Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 SEHEMU YA 6/10

 

 

AISIIIII.....U KILL ME SEASON 2 

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 6 KATI YA 10

 


 

“Hivi una waaamini sana hawa watu?”

“Asilimia kumi, vipi wewe?”

“Mini hata moja siwaamini, kwa maana sijajua ni kwa nini wamemaua kukubali kuungana nawe kirahisi hivi?”

“Ninawafahamu na wananifahamu, ila kwa watu ambao walipanga kuniangamiza sio rahisi kuwaamini”

“Jamani karibuni”

Waziri mkuu alizungumza kwa sauti ya juu huku akiwa amesimama nje ya mlango wa kijumba chake hichi. Tukaanza kutembea kuelekea walipo huku bunduki zetu tukiwa tumezishika vizuri sana.

Waziri mkuu akafungua mlango na taratibu tukaingia ndani, japo kuna giza kiasi ila mwanga unapita katika sehemu ndogo zenye uwezo.

“Itabidi tushuke huku chini”

Waziri mkuu alizungumza huku akiwasha iliyo tufanya tuweze kuona vizuri eneo hili la ndani mwa hii nyumba. Nyumba hii haina chumba chochote zaidi ya seble yenye viti viwili pamoja meza moja tu. Waziri mkuu akasogeza meza pembeni, Martin akamsaidia kusogeza viti hivyo viwili, akafunua kapeti zito, tukaona malango wa kuingilia chini, waziri mkuu akaufungua mlango huu na tukaonga ngazi zinzo elekea chini.

“Huku ndipo ilipo nyumba yangu”

Waziri mkuu alizungumza huku akianza kushuka chini, nasi tukaanza kumfwata kwa nyuma, akawasha taa iliyo tufanya tuweze kuona eneo zuri lililo pambwa kwa vitu vingi vya thamani.

 

“Kwa nini uliamua kujenga chini ya ardhi?”

Martina alimuuliza waziri mkuu huku akitazama eneo hili la hii seble.

“Nilipenda sana staili ya majengo haya niliipata nchini Ujerumani”

“Sasa walio jenga hivi ni kina nani?”

“Nilichukua mafundi kutoka nchini Ujerumani na wao ndio walio ifanya hii kazi iliwachukua miezi zaidi ya kumi na sita”

“Duuu”

Waziri mkuu akawasha tv kubwa iliyopo hapa sebleni.

“Hapa huduma zote za ndani zipo”

Taratibu Babyanka akakaa kwneye moja sofa huku akiwa ameshika tumbo lake. Nikamsogelea na kuchuchumaa mbele yake.

“Unajisikiaje”

“Tumbo langu kwa hapa linauma kidogo”

Babyanka alinionyesha sehemu ya chini ya kitovu chake.

“Pole. Mzee kuna dawa za kutuliza maumivu?”

“Ndio zipo?”

 

“Ninaomba umpatie Babyanka”

Waziri mkuu akaingia kwenye moja ya chumba na kutuacha hapa sebleni.

“Raisi Donald Bush anakuja saa ngapi Tanzania?”

“Leo saa moja moja hivi atakuwa amesha tua uwanja wa ndege”

“Tunatakiwa kumuangusha leo”

“Kivipi Dany?”

“Tunatakiwa kumuua raisi Donald, mke wake pamoja na K2?”

“Dany umechanganyikiwa, hivi unajua ni ulinzi wa wana usalama wangapi ambao wnaamlinda raisi Donald?”

“Hilo kwangu sio dili, ninacho kihitaji mimi ni kuhakikisha kwamba ninawaua”

“Hivi vitu Dany usichukulie hasira utafeli na wewe peke yako huwezi kukamilisha hilo unalo lihitaji kulikamilisha”

Babyanka alizungumza kwa msisitizo, waziri mkuu akatoka huku akiwa ameshika kisanduku chenye rangi nyeupe huku kikiwa na msalaba mwekundu.

 

“Unasikia maumivu sehemu gani?”

Waziri mkuu alimuuliza Babyanka ambaye akamuonyesha sehemu anayo hisi maumivu. Waziri mkuu akafungua kisanduku hichi na kuto sindano pamoja na kichupa kidogo cha dawa.

“Hii dawa itatuliza maumivu kwa kipindi fulani”

“Kwa muda gani?

“Masaa ishirini na nne hadi sabini na mbili”

“Sawa nichome tu”

“Mkuu”

martin alinita, nikamtazama kwa ishara ya kidole akanionyesha Tv na sote tukajikuta tukiitazama. Tukaona picha zangu na Martin zikitangazwa kwamba sisi ni magaidi tuliopo nchini Tanzania na atakaye fanikisha kukamatwa kwetu basi atazawadiwa dola milio moja sawa na bilioni mbili za Kitanzania. Sote tukakaa kimya huku tukiendelea kumtazama mtangazaji wa tangazo hili.

“Inabidi kumtoa madarakani kinguvu K2 amefanya mengi maovu”

 

Waziri mkuu alizungumza kwa msisitizo jambo lililo nifanya nimtazame kwa macho ya mshangao.

“Umetambua uovu wa raisi wako leo?”

“Kwa mfanyakazi wa kawaida kama mimi unahisi ni rahisi kuweza kufahamu kwamba bosi wangu yeye ndio gaidi?”

“Mimi ninafahamu”

Babyanka alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kalia.

“Una muda gani tangu ufahamu kwamba K2 ni gaidi?”

“Kabla hata hajawa raisi, mimi na Dany ndio watu wa pekee tuliye gundua uovu wake hadi akamuua raisi aliye pita ambaye ni kaka yake hii yote ni kwa uroho wa madaraka”

“Sawa ni kwa nini ukuzungumza kabla hajachukua hii nchi?”

“Unahisi maisha anayo ishi Dany kwa mimi mtoto wa kike ngingeweza kuishi.?”

 

Babyanka alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Waziri mkuu alibaki mdomo wazi lile alilo tamani kulizungumza alijikuta akishindwa kabisa kulizungumza.

“Nilikiongoza hichi kikosi cha NSS kwa amri kutoka kwa K2, na jana usiku kama ingekuwa ni kumkamata Dany ningeweza kumkamata kwa maana nilikuwa ni mtu wa kwanza kumuona tangu wakiwa kwenye fukwe za bahari ila kutokana mulikuwa mupo wawili nilihitaji akamatwe mwenzako ili wewe nije kukutana nawe”

 

“Kwa nini uliamua kunishambulia?”

“Kwa sababu ya waziri mkuu, sikuhitaji afahamu kujua kwangu kitu chochote kuhusiana na wewe”

Mimi na Martin tukatazama kwani maneno ya Babyanka kidogo yanaendana na ukweli ila sina imani naye kwa asilimia zote.

“Tuachane na melezo mengi. Tunahitaji kumuua K2”

“Kwa leo itakuwa ngumu”

“Kwa nini?”

“Walinzi wake wanao mlinda si NSS”

“Ni nani?”

“Kikosi chake cha wasichana wauaji, hao leo ndio wanamlinda”

Babyanka alizungumza huku akinikazia macho usoni mwangu. Wasichana hao ninawafahamu vizuri kwani Livna ndio kiongozi msaidizi.

 

“Kikosi cha wasichana?”

Waziri mkuu aliuliza kwa mshangao huku akimtazama Babyanka.

“Ndio, na kikoasi hichi kiongozi wao anaitwa Livna Livba”

“Nina mjua”

Nilizungumza huku nikimtazama Babyanka

“Yupoje huyo msichana?”

Waziri mkuu aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu

“Chotara fulani hivi”

“Hemb ngoja”

Waziri mkuu akakimbilia ndani kwake kisha akarudi na laptop yake mkononi, akaifungua, akaiwasha na baada ya muda akaanza kuminya minya batani za laptop hiyo kisha taratibu akatugeuzia.

 

“Msichana huyu?”

Waziri mkuu alizungumza huku akituonyesha picha ya Livna. Taratibu Martin akaanza kutembea huku akisogelea laptop ya waziri mkuu, taratibu akachuchumaa na kuitazama vizuri picha ya Livna.

“Martin vipi?”

“Ninamfahamu huyu  msichana”

“Unamfahamu vipi?”

Martin akanigeukia na kunitazama kwa macho ya yaliyo jaa wasiwasi mwingi hata swali langu ambalo nimemuuliza anashindwa kulijibu jambo lililo nifanya nijiulize maswali mengi juu ya hili.

“Martin mbona kimya?”

“Huyu msichana ni mke wangu wa ndoa”

Nikabaki nikimshangaa Martin kwani kwa kipindi chote ambacho nimeweza kumfahamu hajawahi kunieleza kwamba alisha wahi kuoa msichana yoyote isitoshe huyo msichana wake nillisha wahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi miaka kadhaa nyuma.



“Mke wako wa ndoa!!?”   

Nilimuuliza Martin huku nikimshangaa usoni mwake.

“Ndio nimemuoa miaka miwili iliyo pita, ila tulikuja kutengena”

“Kutengena kwa sababu gani?”

“Aligundua kwamba nipo katika kikosi cha Boko Haramu”

“Yeye alikuwa anafanya kazi gani?”

“Yeye alikuwa ni mwana chuo cha ualimu pale Lagos”

“Basi sio mwanachuo ni gaidi, tena gaidi kukushinda hata wewe, na ili tumpate K2 ni lazima kumpata Livna la sivyo hatutafanikiwa”

 

Nilizungumza huku  nikikaa kwenye moja ya sofa.

“Mimi ninajua jinsi ya kumpata”

Martin alizungumza huku akinitazama.

“Tutampataje?”

“Kama yupo Dar es Salaam ni lazima turudi Dar es Salaam”

“Dar ulinzi ni mkali kijana na kitendo cha kurudi ni lazima mutakamatwa na watanzania jinsi walivyo na njaa unahisi hiyo dola milioni moja watashindwa kutoboa siri pale watakapo waona?”

“Nitaenda nao, nitaweza kuwakinga pale nitakapo kutana na vizuizi”

 

“Kitambulisho chako unacho?”

“Ndio ninancho”

“Kama unacho unaweza kwenda nao”

“Wewe utakaa hapa?”

“Ndio sihitaji kurudi Dar es Salaam kwa sasa, nahitaji kupanga mipango ya kumpindua K2”

“Mipango hiyo utaipanga wewe mwenyewe?”

“Hapana ninategemea msaada wenu pia nitawawezesha huko muendapo kukutana na watu ambao  wanaweza kuwasaidia”

“Kwa mimi sihitaji mtu wa kutusaidia”

Nilizungumza huku nikimtazama waziri mkuu usoni mwake.

“Kwa nini?”

“Simuamini mtu hata wewe sikuamini mzee wangu, hii oparesheni nitaiendsha mimi na kijana wangu.”

Maneno yangu yakamFanya waziri mkuu kukaa kimya.

“Tutaondoka saa ngapi hapa mkuu”

Martin aliniuliza.

“Saa kumi na mbili jioni tutaianza safari kama kuna chakula mzee tunahitaji kuandaa”

“Njoo huku”

Waziri mkuu alizungumza huku akisimama, taratibu tukaingia kwenye moja ya chumba.

“Hapa ndio jikoni huwa marehemu mke wangu alikuwa anapenda sana kupatumia kupika pika vyakula vyake tukija mapumzikoni huku”

“Ninaweza kukuamini?”

“Unasema?”

“Mzee ninaweza kukuamini kama mwanao alivyo jitunza katika kuilinda bikra yake?”

Waziri mkuu  alinitazama usoni mwangu huku akinitumbulia macho.

 

“Ina maana umemtoa mwanangu usichana wake?”

“Ila ulisha wahi kuniambia hicho kitu “

“Kwamba?”

“Mwanao bado ni bikra, nihakikishe ninaitoa au umesahau”

“Wewe mwana haramu unadhani mwanangu anaweze kuishi na mwanaume kama wewe unaye tafutwa kila kona?”

“Analitambu hilo na nilimtahadharisha ila alikubaliana nami”

Waziri mkuu akatoa mchele kwenye moja ya droo ya kabati kubwa lililopo humu ndani.

“Hiyo si pete ya ndoa?”

“Ndio”

“Umeoa?”

“Ndio maana nimeivaa”

“Hakikisha mwanangu unamtoa mikononi mwa K2, na baada ya hapo ninakuomba uachane naye kabisa, sinto hitaji umuumize moyo kwa mambo ya kihuni huni sawa”

Waziri mkuu alizungumza kwa msisitizo huku  akiwanikazia macho.

“Mzee acha hasira mambo mengine hayahitaji hasira”

“Hapa ninazungumzia kuhusiana na mwanangu, kwenye hilo swala ni lazima niwe na hasira”

 

“Haya nimekuelewa mkuu”

Tukasaidia na waziri mkuu hadi tukamaliza kupika wali  maharage. Tukaandaa chakula hichi na kurudi nacho sebleni na kuwakuta Martin na Babyanka wakizungumza kwa kucheka sana wakionekana kuzoeana sana.

“Jamani nimeshindwa hata kuja kuwasaidia ikiwa mimi ndio mwanamek niliyopo humu ndani”

“Usijali tumesha korofisha msosi. Kuna jipya lolote lililo tangazwa kuhisiana na kupotea kwenu?”

“Mimi na waziri mkuu?”

“Ndio?”

 

“Hapana ila nyinyi ndio munatafutwa kila dakika mutatangazwa”

“Je simu umepigiwa?”

“Hapana simu nimeifunga na si rahisi kwa mtu kuweza kunipata hewani ila mimi ndio ninaweza kumpigia simu mtu”

“Poa”

Tukaaanza kula chakula hichi tulicho kiweka kwenye sinia kubwa. Hatukuchukua muda mwingi tukamaliza kula chakula. Waziri mkuu akaanza kutuchorea ranami na barabara ya kutokea huku shamhbani kwake kwani hata mimi siikumbuki vizuri. Akatupatia namba yake ya siri ambayoa naitumia huku porini. Tukaanza kuzishuhulikia silaha zilizopo kwenye begii kwa kuzisafisha na kuzipanga vizuri kwa ajili ya kazi ambayo tunaiendea mbele yetu.

“Dany hakikisha kwamba unampata Lucy na kunirudi naye huku porini”

 

“Sawa mzee”

“Niwatakie safari njema, na kazi njema na nina imani kwamba baada ya maasaa machache ninaweza kupata habari nzuri”

“Usijali nina imani  utakwenda kuwa raisi ajaye”

Nilizungumza kwa utani na kumfanya waziri mkuu kucheka kidogo kisha akatupa mikono ya kutuaga. Nikazichomeaka kiunoni bastola zangu mbili ambazo zina risasi za kutosha, kisha bunduki yangu kubwa nikaishika vizuri. Martin akabeba begi lenye silaha na tukaanza kutoka humu ndani. Waziri mkuu akatusindikiza hadi lilipo gari.

“Jamani umakini ndio kitu cha muhimu. Tumieni ujuzi wenu wote kuhakikisha kwamba munamuangusha K2 na nina imani kwamba mutaweka historia kubwa kwenye hii nchi”

“Shukrani mzee”

Tukaingia kwenye gari huku Babyanka akiwa amekaas iti ya mbele. Taratibu nikawasha gari na kuanza kuondoka hili eneo. Sikuweza kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kutokana na kuwangalia angalia barabara hiii ambayo kusema kweli inachanganya.

“Jamani haya maharage yananipa usingizi”

Martin alizungumza huku akijinyoosha viongo vya mwili wake.

 

“Pole sana, lala tukifika barabarani nitakustua”

“Asante mkuu”

Safari ikazidi kusonga mbele huku  kazi ya Babyanka ni kunisomea ramani ya kutokea kwenye huu msitu. Hadi inatimi saa mbili usiku tukafnikiwa kutoka katika huu msitu na kuingia kwenye barabara ya lami. Safari ya kuelekea Dar es Salaam ikaanza.

“Dany”

“Naam”

“Uumeoa?”

Babyanka alizungumza huku akinitazama kidole cha upande wa kushoto cha mkono wangu wa kushoto.

 

“Ndio nimeoa”

“Mke wako yupo wapi?”

“Nigeria”

“Ahanafahamu uwepo wako huku Tanzania?”

“Ndio japo tumetengana kwa sasa”

“Kisa nini?”

“Maisha ya hapa na pale”

“Pole”

“Asante. Vipi wewe?”

“Nilibahatika kupata mtoto mmoja wa kike ila alifariki akiwa na miaka miwili”

“Ohoo pole aisee”

“Asante”

“Alifariki na nini?”

“Malaria ilichangia sana kifo chake”

“Pole sana”

“Kuna ukaguzi hapo punguza mwendo”

Nikatazama mbele nikaona kizuizi cha jeshi la polisi. Taratibu nikapunguza mwendo kasi wa gari. 

 

“Martin”

“Mmmmm”

“Amka jiweka sawa”

“Tumefika barabarani?”

“Muda mwingi sana”

Askari aliye valia koti jeupe alitusimamisha, taratibu nikasimamisha gari pembeni, sikushusha kioo upande wangu ila Babyanka aliweza kushusha.

“Njoo huku”

Babyanka alizungumza na kumfanya askari huyo kuzunguka upande alipo yeye, nikatazaama askari wengine waliopo kando kando ya barabara huku wameshika bundiki zao aina ya SMG.

“Habari yako”

Babyanka alizungumza huku akimtazama askari huyu.

“Salama, ninaomba vitambulisho vyeni”

Babyanka akatoa kitambulisho chake, nikamuona askari mmoja akilikagua gari letu akafika katika upande wa kioo changu, taratibu akagonga dirisha taratibu na kuniomba nifungue.

“Mkuu waambie dereva wako afungue kioo”

“Kwani kuna tatizo?”

 

“Tupo kwenye msako mkali wa kuwatafuta magaidi wawili hatari sana”

“Sasa mimi mwenyewe na kitengo changu cha NSS, tupo kwenye mpango wa kuwatafuta hao magaidi, kama umeona kitambulisho changu basi turuhusu tuondoke unatupotezea muda”

Babyanka  alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama askari huyu.

“Mmkuu”

Askari huyu alimuita mkuu wake aliyopo pembezoni mwa barabara upande wa pili.

“Mart”

“Ndio”

“Umakini”

“Sawa mkuu”

 

Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikianza kuivuta taratibu bunduki yangu iliyopo pembeni yangu. Tukamuona mzee mmoja akija kwa mwendo wa haraka, akafika sehemu alipo askari wake, akamkabidhi kitambulisho cha Babyanka, mkuu huyo akatazama kitambulisho hicho kwa sekunde kadhaa, kisha akatoa simu yake mfukoni mwake na kuanza kiminya minya batani zake.

“Mkuu unataka kufanya nini?”

Babyanka alizungumza huku akimtazama kuu huyu wa polisi, ila cha ajabu mkuu huyu wa polisi ndio kwanza akasogea mbali kidogo na gari. Nikaminya batani maalumu ya kutoa ‘lock’ za milango, mlio wa lock za milango kufunguka ikawa ishara tosha kwa Martin kuelewa ni kitu gani kinacho takiwa kufanyika kwa wakati huu. 

 

Tukafungua milango ya gari na kushuka kwa kasi na kuanza kuwashambulia askari wote walio shika bunduki. Shambulizi letu halikuchukua hata dakika mbili tukawa tumewashambulia askari wote wenye silaha na kumbakisha mkuu wao aliye pata kiwewe na bumbuwazi kubwa huku simu yake akiwa bado ameishika mkononi mwake.

“Chukau simu yake”

Nilizungumza na kumfanya Martin kumpokonya mzee huyu simu yake akaikuta ipo hewani, nikaitazama jina la namba aliyo ipigia simu nikakuta jina lililo andikwa  ‘mke wangu’. Nikaminya batani ya kukata simu na kumtazama vizuri mzee huyu.

 

“Dany kwa nini mumewaua hawa?”

Babyanka alizungumza huku akishuka kwenye gari kwani hata hili shambulizi wala hakuhusina na kipindi linaendelea nina imani alikuwa anashangaa shangaa.

“Mzee amewaponza wenzake”

“Ulikuwa unazungumza na nani mzee?”

“Mmmm, mke wangu”

“Hembu simu”

Babyanka alizungumza huku akiichukua simu niliyo ishika, akaanza kuikagua. Nikaona sura ya Babyanka ikibadilika kidogo akionekana kama ana wasiwasi.

“Vipi?”

“Mzee ulikuwa unazungumza na mke wako kweli?”

“Ndio”

“Raisi ni mke wako?”

Babyanka alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama mzee huyu. Hata kabla mzee huyu hajajibu kitu chochote simu yake ikaita na Babyanka akanigeuzia simu hiyo na kuiona namba aliyo  kuwa anazungumza nayo mkuu huyu wa polisi, taratibu nikaichukua simu hii na kuipokea.

 

“Mume wangu”

Sauti ya K2 ikanifanya nimgeukie mzee huyu na taratibu nikasimama mbele yake.

“Sikuhizi umeanzisha mahusiano hadi na wazee?”

“DAANY?”

“Waziri mkuu, na mkuu wa NSS hukuona thamani yao hata  nikiwaua kwako ilikuwa ni POA tuu, sasa huyu mume wako nitamuua kama nilivyo fanya kwa waziri mkuu wako”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiichomoa bastola yangu moja kiunoni mwangu na kuielekeza kwenye kichwa cha mzee huyu aliye zidi kutetemeka hadi mikojo ikaanza kulowanisha suruali yake.

 

“Dany Dany ninakuomba, ninakuomba mpenzi wangu usimuue huyo mwanaumee tafadhalii…………………!!”

K2 alizungumza kwa sauti iliyo jaa woga na majonzi hapa ndipo nikagundua udhaifu wa K2 upo kwa huyu mkuu wa polisi ambaye kwa muonekano wa nje ni mbaya mbaya tu na sijui amempa nini K2 hadi leo hii analia kwa ajili yake.


“Hahaaaa muheshimiwa raisi unaniitaje mimi leo?” “Dany nipo na wageni ninakuomba hili swala tulizungumze wawili nipo tayari kuonana na wewe na niambie chochote nitafanya tafadhali Dany” K2 alizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi na kunibembeleza sana.

‘Huu ni mtego’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama mzee huyu.

“Utaniambia muda na wapi tunaweza kuonana ila una lisaa moja mbele. Andaa sanda yako kwani sinto kwenda kukuacha hai” Nikasikia mihemo ya K2 jinsi anavyo ishusha kwenye simu yake.

“Naomba masaa mawili” “Basi utaongeza hili. Hakikisha kwamba unatangaza kujiudhuru hadharani ili nikikuua ufe kama K2 na si raisi K2”

“Sawa Dany nimekuelewa” Nikata simu na kumtazama mzee huyu.

“Mfunge pingu na tuondoke” “Sawa mkuu”

“Hakikisha unawavua askari watatu nguo zao, zitatusaidia” “Usijali mkuu” Nikaanza kurudi kwenye gari, nikafungua mlango na kuingia kwenye gari, Babyanka akaingia ndani ya gari huku akishusha pumzi nyingi.

“Hatuna raisi kwa kweli” “Mulimchagua kwa kura zenu” “Amesemaje?” “Nimemuambia kwamba atafute sehemu tuonane na nimemuomba masaa mawili ili tuweze kuonana” “Hivi unahisi kwamba K2 ni mjinga wa kukubali kuonana nawe kirahisi namna hiyo?” “Nimemuambia atangaze kujiudhuru nafasi ya raisi ndani ya masaa mawili ya jayo, pasipo kufanya hivyo huyu mzee nina muua” Nilizungumza huku tukiondoka eneo hili kwa kasi sana, kwani hatuna tulicho kibakisha.

“K2 umeanza naye mahisiano lini ikiwa ana mume wake?” Nilimuuliza mzee huyu huku nikizidi kuongeza mwendo kasi wa gari hili.

“N…….ii..i.i.i aa…aaal….i….li…taka” “Zungumza vizuri wewe” Martin alizungumza kwa ukali huku akimtandika ngumi ya mbavu mkuu huyu wa polisi na kumfanya atoe kilio cha maumivu makali sana.

“Alinitaka yeye mwenyewee”

“Umempa nini hadi ana kupapatikia hivi, au ulimla mkund***?” “Weee Dany swali gani hilo?” “Babyanka unashangaa kwa raisi wako kufanya mapenzi kinyume na maumbile?” “Wewe umejuaje?” “Tuachane na hayo” “Au na wewe umesha mla kwa maana kipindi kile nilikuwa siwaelewi elewi”

“Tunaelekea wapi Babyanka tuachane na hayo mazungumzo” “Kwanza zima simu ya huyo mzee toa laini na itupe la sivyo kufwatiliwa ni lazima” Nikamkabidhi Babyanka simu yam zee huyu, akatoa betri pamoja na laini kisha akaitupa. Kunja kushoto” Babyanka alizungumza na kunifanya nipunguze mwendo kasi wa gari na kukunja kushoto.

“Tunaelekea wapi?” “Tukipite barabara hii kukamatwa ni lazima” “Sawa” Tukazidi kusonga mbele huku tukihakikisha kwamba tunaweza kufika jijini Dar es Salaam pasipo kukamatwa na mtu yoyote.

“Kuna rafiki yangu maeneo ya hapo Tegeta inabidi tufike kwake” “Anafanya kazi gani?” “Alikuwa NSS, ila alikuja kuacha na kuunda kikosi chake cha ulinzi”

“Ulinzi gani?” “Hawa walinzi walnao linda kwneye makampuni binafsu” Babyanka alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni, akaminya minya batani na kumpigia rafiki yake huyo.

“Winy upo wapi mama?” “Nipo karibu na getini kwako” “Sawa dakika moja tu nitakuwa hapo” Babyanka alizungumza kisha akakata simu

“Utasimama kwenye nyumba ile pale” Taratibu nikapunguza mwendo kasi wa gari hadi kwenye geti la jumba hili la kifahari, nikasimama getini taratibu geti hili kubwa likafunguliwa, nikaingiza gari hili ndani na kulisimamisha nyuma ya gari jengine.

“Nisubirini” Babyanka alizungumza huku akishuka kwenye gari hili. Akazungumza na dada mmoja mrefu mweusi kiasi na ana umbo jembaba kidogo. Taratibu nigemgeukia mzee huyu aliye kaa siti ya nyuma na Martin. Nikamtazama vizuri kuanzia usoni mwake hadi kifuania mwake, kisha nikajikuta nikitabasamu.

“Mzee una nifahamu mimi?” Mzee huyu akatingisha kichwa akionyesha kunifahamu.

“Unanifahamu mimi kama nani?” “Ehee?” “Mzee wangu unaelewa maswali yangu mbona unajifanya huelewi” Kabla mzee huyu kunijibu kitu chochote Babyanka akagonga kidogo kioo cha upande wangu, taratibu nikashuha kioo.

“Unaweza kushuka” Taratibu nikashuka, dada huyu alipo nitazama akaonekena kushangaa sana.

“Ulihisi ninakutania Winy” “Yaa nilihisi unanitania kwa manaa wewe ndio ulikuwa unaongoza jaramba la kumkamata Dany ila leo hii upon aye yaani siamini” “Ndio uamini. Dany huyu ni rafiki yangu wa damu kabisa, anaitwa Winy. Winy huyu ni Dany” “Nashukuru kukufahamu Dany” Winy alizungumza kwa furaha huku akinipa mkono, taratibu nikaupokea mkono wake huku nikiutingisha kidogo.

“Asante Winy” “Yupo na kijana wake pamoja na fala mmoja hivi tumemkamata njiani” “Waambie washuke” Nikaonyesha ishara ambayo nina imani kwamba Martin anaifahamu, akashuka kwenye gari huku bunduki yake akiwa ameishia vizuri. Akatufwata shehemu tulipo akasalimiana na Winy, kisha akafungua mlango na kumtoa mkuu wa Polisi.

“Wewe fala ulihisi sinto kupata eheee?” Winy alizungumza huku akianza kumfwata mzee huyu jambo lililo tushangaza wote hapa. Akamsukumia mkuu wa polisi kwenye gari huku akilikunja shati la mzee huyu maeneo ya kifuani mwake.

“Ulihisi sinto kupata mjinga wewe” “Vipi shosti?” “Huyu mzee jana amemlaza ndani mdogo wangu, na akakataa asitolewe dhamana” “Kwa nini usiniambie?” “Nilijaribu kukupigia sikukupata hewani” Winy akamtandika makofi mawali mazito mzee huyu hadi machozi yakaanza kumlenga lenga.

“Sasa leo umeingia mikononi mwangu, utaona sasa kama humu utatoka kwa dhamana” “Huyu dada anaonekana na ni mbabe?” Martin alizungumza kwa sauti ya chini chini huku tukimtazama Winy.

“Anaonekana hapendi ujinga” “Ila yupo vizuri” “Umemtamani nini?” “Yaa ingekuwa sio haya matatizo ningemtokea” “Acha uhuni, tufanye kazi” “Sawa bosi” “Jamani samahani kwa kuweza kumshuhulikia mtu wenu ila kwa upande wangu pia ni mtu ambaye nina muwinda” “Usijali” “Kuna chumba tunaweza kumfungia” “Martin chukua uangalizi wa hilo” “Sawa” Martin akamshika mzee huyu na kuanza kuongozana na Winy, wakazunguka nyuma ya jumba hili. Baada ya dakika kadhaa Martin na Winy wakarudi sehemu walipo tuacha mimi na Babyanka, akatukaribisha ndani.

“Karibuni kwangu jamani, japo kupo kimya ila karibuni sana” “Unaishi peke yako hapa?” “Nipo na mdogo wangu wa kiume ambaye kwa sasa yupo polisi kwa ajili ya huyo mjinga muliye kuja” “Shukrani” “Eheee nielezeni mipango yenu kwa maana nina hamu ya kurudi kwenye game, kwa maana ni siku nyingi sijaua mtu” “Shosti mbona una haraka” “Yaani ulivyo niambia kwamba umekuja na Dany, kisim** changu kimenicheza yaani nikiua mtu nyeg** zeto huwa zinaniisha” Tukabaki tukitazamana na Martin kwa mshangao.

“Jamani musinione ninazungumza sana ila huo ndio ukweli”

“Mumzoee ndio alivyo” “Sawa” Nikaanza kumuelezea Winy mpango wa kumuua K2 na kwa sasa nisubiria hotuba yake kwenye Tv ya kujiudhuru, kisha nionane naye.

“K2 hawezi kufanya hivyo hata siku moja” “Ninatambua ila mwanaume tuliye mshika ni kama roho yake” “Roho ya K2 sio huyo mwanume, na atamtumia mwanaume huyo kukua. K2 ana watu ana jeshi, ana mazagazaga ya kila aina” Winy alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. “Dany nilikuambia kwamba K2 hawezi kujisalimisha kwa ajili ya huyo mkuu wapolisi. Ameigiza kupagawa ili mradi uingie kwenye kumi na nane zake kwa maana kila kitu ambacho amekifanya amekukosa” “Mkuu hapo ninashauri tungekaa kwa muda, K2 asipo jiudhuru basi mpango umefeli na huyu mzee tunamuua kama tulivyo waua askari wake”

“Sawa, ila kuna watu bado nipo nao kichwani?” “Kama nani?” “Hawa na raisi Donald Bush” “Unataka kumuua Donald Bush!!!?”

Winy alizungumza huku akinishangaa kwani mtu ninaye mzungumzia analindwa zaidi ya anavyo lindwa K2. “Ndio” “Mmmmm Dany una kazi wewe” “Huo ndio mpango ulio nileta Tanzania, baada ya hapo nitaondoka Tanzania na hata nikifa basi nitakuwa sija jinsi na nitakufa kihaki”

“Winy unatambua kwamba Donald Bush atalala wapi?” “Hapana sijafahamu bado, ila ngoja nimuulize mtu” “Sawa” Winy akachukua simu yake iliyopo kwenye meza ya Tv, akampigia mtu anaye hitaji kuzungumza naye.

“Baby” “Nimekumis jamani” “Ohoo ndio munampeleka raisi Donald hotelini?” “Hoteli gani?” “Ahaa baada ya hapo?” “Hadi dhihara yake iishe?” “Mmmm haya jamani mpenzi wangu, hapa kum** yangu inahitaji mb** yako tu” “Nakupenda mume wangu” “Kazi njema. Mwaaaaa” Winy akakata simu huku akiachia msunyo mkali sana na kuing’ong’a simu yake.

“Mijiwanaume mingine ni usalama wataifa ila mijimbea kama nini” “Kwa nini?” “Alikuwa na haja gani ya kuniambia kwamba wanampeleka raisi Serea Hoteli” “Amesaidia kutufahamisha” “Yaaa. Ehee mutaingiaje Serena kwa maana inalindwa kuliko hata ikulu?”

Sote tukaka kimya huku tukitazamana kwa maana hili jambo ni gumu sana.

“Tanzania hivi hakuna njia za chini ya ardhi?”

Martin alituuliza hukua kitutazama kwenye nyuso zetu.

“Barabara za chini hakuna” Winy akawahi kujibu maswali.

“Hapana sio barabara za chini, anamaanisha mabomba makubwa nayayo pitisha maji machafu” “Hayo yapo, tena tukitumia mabomba hayo tutafika Serena Hoteli pasipo wasiwasi wa aina yoyote.”

Babyanka alizungumza kwa msitizo. Kabla ya mtu yoyote kuzungumza kitu chochotea, taarifa ya dharura(Breaking News) ikakatisha mziki unao onekana kwenye chanel ya Tv kubwa iliyopo humu sebleni. Macho yangu yalipo muona raisi K2 amesimama kwenye sehemu maalumu ya raisi anayo hutubia taifa kupitia vyombo vya habari ikanifanya taratibu kuichukua rimoti iliyopo mezani na kuongeza sauti kwenye hii Tv ili niweze kusikia kwa kile ambacho K2 anakwenda kukizungumza kwa taifa la Tanzania kwa maana nilimpa chaguo la kuachia madaraka kama vile alivyo nipa chaguo hilo mimi kipindi nilipo kuwa jeneral katika kundi la kigaidi la Boko Haramu.



“Habari zenu Watanzania, matumaini yangu ninaimani kwamba mutakuwa muwazima buheri wa afya. Tumeweza kumpokea raisi wa Marekanai kwa shangwe na vifijo nina imani kwamba ziara yake ya siku mbili hizi kwetu itakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa letu”

K2 akakaa kimya huku akionekana kutafakari kitu. Sote sebleni tukabaki tukiwa kimya huku tukimtazama K2 kupitia hii Tv.

“Tunashukuru Mungu, kwamba ulinzi umezidi kuimarishwa katika meeno yote ya nchi. Na nikiwa kama raisi wa Tanzania nitahakikisha kwamba ninamkamata huyu gaidi Dany. Ninaini kwamba kabla ya kupambazuka nitakuwa nimemshika mikononi mwangu. Ninacho waomba Watanzania ni kuhakikisha munatoa taarifa ya kupatikana kwa Dany kupitia simu namba 0657072588. Nasi jeshi langu nitahakikisha kwamba tunafika sehemu ya tukio na kumkamata Dany, kwa maana hatuwezi kuona mtu mmoja anasumbua serikali hii ikiwa, nchi yetu ni nchi ya amani na upendo.”

Nikazima Tv na kuwageukia wezangu, wote macho yao yapo usoni mwangu kwani kile nilicho kuwa nimekitegemea ni tofauti na hichi ninacho kiona hapa.

“Nilisema” Winy alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Mkuu ni nini tutafanya ikiwa muhusika bado anaamini nguvu aliyo nayo inaweza kutuangusha.” “Muacheni kwanza” Babyanka alizungumza baada ya kuniona nimekodoa macho yangu sehemu moja hata pasipo kuzungusha sura yangu. Kila ninacho kifikiria akilini mwangu ninaona hakifai kabisa.

“Ninawazo” Winy alizungumza, na kunifanya taratibu nimtazame huku nikiwa sina matumaini ya kufanya chochote kwa wakati huu.

“Munaonaje tukafanya pigo kwa K2” “Pigo gani?” “K2 ukiachilia huyu mzee, ila ana mtoto wake” “Unahisi mtoto wake ni rahisi kumpata kwa muda huu?” Babyanka alizungumza huku akimtazama Babyanka.

“Hata kwa siku zijazo?” “Unahisi siku zote hizo tutaendelea kuwa huru kama sasa hivi?” “Hapa kwangu kupo salama, hakuna anaye weza kuwakamata” “Mkuu niruhusu nimchinje yule mzee” Macho yakanitoka na kubaki nikiwa nimemtazama Martin.

“Kumchinja!!?” Babyanka akauliza naye akiwa ameshikwa na bumbuwazi.

“Ndio, anamuita gaidi bosi wangu, ili aone kwamba sisi ni magaidi kichwa cha huyu mzee inabidi kipelekwe kama zawadi kwake. Jinsi atakavyo kasirika sisi kwetu ndio itakuwa ni udhaifu mkubwa wa kuweza kumpata kirahisi” “Ila swala la kuchinja jamani hilo ni kubwa?” “Hilo nitalifanya mimi mwenyewe kama bosi ataniruhusu” “Dany zungumza kitu?” Babyanka aliniambia kwani muda wote nilibaki kimya huku nikimtazama usoni mwake kwani muda wote nimeshindwa kuzungumza chochote.

“Mchinje” “Dany!!!!” “Ndio fanya hivyo Martin na kichwa chake niletee hapa” “Hilo ni jambo jema. Usiogope Babyanka” Winy alizungumza huku akitoka sebleni hapa na Martin na kutuacha mimi na Babyanka.

“Dany hili munalo taka kulifanya litazidi kuhatarisha usalama wako” “Unahisi nipo salama?” “Najua haupo salama ila…..” “Ila nini, hivi unatambua ni jinsi familia yangu ilivyo kufa?” Babyanka akaka kimya huku akinitazama usoni mwangu.

“Aliwaua watu wa karibu yangu kwa kuwachinja sasa na mimi nitawaua watu anao wapenda kwa kuwachinja” Nilizungumza huku nikiiwasha Tv, sikukuta hotuba ya raisi tena zaidi ya vipindi vingine kuendelea kwenye hii Tv.

“Dany” Nikamgeukia Babyanka na kumtazama usoni mwake.

“Una, una…..una….” “Nina nini?” “Bado unanipenda?” Tartibu nikajikuta nikiyafumba macho yangu kisha taratibu nikayafumbua na kumtazama vizuri Babyanka.

“Sina hisia za mapenzi moyoni mwangu” Kabla Babyanka hajazungumza kitu chochote Martin na Winy wakaingia huku wakiwa na boksi kubwa. Walilo lizungushia mfuko wa rambo, wakaliweka mezani, taratibu nikalisogelea boksi hili na kulitazama vizuri. Japo mimi ninaroho ya kikatili na swala la kumuua mtu ni kawaida, ila kusema kweli kwa hichi walicho kifanya kwa huyu mzee ni ukatili ulio pitiliza kwani kichwa chake wakekichinja kama kuku aliye chinjwa, ila kilicho nizidisha kuniogopesa ni jinsi walivyo kikata kata kwa kitu chenye makali makubwa.

“Mbona mume mkata kata hivi?” “Aliteta tabu ikabidi nimtandike mapanga kadhaa kichwani” Winy alijibu kwa kujiamini sana, hadi mwili ukanisisimka kwa woga mkali. Babynka wala hakuhitaji kuusogelea hili boksi.

“Haya tutalifikisha vipi kwa muhusika?” “Tutalipeleka mkuu” “Ikulu!!?” “Hapana sio ikulu, hapa cha kufanya ni kupiga simu kwenye namba husika aliyo itangaza K2 kisha tutajidai kama tumekuona kwenye eneo tutakalo hilo eneo sasa hapo utaandika ujumbe ambao wewe utamfikia K2 huko alipo” Nikamtazama Martin jinsi anavyo zungumza kisha nikatingisha kichwa changu kwa kukubaliana naye.

“Naomba karatasi” Winy akachuka moja ya daftari na kalamu vilivyopo kwenye moja ya meza yenye computer ndogo kisha akanikabidhi. Nikachana moja ya karatasi kwenye hili daftari kisha taratibu nikaka kwenye sofa na kuanza kufikiria cha kuandika.

“Mkuu acha tujiandae kuna zile nguo za polisi naamini zitatusaidia” “Sawa” Martin na Winy wakatoka sebleni hapa.

‘HUU NI MWANZO TU, HUWEZI KUNIUA HADI NIHAKIKISHE NINAKUA, ILA USIPO ANGALIA WATU WAKO WOTE WAKARIBU YAKO WATAKUFA KIFO KAMA HICHI. DANY’

Baada ya kuyaandika maneno hayo nikasimama na kuikunja taratibu karatasi yenye maandishi, taratibu nikalisogelea boksi lenye kichwa cha mume wa K2 kisha nikaidumbukiza huku nikiwa nimeikunja vizuri sana.

Winy na Martin wakarudi wakiwa wamevalia mavazi ya askri ambao tuliwaua.

“Ila yana damu ila yataufaa hivi hivi” Winy alizungumza huku akinitazama.

“Mwili wake mumeuweka wapi?” “Mwili wake upo kule kule stoo” “Twende tukauone” Nilumuambia Martin, lengo la kutoka sebleni hapa si kwenda kuuona mwili huo pekee, ila lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba ninazungumza na Martin juu ya huu mpango. Tukaiingia kwenye chumba alichokuwa ameingizwa mkuu wa polisi. Nikaukuta mwili wake ikiwa imelazwa chini huku damu nyingu zikiwa zimesambaa kwenye sakafu. “Unatakiwa kuwa makini na huyu mwanamke” “Sawa mkuu” “Tusimuamini moja kwa moja, ikiawa hatujui ni wapi tulipo tokea, na amekubali kirahisi rahisi kuingia kwenye huu mpango. Ukiona anaenenda kinyume nasi muue” “Usijali mkuu nitalifanya hilo” “Kitu kingine kama ni mtu anaye elekeweka hakikisha unaosha rungu ili asiondoke mikononi mwetu” “Nionshe rungu kivipi?” “Mtomb** hadi apagawe, udhaifu wake huyu msichana nilio uona kwake ndio huo” “Sawa mkuu nitahakikisha ninampa mambo ya kina Jonyyyy” Martina alizungumza huku akiwa ametabasamu kwa furaha kubwa sana.

“Hakikisha humpi nafasi ya kuwa mbali nawe, kosa moja ua asirudie kosa jengine itatugarimu na wakikukamata sasa hivi watakua, hawato kupa hata nafasi ya kukuhoji kwani tayari umesha kuwa most wanted kama mimi” Nilizungumza kwa sauti ya chini sana huku nikimtazama Martin machoni mwake.

“Sawa mkuu” Tukatoka ndani ya chumba hichi na kurudi sebleni na kuwakuta Babyanka na Winy wakiwa wanelekezana kitu kwenye hii computer iliyopo hapa sebleni.

“Tayari bibie tuondoke”

“Ngoja ninamuelekeza Babyanka jinsi ya kuweza kutuona kila tunapo kwenda kupitia satelaiti” “Haito kuwa hatari kwetu?” “Hapana, pia katika hichi kichwa nimechokea kifaa ambacho tutaweza kukiona kila kitakapo kwenda” “Babyanka unaweza kufanya hayo mambo?” “Ndio japo sio sana” “Sawa” Winy na Babyanka wakaelekezana kwa muda kidogo walipo hakikisha kwamba wamemaliza. Martin na Winy wakatuaga na kuondoka huku kila mmoja akiwa ana silaha yake, huku Martin akiwa amelibeba boksi lenye kichwa cha mume wa K2. Nimsogela Babynka alipo kaa, nikatazama anacho kifanya kwenye hii computer, tukawaona Winy na Martina wakingia kwenye gari jengine linalo milikiwa na Winy ana kuondoka katika hili eneo.

“Unahisi huu mpango utafanikiwa?” “Mbona unakuwa na mashaka sana Babyanka upo nasi au haupo nasi?” Ilinibid kuzungumza kwa ukali huku nikimtazama Babyanka machoni mwake. Taratibu Babyanka akasogeza kiti chake cha matairi alicho kikalia, akasimama mbele yangu huku akinitazama kwa macho malegevu.

“Nina mashaka na wewe Dany, sihitaji kukupoteza kama nilivyo kuacha mara ya kwanza ulivyo potea” “Tupo katika kazi mapenzi tuyaweke kando kwanza, tazama wanapo elekea wezetu”

Babyanka akanibusu mdomoni mwangu kisha akarudi na kukaa kwenye kiti. Tukazidi kulifwatilia gari walilopanda Winy na Martin hadi wakafika katika daraja la Sarenda. Wakasimamisha gari pembeni, na Winy akashuka kwenye hili gari, taratibu akashuka hadi chini ya daraja na kuweka boksi hili na kwa haraka akrudi kwenye gari.

“Wanafanyaje?” “Ninahisi watakuwa wanazungumza na simu” “Hembu vuta hiyo video karibu” Babyanka akafanya hivyo na taratibu video ikaanza kuwajia karibu hadi tukamuona Winy akizungumza na simu, baada ya kuzungumza ancho kizungumza, akaitupa simu hiyo pembeni ya barabara na wakaondoka katika eneo hili.

“Unaweza kupata video katika hilo boksi?” “Ndio” “Fanya hivyo” Ikamlazimu Babynka kutoa video inayo onyesha gari walilo panda Winy na Martin, akaonyesha video hii inayo tokea kwa juu, inayo onyesha boksi lenye kichwa cha mume wa K2. Hazikupita hata dakika tano gari zipatazo kumi za NSS, zikafika katika eneo la daraja la Sarenda. Wakashuka na kuanza kulizunguka daraja hilo, huku kila mmoja akiwa naa silaha yake.

“Wamelipata boksi” Babyanka alizungumza huku akinionyesha askari aliye lishika boksi hilo. Askari hawa wakaanza kulizunguka hili boksi huku wakionekana kuwa na woga sana.

“Kwa nini askari wako ni waoga?” “Nahisi wanahisi hilo ni bomu” “Watafikisha kweli mzigo huo?” “Ngoja tuone” Askari hawa wakaliweka bosky hilo katitaki ya barabara na magari yao wakayaweka umbali kidogo kutoka sehemu lilipo boski. Tukawaona askari wawili wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kugegulia mabomu wakianza kulisogela boski hilo taratibu.

“Umeandika huo ujumbe umfikie raisi?” “Hapana” “Watausoma na tulicho kifanya ni kazi bure” “Sio kazi bure ngoja tuone” Askari hao wakalisogelea boksi na taratibu wakalifungua, wote wakaonekana kustula hadi mmoja wao akaanguka chini.

Askari wengine walio kaa umbali kidogo wakaonekana kuwa makini huku wakiwatazama wezao. Askari aliye anguka chini akasimama tarataibu na kuonyesha ishara iliyo wafanya wezake kusogea taratibu. Kila askari aliye tazama ndani ya boksi hilo akaonekana kustuka sana.

“Tunaweza kusikia wanacho kizungumza?” “Hapana hatujatega vinasa sauti”

“Sawa” Tukamuona askari mmoja akizungumza na simu, baada ya muda kidogo akakata simu hiyo na kurudi eneo lilipo boksi. Babyanka akamtazama askari huyo anavyo zungumza na wezake, kisha Babyanka akanigeukia na kunitazama.

“Anazungumza nini jamaa?” “Amewaambia wezake waimarishe ulinzi kwa maana raisi amehitaji kufika eneo la tukio” “Umejuaje?” “Nimetazama mdomo wake jinsi unavyo zungumza na nimeweza kulijua hilo. Umesahau kama nina uwezo mkubwa wa kufahamu jinsi mtu anavyo zungumza hata kama hajatoa sauti” “Nakumbuka” “Niamini basi katika nililo kuambia” “Poa” Baada ya dakika kumi na tano, gari nne nyeusi zenye bendera ya raisi pamoja na bendera ndogo ya nchi hii, zikafika katike eneo la tukio. Wakashuka walinzi wote, walipo hakikisha usalama upo vizuri akashuka K2, aliye anza kutembea kwa kasi kuelekea sehemu lilipo boksi lenye kichwa cha mume wake.

“Laiti kama wangeweka bomu basi hii ingekuwa shabaha yangu ya pekee kuhakikisha kwamba K2 anakufa” “Ni kweli, ila kama mtu mmoja simuoni katika walinzi wake ikiwa wasichana wengine nimewaona” “Nani?” “Livna Livba” Hata kabla sijatazama vizuri, mlango wa hapa sebleni ukafunguliwa. Sote tukajikuta tukigeuka nyuma, tukamuona Martin akiingia humu ndani ila uso wake ukivuja damu na ametulia sana, akaingia na Winy naye jicho moja limemvimba, nikaishika bunduki yangu vizuri huku nikipiga hatua moja mbele. Martin akatingisha kichwa akishiria kunikataza kusogea mbele kwani kufanya hivyo inaweza kuwa hatari kwangu, kwani sifahamu ni nani aliyopo nyuma yao.



Taratibu tukaona viatu vyeusi vya kijeshi, hatukamaliza hata sekunde moja, sura ya Livna ikasimama mbele yetu huku mikononi mwake akiwa ameshika  bastola mbili huku amewanyoshea Winy na Martin kwenye vichwa vyao.

“Halooo Dany”   

Sauti ya Livna haijabadilika kabisa, hata sura yake ni ile ile kabisa.

“Pigeni magoti nyinyi wajinga”

Livna alizungumza kwa kwa ukali, taratibu Winy na Martina wakapiga magoti chini jambo lililo anza kuniumiza akili yangu kwani siwezi kufanya chochote kibaya kwani kitahatarisha maisha ya hawa watu wawili ambao ni muhimu sana kwangu hususani Martin.

“Vijana wako bwana waliingia vibaya kwangu, sikuwa na jinsi zaidi ya kuwafanya hivi japo huyu mseng** hapa alikuwa ni mume wangu”

 

Livna alizungumza huku akimpiga teke la mgongo Martin.

“Sikuja hapa kukukamata ila nimekuja hapa kukusaidia”

“Kunisaidia?”

“Ndio kukusaidia, natambua kiu yako ni kumuua K2 si ndio?”

Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama Livna, taratibu akazichomeka bastola zake kwenye kiuno chake na kuanza kutembea hadi sehemu lilipo sofa na kukaa taratibu.

“Martin unatakiwa kujifunza zaidi maswala ya kupigana, na wewe dada nawe hivyo hivyo”

Uwepo wa Livna humu ndani ukazidi kunishangaza na hata maneno yake yanazidi kunishangaza. Kupigwa kwa Martin na Winy kwangu wala sishangai sana kwani hata mimi nilisha wahi kukutana na kipigo chake nilipo kuwa na Mariana kwenye meli nilipo kuwa ninatoroka nchini Tanzania.

 

“Mbona muna shangaa shangaa vipi nimekuwa kituko eheee”

“Martin mumefanya nini sasa?”

Nilimuuliza Martin huku nikimtazama usoni mwake.

“Samahani mkuu, nilitamani kuonana naye ndio yakatokea haya”

“Kwa nini mumemleta hapa?”

“Dany acha kumkoromea mwenzako. Mshukuru Martin amenishawishi sana kuweza kuungana nawe”

“Livna huwezi kuungana nami ikiwa uliweza kusaliti baba yangu na akafa, leo hii utaungana nami kivipi?”

 

“Baba yako alienenda tofauti na makubaliano yetu na pia K2 ameenenda kinyume na makubaliano yetu je wewe utaenenda kinyume na makubaliano yetu”

“Makubaliano yapi?”

“Moja nahitaji kizazi changu cha wasichana nilio wafunza mafunzo maalumu kubaki kama walivyo na sinto hitaji kuona kuna mkuu yoyote anaye hitaji kujimilikisha kikosi hicho kama alivyo fanya baba yako eti kisa anapesa. Na pia K2 ndivyo anavyo fanya, anawatumikisha wasichana wangu, wanajitolea maisha yao pasipo yeye kufahamu ni thamani gani hao wasichana walivyo na hata akifa msichana mmoja kwangu ni hasara kubwa inayo niumiza sana”

 

 “Mimi kikosi chako sina kisasi nacho na laiti wakihitaji kuendelea kumkumbatia K2 nitahakikisha kwamba ninawaua nao”

“Kuwaua unaweza, na mimi nitakuua kwa maana sishindwi kukuua Dany. Ila bado hujakomaa kwenye vita ambayo ungehitaji kuufanya kwani kumuua msichana wangu basi ineyagarimu maisha yako”

 

Livna alizungumza kwa kujiamini sana. Ili maisha yako yasiende bure nikaamua kukupa hii ofa, ili uweze kulipiza kwa yale yaliyo tokea kwa baba yako na familia yako kwa uzima”

“Una jambo jingine?”

“Ndio ninalo kwa nini nikose. Hakikisha kwamba unanipa orodha ya maadui zako wote sawa”

“Umezungumza ya kwako ngoja na mimi nizungumze yangu. Moja ofa yako nimeikubali. Mbili ukijaribu kunisaliti, nitakuaa, kwa maana Dany wa miaka ile si wa miaka hii ya sasa. Tatu maadui wangu ni watatu na ikiwezekana nitahitaji kabla ya masaa ishirini na nne yajayo wawe wamesha ondoka duniani sawa.”

 

“Sawa hilo ni jambo raisi. Oya bado hamjanyanyuka tu”

Martin na Winy wakanyanyuka, Babyanka akaanza kuwapa huduma ya kwanza kwani nyuso zao zimebadilika kwa kipigo walicho weza kukipata huko walipo toka.

“Jamani ninaombeni maji ya kunywa?”   

Livna alizungumza huku akikaa vizuri kwenye hili sofa. Babyanka akafungua friji na kutoa chupa ndogo ya maji ya kinywa na kukamabidhi Livna.

 

“Kuna sababu nyengine ya kumsaliti K2 zaidi ya hiyo ambayo umeniambia?”

“Sababu zipo ila ni ndogo ndogo sana”

“Kama?”

“Kujiachukulia tu wasichana nao wahitaji kwenye kikundi changu, kuto kuwalipa vizuri pia ni jambo ambalo kidogo limenifanya moyo wangu kila siku niwe na maumivu”

“Kweli?”

Nilimuuliza Livna huku nikiwa nimekazia macho usoni mwake.

“Ndio”

“Kwa nini ulishindwa kumuua ikiwa anaenenda kinyume nawe?”

 

“Sipendi kuua, na kikosi changu nilikiunda kwa sheria ya kulinda wale watakao lipa pesa kwa ajili ya sisi kuwalinda”

“Ilikuwaje K2 akachukau madaraka ya katika kikosi chako?”

“Baba yako na K2 ndio walikuwa walezi wa kile kikosi, walitoa pesa zao nyingi sana. K2 akamgeuka baba yako baada ya kuzidiwa kwa kutoa matumizi, akaamua kumuua, kwa kutumia watu wake wa karibu sana. Sasa yeye ndio akabaki kuwa na nguvu katika kikosi, ila mimi ndio niliachia kikosi hichi na muanzilishi tangu nikiwa mdogo sana.”

“Muanzilishi wa hicho kikosi ni nani?”

“Huwezi kumfahamu ni mama mmoja wa Kijapani na yeye ndio aliye nipatia mafunzo ambayo leo hii ninaweza kuwapatia wezangu”

“Sawa, sasa ninasikiliza mbinu zako ambazo tunaweza kuzitumia kumuangamiza K2, raisi Donald Bush na mke wa raisi bi Hawa Donald?”

“Hao wawili nao wameingia kwenye kumi na nane zako?”

“Ndio”

 

“Ilikuwaje?”

“Hupaswi kufahamu?”

“Basi kwa hao wawili nitajitoa kwa maana siwezi kufanya kazi pasipo kujua huyo ninayetakiwa kumuhudumia amefanya jambo gani kwako”

“Hawa alikuwa mke wangu”

“Ndio  uliye funga naye ndoa, kwa maana kidoleni una pete ya ndoa?”

“Hapana”

“Kwa hiyo alikuwa hawara?”

“Nilipokonywa na raisi huyo baada ya kunipeleka katika mission ambazo ni hatari kubwa. Moja ilikuwa ni kuvuruga kikundi cha Al-Shabab nchini Somalia na nilifanikiwa kukisambaratisha, mbili ilikuwa ni kukisambaratisha kikosi cha Boko haramu nchini Tanzania”

 

“Kweli Dany umebadilika vikosi vyote hiyo viwili uliweza kuvisambaratisha?”

“Niliweza kwenye Al-Shabab, ila kwenye hicho kikosi cha Boko  haramu nilikuwa jeneral wao, baada ya kuona nimesalitiwa na raisi Donald Bush. Nilimsamehe kwa kumchukua mke wangu, ila hakuona kama msamaha wangu una tija akatuma makomandoo wake waniangamize ila nilifanikiwa kuwaua. Nilipata mke mwengine niliye funga naye ndoa, wakaona haitoshi, mke wake akatuma watu wakamuua mtoto wa mke wangu isitoshe wakakisambaratisha kikosi kizima”

 

“Duuu kweli wanahaki ya kuuwawa. Si uliwasamehe kabisa baada ya kuchukuana wao?”

“Ndio”

“Hata kama ni mimi ningewaua”

“Natamani hata kwenda kuwaua leo nasikia wamelala hapo Serena Hoteli?”

“Nani kazungumza?”

Nikamtazama Winy ambaye tayari amefutwa futwa damu usoni mwake.

 

“Hapana hapo Serena wamelala wapambe wake tuu ila raisi na mke wake wapo katika manuari ya jeshi la Marekanani na huko si rahisi kwa mtu yoyote kuweza kuwafikia na kuwaua”

“Mmmmm”

“Ndio hivyo, ukihitaji kumua raisi wao labda kwneye hizo ziara zake anazo anza kesho”

“Anazianzia wapi?”

“Anaanza kutembelea daraja la Kigaoni kukagua kagua mradi huo”

“Sawa na ni saa ngapi?”

“Majira ya asubuhi tu”

“Dany”

 

Babyanka aliniita huku akinitazama, nikamsogelea sehemu alipo kaa kwenye kiti.

“K2 amekipata kichwa cha jamaa yake, na ujumbe ulio andikwa ameusoma tayari?”

Babyanka alizungumza huku akiirudisha video hiyo aliyo irekodi nyuma kidogo.

“Mbona analia K2?”

Livna aliuliza huku akisimama pembeni yangu.

“Tumemchinja mume wake.”

“Eheheee Dany umechokoza moto, mama anakwenda kuvaa gwanda leo”

 

“Shauri yake mkuki kwa nguruwe ndio mtamu ila kwa binadamu ni mchungu sana”

“Mmmm, sasa ilikuwaje mkamchinja jamaa yake?”

“Tulimkamata”

“Mkuu”

Martina aliniita, nikamgeukia na kumtazama.

“Hiyo ndio nafasi ya kwenda kumuua K2 kwa maana hapo amechanganyikiwa tayari”

“Hapana musimue sasa hivi”

“Kwa nini?”

“Kama unahitaji kumpata Donald na mke wake, hakikisha kwamba humuui K2, waue kwanza hao wawili kisha huyo ndio atafwatia na kifo chake kitakuwa ni cha taratibu”

Livna alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

 

“Poa hapa kikubwa ni kupango wa kumuua Donald na watu wake”

“Usijali upo na injini ya kazi hapa, kesho dunia nzima unakwenda kuandika historia ya kugopesha wengi”

Masaa yote yaliyo salia tukayatumia katia kupanga mipango ya kuhakikisha kwamba raisi Donald na Hawa tunawaua huku Livna akiahidi kuongeza wasichana wake wanne ambao anawaamini na wana mfunzo ya hali ya juu anayo amini kwamba ni lazima maraisi hawa wataisoma namba.

 

Hadi kuna pambazuka kila kitu kikawa tayari katika mpango wake, wasichana wa Livna Livba nao  wakawa wamesha fika hapa nyumbani kwa Winy huku wakiwa na mavazi maalumu ambayo wanayatumia walinzi wa Marekani wanao mlinda raisi wao. Nikakabidhiwa suti nyeusi pamoja na jaketi maalumu ya kuzuia risasi ambayo nimeivaa nyuma kwanza kabla ya kuvaa shati langu juu. 

 

Nikavalishwa sura ya bandia ambayo imetengenzwa kwa haraka na mmoja wa wasichana wa Livna mara tuu baada ya kuniona. Sura hii uzuri wake ninaweza kuivaa na si hadi nifanyiwe upasuaji  maalumu(oparesheni).

Kikosi cha watu tisa kikakamilia huku sote tukiwa tumevaa vifaa maalumu vya kuweza kuwasiliana sisi kwa sisi, nikasimama kwenye kioo na kujitazama vizuri, kwa sura niliyo ivaa kusema kweli nimebadilika na si rahisi kabisa kwa mtu kuweza kunitambua. Kitambulisho changu pia kina sura hii, na ukikutana nami ni rahisi sana kuamini kwamba mimi ni mlinzi wa raisi wa Marekanani. Martin, Babyanka na Winy nao wakakabidhiwa vitambulisho vyao kwa ajili ya kwenda kuianza kazi hii.

“Dany ataenda na mimi. Husna utaenda na Winy pamoja na Martin, Babyanka utachukua walio salia”

Livna alipanga majukumu hayo huku tukkiwa tumesimama kwa mfumo wa duara.

 

“Sawa”

“Tukumbuke, mwanachi asife katika hii kazi hapa anaye takiwa ni raisi Donald na mke wake. Tuhakikisheni kwamba tunawaleta eneo hili wakiwa hai na sote tulindane kwenye hii oparesheni”

Livna alizidi kusisitiza huku akitutizama kwenye nyuso zetu.

“Sawa mkuu”

“Jamani nashukuru kwa umoja wenu, hii kazi ni ya kuhatarisha maisha yetu. Na nyote mumefanya kwa ajili ya kunisaidia. Endapo hatuto rudi kwa idadi hii basi ninaimani kwamba tutaonana kwenye dunia nyingine ambayo hakuna mtu aliye wahi kwenda”

Nilizungumza kwa sauti ya upole kwani kusema kweli katika hili swala laiti ningekuwa peke yangu basi siwezi kabisa kufanya hivyo.

 

“Usijali ninaimani sote tutarudi salama, na hakuna hata kati yetu atakaye kufa. Twendeni tukawatandike makalio yao sawa”

Livna alizungumza kwa msitizo ambao unampa hamasa kila mmoja eneo hili.

“Sawa mkuu”

Tukapeana mikono kisha sote tukaaanza kutoka sebleni hapa, kila mmoja akiwa na silaha za kutosha, na kila mtu anajua ni wapi ameingiza silaha hizo. Tukaingia kwenye magari manne yanayo tumiwa na walinzi wa Kimarekani ambayo yamekuja na wasichana wa Livna.

Safari ikaanza taratibu, tulipo fika barabarani gari zikatawanyika na kila gari likapita njia yake ila lengo kubwa ni kufika Kigamboni. Simu ya Livna ikaanza kuita mfukoni mwake, taratibu akaitoa na kuipokea.

 

“Muheshimiwa raisi”

Nikamtazama Livna huku nikiendelea kuendesha gari.

“Ziara imebadilishwa?”

Nikajikuta nikupunguza kasi ya mwendo wa gari.

“Ahaaa inaanzia hapo SPF Tower?”

“Sawa mkuu basi nitaimarisha ulinzi hapo”

Livna akakata simu yake na tukaanza kupeana taarifa watu wote juu ya ziara ya maraisi hawa kubalishwa. Ikatulazimu wote mpango kubadilika haraka inavyo wezekana. Mimi na Livna tukawa wa kwanza kufika katika magorofa haya mawili ambayo ni marefu sana kwenda juu na urefu wake ni sawa na mita 147  kwenda juu.

 

“Sijui wanafika saa ngapi hapa”

Nilizungumza huku nikiendelea kutazama ulinzi ulio imarishwa hapa. Hapakuwa na mtu wa kutukagua kwa maana tunavitambulisho.

“Watafika, siwezi kumpigia K2 simu na kumuuliza inaweza kumpa wasiwasi.”

“K2 alisha wahi kufahamu mahusiano kati yangu mimi na wewe?”

“Hapana hakuwah kufahamu”

“Ahaa sawa sawa”

 

“Tuelekee juu, kwa maana huku ndipo wanapo kagua kagua”

“Wanaanza gorofa gani kwa maana yapo haya mawili hapa?”

“Hili tulilopo ndio wanaanza”

“Babyanka na timu yako hakikisheni munakaa gorofa namba mbili.”

“Sawa”

Baada ya kutoa maelekezo hayo kupitia kinasa sauti maalimu nilicho kivaa, tukaanza kuingia ndani ya hili gorofa ambapo ndio mara yangu ya kwanza kuingia humu ndani. Baada ya lisaa ving’ora vikaanza kusikika, nikasimama kwenye moja ya dirisha na kuchungulia chini nikaanza kuona gari za raisi K2 zikifika katika hili eneo, walinzi wakazidi kuimarisha ulinzi.

“Jaribu kuizuia asira yako utakapo muona K2, tunaye muhiraji leo ni Donald na Hawa sawa Dany”

 

“Nimkuelewa”

Baada ya dakika tano mbeleni gari za raisi wa Marekani nazo zikafika katika eneo hili. Walinzi wote wa Marekani nao wakasogelea gari hili ambalo ni refu, wakamfungulia raisi mlango akashuka huku akipunga mkono. Taratibu nikaona gauni jekundu likianza kutoka ndani ya gari hili, kisha akashuka Hawa huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake, macho yangu nikayashusha hadi tumboni mwake nikaona ujauzito wake ulio nifanya nipatwe na uchungu mwingi sana hadi nikatamani kuanza kufanya mashambulizi nikiwa huku huku juu nilipo.



“Dany tutafeli, unamuonaje malaya tu huyo na unakuwa na hasira kiasi hichi?”

Livna alizungumza huku akitazama mikono yangu jinsi inavyo tetemeka kwa hasira ambayo kusema kweli haina kipimo.

 

“Nahitaji kuwaua sasa hivi?”

“Piga picha ukiwaua sasa hivi kuna midomo mingapi ya bunduki kwa hawa watu na unahisi mwili wako unaonekana vipi. Utafanywa chujio kwa risasi acha ujinga”

Livna aliendelea kuzungumza kwa msisitizo hukua kinishika mkono wangu wa kulia ambao unazidi kutetemeka kwa hasira kali niliyo nayo.

“Tulia nitakuonyesha hii kazi jinsi inavyo fanywa”

“Sawa”

Tukaanza kutembea tembea kwenye gorofa tuliyopo huku tukiendelea kujifanya ni walinzi wanao imarisha ulinzi ila hatuna chochote katika hili.

 

“Hivi unahisi ni kwa nini niliamua kutembea na wewe?”   

“Sijakuelewa?”

“Yaani unatambua kwa nini nimeamua kuongozana nawe kwenye hii oparesheni hii?”

“Sijajua?”

“Kwa sasabu ninakujua vizuri Dany, unafeli kila misheni kwa ajili ya hasira za hapo kwa hapo, ukimuona adui sijui unakuwaje kuwaje. Na isitoshe humu ndani kuna watu wana ujuzi hadi wakuwasoma watu miguu yao jinsi  inavyo tembea wakikuona tembea yako haieleweki lazima wakudandie, sasa piga picha wakikustukizia na jinsi unavyo tafutwa watakufanya nini”

 

Livna alizungumza kwa sauti ya chini, tukasimama pembeni ya lifti inayo fika katika gorofa hili, wakaanza kutoka walinzi kisha akafwatia K2, alipo muona Livna akamkonyeza kama ishara ya urafiki. K2 na walinzi wake wakelea kwenye moja ya sehemu maalumu iliyo andaliwa humu ndani na hapa ndipo maraisi watakapo kutana ili kuanza kukagua gorofa hili lenye huduma mbalimbali.

Waandishi wa habari nao wakazidi kuwa bize kuhakikisha kwamba wanapata picha nzuri kwa raisi ajaye kupitia lifti hii. Tukiwa hapa gafla umeme ukakatika na giza totoro likatawala humu ndani, kelele zikaanza kutawala huku walinzi wakihakikisha kwamba wanamlinda K2 kwani kukatika kwa umeme hili jambo halikuwepo kwenye ratiba yao.

 

“Show time baby”

Livna alizungumza huku akinishika mkono, tutakasimama kwenye lifti hii na kwa haraka Livna akaanza kuifungua milango hii miwili, ambayo haikumpa tabu sana. Mara kwa mara macho yangu yanatazama sehemua lipo kuwa K2 ila kutokana na giza pamoja na wingi wa watu sikuweza kumuona.

“Tunashuka chini unaone lifti ile kule”

Livna alizungumza kwa nguvu huku akinionyesha lifti  iliyo kwama kwa mwanga wa simu yake nikaweza kuiona na lifti hii ndipo alipo raisi Donald pamoja mke wake pamoja na walinzi.

“Ile ni gorofa namba mbili  inabidi kushuka kwa hii kambi”

“Nimekupata”

Akaanza Livna kushuka kwa kasi na hii kamba ngum ili tengenezwa kwa nyanya ndogo dongo za chuma na zimaesukwa sehemu moja na kuifanya kama hii kuwa nene na ngumu sana.

 

Nikachomoa bastola zangu mbili na kuzifanya kama vishikizo katika kamba hii kwani nikishuka chini kwa kutumia viganja vyangu pekee, nikifika hadi lifi ilipo ni lazima viwe vimechubuka. Nikashuka kwa kasi sana hadi nikafika sehemu ilipo lifti.

Tukaanza kusaidiana na Livna katika kufungua mfuniko ulipo juu  ya lifti. Tulipo hakikisha  kwamba umefunguka Livna akamulika ndani na simu yake.

“Muheshimiwa raisi tupo kwa ajli ya kukutoa hapa salama wewe na mke wako”

Livna alizungumza, nikapata nafasi ya kuchungulia ndani, nikawaona walinzi wa raisi Donald wakiwa wamezielekezea bunduki zao kwa Livna.

 

“Sawa”

Livna akaingia kupitia uwazi huo, na mimi nikaingia pia kupitia katika uwazi huu. Cha kushangaza sijamkuta Hawa ila sikuhitaji kuonyesha tofati yoyote katika hili.

“Hii ni gorofa namba mbili, tusaidiane kufungua huo mlango na tumtoe raisi humu ndani”

Livna akawapa maelekezo vijana wa raisi Donald Bush.

“Sawa madam”

Tukaanza kusaidiana kufungua mlango hadi ukafanikiwa kufunguka, tukakuta lifti hii ipo katika usawa wa gorofa ya pili na ya tatu huku kukiwa na uwazi mdogo wa kupita katika  gorofa namba mbili kwani ndio ilikuwa inapanda kwenda juu.

“Unaweza kupita hapo muheshimiwa?”

 ITAENDELEA


0 comments:

Post a Comment

BLOG