Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

DAPHINE SEHEMU YA 1/10

 


DAPHINE
MTUNZI….EMMANUEL F.KWAY(THE STORY MASTER)
AGE…(18+)
Watchstrap…+255718 862176
SEHEMU YA 1 KATI YA 10

 Nelson Magembe alizidi kusonga mbele akikimbia huku mkononi akiwa amemshika mke wake Rebecca Magembe jioni hiyo.


Walizidi kukimbia wote wakihofia maisha yao dhidi ya jeshi kubwa linalo wakimbiza.


Walikua kati kati ya Mbuga ya wanyama ya mikumi iliyopo pembeni ya mkoa wa Morogoro nchini Tanzania.


Furaha ya kutalii na kuangalia mbuga za wanyama iligeuka kuwa majonzi na mateso.


Nelson Magembe hakutaka kumuacha mke wake Rebecca nyuma alizidi kukimbia japo kuwa alisikia kelele za wanyama pori lakini alichokua anakiwaza pale ni kupata usalama na kuokoa maisha yake na ya mke wake kipenzi ambae alimpenda kuliko mwanamke yoyote ulimwenguni.


Rebecca alianza kuchoka sana na kuzidi kuwa mzito kuto kana na mimba kubwa aliyo kua nayo tumboni ambayo wakati wowote ule angejifungua .


hakuweza kutembea tena na kudondoka chini huku ajipiga piga mapaja na kuhisi uchungu wa kuzaa pale pale.

"Rebbeca jikaze gari nimeiacha hapo mbele simama twende tuwahi hospitali"


Aliongea Nelson Magembe ambae alionekana kuchanganyikiwa sana huku jasho jingi likiwa limelowanisha uso wake.


anaaamua kumbeba mke wake mgongoni na kuanza kutembea akizidi kwenda kutafuta alipo paki gari yake .


cha ajabu alishindwa kuliona kutokana na kupotea njia.

hakutaka kuosha hali ya kupotea njia alizidi kusonga mbele huku akisikia miungurumo ya wanyama kama SIMBA ila hakujali sauti hiyo ya mnyama mkali ambae akiunguruma kila mtu hukimbia alicho waza kwa wakati ule ni kuyaokoa maisha ya mke wake na kiumbe alicho beba tumboni..


"Mume wangu nahisi uchungu mtoto anatoka"


Aliongea Rebecca huku akilia kwa uchungu.

****


Upande wa pili wana jeshi hayo waliovalia magwanda ya kijeshi wakiwa ndani ya magari yao walizidi kuwatafuta Nelson na mke wake wakiamini kuwa hawa takuwa mbali na hapo.


Msako unaendelea waki gawanyika kila upande ili waweze kuwa uwa sababu walisikia siri kubwa ya nchi


kutoka kwa wana jeshi wakiamini kuwa uwa ndio wata poteza ushahidi kazi ili kua moja tu kuwa tafuta Nelson na Rebecca na kuwa uwa na ndio kauli aliyo toa kiongozi wao wa jeshi brigedia KARANJE.


***********

"Mke wangu PUSH.PUSH"


Ilikua ni sauti kutoka kwa Nelson akijitahidi kumzalisha mke wake sababu kwa wakati huo hakua na jinsi nyingine wala msaada mwingine wowote ule.

.

Machozi yalianza kumlenga na kujutia kwanini alikuja kutalii mikumi na leo ana mzalisha mke wake kwa shida wakati alikua na uwezo mkubwa kifedha jambo hilo lina mfanya asikie maumivu sana moyoni ila yote alimuachia Mungu aliye juu mbinguni.


Alizidi kumsihii mke wake abane pumzi ili mtoto yule aweze kutoka .


"Mke wangu jitahidi jitahidi bana pumzi jikaze mtoto atoke"


Alisema Nelson Magembe huku akiweka mikono kati kati ya miguu ya mke wake ili kiumbe kile kiweze kutoka .


kweli kwa mbali anaona kichwa cha mtoto kinanza kutoka na kumkazania mke wake azidi kumsukuma mtoto huyo kwa nje.


"Ng'aaaaaa ng'aaaaaa"


Ilikua ni sauti ya mtoto ikilia kwa sauti sana baada ya kuzaliwa huku Nelson akiwa amem shika mikononi mwake.


"Hongera mke wangu ni mtoto wa kike"


Rebecca hakuweza kuongea chochote kutokana na kupoteza fahamu wakati ule.


Alicho fanya Nelson alimchukua mtoto wake na kusonga nae mbele ambapo ana kutana na bara bara ya lami na kumuweka pembeni akimfunika na majani . alivua shati lake na


kulitandika kwa chini na kumfunika nalo mtoto wake ambae ametoka kuzaliwa sekunde chache tu.


"Narudi mwanangu ngoja nika mchukue mama yako"


Aliongea Nelson huku akimwangalia mtoto wake ambae hakuelewa lolote kipindi kile sababu alikua bado mchanga sana.


safari ya kurudi kwa Rebbeca ilianza huku akifurahi mke wake kajifungua salama.


ila akiwa mbali ana muona Rebecca ame piga magoti huku akiwa amezungukwa na kundi hilo la wanajeshi huku wakiwa wamemshikia mitutu waki taka kumuua.


Haku taka jambo lile litokee kwa mke wake tena mbele ya macho yake kilicho mtuma kichwani ni kimoja tu aende, japo kua hakuwa na uhakika kama ange muokoa na kutoka salama..

ila alimuomba sana Mungu afanye miujiza sababu walimuacha mtoto mdogo sana ambae anahitaji malezi yao.


Alitembea taratibu mpaka alipofika walipo simama wana jeshi wale

"Piga magoti hapo"


Aliongea mwana jeshi mmoja wao na

Nelson alitii na kupiga magoti pembeni ya mke wake huku akimwangalia usoni.

.

"Mtoto yupo hai?"

Aliuliza Rebecca kwa sauti ya chini.


"Hongera ume jifungua mtoto wa kike tuta toka salama mke wangu usijali."


Nelson alimfariji mke wake japokua nayeye hakuwa na uhakika kama ange toka akiwa hai ila alitumia kauli ile kama kumfariji mke wake.


"Naomba mtu samehe hatuta sema tulichokiona"


Aliongea Nelson akiwa ame piga magoti.

"Nipatie hio silaha Kobelo"


Aliongea mwana jeshi mmoja wapo huku akiwa ame kinga mkono wake akisubiri apewe silaha.


muda mfupi tayari alikua ameshika mtutu na kuukoki kuashiria kuwa anaenda kuwa uwa Nelson na Rebecca.


"Siwezi kuwaacha muishi . siwezi kuwaacha mkiwa hai"


Nelson na Rebbeca walikombatiana huku wakilia sana na kumuomba Mungu aweze kumlinda mtoto wao mchanga aliye toka kuzaliwa.

kilicho muuma Rebeca ni kitu komoja tu.

haku bahatika kumuona Mtoto wake wala kumshika na leo hii wana enda kufa picha za mizoga iliyo liwa na wanyama ina jijenga ndani ya taswira za bongo zao..


ambapo waliamini kuwa wange uliwa miili yao inge liwa na wanyama pori. Wote walifumba macho kusubiri kifo chao muda mfupi.


Kilicho sikika hapo ili kua ni milio ya risasi ambapo Nelson Magembe na mke wake Rebecca walidondoka chini na kupoteza maisha na huo ndio ulikua mwisho wao.


"ila mkuu alikua ana mimba huyu Mama. ata kua ame jifungua muda mchache naona tumtafute huyo mtoto tummalizie kabisa"

"Achana na huyo mtoto hajui lolote"

"No tuka mmalizie kabisa tumalize kazi"


Mwanajeshi huyo ana kubali wazo na wote kujigawa kuanza kumtafuta mtoto yule mchanga ...




Furaha ya NELSON MAGEMBE NA mke wake REBECCA inaisha ghafla wakiwa mbugani mikumi Mkoani Morogoro,sasa wana kimbizwa na kikundi cha wanajeshi kikiongozwa na Brigedia Karanje mwenye roho mbaya sana, tayari kwa kuwapoteza duniani na kuwauwa, ni baada tu ya kusikiliza siri yao ambayo waliamini kuwa wangekuwa hai ingewafikisha mahali pabaya pengine wasifanikishe zoezi hilo.wana zidi kuwasaka ndani ya mbunga hio ya mikumi yenye wanyama pori wakali, Rebeca anashindwa kusonga mbele kutokana na mimba kubwa aliyokua nayo, Kwa tabu sana mume wake anamzalisha na kwenda kumficha mtoto mbali kidogo, anarudi na kukuta wanajeshi wamemzunguka mke wake tayari wamemuweka chini ya ulinzi. wote wanaungana na kumiminiwa risasi, huo ndio ulikua mwisho wa maisha yao duniani wakimuacha mtoto wao mdogo wa kike yatima.!

SONGA NAYO.


“mama njoo uone!,”

Ilikua ni sauti ya kijana mmoja mdogo akiwa anakojoa mbugani baada ya kutembea safari ndefu sana wakitokea Iringa akiwa na Mama yake japo eneo hilo lilikua hatari kutokana na wanyama wengi lakini hawa kuwa na jinsi yoyote ya kufanya zaidi ya kusimamisha gari.

Sauti ya Mtoto mdogo mchanga aliyekua akilia yupo chini amefunikwa ndiyo iliyo mshtua na kumuita mama yake aliyekua ndani ya Gari aina ya Noah na kutoka nje haraka haraka,

hata yeye alistaajabu baada ya kumuona mtoto mchanga akiwa analia kwa sauti, aliangalia huku na kule na kushindwa kuelewa ni hatua gani achukue.

“jaccob, embu ingia ndani ya gari haraka sana”

Alisema Mama yake, bado alionekana kutafakari hakua na chaguo lingine zaidi ya kumchukua mtoto huyo mchanga na kuingia nae ndani ya gari lake kisha safari ya kuelekea kituo kidogo cha polisi kuanza maramoja, , hawakuelewa kuwa nyuma kuna kikundi cha magari kilichobeba wanajeshi kina wafuatilia, ilikua ni lazima wamuangamize mtoto huyo mchanga ili kupoteza ushahidi ambao utakao waweka sehemu mbaya. walivyofika tu walimkabidhisha kwa polisi aliyekua zamu huku wakitoa maelezeo jinsi walivyo muokota.

“umesema ulimkuta chini kafunikwa na shati?”

Aliuliza polisi aliyekua zamu usiku

“huyu mwanangu Jacob ndiye aliyenionesha, mimi nika muokota na kuamua kumleta hapa kwenu kituoni,”

“sawa mama tuachie namba zako za simu, tutakuhitaji muda wowote ule”

“sawa ahsanteni sana”

Baada ya hayo kufanyika simu ilipigwa moja kwa moja kwa kaminshina mkuu wao wa kituo Kaijage

“basi subiri kidogo nampigia simu detective Ngesa, atakuja hapo mara moja, sasa hivi ni usiku sana mfungulie faili nilikute mezani kwangu asubuhi.”

“sawa mkuu”

Usiku kucha mtoto mchanga alikua akisumbua sana akilia kwa sauti, askari wa kike ilibidi tu akimbie mpaka kwenye duka la maziwa ya Ng’ombe usiku huo huo na kuja nayo mpaka hapo kituoni na kuanza kumpa,.

“VIPI PASCAL?”

“safi tu Ngesa bora umefika”

“ndio ndio, nimepigiwa simu na mkuu, kua kuna mtoto kaokotwa”

Alifika askari aliyevalia kiraia kitengo cha upelelezi baada ya kupigiwa simu na mkuu wake Kaijage usiku huo huo, haraka haraka alipewa maelezo juu ya mtoto huyo mpaka akafikishwa kituoni.

“sasa ina bidi kesho tumtafute huyo Mama aweze kuja tena, hilo faili niachie mimi hapa, mkuu amesema.Nikishakamilisha upelelezi wangu,litaenda ngazi za juu”

“sawa”

Wote walikubaliana wasubiri kukuche ili zoezi lianze ilikua ni lazima wajue ni nani aliye mtupa mtoto huyo ili wamuweke ndani,na ivyo ndivyo walivyoambiwa kutoka ngazi za juu wakipewa vitisho. kama jeshi la polisi ilikua ni wajibu wao kufanya kazi hiyo.

Asubuhi kulivyokucha tayari detective Ngesa alifika kituoni na kuanza mawasiliano na Mama Jacob.

Kwa kuwa alikua mkoani Dar es salaam ndani ya masaa matatu alikua teyari kasha fika Mkoani morogoro akitumia usafiri wake binafsi!. Hapo hawakutaka kupoteza muda Deffender iliwashwa na kunyoosha mpaka mbugani Mikumi sehemu waliyo muokota mtoto mchanga wakiwa na mitutu yao mikononi kwa kujihami dhidi ya wanyama wakali.

“umesema ndiyo hapa?”

Aliuliza Detective Ngesa

“ndio hapa afande”

“una uhakika?”

“asilimia mia”

“sasa mbona hakuna dalili za watu?, itakua sio hapa.”

Huku na kule walianza kupiga macho yao wakitembea na kufatisha majani yaliyo lala wakiamini kuwa kuna watu walipita, walitembea taratibu sana, baada ya kufika mbele kidogo waliona ndege pori wanaruka huku na kule, na mmoja wa maaskari kupiga risasi moja hewani ili kuwatawanya ndege hao ambao walionekana wakiwa wanakula mizoga, taratibu walizidi kusogea mpaka kwenye mizoga iliyo kuwa mbele yao.

“Mungu wangu!”

Alisema askari mmoja wa kike huku akiziba pua zake, ilikua ni miili ya watu waliokufa wamekumbatiana,kila askari alikoki bastola yake na kujihami wakiangaza huku na kule, kila askari aliingiwa na wasi wasi sana. Picha zilianza kupigwa kama ushaidi wa upelelezi wao kisha maiti kuingizwa ndani ya defender mpaka hospitali kwa ajili ya vipimo vya damu za DNA.

Majibu yalionesha kuwa mtoto aliyetupwa hao ndio walikua wazazi wake lakini hawa kuelewa ni nani aliye wauwa, ilikua ni lazima wafanye uchunguzi. Siku ya kwanza ilipita bado walikua wakifanya uchunguzi mtoto mdogo akiwa chini ya usimamizi wa koplo Kapilima akipewa majukumu yote ya kumtunza huku wakiendelea kufanya uchunguzi juu ya maiti walizokuta mbungani Mikumi.

“habari afande!”

Alisalimia mwanaume mrefu mweusi akiwa na kombati za jeshi asubuhi hio na mapema kituoni.

“salama mkuu”

“kuna mtoto aliletwa hapa juzi, namtaka”

“lakini mkuu huo…”

“usitake kubishana nipe mtoto”

Kauli hiyo kutoka kwa mwanajeshi ilimuogopesha koplo kapilima alielewa watu hao walivyokua wakorofi na wakitaka kitu ni lazima wapewe, hakua na chaguo lingine zaidi ya kuingia ndani ya chumba kidogo na kumkabidhisha, hakuelewa alikua anaruhusu mauaji ya mtoto huyo yatendeke, kikosi cha jeshi walishaelewa kuwa mtoto aliyekua amezaliwa angeleta tatizo kubwa ilikua ni lazmia wam-malize ili kupoteza ushahidi, aliingia ndani ya gari na mtoto kisha magari ya jeshi kuondoka kwa kasi tayari kwenda kumtupa mtoto huyo mchanga kwenye maji ya mto ili afe.

Habari alizopata Ngesa zilimkera kitendo cha kuambiwa yaliyotokea muda wa dakika kumi uliopita baada ya kufika kituoni.

“sio utaratibu huo Kapilima, utafanyaje vitu kiholela, mimi nitasema nini ngazi za juu?”

“sasa.. sasa mimi sikua na jinsi”

“wameelekea wapi kwani?”

“kushoto”

“twende tuongozane”

Ngesa Alipenda sana haki ilikua ni lazima amrudishe mtoto mchanga ambaye wazazi wake waliuwawa kwa kupigwa risasi mikononi mwake ili akamilishe ushahidi. faili lilikua tayari mikononi mwake na yeye ndiye anayesimamia kesi hiyo, upotevu wa mtoto huyo au kibaya chochote kingemkuta ilikua ni lazima ajibu mashtaka.

Hakutaka jambo hilo litokee, aliwasha defender harakaharaka huku pembeni akiwa na koplo kapilima anatetemeka jasho linamtoka.

“Lakini wapo wengi Ngesa”

“kwaio, hata wawe mia”

Hiyo ndiyo ilikua sifa ya Detective Ngesa hakuwahi kumuogopa binadamu yoyote Yule duniani isipokua Mungu wake aliye juu mbinguni, japokua alikua na mwili mdogo. Alizidi kuikimbiza Deffenda kwa kasi ya ajabu na kufanya vumbi nyingi kwa nyuma, kwa mbali waliweza kuona Hammer mbili za jeshi huku mbele kabisa ya magari yao ilikua Landrover ya kijeshi pia.

“nafikiri ndio wale?”

“ndio, ndio”

Ngesa alipandisha gia mpaka namba tano na kuanza kupiga honi za mfululizo kuashiria kuwa gari izo za jeshi zisimame lakini hawakuweza kusimama, alijua hata yeye wasingeweza kusimama alichofanya aliwapita kwa mbele na kupiga msele mbele yao,

hapo ndipo gari za jeshi zilisimama pale pale.

Koplo Kapilima mkojo ulianza kumba-na alielewa lazima wangeenda kurushwa kichura kambini.

“Ngesa”

Aliita Koplo kapilima huku akitetemeka na kutamani kumwambia wakimbie.

“vipi?”

“unataka kufanya nini?”

“nisubiri ndani ya gari nakuja”

Detetective Ngesa alishuka ndani ya gari mpaka kwenye gari la jeshi landrover la mbele yao na kusalimia.

“habari zenu wakuu, poleni na kazi”

“toa taka taka yako tupite”

Alisema mmoja wa wanajeshi aliyekomaa sura akiwa amekunja uso wake

“siwezi kutoa gari mpaka mnipe mtoto mchanga mliomchukua, namuhitaji sasa hivi ili nikamilishe kazi yangu, naomba tusiharibiane kazi wakuu”

“mtoto gani?”

“mliomchukua kituoni”

“usitupotezee muda bwana mdogo, unataka kwenda kambini na sisi?”

Watu kwa mbali walishaanza kuzunguka wakiangalia kitakacho tokea, walielewa kuwa vitengo ivyo viwili havipatani jeshi la polisi na wanajeshi. Alishuka mwanajeshi mmoja akikoki bastola yake, Detective Ngesa alitoa bastola yake nayeye kiunoni tayari kaiweka mkononi mwake kwa ujasiri,

japo alijua kama wangerushiana risasi angekufa mara moja sababu alikua peke yake kama jeshi la mtu mmoja.

“Ng’aaaaa ng’aaaaaa”

Mtoto alianza kulia ndani ya HAMMER ya kijeshi na taratibu Ngesa huku akijiamini kuanza kusogea pembeni ya gari hilo na kuanza kugonga kioo cha gari, kioo kilishushwa na sura nyeusi huku begani ikiwa na nyota kuonekana.

“una shida gani?”

Alihoji Brigedia Karanje mkuu wa kikosi cha jeshi akiwa na hasira,



 Kikosi cha jeshi la polisi nacho kilishafika lakini walikua mbali kidogo wakimshuhudia Ngesa akizozana na wanajeshi waliokua wamemchukua mtoto mchanga aliyeokotwa mbugani Mikumi na baadaye kubainika kuwa wazazi wake waliuwawa, bado walikua na maswali mengi yenye kuhitaji majibu, bado walihitaji kufanya uchunguzi wa kina juu ya maiti mbili walizozikuta,walimuelewa ni jinsi gani Ngesa alivyokua kiburi asiyeogopa kitu hata katika Kesi ngumu walimtumia, na katika fujo vile vile, kujiamini kwake kulichangiwa na yeye kujua michezo ya kupigana na mtu wa aina yoyote ile.


Brigedia Karanje aliyevalia gwanda za jeshi alishuka ndani ya Hammer ya jeshi na kumtizama Ngesa kwa macho makali sana.

“usitake matatizo,tupishe tupite”

“hapana siwezi mkuu nipatie huyo mtoto kwanza ili tukamilishe upelelezi wetu”

“sawa, ila naomba nikwambie kitu, utakuja kujutia maamuzi yako”

Amri aliyotoa Brigedia Karanje ni moja tu mtoto mdogo mchanga apewe Ngesa sababu watu wengi walishaanza kujaa na haikuwa picha nzuri hata kidogo, lakini waliapia kuwa wangemtafuta na kumpata mtoto na kumpa vitisho kuwa watamuua,

Kila askari hakuamini kuwa Ngesa amekabidhiwa mtoto na wanajeshi lilikua ni jambo la ajabu sana, kila askari alimpa pongezi na kuanza kuondoka zao wakirudi kituoni huku wakiwaacha wanajeshi wakiwa wenye ghadhabu.

“Yule kijana anaitwa nani?”

Aliuliza Brigedia Karanje

“anaitwa Ngesa”

“fanya upajue kwake namtaka kesho kambini”

“sawa mkuu”

Njia nzima walikua wakimjadili Ngesa hata wao hawakutaka kukubali, walijua ni lazima wangeenda kufanya uchunguzi na wangesumbuliwa, hawakutaka jambo hilo litokee, kila mwanajeshi alishikwa na hasira sana waliona hiko ni kitendo cha aibu kwa wanajeshi wengi kama hao kuzidiwa akili na mtu mmoja tena askari,

Asubuhi na mapema kulivyokucha Ngesa alitafutwa na moja kwa moja kufika kambini, hakua na wasiwasi wowote ule moyoni mwake, alijiamini sana alikubali wito,alishuka ndani ya gari huku nyuma akisindikizwa na wanajeshi wakiongozana mpaka ndani ya nyumba ya mkuu wao wa kikosi Brigedia Karanje iliyokua ina lindwa na wanajeshi nje, waliingia na kuchapa miguu yao chini wakitoa saluti kama heshima.

“Ngesa”

Aliita Brigedia karanje

“Naam,nimekuja”

“M.P Boni mpatie kijana mzigo”

Begi kubwa lililetwa na kufunguliwa mbele yake,ndani kulikua kuna noti za elfu kumi kumi zimejaa.

“hizo milioni mia na hamsini niuzie Yule mtoto”

Ngesa aliwatizama wanajeshi wote saba waliomzunguka wanasubiri jibu lake, lakini kilichowachanganya akili zao ni yeye kutingisha kichwa kuashiria kukataa pesa alizopewa, hapo ndipo Brigedia Karanje alipokunja sura yake kwa hasira sana,

“sikiliza sasa nikwambie kitu, sijawahi kubembeleza mtu katika maisha yangu, hizo pesa utakosa mtoto tutampata na utajiingiza kwenye matatizo makubwa tuna kupa masaa ishirini na manne uje na huyo mtoto hapa, na uende ukashtaki popote pale mimi naitwa Brigedia Karanje sijawahi kumugopa mtu yoyote Yule”

Yalikua ni maneno ya kutisha na kuogopesha hata Kwa Ngesa alishaanza kuingiwa na wasiwasi moyoni mwake aliona mambo yataenda kuwa mabaya sana huko mbeleni kisa mtoto mdogo ambaye hana uhusiano nae. sura ya Brigedia ilizidi kumtisha hakua na mzaa hata kidogo katika maneno aliyozungumza huku akipiga piga meza iliyokua mbele.

“nakupa masaa ishirini na manne nimesema, kesho muda kama huu uwe hapa na huyo mtoto ni lazima sio ombi, mtoeni nje”

Walimsukuma mpaka nje huku wakimsisitiza kuwa watamuuwa endapo asipo fanya wanayo taka ilikua ni lazima afanye ivyo ili kutetea roho yake,

Usiku kucha aliwaza sana bila kupata jibu hakua na wazo lingine zaidi ya kusubiri kukuche ili aende kituoni kumchukua mtoto mchanga aliyekua chini ya uangalizi maalumu,

Kweli kulikucha na kuchukua defender mpaka kituoni, hawakuwa na kipingamizi hata kidogo sababu yeye ndiye alikua na faili ya kesi ya mauaji ya maiti zilizokutwa mbungani Mikumi, maiti hizo mbili zilizokutwa baada ya vipimo vya DNA majibu yalionesha ndiyo wazazi wa mtoto huyo aliyezaliwa.

Maamuzi aliyochukua ni kwenda mpaka kambini na mtoto mchanga,alikua njiani akiwaza sana, baada ya kufika nje aliwaona wanajeshi wakiwa wamesimama nje ya geti la kambi, walitabasamu hata wao walivyomuona.

“Ng’aaaa ng’aaaaa ng’aaaaa ng’aaaaa ng’aaaaaaaaaaaaaa”

Mtoto mdogo alikua akilia sana kwa sauti kubwa bado Ngesa alikua anajishauri alishajua teyari kitendo cha kumuacha hapo kambini angeenda kuuwawa na wanajeshi hao, alishaelewa ndiyo hao waliofanya mauaji baada ya kuchunguza risasi alizokuta ndani ya miili ya maiti alizokuta mbugani Mikumi,alielewa fika maisha ya mtoto huyo sasa yapo mikononi mwake, vitu viwili vilikua vina kinzana ndani ya moyo wake nafsi moja ilimtuma amuache mtoto na nyingine ilimuambia asifanye ivyo kwani ni malaika wa Mungu, ilibidi achague kimoja kati ya hayo mawili kwa wakati huo, japo alielewa kuwa kitendo cha kukubaliana na nafsi ya kwanza ingemgharimu maishani,

“No!”

Alipiga gia na kurudisha gari kinyume nyume kumaanisha kuwa jibu la pili lilikua sahihi kwake, aliweka gia namba moja na kuzungusha usukani na kuondoka eneo hilo kwa kasi ya ajabu sana, hata wanajeshi waliokua nje walishindwa kuelewa ni kitu gani kili mpata.

Akiwa njiani kwa kasi sana alichukua simu yake ya mkononi na kumtafuta rafiki yake wa karibu sana ambaye alimuamini.

“Oyyaaa Hans upo wapi?”

“nipo geto, vipi kwani?”

“naweza nikakuona sasa hivi?”

“ndio upo wapi?”

“chukua begi lako la nguo harakaharaka njoo kwenye ile baa ya juzi”

“mbona sikuelewi Ngesa, sikusikii vizuri upo wapi?”

“nasemaje panga nguo zako vizuri kwenye begi njoo kwenye ile baa ya juzi”

“kwanini kuna safari?”

“ndio, fanya ivyo rafiki yangu”

“sawa, nakuja”

Alishachagua kufa ili kuokoa maisha ya kiumbe mdogo asiyekua na hatia hata kidogo, alifika Mandela Pub na kumkuta Hans kasha fika, hakua na muda wa kupoteza ilibidi amkabidhi mtoto.

“oya sikia mbona sikuelewi kwanza, huyu mtoto wa nani?”

“mtoto ni wangu, sema nimegombana na mama yake, chukua izi laki mbili nenda Dar es salaam, ukifika huko nipigie simu”

Ilibidi Ngesa atumie uwongo.

“sasa mimi Dar es salaam sipajui, nitafikia wapi?”

“wewe ukifika ubungo nipigie, naomba usimwambie mtu wa aina yoyote ile, na usisahau kunipigia simu ukifika”

“sawa nitafanya ivyo”

Walipanda kwenye gari moja kwa moja mpaka stendi kuu Msamvu ili safari ianze mara moja, roho ya Ngesa ili kua nyeupe sasa, alielewa kumuweka mbali mtoto huyo kiasi hiko wanajeshi wasingeweza kumpata kivyovyote vile,

Baada ya kufika kwake ghafla kundi la wanajeshi lilifika wakiwa na mitutu na kuanza kupekua ndani kwake,

“mtoto yuko wapi?”

“sijui”

Walimchukua moja kwa moja mpaka kambini ili wamuhoji na kumpa mateso, mwanajeshi mmoja alipotaka kumpiga ngumi Ngesa aliidaka na kumtizama machoni, alivyotaka kurusha ngumi nyingine aliikwepa kwa kurudi nyuma, hakutaka kufanya ukorofi wa aina yoyote ile, baada ya muda mfupi walianza kumpiga na chuma na ndo hapo alipoamua kukunja ngumi na kuanza kupambana nao, ‘umoja ni nguvu’ wanajshi walikua wengi waliweza kumshinda lakini kwa shida, walimtuliza na kuanza kumpiga sana, ndani ya nusu saa alikua chini anavuja damu hana nguvu zake,

Walimtesa Takribani masaa matatu wakimpiga sana lakini hakuwa tayari kufungua kinywa chake kuongea chochote juu ya mtoto kuwa yupo njiani anasafirishwa kwa siri akielekea mkoani Dar es salaam

“griiii griiii”

Simu ya Ngesa ndiyo ili yowafanya wasitishe zoezi la kumtesa

“pokea simu na uweke laudi spika”

Ngesa alitoa simu yake akiwa chini kwa shida mfukoni alikua ni Hans akipiga alishusha pumzi ndefu alishajua zitakua ni habari za mtoto.

“Oyaa oyaa Ngesa nishafika huyu mtoto ananisumbua sana, analia tu inakuaje sasa?”

Sauti hiyo ilisikika kwa kila mwanajeshi na wote kusogea karibu wakimuekea mitutu kichwani kwake sababu taarifa za upande wa pili wa simu ndizo walizokua wakizihitaji.

“Ha…ns na…kuomba ndu..gu ya..ngu umtunze ka..ma mwa..nao wa kumza..a na usita..je ulipo”

Aliongea Ngesa kwa tabu

“mbona sikuelewi Ngesa?”

“mt..unze mtoto haki..kisha ana..soma,”

Hapo hapo Ngesa alikata simu baada ya kugundua mtoto yupo salama salmin! Alichukua simu na kuipiga chini, hapo hapo alifuata laini ya simu na kuikata kata, kilichofuata hapo kilikuwa ni kipigo kisichokua na maelezo ya kujitosheleza…..




Siku mbili nzima alikua akila mateso ya kila aina ndani ya kambi ya jeshi bila kupewa chakula wala kitu chochote kile,alishalowa damu mwilini mwake lakini hakutaka kufungua kinywa chake kusema lolote juu ya wapi mtoto alipo,ilikua ni bora afe kwani aliamini mwisho wa siku kila mtu atakufa alikua ni bora afe kutokana na kupigania haki ya nchi yake,walimchukua na kumburuza mpaka kwenye chumba kidogo kilichokua na dirisha moja tu lililokua juu sana kisha kumfunga kamba mikono yake yote miwili wakiwa wameitanua,

“kijana unajifanya jasiri? Ngoja nikuhakikishie kitu kimoja utakaa hata miaka kumi humu ndani bila mtu yoyote kujua na utataja tu”

“mn…ajisu…mbuuua mna..potez…a wak..ati we..nu”

“wacha tuone”

Baada ya dakika mbili waliingia watu sita waliojazia mikono yao wakiwa na mikanda ya jeshi,bila kuongea chochote walianza kumchapa na mikanda mwilini mwake huku wakimpiga ngumi nzito za tumboni, mpaka jioni inafika hawakuambulia kitu chochote kutoka kwa Ngesa ambaye kwa wakati huo alikua ameshachakaa sana.

**

Hans akiwa tayari yupo Ubungo keshafika mkoani Dar es salaam. Hakuelewa ni kitu gani akifanye kwa wakati huo, mtoto aliyemshika mikononi mwake alianza kulia sana, habari za Ngesi zilimtisha mno kila alipojaribu kumtafuta hewani hakumpata na kuzidi kuingiwa na wasiwasi,alitembea mpaka kwenye duka la maziwa lililokua mbele yake ili ampatie mtoto,hakuwahi kulea lakini ilimbidi afanye ivyo, hakua na chaguo lingine la kufanya.

“Dada una maziwa fresh?”

“yapo ndio”

“tafadhali naomba”

Mwanamke mwenye rangi maji ya kunde aliyekua anauza maziwa kwenye duka kubwa alitoa maziwa na kumkabidhi mteja wake kisha kumuangalia.

“kaka unataka kufanya nini?”

“kumpa maziwa mtoto”

“hapana hayo sio maziwa ya mtoto”

“sasa maziwa ya mtoto ni yapi?”

“nisubiri nikufuatie”

Mwanamke muuza duka aliingiwa na huruma sana alijikuta anaenda dukani na kuleta maziwa ya mtoto pamoja na kopo, kisha kumchukua na kuanza kumpa.

“kaka samahani nikuulize kitu?”

“ndio”

“huyu mtoto ni wako?”

“haaa hapana ndio ni wangu”

“huyu mtoto bado ni mdogo anatakiwa kupata maziwa ya mama yake,Mama yake yuko wapi?”

“hayupo, hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui nifanye kitu gani dada angu, huyo mtoto mimi nimepewa na rafiki yangu lakini sijui mpaka sasa hivi alipo namimi ni mgeni hapa Dar,yaani sielewi”

Ni kweli alionesha kuchanganyikiwa sana hakuelewa mzigo wa mtoto atampatia nani, historia fupi aliyompa mwanamke aliyejitambulisha Kwa jina Beatrice ilitosha kabisa kumsisimua hata yeye, roho ya huruma ilimuingia sana, kama binadamu ilibidi afanye kitu chochote ili mradi kiumbe cha Mungu kisichokua na hatia akilinde.

“sasa huyo rafiki yako mpaka leo hapatikani?”

“ndio, mara ya mwisho nampigia simu anaongea kwa shida inabidi nisirudi Morogoro hata iweje”

Kwa kuwa Beatrice aliishi mwenyewe kwenye nyumba ya kupanga ya vyumba viwili hapo Mabibo, alikua tayari kumpa hifadhi Hans pamoja na mtoto mchanga, jioni ilipofika walisaidiana kufunga duka na kutafuta dala dala za Kariakoo kisha kushuka Big bon hapo walichukua daladala nyingine za mabibo mpaka mwisho wa kituo na kuanza kutembea wakijaribu kuzoeana,

japo ilikua ni vigumu kwa binadamu kumuamini mtu asiyemjua lakini kwa Beatrice alijikuta akimuamini Hans na kumuonea huruma,waliiacha reli na kuingia kwenye moja ya vichochoro na safari yao kukomea kwenye nyumba ndogo iliyokua na kufuli na hapo ndipo Beatrice yalikua makazi yake,

Mpaka wanafika Hans hakutaka kuamini, hakuelewa ni shukrani gani ampe mwanamke aliyekua mbele yake.

Siku zilizidi kwenda wakiwa na jukumu la kumlea mtoto ambaye walimpa jina DAPHINE, wote walifurahi sana usiku huo baada ya kumpa uji na wao kukaa kitandani wakila chakula cha usiku kwa pamoja.

“kwanini umeamua kumpa jina hilo?”

Aliuliza Beatrice

“hilo jina ni la Mama yangu,alifariki kipindi nipo darasa la saba, aligongwa na nyoka porini, hata yeye pia hakubahatika kulelewa na wazazi wake vilevile”

“pole sana, Pole sana Hans, tutamlea wote ondoa shaka”

“Ahsante!,hakuna kitu kibaya kama umaskini hapa Duniani, Mama yangu alifariki sababu ya umaskini”

Taratibu walianza kuzoeana mwishowe wakawa wapenzi bila kutarajia, wote walipata jukumu la kumlea Daphine walimpa mapenzi yote kama ndio wazazi wake wa kumzaa, na ndo hayo maneno aliyopewa na Ngesa mara ya mwisho alivyofika jijini Dar es salaam kupitia simu.

Miezi ilikatika na miaka kusogea sasa, Daphine alianza kutambaa na kuita jina Mama kutokana na malezi na upendo waliomuonesha alielewa hao ndio wazazi wake, alikua ni mtoto mwenye afya hata uzuri wake ulichangia pia,Upendo ulizidi kwa Hans na Beatrice wakiishi kama wana familia wenye mtoto mmoja Daphine japokua waliishi katika hali ya umaskini wa hali ya chini walihakikisha Daphine halali njaa na anapata kila kitu kuanzia mavazi, malazi mpaka chakula!.

Alivyofikisha umri wa miaka mitatu walimuanzisha shule ya chekechea ili aweze kujichanganya na watoto wenzake, kila mwalimu alimpenda kutokana na uchangamfu aliokua nao,na ndiye mwanafunzi pekee aliyeweza kuelewa masomo darasani kwa haraka sana kuliko mtoto mwingine yoyote Yule, hii iliwashangaza sana walimu wake na kutamani siku wawajue wazazi wake!,

Siku hiyo jioni Daphine alivyorudi shule aliwakabidhi barua aliyopewa kutoka shuleni kwao.

Ikiwataka wazazi wake.

“Mama, Mama nimepewa chuleni na Madam Eliza, kachema mchome”

Aliongea Daphine kwa lugha ya kitoto,lakini Beatrice alimuelewa na kuanza kuisoma barua hiyo iliyowataka waende shuleni kesho yake asubuhi.

Alivyorudi Hans kutoka kibaruani ilibidi amkabidhi usiku wakiwa chumbani kwao.

“sasa kuna nini huko shuleni,lakini si nilitoka kumalizia ile elfu ishirini kuwalipa juzi? Kama ni pesa nyingine hapa sina pesa”

“Hata mimi sijui, inabidi twende tuwasikilize Baba Daphine!”

“sawa wacha tutajua hiyo kesho,kwaio wamesema twende nae?”

“itakua ndio ivyo”

“usisahau kunikumbusha iyo kesho asubuhi”

Baada ya chakula kuiva waliweka mkeka chini na kuanza kula kisha baadaye kumlisha Daphine, walivyo hakikisha yote yamekamilika walilala ili kusubiri kukuche.

***

“Nyie ndio wazazi wa Daphine?”

“ndio sisi, na huyu ndiye Mama yake”

“napenda kuwapa hongera sana mtoto wenu ana I.Q nzuri ya kushika masomo haraka sana darasani ningependa mumsisitize sana kwenye elimu mumpe elimu ya kutosha mumkazanie sana,hata kama mtashindwa kumuendeleza kimasomo sisi kama shule tutakaa ili tujue tutafanya nini”

Yalikua ni maongezi ya Mkuu wa shule,baada ya kuwaita wazazi wa Daphine ofisini kwake waliongea mengi kuhusiana na mtoto huyo mdogo aliyekua akiongoza kwa upeo mkubwa darasani, hata Mkuu wa shule alifurahi sana kuzungumza na wazazi wake.

Jambo hilo liliwafurahisha sana Hans na Beatrice, hapo ndipo walipoanza kumkazania kila siku wakimuuliza juu ya nini alichosoma kila alipotoka shuleni mchana na kumpa kazi za darasani za ziada!.

Hans na Beatrice walichanganyikiwa siku hiyo mpaka jioni inaingia hawakuweza kumuona Daphine akirudi nyumbani,saa kumi na moja ya jioni ilipotimu walinyoosha mpaka shule aliyokua akisoma lakini majibu waliyopata yalizidi kuwachanganya akili zao.

“Mbona tuliwaruhusu wanafunzi wote leo tena mapema sana”

“Lakini Daphine bado haonekani nyumbani,atakua wapi?”

Aliuliza Beatrice akiwa mwenye mashaka sana moyoni mwake,


****

Hans na Beatrice walimtafuta Daphine bila mafanikio yoyote yale,walishasubiri shuleni bila kuambulia chochote kitu.Hakuna mtu yoyote aliyehisi mtoto huyo mdogo yupo wapi kwa wakati huo.Mpaka inafika saa kumi na mbili ya jioni hali ilikuwa ileile hilo ndilo liliwafanya wachanganyikiwe Zaidi.

“Kwanini tusiripoti polisi?”

Lilikuwa ni wazo kutoka kwa Hans.Aliona jambo hilo ni sahihi.Kila mtu alikuwa katika hali ya kupagawa,wakatembea kwa mguu mpaka kituo cha polisi kilichokuwa karibu ili kuyaandikisha maelezo ya kupotelewa kwa Daphine.

“Mtoto ni wenu?”

“Ndio”

“Ana umri gani?”

“Miaka saba”

“Huwa anarudi saa ngapi kutoka shule?”

“Akichelewa sana saa kumi”

“Wewe ni kabila gani?”

“Msukuma”

Kama tabia ama sifa za mapolisi kuuliza maswali ndivyo ilivyokuwa,Beatrice aliulizwa maswali mengi lakini hakuchoka kujibu.Alivyohakikisha kila kitu kipo sawa.Akasimama na kuondoka akihaidiwa na jeshi la polisi kuwa kila kitu kingeenda sawa.


Mpaka inafika usiku wa saa tatu, hali ilikuwa ileile wote walikuwa na mawazo, kutokurudi kwa Daphine kulizidi kuwatia mashaka.Ghafla kila mmoja alishtuka baada ya kusikia sauti ya mtoto mdogo.

“Mamaaa”

Ilikuwa ni sauti ya Daphine,walivyosimama alimanusura wapigane vikumbo mlangoni,haraka wakafungua mlango.

“Habari zenu jamani?”

Mzee mmoja mfupi kiasi aliwasalimia,Hans na Beatrice.

“Nzuri,karibu”

Wakati Hans anadakia salamu,yeye Beatrice alimnyakua Daphine na kumm-wagia mabusu mengi yasiyokuwa na idadi.

“Naomba mniwie sana radhi,kwa yaliyotokea Mwenenu alikuja nyumbani kwangu na mtoto wangu.Wakawa wanacheza,najua mlimtafuta sana”

“Ndio,wewe ni nani?”

“Mimi naitwa Mr.Mwambasi.Kwangu sio mbali na hapa,ni mtaa wa nyuma”

“Ahsante Mr. Mwambasi,ahsante sana”

Hawakuwa na haja ya kumuhoji mzee huyo aliyekuja kumleta mtoto furaha yao ilirudi, ndiyo maana hawakuwa na muda huo kwa wakati huo,walishampata Daphine tayari.

“Nilikuwa kwa rafiki yangu,nilikuwa nachesha kule”

“Umekula Mwanangu?”

“Nimechiba ndio”

“Siku nyingine usifanye hivyo mwanangu,tulikutafuta sana mimi na baba yako”

Daphine suku zote aliamini hao ni wazazi wake wa kumzaa,mapenzi waliyomuonesha yalistaili kabisa kupewa na wazazi.Hakujua lolote kuhusu wazazi wake waliouwawa mbungani Mikumi na wanajeshi akiwa bado mdogo sana.

Hans na Beatrice walifanya kila wawezalo, siku nyingine walidiriki hata kushinda njaa ili mradi Daphine apate madaftari ya shule pamoja na sare.

Uwezo wa Daphine darasani ndiyo uliwafanya wazidi kupata moyo,alikuwa ni mwepesi wa kushika vitu kuliko mwanafunzi yoyote yule.Mpaka anafika darasa la tatu bado aliendelea kushika namba moja tu darasani,hii ilizidi kuwashangaza sana walimu na wanafunzi wengine.Hakuna somo lililomshinda mtoto huyu, mbaya Zaidi hakuwahi kushika daftari na kusoma.

Kumsilikiza mwalimu darasani ilitosha kwake.

“Daphine Hans,embu njoo mara moja”

Siku hiyo mwalimu wake wa hisabati alimuita ofisini.

“Abee Mwalimu”

“Unaishi wapi?”

“Hapo Mabibo”

“Hii hesabu nani kakufundisha?”

“Sio mtu mwalimu,juzi niliangalia kwenye kitabu nikawa najaribu kuifanya”

“Embu niambie,umelifanyaje mpaka ukapata jibu?”

Mwalimu Macha aliogopa,akili za Daphine zilimtisha.

“Hii hapa mbili nimezidisha na tatu,jibu lake nikatoa na hii saba.Jibu nililopata nikagawanya kwa hii namba ya chini”

Daphine alijielezea kama mwalimu anavyoelezea, jambo hilo likazidi kumfanya Mwalimu Macha ashindwe kuelewa hesabu hiyo ngumu ameijuaje.Hivyo ndivyo ilivyokuwa hata katika masomo mengine.


*****

Miaka ilizidi kusogea, alivyofika darasa la saba,aliishangaza shule nzima.Alifumua masomo yote, kila mtu alitaka kumuona mtoto huyo mdogo Daphine,Hans na Beatrice walifurahi sana.Wakazidi kujivunia kuwa na Daphine,siri ya mtoto huyo wapi walimtoa, walijua wenyewe.

***

Uzuri wa Daphine ulianza kuonekana alivyoingia kidato cha kwanza,sura yake ya duara iliendana na macho yake madogo ya kusinzia kama taa za benzi,rangi yake ya maji ya kunde ilikolea vizuri mwilini mwake ikawa kama imepigwa ‘polish’ iling’aa na kumfanya awe maridadi.Mbali na hapo alijaliwa kuwa na mwili mnene kiasi,kiuno chake kilikuwa chembamba na kadri kilivyoshuka chini kilienda kusambaa akatengeneza shepu kama kibuyu,ikamfanya nyuma abinuke,usingekuwa unamjua vizuri ungesema wenda mtoto huyu ni mcharuko au anajibinua mwenyewe, kumbe ndiyo ulikuwa uumbaji wa Mungu.

Kama kawaida ya Daphine darasani,hakukosea alizidi kuwaburuza watu waliomzidi umri,ilikuwa ni aibu kwa wanaume kupitwa na msichana tena mwenye umri mdogo.

Mpaka anafika kidato cha tatu namba yake ilikuwa ile ile,hakuna mtu aliyeweza kumchukulia namba moja.Wasongo walikesha usiku na mchana kuchimba vitabu lakini wapi!Daphine alizidi kuwaburuza darasani.

Mbali na kuwa mzuri wa sura,hata darasani alikuwa vizuri pia.Kila siku uzuri wake ulizidi,kifua chake kikaanza kukuwa taratibu,sauti yake ikaanza kukaa vizuri,ngozi ikawa kama ina mafuta.Hapo ndipo wanaume wakaanza kumsumbua,alipokea barua mbalimbali za wanaume,wakimtaka kimapenzi!

“Lilian,embu angalia huyu naye”

Daphine,alichukuwa kipande cha karatasi na kumuonesha rafiki yake.Nayeye akaanza kuisoma.

“Huyu James huyu,jitu zima.Hana hata aibu”

“Hata mimi kanifurahisha,mwandiko wenyewe mbovu.Sasa anasema akiniona moyo unamdunda.Huu si utoto huu”

Daphine hakutaka kujihusisha na maswala ya wanaume,hali ya umaskini aliyokuwa akiishi aliielewa mwenyewe,alitaka asome kwa bidii ili baadaye awakomboe wazazi wake.

***

Hali ya Hans na Beatrice kimapato ilikuwa mbaya mno,kila kukicha ilikuwa afadhali ya jana.Hans alipigwa chini kazini alikadhalika Beatrice,Kibanda chake cha kuuza vinywaji kilikumbwa na bomoa bomoa Ubungo.Hapo ndipo maisha yalizidi kuwa magumu Zaidi na Zaidi.Hawakupenda jambo hilo Daphine alijuwe lakini ilibidi tu wafanye hivyo.

“Daphine”

“Abee Baba”

“Kuna jambo tunataka kukueleza,wewe ni mtu mzima.Wazazi wako sisi ni maskini nadhani unalijua hilo”

“Ndio Baba”

“Hali unaiona ni mbaya,Baba yako nimefukuzwa kazi,Mama yako sasa hivi hana kibarua”

Daphine alianza kulengwa na machozi,aliwaonea sana huruma wazazi wake.

“Sasa mimi na Mama yako,tunaamua kwenda Mwanza,tutakuacha hapa.Kodi tulilipa ya miezi sita.Daphine usome kwa bidii ili utukomboe wazazi wako”

Hakuna siku iliyokuwa chungu katika maisha yake kama hiyo,Daphine alilia akashindwa kula chakula.Maneno aliyoambiwa kutoka kwa wazazi wake yalimtisha na kumtia simanzi,lakini akapewa moyo ili apambane na maisha ya kuishi mwenyewe ili amalizie elimu ya kidato cha nne.Hivyo ndivyo ilivyokuwa,Hans na Beatrice baada ya siku tatu walisafiri kuelekea mkoani Mwanza huku nyuma wakimuacha Daphine mwenyewe.

****

“Daphine fungua mlango”

“Na na nakuja”

“Nitauvunja huu mlango ujue”

Mlango uligongwa kwa fujo,mtu aliyekuwa nje alionekana kutamani kuingia ndani wakati huohuo.

“Nakuja,nakuja”

Sio kwamba Daphine alishindwa kufungua mlango,alikuwa ana haha kupita kiasi,hakuelewa ashike kipi aache kipi.Ndani alikuwa na mwanaume mwingine.Hilo lilikuwa ni fumanizi.

“Robert,inuka inuka”

Daphine akatembea na kumvuta mwanaume aliyekuwa kitandani anatetemeka,alivyotaka kumuingiza ndani ya kabati alisita,aliona wazo lake sio sahihi.Akamvuta mpaka bafuni na kumuweka.Mlango ulizidi kugongwa kwa nguvu.

“Nakuja Johnson,subiri”

Kazi ya Daphine ikawa ni kuvuta suruali na kuziingiza uvunguni akitumia mguu,jasho lilimtoka akashindwa kuelewa ni kwa namna gani Johnson amewahi kutoka kazini.Akatembea taratibu na kufungua mlango.Jinsi Johnson alivyoingia ni kama aliyekuwa na uhakika kwa kitu kilichokuwa kinaendelea ndani,sababu cha kwanza alifunga mlango na funguo, akauweka mfukoni.

“Hivi unajua kuwa mimi sio bwege,unanifanya mimi fala eh!”

Johnson akaongea kwa hasira,huku akimpita Daphine,akaingia ndani ya makabati na kuanza kupekua.

“Huyo mwanaume umemficha wapi?Najua humu ndani kuna mwanaume.Tafadhali naomba umtoe sababu hatopita popote pale.Daphine,hujanifahamu vizuri nadhani”

Sauti hiyo ilienea chumba kizima,ikamfikia Robert bafuni,akahisi boxa yake inaanza kulowa, hakujua kuwa ni mkojo au jasho la uwoga.

Alijuta kufanya kitu hicho.Hapo ndipo alipoanza kumuomba Mungu afanye miujiza yoyote ile,alijikunja bafuni kwenye kona akiwa anatetemeka na kuzidi kuyasikia maneno ya kutisha kutoka kwa Johnson.

“Hii suruali ya nani?”

Johnson aliuliza kwa hasira baada ya kuinama uvunguni na kuviona,viatu vya kiume pamoja na suruali.Alivyoinuka aligeuka na kelbu lililomfikia Daphine shavuni,akadondoka kitandani.

“Nakulipia ada,kodi ya chumba leo unafanya huu upuuzi.Leo ndio utanitambua.Malaya wewe”

Hasira alizokuwa nazo mtu huyu,hata angekuwa nani asingeweza kumtuliza.Bado aliendelea kuamini kuwa ndani kuna mwanaume,habari alizopewa na marafiki zake aliziamini na ndiyo maana alifanya ziara ya kushtukiza.

Akatembea mpaka mlango wa bafuni na kunyonga kitasa,Mawazo yake yalikuwa sahihi.Bafuni kulikuwa kuna mwanaume aliyevaa boxa,tena ya kwake.

“Simama kijana”

“Ni...nisamehe”

“Simama,kijana”

Johnson aliongea maneno mawili tu,akiwa katika hali ya hasira.

“Ka..ka”

Hakuna neno lingine Zaidi,kilichosikika vilikuwa ni vishindo vya mtu kupigwa,Daphine akiwa kitandani aliogopa.Akaingia bafuni,kipigo alichokuwa anachezea Robert kilikuwa sio cha kawaida.

“Johnson utaua,Johnson uta…”

Daphine alishindwa kumalizia,kofi kali lilitua shavuni kwake.Kichwa chake kikajipiga ukutani akadondoka na kupoteza fahamu hapohapo.

Robert alipigwa mno,Johnson alikuwa na hasira za kuuwa,akaona hiyo haitoshi akatembea mpaka jikoni na kutoa kisu kabatini.

Japokuwa alikuwa hana nguvu lakini ghafla zilimrudia,hakutaka kufa kirahisi ndiyo maana alivyoona kisu kinataka kuzama tumboni mwake,akamshika mkono Johnson, wakaanza kushindana nguvu.

“Chubwiiiii”

Kisu kilikuwa kimezama tumboni,damu zikaanza kutapakaa chini sakafuni.

***

Kwa mbali alihisi harufu kali,ikawa inamchoma puani,kichwa chake kilikuwa kizito mno.Watu walikuwa wakiongea nje,yote hayo alikuwa akiyasikia akiwa anajaribu kuvuta kumbukumbu zake.Taratibu akaanza kuyafumbua macho yake.Moyo wake ukapiga paa,hakutaka kuamini kuwa amelala juu ya mwili wa Johnson tena unavuja damu na ameshika kisu mkononi,kilichojaa damu nyingi.Kabla ya kufanya lolote alihisi kishindo cha mlango ukivunjwa.Kundi la polisi likafika.

“Sija..ua”

Hilo ndilo neno la kwanza kulisema Daphine akiwa na kisu bado mkononi.

“Upo chini la ulinzi,Muuwaji mkubwa”

Polisi alitoa kauli hiyo.

Bado alikuwa ameganda juu ya mwili wa marehemu Mpenzi wake Johnson, hakutaka kuamini kuwa Robert ndiyo kafanya vitu hivyo na kumuachia kesi hiyo kubwa ya mauaji,picha ya nondo za gereza zilianza kujijenga ndani ya akili yake,akaona jinsi atakavyoenda jela.Alipigwa picha hapohapo za ushahidi,akashindwa kuelewa ni kitu gani akiseme ili aepukane na mkono wa sheria.

“Simama”

Daphine,akasimama huku akiangalia maiti ya Johnson ilivyokuwa inatoa macho,akafungwa pingu kwa nyuma ili akajibu mastaka ya mauaji,aliyoyafanya.


 Uchungu aliokuwa anahisi moyoni mwake haukuwa na kipimo chake,kesi iliyokuwa inamkabili mbele yake ilikuwa ni nzito mno,haikuwa rahisi kupindua jambo hilo.Wakati mwingine alijilaumu mwenyewe kwa kutokuwa muaminifu.Alitamani siku zirudi nyuma arekebishe kilichotokea lakini haikuwezekana ukweli ni kwamba alihitajika polisi,kisha akafungwe gerezani.Hicho ndicho kitu kilichokuwa kinapita kichwani mwake.Watu wengi walikuwa wamekusanyika nje,wanamtizama msichana huyo mrembo aliyesadikika kuuwa kwa kutumia kisu.

“Demu mwenyewe ndiyo huyo?”

Kijana mmoja alimuuliza mwenzake.

“Ndio”

“Duu,inakuwaje gashi kama huyu anakuwa katili kiasi hicho”

“Tena hawa mademu ni wabaya hawaaa,usicheze kabisa”

Askari walipata shida kuwapangua watu,mpaka kufika kwenye Deffender.

Daphine akatupwa nyuma na kukalishwa chini na kuendelea kuambiwa yeye ni muuaji.Hapo ndipo kama akili yake ikamrudia,akaanza kulia kwa uchungu.

“Wacha kutuletea uchuro”

“Mi..mi sijaua”

“Kelele,shenzii.Utaenda kuieleza mahakama,hapa sio mahala pake,kenge wewe”

Askari alizidi kumpiga mkwara huku akimuoneshea mtutu,jinsi Deffender zilivyozungushwa kwa mbwembwe na kutimua vumbi iliogopesha utadhani kwamba ndani ya gari kulikuwa na gaidi.Polisi waliondoka kwa mkwara mzito.

***

“Kaka yangu,uwiiiiiii Johnson.Daphine kwanini umemuuwa kaka yangu lakini?”

Miriam Mshana aliangua kilio cha uchungu,habari za kaka yake kuuwawa ziliuchanganya moyo wake.

“Johnsooon,kaka yangu.Nani atanisomeshaa?Daaaaphine jamani kwanini?”

Miriam akazidi kulia kwa uchungu siku hiyo hospitalini kwa sauti ya juu.

“Yuko wapi,huyo muuaji?”

“Bado ameshikiliwa na polisi”

“Yupo kituo gani?”

“Staki shari”

“Sawa”

***

Japokuwa Daphine alianika ukweli wote na juu ya mambo yalivyokwenda lakini aliendelea kuonekana ni mwongo tu,kwanza aliitwa Malaya na kubambikiwa kesi nyingine haramu ya kuuza mwili wake usiku yaani, dada poa.

“Wewe Malaya,unakubali unakataa?”

Askari aliuliza huku akimtisha.

“Hapana,mimi sio”

“Wewe ni Malaya,sasa iweje upande farasi wawili kwa wakati mmoja kama sio umalaya,ni nini?”

“Sikatai lak..”

“Nyamaza,utaozea gerezani.Nyie wasichana mbona hamtuliagi lakini”

Baada ya maelezo kuchukuliwa Daphine akarudishwa nyuma ya nondo.Alilia sana,ndoto zake za kusoma ili aje kuwa mkombozi wa wazazi wake,hakuamini kama ndiyo zilikuwa zinakatishwa na gereza.

***

Hans na Beatrice walifika jijini Dar es salaam kwa basi saa moja ya Jioni,walikuwa hoi bin taaban wamechoka,kutokana na mambo yalivyotokea hawakuhisi uchovu.Habari waliyosikia kuwa Daphine ameuwa na atahitaji kufungwa ziliwachanganya akili zao,walipagawa mno.

Wakatafuta bodaboda baada ya kutoka nje ya lango la ubungo.

“Staki shari”

“Wawili au?”

“Ndio”

“Mshkaki noma,huko mbele kuna matrafiki.Labda mmoja achukuwe nyingine”

“Kwanza shilingi ngapi?”

“Hapo tunaendanga kwa elfu tano”

“Hapana bwana tusaidie”

“Ndio bei yake”

“Mama Daphine una hiyo pesa hapo?”

Beatrice alionekana kuingiza mkono ndani ya mkoba wake,akakosa pesa akafungua upinde wa kanga na kujikuta na shilingi elfu sita peke yake.

“Nina hii elfu sita tu”

“Kaka tuna Elfu sita”

“Yaani,elfu tatu tatu?”

“Ndiyo”

“Hapana”

Hawakuwa na jinsi Zaidi ya kutembea kwa miguu mpaka Ubungo plaza ili kutafuta pikipiki iwawaishe kituo kikubwa cha polisi staki shari kumuona Daphine.Bahati ilikuwa kwao,walivyosimamisha pikipiki bei ikawa imepungua wakapanda na safari ikaanza.

***

Watu wengi walifurika ndani ya mahakama ya kisutu tarehe saba mwezi wa nne, kila mtu alitaka kusikiliza kesi ya msichana mdogo aliyemuuwa mpenzi wake kwa kisu,waandishi wa habari wakubwa kutoka vituo vya kimataifa kama Nipael Mshunga alikuwepo,alimuonea huruma msichana mwenzake,kila alichoongea alikiandika ndani ya kidaftari kidogo.

Kilichowashangaza watu Zaidi ni Daphine kutokuwa na Wakili yoyote yule.Alikuwa amesimama yeye kama yeye.Upande mwingine kulikuwa kuna mashahidi wengi na wakili alikuwepo pia,picha hilo lilimaanisha kuwa gereza linamuhusu,labda ungetokea muujiza wa Mungu.

“Kortiiiiiiiiiiii”

Kila mtu alisimama,jopo la viongozi wa mahakama walipita mpaka mbele.Mtu wa kwanza kupanda alikuwa ni Miriam Msangi,dada wa Marehemu.Kila alichoongea kiliandikwa.

“Ndio nilimuona Daphine,anamchoma kaka yangu kisu,nilikuwa dirishani niliona kila kitu.Kwanza alikuwa ni Malaya,kama anavyodai kuwa sijui alikuwa na mwanaume mwingine huo ni uwongo kabisa,hakuwa na mwanaume mmoja alikuwa na wanaume wengi, siku hiyo walikuwa wawili chumbani yeye na Marehemu kaka yangu.Marehemu kaka yangu alimpenda sana,alikuwa akimlipia ada na pesa ya pango.lak…. lak..sie…lewi”

Miriam aliongea kitu ambacho kilimshangaza sana Daphine,hakuna hata neno moja lililokuwa na ukweli ndani yake,akajifanya kulia na kufuta machozi na kuzidi kuendelea.


Mahakama nzima ilikuwa kimnya inamtizama msichana huyo aliyesadikika kuuwa,bado alikuwa ni mdogo kiumri kufanya mambo mazito kama hayo.

Shahidi wa pili alivyosimamishwa nayeye alimkandia Daphine vilevile.

Daphine alikuwa akilia tu akimuomba Mungu wake kimoyomoyo ili ukweli uwe wazi japokuwa aliamini alifanya dhambi ya kumsaliti Johnson hayo ndiyo aliamini yalikuwa malipo yake.

“Hapana,sikuuwa”

Daphine alimjibu Wakili aliyekuwa anamuuliza maswali.

“Haukuuwa?unaieleza vipi mahakama tukufu,una ushahidi gani wa kujitetea,una mtetezi?”

“Hapana”

“Jielezee”

“Kama maelezo yangu ya mwanzo nilii….”

“Maelezo yapi?”

Wakili Sammy Samson akiwa na suti,alizunguka zunguka kwa mbwembwe akiwa anaweka tai yake vizuri,kila neno aliloongea msichana Daphine, yeye alimkatisha.

“Marehemu Johnson alikuwa ni mpenzi wangu,nakubali kosa la kumsaliti ila….”

“Ila nini?mbona unajiuma uma,nikikwambia wewe una kesi nyingine hapo,utabisha?Kwanza unaidanganya mahakama tukufu,alafu kingine kwanini watu wote wakusingizie wewe,una wazazi?”

“Ndio….”

“Wako hapa?”

Daphine akapiga jicho lake huku na kule,lakini hakuwaona.

“Hapana”

“Wako wapi?”

“Wapo njiani nadhani, wanatokea Mwanza.Walikuja wiki iliyopita wakarudi”

“Unadhani?Ni kwamba huna uhakika na unachokisema,unaona sasa”

“Sina maan…”

“Muheshimiwa jaji,ni hayo tu”

Wakili Sammy Samson alitembea mpaka kwenye kiti chake huku akitabasamu, kesi hiyo aliamini kwamba ilikuwa yake na angeshinda tu,alimuangalia Miriam na kumpa ishara kuwa kila kitu kitaenda sawa.

Daphine bado aliendelea kukataa,hivyo kesi yake ikarushwa mpaka mwezi unaofuata tarehe kumi,kwa maana hiyo aliwekwa mahabusu,ili asubiri siku yake tena.

***

Kila siku alilia na kusaga meno,aliteseka kuliko kawaida,mbu wakubwa walimuuma.Ngozi yake nyororo ikabadilika na kuwa na mabonde mabonde,tangu wiki mbili zinapita maji ya kuoga hakuwahi kuyaona.Chumba kilikuwa kina dirisha moja dogo lililokuwa juu kabisa na kufanya hewa iwe finyu.Wakati mwingine alijilaumu ni kwanini alizaliwa.Mateso aliyokuwa anapata hakustaili kabisa,hata Miriam wifi yake aliyekuwa anampenda sasa amembadilika,afya yake iliporomoka na kupungua uzito,kutokana na kupata lishe duni.

***

Bado Daphine aliendelea kukanusha,japokuwa aliendelea kukandamizwa na upande wa ndugu wa marehemu,wakamchomekea vitu vingine.Pesa ndiyo ilikuwa ikiongea kwa wakati huo,Wakili ndiyo alichachamaa kabisa,Miriam dada wa Marehemu ndiyo usiseme!Moyo wa Daphine ulielemewa hakuwa na mashaidi wala wakili.

Wazazi wake Hans na Beatrice siku hiyo walikuwepo mahakamani waliangua vilio kwa nguvu,hawakutegemea tena ushindi na hata walivyojaribu kumuombea dhamana ilishindikana,nyundo iligongwa mezani na kesi kurushwa tena baada ya miezi miwili na hukumu itolewe,kila mtu aliamini kuwa Daphine atatupwa gerezani.


Jaji Barnabas Kodende,hakuwahi kurusha kesi kiasi hicho yeye alikuwa ni mzee wa kutoa hukumu tu ,alishindwa kuelewa hata yeye imekuaje kesi hiyo aliifanya iwe ndefu,alishindwa kutoa hukumu ya harakaharaka.

“Muheshimiwa Jaji”

Sauti hiyo ilimshtua kutoka katika mawazo,alivyogeuza shingo yake pembeni alimuona Mzee Mfupi kiasi mwenye kitambi kachomekea,amesimama mbele ya Range Rover ya rangi nyeupe.

“Habari za majukumu?”

Mzee alimfuata Jaji Kodende na kumpa mkono.

“Nzuri tu”

“Mimi naitwa Mr. Vital Kamere.Najua hatufahamiani lakini nilikuwa nina mazungumzo nawewe faragha kidogo”

“Sawa,twende ofisini”

“Hapana,sidhani kama maongezi haya yatafaa kuwa ofisini kwako,napendekeza twende sehemu iliyotulia”

“Sawa,naomba unipe dakika thelathini”

“Hakuna shaka,mimi nipo ndani ya gari”

Mwanzo mwisho gari ilikuwa inanguruma,kumaanisha kuwa alikuwa anachoma mafuta.Lakini hakujali alikuwa ana hamu sana ya kuongea na Jaji Kodende,akaingia ndani ya gari ili kumsubiri.

Baada ya dakika arobaini jaji akatokeza na kuingia ndani ya gari.

“Ahsante kwa kukubali ombi langu”

Sauti ya Mzee huyu ilikuwa nene kiasi na kwa haraka haraka umri wake ulikuwa kati ya miaka 50-60.Hakuwa mtu wa maneno mengi.

Kwa kumuangalia harakaharaka alikuwa ni mwenye kujiweza kiuchumi,wakanyoosha barabara ya Ohio na kutokea Posta mpya,alivyofika New African Hotel.Akaweka gari kwenye maegesho.Wote wakashuka.

“Huku Jaji”

Mr.Vital Kamel alitangulia akiwa amevaa suti iliyom-bana kiasi,japokuwa umri wake ulienda lakini alikuwa ni mzee wa kwenda na wakati.Wakaingia ndani na kila mtu kuagiza anachotaka.

“Ulisema unaitwa nani tena Jaji?”

“Jajji Kodende”

“Hakika wewe ndiye unayesimamia kesi ya yule binti muuaji?”

“Nani?Daphine Hans?”

“Sina uhakika na jina lake,nadhani ndiyo huyo.Maji ya kunde.Alimuuwa mpenzi wake na kisu”

“Ndiyo huyo”

“Mimi nahitaji kumtafutia wakili”

“Wakili?kesi inakaribia kufika ukingoni.Na imebaki siku ya hukumu tu”

“Jaji,mimi nimesoma sheria.Nina masters ya sheria na sheria zote za dunia ninazijua,sidhani kama hilo litakuwa tatizo”

Jajji Kodende akakuna kichwa kidogo.

“Mimi sina tatizo,kazi yangu ni kutoa hukumu bwana,ninafuata miiko ya kazi”

“Mimi ninamtafutia wakili,akishindwa sawa.Akishinda heri”

“Sina kipingamizi”

Mr.Vital Kamere alitabasamu,akaingiza mkono ndani ya koti lake na kutoa baasha kubwa ya kaki.

“Milioni saba hizo,ahsante kwa kunisikiliza”

Jaji Kodende macho yake yalimtoka,pesa alizotajiwa zilimtisha,akapigwa butwaa na kuitizama bahasha iliyotuna.

“Hapana,wewe kaa nayo”

“Hii siyo rushwa,maana najua sisi watu wa sheria tunadhani kila pesa ya bure ni rushwa No.Hii ni shukrani yangu kwako”

Kwa kusitasita Jaji Kodende akapokea pesa.

“Ngoja nikutafutie Taxi ikurudishe ofisini kwako,nina kikao kikubwa baada ya dakika arobaini”

Hicho ndicho kilichotokea,Jaji Kodende akajaribu kuziingiza pesa hizo ndani ya suruali yake kubwa kama puto lakini ikashindikana.Akaendelea kuikumbatia baasha hiyo yenye pesa nyingi,alizopata kirahisi.

***

Haukuwa utani wala masihara hata kidogo,Mr.Vital Kamere alimtafuta wakili mkubwa wa kimataifa.Alilazimika kumtoa nchini Urusi kwa dola za kimarekani laki mbili,kumsafirisha na kumlipia hotel na mahitaji yote.Kesi hiyo kwake ilikuwa kama kamali kushinda au kushindwa, kutokana na uzoefu wa wakili Anthony Edson aliamini kwamba kila kitu kingekuwa sawa.

“Shikamoo Mzee”

“Marahaba karibu sana Anthony Edson”

“Nashukuru,juzi ilikuwa graduation nina PHD sasa hivi”

“Hongera”Alikaribishwa siku hiyo uwanja wa ndege baada ya kufika.


Anthony Edson alikuwa ni mtanzania aliyekulia nchi za watu,kila kitu alikifanyia huko.Alijuana na Mr.Kamere mwaka 1991 akamtetea kwenye kesi ya kuziokoa pesa za kimarekani dolla milioni mia mbili,hapo ndipo watu hawa walifahamiana.

**

Baada ya siku mbili Daphine alipewa chumba kimoja na Wakili Anthony ili wazungumze.

“Ongea Daphine ukweli wote,hata kama umeuwa wewe niambie.Mimi ndiyo wakili wako.Haya ni mambo ya kawaida,kuna watu wameuwa na wapo huru sasa hivi”

“Sijaua kaka yangu,wananisingizia tu”

“Ilikuwaje?”

Daphine alitoa kila kitu kilichokuwa ndani ya kifua chake,hakuficha hata kitu kimoja.Anthony akawa ana kazi ya kuandika vitu muhimu pembeni.

“Kisu ulikishika?”

“Ndio”

“Ulisema nani aliua?”

“Mimi nilipigwa kofi,nikajigonga nikapoteza fahamu”

“Huyo muuaji jina lake nani?”

“Robert Kusa”

“Unapafahamu kwao?”

“Ndiyo”

“Je,ulishawahi kuwatajia jina la muuaji.Ili wamtafute?”

“Sio mara moja”

“Ina maana walikuhumu moja kwa moja?”

“Ndio,sijapewa hata nafasi ya kujitetea kabisa”

“Kaa pale”

Anthony Edson,akaingia kwenye laptop yake,na kuanza kupekua vitu anavyovijua yeye.Akamrudia tena Daphine na kumuhoji baadhi ya maswali.

“Wewe endelea kukataa hivyo hivyo,mimi nitajua pa kuanzia.Jihesabie kuwa upo huru”

Daphine aliamini maneno hayo ni ya kumtia moyo tu,bado hakutaka kuamini moja kwa moja kwamba angeshinda kesi.

***

Kazi ya Anthony kuanzia siku hiyo ikawa ni kujifungia chumbani na kusoma vitabu mbalimbali vya sheria vingine akaomba atumiwe kutoka nchini Urusi akasoma na vitabu vya sheria ya Tanzania,akaingia kwenye mtandao na kuangalia kesi mbalimbali.Hata hivyo alitaka kujua sehemu alipouwawa Johnson,alipelekwa na kupakagua vizuri.Bado kulikuwa kuna damu iliyoganda bafuni.

***

“Ndio alimuuwa kaka yangu,nilishasema hilo”

“Ulisema kuwa ulimuona kwa macho yako?”

“Kwa macho yangu ndiyo”

“Kivipi?”

“Kupitia dirishani,nilishuhudia kila kitu”

“Dirisha lipi?wakati marehemu Johnson,aliuwawa bafuni na hakuna dirisha lolote kule”

Swali hilo lilimpagawisha Miriam Mshana,ni kweli alijikuta amejikanyaga.Akaanza kutetemeka,mambo yalikuwa yanaanza kumtokea puani.Wakili Anthony Edson alizidi kumkanyaga maswali mazito tena bila kuonesha uso wa wasiwasi.Mahakama ilikuwa kimnya mno.Ilikuwa ndiyo kama kesi imeanza upya vile,Mr.Vital Kamere alikuwa nyuma kabisa akiangalia na kusikiliza kila kitu.

“Mimi nilimuona kabisa nimesema”

“Ndani walikuwa watu wangapi?”

“Walikuwa wenyewe,wawili tu”

“Huoni kuwa unaidanganya mahamaka tukufu, nikikwambia kuwa ndani kulikuwa kuna mwanaume mwingine vilevile,utakataa?”

“Ndio nitakataa”

“Unajua kuwa unaongea uwongo,dirishani mlikuwa wangapi?Na kwanini hukupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani.Ilikuwa saa ngapi?”

“Saa saa,saaa sikumbuki lakini ilikuwa usiku wa siku hiyo”

“Miriam Mshana,je nikikuambia kuwa siku hiyo ya tukio wakati kaka yako anauwawa, ulikuwa Bagamoyo,Kanajavo Hotel na Mwanaume anayeitwa Richard Mwambe utabisha?”

Hilo ndilo swali,lililomfanya Miriam aishiwe nguvu,akahisi amebanwa na kinyesi.


****


Ni kweli aliua,akili yake ilionesha kuchanganyikiwa kwa kiasi cha kutosha sababu hakuwahi kufanya kitendo kama hicho kabla.Ingawa alikuwa katika hali ya kujitetea, asingejitahidi kushindana nguvu na Johnson yeye ndiye angekuwa maiti anayevuja damu nyingi tumboni.Alijuwa nini maana yake endapo angekutwa eneo hilo usiku huo,jela ingemuhusu.Akasimama taratibu huku nguo zake zikiwa zimelowana na damu alivyotaka kutoka nje akamuona Daphine amelala kandokando,hapo ndipo alipopata akili mpya ya kitu gani cha kufanya,akamburuza Daphine na kumuweka juu ya mwili wa Johnson akachukuwa kisu na kumuwekea mkononi mwake,mpaka hapo alielewa tayari amepoteza ushahidi.

Alimuonea huruma sana Daphine lakini hakuwa na jinsi ya kufanya, ilikuwa ni lazima aitetee nafsi yake,akatoka taratibu mpaka Seblen na kufungua makabati.

Ambapo alitafuta nguo zitakazomfaa za Johnson.Akavua nguo zake na kutafuta mfuko wa nailoni,akazitumbukiza.Yote hayo aliyafanya akiwa mwenye hofu ya kukutwa,usiku ulikuwa ushaingia.

Akabeba mfuko wenye nguo zake zenye damu na kwenda mlangoni.Alihisi kuchanganyikiwa zaidi baada ya kukuta mlango umefungwa kwa funguo.

“Hee!”

Alikema,kazi yake ikawa ni kuangalia huku na kule.Alihisi tumbo linamuuma.Alivyotuliza akili akakumbuka alimsikia Johnson anavyoingia aliufunga,taratibu akaingia bafuni kwa kunyata akamruka Daphine aliyekuwa amezirai juu ya mwili wa Johnson.Hapo ndipo alipoanza kuipekua maiti ya Johnson mifukoni,akashusha pumzi ndefu baada ya kuzikuta funguo ndani ya suruali.

Hakuchelewa haraka akatoka na kufungua mlango,akaufunga kwa nje na kupotelea gizani.

**

“Bibi ukweli ndiyo huo,nimeua”

“Mjukuu wangu,kwanini?”

“Kama nilivyokwambia,inabidi niondoke Dar es salaam.Najua nitatafutwa na Polisi”

“Mjukuu wangu,inakubidi usubiri kwanza”

“Hapana siwezi bibi yangu,nitakamatwa nataka niondoke hata leo usiku”

Johnson alifika Sinza asubuhi sana,hakuwa na jinsi zaidi ya kumueleza Bibi yake kila kilichotokea,sababu ndiye alikuwa akiishi naye na ndiye alimlea tangu utotoni.

Zilikuwa ni habari za kutisha kwa Bibi,Zahra.Alielewa nini maana ya kesi ya kuuwa kama Mjukuu wake angetiwa mikononi mwa sheria.

Hakuwa na jinsi ya kufanya Zaidi ya kumkinga mjukuu wake.

“Sasa inabidi uwende Arusha,ukajifiche.Kwa bibi Khadija”

“Wapi,Alumeru?”

“Ndiyo,sidhani kama huko watakukamata”

“Inabidi niende leoleo”

“Sawa Mjukuu wangu Robert”

Bibi aliongea kwa upole akamsogelea mjukuu wake na kumkumbatia,siku hiyohiyo Johnson alifanya taratibu za kupanga mizigo yake.

kila alipomfikiria Daphine moyo wake ulimuuma,alimuonea huruma jinsi atakavyosota Jela kwa kosa la kusingiziwa,alitamani kumsaidia lakini hakuwa na jinsi yoyote ile.

“Johnson”

“Naam Bibi”

“Usiwe na wasiwasi”

“Ahsante bibi”

“Ukifika huko niambie”

“Nitakutaarifu Bibi,lakini itanibidi nibadili namba za simu”

“Sawa tu”

Alikuwa ni bibi aliyekula chumvi lakini akili yake ilifanya kazi vizuri mno.


Masaa matatu baadaye Johnson alikuwa na kofia kubwa pamoja na miwani, alionekana Ubungo akitafuta mabasi ya kuunga unga,alitafuta basi la Tanga,bahati nzuri ilikuwa kwake.Usiku wa siku hiyo alifika Tanga,akalala na kuchukuwa basi la Arusha kesho yake alfajiri,huko ndipo aliamini kuwa ataanza maisha yake mapya.

***

Mambo yalikuwa juu chini, chini- juu kwa Miriam,kufumba na kufumbua kibao kikageuka kwake,muda wote tumbo lilimuuma.Wakili Anthony Edson alimtwanga maswali yaliyozidi kumfanya ajikanyage,jasho lilimtoka.Siku hiyo ilibidi iwe siku ya hukumu lakini ilirushwa,kutokana na Wakili Anthony Edson kuwapiga mkwara kuwa ataishtaki mahakama.

“Inakuwaje,Mteja wangu analalamika kuwa anamjua aliyeuwa na Mahakama mnalifumbia macho?”

Lilikuwa ni swali lililolenga mahakama nzima,hata jaji mwenyewe alianza kuhisi mambo yanamwendea vibaya.Ndiyo maana akagonga nyundo mezani, kesi ikarushwa tena,ili mtuhumiwa anayeitwa Robert Kusa atafutwe mara moja na kesi iendelee.Kwa maana hiyo Daphine alirudishwa mahabusu,ili msako mkali uendelee.

***

Mr.Vital Kamere atembeza Pesa kwa maaskari,kila deffender iliwekwa mafuta ‘full tank’ili mradi polisi wafanye kazi usiku na mchana.Na ndivyo ilivyokuwa hakuna askari aliyelala, siku hiyohiyo Diffender nane zilipiga msele Sinza nje ya geti la Bibi Zahra,Jinsi walivyotua ardhini kwa mikwara ilitisha.Wakapiga geti teke wakazama ndani.

“Bibi Shikamoo”

“Marahaba Mwanangu”

“Hatujaja kupoteza Muda,tunamuulizia Robert”

“Robert?”

“Bibi,umetusikia.Usituulize mara mbilimbili.Hatujaja kucheza ngoma hapa”

“Mbona Robert hayupo”

“Yuko wapi?”

“Huu ni mwezi wa nne sijamuona”

“Una uhakika?”

“Ndiyo,wanangu”

“Tunaomba tuongozane kituoni”

“Lakini mbona siwaelewi wan..”

“Bibi,usitake tutumie nguvu.Maana hatutoshindwa”

Hakuna hata askari mmoja aliyeonesha kukenua meno yake,waliweka sura za kazi.Ilikuwa ni lazima Robert Kusa apatikane kwa namna moja au nyingine.Bi.Zahra alichukuliwa mpaka kituo kikubwa cha polisi Staki shari ili atoe maelezo yake.

Aliendelea kusimamia jambo aliloliongea.

“Mara ya mwisho alivyoondoka,hakuniaga”

“Na huwa anakuaga siku zote?”

“Ndio”

“Ulisema haukumuona miezi hiyo yote,ulichukuwa hatua gani?”

“Nilimuulizia kwa ndugu zake”

“Hilo tu?”

“Ndio”

“Ukaacha hivyo,Bibi usituletee usanii.Utaozea gerezani”

“Nimechoka kuongea,naombeni mnirudishe”

“Sawa,andika namba zako za simu.Tukitaka maelezo zaidi tutakupigia”

“Ahsante!”

Japokuwa alikuwa ni mkongwe lakini alikuwa ana uwezo wa kuongea,kama walivyomchukuwa ndivyo walivyomrudisha,nyumbani kwake Sinza.

***

“KWAHIYO HUJAWAAMBIA CHOCHOTE?”

“NDIO MJUKUU WANGU”

“AHSANTE SANA BIBI,NAOMBA USIMWAMBIE MTU YOYOTE KUWA NIPO HUKU”

“SIWEZI KWANINI NIFANYE HIVYO,ENDELEA KUKAA HUKOHUKO”

“MIMI NITAENDELEA KUISHI HUKU MPAKA HALI ITAKAPOTULIA”

“SAWA KUWA MAKINI MJUKUU WANGU MIMI NITAENDELEA KUKUKINGA”

Yalikuwa ni maongezi yanayosikilizwa moja kwa moja na maaskari,namba za simu za bibi Zahara zilipelekwa makao Makuu ya kampuni ya mawasiliano Tigo,simu yake ikawa inasikilizwa kuanzia siku hiyo.Baada ya siku mbili wakapata maneno hayo.

Ushahidi ukawa umekamilika kuwa Muuaji Robert Kusa yupo Mkoani Arusha,Alumeru.

Maaskari walifanya kazi kwa haraka,zikatumwa taarifa Arusha siku hiyo hiyo ili mtu huyo aanze kutafutwa haraka iwezekanavyo.


Nyuma ya msako huo alikuwa mwanaume mwenye nguvu kipesa Mr.Vital Kamere,ndiyo maana msako uliendeshwa harakaharaka.Askari wa Arusha waliwasha magofu usiku wa siku hiyo huku wakiendelea kufanya mawasiliano na mitandao ya simu,haikuwa kazi ngumu kumpata mtu wao.

“Ngo!ngo!ngo!”

Siku hiyo usiku mlango wa Bibi.Khadija uligongwa,alivyofungua alikutana na mwanaume mrefu kiasi.

“Robert yupo?”

“Robert gani?”

“Nimepewa mzigo na Bi.Zahra nimpatie nimetokea Dar es salaam”

“Ngoja nikuitie”

Bibi akaingia ndani,baadaye Robert akatokeza.Hapo ndipo kundi la askari lilipomvaa akafungwa pingu,hakuamini kuwa amekamatwa kirahisi hivyo kama bata.

***

Jua lilikuwa kali kupita kiasi jijini Dar es salaam,joto ndiyo usiseme.Msongamano wa magari ulizidi kuwa mrefu Ubungo Mataa,hii iliwafanya abiria watokwe na majasho.Magari yalikuwa yamejaza watu.Japokuwa ilikuwa ni kawaida ya eneo hilo kuwa na msongamano wa magari lakini siku hiyo ilizidi,msululu ulianzia Ubungo mpaka Tabata Relini!

“Jamani,huyo trafiki vipi?”

Abiria walilalamika ndani ya magari wengi wao wakiwa wamesimama wameshika bomba.

“Hii,tangu saa tano mpaka sasa hivi saa nane.Alafu trafiki anaruhusu upande mmoja”

Abiria walizidi kulalamika,foleni ilitisha.

“Huyu ni trafiki au taa?”

“Nadhani ni trafiki mkuu”

“Mbona anatuweka sana?”

Sauti hiyo ya kukwaruza na yenye madaraka ilitoka ndani ya Hammer ya kijeshi,Mwanaume aliyeongea kauli hiyo alikuwa mweusi mwenye mabaka usoni,ungemuangalia kwa mbali usingeweza kugundua ndiye Brigedia Karanje,mwili wake ulikuwa umeongezeka, misuli imemtoka,alikuwa ni mrefu kwenda hewani.

Msongamano wa Magari ulimkuta akiwa Ubungo Mataa,akitokea vitani Urusi,alihisi hasira sana.

Katika orodha ya wanajeshi wenye roho mbaya na wenye hasira basi Brigedia Karanje alikuwa mmoja wapo.Katika historia yake alishawahi kumnyonga mke wake na kumuuwa chumbani,hiyo ndiyo iliwafanya hata wanajeshi wenzake wamuogope.

“Subiri”

Brigedia Karanje,akateremsha mguu chini.Aliteremka kila mtu alimshangaa.


Kutokana na Kombati za Jeshi alizovaa watu waliokuwa pembeni walielewa nini kitakachoenda kumpata trafiki.Hakuelewa amfanye nini trafiki huyo endapo akimfikia,kila alipopiga hatua ndipo hasira zilizidi kumkaba,aliwakumbuka marafiki zake waliokufa vitani,hiyo ndiyo ikamfanya apandishe mori.

Trafiki aliyekuwa anaongoza magari,alivyoangalia pembeni kwa mbali alimuona Mwanajeshi anakuja.Akajifanya hajamuona,hazikupita hata dakika tatu.Alihisi kapigwa kofi kichwani,akasukumwa kando.

“Mpige huyoooo,anazingua”

Abiria walianza kushangilia ndani ya DCM.

Brigedia Karanje,akasimamisha magari yanayotokea mjini,akaanza kuyavuta magari yaliyokuwa kwenye msongamano.Lilivyofika Hammer ya jeshi akaingia na kuondoka zake.

Alivyoingia bado sura yake ilikuwa na makunyazi,akachukuwa simu na kubonyeza namba anazojua yeye.

“Mmefikia wapi?”

“Raisi amekataa kufanya tunavyotaka,tunataka tumuoneshe kazi”

“Mnataka kufanya nini?”

“Kenya itanuka damu,watu watalia na kusaga meno subiri uone”

“Fanya muwezalo,ili asaini”

“Atasaini tu.Atake asitake”

“Sawa,mimi ndio nimeingia Tanzania.Kazi njema.Nitakutafuta”

Yalikuwa ni maongezi ya kutisha,Brigedia Karanje ndiye alikuwa simuni.Safari yake ikakomea Lugalo kambi ya jeshi,hapo ndipo alipotaka kufika.

***

Kufumba na kufumbua maisha ya Daphine yalibadilika,Mr.Vital Kamere alimchukuwa na kumfanya kama mwanaye wa kumzaa.Akiishi ndani ya jumba kubwa la kifahari.Kesi alishinda baada ya Robert Kusa kukamatwa na kukiri makosa,bado aliendelea kuamini kwamba yupo ndotoni japo alitamani isiwe hivyo.


Daphine alisoma shule ambayo watoto wa mawaziri au wenye uwezo kifedha, mbali na hapo alitafutiwa dereva na mlinzi kwa ajili yake.Ilikuwa ni rahisi kumuona mtoto wa Raisi kuliko kuonana na Daphine,alilindwa kama Malkia,alipatiwa kila anachotaka.Kutokana na Mr.Vitale Kamere kuwa na miradi mingi aliwaajiri Hans na Beatrice kwenye moja ya viwanda vyake vya ukataji wa mbao.Kila siku walimpa Shukrani Mr.Kamere kwa kubadilisha maisha yao.

“Wewe ndiye umepata hizi alama?”

Lilikuwa ni bumbuazi kubwa kwa Mr.Vital Kamere.Daphine alikuwa amepata alama za juu shuleni.Haikuwa kawaida,uwezo wake wa kufikiri ulitisha mno.

“Ndio anko”

“Chagua zawadi yoyote ile”

Daphine alikuwa amesimama mbele ya Mr.Vital Kamere siku hiyo seblen,akitafakari ni kitu gani akiseme.Akashindwa kupata jibu la harakaharaka!

“Chochote tu anko”

“Chagua”

“Chochote tu,utakachoamua kunipa”

“Sawa,mnafunga lini shule?”

“Ijumaa ijayo”

“Okay,nenda kaoge chakula kipo mezani ule”

Daphine alipendwa sana akalelewa kama yai,kutokana na matunzo aliyopewa alizidi kunawiri, uzuri wake ukaongezeka ngozi yake ikazidi kuwa laini,alipaka mafuta ya gharama na kuvaa nguo za kisasa.Kila mtu alimtamani Daphine,dereva aliyekuwa anamuendesha alipata tabu, uzuri wa Daphine ulimnyanyasa,alibaki akila kwa macho tu, alimuhofia sana tajiri yake, Kamere.

***

Mr.Vital Kamere hakuwa mzee wa gozigozi!ni kweli alifurahishwa na matokeo ya Daphine na alipanga wasafiri wakizunguka nchi za Afrika Mashariki na kati yaani Burundi,Rwanda,Kenya na Uganda wakitembelea mbunga mbalimbali za wanyama.Ndivyo ilivyokuwa, ndani ya siku tatu Passport ya Daphine ilikuwa tayari.Kwa mara ya kwanza Daphine kupanda ndege,alikuwa akitetemeka.

“Tutafika saa ngapi?”

Daphine alivunja ukimnya wakiwa ndani ya ndege.

“Tutaanzia Kenya,hapo masaa matatu mengi tutakuwa tumefika”

Baada ya matangazo kutolewa,abiria wote walifunga mikanda.Hatimaye taratibu ikaanza kutembea na kuchanganya mwendo,ikaanza kuinuka kwa mbele taratibu kisha kupaa angani.

Walifika uwanja wa kimataifa Jomo Kenyatta saa saba ya mchana,hapo walitakiwa washuke ili utalii uanze.Muda wote Daphine alionesha tabasamu,katika maisha yake hakuwahi kusafiri, mbali na hapo hakuwahi kutoka nje ya Tanzania.

“Nipeleke kwenye Hotel nzuri ya nyota tano”

“Sawa”

Vital Kamere alimwambia dereva taxi,na hicho ndicho kilichotokea.

“Nina dola za kimarekani lakini”

“Hakuna shaka budaa, patia mimi fifty dollar”

Dereva akalipwa pesa yake,Vital Kamere na Daphine wakaingia Hotelini,kila mtu akapewa chumba chake.

***

“Paaaa paaaaaa,griiii griiiiiiii”

Ilikuwa ni milio ya risasi,watu walidondoka na kupoteza maisha yao.

Waliokuwa nje ya jengo la Wastegate walikimbia na kuacha magari yao.

Risasi zilizidi kurindima.Jengo kubwa la Wastegate lilikuwa mateka,kwa harakaharaka ndani kulikuwa kuna watu wasiopungua elfu tatu na mia nane.

“Wote laleni chiiiniiiiiii”

Ilikuwa ni kauli nzito na kubwa,kila mtu aliogopa.Miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya Jengo hilo ni Daphine pamoja na Vital Kamere,kifo ndicho walichoamini kilikuwa mbele yao kutokea.


Kikundi cha watu karibia thelathini ndiyo kilifanya kazi hiyo.Waandishi wa habari walikuwa nje tayari wakipiga picha jengo lililowekwa chini ya ulinzi na watu wasiojulikana.Polisi walilizunguka lakini waliweka magari yao umbali wa mita mia mbili.

“Ushaunganisha mitambo?”

“Bado”

“Nataka moja kwa moja niongee na Raisi,ikulu”

“Sawa”

Majambazi yalisemezana.

“Tayari”

Simu iliita,kisha kupokelewa. Raisi wa Kenya akaunganishwa.

“Mheshimiwa Raisi.Nadhani unajua nini kinachoendelea hapa Wastegate,nina mateka zaidi ya Elfu moja.Usipofanya ninachokitaka kesho mtakesha kuokota maiti”

Kila mtu alimuomba Mungu wake siku hiyo,wenye kutubu walitubu.Maneno ya jambazi yalikuwa ya kutisha.

“Unataka nini?”

Upande wa pili wa Simu ulisikika, Raisi akihoji.

“Hujui?subiri nikukumbushe.Wewe,kuja hapa.Wewe binti uliyevaa shati ya Jeans, yes Come here”

Daphine ndiye alikuwa akiitwa akaishiwa nguvu za kusimama,hofu ikamtanda.Alishaelewa nini maana yake.Alisogezwa na kuwekewa bastola kichwani kumaanisha kuwa alitakiwa apigwe risasi,afe!


Jengo kubwa la ‘Wastegate’ lililokuwa nchini Kenya jijini Nairobi sasa lipo chini ya ulinzi mkali na kwa dakika thelathini tu mamia ya watu walikuwa wameuwawa kwa kumiminiwa risasi.Damu zilitapakaa kila mahali.Waandishi wa habari waliokuwa nje walieneza habari na kwa muda wa lisaa limoja habari hiyo iliweza kuenea karibia Dunia nzima.

Hawakuelewa watu hao walitaka nini hasa mpaka wakaamua kuteka jengo hilo kubwa lililokuwa lina mkusanyiko wa watu wengi.Kazi yao ilikuwa ni kuuwa watu kwa kuwamiminia risasi ikiwa ni kumuonesha Raisi wa Kenya wapo kikazi,hawatanii.

Nia yao ilikuwa ni kuongea na Raisi Odhiambo, kwa maana hiyo alipigiwa simu lakini kilichowakera zaidi ni Raisi Odhiambo kujifanya hajui lolote,hapo ndipo walipoamua kumsimamisha msichana mdogo Daphine ili wampige risasi kama kumkumbusha nini alichotakiwa kufanya Raisi Odhiambo.

Kwa jinsi walivyokuwa na hasira ilikuwa ni lazima wausambaratishe ubongo wa Daphine kwa kukichengua kichwa chake na risasi.


Hakuna kitu alichofikiria zaidi ya kifo chake,alisikitika sana kufa kwa kifo cha kupigwa risasi tena nchi ya watu,hakuwahi kuhisi maumivu ya risasi lakini alishawahi kuona kwenye filamu za kijajusi jinsi inavyofumua vibaya sana,ndiyo maana alianza kulia machozi na kutetemeka,aliziangalia maiti zilizokuwa chini zimelala kwa kupigwa risasi na kuamini kuwa dakika chache kuanzia hapo ataungana na maiti hizo chini,alisikitika sababu alienda kufa bado hajatimiza ndoto zake.

“Relax!”

Jambazi mmoja alijaribu kumtoa hofu Daphine aliyeonekana akitetemeka kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa.

“Taf..adhaa…li msi..niue”

Hakuelewa ni ujasiri gani aliupata mpaka akatamka maneno hayo,aliongea huku akitetemeka, kwikwi imem-bana.

“Tutaenda kuuwa wewe,sisi hatupendi kukuuwa ni Raisi wako.Mlaumu Raisi wako”

Aliyeikamata bastola ndiye aliyeongea maneno hayo kwa rafudhi ya Kikenya,hakuwa na huruma hata kidogo.

“Kacha kacha!”

Sauti ya bastola kukokiwa ndiyo iliyosikika ili kuruhusu risasi zipande kwenye chemba,na kitendo cha jambazi huyo kuvuta triga risasi ingetoka na kufumua fuvu la Daphine aliyekuwa kasimama mbele yake.

“Baba yetu uli..ye Mbi..nguni Ji..na lak..o litukuzwe ufalme wa…”

Daphine alikuwa akisali sala ya ‘baba yetu’ huku macho yake akiwa ameyafumba anabubujikwa na machozi,alielewa hakuwa na msaada mwingine zaidi ya kumuomba Mungu wake amsamehe dhambi zake zote alizozifanya,aliamini kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wake,duniani.

“Captain”

Jambazi mmoja akamnong’oneza mwezake aliyeshika bastola.

“Vipi?”

“Embu kuja hapa”

Majambazi hayo yalionekana kuteta pembeni huku wakimuangalia Daphine aliyekuwa amefumba macho yake anasali.

“Sema”

“Huyu sio Mkenya,Raisi haitomuuma sana.Nimepigiwa simu na Okaka humu ndani kuna binamu wake”

“Binamu wake?Anaitwaje?”

“Jennifer Olamba”

“Are you sure?”(Una uhakika)

Hawakuwa na sura za kuonesha utani,sura zao zilikuwa za kazi tu!

“Yes Captain”

Ulikuwa ni muujiza wa Mungu wala sio kitu kingine,Mawazo ya jambazi huyo aliyejiita Captain yalibadilika hapo hapo,akawa anatafutwa ndugu yake na Raisi Odhiambo,ilionesha watu hao walikuwa na mtandao mkubwa na habari hiyo ilitoka moja kwa moja,Ikulu.

“Kama unajua,jina yako ni Jennifer Olamba,songa mbele”

Ilikuwa ni kauli iliyosikika ndani ya ukumbi mzima,mateka waliokuwa ndani walizidi kuogopa, vichwa vyao vilikuwa chini.Wengine walikuwa teyari wamemwaga mikojo sakafuni,walihofia kifo.

“Nasema tena,kama unajuwa jina yaako ni Jennifer Olamba,Songa mbele hatutoshindwa kufanya msako,mmoja baada ya mmoja hata ichukuwe mwaka mzima,tambua tutakupata tu”

Ulikuwa ni mkwara uliotisha na katika maneno aliyoongea Captain hakukuwa na aina ya utani hata kidogo.

“Paaa paaaa”

Mzee mmoja wa pembeni alipigwa risasi mbili za utosi,hapohapo akapoteza maisha.Hiyo ilifanya watu watandwe na hofu zaidi,Daphine alivyomtizama Mzee huyo alichanganyikiwa zaidi,moyo ulimuuma, kila kitu alishuhudia sababu akiwa chini alichungulia kwa jicho moja,ulikuwa ni unyama ambao hakuwahi kuuona katika maisha yake,hata hivyo aliendelea kumuomba Mungu wake,aliye juu Mbinguni!

***

Kipigo alichokuwa anapigwa Ngesa hakikuwa cha kawaida,aliteswa kupita kiasi,hakuna binadamu yoyote ambaye angeweza kuyamudu mateso aliyokuwa anakula mwanaume huyu jasiri.Wanajeshi walimtesa kwa takribani mwaka mmoja na nusu ndani ya kambi yao bila kuambulia chochote kile.

Alichanwachanwa kila sehemu ya mwili wake na kumwagiwa ‘Spirit’ lakini wapi,hakuwa tayari kutaja ni wapi mtoto mdogo aliyemchukuwa kutoka kwa Brigedia Karanje ni wapi alipo,alilia asubuhi,mchana na Usiku lakini hakuwa tayari kuongea lolote.Alishaapia ni bora afe kuliko mtoto mdogo auwawe kwani aliamini hana hatia.

“Ha.Ha….Haaa mnapot…eza wa..ka..ti we..nu bur…e swal..a ni kwamba ni..po kamili gad..o Hahahahaha! nip..ige.ni mpaka ni..fe lakini…. SISEMI!”

Detective Ngesa alisema kwa tabu huku mdomo na pua yake vikiwa viwelowa damu,jicho limemvimba limevulia damu,usoni hakutofautishwa na nyama ya Ng’ombe lakini cha ajabu hakuwa tayari kuongea lolote na kumtaja Hans alipo na mtoto mdogo,aliyemkabidhi aende naye jijini Dar es salaam!.

“Utataja tu,hatutokuuwa na kwa taarifa yako.Huko unapofanya kazi wanajuwa tayari umekufa kwenye ajali,wewe ni maiti sasa hivi.Utataja tu”

“Ba..si wa..cha tuo..ne”

“Unajifanya Yesu sio?”

Detective Ngesa alikuwa amefungwa mbele ya Senyenge ambazo kwa nyuma zilikuwa na vichuma villivyochongoka,ngumi moja aliyopigwa ilimfanya arudi nyuma na kujichoma navyo mgongoni.Mgongo wake ukawa una vitobo kama neti au nyavu ya kuvulia samaki.Alikula mateso ya kila aina lakini hakuthubutu kutoa siri hiyo nzito.Alipewa chakula mara moja tu kwa siku kama Mbwa.

Siku zilisogea akila mateso ya siri ndani ya kambi ya jeshi lakini wanajeshi hawakuambulia kitu.


Ngesa hakuwa na tofauti na mtu aliyegongwa na roli,sura yake haikutambulika hata kidogo,mateso aliyopewa hata mnyama pori hakustahili, wanajeshi walizidi kumsulubu,walim-mwagia kila siku ‘spirit’ kwenye vidonda vyake lakini Ngesa aliishia kupiga kelele za maumivu tu!

“Bado hajasema chochote?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa M.p Mangia.

“Bado”

“Sasa inakuwaje?”

“Mimi naona haina maana,tuongee na Brigedia Karanje tumsikilize anasemaje”

“Sawa”

Walichoka kumtesa mpaka wao walinawa mikono yao,kila aina ya mateso Ngesa alikula lakini wapi!

Siku hiyo usiku Brigedia Karanje alipigiwa simu akiwa Mkoani Kigoma,hata yeye alishangaa kupewa habari hizo,katika maisha yake hakuwahi kukutana na mtu nunda kama Ngesa.

“Unasema kweli?”

Brigedia Karanje aliuliza kwa mshangao.

“Ndio mkuu”

“Sirgent Mocha anaondoka lini?”

“Kesho mkuu”

“Wampakie kwenye gari wakamtupe huko msituni awe chakula cha Simba”

“Sawa mkuu”

Hicho ndicho kitu kilichofanyika,usiku wa siku hiyo Ngesa alitolewa akiwa hana fahamu na kupakiwa ndani ya lori la kijeshi ili siku inayofuata akatupwe porini.Ulikuwa ni msafara mrefu unaoelekea nchini Uganda,gari za jeshi kumi zilikuwa zinawekwa mafuta na lori alilowekwa Ngesa ndiyo lilikuwa na silaha za moto,nia ya wanajeshi ilikuwa wakamtupe Ngesa msituni kabla hawajavuka boda yoyote ile.

Asubuhi ya saa kumi kulivyopambazuka msafara ulianza kuelekea nchini Uganda.

**

“Sirgent,hivi yule mtu mlimtupa porini?”

“Shit..Nimesahau”

“Umesahau ndiyo nini?”

“Sio mbaya hapo mbele kuna msitu wa mabira,nitamtupa”

Walishafika tayari nchini Uganda,walipita mipaka miwili Namanga na wakati huo walikuwa wanavuka Mpaka wa Kenya na Uganda, Busia. Ndipo Ngesa akakumbukwa.Ulikuwa ni usiku mnene gari za jeshi zilikuwa zikitembea.Msitu wa Mabira ulikuwa mkubwa mno na wenye wanyama wakali wa kutisha,waliamini kama wangemtupa Ngesa asingeweza kupona hata kidogo,maana angeliwa.Waliamini kuwa angetafunwa na wanyama pori.

“Tunakaribia kufika,msitu una wanyama wakali tuwe makini”

“Sawa”

Wanajeshi walisemezana.Baada ya dakika kama ishirini walipunguza mwendo na kuweka lori kando pembeni ya msitu mzito,kila mmoja akashika bastola yake vizuri.Wakapita nyuma na kumbeba Ngesa huku na kule.Hakuna kitu kilichowatisha kama kusikia muungurumo wa Simba usiku huo,wakamteremsha harakaharaka.

“Tumuweke hapa tuondoke”

“Hapana,tusogee mbele kidogo”

“Wewe!humsikii simba huyo?”

“Ndio namsikia”

Sauti ya simba ikaunguruma tena,kitu kilichowachanganya sauti hiyo ilikuwa inasogea, simba hakuwa mbali nao.Wakamtupa Ngesa na kurudi ndani ya gari mbiombio.

***

Baridi alilokuwa anahisi lilitisha,maumivu aliyokuwa nayo mwilini hayakuwa na mfano wa kuyafananisha nayo.Kitu cha kwanza kumjia kichwani ni kukumbuka mateso sababu ndiyo ilikuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku.

Kumbukumbu zake zilichukuwa muda kurudi na kukaa sawa,bado alikuwa ameyafumba macho yake.

Alihisi hakuwa sehemu ambayo siku zote analala.Kitu kilichomchanganya Ngesa akili ni kuhisi kitu kinamlamba usoni,hapo ndipo hofu ikazidi kumtanda.Alielewa kivyovyote vile anayemlamba ni myama mkali ndiyo maana akatulia hakutaka kuyafumbua macho yake.Kwa mbali alihisi sauti za watu lakini hakuelewa ni lugha gani inaongelewa.

Hapo ndipo taratibu alipofumbua macho yake na kuona watu wameshika mishale,wamemzunguka.

Lugha walizokuwa wanaongea hakuzielewa.Mbali na hapo hakuelewa ni kivipi alifika mahali hapo.

“Elinyalio gwa-ne?”(Jina lako nani)

Ngesa hakuelewa lugha mbali na hapo alihisi maumivu makali kupita kiasi mwilini mwake hata shingo akashindwa kuizungusha vizuri,aliamini kuwa yupo sehemu ya hatari na watu hao wangempiga mishale endapo angefanya chochote kile,alibaki akiwaangalia tu.

“Elinyalio gwa-ne”(Jina lako nani)

Mtu huyo ambaye aliyeonekana ana madaraka kuliko wenzake alimsogelea ngesa akiwa ameuvuta mshale,Mbwa wao ndiyo aliwapa dira mpaka wakamfikia.Sio kwamba alishindwa kuwapa jibu la hasha,hakuelewa ni kitu gani akiseme.

“Ova waaa?ovaa waaa”(Unatokea wapi,unatokea wapi)

Jitu hilo likazidi kufoka kwa lugha la kiganda,walivyoona hajibu kitu wote wakamsogelea na kumchukuwa.Wakambe-ba na kuondoka naye.


Ngesa hakuelewa chochote kile,hakujuwa yupo wapi na imekuaje mpaka akawa msituni.Walitembea kwa kama umbali wa kilomita mbili ndipo alipoona vijiji,wakina mama wakikata kuni.Wote walimgeukia na kumshangaa!Ngesa akawekwa kandokando ya jiwe kubwa kisha baada ya dakika tano akatokeza mzee wa makamo mwenye mvi kichwani,akamtizama Ngesa kwa kitambo machoni.

“Who are you?”(wewe ni nani)

Hapo ndipo Ngesa alielewa lakini alipotaka kuongea alihisi sehemu za mbavu zina maumivu makali.

“Ng…esa”

“Say it again!”

Babu aliuliza,hakusikia vizuri kutokana na Ngesa kusema kwa sauti ya chini kwa tabu.

“Ng..esaaaa”

“Where are you from?”(Unatokea wapi)

“Moro..goro”

Bado Ngesa alidhani yupo ndani ya Tanzania.

“Where?” (Wapi)

“Moro..goro, Tanzania”

Babu,akamtizama Ngesa kwa kama sekunde saba akimkagua mwili mzima majeraha yake vizuri.

“Unazungumza Swahili?”

Hapo ndipo Ngesa alipomuangalia Mzee huyo aliyekuwa juu ya kigoda.

“Ndioo”

“Mimi naitwa Mugula”

Mzee Mugula,hapohapo akasimama na kuita vijana wake,Ngesa alianza kupewa matibabu dakika hiyo hiyo akasafishwa vidonda vyake, vikapakwa dawa.Vijana wakaingia msituni kutafuta majani mengine ambapo walivyorudi waliyatwanga kwenye kinu,wakabandika sufuria jikoni wakatumbukiza majani hayo.Dawa ikachemka,baada ya hapo akapewa Ngesa anywe!

“Kunywa,hii hiko ni muzuri itasaidia wewe,kukausha vidonda”

Mzee Mugula alimwambia Ngesa akimtoa wasiwasi.Dawa ilikuwa chungu kama muarubaini,lakini Ngesa alijitahidi akinywa huku akikunja sura yake.

“Nasikia njaa”

“Utakula ondoa shaka,maliza dawa”

Matibabu ya asili yaliendelea kwa takribani nusu saa lizima ndipo Ngesa alipewa chakula,akala akaongeza tena.


Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuishi katika kijiji hiko,kutokana na kukosa nguvu za miguu alipewa magongo aweze kufanyia mazoezi.Mzee Mugula aliwapenda watanzania sababu alikuwa ni rafiki mkubwa wa Hayati Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere miaka mingi iliyopita,kipindi cha vita vya Idd Amin pia alikuwepo, katika watu waliokula mateso ni Mzee Mugula,alishawahi kulishwa ndala za chooni akiambiwa aitafune sababu tu alionekana akiwa amezivaa katikati ya jiji la Kampala,jeshi la Tanzania ndilo lilileta Amani nchini Uganda, kumtoa Nduli Idd Amin Dadaa!Kwa msaada huo hakuweza kumsahau Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Ndiyo mambo yalikuwa hivyo,nilivyotoka mjini kwenda kuchukuwa dawa ya muke wangu,nikaambiwa nitafune slipers zangu”

Mzee Mugula alitoa simulizi hiyo iliyomuacha Ngesa mdomo wazi.

“Siyo hivyo tu,alikuwa akichukuwa Viwete,pamoja na walemavu na kuwatupa Ziwa Victoria,Mujomba wangu alikufa Baba yangu na Mama yangu pia”

“Pole sana”

“Mungu ailaze roho ya rafiki yangu Julius Nyerere pema peponi”

“Amen”

Ngesa akaitikia,siku hiyo waliongea mengi sana na Mzee Mugula.

“Ilikuwaje,ukawa hapa?niliambiwa kuwa ulikutwa porini hali yako ikiwa mbaya sana”

“Mpaka sasa hivi sijaelewa lakini nakumbuka nilivamiwa nyumbani kwangu,wakauwa familia yangu.Baada ya hapo sikujua kinachoendelea ndiyo nikajikuta nipo msituni”

Ngesa alidanganya,bado hakuwa na uhakika ni binadamu gani amuamini.

Baada ya siku saba hali yake ilikuwa nzuri hakutumia msaada wa magongo kutembea,akaungana na vijana kuwinda wanyama pori.

Kijiji kikampenda sababu ya upole wake pamoja na juhudi za kusaidia kazi,alimuheshimu kila mtu mdogo na mkubwa,alishaelewa kuwa yupo nchini Uganda.


Siku moja wakiwa wanawinda ghafla kikatokea kikundi cha watu sita,kikawazunguka kikiwa na mishale.Wakawekwa chini ya ulinzi.Ngesa bado hakuelewa lugha lakini alijua hakukuwa na usalama wowote, alivyoona wavamizi hao wanaongea kwa kufoka huku wakianza kupiga watu kijiji chao makofi,kila mmoja alikuwa akipigwa.

Ilivyofika zamu ya Ngesa ilikuwa tofauti,aliudaka mkono wa mtu huyo aliyekuwa anataka kumpiga.

“Nendeni msitake matatizo”

Ngesa alisema na kuwatizama vijana hao walioshika mishale wamemuoneshea,hata hivyo ilikuwa vigumu kuelewana lugha.


Mbali na Ngesa kuwa na mwili mdogo lakini alikuwa mwepesi na mtundu,alijua kujitetea,mbali na hapo alikua ‘proffesional’ kwenye mchezo hatari wa Judo,alivyoona hakuna maelewano alirusha kofi lililompiga mmoja wao,mmoja akaachia mshale Ngesa akaukwepa na kugeuka na ‘round kick’wawili wakawa wapo chini.Mwingine alimsogelea akitaka kurusha ngumi alimvuta na kumpiga kichwa puani,akamvuta mwingine na kuuzungusha mkono wake akumsukumiza kando.

Ilikuwa ni kama sinema tu,lakini Ngesa aliwapiga wote kimasihala masihala.

****

Swala la Ngesa kupiga watu sita likageuka na kuwa stori kijiji kizima kila mtu alitaka kumuona kijana huyu Ngesa,wakina mama ndiyo usiseme.Kijiji kikazidi kumpenda.

Siku zote Ngesa alimkumbuka Hans hakuelewa kama yupo hai au amekufa,alimkumbuka mtoto mdogo aliyemkabidhi.Ilipita miaka mingi sana,hakuelewa ni kwa njia gani angempata.Alikuwa nyuma ya mambo yote,ilikuwa ni lazima siku moja arudi Tanzania tena jijini Dar es salaam akaonane na Hans rafiki yake kipenzi.

“Hapana Mjukuu wangu,inabidi ukae kae kidogo”

Hivyo ndivyo alivyoambiwa na Mzee Mugula siku hiyo alivyomwambia anahitaji kurejea Tanzania.

“Inabidi nirudi nyumbani lakini”

“sawa utarudi,usijali”

Ngesa hakuwa na sababu ya kuondoka kwa kutoroka sababu uwezo huo alikuwa nao,ilibidi asubiri tena.

Aliendelea kusaidia kazi akijichanganya na wanakijiji.Kitu kilichomchanganya akili yake ni mke wa Mzee Mugula,Deborah.

Alikuwa ni msichana mdogo wa kinyan’kole.Mazoea ya msichana huyu yalikuwa kwa kasi ya risasi! Kwa mara ya kwanza alidhani ni kawaida tu lakini haikuwa hivyo,hakutaka kujiingiza kwenye matatizo na mke wa mwenyeji wake ambaye hata hivyo alikuwa ni mdogo kiumri.Alikuwa ni Mwanamke mzuri,mwenye asili ya Kinyarwanda kwa mbali.Huyo ndiyo mwanamke aliyekuwa anampelekea chakula Ngesa usiku,alijua Kiswahili kwa mbali.

Kutokana na uzee aliokuwa nao Mume wake Mzee Mugula,hakuwa na uwezo wa kumridhisha binti huyo akafurahia tendo la ndoa!Ujio wa Ngesa katika kijiji hicho kilimfurahisha ndiyo maana akaanza mazoea naye ya karibu nayeye ndiye aliyemuomba Mume wake ruksa ya kupeleka chakula chumba anacholala Ngesa kwa kisingizio kuwa wanaongea lugha moja,mumewe hakuwa na tatizo hakuelewa ndani ya kichwa cha Deborah kuna nini.

Kama siku zote ilivyokuwa,Saa mbili Deborah alipakuwa chakula na kutembea mpaka chumbani kwa Ngesa.

“Hodii”

“Karibu Debora”

Deborah aliingia kwa uwoga,sababu hakuelewa ni wapi angeanzia.Akaweka chakula chini na kuanza kuondoka lakini badala ya kutoka nje aliufunga mlango wa majani na kumrudia Ngesa.

“Deborah!”

“Usipofanya nachotaka,nitapiga kelele unataka kunibaka”

Maneno hayo yalimfanya Ngesa atoe macho,hakuelewa ni kitu gani akifanye.Deborah alitupa kanga yake pembeni,akabaki kama alivyozaliwa!




“Nari nari naari”(Moto moto moto)

Kelele za wanakajiji kutokea nje ndizo zilimfanya Ngesa atoke kwenye jaribio hilo la kutaka kuzini na Mke wa Mwenyeji wake,alivyoona moshi ndipo alipomsukumiza Deborah kando na kutoka nje.

Kijiji kilikuwa kikiteketea moto nyumba za nyasi zilikuwa zinaunguzwa na watu wasiojulikana waliendelea kutupa vijiti vyenye moto wakiendelea kukiteketeza.

Ngesa hakutaka jambo hilo liendelee akamfuata mmoja wa watu walioshika mti unaowaka moto na kum-mtwanga kichwa puani,akamvuta na kumpiga kifuti cha tumbo akamsukuma kando.Kila alipozidi kupiga hatua ndipo hasira zilimpanda,akamsukuma mwanaume mmoja aliyetaka kufanya jaribio la kubaka.

Huyu alimpiga vibaya sana mpaka kumvunja mkono wake wa kushoto.Ndani ya dakika tano alikuwa tayari ametuliza gasia na wanakijiji walianza kumwaga maji ili kuuzima moto ulioanza kuwa mkubwa sana,kila mtu alimshangaa Ngesa ambaye hata yeye alikuwa bega kwa bega na wanakijiji kuzima moto.

***

“Hao watakuwa kijiji jirani,wale vijana uliowapiga kipindi kile”

“Lakini Jana nilikutafuta bila kukuona Babu”

“Nilijificha”

Mzee Mugula usiku kipindi moto unateketeza kijiji yeye hakuonekana,alikuwa amejificha mbali akijihami hata hivyo alimshukuru sana Ngesa kwa msaada aliotoa wa kupambana na watu hao wavamizi,Ngesa akawa ameokoa kijiji kwa mara nyingine, akazidi kujizolea sifa.

Licha ya yote alisisitiza kuhusu swala la kuondoka na kurejea Tanzania,haikuwa rahisi kwa Mzee Mugula kukubali swala hilo lakini hakuwa na jinsi,kishingo upande akakubali.

“Wiki ijayo kuna gari la mizigo linaenda Tanzania utaondoka nalo,niliongea na Utingo wa lori”

“Babu ahsante sana”

“Hata ukiondoka naomba usitusahau”

“Usijali babu”

Kuondoka kwa Ngesa ndani ya kijij hicho ilikuwa simanzi kubwa sana hasa kwa Deborah,alihisi uchungu ajabu.

Kwa heshima kubwa, siku hiyo ya kuondoka kwa Ngesa walipika chakula kingi na kufanya sherehe ndogo ya kumuaga,kijiji kizima kilikuwa katika hali ya uzuni mkubwa wengine walilengwa na machozi,Deborah aliumia sana moyo.

Lori lililobeba mbao lilitarajia kupita msitu wa Mabira usiku wa saa nne na yalibaki masaa machache tu.

“Ngesa,kuwa na safari muzuri,huyo utingo anaitwa Chinga”

“Ahsante mzee,usijali nitafika”

Mzee Mugula waliagana na Ngesa na kupeana mikono,wanakijiji walikuwa wamesimama pembeni wanamtizama,akawaangalia na kuanza kuondoka kwa hatua chache kisha akapotelea katikati ya miti akiacha wanakijiji wakiwa katika hali ya majonzi kupita kiasi.


Ngesa alikatiza katikati ya msitu usiku huo,kilichomsaidia ni mwanga wa mbalamwezi.Akatembea na kufika barabarani,hapo hakukaa sana akaliona lori kubwa linatokea upande wake wa kaskazini,linawakaa taa kila mahali,akabaki amesimama kandokando ya barabara,lori likapunguza mwendo na kusimama kabisa.

“Kijana”

Mwanaume mrefu mrefu alimuongelesha Ngesa akiwa ametokea ndani ya lori.

“Naaam”

“Wewe ndiyo Ngesa?”

“Ndio”

“Twenzetu mzee”

Kitendo cha kuitwa hivyo kilimaanisha watu hao walimfahamu,akaingia ndani ya gari na safari ikaanza hapohapo.Kila mtu alijitambulisha na stori zikaendelea.

“Ndio Chinga,ilikuwa juzi hapa nipo Mbeya huko Kyelaa”

Dereva aliyefahamika kwa jina la Bwana Kabumbu alianza kupiga domo na utingo huku akiwa makini juu ya usukani anatafuna mirungi!

“Enheee,Kyela huko!”

“Nilikuwa na Dula,tukatoka fresh kufika kitonga kwenye ule mlima breki zikafeli.Alafu nilikuwa kibati nateremka”

“Sasa ikawaje?”

“Tulia sasa,kupamp breki zikakataa,kupamp zikakaa,Nikamwambia Dula breki zimefeli.Lolote na liwe nikafungua mlango nikaruka nje.Lori likaaribika sema Bosi hakumaindi nilimuelezea si unajua tajiri mzungu yule”

“Hivi ni mtu wa wapi?”

“Amechanganyika Kongo na Rwanda,sijajua kwa kweli.Anaitwa Kamere Vital.Ana pesa nyingi sana”

Dereva na utingo wake waliendelea kupiga stori,Ngesa alikuwa kimnya anayafuatilia mazungumzo yao lakini hakutaka kuchangia mada sababu aliamini mazungumzo hayo hayakumuhusu.

Safari ilizidi kuendelea mpaka wanafika mpaka wa Kenya na Uganda, Busia. Ilikuwa usiku sana,hapo walilazimika kupiga hati zao mihuri.

“Nimeambiwa hauna passpot ndugu, hapa cha kufanya teremka utembee kwa mguu,sisi tutakukuta mbele”

Maagizo hayo alipewa Ngesa,akashuka ndani ya lori na kufanya kama alivyoambiwa tena bila wasiwasi akaanza kutembea kuelekea gizani,akiwaacha bwana Kabumbu na utingo wake uhamiaji wakigonga hati zao za kusafiria mihuri,walivyomaliza waliingia ndani ya lori lao kisha kuanza safari na walivyofika mbele kweli walimkuta Ngesa yupo gizani anawasubiri upande wa Kenya tayari.

“Ingia ndani ya gari ndugu”

Ngesa akapanda.

“Jina lako ni nani?”

“Ngesa”

“Pole na matatizo Mzee alinieleza kila kitu,kwahiyo sasa hivi utaenda kufikia wapi?”

“Popote tu mimi nitafikia”

“Sisi tunaishia Arusha”

“Sawa sio mbaya,mtakuwa mmenisogeza”

Ngesa alikuwa na mwili mdogo wa kawaida lakini akili yake ilikuwa inafanya kazi kwa kasi sana mara nyingi alikuwa ni mtu makini na mkimnya,macho yake yalikuwa mbele anatizama barabara.

Mwendokasi wa lori ulitisha dereva alikimbikiza kupita kiasi.

“Kabumbu”

Utingo alimuita dereva alikuwa ni kama ameona kitu mbele.

“Vipi?”

“Unaona kule mbele”

“Ndio,vipi kwani?”

“Embu subiri kwanza,kuna mwanamke amesimama katikati namuona ana kitambaa”

“Wewe vitu hivyo hujavizoea tu?”

Kila gari lilipozidi kwenda ndipo mwanamke aliyekuwa barabarani walizidi kumuona vizuri,alikuwa katikati ya barabara ameshika kitambaa anakipunga hewani.

“Hapa hasimami mtu”

Dereva akapandisha gia,akakanyaga mafuta ya kutosha gari likazidi kuteleza, Ngesa alimtizama Mwanamke huyo kwa umakini.

“Hawa wanakuwaga majambazi au wakati mwingine wachawi hawa,asipopisha namgonga”

Dereva alizidi kuzungumza na kupiga honi ili kutoa tahadhari, gari lilivyofika karibu Mwanamke aliyekuwa barabarani alipisha,wote wakashusha pumzi ndefu lakini Ngesa aliangalia kioo cha nje na kuzidi kumdadisi

“Kuna kitu nadhani”

Ngesa alitoa hoja.

“Kitu gani?”

“Huyu Mwanamke kuna kitu nahisi alitaka kutuonya”

“Hao mademu majambazi,yaani pale tungesimama wallahi tungevamiwa”

Dereva akampinga Ngesa na kuzidi kunyoosha,aliyapuuzia mawazo yake.

Akashusha gia ili apandishe kilima ndani ya msitu mkubwa uliozungukwa na miti,akaweka gia vizuri ili kuteremsha mlima.


Mbele yake kulikuwa kuna kona kali akajiandaa kukunja,lakini ghafla akaweka mguu kati ili kupiga breki baada ya kuona magogo ya mti yamepagwa katikati ya barabara.Kutokana na mwendo aliokuwa nao gari likamshinda akajikuta amehama barabarani.Gari likaingia msituni,kabla ya kufanya chochote alihisi sauti za watu zinatokea porini.

“Hapo hapo mlipo,hakuna kushuka”

Kwa kasi ya ajabu na jinsi mwili wake ulivyokuwa mwepesi,haraka akaruka nyuma.Chinga alivyotaka kumuiga Ngesa kwa kujificha viti vya nyuma majambazi wakawa tayari wamefika.

“Aroo wewe,shuka shuka upesi.Shuka kabla sijapiga mapanga”

Tayari walikuwa mateka,Kabumbu na Utingo wakashushwa ndani ya lori na kunyoosha mbele huku mikono yao ikiwa juu hewani,Majambazi waliowateka walikuwa wameziba nyuso zao na wanatochi zenye miale mikali,Pembeni yalikuwa yamepaki mabasi mengine matatu yametekwa nyara.Kushoto kulikuwa na abiria waliolala juu ya majani.

“Wewe songa pale upesi”

Chinga akasukumizwa,uwoga ulimtanda akatembea na kulala juu ya majani kisha Dereva wake akafuata wote wakawa wamelala kifudifudi vichwa vyao vinaangalia chini.

“Wewe uliyevaa suti,wewe bwanamdogo.No wewe hapo Embu songa hapa”

Jambazi mmoja aliamuru na mzee mmoja aliyevaa suti akasimama.

“Umetoa pau ngapi pale mlangoni?”

“Shilingi mia mia tano ya Kenya”

“Kwanini?”

“Ndiyo niliyo nayo”

“Sio kweli,haiwezekani uvae suti utoe pesa ya kidogo.Toa pesa mzee”

Majambazi hawakuridhika na pesa walizopewa,hapo ndipo kibao kikabadilika mmoja mmoja akaanza kuitwa.

“Sasa swala ni moja.Unapita pale unaacha nguo yako hapa.Haraka haraka,tuokoe wakati”

Kila mmoja alikuwa mwenye hofu mno na kukiuka amri hiyo kulimaanisha maisha yao kuingia hatarini kama siyo kufa,majambazi walikuwa wakenya na hawakutaka kupotezewa hata sekunde moja,walitaka kumaliza zoezi hilo la kuchukuwa mali za abiria na kuondoka zao.

“Paaaaaaaa”

Abiria mmoja alipigwa risasi ya kichwa kumaanisha kuwa hawakuwa na utani hata kidogo.

“Vueni nguo upesi”

Haikuwa na mzee,kijana,mtoto wala mtu mzima kila mtu alianza kuvua nguo harakaharaka na kuweka mbele kisha kupita upande wa pili wakiwa uchi wa mnyama.


Mlio wa risasi ulisikika kwa sauti kubwa,Ngesa aliyekuwa ndani ya gari alitoa kichwa chake kwa juu na kuchungulia,nafsi yake ilimtuma ajaribu kufanya zoezi la ukombozi.

Akiwa ndani ya gari hakuona mtu yoyote zaidi ya miale ya tochi ikimulika huku na kule,kwa tahadhari kubwa akafungua mlango na kutoka nje,akanyata taratibu kama chui anayenyemelea kitoweo na kujificha nyuma ya mti mkubwa.

Kazi yake ilikuwa ni kuwahesabu majambazi waliokuwa wamesimama.Alivyotaka kutoka kwenye mti haraka akarudi tena baada ya kumuona jambazi mwingine katokea kushoto kwake kashika bastola,huyo ndiye alitaka aanze naye.Akaokota kipande cha mti na kukitupa pembeni, jambazi akageuka na kuanza kusogea alipo,hilo ndilo kosa alilofanya jambazi huyo.Akamvaa haraka na kumziba mdomo,akaukamata mkono wake ulioshika bastola akaukunja,akamvuta kando na kumkaba kohoni kwa nguvu zake zote.

“Argh argh”

Jambazi alikuwa akigugumia akitapatapata, roba aliyopigwa na Ngesa ilikuwa kali.

“Kaaa”

Shingo ya jambazi ilikuwa imevunjwa akapoteza maisha hapohapo,Ngesa akachukua bastola yake akaangalia huku na kule,akaivua maiti soksi aliyoivaa usoni ambayo ilitobolewa machoni na kuivaa yeye.Hakuwa na uhakika kwa kitu anachotaka kukifanya,akatokeza kwa majambazi, wote wakamgeukia.

“Ulikwenda wapi?Njoo hapa tumalize shughuli chapchap”

Jambazi akatoa amri hakuelewa kwamba anaongea na Ngesa, kutokana na usiku kuwa mwingi,hakugundua kabisa.

“Kara kara”

“Unasema?”

Ngesa alijaribu kuongea kitu kisichoeleweka huku akimpungia mkono Jambazi kuwa asogee alipo.Kama nyumbu jambazi huyo akasogea na kwenda na Ngesa gizani hapo ndipo alipopigwa kichwa puani,akatulizwa na kitako cha bastola kichwani.Akavutwa na kuvunjwa shingo jambazi wa pili akawa ameaga dunia,akainama na kumsachi akamkuta na kisu kiunoni akachukuwa na kukiweka kiunoni. Alivyohesabu waliobaki walikuwa wanne na wote walikuwa wameshika silaha kali wanawahamrisha abiria wavue nguo zao kisha wapite kando.

“Vua haraka vua haraka”

Jambazi likaamrisha Ngesa akatokea nyuma yake akajifanya kujiunga nao.Kushoto alisimama jambazi mwingine anatizama huku na kule,taratibu mkono wa Ngesa ulipita kiunoni mwake akawa anachomoa kisu.

“Wewe wenzako wako wapi?”

Lilikuwa ni swali aliloulizwa Ngesa.

“Chopa yuko wapi?”

Ngesa aliogopa kujibu swali hilo sababu sauti yake ingegundulika ndiyo maana alikaa kimnya na kujifanya hajasikia.Kama umeme alichomoa kisu akatumbukiza tumboni mwa Jambazi huyo aliyekuwa anachonga mdomo.

“Paaaaaa”

Mkono wake wa kulia ulioshika bastola alifyaatua kwa jambazi wa kulia kwake.Akarudi nyuma kitaalam na kumpiga kifuti jambazi mwingine.

“Paaaaaa”

Ilikuwa ni kama sinema ya kuigiza kumbe ni kweli,Ngesa alikuwa akipambana kiume alikuwa yupo radhi kufa au kupona ili kuwaokoa wenzake.

“Paa paaaaa”

Jambazi mmoja akatokeza nyuma yake,Ngesa akakimbilia mitini hapo ndipo walipoanza kurushiana risasi.

Katika shabaha Ngesa hakukosea hata kidogo hususani katika maswala na kucheza na silaha za moto,akajificha vizuri nyuma ya mti na kuiweka bastola vizuri,akabana jicho lake la kulia ili kutafuta shabaha ya jambazi aliyekuwa umbali wa mita mbili amechanganyikiwa anatafuta huku na kule.

“Paaaaaaaa”

Ngesa akaachia risasi,jambazi akadondoka chini.Na huyo ndiye alikuwa wa mwisho hata hivyo hakutaka kutokeza kichwakichwa,akatembea kimachale na bastola yake mkononi.

“Inukeni jamani”

Ngesa akasema,kila mtu hakuwa ana amini maneno hayo,baada ya dakika moja abiria waliokuwa wamelala mateka walikimbilia nguo zao.

“Hii sketi yangu”

Dada mmoja alisema,Mzee mwenye mvi nyingi alionekana kuchanganyikiwa na kutaka kuvaa sketi,wengine walivaa nguo sio zao.

Kila mtu alikuwa akimshangaa Ngesa hasa Chinga na dereva wake Kabumbu,dakika thelathini baadaye magofu ya polisi yalitokeza na magari yote yakaelekea kituoni.Kila mtu akatoa maelezo yake.Askari walimuhoji mara mbilimbili Ngesa,hawakutaka kuamini kama mtu huyo mmoja kawaangusha majambazi wote na kuwauwa!

Magari yote yalikesha mpaka kulivyopambazuka ndiyo askari wakawaruhusu,Ngesa na wenzake wakaingia ndani ya lori na safari yao ikaanza,njiani Ngesa alikumbana na maswali chungumzima.Lakini yote aliyajibu.

“Tulikuwa tunafundishwa masjid karate”

Hivyo ndivyo alivyojibu Ngesa hakutaka kuweka wazi kwamba alikuwa ni Detective wa kujitegemea na mafunzo ya kupigana alijifunza nchini Mexico na ndiyo huko alipofuzu mafunzo ya mchezo hatari wa Judo!


Waliingia jijini Arusha kesho yake saa tatu ya Asubuhi,lori likapaki Alumeru hapo ndipo safari ya Ngesa ilipoishia.

“Nawashukuru sana ndugu zangu,wacha mimi niangalie utaratibu”

“Sawa kaka,tunashukuru sana umetuokoa”

Ngesa alikuwa ana begi la mkanda mmoja begani,alivuka barabara na kwenda upande wa pili hakuelewa anaenda wapi ingawa alijua yupo mkoani Arusha.

****

“Mh.Raisi sasa tutafanya nini?”

“Sijui lakini sitoweza kusaini”

“Inabidi usaini,watu watakufa”

“Nimekwambia siwezi”

“Kwahiyo Mh.Raisi upo tayari kuona wakenya wenzetu wanauwawa?”

Raisi wa Kenya alikuwa katika wakati mgumu kupita kiasi,simu aliyopigiwa ilimtisha mno.Jengo la ‘Wastegate’ lilikuwa mateka na mamia ya watu walikuwa wameuwawa tayari.Ndiyo maana akawaita washauri wake ili wamshauri ni kitu gani akifanye.

“Griii griiiii”

Simu ikaita tena,Mh.Raisi akabaki anaitizama ikapokelewa na mmoja wa washauri wake ikawekwa loudspika,Raisi akawa anasikia kila kitu.

“Tuko na ndugu yako Jennifer Olamba”

Sauti hiyo ikamchanganya akili yake.

“Unajua nitakachomfanya usipo saini?”

Jambazi akaongea tena,Msichana mdogo alikuwa mbele yake.Majambazi hao hawakuwa na masihala hata kidogo na ingewezekana kabisa kumtoa uhai Jennifer Olamba kama Raisi ama Mjomba wake angeshindwa kukubali matakwa yao.

Vital Kamere alikuwa miongoni mwa mateka waliokuwa ndani ya Wastegate mara nyingi alikuwa akimuangalia Daphine,aliomba Mungu wasimdhuru japokuwa alikuwa tayari ameachiwa.

“Nitamkataka kiungo chake kimoja kimoja,nitaanza na vidole”

Kidole cha Jeniffer kiliwekwa mezani,kisu kikubwa kikaletwa.

****

Nje ya geti la Wastegate kulijaa polisi chungumzima lakini walikuwa mita kumi wakisubiri amri ya kuingia na kufanya ambush,waliogopa sababu majambazi hayo yalikuwa yamevaa mabomu mwilini,kuingia kwa ghafla ilimaanisha kusababisha hatari zaidi,ndiyo maana walitulia wakifanya mawasiliano.

“Ndio mkuu,bado iko ndani”

“Subiri amri kwanza”

“Sawa”

Polisi walikuwa wanafanya mawasiliano kwa njia ya redio upepo,kitu kama hicho hakikuwahi kutokea nchini Kenya,Wastegate iliwekwa mateka kwa takribani masaaa matano na kilichokuwa kinasikika ni milio ya risasi tu.

“Wengine wapite round haraka,mutasubiri kile nachotaka kusema”

Polisi wakaanza kujigawa,wakaliweka jengo hilo katikati tayari.Kwa tahadhari kubwa wakaingia ndani bila kuonekana.

“griiii giii….polisiiiii”

Hapo ndipo Ambush ilipoanza,jambazi mmoja ndiye aliyeachia risasi,alikuwa ameshika mtutu.Hapo ndipo Polisi walipoingia kufanya ambush,kilichosikika ilikuwa ni milipuko ya mabomu.

“Griiii paaa paaa griiiiiiiii gegegegegegegege”

Risasi zilirushwa askari wa Kenya hawakutaka kurudi nyuma,walishikwa na hasira ndiyo maana wakaingia ndani ya jengo hilo kwa umoja ingawa baadhi yao walikuwa wakipigwa risasi na kudondoka chini.

“Buuuuum”

Ulikuwa ni mlipuko wa bomu,upande mmoja wa jengo ukadondoka na matofali kuwafunika baadhi ya watu waliokuwa mateka ndani ya jengo.

“Nis….aidie”

Daphine alikuwa pembeni ya mtu aliyekuwa amebanwa na tofali kubwa,alikuwa ni mwanaume wa makamo yake,jiwe lilikuwa limemkandamiza mgongoni mwake.

“Nisaaaaidi…e nakuf…a”

Daphine alitetemeka kupita kiasi,aliendelea kusikia milio ya risasi na milipuko.Akamshika mwanaume huyo mkono ili kumvuta akijaribu kumuokoa lakini ilikuwa vigumu.

“Ka….mataaaa hiii Si..mu ina videoo”

Mwanaume huyo aliyekuwa anatoa damu usoni alitoa simu na kumkabidhi Daphine.

“Mta..fute Raisi a..umkabidhi.Mwambie aitizame”

Hapohapo mwanaume huyo akakata kauli,hakuweza kuongea tena.


Daphine alitandwa na hofu hakuelewa simu hiyo ina kitu gani lakini aliiweka mfukoni na kuanza kutambaa kama nyoka ili kuyaokoa maisha yake,milio ya risasi ilizidi kumchanganya akili yake.

Kila dakika askari walizidi kuongezeka,majambazi wakaanza kuzidiwa wengine wakakimbia na wengine walikamatwa.Haikuwa kazi rahisi hata kidogo.

***

Baada ya akili yake kutulia ikiwa tangu siku mbili zipite,alikumbuka simu aliyopewa ndani ya jengo la ‘Wastegate’ akaiwasha na kuanza kuichunguza,hapohapo akaingia ndani ya video na kuangalia,kila kilichotokea ndani ya jengo la wastegate kilikuwa kimerekodiwa tena sura za majambazi zilionekana,akaitizama mara mbili mbili.Hakuelewa hata kidogo ni kwa namna gani ataongea na Raisi akamkabidhi simu kama alivyoambiwa.

“Baba”

“Naaam mwanangu”

Daphine alimuendea moja kwa Moja mlezi wake ama baba kama alivyozoea kumuita,huyo ndiye mtu pekee aliyemuamini.

Bila kuchelewa alianza kumuadithia kila kitu kinagaubaga.

“Embu nitizame”

Mr.Vital Kamere nayeye akaitizama video iliyorekodiwa kupitia simu,akashtuka sana.

“Inabidi tumpe raisi,niachie mimi hilo swala”

Mr.Vital Kamere siku hiyo hiyo alivyokuwa hotelini alisaka namba za ikulu,akampata mmoja wa wafanyakazi aliyeitwa Penina Mtobola.Na kuambiwa kuwa anahitaji kuzungumza na Raisi.

“Raisi ako kwenye meeting”

Penina Mtobola alijibu.

“Sawa nitakupigia baadaye ni muhimu sana”

Bado waliendelea kukaa kwenye Hotel iliyoitwa Shulk jijini Nairobi,kutokana na mambo yalivyotokea waliogopa kuendelea kubaki.

“Daphine”

“Abee”

“Jiandae kesho tunaweza kuondoka”

“Sawa”

Hawakukaa sana simu ya Mzee Kamere ikaita,akawa anaongea moja kwa moja na mshauri wa Raisi, Mr.Bernard Sembe.

“Ndio nilikuwa nahitaji kuongea na Raisi”

“Una shida naye gani?”

“Ni mambo binafsi”

“Ongea shida yako”

Mzee Kamere akashusha pumzi kidogo.

“Kuna simu nataka kumpa ina tukio lote lililotokea wastegate na watu waliohusika”

Kitendo cha kuongea hivyo ukimnya ulitokea wa kama sekunde tano.

“Halloo unanisikia”

“Nakusikia,upo wapi?”

“Nipo Shulk hotel,chumba namba 19”

“Sawa”

Hapohapo simu ikakatwa.

***

Katika watu hatari waliokuwa wanashirikiana na Majambazi walioteka wastegate ni mtu huyu mshauri wa Raisi,Benard Sembe. Habari za kurekodiwa kwa majambazi kulimaanisha mambo kumgeukia kwa maana hiyo ilikuwa ni lazima asawazishe.

“Halloo David upo wapi?”

“Nipo Nairobi”

“Kuna kazi nataka kukupa”

“Nakusikiliza”

Benard Sembe hakutaka kupoteza muda,alimtuma kijana wake aende shulk hotel dakika hiyohiyo,kumchukuwa Mzee Kamere.

“chumba namba ngapi?”

“Kumi na tisa”

“Kisha?”

“Nitakupigia”

Maongezi yalihitimishwa,kijana wa kazi akachukuwa bastola na kuiweka kiuoni tayari kwa kuingia kazini.

David kijana aliyetumwa na Benard Sembe alifika hotelini na kupewa ruksa ya kuingia chumbani.

“Ndiyo nimetumwa kutoka ikulu”

“Sawa”

“Tunaweza kuongozana?”

“Hakuna tabu”

Vital Kamere akiwa na Daphine pembeni yake walitoka nje,hawakuelewa lolote lile.Waliingia ndani ya gari na safari ikaanza.Gari ikatembea mpaka kandokando ya barabara ya vumbi,hapo alitokea mwanaume mwingine mrefu mweusi akawafuata.

“Mimi naitwa Benard,raisi yupo bize.Mnaweza kuongea”

“Sawa,huyu mwanangu alipewa simu na kijana aliyekuwa ndani anarekodi watu walioteka hilo jengo sa…”

“Hiyo simu iko wapi?”

“Hii hapa”

Mzee Vital kamere alitoa simu na kumkabizi Bernad Sembe.

“Ahsante,David fanya kazi yako”

Kauli hiyo ilivyotoka tu,mtu aliyewachukuwa hotelini alitoa bastola na kuwaelekezea Daphine na Vital Kamere.

“Kacha kacha”Bastola ilikokiwa.

Daphine alitetemeka kupita kiasi sababu bastola ilikuwa kichwani kwake.

“Subiri kwanza usiwauwe”

Benard Sembe alitokeza ghafla.

“Memory kadi iko wapi?mbona hakuna video?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Benard Sembe baada ya kukosa alichokuwa anakitafuta!


 Kutokuwepo kwa memori kadi ndani ya simu ndiyo iliyowafanya wawepo hai mpaka dakika hiyo,Mzee Vital Kamere jasho lilimtoka kupita kiasi aliamini maisha yake yalikuwa ukingoni siku hiyo hiyo,alichokifikiria kwa wakati huo ni kuacha utajiri mkubwa na ilikuwa ni mapema kufa tena akiwa ugenini.

“Memori gani iko wapi?”

Lilikuwa ni swali lingine.

“Da.phine Da..phine una memori kadi uwape?”

Vital Kamere aliongea akiwa mwenye kigugumizi ambacho hakuelewa kilitokea wapi hiyo ilitokana na hofu ya kifo cha kufyatuliwa na risasi.

“Sina”

Sijui akili ya kuficha memori kadi aliitoa wapi,alikuwa ni kama alichezwa na machale ndiyo maana akaificha na kitu kilichokuwa kinataka kutokea masaa machache mbeleni ndicho alikiwaza kabla,kichwa cha Daphine kilikuwa kinafanya kazi zaidi ya kompyuta na mpaka wakati huo alielewa kuwa memori kadi ndiyo iliyokuwa inawaweka hai.

“Daph…ine,mbona ilikuwepo?”

“Dad,sina memori kadi”

Watu waliokuwa mbele yao walichukulia maongezi ya Kamere na Daphine ni kama maigizo.

“Msituletee maigizo hapa,leo mtaeleza David funga kamba kisha peleka hii ile sehemu”

“Ok”

Vital Kamere na Daphine walifungwa kamba miguuni na mikononi.Gari likaondoka dakika hiyohiyo, hawakuelewa ni wapi wanapelekwa na kutokana na gari hiyo kuwa na vioo vikali vyeusi yaani ‘tinted’ hakuna mtu yoyote aliyekuwa nje aliyewaona.

“Toeni Memori kadi kabla mambo hayajawa mabaya”

Jambazi David alisema huku akiwatizama mateka wake kupitia kioo cha katikati cha gari lakini wote walikuwa kimnya.

“Hamtaki kusema?nyie viburi.Napenda kuwaambia kuwa mtaitoa kwa njia moja ama nyingine”

Yalikuwa ni maneno ya kutisha na kutokana na jambazi huyo kuwa mweusi mwenye sura ya kutisha hiyo ilifanya aogopeke zaidi.Gari lilitembea kwa umbali wa kama kilomita thelathini wakatoka kabisa nje ya mji wa Nairobi na kuingia Nakuru,kijiji kilikuwa na miti mingi kandokando ya barabara na hakukuwa na rami hata kidogo,barabara ilikuwa na vumbi tu tena la rangi nyekundu jinsi gari lilivyokuwa linatembea kwa kasi ilifanya vumbi litimke juu.

“Kama Una memori kadi Daphine tafadhali naomba uwape”

Mzee Vital Kamere bado aliendelea kutandwa na hofu baada ya kuona gari linazidi kuingia ndani ndani,moyo wake ulipiga kwa kasi muda wote na hakuelewa huko wanapoenda wanaenda kukumbana na shughuli gani.

“Sina”

Daphine alijibu kifupi hakuwa mrahisi kutoa jibu kuwa ana kitu hicho alichoamini kuwa kinawafanya wapumue.Gari likasimama nje ya nyumba kubwa ambayo kwa harakaharaka haikumaliziwa, haikuwa na madirisha na ilikuwa katikati ya pori,hapo ndipo safari yao ilifika kikomo wote wakashushwa na kuingizwa ndani ya jumba hilo bovu bovu.

“Songa mbele”

Kabla hawajakaa vizuri gari aina ya Chaser nyeusi ikapiga msele na kufanya vumbi jingi liruke, ilionekana dereva aliyekuwa ndani ya gari alikuwa na usongo ajabu na alipotoka alikuwa akikimbiza gari kama mwehu,ni kweli Benard Sembe alishuka ndani ya gari akiwa amekunja ndita!amekasirika vibaya sana.

“Umefikia wapi?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa Benard Sembe mshauri wa Rasi wa Kenya!

“Bado hawajataja”

“Watataja,pandisha hiyo takataka juu”

Daphine na Kamere walikuwa mateka na waliingizwa ndani ya jumba bovu wakapandishwa ngazi mpaka juu,wakakunja kushoto ambapo kulikuwa kuna chumba kilichotisha kina mlango na dirisha moja dogo lililokuwa juu.Vitu walivyoviona mbele yao viliwafanya waogope zaidi.

Mikasi,Sime,sindano,marungu,mifuko ya nailoni,pamoja na kamba za manira ndivyo vilikuwa mbele yao,walielewa nini maana ya vitu hivyo.

“Nawapa two minutes za kujifikiria kabla tabu haijawakuta”

Bernad Sembe pamoja na David walitoka nje wakiwaacha Daphine na Vital Kamere ndani ya chumba kidogo chini wamefungwa kamba.

“Daphine,naomba uniambie memori kadi ilipo”

“Dad hii ndiyo inatufanya sisi tuwe hai,ingekuwepo ndani ya simu sasa hivi tusingekuwa tunapumua”

“Wewe nitajie ilipo,hawatoweza kutuua.Hata kama tusipowapa watatuuwa tu”

“Hapan….”

Majambazi yalifika tayari yakiwa yana hasira kupita maelezo yaliyojitosheleza.

“Wewe Songa hapa”

Daphine akaitwa lakini kabla ya kujishauri akabebwa juu juu na kukalishwa juu ya kiti,akawekewa kitaulo kidogo kilichomziba mdomo na pua.Akaanza kumiminiwa maji juu ya kitaulo, hazikupita hata sekunde sita Daphine akaanza kutupatupa miguu yake kama kuku anayechinjwa akijaribu kutafuta pumzi,yalikuwa ni mateso ambayo hakuwahi kuyapata kila alipojaribu kuvuta hewa maji yaliingia puani na alipojaribu kufungua mdomo maji yaliingia mdomoni pia na kumpalia,akakosa hewa kabisa.

Zingeongezwa dakika nyingine mbili Daphine angepoteza maisha yake kwa kukosa hewa.

“Koho kohoooo kohooooooooo kohooo!”

Kitendo cha kitaulo kidogo kutolewa ilimfanya Daphine akohoe mfululizo na kutema maji,alivuta hewa kwa pupa kama mwanariadha aliyetoka kukimbia mita mia saba bila kupumzika.

“Binti Memori kadi iko wapi?”

Lilikuwa ni swali kutoka kwa mtu huyu katili aliyeshika kitaulo na kushoto jagi kubwa lililokuwa na maji.

“Sijui si..ijui koho ko..ho”

Jibu hilo lilifanya alazwe tena juu ya kiti na zoezi likaanza upya.

“Tutaendelea kufanya hivi hivi mpaka unakufa,you will die for nothing kwa sababu memori kadi tutaipata tu,and that is the truth”

Wakati anaambiwa hayo bado maji yaliendelea kum-mwagikia Daphine puani kupitia juu ya taulo dogo akawa anarusha rusha mikono na miguu akijaribu kutafuta Oxygen lakini wapi!mikono na migu yake vilikuwa vimefungwa, Vital Kamere alikuwa chini pembeni anaogopa kupita kiasi.

“Enough David!”(Inatosha David)

Bernan Sembe alitoa kauli hiyo jitu hilo likamuinua Daphine ambapo nguo yake ilikuwa imelowana maji anakohoa na kucheua maji.

“Daphine watajie”

Vital akasema.

“Daa..aad.koho koho…”

Macho ya Daphine yalikuwa mekundu ingawa aliteseka sana lakini hakuwa tayari kutoboa siri, kwa binti kama huyo mdogo kustahimili mateso kama hayo halikuwa jambo la kawaida, hata kwa majambazi walishindwa kuelewa ni kwa namna gani waipate memori kadi.

“Huyu ni Dadii yakee?”

Benard Sembe alimuuliza mwenzake.

“Yes”

“Anhaa,binti nadhani haupo tayari kumuona baba yako anateseka mbele yako,fanya kutueleza mapema.Hatujaja kupoteza muda hapa,patia memori gani otherwise kitakachofuata hutopenda”

Ilikuwa ni kauli ya kutisha kupita kiasi na katika maneno waliyoongea watu hawa hakukuwa na masihara hata kidogo na wala haukuwa mkwara.

“David inua hiyo mzee weka juu ya meza patia mimi ile panga”Bernad akatoa amri kwa rafudhi ya kikwao.

Hicho ndicho kilichofuata, Mzee Vital Kamere alinyanyuliwa msobemsobe mpaka juu ya meza akalazwa chali kama yupo leba.

“Daphine,You have only three minutes to change your mind”(Daphine,una dakika tatu za kubadilisha maamuzi yako)

Panga lilikuwa juu hewani, kushushwa chini kulimaanishwa kichwa cha Vital Kamere kuruka kando kama mpira.

“One,Two, thr….”

“Nata..ja! ila tafadhali naomba msituuwe atutosema chochote”

Daphine aliongea harakaharaka hakutaka kuona mtu aliyemsaidia katika maisha yake anauwawa mbele yake,Kama Vital Kamere angekufa siku hiyo aliamini yeye ndiye alikuwa muuaji sababu ya kuficha ukweli,hakutaka jambo hilo litokee.

“Memori kadi iko wapi?”

“Hotelini, juu ya mlango wa bafuni”

“Kama unadanganya,utakiona cha mtema kuni.David baki nao hawa.Kwanza kuja hapa”

Benard Sembe na David walitoka kando ili kuteta.

“Naenda hotelini,nitakupigia simu.Nikiipata piga wote risasi kisha tupa maiti zao msituni”

“Understood sir”(Nimekuelewa mkuu)

Kama walivyopanga ndivyo ilitakiwa iwe,isingewezekana hata kidogo Vital Kamere na Daphine wawe hai endapo memori kadi itapatikana,Bernad Sembe aliogopa kunyea ndoo gerezani ndiyo maana alitaka kuzima ushahidi kwa njia moja ama nyingine.

Wakiwa ndani wamefungwa kamba kama mateka walisikia muungurumo wa gari kumaanisha gari linaondoka.

“Daaad,I’m sorry”

“Usijali Daphine,tutapona”

Vital Kamere alijaribu kumtia moyo Daphine.

Akili ya binti huyu mdogo haikuwa inachaji darasani tu, hata nje vilevile. Alivyoangalia pembeni aliona vitu vyenye ncha kali,akasogea taratibu akavuta moja ya mkasi mdogo uliokuwa pembeni yake akitumia mikono yake iliyofungwa kwa nyuma,japokuwa alikuwa akiumia lakini alijikaza kisabuni, bado aliamini ana nafasi nyingine ya kuishi na ndiyo maana hakukata tamaa ilikuwa ni bora afe lakini akijaribu kutumia njia ya kujiokoa na kifo,akafanikiwa kuweka mkasi vizuri mkononi mwake kazi yake ikawa ni kusugua kamba ili zikatike amkomboe na Vital Kamere,kamba ilikuwa ngumu kuachia lakini alikazana na katika akili yake alielewa kabisa alifanya makosa ya kutaja ni wapi memori kadi ilipo kumaanisha kuwa ni lazima wangekufa tu.

Vital Kamere aliliona tukio analofanya Daphine lakini hakuwa na uhakika kama kinachofanywa na Daphine kingefanikiwa sababu alikuwa ni msichana mdogo,hata kama wangefanikiwa kukata kamba zao alielewa wasingekimbia popote kuwatoka watu hao waliokuwa na silaha za moto,Vital Kamere alikuwa ni maskini wa fikra!

Daphine alivyosikia parakacha za mtu zinakuja akasitisha zoezi na kutulia,mlango ukafunguliwa jambazi likawatizama na kupiga piga mluzi likatoka nje na kufunga mlango.

“vuku vuku vuku vuku”

Daphine aliendelea kushughulikia zoezi la kukata kamba ya manira iliyokuwa inaendelea kuachia taratibu huku ikipiga kelele.

***

“Griii griiii”

Simu ya jambazi iliita akaitoa haraka mfukoni na kuiweka sikioni baada ya kuipokea.

“Halloo”

“I found the memory card,kill them”(Memori kadi ninayo,wauwe)

Ilikuwa ni kauli kutoka kwa Benard Sembe mshauri wa raisi ikitokea upande wa pili wa simu,David akatoa bastola yake kiunoni ili kufuata amri aliyopewa na mkuu wake ya kuwauwa Vital Kamere na Daphine Nelson Magembe!

 Kitendo cha kumaliza kukata kamba ndipo mlango ulipofunguliwa,Moyo wa Daphine ulipiga kwa nguvu hakuelewa ni kitu gani akifanye kwa wakati huo,ni kweli alikuwa huru lakini alitetemeka, akili yake ilishindwa kutoa hatua yoyote ile akabaki vilevile mikono nyuma,ingawa kamba zilikuwa zimeachia yeye akawa amezishikilia.

“Simameni juu,nasema inuka musonge”

Jambazi likaamuru, aliyekuwa wa kwanza kusimama ni Vital Kamere,akamtizama Daphine kwa kama Sekunde mbili,kupitia macho ya Vital Kamere Daphine aligundua kuna ujumbe,nayeye akasimama hivyohivyo huku mikono yake ikiwa nyuma.

“Wewe songa hapa”

Jambazi likazidi kuamuru wote wakatolewa nje ya mlango na kuanza kushusha ngazi,Jambazi David akiwa nyuma yao na bastola,walivyofika ngazi ya pili Vital Kamere akarudi nyuma na kumpiga kikumbo Jambazi huyu aliyeshika bastola,akajikwaa akadondoka chini bastola ikaenda kando, kama umeme Daphine akaishika akaiweka mkononi mwake akiwa anatetemeka sababu hakuwahi kushika silaha kama hiyo tangu azaliwe ingawa aliwahi kuiona kwenye filamu za kijasusi jinsi inavyotumiwa.Mikono yake ilikuwa inacheza na kutoa jasho.

“Tafadha..li naomba utulie hapo hapo,nitaku..uwa”

Hata jinsi alivyoongea alionekana sio mtumiaji wa silaha hiyo sababu alipata kigugumizi cha ghafla.

“Binti,hiyo silaha sio nzuri ni mbaya sana embu iweke chini taratibu mwanangu najua unaogopa lakini embu weka chini”

David alimsoma Daphine kisaikolojia na kumuona ni jinsi gani anavyotetemeka hata jinsi alivyoishika bastola alionesha hofu mno,hiyo ikamfanya jambazi huyo aanze kumsogelea.Vital Kamere alikuwa chini hawezi kufanya lolote kafungwa kamba kwa nyuma.

“Daphine pull the trigger”

Vital Kamere aliropoka akimwambia Daphine avute kifyatulio cha bastola ili risasi zitoke ndani ya chemba lakini Daphine hakuelewa lolote hata hakujua triga ndiyo nini ingawa alijua kitendo cha kuingiza kidole chake ndani ya tundu la bastola na kuvuta nyuma kidude kilichopinda kidogo kilimaanisha risasi kuchomoka.

“Mwanangu,taratibu weka bastola chini utapata dhambi”

“U..si usisogee nitakuuwa”

Daphine akapiga mkwara lakini Jambazi akazidi kusogea karibu kwa hatua za taratibu huku akimuangalia machoni.Daphine hakuwa na uwezo wa kufyatua risasi hivyo ndivyo akili ya David ilivyomtuma ndiyo maana akawa anasogea mithili ya paka shume!

“Usinisogelee nitakuwaaa…”

“Daphine pull the trigga,Pull the trigga shoot him”Vital Kamere alizidi kusisitiza.

Kwa kutetemeka akaingiza kidole ndani ya triga ingawa kwa hofu, mkono wake ulizidi kutetemeka sana moyo wake ukazidi kumdunda,aliogopa kuuwa ingawa hakuwa na chaguo lingine lolote lile.


Ghafla picha ya jengo la 'wastegate' ikamjia akaona jinsi watu walivyokuwa wanamiminiwa risasi na kudondoka chini,akamuona kijana mdogo akivuja damu mdomoni amebanwa na jiwe kubwa anamkabidhi simu kisha kukata roho,watu wasiokuwa na hatia waliuwawa kikatili kila kitu kilipita kichwani mwake na kutiririka kama mkanda wa filamu.

“Paaaa! paaaa! paaaaa! paaaaa! paaaa! Paaaaaa! paaaaaa!”

Hakuelewa ni kwa wakati gani na ujasiri ulitokana na nini hasira zilimkaba shingoni akahisi uchungu ajabu, akaachia risasi saba zote zikatua kifuani mwa David jambazi aliyekuwa anamsogelea.Bado mkono wake ulikuwa ukitetemeka akaanza kulia machozi ya kwikwi.

Zilikuwa ni hasira kali vitu alivyovikumbuka Wastegate vilimtia uchungu mno.

“Dapine Mwa….”

Daphine aligeuka na bastola akamuelekeza Vital Kamere kwa nia ya kumfyatua pia,alikuwa bado na hasira kupita kiasi,midomo yake ilimcheza kifua chake kilimpanda juu na kushuka mapafu yake yalijaa hewa,akawa analia machozi huku anamtizama Vital Kamere.

Mzee huyu katika maisha yake hakuwahi kumuona Daphine katika hali hiyo hata yeye aliogopa mno akabaki kimnya alimanusura kinyesi kimtoke,Daphine hakutofautishwa na mtu mwenye mapepo au degedege.

“Daphine,Mimi baba yako.Tafadhali weka hiyo hiyo kitu chini.Tuondoke mahali hapa”

“Daaaa.d”

Alivyogeuza macho yake mbele aliona maiti imefumuliwa kifua, damu nyingi zipo chini hapohapo alitupa bastola chini akamfuata Vital Kamere na kumfungua kamba.

“Daaaad nimeu…a nimeuaaaa!”

Kitu kama hicho hakutegemeaa kukifanya ndiyo maana alilia machozi,akamuangalia maiti David aliyekuwa pembeni.

“Usijali,usijali Daphine nyamaza naomba tuondoke mahali hapa”

Wote wakasimama wakashuka ngazi,Vital kamere akazunguka upande wa usukani ambapo gari lililowaleta lilikuwa linaunguruma bado funguo hazijachomolewa akaligeuza na kurudi alipotoka.

“Inabidi turudi Tanzania Daphine tukiendelea kubaki hapa ni hatari”

“Tafadhali Daphine usilie,futa machozi”

Kilio cha Daphine kilichochanganyika na kwikwi kilimfanya Vital Kamere apate kibarua kingine cha kum-bembeleza,dakika mbili baadaye akili ya mtoto huyu ikawa imetulia ingawa bado alikuwa na mawazo.

“Hatuwezi kurudi Tanzania”

Hatimaye akaongea huku akifuta machozi.

“Kwanini?”

“Tukirudi itakuwa kazi bure,naomba mpigie simu raisi umueleze kila kitu”

“Daphine”

“Dad tafadhali,lazima tumalize tulichokianza”

Japokuwa alikuwa ni msichana mdogo lakini alikuwa ana mawazo mapana kupita kiasi jambo hilo lilimshtua sana Vital Kamere lakini hakuwa na jinsi hata yeye aliona Daphine yupo sahihi,alibadili gia na safari yao ilikuwa warudi Hotelini Nairobi.

“Tunaenda wapi Dad?”

“Tunarudi Hotelini”

“Hapana,tusirudi tena pale, tafuta simu yoyote ile ili uongee na Raisi kwanza”

“Daphi..”

“Dad Please”

“Sawa ngoja nipaki nitafute ATM mashine nitoe pesa kidogo”

Hivyo ndivyo ilivyokuwa,Vital Kamere aliendesha gari mpaka walipoingia katikati ya jiji la Nairobi.Akaweka gari kando na kuingia kwenye moja ya mashine akatoa pesa alizoona zitamfaa na kuweka mfukoni.Akarudi ndani ya gari.

“Nisubiri hapa,ngoja nikapige simu”

“Sawa Dad”

Ilieleweka kuwa Daphine ndiye aliyemuokoa katika maisha yake, isingekuwa msichana huyo mdogo aliyemchukulia kama mwanaye basi angekuwa mfu siku hiyo kwa kuchenguliwa na risasi,bado alitafakari kichwani aina ya akili za Daphine,aliingia kwenye kibanda cha simu akiwa na mawazo lukuki,akaingiza shilingi na kuchukua mkonga wa simu,alichofanya kwanza ni kupiga namba za dharura hapo aliomba aunganishwe moja kwa moja ikulu.

“Unaongea na Lulu Oleta kutoka ikulu,shida gani?”

Upande wa pili wa simu ulisikika kwa sauti nyororo yenye rafudhi ya Kikenya.

“Mimi naitwa Kamere”

“Yes Mr.Kamere,nikusaidieje?”

“Nahitaji kuongea na Raisi”

“Una shida naye ngani?”

“Ni muhimu sana,ingekuwa vizuri ningeongea naye moja kwa moja”

“Subiri kidogo”

Mwanamke mwenye weusi wa kung’aa aliyevalia sketi nyeusi na shati jeupe akaweka mkonga wa simu pembeni akatembea mpaka kwenye mlango wa kioo na kugonga.

“Yes Lulu,pita uketi”

Ofisi ilikuwa kubwa na nje kulikuwa kuna walinzi wawili wanalinda,secretary wa Raisi akapita na kukaa juu ya kiti kimoja wapo.

“Kuna mtu anahitaji kuzungumza nawewe Mh.Raisi”

“Ni nani?”

“Amesema anaitwa Kamere?”

“Kamere?”

“Ndio”

“Sawa”

“Nimemuunga laini namba moja”

“Sawa,thank you”

Raisi akanyanyua mkonga wa simu,Vital Kamere bado alikuwa kwenye laini hapohapo akaanza kumuelezea kila kitu kilivyokuwa.

“Sawa,ndio ninakusikia.Yes nitafatilia ahsante sana.Upo wapi?Usiondoke hapo.Thank you”

Vital Kamere alimaliza mazungumzo na Mh.Raisi lakini bado alikuwa mwenye wasiwasi sana,alihofia kubaki nchini Kenya.

Hazikupita hata dakika tano gari tatu nyeusi zikawa zimefika upande wa pili wa barabara, watu wapatao nane wakashuka ndani ya magari,wakatizama huku na kule.Wakafika mpaka kwenye gari waliyoelekezwa na kugonga kioo.

“Tumetumwa na Raisi,wewe ni Kamere?”

Mmoja wa watu hao aliuliza.

“Ndio”

“Shukeni ndani ya gari,msiogope”

Hata kama wangekuwa ni watu wabaya hawakuwa na kitu kingine zaidi ya kushuka ndani ya gari,Daphine hakuwa na raha hata kidogo wakaingia ndani ya gari nyingine safari ikaanza ya kuondoka kuelekea hotelini.Hapo walianza na mapokezi,uzuri hotel hiyo ilikuwa na CCTV camera.Wakaomba picha ya mtu aliyeingia mara ya mwisho,haikuchukuwa hata dakika mbili.Sura ambayo kila mtu ilimfanya ashangae ikatokea.

“Benard Sembe!”

Mmoja wa watu hao alikema kwa mashangao.

“Ndiyo huyu?”

Lilikuwa ni swali alilotupiwa Vital Kamere,akageuziwa kompyuta.

“Ndiyo”

“Okay”

Kilichotokea hapo watu hao walionekana kupiga simu tofauti tofauti na baada ya dakika kumi na tano habari nzuri ikaja kuwa Benard Sembe tayari amekamatwa yupo kituo cha polisi.

“Tayari ameshikiliwa na jeshi la Polisi nyumbani kwake na wamemkuta na Memori kadi,hongereni sana.Umesema unaitwaje?”

“Vital Kamere”

“Dada pale”

“Huyu Daphine ni binti yangu”

Vital kamere halikuwa swali lake lakini alidakia.

“Tutawapa ulinzi wa kutosha”

“Sawa”

Siku hiyo Vital Kamere na Daphine walilindwa kupita kiasi na jeshi la polisi.Kesho yake kulipokucha wote wakaweka mizigo yao tayari kwa ajili ya safari ya kurejea nyumbani, nchini Tanzania.


***


“Silaha zimetosha?”

“Bado”

“Nitajie zipi na zipi ambazo zimepatikana?”

“AK 47,revolver,Shot guns,mabomu ya Grinade na nyingine hizi hapa mkuu”

“Vipi kuhusu General Okwu alipiga simu?”

“Leo?”

“Ndiyo”

“Hapana Mkuu”

“Endelea kukusanya silaha,Ushapata vijana wangapi?”

“Kama hamsini hivi?”

“Wapo wapi?”

“Kambi ya Mbagala na Captain Oyaya”

“Okay”

Jambo lililokuwa linaendelea ndani ya kambi ya Lugalo lilikuwa ni siri kubwa mno na ndani ya chumba kidogo mlikuwa na silaha nyingi za moto zimekusanywa kutoka sehemu mbalimbali na nyingine ziliingizwa kwa njia ya magendo.

Aliyekuwa anaongoza kikosi hicho aliitwa Brigedia Karanje, alikuwa mrefu futi nyingi kwenda hewani mweusi kupita kiasi na alikuwa ana roho mbaya,mara ya mwisho kucheka ilikuwa ni miaka kumi iliyopita.

Na alikuwa ni mtu wa kutoa amri tu,wanajeshi wenzake wote walimuogopa ndiyo maana hata M.P aliyefahamika kwa jina la Isaya Mocha alijibu maswali huku mikono yake ikiwa nyuma hata pumzi zake alizibana na alimuogopa Brigedia Karanje kuliko hata Mungu wake.


Brigedia Karanje alitisha kwa sura sambamba na amri zake, muda wote sura yake ilikuwa inaonyesha makunyanzi,alitoka nje ya kijumba hicho kidogo na kupigiwa saluti na kila mwanajeshi aliyemuona kama kumpa heshima.Alivyofika Kwenye Hammer ya kijeshi akafunguliwa mlango akazama ndani.

“Boscow”

Alimuita dereva wake.

“Naam Mkuu”

“Nitafutie Mr.Vital Kamere simuni unipe niongee naye”

“Sawa mkuu”

Dereva alitoa simu na kuonekana anatafuta majina,alivyopata jina VITAL KAMERE akaipa simu ‘okay’ kisha kugeuka na kumkabidhi mkuu wake,Brigedia Karanje”

“Halloo Kamere”

Simu ilivyopokelewa,Brigedia Karanje alianza maongezi.

“Naam Brigedia”

“Nilikuwa sikupati kwenye simu tatizo nini?”

“Nilisafiri kidogo,nilikuwa nchini Kenya”

“Vipi biashara?”

“Zinakwenda tu mkuu”

“Ile shughuli yetu vipi?”

“Kila kitu kipo sawa”

“Umepata watu wangapi?”

“Kumi”

“Hawatoshi,wasichana wangapi?”

“Msichana mmoja,vijana wapo tisa”

“Endelea na kazi ninahitaji zaidi ya hao”

“Sawa Mkuu”

Vital Kamere alivyokata simu alimuangalia Daphine aliyekuwa juu ya kochi anatizama Luninga kwa macho yaliyojaa huruma sababu hakuwa na hatia lakini hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima atekeleze matakwa ya mwanajeshi huyu gaidi, Brigedia KARANJE!


****

“Derick naomba unisamehe najua nilikuhaidi jana lakini nafasi hakuna,labda ujaribu sehemu nyingine”

Masikioni mwake yalimpenya maneno ya mzee mnene kiasi aliyekuwa na karatasi mkononi mwake nyuma kulikuwa na nyumba kubwa inayofanyiwa ujenzi,hapo ndipo Ngesa alipoamua kutafuta kibarua cha kujishikiza ili apate walau senti mbili tatu za kujikimu.Alitaka kufanya kazi ili ale na kuishi,ndiyo maana alikuwa kila siku anahangaika jijini Arusha kutafuta vibarua.

“Mzee hata zege mimi nitabeba tu”

“Hakuna nafasi Derick”

Ngesa aliweka mikono yake kiunoni alihisi kuchoka akili mpaka mwili hakuelewa siku inayoitwa kesho itakuwaje,akatoka eneo hilo akiwa mnyonge huku analitizama jengo la gorofa ambapo aliona wajenzi wakiendelea na shughuli za kuchanganya zege,alitia huruma kutokana na kukaa bila matunzo ngozi yake ilipauka na alikuwa ana nywele chafu tena ndefu zilizojaa vumbi.

Hakuna hata mtu mmoja aliyejuwa kuwa jina lake ni Ngesa.Alitembea kwa mwendo wa hatua kumi akavuka barabara akijaribu kutafuta vibarua vyovyote vile,kutokana na mambo jinsi yalivyomwendea kombo alikuwa tayari kufanya shughuli yoyote ile ili mradi apate pesa.Bado alikuwa mkoani Arusha na baridi lilikuwa kali lakini alivumilia sana,siku hiyo nzima alizunguka lakini hakuambulia kitu,mfukoni hakuwa na pesa hata moja.


Hata ilivyofika usiku na kutandika gunia kandokando ya mfereji ili alale usingizi haukuja,njaa ilimsumbua kazi yake ikawa kujigeuza huku na kule kutokana na baridi kuwa kali zaidi ikafanya njaa iongezeke maradufu,usiku kwake ulikuwa ni mrefu.

Gari kubwa la kuzolea takataka ndilo lilimshtua, alivyogeuka aliona vijana wawili wachafu wanakusanya takataka na hakujitofautisha nao,hapohapo nayeye akasimama.Akavuka barabara akaanza kuokota uchafu ili kuwasaidia,kazi hiyo ya kuokota takataka ilidumu kwa kama dakika kumi nzima.

“Vipi?”

Mzoa taka alimuuliza Ngesa baada ya kuona amejiunga nao.

“Nahitaji kazi?”

“Utaeza aise chalii angu?”

“Nitaweza ndio”

“Kweli?”

“Kabisa”

“Pakia kwenye gari arif,tupige mzigo”

Ngesa alifurahi akaruka ndani ya gari na kukaa nyuma ya takataka zilizotoa harufu kali kutokana na shida aliyokuwa nayo harufu hiyo hakuisikia kabisa.

“Karibu mkate,mimi naitwa Ndomba,mwenzangu unaitwa nani aisee?”

Bwana Ndomba alikata kipisi cha mkate na kumpa Ngesa, japokuwa maskini huyu alionesha kuwa hana kitu lakini alikuwa ana roho nzuri kupita kiasi alikuwa na ubinadamu na tajiri wa upendo.

“Mimi naitwa Derick”

“Unaishi wapi?”

“Mimi ni mgeni nimekuja kutafuta Maisha hapa Arusha,natokea Njombe”

“Karibu sana aise hapa laifu bomba babake,chukuwa mkate hapo”

Walikuwa wakila huku wakiwa juu ya takataka zinazonuka na gari lilizunguka likikusanya uchafu mji mzima, Ngesa alionesha kuchapa kazi sio masihara alizama mitaroni na kutoa uchafu na kutupa ndani ya gari,ilivyofika jioni alipewa noti ya shilingi elfu moja.Kwake siku hiyo ilikuwa shangwe!

“Ahsante sana Ndomba”

“Usijali,tajiri kanipa buku mbili.Kasema tugawane bukubuku.Kesho basi”

“Sawa mtakuja kunipitia palepale?”

“Ndio tutakuja”

“Unapakumbuka?”

“Mimi kichwa changu kinashika kumbukumbu kuliko sumaku”

“Sawa usiku mwema”

Ngesa hakuamini kama ameshikilia noti ya shilingi elfu moja,usiku huo huo alitembea mpaka kwenye kibanda cha mama Ntilie.

“Ubwawa shilingi ngapi?”

Ngesa aliuliza baada ya kufika ndani ya kibanda cha Mama Ntilie kilichozibwa na mbao pamoja na mabati,ndani humo walikuwa watu wasiokuwa na uwezo yaani makabwela.

“Ubwabwa na nini?”

“Na maharage”

“Shilingi mia saba”

“Sawa,niwekee na ukoko pia jaza mwingi”

“Ukoko shilingi mia”

“Sawa,weka ukoko wa mia mbili”

Siku hiyo Ngesa alikula kwa fujo kama mfungwa,alivyomaliza alilipa na kuondoka zake akiwa ameshiba ndindindi.

****

“Wewe Derick…Derick..”

Siku hiyo Ngesa alilala sio mchezo kutokana na kula vizuri ndiyo maana akachelewa kuamka,mpaka Bwana Ndomba alipomtingisha.

“Amka twende ndugu mbona unalala kama umeridhika na maisha”

“Samahani ndugu yangu”

Akarudi kwenye kibarua chake cha kuokota takataka siku hiyo walizunguka harakaharaka,ilivyofika saa tisa ya alasiri kazi ikawa imekwisha,walimaliza mapema sana.Ngesa akalipwa ujira wake na kuagana na wenzake,kama kawaida siku hiyo akaamua kupitia kwenye mgahawa ili anunue chakula ale.

“Ugali Mama na Maharage”

“Sawa Mwanangu”

Ndani ya kibanda hiko Mama Ntilie huyo alifanya kazi na binti yake aliyekuwa mdogo, ilionekana walikuwa ni maskini wa kutupwa na kutokana na hali hiyo hata mazingira waliyotumia kufanya kazi yalikuwa machafu,alikuwa ni mama mtu mzima lakini kutokana na maisha kumpiga sura yake ilionekana kukomaa kiasi.

“Maji ya Kunawa”

Mtoto mdogo mwenye umri kati ya miaka 10-14 ndiye aliyekuwa na jagi na beseni,Ngesa akakinga mikono yake akanawishwa mikono, alimtizama mtoto huyu mdogo akaingiwa na huruma kupita kiasi sababu mtoto kama huyo alitakiwa awe shuleni anasoma na watoto wenzake.

“Ahsante sana una….”

Kabla ya kumalizia maneno yake mlango wa mgahawa ulipigwa teke bati likaruka kando wakaingia watu watano waliovalia jezi za bluu wenye mabuti makubwa, mikononi wana virungu.

“Wewe Mama muuuza,tulikwambiaje?”

Mmoja kati ya watu hao aliongea kwa sauti ya juu huku akimsogelea Mama Ntilie.

“Lakini ndiyo nilikuwa kwenye taratibu za kuhama hapa”

“Kuhama vipi? tulishasema hapa uhame au pawe pasafi mbona unakuwa kiburi,eeeh”

“Mwan…”

“wewe Mama nyamaza,kwanza umekusanya ngapi leo?”

“Leo sina baba nina elfu mbili tu”

“Embu ilete hapa”

Maneno yote yalipita kwa Ngesa kama yalivyo akawa kimnya ametulia mezani,alijua watu hao walikuwa ni migambo wa jiji.

“Alafu huu wali,hautakiwi”

Mmoja wa mgambo alishika sufuria la wali na kulibinua chakula chote kikamwagika,akashika sufuria la mboga akafanya hivyohivyo.Mama alivyotaka kuingilia alipigwa kibao kikali cha shavu,yote hayo Ngesa aliyashuhudia.

“Mamaaaaaa”

Mtoto alimlilia mama yake na kumkimbilia lakini alisukumizwa kando akadondoka ndani ya sufuria lililokuwa lina maji yanachemka,mambo tayari yalikuwa yameharibika.

“Mshachukuwa pesa,mnataka nini kingine?”

Hilo ndilo swali alilolitupa Ngesa makusudi kwa kujiamini akitaka kurudishiwa jibu litakalo mpandisha hasira zaidi.

“Wewe kibaka unasemaje?”

Mgambo mmoja alijiroga akajibu na kumsogelea Ngesa huku akimpigapiga na kirungu mgongoni,hakuelewa anafanya jambo la hatari kiasi gani kwa kumfanyia kitu kama hicho Ngesa mwenye hasira kali.

Alichofanya Ngesa ni kuudaka mkono wake,akamzungusha na kukiweka kichwa cha mgambo huyu juu ya meza,akakunja ngumi na kuanza kumpiga za puani,kwa sekunde tatu alipigwa ngumi zisizokuwa na idadi kamili.Damu zilitapakaa meza nzima kwa harakaharaka pua ya mgambo ilikuwa imepasuka vibaya sana,alivyokuja mwingine na kirungu alitulizwa na teke akadondoka kwenye mabati hapohapo akatulia.Ngesa akakaa sawa na kukunja ngumi.Aliona kirungu kinakuja akainama kidogo kikapita hewani,alivyoibuka juu akamtwanga kichwa mgambo huyu na kumsindikiza na kifuti cha tumbo,ilikuwa ni kama picha la kuigiza,Ngesa alikuwa mwepesi.Akaokota kirungu kilichokuwa chini na kuanza kupambana na migambo hawa,mmoja alikuja kichwa kichwa akapigwa na kirungu kichwani kikampasua vibaya sana.Ngesa aliwapiga vibaya sana watu hawa waliokuwa waonevu,alivyohakikisha kawafunza adabu bila kuaga aliondoka zake,akimuacha Mama Ntilie anamshangaa.

****

“Gari haliwaki mume wangu”

“Umeangalia maji?”

“Ndio”

“Au injini itakuwa imenock”

“Hata sijui”

“Ukiwasha hapo taa zinawaka?”

“Zinawaka na kuzima”

Mke alijibu na kujaribu kuwasha gari lakini halikuwaka.

“Angalia temino kama zipo vizuri”

Sauti hiyo iliwafanya wote wamgeukie mzoa takataka huyu aliyekuwa kandokando yao anabeba uchafu.

“Umesemaje kijana?”

Lilikuwa ni swali alilotupiwa Ngesa akiwa na rambo la takataka anataka kutoka nje ya geti,akaweka chini mfuko wa Rambo.

“Nimesema mmeangalia temino vizuri kama zimekaza?”

Mzee huyu alimuangalia Ngesa kwa dharau,akampandisha juu mpaka chini jinsi alivyokuwa mchafu na maneno aliyokuwa anaongea vilikuwa ni vitu viwili tofauti,’anajua nini huyu mzoa takataka’haya ndiyo maneno yaliyokuwa yanapita ndani ya fikra za Mzee huyo.

“Embu njoo uangalie baba”

Mwanamke aliyekuwa ndani ya gari alisema kabla mumewe hajasema lolote,Ngesa akasogea mpaka karibu na gari.

“Fungua boneti”

Lilivyofunguliwa akaangalia ndani,akapiga jicho vizuri.Ngesa akaangalia injini na kuanza kushika vitu alivyovijua yeye mwenyewe kila mtu alimuangalia.

“Washa gari”

Bado gari liligoma kuwaka,akajaribu tena kushika shika vitu vingine,akachomoa ‘deepstick’ na kupima oil kama ipo ya kutosha,alivyohakikisha kila kitu kipo sawa,aliomba gari liwashwe.

“Washa”

Kila mtu alimtizama Ngesa gari lilikuwa limewaka tayari.

“Ahsante sana”

Mwanamke akashukuru sana Ngesa alivyotaka kutoka nje ya geti akatulizwa.

“Mimi naitwa Mr.Magembe huyu ni mke wangu anaitwa Elishadai,tunashukuru sana.Ulishawahi kuwa fundi?”

“Hapana mzee ni utundu utundu tu”

“Kwahiyo hukusomea kabisa mambo ya Magari?”

“Hapana sikuwahi kusomea”

“Unaweza kuendesha gari?”

“Ndio naweza”

Mr.Magembe aliendelea kumsaili Ngesa kiundani zaidi, alimuuliza maswali mengi siku hiyo.

“Mzee nasubiriwa nje na wenzangu,tutaonana siku nyingine”

“Waambie kuanzia leo umeacha kazi”

“Unasema?sasa nitakula vipi?”

“Utakuwa unafanya kazi kwangu nimependa ukarimu wako”

Haukuwa utani wala ndoto,kuanzia siku hiyo Ngesa aliajiriwa na Mr.Magembe akawa kama dereva wake,kila alipotaka kwenda Ngesa alikuwa naye.

Ndani ya wiki moja suti zilianza kumzoea Ngesa na alikuwa anaamka asubuhi na mapema anafuta gari na kumsubiri tajiri yake aamke ampeleke kazini,kazi hiyo aliifurahia sababu alilipwa vizuri,mbali na hapo alichukuliwa ni kama miongoni mwa wanafamilia.

“Kesho ninaenda Dar es salaam,hakikisha gari umejaza mafuta ya kutosha Derick, pesa hizi hapa”

“Sawa bosi”

Baada ya kumshusha tajiri yake nyumbani aligeuza gari na kwenda mpaka sheli ya mafuta hapo alijaza mafuta ‘full tank’ kwa ajili ya safari atakayoanza siku inayofuata.

***

Alfajiri na mapema Mr.Magembe na mke wake walikuwa ndani ya gari viti vya nyuma,nyuma ya usukani yupo Ngesa.Hapohapo safari ikaanza,Ngesa aliendesha gari kwa masaa takribani tisa na walipumzika sehemu moja tu Tanga, ‘Liverpool’ kupata kifungua kinywa,waliingia jijini Dar es salaam saa kumi na moja ya jioni.Ilikuwa ni safari ndefu na iliyowachosha sana.

“Derick,unapajua Oysterbay?”

Mr.Magembe aliuliza wakiwa ubungo mataa,jiji hilo lilimkumbusha Ngesa vitu vingi,alimkumbuka Hans na mtoto mdogo mchanga aliyemkabidhi miaka mingi sana iliyopita.Hakuelewa kama rafiki yake kipenzi Hans yupo hai au amekufa tayari.

“Ndio boss”

“Ndio tunaenda huko,Oysterbay polisi pale ukifika utakunja kushoto,au ukifika nitakuelekeza vizuri”

“Hakuna shaka bosi”

Taa za kijani zilivyowaka Ngesa akakanyaga ‘clutch’ akapandisha gia,gari ikaanza kutembea.

Dakika arobaini na tano baadaye walikuwa Oysterbay polisi na Mr.Magembe kazi yake ilikuwa kumuelekeza dereva wake.Mpaka walipofika nje ya geti kubwa la kisasa lenye rangi nyeusi,kwa ndani kulionekana kuna jengo kubwa jeupe la gorofa nne, kifupi lilikuwa ni jumba la kifahari.

“Ndio hapa?”

“Ndio, piga honi”

Ngesa akapiga honi,Mlinzi akatoka nje.Akaliangalia gari kisha kusukuma geti.Gari aina ya NISSAN PATROL likaingia ndani,Ngesa alishangazwa na wingi wa magari ya kifahari nje ya uwanja kama Range rover,Hammer III original,Jaquar na magari mengine ambayo hakuwahi kuyaona katika maisha yake,Nissan Patrol aliyokuwa anaendesha ndiyo ilikuwa ya kimaskini na haikuwa na hadhi kabisa kulinganisha na magari yaliyokuwepo,akaweka gari vizuri kisha kuteremka na kufungua mlango wa nyuma.

“Poleni kwa safari bosi”

“Ahsante”

Mr.Magembe na mkewe wakashukuru wote kwa pamoja huku wakiteremka garini.

“Jimmy karibu sana Dar es salaam jiji la joto”

Mr.Vital Kamere ndiye alisema na kushuka ngazi chache ili kuwapokea wageni wake,akatembea mpaka kwa Mr.Magembe wakakumbatiana na kupigana pigana migongoni kwa furaha kama watu ambao hawakuwahi kuonana siku nyingi.

“Shemeji habari yako?kwanza poleni na safari.Karibuni sana,Kalulu shusha mizigo kwenye gari ipeleke kwenye chumba cha wageni”

“Sawa”

Kalulu alikuwa ni mfanyakazi wa ndani kama alivyoagizwa ndivyo alivyofanya.

“Oh Derick njoo ndani”Mr.Magembe alisema.

Ilionekana walimsahau Ngesa, wote wakaingia ndani.


Ndani seblen hapakutofautishwa na pepo ndogo,kulikuwa na uwazi mkubwa na kila kitu kilikuwa cha thamani huku kiyoyozi kikipuliza kwa mbali.

“Daphine njoo usalimie wageni”

Mr.Vital Kamere alimuita Daphine alivyomuona anapandisha ngazi,kitendo cha kutokeza mbele ya wageni kila mtu alimtizama.Hasa hasa Mr.Jimmy Magembe na Mkewe.

“Huyu mtoto anafanana sana na Marehemu shemeji yangu, Rebeca”

Magembe aliongea akionesha sura ya umakini akiwa anamwangalia Daphine.

“Hata mimi nilitaka niseme hivyo hivyo”

Mkewe Elishadai nayeye akadakia huku wakizidi kumtizama Daphine alikuwa na sura ya kipole, nzuri na mwenye mashavu kiasi.

“Unasemea mke wa Marehemu kaka yako?”

Mr.Vital akatupa swali.

“Ndiyo,Marehemu Nelson”

“Duniani wawili wawili bwana utakuwa umemfananisha”

Daphine alivyomaliza kusalimia akapandisha ngazi na kuingia chumbani kwake.

“Kijana,naomba utupishe kidogo tuna maongezi”

Lilikuwa ni ombi kutoka kwa Vital Kamere,akimtaka Ngesa awape faragha!


 “Vipi Jimmy,kwanza karibu sana pole na safari.Ngoja nikuletee kinywaji”

Vital Kamere akasimama akaliendea friji na kutoa chupa kubwa ya ‘wisky’ akasogea mpaka kwenye kabati akachukuwa glasi mbili akaziweka mezani akawakaribisha wageni wake wanywe mvinyo!

“Shukrani,wewe hutumii?”

“Mimi mlokole siku hizi”

“Ha ha haaaaa tangu lini?”

“Nakutania,nitakunywa nyie pasheni kwanza”

Wote walikuwa wenye furaha siku hiyo na kilichoendelea baada ya hapo ni mazungumzo ya kibiashara,siku zote Vital Kamere alipenda biashara zake zizungumziwe na wahusika tu.Ndiyo maana akataka Ngesa awapishe.

“Lini utaenda kuonana na hao mabosi?”

“Kesho kutwa nadhani, lakini ninahitaji msaada wako”

“Bila shaka,wewe ndugu yangu kila kitu kitaenda sawa.Sisi ndiyo wenye hii nchi”

Vital Kamere alijigamba na jambo hilo lilikuwa kweli,katika matajiri wenye uwezo jijini Dar es salaam Vital Kamere alikuwepo,alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa mwenye malori mengi pamoja na magari mengi ya mizigo yaliyosafirisha mali zake,Afrika Mashariki na kati.Jimmy Magembe na Mkewe Elishadai walifikia nyumbani kwa Vital Kamere,siku hiyo walichelewa kulala walikuwa wana mengi ya kuzungumza!

***

Daphine alifungua shule na kuingia kidato cha nne, mwaka huo ndio ulikuwa wa kumaliza elimu yake ya O’level,alielewa nini maana yake, mtihani mkubwa wa kitaifa ulikuwa ukimsubiria mbeleni ilibidi apambane nao ili asimuangushe mlezi wake Mr.Vital Kamere na hivyo ndivyo alivyomuhaidi.

Siku ya kwanza kufika shuleni kila mtu alimshangaa,Daphine alinawiri na kunenepa kiasi,nyuma akabinuka sketi ya shule ya marinda aliyovaa ilifanya umbo lake lijichore vizuri kabisa.Alikuwa mwenye mwili kiasi chake na macho yake muda wote yalikuwa yamelegea ingawa hakuwahi kula kungu.Tangu siku hiyo Daphine alikuwa makini darasani alihudhurua vipindi vyote na alikuwa akichukuwa masomo ya sayansi,katika majaribio darasani hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyewahi kumfikia.

Daphine alikuwa ana kichwa cha ajabu na aliweza kuchambua kila kitu kuhusu sayansi,hasa hasa masomo ya ‘Physics’ na Chemistry,Biology ndiyo usiseme aliweza kumchambua binadamu kuanzia kwenye nywele mpaka miguuni,kifupi Daphine alitisha na kila mwalimu alijivunia kuwa na mwanafunzi kama yeye.Wanaume wengi shuleni walimsumbua lakini kamwe hakutaka kujihusisha na maswala ya mapenzi aliamini elimu kwake ni kila kitu,hakutaka kumuangusha Vital Kamere na kamwe hakutaka kurudia kosa alilofanya awali,aliyaogopa mapenzi kama ukoma sababu aliujua moyo wake ukipenda unapenda mazima,ndiyo maana aliupiga moyo wake ‘stop’ akajikita kwenye masomo.

“Daphine,unanitesa lakini”

Mwanafunzi mmoja aliyefahamika kwa jina la Lucas Kayahira alimgasi Daphine,uzuri wa msichana huyu ulimzuzua mno.

“Nakutesa kivipi?”

“Hisia zangu”

“Hisia zako zimefanya nini?”

“Mimi nakupenda nilishakwambia tangu mwezi uliopita”

“Nikwambie kitu Lucas”

“Niambie Daphine”

“Sasa hivi soma,wanawake wapo wazuri zaidi yangu.Achana na mapenzi hayatakusaidia kitu”

“Usiseme hivyo Daphine jaribu hata kunifikiria”

“Tunakaribia kufanya Mock exams sasa nikufikirie wewe au nifikirie mitihani?”

“Jaribu kidogo kunifikiria mimi”

“Hapana,naomba niache niende library nikasome kesho tuna test ya Physics”

Swala la mapenzi kwa Daphine halikuwepo kabisa katika akili yake,aliyachukia vibaya sana ingawa alishawahi kupenda kabla,hakutaka tena kurudia makosa yaleyale.


Kitu kilichowachanganya walimu zaidi ni maajabu aliyofanya Daphine kwenye mitihani, aliburuza shule zote zilizokuja kushindana akaibuka kidedea akifuatiwa na mwanafunzi mwingine msichana aliyeitwa Tujaeli Mzava akitokea shule ya Fedha girl’s.Jambo hilo lilizuwa maswali mengi sana wasichana kuongoza na watatu alitupwa mbali sana.Vital Kamere alivyopokea taarifa hizo alifurahi kupita kiasi na alitamani Daphine angekuwa mwanaye wa kumzaa.

Hans na Beatrice walilia kwa furaha na hawakuacha kumshukuru Vital Kamere sababu ndiye alie kuwa kama nguzo ya Daphine.

Wakati siku ya sherehe ya kumpongeza Daphine inaendelea Mr.Vital Kamere alikuwa kambi ya Jeshi ya Mbagala na aliitwa kwa dharura na Brigedia Karanje.Nje kulikuwa kuna uwanja mkubwa wanaume wapatao hamsini walikuwa wakifanya mazoezi huku wanajeshi wengine wakiwa wamezunguka uwanja huo mkubwa sana.

“Unajua kwanini nimekuita hapa Kamere”

Brigedia Karanje akaanza mazungumzo,pembeni walikuwa wanajeshi wanamlinda wakiwa katika sura za kazi.

“Hapana”

“Kuna kitu nataka unisaidie”

“Kitu gani?”

“Najua wewe ni mfanyabiashara mkubwa sana”

“Ni kweli”

“Na unaagiza vitu kutoka nje kila mtu anajua hilo”

“Kabisa”

“Nahitaji unisaidie kitu kimoja lini unaingiza mzigo mwingine?”

“Mwezi ujao nitaagiza magari kutoka Japan”

“Kuna mizigo nataka unipitishie”

“Ipi hiyo?”

“Silaha,ikiwezekana mabomu ya Nuclear”

“Unasema?”

Mr.Kamere alionesha mshtuko wa waziwazi,silaha alizotaja Brigedia Karanje zilikuwa nzito kupita kiasi.

“Kama ulivyonisikia na fanya hima tunakaribia kuwapeleka vijana Urusi jeshini,uliniambia una binti mmoja?”

“Ndio”

“Inabidi ufanye juu chini aende jeshini pia.Lazima hii nchi tuipindue.Raisi Leslie Benjamin lazima nimkomeshe haiwezekani anifanyie mimi mambo ya kishenzi,ama zake ama zangu.Nitahakikisha kile kiti alichokalia anakiona sumu,atajuta katika maisha yake yote lazima nimfanyie kitu kibaya.Mwanzo alikuwa rafiki yangu mkubwa sana lakini sasa hivi ni adui yangu namba moja”

Brigedia Karanje aliongea maneno ya kutisha tena kwa hasira huku akiyabana meno yake,hakukuwa na utani hata kidogo katika maneno aliyoongea, aliongea kwa msisitizo bila kuogopa kuwa anaongea maneno hatari ambayo akisikiwa na serikali atashikiliwa na vyombo vya dola lakini yeye hakuogopa.

Vijana walikuwa wakipokea mafunzo ya kijeshi na walifundishwa jinsi ya kushika silaha,wengi wao walichukuliwa mitaani wakiwa hawana hajira,walipandikizwa mbegu mbaya ya kumchukia raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Leslie Benjamin.Vijana walizidi kuchukuliwa mitaani na kufikia idadi ya mia mbili,hiyo haikutosha kabisa ilikuwa ni lazima wakapewe mafunzo mengine.Brigedia Karanje alikuwa na usongo na Raisi Leslie Benjamin na alitaka kuipindua serikali yake kimabavu ndiyo maana alitafuta vijana wadogo kutokea nchi mbalimbali.

****

Taarifa za habari nchini Nigeria jijini Lagos zilitangaza juu ya upotevu wa wasichana habari hiyo ilitangazwa ulimwengu mzima, baada uchunguzi wa jeshi la Nigeria ilifahamika kuwa watekaji hao wanajiita BOKOHARAM,hiyo haikuishia hapo vijana wadogo walipotea katika mazingira ya kutatanisha.BOKOHARAM ulikuwa ni mtandao mkubwa na wenye mawakala karibia nchi kumi za Afrika,kiongozi wa kundi hilo alifahamika kwa jina General Okwu,alikuwa mweusi tena mwenye roho mbaya kuliko ibirisi,kuuwa kwake ilikuwa ni sawa na kuweka kikombe cha kahawa mdomoni,wengi walizifananisha tabia zake na gaidi Adolf Hilter.

“Omujugu”

General Okwu alimuita mmoja wa wafanyakazi wake siku hiyo wakiwa kambini.

“Naam Mkuu”

“Mbona ulipigiwa simu na Karanje hukunipa taarifa?”

“Nilisahau mkuu”

“Si unajua sipendi uzembe”

“Ndio mkuu lak..”

Kabla kijana huyu mfanyakazi hajamalizia anachotaka kuongea koo lake la hewa lilishikwa na General Okwu aliyekuwa katili,katika uongozi wake hakupenda uzembe hata siku moja hakutaka mwanajeshi wa aina hiyo,vidole vyake vilikuwa vimekomaa na vigumu alizidi kuminya koo la hewa na kuvuta ambapo kilichoonekana hapo zilikuwa ni damu kuruka kama kuku,Kijana aliyefamika kwa jina la Omujugu alidondoka chini na kutupa tupa miguu yake kama mtu anayetaka kukata rohoo.

“Paaa paaaa”

Hapohapo General Okwu alichomoa bastola na kummaliza nayo.

“Tuuuuuuu”

Alitema mate chini kwa dharau,akachukua simu yake na kuanza kubonyeza namba anazojua yeye kisha kuweka simu sikioni.

“Karanje,ulikuwa unahitaji vijana wangapi?”

Lilikuwa ni swali alilouliza General Okwu tena bila salamu kwa lugha ya kiingereza.

“Hata sitini lakini naomba uwapeleke moja kwa moja Urusi,Moscow”

“Watafikia wapi?”

“Nitakupa maelekezo,usijali kesho asubuhi sana nitakupigia simu”

Brigedia Karanje alisikia habari za Bokoharam kupitia kampuni maarufu ya habari CNN,ilichukuwa muda sana kumpata General Okwu na haikuwa rahisi, alimpa dolla elfu saba kwa ajili ya kazi hiyo ya kutafuta vijana.Ilikuwa ni lazima Raisi Leslie Benjamin auwawe kwa njia moja au nyingine,wasingeweza kufanya hivyo bila ya kuandaa majeshi yaliyojipanga.

***

“Nchi yetu ni nchi ya Amani sana,nimejitahidi sana kutoa misaada mingi sasa hivi nipo katika maboresho ya sekta ya usafirishaji nitaanzia na reli,nitahakikisha treni zetu tutazifufua.Kwenye sekta ya viwanda tunakaribia kumalizia”

Raisi Leslie Benjamin alikuwa katika mkutano anahutubia, mamia na maelfu ya watu walikusanyika.Raisi huyu alikuwa ni kipenzi cha watu,kitendo cha kuingia madarakani uchumi ulipanda na aliboresha miundo mbinu.Alikuwa akimsikiliza kila mtu hakujali kabila wala rangi,uwe mweusi au Mweupe.

Rais Leslie angekusikiliza na ndiyo maana hata wakati wake ulivyoisha wananchi hawakumtaka Raisi mwingine walimpenda sana Raisi huyu.Alikuwa ni raisi kijana na mwenye sura ya kipole muda wote alikuwa akicheka hata kama angekasirika isingekuwa raisi kumgundua.

Wakati akiwa anaongea hayo Brigedia Karanje alikuwa anamtizama kwenye luninga,hasira zilimkaba na alikuwa ana usongo naye kupita kiasi chake.

***

Vital Kamere alizidi kumuweka Daphine karibu kwa maana hiyo ilikuwa kila mwisho wa wiki ni lazima atoke na Daphine kula chakula cha usiku ingawa alimuonea huruma lakini hakuwa na jinsi ya kufanya ilikuwa ni lazima siku chache zijazo aungane na vijana wa jeshi la Brigedia Karanje hilo lilieleweka kabisa.

“Mtihani mnaanza lini?”

Vital Kamere alivunja ukimnya akamuuliza Daphine siku hiyo wakiwa Sheraton Hotel wanakula.

“Mwezi ujao”

“Unasoma lakini?”

“Ndio Dad ninasoma,ninakuhaidi sitokuangusha hata kidogo”

“Usome,elimu ndio kila kitu”

Daphine alikuwa ni mwenye furaha siku zote,hakuacha kumshukuru Vital Kamere kwa msaada aliompatia.Aliamini bila mzee huyu ndoto zake zingekuwa zimezimika na asingefika popote pale,hakuelewa lolote linaloendelea ndani ya kifua cha Vital Kamere,alikuwa yupo nyuma ya pazia!

“Ukimaliza mitihani nataka uende jeshini”

“Dad jeshini kufanya nini?”

“Napenda uwe mkakamavu na jasiri”

“Mimi sipendi kuwa mwanajeshi Dad”

“Kwanini sasa?”

“Nataka niendelee na kidato cha tano,nimalize chuo,nipate digrii.Masters na PHD”

Hizo ndizo zilikuwa ndoto za Daphine siku zote,Vital Kamere alimuangalia bila kutoa jibu lolote,hata yeye alitamani Daphine aendelee na masomo lakini hakuwa na jinsi yoyote ile.

Walivyomaliza kula walitoka hotelini na kuingia ndani ya gari tayari kwa safari ya kurudi kupumzika,Vital Kamere alizidi kulipigia debe swala lake la Daphine kutaka kwenda jeshini.

****

Siku zilizidi kusogea na Daphine aliisubiria siku ya mtihani wa taifa kwa usongo sana alihakikisha alikichimba kitabu na kujua kila kitu,wanafunzi waliokuwa walokole walikesha makanisani,wale wa swala tano walikesha misikitini na kupiga ibada.Daphine alimuomba Mungu wake siku hiyo na siku ya siku ilivyofika aliingia ndani ya chumba cha mtihani,kwake ilikuwa ni kama aliyaona maswali kila lililoulizwa alilijua hakuna swali lililokuwa ngeni kwake.Baada ya wiki kukatika mtihani ukawa umekwisha na kilichokuwa kinasubiriwa ni majibu.

***

Hans na Beatrice walibaki vinywa wazi kwa mara ya kwanza walidhani wenda wamesikia vibaya matokeo,Daphine alikuwa ameongoza Dar es salaam nzima kwa kuibuka namba moja.Hawakutaka kuamini moja kwa moja, siku hiyohiyo walipanda daladala mpaka ofisi za NEKTA ili kuhakikisha kuwa taarifa hizo hazikuwa uvumi.

“Mimi naitwa Hans Ukwaju huyu ni mke wangu,tumesikia kwamba Daphine ndiye ameongoza kitaifa?”

Hans ndiye alikuwa akiongea maneno hayo bila breki.Afisa elimu aliyefahamika kwa jina la George Talimo aliwatizama watu hao wawili.

“Daphine aliyekuwa anasoma Kentony?”

“Ndio”

“Ni kweli,nyie ndio wazazi wa huyu mtoto?”

“Ndio”

“Hongereni sana ni kweli”

****

Daphine Hans,Tujaeli Mzava na Jackson Masue.Ndiyo walikuwa wameingia kwenye tatu bora na kwa maana hiyo Raisi Leslie Benjamin aliamua kuwaalika ikulu ili wale chakula cha mchana.Raisi Leslie alifurahi mno na ndiyo maana akawaandalia tafrija ndogo kama kuwapongeza.Moyo wa Daphine ulikuwa ukipiga kwa nguvu muda wote hata siku moja hakuwahi kuota kama atafika ikulu na kuonana na rais wake,jambo hilo kwake lilikuwa ni kama ndoto.

Ikulu kulikuwa na shamra shamra sio masihara na aliyekuwa anasubiriwa ni Raisi Leslie Benjamin aje kupeana mikono na kila mwanafunzi kisha baadaye chakula,baadhi ya waandishi wa habari walikuwa tayari wamefika ndani wanafanya kazi yao.

“TAYARI NISHAINGIA”

“WAPI? IKULU?”

“NDIYO”

“SAFI SANA,USIFANYE MAKOSA”

Mmoja wa watu wa Karanje alikuwa ikulu akijifanya ni mwandishi wa habari,alitoa taarifa na kuiweka simu yake mfukoni,akamuangalia kila mtu aliyekuwa ndani kwa makini nayeye akiwa katikati ya waandishi wa habari.

***

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa chumbani kwake akijiandaa kwa kutoka nje akaonane na wanafunzi watatu akale nao chakula.

“Umependeza mume wangu”

Sauti hiyo ilitoka ndani ya kinywa cha mkewe aliyekuwa mbele yake anamrekebisha tai.

“Ahsante Zuwena”

“Nakupenda sana”

“Mimi pia,sawa twen…”

Kabla hajamalizia sentensi yake simu ilimshtua kutokea mfukoni na alivyoitoa ilikuwa ni namba ngeni,ilielekea aliyekuwa anampigia simu alimjua sababu namba yake walijua watu wachache sana.Akaangalia vizuri na kumtizama Mke wake kisha kuipokea na kuiweka sikioni.

“Halloo Mh.Raisi.Jina langu naitwa Ngesa najua haunifahamu.Tafadhali kama upo ikulu naomba utoke haraka sana wewe na mkeo”


 Ni kweli ni bora asingepuuzia simu iliyopigwa kutoka kwa mtu aliyejitambulisha anaitwa Ngesa,akaikata simu sababu alikuwa ana imani kwamba kwa jinsi ulivyokuwa ulinzi nje na ndani ya ikulu yake hakuna mtu yoyote mbaya angeweza kuingia, hilo aliliamini asilimia mia moja,akamuangalia mke wake akamshika mkono wote wakatoka nje ili kuanza sherehe na watoto waliotingisha Tanzania kwenye mitihani ya kidato cha nne.

“Hamjambo watoto wazuri”

Raisi Leslie Benjamin aliwasalimia wanafunzi watatu waliokuwa mezani wote wakasimama na kumuamkia kwa heshima zote,Mapigo ya moyo ya Daphine yalikuwa yanapiga kwa nguvu.Bado aliendelea kuamini kuwa swala hilo lilikuwa ndoto na wala halikuwa kweli ingawa alitamani isiwe hivyo.Hakutaka kuamini kuwa mbele yake amesimama raisi wake ambaye alipendwa na mamia ya watu yeye akiwa mmoja wapo.

“Tafadhali kaeni chini”

Wanafunzi wote wakaketi kwenye viti na Raisi akaanza kuongea akimpongeza kila mmoja wao,baada ya hotuba fupi chakula kikaletwa na wote wakala na kufurahi huku wakipiga picha nyingi tofauti.

****

“Sasa kwanini uliniambia nighairi?”

“Mkuu ndiye aliniambia”

“Mimi nilikuwa tayari ikulu nifanye mambo yangu”

“Naelewa lakini ulifanya nilivyokwambia?”

“Ndio”

“Vizuri nipatie hiyo ramani”

Swala la kuingia ikulu na kutega bomu lilighairishwa na amri hiyo ilitoka moja kwa moja kwa Brigedia Karanje kumaanisha kuwa hakuwa tayari jambo hilo litokee kwanza ndiyo maana akasitisha zoezi.Ilikuwa ni lazima Raisi Leslie aonje joto la jiwe, alimchukia kuliko kinyesi ingawa walishawahi kuwa marafiki wakubwa sana siku za nyuma.Silaha ziliendelea kupitishwa kwa njia za magendo chini kwa chini pasipo serikali ya Tanzania kujua lolote lile.

“Hii hapa ramani”

Ilikuwa ni karatasi kubwa sana nyeupe juu ilionekana picha ya milango ya jengo la ikulu lilivyokuwa na kila kipimo.

“Pablo,hii ndiyo nini?”

“Huu mlango wa nyuma hapa ukipita unatokea kwenye korido chumba hiki hapa ndiyo analala Raisi Leslie”

“Sawa kwahiyo nimtumie mkuu?”

“Ndio mtumie yeye ataelewa”

“sawa”

Mambo yaliyokuwa yanaendelea chini kwa chini yalitisha,ndani ya ofisi hiyo kulikuwa na kompyuta nyingi.Karatasi ikawekwa vizuri kwenye mashine na kutumwa kwa njia ya barua pepe ambapo iliingia moja kwa moja ofisini kwa Brigedia Karanje ulikuwa ni mchoro wa ramani ya ikulu jinsi watavyoingia na kufanya ‘ambush’

“Grii griiii”

Simu ya Brigedia Karanje iliitia akiwa ndani ya ofisi yake.Akaipokea na kuiweka sikioni.

“Pablo,Ongea”

“Mkuu nishatuma tayari”

“Ndio nimeiona hapa,kazi njema”

“Ahsante”

Brigedia Karanje hakuongea maneno mengi alivyokata simu alibonyeza keybord na kuingia kwenye barua pepe akaona mchoro haraka akauchapa na kuanza kuukagua.Aliitizama karatasi kubwa kwa hasira mno,alitamani hata kesho aingie ikulu na kuipindua nchi ya Tanzania kwa njia yoyote ile.Hapohapo akavuta kiti chake nyuma na kutoka nje ya ofisi yake.

“Nipeleke Lugalo”

Alimuamuru dereva wake baada ya kuingia ndani ya Hammer yake ya jeshi,gari ziliondoka mara moja na kuelekea alipopataka yeye,Brigedia Karanje siku zote alikuwa ni mtu mwenye kauli za kutisha na mwenye amri tu.Na siku zote alitembea na msafara licha ya hayo alilindwa vibaya sana, ilikuwa ni rahisi sana kuonana na Raisi Leslie kuliko Brigedia huyu katili, Karanje.

***

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG