Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 8/10

 

 


 MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE)

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 8 KATI YA 10

 


“Salama habari yako”

“Nina habari njema, nimeweza kumpata mwanao na watu wote ambao uliniagiza kwamba niweze kuwaua nimewaua”

“Apia Adrus”

“Haki ya Mungu dini yangu Muislam”

Eddy akajikuta akishangilia na kusahau kwamba yupo katikati ya kipindi kingine ambacho ni kigumu. Viongozi wote wakabakiw akimkodolea macho akiwemo Rahab.

“Mupo wapi kwa sasa ?”

“Ndio tupo kwenye harakati za kuondoka nchini Madagacar”

“Basi moja kwa moja njooni Tanzania sawa”

“Sawa muheshimiwa”

“Kazi nzuri na ninashukuru sana”

“Ni jikumu langu muheshimiwa makamu wa raisi”

“Basi mukifika tu muwasiliane nami”

“Sawa muheshimiwa”

Simu ikakatwa na kumfanya Eddy kumfumba macho yake kwa sekunde kadha na kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kile alicho weza kukifanya kwa muda huu.

“Eddy kuna nini kinacho endelea?”

Raoso Rahab ilimbidi aulize kwa shahuku kubawa ya kuhitaji kuweza kufahamu ni kitu gani ambacho kimetokea kwa makamu wake hadi ajawe na furaha kubwa sana.

“Mwanangu amepatika”

“Kweli ni nani ameifanya kazi hiyo?”

“Adrus”

“Ohoo asante Mungu. Haya jamani kazi iendelee”

Rahab naye alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana. Furaha ikakatika mara baada ya kuanza kuhushudia vijana helicopter moja ya polisi ikilipuka, hata kabla hawajakaa sawa wakashuhudia helicoptwe nyingine ambayo si ya Tanzania ikiwa usawa wa gorofa la Tanesco kwa juu, wakaanza kushusha watu wengi kwa kutumia kamba ndefu.

“Ni kina nan…..”

Hata kabla Rahab hajauliza swali hilo, tv zote mbili zitatawala chenga chenga jambo lilio wafanya wote wamtazame kijana waliye naye ndani humo.

“Kumetokea nini?”

“Mawasiliano yote ya satelaiti yamekatika?”

“Nini?”

Eddy aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

***

“Wamesha fika”

Livna alizungumza huku akikata simu aliyo pigiwa na vijana wake. Wakakimbilia hadi kwenye lifti, wakafungua na kuingia ndani. Lifti ikawapeleka hadi gorofa la mwisho. Wakatoka na kukimgilia juu kabisa ya gorofa hilo na kuwakuta vijana wake wapatao sita wakijibu mashambulizi yanayo toka kwa askari walipo kwenye helicopter ya pili ambayo kwa ndani yake yupo bwana Mabula.

“Acheni kushambulia”

Bwana Mabula alizungumza kwa ukali na vijana wake wakatii amri hiyo. Macho ya K2 yakakutana na bwana Mabula ambaye yupo kwa mbali kodogo.

“Twendeni twendeni”

Livna alizungumza huku akikimbilia kwenye helicoptwe hiyo. Wakaingia ndani ya helicopter hiyo wakiwa na bwana K2 taratibu wakaanza kuondoka katika jengo hilo na kuwaacha askari walipo chini kushangaa tu.

“Muheshimiwa kwa nini umetukataza?”

“Ehee?”

“Kwa nini umetukataza tusiwashambulie”

Kijana mmoja alizuliza kwa sauti ya ukali sana huku akimtazama bwana Mabula usoni mwake.

“Sio muda wa kuulizana maswali sawa”

“Nina haki ya kuuliza maswali ka maana maadui wametoroka mbele yetu na huonyeshi dalili ya kusema tuwafukuzie au tufanyaje”

Kijana huyo mwenye asili ya kikuria alizungumza kwa hasira kali sana huku akimshika shati bwana Mabula na kuuanza kumlaza chini. Askari walio salia ikawabidi kuanza kuuamua ugomvi huo kwani wapo angani kwenye helicopter na endapo watafanya ujinga wa ina yoyote basi wanaweza helicopter hiyo kuanguka chini.

“Unamfahamu yule?”

Livna alizungumz ahuku akimtazama K2 usoni mwake.

“Yaa nina mfahamu ndio maana vijana wake wakashindwa kunishambulia”

“Alikuwa nani yako?”

“Mpenzi wangu, nashukuru kwa msaada wenu ila ninaombi moja”

“Ombi gani?”

“Nahitaji kumuua raisi na makamu wake, vifo vyao vitaweza kutupa sisi nafasi nzuri ambayo sisi na nyinyi tunaweza kuwa pamoja kwa miaka mingi na musipate buguzi ya aina yoyote.”

Livna kaka kimya kwa muda huku akiwatazama vijana wake usoni mwake.

“Nashukuru kwa kuweza kuja kutuokoa”

“Ni jukumu letu, ila muheshimiwa tuna habari njema”

“Habari gani?”

“LIZZY bado yupo hai ila ameshikiliwa nyumbani kwa makamu wa raisi”

“Muna uhakika na munacho kizungumza?”

“Ndio muheshimiwa”

“Munapafahamu nyumbani kwa makamu wa raisi?”

“Ndio”

“Geuzeni helicopter tunaelekea nyumbani kwa makamu wa raisi, siwezi kuondoka Tanzanai na kumuacha Lizzy nyuma”

Livna Livba alizungumza kwa msisitozo na kuwafanya vijana wake kujiweka tayari kwa kazi nyingine wanayo kwenda kuifanya huku K2 akijawa na mshangao mkubwa sana, kwani alijua hiyo ndio nafasi ya pekee ya yeye kutoroka nchini Tanzania na hio ndio ingekuwa nafasi yake ya pekee ya kwenda kujipanga kivingine kwa ajili ya kuja Tanzania kuhakikisha kwmaba wana ingia madarakani yeye na kaka yake.



“Livna ninahisi hili sio wazo zuri kwa sasa, utakwenda kupoteza vijana wako bure na utashindwa kutimiza malengo yako. Kwa maana hivi sasa lazima kila mlinzi jicho lake lipo makini kuhakikisha kwamba wanalinda kile walicho pewa jukumu la kukilinda”

K2 alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Livna usoni mwake.

“Kumbuka mimi ndio nilikuja kurusha karata yanug ya mwisho kuja kukuokoa pale ambapo ulokuwa umesha ingizwa kwenye kumi na nane na jeshi, so nakuomba tukajipange kivingine, baada ya hapo tutakuja kuhakikisha kwamba tunafanya shambulizi lenye nguvu. Fikiri hilo, usipoteze damu zaidi, na kama ndio huyo kijana wako kuna mipango na mbinu nyingine ambazo unaweza kuzifanya kuhakikisha kwamba unamuokoa”

Livna akakaa kimya huku akijifikiria, akakumbuka jinsi vijana wake walivyo jitolea maisha ya ajili yake, taratibu akashusha pumzi na kumtazama K2 usoni mwake.

“Nimekuelewa dada. Turudini kambini”

“Sawa mkuu”

Taratibu rubani anaye iendesha helicoptwe hiyo akaiigeuza taratibu na safari ya kuelekea katika makao makuu ya kikosi chake ikaanza.

***

“Huku tunapo elekea nitakuja kujiudhuru madaraka yangu”

Raisi Dustan alizungumza huku akiwa amechoka sana, akajbwaga kwenye sofa lililopo ndani ya ofisi yake, kwani mauaji ya vijana wake alio watuma nchini Madagascar ni pigo jengine tena kwake na taifa zima.

“Muheshimiwa ila vijana hawa tunatakiwa tuweze kuwatafuta kama Magaidi sasa wa kimataifa?”

“Hembu tuachane nao kwanza, mtoto wangu hadi sasa hivi sijui ni wapi alipo, sijui anafanywa nini, sijui anakula nini, unataka kuniambia kwamba niendelee kumtafuta tu Adrus, yeye ni nani, nina wanajeshi na makomandoo wangapi ndani ya nchi yangu?”

Raisi Dustan alizungumza kwa uchungu sana, kwani kila mpango ambapo amejaribu kuupanga kwenye maisha yake umekwenda vibaya.

“Sisi ni taifa kubwa, hatuwezi kutegemea mtu wa taifa dogo kama Tanzania, kitu cha kufanya, nahitaji kuwaona vijana wangu, nina imani hii kazi wataweza kuifanya vizuri kama ninavyo hitaji mimi mwenyewe”

“Ni kina nani hao?”

“Niandalie msafara wangu, nahitaji kutoka muda huu”

“Muda huu muheshimiwa, mbona ni usiku sana?”

“Ndio nahitaji kutoka muda huu”

“Sawa muheshimiwa”

Maandalizi ya msafara wa Raisi Dustan kwa majira haya ya saa tisa uskiku yakawashangaza hadi walinzi wake, ila kutokana mkuu wao ndio ameamua hawakuwa na budi ya kufwata maelekezo yake. Safari ya kuelekea katika eneo Mclean Garden ikaanza. Gari zipatazo kumi pamoja na pikipiki nne zikaliweka katikati gari la raisi Dustan, msafara huo ukafika katika jengo liitwalo Vaughn Mc Lean. Walinzi wake wa kikosi cha secrety servise, wakashuka na kuanza kuimarisha ulinzi katika kila eneo, walipo hakikusha kwamba usalama upo wa kutosha katika magorofa hayo, raisi Dustan akashusha kwenye gari na moja kwa moja akaeleke hadi kwenye moja ya mlango wa hilo gorofa.

“Nisubirini hapa”

“Muheshimiwa jukumu letu ni kululinda popote uendapo”

Mlinzi wake wa karibu alizungumza huku akimtazama raisi Dustan usoni mwake.

“Nimekuambia kwamba munisubiri hapa sawa”

“Sawa muheshimiwa”

“Naomba bastola”

Mlinzi wa raisi Dustan akachomoa bastola yake moja kiunoni na kumkabidhi raisi Dustan.

“Nitakaa dakika kumi mara baada ya dakika kumi munifwate”

“Sawa muheshimiwa”

Raisi Dustan akafungua mlango huo, akatembea hatua chache hadi kwenye mlango mwengine ulio kuwa kushoto kwake, akatazama huku na kule, alipo hakikisha hakuna mtu, akatoa funguo ndogo na kufungua mlango huo. Akaingia ndani na kufunga kwa funguo, akaanza kushuka ngazi zilizo elekea chini ya ardhi. Akazidi kusonga mbele kwenye kordo nyembamba nyenye taa mbili. Akasimama kwenye mlango wa chuma, akatazama kamera iliyopo juu ya eneo hilo, huku pembeni ya mlango kukiwa na kiboksi kidogo kilicho jaa batani za zenye namba. Akaminnya batani kadhaa na mlango huo ukafunguka, akaingia ndani na kukutana na wauame wawili walio simama wima huku nyoso zao zikiwa zimejaa ndevu nyingi sana, na wanaonekana wanamsubiria kwa hamu sana.

***

“Tumewapoteza waheshimiwa”

Sauti ya bwana Mabula ilisikika vizuri katika masikio ya kila mtu aliyo ndani ya ukumbi wa mkutano katika ikulu ya Tanzania. Eddy akawatazama viongozi hawa wa vitengo mbalimbali vya kijeshi.

“Kinacho takiwa kufanyika hivi sasa, hakikisheni kwamba ulinzi unaimarika katika kila eneo.”

“Sawa mkuu”

“Na kitu kingine cha ziada, andaeni mazishi ya vijana wote walio poteza maisha yao kila familia ya mfiwa itakabidhiwa milioni kumi kumi, hilo zoezi ninaomba liendek ikamilifu, na lisimamiwe kikamilifu, isije ikatokea idada ya maiti ambazo hazipo, naamini munafahamu ni nini amacho nina kimaanisha”

Raisi Rahab alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama viongozi hao walio izunga meza hiyo kubwa.

“Sawa mkuu”

“Makamu una kitu cha kuongezea?”

“Cha kuongezea hapo tuhakikishe kwamba tunakuwa zaidi ya makini, kwa mana maadui zetu wapo kila mahali, anahitaji kutuvuruga, wanahitaji kutuangusha na utawala huu, nahitaji uwe ni utawala wa amani na usiwe kama utawala ulio pita wa baba yangu Mzee Godwin. Ninacho watakia hivi sasa ni utendaji na uwajibikaji mwema na niwatakie asubihi njema”

“Shukrani”

“Kuna mwenye maoni?”

Viongozi wote wakatazamana, hapakua na aliye nyoosha mkono wake.

“Basi nami nitawakie asubuhi njema”

Raisi Rahab mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akasimama, na kuwafanya viongozi wengine wote kusimama na kumpigia saluti. Rahab akaanza kukisukuma kiti cha Eddy taratibu.

“Unaonaje leo ukalala hapa ikulu”

“Mmmmm”

“Yaa, unalala na mimi huku tukiwa na maandalizi ya kuandaa walinzi wapya”

Rahab alizugumza kwa sauti ya chini sana huku akiendelea kukisukuma kiti hicho cha Eddy kuelekea sebleni kwake.

“Sawa”

“Umekubali ulale chumbani kwangu”

“Yaa ila tuna lala bila kufanya chochote”

“Hahahaa kwenda zako huko”

“Nini sasa”

“Wewe huyo”

“Ndio mimi huyo, au unatakaje?”

“Mmmmm haya bwana”

Wakafika sebleni, Rahab akawaruhusu walinzi wake waende kupumzika kwani wameshinda usiku kucha pasipo ya kupata hata mapumziko.

“Jane subiri mara moja”

Rahab alimzuia sekretari wake wambae naye alianza kuondoka.

“Ndio madam”

“Yule mjinga hakikisha kwamba anapatiwa chakula kama kawaida, nikiamka nitakuja kumuona”

“Sawa muheshimiwa”

“Pia kesho utaniandalia hutoba ambayo niahitaji kuzungumza na wanachi”

“Sawa, itahusiana na nini?”

“Tukio la leo, na mambo ya ulinzi”

“Sawa muheshimiwa, ngoja nikaiandae muda huu”

“No kichwa chako kimechoka, watangazie kesho kwamba muda wa kuingia ofisi utakuwa ni saa nne asubihi na si saa moja”

“Sawa muheshimiwa”

Jane akaondoka na kuwaacha Eddy na Rahab.

“Nikuandalie kinywaji?”

“Hapana nipo vizuri”

“Nahitaji tunywe hata mvinyo kidogo tuchangamshe kichwa”

“Tutakunywa siku nyingine, kesho nahitaji kwenda kumpokea mwanangu”

“Atafika, ila huyu kijana inabidi tumpatie japo kitengo”

“Kitengo cha nini?”

“Chochote akiongoze japo kidogo”

“Hapana bado ni mapema sana”

“Kwa nini unazunumza hivyo ikiwa amefanya kazi nzuri ya kumuokoa mtoto wako?”

“Tukumbuke kwamba bado Marekani wana hasira nasi, mbili wanamtafuta sasa endapo tunampatia mamlaka au madaraka ya eneo lolote katika hii serikali. Moja kwa moja tutachukuliwa vibaya mataifa mengine yanayo tuzunguka”

“Sawa baba nimekuelewa twende chumbani”

Rahab akaanza kukisukuma kiti hicho alicho kikalia Eddy ndani kwake. Eddy taratibu akajikaza na kunyanyuka. Akaanza kuvua nguo moja baada ya nyingine alipo bakiwa na boksa tu akapanda kitandani.

“Bado kidonda kinauma?”

“Yaa kinauma kiasi”

“Pole mwaya”

Rahab alizungumza huku naye akivua nguo zake, akabaki kama alivyo zaliwa na kuingia bafuni kujimwagia maji huku akilini mwake, akiwazia penzi atakalo pewa usiku kucha na makamu wake wa raisi Eddy Godwin.

***

Hadi inafika majira ya saa mbili asubihi, mlango wa chumba cha ambacho dokta Ranjiti na familia yake wamo haujafunguliwa jambo ambalo kwao ni ngeni kidogo kwani walisha zoea kumuona bosi wao akitoka alfajiri na mapema na kueleka katika ukumbi mkubwa wa Gym ulipo katika hoteli hiyo.

“Vipi leo?”

Mlinzi mmoja aliuliza hukua kimwatazama wezake wanne walio simama nje ya mlango huo.

“Hatujajua, jana nahisi alichelewa kulala”

“Ila si kawaida yake, ninamfahamu vizuri mkuu John”

“Tuangalie angalie itakavyo kuwa, labda haitaji kwenda kufanya mazoezi kwa leo”

“Ngoja nijaribu kumpigia simu labda atakuwa amejisahau”

Mlinzi huyo alizungumza huku akianza kuitafuta namba ya simu ya bosi wake alipo iona taratibu akaipiga na kuiweka simua yeke hiyo sikioni mwake. Kwa bahati mbaya akakuta simu ikiwa haipatikani.

“Hapatikani”

“Kalala kwa maana ameanza mahusiano na binti wa mzee”

“Weee”

“Yaa wana mahisiano ya kimapenzi kwa sasa”

“Basi sijalijua hilo”

Wakandelea kulinda katika eneo la mango huo wakiamini kwamba hakuna mtu yoyote ambaye anaweza kuingia. Baada ya dakika arubaini, akafika sekretari wa kikosi hicho cha D.F.E. Wakasalimiaana na mzee huyo machari sana katuka kuzungumza.

“Nahitaji kuzungumza na mkuu”

“Amelala”

“Hadi muda huu?”

“Ndio, na simu yake amezima”

“Ndio maana nikimpigia huwa hapatikani, so aliwapa taarifa kwamba haitaji usumbufu?”

“Hapana hatatupa”

“Hajawapa?”

“Ndio”

“Na dokta Ranjiti je?”

“Hatujampigia”

“Hembu mpigieni simu ya humo ndani”

Sekretari huyo akawatajia namba hiyo ya simu ya mezani iliyomo ndani humo, wakaipiga zaidi ya mara tano haikupokelewa na hapo ndipo wakaanza kupata wasiwasi.

“Fungueni mlango”

Mzee huyo aliwaamuru, mlinzi mmoja akatoa kadi yake mfikoni na kufungua mlango huo unao tumia kadi katika kufunguliwa. Wote hawakuamini kukuta maiti ya Anna ikiwa imelala sakafuni huku ikiwa imeanza kuvimba, kila mmoja akachomoa bastola yake, wakakimbilia chumbani kwa John na kumkuta amelala chini, huku akiwa kimya, walinzi wengine wawilio wakio ingia chumbani kwa dokta Ranjiti hawakuamini kukuta mzee huyo akiwa emakufa huku mwili wake nao ukiwa umesha vimba.

“Mkuu mkuu”

Sekretari huyo aliita hukua kimtingisha John. John akafumbua macho yake kwa haraka akaka kitako.

“Mkuu ni nini kimetokea.”

“Pesa, zuieni pesaa”

“Pesa gani?”

“Kuna magaidi wamendoka na pesa zangu”

“Mungu wangu”

“Wee lete simu yako”

Sekretari huyo akatoa simu yake na kumakabidhi John, kwa haraka akaingia kwenye akaunti ya kikosi chake cha D.F.E, akakuta pesa aliyo iidhinisha jana ikiwa imetolewa cha kushangaza akakuta pesa nyingine zaidi ya dola mia mbili na tisina na tisa zikiwa hazipo, na akaunti hiyo inayo changiwa na wanachama wapatoa elfu moja kutoka duniani kote, imebaki na dola sifuni nukta sifuri sifuri, jambo lililo mfanya John azidi kuchanganyikiwa kwani anacho kikumbuka yeye ni kwamba ameidhinisha kutoa dola bilioni moja tu na si pesa zote kwenye akaunti hiyo.



“Mkuu”

“Niacheeee”

John alizungumza kwa hasira huku mikono yote ikimcheza, jasho likazidi kumwagika usoni mwake. John akatoka chumbanihumo akazidi kupata pigo mara baada ya kumuona Anna akiwa amelala chini huku ameuwawa.

“Eddy, Eddy sasa umevuka mpaka, nilazima nikuue”

John alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, na alicho kizungumza amekidhamiria kabisa kutoka moyoni mwake.

***

“Adrus pesa imeidhibitisha kuingia kwenye akaunti yako?”

Lee Ji alizungumza huku akimtazama Adrus wakiwa ndani ya boti hiyo inayo endeshwa na Jing kwa mwendo wa kasi sana.

“Ndio”

“Hembu naomba unitajie akaunti yako”

“Kwa nini akanti yangu?”

“Kuna kitu nahitaji kukifanya”

Adrus akaanza kuitaja namba ya akanti yake hiyo iliyopo nchini Uingereza, Lee Ji akaiingiaza namba hiyo kwenye program yake moja katika laptop yake ambayo hutumika katika kuhamisha pesa kwa njia ya wizi kutoka akaunti moja kwenda nyingine.

“Utanataka kufanyaje?”

“Nataka niangalie akauntia ambayo imekuingizia pesa ina kiasi gani”

“Ukifahamu?”

“Ninawaibia pesa zao zote”

“Kumbe inawezekana?”

“Yaa inawezekana”

“Hembu”

Lee Ji akaanza kutafuta namba ya siri ya akaunti ya D.F.E, alipo hakikisha ameipata, akaidhinisha pesa zote zilizo salia katika akauti hiyo, akazihamishia kwenye akauti ya siri iliyopo nchini China, na ahakunti hiyo haionyeshi imetokea kwenye benki gani.

“Waoooo done”

“Unataka kuanimbia kwamba pesa hizo zote zimehamia kwenye hiyo akaunti yako?”

“Ndio nimeziamisha hapa ni laizma walie wenye akaunti yao. Ngoja nikuongezee dola bilioni tatno”

“Duuu”

“Au hutaki?”

“Haaa, sitaki ndio nini, yaani sifanyi kazi za kijinga kama hiz tena, baada ya kumkabidhi huyu mtoto kwa baba yake, ninapotea Tanzania, ninaondoka na mama yangu”

“Inabidi uhakikishe kwamba unakwenda sehemu ambayo Wamrekani hawato weza kukukamata”

“Hilo wala usijali, najua jinsi ya kujiepusha nao”

“Sawa, nakuaminia, hapa nataka nifanye mgao, wewe bilioni tano, Jing Lee naye bilioni tano na Cookie naye bilioni tano”

“Nashukuru sana”

Lee Ji akamuingizia Adrus kiasi hicho cha pesa, kisha aakelekea katika chumba ambacho yupo Jing, Cookie pamoja na mtoto. Akawaelezea jinsi alivyo weza kuiba pesa hizo.

“Una uhakika hawato tutafuta?”

Cookie aliuliza kwa mshangao huku akomtazama Lee Ji usoni mwake kwani haamini kwamba anakwenda kuwa tajiri mkubwa sana.

“Hawato weza kututafuta kwa manaa hizo pesa ninaziamisha kutoka kwenye akaunti yangu mimi ambayo ni ya siri sana, hadi waje kuitafuta na kuipata itawachukua zaidi ya miaka kumi. Sasa miaka kumi hiyo sijabadilisha kweli maisha yangu na kujitengenezea ngome yenye nguvu sana”

“Sawa, mama”

Akaanza Cookie kutaja akaunti yake ya pesa iliyopo inchini Sweden. Jing naye akataja akaunti yake ya pesa iliyopo nchini China, akaingiziwa kiasi chake cha pesa na wakaendelea na safari yao. Kuelekea nchini Tanzania huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha kubwa na kuwazia ni kitu gani ambacho atakifanya baada ya kuwa na kiasi hicho kikubwa cha pesa.

***

Raisi Rahab akatoka bafuni huku mwili mzima ukiwa unamwagika maji, hakuona hata haja ya kujifuta maji hayo kwa taulo, taratibu akatembea kwa mapozi hadi kitandani huku wakitazamana na Eddy.

“Umbo lako haliishi mvuto”

Eddy aluzungumza huku akimshika mkono Rahab, akamvutia kitandani na akamlaza kifuani mwake.

“Mwili wangu mzuri, hauzeeki mapema”

Taratibu Rahab akaanza kuzinyonya lipsi za Eddy, msisimko wa mapenzi ukaaanza kuawala kati kati yao, Eddy akakishika kiuno cha Rahab na kuanza kukitomasa taratibu.

“Aii..ssii…aa…”

Rahab alilalama huku akikiminya minnya kifua cha Eddy.

“Unajisikiaje?”

“Mmmm?”

“Unajisikiaje?

“Jamani Eddy hilo ni swali gani, unahisi ninajisikiaje?”

“Numekuuliza tu”

“Mmmmm najisikia raha”

Taraibu Rahab akaivua boksa ya Eddy.

“Ngoja”

Eddy alizungumza na kumfanya Rahab kusitisha zoezi hilo.

“Vipi baby”

“Tusifanye”

“Hee, kwa nini?”

“Tusifanye chochote tafadhali”

Eddy alizungumza huku akianza kupandisha boksta yake taratibu.

“Jamani Eddy mbona hivyo?”

“Unajua ni nni?”

“Sijui, ningejua ningesema?”

Rahab alizungumza huku akiwa amenuna na kujilaza pembeni ya Eddy.

“Najua hichi tunacho kifanya sio kitu sahihi, nimegundua siri moja ambayo inaniletea matatizo mengi kwenye familia yangu”

“Ni siri gani?”

“Pesa ninanyo, maisha mazuri ninayo toka nikiwa mtoto, kitu kikubwa kinacho leta mamatizo haya ni umalaya. Umalaya wangu ndio unanipoza katika mambo mengi, leo hii Phidya na Shamssa wasinge kuwa maadui kama si uadui, leo hii nisinge kuwa hapa kitandani kwako, kama sio umalaya. Natakiwa kubadilika sasa, natakiwa kukua kiakili, kama ni umri nimesha kua tu”

Eddy alizungumza kwa upole ila kwa msisitizo ulio mfanya Rahab kukaa kimya kwa muda.

“Sisi ni viongozi sasa, kwa nini serikali yetu inakubwa na matukio makubwa na mengi yanayo poteza vijana na nguvu kazi ya taifa? Tumeweka mambo yetu binafsi mbele Rahab, haya madaraka hayakuja kama chafya, tulipanga, tukapambana na tukamng’oa aliye kuwa ameyashikilia haya madaraka. Wananchi wanatarajia kupata vitu vizuri kutoka kwetu, kama pesa tunazo Rahab, ni nini ambacho tunakihitaji?”

Rahab akazidi kukaa kimya.

“Nahitaji sasa tuijenge Tanzania yetu, tusiendekeze kutomb** ikia nchi inatetereka kila siku, ipo siku tutakuja kudaiwa huko mbinguni na kuulizwa tulivyo kuwa viongozi tuliwafanyia nini Watanzania.”

Rahab akashusha pumzi nyingi, akavuta shuka taratibu na kujifunika.

“Nimekuelewa, tulale, kwa maana ninaona hata kupeana raha inategemea na kuwatumia wananchi, sawa bwana”

Rahab alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwke.

“Laiti mume wangu angekuwa hai, wala yasinge pata tabu kama hii Eddy unanionea, uninionea kweli”

Maneno ya Rahab yakamfanya Eddy kukaa kimya kwa muda kisha kwa nguvu akalivuta shuka alilo jifunika Rahab na kulitupia pembeni, akaipanua miguu yake, akaanza kuyanyonya kitumbua cha Rahab na kumfanya Rahab kuendelea kutoa miguno ya kimahaba.

***

“Umefwata nini?”

Watu hao walio walimuuliza Raisi Dustana mara ya kuingia katika chumba hicho.

“Nina kazi ambayo ninahitaji kuwapatia?”

“Zungumza”

“Mwanangu ametekwa, ni wiki kadhaa hivi sasa nahitaji mukamuokoe”

“Yupo wapi na ni kina nani ambao wamemteka?”

“Al-quida”

“Tunaifanya hii kazi ila kwa sharti moja”

“Sharti gani?”

“Tukiimaliza hii kazi tunahitaji kuwa huru sasa, tunahitaji kufanya kazi zetu binafsi za hatuto hitaji kuendelea kupokea oda kutoka kwako na laiti ukiendelea kutukatalia katika hili tutakuua na wewe umetuelewa?”

Raisi Dustana akaka kimya huku mwili mzima ukimtetemeka kwani anawatambua vizuri watu hawa wawili kwani nai wauaji wenye uwezo wa hali ya juu ambao wakiwa huru tu wanaweza kufanya mauaji makubwa kupita hata mauaji mia moja na hamsini walio wahi kuyafanya kabla hawajakamatwa na kuwekwa katika eneo hilo maalumu ambalo wameishi humondani kwa miaka zaidi ya kumi na mtu pekee ambaye anaweza kuzungumza nao ni raisi Dustan pekee.



“Nimewaelewa”

Raisi Dustan alizungumza kwa sauti ya upole huku akiwatazama wanaume hawa.

“Safi picha yake ipo wapi?”

Raisi Dustan akatatoa simu yake mfukoni akaitafuta picha ya mwanaye, alipo hakikisha kwamba ameipata, akawaonyesha. Wakaitazama picha hiyo kwa muda kisha mmoja wao akatingisha kichwa.

“Tumemuona, tupe leo na kesho sawa”

“Sawa”

Raisi Dustan mara baada ya kumaliza kuzungumza hiyvo akaiingiza simu yake mfukoni mwake na kutoka katika chumba hicho huku akiiacha milango hiyo wazi ili watu wake waweze kutoka na kwenda kuifanya kazi hiyo aliyo waagiaza.

***

Eddy na raisi Rahab wakendelea kupeana utamu hadi ikafikia hatua, wote akajikuta wakiwa wamechoka sana kwani shuhuli walio weza kuifanya ni nzito sana.

“Saa ngapi?”

Eddy aliuliza huku akihema na jasho jingi likimwagika mwilini mwake. Rahab akaichukua simu yake iliyopo pembeni mwa kitanda chake na kuitazama kwa sekunde kadhaa.

“Ni saa kumi na mbili kasoro”

“Nahitaji kwenda kufanya maandalizi ya kuonana na Adrus ili aweze kunikabidhi mwanangu”

“Si usubiri kupambazuke japo kidogo?”

“Muda umekwenda”

“Mmmm haya mwaya”

Eddy akashuka kitandani, akajikaza na kutembea hadi bafuni, taratibu akafungua bandeji alilo fungwa kwenye mguu wake, akaliweka pembeni na kutazama majeraha ya risasi ambayo ameyapata. Akachukua kitaulo kidogo chenye rangi nyeupe na kuanza kujifuta kando kando ya majeraha hayo, alipo maliza, akafungualia bomba la maji ya mvua na kuanza kuoga. Hamu na shauku kubwa ya kumuona mtoto aliye zaa na Shamsa, ikazidi umtawala. Akamaliza kuoga na kutoka bafuni humo.

“Mbona umefungua bandeji?”

“Ningeoga nalo vipi, si kidonda kingekuwa kibichi”

“Ngoja basi nikufunge bandeji jengine”

“Sawa”

Rahab akashuka kitadani mwake, akafungua kabati kubwa akatoa kisanduku kidogo chenye rangi nyeupe huku kikiwa kimechorwa msalaba wa rangi yakundu. Akakifungua, akatoa pamba na kuanza kukausaha maji yaliyo juu ya vidonda hivyo vya Eddy, alipo maliza zoezi hilo akampaka dawa ya kukausha vidonda hivyo, kisha akamfunga na bandeji.

“Kazi ya udaktari inakufaa sana”

“Mmmm”

“Yaaa inakufaa”

“Kweli, unajua kipindi nilipo kuwa mtoto nilikuwa ninatamani sana kuwa daktari, ila mama yangu alivyo kuja kufariki na yeye ndio alikuwa tegemezi langu basi kika kitu kikaharibika, nikajikuta nikiingia kwenye maisha ambayo sikuyatarajia, ila maisha hayo naamini leo hii nio yajmenifanya mimi na wewe kuwa hapa, ila ningekuwa dokta sidhani kama leo hii ningekuwa raisi”

“Unajua kufeli katika kitu ambacho mtu unakitarajia au unakiona ndio kinaweza kukupelekea katika sehemu ambayo unahitaji, watu wengi wanakata tamaa pasipo kufahamu kama Mungu naye anaweza kukupangia maisha ambayo ni mazuri kuliko hata hayo uliyo kuwa unayataka”

“Ni kweli lakini, ila watu wengi wanaogopa changamoto za maisha hayo, na ndipo wengi wao wanapo kata tamaa”

“Kwa mfano mimi, mama alikuwa ni waziri, baba alikuwa na cheo kikubwa tu jeshini. Sasa mapenzi ya mama yangu alitamani sana siku na mimi nije kuwa daktari ila kutokana na ukorofi wangu, sikufanikiwa hata kumaliza form six, nikapitia majanga mengi kwa kweli, nilijikuta kuna nchin ina kwenda pasipo hata kupenda au kutarajia”

“Ndio hivyo, kila kitu Mungu yeye mwenyewe ndio anaye panga”

Rahab alizungumza hukua akimalizia kukifunga vidonda vya Eddy vizuri.

“Unaonaje siku tukaandaa kongamano la kuhamsisha vijana kwamba wasikate tamaa hata kwa maisha gani magumu ambayo wanaapitia”

“Mmmmm….mimi maisha yangu hayafai kuhamasisha vijana”

“Kwa nini?”

“Siwezi kusimama na kuwaaambia watu kwamba nilikuwa malaya, nilikuwa jambazi. Nimemuua huyu na huyu leo nimekuwa raisi, unahisi kweli watu watahamasika na historia yangu au ndio kwanza watakuwa wakiniponda katika mitandano ya kijamii na sehemu nyingine nyingi”

“Mmmm hilo nalo neno”

Eddy akaichukua suruali yake na kuivaa.

“Umesahau kuvaa boksa yako, ukienda huko kwa mke wako akikuuliza boksa ipo wapi utasemaje?”

“Ohoooo ipo wapi?”

Wakaanza kutazama chini na kwa bahati nzuri wakaikuta ikiwa ipo pembezoni mwa kitanda. Rahab akaichukau nguo hiyo ya ndani na kumkabidhi Eddy, aliye lazimika kuivua suruali yake kwanza ili aweze kuvaa boksa.

Eddy akamaliza kuvaa nguo zake, akasindikizwa na Rahab hadi nje, msafara mdogo ukaandaliwa, kutokana ni alfajiri na mapema asubuhi hapakuwa na haja kubwa ya kuandaa msafara mkubwa sana.

“Kuwa makini huko uendapo”

“Usijali baby”

Eddy na Rahab wakakumbatiana kwa muda kidogo kisha Eddy akaingia ndani ya gari na kuondoka ikulu hapo na kumuacha Rahab akimsindikiaza kwa macho.

***

Majira ya saa moja asubuhi, Adrus na wezake wakafika katika bandari ya jijini Dar es Salaam. Wakakuta makamu wa raisi Eddy Godwin akiwa tayari amesha fika huku ulinzi katika bandari hiyo ukiwa umeimarishwa kila kona.

“Habari yako muheshimiwa”

Adrus alisalimia huku akimpa mkono Eddy aliye upokea kwa furaha sana.

“Salama pole kwa majukumu”

“Nashukuru sana, nafurahi kuweza kuonana nawe tena kwa wakati kama huu”

“Hata mimi”

Eddy alizungumza huku macho yake akiwatazama Cookie, Jing pamoja na Lee Ji ambao wamesimama nyuma yake huku Cookie akiwa amembeba Junion Jr mikononi mwake. Cookie akatembea kwa hatua za taratibu hadi alipo simama makamu wa raisi Eddy Godwin na kukabidhi Junion Jr aliye lala fofo. Eddy mikono ikaanza kumtetemeka kwa furaha, kwani Junion Jr amefanana naye sana, japo kwa mara yake ya kwanza alimuona kwenye picha ila kwa sasa anamuona akiwa mikononi mwake. Eddy macho ya furaha yakaanza kumwagika, jambo lililo wafanya Adrus na wezake kutabasamu.

“Nashukuru sana, nashukuru sana kwa kazi ambayo mumeifanya”

“Usijali muheshimiwa ni jukumu letu hilo, hawa ni wezangu nilio saidiana nao kwenye kazi hii. Huyu anaitwa Jing, yule pale anaitwa Lee Ji, na huyu hapa ni mke wangu mtarajiwa anaitwa Cookie”

“Nashukuru sana jamani kwa kuweza kuwafahamu”

“Shukrani”

“Jamani huyu ndio makamu wa raisi aitwa, Eddy naamini nilisha waeleza eleza juu ya habari zake”

“Ndio”

“Jamani twendeni nyumbani kwangu japo mukapafahamu tu”

“Usijali muheshimiwa, sisi kazi yetu ilikuwa ni kumlete amtoto hapa, na tuna imani kwamba amesha kamilisha jukumu letu”

“Hapana jamanani hivi hivi tukiachana hewani sio jambo zuri, ninawaomba sana twendeni nyumbani kwangu”

Eddy alizungumza kwa msisitizo na kuwafanya Adrus na wezake kutazamana kwa sekunde kadhaa. Jing akakubali ombi hilo la makamu wa raisi Eddy Godwin. Wakaingia kwenye magari ya msafara wa makamu wa raisi huku Adrus akipanda gari moja na Eddy aliye mbeba mwanye vizuri.

“Adrus”

“Ndio muheshimiwa”

“Umeirudisha furaha yangu ambayo ilisha potea kwa kipindi kirefu sana, ila leo hii nina imani hata nyumbani kwangu furaha hiyo itafufuka upya”

“Usijali muheshimiwa jukumu langu likikuwa ni kuhakikisha kwamba ninafwata amri ya kazi yako ambayo umeweza kunipatia”

“Naamini hata mama yako ataweza kujawa na furaha, kwa maana mabinti wangu walimuokoa kutoka mikononi mwa Wamarekani kwani waliwahi kumteka kabla vijana wangu hawajafika”

“Duuu, ilikuwaje?”

“Naamini unamfahamu Shamsa?”

“Yaaa nilikutana naye kwenye dnege kipindi ninatoka nchini Uingereza nilikaa naye siti moja”

“Yaa yeye ndio aliye lishuhulikia swala la kumuokoa mama yako kutoka mikononi mwa majasusi wa Marekani, hadi ninavyo zungumza hivi sasa kuna hali mbaya kati yetu na Marekani”

“Na sisi watakuwa wanatutafuta, kwa maana kitu tulicho kifanya huko Madagascar nina imani itaukuwa ni historia kwao nchi ile”

“Mmmm niambie dokta Ranjiti na mwanaye imekuwaje?”

“Nimefwata lile ulio niambia, nimewaua pasipo huruma kwa bahati mbaya usiku ule hatukuweza kumkuta John kwenye hoteli ambayo walikuwa wapo”

Adrus ilimbidi kuongopea kuhusiana na swala zima la kumuua John.

“Kwanza hongereni kwa kumuua huyo mzee, mbili John nitaendelea kushuhulika naye, nitajua ni wapi kwa kumuangamiza”

“Nashukuru”

“Ila nina ombi moja, naona nilizungumze mapema kabla sijalisahau”

“Ombi gani muheshimiwa?”

“Kuma kikundi kipya cha magaidi ambacho jana usiku kimeweze kuvamia msafara wangu na kuwaua vijana wangu wote, tumeweza kufahamu muhisika wa tukio hilo anaitwa Livna Livba….”

“Livna……!!!?”

“Ndio, Livna vipi unamfahamu?”

“Ninamsikia tu na yeye ndio alihusika katika uvamizi wa ndege ambayo nilitoka nayo hapa Tanzania na alituma vijana wake ndani ya ndege hiyo waweze kuniangamiza, ila kwa kudra za mwenyezi Mungu hawakufanikiwa na ndege iliweza kupata ajali mbaya sana”

“Ohooo pole sana, kumbe huyu binti ni mshenzi kiasi hichi eheee?”

“Ndio muheshimiwa, tulikuwa na mpango mimi na wezangu tuweze kumfanyia cha kumfanyia mara baada ya kumaliza hii kazi yako ambayo umetupatia ila tuliamu kumsamehee tu”

“Ohoo basi ninawaomba muweze kumshuhulikia na yeye”

“Tutalizungumza muheshimiwa kwa maana mtu huyo ana mtandao mkubwa sana na watumishi wake wote ni wanawake kwa hiyo tunatakiwa kuwa makini sana kwenye hilo swala”

“Hapo sasa ninaanza kupata picha”

“Picha…..?”

“Ndio ninanaza kupata picha, kwa maana kuna msichana mmoja ambaye tumemkamata na yupo nyumbani kwangu naye alimteka mtoto wangu yule wa kike, sasa tumemshikilia sema sijapata tu muda wa kumuhoji, na hata hapa ninavyo zungumza nilipata jaraha la kupigwa risasi kwenye paja langu hili”

“Pole sana muheshimiwa”

“Nimepoa”

Wakafika katika jumba mpya anayo ishi Eddy, ni jumba kubwa na lililo jaa ulinzi katika kila kona ya jumba hilo.

“Karibuni sana nyumbani kwangu”

Eddy alizungumza huku akishuka, hii ni mara baada ya mlinzi kumfungulia mlango na kushuka. Wakashuka wote kwenye magari. Wakaingia sebleni, Adrus hakumini kumkuta mama yake akiwa amekaa sebleni hapo akitazama vipindi vya asubuhi, mama Adrus akashindwa kujizuia, kupiga yowe la shangwe lililo wafanya Shamsa na Sa Yoo walipo jikoni wakiandaa kifungua kinywa kutoka kwa haraka ili kuweza kufahamu ni kitu gani kilicho tokea katika eneo hilo la sebleni.

Shamsa hakuamini kumuona Eddy akiwa amembeba Junion Jr, Shamsa akakitupa kitambaa alicho kuwa anashikia sufuria jikoni na kwa haraka akakimbilia sehemu alipo simama Eddy, akamchukua mtoto wake na kumkumbatia kwa nguvu sana huku machozi yakimwagika usoni mwake. Adrus na mama yake wakendelea kukumbatiana kwa furaha huku mama Adrus akilia kwa furaha sana.

***

Livna na vijana wake huku wakiwa wameongozana na K2 mara tu ya kufika katika katika ngome yake, akaelekea moja kwa moja katika ukumbi wa mkutano ili kufanya kikao cha dharura.

“Nahitaji kusikia mawazo yenu ni jinsihani tunaweza kulipiza kisasi hichi”

“Tuvute muda Livna, mimi naifahamu Tanzania vizuri, huwa viongozi wao wana mtindo wa kujisahau kuanzia kwenye swaala zima la usalama wa baadhi ya maeneo katika nchi yao, tunaweza kufaya mashambulizi ya kujistukiza katika eneo lolote ambalo wahusika watakuwepo na itakuwa ni vizuri sana kwetu”

K2 alizungumza huku akimtazama Livna usoni mwake, mlango ukafunguliwa, akaingia binti mmoja, moja kwa moja akamfwata Livna sehemu alipo kaa.

“Mkuu unatakiwa kuona hichi”

Msichana huyo alizungumza huku akiwasha Tv iliyopo humo ndani ya chumba hicho. Livna akajikita akinyanyuka kwenye kiti na kuisogelea tv hiyo ili kumtazama vizuri Cookie na Jing vijana wake alio amini kwamba hivi sasa wamekufa, kwenye ajali ya ndege ila leo hii anawaona wakiwa pamoja tena na Adrus ambaye aliwaagiza waende kumuua.



“Fuc****”

Livna alizungumza kwa hasira huku akitazama jinsi wanavyo zungumza na Eddy ambaye ni makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania.

“Hii video imechukuliwa muda gani?”

“Kama dakika tano zilizo pita muheshimiwa”

“Hakikisheni kwamba hao kunguni hawatoki ndani ya Tanzania mume nielewa?”

“Sawa mkuu”

***

“Jamani leo ni siku ya furaha kwetu sote, tule tunye tusherekee”

Eddy alizungumza mara baada ya Phidaya kujumuika katika eneo hilo la sebleni. Phidaya akamchukua Junion Jr na kumbeba, machozi ya furaha yakaanza kumwagika, kwani taswira ya mwanaye Junio aliye fariki miaka mingi ya nyuma imerudi sasa mbele ya macho yake.

“Mtoto ni mzuri, ni mzuri sana”

Phidaya aliendelea kuzungumza huku akifurahi.

“Kweli ehee?”

Sa Yoo alizungumza huku akiwa amemuinamia Phidaya aliye kaa kwenye kiti chake.

“Ndio ni mzuri sana. Nashukuru Mungu ameweza kuirudisha furaha ya nyumba hii. Baba watoto, kweli leo tufanya sherehe”

Kila mtu ndani ya seble hiyo akakubaliana na swala la kufanyika kwa sherehe kubwa ya kumshukuru Mungu kwa familia hiyo kuwa hai.

“Ahaa muheshimiwa unaweza kunionyesha huyo binti ambaye umemshikilia?”

Adrus alizungumza kwa sauti ya chini.

“Ohoo yupo huku”

Adrus kwa ishara akawaomba Cookie, Jing na Lee Ji, kuongozana na makamu wa raisi. Wakaingia katika nyumba ambayo Lizzy amehifadhiwa na kuna ulinzi mkali sana unao. Lizzy akastuka sana kumuona Cookie na Jing kwani anawafahamu vizuri sana, niwezake alio wahi kufanya nao kazi nyingi za hatari.

“Lizzy”

Lee Jing aliita huku macho yakimtoka.

“Muna mfahamu?”

Eddy aliuliza.

“Ndio tunamfahamu, ni mwezetu, yamekukuta yapi hadi kuwa huku”

Lizzy hakujibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kumtazama Eddy kwa hasira, sehemu aliyo fungwa, mikono yake kwa kutumia nyororo ngumu na nenen kiasi ina mfanya ashindwe hata kupiga hata hatua moja mbele.

“Mkuu huyu niachieni atataja ni wapi alipo bosi wake”

Adrus alizungumza huku akimtazama Lizzy usoni mwake.

“Kuna nini kinacho endelea?”

Cookie aliuliza ili naye aweze kutambua.

“Huyu amehusika katika kumteka mwanagu yule wa kike muliye muona kule ndani ila kabla hawajafanikiwa niliweza kumuokoa na kwa bahati mbaya wakanipiga risasi hii ya paja ndio maana unaweza kuona nikitembea nina chechemea”

Eddy alitoa maelezo yaliyo weza kueleweka kwa kila mmoja wao.

“Sasa Adrus ukimuuliza Lizy hilo swali hawezi kukijibu, siis tunafahamu ni wapi makao makao makuu ya Livna yalipo”

Cookie alizungumza maneno yaliyo mshangaza sana Eddy.

“Unafahamu?”

Eddy aliuliza kwa herufi kubwa huku akizidi kushangaa.

“Muheshimiwa kama nilivyo kuelewaa kwamba hawa wezangu walikuwa wakifanya kazi chini ya huyo Livna na alisababisha mambo mengi yaliyo pelekea hadi wao kuamua kuungana nami”

“Ila Adrus si tumekubaliana kuendelea na maisha yetu, kwa maana kila mmoja sasa hivi ana pesa zake na anahitaji kuendelea na harakati zake za kimaisha”

Jing alizungumza kwa msisitizo.

“Hilo nalitambu, ila kuna matatizo ambayo yamejitokeza”

“Matatizo gani?”

“Jana Livna na kundi lake wameweza kusababisha matatizo makubwa mojawapo ikiwemo la kuvamia msafara wa makamu wa raisi na kuua walinzi wake wote”

“Heee”

“Yaaa na hawakuishia hapo waliweza kuua askari wengine, kwa hiyo inavyo onyesha Livna anahiyaji kufanya mambo ambayo yatazidi kupelekea nchi hii kukosa amani kanisa.”

“Munahisi kumsaliti Livna mutaweza kuwa hai ni lazima awaue”

Lizzy alizungumza kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo itokanayo na kugoma kwake kula kwa siku kadhaa sasa. Cookie na Jing wakamtazama Lizy kwa muda kisha Jing akamsogelea.

“Unahisi kwamba utaendelea kuwa mbwa wa Livna hadi lini, utaendeleak uhatarisha maisha yako pasipo maslahi ya aina yoyote hadi lini, ni muda sasa wa kuamka ni muda wa kufumbua hayo macho yako ya akilini mwako na kuamua kufanya maamuzi sahihi. Tanzama jinsi ulivyo, unatia huruma ila huruma ambayo inaongeza chuki kwa yule anaye kutazama. Lizzy nina kufahamu wewe vizuri sana, hembu achana basi na huo ujinga ambao una uendea”

“Lazima Livna aweze kuja hapa na nitawahakikishia kwamba lazima mufe, mbwa nyinyi”

Jing akafumba macho yake kwa muda kidogo kisha akayafumbua, akamtandika ngumi ya uso Lizzy na kumsabishia kutoa mguno mzito wa maumivu. Akaichukua saa aliyo ivaa Lizy mkononi mwake kisha akawageukia wezake.

“Hii saa ukiminya batani hii inaweza kumuashiria Livna na watu wake wafahami ni sehemu gani alipo. Na hapa ipo on, hivyo basi muheshimiwa muda wowote na wakati wowote ujiandae kuvamiwa kwenye hii nyumba yako”

Maneno ya Jing yakaanza kuufanya moyo wa Eddy kubadilisha utaratibu wake wa mapigo ya moyo. Kajasho kakaanza kumwagika usoni mwake, kwani hali mbaya sasa inaanza kumkabili, furaha na amani aliyo ipata kwa muda mchache ulio pita umetoweka kabisa.

“Lee Ji, unaweza kulishuhulikia hili?”

Jing alizungumza huku akimkabidhi rafiki yake saa hiyo. Lee Ji akaitazama kwa muda kisha akatingisha kichwa akimaanisha kwamba kazi hiyo anaweza kuifanya.

“Laptop yangu nimeicha kwenye boti kule”

“Tunaweza kutuma vijana kwenda kuichukua”

“Hakuna haja ya kutuma vijana, nahitaji kwenda kuichukua mimi mwenyewe, nipeni dereva tu”

“Nitakusindikiza”

Jing alizungumza huku akimtazama Lee Ji.

“Hahaaaa………”

Lizy akaachia kicheko kikali sana kilicho wafanya watu wote kumtazama.

“Wanakujaaaa”

Akamalizia maneo hayo yaliyo mfanya Jing kumpiga teke zito la kisho na kumfanya apoteze fahamu hapo hapo. Wakatoka nje, Eddy akawakabidhi Lee Ji na Jing kwa dereva wake anaye muamini, kisha akaitisha kikoa cha dharura cha walinzi wake wote wanao linda nyumba yake hiyo kuhakikisha kwamba ulinzi unazidi kuimarisha na unakuwa ni ulinzi wa masaa ishirini na nne.

“Mkuu kuna haja ya kuihamisha familia kwa siri kwenye hii nyumba”

Adrus alishauri mara baada ya kikao hicho kumalizika.

“Nitawapeleka wapi, kwa maana sifahamu ni wapi ni salama”

“Hii nyumba haina mahandaki ya chini ya siri?”

“Yapo?”

“Basi kukitokea tatizo la ina yoyote tutahakikisha kwamba familia inakuwa salama katika mahandaki hayo”

“Sawa, je na yule msichana tuliye mshikilia itakuwaje?”

“Yule atakuwa chambo kwa wezake watakao kuja”

“Chambo kivipi”

“Usioogope muheshimiwa, hakikisha kwamba unawasiliana na raisi ili kuweza kumueleza hili jambo”

“Sawa”

***

“Unahisi huyo Livna sijui Livna gani munaweza kupambana naye?”

Lee Ji aliuliza huku akimtazama Jing usoni mwake.

“Inabidi tuweze japo ana kundi kubwa la watu hatari ila inaidi kufanikiwa katika hilo”

“Sidhani”

“Kwa nini?”

“Kama ni mtu mwenye kundi kubwa basi ujue hata ufwatiliaji wake ni mkubwa, kama ni mtu ambaye ameweza kuuvamia msafara wa makamu wa raisi na kuuwa walinzi wote hapo wewe unafikiriaje, kwa maana ile ni serikali na nyinyi ni watu”

“Tukikimbia ni lazima aweze kutua mmoja baada ya amwengine, kipi ni bora, kuungana pamoja au kila mmoja akaenda kuishi maisha yake na yakawa mfupi kama jinsi Livna atakavyo panga?”

Lee Ji kaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akiyafikiria maneno ya Jing.

“Inabidi kuwa pamoja”

“Basi tuwe hivyo, kwa sasa hatuwezi kukimbia kabisa, na kwenda sehemua mbayo tunajua kila mmoja maisha yake yatakuwa matatatani”

“Una iamini hii serikali?”

“Ndio, sina wasiwasi kabisa”

“Kweli?”

“Ndio”

“Sawa tuifanye kazi hii kwa moyo mmoja”

Lee Ji alizungumza huku akiushika mkono wa Jing huku wakitazama majengo ya jiji la Dar es Salaam kwa maana hii ndio mara yao ya kwanza kufika katika jiji hilo na nchi ya Tanzania.

***

Heka heka za kuwatafuta ni kina nani wamesuhika katuaka mauaji ya dokta Ranjiti na mwanaye Anna yakazidi kupamba moto. Wataalamu kutoka nchi kubwa kama Marekani wakafika katika visiwa vya Madagascar. Kwa bahati mbaya kamera za ulinzi za barabani ziliweza kunasa tukio la Adrus na wezake wakishuka katika gari hili.

“Munaweza kuziotafuta sura zao?”

John alizungumza huku akiwa katika chumba kimoja na maafisa wa FBI kutoka nchini Marekani walio weka kambi katika hoteli hiyo kuhakikisha kwamba wanafanya uchunguzi wa kija juu ya mauji hayo ya daktari Ranjiti na mwanaye.

“Ndio tunalo lishuhukikia kwa hivi sasa”

“Tafuteni basi haraka haraka”

“Mkuu kuna simu yako hapa”

Sekretari wa John alizungumza huku akimtazama John usoni mwake.

“Umetoka wapi?”

“Sijanajua”

John akamtazama sekretari wake huyo kwa macho makali, kisha akaichuku simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Haloo”

John alizungumza huku akiingia chumbani kwake.

“Najua tulisha wahi kuzungumza, ila hivi sasa ni muda wa mimi na wewe kuungana kuhakikisha kwmaba tunawaangamiza watu walio sababisha matatizo kwako”

Sauti ya kike ilisikika na kumfanya John kufikiria kwa muda kido akitafakari ni wapi aliisikia hiyo sauti.

“Wewe ni nani?”

“Unazungumza na Livna, Livna Livba, kwa pamoja nahitaji tufanye kazi pamoja sasa.”



“Sikufahamu na sina muda wa kufanya na wewe sawa”

John baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo akakata simu na kumrudishia sekretari wake.

“Sihitaji usumbufu kwa sasa hadi hii kazi iweze kukamilia umenielewa”

“Ndio mkuu”

John akarudi katika sebleni na kuwakuta wana FBI, wakiwa wamejawa na heka heka.

“Ni nini kinacho endelea hapa?”

“Tumewapata wauaji”

“Ni kina nani hao”

John akaonyeshwa picha ya mwanaume mmoja ambaye ni Adrus pamoja wasichana watatu, wawili wana asili ya kichina na mmoja ana asili ya kiafrika.

“Ni kina nani hao!!!?”

Adrus aliuliza huku akiwa ameshikwa na mshangao mkubwa sana. Jamaa mmoja akanyanyuka kidogo na kumtazama John usoni mwake huku akishusha pumzi.

“Hawa ni watatu ni magaidi wana tafutwa sana na nchi yetu ya Marekani. Huyu mwanaume anaitwa Adrus Maldin ni mtu gaidi sana na pia ana mafunzo makubwa ya ukombandoo, ndio maana hata mauaji haya yalivyo fanyika basi yamefanyika kwa akili kubwa na ustadi wa hali ya juu na hata kuwa hai kwako basi ujue kwamba mtu huyu ni hatari kama hadi sasa Marekani haijafanikiwa kumkamata, basi pia kwa upande wako itakuwa ngumu kumkamata”

“Najua ni nani anaye mpa jeuri mtu huyo, tukifanikiwa kumdhibiti mtu basi tutafanikiwa kuwapata watu hao”

“Ni mtu gani huyo?”

“Ni Eddy, Eddy Godwin, makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania”

Wana FBI wote macho yakawatoka kwani kitu ambacho anakizungumza John ni hatari sana ambacho kinaweza kupelekea mataizo makubwa sana kwa hapo badaye.

***

“Vipi?”

K2 alimuuliza Livna mara baada ya kumuona akiirudisha rudisha simu yake sikoni mwake.

“Amekata simu na kuizima, mshenzi huyu”

“Amekataa kushirikiana nawe”

“Ndio”

“Ni nini tutafanya kwa maana historia inaonyesha hawa watu wanajua vizuri sana na mahusiano yao kwa sasa sio mazuri”

“Nitajitajidi kumshawishi kuhakikisha kwamba anakubaliana kufanya kazi na mimi”

“Mmmm kweli itawezekana kweli hiyo?”

“Itawezekana”

“Kwa njia gani?”

“Hapa kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunafunga njia zake zote za yeye kuhitaji kufanikiwa katika pinago yake dhini ya Eddy”

“Sijakuelewa hapo, ina maana unataka kwa namna moja ama nyingine tumlinde Eddy”

“Ndio”

“Kwa nini ikiwa kuna uwezekano wa kumuua”

“Angalia malengo yangu, kumbuka hapa umekuja kuungana na mimi na kusema unahiyaji kaka yako awe raisi wa nchi ya Tanzania, sasa leo ikisadikika kwamba kaka yako amemuua Eddy au wewe umemua Eddy unahisi watu ambao munakwenda kuwaongoza watawaelewa?”

Swali la Livna likamfanya K2 kukaa kimya kwa muda huku akitafakari.

“Ni lazima kumtumia John kuhakikisha kwamba tunakuwa nyuma ya hili swala, na hata ikiwezekana kwa sasa hakikisha kwamba unamuwinda Eddy anakuwa mtu wako wa akribu”

“Samahani?”

“Ndio maana yake, ukihiataji tusaidiane hadi dakika ya mwisho ni lazima uhakiksihe kwamba unamteka Eddy katika hisia za mapeni kwa maana yeye”

Maneno ya Livna Livba yakazidi kumshangaza K2, kwani hiyo kazi aliyo kabidhiwa ni ngumu kuliko hata na anavyo tegemea, kwani anaamini kwamba uasi alio ufanya ndani ya Tanzania lazima viongozi hao watakuwa wameufahamu na yeye ayakuwa anasakwa.

***

Majasuri wawili hatari wajulikanao kwa jina la Dump na Dumbe, ambao kwa kipindi chote walikuwa wapo chini ya uangalizi wa Raisi Dustan, wafika nchini Pakistani, huku wakiwa wamevalia kanzu nzuri nyeupe na kijifunga vitambaa vichwani mwao. Huku wakionekana kama kama waislamu safi kanisa, na jinsi ndefu zao ndefu walizo zifuga ni jambo gumu sana kuweza kufahamu kwamba ni watu wenye roho mbaya kuliko hata roho mbaya ambayo inasadikika kuwa nayo gaidi aliye wahi kuitingisha dunia Osama Bin Laden. Wakapolewa na msaidizi wa balozi wa Marekani nchini humo, akawapeleka hadi kwenye nyumba ambayo wakakuta mabegi ya silaha na gari ambalo walihitaji kupatiwa.

Moja kwa moja wakaelekea katika jangwa liitwalo Indus Valley lipatikanalo Kaskazini mwa nchi hiyo ya Pakistan. Wakatengeneza hema lao moja kubwa, na kuanza kupanga vitu vyao ambavyo.

“Tunaanzai wapi?”

Dump alimuuliza mwenzake huku akimtazama usoni mwake.

“Kutoka hapa tulipo hadi katika kambi ya Al-quida, ni kilomita mia mbili, hii kazi inabidi kuifanya usiku wa siku ya leo”

“Sawa kazi ni kumchukua Charity au kutakuwa na jambo la ziada unahitaji tulifanye?”

“Tutamuua kila mtua ambaye atajariku kutuua”

“Sawa sawa”

Wakaanza kakaendelea kufanya maandalizi yao waliyo yahiditaji, wakapata chakula cha usiku, kisha wakaingiaza silaha zao kwenye gari hilo aina ya Hammer, ambalo lina uimara mkubwa sana wa kuweza kupita jangwani pasipo kukwama au kupata tatizo la aina yoyote.

Usiku wa siku hii kitu cha kumshukuru Mungu, hakuna mbalamwezi, wala nyota na hali ya joto kali ndio inatawala katika jangwa hili. Safari yao ikawachukua lisaa moja hadi kupika katika eneo ambalo ndipo zilipo ngome za siri za kundi la Al-quida, wakasimamisha gari lao nyuma ya kilima kirefu kiasi cha mchanga wa jangwa hilo. Kila mtu akabeba silaha yake pamoja na mabomu ya kutosha. Dump akatoa simu yake ndogo na kutazama ni wapi watakuwa wamemficha, alama maalumu inaonyesha kwamba Charity yupo kwenye eneo hilo ila ni katika mahandaki maalumu yaliyopo chini ya ardhi.

***

“Muheshimiwa raisi naomba unipe ruhusa ya kwenda kumleta Ardus”

Naomi alizungumza mara baada ya kukaribisha ndani ya ofisi ya raisi Dustan.

“Hali yako inaendeleaje?”

“Ninaendelea vizuri muheshimiwa”

“Unatakiwa kupumzika kwa mwaka mzima pasipo kujishusisha na hizi kazi kwa sasa. Nikupa majukumu mepesi mepesi ndani ya hii ikulu”

“Hapana muheshimwia, nilizaliwa kuwa mwanajeshi, na nimekuwa mwanajeshi. Tafadhali ninakuomba unipe jukumu hili”

“Ningekupa hili jukumu Noami ila huyu Adrus kwa sasa simuhitaji kwa maana kazi kama yake tayari nimesha mpatia mtu mwengine”

“Sawa muheshimiwa, ila ninakuomba niweze kwenda nchini Tanzania”

Raisi Dustan akamtazama kwa muda Naomi na kutambua kwamba kitu ambacho kinamsumbua hivi sasa ni wivu wa mapenzi juu ya mpenzi wake Adrus ambaye alimpenda kuliko kitu chochote.

“Nakuruhusu kwenda Tanzania ila kwa kwazi moja”

“Niambiae muheshimiwa”

“Kuna mauji ya majasusi wetu waliuwawa nchini Tanzania na wauaji wanakumbatiwa na serikali ya Tanzania, hakikisha kwamba ukifika unawaangamiza wauaji hao kimya kimya”

“Nitafwata amri yako muheshimiwa na nitaifanya hiyo kazi kikamilifu kabisa, ninaomba unionyeshe picha zao”

Raisi Dustan akawamonyesha Naomi picha hizo. Naomi akazitazama picha hizo zilizopo katika computer ya raisi Dustan kisha akatingisha kichwa.

“Nimekuelewa nitawasaka”

“Taarifa zao zote utaingizwa kwenye email zako”

“Sawa muheshimiwa raisi”

“Nakuangalia safari yako na kiasi cha pesa ambacho utakwenda kukitumia ukiwa katika safari yako”

“Sawa muheshimiwa.”

Cookie akatoka katoka ofisi ya raisi Dustan huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana, kwani sasa ni muda wa kwenda kumrudisha Adrus wake ambaye amekaa naye mbali kwa kipindi kirefu sana hii yote ni kutokana na kuugua.

***

Maandalizi ya kuandaa sherehe ndogo ikazidi kupamba moto huku Cookie, Sa Yoo, mama Adrus, Phidaya wakijitahidi kuandaa chakula kizuri kwa ajili ya sherehe hiyo.

“Mama Junion Jr yupo wapi?”

Phidaya alimuuliza Sa Yoo huku akimtazama usoni mwake.

“Yupo chumbani na watoto yaani leo hatoki huko kwa furaha”

“Hahaaa”

“Ila jamani kuwa na watoto raha sana”

Sa Yoo alizungumza kwa sauti ya chini huku akimtazama Phidaya.

“Hahaa, ndio ufanye upate mwanaume uzae naye, umri unakwenda”

“Nitazaa tu, Mungu ni mwema”

“Na wewe Cookie unatarajia kupata lini mtoto?”

Phiadaya aliuliza huku akimtazama Cookie

“Mimi namsikilizia Adrus, akihitaji mtoto hata leo basi mimi nipo tayari kumpatia kwa maana nina mpenda sana. Mama najua nitakuwa labada nimefanya kosa kuzungumza hizi hisia za kimapenzi mbele yako pasipo mwanao kizizungumza kwako, ila ukweli nina mpenda sana”

“Ahaaa, sawa ni vizuri sana”

Mama Adrus alizungumza huku akitabasamu. Akaweka kitunguu alicho kuwa akikikata kata juu ya kibao maalmu ndani humo, kisha akatoka jikoni humo na kukitana na Adrus sebleni.

“Adrus nahitaji kuzungumza nawe”

Mama Adrus alizungumza kwa sauti ya chini mara baada kutoka jikoni alipokuwa anapika akishirikiana na Cookie na wengine.

“Kuna nini mama?”

“Kwani kuzungumza na wewe siku hizi ni hadi uniulize?”

Mama Adrus alizungumza kwa hasira kidogo, jambo lililo mshangaza sana Adrus. Wakatoka nje na kwenda kukaa kwenye kibanda kidogo kilichopo katika eneo hilo la nje.

“Niambie kuna kitu gani kunacho endelea na yule msichana”

“Msichana yupi tena mama?”

“Yule sijui Cookie sijui nani”

Adrus akashusha pumzi nyingi huku akitabasamu.

“Mama yule ni mkwe wako mpya”

“Mkwe?”

“Ndio mama ni mwanamke ninaye mpenda kutoka moyoni mwangu na amekuwa msaada mkubwa sana kwenye maisha yangu”

Adrus akastukia akitandikwa kofi zito usoni mwake na mama yake jambo lililo mstusha sana Adrus pamoja na Cookie ambaye alikuwa akiwafwata hapo ili Adrus aweze kumtambulisha kwa mama yake kwani hiyo ndio ilikwa nafasi yake ya pekee kwa kutambulishwa.

“Simuhitaji huyu mwanamke na kamwe usirudie kuzungumza maneno ya kipuuzi mbele yangu”

Mama Adrus baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo ambayo Cookie hakuyasikia, akaondoka katika eneo hilo huku akimpita Cookie pasipo kumsemesha neno la aina yoyote.



Cookie akanifwata kwa haraka huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa.

“Baby kuna kuna nini kinacho endelea?”

Cookie alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana.

“Usijali hakuna tatizo?”

“No….Adrus haiwezekani mama akakupiga kibao kama hichi alafu unaniambia kwamba hakuna tatizo?”

“Mimi na mama yangu ni watu wa kutaniana sana, muda ule ulivyo kuwa unakuja hapa, akaniambia ngoja anipige kibao aone jinsi utakavyo jisikia, ila kila kitu kipo sawa mpenzi wangu”

Cookie akashusha pumzi nyingi sana huku akimshika Adrus shavu lake.

“Jamani pole mke mume wangu”

“Pole ya nini tena hapo jamani?”

“Kwa kupigwa kibao hichi na mama”

“Haha usijali ni utani tu”

“Sawa basi ngoja nikaendelee kusaidiana nao jikoni kwa maana ni siku nyingi sikuingia jikoni na kutengeneza madiko diko”

“Hahahaa……Unajua kupika lakinia?”

“Saanaaaaaa”

Cookie alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa snaa usoni mwake. Akakimbilia ndani na kumfanya Adrus kushusha pumzi nyingi na taratibu akaanza kutembea kuelekea kwenye moja ya kibanda cha mapumziko. Taratibu akaka kwenye kiti, huku akiyatafakari maeno ya mama yake juu ya kumkataa Cookie kuwa mkwe wake.

‘Kwa nini hamtaki?’

Swali la Adrus halikuweza kupata jibu kabisa, kwani toka kuzaliwa kweka hakuwahi kumuona mama yake akimkatalia jambo ambalo kwake analifanya na kuonona ni sahihi.

“Umemfanya nini mama?”

Sauti ya Eddy ikamstua sana Adrus na kujikuta akikaa sawa na kumtazama.

“Eheee?”

Eddy akaka katika kiti cha pembeni huku akiwa ameshika chupa mbili za soda, akamkabidhi Adrus moja.

“Nimeona mama amekutandika kofi, nilikuwa gorofani nikiwatazama. Chumba changu ni kile pale”

Eddy alizungumza huku akimonyesha Adrus chumba kilichopo gorofani. Adrus akakaa kimya kwa muda kidogo huki akifikiria ni kitu gani cha kumjibu makamu wa raisi.

“Aha…mama hamuhitaji mpenzi wangu wa sasa”

“Hamuhitaji kwa nini?”

“Sijajua kwa nini hamuhitaji, ikiwa ni mwanamke anaye thubutu kujitoa maisha yake kwa ajili yangu”

“Hapo awali ulisha wahi kumtambulisha mama mchumba?”

“Ndio, naamini unakumbuka yule mpenzi wangu aliye kuwa ni mlinzi wa mtoto wa raisi wa Marekani”

“Ohooo ni mekumbuka ni yule aliye pigwa risasi kipindi fulani na wale magaidi?”

“Ndio, ni mwanamke ambaye nilimpenda snaa”

“Kwa sasa humpendi?”

Swali la Eddy likamfanya Adrus kukaa kimya kwa muda.

“Ukimya wako una ashiria kwamba unampenda sana mwanamke huyo uliye mtambulisha kwa mama”

“Ni kweli muheshimiwa hisia zaungu bado zipo kwa Naomi, nina mpenda sana”

“Cookie je?”

“Ninampenda pia”

“Haumpendi, ila umemzoea.”

“Ahaa….”

“Yaa umemzoea, kuna tofauti kati ya kupenda na kumzoea mtu kwa muda au kipindi ambacho upa naye. Ngoja nikuadisie historia yangu kwa ufupi sana, katika upande wa mahusiano”

“Eheee”

“Nakumbuka nilianza mahusiano nikiwa na miaka kama kumi na sita hivi, unajua niliwahiswa shule mapema sana, kipindi cha O level niliuwa na msichana wangu mmoja huyo, ila tulikuwa na yela mapenzi ya kishule shule”

“Ila nilivyo kuja kuingia A level ndipo hapo nilipo jikuta nikijua nini maana ya kupenda, huwezi amini nilimpenda mwanamfunzi mwenzangu amanye anaitwa Sheila. Sheila yeye ndio alichangia uadui mkubwa sana na John. Kwa maumivu hayo nilikuja kuapia na kuamini kwamba mwanamke kwangu ni kama chombo cha starehe tu, na kweli niliwala wanawake, nilikuwa sichagui ni mzuri au ni mbaya, mimi kwangu ilikuwa chapa ilale”

“Ila nilipo kuja kukutana na Phidaya hapo ndipo nilipo kuja kujua na kufahamu nini maana ya kupande. Phidaya alinibadilisha sana moyo wangu, alijitahidi sana kuhakikisha kwamba kila hatua ninayo piga, iwe mbaya au nzuri basi alikuwa pembeni yangu. Ubaya na tabu ilikuja pale mama yangu alipo mkataa Phidaya, kisa asili yake ni mtu wa Asia.”

“Niliumia sana kuona mama yangu hampendi mke wangu, hampendi mwanamke ambaye nilizaa naye. Ila kutokana ninampenda nilipambana kwa ajili ya penzi langu, nilihakikisha kwamba ninamshawishi mama anakubaliana na penzi langu, japo ilifikai hatua mama alinichagulia hadi mwanamke wa kuoa na aliolewa”

“Na wewe?”

“Hapana na mtu anaye fanana na mimi?”

“Duu unataka kuniambia kwamba hapo mkuu ulicheza rafu?”

“Tena rafu ambayo hapakuwa na mtu aliye weza kuelewa wala kufahamu kwamba jamaa anaye oa si mimi”

“Aisee”

“Yaa yote niliyafanya kwa ajili ya upande, ilifikia hatua ikabidi kwamba mama aweze kukubaliana na matakwa yangu”

“Na Sheila ilikuwaje?”

“Sheila nilimuua”

“Hee?”

“Yaa nilimuua tena kifo cha kinyama sana, nilimuua mbele ya John na John naye nilimuua ila mizimu ya kwao ikamuokoa kwa kweli”

Adrus akatabasamu tu kwani anafahamu kwamba John anaye zungumziwa hapa yupo hai na wamemfilisi kiasi chote cha pesa alizo kuwa akizitegemea.

“Kitu cha kukushauri hapo hakikisha kwmaba unafanya chagua lililo sahihihi na maisha yako kwani mimi nilibisha ila mwishowe maisha yangu na familia yangu hadi sasa hayana amani, ukiachilia mbali pesa, vyeo ila sina amani kabisa na familia yangu maadui zangu wamenizingira kila upenda. Hadi watoto wadogo ambao hawana hatia nao wanakuja kukutan ana makosa ambayo niliyafanya hapo nyuma”

Eddy alizungumza kwa sauti ya upole ila iliyo jaa msisitizo mkubwa ndani yake.

***

Dump na Dumbe wakaanza kufanya mashambulizi ya kimya kimya pasipo wanajeshi wa kundi hili la Al-quida kuweza kufahamu kwani ni utaalamu mkubwa ambao wanao utumi akatika kuhakikisha kwamba wanampata Charity. Dump akaingia katika gandani lililopo chini ya ardhi na hapo ndipo baadhi ya wanajeshi wa Al-quida walipo weza kugundua kwamba wamevamiwa. Kufahamu kwao haikuwa sababu yoyote ambayo ingemfanya Dump kushindwa kutekeleza kile kilicho muingiza ndani ya gandaki hili, ndani ya dakika mbili akafanikiwa kuwaua wanajeshi wote walimo ndani ya handaki hili, akaelekea hadi kwenye chumba alicho fungiwa Charity na kumkuta akiwa amelala huku amechakaa na kukondeana kwani siku zote hizo alizo kuwa anashikiliwa kula yake ilikuwa ni ya shida sana.

Akanyanyua na kumuweka begani mwake, na kuanza kutoka nje. Dumbe naye hakusita katika kuhakikisha kwamba anawamaliza wanajeshi wote walipo nje. Wakaingia katika gari lao na kuondoka eneo hilo.

Wakafika katika eneo walipo weka hema lao, wakakusanya kila kitu kilicho na umuhimu kwao na kuendelea na safari ya kutoka katika jangwa hilo.

“Unaonaje ukawasiliana na raisi”

Dump alishauri.

“Sasa hivi?”

“Ndio, mimi sina mpango wa kurudi Marekani tena”

Dumbe akajifikiria kwa muda kisha akachukua simu yake na kumpigia raisi Dustan. Simu ya raisi Dustan ikaanza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.

“Ndio muheshimiwa”

“Nipeni habari?”

“Mwanao tumempata”

“Ohoo asante Mungu, ehee niwaandalie private jet muweze kumletea huku?”

“Hapana hatuhitaji private jate, kinacho hitajika hivi sasa ni kukukabidhi mtoto wako hatufikirii kurudi Marekani”

“Ahaa….sijawalewa hapo?”

“Nimezungumza kilugha au, tutamkabidhi mwanao katika watu ambao wanaweza kumfikisha Washington D.C”

Raisi Dustan akashusha pumzi nyingi sana kwani mpango wake alio uweka nyuma ya pazia ni kuhakikisha kwamba Dump na Dumbe wanapo maliza kufanya kazi hiyo anawarudisha mikononi mwake na anaendelea kuwaweka chini ya ulinzi mkali sana, kwani ni watu hatari sana duniani pale watakapo kuwa huru.

***

Naomi akapanga nguo zake kadhaa kwenye begi lake. Akatoka katika chumba chake na kukabidhiwa tiketi na sekretari wa ofisi ya raisi.

“Ndege inaondoka baada ya nunu saa kuanzi hivi sasa, utapelekwa na helicopter hadi uwanja wa ndege”

“Sawa sawa”

“Hii ni kadi ambayo unaweza kuchukua kiasi cha pesa katika benki yoyote duniani, katika akaunti yako kuna kiasi cha dola milioni moja, utaweza kukitumia katika kazi uliyo weza kukabidhiwa”

“Sawa”

Naomi akasindikizwa hadi kwenye uwanja mdogo wa helicopter ulipo katika ikulu hiyo ya Marekani, akaingia ndani ya helicopter hiyo na moja kwa moja safari ya kuelekea uwanja wa ndege ikaanza, hawakuchukua muda mrefu sana, wakafika katika uwanja huo. Moja kwa moja akaeleka katika ndege ya shirika la KLM, akaa kwenye siti yake na kujifunga mkanda wa siti hiyo. Akachuku laptop ndogo iliyo kwenye begi lake dogo kisha akaifungua. Baada ya kuiwasha akaanza kusoma malezo ya wasichana wawili alio kabidhiwa kwamba ahakikishe kwamba ana waangamizi pale atakapo fika nchini Tanzania

‘Nitawaua kabla kumpata Adrus wangu’

Noami alizungumza kimoyo moyo huku akimitazama picha ya Shamsa na Sa Yoo.

Taratibu ndege hiyo ikaacha ardhina kupaa angani na kuiaza safari ya kukatiza baadhi ya nchi na safari yake ya mwisho itaishia nchini Tanzania.

***

Jing na Lee Ji wakarudi nyumbani mara baada ya kuichukua laptop waliyo kuwa wameifwata kwenye boti walio jia nayo nchini Tanzania. Walipo waona Eddy na Adrus wamekaa kwenye moja ya kibanda cha kupumzikia, wakawafwata.

“Vipi mumefanikiwa?”

Adrus aliuliza huku akiwatazama kwenye nyuso zao.

“Ndio, asiee kumbe Tanzania ni nzuri ehee?”

Jing alizungumza huku akikaa kwenye kiti kilichopo pembeni ya Adrus.

“Yaa ni nzuri kwa kiasi chake”

“Nimeipenda, haina mambo mengi, ni tofauti na kule kwetu chini, yaani kila kitu mambo ni mengi sana.”

“Ni kweli”

“Jing naomba unipe maelekezo ya nini nifanye kumpata Livna?”

“Si unaweza ku hack system nzima ya makamo makuu yake”

“Inawezekana ila ni kazi ngumu sana ambayo itachukua muda kidogo”

“Hapa Cookie anatakiwa awepo kwa maana yeye anafahamu mambo mengi ya mule ndani”

“Ngoja nikamuote”

Jing alinyanyuka na kuingia ndani, baada ya dakika mbili akarudi akiwa wameongozana na Cookie. Wakamueleza nin ini anacho takiwa kukifanya. Cookie akaanza kutaja code ambazo zinaweza kuwawezenye ku hack kila mfumo wa computer zilizopo ndani ya makamo makuu ya Livna.

“Vipi?”

Adrus aliuliza huku akimtazama Lee Ji anaye ifanya shuhuli hiyo.

“Inasoma, hii baada ya muda kidogo itatupa majibu”

“Hivi hivyo munavyo hack, mutaweza kufahamu nini kinacho fanyika ndani ya makao makuu yao?”

Eddy aliuliza.

“Ndio muheshimiwa, tunaweza kujua kila kitu, mipango yao, mazungumzo yao kwa njia ya simu vyote tutaweza kuf…..”

Kabla Lee Ji hajamalizia sentensi yake, zoezi alilo kuwa akilifanya likafanikiwa kwa asilimia mia moja. Hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kuanza kuchunguza ni kitu gani ambacho kimefanyika ndani ya muda mchake. Akafanikiwa kuyadaka mazungumzo ya Livna aliyo kuwa akizungumza na John. Akawasikilizisha watu wote alio kaa nao katika eneo hilo.

“Ina maana wanataka kumtumia John kutukabili sisi?”

Eddy aliuliza huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Ndio muheshimiwa”


“Shitiii, John hamkufanikiwa kumona?”

Adrus kidogo akastuka kwa swali alilo ulizwa na makamu wa raisi. Eddy akayafumba macho yake kwa muda huku akitafakari ni kitu gani cha kufanya kwa maana John ni mtu ambaye uadui wao bado una pamba moto kadri siku zinavyo zidi kwenda mbele.

“Nife mimi au afe John ni lazima ushinde upatikane kati yetu”

Maneno ya Eddy yakawafanya watu wote kukaa kimya kwani hii ni vita inayo onyesha kwamba ni mbaya sana.

***

Dump na Dumbe wakafika hadi katika ubalozi wa Marekani. Dump akafungua mlango na kumshusha Charity akamkabizisha kwa wanajeshi waliopo katika geti hilo la makao makuu ya ubalozi. Wanajeshi hao ni wakabaki kujawa na mshangao kwa maana wana mfahamu sana mtoto wa raisi Dustan na wanafahamu juu ya kupotea kwake.

“Hakikisheni anakuwa salama na anafika nchini Marekani”

Dump alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama wanajeshi hao walio endelea kumshangaa.

“Wewe ni nani?”

“Hupaswi kufahamu kwamba mimi ni nani, kazi tuliyo pewa tumeifanya, sasa jukumu lenu ni kumlinda mtoto huyo na kuwa salama. Tumeelewana?”

“Ndio”

Dump akarudi kwenye gari na kuingia, na wakaondoka katika eneo hilo kwa mwendo wa kasi. Wanajeshi hao wakamchukua Charity na kumuingiza ndani ya ubalozi huo na moja kwa moja wakampeleka hadi ofisi ya balizi bwana Tom Sand.

“Ameletwa na nani?”

“Hatuwafahamu ila wanaonekana ni Wamarekani”

“Nileteni video iliyo rekodiwa na kamera za getini na hakisheni kwamba daktari anampatia mtoto huduma ya kwanza”

“Sawa muheshimiwa”

Balozi bwana Tom Sand akchukua simu yake na kumpigia raisi Dustan aliyopo nchini Marekani. Simu yake kwa haraka ikapokelewa na sekretari wa raisi Dustan na moja kwa moja kakabidhiwa raisi Dustan

“Niambie Tom”

“Muheshimiwa mwanao hadi sasa hivi yupo mikononi mwatu ameletwa na watu wambao inasadikika kwamba ni wamarekani”

“Ohoo asante Mungu, hakisheni kwamba unatuma vijana na watu hao wanakamatwa na kuwekwa nchi ya ulinzi haraka iwezekanavyo”

“Sawa muheshimiwa raisi ila samahani wanakamatwa kisa nini kwa maana wanaonekana ni watu wema?”

“Fwata amri yangu na usiulize maswali yoyote juu ya hilo sawa”

“Sawa muheshimiwa raisi”

Balozi Tom Sand akakata simu yake na kumtazama msaidizi wake.

“Niitie mkuuwa jeshi”

“Sawa”

Bwana Tom Sand akaka kwenye kiti chake huku akitafakari juu ya amri aliyo kabidhiwa na raisi Dustan ambaye ndio msamaji wa mwisho wa maamuzi yote yanayo husiana na kazi yake. Akaingia mkuu wa kikosi cha jeshi la Marekani kinacho linda ubalozi huo ambao upo katika nchi hatari inayo sifika kwa matukio mengi ya ugaidi.

“Kuna watu wawili wamemleta Charity mtoto wa raisi Dustan, ninahitaji muweze kuwafwatilia na muweze kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi”

Mkuu huyo wa jeshi bwana Lindagard akamtazama balozi Tom Sand, kisha akatoa simu yake mfukoni aina ya iphone 7 na kumuonyesha balozi huyu picha za Dump na Dumbe.

“Muheshimiwa ninawapenda sana vijana wangu na wengi wapo hapa kwa ajili ya kukulinda wewe muheshimiwa, hawa watu hatari sana katika majeshi ya Marekani, kama waifanya kazi ya kumleta huyu binti hapa ikulu. Chukua simu yako mpigie raisi na umuambie kwamba kazi hiyo huto weza kuifanya”

“Samahani”

“Umenisikia vizuri, siwezi kumtoa mwanajeshi wangu hata mmoja kwenda katika kuwafwatilia hao watu. Muambie muheshimiwa raisi kwamba nimekataa, kwa maana yeye ndio mtu aliye waachilia na yeye ndio mtu atakaye warudisha”

Siri ya raisi Dustan katika kuwashikilia Dump na Dumbe, General Lindagard anaifahamu vizuri sana, na hata uhatari wa watu hao anaufahamu vizuri na anafahamu matukio yao ambayo wamesha wahi kuyafanya huko nyuma.

“General ni kosa kubwa la kikatiba kukataa amri ya raisi”

“Ni kwako ila si kwangu, wewe muambie raisi Dustan kwamba General Lindagard amekataa kabisa katika kuiendesha oparesheni”

Balozi Tom Sanda akashusha pumzi nyingi sana kwani ukiachilia kwamba ni amri ya raisi ila hata yeye mwenyewe anamuogopa General Lindagard kwani ni mtu asiye penda masihara na ana maamuzi yake ya kipekee juu ya vijana wake ambao ana waongoza katika ubalozi huu.

Taratibu balozi Lindargard akainyanyua simu yake na kumpigia raisi Dusta, ndani ya muda mfupi simu yake ikapokelewa.

“Ndio”

“Muheshimiwa raisi General Lindagard amekataa kazi”

Balozi Tom Sand alizungumza huku akimtazama general Lindagard ambaye amesimama wima huku mikono yake akiwa ameikunja kwa kuielekezea nyuma.

“Amekataa…….!!”

General Lindagard akapiga hatua hadi kwenye meza ya balozi Tom Sand, akampokonya mkonga wa simu alio ushika na kuuweka sikioni mwake.

“Muheshimiwa raisi, ninajua unajua nini nina zungumzia, nina wapenda vijana wangu na kama ulikuwa na mipanngo mibaya na watu wale, kwa ushauri wangu. Kwa usalama wako na usalama wa nchi ni vyema ukaachana nao kwani itawagarimu katika maisha yako. Kikubwa tufanye mpango wa kumrudisha mwanao nchini Marekani na uandelee na maisha yako. Umenielewa muheshimiwa raisi”

General Lindagard alizungumza kwa msisitizo na kumfanya raisi Dustan kupatwa na kigugumizi cha kumjibu general huyo.

“Ukimya pia ni jibu moja zuri hivyo basi sahau kama ulitoa amri hiyo ya kuwatafiya Dump na Dumbe.”

Mara baada ya General Lindagard kumaliza kuzungumza maneno hayo akaka simu hiyo.

“Vinana wangu wawili wana msindikizi binti wa makamu wa raisi hadi nchini Marekani huo ndio msaada wangu wapekee nilio utoa kwa ajili ya binti huyo sawa”

“Sawa”

“Maandalizi yote mengine ni wewe na nchi ofisi yako. Asante”

General Lindagard mara baada ya kuacha maagizo hayo kwa Balozi Tom Sand akatoka ofisini humo na kumuacha Balozi Tom Sand akiwa na mshangao sana kwani inakuwaje jeneral wa jeshi tena katika ubalozi anakuwa na nguvu kubwa na amari kuliko yeye na raisi Dustan.

‘Kuna kinacho endelea hapa si bure’

Nalijsema kimoyo moyo huku akitingisha kichwa chake.

***

“Nina kitu ninahitaji kukushauri Livna?”

K2 alizungumza mara baada ya kumaliza kuoga na kuingia chumbani kwa Livna ambaye tayari amesha amua kumpa makazi ya kuweza kuendelea kukaa hapo hadi pale mambo yatakapo kuwa sawa.

“Ushauri gani?”

“Nahitaji tumuue kwanza raisi Rahab kisha ninajua ni nini cha kufanya juu ya Eddy najua itakuwa ni raisi kuwa karibu sana na Eddy na nitamshawishi sana kuiachia nchi kwa amani na hapo tutapata ushindi mnono”

K2 alizungumza huku akikaa kitandani kwa Livna aliye valia bikini tu na sidiria.

“Hayo mambo kwa sasa nimechoka kuyasikia, ninahiaji kukipumzisha kichwa changu na sitaki fujo”

Jibu la Livna likapnyesha dhairi limemkatisha tamaa K2 aliye tamani sana kuweza kijibiwa vizuri na kukubaliwa.

“Samahani kama nitakuwa nimekuudhi”

“Nataka nipumzike, toka chumbani kwangu”

Livna alizungumza kwa hasira kidogo. K2 akasimama akapiga hatua mbili mbele kisha akageuka na kumtazama Livna jinsi alivyo jilaza kihasara hasara hapo kitandani. Taratibu K2 akamsogelea Livna na kukaa tene pambeni yake.

“Nimekuambia kwamba ninahitaji kupumzika vipi?”

Livna alizungumza huku akiwa amekunja sura yake akionyesha dhairi kwamba amekasirika.

“Shiii…….”

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG