Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 6/10

 

 


 MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE)

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 6 KATI YA 10

 


Hata kabla Sa Yoo hajaendelea kuzungumza, wakamuona mlinzi mkuu anaye husika na kulinda eneo la jumba hili la makamu wa raisi, akiwafwata.

“Samahani muheshimiwa, kuna simu yako ya kikazi”

“Naomba”

Eddy akaichukua simu hiyo na kiiweka sikioni mwake.

“Haloo”

“Muheshimiwa, kuna waziri wa kilimo kutoka nchini Brazili anahitaji kuzungumza na wewe”

Eddy akashusha pumzi taratibu huku akijiweka ksawa kuhakikisha kwamba anayafuta mawazo ya familia yake kwa muda.

“Muunganishe”

Eddy alimruhusu sekretari wake kuweza kumuunganisha na waziri huyo.

“Haloo”

Sauti ya Adrus haikuwa ngeni masikioni mwa Eddy.

“Hahaa, Adrus umekuwa waziri nchini Brazil”

“Hapana muheshimiwa hii ni mbinu raisi ya mimi na wewe kuweza kufanya mawasiliano”

Adrus akaanza kumuelezea Eddy matatizo yote yaliyo tokea, kwa ufupi sana. Akaeleza hadi amari ambayo raisi Rahab ameitoa dhidi yake ili aweze kuuwawa kutokana na kuipinga kazi aliyo kabidhi na nchi hizo mbili.

“Fuc***hayo ndio maamuzi ya Rahab si ndio?”

“Ndio muheshimiwa, ninaimani kwamba Wamarekani watamteka mama yangu ili nijisalimieshe kwao, ninakuomba msaada wako muheshimiwa umsaidie mama yangu, kwa maana muda wowote anaweza kutekwa?”

“Ulisha wasiliana naye?”

“Hapana wewe ndio mtu wa kwanza kukuomba msaada”

“Sawa Adrus, ninatuma vijana sasa hivi waweze kumsaidia mama yako, nitajie namba yake”

Adrus akaanza kiitaja namba ya mama yake.

“Nimeipata, nitamchukulia uangalizi sawa”

“Sawa muheshimwa”

“Ila ninaomba msaada wako Adrus?”

“Masaada gani tena muheshimiwa?”

Eddy akamtazama Phidaya aliye fura kwa hasira.

“Mwanangu hadi hivi sasa ahajapatika, kama ikiwezekana ninakuomba uweze kunisaidia, kwa maana wahusika nnasikia kwamba wapo nchini Madagascar katika kisiwa cha Antananarivo”

“Sawa muheshimiwa, je unahitaji wahusika walii mteka mwanao wakiwa hai au wamekufa?”

Eddy akatabamu kidogo.

“Fanya kama chochote unacho kiweza ninacho kihitaji ni kumpata mwanagu.”

“Sawa mkuu”



Eddy akakata simu huku akijawa na tabasamu usoni mwake.

“Tupishe kwa muda”

Eddy alimuambia mlinzi wake huyo.

“Hembu nyinyi wanawake nisikilizeni kitu kimoja. Wote nyinyi wawili hamuijui historia yangu ya nyuma vizuri zaidi ya kuwasimulia juu juu. Sitaki ujinga na upumbavu kwenye familia yangu, Ninaweza nikawaacha nyinyi nyote na kila mtu akaendelea na hamsini zake, sijui munanielewa, na hakuna atakaye ondoka na mtoto”

Eddy alizungumza kwa msisitizo hadi Shamsa akashangaa, kwani maringo yake yote akajikuta yakiyayuka moyoni mwake.

“Wewe muheshimu Phidaya, maswala ya uswahili wa kupandishiana macho na kushusha ndani ya familia yangu sihitaji kuona hilo swala linajitokeza tena umenielewa Shamsa?”

“Eheee?”

“Na wewe Phidaya, maswala ya kuwekeana shonde na mtoto mdogo, sitaki. Mpendane kama ilivyo kuwa pale mwanzoni sijui umenielewa”

“Ndio nimekuelewa”

“Sasa nije nione sijui wewe Phidaya au Shamsa munaleteajae nyodo za kijinga, mutanielewa mimi ni nani sawa”

“Sawa”

Shamsa na Phidaya wakajikuta wakiitikia kwa pmoja kila mtu akiwa ameielewa amei ya kiongozi wa familia hiyo. “Kumbatianeni sasa”

Sa Yoo alizungumza huku akiwa amejawa na furaha, Phidaya na Shamsa wakatazamana kisha taratibu wakakumbatiana huku wakiwa na tabasamu pana kila mmoja kwenye uso wake.

“Waooo, umeona sasa, hadi rahaa, na mimi ngoja nijiunge”

Sa Yoo alizugumza kisha akawakumvatia Shamsa na Phidaya ambao kila mmoja anajiona mpuuzi na mjinga kwa kile kitu alicho kuwa amekitengeneza katika akili na moyo wake.

***

“Vipi?”

Cookie alizungumza huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Makamu wa raisi amekubali kuifanya kazi yangu, ila amenikabidhi kazi ambayo ningewaomba muweze kunisaidia na mimi”

“Kazi gani?”

“Kabla sijapangiwa kazi ya kuja nchini Marekani. Makamu wa raisi aliweza kunipatia kazi ya kwenda kumkomboa mtoto wake ambaye alitekwa nchini Uingereza na hadi sasa hivi anavyo zungumza ni kwamba hajampata mwanaye. Sasa raisi yeye mwenyewe ndio alitoa maamuzi ya mimi kujumuika na Wamarekani kuongoza nao katika kazi ya kwenda kumkomboa mtoto wa raisi wao”

“Sasa unafahamu ni wapi mtoto huyo alipo?”

‘Sijafahamu, ila nitamuomba makamu wa raisi aweze kutupatia detail za wapi mwanaye alipo”

“Sawa, inabidi kuweza kufahamu mapema ili kama kazi itaanza basi iweze kufanyika kwa umakini”

“Ngoja niwasiliane na mama yangu kwanza”

“Sawa”

Adrus akaandika namba ya mama yake katika simu hiyo kisha akaipiga. Kwa bahati nzuri simu hiyo ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.

“Halooo”

Adrus aliisikia sati ya mama yake iliyo mfanya ajawe na tabasamu pana usoni mwake.

“Mama Shikamoo”

“Marahab, Adrus umefika salama mwanangu?”

“Yaa ila kwa sasa nipo nchini Brazili”

“Brazil tena na sio Marekani?”

“Hapana mama, kuna kuna sababu nyingi za kiusalama zimenifanya niweze kuja nchini Brazil ila mama kuna jambon ninahitaji kukuomba”

“Jambo gani tena mwanangu?”

“Nahitaji uweze kujifiacha eneo ambalo Makamu wa raisi anaweza kutuma watu watakao kuja kukuchukua na kukuweka mafichoni”

“Adrus, ni nini kinacho endelea?”

Mama Adrus alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana, ulio weza kumdhihirishia Adrus kwamba mama yake huyo amejawa na woga mwingi sana.

“Mama kwa sasa sina muda wa kuweza kukuelezea hayo mambo yote, ila ninakuomba sana uweze kuwa sehemu ambayo nitampatia Makamu wa raisi namba yako na atawasiliana nawe moja kwa moja na utachukuliwa na vijana wake na atakuweka katika sehemu ambayo ni salama.”

“Ila na wewe upo salama mwanangu?”

“Nipo salama mama yangu, ila ninakuomba mama yangu uweze kufanya hivyo. Zile safari za kwa mashosti wako, au wale wanao kuja hapo nyumbani ninakuomba tafadhali uzisitishe kwa kipindi hichi, sawa mama?”

“Sawa, ila kule nilisha hama nimenunua jumba huku Mbezi”

“Ahaaa, sawa jambo zuri, ila ninakuomba ufanye kama vile nilivyo kueleza”

“Sawa mwanangu”

Adrus akakata simu, kwa haraka akaipiga namba ya ofisini mwa makamu wa raisi ili weze kuto amalekezo hayo juu ya ulinzi wa mama yake kuimarishwa.

***

K2 na kaka yake hadi inatimu saa mbili asubuhi, ndio wanamaliza zoezi la kuchimba kaburi kubwa. Wakanaza kuuzika mwili wa mlinzi wao mmoja baada ya mwengine. Walipo hakikisha kwamba wamemaliza wakaifukia sehemu hiyo.

“Hii miili haito julikana kweli?”

“Usiwe na shaka kaka haiwezi kujulikana kwani nin nani ambaye atakuja huku na kuanza kufukua fukua”

“Ila tukumbuke kwamba hawa vijana wana familia zao ambazo zinawategemea?”

“Uzuri nilisha wapa onyo kwamba mtu asije akaiambia familia yake kwamba anafanya kazi gani na eneo gani, nina imani kwamba onyo langu halito leta maswali mengi kwa familia yao hata wakigundua wapendwa wao wamepotea”

‘’Sawa, ila nini kinacho fwata?”

“Lazima tuingie serikalini kwa mbinu nyingine”

“Mbinu gani?”

“Lazima tuanzishe kitengo cha ulinzi, kitengo kinacho weza kutulinda na itakuwa ni nafasi ya pekee kwa wewe kuingia madarakani”

K2 alizungumza huku akiwa amjawa na tabasamu pana usoni mwake.

***

“Shamsa, ninakazi ninahitaji kuwapatia”

Eddy alizungumza huku akiwatazama Shamsa, Phidaya na Sa Yoo.

“Kazi gani tena?”

“Kuna mama yake Adrus yule mlinzi wa Phidaya, anatakiwa kuchukuliwa na kuletwa hapa nyumbani, tutaishi naye kwa siri”

“Kwa siri kwa nini?”

Phidaya alimuuliza huku akimtazama mume wake.

“Kuna maswala ya kiusalama, ninatakiwa kuyaweka kwa mwanamama huyo, ili kazi ya kumuokoa mtoto wetu iweze kwenda vizuri”

“Sawa, yupo wapi?”

“Hajaniambia bado ila ngoja nifanye naye maswaliano”

Eddy kabla hajazungumza chochote simu aliyo letewa na mlinzi wake ikaanza kuita, kwa haraka akaipokea kwani ni namba kutoka ofisini kwake.

“Ndio”

“Mkuu waziri anahitaji kuzungumza nawe”

“Waziri gani?”

“Kutoka nchini Brazil”

“Okay muunginishe”

“Mkuu”

“Ndio Adrus”

“Naweza kukutajia namba ya mama yangu kwa maana ameniambia kwama amehama nyumbani alipo kuwa anaishi”

“Okay nitajie namba yake”

Eddy akamnyooshea Sa Yoo mkono na kumiomba simu yake, Adrus akaitaja namba hiyo na Eddya akainakili namba hiyo katika simu ya Sa Yoo.

“Nimeipata”

“Sasa mkuu ninahitaji kuweza kufahamu kwa sasa mwanao yupo wapi?”

“Kwa detail za mwisho kuna watu nilikuwa ninawashikili, ambao kuna makosa kidogo yalijitokea na wakatoroka, ila watu hao wanaweza kuwa ndio dira sahihi ya wewe kuweza kumpata mwanangu. Hii namba yako si ina huduma za WhatSapp?”

“Ndio mkuu”

“Basi nitakutumia picha za wahusika na eneo walipo. Ndani ya dakika kama kumi na tano nitakuwa nimesha kamilisha zoezi hilo”

“Sawa muheshimiwa, ila shukrani sana kwa msaada wako”

“Usijali, hakikisha kwamba hii kazi inakuwa kati yangu mimi na wewe na baada ya hapo nitahakikisha kwamba ninakuwekea ulinzi wa kutosha”

“Shukrani muheshimiwa”

“Sawa”

Eddy akakata simu, akaitazama namba ya mama Adrus, kisha akaipiga. Simu hiyo ikaanza kuita baada ya muda kidogo ikapokelewa.

“Habari yako”

“Salama nani?”

Mama Adrus alizungumza kwa wasiwasi mwingi sana.

“Unazungumza na Eddy Godwin makamu wa raisi hapa nchini Tanzania”

“Ooohoo asante Mungu, niambie baba yangu”

“Kuna mabinti wangu nitawatuma hapo waje kukuchukua, utawasiliana nao kupitia namba hii niliyo kupigia utawaelekeza ni wapi ulipo sawa”

“Sawa baba yangu nashukuru sana”

“Sawa mama yangu”

Eddy akakata simu na kumrudishia Sa Yoo simu yake.

“Jiandaeni haraka mukamchukue huyo mama”

“Samahani Eddy, kwa nini tunakwenda kumchukua, labda ungetueleza maelezo mafupi?”

“Majasusi wa nchini Marekani wanamuhitaji mama huyu ili waweze kushurutisha Adrus kujiunga nao katika kwenda kufanya oparesheni ya kumchukua mtoto wa raisi wa Marekani aliyetekwa na magaidi wa kundi la Alquida”

“Sasa kwa nini sisi tunamchukua?”

Sa Yoo aliuliza.

“Huyu ndio shabaha ya pekee ambayo tunaweza kuitumia kumuokoa JJunion, kwa manaa hii vita yangu na John inabidi nipambane naye kimya kimya na kuhakikisha kwamba nina muharibu pasipo tete kufahamu kwamba ninamuharibu. Na wakati huu sinti mkata miguu wala miguu yake, nitaikata shingo yake”



Shamsa na Sa Yoo wakabaki wakiwa wamekodolea macho Eddy kwani kitu walicho kisikia hawakuwahi kukisia hapo awali.

“Sa Yoo twende”

Shamsa alizungumza hukua kinyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekali.

“Silaha zinatakiwa?”

Shamsa alizungumza huku akisimama na kumtazama Eddy.

“Yaaa, hamuwezi kujua ni kitu gani kinacho weza kwenda kutokea mbele ya safari”

“Inabidi kwenda na mlinzi mmoja?”

“Nendeni nyinyi, hii sio oparesheni ya kiserikali. Ni ishu ya kifamilia na hata walinzi wakiwauliza munakwenda wapi waambieni kwamba waje kupata majibu kutoka kwangu sawa?”

“Yes Boss”

Shamsa na Sa Yoo wakaondoka na kuwaacha Eddy na Phidaya wakiwasindikiza kwa macho.

“Nina amani sasa”

Phidaya alizungumza huku akitabasamu.

“Kweli?”

“Haki ya Mungu”

“Tumuombe Mungu tumpate mtoto wetu”

“Ila ninaombi moja kwako mume wangu”

“Ombi gani?”

“Ninaomba siku za mbeleni ugombanie uraisi, kwa manaa ungekuwa ni raisi ungeweza kupingana na amri za Rahab”

“Mimi mbona ninafirikia kuachia madaraka, ninahitaji kupumzika sasa. Tangu shule nimekuwa ni mtu wa kuhangaika hadi nimefikia umri huu mke wangu, kuna haja ya mimi kupumzika sasa”

“Usipumzike kabla ya kuwa raisi, uwe hata miaka mitano tu, mbeleni watoto wetu watakuja kuishi na historia ya kujisifu kwamba baba yao alisha wahi kuwa waziri, akawa makamu wa raisi na mwishowe akawa raisi”

Eddy akamtazama Phidaya kwa macho yaliyo jaa furaha taratibu akamsogelea Phidaya, kisha akamshika Shingo yake na kumvuta karibu yake na kumnyonya lipsi zake.

Shamsa na Sa Yoo akaingia kwenye gari, mlinzi mmoja akawafwata, ikamlazimu Shamsa kufungua kioo ili kumsikiliza.

“Ahaa…samahani, unakwenda wapi?”

“Kuna sehemu baba ametuagiza”

“Tunaweza kuwasindikiza?”

“Hapana, tutakuwa salama, ila unaweza kutuazima silaha yako?”

Mlinzi huyo akaka kimya kwa muda huku akiwatazama Shamsa na Sa Yoo.

“Aha..huku nyuma ya gari kuna silaha”

Mlinzi huyo alizungumza huku akizunguka nyuma ya gari hilo. Ikawalazimu Sa Yoo na Shamsa kushuka kwneye gari hilo, wakazunguka nyuma ya gari hilo. Mlinzi akafungua mlano wa gari hilo na kuwaaonyesha silaha zilizo pangiliwa vizuri.

“Munaweza kuchangua silaha ya aina yoyote”

“Hivi kumbe kwenye haya magari yenu munatembea na silaga?”

Sa Yoo aliuliza huku akimtazama mlinzi huyo.

“Yaa hizi zinakuwa kwa ajili ya dharua”

Sa Yoo akachukua moja ya bastola aliyo ipenda, akaigua kwa kutoa magazine yake, akakuta ikiwa imejaa silaha za kutosha. Akairudisha na kuichomeka kiunoni mwake, akachukua magazine mbili na kuzichomeka kwenye mifuko ya suruali yake hiyo ivaa na kuubana mwili wake vizuri. Shamsa akachukua bastola mboli, moja akaichomeka kiunoni, na nyingine akaichomeka kwenye kiatu chake aina ya travota, nyenye zipu ndefu iliyo fika nusu ya mguu wake.

“Kuna haja ya kuvaa bullet proof?”

Shamsa alimuuliza Sa Yoo.

“Tuchukue za dharura”

“Samahani muna kwenda wapi kwani….!!!?”

Mlinzi huyo aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao kwani maandalizi wanayo yafanya Shamsa na Sa Yoo kusema kweli ni maandalizi yanayo mshangaza sana.

“Tunakwenda kununua baashi ya vitu mjini, kwa hiyo inabidi kuvaa hivi kwa ajili ya usalama wetu”

Shamsa alizungumza hukua kivaa jaketi la kuzuia risasi.

“Ila si mungepata ulinzi wetu?”

“Hapana, sisi wenyewe inatosha kujilinda”

Shamsa akaufunga mlango huo wa gari kisha wakarudia mbele.

“Ukihitaji maelezo zaidi nenda kwa Eddy”

Shamsa alimuambia mlinzi huyo huku akiingia ndani ya gari hilo na kufunga mlango. Shamsa akawasha gari, taratibu akalirudisha nyuma, akaliweka sawa na kuanza kutoka katika geti la kwanza.

“Mpigie huyo mama?”

Sa Yoo akaitoa simu yake mfukoni na kuitazama namba ya mama Adrus, akaipiga. Hazikupita muda sekunde nyinngi simu ikapokelewa.

“Haloo mama, ninaitwa Sa Yoo tupo njiani tunakuja kukuchukua huko, ninakuomba uweze kunielekeza ni wapi ulipo?”

“Nipo Mb……”

Mama Adrus hakubalizia kuzungumza sentensi yake, simu ikakatika, jambo lililo mfanya Sa Yoo kuipiga tena namba hiyo. Simu ikaita kwa muda na haikupokelewa.

***

Majasusi kutoka nchini Marekani, wakafika nchini Tanzania majira ya saa moja asubihi. Moja kwa moja wakaelekea katika ubalozi wa Marekani, kutia saini kwa balozi huyo anaye iwakilisha nchi yake nchini Tanzania. Baada ya kukamilisha zoezi hilo wakakabidhi gari na kazi ya kuelekea kwa muhusia waliye mfwata nchini Tanzania ikaanza.

Teknologia kubwa ambayo ipo nchini Marekani, iliweza kuwawezesha majasusi walio agizwa na mshauri wa raisi Dustan, kuweza kutambua ni wapi mama Adrus alipo. Kwa kutumia namba yake ya simu ikawa ni kazi rahisi sana kuanza kufwata alama inayo onyesha eneo alipo mama Adrus. Wakafika katika jumba la mama Adrus hawakuwa na haja ya kuweza kugonga, walicho kifanya ni kuruka ukuta na kuingia ndani. Majasusi hao wanne wakiwa wanaongozwa na mwanamke mmoja aitwaye Angelina Thomssend, wakazidi kusonga mbele kwa umakini sana huku wakiwa na bunduki mikononi mwao.

Machale yakamcheza mama Adrus, kwa haraka akanyanyuka kitandani alipo kaa. Simu yake ikaita, akaitazama kwa muda, kisha akaipokea na kupiga hatua dirishani, akafunga pazia kidogo na kuwaona watu wanne walio valia suti nyeusi wakizidi kusogelea mlango wa kuingilia ndani kwake. Kwa haraka akapoea simu ya yake, akasikia sauti msichana ikimtaarifu kwamba wanakuja kumchukua.

Woga ukaanza kumtawala kwani hawa watu walio ingia nyumbani kwake pasipo hata kubisha hodi akaamini moja kwa moja kwamba watakuwa ni watu wabaya. Kwa haraka akaikata simu hiyo, kisha akapunguza sauti ya simu hiyo hadi mwisho. Simu hiyo ikaanza kuita tena, ila hakulijali hilo swala zaidi ya kaunza kupapasa papasa macho ni sehemu gani ambayo anaweza kujificha.

Sehemu salama ambayo aliweza kuiona kwa wakati huo ni chini ya uvungu wa kitanda chake, kwa haraka akaingia chini ya uvungu wa kitanda huku mwili mzima ukimtetemeka. Wazo jengine lililo mjia kichwani mwake ni kutuma meseji kwa msichana ambaye amepigia simu akimuomba amuelekeze ni wapi anapo ishi ili waende kmchukua.

‘Naishi Mbezi beach, kuna watu wameingia nyumbani kwangu, wana silaha na nimejificha chini ya uvungu’

Mama Adrus akasikia mlango wa chumbani kwake ukingogwa kwa nguvu. Mama Adrus akatamani hata dunia nyumba yake hiyo ianguke na wote wafie humu. Mlango ukaendelea kugungwa kwa nguvu, kilicho mchanganya kabisa, ni milio yadhaa ya risasi, iliyo pelekea hadi haja ndogo kumtoka. Mlango ukafunguliwa, kwa kupitia uwazi wa shuka la kitanda hicho, akaanza kuona miguu ya watu wawili wakiingia ndani humo. Majasusi hao, wakasimama pembeni ya kitanda cha mama Adrus, mmoja wao akatabasamu kwani wanajua fika muhusika atakuwa amejificha chini ya kitanda.

“Kuwa makini”

Jasusi mmoja alizungumza mara baada ya mwenzake kushika godoro ili alifunue. Jasusi huyo akaishika vizuri bastola yek akiielekeza katika eneo hilo la kitandani. Akafunua godoro hilo kwa haraka, wakamkuta mama Adrus akiwa amefumba macho yake.

“Toka chini kabla hatujakuvuruga kichwa chako”

Mama Adrus hakujali umri wake, hakujali kitendo cha kujikojolea alicho kifanya. Ila alicho kijali hapo ni kuhakikisha kwamba anatii amri aliyo ambiwa ili maisha yake yaendele kuwepo hapa Duniani.

“Amejikojolea”

Jasusi mmoja alizungumza huku akimtazama mama Adrus aliye lowa eneo la mbele ya suruali yake aliyo ivaa.

“Hatuwezi kwenda naye hivi”

“Tunafanyaje sasa”

“Mkuu kuna tatizo”

Jasusi mmoja aliwasiliana na mkuu wake Anjelina kwa kutumia vinasa sauti maalumu walivyo vivaa masikioni mwao,aliye muacha sebleni akiimarisha ulinzi.

“Tatizo gani?”

“Huyu mama amjikojolea”

“Hilo ndio tatizo”

“Njoo uone mkuu”

Anjelina ikamlazimu kuingi akatika chuma walicho wezake, akamkuta mama Adru sakiwa amesimama huku mwili mzima ukiendelea kumtetemeka kwa woga.

“Mama ingia bafuni, tusubirini hapo nje”

Angelina alizungumza na kuwafanya vijana wake kutoka nje. Mama Adrus hakuweza hata kupi hatua, kwa msaada wa kushikwa mkono na Angelina wakaingia bafuni, akaamrishwa kuvua nguo zake zote ili aweze kuoga na avae nguo nyingine. Angelina akaichukua simu ya mama Adrus na kuizima.

Mama Adrus akaoga kwa woga sana, katika maisha yake alisha wahi kusikia mtukio ya kutekwa tu aliyo kuwa anasimuliwa na marehemu mume wake, mzee Maldini, ila hakuwahi kukutana nayo oso kwa uso.

“Mama fanya haraka, sina muda wa kupoteza hapa”

Anjelina alizungumza hukua kiwa amekuja sura yake.

“Sa…sa….aa…a.saa..waa”

Mama Adrus alizunguzma huku sauti ikikatika katika. Mama Adrus akamaliza kuoga, wakatoka bafuni humo.

“Haraka haraka, vaa, vaa mama”

Msisitozo wa Anjelina, ukazidi kumpagawisha mama Adrus, badola ya kufungua kabati la nguo akajikuta akifungua droo ya dressing table yake aliyo hifadhia vipodozi tu.

“Unafanyaje hapo?”

“Nataf….u…u….t…aa ng….u….ooo…”

“Pumbavu, ngoo zinakaa kwenye kijidroo hicho kidogo. Mama unanitania eheee, nitalipua kichwa chako hicho”

Mama Adrus akajikuta akimwagikwa na mchozi, kwani binti anaye mfokea ni mdogo sana ambaye anaweza kumzaa, ila hana jinsi ya kufanya zaidi ya kukubaliana na kile anacho amarishwa.

***

Sa Yoo akaisoma meseji aliyo tumia na mama Adrus, akamsomea Shamsa na wakajikuta wakiatazamana.

“Jaribu kumpigia tena”

Shamsa alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake.

“Hapana, tukumpigia tunamzidishia matatizo, kumbuka kwamba amesema kwamba amejificha chini ya kitanda”

“Masikini, sasa chini ya kitanda kweli si ataonekana”

“Ohoo, sijui ni kina nani hao?”

“Watakuwa ni Wamarekani, wametuwahi”

“Tukumbuke kwamba wakiondoja naye tu, mwanao hato weza kukombolewa na Adrus”

Kauli hiyo ya Sa Yoo ikampa hamasa Shamsa ya kuongeza mwendo kasi wa gari lake.

“Ngona nina itafuta namba yake hapa, itatuoshesha ni sehemu gani alipo”

Sa Yoo alizungumza. Zoezi hilo halikuchukua hata dakika mbili akawa amefanikiwa kuweza kufahamu ni wapi mama Adrus alipo. Akaanza kumuelekeza Shamsa wapi apite. Shamsa kutokana na utaalamu na uwezo wa undeshaji wa gari, haikuwa kazi ngumu kuweza kupita njia za mkato mkato, japo nyingine sio nzuri, ila aliweza kuhimili mabonde mabonde huku akiwa katika mwendo wa kasi.

“Kunja kulia?”

Sa Yoo alizungumza hukua akiitazama simu yake. Shamsa, akakanyaga breki huku akikunja kona ya kuingia kulia na kusababisha tairi za nyuma kuserereka kidogo, na wakaendelea na safari.

“Ni mtaa huu”

Sa Yoo alizungumza huku wakikatika mtaa wenye majumba makubwa na ya kifahari sana. Signal walio kuwa wanaitumia kuweza kufahamu ni wapi alipo mama Adrus, sikapotea.

“Shitiii”

Sa Yoo alizungumza kwa hasira huku aking’ata meno yake.

“Nini?”

“Watakuwa wamezima simu yake kwa maana singal yake imepotea”

“Ila si imeonyesha ni mtaa huu?”

“Ndio mtaa huu huu”

Shamsa akatazama barabara hii ndefu ya lami iliyo tulia sana. Akaoga gari kubwa aina ya FORD, likiwa limesimisha pembeni ya geti kubwa. Taratibu akaanza kupunguza mwendo kasi wa gari lake. Wakalipita gari hilo huku akiendelea kulichunguza sana, akafika mbele kigo akasimamisha.

“Vipi?”

“Nina mashaka na gari hilo, watakuwa ni gari la watekaji na kama ni lao basi ujue nyumba hiyo ndio tumeipita”

“Tunafanyaje sasa?”

“Andaa silaha yako mapema”

Sa Yoo akachomo abastola yake, akaliweka vizuri jaketi la kuzuia risasi. Shamsa akaligeuza gari hilo na kulisimamisha mita kadhaa kutoka eneo lilipo gari walilo liona. Shamsa akafungua mlango wa gari lake kwa haraka akazunguka kwa nyuma gari lao, akafungua mlango na kuchukua kisu kikubwa alicho kiona, kisha akafunga.

“Kisu cha nini?”

Sa Yoo alizungumza huku akimtazama Shamsa anaye chomoa kisu hicho kutoka katika sehemu maalumu kilipo chomekwa.

“Nilinde”

Shamsa alizungumza huku akianza kukimbia kuelekea lilipo gari hilo. Sa Yoo macho yake yote yakawa na kazi ya kutazama katika geti la nyumba hiyo ili hata kama kuna mtu ataweza kutoka aweza kumstua Shamsa.

Shamsa akalifika gari hilo, kitu alicho kifanya ni kutoboa tairi la upande wa nyuma la gari hilo kwa kutumia kisu chake na kusababisha upepo wa tairi wote kutoka. Akalitazama gairi la upande wa mbele, akalisogelea kwa umakini huku macho yake kwa mara kadhaa yakiwa getini. Akalitoboa tairi la gari hilo kisha kwa garaka akarudi katika gari lao.

“Kwa mfano likiwa sio gari la hao watekaji itakuwaje?”

“Atakwenda kuweka matairi mapya kwani atajua ni sisi ndio tumemtobolea”

“Hahaa, Shamsa unavituko rafiki yangu”

“Aaahhh ndio hivyo”

Hazikupita hata dakika tano, wakaona wanaume wawili walio valia suti nyeusi na wenye asili ya Kimarekani. wakitoka katika kigeti kidogo cha nyumba hiyo. Sa Yoo akataka kuwapiga risasi, ila Shamsa akamzuia.

“Tulia kwanza”

Shamsa alizungumza huku wakiwa wamekaa siti ya nyuma ya gari hilo. Wakawaona wanaume hao wakishangaa kuona gari lao likiwa limeisha upepo tairi mbili.

“Wanafanyaje?”

Sa Yoo aliuliza mara baara ya kumuona mwanaume mmoja akiwa ameusogeza mkono wake wa kulia karibu kabisa na mdomo wake.

“Anawasiliana na wezake, inaonyesha hawapo peke yao”

Wakawaona wanaume hao wakitoa silaha zao huku wakiotazama huku na kule. Wakalitazama gari walilomo Shamsa na Sa Yoo.

“Wanakuja huku”

Sa Yoo alizungumza hukua kiwa ameshika bastola yake vizuri.

“Yaa”

Shamsa alijibu kwa ufupi huku naye akichomoa bastola yake. Majasusi hao kutoka nchini Marekani wakazidi kulisogelea gari la kina Shamsa. Shamsa kwa ishara ya vidole vya mokoni mwake, akaanza kuvihesabu kuanzia moja, ishara ambayo Sa Yoo aliweza kuielewa kabisa. Shamsa alipo nyanyua kidole cha tatu tu, kwa haraka wote kila mmoja akafungua mlango wa upande wake, hapakuwa na majadiliano wala mahojiano. Kitu walicho kifanya ni kuwafyatulia risasi majasusi hao, na kufanikiwa kuwachakaza vibaya sana, kwani ni shambulizi la kustukiza na wamekosa sehemu ya kujificha kwani walijikuta wakiwa katika kati ya barabara. Milio hiyo ya risasi ikamstua Anjelina na mama Adrus anaye malizia kuvaa suruali yake.

“Hei ni nini kinacho endele?”

Anjelina alizungumza huku akisikilizia jibu kutoka kwa vijana wake.

“Sifahamu mkuu, ila Fredy na Luka ndio wametoka nje”

“Luka ni nini kinacho endelea?”

Anjelina alizungumza kwa wasiwasi mwingi, ila hakuweza kupata jibu la aina yoyote jambo lililo anza kumchanganya yeye kijana wake aliye baki naye, kwani anacho kifahamu yeye, oparesheni hii ni ya siri sana na hata hawajaishirikisha serikali ya nchini Tanzania, kitu kilicho zidi kuwapa hofu kubwa sana na maswali yaliyo kosa majibu kabisa vichwani mwao.



“Tuitoe hii miili hapa”

Shamsa alizungumza, kwa haraka wakaanza kuivuta miili hiyo na kuikalisha pembezoni mwa gari letu.

“Mimi naruka ukuta wewe simama getini hapo sawa”

Shamsa alitoa melekezo hayo huku akimtazama Sa Yoo usoni mwake.

“Sawa”

Sa Yoo kwa haraka akakimbilia hadi getini, Shamsa akaupande ukuta huo kwa haraka sana. Akachungulia ndani na hakuona dalili yoyote. Akashuka ukuta huo kwa umakini sana, akaanza kukimbilia ndani, Sa Yoo akafungu geti dogo na kuchungulia ndani, alipo muona Shamsa akikimbia kwa mwendo wa haraka. Sa Yoo na yeye akaingia ndani.

Anjelina kwa haraka kamshika mama Adrus mkono, akamuwekea bastola ya kichwa na kumuamrisha kutoka ndani humo. Mama Adrus akatii amri huku bado woga ukiwa umemtawala, wakaanza kushuka kwenye ngazi za kuelekea sebleni. Shamsa kwa haraka akaingia ndani humo, risasi iliyo mpunyua na kupiga mlangoni ikamfanya kwa haraka kuinama chini. Akajiviringisha hadi kwenye moja ya nguzo. Msaidizi wa Anjelina akaendelea kufyatua risasi kwenye nguzo aliuo jificha Shamsa.

Anjelina kwa haraka akamkalisha mama Adrus kwenye moja ya ngazi na yeye akaanza kuelekeza mashambulizi kwenye nguzo ya hiyo iliyo tengenezwa kwa saruji. Shamsa akashusha pumzi huku akisikilizia jinsi risasi zinavyo endelea kupigwa. Sa Yoo kwa umakini akachungulia ndani kupitia dirisha la hapo sebleni akamuona mwanaume huyo jinsi anavyo pambana kumuua Shamsa. Taratibu Sa Yoo akafungua dirisha hilo la kioo, akamuweka mwanaume huyo kwenye tageti ya bastola yake, akarudhusu risasi kadhaa zilizo mpata mwanaume huyo mwilini mwake barabara.

Mama Adrus alipo ona msaada umepatikana, hakuhitaji kujilegeza akamtazama Anjelina aliye simama pembeni yake huku akifyatua risasi. Kwa haraka akamsukuma Anjelina aliye pepesuka na kuanguka na kubingiria kwenye ngazi hizo. Shamsa aliweza kuliona tukio hilo ikawa ni nafasi yake ya pekee kujitokea kwenye ngazi hiyo, kwa har aka akaliruka sofa lililopo mbele yake na kuiwahi kuipiga teka bastola ya Anjelina ambayo aimeangukia mbali kidogo.

Shamsha akamuelekezea Anjelina bastola ya kichwa.

“Huwa ninajisikia vibaya sana kumua msichana mwenzangu, ila kumuua mwanaume yoyote kwangu ni jambo rahisi sana, hivyo ninakuonya usifanye ujinga wa namna yoyote umenielewa dada”

Shamsa alizungumza huku akimkazia macho Anjelina aliye lala chini na kukubalian ana hali halisi inayo endelea katoka eneo hilo kwani kama vijana wake wote watatu wameuwawa na wasichana hawa basi hata yeye kuuwawa ni jambo rahisi sana.

***

“Muda tulio wapatia Marekani nahisi unazidi kwenda, tunafanyaje mkuu?”

“Nahitaji kufanya shambulizi moja la mwisho, wametuulia vijana wetu vya kutosha, sasa ni muda wa kuhakisha kwamba tuna wapa fundisho jengine”

Mkuuw a kundi la Al-quida alizungumza huku wakitazama tv dogo inayo muonyesha Charity mtoto wa raisi Dustan akiwa ndani ya chumba maalumu walicho mfungia na kina kamera mbili za ulinzi zinazo muonyesha Charity kila kitu ambacho anaweza kukifanya ndani ya chumba hicho.

“Ni shambulizi gani mkuu utalifanya kwa maana ndege wameweza kuiokoa na hakuna abiria yoyote aliye weza kufa. Na habari nilizo zipata kwa mtu wetu ndani ya ikulu ya Marekani wanadai kwamba Adrus ndio amehusika katika kuikoa”

“Shii……tiii huyu mtu ni hatari sana endapo wakishirikiana naye”

“Hilo halina shida muheshimiwa ila ukweli ni kwamba mtu huyo ameweza kuwasaliti wa Marekani na hadi inavyo zungumza hivi sasa wanamtafuta kwa udi na uvumba”

“Weeee”

“Ndio mkuu, inavyo onyesha kuna jambo ambalo linaendelea”

“Tutampatua wapi mtu huyo”

“Kama Wamarekani wameshindwa kumpata basi hata kwetu inaweza kuwa ni kazi ngumu sana kumpata”

“Wamarekani ni Wamaeekani na sisi ni sisi, hatuwezi kujifananisha nao sawa. Hakikisha kwamba unampata Adrus haraka iwezekanavyo umenielwa”

“Sawa mkuu, ila tunamtafuta kwa mema au mabaya?”

“Kwa mabaya yatatukuta mabaya, ila inabidi tymtafute kwa mema, ili tuweze kupata yaliyo mema zaidi”

“Ila ninaushauri mkuu”

“Zungumza”

“Kama itawezekana ninakuomba tusishambulie Marekani kwa sasa kwa maana nina imani kwamba wameimarisha ulinzi mkali sana katika kila eneo. Tujitahidi nasi kwa njia yetu tuweze kumpata huyu kijana”

“Sawa, ila hakikisha katika kumtafuta kwenu munakuwa makini kwa maana si unajua muda wowote na wakati wowote anaweza kuwa adui yetu”

“Nalifahamu hilo mkuu”

“Sawa”

***

John akiwa ameambatana na vijana wake wapatao ishirni, wakafika nchini Marocco ambapo ndipo ameamua kuweka makazi yake kwa kipindi hichi anacho jaribu kuhakikisha kuunda upya kikosi chake cha kazi.

Baada ya kupokelewa kwenye bandari ya siri, moja kwa moja wakaelekea katika hoteli waliyo fikia dokta Ranjiti na mwanaye Anna.

“Habari yako mzee”

“Salama karibu sana mkuu”

“Shukrani”

John alizungumza huku akiwa amembaba Junion Jr ambaye tayari amesha mzoea John.

“Huyu ndio mtoto wa Eddy?”

Dokta Ranjiti alizungumza huku akimtazama Junion Jr

“Yaa ndio mtoto wake huyu”

“Jamaa sura zake hazipotei”

“Kweli kabisa”

Wakaka kwenye sofa zilizopo hapo sebleni.

“Pole na safari”

“Nashukuru, vipi katika siku mbili tatu hizi ulizo kaa hapa kuna usumbufu ambao umeupata?”

“Hapana mkuu, nimekaa salama. Huku sidhani kama Eddy anaweza kufika”

“Usizungumze hivyo kwa maana ninamulewa Eddy, huku anaweza kufia ila jambo la muhimu kwa muda huu ni kuhakiksha kwamba ulinzi unakuwa mzuri”

Anna alipo sikia mazungumza hayo akatoka chumbani kwake, macho yake yakakuta na macho ya John, wakatazamana kwa sekunde kadhaa, kisha wote kwa pamoja wakajikuta wakiweka tabasamu pana.

“Habari binti”

“Salama”

“Ahaa…Anna huyu ndio yule mkuu wangu niliye kuwa ninakuambia, na mkuu huyu ndio binti yangu wa pekee kabisa katika maisha yangu”

“Nashukuru kumfahamu”

“Una mtoto mzuri”

Anna alizungumza huku akimtazama John

“Mchukue ucheze cheze naye”

“Na ninavyo pemba mtoto, niuzie”

“Hahaaa, usijali”

Anna akambabe Junion Jr na kuingia naye chumbani kwake.

“Mzee umekuza, unaonaje nikawa mkweo”

“Mkwe tena mkuu”

“Yaa kwani kuna tatizo hapo mkuu wangu?”

“Hapana ni heshima kubwa sana ambayo umenipatia”

“Kwa hiyo umekubaliana nami?”

“Asilimia mia moja”

Dokta Ranjiti alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

***

“Hivi ile laptop uliweza kuibeba?”

“Ipi baby?”

“Ile Laptop iliyokuwa ya mzee”

Eddy alizungumza huku akimtazama Phidaya usoni mwake.

“Yaa ipo ndani kule kwenye kabati”

“Twende ndani”

Eddy kwa ishara akawaita walinzi wake ambao walianza kuvisukuma viti hivyo vya matairi walivyo vikalia. Wakaingizwa hadi sebleni na kuwakuta dokta Benjamini na nesi wakiwa wamekaa kwenye sofa za eneo hilo.

“Dokta kumbe bado upo?”

“Ndio muheshimiwa”

“Inabidi sasa uende kwako ukapate mapumziko”

“Shukrani muheshimiwa”

“Walinzi wangu watakupelekea hadi kwako”

“Inabidi nirudi kwanza hospitali ili niweze kusaini mapumziko ya siku hii”

“Hapana, chukua mapumziko ya wiki nzima”

“Shukrani muheshimiwa”

Dokta Benjamini akaaga na kuaondoka akiwa ameongoza na wauguzi wake alio kuja nao katika eneo hilo.

“Ngoja nikaumuangalie mtoto”

Phidaya alizungumza huku akielekea katika chumba alicho lazwa Camila, Eddy moja kwa moja akaeleka katika chumba chao. Akafungua kabati kubwa la nguo, akaiona laptop ya mzee Godwin. Akaichukua na tataratibu akaifungua na kuipakata kwenye mapaja yake. Akaiwasha, akashusha pumzi taratibu, kwani anatakiwa kuingiza namba za siri. Zoezi hilo la kuingiza namba za siri siku zote huwa linamshinda pale anapo kuwa ameishika laptop hiyo. Akajaribu kuandika jina la mama yake, ila halikuwa neno sahihi lililo weza kuifungua laptop hiyo.

‘Baba alikuwa anapenda nini?’

Eddy alijiuliza huku akijikuna kichwa chake.

‘VANILA’

Eddy akaliingiza jina hilo, kwa bahati nzuri akafanikiwa kufungua. Akaanza kushangilia kwa furaha kwani kwa kupitia laptop hiyo anakwends kusambaratisha kikosi kizima cha D.F.E kwani wanachama wake wengi ni wa siri sana na wengine wapo katika serikali anayo iongoza.



Eddy taratibu akaanza kupitia faili moja baada ya jengine. Mafaili hayo yote yamehifadhiwa siri nzito pamoja na majina ya viongozi wengi sana ambao ni wanachama wa kikosi hicho. Phidaya akaingia ndani ya chumba hicho huku akiwa amempakata Camila miguuni mwake.

“Eddy”

“Mmmm”

“Mtoto anaumwa”

Phidaya alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.

“Anaumwa?”

“Ndio hembu mshike”

Phidaya alizungumza huku akimsogelea Eddy, Eddy akakiweka kiganja chake shingoni mwa Camila na kukuta akiwa na joto kali sana. Zoezi la kuendelea kutafuta ni nani mwanachama wa D.F.E katika laptop hiyo likaishia hapo. Heka heka za kutoa chumbani humo zikaanza huku wakijitahidi kuendesha viti vya matairi walivyo vikali ili wafike nje na kuweza kuwataarifu walinzi wao juu ya hilo tatizo la Camila ili awahishwe hospitalini haraka iwezekanavyo

***

Gari za polisi zipatazo kumi zikafika katika eneo la nje ya jumba la mama Adrus, hii ni baada ya wasamaria wema kuweza kupiga simu katika kitua kioo cha kati, na kuwataarifu kwamba kuna milio ya risasi imeweza kusikika eneo hilo. Ving’ora hivyo vya gari za polisi vikwafanya Sa Yoo na Shamsa kustuka sana, kwani Eddy aliwaeleza kwamba tukio hilo waweze kulifanya kisiri sana kwani halihusiani kabisa na serikali. Sa Yoo kwa haraka akapandisha hadi gorofani, akaingia kwenye chumba cha mama Adrus alicho kikuta kipo wazi, akafungua pazia na kuchungulia nje, hakuamini kuona kundi kubwa la askari wenye silaha. Kwa haraka akatoka chumbani humo na kurudi sebleni na kumkuta Shamsa akiwa emeendelea kumdhibiti Anjelina.

“Vipi?”

“Kuma polisi wengi sana wapo nje”

“Shiti unakuwaje sasa?”

“Hata mimi sielewi itakuwaje”

“Mpigie Eddy”

“Nitampigia kwa namba gani ikiwa namba yake siifahamu”

“Na simu yake sijui atakuwa ameiweka wapi”

“Oohoo sasa tunafanyaje?”

Mama Adrus akaendelea kuwatazama Shamsa na Sa Yoo ambao tayari wamesha changanyikiwa.

“Kuna sehemu ambayo tunaweza kutokea humu ndani pasipo watu kutuona”

Maeno ya mama Adrus kidogo yakamwapa matumaini Sa Yoo na Shamsa.

“Ni wapi?”

“Huku”

“Nyanyuka”

Shamsa alizungumza huku akimtazam Anjelina, wakaingia kwenye moja ya chumba. Mama Adrus akafungua mfuiko mkubwa sana wa chumba.

“Kuna ngazi za kuingia huko chini”

Mama Adrus alizungumza, Sa Yoo akaingia taratibu huku akiwa ameishika bastola yake kwa umakini sana. Shamsa kwa ishara akamumrisha Anjeliana kuingia chini humo. Mama Adrus akaingia kisha akamalizia Shamsa na kuufunga mfuniko huo ambao kwa haraka haraka mtu akiingia ndani ya chumba hicho wala hawezi kihisi kama kuna mlango wa kuingilia chini ya ardhi. Mama Adrus akaanza kuongoza njia ili kutoka ndani ya hili jumba lake.

“Mumefanya kosa kubwa sana, musihihisi kama taifa la Marekani litakuja kuwaacha hivi hivi”

Anjelina alizungumza huku Shamsa akiwa nyuma yake.

“Hahaaa, eti eheee. Siogopi kufa, kwani kama ni kufa ningekufa jana usiku na si leo”

“Huku”

Mama Adrus alizungumza huku akikinja kona, uzuri wa njia hiyo ya chini ya ardhi ina taa zeenye mwanga hafifu ambazo zinawawezesha kuona ni wapi wanapo kwenda.

“Hii uliitengeneza wewe?”

Sa Yoo alizungumzahuku akimfwata mama Adrus kwa nyuma.

“Hapana, mzungu aliye niuzia hii nyumba aliweza kunionyesha hii njia. Akaniambia enepao inatokea ninapata tatizo basi ninaweza kutorokea huku na tunatokea ufukweni”

“Ahaa sawa sawa”

Kama maelezo ya mama Adrus alivyo zungumza, wakatoka katika ufukwe mkubwa wa bahari, ulipo katika eneo la hilo la Mbezi Beach.

“Kule ndipo tulipo tokea”

Mama Adrua aliwaonyesha nyumba yake inayo onekana kwa mbali sana.

“Duu kweli, wazungu huwa wanajiongeza”

“Sa Yoo fanya utaratibu wa usafiri basi”

“Poa”

Sa Yoo akaanza kutembea kwenye ufukwe huo, akafika katika barabara ya lami iliyo tulia na ni magari machache sana ambayo yanapita katika eneo hilo. Akaona gari aina ya Alteza ikija kwa mwendo wa taratibu, kwa haraka akasimama barabarani huku bastola yake akiwa ameificha kwa nyuma. Akapunga mkono kama wafanyavyo maaskari usalama barabarani, dereva wa gari hilo mwenye asili ya kihidi, akasimamisha gari pembeni ya barabara, huku akimtazama binti hiyo mzuri aliye msimamisha. Sa Yoo akamsogelea hadi katika kioo chake, taratibu akainama huku macho yake akiwa ameyaweka katika hali ya kimtego ya kimahaba.

“Hii”

“Hii..hahaaahhaa”

Muhindi huyo mwenye kitambi kikubwa kinacho karibia kugusa mmskani wa gari hilo, alizungumza huku akijichekesha chekesha akirogeka kwa jicho zuri la Sa Yoo.

“Kwa haraka Sa Yoo akamminya mshipa wa fahamu baba huyu na kumfanya azimie hapo hapo. Akatazama eneo hilo la barabarani lililo jaa minazi mingi, kwa haraka akafungua mlango akamza kumtoa mwanaume huyo. Tukio hilo, Shamsa na wezake waliweza kuliona. Wakafika katika eneo hilo na kumkuta Sa Yoo akimalizia kumshusha mbaba huyo ndani ya gari.

“Hee ni lizito hilo akhaaa, sijui linakilo ngapi?”

Sa Yoo alizungumza huku akishusha pumzi nyingi sana kwa kuchoka”

“Pole, endesha”

“Poa”

Shamsa na Anjelina wakaingia siti za nyuma za gari hilo huku Sa Yoo na mama Adrus wakikaa siti za mbele. Kwa mwendo wa haraka wakaondoka katika eneo hilo.

“Yule mwanaume muliye muacha pale chini inakuwaje?”

Mama Adrus aliuliza kwa sauti iliyo jaa mtetemesho wa woga mwingi ulio mjaa.

“Atapata msaada”

Sa Yoo alizungumza huku akitazama kioo cha pembeni cha gari hilo.

***

K2 na kaka yake wakafika ikulu. Moja kwa moja wakapelekwa katika sehemu maalumu ya kupumzikia. Ili waweze kumsubiria raisi Rahab aweze kumaliza kikao na wakurugenzi wote wa mikoa.

“K2 unahisi wazo lako linaweza kuzaa matunda?”

“Kaka kila kitu niachie mimi. Mimi nitajua nini cha kuzungumza nini cha kupangilia. Siku moja lazima uje kukaa hapa ikulu”

“Usijali mdogo wangu, ninakuaminia. Kichwa chako kina mipango uliyo madhubuti. Mungu atujalie katika hili”

Wakaka zaidi ya robo saa, dada mrefu aliye valia suti nyeusi iliyo mkaa vizuri mwilini mwake, akaweza kufika katika eneo hilo walilo kaa.

“Munaweza kunifwata”

“Sawa”

K2 na kaka yake wakanyanyuka kwenye viti vyao, na kuanza kumfwata msichana huyo anaye tembea kwa mwendo wa haraka. Wakafika kwenye moja ya mlango, akagonga kidogo na suati ya Rahab ikasikika ndania akimruhusu aweze kuingia ndani. Msichana huyo akawafungulia mlango na wakaingia ndani.

“Habari yako muheshimiwa raisi”

K2 alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Salama tu karibuni”

“Habari muheshimwia”

“Salama tu, karibuni mukae kwenye viti”

“Asante sana”

“Tunaweza kutambuana kwa majina na nafasi labda mulizo nazo kwenye jamii nzima ya Watanzania”

“Akaa mimi ninaitwa John Kardin, huyu ni mdogo wangu anaitwa Khatherina Kardin kwa juna la kifupi anaitwa K2. Sisi ni waduau wa maendeleao hapa nchini. Pia mimi nina miliki baadhi ya biashara kubwa, kama vile Sheli, hoteli, mabasi na mambo mengi sana”

“Sawa sawa nashukuru sana kuweza kulifahamu hilo, vipi dada kwa upande wako unamiliki nini?”

“Mimi nina kampuni yangu inayo jishuhulisha na ulinzi wa makampuni binafsi pamoja na ulinzi wamtu mmoja mmoja yule mwenye haja na hitaji la kuweza kupata ylinzi”

“Waooo ni safi sana kwa mwanamke kuwa na maendelea kama hayo nina imani kwamba si wanawake tu unao wamiliki, hata wanaume pia unawamiliki”

“Yaa ni kweli muheshimiwa raisi”

“Sawa sawa, labda ni nini haswa kilicho waleta hapa?”

Rahab alizungumza huku akiwatazama usoni mwao.

“Lengo kubwa lililo tuleta hapa, ni kushauri jambo moja ambalo nina imani kwamba linaweza kuimarisha ulinzi mzima wa taifa kwa ujumla. Nimeweza kufwatilia baadhi ya matukio ya uhalifu yanayo tokea hapa Tanzania, nimeweza kugundua vyombo vya usalama, kama jeshi la polisi, usalama wa taifa vinahitaji kuongezewa nguvu ya ziada, nilikaa nikaona kwamba kama ukiridhia, serikali yako iweze kuanzisha kikosi ambacho kitakuwa kinayafwatilia matatizo ya kiserikali kwa utandani zaidi na kwa haraka kuliko, jeshi la polisi au usalama wa taifa”

Rahab akaka kimya huku akimtazama K2 usoni mwake kwa umakini sana.

“Chombo hicho kitakuwa kina weza kuimarisha ulinzi kuanzia kwako. Vijana wa kikosi hicho watakuwa wanapata mafunzo makali na ya uwezo wa juu ambayo yanaweza kuwafanya vijana hao kuwa ndio kikosi bora cha ulinzi hapa nchini Tanzania”

“Nimekuelewa K2 ila swala kama lako, hilo sio la kwangu peke yangu kwamba nitalianzisha tu, hapana ni lazima nikae na wa kuu wa vyombo ya ulinzi, tulijadili tulipitie kisha tutafahamu ni nini cha kufanya baada ya hapo”

“Sawa muheshimiwa raisi nimekuelewa sana, nitatoa msaada wa hali na mali kuhakikisha kwamba nchi yangu inaendelea kuwa salama siku hadi siku”

“Sawa shukrani kwa mawazo yako na kujitoa kwako”

“Shukrani nawe pia”

K2 na kaka yake wakaagana na raisi Rahab na kutoka nje ya ofisi yake.

“Ila mbona kama anauonekana mgumu sana?”

“Usijali kaka yeye mwenyewe atakubali”

“Ila kama simuamini”

“Usijali kaka tusubirie tuone ni kitu gani ambacho kitatokea na kuendelea”

***

“Muheshimiwa ninaona ni vyema daktari akaletwa hapa nyumbani kwa maana dokta Benjamini bado hajafika mbali”

Mlinzi mmoja wa Eddy alishauri huku akiwatazama usoni Eddy na mke wake.

“Mpigie sasa aje hapa nyumbani”

“Sawa muheshimiwa”

Mlinzi huyo akafanya kamaa alivyo agizwa na Eddy. Baada ya taarifa kumfikia dokta Benjamini, ikawalazimu dereva wa gari lao hilo la wagonjwa kugeuza na kuanza kurudi nyumbani kwa makamu wa raisi huku akiwa amewasha ving’ora vya hari hilo vilivyo sababisha gari nyngine kuweza kulipisha barabarani.

“Baby mtoto wangu atapona kweli?”

Phidaya alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Atapona mke wnagu usiwe na wasiwasi”

“Anazidi kuwa wa moto hembu mshike”

Eddy akamgusa mwanaye, wasiwasi kwa upande wake naya ukaanza kumpanda kwani hali ya mtoto wao Xamila inazidi kuwa mbaya kadri muda unavyo zidi kuongezeka.

***

Taarifa ya kuuwawa kwa majasusi watatu wa Kimarekani, zikafika ikulu kwa raisi Rahab.

“Kwani kulikuwa na taarifa ya wao kuja nchini hapa Tanzania?”

Rahan aliuliza huku akimtazama sekretari wake wakielekea katika chumba cha mawasiliano.

“Hapana muheshimiwa”

“Sasa nao wataingiaje kufanya kazi nchini pasipo idhini ya nchi kuweza kufahamu”

Rahab aliuliza hukua kiingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta wataalamu wa computer wakiendelea kufanya kazi za kuweza kuwatafuta ni kina nani wahusika wa tukio hilo.

“Mume wapata?”

“Ndio muheshimiwa raisi”

“Nionyesheni picha zao”

Kijana huyo akaminya minya batani za laptop yake na picha za Shamsa na Sa Yoo zikaonekana kwenye tv kubwa iliyomo ndani ya chumba hicho, jambo lililo mfanya Rahab kushanganaa na kushindwa hata kumeza mate mdomoni mwake, kwani anawaelewa vizuri sana wasichana hawa.



Rahab kwa haraka akatoa simu yake mfukoni, akaitafuta namba ya Eddy. Kwa haraka akaipiga, ila kwa bahati mbaya akakuta haipatikani. Akaitafuta namba ya Phidaya akaipiga, ikaanza kuita hadi ikakatika.

“Nitafutie namba ya mkuu walinzi katika nyumba ya makamu wa raisi”

“Sawa muheshimiwa”

Haikuchukua muda namba hiyo ikapatikana, wa haraka Rahab akaipiga, ikaita kwa muda na ikapokelewa.

“Unazungumza na raisi”

“Vipi?”

Rahab akastuka kidogo, baada ya kuisikia sauti ya Eddy akizungumza.

“Eddy kuna tatizo, tena ni serious issue”

“Inahusian ana nini tena jamani?”

Eddy alizungumza kwa kulalamika.

“Mabinti wako wamefanya mauaji ya wanausalama watatu wa Marekani, sasa unaweza kunieleza juu ya hili swala?”

“Mauaji!!?”

“Ndio wamewaua wanausalama”

“Hembu ngoja kwanza nakupigia”

***

Eddy akakata simu mara baada ya kuona gari aiana ya Alteza ikisimama kweye maegesho ya magari katika eneo hilo, akawaona Shamsa, Sa Yoo, mama Adrus na binti wa Kimarekani wakishuka katika gari hilo.

“Waambie wanione hao mabinti sawa”

Eddy alimuambia mlinzi aliye simama karibu naye.

“Sawa mkuu”

Gari la wangojwa nalo likaingia katika eneo hili, dokta Benjamini kwa haraka akashuka kwenye gari akapelekwa hadi katika chumba alichopo Phidaya na mwanaye Camila.

Shamsa, akamfwata Eddy sehemu alipo kaa.

“Mumefanya nini huko?”

“Kivipi?”

“Kwa nini mumefanya mauaji ya watu ambao hawpao kwenye mpango kama tulivyo zungumza?”

“Eddy ulitaka uje kuona maiti zetu au, tumefanya kama vile ilivyo tubidi sisi kuweza kufanya”

Eddy akaka kimya huku akimtazama Shamsa usoni mwake.

“Haikuwa kazi rahisi kama ulivyo hisi, tuliwakuta hao Wamarekani wakiwa tayari wamesha mchukua huyo mama, unahisi sisi tungefanyaje, ikiwa sio swala la kwenda kuobembelezana au kukubaliana. Walifyatua risasi na sisi tukafyatua. Ikawa hivyo ilivyo kuwa”

“Picha zenu zimeweza kuonekaa mukiwa munafanya tukio la mauaji ya hao majasusi”

“Mmmmmm”

“Ndio hivyo hii, ishu inakwenda kuwa kubwa sasa.”

“Ahaa utajua jinsi ta kutulinda sisi. Mama yule pale, na yule pale ni kiongozi wa hao majasusi, ikiwezekana naye tumuua ili kuibeba kesi mazima”

“Acha usimuu, muwekeni katika chumba cha siri, hakikisheni hana simu, hana chochote kinacho weza kuwaashiria wezake eneo ambalo yeye yupo”

“Sawa”

Shamsa akaondoka, Eddy akampigia simu Rahab, ili waendelea na mazungumzo aliyokuwa ameyakatisha.

“Ndio”

“Ndio hiyo, mabinti wako wamefanya mauaji ambayo yatakwenda kutuingiza sisi na Marekani katuka kipindi kigumu cha urafiki wetu”

“Walikuja labda kufanya nini Tanzania, uliidhinisha juu ya hilo?”

“Lipi?”

“Hilo lililo waleta huku?”

“Hapana sikuidhinisha mimi, kila kitu wamekifanya kama walivyo kifanya wao wenyewe”

“Basi tuna ponti ya kujitetea katika hilo, sisi hatuwezi kutuma vijana wetu kwenda Marekani pasipo idhini yao wao na kama wao walihisi hii ni nchi yao basi yametokea ya kutokea, wakaushe”

“Hii yote imetokana na yule kijana Adrus kukataa kufanya kazi na Wamarekani?”

“Lazima akatae kwa maana ulimlazimisha kufanya kazi ya ajabu. Marekani na ukubwa wao wote katika kila taasisi wanashindwa kwenda kumtafuta huyo binti wa raisi wao hadi wamtumie Adrus, kumbuka kwamba wanao walio kuwa wanakwenda kudili nao si watu wa kawaida, ni magaidi, ambao ndio waliiangusha ndege aliyo kuwa amependa Adrus”

“Sasa Eddy hapo tunafanya nini?

“Hakuna kunzungumza na kiongozi wowote wa Marekani kwa sasa, acha kwanza tufanyek kazi ya kulijenga taifa letu, kwa maana walio ufanya wao ni uharamia katika nchi yetu”

“Ila Eddy kuna kosa moja ambalo nimelifanya, ninakuomba nikueleze tu”

“Zungumza?”

“Niliweza kuidhinisha kwa maneno Wamarekani wafanye chochote kwa Adrus”

“Hata kumuua?”

“Ndio”

Eddy akashusha pumzi taratibu.

“Unahitaji msaada mkubwa sana katika utendaji wako wa kazi”

“Ni kweli Eddy, yaani hapa natamani kuiacha hii kazi, hii kazi inanishinda Eddy wangu”

“Cha kufanya hivi sasa, hakuna kuzungumza na kiongozi wa Marekani, awe ni raisi wao, makamu au balozi wao hakuna kuzungumza nao. Umenielewa?”

“Eddy ninakuomba uje ikulu, nakuomba uje unisaidie, ninaogopa Eddy”

“Ngoja niangalie hali ya mtoto wangu, kisha baada ya hapo nitakuja?”

“Sawa Eddy”

“Poa badaye”

Eddy akakata simu yake na kumtazama mkuu anaye simamia kikosi cha ulinzi katika nyumba yake hii.

“Baada ya nusu saa niandalie msafari ninaelekea ikulu”

“Sawa muheshimiwa”

Eddy akaingia ndani ya chumba alichopo Phidaya na dokta Ranjiti. Akamkuta Phidaya akiwa amemkumbatia Camila huku akilia jambo lilio yafanya mapigo ya moyo ya Eddy kuanza kumuenda mbio.

***

Mshauri wa raisi Dustan akaingia ofisini mwa raisi Dustan huku akiwa amejawa na huzuni iliyo changanyikana na hasira.

“Vipi umefanikiwa?”

Raisi Dustan aliuliza huku akiacha kile anacho kiandika.

“Samahani muheshimiwa, hawajafanikiwa na kwa bahati mbaya wameweza kuuwawa watatu na mmoja hadi hivi sasa hajulikani ni wapi alipo”

“Ohooo Mungu wangu, ni nani ambaye amehusika katika hilo swala?”

“Kuna picha ya wasichana ambayo imeweza kupatikana, kwa maelezo ya ufupi wasichana hao wawili wana mahusiano ya karibu kabisa na makamu wa raisi wa Tanzania”

“Mmmmmm”

“Yaa”

“Inabidi wasichana hao waweze kupatika, lazima tuwachukulie sheria”

“Muheshimiwa tukumbuke kwamba majasusi wetu waliweza kwenda kimya kimya, hatukuweza kuitaarifu serikali ya Tanzania”

“Hata kama hatuwezi kupoteza vijana wetu, kumbuka kwamba wana thamani kubwa kuliko hivyo unavyo fikiria, isitoshe hata huyo mtu tuna muhangaikia kwa kiasi hicho hana msaada wowote na sisi kwa hivi sasa”

“Sasa tunafanyaje muheshimiwa?”

“Mpigie simu raisi Rahab, na umuambie nahitaji kuzungumza naye sasa hivi?”

“Sawa mkuu”

***

Simu ikaanza kuita na kuwafanya Jing, Cookie na Adrus kuitazama simu hiyo iliyo wekwa mezani na Adrus.

“Pokea”

Jing alimuambia Adrus huku akimtazama usoni mwake. Adrus akaichukau simu hiyo na kutazama namba hiyo na kugundua kwamba inatoka nchini Tanzaniaa, akaipokea na kuweka sikioni mwake.

“Haloo”

“Adrus zungumza na mama huyu hapa”

Adrus alisikia sauti ya Eddy, kauli hiyo ilimfurahisha.

“Mama”

“Mwanangu upo salama?”

“Nipo salama mama yangu, unaendeleaje?”

“Ninaendelea salama, na nipo salama na nimesha okolewa na hawa wasichana”

“Oooh asante Allah, utakaa hapo kwa muheshimiwa kwa kipindi chote adi hata matatizo yatakapo kwisha”

“Ila upo wapi mwanangu?”

“Nipo salama mama yangu, ila atakuambia muheshimiwa”

“Sawa mwanangu kuwa makini huko ulipo sawa”

“Sawa mama, naomba nizungumze na muheshimiwa”

“Ndio Adrus”

“Muheshimiwa ninaomba unitumie details za wahusika, ili kama ni kazi nianze kuifanya hivi sasa”

“Sawa, ninakutumia sasa hivi kwenye email”

“Sawa muheshimiwa”

“Utakapo wapata hakikisha kwamba unamuua dokta Ranjiti na mwanaye, ila kama utafanikiwa kumpata John hakikisha kwamba unamshikilia hadi pale nitakapo kutana naye mimi”

“Nimekuelewa muheshimiwa”

“Sawa, ndani ya dakika tano nitakuwa nimesha kutumia”

“Okay”

Eddy akakaya simu, Adrus akairudisha simu hiyo mezani.

“Ninaweza kupata computer iliyo unganishwa na Internet?”

“Nahisi inaweza kupatikana”

Jing akatoka chumbani humo na kuzungumza na mfanyakazi wa baba yake aliye wapokea katika kisiwa hicho. Baada ya muda kidogo akarudi akiwa amebeba laptop, akamkabidhi Adrus, aliye anaza kuifungua, akaingia kwneye email yake na kukuta ujumbe kutoka kwa Eddy, akafungua na kukuta picha na maelezo yanayo muelekeza ni eneo hani ambalo wahusika ambao anatakiwa kuwatafuta walipo.

***

Eddy akashusha pumzi nyingi sana baada ya kumuona Phidaya akitabaamu huku akimtazama Camila usoni mwake, kumbe machozi ambayo yalikuwa yakimwagika Phidaya yalikuwa ni machozi ya furaha.

“Baby mtoto anaendelea vizuri”

“Kweli?”

“Ndio mume wangu?”

“Dokta mtoto alikuwa na tatizo gani?”

Kabla dokta Benjamini hajazungumza chochote, mlango wa chumba hicho ukafunguliwa, akaingia Sa Yoo.

“Oohoo samahani”

“Bila samahani”

“Eddy tunaweza kuzungumza?”

“Ndio”

“Nakuomba nje, jamani samahani”

“Usijali?”

“Phidaya vipi mbona machozi yanakutoka?”

“Hapana Jojo, tutazungumza baadaye”

Sa Yoo akamsukuma Eddy hadi sebleni na kumkuta mama Adrus akiwa amekaa kwenye moja ya sofa.

“Habari yako mama”

“Salama baba, nashukuru sana kwa msaada wako”

“Usijali mama yangu, jisikie upo huru sana”

“Asante baba”

“Tena ngoja uzungumze na kijana wako”

“Sawa”

Eddy akaipiga namba ambayo Adrus anaitumia, simu ikaanza kuita baada ya muda ikapokelewa, akazungumza naye kidogo kisha akamkabidhi mama Adrus. Kwa ishara Eddy akamutia Sa Yoo aliye kaa kwenye moja ya sofa.

“Ndio”

“Ingia katika chumba changu cha kulala kuna laptop pale juu ya meza ninakuomba uniletee”

“Saswa”

Sa Yoo akingia katika chumba cha Eddy, kwa bahati nzuri akaikuta laptop hiyo juu ya meza,a akaichukua na kutoka chumbani humo na kumkuta Eddy akimalizia kuzungumza na simu. Eddy alipo kata simua kamkabidhi laptop hiyo.

“Sa Yoo nisaidie katika hili, hii laptop ina kila kitu cha siri kinacho husiana na D.F.E, sasa nahitaji unisaidie kutafuta location ya dokta Ranjiti sehemu alipo”

“Sawa”

Sa Yoo akaichukau laptop hiyo na kuipakata kwneye mapaja yake, akaanza kufanya kazi aliyo kabidhia na Eddy. Baada ya dakika tano akawa amefanikiwa kutambua ni wapi dokta Ranjiti alipo.

“Done”

Sa Yoo alizungumza huku akimgeuzia Eddy laptop hiyo.

“Ok mtumie Adrus kwenye hii email”

Eddy alizungumza huku akimtajia Sa Yoo email ya Adrus.

“Tayari”

“Poa”

“Samahani baba yangu, Adrus amaniambia niweze kukulize kwamba yeye yupo wapi?”

“Kwa sasa yupo nchini Brazil kuha kazi ataifanya huko baada ya muda atarudi nchini Tanzania”

“Sawa baba yangu nashukuru sana”

“Asante”

“Sa Yoo muangalieni yule muliye mteka, mimi ninaelekea ikulu sasa”

“Sawa”

Eddy akaingia katika chumba alipo Phidaya, alipo hakikisha kwamba afya ya mwanaye ipo vizuri, akatoka nje na kukuta msafara ukiwa tayari umesha andaliwa. Akaingia ndani ya gari na kuondoka katika nyumba yake.

***

“Muheshimiwa raisi kuna simu yako kutoka ikulu ya Marekani”

Sekretari wa Rahab alizungumza na kumfanya Rahab mapigo ya moyo kuanza kumuenda mbio.

“Waambie raisi kwamba yupo kwenye kikao”

“Sawa muheshimiwa, niwaambie baada ya muda gani utakuwa free?”

“Wewe waambie nipo kwenye kikao muhimu na siwezik uzungumza na sisi hivi sasa”

“Sawa”

Sekretari huyu akatoka na kumjibu mshauri wa raisi Dustan juu ya jibu ambalo amepewa na raisi Rahab. Rahab taratibu akasimama na kusimama kwenye dirisha kubwa lililipo katika ofisi yake, akatazama nje ambapo kuna bustani nzuri sana iliyo ja amaua ya kila aina ya rangi. Mlango wa ofisini kwake ukagongwa, akaugeuka na kukuta mlango ukifunguliwa pasipo idhini yake, akamuona Edd akiingia ndani humO.

“Ohoo afahadhali umekuja mpenzi, nilikuwa nakufikira hapa”

Rahab alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Ehee niambie hao wajinga wanasemaje?”

“Wametoka kupiga sasa hivi hapa na walikuwa wanahitaji kuzungumza nami ila nimefanya kama vile ulivyo niambia”

“Safi, nahitaji kuzungumza na raisi wao kwa video call”

“Kwa hiyo tumuambie sekretari azungumze nao?”

“Ndio muambie afanye hivyo”

“Ndio”

Rahab akanyanyua simu yake ya mkonga akampa malekezo sekretari wake, baada ya muda sekretari akaingia ndani ya ofisi hiyo.

“Tayari muhesimiwa unaweza kuwasha tv yako”

Eddy akaka mbele ya tv hiyo, Rahab akaiwasha na wote wakamuona raisi Dustan akiwa anasubiri kuzungumza.

“Nilikuwa ninahitaji kuzungumza na raisi Rahab na si wewe?”

“Mimi pia ni raisi, unaweza kuzungumza na mimi”

Raisi Dustan akatazamana na Eddy kwa sekunde kadha huku wote sura zao zikiwa zimejawa na hasira.

“Nahitaji kujua ni kwanini majasusi wangu wameweza kuuwawa katika ardhi ya nchi yenu?”

“Na mimi nahitaji kujua hao majususi wako, walikuja kufanya nini ndani ya nchi yangu pasipo idhani ya serikali yangu?”

Eddy hakujibu swali alilo ulizwa zaidi ya yeye kuuliza swali lililo mueweka raisi Dustan katika kigugumizi kizito kiliachoa mbatana na hasira kali hadi akatamani kumtukana makamu wa raisi Eddy Godwin.



“Ndio maana nilihitaji kuzungumza na raisi na si wewe makamu wa raisi ufahamu ni makubaliano gani ambayo niliingia mimi na raisi wako?”

“Makubaliano hayo hayakuwa si ya vijana wako kuingia katika nchi yangu, umekiuka maadili na mipango ya nchi yangu hivyo basi kaa ukifahamu kwamba hakuna kosa lolote ambalo vijana wangu wamefanya.”

“Ninakuambia makamu wa raisi hili swala litakwenda kuigarimu nchi yako”

“Hata wewe hili swala litakwenda kuigarimu nchi yako. Na labda nikupe onyo, usihisi kwamba nchi yako jni kubwa sana na unaleta mamlaka yako kwa nchi kama hii, kumbuka kwamba hii ni Tanzania, na si Marekani. Asante”

Eddy mara ya kumaliza kunzungumza hivyo akazima tv hiyo na kumtazama Rahab ambaye amakaa pembeni akiyasikilia majibizano hayo.

“Itisha kikoa na wakuu wote wa vikosi vyote vya kijeshi”

“Sawa”

Rahab akanyanyua mkonga wa simu yake na kuwasiliana na secretary wake. Akampa maelekezo ya kuwasiliana na wakuu wote wa jeshi ili kuhakikisha kwamba hadi inafika jioni ya siku hiyo wanakutana na kikao kinafanyika.

“Eddy”

“Mmmmm”

“Kuna watu walikuja hapa, mida ya asubihi na walinishauri juu y kitu kimoja ambacho kwa namna moja ama nyinine nimegundua kwamba ni kizuri”

“Kitu gani?”

“Wamehitaji tuanzieshe kikosi ambacho kitaweza kuilinda serikali kwa namna moja ama nyingine”

“Kwani vikosi vyote vya ulinzi havitoshi?”

“Lengo sio kwamba havitoshi, hapana. Ishu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunakuwa na nguvu. Kikosi hicho kitadili na mambo mengi sana hususani matukio ya siri ambayo ikulu kama ikulu ni lazima yayafanye”

“Utaalizungumza kwenye kikao cha leo”

“Sawa”

***


“Ni wapi walipo wahusika?”

Jing alizungumza huku akimtazam Adrus usoni mwake.

“Wapo Afrika katika kisiwa cha Magascar katika mji mkuu unaitwa Antananarivo”

Adrus alizungumza huku akinedelea kusoma malezo aliyo tumiwa na makamu wa raisi.

“Kutoka hapa Brazil hadi huko itatuchukua masaa mangapi?”

Cookie naye aliuliza

“Kwa upande wangu siwezi kufahamu kwa kweli”

“Labda nizungumze na baba, na tunaweza kutumia hata private Jet kwenda huko, nina imani kwamba Wamarekani watakuwa bado wanatutafuta”

“Yaa hilo litakuwa ni wazo zuri, itabidi pia nifanya mawasiliano na makamu wa raisi, ili aweze kunitumia pesa ambayo itanisaidia kuhakikisha kwamba tunaweza kuwa katika eneo hilo huku tukiendelea kufanya uchunguzi wetu wa kujua wahusika wapo wapi?”

“Pesa sio tatizo, nitajitoa kwa kila jambo kuhakikisha kwamba oparesheni hii infanikiwa na inakwenda vizuri sana”

“Asante Jing, umejitoa sana kwa ajili yetu”

“Musijali, nyinyi kwa sasa mumesha kuwa familia yangu, kwa maana tumeepuka kifo pamoja, tumepita katika hali ya hatari pamoja”

Jing alizungumza kwa upole huku akiwatazama kwenye nyuso zao

“Ninashukuru sana, kwa maana nyote mumewaza kujito kwa ajili yangu”

“Musijali, nimezungumza na huyu aliye tupokea, atatupeleka katika nyumba ya kumpumzikia ninaimani hapo tunaweza kupata huduma zote, ikiwemo chakula na maviazi”

“Sawa”

Wakatoka katika chumba hicho na wakapelekwa kwenye moja ya jumba kubwa la kifahri lililopo ndani ya kisiwa hicho.

“Hii laptop ninaweza kuendelea kuitumia?”

“Ndio hakuna tatizo”

“Nashukuru”

Adrus alijibu mwanaume huyo aliye wapokea katika kisiwa hicho.

“Kuhusiana na chakula kuna mpishi atakuja kuwapikia”

“Hapana mimi nipo vizuri kwenye swala zima la kupika chakula”

Adrus alizungumza na kuwafanya Cookie na Jing kumshangaa

“Yaa nipo vizuri wewe nenda tusikusumbue sana”

“Sawa niwatakie muda mwema”

“Nawe pia”

Mwanaume huyo akatoka chumbani humo na kuwaacha. Adrus akaanza kuzunguka eneo la ndani ya nyumba hiyo, alipo hakikisha kwamba ulinzi upo wa kutosha akarudi sebleni.

“Hii nyumba ipo poa”

“Yaa baba yangu amewekeza billions of dollar kuhakikisha kwamba anakijenga kisiwa hichi na kimekuwa hivi kilivyo kuwa”

“Amefanya kazi nzuri”

“Jikoni umepaona?”

“Yaa nimepaona, munataka niwapike chakula gani?”

“Mmmm ukipendacho wewe mpishi”

Jing alizunngumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Nawapikia chakula kimoja kinaitwa Ugali, samaki, mumesha wahi kukila?”

“Mimi bado”

“Hata mimi bado”

“Basi jiandaeni kula”

Adrus alizungumza huku akielekea jikoni na kuwaacha Cookie na Jing wakitazamana huku wakiwa wamejawa na hamu kubwa sana ya kula chakula hicho.

***

“Naweza kuingia?”

John alizungumza huku akimtazama dokta Ranjiti usoni mwake. Dokta Ranjiti akautazama mlango wa chumba cha Anna.

“Yaa unaweza kuingia hakuna tabu mkuu”

John taratibu akanyanyuka kwenye sofa na kuingia ndani ya chumba cha Anna na kumkuta akiwa amekaa kitandani akicheza chenza na Junion Jr.

“Mumependeza na mtoto”

“Hahaa, huyu mtoto kusema kweli nimempenda sana”

“Haa unaweza kuwa mama yake wa hiyari”

John alizungumza huku akijlaza pembeni yao.

“Mama, si ana mama yake na ninaimani kwamba atakuwa bado anatafutwa”

“Hawato weza kumpata kabisa”

John alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akitazama kifuani mwa Anna, ambapo kanguo alicho kivaa, kidogo kimeyaacha maziwa yake makubwa kiasi wazi. Uchu wa mahaba ukamjaa John, hakuhitaji kuyakwepesha macho yake hadi Anna akalistukia hilo.

“Ahaaa, ngoja nimpeleke mtoto kwa baba”

Anna alizungumza huku akishuka kitandani, akambeba Junion Jr na kutoka naye chumbani kwake, akamkuta dokta Benjamini akiwa amekaa kwenye sofa.

“Baba mchukue mtoto mara moja”

Dokta Benjamini akayatazama macho ya Anna na kugundua kinahco endelea, kama mtu mzima hakuwa na haja ya kungumza maneno mengi ikiwani muda mchache John alikwenda kumueleza juu ya ombi lake la kummuhitaji binti huyo mwenye urembo wa hali juu.

“Sawa”

Anna akaingia chumbani alipo muacha John, akaufunga mlango na kupanda kitandani, hapakuwa na haja ya kuelezana maneno mengi sana, wakajikuta wakiikutanisha midomo yao na kuanza kulana denda, lililo wapelekea kuanza kuchojoa nguo zao moja baada ya nyingine.

***

“Una nafasi ya kujieleza la sivyo utapotelea jela”

Mkuu wa upelelezi alizungumza huku akimtazama madam Mery, wakiwa ndani ya chumba maalumu cha mahojiano.

“Mumenikatalia kuniletea mwanasheria wangu, siwezi kuzungumza chochote hadi nimuone makamu wa raisi”

Madam Mery alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama mkuu huyu wa upelelezi.

“Makamu wa raisi hawezi kuja kukusikiliza gaidi kama wewe”

“Wewe kijana chunga mdomo wako, huyo makamu wa raisi unaye mzungumza hapa alikuwa ni mwanafunzi wangu, sasa tazama unacho kizungumza sawa?”

“Hahaaa, wewe umfundishe makamu wa raisi, unaota mama eheee?”

“Sioti ila ninacho kuambia ni kitu cha ukweli, sasa chunga kinywa chako usije ukapoteza kibarua chako”

“Nahisi utazungumza tu”

Kijana huyo kwa aishara akanyoosha mkono wake juu, wakaingia wanawake wawili warefu walio valia suti nyeusui, huku mmoja wao akiwa ameshika brufcase yenye vivaa malumu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba madama Mery anakwenda kuzugumza ukweli ni kwa nini alihusika katika tukio la kuwatorosha magaidi dokta Ranjiti na mwanaye.

“Hakikisha kwamba anazungumza ukweli”

“Sawa mkuu”

“Kijana hii ndio nafasi yako ya mwisho hakikisha kwamba unakuwa makini kwa hili unalo lifanya, endapo nitatoka humu ndani salama salami, nitahakikisha kwamba hicho kichwa chako kinakuwa chakula cha mbwa wangu”

Madam Mery alizungumza kwa hasira huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake, jambo lililo mfanya kijana huyo kuuanguka kicheko kizito kilicho washangaza hadi vijana wake walio ingia ndani ya chumba hicho.



“Munanishangaa nini, fanyeni kile nilicho waleza”

“Sawa mkuu”

Msichana mmoja akafungua brufacase hiyo, akatoa plaize, akamtazama madam Mery aliye anza kutetemeka mwili wake, akamsogelea hadi sehemu alipo, akalishika sikio la upande wake wa kushoto, na kuanza kulibana na plaize hiyo. Madam Mery akaanza kulia kwa uchungu sana kwani maumivu anayo yahisi ni makali kupindukia.

***

Jina la Mery, likapita kichwani mwa Phidaya kwa kasi sana. Akamtazama Camila aliye mshika mkononi mwake.

“Sa Yoo hembu mtazame mtoto”

Phidaya alizungumza huku akimkabidhi Camila kwa Sa Yoo aliyopo ndani ya chumba hicho.

“Vipi unakwenda wapi?”

“Ninataka kwenda nje”

Phidaya alizungumza huku akianza kusukuma magurudumu ya kitanda chake kwa kutumia mikono yake. Akafika nje, na kumuita mlinzi mmoja.

“Ndio madam”

“Unafahamu kuhusiana na yule mwanamke aliye watorosha magaidi, Ranjiti na mwanaye?”

“Hapana madam labda nifwatilie”

“Hembu fwatilia na uhakikishe kwamba unaniletea ripoti muda huu, nipo hapa ninakusubiria”

“Sawa madam”

Mlinzi huyo akaondoka, akamfwata mwenzake mmoja akauzungumza naye, kwa bahati nzuri huyo aliweza kufahamiana ni tukio hilo na anafahamu ni wapi madam Mery alipo.

“Yule mwenzangu anasema kwamba amechukuliwa na wana usalama wa kitengo cha upelelezi”

“Ni wapi alipo?”

“Makao makuu”

“Nipelekeni sasa hivi”

Mlinzi huyo akaka kimya kwa muda, kisha akatingisha kichwa cha kukubaliana na kile Phidaya alicho kizungumza.

“Unaitwa nani?”

“Peter”

“Haya”

Peter akawasiliana na wezake, na kuwaleeza juu ya safari hiyo ya dharura iliyo tokea. Wakaingia kwenye gari wakiwa na Phidaya mke wa makamu wa raisi. Safari ya kueleeka katika kitengo hicho ikaanza huku ukiwa ni msafara wa gari tatu, ambazo moja ilitangulia mbele na moja ipo nyuma ya gari alilo panda Phidaya.

“Madam samahani, ninaweza kukuuliza tunakwenda kufanyaje huko?”

Peter aliuliza kwa sauti ya upole sana, huku akimgeukia Phidaya aliye kaa siti ya nyuma.

“Ninahitaji kuonana na muhisika”

“Ahaaa….sijaelewa hapo”

“Mutajua huko huko”

“Sawa madam”

Hawakuchukua muda mrefu sana, wakawa wamefika katika kitengo cha upelelezi. Wakamshusha Phidaya kwenye gari na kukaa kwenye kiti chake hicho cha magurudumu kwani bado mguu wake ulio na jeraha la risasi bado haujapona vizuri. Wakaingia ndani, katika kitengo hicho chenye ulinzi mkali, na wafanyakazi wengi sana.

“Nipelekeni ofisini kwa mkuu wenu”

“Sawa”

Wakampeleka Phidaya hadi kwenye ofisi ya mkuuw a kitendo hicho cha upelelezi.

“Habari yako madam”

Kijana huyo alizungumza, Phidaya akasoma kibao kidogo kilichopo mezani na kimeandikwa jina la kijana hiyo.

“Mngulo si ndio?”

“Ndio madam”

“Nimekuja kuonana na madam Mery”

Kauli hiyo ikamstua sana Mngulo, kauli ya madam Mery aliyo zungumza kwamba alimfundisha makamu wa raisi ikaanza kumrudia kichwani mwake.

“Vipi mbona umestuka?”

“Ahaaa….muheshimiwa huyo mtu ni hatari sana”

“Uhatari wake ni upi?”

“Ahaa….kuwatorosha magaidi si jambo dogo muheshimiwa, atakuwa na mtandao mkubwa sana”

“Okay nahitaji kuonana naye sasa hivi, hii ni amri kutoka kwa mume wangu, nimekuja kumuwakilisha hapa”

“Sawa madam”

Ngulo akatoa simu yake na kumtumia kijana wake mmoja na kumsisitizia kwamba wasitishe zoezi la kumpa mateso madam Mery haraka iwezekanavyo.

“Mbona una mashaka masaka vipi?”

“Hapana madam”

Wakatoka ndani humo, huku Phidaya akilindwa na vijana wake alio kuja nao, kwani wao ndio wanajukumu la kulinda mke huyo wa makamu wa raisi. Wakaingia kwenye chumba cha mahojiano. Phidaya akamkuta madam Mery akiwa analia kwa uchungu sana, huku wasichana wawili wakiwa wamesimama pembeni yake.

“Phidaya asante kwa kuja, kwa nini ninanyanyasika kiasi hichi kwa nini wananibana kama gaidi, kwa nini lakini, kosa langu mimi lipo wapi jamani?”

Madma Mery alizungumza huku akiendelea kulia, Phidaya akamtazama Mngulo, akawatazama wasichana hao walio simama pembeni ya madam Mery, akamtazama mmoja wao akaona plaizi aliyo ishika mkononi mwake.

“Peter”

“Ndio madam”

“Wasiliana na makamu wa raisi na umueleze kila kitu juu ya hili swala”

“Sawa madam”

“Tena hakikisha kwamba unapiga picha wahusika wa hili tukio kisha mtumia Eddy”

“Ahaa….samahani madam mbona tunaweza kulizungumza hili swala na likawa sawa tu”

“Tena wewe usizungumze, si nilikuambia mimi, ukanicheka kwa dharau sana. Phidaya mdogo wangu, mtu wa kumshuhulikia hapa ni huyo kijana hapo, hawa mabinti wamefwata amri tu”

“Peter mpigie simu makamu wa raisi sasa hivi”

Phidaya alizungumza kwa ukali sana. Mngulo mwili mzima ukaanza kumtetemeka, akajikuta akitamani kurudisha muda nyuma ili ile dharua aliyo muonyeshea madam Mery aweze kuizuia, kwani hivi sasa inakwenda kumgarimu maisha yake na kibarua chake kwa umoja.

***

Mlango wa ofisi ya raisi Rahab, ukagongwa. Wakautazama kwa muda, kisha Rahab akamruhusu mtu anaye gonga kuingia. Akaingia mlinzi wa Eddy.

“Muheshimiwa kuna simu yako hapa”

“Kutoka wapi?”

“Kwa mrs”

Eddy akaichukua simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio”

“Eddy kuna kitu kimetokea kwneye sekta za watu wako kusema kwelis ijazipenda”

“Phidaya ni nini tena hicho”

“Madam Mery amekamatwa, na ameteswa kiasi kwamba anakaribia kufaa kweli ndivyo jinsi serikali yako inavyo endeshwa?”

“Amekamatwa na nani tena?”

“Na sijui wapepepelezi gani, na amepondwa amechakaa mama wa watu”

Eddy akafumba macho yake kwa muda kidogo kisha akayafumbua huku akimtazama Rahab usoni mwake.

“Mkuu wao ni nani?”

“Some body Mngulo, na amemkejeli sana madam Mery”

“Mpe simu kama yupo hapo”

“Wewe mjinga chukua simu”

“Halooo”

Eddy alisikia sauti ya kiume iliyo jaa mitetemesho mingi sana.

“Huyo mwanamama mume mfanyaje?”

“Aha…..tulikuwa tunamuhoji tu muheshimiwa”

“Kwa idhini ya nani?”

“A…aha……”

“Idhini ilibidi itoke kwangu, ya yeye kuhojiwa si matukio ameyafanya kwangu, ila kwa nini memejichukulia jukumu ambalo haliwahusu?”

Ukimya ukatawala Mngulo akakosa kabisa cha kujibu.

“Hakikisha kwamba munamuachia huyu huyo mama, mbili hakikisha kwamba anapata matibabu. Tatu andika barua ya maelezo ya kwa nini ulichukua jukumu masipo hidhini yangu, barua yako niikute kesho ofisini kwangu sawa?”

“Sawa muheshimiwa”

“Mpe simu mke wangu”

“Eheee?”

“Hakikisha kwamba madam anapatiwa matibabu”

“Na hili chini vipi umelisamehe?”

“Niyashuhulika naye, wewe hakikisha kwamba madam anapata matibabu kama ameumia sana”

“Sawa mume wnagu nashukuru sana”

“Sawa”

Eddy akakata simu na kumkabidhi mlinzi huyo.

“Kuna nini kinacho endelea?”

“Wamemshikilia madam Mery, wamempa mateso”

“Mmmmmm”

“Yaani kuongoza nchi jamani ni mateso”

“Sasa wewe Eddy unazungumza hivyo, mimi je. Yaani hapa natamani miaka mitano ifike nikukabidhi nchi, haki ya Mungu sinto hitaji hii kazi tena. Nataka muda wa kupumzika na kuachana na haya mambo ya kipuuzi aisseii”

“Ndio hivyo inabidi kujikata katika kuhakikisha kwamba hata tunapo kuja kuiachia nchi kwa watu wengine basi tumetengeneza mazingira mazuri ya kuhakikisha kwamba hawapati shida kama zile tulizo zipata sisi”

“Mmmm acha tu wapate tabu bwana, Eddy mimi nakuachia nchi kwa kweli, ninachoka. Sina muda wa kutulia, sina muda wa kulala. Sina muda wa kusema ninampango wa kupata mtoto jamania khaaaa, it’s too much”

Rahab alizungumza kwa msisitizo, ikonyesha dhairi kwamba amechoka kwa kweli katika kuongoaza nchi hiyo.

***

Adrus akamaliza kupika chakula na kukiandaa mezani, Cookie na Jing wakabaki kushangaa chakula hicho ambacho hawakuwahi kukila au kukiona tangu kuzaliwa kwao.

“Adrus umesema hiki chakula kina itwaje?”

“Ugali”

“Heee, tunakula kwa kijiko kwani?”

“Hapana, tunakula kwa kutumia mkono, ngoja niwaonyeshe”

Adrus akakata kipande kidogo cha ugali akaanza kukifinyanga taratibu. Alipo hakikisha tonge hilo limekaa sawa, akachovyo kidogo kwenye mboga na kulila. Jing naye akakata kipande kidogo cha ugali, akaanza kulifinyanga tonge hilo, ila hali kwake haikuwa nzuri kwani ugali huo uliweza kujitokeza kwenye nafasi za vidole vyake.

“Hahaa usitumie nguvu kufinyanga tonge, yaani ni taratibu tu”

“Jamani mimi linanishinda khaaa”

Adrus akaendelea kuwafundisha jinsi ya kufinyanga ugali, hadi wakafanikiwa kuweza. Wakaanza kula taratibu huku kila mmoja akimsifia Afrus kwamba anaweza kupika, na chakula wanacho kila ni kitamu sana.

“Jamani huyo Livna wenu tutaanza kumshuhulikia lini?”

Adrus alizungumza huku akiwatazama Cookie na Jing.

“Tumalize kwanza hiyo kazi uliuo pewa na makamu wako wa raisi”

“Kweli, kwa maana Livna ana kikosi kikubwa, hadi kumfikia yeye inahitaji akili nyingi sana”

“Munaweza kupata data za ndani ya kambi yake”

“Kivipi?”

“Kujua ni mipango gani ambayo ameipanga au ni watu gani ambao ameshirikiana nao”

“Mmmmm…..inawezekana, ila ana watu wengi wenye uwezo mkubwa wa kimtandao, ambao kazi yao masaa ishirini na nne ni kuhakikisha kwmaba wanalinda data za kikosi chao.”

“Ila kuna watu wa baba ambao nao pia wapo vizuri, kama ni kuiba data zao tunaweza kuwatumia hao na tukafanikiwa na sisi”

“Basi nitawaomba uweze kuwaanda”

“Sawa, safari ya kwenda Madakascar si kesho?”

“Yaa inabidi iwe kesho”

“Basi nitawasiliana na rafiki yangu wa muda mrefu anaishi huko, nitamuambia atuandalie kila kitu ambacho tunakihitaji”

“Sawa”

Wakaendelea kupanga mikakati yao, walipo hakikisha kwamba wamemaliza, Jing akaingia katika chumba chake cha kulala na kuwaacha Adrus na Cookie wakiwa wamekaa kwa pamoja katika seble kubwa iliyopo katika eneo hilo.

“Adrus”

“Mmmmm”

“Unanipenda kweli?”

“Yaa huamini?”

“Ninaamini ila nina wasiwasi kwamba unaweza kuniacha siku”

“Siwezi kufanya hivyo mpenzi wangu”

“Kweli”

“Ndio”

Cookie akamtazama Adrus, kwa muda kisha akamsogelea taratibu, wakaanza kunyonyana midomo yao. Adrus, taratibu akaifungua zipu ya suruali ya Cookie, akaingiza mkono wake ndani na kuanza kuchezea kitumbua cha Cookie na kumfanya aanze kutoa miguno ya kimahaba. Cookie, kwa haraka akamvua Adrus tisheti aliyo ivaa, akakitazama kifua cha Adrus kilicho gawanyika vizuri, tartaibu akaanza kukilamba kwa mahaba mazito huku akisikilizia utamu anao upata kwa kuchezewa kitumbua chake.

***

“Muheshimiw raisi tuwafanyaje?”

Mshauri wa raisi Dustan alimuuliza raisi Dustan huku akimtazama usoni mwake.

“Tunakwenda kuwawekea vikwazo vya kiuchumi”

“Hapana muheshimiwa hilo sio wazo zuri, dunia nzima itakwenda kulijua hili swala. Na kumbuka kwamba bado Charity hajapatikana”

“Unanishauri tufanye nini?”

“Hapa muhesimiwa kitu ninacho weza kukushauri, tutafute kikundi cha kigaidi, ambacho tunakwenda kukipa nguvu ya utendaji kazi, kikundi hicho kitakuwa kinafanya kazi kwa niaba yetu”

“Una akili kweli wewe, hilo ndio jukumu ambalo nimekupa la kunishauri?”

Raisi Dustan alizungumza kwa hasira huku akimtazama mshauri wake huyu.

“Samahani muheshimiwa raisi kama nitakuwa nimekuudhi, ila kitu ambacho nimekizungumza hapa kina maana kubwa sana. Nchi ya Tanzania ina maliasili nyingi sana ambazo wao wenyewe hawajui jinsi ya kuzitumia. Hapa tukihakikisha kwamba tunaweza kuwadhibiti basi kila kitu kinaweza kwenda vizuri muheshimiwa”

“Unajua siku zote nimekuwa nikipambana na magaidi, nimekuwa nikihitaji kufuta hawa watu wanao jiita magaidi, leo hii unakuja kuniashauri kwamba niweze kuinga nao mkataba, ili iweje sasa?”

“Muheshimiwa, kwa upande mmoja hawa watu hawana faida hapa dunia, ila kwa upande mwngine wana faida. Hembu kwa mfano tukifanikiwa kutoa hichi kizazi cha Gowin kwenye nchi ya Tanzania, wale wengine wote watakao kwenda kuichukua nafasi hiyo watakuwa watu wetu, wanatoka mikononi mwetu, na kila tutakacho kuwa tunawaambia basi wao watakuwa wnafanya kwa kufwata amri yetu sisi”

“Siwesi kufanya ujinga wa namna hiyo, nimekupa nafasi ya kuwapelekea vijana Tanzania wameshindwa, na hata hilo ambalo unakuja kuniambai litashindwa, mimi ndio raisi, nitajua ni kitu gani cha kufanya umenielewa?”

Raisi Dustan alizungumza kwa ukali sana.

“Sawa muheshimiwa raisi, samahani kama nitakuwa nimekuudhi”

“Toka ofisini kwangu, nikikuhitaji nitakuita”

***

Livna Livba akasimma mbele ya kisoso cha wasichana nane alio wateua katika kazi ya kwenda kuhakikisha kwamba wanamuangamiza makamu wa raisi wa Tanzania, Eddy Godwin aliye husika katika kuwaua vijana wake alio wapenda sana.

“Hii kazi mimi mwenyewe nitaiongoza, mimi mwenyewe nitakikisha kwamba tunamuua yeye na familia yake yote. Kitu kikubwa cha kuzingatia ni umakini, kwa maana hatuendi kupambana na mtu mmoja tu bali tunakwenda kupambana na nchi pia. Nimeeleweka?”

“Ndio muheshimiwa”

“Tuondokeni sasa”

Livna alizungumza huku akiongoza vijana wake kuelekea kwenye boti ndogo, huku mikononi mwake akiwa ameshika bastola mbili tayari kwa kukikisha kwamba anakwenda kuitoa roho ya Eddy Godwin na famili yake, akiwemo Shama.

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG