Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

POWER SEHEMU YA 10 MWISHO

 

 


 POWER

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 10 KATI YA 10

 


“Sihitaji kuendelea tena na huyo mwa na mama. Hivi sasa niandalie mazingira mazuri ya kutoka nje ya Tanzania na nina hitaji kuelekea Ujerumani leo na nitapandia ndege nchini Kenya”

“Nina weza kufahamu Ujerumani una kwenda kufanya nini?”

“Kuna kazi muhimu nina hitaji kwenda. Fanya kama nilivyo kueleza”

“Sawa mkuu”

Nikakata simu, nikachukua begi dogo la mgongoni na kuingiza nguo kadhaa.

“Una safari”

Sauti ya Latifa ikanistua kidogo na kujikuta nikimgeukia na kumtazama usoni mwake.

“Ndio”

“Unakwenda wapi mume wangu”

Latifa aliniuliza huku akiwa amejawa na maswali mengi sana kichwani mwake.

“Nina kwenda Ujerumani kuna kazi ninahitaji kuifanya”

“Unakwenda Ujerumani kwenye wakati kama huu tulio nao Ethan?”

“Sina jinsi ila kuna kazi ya umuhimu nina taka kwenda kuifanya”

Kwa haraka Latifa akanifwata na kunikumbatia kwa nyuma. Kitu nilicho kigundua ni kwamba Latifa hajafahamu chochote kuhusiana na ramani ambayo ipo mgongoni mwangu.

“Ethan mbona umefanya maamuzi ya wewe kama wewe. Tafadhali nakuomba sana twende wote kwenye hiyo safari”

“Hapana nitatakiwa kwenda mwenyewe”

Simu yangu ikaanza kuita, nikaichukua kitandani na kukuta ni namba ya Piyanka.

“Ndio Ethan”

“Niambie”

“Nimefanya booking kwa Kenya tiketi mbili. Ethan alinieleza kila jambo”

“Sawa nipo kwenye maandalizi ya kuondoka”

“Sawa nitatangulia kukuandalia maandalizi”

Nikakata simu huku Latifa akiwa amepoteza furaha kabisa kwenye uso wake.

“Hakikisha kwamba una jilinda na kuwa salama”

“Ethan ila kwa nini una nitesa moyo wangu?”

“Ninakutesa na nini?”

“Hivi unavyo ondoka. Si uliniambia kwamba kila unapo kwenda utakubali kwenda na mimi?”

“Latifa nisikilize mke wangu. Kuna wakati mwengine inabidi uweze kuelewa hali halisi tunayo pitia hivi, inabidi nihakikishe kwamba mambo yote yaaisha kabla ya mwaka huu kuisha.”

“Sawa Ethan ila kumbuka hii safari haikuwepo, sasa ina kuwaje una ipanga tu’

“Kampuni zangu zilizopo Ujerumani zinataka kubinafsishwa. Hivyo nina hitaji kwenda haraka iwezekanavyo kuhakikisha nina zuia swala hilo”

Ikanilazimu kumdanganya Latifa ambaye anaonekana kuumizwa na habari ya kuondoka kwangu.

“Kweli?”

“Ndio maana umeniona nina ondoka gafla”

“Utakaa huko kwa muda gani?”

“Sijajua ila tutakuwa tunawasiliana. Ila ninacho kihitaji kampuni ya mawasiliano izidi kusonga mbele sawa”

“Sawa Ethan. Hunipi hata cha kuniagia?”

Latifa alizungumza huku akimshika jogoo wangu taratibu.

“Mke wangu Romani yupo njiani ana kuja huku nahitaji kuondoka”

“Hata kama mume wangu naomba haki yangu”

Latifa alizungumza huku akimtoa jogoo wangu kwenye suruali. Akaanza kunyonya taratibu na kunifanya akili zangu zihame kwa muda kwa maana eneo hili. Taratibu tukajikuta tukizama kwenye penzi zito na kuanza kupeana haki ambayo kila mmoja ana stahili. Baada ya mzunguko wa kwanza kuisha, Latifa akaniandalia nguo za kuondokea. Hadi Romani ana fika tayari nikawa nimesha jiandaa.

Majira ya saa mbili usiku tukaanza safari ya kueleeka nchini Kenya kwa kutumi helicopter hii.

“Hakikisha hawa mabinti wana kuwa katika ulinzi mzuri sawa”

Tukafika nchini Kenya na nikapolewa na Piyanka, tukalala kwenye holeti tuliyo fikizia na asubuhi na mapema tukaelekea uwanja wa ndege huku akiwa amenikabidhi hati yangu ya kusafiria.

“Hii sio feki?”

“Ni O’G hiyo. Nimeikatia hapa Kenya hivyo hakuna ambaye ana weza kukutulia mashaka”

Tukafanikiwa kuingia kwenye ndege na uzuri siti zetu zipo karibu. Karibia watu wengi ndani ya ndege hii wana nitazama kwa umakini sana.

“Watu wana kutazama sana laiti kama ningejua ningekununulia kofia na miwani”

“Usijali”

Safari ikaanza tararibu huku nikiendelea kuwazia ni jinsi gani nitakavyo anza kuishi nchini Ujerumani ikiwa Camila na Biyanka wameungana na wote wana iwinda roho yangu.

“Mbona una mawazo sana?”

“Ninafikiria jinsi ya kucheza na maadui zangu”

“Maadui wapi?”

“Ethan hakukuambia?”

“Aliniambia juu ya hili swala tunalo kwenda kulifwata huku tu”

“Basi huku tunapo kwenda ni vitani. Tutakumbana na matatizo mengi, tutakumbana na shida nyingi sana katika hili. Hakikisha kwamba una kuwa mstamilivu na mjasiri”

“Mmmm mbona una nitisha?”

“Sikutishi ila hichi tunacho kifwata huku kina sakwa na waty wengi sana”

Nilizungumza kwa sauti ya chini ili watu wa pembeni yetu wasiweze kusikia ni kitu gani kinacho endelea.

“Samahani muna tumia vinywaji gani?”

Muhudumu wa ndege alituuliza huku akitutazama kwenye nyuso zetu.

“Maji”

Nilizungumza na muhudumu huyu akanipatia chupa ndogo ya maji.

“Juisi ya mango”

Piyanka naye aka kabidhiwa kitu anacho kihitaji.

“Samahani kaka nina weza kukuuliza swali?”

“Uliza tu”

“Wewe ni Ethan?”

“Hapana si Ethan mume mfananisha”

Piyanka aliwahi kujibu swali hilo na kumfanya muhudumu huyo atabasamu na kuondoka na kuendelea na zoezi la kugawa vinywaji kwa abiria wengine.

“Nipe mpango juu ya kupambana na adui zako?”

“Tukifika Ujerumani basi tutajua ni wapi kwa kuanzia”

“Ila kutokana Ujerumani umeishi kwa muda mrefu sana basi sina wasi wasi na swala hilo”

Baada ya masaa kadhaa angani tukafika nchini Ujerumani. Tukafika katika hoteli ya kawaida ambayo si rahisi kwa watu kuhisi kwamba mtu maarufu na mwenye hadhi kama yangu ana weza kukaa katika hoteli hiyo.

“Ethan”

“Naam”

“Njoo uone”

Kwa haraka nikamfwata Piyanka katika dirisha la chumba chetu tulicho pangisha. Nikachungulia nje na nikashuhudia gari mbili nyeusi aina ya bmw zikisimama huku wakishuka watu walio valia suti nyeusi na miwani nyeusi na wakaanza kuingia kwenye hoteli.

“Shiti”

Nilizungumza kwa kutahamaki.

“Nini?”

Sikumjibu chochote Piyanka zaidi ya kumuonyesha jinsi Camila anavyo shuka kwenye moja ya gari hilo huku walinzi wengine wakiwa wamemzunguka kwa kumuwekea ulinzi mkali sana.



“Yule ndio Camila niliye kuwa nina kuadisi kwenye ndege”

“Mungu wangu sasa si amegundua kwamba tupo hapa”

“Ndio maana yake inabidi tufanye mpango wa kuondoka eneo hili”

Piyanka akavaa tisheti yake ambayo alisha ivua mara baada ya kuingia ndani humu. Nikafungua mlango na kuchungulia nje na nikaanza kusikia vishindo vya miguu ya watu wakipandisha ngazi za gorofa hili tulipo. Sikutaka kujioa matumaini kwamba watu wanao kuja si watu wa Camila. Nikaufunga mlango huu kwa ndani, kisha nikavuta sofa la karibu yangu na kuliweka mlangoni ili hata kama ikitokea wakijitahidi kufungua mlango kwa nguvu wapate kizuizi kidogo.

“Dirishani inabidi tupitie”

“Ethan jua tupo gorofa ya tano!!”

Piyanka alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.

“Hatuna jinsi kwa maana watu hao wana kuja”

Hata kabla Piyanka hajazungumza kitu chochote, mlango ukabamizwa kwa nguvu. Piyanka hakuhitaji hata kujishauri kabisa na alicho kifanya ni kunifwata dirishani hapa huku akiwa amevalia kibegi chake cha nguo mgongoni. Akanikabidhi begi langu la nguo, nikalivaa, nikafungua kioo cha dirisha hili na kuchungulia nje. Hapakuwa na watu ambao wana tufwatilia kabisa. Nikawa wa kwanza kutoka dirishani humu na kujibanza kwenye kanjia kadogo sana kalichopo hapa ukutani na endapo nitafanya kosa la aina yoyote basi nitaanguka na kuvunjika vunjika. Piyanka naye akatoka na sote tukawa ytumesimama kwa kujikaza katika kinjia hichi. Kwamwendo wa taratibu sana tukaanza kutembea kwenye kanjia haka hadi katika dirisha la chumba kingine, nikalifungua dirisha hilo na kuchungulia ndani na kwa bahati nzuri ndani ya chumba hichi hakuna mtu yoyote. Tukaingi katika chumba hichi na moja kwa moja tukaelekea mlangoni. Nikaufungua mlango na kuchungulia nje na kuwaona watu wa Camila wakimalizia kuufunja mlango huo kwa nguvu sana na wakaingia ndani. Kutokana katika hoteli hii kuna kordo mbili, ikatulazimu kupita katika kordo nyingine huku tukikimbia kwa kasi sana.

“Jibanze”

Nilimuambia Piyanka huku nikipunguza mwendo wangu wa kukimbia na tukajibaza kwenye ukuta ambao pembeni yake kuna ngazi za kushukia chini, nikachungulia vizuri katika ngazi hizo na hakuna mtu ambaye ana pandisha. Tukaanza kushuka kwa kasi sana hadi ntukafanikiwa kufika gorofa ya mwisho na kukuya mlango wa dharura wa kutoka katika hoteli hii. Tukatokea nje mtaa wa pili katika hoteli hii na tukaanza kutembea kwa kasi huku tukiwa makini sana kuhakikisha kwamba hatufwatiliwi.

“Walijuaje kwamba tupo pale?”

“Nahisi habari hizo zimevuja uwanja wa ndege na kumbuka kwamba baba yake ndio raisi wa hii nchi hivyo ana watu wengi sana ambao anaweza kupata taarifa zangu”

“Sasa kama ni hivyo tunajisumbua tu kukimbia”

“Kwa nini?”

“Tazama barabara nzima kuna security camers. So unahisi kwamba iatakuwa ni ngumu kwa yeye kuweza kutupata?”

“Hatuwezi kujirahisisha na kukamatwa kirahisi hivyo”

Nikasimamisha taksi na kumuomba atypeleke kwenye kituo cha dreni za mwendo wa kasi wa umeme. Dereva taksi akafanya hivo na tukafanikiwa kufika katika kitua cha treni, nikamlipa kisha tukashuka katika subway. Tukakata tiketi na hatukukaa hata dakika tano treni ikafika. Tukaianza safari ya kuelekea katika mji ambao nimeishi kipindi cha utoto wangu na ndipo ilipo nyumba ya mzee Klopp.

“Niliamini kwamba tukifika tutaishi maisha ya furaha. Kumbe kuna majanga kiasi hichi daa”

Piyanka alilalama kwa sauti ya upole sana.

“Ndio maana nilikueleza kabisa tukiwa kwenye ndege ili uweze kujiandaa kisaikolojia”

“Mmmm kuna na kuja, yaani hata hatujalala”

“Ndio hivyo mama kaza moyo.”

Tukafika katika kituo kimoja, abiria kadhaa wakashuka na wengine wakapanda. Nikastuka sana mara baada ya kuwaona vijana wanne wa Camila ambao sura zao niliziona kupitia dirishani, nao wakipanda ndani ya treni hii.

“Inama”

Nilimuambia Piyanka ambaye ana onekana kujawa na mawazo mengi sana kichwani mwake. Taratibu Piyanka akainama pasipo kujua ni nini kinacho endelea. Kutokana na wingi wa tatu ndani ya treni hii basi ikawa ni ngumu sana kwa watu hawa kutuona kwa haraka.

“Sasa sikia. Ukifika kitua cha pili kutokea hapa. Yaani kitua kinacho fwata hicho kingine. Shuka na piga simu kwa dada yangu na utamuambia ni wewe atakuja kukuchukua sehemu ulipo”

Nikamtajia Piyanka namba ya dada yangu Mary ambaye hajui kama kwa sasa nipo nchini Ujerumani.

“Unataka kwenda wapi?”

“Kuna wale watu wanao tutatufa wamepanda ndani ya treni hiyo. Nahitaji ufanya kama nilivyo kuambia mimi nitabaki peke yangu na nitawatoa nje ya treni hii kiujanja kwa maana mtu muhimu anaye sakwa hapa ni mimi na wala sio wewe”

“Ethan ila kumbuka kwamba tumekuja pamoja ni lazima tupambane pamoja”

“Hata kama ila wasiliana na dada yangu ana itwa Mary Klopp. Make sure una muambia mimi Ethan Klopp ndio nime kuagiza. Ukiwasaliana naye basi nita pata msaada mimi sawa”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Piyanka usoni mwake.

“Sawa”

“Haya fanya hivyo”

Nikanyanyuka na kwa bahati mbaya mmoja wa vijana hao aliweza kuniona. Taratibu nikaanza kujichanganya na watu huku nikielekea kwenye behewa jengine. Watu hawa wakampita Piyanka pasipo kumfanya jambo la aina yoyote. Nikaingia kwenye behewa la pili, kitendo cha treni hii kusimama kituoni na milango kufunguka. Nikawa wa kwanza kutoka na kuanza kukimbia. Watu wa Camila hawakuniacha, wakaanza kunikimbiza kwa nyuma. Kitendo cha kutoka katika subway nikakutana na gari nne nyeusi zikiwa zimepaki mbele yangu na walinzi karibia kumi wenye bastola mikononi mwao wakanifanya nisimame na nikose kwa kukimbilia.

Wakaniiingiza ndani ya gari moja na tukaondoka katika eneo hili na kuwaacha watu wakiendelea kushangaa shangaa na kukosa majibu.

“Nyinyi ni kina nani?”

“Hatuna majibu ya maswali yako”

Jamaa aliye kaa pembeni yangu alinijibu huku akinitazama kwa macho makali sana. Safari ya kupelekwa pasipo kulikana ikachukua masaa kama manne hivi, huku gari hizi zikipita katika vizuizi kadhaa vya askari pasipo kukaguliwa. Tukafika nje ya mji wa Berlin na kupelekewa kwenye moja ya jumba kubwa sana ambalo ulinzi wake katika eneo hili ni mkali sana.

Nikamkuta Camila pamoja na walinzi wengine wakinisubiria. Nikaamrishwa kushuka ndani ya gari na nikatii amri.

“Waoo umebadilika sana Ethan toka ulipo toka kwenye kifo”

Camila alizungumza huku akiwa amejawa na furaha usoni mwake. Akilini mwangu nikagundua moja kwa moja kwamba hili ni tabasamu feki. Tafasabu ambalo haliendani kabisa na matakwa ya moyo wake.

“Karibu ndani.”

Tukaingia sebleni huku nikiendelea kuwa na wasiwasi mwingi sana. Tukapitiliza moja kwa moja hadi kwenye meza ya chakula.

“Kula ushibe kwa maana una siku chache za kuishi hapa duniani”

Camila alizungumza kwa kuzudi kujiamini huku akinitazama usoni mwangu.

“Unahisi kwamba ukiniua unaweza kufaidika kwa jambo lolote”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimkazia macho Camila.

“Kaa kwenye kiti”

Nikakitazama kiti hichi ambacho Camila ananielekeza niweze kukaa. Kisha nikakivuta nyuma taratibu na kukikalia huku nikimtazama machoni mwake.

“Kuna kila aina ya chukula hapo. Nilipo kaa Tanzania niliweza kujifunza aina ya vyakula vingi ikiwemo ugali, bada, mtori na mapure na kila kitu kime andaliwa hapo chagua ni nini unahitaji uweze kula”

“Nashukuru sina hamu ya kula kitu chochote”

“Ethan….Tambua ni mambo mengi sana tumeweza kupitia mimi na wewe”

“Kwahiyo?”

“Hivyo nina mamlaka juu yako”

“Ulisha wahi kuona wapi mwanamke akiwa na mamlaka juu ya mwanamke Ehee?”

Nilimuuliza Camila huku moyoni mwangu nikiwa nimekosa amani kabisa.

“Kwangu ndio itakavyo kuwa”

“Kwasababu nipo hapa ndio utasema nipo chini yako. Ni nini unahitaji”

“Okay acha niende kwenye pointi. Nahitaji kujua ni wapi ilipo black boksi. Nikwakipindi kirefu sana nilikuwa nina isubiria siku kama ya leo niweze kufahamuni wapi lilipo boksi hilo. Nahitaji Ujerumani ipande tena ikiwa mikononi mwa baba yangu. Nahitaji turudi kwenye uongozi wa dunia na tuwe namba moja”

“Kwahiyo haya yote unafanya kwa ajili ya tamaa zako za nguvu kuhusiana na uongozi wa baba yako?”

“Ndio maana yake.”

“Camila”

“Bee”

“Natambua kwamba wewe na Biyanka mume ungana kwa ajili ya kuniangamiza, ili mradi kila mmoja aweze kulipiza kisasi kwa wakati wake. Wewe unahitaji Black boksi na mwenzako anahitaji kulipiza kisasi cha baba yake akiamini kwamba mimi ndio nime muua. Sasa wewe ndio wa kwanza kunipata nipo tayari kufa mikononi mwako. Sinto jutia kufa mikononi mwako ila ukweli ni kwamba huto weza kupata kitu chochote ambacho kuhusiana na black boksi”

Nilizungumza kwa kujiamini sana na kumfanya Camila kunirushia glasi ya maji aliyo ishika na ikatua usoni mwangu na kupasuka vipande vipande na kusababisha damu ianze kunichuruzika kwenye baadhi ya maeneo taratibu.



Nikashusha pumzi taratibu huku nikijipangusa damu inayo nimwagika kutokana na majeraha ya kukata na glasi hii. Camila akatoa ishara walinzi wake wanikamate na waniondoe hapa sebleni. Hakika Camila amebadilika, amekuwa si binadamu tena kwangu, bali ni mnyama mkali na wa kuogopewa. Walinzi wake wakaninyanyua kwenye kiti hichi na kuniondoa sebleni hapa. Wakanitoa nje ya jumba hili na kuniingiza katika nyumba ndogo ya iliyopo pembezoni mwa jumba hili. Katika nyumba hii ina hifadhia vyakula vya farasi.

‘Ethan hichi ni nini?’

Nilizungumza kimoyo moyo, Ethan hakuweza kunijibu kitu cha aina yoyote.

‘Hei’

Ethan alijitokeza mbele yangu huku akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake.

“Mbona una sononoka?”

“Unahisi kilicho nitokea ni kizuri au nimekipenda?”

“Hahaaa inakuwaje unashindwa kumshawishi mwanamke ambaye ulimtoa usichana wake?”

“Hata kama nimemtoa usichana wake ila huyu mwanamke amekuwa ni gaidi. Si yule Camila niliye kuwa nina mjua.”

“Sawa tuachane na hayo. Imekuwa hivi ili uweze kupata njia ya kuelekea katika eneo lililo hifadhi hilo boksi”

“Hiyo njia ipo wapi?”

Ethan akasogeza moja roba kubwa la chakula cha farasi. Akafunua eneo hili ambalo lina mfuniko wa chuma. Tukashuhudia ngazi ndevu zinazo shuka chini.

“Huku ndipo lilipo boksi hilo”

“Twende”

Ethan akatangulia na mimi nikamfwata kwa nyuma huku nikifunga mfuniko huo ili hata walinzi wakija iwe ni ngumu kwa wao kuweza kugundua ni wapi nilipo elekea. Tukaanza kutembea kwenye miamba hii iliyo chongwa na tukafanikiwa kutokae eneo la nje kabisa la jumba hili.

“Sasa huku ni wapi?”

Nilimuuliza Ethan mara baada ya kuona shamba hili kubwa.

“Jambo la kwanza ni wewe kuwa salama. Twende huku”

Tukaendelea kutembea katikati ya shamba hili la maindi. Tukakuta gari moja, tukaingia ndani ya gari na kuanza kuoendoka eneo hili.

“Umenitorosha au tuna kwenda kutafuta hilo boksi”

“Mbona una papara. Tulia”

Safari hii ikatuchukua masaa mawili na kufika katika moja ya msitu na nikamkuta Piyanka pamoja na dada Mery ambaye kwa haraka akanikimbilia na kunikumbatia huku akiangua kilio kizito sana.

“Kwa nini, kwa nini Ethan umetesa hisia zangu hivi. Nimekuwa na wasiwasi mwingi sana juu yako”

Da Mery aliendelea kulalama huku akiwa amenikumbatia.

“Nisamehe”

“Ingekuwa sio Ethan ninge amini kwamba umesha kufa”

“Sijakufa dada nipo hai”

Taratibu tukaachiana huku nyuso zetu zikiwa zimelowana kwa machozi ya furaha kwa maana ni kwa muda mrefu tumeishi mbali na hakuna mtu ambaye aliwasiliana na mwenzake hii yote ni kutokan na matatizo ambayo yalikuwa yakinikabili.

“Niliacha uweze kuingia mikononi mwa Camila ili uweze kufahamu lengo lake juu ya hilo boksi jeusi. Nina imani kwamba umeweza kufahamu?”

“Ndio”

“Vua tisheti yako. Piyanka andaa kalamu yako na karatasi”

Piyanka akafungua kibegi chake na kutoa karatasi nyeupe pamoja na kalamu. Nikavua tisheti yangu na Ethan akafanya kama nilivyo kuwa nchini Tanzania. Dada Mery na Piyanka wote wakabaki kushangaa ramani iliyopo mwilini mwangu.

“Anza kuichora”

Ethan alizungumza huku akinimulika mgongoni mwangu kwa maana tupo msituni na sasa ni majira ya usiku sana. Piyanka akainza kazi ya kuichora ramani hii kwa kasi sana.

“Imewekwaje wekwaje hiyo ramani?”

Da Mery aliuliza huku akimtazama Ethan usoni mwake.

“Kipindi baba yako ana hangaika na kutafuta jinsi ya kuificha siri yake boksi hili. Niliweza kumtokea wakiwa nchini Tanzania. Nikamletea kijana huyu na kumuagiza aweze kuichora ramani hiyo mgongoni mwake. Kutokana nina uwezo wa kucheza na ufahamu wa ubongo wa binadamu, basi aliweza kutii na kuichora ramani hiyo mgongoni mwa Ethan toka akiwa mdogo. Alipo maliza kuifanya kazi hiyo niliificha kwa jinsi ninavyo jua mimi mgongoni mwa Ethan na ramani mbayo alikuwa nayo baba yako niliweza kuiteketeza kwa moto kisha nikafuta kumbukumbu zote juu ya kichwa chake kuhusiana na ramani iliyopo mwilini mwa Ethan”

“Ahaaa sasa hii ramani ndio itatupelekea eneo hili ambalo ndipo lilipo hifadhiwa boksi hilo?”

“Ndio mpenzi wangu”

Ethan alimjibu dada Mary huku akimtazama usoni mwake.

“Mumefikia wapi?”

Niliwauliza dada Mery huku nikimtazama usoni mwake.

“Wapi?”

“Kwenye mahusiano yenu?”

“Mmmmm!!!”

“Ethan una guna nini?”

“Hakuna kitu”

“Eti dada ana kupa furaha?”

“Sana tu. Toka nimekuwa naye maisha yangu yamebadilika sana. Nimekuwa ni mwenye furaha na kujiamini. Hakika nina mpenda sana mume wangu Ethan”

“Lini muna niletea mjomba”

“Piyanka hujamaliza bado”

“Bado Ethan”

“Musipotezee mada, lini mutanitafutia mjomba?”

“Ethan bwana tupo hapa kwenye maswala ya kutafuta hilo boksi. Mambo ya mtoto ni ya kupanga mimi na dada yako”

“Mmmmm! Sawa bwana”

Piyanka akamaliza kuichora ramani hiyo na Ethan akaifananisha na ramani iliyopo mgongoni mwangu na akakiri kwamba ameipatia kama ilivyo chorwa.

“Tunatakiwa kuondoka sasa na kesho tutaelekea kwenye milima ilipo fichwa boksi hili”

“Kwa nini tusiende usiku huu?”

“Hatuwezi ni lazima muweze kujipanga. Nyinyi ni binadamu na sehemu ambayo muna kwenda ina kila aina ya ubaya. Hivyo munatakiwa kujiandaa kisaikolojia, kimwili na kisilaha”

Ethan alizungumza kwa msisitizo na sote tykakubalian ana hilo na hapakuwa na mtu ambaye aliweza kubishana katika hilo. Safari ya kuelekea nyumbani ikaanza. Tukafanikiwa kufika katika nyumba ya mzee Klopp.

“Ni muda mrefu sana sijafika hapa.”

“Yaa ni muda mrefu Ethan, kuna kipindi nilitamani kuhama nyumbani hapa, ila Ethan alijitahidi kuwa pamoja nami hadi upweke ukapotea kwenye maisha yangu”

Da Mery alizungumza kwa upole sana. Nikaendelea kuitazama nyumba hii hakika hakuna vitu vilivyo badilika japo nimeishi nje ya nchi hii kwa miaka mingi sana.

“Ethan”

“Naam”

“Hivi Camila atafikiria kwmaba nipo huku?”

“Hawezi kuhisi kama una weza kuwepo huku.”

“Na nini tumfanye?”

“Nani?”

“Camila kwa maana kama ni lengo lake umeweza kuliona”

“Tupate kwanza hilo boksi kisha mengine yatafwata”

Piyanka na da Mery wakaandaa chakula cha usiku huku nami nikijipatia matibabu katika majeraha yangu madogo madogo usoni mwangu. Baada ya chakula cha usiku tukaingia kulala huku Piyanka akilala chumba tofauti.

‘Lazima niwaue wote ili niweze kuishi kwa amani’

Niliwaza akilini mwangu huku katika hisia zangu nikiwashuhudia Camila na Biyanka jinsi wanavyo niwinda.

‘Lakini kwa nini wamekuwa ni maadui zangu ikiwa walikuwa ni wake zangu? Wapi nilipo kosea?’

Niliendelea kuwaza akilini mwangu huku nikijitahidi sana kuweza kupata jibu juu ya wanawake hawa wawili. Msongamano wa mawazo ukanifanya nishindwe kabisa kupata hata lepe la usingizi. Nikashuka kitandani na kutoka nje ya chumba changu. Nikaelekea hadi sebleni na kuwasha tv ili mradi niweze kupoteza muda ili kupambazuke.

Nikajikuta machozi yakianza kunilenge lenga mara baada ya kumshuhudia rafiki yangu wa zamani sana Frenando akiwa ana idakia timu ya Real Madrid ya nchini Spain.

‘Well broo”

Nilizungumza huku nikitabasamu jinsi anavyo jituma kuokoa mashuti makali yanayo pigwa langoni mwake.

‘Nahitaji kurudi uwanjani sasa. Nimechoka na kazi za nje’

Niliendelea kutafakari tu moyoni mwangu.

“Bado hujalala”

Sauti ya Da Mery ikanifanya nitazame kwenye ngazi za kushukia kutoka gorofani.

“Yaa kichwa changu nina ona hakipo sawa”

“Pole sana. Unatumia wisky?”

Da Mery alizungumza huku akimimina pombe hiyo kali kwenye glasi yake. Nikatingisha kichwa nikimaanisha kwamba nina tumia.Akanimiminia kisha akaka pembeni yangu huku sote tukiendelea kutazama mechi hii ya marudio.

“Huyu si Frenando?”

“Ndio”

“Waooo amekuwa mkubwa sasa”

“Yaa natamani sana maisha ya kuzungukwa na mashabiki. Natamani kurudi kusimama katika namba yangu ya ufungaji pale mbele. Nimeamini kwamba pesa sio kila kitu kwenye maisha, ila amani ndio jambo kubwa sana la msingi kwenye maisha yetu”

“Ni kweli Ethan. Pole mdogo wangu kwa maana maisha yako hayajakwenda kama vile ulivyo kuwa una panga. Pole sana”

“Nashukuru ila nina imani nitarudi uwanjani tu. Bado umri wangu una ruhusu”

“Kikubwa ni kumuomba Mungu, kujiamini na kuto ongeza maadui. Sasa hivi ni wakati wa wewe kupunguza au kufuta kabisa maadui. Wabaki wale maadui ambao wana kuchukia tu pasipo wewe kuwafanyia jambo lolote”

“Dada”

“Bee”

“Hivi una amini katika kuua ndio njia sahihi ya kupunguza au kufuta maadui?”

“Siamini katika hilo, kwa maana wale unao waua. Nao watakuwa na wapendwa wao na hao wapendwa wapo nao watajikuta wakihitaji kuja after you or your family. Hivyo utajikuta una poteza amani yako”

“Kwa mfano kama Camila nitapanaje naye ikiwa kuingia tu hapa Ujerumani ame niteka na hizi alama huku usoni mwangu ni glasi aliyo nipiga nayo”

“Unajua Ethna bado hujatujua sisi wanawake insi tulivyo”

“Una maana gani?”

“Unajua Camila alikupenda sana toka alipo kuwa binti mdogo sana. Aliamini kwamba kwenye maisha yake wewe ndio utakuja kuwa mwanaume wa maisha yake yote. Ila sivyo jinsi ilivyo kuja kutokea. Hivyo sisi wanawake tuna uwezo wa kutumia asilimi kumi tu ya akili zetu kwenye swala zima la mahusiano ila silimia tisini iliyo baki hatuaminiki. Huwa tuna weza kufanya jambo lolote ili mradi kuridhisha nafsi zetu tu. Anayo yafanya Camila si kwamba eti ana penda kufanya hivyo ila ni hisia zake za kimapenzi zimechanganyikana na hasira ndio maana ana fanya mambo ya ajabu”

“Ila kwa Camila ni tofauti sister. Camila toka alipo kuwa mdogo mdogo alisha pandikizwa roho ya kijasiri. Hivi kuna siku una jua alisha wahi kunidhuru kwa ajili ya hili swala la boksi jeusi. Kama angekuwa si Ethan basi ile siku tungekuwa sasa hivi tumebakia kuwa story tu”

“Alitaka kukua?”

“Sio alitaka ila alidhamiria kufanya hivyo na akafanya ila Ethan ndio aliye niokoa”

“Duu basi huyu binti sio mtu mzuri”

“Ndio maana yake, zile mbwembwe za uwifi wifi zife tafadhali dada yangu usije ukamkaribia huyo binti ni shetani mbaya sana”

“Nimekuelewa Ethan, ila piga picha kwamba endapo utamuua. Je baba yake atakuacha hai, je Ujerumani ita kuacha hai? Je mali zote ambazo tunazipigania kila siku kuhakikisha kwamba zina simama na kuwa katika mstari mzuri je zitaachwa salama?”

Da Mery alizungumza kwa hisia kali sana huku akigugumia fumba la pombe hii kali huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Kama ni vita hii Ethan bado hatujashinda ndio kwanza ina anza”

“Nini tufanye dada yangu ikiwa ni lazima amani ipatikane kwenye maisha yetu”

“Ethan ukihitaji amani ni sawa sawa na sisimizi kupambana na tembo. Sisi ni sisimizi hatuna uwezo wa kumuangusha tembo. Ili tulinde vile tulivyo vishikilia ni lazima tuendeleze uchumi walio tuachia wazazi wetu Ethan”

Maneno ya da Mery kwa namna moja ama nyingine nikajikuta yakinikatisha tamaa. Ukiangali kwa jicho la tatu ni kweli Camila na familia yake wana nguvu ya kutusambaratishia kila kitu ambacho tumerithi kutoka kwa mzee Klopp na mke wake na endapo wakifanya hivyo basi maisha yetu yatakuwa ni ya kimasikini sana na tutaanza moja katika kutafuta maisha jambo ambalo litatuwia ugumu sana kuweza kupanda tena kiuchumi.


ENDELEA

“Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama da Mery usoni mwake. Taratibu nikamvuta na kukilaza kichwa chake begani mwangu.

“Tutashinda tu, haijalishi kwamba dunia ita tutazama vipi ila ni lazima tushinde katika hili”

Nilizungumza kwa kujiamini.

“Ngoja nikalale”

Dada Mery alizungumza huku akisimama. Akanipiga busu la shavuni na kuondoka sebleni hapa. Hadi kuna pambazuka sikuweza kupata hata lepe la usingizi. Nikaingia chumbani na kumkuta Piyanka akijigeuza geuza kitandani.

“Hei”

Nilimuita kwa sauti ya chini sana huku nikikaa pembeni ya kitanda hichi.

“Hai vipi ulikwenda wapi?”

“Nilikuwa sebleni kidogo nikituliza tuliza mawazo”

“Come here”

Piyanka akanivuta na kukilaza kichwa changu kwenye kifua chake kilicho beba maziwa yaliyo jazia vizuri.

“Natambu kwa sasa Ethan upo kwenye wakati mgumu sana. Ila nimejaribu kufikiria jinsi gani tunaweza kufanya mara baada ya kuipata hiyo fumular, ila nimepata wazo moja?”

“Wazo gani?”

“Natambua kwamba Camila ana kuwinda kwa ajili ya hiyo fumular. Ikitokea kwamba tumeipata, kutokana nina uwezo mkubwa sana katika mambo haya nitajaribu kutengeneza fomular nyingine inayo fanania na fomular hiyo na nita ibadilisha kidogo na wakiitengeneza bomu litakalo tokea hapo lita waangamiza wao wenyewe”

“Unahisi wanaweza kufikia kutengeza bomu ambalo litawateketeza wao wenyewe?”

“Kwa jinsi ambavyo nitaibadilisha hiyo fomular hakuna ambaye atafahamu kwamba ime badilishwa. Wewe niamini katika hili.”

Nikanyanyua kichwa changu kidogo na kumtazama Piyanka usoni mwake.

“Nakuamini katika hili”

“Nashukuru”

Baada ya kupata kifungua kinywa, tukaanza kujiandaa kwa ajili ya safari kuelekea katika milima ambapo ndipo ilipo fichwa boksi jeusi lililo hifadhia fomular ya kutengeneza bomu kubwa sana la nyukilia ambalo linaweza kuisambaratisha dunia katika wakati mdogo sana. Majira ya saa kumi na mbili jioni tukaianza safari ya kuelekea katika misitu hiyo huku nikiwa dereva na da Maery akiwa na kazi ya kunisomea ramani ya wapi tupite hadi tufike kwenye milima hiyo.

Majira ya saa nne usiku tukafika kwenye milima hiyo. Tukatafuta sehemu ambayo tukisimamisha gari hili hakuna mtu ambaye anaweza kuliona. Tukashuka kwenye gari huku tukiwa tuna bunduki pamoja na tochi kubwa. Makoti makubwa tuliyo vaa kidogo yana tusaidia kuweza kupambana na baridi kali sana iliyopo kwenye hii milima.

“Ethan hajafika bado”

Da Mery aliuliza huku akiangaza angaza katika eneo hili ambapo Ethan aliahidi kwamba tunaweza kukutana naye hapa.

“Atafika”

Nilizungumza huku nikiichukua ramani hii kutoka mikononi mwa da Mery na kuifungua, nikaanza kutazama njia ambayo tunapaswa kupita.

“Kumbukeni kufunga bastola zenu viwambo vya kuzuia sauti kwa maana kwenye misitu kama hii kuna patrol za askari wa misitu. Pia mukumbuke kuna wanayama wakali sana hivyo. Tutatembea kwa ukaribu hakuna kupeana nafasi kubwa ya kutembea sawa”

Maagizo yangu yakawafanya Piyanka na da Mery kutingisha vichwa vyao wakimaanisha kwamba wamenielewa kwa kile ambacho nina kizungumza. Tukaanza safari ya kupandisha katika misitu hii ambayo ina mapango mengi sana.

‘Kuna sehemu inabidi uweze kumwaga damu yako ili mizimu iweze kuwakubalia kupita katika eneo hilo”

Niliisikia sauti ya Ethan ikiniongelesha mimimi mwenyewe.

‘Damu kiasi gani?”

‘Kidogo tu kwa maana ina hitaji damu’

‘Hivi na hao wanyama’

‘Nipo nanyi hakuna mnyama ambaye anaweza kuwadhuru ila tukifika katika hilo pango ni lazima uweze kumwaga damu katika hilo pango ili muweze kuingia ndani.’

‘Sawa’

Tukazidi kupandisha katika majabali makubwa. Tukafanikiwa kufika katika katika pango moja kubwa mabalo ndani ya pango hili ndipo lilipo hifadhiwa boksi hilo.

“Ramani inaonyesha ni hapa”

Da Mery alizungumza huku akihema sana. Nikamtazama Piyanka na kumuona akiwa ameinama huku ameshikilia magoti yake kwani shuhuli ya kupandisha mlima huu sio ndogo. Nikachomoa kisu kidogo kwenye mfuko wangu wa suruali nilio uvaa. Nikajikata sehemu ndogo kiasi na damu zikaanza kunimwagika na nikaanza kuzimwaga katika mlango mkubwa wa pango hili.

“Mbona una fanya hivyo?”

Da Mery aliniuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana usoni mwake.

“Ndio masharti yanavyo hitaji. Hatuto weza kuingia ndani ya pango hili pasipo kufanya hivyo”

Gafla tukaanza kuona mwaga wa njano ukianza kuwaka ndani ya pango hilo ambalo hapo awali tuliona gaiza kubwa sana.

“What’s fuc**!!”

Da Mery alizungumza huku akiwa amejawa ana mshangao kwa maana hili jambo ni la kutushangaza sisi sote.

“Tuingieni ndani”

Nilizungumza huku nikianza kutangulia mimi. Milio ya ajabu ajabu ikazidi kutupa wasiwasi na woga mwingi sana. Hata kama una silaha ila ukisikia milio ambayo haieleweki na hujui ina tokea wapi hakika ina ogopesha sana.

“Ni nini hivyo?”

Piyanka alizungumza huku akiwa amelishikilia koti langu kisawa sawa.

“Twendeni”

Nilijikaza kuzungmza hivyo ila kiukweli hata mimi mwenyewe nina ogopa. Tukakafika kwenye eneo lenye ukumbi mkubwa sana wa pango hili huku kikiwa kumejaa masanamu ya watu maarufu wa zamani sana akiwemo adolf Hitler. Katika ukumbi huu kuna eneo lina jukwa dogo ambalo kwa juu yake kuna boksi hili jeusi.

‘Nenda mwenyewe ukalichukue’

Niliweza kuisikia sauti ya Ethan. Nikawapa ishara ya kunisubiria Piyanka na da Mery. Nikapiga hatua za taratibu na zilizo jaa umakini wa hali ya juu, nikapandisha ngazi sita za jukwaa hil. Nikalifikia boski hili ambalo kwa miaka mingi nimekuwa nikiandamwa nalo pasipo hata mimi mwenyewe kufahamu ni wapi lilipo.

Taratibu nikausogeza mkono wangu wa kulia na kulishika boski hili, nikalinyanyua na kushuka kwenye ngazi kwa hatua hizi za taratibu. Gafla mwili wangu ukaanza kusisimka, tukaona watu walio mavazi meupe wakikatiza katika katika ukumbi huu jambo lililo tufanya tutamani kukimbia ila nguvu za miguu zikatuishia kabisa. Watu hawa ambao hawakanyagi ardhi wakaendelea kututesa kwa kukatiza katiza karibu yetu.

“Ethan”

Niliisikisa sauti ya mzee Klopp nyumba yangu, nikageuka gafla na kumuona mzee Klopp akiwa ana elea elea hewani huku naye akiwa amevalia mavazi meupe. Nikamtazama da Mery kwa jicho la kuiba naye nikamshuhudia akimtazama baba yake aliye simama mbele yangu.

“Musiogope”

Mzee Klopp alizungumza huku akiendelea kunitazama.

“Fungua hilo boksi”

Nikafungua boksi hili huku mikono yangu yote ikinitetemeka kwa woga mwingi sana. Nikakuta karatasi ambayo imekunjwa vizuri na kufungwa na kama nyeusi. Karatasi hii kwa kuitazama inaonyesha ni ya miaka mingi sana.

“Fungua hiyo karatasi”

Nikaifungua karatasi hii na kuona michoro ambayo sikuwahi kuiona hapo awali. Mzee Klopp taratibu akanisogelea na kuichukua karatasi hii na kuniomba niweze kuvua koti na tisheti. Nikatii, na kubaki tumbo wazi. Akanibandika karatasi hii kifuani mwangu na nikahisi maumivu makali sana na baada ya muda nikaona michoro yote iliyopo kweye hii karatasi ikiwa imehamia mwilini mwangu. Haya yote yakiendelea, Piyanka na da Mery wana shuhudia.

“Wewe ndio fumular sasa hivi. Kupitia wewe una weza kuitawala dunia”

Mzee Klopp alizungumza huku aki ikunja kunja karatasi hii ambayo bado ina michoro hiyo. Akairudisha ndani ya boksi hilo na kunikabidhi. Baada ya muda mchache maandishi yote yakapotea mwilini mwangu.

“Hakikisha una wapatia wanacho kihitaji”

“Kina nani?”

“Utawaona”

Maneno ya mzee Klopp yakaniweka katika hali ya sinto fahamu. Nikavaa nguo na tukapewa ishara ya kutoka katika pango hili, kila kilicho tokea kwenye macho yetu ni kama ndoto ila ni hali ya kweli kabisa. Tukatoka ndani ya pango hili na taa zote za ndani ya hili pango zikazima. Tukaanza kushuka kilima hichi huku sote tukiwa kimya, hapakuwa na mtu aliye weza kumuuliza mwenzake swali. Tukafika eneo tulilo acha gari letu na tukaingia ndani ya gari na kuondoka katika eneo hili.

“Ethan”

“Naam”

“Nini utafanya juu ya hiyo fomula?”

“Sijui”

Nilimjibu Piyanka kwa kifupi. Tukiwa barabarani, nikajikuta nikipunguza mwendo kasi wa gari hili hii ni mara baada ya kuona kizuizi cha wanajeshi kilichopo mbele yangu. Sikuta kuleta ubishi wa aina yoyote zaidi ya kukubali kusimama. Wanajeshi wanne walio shikilia bunduki zao vizuri wakalisogelea gari letu na kutuamrisha kushuka.

“Ethan Klopp upo chini ya ulinzi”

Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akinionyooshea bunduki ya kichwa. Hapa sasa kidogo ndipo nikaanza kupata maana ya maneno ya mzee Klopp aliyo yazungumza kwangu. Mwanajeshi huyu akanisogelea na kunifunga pingu za mikononi mwangu.

“Tunahitaji boksi jeusi”

Mwanajeshi huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kama muna lihitaji boksi hilo, nahitaji dada yangu na rafiki yangu waweze kuondoka eneo hili”

“Hapana Ethan tutakuwa pamoja”

Da Mery alizungumza kwa sauti ya majonzi.

“Hapana munapaswa kuondoka. Niacheni mimi peke yangu natambua kabisa kwamba Camila ndio alio waagiza si ndio”

“Ndio”

“Basi waachieni waondoke”

Wanajeshi hawa wakashauriana kisha wakakubaliana na pendekezo langu. Nikachukua boski hilo ndani ya gari na Piyanka na Da Mery wakaondoka eneo hili na kuniacha na wanajeshi hawa. Baada ya robo saa helicopter moja ya jeshi ika tua katika barabara hii ya magari na muda huu unao endelea alfajiri hakuna magari yanayo katika katika barabara hii. Camila na wanajeshi kadhaa wakashuka kwenye helicopter hii na kunifwata hapa nilipo simama.

“Ethan, unahisi kwamba una weza kunikimbia?”

“Natambua kwamba siwezi kukimbia ikiwa nipo chini ya kivuli cha mwamvuli wako. Nimekufanikishia kile ambacho unakihitaji na waambie watu wako waweze kukupatia”

Camila akatabasamu huku mwanajeshi mmoja akimkabidhi Camila boksi hili dogo. Camila akafungua boksi hilo na kutoa karatasi hiyo, akaifungua na kuitazama kwa sekunde kadhaa na akafurahia sana.

“Sasa Ujerumani kuitawala dunia tena”

“Una maana gani?”

“Nilazima tumshushe Marekani na sisi tuwe juu ya nchi zote duniani.”

“Una maanisha unataka kwenda kuanzisha vita ya tatu ya dunia?”

Camila akaanza kucheka kicheko cha kinafiki huku akiikunja vizuri karatasi hii.

“Ninakupa nafasi ya mwisho kwenye maisha yako. Potea nchini Ujerumani na nisikuone tena kwenye ardhi ya nchi hii. Endapo nitakuja kukuona basi nitakuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe. Umenielewa?”

Camila alizungumza kwa msisitizo. Wanajeshi hawa wakanifungua pingu kisha Camila na wanajeshi alio kuna nao wakingia ndani ya helicopter yao na kuondoka huku wanajeshi walio kuwa wameweka kizuizi barabarani wakiingia kwenye magari yao na kuondoka na nikabaki peke yangu.

“Vipi”

Niliisikia sauti ya Ethan pembeni yangu. Nikamtazama na kumuona akiwa ana tabasamu.

“Huyu binti ana maanisha kwa kile anacho kwenda kukifanya?”

“Yaa ila hato weza kufanikiwa”

“Kivipi?”

“Kitu wanacho kwenda kukitengeneza ndio kitakacho waua”

“Waua hadi wananchi wasio na hatia?”

“Hapana ila yeye na watu watakao ungana nao kwenda kufanya majaribio ya mwisho katika kulijaribu bomu hilo”

“Hadi kutengeneza bomu hilo itawachukua muda gani?”

“Miezi arobaini na nane”

“Miaka miwili?”

“Ndio”

Nikaona gari ndogo ikija kwa mwendo wa taratibu katika barabara hii. Nikasimamisha gari hili na kwa bahati nzuri dereva wa hili gari akakubali kusimama. Nikainama na kuchungulia ndani ya gari hili na kumuona mzee mmoja wa makamo.

“Klopp mbona upo hapa?”

“Mzee huyu aliweza kunitambua kwa haraka sana.

“Ahaa niliharibikiwa na gari langu hivyo nimekosa msaada wa kurudi mjini”

“Ingia ndani ya gari tuondoke kwa maana alfajiri hii, sio salama kuwa peke yako kwenye hili eneo.”

“Nashukuru mzee”

Nikazunguka upande wa pili wa gari hili na kuingia ndani. Taratibu tukaondoka eneo hili na kumuacha Ethan peke yake barabarani. Nilicho weza kugundua kwamba mzee huyu hakuweza kumuona Ethan. Taratibu mzee huyu akaongeza sauti ya redio yake iliyomo ndani ya gari hili.

“Naitwa Mullar, nilicheza na baba yako timu moja miaka mingi ya nyuma”

“Weee”

“Yaa ni nilikuwa nina cheza kiongo wa timu. Ila ni miaka mingi sana ya nyuma na baada ya hapo nilihama timu na kuhamia ligi ya nchini Uingereza katika klabu ya Chelsea.”

“Sawa sawa”

“Ila vipi wewe mbona hadi sasa huja jiunga kwenye club yoyote, ikiwa una kipaji kizuri sana cha mpira au huhitaji kucheza tena mpira?”

“Nina hitaji ila nitaanza kucheza kwa msimu huu unao anza mwaka huu”

“Fanya hivyo bwana kwa maana ulimwengu una kuhitaji burudani yako. Mimi ni shabiki yako mkubwa sana”

“Kweli?”

“Kweli kabisa, yaani nimekuwa nikikufwatilia toka ulipo kuwa shule ya msingi”

“Nashukuru sana mzee wangu”

“Nina imani Ujerumani tuna jivunia wewe, kwenye world cup lazima tuchukue kombe kwa mara nyingine”

Mzee huu alizungumza kwa furaha sana pasipo kufahamu kwamba moyo wangu kwa sasa hauipendi kabisa Ujerumani na hata ikitokea nimeitwa kwenye timu ya taifa ya nchi hii sinto kubali kabisa. Mzee huyu akanipelekea hadi nyumbani na kuwakuta da Mery na Piyanka wakiwa wamejawa na wasiwasi. Nikaagana na mzee Muller na nikawaelezea kili kitu da Mery na Piyanka.

“Inakuwaje sasa?”

“Kwa sasa nahitaji nielekee nchini Spain. Piyanka na dada mutaelekea nchini Tanzania”

“Spain unakwenda kufanya nini Ethan?”

“Nahitaji kurudi kiwanjani. Maisha yangu sasa nataka kuyaweka kweye soka. Sitaki kuhangaika tena na matatizo haya ya dunia”

“Ila Ethan kumbuka kwamba na sisi tunatakiwa kutengeneza bomu kwa kupitia ramani iliyopo mgongoni mwako ili kuhakikisha kwamba tuna pambana na Ujerumani”

Piyanka alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama machoni mwangu kwa umakini sana.

“Ulicho kizungumza umekifikiria mara mbili mbili au umezungumza ili mradi na wewe uwe ume zungumza?”

“Ila Ethan anacho kizungumza Piyanka ni kweli?”

“Sikilizeni nyinyi, ni damu za watu wangapi zitakwenda kumwagika kwa ajili ya mapambano haya ya kipuuzi. Damu zilzo mwagika kwa ajili ya haja mambo sasa zimetosha. Fungasheni kila kilicho chenu muelekee nchini Tanzania leo hii sawa”

Nilizungumza kwa hasira na kuwafanya da Mery na Piyanka kubaki midomo wazi kwani hawakutarajia mara baada ya kupata hii fomula kama nitakuja kuaamua maamuzi kama haya.



Piyanka na da Mery wakaonekana kukubaliana nami kwa shingo upande. Hapakuwa na hata mmoja wao aliye diriki kufungua kinywa chake juu ya hili. Taratibu za kuelekea nchini Tanzania zikaanza, hadi inafika majira ya jioni kila kitu kikawa kimekamilika na wakapata tiketi ya ndege itakayo ondoka siku inayo fwata.

“Utaondoka lini Ujerumani?”

Da Mery aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nahitaji kuziweka sawa kampuni kisha nitaondoka”

“Sawa. Mimi ninaelekea Tanzania je ninakwenda kufanya kazi gani katika nchi hiyo ya ugenini?”

“Utakuwa mmiliki wa kampuni ya mawasiliano niliyo ianzisha huko”

“Ila Ethan kumbuka kwamba professional yangu mimi ni daktari na si mfanya biashara”

“Sawa utasimama katika kapuni hiyo huku tukijenga hospitali kubwa ambayo uta isimamia. Nina imani kwamba Ethan atasaidia katika hilo”

“Sawa alafu nilikuwa nina omba ushauri wa jambo moja”

Da Mery alizungumza kwa upole na kwa haraka haraka nikamdadisi na kutambua hilo jambo analo hitaji niweze kumshauri hakika linamsumbua sana akilini mwake.

“Jambo gani?”

“Nahitaji kuwa na mtoto kwa sasa. Umri wangu una kwenda, wezangu ambao nilisoma nao mavyuoni huko ssa hivi wana familia zao. Mimi pekee tu ndio sina, hembu niambie nina fanyaje?”

“Umezungumza na Ethan juu ya swala hilo la mtoto?”

“Ndio nilisha wahi kuzungumza naye ila hakunipa majibu ya kueleweka na mwisho akaniambia kwamba yeye si binadamu na endapo ata nipatia ujauzito mimi basi mtoto atakaye zaliwa ana weza kuleta madhara kwenye jamii au ana weza kuwa wa tofauti kabisa na watoto wengine”

“ Mmmm utafanyaje?”

“Ndio hapo nilikuwa nafikiria niweze kumuomba Ethan nizae na binadamu mwenzangu huku mahusiano kati yangu na yeye yaendelee kama kawaida”

“Unahisi ata kubali?”

“Ndio maana nikakuomba ushauri kwani yeye ni rafiki yako na muna urafiki wa miaka mingi”

“Sawa nitazungumza naye kisha nitakujulisha”

“Nitakushukuru katika hilo”

“Sawa kapumzike”

Dada Mery akaelekea chumbani kwake. Nikaanza kufanya mawasiliano kwa wakurugenzi wote wanao simamia kampuni zangu na kuahidi kukutana nao kesho majira ya saa nne asubuhi.

Siku iliyo fwata nikawasindikiza Piyanka na da Mery hadi uwanja wa ndege, nilipo hakikisha wamepanda ndege na imeondoka uwanjani nikaelekea katika kampuni yangu inayo shuhulika na maswala ya utengenezaji vifaa vya michezo ambapo hapo ndipo nilipo ahidiana na wakurugenzi wangu wa kampuni zangu zote kuonana. Kila mfanyakazi aliye bahatika kuniona, akajawa na furaha kubwa sana, kwani ni kwa kipindi kirefu sana sija onekana kwenye upeo wa macho yao. Saa tano kamili asubuhi tukaanza kikao hichi ambcho lengo kubwa kufahamu juu ya ripoti za kiuchumi kwa kipindi chote ambacho nilikuwa sipo kazini.

Hakika wakurugenzi wangu hawa wameweza kufanya kazi ambayo inahitaji kupongezwa, kila kampuni imepanda kiuchumi kwa asilimi nyingi sana.

“Nina waamini sana na nina omba tuzidi kujitanua katika uzalishaji.”

“Tumekuelewa muheshimiwa raisi”

“Basi niwatakie mchana mwema na kikao kimeishia hapa”

Nilizungumza huku nikinyanyuka na kuwafanya wa kurugenzi wangu wote kunyanyuka. Tukapeana mikono kisha nami nikaondoka huku nikiwa tayari nimesha wasiliana na marubani wangu ambao nitaondoka nao na ndege yangu binafsi kuelekea nchini Spain.

“Hei”

Ethan alinistua huku akiwa amekaa katika siti ya pembeni ambayo nimekaa.

“Naendesha Ethan maswala ya kunistua nina weza kupata ajali”

“Ila huwezi kupata ajali ukiwa na amimi”

“Haya bwana. Eheee nimeongea na Mery anahitaji mtoto vipi?”

“Nimewasililiza kila munacho kizungumza”

“So umeamuaje juu ya hatima ya dada yangu. Umri wake ni kweli una kwenda?”

“Nitampatia”

“Sawa utampatia je huyo mtoto ata kuwaje?”

“Siwezi jua ila nita mpatia, sinto mruhusu azae na mwanaume mwengine”

“Haya, mimi nina kwenda Spain hembu niambie safari yangu je itakuwa ya mafanikio au?”

“Ndio itakuwa na mafanikio”

“Poa, acha nielekee nyumbani kisha nitaelekea uwaja wa ndege”

“Hakuna tatizo.”

Nikafika nyumbani na kubaba kila kilicho changu kisha nikaelekea uwanja wa ndege na kukuta ndege yangu ikiwa tayari imesha andaliwa kwa safari. Majira ya saa mbili usiku safari ya kuelekea nchini Spain ikaanza huku ndani ya ndege hii nikiwa na rubani wangu wawili tu. Nikafanya mawasiliano na kocha wa timu ya Real Madrid na akafurahi sana juu ya ujio wangu akaniahidi kwamba ata hakikisha kwamba ana nipokea katika kiwanja cha ndege.

Nikafika nchini Spain na nikapolekewa na kocha huyu kwa siri sana pasipo waandishi wa habari kuweza kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea. Tukaelekea nyumbani kwake ambapo niliweza kupokelewa kwa furaha kubwa sana na mke wake pamoja na wajukuu wake wawili nilio wakuta hapa.

“Karibu sana”

“Nashukuru mama”

Nikapewa chumba changu ambacho nitakitumia kwa kipindi chote ambacho nitakaa nyumbani hapa, na pale nitakapo nunua nyumba yangu basi nitahamia kwenye nyumba yangu hiyo. Siku iliyo kwa kusaidiana na kocha wangu tukaanza kufwatilia kibali cha mimi kuishi nchini Spain na kucheza soka katika nchi hii. Kutoana na umaarufu wa kocha pamoja wa umaarufu wangu vikatusaidia sana kuweza kupata vibali vyote ambavyo tulivitafuta. Baada ya kumaliza hatua hiyo, nikapelekewa katika bodi ya usajili ya club hii kubwa hapa Spain na duniani kwa ujumla.

“Kabla ya kumsajili inabidi akapimwe vipimo vyote”

Mmoja wa wakurugenzi wa usajli alizungumza.

“Hilo kwa upande wangu halina shida kabisa.”

“Sawa madaktari wetu wapo tayari kwa ajili ya zoezi hilo na ukimaliza kufanya hivyo basi tutakaa mezani na kujadili juu ya maslahi yako”

“Sawa sawa”

Kutokana siku ya leo muda umekwenda sana, ikatulazimu kufanya vipimo hivi vya afya siku iliyo fwata. Jopo la madaktari na manesi wakaanza kazi yao kunipima kuanzia damu hadi magonjwa mengine ambayo sio ya kuambukiza kama kisukari na saratani. Jambo la kumshukuru Mungu, hali yangu ya Afya ipo vizuri sana na sina tatizo la aina yoyote.

“Karibu Madrid”

Daktari mkuu alizungumza huku akinipa mkono.

“Nashukuru sana dokta”

Vipimo vyangu vikarudishwa kwenye bodi ya wasajili. Kutokana vimedhibitishwa na daktari wao kwamba sina tatizo lolote, wote wakaridhika.

“Nina imani kwamba mashatri yangu niliweza kumueleza kocha kwa kipindi cha nyuma. Jambo moja kubwa nina hitaji kulipwa mshahara mkubwa kupita wachezaji wote hapa duniani. Pila kodi za mapato ya nchi zisiingie kwenye mshahara wangu na kutokana sijatoka kwenye club yoyote, hivyo sinto hitaji pesa za usajili”

Viongozi hawa wa bodi ya usajili wakatazamana huku wakionekana kufurahishwa kwa masharti yangu kwani si magumu sana.

“Tutakulipa paun laki sita kwa wiki?”

“Sihitaji mshahara huo kwa maana nimekuja hapa kuhakikisha kwamba nina weka rekodi ya kipekee katika timu hii”

“Basi tunakupa nafasi ya wewe una hitaji kulipwa kiasi gani?”

“Paun milioni moja na nusu kwa wiki”

Watu wote wakatazamana huku wakiwa wamejawa na mshangao mkubwa sana kwani ni kiasi kikubwa sana cha pesa kwa mchezaji kulipwa.

“Kama hamto hitaji basi kuna club kubwa zina nihitaji nina weza kuelekea huko na wapo tayari kunilipa kiasi kikubwa zaidi ya hicho. Jambo lililo nifanya nije hapa ni kutokana na ahadi niliyo iweka kwa kocha kama ingekuwa sio hivyo nisinge kuja”

Nilizungumza kwa msisitizo na kuwafanya viongozi hawa kushusha pumzi huku wakitafakari. Ikawalazimu kuzungumza na raisi wa timu hiyo, japo naye aliweze kustushwa kwa kiasi hicho cha pesa, ila ikabidi akubaliane na viongozi hao ili kuinasa saini yangu. Makubaliano yalipo fikia muafaka, wakanipa mkataba wa miaka minne. Kutokana ni utaratibu wa club zote zinapo msajili mchezaji ni lazima wawaeleze waandishi wa habari na mchezaji asaini mbele ya waandishi wa habari, ndivyo jinsi ilivyo kuwa kwangu. Nikakabidhiwa jezi yenye namba tisa mgongoni huku ikiwa imendikwa jina la Ethan. Picha nyingi sana zikapigwa na waandishi wa habari, nikasaini mkataba huu wenye vipengele ambavyo, endapo mkataba wangu ukiisha baada ya miaka hii minne nina weza kuongeza au kuondoka katika club hii. Kipengelea kingine kina elezea endapo itajitokeza club yoyote duniani kuamua kuni nunua kabla ya mkataba wangu kuisha basi wata ninunua kwa kiasi cha pauni bilioni moja, kiasi ambacho sidhani kama kuna club yoyote duniani kitaweza kuni nunua.

Habari ya mimi kusajiliwa na club kubwa ya Real Madrid zikazidi kusambaa duniani, mashabiki wangu wa mpira ambao kwa kipindi kirefu walikuwa na hamu na mimi wakazidi kuongezeka katika account zangu za Instergram na Twitter. Nikanunua jumba la kifahari katika mji huu wa Madrid, jumba ambalo lina kila aina ya starehe niliyo ihitaji, ikiwemo kiwanja cha mpira. Nikaipa tenda kampuni kubwa ya ulinzi kuhakikisha kwamba nyumba yangu ina wekewa ulinzi mkubwa na hakuna adui ambaye ana weza kunivamia. Nikanunua gari nne za kifahari, BMW i8, Ferrari 458, Lamborghini huracan na Audi r8.

“Hei ni mimi”

Nilizungumza kwa sauti ya upole sana huku simu yangu ikiwa sikioni mwangu.

“Ethan”

Latifa alizungumza kwa shahuku kubwa sana, kwani kwa kipindi kirefu sana toka niondoke nchini Tanzania sikuwahi kuzungumza naye.

“Yaa ni mimi”

Latifa akaanza kuangua kilio cha furaha.

“Nimeona kwenye tv mume wangu ndoto zako zime fanikiwa”

“Yaa, kesho nitajaribu kuzungumza na ubalozi wa Tanzania kwa huku wakufanyia juu chini uweze kupata visa na uje huku. Nahitaji uishi nami sasa. Nina amani moyoni mwangu”

“Ethan utaulipua moyo wangu kwa furaha”

“Niamini mimi nitayafanya hayo usiku wa leo”

“Nitashukuru sana mume wangu. Nina kupenda sana”

“Nina kupenda pia mke wangu. Msalimie Romani, Qeen la Claudia”

“Usijali zimefika mume wangu. Nimempokea dada yako na nilimtambulisha kwenye kampuni yako na amechukua usukuni wa kuiongoza kampuni yako”

“Nashukuru kwa hilo, acha niwahi mazoezini tutawasiliana kesho”

“Sawa mume wangu. Nina kupenda sana”

“Ninakupenda pia mke wangu”

Nikakata simu, na kuingia kwenye gari langu aina ya Audi r8 na kuelekea katika kiwanja cha mazoezi. Kitendo cha kufika katika kiwanja hapo ikiwa ni mara yangu ya kwanza kuanza mazoezi rasmi, waandishi wa habari wakanivamia na kuanza kunipiga picha za kutosha huku wengine wakunihoji juu ya usajili wangu. Sikuwajibu kitu cha ina yoyote zaidi ya kujumuika na wachezaji wezangu, ambao kwa hapo awali niliweza kuwaona kwenye televishion.

Mazoezi kwa siku ya leo yakaenda vizuri sana. Baada ya wiki tatu za mazoezi, nikazoeana na wachezaji wezangu huku wote wakifurahia juu ya uwepo wangu katika timu hii. Uzuri ni kwamba katika kikosi cha kwanza mimi ndio mwenye umri mdogo kuliko wachezaji wote.

“Mechi ya kombe la hisani tunaanza na wapinzani wetu Barcelona. Tunahitaji kuchukua kombe hilo ili kuanza msimu huu vizuri”

Kocha alizungumza huku akiwa amesimama katikati yetu.

“Ethan japo kwa sasa tunapata maoni mengi sana kutoka kwa wachambazi wakubwa wengine wakilalama kwa kiasi tunacho kulipa, ila hii ndio mechi yako ambayo unatakiwa kuonyesha thamani yako. Hakikisha hufanyi makosa”

“Usijali kocha nitafanya hivyo”

“Kocha kwa huyo wala huna haja ya kumueleza afanye nini nina mjua sana Ethan”

Rafiki yangu Frendando ambaye kwa sasa ndio kipa namba moja wa timu hii alizugumza na kuwafanya wachezaji wezangu kutabasamu.

“Sawa, mutapumzika kwa siku ya kesho kesho kutwa ni siku ya mechi hivyo munapaswa kuhakikisha kwamba munawahi mapema na tunaelekea katika jiji la Barcelona mapema iwezekanavyo ili kuzoea mazingira ya mji huo”

“Sawa kocha.”

Baada ya maelezo hayo, tukaruhusiwa kuondoka kiwanjani. Tukaongozana na Frenando hadi nyumbani kwake na kumkuta mke wake ambaye ni Mmexcan mwenzake. Akanitambulisha kwa furaha na tukaapata chakula cha jioni kwa pamoja huku tukikumbushana juu ya mambo mengi tuliyo yafanya kipindi tukiwa shuleni.

“Unajua kitu ambacho sikiamini hadi sasa hivi Ethan, ni wewe kuachana na Camila. Yaani bado kabisa”

“Ndio hivyo uamini ndugu yangu yule mwanamke ni nyoka”

“Duu, ila kutokana amesha olewa basi inabidi kwa sasa kuhakikisha kwmaba maisha yana songa mbele, ionyeshe thamani yako rafiki yangu. Vyombo vya habari vya hapa Spain, vinajua kupiga madongo wachezaji, hivyo usije ukaingia katika kipindi kigumu cha kuandamwa na vyombo vya bahari”

“Usijali rafiki yangu. Mungu atusaidie katika hili”

“Sawa kaka”

Majira ya saa mbili usiku nikaondoka nyumbani kwa Frenando na kurudi kwangu. Ukumbwa wa jumba langu hakika nina hitaji mke wa kuishi naye. Siku iliyo fwata kama nilivyo muahidi Latifa nikafwatilia juu ya kupata visa ya yeye kuja huku. Balozi wa Tanzania hapa Spain aka niahidi kulishuhulikia jambo hili ndani ya wiki hii.

Siku iliyo fwata asubuhi na mapema wachazaji wote tukakuatana katika club yetu. Tukapanda basi lililo tupeleka hadi uwanja wa ndege kisha tukapanda ndege ya kutupeleka katika mji wa Barcelona. Ikatuchukua saa moja na dakika kumi na tano kufika katika mji huu. Moja kwa moja tukaelekea hotelini kwa ajili ya kujipumzisha hadi majira ya saa kumi jioni ambapo ndipo mechi yetu ita chezwa katika kiwacha cha Camp Nou.

“Ethan huta anza katika mechi hii”

“Sawa kocha”

Kocha akapanga mipango yote ya jinsi tutakavyo kwenda kucheza kiwanjani hapa. Majira ya saa tisa, tukaingia katika basi letu na kuelekea kiwanjani, kila mchezaji amevalia trakc suit nyeupe. Tukapokelewa uwanjani hapo kwa shangwe za mashabiki wetu ambao wamesafiri nao kutoka katika mji wetu ili kuja kushuhudia mechi hii ambayo ni kubwa sana kwa nchi hii. Tukavalia jezi zetu, huku kwa mara ya kwanza nikivaa jezi ya timu hii, wachezaji walio pangwa kuanza wakatangulia katika kupanga mstari wa kuelekea uwanjani huku sisi ambao tutaingia kwa mapendekezo ya kocha, moja kwa moja tukielekea katika viti vya bechi la ufundi. Waandishi wa habari hawakusita kunipiga picha huku wengine wakiendelea kunirekodi. Hakika huu uwanja ni mkubwa na una watu wengi sana.

“Vipi una wasiwasi”

Mchezaji mwenzangua aliniuliza mara baada ya kuniona nikitazama tazama uwanja huu.

“Hapana”

“Kuwa na amani hawawezi kutufunga”

“Nashukuru Nacho”

Wachezaji wezetu wakaingia kiwanjani huku vifijo na shangwe vikitawala uwanja mzima. Wachezaji wakapeana mikono na kutawanyika. Kipenga cha muamuzi kikalia na mpira huu ukaanza kwa kasi ya ajabu sana huku wachezaji wa Barcelona wakitushambulia kwa spidi kali. Dakika ya tano Messi akafunga goli la kwanza kwa faulu nzuri ambayo Frenando alijitahidi kuruka ila akashindwa kabisa kuupata mpira huo. Kocha akazidi kutoa maelekezo na wachezaji wezetu wakajitahidi katika kishambulia, ila kila walicho kifanya kikawawia ugumu. Dakika ya ishirini na mbili Luis Suarez akatufunga goli la kichwa, baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Iniesta.

Nikashusha pumzi nyingi sana kwani kwa jinsi wachezaji wa Barcelona wanavyo piga pasi nyingi na zenye kasi, zimewawia wachezaji wezangu kushindwa kabisa kumiliki mpira. Kona ya dakika ya arobaini na tano Pique akatufunga goli la kichwa. Hadi tunakwenda mapumziko, tupo nyuma ya goli tatu.

“Benzema utapumzika, Ethan utaingia. Ronaldo na Bale hakikisheni kwamba munaingia kwenye boksi la wapinzani”

“Sawa kocha”

Tukarudi uwanjani huku nikiwa nimeivaa jezi yangu vizuri. Mashabiki wa timu yangu karibia wote wakasimama na kuanza kunishangilia. Refa akapiga filimbi na mchezo huu ukaanza, huku karibia timu nzima ikiniangalia mimi. Nikapata pasi moja maridadi kutoka kwa Isco, nikawazunguka mabeki wawili wa Baecelona ambao wananifwata kwa kasi ya ajabu sana, nikapata nafasi ya kulitazama goli, kwa mguu wangu wa kushoto nikaachia shuti moja kali ambalo halikukosea kuelekea nilipo hitaji, moja kwa moja mpira ukamshinda kipa na ukazama golini. Shangwe zikatawala huku wachezaji wezangu wakinifwata na kunikumbatia kwa furaha. Goli hili likanyanyua morali wa wachezaji wezangu, tukaanza kuwaandama wachezaji hawa wa Baecelona huku miguu yangu ikiwa na kazi ya kuwakimbiza na kuwapiga vyenga vya uzalilishaji. Nikatoa pasi moja ambayo ikamfikia vizuri Ronaldo kichwani mwake na kupiga kichwa kizuri sana kilicho mshinda kipa na mpira ukaingia golini. Kuingia kwangu ndani ya kiwanja hichi kukazidi kuzaa matunda, kwani nilipiga shuti jengine ambalo likababatiza beki na kuingia golini na hadi dakia ya sabini goli ni tatu kwa tatu. Dakika ishirini zilizo baki zitaamua ni nani atakuwa mshindi wa kombe la hisini.



Barcelona wakaanza mpira kwa kasi sana huku kila mchezaji akihitaji kupata ushindi. Viungo wa timu yangu wakisaidiana na mabeki, hawakukubali tushambuliwe sana, hivyo wakakaba kwa juhudi zote na mipira wakaipandisha kwetu, Bale akampita beki wa kushoto na kuingiza krosi moja ya juu. Sikujali kuumia, nikajigeuza kwa kasi kubwa sana na kupiga tikitaka na kwa bahati nzuri mpira huo niliweza kuupata vizuri mguuni mwangu. Hadi ninatua chini na kutazama golini, nikashuhudia nyavu zikitingishika huku mashabiki wote wakinyanyuka na kushangilia. Wachezaji wezangu wakaja kunilalia hapa hapa huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana. Tukanyanyuka huku sasa tukiwa tunaongoza kwa goli nne. Wapinzani wetu wakaanza mpira, ila kutokana tayari tumesha wazidi nguvu, hivyo kuwapokonya mpira ikawa ni jambo rahisi sana. Nikafanikiwa kupata mpira, nikiwa katikati ya uwanja, nikamtazama golikipa na kumuona akiwa ametoka golini, nikakunjua mguu wangu wa kushoto na kuachia shuti kali, mpira ukaanza kuambaa ambaa hewani huku golikipa akianza kurudi nyuma. Kitendo cha kufika golini ili aokoe mpira huo, akajikuta akizama nao nyavuni.

Hakika ni siku yangu nzuri sana kwenye maisha yangu ya soka, wachezaji wezangu, wakanikumbatia kwa furaha. Goli hili, limewanyong’onyeza wapinzani wetu na hadi sasa ni tano kwa tatu. Ronaldo akachezewa madhabi nje kidogo ya boksi la wapinzani wetu na refarii akaweka faulu inayo elekea golini mwa Barcelona.

“Dogo piga hii faulu”

Ronaldo aliniambia huku akiwa ameuweka mpira sehemu ambayo refarii ameagiza uwekwe. Refarii mara baada ya kupiga hatua zake akachora mstari na mimi nikarudi nyuma hatua nne huku nikitazama ukuta wa wachezaji hawa wa Barcelona. Refa akapiga filimbi, kwa mguu wangu wa kulia, nikapiga shuti zito la chini chini, wachezaji wa Barcelona wakajikuta wakiruka juu, na mpira ukapita chini ya miguu yao na kuingia nyavuni jambo lililo zidi kunyanyua shangwe kwa mashabiki wa timu hii.

“Hongera sana”

Wachezaji wangu walinipongeza sana kwani hadi sasa nimefunga goli tano peke yangu. Wapinzani wetu wakaanza mpira, kitendo cha Messi kutoa pasi ambayo sikujua alikuwa anampatia nani, nikaudaka mpira huu, nikaanza kukimbizana na mabeki pembezoni mwa uwanja. Mabeki japo wana nguvu, ila nami niliweza kutunisha misuli yangu na wakashindwa kuuchukua mpira miguuni mwangu, nikapata nafasi ya kuingia katikati ya mpira, kisha nikapiga shuti moja lililo kuja mithili ya ndizi na mpira ukamshinda goli kipa na kuingia wavuni. Mashabiki wote wa Barcelona wakaka kimya huku mashabiki wetu walio valia jezi nyeupe na kurusha rusha bendera nyeupe, wakazidi kushangilia kwa furaha kubwa sana. Hadi mpira unakiwsha, goli ni saba kwa tatu. Refa akanikabidhi mipira yangu miwili kwani nimefunga goli sita katika mechi moja.

“Hongera dogo naomba jezi yako”

Messi alizungumza huku akinifwata, nikavua jezi yangu naye akavua jezi yake na kunikabidhi.

“Ukiendelea hivyo utavunja rekodi ya Pele pambana”

Baada ya Messi kuzungumza maneno hayo akaondoka. Wachezaji wezangu wakanipa mikono ya kunipongeza, kocha akanifwata na kunikumbatia kwa nguvu sana.

“Hongera sana Ethan”

“Nashukuru”

“Umenionyesha kwamba sijakosea kukuleta kwenye timu hii”

“Asante kocha”

Nikawakabidhi jezi hii wasaidizi wa kocha pamoja na mipira, tukapewa tisheti nyingine kwa ajili ya kwenda kupokelea medali pamoja na kombe la hisani. Jukwaa baada ya kuandaliwa, wachezaji wa Barcelona wakakabidhiwa medali zao kisha tukafwatia sisi na kuanza kukabidhiwa medali na raisi wa shirikisho la mpira katika nchi hii ya Spain. Kila kiongozi hakusita kunipa hongera kwa juhudi nilizo zionyesha. Nikavalishwa medali na raisi huyu kisha tukakusanyika katika jukwaa hili kusubiri kapteni wetu kukabidhiwa kombe hili.

Kapteni wetu Ramos, akakabidhiwa kombe hili na kuja sehemu tulipo, akalinyanyua kwa nguvu juu na baruti zenye vikaratasi vingi sana zikaanza kulipuka. Kila mchezaji akaanza kulishika kombe hili na kulinyanyua juu, ikafika zamu yangu nami nikalishika na kulinyanyua juu huku wachezaji wezangu wakishangilia kwa furaha sana.

Baada ya shamra shamra hapa uwanjani tukaelekea kwenye vyumba vyetu vya kubadilishia nguo. Tukabadilisha nguo na kuondoka uwanjani hapa, moja kwa moja tukaelekea uwanja wa ndege na kurudi katika mji wetu wa Madrid. Mapokezi ya uwanja wa ndege ni makubwa sana kiasi cha kumshangaza kocha.

“Nimecheza kwenye timu hii na hadi sasa hivi nimekuwa kocha. Hakiksa sijawahi kuona mapokezi makubwa kama haya”

Kocha alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Mashabiki wengi wamashika mabango yenye jila langu huku wengi wakionekana kunipenda.

“Usije ukavimba kichwa kwa mechi moja. Kuna mechi nyingi sana mbele yetu”

Kocha alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Usiku huu hapakuwa na mchezaji aliye ondoka eneo la club yetu ilipo. Shangwe na furaha zilitawala huku wenye wake na wachumba zao wakijumuika nasi katika kusherekea ushindi huu mkubwa tulio upata kutoka kwa wapinzani wetu wa jadi.

“Hei naitwa Xaviela”

Dada mmoja mrefu na mwembaba, aliye na nywele ndefu zilizo karibia kufika mdogoni aliniongelesha huku akinipa mkono. Nikautazama mkono wake kisha nikaupokea.

“Nashukuru kukufahamu naitwa Ethan”

“Usijali ninakujua”

“Ninashukuru”

“Una mtu yoyote unaye msubiria kwenye hii party?”

“Hapana nipo mwenyewe”

“Naweza kujumuika nawe?”

“Hakuna tatizo, kwani umekuja na nani?”

“Nimekuja na mke wa Ramos, mimi na yeye ni marafiki”

“Sawa”

Wanao kunywa wakaendelea kunywa, wanao vuta nao wakendelea kuvuta shisha na sigareti. Hakika maisha ya ushindi ni mazuri sana. Kwa kumtazama kwa haraka haraka Xaviela, amenitamani ila anashindwa kuzungumza ukweli wa moyo wake.

“Mbona upo kimya?”

“Ahaa hakuna, ila nina weza kukuuliza swali”

“Uliza”

“Una msichana?”

“Ndio ninaye ila yupo nchini Tanzania kwa sasa”

“Ohoo ana itwa nani?”

“Mmmmm mbona ume muuliza”

“Kama ni vibaya nina omba unisamehe?”

“Hapana nilihitaji kujua kwa nini una muulizia”

“Ningependa kufahamu tu hilo”

“Anaitwa Latifa”

“Ahaa nashukuru kukufahamu”

“Samahani Ethan, ninaitwa Jonathan ni muandishi wa Madrid tv. Nina mahojiano mafupi na wewe, je tunaweza kuzungumza”

“Mmmm sawa. Xaviela samahani nina omba niweze kuzungumza kidogo”

“Hakuna tatizo”

Tukasoegea pembeni na muandishi huyu wa habari wa club hii. Kamera man akaanza jukumu la kunirekodi.

“Unajisikiaje kuhisiana na ushindi huu mkubwa kwanza wa club yako na wewe kufunga hat trick mbili mfululizo ikiwa ni rekodi ya pekee ambayo umeiweka katika kiwanja cha Barcelona.

“Ahaa…nina jisikia vizuri kwa kweli. Ni jambo kubwa sana kwenye maisha yangu. Sikutarajia kama tuna weza kutoka nyuma kwa goli tatu hadi kufikisha goli saba. Nina mshukuru Mungu kwa hilo”

“Je una waambiaje mashabiki wa Real Madrid kwa duniani?”

“Ninacho waomba waniamini, haijalishi ni magumu gani ambayo yanaweza kutokea katika msimu tunao kwenda kuuanza, ila waniamini”

Gafla nikajistukizia nikimwagiwa maji mwili mzima na Frendando.

“Happy birthday Ethan”

Frenando alinistua sana kwani hakika sikuweza kuikumbuka siku yangu ya kuzaliwa.

“Saa sita usiku sasa, siku yako ya kuzaliwa imesha fika”

Frenando alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Wachezaji wezangu wakajumuika kuungana na Frenando katika kunimwagia maji, pombe kali pamoja na vinywaji vingine.

“Hongera sana”

Kila mchezaji alinipongeza kwa jinsi alivyo hitaji.

“Jamani kukipambazuka sherehe ya Ethan ya siku yake ya kuzaliwa, itakuwa nyumbani kwake”

Frenando aliwatangazia watu jambo ambalo hakika sikuweza kujipanga.

“Wewe mimi mbona sija andaa chochote”

“Usijali Ethan, nilisha andaa watu wa kuandaa kila kitu katika sherehe yako. Wala usijali katika hilo”

“Kumbe bado una kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa?”

“Nitaachaje kukumbuka. Yaani katika watu ambao siwezi kusahau siku zao za kuzaliwa. Wewe, mama yangu na mke wangu”

“Hahaaa haya bwana nashukuru sana rafiki yangu. Ngoja nikabadilishe nguo”

“Sawa”

Nikaelekea katika vyumba ya kubadilishia nguo. Nikafungua kabati langu na kutoa taulo langu na kulishika mkononi.

“Hei”

Sauti ya Xaviela ikanistua sana na kunifanya nigeuke nyuma.

“Hei umefwata nini huku?”

“Ahaa…nili…nili nilikuona ulipo kuwa una kuja huku nikaona nikufwata labda nikahisi kwamba ume kasirishwa na swala la kumwagiwa maji”

“Hapana nimekuja kubadilisha nguo. Hapa nina hitaji kwenda kuoga.”

Xaviela taratibu akaanza kutembea kwa mwendo wa madoido hadi akanifikia sehemu nilipo simama.

“Ethan, nakuomba ninacho kwenda kukiomba kwako usinichukulie vibaya”

Xaviela alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa mahaba mengi. Akanishika tisheti yangu eneo la kifuani mwangu na kunivutia kwake, akataka kuninyonya lipsi zangu ila nikaukwepesha mdomo wangu.

“Tafadhali nakuomba nikaoge”

Nilizungumza huku nikirudi nyuma kidogo.

“Ethan moyo wangu umefunikwa na pendo lako. Tafadhali nina kuomba unikubalie”

“Nipe muda tafadhali nahitaji kwenda kuoga”

Baada ya kuzungumza hivyo nikaondoka na kuingia kwenye mabafu ya kuogea. Nikavua nguo zangu zote na kuanza kuoga huku moyoni mwangu nikiamini kwamba Xaviela amenipenda kutokana na umaarufu wangu pamoja na utajiri nilio nao.

Nguo hizi nikaziweka kwenye dustbin, kisha nikarudi katika chumba cha kubadilishia nguo na kumkuta Xaviela akiwa amekaa kwenye moja ya benchi huku akilia. Nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikasimama mbele yake.

“Hei una umwa?”

Taratibu Xaviela akanyanyua uso wake na kunitazama usoni mwangu.

“Ethan natambua kwamba utanichukulia mimi ni malaya. Ila ukweli ni kwamba nina kupenda sana Ethan. Moyo wangu unahisi maumivu makali sana kiasi cha kushindwa kuvumilia katika kushindwa kuacha kukupenda na kukueleza hisia zangu”

“Xaviela, ila nilisha kueleza kwamba nina mwanamke ninaye mpenda kwenye maisha yangu. Kwa nini unahsindwa kunielewa”

“Sawa, ila nipo tayari nipate japo hifadhi nje ya moyo wako. Niambie chochote Ethan kitakacho nifariji”

“Nikueleze nini ikiwa nina kuambia kwamba sina upendo nawe na sina hisia na wewe. Kwa nini niwe mnafki katika hili. Sihitaji kukutesa wala sihitaji kumtesa mwanamke ninaye mpenda”

Nilizungumza kwa msimamo huku nikimtazama Xaviela usoni mwake.

“Naomba unipishe nahitaji kuvaa”

Xaviela akanitazama kwa unyonge kisha akatoka ndani humu na kuniacha peke yangu. Nikavaa suti yangu kisha nikatoka ndani humu.

“Frenando”

“Ndio ndugu yangu”

“Nahitaji kuelekea nyumbani kuanza kuandaa sherehe ya kuzaliwa kwangu”

“Sawa kaka. Majira ya saa kumi nambili wale watu nilio wapa tenda ya kuandaa kila kitu watafika nyumbani kwako”

“Si wana vitambulisho kwa maana kwangu hawawezi kuingia pasipo vitambulisho”

“Ndio ni kampuni maalumu ambayo ina shuhulika na maswala ya uandaaji wa mashere”

“Sawa rafiki yangu, idadi ya waalikwa itakuwa ngapi?”

“Tutakuja kuzungumza, nikitoka nyumbani kwangu”

“Hakuna tatizo”

Nikaagana na wachezaji wezangu kadhaa kisha nikaondoka eneo hili. Nikafika katika eneo la maegesho ya magari, nikastuka sana baada ya kukuta gari langu katika eneo la kioo cha upande wa dereva likiwa limeandikwa maandishi mekundu yanayo sema I LOVE YOU ETHAN. Nikagusa herufi moja ya maandishi haya na kuinusa kidogo, nikastuka baada ya kugundua kwamba maandishi haya yameandikwa kwa kutumia damu. Nikatazama eneo zima la maegesho haya, hakuna mtu yoyote. Nikataka kufungua mlango wa gari langu ila moyo wangu kidogo ukasita, nikapiga hatua za umakini hadi nyuma ya gari langu na nikamkuta Xaviela akiwa amekaa huku ameliegemea gari langu. Pembeni yake kuna chupa ya pombe kali iliyo pasuliwa huku mkono wake wa kushoto ukiendelea kumwagikwa na damu.

“Xaviela ni nini unacho kifanya!!?”

Nilimuuliza Xaviela huku nikiwa nimejawa na mstuko mkubwa sana. Xaviela alinitazama kwa macho yaliyo mlegea, kisha taratibu akaanguka chini na kupoteza fahamu, kwani mwili wake umepoteza damu nyingi sana iliyo toka katika jeraha hilo la mkononi mwake.



Kwa haraka nikatoa simu yangu na kupiga namba ya dharura, uziri wa nchi hii vyombo vya usalama na wale wanao shuhulika na maswala ya afya wapo haraka sana kwenye humuda zao. Hazikuisha hata dakika tano, gari la wagonjwa likafika eneo hili na kuwafanya baadhi ya wachezaji wezangu kutoka ukumbini na kuja kushuhudia hili tukio.

“Amefanyaje?”

Frenando aliniuliza huku akimshangaa Xaviela anaye ingizwa kwenye gari la wagonjwa na kukimbizwa hospitalini. Nikawaonyesha watu jinsi alivyo lichora gari langu kwa kutumia damu yake.

“Kweli ana kupenda”

Frenando alizungumza huku akinitazama usoni mwake. Wachezaji wezangu pamoja na wake zao wakaanza kutawanyika na kurudi ukumbini. Nikataka kufuta maandishi haya ila roho ikasita kwani kwa jambo alilo lionyesha Xaviela hakika ni kubwa na halikuwahi kunitokea siku hata moja kwenye maisha yangu. Nikaingia ndani ya gari na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwangu. Haikunichukua dakika nyingi nikafika nyumbani kwangu, nikashuka kwenye gari langu na mwana mama ambaye nina ishi naye hapa kama mfanyakazi mkuu wa maswala ya usafi akanipokea koti langu la siti ambalo nimelishikilia mkononi mwangu.

“Bosi mbona kioo kina maandishi ya damu?”

“Ahaa musilisafishe gari liache hivyo hivyo. Asubuhi kuna watu watakuja kuandaa sherehe yangu ya kuzaliwa. Hakikisha una wasimamia vizuri, si unajua kwamba si kila mtu ni wa kumuamini”

“Sawa Ethan”

“Nipo chumbani”

Nikaelekea chumbani, kwangu na kujitupa kitandani. Hata sikujisumbua kuvua viatu, usingizi mzito ukanipitia na nikalala fofofo.

***

Mlio wa simu yangu ukanistua kutoka usingizini, nikajipapasa mifukoni mwa suruali yangu na kuitoa simu yangu. Nikakuta ni namba ya Frenando ndio anaye nipia.

“Hei Ethan bado umelala hadi sasa hivi?”

“Yaa ndugu uchovu”

“Hembu amka bwana. Mimi nipo sebleni kwako hapa.”

“Poa”

Nikakata simu huku nikitazama dirishani, nikashuka kitandani na kujikongoja hadi sebleni.

“Aisee hukubadilisha hata nguo?”

“Yaani wee acha tu, nimechoka si mchezo”

“Ehee nimekuja kukuletea list ya wageni nilio waalika. Ni wagani hamsini na tano na kila mtu ana mke wake”

“Sio mbaya”

“Wewe huna wageni wengine wa kuwaalika?”

“Hapana sina wageni. Huku bado sijajua na watu…..No nimekumbuka kuna mgeni mmoja nitamualika”

“Nani huyo?”

“Ni balozi wa Tanzania hapa Uingereza ana itwa Mzee Ngeleja”

“Ahaa sawa fanya hivyo basi. Ili tukisha submit hii listi kwa walinzi basi pale getini asi ruhusiwe mtu mwengine kuingia ndani humu”

“Ila ngoja kwanza nimpigie simu”

Nikampigia mzee Ngeleja, simu yake ikaita na baada ya muda mchache ikapokelewa.

“Habari za asubihi mzee”

“Salama tu Ethan. Tena afadhali umeniwahi, nilikuwa nina taka kukupigia simu muda si mrefu.”

“Ndio mzee wangu na kusikiliza”

“Visa imepatikana hivyo basi unaweza kumualika mchumba wako na akaja huku”

“Sawa basi nitawasiliana naye na mambo yote hayo nitakupatia email yake muweze kumtumia maelezo husika. Ilia ajiandae na safari”

“Sawa hakuna tatizo Ethan na hongera sana kwa uwezo mkubwa ulio uonyesha jana. Japo mimi ni mshabiki wa Liverpool ila kama Mtanzania mwenzako hakika nina jivunia juu ya uwepo kiwango chako”

“Nashukuru sana mzee wangu. Leo ni siku ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa hivyo nina kuomba kama huto jali basi uweze kufika nyumbani kwangu”

“Ohoo sawa sawa hakuna tatizo. Je sherehe ina anza muda gani?”

Nikamtazama Frenando na nikamuuliza kwa sauti ya chini na kwa ishara akanionyesha vidole kwamba ina anaza saa mbili usiku.

“Ina anza saa mbili usiku mzee”

“Basi nitafika hapo na mama yako. Ana hamu kubwa sana ya kukuona na nilivyo muambia kwamba wewe ni Mtazania alikataa, ila nahitaji uje kumdhibitishia kwamba wewe ni Mtanzania mwezetu”

“Haaaa sawa mzee wangu karibu sana”

“Nashukuru”

Nikakata simu na kumtumia mzee Ngeleja email ya Latifa. Nikampigia Latifa na kwa bahati mbaya simu yake haipo hewani.

“Mzee atakuja hivyo muingize kwenye list”

“Ana itwa nani?”

“Anaitwa Ngeleja”

“Mmm hili jina kweli ni la kiafrika”

“Kwa nini?”

“Ngeleja kwa watu wengine itawawia ugumu kulitaja”

“Yaa sijui kwa Tanzania ni kabila gani. Ila muandike.”

Tukasaidiana na Frenando kupanga mfumo mzima wa ratiba ya sherehe kisha nikamuacha sebleni na kuelekea chumbani kwangu, nikaoga na kubadilisha nguo nyingine. Wazo la kwenda hospitalini kumuona Xaviela likanijia kichwani.

“Frenando mwanangu hembu tuelekee hospitalini kumuaona yule dada wa jana”

“Mmmm kuna mambo bado sijayaweka sawa hapa ndugu na nikiondoka yatasimama. Wewe nenda kamuone si unatambua ile gari ni ya hospitali gani?”

“Ndio”

“Wewe nenda kamuone ila kuwa makini si unajua leo vyombo vya habari umevichafua wewe”

“Duu toka niamke sijaingia kwenye mtandao wa kijamii wala kusoma gazeti”

“Yaani asikuambie mtu ndugu yangu ume chukua head line ya vyombo karibia vyote hapa Spain na duniani”

“Itabidi nivae miwani na kofia ili isiwe ngumu kwa watu kukufahamu”

“Hapo umeongea pointi”

“Habari ya binti huyu ime tangazwa?”

“Sijaifwatilia, ila kwa pale hapakuwa na mtu aliye piga picha yoyote wala kurekodi lile tukio”

“Basi hakuna tabu”

Nikavaa kofia nyeusi pamoja na miwani. Kisha nikawasha gari na kuelekea katika hospitali aliyo lazwa Xaviela. Hadi nina ingia ndani ya hospitali hii hakuna mtu hata mmoja aliye weza kunifahamu kwa urahisi. Nikafika mapokezi na kumuulizia Xaviela. Nesi huyu akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akatupia macho yake kwenye tv kubwa iliyopo katika eneo hili na kutazama taarifa ya habari inayo husiana na mimi.

“Ethan”

Nikapata kigugumizi cha kumjibu nesi huyu. Kwa haraka nesi huyu akasimama na kutoka katika chumba alicho kaa na kunikumbatia. Akatoa simu yake na kuniomba niweze kupiga naye picha. Watu wengine walio gundua kwamba nipo hospitalini hapo, nao wakaanza kunisogelea na kuanza kuiomba nipige nao picha huku wengine wakioniomba niweze kusaini katika nguo zao wengine vitabu vyao. Nguvu hii ya mashabiki kunizunguka, ikawalazimu walinzi wa hospitali hii kuingilia kati na kuniondoa eneo hili la mapokezi. Nikaingizwa katika chumba cha kupumzikia na ulinzi mkali sana ukaimarishwa nje ya mlango huu.

Akaingia mwana mama aliye enda umri kidogo. Nikawaweza kumfahamu kwa haraka kwamba yeye ni daktari hii ni kutokana na koti lake alilo livaa.

“Habari yako bwana Ethan”

“Nashukuru sana”

“Ninaitwa dokta Maria. Mimi ndio daktari mkuu wa hii hospitali”

“Nashukuru kukufahamu dokta Maria. Kuna mgojwa wangu nimekuja kumtembelea ana itwa Xaviela sijui nina weza kumpata”

“Mmmm majina ya wagonjwa hao yapo mengi labda ana itwa Xaviela nani?”

“Kwakweli sifahamu jina lake la mbele ila nina mtambua kwa jila lake hilo moja tu”

“Je unajua tatizo la ugonjwa wake, labda tumtafute kwa kutumia mfumo huo?”

“Jana alijikata mkononi mwake kwa chupa katika ukumbi wetu wa Club kule”

“Ahaa nimemfahamu huyo binti. Twende nikupeleke”

Tukatoka katika chumba hichi na walinzi karibia sita wakatuweka katikati ili asitokee shabiki yoyote akanigusa. Waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma kuhakikisha wana pata cha kuandika. Umaarufu wangu hakika ume ongezeka mara dufu. Nikaingia katika chumba kilicho tulia sana. Nikawakuta wazee wawili ambao kidogo umri wao umekwenda kwenda. Nikamshuhudia Xaviela akiwa ame lala kitandani huku akiwa ametundikiwa dripu la maji pamoja na dripu la damu.

“Karibu sana”

Mama huyu alitukaribisha, huku wote wakinitazama usoni mwangu.

“Tunashukuru. Huyu ana itwa Ethan, amejitambulisha ni rafiki wa mtoto wenu”

“Wewe ndio kijana uliye mfanya atake kujitoa maisha yake kwa ajili ya kumkataa?”

Mzee huyu alinikoromea huku akinifwata sehemu nilizo simama. Dokta Maria ikamlazimu kusimama mbele yangu na kumzuia mzee huyu.

“Mzee wangu kumbuka mupo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi hivyo nakuomba uweze kutuliza jazba.”

“Ethan….Ethan”

Sauti ya Xaviela aliye kuwa ame lala ikatufanya sisi sote kumtazama. Mama yake kwa haraka akamsogelea na kuanza kumtazama kwa ukaribu.

“Xaviela mwanangu. Mama yako nipo hapa”

Mama huyu alizungumza kwa sauti ya upole sana.

“Ethan mama, Ethan mama anitaki”

Xaviela alizungumza pasipo kuniona. Taratibu nikaanza kusogelea kitanda hichi. Xaviela akanitazama kwa unyonge kisha akaanza kutabasamu. Nikaka katika kiti cha pembeni yake na kumtazama usoni mwake.

“Hei”

Nilimuita Xaviela kwa sauti ya upole.

“Umekuja Ethan”

“Yaa una jisikiaje?”

“Uwepo wako tu hapa umenifanya nijisikie amani moyoni mwangu”

Xaviela alizungumza kwa sauti iliyo jaa mahaba mazito. Nikatupia jicho la kuiba kwa baba yake na kumuona jinsi alivyo fura kwa hasira.

“Vipi ume kula”

“Mmmm bado”

“Kama kuna chakula jamani nina ombeni ili niweze kumlisha”

Mama Xaviela akaniwekea chakula cha kutosha kwenye kibakuli na taratibu nikaanza kazi ya kumlisha binti yao ambaye anaonekana kujawa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Xaviela akanipa ushirikiano mzuri sana wa kula chakula hichi hadi aka maliza.

“Asante Ethan”

“Asante nawe pia. Hakikisha hufanyi jambo ulilo lifanya leo”

“Siwezi hakika uwepo wako kwangu ume nipa furaha kubwa sana mayoni mwangu. Ninakupenda sana Ethan, sitamani kuwa mbali nawe”

“Usijali, kuanzia hivi sasa nitakuwa nawe karibu”

“Kweli”

“Haki ya Mungu”

Tartaibu Xaviela akanikumbatia na pasipo kujali uwepo wa wazazi wake, akaninyonya lispi taratibu. Sikutaka kukataa kwani hi jambo ambalo linge wakasirisha wazazi wake.

“Kijana nahitaji kuzungumza na wewe”

Mzee huyu alizungumza kwa sauti ambayo bado ana onekana ana hasira na mimi. Nikanyanyuka kwenye kiti na kumfwata nje mzee alipo elekea. Tukasimama kwenye kordo hii liyo jaa walinzi ambao wana hakikisha kwamba hakuna shabiki anaye ingia kwenye eneo hili la vyumba vya wagonjwa mahututi.

“Kijana naomba unisikilize”

Mzee huyu alizungumza kwa jazba.

“Binti yangu ni mmoja tu na ndio mtoto pekee niliye naye na ninampenda kuliko hata ninavyo mpenda mwanangu. Hivyo kwa kitendo ambacho umemfanyia ni lazima ulipe”

“Nilipe. Nilipe kiasi gani?”

“Sitaki pesa zako kijana. Nina pesa nyingi kuliko wewe. Na usijione umaarufu wako ukautumia kama fimbo ya kumchapia mwanangu kwako. Umenielewa?”

“Nakuelewa mzee”

“Sasa nataka umueo mwanangu na uhakikishe kwamba una mpa raha katika maisha yake la sivyo maisha ya hapa Spain utayaona machungu sana”

Nikamtaza baba Xaviela kwa mcho makali sana kwa maana anacho kizungumza sidhani kama ame kielewa vizuri.

“Unanitishia au?”

“Sikutishii ila nina kueleza ukweli. Kwa ujinga wako umepelelekea mwangu kutaka kujiua. Hilo siwezi kuliruhusu litokee tena na garama zote za ndoa niachie hatuhitaji pesa yako yoyote sawa”

“Mzee nahisi utakuwa umekosea”

“Nini?”

“Ndio umekosea. Mimi ni kijana ninaye jiamini, na siwezi kufanya mambo kwa kushinikizwa. Swala ni hivi sina hisia za kimapenzi na mwanao na wala simpendi mtoto wako. Kama atakufa eti kwa ajili ya kunikosa mimi acha afe na kama ata ishi basi acha aishi ila huo upuuzi na unao uzungumza masikioni mwangu. Usirudie tena kuuzungumza sawa”

Maneno yangu yakaufanya uso wa baba Xaviela kujaa mikunyo mingi ya hasira. Akarusha kofi, nikalikwepa na nikaanza kuondoka eneo hili kwa kujimini sana na hata hamu ya kurudi katika chumba alicho lazwa mwanaye ikaniishia.


Nikaishusha kofia yangu vizuri na ikaficha uso wangu kwa kiasi kidogo na nikaanza kutembea huku walinzi wa hospitali hii wakiwa wameniweka katikati. Mashabiki wa na waandishi wa habari ambao walikuwa wakinisubiria eneo la nje, hawakusita kunifwata huku mashabiki wengi wakiniomba niweze kusaini kwenye tisheti zao pamoja na daftari zao. Walinzi walipo ona vurumai la mashabiki limekuwa kubwa sana, wakanisindikiza hadi kwenye gari langu na nikaondoka hapa huku akilini mwangu nikimfikiria sana baba Xaviela. Nikafika nyumbani kwangu na sikuzungumza na mtu yoyote, moja kwa moja nikaelekea chumbani kwangu. Haikupita hata dakika moja, mlango wangu ukagongwa.

“Nani”

“Frenando”

“Ingia”

Frenando akaingia ndani humu na akasimama mbele yangu huku akionekana kunichunguza vizuri usoni mwangu.

“Mbona umekasirika huku utokapo ni kwema?”

“Kwema kiasi”

“Kuna jambo gani lime kukumba?”

“Baba Xaviela amenikera sana.”

“Baba ya yule mtotpo?””

“Ndio”

“Kwa nini akukere”

Nikamuelezea Frenando kila kitu kilicho tokea. Frendando akatoa simu yake na kutafuta familia ya Xaviela akasoma maelezo ya familia yake kisha akanionyesha picha ya mzee huyo.

“Ni huyu?”

“Ndio”

“Ni waziri wa mambo ya uhamiaji hapa Spain ila asikutishe kwa maana kila raia wa hii nchi, awe muhamiaji halali au mzawa ana misingi wa kuistaki serikali au kiongozi yoyote wa serikali endapo pala atakapo onewa au kunyanyapaliwa kwa rangi. Hivyo endapo atakwenda mbali zaidi, basi nitakuonyesha makampuni bora ya wana sheria na utawapatia kesi yako na nina imani utafanikiwa kushinda”

“Nashukuru ndugu yangu”

“Maandalizi ya sherehe yamekwenda vizuri na watu wote nilio waalika wameniahidi kuweza kufika”

“Asante ndugu yangu.”

Hadi inafika usiku maandalizi yote yakawa yamekwisha huku shuhuli iliyo bakia ni juu ya wageni kuweza kufika. Marijara ya saa moja usiku waalikwa wakaanza kufika kwangu huku mimi na Frenando tukiwa na kazi ya kuwaokea. Wageni waalikwa walipo fika wote, akiwemo balozi wa Tanzani nchini hapa Spain, shuhuli ikaanza rasmi. Muendesha sherehe huyu akajitahidi kwenda na ratiba na watu wote wakaendelea kusherekea siku yangu hii ya kuzaliwa.

“Hei Ethan”

Nilistuka sana kumuona Xaviela akiniita, kwani hali niliyo mkuta nayo asubuhi hospitalini, hakupaswa kuwepo hapa. Nikamshika mkono na tukasimama eneo ambalo hakuna watu wanao weza kutusikiliza mazungumzo yetu.

“Umefwata nini hapa ikiwa una umwa?”

“Ethan nimetoroka hospitalini kwa ajili yako. Nina kupenda na sijajisikia vizuri maneno mabaya ambayo baba aliyazungumza mbele yako”

“Usijali katika hilo, ila nina kuomba uweze kurudi hospitali tafadhali. Natambua kwamba baba yako ana cheo kikubwa sana serikali, ninaogopa akanisababishia matatizo ikiwa ndio kwanza nimeanza maisha yangu ya soka”

“Ethan tafadhali, baba yangu hata aseme nini hato weza kufanya chochote juu yako. Nilisha muambia endapo atakudhuru basi hakika na mimi nitakufa akishuhudia”

“Hayo ni maneno Xaviela ila nina kuomba sana urudi hospitalini”

“Siwezi kurudi”

“Kwa nini?”

Nilizungumza kwa hasira kidogo huku nikimkazia Xaviela macho. Xaviela akanikumbatia kwa nguvu na akaanza kuangua kilio.

“Nakupenda Ethan, nakuhitaji Ethan”

“Ohooooo……!!!”

Nilizungumza huku nikishusha pumzi taratibu.

“Ethan nikiondoka hapa nyumbani kwako, haki ya Mungu nina kuapia nitajiua tu na hii ndio itakuwa ni siku yako ya mwisho kuniona”

Xaviela aliendelea kuzungumza huku akilia kwa uchungu sana. Nikawaza kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama usoni mwake.

“Xaviela”

“Mmm”

“Una nipenda?”

“Ndio”

“Nakuomba ukachukue chumba kwenye hoteli yoyote hapa Madrid, nitalipia kwa njia ya mtandoa. Nisubirie hapo hadi sherehe itakapo kwisha, nitakuja kulala na wewe”

“Kweli Ethan”

“Ndio”

“Basi hakuna haja ya wewe kulipia. Nina pesa ya kufanya hivyo. Nitakutumia ujumbe wa meseji pale nitakapo pata hiyo hoteli”

“Nashukuru kwa hilo Xaviele”

Xaviela akanibusu shavuni mwangu kisha kisha akaanza kukimbilia eneo la maegesho ya magari. Nikabaki nikimtazama binti huyu kwa jinsi alivyo data kwa upendo wake kwangu.

“Kichaa huyu”

Nikarudi na kujumuika na wageni waalikwa kwenye sherehe. Baada ya dakika kumi na tano meseji ikaingia kwenye simu yangu.

‘Nimepata hoteli nakuomba uweze kuja, nipigie nikuambie ni hoteli gani’

Ujumbe huu ukanifanya nishushe pumzi huku nikimtazama Frenando anaye endelea kuburudika katika na wachezaji wengine. Nikamfwata Frenando na kumnong’oneza sikioni mwake, tukapandisha gorofani.

“Kaka nina matatizo”

“Matatizo. Matatizo gani mengine?”

Nikamuonyesha Frenando meseji hii akaisomoa na kunitazama usoni.

“Imetoka kwa nani?”

“Kwa yule binti wa jana aliye jiumiza na kupakaza damu kwenye gari langu”

“Weee si umetoka kuniambia kwamba yupo hospitalini na hali yake uliikuta ikiwa ni mbaya?”

“Ndio ila ametoroka na ameingia hapa nyumbani pasipo mualiko wa mtu yoyote”

“Mmm nahisi kuna mbinu ameitumia kwa maana ulinzi ni mkubwa sana nilio uweka”

“Yaa ila tuachane na hilo. Ameniomba niweze kufika hotelini alipo”

“Isije ikawa ni mtego ndugu yangu na kesho ukajikuta upo kwenye scendo, kwani toka uje hapa Spain magezeti yanauza kutokana na habari zako”

“Ila ameniambai kwamba nisipo kwenda itakuwa ndio mara ya mwisho mimi na yeye kuonana”

“Bora iwe hivyo kaka”

“Maana ya yeye kusema hivyo ni kujiua”

“Mmmmm!!!”

“Yaani hapa nilipo ndugu yangu sijui hata nifanye nini nina hisi kuchanganyikiwa kabisa”

“Nenda kaonane naye”

“Alafu?”

“Uwe makini, ila mpigie kwanza”

Nikampigia Xavila kwenye simu yake.

“Hei”

“Niambie Ethan wangu”

“Upo hoteli gani”

Xaviela akanitajia jina la hoteli hiyo na kwa bahati nzuri nina ifahamu.

“Basi sherehe ikiisha nitakuja”

“Sawa nakusubiria kwa hamu”

Nikakata simu, tukaendelea na sherehe na ilipo isha na waalikwa wote kuondoka nyumbani kwangu. Tukaondoka nyumbani hapa na Frenando pamoja na mke wake, wakanifikisha hadi kwenye hoteli aliyo lala Xaviela.

“Kuwa makini kaka”

“Usijali ndugu yangu. Shemeji nashukuru sana kwa kujitoa kwenu hakika mumefanya jambo ambalo hakika sinto lisahau kwenye maisha yangu”

“Usijali shemeji, tupo kwa ajili yako”

“Nafurahi kwa kusikia hivyo. Frenando niwatakie usiku mwema na safari njema rafiki yangu”

“Nashukuru nawe pia burudani njema”

Maneno ya Frenando yakanifanya nishuke kwenye gari lao huku nikiwa nina cheka. Nikaanza kuingia ndani ya gari hoteli hii kubwa ya kitali. Kutokana nimevaa kofia na miwani kubwa kiasi hakuna muhudumu aliye weza kunifahamu, nikaingia moja kwa moja kwenye elevator(lifti) na moja kwa moja nikapandisha hadi gorofa ya ishirni na tano. Nikatembea kwenye kordo hii ndegefu hadi kwenye chumba namba elfu sita na moja. Nikagonga na baada ya sekunde kadhaa ukafunguliwa.

Xaviela akasimama mbele yangu huku akiwa amevalia taulo lillo acha sehemu kubwa ya mapaja yake kuwa wazi. Macho malegevu anayo nitazama nayo hakika yakanifanya niishiwe pozi kabsia. Akanishika kifuani mwangu na kwa kutumia tisheti yangu akanifuta ndani ya chumba hicho na mlango ukajifunga.

Xaviela hakuhitaji kunipa hata nafasi ya kuzungumza, wala kumuuliza ana endeleaje. Akaanza kuniyonya lispi zangu kwa ndimi yake ambayo ni laini sana na iliyo jaa msisimko mkali sana wa kimabaha.

Jogoo wangu hakusita kusimama, ila nilipo kumbuka kwamba binti huyu asubuhi ya siku ya leo alikuwa ni mgonjwa sana. Kengele ya hatari ikalia kichwani mwangu na kujikuta nikimuachi taratibu huku nikimtazama usoni mwake.

“Hei”

“Nashukuru kwa kuja Ethan”

“Yaa nahitaji tuzungumze”

“Nini una hitaji tuzungumze”

“Niachie kwanza”

Taratibu Xaviela akaniachia, kitu kilicho nichanganya ni pale alipo liachia taulo lake hili na akabaki kama alivyo zaliwa. Maziwa yake yaliyo simama sawia hakika yakaufanya mwili wangu wote kujawa na msisimko mkali sana.

“Ehee zungumza Ethan wangu”

Xaviela alizungumza huku akinisogelea, nikaushika mkono wake na kutazama sehemu aliyo jikata kwa chupa. Bandeji alilo fungwa eneo hili, likanifanya nishindwe kutambua ukubwa wa kidonda hicho.

“Kwa nini uliamua kujikata kwa chupa?”

Niliuliza swali hili ili kuifukuza hali ya kimapenzi ambayo imenitawala kisawa sawa kwenye mwili wangu.

“Ethan kwenye maisha yangu nimekata tamaa kabisa. Nina jisikia hamu ya kujiua, nilikuwa ninataka kujiau. Ila nilipo kuona wewe nikapata matumaini ya kuendelea kuishi. Ulipo nikataa kimapenzi hali ya kujiua ikanitawala na kufanya vile nilidhamiri kabisa nife ili usinione tena”

Xaviela alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nini kinacho kufanya utamani kujiua?”

“Miezi kadhaa iliyo pita nilimpoteza mpenzi wangu niliye mpenda sana”

“Pole sana, alikuacha?”

“Hapana alifariki kwa ajali ya gari hivyo kuanzia hapo nimekuwani mtu mnyonge na wa kukata tamaa. Siku ambayo ninakuja kwenye sherehe yenu nikiwa na rafiki yangu. Nilipo kuona wewe moyo wangu ulisikia ubaridi ambao sikuwahi kuuona kwenye maisha yangu”

“Nilijizuia nikashindwa, na niliamua kukueleza ukweli kwamba nina kupenda sana Ethan”

Nikakichunguza chumba hichi kwa umakini sana na nilipo hakikisha kwamba hakuna kamera yoyote inayo rekodi matukio ya humu ndani nikajitupia kitandani huku nikimtazama Xaviela ambaye muda wote huo yupo kama alivyo zaliwa.

Xaviela akapanda kitandani hapa huku akiniendelea kunitazama kwa macho yaliyo legea. Akanikalia mapajani mwangu na taratibu tukazikutanisha lipsi zetu. Tukaanza kunyonyana huku macho yetu tukiwa tumeyafumba kwa hisia kali sana. Xaviela akanivua tisheti yangu kisha akanivua suruali yangu na nikabakiwa na boksa tu. Nikavua miwani na kofia na kuvitupia pembeni. Nikaanza kumnyonya binti huyu kila kona ya mwili wake. Nikamlaza chali kitandani, nikaipanua miguu yake na kuanza kunyonya kitumbua chake na kumfanya atoo kelele za mayowe ya kimahaba. Nilipo hakikisha kwamba ame legea kisaswa sawa, nikaingia mkono wangu wa kulia ndani ya boksa yangu ili kumtoa jogoo wangu aliye jiandaa tayari kwa mashambulizi. Gafla mlango ukaanza kugongwa kwa nguvu na kutufanya sote tukurupuke.

“Xaviela fungua. Mimi baba yako nimekutafuta sana mwanangu hadi nimetoa taarifa polisi ya kupotea kwako”

Macho yakatutoka huku mapigo ya moyo wangu yakinienda kasi kiasi cha kunifanya nitamani ardhi ya eneo hili ipasuke na inimeze kwani kama ni fumanizi basi hili litakuwa ni fumanizi kubwa sana kwenye maisha yangu na litanizalilisha katika vyomba vya habari hapa Spain na duniani kote



“Tunafanya nini?”

Nilimuuliza Xaviela huku mwili mzima ukinitetemeka kwa woga. Xaviela akakosa hata cha kunijibu zaidi ya kuzunguka zunguka ndani humu. Nikavaa nguo zangu kwa haraka, nilipo hakikisha kwamba nipo vizuri nikachungulia chooni ili niweze kuona kama kuna sehemu ya kujificha, ila ubaya hakuna sehemu ambayo nitajificha na kushindwa kuonekana. Jinsi umlango unavyo endelea kugongwa ndivyo jinsi tunavyo zidi kuchanganyikiwa. Nikafungua dirisha la chumba hichi na kuchungulia nje, umbali wa kutoka hapa juu nilipo hadi chini, endapo nitajirusha basi kitendo hicho kitapelekea kuwa huo ndio mwisho wa maisha yangu au nivunjike vunjike vipande vipande ambavyo vitanifanya nishindwe kucheza mpira maisha yangu yote.

“Ingia chini ya kitanda”

Xaviela alainishawishi, kwa haraka nikachungulia chini ya kitanda na nikaona nafasi ambayo ninaweza kuingia na kujibanza vizuri. Sikuhitaji kupoteza muda, nikaingia chini ya kitanda na kijikausha kimya. Baada ya sekunde kadhaa nikasikia sauti ya baba Xaviela akimfokea mwanaye ni kwa nini ametoroka hospitalini.

“Upo na nani humu ndani?”

“Peke yangu baba”

“Peke yako, muda wote ulikuwa una fanya nini ushindwe kufungua mlango?”

“Baba nahitaji kupumzika, sitaki kurudi hotelini na hawa polisi wako ulio ingia nao humu ndani sitaki niwaone. Tokeni”

Xaviela alizungumza kwa kufoka. Kijiupenyo kidogo cha shuka ambalo limegusa ardhini likitokea kitandani, nikashuhudia askari hao wakitoka ndani humu. Xaviela akabaki peke yake na baba yake.

“Mwanangu kwa nini una nipa wasiwasi. Unajua ni jinsi gani ninavyo kupenda. Hembu tazama hali yako, tafadhali twende nyumbani”

“Baba”

“Naam”

“Fika unatambua kwamba ninahamu ya kufa”

“Ndio natambua mwanangu”

“Hivyo nahitaji kuwa peke yangu. Jinsi unavyo endelea kunisumbua na kunifwatilia mambo yangu, nitajiua mimi. Nitakufa na utashuhudia maiti ya mwili wangu mbele yako”

“Usiongee hivyo Xaviela mwangu. Unataka nibaki peke yangu, unataka nimpende nani zaidi yako mwangu.”

“Kwa nini Ethan aliondoka hospitalini pasipo kuniaga”

“Yule mwana haramu achana naye. Hana hadthi ya kuwa na mwanamke mzuri kama wewe. Sitaki uwe na mahusiano na kinana mweusi. Ataharibu sifa na rangi ya wajukuu wangu ambao ninataka wawe”

Maneno ya baba Xaviela yakanifanya nishushe pumzi taratibu. Kwenye maisha yangu toka nilipo kuwa mtoto, nimepitia maisha ya ubaguzi wa rangi.

“Baba toke nje”

“Xaviela”

“Nimesema toka nje baba na sitaki nikuonea tena kwenye maisha yangu. Una mdharau mwanaume ninaye mpenda. Mwanaume anaye nifanya niishi kwa ajili yake. Na kuanzia sasa usinitafute baba nakuchukia nakuchukia”

Xaviela aliendelea kulalama kwa hasira huku akilia kwa uchungu mwingi sana.

“Wewe ni mwanangu na nina mamlaka juu yako. Huwezi kuniletea mambo ya kujinga nikakutazama. Ingieni ndani”

Nikashuhudia miguu ya watu kama wanne wakiingia ndani humu. Nikasikia kelele za Xaviela akiomba aachiwe na baada ya sekunde kadhaa nikasikia ukimya.

“Hiyo sindano ya usingizi itachukua masaa mangapi hadi aamke?”

“Masaa sita mkuu”

“Sasa safari iwe moja kwa moja hadi uwanja wa ndege. Hakikisheni kwamba anafika Marekani akiwa hajitambui, kila mutakapo ona dalili ya kuzinduka kwake basi mchomeni sindano ya usingi”

“Sawa mkuu”

“John wewe utabaki hapa kuna kazi nina hitaji nikupatie”

“Kazi gani”

“Kuna huyu mwana haramu amesajiliwa na timu ya Real Madrid. Nataka uhakikishe kwamba muna msababishia ajili ambayo itamuondoka hapa duniani sawa”

Nikastuka sana kwa kusikia mazungumzo haya. Mwili ukazidi kutetemaka, nikashindwa hata nianzie wapi katika jambo hili.

“Sawa mkuu”

“Hii itakuwa ni siri, na endapo utafanikiwa kumuua kwa ajali. Toweka hapa Spain haraka iwezekanavyo”

“Nimekuelewa mkuu”

“Haya twendeni”

Nikasikia mlango ukifungwa, nikasubiri kama dakika tano hivi. Nilipo ridhika kwa ukimya uliopo ndani humu, nikatoka uvunguni humu huku nikiwa na wasiwasi mwingi sana. Nikakaa kitandani huku nikitafakari maneno ya mzee huyu na kijana wake ambaye sijamuona sura yake.

‘Ethan ni nini hichi’

‘Usiogope vita yake huyu inaisha mapema sana’

Etthan alizungumza huku akiwa amekaa kwenye moja ya kiti.

‘Sasa ni nini ambacho tutafanya’

‘Ipo hivi, ili kumuondoa kabisa kwenye madaraka yake na kumpeleka jela moja kwa moja. Nitabadilisha sura yangu na kuwa sura yako. Nitatumia gari lako na kutokana wamepanga kukuua, endapo watakugonga na lori basi itakuwa ni mwanzo wa kuianza kesi yako ya kumstaki yeye”

“Nitamstaki vipi ikiwa sina kidhibitisho kwamba yeye ndio kafanya?”

Ethan akanirushia simu. Nikaona faili la audio, nikalifungua na nikaanza kusikia mazungumzo ya mzee huyu akibishana na mwanaye hadi alipo toa kazi ya kuuwawa kwangu.

“Hicho ndio kidhibitisho cha kumfunga yeye na kumuangamiza kabisa”

“Sawa nashukuru kwa hilo rafiki yangu”

“Wala usijali ndio jukumu langu”

Tukatoka hotelini hapa mimi na Ethan, pasipo mtu yoyote kufahamu kwamba nilikuwepo kwenye hoteli hii. Kwakutumia usafiri wa taksi ya kukodi nikarudi nyumbani kwangu, huku nikimfikiria mzee huyu ni kwa nini amejawa na chuki kubwa sana juu yangu.

Alfajiri na mapema Ethan akafika nyumbani kwangu. Akachukua fungua ya gari langu moja la kifahari.

“Leo usitoke kabisa nyumbani kwako”

“Kwa nini?”

“Hili ninalo kwenda kulifanya litatingisha ulimwengu”

“Usije ukafanya nimeonekana nimekufa?”

“Hapana huto kufa ila ni kazi ya kumtowesha huyu mzee. Kaa vizuri kwenye tv yako”

“Sawa”

“Walinzi wako nitawaaga kwamba nina kwenda mazoezini”

“Haya.”

Ethan akaondoka na kuniacha ndani humu. Nikamshuhudia akitoka getini na gari langu aina ya BMW. Hapakuwa na mlinzi wangu aliye mgundua kwa maana amebadilika na kuwa katika sura yangu. Kitu nilicho gundua ni kwamba Ethan ameondoka na simu yangu na kuniachia simu ambayo alinikabidhi jana usiku. Simu hiyo ikaanza kuita, nikaitazama vizuri na kufahamu ni simu yangu.

“Vipi mbona umeondoka na simu yangu?”

“Nimefanya hivyo ili kuzidi kuweka udhibitisho wa hili tukio. Kuna gari nyeusi ndogo ina nifwatilia nyuma yangu.”

“Ni gari ya kina nani?”

“Hawa watu”

“Kuwa makini”

“Natambua ni wapi watakapo nivamia ila usijali”

Ethan akakata simu na kuniacha katika alama kubwa ya kujiuliza. Nikawasha tv huku nikijaribu kusubira habari hiyo kwa umakini sana. Baada ya dakika kumi na mbili. Habari ya dharura ikaanza kutangazwa kutoka katika kituo cha habari cha taifa kikionyesha habari ya mimi kupata ajali kubwa ya gari huku gari yangu ya garama ikiwa imepondeka pondeka vibaya sana.

Nikashusa pumzi huku nikiendea kuona waokoaji wakifanya juhudi za kuhakikisha kwamba wana niokoa kutoka ndani ya gari langu. Nikamshuhudia Ethan akichomolewa ndani ya gari hilo huku akiwa hoi bin taabani.

Nikachungulia dirishani na kuona gari mbili za walinzi wangu zikitoka kwa kasi na nina imani wana elekea eneo la ajali ilipo tokea.

‘Kazi kweli kweli’

Nilijisema kimoyo moyo huku nikitazama jinsi Ethan anavyo ingizwa ndani ya gari na kukimbizwa hospitalini. Nikaanza kubadilisha cheneli za tv na kila kitua ninacho fungua habari yake kina elezea juu ya ajali yangu huku wengi wao wakisema. STAR MPYA WA MADRID APATA AJALI MBAYA SANA.

Baada ya dakika kumi hivi, vyombo vya habari vikaripoti hospitali niliyo pelekwa. Mashabiki wengi sana wakiungana na waandishi wa habari wakajitokeza katika hospitali hiyo huku wakiwa na mashada ya maua pamoja na makadi makubwa. Wengi wao tayari wamesha shapisha tisheti na mabango wakiniombea niweze kupona.

‘Kazi imekwisha’

Ethan alitokea humu ndani huku akinitazama usoni mwangu’

‘Ehee imekuwaje?’

‘Sasa hivi mwili huo wa bandia upo katika chumba cha upasuaji. Hapa madaktari wanajitahidi kuyastua mapigo yako ya moyo’

‘Tunaweza kwenda?’

‘Yaa ndio nimekuja kukuchukua’

Ethan akanishika mkono. Kufumba na kufumba, sote wawili tukatokea katika chumba cha upasuaji. Nikawaona madaktari jinsi wanavyo jitahidi kuyastua mapigo yangu ya moyo kwa kutumia mashine maalumu. Nikatazama mashine ya mapigo ya moyo na nikayashudia yakiwa katika asilimia sifuri.

‘Si watasema nime kufa?’

‘Ngoja kwanza’

Ethan alizungumza huku madaktari hawa wakizidi kujitahidi kustua mapigo ya mwili. Walipo anza kutingisha vichwa wakiamini kwamba nimekufa. Ethan akaingia katika mwili huo na mashine ya mapigo ya moyo taratibu ikaanza kupandisha mapigo ya moyo.

Madaktari wote wakashangaa mara baada ya kumuona Ethan anaye fanana na mimi amefumbua macho. Ethan akakaa kitandani na kuzidi kuwashangaza madaktari.

“Nipo wapi hapa?”

Ethan aliwauliza na madaktari wakamuomba aweze kulala kidogo.

“Nipo wapi?”

“Upo hospitali ni muda mchache ulipata ajali”

“Nimeumia?”

“Tumekupa kwanza huduma ya kwanza na baada ya hapo tutahakikisha kwamba tuna kufanyia vipimo vya X ray ili tuweze kujua kama kuna eneo lenye tatizo”

Daktari mmojaa lizungumza na kumfanya Ethan kutingisha kichwa akionyesha kukubaliana na wazo hilo. Ethan akaniita na nikasogea katika kitanda hicho na hapakuwa na daktari yoyote aliye weza kuhisi uwepo wangu. Ethan akaniomba nilale hapa kitandani na nikafanya hivyo huku yeye akijitoa kitandani hapa na kusimama pembeni.

“Mapigo yake ya moyo yamerudi kama kawaida, tunaweza kumpeleka chumba cha X ray”

Daktari mwengine alishauri, wakanitoa chumbani hapa. Nje ya chumba hichi nikakuta baadhi ya wachezaji wezangu pamoja na walinzi wangu wakiwa wana subiria kupata taarifa ya madaktari.

“Hali yake ipo vipi?”

Kocha alimuuliza daktari mmoja huku kitanda nilicho lazwa kikiendelea kusukumwa.

“Tutawapa taarifa kamili ila kwa sasa tunaomba mutupe nafasi ya kuifanya kazi yetu”

Nikaingizwa kwenye moja ya chumba, nikalazwa kwenye mashine maalumu ambayo hata siifahamu inaitwaje. Uzuri ni kwamba mwili wanao ufanyia X rays ni mwili wangu halisi ambao haujaumia. Wakaanza kunifanyia vipimo vyao na madaktari wote wakabaki wakiwa wameshangaa. Kwani hakuna hata mfupa mdogo ambao umevunjika.

“Hili haliwezekani, rudieni tena”

Wakarudia zaidi ya mara tatu kunifanyia vipimo hivyo vya X rays na hawakuweza kuona kitu chochote.

“Ikiwezakana nina omba muniruhusu nirudi nyumbani kwangu”

“Hapana kwa leo utakaa hapa hospitalini ili kuendelea kuichunguza afya yako. Kunaweza kutokea mabadiliko yoyote usiku ikawa ni tatizo”

“Ni kweli Ethan inabidi iwe hivyo. Tupe nafasi nyengine ya kuendelea kuichunguza afya yako kwa maana jinsi picha ya gari inavyo onyesha ilivyo pondeka hadi sasa hatuamini kama hakuna jambo lolote baya ambalo limeweza kutokea mwilini mwako.”

“Sawa kazi ni kwenu, ila musiwaeleze mashabiki chochote juu ya hali yangu. Ila wachezaji wezangu ninaomba muweze kuwapatia taarifa”

“Usijali tutafanya hivyo”

Nikatolewa katika chumba hichi na kupelekwa kwatika chumba cha kupumzikia. Wachezaji wezangu wakanitembelea na kunijulia hali. Baadhi yao hawakusita kupiga picha zikionionyesha kwamba nipo salama na kuwatoa hofu mashabiki. Mkuu wa polisi wa jiji hili la Madrid akafika katika chumba changu kwa ajili ya kunihoji maswali mawii matatu.

“Ajali inaonyesha lori ndio lilikufwata na kukugonga. Upelelezi unazidi kuonyesha kwamba ajali hii ni ya kupangwa na si yakawaida au bahati mbaya. Je unaweza kujua ni nani ambaye yupo nyuma ya ajali hii ili tuweze kumshuhulikia?”

“Ndio nina mfahamu”

Mkuu huyu wa polisi pamoja na kocha wakastuka kidogo kwani hawakutarajia kama ninaweza kumfahamu muhusika aliye nisababishia ajali hii.




“Aha…bwana Ethan una weza kuniambia ni nani huyo ambaye yupo nyuma ya hili tukio?”

“Sinto weza kulizungumza, nikiwa hapa kitandani. Ila nitahitaji ulimwengu mzima uweza kufahamu ni nani ambaye yupo nyuma ya hili tukio”

“Una maanisha nini?”

“Wewe ni mkuu wa polisi. Agiza vijana wako kufanya upelelezi katia hili tukio la sivyo nita uwawa hata nikiwa hapa hospitalini”

Mkuu huyu wa polisi akatazamana na kocha kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa na kukubaliana na kile nilicho mueleza.

“Sawa hii ni kadi kadi yangu, namba zangu za simu zote zipo hapo. Ukiwa tayari utawasiliana nami”

“Nashukuru”

Mkuu huyu wa polisi akatoka chumbani hapa na kuniacha na kocha.

“Ethan una mfahamu kweli msababishaji wa ajali hii?”

“Ndio kocha”

“Ni nani?”

“Usijali nitakuambia pale muda utakapo fika”

“Inabidi ulinzi uzidi kuimarishwa kwako”

“Usijali katika hilo kocha. Nipo fiti na mechi ya kwanza kwenye ligi nina weza kucheza”

“Una uhakika?”

“Ndio kocha nina uhakika, nina weza kucheza mechi ya kwanza”

“Basi tutaangalia ripoti ya madaktari wa hapa na madaktari wa timu watakapo ridhika juu ya afya yako basi nitakupanga kwenye kikosi cha kwanza kitakacho kwenda kupambana na watani wetu Atletico Madrid.”

“Sawa kocha”

Kocha akaniaga na kutoka ndani hapa na nikabaki na Ethan.

“Ukiruhusiwa kutoka hospitalini, andaa mkutano na waandishi wa habari kisha hiyo sauti uiweke hadharani”

“Sawa, hivi yule mzee anaitwa nani?”

“Alex Alvandor”

Mlango ukafunguliwa na akaingia Frenando na mke wake.

“Broo vipi upo salama?”

“Nipo salama ndugu yangu.”

“Pole sana kaka, unajua nimeipata habari hii nikiwa katika ndege. Tulikuwa tunampeleka shemeji yangu kwenye hospitali moja jijini Barcelona”

“Ahaa”

“Shemeji vipi ume umia?”

“Hapana shemeji nipo safi”

“Kweli?”

“Ndio shemeji wala usijali hapa madaktari wamenipumzisha kwa muda nikikaa sawa wataniruhusu kutoka hapa hospitalini”

“Unajua nilijikuta nikilia shemeji yangu. Kwajinsi habari ilivyo tufikia tulitamani ndege iweze kugeuka hewani turudi ila kwa bahati mbaya hatukuwa na uwezo huo”

“Nashukuru kwa kunijali pia”

“Ehee vipi ni ajali ya bahati mbaya au ya kupangwa?”

“Ajali ya kupangwa”

“Usitake kuaniambia kwamba mzee Alex Alvandor ndio muhisika”

“Huyo huyo ndio muhusika mkuu”

“Unaona mke wangu nilikuambia. Na mzee yule nimejaribu kufwatilia mambo yake ya nyuma ya pazia. Nimegundia kwamba mzee yule ni mshenzi sana”

“Shemeji inabidi ukamstaki mahakamani”

“Sema yule mzee ana nguvu serikalini, ndio maana baadhi ya viongozi wana mtazama tu na pia ana undugu na raisi”

“Mmmmm”

“Yaa kama ni kupambana basi inabidi utumie akili kubwa sana na pia huwezi kwenda kumstaki mahakamani pasipo kidhibitisho cha aina yoyote”

“Shemeji mimi ni mwana sheria, endapo una kidhibitisho chochote nipo tayari kusimama mahakamani kwa ajili ya kuipigania kesi yako”

“Frenando mbona hujaniambia kwamba shemeji ni mwana sheria?”

“Ahaa kaka mambo mengi kichwani, ila ndio kazi yake na ana kampuni yake kubwa inayo miliki jopo kubwa sana la wanasheria”

“Na kampuni yangu kwa mwaka huu ndio kampuni namba moja hapa Spain na Uingereza kwa kushinda kesi nyingi tulizo letewa na wateja wetu”

“Hongera sana shemeji”

“Asante, na kuanzia sasa nitaanza utaratibu wa kumfungulia mashtaka mzee Alex”

“Nashukuru kwa msaada wenu munao endelea kunipatia”

“Usijali shemeji”

Frenando na mke wake wakalala hospitalini hapa hadi siku iliyo fwatia. Asubuhi na mapema madaktari wakaniruhusu kutoka hospitalini. Moja kwa moja tukaelekea kwenye ukumbi ambao tulipanga kuonana na waandishi wa habari kwa ajili ya kuzungumza nao. Ulinzi mkali umeimarishwa katika ukumbi huu, kitendo cha kuingia ndani ya ukumbi huu, mianga ya picha za waandishi wa habari ikaanza kurindima. Tukapia moja kwa moja hadi katika meza maalumu iliyo pangwa maiki nyingi.

“Habari za mchana”

Frenando alianza kuzungumza na waandishi wote wakaitikia.

“Japo wengi wenu muna nifahamu, ila acha nijitambulishe. Ninaitwa Frenando ni mchezi wa Real Madrid. Kushoto kwangu ni mke wangu anaitwa Maria Frenando na kulia kwangu ni rafiki yangu na mchezaji mwenzangu anaitwa Ethna Klopp”

“Nina imani kwamba wengi wenu jana muliweza kushuhudia juu ya ajali iliyo weza kutoka kwa rafiki yangu Ethan. Japo ni ajali mbaya sana ila Mungu alikuwa upande wa rafiki yangu, na alifanikiwa kutoka hai na hadi hapa munapo muona, hakika yupo fiti kabisa.”

“Aha…Nisiwe mongeaji sana labda nimkaribishe Ethan aweze kuzungumza”

Nikawatazama waandishi hawa wa habari kwa sekunde kadhaa, kisha nikatabasamu.

“Namshukuru Mungu kwa kuniokoa kutoka katika kifo. Nashukuru sana wale wote ambao waliguswa na ajali yangu. Waliniombea na wengine waliweza kufika hospitalini muda mchache baada ya kusikia kwamba nime pata ajali.”

“Ajali ya jana iliweza kupangwa na mtu aliye panga alidhamiria kabisa kuweza kuniondoa duniani”

Sura za waandishi wengi wa habari zikajawa na mshangao.

“Nina uhakika wa asilimia mia moja muuaji ana nitazama kwenye televishion kwa sasa na nina imani kwa kuwa hai kwangu atajaribu kufanya shambulizi la pili ambalo hakika sifahamu litakuwa nia la aina gani”

“Nina ushahidi wa suati ya mtu huyo. Wengi wenu nina imani kwamba mutakuwa muna mfahamu. Japo mimi ni mgeni kwenye hii nchi ila wengi mutamfahamu”

Nikatoa simu aliyo nipatia Ethan na kuiweka mezani. Nikawasikilizisha mazungumzo ya mzee Alex na Xaviela kisha na kijana wake aliye mpa kazi ya kuniangamiza.”

Waandishi wote wakazidi kushangaa huku wengine wakijawa na masikitiko.

Huyu ndio aliye panga kuniua. Nina imani kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimesikia hili lililo kuwa limepangwa na kweli limetoka. Naomba sheria iweze kufwata mkondo wake.”

“Ahaa mimi nikiwa kama mwanasheria wa Ethan. Huu ushahidi tutaupelekea mahakamani ili sheria iweze kufanya kazi yake”

Shemeji alizungumza kwa kujiamini. Waandishi wa habari wakaanza kunyoosha mikono kwa ajili ya maswali. Nikamchangua muandishi mmoja wa habari ili aulize swali lake.

“Hadi kufikia maamuzi ya kuhitaji kukuua. Je kuna jambo gani ambalo uliweza kumfanyia mzee Alex”

Nikajifikiria kwa muda huku nikimtazama Frenando na mke wake. Shemeji akanipa ishara niweze kuzungumza ukweli wote. Nikaanza kuwaadithia waandishi wa habari kianzia siku niliyo kutana na Xaviela, jinsi aliavyo jaribu kunieleza hisia zake na majibu niliyo mpatia. Nikawaeleza jinsi nilivyo kwenda kumuona Xaviela hotelini kwa ajili ya kumzuia asiweze kujiua. Nikawaeleza jinsi baba yake alivyo fika hotelini hapo na kuondoka na mwanaye na kufika hatua ya kuzungumza maneno hayo.

Waandishi wote wa habari wakakosa maswali kwani majibu ya maswali yao nimeyajibu kwenye historia hiyo fupi.

Baada ya mkutano huu kuisha tukatoka nje ya ukumbi huu na kukutana na mkuu wa polisi akiwa na askari wenginie.

“Muhusika tumeweza kumuweka chini ya kizui na tuna hitaji ushahidi”

Mkuu wa polisi alizungumza huku akitutazama usoni. Waandishi wa habari hawakusita kuendelea kurekodi kila jambo linalo endelea hapo. Nikawakabidhi simu hii na tukapeana mikono.

“Nina imani sheria itafwata mkondo wake”

“Ndio usijali katika hilo”

“Ninashukuru”

Tukaingia kwenye gari na kuondoka eneo hili. Moja kwa moja tukaelekea kwenye makao makuu ya club. Madaktari wakanifanyia vipimo vya mwili mzima ili kujiridhisha na majibu yaliyo toka hospitalini. Majibu yakatoka salama na wala sina matatizo ya aina yoyote na wakaniruhusu kucheza katika mechi yetu ya ufuguzi katika ligi ya La Liga.

“Inabidi ukake kwangu kwa siku mbili hizi unazo jiandaa kwa kombe. Unajua waandishi wa habari watakuwa wana kuandama, kwa maswali mengi”

“Ni kweli shemeji. Unajua kipindi hichi unatakiwa upate mwana saikolojia atakaye weza kukuweka sawa na ukaisahau ajali iliyo kupata. Itakuwa ni vizuri zaidi ukikaa nasi”

Sikuona sababu ya kuwakatalia Frenando na mke wake katika hili. Tukaelekea nyumbani kwao na shemji akanitafutia dada mmoja ambaye ni mwana saikolojia.

“Vivy kutana na Ethan. Ethan huyu anaitwa Vivy ni mwana saikolojia mzuri sana. Hivyo atakuwa nawe kweye kipindi hichi kigumu unacho pitia”

“Nashukuru kukufahamu Vivy”

“Hata mimi nashukuru kukufahamu Ethan”

“Vivy nakuamini, utahakikisha shemeji yangu ana rudi katika hali yake ya kawaida na Jumamosi aweze kutufungia magoli mengine kama siku ile”

“Hahaaa”

“Ni kweli shemeji, wee hujui tu. Mume wangu akiwa ame fungwa, ana poteza furaha kabisa na kujisikia vibaya. Ila akishinda huwa anajawa na furaha sana.”

“Usijali nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kwa msimu huu, kuhakikisha kwamba nina mpa furaha ndugu yangu”

“Nitashukuru sana shemeji. Sasa Vivy kuweni huru”

“Sawa”

Shemeji akaondoka sebleni hapa na kutuacha wenyewe. Vivy akanitazama kwa macho yake makubwa kiasi kisha akatabasamu kidogo.

“Tunaweza kutembea pamoja?”

Vivy alizungumza huku akisimama.

“Ndio hakuna tatizo”

Tukatoka sebleni hapa na kuelekea eneo lenye bustani kubwa nyumbani hapa kwa Frenando.

“Ethan”

“Naam”

“Huwa una pendelea vitu gani?”

“Mmm vya kimaisha ua?”

“Yaa ukiwa mwenyewe huwa una penda kufanya vitu gani?”

“Napenda kusikiliza nyimbo za rnb, kucheza games hususani za mpira pamona na mapigano”

“Ahaaa. Nimsanii gani ambaye huwa una msikiliza nyimbo zake”

“Bruno Mars, Adela, Michael Jackson, West life. Ni wengi wegi huwa nina penda kusikiliza nyimbo zao”

“Ahaa je games unapenda kuchezesha timu gani?”

“Hahaaa napenda kuitumia timu ya Liverpool”

“Kwa nini Liverpool ikiwa wewe ni mchezaji wa Madrid?”

“Ahaa toka nilipo kuwa mdogo nilikuwa naipenda sana Liverpool kipindi hicho wanacheza kina Gerrad, kina Xavi Alonso, kina Torres na wengine wengi. Hapa Madrid ninatengeneza jina na kipato”

“Ahaa hapo nimekuelewa. Je unapenda kujichanganya na watu au unapenda kuwa mwenyewe?”

“Napenda kujichanganya na watu japo sio sana. Unajua unapo kuwa maarufu ni ngumu sana kutembea barabarani kwa miguu. Watu watakuzonga zonga sana”

“Chakula una pendelea chakula gani?”

“Napendelea ndizi na chakula kimoja hivi kipo nchini kwetu Tanzania kinaitwa Ugali”

“Ahaa nimekifahamu, nilisha wahi kukila siku nilipo kwenda kutembelea mlima Kilimanjaro Tanzania”

“Oho kumbe ulisha wahi kufika Tanzania?”

“Ndio, ni nchi nzuri na ninatamani sana kuweza kurudi kwa mara nyingine nikaitembelee”

“Usijali”

Nikamshika Vivy mkono wake wa kulia na kutazama pete yake ya ndoa.

“Mume wako ana endeleaje?”

“Ahaa…….ahaa…safi”

“Mbona una kigugumizi, au nimefanya vibaya kukuuliza swali hilo?”

“Hapana, ila kidogo ndoa yangu ina matatizo na kwa sasa mimi na mume wangu tumetengana kidogo”

Vivy alizungumza kwa sauti ya upole. Nikamtazama Vivy kwa umakini sana, ni mwanamke mzuri. Mwanamke ambaye ana kila aina ya vigezo vya kuwa mke mtu.

“Kwa nini ina matatizo”

“Mume wangu ana nilaumu kwamba sina uwezo wa kumbebea ujauzito na ameamua kuwa na kimada wa nje kwa ajili ya kubebewa ujauzito”



ENDELEA

“Mmmm ila swala la mtoto ni majaliwa ya Mungu. Je huyo kimada wa nje amempatia mtoto hadi sasa?”

“Hapana ni miezi nane sasa toka tutengane na sijawahi kumuona huyo mwanamke hata kuwa na ujauzito. Ila tuachane na hayo kwa maana sihitaji kuyazungumzia kwa kipindi hichi.”

Vivy alizungumza kwa upole sana.

“Kuna kitu chochote ambacho kinakusumbua kwenye uwepo wako wa akili ambalo limetokana na ajali ambayo umeipata?”

“Hapana nipo sawa. Akili yangu ipo vizuri na wala sina tatizo la ina yoyote. Hapa ninacho kifikiria ni kuhusiana na mechi ya ufunguzi wa ligi. Hivyo nahitaji kuwa katika kiwango kizuri zaidi ya kile ambacho nilikuwa nacho pale awali”

“Vizuri naweza kuwa karibu yako kwa muda mrefu”

“Kivipi?”

“Unajua kazi hii niliyo kabidhiwa, inanipasa niweze kuwa karibu nawe. Nifahamu mambo mengi sana kutoka kwako. Inawezekana hapa unazungumza kwamba upo sawa. Ila kwa ndani katika akili utakuwa haupo sawa. Unajua watu wanao kutana na matatizo kama yako kwa mara nyingi huwa wanaota njozi ambazo zinawakumbusha tukio hilo la ajali. Jambo hilo ni baya na linaweza kupeleka uwezo wako uwanjani ukashuka kwa kasi sana”

“Usijali katika hilo, ila unaweza kufanya chochote unacho amini kitakuwa ni kizuri kwangu”

“Nashukuru kwa kunipa nafasi hiyo.”

Siku iliyo fwata, nikarudi nyumbani kwangu huku nikiwa nimeongozana na Vivy. Kutokana jukumu lake ni kunitazama katika kila mwenendo ambao nina piga, nikampatia chumba kimoja katika nyumba yangu.

“Ina bidi baadhi ya vitu vyangu niweze kuvihamishia hapa”

“Sawa hakuna shida. Ngoja nikukabidhi kwa walinzi wangu waweze kukupeleka nyumbani kwako ukachukua vitu unavyo hitaji kuhamia navyo hapa kisha mutarudi”

“Nashukuru kwa hilo”

Nikamkabidhi Vivy kwa mkuu wawalinzi wangu na akaondoka naye. Nikampigia Latifa simu, na kwabahati nzuri nikakikuta ikiwa hewani.

“Ethan mume wangu nina ogopa upo salama kweli?”

“Ndio nipo salama mke wangu, usihofie juu ya uslama wangu”

“Nimeruhusiwa niweze kuja nchini huko wiki ijayo”

“Ndivyo ubalozi wa Spain huko ulivyo sema?”

“Ndio mume wangu kidogo visa ilikuwa na shida ila mambo yamekuwa sawa”

“Sawa mke wangu. Ngoja tutawasiliana baadae”

“Haya”

Nikakata simu na kuisogelea tv kubwa iliyo chumbani kwangu ambayo inaonyesha video zote zinazo rekodiwa na kamera za hapa nyumbani kwangu. Gari hili la kifahari ina ya Roll Royce lililo simama nje ya geti langu, likanifanya ninyanyue mkonga wangu wa simu ya mezani ili niweze kuwasiliana na walinzi wa getini wanao endelea kuzungumza na mtu aliyomo ndani ya gari hilo

“Ni nani huyo mgeni?”

“Ahaa amejitambulisha kwa jina la Hawa. Anasema yeye nimke wako na hapa ana mtoto wako”

“Hembu igeuzeni kamera ya hapo niweze kumuona vizuri”

Mlinzi wangu, akafanya kazi hiyo na kweli nikamuona Hawa, mwanamke aliye nizalia mtoto wangu.

“Mruhusini kuingia”

“Sawa mkuu”

Gari hiyo ikaruhusiwa kuingia. Nikatika chumbani kwangu kwa haraka na kukimbilia nje. Nikamkuta Hawa akifunguliwa mlango na dereva wa gari hilo. Taratibu Hawa akashuka huku akiwa amemshika mtoto wangu. Tabasamu lake alilo nipatia usoni mwake, kwa haraka likanifanya nimkimbilie na kumkumbatia kwa nguvu huku nikimbusu kwenye lipsi zake.

“Ethan mume wangu nimekukumbuka”

“Hata mimi mke wangu. Umejuaje nina ishi hapa?”

“Habari niliyo isikia juu ya kupata kwako ajali ilinichanganya kwa kweli na nimejikuta nikifunga safari kuja huku bila hata ya kukuambia. Sikutaka mtoto wetu afe pasipo kukuona wewe.”

“Nashukuru sana mke wangu”

Nilizungumza huku nikiendelea kumkumbatia Hawa. Taratibu nikamtazama mwanangu, hakika hakuna sehemu ambayo nimeibiwa. Mtoto huyu ana fanana snaa na mimi.

“Karibu ndani, kuna mizigo yoyote kwenye gari?”

“Ndio kuna mabegi ya nguo

Wafanyakazi wangu wa ndani wakasaidiana na dereva kushusha mizigo kwenye gari hilo. Hakika kama ni suprize basi hii ni suprize kubwa kwenye maisha yangu. Kwasiku kama ya leo sikutarajia kuonana na Hawa pamoja na mwanangu niliye mpatia jina la Ethan Jr. Haukupita muda mrefu sana, Vivy akafika nyumbani hapa na kukuta ugeni huu ambao kidogo ukamstua.

“Vivy, kutana na Hawa, ni mama wa mwangu huyu anaye itwa Ethan na Hawa huyu ni mwana saikolojia wangu ambaye toka nilipo pata ajali basi ameweza kuwa karibu yangu ili kuhakikisha akili yangu ina kuwa sawa”

“Ohh nashukuru kukufahamu Vivy na asante kwa kuhakikisha mume wangu ana kuwa sawa”

Hawa alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake. Japo Vivy ana jitahidi kutabasamu, ila kwa namna moja ama nyingine hajapendezwa na ugeni huu.

“Nashukuru kukufahamu nawe pia”

“Asante”

“Waoo muna mtoto mzuri”

“Kweli ehee?”

“Yaa mune mtoto mzuri sana. Amefanana na wewe baba yake”

“Hahaaa nashukuru Vivy”

“Basi mimi nipo juu”

“Sawa Vivy”

Vivy akaondoka sebleni hapa akiwa na mabegi yake na kupandisha gorofani na kumfanya Hawa kumsindikiza kwa macho.

“Mbona ana onekana kama hajafurahi mimi kuwepo hapa?”

“Sijajua”

“Ana kutaka huyu mwanamke”

“Nini?”

“Ndio ana kutaka kimapenzi. Hakika nimekuja kuishi na wewe na wewe ndio mume wangu na sinto kuacha kamwe na huyu ni mwanao na nina kupenda Ethan. Namuomba aweze kuchungu hisia zake kwa maana hatambu ni wapi mimi na wewe tumetokea”

Hawa alizungumza kwa msisitozo na nikajikuta nikikosa cha kuzungumza. Nikayanyuka na kumshika mkono Hawa na kuanza kuelekea juu gorofani kikipo chumba chetu, huku mkono mmoja nikiwa nime mbaba mwanangu.

“Woo una nyumba kubwa sana Ethan”

“Nashukuru mke wangu”

“Katika siku zote za kuishi peke yako humu ndani, kweli hujaleta mwamke?”

“Mmmm hapana”

“Mbona umeanza kwa kuguna?”

“Nimeguna kwa kuwa hilo ndio jambo unalo waza akilini mwako au?”

“Ndio, unahisi sijasikiliza stori iliyo kuwa una waambia waandishi wa habari jinsi mwanamke alivyo kupenda hadi ana taka kujia kwa ajili yako”

“Sasa hiyo ndio ina kufanya uwe na wivu na mimi?”

“Ndio nina wivu na wewe Ethan. Laiti kama ningekuwa sijabeba ujauzito wako. Hakika nisinge kuwana muda na wewe na ingekuwa imebaki kumbukumbu kwenye maisha yangu kwamba wewe ndio mwanaume uliye nitoa usichana wangu tu. Ila nimebeba ujauzito wako na nimekulelea mwanao na sasa ana miazi nane, hapo una hisi kwamba nitakusahau?”

Hawa alizungumza huku akiendelea kuzunguka zunguka ndani ya chumba changu hichi ambacho ni kikubwa sana.

“Najivunia kuwa mke wako Ethan. Tambua kwamba wewe kwa sasa ndio baba yangu na ndio mama yangu nina kupenda sana na nitakusikiliza kwa kila jambo ambalo uta niambia”

Maneno ya Hawa yakazidi kuniacha kinywa wazi, sijui hata ninaazia wapi kumzuia Latifa asije nchini Spain ikiwa kila jambo nimesha liweka sawa kwake. Hawa naye ana hitaji kuishi namimi. Nikajikuta nikijikuna kichwa na kukosa cha kufanya.

“Ethan”

“Naam”

“Una nipenda?”

“Ehee?”

“Una nipenda?”

“Ndio”

“Kweli?”

“Ndio nina kupenda”

“Basi nina furahi kusikia hivyo. Nita ihamishia kampuni yangu ya sheria nchini Spain na kazi zangu zote nitakuwa nina fanyia hapa Spain na si Marekani tena”

“Hawa mbona mambo una taka kuyapeleka haraka haraka. Kumbuka hapa mimi ndio mume na si wewe na kila jambo unalo hitaji kulifanya mimi ninatakiwa kuweza kulipisha au kulikataa na si kuja kwamba na kuhitaji kuamua kila jambo”

Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nikimtazama Hawa usoni mwake kwa maana kwa kila jambo alilo lizungumza kwangu kidogo lina ugumu katika utekelezaji.

“Kwa hiyo Ethan unahitaji kuishi peke yako na si mimi na mwanangu?”

“Hilo umelizungumza wewe Hawa. Ila kumbuka akili yangu jinsi ilivyo na kwa sasa ninatakiwa kuhakikisha nina shuhulika na mpira kiwanjani. Sasa ukianza kuniingizia maswala ya ndoa ikiwa bado sijajipanga kuoa kwa kipindi hichi, utakuwa una nichanganya”

“Nimekuelewa Ethan. Kesho nitakata tiketi ya ndege na tutarudi Marekani mimi na mwangu na kama utahitaji kuonana nasi basi utatafuta”

Hawa alizungumza kwa jazba kidogo.

“Hawa nisikilize mke wangu. Kila jambo linahitaji utaratibu hivyo unavyo zungumza kwa hasira utakuwa una kosea mke wangu”

“Hapana Etha. Una kumbua ni kwa kipindi gani nimekaa mbali na wewe?”

“Kirefu”

“Unahisi kwamba mimi kwa kipindi chote hicho sikuwa na hisia na wewe?”

“Ulikuwa nazo?”

“Kwa nini hutaki kunisikiliza hisia zangu. Kumbuka mtoto wako ana hitaji malezi ya baba na si kukimbia kimbia. Kama ni pesa haziwezi kutengeneza upendo kwa mwanao. Ukaribu wako ndio unatakiwa kuhakikisha kwamba mtoto ana kaa katika malezi yako mume wangu”

Hawa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Akaka kitandani huku akiwa amejiinamia, kama ni vituko basi leo Hawa ameamua kunifanyia vituko. Nikamsogelea na kukaa pembeni yake.

“Mke wangu hembu niambie kwa nini unakuwa hivi”

“Ethan ninakuwa hivi kwa sababu nina kupenda”

“Kunipenda tu ndio kuna kufanya uwe hivi?”

“Ndio mume wangu”

“Basi mutakaa hapa na mwanangu”

“Sawa na nina ombi jengine”

“Ombi gani?”

“Ninataka mwanangu umuandikie urithi wake kabisa. Kwa maana maadui wanao kuwinda wewe ni wengi na endapo ukifa ni nani ambaye atatuambua juu ya uwepo wangu na uwepo wa huyu mtoto”

Maneno ya Hawa yakanistua sana na kujikuta nikisimama huku nikimtazama usoni mwake.

“Sijakuelewa Hawa”

“Nielewe tu Ethan. Nataka mwanangu umuandikishe mrithi wa mali zako”

“Nikiwa bado hata sijafikisha miaka ishirini na tano, niandike urithi kweli?”

“Ndio Ethan, je juzi ungekufa ingekuwaje. Nani ambaye ninge muaminisha kwamba huyu ni mwanao. Wengi si wangesema kwamba nina jipendekeza kwako na ikiwa kwamba wewe na mimi hatunawahi kuonekana wala kuhisiwa kwamba tuna mahusiano ya kimapenzi?”

“Una kumbuka nilikuambia kwamba nikutumie pesa kwa ajili ya kumlea mwangu, ulinijibu nini?”

“Nakumbuka ila kipindi kile ulimwengu mzima ulikuwa unajua kwamba wewe ni mfu”

“So kama ni mfu kwa hiyo una hitaji sasa hivi kupata urithi kwa ajili ya mwanao?”

“Ndio”

“Hawa”

“Beee”

“Nilikuamini sana na sikuwahi kufiria kwamba ipo siku utakua kuniambia upuuzi kama huu. Mimi ndio baba wa Ethan Jr na ninajua nini napaswa kukifanya. Kuja kwako kwangu bila ya taarifa si kwamba una nipenda. Ila umekuka kutokana na kuhitaji kitu hususani pesa na umemtoa mwanangu kama chambo ili uweze kufanikisha kile ambacho unakitaka.”

“Sasa katika haya mawili chagua moja. Kumuacha mwanangu mikononi mwangu na kuondoka zako hapa Spain mikono mitupu au niambie unahitaji kiasi gani cha pesa na uondoke na kuniachia mwanangu na nitamlea mimi mwenyewe? Chagua moja kati ya hayo.”



Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Hawa usoni mwake. Kitu nilicho kiongea hakika kimetoka kabisa moyoni mwangu. Sijajua ni kwa nini Hawa amebadilika kwa kiasi hichi, hadi kufika hatua ya kung’ang’aniza kumuandika mtoto wangu kwenye urithi wangu, kana kwamba anafahamu siku yangu ya kufa.

“Ethan una una jua kuwa”

“Mmm nimekuambia chagua, nikupe pesa umuache mwanangu hapa ukaendelee na maisha yako nchini Marekani au uniachie mwanangu na uondoke mikono mitupu. Nyinyi ndio wanawake ambao munakuja kuwaua waume zenu kwa ajili ya pesa. Tena wewe ni mchaga mwezangu, hakika sina imani kabisa na wewe.”

“Nahitaji hili swala lipelekwe mahakamani?”

“Kufanya nini?”

“Lazima nami nipate haki zangu za msingi kama mama wa huyo mtoto.”

“Hii ndio maana ya msingi uliyo hitaji kuzaa na mimi, sikukulazimisha wala kukuomba kuzaa na mimi. Ila unavyo nifayia hakika siwezi kuvumilia. Nyinyi wanawake wa Kitanzania mupo vipi, inakuwaje una hitaji urithi wa mali zangu kwa kigezo cha kuzaa na mimi eheee?”

“Hili swala tutalizungumzia mahakamani. Tena nina kwenda kufungua kesi Marekani, kwani huyo mtoto amezaliwa Marekani na niraia wa Marekani”

“Sawa hakuna shida, kafungua kesi, ila mwanangu atakuwa chini ya uangalizi wangu kuanzia hivi sasa. Nitampatia huduma zote azitakazo sawa”

“Siwezi kuondoka na kumuacha mwangu hapa nina ondoka naye kwa maana mimi ndio nina jua uchungu wake na nilikaa leba kwa kipindi chote hicho na wewe wala haukuwepo”

“Poa ondoka na nitakuja na mwanangu”

“Ethan siondoki bila mwanangu na nitafungua kesi ya umiliki wa huyu mtoto na kama urithi wake utautoa makahakani”

Hawa akanipokonya mwanangu, akashika begi lake la mkononi na kutoka ndani hapa. Nikaanza kumfwata kwa nyuma huku nikijaribu kumzuia ila hakuweza kusimama. Akafika katika gari aliko kuja nalo na dereva wake akafungulia mlango na kuingia.

“Nahitaji mabegi yangu”

Hawa alizungumza huku akiwa ameshusha kioo cha gair hilo kidogo.

“Kalete mabegi yake”

Nilimuambia mfanyakazi wangu wa ndani. Baada ya dakika chache akatoka mabegi ya Hawa. Yakapakizwa kwenye gari.

“Ninaishi New York na kampuni yangu inaitwa H.I.L”(Hawa International Laywers)

Hawa akafungua pochi yake na kutoa business card na kunipatia.

“Utanitafuta ukoja Marekani kwa maana nimezungumza kwa ustarabu ila una onekana kubisha. Utaandika urithi wa mwanao Mahakamani. Dereva tuondoke”

Hawa baada ya kuzungumza hivyo akafunga kioo cha gari na kuondoka. Nikalisindikiza gari hili kwa macho hadi lilipo tokomea nje ya geti langu.

“Pole ETHAN”

Sauti ya Vivy ikanifanya nigeuke nyuma kwa unyinge sana.

“Asante”

“Imekuwaje mgeni ameondoka kwa hasira na kwa haraka sana. Hajamaliza hata lisaa ndani ya nyumba yako?”

“Tumepishana kwenye swala la Urithi na kuishi naye”

“Urithi wa nini?”

“Anahitaji niweze kumuandika mwanangu kama mrithi wa mali zangu zote. Jambo ambalo sijakubaliana nalo”

“Mmmm bora ambavyo hujakubaliana nalo. Kwani wanawake wengi huwa wanakimbilia kuwazalia watu maarufu kwa ajili ya kuweza kupata pesa na wengine hufika mbali kama huyo anaye hitaji urithi mapema sana na ikiwa mtoto bado ni mdogo”

“Yaaa anahitaji kufungua kesi mahakamani na ameniambia urithi nitautolea mahakamani”

“Mmmm japo sija utaalamu kwenye maswala ya sheria, ila sidhani kama hapa Spain wana weza kutoa hukumu kama hiyo kwako”

“Anafungulia kesi Marekani”

“Duu! Hapo inabidi uweze kuzungumza na mke wa Frenando juu ya hili swala ili kama ni kisheria waweze kujipanga vizuri”

“Sawa”

“Ila upo sawa kweli?”

“Sipo poa”

Baada ya kumjibu hivyo Vivy nikaingia ndani, na moja kwa moja nikapitiliza hadi chumbani kwnagu. Nikampigia Frenando na kumuelezea kwa kila jambo lililo weza kutokea.

“Duu kaka pole, shemeji yako ameweza kusikia kila kitu hembu ongea naye”

“Shem”

“Naam shemeji”

“Muache afungue kesi, nina imani kwamba mahakama itatoa maamuzi mazuri kuliko kutoa maamuzi yako binafsi ya kumrithisha urithi mtoto ambaye hata mwaka mmoja hajafikia. Ina maana katika hiyo miaka kumi na nane mbeleni ni lazima mama mtu awe ndio msimamizi mkuu wa mali hizo. Hapo unahisi kitatokea kitu gani kama si utapeli wa mama mtu”

“Ndio jambo nililo lihisi shemeji”

“Wewe kaa kwa amani, ukitumiwa fax ya kutakiwa kufika mahakamani, basi nasi ndio tutakapo jiandaa. Uzuri kampuni yangu inaweza kufanya kazi duniani kote. Hivyo kuwa na amani shemeji yangu”

“Nashukuru kwa kunitia moyo shem”

“Usijali na yule waziri amekamatwa. Hapa nimetumiwa email na mahakama, watatuhitaji jumatatu ijayo. Nina imani kwamba hata wewe umetumiwa email hiyo”

“Sijafungua email yangu, acha nifungue niweze kuiangalia”

“Hakuna tatizo. Wewe kuwa na amani hakuna linalo weza kukupata baya katika kesi hizi mbili”

“Nashukuru shemeji”

Baada ya siku mbili, nikapokea email kutoka mahakama kuu nchini Marekani, ikinipa wito wa kwenda kusikiliza kesi ambayo imefunguliwa dhidi yangu. Nikamtumia shemeji email hii na baada ya kuisoma akapeleka pendekezo kwenye club yangu ya Real Madrid, juu ya mimi kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kushuhulikia kesi hii.

“Uongozi wako wa timu wamekuomba uweze kucheza mechi hii ya jumapili kisha ndio uweze kuondoka”

“Nashukuru shemeji”

Nikaendelea kufanya mazozi na wachezaji wezangu kama kawaida. Siku ya mechi na wapinzani wetu wa mji mmoja ambao ni Altetico Madrid ikawadia. Kocha akanipa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, huku Benzema akiwa benchi. Uwanja wetu wa Santiago Benabeu, umejaa mashabiki wengi sana.

‘Mungu nisaidie’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikitazama washambuliaji wawili wa timu pinzani ambao ni D.Costa na A.Grizman. Mpira ukaanza kwa kasi sana huku mashambulizi yakielekea golini kwetu. Frenando kwa ubora wake aliweza kunyaka shuti kali la Diego Costa. Akaupiga mpira mbele, ukatua kifuani kwa Madric ambaye hakuuweka mguuni, akapiga pasi ndefu iliyo weza kunifikia mimi. Kasi na nguvu aliyo nibariki mwenyezi Mungu, nilijikuta nikiambaa ambaa na mpira huu pembezoni mwa uwanja, nikamtisha beki wa kulia kama ninapiga krosi, ila nikausogeza mpira huu kwenye mguu wangu wa kulia na kumfanya beki huyu kupita kwa kasi huku akiburuzika kwenye nyasi za uwanja huu.

Nikanyanyua uso wangu mara moja kumtazama kipa jinsi alivyo kaa golini. Nikapiga shuti kali, mpira ukaanza kuambaa ambaa hewani na kuingia katika katika kona ya mwamba wa juu, japo kipa alijaribu kuufwata ila hakuweza kuupata na nikaiandikia timu yangu goli la kuongoza katika dakika ya tisa. Wachezaji wezangu wakanikumbatia na kunipongeza kwa goli hili.

Mtanange ukaendelea huku mashambulizi yakiwa ni makali sana. Hadi zinatimia dakika arobaini na tano, goli ni moja bila. Tukaingia kwenye vyumba vya mazoezi kwa ajili ya maelekezo kutoka kwa makocha wetu.

“Mumecheza vizuri. Ila wapinzani wetu wote macho yao ni kwa Ethan. Jambo la kufanya, Ethan utashuka kidogo na kicheza kumi. Bale na Ronaldo nyinyi mutasimama winga. Ethan hakikisha kwamba mipira utakayo pata kutoka katikati unaitawanya kwa hawa watu wawili.”

“Sawa kocha.”

“Beki ipo safi. Hakikisheni kwamba Costa wala Grizman hawashiki mpira wala kukaa nao. Marcelo hakikisha unaendelea hivyo hivyo kumkaba Costa. Naona amesha anza kupaniki, akiendelea hivyo kadi nyekundu itamuuhusu”

“Kiwango ni kizuri. Goli moja halitoshi kwa maana muda wowote linaweza kurudi na likirudi basi itatuwia ugumu kupata goli la ushindi. Tunatakiwa kupata pointi tatu muhimu. Tusiwape nafasi Barcelona kuongoza ligi, kwani hadi sasa hivi walempiga Valencia goli nne”

“Tumekuelewa kocha”

“Frenando, hakikisha kwamba mipira ya juu unaidaka kwa uangalifu, kwa maana wanaweza kukurikia kwenye mbavu, ukapata majeraha yatakayo kuweka nje kwa kipindu kirefu. Sawa”

“Sawa kocha”

“Haya turudini uwanjani”

Tukaanza kurudi uwanjani huku nikifikiria ni jinsi gani nina weza kung’aa leo, kwani kocha amesha nihamisha nafasi ya uchezji. Mpira ukaanza kwa kasi, nikafanikiwa kuupata mpira, nikaanza kuwatoka mabeki wa upinzani, nikamtazama Ronaldo na kumuona akiwa katika kasi, nzuri. Nikamtangulizia pasi ambayo iliweza kumfikia katika wakati. Ronaldo hakufanya kosa, akaachia shuti kali lililo weza kuzaa goli la pili na kutupa nguvu na ujasiri wa kuhakikisha kwamba tuna pata ushindi mzuri.

Mori ya uchezaji ikazidi kupamba moto, mimi na wachezaji wezangu tukazidi kulishambulia goli la wapinzani wezetu na pasi yangu ya mwisho ikafanikisha Ronaldo kufunga goli lake la pili na kufanya tuongoze kwa goli tato bila.

“Safi sana Ethan”

Ronaldo alizungumza huku akinikumbatia. Tukaendelea na mashambulizi, dakika ya sabini na moja nikafanikiwa kuudumbukiza mpira golini kwa kutumia kichwa, nikiunganisha krosi kutoka wa Bale. Shangwe zikazidi kutawala uwanjani hapa. Dakika ya sabini na tano nikaweza kuwatoka mabeki na kipa wao na kufanikiwa kufunga goli la tano huku kwa upande wangu nikiwa nimefunga hatrick yatatu katika mechi mbili nilizo ichezea timu hii.

Baada ya kumaliza kushangilia goli hili, kocha akanitoa na akaingia Benzema.

“Hongera sana Ethan”

Kocha alizungumza huku akinipa mkono na kunikumbatia.

“Nashukuru sana kocha”

Nikawapa mikono wachezaji wezangu waliopo benchi, kisha nikakabidhiwa koti langu kubwa na kukaa katika siti yangu.

Hadi mpira una fika dakika ya tisini na tatu. Tumeongoza kwa goli sita kwa sifuri, nikakabidhiwa mpira na refarii. Waandishi wa habari wakaniomba wanihoji.

“Ethan ni goli tisa sasa umefunga kwenye mechi moja huku ume saidia kufungwa kwa goli nne katika hizi mechi mbili. Je unajisikiaje kwa kiwango hichi kizuri ulicho barikiwa na MUNGU”

Dada huyu mrembo ambaye ni muandishi, alinifanya nitabasamu kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama usoni mwake.

“Ni jambo zuri sana. Ninamshukuru Mungu kwa kuweza kuniweka sawa, kutoka kwenye ile ajali hadi hapa sasa nilipo.”

“Una waahidi nini mashabikir wa Madrid?”

“Jambo kubwa wazidi kutuunga mkono kwa maana ligi imeanza vizuri. Furaha kubwa ni kuona timu ina pata matokeo mazuri na kushinda makombe mengi”

“Hongera sana hii ni tuzo yao ya mchezaji bora wa mechi”

Dada huyu alinipa kiboksi kizuri”

“Nashukuru sana”

“Asante”

Nikavua jezi yangu kumpatia dada huyu na kumfanya akose cha kuzungumza huku macho yakimtoka kwa furaha. Nikaondoka na kumuacha akinisidikiza kwa mcho yaliyo jawa furaha.

“Ila wewe mjinga upo kwenye kiwango kizuri. Aisee sikutaraji”

Frenando alizungumza huku akinikumbatia kwa nyuma.

“Hahaaa. Timu ipo kwenye kiwango kizuri”

“Lile goli la kwanza hakika hata mimi siwezi kulinyaka na hata nikiufwata mpira basi nitaufwata kiushahidi tu ila mmmmm”

“Hahaaa”

Tukaingia katika chumba cha kubalidilishia nguo. Tukapiga piga picha za ushindi wa leo kisha tukaanza kuelekea kwenye basi letu ili turudishwe kwenye kiwanja kidogo cha mazoezi ambapo ndipo zilipo ofisi za makao makuu ya timu yetu.

“Ethan Ethan Ethan”

Sauti ya kike ikanifanya niweze kusimama na kugeuka nyuma. Nikamuona yule muandishi wa habari niliye mpatia jezi yangu akinifwata kwa kasi. Safari hii hana maiki wala hajaongozana na kamera mani wake. Mkononi mwake ameshika jezi yangu niliyo mkabidhi.

“Samahani sana Ethan, naomba upokee jezi yako sinto weza kuichukua. Samahani sana”

Maneno ya muandishi huyu wa habari yakawafanya hadi baadhi ya wachezaji wezangu ambao nimeongozana nao kumshangaa sana, kwani hakuna zawadi kubwa kwa shabiki kama kukabidhiwa jezi ambayo mchezaji ameitumia kiwanjani.



“Natambua kwamba nitakuwa nime kuudhi na kukuzalilisha mbele ya wezako. Ila samahani pokea jezi yako”

“Kwa nini?”

“Hakuna sababu Ethan pokea”

Nikamtazama kwa sekunde kadhaa muandishi huyu na kuipokea jezi hii. Akaanza kuondoka eneo hili huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Ana jambo linalo msumbua”

Navas alizungumza huku sote tukimtazama dada huyu. Sikuwa na budi zaidi ya kukubaliana na ukweli kwamba jezi yangu imerudishwa. Nikainagia kwenye basi na kurudishwa makao makuu ya timu, baada ya maelezo mafupi ya kocha juu ya utaratibu wa mazoezi kwa wiki hii. Nikapewa rushusha ya maandishi ambayo itaniweka nje ya kikosi kwa siku tano kunzia kesho.

Tukaelekea nyumbani kwa Frendando, kutokana mke wake ni mwanasheria wangu. Ikatulazimu kupanga juu ya safari ya kuelekea nchini Marekani. Mipango ya kwenda nchini Marekani ikakamilika katika siku ya leo, kutokana ndege yangu ipo hapa hapa nchini Spain, hatukuwa na haja ya kukata tiketi kwenye mashirika ya ndege. Nikarudi nyumbani kwangu na kujiandaa.

“Ethan ninakuomba tuweze kwenda pamoja Marekani”

Vivy alizungumza huku akinitazama jinsi ninavyo panga baadhi ya nguo zangu ndani ya begi langu la mgongoni. Nikatazama saa yangu ya mkononi.

“Saa tatu na nusu sasa hivi. Wasiliana na ubalozi wa Marekani wakupatie visa. Uwaambie wewe ni mwana saikolojia wangu, wanaweka kukupatia visa kwa masa haya machache”

“Sawa”

Vivy akaanza kufanya taratibu hiyo, haikuchukua muda mrefu sana akafanikiwa kupata visa ambayo itatuwezesha kukaa Marekani kwa siku saba. Siku iliyo fwata, majira ya saa mbili asubuhi tukaondoka jijini Madrid kwa ndege yangu binafsi na kuianza safari ya kuelekea nchini Marekani. Safari ambayo itatutoa bara moja kwenda bara jengine na uzuri ni kwamba ndege yangu ina uwezo wa kusafiri kwa masaa sabini na mbili angani pasipo kutua ardhini.

“Nimesha anda taratibu za kimahakama hivyo tukifika kesho asubuhi, itatulazimu mchana tuwasilia mahakamani”

“Sawa”

“Ethna”

“Naam”

“Hii ndege uliinunua mara baada ya kusaini mkataba Madrid?”

Vivy aliniuliza swali lililo nifanya niweze kumtazama kwa sekunde kadhaa usoni mwake.

“Hapana. Mimi toka nilipo kuwa mtoto mdogo nilirithi utajiri wa mzee Klopp na niliweza kuuendeleza na kuniletea mafanikio makubwa. Hivyo siishia kwa mshahara ambao nina pokea kutoka Madrid”

“Ahaa sawa sawa. Inabidi siku ukipata muda uweze kunielezea back ground yako ili niweze kukuelewa kwa kila jambo”

“Usijali Vivy. Jamani kama muna jisikia njaa, munaweza kupata vinywaji, matanda pia munaweza kupika. Kuna kila aina ya chakula ndani ya ndege yangu”

“Tunashukuru”

Siku iliyo fwata tukafika nchini Marekani katika jiji la New York. Ujio wangu hapa Marekani sijui ni nani aliweza kuuvujisha kwa waandishi wa habari. Kitendo cha kutua katika kiwanja cha ndege waandishi wa habari wakanivamia na kuanza kunihoji maswali. Walinzi ambao walisha andaliwa na shemeji waliweza kutusaidia kuingia kwenye gari lililo andaliwa. Moja kwa moja tukapelekwa katika hoteli ambayo tuliweka oda ya vyumba vitatu.

“Ethna masaa yetu ni machache sana. Hivyo jitahidi sana kuhakikisha una jianda haraka ili tuweze kufika mahakamani”

“Sawa”

Tukajindaa na saa nane kasoro tukaelekea mahakani. Hadi inafika saa nane kamili, tayari tulisha wasili katika mahakama kuu hapa nchini Marekani. Nikamkuta Hawa, akiwa ana hojiwa na waandishi wa habari, ambao mara tu baada ya kuniona, wakatufwata na kutuzunguka.

“Usizungumze chochote Ethan”

Shemeji Maria alizungumza huku tukiingia katika ukumbi wa mahakama. Nikakuta watu wengi sana wakiwa wana isubiria kesi hii kwa hamau.

“Hee kesi ya urithi ndio imejaza watu namna hii?”

“Hawa ameandaa hili, ila usihofie. Wewe niamini katika hili”

“Sawa”

Tukaonyesha sehemu ya mimi na shemeji kukaa, huku Vivy, akikaa na mashuhuda wengine katika mahakama hii. Nikamuona Hawa akiwa ameongozana na mwana sheria wake, akanitazama kwa jicho la husda kisha wakaka nao katika sehemu yao. Jaji akaingia katika sehemu yake na kesi ikaanza kusikilizwa. Upande wa mlalamikaji ambaye ni Hawa, ana dai kwamba toka azae na mimi sijawahi kutoa hata senti tano ya matumizi na walipo kuja nchini Spaini niliwafukuza kama mbwa.

Nikastuka sana kwenye swala la kuwafukuza wao kama mbwa. Nikageuka nyuma na kutazamana na Vivy ambaye siku ile aliwekuwepo nyumbani kwangu.

Staka jengine la walalamikaji ni kwamba nimekataa kabisa kutoa huduma kwa mtoto huyo kitu ambacho si kweli. Haya yote yanayo fanywa na Hawa ni moja ya mpango wa kunichafua, mbili, jinsi ninavyo mjua Hawa, basi kutakuwa na mtu nyuma yake ambaye ana mshinikiza katika kunichafua. Nikaitwa kizimbani, nikaapa kwa kutumia biblia kisha nikaanza kuhojiwa.

“Je unakubaliana na mastaka yote yaliyo somwa mbele yako?”

“Hapana sikubaliani nayo”

“Bwana Ethan, wewe ni kijana tajiri, mwenye pesa zake na pia ni star katika timu ya Madrid inakuwaje unashindwa kumlea mwanao?”

Mwanasheria wa Hawa alinihoji huku akinitazama usoni mwangu.

“Sijawahi kukataa kumuhudumia mwangu. Hawa alinikumbia nchini Tanzania nakuja kuishi huku Marekani. Aliondoka pasipo kunijulisha chochote juu ya kuondoka kwake Tanzania”

“Kama alikukimbia ndio uliona nawe ulipize juu ya kuto kumtunza mwanao?”

“Ningejuaje eneo alipo ikiwa aliondoka pasipo kuniambia anakwenda wapi?”

“Katika kumbukumbu zangu za nyuma. Kipindi Hawa ana kuja nchini Marekani, ni kipindi ambacho mama yake ambaye alikuwa ni raisi wa Tanzania alishambuliwa na kuuwawa. Ninaweza kusema kwamba alikimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake na kimbe ambacho kilikuwepo tumboni mwake wasiuwawe.”

“Haya umeyasema wewe. Ila kama baba wa mtoto huyo ilipaswa kuweza kufahamu ni wapi alipo”

“Kwajuhudi zake aliweza kuja nchini Spain kwa ajili ya kukutana na wewe. Ila uliwafukuza kwa nini?”

“Sikuwafukuza, waliondoka wenyewe. Jambo ambalo nilio muambia ni kwamba siwezi kuandikisha mali zangu zote kwa mwanae. Mimi bado ni kijana, nina tafuta na si kwamba nitaishia kuzaa mtoto mmoja ni lazima nitazaa mtoto wa pili wa tatu na wengine mbeleni. Itakuwaje kwa hao ambao watazaliwa?”

Maelezo yangu haya yakawafanya watu waliopo ndani ya mahakama hii kuanza kunong’ono nong’ona hadi wakamfanya jaji kugonga nyundo mezani ili watu waweze kukaa kimya.

“Muheshimiwa sina swali jengine”

Mwanasheria wa Halima akaondoka. Ikawadia zamu ya Hawa kuhojiwa maswali na mwanasheria wangu ambaye nia shemeji yangu.

“Ahaa unaitwa Hawa Ramadhani”

“Ndio”

“Mtoto wa raisi aliye pita nchini Tanzania?”

“Ndio”

“Ulijuana vipi na Ethan?”

Hawa akaka kimya huku akinitazama.

“Nilimfahamu kupitia mama yangu. Aliweza kumsaidia mama yangu katika kiny’ang’anyiro cha kugombani uraisi na mama akashinda.”

“Baada ya kumsaidia mama yako kuwa raisi ukaona ndio nafasi nzuri ya kumtongoza”

“Ehee”

“Ndio ulimtongoza unabisha”

“Ahaa….nakumbua iikuwa chumbani”

“Hadi anaingia katika chumba chako, ikulu ni kwamba ulimkaribisha na hakuingia kwa bahati mbaya au kukosea njia”

“Ndio nilikaribisha”

“Baada ya kumkaribisha ukaanza kumshawishi ili azae na wewe kwa manaa uliona ni mtu maarufu na mwenye pesa?”

“Nilimueleza kwa upendo, azae na mimi”

“Imekuwaje upendo wako leo umehamia kwenye pesa zake. Nikisema kwamba ulikuwa ni mpango wa muda mrefu kuhakikisha kwamba una pata ujauzito ili uje kumfilisi?”

“Haukuwa mpango wangu. Nilimpenda Ethan tena sikuweza kufikiria juu ya pesa zake kwa maana hata mimi ninazo pesa zangu”

“Ila sio nyingi kama za Ethan”

“Ndio”

“Kila binadamu hapa duniani ana taka pesa. Kila mtu anaye tafuta ana hitaji pesa. Hivyo na wewe ulimtafuta mtoto ili upate pesa. Katika kipindi hicho Ethan alikuwa kwenye mahusiano na Biyanka na wewe ulikuwa una lifahamu hilo. Nikisema kwamba umezaa na mume wa mtu nitakuwa nimekosea?”

Hawa akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akimtazama shemeji usoni mwake.

“Baada ya kuzaa naye ukakimbia Marekani ili baba wa mtoto asiweze kumuona mwanaye. Baada ya maisha kukupiga na mama yako kuondoka duniani ukaona mtumie kiumbe wa watu ambaye hajui hata kinacho endelea uweze kujipatia tena pesa si ndio”

“Muheshimiwa pingamizi”

Mwanasheria wa Hawa alizungumza hukua kisimama.

“Pingamizi limekataliwa. Endelea na maswali”

“Ethan alipitia matatizo ya kutaka kuuliwa, ila hukumtafuta. Ila juzi ulipo sikia amepata dili la kuichezea Madrid ndio ukatoka huko ulipo toka kwa ajili ya kuja kurithi kirahisi mali zake anazo endelea kutafuta?”

“Hapana mimi nilipo sikia kwamba Ethan amepata ajali ya kusababishiwa. Nikaona nije Spain ili hata ikitokea akifa basi mwanangu ame pata haki kutoka kwa baba yake na hiyo ndio maana yangu kubwa.”

“Kwahiyo una muombea afe ili mwanao apate mali zake. Je mtoto wenu akifa mali atarithi nani?”

“Mwanangu hawezi kufa”

“Hakuna mwenye garentii ya kujua lini atakufa. Mamia ya watoto huwa wana kufa je mwanao ni nani asife?”

Maswali ya shemjeji yakazidi kumbana Hawa kwenye kona ambayo hakuitarajia.

“Muheshimiwa nina ushihidi ambao una muonyesha Hawa akishirikiana na x wife wa Ethan ambaye naye ana mipango madhubuti ya kumshusha chini Ethan kiuchumi”

Nikastuka sana kwani sijafuhamu ni wapi amepata ushahidi huu.

“Naomba niuwasilishe mbele ya mahakama yako”

“Unaweza”

Shemeji akafungua brufcase yake na kutoa flash. Akampa msimamizi wa mahakama , akaichomeka flash hiyo kwenye tv kubwa iliyopo hapa mahakamani.

Zikaanza kuonekana picha za Hawa na Biyanka wakiwa kwenye moja ya mgahawa, hapa nchini Marekani.

“Huyo ni Biyanka, mtoto wa aliye kuwa mgombea uraisi mzee Poul Mkumbo. Alikuwa ni mke wa Ethan, kwani walisha funga ndao kanisani. Biyanka na baba yake walikuwa na lengo la kumuua Ethan na kweli katika kipindi cha miezi takribani sita ambacho Ethan alisadikika kufa kwenye boti, yeye na baba yake ambaye kwa sasa ni marehemu waliweza kuhisika.”

“Hadi leo Biyanka ana kisasi cha kumuangamiza ETHNAN. Biyanka aliungana na Hawa ili waweze kujivunia utajiri wa Ethan. Ukisogeza mbele kuna ushahidi wamaneno naomba mahakama yako waweze kuusikiliza”

Shemeji alizungumza kwa kujiamini na kumfanya Hawa macho kumtoka. Wasiwasi anao uonyesha hakika unapekelea ushindi katika kesi hii.

“Habari”

“Salama nani mwenzangu”

“Biyanka, nina imani wewe ni Hawa”

“Ndio umejuaje mimi ni Hawa”

“Mimi na wewe tulisha wahi kuhudumiwa na mb** moja. Ila wewe mwezangu ulifanikiwa kupata mtoto. Nina imani kwamba umenifahamu”

“Yaa unataka nini Biyanka”

“Natambua unapo ishi, natambua mtoto wako anaye itwa ETHAN Jr. Kwaufupi nakujua wewe kwa silimia tisini na tisa. Moja uliniibia mume wangu kabisa wa ndoa na kuwa naye kimahusiano.”

“Jambo ambalo nina hitaji kukuomba Hawa. Nataka kuhakikisha nina mshusha chini Ethan. Ili niweze kukusamehe kwa kosa la kuniibia mume wangu wa ndoa. Ninahitaji ushirikiane nami”

“Biyanka ila Ethan yeye hajanikosea chochote mimi”

“Ila wewe umenikosea. Hivi unahisi ni adhabu gani ambayo ina kufaa wewe uliye niibia mume wangu wa ndoa na kuzaa naye?”

“Mmmmm!!!”

“Usigune. Kama nina jua ulipo, nini una fanya na mwanao hadi mahudhurio yake ya Cliniki ninayo. Basi nahitaji ushirikiane nami kwenye hili”

“Naomba muda wa kulifikiria”

“Katika hili hakuna muda wa kulifikiria. Ninacho kihitaji unipe jibu sasa hivi. Unashirikiana nami au hushirikiani nami”

“Kwa ajili ya mwanangu nipo tayari kushirikiana nawe. Niambie nini napaswa kufanya.”

“Nahitaji uende nchini Spain alipo Ethan na nina hitaji umshinikize aweze kumrithisha mwanao mali zake zote na endapo ata kubali, basi tutagawana. Asilimia stini ya mali itakuwa ni yangu na asilimia arobaini itakuwa ni mali zako na mwanao. Tukifanikisha hilo basi Ethan tutamuacha na nguo alizo vaa na atakuwa maskini wa kutupa”

Nikamtazama Hawa na kumshuhudia jinsi uso wake unavyo mwagikwa na machozi. Kama vile nilivyo hisi kwamba kutakuwa na mtu nyuma yake kumbu ni kweli, Biyanka bado ana endesha vita yake ya chini chini ili mradi anifilisi.



“Sawa je unahisi kwamba Ethan ana weza kukubaliana na mpango huo?”

“Huyo ni mwanaye na nilazima atakubaliana na wazo hilo. Hana ujanja na wala hato weza kupindua kwenye jambo hilo”

“Sawa nitafanya hivyo. Ila nisinge penda kuingia kwenye uhasama na Ethan kwa maana sina ugomvi naye”

“Ila kumbuka kwamba upo kwenye uhasama na mimi na endapo utakataa kulitekeleza hilo basi wewe na mwanao wote nita hakikisha hamuumalizi huu mwaka ni lazima niwaue”

Kauuli hiyo ya Biyanka iliyo rekodiwa, ikawafanya watu wote mahakamani kuanza kunong’ona tena na kumfanya muendesha mastaka kupiga nyundo mezani ili watuu wakae kimya”

“Sawa nitafanya hivyo”

“Nashukuru na mimi ndio nitakuwa nina kupigia ili niweze kufahamu ni nini kinacho endelea”

“Sawa”

Mwahojiano yakaishia hapo.

“Muheshimiwa nina imani kwamba umeweza kusikia juu ya mpango mbaya alio nao huyu msichana pamoja na mke wa zamani wa Ethan. Wanatumia kigezo cha mtoto kuhitaji kumfilisi. Nina imani kwamba mahakama yako ita toa haki katika hili. Ninawasilisha na sina swali jengine kwa Hawa.”

Baada ya shemeji kuzungumza hivyo, akarudi kukaa pembeni yangu huku akiwa na furaha sana kwa maana hadi hapa ilipo fikia basi mimi ndio mshindi wa hii kesi na tuna subiria maamuzi ya mahakama. Machozi yakaanza kunilenga lenga kwa kumuonea huruma Hawa. Masikini ameingia kwenye vita ambayo hata hakujua chanzo chake ni nini, mwisho wa siku ana ishia kwenye wakati mgumu sana.

“Nimeihahirisha mahakama, na hukumu itatolewa baada ya siku mbili zijazo.”

Jaji akagonga nyundo mezani na akasimama na kutufanya sote tusimame. Alipo weza kutoka tu mahakamani, waandishi wa habari wakaruhusiwa kuingia ndani ya chumba hichi na wakaanza kutuandama kwa kutupiga picha huku wakijaribu kutuhoji. Kwakusaidiwa na walinzi wetu tulio ambatana nao, tukaanza kutolewa ukumbini humu huku waandishi wa habari wakianza kutufwata kwa nyuma. Nikatamani hata kusimama ili niweze kusikia neno la Hawa atakalo niambia ila nikashindwa kabisa. Tukaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hili huku ulinzi ukiwa umezidi kuimarishwa. Mbele imetangulia gari inayo fanana na gari letu huku nyuma yetu kukiwa na gari jengine ambalo lipo sawa na gari letu. Magari haya yote yamejaa walinzi wanao hakikisha kwamba tuna kuwa salama ndani ya jiji hili la New York.

“Ethan, Ethan”

Sauti ya shemeji ikanistua sana kutoka katika dimbwi hili la mawazo na nikamtazama usoni mwake kwa macho yaliyo jaa machozi. Vivy akampa ishara shemeji asiniongeleshe jambo lolote.

“No zungumza”

“Ahaa niwemeza kuzungumza na kitengo cha CIA, na nimewaomba waweze kumfwatilia Biyanka popote pale duniani na wamkamate. Kwani ni lazima ata idhuru familia yako”

“Je Hawa ata fungwa?”

“Kwa mujibu wa sheria ni lazima aweze kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa maana ame panga mpango wa kuhitaji kudhulumu mali ya mtu. Ila kifungo chake yeye kitakuwa ni kidogo kwani ameshirikishwa kwenye mpango kwa kushinikizwa”

“Kifungo chake kidogo kitakuwa ni muda gani?”

“Ndio hiyo miaka miwili”

“Ohoo Yesu wangu. Kwa hiyo daaaa……. Mwanangu ataishije?”

“Hapa mahakama ni lazima itakukabidhi wewe mwanao”

“Ushahidi ule umeupatia wapi na ni kwanini hukuweza kunijulisha juu ya ushahidi huo”?

“Ethan, kampuni yangu ina vyanzo vingi sana vya kujipatia ushahidi nyeti kama huu. Pia sikuweza kukusikilizisha huu ushahidi kwa maana kuna mambo mawaili ambayo ungeweza kuyafanya. Moja kukubaliana ushahidi ufikishwe mahakamani, au mbili uweze kuusitisha ushahidi kufikishwa mahakamani kwa lengo la kumlinda tu Hawa. Ninaelewa ni jinsi gani ambayo una jisikia ndani ya moyo wako, ila hatuna jinsi ni lazima tuweze kukubakiana na hili ambalo limetokea”

Sikuwa na jambo la kuzungumza zaidi ya kumtazama shemeji usoni mwake. Tukafika hotelini na kukuata waandishi wa habari wakihitaji japo kunihoji maswali kadhaa. Walinzi wakatuzuia na tukafanikiwa kuingia kwenye lifti. Moja kwa moja tukapelekwa hadi katika vyumba vyetu.

“Nahitaji kupumzika. Baada ya masaa matatu ndio muniamshe”

Nilimuambia shemeji na Vivy huku nikiwa nimesimama mlangoni mwangu.

“Sawa”

“Ethan nina weza kuzungumza na wewe jambo?”

Nikamtazama Vivy usoni kwa macho makali hadi akaniogopa. Nikafungua mlango na kuingia ndani na kuufunga kwa ndani. Huku nje ya chumba changu nikiwaacha walinzi wakie wana linda eneo zima la hii kordo.

“Hei”

Sauti ya Ethan aliye simama kwenye moja ya kona katika hichi chumba ikanistua sana na kujikuta nikimtazama pasipo kuzungumza chochote.

“Nimekuja kukuaga rafiki yangu”

“Kuniaga kivipi?”

“Hatuto weza kuonana na mimi tena kwenye maisha yako yaliyo baki. Nimeweza kufanikisha ile haja ya moyo wako ambayo ulikuwa nayo toka utotoni”

“Haja gani Ethan, mbona na wewe una taka kuni changanya?”

Ethan akatabasamu huku akinisogelea. Akanishika begani huku akinitazama.

“Unakumbua siku ulipo kuwa mdogo, katika chumba kimoja ndani ya hoteli jijini Dar es Salaam. Ulikuwa na hamu ya kufanya nini?”

Swali hili la Ethan likanirudisha katika kumbukumbu zangu za miaka mingi sana ya nyuma. Nikakumbuka jinsi nilivyo kuwa na hamau ya kuweza kupata NGUVU(POWER) katika jamii ya Tanzania na dunia kwa ujumla.

“Ndio nimekumbuka”

“Hadi sasa hivi dunia nzima imeweza kukufahamu. Umekuwa na nguvu kubwa ya ushawishi katika dunia, umekuwa ni mtu ambaye una tazamiwa kama kijana mwenye mafanikio makubwa sana. Hivyo hakikisha kwamba huo urithi ulio nao una warithisha kizazi chako. Nguvu uliyo itengeneza kwenye familia yako hakikisha kwamba haipotei. Hakikisha kwamba una kuwa zaidi ya mtu bora duniani ambaye alisha wahi kutokea.”

Ethan alizungumza kwa upole na unyonge sana. Hii ni mara yangu ya kwanza kumuona Ethan akialengwa lengwa na machozi. Machozi ya Ethan yapo mithili ya damu ni tofauti na machozi ambayo sisi binadamu wa kawaida yametutoka.

“Kwenye kipindi chote nilicho kuwa na wewe. Nilihakikisha kwamba nina timiza haja ya moyo wako. Nina kutenga mbali na maadui zako na unafanikiwa kuwaangusha maadui zako. Baada ya Biyanka sasa huto kuwa na adui mwengine yoyote”

“Ila Camila ume msahau?”

“Hahaaa….Camila hato weza kukugusa tena kwani naye haja ya moyo wake ilisha weza kutimia. Bomu linalo litengeneza kama nilivyo kupa ahadi, litawasambaratisha wao wenyewe siku ya majaribo hivyo stori yake kwenye uso wa dunia itakuwa imeishia hapo.”

“Ahaa kwa nini sasa huto unana na mimi, ikiwa wewe na dada yangu muna mahusiano?”

“Nimeweza kumpa ruhusa dada yako kuolewa na mwanaume mwengine. Nimpa ruhusa ya kuisha maisha yake ya kawaida na kutengeza familia kama haja ya moyo wake ulivyo kuwa una hitaji. Mimi nitapotea kwenye uso wa ulimwengu na huto niona tena rafiki yangu”

Nikajikuta nikishusha pumzi huku nami machozi yakianza kunimwagika. Hakika Ethan amekuwa ni rafiki aliye nisaidia kwenye mambo mengi sana.

“Ethan mimi ni jini, japo nina jiweka katika umbo la kibinadamu kama wengine, ila mimi ni jini. Sisi pia majini tupo chini ya Mungu. Huwa hatufi ila tunatoweshwa tu katika ulimwengu huu, duniani hatuwezi kuwepo, wala kuzimu hatupo, hivyo tuna eneo ambalo tunafungiwa na hatuto weza kutoka hadi mwisho wa ulimwengu huu. Muda huo sasa kwangu umekaribia ndio maana nimekuja kukuaga rafiki yangu”

Maneno ya Etha yakanifanya nizidi kushindwa kujizuia. Nikaangua kilio kizito, akanikumbatia na kuanza kunipiga piga mgongoni mwangu.

“Zoea rafikia yangu ila nina zawadi moja ya mwisho ambayo nitakuachia”

Ethan alizungumza huku akiniachia taratibu. Akanitazama usoni mwagu kwa sekunde kadhaa pasipo kuzungumza chochote kisha akanishika kwenye paji langu la uso kwa mkono wake wa kulia. Nikahisi ubaridi mkali ukipita kwa kasi kuanzia kichwani mwangu hadi kwenye nyanyo za miguu yangu.

“Ninakupatia nguvu ya kuweza kuona mambo yajayo. Ninakupatia nguvu ya kuweza kucheza soka kuliko wachezaji wote walio wahi kutokea hapa duniani. Si Pele, si Maradona wala Mesi. Utaweka historia kwenye ulimwengu wa soka ambayo mwanao pekee tu ndio atakuja kuifunja. Utazaa watoto wenye vipaji vikubwa sana duniani na wataheshimika na kuogopewa kwa uwezo wa vipaji vyao walivyo navyo. Utaishi miaka mingi pasipo kuumwa wala kukumbwa na maradhi yatakayo kuondoka duniani. Pokea hivyo”

Gafla nikahisi mwili mzima ukiishiwa na nguvu na kujikuta nikianguka chini na kupoteza fahamu.

***

Kengele ya mlangoni inayo ashiria kuna mtu ana bisha hodi ikanistua sana, nikafumbua macho yangu na kuchunguza eneo hili na kugundua kwamba nipo ndani ya chumba changu, katika hoteli hii tuliyo kodisha. Nikajikuta nikiwa nimelala kitandani, nikiwa na nguo zangu zote. Nikashuka kitandani huku nikipiga miyayo ya uchovu. Nikajinyoosha viungo vyangu kwa sekunde kadhaa kisha nikatembea hadi mlangoni na kuufungua.

“Ohoo asante Mungu umefungua”

Vivy alizungumza huku wakiingia ndani humu na shemeji.

“Kuna nini?”

“Ethan masaa matatu uliyo tuambia tukuamshe yamesha pita. Tumesimama hapo mlangoni tukigonga kwa zaidi ya robo saa. Hadi tukahisi kuna tatizo ambalo limekukumba. Nikata kuwajulisha uongozi wa hoteli il anikaona nitatengeneza tetesi nyingine ambazo sio nzuri kwa sasa”

Shemeji alizungumza huku akitazama tazama ndani ya chumba hichi.

“Woga wenu. Hakika nimechoka sana”

Nilizungumza huku nikiendelea kupiga miyayo mingi sana. Nikaka kitandani huku nikiwatazama.

“Lazima tuwe waoga. Kwahali jinsi ilivyo ni lazima tujawe na wasiwasi”

“Ethan nimepoke simu kutoka kwa mkuu wa kitengo cha CIA. Kina hitaji uweze kudhibitisha kwa kinywa chako kwamba Biyanka aweze kukamatwa”

“Mimi niidhinishe juu ya kukamatwa kwake. Sasa hapo mimi ni nani hadi niidhinishe?”

“Wewe ni mume wake wa ndoa ambaye unajulikana. Pia kumbuka Biyanka ni Mtanzania na wala si Mmarekani, hata wanapo kwenda kufanya kazi yao nje ya Marekania, basi wanahitaji idhini yako”

“Waambie nimekubali”

Shemeji kwa kutumia simu yake ya mkononi. Akapiga video call kwa mkuu wa kitengo cha CIA. Baada ya simu hiyo kupokelewa, akanikabidhi na nikaonana na mwana mama huyu mwenye asili ya Afrika na ana sura mbaya kiasi. Sauti yake nzito ikanifanya nimtazame pasipo kuijibu salamu yake.

“Ethan nina subiria jibu lako”

“Ohoo salama, juu ya swala la kukamatwa kwa mke wangu nimekubaliana nalo”

“Basi tutaswasiliana na wewe pale tu zoezi hili litakapo kwisha”

“Nashukuru”

Simu hiyo ikakatwa na kumrudishia shemeji simu.

“Huyu mwana mama mbona kama mwanaume?”

“Wee acha tu, ila ndio majukumu yao. Kwenye vitengo kama hivyo huwezi kuwa kiongozi, ukwia lege lege”

“Mmmm haya”

“Ila sijawauliza ni wapi alipo Biyanka kwani waliniambia wana taka kwenda nchini Tanzania”

Nikajikuta nikifumba macho na kuanza kumfikiria Biyanka eneo alipo. Kama jinsi computer inavyo tafuta mafaili yaliyo hifadhiwa ndani ya computer hiyo, ndivyo jinsi akili yangu nayo ilivyo fanya kazi kwa kasi sana. Nimashudia Biyaka akiwa nchini Afrika Kusini katika mji wa Cape Town, akili maisha na mume wake.

“Hayupo Tanzania”

“Nani?”

“Biyanka”

“Umejuaje?”

Nikafumbua macho yangu na kumtazama shemeji usoni mwake.

“Waambie CIA, waelekee nchini Afrika kusini katika mji wa Cape Town ndipo watakapo mpata Biyanka na wasijishumbe kwenda Tanzania”

Shemeji akampigia mwana mama huyo na kumpa taarifa hiyo na akashukuru sana na kuahidi atatuma kikosi chake kwenda nchini humo. Mlango ukagongwa na sote tukautazama.

“Kuna mgeni yoyote ambaye mulipanga aonane na mimi?”

“Hapana”

“Je muliagizia chakula?”

“Hapana”

“Sasa atakuwa ni nani?”

“Sijajua kwa kweli”

Shemeji akataka kwenda kufungua mlango ila nikamzuia. Nikawaomba waweze kukaa eneo ambalo mtu ninaye kwenda kumfungulia mlango hato weza waona. Nikatambea kwa hatua za kujiamini hadi mlangoni, taratibu nikaufungua mlango huu. Nikajikuta nikistuka sana mara baada ya kumuona Hawa akiwa amesimama huku mikononi mwake akiwa amemembeba mwanangu Ethan Jr. Tukatazamana na Hawa kwa sekunde kadhaa na machozi yakaanza kumbubujika huku walinzi wanao tulinda wakiwa wamemzunguka kuhakikisha kama ana jambo lolote baya analo hitaji kunidhuru nalo asiweze kufanikiwa kulitekeleza.



“Ni sawa.”

Niliwaambia walinzi hawa na taratibu wakatawanyika, ila umakini wao wote upo kwa Hawa.

“Ingia ndani”

Shemeni na Vivy wakabaki wakiwa wamejawa na mshangao mkubwa . Hapakuwa na mtu aliye weza kutaraji ujio wa Hawa katika eneo hili. Nikamkaribisha Hawa kwenye kiti, na taratibu akaka huku akiwatazama Vivy na shemeji. Kwaishara nikawaomba Vivy na shemeji waweze kutoka nje na waniache na Hawa tuweze kuzungumza.

“Ethan”

“Naam”

“Kuna ule usemi ambao unasema kwamba. Mwanamke mjinga ata ivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe”

Hawa alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio”

“Mimi ni miongoni mwa wanawake hao wajinga. Ethan sikupanga kukusaliti siku hata moja wala sikufikiria kuenenda kinyume na wewe. Nina nina imani kwamba moyoni mwako unanijua na ninahisi ulinishangaa kwa nini nimekuwa nikifanya mambo haya yote. Nakumbuka kipindi nilipo kuwa nina fanya mambo hayo sikuweza kukutazama machoni mwako. Kwani nilifanya kwa kushinikizwa.”

“Kwa nini hukuniambia kwamba Biyanka yupo nyuma ya hili jambo?”

“Kila nilicho kuwa nina kifanya, kila nilipo kuwa nina kwenda aliweza kuweka watu wake ambao walinichunguza na kunifwatilia kwa kila hatua na sikuweza kufanya jambo lolote. Hata simu zangu zote ni lazima zilipitie kwake ndio zimfikie muhusika. Hata kuja kwako Spain ni yeye aliye weza kunipa watu wa kunileta huko na hata yule dereva, hakuwa dereva kama ulivyo muona ila ni mtu wake. Ndani ya moja ya begi kulikuwa na laptop ambayo ndani yake kulikuwa na bomu. Si jambo rahisi kwa mashine au askari wote wa uwanja wa ndege kuweza kufahamu kwamba ndani ya hiyo laptop kuna bomu. Hivyo siku ile ningeenenda kinyume na wewe, basi angelilipua bomu hilo na mimi, wewe na mtoto tungekufa kwa pamoja”

Hawa alizungumze huku akiendelea kumwagikwa na mchozi.

“Ili kukulinda wewe ilinilazimu kuondoka nyumbani kwako. Ila njia nzima nilikuwa nina lia kwa uchungu sana. Si kwa uchungu wa kushindwa kukubaliana na maamuzi yako. La hasha, nilikuwa nina umia kwa maana nina mzigo mkubwa sana kwenye maisha yangu. Niwalinde wewe na mwanao. Nisamehe Ethan, hata mama yangu huko alipo nina imani kwamba ana fahamu hali ngumu ambayo mwanaye nina pitia”

Maneno ya Hawa yakanifanya nianze kulengwa lengwa na machozi huku nikijizuia kuulainisha moyo wangu kwa haraka kutoa msamaha ambao sijajua kwamba una faida gani au madhara gani kwangu.

“Mimi kwa sasa ni mfungwa. Nipo tayari kupokea kifungo ambacho nina stahili kwa hili kosa ambalo nimekufanyia. Ila ninacho kiomba ni kukuachia mwanangu kwa mema tu. Huyu ni mtoto wetu sote japo hapo mwanzo nimetanguliza ubinafsi wa mwanangu. Mlee kwenye maadili ya kupendeza, hakikisha kwamba ana kuwa ni kijana mwema. Hakikisha una mueleza mema juu yangu na bibi yake. Tafadhali usije kupandikiza chuki dhidi ya familia ya mama yake.”

Hawa taratibu akanyanyuka kwenye hichi kiti na kunikabidhi mtoto.

“Mtoto ana penda sana kuangalia katuni, kucheza na midoli pia kuangalia mpira. Anapenda sana maziwa ya choclate pamoja na ndizi zilizo pondwa. Ambazo sisi kule Moshi tunaziita mtori”

Nikampokea mwanangu huku nikiendelea kushangaa maamuzi haya ya Hawa.

“Natambua miaka miwili ambayo nina weza kuhukumiwa na kukaa jela, mwanangu atakuwa ana kuwa vyema mikononi mwako. Nina kuamini sana Ethan na wewe ndio mwanaume wa pekee ambaye nina kupenda. Haito kuja kukaa itokee nimpende tena mwanaume mwengine.”

Hawa mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akaanza kutembea kuelekea mlangoni, kwa haraka nikamuweka kitandani mtoto na kumuwahi kumzuia.

“Unaondokaje pasipo kusikia neno langu”

“Ethan mimi ni mkosaji kwako. Natambua kwamba huwezi kunisamehe tena kwenye haya maisha. Ila zawadi ya mtoto hiyo hapo, tafadhali mlee vizuri mwanangu.”

Nikaufunga mlango wa chumba hichi kwa ndani na kuiweka fungua mfukoni. Nikamshika Hawa mkono na kuingia naye bafuni, nikafungulia maji ya bomba ili hata kama Vivy na shemeji watakuawa wana sikilizia mazungumzo yetu, basi watashindwa kusikiliza kinacho endelea. Nikafungua zipu ya gauni hili refu alilo livaa Hawa na kumfanya ajawe na mshangao.

“Ethan una hitaji kufanya nini?”

Hawa alizungumza huku akinigeukiwa kwa haraka na kunitazama usoni mwangu. Sikumpa muda wa kutoa swali jengine kinywani mwake. Nikaanza kumnyonya lispi zake kwa hisia kali, japo kwa awali Hawa alijifanya kuleta vipingamizi vya hapa na pale ila mwisho akajikuya akilegea kabisa. Nilipandisha gauni lake hili juu huku chupi yake nikiishusha chini. Nikafungua zipu ya suruali yangu na taratibu nikaanza kukumbukia enzi zetu za mahusiano. Hakika utamu wa Hawa bado upo vile vile, japo amejifungua, ila tunda lake bado lina ubora mkubwa sana kwangu.

“Umekutana na mwanaume gani baada ya mimi?”

“Sijawahi kuwa na mwanaume yoyote zaidi yako Ethan. Wewe ndio mwanaume wangu kwa kwanza na wa mwisho”

Hawa alizungumza huku akilalama kwa sauti ya mahaba. Dakika thelathini, zikatutosha kuridhishana kwa shuhuli hii kabambe.

“Kwa nini umeamua kunitomb** ikiwa kwako ni mkosaji?”

“Mkosaji ni kwa macho yaw engine. Ila mimi nina kujua, mama yako nina mjua na laiti kama ingekuwa si Biyanka usinge fanya haya yote”

“Nashukuru kwa kulitamba hilo”

“Nitahakikisha kwamba hii kesi ina fungwa kabla haijafika tamati”

“Hapana Ethan, acha nitumikie hichi kifongo. Hichi kifungo ni haki yangu tafadhali sana baba Ethan Jr acha nikitumikie hichi kifungo”

Hawa alizungumza kwa upole sana huku akiziweka sawa nguo zake.

“Una uhakika una hitaji kuhukumiwa?”

“Ndio Ethan acha sheria ifwate mkondo wake. Huwezi jua Mungu ana makusudi gani juu ya hili”

Tukakumbatiana na Hawa kwa dakika kadhaa, hichi ni kipindi kigumu sana kwa Hawa anacho kipitia kwenye maisha yake. Tukarudi chumbani na kumkuta Ethan Jr akiwa ana jigeuza geuza kitandani kwa furaha.

“Naomba tupige picha ya ukumbusho”

Nilizunugmza na kumfanya Hawa kutabasamu. Tukaanza kupiga picha kadhaa kwa kutumia simu yangu. Zoezi hili lilipo isha. Hawa akaniomba aweze kuondoka na kurudi nyumbani kwake.

“Je naweza kupafahamu kwako?”

“Hapana”

“Kwa nini?”

“Hapana Ethan. Waandishi wa habari wapo kila sehemu. Sihitaji kukuchafua kama nilivyo fanya hivi. Nakuomba niweze kurudi nyumbani”

Sikuhitaji kuyapinga maamuzi ya Hawa, nikamfungulia mlango na akatoka ndani humu na kuwafanya Vivy na shemeji kuingia kwa haraka huku wakiwa wamejawa na mshangao kumuona mtoto amebaki kitandani.

“Imekuwaje amemuacha?”

“Ni maamuzi yake binafsi, nitamlea huyu mtoto”

“Ethan kweli huu sio mtego?”

“Hapana, nina mfahamu Hawa na hili alilo lifaya ni kwa ajili ya usalama wangu na mwanangu. Hivyo musimuhukumu kwa kumtazama tu”

“Ila Ethan huyu mwanamke ni mshenzi sana hakupaswa hata kukuona”

Vivy alizungumza kwa jazba kidogo.

“Vivy kumbuka huyo mwanamke unaye mzungumzia ni mama wa mwanangu. Mwanamke aliye hakikishana ana pambana kulinda familia yake. Na siku nyingine nisikusikie una mzungumzia vibaya Hawa. Si wewe wala si shemeji, mumenielewa?”

Nilizunugmza kwa kufoka kidogo na kila mtu akaitikia kwa unyonge kwani mimi ndio mwenye maamuzi ya mwisho.

Siku ilivyo fwata mkuu wa kitengo cha CIA, akatupa taarifa kwamba wamefanikiwa kumkamata Biyanka na yupo njiani kuletwa nchini Marekani kwa ajili ya kusomewa mashtaka. Kwaupande mmoja ama mwengine, ni jambo lililo jaa furaha sana kwetu. Ila moyoni mwangu, nina hamu sana ya kuweza kupata nafasi ya kuzungumza na Biyanka, ili niweze kumuuliza ule upole wake na unyenyekevu wake alio kuwa ana nionyesha umeishia wapi.

“Ethan kesho ndio siku ya mahakama. Je unahitaji kushikilia msimamo wa kumuweka kizimbani Hawa, ikiwa mtoto amemuacha hapa?”

Shemeji aliniuliza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni.

“Acha mahakama ifanye kazi yake”

“Sawa”

“Ila nipangie utaratibu wa kuonana na Biyanka mara baada ya kufikishwa hapa Marekani”

“Sawa”

Shemeji akaanza kushuhulikia jambo hilo. Kwabahati nzuri tukapewa nafasi ya kuonana na Hawa. Majira ya saa sita usiku, tukaja kuchukuliwa hotelini hapa na askari wa kitengo cha CIA. Kwakutumia helicopter yao, moja kwa moja tukaeleka hadi makao makuu ya kitengo hicho. Mimi na shemeji tukaruhusiwa kuingia katika chumba alicho fungiwa Biyanka, ambaye mara baada ya kuniona alistuka sana.

“Umekuja kunikejeli au?”

Biyanka aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Shemeji naomba utupishe”

“Sawa Ethan”

Kwenye kila kona ya chumba hichi kimefungwa kamera ambazo zina rekodi kila kitu ambacho kina endelea ndani humu.

“Itakuwaje nikukejeli ikiwa ulihitaji kuchukua mali zangu kwa kumtumia mwanamke niliye zaa naye. Kwa nini umekuwa hivi Biyanka. Ile hekima kama mke ilipotelewa wapi, au ulikuwa una igiza?”

“Kama vile ulivyo kuwa una tuigizia sisi kwenye yetu familia ndivyo jinsi nami nilivyo fanya. Alafu nina jilaumu ni kwa nini sikukuu toka kipindi kile. Nisinge kuwa nina sumbuliwa kama hivi”

“Biyanka isiwe hivyo. Bifu la baba yako na mimi kwa nini ulihitaji kulita kwangu. Baba yako aliniulia wazazi wangu na kuwapokonya ardhi yao yenye madini. Kwanini sasa wewe umeamua kunirudi mimi”

“Ethan sijakuja kusikiliza stori za nyuma hapa. Ondoka na wala usihisi kwamba nina jutia kwa kila nililo lifanya kwako. Hapana, sina majuto ya aina yoyote.”

Maneno ya Biyanka yakazidi kunishangaza. Hakika wanawake ni watu wa ajabu sana, kwa jinsi alivyo kuwa ananifanyia Biyanka wala sikudhani kama ana weza kubadilika na kuwa mkatili hivi.

“Ombea nife ila kama sinto kufa nitahakikisha kwamba sikuachi uwe na amani na nilazima nikuue tu Ethan Klopp. Ulizifuta ndoto za wazazi wangu, na mimi nilazima nifute ndoto zako”

Biyanka alizungumza kwa ukali saha huku akihangaika hangaika kwenye kiti hichi, huku miguu yake na mikono yake vikiwa vimefungwa pingu. Machozi yakaanza kunilenge langa, hakika roho ya kikatili aliyo pandikizwa Biyanka haito weza kubadilika.

“ETHAN KLOPPP NI LAZIMA NIKUUEEE WEWEEEEE”

Biyanka aliendelea kuzungumza kwa ukali hadi askari wawili wakaingia ndani humu ili kuhakikisha kwamba Biyanka hanidhuru kwa lolote. Sikuwa na jambo lolote la kuzungumza zaidi ya kusimama na kutoka ndani humu huku macho yangu yakiwa yamejawa na ukungu wa machozi.

“Nahitaji kurudi hotelini”

“Ila umridhika kwa kumuona?”

Mkuu wa kitengo hichi cha CIA, aliniuliza.

“Ndio”

“Basi safari njema”

Tukaingia kwenye helicopter, Vivy akanikabidhi mwanangu na kumpakata mapajani. Tukafika hotelini na moja kwa moja nikelekea chumbani kwangu. Asubuhi na mapema nikwa wa kwanza kuamka, nikafanya mazoezi ya viongo kama kawaida. Baada ya kupata kifungua kinywa majira ya saa nne kasoro tukaelekea mahakamani kusikiliza hukumu ya mahakama. Nikaonana na Hawa ila safari hii amekuwa ni mnyonge sana kiasi cha kumfanya apoteze furaha. Muda wa kuendeshwa mastaka ukaanza huku makosa ambayo nilistakiwa nayo hapa mahakamani yakianza kusikilizwa.

“Mahakama imechukua maamuzi ya kumrejesha mtoto Ethan Jr, mikononi mwa baba yake. Pia mahakama imemkuta na hatia bi Hawa Ramadhani na atahukumiwa kifungo cha nje kwa miaka miwili. Hato ruhusiwa kukutana na mwanaye kwa kipindi hicho cha miaka miwili wala kutoka nje ya jiji la New York wala Marekani”

Baada ya maamuzi hayo jaji akagonga nyondo mezani akimaanisha kwamba maamuzi yamesha pitishwa. Jaji alipo toka mahakamani, nikamfwata Hawa alipo simama huku askari wa kike wakiwa tayari wamemzunguka.

“Naomba niweze kuzungumza naye”

Maaskari wakaniruhusu. Nikamsogelea Hawa, huku nikiwa nimejawa na tabasamu usoni mwangu.

“Wewe bado ni familia yangu. Kuwa huru kunipigia muda wowote”

“Sawa Ethan, nashukuru kwa hukumu hii pia.”

“Nina imani kwamba namba yangu una ifahamu”

“Ndio”

“Haya”

Hawa akambusu mwanaye kwa mara ya mwisho kisha akanikumbatia kwa nguvu, huku watu wengi mahakamani wakiwa wana shangaa ni kwa nini tuna kumbatiana ikiwa Hawa ndio mkosefu. Hawa akondoka mahakamani hapa chini ya ulinzi wa askari na katika kipindi cha miaka miwili atakuwa ana lindwa na askari popote aendapo katika jiji hili la New York na itampasa kuhasaini mahakamani kila siku, asubihi na jioni kwamba yupo ndani ya jiji hili. Tukarudi hotelini na kuchukua kila kicho chetu na kuelekea uwanja wa ndege. Waandishi wa habari wakatuvamiwa uwanja wa ndege huku wengi wao wakihitaji kusika japo neno kuhusiana na keshi hii.

“Ni maamuzi mazuri waliyo yatoa mahakama. Nitahakikisha kwamba nina ishi na mwanangu katika mazingia mazuri”

“Je mama yake hato onana naye?”

“Inabidi kufwata sheria za mahakama. Siwezi kukiuka maamuzi hayo hivyo kila jambo kuanzia sasa litaenda kama vile sheria ilivyo hitaji. Ninashukuru sana ninaomba niweze kuwahi ndege”

Walinzi wakanisaidia kunipitisha katikati ya waandishi hawa wa habari ambao kila mmoja ana jitahidi kuchukua picha ya ukumbusho. Tukaingia kwenye ndege huku nikiwa nimebeba mwanangu, nataratibu safari ya kurudi nchini Spain ikianza.

***

Jina langu la ETHAN KLOPP, likazidi kutawala ulimwenguni. Uwezo wangu wa kupachika magoli kwa timu pinzani, ukaanza kufifisha stori za Messi na Ronaldo katika ulimwengo wa soka. Hakika uwezo alio nipatia Ethan, umenifanya kila mechi nina funga magoli matatu kuelekea juu. Timu pinzani, zikazidi kuniogopa mimi pamoja na timu yangu ya Real Madrid. Mabeki na makipa wa timu zote za Spain na timu zinazo shiriki kombe la UEFA, nao waliweza kunigopa. Katika ishirini za mzunguko wa kwanza wa ligi hii ya Laliga Santander, nimefanikiwa kufunga magoli stini ikiwa ni histori kubwa na ya kipekee ambayo nimeweza kuiweka katika ligi hii na dunia kwa jumla.

Miezi miwili iliyo pita nimeweza kuihamishia familia yangu, dada yangu pamoja na Latifa nchini hapa Spain na wote wana ishi na mimi huku Qeen akibaki nchini Tanzania kama msimamizi wa mali zangu zote ikiwemo mgodi wambao hapo awali ulikuwa una mikikiwa na mzee Mkumbo.

“Ethan”

Hawa alinitaza kwa sauti ya upole huku tukiwa tuna zungumza kupitia video call

“Naam”

“Unakumbuka siku ambayo tulifanya mapenzi pale hotelini?”

“Ndio nina kumbuka”

“Basi siku ile nilikuwa kwenye siku zangu za hatari na niliweza kutoka na ujauzito”

“Weee”

“Ndio Ethan”

“Sasa kwa nini hukunieleza siku zote hizo na tunazungumza mara kwa mara”

“Nilikuwa nina tafuta nafasi hiyo ya kukueleza. Madaktari wameniambia kwamba mtoto atakaye zaliwa ni mtoto wa kike”

“Ohoo asante Mungu”

“Ndio, nina imani huyu atakuwa ni zawadi yangu kwa maana kwa sasa umenieleza una ishi na mwanamke mwengine”

“Ndio ila haijalishi wewe ni mke wangu na una mimba yangu na kama ingekuwa sio kifungo basi ningehakikisha una kuja kishi nchini Spain. Ila hakikisha kwamba una linda mimba yangu”

“Sawa mume wangu”

Baada ya kupata taarifa hii sikuhitaji kumficha mtu yoyote wa familia yangu. Latifa akafurahia kwa ujia wa mtoto huo wa mwanamke mwenzake huku naye tumboni mwake akiwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na nusu. Baada ya miezi kadhaa, Hawa akajifungua mtoto huyo wa kike na nikaenda kumuona nchini Marekani na nikawatangazia ulimwengu kwamba kwa sasa nina mtoto wa pili niliye zaa na Hawa. Kila mtu aliweza kunipongeza kwa hilo. Wanasheria wangu wakiongozana na shemeji yangu wakafwatilia juu ya hukumu ya Hawa aliyo patiwa. Wakakata rufaa na kuomba mahakama iweze kumuachia huru Hawa, kutokana mimi na Hawa tumebahatika kupata mtoto mwengine, hakuona haja ya kuendelea kumshikilia Hawa na wakaamuachia Huru. Kutokana Marekani hakuna makazi yangu, nikarudi na Hawa pampja na mwangu nchini Spain na tukaendelea na maisha yetu ya kila siku.

Hapakuwa na ugomvi wowote kati ya Hawa na Latifa na wote ninaishi nao nyumba moja. Nikaushangaza ulimwengu pale nilipo funga nao ndoa siku moja wote wawili jambo ambalo watu wengi waliweza kunisifu kwa kuweza kuwaweka wanawake hawa chini ya uangalizi wangu na wote wana nitii na kunijali.

Makombe mfululizo ninayo ishaida timu yangu kuchukua, yakaambana tuzo nyingi, huku nikiwa mchezaji wa pili kuchuku tuzo ya mchezaji bora wa duniani(ballon d’or) kutoka katika bara la Afrika.Wakwanza akiwa ni Geogre Weah. Mafanikio yangu katika soka, yakaisadia timu yangu ya taifa ya Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza katika kombe la dunia.

Mamilio ya watu nchini Tanzania, mategemeo yao na matumaini yao wameyaweka kwangu katika mashindano haya ya kombe la dunia. Si watanzani tu, ila hata waafrika wana tazamia timu yetu ya taifa ya Tanzania iweze kuchukua kombe hili. Mimi na timu yangu ya taifa tukaeleka nchini Russia kwa ajili ya mashindano haya huku wake zangu na wanangu, wanangu na wifi yao wakija nchini Russia kushuhudia kombe hili.

Mashindano haya yakanza huku kundi letu tukiwa tumepangwa na Ujerumani, Mexco na Canada. Katika mzunguko wa mandi tukafanikiwa kumaliza wa kwanza huku nyuma yetu tukifwatiwa na Ujerumani. Mashindano haya yakazidi kutuendea vizuri hadi tukafanikiwa kufika fainali huku tukiwa tumekutana na timu ya Spain ambayo kwa asilimia kubwa wachezaji wake wanacheza timu ya Madrid na Barcelona.

Mtangange huu wa mwisho katika mashindano haya ya kombe la dunia, umesheheni mashabiki wengi sana. Katika siku zote za maisha yangu ya soka leo, ndio nimecheza kwa kiwango changu chote. Hakika nimekuwa mwiba sana kwa wapinzani wezangu, ambao kwa mara kadhaa walijikuta wakinicheza rafu za makusudi ili kuhakikisha wana nitoa nje ya kiwanja kabla hata ya dakika tisini kuisha.

Faulu niliyo chezewa nje kidogo ya boksi la kipa upande wa upinzani, dakika ya tisini ikanifanya nitulize akili yangu sana kwani hadi sasa hakuna timu iliyo ona goli la mwezake kwa kufunga. Nikauweka mpira sehemu ambayo refarii aliagiza mpira huo uwekwe. Nikarudi nyuma kwa hatua nne huku nikiwatazama wachezaji wa Spian wakijipanga vizuri kuhakikisha kwamba mpira huo hauingii golini.

“Ethan una piga au nipige?”

Mchezaji mwezangu aliniuliza.

“Nianzie huu mpira kidogo”

“Sawa”

Refa akapiga filimbi, mchezaji mwezangu akafanya kama nilivyo muagiza, nikapiga shuti la chini chini la likaingia katika mwamba wa chini kabisa na kuwafanya mashabiki waliopo hapa uwanjani kunyanyuka kwa furaha. Nikakimbia karibu na neo la konana nikaanza kuserereka kwa magoti huku machezaji wezangu wakinifwata kwa nyuma. Wakaniangukia kwa juu huku nikiwa nimelala chali. Dakika tano zilizo ongezwa, zikwa ni ngumu sana kwetu kwani wapinzani wetu wana leta mashambulizi kuhakikisha kwamba wana komboa goli hili. Ikatulazimu wachezaji wote kurudi nyuma kuhakikisha kwamba goli hilo alirudi. Mapambano haya yakaamuliwa na refa dakika ya tisini na tano. Wachezaji wezangu wote wakanikimbilia na kuanza kuninyanyua juu huku ndoto ya Watanzania na waafrika wengi kwa timy moja barani hapa kuchukua kombe la Dunia. Hadi nikamabidhiwa kombe hili ambalo sikuwahi kulishika maishani mwangu, ndio nikaamini kwamba nimeshinda kombe hili. Hakika nimekuwa mchezaji wa kwanza wa bara la Afrika kushika kombe la Dunia. Tukarudi nchini Tanzania huku tukipewa heshima kubwa sana na kupokelewa mithili ya wafalme. Raisi kwa heshima niliyo iletea nchi yangu ya Tanzania, akanizawadia mji mzima wa Kigamboni na ukabadilishwa jina na kuitwa ETHAN LAND huku kukiwa na sanamu langu kubwa sana lililo jengwa katika mji huo.

Baada ya miaka miwili nikajenga kiwanja kikubwa cha mpira katika mji wangu wa ETHAN LAND. Huku nikimiliki timu ya mpira iitwayo KIGAMBONI FC.

Maisha yangu ya soka yakendelea kung’rata siku hadi siku, katika mufa mfupi sana nikafanikiwa kuvunje rekodi ya magoli ya nguli wa mpira duniani Pele na nikwa mchezaji wa pekee ambaye nina tazamiwa kuweka rekodi ambayo hakuna mchezaji mwengine ambaye atakuja kuifunja. Habari ya kulipuka kwa vyungu vya nyuklia nchini Ujerumani, vikaistua sana dunia huku habari ya Camila kuwa miongoni mwa watu walio fariki katika visima hivyo ikazidi kunistua sana. Hapa ndipo nikakumbuka maneno ya rafiki yangu Ethan kwamba endapo wakijaribu kulijaribu bomu walilo litengeneza kutokana na fomula ambayo niliwapatia, basi matokeo yao ni wao kufa.

‘Asante Mungu na ninaomba uendeleaa kuniongoza mimi na familia yangu’

Nilizungumza man ohayo kimoyo moyo huku nikizima tv ya chumbani kwangu mara baada ya kuitazama taarifa hiyo ya habari. Nikapanda kitandani na kumkumbatia Latifa kwa nyuma huku nikipapasa tumbo lake lililo beba ujauzito wa mtoto wangu mwengine ambaye atakuwa wa nne kati ya Ethan Jr, Agnes, Tonny na huyu anaye fwatia ni wakike na tumepanga kumpatia jina la Christina.


MWISHO

0 comments:

Post a Comment

BLOG