Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MY LIFE SEHEMU YA 6/10

 

 


 MY LIFE

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 6 KATI YA 10

 


“Hakikisheni kwamba munamkamata Nuru akiwa hai”

“Sawa na mwanangu pia awe hai”

“Sawa”

Mama mkwe akakata simu.

“Endapo Nuru na Eddy watakiri hicho ulicho kizungumza ni ukweli, utarudi kwenye familia yangu, ila kama wakikiri kwamba ni uongo basi sahau kurudi kwenye familia yangu kwa mana utakuwa umenisaliti kwa mara nyingine kwa uongo wako”

“Nashukuru mama kwa nafasi yako ya pekee”

Mama mkwe hakunijibu chochote zaidi ya kukaa kimya. Tukafika kwenye moja ya kilima na gari zote nne zikasimama. Walinzi wa mama kwe wote wakashuka huku wakiwa na silaha, mlinzi mmoja akafungulia mama mkwe mlango wa gari, akashuka, akamkabidhi mama mkwe jaketi la kuzui risasi. Akalivaa vizuri kisha akakabidhiwa bunduki kubwa ambayo mara ya mwisho kumuona nayo ni siku ambayo tulikuwa jijini Tanga tulipo kwenda kumuokoa mwanye Eddazaria.

Kwa ishara mama mkwe akaniambia nishuke, taratibu nikashuka kwenye gari. Mama mkwe kwa ishara ya kidole chake cha mkono wa kulia akakizungusha hewani, ishara iliyo wafanya walinzi wake wote kutawanyika na kutuacha sisi wawili.

Katika eneo hili la mlima kwa chini kuna daraja kubwa. Mama mkwe akanitolea rarubini ndogo kwenye mfuko wa suruali yake aliyo ivaa. Kisha tukajificha kwenye moja ya gari na mama mkwe akaiweka sawa bunduki yake hii ambayo nayo ina lenzi ambayo husaidia kumvuta mtu karibu sana.

Baada ya dakika kama tano hivi gari ambazo zilikuwa zimembeba Jojo faki zikasimama mwanzo wa daraja hilo. Walinzi wakashusha na kuimarisha ulinzi. Mama mkwe akatoa vifaa vidogo viwaili vinavyo nasa sauti, akakivaa kimoja sikioni mwake, kisha akanivalisha na mimi kingine.

“John kuna dalili yoyote ya kumuona Nuru na watu wake?”

“Hapana mkuu”

“Kuweni makini sawa”

“Sawa mkuu”

Mama mkwe alizungumza huku jicho lake moja akilielekezea kwenye lensi ya bunduki yake. Tukaona gari nne aina ya roll Royce zenye rangi ya kijivu zikisimama mwanzo wa daraja hilo kwa upande wa pili. Nikazidi kuzivuta karibu na nikamuona Nuru akishusha kwenye gari moja wapo, huku walinzi wake nao wakiwa makini sana kuimarisha ulinzi. Nuru akatoa simu yake na kupiga, simu ya mama mkwe ikaanza kuita, kwa haraka akaitoa mfukoni mwake na kuipokea na kuweka loud speaker.

“Shuka kwenye gari tukabidhiane, Jojo kwa Eddy, mimi na wewe tu”

Maelekezo ya Nuru kidogo yakampa mama mkwe kigugumizi cha kumjibu kwa maana yeye hayupo kwenye eneo la daraja na eneo ambalo tupo ni juu sana na si rahisi kwa mama mkwe kushuka hadi katika daraja hilo na kufanya makabidhiano hayo anayo yahitaji Nuru.



“Namuachia Jojo na wewe muachie Eddy, wakutane katikati”

Mama mkwe alizungumza kwa kujiamini sana. Nuru akaka kimya kwa muda huku kazi yangu ikiwa ni kuhakikisha ninafwatilia kila hatua ambayo inaendelea kwenye daraja hili, hususani upande wa Nuru na watu wake.

“Sawa muachie Jojo”

Nuru alikubwali, mama mkwe akakata simu na vijana wake tayari walisha weza kuelewa. Jojo wa feki akashusha kwenye gari na nguo alizo zivaa ni sawa na nguo zangu nilizo zivaa. Simu ya mama mkwe ikaita tena na akapokea.

“Ndio”

“Shuka na wewe kwenye gari nahitaji kukuona”

Mama mkwe akanitazama kwa sekunde kadhaa kwa maana hayo ni masharti ambayo ni magumu kwa yeye kuweza kuyatimiza kwa muda huu.

“Mabadilishano ni ya Jojo na Eddy, mimi hapo wa nini, kama huitaji kumchukua mshenzi wako, mabadilishano yanakufa, umenielewa?”

Mama mkwe alizungumzza kwa jazba kidogo na kumfanya Nuru kukaa kimya kwa sekunde kama ishirini hivi, huku akionekena kutazama tazama kila eneo la daraja hili, akihisi kama huu unaweza kuwa mtego.

“Sawa namuachia mwanao na wewe muachie Jojo”

“Poa”

Mama mkwe akakata simu, akaamuru Jojo faki aanze kutembea. Nikamtazama Eddazaria naye nikamuona akianza kutembea huku watu wa Nuru wakiwa wamemuelekezea bunduki zoa na endapo kuna tukio lolote la kijinga linaweza kutokea basi Eddy watamuangamiza.

“John”

“Ndio mkuu”

“Kila mmoja aondoke na wa kwake”

“Nimekupata mkuu”

Nikaendelea kutazama jinsi Eddazaria anavyo tembea kwa kuchechemea, machozi yakaanza kunilenga lenga, kwani amepigika sana na ametekeka sana hata ule mvuto wake umepotea, na anaoneonekana ni mtu aliye kata tamaa kabisa na maisha yake ya hivi sasa. Wakakaribiana kabisa hatua chache kufikiana na Jojo faki.

“Hei Eddy”

Jojo huyu alizungumza kwa sauti nzito kidogo ambayo ni tofauti ya na kwanguna kumfanya Eddzaria kama kugoma kidogo katika kutembea huku akimkazia macho.

“Mimi siye, ila cha kufanya hapa hakikisha kwamba unalala chini haraka iwezekanavyo sawa”

“Eddy akatingihsa kichwa”

“Haya sasa kazi kwenu”

Mama mkwe alizungumza huku akiikoki bunduki yake, nikashuhudia vijana wa Nuru wakianza kuanguka mmoja baada ya mwengine. Nuru akachachawa, kwani shuambulizi hili ni zito, akajaribu kukimbia ila mama mkwe akamtandika risasi ya paja la upande wa kulia na kumfanya aanguke chini, akajaribu kujitahidi kukimbilia kwenye gari lake, ila akatandikwa risasi nyingine ya paja la upande wa kushoto na kumuangusha chini kabisa. Vijana wa mama mkwe walio kuwa mwanzo wa daraja kwa haraka wakaanza kukimbilia katika eneo ambalo Jojo faki na Eddy wapo.

Vijana wengine wakawachukua, Eddy na Jojo fake, huku vijana wengine wakikimbilia katika eneo ambalo Nuru ameanguka. Nikaendelea kuwasindikiza Eddy na Jojo fake kwa macho hadi walipo ingia kwenye gari moja wapo, kisha nikamuona jinsi Nuru anavyo kokotwa na akaingizwa kwenye gari jengine na vijana hao wa mama mkwe wakaondoka.

Vijana wa mama mkwe walio kuwa wametawanyika wakaja kwa haraka katika eneo tuliopo, tukaingia ndani ya gari na kuanza kuondoka kwa mwendo wa kasi sana katika eneo hili.

“John”

“Ndio mkuu”

“Mpeni huduma ya kwanza mwaangu na huyo Nuru”

“Sawa muheshimiwa”

Mama mkwe akavua kifaa cha kusana sauti alicho kivaa sikioni mwake, kisha akashusha pumzi nyingi sana kwani kazi imekwenda kama vile ilivyo pangwa. Tukawahi kufika katika nyumba hii iliyopo msituni.

“Mama hivi hapa ni wapi?”

“Unahitaji upajue ili iweje?”

Jibu la mama mkwe likanifanya niweze kuamini kwamba bado nipo kikaangioni na sijasamehewa, nikiwa katika hali ya kujadili hili, gari zilizo wabeba Eddazaria na Nuru zikafika, walinzi wakashuka, kwa haraka wakamshusha Eddazaria, nikatamani kushuka ndani ya gari ila mama mkwe akanishika mkonona kunizuia.

Mama mkwe akashusha kwa haraka, akamfwata Eddzaria na kumkumbatia kwa nguvu. Wakaendelea kukumbatia kwa dakika kama tano. Mama mkwe akaanza kumchunguza Eddy jinsi mwili wake ulivyo jaa majareha ya kupigwa. Taratibu nikashusha kioo cha gari hili, macho yangu yakakutana uso kwa uso na Eddazaria. Akanitazama kwa hasira sana, akaanza kutembea kwa haraka huku akizidi kuchechemea. Akafungua mlango kwa haraka na kunishika mkono, na kunivuta nje kwa nguvu. Nikayumba yumba kabla ya kuanguka, akanishika mkono na kunigandamiza kwenye gari huku akinikaba koo kwa nguvu, na machozi yakimwagika usoni mwake.

Sikuhitaji kuonyesha juhudi yoyote ya kuutoa mkono wa Eddazaria unao zidi kunikaba koo langu na kuifanya pumzi yangu izidi kupungua.

“Kwa nini eheeeeee?”

Eddazaria alizungumza kwa kufoka sana huku akiendelea kunikaba.

“Eddy, Eddy”

Mama mkwe alimuita Eddy huku akitufwata hapa tulipo. Kwa nguvu akautoa mkono wa Eddy katika shingo yangu na kunifanya niaanze kuvuta pumzi kwa wingi huku nikihema sana na kukohoa sana.

“Ni nani laikuambia na wewe ufungue kioo eheee?”

Mama mkwe alifoka huku akinitazama kwa ukali.

“Mpelekeni ndani”

Mama mkwe alizungumza, walinzi wake wawili wa kike wakanishika mikono yangu huku na huku, kisha wakaanza kunipelekea ndani huku kwa mara kadhaa nikigeuka nyuma nikimtazama Eddazaria jinsi anavyo nitazama kwa macho makali sana na yaliyo jaa jazba kubwa mno.

Nikaingizwa ndani ya chumba ambacho nikikuwemo, walinzi wakatoka na wakaufunga mlango kwa nje na kuniacha nikiwa peke yangu. Machozi ya uchungu na lawama yakazidi kunimwagika usoni mwangu.

‘Kwa nini mimi, kwa nini mimi jamani. Ohoo Mungu niasaidie mimi. Nitaishi wapi, nitaishi na nani?’

Niliendelea kulia na kumuomba Mungu wangu, nikanyanyuka kitandani na kuelekea mlangoni na kujaribu kuufungua ila nikashindwa, taratibu nikajikalisha pembeni ya mlango huo. Galfa nikaanza kuhisi maumivu makali chini ya kitovu changu, nikajaribu kusimama ila nikashindwa, na maumivu yakazidi kuniuma.

“Nakufaaaaaa, mamamaaaa”

Nililiza kwa nguvu sana huku nikijilaza chali, kila aina ya kulala ninayo jaribu nikajikuta nikishindwa na maumivu ndivyo jinsi yanavyo zidi kuongezeka.

“Mamaaaaaaaa”

Nilita kwa sauti ya kukoroma, na kadri jinsi muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nguvu za mwili wangu zinavyo zidi kuniishia.

Mlango ukafunguliwa, akaingia mama mkwe, kwa haraka akaanza kujitahidi kunyanyua, akawaita walinzi wake wawili wa kike ambao wakasaidiana naye kuninyanyua na kuniweka juu ya kitanda.

“Nakufa mama, nakufaaaa…….”

Nilizungumza huku macho yangu yakizidi kuniishia nguvu, na sikuchukua muda mwingi snaa nikajikuta nikitawaliwa na giza nene kwenye macho yangu na kulala fofofo.

***

Mtu wa kwanza kumuona baada ya kufumbua macho yangu ni daktari ambaye alikuja kunipima siku ya kwanza tumbo langu akiwa na mama mkwe. Akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akaachia tabasamu pana usoni mwake.

“Unaendeleaje?”

Sikumjibu chochote zaidi ya kuendelea kutathimini eneo hili nilipo na nikagundua kwamba nipo katika eneo jengine tofati kabisa na nyumba ile niliyo kuwepo.

“Nipo wapi?”

“Upo hospitali”

“Ya wapi?”

“Hapa ulipo ni Mumbai nchini India”

“Mumbai?”

“Ndio tulikusafirisha kwa ndege ya haraka, kuhakikisha kwamba tunayaokoa maisha yako na mwanao.”

Kwa haraka nikajishika tumbo langu na kujikuta tumbo langu likiwa salama na ujauzito wangu upo. Wasiwasi nilio kuwa nao kidogo ukapungua taratibu.

“Laiti kama tungekuchelewesha basi maisha yako yangekuwa hatarini”

“Asante dokta”

“Kitu kikubwa hivi sasa ni kuhakikisha kwamba, huwi na msongamano mkubwa wa mawazo. Mbili hakikisha kwamba hufikiria matukio yoyote mabaya ya nyuma ambayo yanaweza kukupa msongamano wa mawazo”

“Sawa dokta, mama na mume wangu wapo wapi?”

“Watafika usiwe na shaka”

“Mwanangu lakini yupo vizuri?”

“Yupo vizuri na ni mtoto wa kike, naamini atakuwa mzuri kama wewe mama yake pale utakapo mzaa”

“Hahaaa asante sana dokta. Je baba yake amesha pata matibabu?”

“Ahha….mimi jukumu langu ni kukuangalia wewe kwa asilimia mia moja, baba yake bado sijafahamu kama amepata matibabu au laa”

“Una simu nizungumze naye?”

“Hapana kwa sasa unatakiwa kupata muda wa kupumzika. Na huwa unapendelea nini ukiwa peke yako?”

“Kivipi?”

“Yaani kitu unacho kipende, kwa mfano kama kutazama movies, kusikiliza mziki, nini unacho kipenda?”

“Mmmmm labda kutazama movie”

“Movies za aina gani?”

“Kuna zile tamthilia za kikorea hizo huwa ndio ninazo zipenda”

“Unapenda love story, au za mapigano?”

“Za mapigano sana”

“Chakula je unapenda chakula gani?”

“Ndizi na nyama, pamoja na juisi ya machungwa, kama ipo”

“Okay sawa nakuleea”

Daktari huyu akatoka ndani ya chumba hichi kizuri cha hapa hospitalini, ambacho ni kikubwa na kina huduma zote ambazo zinapatika katika hoteli za nyota tano. Baada ya muda kidogo daktaria akarudi akiwa amebeba sinia kubwa kidogo huku likiwa na sahani pamoja na kibakuli.

“Unatakiwa ule hichi chakula hadi umalize sawa Jojo”

“Ni kingi eheee?”

“Ahaaa kiasi, mtoto anatakiwa kupata chakula sasa”

Dokta alizungumza huku akiniwekea kiji stuli kidogo juu ya mihuu yangu, akaniweka sahani iliyo jaa ndazi, kisha akaniwekea kibakuli kikiwa kimejaa nyama pamoja na mchuzi.

“Hawajazipika kwa pamoja?”

“Nikahisi hivyo ndiyo utakavyo penda, au hujapenda?”

“Nimependa, ila kule Tanzania tumesha zoea kula zikiwa zimechanganywa mara nyingi wachaga ndio wanavyo penda kupika”

“Ahaaa, usijali wakati mwengine nitawaambia wapishi wapike kwa mfumo una uhitaji wewe”

“Sawa”

“Nimekueletea hii CD inaitwa, the love moon, naamini utaipenda”

“Ni nzuri?”

“Nesi anaye shuhulika na maswala haya anasema ni nzuri”

“Sawa niwekee”

Daktari akaniweka CD hii na taratibu nikaanza kuitazama, mlango ukafunguliwa na akaingia mama mkwe. Taratibu mama mkwe akatufwata hadi hapa kitandani, akatabasamu kidogo mara baada ya kuniona nikiwa nimekaa.

“Shikamoo mama”

“Marahaba, vipi unaendeleaje?”

“Najisikia vizuri sasa”

“Safi, dokta habari ya wewe”

“Nipo salama mkuu, sikui wewe?”

“Mimi nipo salama”

“Ngoja niwaache muweze kuzungumza mawili matatu”

Dokta mara baada ya kumaliza kuzungumza hivyo akatoka na kutuacha ndani humu sisi wawili.

“Mama Eddy anaendeleaje?”

Mama mkwe akaka kimya huku akinitazama usoni mwangu kwa macho yaliyo jaa masikitiko. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi, kwa maana swali langu limptezea mama mkwe furaha kabisa.

“Mama, niamabie mume wangu anaendeleje?”

“Hali yake sio nzuri”

“Ameumia sana?”

“Bora hata angeumia sana, tungejua”

“Ila ana nini?”

“Mumeao…..mumeo amekuwa KICHAAAA WA AKILI”

Mwili mzima ukaniishia nguvu, hamu yote ya kula ikaniishia, furaha ya muda niliyo kuwa nayo ikaniishia kwani taarifa hii sikutarajia wala kuifikiria kwamba inaweza kuja kutoka kwa mwanaume ninaye mpenda.



“Walimtesa sana mwanangu, walimpiga shoti nyingi za umeme, ili mradi kumuahibu mfumo wake wote wa akili”

Mama mkwe alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Nikakaa kimya kwa muda huku nami huzuni iliyo ambatana na machozi ikinitawala mwili mzima.

“Mama”

Niliita kwa uchungu sana, mama mkwe akanijibu kwa kunitazama tu usoni mwangu tu.

“Mama mimi ndio mkosefu katika hili, mimi ndio chanzo cha mwanao kuwa katika hali kama hiyo. Nakuomba unisamehe mama yangu”

Nilizungumza huku nikiangua kilio kizito. Mama mkwe taratibu akanisoegele karibu kabisa na kunishika kichwa changu na taratibu akakilza katika bega lake na kuanza kunibembeleza.

“Usijilaumu kwa vitu ambavyo vimesha pita, niliielewa maana yako ndio maana nipo hapa kwa ajili yako. Wewe ni mwanangu sasa, nilazima nikuangalie wewe kwa uangalizi mzuri sana.”

“Sasa mama yupo wapi mume wangu?”

“Ametangulia nchini Tanzania, kuna daktari mmoja anatakiwa kwenda kuonana naye kule”

“Huyo daktari kweli ataweza kumsaidia?”

“Sijajua, ila inabidi tujaribu kila mahali?”

“Ila mama kwa nini asiletwe hapa India?”

“Alikuwepo hapa India ila kila daktari amekiri kwamba hawezi kumshuhilikia hilo jambo kwa maana ni tatizo kubwa sana na wameniambia kwamba litachukua muda mrefu sana hadi yeye kupona”

Maneno ya mama mkwe yakazidi kunikatisha amani na furaha ikazidi kutoweka. Mama mkwe akatoa simu yake mfukoni na kuanza kunionyesha picha za mume wangu jinsi alivyo, machozi yakendelea kunimwaika usoni mwangu, kwa maana amekuwa ni mwenda wazimu kama wale wanao onekana wakiwa katika mitaa, japo amevaa nguo nzuri na za thamani kubwa ila macho yake tu yanaonyesha dhairi ana mapungufu ya akili.

“Uzuri wote wa mwanangu umeondoka, maisha yake sasa hivi ni kufungwa tu. Akiachiliwa huru basi anapigana sana, hajali kama huyu ni mama, au ni nani, amekuwa ni mtu hatari hata mimi ninamuogopa kwa kweli”

Mama mkwe aliendelea kuzungumza kwa upole na unyonge mwingi sana.

“Mama nahitaji kwenda nchini Tanzania kukaa na mume wangu”

“Kukaa naye”

“Ndio mama, najua Eddy ananipenda, najua hawezi kufanya jambo lolote baya juu yangu”

“Umesahau jinsi alivyo kushusha kwenye gari?”

Swali la mama likanifanya nikumbuke kitendo alicho nifanyia Eddzaria ambacho nilinusurika kufa, na laiti kama kusingekuwa na walinzi wa mama mkwe basi ile siku ningekufa mimi.

“Mama nitajaribu kuishi naye?”

“Jifungue kwanza, vumilia hiyo miezi yako michache iliyo salia, sihitaji hasara zaidi iendelee kutoke kwenye kizazi changu”

“Ina maana mama umekata tamaa katika kumsaidia Eddy?”

“Siwezi kukata tamaa kwa ajili ya mwanangu, ila endapo akikiudhuru hapo itakuwaje, hembu tazama jinsi alivyo nijeruhi hapa”

Mama mkwe alizungumza huku akifungua vifungo vya shati lake aliko vaa, akafunua upande wa bega la kulia na kuona sehemu ikiwa imezibwa na plasta maalumu, taratibu akaitoa plata hiyo taratibu na kunionyesha jeraha kubwa kiasi.

“Hapa alinichana na kisu, siku ile ambayo ulipoteza fahamu. Alihitaji kukuua tulipo kuwa tunakukimbiza kwenye helicopter ili kuwahishwa hospitali, ila nilipo kuwa ninajaribu kukuzuia ndio kisu kikatua hapa. Sasa pata picha alihitaji kukuaa, huku akihitaji kuitoa mimba yako kwa mikono yake yeye mwenyewe, je akikuona atakufanya nini?”

Swali la mama mkwe likazidi kunifanya nikae kimya na woga mwingi ukazidi kunitawala.

“Ila haya yote yule mshenzi ni lazima aweze kulipa hili”

Mama mkwe alizungumza kwa msisitizo.

“Kwani Nuru bado yupo hai tu mama?”

“Ndio yupo hai”

“Kwa nini hujamuua lakini, atafanya vitu vingine vya kijinga”

“Serikali ilikuwa inamuhitaji na nilishindwa kuweza kufanya hivyo?”

“Ila maam……”

“Najua ni nini unahitaji kuzungumza, ila kila kitu kinahitaji utaratibu, wale walinzi hawakuwa wangu wote, ni kikosi maalumua ambacho nilikabidhi na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha kwamba tunamuingiza mikononi Nuru kwa sababu nyingi sana”

Mama mkwe alinyamaza kidogo kisha akaendelea kuzungumza.

“Sababu kubwa na ya kwanza ni kuhusiana na utengenezaji wake wa madawa ya kulevya, ana mtandao mkubwa sana ambao unamuingizia mabilioni ya dola kwa biashara hiyo, na yeye ndio alikuwa kinara mkubwa. Sasa ukiachana na maswala ya kifamilia tu basi hata maswala hayo yamenifanya nishindwe kulipita kisasi kabisa juu yake ila nina imani kwamba sheria itachukua mkondo wake”

“Mama bado haitoshi kwa Nuru kuchukuliwa sheria, mama Nuru sio mtu mzuri”

“Nalitambua hilo Jojo, ila niliifanya kazi yangu kama nilivyo ombwa na serikali na sikuweza kuikataa kwa maana wanangu nyinyi pia ni miongoni mwa watu muliokuwa mumeshikiliwa na Nuru ndio maana niliifanya kwa moyo mmoja japo hii kazi ya kiserikali nilikuwa nimeiacha”

‘Ehee Mungu nisaidie, nikitoka hapa ni lazima nihakikishe kwamba nina muangamiza Nuru, siwezi kukubali aishinde hii vita kwa maana ana pesa na kwa kutumia pesa yake anaweza kufanya kitu chochote kuiweka sheria chini yake’

Nilizungumza kimo moyo huku nikimtazama mama mkwe.

“Nuru atakwenda kutaja watu wote anao shuhulika nao kwenye swala zima la uuzaji wa madawa ya kulevya”

“Sawa mama ila kama ingekuwa sio sheria basi leo hii nina imani kwamba Nuru angekuwa marehemu”

“Ndio hata mimi ningetamani iwe hivyo ila sheria ndio kila kitu kwenye maisha yetu na mimi nimeishi nikiifwata sheria ya nchi yangu hadi umri huu. Usije siku ukavunja sheria na ukategemea kwamba itakuacha huru, naamini kwamba unalifahamu hilo, ulipunyuka punyuka inchini China, si unakumbuka?”

“Ndio mama ninakumbuka ila ni kwa nini umeamua kuniambia hilo jambo?”

“Kwa sababu nina kupenda, na kwasababu najua ni kitu gani ambacho unacho moyoni mwako”

Mama mkwe alizungumza hukua akiniachia taratibu.

“Vipi Judy mumefahamu ni wapi alipo?”

“Yaa naye yupo Tanzania kwa sasa aliondoka siku tu ile ya harusi alirudishwa nchini Tanzania na anaendelea vizuri”

“Ninaweza kuzungumza naye?”

“Yaaa ngoja baadae nitajaribu kufanya naye mawasiliano uzungumze naye.”

“Sawa mama”

Mama mkwe taratibu akaanza kunilisha chakula hichi jambo lililo zidi kunishangaza sana kwani kwa upendo huu kusema kweli sikuustahili baada ya matukio yangu ya kipuuzi ambayo niliwahi kuyafanya na yalileta matatizo mengi sana.

“Mama”

“Beee”

“Kwa nini una nipenda na kunijali kama hivi, kwa nini umekuwa ni mtu wa kusahau mambo mabaya niliyo yafanya dhidi yako?”

“Mimi ni mama, wewe sio wa kwanza kunikosea. Kina Eddy wenyewe na ndugu zake hao wawili walisha nikosea, tena sana, ila nikiwa kama mama nilazima nihakikishe kwamba ninawaelekeza wanangu katika njia sahihi, njia ambayo itawajenga maisha yao yote hata kama wananikosea. Hivyo hivyo itakuwa sawa kwako wewe, yale ulivyo fanya natambua kwamba ule ulikuwa ni utoto. Naamini utakuwa umejifunza mengi sana na huto rudia makosa tena”

“Nashukuru sana mama, sinto weza kufanya ujinga kama ule, na nakuahidi mama nitaku ni msicha mzuri na bora sana kwenye maisha yangu yote”

“Nafurahi kusikia hivyo”

“Ila mama nina swali moja?”

“Swali gani?”

“Kwa nini usimtafute Gody, nina tamani kuishi naye, ninatamani kuwa na wanangu wote wawili. Gody na huyu ambaye nitakwenda kumzaa?”

Mama mkwe akanitazama usoni mwangu kwa sekunde kadhaa kisha akashusha pumzi taratibu.

“Hilo ni swala ambalo sikuwahi kulifikiria, ila utanifanya niweze kulifikiria kwa sasa”

“Ndio mama, nataka niishi na wanangu wote, nitampenda, nitamjali nitamuheshimu na nitampa haki sawa sawa na nitakayo mpa huyu aliyopo tumboni mwangu”

“Kwa mara ya kwanza sikutaka kuliingilia hili swala la mume wako juu ya mtoto wake wa kwanza kwa manaa mama wengi wa kambu hususani wa Kitanzania, hujenga chuki na roho mbaya juu ya watoto ambao hawajawazaa wao. Ila kutokana umeniahidi basi nitahakikisha kwamba mjukuu wangu anarudi mikononi mwa familia yangu”

“Nashukuru sana mama mkwe”

“Ila nina kuomba usije ukamtesa”

“Mama ni ahadi yangu sinto weza kufanya jambo lolote baya juu ya Godlove”

“Sawa ninashukuru”

Tukaendelea kukaa siku nzima hapa hospitalini na mama mkwe.

***

Kama waswahili wanavyo sema kwamba siku hazigandi kweli kwa upande wangu siku hazikuganda. Tarehe ambayo madaktari wa hospitali hii waliniandikia kwamba itakuwa ni siku yangu ya kujifungua ikafika. Nashukuru Mungu kwa kipindi chote mama mkwe yupo pamoja nami, tabu na shida zote ambazo nilikuwa ninapitia hakusita hata siku moja kusema kwamba amechoka. Ni mara nyingi tulikaa pamoja na kukesha usiku pamoja. Katika mama wakwe ambao ni mfano wa kuigwa ni mama yangu huyu.

“Usiogope”

Mama mkwe alizungumza hukua kinishika mkono nikwia juu ya kitanda cha kuingizwa katika chumba cha kujifungulia.

“Mama naomba uniombee”

“Nakuombea mwanangu, kikubwa tuliza akili sawa, utajifungua salama”

“Nashukuru mama”

Mam amkwe akafungua cheni ndogo ya dhahabu ambayo siku zote ninaiona kwenye mkono wake wa kulia, akanifunga na mimi kwenye cheni hiyo ya dhahabu.

“Hii cheni alinipa mama yangu, kipindi ninajifungua mtoto wangu wa kwanza, sikuwahi kuivua hadi siku hii ya leo, nina imani kwamba itakulinda”

Mama mkwe alizungumza huku akitabasamu.

“Nashukuru sana mama”

“Mama ndio muda sasa”

Nesi alizungumza na kumfanya mama mkwe atingishe kichwa kukubaliana na nesi huyu. Taratibu kitanda kikasukumwa na kuingizwa katika chumba hichi cha kujifungulia. Manesi wanne wakanizunguka, wakaanza kunipima pima. Taratibu nikaanza kujihisi maumivu makali sana ambayo yakapeleka jasho jingi kuanza kunimwagika usoni mwangu.

“Sukuma”

Nesi alinisisitizia nizidi kumsukuma mtoto nje. Kusema kweli ule usemi wa kusema kwamba uchungu wa mwana aujue ni mama, kweli leo hii ndio ninauamini kikweli kweli. Zaidi ya dakika kumi na tano ninazidi kuminyika tu kumtoa mtoto nje ya tumbo langu ila ninashindwa kabisa kufanya hivyo. Nikachomwa sindano ambayo ikazidisha maumivu makali yaliyo nipa nguvu ya kujikuta mtoto akianza kutoka taratibu.

“Sukuma mtoto anakuja, jikaze”

Nesi huyu alizidi kunisisitizia, nikaendelea kujitahidi huku nikiwa nimeshika bomba mbili za chuma zilizopo pembeni ya kitanda hichi.

“Jojo jikaze, mtoto ameanza kutoa kichwa jikaze”

Nesi alizidi kunisisitizia, kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo nikaanza kuhisi nguvu na pumzi zikaanza kuniishia.

“Ohoo nakufa mie”

Nililalama huku nikizidi kujitahidi ila nguvu na uwezo wa kuendelea kumsukuma mtoto wangu nje, giza totoro likaanza kunikamata, taratibu nikatazama kicheni alicho nifunga mama mkwe upande wangu wa kulia na taratibu nikajikuta macho yangu yakijifunga na kushindwa kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea.


‘Hapana siwezi kufa, siwezi kufaa, lazima nizae’

Nijipa moyo katika ufahamu wangu wa akili, nikabana pumzi zangu kwa nguvu na kuyafumbua mabcho, sikuhitaji udhaifu wa kushindwa kujifungua unitawale. Manesi wote wakabaki wakinishangaa, kwani tayari walisha anza katika harakati za kuomba msaada wa kufanyiwa upasiaji.

“Jikaze Jojo”

Nimaumivu makali sana kwa kweli, ila sina jinsi ya kufanya zaidi ya kuhakikisha kwamba ninamtoa mtoto wangu nje ya tumbo langu. Juhudi zangu hazikuwa za bure, kwani taratibu mtoto wangu akapokelewa na manesi hawa huku wote wakiwa wamejawa na tabasamu pana usoni mwao.

“Ni wa kike”

Nesi mmoja alizungumza huku wakimfuta futa mtoto wangu. Taratibu wakanikabidhi mwanangu, machozi ya furaha yakaanza kunibubujika usoni mwangu. Ni mtoto mwenye afya njema na mwili mnene kiasi kwamba ninatamani hata kujua ana uzito kiasi gani.

“muiteni mama”

Nesi mmoja kwa haraka akatoka katika chumba hichi, hazikuisha hata sekunde thelathini mama mkwe akaingia huku uso wake ukionyesha dhairi kwamba mama mkwe anatamani sana kuweza kumuona mjukuu wake. Mama mkwe kwa haraka akanisogelea, taratibu nikamnyanyua mjukuu wake na kumkabidhi mikononi mwake. Mama mkwe kwa furaha aliyo nayo machozi yakaanza kumbubujika usoni mwake, kwani ni mtoto mwenye afya bora.

“Ahhaa…..rekodi zote zipo tayari. Hapa bado jina lake na kilo zake tu”

Nesi alizungumza hukua kitutazama mimi na mama mkwe.

“Sawa muneweza kumfanyua hivyo”

Mama mkwe alizungumza huku akimkabidhi nesi huyu mtoto. Taratibu nesi huyo akamuweka mwanangu katika mizani ya kupimia watoto. Nesi huyo akatugeukia na kututazama kwa mshangao ulio nifanye nistuke kidogo.

“Mume weka rekodi katika hospitali yetu. Jojo umeweka rekodi ya kuzaa mtoto mwenye kilo sita na nusu”

“Kweli?”

Mama mkwe alizungumza hukua kimfwata nesi alipo simama. Mama mkwe akadhibitisha kwa macho yake juu ya kilo hizo ambazo amezaliwa mwanangu.

“Ohoo asante Mungu wakwe zangu wote huwa wanazaa watoto wenye kilo zaidi ya tano”

“Duuu hongera sana mama, inavyo onekana wanao sio watu wa mchezo mchazo”

“Hahaaaa”

Furaha ikatawala sana ndani ya chumba hichi. Baada ya maandalizi yote kumalizika, moja kwa moja nikapelekewa katika chumba changu maalumu huku nikiambatana na mwanangu. Katika siku ambazo nimemuona mama mkwe wangu akiwa na furaha mara dufu ni siku hii ya leo.

“Mama tmuite jina gani?”

“Mmmmm kwenye jina hapo kusema kweli siwezi kuzungumza chochote, ila itakuwa ni vizuri endapo tukashauriana na wifi yako, kwa niaba ya baba yake”

“Sawa ukimpigia utamshirikisha”

“Au unaweza kuwapa kazi mashabiki wako wakakuchagulia jina la mwanao”

“Hivi bado mashabiki wangu wapo tu mama?”

“Wapo na maswali kila siku yapo mengi sana, wabaya pia wapo wanao zungumza maneno mengi mengi, wengine wanasema kwamba filamu ilikuwa ni nguvu ya sada hadi leo haitoki. Sasa ukiwafunga mdomo kwa hili jambo hakikia hakuna ambaye ataendelea kukuzungumzia vibaya na kila mmoja atagundua kwamba ulikuwa katika hali gani kama mama.”

“Sawa mama ila nitakakiwa kuwa na simu yangu, au unataka nitumie hiyo simu yako?”

“Hilo swala la kuwa na simu hata sasa hivi ukiseme kwamba nikakununulie ninakwenda”

“Sawa mama nitashukuru”

Mama mkwe akatoka chumbani humu, sikuhitaji hata sekunde moja kumuachia mwanangu, kila muda ninamtazama kwa macho yaliyo jaa furaha kubwa sana. Baada ya kama nusu saa mama mkwe akarudi akiwa ameshika mfuko mweupe ambao ndani una boksi. Akatoa simu aina ya iphone 7 plus, akanikabidhi.

“Ina laini humo ndani na vocha ya kutosha”

“Nashukuru sana mama”

Kitu cha kwanza kukifanya, nikaingia instergram na kuangalia ni nini kinacho endelea kwenye akaunti yangu, kwanza nikakutana na suprize kubwa, kwani idadi ya mashabiki imeongezeka na kufikia zaidi ya watu milioni mia mia mbili sabini.

“Ila hakikisha kwamba huiweki sura ya mtoto kwenye mtandao, si unajua waswali”

Mama mkwe alizungumza huku akiendelea kunipiga picha taratibu kwa kutumia simu yake.

“Sawa mama”

“Picha hii ni nzuri”

Mama mkwe alizungumza huku akinionyesha picha nikiwa nimemshika mtoto huku sura ya mtoto ikiwa haionekanani kwani kidogo tumeizima na kitaulo hichi nilicho mfunika, ila mikono yake na miguu inaonekana.

“Naiweka sasa hivi hii hii”

“Yaaa”

Mama mkwe alanitumia picha hiyo kwa kutumia Bluetooth, nikaichunguza tena picha hii kwa sekunde kadhaa kisha nikaiweka kwenye akaunti yangu ya instergram, huku nikiandika maneno ‘MUNGU ASANTE KWA MTOTO HUYU MZURI WA KIKE ULIYE NIPATIA’. Ndani ya dakika moja nikajikuta nikichanganyikiwa kwa furaha, kwani zaidi ya watu milioni tatu wakwa wameipenda picha yangu, huku hongera zikizidi kumiminika.

“Mjukuu wangu amekaribishwa vizuri”

Mama mkwe alizungumza huku akitazama simu yake.

“Umeona eheee mama”

“Yaa nimeona, ndani ya dakika tano watu milioni thelathini, wame ipenda picha yako, ujue ni jambo kubwa sana hilo”

“Sana mama yangu.”

Simu ya mama mkwe ikaanza kuita, mama akatoka nje na kwenda kuzungumza na simu hiyo. Maoni ya mtu mmoja yakanifanya nistuke na moja kwa moja nikajikuta nikiingia kwenye akaunti yake na kuitazama vizuri. Maoni haya ya kunipongeza yaliyo toka kwa raisi mstafu wa nchi ya Marekanani Barack Obama yakanifanya nizidi kulengwa lengwa na machozi na kuona kwamba si Watanzania tu ndio wananifwatilia mimi kumbe hata watu wakubwa duniani wananifwatilia kwa ukaribu sana. Nikarudi kwenye picha yangu na kuyajibu maoni ya raisi mstafu Barack Obama jambo lililo zidi kuongeza muamko wa watu katika kunipongeza. Mama mkwe akaingia humu ndani huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Jojo, Jojo”

Mama aliniita huku akikaa karibu kabisa na kitanda changu.

“Mmmmm”

“Pokea salamu kutoka kwa raisi wa Tanzania”

“Raisi……!!!?”

“Ndio, hapo ndio nilitoke kuzungumza naye, amekupongeza sana kwa hatua nzuri ya kuwa na familia uliyo fikia”

“Asante sana mama, umeona pongezi za raisi Obama”

“Weee…..”

“Hiii hapa mama”

“Ni yeye mwenyewe au matapeli?”

“Ni yeye mwenyewe, si unaona page ina tiki la blue”

“Yaa ni mwenyewee. Mwanangu hii ni nafasi nzuri sana kwa wewe kufuta makosa yako yote uliyo wahi kuyafanya hapo nyuma. Mwanao amesha kufungulia milango ya baraka, kuwa mama bora, kuwa mama wa kuigwa. Umenielewa”

“Nimekuelewa mama nahakikisha kwamba nitakuwa ni mama bora mama mwenye uangalizi mzuri sana kwenye familia yake.”

“Mungu abariki”

Baada ya siku mbili tukawatangazia wale mashabiki wangu walipo nchini India kuja , kuja kunitembelea hospitali. Kila kitu kwenye maisha yangu naona vinatokea kama ndoto, kwani nilihisi katika nchi hii kutakuwa na mashabiki wachache sana, ila watu zaidi ya elfu kumi wakamininika hapa hospitalini huku wengi wao wakiwa wamechanganyikana na waafrika wanao ishi katika nchi hii ya india. Polisi pamoja na ongozi wa hii hospitali ikabidi waandae ukumbi mkubwa wa hapa hospitalini ili niweze kukutana na mashabiki wangu walio kuja kuniona.

“Jojo kuna wageni”

Mama mkwe alizungumza mara baada ya kuingia katika chumba hichi ninacho kaa huku nikiwa tayari nimesha jitayarisha kwenda kuonana na mashabiki wangu.

“Ni kina nani mama?”

“Wewe subiri tu umuone”

Mama mkwe akafungua mlango taratibu, sikuamini macho yangu mara baada ya kumuona Shah Rukh Khan na Kajol, wasanii wa filamu maarufu sana duniani. Mwili mzima ukahisi kupigwa ganzi kwa mshangao. Wakanisalimia kwa heshima kubwa ya kunamisha kichwa kama wanavyo salimia wahindi wengine, na mimi nikawajibu kwa kuwasalimia kwa kuinama kidogo.

Shah Rukn Khan akaanza kuzungumza kwa lugha ya kihindi na kumfanya mama mkwe anitafsirie.

“Anasema kwamba wana furahi kuoana na wewe, na kupata nafasi ya kipekee ya kukutana na wewe”

“Hata mimi ninashukuru kwa kuonana nao, kwa kweli ni suprize kubwa sana walio nifanyia sikutaraji wala kutegemea kama ipo siku nitakuja kuonana nao”

Mama akawajibu kwa kihindi, wakatabasamu. Kajol naye akazungumza.

“Wanasema kwamba wamekuja na jambo jengine kubwa sana ambalo nina imani kwamba utalifurahia”

“Jambo gani hilo?”

Mama akawatafsiria kwa kihindi. Shah Rukn Khan akatoa karatasi na kunikabidhi. Karatasi hii imeandikwa kwa lugha ya kingereza, inaonyesha kwamba ni project ya filamu kubwa ambayo Shah Rukn Khan anaiandaa siku za hivi karibuni na huu ni mkataba unao onyesha juu mimi kuhitajika kuingia katika filamu hiyo.

“Wanasema kwamba huo ni mkataba wa filamu yao mpya, wanahitaji uweze kushiriki wewe na mtoto wako na nyote wawili mutalipwa kiasi kikubwa cha pesa”

“Mama ila ni jambo la kulijadili mimi na wewe, siwezi kufanya maamuzi ya kwangu mimi peke yangu”

“Kwa upande wangu, mimi nimekukubalia kama mama, ila sijajua kwa upande wako”

“Waulize filamu inakwenda kuanza baada ya muda gani?”

Mama akawauliza kwa kihindi.

“Wanasema baada ya mwenzi mmoja na nusu”

“Kwa hiyo mtoto atakuwa amesha timiza arubaini eheee?”

“Yaa atakuwa amesha timiza na atakuwa na siku kadhaa”

“Sawa mimi nipo tayari”

Mama akawajibu na kuwafanya wafurahi sana na kunikumbatia. Nikamnyanyua mwanangu kitandani na kuwakabidhi waweze kumuona.

“Wanasema kwamba mtoto ni mzuri sana kama vile walivyo kuwa wanategemea”

“Nashukuru sana”

Kajol akatoa kadi mbili zinazo onyesha zamba za simu zao pamoja na namba ya simu ya kampuni yao wanayo itumia. Na mimi nikawakabidhi namba yangu ya simu pamoja na namba ya mama mkwe. Kutokana muda wa kwenda kuonana na mashabiki wangu ulisha wadia, ikawalazimu Shah Rukn Khan na Kajol kutoka ndani ya chumba changu.

“Utunze huo mkataba vizuri, baadae ukirudi uje kuusoma”

“Sawa mama”

Nikauweka mkataba huu ndani ya kabati langu la nguo, kisha tukatoka ndani ya chumba hichi huku nikiwa nimembeba mwanangu amaye hadi sasa hivi hatujampatia jina kamili. Walinzi na askari wakatuzunguka kuhakikisha kwamba waandishi wanao tuzonga zonga kuto kutusogelea, ila kitu ninacho jitahidi ni kuhakikisha kwamba sura ya mwanangu ninaificha kwa kuifunika na babyshow. Tukafika ukumbina na kuwafanya mashabiki wangu walio kuwa wamekaa kwenye viti kunyanyuka kwa furaha na kupiga makofi. Tukaonyeshwa sehemu ya kukaa mimi na mama mkwe. Tukaka huku tukiwatazama watu wote ndani ya hichi huu ukumbia. Maiki zilizo wekwa mbele yetu juu ya meza, zikawashwa, huku waandishi wa habari wakiwa makini katika kuhakikisha kwamba wana daka kila tukio na neno ambalo nitalizungumza. Machozi ya furaha yakaanza kunimwagika kwani upendo ninao onyeshwa ni mkubwa sana kwenye maisha yangu.

“Habari zenu”

Nilisalimia na mama mkwe akaendelea kuwa mkarimani wangu, kwa hawa Wahindi.

“Ninafurahi kuwapo hapa, kusema kweli ni heshima kubwa na upendo mkubwa sana ambao mumenionyesha. Sikuwahi kufikiria kwenye maisha yangu kama ipo siku kama hii itakuja kutokea, ninawapenda sana”

Mama mkwe akazungumza kwa kihindi na baada ya yeye kumaliza watu wakapiga makofi.

“Ningependa kukaribisha maswali matano tu kutoka kwenu nyinyi”

Mama mkwe akawatafsiria na kuwafanya watu kuanza kunyoosha mikono huku kila mmoja akitamani kuwa wa kwanza kuniuliza swali. Nikamchagua mtoto mmoja wa kiafrika mwenye umri kama miaka kumi au kumi na moja hivi. Mtoto huyo akakabidhiwa maiki na kuanza kuzungumza.

“Ninaitwa Jane, ninatokea nchini Kenya. Eti dada Jojo WASAGAJI wanazaa kama wewe?”

Swali la mtoto Jane likaufanya ukumbi mzima kuzizima kwa ukimya huku watu wote wakinitazama usoni mwangu, kigugumizi cha galfa kikanitawala na kujikuta nikitetemeka mwili mzima, hadi mama mkwe akawahi kumchukua mtoto na kumbeba yeye.



Kusema kweli moyoni mwangu nikazidi kujihisi vibaya sana. Nikawatazama watu wote waliomo ndani ya ukumbi huu, mama mkwe taratibu akanishika mkono wangu wa kushoto katika eneo la kiganja na kuanza kuniminya minya taratibu. Kila nikijaribu kunyanyua kinywa changu ninajikuta nikishindwa na kigugumizi kikubwa kikinitawala.

Nikajikuta nikisimama na kuanza kuondoka katika eneo hili, mama mkwe akazungumza kihindi kisha akanyanyuka akiwa amembeba mjukuu wake na kuanza kunifwata kwa nyuma.

“Mama”

Niliita huku nikipungumza kasi ya kupungua na mama mkwe akanikaribia.

“Ndio”

“Nahitaji kuondoka hapa India”

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga.

“Sawa, ila inabidi nianze kuandaa maandalizi ya ndege ya kukodi, hatuwezi kusafiri katika ndege ya abiri, si unajua mtoto wako haitajiki kuonekana sura na watu kwa sasa”

“Sawa mama”

Tukarudi katika chumba chetu, na mama mkwe akaanza kuwasiliana na shirika moja la ndege ambalo hukodisha ndege kwa watu wana hitaji kupata huduma za ndege zao.

“Tumependa ndege moja, kututoa hapa hadi Tanzania itagarimu dola kaki moja na nusu”

“Hiyo pesa si ipo mama?”

“Ndio ipo, wala usijali”

“Sawa”

“Tutaondoka saa ngapi?”

“Ngoja nielekee huko, nikirudi nitakupa jibu sahihi, nilazima niweze kufahamu ndege tunayo safiria ina ubora gani”

“Sawa”

“Nje watabaki walinzi kadhaa watakulinda hadi pale nitakapo kuwa nimerudi”

“Nashukuru mama kwa kunijali, kuwa makini huko uendapo”

“Usijali, hakikisha kwamba mtoto na wewe munakuwa salama”

Baba mkwe akanipiga busu katika paji langu la uso ikiwa ndio mara yangu ya kwanza kapata upendo kama huo kutoka kwa mama mkwe. Mama mkwe akamtazama mwanangu kidogo kisha akaondoka ndani ya chumba hichi.

‘…….dada Jojo WASAGAJI wanazaa kama wewe?’

Swali la mtoto yule mdogo likajirudia tena kichwani mwangu.

‘Kwa nini amenifikiria hivyo?’

Niliendelea kujiwazia mimi mwenyewe ndani ya chumba hichi, nikachukua simu yangu na kuanza kuperuzi katika mitandao ya kijamii. Jinsi mashabiki wangu wanavyo zidi kutoa pongeze nyingi, juu ya ujio wa mwanangu hapa duniani, kusema kweli ninazidi kujihisi furaha sana. Baada ya saa moja na dakika kadhaa mama mkwe akarudi akiwa ameshika bahasha ya kaki.

“Nimefanikiwa, asante Mungu”

Mama mkwe alizungumza huku akikaa pembeni yangu.

“Ndege ni nzuri?”

“Yaa ni nzuri sana, nimeikagua ndani. Na hapo inafanikwa uangalizi wa hapa na pale, kisha majira ya saa saba usiku tunatakiwa kuripoti uwanja wa ndege na saa nane usiku tutaondoka”

“Ni usiku sana mbona mama”

“Yaa sihitaji tukiondoka hapa watu wengi waweze kufahamu. Si unajua si kila binadamu anaweza kukufikiria jambo jema”

“Ni kweli mama”

“Mumepata chakula sasa?”

“Hapana”

“Jojo unatakiwa kula mtoto ananyonyoa huyo, atakukondesha”

“Sasa mama ningekula nini, ikiwa wewe haupo. Simuamini mtu mwengine humu ndani zaidi yako”

Nilizungumza kwa kudeka deka.

“Ila ni kweli usimuamini mtu usije ukawekewa sumu bure ukafa wewe na mjukuu wangu”

Kama kawaida mama mkwe kaniandalia mtori mzuri ambao siku zote nikiunywa huwa ninajisikia vizuri. Uzuri katika chumba chetu hichi cha hapa hospitalini kimegawanyika katika kuu nne, amabzo ni seble, jiko, bafu na choo.

“Mama umejifunza wapi kupika chakula kitamu kama hichi.?”

“Hahaa, kwa nini umeniuliza?”

“Nimeuliza tu , umejifunzia wapi mama, kwa maana siku zote ninakula chakula chako, najaribu kutafuta kasoro hata ya chumvi kuzidi ila sijawahi kuipata”

“Hahaaaa…..acha kunifurahisha Jojo”

“Kweli mama, najaribu kuangalia labda mafuta yamezidi ila hakuna yaani ni full utamu tu”

“Unajua kipindi nilipo kuwa ninasoma Ashira Gilrs, tulikuwa na somo moja la upishi. Nilikuwa ninalipenda sana hilo somo ambalo nilikuwa ninalifaulu kwa ustadi wa hali ya juu sana ndio maana unaona hata mapishi yangu ninayapika ki professional sana”

“Hapo nimekuelewa ila nataka na siku na mimi unifundishe kupika kama hivi mama”

“Kweli?”

“Ndio mama, mim inajua kupika kawaida, ila machopo pocho kama haya siwezi mama yangu”

“Kipindi unaishi na mume wako nani alikuwa anapika?”

“Mmmmm, asilimia kubwa tulikua tuna nunua”

“Hahaa, nilijiua kwa maana mumeo najua anacho weza kupika ni chai tu”

“Hahaaaa mama jamani?”

“Ahaa….si namjua Eddy, alikuwa anakimbia sana zamu zake za kupika”

“Ila anaweza kukaanga mayai”

“Machizi kweli nyinyi, kukaanga mayai sasa huko ni kupika”

Mama mkwe alizungumza huku akicheka na kunifanya na mimi kucheka. Tukaendelea kula taratibu, muda ukazidi kuyoyoma. Mama mkwe akaendelea kukusanya kila kitu chetu kwa ajili ya safari ya kuondoka ofisini hapa. Simu ya mama mkwe ikaanza kuita, kutokana ipo kitandani na nipo nayo karibu, ninakichukua na kumpatia. Mama mkwe akaitazama kwa muda, nikaona sura yake kama ikiwa imebadilika kidogo. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake.

“Haloo”

“Ametoroka?”

Maneno ya mama mkwe yakanifanya nistuke kidogo huku nikimtazama mama mkwe.

“Imekuwaje ametoroka?”

“Narudi leo usiku, hakikisheni munaniandalia statement ya kueleweka, mumenielewa”

“Poa, ila ni upumbavu wa hali ya juu mulio ufanya”

Mama mkwe alizungunza kwa hasira kisha akakata simu.

“Pumbavu”

“Mama kuna nini?”

Mama mkwe akanyamaza kwa muda, kisha akashusha pumzi taratibu.

“Nuru ametoroka”

Nikahisi kama kisu kikali kikikata maini yangu pasipo huruma yoyote. Wasiwasi mwingi ukanitawala, nguvu za mwili nikahisi zikinishia kabisa.

“Aha….ame….torokaje?”

“Sielewi kwa kweli, kuna njama zitakuwa zinaendelea katika serikali, haiwezekania mtuhumiwa mkubwa kama Nuru kutoroka”

“Mama sina amani kabisa”

“Usijali ni swala ambalo nitalishuhulikia kwa umakini sana. Safari hii hato weza kukugusa kwa namna yoyote. Umenielewa?”

“Ndio mama”

“Wewe kuwa na amani kabisa, nitahakikisha kwamba nikimkamata safari hii nitamuua pasipo kumfikisha katika vyombo vya sheria”

Nikakosa la kumjibu kabisa mama mkwe kwani hapa ujasiri na furaha yangu vyote vimepotea na kusema kweli siwezi kuyarudia maisha ambayo Nuru siku zote anahitaji niyaishi. Muda wa kuondoka hapa hospitalini ukawadia. Walinzi zaidi ya kumi na mbili wakaambatana nasi huku tukiwa katika msafara wa magari zaidi ya manne yanayo fanana.

“Usiwe na wasiwasi”

Mama mkwe aliniambia huku akinitazama usoni mwangu.

“Naogopa mama”

“Usijali kutoroka kwake kusikuumize kichwa sawa”

Nikamjibu mama kwa kutingisha kichwa nikimaanisha kwamba nimemuelewa.

“Itatuchukua muda gani kufika uwanja wa ndege?”

Mama mkwe akatazama saa yake ya dhahabu mkononi.

“Kama dakika kumi na mbili hivi”

“Sawa”

“Bibie amelela?”

“Yaa amelala muda mrefu sana, toka nilivyo mnyonyesha muda ule saa nne usiku”

“Uzuri wa mwanao sio msumbufu, halii lii”

“Yaani namshukuru Mungu kwa hili, angekuwa analia lia ingekuwa shida sana”

“Ni kweli, ila hata mimi watoto wangu wote wanne, hakuna ambaye alinisumbua, japo mumeo nilimzaa na miezi saba ila hakuwahi kunisumbua katika malezi ya utoto kabisa”

Galfa gari linalo ogoza msafara tunaliona likipaa angani huku mlipuko mkubwa ukitokea. Dereva wetu kwa ustani mkubwa akafunga breki na kulikwepa gari ambalo lipo mbele yetu, kwani dereva wake amefunga breki za gafla.

“Ni nini kinacho endelea?”

Mama mkwe aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.

“Ni ambush mkuu”

Mlinzi aliye kaa siti ya mbele pamoja na dereva alizungumza huku tukishushudia gari kama nne nyeusi zikiwa zimeifunga barabara kwa mbele. Risasi zikaanza kuvurumishwa kwenye gari zetu, ikamlazimu dereva wa gari la nyuma yetu kupita mbele yetu na wakatukinga pamoja na gari jegine ambalo halikulipuka. Risasi zikazidi kumiminika huku watu hao wakionyesha dhairi kwamba wamejifunga.

“Hakuna sehemu nyingine ya kupita?”

Mama mkwe aliuliza kwa sauti kubwa, dereva akageuza gari kwa utaalamu mkubwa sana hadi tukayumba wote ndani ya hili gari, ila sikudhubutu kumuachia mwanangu. Gari lilipo kaa sawa, tukaondoka kwa mwendo wa kasi sana kiasi kwamba hadi mwangu akafumbua macho.Gari moja ambalo tulikuwa tumeongozana nalo, likaanza kutufwata kwa nyuma.

“Nipatie silaha”

Mama mkwe alizungumza huku akifunga mkanda wa siti. Mlinzi akamkabidhi mama mkwe ambaye kwa haraka akashusha kioo kidogo na kuchomoka kidogo. Akaanza kufyatua risasi kuelekea nyuma. Mlinzi alipo ona juhudi za mama na yeye akaanza kufanya kama vile mama mkwe anavyo fanya, huku jukumu la dereva likiwa ni kuhakiksha kwamba anawatoroka wavamizi hao walio tuvamia. Nikatazama nyuma na kuona gari za wavamizi zikizidi kutufwata kwa kasi sana.

“Ni kina nani hao?”

Niliuliza huku mapigo ya moyo yakizidi kwenda mbio. Mwanangu akaanza kulia jambo lililo nifanya nimkumbatie na kuanza kumbembelaza.

“Risasi zimekwisha”

Mama mkwe alizungumza huku akirudi ndani ya gari na kukaa vizuri. Gari la nyuma yetu tukalishuhudia likiacha njia na kuingia maporini na likalipuka.

“Mshike vizuri mtoto”

Mama mkwe alizungumza na kinifanya niendelee kumkumbatia mwanangu kisawa sawa, huku nikimrusha rusha ikiwa ni ishara ya kubembeleza.

“Madam nimeishiwa risasi”

Mlinzi aliye kaa siti ya mbele na kumfanya mama kukaa kimya kwa sekunde kadhaa akionekana anajambo la kufikiria.

“Umeweka wapi zile kadi ulizo pewa na wale rafiki zako?”

Nikaanza kujipapasa, nikakumbuka kwamba nimeziweka katika kipochi changu kidogo.

“Kwenye hicho kijipochi changu kidogo, na simu pia ipo humo humo”

Mama mkwe akafungua pochi kubwa ambayo tumeiweka baadhi ya nguo za mtoto. Akakitoa kipochi changu kidogo na kukifungua. Akatoa simu yangu pamoja na kipochi hicho akaanza kunakili namba za moja ya kikadi nilicho pewa, kisha akaiweka simu yangu sikioni mwake.

Mama mkwe akaanza akaanza kuzungumza kihindi huku risisi zikizidi kutuandama. Nikatazama nyuma nikaona jinsi gari za wavamizi hao zikizidi kutukaribia huku wavamizi hao walio jiziba sura zao kwa vinyago vyeusi wakiendelea kutushambulia kwa risasi.

“Mama, mama?”

Nilimuita mama mkwe huku nikimtingisha begani mwake, nilishindwa kuzungumza kwa kile ninacho kiona. Mama mkwe akatazama nyuma tukamshudia mmoja wa wavamizi akiwa ameshika bumo aina ya Beggar’s Bazooka akituelekezea sehemu gari letu linapo kwenda na endapo atalifyatua bomu hilo basi maisha yetu watu wote ndani ya gari hili akiwemo na mwanangu leo ndio itakuwa ni mwisho wetu.



‘Eheee Mungu tusaidie’

Nilizungumza huku nikiyafumba macho yangu kwa maana hii ndio sala yangu ya mwisho ya kujikamizi mikononi mwa mwenyezi Mungu.

“Ohoo shitiiiiii”

Nilisikia sauti ya mama mkwe na ikanifanya nifumbue macho yangu, nikaona gari la wavamizi likibingiria bingiria barabarani huku magari mengine ya wavamizi hao, wakijitahidi kulikwepa gari hilo la wezao. Mwanga mkali unao tokea juu ukiashiria kwamba kuna helicopter ambayo imekuja kutusaidia katika mapambano haya, ukaendelea kumulika magari haya ya wavamizi na kuwafanya wavamizi hao kuelekezea mashambulizi yao katika helicopter hiyo.

“Asante Mungu”

Mama mkwe alizungumza huku tukiendelea kutazama nyuma jinsi gari hizo zinavyo zidi kuzuiliwa moja baada ya nyingine.

“Mama ni kina nani?”

“Ni kikosi cha ulinzi cha yule rafiki yako muigizaji wa kiume”

“Wao ndio wamekuja kutusaidia?”

“Ndio”

Ikaongezeka helicopter ya pilia mbayo inaenda sambamba na sisi. Taratibu helicopter hiyo ikaanza kushuka chini.

“Simamisha gari”

Mama mkwe alimuamuru dereva na akatii amri. Helicopter hiyo ikasimama mita kadhaa kutoka gari letu lilipo. Wakashuka watu wanne kwenye gari hilo huku wakiwa wamevalia nguo nyeusi pmoja na kofia nyeusi na mikononi mwao wameshika bunduki. Mama mkwe akawa mtu wa kwanza kushuka, kisha akashuka dereva na mlinzi wake. Wakazungumza kidogo na mama mkwe kisha mama mkwe akafungu mlango, akamchukua mtoto na tukaanza kukimbia kuelekea kwenye helicopter hiyo. Tukaingia wote na taratibu helicopter hiyo ikaanza kunyanyuka taratibu na kupaa angani.

“Mama hawa ni kina nani?”

“Walinzi wa Kajol”

“Ahaaa”

“Yeye tayaria amesha tangulia uwanja wa ndege”

“Ahaaa sawa”

Hatukuchukau mud asana tukafika katika kiwanja cha ndege cha Indira Gandhi Intertantiona. Helicopter kwa haraka ikatua katika kiwanja hichi cha ndege kisha taratibu tukaanza kushuka huku mama mkwe akiwa amemshikilia mtoto vizuri na kumfunika kuhakikisha kwamba upepo huu utokanao na helicopter usimdhuru. Tukaingia katika jengo la ukaguzi huku tukiwa katika ulinzi mkali sana na walinzi hao wanne walio kuja kutusaidia. Tukakuata na Kajol akiwa na walinzi wake wengine sita wakitusubiria. Mam amkwe akapena naye mkono kisha taratibu Kajol akanikumbatia kwa nguvu, akazunguma maneno kadhaa.

“Anasema pole kwa matatizo yaliyo tokea India ni nchi salama japo kuna magaidi wachache kamahao walio kuwa akihitaji kutuuangamiza”

Mama mkwe alinitafsiria kwa maana ana kifahamu kihindi vizuri sana.

“Nakushukuru kwa msaada wako ulio weza kutupatia”

Mama akazungumza kwa lugha ya kihidi, kisha tarayibu tukaachiana na Kojol, tukaagana na walinzi wa Kajoli kisha tukaondoka na mlinzi wa mama mkwe huku dereva akiwa amebaki hapa hapa India.

“Mbona yule dereva amebaki?”

Nilimuuliza mama mkwe huku tukipandisha ngazi za ndege hii tuliyo kodisha, japo tupo nyuma ya muda ambao tulipaswa kuondoka katika kiwanja hichi.

“Yule dereva atafwatilia ni kina nani ambao wamehusika katika kutuvamia”

“Ahaa, ila si Mtanzania?”

“Yaa ni Mtanzania, ni miongoni mwa vijana wangu.”

Tukaka kwenye siti zetu ambazo zimetengenezwa katika muundo wa sofa. Mama mwke akamlaza mwanangu kwenye kiti chake maalumu kilicho kaa muundo wa kitanda. Taratibu ndege ikaanza kuondoka katika kiwanja hichi na baada ya muda ikapaa angani.

Mama mkwe akafungua mkanda wa siti yake na kunyanyuka, akafungua kiji friji kidogo kilichopo ndani ya hii ndege ya kisasa. Akatoa tunda moja, kwa ishara akaniuliza kama nina hitaji tunda hilo aina ya apple, ila nikatingisha kichwa nikimuashiria kwamba nipo vizuri na sihitaji kula kitu cha kula kwa muda huu.

“Mlinzi wako yupo wapi?”

“Yupo huko sehemu ya pili napo kuna sehemu kama hii ila ni ndogo kiasi”

“Ahaa, hivi mama maisha yetu yatakosa amani hadi lini?”

“Kwa nini umeuliza hivyo?”

“Kama vile tumetoka hospitalini, tumevamiwa ni nani ambaye alikuwa anajua kwamba sisi tunasafiri”

“Unajua wewe ni maarufu na ninaamini kwamba kuna waty walikuwa na njama za kukuteka ili waweze kupata chochote, ila hiy ni kwa mawazo gani ngoja uchunguzi uweze kufanyika kisha ndio tunaweza kufahamu kwamba ni kina nani ambao walikuwa nyuma ya uvamizi ule”

“Sawa, ila mama nina ogopa. Tunakwenda Tanzania huko ila nahisi kwamba hali inaweza kuwa mbaya kwa maana Nuru ndio amesha toroka”

“Usijali tutakuwa salama”

“Sawa mama”

Tukaendelea kuzungumza mambo mawili matatu na mama mkwe akapitiwa na usingizi. Mwanangu pia amelala, taratibu nikasimama na kunza kujinyoosha viungo vyangu vya mwili. Baada ya kujiweka sawa, nikafungua friji na kutoa chupa ya soda aina ya fanta na taratibu nikaanza kunywa soda hii.

Nikaingia upande wa pili alipo mlinzi wa mama na kumkuta akiwa amejilaza kwenye moja ya siti.

“Hei”

Niliita huku nikiaa katika siti nyingine.

“Naam”

Aliitika huku akijiweka sawa kwenye siti hiyo.

“Samahani kwa kuuamsha”

“Hapana usujali nilikuwa nimejilaza tu kidogo”

“Unafahamu ni kina nani walio endesha shambulizi lile?”

“Hapana kama mkuu alivyo zungumza mimi siwezi kuelewa ni kina nani, ila uchunguzi ukifanyakika basi tunaweza kufahamu ni kina nani?”

“Ahaaa sawa.”

Ukimya ukatawala kidogo huku nikimchunguza mlinzi huyu, ni kijana mtanashati mpole na anaye fahamu nini anafanya.

“Soda”

Nilizungumza huku nikimuonyesha chupa yangu ya soda niliyo ishika. Akatingisha kichwa akikubaliana nami. Nikanyanyuka na kwenda katika katika sehemu ya pili nilipo muacha mama mkwe na mtoto, nikafungua friji na kuchukua chupa nyingine ya soda na kurudi nayo sehemu alipo kaa mlinzi huyu wa mama.

“Ila pole”

“Pole kwa nini?”

“Kwa kuwapoteza wezako wengi yote yalikuwa ni kwa ajili yetu”

“Usijali yote ni maisha na ni jukumu la kazi yetu, kufa au kupona ni moja ya matokea ya maisha yetu”

“Kwa nini uameamua kufanya kazi kama hii hatari?

“Niliipenda toka nikiwa utotoni. Na mkuu wangu alihakikisha kwamba ananipa nafasi kuhakikisha kwamba ninatimiza malengo yangu na ni kweli nilifanikiwa na akaona kwamba nisiwe mbali naye, akanipa jukumu la kumlinda kila ninapo kwenda”

“Ahaaa sawa sawa”

Tukaendelea kunywa soda taratibu huku nikiendelea kumtazama huyu mlinzi wa mama mkwe kwa umakini sana.

“Una familia?”

Nilimuliza mlinzi huyu kwa sauti ya upole huku nikimtazama usoni mwake.

“Hapana, nilikuwa ni yatima, mkuu alinichukua na kunilea pamoja na vijana wake”

“Kina Eddy?”

“Ndio”

“Unamfahamu vizuri mume wangu”

“Yaa ninamfahamu vizuri”

“Unaweza kunielezea maisha yake ya nyuma”

“Hahaaa, kwa nini unahitaji kufahamu maisha yake ya nyuma?”

“Napenda tu nizidi kumfahamu mume wangu”

“Alikuwa mpole sana”

“Hivyo tu”

“Yaaa”

“Hahaa kuna mambo unanificha”

“Mambo gani?”

“Hutaki kuniambia historia yake ya nyuma”

“Hicho nilicho kueleza ni ukweli kabisa”

“Ulisha wahi kumuona mume wangu katika kipindi hichi kifupi?”

“Ndio”

“Anaendeje?”

Jamaa akaka kimya kwa muda huku akionekana kama kuwaja jambo fulani ambalo kwa haraka haraka likaanza kuweka hisia mbaya katika akili yangu.

“Anaendeleaje?”

“Hali yake sio nzuri kwa kweli”

Jibu la mlinzi huyu likanifanya nikae kimya kwa muda huku nikimtazama. Akatoa simu yake mfukoni akanikabidhi huku ikiwa ina picha kadhaa za mume wangu Eddazaria. Machozi yakaanza kunilenge lenge kwa jinsi alivyo chakaa.

“Hatujui ni lini atapona hiyo hali inasikitisha kwa kweli”

“Ni kitu gani jamani alicho fanywa?”

“Kwa mimi siwezi kuelezea, ila mama mwenyewe anafahamu”

Sauti ya mwanangu aliye anza kulia ikianifanya niyakatishe mazungumzo yangu, nikasimama na kurudi alipo mtoto, nikanyanyua na kukaa naye kwenye siti niliyo kuwa nimekaa. Nikaanza kumnyonyesha taratibu huku nikimbembeleza.

“Ameamka?”

Mama mkwe aliniuliza hukua kijiweka sawa

“Yaaa ameamka”

Mama mkwe akaitazama saa yake ya mkono.

“Ohoo safari bado ndefu, tuna msaa kede kede ili tuweze kufika”

“Mama”

“Beee”

“Hivi mume wangu atapona kwa kweli?”

“Kila jambo ni kumuomba Mungu, kwa maana madaktari wote bingwa ambao ninawafahamu wanao jishuhukisha na maswala ya kutibu watu wenye matatizo ya akili ila imeshindikana kabisa”

“Mmmmm sasa tutamsaidiaje?”

“Ngoja tufike nchini Tanzania tutajua nini cha kufanya.”

“Sawa mama”

Safari ikazidi kusonga mbele huku masaa nayo yakizidi kuyoyoma. Majira ya saa kumi na mbili jioni tukafika katika uwanja wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Nenda katuandalie maandalizi ya kutoka kwa manaa naamini watu wakituona inaweza kuwa tabu kidogo”

“Sawa mkuu”

Mlinzi wa mama akaondoka na kutacha sisi ndani ya hii ndege, baada ya nusu saa akarudi na kututaarifu kwamba kila kitu kipo tayari. Tukashuka na kupitia katika njia za siri na kufanikiwa kufika katika maeneo ya maegesho ya magari, tukaingia kwenye garia ina ya V8 na kuondoka katika uwanja huu wa ndege. Ukimya ukatawala ndani ya gari huku nikitazama majengo mbali mbali ya jiji hili la Dar es Salaama ambalo niliondoka zaidi ya mizi saba iliyo pita.

“Hembu ongeza sauti nisikie anasemaje”

Mama mkwe alizungumza na kumfanya mlinzi wake kuongeza sauti ya redio hii tunayo isikiliza ndani ya magari haya.

‘Huyu ni mdogo wangu anaitwa Jojo ni mmiliki wa hii kampuni ya J Entertiment, keso naye afike kituo cha Polisi kwa mahojiano zaidi”

Taarifa hii ikanistua sana, kwani niliye tajwa hapa ni mimi na kampuni iiyo tajwa hapa ni yangu. Yaani kuingia tu Tanzania ninakaribishwa na kwenda kituo cha polisi ambapo hadi sasa hivi sifaamu nimeitwa nikahojiwe nini huko kituoni.



“Mahojiano ya nini?”

Mama mkwe aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, mara tu ya kuisikia sauti hiyo ya mkuu wa mkoa.

“Sijui ninaitwa nikafanyaje?”

“Wamejuaje kama upo Tanzania?”

“Sijui mama”

“Ngoja tufike nyumbani”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi. Tukafika nyumbani majira ya saa tano kasoro usiku. Tukawakuta wifi na Judy wakiwa wanatusubiria huko wote wakiwa na shauku ya kutuona. Wakatukumbatia kwa shangwe sana huku kila mmoja akitamani sana kumuona mtoto wangu. Kwa kipindi cha miezi hii niluyo kaa njena Tanzania jumba langu limerekebishwa kwa kiasi kikubwa. Imepakywa rangi za kupendaza na imeandaliwa maeneo mengi ya watoto kuchezea ikiwemo mabembea maftuza mengi sana.

“Jojo umetoka shavu”

Wifi yangu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hahaaa, kweli wifi?”

“Haki ya Mungu vile”

“Hahaaa asante”

Judy akamkabidhi wifi mtoto wangu. Akampokea taratibu.

“Weee Jojo umemzaa lini huyu?”

“Leo ana siku ya nne anakwenda siku ya tabo”

“Aiissee mbona mzito sana hivi eheee?”

“Wee ulihisi utani nilivyo kuwambia kwamba Jojo amejifungua mtoyto ana kilo nyingi”

“Ahaa…nimi niijua kilo mbili tatu hivi”

“Mmmm ana kilo nyingi. Mumetuandalia chakula?”

“Yaa na hatujakula tilikuwa tunawasubiria mufike ndio tule pamoja”

Wifi alizungumza kwa furaha. Judy akapelekea mizigo yetu chumbani na kurudi sebleni.

“Ma mdogo wangu anaitwa nani?”

“Bado hatujampatia jina”

“Kwa nini?”

“Mimi nataka baba yake ndio ampe”

Nilizungumza na kuwafanya watu wote kukaa kimya hususani wifi yangu. Akanitazama usoni mwangu kwa sekunde kadhaa na akaonyesha kama mtu aliye katishwa tamaa na jambo fulani.

“Hivi umemuoana huyo baba yake?”

Wifi alizungumza kwa suati ya upole sana huku akinitazama.

“Sijamuona ila hajilisha anaonekana vipi, ila nitapenda yeye ndiio amchagulie mtoto wake jina kwa sababu ni damu yake”

“Twendeni tukale bwana hayo maswala ya jina yatakuja baadaye”

Judy alizungumz huku akitangulia mezani, sote tukatangulia mezani. Mlinzi wa mama akatoka nje.

“Mbona unatoka”

Nilizungumza na kumfanya mlinzi huyo kusimama huku kutugeukia.

“Njoo ule”

Mlinzi akamtazama mama usoni mwake, na mama mkwe akatingisha kichwa kumkubalia na akajua kujumuika nasi.

“Yaa we ka Musa una aibu sana”

Wifi alizungumza na kunifanya hapa ndio nilifahamu jina la huyu mlinzi wa mama.

“Kumbe unaitwa Musa?”

“Ndio”

“Unataka kusema kwamba siku zote ulikuwa humfahamu?”

Mama mkwe aliuliza huku akinitazama.

“Hapana nilikuwa simfahamu jina lake”

“Anaitwa Musa, ni kijana nimemkuza mwenyewe toka alipo kuwa mdogo, aliishi na hawa wifi zako”

“Ahaa….sawa sawa mama”

Tukaanza kula taratibu huku wifi akiwa amembeba mwanangu.

“Jamani nimesikia jina langu likitajwa kwneye vyombo vya habari kwamba nahitajika kwenda kituoni kujojiwa kuna nini kinacho endelea”

Judya akastuka kidogo na kurudisha chini glasi ya juisi aliyo kuwa amekusudia kuipeleka mdomoni mwake.

“Na wewe umetajwa?”

“Ndio nimesikia nimetajwa”

“Mungu wangu!!”

“Nini kwani kuna tatizo ambalo limetokea?”

Niliendelea kumuuliza Judy maswali huku nikimtazama usoni mwake.

“Ndio walio tajwa wote wanaambiwa kwamba wanajishuhulisha na madawa ya kulevya, sasa kama na wewe jina lako upo ujue huto toka”

Nikahisi utumbo ukinicheza kwa taarifa hii. Wasiwasi mwingi sana ukanijaa moyoni mwangu, mikono ikaanza kunitetemeka hadi kushika kijiko nikajikuta nikishindwa kabisa.

“Kwani wifi ulisha wahi kufanya biashara hiyo ya madawa ya kulevya?”

Swali la wifi likaniweka njia panda, kusema kweli nimesha wahi kufanya biashara hii ya madawa ya kulevya ila ni mama mkwe tu ndio alisha wahi kuniambia kwamba anaifahamu historia yangu toka nilipo kuwa nipo kamatwa nchini China na nina imani hata wifi fununu fununu hizo alisha wahi kuzisikia kwamba nilisha wahi kukamatwa nchini Chini, ila nahisi anahitaji niweze kumdhibitishia.

“Eti wifi ulisha wahi kuifanya?”

“Ndio”

Wifi akashusha pumzi nyingi ankionekana kustushwa sana na jibu langu.

“Mama tunafanyaje sasa?”

Wifi alizungumza huku akimtazama mama mkwe ambaye anaonyesha kuto kuwa na wasiwasi wa aiana yoyote.

“Hakuna kwenda mahala popote”

“Mama kuna wengine wengi wametajwa na wamesha kwenda, wapo watu matajiri nao pia wamsha jisalimisha?”

“Nimesema kwamba Jojo hakuna kwenda popote, na kama kwenda polisi, waje kukuchukua hapa nyumbani na si kuitana itana tu polisi. Munahisi polisi ni disco pale, akienda lazima wamlaze ndani, unahisi mtoto atahudumiwa na nani, atanyonya nini?”

Mama mkwe alizungumza kwa msisitizo kidogo ambao ukanifanya niwe na matumaini kidogo na usalama wangu. Nikajuta ni kwa nini nimekuja Tanzania. Akili yangu moja kwa moja nikaanza kuhisi kwmaba Nuru ndio mtu aliye nitaja kwa manaa anafahamu siri zangu nyingi za miaka ya nyuma.

“Tena kuanzia kesho hakuna kumruhusu mtu yoyote kuingia humu ndani pasipo idhini yangu. Mumenielewa?”

“Ndio mama”

Mama mkwe akaacha kula na kunyanyuka. Akamchukua mtoto kutoka mikononi mwa wifi na kupandisha naye gorofani.

“Majina yameanza kutajwa lini?”

Niliuliza kwa kujikazatu ila kujiamini kwangu kote kumepotea.

“Wiki kama tatu hivi zilizo pitwa, yaani wanatjwa tajwa tu watu, wapo wanao kwenda na kuachiliwa. Ila wapo wanao kwenda moja kwa moja”

“Mmmmm”

“Yaani wee acha tu inaogopesa, kuna watu ukiwasikia masikio yaani yanawasha, hutegemei kama wanahusika”

“Ni kina nani hao walio tajwa?”

“Wee ingia kwenye mtandao utawaona ni wengi sana”

Yaani hata hamu ya kuishika simu yangu sina kabisa. Yaani wee sikia tu kwamba fulani katwajwa ila usiwe wewe.

“Ngoja nikutafutie”

Judy alizungumza huku akinitazama usoni mwake, akanyanyuka na kukimbilia sebleni baada ya dakika moja akarudi huku akiwa ameshika simu yake mkononi. Akakaa kwenye kiti chake na kuendelea kuipekua pekua simu yake. Akanikabidhi simu yake na nikaichukua taratibu na kuanza kusoma majina ya watu ambao wametajwa ikisemake wanajishuhulisha na madawa ya kulevya.

“Mmmmmm”

Nilijikuta nikiguna baad aya kukutana na majina ya watu maarufu.

“Wengine wamsha fikishwa mahakamani na wengine wapo nje kwa dhamana”

“Kumbe ni ishu serious kiasi hichi?”

“Ooohoo mkoa umekuwa mchungu kwa baadhi ya watu sasa”

Judy aliendelea kutia msmsitizo ambao ukazidi kunipa wasiwasi mwingi.

“Ila litashuhuliwa”

Kaka Musa alizungumza kwa sauti ya upole na kutufanya tumtazame sote.

“Kweli?”

Nilimuuliza huku macho yakiwa yamenitoka kisawa sawa.

“Ndio wala usiwe na wasiwasi”

Tukamaliza kupata chakula, sikuona hata haja ya kuendele akukaa hapa sebleni, nikapandisha gorofani kilipo chumba changu, nikamkuta mama mkwe akiwa amelala kitandani huku pembeni yake akiwemo mjukuu wake. Nikaingia bafuni na kuvua nguo zangu, nikasimama mbele ya kioo kilichopo humu bafuni na kuanza kujichunguza mwili wangu huu. Taratibu nikaanza kuoga huku wazo la kesi ya madawa ya kulevya likizidi kuniumiza kichwa changu.

“Unawaza nini?”

Sauti ya mama mkwe ikanistua sana, nikajikuta nikigeuka huku mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi sana.

“Mama naogopa kwa nini matatizo yanakuwa mengi kiasi hichi jamani”

“Usijali hilo swala mimi nitashuhulikia, nitatazama ninaweza kuzungumza vipi na viongozi wakubwa serikalini”

“Kweli litakwisha mama?”

“Litakwisha na wala hakuna ambaye anaweza kuja kukukamata, kwa maana hakuna mwenye udhibitisho kwamba unatumia au una uza madawa ya kulevya”

“Mama nakuomba unisaidie mtoto wangu bado mdogo sana, na baba yake unaona jinsi alivyo?”

“Wala usiwe na mawazo hayo kabisa umenielewa, nitakulinda kwa namna yoyote nitakavyo weza, najua kuna njama zimefanywa hapo”

“Ila ni kweli nilisha wahi kufanya mama hiyo biashara”

“Natambua ila isikuumize kichwa, kikubwa unacho yakiwa kukifanya hivi sasa muangalie mtoto basi, hayo mambo mengine achana nayo sawa”

“Sawa mama”

“Oga uje kujipumzisha, muda umekwenda sasa”

Mama mkwe akatoka bafuni humu, taratibu nikaanza kuoga. Nikamaliza kuoga na kurudi chumbani kwangu, nikajifuta maji kwa kutumia taulo kisha nikachuka nguo ya kulala na kupanda kitandani huku mwanagu akiwa amelala pembeni. Mlango ukafunguliwa, akachungulia mama mkwe.

“Usiwashe AC(air condition) kwa upepo mkali sana, mtoto hato weza kuhimili ubaridi mkali”

“Sawa mama”

“Ulale salama”

“Nashukuru”

“Usisahau kusali”

“Sawa”

Mama mkwe akafunga mlango. Nikaichukua simu yangu juu ya dreasing table. Nikaanza kuperuzi mitandaoni na habari kuba nikaikuta ni juu ya jina langu kutajwa. Nikaanza kupitua maoni ya baadhi ya mashabiki wangu walio iweka picha yangu kwenye akaunti zao. Asilimia kubwa ya mashabiki wanaonekana kuchukizwa snaa na jina langu kutajwa huku wengine wakishindwa kujizuia kabisa na kujikuta wakiporomosha matusi kwa vyombo maalumu vilivyo nitaja.

‘Ehee Mungu niepushie kikombe hichi jamani, mbona mambo ya aibu aibu inanikuta mimi jamani’

Niliendelea kuzungumza kimoyo moyo huku huzuni kubwa nikiwa imenitawala kwa maana maisha ya gerezani nimesha wahi kuyapitia na ilinibidi kufanya matendo ya ajabu ili mradi niweze kuwa huru. Hadi inafika saa kumi na mbili alfajiri, sijapata hata lepe la usingizi. Mwanangu akaanza kulia, taratibu nikamchukua na kumpakata, nikaanza kumnyonyesha taratibu. Alipo ridhika usingizi ukampitia tena. Nikanyanyuka kitandani na kuingia chooni na kujisaidia haja ndogo, nikaoga na kurudi chumbani kwangu. Nikamtazama mwanangu kwa muda kisha nikaelekea sebleni huku nikiwa nimevaa kanga moja tu na nyepsi.

Nikiwa ninashuka kwenye ngazi, nikakutana na ka Musa akipandisha ngazi hizi kwa haraka haraka sana.

“Rudi chumbani kwako haraka”

Kaka Musa alizungumza huku akinishika mkono wangu na kuanza kunivuta mkono.

“Kuna nini kaka Musa”

“Wewe Rudi chumbani”

Kaka Musa akanikimbiza kwenye kordo hii ya kuelekea chumbani kwangu haraka haraka akafungua mlango na kuniingiza ndani, kitendo cha kuniachia mkono wangu ili nikiweka sawa, kwa bahati mbaya kanga yangu ikanianguka na nikabaki kama nilivyo zaliwa, tukiwa katika hali ya kushangaa, mama mkwe akaingia chumbani humu bila hata ya kubisha hodi na kunikuta nikiwa katika hali kama hii jambo lililo tushtusha sana na kaka Musa.


“Mama imemuanguka bahati mbaya”

Ka Musa alijiwahi katika kuzungumza, kwa haraka nikaikota kanga yangu na mama mkwe hakuzungumza chochote zaidi ya kuufunga mlango kwa ndani.

“Kuna nini, mbona munakimbia?”

“Mama askari wapo nje ya gati pale wamezuiwa na walinzi kuweza kuingia ndani huku”

“Ohoo Mungu wangu!!?”

Nilihamaki huku mapigo ya moyo yakianza kunianda kasi sana, nikambilia dirishani na kufungua pazia kidogo, nikachungulia nje, na kweli nikaona defender mbili zilizo jaa askari zikiwa zimesimama huku walinzi wakijaribu kuzungumza na askari hao.

“Kaa ndani na usitoke humu umenilewa?”

Mama mkwe alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu

“Sawa mama”

Mama na kaka Musa wakatoka chumbani kwangu, kwa haraka nikaufunga mlango kwa ndani na kurudi dirishani. Nikafunua pazia kwa uwazi mdogo snaa na kuendelea kuchungualia na kufahamu ni kitu gani kinacho endelea. Nikamuona mama mkwe akiongozana na kaka Musa hadi getini. Wakaingia askari watatu huku wawili wakiwa na silaha na mmoja wao akiwa hana chochote na ana vyeo kuliko askari hawa wawili walio ingia. Wakaanza kuzungumza na mama mkwe huku walinzi wengine wa mama wakiendelea kudumisha ulinzi katika eneo la geti wakihakikisha kwamba askari wengine hawaingii ndani.

Wakazungumza kwa muda na mama mkwe, kisha nikawaona wakianza kupiga hatua za kuja huku ilipo nyumba na inaonyesha dhairi kwamba wanaelekea sebleni. Mwili mzima ukaanza kunitetemeka, nikamtazama mwanangu aliye lala kitandani masikini ya Mungu hafahamu ni nini kinacho endelea kwa mama yake.

Nikapiga hatua hadi kitandani, nikapanda na kumchukua mwangu na kumshikilia mikononi mwangu huku machozi yakinilenga lenga sana.

“Jojo fungua mlango”

Niliisikia sauti ya mama mkwe, hapo ndipo mapigo ya moyo yakazidi kuniende kasi kiasi kwamba nikajikuta nikishindwa hata kushuka kitandani.

“Jojo”

Mama mkwe akaendelea kuniita, ila ujasiri wa kufungua kinywa changu nikashindwa kabisa.

“Jojo fungua mlango”

Safari hii mama mkwe alizungumzakwa sauti ya juu huku akigonga kwa nguvu mlango. Nikameza mate taratibu, nimkamlaza mwanangu pembeni, nikashuka kitandani huku mwili mzima ukinitetemeka. Nikaufungua mlango, mama mkwe akawa wa kwanza kuingia.

“Vaa nguo nyingine”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa ameshikilia kitasa.

“Mama kuku…..k….k…”

Kigugumizi cha galfa kikanitena na kujikuta nikishindwa kuzungumza kitu kabisa.

“Vaa nguo, jamani musiingie hadi mkwe wangu avae nguo sawa”

“Sawa”

Nilisikia sauti ya mwanaume mmoja akiitikia jambo lililo nifanya nizidi kuishiwa nguvu. Nikatembea kwa woga hadi kwneye kabati kubwa la nguo, nikafugua, sikutaka hata kuchagu, nguo nilizo iona mbele ya macho yangu ndio niliyo ichukua. Nikavaa suruali nyeusi pasipo kuva akitu chochote ndani, kisha nikavaa na tisheti nyeupe.

“Ingieni kimya kimya, mjukuu wangu amelala”

Wakaingia askari hao watatu huku wakionekaa wakihiyaji kufanya jambo fulani. Wakaanza kukagua kwenye kabati langu langu na kila sehemu ya chumba changu.

“Musichangue vitu vya mwanangu”

“Tunahiytaji kukagua acha tuifanye kazi yetu mama”

“Nimewaambia kwamba sihitaji muchangua nyinyi jidaini kwamba munafanya kazi yenu, mutafanya kazi ya kuzipanga hizi nguo”

“Mama mbona unaongea sasa vipi?”

Mkuu huyo wa polisi alizungumza huku akimtazama mama mkwe kwa macho makali sana.

“Ninaongea sana kwa sababu najua upuuzi ambao munataka kuufanya”

“Mama angalia kinywa chako”

“Na wewe angalia maneno yako wewe mzee. Tuheshimiane sawa”

Mama mkwe alizungu huku akimtunishia askari huyu kifua.

“Pigeni pungu huyu mama mpelekeni kwenye gari”

“Ndio mkuu”

“Acheni ujinga hafungwi pingu mtu hapa”

“Unasemaje mama?”

“Hafungwi pingu hapa”

“Mshuhulikieni mara moja”

Mkuu wa polisi akatoa amri, kwa haraka ka Musa akasimama mbele ya mama mkwe, askari mmoja akajaribu kumshika mama mkwe, ila nikastukia kumuona askari huyo akianguka chini kofia na bunduki yake vikaangukia kila kimoja aneo leka, na wala sijafahamu hata amepigwa pigwa vipi.

“Khaaa…..!!! Unampiga jeshi la polisi?”

Mkuu wa jeshi la polisi alizungumza kwa ukali, kijaja wake mwengine akajaribu kumshambulia Ka Musa, ila akakutana na kigoti cha kifua kilicho myumbisha, kabla hajakaa sawa, ka Musha akazunguka hewani na kurusha teke moja lililo mpiga askari huyu anaye yumba sana na kumsindikiza kwenye dreasing table yangu na kuanguka nayo na kuvunyikiwa na kioo cha dreasing table jambo lililo mfanya hadi mwanangu kustuka na kuanza kulia. Nikamuwahi kumbeba mwanangu na kujibanza naye pembeni ya kona moja ya chumba changu.

“Nisikilize wewe, hizi gwanda zako nilizivaa kipindi hicho ni msichana mdogo sana, umenielewa. Leo mtu kama wewe huwezi kunyanyua sauti yako ya kipuuzi na ukajidai kwamba unakua kumkamata mkwe wangu umenielewa?”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amemsogelea mkuu huyu wa polisi karibu kabisa nauso wake.

“Umenielewa mzee?”

“Ndio”

“Mumempa wito aje leo kituoni, asubuhi yote hii mumekuja kufanya nini eheee, au munaaka kuja kupandikaza ushahidi wa madawa ya kulevya ili muje kumtia hatia si ndio?”

“Mumetufikiria vibaya mama”

“Unataka niwafikiriaje labda? Michezo yote ambayo nyinyi umesha icheza sisi tayri tumesha icheza sawa. Waondoe vijana wako na baadae nitamleta mimi mwenyewe mkwe wangu kituoni kwenu sawa”

“Sawa”

“Na nenda kawaambie vijana wako kwamba hapo getini sio disko, musitake kunijazia waandishi wa habari kwanza sihitaji mkwe wangu ajulikane kama yupo nchini sawa”

“Sawa”

“Haya nyanyua kunguni wako uondoke nao”

“Ila nakuambia nilazima hili nilipize?”

“Wewe mzee hivi unajua ninaweza kukufanyia umafia na musitoke humu ndani hadi nipate amri kutoka kwa raisi unalielewa hilo?”

Maneno ya mama mkwe yakamfanya mkuu huyu wa polisi kunywea kidogo. Akanyanyua vijana wake na kutoka nao humu ndani.

“Musa hakikisha kwamba wanatoka nje hao, wasidondoshe hata kifungo vya mashati yao”

“Sawa mkuu”

Ka Musa akatoka ndani humu, mama mkwe akanifwata na kumchukua mjukuu wake na kaunza kumbembeleza kwani kwa muda wote huo nilikuwa nimeshikwa na kigugumizi kizito sana hata mwanangu analia ila ninashindwa kufanya jambo lolote lile.

“Usiwe na wasiwasi hakuna kitakahcho aribika”

“Mama hawat kwenda kunifunga kweli?”

“Hawawezi kukufunga”

“Mama naogopa kufungwa”

“Najua hilo, nitakupigania hadi mwisho wa uhai wangu sawa”

“Sawa mama nashukuru”

“Kuna nini jamani kilicho tokea”

Wifi alizungumza huku akiingia ndani ya chumba hichi. Akaanza kushangaa jinsi dreasing table ilivyo haribika kwa kuvunjika vunjika.

“Ni polisi”

Mama mkwe alijibu wifi kwa sauti ya upole sana.

“Polisi wamekuja kumbe?”

“Na nyinyi munalala kama mapono, hujasikia vishindo vishindo?”

“Nitasikiaje mama, nilikuwa nimelala fofofo”

“Ndio hivyo wamekuja”

“Sasa walikuja kufanyaje?”

“Kukagua, ni upuuzi tu ambao wameuleta humu ndani”

“Wifi”

Wifi aliniita huku akinishika mkono, na kukaa pembeni yangu, akanigeukia huku akinitazama usoni mwangu.

“Bee”

“Usijali haya ni mapito, usiogope sana, naamini kwamba mama atakusimamia katika hili swala na utashinda”

“Sawa wifi nashukuru kwa kunifariji”

“Usijali tupo nyuma yako.”

“Nenda kamuandalie mwenzio uji wa ulezi”

“Sawa mama”

“Niitie na Musa”

“Sawa”

Wifi akatoka hapa chumbani kwangu. Tukaanza kusikia mlio wa simu ya mama mkwe ukikaribia kuja katika chumba changu, akaingia Judy huku akiwa na wenge la usingizi.

“Simu inaita mama”

Judy alizungumza huku akipiga miyayo mingi sana. Mama mkwe akaichukua simu yake na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio muheshimiwa”

Mama mkwe alizungumza huku kwa ishara akimuomba Judy kumbeba mtoto. Judy akafanya kama mama mkwe anavyo hitaji, kishaa katoka chumbani humu na kutuacha mimi na Judy pamoja na mtoto.

“Hee vipi kioo mbona kimevunjika?”

Nikamueleza Judy kila kilicho tokea, naye wasiwasi mwingi sana ukamjaa kwa maana hili swala sio dogo na lilipo fikia ni pabaya sana.

“Dada ni bora ukatoroka nchini?”

“Siwezi, sitaki matatizo niliyo yapata kipondi nilipo toroka mara ya kwanza yanikute sasa hivi”

“Sasa unahisi hapa dada ni nini kitakacho kwenda kutokea ikiwa askari wamesha anza kukufwata hadi humu ndani?”

“Haijalishi hilo ila sinto ondoka, hapa ni kwangu na nipo tayari kwa lolote litakalo jitokeza, kama watanishika na hatia yote sawa, ila kama hawato nishika kwa hatia yote pia sawa”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimedhamiria kabisa kutoka moyoni mwangu. Judy akanitazama kwa muda huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Dada”

“Beee”

“Nipo tayari kukusaidia katika hili, nawajua watu wengi wakubwa, wenye vyeo vyao na bado wapo serikalini, wakikusumbua tu, na mimi nitamtaja mmoja baada ya mwengine tena hadharani na ushahidi wa kudhibitisha kwamba wao ni wahusika wa madawa ya kulevya najua ni wapi ulipo fichwa na Chibidu”

Maeno ya Judy kidogo yakanipa matumaini, na taratibu nikaupitisha mkono wangu wa kulia nyuma ya shingo yake na kumkumbatia kidogo huku machozi yakitumwagika kwa uchungu sana.



Tukaachiana mara tu baada ya mlango kufunguliwa, akaingia mama mkwe ambaye anaonekana kujawa na hasira. Akavuta kiti kimoja kilichopo ndani ya chumba hichi na kukaa huku akinitazama usoni mwangu. Ukimya ukatawala kama dakika mbili hivi.

“Ina bidi baadaye twende kituoni”

“Sawa mama”

Nilijibu kwa sauti ya upole na unyonge sana.

“Pata kifungua kinywa kisha ujiandae tutaondoka hapa saa sita mchana”

“Sawa”

Mama mkwe akatoka ndani humu akionekana kuchoka sana.

“Dada ngoja nikaanze kutafuta ule udhibitisho”

“Upo wapi?”

“Kwenye ile nyumba ya Chibidu kule Mbezi Mwisho”

“Unataka kwenda sasa hivi?”

“Ndio”

Nikaka kimya huku nikitafakari juu ya usalama wa mdogo wangu.

“Usiende sasa hivi”

“Kwa nini dada?”

“Subiri kwanza niende huko polisi, endapo nitawekwa ndani basi hakikisha kwamba unatafuta na usimuamini mtu wa aina yoyote zaidi ya mama”

“Sawa”

“Nikiondoka, hakiksha kunafanyiwa usafi humu ndani”

“Poa”

Nikanyanyuka na kuelekea bafuni, nikaoga kwa mara nyingine huku nikiwa nimejawa na mawazo mengi sana. Nikarudi chumbani na kuvaa nguo nyingine, nikatoka chumbani kwangu na kumuacha Judy akiwa amembeba mtoto. Nikakutana na wifi kwenye kordo.

“Kifungua kinywa kipo tayari”

“Sawa sawa”

“Mtoto yupo wapi?”

“Yupo na Judy ndani”

Wifi akaelekea chumbani, nikashuka gorofani, nikapitiliza hadi jikoni, nikajitengea kifungua kinywa na kuanza kula taratibu. Kwa msongamano wa mawazo nikajikuta nikishindwa kabisa kuhisi ladha ya hichi ninacho kila. Sikuweza hata kumaliza kifungua kinywa hichi. Ka Musa akaingia sebleni huku akiwa ameongoza na wazee wawili ambao sikuwahi kuwaona siku hata moja. Akawakaribisha kwa ukarimu mkubwa sana, baada ya muda kidogo mama mkwe akashuka gorofani akiwa amesha jiandaa. Akasalimiana na wazee hao kisha akaniita nisalimiane na wazee hao. Nikawasalimia kwa heshima zote.

“Jojo hawa ni wanasheria, ni rafiki zangu wa siku nyingi sana, tutaambatana nao kwenda polisi kushuhuhulika na hii ishu”

“Sawa mama”

“Mkweo ni nyeyekevu sana”

Mzee mmoja alizungumza huku akinitazama na kujawa na tabasamu pana sana.

“Yaa ndio maana nipo naye bega kwa bega”

“Hili swala ni dogo sana, litakwisha kisheria”

“Kweli mzee wangu?”

“Asilimia mia moja ikiwa hakuna kitu chochote kibaya ambacho wamekumamata nacho basi nina imani tunakwenda wote na tutarudi wote”

“Nashukuru sana mzee wangu”

“Karibu sana.”

“Mama ninakwenda na mtoto?”

“Hapana muache na wifi yako pamoja na Judy”

“Sawa, ngoja nikamuone mara moja”

Nikakimbilia gorofani na kuingia ndani kwagu na kuwakuta wifi na Judy wakiwa wamekaa kitandani huku wifi amemshikilia mtoto na wote wanaonekana kujawa na wasiwasi.

“Vipo mbona mbio mbio?”

“Nimekuja kumtazama mtoto”

Nilizungumza huku mchozi yakinilenga lenga usoni mwangu, nikambeba kidogo mwanangu kisha nikamrudishia wifi.

“Jamani naombeni mumuagalie mtoto jamani”

“Usijali tutamtazama”

Wifi alinijibu, nikashusha pumzi kidogo, kisha nikatoka chumbani humu, nikashuka hadi sebleni na kuwakuta mama na wazee hawa wakiwa wamesha simama tayari kwa kutoka sebleni humu. Tukatoka ndani humu humu, tukaingia kwenye gari aina ya VX V8 ambayo naamini ni mali ya mmoja wa hawa mawakili.

“Musa hakikisha kwamba nyumba inabaki na usalma na kama watakuja hakikisha kwamba kila hatua wanayo piga ndani ya hii nyumba unawafwatilia na usiwaachie nafasi hata moja wasije wakapandikiza ushahidi wa kijinga”

“Sawa mkuu”

“Na watazame kina Love na wengine huko ndani”

“Sawa”

Taratibu mama mkwe akafunga kioo cha upande wake na taratibu tukaanza kuondoka hapa nyumbani.

“Jojo”

“Beee”

“Umesha wahi kujisisha na hiyo biashara uliyo itiwa?”

Mzee anaye endesha hili gari aliniuliza huku akinigeukia kidogo. Nikamtazama mama mkwe, akatingisha kichwa kidogo akiniashiria kwamba nikiri kila kitu.

“Ndio”

“Okay, unawakumbuka ambao walikupatia huo mzigo?”

“Ndio, ni kibopa”

“Kibopa yupi kwa maana kibopa wapo wawili?”

“Yule mmiliki wa shirika la ndege la K Airways”

“Duuu, una hakika na unacho kizungumza Jojo?”

“Laiti kama ningekuwa sina uhakika nisinge zungumza, na toka nilipo kuwa nimepatwa na matatizo nchini China, sikuwahi kumuona hadi leo, ni mwaka wa nne sasa”

“Ila huu mtandoa ni mkubwa sana”

Mama mkwe alizungumza.

“Kweli ni mkubwa sana kwa maana kama huyo uliye mtaja ni nyangumi”

“Jamani hii nchi akhaaa, sijui huko nyuma watu walikuwa wanafanya vituko vya aina gani”

“Usimamizi ulikuwa ni mdogo sana, wewe unajua ni kwa nini niliamua kutoka katika kitengo cha usalama baada ya kurudi Marekani na kuingia katika taaluma ya ualimu?”

“Sijajua?”

“Usimamizi ulikuwa ni mbovu, laiti ningekuwa nimesimama kwenye mambo ya usalama, hadi leo wanangu wasinge kuwa hai au hata mimi mwenyewe. Ninapenda haki, ila kuna watu wanaipindisha haki na maovu yao ndio wanataka wayafanye yawe haki. Ona nimetia nguvumi Nuru amekuja huku amekaa miezi kadhaa sijui kuna mshenzi gani amemaua kumuachia na kumtorosha, ona sasa ni nini kitakacho fwatia hapo”

“Mmmmm”

“Yaani wewe ngoja tu, mbona kwa kupitia Jojo watajibeba mwaka huu, na nitasimamia hili swala hatua kwa hatu”

“Watakubali sasa”

“Inabidi nitumie kofia yangu ya pili, nyinyi subirini mutaona kitakacho endelea”

Mama mkwe alizungumza kwa msisitizo huku gari likizid kusonga mbele. Tukaifika kitua kiokuu cha polisi hapa jijini Dar es Salaam, sikuamini macho yangu kukuta watu wengi waiwa wamekusanyika kana kwamba kuna tukio laajabu. Cha kumshukuru Mungu hili gari tulilo panda sio rahisi kwa mtu wa nje kuweza kuona ndani ila sisi tulipo ndani ni rahisi sana kuweza kuwaona wa nje. Gari likasimamishwa kwenye maegesho maalumu yaliyopo katika eneo hili ambapo ni nje kidogo ya uzio wa jengo hili la kituo cha polisi kati, nikatazama nje nikawaona watu hao walio changanyikana na waandishi wa habari wakilitazama sana hili gari letu.

“Mama watu ni wengi sana”

“Yaa alafu nimesahau hau kukumbusha uvae miwani na kofia”

“Ila haina shida unaweza kushuka”

Mzee aliyekuwa anaendesha gari alishauri na kutufanya tukae kimya kwa muda huku tukitafakari nini cha kufanya.

“Ila nisinge penda mkwe wangu aonekane sura yake”

“Hatuna jinsi tumesha fika polisi, ni lazima tushuke kwenye gari”

“Nitashuka mama”

“Huoni kama unaweza kusabisha vurumai?”

“Hakuna shaka mama”

Nilizungumza kwa kujiamini sana kwa maana natambua wingi wa watu walio weza kuja katika eneo hili, wengi wao wana hamu na kuweza kuniona uso kwa uso kwa nimekuwa ni mtu mmoja maarufu sana, ndani na nje ya Tanzania. Wazee hawa wakashuka na waandishi wa habari wakaanza kuwasogelea huku wengi wao wakiwa hawajiamini katika kuwafwatwa kwao, kwa maana hawajui kama nao ni wahusika walio tajwa kwenye hili sakata la madawa ya kulevya au laa.

“Unauhakika na hichi unacho hitaji kukifany?”

“Ndio mama”

Mama mkwe akafungua mlango wa upande wake na kushuka, sasa hapa ndipo waandishi wa habari wakaanza kumzonga zonga mama kwa maana nina imani wanamfahamu kwamba ni mama yangu mkwe, kwani katika picha zangu kadhaa nilizo ziweka instergram na mitandao mingine zinanionyesha nikiwa naye. Nikashusha pumzi nyingi kisha nikafungua mlango na kushuka ndani ya gari.

Watu na waandishi wa habari wakaanza kunikimbilia, polisi walipo hapa katika eneo hili la kuingilia kwa haraka wakanifwata sehemu nilipo simama na kunizunguka, shangwe na kelele za watu zikazidi kutawala. Si wadada wala wakaka, kila mmoja akaanza kuniita jina langu kwa nguvu sana. Nilicho kifanya ni kiwapungia mkono huku askari wakisaidia na na wazee hawa kuigia ndani ya uzio wa eneo la kituo hicho ambapo watu wa kawaida au wanadishi wa habari hawawezi kuingia. Cha kushanga watu wakaruka uzio huo na kuendelea kunifwata huku wakinishangilia kwa shangwe kubwa sana.

“Wazuieni hao”

Polisi mmoja alizungumza na kuwafanya askari wengine kutoka ndani ya kitua cha polisi kuanza kutoka nje kwa kasi ili kuzuia wananchi hawa ambao wamesha vamia kituo hichi cha polisi. Polisi wakapiga risasi nne hewani ili kuwatawanyisha watu hawa, ila ndio kwanza raisi wakazidi kuingia kana kwamba hiyo miliyo ya risasi waliyo isikia ni kama honi za gari au pikipiki.

“Hili ni tatizo sasa”

Mama mkwe alizungumza huku tukiingia ndani ya kituo cha polisi. Nikashuhudia jinsi askari wanavyo pewa kichapo na raisi hawa wanao onekana kama kuchanganyikiwa na ushabiki. Hawakujali kufa, hawakuli kama hii ni sehemu ya sheria, ila wao anacho kijua ni kutaka kuniona huku wengine wakishambulia kwa mawe kituo hichi.

“Twendeni huku”

Askari mmoja alizungumza huku akitangulia akihitaji tupande ngazi kuelekea goroani. Nikasimama baada ya kumkuta yule mkuu wa askari aliye kuja nyumbani akiwa anashuka kwenye ngazi kwa haraka kwani vijana wake tayari wamesha shindwa nguvu na raia hawa wenye nguvu na tayri wamesha ingia hadi mapokezi.

“Jojo twende”

Mama mkwe alizungumza huku akipandisha ngazi. Nikatingisha kichwa huku nikiwaangalia askari hawa wanao pokea kichapo hila hatia ya aina yoyote, kisha chote ni mimi tu kuwepo ndani ya kituo chao.



“Heeeiiiiiii”

Nikapata sauti kwa ukali na kuwafanya watu wote wanao leta vurugu ndani ya hichi kitua kuka kuacha kile wanacho kifanya. Nikaanza kutembea kuelekea nje na kusimama eneo la juu kidogo na kwa ishara ya mkono nikawaomba wananchi wote kushuka chini na wakatii amri yangu jambo lililo nishangaza mimi hata na askari walio kuwa wakijaribu kupambana na nguvu ya wananchi wote walipo katika eneo hili.

“Naomba tusikilizane”

Nilizungumza kwa sauti ya juu na kuwafanya wananchi wote kukaa kimya. Nikashusha pumzi huku nikitazama wingi wa wananchi hawa.

“Najua kwamba munanipenda, nimekuja hapa kwa wema tu, ninawaomba muweze kuwa wapole na wastaarabu katika hili, nakuomba mukanisubirie nje ya hili eneo. Munanielewa jamani”

Wananchi wote wakaitikia huko wote wakiwa wamejawa na furaha sana. Wakaanza kuondoka huku askari wakiendelea kumiminika. Nilipo hakikisha kwamba wananchiwote wameondoka katika eneo la mbele ya kitua hichi, nikarudi eneo alipo simama mama mkwe, askari na wanashiria tulio ambatana nao katika kuja katika eneo hili.

“Hasira ya wananchi haizuiwi kwa nguvu ya silaha, kuweni makini katika hili”

Baada ya kuzungumza maneno hayo, nikaanza kupandisha ngazi kuelekea gorofani. Nikaingia katika chumba cha mahojiano pamoja na wanasheria hawa wawili.

Wakaingia askari wawili wakiwa wamevalia nguo za kiraia. Wakaweka faili moja mezani na mmoja akaka kiti cha mbele huku mwengine akisimama kisimama.

“Jojo, unajihusisha na baishara za madawa ya kulevya si ndio?”

“Unaniuliza au unadhibitisha kwa maneno?”

“Nimeuliza?”

“Nikisema kwamba sijiusishi nitakuwa nina hatia eheee?”

Askari hawa wakatazamana. Kisha mmoja wao akafungua faili alilo liweka mezani.

“Ulikamatwa na madawa ya kulevya nchini China miaka kadhaa iliyo pita na ukahukuumiwa kufungwa jela”

“Sahamani sikuhukumiwa kufungwa, ila niliwekwa magereza kama nyinyi munavyo weka watu mahabusu”

Nilizungumza kwa kijiamini na kuhakikisha kwamba ninakatisha askari huyu mpelelezi.

“Tuambie ni nani ambaye alikupatia mzigo?”

“Mzigo?”

“Ndio mzigo wa madawa ya kulevya”

“Unauhakika kwamba nilipatiwa huo mzigo, una kidhibitisho. Ngona nikuambie kitu kimoja, nahitaji kuzungumza na huyo mkuu wenu ambaye amewaagiza katika hilo, kupitia yeye nitaweza kuzungumza kila kitu, ila sio nyinyi”

Akaingia mkuu wa polisi, akanitazama kwa macho amakali sana ambayo yanaonyesha dhairi kwamba yamejawa na hasira kali sana.

“Mpelekeni chumba cha mateso”

Kauli ya askari huyu ikawastua wana sheria hawa.

“Hatuwezi kukubalina na hilo, mteja wetu ni juzi juzi tu ametoka kujifungua, leo hii munataka kumpeleka katika chumba cha mateso”

“Kwanza nyinyi hamutakiwa kuingia humu ndani, tokeni nje”

Mkuu wa polisi alizungumza kwa ukali sana. Mlango ukafunguliwa na akaingia mama mkwe.

“Una akili gani wewe mzee?”

Mama mkwe alilizungumza kwa ukali.

“Toka nje na wewe?”

“Siwezi kutoka nje, fwateni kile alicho kizungumza Jojo”

“Mama hili ni jeshi la polisi huruhusiwi kulete papara”

Mama mkwe akafungua pochi yake na kutoa kitambulisho kidogo na kumkabidhi mkuu huyu wa polisi, akakisoma kwa muda, macho yakamtoka, nikaanza kumuona mkuu wa polisi mikono ikianza kumtetemeka kisha akapiga saluti iliyo tushangaza sisi sote.

“Sasa kesi inaweza kubadilika kwenu, nyinyi ndio mulikabidhi Nuru, imekuwaje ametoroka?”

“Ahaa..aha….unajua….unajua muheshimiwa “

“Nini, hii kesi ianzie hapa, munashuhulika na watu ambao mwisho wa siku hawana kitu cha kufanya juu ya biashara hiyo, wale wakubwa wanaranda randa. Nileteeni faili la Nuru hapa”

“Sawa mkuu”

“Mchukueni Jojo na kurudi naye nyumbani sasa hivi”

“Sawa”

Wanasheria waliitikia na kunifanya nishangae sana. Tukasimama sisi na wanasheria kisha tukatoka katika chumba hichi, mama mkwe naye akatoka ndani ya chumba hichi na kuniita, tukasimama katika kordo hii ndefu ambayo haina watu.

“Mama kuna kitu gani kinacho endelea?”

“Nilipigiwa simu na muheshimiwa raisi asubuhi ya leo pale tulipo kuwa chumbani, ameweza kuniteua kuwa mkuu wa kikosi cha ufwatiliaji wa hili swala la madawa ya kulevya hivyo basi nakuomba uende nyumbani ukatilie sawa”

“Sawa mama”

“Naamini baadae nitapitia ikulu kuapishwa katika hili swala, ila nahiji kwanza nianze na Nuru niweze kutambu ilikuwaje hadi akaondoka na yule Kibopa uliye nitajia basi nitamfwatilia”

“Sawa mama, ila kuna jambo moja ambalo sikukuambia”

“Jambo gani?”

“Judy anafahamu ushahidi na udhibitisho wa watu wanao husika na madawa ya kulevya na anasema kwamba wapo watu wakubwa sana serikalini na bado wapo”

“Una uhakika na unacho kizungumza?”

“Ndio mama”

Mama mkwe akaka kimya kwa muda, akashusha pumzi kisha akanishika mkono.

“Nenda nyumbani ukapumzike sasa hivi, hili swala ni gumu na sihitaji uliingilie”

“Mama ila huo ushahidi Judy amenihakikishia kwamba anafahamu sehemu ulipo, unataka kuniambia kwamba tuna uachia hivi hivi?”

“Pangeni na Judy mukautafute”

“Sawa mama”

“Haya nenda nyumbani ukajipumzishe sasa”

Nikaanza kuondoka taratibu ila kabla sijafika mbali sana, nikageuka na kumtazama mama mkwe akiwa amesimama kwenye kordo hii ndefu huku akinitazama. Kwa haraka nikaanza kumfwata mama mkwe na kumkumbatia kwa nguvu huku machozi yakinilenga lenga, kwa madhaifu yangu mengi niliyo nayo ila mama huyu ananikingia kifua na kuendelea kuniweka karibu kabisa na maisha yake.

“Nakupenda sana mama yangu”

Nilizungumza huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu.

“Ninakupenda pia mwanangu”

“Mama naomba niende kumuona Eddy, nimemiss mume wangu”

Taratibu mama mkwe akaniachia na kunitazama usoni mwangu kwa umakini.

“Kweli unataka kumuona?”

“Ndio mama”

Mama mkwe akajikuna kidogo kwenye paji lake la uso.

“Eddy, Eddy yupo kigamboni, kuna nyumba moja kule nimeinunua, yupo chini ya uangalizi wa madaktari”

“Nahitaji kumuona”

Mama mkwe akatoa simu yake kwenye kipochi kidogo.

“Musa, njoo hapa makao makuu ya polisi, umchukue Jojo umpeleke Kigamboni”

Mama mkwe akakata simu na kuirudisha simu yake mfukoni.

“Musa atakuja atakupeleka Kigamboni ila nakuomba uwe makini sana Eddy hayupo sawa”

“Nimekuelwa mama”

“Nenda kasubirie katike eneo lile la mapokezi”

“Sawa”

Nikaachana na mama mkwe na kuelekea eneo la mapokezi, askari na watu wengine walio fika hapa kituoni kwa ajili ya matatizo yao wakabaki wakiwa wananitazama, wapo ambao wanatamani

kunisemehesha ila wanashindwa. Baada ya Nuru saa nikamuona Musa akiingia ndani eneo hili, kwa aishara akaniita, nikasimama. Akanikabidhi miwani pamoja na kofia, nikavaa kisha tukatoka katika eneo hili na kwa haraka nikaingia ndani ya gari, kisha tukoandoka katika eneo hili kwa kupitia geti la upande wa pili na kuondoka. Ukimya ukatawala ndani ya gari hili huku kila mmoja akiwa kimya.

“Watu wanakupenda sana”

“Yaa kweli”

Nilimjibu ka Musa kiufupi na kuendeea kukaa kimya huku akili yangu kwa sasa ikimuwaza mume wangu Eddazaria. Tukafanikiwa kufika Kigamboni na kuingia katika moja ya jumba kubwa, nje ya jumba hili kuna walinzi wakizunguka zunguka wakiwa na silaha mikononi mwao. Tukashuka kwenye gari hili na kuingia ndani tukiwa na kaka Musa. Tukakutana na madaktari wawili wakiwa sebleni wanatazama Tv. Tukasalimiana nao, nikawaeleza nia iliyo nileta hapa, daktari mmoja akanitazama kwa macho yaliyo jaa wasiwasi mwingi sana.

“Mimi ni mke wake, chochote atakacho kifanya dhidi yangu mim nipo tayari”

“Sawa naomba unifwate”

Daktari huyo alizungumza na kunifanya nianze kumfwata kwa nyuma, tukafika kwenye moja ya mlango wa chumba, tukasimama kwa muda huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu akafungua mlango huo huku akishusha pumzi akionyesha dhairi kwamba ana wasiwasi mwingi sana. Kwa ishar daktari akaniomba niweze kuingia ndani, nikapiga hatua moja mbele, nikasikia suati ya kukoroma kama mtu ambaye anakata roho. Kwa woga nikachungualia, sikuamini macho yangu mara baada ya kumuona Eddazaria akijikaba na shuka lake akidhamiria kujiua kwa kujinyonga.


Japo ninasikia kwa watu kwamba mume wangu amechanganyikiwa na huwa anapiga watu kutokana na kuchanganyikiwa hiko, sikulijali hilo, kwa haraka nikaingia ndani ya chumba hichi na kumshika Eddazaria mikono yake na kuanza minyana naye huku nikimsihi kwa nguvu kwamba aweze kuacha kujiua. Haikuwa shuhuli ndogo ya kuiachanisha mikono ya Eddazaria na shuka lake.

“Eddy, Eddy niangalie mume wangu”

Nilizungumza huku nikimshika Eddazaria mashavu yake yaliyo jaa ndevu nyingi sana zilizo ambatana na nywele nyingi ambazo zimechanguka changuka na dhairi anaonyesha kwamba ni mtu aliye changanyikiwa.

“Weee nani?”

Swali la Eddazaria likanishangaza kwa kweli.

“Wewee naniiiiiiiiii?”

Eddazaria alizungumza huku akiwa amenikazia macho. Akanisukuma na nikaangukia pembeni, kwa haraka akanyanyuka na kuanza kunifwata huku akikoroma kama Simba nyikani anaye linda himaya yake na wanyama wengine.

“Eddy mimi ni jojo”

Nililuzungumza huku nikianza kurudi nyuma. Eddazaria akendelea kunifwata, alipo nikaribia, akanishika akainama na kunishika mkono wangu, akaninyanyua kwa haraka na kunikandamiza ukutani huku akinikaba koo langu, tukio hili likanikumbusha siku tulipo kuwa tumetoka kumuoka baada ya kushikiliwa na K2 kwa kipindi kirefu sana.

“Eddy, Eddy ni mimi, ni mimi Jojo, nimesha za mume wangu”

Nilizingumza kwa shida sana huku nikijitahidi kuutoa mkono wa Eddazaria, anaye zidi kuniminya koo langu.

“Nime….ni…..me…jifu…ngua mtoto mtoto wa kike mume wangu”

Sauti ya mingurumo kama Simba ya Eddazaria ikaanza kupungua taratibu huku akinitazama usoni mwangu, akaiachia shingo yangu na kunifanya nianze kuhema sana huku mapigo yangu ya moyo yakianza kunienda kasi.

“Ni mimi mume wangu, nimekuzalia mtoto wa kike”

Eddazaraia kwa haraka akafunua tisheti yangu na kuanza kulipapasa papasa tumbo langu, akaweka sikio la upande wake wa kulia kana kwamba kuna kitu anakisikilizia tumboni mwangu.

“Mtoto hahahaaaaaaaa”

Eddazaria alizungumza huku akicheka sana hadi akalala chini na kujizungusha zungusha kwa furaha.

“Mtoto hahahahahaaaa. Mtotoooooooooo”

Machozi yakaanza kunilenga lenga, kwa kweli mume wangu si yule ninaye mtambua, mtu mtanashati, mpole, mcheshi na mwenye kujali kila mtu. Eti leo hii amekuwa mwenda wazimu tena wa kugara gara chini. Gafla akanishika kiuno changu na kuanza kuivua suruali yangu.

“Eddy, Eddy”

Niliita huku nikijaribu kuizuia mikono yake isiendelee kunivua suruali yangu kwa maana daktari wa kiume amesimama mlangoni. Daktari akataka kuingia, ila kwa macho aliyo tazamwa na Eddazaria akajikuta akisimama na kuanza kurudi nyuma taratibu. Eddazaria akaanza kunguruma tena kama samba na kuanza kumfwata daktari huyu huku akitembea kwa kutambaa kama wanavyo fanya watoto wanao jifunza kutembe. Daktari akatoka nej kwa haraka, Eddazaria akaufunga mlango wa chumba hichi kwa ndani na kuanza kucheka sana huku akibingiria bingiria chini.

“Hahahaaaa eheheeeeheee”

Vicheko vya Eddazaria vikazidi kunisikitisha, akanisogelea hapa ukutani nilipo egemea huku nikiiweka suruali yangu vizuri.

“Mtoto”

Alizungumza tena huku akifunua shati langu, akanza kuliminya minya tumbo langu kwa nguvu.

“Eddy. Eddy utaniuaaa mwenzio”

Nilizungumza kwa nguvu huku nikiendelea kuitoa mikono yake, Eddazaria akaniachia, akaanza kuninyonya kitovu changu.

“Tamuuuuu”

Alizungumza huku akianza kuupandisha mkono wake wa kulia hadi kwenye maziwa yangu, akaanza kuyatomasa tomasa taratibu.

“Eddy mwenzio nimejifungua juzi tu, sipaswi kufanya mapenzi”

Nilizungumza huku nikiutoa mkono wake.

“Eheee?”

“Eheee nini, sitakiwi kufanya mapenzi”

Nilizungumza kwa ukali na kumfanya Eddzaria kuutoa mkono wake. Akatabasamu kisha akasimama mbele yangu. Kwa jinsi alivyo chakaa, umaridadi wake kama mwenaume wote umemuondoka. Akaanza kuninusa nusa nywele zangu, woga ukaanza kunitawala, ujasiri wa kukaa naye mwanaume kama huyu ukaniondoka kabisa. Kwa haraka Eddazaria akanibeba na kunilaza kitandani kwake.

“Eddy nini lakini jamani, doktaaaaaaa”

Niliita kwa nguvu huku nikijitahidi kuitoa mikono ya Eddazaria anaye ng’ang’ania kunivua tisheti yangu. Akafanikiwa kutokana ana nguvu kuilo mimi, akaikata mikanda ya siridia yangu huku akiendelea kukoroma.

“Dokta nabakwaaaaa”

“Na nani?”

Eddazaria alinijibu huku akinitazama usoni mwangu.

“Na wewe”

“Mimi”

“Ndio”

“Mimi nani?”

“Eddy una nini lakini, nimekuambia sijapona vizuri mwenzio, nimejifungua majuzi tu na unataka kuendelea kunifanyia vitu vya ajabu, kwa nini lakini eheee?”

Nilizungumza huku nikilia, Eddazaria akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha taratibu akaanza kunifuta machozi yangu, akaninyanyua na kunikalisha kitandani vizuri.

“Wewe nani?”

Aliniuliza kwa sauti ya upole huku akiendelea kunitazama usoni mwangu.

“Eheee?”

“Wewe nani?”

“Mimi ni Jojo. Jojo mke wako”

“Mke wangu?”

“Ndio Eddy, ina maana umenisahau?”

“Eddy, Eddy ndio nani?”

“Kwani umelisahau jina lako”

“Mimi naitwa Simba”

Nikashusha pumzi nyingi za kukata tamaa kwani ninaye zungumza naye ni kichaa kabisa.

“Nina njaaa”

Eddazaria alizungumza kwa sauti nzitio na sauti ya upole yote ikapotea.

“Unataka kula nini?”

“Simba anakula nini?”

Nikaka kimya kwa muda huku nikisogea pembeni taratibu.

“Nyama”

“Yaaa nataka nyama”

“Ngoja nikakuletee”

Nilizungumza huku nikivaa tisheti yangu na ninashindwa kuvaa sidiria kwa maana imekatwa katwa.

“Niletee nyama mbichi”

“Nyama mbichi!!!?”

“Ndio”

“Sawa”

Nikaanza kutembea hadi mlangoni.

“Simama”

Eddazaria alizungumza kwa sauti nzito. Nikasimama na kugeuka huku mwili mzima ukianza kunitetemeka. Akanifwata hadi sehemu nilipo simama, akanigandamiza ukutani huku akinitazama kwa macho makali.

“Mwangu muite kwa jina la Cleopatra”

Eddazaria alizungumza kwa sauti yake ya kawaida kabisa ambayo siku zote huwa ndio anayo zungumza nayo jambo lililo nifanya nishangae hadi nikamtazama kwa umakini sana usoni mwangu.

“Nimuite Cleopatra”

Eddazaria hakunijibu zaidi ya kuanza kunguruma tena kama samba, taratibu nikafungua kitasa cha mlango huu na kutoka ndani ya hichi chumba huku nikiwa na maswali mengi sana kichwani mwangu. Nikafika sebleni na kila mtu akabaki akinitazama kwa macho ya mshangao, ka Musa akanifwata huku yeye akionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.

“Jojo upo salama?”

“YaaH”

Nilijibu kwa ufupi huku nikitafuta sehemu ya kukaa. Nikakaa kwenye moja ya sofa huku nikiwa nimechoka kwa kweli kwa mawazo juu ya mume wangu, kusema kweli amebadilika na amekubwa ni kituko cha ajabu saa.

‘………Mwangu muite kwa jina la Cleopatra…..’

Sauti ya Eddazaria ikaanza kujirudia kichwani mwangu na kunifanya machozi yaanze kunibubujika kwa wingi sana. Kwa upande mmoja nina furaha kwa kuweza kupewa jina la mwanangu ambaye hadi sasa sikufanikiwa kuweza kumpatia jina lolote, ila kwa upande wa pili nina huzuni kwa maana hali ya mume wangu ni mbaya sana.

“Dokta”

“Ndio miss”

“Nyama za mume wangu zipo wapi?”

“Zipo kwenye friji”

“Niinyeshe”

Daktari akasimama na nikaanza kuongozana naye kuelekea jikoni, akanionyesha friji la nyama, akafungu na kunionyesha vifuko vingi vikiwa na nyama.

“Ameniambia kwamba anahitaji kula nyama mbichi”

“Yaa ndivyo anavyo kula kila siku”

“Nini?”

“Ndio, hali chakula cha kawaida”

“Muna akili lakini nyinyi, mume wangu inakuwaje mumlishe chakula kama hicho eheeeee?”

Nilizungumza kwa kufoka sana hadi daktari akaanza kujawa na wasiwasi.

“Madam tupo hapa kwa kumuangalia mume wako na kujitahidi kurudisha katika hali yake ya kawaida. Tunafanya kuie ambacho anakihitaji yeye na laiti kama tukifwata kile tunacho kihitaji sisi ni hadi sasa hivi angekuwa amesha kufa”

Daktari naye alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu.

“Na nyama hiyo tumeifanyia vipimo vya kutosha na haina madhara kwa mtu akila”

“Nampikia mume wangu”

“Sawa”

Daktaria alinijibu kwa kifupi kisha akatoka jikoni hapa na kuniacha peke yangu. Nikachukua vifuko viwili vya nyama kisha nikaanza kuvikata kata, nakuvikaanga jikoni. Nilipo hakikisha kwamba vimeiva vizuri nikaviweka kwenye sahani.

“Harufu nzuri ya madiko diko yako imenifanya niingie humu chumbani”

Ka Musa alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana.

“Kweli?”

“Yaa huko sebleni kila mtu pua ipo juu juu yaka mgiriki”

“Hahaaa, onja kidogo”

Ka Musa akachukua kipande cha nyama na kukila taratibu, akakisikilizia kwa muda kisha akatabasamu, akataka kuokota nyama ya pili ila nikamuwahi kumshika mkono wake.

“Ahaahahaa…..nilikuambia kipande kimoja tu, nyingine ni nyama ya mume wangu”

“Ila vipi jamaa anaendeleaje?”

“Mmmmm sio nzuri kwa kweli, humo ndani nimepunyuka kuuwawa, kubakwa yaani shida juu ya shida”

“Pole sana”

“Yaani ngoja nimpekekee chakula ninakuja”

Nikabeba sahani yangu ya chakula, nikaanza kutembea hadi katika chumba cha Eddazaria, nikashika kitasa taratibu na kuufungua taratibu. Nikamkuta Eddazaria akiwa amesimama katikati ya chumba huku akiwa uchi kama alivyo zaliwa na mikono yake yote akiwa ameinyoosha juu kama mtu anaye Sali.

“Eddy nimekueletea chakula”

Eddy hakujibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kuinyoosha mikono yake juu huku macho yake akiwa ameyafumba. Nikaweka sahani hii ya chukula kwenye meza kisha nikaanza kutoka ndani ya chumba.

“Kaniletee Cleopatra”

Eddazaria alizungumza huku akifumbua macho yake, akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha kwa ishara akaniamrisha nitoke ndani ya chumba hichi. Nikatoka chumbani humu na nikakutana na ka Musa kwenye kordo.

“Vipi?”

“Twende nyumbani”

“Kuna nini?”

“Eddy anahiji kumuona mwanaye”

Nilizungumza huku nikielekea nje, nikaingia ndani ya gari, Ka Musa naye akaingia, akawasha gari na taratibutukaanza kuondoka eneo hili.

“Hivi haito kuwa hatari kumleta mtoto huku kwa baba yake?”

“Kwa nini?”

“Naamini hali ya baba mtu umeiona”

“Ndio ila naamini anataka kweli kumuona mwanaye kwa maana hata jina la mtoto ameweza kuniambia”

“Amekuambia jina gani?”

“Amesema kwamba nimuite Cleopatra”

Galfa Ka Musa akafunga breki za gari hili na kunifanya nistuke sana kwa maana mbele hakuna gari wala kikwazo cha namna yoyote kinacho weza kumfanya yeye kufunga breki hizi za galfa namna hii.



“Mb….o…na umefunga breki gafla?”

Nilimuliza ka Musa huku nikiwa na wasiwasi kidogo.

“Cleopatra ndio mtu wa pekee anaye weza kuirudisha akili ya dogo ikawa sawa”

“Kweli kaka Musa?”

Nilizungumza huku nikiwa na furaha kubwa sana moyoni mwangu, kwani mwanangu ndio dawa ya mume wangu.

“Sio Cleopatra mwanao”

Kidogo nikastuka na kujikuta nikijitahidi kuziongoza pumzi zangu zisiweze kusgindwa na mstuko huu nilio sikia kwamba sio mwanangu Cleopatra.

“Ni nani huyo?”

“NI mwanamke wake wa kwanza kumpenda kwenye maisha yake. Ni mwanamke ambaye nimeweza kuyaona mahusiano yao toka walipo kuwa watoto wadogo sana, walidumu kwa kipindi kirefu sana”

Habari hii kidogo ikaanza kunipotezea furaha yangu. Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kugundua kwamba mpenzi wako anampenda mwanamke wake wa kwanza kuliko wewe.

“Kwa hiyo jina alilo mpa mwanangu ni kutokana na huyo mwanamke wake wa kwanza”

“Yaa hujakosea”

“Eddy ana akili zake basi, na hali hiyo aliyo nayo anajifanyisha makusudi”

“Huwezi kufahamu kama ni makusudi au si makusudi.”

“Ni makusudi Ka Musa kwa nini amkumbuke mpenzi wake wa kwanza?”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenga usoni mwangu, kusema kweli wivu mwingi umenitawala kiasi cha kuanza kujisiia vibaya. Ka Musa akaanza kuendesha gari taratibu taratibu.

“Jojo”

Ka Musa aliita kwa sauti ya upole sana.

“Beee”

“Unahisi ulicho mfanyia Eddy kilikuwa sahihi?”

Nikaka kimya huku akili yangu na hisia zangu zikirudi siku nilipo msaliti Eddazaria mbele ya Nuru, hii yote ilikuwa ni kuhakikisha kwamba ninayaokoa maisha ya mwanangu pamoja na maisha yake mwenyewe.

“Ila ka Musa sikufanya makosa mimi”

“Kivipi?”

“Nilifanya kwa ajili yake yey mwenyewe pamoja na mwanaye”

“Kwa nini yeye alikuwa anapambana kufa na kupna na wewe ulishindwa kupambana kufa na kupona kwa ajili yake?”

“Ka Musa…..”

“Jojo dogo amekuwa vile kwa ajili yako. Alikuwa haambiliki wala ashikiki kwa ajili yako. Alikupenda kuliko maisha yake mwenyewe kwa nini wewe ulishindwa?”

Ka Musa alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, nikajikuta nikishindwa cha kuzungumza kabisa na machozi yakaanza kumminika usoni mwake.

“Eddy alikupenda sana, usha wahi kumuona mwanaume wa Kitanzania akijitoa maisha yake kwa ajili ya mwanamke wake. Mimi hapa na mafunzo yangu yote ya kijasusi siwezi kufanya hivyo kutookana na michepuko yangu. Ila yeye aliweza, kwa nini lakini ulimfanyia hivyo mwenzako”

“Ka Musa stop talking”

Nilizungumza kwa kufoka kwani maneno ya ka Musa yanazidi kuniongezea uchungu mwingi sana.

“Jambo moja la mwisho, akili ya mume wako haiwezi kukaa sawa kama hajamuona huyo Cleopatra. So unaweza kuchagua wewe mwenyewe, tumtafute huyo Cleopatra au mumeo aendelee kuwa mbumbumbu kama ulivyo muona”

Ka Musa alizungumza kwa msisitizo huku akiongeza mwendo kawsi wa gari. Baada ya hapo hakuna ambaye aliweza kumsemesha mwenzake. Tukafika nyumbani, na kukuta waandishi wa habari wakiwa wamekusanyika wengi, nina imani kwamba kila mmoja anahitaji kuweza kusikia neno kutoka kwangu.

“Simama hapo nje nizungumze nao”

“Huwezi kuzungumza kitu cha aina yoyote kwa sasa ni vyema tukaingia ndani sawa”

Ka Musa alizungumza huku akipiga honi, geti ikafunguliwa na taratibu tukaingia ndani ya geti huku waandishi wa habari kila mmoja akijitahidi kupata picha yangu anayo weza kuitumia kwenye mtandoa wake anau weza kupasha watu habari. Geti likafungwa nikawa ni mtu wa kwanza kushuka kwenye gari, sikuhitaji hata kumuaga ka Musa, moja kwa moja nikaingia ndani na kumkuta Judy akiwa amekaa sebleni huku akiwa amembeba mwanangu.

“Jojo vipi?”

Judy aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu, nikaka kwenye moja ya sofa huku nikiwa nimechoka sana, msongamano wa mawazo kichwani mwangu na mtukio mabaya niliyo wahi kuyafanya, yakanifanya hadi nishindwe kumjibu Judy salama yake.

“Jojo”

“Mmmmmm”

“Mbona una mawazo mengi sana, wamekusumbua sana?”

“Hapana”

“Sasa mbona upo hivyo, na wale wafuasi wako wote wamekwa chini ya ulinzi”

Judy alizungumza huku akitazama taarifa ya habari inayo endelea kwenye tv.

“Mtoto amesumbua?”

“Hapana, yaani toka uondoke yupo poa”

“Wifi yupo wapi?”

“Yupo jikoni anaandaa chakula cha mchana”

Nikanyanyuka na taratibu nikaeleke jikoni pasipo kumshika mwangu, kila ninapo kifikiria jina la Cleopatra ninahisi kama moyo wangu unahitaji kunichomoka.

“Hakikisha mahesabu ya dukani unayapitia kia saa kumi jioni, na uchukue pesa zote na upeleke NMB ya pale Mkwakwani sawa”

“Alafu sikia, kuna yule fundi alikuja?”

“Ulimsimami vizuri eheee?”

“Ahaa, hapo sawa. Baadae”

Wifi akakata simu yake na kuiweka pembeni.

“Vipi mbona umekuwa mnyonge, unaumwa au wamekusumbua huko polisi?”

“Yaani wee acha tu ni bora ningesumbuliwa polisi basi ningefahamu kwamba ni polisi ndio wamenifanya hiwe hivi?”

“Ni nini sasa kinacho kusumbua?”

“Nimetoka kuonana na Eddy”

“Mungu wangu, hajakupiga!!?”

Wifi aliniuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Hivyo hiyo”

“Jamani masikini weee, amekuumiza?”

Wifi alizungumza huku akinitazama tazama mikono yangu.

“Alinikaba koo kwa nguvu”

Nilizungumza kwa unyonge sana huku machozi yakinilenga lenga.

“Jamani pole, mwenzio sasa hivi hayupo vizuri kiakili, inabidi uwe makini naye sana”

“Ila wifi nimeambiwa kwamba dawa ya Eddy kurudi katika akili yake ipo”

“Ipo…..!!! Dawa gani?”

“Mwanamke wake wa kwanza”

Wifi macho yakamtoka huku akinitazama, taratibu akakirudisha kitunguu alicho kishika alicho kuwa anahitaji kukikaanga. Akazima jiko hili la gesi na akabaki akiwa amenitazama usoni mwangu kama mtu aliye jawa na tahamaki kubwa sana.

“Wee nani aliye kuambia hivyo?”

“Ni kweli kwani?”

“Weee niambie ni nani aliye kuambia hivyo?”

Wifi alizungumza kwa jazba kidogo huku akinitazama usoni mwangu.

“Eddy ameniambia nimuite mtoto jina la Cleopatra”

Wifi akashusha pumzi nyingi, jazba alio nayo yote ikayayuka kwa sekunde hizi chache nilizo mtajia jina hilo.

“Eti Cleopatra ndio mwanamke anaye mpenda kwenye maisha yake kulili mimi?”

“Aha…ah….”

Wifi alipata kigugumizi ambacho kwangu kikaanza kunipa wasiwasi mwingi sana naamini haya yeye anafahamu juu ya moyo wa mdogo wake ni mahali gani upo.

“Anakupenda wewe?”

“Wifi unanidanganyaa”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenga usoni mwangu.

“Sikudanganyi Jojo, kama angekuwa hakupendi asinge weza kujitoa maisha yake kwa ajili yako”

Nikakaa kimya huku machozi yakinibujika, wifi akanitazama kwa muda kisha akanivuta karibu yake na kunikumbatia.

“Najua ni jinsi gani unavyo umia kwa ajili ya mume wako. Tumejaribu kila njia na namna ila hatujaweza kupata dawa ya kumponya. Watu tumefunga, tumeomba na tunaendelea kumuombea ila hata dalili hajaweza kupata”

Wifi alizungumza kwa sautii ya upole na iliyo jaa faraja ndani yake.

“Wifi”

“Beee”

“Unajua ni wapi huyo Cleopatra anapo patikana?”

Wifi taratibu akaniachia na kunishika mabegani mwangu huku akinitazama. Tartaibu akatingisha kichwa akiashiria kwamba hafahamu.

“Kweli wifi?”

“Ndio sifahamu. Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni miaka kama kumi na mbili hivi iliyo pita na enzi hizo bado alikuwa anasoma”

“Naomba unisaidie kwa kumpata”

“Muulize Musa, yupo kwenye hivyo vitengo vya usalama hivyo ni rahisi kuweza kumsaidia kumtafuta”

“Kweli?”

“Ndio niamni katika hilo, Musa anaweza kufahamu”

Nikatoka ndani humu nikiwa mnyonge sana. Nikamkuta Ka Musa akiwa sebleni amembeba mwanangu.

“Ka Musa tunaweza kuzungumza mara moja”

“Yaa tunaweza”

Nikatangulia kutoka nje, ka Musa akatoka huku mtoto akiwa amekabidhi kwa Judy.

“Wifi anasema aunaweza kufahamu ni wapi Cleopatra anapo ishi, tunaweza kwenda?”

“Una uhakika na maamuzi yako uliyo yachagua?”

“Ndio ka Musa, ninamuhitaji mume wangu apone, sihitaji jambo jengine kwa sasa zaidi ya hilo. Ninakuwa ni mama gani nitakaye mlea mdanangu pasipo baba yake, haya baadae mwanangu akija kuniuliza kwamba nilikuwa na msaada gani kwa baba yake na hali yake aliyo kuwa nayo hivi sasa unahisi kwamba nitamjibu jibu gani?”

Nilizungumza kwa uchungu mwingi sana. Ka Musa akaka kimya kwa muda kisha akatingisha kichwa kidogo.

“Nitakusaidia kwenda kumtafuta mkoni Arusha”

“Nahitaji twende sote”

“Na mtoto je?”

“Nitazungumza na mama akirudi, ila nataka kwenda na wewe kumuona huyo msichana”

“Sawa subiri mama arudi”

“Poa ila anza kufanya maandalizi ya kumtafuta”

“Usijali”

Kidogo nikapata moyo wa matumaini. Masaa yakayoyoma hadi majira ya saa tatu usiku mama mkwe akarudi huku akwia na walinzi wengine wapya ambao sijawahi kuwaona. Tukamsalimia na tukapata chakula cha usiku kwa pamoja, baada ya kumaliza kula nikamuomba niweze kuzungumza naye. Nikamuelezea hali halisi na jina ambalo mjukuu wake amechaguliwa na mwaanye.

“Je mama unaniruhusu niweze kwenda kumtafuta huyo msichana?”

Mama mkwe akaka kimya kwa mdua huku akitafakari ombi langu.

“Unafahamu ni wapi alipo?”

“Kaka Musa amesema kwamba anafahamu ni wapi alipo huyo msichana”

“Sawa mtoto je?”

“Nitamuacha na wifi pamoja na Judy”

“Sawa ila iwe ni safari ya siku moja, musije mukaenda na kukaa huko kwa muda mrefu sawa”

“Sawa mama”

“Ila kitu kimoja…….au basi”

Mama mkwe aliikatisha sentensi yake akanyanyuka na kupandisha goforani. Nikamfwata kaka Musa nje alipo na wezake wakizungumza, nikamuita pembeni na kumueleza maamuzi ya mama mkwe.

“Sawa, inabidi tuondoke saa tisa usiku”

“Kuelekea huko Arusha?”

“Ndio tunatakiwa kufika mapema sana na tuianze shuhuli hiyo.”

“Sawa”

Nikarudi ndani na kumueleza wifi na Judy juu ya safari yangu ya kuelekea mkoani Arusha, kila mmoja akakubaliana nami kwani ni jambo la kumsaidia mume wangu na wakaniahidi kumuangalia mwanangu kwa ukaribu kwa kipindi chote ambacho sinto kuwepo ndani ya jiji la Dar es Salaam. Tukaingia na Judy chumbani na akaanza kunisaidia kupanga kuo chache za kuondokea. Kwa siku ya pili sikuweza kulala usingizi fofo kutokana na mawazo, kila ninacho kipanga ninaona hakikai sawia kichwani mwangu. Hadi inafika saa tisa kasoro nikaingia bafuni na kuoga kisha nikarudi chumbani kwagu na kujiandaa vizuri. Nikamuasha Judy niliye lala yake ili amuangalie mtoto kwa kipindi chote ambacho sinto kuwepo. Mama mkwe na wifi nao wakamka na kututakia safari njema. Tukaingia ndani ya gari na kaka Musa na safari ikaanza, ndani ya gari hili nikapata nafasi ya kulala kwani mwili wangu umechoka sana.

“Hei amka”

Taratibu nikafumbua macho yangu na kukuta tukiwa katika mji mmoja wenye watu wengi.

“Tupo wapi?”

“Moshi?”

“Saa ngapi?”

“Saa tano asubuhi”

“Mmmmm umetumia msaa mgapi?”

“Kama sita au saba”

“Umetembea eheee”

“Sana, kutoka hapa hadi Arusha ni muda mchache sana”

“Sawa”

“Nikuletee nini?”

“Maji tu”

“Hujakula chochote ibaidi upate kitu kama chai hivi”

“Kwani si umesema kwamba hapa na Arusha ni karibu?”

“Ndio”

“Basi twende tukalie chakula Arusha”

“Poa”

Tukaendelea na safari hadi jijini Arusha. Tukafikia kwenye moja ya hoteli na tukachukua vyumba viliwili huku kila mmoja akiwa na chake. Tukapata chakula cha mchana kisha tukaelekea katika eneo ambalo Ka Musa ameniambia kwamba ndipo anapo ishi huyo Cleopatra. Tukasimama kwenye moja ya nyumba ambapo nje tukakuta magari mengi pamoja na watu wakiwa wamevalia vizuri sana.

“Ni hapa?”

“Ndio”

“Mbona kuna watu wengi sana?”

“Sijui ngoja nikaulize”

“Twende wote”

“Kuna kofia siti ya nyuma, vaa usije ukanijazia watu bure”

“Sawa”

Nikavaa kofia hiyo na tukashuka kwenye gari, tukajisogeza karibu kabisa na eneo hilo ambalo limejaa shangwe na nderemo. Ka Musa akamuita kijana mmoja na kumuuliza kuna nini kinacho endelea hapa.

“Nynyi ni wageni chalii zangu?”

“Yaaa?”

“Sisteriiii anaolewa aisee”

“Nani huyo?”

“Cleopatra”

Tukajikuta tukitazamana na ka Musa huku sote tukiwa tumechoka na kujikuta tukishindwa kujuani nini tunaweza kukifanya kwani mtu anaye takiwa na Mume wangu ndio tumekuta leo siku yake ya kuolewa na watu wamefurika kwa wingi nyumbani hapa kwao nikimini wanamsubiria bibi harusi kutolewa nje kuelekea kanisani.



“Anaolewa….!!?”

Niliuliza huku nikiwa na mshangao mkubwa sana.

“Yaaa mbona umehamakia dada ake vipi?”

“Aah…hamna ni rafiki yangu nashangaa hajanialika kabisa”

“Ohoo ngoja nimuite mdogo wake hapa uje kuhakikisha”

Kijana huyo na kuniacha na ka Musa tukiendelea kuangalia angalia baadhi ya watu, nashukuru kofia hii niliyo ivaa imeniziba nusu ya uso wangu hivyo watu wengi hawakunifahamu kwa haraka japo watu ambao walinikodolea macho.

“Wadogo zake wote wananifahamu”

“Wanakufahamu?”

“Yaa”

Tukamuona kijana huyo akirudi na msichana mrefu kiasi aliye valia vizuri.

“Ka Musssaaaa msichana huyo alizungumza huku akikumbatia Ka Musa kwa furaha sana.

“Hujambo Dotto?”

“Sijambo karibu sana”

“Asante vipi hamjanialika jamani”

“Hahaaa….mimi nikajua da Cleo amekupa kadi?”

“Hapana hajanipatia”

“Jamani, ngoja nikakuibie kadi ya wana familia moja ndani uje”

“Sawa”

“Huyu ni wifi yetu?”

Tukatazamana na ka Musa kwa sekunde kadhaa.

“Ehee”

Nilijiwahi kujibu swali hilo na kumfanya msichana huyu anaye itwa Dotto kufurahi sana.

“Jamani twende ndani wifi uakajiandae andae kwa maana bi harusi naye yupo ndani huku anamaliziwa kupambwa”

“Usijali nipo vizuri”

“Kweli wifi?”

“Yaa nipo vizuri”

“Haya. Ka Musa dakika sifuri nakuja sasa hivi”

“Sawa”

Dotto akandoka na kutuacha na kijana huyu aliye tusaidia kumleta.

“Huyu manzi nina mfili sana, sema ananichomoleaga, kumbe ni mdogo wako?”

“Yaa ni wadogo zangu wote hao”

“Aissee chalii yanug unaonaje ukaniunganishia japo nikaa naye usiku wa leo kwa maana hapa kwao ni mageti kali sana”

“Hahaaa…..usijali, unaitwa nani?”

“Reymond”

“Okay”

Msichana huyo akarudi huku akiwa ameshika kalamu nzuri. Akamkabidhi ka Musa kalamu huyo.

“Ukivuta hapa kwa pembeni, utaona kijikaratasi hicho ndio kadi”

Dotto alimuelekeza ka Musa.

“Okay nimekiona. Kanisani ni wapi?”

“RC”

“Ahaa hii ya hapa mjini?”

“Yaaa, tunaingia saa tisa pale”

“Anaolewa na nani?”

“Kuna mwanajeshi mmoja hivi alikuwa Cuba huko kwenye mafunzo ya kijeshi ndio amerudi kama mwezi ulio pita, leo ndio siku yenyewe”

“Sawa sawa, ngoja nimpeleke wifi yako hotelini kwa maana tumefikizia hotelini”

“Ahaaa sawa sawa.”

“Maharusi wanakwenda kupumzikia wapi mara baada ya sherehe?”

“Mmmm sijajua, naomba namba ya simu, nikisikia sikia fununu basi nitakutext”

Ka Musa akamtajia Dotto namba ya simu yake, kisha akaiingiza na baada ya kufanikiwa akamoigia ka Musa simu.

“Ndio hii inayo ishia na themanini na sita?”

“Yaa ndio hiyo”

“Poa Dotto asante”

“Poa ka Musa ngoja niende ndani wasije wakanitafuta bure”

“Poa poa”

Dotto akaondoka huku akiwa amejawa na furaha sana.

“Aiseee kaka, naomba uniganjie hiyo namba basi nimcheki manzeriii”

“Kumbe hata namba yake ulikuwa huna?”

“Ndio aissee mtoto yaani ana bana kama vile yaani daaa”

Ka Musa akamuonyesha Raymond namba hiyo kwa sekunde kama tano hivi kisha akiingia mfukoni simu yake.

“Aisee broo, sijamalizia kuishika aisee”

“Shauri yako, si nimekuwekea utazame umeshindwaje sasa”

“Aiisee broo msaada basi”

“Dogo umepoteza si nimekupa uangalie. Umeshindwaje sasa. Twende zetu”

Tukaondoka na kumuacha Raymond akiwa emeduwaa asijue ni nini cha kufanya. Tukaingia ndani ya gari, ka Musa akawasha gari na taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili.

“Tuna kazi moja ngumu mbeleni”

“Kwa nini?”

“Cleopatra mwenyewe ndio hivyo anaolewa, tena na mwanajeshi unahisi tunamshawishi vipi hadi kumpeleka kwa Eddy?”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Ka Musa usoni mwake.

“Tutaona itakavyo kuwa”

“Ka Musa”

“Mmmmmm”

“Kwani huyo Cleopatra mwenyewe ni mzuri kuliko mimi?”

Ka Musa akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaka kimya pasipo kuzungumza chochote.

“Niambie basi”

“Jojo siwezi kuzungumza katika hilo, wewe mwenyewe utaweza kujionea kama ni mzuri ama laaa”

Tukafika katika moja ya benki ka Musa akasimamisha gari nje ya maegesho. Akaniomba nisuburi ndani ya gari kisha yeye akashuka na kuingia ndani ya benki hiyo. Nikatoa simu yangu mfukoni na kuitazama kwa sekunde kadhaa kisha nikairudisha mfukoni. Baada ya kama robo saa Ka Musa akarudi akiwa na bahasha moja iliyo jaa pesa na kunikabidhi.

“Pesa zote za nini?”

Nilizungumza huku nikiwa nimeifunua bahasha hii na kukuta vibunda viwili vya dola za kimarekani pamoja na kibundu kimoja cha shilingi ya Kitanzania.

“Zitatusaidi katika harakati za kumuweka karibu Cleopatra na kurudi naye Dar es Slaam”

“Una hisi pesa inaweza kumshiwishi kurudi?”

“Si pesa kwamba inaweza kumshawishi, ila tulia utaona”

Taratibu tukaondoka katika eneo hili, Ka Musa akasimamisha gari kwenye moja ya duka kubwa la nguo za kike. Akanitazama usoni mwangu kwa sekunde kadhaa.

“Nini?”

“Kanunue nguo”

“Za nini?”

“Unahisi usiku utakwenda hivyo kwenye sherehe ya watu”

“Akhaa kwani kuna ulazima wa mimi kuvaa vizuri”

“Ulazima upo?”

“Watu wakianza kunisumbua, kumbuka ninajulikana sana na watu”

“Sawa, ila nenda kanunue nguo nzuri nzuri”

Nikashusha pumzi, nikachukua kibunda hichi cha pesa za kitanzania, nikavuta noti kadhaa kisha nikashuka kwenye gari, nikaingia kwenye duka hili kubwa, nikaanza kuzunguka huku na kule, nikabahatika kupata gauni moja lenye rangi ya gold inayo ng’aaa vizuri.

“Bei gani hili?”

“Laki tatu na nusu”

“Naliomba”

“Nikupatie pamoja na mtandio wake?”

“Ndio kwani vinauzwa tofauti?”

“Ya mtandio wake ni elfu hamsini nao”

“Poa nipatie”

Muhudumu huyu wa kike niliye ongozana naye akanibebea gauni hili na mtandio wake, nikatafuta na viatu vya juu pamoja na miwani nzuri, kisha nikavilivipia vyote na kurudi kwenye gari.

“Inabidi tupitie hapo mtaa wa pili na mimi ninunue suti kali hivi”

“Sawa”

“Mbona umejibu kinyonge, namna hiyo?”

“Hamna”

“Una uhakika?”

“Yaa”

Tukaondoka eneo hili na kufika katika maduka ya nguo za kiume, ka Musa akashuka na kuingia kwenye moja ya duka, akachagua licho kichagua kisha akarudi kwenye gari. Tukarudi hotelini na kila mmoja akelekea katika chumba chake. Nikaliweka gauni hili kitandani pamoja na viatu na mtandio wake. Nikavitazama kwa sekunde kadhaa, nikavua nguo nilizo zivaa na kuvijaribisha, kusema kweli nimependa na kuvutia kwa kweli. Nikajifunia mtandio huu kichwani mwangu na kujikuta nikizidi kupenda na kuvutia. Nikazichana nywele zangu mtindo anao penda kuuweka msanii mkubwa wa Marekani Rihan, wa kuziba jicho lake moja kwa nywele zake ndefu, kisha nikavaa miwani. Nikasimama mbele ya kioo kilchomo humu ndani kwa hakika nimebadilika kwa asilimia kubwa sana, nina uhakika wa asilimia mia moja kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kunifagamu kwamba mimi ni Jojo.

Nikavua nguoa zangu hizi mpya, kisha nikaingia bafuni na kuoga. Nikajifunga taulo na kurdi kitandani huku nikisubiria muda uzidi kwenda mbele. Simu yangu ya mezani ikaanza kuita , nikaipokea.

“Jojo”

Niliisikia sauti ya ka Musa.

“Ndio”

“Unahitaji chochote?”

“Hapana”

“Saa mbili usiku tunaondoka, ngoja niale kidogo ikifika mida ya saa moja usiku nistue niamke”

“Poa poa”

Nikaurudisha mkonga wa simu hii kwenye sehemu yake maalumu nilipo itoa. Masa yakazidi kusonge mbele huku kichwani mwangu nikipanga mipango mingi ya maisha ya sasa na baadae. Majira ya saa moja usiku nikampigia ka Musa kwa simu ya chumbani kwake, nikamtaarifu kwamba muda wa kujianda umefika. Nilipo maliza kuzungumza naye, nikashuka kitandani na kuingia bafuni nikaoga kwa mara nyingine kisha nikaanza kuvaa nguo zangu. Nywele zangu nikaziweka kama nilivyo ziweka mara ya kwanza, kisha nikavaa miwani yangu. Nikaufunga mtandio wangu vizuri kichwani mwangu. Nikaiweka simu yangu kwenye kijipochi kidogo kisha nikatoka chumbani humu, kwa bahati nzuri nikakutana na ka Musa akitoka chumbani kwake.

Ka Musa akaonekana kama kuto nitilia maanani sana.

“Habari yako dada”

Kaa Musa alizungumza huku akielekea kwenye mlango wa chumba changu nilicho toka, nikajikausha na kumuangalia ni nini atakacho fanya. Akafika kwenye mlango wangu na kuanza kugonga huku akijiweka weka sawa suti yake iliyo mkaa vizuri mwilini mwake.

“Wee ka Musa umechanganyikiwa au?”

Sauti yangu ikamstua na kujikuta akinitazama.

“Jojo ni wewe?”

“Ina maana hujanijua au?”

“Haki ya Mungu sijakufahamu heeee mbona umebadilika hivyo?”

“Acha wenge twende zetu”

Nilizungumza huku nikitabasamu.

“Yaani sijakujua kabisa”

Tukaingia kwenye lifti, tukashuka chini na kelekea eneo tulipo acha gari letu. Tukaingia na taratibu tukaanza kuondoka hapa hotelini.

“Yaani Jojo sijakufahamu kabisa mdogo wangu”

“Ndio hivyo, ninaweza kujibadilisha mimi”

“Kweli sana, unajua na hivyo viatu vimekufanya uzidi kuonekana mrefu ndio, maana sikuhitaji hata kukusumbua”

“Hahaa, inabidi siku nyingine unikremishe kitu chochote mwilini mwangu”

“Kweli asiee”

Tukafika kwenye moja ya ukumbi mkubwa, tukakuata magari mengi huku kukiwa kumeimarishwa na ulinzi wa jeshi. Tukaonyesha kadi yetu, kisha tukaruhusiwa kuingia ukumbini humu. Tukapata eneo la kusimamisha gari letu na kushuka. Nikazunuka upande wa pili wa gari hili na mkono wangu wa kulia nikaushika mkono wa kushoto wa ka Musa.

“Inabidi tutembee hivi, leo kama kuna vijimchepuko vyako humu ndani vinakupiga vibuti”

“Hahaa umejuaje”

“Etiie ehee, visije vikaja kunibabaisha, kwa maana nitavivunja miguu”

“Hahaa haya mwaya”

Tukaingia ndani ya ukumbi, kila tunapo pita si wanaume wala wanawake, wakabaki wakitukodolea macho. Dada m moja akatufwata na akasalimiana na ka Musa kwa furaha.

“Ndio wifi yetu huyu nini?”

“Yeah”

“Aisee mume endana, karibu ukae hapa”

Msichana alituonyesha moja ya viti vilivyo kaa eneo la mbele karibu kabisa na sehemu ya watakapo kaa maharusi.

“Ehhee Musa umemtoa wapi mtoto mkali kama huyu?”

“Ahaa Lily acha hizo bwana”

“No tuambizane”

“Mbona wapo wengi sana”

“Mmmmm”

“Yaa niamini”

Muongoza sherehe akatuomba sote tusimame kwa maana upande wa familia ya wamaume dio wanaingia ukumbini. Tukasimama na ukapigwa mziki wa kilugha cha kisukuma. Wakakaa kwenye eneo lao walilo andaliwa, hazikupita dakika nyingi, famili ya upande wa mume wakaombwa na mshereheshaji kwenda kuwapoke familia ya upande wa wanawake. Dada huyu akaondoka na kwenda kujumuika na ndugu zake.

“Huyu ni nani?”

“Ni dada yao mkubwa”

“Ahaa”

Tukaa kwenye viti vyetu huku tukiwaacha ndui wa familia hizo mbili wakiserebuka kwa mziko walio wekewa na Dj. Muda wakuwakaribisha maharusi wetu ukawadia, wakaanza kutangulia wasichana na wavulana kama sita hivi wanao cheza cheza na kumwaga maua katika kapeti jekundu watakalo pita maharusi. Wakaingia wasimamizi wa maharusi, kisha wakaanza kuingia maharusi wenyewe. Kutokana na kuzonga zongwa na watu wana jitahidi kuwapiga picha na wengine kuwachukua video camera sikuweza kuwaona vizuri ila walivyo fika karibu, mwili mzima ukaanza kunitetemeka kwa hasira, wivu mwingi ukanijaa, kwani mwanaume huyu anaye muoa huyu Cleopatra ni mume wangu Eddazaria.

 

0 comments:

Post a Comment

BLOG