SIN SEASON 1
WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+
SEHEMU YA 6 KATI YA 10
“Mwanangu vipi?”
“Yaani baba na Evans wametembea na yule malaya pale eheee?”
Mrs Sanga akashusha pumzi kwa maana swali hilo lina uponda ponda sana moyo wake.
“Mama yaani nimetoa bikra yangua mbayo nilipanga kumpa Jery ila leo hii nime mpa yule mjinga. Ahaa……inaniuma mama”
Julieth alizidi kulia na kumfanya mrs Sanga kumkumbatia mwanaye huyo wa kike.
“Wanaume ni watu wabaya. Mwanangu huu ni wakati wa kufanya jambo juu ya maisha yako. Achana na huyo Evans, mtazame Jery ndio mwanaume sahihi kwenye maisha yako”
Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya upole hukua akimtazama Julieth usoni mwake. Julieth akajipangusha machozi yake kwa pamoja na kumkazia macho mama yake.
“Mama nina hitaji kumua Evans”
“Kwa nini?”
“Hawezi kunitoa bikra yangu na nikamucha hai ikiwa ni msaliti kwenye maisha yangu”
Mrs Sanga macho yakamtoka kisha baada ya muda akatabasamu kwani roho yake ya ukatili sasa ana anza kuiona ndani ya mwanaye huyo.
“Kamueleze huyo kunguni wako aniambie ni wapi alipo mume wangu. Nikamchukue la sivyo sinto ondoka hapa”
“Hivi wewe binti una jiamini nini, ikiwa mimi ndio nilikutoa kule uswahilini na kukupeleka kwenye maisha mazuri. Hivi una jua nina weza kukupokonya kila kitu”
“Hahaa hakuna tabu una weza kunipokonya. Ila kabla ya kunipokonya ulimwengu mzima utajua madhambi yako”
Nabii Sanga akafumba macho kwa sekunde kadha akisha akamatazama Magreth.
“Kitu unacho jaribu kukifanya wewe ni sawa na paya kuanzisha vita na panya ikiwa anatambau fika kwamba hana uwezo wa kuoambana na paka”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka na kuondoka sebleni hapo na kuelekea chumbani kwa binti yake.
“Hei Julieth yupo wapi Evans?”
Nabii Sanga aliuliza huku akikaa pembeni ya binti yake.
“Baba”
“Naam”
“Ninawaomba munisamehe kwa yale niliyo yazungumza jana”
“Tume kusamehe kwa maana tuna jua ulikuwa hujui kinacho endelea”
“Ni kweli, ila baba nina hitaji kufanya jambo moja”
“Jambo gani?”
“Nataka kumuua Evans. Hawezi kunitoa usichana wangu na nikamuacha hai. Atakuja kuniharibia kwa Jery”
Nabii Sanga akamtazmaa mke wake huku akishindwa kutoa jibu sahihi.
“Kwa sasa yupo wapi?”
“Hotelini”
“Hoteli gani na yupo chumba namba ngapi?”
Julieth akakaa kimya kidogo kisha akamtazama baba yake.
“Yupo hoteli ya X Royal chumba namba elfu moja na tatu?”
“Sawa”
Nabii Sanga akanyanyuka na kutoka chumbani hapo. Akarudi sebleni na kumkuta Magreth akiwa amesimama.
“Yupo hoteli ya X Roya chumba namba elfu moja na tatu. Kaishi maisha ya amani na huyu kijana wako, sinto hitaji uingilie tena kwenye maisha yangu umenielewa”
Magreth akanyanyua begi lake, akamtazama nabii Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akamsogelea.
“Endapo kuna jambo lolote litamtokea Evans au mimi, basi nita hakikisha watu wa kwanza kushuhulika nao ni wewe na familia yako. Umeona uwezo wangu kidogo tu, ila nina uwezo hata wa kupigana ana wanaume kumi wenye uwezo mkubwa na nikawapiga hiyo kuwa makini na mimi”
Magreth akampiga nabii Sanga busu la shavuni kisha akaondoka nyumbani hapo. Breki ya kwanza akasimama katika hoteli hiyo, akashuka na moja kwa moja akaingia kwenye lifti na kupandisha gadi gorofa ya nne. Akatembea kwenye kordo hiyo na akaona chumba namba elfu moja na tato. Akasimama malangoni hapo kwa sekunde kadhaa na kuanza kuminya kitufe cha kengele.
***
Evan mara baada ya kukaa dakika ishirini ndani ya chumba hicho, akatoka na kuingia kwenye mgahawa ulipo katika hoteli hiyo. Akaanza kunywa juisi huku akitazama mechi ya mpira pamoja na mashabiki wengine waliomo katika mgahawa huo.
‘Nina kwenda kuwa tajiri sasa’
Evans alizungumza huku akitengeneza picha za muono wa jumba walilo kubaliana yeye na Julieth kulinunua.
‘Sijui nimuambie aniadikishe jina langu?’
Evans alizidi kuwazia mafanikio hayo ambayoa amebakisha masaa kadhaa kabla ya siku hii ya keo kuisha.
“Habari yako kijana?”
Sauti ya mzee Mbogo ikamstua sana Evans aliye jikuta akimshangaa mzee huyo kwa maana hajawahi kumuona sehemu yoyote kwenye maisha yake.
“Salama. Shikamoo”
“Marahaba nina weza kukaa?”
“Ndio karibu”
Mzee Mbogo akaka katika kiti kichopo pembeni ya meza hiyo. Akaweka bahasha yenye rangi ya kaki, mezani hapo.
“Fungua ndani ya bahasha kuna zawadi yako”
“Samahani sana mzee. Una nifahamu mimi?”
Mzee Mbogo akatabasamu kidogo, akapiga fumba la maji aliyo fika nayo hapo mezani.
“Evans Richard Shika si ndio?”
“Nd….i…ioooo”
“Basi fungua ndani ya bahasha hiyo kuna zawadi yako”
Taratibu Evans akaichukua bahasha hiyo huku mikono ikimtetemeka mwili mzika. Akaifungua bahasha hiyo, picha ya kwanza kuitoa, ni picha yake na Julieth. Akastuka sana kwa maana picha hiyo ime pigwa wakiwa katika mgahawa ambao walikuwa wakipata chakula mchana wa siku ya leo. Akafungu picha ya pilis na kumshuhudia Julieth akiwa ameshika mikono na mwanaume mwengine ambaye hamtambui ni nani. Taratibu akatoa picha nyingine huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi, akamshuhudia Julieth akiwa amekumbatiana na mwanaume huyo huku wakinyonyana lispi zao na nguo ambazo amevaa Julieth ndio nguo hizo hizo alizo ondoka nazo leo.
“Mzee ume zitoa wapi hizi picha?”
“Huyo binti anaitwa Julieth Sanga. Ni mtoto wa nabii mkubwa sana waha Tanzania, nabii Sanga nina imani kwamba una mfahamu. Pili huyo wa pembeni ni mwanaume wake anaitwa Jery Mtenzi, ni mtoto wa raisi Mtenzi aliyopo madarakani kwa sasa. Hivyo Evans kama ulikuwa na ndoto za kumuo huyo binti basi kaa naye mbali kwa maana kinacho fwata kwako ni kifo. Kwausalama wako ondoka kabisa ndani ya jiji la Dar es Salaam.”
Mzee Mbogo mara baada ya kuzumguza hivyo akaondoka huku vijana wake wanne wanao mlinda nao wakaanza kunyanyua kwenye meza walizo kuwa wamekaa na kuondoka naye na kumuacha Evans akiwa amenyong’onyea huku akihisi moyo wake ukichwanjwa chanjwa na viwembe kwani maumivu anayo yahisi hapo ni mara mbili ya maumivu aliyo sababishiwa na Magreth.
Machozi yakaanza kumlenga lenga Evans huku akishuhudia jinsi matumaini ya mafanikio yakianza kuyayuka mithili ya barafu. Akatoa noti ya shilingi elfu tano na kuiweka chini ya glasi hiyo ya juisi ambayo imesalia kidogo. Akanyanyuka na kuishika bahasha hiyo mkononi mwake. Akaanza kupandisha ngazi za kuelekea gorofani, akafika kwenye kordo ya chumba alicho panga. Akastuka sana mara baada ya kumuona Magreth akiwa amesimama mlangoni kwake. Kwa haraka akarudi nyuma na kuanza kushusha ngazi huku woga mwingi ukiwa umemtalawala kwa maana ana amini kwamba Magreth ni lazima atakuwa ameambatana na nabii Sanga na kitendo cha kufika hapo ni kuhakikisha kwamba ana muangamiza. Kutokana mfukoni ana simu yake pamoja na wallet yenye kiasi cha shilingi laki tatu, hakuona haja ya kuendelea kurudi chumbani kwake. Akatoka nje na kusimamisha muendesha pikipiki, na akamuomba ampelekea katika stendi ya mabasi Ubungo.
Magreth akaendelea kuminya kitufe cha kengele hiyo, ila mlango haukufunguliwa. Baada ya dakika tano akamua kuelekea mapokezi.
“Habari yako dada”
“Salama”
“Ahaa una weza kuwasiliana na mgeni aliyopo katika chumba namba elfu moja na tatu?”
“Wewe ni nani yake?”
“Ni mgeni wake, alinieleza kwamba yupo hapa ila nimefika mlangoni hapo nimebisha hodi sana ila hajafungua”
“Muhudumu huyo akafunua daftari la wageni. Akatazama jina lililo andikwa katika chumba hicho.”
“Nahisi huyu kaka amepita hapa kama dakika saba hivi”
“Dakika saba ?”
“Ndio amepita hapa”
“Mrefu hivi, maji ya kunde?”
“Ndio dada”
“Amesema kwamba atarudi?”
“Hapana hajakabidhi hata fungua. Nahisi hajakwenda mbali sana ana weza kurudi”
“Sawa nina shukuru”
Magreth akatoka nje hoteli hiyo na kuanza kuangaza kila sehemu, ila hakuweza kuona dalili yoyote ya Evans. Akamfwata mlinzi wa geti.
“Shikamoo mzee”
“Marahaba”
“Kuna kijana hivi mrefu, maji ya kunde ametoka hapa kama dakika kadhaa zilizo pita je ameelekea uwepo gani?”
“Hivi, emekodisha pikipiki hapa na kuelekea kule”
“Asante”
Magreth akafuka upande wa pili wa barabara ambapo kuna kituo cha waendesha pikipiki.
“Habari zenu”
“Salama dada. Wapi una kwenda”
“Ahaa kuna kijana emetoka pale hotelini ni mrefu maji ya kunde, dakika kama kumi hivi amepanda pikipiki pale nje”
“Yaa nimeona, amepanda pikipiki ya Jose”
“Una weza kuwasiliana na huyo Jose na kumueleza ana elekea wapi?”
“Mmmm kwema sister?”
“Kwema ni mume wangu jamani yule nimegombana naye hivyo ameondoka kwa hasira”
Bodaboda hao wawili wakatazamana.
“Sister unajua hili tunalo fanya ni kukiuka sheria za kijiwe chetu. Tusije tukawa tuna mchomesha mchizi wetu”
Magreth akatoa elfu arobaini na kuwakabidhi vijana waha kila mmoja elfu ishirini.
“Nina waomba sana muweze kunisaidia kuwasiliana na huyo Jose ili nifahamu tu, niwapi ana elekea mume wangu”
Kijana mmoja akatoa mfukoni simu yake na kumpigia Jose.
“Oya kaka wapi hiyo?”
“Nina kwenda Ubungo stendi”
“Ahaa poa mwanangu”
“Fresh”
Kijana huyo akakata simu.
“Panda amekata simu anasema kwamba ana elekea Ubungo”
“Sawa nipeleke nipeleke”
Kijana huyo akamkabidhi Magreth kofia ya usalama kwa ajili ya kichwa chake kisha na yeye akavaa kofia hiyo na kuwasha pikipiki na kuondoka eneo hilo.
Njia nzima Evans akazidi kutafakari ni sehemu gani ambayo ana weza kwenda kutulia na kujipanga vizuri kama ni kurudi Dar es Salaam basi atarudi kwa siku nyingine akiwa na akili mpya.
“Oya hivi Ubungo kwa sasa nina weza kupata magari ya kuelekea Dodoma?”
“Kwa sasa ni uongo kaka. Ila labda upande gari kutoka hapa hadi Morogoro. Ulale Moro, au ubahatike kupata gari za kuelekea Dodoma za usiku”
“Eti ehee?”
“Ndio ila kwa urahisi zaidi una weza kupata gari za kuwahi Morogoro, Mbezi mwisho stendi”
“Sawa nipeleke Mbezi mwisho”
Kama walivyo kubaliana ndivyo jinsi safari ilivyo badilika na kuianza safari ya kuelekea Mbezi mwisho Stendi. Kutokana na pikipiki kuto kusimama kwenye foleni, ndani ya muda mchache wakafika Mbezi mwisho stendi na Evans akamlipa dereva huyo kiasi anacho kihitaji kisha akapanda kwenye gari aina ya costa na safari ya kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam ikaanza.
***
Magreth na muendesha pikipiku huyo wakafika katika stendi kuu ya mabasi Ubungo.
“Una weza kunisubiria kaka”
“Pesa ita kuwa kubwa au unaweza kunilipa nauli ya kutoka kule hadi hapa”
“Ni kiasi gani?”
“Elfu kumi na tano”
Magreth akamkabidhi elfu ishirini na kuingia ndani ya kituo hicho kikubwa cha mabasi. Akaanza kuangaza macho huku na kule ila hakuweza kumuona Evans. Akajaribu kumpigia simu, ila jibu la kuto kupatikana kwa simu hiyo, likazidi kumchanganya Magreth. Magreth akaanza kumuuliza kila aliye ona ana weza kumfahamu Evans, ila kila mtu akakiri kwamba hamfahamu kabisa Evans. Baada ya dakika hamsini, Magreth akatoka ndani ya kituo hicho huku akiwa amechoka sana.
“Vipi ume mpata?”
“Hapana kaka”
“Ngoja basi nimcheki jamaa nimuulize ni wapi alipo mpeleka jamaa”
“Fanya hivyo, labda hakumleta Ubungo hapa stendi”
Kijana huyo akawasiliana na rafiki yake huyo aliye kuwa amembeba Evans.
“Kaka hivi yule abiria uliye ondoka naye pale hotelini umempeleka wapi?”
“Kwani vipi ndugu?”
“Nipo na mke wake hapa, ana mtafuta balaa. Wamegombana hivyo ameomba sana aweze kufahamu ni wapi alipo jamaa”
“Daa jamaa kwa sasa atakuwa anaitwafuta Kibaha kama si kuitafuta Kibaha basi atakuwa anainusa nusa Chalinze”
“Duu ana elekea wapi?”
“Dodoma, ila kutokana muda umekwenda, ana weza kulala Morogoro kisha kesho akaelekea Dodoma. Jamaa amepandia gari Mbezi Mwisho”
Muendesha pikipiku huyo akamtazama Magreth ambaye bado anaendelea kuangaza kila sehemu ya eneo hilo la Ubungo.
“Poa kaka”
Muendesha pikipiki huyo akakata simu na kumgusa Magreth bega.
“Sister jamaa amesha toka nje ya mji huu. Jamaa anasema kwamba alimpeleka stendi ya Mbezi mwisho na anadai kwamba jamaa ana elekea Morogoro na kesho ana sepa kwenda Dodoma”
Habari hiyo ikamyong’onyeza sana Magreth kwa maana haamini kwamba ndio ana kwenda kumpoteza Evans milele.
***
“Mkuu kuna habari nyeti nime ipata hapa”
Mlinzi wa karibu wa Jery alizungumza huku akimtazama usoni mwake.
“Habari gani?”
“Kuna rafiki yupo NSA. Amenitumia hizi picha kwenye simu ambazo zina muonyesha Magreth na mpenzi mwanaume mwengine”
Jery akakurupuka kwenye kiti alicho kikalia huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.
“He….he….e…mbu nione”
Mlinzi huyo akamkabidhi Jery picha zinazo muonyesha Julieth na Evans wakiwa maeneo mbalimbali. Jery akahisi kifua chake kina kwenda kupasuka kwa maumivu ya wivu yaliyo ambatan ana hasira kali itokanayona kitendo hicho.
“Huyo jamaa ana fanya kazi gani?”
“Amemaliza chuo na hana kazi yoyote na hata leo hii kabla ya kuja hapa alikuwa naye”
“Nitafutie huyo kijana haraka iwezekanavyo na ikiwezekana mtekeni na nitahitaji kuonana naye. Jambo hili hakikisha baba halitambui. Umenielewa?”
“Ndio mkuu”
“Niandalie mazingira nina hitaji kwenda tena nyumbani kwa kina Julieth”
“Peke yako”
“Twende wote ila sinto hitaji ulinzi wa mtu mwengie yoyote”
“Sawa mkuu”
Jery akaendelea kuzipitia picha hizo, ambazo zilipigwa na mtu maalumu aliye wekwa na kitendo cha NSA kuhakikisha wana mfwatilia Evans popote pale anapo elekea. Richard akawakabidhi vijana wawili walipo chini yake kazi ya kumtafuta Evans, kisha akandaa mazingira ya kumtoa Jery eneo hilo la ikulu pasipo mlinzi mwengine yoyote kufanikiwa kufahamu. Wakafanikiwa kutoka ikulu na kuianza safari ya kuelekea nyumbani kwa nabii Sanga.
“Jery”
“Naam”
“Uta kwenda kumfanya nini Julieth?”
“Sijui hata nitamfanya nini. Ila ngoja tufike”
Jery alizungumza huku machozi yatokanayo na hasira yakimwagika taratibu usoni mwake.
***
“Mkuu nime mpoteza Evans”
Kijana aliye pewa kazi ya kumfwatilia Evans popote anapo kwenda alitoa ripoti kwa mzee Mbogo.
“Imekuwaje ume mpoteza?”
“Alikuwa kwenye pikipiki na mimi nipo kwenye gari hivyo foleni hapa Ubungo ndio ime sababishia nimempoteza.
“Hakikisha kwamba una mtafuta na kumpata. Umenielewa?”
“Sawa muu”
Kijana huyo akakata simu huku akiangaza kila sehemu hapo Ubungo na hakuweza kuona pikipiki aliyo kuwa amepanda Evans sehemu ilipo elekea. Mpelelezi huyo akasimamisha gari lake kwenye sheli iliyopo hapo eneo la Ubungo, akaanza kutafakari ni wapi ambapo Evans anaweza kuwa ameleelekea. Kwa bahati nzuri akamuona dereva pikipiki aliye kuwa amempakiza Evans akisamama hapo sheli na kuanza kuongeza mafuta kwenye pikipiki yake. Mpelelezi huyo akashuka kwenye gari lake na kumfwata muendesha pikipiki huyo. Akamuonyesha kitambulisho chake.
“Ume mpeleka wapi yule jamaa aliye ondoka naye pale hoteli ya X Royal”
Kijana huyo akaanza kuhisi abiria aliye kuwa amempakiza atakuwa ni muhalifu kwa maana si kwa kuuliziwa huko.
“A…aa nimempeleka Mbezi Mwisho stendi”
“Ana elekewa wapi?”
“Aliniambia kwmaba ana kwenda Dodoma. Ila kutokana ni jioni sasa hivi nilimshauri kulala Morogoro na kesho aweze kuelekea huko Dodoma”
Mpelelezi huyo akamtazama dereva huyo pipikipi na kumuamini kile alicho kizungumza.
“Amepanda gari gani?”
“Sijajua kwa maana mimi nilimshusha pale stendi na mimi nikaondoka zangu”
Mpelelezi huyo kwa haraka akarudi ndani ya gari lake na kuondoka eneo hilo na kuianza safari ya kuelekea mkoani Morogoro.
***
“Mama Jery akifahamu kwamba mimi sio bikra itakuwaje mama?”
Julieth alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Kabla ya mama yake kumjibu kitu chochote mlango ukafunguliwa na nabii Sanga akaingia ndani hapo.
“Jery amerudi na anahitaji kuonana nawe”
Julieth akastuka sana. Julieth kwa haraka akayafuta machozi yake na kujiweka sawa. Jery akaingia ndani hapo na kuwafanya nabii Sanga na mke wake kutoka ili kuwapisha waweze kuzungumza.
“Jery”
Julieth alizungumza huku akitabasamu. Jery akaufunga mlango huo kwa ndani na kumshika Julieth kwa hasira sana na kumsukumia kitandani. Kitendo hicho kika mstua sana Julieth na katika maisha yake yote hakuwahi kumuona Jery akiwa amekasirika kwa kiasi hicho.
“Kabla sijakuoa nina hitaji kufahamu, je wewe ni bikra au si bikra?”
Swali la Jery likamstua sana Julieth pamoja na mrs Sanga aliye simama mlangoni hapo akihitaji kusikia ni kitu gani Jery ana zunugmza na mwanaye kwa maana alipo weza kumuona Jery aligundua kwamba amekasirika sana.
Julieth akapatwa na bumbuwazi, akatamani kuzungumza ila mdomo wake ukakosa uwezo kabisa wa kuzungumza.
“ZUNGUMZAAAA”
Jery alizungumza kwa ukali sana huku akimkazia macho Julieth ambaye mwili mzima una mtetemeka kwa woga.
“Mimi ni bikra Jery”
Julieth aliongopea ili kuepukana na kipigo ambacho ana weza kukipokea kutoka kwa Jery ambaye amefura kama Mbogo aliye jeruhiwa na muwindaji. Mrs Sanga naye mapigo yake ya moyo yakazidi kumuenda kasi hadi akatamani kuingia ndani humo, ila akaona sio jambo zuri kuingilia mazungumzo ya watoto. Jery akatoa simu ya mlinzi wake, akamuonyesha Julieth picha alizo pigwa akiwa na Evans.
“Unaweza kunipa maelezo juu ya huyu mtu”
Julieth akatamani ardhi ipasuke na immeze kwani limekuwa ni jambo la haraka sana kwa Jery kufahamu mahusiano yake na Evans ambaye amepanga kumuua.
“Huyo kijana ana itwa Evans”
“Ni nani yako?”
“Majuzi hapa mimi na mama tulikuwa tuna alekea Bagamoyo. Ia tulipo fika pale mataa na ya Mwenge tuli mgonga muendesha pikipiki akiwa amempakiza abiria ambaye ndio huyo kijana”
Jery akashusha pumzi kwa nguvu huku akijaribu kuiweka sawa hasira yake.
“Baada ya kumgonga ikawaje?”
“Dereva alifariki pale pale ila huyo kijana alifanikiwa kupona. Ili kumuweka sawa asiende kutufugulia kesi mahakamani ilinibidi niwe naye karibu sana.”
“Ina maana huna mapenzi na huyu kijana?
“Sina mapenzi naye na una nijua jinsi nilivyo na msimamo na maisha yangu. Siwezi kukutana na mwanaume tu alafu nikawa naye kwenye mahusiano”
Julieth alizungumza kwa kujiamini sana. Kujiamini kwake kuka ufaifanya hasira ya Jery taratibu kuanza kushuka huku akianza kumuamini Julieth.
“Una nihakikishia kwamba sio mpenzi wako kabisa?”
“Ndio na hizi picha aliye zipiga ana malengo mabaya na sisi. Hivi una hisi miaka yote minne uliyo kaa Marekani bila ya kuwasiliana na mimi una hisi kwamba nilikuwa nina jiachia jiachia eheee?”
“Hapana mpenzi wangu. Una jua ni lazima niwe na wivu na wewe. Na swala la kuto kuwasiliana nawe mbona tulisha lizungumza”
Jery alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Julieth usoni mwake.
“Ndio hivyo huyo kijana mimi sina mahusiano naye kabisa na wala usihisi kwamba nina weza kukusaliti wewe na kama ni zawadi yako ya bikra utaipata ukisha nioa”
“Nashukuru sana mpenzi wangu. Nina kupenda sana mke wangu”
“Nina kupenda pia mume wangu”
Jery na Julieth waka kumbatiana kwa sekunde kadhaa kisha, taratibu wakaanza kunyonyana lipsi zao huku wakizama katika hisia nzito za kimapenzi. Jery akataka kuingiza kiganja chake cha mkono wa kulia katika suruali aliyo vaa Julieth ila Julieth akakiwahi kiganja hicho kwa maana kina weza kwenda kushika kitumbua chake na hilo lina weza kumpelekea Jery kufahamu kwamba mke wake sio bikra tena.
“No baby, muda haujafika”
“Oho sory nimejisahau mke wangu”
“Usijali natambua una hamu na mimi”
“Ni kweli je upo tayari kuolewa na mimi?”
“Ndio mume wangu nipo tayari”
Jery akajawa na furaha ya ajabu sana. Hata mrs Sanga ambaye muda wote alikuwa amesimama hapo mlangoni pasipo Jery wala Julieth kufahamu, naye alijawa na furaha kubwa sana. Baada ya mazungumzo ya hapa na pale, Jery akaaga na kurudi zake ikulu.
“Mama nitafanya nini ikiwa nime mdanganya Jery kwamba nina bikra?”
“Wala usijali kuna bikra za kutengeneza nita hakikisha una ipata hiyo na hato weza kufahamu kama bikra yako alisha tolewa”
“Nashukuru sana mama yangu ukinisaidia katika hilo”
“Ehee na huyo kichaa una mshuhulikia lini kwa maana ikitokea aka weka pingamizi katika ndoa yenu kanisaini ita kuwaje?”
Julieth taratibu akashusha pumzi huku akimtazama mama yake.
“Nisaidie katika hilo kwa maana Jery amekuja na picha za ushahidi nikiwa na kijana huyo”
“Kweli?”
“Ndio mama sijui nita fanya nini?”
“Nita kuambi nini cha kufanya kwa maana sasa hivi yule malaya wake atakuwa amekwenda kumchukua hotelini”
“Nani?”
“Si umemueleza baba yako ni hoteli gani alipo Evans hivyo utambue kwamba ni lazima atakuwa amemuambia Magreth ni wapi alipo huyo kunguni wake.”
“Mama siwezi kukubali Magreth ampate Evans”
“Kwa nini ikiwa una hitaji kumua?”
“Ndio ila sitaki awe na huyo Mage”
Julieth alizungumza huku akinyanyuka kitandani hapo.
“Sasa una kwenda wapi?”
“Nina kwenda hotelini”
“Hembu rudisha makalio yako hapa. Acha ujinga wewe, kumbuka upo kwenye kipindi gani. Kama Jery amesha kuonyesha picha upo na huyo mwenda wazimu wako ni lazima utambue kwamba una fwatiliwa na kama una fwatiliwa basi ina kupasa kuwa makini. Umenielewa?”
Mrs Sanga alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Julieth kuwa mpole kwa maana hasira aliyo iona kwa Jery hatamani tena kuiona kwenye maisha yao ya ndoa.
***
Amani ikazidi kupotea moyoni mwa Evans, njia nzima ana tafakari ni kitu gani ambacho kina weza kumkuta kwa kujihusisha kimanusiano na Julieth, mtoto wa nabii Sanga. Akazitoa picha kwenye bahasha aliyo achiwa na mzee Mbogo. Akaanza kutazama picha moja baada ya nyingine.
‘Julieth nina kuchukia ume yayumbisha maisha yangu’
Evans alizungumza kimoyo moyo huku machozi ya hasira yakimwagika usoni mwake. Safari ikazidi kusonga mbele hadi wakafika katika stendi ya Msavu mkono Morogoro. Evans akashuka kwenye gari huku akishangaa shangaa magari mengi yaliyopo kwenye stendi hiyo kubwa.
“Oya mambo vipi”
Evans alimuambia muuza maji vinjwaji kwenye boksi aliye simama pembeni yake.
“Poa kaka”
“Nina omba Coca take away”
“Poa ni buku”
Evans akatia noti ya shilingi elfu mbili na akachukua na pakti ya biskuti ya elfu moja.
“Oya hapa kuna gari za kwenda Dodoma usiku huu?”
“Ahaa hapana kaka mabasi yoyote yamesha pita kaka”
“Duu hapa hoteli nina weza kupatia wapi?”
“Zipo loge nyingi tu kaka”
“Nielelekeze”
“Njoo nikuonyeshe”
Muuza vinywaji huyo alizungumza huku wakisogea katika eneo ambalo wana weza kuona gorofa moja la hoteli.
“Kwenye lile gorofa pale una weza kupata vyumba kaka”
“Shukrani sana ndugu”
“Hapa chukua bodaboda ata kupeleka hadi pale”
“Poa”
Evans akaagana na muuza vinywaji huyo kisha akakodisha pikipiki iliiyo mpeleka hadi kwenye hoteli hiyo. Kwa bahati nzuri akafanikiwa kupata chumba. Usiku mzima Evans hakupata usingizi kabisa, maneo ya mzee Mbogo yakaendelea kujirudia kichwani mwake.
‘Mtoto wa raisi. Daaa kwa nini Julieth ali nipumbaza kiasi hichi hadi nika muamini sana?’
Evans aliendelea kuwaza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
‘Mimi ni mwanaume, nilazima nihakikishe nina pambana kwenye haya maisha na kuanzi hivi sasa sinto mpenda mwanamke wa aina yoyote. Nitakuwa nina chapa ilale tu’
***
Mpelelezi anaye amfwatilia Evans, akafika mkono Morogoro majira ya saa saba kasoro usiku. Akasimamisha gari karibu na stendi ya mabasi. Akawafwata waendesha pikipiki walipo eneo hilo.
“Waskaji mambo vipi?”
“Safi kaka”
“Aisee gari za kuelekea Dodoma hapa za mwisho huwa zina pita saa ngapi?”
“Mmmm saa nne hivi zikichelewa sana zina pita hapa saa tano kaka”
“Ahaa sawa nina shukuru”
“Poa poa”
Mpelelezi huyo akarudi ndani ya gari lake na kuanza kupiga mahesabu ya gari la abiri likitoka Dar es Salaam hususani costa zinazo simama simama barabarani, akagundua kwamba costa aliyo ipanda Evans ni lazima itakuwa ime chelewa kufika Morogoro hivyo ame kosa usafiri wa kuondoka Morogoro hapo.
‘Ata kuwa wapi huyu jamaa’
Mpelelezi huyo alijiuliza huku akitazama majengo ya gorofa yaliyopo katika mji huo. Kabla hajapata jibu akapokea simu bosi wake Mzee Mbogo.
“Habari mkuu”
“Upo wapo?”
“Nimefika Morogoro usiku huu”
“Sasa tume nasa video za CCTV kamera zilizopo hapo kwenye hiyo stendi. Dakika arobaini na nne Evans aliondoka hapo”
“Muheshimiwa una weza kunitumia hiyo video?”
“Ndio”
“Nashukuru sana”
Simu ikakatwa, hazikuisha hata dakika mbili, video hiyo ikaingia kwenye simu yake. Akamshuhudia Evans akishuka kwenye moja ya costa. Akamshuhudia akizungumza na kijana wa maji huku akinunua soda pamoja na biskuti. Akaendelea kuitazama video hiyo na kumuona kijana huyo akimuelekeza Evans sehemu ya kwenda na Evans akatoka nje ya stendi hiyo na kupanda pikipiki na kuondoka eneo hilo. Mpelelezi huyo akarudi sehemu ya maelekezo anayo pewa Evans na kijana muuza maji.
‘Akiwa upande ule pale, akielekezwa kule sehemu aliyo fikia ni ile pale’
Mpelelezi huyo alijikuta akitabasamu mara baada ya kugundua ni wapi Evans ameelekea.
‘Kazi imekwisha sasa’
Mpelelezi huyo alizungumza huku akiwasha gari lake. Akafika hotelini hapo na moja kwa moja akaelekea mapokezi. Akamasalimia muhudumu huyo wa kiume kisha akamuonyesha video inayo muonyesha Evans.
“Huyu kijana amefika hapa hotelini kwenu?”
Muhudumu akaitazama video hiyo, kisha akamtazama mpelelezi huyo.
“Ahaa kwa nini una muulizia?”
“Ni rafiki yangu”
“Basi acha niwasiliane naye ili nifahamu kama una miahadi naye”
“Hapana. Wewe niambie ni chumba kipi alichopo ili niweze kuingia na kuonana naye”
“Utaratibu wa kazi yangu hausemi hivyo. Isitoshe sasa hivi ni usiku na nina ogopa sana endapo ikatokea mteja akauwawa ndani ya hoteli yetu, ita tutia matatizoni”
“Mimi sio muaji ila ni mlinzi wake”
“Mlinzi wake? Nitaamini vipi?”
“Amini hilo”
“Ndio uniaminishe, siwezi kuamini tu maneno”
Mpelelezi huyo akashusha pumzi huku akimtazama muhudumu huyo. Akatoa kitambulisho chake na kumkabidhi muhudumu huyo ambaye mara baada ya kukisoma, akajikuta akianza kutetemeka.
“Haya nipelekea chumbeni kwake”
Muhudumu huyu hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na mpelelezi huyo. Wakafika katika chumba cha Evans, mpelelezi huyo akampa ishara muhudumu huyo kungonga na akatii agizo hilo.
Evans akastuka sana mara baada ya kusikia mlango ukigongwa. Akatazama saa ya ukutani inamuonyesha ni saa saba kasoro usiku. Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda kasi huku wasiwasi mwingi ukimtawala. Taratibu akashuka kitandani.
“Nani?”
Evans alizungumza huku akijibanza mlangoni.
“Room service”
“Muda huu una hitaji nini?”
“Tuna utaratibu wa kukagua wateja wetu kila usiku”
Evans akaanza kupata mashaka kwa maana amelala latika mahoteli makubwa na ya kifahari kuliko hata hoteli hii ila hajawahi kukutana na utaratibu wa aina kama huo.
“Nita kuamini vipi kama wewe ni room service”
“Mimi ndio yule niliye kupa chumba pale mapokezi. Ume sahau sauti yangu?”
Evans akaka kimya kwa sekunde kadhaa, akaikumbuka sauti ya kijana, akaufungua mlango huo. Kwaharaka mpelelezi huyo akaingia ndani hapo na kumstua sana Evans kwa maana alicho kitegemea ni tofauti kabisa na hichi anacho kiona.
“Wewe ni nani?”
“Vaa nguo zako sasa hivi na tuondokea, eneo hili sio salama”
Mpelelezi huyo alizungumza huku akikimbilia dirishani, akachungulia na kushuhudia kundi kubwa la watu walio valia suti nyeusi, wapatao ishirini, wakishuka katikamagari mawili aina ya Toyota VOXY. Mpelelezi huyo akachomoa bastola yake na kuwafanya Evans na muhudumu huyo kustuka sana.
“Una shangaa nini, nimekueleza vaa nguo zako na tundoke humu ndani?”
“Wewe ni nani?”
“Utanijua baadae ila kwa sasa fanya kile ninacho kihitaji. Umenielewa?”
Evans akamtazama muhudumu huyo, kisha kwa haraka akairudia suruali yake iliyopo kitandani na kuivaa haraka haraka. Akavaa na viatu vyake, kisha mpelelezi huyo akachungulia mlangoni hapo. Alipo hakikisha kwamba hakuna mtu yoyote, kwa haraka akamshika Evans mkono na wakaanza kutembea huku bastola yake ikiwa mkononi mwake.
***
“Maelezo ya Julieth bado hayajanitosheleza”
Jery alizungumza huku akimtazama mlinzi wake.
“Nimepata habari kwamba kijana huyo amekimbilia Morogoro”
“Amekimbilia Morogoro?”
“Ndio mkuu”
“Sasa kama angekuwa sio muhalifu nina imani kwamba asinge kimbia. Una timu gani ambayo ina weza kwenda Morogoro na kuhakikisha wana mleta Evans mikononi mwangu”
“Nimewakabidhi wale vijana wangu wawili na wamepata viajana wengine kama kumi na nane hivi wenye uwezo wa mapigano. Nina imani kazi ita fanyika”
“Waambie kabisa kwamba hiyo kazi ni ya siri. Haihusiani kabisa na serikali ya baba yangu na hakikisha kwamba atakaye kamatwa basi ana kunywa kidonge cha sumu na kujiua yeye mwenyewe. Umenielewa?”
“Nimesha toa hayo maelezo mkuu”
“Na nitahitaji kumpata huyo mpelelezi anaye mfwatilia Evans na kutupiga hizi picha”
“Sawa mkuu ata patapatikana”
Jery akamimina glasi ya pombe kali aina ya wisky kwenye glasi yake na taratibu akaanza kuinywa huku akitamani sana kumtia Evans mikononi mwake, kwani ana amani endapo ata mbana Evans basi ata pata ukweli ju ya bikra ya mpenzi wake Julieth.
“Mkuu nimepata ujumbe kwamba kikosi kipo njiani kuelekea Morogoro na nime tumiwa video ya CCTV Camera iliyo muonyesha Evans katika stendi ya Msamvu Morogoro.”
“Hembu niione”
Jery alizungumza kwa pupa. Mlinzi wake akamkabidhi simu hiyo na kuanza kuitazama video hiyo inayo muonyesha Evans akishuka kwenye gari pamoja na abiria wengine.
“Jamaa mwenyewe kumbe ni mbaya hivi”
Jery alizungumza kwa kejeli.
“Ndio mkuu”
“Umesema ume tuma kundi la vijana wangapi?”
“Ishirini mkuu”
“Waambie wasimuue nahitaji kuonana naye uso kwa uso. Endapo ata kiri kwamba Julieth ni mpenzi wake basi haki ya Mungu nita muua”
“Usijali mkuu, wameniambia ndani ya dakika ishirini wata kuwa wamefika hoteli ambayo amefikizia Evans”
“Sawa”
Gari mbili aina ya Toyota VOXY zenye rangi nyeusi zinazo endeshwa na madereva wenye umahiri mkubwa sana mithili na mr transpoter. Zina zidi kuongezwa mwendo huku vijana wenye siha za moto wakitazama picha za watu wawili wanao kwenda kuwafwata mkoani Morogoro. Picha ya kwanza ni ya Evans huku picha ya pili ikiwa ni picha ya mpelelezi kutoka kiyengo cha NSA.
“Nisikilizeni, kwa umakini”
Kiongozi wa kikundi hicho alizunugmza wa kutumia kinasa sauti chake mkononi ambacho kina wafanya waweza kusikilizana viziuri.
“Mission yetu ni kumkamata Evans. Ila huyo wa pili sio jukumu letu, hivyo endapo ata ingia kwenye mpango wetu basi tuhakiksihe tuna muangamiza. Mume nielewa?”
“Ndio mkuu”
Kutokana na kuto kuwa na magari mengi njiani, ika wawezesha kufika Morogo katika muda mfupi sana. Moja kwa moja wakaeleka katika hoteli aliyopo Evans.
Ujumbe mfupi ulio imgia katika simu ya mpelelezi anaye mfwatilia Evans uka mstua sana. Ujumbe huo ulio tumwa kutoka makao makuu ya kitengo chake cha NSA ambacho wataalamu wake wamefanikiwa ku-hack kamera za hotelini hapo, waliweza kumfahamisha kwamba kuna gari mbili zime fika hotelini na ikamfanya aanze kuwa makini kuhakikisha kwamba ana mlinda Evans kwa garama yoyoe ile.
“Kaa nyuma yangu sawa”
Mpelelezi huyo alizungumza huku wakiendelea kutembea kwenye kordo hiyo. Lifti ina onyesha kwamba ina kuja gorofa ya juu jambo lililo mfanya mpelelezi huyo kujiongeza na kwa haraka wakaanza kushuka kwenye ngazi za gorofa hilo huku akiendelea kuwa makini sana.
“Ni kitu gani kinach……..”
Kabla hata Evans hajamalizia sentensi yake. Gafla risasi ikapiga katika ukuta wa pembeni yao na kumfanya mpelelezi huyo naye kuanza kujibu mashambulizi kwa mtu huyo aliye mfyatulia risasi.
***
Magreth usiku kucha hakupata usingizi. Kila muda mapigo yake ya moyo yana mstuka hadi ikafikia kipindi akajishisi moyo huo una weza kuchomoka muda wowote. Magreth akakumbuka namba ya rafiki yake ambaye alikuwa ana Sali naye katika kanisa la nabii Sanga. Akampigia na kwa bahati nzuri simu yake ikapokelewa.
“Josephine samahani rafiki yangu kwa kukusumbua usiku huu”
“Bila samahani. Vipi kwema Mage”
“Sio kwema rafiki yangu”
“Kuna tatizo gani?”
“Nina kuomba unisaidie kuomba ili kufahamu ni wapi mume wangu alipo”
“Mume wako? Mbona huja wahi kuniambia kama una mume Mage?”
“Ni stori ndefu sana ila nina kuomba unisaidie rafiki yangu katika hilo”
“Sawa mume wako ana itwa nani?”
“Evans Shika”
“Sawa acha nianze kuomba nita kupa majibu”
“Nashukuru sana Josephine”
“Mungu atuongoze katika hili”
“Amen”
Magreth akakata simu na kukaa kitandani kwake huku akisubiria majibu kutoka kwa binti huyo ambaye ana kipawa cha kuomba mbele za Mungu na kuonyeshwa ni mambo gani ambayo yana weza kumpata mtu katika muda fulani au kutambua ni sehmu gani alipo. Baada ya dakika kumi na tano simu ya Magreth ikaanza kuita na kwa haraka akaipokea kwa maana simu hiyo ina toka kwa Josephine.
“Mmm rafiki yangu mbona mume wako yupo kwenye matatizo makubwa”
“Ohoo Mungu wangu matatizo gani?”
“Kuna watu kama ishirini hivi wenye bunduki mikononi mwao wana mshambulia yeye na kama mmoja ambaye sija pewa jina lake na Mungu, ila kaka huyo ana onekana ndio ana msaidia Evans”
“Wapo wapi?”
“Morogoro”
“Samahani sana rafiki yangu nina weza kukupitia kwako usiku huu tuka enda pamoja”
“Mmmm tukaenda kufanya nini?”
“Tukamsaidie mume wangu”
Josephine akaka kimya huku akitafakari juu ya ombi hilo alilo pewa na rafiki yake kipenzi.
“Sawa nipitie si una gari?”
“Ndio ninalo”
“Sawa nipitie”
Magreth kwa haraka akakata simu, akajianda kwa haraka na kutoka nje. Akawasha gari lake na kuondoka nyumbani kwake. Kutokana rafiki yake huyo ana ishi hapo hapo Kigamboni, ikawa ni rahisi kwa yeye kumfikia. Josephine akaingia kwenye gari na wakaianza safari ya kuelekea mkoani Morogoro huku mara kwa mara Josephine ana omba ili kufahamu ni kitu gani kinacho endelea eneo hilo la tukio.
***
“Wametokea wapi hawa?”
Mzee Mbogo alizungumza huku akitazama tv kubwa iliyopo katika chumba cha mawasiliano ikionyesha jinsi watu hao walio funika nyuso zake wanavyo shambuliana kwa na mplelezi wake anaye mlinda Evans.
“Hatufahamu mkuu kwa maana hatuwezi kuwatambua kutokana na sura zao zime funikwa”
Mzee Mkumbo aka ichekecha akili yake kwa haraka na jina la nabii Sanga likamjia kichwani mwake. Akaondoka ndani ya chumba hicho na kuingia ofisini kwake. Akahakikisha kwamba hakuna mtu yoyote anaye weza kusikia mazungumzo yake hayo, akampigia simu nabii Sanga. Simu yake ikaita kwa sekunde kadha kisha ikapokelewa.
“Ndugu yangu vipi?”
“Sanga niambie hawa vijana ni wewe ulio watuma kumuangamiza Evans?”
“Vijana gani?”
“Kuna watu wanao mvamia Evans muda huu ninavyo zungumza. Sasa niambie ukweli ni wewe ulio waagiza au?”
“Hapana ndugu yangu siwezi kufanya hivyo japo nilizungumza kwa hasira kauli kama hiyo mbele yako ila ukweli ni kwamba sijafanya mpango wowote na wala sijui ni kitu gani kinacho endelea”
Mazungumzo ya nabii Sanga kidogo yaka mfanya mzee Mbogo kuamini.
“Una nihakikishia kwamba sio vijana wako?”
“Haki ya Mungu sio vijana wangu”
“Wakiwa ni vijana wako nini nifanye?”
“Nifanye kitu chochote rafiki yangu. Yaani hata sielewi ni kitu gani kinacho endelea”
“Sawa nimekulewa”
Mzee Mbogo akakata simu yake huku akiwa amejawa na hasira sana. Akatoka ofisini hapo na kurudi katika chumba hicho kikubwa cha mawasiliano.
“Ame waangusha wangapi?”
“Wanne mkuu”
“Kuna dalili yoyote ya askari kufika eneo la tukio?”
“Hapana mkuu”
“Niunganishe na RPC wa Morogoro”
“Sawa mkuu”
Baada ya dakika moja RPC wa Morogoro akapokea simu hiyo kutoka kwa mzee Mbogo.
“Unazungumza na Martin Mbogo mkuu wa kitengo cha NSA. Kuna kijana wangu ame uzungukwa na wavamizi katika hoteli ya HIGH CLASS hapo mjini”
“Nimekuelewa mkuu, nina agiza vijana wangu kuelekea huko sasa hivi”
“Wahakikishe wana kamata japo mmojawao akiwa hai”
“Nimekuelewa mkuu”
Mzee Mgogo akakata simu hiyo huku akizidi kumuangalia kijana wake jinsi anavyo jitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ana yaokoa maisha ya Evans kama alivyo agizwa na mku wake wa kazi.
***
“Vipi mume wangu ni nani?”
Mrs Sanga alimuuliza mume wake huku akiwasha taa kwa kutumia swichi iliyopo pembezoni mwa kitanda chao.
“Ni Mbogo amenipigia ana dai kwamba kuna watu wana mvamia Evans hivyo wana hisi kwamba mimi ndio nime waagiza.”
“Mungu wangu, kama kitengo cha NSA wame tambua hilo si itakuwa ni matatizo”
Nabii Sanga akamtazama mke wake kwa macho ya mshangao.
“Mimi sija mtuma mtu yoyote mume wangu”
Mrs Sanga alijishuku.
“Kwani nime kuuliza?”
“Ila Julieth alidhamiria kumuua Evans. Mungu wangu sijui ni yeye ndio aliye waagiza”
Mrs Sanga alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Kwahiyo una taka kuniambia kwamba Julieth ndio aliye waagiza hao watu?”
“Sina uha kika ila twende tuka muulize”
“Akaghaa!!”
Nabii Sanga alishuka kitandani huku akiwa amegadhibika. Akavaa suruali yake huku mke wake akijifunga tenge. Wakatoka ndani kwao na moja kwa moja wakaelekea chumbani kwa Julieth. Wakagonga mlango kwa muda huku wakimuita jina lake. Julieth akafungua mlango huku akipiga miyao itokanano na uchovu wa usingizi.
“Vipi kuna tatizo?”
Julieth aliuliza huku akiwatazama wazazi wake hao walio simama hapo mlangoni.
“Ndio kuna tatizo, tuingie ndani tuzungumze”
Nabii Sanga alizungumza huku akitangulia kuingia ndani humo. Julieth na mama yake wakafwata kwa nyuma na wakaka kitandani.
“Julieth kwa nini una hitaji kumua Evans?”
“Baba maswala ya Evans usiku wote huu yana fwata nini bwana?”
“Tafadhali Julieth nijibu sipo kwenye wakati wa masihara?”
“Nitaka kumua kwa sababu yeye amenitoa usichana wangu ambao nilikuwa nina utunza kwa ajili ya mume wangu. Mbaya zaidi yeye ametembea na Magreth ambaye wewe pia ume tembea naye. Hapo una hisi nita muacha hai ili aje kunivunjia ndoa yangu na Jery kwa kuleta vipingamizi kanisani”
Nabii Sanga akashusha pumzi huku akiwa amejawa na hasira.
“Hivi unajua unacho kifanya kina weza kukupeleka jela kwa maana sio siri tena”
“Sio siri ikiwa nime waeleza nyinyi wazazi wangu au muta nisaliti kwa kwenda kuni staki polisi kwamba nina mpango wa kumua Evans?”
“Sio hivyo mwanangu. Ila kitengo cha NSA kime fahamu kwamba Evans ana pangwa kuuwawa”
Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akimtazama Julieth usoni mwake.
“Julieth sina muda mwingi wa kupoteza katika hili. Chukua simu yako hapo, wapigie hao majambazi wako wanao mvamia Evans sasa hivi, waambie wasitishe mpango wa kumuua Evans la sivyo utasababisha NSA kuja hapa na kunikamata mimi kwa kauli yangu tu ya mashaka niliyo zungumza mbele ya mbosi wao kwamba nita muua Evans kwa mikono yangu mimi mwenyewe”
Julieth akastuka sana kwa maana ni kweli ana mpango wa kumuua Evans ila haja mtuma muuaji wa aina yoyote na wala hamjui mtu yoyote ambaye ana weza kufanya kazi ya mauaji.
“Mimi mbona sija muagiza mtu yoyote kwenda kumvamia Evans”
“Nini?”
“Haki ya Mungu vile baba nina kuambia ukweli, sijamuagiza mtu yoote kwenda kumvamia Evans, japo nina mchukia na nina mpango wa kumua, ila sija fanya hatua yoyote ile.”
“Mmmm sasa ni nani ambaye ata kuwa ametekeleza jambo hilo?”
Nabii Sanga alizungunza huku akiwa amejawa na mashaka mengi sana.
“Ila mume wangu hawawezi kukutia hatiani kwa maana huja lifanya hilo jambo wewe usiwaze sana”
Nabii Sanga alizungumza huku akimpapasa papasa nabii Sanga mgongoni mwake.
“Julieth kweli huja fanya hivyo mwanangu?”
“Baba nime apia kwa jina la Mungu, sija fanya kitu kama hicho.”
“Haya usiku mwema”
Nabii Sanga akanyanyuka kwa unyonge na kutoka chumbani hapo, huku mke wake akimfwata kwa nyuma.
***
“Una weza kutumia bastola?”
Mpelelezi huyo alimuuliza Evans ambaye mwili mzima una mtetemeka kwa woga.
“Si…si…si…wezi”
Evans alizungumza huku akihisi haja ndogo ikianza kumwagika taratibu. Mpelelezi huyo hakuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuhakikisha ana pambana na wavamizi hawa wanao endelea kuzivurumisha risasi katika chumba cha jiko walicho jificha Evans na mpelelezi huyo. Jambo la kumshukuru Mungu mlango wa kuingilia katika chumba hicho ni mlango wa chumba na kwa ndani wame weka vitu vizito ambayo hata wavamizi hawa wakijaribu kuvamia hawawezi kuingia ndani ya chumba hicho. Kila mtu aliyomo ndani ya hoteli hiyo alijificha sehemu anayo ijua yeye mwenyewe kwa maana hakuna anaye hitaji kufa. Wavamizi wanne walio baki nje ya hoteli hiyo walipo ziona gari za polisi zikija eneo hilo, hawakuhitaji kupewa amri kutoka kwa mkuu wao na kitu walicho kifanya ni kuhakikisha wana wazuia askari hao kadri wanavyo weza.
“Bro una itwa nani?”
Evans alimuuliza mpelelezi huyo huku akimtazama usoni mwake.
“Dogo una muda wa kuulizana jina langu”
Evans ikambidi kutulia kwa maana hajibiwa hivyo kuna tosha. Evans akachukua meza ya chumba iliyopo jikoni hapo na kupanda juu.
“Una fanya nini?”
“Katika hizo gorofa ni lazima kuna njia za juu zinazo tumiwa kupitishia hewa tuna weza kupita”
Evans alizungumza huku akiangaza angaza sehemu ambayo ima kimfuniko cha wavu ambacho kime fungwa kwa kutumia nati hivyo sio rahisi kwa wao kuweza kupitia kirahisi.
“Nyinyo mbona muna shambulia nje”
Mkuu wa kikundi hicho alizungumza kwa kutumia kinasa sauti chake.
“Mkuu kuna kundi kubwa la askari wame fika hapa, imetulazimu kuwazuia”
“Hakikisheni kwamba hakuna askari anaye ingia humu ndani. Sawa”
“Sawa mkuu”
“Ikiwezekana tumieni mabomu au kitu chochote ili mradi moango wetu uende kama tulivyo panga’
“Nime kupata”
Mkuu wa kikundi hicho akaendelea kuwahimiza vijana wake kujitahidi kuhakikisha wana uvunja mlango huo wa chumba. Mmoja wa wavamizi hao, akafungua nyuma ya gari moja wapo walilo kuja nalo, akachukua bomu aina ya RPG, akaoiga goti moja chini huku bomu hilo akiwa ameliweka begani mwake. Akailenga moja ya gari la polisi linalo wasili hapo na kulifyatua.
“RPG……..”
Dereva wa askair wa gari hilo alipiga kelele huku akifungua mlango wa gari hilo na kujirusha, kila askari alijirusha upande wake na ndani ya sekunde chake bomu hilo kika lichangua changua gari polisi hilo na kuwajeruhi baadhi ya askari walio kuwa karibu na gari hilo.
***
Mlango wa chumba cha raisi Chinas Mtenzi ukagongwa na mlinzi wake namba moja. Raisi Mtenzi akafungua huku akiwa amevalia nguo zake za kulalia.
“Samahani muheshimiwa raisi kuna tatizo lime tokea mkoni Morogoro.”
“Tatizo gani?”
“Kuna majambazi wame vamia katika moja ya hoteli na wamewashambulia askari hivyo muheshimiw auna hitajika katika chumba mawasiliano”
Raisi Mtenzi akashusha pumzi, akaingia chumbani kwake, akachukua koti lake na kuvaa kisha akaongozana na mlinzi wake hadi katika chumba hicho kikubwa cha mawasiliano kilichopo chini ya ikulu hiyo na ndani ya chumba hicho watendaji wote wa kazini ni watu walio jaliwa ufahamu mkubwa wa akili(IQ) hivyo ina kuwa ni rahisi kwa wao kuju kila jambo linalo endelea ndani na nje ya nchi ikiwemo ulinzi wa mikaka ya nchi kwa kutumia satelaiti.
“Muheshimiwa raisi”
Mmoja wa fanyakazi alizungumza na kuwafanya wafanyakazi wote wapatao hamsini kusimama.
“Kaaeni, kuna kitu gani kinacho endelea?”
“Muheshimiwa hizi ni baadhi ya video zilizo rekodiwa na satelati zetu zina onyesha jinsi wavamizi walivyo tumia silaha ya RPG kuwavamia askari”
“Kuna askari yoyote aliye fariki?”
“Bado hajujafahamu muheshimiwa ila tuna amini kwamba kuna walio jeruhiwa vibaya sana kwa maana walivyo shambuliwa gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi sana”
“Jambazi wa Kitanzania kumiliki RPG sio jambo la kawaida.”
“Ndio muheshimiwa raisi ila tuna hisi kuna kitu ambacho kina endelea hapa”
“Hembu wavuteni sura zao karibu”
Sura ya mmoja wa majambazi walipo nje ya hoteli ikavutwa karibu kabisa ila kitu ambacho ni kigumu ni kuweza kuona sura kamili kwa maana nyoso zao zime funikwa.
“Niunganishe na mkuu wa NSA”
“Sawa muheshimiwa raisi.”
Raisi Mtenzi akashuhudia jinsi askari wake wakiangushwa kwa risasi.
“Muheshimiwa, Mbogo yupo kwenye laini namba moja”
Raisi Mtenzi akanyanyua mkonga wa simu na kuweka sikioni mwake.
“Muheshimiwa raisi”
“Hivi una ona hichi ninacho kiona hapa mimi au?”
“Ndio muheshimiwa raisi ila tuna endelea kuhakikisha majambazi hao wana dhibitiwa haraka iwezekanavyo”
“Unafahamu chanzo cha uvamizi wao?”
“Ndio muheshimiwa”
“Ni kitu gani?”
“Kuna mpelelezi wangu mmoja nilimpatia jukumu la kuhakikisha ana mfwatilia kijana mmoja ambaye ana itwa Evans. Hivyo hao majambazi tuna imani kwamba wame agizwa kumuangamiza kujana huyo”
“Kijana huyo ni nani?”
“Ehee?”
“Kijana huyo ni nani?”
“Ni mpenzi wa Julieth Sanga. Mtoto wa nabii Sanga”
Raisi Mtenzi akasstuka sana kwa maana binti huyo ni mkwe wake mtarajiwa.
“Una uhakika na hicho unacho kizungumza?”
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Nitumieni picha ya huyo kijana nimuone”
“Sawa muheshimiwa”
Hazikuisha hata sekunde ishirini, picha ya Evans ikaonekana katika tv kubwa ambayo ipo katika chumba hicho. Baadhi ya wafanyakazi wakajikuta wakimtazama muheshimiwa raisi kwa maana hawajui ni kwa nini picha ya kijana huyo ime tumwa kwa wakati huo.
“Toeni hiyo picha. Niunganishe na RPC wa Morogoro”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Raisi mtenzi akajikuta akijawa na hasira sana moyoni mwake kwa maana katika vitu ambavyo havipendi kwenye maisha yake ni kudanganywa. Kitendo cha Evans kuwekewa ulinzi ambao una sababisha askari wasio na hatia kujeruhiwa vibaya ina zidi kumuumiza roho.
“Muheshimiwa raisi RPC yupo kwenye mtandao”
Raisi Mtenzi akauweka mkonga wa simu sikioni mwake.
“Habari za usiku muheshimiwa raisi”
“Sio salama, nipe ripoti ni hali gani ambayo ina endelea huko Morogoro?”
“Vijana wanne wamejeruhiwa vibaya na mashambulizi bado yana endelea muheshimiwa”
“Waambie vijana wako wote warudi nyuma”
Kauli hiyo ika washangaza hadi baadhi ya watu waliomo ndani ya chumba hicho.”
“Samahani muheshimiwa ume sema?”
“Nimesemaa warudishe vijana wote nyuma na ikiwezekana waondoke eneo hilo la tukio”
“Sawa muheshimiwa”
Kutokana ni amri ikamlazimu RPC kufwata agizo hilo. Raisi akampigia simu mkuu wa NSA mzee Mbogo.
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Huyo kijana wako muambie amsalimishe huko kijana kwa hao watu”
“Nini?”
“Ni amri na sio majadiliano”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Raisi Mtenza akaurudisha mkonga huo wa simu sehemu alipo utoa na kuanza kutoka ndani hapo.
“Samahani muheshimiwa raisi mbona ume fanya maamuzi hayo?”
Mshauri wa maswala ya ulinzi alimuuliza raisi Mtenzi ambaye ana onekana kugadhibika sana.
“Hatuwezi kupoteza maisha ya vijana wangu kisa kijana mmoja ambaye hana impact yoyote kwenye hii nchi.”
“Samahani muheshimiwa raisi. Ila kijana huyo ni Mtanzania na ana haki ya kulindwa kama Watanzania wengine”
“Mark nime make my final decision. Good night”
Baada ya raisi mtenzi kuzungumza hivyo akaondoka ndani hapo na kuwaacha watu wote wakiwa hoi kwani walicho kitarajia sio hicho walicho kiona kutoka kwa raisi Mtenzi.
Mlinzi wa karibu wa Jery akaingia ndani kwa Jery ambaye ana subiria kupata ripoti ya hali halisi inavyo endelea mkoni Morogoro.
“Jery mambo yame haribika”
“Kwa nini?”
“Mzee amefahamu juu ya vijana wetu walipo kule Morogoro”
Jery akastuka sana na mapigo yake ya moyo yakaanza kubadilika na kumuenda kasi tofauti na mfumo wa kawaida. Katika siku zake zote za maisha ya kuishi na baba yake ana fahamu jinsi baba yake alivyo kuwa mtu wa maamuzi magumu sana kwani ana fahamu jinsi baba yake alivyo toa amri kwa kaka yake wa kwanza kuuwawa kutokana na shuhuli zake za ujambazi.
“Ohoo Mungu tuta fanya nini?”
“Usi panic mkuu. Tusubiri tuoe na wala usionyeshe dalili yoyote ya kuhusika na tukio hilo”
Gafla mlango wa chumba hicho uka gongwa na kuwafanya wastuke sana. Raisi Mtenzi akaingia ndani humo na kumfanya Jery azidi kujawa na mshangao ulio changa nyikanana woga. Macho makali aliyo tazamwa nayo mlinzi huyo yakamfanya atoke nje pasipo kuambiwa chochote.
“Jery ume kosa wasichana hadi una kwenda kujichanganya na wanawake ambao wana tembea na watu hata wasio julikana”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka sana huku akiwa amevimbiana kwa hasira.
“Ba..ba….ba…mbona sielewi?”
“Huyo Julieth wako ni mtu wa kutembea na kijijaa ambacho hakaeleweki mbele ni wapi na nyuma ni wapi na wewe una taka uka jichanganye humo humo?”
“Ba…ba….ba….Ju…liee..t ni birka”
“Ahaa ndivyo alivyo kudanganya? Sasa ni hivi asubihi nina hitaji ukamlete huyo binti asubuhi. Atapimwa na madaktari wa hapa ikulu. Akionekana ana bikra utamuoa ila akionekana hana bikra basi sahau kumuona na uhusiano wetu na ile familia utakuwa umekufa”
Raisi Mtenzi mara baada ya kuzungumza hiyvo akatoka chumbani hapo humo na kuubamiza mlango huo kwa nguvu na kumuacha Jery katika njia panda asijue afanye nini.
***
Evans kwa haraka akachukua kisu kikubwa ila chenye ncha ambayo ana amini kwamba ana weza kufungua nati za kijimlango hicho cha nyavu ambacho kina pita katika bomba moja kubwa ambalo lina muwezesha mtu kupita akiwa ana tambaa mithili ya mtoto mdogo.
“Una hisi kwamba kisu kita fungua?”
“Ndio kaka wewe subiri”
Simu ya mpelelezi huyo ikaanza kuita, akaitoa mfukoni mwake na kuitazama kwa sekunde kadhaa na kukuta ni namba ya mkuu wake mzee Mbogo.
“Ndio muheshimiwa”
“Bony mupo wapi?”
“Bado tupo ndani ya hoteli mkuu tuna tafuta njia ya kujiokoa kwa maana hawa watu ni wengi sana na hapa nilipo risasi zina karibia kuniishia”
“Kama upo na huyo kijana mkabidhishe kwa hao majambazi”
“NINI!!!?”
“Kama ulivyo nisikia hiyo ni amri kutoka moja kwa moja kwa raisi hivyo fwata amri ya muheshimiwa”
Simu hiyo ikakatwa na kumfanya Bony kushusha pumzi taratibu kwani kazi yake siku zote ni ya kufwata amri kwa wale walio mpita cheo na mamlaka.
“Sawa mkuu nime kuelewa”
Bony akakata simu huku akimtazama Evans. Bony akatazama ndani ya chumba hichi cha jiko, akachukua fagia lenye mti mrefu, akachukua moja ya nguo nyeupe inayo tumiwa na wapishi. Akaiweka nguo hiyo mbele ya mti huo kisha akaanza kusogeza kabati zito kililopo hapo mlangoni.
“Una fanya nini kaka?”
Evans aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Bony hakumjibu chochote zaidi ya kuufungua mlango huo taratibu, akautoa mti huo ambao mbele ume tanguliza nguo hiyo nyeupe. Kwa watu waelewa huwa wana tambua kwamba ishara hiyo ina ashiria amani au muhusika ame amua kujisalimisha. Wavamizili walio agizwa na Jery waliweza kuielewa ishara hiyo na wote wakaacha kuushambulia mlango huo. Bony akaitoa bastola yake ikiwa ni ishara ya kuonyesha kwamba haitaji kuendelea na mapambano hayo.
“Fungua mlango”
Bony akatii amri hiyo na kuufungua mlango wote
“Munyae muhitaji sio mimi si yule?”
Bony alizungumza huku mikono yake ikiwa juu. Wakatazamana huku wote wakiwa hawaamini kwamba mtu huyo amejisalimihsa. Evans mwili mzima ukazidi kumtetemeka, hakutarajia kama ana weza kuachwa peke yake na kukabidhiwa kwa watu hao wana iwinda roho yake. Mmoja wa vavamizi akampiga Bony kisogoni kwa kutumia kitako cha bunduki na kumfanya apoteze fahamu hapo hapo. Evans akajaribu kupambana na vijana hao ila hakuweza kabisa kwa maana wame mzidi kwa wingi na pia hata kwa mafunzo ya kupigana wamemshinda. Ndani ya dakika moja wakamzimisha Evans na hakuweza kuelewa ni kitu gani kinacho endelea.
“Mkuu polisi wana ondoka”
Kijana mmoja aliyopo nje alitoa ripoti hiyo.
“Kwa nini?”
“Hatufahamu mkuu”
“Isije ikwa ni mtego”
“Hatufahamu mkuu”
“Hakikisheni tuna ondoka na miili yote ya wezetu kufupa ushahidi”
“Sawa mkuu”
Kazi ya kuikusanya miili ya wezao walio fariki ikaanza walipo hakikisha wame ipata kazi hiyo, wakatoka ndani hapo huku wakiwa ameubeba pia na mwili wa Evans. Wakaingia kwenye gari zao na kuanza kuondoka hotelini hapo.
***
Magreth na Josephine wakafika hotelini na kuhuhudia moja ya gari la likiteketewa kwa moto huku gari nyingine za polisi zikianza kurudi nyuma na kuondoka eneo hilo.
“Evans wako yupo hapa”
“Wale si majambazi?”
“Ndio ni majambazi”
“Sasa tuta fanya nini?”
“Tusishuke kwenye gari kwa maana kama askari wenyewe wameshindwa na kuondoka basi tuangalie ni kitu gani kitatokea”
Josephine alizungumza huku wakiendelea kuwaangalia majambazi hao jinsi walivyo imarisha ulinzi nje ya hoteli hiyo. Hazikuisha hata dakika tano wakatoka watu walio bebe miili ya watu ambao wame valia kama wao.
“Evans yule pale”
Magreth alizungumza mara baada ya kumuona Evans akiwa ame bebwa begani na mmoja wa watu.
“Tulia una shuka una taka kwenda wapi?”
“Kumuokoa mume wangu”
“Acha ujinga Mage wewe, uta uwawa”
“Hapana nina jua nini cha kufanya”
“Hapana”
Josephine alimzuia Magreth hadi gari hizo zikaanza kuondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi. Magreth akageuza gari lake kwa kasi na kuanza kuwafwatilia watu hao. Gari hizo hizo zikashika njia ya kuelekea jijini Dar es Salaam. Magreth naya hakutaka kuwapa nafasi ya kuwaacha kwa umbali mrefu kwa maana hiyo ndio nafasi ya pekee kwa yeye kumpata Evans.
“Mkuu kuna gari nyuma yetu ina tufwata kwa kasi sana”
Mmoja wa kijana alizungumza huku akitazama jinsi gari ya Magreth inavyo kuja kwa mwendo wa kasi sana.
“Hatuelekei Dar tukifika Mikese tuelekee huko hii gari inayo tufwatilia tuta malizana nayo huko huko”
“Sawa mkuu”
Gari zikazidi kuongeza mwendo.
“Wanaongeza mwendo”
Josephine alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.
“Hamia siti ya nyuma”
“Mmm”
“Hamia siti ya nyuma”
“Ehehee”
“Hamia siti ya nyuma”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akizidi kuzifukuzia gari hizo kwa mwendo wa kasi sana. Josephine akahamia siti ya nyuma na kufunga mkanda.
“Un ampango gani Mage?”
“Wewe tulia”
Gafla gari hizo zikaachaa barabara ya lami na kukunja kulia na kushika barabara ya vumbi. Magreth naye akapungza mwendo na kukunja katika marabara hiyo huku akisoma kibao cha pembeni kilicho andikwa Mikese.
“Magreth wana kwenda wapi kule”
“Sijui ila tuta wafwata hadi mwisho wao”
“Huogopi?”
“Mbele ya mume wangu siwezi kuogopa jambo la aina yoyote”
Magreth alizungumza huku akikunja kona moja kali hadi gari lika karibia kuacha njia ila, ila akajitahidi kadri ya uwezowake na kuliweka sawa na kuendelea na kuwakimbiza majambazi hao.
***
Mlio wa simu uka mstua Julieth ambaye bado ana hangaika kuutafuta usingizi. Akaichukua simu yake na kukuta ni namba ya Jery. Akatazama saa yake simu hiyo ina onyesha muda huu ni saa tisa kasoro usiku. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Baby vipi?”
“Sio kwema, baba ametambua juu ya mahusiano yako na sijui Evans na hapa ninapo kuambia ameniaeleza kwamba kesho asubuhi nije kukuchukua na tunakupeleka kwa daktari ili akupime kama wewe ni bikra au sio bikra”
Moyo wa Julieth bado nusu tu usimame kwa mstuko. Katika maisha yake hakuna habari ya mstuko aliyo ipokea kama hiyo.
“Julieth”
“Mmmm”
“Hivyo jiandae kesho asubuhi nina kuja hapo. Sawa”
“Sawa baby”
Jery akakata simu na kumfanya Julieth akae kimya kama dakika kumi hivi akitafakari ni kitu gani ambacho ana weza kukifanya ili kufanikiwa katika mtihani huo. Akanyuka kwa haraka na moja kwa moja akaelekea katika chumba cha wazazi wake. Akagonga kwa muda kisha mlango ukafunguliwa na nabii Sanga.
“Julieth kuna nini?”
“Baba nina hitaji kuzungumza na mama”
“Kuna tatizo”
“Wewe nina omba kuzungumza na mama”
Mrs Sanga akasimama mlangoni hapo, akamtazama Julieth kwa sekunde kadha ana akatambua kuna jambo ambalo lina msumbua mwanaye huyo. Wakatoka ndani hapo na kuelekea chumbani kwa Julieth.
“Kuna nini mwanangu””
“Jery amenipia na kuniambai kwamba baba yake ame tammbua kuwa nina mahusiano na Evans”
“What….imekuwjae?”
“Sifahamu mama ila jambo baya zaidi ni kwamba baba yake ana hitaji kunipima bikra na kesho asubuhi hapa Jert ana kuja kunichukua kuelekea Ikulu”
“Mungu wangu sasa tuta fanya nini ikiwa sio bikra wewe kwa sasa?”
“Ndio hivyo mama nina ogopa”
“Aha…nimekumbuka ngoja nina kuja”
Mrs Sanga akatoka chumbani hapo, akaelekea chumbani kwake na baada ya muda akarudi akiwa ameshika simu yake mkononi. Akamtafuta mmoja wa madaktari wa kichina ambao kazi yao kubwa ni kutengeneza bikra za bandia kwa wasichana. Simu ya daktari huyo ikaanza kuita kisha ikapokelewa.
“Dokta Jing”
“Habari mrs Sanga”
“Salama na samahani sana kwa kukupigia muda huu”
“Bila ya samahani”
“Nina shida je nina weza kukuona usiku huu”
“Sawa nipo hospitalini kwangu una weza kuja”
“Nashukuru”
Mrs Sanga akakata simu na kumueleza Julieth ajiandae kwa safari hiyo. Akaelekea chumbani kwake na kumueleza mume wake hali halisi.
“Tuna kwenda wote”
Nabik Sanga alizungumza na wote kwa pamoja wakajiandaa na kuianza safari ya kuelekea hospitalini kwa dokta Jing. Wakafika hospitalini hapo na moja kwa moja wakaelekea ofisini kwa daktari huyo.
“Karibuni sana”
“Tuna shukuru. Tuna shida, binti yangu hapa ame tolewa usichana wake. Mwanaume aliye hitaji kumuoa ana hitaji amkute akiwa na bikra. Je hapo uta weza kutusaidia?”
“Kuwasaidia mrs Sanga ina wezekana. Binti ume wahi kufanya tendo la ndoa mara ngapi?”
Julieth akamtazama mama yake na baba yake.
“Zungumza una toa toa nini macho”
Nabii Sanga alizungumza kwa ukali huku akimtazama mwanaye huyo.
“Mara sita”
“Ni mwanaume mmoja au tofauti?”
“Mwanaume mmoja tu”
“Sawa hiyo kazi ina weza kufanyika usiku huu”
“Itachukua muda gani dokta?”
“Mmm lisa amoja na nusu kumuingizia katitika chumba cha upasuaji. Nina imani mupo tayari kwa hili”
“Ndio dokta tupo yari, Garama zake ni kiasi gani?”
“Dola mia sita”
“Sawa hakuna shaka dokta”
Julieth akaingizwa kwenye chumba cha upasuaji na daktari Jing akishirikiana na manesi wake wawili wakichina wakaianza kasi hiyo ambayo wana taaluma nayo kubwa sana na niidadi kubwa sana ya wanawake waliomo ndani ya ndo nyingi kabla ya kuolewa na wanaume wanao wapenda walijikuta wakiwekewa bikra hizo feki ambazo ni ngumu sana kwa mwanaume kuweza kufahamu kwamba bikra hizo ni feki.
***
“Hawa ni lazima niwapate”
Magreth alizungumza huku akizidi kukanyaga mafuta. Uzuri wa gari lake ni imara na lina uwezo mkubwa wa kukimbia.
“Washambulieni”
“Sawa mkuu”
Vijana wawili walio panda gari la nyuma wakajitokeza kwenye madirisha ya gari hilo na kuanza kuwashambulia kina Magreth. Jambo jengine la kumshukuru Mungu ni kwamba gari la Magreth haliingii risasi hivyo ime kuwa ni ngumu sana kuwadhuru. Josephine akajikuta akianza kulia kwa uchungu sana huku akimuomba Mungu kwa maana hajui kama wana weza kutoka salama kwenye mapambano hayo.
“Magreth wata tuua hao”
“Tulia Josephine usilie wewe muombe Mungu tu”
Magreth alizungumza huku akizidi kujiamini kuongeza mwendo wa gari lake. Akalifikia kwa ukaribu gari hilo la nyuma ambalo lina vijana wanao mshambulia kwa risasi. Akaanza kuligongwa kwa nguvu huku akiamini kabisa kwamba Evans yupo gari la mbele. Gari hilo likaanza kuyumba, Magreth akaongeza tena mwendo wa gari lake hukua kiwa amejikaza mwili mzika. Akaligonga tena gari hilo na kulisababishia lipoteze muelekeo kabisa na likaanza kubingirika kwenye maporomoko ya kilima kiitwacho Chamanyani. Ikabaki gari moja tu na Magreth hakuhitaji kulipoteza gari hilo wala kuligonga kwa nyuma kwa maana kufanya hivyo kuna weza kukasababisha ajali mbaya sana na ina weza ikapoteza maisha ya mwanaume ampendaye Ethath.
“Walipueni”
“Sawa mkuu”
Kijana mmoja akavunja koo cha nyuma cha gari hilo aina ya Toyota Voxy akaweka begani kwake bomu aina ya RPG. Bila hata ya kujishauri akafyatua bomu hilo, Magret kwa haraka akalikwepesha gari hilo ila kwa bahati mbaya gari ikamzidi nguvu, ikapinduka na kuanza kuserereka kwenye gema lililopo pembeni mwa barabara na safari ya kumuokoa Evans wake ikaishia hapo.
Kelele za maumivu za Josephine zikamfanya Magreth kuufungua mkanda wa siti yake aliyo kalia. Akaufungua mlango wa upande wa abiria kwa maana katika upande wake ndipo gari lilipo angukia.
“Mguu wangu”
Josephine aliendelea kulalama huku maumivu makali ya mguu wake wa kulia ulio vunjika mara mbili, yakiendelea kumtafuna mwili wake. Magreth akaanza juhudi za kumtoa kwa uamkini Josephine na akafanikiwa. Akamlaza pembeni ya barabara huku akiendelea kulia sana
“Mage nina kufa mimi”
Josephine alilalama na kuzidi kumpa wasiwasi Magretha ambaye naye ame chubuma katika mkono wake wa kulia.
“Huwezi kufa rafiki yangu. Vumilia nitafute msaada”
Julieth alizungumza huku akiendelea kuangaza angaza eneo hilo ambalo kwa habahati mbaya halina nyumba hata moja zaidi ya miti mirefu iliyo fungamana na kusababisha msitu mkubwa na kutisha. Magreth akajipapasa mfukoni mwake na kuitoa simu yake. Akajikuya akishusha pumzi kwa maana simu hiyo ime pasuka kioo chake hivyo hawezi kuitumia kwa wakati huo.
“Mage”
Josephine alimuita Magreth kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge. Akamsogelea rafiki huku woga na wasiwasi vikiwa vime mtalawa.
“Tuombe”
Josephine alizungumza huku akimshika Magreth kiganja cha mkono wa kulia. Taratibu Josephine akaanza kusali huku akikishika kwa nguvu kiganja cha mkono huo wa kulia. Baada ya dakika nane akamuachia Magreth na akapoteza fahamu. Magreth akaanza kuangua kilio huku akihisi kuchanganyikiwa kwa maana kama ni Evans ame mpoteza na rafiki yake hapa ana hali mbaya sana na sehemu walipo hakika hamjui mtu wa aina yoyote.
***
Zoezi la kumtempandikiza Julieth bikra ya bandia ikafanikiwa kwa asilimia tisini na tisha. Wakatoka katika chumba hicho huku dokta Jing akiwa na furaha sana.
“Ndio dokta tupe ripoti”
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama daktari huyo.
“Zoezi letu lime kwenda vizuri na nina uhakika kwamba hata akifanyiwa kipimo na kifaa cha aina yoyote basi hakuna anaye weza kugunda kwamba hiyo ni bikra feki”
“Kweli dokta?”
Mrs Sanga alizungumza huku akiwa na furaha sana.
“Ndio mama Sanga”
“Ohoo asante Mungu. Ehee malipo tuna yafanya by casha au kwa njia ya benki?”
“Mmmmm ni nzuri sana mukifanya kwa njia ya benki kwa maana ndio njia salama zaidi ya hii”
“Sawa basi kama huto jali dokta nina omba nipatie akaunti namba yako”
Dokta Jing akaiandika namba hiyo kwenye kikatasi kidogo. Mrs Sanga akahamisha kiasi hicho cha pesa kwa kutumia njia ya simu kisha wakaaga na kuondoka eneo hilo.
“Sasa ukakutane na huyo mjinga wako akuvunje bikra kwa mara ya pili, uta tutambua sisi ni kina nani”
Nabii Sanga alizungumza huku akizidi kuongeza mwendo wa gari hilo kwa maana kama kuna karibia kupambazuka. Wakafika nyumbani na kika mmoja akaelekea chumbani kwake. Julieth akaa kitanda ni huku akiwa na furaha sana, akakumbuka akiwa ndani ya chumba dokta Jing alimueleza kwamba ame mpaka dawa ambayo ita mfanya uke wake kubana na kuwa mtamu sana kwa mwanaume ambaye ata kutana naye katika ndoa yake.
Julieth akachukua kioo kikubwa, akavua nguo zake zote kisha akachukua kioo hicho na kukiweka kwa mbele na kuanza kujichungua, hakika uke wake ume badilika kwa asilimia kubwa sana.
Furaha ikazidi kumtawala na wala hakupata usingizi kwa maana ule wasiwasi ambao alikuwa nao kwa sasa ume kwisha. Majira ya saa kumi na mbili asubuhi gari nne kutoka ikulu, zikafika nyumbani hapo. Jery akiwa ameongozana na walinzi, wakashuka katika gari hizo. Mrs Sanga akawakaribisha kwa maana na yeye hakuweza kupata usingizi kabisa akilifikiria tukio hilo.
“Shikamoo mama”
Jery alisalimia kwa heshima zote.
“Salama mwanangu. Karibu sana”
“Nashukuru sana mama yangu. Nimekuja kumchukau Magreth baba ana hitaji kwenda kukutana naye”
“Ahaa basi acha nika muamshe kwa maana amelala. Au uliwasiliana naye?”
“Hapana mama”
“Basi nisubiri. Vipi nikuandalie kifungua kinywa?”
“Hapana mama nipo vizuri”
“Sawa mwanangu nina kuja”
Mrs Sanga akapandisha gorofani na kuingia chumbani kwa Magreth na kumkuta akiwa ana malizia kuvaa nguo.
“Umemuona Jery?”
“Yaa nime ziona gari zao”
“Sasa nimemuambia kwamba ume lala. Hivyo chelewa chelewa kidogo”
“Sawa mama, ila mbona leo wame kuja na gari nyingi hivi?”
“AHaa….Si wamekuja kumchukua mkwe wa raisi”
“Hahaaa”
Wingi wa walinzi hao, baadhi yao ni walinzi wanao mlinda raisi, ambao jukumu lao walillo pewa na raisi Mtenzi ni kuhakikisha kwamba wana mlinda Jery asiwasiliane na mtu wa aina yoyote hadi pale watakapo rudi na Julieth ikulu. Walinzi hao hawakumruhusu kabisa Jery kupandisha chumbani kwa Julieth. Baada ya dakika kumi na tano, Julieth na mama yake wakashuka kwenye ngazi huku, Julieth akiwa amevalia gauni refu jeupe huku nywele zake akiziweka katika mtindo mzuri na wa kuvutia sana.
Wakaagana na mrs Sanga kisha wakaondoka nyumbani hapo, huku Julieth akipandishwa kwenye gari jengine tofauti na gari alilo panda Jery.
***
Gari la abiria linalo toka katika mji wa Dutumi na kuelekea Morogoro mjini, likawa ndio gari la kwanza kufika eneo walilo pata ajali Magreth na Josephine. Abiria wakashuka huku wakishangaa shangaa jinsi gari hilo lililo pinduka.
“Dada mupo salama?”
Dereva wa gari hilo alizungumza.
“Hapana mwenzangu hapa amevunjika mguu nina waomba mumsaidie”
“Sawa oya Jafari, muingizeni kwenye gari na tumlaze siti ya nyuma”
Dereva huyo alitoa maagizo kwa makonda wawili wa gari hilo. Wakanza kumbeba Josephine na kumlaza siti ya mwisho huku watu walio kuwa wamekaa kwenye siti hizo wakihamia siti za mbele kidogo.
“Kama huto jali naomba mumfikishe katika hospitali kubwa na ninakuomba unipatie naomba uni andike namba zako za simu, ili nikipata msaada wa gari langu kulitoa hapa basi iwe rahisi kwa mimi kuwasiliana nawe”
Magreth alimuambia dereva wa basi hilo dogo la abiria.
“Sawa ila hii gari hapa mbona ina weza kusukumwa na kukaa sawa”
“Kweli?”
“Ndio”
“Hembu naombeni munisaidie”
Wanaume wapatao kumi na tano, wakaanza kujiahidi kulisukuma gari la Magreth lililo pindukwa kwa ubavu wa kulia. Nguvu za wanaume hao zikazaa matunda. Gari la Magreth likaa sawa.
“Hembu jaribu kuliwasha”
Magreth akaingia ndani ya gari lake, akajaribu kuliwasha ila halikuweza kuwaka.
“Hapa tuna fundi wetu hivyo ngoja tukuachie kisha sisi tumuwahishe hospitali huyu mgonjwa”
“Nashukuru sana kaka”
“Usijali”
“Hivi huko mulipo toka hamjaona gari moja aina ya Toyota Voxy?”
“Hapana sijakutana na gari lolote”
“Nashukuru”
Dereva na abiria wake wakaondoka eneo hilo huku wakimuacha fundi wa gari hilo akianza kutafuta ni wapi gari la Magreth lime lete itilafu.
“Ilikuwaje dada hadi mukapinduka?”
“Kuna gari la majambazi nilikuwa nina lifukuzia. Hivyo waliweza kunichezea mchezo mbaya wa kunipindua”
“Majambazi!!?”
“Ndio mbona una shangaa?”
“Mmmm nashangaa kwa maana majambazi ni watu hatari na nina sikia kwamba jana wamevamia hoteli moja pale Morogoro mjini”
“Yaa ndio hao hao nilikuwa nina wafukuzia”
“Mmmm wewe ni askari?”
“Hapana, ila wame mteka mume wangu hivyo nilikuwa katika harakati za kuhakikisha kwamba nina muokoa mume wangu”
“Mmmmm”
Fundi huyo alijikuta akiguna huku akimtazama Magreth kwa macho ya kuiba kwa maana si kwa maelezo hayo ya kujiamini. Baada ya dakika kumi na tano za matengenezo madogo, gari hilo likafanikiwa kuwaka.
“Dada una bahati sana kwa maana taaluma yangu hii ya kutengeneza magari ya aina hii niliipata kwa Mahindi fulani pale Dar”
“Nashukuru sana kaka yangu. Tuelekee mjini nita kupatia zawadi nzuri sana”
“Usijali dada. Mafundi hawa wa gereji bubu, hawawezi kutengeneza hizi gari kwa maana ni garama sana na zina mifumo yao ya uundwaji ni ya kipekee sana, tofauti na hizi Toyota ambazo mifumo yao ina ingiliana ingiliana”
“Ni kweli nashukuru sana”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana. Fundi huyo akaingia kwenye gari, Magreth akaligeuza na kuanza safari ya kueleeka mjini Morogoro huku akipewa maelekezo na fundi huyo ni barabara ipi apite.
***
Kwa mara yake ya kwanza maishani kuingia katika jengo linalo lindwa kupita majengo yote nchini Tanzania. Julieth akaendelea kushangaa shangaa jinsi Ikulu ilivyo pambwa na bustani nzuri za maua huku walinzi wenye bundukiwa wakiwa wamezagaa kila mahali ndani ya ikulu hiyo.
“Jery mzee ana kuita ofisini kwake”
Mlinzi mmoja alizungumza na kumfanya Jery anze kujiuliza maswali mengi sana kichwani kwake. Julieth moja kwa moja akapelekwa anapo ishia raisi na familia yake akisubiria kunza kufanyiwa vipimo. Jery akaingia ofisini kwake na kumkuta raisi Mtenzi akitwa amesimama hukua kitazama dirishani.
“Baba nime rudi”
Raisi Mtenzi akaendelea kukaa kimya kana kwamba hajasikia chocote.
“Baba”
“Jery hivi niki kufunga au nikikupa adhabu kubwa sana nita kuwa nina makosa?”
Mapigo ya moyo ya Jery yakaanza kumuenda kasi sana huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga sana. Raisi Mtenzi akageuka huku akiwa ameshika picha zipatazo kumi. Akaanza kutembea hadi sehemu alipo simama Jery ambaye kujiamini kwake kote kume muisha.
Raisi Mtenzi akamzaba Jery kofi zito hadi akayumba nusura aanguke chini.
“Kuwa mtoto wa raisi si kuwa na mamlaka ya kutumia rasilimali zangu au za nchi hii jinsi unavyo jisikia. Umenielewa?”
“Nd…iooo baba”
Raisi Mtenzi akamkabidhi Jery picha zinazo onyesha maiti za baadhi ya watu alio waagiza kwenda kumteka Evans. Picha hizo zote ni maiti za vijana hao walio pata ajali katika moja ya maporomoko katika mkoa wa Morogoro.
“Kuanzia sasa nime kubadilishia mlinzi na huto ruhusiwa kutoka na kwenda sehemu yoyote nje ya ikulu pasipo idhini yangu. Simu yako pia nime iunganisha tambua kwamba chochote ambacho una zungumza na mtu yoyote, nitakuwa nina kisikia na mimi pia kwenye hii simu yangu. Umenielewa”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa sauti ya chini ila ya kukoroma sana inayo dhihirisha kwamba ame jawa na hasira sana.
“Nimekuelewa baba”
“Huyo mwanamke wako amesha fika?”
“Ndio baba”
“Kamlete hapa ofisini kwangu”
Jery akatoka ofisini hapo huku akishika shika shavu lake kwa maana kofi hilo lime muingia kisawa sawa. Jambo analo jivunia Jery ni kwamba ana pendwa sana na baba yake. Jery akaingia ndani kwao na kumkuta Julieth akizungumza na mama yake.
“Baba ana kuhitaji”
Jery alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Wewe mbona haupo sawa”
Mrs Mtenzi alimuuliza mwanaye huku akimtazama usoni.
“Nipo sawa mama”
“No nina kufahamu niambie una nini?”
“Hapana mama. Julieth twende”
“Mama baadae”
Jery na Julieth wakatoka ndani hapo huku njia nzima wakiwa kimya.
“Mume wangu kuna nini?”
Jery hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kutembea. Wakaingia ofisini kwa raisi Mtenzi na kumkuta akiwa amekaa kwenye kiti chake. Julieth akasalimia kwa heshima zote, raisi Mtenzi hakuitikia salamu hiyo zaidi ya kumpandisha na kumshusha Julieth.
“Baba tumefika”
“Toka ndani hapa”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo, Jery akamtazama Julieth na kuanza kuelekea mlangoni, kabla hajatoka raisi Mtenzi akampa ishara Jery ishara ya kurudisha picha hizo, kisha akatoka ndani hapo. Raisi Mtenzi akampatia Julieth picha hizo na kumfanya astuke kidogo kwa maana zina tisha sana na watu hao wame kufa vifo vibaya sana.
“Hao watu wame kufa kwa ajili yako”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akimtazama Julieth kwa macho makali. Julieth macho yakamtoka huku akiwa hajui ni kwa nini watu hao wame kufa kwa ajili yake.
“Upuuzi wa huyo bwana wako, ameagiza watu wangu waende kumteka huyo mjinga wako Evans na mwishowe wame aishia kwenye vifo. Watu hao wana familia ambazo zina wategemea. Upuuzi wa mapenzi yenu ya kijinga una wagarimu watu wengine ambao hawana hatina na wala hawato kuwepo pale mutakapo kuwa muna panuana miguu kitandani”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa ukali sana na lumfanya Julieth kutetemeka sana kwa woga kwa maana siku ya kwanza kukutana na baba mkwe ana fokewa kwa kiasi chiho.
“Sasa nina taka kujua ukweli, ukinidanyanya nita fanya kitu kibaya ambacho huja wahi kufanyiwa na mtu wa aina yoyote”
Julieth akatamani ardhi ipasuke ili mmeze.
“Evans amekutomb** au haja kutomb**”
Raisi Mtenzi alizungumza maneno ambayo Julieth hakutarajia kama yana weza kutoka kwenye kinywa cha mkwe wake huyo. Julieth akahisi kuchanganyikiwa kwa maana hajui hata amjibu kitu gani raisi Mtenzi.
“Nijibu”
Raisi Mtenzi alizungumza huku akipiga kofi zito juu ya meza yake na kumfanya Julieth kustuka kwa woga huku akiziachia picha hizo na kuanguka chini. Mlango wa raisi Mtenzi ukafunguliwa na akaingia mlinzi wake namba moja.
“Muheshimiwa muda ume fika, kuelekea airport”
Raisi Mtenzi akashusha pumzi huku akimtazama Julieth aliye inama chini huku akihisi kuchanganyikiwa kama si mlinzi huyo kuingia ndani hapo basi angezungumza ukweli wote wa mahusiano yake na Evans.
“Sawa mpelekeni huyu binti kwa daktari na nime muachia maelekezo yote. Waambie wahakikishe asionane na Jery wala mtu yoyote hadi pale nitakapo rudi”
“Sawa mkuu”
Wakaingia walinzi wawili wa kike, wakaondoka ofisini hapo na Julieth ambaye ana mwagikwa na machozi. Wakiwa njiani wakakutana na Jery.
“Baby vipi mbona un alia?”
Jery alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi. Walinzi hao wakamzuia Jery kuzungumza na Julieth na wakampita kama sio yeye. Julieth akaingizwa kwa daktari wa kike na ambaye amepewa maagizo ya kumpima Julieth vipimo vyote. Jery akaingia ofisini kwa baba yake huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.
“Baba ume mfanya nini Julieth?”
Jicho jali alilo tazamwa nalo likawa ni jibu tosha kwa Jery kukaa kimya. Raisi Jery na walinzi wake wakatoka ndani hapo na kumkuta mke wake akiwa tayari amesha ingia ndani ya gari.
“Baba Jery kuna nini kinacho endelea kwa watoto”
“Tuna ongea tukimaliza majukumu ya kiserikali”
Raisi Mtenzi alizungumza hukua kifunga mkanda wa siti yake na kuianza safari ya kuelekea uwanja wa ndege kumpokea raisi wa Marekani anaye kuja kwa ziara ya siku mbili nchini Tanzania.
***
Watu wa Evans wakafika kwenye moja ya msiti mkubwa sana ulipo katika miliya ya Uruguru. Wakasimamisha gari lao na kumtoa Evans ambaye bado amepoteza fahamu.
“Simu za wakuu wote wawili hazipatikani”
Mmoja wao alizungumza mara baada ya kuwasiliana na Jery pamoja na mlinzi wake.
“Tuna fanyaje na huyu boya?”
“Sijajua kabisa mkuu, isitoshe wezetu watakuwa wame kufa”
“Jaribuni kuwatafuta na ikishindikana tuna muua”
“Sawa mkuu”
Mmoja wa walinzi huyolizungumza na kuendelea kutafuta mawasiiano na mlinzi wa Jery ambaye ndio amewapatia kazi hiyo. Mmoja wa walinzi ambaye ana laptop inayo msaidia kuperudi katika mtandoa wa NSA wanao ili kufahamu ni kitu gani kinacho endelea.
“Mkuu”
“Ndio”
Akamuonyesha mkuu wake picha za wezao ambao wamefariki katika ajali waliyo ipata jana usiku. Kila mmoja wao akajawa na wasiwasi mkubwa sana kwa maana jambo hilo kama lime weza kujulikana ndani ya kitengo chao ni lazima na wao wata kuwa wana tafutwa na endapo wata kamatwa badhi adhabu yao ni kifo kwa maana kitendo cha kuwadhuru askari polisi basi ni moja ya kosa kubwa sana katika katiba ya kitengo chao.
“Mkuu tuta fanya nini?”
“Hadi sasa hivi tuna hesabika ni waasi wa serikali. Ina bidi kuhakikisha kwamba hakuna hata mmoja wetu ambaye ana ingia mikononi mwa vyombo vya usalama”
“Na huyu”
Mmoja wao alizungumza huku akimtazama Evans. Mkuu wao akachomoa bastola yake na kumuelekezea kichwani mwake.
“Usimuue kwa risasi uta poteza risasi zako bure mkuu”
“Tufanye nini?”
“Huyu tuna mzika akiwa hai”
“Muda wa kuchimba kaburi sisi hatuna”
Mkuu wao alizungumza, akaifunga bastola yake kiwamboa cha kuuzia sauti. Kabla hajafyatua risasi, simu yake ikaanza kuita. Akaitoa mfukoni na kukuta ni namba ngeni, akaipokea na kuiweka sikioni mwake.
“Ndio”
“Ni mimi Jery”
“Mkuu”
“Mume mpata huyo mjinga?”
“Ndio tunaye”
“Hakikisheni muna kuwa naye hai na nita dili naye mimi mwenyewe, Kajiificheni sehemu ambayo hakuna mtu ambaye ata wapata. Nitakuja kuwacheki”
“Sawa mkuu”
Simu ikakatwa, mkuu huyo akamtazama Evans kisha akawaagiza wezake wamuingize kwenye gari na wakaondoka eneo hilo na kutokomea wanapo pafahamu wao wenyewe.
***
Magreth na fundi huyo wakaifka katika hospitali ya mkoa aliyo pelekewa Josephine na kumkuta akiwa bado yupo katika chumba cha upasuaji.
“Hapa mjini ni wapi kuna fundi wa hizi iphone?”
“Yupo jamaa yangu mmoja ana tengeneza hizo simu”
“Una weza kunipeleka?”
“Ndio”
Wakaelekea kwa fundi huyo na simu ya Magreth ikaanza kutengenezwa. Hawakuchukua muda mrefu fundi huyo akamaliza kuitengeneza simu hiyo. Magreth akatoa kiasi cha milioni mbili kwa wakala wa mtandoa mmoja wa simu, akamlipa fundi hiyo kisha akampatia fundi huyo wa gari kiasi cha laki tatu na kuagana naye. Magreth akarudi hospittalini hapo na kumkuta Josephine akipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa.
“Vipi dokata hali yake ina endeleaje?”
“Ni mguu ume vunjika mara mbili, ila tume jitahidi kwa kadri ya uwezo wetu na tumefanikiwa kuuweka sawa”
“Ahaa je nina weza kupata msaada wa kumuhamishia katika hospitali ya Dar es Salaam.”
“Wewe ni nani yake?”
“Mdogo wake”
“Sawa ila kuna garama kwa maana ina bidi atumie usafiri wa hapa hospitalini”
“Hakuna shaka dokta, je ni kiasi gani?”
“Laki mbili”
“Sawa nina weza kulipia kwa sasa”
“Hakuna shaka. Uta elekea pale kwa muhasibu na utalipia”
“Sawa”
Magreth akamaliza taratibu zote za kulipia gari hilo la wagonjwa na safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam ikaanza huku na yeye akifwata kwa nyuma gari hilo la wagonjwa. Kutokana na king’ora kinacho pigwa na gari hizo kika wapa wepesi mkuwa wa kupishwa barabarani na gari nyingine hivyo ikawasaidia kuto kusimama kwenye foleni na wakafika Dar es Salaam ndani ya muda mchache. Moja kwa moja Josephine akapelekwa kwenye hospitali ya Muhimbili na kupokelewa na madaktari wa hospitali hiyo, wakamfanyia uchunguzi na walipo hakikisha kwamba yupo salama wakampelekea kwenye wodi ya kwake peke yake huku Magreth akiendelea kulipa huduma za matibabu yote hayo. Vyombo vyote vya nchini Tanzania na jirani ya nchi ya Tanzania vime jawa na habari ya shambulizi lililo tokea katika mkoa wa Morogoro. Habari hiyo ikaendelea kumuumiza Magreth kwa maana ame jitahidi kwa kadri ya uwezo wake ila hajafanikiwa kumuokoa mume wake.
‘Mungu msaidie Josephine aamke anisaidie kumtafuta mume wangu kwa maombi yako’
Magreth aliendelea kuomba kimoyo moyo huku akiwa amejiinamia katika kiti alicho kalia. Simu yake ikaanza kuita, akaitazama na kuipokea.
“Juma”
“Naam bosi habari ya mchana”
“Salama za wewe”
“Safi mbona huonekani ofisini, vipi kwema?”
“Yaa kwema kiasi ila nita pita hapo ofisini baadae kidogo”
“Sawa bosi”
Magreth akakata simu, kisha taratibu akanyanyuka na kuingia katika chumba alicho lazwa Josephine ambaye bado yupo katika usingizi mzito utokanao na sindano ya usingizi alio chomwa kipindi anafanyiwa upasuaji.
***
Daktari wa raisi akamaliza kumfanyia Julieth vipimo vyote kisha akampelekwa katika chumba cha mapumziko. Jery akafika katika chumba hicho alicho kaa Julieth ambaye bado ana msongamano wa mawazo ulio ambatana na woga mwingi sana. Walinzi wawili walipo mlangoni hapo wakamzuia.
“Hamuna nguvu ya kunizuia. Mume nielewa?”
Jery alizungumza kwa hasira huku akiwatazama wadada hao.
“Jery tuna kuheshimu, ila hatufanyi kazi kwako. Tuna fwata amri ya muheshimiwa raisi”
“Ila kumbukeni kwamba mimi ni mtoto wa raisi?”
“Ndio tuna lijua hilo, ila hatufwati amri yako”
Walinzi wengine wawili wakafika sehemu hiyo.
“Samahani mkuu una itwa”
“Na nani?”
“Mlinzi wako”
“Yupo wapi?”
“Tufwate”
Jery akawatazama kwa sekunde kadhaa wadada hao kisha akaongozana na walinzi hao hadi eneo la chini ya ikuli ambapo toka anze kukaa hapo ikulu hajawahi kuiona sehemu hiyo. Eneo walilo ingia ni sehemu iliyo jengwa kwa ajili ya kuwafunga walinzi wana kiuka sheria za eneo hilo. Akamkuta mlinzi wake akiwa amepigwa sana hadi mwili ukamsisimka kwa woga.
“Bosi samahani”
Mlinzi huyo alizungumza kwa shida sana huku jicho lake moja likiwa lime ziba kwa kupigo hicho.
“Kime kupata nini?”
Jery aliuliza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Ni..same…he…Mzee amegundua mpango wetu”
“Ndio akupige hivi?”
“Nisamehe kwa kushindwa kutunza siri mkuu”
Mlinzi huyo alizidi kumtia huruma Jery na kumpandisha hasira.
“Kama nikifa mkuu nakuomba umlee mwanangu”
“Huwezi kufa”
“Hapana mkuu nime iasi katiba yangu ni lazima nife”
“Hapana uzingumze hivyo. Nitahakikisha nina zungumza na baba”
Jery alizungumza kwa msisitozo, taratibu mlinzi wake huyo ambaye ame kuwa naye kwa kipindi kirefu, akamshika Jery viganja vyake vyote viwili na kumfanya ajawe na hasira na uchungu mwingi sana kwa maana tukio hilo ni la kikatili sana kwa mlinzi wake ambaye ana mpenda na amejitoa sana kwa ajili ya maisha yake.
“Mleteni daktari apewe matibabu?”
“Hatuwezi kufanya hivyo kwa maana hii ni amri ya raisi na ume ingia hapa kwa heshima yako ila pia ulikuwa huruhusiwa kuingia hapa”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akimtazama Jery usoni mwake. Jery akazidi kujawa na hasira sana kwa maana endapo ata muacha mlinzi wake katika mazingira hayo basi ana weza kupoteza maisha. Jery akamnyanyua mlinzi wake huyo, akataka kutoka naye ndani hapo ila akazuiwa.
“Tafadhali Jery usitulazimieshe kutumia nguvu”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akimzuia Jery kwa kumshika kifuani mwake. Jery akautazama mkono wa mlinzi huyo na kumfanya autoe.
“Nina mtoa sasa ole wake mtu aniguse, huo ugeni wenu leo wote uta vurugika na muta jua kama mimi ni kishaa au nina akili timamu”
Jery alizungumza na kuwafanya walinzi hao kutazamana huku wakijuliza ni kitu gani ambacho Jery amekidhamiria kukifanya kwao.
“Kama leo muna mfanyia mwenzenu hivi ambaye amjitoa maisha yake yote kwa ajili yangu. Kumbukeni huyo huyo ambaye alimfanya awe hivi ipo siku nanyi ata wafanya kuwa hivi. Ana stahiki kuishi ana mtoto wa kike ni mdogo na ana miaka mitatu ana stahili maleze ya baba yake. Nina mjua baba yangu sio mtu mwenye utu kabisa.”
Jery alizungumza maneno ambayo yaliwaingia walinzi hao wawili mioyoni mwao.
“Ana hitaji kuishi mwenzenu”
“Sawa ila daktari aletwe hapa hatutoa hitaji atoke hapa ndani kwa maana na sisi hatuhitaji kupata adhabu kama hiyo”
“Sawa nita mtibu mimi mwenyewe. Nisubirini nina kuja”
Jery akatoka ndani hapo kwa haraka, akaingia chumbani kwake na kuchukua kibegi chake kidogo chenye vifaa vya kidaktari kisha akarudi eneo hilo na kuanza kumpatia matibabu ya siri mlinzi wake huyo.
***
Ulinzi ukazidi kuimarishwa katika kiwanja cha ndege cha mwalimu Jk Nyerere na majeshi ya nchi za pande mbili, Marekani na Tanzania. Umakini haukuwa tu kwenye maeneo ya ardhini, bali hata eneo la anga, ndege za kijeshi aina ya Jet zipatazo kumi zime uzingira uwanja huo huku zikisubiria ndege kubwa ya raisi wa Marekani, ali maarufu kwa jila la Air Force One itue katika kiwanja hicho.
Raisi Chinas, mke wake pamoja na viongozi wengine wa kitaifa, wamekusanyika katika kiwanja hicho kuusubiria ugeni huo ambao kwa nchi ya Tanzania ni ugeni mmoja mkubwa sana. Hazikupita dakika kumi na tano ndege hiyo ikaanza kuonekana kwenye anga la uwanja huo wa taifa. Wananchi wengi walio jitokeza wakaanza kushangilia huku kila mmoja akiwa na hamu kubwa sana ya kumuona raisi wa Marekani. Taratibu ndege hiyo ikaanza kutua na kupunguza mwendo wake wa kasi, ilipo kaa sawa, ikaendeshwa hadi katika zulia jekundu lililo wekewa ngazi maalimu kwa ajili ya raisi wa Marekani na timu yake kushuka. Raisi Chinsa Mtenzi mpamoja na mke wake wakasogelea katika eneo hilo la ngazi huku kukiwa na vitoto viwili vya kike vikiwa vime beba maua ambayo wata mpatia raisi huyo ambaye naye ameambatana na mke wake pamoja na mtoto wake wa kike.
Raisi Minler Thomas akaanza kushuka na mke wake katika ngazi hizo huku wakiwa wame jawa na furaha kubwa sana. Wakapeana mikono na raisi Chinas Mtenzi huku wakiwa na furaha kubwa snaa. Wakatambulishana wake zao kisha wakaeleka kwenye kijukaa maalumu. Ukaanza kupigwa wimbo wa Taifa wa nchi ya Tanzania kisha ukafwatia wimbo wa taifa wa nchi ya Marekani. Baada ya hapo, wakakagua kikosi cha jeshi kilichopo hapo uwanjani kisha wakaelekea katika eneo la wacheza ngoma. Wakatazama ngoma hizo kwa dakika tano kisha wakaingia kwenye gari maalumu ambalo lina tumiwa na raisi wa Marekani.
“Nchi yako ina watu wakarimu sana”
“Nashukuru sana ndugu yangu. Karibu sana Tanzania”
“Nashukuru sana ndugu yangu. Nime jawana furaha sana kufika hapa. Kipindi chote cha misha yangu nime kuwa na hamu kubwa sana ya kufika nchini hapa na leo ndoto yangu ime kamilika”
“Nafurahi kusikia hivyo ndugu yangu”
Msafara huo moja kwa moja ukafika ikulu. Raisi Mtenzi akamuagiza mmoja wa walinzi wake waende kumuita Jery kw amaana na yeye ana paswa kutambulishwa kwa familia ya raisi Minler. Mlinzi huyo akaanza kuulizia ni sehemu gani aliyopo na akaelezwa kwamba yupo katika gereza alilo fungwa mlinzi wake. Akafika katika gereza hilo na kumkuta Jery akimalizia kumuhudumia mlinzi huyo.
“Jery baba yako ana kuita”
“Wameshafika?”
“Ndio”
“Ndugu yangu hii sindano niliyo kuchoma ita saidia sana katika kukausha majeraha ya vidonda.”
Jery alizungumza kisha akaondoka eneo hilo, moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, akaoga haraka haraka ana kuvaa suti nzuri kisha akeleeka katika eneo walipo wazazi wake. Jery akasalimia na riaisi Minller, mkewe pamoja na mwanaye wa kike.
“Huyu ni mwanangu wa mwisho”
“Ohoo nashukuru sana kumfahamu”
“Jery una weza kumtembeza mwanangu na muka zungumza mambo mawili matatu”
Raisi Minler alizungumza na kumfanya Jery atabasamu. Wakatoka eneo hilo pamoja na mtoto huyo wa kike wa raisi Minler ambaye ana umri mmoja na Jery.
“Una itwa nani?”
“Naitwa Godliver”
“Wao ni jina zuri sana”
“Nashukuru hata na wewe pia jina lako ni zuri sana.”
Jery akampeleka msichana huyo kwenye bwawa kubwa ambalo lime zungukwa na maua mazuri pamoja na bata mzinga wengi ambao wame kuwa ni kivutia kizuri sana kwa Godliver.
***
“Nimejarubu kumpigia Julieth simpati hewani vipi wewe ume mpata?”
Mrs Sanga alimuuliza mume wake ambaye amekaa sebleni akisoma biblia yake.
“Hawezi kuwa hewani, leo ikulu kuna ugeni mkubwa hivyo ni lazima simu yake itakuwa off. Si unajua jinsi wezetu Wamarekani wanavyo jali sana kwenye mambo ya usalama”
“Ahahaa….Nilijawa na wasiwasi mwingi, nikihisi labda ule mpango wetu ume julikana”
“Hapana, yule dokta yupo vizuri sana”
“Mume wangu, haya sasa tuna nafasi ya ukaribu na raisi, ehee je tuna fanyaje juu ya mipango yetu?”
“Subiri kidogo muda uta amua. Unajua inabidi tuvumilie hadi pale utakapo ingia bungeni na mambo yakiwa vizuri basi kila jambo tutakalo lipanga litakwenda poa”
“Sawa mume wangu mimi nina kusikiliza wewe. Vipi leo una kwenda kwenye ibada?”
“Yaa nina hamu sana ya kurudi mazabahuni.”
“Mungu akutangulie”
“Vipi hutaki kwenda na mimi?”
“Mmmm hapana kuna mahala nina kwenda mara moja kisha nina rudi nyumbani. Nahitaji kuwandalia chakula kizuri kwa leo usiku”
“Sawa mke wangu”
Mrs Sanga akambusu mume wake mdomoni kisha akaondoka nyumbani hapo. Nabii Sanga alipo hakikisha ameandaa somo zuri la kwenda kuhubiri kanisani akajiandaa na kuanza safari ya kuelekea kanisani kwake. Wingi wa watu walio kusanyika kanisani hapo, uka zidi kumfanya nabii Sanga aamini nguvu alizo nazo zina zidi kufanya kazi. Kila muumini aliye muona nabii Sanga alizidi kujawa na wa furaha kwa maana ni kipindi kirefu hawajamuona mtumishi wao huyo. Shangwe na nderemo zikazidi kupambam moto kanisani hapo huku wana kwaya wakizidi kutumbuiza kisawa sawa. Nabii Sanga akaanza makeke yake ya kuhubiri huku waumini wake wakizidi kujawa na imani mioyoni mwao pasipo kufahamu kwamba siri ya mambo yote nyuma ya nabii wao huyo ina tokana na nguvu za giza na wala si kwa nguvu za Mungu.
***
Kadri muda unavyo zidi kusonga mbele ndivyo jinsi Julieth anavyo jawa na wasiwasi.Hatambu lengo la yeye kuweka ndani ya chumba hicho ambacho kina kila aina ya huduma. Kitu kibaya zaidi ni simu yake ameicha alipo kuwa ana ingia ofisini kwa raisi. Akasimama na kugonga mlango huo. Mlango ukafunguliwa na akachungulia mlinzi mmoja wa kike.
“Ndio”
“Nahitaji kumuona Jery”
“Kwa sasa Jery yupo na wageni”
“Tafadhali nin kuomba umuombe aweze kuja humu”
“Hapana dada. Raisi wa Marekani yupo hapa hivyo kila mmoja yupo busy”
“Sasa kwa nini nime fungiwa humu ndani kama mfungwa?”
“Haujafungiwa kama mfungwa ndio maana hauna pingu mkononi mwako.”
“Ila nina kuomba unisaidie kumuita yule ni mume wangu mtarajiwa na nina kila haki ya kumuona”
Mlinzi huyu kidogo akastuka baada ya kusikia kwamba Julieth ni mke mtarajiwa wa Jery. Wakashauriana walinzi hao na mmoja wapo akaondoka na kuanza kumtafuta Jery. Akafanikiwa kumuona Jery, akamsogelea na kumgong’oneza sikioni mwake.
“Sawa muambie nina kuja”
Mlinzi huyo akaondoka na kumuacha Jery akiendelea kuzungumza na mgeni wake.
“Ana kuja”
“Sawa”
Kidogo Julieth akaanza kujawa na furaha kwa maana ana weza kupata fumbo la yeye kuwekwa ndani hapo. Baada ya nusu saa Jery akaingia ndani hapo. Wakakumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akiwa na hisia kali za kimapenzi kwa mwenzake.
“Jery nime choka kukaa peke yangu humu ndani”
“Usijali twende chumbani kwangu. Unajua kuna ugeni mkubwa sana wa raisi kutoka Marekani”
“Ahaa kumbe ni leo”
“Yaa ni leo. Pia si una jua kwamba wewe ni mke wangu mtarajiwa hivyo baba haja penda uwe una onekana onekana kwa watu hadi pale tutakapo oana”
Jery alimuomgopea Julieth ili mradi ajawe na amani ambayo anatambua kwamba ilisha mtoweka.
“Nime kuelewa mume wangu”
“Nashukuru kusikia hivyo. Twende”
Jery akatoka na Julieth na walinzi hao wakashindwa kuwazuia, walicho kifanya ni wao kufwata kwa nyuma. Jery akamuingiza Julieth chumbabi kwake.
“Kila kitu kipo humu ndani mke wangu. Ukihitaji games zipo kuwa na furaha”
“Simu yangu”
“Ohoo simu nita mtafuta yule mlinzi kisha nita kuletea”
“Sawa mume wangu”
“Vipi una jihisi njaa?”
“Kwa mbali?”
“Basi nita muagiza mpishi akuletee. Ila nisamehe sana mke wangu kwa maana kuna baadhi ya wageni ambao baba ame nikabidhi niwe nao hivyo sipaswi kuwa nao mbali”
“Usijali mume wangu, huo ndio wakati wa wewe kuji funza baadhi ya mambo. Huwei jua huko mbele nawe ukaja kuwa raisi”
“Hahaa sawa mke wangu. Nina kupenda sana”
“Nakupenda pia”
Jery akambusu Julieth mdomoni mwake kisha Jery akatoka ndani hapo. Akamuaagiza mpishi wa familia ya kumuandalia Julieth chakula, kisha yeye akaelekea alipo muacha mtoto wa raisi wa Marekani.
***
“Mkuu gari ina elekea kukata mafuta na huku tulipo ni porini”
Dereva alizugumza huku akimtazama mkuu wake aliye kaa siti ya pembeni.
“Daa na huku hakuna hata dalili ya mtu kuishi?”
“Yaaa”
“Dogo endapo mafuta yatatuishia, damu yako ita kuwa ndio mafuta yetu”
Jamaa huyo alizugumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Kwa nini jamani mume niteka?”
“Wewe una kulaje sahani moja na wenye nchi. Hili ndio linalo kutokea”
Mkuu huyo alizungumza huku akimtazama Evans kwa macho ya dharau. Evans machozi yakaanza kumlenga lenga na hapa ndipo akaanza kupata picha kwamba mateso haya yote anayo yapitia kwa sasa ni kutokana na kuwa na mahusiano na Julieth.
‘Wanawake kweli ni wauaji’
Evans alizungumza kimoyo moyo huku akiwatazama wanaume hawa watano alio kaa nao ndani ya gari hilo linalo elekea asipo pajua.
“Naombeni kujisaidia haja ndogo”
Evans alizungumza huku akijaribu kutazama maporomoko yaliyopo pembezoni mwa hii barabara.
‘Una zingua una jua?”
“Ni kweli naombeni sana nijisaidie”
Kwa ishara mkuu wa kikosi hicho akamuomba dereva huyo kusimamisha gari hilo pembezoni mwa barabara.Vijana wawili walio kaa siti ya nyuma na Evans waka shuka ndani ya gari hilo, walipo hakikisha kwamba ulinzi upo vizuri wakamshusha Evans ambaye ni kweli ame banwa na haja kubwa.
“Mkuu una jua kwamba tuna songa tu mbele na hatujui ni wapi tunapo elekea?”
“Huku mbele kuna kijiji ana ishi babu yangu, nina imani tuna weza kukaa pale hadi mkuu atakapo kuja”
“Ila mkuu tume poteza sana wezetu. Sisi tulio baki hatujui tuna ishi vipi, hatuelewi familia zetu zita kuwa kwenye hali gani”
“Ni kweli nina wasiwasi hata mimi, Ila hii ndio njia tuliyo ichagua. Hatuna namna ya kurudi nyuma tena”
“Daa kazi kweli kweli kaka. Ila huyu dogo sijui ata fanywa nini na Jery?”
“Atamuu “
“Ila mapenzi ni mambo ya kijinga sana. Sisi tuna hangaika ila wao wakipatana mambo yana endelea”
“Tuta fanyaje sasa ikiwa ndio kazi yetu”
Evans akasogea pembezoni kabisa kwa barabara hiyo, akafungua zipu ya suruali yake na kuanza kujisahidia haja ndogo huku macho yake yote yakitazama katika eneo hilo lenye bonde kubwa. Chini kabisa ya hilo bonde ambalo ni refu sana akaona mto mkubwa sana una tirisha maji. Akageuka nyuma na kuwatazama watu hao walio mteka. Wawili alio shuka nao kwenye gari wame simama eneo moja huku wakipiga stori zao na kucheka. Wengine watatu wapo ndani ya gari wakiendelea na mazungumzo yao.
‘Ni heri kufa kuliko kuendelea kushikiliwa na hawa watu ambao sijui hatima ya maisha yangu itakuwa ni nini mikononi mwao’
Evans alizungumza huku akiifunga zipu ya suruali yake. Akarudi hatua mbili nyuma kisha akakimbia kwa kasi na kujirusha kuelekea chini katika bonde hilo kubwa na kuwafanya walinzi hao wote kustajabu kwa maana hakuna hata mmoja wao aliye tarajia kuona Evans akifanya tukio kama hilo.
“Huu ni using** gani”
Kiongozi wa kikundi hicho alizungumza huku akishuka kwenye gari kwa haraka na kukimbilia sehemu walipo simama wezake wana. Wakamshuhudia Evans akidumbukia katika mto mkubwa wa maji ambao una pita katika mabonde hayo. Mkuu wao akavua koti lake la suti kisha na yeye akajirusha ndani ya mto huo kwa maana haitaji kumkosa Evans, kwani kumpoteza kwake kutazidi kuyaweka maisha yao hatarini.
“Baki na gari”
Mmoja wao alimuambia dereva wa gari abaki eneo hilo huku nao wakianza kujirusha kwenye mto huo. Evans akajigeuza taratibu ndani ya maji na kuanza kupanda juu kwa maana kina cha mto huo ni kirefu sana. Evan akawaona watu walio mkamata nao wakijirusha katika mto huo. Hapakuwa na haja ya kujishauri mara mbili na kitu pekee alicho kifanya ni kuhakikisha kwamba ana ogelea kadri ya uwezo wake. Wingi wa maji hayo ambayo yana kasi kubwa, yakamzidi Evans na kujikuta akianza kupelekwa mbele huku akijibamiza kwenye baadhi ya majabali yaliyomo ndani ya mto huo. Evans akafanikiwa kushikilia moja ya jabali moja kubwa na taratibu akanza kupanda katika jabali hilo ambalo kwa juu kuna sehemu unayo weza kukaa vizuri. Jitihada zake zikazaa matunda na akakaa eneo hilo huku akiwashuhudia jinsi watu walio mteka nao wakipambana na hali zao kwa maana maji hayo yana nguvu kubwa kuwashinda hata wao wenyewe. Evans akashuhudia kiongozi wa kikosi hicho akipita pembezoni mwa jabali hilo huku akiwa ana mwagikwa na damu nyingi kichwani mwake ikiashiria kwamba ame pigiza kichwa chake kwenye moja ya jabali.
***
Raisi Mtenzi na raisi Minler wakakutana na waandishi wa habari na kuanza kutoa hotuba fupi zinazo husiana na uhisiano mzuri wa nchi hizi mbili, Tanzania na Marekani. Pia wakazungumzia juu ya miradi mikubwa ambayo Marekani wana mpango wa kuwekeza nchini Tanzania ikiwemo kiwanda kikubwa cha utengenezaji wa magari ambayo yatauzwa ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Mkutano huo wa dakika ishirini ukamalizika na raisi Mtenzi akamkaribisha raisi Minler kujumuika naye kwenye chakula cha jioni kilicho andaliwa hapo hapo ikulu.
“Baba tuna weza kuzungumza”
Jery alimnong’oneza baba yake sikioni mwake mara baada ya kumaliza kupata chakula hicho.
“Kuna nini?”
“Ni kuhusiana na Julieth. Si una tambua kwamba yupo tu ndani na hana pa kwenda”
“Kumbe bado yupo?”
“Ndio au ulisahau kama yupo?”
“Ahaa vipimo vyake vime tokaje?”
“Sijajua kwa maana sijakutana na daktari”
Raisi Mtenzi akaomba ruhusa ya kuondoka eneo hilo na akamuacha raisi Minler na familia yake. Wakaelekea moja kwa moja katika chumba cha daktari.
“Muheshimiwa raisi”
Dokta alizungumza huku akinyanyuka na kwenye kiti chake
“Majibu ya mkwe wangu yapo tayari?”
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Nayaomba”
Daktari akamkabidhi raisi Mtenzi faili lenye majibu hayo. Akaanza kupitia kitu kimoja baada ya kingine, Jery akatamani kusoma ila akashindwa kwa maana wana tazamana na baba yake. Raisi Mtenzi akapitia neno moja baada ya jengine, majibu yote yana onenyesha kwamba Julieth yupo sawa na bado ni bikra.
“Mke wako yopo salama. Uta mchukua na kumpeleka kwao na tuta jua ni taratibu gani nyingine za ndoa zitakavyo fwata”
“Kwa hiyo baba ume mkubali?”
“Ndio si muna pendana?”
“Ndio baba”
“Basi tusubiri huu ugeni uondoke kisha tuta jua ni nini cha kufanya”
“Nashukuru sana baba”
“Jambo jengine wale wajinga wako ulio watuma wasilina nao na waambie wajisalimishe na wasiendelee kuichafua sifa ya serikali yangu”
“Sawa baba”
Jery akatoka ndani hapo huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Akaingia chumbani kwake na kumkuta Julieth akiendelea kula taratibu. Akamkabidhi Julieth faili hilo la majibu ya daktari.
“Waoo”
Julieth alizungumza huku akiwa wamejawa na furaha kubwa sana, moyoni mwake. Wakakumbatiana na Jery huku wakimwagikwa na machozi ya furaha kwa maana ndoa yao ina anza kunikia taratibu.
“Ina bidi nikupeleke nyumbani sasa”
“Baba amekubali niondoke hapa?”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment