MY LIFE
WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+
SEHEMU YA 10 KATI YA 10
“Eddy STOPPPPPPP”
Nilizungumza kwa sauti ya juu huku mwili mzima ukinitetemeka kwa woga, Eddazaria akajitahidi kwa kulizuia jambia lake hilo ambalo limebakisha sentimita kama mbili kutua shingoni mwa mke wa raisi. Nikamtazama mke wa raisi na nikamuona jinsi alivyo yafumba macho yake huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi kifuani mwake. Nikamfwata mume wangu anaye tetemeka kwa hasira sana, taratibu nikamshika mkono wake na kulichukau jambia lake.
“Eddy, Eddy”
Eddy kwa hasira akachukau kiti kimoja na kukitupa ukutana hadi kikavunjika vunjika, na kumfanya mke wa raisi kutetemeka sana. Eddazaria kaapiga kelele huku akikaa chini na kuangua kilio kikali kilicho changanyikana na hasira. Sikuhitaji hata kumshika kwa maana mume wangu akiwa katika kipindi kama hichi mara nyingi hupenda kwua peke yake.
Nikamfungua mke wa raisi kamba nilizo mfunga mwilini mwake.
“Ni lazima nikakukabidhi kwa mume wako na atupatie mama yetu”
Nilizungumza kwa kujiamini huku nikimtazama mke wa raisi usoni mwake.
“Jojo”
Eddazaria aliniita kwa sauti nzito na kutufanya tumtazame. Taratibu akanyanyuka na kutusogelea karibu.
“Hakikisha kwamba unarudi na mama yangu hapa sawa”
“Sawa mume wangu”
Eddazaria akanikabidhi funguo ya pikipiki, kisha akavuta kiti alicho kuwa amekalia mke waisi na akakikalia yeye. Nikamtazama kwa muda kisha tukatoka ndani humu, moja kwa moja tukaelekea chumbani huku nikiwa nimemuweka kwenye ulinzi mkali sana.
“Jojo kwa nini munafanya jambo la hatari kama hili”
“Mama wewe ndio unamjua Eddy, ila mimi sikujui, ninafanya kile alicho niambia mume wangu nifanye sawa”
Nilizungumza huku tukipandisha ngazi za kuelekea gorofani, tukaingia chumbani na nikamkabidhi dera ambalo ni kubwa kiasi. Akaliva na kwa bahati nzuri likamuenea mwilini mwake. Nikachukua saa mbili ambazo tunazitumia mimi na mume wangu hususani kwenye swala la kuwasiliana. Nikaivaa saa moja na tukaanza kutoka chumbani humu, tukafika sebleni na kumkuta Eddazaria akiwa amesimama huku amevaa kinyago chake huku mkononi mwake akiwa ameishika laptop.
“Mume wako akifanya usaliti wa aina yoyote, ninakwenda kuiangamiza nchi hii, umenielewa?”
Eddazaria alimuambia mke wa raisi na kumfanya atingishe kichwa chake akimaanisha kwamba amemuelewa vizuri mume wangu.
Tukaongozana na Eddazaria hadi kwenye gereji ilipo katika nyumba yetu hii. Akanishika mkono na kunisogeza pembeni, nikamkabidhi saa na akaivaa mkononi mwake.
“Hii ni kalamu ina GPRS, popote utakapo kwenda nitakuwa ninakufwatilia na kukuona. Mini nina yaandaa haya mabomu ya nyuklia endapo kutatokea tatizo lilote nitampa onyo”
“Onyo la namna gani?”
“Nitaachia bomu moja”
“Mume wangu usije ukaua raia wasio na hatia ya aina yoyote, kumbua kwamba familia zetu bado zipo ndani ya Tanzania”
Nilizungumza kwa sauti ya chini kidogo huku nikimtazama mume wangu usoni mwake.
“Nalitambu hilo na wala usiwe na wasiwasi katika hilo”
“Niambie ni wapi tuatalipelekea bamu hilo?”
“Baharini”
“Una uhakika?”
“Ndio, niamini mke wangu, nitalipeleka baharini”
“Sawa, nina kuamini mume wangu. Ninakupenda sana”
“Ninakupenda pia. Ila kama huyu mama ataonyesha dalilili ya usaliti either kwa kukupiga au kutoroka muue”
“Ni muue……!!!?”
Niliuliza huku nikiwa nimejawa namshangao mkubwa sana.
“Ndio hakikisha kwmaba una muua hilo sio ombi ni amri”
“Sawa mume wangu, swala moja la mwisho. Hivi unamfahamu huyu mama?”
“Ndio”
“Kwa nini hukuniambia toka hapo awali?”
“Tutayazungumza hayo mambo ukirudi mke wangu sasa hivi fanya hii kazi”
“Sawa”
Tukakumbatiana kidogo na mume wangu, kisha nikapanda kwenye pikipiki. Nikavaa helment, kisha nikamkabidhi na mke wa raisi helment, na yeye taratibu akapanda. Eddazaria akatufungulia geti la gereji hii na taratibu nikaanza kuondoka huku kichwani mwangu nikiwa na mawazo mengi ya kujiuliza ni namna gani kazi hii inavyo weza kuwa.
Uzuri katika eneo ambalo tunakatika kuvuka kwenda ng’ambo ya pili hakuna wingi wa watu ambao wanapita na waokoaji wengi wamekuja kwa kupitie eneo jengine ambalo ni rahisi sana kwa kuweza kufika katika jiji la Dar es Salaam. Nikaipandisha pikipi hii kwenye boti, yetuu ndogo, kisha taratibu nikaanza kuiendesha kuelekea upande wa pili wa bahari.
“Jojo”
Mke wa raisi aliniita kwa sauti ndogo na ya upole sana. Nikavua kofia hili la pikipiki ili kumsikiliza kwa umakini sana.
“Kwa nini munafanya haya yote, kwa nini musiamue kulimaliza hili jambo kwa amani?”
“Amani, hahaaaa. Labda nikuulize swali moja, je unamfahamu mume wako vizuri?”
“Si kumfahamu tu ila nina mjua vizuri mume wangu”
“Unajua kwamba amefanya mambo mangapi mabaya, unalitambua hilo?”
“Mume wangu ni mtu mwema, mume wangu ni mtu mpenda amani hana tatizo na mtu”
“Eti eheee?”
“Ndio”
“Ngoja nikuambie kitu kimoja na ukiweke akilini mwako kabisa. Mimi sio Eddy, mimi hukuwahi kunishuhudia nikizaliwa. Hadi kufika haapa nimepitia mambo mengi sana mabaya. Jambo moja ambalo ninaweza kukutahadharisha tu, endapo utaniletea ujinga, nitahakikisha kwamba ninakikata kichwa chako, sina huruma nikiwa katika kazi hii”
Nilizungumza kwa msisitozo huku nikimtazama mke wa raisi usoni mwake.
“Nimekuelewa Jojo, ila namjua mume wangu hapa lazima atahakikisha kwamba unakamatwa, hawezi kumuachia mama mkwe wako kirahisi namba hiyo kama kweli yeye ndio amemkamata”
“Atamtoa, najua unahisi mume wakko ni hodari na jeuri, ila ni kwa wengine ila si sisi”
Nilizidi kuzungumza kwa kujiamini sana hukua kilini mwangu nikiwa ninatafakaji mbinu na namna gani ambayo ninaweza kufanya kuhakikisha kwamba leo hii ninaondoka na mama mkwe.
Tukafika pembezoni mwa bahari, nikaitoa pikipiki kwenye boti, nikaifunga kamba ya boti hii eneo la pembeni kwenye jiwe. Nikapanda kwenye pikipiki na mke wa raisi hakuwa na jinsi zaidi ya kupanda kwenye hii pikipiki. Tukaondoka eneo hili na kuinza safari ya kuelekea kwenye daraja la Kigamboni. Safari ikatuchukua daika ishirini na tano kufika. Kitu cha kwanza nikicho kifanya ni kuiwasha saa yangu na nikamuona Eddazaria akinisubiria kwa hamu.
“Simama hapo mwanzo wa daraja”
Eddazaria aliniambia huku akinitazama.
“Unaniona”
“Yaa ninatumia satelaiti kukufwatilia”
“Umesha wasiliana na raisi?”
“Ngoja nizime taa zote za daraja”
Eddazaria alizungumza huku mikono yake ikicheza cheza dhairi anaonekana akicheza na laptop yake ule ujanga ambao aliitumia katika jengo la Mlimani City ndio ujanja anao utumia hapa. Baada ya dakika kama moja na sekunde kadhaa hivi taa zote za hili daraja zikazima. Nikajipapasa mfukoni mwangu na kwa bahati nzuri nikauiona miwani ambayo tunazitumia kwenye giza na hutusaidia kuona vizuri kila kitu. Taratibu nikaivaa na kuzidi kuwa makini nikitazama eneo hili la daraja.
“Msafara wa raisin a watu wake wapo njiani wanakuja, baada ya dakika mbili watatukwa wamesha fika”
“Sawa mume wangu, naomba uzidi kunipa maelekezo”
“Sogea mbele hadi katikati ya daraja”
“Sawa”
Nikawasha pipikipi na taratibu tukaanza kusogea hadi katikati ya daraja na nikasimamisha tena pikipiki.
“Eddy”
“Mmmmmm:
“Mbona hamna gari hata moja linalo kuja?”
“Wao wenyewe ndio wamepanga magari yasipite kwenye eneo hilo”
“Sawa, nitafanyaje baada ya wao kufika”
“Kuna maelekezo nimempa raisi, na yeye mwenyewe ndio atashuka kwenye gari andapo ataleta ubishi, unajua nini cha kumfanya mkewe”
“Je mama yupo naye?”
“Ndio”
“Umemuonaje”
“Ngoja nikutumie picha kwenye saa”
“Kwani ina uwezo wa kupokea picha?”
“Ndio wewe, subiria”
Baada ya sekunde kadhaa nikaiona picha ya mama mkwe, mwili mzima ukaanza kufura kwa hasira, kwani mama mkwe amechakaa kwa mateso, amekuondeana kiasi kwamba anatia huruma.
“Mungu wangu, unaona unaona weweeeee”
Nilizumnguza kwa hasira huku nikimuonyesha mke wa waisi picha ya mama mkwe. Mke wa raisi akazidi kuogopa kwani hali ya mama mkwe hata yeye inamuogopesha.
“Huyu ndio mume wako, unaona kitu alicho kifanya, unaonaaaa?”
“Samahani sana, si….si……sikujua kama inaweza ikatokea hivyo”
“Ndio uje kwamba mume wako sio mtu ni jini”
Nilizidi kuzungumza kwa ukali huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
“Jojo tulia raisi na watu wake wanafika darajani”
Niliisikia sauti ya Eddazaria kwa haraka nikatoa bastola zangu zote mbili nilizo kuwa nimezichomeka kiunoni mwangu, huku nikihema kwa hasira.
“Jojo unanisikia”
“Nakusikia zungumza”
“Hakikisha mke wa raisi anaanza kutembea mara atakapo muona mama mkwe akitembea”
“Sawa”
“Kitu kingine kwenye hiyo miwani yako upande wa kulia kwenye kishikizo cha sikioo kilicho ungana na kioo kuna kimviringo kidogo, hakikisha kwamba cha duara uki kizungusha unaweza kuwaona kwa ukaribu kabisa, kwa maana nimesha wapa amri wasimame mwanzoni mwa daraja”
“Sawa”
Nikaona gari sita aina ya range rover zikisimama mwanzoni mwa daraja. Nikaanza kuzungusha kifaa alicho niambia mume wangu na taratibu nikaanza kuwaona kwa ukaribu kabisa raisi na mama mkwe wakishuka kwenye gari moja wapo. Raisi akasimama mbela ya moja ya gari huku akiwa ameshika simu yake sikioni mwake.
“Mruhusu atembeee”
“Sawa. Oya tembeea”
Nilizugumza huku nikiwa nimenyooshea mke wa raisi bastola ya kichwa. Kila jinsi mke wa raisi anavyo tembea kwenda mbele ndivyo jinsi taa za barabarani zinavyo waka na akiipita nguzo ya taa aliyo nayo usawa wake inazima na inawaka nyingine.
“Mbona taa zinawaka na kuzima”
“Ninawaonyesha kwamba nina uwezo wa kumdhuru mke wake, hapo mimi ndio muongozaji wa hilo eneo”
Nikajikuta macho yakinitoka kwani mama mkwe anatembea kwa kuchechemea, huku akionekana kuuburuza mguu wake wa kushoto unao unyesha dhairi umepata matatizo nikatamani kwenda kumchukua ila Eddazaria akanizuia kabisa.
“Usifanye hivyo”
“Kwa nini Eddy mama anaumia?”
“Najua ila usifamye hivyo?”
Mke wa raisi na mama mkwe wakakutana katikati. Nikamuona mama mkwe akimtazama mke wa raisi kwa macho makali yanayo onyesha dhairi kwamba ana hasira naye. Mke wa raisi akajaribu kumshika mama mkwe mkono wake wa kushoto ila mama mke akakataa kabisa asishikwe. Mama mkwe akaendelea kujikokota taratibu huku akionyesha dhairi kwamba ana maumivu makali sana kwenye mguu wake.
Mama mkwe akafanikiwa kufika sehemu niliyo simama mimi kwa haraka akanikumbatia na kuangua kilio kikali sana. Jambo lililo nifanya na mimi nishindwe kabisa kujihimili na kulila.
“Acheni kulioa ondokeni haraka”
“Mama twende”
Nilizungumza huku nikimuachia mama mama mkwe. Mamam mkwe akanitazama uosni mwangu kwa macho yanayo endelea kutiririkwa na machozi.
“No nipe bastola”
Mama mkwe alizungumza kwa hasira huku mwili mzimama ukimtetemeka. Kabla sijazungumza chochote mama mwe akanipora bastola moja mkononi mwangu na kuanza kufyatua risasi kuelea katika eneo zilipo gari za raisi na watu wake.
“Shitiii Jojo munafanya nini, mpokonye mama hiyo bastola”
“Mama acha, achaa mama yangu”
“Pumbavu pumbavu nyinyi, wajinga hamna akili nyinyi”
Mama mkwe alifoka huku akiendelea kufyatua risasi hadi risasi zilizomo kwenye bastola hiyo zikaisha. Gari mbili zikaanza kutufwata kwa kasi huku walinzi wakiwa amejichomoza kwenye vioo vya gari hizo huku wakitushambulia kwa risasi jambo lililo nifanya nimshike mama mkwe kwa haraka na kumsogeza eneo ilipo pikipiki, nikapanda na yeye akapanda, nikaiwasha na kwa kasi ya ajabu nikaigeuza na kuanza kuondoka katika eneo hili. Kitu kilicho zidi kunichananya zaidi ni gari nne za jeshi zilizo ifunga daraja katika eneo tunalo elekea na huku nyuma gari na raisi zinazidi kutufukuzia kuhakikisha kwamba wanatukamata mimi na mama mkwe au kutuua kabisa.
Kadri jinsi ninavyo zidi kusonga mbele ndivyo jinsi ninavyo zidi kuchanganyikiwa. Mama mkwe akachomoa magazine niliyo ichomeka kwenye mifuko ya suruali yangu. Akabadilisha magazine na kuanza kujibu mashambulizi ya walinzi wa raisi wanao endelea kutufukuzia. Kwa kupitia kioo cha pembeni cha pikipiki yangu nikashuhudia kuona gari hizi mbili zikipoteza muelekeo huku gari nyingine ikipinduka vibaya na kuvunja uzio wa daraja na kutumbukia baharini. NikuhIfuhuafunga breki za gafla huku tairi za pikipiki zikiserereka kwenye hii lami.
“Mbona umesimama?”
Mama mkwe aliniuliza huku akiwa bado amendelea kunishikilia kwa mkono mmoja kiunoni mwangu.
“Tazama mbele mama”
Nilizungumza huku nikitazam gari hizo za jeshi ambazo zimetuzuia njia darajani. Tukiwa katika majadiliano na mama mkwe tukastukia gari hizo za jeshi zikilipuka jambo lililo tustua sana. Tukaona helicopter moja ya kijeshi ikifanya mashambulizi hayo ya anga.
“Ni nani?”
Nilimuuliza mama mkwe huku nikimtazama usoni mwake.
“Sifahamu kwa kweli ni nani”
Mama mkwe alinijibu kwa sauti yaupole huku tukiendelea kuhusidia jinsi helicopter hii inavyo zidi kufanya mashambulizi ya mabomu na risasi kwenye gari hizi za wanajeshi. Baada ya mashambulizia haya kuisha helicopter hii taratibu ikaanza kushuka taratibu na kutua katikati yadaraja. Wakashuka watu wanne walio valia nguo nyeusi huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Sura zao wamezifunika, taratibu mama mkwe akashuka kwenye pikipiki.
“Mama unakwenda wapi?”
Nilimuuliza mama mkwe huku na mimi nikishuka kwenye pikipiki. Watu hao wakaanza kutembea kwa umakini huku wakitufwata, kwa haraka nikaichoma bastola yangu moja niliyo salia nayo na kuwanyooshea ili hata kama kuna lolote watako lifanya basi nijibu mashambulizi japo tutakufa, ila si kizembe. Watu hawa wakasimama mbele yetu na kumpigia mama mkwe saluti.
“Mkuu tumekuja kukuchukua”
Mama mkwe akawatazama kwa muda kisha akaanza kupiga hatua ya kupita katikati yao akimaanisha kwamba amekubali kuondoka nao.
“Twende”
Mama mkwe aliniambia huku akinigeukia na kunitazama. Nikaitazama pikipiki ya mume wangu.
“Achana nayo”
Mama mkwe alizugumza kwa kujiamini. Nikajumuika na mama mkwe na tukaanza kutembea kuelekea sehemu ulipo helicopter hiyo huku kitika hali ya umakini sana. Tukaingia ndani ya helicopter hii na taratibu tukaanza kuondoka huku muda wote nikiwa makini sana kwani hadi sasa hivi sina uhakika na hawa watu.
“Mama tunaelekea wapi?”
Nilimuuliza mama mkwe kwa sauti ya kumnong’oneza ila hakunijibu chochote zaidi ya kunitazama usoni mwake. Nikajaribu kuiwasha saa yangu ili niweze kuwasilian ana mume wangu ila hapakuwa na mawasiliano ya aina yoyote.
“Samahani hakuna mawasiliano yoyote unayo weza kuyapata humu ndani”
Niliisikia sauti ya kike ya mmoja wa hawa watu walio kuja kutusaidia. Mama mkwe akanishika kiganja cha mkono wangu wa kushoto na kukiminya kidogo ikionyesha ni ishara ya kunitoa wasiwasi nilio nao.
Safari ikatuchukau zaidi ya masaa matatu kutokana ni usiku na tupo angani wala sikuweza kutambu ni wapi tunapo elekea. Nikaona eneo lililo jaa taa zilizo izunguka herufi kubwa ya ‘H’ huku herufi hiyo nayo inawaka taa nyeupe zikiashiria kwamba hicho ni kiwanja cha helicopter. Taratibu helicopter hii ikaanza kushuka, ikatua ardhini na mlango ukafunguliwa kwa nje, tukakuta wanaume watatu na mwanamke mmoja walio valia makoti meupi wakishiaria kwamba wao ni madaktari.
Wakakiandaa kitanda cha matairi na taratibu mama mkwe akalala juu ya kitanda hicho na kikaanza kusukumwa kupelekwa ndani huku nami nikifwata kwa nyuma. Katika eneo hili kuna jumba kubwa la kifahari ambalo ulinzi wa eneo hili umeimarishwa vizuri sana kuanzia nje hadi nje.
“Mama hawa ni watu gani?”
“Utajua”
Mama mkwe alinijibu kwa ufupi huku kitanda kikindelea kusukumwa. Akaingizwa kwenye moja ya lifti, nikaingia naye cha kushangaza badala ya lifti hii kwenda juu ikaanza kuelekea chini. Lifti ikafunguka, tukatoka kwenye lifti hii na kuanza kutembea kwenye kordo hii yenye vyumba kadhaa huku kukiwa na walinzi wakiwa wamesimama vizuri na bunduki zao.
Mama mkwe akaingizwa kwenye moja ya chumba, na nesi akaniomba niweze kukaa nje niweze kuwasubiria waweze kumshuhulikia. Sikuhitaji kubisha zaidi ya kusimama pembeni ya chumba hichi kwa maana hakuna sehemu yoyote ya mimi ninayo weza kukaa.
Nikajaribu kutumia saa yangu ili kuweza kuwasiliana na mume wangu, ila hali ya kuto kuwa na mawasiliano ikaendelea kunichanganya zaidi. Nikatamani kumuuliza mmoja wa walinzi ila kwa ukimya wao nikashindwa kabisa kufanya chochote huku nikijipa moyo kwamba mama mkwe atakapo toka katika chumba hichi anaweza kunielezea hapa tulipo ni wapi. Nikakaa eneo la hapa nje zaidi ya lisaa na dakika kama ishirini hivi mlango wa chumba cha mama mkwe ukafuguliwa na akatolewa huku akiwa amefungwa bandeji kwneye mguu wake ambao ulikuwa umepata majeraha.
“Zoezi limeendaje dokta?”
“Limekwenda vizuri”
“Anasumbuliwa na nini mama yangu?”
“Ni mguu kidogo ulikuwa na itilafu, ila kitu kingine anatakiwa apate chakula kizuri”
“Sawa sawa”
Tukazidi kusonga mbele na kuingia katika chumba ambacho mama mkwe atakitumia katika kipindi hichi chote cha matibabu yake. Madaktari wakanipa malekezo machache ya jinsi ya kumshuhulikia mama mkwe, kisha wakaondoka. Saa yangu inanionyesha muda huu ni saa kumina moja alfajiri. Uchovu wa mishemishe zote za usiku ukanifanya niweze kupata usingizi mzito sana huku nikiwa nimekaa kwenye sofa lililopo pembeni ya kitanda hichi cha mama mkwe.
“Habari yako Jojo”
Sauti hii ya kike ikanistua sana na kufumbua macho yangu, nikakutana na sura ya Nuru akiwa amesimama mbele yangu, kwa haraka nikaupeleka mkono wangu kiunoni ambapo nimeichomeka bastola yangu ila sikuweza kuikuta. Nuru akanionyesha bastola yangu huku akizungusha zungusha hewani. Nikamtazama mama mkwe na kumkuta akiwa amekaa kitako, taratibu Nuru akainamisha kichwa chake chini kwa ishara ya kumsalimia mama mkwe kwa heshima zote jambo lililo zidi kunichanganya.
“Ni siku nyingi hatujaonana Jojo?”
“Umefwata nini humu”
Niluuliza kwa ukali huku nikinyanyuka kwenye hili sofa, nikataka kumsogelea Nuru, ila mama mkwe akanyoosha mkono mmoja wa kulia akiashiria kwamba nisifanye jambo lolote kwa Nuru.
“Bado hujaacha hasira nami, nilihisi kwamba ukiwa na mtoto kwamba unaweza kujizuia hasira zako kwangu”
“Nimekuuliza umefwata nini humu?”
“Jojo”
Mama mkwe aliniita kwa sauti ya upole sana huku akinitazama.
“Bee mama”
“Nuru kwa sasa anafanya kazi chini yangu”
“Kivipi mama?”
“Ni maelezo marefu sana, ila kwa ufupi kwa sasa unaweza kushirikiana naye katika hatua zote za kuweza kulipa kwa hili ambalo nimefanyiwa na raisi”
“Samahani mama, sikuwahi kupinga chochote kile ambacho uliwahi kuniambia ila kwa hili ninakuomba sana, uweze kunisamehe siwezi kufanya naye kazi mtu fedhuli kama huyu ambaye hajui ni jinsi gani nimekaa nikiteseka kwenye jamii kwa ajili yake”
Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama mama mkwe usoni mwake.
“Hilo Jojo ninalitambua ila tambua kwamba kwenye maisha yako, adui yako anaweza kuja kuwa adui yako na rafiki yako anaweza kuja kuwa adui yako. Mambo hayo yote yametokea kwako. Kikubwa ni kupiga moyo konde na kusahau kila kitu kilicho pita”
Mama mkwe alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu. Mlango ukafunguliwa na kutufanya sote tugeuke na kutazama. Nikamuona mume wangu Eddazaria akiwa katika mavazi yake niliyo muacha nayo. Kwa haraka nikamkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu.
“Upo poa?”
“Ndio mume wangu”
Eddazaria akaniachia na kumsogelea mama kitandani pasipo hata kumtazama Nuru aliye simama pembeni ya chumba hichi, taratibu Eddazaria akakaa kitandani na kumkumbatia mama yake kwa nguvu huku akisikika akilia kwa uchungu. Tukatazamana na Nuru kidogo ila, nikawahi kuyakwepesha macho yangu kwani nina mchukia na nina kisasi naye kikubwa sana kwenye moyo wangu.
“Hei nipo sawa, nipo sawa”
Mama mkwe alizungumza huku akimuachia mume wangu.
“Mama ni lazima nimuue yule mshenzi, hawezi kukufanyia hivi”
“Najua una hasira ila ni lazima ujipange upya mwanangu.”
“Huu mguu wamekuvunja au wamefanyaje?”
“Walinipiga na ukatenguka vibaya”
“Mama naomba unipe amri mmoja ya kufanya”
“Amri gani?”
“Nina flash ambayo inaonyesha hatua zote za kuweza kulipua mabomu ya nyuklia, ninakuomba niweze kuyatumia hayo”
“Eddy, chuki ya mtu mmoja isiwagarimu watu wengine ambao hawana ugomvi na hii familia. Kuna mtu ambaye nahitaji muweze kushirikiana naye katika kuikamilisha hii kazi”
“Ni nani?”
“Ni Nuru huyo hapo”
Eddazaria akageuza sura yake na kumtazama Nuru, tukastukia Eddazaria akinyanyuka kwa kasi ya ajabu na kumshikia Nuru shingo yake na kumsukimia hadi ukutani huku akiendelea kumkaba koo lake akiashiri dhairi kwamba mpango wa mama mkwe kutuweka sehemu moja na Nuru mtu aliye tuyumbisha kwa kiasi kikubwa kwenye maisha yetu ni ndoto za aliniacha.
“Eddy, Eddy”
Mama mkwe aliita kwa sauti ya ukali kidogo, ila Eddazaria hakuhitaji kumsikiliza na akaendelea kumkaba Nuru koo lake.
“Eddy kama mimi ni mama yako muachie Nuru”
Eddazaria akamgeukia mama yake na kumtazama kidogo, taratibu akamuachi Nuru ambaye akaanza kujiweka weka sawa.
“Mama kwa nini unatuwekea huyu shetani?”
“Naombeni nyote munisikilize”
Mama mke aliendelea kuzungumza kwa hekima huku akijitahidi sana kuzuia hasira zetu dhidi ya Nuru.
“Nuru alifanya makosa hapo nyuma. Makosa yake ameyarekebisha kwa hili alilo lifanya kabla na baada ya nyinyi kufahamu ukweli huu ambao ninakwenda kuwaambia”
Mama mkwe akaka kimaya kidogo huku akitutazama kwenye nyuso zetu
“Nafuraha kuwa na watoto wapambanaji, nafurahi kupata mkwe mpambanaji. Ni kweli Nuru aliweza kuwakosea sana, si nyinyi bali hata mimi pia. Jojo nahisi unakumbuka kuna siku nilikuambia kwamba Nuru alitoroka kwenye mikono ya serikali mara baada ya kumkamata”
“Ndio mama nina kumbuka”
“Kuna watu ndani ya serikali ni wasaliti. Japo nilifanya kazi kubwa sana ila kuna wajinga wachache waliweza kuirahisisha. Kitu ambacho hata kwa Nuru yeye mwenyewe alisha wahi kunipigia simu siku tu niliyo teuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha kufwatilia madawa ya kulevya.”
“Nuru aliniambia kwamba, kitengo nilicho pewa ni geresha, na alinisihi sana niweze kukataa cheo hicho. Hapo awali nilihisi kwamba ananikejeli, ila hakuishia hapo aliweza kunitumia faili lenye siri nyingi mbaya sana za riaisi. Siri ambazo zilinichanganya na kunishangaza hata mimi. Nililitunza lile faili kwa umakini sana na wewe Jojo ndio mtu niliye kuelekeza ni wapi kwa kulipata japo sikukumalizia ni jinsi gani ufanye ili kulipata faili hilo ila yote katika yote sikufahamu kama uliweza kufanikiwa au hakufanikiwa kulipata?”
“Nililipata mama”
“Ila hukulifanyia kazi”
“Samahani mama kuna matatizo yalijitokea, tukashindwa”
“Okay. Nuru hakuishia hapo, aliendelea kuhakikisha kwamba ninafanikiwa kuweza kutoka kwenye mikono ya raisi”
“Lilikuwa jambo gumu sana kwao kwani nilikuwa ni mtu wa kuhamishwa hamishwa kutoka sehemu moja na kwenda nynyingine. Nuru hakukata tamaa, na hadi jana usiku kwa kutumia vijana wake”
“Kwa nini ulimsaidia maam yangu?”
Eddazariaalimuuliza Nuru huku akiwa amekazia macho ya hasira.
“Mimi ni Mtanzania, japo machoni mwenu muliniona ni mkosaji ila kwa namna moja ama nyingine nina nia nzuri na nchi yangu. Ninaipenda nchi yangu na ninahitaji nchi yangu iweze kwenda kwenye haki na misingi mizuri. Sipendi vitu vinavyo fanywa na baadhi ya viongozi, ni muda wa kuhakikisha kwamba wana step down wote ambao hawana sifa ya kuiongoza nchi yetu”
“Hiyo ndio sababu?”
“Ndio muheshimiwa”
Nuru alijibu kwa heshima zote hadi nikajikuta nikishindwa kuelewa kabisa, hekima hii na upole huu ameutolea wapi.
“Mama ninahitaji muda wa kulifikiria hili”
Meseji ikaingia kwenye simu ya Nuru, akaitoa mfukoni mwake na kusoma ujumbe huo.
“Muheshimiwa familia yako imefika”
Nuru alizungumza huku akimuambia mama mkwe.
“Nenda kawachukue na uwalete huku”
“Sawa mkuu”
Nuru akatoka ndani humu na kutuacha sisi watatu.
“Mama hivi kweli unamuamini huyu jini kweli?”
“Ndio nina muamini?”
“Mama kweli, hivi huoni kama anaweza kuja kutuulia humu ndani, yaani kirahisi rahisi tu una muamini au kuna mambo mengi chini ya haya ambayo yametokea eheee?”
Eddazaria aliendelea kuzungumza kwa ukali kidogo.
“Eddy kumbuka kwamba unazungumza na mama?”
Nilizungumza kwa upole na unyonge mkubwa sana huku nikimshika mume wangu bega la mkono wake wa kulia.
“Najua ni jinsi gani unavyo umia ila lengo letu sisi na Nuru ni kuweza kuiona nchi yetu inakuwa kwenye hali nzuri, yenye misingi mizuri na amani. Acha tusimame kwenye swala zima la nchi hayo mambo mengine ya chuki tawekeni kando kwanza, umenielewa Eddy”
“Mama…..”
“Unielewe, hii sio ombi sasa ila ni amri nikiwaka kama mkuu wako wa kazi”
Mama mkwe alizungumza kwa ukali na kumfanya mume wangu kunyong’onyea, mlango ukafunguliwa, anakingia wifi, mume wa wifi na mtoto wao, Judy ameongozana na mwanangu huku, shem akiongozana na watoto wake na mke wake. Tukaanza kusalimiana huku tukiwa na furaha tena ya kuonana tena kwa wingi wa namna hii.
“Jojo nakuomba”
Nuru alizungumza huku akitoka chumbani humu, nikamfwata kwa nyuma. Tukasimama kwenye kordo hii, akajaribu kunikumbatia ila nikamzuia asiweze kunigusa hata mkono wangu.
“Zungumza kitu ulicho weza kuniitia hapa”
“Jojo nimekumiss sana, natamani hata kukushika mkono wako tu nafsi yangu iweze kuridhika”
Nikatabasamu kwa kejeli huku nikimtazama usoni mwake.
“Hiyo ndio sababu iliyo kufanya uweze kumsaidia mama mkwe na sisi sote eheee?”
“Hapana Jojo, nimefanya haya yote kuyafuta matatizo yaliyo weza kutokea kati yetu sisi wawili. Sihitaji kuendelea kuishi kwa chuki, nimejifunza Jojo, nakumbuka kamaisha niliyo kukuta nayo kule China, nikakumbuka juhudu zako zote ulizo kuwa unazifanya, nikagundua zote ni kwa ajili ya maisha ya mazuri. Wewe jiulize ni kwa nini nilipo achiwa huru sikuhitaji kufanya jambo lolote baya hadi leo hii ndio umekuja kuniona hapa”
Nuru alizungumza kwa unyonge huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Jojo nisamehe, nahitaji msamaha wako wa kweli kabisa”
Nuru kwa msisitizo akapiga magoti chini jambo ambalo liliwashangaza hadi walinzi wake ambao wamesimama kwenye kordo hii ndefu.
“Najuta kuwa mpumbavu kwako, najutia kw amabaya na maovu yote ambayo niliyafanya. Jojo naomba unisamehe?”
Eddazaria akatoka katika chumba alipo mama mkwe na wanafamilia wengine, hali aliyo mkuta nayo Nuru hata yeye ikamshangaza na kujikuta akisimama huku akituzama kwenye nyuso zetu.
“Sihitaji kuwa na mwisho mbaya. Najaribu kutengeneza mwisho wangu, najaribu kuwa sawa kwa kila ambaye nimemkosea kwa maana siku zangu za kuishi hapa duniani zina hesabika”
Nikastuka sana kuweza kusika kwamba Nuru siku zake za kuishi hapa duniani zinahesabika.
“Zinahesabika kivipi?”
Nilizungumza huku nikiendelea kumtazama Nuru usoni mwake. Eddazaria kwa haraka akatembea hadi sehemu alipo Nuru, akachuchumaa na kumshika shati lake na kumtazamana usoni. Walinzi wake kwa haraka wakakoki silaha zao na kuuelekezea sisi. Nuru kwa ishara akawaomba walinzi wake waweze kushusha silaha zao chini na wakatii amri yake.
“Nijibu wewe shetani”
Eddazaria aliendelea kuzungumza kwa hasira huku akiendelea kumshikilia Nuru shati lake.
“Nina Kansa ya damu, siku yoyote na muda wwote ninaweza kufa”
Nuru alizungumza huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake, taratibu Eddazaria akamuachia Nuru na akaonekana kuishiwa na nguvu kabisa kwani ugonjwa ambao aunao Nuru kusema kweli kwa sasa ni ugonjwa ambao ni hatari sana duniani.
“Najua siku yoyote nitakufa, ila sitaki kufa kwa hasara, nahitaji nife kwa faida, nife na faidia ya kizazi kilichopo na kijacho ni lazima iwe hivyo Jojo”
“Eddy usinichukue kwa makosa niliyo yafanya. Nakuomba unisamehe, nilikutesa na kukuhangaisha kwa ajili ya mpenzi wako ila kwa sasa naomba unisamehe sana”
Taratibu Eddazaria akamshika Nuru mkono na kumnyanyua, wakakumbatiana kisha nami nikajumuika nao na kukumbatiana kwa pamoja.
“Nimekusamehe”
Nilizungumza kwa upole huku nikiwa ninaendelea kumkumbatia Nuru na mume wangu
“Hata mimi pia nimekusamehe, ila sihitaji utusaliti, ukifanya hivyo safari hii nakuhkikishia kwamba ni lazima nitakuua sawa.”
“Nimekuelewa Eddy”
Tukaachia na kurudi chumbani na nikawakuta mama akicheza cheza na wajukuu zake kitandani.
“Jamani naomba nikawaonyeshe nyumba ya kupumzikia”
Nuru alizungumza na watu wote tukakubaliana, nikamchukua Cleopatra kutoka kwa Judy, kwa ni kwa muda mrefu sana hatukuweza kuonana.
Tukaongozana na Nuru hadi kwenye nje ya jengo hili la gorofa ambalo limezungukwa na miti mingi sana.
“Hivi Nuru huku ni wapi?”
Nilimuuliza Nuru huku nikitembea naye.
“Tupo Kenya, huu mlima niliununua na kuwekeza katia hospitali hii kubwa pia kuna majengo yangu mengi sana ambayo nimeyajenga huku, huwa ninayatumia kupiumzika”
“Ahaaa, sasa kwa nini umeamua kutuleta huku?”
“Tanzania kwa sasa sio salama kwenu nyinyi. Munacho takiwa kukifanya hivi sasa ni kufanya mashambulizi ya kuwatoa maadui zenu mikiwa nje ya nchi na sio ndani ya nje na isitoshe ni kwamba maadui zenu wana nguvu, na nyinyi hamuna nguvu”
“Hapo sawa nimekuelewa, niambie tutaanza kuifanya vipi kazi?”
“Ngoja tutulie na tutajua ni jinsi gani tuna weza kuifanya hiyo kazi kwa maana ni kazi ambayo inahitaji akiuli na si kutumia tena nguvu ya damu za watu ili kuwatoa wao madarakani”
“Sawa sawa”
Nuru akaniomba ambebe mwanangu, nikamkabidhi na tukazidi kutembea hadi kwenye moja ya jumba moja la gorofa. Tukaingia ndani na akaanza kutuonyesha mandhari ya jumba hili ambalo lina wafanyakazi pekee. Kila mtu akachagua chumba chake anacho kuhitaji kwani kila chumba kina kila huduma inayo hitajika ndani ya chumba.
“Nyumba yake ni nzuri ehee?”
Nilimuuliza Eddazari huku nikimlaza mtoto kitandani.
“Yaa ni pazuri kwa kweli amejitahidi katika kujenga”
“Ni kweli, sasa Eddy unaonaje ukaitumia hiyo flash kumpatia Nuru ili tujue ni njia gani raisi anaweza kuachia madaraka?”
“Bado mapema hiyo itakuwa ni njia ya mwisho kabisa pale tu njia zote zitakazo pangwa zitakwenda kushindikana”
“Hivi mke wa raisi kweli si anaweza kututaja na kututangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba sisi ni wahusika wa tukio la kumteka”
“Hilo siwezi kusema atafanya au hato fanya, ila meseji ya mume wake kuachia madaraka nina imani kwamba anayo na ataifanyia kazi kwa umakini sana.”
“Mmmm ila hadi sasa hivi japo Nuru tumekuwa naye pamoja ila sijaiuingiza moyo wangu moja kwa moja katika kumuamini”
“Usimuamini mtu kabisa, tujiandae kisaikolojia chochote kibaya ambacho atahitaji kukifanya dhidi yetu basi nasi ni lazima tuweze kufanya jambo dhidi yake umenielewa hapo”
“Nimekuelew amume wangu”
“Vipi mtoto yupo poa?”
“Yaa kama unavyo muona hapo, japo namuonea huruma, kwani baba na mama yake tupo bize kiasi cha kuogopesha”
“Ni kweli kabisa”
Mlango ukagongwa, Eddazaria akatembea hadi ulipo na kuufungua.
“Dogo tunaweza kuzungumza?”
“Ndio tunaweza kuzungumza, baby nina kuja”
“Poa”
Nikaingia bafuni, nikavua nguo zangu zote na kuingia kwenye sinki la kuogea, nikafungulia maji kiasi yenye uvuguvugu kidogo, nikaweka sabuni ambayo ndani ya muda mchache ikatoa povu jingi sana. Taratibu nikaanza kuoga huku nikijisigua kila sehemu ya mwili wangu.
“Jojo jojo?”
Niliisikia sauti ya mume wnagu akiniita kwa nguvu, jambo lililo nishangaza sana.
“Nipo huku”
Eddazaria akaingia chumbani humu huku akiwa ameshika simu aina ya tablate.
“Kuna nini mume wangu”
“Huyu mseng*** lazima nimue haki ya Mungu vile”
Maneno ya mume wangu yakanitisha na kuniogopesana sana, kwani anayazungumza kwa hasira sana dhairi anaonekana kitu anacho kizungumza kimemkera sana na sijui ni nani ambaye amemkera kiasi cha kujikuta akitukana sana
Mume wangu akanionyesha picha ya pacha wake akiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi huku kukiwa na maelezo kwamba yeye ndio anaye husika na swala zima la kuwaua wanajeshi katika daraja la Kigamboni.
“Amekamatwaje?”
Nilijiuliza huku nikimtazama Eddazaria usoni mwake kwa maana natambua sehemu ambayo tulimpelekea pacha wake, ni porini na eneo hilo sio rahisi kwa mtu wa kawaida kuweza kwenda kabisa.
“Amekamatwaje, hilo ni swali gani sasa na wewe?”
“Nauliza hivyo kwa maana mimi na dokta tulimpeleka kule kwa babu yake?”
“Wapi?”
“Kwa babu yake”
“Fuc*** unamuaminije doktaaaa?”
Eddazaria alizungumza kwa hasira kubwa sana huku akinitazama usoni mwangu.
“Kwani si rafiki yako?”
“Mimi na yeye urafiki ulisha isha siku nyingi na ni msaliti, umesahau ni kitu gani ambacho alitufanyia siku ile pale hospitalini?”
Nikakosa cha kuzungumza kwani siku hiyo yeye ndio aliye tuchomesha kwa Nuru na watu wake na kama ingekuwa si shemeji basi siku hiyo tungeuwawa.
“Dokta amenisaliti katika mambo mengi sana, na siku ile ndio ilikuwa ni siku yangu ya mwisho kumuamini”
“Ila babu yake aliahidi kumsaidia mwenzio”
“Angeanza kujisaidia yeye kwanza alafu angefwata doto”
“Eddy, Eddy”
Tuliisikia sauti ya wifi ikimuita mdogo wake, akatoka bafuni.
“Hembu hiyo taarifa”
Niliisikia sauti ya wifi naye akiuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi. Kwa haraka nikamaliza kuoga kisha nikajifunga taulo na nikatoka bafuni humu, nikamkuta wifi akwia anaisoma habari hiyo ya kukamatwa kwa pacha mwenzie.
“Huyo ni raisi na watu wake ndio wamefanya hilo swala”
“Sasa tutuamuokoaje?”
“Mimi ninajua ni nini cha kufanya”
Eddazaria mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akatoka na kutuacha mimi na wifi.
“Wifi”
“Beee”
“Hivi pacha wake anaitwa nani?”
“Azaria na huyu ni Eddy”
“Eddazaria ni nani kati yao sasa”
“Kutokana na hali ya Azaria kuwa vile ilbidi tuwape jina moja la Eddazaria, ambalo mmoja anasimama kama Azaria na mwengine kama Eddy”
“Ahaa, kwa hiyo mume wangu ni Eddy na Azaria ni shemeji yangu?”
“Ndio”
Nikashusha pumzi taratibu kwa kushukuru kwa kupata ufafanuzi huu ambao kwa hapo awali ulinichanganya sana.
“Inabidi ukae uzungumze na mume wake asije akafanya maamuzi ya kijinga kwa maana si unaju halisi familia nzima inaswakwa”
“Sawa wifi”
“Kama bado hujapata kifungua kinywa, uje mezani huku sawa”
“Sawa:
Wifi akatoka chumbani humu, nikafungua kabati la nguo lililopo ndani humu na kukuta mataulo tu ndio yamening’inizwa. Nikamnyanyua Cleopatra kitandani na kutoka naye humu chumbani huku nikiwa nimejifunga taulo langu. Nikawakuta watu wote sebleni wakiwa wamekaa wakionekana wakijadiliana jambo.
“Jojo umekosa nguo?”
Mke mwenzangu kwa shemeji yangu aliniongelesaha
“Ndio best”
“Njoo”
Tukaondoka na mama Gody na kuingia chumbani kwao. Kutokana mwili wake hauna tofauti kubwa sana na mwili wangu haikuwa kazi ngumu kwa mimi kuweza kuvaa nguo zake.
“Hivi imekuwaje kuwaje nyinyi kuja kuchukuliwa na kuletwa huku”
“Yaani wee acha tu shosti. Baba Gody alirudi tu na kuniomba nikusanye kila kilicho changu pamja na vya watoto. Tukaingia kwenye gari hadi kwneye msitu mmoja tukakuta helicopter tukapanda na kuondoka, kila nilipo kuwa ninamuliza ni wapi tunakwenda hakuhitaji kunijibu”
“Mmmmm”
“Yaani wee acha tu, hii misuko suko sijui itaisha lini?”
“Itaisha tu”
“Yaani hadi nina ogopa sana, wanangu wanakosa malezi mazuri kwa ajili ya kuwahofia watu fulani serikalini”
“Hivi unafahamu juu ya swala la mume wangu kuwa na pacha mwenzake?”
“Ndio nafahamu?”
“Siku nyingi?”
“Hapana siku za hivi karibuni tu ndio nimefahamu, kwani wewe ulikuwa hujafahamu?”
“Sikuweza kulijua hili hadi juzi juzi tu hapa”
Tukatoka chumbani humu na kuwaacha watoto wetu na tukarudi sebleni. Tukapata kifungua kinywa cha pamoja huku mume wangu dhairi akionyesha kwamba hana furaha.
“Hili swala nitatuma vijana wangu waweze kwenda kulishuhulikia wala musijali?”
Nuru alizungumza huku akitutazama mimi na mume wangu.
“Hili swala niachieni mimi kwa maana nimesha chafuliwa vya kutosha”
“Sawa tunajua kwamba umechafuliwa, na watu wote watakuw awamefahamu kwamba ni wewe, ila vita iwe ya kisaikolojia na isiwe ya damu”
“Kivipi?”
“Ule ushahidi ambao mume upoteza, mimi bado ninao. Kupitia akaunti zako za Twitter, Facebooka na Istergram, zitumike katika kuachia uhushidi mmoja baada ya mwengine, kwa kufanya hivyo nina imani kwamba wananchi watakuwa pamoja nawe na sidhani kama kutakuwa na mwananchi amabye anaweza kupinga kile ambacho umekizungumza”
Nuru alizungumza pointi iliyo mfanya hata shemeji kutingisha kichwa.
“Ninakuunga mkono hapo. Huwezi kujitutumua na mtu ambaye anashikilia majeshi yote, cha kufanya kama alivyo sema dada hapo tumia ushahidi huo kutengeneza mioyo ya watu ambao kwa hivi sasa watakuwa wanakufwatilia kuhitaji kufahamu juu ya kukamatwa kwako”
“Alafu ni kweli Eddy, na wengi wao hawajui kama mupo mapacha, hiyo ndio nafasi ya wewe kuweza kuzungumza ukweli”
Wifi naye alizidi kuchangia mada hii.
“Unahisi wananchi wanaweza kunisaidia katika hili?”
“Asilimia mia moja. Wananchi ndio wenye nchi, walio wateua kwa umoja wao wanaweza kuwatengua muda wowote na wakati wowote ule ambao watataka watoke madarakani.”
Nuru aliendelea kzuungumza maneo ambayo yakazidi kunipa moja na kweli amebadilikika kwa asilimia kubwa sana.
“Baby huo ushauri hata mimi nina uunga mkono”
“Shem fanya hivyo, watu wote yupo pamoja nawe, tunakusaidia kusambaza kila post ambayoutaitoa kwenye mtandao wa kijamii na zitawafikia watu wengi sana”
Shemeji naye alizungumza kwa upole huku akimtazama mume wangu.
“Nitafanya hivyo, ninaomba uweze kunipatia ushiadi wa matukio yake yote mabaya, kama kuna mambo mengine ambayo Nuru unayafahamu ninakuomba uweze kunipatia”
“Usijali, nitakusaidia kutafuta zaidi na zaidi”
“Sawa”
Tukamaliza kula na Nuru akaanza kazi ya kumpatia kila mmoja simu pamoja na laptop yake kwa kazi hii ya kuutoa ushahidi unao onyesha matukio mabaya aliyo weza kuyafanya raisi kwa kipindi cha nyuma. Nuru akamkabidhi Eddy faili lenye mambo mengi sana kuhisiana na raisi.
“Niazie wapi?”
“Ingia facebook, kisha kanusha juu ya kukamatwa kwako”
“Ila zile picha zilizo samba ni za pacha wangu?”
Nuru alishauri.
“Ndio ni za pacha wako, ila si hakuna watu wengi huko nyuma wanao weza kufahamu juu ya pacha wako si ndio?”
“Ndio”
“Basi anza kuandika hivyo, akaunti yako ipi ina watu wengi?”
“Instergram”
“Ina watu wangapi?”
“Milioni tano”
“Jojo?”
“Mimi wanafika milioni mia sasa”
“Sasa Jojo anza kukanusha wewe?”
“Mimi?”
“Ndio”
“Huoni watu wanaweza kuhisi kwamba nina tumia akaunti ya mume wangu”
“Angeanza dogo kukanusha”
Shem alichangia mada hii.
“Sawa anza wewe”
Eddy akaandika post(ujumbe) wa kukanusha kukamatwa na jeshi la polisi pamoja na kuhusika na shambulizi la kuwaua wanajeshi katika daraja la Kigamboni.
“Tayari”
“Sasa tuanze kazi”
Nuru alizungumza na kila mmoja akaanza kuusambaza ujumbe huo. Ndani ya dakika kama tano ujumbe huo ukapata watu milioni ishirini walio usoma huku maoni yakianza kuminika. Hapa ndipo nikaona nguvu ya mitandoa ya kijamii, kwani watu wamefikiwa na ujumbe huo kwa haraka sana.
“Eddy ungewaongezea na video ukaituma instergram”
“Yaa hilo pia ni wazo zuri sana, tena mungekuwa wawili wewe na Jojo mukaenda live video, ingependeza sana”
“Basi ngoja nitumie akaunti yangu mimi”
Nilizungumza huku nikimtazama Nuru
“Sawa”
Eddazaria akanisogelea, nikaingia katika mtandoa wa Instergram ambao kwa sasa unaweza kurusha video hewani na watu wakawaona moja kwa moja(mubashara).
“Habari ndugu mashabiki, kuna taarifa zinaenea kwenye mitandao ya kijamii juu ya kukamatwa kwa mume wangu, Eddy na kupewa tuhuma za mauaji yaliyo tokea siku ya jana. Ila kusema kweli mimi kama mke wake nina kanusha hilo swala”
Nilizungumza huku nikiwa nimejielekezea simu mimi mwenyewe. Nikajisogeza pembeni ya mume wangu na tukaonekana wote kwa pamoja kwenye hii video. Maoni ya watu yakazidi kuongezeka huku wengi wakiwa waneonyesha furaha zao juu ya uwepo wetu wawili.
“Jamani hizo habari zilizo samba ni uongo, mimi nipo na mke wangu pamoja na mtoto wetu amelala chumbani. Sasa inapo tokea kikundi cha watu wanajaribu kunichafua, basi musikae mbali sana na akauti zangu, nitakwenda kuachia ushahidi wa kwa nini wameamua kunichafua, na ninawapa lisaa moja kama hawato nitafuta, nitahakikisha kwamba ubaya na mambo yote mabaya ambayo waliyafanya, ninakwenda kuyatoa hewani. Nina imani kwamba wengi wenu mutakuwa munajiuliza ni kina nani, ila woa wenyewe wanajijua. Asanteni”
Baada ya Eddy kumaliza kuzungumza maneno hayo akasogea pembeni.
“Jamani kama mulivyo weza kuona, mume wangu nipo naye hapa na tunaendelea na maisha yetu kama kawaida. Ninawapenda sana na tutakutana na muda mchache tu baada ya hili video”
Nikakatisha video hii na kuwatazama watu walipo humu sebleni, kabla sijataka kuzungumza chochote simu ya Nuru ikaanza kuita, akaipoke ana kuiweka sikioni mwake.
“Ndio”
“Poa nitumie sasa hivi”
Nuru baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akakata simu na kututazama.
“Kuna mpelelezi wangu ameniambia kwamba ana nitumia video ya siria ameipata sasa hivi ambayo itashangaza dunia nzima”
“Ni video gani?”
Niliuliza huku nikiwa na shauku ya kutaka kujua ni video gani
“Sifahamu ni video gani, ila tuwe wapole na tusubirie tuione”
Ujume wa meseji katika mtandao wa whatsapp ukaingia katika simu ya Nuru na kutufanya sote tumtazame. Nuru akaitazama simu yake kwa dakika kadhaa tukamuona akiweka mdomo wake mdomoni huku macho yakiwa yamemtoka. Jambo hili likanifanya nisimama ili niweze kutazama ni kitu gani anacho kitazama ila akanizuia kwa ishara ya kuninyooshea mkono.
“Ninawatumia kila mtu kwenye whatsapp yake”
Nuru alizungumza, kila mtu akaanza kuingiziwa video hii, nikaifungua video hii kwa haraka, nikaitazama kwa sekunde kadhaa na kujikuta mapigo ya moyo yakianza kunienda kasi. Video hii inamuonyesha mama mkwe akiwa katika chumba cha mateso, huku mtu ambaye anampatia mateso ni raisi mwenyewe. Nikamuona shem machozi ya hasira yakianza kumlenga lenge, nikalitupia jicho langu kwa wifi na kumuona akiishusha simu yake akionekana ameshindwa kabisa kuendelea kuitazama video hiyo. Nikamgeukia mume wangu, huyu ndio hana nafuu kabisa, kwani ana tetemeka hadi meno yake ya mdomoni yana gongana gongana kana kwamba amefungiwa katika sehemu yenye barafu tupu.
Nikazidi kuumia moyo wangu pale nilipo muona raisi akipiga mguu wa mama mkwe kwa kutumia fimbo nene huku akiukanyaga. Kwa bahati mbaya hii video haina sauti na imerekodiwa na CCTV kamera.
“Njia muliyo nipa nina hisi sio nzuri, njia hii ndio nzuri”
Eddy alizunguumza huku akitoa flash tuliyo ikuta kwenye kisanduku cha dhahabu kilicho kuwa kimeanguka kwenye ajali ya ndege. Kwa haraka nikampokonya Eddy flash hii kwani mimi na yeye ndio tunafahamu ni kitu gani ambacho kipo ndani ya flash hii. Eddy akaanz akunipokonya ila nikajitahidi kwa juhudi zangu zote kuto kumuachia hii flash hadi watu wakaaanza kutuachanisha wakiamini kwamba tunagombana.
“Nipe flash hiyo”
“Hapana Eddy huwezi kuwaona raisi wasio na hatia, kwa nini lakini?”
“Nimekuambia nipe”
“Dogo tulia”
Shemeji alizungumza kwa ukali huku akimtazama Eddy. Eddy taratibu akawa mnyonge huku akigema kwa hasira.
“Hiyo flash ina nini Jojo?”
“Ina activation code za kuruhusu mabomu ya Nyuklia ambayo yametengenezwa hapa Tanzania”
“Tanzania ni wapi kunatengenezwa mabomu ya Nyuklia?”
Wifi aliuliza huku macho yakimtoka.
“Kuna kambi moja ya jeshi inafanya hivyo”
“Nipe”
Shem alizungumza hukua kinyooshea mkono, nikamkabidhi flash hii, akarudi kwenye kiti alicho kuwa amekaa. Akaichomeka flash hiyo kwenye laptop yake.
“Hivi tunaweza kuunganisha laptop yangu na tv yako Nuru?”
“Ndio, uzuri ni wireless hiyo tv”
Nuru alizungumza huku akisogelea laptop ya shemeji, akaanza kuminya minya baada ya muda kile kinacho onekana kwenye laptop ya shemeji, vinaonekana kwenye tv hii kubwa sana iliyo hapa sebleni.
“Ohoo Mungu wangu”
Mke wa wifi alizungumza kwa mshangao huku akiiosogelea tv hii huku akishangaa michoto michoro hiyo ya mabomu hayo makubwa sana.
“Rich si unaweza ku activate hizi code?”
Shema alimuuliza shemeji yake kwa mdogo wake.
“Ndio”
Shema kamgeuzi mume wa wifi laptop hiyo. Taratibu Rich akaanza kuminya minya batani za laptop hiyo, mwili mzima ukaanza kunitetemeka kwani endapo watayatumia mabomu hayo basi yanaweza kwenda kuwaua wananchi wengi sana ambao hawana hatia.
“Mabomu yapo tayarik wa kutumia”
Rich alizungumza na kumfanya Eddy kutabasamu.
“Hawawezi kweli kuyazuia?”
“Hakuna ambaye anaweza kufanya hivyo kwa maana hii ndio funguo ambayo inatumika katika kuyarusuhu kufanya kazi”
“Jamani hilo sio swala ambalo tunatakiwa kulifanya, kumbukeni kwamba kuna wamama na watoto ambao wanaweza kuathirika na bomu hilo na mukiyatumia kumbukeni hatuendi kuwa maadui na Tanzania pekee, ila dunia nzima inaweza kutushuhulikia, hatuwezi kupambana na dunia, tutakufa vifo visivyo na faida yoyote kwenye maisha yetu”
Nuru alizungumza kwa upole sana huku akitutazama kwenye nyuso zetu.
“Tujaribu kuzuia hasira zetu, aliye fanya hili jambo ni mtu mmoja na si watu wote, hembu tujaribuni kuwa wapole?”
Wifi alizungumza kwa upole sana.
“Unaona alicho fanyiwa mama ni kitu kizuri si ndio?”
Shem aliuliza kwa ukali.
“Hakuna anaye weza kusema kwamba ni sahihi. Ila tujipe muda, hayo maamuzi ya kutumia mabomu hayo ya nyuklia sio mazuri kwa maana hayamgusi mtu mmoja mmoja yanawagusa watu wengi”
Wifi aliendelea kujibu kwa upole na hekima kubwa.
“Rich ruhusu moja na lielekezee ikuku”
“Richa kama mimi ndio mke wako na uananipenda usifanye hilo jambo ni hatari sana”
“Nimekuambia elekezea ikukulu sasa hivi”
“Usifanye, mbona munakuwa na roho mbaya kama wanyama. Mbona munakuwa hamuna utu kati yenu ni damu za watu wangapi munataka kuzimwaga. Munahisi hilo bomu ni andazi na litakwenda kumuua raisi peke yake eheee?”
Wifi alizungumza kwa ukali sana huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na kusogea sehemu aliyo kaa mume wake. Shemeji akasimama na kumsogelea wifi, dhairi inaonyesha kwamba tayari hali ya kuto kuelewana imeingia katikati.
“Nionyeshe ni wapi ambao ninatakiwa kuminya ili niyaruhusu mimi mwenyewe?”
Shem aliendelea kuzungumza kwa ukali na jazba kubwa.
“Usimuonyeshee”
“Unanijua, kaa mbali na mimi nitakubamiza hata kama mume wako yupo hapa”
“Dhubutu, unahisi mimi ndio yule uliyekuwa ukiionea kipindi nikiwa mtoto eheee?”
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio na wasiwasi mwingi ukazidi kunitawala. Nikamtazama mke mwenzangu, nikamuona jinsi alivyo jawa na mshangao mkubwa huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Jamani tuelewane basi”
Nuru alizunguzungumza kwa upole.
“Wewe koma hili swala ni la kifamilia na si la kwako, umenielewa?”
Shem alizungumza kwa ukali sana hadi Nuru akaijikuta akikaa kwenye sofa lililopo pembeni yake.
“Nimekuambia kwmaba yaelekezee mabomu hayo ikuku sasa hivi?”
“Nimekuambia usifanye hivy……”
Kabla wifi hajamalizia sentensi yake tukastukia kumuona akipepesuka na kuanguka chini, hii ni mara baada ya kusukumwa na shem. Rich akataka kusimama ila akazuiwa na shem na kukalishwa kwenye kiti chake ili afanye kile alicho kizungumza shemeji. Wifi akanyanyuka kwa haraka huku akiwa amefura kwa hasira, uzuri wa sura na upole wote ambao siku zote nilikuwa nikimuona nao umepotea usoni mwake.
Akarusha ngumi kadhaa zilizo mpiga shemeji kifuani na kumfanya na yeye kujibu mashambulizi hayo ambayo ni makali sana. Ugomvi wa ndugu siku zote huwa hauingiliwi. Wakaangushana chini na kuanza kubingirizana huku kila mmoja akionyesha kuwa na nguvu sana na mwenzie, japo wifi yangu ni mwanamke, ila ana nguv nyingi sana za kupambana na mwanaume. Mke mwenzangu akaangua kilio cha sauti huku akiwa amenijikunyata. Rich akashindwa kunyanyuka kwenye kiti chake naye mwili mzima una mtetemeka. Nuru naye alipo kaa hajitingishi hata mkono. Nikamgeukia mume wangu nikamuona akiwa amewakazia macho dada yake na kaka yake hao wanao endelea kuparangana hapo chini huku wakishindiliana magumi mazito. Eddy akashusha pumzi taratibu, akaurudisha mkono wake wa kulia nyuma ya kiuono na kuchomoa bastola, akaikoki, jambo lililo nifanya nianze kuhisi haja ndogo. Eddy akafyatua risasi mbili juu hewania na kusababisha wifi na shemeji kuachiana huku kila mmoja akiwa anamwagikwa na damu za mdomoni. Eddy akatembea hadi kwenye laptop yenye flash, akaichomoa flash hii na kuishia na mkono wa kulia.
“Mimi ndio mwenye mamlaka ya kufanya chochote na hii flash. Acheni using** wa kupigana pigana, mama ni mgonjwa, kila mtu ana mtoto mdogo hapo. Munataka muuane ili munipe mimi shida ya kuwalelea watoto wenu si ndio?”
Eddy alizungumza kwa hasira huku akiwatazama kwenye nyuso zao. Taratibu shem akanyanyuka huku akijipangusa damu zake mdomoni.
“Acheni ufal** muda huu ni muda wa kuhakikisha kwamba tunamtetea vipi mama na doto, nyinyi munaleta maswala ya kupimana ugali, tena mbele ya watu ambao hata historia ya utoto wetu hawajawahi kuiona. Hayo mambo ya kitoto hakuna kuyafanya tena sawa?”
Eddy aliendelea kuzungumza kwa ukali, taratibu shem akampatia wifi mkono na wakanyanyuana.
“Kazi iendelee”
Eddy alizungumza huku akirudi kwenye kitu alicho kuwa amekaa. Watu wote tukawa kama tumepigwa na bumbuwazi.
“Munanikodolea nini macho, tuendelee na kazi iliyo tuweka hapa”
Taratibu nikarudi kwenye kiti changu na nikakaa, nikaichukua simu yangu na kutazama meseji nyingi nilizo zipata kupitia hii Instergram.
“Hii video ninaiweka hewani”
Eddy alizungumza huku akiminya minya simu yake.
“Hewani, Eddy huko ni kumdhalilisha mama”
Nikajitahidi kuchangia mada hii kwa maana naona watu tayari wamesha rudi kwenye hali zao za kawaida.
“Story itaanzia hapa, kabla ya kufukunua mambo ya ndani, basi nilazima raia waweze kufahamu hili jambo kwanza”
“Rusha”
Shem alizungumza kwa sauti ya upole, na nikakosa cha kuzungumza kwani wezangu ambao ninategemea waweze kunisaidia katika kunishauri wamenizidi nguvu na hata mke mwenzangu bado anaendelea kulia kwa uchungu tu. Eddy akaiweka video hii kwenye akaunti zake zote katika mitando ya kijamii huku akiandika maandishi yanayo someka ‘Story yetu inaanzia hapa, naamini wote munamuona ni nani ambaye amenzisha vita na bado amekwenda mbali na kunisingizia kwamba mimi ndio muhusika wa mauaji ya wanajeshi wake, sasa mutaendelea kuyaona mengi sana kwenye siku hii yaleo.’
Kama jukumu letu, tukaanza kusambaza video hii ambayo ndani ya muda mfupi sana ikaanza kurushwa na vyombo vikubwa vya habari duniani, ikiwemo BBC, SKY NEWS, CNN na ALJAZIRA
Wananchi wakaanza kucharukwa kwenye mitando ya kijamii huku kila mmoja akiendelea kutoa maoni yake na katika kupitisha kwangu macho sikuona hata mmoja ambaye aliweza kusifia kitendo hicho, kila mmoja anaonyesha kusikitishwa kwa kitendo hicho kibovu sana cha unyanyasaji.
“Video ndani ya dakika hizi ishirini katika chaneli yangu ya Youtube imeangaliwa na watu zaidi ya bilioni mbili na nusu duniani kote”
Nilizungumza huku nikiwa nimeshangazwa na muitikio huu mkubwa sana wa watu ambao wengi wao ni wapenda haki.
“Jamani tunaifanya hii kazi hivi IP Adress zetu hawawezi kuzitafuta kweli na mwishowe tukakamatwa?”
Niliuliza huku nikimtazama Nuru usoni mwake.
“Hakuna satelait ya nchi yoyote duniani inayo weza kunasa hili eneo wala mawasiliano yanayo toka katika eneo hili. Hivyo hawawezi kufanya chochote, katika jambo hilo nina waomba muweze kuwa na maani tu”
“Jamani kuna sehemu ambayo mumeona maoni ya kiongozi yoyote?”
“Mmmm viongozi wanafunguka nao ni balaa”
Richa alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu kana kwamba hapakuwa na ugomvi wowote ambao umetokea.
“Nuru”
“Bee”
“Ninaweza kuzungumza na raisi sasa hivi?”
“Ngoja nijaribu kumtafuta”
“Unampigia kupitia simu yako?”
“Hapana ninampigia kijana wangu mmoja mwenye uwezo wa ku-hack mawasiliano yoyote ya kimtandao”
“Ahaa, sawa sawa”
Nuru akazungumza na kijana wake huyu kupitia simu ya mkononi, baada ya dakika kadhaa akaingia kijana mwenye hasili ya Kihindi na usoni mwake amavalia miwani kubwa kidogo huku mkononi mwake akiwa ameshika laptop yake.
“Eddy pale anataka kuzumza na raisi wake je unaweza kufianya hiyo kazi?”
“Ndio, je anataka kuzungumza naye kwa video au simu?”
Tukatazamana mimi na Eddy.
“Video”
“Wewe unataka sura yako iuonekane?”
Nilijikuta nikiuliza swali lililo lenye jibu lake.
“Sasa ionekane mara ngapi mke wangu?”
“Ohoo sorry nimekosea”
“Kama ni video basi naomba munipe dakika kumi na tano kwani ninataka ku=hack signal za tv broadcast zote duniani, kisha nina hack white house call zote na tutazitumia sisi kwa muda wote ambao utakuwa unazungumza na raisi”
“Ngoja mara moja hapo sijakuelewa.”
Eddy aliuliza huku sote humu ndani tukimtazama kijana huyu wa kihisi.
“Yaani ukipiga video hiyo call kwa ikulu ya Tanzania watapokea kuona inatoka kwa raisi wa Marekani kwa hiyo hawawezi kuikataa, lazima wataipokea tu”
“Ahaa hapo nimekuelewa hembu fanya mambo sasa”
Kijana huyu akafungua lapotop yake na kuanza kufanya kazi anayo ijua yeye mwenyewe. Ni kijana ambaye kwa kumuangalia hivi unaweza kumuona ni kama zezeta fulani hivi ila uwezo wake ni mkubwa sana.
“Utazungumza nini mume wangu?”
“Wala usijali”
“Inabidi sasa hivi nywele uziweke vizuri bwana si unajua dunia nzuma inakwenda kukuatazama”
“Wala usijali, hivi hivi tu kila jambo linakwenda kuwa sawa.”
Tukaendelea kusubiria huku kwa muda huu nikiwa nipo bize nikipitia pitia maoni ya watu wengi duniani.
“Tayari kila kitu njoo ukae hapa”
Kijana huyo alizungumza na Eddy akanyanyuka na kutembea hadi kwenye sehemua lipo kaa kijana huyo. Kijana huyoa kampisha Eddy kwenye kiti na akaka.
“Wakeni Tv katika upande wa chaneli”
Kwa haraka Nuru akiwa na shahuku kubwa sana akabadilisha mfumo wa tv na kuweka upande wa chanel. Kijana huyu akaminya batani moja ya laptop yake kisha akasimama pembeni kwa ishara ya vidole akaanza kuhesabu hadi tatu. Chaneli ambayo ilikuwa ikionyesha miziki kwenye hii Tv ikabadilika na kuonyesha picha ya nembo inayo tumiwa na ikulu ya Marekani. Baada ya muda tukamuona raisi wetu kwenye kipicha kidogo cha pembeni akionekana yupo tayari. Hazikuisha hata sekunde kumi akaonekana Eddy mume wangu na kumfanya raisi kustuka sana.
“Usihangaike kukata wala kufanya chochote kwa maana dunia nzima inatutazama hivi sasa. Nahitaji ufanye kile ambacho nitakuambia uweze kukifanya. Umenielewa muheshimiwa raisi?”
Swali la mume wangu likamfanya raisi ashushe pumzi taratibu, huku jasho likianza kummiminika usoni mwake kwa woga.
“Dunia nzima ina imeweza kuona ukatili wako, ulio weza kumfanyia mmoja wa wateule wako, ulio wateua kwa kinya chako na maamuzi yako wewe. Una maelezo yoyote ambayo unaweza kuyatoa kwa dunia kwa nini uliweza kumfanyia hivyo mama yangu?”
Watu wote tukashuhudia jinsi raisi koo la raisi linavyo cheza ikiashiria kwamba amemeza fumba zito la mate.
“Bwana mdogo unaniuliza maswali wewe kama nani?”
“Kama mtoto wa Bi Joyce”
“Hahaaa…..sina muda wa kumjibu mpumbavu mmoja kama wewe. Hata kama dunia inanitazama ila wewe ni mpuuzi mmoja ambaye unataka kuiyumbisha nchi. Unahisi kwamba Watanzania watakuelewa kwa ujinga wako unao uhitaji eheeee?”
Raisi alimjibu Eddy kwa dharau na kutufanya sote tumgeukie na kuacha kuitazama Tv hii kubwa iliyopo hapa sebleni.
“Kitu kingine nikuambie bwana mdogo, unahitaji kuzisafisha dhambi zako kwa kunichafua mimi. Hahaa bado hujafanikiwa bwana mdogo na nina kuhakikishia kwamba serikali ninayo iongoza lazima itakutafuta na itakustaki kwa makosa yote uliyo yafanya”
Wasiwasi sasa ukahamia kwa mume wangu, akashusha pumzi nyingi sana huku akionyesha dhairi kwamba anaelekea kushindwa. Nikamsogelea Nuru na kumgong’oneza sikioni mwake.
“Lile faili lenye ushahiri wa mambo mabaya aliyo yafanya raisi lipo wapi?”
“Lipo ofisini kwangu?”
“Kwenye hii hii nyumba?”
“Ndio”
“Naliomba sana, kwa maana Eddy pale tayari amesha shindwa kuzungumza si unamuona akiwa anaweweseka”
“Sawa”
Nuru akatoka kwa haraka sebleni humu, nikasimama yumba ya laptop hii ambapo Eddy ananiona vizuri. Nikamuita kwa ishara na akanitazama.
‘Kuna mafaili yale ya dhambi zake alizo zifanya Nuru anakwenda kulichukua’
Nilizungumza kwa kwa sauti ya chini sana na Eddy akatingisha kichwa huku akitabasamu.
“Serikali initafute na kunihukumu kwa makosa gani ambayo nimeyafanya. Unahisi kwamba nchi ya China inaweza kwenda kukuacha hai kwa kumuua waziri mkuu kwenye ajali ya ndege?”
Raisi macho yakamtoka, hali ya wasiwasi ikahamia kwake.
“Unahisi kwamba Russia nayo inaweza kukuacha madarakani kwa dhambi zao mashambulizi ambayo uliwahi kuyafanya chini chini juu ya nchi hiyo Eheeee……?”
Raisi akakaa kimya.
“Kuna dhambi nyingi sana ambazo raisi wa nchi unayo iongoza hawakuwahi kuzifahamu. Ngoja niiambie dunia kitu kimoja ambacho ilikuwa haikifahamu juu yako. Video ya kumpiga mama yangu na kumdhalilisha, ilitokana na ushahidi ambao aliiushikilia na ulimpiga ili kuonak wamba ushahidi huo unakwenda kupotea. Na umekuwa ni mtu wa kuyawinda maisha ya sisi watoto wake kwa maaana unaona kwamba tumekushika pabaya. Sasa ili kuwahakikishia Watanzania wote, sasa kila kitu tunakwenda kukiweka hadharani, na baada ya kuweka kila kitu hadharani, ninawaomba wananchi wote wa Tanzania kupiga kura ya kumtoa raisi madarakani kwa maana hufai kuwaongoza watu ambao hawajui hata nini maana ya vita. Watanzania mukimuacha madarakani, nchi kama hizo mbili nilazima zitaanzisha vita juu ya Tamzania, je mupo tayari mufe, mupo tayari makazi yenu na mali zenu zipoteee kwa ajili ya mjinga mmoja? Najua majibu yenu ni hapana, sasa ninawaomba hakikisheni kwamba muna mtoa mdarakani.”
“Hakuna kitu kama hicho mpumbavu weweeeee”
Raisi alifoka sana huku akinyanyuka kwenye kiti chake.
“Unakwenda wapi muheshimiwa, kaa uweze kuona ni nini ninacho kuonyesha”
Raisi akamtazama Eddy kisha akarudi kwenye kiti chake.
“Sikuzote hasira haijengi, ila hekima ndio hujenga. Ulihisi ukitumia nguvu ndio unaweza kushinda kwenye kila kitu. Kwa haya ninayo yazungumza ninakuambia kwamba huwezi kushinda mioyo ya Watanzania ambao wanakwenda kujua ukweli wa upuuzi wako wote ulio ufanya.”
Nuru akaingia ndani hapa akiwa na faili, moja kwa moja akatembea hadi kwenye kiti alicho kaa Eddy, akamkabidhi faili hilo na Eddy akalishika na kuanza kulizungusha zungusha.
“Humu ndipo ulipo ushenzi wako wote. Sasa tuanze kuchambua moja baada ya jengine. ICC ninaiomba nayo iweze kukaa macho kwa maana lazima ukafunguliwe mastaka”
“Bwana mdogo, hembu tuzungumze kwa herufi kubwa kidogo. Hembu disconnect hayo mambo uliyo yaweka kwenye matv?”
Raisi alizungumza kwa unyonge akionyesha dhairi kwamba anaelekea kushindwa na kuogopa.
“Ulimwaga ugali, acha nimwage ugali, ili kama ni kulala njaa tulale wote”
Simu ya Nuru ikaita, akaitoa mfukoni na kuiweka sikioni mwake.
“Sawa mkuu”
Nuru akaanza kutembea hadi sehemu alipo Eddy na kumkabidhi simu.
“Nani?”
“Chukua”
Eddy akaichukua simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Mama”
“Sawa mama”
“Nimekuelewa”
Eddy akakata simu hiyo na kuiweka pembeni.
“Una bahati mama amenizuia kufanya chochote nilicho kusudia kukifanya. Ila una masaa ishirini na nne ku step down kwenye madaraka yako. Yakipita masaa hayo ishirini na nne basi ninakwenda kuweka kila kitu wazi na ushahidi wote nitautuma kwenye mitandoa ya kijamii kuanzia picha, maandishi na sauti. Mchana mwema muheshimiwa raisi. Na ninawaomba watu wote kwua wavumilivu hadi kesho muda na wakati kama huu nitarudi tena hewani”
Eddy mara baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na kijana aliye shuhulikia swala hilo akakata mawasiliano hayo na tv zote zikarudi kwenye vipindi vyao vya kawaida.
“Mama akhaaaa”
Eddy alizungumza huku akitoka sebleni humu, nikaanza kumfatwa kwa nyuma.
“Imekuwaje?”
“Mama amenizuia kufanya chochote”
“Kwa nini?”
“Ndio ameniambia kwamba nikatishe nikazungumze naye”
“Au hajapenda wewe kufanya vile?”
“Sijuia”
Tukaelekea katika hospitali aliyopo mama na moja kwa moja tukaelekea katika chumba chake alicho lala na kumkuta akiwa na Gody wakizungumza na kucheka.
“Mama”
“Ni nini ambacho unataka kufanya?”
Swali la mama mkwe likatufanya sote tuwe kimya.
“Unahisi njia ya kutumia vyombo vya habari inaweza kumtoa madarakani raisi?”
“Mama ila……”
“Ila nini. Wewe Jojo si nilikuambia kwamba hilo faili mulipeleke kwenye mahakama kuu ya dunia na kama kufunguliwa mastaka afunguliwe huko si ndio?”
“Ndio mama?”
“Sasa kujianika sura yako kwenye vyombo vya habari hiyo ndio mahakama kuu eheee?”
Mama mkwe alizungumza kwa ukali.
“Gody kacheze nje?”
“Muache mjukuu wangu, yaani ana akili kukushinda hata wewe jibaba lizima. Unahisi huyu ataiga mfano gani?”
“Ila mimi ni wapi nilipo kosea?”
“Hujui ulipo kosea, umakalia kuwashinikiza watu waweze kupiga kura za kumtoa raisi madarakani, unahisi hii vita ni ya wananchi eheeee. Tayari umesha yataya mataifa makubwa China na Russia kwamba raisi amehusika kwenye matukio ya kigaidi yaliyo yalenga mataifa hayo, je unahisi sasa hivi wapo kwenye attention ya namna gani juu yako na kutaka kufahamu ukweli wa hicho ulicho kizungumza?”
Mama mkwe aliendelea kuzungumza kwa kufoka na kutufanya mimi na mume wangu kunywea sana japo mashambulizi anapelekewa yeye mwenyewe, ila kwa namna moja ama nyingine watu wote tulio kuwa sebleni tulikubaliana naye kwa kile alicho kifanya.
“Mama kwa nini unamtetea?”
“Nina mtetea nani, unahisi nilicho fanyiwa ni kizuri. Kila kitu kina utaratibu, kumbuka raisi haongozi familia anaongoza nchia mbayo ina watu wa kila aina. Wenye akili na waiso na akili. Unahisi wale wasio na akili ulivyo wajaza ujinga wako, wakiamua kuandamana ni nini kitatokea, mbona mwanangu Eddy haukui wewee. Jojo na wewe umeshindwa kumshauri mume na umekaa naye unamuacha anazungumza blaa blaaa tu huko duniani?”
“Mama ila tulijadiliana na kila mtu kule sebleni?”
Nilizungumza kwa upole kwa maana yupo kikaangioni.
“Kina nani?”
“Shemeji, wifi yaani watu wote”
“Pumbavu kwa hiyo akili zenu zote ziliishia kwa kumuagiza mpuuzi mwezenu akajianike lisura yake. Hivi unahisi ukitoka katika eneo hili ni watu wangapi watakuwa wanakuwinda ili wakuue. Kuna watu wamewekeza kwa raisi huyo ili mambo yao yaende. Ukimuaribia yeye kuan kundi kubwa la watu nyuma yake wanapata shida. Wewe si ulikuwa shahidi kwa Kibopa si ndio?”
“Ndio mama”
“Yeye si ndio aliye mshinikiza raisi anitoe katika safasi aliyo niteua?”
“Ndio mama?”
Niliendelea kuwa mnyonge
“Sasa ilimuacheje mpumbavu mwenzio akafanya ujinga huo”
“Ila mama hembu fikiria mtu anakupiga ana kudhalilisha namna hiyo je angekua?”
“Ila hajaniua?”
“Ndio hajakuua, ila ni wakati wa yeye wananchi wakatambua kabisa, kwamba hatufai”
“Sogea hapa”
Eddy akamsogelea mama yake karibu. Tukastukia kofi zito likitua shavuni mwake na kutufanya mimi na Gody kushangaa.
“Pumbavu wewe, tumia akili yako niliyo kukuza nayo na si ujinga, ujinga”
“Kwa hiyo mama unanipiga kwa kuitetea haki yako si ndio?”
“Sijakukuza kuwa mjinga”
“Ni kitu gani ambacho kinakufanya mama umteteee?”
Eddy naye alikuja juu na upole wote ukaisha.
“Tumekuwa ni watu wa kuzunguka zunguka kama kunguru kwa ajili ya fala mmoja. Mama umenikuza kuwa jasiri na si kutumia akili kwa mpumbavu ambaye najua ni mpumbava. Amefanya ujinga nilazima na sisi tumuadamishe, la sivyo akikataa kutoka madarakani kwa njia ya makubaliano, ninakwenda kutumia nguvu, ambayo itagarimu damu za maelfu ya watu. Umenielewaaa?”
Eddy alizungumza huku akimsogelea mama yake usoni na kumfanya mama mkwe kuanza kulengwa lengwa na machozi. Eddy akatoka ndani humu na kutuacha na mama mkwe ambaye taratatibu machozi yakanaza kumwagika usoni mwake.
“Ohoo Mungu sijalea wanangu kuwa makatili namna hii. Ni wapi nilipo kosea Mungu wangu”
Mama alizungumza huku akilia, taatibu Gody akamsogela bibi yake na kumkumbatia.
“Bibi, ba mdogo ana hasira tu zitaisha”
Gody alizungumza kwa upole sana huku naye akimwagikwa na machozi usoni mwake. Nikatamani kutoka kumuwahi mume wangu ila nikashindwa kumuacha mama mkwe kwenye hali kama hii.
“Au kwa sababu baba yao amefariki eheee?”
Mama mkwe alizungumza kwa uchungu na kijikuta taratibu nikiaa kitandani hapa.
“Mama, usiseme hivyo. Kile ulicho fanyiwa hakuna ambaye amependezeshwa nacho. Kwa nini unataka kuwa mnyonge na kuwaacha maadui zao wakashindwa, ikiwa hapa ulituambia kwamba tusaidiane na Nuru katika kulipa kisasi ehee mama?”
“Jojo?”
“Beee mama”
“Hadi nilipo kuachia faili lile nilitambua kwamba una akili kumshinda hata mwanangu. Sikukuachia tu, nilijua kwamba lazima utafwata kile nilicho kuambia. Wanangu ni wendawazimu wakiamua ya kwao wameamua. Sasa hembu ona anavyo sema kwamba atatumia nguvu ya kumtoa raisi madarakani. Anataka kumwaga damu kwa nini lakini?”
Mama mkwe alizungumza kwa kulalama.
“Yeye kama yeye ana nguvu gani za kupingana na serikali jamani?”
Nikaka kimya kwa muda huku nikimtazama usoni mama mkwe.
“Nguvu anayo”
Nilizungumza kwa kifupi na kumfanya mama mkwe anitazame kwa mshangao mkubwa sana.
“Nguvu anayo. Nguvu gani?”
“Ana flash ambayo ndio ina weza kuendesha mabomu yote ya nyuklia yanayo tengenezwa kwa siri hapa Tanzania”
“MUNGU WANGUUUU………..”
Mama mkwe akataka kushuka kitandani ila kwa haraka nikamzuia, asishuke.
“Niache, Jojo huwezi kunizuia ikiwa chizi wangu anakwenda kumwaga damu za watu niache nishuke”
“Hapana mama, hawezi kufanya hilo jambo”
“Eddy ni mwanangu, ninamjua vizuri sana, atakwenda kufanya upumbavu huo”
“Basi mama ngoja nikamtafute, ila nina uhakika hawezi kufanya jambo hilo”
“Hakikisha una mzuia hata ikiwezekana umuue, damu yake itakuwa mikononi mwangu. Ila sitaki kuona damu ya Watanzania wasio na hatia ikimwagika kutokana na uzao wangu. Sijazaa gaidi mimi”
Mama mkwe alizungumza kwa hasira maneno yaliyo nifanya nitetemeke mwili wangu mzima, kama imefikia hatua ya kunipa amri ya kumuua mume wangu ili asifanye ujinga wowote, basi akinyanyuka yeye hapa kitandani basi Eddy wangu hato kuwa na bahati ya kuendelea kuishi tena hapa duniani.
“Sawa mama ninakwenda”
Kwa haraka nikafungua mlango, mapigo ya moyo yakazidi kunienda kasi mara baada ya kumkuta Eddy akiwa amesimama pembeni ya mlango huku machozi yakimwagika usoni mwake. Kwa asilimia tisini nina imani kwamba atakuwa amesikia kila kitu ambacho tulikuwa tunakizungumza na mama mkwe.
“Ma….a…….”
Nikajikuta nikipata kigugumizi kizito sana na nikashindwa kuzungumza kabisa. Eddy akanishika mkono wangu wa kulia na tukaanza kutembea kwa kasi sana kuelekea nje, tukafika kwenye moja ya busta na akanitole bastola na kunikabidhi mkoboni mwangu.
“Umetumwa kuniua, niue”
Maneno ya mume wangu yakanifanya nitetemeke mwili mzima. Ujasiri hata wa kuishika hii bastola ukaniishia na kujikuta nikiiangusha chini.
“Okota uniue”
“Eddy mume wangu fika unatambua kwamba siwezi kufanya hivyo. Ukifa wewe na mimi ni lazima nife mume wangu, siwezi kubaki peke yangu kwenye maisha haya yaliyo jaa visa, mikasa na tabu za kila aina. Wewe ndio mtu ambaye uliweza kunishika na kunifanya niwe Jojo, kwa nini nikuue mume wangu”
Nilizungumza kwa unyonge huku nami machozi yakinimwagika usoni mwangu.
“Najua mama amekasirika kwa msimamo wako, ila nahisi kuna kitu ambacho mama amefanyiwa, kwa maana hawezi kuwa kama yule niliye mzoea. Nimefanya vitu vingi na mama na wala hakuna sehemua mbayo alihitaji kushindwa, imekuwaje kwa raisi. Mume wangu mimi nipo na wewe kwenye kila jambo. Simsikilizi mtu mwengine zaidi yako wewe”
Nilizidi kuzungumza maneno yenye ushawishi ili kuhakikisha kwamba nina ishusha hasira ya mume wangu.
“Kwa nini mama ananiita gaidi, ikiwa tunapigania haki yake?”
“Ndio maana Eddy nikakuambia kwamba mama kuna kitu ambacho watakuwa wamemfanya, nakuomba mume wangu uwe mvumilivu. Ina maana unataka kusema kwamba hujamzoea tu mama?”
“Nimemzoea”
“Sasa kwa nini unapata naye shida mume wangu. Tufanye lile ambalo sisi tunaliona ni sahihi kwetu, sawa mume wangu”
Eddy akashusha pumzi nyingi taratibu.
“Sawa nimekuelewa”
“Ila kumbuka kwamba ninakupenda sana mume wangu”
“Ninakupenda pia mke wangu”
Taratibu Eddy akaninyonya lispi zangu kwa hisia kali.
“Umenimiss”
“Yaaa”
Eddy akanyanyua na kunibeba na tukaanza kuelekea ndani, kwenye kordo tukakutana na wifi na ikakamlazimu kunishusha.
“Inabidi tuanze kutuma ushiahidi kwenye kila nchini ambayo umewaeleza kwamba raisi anahusika katika mabyo mabata aliyo wafanyia”
Wifi alizungumza huku akimtazama Eddy usoni mwake. Eddy akamkabidhi faili lenye ushahidi wote wa maofu ya raisi, taratibu wifi akaanza kulipitia.
“Mmm hili mbona kama kuna vitu viongezeka?”
“Vipi?”
Ikatubidi wote tulitazame fiali hili.
“Huyu si mama?”
Wifi alizungumza huku tukiitazama picha ya miaka mingi ya nyuma, imauonyesha raisin a mama mkwe wakiwa wamekumbataiana.
“Ndio yeye”
Eddy alijibu huku akinitazama usoni mwangu kwa macho ya kuiba iba. Tukatazama picha ya pili na kuwaona wakiwa wananyonyana midomo hapo ndipo tukapata jibu kabisa kwamba mama mkwe na raisi ni watu walio kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
“Munatazama nini?”
Shem alitufwata sehemu tulipo simama, wifi pasipo hata kumjibu shemeji, akamkabidhi picha hiyo ambayo mama na mkwe wanapena denda. Shem akaitazama kwa muda na kujikuta kichwa huku hata yeye mwenyewe akionekana kujawa na mshangao mwingi juu ya hili swala.
“Dogo ulivyo kwenda kuzungumza na mama amesemaje?”
“Eti tusitishe mpango wa kumtoa raisi madarakani”
“Kwa ajili ya ujinga huu au kuna sababu aliyo kuambia?”
“Zipo ila hazina nguvu ya kusitisha”
“Hili alikuambia?”
“Hapana”
“Lazima atoe ufafanuzi, maisha yetu ameyaweka kwenye mstari wa kufa tayari, na tumesha jitoa kwa ajili ya jambo hilo inakuwaje asitishe, ina maana anamtetema mpenzi wake au?”
“Ila kumbuka kwamba mama ana umwa”
Wifi alizungumza kwa upole
“Hajaumwa kiasi cha kushindwa kutoa maelezo ya hili swala”
Shem baada ya kuzungumza hivyo akapita katikati yetu na kuelekea nje, wifi akaanza kumfwata, kutokana na sisi tunahitaji kufahamu ukweli wa hili jambo ikatulazima twende huko huko wanapo elekea wezetu. Tukawakuta wifi na shem wakiwa tayari wamesha ingia ndani ya chumba cha mama, tukaingia na sisi na kumfanya mama mkwe kujawa na mshangao kwani ujio huu hakuna hata mmoja ambaye ana sura ya furaha usoni mwake.
“Ina maana umekwenda kuwaita wezioa baada ya kukataa mpango wenu si ndio?”
Mama alizungumza huku akimtazama Eddy usoni mwake.
“Gody toka humu chumbani”
Shem alizungumza kwa sauti nzito kidogo.
“Mjukuu wangu munataka mumpeleke wapi, Gody baki humu humu ndani”
Shem akamtazama mwanaye kwa macho makali, ambayo taartibu yakamfanya Gody kushuka kitandani na kutoka nje ya chumba hichi huku akiwa amejawa na woga ulio ambatana na wasiwasi mkubwa sana. Shem akamkabidhi mama mkwe picha hiyo ya inayo waonyesha yeye na raisi enzi za ujana wao wakipeana mabusu motomoto. Mama mkwe akaishika picha hiyo na kuitazama kwa muda huku mikono ikimtetemeka, uso wa hasira wote ukamtoweka usoni mwake.
“Hiyo ndio sababu iliyo kufanya ukatae juu ya mpango wa kumtoa raisi madarakani kwa njia ya kumtangaza maovu yake kwenye vyombo vya habari, eheee?”
Shem aliendelea kuzungumza kwa sauti nzito inayo onyesha dhairi kwamba amekasirishwa.
“Mama tupatie jibu, sisi ni watoto wako, je hiyo ndio sababu inayo tuzuia tusiendelee na mpango wetu?”
“Mumeipata wapi?”
“Hilo sio jibu mama, tujibu?”
“Baba Gody acha kumfokea mama, tazama na afya yake?”
Wifi alizungumza kwa upole.
“Sijamfokea, nimemuuliza”
Mama mkwe akafumba macho kwa muda, hadi nikamuonea huruma kwa maana amebananishwa na watoto wake na mimi nipo hapa kama shahidi tu japo muda wowote mambo yanaweza kubadilika nanikaambiwa nitoke humu ndani ya chumba hichi.
“Ndio”
Mama mkwe akajibu kwa sauti ya unyonge kabisa.
“Mama umeshindwa hata kutudangaya, kweli mapenzi yanakuyumbisha, eheee?”
Wifi alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Mimi nami ni binadamu na ninapaswa kupenda”
“Kupenda, kumpenda yule shetani mama, ambaye amekupiga piga vile alafu unasema kwamba unampenda mamaaa”
Wifi aliendelea kulalama, taratibu wifi akakaa kitandani na kumtazama mama usoni mwake.
“Ni nini kilicho tokea kati yenu mama?”
“Mama katika kuadisia kilicho tokea, tusije kuja kusikia kati yetu kuna mtu ni mtoto wa yule mshenzi, sinto kuelewa mama”
Shemeji alizungumza kwa msisitizo mzito sana na kuzidi kumuweka maam kwenye mabano na wakati mgumu sana.
“Mama hembu tuambie ukweli basi, nini kilicho tokea kati yetu hadi ikawa hivi inavyo kuwa hivi sasa”
“Kipindi nipo sekondari……”
Mama mkwe alizungumza sentensi hiyo kisha akakaa kimya kwa muda huku machozi yakimtiririka usoni mwake.
“Nilikutana na Henrry. Kipindi nipo kidato cha tano, yeye alikuwa kidato cha sita……Tulipenda sana kwa mana yeye ndio alikuwa mwanaume wangu wa kwanza na yeye ndio mwanamke wake wa kwanza.”
“Kwa kipindi cha mwaka mmoja mzima tulio ishi na Henrry pale shule kusema kweli nilijua nini thamani ya mapenzi, na tuliweza kuzungumza mambo mengi sana na kupanga mambo mengi katika maisha, ikiwemo ya ndoto yake ya kuwa raisi na kweli amekuwa raisi”
“Mama ngoja kwanza, unataka kusema kwamba raisi Hennry ndio aliye kutoa bikra?”
Swali la Eddy likatufanya sote tumtazame usoni mwake, kwani ni swali ambalo kwa mtoto kumuuliza mama ni gumu kidogo na hata majibu yake ni magumu.
“Na wewe swali gani la kijinga hilo”
Shem alizungumza kwa hasira kidogo.
“Ndio yeye ndio aliye nitoa usichana wangu”
Jibu la mama mkwe likaturudisha akili zetu kwake na kuendelea kumsikiliza.
“Katika siku yao ya graduation ndio tulipiga hizo picha ambazo sikujua kama zinaweza kuduma kwa kipindi kirefu hadi leo hii”
“Henrry siku zote alinisisitizia upendo wetu udumu, hata kama kuna kitu chochote kibaya kinaweza kutokea kati yetu basi ni lazima tuendelee kuwa wapenzi, na tukaweka kiapo cha damu katika siku hiyo?”
“Ndio kiapo gani hicho?”
Eddy aliuliza swali jengine ambalo hata mimi nina hitaji kupata ufafanuzi.
“Alinitoa usichana wangu, endapo mwanamke akitolewa usichana na mwanaume hicho ni kiapo cha damu ambacho hakita sahaulika kichwani mwa wanamke wala mwanaume katima maisha yao yote hadi wanakufa”
“Eheee, ikawaje?”
Wifi aliona akatishe maelezo hayo ya mama ili kuendelea kupata kusimuliwa hadithi hiyo.
“Ule mwaka wangu wa mwisho kuishi pale shule nilipata shida sana, shida ya kumkumbuka mpenzi wangu Henrry na kwa kipindi kile kulikuwa hakuna simu na kama ni mawasiliano ni barua, na Henrry hakuweza kutuma barua pale shule kuepuka kuniweka kwenye matatizo kwa maana mtu ambaye alipaswa kutuma barua shuleni alikuwa ni baba tu au mama”
“Mmmmm”
“Hiyo ilikuwa ni kwa kila mwanafunzi wa shule hiyo. Nikiwa hapo shule ndipo nilipo anza urafiki na yule mkewe, nilikuwa nina lala naye kwenye bweni moja”
“Mulikuwa darasa moja?”
Wifi aliuliza.
“Hapana, yeye alikuwa kidato cha tano na mimi kidato cha sita na pale shule nilikuwa kama ni dada yake kwa maana mim ndio niliye mpokea siku wanakuja shuleni”
“Babu yenu aliamua kiniingiza kwenye maswala ya usalama mara baada ya kumaliza kidogo cha sita. Niliweza kwenda sehemu nyingi duniani nikiwa kama mwana usalama, nilifanya vitu vingi sana na hata zile hisia juu ya Henrry ziliisha kwani ni miaka mingi sana ilipita na hata mambo mengi ya hatari niliyo kuwa nina yapitia yakanifanya niweze kushindwa kuwa na hisia dhidi yake.”
“Kipindi ninarudi Tanzania ndiopo nikakutana na baba yenu, nikakuzaa wewe, wewe na wewe”
Mama mkwe alimalizia kuzungumza kwa kuwanyooshea vidole shem, wifi na mume wangu.
“Sasa mama kama hisia ziliisha juu yake, inakuwaje kwenye hili la sasa hivi, ni hisia gani ambazo zipo ikiwa amekupiga kiasi cha kukufanya muda huu uwe hapa kitandani”
“Siku ambayo alinipiga ni siku ambayo nilikataa kula, nilikuwa nipo tayari kukaa na njaa ili mradi tu nife kwa njaaa, walinilazimisha kula ila nilikataa hadi pale alipo amua kunipiga”
“Kwa hiyo umekuwa kina Cleopatara hadi tuwazibe pua ndio wale?”
Wifi alizungumza huku akimtazama mama usoni mwake.
“Maana yangu sio hiyo?”
“Ni ipi sasa?”
“Nilikata tamaa kabisa, sikuona msaada wowote hadi pale nilipo pata matumaini ya Nuru kwamba yupo tayari kunisaidia”
“Okay sasa hapo mama bado sijaona sababu ya wewe kunizuia kumtoa huyo chizi madarakani”
Mume wangu alizungumza huku akimtazama mama mkwe usoni mwake.
“Sababu ipo?”
“Ipi hapo au ulichepuka naye alipo kukamata?”
Swali hili likanifanya nimfinye Eddy mkononi mwake, kwani ni kumkosea mama heshima hata kama kuna udhaifu kidogo ameufanya ila si kwa maswali haya.
“Bado anaonyesha ananipenda?”
“Mama huo ni uongo. Tazama umri usmesha kwenda, aache kukubabaisha bwana”
Wifi naye alizungumza kwa ukali kidogo.
“Mama najua unaogopa kutokana ni mwanaume wako wa kwanza, inaonyesha alikupa vitisho, si ndio”
Shem aliuliza huku akimkazia mama mkwe macho.
“Hajanipa vitisho vyovyote?”
“Kama hajakupa vitisho vyovyote tunaendelea na lile tulilo likusudia kulifanya, na dogo hapa ana flash ambayo inatumia katika kuongoza mabomu ya nyuklia, sasa kama hato jiuzuru kesho, tunakwenda kutumia nguvu na oparesheni hii nitaiongoza mimi kama kiongozi wa wadogo zangu, umenielewa mama?”
‘Ehee gaidi mwengine’
Nilijiseme kimoyo moyo huku nikimtazama mama mkwe akijiweka sawa kitandani mwake.
“Nimemkaza mdogo wako kutumia hizo silaa, kuna raia wasio na hatia wataangamia na kumbukeni amamshikilia Doto unahisi ni nini kinacho kwenda kutokea?”
“Kwenye ushindi wowote ni lazima damu imwagike, tumejitoa sadaka na nilazima tumtoe madarakani”
“Sitaki kusikia ujinga kama huo, kama mimi sio mama yanu niliye waza jaribuni kufanya ushenzi huo”
“Utafanyaje, utatupiga au? Sasa kama sisi sio wanao wa kutuzaa, endelea kukataa kumshuhulikia huyo mpumbavu anaye tumia madaraka yake kututesa. Ni nani yupo nami kwenye hili?”
Shema alizungumza huku akinitutazama usoni mwetu. Taratibu Eddy akanyoosha mkono, macho yote tukamtazama wifi, wifi akamtazama mama usoni mwake kisha taratibu naye akanyoosha mkono kuonyesha msisitozo kwamba amri ya mama yao wameipinga na wapo pamoja na kaka yako kuhakikisha wanamtoa raisi Henrry madarakani.
Taratibu nikanyoosha na mimi mkono wangu kuashiria kwamba nipo na wezangu, mama mkwe akabaki akiwa ametokwa na macho huku akitutazama.
“Acha tuifanye kazi yetu mama, wewe kaa hapo uuguze majeraha yako”
Shemeji baada ya kuzungumza hivyo akaanza kutoka humu chumbani, akafwatia mume wangu na akamalizia wifi.
“Jojo hata wewe umeungana na hao wajinga”
“Mama una……”
“Una una nini, hembu toka ndani humu na ukaungane na wajinga wezio”
Mama mkwe alizungumza kwa ukali na kunifanya nitoke chumbani huku pasipo kuzungumza chohcote, nikapishana na Gody kwenye kordo huku akionekana kuto jawa na furaha ya aina yoyote. Tukaelekea sebleni ili kuanza kupanga mipango na mikakati ambayo tunaweza kuitumia.
“Plan A tayari tumesha itumia, plan ya kumshinikiza raisi kuachia madaraka. Je akikataa Plan B itakuwa ni ipi?”
Shemeji alizungumza huku akiwa amekaa kwenye kiti alicho kuwa amekikalia hapo awali.
“Tunamlipua na nchi yake”
Eddy alijibu huku akiwa ameniwekea miguu yake pamajani mwangu na kijilaza kidogo.
“Hiyo sio ponti kwa sasa ni lazima tuweze kufikiria njia mbadala ambayo ni salama na haito wagusa watu wa aina yoyote, iwe wenye hali ya chini au ya juu”
Wifi alizungumza kwa upole.
“Inabidi tuunde kikosi maalumu ambacho tutakituma kwanza kumkomboa pacha wa Eddy pale. Pili kikosi hichi kiwe na uwezo wa kumteka raisi na kumuweka chini ya ulinzi ili kuhakikisha kwamba analitangazia taifa katika kuiachia nchi”
Nuru alishauri naye.
“Jamani mimi nilikuwa serikalini katika kitengo cha usalama, kwa sasa ni vigumu sana kuweza kumfikia raisi, ni lazima ulinzi wake utakuwa ni mzito na hatuwezi kupoteza vijana ambao watakuwepo kwenye kiosi hicho kwa ajili ya mtu mmoja”
Shemeji alizungumza huku akitutazama sote.
“Kuna kitu nilikizungumza muda ule alafu sikuona kama watu mulikitilia msisitizo”
“Kitu gani?”
“Nilisema tuandae ushahidi wote wa zile nchi ambazo zilifanyiwa matatizo na huyu jamaa, tukiziweka sawa basi kinacho fwata baada ya raisi kukataa kuachia madaraka ni lazima tutume ushahidi kwenye kila nchi ambayo Eddy alizitaja, baada ya hapo nina imani kwamba tutakuwa na na nguvu ya kufanya chochote juu ya raisi”
Wazo la wifi likatufanya tukae kimya kwa muda.
“Ishu ni kwamba je nchi hizo kama zikikataa juu ya kufanya upepelezi wowote juu ya raisi?”
“Si kwa nchi kama China wala Urusi, nyingine hapo sawa. Ila nchi hizo mbili ni nchi zilizo jaa watu imara kuanzia viongozi wao hadi watu wakawaida.”
“Sawa hilo ni wazo zuri”
“Jamani mimi naomba tuzungumze”
Mama Gody aliomba kuzungumza na sote tukakaa kimya.
“HIli swala tutalo kwenda kulifanya ni kubwa sana. Ukubwa wake ni lazima tulichukulie katika njia nyingine ya kirogo. Je haya tunayo yafanya Mungu atayatia muhuri wake, Je Mungu atakubali tuweze kumuangusha raisi Henrry. Tunaweza kupanga kwa akili zetu sisi hapa, kumbe tunapoteza muda tu na tukja katika swala la utendaji wa kazi tunashindwa kufanya jambo lolote na tukakwama”
“Mmmm hili wifi yangu nalo ni neno”
“Sasa shem tutazungumza vipi na Mungu, mimi kama mimi mikono yangu ina dhambi, Jojo hapa sijui siku yake ya mwisho kusali ni lini? Kwa baba Gody naye hapo naye ndio hivyo hivyo tu. Labda shemeji yangu Rich hapo kidogo ndio anaweza akawa ameokoka kidogo”
“Mimi nipeni muda huu hadi kesho asubuhi nitawapa jibu. Nitasali usiku kucha na kumuuliza Mungu kama tufanye huu mpango au tusiufanye”
“Sawa shem, niombee na mimi dhambi zangu ziweze kusamehewa”
“Hahaaa….”
Mama Gody akanyanyuka na kutoka eneo hili la sebleni na kuelekea chumbani kwao na kutuacha sisi wengine tukiwa kimya.
“Eheee tuendeleni?”
Eddy alizungumza huku akishusha miguu yake chini na kukaa vizuri kwenye hili sofa.
“Hatuwezi kuendelea na chochote hadi mama Gody aombe”
“Heee”
“Hee nini, ngoja aombe tujue ni nini kinacho endelea.”
Eddy akanyanyuka na kunishika mkono wangu wa kuliana kuninyanyua na tukaondoka sebleni hapa bila ya hata kuaga. Tukaingia chumbani kwetu, kwa haraka Eddy akaninyanyua na kuanza kuninyonya midomo yangu.
“Baby ngoja nifunge mlango jamani”
“Mmmmmm”
“Ndio tukumbuke hatupo kwetu”
Eddy akaniachia, kwa haraka nikaelekea mlangoni na kuufunga kwa ndani, nikavua nguo zangu na kupanda kitandani, kwa haraka nikaanza kumvua nguo mume wangu.
“Mmmm Eddy unanuka jasho kaoge kwanza”
“Mmmm hayo mambo yameanza lini lakini Jojo?”
“Yameenza leo, una nuka jasho, nenda kaogo”
“Khaaaaaa……………..”
Eddy alizungumza huku akishuka kitandani na kuingia bafuni, nikajilaza kitandani huku nikifikiria jambo hili la kumtoa raisi madarakani. Baada ya muda Eddy akarudi na kujirusha kitandani.
“Jamani Eddy utavunja kitanda cha watu?”
“Kivunjike tutawalipa”
Eddy alizungumza huku akinipanua mapaja yangu, akaanza kuninyonya kitovu changu na kuufanya mwili wangu kujawa na msisiko. Akaushusha mdomo wake hadi kwenye kutumbua changu, hapo ndipo nilipo zidi kuchanganyikiwa na kijikuta nikitoa vilio mfululizo vya utamu wa penzi la mwanaume huyu.
“Leo unalalamika vizuri mke wangu”
“Eddy jamani niniiii akhaaaa”
Maneno ya mume wangu nilihisi yakinikatisha utamu wote ambao nilikuwa nikiuhisi mwilini mwangu. Taratibu tukaanza kupeana utamu huku mtanange wa leo ukiwa ni mzito kwa kila mtu. Nahisi hata watu walipo nje wanaweza kusikia fujo zetu. Tukamaliza mizunguko kwa siku ya leo, hadi tunakuja kustuka ni saa tatu kasoro usiku.
“Eddy muda umekwena mume wangu”
“Kwani kuna sehemu unataka kwenda?”
“Hatujakula bwana”
“Tutakula tu”
“Nyanyuka tukaoge”
“Eheee?”
“Nyanyuka bwana tukaoge”
Nilizungumza huku nikishuka kitandani, nikaanza kumvuta mume wangu taratibu hadi nikamuanguka chini.
“Jojo utanivunja”
“Twende bwana tukaoge”
Eddy akajikokota taratibu na kusimama, tukaingia bafuni na kunza kuoga.
“Twende mechi nyingine”
“Hee unataka kum** yangu iwake moto zaidi ya huu ninao uhisi sasa hivi au?”
“Njoo nikupulize”
“Hembu acha mambo yako bwana, tuoge tukale”
“Hivi mimi unajua sina nguo za kubalisha?”
“Utakwenda kumuomba baba Gody, si mnavaliana?”
“Yaa”
Tukamaliza kuoga, Eddy akajifunga taulo na kutoka chumbani humu. Nikajiandaa vizuri na kuelekea sebleni, nikapishana na Eddy kwenye kordo huku akiwa ameshika pensi.
“Watu wanakula wahi”
“Wanakula nini?”
“Mimi naona kuna nukia nukia tu huko sebleni”
“Nawe fanya uje”
“Poa”
Nikafika katika meza ya chakula na kuwakuta watu wote, nikaka pembeni ya Judy ambaye muda wote wa mchana alikuwa amelala chumbani kwake.
“Vipi upo poa?”
Nilimuuliza Judy kwa kunong’oneza.
“Yaa nipo poa, nimemlisha Cleopatra na amesha lala tena”
“Ahaa sawa sawa”
Nikajitengea chakula ninacho kihitaji na kuendelea kula taratibu, mume wangu akaja naye, nikachukua jukumu la kumsaidia kumtengea chakula.
“Shem vipi umepata jibu katika maombi yako”
“Bado shem”
“Sawa sawa, kuna mpya zozote?”
“Hakuna”
Wifi alijibu kwa kifupi huku akiendelea kupata chakula huku amempakata mwanaye mapajani.
“Gody yupo wapi?”
“Yupo kule kwa bibi yake, si unajua Gody na bibi yake picha zinaiva”
Mama Gody alijibu, nikapata wazo moja ambalo nikatamani kumuambia mume wangu hapa hapa ila kutokana na watu nikaona ni bora ninyamaze hadi pale tutakapo pata muda wa kuweza kufanya hivyo. Tulipo maliza kupata chakula cha usiku, Nuru akaomba azungumze nami, tukatoka nje na kukaa kwneye bustani ya kumpunzikia ambayo ina mabembea maalumu, ya kujiburudisha.
“Naona hatujapata muda wa kuzungumza tangu tuonane”
Nuru alizungumza kwa sauti ya upole huku akibembea taratibu.
“Yaa ni kweli, vipi lakini unajisikiaje na tatizo lako?”
“Tatizo langu bado linanisumbua, ndio maana makazi yangu nimeamua kuyaweka kwenye hii hospitali yangu, kwa maana huwa kila baada ya muda huwa nina badilishiwa damu”
“Pole sana”
“Nashukuru.”
Upole wa Nuru ukazidi kunipa maswali mengi sana kichwani mwangu. Nikamtazama jinsi anavyo vikunja kunya vidole vyake, dhairi anaonyesha ni mtu ambaye amakata tamaa kabisa ya kuishi hapa duniani.
“Madaktari wameniambia kwamba nimebakisha mwenzi mmoja wa kuishia hapa duniani, na baada ya wiki kadhaa sinto kuwa na uwezo hata wakutembea mwenyewe kama hivi unavyo niona nikitembea”
“Mmmmmm”
“Yaaa. Jojo huu ugonjwa ni mbaya sana. Usikie tu hivi kwa watu, ila ni mbaya sana”
“Ni kweli kwani kuna siku Eddy aliniambia kwamba baba yake naye alikuwa kwa Canser”
“Ni kweli, ila nina jambo ninahitaji kukuomba kabla sijakufa?”
“Jambo gani?”
“Kutokana sina mwana familia, sina mtu ninaye mpenda zaidi yako. Ninakuomba uwe mrithi wa mali zangu zote, na leo usiku nina kikoa cha mabosi wote nilio waajiri kwenye kapuni zangu zaidi ya mia moja hapa duniani. Ninataka kukutambulisha kwao kwama mmiliki halali wa kampuni zangu zote je upo tayari kwa hilo?”
Swali la Nuru likanipa bumbuwazi kubwa sana kwani sikutarajia kwa yale yote ambayo tulifanyiana hapa duniani, uadui wote alio kuwa akinifanyia mimi na mume wangu, leo hii anataka niwe mrithi wa mali zake.
“Najua kwamba unashangazwa na maamuzi yangu Jojo, ila kama nilivyo kuambia sina ndugu, sina mtoto wa kuweza kumrithisha hizi mali. Nakuomba uwe mrithi wangungu, naogopa kufa na kuacha miradi niliyo ipigania usiku na mchana ili mradi iweze kukua, ila mwisho ninakufa kama hivi”
Nuru alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Taratibu nikaushika mkono wake wakulia na kuanza kuuminya taratibu taratibu. Kitendo hichi kikamfanya Nuru kuzidi kulia kwa uchungu sana.
“Noo usilie Nuru, wangapi wamekufa. Wangapi wapo mahospitalini hawajiwezi. Kwa afya yako ulio nayo hadi sasa hivi ni jambo la kumshikuru Mungu”
“Jojo sio kama ninaogopa kufa, hapana. Ila ninajutua maisha ya kijinga na kipuuzi ambayo niliyafanya hapo nyuma”
“Kama umetubu dhambi zako na kusamehana na watu wote, hakuna haja ya wewe kuendelea kuumia, acha yaliyo pita yapite Nuru. Ni wakati wa kusimama kwa Mungu na kama ni kweli hao madokta wamesema maisha yako yataisha baada ya mwenzi mmoja, basi huna budi kuhakikisha kwamba unakuwa karibu sana na Mungu wako ili hata hiyo siku ikifika basi utaweza kwenda mbinguni moja kwa moja”
Nilijitahidi kuzungumza maneno ya kumfariji Nuru huku nikimtazama usoni mwake.
“Sawa Jojo, ila upo tayari kwa hilo, kwa maana kikao ni saa sita usiku wa leo?”
“Unaweza kunipa muda wa kuzungumza na mume wangu?”
“Sawa, ila ninaomba unijibu ili niweze kujua ni nini ninaweza kufanya, pia kama utahitaji fundi wa kukushonea nguo kwa haraka utaniambia akushone gauni”
“Sawa”
“Nenda kazungumze na Eddy ila nakuomba usiniangushe Jojo”
“Nimekuelewa”
Nikanyanyuka na kurudi sebleni, nikamkuta Eddy na shemeji wakicheza game ya mpira kwenye tv.
“Samahani, Eddy tunaweza kuzungumza?”
“Sasa hivi?”
“Ndio”
“Weka pause, nije kukufunga”
“Nenda huko, michezaji yako yenyewe mizitoo”
Shemeji alizungumza kwa utani, tukaongozana na mume wangu hadi chumbani kwetu. Tukaka kwneye masofa yaliyomo ndani ya hichi chumba.
“Vipi kuna tatizo?”
“Hapna ila nimekuja kukuomba ushauri”
“Zungumza”
“Nimezungumza na Nuru, kuna kitu ameniomba, nikaona si vyema nikafanya maamuzi ya kwangu peke yangu ikiwa wewe upo hapa na nilisha ahidi kwamba wewe ndio nitakaye kusikiliza”
“Ni kweli”
“Kama Nuru alivyo tuambia kwamba ana umwa na saratani ya damu. Habari mbaya ni kwamba madaktari wamemuambia kwamba ana mwenzi mmoja tu wa kuishi hapa duniani….”
“Mungu wangu.....Eheee?”
“Nuru ameniomba niwe mrithi wa mali zake zote, ana kampuni zaidi ya mia moja hapa duniani kwa hiyo amenisisitizia sana nisimuangushe katika hili”
“Mmmmmm hayo maneno aliyazungumza akiwa na akili zake timamu au kwa hisia kutokana ana kupenda penda tu?”
“Kwa akili zake yeye mwenyewe, na si kwa hisia za kimapenzi. Na amefanya hivyo kutokana hana ndugu wala familia na mimi ndio mtu pekee wa karibu yake”
“Mmmmm…..Unajua kuongoza kampuni zaidi ya mia moja duniani, ni jambo zito sana. Jambo ambalo kama utakubali kuchukua jukumu hio inabidi uwe mchakarijikaji na mpambanaji sana”
“Ni kweli mume wangu”
“Haya, wewe kama wewe umeamuaje?”
“Mimi kama mimi siwezi kukataa hiyo nafasi mume wangu, na leo usiku saa sita amesema kwamba mabosi wake wote duniani, alio waajiri kwenye kampuni zake hizo wana kikao. Anataka kunitambulisha mimi kama mmiliki wa mali zake”
Eddy akashusha pumzi taratibu huku akinitazama.
“Mume wangu najua sisi tumekuwa zaidi ya mwili mmoja, japo hatujahalalishwa kanisani, ila hii ni nafasi mume wangu, hatuto kuja kuwamatajiri kama hivi tunavyo endea”
“Kutokana wewe mwenyewe umekubaliana na jambo hilo kwa upande wangu mimi siwezi kulikataa, ila kuwa makini sana mke wangu. Kwenye maswala ya makampuni kampuni haya kuna mambo mengi ya kishenzi, hususani kama wafanyakazi watajua kwamba bosi wao ana muda mfupi wa kuishi, sasa asije akakuachia kizaa zaa, baada ya kukabidhiwa utajiri huu, ukatutokea puani mke wangu”
“Ni kweli, najua wewe utakuwa nami”
“Ndio nitakuwa nawe kwenye kila jambo, ila tusije tukajiongezea matatizo juu ya matatizo”
“Tupambane kwa ajili ya watoto wetu. Gody na dada yake Cleopatra, ni lazima waweze kuishi maisha mazuri hapo baadae. Alafu muda ule nilipo kuwa nina kula niliwaza kuhusiana na swala la Gody, hivi ni kwa nini hufaji jambo kwa ajili ya Gody. Unataka umuache aendelee kukaa na mama yake unahisi anajazwa roho gani juu yako ikiwa mama yake muliachana kwa kuchomeana nyumba”
“Muda wake wa kumchukua utafika tu mke wangu?”
“Lini Eddy, miaka ina kwenda na kumbuka mama yake ni adui yako. Atamjaza mtoto roho ya kuchukia, Hembu fanya basi mchukue, nakuahidi nitakuwa mama mzuri kwake. Nitamlea kwneye misingi yote ambayo mtoto anapaswa, au una mashaka na mimi juu ya kumlea mwanao?”
“Mashaka gani sasa?”
“Ya kumtesa kama ilivyo zoeleka kwa mama wa kambo wengi?”
“Weee ukimtesa si ninakukata hicho kichwa”
“Sawa, hembu mchukue, yule ni mwanangu pia siwezi kumnyima chochote atakacho”
“Nimekuelewa, nitafanya utaratibu wa kumtafuta mama yake”
“Kumbe kwa kipindi chote hujui hata ni wapi alipo mtoto?”
“Ndio”
“Eddy mbona unajisahu hivyo mume wangu”
“Ninajisahu vipi, kwani haya matatizo yote wewe hutajui au. Unahisi ninataka nijionyeshe onyeshe kwa watu juu ya Gody ili wamtumie yeye kunipata mimi. Nina akili Jojo kufanya hivi nawapenda wanangu wote ndio maana sihitaji matatizo juu yao. Acha msalaba huu niubebe mimi kama baba”
Eddy alizungumza kwa uchungu huku machozi yakimlenge lenga usoni mwake. Taratibu nikanyanyika na kukaa karibu yake.
“Samahani kama nimekuudhi mume wangu”
“No hujaniudhi Jojo, ila hili swala la watoto ni gumu, tusijichanganye siku hata siku moja watoto wetu wakaingia kwenye hizi vita za kijinga. Tutaumia zaidi ya kumia, tutaacha kila kitu na kuanza kuwashuhulikia wao, nina imani kwamba unafahamu uchungu wa mtoto?”
“Ndio mume wangu nina fahamu”
“Ndio hivyo watoto kama watoto sio nafasi ya vita yetu. Ndio maana sitaki mwanangu hata mmoja sura yake ionekane kwenye social media kama watu wengine wanavyo fanya”
“Nimekuelewa mume wangu”
Taratibu nikamkumbatia mume wangu kwa muda, kisha tukaachiana.
“Nenda kampe mwenzio jibu, ila usimuambie mtu yoyote kama kuna swala hilo unalo hitaji kufanya na Nuru”
“Sawa mume wangu, je mama nimuambie”
“Bwana nimekuambia usimuambie mtu yoyote. Mama alipo pale amesha vurugwa, anamfikiria tu huyo mtu wake tutakavyo mtumbua. Sasa ukimuongezea na hilo anaweza kukuambia usikubali bureee, mamabo yakawa sio mazuri”
“Sawa je kwenye hicho kikoa unaniruhusu niweze kwenda?”
“Ndio nenda, siwezi kukubania, ndio nafasi ya kutusua kwenye maisha yako. Kuna leo na kesho, ninaweza nisiwepo duniani, unaisi watoto wangu ninataka kuwaacha wakishindia ugali, dagaa na matembele. Ndio maana ninapambana kila kukicha”
“Sawa baba nimekuelewa”
Tukatola chumbani humu na kurudi sebleni, nikamkuta Nuru akicheza game na shemeji huku wakiwa wanacheka sana, hadi nikajikuta nikijawa na amani sana moyoni mwangu kwa maana ana furaha.
“Nuru nakuomba”
Nilizungumza huku nikiwatazama
“Wewe Jojo muna ajenda gani ya siri, mbona umemchomoa dogo hao mukaondoka, hapa unamchomoa Nuru munataka kuondoka, hembu niambie shemeji yangu kuna nini?”
Shemeji alizungumza kwa kutania.
“Hapana shem si unajua mambo mambo yanayo endelea hivi sasa yanaumiza kichwa”
“Sawa, ila kama kuna tatizo usiache kuzungumza”
“Usijali shemeji yangu mimi na wewe tena, ni lazima nitakuambia kila kitu kinacho endelea”
“Sawa”
Tukatoka na Nuru nje na kukaa kwneye mabembea ambayo tulikuwa tumekaa
“Ehee niambie”
“Amekubali”
Nuru akashusha pumzi nyingi huku akitabasamu, akatazama saa yake ya mkononi.
“Muda unatosha, sasa tupite kwa fundi akupime na uchague ni nguo gani utavaa usiku huu, kisha tuelekee ofisi kwangu”
“Sawa”
Tukaondoka katika eneo la jumba hili tunalo ishi na kuingia katika jumba jengine, tukaingia katika chumba kikubwa ambapo wapi washonaji nguo kama kumi hivi huku kila mmoja yupo na mashine yake ya kisasa. Tukawasalimia na tukamfwata mzee mmoja wa kamamu, nikamueleza ni gauni ya aina gani ninalo hitaji kuvaa kw usiku huu. Baaada ya kunielewa akanipima vipimo vyote kisha tukaondoka.
“Hivi hao wafanyakazi wanashona nguo usiku kucha?”
“Hapana huwa wanaingia kwa shifti, hao ndio wanao shone nguo za walinzi wote, madaktari na masesi, hata nguo za wagonjwa wao ndio wanashona”
“Ahaa, kwa hiyo kila kitu kinafanyika ndani humu humu?”
“Yaa hakuna kazi ambayo inatoka nje ya eneo hilo na kwanza ili mtu aweze kufika au kuondoka katika eneo hili nilazima watumie ndege ama helicopter kwa maana hakuna barabara ya kutoka kwenye hii milia”
“Duu kwa nini mume fanya hivyo?”
“Ni kutokana na usalama zaidi, na sehemu hii huwa wanatibiwa watu muhimu sana na kwa siri kubwa sana, huwa watu wakawaida hawawezi kutibiwa”
“Unataka kuniambia kwamba hospitali hii haijulikani na hapa Kenya?”
“Sio Kenya, wala duniani haijulikani, na wafanyakazi wake pia ni watu wangu muhimu sana”
“Sawa sawa”
Tukaingia kwneye jengo moja la gorofa kama sita hivi, tukaingia kwenye lifti, tukapandisha hadi juu gorofani. Tukaingia kwenye ofisi kubwa ya Nuru, ni ofisi nzuri snaa na iliyo pangiliwa vizuri.
“Ofisi yako ni nzuri?”
“Asante ila kuanzia leo haito kuwa ya kwangu. Wewe ndio utakuwa mmiliki wa hii ofisi”
Nuru alizungumza kwa unyonge huku akitazama vitu vya thamani vilivyomo ndani ya hii ofisi.
“Najua wewe ni mpambanaji zaidi yangu. Kwanza bado ni mdogo, una maisha marefu ya kuishi, una akili nyingi. Sasa ni wakati wa wewe kusimama na kuhakikisha kwamba unafikisha malengo ambayo nitakuachia na utakayo yaweka”
Nuru baada ya kumaliza kuzungumza hivyo akaka kwenye kiti chake cha kuzunguka. Akanyanyua mkonga wa simu iliyopo hapa mezani.
“Kaa mbona umsimama, au unaogopa ofisi yako?”
“Hamna, ninashangaa jinsi ukubwa wa hii ofisi ulivyo”
“Sasa hii ni ndogo, nchini China kuna ofisi kubwa mara mbili ya hii. Naamini sikuwahi kukuonyesha, sasa hapo ndipo makao makuu ya kampuni zangu za N GROUPS”
“Maana ya N2 ni nini?”
“Ni jina langu NURU’S GROUP”
“Ahaaa, ila mali ikiwa mikononi mwako, basi unaweza kubadilisha majina ya makampuni yote”
Nuru akaweka mkongo huo wa simu sikioni mwake na kuanza kusikiliza kwa muda.
“Ehee Basil, nipo gorofani, njoo sasa”
Nuru akarudisha mkonga huo wa simu kwenye sehemu alipo utoa.
“Basil ni nani?”
“Ni mwanasheria wangu anaye fahamu mali zangu zote, na hapa unakuja kujaza Power of attorney ambayo itakuhalalisha kuwa mmiliki wa kila kitu. Badae tukienda kwenye kikao huko ni kuwapa tu watu taaria”
“Sawa, ila nina swali ambalo nina hitaji kukuuliza”
“Uliza tu?”
“Katika kuendesha kampunzi zote hakuna watu ambao una matatizo nao ya kibiashara kwa maana isije ikatokea nimerithi matatizo ambayo yanaweza kupelekea maisha yangu na familia yangu kuwa kwenye shida za kila siku”
”Hakuna kampuni yoyote kubwa inayo kosa washindwanishaji na hakuna kampuni inayokosa maadui wa kibiashara ambao ukikaa vibaya wanaweza hata kukuua, ndio maana tunakuwa na walinzi lukuki”
“Kwa hiyo maadui wako bado unao?”
“Ndio zipo kampuni nina uhasama nao wa kibiashara na wapo ambao wanataka kuona N GROUPS inaanguka chini, ila nina imani nimepata kiongozi bora. Ngoja nikuambia siri moja katika kutafuta nguvu kwenye maisha yoyote hapa duniani nilazima uwe na maamuzi magumu na roho mbaya katika kila maamuzi iii mradi ifikie hatua ile nguvu unayo ihitaji inakuwa”
“Sijakuelewa hapo?”
“Kwa mfano mimi ni mwanamke, ila nina ongoza wanaume nilio waajiri kwenye makampuni yangu zaidi ya milioni tisa na wanawake milioni sita jumla ni watu milioni kumi na tano na wapo ambao hawanijui kabisa”
“Laiti kama ningekuwa mtu wa kulegelega tena kutokea Tanzania, nchi masikini leo hii ningekuw aninatawala chupi zangu na vipodozi katika chumba changu na hata mwanaume ambaye ningekuwa naye angekuwa ananitawala. Ila nilipambana, nikahakikisha kwamba ninaitafuta nguvu na watu hao wote na hata hawa watakao kuja leo hii hapa nikiwambia jambo ni lazima wafate na kutii.”
“Hivyo nilazima uwe na nguvu ya kuwaamrisha watu wote hao na wakusikilize wewe kama kiongozi umenielewa?”
“Nimekuelewa, nitahakikisha kwamba wote wanatii kile ninacho wamabia”
“Nafurahi kusikia hivyo, ila jambo la kuongezea hapo. Ninajitoa kwenye mpango wa kumtoa raisi madarakani, ila sasa simama kwa kutumia pesa na nguvu ninayo kupatia ya pesa, hakikisha kwamba unamtoa raisi Henrry madarakani kabla sijaiaga hii dunia, umenielewa”
Nuru alizungumza kwa msisitozo huku akinikazia macho usoni mwangu, nikatingisha kichwa ikiwa ni ishara ya kumkubalia kwamba alicho kizungumza nitakitekeleza kwa kutumia pesa ambayo ninakwenda kuirithi.
Akaingia kijana mwenye asili ya kiarabu. Nuru akanitambulisha kwake kwamba huyo ndio Basil mwanasheria wake. Kwa Basil hakuwa na haja ya kutambulishwa kwa madai yake anasema ana nifahamu vizuri. Basil akaka kwenye kiti cha pembeni yangu.
“Wamesha anza kufika?”
“Ndio mkuu”
“Sawa tuanze majukumu”
Basil akafungua kibegi chake cheusi na kutoa karatasi na kuziweka mezani. Akanikabidhi karatasi hizo zilizo banwa vizuri na zenye uzito na ugumu mzuri. Nikaanza kusoma maelezo yake, taratibu na kiapo alicho kiingia Nuru kwa kunikabidhi mali zake zote.
“Umesoma vizuri na kuielewa?”
“Ndio”
“Sasa sijui nani anze kuweka muhuri?”
Nuru akanyoosha mkono akimaanisha kwamba anataka kuanza yeye. Basil akamkabidhi karatasi hizo na Nuru akatia saini katika kila eneo ambalo alipaswa kutia saidi, kisha nikabishiwa mimi na kutia saidi kwenye kila karatasi.
“Hongera sasa hivi wewe ndio raisi wa N GROUPS”
Basil alizungumza huku akisimama na kuinamisha kichwa chini kidogo ikiwa ni ishara ya heshima. Nuru naye akasimama kwenye kiti chake huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake na kuinamisha kichwa chake kidogo.
“Karibu muheshimiwa raisi”
“Nashukuru”
Bassil akanikabidhi karatasi hizi kisha akaomba kutoka ndani humu, Nuru akamruhusu na tukabaki sisi wawili, taratibu Nuru akanishika mkono wangu wa kulia na kunizungusha kwenye meza yake hii kubwa, akanikumbatia kwa muda huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Jojo”
“Beeee”
“Nashukuru kwa kunitua mzigo huu ulio kuwa ukiniumiza kichwa kwa kipindi chote hichi, najua nimeacha mali zangu kwa mtu sahihi”
“Yaa ni kweli, usiwe na wasiwasi, naamini nafsi yako itakuwa nami kwa kipindi chote ambapo mwili wako hato kuwepo duniani. Utanisimiamia na kuniongoza, utanishauri muda wowote ambao nitakuhitaji”
Maneno yangu yakamfanya Nuru kunikumbatia kwa nguvu na kuangua kilio cha uchungu sana, hata mimi nikajikuta nikishindwa kuvumilia na machozi yakazidi kunimwagika usoni mwangu. Tukakumbatiana kwa dakika kama kumi kisha tukaachiana, taratibu Nuru akazunguka na kukaa kwenye kiti nilicho kuwa ni nimekalia mimi.
“Kaa sasa hicho kiti ni chako”
Nuru alizugumza hukua kijipungusa machozi usoni mwake. Taratibu nikaa huku nikikitazama hichi kitu usoni mwangu.
“Namba ya siri ya computer ni Jojo93Jojo, niliibadilisha leo asubihi, na hiyo ndio itakuwa namba yako ya kufugulia kila kitu kinacho hitaji namba za siri ikiwemo na akaunti zote za makampuni yote, wewe utatumia neno hilo la siri”
“Duuu, kwa hiyo kuna akauti ngapi kwenye kampuni zote?”
“Kuna akaunti binafsi ambayo sasa ni yako, ina kiasi cha dola bilioni thelathini, kuna akaunti zaidi ya mia tatu za makampuni na vitengo mbali mbali nazo zina pesa zao, kwa haraka haraka siwezi kukumbuka ni kiasi gani cha pesa kitakuwemo kwenye akaunti hizo.”
Nuru akatoa flash iliyo tengenezwa kwa madini ya dhahabu.
“Hiyo flash ndio ufunguo wa kila data zaote za makampuni ukichomeka kwenye hiyo computure, au laptop nyingine utaweza kuona hizo data, kila linalo tendeka kwenye kila kampunini utaweza kuona data zake, hadi record ya CCTV kamera, hakikisha kwamba huipotezi hiyo flash kwani hiyo ndio msema kweli. Hembu jaribu kuichomeka kwenye hilo computure”
Nikachomeka flash hii na kukuta ikinihitaji kuingiza neno la siri, nikaingia jina langu kama vile Nuru alivyo nitajia na kweli ikafunguka, nikakuta mafaili zaidi ya elfu moja.
“Click kwenye fail lililo andikwa CCTV Camera?”
Nikafungua faili hilo.
“Umeona nini?”
“Kumekuja picha za majengo mengi hapa?”
“Click katika picha ya jengo hili?”
“Ni namba ngapi?”
“Mia tatu?”
Nikafungua faili hili na kuniletea vipande vya picha za video zaidi ya mia moja huku kila video ikionionyesha eneo lake.
“Hapo ukiwa sehemu yoyote duniani, unaweza kufwatilia kila kinacho endelea katika jengo hili au unaweza kupata kumbukumbu zote za matukio yaliyo weza kutokea katika siku chache za nyuma au dakika chache za nyuma”
“Sawa sawa, imefanywaje fanywaje?”
“Ni mambo ya kisayansi hayo. Pia kupitia flash hiyo utaweza kupata data za mfanyakazi yoyote kuanzia hawa tunao kwenda kuonana nao hadi mfagiaji wa maeneo haya. Utapata ripoti yake”
“Nashukuru sana Nuru”
Nuru akaendelea kunipa maelekezo ya vitu vingine hadi inatimu saa sita kasoro tukawa tumemaliza maelekezo ambayo amenipa. Tukarudi kwa mafundi chereheni na kukuta wakiwa tayari wamesha maliza kunishonea nguo yangu. Nikachukua na kurudi kwenye jumba tunalo ishi.
Nikamkuta Eddy akiwa mwenyewe sebleni akicheza game.
“Vipi kikao kimesha kwisha?”
“Hapana ndio tunakwenda kukianza?”
“Mmmm saa sita hivi?”
Ndio mume wangu, nitakuelezea kila jambo nitakapo rudi”
Eddy akanisindikiza kwa macho hadi nilipo potea kwenye macho yake, nikaingia chumbani na kuoga haraka haraka huku flash nikiwa nimeivaa shingoni mwangu kwa maana ina cheni yake na imekaa kama pambo pale ninapo ivisha kifuniko chake. Mlango wa bafuni humu ukafunguliwa na Eddy akasimama mlangoni huku akinitazama jinsi ninavyo oga.
“Umeniambia kwamba kikao ndio munakwenda kukifanya?”
“Ndio mume wangu?”
“Muda wote mulikuwa munafanyaje?”
“Kuna maelekezo ambayo Nuru alikuwa akinipatia, pia nilikuwa nina saini kwa mwanasheria wake na nimesha kuwa raisi wa kampuni zake zote”
Eddy akanitazama kwa macho ambayo dhairi yanaonyesha kwamba ana wivu na ana hisi jambo baya.
“Hamjafanya chochote?”
“Jamani mume wangu, hatujafanya kitu cha aina yoyote zaidi ya hivyo nilivyo kuambia”
“Na hiyo cheni hapo shingoni umeitoa wapi?”
“Mume wangu hii ndio utajiri wetu, tayari tumesha kuwa matajiri”
“Mmmm haya”
“Nini lalikini mbona unajibu kiunyonge mume wangu”
“Umekwenda huko na kukaa muda wote wewe unahisi mimi nitahisije wakati watu wenyewe hapo awali mulikuwa……kama hivyo”
“Mume wangu, nimesha kumabia kwamba ule mchezo tumesha uacha, achilia mbali tu kuacha kwa jinsi leo ulivyo nitomb** hapa sina hata nyeg** na mwanaume wa auna yoyote”
“Ila yeye ni mwanamke”
“Sawa hata yeye sina hisian naye, isitoshe anaumwa yeye. Mambo hayo akianza kuyafanya hivi sasa anaweza kufa hata kabla ya siku zake”
“Sawa, basi nataka niwe mlinzi wako huko unapo kwenda kufanya kikao”
“Eddy”
“Nini, kwani kazi ya mume ni nini, si kumlinda mke wake?”
“Wivu huo sasa”
“Ukienda utarudi saa ngapi?”
“Sijajua ila kikao kikiisha tu nitakuja”
“Okay, kuwa makini sana”
“Poa”
Nikatoka bafuni na kujifuta maji mwili mzina.
“Jojo”
“Beee”
“Wewe ni mzuri mke wangu”
Eddy alizungumza huku akinitazama mwili wangu wote.
“Achante ma huby”
Nikavaa gauni hili na Eddy akanisaidia kunifunga zipu mgongoni mwanngu. Baada ya kumaliza, nikavaa na viatu virefu vyangu virefu kiasi. Nikaziweka nywele zangu vizuri huku nikijitazama kwenye kioo.
“Umependeza, hapo hakuna haja ya vipodozi?”
“Yaa wala sipaki chochote usoni mwangu”
Tukatoka ndani humu na moja kwa moja tukaelekea hadi sebleni na kumkuta Nuru akinisubiria. Tukatoka nje na kuwakuta walinzi sita walio valia suti nyeusi wakitusubiria, nikamkumbatia mume wangu.
“Kuwa makini, nitakusubiria hapa hadi urudi”
“Sawa mume wangu”
Tukaondoka katika eneo hili na kuelekea katika eneo moja lenye lifti zinazo tembea juu ya nyanya maalumu, inayo toka katika mlima mmoja na kwenda katika mlima mwengine.
“Ulisha wahi kupanda mashine hizi?”
Nuru aliniuliza huku tukiwa tunaingia katika mashine hii iliyo kaa kama kijumba, ila kimetengenezwa kwa vioo vigumu sana.
“Hapana leo ndio mara yangu ya kwanza kuipanda”
“Ahaa, tunaelekea kule ndipo ulipo ukumbi wa mikutano na ndipo kuna hoteli ambayo watu wote wanafikia kule”
“Ahaa, kwa hiyo kwenye hilli eneo la milima kuna majengo mangapi?”
“Nane ya gorofa ni saba na la nane ni la kawaida tu”
Tukafika katika jengo hilo na kukuta walinzi walikiwa ni wengi sana tofauti na eneo tuliko kuwepo. Tukaingia moja kwa moja hadi kwenye moja ya chumba cha mapumziko, Nuru akajiweka vizuri.
“Hivi uliwaambia kwamba leo unamteua mrithi wa mali zako?”
“Hapana?”
“Haaa….!!! Kwa nini sasa?”
“Wangejipanga kufanya mambo mabaya. Leo hii yenyewe ni lazima kuna viongozi ambao nitawafuta kabisa kwenye kampuni zangu. Watakupa shida”
“Wamefanyaje?”
“Ni watu wenye tamaa na uchu wa madaraka. Mtu umemuajiri ila bado anakuwa na uchu wa madaraka jambo ambalo sio zuri kabisa kwenye biashar”
“Ahaaa, mmm inabidi unionyeshe kabisa leo”
“Wala usijali, hao mimi ndio ninao maliza nao kwenye wakati wangu wa kuongoza”
“Sawa”
“Nitaanza kuingia kwenye chumba cha mkutano na baada ya muda atakuja sekretari kukuchukua sawa”
“Sawa”
Nuru akatoka chumbani humu na kuniacha peke yangu. Kila muda nikajikuta nikizunguka zunguka kwenye chumba hichi huku nikivuta taswira ya jinsi nitakavyo tangazwa kama raisi wa makapuni yote ya Nuru.
‘Nitaongea nini?’
Nilijiuliza na kukosa jibu kabisa. Zikapita dakika kama ishirini hivi, mlango ukafunguliwa na akaingia dada mmoja mrefu na aliye valia suti.
“Habari yako mkuu”
“Salama”
“Tunaweza kuongozana sasa”
Dada huyu alizungumza huku akianza kutangulia mbele. Tukatoka katika chumba hichi na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu ambayo imetulia sana, na vitu vinavyo sikika ni milio ya viatu vyetu aina ya kokoko tulivyo vivaa. Tukafika katika mlango mkubwa ulio andikwa N GROUPS. Dada huyu akaufungua na tukaingia ndani, nikakuta watu wengi wakiwa wamekaa kwenye viti na meza kubwa zilizo kaa mfumo wa duara. Tukaanza kutembea hadi kwenye eneo aliko kaa Nuru, na ni kiti kimoja ambacho kipo pembeni. Nuru akasimama huku akiwa na tabasamu, akanipa mkono na kunikaribisha kwenye kiti cha pembeni kisha kwa pamoja tukaa. Nikaanza kuangaza macho yangu kwa mtu mmoja baada ya mwengine ila nilipo fika kwa mtu wa kumi na mbili moyo wangu ukastuka sana, kwani sikutegemea kumuona adui yangu Kibopa akiwa katika ukumbi huu naye akihesabika kama mtu bosi aliye ajiriwa na Nuru.
ENDELEA
Kiboma naye akaonekana kustushwa sana, nikatabasamu huku nikiendele kutazama watu wengine.
“Kama nilivyo watangazia hapo awali kwamba nimepata mrithi wa mali zangu. Basi sina mudi kumtangaza Jojo Jery kuwa mrithi wa mali zangu, ninakuomba usimame”
Taratibu nikasimama na watu wote wakaanza kupiga makofi huku wakisimama na kuinamisha vichwa vyao chini ikiwa ni ishara ya heshima.
“Unaweza kuzungumza kitu”
Nuru aliniambia huku akinitazama usoni mwangu.
“Nitazungumza nini Nuru”
Nilimnong’oneza Nuru kwa sauti ya chini
“Chochote kila ambacho unahitaji kukizungumza”
“Sawa”
Kwa ishara nikawaomba watu hawa kukaa chini. Nikashusha pumzi taratibu huku nikitazama watu hawa walio toka mataifa mbalimbali duniani.
“Habari za muda huu?”
“Salama”
Waliitikia kwa pamoja, hapa ndipo nikagundua kwamba wote wanafahamu Kiswahili.
“Mimi kwa muda huu sina mengi sana ya kuzungumza, ila ninacho taka kuwaomba ni muweze kunipa usihirikiano kama mulio uonyesha kwa mama hapa. Na kitu cha kusisitizia tufanye kazi kwa juhudi ili kuzidi kukuza makampuni yote. Ila angalizo, msaliti kwangu hana nafasi na kama unaweza kujijua wewe ni msaliti au ulisha wahi kunifanyia mambo mabaya hapo awali ni vyema ukajiengua kwenye kampuni yangu, kwani ukisubiri mimi kufanya hivyo, nilazima nitakuua. Asanteni”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo nikakaa chini na kuwafanya baadhi ya watu kupiga makofi ila Kibopa na watu walio kaa karibu naye wote hawakupiga makofi na wanaonekana kujawa na wasiwasi mwingi sana, japo kauli yangu kwa namna moja ama nyingine ina mlenga Kibopa yeye mwenyewe. Nuru akasimama huku akiwa amejawa na tabasamu.
“Kama mulivyo weza kumsikia raisi mpya wa N GROUPS, msaliti kwake hana nafasi, ila nitawaombea nafasi moja ya kukutana na raisi huyu ili kama kuna mambo mabaya ulisha wahi kunifanyia au kumfanyia yeye basi munaweza kumuomba msamaha, akikubali, basi ni bahati yako ila akikataa mimi sina cha kuzungumza zaidi ya kusubiria hukumu yako. Muheshimiwa Jojo, nafasi ni yako ya kuvunja kikao”
“Kuna mtu mwenye mawazo au maoni?”
Nilizungumza huku nikiwatazama, zikapita kama sekunde thelathini hivi, bibi mmoja wa kichina akanyoosha mkono. Nikamruhusu kusimama ili azungumze kile ambachoa anahitaji kukizungumza.
“Mimi penda sana wewe ongoza kampuni hii, kiwa bado upo katika umri mdogo. Ila je tambua juu ya uzalishaji wa Cocain yetu kule Colombia na je utasaidia vipi kukuza soko letu?”
Bibi huyu alizungumza kwa Kiswahili kibovu kibovu, swali lake likanifanya nikae kimya kwa muda huku nikimtazama Nuru.
“Kwa sasa ni ngumu kuzungumza chochote juu ya hiyo biashara. Nitahitaji wanao shuhulika na biashara hiyo tuweze kuonana usiku huu huu mara baada ya kumaliza kuonana na wale ambao watahitaji nizungumze nao kwa kuomba msamaha, au walikuwa wakihitaji kuzungumza nami”
“Nitamke rasi kwamba kikao kimevunjwa, ila kesho saa nne asubuhi nitahitaji tuonane tena ili niweze kuwatangazia sheria zangu kumi ambazo nitahitaji kila mmoja wenu aweze kuzizingatia na akizikiuka, basi adhabu yake ni kifo. Asanteni”
Baada ya kumaliza kuzungumza hivyo nikasimama, na watu wote wakasimama akiwepo na Nuru. Tukaongozana na Nuru na kutika katika ukumbi huu huku mapigo ya moyo yakinienda kasi kwa maana siamini kama kweli nimeweza kuwaongoza watu wengi namna hii na wengi wao nina imani mimi ni sawa na mtoto wao.
“Nuru hivi watu hawa wote uliwatoa wapi?”
“Hahaa, kila kitu ni nguvu, unahisi ninawatafuta. Walikuja wao wenyewe”
“Mmmmm, ila niliogopa nilipo kuwa nina ingia, ila kuna mjinga mmoja baada ya kumuona humo ndani, ndio amenifanya niwe jasiri hata katika kuzungumza”
“Mjinga gani huyo?”
“Kibopa”
“Kibopa, Kibopa…….”
“Ina maana humfahamu?”
“Hapana, unahisi mimi ninawajua wote hao. Ila nikihitaji kumfwatilia mtu hapo ndipo ninapokwa ninamfwatilia kwa undani na kumfahamu”
Nuru alizungumza huku akifungua mlango mmoja na tukaingia ndani. Katika chumba hichi kuna meza moja ya duara iliyo zungukwa na viti.
“Utazungumza na watu wote hao ambao ulihitaji kuzungumza nao humu ndani, ila kama unahitaji unaweza kumuita mmoja mmoja au ukazungumza nao wote”
“Unataka nizungumze nao peke yangu”
“Ndio, kwa maana wewe ndio mmiliki wa makampuni yote”
“Hapana, nahitaji uwepo pembeni yangu hapa, nahitaji kumuanza huyo Kibopa kwa maana kuna kazi nahitahi kumkabidhi”
“Sawa”
Tukaaa kwenye viti, sekretari akaingia na nikampa maagizo ya kuweza kumuita kibopa. Baada ya dakika kama tano hivi wakaingia wote wawili, kwa ishara nikamuomba Kibopa kukaa kwenye kiti na sekretari akatoka. Nikamtazama Kibopa kwa macho makali sana jambo lililo mfanya kuyakwepesha macho yake mara kwa mara ili asiyakutanishe na macho yangu.
“Kibopa niambie”
Nilizungumza kwa sauti ya kawaida, ila yenye msisitizo ndani yake.
“Mmmmm”
“Naona hukutegemea kuonana na mimi hapa si ndio?”
Swali langu kikazidi kumpa wasiwasi Kibopa.
“Sihitaji kurudia yale ambayo ulisha yafanya kwangu. Ila ninataka kukupa kazi moja ambayo itakuwa ni msamaha kwenye maisha yako, la sivyo huto iona Tanzania tena na nitakuua, umenielewa?”
Nilizungumza kwa msisitozo na kumfanya Kibopa kutingisha kichwa huku akinitazama usoni mwangu.
“Nipo tayari kufanya kazi yoyote mkuu ila unisamehe maisha yangu”
“Henrry ni rafiki yako sana, si ndio?”
“Ndio mkuu?”
“Na uliona kilicho tengenda machana si ndio?”
“Ndio muheshimiwa?”
“Kama ulivyo shinikiza mama mkwe wangu kutolewa madarakani, basi kwa nguvu na amri ile ile hakikisha kwamba raisi Henrry hadi ina fika saa sita mchana kukipambazuka awe ameachia madaraka umenielewa?”
Kibopa macho yakamtoka, dhairi anaonekana kwamba kitu nilicho muambia ni jambo zito kwa yeye kulifanya.
“Umenielewa?”
“Ndio mkuu”
“Cha kuongezea hapo, kumbuka sheria zetu zipo vipi na nimesha muachia Jojo kila kitu kwa hiyo ana mamlaka ya kukufanya jambo lolote hivyo basi kuwa makini sana kwa kila jambo unalo likusudia kulifanya”
Nuru naye alitilia uzito katika kazi hii niliyo mkabidhi.
“Sawa mkuu”
“Unaweza kwenda”
Taratibu Kibopa akasimama huku akionyesha dhairi haamini kabisa, kwamba yule msichana ambaye nilikuwa ninafagia katika nyumba yake na kumfuta futa jasho mwilini mwake, leo hii nimekua bosi wake tena katika kikundi kikubwa sana ambacho kimeyashikilia maisha yake. Wakaingia viongozi wengine ambao wamekuja kuomba msamaha kwa yale mabaya waliyo yafanya kwa Nuru. Zoezi la kuzungumza nao likaisha saa kumi na moja alfajiri, huku sote tukiwa tumechoka sana. Tukarudi karika jumba tunalo ishi na nikamkuta mume wangu akiwa amelala sebleni kwenye sofa, ahadi yake ya kunisubiria hadi niyakapo rudi ameikamilisha.Taratibu nikainama na kumbusu mdoni mwake na kumfanya afumbue macho yake.
“Baby mbona umelala hapa”
“Mmmmmmm”
“Amka mume wangu tukalale”
“Ni saa ngapi sasa hivi?”
“Saa kumi na moja”
“Mmm….mbona umechelewa hivyo?”
“Tutazungumza ndani?”
Nikamshika mume wangu mkono na kuingia chumbani kwetu, hakuhitaji hata kuzungumza, moja kwa moja akajibwaga kitandani na kuendelea kulala. Nikavua nguo zangu zote na kuingia bafuni, nikasimama mbele ya kioo na kujitazama kwa muda huku nikiya tathimini maisha yangu toka nilipo tokea, misuko suku mingi sana niliyo ipata hususani nchini China, ambapo huko ndipo nilipo pata ujasiri wa kuhakikisha kwamba nina pambana na maisha. Kitu kimoja nilicho kigundua maishani mwangu ni kuto kukata tamaa, laiti ningeyakubali maisha ya uswahilini ningeishia kuwa mama ntilie na huu uzuri wangu nilio nao, wala nisinge kuwa nao kwani vijana wa mtaani wangenivuruga kwa kutomb** hadi ninge zeheka kabla ya umri wangu wa kuzeeka kufika. Nikaoga kisha nikarudi kitanda na kukumbatia mume wangu kwa nguma, hazikupita dakika nyingi usingizi ukanichukua na kulala fofofo.
***
Asubuhi wote tukakusanyika sebleni kwa kupata kifungua kinywa. Nuru akaitumia nafasi hii kwa kuwaambia watu wa familia wangu juu ya urithi wa mali zake alizo nirithisha. Kila mmoja akapendezwa na uamuzi huo alio ufanya.
“Hongera wifi”
“Asante”
“Inabidi uniajiri”
Shemeji alizungumza huku akitabasamu.
“Haaha usijali shemeji yangu”
“Haya jamani nimepata jibu la maombi ambayo nilikuwa ninaomba jana usiku”
Mama Gody mkubwa alizungumza kwa upole huku akitutazama usoni watu wote.
“Ehee majibu shem ni yapi?”
Mama Gody akakaa kimya kwa muda kisha akashusha pumzi nyingi sana kisha akaanza kuzungumza.
“Maombi nilivyo jibiwa ni kwamba, raisi hatotoka madarakani kwa njia kama tuliyo hitaji sisi wenyewe”
Habari hii ikatushua sote na kila mmoja akakaa kimya ili kuweza kumsikiliza mama Gody ambaye kwa imani tunaamini ni mwanamke mwenye mahusiano mazuri na Mungu, toafuti na sisi ambao maisha yetu yamejaa dhambi nyingi.
“Maono niliyo onyeshwa na mwenyezi Mungu ni kwamba, ili raisi aweze kutoka madarakani, ni lazima damu itamwagika”
“Mmmmm”
Eddy aliguna kidogo.
“Na si damu ya watu wengi, ila ni damu ya mtu mmoja ndani ya hii familia tukimtoa Nuru”
Nyuso za watu wote zikapoteza furaha, hamu hata ya kuendelea kunywa hii chai nayo ikapotea kabisa.
“Shem ni nani atakufa?”
“Hapo ndipo lilipo fumbo nililo fumbwa, sijui ni nani atafarikia, ila nimehakikishiwa kwamba raisi ni lazima atoke madarakani kwa damu ya mmoja wetu kumwagika, sasa sijajua ni mimi au ni nani?”
Tv iliyopo hapa katika eneo la kupatia chakula, ikaweka taafira ya dharura kutoka nchini Tanzania, jambo lililo tufanya tuzidi kuwa wasikivu. Chaneli hii ya Kenya, ikaonyesha matangazo ya moja kwa moja kutoka ikuli ya raisi Tanzania. Tukamuona raisi Henrry akisimama katika maiki kadhaa zilizo pangwa kwenye kwenye sehemu yake maalumu ya kuzungumza.
“Hivi ndivyo nilivyo onyeshwa”
Mama Gody alizungumza huku akiwa ameyafumba macho yake.
“Raisi hato kubali kutoka madarakani”
Mama Gody aliongezea na kutufanya tuzidi kujawa na hofu na wasiwasi mwingi sana.
“Ndugu wananchi, ninaimani wengi wenu jana muliweza kuona kile kilicho tokea kwenye televishion zote duniani”
“Nilitishwa, niliogopeshwa tena na kijana mmoja ambaye hapo mwanzoni taifa lilimuangalia kama maundishi mzuri mashuhuri na mbunifu pia?”
Nikamtazama mume wangu kwa maana mtu anaye ambiwa hapa ni mume wangu.
“Nilikaa sana na kutafakari maneno ya kijana huyo, ambaye siku za hapo nyuma alimteka mke wangu akiwa na mchumba wake yule Jojo, ambanye naye pia taifa lilimuangalia kama mcheza filamu mzuri na aliye zalisha ajira kwa vijana wezake na hata watu wengine”
Raisi alizungumza kwa upole na unyenyekevu mkubwa sana.
“Nilizidi kutafakari usiku kucha ni kwa nini vijana hawa wamefanya hivi au wanafanya hivi, kwa nini anataka kutishia taifa na kulipeleka taifa katika mstari ambao sio mzuri, mshari utakao sababisha fujo na vurugu nyingi nchini Tanzania”
“Je nikiwa kama raisi niliye chaguliwa na watu nijiudhuli kwa ajili ya mtu mmoja na mchumba wake ambao hata wahawajafikia hatu ya kugombania uraisi. Je wale wafuasi wangu wa chamba changu walio niamini na kunisimamisha nigombanie nafasi hii je niwasaliti kwa kujiudhulu. Nikakaa na kamati yangu na washauri wangu, hakuna hata mmoja aliye kubali niweze kujiudhulu na kuachia madaraka yangu. Nami nikiwa kama raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ninasema kwamba sinto jiudhuru na vijana hao wawili Jojo na Eddy, ninawatangaza kama magaidi na popote wanakapo onekana basi mutoe taafira kwa chombo chochote cha usalama zawadi ya dola milioni moja itatolewa kwa kila atakaye fanikisha kukamatwa kwa vijana hao. Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Afrika asanteni kwa kunisikiiza”
“Pumbavu lazima niende kumuua huyu fala kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Eddy alizungumza kwa hasira huku mwili ukimtetemeka kwa hasira.
“Shem usiende na usifanye hivyo kwani utakufa”
Maneno ya mama Gody yakazidi kutupa wasiwasi ulio nifanya nianze kuhisi kukata tamaa kwani sinto hitaji kumpoteza mume wangu katika swala hili la kumtoa raisi madarakani.
“Huwezi kukurupuka na mahasira yako na kutaka kwenda kumvamia raisi, ikulu sio sokoni”
Shem alizungumza huku akimtazama mume wangu usoni mwake.
“Plan A, imefeli, inabidi twende na Plan B?”
Plan alizungumza, ila kabla ya mtu yoyote hajachangia tukamuona mama mkwe wakiingia ndani humu na Gody huku akisukumwa kwenye kiti cha magurudumu na mjukuu wake huyo. Wakafika katika sehemu hii na watu wote tukamsalimia. Mama mkwe akaitikia huku akiwa na tabasamu pana sana usoni.
“Naona Henrry amewakosmesha, sasa muache viranga vyenu na mutulie na muendelee na maisha yenu”
“Mama unazungumza kitu gani jamani?”
Wifi alizungumza kwa kulalama.
“Kuna nini ambalo munaweza kulifanya ikiwa amekataa kuachia madaraka”
“Mama katika hili, pasipo kukuvunjia heshima, tunakuomba uliache kama lilivyo. Tulia uone ni kitu gani ambacho tunakwenda kukifanya”
Shemeji alizungumza kwa ukali kidogo huku akimtazama mama mkwe
“Haya mimi yangu macho”
Wifi akanyanyuka kwenye kiti na kuondoka katika eneo hili na kuelekea chumbani kwake. Baada ya dakika kadhaa akarudi huku akiwa ameshika laptop yake, akaifungua na kuanza kuminya minya.
“Ninaanza kutuma ushahidi wa kwanza katika serikali ya China na ushahidi wa pili ninatuma katika serikali ya Urusi. Nitawapa muda wa masaa mawili ili kuweza kufanya maamuzi kwa ushahidi ambao wanakwenda kuuona”
Wifi alizungumza huku akiminya minya batani za laptop hiyo kwa kasi sana. Baada ya muda kidogo wifi akatujibu kwamba tayari ushahidi wote amasha tuma kwenye serikali hizo na ameahidiwa kupewa majibu baada ya mdua kidogo.
“Rich anza kushuhulikia ile flash”
Shemeji alizungumza huku akinyanyuna na kuelekea sebleni, watu wote tukahamia sebleni kutazama mipango yote ambayo inatakiwa kufanyika.
“Nuru yule kijana wako yupo wapi?”
“Ngoja nimpigie simu aje”
“Tunaweza kupata Tv kubwa tofauti na hii?”
“Labda niwapelekee katika ofisi anayo fanyia kazi yule kijana”
“Sawa itakuwa vizuri”
Hapakuwa na mtu hata mmoja aliye baki sebleni, sote tukaelekea katika katika ofisi hiyo. Tukaingia katika ofisi hii ambayo ni ukumbi mkubwa na kuna Tv nyingi ukutana na kijana huyu yupo peke yake akishuhulikia kila kitu anacho kijua yeye ndani ya chumba hichi.
“Tunaweza kwenda online?”
Eddy aliuliza.
“Na leo unataka kujianika kwneye mitandao televishion?”
Mama mkwe aliuliza huku akitutazama.
“Mama hili swala halihitaji ushauri wako, acha tufanye kazi yetu”
Eddy alimjibu mama mkwe huku akimtazama kijana huyu.
“Ndio inawezekana”
“Basi nahitaji kusema jambo na dunia”
“Dakika kumi naomba”
Kijana huyu akaburuzika na kiti chake hichi za matairi hadi kwenye compure nyingin na akaanza kuminya minya batani hizo huku akitingisha tingisha kichwa chake. Akanayanyuka na kuchukua camera ndogo aina ya Panasonic HD. Akaisomamisha kwenye viguu vitatu vya kusimamishia kamera.
“Mmmm ukataa pale”
Kijana huyo alizungumza huku akimonyesha Eddy sehemu ya kukaa ambayo kwa nyuma kuna Tv kubwa”
“Sawa”
Eddy akavuta kiti kimoja na kukaa katika eneo hilo huku kamera hiyo ikiwa imeelekezewa kwake.
“Sister ule ushahidi unao?”
“Nitampa huyu kijana awe anaurusha kila utakapo kuwa unazungumza”
“Inawezekana?”
“Ndio”
“Hembu naomba niuusome ili nikizungumza nisijing’ate ng’ate”
“Sawa”
Wifi akamkabidhi Eddy laptop yake na akaanza kusoma ushahidi huo.
“Haki ya Mungu nimezaa watoto wendawazimu”
Mama mke walizungumza huku akitabasamu. Nikamtazama ila sikumjibu kitu chochote.
“Chukua”
Eddy alizungumza huku akinikabidhi laptop ya wifi, nikaichukua, akajiweka vizuri shati lake na sote tukamtazama kijana huyu wa Nuru.
“Bado dakika moja”
“Sawa”
“Baby”
“Mmmm”
“Utazungumza nini?”
Nilizungumza kwa kunong’oneza huku nikiwa nimeinama pembeni ya Eddy
“Usijali mke wangu, kila kitu kinakwenda kuwa poa, sawa baby”
“Sawa mume wangu”
Nikarudi katika sehemu niliyo kuwa nimesimama. Kijana huyo akaanza kuhesabu vidole kuanzia no moja hadi tatu na Tv zote zilizomo humu ndani zikaanza kuonyesha video ya mume wangu.
“Habari za muda huu. Ni muda mchache raisi wa Tanzania, bwana Henrry amekataa kufwata kile ambacho nilimuagiza jana. Kwa kuongezea ameweza kutubatiza jina jipya na mke wangu Jojo eti sisi ni magaidi, na tena tulimteka mke wake, jambo ambalo kusema kweli mimi na mke wangu hatukuwahi kulifanya wala kulifikiria kulifanya.”
“Tukwia kama wananchi wema na watetezi wa wanyonge ambao hawawezi kusimama na kudai haki zoa kama sisi tunavyo fanya, nilazima leo hii niweze kuweka kile watu wengi mulikuwa mukikisubiria kwa hamu. Dhahiri itawaonyesha kwamba raisi Henrry hafai kuiongoza nchi na si mtu wa kawaida”
“Mwaka 2001 mwezi wa tano, aliweza kuagiza vijana kutega bomu kwenye ndege ya makamu wa raisi wa nchi China”
Picha za raisi Henrry akiwaagiza vijana wake kutegesha mabomu kwenye ndege hiyo zikaanza kuonekana.
“Alimiliki vijana watano ambao walikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuua. Wawili kati ya hao munao waona kwenye hizo picha hapo ni walinzi wake wa karibu, huku watatu walio salio akiwa amewaua kwa sababu zake anazo zifahamu yeye mwenyewe”
Picha za raisi Henrry alipo kuwa akiwapiga risasi vijana wake hao watatu zikanekana kwenye tv hizi, picha ambazo hata mimi mwenyewe sikuwahi kuziona kwenye faili ambalo alitupa Nuru na hata lile alilo kuwa nalo mama mkwe.
“Je kama ni mtu ambaye anaweza kuwau vijana wake, je atashindwa kuwaua wananchi wa kawaida, kama sisi ambao ametubatiza eti ni magaidi. Jibu ni kwamba hato shindwa. Turudi kwenye pointi ya China.”
“China waliomboleza kilio, na uchunguzi wao walipo ufanya hawakuweza kupata chochote cha msingi kwa maana jambo hilo lilifanyika kwa akili sana, ila huu ni ushidi wa video wa maandalizi ya mpango huo wa mauaji hadi kukamilika kwake”
Tukahamishia macho yetu kwenye tv, japo ni video iliyo rekodiwa kwa ubora wa chini ila uliweza kuonyesha sura sahihi za watu walio usika katika mpango huo, akiwemo raisi Henrry na kipindi hicho alikuwa bado ni kijana kama wa miaka thelathini hivi”
“Hao vijana wake walitega bomu kwenye moja ya zawadi la ua alilo kabidhi makamu wa raisi wa nchi kipindi akiondoka nchini Tanzania mara baada ya kumaliza ziara yake iliyo mleta”
“Dakika thelathini maara baada ya ndege hiyo kupaa angani, ikalipuka na kila mtu ndani ya ndege hiyo akafa, kama hivyo munavyo ona mabaki ya ndege hiyo yakianguka chini”
Video hiyo ikaishia hapo.
“Sasa hadi hapo munaweza kujua gaidi ni nani, mimi na mke wangu au yeye aliye shiriki katika mauaji hayo”
“Tukiachana na hilo, tuangalie waziri mkuu wa Urusi alivyo uliwa mwaka 2004 hapa nchini Tanzania akiwa katika ziara yake ya siku mbili”
“Mmoja wa walinzi wake ambao amesha muua, alijifanya muhudumu wa hoteli ya Senah kwa kipindi hicho kabla ya kuvunjwa na kujengwa Serena. Akaingia katika chumba cha waziri huyo huku akiwa na sumu ambayo ilikaa katika mfumo wa gesi, ambayo aliiweka katika kichupa cha mafuta ambacho ndani hakikuwa na mafuta, na baada ya kuifungulia gesi hiyo, waziri huyo alikufa pamoja na mkewe na ushahidi wa kikopo hicho cha mafuta wakauiba, na siku hiyo ndiyo kijana wake hiyo naye akapoteza maisha mara baada ya kuikamilisha kazi hiyo ili kuepuka uchunguzi wa kika kufanyika. Kama hapo munapo muona raisi akimtandika risasi kijana wake”
“Tukiacha hayo yote ambayo yamewagusa watu wa nje. Kuna hili lililo wagusa watanzania wengi na nina imani kwamba wengi wenu muna likumbuka. Jumatatu ya tarehe 24 mwenzi wa sita mwake 2002, naamini wengi wenu munaikumbuka ajali ya treni Dodoma. Ajali iliyo poteza mamia ya ndugu zetu waztu zaidi ya 281 walipoteza maisha, hapo ukiachilia walio pata vilema kwa kupoteza viungo mbalimbali kwenye miili yao”
Zikaanza kuonekana picha za Herrny na vijana wake wakizungumza, na ikaonyesha jinsi walivyo muua muendesha treni kisha wao wakaruka na kuacha treni kwenda bila ya muongozaji na baada ya muda mchache ikapata ajali.
“Zile damu zilizo mwagika mwaka ule si damu za kuku wala panya. Ni watu, ni ndugu zetu, watu walipoteza baba, mama, dada, kaka watoto na kadhalika. Leo hii jini huyo anaongoza nchi na bila haya wala aibu anasema kwamba eti mimi na Jojo ni magaidi. Huo ni ujinga, ilipo ifikia inatosha jamani. Nilazima raisi uachie madaraka, ni wakati wa kusimama kwa pamoja wananchi na kuwa na kauli moja. Sisi ndio tuliye mpa hiyo nafasi ya kuwa hapo alipo na sisi ndio tuna nafasi ya kumuangusha chini. Ninatangaza maandamano ya amani, leo hii niyajumuika nanyi kwenye maandamano ya amani kumshinikiza raisi kuachia madaraka. Maandamano yafanyike nchi nzima kwa pamoja tunaweza”
Kauli ya maadamano ikatustua sote katia eneo hili.
“Ninawapenda sana Watanzania wezangu, sasa leo nitashangaa pale chombo chochote cha usalama kikiinua mkono wake na kumuadhibu mwananchi yoyote kisa ni kuandamana, mukumbuke hata nyinyi muna watoto ambao kesho na kesho kutwa wanatakiwa kuishi kwenye nchi iliyo salama, nchi yenye kiongozi mwenye hofu na Mungu na si kiongozi mwenye mamlaka ya kishetani”
Wifi akaanza kutoa maelekezo ya vitendo kwa Eddy, kisha akamuonyesha kitu ambacho sisi hatukikiona.
“Kuna kitu kimoja nimekisahau”
Eddy alizungumza kwa upole huku akimtazama kamera hiyo inayo endelea kumrekodi.
Zikaonekana picha za watoto wenye ulemavu wa ngozi(zeruzeru).
“Hao ni watoto sita ambao walipotea kwenye mazingira ya kutatanisha, nchi iliingia kwenye vita ya mauaji juu ya Albino, na kweli albino wengi walikufa, wengi waliyeketea na wengi walijawa na hofo na wengine walipoteza miguu au viganja vya mokono au mikono yao kabisa.”
Zikaonekana picha za raisi Henrry akiwa ameshika kichwa cha mmoja wa mtoto aliye chinjwa, jambo ambalo hata mama mkwe lilimstusha sana.
“Oneni, huyo ni kiumbe wa Mungu. Kiumbe ambaye alitarajia siku moja aje kutimiza ndoto zake, awe na elimu bora au familia bora, ila jini huyo alimchinja, jini huyo alitumia viungo vya watoto hao ili kujipatia nguvu za kishirikina ili mradi tu apate nguvu ya kisiana. Je kwa hili bado tutaendelea kuwa na hofu ya kumuogopa mjinga mmoja. Jibu ni hapa, nipo tayari kufa kwa ajili ya haki watu wengine. Baada ya kumaliza kuzungumza hayo maandamano yataanza saa nane mchana nchi nzima. Ninashukuru kwa kunisikiliza”
Kijana wa Nuru akakata mawasiliano hayo ya moja kwa moja na tv zikaendelea na vipindi vyake vya kawaida.
“Unataka kusema kwamba mutakwenda kuandamana si ndio?”
Mama mkwe aliuliza kwa ukali kidogo.
“Mimi ndio nitakwenda kuandamana, watu wengine humu ndani hawana haja ya kwenda kuandamana”
“Mimi nitakwenda”
Nilizungumza huku nikimtazama mume wangu usoni.
“Mimi pia nitakwenda”
Wifi naye alizungumza na kujumuika nasi.
“Mimi nitakuwepo ila nitaandaa vijana wa kuwalinda musiweze kuudhurika”
Shemeji alizungumza.
“Nimepata wazo moja. Kutokana watu wengi wanamfahamu Mr Z, itakuwa ni vizuri yakashoneshwa mazazi mengi yanayo fanana na Mr Z, na wapewe vijana wengi ili kuwachanganya walinzi wake kwani nina imani watakuwa wamejipanga kwa ajili ya kuwashambulia”
Nuru alitoa wazo hilo ambalo hapakuwa na mtu wa kulipinga na kutokana ana mafundi wake basi, ikawa ni rahisi kupeleke oda ya nguo zaidi ya elfu kumi zinazo fanana na nguo za Mr Z zishonwe.
“Sasa hivi nisaa tano asubuhi, nina imani hadi saa saba kasoro nguo hizo zitaweza kwua tayari?”
“Je katika kuzisambaza hapo itakuwaje Nuru?”
“Tanzania nzima nina matawi ya watu wengi, nina imani ndani ya muda mchache zitakuwa zimesambaa na tutaandaa vijana watakao vaa nguo hizo”
“Itakuwa ni jambo zuri, basi kazi ianze sasa”
Nuru akatoka chumbani humu, nikakumbuka kwamba leo nina kikao watu wote ambao ninawasimamia kwenye kampuni zangu. Nikatoka chumbani humu na kuanza kutembea kwenye kordo hii huku nikimuita Nuru ambaye kidogo amesha fika mbali kidogo. Nuru akasimama na kunisubiria.
“Vipi?”
“Kuna kile kikao nilicho wataarifu wale watu, na sasa ni saa tano”
“Duuu, watakuwa wanakusubiria, sasa wewe nenda kwenye kikao hicho acha sisi tushuhulike na hili swala”
“Poa”
Nikaongozna na walinzi wanne hadi katika ukumbi wa mikutano na kukuta watu wote wakiwa wana nisubiria huku wakionekana walikuwa wakijadiliana mambo kadhaa. Walipo niona wote wakasimama na kukaa kimya, wakatoa salamu ya heshima kisha nikawaruhusu kukaa chini.
“Samahani kwa kuchelewa, naamini kwamba mumeweza kuona hali ambayo mume wangu ameitangaza ya maandamano ya amani nchini mwetu si ndio”
“Ndio mkuu”
“Nina imani kwamba nyinyo wote mutakuwa pamoja nami katika kuhakikisha kwamba hili swala linakamilika, nitahitaji muweze kutoa ushawishi katika nchi zenu, kuhakiksiha wanamshinikiza raisi Henrry anaachia madaraka. Hilo ni moja, mbili kama kuna muwekezaji mkubwa aliye wekeza Tanzania, hakikisheni kwamba muna mshawishi kutoa uwekezaji wake Tanzania, hadi pale raisi atakapo kubali kuondoka madarakani”
“Je mumenielewa na mupo pamoja nami?”
“Ndio muheshimiwa?”
“Angalizo, sinto hitaji msaliti na wala sinto hitaji makosa kufanyika katika maelekezo yangu. Mimi ni mtu ambaye ninapenda kunyoosha melezo na si mtu ambaye ninapenda kuyumba yumba, sawa”
“Umeeleweka muheshimiwa”
“Sawa munaweza kutawanyika”
Mara baada ya kumaliza kuzungumza hivyo nikatoka ukumbi huu, nikiwa njiani kuelekea nje, Kibopa akaniwahi na kuniomba tuzungumze.
“Ndio”
Nilizungumza huku tukisogea pembeni na kibopa.
“Jana nilizungumza na raisi Henrry”
“Ehee”
“Kama ulivyo sikia alicho kizungumza, alikataa.”
“Wewe una vijana wangapi Tanzania wanao fanya kazi zako haramu?”
“Mmmm”
“Vijana wangapi unao?”
“Kama mia na hamsini?”
“Wahamasishe wakuu wao wote kwamba wanatakiwa wawe kwenye maandamano na waweze kushika mabango ya kumuhamasisha raisi kuachia madaraka sawa”
“Sawa, ila pia nina watu maalumu ndani ikuku ambao wanaweza kuhakikisha kwamba pacha wa mume wako anakombolewa kwa maana ameniambai atamtumia pacha huyo kuwatishia mumuache aendelee na madaraka yake”
Nikaa kimya kwa muda huku nikitafakari cha kuzungumza.
“Una uhakika na hicho ulicho kizungumza?”
“Ndio amesema kupitia pacha huyo atamshinikiza mume wako kuto kumtolea siri zake, ila nimeshangaa kuona kwamba mume wako ametoa siri zake za ndani sasa sijajua hakumpata au laa?”
“Twende huku”
Nilizungumza na Kibopa na tukaingia kwenye lifti hii na kurudi katika upande wa pili tunapo ishi, moja kwa moja tukaelekea kwenye ofisi ambayo niliwaacha Eddy na ndugu zake. Tukawakuta wakiendelea kufanya mipango yao. Mama mkwe alipo muona Kibopa hasira zikaanza kumpanda.
“Huyu mshenzi umemtolea wapi?”
Mama mkwe alizungumza kwa ukali, huku akiyazungusha matairi ya kiti chake hichi alicho kikalia huku akimfwata Kibopa sehemu alipo simama.
“Mama mama huyu ni msaada wetu wa kumpata Azaria ndani ya ikulu, kwa maana ameshikiliwa na raisi”
Nilizungumza kwa haraka na kumfanya mama mkwe kupunguza kasi ya kumsogelea Kibopa na kuniangalia.
“Yaa ninaweza kuwasaidia kumpata pacha wa jamaa hapo”
“Kivipi?”
Eddy aliuliza huku akitufwata sehemu hii tulipo simama.
“Raisi Henrry ni rafiki yangu wa karibu sana, jana Jojo aliniambia nimshawishi ili kuachi madaraka hivyo ninataka kuwasaidia nyinyi”
“Ina maanisha unataka kumsaliti rafiki yako si ndio?”
“Ndio”
Nikastukia Eddy akimpiga Kibopa ngumi ya shavu na kumfanya aweweseke na kuanguka chini.
“Kama unaweza kumsaliti huyo mshenzi mwenzako utashindwaje kutusaliti sisi?”
Eddy alizugumza kwa ukali.
“Dogo, dogo hembu ngoja kwanza. Hujui ni sababu gani zinazo pelekea kumsaliti rafiki yako?”
“Ni kwa ajili ya Jojo mkuu wangu, kwa kufanya hivi ameniahidi kunisamehe dhambi zangu nilizo mfanyia kwenyemaisha yangu na kuniacha hai na mimi ninapenda kuishi.”
Kibopa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Sawa tupe maelekezo ya kufanya ili niweze kumkomboa mdogo wangu”
“Kuna dada yupo ikulu mule ni mlinzi wa mke wa raisi ameweza kunipa maelezo ni wapi ambapo mdogo wako amefungiwa”
“Una mawasiliano naye?”
“Ndio”
“Mpigie simu?”
Kibopa akatoa simu yake mfukoni na kumpigia msichana huyo. Nuru akaingia ndani humu na kushangaa kumkuta Kibopa humu ndani, ila hakuhitaji kuzungumza chochote.
“Jojo”
“Beee”
“Nakuomba”
Tukatoka nje na Nuru na kusimama kwenye kordo.
“Amefwata nini huyu chizi?”
“Anafamu sehemu alipo pacha wa mume wangu”
“Ahaa…..sasa nguo ambazo tumeweka oda mafundi wamesema kwamba kwa leo itakuwa ni ngumu kuzimaliza, hivyo labda kwa kesho sasa sijajua itakuwaje juu ya maandamano hayo?”
“Mmmm unataka kuniambia kwamba tusitishe mpango wa maandamano hadi kesho?”
“Nilikuwa nina waza jambo hilo, ila sijajua kama mume wako anaweza kulikubali”
“Ngoja nimuite”
Nikaingia ndani, kwa ishara nikamuomba Eddy na akanifwata na tukatoka nje na kusimama alipo simama Nuru.
“Vipi?”
“Nguo ambazo tulikuwa tunazihitaji kwa leo hatuto weza kuzipata, mafundi wangu wameniambia kwamba kwa kesho zinaweza kuwa tayari”
“So munataka tusitishe maandamano?”
“Ndio, ingekuwa ni vizuri yakafanyika saa kumi na mbili asubihi, nina imani nguo pia tutakuwa tumezitawanya katika nchi nzima”
Eddazaria akajikuna kichwa kidogo huku akionekana kujawa na mawazo kidogo.
“Sasa tutawatangazia wananchi juu ya hili si watatuona watu wenye vigeu geu na hatuna msimamo kwenye maamuzi yetu?”
“Jaribu hata kuwadanganya nina imani unaweza kuwatangazia jambo lolote na waka kuelewa”
“Mmmmm”
“Eddy mume wangu nakuomba tufanye hivyo ili swala hili liende endapo tukashindwa kujipanga leo mambo yanawea kuwa mabaya”
“Sawa nimewaelewa”
Eddy akarudi ndani na kwa kushirikiana na kijana wa Nuru akawatangazia wananchi kwamba maandamao yatafanyika kwa siku ya asubuhi, inayo fwata, anatoa nafasi kwa wananchi kujipanga katika swala zima la maanadamo. Pia akawaeleza maandamano yote yataelekea ikulu kwa wale walipo Dar es Salaam.
***
Usiku wa saa kumi, tukatoka nchini Kenya na kuingia nchini Tanzania kwa helicopter huku tukiwa tumejipanga kwa maandamano, tukafika katika nyumba ya Nuru ya siri iliyopo jijini Dar es Salaama maeneo ya Mbagala. Nguo zote ambazo hutumia Mr Z, zikasambazwa nchi nzima.
“Shem”
“Naam”
“Ulifanikiwa kuweza kujua ni wapi alipo Azaria?”
“Bado kwa maana mtu ambaye tulikuwa tunamtegemea atupatie taarifa amekamatwa”
“Mmmmmm”
“Yaa ila tutampata tu”
“Sawa”
Ilipo fika majira ya saa kumi na moja alafajiri tukaianza safari ya kuelekea ikulu, hadi inafika saa kumi na mbili tukakuta watu wengi sana wakiwa wamefunga barabara ya kuelekea ikulu jambo lililo tupa matumaini sana, kwani kwa kile tilicho kikusudia tumekipata. Vijana wengi wamevaa nguo za Mr Z huku mimi na mume wangu nasi tukiwa tumevaa nguo hizo. Tukajichanaganya na watu, tukajitahidi na kufika mbele kabisa ya maandamano kabisa na kuendelea kuhimiza watu wazidi kusonga mbele. Mita chache kutoka ikulu tukakuta wanajeshi wakiwa wamezuia barabara kwa kusimamisha magari na vifaru vya mizinga huku ikulu ikiwa imezungukwa na wanajeshi na inalindwa kwa ulinzi mkali sana.
“Eddy”
“Mmmmm”
“Umeona?”
“Yaa”
“Tunafanyaje mume wangu?”
“Ngoja?”
Kutokana tumevaa vifaa vya mawasiliano kila mtu kwenye sikio lake, ikawa rahisi kuweza kuwasiliana na shemeji pamoja na wifi ambao wao wapo upande mwengine.
“Tunafanayaje kaka?”
“Hao wanajeshi ngoja kuna mawasiliano Love anamalizia hapa, kisha tutajua nini cha kufanya”
“Sawa”
Baada ya dakika kama nne hivi, wanajeshi wakatupisha barabarani jambo lililo washangaza hata raisi wa kawaida. Tukazidi kusonga mbele hadi kwenye mageti ya ikulu. Eddy akavua kinyago chake na mimi ikanilazimu kuvua na kuwafanya wananchi walipo karibu yetu kutushangaa kwa maana kwa muda wote hawakuweza kufahamu kama ni sisi. Tukamuona raisi akitoka ndani ya ikulu huku akiwa amepiga kabali kwa nyuma Azaria pacha wa Eddy na mkononi mwake amashika bastola.
“Ondokeni”
“Alizungumza kwa ukali huku akiwa amemuakea pacha wa mume wangu bastola ya kichwa. Eddy akatka kwenda ila nikamuwahi kumshika mkono.
“Ngoja”
“Ningoje nini yule ni mwenzangu”
“Najua Eddy ila ngoja kwanza”
Waandishi wa habari nao hawakuwa mbali kila mmoja yupo makini katika kurekodi tukio hili.
“Wewe mtoto mshenzi ondoka, siwezi kuachia madaraka”
Wananchi hawakuogopa, wakaanza kung’ang’ania kuvunja geti la ikulu na haikuchukua muda sana geti likavunjia na raisi akanaza kushambulia wananchi kwa risasi. Azaria kwa haraka akamuwahi kumng’angania mkono alio shika bastola yake, katika kuminyana minyana na raisi nikashuhudia shemeji yangu Azaria akianguka chini, jambo lililo tufanya kukimbilia kakika eneo hilo huku wananchi wakiwa tayari wamesha mtia raisi mikononi na kuanza kumpiga kipicho kama cha mbwa mwizi. Eddy kwa haraka akamnyanyua pacha wake, hapa ndipo nikapata nafasi ya kuwaona jinsi wanavyo fanana.
“Amepigwa risasi”
Eddy alizungumza huku akipizidi kukimbia huku amembeba mwenzake na mimi nikimfwata kwa nyuma.
“Kurwa”
“Mmmmm”
“Siwezi pona, niweke chini”
“Hapana unatakiwa upate mataibabu”
“Nooo, niweke chini”
Eddy akasikiliza anacho kizungumza mdogo wake. Doto akanitazama usoni mwangu huku akiwa amejawa na tabasamu.
“Shem eheee”
“Beee”
“Asante, kwa kunipeleka kwa babu nipo sawa”
Doto alizungumza huku akiwa amejishika tumboni mwake, eneo alilo pigwa risasi huku damu nyingi zikimwagika.
“Muambie mama nampenda, na muambie kina Gody na wezake kwamba nina wapenda sawa”
Eddy alitingisha kichwa huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Shem”
“Beee”
“Mpende kaka yangu, ana kupenda. Japo tulikuwa tunacheza game ya kujifanya ni mtu mmoja ila tulifanya ili kuweza kujau kwamba wewe ni mwanamke sahihi kwetu au laa. Ila nina imani kwamba kaka yangu nimemuacha sehemu sahihi na mtu sahihi”
“Eddy funga ndoa bwana na Jojo, wewe ndio umebaki tu kwenye familia”
“Hapana hata wewe”
“Hamna bawana mimi siwezi…….si…we..z…..”
Doto alizungumza huku damu zikimtoka mdomoni mwake.
“Siwezi ku….ishi…..ill….ii….kuwa ni lazima iwe hivi ili hili la leo litokeee”
Machozi yakazidi kutumwagika kwani ule utabiri alio uzungumza mama Gody ndio huu ambao unakwenda kukamilika.
“Kaka na dada waambie ninawapenda”
“Wanakusikia hapa”
Eddy alizungumza huku akitoa kinasa sauti chake alicho kichomeka sikioni mwake. Akamvisha pacha wake.
“Ba Gody”
Doto aliita huku akitabasamu.
“Mmmmm”
Shem alijikaza kuitikia ila sauti yake imejawa na majonzi.
“Nakupenda kaka, Sister ehee?”
“Beee”
“Una….un…ku…..mb…..uka utotoni ulivyo kuwa una….una…ni….adisia…..aa kuhusu mbinguni?”
“Nakumbuka doto”
“Naenda dada”
“Hapana usiseme hivyo”
“Haha…haa….muda umefi….ka……nataka nikakae na baba namuona ana niita”
Waandishi wa habari wakatuzunguka huku wakiendelea kurekodi tukio hili. Hapakuwa na hata mtu mwenye nguvu ya kuwazuia hawa waandishi wa habari kuturekodi.
“Huwezi kwenda mdogo wangu, utapelekwa hospitali”
“Hamna si unajua jisni nisi….vyopend…….a dawa”
“Ndio najua mdogo wangu ila uakuwa sawa, muambie Kurwa akupelekea sasa hivi?”
“Haa….Kurwaa hawezi, hei mpe mwanao mmoja jina langu lisimame kama baba yake”
“Usijali nitampa”
“Kweli”
“Haki ya Mungu vile nina kuhahidi”
“Haya nivue kidude chako nataka munipeleke hospitali”
Gari la wagonjwa kumbe lilikuwa limesha fika, kwa haraka madaktari wakamnyanyua na akaingizwa kwenye gari la wagonjwa na sisi tukaingia pia. Safari ikaanza kwa kasi, ila shem akatutazama kwa pamoja kisha akatuomba mikono yetu na kuishika kwa pamoja huku akitabasamu, taratibu nguvu ya kuandelea kuishika mikono yetu ikamuishia na akaiachia kwa pamoja na kuyafumba macho yake jambo lililo mfanya mume wangu kuzidi kulia kwa uchungu, daktari akajitahidi kutoa huduma ila hadi tunafika hospitalini shemeji yangu Doto akawa tayari emefariki duniani.
***
Wiki mbili baada ya kufanya mazishi ya doto, turudi rasmi nchi Tanzania huku makazi ya kampunzi zangu nikiyaweka hapa hapa jijini Dar es Salamaa katika maeneo ya posta. Makamu wa raisi akaapishwa kuwa raisi wa nchi hadi pale uchaguzi mpya utakapo pangwa huku mume wangu akishuulikia swala zima la uzinduzi wa filamu yetu pamoja na ndao. Wingi wa watu kutupenda ukazidi kuongezeka na watu wengi waka ahadi kuinunua filamu niliyo cheza mimi Love Mask.
Tarehe ya uzinduzi ikafika, familia nzima tukajumuika katika ukumbi mkubwa sana wa kampuni zangu tulio ujenga. Idadi ya watu wengi wakafurika katika siku hii, huku ulinzi ukiwa umemarisha, na makamu wa raisi ambaye sasa ni raisi, akatupatia ulinzi madhubuti. Muendesha sherehe akamuita mume wangu ili aje kuzungumza mambo mawili matatu akiwa kama mtunzi na muongozaji wa filamu hii kabla haijazinduliwa rasmi na waziri mkuu. Mume wangu akanibusu mdoni na kusimama huku akiwa amevalia suti nzuri sana iliyo mpendezesha sana. Akasima mbele ya kipaza sauti.
“Habari za usiku mabibi na mabwana?”
“Salama”
Watu ukumbi mzima wakaitikia kwa furaha.
“Kwanza nipende kumshukuru Mungu kwa kutuweka hai hadi leo, kwani ni siku nyingi sana hii filamu tuliitengeneza hapo kati kati yakatoke mambo mengi sana yaliyo tufanye tuwe bize sana, ila leo Mungu ameweza kutusimamia na kufanikiwa kuizindua.”
Watu wakapiga makofi na kumfanya mume wangu kutulia kwa muda hadi makofi yalipo nyamaza akaendeea kuzungumza.
“Kabla sijasonga mbele ninaomba niweze kumuita mama Cleo, japo wengi mumezoea kumuia Jojo, ila mimi ninamuita mama Cleopatra, njoo mbele laazizi wangu, asali wa moyo wangu. Usingizi wangu”
Maneno ya mume wangu yakaufanya ukumbi mzima kujaa shangwe nyingi ambazo kusema kweli zikazidi kunipa furaha. Nikanyanyuka taratibu huku nikiwatazama wanangu wawili Godlove ambaye tayari mume wangu alisha mchukua kutoka mikononi mwa mama yake huku na Cleopatra ambaye amekaa kwenye kiti chake maalumu."
Nikalishika gauni langu hili redu kidogo na nikaanza kutembea, nikapandisha ngazi hadi jukwaani, mume wangu akanipokea kwa kunikumbatia na kunipiga mabusu mfululizo.
“Nampenda sana mke wangu. Miaka na miaka ninazidi kumuona mzuri na hachakai hata kidogo. Kwa kweli Mungu amenipa Malkia wa Nguvu, tena shupavu na mpambanaji”
Eddy kwa ishara ya vidole akanyoosha kidole cheka kwa mtu ambaye watu wote tukamtazama, tukamuona mchungaji aliye valia mavazi meupe akiingia jukwaani hapa. Mapigo ya moyo yalivyo changanyikana na furaha yakaanza kunienda mbio.
“Ninawatangazia rasmi kwamba leo ndio siku ya harusi yangu mimi na Jojo na mchungaji yupo kwa ajili ya kutufungisha ndoa”
Ukumbi mzima ukafurika kwa kwa furaha, nderemo na vifijo. Furaha yangu ikazidi kipimo hadi nikajikuta nikiangua kilio, kwani sikutegemea wala kutarajia siku kama ya leo ninaweza kufunga ndoa na mume wangu.
Ukumbi ulipo tulia mchungaji akaanza kuongoza ibada ya ndoa yetu. Mama mkwe na Nuru nikawaona nao machozi yakiwamwagika usoni mwao kwani ni furaha kwa kila mtu. Mchungaji akaniuliza je nimekubali kumpokea Eddy awe mume wa maisha yangu kwenye shida na raha, tabu na mateso.
“NDIO NIMEKUBALI….”
Nilizungumza huku sauti yangu ikiwa aimetawaliwa na machozi mengi ya furaha. Taratibu nikamvisha mume wangu pete ya ndoa na furaha ikazidi kutawala ukumbini. Waziri mkuu kwa haraka akapanda jukwaani, akaomba kipaza sauti huku akiwa amejawa na furaha.
“Nikiwa kama mgeni rasmi kwa tukio hili lililo tushangaza sote ninatangaza kwamba filamu yetu imezinduliwa na wana ndoto wetu wakate utepe”
Furaha zikazidi kutawala, tukakabidhi mkasi tukaushika kwa pamoja na kukata utepe ulio zunguka picha kubwa ya filamu hii iliyo funikwa na tambara kubwa la rangi ya blue. Mara baada ya kumaliza kuukata kwa kushirikiana na waziri mkuu tukalivuta tambara hilo chini na tukaona kava la filamu hii lilo tengenezwa kwenye ubora wa hali ya juu huku picha yangu ikionekana, jambo lililo wafanya watu wote hapa ukumbini kusimama na kushangilia kwa fura, taratibu nikamgeukia mume wangu, tukaanza kunyonyana midomo yetu pasipo aibu ya aina yoyote na watu wakazidi kufurahia mwanazo mpya wa maisha yetu ya ndoa.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment