mtu mzima sasa baba sasa maisha ya kuongozwa na wewe”

Anna aliendelea kuzungumza kwa ukali sana na kumfanya dokta Ranjiti kumtazama Anna kwa macho makali sana.

“Mimi bado ni baba yako na unatakiwa kunihsehimu sawa”

Dokta Ranjiti alizungumza kwa ukali sana huku akimkazia macho Anna. Anna akachia msunyo mkali na kuingia katika chumba kilichopo katika eneo hilo.

***

Kutona ni usiku na magari mengi yamepungua, haikumuwia ugumu kabisa Shamsa naye kuanza kujiunga kwenye mbio za kulifukuzia gari la Lizzy na wezake. Umahiri wake katika uendeshaji nao umeukuwa msaada mkubwa sana kwake kwa kuwea kuwafikia.

“Mumemuka nyinyi malaya”

Shamsa alizungumza huku akizidi kuongeza mwendo, alipo likaribia gari hio karibu sana. Shamsa akajaribu kulipita gari hilo ila Dora akamzuia kwa kumzibia Shams a njia.

“Mkuu kuna mwengine”

“Fuc**”

Lizzy alizungumza huku akigeuka nyuma na kuona gari jeusi ambalo mara nyingi hutumia na walinzi wanao mlinda raisi au makamu wake. Shamsa pasipo kufahamu kwamba ndani ya gari hilo yupo mtoto Camila, alicho kifanya ni kuligonga kwa nyuma na kulifanya gari hilo kuanza kuyumba.

“Mshambulieni”

Lizzy aliwaambia wezake, hata kabla hawajafungu vioo, Shamsa akarudia tena kuligonga kwa nguvu gari hilo na kulisababishia kuzidi kuyumba na kumpa ugumu Debora katika kuliendesha. Gari hilo likaanza kuoka barabani na kuingia vichakani huku likiserereka. Eddy akashuhudia tukio la gari hilo jinsi linavyo tokemea vichakani, kwa haraka akafanha breki za gari lake, na kuligeuza kwa utaalamu mkubwa. Shamsa hakuhitaji kumuacha mtu zaidi na yeye kunaza kulingiza gari hilo vichakani. Mwanga wa helicopter ukazadizi kumchanganya Debora na kujikuta wakiparamia mti mkubwa aina ya mkuyu na gari likatulia hapo hapo.

“Mupo sawa?”

Lizzy aliuliza huku akimtazama Dora anaye sumbuka kutoa ftuza kubwa lililo toka kwenye mskani wake kwa jila la kitaalamu linaitwa Air bag.

“Yeea”

Msicha mmoja aliye kaa siti ya nyuma aliitikia.

“Tuwaonyesheni hawa washenzi kwamba sisi ni mbwamitu malaya”

Lizzy alizungumza huku akiikoki bunduki yake, akafungua mlango na kumuweka Camila juu ya siti aliyo kuwa amekali. Kwa kasi ya ajabu akaanza kulishambulia gari la Shamsa, huku wezake nao wakishuka na kuishambulia helicopter inayo wamulika kwa mwanga. Shamsa naye hakuwa mzeembe akajirusha siti ya nyuma kitaalamu mara baada ya kuona jinsi koo cha gari lake ikinayvo jaa matundu yanayo sababishwa na risasi anazo vurumushiwa. Akaufungua mlango wa siti za nyuma, kwa kasi akashuka na kuzunguka nyuma kabisa ya gari. Akiwa hapo akashuhudia gari dogo kikisimama, hakuamini macho yake baada ya kumuona Eddy akishuka katika gari hilo na kuanza kuivirigisha kama tairi la gari. Akajibanza kwenye gari alilo jibanza Shamsa.

“Umefikaje hapa?”

Shamsa alimuuliza Eddy huku akimshangaa jinsi alivyo vaa kwani asubuhi alivyo kuwa ameondoka hospitalini alimuacha Eddy akiwa mahututi.

“Sio muda wa maswali, wamemteka Camila”

“Camila?”

“Ndio na wanaye kwenye lile gari”

“Pumbavu”

Shamsa alizungumza na kujitokeza kwenye gari hilo nakuanz akujibu mashambulizi ambayo kadri muda unavyo szidi kwenda ndivyo jinsi hali inavyo zidi kuwa ngumu kwao kwani Lizzy hizo zirasi wanazo wamiminia kusema kweli ni kama wendawazimu. Eddy akavunja kioo cha nyuma cha gari hilo kwa kutumia kitako cha bastola yake. Akaokota moja ya kipande cha vioo hivyo vilivyo pasuka. Akakisogeza pembeni na kushuchungulia nyuma, akamshuhudia msichana aliye kuwa amening’iniza Camila kichwa chini mguu juu, akiedenelea kushambulia gari lao. Eddy na Shamsa wakashuhudia helicopter iliyopo angani ikianza kuyumba huku kiyoa moshi mwingi na rubuani akajitahidi kuondoka katika eneo hilo. Ila kutokana na helicopter hiyo kushambuliwa sana kwa risasi, hazilipia hata dakika mbili kikaanguka chini na kulipuka huku rubuani akijiwahi kuruka na parachute lake.

“Waoooooo”

Eddy na Shamsa walisikia shangwe za wasichana hao wakishangilia juu ya tukio walilo lifanya.

“Washenzi wana silaha kubwa hawa?”

Shamsa alizungumza, Eddy akatazama tena kioo chake, na kuwaona wasichana hao wakijipanga vizuri kwa shambulizi jengine. Taratibu Eddy akalala chini, kutokana sasa mwanga wa helicopter haupo na ni mbalamwezi ndio imatawala kwa mwanga hafifu, akaingia chini ya gari hili akiamini kabisa hato weza kuonwa na wasichana hao.

“Unafanyaje Eddy?”

Shamsa alizungumza kwa sauti ya chini sana.

“Endelea kushambulia mfululizo”

Shamsa akatii amri aliyo ambiwa na Eddy. Akaanza kujibu mashambulizo hiyo na kuwafanya Lizzy na wezake waendelee kumimina risasi katika gari hilo. Eddy akazidi kutamba hadi akafanikiwa kufika katikati ya gari hilo na kushuhudia miguu ya wasichana wote. Akaishika bastola yake vizuri huku akisali sala yake ya mwisho kwani tukio hiko ni hatari sana hajui ni kitu gani kitatokea baada ya yeye kuanza kuwashambulia wasichana hao..

Eddy akampiga risasi Dora ya mguu na kumfanya apige ukelele mkali na kuanguka chini, hata kabla hajasaidia na wezake walio changanyikiwa kwa shambulizi hilo. Akapigwa sirisasi ya kichwa iliyo yakatisha maisha yakehapo hapo.

Lizzy akawa kama mwenda wazimu mara baada ya kumuona Dora akimwagikwa na damu kichwani mwake. Kuichanganyikiwa kwao ikawa nafasi nyingine kwa Shamsa kumtungua msichana mwengine kwa kumpiga risasi ya kcihwa na kumuangusha chini.

“Mkuu chukua mtoto na ukimbie”

Msicha aliye salia alizungumza huku akimtaza Lizzy usoni mwake na wakiwa nyuma ya gari lao. Lizzy machozi ya hasira yakaanza kumtoka. Katika maisha yake yote ya ujasusi toka alipo kuwa binti mdogo wa mika sita hakuwahi kushindwa siku hata moja wala hakumuogopa mtu wala kukimbia.

“No mchukuee mtoto wewe na ukimbie sawa”

“Hapana mkuu…..”

“Hii ni amri sio ombi sawaaa”

Lizzy alizungumza kwa ukali sana, msichana huyo akamtazama Lizzy usoni mwake. Wakakumbatiana kwa nguvu sana huko wote wakilia, kwani wezao wawili tayari wamesha poteza maisha.

“Nimekuambia mchukue mtotooo”

Msicha huyo kwa haraka akamchukua Camila anaye endelea kulia, akamtazama Lizzy usoni mwake.

“Goooooo”

Lizzy alizungumza na kumfanya mwenzake huyo kukimbia na kutokoea msituni. Shamsa aktazama eneo hilo kwa haraka sana kwa mahesabu ya haraka haraka akaona moja ya njia ambayo anaamini kwamba akiipita hiyo ni laizma ataweza kukutana na msichana huyo kwa mbele.

“Ninakwenda kumchukua Camila”

Shamsa alizungumza huku akichuchumaa, na kumtazama Eddy anaye jitoa chini ya gari hilo.

“Asante, kuwa makini Shamsa”

Shamsa akamshika Eddy shongoni mwake na kuanza kumnyonya midomo yake, kisha akamuachia na kuanza kukimbilia katika kinjia hicho anacho amini kwamba atafanikiwa kumpata msichana aliye mbeba Camila.

Eddy akachomoa magazine ya bastola yake na kukuta zimebaki risasi tano tu. Akairudisha, huku akijibapasa kwneye mifuko ya suruali na kukuta magazine alizo zichomeka zikiwepo.

Lizzy alipo hakikisha kwamba kijana wake ameondoka eneo hilo salama salmini. Akavua kitambaa kilicho ificha sura yake, akazifunga nywele zake ndefu kwa nyuma. Kisha akaishika bunduki yake vizuri, kukabiliana na adui yake, afe yeye au afe Eddy hao ndipo ushindi wa mmoja wapo utapatikana.



Mashambulizi ya Lizzy kuelekea lililo gari alilo jificha Eddy yakaanza kupamba moto. Uwezo wa bundukia AK-47, anyo itumia Lizzy unamfanya Eddy kwa mara kadhaa kuwa msikilizaji wa mashambulizi hayo makali sana. Eddy akasikilizia hadi pale alipo sikia mlio wa kubadilisha magazine. Ni sekunde chache za tukio hilo ila ndio ikawa nafasi ya pekee kwa Eddy kumdhihirishia Lizzy kwamba na yeye ana uwezo wa kufanya mashambuli. Risasi za Eddy kwa bahati mbaya hazikuweza kumoata Lizzy zaidi ya gari alilo jificha.

“Wewe malaya wa kiumea kama unajiamini njoo upambane na mimi”

Lizzy alizungumza maneno ya kejeli ilu kumshawishi Eddy aweze kutoka katika eneo alilo jificha ili iwe ndio nafasi yake ya pekee kuumaliza mchezo huo. Eddy hakuwa mjinga kwani matukio kama hayo alisha wahi kukutana nayo katika maisha yake.

Eddy akaanza kunyata huku akijibanza banza katika gari hili. Lizzy aliweza kuliona tukio hilo na kuanza kushambuli kwa risasi mfululilo na kumfanya Eddy kurudi kwa haraka na kujificha katika eneo alilo kuwepo. Katika mashambulizi yao yote haoakuwa na hata mmoja aliye weza kumpiga mwenzake risasi, zaidi ya kujikuta risasi zikiwaishia na hakuna hata mmoja wao aliye weza kubahatika kuwa na risasi za akiba.

“Wewe malaya wa kiume jitokeze, tupambane mkono kwa mkono”

Eddy akajishauri kwa sekunde kadhaa kisha akatoka katika eneo alilo jificha, taratibu wakaanza kutembea hadi wakakutana katikati. Eddy hakuamini macho yake baada ya kumkuta mtu anaye pambana naye ni mrembo sana, mwanamke ambaye kwa haraka haraka ukimtazama usoni mwake wala huwezi kudhani kwamba ni gaidi mwenye roho mbaya kupita maelezo.

“Sali sala yako ya mwisho kabla sijaling’ofoa koromeo lako”

Lizzy alizungumza kwa kujiamini sana huku akivikunja vidole vya viganja vyake tayari kwa kupigana na mwaume ambaye hamfahamu vizuri kama hadi hapo alipo fika ni mamia ya watu amesha pambana nao na hakuna hata mmoja ambaye alifanikiwa kuitoa pumzi yake.

***

Shamsa akazidi kukimbia na kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona msichana aliye mbabe Camila. Shamsa hakuhitaji kumshambulia msichana huyo kuhofia kuharibu maisha ya Camila ambaye anampenda kama mwanaye. Shamsa kwa haraka akajitokeza kwa mbele, na kumfanya msichana huyo kusimama gafla huku macho yakimtoka. Wakanyoosheana bastola zo walizo zishika na endapo yoyote kati yao atavuta traiga na kuruhusu risasi yake kutoka, basi hata mwenzake naye atafanya hivyo kabla hata risasi haijamfikia.

“Yupo wapi dokta Ranjiti?”

Shamsa alimuuliza msichana huyo, ambaye sura yake ameificha kwa kitambaa cheusi na ni macho yake tu ndio yanaonekana.

“Upoa hapa kwa ajili ya dokta Ranjiti na si mtoto?”

“Vyote vyote”

“Hahaaa kama ni vyote vyote, huto weza kupata hata kimoja kutoka kwangu”

“Etiii eheeee?”

“Ndio”

Msichana huyo akamrushia Shamsa, mtoto na kumfanya Shamsa umakini wake wote kuupeleka kwa Camila, akamtada, ila akasindikizwa na teka la tumbo lililo muangusha chini ila hakujaribu hata kumuachia Camila anaye endelea kulia. Shamsa kwa haraka akamuweka Camila kwenye nyasi zilizopo pembeni kisha kwa utaalamu mkubwa, akajizungusha hapa chini na kupiga mtama msicha huyo na yeye akaanguka chini n a kuonja vumbi jingi lililopo katika eneo hilo. Shamsa akasimama kwa haraka huku akimtazama msichana huyo, taratibu msichana huyo akasimama huku bastola yake akiitupa pembeni akiashiri kwamba wanataka wapigane mkono kwa mkono. Shamsa akajifikiria kwa sekunde kadhaa kutokana anajiamini na yeye akatupa bastola yake pembeni na kujipanga. Binti nuyo kwa kasi ya ajabu akanza kurusha mateke mfululizo ambayo baadhi ya mateke hayo yaliweza kumpata Shamsa ila mengine Shamsa alifanikiwa kuyakwepa.

Mparangano wa mapigano hayo yakazidi kupamba moto, huku Shamsa akianza kujipa matumaini ya kumshinda binti huyo kwani ni vitu vingi sana amaweza kumzidi, hususani pumzi ambayo mara kwa mara binti huyo hujikuta akichoka sana baada ya kumsambulia sana Shamsa.

Shamsa akafanikiwa kumpiga kabari takatifu binti huyu. Kabali hiyo ikamwafanya hadi waanguke chini, kwa kurupushani za binti huyu kujaribu kuitoa hiyo kabali, ila anashindwa, kwani Shamsa mikono yake ameikaza kisawa sawa.

“Niambie ni wapi alipo dokta Ranjiti”

Shasma alizungumza huku jicho la upende wake wa kuliwa likimwagikwa na damu.

“Sijui….”

Shamsa bila ya huruma huku akiwa amenyang’ata meno yake, akaanza kuingiza kidole gumba kwenye icho la kushoto la binti huyo na kumsababishia mauivu makali ambayo tangu kuzaliwa kwake hakuweza kuyapata maumvu hayo.

“SEMA YUPO WAPI DOKTA RANJITIIIII”

Shamsa alizungumza huku akiendelea kugandamiza kidole chake kwenye jicho la msichana huyo huku kabali yake akiendelea kuikaza kisawa sawa.

“Yu….yu…..p….o”

“Wapi?”

Shamsa alizungumza kwa ukali huku akilegeza kidogo mkono ulio mkaba shingo msichana huyo ili aweze kumsika vizuri ni wapi alipo dokta Ranjiti.

***

Risasi za wanajeshi wa Marekani wanazo zielekezea helicopter waliyo panda Jing, Adrus na Cookie hazikuweza kufua dafu, kwani wamejisahau kabisa kwamba helicopter hiyo imetengenezwa kwa vyuma vizito ambavyo haviwezi kuingiza risasi kirahisi. Wanajeshi hao wakashuhudia helicopter hiyo

“Woooooo”

Cookie alipiga kelele baada ya kuona wamefanikiwa kuondoka katika eneo hilo.

“Ooohoo asante Mungu”

Jing alizungumza huku akipiga ishara ya msalaba.

“Bado hatujafanikiwa”

Adrus alizungumza huku akionekana kuto kuwa na furaha yoyote usoni mwake.

“Kwa nini?”

“Wamarekani si watu wa kukata tamaa kiasi hicho”

“Kivipi?”

Kama alivyo zungumza Adrus, ndege mbili aina ya Jet ambazo zinakwenda mwendo kasi, zikaiweka katikati helicopter hiyo.

“Onyo munatakiwa kujisalimisha haraka iwezekanavyo, tunarudia munatakiwa kujisalimisha haraka iwezekanavyo”

Satuti ya rubani mmoja wapo ya ndege hizo za kivita ilisikika vizuri kwenye spika ndago zilizopo ndani ya helicopter hii.

Cookie macho yakamtoka, akatamani kuzungumza kiti ila anajikuta akishindwa kabisa kuzungumza. Akawatazama Adrus na Jing ambao ndio marubani wa helicopter hii, nao pia wanaonekana kukaa kimya wakitafakari nini wafanye, wajisalimiesha au wakubaline kwa lolote ambalo litatokea.

***

Livna machozi yakaanza kumwagika baada ya kuhushudia vijana wake jinsi wanavyo endelea kutekezwa kwa kupigwa risasi. Akashushudia jinsi kijana wake mmoja akiondoka na kumuacha Lizzy mfanyakazi wake bora kabisa, anaye mpenda kulio wengine.

Wasichana wote waliomo ndani ya chumba hicho hakuna ambaye aliweza kuzungumza kitu chochote zaidi ya kuanza kumuokoa Lizzy kimoyo moyo ili aweze kufanikiwa kumzidi mwanaume anaye pambana naye

‘Lizzy akifa, John na mpumbavu wako lazima niwaue’

Livna alijiapiza moyoni mwake huku akiendelea kutazama jinsi Lizzy anavyo jiweka sawa kupambana na Eddy. Lizzy akaruka hewani na kurusha teke ambalo Eddy aliweza kuuwahi mguu wake huo na kumzungusha kwa nguvu na kumuangusha chini kama mzigo. Tukio hilo likamfanya Livna kufumba macho yake, kwani maumivu anayo yapata Lizzy anahisi ni kama maumivu anayo yapata yeye mwenyewe.

Lizzy akanyanyuka na kumtazama Eddy aliye simama huku sura yake ikiwa imejaa mikonjano ya hasira aliyo nayo. Lizzy akarusha ngumi kadhaa mwilini mwa Eddy, ila cha kushangaza Eddy hakuweza kuonyesha dalilili yoyote ta kuumia.

Eddy kwa haraka akamshika Lizzy na kumbamiza kwenye gari walilo kuwa walo Lizzy na wezake. Vigoti vya tumbo anavyo shidiliwa Lizzy vikakmfanya aanze kumwagikwa na damu mdomoni mwake. Lizzy akajaribu kujitetea ila tayari alisha taitishwa kwani mtu anaye pigana naye ni hatari sana.

“Lazima anilipeee. Lazimaaa Eddy naye afeeeeeeeeeeeeeeee”

Livna alizungumza kwa hasira huku akivunja moja compture iliyopo ndani humo. Kwani tayari Lizzy alisha kabwa shingo yake kwa nguvu sana.

***

Japo kwenye maisha yake Lizzy alisha pambana na wanaume wengi wenye miili yao na wenye uwezo wao. Ila anajishangaa kujikuta akishindwa mpambano huu mapema sana. Eddy hakuwa mwanaume wa mchezo mchezo na anafahamu ni maeneo gani ya kumpiga mtu na kumlegeza kabisa. Hali hiyo ikazidi kumchanganya na kumdhohofisha Lizzy ambaye tayari damuza mdomoni mwake zimesha anza kumwagika.

“U….u….si…..niue, nita….kuaa…..mbia ni wapi alipo dokta Ranjiti”

Lizzy hakuwa na namna zaidi ya kuomba msaada huo ambao anahisi unaweza kumsaidia kwa namna mmoja amma nyingine, kwani kama kupigwa tayari amesha pigwa, na mkono wa Eddy ulio kikaba koo lake, kama alivuo kuwa akidai kwamba atamng’ofoa mwanaume hiyo koromea, sasa kibao kimemgeukia yeye koromeo lake ndio lipo katika hatua za mwisho mwisho katika kung’ofolewa.

Eddy huku mwili ukimtetemeka na machozi yakimwaika usoni mwake, akamtazama Lizzy ambaye ndio yupo katika hatua za mwisho mwisho katika kupoteza maisha. Taa za gari za wanajeshi wanao fika katika eneo hilo, zikamfanya Eddy kiminya Lizzy mshipa ambao ukamfanya apoteze fahamu, na hata wanajeshi hao wakija na kumpima basi watangundua kwamba msichana huyu amefariki dunia.

“Mkuu mkuu”

Kiongozi wa kikosi hicho cha jeshi aliita huku wakimzunguka Eddy. Taratibu Eddy akanyanyuka na kutazama angani akiamini lazima satelaiti za nchi hii zitakuwa zimeweza kushuhudia kila kitu kilicho toke.

“Pole sana mkuu, zichukueni hizo maiti”

“Maiti ya huyo binti muitunze vizuri”

“Sawa mkuu”

Eddy akaegemea kwenye mti huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana. Maumivu ya majeraha kwenye mguu wake yakaanza kuyasikilizia jinsi yanavyo muuma.

“Wapi?”

Shamsa alizumuuliza msichana huyo

“Madagasca, Antananarivo”

“Asante”

Kwa nguvu zake zote Shamsa akaivunja shingo ya msichana huku akitoa kidole kilicho jaa damu kwenye jicho la msichana huyo. Taratibu Shamsa akajipangusa kidole chake hicho kwenye nguo ya msichana huyo, akasimama taratibu na kuanza kutembea kuelekea eneo alilo muweka Camila. Taratibu akamnyanyua Camila na kumtazama mtoto huyo aliye jaliwa uzuri wa asili.

“Yamekiwsha mtoto mzuri”

Shamsa alizungumza huku akichechemea akielekea katika eneo alipo muacha Eddy. Akafika na kukuta wanajeshi wangi wakiwemo katika eneo hilo. Eddy alipo muona Shamsa akiwa na mtoto kwa haraka akamkimbilia na kuwakumbatia wote.

“Mupo salama”

“Ndio Eddy”

Eddy akamchukua Camila na kumtazama usoni mwake na kujikuta machozi yakimwagika usoni mwake.

“Mkuu inabidi sasa muende sehemu salama”

Mkuu wa kioso hicho cha jeshi alizungumza huku akiwatazama Shamsa na Eddy.

“Sawa”

Eddy taratibu akaupitisha mkono wake kiunoni mwa Shamsa na kumkumbatia, taratibu wakaanza kutembea kuelekea barabarani walipo elezwa kwamba ndipo lilipo gari maalumu litakalo warudishia katika eneo salama.

“Ni saa napi sasa?”

Shamsa alimuuliza mwanajeshi mmoja ambaye anawalinda pembeni yao.

“Ni saa nane usiku”

“Duuu siku ya leo imekuwa ni ndefu kuliko ya urefu tulio utarajia”

“Kweli cha kumshukuru Mungu familia yangu ipo salama, nikimpata na Junion nitafurahi sana”

Eddy na shamsa wakafunguliwa mlango na kuingia ndani ya gari aina ya Benzi Compresa. Eddy hakuhitaji hata kumpa Shamsa nafasi ya kujifunga mkanda wa siti ya gari hilo, taratibu akaanza kumnyonya mdomo mdomo wake, dereva wa gari hilo akabaki kumeza mate huku akiwatazama kwa kuiba iba kwa kioo kilichopo mbele yake.

“Shamsa nakupenda sana”

“Nakupenda pia Eddy”

“Nahitaji kukuona, nahiji uwe mama wa wanangu, Camila na Junion Jr?”

Maneno ya Eddy yakamshangaza sana Shamsa ambaye anatambua kwamba uhusiano wao ni wa siri na hapendi hata watu wa nje waweze kufahamu ili kulinda heshima ya makamu huyo wa raisi.

“Na PHIDAYA JE?”

Swali la Shamsa, kikamfanya Eddy kujibu kwa ishara ya kupitisha kidole chake gumba cha mkono wa kulia katika shingo yake akimaanisha kwamba atamchinjilia mbali mke wake hiyo, Phidaya Eddy.



Dereva akataka kuondoa gari ila Eddy akamuomba asubiri kwanza.

“Unakwenda wapi?”

“Kuna kitu nahitaji kuzungumza na mkuu wa hichi kikosi”

“Sawa”

Eddy akashuka kwenye gari, akamuagiza mwanajeshi mmoja kuwasiliana na mkuu wake huyo ambaye yupo eneo la msituni. Mwanajeshi hiyo akafanya hivyo, baada ya muda mkuu huyo akafika.

“Kuna maiti ya yule msichana muliye nikuta naye hakikisheni kwamba munaipeleka katika nyumba nitakayo pelekwa”

“Aha…samahani muheshimiwa maiti tuilete nyumbani kwako?”

“Ndio fanyeni kama nilivyo waambia”

“Sawa, nimepata amri kutoka mwa mweshimiwa raisi, kwamba vijana wangu wakuepeleke kwenye nyumba salama uliyo kuwa unaishi kabla ya kurudi kwako”

“Hilo halina tatizo, mimi ninacho kihitaji ni huyo msichana sawa”

“Sawa mkuu”

Eddy akarudi kwenye gari. Msafara wa magari yapatano naye ya kijeshi wakaliweka gari la makamu wa raisi katiti, huku gari hizo zikiwasha ving’ora vilivyo waashiria madereva wengine kupisha msafara huo.

***

Furaha ikazidi kutawala katika chumba cha wafanyakazi wa ikulu, kila mtu akijikuta akimpongeza makamu wa raisi kuweza kupambana na magaidi hao na kuweza kumuokoa mwaye. Japo Rahab moyoni mwake naye ametawaliwa na furaha ya ushindi huo, ila denda walilo peana Shamsa na Eddy bado linamuumiza kichwa japo anatambua kwamba walisha wahi kupata mtoto, ila hakuweza kuona wakifanya hilo jambo. Raho ya wivu ikaanza kumtawala. Taratibu akatoa simu yake mfukoni na kumpigia mkuu wa kikosi cha ukoaji na kumpa maelekezo ya ya kumpeleka Eddy katika nyumba aliyo kuwa amamtafutia. Alipo maliza kuzungumza na simu akatoka chumbani humo na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, kwa maana siku hiyo imekuwa ni siku ndefu sana kwao, kwani tangu asubuhi alikuwa katika ngija ngija za kuongoza taifa.

Kabla hajaingia katika mlangowa sebleni kwake, mshauri wake akamfwata huku akiwa ameshika simu mkononi mwake na kuiziba katika sehemu ya kuzungumzia.

“Muheshimiwa raisi kuna tatizo”

“Tatizo gani tena?”

“Adrus ameamua kuwasaliti wa Marekani na kutoroka”

“What…..?”

“Raisi wa Marekani bwana Dustan yupo hewani kwa sasa anahitaji kuzungumza na wewe”

Raisi Rahab akaichukua simu hiyo na kuiweka sikoni mwake.

“Madam President”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Kinana wako amekuwa msaliti na amebadilika, na hivi sasa ninavyo zungumza na wewe ameiba helicopter ya kijeshi, na yupo na wasichana wawili ambao kwa rekodi zoa zinaonyesha kwamba ni majasuri wa kikosi kimoja cha siria sana na wamefanya matukio mengi ya kigaidi.”

“Ohooo Mungu wangu, ni kwa nini amefanya hiyvo?”

“Hata sisi hatujaui, na inavyo onyesha kuna ushawishi ulio fanyika kwa maana ndege aliyo kuwa amepanda ilipaya ajali na wameokolewa na tukio hilo ndipo lilipo jitokeza”

“Munaweza kuniunganisha naye nikazungumza naye?”

“Ndio madam President”

***

“Habari bwana Adrus, unaongea na sekretari kutoka ikulu ya Marekani, raisi Rahab kutoka nchini Tanzania anahitaji kuzungumza na wewe”

Cookie na Jing wote wakamtazama Adrus, mara baada ya kusikia sauti ya mwanaume huyo. Adrus akashusha pumzi nyingi huku akitazama ndege mbili za kijeshi zilizo waweka katikati.

“Sawa”

“Adrus ni nini unacho kifanya?”

Sauti ya ukali ya raisi Rahab ilisikika katika simu hiyo.

“Muheshimiwa nimefanya kilicho bora kwa ajili ya familia yangu. Familia yangu kwanza nchi nayo itafwata”

“Nikiwa raisi wako wa Jamuhuria ya muungano wa Tanzania, ninakuamrisha kujisalimisha mara moja na urudishe helicopter uliyo iiba”

Adrus akaka kimya kwa sekunde kadhaa, hukuakimtazama Jing na Cookie ambao tayari walisha anza kupata matumaini mapya ya kutoroka katika eneo hilo.

“Muheshimiwa raisi, nimeisikia amri yako ila samahani sinto weza kufanya hiyo”

“Kitakacho tokea juu yako, hakito nihusu mimi na kitakua nje ya mikono yangu sawa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Simu hiyo ikakatwa, baada ya dakika moja wakashuhudia ndege hizo za kijeshi(Jet), zikigeuza, jambo lililo wafanya Cookie na Jing kushangaa.

“Kila mtu afunge mkanda wake”

Adrus alizungumza na kumfanya Cookie kufaunga mkanda wa siti aliyo kalia.

“Kwa nini wameondoka?”

Jing alizungumza huku akimtazam Adrus usoni mwake.

“Wamekwenda kuchukua kasi tujiandae kwa lo……”

Hata kabla Adru hajamalizia sentensi yake tabata maalumu pembeni yao ikaanza kuwaka taa nyekundu, huku kwenye screan ndogo ikionyesha mabomu mawili yakiwafwata nyuma yao kwa kasi kubwa sana.

***

Kama alivyo ahidiwa na katibu mkuu wa chama cha D.F.E, majira ya saa mbili usiku. Dokta Ranjiti akakabidhiwa laptop maalumu na katibu huyo, kwa ajili ya kuwasiliana na John mkuu wa chama hicho. Dokta akaka kwenye sofa lilipo hapo sebleni kwenye hoteli waliyo fikizia. Akajiweka sawa shati lake jeupe alilo livaa mara baada ya kutoka kuoga na kufanyiwa matibabu. Dokta Ranjiti akaminya batani moja aliyo elekeza aweze kuminya, akamuona John akiwa amekaa sehemu yeye mabomba ya vyuma vyuma.

“Muheshimiwa habari yako”

“Sio nzuri, niambie mume rudi na binti huyo?”

“Binti gani muheshimiwa?”

“Camila?”

“Hapana hatukumteka sisi, habari nahisi ulizo ziona si sahihi”

“Pumbavu sana wewe, ni ujinga gani ulio ufanya. Nimepoteza mamilio ya mapesa kwa ajili yako kumbe hakuna kitu cha maana ulicho kifanya”

“Samahani muheshimiwa, sikufahamu hilo”

“Hujafahamiu vipi, lengo na nia ya kukupeleka wewe nchini Tanzania ilikuwa ni nini?”

“Kumachukua Phidaya”

“Yupo wapi hiyo Phidaya?”

Dokta Ranjiti akaka kimya huku akimtazama John liye jawa na jazba usoni mwake.

“Sijampata mkuu, ila yeye ndio ameweza kufanikisha mimi kutoroka kutoka mikononi mwa mume wake na inavyo pelekea hivi karibuni basi anaweza kuwa wa kwangu, kwani tayari anafahamu ukweli kwamba Shamsa na Eddy wana mahusiano ya kimapenzi na wamesha zaa mtoto.”

John akaka kimya kidogo huku akitafakari maneno aliyo yazungumza dokta Ranjiti.

“Phidaya umemuacha kweney mazingira gani?”

“Tulimpiga risasi ili kufuta ushahidi wa kuobekana kama yeye ndio ametutorosha”

“Phidaya atakuwa silaha yetu ya siri”

“Una maanisha nini mkuu?”

“Kupitia Phidya tutamuharibu Eddy taratibu hadi kufa kwake”

“Je ikitokea akifahamika kwamba yeye ndio amsaliti huoni kwamba tunaweza kumuwekea mazingira magumu kwake na kama unavyo kifahamu kichwa cha Eddy anaweza akamchinjilia mbali”

“Unashurije wewe?”

“Ninacho shauri hivi sasa ninakuomba Phidaya ufanye utaartibu atoroshwe na kuja huku nilipo na kupitia yeye tunaweza kufahamu udhaifu wa Eddy pamoja na serikali yake kwa ujumla”

“Sawa, nitalifanyia kazi”

“Asante sana mkuu”

***

Kumbukumbu ya maneno ambayo aliyazungumza kwa mume wake ikaanza kujirudia kichwani mwake taratibu. Phidaya macho yakamtoka, kwani anakumbuka vizuri alikiri kwamba alikiri amemtorosha dokta Ranjiti na mwanaye Anna.

‘Mungu wangu ni nini nimefanya ahaaa…..’

Phidaya alijisemea kimoyo moyo huku akizichangua changua nywele zake.

‘Siwezi kuendelea kukaa hapa, lazima Eddy atanifanyia kitu kibaya.’

‘Noo siwezi kuondoka kama ni kuniua aniue mimi na mwanangu, yeye ndio mkosaji na yeye ndio amenzisha matatizo haya’

Phidaya aliendelea kujiushauri yeye mwenyewe katika fikra zake.

‘Mama, mama, mama’

Phidaya aliisikia sauti ya marehemu mwaye ikimuita kwenye ufahamu wa kicha chake, akajaribu kutingisha kichwa ili kuizuia sauti hiyo isiendelea kumuita, ila sauti hiyo ikazidi kumuita.

‘Mama, kimbiaaaaa’

“Nini?”

Phidaya alizungumza huku akijichokoa sikio la upande wa kulia kwa kidole chake.

‘Kimbiaaaaaaa’

“Niende wapi?”

‘Mama KIMBIAAAAAA’

“Junio?”

Phidaaya aliita ila sauti hiyo haikuweza kumjibu kabisa. Mlango ulio funguliwa na nesi, ukamstua sana Phidaya ya kujikuta akimtolea macho nesi huyo, hadi nesi yeye mwenyewe akabaki akitawaliwa na mshangao.

“Muheshimiwa kuna nini?”

Nesi huyo alizungumza huku akiweka chupa ndogo ya dawa pamoja na glasi yenye maji mezani

“Nisaidie kuondoka humu ndani?”

“Unahitaji kwenda wapi madam”

“Kuondoka hapa hospitalini”

“Kwa nini mkuu?”

“Nahitaji kuondoka”

“Ahaa, ila mkuu sasa hivi ni usiku wa manane, na walinzi wamepewa amri ya kuto kukuruhusu wewe kuondoka”

“Wamepewa na nani?”

“Na mume wako”

Phidaya mwili mzima ukaanza kumtetemeka, kile alicho kuwa anakiwaza ndicho hichi anacho kihisi kwamba kinakwenda kutoka.

“Mkuu kuna tatizo gani?”

Phidaya akamtazama nesi huyu kwa macho makali, akamdadisi kwa umakini sana na kufahamu kwamba huyu nesi ana huruma naye na chochote anacho weza kumuambia basi nesi huyo atakiamini bila ya kumpinga.

“Mume wangu anataka kuniua”

“Samahani madama unasema……!!?”

Nesi huyo aliuliza huku macho yakimtoka kwani alicho kisikia kidogo kina mstajabisha na kumshangaza.

“Niamini mimi, nitakupa chochote ukitakacho, chochote ukisemacho mimi nitakupa ila ninakuomba tu unitoroshe eneo hili la hospitalini”

Nesi huyo akashusha pumzi nyingi sana huku akimtazama Phidaya ambaye kusema kweli anasikitisha.

“Madam mimi siwezi kupigana wala siwezi kutumia silaha nitakutorosha vipi?”

“Nisaidie, tafadhali. Ikifika hadi asubuhi na mume wangu akinikuta hapa ni lazima ataniua, ni lazima ataitoa roho yangu”

“Kwani madam umefanya kitu gani hadi muheshimiwa akuue”

“Nitakuambia ukinitoa hapa?”

“Hapana madam, naomba uniambie ukweli. Hata nikifanya kitu nifahamu ni nini kinacho endelea?”

Phidaya akaka kimya huku akisikilizia msukomo wa sauti ya nafsi yake inayo mshauri amueleze nesi huyo ukweli wote kwani yeye ndio msaada wake kwa sasa utakao muwezesha kuondoka katika eneo hilo.

“Mimi ndio nilio watorosha Ranjiti na mwanaye, niliwauwa wanajeshi wanne ili kuokoa maisha ya hao watu wawili”

Nesi huyo akazidi kujawa na mshangao kwani kila anacho kisikia masikioni mwake ni cha kushangaza kwani Phidaya kwa kumtazama huwezi amini kwamba hayo matukio ameyafanya yeye na kama hata ukisikia kwa mtu mwengine kwamba hajahusika katika matukio hayo basi unaweza kuamini kwamba ni kweli hajauhusika. Nesi huyo akasimama, akamtazama Phidaya kwa macho yake hayo madogo kiasi.

“Ninakuja”

Nesi huyo akatemeba hadi mlangoni, akafungua mlango na kuchungulia nje, kwa haraka akarudi ndani huku akiufunga na kumfanya Phidaya astuke sana.

“Vipi?”

Makamu wa raisi anakuja, na ameshika bastola mkononi mwake”

Phidaya akahisi utumbo ukijikunja kunga tumboni mwake na kusababisha maumivu makali ambayo yamemfanya aanze kusali sala yake ya mwisho kabla ya kifo chake hakija mfikia.



Hata kabla hawajafikiria ni kitu gani wanaweza kukifanya, wakastulia mlango ukifunguliwa na wote wakajikuta wakizidi kutetemeka huku wakimtazama Eddy aliye shika, bastola yake.

***

“Simamisheni msafara”

Eddy alimuambia dereva wa gari walilo panda

“Kwa nini wasimamishe”

“Nahitaji kwenda Muhimbili?”

“Kufanyaje tena Eddy ikiwa ni usiku, tunatakiwa kwenda kumpumzika”

“Kuna kazi ninahitaji kwenda kuimalizia muda huu, sihitaji siku hii iweze kupita pasipo kuweza kuifanya”

Shamsa macho yakamtaka, kwa maana ni muda mchache Eddy alimueleza kwamba ni lazima atamuua Phidya ili mradi wabaki wao wawili kwenye mahusiano yao ya kimapenzi. Dereva akawasiliana na madereva wote wa msafara huo na ukasimamisha, Eddy akamnyonya Shamsa midomo yake, kisha akambusu Camila ambaya tayari amesha pitiwa na usingizi.

“Kuwa makini mpenzi wangu”

“Usijali”

Eddy akashuka kwenye gari na kuingia katika gari jengine, lenye wanajeshi wawili walio kaa siti ya mbele. Safari ya kuelekea katika hospitali ya Muhimbili ikaanza. Kumbukumbu ya maneno ya Phidaya kukiri kwamba amemtorosha dokta Ranjiti na Anna, yakaanza kumpa Eddy jazba ambayo hadi ikafikia hatua mkono wake wa kulia ukaanza kumtetemeka, roho ya chuki na mauaji ikazidi kuutawala moyo wake. Hata wanajeshi walio kaa siti ya mbele ya gari hili waakaanza kutambua hali hiyo ya makamu wa raisi.

“Mkuu”

“Nini?”

Eddy aliuliza kwa jazba sana.

“Aha….unaonekana kama haupo sawa mkuu”

“Kwa hiyo?”

“Samahani kama nitakuwa nimekuudhi”

Mwanayeshi huyo aliye jawa na busari ilimbidi kukaa kimya kwa maana majibu ya mkuu wake huyo sio mazuri kabisa. Wakafika katika hospitali ya Muhumbili, Eddy kitu cha kwanza kukifanya akaichomoa bastola yake kiunoni na kuanza kutembea kwa mwendo wa haraka hadi akafika katika katika kordo ya chumba alicho lazwa Phidaya, walinzi wote wakashangaa kumuona makamu wa raisi akiwa katika mavazi ya kijeshi huku mkononi mwake akiwa amehsika bastola. Walinzi wote walipo muona wakampigia saluti, ila Eddy hakujali saliti zao zaidi ya kuufungua mlango wa chumba alichopo Phidaya kwa nfugu na kuwafanya Phidya na nesi aliye mkuta humo ndani wogte kustuka.

“Toka nje”

Eddy alizungumza kwa sauti nzito hadi nesi huyo akahisi haja ndogo ikimbana. Nesi huyo huku macho yakimtoka, akaanza kutembea kwa hatua za taratibu taratibu huku akitetemeka.

“Nimesema poteaaa”

Neno hilo likamfanya nesi hiyo kuongeza kasi ya kutembea kwake na kutoka chumbani humo hadi walinzi waliopo mlangoni wakashangaa. Eddy akaifunguka mlango wa chumba hicho, akaanza kutembea taratibu hadi kitandani na kumfanya Phidaya kuzidi kujikunyata na kujibanza ukutani. Eddy akaka kitandani hapo huku macho yake yakiwa yametawaliwa na uwekundu ambao Phidaya anautambua vizuri sana.

“Eddy……na…..ata…amb….ua kwamba unataka kuniua. Niue haraka ili nife tu nimfwate mwanangu Junio kule alipo, sina haja ya kuendelea kuishia, sina haya ya kuendelea kuwa hapa duniani, ikiwa mimi ni mkosaji mbele yako”

Phidaya alizungumza huku machozi yakimtoka usoni mwake.

“Eddy kosa langu moja tu nililo lifanya linatoshaa wewe kuniu, ni makosa magapi wewe uliyo yafanya ila sijadhubutu kunyanyua hata mkonow angu kukupiga hata shavu lako. Ulihisi kwamba kuzaa na Shamsa, mimi sinto jua, nimejua Eddy, nimeelewa Eddy unampenda Shamsa, na mimi nipo tayari kuwaachia. Ila kumbuka Eddy, Shamsa ni wapi ulipo mtoa, kumbuka kipindi tunamlea hata maziwa kifuani mwake hayakuwepo. Alikuita baba, na mimi aliniita mama. Leo emekuwa mama mwenzangu, leo anakuita Eddy, kweli. Kweli Eddy hii ni haki ambayo umekusudia wewe kuifanya mbele yangu na kwenye maisha yangu”

Maneno ya Phidaya yakapenya hadi kwenye moyo wa Eddy na kuanza kulainisha hasira na chuki iliyo tawala kwenye moyo huo.

“Eddy kumbuka kipindi unataka kuuliwa na madam Mery kwa kukatwa katwa vipande vipande, ila kumbuka jinsi nilivyo dhalilika mbele yako, kumbuka jinsi nilivyo zalilisha na mimba ya mwanao, kwa nini lakini Eddy. Najua wewe sio mnyama, najua wewe ni mbwa mwitu ambaye huwezi kuyasikia maneno yangu, natambua wewe ni mtu, ndio maana ulipigana, ulipambana ili mradi kunirudisha kwenye himaya yako. Je kujitoa kwako kote ni bure, eheee?”

Eddy machozi yakanza kumririka usoni mwake, maneno ya Phidaya yanamkumbusha maisha ya nyuma waliyo yapitia kwa pamoja.

“Eddy kumbuka nimekubeba mimba za watoto wawili, japo mmoja alikufa ila ni kwa mapenzi ya Mungu, je Camila ataishi maisha ya kumkosa mama yake, ataishi kwa kukosa mapenzi yangu Eehee?”

“Je Camila akikukua, ni nini utamuambia. Mikono yako ilitumika katika kuimwaga damu ya mama yake? Kama ni ndio nipo tayari sasa hivi uniue, niue Eddy”

Silaha ya maeno aliyo itumia Phidaya, ikazidi kumlainisha Eddy, msimamo alio ukusudia kuufanya kwa Phidaya ukapotea. Eddy kwa haraka akamshikisha Phidaya bastola yake na kuunyanyua mkono wa Phidaya na kuielekeza bastola aliyo mshikisha Phidaya kwenye paji lake la uso.

“Kill me”

Eddy alizungumza kwa uchungu, huku akikilazimisha kidole cha Phidya kuvuta traiga ili kuruhusu risasi itoke na kumpiga Eddy usoni mwake.

***

Si Jing wala Cookie wote wamejawa na wasiwasi mkubwa sana. Adrus akameza fumba zito la mate huku akitazama mabomo hayo ambayo kadri sekunde zinavyozidi kwenda ndivyo jinsi yanavyo zidi kuwasogelea. Yakiwa yamekabisha mita chache sana kuwafikia, kwa haraka Adrus akaipeleke helicopter hiyo chini na kusabaisha mabomo hayo kupita kwa kasi na kulipuka kwa mbele. Kitendo hicho kikamshangaza Jing ambaye anamchukulia Adrus ni mtu wa kawaida sana.

“Hatuwezi kusonge mbele”

“Kwa nini?”

“Lazima tupambane na hizi jeti”

“Tutaziweza kweli?”

“Ndio, tutaziweza hii helicopter ina uwezo mkubwa sana”

Adrus alizungumza huku akiigeuza helicopter hiyo, akanaaza kuminya batani za kuandaa mambomu ya ndege hiyo tayari kwa mashambulizi.

“Unaweza kupima shabaha?”

Alimuuliza Jing aliye kaa pembeni yake.

“Ndio”

“Poa shuhulika nao, mimi kazi yangu ni kukwepa mashambulizi yao”

“Sawa”

Mashambulizi kati ya ndege hizo za kishe pamoja na helicopter anayo iendesha Adrus yakazidi kupamba moto. Marubani wa ndege hizo wakajikuta wakishangaa sana uwezo wa Adrus, kwani kila walivyo jaribu kumshambulia walijikuta wakitoka hola.

“Jing hakikisha kwamba unakaridiria kuwaweka kwenye target kwa maana kulipua ndege hizi ni shuhuli sana”

“Sawa”

Jing alijibu huku jasho la usoni kimmwagika, kwani naye tangu aanze kuwashambulia hajabahatika kuilipua ndege hata moja.

***

Kila mtu katika chumba cha mawasilino kilichopo katika meli hiyo kubwa inayo milikiwa na Livna Livba, akaka kimya wakisililizia kauli ya bosi wao, kwani wote wamashuhudia jinsi Lizzy na wezake wakiuwawa kikatilia. Livna taratibu akajifuta machozi yake usoni, akaziweka sawa nywele zake, kisha taratibu akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia.

“Minya kengele ya dharura”

“Sawa mkuu”

Kengele ya dharura ikaanza kusikika eneo zima la meli hiyo. Watu wote walio kuwa wamelala, wakanayanyuka kwenye vitanda vyao na kuelekea katika ukumbi kubwa kusikiliza ni kitu gani ambacho kimetokea.

“Tayari mkuu”

“Hiyo video niwekee kwenye big screan kule ukumbini”

“Sawa”

Livna akatoka katka chumba hicho huku akiongozana na wasina wawili. Akafika katika ukumbi huo na kukuta wasicha wote wakiwa wamesimama katika mistari iliyo nyooka.

“Tmepata msiba mkubwa sana, msiba ambao sisi kama sisi hatuwezi kuendelea kukaa kimya kusikilizia kwa kile kilicho tokea”

Livna alizungumza kwa sauti ya upole huku akiwatazama wasichana hao. Kwa isha akaomba video hiyo kuonyeshwa kwenye Tv kubwa iliyopo katika ukumbi huo. Kila msicha akashuhudia jinsi wezao walivyo uwawa kiukatili sana.

“Tuna vita iliyopo mbele yetu. Hao ni wezetu walio tangulia mbele za haki. Hatuwezi kuendelea kukaa kimya pasipo kufanya kitu chochote dhidi ya wahusika, kusema kweli itakuwa ni dhambi hata kwa mwenyezi Mungu”

“Tuna wahusika wengi sana katika hii vita yetu. Kuna makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania, anaitwa Eddy Godwin, mtoto wa Mzee Godwin aliye kuwa raisi wa Tanzania kabla raisi huyu wa sasa”

Livna alizungumza huku akiinyooshea kidole picha ya Eddy inayo onekena katika eneo hilo.

“Pia yupi Shamsa Eddy, huyu naye amehusika katika mauaji ya wezetu. Lengo la mimi kuwaonyesha hawa watu ni kuhakikisha kwamba tuna waangamiza kabla ya hii wiki kuisha. Nimeeleweka?”

“Ndio mkuu”

“Oparesheni hiyo nitaiongoza mimi mwenyewe, baada ya kumaliza kwaangamiza hawa watu. Tutafwata kwa wale ambao wametupatia kazi hii kwani nao pia lazima wafe. Nimeeleweka?”

“Ndio”

Wasichana wote wakajibu kwa pamoja, Livna akaondoka eneo hilo huku akijaribu kufikiria ni njia gani ambayo anaweza kuitumia kuhakikisha kwamaba anawawaangamiza Eddy na Shamsa.

***

“Naona umesha ongea na mkuu wako”

Anna alizungumza huku akiwa amesimama mlangoni mwa chamba chake akimtazama baba, dokta Ranjiti aliye maliza kuifunga laptop aliyo tumia kuzungumza na John.

“Ulisha wahi kunifundisha maisha ya utotoni kwamba nisiwe mtu wa kumnyenyekeza au kuongozwa na binadamu mwenzangu, inakuwaje leo, unaongea kiustarabu na kumnyenyekea mtu”

“Anna mwanangu najua hujui kinacho endelea ndio maana unazungumza hivyo?”

“Kweli sijui na sinto acha kuzungumza maneno haya hadi nijiue”

“Njoo ukae hapa”

Anna akatembea taratibu na kukaa kwneye sofa sehemu aliyo ombwa na baba yake akae.

“Maisha yanabadilika mwanangu, hapo mwanzo niliamini taaluma yangu na pesa, vinaweza kutatua kila ktatizo kwenye maisha yangu, ila si hivyo.”

“Mapenzi yangu juu ya Phidaya ndio yameweza kuniigiza kwenye mamatizo kama haya unayo yaona ila sinto weza kumuacha Phidaya hadi pale nitakapo hakikisha kwamba nimempata”

“Kwani Phidaya ana kitu gani cha maana ambacho baba kimekupagawisha?”

“Sio kitu, ila ni upendo. Ninampenda sana Phidaya na nilisha apa kwamba nitafanya chochote kuhakikisha Phidaya anakuwa ni mke wangu peke yanug”

“Baba huyo Phidaya ulimtongoza?”

“Hapana”

“Haaa…..ulimpataje sasa?”

Dokta Ranjiti akatabasamu huku akimtazama mwanaye.

“Siku ambayo nilimpata Phidaya, nilikuwa katika hospitali ya Agaghakan, ambapo nilienda pale kwa kazi maalumu ya upasuaji ambayo niliweza kuombwa. Siku hiyo nakumbuka niliweza kumuona Phidaya, kusema kweli nilijisikia msukumo mkubwa sana moyoni mwangu wa kuweza kumpata. Ila ubaya ni kwamba aliku ni mkwe wa waziri, ambaye ndio mama yake Eddy”

“Eddy yule aliye kuwa amenikamata”

“Ewalaaa”

“Ehee”

“Hiyo siku nakumbuka ilikuwa ni siku mbaya kwa Eddy, kwani siku hiyo alifariki mama yake, akafariki na mtoto wake, ili niweze kupata bingo ya kumpata Phidaya ilibidi na yeye nimchome sindano fulani hivi, ambayo inaweza kuyasimamisha mapigo ya moyo kwa kipindi fulani na mtu akiweza kumuona mtu katika muda huo ni lazima ataamni kwamba mtu huyo amefariki dunia”

“Hee huoni kwamba ulikuwa unafanya jambo la hatari?”

“Yaa ni hatari ila muda huo sikujali kama kuna hatari au laa, nilicho kuhitaji kwa wakati huo alikuwa ni Phidaya tu. Nilipo hakikisha kwamba zoezi langu linakwenda vizuri, nikajiweka karibu sana na wale wachima makaburi, katika kaburi la Phidaya, kulichibwa shimo refu lilo tokelezea katika ufukwe ulipo karibu kabisa na ile nyumba ya Eddy. Baada tu ya mazishi, kuna vijana nilisha waandaa, wakalitoa lile jeneza na siku hiyo hiyo nikaondoka na Phidaya nchini Tanzania”

“Sasa uliondoka naye kama maiti au?”

“Hapan niliondoka naye kama mgojwa, nikiwa kwenye ndege, nilimchoma siindano ya kuuwezesha moyo wake kufanya kazi kama kawaida, baada ya hapo nikamchoma sindano ya kufuta kumbukumbu zake zote”

“Mmmm ila baba hiyo ilikuwa ni hatari sana. Haya sasa hivi si bora uachane naye tu kwa maana kumbukumbu zake zimerudi kama kawaida”

“Siwezi kumuacha”

“Kwa nini sasa baba, ikiwa ilikuwa bado theluthi tu, tukionje kifo?”

“Phidaya ndio silaha ya pekee ya kumuangamiza Eddy”

“Baba bado unahitaji kuendelea na hayo mashindano yasio ya msingi kweli baba?”

“Usijali, utaona tu kitu kitakacho tokea”

***

Shamsa na Camila wakafikishwa katika nyumba maalumu iliyo andliwa. Si nyumba ngeni kwa Shamsa, kwani ni siku chache tu walihama kwenye nyumba hiyo. Camila moja kwa moja akaelekea jikoni, akanadaa chakula kwa ajili ya Camila ambaye anaamini kwamba ana njaa kali. Alipo maliza kuandaa chakula hicho, ikamlazimu kumuasha Camila na kuanza kumlisha chakula hicho.

‘Yupo Madagascar, mji wa Anatananarivo’

Meneo ya msicha aliye muua, yakajirudia akilini mwa Shamsa, ambaye hadi sasa hivi hajampata mwanaye. Akamaliza kumliza Camila, akamuogesha na kumpeleka katika chumba chakena kumlaza. Shamsa akatoka nje na kuwakuta walinzi wakiendelea kuimarisha ulinzi.

“Nahitaji kwenda ubalozi wa Uingereza”

“Usiku huu?”

“Ndio, kwani kuna tatizo?”

“Ahaa…muda umekwenda, na jukumu letu ni kukulinda”

“Ninahitaji kwenda huko, kama mutashindwa kunipekeka nitakwenda mimi mwenyewe”

Walinzi hao wakatazamana, wakawasiliana na mkuu wao na kumueleza ombi hilo. Mkuu wao hakuwa na namna zaidi ya kumruhusu binti hiyo kwani eneo wanalo elekea ni salama.

***

Phidaya akaendelea kukikaza kidole chake kuhakikisha kwamba hafanyi kitu ambacho Eddy amehitaji amfanyie.

“Niue Phidaya”

“Siwezi, siwezi Eddy kufanya hivyo”

Phidaya aliendelea kuzungumza huku machozi yakimgika. Phidaya kwa nguvu akaitupa bastola hiyo chini na kwa nguvu akamkumbatia Eddy huko wote wakilia.

“Ninakupenda Eddy, kwa nini unanisaliti jamani?”

“Ninaomba unisamehe mke wangu, ninakupenda pia”

“Kweli”

“Ndio mke wangu, ninakupenda sana”

“Nimekusamehe mume wangu, nipo tayari kuwasidia wewe na Shamsa kumtafuta huyo mtoto wetu mwengine”

“Kweli”

“Ndio mume wangu, na kupitia mimi itakuwa rahisi kumkamata John na Ranjiti na huo ndio utakuwa mwisho wao”

Maneno ya Phidaya yakamfanya Eddy kuanza kumnyonya mdomo wake huku akiwa amejawa na raha sana, kwani matumaini ya kuwapata maadui zake na mwanaye kwa sasa yapo kwa Phidaya pekee.


Taratibu wakaachiana, kwa kutimia viganja vyake, Eddy akaanza kumfuta Phidaya machozi yanayo endelea kumtiririka mashavuni mwake.

“Phidaya sihitaji kukupoteza maishani mwangu, na huyu shetani aliye kuwa ameningia ninamkemea ashindwe na kulegea”

Phidaya akatabasamu kidogo, tabasamu lilio mfanya Eddy azidi kuuona uzuri wa mke wake huyo.

“Baby kuna haja ya mimi kuendela kuka hapa hospitalini?”

“Ah….sijajua jeraha lako lipo vipi, ila inabidi kuzungumza na daktari”

“Sawa”

“Nina habari nzuri”

“Habari gani?”

“Nimempata Camila wetu”

“Kweli mume wangu”

“Ndio mke wangu, nimempata, nimesaidiana na Shamsa katika kuwamakata watekaji walio kuwa wamemuiba mtoto wetu”

“Ni kina nani?”

“Ni wasichana ambao hadi sasa hivi sifahamu wametokea wapi, ila kuna mmoja ambaye yupo hai, nitamuhoji maswali hili niweze kufahamu ni wapi alipo tokea”

“Sawa mume wangu, haujaumie sehemu?”

“Ni jeraha tu la mguuni hili nililo pigwa risasi ila nilifungwa vizuri na sindano za kupunguza maumivu ndio zinazo nisaidia hadi sasa hivi ninajisikia vizuri”

“Sawa mume wangu pole sana, na nina kuahidi kwamba kila jambo litakwenda salama”

“Asante mke wangu, sogea huko tulale pamoja”

Phidaya akasogea upande wa ukutani na Eddy akajilaza kitandani hapo huku akikiweka kichwa cha Phidaya kifuani mwake.

***

Jing akafumba jicho moja huku akiitazama ndege ya kijeshi inayo kuja mbele yao, akameza fumba zito la mate, kisha akafyatua bomu moja lililo lililo toka kwa kasi na kulipua ndege hiyo ya kijesho.

“Waooooooooooooo, huuuuuuuuuuuu”

Jing alishangilia huku akigonganisha kiganja chake cha mkono wa kulia na Adrus kisha akamgeukia Cookie aliye kaa siti ya nyuma na kugonganisha naye kiganja.

“Kazi nzuri”

“Asante”

Adrus akazidi kusonga mbele huku wakiendelea kushambuliana na ndege moja ya kijeshi iliyo bakia. Wakafanikiwa kuiangusha ndege hiyo, furaha na amani zikazidi kutawala.

“Tunaelekea wapi kwa sasa?”

Adrus alizungumza huku akimtazama Jing usoni mwake.

“Tunatakiwa kuua signal zote za satelaiti zinazo weza kuinasa hii helicopter kwa maana tunaweza kukimbia mwisho wa siku tukakamatwa kama kuku wenye videri.”

“Unaziua vipi?”

“Mimi ninaweza”

Cookie alizungumza.

“Hata mimi naweza, kuna nyaya fulani vipo hapa mbele tunatakiwa kuzikata”

Jing alizungumza huku akimonyesha Adrus sehemu yenye nyaya hizo. Cookie akafungu kisanduku cha chuma kilichopo ndani ya helicopter hiyo na kukuta bisisibi zenye ukubwa zenye ukubwa tofauti tofauti. Cookie akatazama nati zilzo fungia eneo alilo lizungumzia Jing, akachukua bisibisi inayo endana na nati hizo na kumkabidhi Jing. Jing kwa haraka akaanza kufungua eneo hilo. Alipo maliza, akatoa nyaya zipatazo sabini na sita zenye rangi tofauti tofati.

“Mbona nyaya zenyewe zipo nyingi sana”

Adrus alizungumza huku akishangaa sana.

“Hii helicopter ipo tofauti na nyingine, nyaya hapa huwa zinakuwa ishirini”

Jing naye alizungumza huku akishangaa. Cookie akaendelea kutazama nyaya hizo.

“Nipishe hapo”

Cookie alizungujmza huku akifungua mkanda wa siti aliyo kali, Jing akahamia siti ya nyuma na Cookie akaka siti ya mbele, taratibu akaanza kuzichambu nyanya hizo, ila kila anayo ishika anahisi sio sahihi

***

Raisi Dustan na wafanyakazi wake wote walipo katika ukumbi wa mawasiliano katika ikulu ya White House wakakaa kimya wakishushudia ndege zao za kijeshi jinsi zinavyo teketea hewani.

“Son of bic**”

Raisi Dustan alijikuta akitukana huku akikunja ngumi ya mkono wa wake wa kulia ikiashiria kwamba amekasirishwa sana na tukio lililo jitokea.

“Tuna fanyaje?”

“Muheshimiwa raisi bado tuna tafasi ya kumrudisha mikononi mwetu”

Mshauri wa raisi Dustan alizungumza huku akimtazama usoni mwake.

“Nafasi gani?”

“Tunaweza kumtumia Naomi kuweza kumshawishi Adrus aweze kubadilisha maamuzi yake, kwa maana hawa watu wawuli wana mahusiano ya kimapenzi”

“Sasa huyo Naomi mwenyewe unaye mzungumzia si hali yake ni mbaya”

“Hapana mkuu hali yake kwa sasa inaendelea vizuri na hadi ninavyo zungumza hivi sasa tayari amesha zinduka na anazungumza vizuri”

“Kumbu kumbu zake je zipo vizuri?”

“Ndio muheshimiwa”

Raisi Dustan akawatazama viongozi wa kijeshi walio pokatika eneo hili.

“Muna ushauri gani?”

“Mkuu kuna tunaweza kutumia signal inayo weza kuwaonyesha ni eneo gani wanapo elekea na itakuwa ni rahisi kwa sisi kuweza kuwakamata”

“Hilo swala la Naomi kwa sasa hembu achana nalo kwanza”

Raisi Dustan alizungumza huu akitazama signal ya helicopter hiyo, ila hata kabla hawajajipanga ni jinsi gani wanavyo weza kuwakamata Adrus na wezake, wakashuhudia signal hiyo ikipotea.

“Mbona imepotea?”

Raisi Dustan alizungumza hukua kinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia, kila mtu hakujua ni nini kilicho tokea. Wataalamu wanao shuhulika na maswala ya satelaiti, wakaendelea kujitahidi kuhakikisha kwamba wanaipata signal hiyo.

“Mbona hamuongei kitu cha kueleweka?”

“Muheshimiwa raisi, wameweza kuua signal za satelait na hatuto weza kuwaona”

“Shiti’

“Ila mkuu tuna mawasiliano nao”

“Mkuu kama nilivyo kushauri, tumtumie Naomi kuweza kumpata Adrus, pasipo kufanya hivyo kila kitu kinakwenda kumpoteza hivi hivi, kwa maana kama ulivyo jionea huyo mtu ana uwezo mkubwa sana, ambao si wakawaida, kuupata kwa mwanajeshi yoyote hapa nchini”

“Naomi mwenyewe yupo wapi?”

“Yupo kwenye hiii hospitali ya Ikulu”

“Twende”

Wakatoka katika eneo hilo na kueleke katika chumba maalumu alicho lazwa Naomi, wakamkuta Naomi akiwa amekaa kitako kitandani huku akinyweshwa uji na mmoja wa manesi wanao muhudumia.

“Muheshimiwa raisi”

Naomi alizungumza huku akitabasamu..

“Ninafurahi kukuona ukiwa katika hali hii”

“Nashukuru muheshimiwa raisi, nashukuru pia kwa kuweza kuja kuniona”

Naomi alizungumza kwa sauti ya chini sana kwa maana bado ana maumivu kwenye kifua chake.

“Usijali, samahani kama tunatakuwa tumekusumbua, kwa hii hii kazi ambayo ninakuomba ukiwa katika hali kama hii”

“Usijali muheshimiwa raisi, jukumu langu ni kuhakikisha kwamba ninailinda nchi yangu, na kuhakikisha kwamab taifa langu linakuwa salama”

“Nashukuru kwa hilo, kuna tatizo limetokea, na wewe tunaamini ndio utakuwa ni mtu utakaye weza kutusaidia”

“Tatizo gani muheshimiwa”

“Ni kuhusiana na mpenzi wako Adrus”

Naomi kidogo akastuka huku akimtazama raisi.

“Sio tatizo baya, hapana”

Mshauri wa makamu wa raisi alizungumza ili kumtoa wasiwasi Naomi. Akaanza kumsaidia Naomi kila jambo lililo fanywa na Adrus.

“Bado tunamuhitaji, naamini hata wewe unamuhitaji pia”

“Ndio”

“Tunahitaji uwasiliane naye na umshawishi kuhakikisha kwamba anabadilisha mawazo yake, kwa maana anakupenda”

“Sawa, mpigieni simu”

Mshauri wa raisi akamtazama raisi Dustan usoni mwake, kwa ishara ya macho, raisi Dustan akamruhusu mshauri wake huyo kufanya mawasiliano na Adrus.

***

“Hii maiti inabidi itolewe humu ndani?”

Madam Mery alimuambia mlinzi wa Shamsa, aliye baki naye humo ndani mara baada ya Shamsa kuondoka katika eneo hili yeye mwenyewe.

“Ngoja papambazuke”

“Ataozeana humu ndani bwana”

“Inabidi nifanya mawasiliano na mkuu wangu, siwezi kufanya chochote juu ya hii maiti”

“Bora ufanye hivyo”

Mlinzi wa Shamsa akaitafuta namba ya mkuu wake, akampigia.

“Ndio”

“Mkuu kuna tatizo limetoke, ninaomba msaada wako”

“Tatizo gani?”

Mlinzi huyo akaelezea kila kitu kilicho tokea, katika nyumba hilo, mkuu wake akamuahidi ndani ya muda mfupi atamtumia msaada wa kuwaondoa maiti hao na ahakikishe kwamba madam Mery anakuwa chini ya ulinzi hadi pale watakapo pokea amri kutoka kwa makamu wa raisi

***

K2 taratibu akajinyanyua chini alipo anguka na kukaa kitako. Akashusha pumzi nyingi sana huku akisikilizia maumivu ya mwili wake kwani kipigo alicho patiwa ni kikali na kimemfanya kila sehemu anayo jishika imuume. Akanyanyuka na kuingia jikoni alipo muacha kaka yake ambaye kabla ya uvamizi alilewa sana hadi hadi akapitia na usingizi.

“Kaka, kaka, kaka amka”

K2 aliita huku akimtingisha kaka yake huyo anaye endelea kukoroma kwa usingizi wa pombe. K2 akafungua friji kunwa lililomo ndani humu, akachukua kidungu kidogo cha lita tano chenye maziwa ya baridi na kuanza kumwagika kaka yake usoni na kumfanya akurupuke kitandani kwa haraka huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi.

“Vipi”

“Tumevamiwa na mtoto amechukuliwa”

“Amechukuliwa, kivipi?”

“Mtoto ameibiwa, na walinzi wote nahisi wamesha uwawa”

K2 alizungumza huku akimsaidia kaka yake kunyanyuka chini, wakatoka jikoni humo na kutoka nje, kila sehemu wanayo pita katika nyumba yao hiyo wanakutana na maiti ya walinzi wao.

“Ni kina nani walio fanya hivyo?”

“Yaani hata mimi sielewei kabisa, na sifahamu ni nani aliye watuma”

“Au atakuwa ni makamu wa raisi?”

“Sielewi kaka, yaani kichwa changu hapa nahisi kuchanganyikiwa”

“Ohoo Mungu wangu kila kitu kimeharibika sasa”

“John nitahakikisha ninawafahamu wale wasichana na nikiwashika nitawaua wote”

“Na hizi maiti je?”

“Tutawazika wote katuka kaburi moja hata kabla ya kujapambazuka.

***

Shamsa akafika katika ubalozi wa Uingereza, akahojiwa maswali kadhaa na walinzi wa getini, kutokana na vitambulisho vya walinzi alio ongozana nao, ikawa ni rahisi kwa yeye kuruhusiwa kuingia katika ofisi hizo za Ubalozi wa Ungereza hapa nchini Tanzania. Shamsa akasindikizwa moja kw amoja hadi kwenye chumba alicholala Sa Yoo.

“Sa Yoo”

Shamsa aliita mara baada ya kuingia katika chumba hicho na kumkuta Sa Yoo akiwa amejilaza kitandani, taratibu Sa Yoo akafumbua macho yake baada ya kuisikia sauti ya Shamsa safiki yake anaye mpenda sana. Kwa haraka Sa Yoo akashuka kitandani na wakakumbatiana na Sa Yoo.

“Samahani Shamsa, sikuweza kumsaidia mwanao, sikufanikiwa kumsaidia Junion Jr”

“Usijali, tutampata, ikiwa tumetambua muhisika halisi basi tutamsaka duniani mzima na kumkamata na kumrudisha mtoto”

“Asante rafiki yangu kwa kunielewa”

***

“Asante Mungu”

Cookie alizungumza mara baada ya kufanikiwa kukata nyanya baadhi zinazo ifanya ndege hiyo kuto weza kunaswa na satelaiti ya nchi yoyote na popote pale wanapo kwenda.

“Umefanikiwa?”

Adrus alizungumza huku akimtazama Cookie

“Ndio mpenzi wangu”

Adrus, akavuta karibu Cookie na kumnyonya midomo yake. Jing akajikoholesha kidogo na kuwafanya Adrus na Cookie kuachiana.

“Aaha……”

“Haya mama najua unataka kuzungumza kitu gani rudi kwenye siti yako, umuelekeze rubani wetu hapa”

Cookie alizungumza kwa sauti iliyo jaa furaha.

“ADRUSDDD…….”

Sauti iliyo sikika kwenye vipaza sauti ndani ya helicopter hiyo, ikawashangaza Cookie na Jing ila Adrus ilimstua sana kwani kwa muda na wakati kama huu hakutarajia kuweza kuisikia sauti ya Naomi mwanamke wa kwanza kumteka moyo wake na kumfundisha nini maana ya kupenda.



Cookie na Jing wakamtazama Adrus alite endelea kuwa katika hali ya bumbuwazi.

“Adrus mume wangu, natambua kwamba uninisikia. Nipo hai mpenzi wangu”

“NAOMI?”

“Ni mimi Adrus wangu, kwa nini unafanya hivi. Kumbuke tulipo toka, tulipambana pamoja , tuliahidi kufa pamoja, ila kwa nini unanisaliti Adrus. Kwa nini unasaliti taifa laki, kumbuka kwamba tulikula kiapo cha kutetea nchi pamoja na heshima ya nchi zetu. Kwa nini lakini Adrus unafaya hivyo”

Sauti ya Naomi ilisikika ikiwa imetawaliwa na majonzi mengi sana. Adrus akajikuta akikosa jambo la kuzungumza kabisa kwa maana maneno hayo yanamuumiza sana moyo wake. Macho ya Jing yakakutana na macho ya Cookie ambaye maneno hayo kwa namna moja ama nyingine yanamkera sana kwani wivu umeanza kumtawala. Jing akamkonyeza Cookie kukata nyaya za mawasiliano. Cookie akamtazama Adrus na kumuona jinsi anavyo lengwa lengwa na machozi usoni mwake. Cookie taratibu akashika nyaya moja ya rangi nyeupe.

“Adrus kumbuka ninakupenda mpenzi wangu kwa ni…….”

Mawasiliano yakakatika, Adrus akamgeukia Cookie na kumkuta akiitoa mikono yake kwenye waya anao amini kabisa kwamba huo ndio waya wa mawasiliano. Adrus akayang’ata maeno yake kwa hasira huku akimtazama Cookie kwa jicho ambalo hata Cookie yeye mwenyewe alitambua hasira iliyo kifuani mwa Adrus.

“Baby kumbuka tumesha fanya maamuzi huwezi kurudi kwao tena kumbuka sio watu wazuri hao kwako wanamtumia msichana huyo kukurudisha katika himayo yao na ukirudi watakufanyia kitu kibaya, hata kukuua”

“Ni kweli kabisa, kitu alicho kizungumza Cookie kina ukweli Adrus, umesha amaua maisha haya usirudi nyuma, ushawishi wa huyo msichana utakugarimu maisha yako kwa asilimi kubwa sana, ninakuomba sana Adrus, uachane na mawazo hayo, hata kama anakupenda ila ninakuomba u……”

“Fungeni mabakuli yenu”

Adrus alizungumza kwa ukali na kuwafanya Cookie na Jing kukaa kimya

***

“Eddy…..Eddy kumepambazuka”

Phidaya alizungumza huku akikinyanyua kichwa chake kifuani mwa mume wake Eddy.

“Mmmmmm”

“Pamepambazuka”

Eddy taratibu akajinyanyua na kukaa kitako kitandani.

“Aiissiii…..”

“Nini baby?”

“Muguu una niuma”

“Wapi?”

“Hapa kwenye jeraha”

“Inabidi kumuita dokta?”

“Mmmmhhmmm…….”

Eddy alizungumza huku akishusha mguu wake wa kwanza chini, akajaribu kuushusha mguu wenye jeraha, ila anashindwa kabisa, kwa maana maumivu yanazidi kuongezeka.

“Baby mguu unamwagikwa na damu!!!”

Phidaya alizungumza huku akimuonyesha Eddy damu zilizo samba kweney shuka.

“Doctaaa”

Phidaya aliita kwa sauti ya juu, walinzi wawlili wakaingia ndani humo.

“Muiteni daktari haraka”

Walinzi hao wakatoka, baada ya muda mfupi dokta Benjamini akafika akiwa ameongozana na nesi mmoja.

“Habari yako muheshimiwa?”

Dokta Benjamini alizungumza huku akiushika mguu wa Eddy na kuutazama.

“Naomba mkasi”

Dokta Benjamini alimuambia nesi huyo, ambaye kwa haraka akatia mkasi kwenye kibegi kidogo walicho ingia nacho katika chumba hicho. Kwa haraka dokta Benjamini akaanza kuichana suruali ya Edddy.

“Ohooo Mungu wangu”

“Nini dokta?”

Phidya aliuliza huku macho yakimtoka, na wasi wasi mwingi ukiwa umemjaa.

“Nyuzi zote zimeichia”

“Jamani Eddy kwa nini ulikwenda kupambana huyo ukiwa unajua unaumwa jamani?”

Phidaya alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Yote nilifanya kwa ajili ya familia yangu”

Maneno hayo ya Eddy yakazidi kumpandisha Phidaya uchungu na kujikuta akiangua kilio hadi nesi aliyomo humo ndani akabaki akiwa amejawa na mshangao kumuona mke wa makamu wa raisi akili kama mtoto mdogo.

***

“Amelala bado”

Shamsa alizungumza huku akiufunga mlango wa chumba alicho mlaza Camila.

“Amekuwa mkubwa sana”

Sa Yoo alizungumza hukuakiwa amejawa na tabasamu usoni mwake.

“Yaa ila jana ilikuwa ni siku mbaya sana”

“Poleni sana”

“Aahhaa,tumesha poa. Ila kuna majanga mengine”

“Yapi tena?”

Shamsa na Sa Yoo wakaka kwenye sofa zilizopo eneo la hapo sebleni.

“Ni kuhusiana na ukweli juu ya mtoto nilio zaa na Eddy, Phidaya ameweza kufahamu ukweli”

“Weeeee…….!!?”

“Haki ya Mungu vile, na hapa ninavyo kuambia kuna vita ya vuguvugu inaoyo endelea kati yangu mimi na Phidaya”

“Ila Shamsa kumbuka Phidaya ni mama yako?”

“Sio wa kunizaa, mimi asili yanu ni Somalia yeye sijui ni Iraq huko”

“Hata kama Shamsa, mumeishi miaka yote hiyo mukiheshimiana kama mama na mtoto”

“Sa Yoo, ninampenda Eddy na Eddy mwenyewe ananipenda kupita maelezo”

“Mmmmm”

“Kweli na hapa ameniambia kwamba anakwenda kumuua Phidaya”

“Hahahaaa…….Shamsa mbona unanichekesha rafiki yangu, unahisi kumuua mke wake ni jambo rahisi sana au?”

“Hiyo ndio ahadi ambayo ameweza kunipatia?”

“Shamsa wewe ni rafiki yangu, ninakupenda sana zaidi ya sana. Kwa hilo jambo unalo taka kuliingiza moyoni mwako sio zuri. Umekosa nini Shamsa, kama nipesa ipo, kama ni maisha mazuri unayo. Kwa nini unamng’ang’ania Eddy, kama muliteleza hadi mukampata Junion Jr basi jaribu kumsahau Eddy na muachie Phidaya awe na amani ya moyo wake. Nimeishi nanyi nyote kwa kupindi chote, Phidaya hakuwa na tatizo lolote kwenu, ila nyinyi ndio mumeyaanzisha matatizo”

Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyenyekevu mwingi sana.

“Najua maneno yangu huto yapenda, ila pale ninapo kuona rafiki yangu unakwenda kupotea, unapokwenda kuanzisha matatizo mapya ikiwa tatizo moja halijaisha, lazima nitakuambia tu Shamsa”

Shamsa akashusha pumzi taratibu, maneno anayo yazungumza Phidaya yana ukweli mtupu ndani yake.

“Ila Sa Yoo hujui maana ya mapenzi, hujui nini maana ya kupenda”

“Hata nisipo jua Shamsa, ila si kwa mwanaume ambaye amekukuza wewe. Ingekuwa ni furaha kubwa sana siku Eddy unamletea mkwe na munapata mtoto…..”

“Mmmmm humjui Eddy wewe”

“Sisemei kwa kipindi cha sasa, kipindi ninacho kizungumzia ni kile kipundi ambacho hamkuba mumeingia kwenye mahusiano ya siri.”

“Ahaa….tuachane na hizo mada”

“Sawa tunaachana nazo ila jaribu kabisa kuachana na maswala ya hayo na Phidaya, kwa maana unakwenda kutengeneza vita ambayo itawatafuta hadi watoto wenu kwa maana Camila na Junion Jr ni mto na dada yake, endapo, wewe au Phidaya mmoja wao atamuua kumuua mwenzake lazima watoto wenu watakuja kuuana na wao kuendelea visasi vya kijinga ikiwa wao ni damu moja”

“Nimekuelewa Sa Yoo, ila kninampenda Eddy”

“Mpende kama baba na si mpenzi”

Shamsa hakuwa na pointi ya msingi zaidi ya kunyanyuka na kuelekea jikoni kuandaaa kifungua kinywa.

***

Naomi machozi yakaanza kumwagika usoni mwake huku akimtazama raisi Dustan aliye simama pembeni ya kitanda chake.

“Mkuu mawasiliano hayapatikani tena”

Mshauri wa raisi Dustan alizungumza huku akitoa sikioni simu aliyo itumia kuwasiliana na Adrus.

“Jaribu tena?”

Naomi alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi.

“Ahaa samahani muhesimiwa, mgonjwa akiendela kuwa na hali kama hii, basi damu inaweza kuendelea kumtoka kwa ndani na kumsababishia matatizo mengi ya ndani kwa ndani”

Nesi aliyomo katika chumba hichi alimshauri raisi Dustan pamoja na mshauri wake.

“Ahaa, basi ngoja tumuache kwa muda kidoho ili aweze kukaa sawa”

“Sawa”

“Muheshimiwa raisi”

Noami aliita huku akijapangusa machozi usoni mwake.

“Naam”

“Ninakuomba kitu kimoja”

“Kitu gani?”

“Hata mukimkamata Adrus ninawaomba musimuumize wala kumuua, yule ndio roho yangu, nina imani kuna kitu kitakuwa kimempitia tu, ila ninawaomba sana”

“Nakuahidi hilo hato umia, kwa maana umeyasaidia maisha ya mwanangu, japo hatujampata bado ila tutahakikisha kwamba na Adrus anapatukana akiwa asalama salmini”

“Asante muheshimiwa raisi”

“Asante nawe pia, nikitakie kuugua kwema”

“Asante”

Raisi Dustana na mshauri wake wakatoka chumba alicho lazwa Naomi.

“Muheshimiwa nimepata wazo jengine”

“Wazo gani?”

“Tuliingia mkataba na Adrus na amepatiwa kiasi kikubwa sana cha pesa, na pesa hiyo kwa asilimia mia moja amemiachia mama yake”

“Kwa hiyo?”

“Tumtumie mama yake kuwa chambo wa kumrudisha Adrus mikononi mwatu tena”

“Fanya mawasiliano na raisi wa Tanzania na umueleze juu ya huo mpango mpya ambao umeamua tuufanye”

“Ila muheshimiwa raisi, ninaona hili swala si la kuomba ruhusa tena”

“Kivipi?”

“Raisi Rahab alisha toa ruhusa ya sisi kuweza kufanya kitu chochote juu ya Adrus hata kumuua pia alizungumza nawe, kama ni hivyo bado tunamuhitaji kwa maana ndio mtu wa pekee ambaye anaweza kumuokoa mwanao na yeye ndio mtu wa pekee anaye fahamu maeneo hayo ya Al-quida vizuri sana. Tumteke mama yake, aja hapa nchini Marekani na tutajua ni jinsi gani tunaweza kumtafuta Adru na kumpata”

Raisi Dustan akasimama kwa muda huku akimtazama mshauri wake huyu anaye muamini sana.

“Simamia hilo swala na hakikisha kwamba linakwenda vizuri sawa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

***

“Inabidi twende nchini Tanzania”

Kauli ya Adrus ikawashangaza Jing na Cookie ambao hawajatarajia kusikia hicho walicho kisikia.

“Samahani, nimesikia vibaya au?”

Jing aliuliza huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Tnatakiwa kurudi nchini Tanzania sasa hivi?”

“Ila kwa hii helicopter sidhani kama tunaweza kufika?”

“Tunaweza kufika”

“Mafutu hatuna ya kutosha, na tunarudi nchini Tanzania kufanya nini Adrus?”

“Ninakwenda kumlinda mama yangu, mama yangu ndio kilakitu kwa sasa, hisia zungu zinahisi kwamba, kama wameshindwa kumtumia Naomi, mtu anaye fwata katika kumtumia kwamngu ni mama yangu mzazi, na hapo hakuna kati yenu ambaye anaweza kunishauri kitu nikamuelewa, kwa maana ninampenda mama yangu kuliko kitu chochote”

“Umejuaje hilo?”

Cookie alizungumza huku akimtazama Adrus akwa mshangao usoni mwake.

“Mumeshau kwamba mimi ni nani?”

Adrus alizungumza huku akiitazama ramani inayo onekeana pembeni yake, taratibu akaigeuza helicopter hiyo na kuzii kuwafanya Cookie na Jing kuzidi kushangaa maamuzi anayo yafanya Adrus.



“Adrus naomba nikushauri kitu”

Jing alizungumza kwa sauti ya upole

“Kitu gani?”

***

Kila mtu ambaye anamfahamu mama Adrus alizidi kushangazwa na maendeleo ya kasi ambayo anayafanya. Kununua jumba la kifahari Mbezi beach na kuhamia huko, kukazidi kuwafanya watu wanamfahamu kujiuliza maswali ambayo hakuna hata mmoja wao aliye weza kupata jibu la kueleweka. Wapo walio anza kuisi mama huyo amejiunga na chama cha freemason.

“Shosti kwako ni kuzuri”

Mama Baraka alizungumza huku akitazama tazama seble ya jumba hili kubwa la mama Adrus, aliye mkaribisha hapo nyumbani kwake.

“Asante shosti”

“Basi kule Ubungo umetuachia story kila mtu mama Adrus, mama Adrus hembu shosti yangu niambie siri ya huu utajiri wako ni nini kwa maana mmmm”

“Hahaa najua tu waswahili lazima watazungumza kwa maana walizoea kuniona natembeza vitenge vyangu eheee?”

“Yaani watu wengine umesha kuwa mwanachama”

“Mwanachama wa nini?”

“Ahaaa si wa Freemason”

“Wendawazimu hao wanao sema hivyo. Shost siri kubwa ya maisha haya ni kuwa na mtoto anaye jituma na kujitambua. Kwa nini hawamfikirii mwanangu kama anaweza kufanya jambo juu yangu?”

“Ahaa…hayo ni maneo ya waswahili shosti yangu, ila sio mimi”

“Haya mwaya”

“Hayo magari mawili hapo nje niliyo yaona ni ya kwako?”

“Ndio ya kwangu”

“Ahaaa wewe sasa hivi sio mwezetu kwa kweli”

Mama Baraka alizungumza huku akiendelea kutazama jumba hilo

***

Dokta Benjamini na nesi wake wakasiaidiana kuhakikisha wanayatimu majeraha ya makamu wa raisi Eddy. Zoezi hilo halichukukua muda mrefu wakamaliza.

“Muheshimi, itabidi tukupe mapumziko ya siku nzima, ukiendelea kuusumbua huu mguu itafika hatua ya mguu kukatwa”

Maneno hayo ya dokta Benjamini yakamstua sana Phidaya pamoja na Eddy.

“Ukatwe kwa nini dokta?”

“Anaweza kupata saratani, kidonda kinahitaji utulivu, hadi kikikauka basi anaweza kuendelea kuwa salama”

“Dokta siweikuendelea kukaa hapa hospitalini, nahitaji kuelekea nyumbani kwangu”

Eddy alizingumza na kumfanya dokta Benjamini kushangaa sana.

“Ila mkuu nimekuambia kidonda chako hakihitaji mapumziko”

“Munanipeleka kwangu nanitatulia kwangu, si jui umenielewa hapo”

“Lakini Eddy mume wangu, msikilize dokta?”

“Siwezi kuendelea kuwasimamisha vijana wa watu hapo nje, usiku na mchana kisa kunilinda mimi na wewe. Andaa gari la wangojwa munipeleke nyumbani”

“Sawa mkuu”

Dokta Benjamini alijibu kishingo upande tu, akatoka chumbani humo na kwenda kuandaa usafiri wa makamu wa raisi kuondoka hapo hospitalini. Msafara wa gari za walinzi ukaandaliwa, huku askari wa usalama barabarani walipo kwenye barabara ambazo msafara wa makamu wa raisi utapita wakianza kufanya utaratibu wa kusimamisha magari ili kuepusha msafara huo kusimama. Baada ya maandalizi hayo kufanyika, taarifa ikarudishwa hospitalini.

“Muheshimiwa makamu wa raisi tunaweza kuondoka sasa”

Mkuu wa walinzi wanao mlinda Eddy na mke wake hapo hospitalini alizungumza. Eddy akapanda juu ya kitanda maalumu liliocho andaliwa, huku Phidaya akikaa kweney kiwenye kiti cha magurudumu. Wakatoka ndani ya chumba hicho, Eddy akaingizwa kwenye gari la wagonjwa huku Phidaya akiingizwa kwenye garia aina ya Van, lililo tengenezwa na kampuni ya Masedez Benz, ambapo ndani ya gari hilo, moja ya siti zake inauwezo wa kukunjuka na kuwa kitanda.

Msafara ukaondoka katika eneo hilo la hospitali ya Muhimbili kwa mwendo wa taratibu. Wakatumia dakika kumi na saba kufika katika nyumba maalumu ya makamu wa raisi.

Sa Yoo na Shamsa, wakatoka nje kushuhudia magari hayo jinsi yanavyo ingizana katika magati makubwa mawili yaliyopo katoka jumba hilo.

“Eddy amamua kweli mke wake nini?”

Sa Yoo alimuliza Shamsa huku wakilitazama gari la wagonjwa linalo simama katika eneo laegesho ya magari.

“Sijajua kwa kweli”

Walinzi wakashuka kweney magari yao. Dokta Benjamini na manesi wake wawili alio ongozana nao, wakashuka kwenye gari hiyo ya wagojwa na kumshusha Eddy kwenye kitanda chake, jambo lililo mfanya Shamsa na Sa Yoo kushangaa sana.

“Eddy”

Shamsa alizungumza huku akikimbilia katika kitanda alicho lazwa Eddy.

“Vipi?”

Eddy alizuungumza huku akimtazama Shamsa usoni mwake.

“Ni nini kilicho tokea?”

Eddy akashindwa kujibu swahi hilo baada ya kumuona Phidaya akishushwa kwenye gari hilo na kukalishwa kwenye kiti cha magurudumu. Shamsa akatatabasamu kinafki huku akimtazama Phidaaya kwa macho ya kejeli. Sa Yoo akalio tukio hilo, kwa haraka akawasogelea eneo hilo.

“Phidayaaaa”

Sa Yoo alizungumza kwa furaha hukua kimkumbatia Phidaya.

“Umekuja lini kwetu jamani?”

“Tangu jana usiku nipo hapa”

“Karibu sana mpenzi nimekumissije?”

“Hata mimi nimewamiss sana”

“Sa Yoo karibu”

Eddy alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Sa Yoo.

“Asante mwaya mr vice President”

“Hahaaa, hujaacha vituko vyako tu?”

“Hahaaa niachie wapijamani, ikiwa mimi ndio yule yule”

“Sawa, nipeleke ndani”

Menesi hao wawili wakakisukuma kitanda hicho, huku Shamsa na dokta Ranjiti wakiwafwata kwa nyuma. Sa Yoo akakishika kiti cha Phidaya na kuanza kukisukuma taratibu kuelekea ndani.

“Twende kwenye ile bustani”

Phidaya alizungumza huku akinyooshea kidole bustan nzuri iliyo katika jumba hilo.

“Kwa nini?”

“Wewe twende”

Sa Yoo na Phidaya wakafika katika bustani hiyo.

“Mtoto yupo ndani?”

“Yaa yupo amelala”

“Sitamani kuishi humu ndani?”

“Samahani, sijakusikia vizuri?”

“Sitamani kuishi humu ndani kwa sasa, kichwa changu hakipo vizuri, kila ninapo muona Shamsa, roho yangu inatawaliwa na ukatili ambao utaisababishia familia yangu matatizo ambayo sihitaji yatokea kwa wakati huu”

“Kwani kuna nini kinacho Endelea kati yenu?”

Sa Yoo aliuliza huku akijifanya kama haelewi kitu kinacho endelea. Phidaya akamtazama Sa Yoo, kisha akatabasamu kidogo.

“Sa Yoo ninaamini kwamba unafahamu, kwa maana Shamsa ni rafiki yako na atakuwa amekueleza kila kitu?”

“Hatujapata muda wa kukaa na Sa Yoo na kuzungumza mambo mengi, labda unieleze wewe, kwa maana leo nimeona utofauti kati yenu ambao kidogo umenipa wasiwasi na mashaka”

“Unafahamu kwamba Eddy na Shamsa wana mtoto?”

“Mtoto…..!!!?”

“Ndio, wana mtoto wa kiume”

“Mungu wangu!!!”

“Swala la mtoto, kwa upande wangu mimi sina matatizo, ila shida, inakuja pale wanapo endeleza mahusiano yao, ya kimapenzi, kwa kweli inaniuma sana, basi wafanye kisiri siri, ila huyo rafiki yakoi ananidharau mimi, anaona mbo** ya Eddy ndio kila kitu kwake, amesahau wapi tumetoka”

Phidaya alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, jambo lililo mfanya hata Sa Yoo mwenyewe kumwagikwa na machozi.

***

“Niitie mkuu wenu”

Eddy alizungumza huku akimtazama mwanajeshi mmoja aliye simama hapo sebleni. Mwanajeshi huyo akatoka nje na baada ya muda akarudi akiwa ameongozanana mkuu wa kikosi chake.

“Ulifanya kama nilivyo kueleza jana?”

“Ndio muheshimiwa”

“Yupo wapi?”

“Katika nyumba ya nje muheshimiwa”

“Nipelekeni sasa hivi”

“Sawa muheshimiwa”

Dokta Benjamini hakuhitaji kuingilia kati maamuzi ya Eddy, kwani hadi sasa amesha zungumza hadi amechoka. Kwa kusaidiwa na wanajeshi hao wawili Eddy akakalishwa kweney kiti cha magurudumu alicho telewa.

“Eddy unaenda kutazama nini?”

Shamsa alimuuliza Eddy.

“Kuna kitu ninakitazama, niandalie chakula”

“Sawa”

Eddy akaongozana na mkuu huyo wa jeshi hadi kwenye nyumba ndogo iliyopo pembezoni mwa jumba hilo. Wakaingia ndanina kumkuta Lizy akiwa ametundikiwa dripu la maji huku akiwa amelala huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na wanajeshi wapatao sita.

“Tuliweza kumuhudumia baada ya kugundua kwamba bado yupo hai”

“Sawa sawa, hakikisheni kwamba munamlinda hadi pale hali yake itakapo kaa sawa, mutanifahamisha”

“Sawa muheshimiwa”

Eddy kwa ishara akamuamuru mkuu huyo wa jeshi kumtoka katika eneo hilo. Wakiwa wanaelekea ndani, wakamuona Sa Yoo akiwakimbilia, ikawabidi kusimama na kumtaza.

“Samahani ninamuomba muheshimiwa”

Sa Yoo alizungumza huku akiitia mikono ya mwanajeshi huyo kwenye kiti cha Eddy. Akaanza kumsukuma kuelekea katika bustani aliyo muacha Phidaya.

“Unanipeleka wapi tena Sa Yoo”

“Twende tu hapa si kwako”

Wakafika katika bustani hiyo, Eddy akamkuta Phidaya akijifuta machozi usoni mwake.

“Baby mbona unalia?”

Eddy alizungumza huku akimtazama Phidaya usoni mwake.

“EDDY KAMA UNANIPENDA, NAOMBA UMUONDOE SHAMSA HAPA NYUMBANI, SINTO INGIA NDANI HADI PALE SHAMSA AKIONDOKA KABISA KATIKA ENEO HILI”

Phidaya alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Sa Yoo na Eddy wakabaki midomo wazi kwani maamuzi ya Phidaya ni magumu sana kwa Eddy kuweza kuyatoa kwa wakati huu ambao bado ni kitendawili kigumu cha kumpata mwanaye Junion Jr ambaye hadi sasa hivi yupo mikononi mwa adui yake namba moja duniani John.



“Ahha…..samahani Phidaya, kama sijakusikia vizuri?”

Sa Yoo alizungumza huku akitabasamu, japo amemsikia vizuri Phidaya kitu alicho kizungumza. Eddy akaka kimya huku akitafakari maneno ya mke wake.

“Phidaya na Eddy, pasipo kuwavunjia heshima au kuwaingilia kwenye mambo ya ndani ya kifamilia yenu, kwanza ninawaomba munisamehe kwa haya nitakayo kwenda kuyazungumza”

“Hembu jitazameni sasa hivi, kila mmoja kwenye mguu wake ana jeraha la risasi, kwa nini imetokea hivyo. Sababu nyinyi wenyewe munazijua au kwa kuwasaidia haraka haraka sababu kuu ni maadui”

“Mumetengeneza mabifu ya kijinga ambayo Eddy kama baba unataka yaingie ndani ya familia yako, ikiwa watu wa nje tu hujawamaliza hata theluthi. Tangu nimewajua nyinyi kila siku ni kukimbizana na roho mikononi, kwa nini lakini, mumeshindwa kujitambua kwamba munahitaji maisha ya amani na furaha. Hembu mtazameni mtoto wenu ana miezi mingapi tangu azalie, leo hii amekuja kukutana na heka heka ambazo bado kidogo tu ampoteza maisha”

Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku akiwakazia macho Eddy na Phidaya ambao wamekaa kimya wakimsikiliza.

“Eddy simama kwenye zamu yako, unataka uje kulelewa familia yako na mwanaume mwenzio? Najua jibu ni hapana, je na wewe Phidaya unataka kuja kulelewa na mwanamke mwenzio watoto wenu baada ya kufa kipuuzi pasipo na sababu ya msingi?”

“Eddy utakumbukwa duniani kwa lipi, ikiwa watu wambao uliwaweka katika nafasi kubwa ya maisha yako wakiwa wanagombana kama wendawazimu?”

“Ngoja Eddy nikuambie siri moja, usijaribu wala kuthubutu kumpoteza kati ya Phidaya au Shamsa, kwa nini ninazungumza hivyo? Watakuwa ni watu ambao watakuangamiza kimya kimya pasipo wewe kutarajia, na utakufa kipuuzi”

“Siwajui sana nyinyi, ila kwa kipindi nilicho kaa nanyi nimewajua. Phidaya hembu acha wivu wa kijinga wewe ni mama sasa na ni mtu mzima sasa. Eddy acha kutomb**n** kwa kijinga na kipuuzi wewe hivi sasa ni mtu mzima, ukiachilia mbali kuwa baba tu, wewe ni makamu wa raisi. Kama utashindwa kuiongoza familia yako nchi utaiongoza saa ngapi?”

Maneno makali ya Sa Yoo yakawafanya Phidaya na Eddy kutazamana na kuendelea kukaa kimya.

“Nimesha mueleza Shamsa, upuuzi na ujinga ambao wewe Eddy mulishirikiana kwa pamoja na kuufanya. Haya sasa iwe mwisho. Maswala ya sijui ya kusema kwamba sijui unampenda Shamsa, sijui unamfanyaje mwisho siku hiyo muliyo tomb**n**. Wewe Phidaya najua hawa ndio wamekuchokonoa chokono hadi ukafikia hapo ulipo fikia, kausha sasa, acha mambo yapite na maisha yasonge mbele. Musipo kuwa makini Camila naye atakufa akiwa binti mdogo kabisa na hato ona faida ya kuwa na baba makamu wa raisin a mama siju nikuiteje. Ninawapenda sana, mimi sio Mtanzania, ila Eddy nahitaji uwe baba bora, Phidaya na wewe uwe mama bora. Tumelewana?”

Eddy akatingisha kichwa akiashiria kwamba amemuelewa vizuri Sa Yoo.

“Mimi nimekuelewa Sa Yoo, ila ninaombi moja?”

“Omba”

“Ninakuuomba umuite Shamsa hapa nimkanye juu ya hili analo lifanya na mume wangu, haya sio malipo ambayo anapaswa yeye kunifanyia, ninampenda Eddy ndio maana kwenye kila hatari ya maisha yake mimi ninakuwa karibu yake, na isitoshe tumefunga ndoa kabisa halali ambayo inatambulika na hata yeye alikuwa ni shahidi”

“Hilo halina shida”

Sa Yoo akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Shamsa.

“Yeea”

“Unaweza kushuka huku chini, ukazunguka huku nyuma kwenye bustani?”

“Ndio, ila nimuandalia husband chai”

“Acha hizo mambo njoo sasa hivi”

“Mmmm mboa unanitisha kuna nini?”

“Fanya uje bwana”

“Sawa”

Sa Yoo akakata simu na kuirudisha kwenye mfuko wa suruali yake. Hazikupita hata dakika tatu Shamsa akafika katika hiyo bustani, akamtazama Phidaya kwa macho ya dharau, ila Sa Yoo ili kuipoteza hiyo hali, akavuta moja ya kiti kilicho tengenezwa ka mkeka, kisha kwa ishara akamuomba Shamsa kukaa. Shamsa akajishauri kwa sekunde kadha kisha akaka chini.

“Umeamua kunikalisha kikao na mke mwenza?”

Shamsa alizungumza kwa dharau jambo lililo ibua harisa ya Phidaya upya, laiti kama angekuwa na uwezo wa kusimama kwa wakati kama huu basi angeapambana na Shamsa kuhakikisha kwamba anamfundisha adabu.

***

“Unaonanaje tukaelekea katika himaya ya baba yangu, tukapata msaada mkubwa zaidi kuliko kuelekea Tanzania na helicopter hii”

“Baba yako himaya yake ipo wapi kwa sasa?”

“Ipo nchini Chini, ila ana mako yake mengine inchini Brazil, na tunaweza kufika katika nchi hiyo na ita kuwa ni rahisi kwa sisi kuweza kufanya hata mawasiliano nchini Tanzania na mama yako na tukampatia tahadhari”

Maneno ya Jing kidogo yakaanza kuingia akilini mwa Adrus kwani hakuna namna nyingine zaidi ya kufwata ushauri wa Jing, kwani nchini ya Brazili ndio ipo karibu yao.

“Tuna uwezo wa kutumia masaa mawili hadi kufika nchini Brazili”

“Sawa nimekuelewa”

Taratibu Adrus akabadilisha mkueleko wa helicopter hiyo, na kuanza kueleeka nchini Brazili. Kama walivyo weza kutarajia ndani ya masaa mawili wakatua kwenye moja ya kisiwa kilicho jitenga kidogo na nchi hiyo ya Brazil. Kisiwa hicho kinamilikiwa na baba yake Jing, bwana Lee Sing, na amewekaza katika kiwanda cha utengenezaji wa ndege kubwa na ndogo ndogo.

Kutokana na ulinzi mkali ambao upo katika kisiwa hicho ikamlazimu Jing kuwa mtu wa kwanza kushuka kwenye helicopter hiyo huku akiwa ameinyoosha mikono yake juu. Adrus na Cookie nao wakajamuika na Jing. Walinzi wapatao thelathini walio shikilia bunduki wakawazunguka huku helicopter hiyo ya kijeshi wakiwa wameiweka katikati.

“Ninaitwa Jing Lee Sing. Ni mtoto wa mmiliki wa hii kampuni?”

Walinzi hawakutaka kujiaminisha kiharaka namna hiyo, wakawafunga pingu na moja kwa moja wakawapeleka katika chumba cha mapumziko huku meneja wa kampuni hiyo akifanya mawasiliano na mzee Lee Sing.

Meneja huyo akamueleza mzee Lee Sing, sifa zote za Jing jinsi alivyo.

“Niunganishe naye kwenye skype”

“Sawa”

Meneja huyo akafanya kama alivyo agizwa, akamkabidhi Jing simu yake. Mzee Lee Sing macho yakaanza kumwagika usoni mwake baada ya kumuona mwanye kwa mara nyingine tena, kwani kwa ripoti alizo nazo hadi muda huo ni kwamba ndege ambayo alipanda mwanye ilianguka muda mchache sana mara baada ya kuzungumza naye akiombwa msaasa wa kuwaongezea mafuta kwani ndege walio kuwa wakijitahidi kuiokoa isianguke ilisalia na mafuta machache sana.

“Baba”

“Jing mwanangu upo hai?”

“Ndio baba nipo hai”

“Ohoo asante Mungu”

“Baba naendelea kukusumbua, ninaomba msaada wako”

“Msaada gani mwanangu?”

“Kuna rafiki yangu mpya anaitwa Adrus nilisaidiana naye katika kuhakikisha kwamba ndege ile tunaiokoa salama”

“Upon aye hapo?”

“Ndio baba, kuna mamtatizo ya……”

Jing akakatisha sentensi yake baada ya kumtupia jicho Adrus, aliye fanya ishara ya kutingisha kichewa akimuomba Jing asizungumza chochote.

“Ahaa baba ngoja tutazungumza vizuri, kuna jamnbo ambalo tunahitaji kujadiliana mara moja”

“Sawa mwanangu, mukihitaji msaada wa aina yoyote nipo kwa ajili yenu nitawasaidia”

“Asante sana baba”

Jing akamrudishia meneja huyo mwenye asili ya kizungu, simu yake. Meneja huyo akawaamru walinzi wake kuwafungua pingu. Adrus na Cookie kisha wakatoka nje ya chumba hicho, wakiwaacha waweze kujadili.

“Njing ninacho hitaji kwa hivi sasa ni kuweza kupata simu na kuwasiliana na mama yangu tu, huo ndio msaada wangu wa kwanza ambao ninaweza kukuomba”

“Sawa, je tutampatia vipi usalama au kuna sehemu ambayo anaweza kujificha?”

“Sidhani”

“Baby kwani huna mtu ambaye unamuamini nchini Tanzania?”

Adrus akaka kimya huku akijaribu kuitathimi sirikali yake kuanzia raisi, ila alipo fika kwenye cheo cha makamu wa raisi, kidogo moyo wake ukapaya amani.

“Ninaye ila mmoja ila inabidi niweze kuwasiliana naye?”

“Ni nani?”

“Ni makamu wa raisi?”

“Haaa….Adrus kama raisi alisha toa amri ya wewe kufwanya chochote inakuwaje unamuamini makamu wa raisi?”

“Ninamuamini, kwa kwani hata yeye aniamini, na katika serikali ya sasa maamuzi ya raisi ni maamuzi yake na maamuzi ya makamu wa raisi ni maamuzi yake mwenyewe”

“Sawa tujaribu kuanza na yeye, tusikie anatusaidiaje?”

“Niombee simu”

“Sawa”

Jinga akanyanyuka na kugonga mlango kidogo, ukafunguliwa na akaingia meneja.

“Ninaomba simu yako”

Meneja akamkabidhi Jing simu hiyo.

“Si ina salio la kutosha?”

“Ndio madam?”

“Okay asante”

Jing akakmabidhi Adrus simu hiyo, taratibu Adrus akaanza kuingiza namba za simu ya mkononi ya Eddy, ajajarihbu kuipiga simu hiyo ila akakuta haipo hewani. Akapiga namba ya ofisini kwa mamaku wa raisi, simu ikaita baada ya muda ikapokelewa na sekretari wa ofisi hiyo.

“Ninaitwa bwana Diego deo Santos, mimi ni waziri kililo nchini Braziil nahitaji kuzungumza na makamu wa raisi”

Adrus alizungu na lafudhi ya kibrazili na kumchanganya sekretari huyo alaiye weza kuamini kwamba yeye ni waziri wa sekte hiyo kutoka nchini Brazili.

“Karibu sana muheshimiwa, ninaweza kukusaidia nini?”

“Ninahitaji kuzungumza namakamu wa raisi”

“Okay sawa ninaomba dakika moja niweze kukuunganisha naye”

“Shukrani”

Cookie na Jing wote wakabaki wakitabasamu huku wakimtazama Adrus anaye subiria kuunganishwa na makamu wa raisi.

***

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG