Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MY LIFE SEHEMU YA 7/10

 

 


 MY LIFE

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 7 KATI YA 10

 


Nikamtazama Ka Musa huku nikizidi kutetemeka kwa hasira, ka Musa naye anaonekana kujawa na mshangao mkubwa sana. Nikataka kupiga hatua ya kumwafwata maharusi hawa, ila ka Musa akawahi kunishika mkono wangu.

“Nini?”

“Sio Eddy”

Ka Musa alizungumza huku akitingisha kichwa.

“Tazama shingoni mwake”

Ka Musa alizungumza huku akinionyesha eneo la shingo la mwanaume huyu. Nikaona jeraha kama la kushonwa na nyuzi, ila ni jeraha lililo pona na linalo onekana ni la muda mrefu sana ila kwa upande wa mume wangu yeye hana jeraha kama hilo. Kidogo nikashusha pumzi huku nikiendelea kumchunguza mwanaume huyu. Kitu kingine ambacho kina utofauti kati ya mume wangu na huyu mwanaume wa Cleopatra ni mguu wake wa upande wa kulia kidogo anaonekana kuchechemea japo anajitahidi kutembea vizuri. Hapa sasa amani ndio nikaanza kuipata taratibu sikuhitaji hata kuendelea kusimama, nikaa kwenye kiti changu japo watu wengine wanaendelea kusimama. Ule msemo wa watu duniani ni wawili wa wili sasa leo ndio ninauona, mwanaume huyu kusema kweli ni ngumu sana kutofautisha na mume wangu kama huwafahamu kwa haraka haraka.

“Ka Musa”

Nilimuita Ka Musa kwa sauti ya chini, taratibu akaka chini na kunisogezea sikio lake karibu.

“Una namba yoyote ya daktari kule alipo hifadhiwa mume wangu”

“Ndio ninayo”

“Naomba unipatie?”

Ka Musa akaitoa simu yake mfukoni mwake akanionyesha namba ya daktari huyo. Nikaitazama na kuinakili kwenye simu yangu. Taratibu nikaipiga namba hii, japo kuna mziku mkubwa sana unao endelea hapa ukumbini ila nikainama chini taratibu. Simu ya daktari huyo ikaanza kuita taraibu na kwa bahati nzuri ikapolekewa.

“Haloo”

“Haloo habari yako”

“Salama, nani?”

“Mimi Jojo”

“Jojo gani, mbona kuna kelele sikusikii vizuri”

Nikakata simu kisha nikanyanyuka kwenye kiti hichi nilicho kikalia, nikatoka na kuelekea eneo la vyoo vya wasichana. Nikaingia ndani ya chuoo hichi na kujifungia kwenye moja ya kijichumba kidogo cha choo hichi. Nikampigia tena daktari na simu ikapokelewa.

“Ndio”

“Unazungumza na Jojo, ni mume wa Eddy”

“Ahaaa nimekufahamu”

“Mume wangu yupo hapo nyumbani?”

“Ndio yupo”

“Nahitaji kukupigia video call kupitia whatsapp, hii namba yako si inauwezo wa kutumia mtandao huo wa whatsapp?”

“Ndio nakupigia sasa hivi”

“Poa”

Nikakata na kupiga simu katika mfumo wa video. Ikapokelewa na nikawa ninaonana na daktari moja kwa moj.

“Nahitaji kumuona mume wangu”

Nilizungumza huku nikiwa nimeivua miwani yangu.

“Sawa kwa sasa atakuwa yupo ndani amelala kwa maana nimesha mchoma sindano ya usingizi”

“Nionyeshe kama yupo”

“Sawa madam”

Daktari huyo akatembea hadi chumbani kwa Eddazaria na kuigeuzia kamera katika kitanda cha mume wangu na nikamuona akiwa amelala fofofo. Amani ikazidi kububujika moyoni mwangu.

“Sawa nashukuru”

“Ila kwa nini umeniomba nifanye haya yote?”

“Huyo ni mume wangu na nitakuwa ninakupigia kila siku ili unionyeshe juu ya maendeleo yake na nitakuwa ninakulipa kwa jambo hilo sawa”

“Sawa madam nashukuru sana”

“Asante”

Nikakata simu na kuirudisha kwenye kipochi changu kidogo. Nikarudi ukumbini na kukaa kwenye kiti changu huku kila nilipo kiwa nimepita si wasichana wala wavulana walikuwa wakinitazama kwa macho amabayo ninaamini kwamba katika swala la uzuri na uvaaji wangu nimewapiga bao wasichana wengi sana humu ndani ya ukumbi.

“Jojo”

“Mmmmm”

“Utavuruga shereha ya watu”

“Kwa nini?”

“Kila unapo pita watu wanakukodolea macho mmmm umependeza”

Ka Musa alizungumza kwa sauti ya chini sana huku akiwa amejawa na tabasamu.

“Hahaa shauri yao bwana si wangevaa na kupendeza”

“Mbona wamependa ila umewazidi”

“Tuachane na hizo stori. Hujapata habari yoyote ya wapi wanaweza kwenda baada ya kutoka hapa ukumbini?”

“Bado dogo hajanijulisha”

“Basi hakikisha basi unafahamu, kwa maana tunamuhutaji huyo msichana”

Tulizungumza kwa sauti ya chini snaa na hata watu tulio kaa nao karibu hakuna ambaye anaweza kutusikia. Nikaanza kumfwatilia bibi harusi huyu ambaye ndio Cleopatra. Ni msichana mzuri kwa kweli kwa kuchagua basi mume wangu anachagua, ila kama ni vigezo mimi na yeye tutakuwa tumetofautiana kidogo sana, ila kwa namna moja ama nyingine mimi ndio nimemzidi mwenzangu kidogo. Sherehe ikazidi kusonga mbele huku shuhuli muhimu zikiendelea kufanyika.

“Una pesa kiasi gani hapo mfukoni?”

“Nina dola elfu hamsini”

“Naomba dola elfu ishirini”

“Ya nini?”

“Wewe naomba kama unahitaji nikurudishe basi nitakurudishia”

Ka Musa akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akachomoa kibunda cha pesa hizo na kunitolea vibunda viwili.

“Kila kubunda kina dola elfu kumi kumi”

“Sawa sawa”

Muda wa zawadi ukawadia, wakatoa wazazi zawadi zao wa pande zote mbili, kisha wakafwata wageni, nikawa wa kwanza kunyanyuka na kumaucha ka Musa akinishangaa sana. Nikafika sehemu walipo kaa maharusi kwenye viti vyao, nikatoa kibunda cha dola elfu ishirini na kuanza kutoa dola moja baada ya nyingine jambo lililo sababisha, vifijo na nderemo kuendelea kurindima ndani ya ukumbi huu. Nikaendelea kuwamwagia pesa hizi za kigeni, kilipo isha kubunda hichi cha kwanza nikatoa kibunda cha pili na juendelea kuwamwagia naharusi hawa jambo lililo zidi kuwapagawisha watu ndani ya ukumbi huu. Nilipo hakikisha kwamba nimemaliza kutoa pesa hizi nyingi ambazo kwa haraka haraka ni sawa na kama milioni arubaini hivi za kitanzani, nikarudi katika kiti changu na kumkuta ka Musa akiwa amenuna sana.

“Ni ujinga gani ule ulio ufanya Jojo?”

“Kwani tatizo ni nini?”

“Ni milioni arubaini zile unajua?”

“Ndio najua, kwani tatizo lipo wapi. Tulia na utajia ni nini maana ya mimi kufanya hivi”

Watu wengine wakafwata katika kutoa chochote kitu. Tukapata chakula cha usiku kisha muda wa maharusi kutoa ukumbini ukawadia, huku wakiwa wanaelekea katika hoteli ‘LAKE MANYARA SERENA LODGE’ kwa mapumziko ya wiki moja.

“Tutaelekea kwenye hiyo hoteli ambayo wanakwenda kupumzika?”

“Tutakwenda kesho asubihi”

“Kesho asubuhi, kwa nini isiwe ni usiku wa leo?”

“Leo ni lazima watakuwa wanalindwa lindwa”

Ka Musa alizungumza huku tukiingia ndani ya gari. Tukaondoka eneo hili na safari ya kurudi hotelini ikaanza taratibu.

“Jojo kusema kweli leo umeniudhi sana”

“Nimekuudhi na nini ka Musa jamani?”

“Kwa nini utoe pesa zote zile unajua zilikuwa na mipango gani?”

“Hilo ndio lililo kukera si ndio?”

“Ndio”

“Tupitie bank nikupatie hicho kiasi, si milioni arubaini eheee?”

Nilizungumza kwa ukali kidogo.

“Ndio”

“Basi pitia banki sasa hivi nitakupatia”

Nilizungumza kihasira kidogo kwa maana ninaona ka Musa ana uchungu mkubwa sana wa pesa ambazo nimezitoa.

“Kesho”

Ka Mus alinijibu kwa ufupi sana. Tukafika hotelini na kika mmoja akaelekea chumbani kwake. Nikapanda kitandani huku nikitafakari juu mbinu gani ambayo ninaweza kuifanya kwa ajili ya kumuweka Cleopatra karibu yangu ili niweze kumshawishi juu ya uhitaji wa mume wangu. Nikiwa katikati ya mawazo hayo bila ya hata kubadilisha nguo zangu wala kuvua viatu, usingizi mwingi ukanipitia na nikalala fofofo. Mlio wa simu yangu ndio ukaniamsha, nikafumbua macho yangu na kuichukua pembeni ya kitanda nilipo iweka, nikaitazama namba hii na kukuta ni mama mkwe ndio anaye nipigia, kwa haraka nikanyanyuka na kukaa kitako kitandani.

“Shikamoo mama”

“Marahab ehee nipe ripoti”

“Tumefanikiwa kumuona Cleopatra”

“Eheee anasemaje?”

“Bado hatujafanikiwa kuzungumza naye kwa maana jana ndio siku yake ya kuolewa.”

“Ameolewa!!!?”

“Ndio mama”

“Mmmmm, sasa mutampataje kama jana ndio kwanza ameolewa?”

“Leo ndio tunajiandaa kwenda kwenda kwenye hoteli ambayo wamefikizia, naamini hapo ndipo tunaweza kufanya lolote linalo wezekana kuweza kumpata”

“Sawa, kama mutahitaji msaada wa vijana basi niambieni niweze kuwapatia.”

“Usijakki mama, ila mama ninaweza kukuuliza swali”

“Niulize?”

“Eddy uliwazaa mapacha?”

“Mapacha, mapacha kivipi?”

“Ahaa……basi tutazungumza baadae mama”

“Sawa kuweni makini sana katika hilo swala”

“Haya mama”

Nikakata simu, nikanyanyuka kitandani, nikavua nguo zangu zote na kuingia bafuni na kuoga. Nikarudi chumbani na kujiandaa kwa kuva anguo nyingine, nikakusanya kila kilicho changu na kutoka chumbani humu. Nikamgongea ka Musa mlangoni mwake na kumkuta akiwa na yeye tayari amesha maliza kujiandaa.

Tukaondoka eneo hili na safari ya kulekea katika mbuga ya wanayama ya Manyara ikaanza. Njiani ka Musa hakuwa mzungumzaji sana kama siku iliyo pita.

“Tumepata chumba kimoja huko tunapo kwenda”

Ka Musa alizungumza kwa ufupi na sauti nzito kidogo.

“Sawa”

Nami nilimjibu kwa ufupi. Ka Musa akapunguza mwnedo kasi wa gari lake na taratibu akalisimamisha pembeni ya barabara.

“Vipi mbona umesimamisha gari?”

Ka Musa akanitazama kwa macho ya upole na unyonge mwingi sana.

“Jojo ninakupenda kutoka moyoni mwangu, nakuomba twende mbali, achana na familia ya yule mama twende tukaishi maisha yetu mbali na hapa. Nipo tayari hata kufa kwa ajili yako Jojo nakupenda sana”

Ka Musa alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake jambo lililo nishangaza sana na kujikuta nikiwa na bumbuwazi kwani sikutarajia kwa kipindi kama hichi ka Musa anaweza kunieleza maneno ya kipuuzi kama haya.



Nikajikuta nikitabasamu kwa dharau sana huku nikito kicheko cha chini chini.

“Unaweza kuendelea kuendesha gari au niendeshe mimi mwenyewe”

“Jojo, hisia hazijali mtu anafanya kazi gani au anaonekana vipi u…..”

“Acha uongo wako, hujanipenda na umenitamani tu kwa jinsi nilivyo. Mbona nyinyi wanaume hamuwi kama mume wangu, mbona munapenda kuona kwa macho na si kwa moyo. Nilimtesa sana Eddy na hadi kuwa katika hali kama ile ni kutokana nami. Unahisi kwamba sifahamu kwamba mimi ndio chanzo cha matatizo. Leo hii wewe ambaye nimeona utakuwa ni msaada kwangu kumpata msichana anaye hitajika na mume wangu umekuwa ndio mtu wa kwanza kunishawishi eti tukimbie mbona unazungumza upumbavu eheee?”

Nilizungumza kwa kufoka sana huku hasira ikiwa imenitawala sana usoni mwangu na moyoni mwangu. Ka Musa akakaa kimya huku akitazama chini, inaonyesha dhairi anajutia ni kwa nini amezungumza hisia zake kwa muda na wakati kama huu.

“Sihitaji kuwa msaliti tena kwa mume wangu na ukumbuke kwamba nina mtoto, nina mtoto nyumbani kwangu hivyo siwezi kumuacha yeye niambatane nawe kwa kipi cha ajabu eheee?”

“Au una mbo** ya dhahabu na si ya nyama kama wanaume wengine eheee?”

Kusema kweli ka Musa amenivurugia siku yangu asubuhi yote hii.

“Jojo”

“Jojo nini, unahisi mimi mwanamke rahisi rahisi eheeee?”

Ka Musa akazidi kukaa kimya huku akitamani kitu ila ninamnyima uhuru wa kuzungumza neno lolote.

“Washa gari tuondoke, kama unashindwa pisha niendeshe mwenyewe”

“Nisamehe”

“Wanasha tuondoke usinichefue”

Ka Musa kwa unyonge akawasga gari na taatibu tukaanza kuondoka eneo hili huku akijifuta machozi yake. Nikafungua mkanda wa siti ya mbele niliyo kalia na kuhamia siti ya nyuma huku mwili wangu ikichemka kwa hasira kali kwani katika maisha yangu sipendi ninapo kuwa na tatizo fulani na mtu naye ananiletea tatizo lake binafsi ambalo kwa namna moja ama nyingine halina msingi wowote kwenye maisha yangu. Nikatoa simu yangu kwenye mfuko wa suruali na kuitafuta namba ya mama mkwe, nikaitazama kwa sekunde kadhaa huku nikihema, kisha nikaipiga. Simu ya mama mkwe ikapokelewa.

“Mama”

“Nipo ikulu Jojo baade”

Mama mkwe alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza akionekana dhairi kwamba yupo kwenye swala muhimu sana. Nikakata simu pasipo kuzugumza kitu chochote.

“Jojo”

“Nini?”

“Naomba unisamehe”

“Bwana weee endesha gari usizidi kunitibua yaani ninakuchukia, najuta kwa nini nimekuja na wewe huko ulihisi yake maneno ya kukuambia kwamba mimi ni mpenzi wako mbele za watu ulihisi kwamba ni kweli eheee?”

“Hapana Jojo ila….”

“Ila nini hembu endesha tuwahi kufika mimi nimesha jichokea”

Ka Musa akanitazama kwa kupitia kioo kilichopo humu ndani ya gari, nikatoa earphone zangu kwenye begi la langu la nguo, nikazichomeka kwenye simu na kuweka mziki mzuri ninao upenda kisha nikazivaa masikioni mwangu. Kadri ya muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi ninavyo ona jinsi miti ya inavyo rudi nyuma kwa kasi, ikiwa ni kipimo tosha cha macho kwamba dereva anaendesha gari hili kwa mwendo wa kasi sana. Nikachungulia kwenye sehemu yenye mshale unao hesabu mwendo wa dereva, nikashuhudia mshale huo mwekundu ukielekea kwenye spidi ya mia na themanini.

“Wee ka Musa huoni mwendo ni mkali huo?”

Ka Musa hakunijibu chochote zaidi ya kuendelea kuongeza mwendo kasi, tukaona roli mbili mbele za kokoto zikiwa zimeongozana ka Musa akaanza kupita lori moja kwa mwendo huu huu wa kasi, tukiwa tupo katikati ya kulipita lori la pili tukaona gari aian ya Noah, ikija kwa kasi mbele yetu. Ka Musa hakupunguza mwendo wa gari, dereva wa Noah akawasha taa zake zote akimuashiria Ka Musa kwamba upande alipo sio wake na wote wapo kasi. Chakumshukruu Mungu dereva wa roli akapunguza mwendo kidogo na kumpa Ka Musa nafasi ya kurudi upande wake na Noah hiyo ikapita kwa kasi sana yaani bado kidogo tu tugongane uso kwa uso.

“Mpuuzi wewe unataka kufa eheeeee?”

Nilimuuliza Ka Musa huku nikimpiga piga kwenye bega lake la upande wa kushoto. Ka Musa hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuzidi kuendesha gari kwa mwendo wa kasi sana huku akikunja kona kasha kwa mwendo huo huo hadi gari linayumba kwa kweli.

“Wee ni chizi ehee punguza mwendo bwanaa”

Ka Musa akanitazama kidogo kisha akaachia mikono yake miwili huku gari likiwa katika mwendo wa kasi, kwa mbele kuna kona moja kubwa sana. Macho yakanitoka huku machozi yakinilenge lenge kwani ka Musa amedhamiria kufa pamoja na mimi. Nikafumba macho yangu huku mapigo ya moyo yakinienda kasi sana, jasho likaanza kunimwagika usoni mwangu.

“Hahahaaaa hahaaa”

Nilisikia sauti ya kichecho cha ka Musa na kunifanya nifumbue macho yangu, nikamkuta akiwa ameshikilai mskani wa gari huku akiimalizia kuikunja kona hiyo ambayo angeendelea kufanya ujinga wake basi sasa hivi tungekuwa tunazungumza mambo mengine.

“Waoooooo.”

Ka Musa alishangilia na kuzidi kunikasirisha.

“Musa ninasehema simamisha gari niendeshe mimi mwenyewe”

Nilizungumza kwa sautu ya chini ila iliyo jaa hasira huku nikiwa nimeyang’ata meno yangu kwa hasira kali sana.

“Si sisimamishi na utakoa na jeuri yako. Mtu ninakualeza hisia zangu bado unaendelea kuwa mpuuzi na mjinga na unanifokea kama mtoto, haya huyo mume wako ananiheshimu na kunisalimia kwa heshima na hata siku moja hakuwahi kunivunjia heshima ila wewe kunguni mdogo ndio unaleta dharau eheee?”

Ka Musa alizugumza kwa kufoka na kujikuta nikinyamaza chini huku nikutazama mbele.

“Nakueleza hisia zangu unajiadai kufoka, foka. Hivi jana kwa kukaa na wewe kwenye sherehe umejua nimeachana na wanawake wangapi, unalifahamu hilo mseng*** wewe…..?”

Ka Musa aliendelea kuzungumza kwa hasira huku machozi yakimwagika usoni mwake.

“Mwanamke ninaye mpenda nimeachana naye kwa ajili yako wewe, nimekueleza kwamba ninakupenda unahisi kwamba ninaitamani kum** yako eheee?”

Nikaendelea kukaa kimya na kutulia kama maji yaliyomo ndani ya mtungi.

“Siogopi kufa mimi, siogopi kabisa kufaaa. Kama ni kufa ningesha kufa kwa ajili yako mpuuzi wewe. Ila bado unazidi kuleta swaga za kiseng** Unahisi pesa zako zinaweza kupelekesha kila mtu eheee?”

“Ka Musa yaishe basi”

Nilizungumza kwa unyonge.

“Ka Musa yaishe basiiiiii kenge wewee”

Ka Musa alizungumza huku akiwa ameibana pua yake.

“Nisikilize wewe mtoto wa juzi juzi, unaipenda au hunipendi niliangushe gari tuvunjike vujike au hata kufa sasa hivi ili mbwembwe zako zote ziishe”

Ka Musa alizungumza huku akianza kuliyumbisha yumbisha gari hili. Mwili mzima ukaanza kunitetemeka.

“Unaliona lile bonde mule, ninakwenda kulitosa hili gari, niambie unanipenda au hunipendi”

“Ila Ka Musa haya sio mapenzi ya dha….”

“Kum** wewe unataka kufa sirudii tena”

Ka Musa alizungumza kwa ukali huku akienelekea kwenye bonde hili.

“Nakupenda, nakupenda”

Nilizungumza kwa woga kwani tumebakisha mita chache sana kulifikia bonde hili.

“Unanipenda kama nani?”

“Mpenzi, mpenzi wangu”

“Nipe denda”

Ka Musa alizungumza huku akiendelea kuyumbisha gari hili, kwa haraka nikamsogelea na kushika mashavu yake na kuanza kunyonya midomo yake ikiwa ndio mara yangu ya kwanza toka kuzaliwa kwangu kufanya kitendo hicho kwa mwaume tofauti na mume wangu Eddazaria.

“Ewalaaaaa hapo sawa”

Ka Musa alizungumza na kupunguza mwendo wa gari hili na taratibu akaliweka sawa barabarani na kuendele na safari hii.

‘Haki ya Mungu denda hilo litakugarimu mseng** wewe’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama ka Musa usoni mwake. Ukimya ukatawala ndani ya gari hili huku nikiwa nina mawazo mengi sana huu ya ka Musa kiasi kwamba hata mawazo ya kumfikira Cleopatra yakaanza kunipungua kichwani mwangu.

“Baby mbona umekaa kimya?”

Ka Musa alizungumza kwa sauti ya upole, jina alilo niita likazidi kuipandikiza chuki ya kumchukia ndani ya moyo wangu.

“Hatujafika tu”

“Tutafika baada ya kama dakika kumi na tano hivi”

“Okay”

“Duu Jojo mate yako ni matamu sana, yaani sijui hiyo kum** yako itakuwa na utamu gani, natamani tuwahi kufika unipe utamu mtoto wa kike”

‘Kum*****ko nitakacho kufanya wewe kenge utajuta kunijua’

Niliendelea kujiapiaza moyoni mwangu.

“Etii Jojo, kum** yako si itakuwa ni tamu kuliko hata mate yako”

“Hivi umekosa mada ya kuzungumza?”

“Nimekuliza tu mpenzi wangu”

“Basi nakuomba ukaushe basi”

“Mbona unanijibu kwa hasira sasa”

“Ka Musa……….”

“Sio ka Musa niite baby”

Nikatamani hata kumnyongea ndani ya hili gari kwani kila neno linalo toka kinywani mwake linanikasirisha na kunikera kwa kweli.

“Okay baby”

“Ewalaaaa niambie mama watoto”

“Hamna”

“Hamna, mbona unaonekana kama unahitaji kuniambia kitu kizuri mpenzi wangu”

“Usijali, nitakuambia kitu hicho tikifika hotelini”

“Kweli mpenzi wangu?”

“Yaa wewe jiandae kupata utamu wangu mwanana”

“Ohoo yaani umezungumza hivyo hadi mbo** yangu imesimama, njoo uione”

Ka Musa alizungumza huku akifungua zipu ya suruali yake, cha kushangaza akautoa uume wake wote nje ukiwa umesimama.

“Umeuona umeuona eheee?”

Yaani nikatamani kuwa samba niung’ofoe ili nimfundishe adabu ya tabia mbaya na ya kishenzi ambayo ameninyesha.

“Yaa”

“Njoo uunyonye basi mpenzi wangu”

“Tupo barabarani mpenzi wangu, tukifika tu tunaingia ndani na kupeana mautamu”

“Ohoohooo kweli mpenzi wangu”

“Asilimia mia moja kabisa”

Kwa Musa akaurudisha uume wake ndani ya suruali yake huku akionekana kujawa na hamu kubwa ya kutaka kufanyiwa kile nilicho muahidi kwamba nitamfanyia. Tukafika katika geti la hoteli hii ya kitalii inayo itwa LAKE MANYARA SERENA, ka Musa akafanya malipo yanayo takiwa kulipiwa hapo getini, kisha moja kwa moja tukaelekea eneo zuri la magesho. Tukashuka ndani ya gari hili, ka Musa akazunguka upande wa pili wa gari nilipo simama, akachukua begi langu la nguo na kunishika kiuno changu. Sikutaka kumkatalia kwa maana kuna wazungu kadhaa wakitutazama. Tukafika mapokezi, ka Musa akaulizia chumba chake akalipa kiasi cha pesa kilicho kuwa kimesalia kisha muhudumu wa ziada akatuongoza hadi kwenye kijumba chetu ambacho kina chumba, seble na kina kila kitu kinacho takiwa kuwemo ndani ya vymba hivi.

Ka Musa kwa haraka akanza kuvua koti lake la suti, akafwatia shati lake huku akionyesha dhauri kwamba ana uchu wa penzi langu, nikatazama eneo hili la sebleni kama ninaweza kupata kitu hata cha kumpiga nacho kichwani ila sijaona.

“Vua basi baby”

Ka Musa alizugumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nitavua”

Akanisogelea na kunishika mkono wangu wa kushoto na kunivuta karibu yake. Akaanza kunishika maziwa yangu kwa papara huku mkono wake mwengine ukinishika kiuno changu na kuzidi kunigandamiza kifuani mwake jambo lililo nifanya nizidi kupandwa na hasira na nikaanza kukiria ni pigo gani ambalo ninaweza kumpiga ka Musa na kumdhibiti mazima na ashindwe kuendelea na upumbavu wake huu ambao anaendelea kuufanya kwangu.



Akili yangu ikafanya kazi haraka sana, nikakumbuka mafunzo yote aliyo nipatia bibi Sosiono kipindi nilipo kuwa naye nchini China. Nikampiga ka Musa kigoti katika sehemu zake za siri na kumfanya atoa mguno mzito wa maumivu huku mikono yake yote ikishika sehemu zake hizo za siri. Kosa kubwa ni kwa yeye kuinama kwani, ikanipa fursa ya mimi kumpiga ngumi ya shingo eneo ambalo mtu yoyote anapo pigwa ni lazima apoteze fahamu kwa muda kidogo na ndivyo jinsi ilivyo tokea kwake na taratibu akaanguka chini na kutulia tuli.

“Hichi ndicho ulicho kuwa ukikihitaji”

Nilizungumza huku nikijiweka sawa nguo zangu, nikafungua begi la ka Musa na kuchukua kiasi cha pesa, sikuhitaji hata kuzihesabu, nikachukua na swete langu lenye kofia kisha nikatoka humu ndani. Nikaelekea kwenye moja ya baa iliyopo ndani ya hoteli hii ya kitalii. Nikaaa kwenye moja ya kiti kirefu na kuagizi soda ya baridi sana japo eneo hili lenyewe lina baridi kali. Muhudumu akanipatia soda hii niliyo ihitaji na nikaanza kuinywa haraka haraka.

“Hei mambo”

Nilisikia sauti ya kike ikizungumza nyuma yangu, kwa haraka nikageuka na kumtazama msichana huyu ananisalimia. Nikamkuta na Cleopatra akiwa na mume wake ambaye anafanana kama Eddazaria. Taratibu nikatabasamu huku nikimtazama usoni mwake

“Habari yenu”

“Safi tu kumbe na wewe umekuja huku?”

“Yaa, nimekuja kutuliza akili kidogo.”

“Kweli, wewe si Jojo?”

“Yaa ni Jojo”

“Waooo, mume wangu huyu ndio yule dada nilitekuwa nikikusimulia kipindi kilee”

“Ahaa nashukuru kukufahamu Jojo”

Mume wa Cleopatra alizungumza huku akinipa mkonno, Taratibu na mimi nikampatia mkoo wake.

“Jojo mimi ninaitwa Cleopatra na huyu ni mume wangu anaitwa Ben”

“Ohoo asante sana Ben kwa kukufahamu”

“Ninashukuru”

“Jana ndio ilikuwa ni harusi yetu na leo ndio tumeamua kuja huku kujipumzisha”

“Ahaaa…sawa sawa”

“Sijui unaweza kujumuika nasi kwenye ile meza pale?”

Cleopatra alizungumza kwa uchangamfu sana, nikaitazama meza yao kisha nikatingisha kichwa nikiasihiria kwamba nimekubaliana naye. Nikaibeba chupa yangu ya soda na kujumuika naye kwenye meza yao. Muhudumu akatufwata na kutuuliza tunatumia nini kwa muda huu.

“Mimi hii hii soda inatosha”

“Ahaa..Jojo agizia chakula bwana”

“Hapana shemeji, nipo sawa”

Wakaagizia chakula chao na mimi nikaendelea kunywa soda yangu taratibu huku nikifikiria ni jinsi gani ninavyo weza kuondoka na Cleopatra katika eneo hili la Arusha.

“Jamani Jojo, sisi tunakula huku wewe unakunywa soda tu, hadi najisikia vibaya”

Cleopatra alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Usijali mimi nipo vizuri”

“Laiti kama ningekuwa na namba zako za simu ningekualika une kwenye harusi yangu”

Hapa kidogo nikaanza kupata picha kwamba uwepo wangu jana kwenye harusi yake hakuweza kunifahamu kabisa.

“Hahaaa usijali, ila kusema kweli mumependeza”

“Etii ehee?”

Ben naye alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake. Cleopatra akaonekaa kama aja jambo la kuzungumza ila akaka kimya.

“Filamu yako Jojo, mbona hadi leo haitoki”

“Itatoka tu”

“Lini sasa ni mwaka na kitu tangu muanze kuitangaza?”

Cleopatra aliendelea kuzungumza.

“Usijali itatoka kuna mambo kidogo yalingiliana ila itatoka tu”

“Jamani ninakuja mara moja”

Ben alizungumza huku akinyanyuka, akambusu Cleopatra mdomoni mwake na akaondoka eneo hili na kutuacha sisi peke yetu. Ukimya ukatawala katikati yetu huku kila mmoja akionekana kwamba anahitaji kuzungumza jambo kwa mwenzake.

“Mume wako anaendeeaje?”

Cleopatra alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Mume wangu…….”

“Eddy, ninatambua kwamba wewe na Eddy muna mahusiano si ndio?”

Cleopatra alizungumza huku akiwa na msisitizo ulio nifanya nianze kushikwa na mshangao kidogo dhidi yake.

“Ndio na tumejaliwa kumpata mtoto, na nimekuja huku kwa ajili yako”

“Umejaliwa kupata mtoto, umekuja huku kwa ajili yangu, una maanisha nini?”

“Eddy anakuhitaji, anahitaji akuone”

“Hahaaa amechekewa, wewe si upo au anataka nini kwangu. Hajui ni jinsi ganin ilivyo teseka, hajui ni jinsi gani alivyo niacha na makovu ya mamivu kwenye moyo wangu, sasa mimi wa nini kwake?”

Cleoptara alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikatazama eneo alipo elekea Ben na sikumuona akiwa anakuja huku.

“Cleopatra sijui ni kitu gani kilicho weza kutokea kati yako wewe na Eddazaria. Ila mimi jana nilikuwa kwenye sherehe yako, mimi ndio yule niliye wapitia pesa za kimarekani.”

“Kwa hiyo ulikuwa unanipatia pesa ili iweje?”

“Ni zawadi kama kawaida, ila tambua kwamba Eddazaria anakuhitaji, najua unampenda mume wako, ila nakuomba unisaidie kama mwanamkwe mwenzio katika kuirudisha akili ya mume wangu na kuwa sawa kwa maana hivi sasa amekuwa kama mwendawazimu amaechanganyikiwa. Yeye ndio amekuita nakuomba ulifikirie hilo”

Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo nikanyanyuka, nikataka kuondoka ila Cleopatra akawahi kunishika mkono.

“Unasema kwamba amechanganyikiwa?”

Cleopatra alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingis ana.

“Ndio”

Taratibu akashusha pumzi nyingi sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Japo nipo na Eddy, japo nimezaa naye ila wewe ndio daktari wake, wewe ndio daktari wake wa mapenzi, lifikiria hilo na uendelee kuliweka akilini.”

Nikautoa mkono wangu na kuondoka eneo hili nikaurudi katika chumba ambacho nilimuacha ka Musa. Nikaingia ndani, ila cha kunishangaza sikumkuta ka Musa katika eneo ambalo alikuwa ameanguka. Nikaingia katika chumba cha kulala napo sikuweza kumkuta, nikapitiliza moja kwa moja hadi bafuni napo pia sijamkuta.

‘Atakuwa amekwenda wapi?’

Nilijiuliza swali hili huku nikurudi sebleni. Jinsi mageni nilivyo yaacha ndivyo jinsi ninavyo yaona hapa. Nikatoa simu yangu mfukoni na kuitafuta namba yake, nikataka kumpigia simu ila roho ikasiti kidogo, nikatoka ndani humu na kuanza kuelekea kwenye eneo la maegesho ya magari cha kushangaza napo sikuweza kukuta gari letu. Hapa sasa nikaanza kuhisi hali ya hagtari kwamba inaweza kutokea, kwa haraka nikampigia simu mama mkwe, simu ya mama mkwe ikaanza kuita hadi ikakata, nikarudi tena kuipiga na ikapokelewa.

“Mama shikamoo”

“Marahaba vipi mbona unazungumza kwa wasiwasi mwingi, kuna tatizo gani tena?”

“Mama ka Musa simuoni ameondoka”

“Ameondoka kivipi?”

“Tulifika hapa hotelini, kuna mambo akawa anataka kuyafanya sasa nimerudi ndanin ilipokuwa nimeuacha sijaweza kumuona na sifahamu ni wapi alipo”

Nilizungumza haraka haraka dhairi inaonyesha ni kwamba nimajawa na wasiwasi mwingi sana.

“Ni mambo gani alikuwa anataka kuyafanya?”

“Mambo yake tu”

“Ndio ni yake ni mambo gani?”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikitafakari ni nini cha kuzungumza.

“Alitaka kunibaka”

“Nini?”

“Ndio mama, ila niliweza kumdhibiti na kumpiga akawa amepoteza fahamu”

“Pumbavu zake, sasa sikia ninakutumia namba ya simu ya mkuu wa mkoa wa Arusha, ni ndugu yangu mpigie muelezee juu ya hilo swala, kisha atakutumia gari akuchukue eneo hilo sawa’

“Sawa mama”

“Pumbavu huyu musa, nilijua tu atafanya upuuzi”

Mama mkwe alizungumza huku akiachia msunyo mkali sana. Akakata simu, nikajukuta mwili mzima ukinitetemeka. Nikatazama eneo hili nililo simama, hakuna mtu anaye jishuhulisha na mimi. Hata kabla sijaondoka ikaingia meseji kwenye simu yangu, nikaifungua na kukuta ni meseji ya namba ngeni.

‘Najua umenichafulia tayari kwa mama, sasa nilazima nitakukomesha’

Mesji hii dhairi inaonyesha inatoka kwa ka Musa ambaye tayari amesha kuwa msaliti kwangu na kwa mama kwa ujumla. Ikaingia meseji nyingine kutoka kwa ka Musa.

‘Tegemezi lako huku si Cleopatra, naye ninamuua na mumeo ayaendelea kuwa mwendawazimu hadi kufa kwake’

Nikajukuta nikichanganyikiwa huku nikimfikiria Cleopatra. Kwa haraka nikaanza kuelekea katika eneo nilipo muacha Cleopatra, nikafika katika meza ambayo alikuwa amekaa, sikumkuta.

“Samahani dada, kuna msichana mmoja alikuwa amekaa hapa pamoja na mume wake sijui umewaona?”

“Ulivyo ondoka, naye aliondoka na kijana mmoja mwengine”

“Yupoje yupoje?”

“Mrefu kiasi na nimaji ya kunde”

Kwa sifa hizo tu alizo nieleza muhumu huyu kwa haraka nikatambua kwamba ni ka Musa ndio ameondoka na Cleopatra.

“Hili eneo lina kamera?”

“Ndio, kunai le pale na ile pale”

Muhudumu alizungumza huku akinionyesha kamera mbili zilizopo kwenye kona mbili tofauti za ukuta.

“Ninaweza kuona video zilizo rekodiwa kwa muda mfupi ulio pita?”

“Hapana ni vigumu kwa sisi kuweza kumuonyesha mtu yoyote rekodi za kamera pasipo kuwa na kitambulisho sahihi”

“Tafadhli dada yangu ninakuomba sana unisaidie katika hili”

“Siwezi mdogo wangu”

“Unahitaji kiasi gani nikupatie?”

“Hata ukinipatia pesa siwezi kufanya hivyo dada yangu, hilo jambo lipo kinyume na maadili ya kazi yangu”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia mama mkwe na akapokea.

“Mama Ka Musa amemchukua mateka Cleopatra”

“Nini?”

“Ndio mama”

“Ohoo Mungu wangu”

“Na amenitumia meseji kwamba ni lazima kwamba atamuua”

Nikiwa ninazungumza hapa nikamuona Ben akija aneo hili huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.

“Nakutumia namba ya mkuu wa mkoa na ninampa maelekezo ya kuweza kumdhibiti huyo mshenzi”

“Sawa mama”

“Jojo umemuona Cleopatra?”

Ben aliniuliza mara baada ya kufika katika eneo hili nililo simama.

“Hata mimi nilikuwa nimemuuliza huyu muhudumu hapa ananiambia kwamba ameondoka na ka Musa”

“Ka Musa ndio nani?”

“Alikuwa ni mlinzi wa mama yangu”

“Mlinzi?”

“Ndio na inavyo onyesha ni kwamba Ka Musa amemteka Cleopatra”

Nikaanza kukiona kifua cha Ben kikianza kupanda na kushuka kwa kasi huku kikivimba, ikiashiria kwamba ana hasira kali sana.

“Yupoje yupoje huyo Musa?”

“Dada hapa amemuona na kuna kamera zile pale nimemuomba niweze kuona rekodi iliyo rekodiwa ila amenikatalia”

Ben aakatoa kitambulisho chake na kumonyesha huyu muhudumu. Muhudumu akakitazama kwa muda kitambulisho hicho kisha kwa ishara akatumba tumfwate. Tukaingia kwenye moja ya chumba chenye Tv nyingi sana. Tukamkuta kijana mmoja muhudumu huyu akampa maelezo ya kile tunacho kihitaji na kijana huyo akatuonyesha rekodi za video zilizo rekodiwa eneo lile muda mchache ulio pita. Kweli tukamuona Ka Musa akiwa akizungumza na Cleopatra huku wakiwa wanacheka sana japo mazungumzo yao hayasikiki kwetu.

“Huyu jamaa jana si alikuwepo kwenye harusi yangu?”

“Ndio”

Tukaowana wakiondoka katika eneo hilo na kuelekea katika eneo la maegesho ya magari na wakaingia kwenye gari ambalo tulikuja nalo katika eneo hilo na kuondoka hotelini hapa.

“Nikimkamata huyu ngedere Musa ni lazima nitamuua kwa mkono wangu mimi mwenyewe hawezi kuondoka na mwanamke wa maisha yangu”

Ben alizungumza huku akiwa amejawa na hasira kiasi kwamba watu dada huyu muhudumu pamoja na kijana huyo wakastuka sana kwani hawakutaraji kuskia kauli kama hii kutoka kwa Ben.



Ben akatoka ndani ya chumba hicho huku akiwa amejawa na hasira sana. Nikaanza kumfwata kwa nyuma huku nami nikiwa ninasikilizia ni kitu gani ambacho atakiamua kwa muda huu. Tukiwa tunaelekea katika maeneo ya maegesho ya magari simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa katika mfuko wa suruali yangu. Nikakutana na namba mpya ambayo sijawahi kuiona kwenye simu yangu, nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Haloo”

“Jojo nisikilize kwa umakini mimi sana”

Niliisikia sauti ya Cleopatra akizungumza jambo lililo nifanya nistuke sana.

“Nimeondoka hapo kutokana na nguvu ya mapenzi yangu juu ya Eddy ninampenda sana kuliko hata ninavyo mpenda Ben. Najua kwamba Ben anafanana sana na Eddy sana nakuomba tufanya mabadilishano ya kutosha tu. Wewe baki na Ben na mimi nibaki na Eddy wangu ambaye nimetoka naye mbali kuliko unavyo fikiria sawa”

“We….ew……eeee uu…”

Nilijikuta nikipatwa na kigugumizi kikali sana kiasi kwamba hata kasi yangu ya kutembea kumfwata Ben anaye onekana kuwa na haraka sana.

“Usipatwe na kiguhumizi, Ka Musa ndio ananipelekea kuonana na mume wangu ninaye mpenda kuliko chochote kwenye maisha yangu”

“Wewe acha upumbavu huyo ni gaidi anataka kukuua”

“Mimi ndio niliye muambia akutumia hizo meseji na wala usihi kwamba ni msaliti kwa bosi wake kwa maana hufahamu ni wapi tulipo toka”

Nikahisi kama kuchanganyikiwa kumbe meseji zote ambazo kaka Musa amezituma kwangu amepata maelekezo kutoka kwa Cleopatra.

“Ukifanya chochote kwa mume wangu, nakuapia haki ya Mungu sinto kwenda kukuacha mzima na nitakuwinda popote na kukuua malaya wewe”

“Hahaaa, malaya ni wewe laiti angekuwa ni mume wako hadi sasa hivi ungekuwa na pete ya ndoa mkononi mwako, ila hadi sasa hivi huna cha ndoa wala ushuzi kwa hiyo sio mume wako ni boyfriend wako tu”

Maneno ya Cleopatra yaliyo jaa dharau yakazidi kunichanganya na kunizidisha jazba niliyo nayo.

“Kumbuka nina mtoto naye hivyo basi ni mume wangu”

“Hahaaa, hata mimi ninaweza kubeba ujauzito wake na kumbua huyo panya wako uliye mzaa sio mwanae wa kwanza na alikuwa na mwanaye mwengine kabla ya huyo kwa hiyo usijishaue”

Nikajikuta nikikata simu huku mapigo ya moyo yakinienda kasi sana.

‘Nitakuua wewe mbwa, huwezi kumchukua mume wangu mpuuzi wewe’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikielekea eneo la mapokezi. Nikawakuta vijana wawili wa kiume na wakaonekana kujawa na furaha mara baada ya kuniona.

“Samahani”

“Bila ya samahani Jojo, tunaweza kukusaidia nini?”

“Munatoa huduma ya ndege?”

“Tunatoa huduma ya usafiri wa magari gadi Kia sasa kuanzia hapo unaweza kupata ndege ya kukupelekea kule utakapo”

“Okay usafiri wenu unagarimu kiasi gani?”

“Laki moja na nusu, na tukikuwekea booking ya ndege ya kukodi itakuwa ni laki mbili na nusu”

Nikatoa dola mia mbili na kuwapatia.

“Ninakwenda kuchukua mizigo yangu hivyo basi hakikisheni kwamba muniandalia kila kitu sasa hivi mumenielewa”

“Sawa”

Nikaanza kueleka katika chumba ambacho tulikodisha. Nikachukua pesa zote zilizomo ndani ya begi la ka Musa kisha nikaziweka kwenye begi langu, nikaondoka na kila kitu kilicho changu na kurudi mapokezi.

“Samahni tunaweza kupiga picha hata moja”

Kija mmoja alizungumza huku akiwa amejiandaa vizuri na simu yangu. Akasimama pembeni yangu na akapiga picha kadhaa.

“Mumesha andaa?”

“Ndio kila kitu kipo tayari na dereva yupo tayari na tumepata ndege moja. Katika shirika la ST Air ukifika hapo utawapa maelekezo”

“Sawa”

Kijana niliye piga naye picha akanisindikiza hadi kwenye gari la kuampuni yao. Nikapanda gari na taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hilo.

“Unaweza kwenda haraka kidogo, kwa maana nina haraka?”

“Sawa madam”

Mzee huyu anaye endesha hili gari alinijibu kwa ustarabu huku akianza kuongeza mwendo kasi wa gari. Nikampigia Judy simu, simu yake ikaanza kuita na baada ya muda ikapokelewa.

“Judy”

“Ndio”

“Nisikilize, elekea Kigamboni, nenda kahakikihe kwamba Eddy unamuondoka katika eneo hilo”

“Jojo, unataka nikamuondoe Eddy, si unaifahamu hali yake?”

“Ndio naifahamu ila hakikisha kwamba unakwenda kumtoa eneo hilo tafadhali fanya hivyo”

“Ila Jojo huo unao nitapatia wewe ni mtihani dada yangu”

“Nisaidie tafadhali”

“Kwani kuna nini kinacho endelea?”

“Ka Musa ameamua kuondoka na msichana mbaye tumemfwata huku na msichana huyo amepanga kumchukua Eddy wangu na kuondoka naye”

“Ohooo”

“Yaaa fanya hivyo mdogo wangu naomba unisaidie tafadhali”

“Sawa, ngoja nimuachie wifi mtoto”

“Hajasumbua?”

“Hapana yupo poa hajasumbua”

“Sawa, ukifika nakuomba uweze kunijulisha juu ya hilo”

“Poa poa”

Nikakata simu na kukaa kimya kwa muda huku nikimtazama mzee huyu jinsi anavyo jitahidi kadri ya uwezo wake kuendesha gari hili.

“Shikamoo”

“Marahaba binti”

Mzee huyu aliitikia huku akitabasamu.

“Ni nani amekupa mawazo kiasi hicho binti yangu?”

“Kuna mambo yangu binafsi tu yananichanganya”

“Pole sana binti yangu”

Mzee huyu alizungumza huku akizidi kuonyesha amejawa na furaha kubwa sana.

“Unaitwa nani binti”

“Jojo”

“Jojo nani?”

“Mzee mbona unamswali mengi sana, kichwa changu kwa sasa hikipo vizuri bwana”

“Samahani binti kama nitakuwa nimekukwaza kwa maswali yangu ya kipumbavu”

Mzee huyu alizungumza kwa upole sana huku machozi yakimlenga lenga. Nikamtazama kwa muda kisha nikageuzia uso wangu na kutazama nje,

“Mama yako anaendeleaje?”

Swali la mzee huyu likanistua sana na kujikuta nikimkazia macho.

“Yaa mama yako anaendeleaje?”

“Umemjuaje mama yangu?”

“Au basi”

“Basi nini, umemjuaje mama yangu na inakuwaje umemuulizia mama yangu ikiwa hunijui na wewe sikujui?”

“Mimi ninakufahamu”

“Kivipi?”

Nilizidi kuzungumza kwa hasira huku nikimkatazama mzee huyu. Mzee huyu akapunguza mwendo wa gari huku akitoa wallet yake kwenye mfuko wa suruali ya nyuma. Mzee huyu akaifunga wallet yake hiyo huku akiendesha gari hili kwa mkono mmoja. Akatoa picha moja ndogo yazamani kidogo. Akanikabidhi picha hiyo ambayo inamuonyesha yeye na mama yangu wakiwa wamesimama, huku mzee huyu akiwa amemshika mama yangu kiuno. Nikajikuta nikimeza fumba kubwa la mate huku nikimtazama mzee huyu kwa umakini sana kuanzia usoni mwake.

“Naamini hivi sasa utakuwa umefahamu ni kwa nini nimemuulizia mama yako”

Nikazidi kukaa kimya huku nikiwa nimechanganyikiwa kwamaana ninamuona huyu mzee ananichanganyia mada ambazo sijazitarajia kwa muda huu.

“Mama yako anaendeleaje?”

“Mama yangu amefariki dunia?”

Taratibu huyu mzee akaanza kupunguza mwendo kasi wa hili gari na mwishowe akalisimamisha kabisa.

“Mzee nina haraka bwana kwa nini umesimamisha gari?”

Mzee huyu hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kushuka ndani ya gari hili huku machozi yakimwagika usoni mwake. Akasimama mbele ya hili gari huku akiwa amenipa mgongo. Nikatazama mskani wa hili gari kwa muda kidogo, nikamfikiria mume wangua mbaye anakwenda kuchukuliwa.

“Asinicheleweshe bwana”

Nilizungumza huku nikiufungua mkanda wa siti yangu niliyo kalia. Nikahamia kwenye siti ambayo alikuwa amekaa mzee huyu. Nikawasha gari na kulirudisha nyuma kidogo, nikamkwepa mzee huyu na kwa mwendo wa kasi nikaanza kuondoka katika eneo hili kwa kasi. Nikatazama kioo cha pembeni ila sikumuona mzee huyu kutingisha wala kuhamasika katika kunifwatilia. Nikafunga breki za gafla, huku nikitafakari ni kitu gani ambacho kimfanya huyu mzee kumwagikwa na machozi. Nikaanza kulirudisha nyuma gari hili hadi sehemu nilipo simama, nikafungua kioo na kumtazama.

“Mzee unanipeleka au hunipeleki?”

Mzee huyu taratibu akanigeuka na kunitazama huku uso wake ukiwa umejawa na huzuni kubwa sana.

“Nakuuliza unanipeleka au hunipeleki?”

“Jojo”

“Nini”

“Mimi…..mimi ni baba yako”

Nikastuka kidogo kisha nikajikuta nikitabasamu kwa maana mama yangu alisha niambia kwamba baba yetu mimi na Judy amesha fariki kipindi kirefu, sasa baba kama huyu ametoka wapi.

‘Au kwa sasabu amejua mimi ni super star na nina hela?’

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama mzee huyu usoni mwake.

‘Wazee wengine sijui wametokea wapi jamani’

“Mzee sipendi kuigiziwa, mimi mwenyewe pia ni msanii sawa. Ingia ndani ya gari ufanye kazi yako kwa maana huko Kia kwenyewe sipafahamu sawa mzee?”

“Jojo hili jambo ninalo lizungumza hapa ni muhimu sana binti yangu naomba unielewe?”

“Mzee wangu, najionea mapicha picha, unahisi nitakukubali kirahisi kwambwa wewe ni baba yangu eheee?”

“Najua ni ngumu kunielewa ila tambua kwamba wewe ni mwanangu uliye toka kwenye kiuno changu”

“Mzee usinichanganyia habari aisee, ingia kwenye gari ufanye kazi yako uliyo ajiriwa. Ninaharaka Nanina muwahi mume wangu. Sasa ukinichelewesha sinto kuelewa”

Mzee huyu akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akafungua mlango, nikahamia kwenye siti yangu niliyo kuwa nimekaa. Taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hil huku mzee akijipangusa machozi yake usoni mwake.

“Mzee kuwa makini barabarani, maswala yakujitia mawazo yasiyo na kichwa wala miguu nakuomba usahau. Umenielewa kama ni pesa sema nitakupatia ila si kwa kuigiziwa”

“Jojo?”

“Sina baba mimi”

“Mama yako si anaitwa Mariana”

“Ndio anaitwa hilo jina si nimekuona naye kwenye picha hapa, sasa unahisi kwamba utakuwa hufahamu jina lake au kunitajia jina lake unahisi kwamba mimi ndio nitakuubalia. Mimi na mdogo wangu hatuna baba”

“Una mdogo wako?”

“Ona sasa unashangaa nini sasa. Umekurupuka mzee, nimesha kuambia kwamba sina baba mimi na tafadhali hizo mada zako za kipuuzi kausha basai”

Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama mzee huyu. Tukazidi kusonga mbele huku ndani ya gari tukiwa tumetawaliwa na ukimya mkali sana. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitazamana kumkuta ni Judy ndio anaye nipigia.

“Niambie”

“Dada nimefika huko kigamboni, sijamkuta mtu yoyote kwenye hii nyumba”

“Ngoja kwanza, umekwenda kwneye nyumba iliyo sahihi au umeingia kwa jirani?”

“Jamani Jojo, mimi hapa napafahamu vizuri, sijakuta walinzi, sijakuta madaktari wala sijamkuta Eddy mwenyewe”

“Ohoo Mungu wangu, sasa umeulizia ulizia huko”

“Hapana sijaulizia kwa majirani na eneo lenyewe lilivyo tulia hivi kuna jirani gani ambaye anaweza kuona kama kunakuwa na tatizo ambalo limetokea?”

“Okay naomba ufanye hivyo ulizia kwa majirani”

“Sawa”

Nikakata simu na kuana kuitafuta namba ya mama mkwe.

“Kuna kitu gani kinaendelea mwanagu”

“Mzee KOMAAAAAA MIMI SIO MWANAOOOOO”

Nilizungumza kwa ukali na sauti ya juu hadi mzee huyu akaanza kutetemeka mwili wake. Nikaipata namba ya mama mkwe na kumpigia.

“Mama”

“Niambie uliwasiliana na mkuu wa mkoa?”

“Hapana mama kuna tatizo limejitokea”

“Nini tena?”

“Nimemuagiza Judy kwenda kumtazama Eddy kule kwenye ile nyumba Kigamboni na anadai kwamba hakuna mtu ndani ya nyumba hiyo, si walinzi na wala si madaktari na hata Eddy mwenyewe hayupo”

“Unasemaje?”

“Ndio mama, Judy ndio amenieleza”

“Hembu kata simu nimpigie Judy”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi sana huku jasho likinimwagika usoni mwangu. Tukafika katika kiwanja kikubwa cha ndege Kia. Nikawa wa kwanza kushuka kwenye gari hili huk nikibeba kila kilicho changu, mzee huyu akashuka naye kwenye gari na kuanza kunikimbilia huku akiniita jina langu. Nikasimama huku nikimtazama kwa macho makali na yaliyo jawa na hasira kali sana kwa maana naona na yeye ananichanganya.

“Kwa nini unanidanganya ikiwa nimekusikia unazungumza na mama yako, nampenda sana mama yako, namuhutaji sana mama yako. Yeye ndio mwanamke wa maisha yangu na wewe ni mwanangu kwa nini lakini Jojo unanitenga na upendo wa mama yako eheee?”

Mzee huyu alizngumza huku akipipigai magoti na kunishika mguu wa kushoto na machozi yakimwagika usoni mwake kiasi kwamba hata watu kadhaa walipo karibu yetu wakaanza kunishangaa na wengijne hawakuishia hapo wakatoa simu zao na kuanza kurekodi tukio hili linalo endela kati yangu mimi na huyu mzee.



Nikashusha pumzi nyingi huku nikijiuliza maswali mengi kichwani mwangu. Kusema kweli kila anacho kizungumza huyu mzee kwangu ninaona kama mapicha picha ambayo sijui yataisha saa ngapi.

“Mzee wangu”

“Ndio mwanangu”

“Nakuomba usimame si unaona jinsi watu wanavyo kusangaa baba yangu”

Nilizungumza kwa upole mkubwa saba huku nikimtazama mzee huyu usonimwake. Taratibu mzee huyu akasimama, nikamshika mkono na kuanza kutembea naye kuelekea kwenye moja ya ofisi.

“Samahani dada vyoo vipo wapi?”

“Aha…nyoosha hivi kuja kulia utaona kuna sehemu ina vyoo vya kiume na wanawake”

“Nashukuru”

Uzuri vyoo nilivyo onyeshwa vipo ndani ya hili hili jengo hapa. Nikaanza kutembea huku nikiwa ninaendelea kuishika mkono wa huyu mzee. Tulipo fika katika eneo ambalo hakuna watu na nikwenye kordo nyembaba kiasi. Nimapiga kisuku suku cha tumbo mzee huyu na kumfanya ajikunje na kugugumia kwa maumivu makali sana.

“Ukome kuparamia watu usio wafahamu. Sipendi kuigiziwa ujinga sawa wewe fala?”

Nilizungumza kwa ukali kisha nikaanza kurudi eneo la mapokezi nikimuacha huyu mzee akinitazama kwa macho ya kuto kuamini kama kweli mimi ndio nimeweza kumfanya hivyo. Nikaulizia juu ya ndege ambayo nimekodisha inirudishe jijini Dar es Salaam. Nikalipa kiasi ninacho takiwa kulipia kisha nikasindikizwa na muhudumu wa ndege hiyo hadi sehemu ilipo ndege hiyo.

“Kuna yule mzee niliye ingia naye kwenye lile eneo lenu pale. Samahani chukua hii pesa ukampatie, muambie aende hospitalini”

Nilizungumza huku nikimkabidhi muhudumu huyu dola mia tano.

“Sawa”

“Na wewe chukua hii kuwa muaminifu sawa”

“Nashukuru sana dada”

Muhudumu huyu wa kiume alishukuru sana mara baada ya kumpatia dola mia mbili. Nikaingia ndani ya hii ndege ndogo ambayo kwa udogo wake ina beba abiria kama watano hivi au sikta, ila kutokana nipo peke yangu, sijaona haja ya kupanda na watu wengine kwani nina haraka.

“Funga mkanda wako dada”

Rubani aliniambai, nikafunga mkada wa siti yangu huku akianza kuiwasha ndege hii. Taratibu tukaanza kuondoka na kadri jinsi kasi ilivyo zidi kuongezeka ndivyo jinsi inavyo zidi kupaa angani. Nikatoa simu yangu mfukoni na kuanza kumpigia mama mkwe. Simu yake baada ya muda ikapokelewa.

“Mama”

“Ndio mwanangu”

“Umeweza pata habari yoyote kutoka kwa Judy?”

“Ndio ameniambia kwamba kule alipo kuwa mume wako, amekwenda na kukuta hakuna mtu”

“Ndio mama, atakuwa amekwenda wapi jamani?”

“Usijali, niliwaambiwa wamuondoke katike eneo lile na kumpeleka eneo jengine”

“Eneo gani?”

“Sio vizuri nikazungumza kwenye simu kutokana mawasiliano yangu mimi na wewe kuna watu wanayasikia hivi sasa ukifika nyumbani basi tunaweza kuzungumza kwa kirefu, hii yote ni kwa ajili ya usalama”

“Sawa mama”

“Kitu kingine ukimaliza kuzungumza nami, toa betri na laini ya simu yako kabisa. Kwa maana watakutafuta kwa sattelaiti ili wakuchukue”

“Kina nani mama?”

“Fanya hivyo, kitu kikubwa ni uhakikishe kwamba unafika nyumbani salama sawa”

“Sawa mama ila nip……”

“Usiseme eneo ulipo Jojo, sawa mwanangu”

“Sawa mama”

“Kuna mzee umekutana naye?”

Nikastuka kidogo kwa maana ninajiuliza mama mkwe amejuaje kama nimeonana na mzee huyo.

“Ndio mama”

“Basi jikague mwilini mwako mwote, ukiona kitu chochote kidogo hivi hakikisha kwamba unakitoa. Pia kagua kwenye mabegi yako”

“A…ameniwekea nini mama?”

“GPRS, popote utakapo kwenda wanakuona”

“Heee?”

“Ndio fanya hivyo sasa hivi”

Sikujali kama kuna huyu rubabi ni mwanaume nikaanza kuvua sweta nililo vaa, nikalichukuguza na sikuona kitu chochote, nikavua tisheti niliyo ivaa, nayo nikaikagua na sikuona kitu cha ina yoyote”

“Kipo wapi?”

Nilijiuliza huku nikijipapasa mifuko ya suruali yagu niliyo vaa. Katika mfuko wa nyuma ya suruali yangu nikakuta kifaa kidogo sana kinacho waka alama nyekundu, jambo lililo nifanya nijawe na woga mkubwa sana. Nikavaa tisheti yangu pamoja na sweta.

“Hei hivi vijidirisha vinafunguka”

Nilimuuliza rubani, akageuka na kunitazama huku akivua earphone kubwa alizo zivaa masikioni mwake.

“Unasema”

“Haya madirisha ninaweza kuyafungua?”

“Hapana, tupo hewani, kufanya hivyo unaweza kuangusha ndege kwa maana upepo utaingia mwingi sana”

“Ohoo Mungu wangu”

“Kwani kuna nini?”

“Hakuna tatizo”

Rubani akageukia mbele na kuvaa earphone zake na safari ikaendelea. Nikajifikiria kwa muda kisha nikampigia Cleopatra aliye nipigia kwa namba ambayo haipo kwenye simu yangu. Simu yake ikaanza kuita hadi ikakata, nikarudi tena kuipiga namba yake na ikaanza kuita tena hadi ikakata.

‘Malaya wewe pokea simu’

Nilizungmza kimoyo moyo huku nikiendelea kujitahidi kumpigia simu hii ila haikupokelewa. Nikakumbuka kumpigia Judy, simu ya Judy ikaita kwa sekunde kadha kisha ikapokelewa.

“Judy”

“Bee”

“Upo wapi?”

“Nimesha rudi nyumbani”

“Mtoto anaendeleaje?”

“Safi, ila nimemuambia mama kwamba Eddy kule hayupo na watu wote waliokuwa wanamlinda”

“Usijali, sasa nakuomba kitu”

“Kitu gani?”

Nikataka kumuambia kwamba anifwate uwanja wa ndege ila nikakumbuka kwama mama mkwe amenionya nisiweze kutaja eneo ambalo nipo.

“Au basi, tutazungumza baadae”

“Kuna tatizo?”

“Hapana tutazungumza baade”

“Sawa”

Nikakata simu, nikatoa berti pamoja na laini na kuviingiaza kila komoja kwenye mfuko wangu wa suruali, huku nikiendelea kuishika hii GPRS niliyo wekewa mfukoni na yule mzee.

‘Yule mzee ni mtu mbaya ila kwa nini ana picha ya mama yangu na wamepiga picha pamoja?’

Nilijiuliza swali hilo kimoyo moyo huku nikiendelea kujishauri kichwani mwangu. Hadi tunafika katka uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, sikuweza kupata jibu lolote juu ya mzee yule. Nikavaa kofia la sweta langu, kisha begi langu la nguo nikalivaa mgongoni, kabla sijashuka nikakumbuka kwamba nina miwani, nikaichukua miwani hiyo ndani ya begi langu na kuivaa. Nikaanza kutembea kwa kujiamini kuelekea nje, ya uwanja huu, nikapita eneo la ukaguzi na kuanza kutembea kwa hatua za umakini huku macho yangu yakiwa yanamtaama kila mtu aliyopo mbele yangu kwani GPRS bado nimeishika mkononi mwangu.

Nikawaona wanaume watatu walio valia suti nyeusi huku macho yao yote yakiwa kwangu. Kwa haraka sana nikatambua kwamba watu hawa wapo hapa uwanja wa ndege kwa ajili yangu. Sikaanza kutembea usawa mmoja na mzungu aliye valia begi kubwa mgongoni mwake. Nikaigandisha GPRS hiyo kwenye begi lake kisha nikaanza kutembea kwa hatua za haraka kueleka nje. Wanaume hao wakaendelea kunifwata.

“Taksi”

Nilimuita muendesha taksi mmoja, kwa haraka akanifwtaa na kusimama mbele yangu na kusimama mbele yangu.

“Tuondoke”

“Tunaelekea wapi dada?”

“Nimekuambia kwamba tuondoke”

Nilizungumza huku nikitazama nyuma nikawaona wanaume wale wakikimbilia eneo la maegesho.

“Unaweza kundesha gari kwa haraka”

“Dada yangu si unaona bado kuna foleni, inabidi tufwate utaratibu”

Nikageuka nyuma na kuona gari aina ya BWM ikitufwata kwa kasi.

“Vipi kuna watu wanao kukimbiza?”

“Ndio maana nikakuambia uendeshe gari kwa kasi, ila unataka kufwata utaratibu, sijui ni utaratibu gani unao utaka wewe”

Dereva taksi akatazama kwenye kioo chake cha pembeni na kuona jinsi gari hiyo inayo kuja kwa kasi.

“Una kiasi gani cha pesa ambacho ninaweza kuwatoka watu hawa”

“Ehee?”

“Pesa dada niweze kuwatoka watu hao wanao kufwatilia”

“Wewe endesha gari pesa ipo”

“Nahitaji kuiona kwanza”

Nikachomoa noti tano za dola mia kwenye begi langu na kumpatia. Akatabasamu huku akinitazama.

“Hamia siti ya mbele hapa”

Nikafwata maenekezo yake na kukaa siti ya mbele.

“Hujafunga mkanda”

Nikafanya kama anavyo hitaji, dereva taksi akaanza kuongeza mwendo kasi wa gari lake huku akianza kuzipita gari zilizipo mbele yetu. Kwa jinsi mwendo anao uendesha dereva huyu nikaanza kupata matumaini ya kuwaacha mbali watu wanao nifwatilia ambao hadi sasa hivi sifahamu wameagizwa na nani na ni kwa nini wananifwatilia.

“Unaelekea wapi?”

“Eheee?”

“Unaelekea wapi dada?”

“Tegeta”

“Okay”

Nikayaona macho ya dereva huyu akitazama mataa ambayo yamesimamisha magari ya eneo tunapo tokea, akaanza hesabu videole vyake, kitendo cha taa hizo kubadilika kutoka katika rangi nyekundu na kuwa rangi ya kijani, ikimaanisha kwamba wamaturuhusu akazipita gari mbili zilizopo mbele yetu na tukaanza kuondoka kwa mwnedo wa kasi sana katika eneo hili hadi nikahisi kuna watu watakuwa wanashangaa kwa kile anacho kifanya dereva huyu.

“Wajinga wale wageni na Dar”

Dereva huyu alizungumza huku akicheka cheka. Nikatazama nyuma na siwaoni watu wale walio kuwa wanatufukuzia.

“Huku unapita wapi?”

Nilimuuliza Dereva huyu mara ya kumuona akibadilisha njia tofauti na ile ambayo nimeizoea.

“Hatuwezi tukapita hii one way, kwa maani ni lazima watakuja kutukamata hapo mbele.

Dereva alizungumza huku akiendelea kukatiza katika mitaa ya jiji hili la Dar es Saalam.

“Jojo hivi ile ishu yako ya madawa imeishiaje?”

Swali la dereva huyu kidogo likanistua kiasi cha kujikuta nikipata kigugumizi katika kumjibu swali lake.

“Kwa nini umeniuliza hivyo?”

“Nimekuuliza tu, si unajua wewe ni mtu maarufu na kuna stori nyingi sana zinaendelea mtaani”

“Stori zipi?”

“Watu wanasema ni kweli kwamba unatumia dawa hizo, wengine wanasema kwamba unauza. Si unajua waswahili”

“Siuzi wala situmii”

“Yaa ni kweli kwa maana mtoto unaonyesha bado mbichi”

Sikutaka kuendelea kuzungumza chochote kwa huyu dereva zaidi ya kukaa kimya. Kwa njia anazo zipita huyu dereva tukatokea Mbezi kwa Msuguri, akanyoosha na barabara kuu ya kuelekea mikoani, akafika Mbezi mwisho na tukapita njia ya Mbezi luis na tukaanza kuitafuta Tegeta.

“Jojo”

“Bee”

“Mbona ile filamu yako haitoki imekuwaje?”

“Itatoka pale muda utakapo fika”

“Wengine tumeisubiria hadi tumechoka dada yangu”

“Usijalo itatoka”

“Ila kwa yale ma trela niliyo yaona youtube, nina uhakika kwamba filamu yako inakwenda kuvunja historia ya filamu Tanzania au hata Afrika mashariki kwa ujumla”

“Asante”

Nikamueleza dereva huyu hadi nyumbani kwangu ninapo ishi. Nikampa dola mia nyingine, akanishukuru sana na kuondoka zake. Nikaminya kitufe cha kengele, baada ya muda geti likafunguliwa na walinzi wanao linda hapa nyumbani kwangu. Nikaingia ndani na moja kwa moja nikaeleka ndani na kumkuta wifi sebleni.

“Shikamoo”

“Maraba vipi, umerudi na ka Musa?”

“Hapana”

“Kwa nini?”

“Mama hajakuambia kitu alicho taka kukifanya kwangu?”

“Hapana hajaniambia”

“Alitaka kunibaka kwenye hoteli tuliyo fikia”

Wifi macho yakamtoka, akaonekana kujawa na mshangao mkubwa sana kiasi kwamba furaha ikamuishia usoni mwake.

“Jamani kwa nini anajitafutia matatizo?”

“Ndio hivyo wifi”

“Kwa hiyo ulimuambia mama?”

“Ndio nilimuambia”

“Mmmmmm sijui itakuwaje”

“Judy yupo wapi?”

“Alitoka mida fulani hivi kama dakika ishirini zilizo pita”

“Amekwenda wapi?”

“Aliniambia kwamba kuna mtu amempigia anahitaji kuonana naye maeneo ya Posta”

“Nani huyo?”

“Hakuniambia”

“Una simu yako”

“Ndio”

“Naomba nimpigie”

Wifi akanipatia simu yake, nikaanza kumpigia Judy, simu yake. Ikaanza kuita na baada ya muda ikakata, nikarudi kupiga zaidi ya mara tano ila haikupokelewa jambo lililo anza kunipa wasiwasi mwingi kwani kama watu wanao nitafuta mimi wamenikosa basi mtu mwengine wanaye weza kumchukua kwa urahisi sana ni Judy mdogo wangu jamo ambalo ni tatizo jengine tena kwenye maisha yangu.



“Vipi?”

Wifi alizungumza huku akinitazama usoni mwangu?”

“Hapokei simu”

“Labda atakuwa ameiweka silent?”

“Hakuna wifi kitu kama hicho, kwa maana nilipo kuwa ninatoka uwanja wa ndege kuna watu walikuwa walinifwatilia kwa nyuma na gari lao”

“Watu gani?”

“Hata mimi sielewi wifi ni kina nani?”

“Mmmmm jamani mbona matatizo hatajishi kwenye familia hii”

Wifi alilalama akionyesha dhairi kwamba amechoshwa na matatizo ya kifamilia yanayo endelea.

“Mtoto yupo wapi?”

“Gorofani”

Nikamkabidhi wifi simu yake na nikaanza kupandisha gorofani. Nikaingia chumbani kwangu na kuwakuta watoto wawili, mmoja akiwa wa wifi yangu na mwengine akiwa wangu. Nikawatazama kwa muda kidogo na kujikuta nikitabasamu kwa maana hawa ndio faraja iliyo salia kwenye familia yetu. Kutokana wote wawili wamelala, sikuona haja ya kuwasumbua, nikaingia bafuni, nikavua nguo zangu zote na nikaitoa simu yangu niliyo toa betri, lain na kuiweka pembeni kwenye sinki la kunawia mikono. Nikatamani kuoga ila kutokana na mawazo ambayo yananikabili kichwani mwangu, nikajikuta nikikaa kwenye choo hichi cha kukaa.

‘Huyu naye atakuwa amekwenda wapi jamani?’

Nilijiuliza swali hili kichwani mwangu na kukosa jibu la maana. Mlango wa bafuni humu ukagongwa.

“Wifi”

“Beee”

Nikashusha pumzi kidogo kwa maana nilimuita kwa mshtoko kidogo.

“Vipi?”

“Judy anapiga simu, sijapokea lakini”

Nikanyanyuka kwa haraka, nikafungua mlango kidogo nikatoa mkono nje na wifi akanikabidhi simu yake, kwa haraka nikaipokea simu ya Judy.

“Wewe upo wapi mbona nakupigia simu muda wote hupokei?”

Swali langu halikuweza kujibiwa jambo lililo nifanya nitege masikio kwa umakini sana ili niweze kusikia nikitu gani kinacho endelea upande wa pili. Nikaanza kusikia kama mikurupushano ya watu wanao pigana huku baadhi ya vitu vyenye milio kama sahani za dongo vikianguka chini.

“Haloooo, haloooo”

Niliita huku nikiendelea kusikilizia vurumai hilo. Nikaisikia sauti ya Judy akiugulia kwa maumivu huku akionekana kama kuminywa hivi. Kwa haraka nikatoka bafuni humu huku jasho na wasiwasi vikiwa vimenikamata kisawa sawa.

“Vipi mbona umetoka uchi?”

Wifi aliniuliza huku akiwa amekaa kitandani akiwawaweka sawa watoto.

“Wifi sikiliza?”

Nilizungumza huku nikimkabidhi simu yake, akaiweka sikioni na kusikiliza kinacho endelea, kwa haraka akaanza kurekodi sauti hizo huku simu akiwa ameiweka loud speaker.

“Pumbavu simu kumbe simu uliiweka hewa……..”

Sauti hiyo ya mwanaume iliishia hapo na simu ikakata. Wifi akajaribu kupiga simu, ila kwa bahati mbaya simu haipatikani hewani.

“Ohoo Mungu wangu mdogo wangu anafanywa nini jamani?”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenga usoni mwangu. Wifi hakunijibu kitu chochote zaidi ya kuiweka simu yake sikioni mwake.

“Mama”

“Kuna sauti hapa nataka kukutumia naomba uagize watu wako wamtafute Judy kwa maana ametoka nyumbani na tunahisi kama kuna tatizo limemkuta”

“Aliniaga tu mama sasa hivi ndio tulikuwa tunampigia simu akawa hapokei”

“Sawa nakutumi”

Wifi akamtumia mama mkwe sauti ya mwanaume huyo ambaye tulimsikia. Amani moyoni mwangu ikazidi kupotea na kujikuta nikiwa mnyonge kwani sifahamu ni wapi ninapo anzia kumsaidia mdogo wangu. Wifi akanyanyuka kitandani na kunikabidhi tenge, nikajifunga kwa manaa nipo uchi kama nilivyo zaliwa.

“Mama amesemaje?”

Nilimuuliza wifi kwa sauti iliyo jaa unyonge.

“Anasema analishuhulikia”

“Hembu mpigie tena?”

Wifi akajaribu kupiga, akatingisha kichwa akimaanisha kwamba hapatikani.

‘Hee Mungu ninakuomba uweze kumsaidia mdogo wangu’

Niliomba kimoyo moyo huku nikizunguka zunguka ndani ya chumba hicho. Wifi akatoka ndani ya chumba hichi na kuniacha peke yangu. Majiria ya saa mbili hivi usiku nikasikia mngurumo wa gari, kwa haraka nikakimbilia dirishani na kufungua pazia. Nikamuona mama mkwe akishuka kwenye gari huku aiwa ameongozana na wanaume wawili ambao siwafahamu ni kina nani.

Nikajifinga vizuri tenge langu na kutoka chumbani humu na kuanza kuelekea sebleni. Kabla sijaanza kushuka ngazi nikakutana na mama mkwe akipandisha ngazi hizo.

“Shikamoo mama”

“Marahaba, twende juu”

Mama mkwe alizungumza huku usoni mwake akioneakana kuto kujawa na furaha ya aina yoyote. Tukaingia chumbani kwangu, akawatazama wajukuu wake walio lala.

“Mama vipi umeweza kumpata Judy?”

“Hapana bado polisi wanaendelea kumtafuta, ila tumeweza kufahamu picha ya mwanaume ambaye alikuwa akizungumza”

“Ni nani?”

Niliuliza kwa shahuku kubwa huku nikimtazama mama mkwe usoni mwake. Mama mkwe akatoa simu yake na kunionyesha picha ya mwanaume huyo. Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi, kwani mwanaume huyu ninamfahamu vizuri, ni Juma, mdogo wake Kibopa, bosi ambaye nilikuwa nikifanya kazi kwake na yeye ndio alinipatia mzigo wa madawa ya kulevya na kuyapeleka nchini China jambo ambalo lilisababisha kukamatwa na kuingia kwenye matizo ambayo hapo awali sikuyakusudia kuweza kuingia kabisa kwenye maisha yangu.

“Unamfahamu huyo mwanaume?”

“Ndio mama, ninamfahamu”

“Ni nani?”

“Anaitwa Juma kwa jina lake maarufu alikuwa anaitwa Njiga”

“Unamfahamu fahamu vipi?”

“Ni mdogo wake Kibopa yule mzee ambaye nilikuwa ninafanya kazi kwake na aliniagiza kwenda nchini China”

“Okay, unafahamu ni wapi anapo ishi?”

“Kwa kaka yake kule ndipo alikuwa akiishi?”

“Wapi?”

“Masaki”

“Vaa twende sasa hivi”

“Sawa mama”

Mama mkwe akanyanyuka na kutoka chumbani humu, nikavua tenge pamoja na tisheti hii kisha nikachukua suruali yangu moja ya jinzi na kuivaa pasipo kuva hata chupi ndani. Nikachukua tisheti yangu nyingine na kuvaa. Nikavaa raba zangu nyepesi, nikasimama kwenye kioo na kuzibana nywele zangu ndefu vizuri. Nikachukua kofia nyeusi na kuvaa. Nikapiga hatua hadi kitandani, nikambusu mwanangu mdomoni kisha nikambusu mtoto wa wifi shavuni mwake.

“Unaondoka?”

Niliisikia sauti ya wifi na kujikuta nikinyanyuka na kumtazama usoni mwake.

“Ndio kuna sehemu mama ameniambie twende kuna mtu ambaye tunatakiwa kumtafuta”

“Mtu gani?”

“Kuna jamaa mmoja anaitwa Juma, ni muuza madawa ya kulevya sasa ndio yupo na Judy”

“Ahaa sasa beba simu yako kwa maana ninahitaji muweze kunijulisha kila kinacho endelea.”

“Sawa”

Nikaingia bafuni na kuichukua simu yangu. Nikatoka chumbani humu na kumkuta mama mkwe akinisubiria nje kabisa. Tukaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hili. Ukimya ukatawala ndani ya hili gari na mama mkwe anaonekana kuchoka sana kwa kazi nyingi hadi nikajikuta nikimuonea huruma mama wa watu, kwani kwa umri wake sasa hivi alipaswa kukaa nyumbani na kutulia na kufurahia na wajukuu wake alio barikiwa kupewa na mwenyezi Mungu.

“Mama”

“Mmmmm”

“Samahani”

“Kwa……”

“Tunakubebesha matatizo ambayo hustahili kuyabeba kwa muda huu”

“Usijali, ikiwa baba yenu hayupo, mimi ndio baba na mama, nilazima niiangalie famillia yangu kwa kipindi chote cha uhai wangu”

“Ni kweli mama ila nakuomba haya yakiisha mama yangu uweze kupumzika na kuachana na hizi kazi mama yangu”

“Hahaaa Jojo hizi kazi haziachwi”

“Ila nakuomba wewe mama uweze kuacha. Tunatakiwa sisi hapa tukuangalie na kukutunza ila sasa hivi wewe ndio unahangaika mama yangu”

“Usijali, muda ukifika basi kila jambo litakuwa sawa mwanagu, sawa”

“Sawa mama”

Nilizungumza kinyonge huku nikimtazama mama mkwe usoni mwake. Vijana hawa walio kaa siti ya mbele huku mmoja akiwa ni dereva, hakuna hata mmoja ambaye anazungumza jambo lolote.

“Vipi kuhusiana na Eddy?”

“Eddy yupo kwa kiongozi wangu mmoja hivi, nimemuweka huko hadi hali ya hewa itakapo tulia kwa maana sasa hivi hali ya hewa haieleweki kwa kweli?”

“Ka Musa je?”

“Hajarudi na wala sijapata mawasiliano naye hadi sasa hivi na sijui anajipangaje, kwa maana ananiumiza kichwa na yeye”

“Ila kwa nini ka Musa amebadilika kiasi hichi?”

“Hili ni swali gumu ambalo mimi nikijiuliza ninachanganyikiwa kabisa, kwa maana Musa ni kijana niliye mlea toka akiwa mdogo sana. Mama yake alikuwa ni rafiki yangu sana, kwa ule urafiki tukawa kama ndugu. Sasa kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali, kutokana Musa alikuwa peke yake tu, ikanibidi nimchukue na kumlea kama mwanangu.”

“Kipindi cha huko nyuma alisha wahi kukufanyia jambo lolote baya ikiwemo kukusaliti?”

“Hapana ila udhaifu wake ni wanawake, kuna kipindi alikuwa anamtaka wifi yako. Ila nilimkanya vikali sana asifanye jambo hilo kwa binti yangu kwa maana sikuhitaji aniharibie maisha ya msichana wangu”

“Ahaa….kumbe ndivyo alivyo?”

“Yaa hata mulipo kuwa munakwenda hivi, nikasema ngoja niangalie labda atakuwa amebadilika. Kumbe bado akili yake ipo vile vile”

Simu ya mama yake ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaipokea na kuweka sikioni mwake.

“Ndio”

“Mimi nipo njiani tunaelekea katika eneo la tukio”

“Hakikisha kwamba vikosi vyako unaviweka sawa, sinto hitaji uzembe kujitokea tena”

Mama mkwe akakata simu na kunitazama.

“Niliwataarifu askari waweze kutusaidia kwenye hili jambo kwa maana lipo nje kwa kazi ya ofisi yangu”

“Ahaa….sawa sawa”

“Ila Judy naye asubuhi nilimuambia kwamba acha kuhangaika hangaika ila amekuwa mzembe na yamemkuta”

“Ila wifi anasema kwamba huyo mtu hafahamiani naye?”

“Afahamiani naye kivipi?”

“Anadai kwamba alipigiwa tu simu na akaamua kwenda huko”

Nikawalekeza askari hadi kwenye jumba moja la kifahari. Tukasimamisha gari umbali kidogo kutoka katika jumba hili lililo tulia sana.

“Una uhakika kwamba hapo ndipo anapo kaa huyo Kibopa”

“Ndio”

“Twende”

“Ndani….!!?”

Niliuliza huku nikiwa nimejawa na mshangao mkubwa sana.

“Ndio ndani”

Nikashusha pumzi nyingi sana huku nikiwa nimejawa na mashaka kwani nina amani kitendo cha Kibopa kuniona mimi, tena nikiwa nimeongozana na mama mkwe ambaye kwa sasa ni mkuu wa kitengo cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya. Ataamini kwamba nimemlengesha makusudi ili aweze kukamatwa kitu kinacho weza kuyagarimu hata maisha yetu kwani nina muelewa ni mtu mwenye roho mbaya na asiye penda mchezo mchezo na biashara zake na isitoshe ndani ya hili jumba lake kuna ulinzi mkali sana ambao si rahisi kuingia ndani kama jinsi mama mkwe anavyo dhania



“Mama kwenye hilo jumba kuna ulinzi mkali sana na nihatari kwa sisi kuingia ndani humo kwa maana huyo mtu ananifahamu mimi vizuri sana”

Nilizungumza huku nikimtazama mama mkwe usoni mwake.

“Wewe twende ndani”

Nikashusha pumzi, taratibu mama mkwe akafungua mlango wa upande wake.

“Tusubirini”

“Sawa mkuu”

Nikafungu mlango wa upande wangu kisha nami nikashuka. Tukaanza kutembea kueleka kwenye jumba hilo na kadri jinsi ninavyo zidi kupiga hatua mbele ndivyo jinsi mapigo ya moyo yanavyo zidi kunienda mbio huku nguvu za miguu zikiniishia. Tukafika getini na mama mkwe akatazama eneo la kamera ilipo, taratibu geti hilo likafunguka, jambo lililo nishangaza kidogo kwa maana watu tumezoa kuminya kitufe cha kengele kisha ndio tufunguliwe tena kwa kuhojiwa maswali. Ila kutoka nina miaka kadhaa sijakanyaga kwenye hii nyumba basi nahisi kwamba utaratibu utakuwa umebadilika.

Tukakutana na wanaume wawili wakiwa wameshika mitutu ya bunduki huku kila sura zao zikionyesha kuto kuwa na masira hata kidogo. Mmoja wao akaanza kutupitishia kifaa malumu ambacho tuhumika katika kuwakagua watu wanao ingia ndani ya jumba hili na endapo kama utakuwa na silaha au kitu chochote cha chuma basi kinaanza kupiga kelele ambayo inaweza kuwaashiria wakaguzi kwamba una silaha umeificha.

Mama mkwe kwa upande wake hakuwa na kitu chochote jambo lililo nifanya nizidi kuingiwa na woga, kwani inakuwaje mama mkwe anaingia eneo hili pasipo kuwa na silaha ya aina yoyote. Nikakaguliwa na mimi, kutoka sina kutu chochote, nikaruhusiwa kuingia ndani. Tukakutana na mlinzi mwengine mwenye silaha. Akatangulia mbele huku kwa ishara akituashiria kwamba tumfwate kule anapo elekea.

“Mama”

Niliita kwa sauti ya chini sana huku nikimongeza hatua mbili na kumfikia mama mkwe.

“Mmmmm”

“Mbona huna silaha tutatoka kweli?”

“Ndio”

Ikabidi nijipe matumaini ambayo hayana uhakika wowote kwenye maisha yangu. Kwani sidhani kama Kibopa atahitaji kuniacha mimi hai, ikiwa kwa kipindi chote tangu niupoteze mzigo wake wa madawa ya kulevya nimekuwa ni mtu wa kuishi kwa tahadhari kubwa sana. Tukaingia kwenye seble kubwa sana ambayo kwa miaka ya nyuma mimi ndio nilikuwa nikifanya usafi wa kufagia fagia na kupanga vitambaa vizuri. Seble hii kwa sasa imebadilika kwa silimia nyingi sana kwani vitu vya thamani vimeongezwa ndani ya hii seble. Tukatembea hadi kwenye sofa zilizopo hapa sebleni, mlinzi huyu kwa ishara akatuomba tusimama hadi pale bosi wake atakapo kuja. Mlinzi akasogea hatua chache na kutulinda huku mtutu wake wa bunduki yake aina ya SMG akiwa ametuangalizia sisi.

“Mama ninaogopa?”

“Kwa nini?”

“Basi tu, huyu baba sio mtu mzuri kabisa”

“Usijali hakuna kibaya kiyakacho tokea”

“JOJOOOOOOOO…..”

Niliisikia sauti nzito ya kiume iliyo nistua sana. Nikaanza kumuona Kibopa akishuka kwenye ngazi za jumba lake zinazo tokea gorofani, huku pembeni yake akiwa na wasichana wawili walio valia chupi aina ya bikini huku vifuani mwao wakiwa hawana chochote.

“Ni muda mwingu hatujaonana eheee?”

Kibopa alizungumza huku akiwa amejwa na tabasamu pana usoni mwake. Taratibu akaka kwenye sofa lake analo lipenda sana na wasichana hawa wakaka pembeni yake huku wakiwa wanatabasamu na ninatambua kabisa wanatabasamu kinafki na kinacho waweka hapa ni shida ya maisha na kama wangekuwa napesa wala wasinge jidhalilisha namna hiyo.

“Kaeni”

Taratibu tukaka kwenye sofa lililopo nyuma yetu.

“Aha….nakuona mama umekuja kunikamata au kunihoji?”

“Leo sijakuja na swala hilo, laiti kama ningekuja kwa swala hilo wala nisinge kuwa na sura kama hii”

“Hahaaaaaa…….acha kunichekesha unataka kuniambia kwamba ugekuwa na sura kama samba au chuiiii”

Kibopa alizungumza kwa dharau sana huku akicheke kicheko kinacho onyesha dhairi ni kwamba anaudharua uwepo wetu hapa.

“Nimekuja kwa ajili ya Juma ama jinga jengi…..”

“Chiga”

Kibopa alimalizia sentensi ya mama mkwe.

“Namuhitaji huyo kijana kwa maana ana mwanangu”

“Hahaa unahisi ni rahisi kiasi hicho?”

“Itakuwa ni rahisi endapo utapenda iwe rahisi na inaweza kuwa ngumu kama utapenda iwe ngumu, sasa jawabu unalo wewe mwenyewe”

Mama mkwe alizungumza kwa kujiamini sana na kunifanya nizidi kujawa na uwoga mwingi kwa maana nimesha wahi kuona matukio kadhaa ya ukatili ambayo alikuwa akiyafanya bwana Kibopa. Kipoba akatabasamu kidogo kisha akaanza kushika shika ziwa la msichana aliye kaa kushoto kwake, kisha tartibu akaanza kulinyonya na kumfanya mama mkwe kufumba macho huku nikishuhudia mkono wake wa kulia akikunja ngumi kwa hasira.

“Ahaa……maziwa ya hawa watoto ni matamu sana, tena sana na ni malaini kwa namna moja ama nyingine.”

Kibopa alizungumza huku akiyafumbua macho yake.

“Una watu wangu wawili muhimu umewakamata, sasa nahitaji kufanya makubaliano mimi na wewe. Nikupe huyo unaye muita mwanao, kisha nami unipatie watu wangu”

“Hahahaaa…..hahaaaaa…..”

Mama mkwe alicheka hadi machozi yakaanza kumwagika, kitu kilicho tusababisha watu wote kubaki njia panda hususani mimi.

“Unahisi mimi ni kama wale wajinga wengine walio pita kwenye hii nafasi”

“Hahahaaaaa….nafasi. Nisikilize wewe mwanamke, ninauwezo wa kukutoa kwenye hiyo nafasi kwa pesa yangu niliyo nayo na huyo raisi wako asifanye jambo la ina yoyote kama unakataa sema nifanye hivyo”

“Fanya”

Mama mkwe alizungumza kwa kujiamini na kuisababisha haja yangu ndogo kuanza kunibana huku nikisikia tumbo likinikata kata kama vile ninaihisi haja kubwa ikinijia kwa mbali. Kibopa akatoa simu yake na kuanza kuminya minya namba anazo ziona yeye mwenyewe kisha baadaya muda akaiweka sikioni mwake.

“Habari yako kiongozi”

Bwana Kipoba baada ya kuzungumza maneno hayo akaweka loud speaker.

“……lama ndugu yangu”

Tuliisikia sauti ya raisi akizungumza.

“Sasa kiongozi kuna teuzi kwenye serikali yako sisi kama sisi hatujazipenda kwa kweli”

“Kama ipi?”

“Kuna huyu mama ulimchagua kama msimamizi wa kitengo hichi cha madawa ya kulevya naona hafanyi kazi yake vizuri na mimi kama mimi simtaki bwana”

Raisi akaka kimya pasipo kujibu chochote, tukasikia akishusha mihemo ya kuonyesha kwamba hili swala sasa linaanza kumshinda.

“Mtoe haraka iwezekanavyo”

“Lakini ni juzi tu nimemteua?”

“Ni wewe ndio umemtea ila sisi hukutushirikisha”

“Niliamua kumuweka mwanamke ili muweze kuona mambo maraisi kidogo kwa upande wenu”

“Aisee kaka unajua mimi na wewe hatupendagi kubishana si ndio”

“Ndio ndugu”

“Na unajua ninakujua wewe A hadi Z si ndio”

Kibopa alizungumza kwa ukali.

“Ndio”

“Sasa fanya ninacho kueleza la sivyo nitakung’oa hapo madarakani na siri zote nitaziachia”

“Sawa ndugu”

“Unalifanya lini?”

“Nitampigia simu kesho aje ofisi kwangu nimpe onyo asiwaguse watu kama nyinyi”

“Nimsema umtoe au umpe onyo mbona unataka kutibua mavuz*** yangu muda huu ikiwa sitaki kupigizana kelele na wewe bwana?”

“Sawa, sawa ninamtoa”

“Sasa hivi mtoea”

Kibopa akakata simu na kuanza kucheka na wasichana wake hawa wawili wakaungana naye kucheka kicheko cha dharau sana. Nikamtazama mama mkwe usoni mwake na kumuona jinsi machozi yanavyo endelea kumwagika. Hazikuisha hata dakika mbili, simu ya mama mkwe ikaanza kuita jambo lililo nifanya nizidi kupatawa na wasiwasi. Mama mkwe akaitazama simu yake kwa muda na nikachungulia ili kuona ni nani anaye piga na lile ninalo lifikiria ndilo ninalo liona kwani ni raisi. Taratibu mama mkwe akaipokea simu yake na kuiweka sikioni.

“Ndio muheshimiwa”

“Nimekuelwa muheshimiwa”

“Nashukuru muheshimiwa kwa maamuzi yako. Ila ninajambo moja ninalo hitaji kukuambia, una wiki moja tu la sivyo kila kitu ninacho kijua kuhusiana na wewe nitakipeleke ICC sawa”

Mama mkwe alizungumza kwa hasira kiasi kwamba hadi machozi yakazidi kumwagika.

“Sina cha kujadili na wewe. Safari hii wewe na huyu nguruwe wako wote mutakwenda jela”

Mama mkwe akakata simu na kusimama. Kibopa macho yakamtoka sana dhairi naye naona amepata woga kiasi katika maneno ya mama mkwe.

“Twende”

Mama mkwe alizungumza taratibu nikanyanyuka huki nikijikataza kutembea kwani miguu yangu inagongana gongana kwa wasiwasi.

“Unahisi utaweza kufanya hicho unacho taka kukifanya?”

Maneno hayo ya Kibopa yakamfanya mama mkwe kusimama, kisha taratibu akageuka na kumtazama.

“Unahisi ninashindwa kukuua humu ndani kwako?”

“Heee”

Nilijikuta nikiropoka tu, kwani kauli hiyo ya mama mkwe itatufanya tusitokea humu ndani salama.

“Umeona wapi mtu akapigwa na kwake?”

“Etiee eheee?”

“Jojo muambie huyo sijui mama yako, sijui msagaji mwenzio asikurupuke. Unanifahamu vizuri?”

Maneno ya Kibopa kwa namna moja ama nyingine yakanikera sana, woga nilio nao sasa ukaanza kupunguzwa na hasira iliyo anza kunipanda taratibu. Mama kwe kwa haraka akafungua kibanio cha nywele zake. Akamrushia mlinzi aliye tuingiza humu ndani, nikastukia mlinzi akianguka chini mzima mzima huku akiwa ameshika koo lake na damu nyingi zinaruka. Tukiwa katika hali ya kushangaa, nikastukia kumuona mama mkwe aliwa ameishika bunduki ya mlinzi ambaye anahangaika katika kuyapapigania maisha yake ambayo muda wowote kuanzia hivi sasa yanakwenda kutoka endapo tu atakosa huduma ya kwanza.

“Jojo kafunge mlango”

Mama mkwe alizungumza huku akimfwata Kibopa alipo kaa. Mlio wa risasi nilio usikia ukanichanganya na kujikuta nikiwashangaa wasichana walio kaa pembeni ya Kibopa kila mmoja kuruka upande wake na kumuacha Kibopa mwenyewe kwenye sofa huku akipiga makelele huku mikono yake ikiwa imelishika paja la mguu wake wa kulia. Nikastukia nikipigwa kikumbo kizito na kuanguka chini mzima mzimwa, wakaingia walinzi kama sita wakiwa na bunduki zao na wote wamenyooshea mama mkwe bunduki zao huku mama mkwe akiwa amenyooshea Kibopa bunduki usawa wa kichwa chake.



Macho yakanizidi kunitoka kwani kila mtu yupo makini kwa kumtazama mama mkwe. Nikaanza kunyata hadi sehemu alipo lala mtu mlinzi huyu anaye endelea kumwagikwa na damu, hapa ndipo nikagundua kwamba kibanio hicho cha mama mkwe kina ncha kali na kina uwezo wa kumtoboa mtu sehemu yoyote katika mwili wake. Kwa haraka nikakichomao kwenye koo la mtu huyu. Kisha nikawatazama walinzi wa Kibopa jinsi wanavyo jishauri katika kufanya maamuzi ya kumshambulia mama mkwe kwani wakifanya kosa wao basi kinacho fwata ni kushuhudia ubongo wa bosi wao ukimwagika chini.

“Waambie watu wako waweke silaha zao chini, la sivyo tunakufa wote sasa chagua kati ya kuishi ama kufa?”

Swali la mama mkwe likanifanya nisite kidogo kufanya maamuzi ya kuwashambulia walinzi hawa wa Kibopa.

“Wekeni silaha zenu chini, munataka nife wajinga nyinyi?”

Kibopa alizungumza kwa kufoka sana na kwuafanya walinzi wake kuweka silaha zao chini.

“Jojo zikusanye hizo na hakikisha kwamba unamkagua kila mmoja sawa”

Mama mkwe alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo na kwa haraka nikaanza kukusanya silaha zote zilizop latika eneo hili.

“Zitupe nje”

“Sawa mama”

Nikazibabe, japo ni nzito sana hizi silaha ila nikajikaza hivyo hivyo hivyo. Nikatoka nje na kuona gari moja aina ya Mark X ikiwa iemsimamishwa karibu kabisa na eneo nilipo simama. Nikalichunguza vizuri na kugundua kwamba ndani ya gari hilo hakuna mtu yoyote. Nikalisogelea na kushika kitasa cha mlango wa upande wa dereva. Nikauvuta kwa bahati nzuri nikaukuta upo wazi, na pembeni kuna fungua yake, nikafungu buti ya nyuma katika gari hilo kisha silaha zote nikazingiza ndani ya buti na kulifungua. Nikakimbilia ndani na kukuta watu wamesimama vile vile, nikaanza kumpapasa mmoja baada ya mwengine. Nikawakuta wawili wakiwa na bastola ambazo zimejaa risasi za kutosha.

“Mama tayari”

“Mwanangu Judy yupo wapi?”

Mama alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka kwa hasira.

“Sifahamu”

Mama akaikoki bundiki vizuri na kumfanya Kibopa kuzidi kutetemeka, jeuri dharau zote alizo kuwa akituonyeshea zimeyayuka kama barafu juani. Kusema kweli nimeamini kifo ni kibaya na katika maisha yangu sikuwahi kushuhudia huyu mbaba akibabanishwa kama leo.

“Chu…ch…ukua namba yake hii hapa utajua ni wapi alipo”

Kipoba alizungmza huku akimkabidhi mama mkwe simu, kwa ishara mama mkwe akaniomba niichukue namba hiyo ya simu hiyo ya Kibopa, taratibu tukaanza kurudi nyuma huku mama mkwe akiwa amewaonyooshea bunduki watu hawa wa Kibopa. Nikawa wa kwanza kutoka humu ndani, walinzi wale tulio kuwa tumewakuta getini kipindi tunaingia humu ndani nao wapo ndani kwani nahisi ule mlio wa bunduki uliwastua sana.

“Mama kuna gari pale”

“Kafungue geti”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amesimama mlangoni huku akitazama ndani. Nikakimbilia hadi getini, nikalifungua kisha nikarudi katika gari. Mama mkwe akarudi kwa umakini hadi katika mlango wa mbele katika gari hili, akafungua na kuingia ndani. Nikawasha gari na kutoka katika uzio wa jumba hili.

“Simama kwenye gari letu pale”

Nikasimamisha gari pembeni ya gari walipo vijana wawili wa mama mkwe.

“Chukueni hii gari ndogo na muondoke nayo niachieni hilo gari kubwa”

“Sawa mkuu”

“Pia kuna silaha humu ndani. Kibopa na watu wake watawafukuzia naamini kwamba munajua ni nini cha kuwafanya”

“Sawa mkuu”

Tukabadilishana magari, walinzi hawa wakaanza kuondoka kwa mwendo wa kasi katika eneo hili.

“Mbona hatuondoki”

Nilimuuliza mama mkwe huku nikimtazama usoni mwake. Akanionyesha kwa kidole, nikaona gari mbili nyeusi zikitoka ndani ya uzio wa jumba la Kibopa. Gari hizo zikaanza kuifukuzia ile gari ndogo ambayo niliichukua ndani ya jumba hilo. Mama mkwe akachukua simu yake na kupiga namba kadhaa, kisha akaiweka sikioni mwake.

“Mumeuona huo mkia unao wafwata”

“Basi hakikisheni kwamba munaukata”

Mama mkwe akairudisha simu yake kwenye mfuko wa suruali, kisha akawasha gari na taratibu tukaondoka katika eneo hili kana kwamba sio sisi ambao tumefanya tukio ndani ya jumba la Kibopa. Tukapishana na gari la wagongwa, mama mkwe kidogo akapunguza mwendo huku akitazama gari hilo la wagonjwa ni wapi linapo elekea. Ikanilazimu na mimi kugeuka kabisa nyuma, nikaona gari hilo likiingia katika jumba la Kibopa. Tartaibu mama mkwe akasimamisha gari pembeni ya barabara.

“Tutanatakiwa kuhakikisha kufahamu ni hospitali gani anapelekwa”

“Mama huoni kama inaweza kuwa hatari”

“Hadi sasa hivi imesha kuwa hatari kwa upande wa familia yangu kwa ujumla. Nahitaji kukufundisha umafia ambao hukuwahi kufundishwa sehemu yoyote kwenye maisha yako”

Mama mkwe alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Kwa nini mama unahitaji kunifundisha?”

“Najua sasa hivi nimeingia kwenye vita na serikali. Siku yoyote ninaweza kuingia kwenye matatizo makubwa, je wewe, mwanao na mdogo wako mutaishi vipi? Je mutakuwa ni watu wa kuonewa na watu wengine na musipo angalia muna weza kufilisiwa pesa zote na mukafulia kabisa na kurudi sijui wapi kule uswahilini mulipo kuwa munaishi. Je unapenda kurudi kwenye maisha hayo?”

“Hapana mama”

“Basi fwata kile ninacho kuambia”

“Vipi kuhusiana na Eddy?”

“Eddy anajimudu, wifi yako anajimudu na shemeji yako anajimudu”

“Wifi anajimudu kivipi?”

“Ni undercover wa CAI, hapa Tanzania. Hakuna mtu nje ya familia yangu anayawe weza kufahamu hilo na wewe utakuwa ni mwengine ambaye unaweza kufahamu”

Nikajikuta nikishangaa sana kwa maana wifi yangu ukimtazama ni mpole na anaonyesha ni kama mzembe mzembe fulani asiye penda makuu na mtu yoyote.

“Mama kwa nini familia yako umeifanya wawe katika vitengo kama hivyo vya siri sana?”

“Wanangu uzuri wao kwamba mimi ndio role model wao. Hivyo kila mtu anapenda kupita katika nyanyo zangu nilizo wahi kupita katika usichana wangu, japo kila mmoja ameamua kufanya kile anacho kipende, ila upande wa pili ana kazi ya ziada ambayo yakitokea mambo kama haya basi hawato ogopa zaidi ya kupambana.”

Simu ya mama mkwe ikaanza kuita, akaipokea na kuiweka sikoni mwake.

“Ndio”

“Safi wapo wangapi?”

“Muhojini mmoja baada ya mwengine wakishidwa kujibu ni wapi alipo Judy, tumieni plan B”

“Okay”

Mama mkwe akakata simu.

“Wamekamatwa?”

“Ndio”

“Mmm kumbe vijana wako wapo makini sana ehee?”

“Kwenye maisha yako yote hakikisha kwamba unakuwa na karata ya siri. Watu wengi sana walihisi kwamba Mussa ndio karata yangu ya siri, wamemrubuni kwa pesa na kumchukua ila wamebugi kwa maana hawato pata chochote kwake zaidi ya maneno mengi”

“Ila ka Musa ameondoka na Cleopatra sasa hapo awali ka Musa alisema kwamba atamnyonga na kumua, badae wakabadilika na Cleopatra akadai kwamba anahitaji kuondoka na Eddy Tanzania, sasa nikashindwa kuelea na nikabakki njia panda”

“Cleopatra ni……”

Mama mkwe alikaa kimya huku akitazama gari la wagonjwa linalo toka katika jumba la Kibopa.

“Wanatoka”

Tukashuhudia gari la wagonjwa likipita pembeni yetu huku kukiwa na gari jengine aina ya Range Rover Sport ikiwafwata kwa nyuma. Mama mkwe akasubiria yafike mbali kidogo kisha taratibu tukaanza kuwafwatilia.

“Mama unaziacha gari hizo mbeli sana, si watatupotea?”

“Hakuna kitu kma hicho, ila gari inaonyesha kabisa inatokea Regency medical Centre. Kwa hiyo sio rahisi kwa wao kutupotea”

“Sawa mama”

Ukimya ukatawala ndani ya gari na mama mkwe akaendelea kuendesha gari kwa umakini hadi tukafika kwenye kwenye jengo refu la hospitali hii. Tukamshuhudia Kibopa akishusha kwenye gari hilo la wagonjwa huku walinzi wake walimo kwenye gari ina ya Range Rover Sport nao wakishuka huku ili kuendeleza ulinzi kwa bosi wao. Taratibu mama mkwe akageuza gari na tukaanza kuondoka eneo hili.

“Mama mbona hatujaingia ndani?”

“Kuna kazi ambayo tunatakiwa kuifanya kwa muda huu, kumbuka kwamba bado Judy hayupo mikononi mwetu”

Nikakosa cha kuzugumza, tukazidi kusonge mbele hadi kwenye msitu mmoja ambao siufahamu ni wapi kwa maana hii ndio mara yangu ya kwanza kufika huku.

“Unashuka au unanisubiri ndani ya gari?”

Mama mkwe aliniuliza huku huku akinitazama usoni mwangu”

“Ninashuka mama”

Mama mkwe akawa wa kwanza kushuka nami nikafwatia. Nikaanza kuuongozana naye hadi kwenye moja ya mtu, tukakuta vijana wote wa Kibopa wakiwa wamepigisgwa magoti chini huku wakiwa wamedungwa kamba mikono yao kwa nyuma na miguu yao pia ikiwa imefungwa kama. Kila sura ya ninaye mtazama hapa imebadilika kwa kuvimba na inaonyesha dhairi ni kwamba wamepogea kipigo kimoja kikali sana.

“Wamezungumza?”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amesimama mbele yao?”

“Hapana mama”

“Hata mmoja?”

“Ndio”

“Jojo naomba ile simu”

Nikajipapasa katika mifuko yangu ya suruali na kuiona simu hiyo. Nikamkabidhi mama mkwe simu hiyo. Akatoa simu yake na kuonekana kama ana nakili namba fulani kutoka katika namba ya Kibopa, alipo hakikisha kwamba ameipata akampiga.

“Ulinifanyia kosa, ila bado unaendelea kufanya kosa la kutuma vijana wako unahisi kamba mimi ni fala sana ambaye sito tambu juu ya hawa vijana wako?”

Mazungumzo ya mama dhairi yanaonyesha anazungumza na Kibopa.

“Nikusamehe nini sasa, nimekuomba kitu kimoja, nikabidhi kijana wangu nami nikupatie vijana wako”

“Kwa hiyo huwezi kumuachia si ndio?”

Mama mkwe alizungumza huku simu akiishusha sikioni mwake na akaweka loud speaker.

“Siwezi kufanya ujinga huo malaya mkubwa wewe, tena ninakuambia kitu kimoja ukiua hata kijana wangu mmoja basi nitamuua kunguni wako”

Mama mkwe akamnyooshe kijana wake mmoja, akakabidhiwa bastola. Pasipo hata kufikiria akafyatua risasi kwa kijana mmoja na akaanguka chini na kufa hapo hapo”

“Nimemuua mmoja, zungumza ujinga tena nimuue mwengine”

“Pumbavu wewe nitakuuaa, haki ya Mungu, nitakuuaaa”

Tuliisikia sauti ya Kibopa akizungumza kwa mashaka mengi sana. Mama mkwe akampiga risasi mtu mwegine wa Kibopa.

“Nikimalizana na hawa, kabla ya kupambazuka. Nitakuletea kichwa cha mdogo wako hapo hospitalini ulipo lazwa”

Mama mkwe baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akawapiga risasi wa vijana wote wa Kibapo hadi nikajikuta mwili mzima ukinitetemeka kwa woga mwingi kwani ni tulio la kutisha japo hata mimi nilisha wahi kufanya matukio mabaya ya mauji ila dhairi mama mkwe anaonyesha ni mwanamke asiye na huruma hata kidogo kwa adui yake.



Mama mkwe baada ya kumaliza kufanya tukio hilo, taratibu akamrudishia kijana wake bastola hiyo.

“Hakikisheni kwamba hii miili haionekana maisha yote yaliyo baki hapa dunia”

“Sawa mkuu”

“Mukimaliza kazi hiyo tangulieni nyumbani ninapo ishi na muhakikishe kwamba usalama unaendelea kuimarika”

“Sawa mkuu”

Mama mkwe akaanza kutangulia kwenye gari na mimi nikaanza kumfwata kwa nyuma huku kwa mara kadha nikigeuka nyuma nyuma na kutazama ni miili hiyo itafanywa nini na watu hao. Tukaingia ndani ya gari, kitu cha kwanza kukifanya mama mkwe ni kuitazama simu ya Kibopa. Akachukua simu yake na kumpigia mtu anaye mfahamu yeye.

“Jane”

“Marahaba, upo ofisini au wapi?”

“Okay kuna namba nahitaji unisaidie kuitafuta sasa hivi hapa na unifahamishe huyo mtu ninaweza kumpata wapi”

“Sawa”

Mama mkwe akaimtajia huyo Jane namba hiyo, alipo maliza, akakata simu, akawasha gari, akalirudisha nyuma kwa haraka huku akiligeuza kasi hii hii hadi gari likauyumba kidogo kisha akaliweka sawa na tukaanza kuondoka eneo hili kwa mwendo wa kasi sana. Mama mkwe akaanza kuachia misunyo ambayo sikuweza kujua nini maana yake.

“Watu wengine wanakufanya mtu unatenda dhambi ambayo hujakusudia kuifanya kabisa. Sikupanga kuua mimi akhaa”

Mama mkwe alilalama huku akiendelea kusunya, dhairi anaonyesha kwamba ana hasira na amekwerwa na kila jambo ambalo linatokea hivi sasa. Kusema kweli mimi kwa namna moja ama nyingine mimi ndio niliye leta matatizo kwenye hii famili ya watu. Laiti kama ingekuwa si kumpenda Eddazaria na kunitambulisha kwao, sidhani kama leo hii huyu mama wa watu angekuwa anapitia vipindi vigumu kama hivi. Kwa mawazo yangu nikajikuta nikimwagikwa na machozi usoni mwangu, mama mkwe akaniangalia huku akiendelea kuendesha gari hili kwa mwendo wa kasi sana. Simu ya mama mkwe ikaanz akuita.

“Ndio”

Mama mkwe alizungumza mara baada ya kuipokea simu hiyo

“Triple 7?”

“Sawa, nitumie na picha za nguo aliyo ivaa sasa hivi”

Mama mkwe akakata simu na kuiweka pembeni.

“Mama”

“Mmmmm”

“Nakupenda sana mama yangu”

Mama mkwe alizungumza huku akitabasamu tu usoni mwake.

“Akili yako Jojo sasa hivi tuiweke kwanza kwenye kumtafuta Judy hayo mambo mengine tutazungumza baadae”

“Sawa mama yangu”

Tukafika Triple 7, mama mkwe akasimamisha gari kwenye maegesho ya magari. Akaitoa simu yake mfukoni na kutzama picha ya Juma.

“Ukimuona si unamfahamu?”

“Ndio mama”

“Naomba bastola moja”

Nikamkabidhi mama mkwe bastola moja kisha akawa wa kwanza kushuka kwenye gari, nikaichomeka bastola niliyo baki nayo nyuma eneo la kiunoni mwangu. Tukaanza kutembea kuelekea ndani ya eneo hili huku mama mkwe simu yake akiwa ameishika mkononi. Tukaingia kwenye moja ya sehemu na kukuta wasichana wengi wa kiwa wamekusanyika huku wakiwa wamemuweka Juma katikatati.

“Mama Juma ana walinzi wengi”

“Tunamchukua”

Mama mkwe alizungumza huku akianza kupita katikati ya wasichana hao. Akamshika Juma shati lake na kumpiga kichwa cha uso kilicho mfanya kupagawa kiasi kwamba akaanza kupepesuka. Walinzi wake wakaanza kutoa silaha zaoa wakihitaji kumshambulia mama mkwe, ila mama mkwe kwa haraka akampiga Juma kabali na kumuweka mbele yake, huku akimuwekea bastola ya kichwa. Nikachomoa nami bastola yangu, safari hii sihitaji udhaifu wowote kwa kasi ya ajabu, nikaanza kuwashambulia walinzi hawa walio simama wakishangaa shangaa. Milio ya risaisi ikakawafanya wadada na watu wengine walipo katika eneo hili kuanga kugawanyika na kukimbia kila mtu akijaribu kuyaokoa maisha yake. Kwa shambulizi langu nililo lifanya hapakuwa na mlinzi wa Juma aliye baki akiwa amesimama.

“Kazi nzuri”

Mama mkwe alizungumza huku akianza kumkokota Juma na kutoka naye nje. Mama mkwe akamuingiza Juma ndani ya gari huku mimi nikikaa siti ya mbele upande wa dereva na nikaanza kuondoka eneo hili kwa kaisi.

“Judy yupo wapi?”

Mama mkwe alizungumza huku akiwa amemuwekea Juma bastoka ya kichwa chake.

“Sijui mimi”

Mama mkwe hakurudia swali mara mbili zaidi ya nilicho kisikia ni mlio wa bastola ukiambatana na makelele mengi ya Juma kama aliyo kuwa akiyatoa kaka yake.

“Yupo wapi Judy”

“Yupo hotelini”

“Hoteli gani?”

“Kule…kule Kariakoo”

“Twende”

Juma akaanza kunielekeza ni eneo gani ilipo hoteli aliyo muhifadhi mdogo wangu. Tukafika Kariakoo katika hoteli moja ambayo hata sikujishuhulisha kutazama jina lake ina itwaje. Mama mkwe akamshusha Juma kwenye gari kisha nami nikashuka. Tukanza kuingia ndani hoteli hii, tukapita mapokezi na kumkuta kijana mmoja na wala hatukumsalimia. Michirizi ya damu ya Juma inayo mdotoka katika mguu wake wa kulia kidogo ikanitisha kwa maana kama kuna watu watakuwa wanatufwatilia wanaweza kuitumia michiziri hii kutufwatilia kwa maana tumesha panda gorofa ya kwanza tayari.

“Mama anamwaga sana damu huyu”

Mama mkwe akamtazama Juma, kisha akamgandamiza ukutani.

“Yupo gorofa namba ngapi?”

“Namba tano?”

Tukaanza kusikia vishindo vya watu wakipandisha katika hii gorofa, kwa haraka nikachungulia kwa chini na kuona wanaume kama sita, wakiwa wamebeba silaha wakipandisha ngazi hizi kwa umakini sana.

“Mama wanakuja, ingia naye kwenye lefti mimi nawazuia hawa”

“Jojo”

“Ndio mama fanya hivyo”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenge. Mama mkwe akaingia akaminya batani ya lifti, ilipo funguka akamsukumia Juma ndani ya lifti hiyo kisha na yeye akaingia ndani. Nikajibanza kwenye moja ya kona huku nikisubiria kuangali watu hawa mwenendo wao. Katika watu hawa mmoja wao nikaweza kumgundua kwamba ni mtu wa Kibopa hapa ndipo nikapata uhakika kwamba hawa sio watu wazuri.

Nikashushu pumzi taratibu kisha nikaibana vizuri na kuanza kuwashambulia wawili ambao wametangulia mbele na kwa bahati nzuri nikafanikiwa kuwaangamiza. Mashambulizi yakaanza huku watu hawa wakijitahidi kujakikisha kwamba wananiua. Milio hii ikasabisha watu waliomo ndani ya hoteli hii kuanza kutoka kwa kuchanyikiwa.

“Rudini ndani”

Niliwaambia wadada wawili walio toka uchi kama walivyo zaliwa kwenye chumba kimoja. Mashambulizi yakazidi kupamba moto. Mashambulizi kwa upande wangu yakazidi kuwa mazito sikiona sababu ya kuendelea kujibanza katika eneo hili. Nikaaanza kupandisha ngazi huku nikikimbia kwa uwezo wangu wote ninao jitahidi.

Kukaa kwa muda mrefu pasipo kufanya mazoezi nalo ni tatizo lililo nipelekea kwa mara kadhaa kujikuta nikiishiwa na pumzi na inanilazimu kujibanza kwenye kona yoyote ambayo kwangu nitaona ni salama kwa maana kupandisha gorofa tano kwa kukimbia sio jambo jepesi.

Watu hao wakazidi kupandisha ngazi huku wakishambulia eneo nililipo kwa risasi, ubaya ni kwamba bastola yangu imeniishia risasi na sina magazine ya ziana ambaye ina ridsasi. Nikazidi kupandisha juu huku nikimuomba Mungu nisipigwe risasi ya aina yoyote.

Nikafanikiwa kufika katika kordo ya gorofa ya tano na kukuta maiti kama nne za wanaume wenye silaha wakiwa wamelala chini. Ina ashiri kwamba mama mkwe yeye ndio alio wafanya hivi.Nikaokota bunduki moja, nikatoa magazine na kukuta ina risasi kadhaa. Nikaanza kurudisha mashambulizi kwa wale ambao walikuwa kinikimbiza toka goroa ya kwanza, cha kumshukuru Mungu nikafanikiwa kuwaua kila mmoja kwa namna yake. Nipo hakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha nikaanza kufwata michiri ya damu ambayo natambu ni ya Juma. Nikafika kwenye moja ya chumba na kumkuta mama mkwe akiwa amekumbatiana na Judy huku wote wakilia kwa

huzuni na Juma naye yupo chini akimwagikwa na damu za kichwani.

Nikaitupa bunduki hiyo pembeni na kuwakumbatia kwa pamoja huku nami machozi ya furaha yakinimwagika usini mwangu.

“Nashukuru kwa kuja”

Judy alizungumza huku machozi yakimwagika, usoni mwake amejaa michirizi ya kupigwa makofi mazito mazito, inaonyesha dhairi kwamba amepitia kipindi kigumu sana.

“Tupo kwa ajii yako”

Nilizungumza huku nami machozi yakinimwagika usoni mwangu.

“Jojo”

Mama mkwe aliniita huku akijifuta machozi yake usoni mwake.

“Ndio mama”

“Mchukue Judy na moja kwa moja uelekee nyumbani”

“Na wewe je mama?”

“Mimi nitabaki hapa”

“Mama hatuwezi kukuacha peke yako hapa”

Nilizungumza huku nikimtazama mama mkwe usoni mwake.

“Hii ni kesi ambayo mukikutwa hapa wewe na Judy munaweza kusumbuliwa na askari. So mchukue mdogo wako na muondoke eneo hili haraka iwezekanavyo sawa”

Mama mkwe alizungumza kwa ukali huku akinitazama usoni mwangu.

“Mama twende nyumbani”

Judy alizungumza huku akiwa amejichokea.

“Tutaonana asubuhi”

Mama mkwe alizungumza huku akitabasamu. Nikamshika Judy mkonona kuanza kutoka naye humu ndani huku nikimtazama mama mkwe. Kabla ya kutoka ndani ya chumba hichi mama mkwe akanita sehemu alipo simama. Nikamsogelea na kusimama mbele yake.

“Kama unavyo jua raisi amenitoa katika madaraka ya kusimamia kitengo cha madawa ya kulevya. Endapo nitakamatwa, nenda nyumbani kwangu mkoani Tanga, katika chumba changu chini ya kitanda changu, kuna mlango wa chini ya ardhi, shuka chini ya ardhi utakuta vitu vyenye siri muhumu kabisa nakuomba uvichukue na wewe ndio utakuwa ni mtetezi wangu, ninakuomba usije ukaniangusha katika hilo sawa”

Mama mkwe alizungumza kwa unyonge mkubwa sana huku machozi yakimwagika usoni mwake, nikajikuta nikishindwa kuitikia chochote zaidi ya kuangua kilio kizio kilicho mfanya mama mkwe kunikumbatia kwa nguvu na kuendeea kulia na yeye.



“Nenda sasa hakikisha munakuwa salama”

Mama mkwe alizungumza huku akiniachia, nikatamani kuendelea kumkumbatatia ila mama mkwe akanisukuma kilazima na kwa ishara akaniomba niweze kuondoka na Judy. Nikatoka ndani humu na kumkuta Judy akiwa anashangaa maiti za watu walio lala chini. Nikamshika mkono na kuanza kukimbia naye huku tukijitahidi kushuka kwenye ngazi hizi. Tukakutana na watu wanao kimbia kuyoka kwenye vyumba vyao kuyaokoa maisha yao. Tukajumuika nao, tukiwa katika goroa ya pili, tukakutana na askari wakiongozwa na yule kamanda wao ambaye yeye na mama picha haziendani kabisa. Tukapita pembeni yake na kwa bahati nzuri hakuweza kutuona, tukafanikiwa kutoka nje ya hoteli hii, nikatazama eneo nilipo liacha gari tulilo kuja nalo ila sikuweza kulisogelea kwa manaa tayari polisi wamesha tanda eneo hili na endapo nitathubutu kuondoka na gari hili nina imani nilazima kuna mambo ambayo yanaweza kupelekea kutiliwa mashaka jamba ambalo mama mkwe hapendi litokee.

“Tujibaneze hapa”

Nilimuambia Judy huku nikihema sana. Tukajibanza kwenye moja ya duka ambalo linatazamana na eneo la mbele la hii hoteli. Hazikupita hata dakika kumi, tukamshuhudia mkuu wa polisi na vijana wake kadhaa wakiwa wamemshikilia mama mkwe huku wamemfunga pingu mikono yake kwa nyuma. Machozi yakanimwagika kwani ninatambua ni shida gani ambayo mama mkwe anakwenda kuipata kwa kipindi hichi ambacho tayari ameamua kumwaga mboga ikiwa raisi na Kibopa waliamua kumwaga ugali.

“Wanampeleka wapi mama”

Judy aliniuliza huku akionyesha dhairi kwamba amejawa na mashaka makubwa sana.

“Ehee?”

“Anapelekwa wapi?”

“Twende nyumbani”

“Dada Judy mama anapekekwa wapi?”

Judy aliendelea kuning’ang’aniza katika kuniuliza maswali ambayo jibu ninalo kichwani mwangu ila sijui nianze vipi katika kumjibu.

“Twende bwana nyumbani”

Niliendelea kuzungumza huku tukianza kutembea katia mitaa hii ya Kariakoo usiku huu huku nikitambua kwamba kwa watoto wa kike ni jambo hatari kwa maana kuna vibaka wa kila aina.

“Dada kuna watu wanatufwatilia kwa nyuma”

Judy alizungumza na kunifanya nigeuke nyuma haraka, ila sikuweza kuona watu wakitufwata.

“Wapo wapi?”

“Walikuwa wanakuja wanaume wawili”

Judy alizungumza huku mwili mzima ukimtetemeka. Nikakiminya kiganja chake kwa nguvu na kumfanya anitazame usoni mwangu.

“Upo nami usiwe na mashaka mdogo wangu”

Baada ya kumaliza kuzungumza sentensi hiyo tukaendelea kutembea huku nikijiamini. Hisia zangu zote nikazielekezea kwenye masikio yangu, na nikaanza kusikia vishindo vya watu vikitufwata kwa nyuma. Idadi ya watu hao ambao hapo awali walikuwa wa wili, inazidi kuongezeka na kufikia watu watano.

“Jojo wanazidi kuja”

“Usijali”

Nilizungumza huku nikikunja ngumi ya mkono wangu wa kulia. Mbele yetu wakatokea wanaume wengine wanne wakiwa wameshika magongo pamoja na visu, ikatulazimu kusimama.

“Hei nyinyi malaya usiku huu munakwenda wapi hamujui hichi kitaa ni cha manyani?”

Jamaa mmoja anaye zidi kutosogelea na wezake mbele yetu alizungumza huku akizidi kutusogelea.

“Judy?”

“Mmmm”

“Hakikisha kwamba husogei mita mbili kutoka hapa nilipo sawa”

“Unataka kufanya nini dada?”

“Usijali”

Nilizungumza huku nikiwatazama wanaume hawa, vibaka jinsi wanavyo tuzunguka na kutuweka katikati.

“Kama kuna mtu mmoja wenu anahitaji kufa au kwenda Muhimbili akiwa amevunjika vunjika basi atusogelee na kwa usalama wenu ninawaomba muweze kuondoka eneo hili kabla hali hajibadilika”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwatazama.

“Hahaaaa………”

Baadhi yao walicheka kwa dharau, dhairi wanatuzarau jinsi yetu kwani siku zote wanaume wa Tanzania baadhi yao huwa wanaamini kwamba mwanamke kwao ni kitu chepesi na hawezi kufanya lolote hususani katika swala la kupambana nao.

“Hahaahahaa haki ya Mungu, malaaya wa bongo wana biti aiseee. Sasa ukitaka kutujua sisi ni manyani tunawabaka na asubihi nyinyi ndio mutakwenda Muhimbili kuzibwa kum** na mikund** yenu kwa maana tunakuwa tumeichana chama”

Kibaka mmoja ambaye ndio anaonekana ndio kiongozi wao alizungumza huku akianza kunisogelea. Sikuhitaji afike katika eneo ambalo amesimama Judy kwa maana ninatambua mdogo wangu hajimudu kwenye swala la kupambana. Kitendo cha kibaka huyu kufika mita chache toka nilipo nikajirusha hewani huku mguu wangu wa kulia nikiuntanguliza mbele. Nikampiga teke la kifua na kumfanya apepesuke huku akirudi nyuma na akaanguka chini kama zigo la kuni.

Wezake wakamtazama mwenzao jinsi anavyo jitahidi kusimama ili kufuta aibu kwani toka tumekutana nao hapa yeye ndio alikuwa kihere here wa kuzungumza.

Bila ya kujiuliza mara mbili kwamba mimi ni mtu wa aina gani akanisogelea huku akikunjua kisu chake ambacho ni cha kukunja. Akaanza kunishambulia, ila kibaka ni kibaka tu na ubaya vibaka wetu wa Tanzania hawana mafunzo ya kupambana, na bangi wanazo zivuta basi zinawaaminisha kwamba wanaweza kupambana na kila mtu.

Nikaudaka mkono alio shika kisu, bila ya huruma nikauvunja kama vile mtu anavyo vunja kuni na kusabisha kisu kumuanguka chini. Makelele ya maumivu yakawa hofu kidogo wezake ambao macho yao yoye yapo kwenye kushuhudia mtanange huu unao endelea. Nikamuwekea kisu cha shingo kibaka huyu huku mkono wake wa kuliaa ukiwa unaning’inia.

“Kuna yoyote kati yetu anahitaji kwenda Muhimbili kwa maana huyu tayari kesho anakwenda”

“Hapana bwana sister Jojo”

Hapa kidogo nikastuka kwa maana tayari wamesha nigundua.

“Siku nyingine usimkurupikie kila mwanamke, utakuja kufa, sawa wewe mwehu?”

Nilizungumza huku nikikigandamiza kisu hichi taratibu kwenye shingo ya huyu kibaka.

“Ndio ndio”

Alizungumza huku akilia kwa maumivu ambayo anaendelea kuyapata. Nikamsukumia chini na nikabaki na kisu chake.

“Pisheni”

Nilizungumza na wote walio kuwa wametengeneza duara, wakatupisha. Nikamshika Judy na tukaanza kutembea katikati yao huku nikiwa nimekishika kisu hichi.

“Sister Jojo”

Niliisikia sauti ya kijana mwengine ikiniita nyuma yetu na akanifanya nisimame na kugeka taratibu.

“Asante bwana kwa maana huyu mseng** alikuwa akitukoromea na kujiona mtemi kumbe boya tu”

“Dogo dogo unaniita boya mimi”

Jamaa niliye mpiga alijitahidi kuzungumza huku akisimama. Ila kijana huyo mwenye mwili mwembamba sana akampiga mtama na akaangukia mkono ule ule nilio uvunja.

“Tulia boya wewe, unanyanyuka unakwenda wapi?”

“Dogo Amidu nikinyanyuka ha……”

Kijana huyo akamkanyaga kifuani.

“Mseng** wewe utaniambia nini wewe, unakumbuka asubihi ulinifanya nini wewe kum** eheeee.”

Kijana huyo aliendelea kumkanyaga kanyaga jamaa huyo kifuani mwake na cha kushangaza hakuna kibaka mwengine aliye msaidia huyo anaye kajagwa.

“Na nyinyi munashangaa nini, huyu tunamzika hapa hapa hakuna haja ya kumpeleka Muhimbili, njooni mumpige”

Vijana wengine wanakafwata amri ya kijanahuyo mwembaba, wakanaza kupiga mateke mwenzao huyo anaye endeea kuugulia kwa maumivu makaki. Mwanga mkali wa gari linalo kuka katika barabara hii ukawafanya vijana hawa kuanza kutawanyika.

“Pira pira”

Ilisikika sauti ya kijana mmoja akimaanisha kwamba gari hilo linalo kuna ni gari la polisi. Nikamshika Judy mkono na tukaanza kukimbia huku nyuma yetu tukifwata na vijana wawili akiwemo huyo dogo Amidu.

“Sister huku”

Dogo Amidu alizungumza huku akipita kwenye kichochoro chembaba hicho ambacho naamini kwa mtu mnene hato weza kupita. Tukaanza kuwafwata kwa nyuma huku tukisikia milio ya risasi zinazo pigwa hewani zikisikika. Tukazidi kufwata kichochoro hicho, ambacho dogo Amidu ndio anakifahamu vizuri. Tukaingia kwenye moja ya godauni lenye giza giza kidogo ila mwanga hafifu wa mbalawezi inayo mulika vizuri, tunaweza kuona ona baadhi ya magunia yaliyo pangwa ndani ya godauni hili.

“Sister eneo hili ni salama”

“Kweli?”

Nilizungumza huku nikiwa nimekishika kisu changu vizuri.

“Ndio”

“Saa ngapi sasa hivi?”

Dogo Amidu akatoa kijisimu kidogo kilicho fungwa na mipira, kiufupi ni simu mbaya.

“Ni saa kumi na dakika ishirini”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikianza kupiga mahesabu ya kujiuliza ni jinsi gani ambavyo tunaweza kuelekea Tegeta nyumbani kwangu muda huu.

“Dogo Amidu”

“Ndio sister?”

“Tunaweza kupata usafiri wa pikipiki usiku huu?”

“Ndiom kuna mchizi wangu mmoja nimemuachia pikipiki yangu apiga deiwaka usiku huu”

“Unaweza kupigia simu na akaja hapa tulipo?”

“Ngoja nimcheki”

Dogo Amidu alizungumza huku akiminya minya batani za simu yake. Akaiweka sikioni na kusikilizia kwa muda.

“Oya upo wapi?”

“Njoo maskani”

“Kimenuka nini, njoo niletee pikipiki yangu bwana”

“Oya usiniletee using** wewe kama upo kwa huyo malaya wako na unajifanya unashindwa kutoka, nitakufanya kitu mbaya sawa, niletee pikipiki yangu”

Hamidu alizungumza kwa hasira huku akikata simu yake.

“Kum**k** huyu choko kasha kumbatia malaya wake basi analeta porojo za kiseng***”

“Oya dogo Amidu mwera mwera”

Kijana mwengine alizungumza huku akiwa anachungulia nje, kwa haraka nikamuona dogo Amidu na mwenzake wakijificha kwenye magunia, ikatulazimu mimi na Judy nasi kukimbilia kwenye eneo jengine lenye magunia mengi nasi tukajificha. Yaani hata sekunde kumi hazijaisha tukashutukia mlango ukifunguliwa kwa nguvu huku matochi makubwa yakimulika.

“Hawa washenzi lazima tuwakamate, tafuteni kila sehemu, iwe ndani ya gunia au ndani ya pipa funuenii funueni lazima tuwakamate, hawawezi kufanya jeshi la polisi kama mgambo. Pumbavu”

Sauti hii ya kiume na yenye ukali ikatutisha sote hususani Judy ambaye taatibu akanikumbatia kwani nafasi ya sisi kutoka ndani ya hili eneo ni ndogo sana ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.



Mianga ya tochi ikaanza kuangaza kila upande wa godauni hili. Tukaanza kuona kivuli cha mtu kikija katika eneo ambalo tumejificha, Judy akazidi kutetemeka hadi meno yake yakaanza kujigonga gonga jambo lililo nifanya nimzibe mdomo wake kwa nguvu. Mtu huyo ambaye ni askari aliye valia sare zake na koti lake akakaribia kabisa katika eneo la gunia ambalo tumejificha, gafla tukasikia mlio wa simu ikitokea kwenye eneo ambalo dogo Amidu na wezake walikimbilia kujificha.

“Hawa huku”

Ilisikika sauti ya kiume ikimfanya askari huyu ambaye anakuja katika eneo hili kugairisha kabisa kumulika eneo tulipo. Taratibu nikamuachia Judy mdimo wake na kuchungulia, nikamshuhudia dogo Amidu na wezake wakiwa wamebebwa juu juu huku wakitandikwa virungu vya kila sehemu za mwili mwilini mwao pasipo huruma yoyote. Polisi wakatoka ndani ya godauni hili na kutuacha mimi na Judy.

“Ohoo Mungu wangu”

Nilijikuta nikizungumza kwa sauti ya chini. Nikamkumbatia mdogo wangu kwa maana tumeokoka kwenye sekeseke hili sipati picha kama ningekamatwa, magezeti ya udaku sijui yangeandikaje juu yangu.

“Nisubiri hapa”

Nilimuambia Judy huku nikinyanyuka, nikatembea kwa tahadhari hadi kwenye mlango wa kuingilia katika godauni hili, nikachungulia kwenye kichochoro ambacho tunapita, sikuona mtu wa aina yoyote.

“Judy”

Niliita kwa sauti ya chini kidogo, Judy akasimama na kuniangalia.

“Njoo”

Judy kwa mwendo wa wasiwasi akafika hadi eneo ambalo nimesimama, nikachungulia nje, nilipo hakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha tukatoka kwenye godauni hili na tukaanza kutembea kukifwata hichi kichochoro hadi tukatokea mtaa wa pili.

“Naufahamu huu mtaa”

Judy alizungumza huku kidogo akiwa amejiamini.

“Twende huku, kuna sehemu pale mbele kuna waendesha taksi”

“Sawa”

Tukaanza kutembea kwa haraka haraka, tukafanikiwa kufika katika eneo la maegesho ya taksi na tukamkuta dereva mmoja akiwa amesimama nje ya taksi yake huku akivuta sigara.

“Habari yako kaka”

Nilimsalimia huku nikimtazama usoni mwake kwa kumkazia macho.

“Salama aisee”

“Tunahitaji kuelekea Tegeta usiku huu”

“Aisee Tegeta muda huu, mbona mbali sana masiteriii”

Jamaa huyu alizungumza kwa lafudhi ya kichaga.

“Unataka pesa au huhitaji pesa”

“Pesa aisee nahitaji ila huko mbali sana na ukicheki ngoma saa hizi ni kitu kumi aisee, musije kwenda nifanya kitu mbaya”

“Kuna sura za kufanyia watu kitu kibaya na sura nyingine sio za kuzifanyia kitu kibaya”

“Nyinyi muna bei ngapi?”

“Hamsini”

Judy alidakia.

“Haahaa aisee hamsini siendi hiyo ni pesa ya pikipiki”

“Wewe unataka sh ngapi?”

Nilimuuliza kwa msisitizo.

“Nyinyi semeni mutanipa sh ngapi”

“Nitakupa laki”

“Laki siendi”

“Sister tuachane naye naona hataki pesa, wewe usawa huu ulivyo mgumu unakataa laki”

Judy alizungumza kwa jazba kidogo kana kwamba amesahau sehemu tulipo na ni nini kilicho tukosa kosa.

“Nitakupa laki mbili twende”

“Lete kitangulizi”

“Hapa sina, unanipekea hadi nyumani kwangu na nitaingia ndani na kukupatia hiyo pesa”

“Khaa kumbe hata pesa yenyewe hamna”

“Jamani wee kaka mbona muongeaji au ni hiyo bangi unayo ivuta ndio inakuuzua. Humjui huyu Jojo msanii maarufu eheee?”

Judy alizungumza kwa hasira huku machozi yakimlenga lenga. Jamaa akanitazama kwa umakini, kisha akatabasamu.

“Aissee nilikuwa nakufananisha aiseee”

“Twende basi”

“Sawa ila ngojeni kwanza”

Jamaa huyu akafungua mlango wa nyuma.

“Aisee nyinyi waseng*** kama hamjamaliza kutomb***a tokeni kwenye gari yangu”

Maneno ya huyu dereva huyu yakatufanya tuchungulie katika siti za nyuma, tukamuona jamaa akiwa na mwanamke wakifanya mapenzi.

“Kaka nipe dakika moja, namwaga sasa hivi”

“Unamwaga nini aisee hembu tokeni na malaya wako huyo”

“Jamani na wewe mchaga si umuache mwenzako amwage, unajua hapa nahesabu mabao wewe, asipo mwaga hilo bao moja utanilipa pesa ya hilo bao”

Dada huyo ambaye anaonyesha dhairi ni changudoa alizungumza.

“Acha ukum** wewe, mulinisaidia kununua hii gari. Oya toka bwana nawachelewesha warembo hapa”

“Oya Kimaro mimi si ndugu yako kabisa, nipe dakika moja tu”

“Waache wamalizie”

Nilizungumza kwa upole huku nikimtazama dereva taksi huyu. Taratibu akaniufunga mlango huo na tukasimama pembeni ya taksi hii na tukaishuhudia jinsi inavyo tikisika tikisika.

“Aisee limekuwa bao la tembo nini, hembu shukeni musije mukanivunjia tairi zangu”

Derva alizungumza huku akifungu mlango wa gari hili, akaanza kushuka jaa huyo huku akivua kondom yake iliyo jaa shahawa na jasho likimwagika mwilini mwake. Akashuka dada huyu ambaye amejaliwa uzuri kwa kweli, naye bila ya aibu akaanza kupandisha chipi yake huku suruali yake akiwa ameishika mkononi.

“Nipatie changu nisepe nikawahi wateja wengine”

“Ngoja kwanza nivue kondom bwana”

Mwnaume huyu alizungumza kwa kokoroma.

“Uvue kwani nilikuvisha mimi, nipe changu”

“Hivi umeniambia bao moja ni shilingi ngapi?”

“Usijifanye mseng** wewe. Kila bao ni sh elfu tano. Nipe elfu kumi yangu niondoke”

“Aisee nyinyi kadaieneni kule kwanza taksi yangu inanuka ubeberu ubeberu”

Dereva taksi alizungumza huku akipulizia airfresh ndani ya gari lake.

“Na wewe Kimaro acha using** kudai pesa yangu kuna kukera nini?”

“Mwajua chukua hii buku saba, buku tatu nitakumalizia”

“Weee weeee weee, Rama unanijua, Rama unanijua ohoooo?”

“Sasa ndio pesa niliyo nayo”

“Nimekuambia nipe pesa yangu”

Dada huyu alizungumza huku akimshika mwanaume huyo mkono wake. Hali hii kusema kweli ikanisikitisha sana.

“Ukilete ujuaji hata hii buku saba sinto kupa”

“Labda sio mimi Mwajuma. Kunitomb** unitomb**. Kunifir** pia unifir*** alafu unanipa buku saba, haki ya Mungu nitakwenda kuidai kwa mkeo ndio utanijua mimi ni kicha au mwenda wazimu wa Mirembe”

“Aisee Jojo ingieni kwenye gari tuondokeni”

Judy akawa wa kwanza kuingia ndani ya taksi, nikataka kuingia ila roho ikasita kabisa kwani anaye dhalilisha hapa ni mwanamke kama mimi. Kwa namna moja ama nyingine maisha yake yatakuwa ni magumu sana kiasi cha kujikuta akiingia kwenye biashara hii.

“Kaka mpe pesa yake”

“Oya na wewe maindisha ishu zako, ingia kwenye gari na usepe, hayakuhu haya”

Nikakichomoa kisu nilicho mpokonya kibaka niliye toka kupambana naye na kumfwata mwanaume huyu. Dereva taksi akashuka kwenye gari na kunishangaa jambo lililo mpelekea hata Judy naye kushuka kwenye gari.

“Unampa pesa yake au humpi?”

Nilizungumza kwa hasira sana hadi mwanaume huyu akaanza kunywea, akaanza kuipandisha suruali yake na kujipapasa mikoni mwake. Akatoa wallet, kabla ya kuifungua nikampokonya. Nikaifungua mimi, nikakuta noti mbili za shilingi elfu kumi, nikazichomoa zote na kukabidhi dada huyu, kisha wallet nikampiga nayo usoni mwanaume huyu.

“Uyoooo liangalie dume zima hadi ushikiwe visu, nyooo. Asante sana dada yangu”

“Vaa suruali yako”

Dada huyu akaanza kuvaa suruali yake, akajiweka sawa kishati chake alicho kivaa na kumuacha tumbo lote wazi.

“Potea na wewe hapa, au unataka nikuchinje chinje?”

Nilimuambia mwanaume huyu huku nikimtishia kisu hichi, kwa unyonge mkubwa akaokota wallet yake, taratibu akaanza kuondoka huku shati lake akiwa amelibeba begani.

“Judy kaa mbele”

“Sawa”

“Ingia kwenye gari na wewe”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama dada huyu usoni mwake. Akaingia siti ya nyuma kisha nami nikaingia na kuufunga mlango. Dereva akawasha gari na tukaanza kuondoka katika eneo hili.

“Judy muelekeze njia ya kwenda nyumbani”

“Sawa”

“Kwa nini na wewe unahatarisha maisha yako. Dada mzuri, mwenye umbo zuri, sura nzuri unaranda randa usiku wa manane barabarani huku?”

Swali langu likamfanya dada huyu kukaa kimya huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Nakuuliza nijibu?”

“Maisha tu dada yangu”

“Maisha ndio yanakufanya ujidhalilishe mbele zawatu namna hii, uchi wako wewe huuonei aibu, sijui Kimaro hapa amekuona, sisi tumekuona yaani na bora sisi ni wanawake wezio je hao wanaume je?”

Dada huyu akaka kimya na kukosa cha kuzungumza

“Unaishi wapi?”

“Mbagala Chamanzi”

“Yaani unatoka Mbalaga, unakuja kujiuza huku Kariakoo?”

“Kijiwe changu kipo pale Sinza”

“Jojo huyo awezi kukuelewa unacho kizungumza”

Dereva naye alidakia mada hii.

“Atanielewa tu, mambo mengine wanawake wa Kitanzania ni kujiendekeza, unahisi kwamba kum** yako ndio mtaji wako si ndio?”

“Sasa dada yangu, sina ajira, sina elimu. Wazazi wangu walifariki nikiwa mdogo sana, unahisi nitaishije ehee?”

Dada huyu alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikaka kimya huku nami nikifikiria jinsi nilivyo jitoa maisha yangu na kuwa msagaji kwa ajili tu ya kuweza kupata pesa na maisha bora ambayo ndio ninayo hivi sasa.

“Sasa hivi unaishi na nani?”

“Nipo tu naishi na marafiki zangu”

“Una kwako?”

“Sina dada yangu”

“Judy unasemaje?”

“Twende naye nyumbani, hadi kesho basi tunaweza kujua ni nini cha kufanya”

“Sawa”

“Alafu wewe Mwajua uachee umalaya aisee utakuja kufa ohoooo”

“Na wewe koma, kwani tutaishi milele sote”

“Weee niletee dharau ni wanaume wangapi wanakuja kukutomb** ndani ya taksi yangu”

“Kimaro nini lakini, kwani lazima unipe ushauri, sikulipagi pesa yako wewe”

“Hata kama, ila kama umepata dada wa kukusaidia, tena huyo dada ana mavumba yake ya kutosha wewe achana na hizo mambo, wanaume wenyewe wakukupa buku tano tano kwa bao, unahisi watakusaidia ukiumwa”

“Hembu niache basi Kimaro”

Mwajuma alizungumza kwa hasira hadi Judy akageuka nyuma na kumtazama.

“Sawa bosi wangu, nisamehee. Ila leo umesikia Kariakoo kimenuka chalii yangu”

“Kimenuka saa ngapi?”

“Ohoo kwenye hile hoteli pale karibu na sheli, nasikia kwamba kuna majambazi wameingia wametembeza risasi yaani watu wametapishwa utumbo ile mbaya”

Judy akageuka na kunitazama, nikamkonyeza ili ajifanye kwamba hiyo story haifahamu kabisa.

“Umeonaaaaa…..?”

“Nimesikia tu, unazani kwa nini leo kijiwe nipo peke yangu, kila raisi amekwenda kulala mapema aisee, nimebaki tu mimi”

“Shauri yao bwana, wakifa mimi wananihusu nini”

Mwajuma alizungumza kwa dharau.

“Acha dharau Mwajuma aiisee wale walio kufa ni watu na si kuku”

“Tatizo lako wewe Kimaro unapenda sana umbeaa, yaani hilo tu. Haya kwa nini sasa wakati unasikia milio ya risasi usiende ukawatetee, wewe si unajifanya Jet Lee wa Marangu wewe”

Maneno ya Mwajuma yakanifanya nicheke kichini chini.

“Kuna ujet lee mbele ya shaba wewe”

“Ndio hivyo ungeenda uone mziki wake, ungepelekwa Marangu ukiwa umelala kwenye jeneza”

“Hembu Mwajuma acha hizo mambo bwana, swala la kufa ni jengine aisee”

“Nyoo bwege wewe, unaogopa kufa ehee”

Mazungumzo ya Kimaro na Mwajuma yakanifanya hadi nisahau kwamba nina matatizo makubwa kuliko ya wanavyo niona. Kimaro akakunja kona ya mtaa ninao ishi, kadri jinsi inavyo zidi kwenda mbele ndivyo jinsi nilivyo anza kupatwa na wasiwasi mwingi sana kwani katika usawa wa nyumba yangu kuna gari kama nne za polisi zimesimama huku askari wapatao kumi na tano hivi wakiwa wamezagaa eneo la nje ya jumba langu wakiwa na bunduki pamoja na mbwa wakubwa. Kigugumizi kikanifanya nishindwe kumuambia Kimaro kusimamisha gari hadi alipo simamishwa na askari walio anza kuisogelea taksi hii tuliyo panda huku kila mmoja akiwa ameshika bunduki yake kwa ukini sana wakionyesha wanahitaji kukagua gari taksi hii na kwa namna mmoja ama nyingine ninahisi mtu wanaye mtafuta ni mimi.



“Rudisha gari nyuma barabara imefungwa”

Askari mmoja alizungumza kwa ukali sana na kumfanya Kimaro kuanza kurudisha gari hili nyuma taratibu hadi katika barabara tuliyo ingilia.

“Kuna nini pale?”

Mwajuma aliuliza huku akichungulia chungulia mbele.

“Kuna ibada”

Kimaro alijibu kwa kejeli, Judy akanitazama huku akionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.

“Jojo tunapita njia gani dada yangu?”

Swali la Kimaro likaanza kuifanya akili yangukuanza kufikiria ni wapi kwa kwenda na ni mtu gani kwa sasa ambaye ninaweza kumuamini. Wazo la kumpata dokta Clara likanijia kichwani mwangu, kutokana simu yangu ninayo mfukoni na japo nimeitoa betri na laini, nikaona huu ndio wakati wa mimi kuwasiliana naye.

“Hembu simamisha gari hapo”

Kimaro akasimamisha gari pembezoni mwa babara eneo ambalo polisi walipo mtaani kwetu hawato weza kuliona. Nilipo hakikisha kwamba nimerudisha kila kitu kwenye simu yangu, nikaiwasha huku mapigo ya moyo yakinienda mbio sana. Nikaanza kukagua jina moja baada ya jengine kwenye simu yangu na kwa bahati mbaya katika simu hii sina namba ya dokta Clara na wala kichwani siifahamu.

“Judy”

“Mmmm”

“Unaifahamu namba ya simu ya dokta Clara”

“Hembu lete simu yako”

Nikamkabidhi Judy simu, akaanza kiminya minya namba za simu kisha akanirudishia. Nikaitazama kwa umakini namba hii na kugundua kwamba ndio yenyewe, japo ni muda mrefu sana sijawasiliana naye ila hii namba ndio yenyewe. Nikaipiga na kuiweka simu sikioni, simu ya dokta Clara ikaanza kuita taratibu kisha ikapokelewa.

“Clara”

“Mmmmm”

Alizungumza huku akionekana kujawa na malepe ya usingizi mwingi sana.

“Naamini kwamba umenifahamu”

“Yaa si….”

“Ndio, upo wapi?”

“Nipo ofisini”

“Okay ninakuja sasa hivi”

“Kwema?”

“Tutazungumza”

Nikakata simu, nikatoa betri kisha nikamalizia na laini yenyewe, nikampa Kimaro maelekezo ya kunilepeleka kwenye gorofa ambalo lina ofisi za kampuni yangu. Hatukuchukua muda mrefu sana, tukafanikiwa kufika katika ofisi za kampuni yangu na Kimaro akasimamisha gari lake pembeni kabisa ya geti kubwa la kuingilia katika eneo la magesho ya ofisi hizi, kutokana ni usiku hapakuwa na gari hata moja na wala walinzi hawaruhusu magari kuingia kwa muda huu.

“Judy nisubirini hapa nina kuja sawa”

“Sawa”

Judy alinijibu kinyonge.

“Kimaro naomba uwe makini na hawa watu wawili hapa”

“Haina shida sister niamnini aisee”

“Alafu ungeenda kupaki sehemu ambayo sio rahisi kuonekana, ila liwe eneo ambalo nikitoka hapa getibi basi munaweza kuniona”

“Sawa”

Nikashuka kwenye gari, kisha nikazunguka hadi upande alio kaa Judy nikamkabidhi kisu hichi cha kukunjua na endapo kutatokea jambo lolote baya ninaamini kwamba hato kuwa mzembe wa kujitetea. Nikaanza kuelekea getini, walinzi wanne wanao linda katika eneo hili wakiwa na bunduki zao wakaanza kunimulika na tochi usoni.

“Ni mimi”

“Nani wewe?”

“Jojo”

Nilizungumza huku nikizidi kusonga mbele na mkono wangu mmoja nikiwa nimekinga mianga hiyo ya tochi zenye mwanga mkali wanazo nimulika nazo usoni mwangu.

“Bosi”

“Yaa ndio mimi”

“Mbona usiku wote huu kwema?”

“Kwema, Clara si yupo juu?”

“Ndio yupo”

“Basi nashukuru”

Nilizungumza huku nikiingia getini. Nikaanza kutembea kwa tahadhari huku nikitazama eneo hili kwa umakini mkubwa sana, kwa maana ni eneo lililo tulia sana. Nikaingia ndani ya lifti na moja kwa moja nikapandisha hadi kwenye gorofa ya kampuni yangu. Nikakuta baadhi ya wafanyakazi kwenye kampuni yangu hususani matu wanao shuhulika na upangaji wa vipande vya filamu wakiwa wapo bize na kufanya kazi.

“Jojo”

Clara alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu na kwa furaha sana kwani ni ni siku nyingi hatujawahi kuonana na kuzungumza.

“Nimekumiss mumy”

“Hata mimi jamani, yaani ubize umenifanya hadi nimeshindwa kuja kumuona mwanao”

“Usijali mwaya niambie lakini”

“Safi, mpenzi ninashida”

Nilizungumza huku nikitembea na kueleka kwenye ofisi yangu. Nikafungua mlango na kukuta picha kubwa ya Clara ikiwa ukutani huku juu ya meza kukiwa na kibao kinacho muonyesha kwamba yeye ndio mkurugenzi wa kampuni yangu.

“Ohoo samahani mwaya kwa mabadiliko haya”

“Hapana, hapana. Si unajua kwamba bosi mwenyewe nipo bize. Bila ya wewe nahisi kwamba leo hii kampuni ingekuwa imefungwa kabisa”

“Ni kweli, na hadi sasa hivi tumefikia kiwango cha kutengeneza filamu karibia ishirini na nyingine zimesha anza kutoka”

“Weee”

“Haki ya Mungu vile”

“Okay tuachane na mambo hayo. Nimekuja hapa kutokana na ombi moja au mawili”

“Zungumza mwanya rafiki yangu”

“Ninahitaji pesa kama dola elfu kumi hivi”

“Ahaa hizo utapata hapa hapa ofisi, ehee kingine?”

“Kingine nahitaji gari, kuna gari gani la kapunzi kwenye maegesho”

“Kuna Benzi mbili, moja ninaitumia mimi na nyingine ipo tu”

“Si ina mafuta ya kutosha?”

“Yaa”

“Naomba unisaidie mpenzi”

Clara akazunguka hadi upande wa pili wa meza kubwa iliyopo hapa ofisi kwake, akafungua na kutoa vibunda vya dola kadhaa vilivyo fungwa vizuri.

“Una begi lolote?”

“Ngoja nikakuulizie kwa wale vijana”

“Naomba funguo ya gari”

“Ohoo nilijisahau, chuku gari langu kwa maana hiyo nyingine sijaipeleka service, lisije likakuletea shida hapo baade”

“Sawa”

Clara akanikabidhi funguo yake na kutoka ndani humu. Nikatazama mazingira ya hii ofisi, kwa namna moja ama nyingine amajitahidi kuyaboresha. Nikapiga hatua hadi dirishani, cha kushangaza nikaona gari mbili nyeusi aina ya Range Rover zikiingia getini, zikasimama eneo la megesho na wakashuka wanaume kama kumi wakiwa wamevalia suti nyeusi tupu, kwa namna moja ama nyingine wanaonekana si watu wazuri. Nikaichomekea tisheti yangu kwenye suruali hii niliyo ivaa. Kisha nikaanza kuviingiza vibunda hivi vya pesa kwenye hii tisheni nilipo hakikisha kwamba vimekaa sawa, nikatoka ofisi humu huku nikiwa nimeishika funguo yangu. Nikatembea hadi kwenye lifti na kukuta lifti inaonyesha kwamba inapanda juu, kwa namna moja ama nyingine watu hao watakuwa wanapanda huku gorofani. Nikautazama mlango wa kuelekea kwenye ngazi, nikaanza kutembea kwa haraka, ila kabla sijaufungua nikaisikia sauti ya mnong’ono, ikanibidi nitege siko langu vizuri.

“Pandeni haraka haraka, mimi nina mzuga tu, hakikisheni hamufanyi makosa ya kipuuzi. Hakikisheni munamuua sawa”

Nikahisi kuishiwa nguvu za mwili, kwani maneno haya yanazungumzwa na dokta Clara, mtu ambaye nilimuamini kutokana na kuaminiwa na mume wangu kipenzi Eddazaria. Nikatamani kwenda kumfwata kwenye kona aliyo jibanza, ila nikashindwa mara baada ya kumkumbuka mdogo wangu Judy na kutambua kwamba hayupo kwenye mikono salama. Nikaufungua mlango huu taratibu kisha nikaufunga taratibu pasipo kutoa mlio wa aina yoyote. Nikachungulia chini kwenye ngazi ili niweze kuona kama kuna watu watakuwa wanapandisha, ila ukimya uliopo ukanishiria kwamba watu hao wanao nitafuta wametumie lifti kupanda huku gorofani.

Nikaanza kushuka kwa haraka, cha kushukuru zaidi Mungu ni raba zangu hizi nilizo zivaa, kwani ni nyepesi, na hazitoo mlio wa kishindo hata pale ninapokuwa nimekanyaga mahali ninapo pita. Nikafanikiwa kufika eneo la maegesho ya magari nikaingia ndani ya gari la Clara, nikaanza kuliendesha kwa kasi kutoka chini ya ardhi ambapo kuna haya maegesho ya magari ya wafanyakazi maalimu waliomo ndani ya hili gorofa.

Nikafika eneo la yalipo egeshwa magari ya watu hawa walio kuja kuniletea fujo, nikasimamisha gari na nikashuka, nikatazama matairi ya magari haya nikatamani kuyatoboa ila kwa bahati mbaya sina kisu. Nikarudi ndani ya gari, nikaliendesha gadi getini, walinzi wakanifungulia geti nikatoa gari hadi barabarani, kisha nikashuka na kupunga mkono. Hazikuisha hata dakika moja, nikaiona taksi ya Kimaro ikitokea kwenye moja ya uchochoro wenye giza. Macho yangu yote yapo kwenye magari mawili ya watu wanao nitafuta. Kimaro akasimamisha gari lake pembeni ya hili gari.

“Judy shuka”

Nilizungumza huku nikitoa kibunda cha dola mia mia zilizo fungwa vizuri. Nikamkabidhi Kimaro pasipo hata kukihesabu. Kimaro macho yakamtoka, kigugumizi kikampata.

“Mwajuma upo nasi au unabaki?”

“Hata sijielewi mimi naona raha raha tu kupanda magari”

Nikaoa kibunda kingine nikachomoa noti kumi za dola mia na kukabidhi.

“Ujitunze”

“Sawa dada asante”

Nikawaona watu wale walio valia suti nyeusi wakikimbilia katika magari yao.

“Ondokeni haraka sana Kimaro, wale watu wanifwatilia mimi”

“Sasa sister?”

Kimaro alizungumza huku akiwasha gari lake na kuondoka katika eneo hili kwa mwendo wa kasi. Nikaingia ndani ya gari ambalo nimelicha likiwa linawaka, kwa kasi ya ajabu nikaanza kuondoka katika eneo hili la Morroco zilipo hizi ofisi zetu

“Ni kina nani wale dada?”

Judy aliuliza huku akitazama nyuma.

“Ni watu wa Clara”

“Clara!!?”

“Ndio mdogo wangu”

Nilimjibu Judy huku nikiongeza mwendo kasi wa gari hili. Nikaanza kuziona gari hizo zikinifwata nyuma kwa mwendo wa kasi sana jambo lililo zidi kunipa wasiwasi.

“Sasa wanataka nini kwako?”

“Roho. Roho yangu mdogo wangu”

Nilizungumza huku machozi yakinilenge lenga kwa maana nilimsikia Clara kwa masikio yangu yote mawili. Mabadiliko aliyo yafanya kwenye ofisi yangu nayo yananizidi kunidhibitishia kwamba sasa Clara amedhamiria kunipokonya kampuni yangu na ninahisi ni mtu ambaye atakuwa na mtandao mkubwa kwa sasa ambao anatumia kuniangamiza taratibu. Judy machozi yakaanza kumwagika usoni mwake.

“Hata nikifa leo Judy hakikisha kwamba unamuangalia mwanangu, yule ndio ndugu yako, yule ndio mwanao wa pekee sasa sawa”

“No usiongee hivyo Jojo”

“Hakuna jinsi mdogo wangu, kila kona ninawindwa. Nitaishi wapi mimi, nitakaaje na amani mimi?”

Niliendelea kuzungumza kwa hasira huku nikijitahidi kardi ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba ninaendesga gari hili kwa mwendo wa haraka sana. Simu maalumu iliyomo ndani ya gari hili ikaanza kuita. Nikaitazama kisha nikaminya kitufe maalumu na kuipokea kisha nikaiweka loud speaker.

“Jojo unahisi kwamba utatoka hai ndani jiji hili la Dar es Salaam?”

Niliisikia sauti ya Clara akizungumza huku akicheka.

“Clara, naamini unacho kifanya hujashawishiwa na mtu na umekusudia. Sasa ngoja nikuambie jambo moja endapo ikatokea nikatoka hai katika kifo hichi nakuahidi kwamba, nitakuua kifo ambacho sidhani kama kuna mtu alisha wahi kuuwawa”

Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nikipunguza mwendo kasi wa gari, kwani kwa mbele kuna lori kubwa linakatika zarabara jambo lililo sababisha kukosa upenyo wa kupita. Cha kushangaza zaidi lori hilo kikasimama na kutuzuia kabisa, kitu kilicho nifanya nijawe na wasiwasi mwingi sana kwani gari mbili za watu walio tumwa na Clara wakizidi kutusogelea kwa ukaribu sana.


Nikafunga breki za gafla huku nikirifikia ni nini cha kufanya. Magari yanayo tufukuzia yakasimama mita chache kutoka gari letu lilipo. Wakashuka watu hao wakiwa na bunduki.

“Tutafanyaje dada?”

Judy aliniuliza huku akiwa anaweweseka sana. Tukashuhudia dereva wa roli hiyo akishuka huku akiwa amevaa kinyago kilicho ificha sura yake huku akiwa akiwa amebeba bunduki kubwa mkononi mwake.

“Tunakufa dada”

Nikapata kigugumizi kwani macho ya mtu huyo yote yapo kwetu. Nikamuinamisha chini Judy hata kama basi mtu huyo akiamua kutushambilia basi mimi niwe wa kwanza kufa kabla ya mdogo wangu. Mtu huyo akaanza kuwashambulia watu wa Clara jambo lililo nishangaza sana. Nikaanza kuona jinsi watu wa Clara wanavyo changanyikiwa huku wengine wakikimbilia kwenye magari walio kuja nayo. Mwanaume huyu aliye valia nguo nyeusi pamoja na jaketi la kuzuia risasi(Bullet proof) akazidi kuwashambulia watu hao huku akisimama pembeni ya gari letu. Kwa ishara akaniomba niweze kufungua mlango wa upande wangu. Kwa mara ya kwanza nikajifikiria kwa sekunde kama hamsini huku nikiwa ninamtathimini.

Akaendelea kuniomba kwa ishara nifungue mlango wa gari huku akizidi kuhakikisha anawamaliza watu wa Clara. Nikaminya batani na ya kuruhusu loki za milango kufunguka, akafungua mlango na kwa ishara akaniomba niweze kukaa siti ya nyuma. Nikafungua mkanda wa gari hili na kukaa siti ya nyuma, akaitupa bunduki yake chini kisha akakaa kwenye siti yangu na kufunga mlango kwa nguvu.

Akalirudisha gari nyuma kwa hadi likagonga magari ya watu wa Clara ambao wengi wao wamefariki dunia. Akaliweka gari sawa na tukaondoka eneo hili kwa kasi kubwa sana. Judy taratibu akanyanyuka na kumtazama mtu huyu na kuanza kupiga kelelea.

“Judy, Judy nipo hapa”

Ilinibidi nizungumze huku nikimshika mdogo wangu kwa maana anahisi kwamba mtu huyu aliye tusaidia ameamua kumteka.

“Ni nani huyu?”

Judy aliuliza huku macho yakiwa yamemtoka.

“Ametusaidia”

“Ametusaidia, unamjua?”

“Hapana ila tulia”

Nilizungumza huku nikimtazama mwanaume huyu jinsi anavyo endelea kuendesha gari hili kwa mwendo wa kasi.

“Samahani wewe ni nani?”

Mwanaume huyu akanigeukia na kunitazama tu kisha hakunijibu kitu cha ina yoyote zaidi ya kuendelea kuendesha gari hili. Nikatamani kumvua kinyago chake ila wasiwasi mkubwa ukanifanya nishindwe kufanya hivyo kabisa.

Tukapita mkoa wa Pwani, tukaingia kwenye barabara iendayo kwenye mikono ya Tanga, Arusha. Akasimamisha gari kwenye njia panda ya eneo hili, kisha akafungua mlango wa gari hili na kushuka. Kutokana kumesha anza kupambazuka, mazingira ya hapa yanaonekana vizuri, nikashuka kwenye gari na kumtazama. Akainamisha kichwa chake kidogo chini kwa ishara ya kuniheshimu kisha kwa ishara ya mikono akaniomba niendelee na safari huku akinionyeshea barabara ya kuelekea mkoani Tanga.

“Samahani wewe ni nani?”

Akatingisha kichwa kisha akaanza kutembea hadi kwenye moja ya kibanda kilichopo pembezoni mwa barabara, akafunua moja turubai na nikaishuhudia pikipiki kubwa yenye rangi nyeusi. Kwa haraka nikakimbilia hadi sehemu alipo.

“Samahani naomba niweze kukufahamu wewe ni nani?”

Mwanaume huyu akaingiza mkono wake mfukoni na kutoa kijiherufi kilicho undwa kwa mfumo wa herufi Z. Akawasha pikikipi yake yenye mlio mkubwa kisha akaondoka katika eneo hili na kurudi katika njia tuliyo tokea. Nikamsindikiza kwa macho mtu huyo hadi akapotelea, nikageuka nyuma na kumkuta Judy akiwa amesimama nje ya gari huku akinitazama.

“Amekuambia ni nani?”

“Hapana, ila ameniachia herufi hii Z”

Nilizungumza huku nikiingia ndani ya gari. Nikaichomoa tisheti yangu na kuvitoa vibunda vya pesa ambavyo nilikuwa nimevizokomeza ndani ya tisheti yangu. Nikawasha gari na taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili.

“Tunaelekea wapi?”

“Tanga, Dar kwa sasa kwa upande wetu imesha chafuka”

Nilizungumza huku nikiangalia kijialama hichi za herufi ya Z nilicho kabidhiwa na mtu ambaye simfahamu na sijui ni kwa nini ameamua kunisaidia. Tukazidi kusonga mbele, Judy akapitiwa na usingizi, japo hata mimi nina uchomvu mwingi ila sikuhitaji kusimama njiani hadi pale nitakapo fika mkoani Tanga. Chakumshukuru mwenyezi Mungu sikusimamisha njiani, hadi nikafika jijini Tanga, kutokana nilisha wahi kufika huku sikuwa na wasiwasi mwingi sana. Moja kwa moja nikaelekea hadi nyumbani kwa mama mkwe. Nikasimamisha gari nje ya geti kwa maana nimekuta utulivu mkubwa sana.

“Judy, Judy”

“Mmmmm”

Judy akafumbua macho yake huku akipiga miyayo ya uchovu, akaanza kutazama tazama eneo hili.

“Huku ni wapi?”

“Kwa mama”

“Mama gani?”

“Mama mkwe, hapa ndipo nyumbani kwake, tumesha fika Tanga”

“Huku ndio Tanga?”

“Ehee”

Nikafungua mlango na kushuka kwenye gari, nikapiga hatua hadi getini. Nikaminya kitupe cha kengengele ambayo inaweza kumuashiria mtu aliyomo ndani kugundua kwamba getini kwamba kuna mtu.

“Nani?”

Niliisikia sauti ya wifi akiniuliza.

“Mimi”

  ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG