Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

AIISSII U KILL ME LEGACY SEHEMU YA 8/10

 


AIISSII U KILL ME LEGACY

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+

SEHEMU YA 8 KATI YA 10

 


Jojo alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Sitaki kuona hayo maisha yanageukia kwako. Sipendi kukuona siku unakufa au unafika uzeeni ukiwa huna mbele wala nyuma.”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama Jojo kwa macho yaliyo jaa masikitiko sana. Jojo taratibu akakilaza kchwa chake kwenye bega langu la kushoto huku akiichezesha chezesha miguu yake ndani ya swimming pool hili.

“Kwenye maisha yangu hakuna kitu ambacho nina kipenda kama familia. Hususani watoto, alafu Randy unatambua kwamba una mtoto”

“Nina mtoto!!?”

“Kwani mama yako hakukuambia hilo jambo?”

Nikavuta kumbukumbu za swala hili na nikamkumbuka Marieta.

“Kuna binti anaitwa Marieta ana mtoto wako wa kike hembu jaribu kujiweka karibu naye. Au unahitaji kuishi maisha kama aliyo kulea Yemi ya kukaa mbali na baba yako?”

“Hapana”

“Kesho hembu jaribu kumtafuta huyo binti”

“Hivi yupo wapi?”

“Mama yako nina imani kwamba anaweza kuwa na majibu kamili sana. Ila sasa ni saa sana usiku na wamesha lala hakuna haja ya kumsumbua”

“Sawa nitafanya hivyo”

Jojo akakaa vizuri na kujinyoosha viungo vyake huku akipiga miyoyo.

“Nimechoka mimi ninakwenda kulala”

“Sawa usiku mwema. Mimi sina hata usingizi kabisa kwa maana nililala muda mrefu”

“Poa”

Jojo akaondoka na baada ya dakika kama tatu, Tatiana akafika katika eneo hili huku akiwa amejifunga taulo kubwa ambalo hupatikana kwenye vyumba vya kila mteka katika hoteli hii.

“Mbona hujalala”

Niliwahi kumuuliza Tatiana kabla hata hajanisemehesha. Akavua taulo hili na kubakiwa na bikini pamoja na sidiria.

“Nimeishiwa na usingizi ndani, nimeona nije kuoga oga kidogo nahisi mwili wangu utachangamka”

Tatiana akajirusha ndani ya swimming pool hili na kuanza kuogelea taratibu. Sasa hapa ndipo nikapata nafasi ya kuuchunguza vizuri mwili wa mwanamke huyu. Mapaja ya Tatiana yamejazia kiasi na yameshikilia makalio yake makubwa kiasi ambayo kwa namna moja ama nyingine yanamvutia kila mwanaume ambaye ana mtazama. Kiuno chake chembaba kimeshikilia tumbo lake ambalo si kubwa kama ilivyo kwa wanawake wengi wanao jaliwa shepu nzuri kuwa na matumbo makubwa. Kwa haraka haraka mtu akikuambia kwamba Tatiana ni mlimzi mwenye uwezo mkubwa sana katika maswala ya upambanaji unaweza ukakataa kwani haendani kabisa na sifa hiyo.

“Njoo uogelee”

“Wewe endelea tu”

Nilimjibu Tatiana huku nikimtazama jinsi anavyo geuka tena na kuanza safari ya kuelekea upende mwengine wa hili swimming pool ambalo ni kubwa sana. Kila jinsi Tatiana anavyo zidi kuogelea ndani ya swimming pool hili akazidi kunipa hamasa na mimi, nikavua pensi niliyo ivaa pamoja na tisheti kisha taratibu nikaingia ndani ya swimming hili, ila kitu ambacho nimekifanya ni kuingia chini kabisa ya swimming hili na kuanza kuogelea kwa kasi hadi sehemu alipo Tatiana na nikijaitokeza mbele yake jambo lililo mfanya kustuka sana.

“What the fuc**……..!!!!”

Tatiana alizungumza huku akinitazama kwa mshangao mkubwa sana. Sikumjibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kucheka. Tatiana akanipia vibao ambayo si vya kuniumiza sana mwilini mwangu.

“Wewe si kamanda, mbona una ogopa hivyo?”

“No…sikutarajia kukuona hapa na wala sikuwa na wazo hilo Randy”

“Pole”

Tatiana hukunijibu kitu chochote zaidi ya kunitazama usoni mwangu kwa macho makelegevu ambayo hakika yanazidi kuuonyesha uzuri wake wa asilia. Uvumilivu ukatushinda sote wawili na kujikuta tukianza kunyonyana lipsi zetu huku kila mtu akimkumbatia mwenzake ndani ya maji haya.

“Mmmmm”

Sauti ya mlinzi aliye shika tochi mkononi mwake, ikatufanya tuachiane huku tukitazamana.

“Samahani kwa kuwashutua”

“Bila ya samahani”

“Ahaa ninaomba muweze kuelekea ndani kwa maana muda wa mwisho kuogelea kwenye swimming pool ni saa sita usiku na hivi sasa inaelekea saa tisa”

“Ohoo sawa sawa kiongozi tunatoka. Samahani kwa hilo”

Nilizungumza huku nikianza kuogelea hadi zilipo ngazi za kutokae ndani ya swimming pool hili. Nikachukua nguo zangu pamoja na taulo la Tatiana. Tukaondoka eneo hili huku mlinzi akitusindikiza kwa macho. Tukaingia kwenye lifti na kuendelea kunyonyana lipsi zetu huku kila mmoja akionekana kujawa na hamu ya kuhitaji kupata raha ya mwezake. Lifti ikafunguka na moja kwa moja tulaekekea chumbani kwa Tatiana, nikamnyanyua na kuendelea kunyonyana naye.

“Mmmm…..aiiisii”

Tatiana alitoa miguno hiyo mara baada ya kuanza kukichezea kitumbua chake. Nikafungua mikanda ya bikini yake kumlaza kitandani huku nikivua boksa yangu.

“Randy”

“Mmmmm”

“Mimi ni bikra?”

“Kweli?”

“Haki ya Mungu, na sheria za kikundi chetu ni lazima sote tuwe bikra”

“Unaogopa nikiitoa bikra yako?”

“Nahofia mkuu wangu akifahamu”

“Usijali nitamueleza kila jambo”

“Kweli?”

“Ndio mpenzi wangu”

“Sawa”

Nikaendelea na zoezi langu la kuutomasa mwili wa Tatiana na nilipo hakikisha kwamba yupo tayari kwa kuliwa, taratibu nikaanza kumpa kitu ambacho wanawake wote nina imani wanapenda.

***

Asubuhi nikawahi kuamka ila cha kushangaza sikuweza kumkuta Tatiana chumbani humu, nikaingia bafuni ila pia sikuweza kumkuta. Nikavaa nguo zangu na kutoka chumbani humu na kuingia katika chumba changu. Kabla sijamaliza kufanya jambo lolote, akaingia Livna huku usoni mwake akionekana kama mtu mwenye jambo ambalo limkera.

“Mama karibu”

Nilizungumza kwa kujistukizia, Livna hakunijibu jambo lolote zaidi ya kunisogelea karibu yangu. Nikameza fumba zito la mate kwani katika siku zote ambazo nina mfahamu Livna sikuweza kumuona akiwa katika hali ya kugadhibika kama hii.

“Unahisi nimeleta walinzi wangu hapa kwa ajili ya kutomb** na wewe si ndio”

Livna alizungumza huku akinishika sehemu zangu za siri kwa kiganja chake cha mkono wa kulia na kuanza kuziminya kwa nguvu jambo lililo nifanya nianze kugugumia kwa maumivu makali sana ambayo hayana lugha nzuri ya kuelezewa.



Livna akazidi kunitazama usoni mwangu kwa ukali sana.

“Ni….n…sa…mehe mama”

Nilizungumza kwa kubabaika kwani bado ninaendelea kuyasikilizia maumivu ambayo Livna ananipatia. Taratibu Livna akaziachia sehemu zangu za siri kisha akatoka chumbani humu na kuniacha nikimsindikiza tu kwa macho. Nikatoka chumbani humu huku nikiwa nina chechemea.

“Wewe vipi mbona una chechemea?”

Mama aliniuliza na kunifanya nistuke sana, nikageuka na kumtazama na kumkuta akiwa ametoka katika chumba chao.

“Ahaa..nipo poa”

“Una uhakika?”

“Ndio mama kwani vipi?”

“Unatembea kama umeumia sehemu”

“Nipo sawa mama yangu, niamini”

“Sasa baada ya kupata kifungua kinywa nina hitaji tuelekee sehemu mimi na wewe”

“Sehemu gani?”

“Utaijua mara baada ya kueleka hiyo sehemu”

“Sawa”

Nikaachana na mama na kugonga chumba cha Jojo, baada ya muda kidogo mlango ukafunguliwa.

“Dogo vipi?”

“Bado umelala?”

“Yaa si unajua jana usiku tulichelewa kulala eheee niambie vipi mbona mapema sana”

Jojo alizungumza huku akinipisha mlangoni. Nikapitiliza moja kwa moja na kukaa kitandani kwake.

“Mbona una chechemea, umekumbwa na jambo gani?”

“Yaani wee acha, Livna amenibana sehemu zangu za siri kwa sababu ya msichana wake”

“Tatiana?”

“Ndio, jana usiku nililala naye”

“Weee ehee?”

“Ndio hivyo sijui imekuwaje Livna amefahamu na mbaya zaidi nimemkuta na bikra yake kabisa”

“Nilikuambia yule msichana naa kupenda ana mejitunza hadi kufika hatua hiyo. Hembu tazama ni wanawake wangapi ambao umetembea nao na hukuwahi kukuta hili jambo”

“Ni wengi ila sijajua ni kitu gani ambacho Livna amemfanya Tatiana kwa maana niliamka asubuhi sana ila sikuweza kumkuta kitandani”

“Mmmm labda kuna sehemu atakuwa ameagizwa na mkuu wake”

“Ehee mbona swala la kwenda katika nchi ambazo Danya alitupangia halitiimii kuna nini kinacho endelea?”

“Kuna maswala ambayo Dany ana yafwatilia yakikamilika basi tutakwenda”

“Poa acha nikapate kifungua kinywa kwani kuna sehemua mbayo mama ameniambia anahitaji tuweze kwenda”

“Haya mimi nina endelea kulala kidogo kwa maana bado nimechoka sana.”

Nikatoka ndani kwa Jojo, nikaingia ndani ya lifti, nikashuka hadi katika eneo ambalo wateja wa hii hoteli hupata kifungua kinywa. Nikakutana na bi Jane akiwa anazungumza na wazee wawili, alipo niona akaniita kwa ishara na nikawafwata katika sehemu waliyo kaa.

“Habari yako Randy”

“Salama”

“Naomba uketi hapo”

Nikaka katika kiti ambacho hakina mtu na kuwatazama wazee hawa.

“Randy kutana na bwana Juma Kiiti pamoja na bwana HassanTola. Hawa ni wafanya biashara wakubwa hapa nchini Tanzania na wamewekeza katika katika biashara ya mahoteli makubwa ya kitalii katika jiji la Arusha na Mwanza”

“Nashukuru kuwafahamu”

“Hata sisi kijana, pia pole sana kwa kuodokewa na mke wako kwani siku ya harusi yako tulipanga kuja ila kuna matizo kidogo yalitoke ana kwa bahati mbaya tukasikia jambo lililo jitokeza hivyo pole sana”

“Ninashukuru sana wazee wangu”

“Randy kuna maswala ya kibiashara nilikuwa nina jadiliana na waheshimiwa hapa ila baadaye nikimaliza nitakushirikisha sawa”

“Sawa, ninashukuru”

Nikaagana na wazee hawa na kukaa katika meza nyingine, nikaagiza kifungua kinywa. Danya akaka kiti cha mbele yangu na kunitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatabasamu.

“Dogo ndio umemfanya nini binti wa watu?”

‘’Ehee?”

“Siku nyingine kabla ya kufanya jambo inabidi uwe una niuliza sawa”

“Sawa”

Dany akanyanyuka na kuondoka na nikabaki nikiwa nina maswali mengi sana kichwani mwangu kwani sikutarajia kwamba jambo hili linaweza kuwa kubwa kiasi hichi. Nikanyanyuka na kufwata Dany sehemi anayo elekea.

“Baba”

Nilimuita Dany, akasimama na kunigeukia.

“Kwani hili swala ndio limekuwa kubwa kiasi hichi?”

Dany taratibu akashusha pumzi huku akinitazama usoni mwangu.

“Ndio limekuwa ni jambo moja kubwa sana japo nilijaribu kuzungumza na Livna ila bado anaonekaja kujawa na hasira”

“Sasa baba kwanini inakuwa hivi?”

“Unajua wale wasichana wameandaliwa kwa ajili ya kazi moja tu dunia. Kulinda watu au kufanya mission wanazo pewa na watu wanao wahitaji waweze kupewa. Ila hawapo kwa ajili ya mapenzi na wote wale wasichana ulio kuwa ukiwaona nyumbani ni ma bikra hivyo kufanya hivyo kumtoa msichana huyo ni tatizo moja kubwa sana ambalo linaweza kupelekea msichana huyo kupewa adhabu kali sana ikiwemo ya kuuwawa”

Nikastuka kidogo huku nikimtazama Dany usoni mwake.

“Usistuke huo ndio ukweli ndio maana binti yule alijaribu kutoroka ila Livna aliweza kudhibiti na hivi ninavyo zungumza amerudishwa kambini kwao kwa ajili ya adhabu inayo stahili”

Nikahisi mwili mzima ukiishiwa na nguvu huku nikimtazama Dany.

“Sasa baba kambi yao ipo wapi?”

“Siwezi kukuambia na hili swala si la kuliingilia acha Livna afanye anacho kifanya kwa wafanyakazi wake. Sihitaji tuweze kumuingilia kwenye mamlaka yake japo nina mahusiano naye ila acha iwe hivyo?”

“Kwani Livna yupo wapi?”

“Ameshaondoka muda mrefu sana”

“Kwenda wapi?”

“Huko kwenye kambi yake”

“Baba tafadhali ninakuomba niweze kuzungumza na Livna. Tatiana alisha nieleza juu ya hili swala ila nilishindwa kujizuia. Hivyo matatizo hayo yote ni kwa ajili yangu baba. Tafadhali ninakuomba unipe nafasi niweze kuzungumza na Livna”

“Siwezi kuzungumza hivyo kwa maana laiti kama wewe ungekuwa si mwangu, angekua kwa manaa umemkosea sana”

Nikajikiya Nikiwa nimeishiwa hata hamu ya kumuona Livna kwani siku zote nilizo ishi naye na kucheka naye kumbe ni mwanamke asiye hitaji masiraha kabisa na vitu vyake.

“Kuwa makini sana na walinzi wa Livna si wakuchezea kabisa”

Dany alizungumza huku akinipiga piga begani, akaondoka na kuniacha nikiwa katika hali ya sinto fahamu.

“Nenda kajiandae twende”

Yemi alinongelesha huku akinitazama usoni mwangu. Nikabaki nikimtazama bila ya kumjibu kitu chochote.

“Unanielewa au?”

“Umesema?”

“Nenda kajiandae tutoke nina kunywa chai nikimaliza uwe umesha jiandaa”

“Tunakwenda wapi kwani?”

“Wewe nenda bwana, mbona maswali Mengi Randy”

Mama alizungumza kwa msisitozo huku akinitazama usoni mwangu. Nikarudi chumbani kwangu, nikaoga kisha nikajianda na safari ambayo mama anahitaji tuelekee ila kusema kweli kichwani mwangu nina mawazo mengi sana ambayo yananikosesha raha na amani. Nikarudi sehemu nilipo muacha mama na kumkuta akizungumza na bi Jane.

“Umependeza mwanangu”

Yemi alinisifia huku akinitazama kuazia juu hadi chini.

“Tuondoke”

“Mbona unazungumza kinyonge kiasi hicho mwanangu”

“Twende bwana mama”

Tukaelekea eneo la maegesho ya magari.

“Unaendesha nikuendeshe?”

“Niendeshe tu mama”

Tukaingia ndani ya gari na kuondoka eneo hili. Ukimya ukazidi kutawala ndani ya gari huku mama akizidi kuendesha gari hili na kueleeka sehemu ambayo siifahamu.

“Mbona umekuwa kama mtu aliye poteza raha mwanangu?”

“Nipo poa tu”

“Mimi ninakujua kuliko mtu yoyote wala haupo poa, hembu niambie tatizo ni nini?”

“Mama nielewe bwana. Tunaelekea wapi kwani?”

Mama akanitazama na kuto kunijubu jambo la aina yoyote. Tukafika kwenye moja ya mtaa wa uswahilini ambao nyumba zake ni za watu wenye maisha ya kati. Mama akasimamisha gari hili nje ya moja ya nyumba ambayo nje ya baraza pamejaa wana mama wengi wakizungumza zungumza.

“Hapa ni wapi mama?”

“Wewe twende ndani”

“Humo ndani!!?”

“Ndio unaogopa nini, hembu shuka kwenye gari twende”

Nikawatazama wanamama hawa ambao wanacheka cheka huku wote macho yao yakiwa katika gari letu. Tukashuka wote wawili, tukawasalimia wana mama hawa na kuingia ndani ya hii nyumba ambayo eneo la kordo limejaa ndoo za maji pamoja na madungu. Mama akasimama kwenye moja ya chumba na kugonga baada ya muda mlango ukafungulia na kujikuta nikistuka sana mara baada ya kumuona Marieta akiwa amesimama mlangoni hapa huku akiwa amembeba mtoto wa kike ambaye kitendo cha kumtazama usoni mwake nikaiona sura yangu jambo lililo nifanya mwili mzima unisisimke huku machozi yakinilenga lenga.



“Karibu mama”

Marieta alizungumza huku akiufungua mlango wote, mama akawa mtu wa kwanza kuingia ndani kisha nikafwatia mimi huku macho yangu yote yakimtazama mtoto huyu wa kike. Chumba anacho ishi Marieta ni kidogo kiasi, kina kitanda kimoja, sofa la mtu moja pamoja na meza ya kioo. Mama akaka kwenye sofa kisha mimi na Marieta tukaka kitandani. Marieta akamkabidhi mama mtoto.

“Anaendeleaje Yemi wangu”

Mama alizungumza huku akimtazama mtoto huyo ambaye ni wa kwanza kwa asilimia mia moja na wala sina sababu ya kumkataa wala kumkana.

“Leo kidogo ameamka na viji homa homa”

“Ahaa, ila umempeleka hospitalini?”

“Hapana mama sijampeleka”

Marieta alizungumza katika hali ya woga, nikaitazama nikono yake na kuona alama ambazo alishambuliwa na mama kipindi alipo tekwa.

“Randy huyu ni mwanao nimempatia jina langu la Yemi”

Mama alizungumza kwa furaha huku akinikabidhi mwanangu. Kwa mara yangu ya kwanza maishani kumshika mtoto ambaye ni wangu. Ni mtoto mzuri na aliye jaliwa afya njema.

“Ninawapa nafasi muzungumze”

Mama alizungumza hukua kinyanyuka, akatoka ndani humu na kuniacha na Marieta ambaye akanitazama kwa woga na machozi yakaanza kumwagika. Yemi akanikumbatia taratibu huku akiangua kilio kikubwa sana.

“Randy ninaogopa, nina muogopa mama yako”

Yemi alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu.

“Imekuwaje unaishia kwenye mazingira kama haya?”

“Nimekuja kujificha huku, hata sifahamu amejuaje”

Yemi alizungumza huku akiwa emenikumbatia. Yemi akaniachia na kuelekea mlangoni, akaufunga mlango kwa ndani kisha akavua dera lake alilo livaa. Macho yakanitoka kwa jinsi alama za makovo zilivyo mtawala mwilini mwake.

“Hichi ndicho alicho nifanya mama yako. Randy maisha yangu yamekosa muelekeo asinge kuwa ni mwanangu. Haki ya Mungu sasa hivi ningekuwa nimesha jiua”

Marieta alizungumza kwa uchungu sana huku akiwa uchi kabisa. Nikamuweka Yemi pembeni na kusimama, nikamsogelea sehemu alipo simama na kuanza kuuchunguza mwili wake, hasira kali dhidi ya mama yangu ikazidi kunitawala kwani si kwa unyama huu alio mfanyia binti huyu. Msichana ambaye amejaliwa uzuri mkubwa ila ndio hivyo amekumbana na mateso makali ambayo hakustahili kuweza kuyapata.

“Yote haya ni kwa ajili yako. Mama yako aliniweka mbali na wewe. Mama yako alininyanyasa kiasi cha kunifanya nikate tamaa. Hakuishia hapo akanileta hadi kanisani niweze kushuhudia hasuri yako akinidhihirishia kwamba sina hadhi ya kuwa na wewe. Randy moyo wangu hauwezi kukusaha, kwani bila ya wewe sasa hivi mimi nisinge kuwa hai”

Marieta alizungumza kwa uchungu sana huku akinitazama usoni mwangu. Nikamkumbatia kwa nguvu sana huku nikiungana naye katika kilio hichi ambacho kusema kweli kina toka moyoni.

“Nitazunumza na mama yangu. Nahitaji kuijenga amani yetu”

“Hapana Randy, siwezi kumpenda mama yako. Randy nilikuwa na maisha mazuri, nilikuwa na familia nzuri ila wazazi wangu na ndugu zangu ambao niliwajengea maisha mazuri kutokana na pesa ambayo ulinipatia wote wamewawa”

“Nini?”

“Ndio, mama yako aliwaua katika kifo kibaya sana. Aliwachoma moto kama wanyama”

Yemi aliendelea kuzungumza kwa uchungu uhuku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga. Marieta kwa hali aliyo nayo amekuwa ni mtu aliye athirika kisaikolojia. Kilio cha mtoto wetu niliye mlaza kitandani kikatufanya tukatishe mazungumzo yetu. Marieta kwa haraka akaikimbilia kitandani na kumtazama mtoto.

“Kuan kitu gani cha muhimu hapa?”

“Eheee?”

“Kuna jambo gani la muhimu hapa nyumbani kwako. Nahitaji tuhame sasa hivi”

“Randy kutoka kwangu humu ndani ndio kufa kwangu, nina shukuru hata hii nyumba kuna watu wengi kidogo sinto weza kuudhurika”

“Nisikilize mimi, nna kuhakikishia kwamba hakuna mtu ambaye ataweza kukushika”

“Hapana Randy”

“Niamini Marieta. Kama nilikuakoa kwenye maisha yako siku ambayo ulitaka kubakwa na kuuwawa basi wewe na wanangu ni watu muhimu. Vaa nguo tuondoke”

Nilizungumza kwa msisitizo ulio jaa hasira. Taratibu Marieta akavaa dera lake. Kusema kweli Marieta ana hali ngumu kwani amekonda kiasi cha kunifanya nijawe na huruma kubwa. Nikambeba mtoto na kufungua msumari ulio fungia mlango huu.

“Mama Asha nitazamie chumba changu ninampeleka mwanagu hospitalini”

Marieta alimuambia mwana mama mmoja tuliye mkuta akiwa amekaa kwenye kordo hii akipiga mboga.

“Sawa ana umwa na nini mtoto?”

“Homa tu rafiki yangu. Nitazamie”

“Sawa”

Nikamshika Marieta mkono na kutoka naye nje, nikamkuta mama akiwa ameegemea gari tulilo jia huku akizungumza na simu. Alipo tuona akaka simu.

“Munakwenda wapi?”

Mama alizungumza huku akitutazama, nikamtazama kwa macho ya ukali ambayo nina imani hii sio mara ya kwanza kwa mama kuweza kuyaona.

“Kwa jinsi ulivyo mfanya mama wa mwanangu, siwezi kukusamehe hata kidogo mama”

Nilizungumza kwa hasira sana na mama akabaki akiwa ameduwaa. Nikasimamisha moja ya bajaji na sote tukaingia.

“Wewe Randy umechanganyikiwa”

Mama alizungumza huku akituchungulia ndani ya hii bajaji.

“Dereva tuondoke”

Dereva akatii amri yangu na kuondoka eneo hili, nikageuka nyuma na kuliona gari la mama likija kwa kasi. Mama akaipita bajaji hii na kuizuia kwa mbele na kusababisha dereva bajaji kufunga breki za gafla. Mama akashuka kwenye gari huku akiwa amejawa nahasira kali.

“Usitake kuniabiasha kijinga. Ingia kwenye gari”

“Niingie kwenye gari na si tuingie kwenye gari?”

“Randy unanijua nitakutia vibao hapa mbele za watu sinto jali wingi wa watu wa hili eneo.”

Mama alizungumza kwa ubabe ambao siku zote mimi na yeye tumekuwa tukipingana kabisa. Nikamkabidhi Marieta mtoto kisha nikatoka ndani ya bajaji.

“Mama unahisi kwamba nina kuogopa, au unahisi kwamba nina kuhofia eheee?”

Nilizungumza huku nikimkazia macho mama na akaanza kurudi nyuma nyuma kwani mwili wangu wote umevimba kwa hasira.

“Nilihisi umebadilika rohoni mwako. Umemueweka majeraha makubwa mke wangu, umemfanya aishi masha ya woga na wasiwasi kila mara una hisi kwamba ninafurahi kwa vitendo vyako?”

“Randy niliyafanya hayo yote kwa ajili yako mwanagu”

“Acha uongo mama kwa ajili yangu. Vileee eheee?”

Watu wa hapa uswahilini wakaanza kukusanyika taratibu huku wakishangaa majibizano haya na mama yangu. Mama alipo ona kundi kubwa la watu, akatingisha kichwa kisha akaingia ndani ya gari na kuondoka kwa kasi sana. Nikaingia ndani ya bajaji na kumkuta Marieta akiendelea kumwagikwa na machozi huku akitetemeka sana.

“Tuelekee hospitali yoyote nzuri”

“Ipi?”

“Yoyote nzuri hapa Dar kwani wewe hufahamu hospitali nzuri?”

“Sawa muheshimiwa”

Dareva akawasha bajaji na kuendelea na safari. Tukafika kwenye moja ya hospitali kubwa na nikashuka kwa haraka, nikajipapasa mifukoni mwangu na kwa bahati mbaya sina hata shilingi moja.

“Unadai kiasi gani?”

“Elfu kumi na tano”

“Ndo unayo nidai?”

“Ndio”

Niakjichunguza mwilini mwangu na nikaivua saa yangu ambayo nimenunua kwa kiasi cha shilingi laki mbili na nusu.

“Kama unaweza kuniamini, chukua hii saa yangu, niwasiliane na mtu ambaye anaweza kunletea pesa hapa hospitalini kisha nitakulipa kwa maana kama ulivyo weza kuona mambo yaliyo tokea kati yangu mimi na mama yangu pesa nmeacha ndani ya gari mule”

Dereva huyu bajaji akatazama saa yangu kwa muda kisha akaipokea.

“Una simu?”

“Ndio”

“Naomba uniazime”

Dereva bajaji akatoa simu yake na kunikabidhi.

“Ina sekunde za kukopa, labda ubipu tu”

“Sawa. Marieta usishuke”

Nilizungumza huku nikimtazama Marieta na mwanangu. Nikaiandika namba ya bi Jane, nikaibipu kisha nikasubiria ili anipigie. Zikapita dakika mbili bila ya bi Jane kunipigia, nikambipu tena, baada ya sekunde kama kumi hivi akapiga.

“Nipo kwenye kikao nitakupigia”

“Usikate simu Jane”

“Randy!!!”

“Ndio ni mimi”

“Jamani samahani, ninasimu muhimu hapa”

Nilimsikia bi Jane akizungumza nina imani kwamba yupo na wafanya biashara.

“Randy vipi mbona namba mpya”

“Nina matatizo nipo katika hospitali ya…..”

Nikaanza kutafuta jina la hospitali hii.

“BIAFRA. Ninahitaji uje haraka kama inawezekana”

“Ohoo Mungu wangu, una tatizo gani Randy”

“Ninakuomba uweze kuja”

“OKAY dakika kumi nitakuwa hapo”

“Sawa”

Nikakata simu na kurudi ndani ya bajaji.

“Jamaa unaweza kumsubiria mtu ambaye atakuja kuniletea pesa”

“Ila pesa itaongezeka ya kukusubiria”

“Haina shida ndugu ila kama inawezekana nina kuomba uweze kumsubiria kama dakika kumi na tano hivi”

“Poa”

Nikamtazama Marieta, taratibu akakilaza kichwa chake begani mwangu, nikamtazama mwanangu na kumkuta akiwa amejawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Nitahitaji tuondoke twende mbali na hapa”

“Wapi?”

“Popote ila ninahitaji tuondoke hapa na kwenda mbali kabisa. Ni muda wa mimi kuweza kuilinda familia yangu sasa”

Taratibu Marieta akashusha pumzi. Baada ya dakika kama kumi na mbili hivi, nikaoga gari la bi Jane likisimama kwenye maegesho ya magari. Nikashuka kwenye bajaji na kumfata sehemu alipo.

“Randy kuna tatizo gani?”

“Una elfu thelathini hapo?”

“Ndio”

Bi Jane akafungua pochi yake na kunikabidhi noti tatu za shilingi elfu kumi. Nikamfwata dereva wa bajaji na kumkabidhi noti hizi pasipo hata kumdai chenchi, akanikabidhi saa yangu kisha nikamuomba Marieta ashuku ndani ya bajaji na mtoto. Bi Jane akaonekana kumshangaa mtoto aliye bebwa na Marieta.

“Mwanangu ana umwa pamoja na mama yake nitahitaji unisaidie”

“Sawa hakuna tatizo, twendeni ndani wakapatiwe matibabu”

Tukaingia ndani ya hospitali hii, wahudumu wa hapa wakaanza kumchangamkia bi Jane huku wengi wao wakionyesha kumfahamu bi Jane. Tukaingia kwenye chumba cha daktari mkuu, mtoto akaanza kupewa matibabu ya haraka.

“Randy tunaweza kuzungumza?”

Bi Jane alizungumza huku akinitazama usoni mwangu. Tukasimama na kutoka katika chumba hichi cha matibabu.

“Randy kwa nini hukuwahi kuniambia kwamba una mtoto?”

“Ni stori ndefu sana ambayo kichwa changu kikitulia nitakuambia. Ila kwa sasa ninakuomba unisaidie kiasi cha pesa na ninaomba niweze kupata hati ya kusafiria kwa maana ninahitaji kuelekea nchini Afrika kusini. Nahitaji kwenda kuanza maisha mapya huko na familia yangu. Swala la kumtafuta Farida kwa ajili ya kulipiza kisasi limeishia leo. Sitaki kuipoteza familia yangu sawa”

Bi. Jane akabaki akiwa amejawa na mshangao kwa jinsi nilivyo kuwa nimejawa na hasira ya kulipiza kisasi dhidi ya Farida, si rahisi kwa watu wanao nifahamu kuamini kwamba nimeweza kusamehe yale yote yaliyo tokea dhidi ya mke wangu wa ndoa Victoria.



“Sawa”

Bi Jane alinijibu kwa unyonge mara baada ya kuona nimesimama kwenye msimamo ambao hakuna mtu amabye anaweza kuupinga.

“Nahitaji kuwa ndani sasa”

Nilizungumza na kurudi katika chumba cha matibabu, nikakuta manesi na madaktari wakimpatia matibabu Marieta.

“Mr tunakuomba uweze kutoka nje”

“Ila huyo ni mke wangu”

“Tunalifahamu hilo ila tunakuomba uweze kutupa muda”

Daktari alizungumza kwa msisitizo, taratibu nikafungua mlango na kutoka nje ya chumba hichi. Nikaka kwenye moja ya kiti kilichopo kwenye kordo hii. Haukupita muda mrefu sana nikamuona Bi Jane akiwa ameongozana na Jojo pamoja na Dany.

“Dogo kuna nini kinacho endelea?”

Dany aliniuliza na kunifanya nisimame. Nikapata kigugumizi cha kuwajibu kwa maana sifahamu nianze kuwaadisia wapi.

“Ehe….!!”

“Ni hivi Dany. Randy alinipigia simu akaniomba niweze kufika hapa hospitalini. Nilimkuta akiwa an msichana mmoja hivi pamoja na mtoto ambaye kwa kumtazama tu ni copy na paste ya Randy”

“Unataka kusema kwamba yule mtoto ambaye mama yako aliniambia yupo hapa hospitalini?”

“Ndio”

“Sasa ni yeye ndio anaumwa au ni mama yake?”

“Wote”

Nilijibu kwa kifupi. Dany akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaomba kuonyeshwa ni chumba gani walipo. Akaingia kwenye chumba hicho bila hata ya kubisha hodi. Zikapita kama dakika tano bila ya Dany kutoka ndani ya chumba hicho. Nikataka kwenda ila Jojo akanishika mkono.

“Tulia”

“Kuna nini kinacho endelea huko ndani?”

“Sijui ila tulia, kama wapo katika matibabu jaribu kutuliza munkari.”

Baada ya muda kidogo Dany akatoka huku akiwa amejawa na tabasamu sana. Akanifwata sehemu nilipo na kunipa mkono wake wa kulia, nikautazama kwa sekunde kadhaa kisha nikaupokea.

“Hongera sana, sasa nimemuona mjukuu wangu”

“Nashukuru”

“Ehee matibau wamesema ni kiasi gani?”

“Nimesha walipa”

“Safi, umekua mwanangu. Sasa hivi akili yako inatakiwa ufikirie kama baba. Umenielewa?”

“Ndio maana nina hitaji kuondoka Tanzania na familia yangu na kwenda mbali kuanza maisha mapya”

Kauli yangu ukamshangaza sana Jojo, huku Dany naye akinitazama kwa kunikazia macho.

“Nataka kujenga amani ya familia yangu. Nahitaji kumkuza mwanangu mikononi mwangu. Maswala ya kuishi kwa kulipiza visafi siyahitaji tena. Sitaki kumpoteza Marieta kama ilivyo tokea kwa Victoria”

Dany taratibu akauachia mkono wangu. Hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kukaa katika kiti cha pembeni na kujiinamia.

“Hayo unayo yazungumza yanatoka moyoni mwako. Au kuumwa kwa familia yako ndio kume kuzuzua?”

Jojo aliniuliza kwa umakini.

“Moyoni mwangu na sihitaji maamuzi yangu yapingwe na mtu wa aina yoyote”

“Mmmmm!!!”

Jojo aliguna na kukaa taratibu pembeni ya Dany. Baada ya dakika ishirini daktari ambaye alinisisitizia niweze kutoka katika chumba cha matibabu.

“Dokta vipi hali ya mwanangu na mke wangu”

“Ahaa..tunaweza kwenda kuongelea ofisini kwangu”

“Hakuna tabu”

Tukaanza kuondoka eneo hili, Dany, Bi Jane pamoja na Jojo nao wakaanza kutufwata kwa nyuma. Tukaingia ofisini kwa daktari huyu.

“Hali ya mtoto inaendelea vizuri, hata matatizo makubwa sana.”

“Ohoo asante Mungu”

Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi taratibu.

“Ila shida kubwa ipo kwa mama yake.”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi mithili ya mtu ambaye anapokea majibu ya vipimo vya HIV kwa mara ya kwanza huku nyuma yake akikumbuka listi ya watu alio tembea nao.

“Mama yake moja ameathirika sana kisaikolojia. Ni mtu ambaye amepitia mateso Makali sana japo sifahamu ni mateso gani ambayo alipitia kwa maana mwili wake umejaa alama nyingi sana ma majeraha kama munavyo ziona hapa”

Daktari alizungumza huku akitugeuzia compture yake iliyopo mezani.

“Mmmm jamani”

Bi Jane alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Pia amepoteza kiasi kikubwa sana cha damu, maji. Hivyo tumeweza kumtundikia dripu la maji”

“Jambo jengine kubwa sana ambalo ni zito, inabidi muweze kujiandaa kisaikolojia kabla sijaweza kulizungumza hili”

Mapigo ya moyo yakazidi kunienda kasi hadi jasho likaanza kunimwagika usoni mwangu. Nikastukia tu Jojo akinikabidhi kitambaa chake ili nijifute jasho japo ndani ya chumba hichi kunahewa ya A/C.

“Dokta kama inawezekana naomba uniambie hilo jambo. Watu wote tokeni muniache mimi na daktari”

Dany alizungumza kwa kujiamini na kujikuta nikumtazama kwa mshangao sana kwa maana hili jambo ni la kifamilia na watu wote tunatakiwa tuweze kulisikia.

“Baba hatoki mtu hapa. Daktari endelea?”

“Hapana Daktari, yule ni mkwe wangu na mimi ndio babu wa yule mjukuu kama nilivyo weza kuwaeleza mule ndani. Jojo mchukue mwezako utoke naye”

“Baba ila hili jambo inabidi sote tuweze kufahamu”

Jojo naye akalitilia msisitizo jambo hili na kumfanya Dany kutulia.

“Dokta hembu zungumza, mke wangu ana tatizo gani?”

“Mmmmm….tumeweza kugundua mambo mawili makubwa sana kwa mgonjwa. Jambo la kwaza ni kwamba figo yake moja haifanyi kazi, it’s mean kwamba imekufa”

Nikahisi kama mwili mzima ukianza kuishiwa nguvu, ila nikajikaza ili nisiweze kuonyesha udhaifu wangu kwake.

“Figo hiyo nyingine nayo ina elekea kuishiwa nguvu kwa maana vipigo au mateso aliyo kuwa akikutana nayo kidogo yameweza kumuadhiri sana vitu vya ndani”

“Jambo la pili, tumeweza kugundua kwamba ana saratani ya damu ambayo ni hatari sana na ilisha anza kumtafuna taratibu na kwa kuwapa miezi ya kukadiria tu. Mgonjwa wenu hato weza kumaliza miezi minne au sita lazima ataiaga dunia”

Nikajikuta nikijishika kichwa changu na kushindwa kabisa kujizuia hisia zangu za machozi. Dany akampa ishara Jojo, taratibu Jojo akaninyanyua na tukatoka chumbani hapa na akaanza kunikokota kuelekea nje ya hospitali hii, akaniingiza kwenye gari walilo kuja nalo, kisha na yeye akaingia.

“Wewe si jini?”

Nilimuuliza Jojo kwa upole sana huku mwili mzima ukitetemeka kwa woga.

“Hapana Randy, natambua ni nini unacho taka kukizungumza ila sina uwezo nacho. Siwezi kuzuia binadamu kuweza kufariki dunia”

“Alicho ki..kizu…ungu…mz…a dok…ta…aaa ni cha kweli?”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na kigugumizi kikubwa.

“Ndio mdogo wangu”

“Yote haya ameyasababisha mama”

“Kivipi?”

“Mama alimteka Marieta, ni kile kipindi ambacho tulikuwa na uaduia mkubwa ndio maana mambo yamekwenda kama hivyo yalivyo kwenda”

“Masikini weee, dunia hii”

“Ila kwa hili mama sinto weza kumsamehe kabisa. Haki ya Mungu nina apa kwa jina la mwenyezi Mungu sinto weza kumsaheme”

Nilizungumza kwa msisitizo na Jojo hakuwa na jambo la kufanya zaidi ya kuendelea kunibembeleza. Hadi inafika jioni bado tupo hospitalini hapa. Daktari akanipatia nafasi ya kuingia katika chumba maalumu alicho lazwa Marieta. Nikamkuta akiwa amezungukwa na mashine kadhaa ambazo kwa mimi sina utaalamu zina msaidia nini mwilini mwake. Marieta akatabasamu huku akinipa mkono wake wa kulia ili niweze kuushika.

“Mbona umekuwa mnyonge Randy, au nimekuchosha kwa mimi kuumwa?”

Swali la Marieta bado nusu linitoe machozi ila nikajikaza kiume kwa maana siku nzima ya leo nimeshinda nikimwagikwa na machozi.

“Hamna, ni jukumu langu kuhakikisha kwamba una kuwa salama”

“Kweli mume wangu?”

“Ndio”

“Ila mimi mbona nina jisikia vizuri, imekuwaje madaktari wameweza kunilaza na kuniwekea mamashine haya yote?”

Nikaka kwa sekunde kadhaa huku nikitamani sana kumueleza ukweli Marieta, ila nikahisi endapo nitafunguka kila jambo basi ninaweza kumsababishia kifo chake na kikawa karibu sana.

“Hapana ni hali ya uangalizi tu wa afya yako mpenzi wangu. Wanahitaji hayo majeraha yaweze kupungua sasa”

“Kweli?”

“Ndio”

Nilidanganya kitu ambacho dhairi kinaonekana kwamba nina danganya.

“Mtoto hajawasumbua?”

“Hapana, yupo na shangazi yake”

“Ahaa ndio yule Jojo aliye kuja muda fulani hapa ndani?”

“Ndio mpenzi wangu”

“Kama ni yule sawa”

Tukajikuta tukizungumza mambo mengi sana na Marieta hadi akapitiwa na usingizi, nikamfunika shuka vizuri kisha nikatoka chumba hichi huku kichwa changu kikiwa kimejaa mambo mengi sana ambayo nina hitaji niweze kuyafanyia kazi. Jambo kubwa ambalo Marieta amenisisitizia kila baada ya muda mfupi nilipo kuwa nina zungumza naye ni kuhusiana na msahama.

“Dany na Jojo wapo wapi?”

Nilimuuliza bi Jane mara baada ya kumkuta akiwa amekaa kwenye kordo hii peke yake.

“Wamerudi hotelini, nimekusubiria ili tuweze kwenda nyumbani”

Nikaitazama saa yangu ya mkononi inaoyesha sasa hivi ni saa saba kasoro usiku. Tukaingia kwenye gari na safari ya kuelekea hoteli ikaanza.

“Hali ya mgonjwa inaendeleaje?”

“Anazungumza na kucheka vizuri. Hivi hufahamu madaktari wazuri huko duniani?”

“Nimewasiliana na daktari mmoja yupo nchini India ameomba aweze kutumia vpimo vya majibu ya mgonjwa na madaktari walimtumia, ila bado hajarudisha majibu. Ila kama wakimuhitaji basi nimesha andaa taratibu za kumpeleka nchini India akafanyiwe matibabu ya kina zaidi. Huwa sipendi sana kuwaamini madaktari wa hapa nchini kwetu”

“Ohoo nina shukuru sana Jane, sikutarajia kwa haya yote ambayo nimeyafanya kwako. Umeweza kunisaidia kwa shida na raha”

“Usijali Randy, wewe ni kijana ninatambua kwamba ni lazima utakuwa umepita sehemu mbili tatu ambazo si rahisi kwa wewe kunieleza kwa kina. Pia isitoshe haya ni maisha, leo Marieta anaumwa, huwezi jua kesho ninaweza kuumwa mimi au wewe, sasa kama tusipo onyesha upendo na juhudi katika kusaidiana nyakati za shida basi hata Mungu mwenyewe atakuwa hatukumbuki”

“Ni kweli, ila kwa haya yote aliyo fanyiwa ila Marieta ameniomba niweze kumsamehe mama”

“Mama nani?”

“Yemi?”

“Yemi ana husika nini na matatizo ya Marieta?”

Nikamtazama bi Jane kwa sekunde kadhaa.

“Yemi umefahamiana naye lini?”

“Mikaa kama miwili iliyo pita hivi?”

“Ahaa…ndio maana”

“Randy hembu niambie ussinifiche, wewe ni mpenzi wangu na Yemi ni rafiki yangu hembu niambie ni nini alicho kifanya kwa Marieta mpenzi wako”

“Kabla sijakueleza chochote, je una ifahamu historia ya Dany vizuri?”

“Ndio, alinisimulia Professa?”

“Ya Yemi?”

“Sikubahataika kuweza kuifahamu, zaidi ninamfahamu kama mwana mitindo hodari Afrika na mwanamke aliye fanikiwa kiuchumi kwa kiasi kikubwa katika bara hili la Afrika”

“Hivyo tu?”

“Ndio hayo mengine mimi siyafahamu kabisa”

“Mimi na mama yangu tulikuwa ni maaduia na nina imani leo pia uadui umezaliwa upya?”

“Kwa nini?”

“Mama yangu ni GAIDI wa kisirisiri”

Bi Jane akabaki akiduwaa hadi akafunga breki za gafla kwani hakutarajia kuweza kusikia jambo hili ninalo mueleza kwa maana yeye na mama ni mashosti wakubwa sana na wanasaidiana kwenye mambo mengi sana ya kibiashara.



“Randy upo serius na hilo jambo unalo lizungumza?”

“Asilimia mia moja na ziwezi kuzungumza kitu ambacho sikifahamu hususani kuhusiana na mama yangu”

Bi Jane taratibu akashusha pumzi huku akinitazama.

“Yaana hadi nguvu ya kuendesha gari imeniishia jamani””

“Ila tutajua nini cha kufanya”

“Randy yaani jambo ulilo niambia kwa kweli limeniweka njia panda. Sijui nifanye nini jamani”

“Njia panda kivipi?”

“Mama yako ana fahamu mambo mengi sana ya kibiashara hususani mipango yangu ya muhimu, je akitumia mipango hiyo kunizunguka si atakuwa ameniua kwa presha?”

“Sijui ila ngoja tuone. Endesha gari tuondoke”

“Siwezi, nina mawazo mengi sana tusije tukapa ajali nakuomba uje kuendesha”

Tukabadilishana siti na kuendelea na safari yetu. Tukafika hotelini na kuwakuta Jojo na Dany katika eneo la mapumziko.

“Mama yupo wapi?”

Nilimuuliza Jojo huku nikimtazama usoni mwake.

“Toka ulipo ondoka naye asubuhi hatufahamu ni wapi alipo na ukipiga namba yake ya simu imezimwa”

“Baba inabidi tyumtafute mama”

Dany akanitazama kwa sekunde kadhaa na akashindwa kujibu chochote.

“Kwa nini?”

Jojo aliniuliza kwa upole.

“Yale yote uliyo yaona kwa mke wangu, yamesababishwa na mama”

“Randy sasa hivi ni muda wa kuangalia ni jinsi gani mke wako anaweza kupona. Kama mama yako alifanya makosa na kumpelekea mpenzi wako kuwa hivyo, hatuna jambo la kufanya zaidi ya kuhakikisha kwamba tunasamehana. Umenielewa?”

“Lakini baba”

“Randy hukuna jambo la lakini. Yule ni mama yako atabaki kuwa mama yako. Hata kama kuna mapungufu au dhambi alizo wahi kuzifanya kwa maisha hayo ya nyuma ila jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba amani inatawala. Mambo ya kuwindana familia kama familia mimi siyahitaji umenielewa?”

Dany alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Sikuona haja ya kuendelea kukaa hapa, nikaelekea chumbani kwangu, nikajitupa kitandani huku nikitafakari ni jinsi gani ninaweza kufanya. Usingizi taratibu ukaanza kuniandama na haikupita mud asana nikajikuta nikilala usingizi fofofo.

***

Asubuhi na mapema mara baada ya kupanda kifungua kinywa nikaelekea hospitalini. Nikamkuta Marieta akiwa bado amelala, taratibu nikakaa pembeni ya kitanda chake huku nikimtazama usoni mwake. Uzuri wake bado upo usoni mwake.

“Hei”

Marieta aliniita mara baada ya kufumbua macho yake.

“Hai, umeamkaje?”

“Mmmm poa, japo mwili una uma kiasi”

“Utakaa poa mpenzi wangu”

Taratibu nikambusu Marieta mdomoni mwake.

“Vipi mtoto ana endeleaje?”

“Yupo na wifi yako, ila anaendelea vizuri japo nimeamka asubuhi na mapema kabla hata sijamuona”

“Ahaa sawa sawa”

Akaingia daktari, tukasalimiana naye. Akamchoma Marieta sindano ya mkononi kisha akaniomba niweze kuelekea naye ofisini kwa mazungumza zaidi.

“Nina kuja mpenzi wangu”

Nilizungumza huku tukitoka chumbani humu na daktari. Tukaingia ofisi kwake na daktari akanikaribisha kwa ukarimu mkubwa.

“Ndio dokta”

“Ahaa..majibu yale tuliyo yatuma nchini India yameweza kurudishwa. Hivyo wametuomba ndani ya siku mbili hizi mgonjwa aweze kusafirishwa na kupelekwa nchini India kwa matibabu ya haraka sana. Sasa hatutajua kwa nyinyi upande wenu mume jipangaje?”

“Mmmm….ngoja nitazungumza kwanza na familia kisha nitakujulisha dokta”

“Sawa ni vyema mukawapelekea na wezetu kule, inawezekana mgonjwa akapona”

“Akapona?”

“Ndio, wezetu kidogo wapo mbele sana kwenye taaluma hii ya udaktari”

“Sawa, namba kama dakika tano hivi kisha nitakujulisha”

“Haya”

Nikatoka ofisini hapa, nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia bi Jane, nikamuelezea kila kitu nilicho elezwa na daktari.

“Inawezekana ukaenda naye leo. Kwani kila jambo nilisha lipanga”

“Sawa sawa”

“Basi acha mimi nielekee uwanja wa ndege, nikashuhulikie maswala ya usafiri baada ya hapo nitakuja hapo hospitalini”

“Sawa”

Nikakata simu na kurudi chumbani kwa daktari, nikamueleza inawezekana kwa sisi kuondoka leo.

“Sawa basi ngoja niandae ripoti ambayo ikifika kule iwe rahisi kwa madaktari wa kule wajue wanaanzia wapi”

“Nashukuru sana dokta kwa juhudi zako zote juu ya jambo hili”

“Usijali kila kitu ni jukumu letu sawa”

“Sawa”

Nikarudi chumbani kwa Marieta huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana.

“Mke wangu, leo tunaondoka na kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu”

“Weee”

“Ndio mpenzi wangu. Mungu atatusaidia afya yako itarudi kwenye ubora wake”

Marieta akanitazama kwa tabasamu huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.

“Kuna mchungaji wangu naomba uweze kumpigia kama inawezekana aje anifanyie maombi”

“Namba yake ya simu una ifahamu?”

“Ehee”

“Nipatie”

Marieta akanitajia namba ya mchungaji huyo wa kiroho, nikampigia na kumueleza juu ya uwepo wa Marieta hapa hospitalini, mchungaji aka niahidi baada ya lisaa moja atakuwepo hospitalini hapa.

“Randy”

“Naam”

“Nimekuzalia mtoto mzuri eheee?”

“Yaa nashukuru sana mpenzi wangu”

“Naomba umkuze kwenye mazingira bora ya kuwa binti mzuri sana kwenye maisha yake”

“Usijali sna ampemzi wangu, nitahakikisha kwamba ana kuwa ni binti bora mwenye hekima na tabia njema”

“Nashukuru sana mpenzi wangu”

Mlango wa chumbani hapa ukafunguliwa na akaingia Jojo huku akiwa amembeba mtoto. Wakasalimiana na wifi yake kwa furaha sana.

“Hajakusumbua usiku?”

“Wala, yaani nilipo toka naye hapa hospitalini, nikapita naye kwenye maduka ya nguo. Nikamnunulia nguo mpya na kurudi naye nyumbani, yaani amenipenda bure jamani”

“Hahaa damu zimeendana wifi yangu”

“Ni kweli”

Jojo akamkabidhi Marieta mtoto.

“Sister tunaweza kuzungumza kidogo hapo nje”

“Sawa”

Tukatoka nje ya chumba hichi na kusimama pembeni ya mlango.

“Leo tunaelekea Inda kwa matibabu zaidi. Sasa naomba unisaidie jambo moja”

“India?”

“Ndio”

“Ehee…Nikusaidie nini?”

“Nahitaji unisaidie kupita pita madukani huko na ukamnunulia wifi yako nguo za kwenda kuvaa huko, nguo za ndani, si umeweze kuuona mwili wake?”

“Yaa nimeweza kuuona”

“Naomba unisaidie katika hilo basi dada yangu”

“Sawa”

Tukarudi ndani ya chumba hichi na Jojo akamuaga Marieta na kumuahidi atarudi baada ya muda mfupi. Hauikupita muda mrefu sana simu yangu ikaita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni namba ya mchungaji. Nikaipokea simu hii na kumuelekeza ni chumba gani ambacho tumelazwa kisha nikaka simu. Baada ya dakika tatu hivi, mlango wa chumba hichi ukagongwa, na nikaufungua. Akaingia mzee aliye valia suti nyeupe pamona na shati jeusi huku mkononi mwake akiwa ameshika biblia ndogo.

“Bwana Yesu asifiewe”

Mchungaji huyu alisalimia na Marieta akaitikia kwa furaha. Nikampa mkono mchangaji huyu.

“Mama Charity una endeleaje?”

“Mama Chariy…!!”

Nilijikuta nikilirudia jina hilo huku nikimtazama mchungaji huyu.

“Randy hilo ni jina jengine la mtoto wetu ambalo ndio nilimbatiza nalo. Sikuhitaji mtoto wetu arithi jina la mama yako, kwani nina hofia asije kurithi matatizo ya mama yako”

Marieta alizungumza kwa upole sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Ohoo huyu ndio baba wa mtoto?”

“Ndio mchungaji”

“Kuna jambo ndani yako kijana, nitahitaji kuweza kufanya maombi kwa ajili ya familia yako kwani bila ya kufanya hivyo kila kizazi chako kitakwenda kutetekea. Kuna roho ya mauti ninaiona ndani yako, imesha anza kukutafuna na usipo izuia itaendelea kukutafuna. Una roho ya kisasi, usipo uachalia moyo wako na kumpa bwana maisha yako basi damu za watu ulio waangamiza zitaendelea kukifwata kizazi hadi kizazi”

Maneno ya mchungaji huyu kidogo yakaniweka njia panda na kuniacha mdomo wazi.

“Charity bado ni mdogo sana. Hajui ni nini kinacho endelea kwenye huu ulimwengu, ila neno la bwana linasema waacheni watoto wadogo waje kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wao. Ila kama baba utashindwa kusimama kwenye mstari wa kumuamini Mungu, hakika mwanao hato weza kufwata njia iliyo bora ni lazima atarithi mambo yote mauvo kwako”

“Samahani mchungaji. Lengo la wewe kuja humu ndani ni kuonana na mke wangu. Ila si kuja kuhubiri. Nakuomba sana uweze kufanya unacho kifanya kisha uondoke”

Marieta akabaki mdomo wazi kwa mshangao. Mchungaji akatabasamu huku akiniangalia.

“Vipimo vya mke wako nina imani kwamba univifahamu na hapa mupo kwenye harakati za kwenda nchini India kwa matibabu. Unahsii hili ulilo ambiwa Tanzania, ukifika India litabadilika?”

Nikamtazama mchungaji usoni mwake kwa wasiwasi kidogo kwa maana swala hili la kuumwa kwa mke wangu na mipango yote ya kwenda India hatujamueleza mtu yoyote wa nje ya familia yangu.

“Unajua ni nini kinacho msumbua mke wako si ndio?”

“Umejuaje hayo yote?”

“Ni maono. Ngoja nikuambie kijana Mungu ndio daktari wa madaktari. Mungu ndio muweza wa yote, hakuna jambo linalo weza kushindika kwake. Hivyo nipe nafasi niweze kufanya jambo juu ya masha yako”

Marieta akanitazama, kwa ishara ya macho akaniomba niweze kukubaliana na kile anacho kizungumza mchungaji. Kusema kweli kwenye maisha yangu yote ya kukua, swala la kuwaamini wachungaji limekuwa ni dogo sana moyoni mwangu na nimekuwa ni mtu wa kuishi kwa kutegemea uwezo wnagu tu wakibinadamu.

“Mama Charity ninakuhakikishia leo unakwenda kupona kila jambo lililopo ndani ya mwili wako. Mungu ana makusudi makubwa sana na hii familia yako kuikutanisha nami siku ya leo”

“Sawa mchungaji”

Mchungaji kwa ishara akaniomba niweze kumchukua mwanangu. Nikambeba mtoto na kusimama naye pembeni ili niweze kuangalia ni kitu gani ambacho mchungaji anakwenda kukifanya. Mchungaji akamuwekea Mareta mkono wake wa kulia kwenye paji la uso. Mchungaji akaanza kuomba taratibu, baada ya muda kidogo nikaanza kumuona Marieta akitetemeka mwili mzima. Marieta akaendelea kutetemeka huku akirusha rusha miguu jambo lililo mfanya hdi mtoto akaanza kulia.

Mchungaji akazidi kuomba huku akiendelea kumuombea Marieta aliye anza kujikunja kunja mwili wake mithili ya nyoka, kitu ambacho kina zidi kunishangaza. Marieta akachomoa sindao za dripu mbili alizo tundikwia.

“Mchungaji mke wangu atakufa huyo”

Nilizungumza huku nikimvuta mchungaji koti lake. Mchungaji hakutaka kunisikia na lugha anayo izungumza kwa sasa wala siielewi kwa maana lugha hii ni ngeni sana kwangu.

“Huto kufa ukiwa bado kijana, huto kufa na kumuacha binti yako mdogo. Pokea uponyaji”

Mchungaji sasa alizungumza kwa kiswahili fasaha ambacho nimeweze kukielewa. Gafla tukashuhudia Marieta akitema kitu kilicho fungwa fugwa kwa kitambaa cheusi na kikaanguka chini.

“Irithi, majini, mapepo, magonjwa yote uliyo tumiwa na watesi wako nina yatoa in the nama of Jesus Christ.”

Mchungaji alizidi kupiga mambo na Marieta akaendelea kutingishika hapa kitandani hadi akaanguka chini. Madaktari wawili wakaingia ndani ya chumba hichi nao wakabaki kujawa na mchangao kwa kumuona jinsi Marieta anavyo endelea kupata shida hapa chini.

“Pepo la mauti toka”

Mchungaji alizungumza kwa nguvu huku akiendelea kumnyooshea Marieta mkono.

“Sitoki”

Marieta alizungumza kwa sauti nzito ya kiume hadi sisi sote tukabaki na mshangao.

“Nimepewa mamlaka ya kuwasambaratisha, kwenye maisha yenu. Huna mamlaka ya kukaa katika mwili huuu”

“Nimesemaaaa SITOKI hadi niondoke na roho ya mmoja wao. Mama, baba au mtoto”

Marieta alizungumza huku akinikazia macho mimi na mwanangu, galfa akasimama wima huku mikono yake akiwa ameichanua na akaanza kutembea kutufwata tulipo mimi na mwanangu jambo lililo nifanya nianze kutetemeka mwili wangu wote na mwanangu akaanza kuangua kilio akishiria kuogopa sana.



Mchungaji kwa haraka akwahi kumshika Marieta huku akiendelea kumuombe kadri awezavyo. Marieta akaanguka chini na kutulia kimya. Mchungaji akazidi kuendelea kusali huku jasho likimtiririka usoni mwake. Nikatoka nje ya chumba hichi na mwanangu, huku mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi sana na wasiwasi ukinitawala. Tukiwa katika kordo inayo elekea nje, nikakutana na Dany akiwa ameongozana na Livna.

“Vipi mbona kama una wasiwasi”

Baba aliwahi kuniuliza mara ya kusimama mbele yao.

“Kuna…ku…na mchungaji ndani”

“Ndani wapi?”

“Chumba cha Marieta ana sali”

“Nani amemruhusu kusali”

Dany aliniuliza kwa msisitizo kidogo huku akionyesha kuto pendezewa na jambo hili. Sikumjibu zaidi ya kupita katikat ia yao na kutokatoa nje kabisa. Nikakaa kwenye moja ya bustana huku nikijaribu kuurudisha moyo wangu katika hali ya kawaida kwani yale niliyo yaona ndani, toka kuzaliwa kwangu sikuwahi kuyaona siku hata moja.

“Heim bona upo hapa?”

Jojo alinistua na kunifanya nigeuke nyuma kwa kasi sana.

“Ehee?”

“Mbona upo hapa?”

“Kuna maombi chunbani kwa mke wangu”

“Maombi?”

“Ndio”

“Nani ana sali?”

“Mchungaji wa mama watoto”

“Mmmmm….”

“Yaa Dany amekwenda huko chumbani”

“Dany?”

“Ndio”

“No…no hapaswi kwenda”

Jojo alizugumza huku akianza kukimbia kuelekea ndani. Gafla kioo cha gorofani kikavunjika, nikamshuhudia mchunhaji akiambaa ambaa hewani na suti yake kisha akatua kwenye moja ya gari hapa chini lilipo kwenye maegesho na kutufanya watu wote hapa nje kushangaa sana. Wamama na wadada walio shuhudia tukio hilo wakaanza kulia vilio vya kupayuka. Madaktari na manesi wenye ujasiri wakasogelea eneo hilo kwa kasi. Nikapiga hatua nne za haraka kuelekea kwenye eneo hilo, ila nilipo kumbuka kwamba nimembeba mwanangu ambaye hastahili kushuhudia mambo kama hayo kwenye umri huu mdogo nikasita na kuendelea kushuhudia jinsi watu wanavyo endelea kukusanyika katika gari hilo lililo bonyea kwa juu. Nikamshuhudia Jojo akichungulia dirishani, hapa ndipo nikazidi kuchanganyikiwa kwa maana sijui ni nani ambaye amesababisha mauaji hayo.

“Hapana”

Nikaanza kurudi ndani kwa haraka huku mwanangu nikiwa nimemshikilia vizuri. Nikapishana na madaktari walio funika nyuso zao huku wakisukuma kitanda cha mgonjwa aliye funikwa hadi usoni. Nikakimbilia hadi chunba alicho lazwa Marieta, nikaingia ndani na kujikuta nikishangaa sana kuwaona wauguzi wawili nilio waacha katika chumba hichi wakiwa wameuwawa kwa kuvunjwa shingo huku kitanda cha Marieta kikiwa hakipo. Akili nia kumbukumbu zangu zikawakumbuka madaktari hao nilo kutana nao na moja kwa moja nikajua watakuwa ni Dany, Livna na Jojo.

“Fuc**”

Nilizungumza huku nikitazama dirisha hili la vioo jinsi lilivyo vunjika. Nikaanza kukimbia kuelekea nje nilipo pishana nao na kuona gari moja la wagonjwa likitoke getini huku gari ya Dany ikiwa imetangulia mbele.

“Kwa nini wamefanya hivi?”

Niljikuta nikijilaumu huku nikitazama gari hizo jinsi zinavyo tokomea getini. Mchungaji aliye angushwa dirishani nikamuona akipakiwa kwenye kitanda cha matairi huku akiwekewa mashine maalumu inayo msaidia kuingiza hewa ya oksijeni kwenye mapafu yake.

“Dokta atapona?”

Nilimuuliza daktari mmoja aliye tangulia huku wezake wakisukuma kitanda hicho kwa nyuma.

“Hatujui”

Ujumbe mfupi wa simu yangu, ukanifanya nisite kuuliza swali jengine. Nikatoa simu yangu mfukoni na kusoma ujumbe huo.

‘Ondoka hospitalini na uje uwanja wa ndege’

Meseji hiyo imetoka kwa Jojo, nikashusha pumzi taratibu na kuanza kutazama tazama hapa nje ni usafiri gani ambao ninaweza kupanda kwa ajili ya kuelekea uwanja wa ndege. Nikawaona waendesha bajaji kadhaa wakiwa wamekusanyika katika eneo la karibu na geti la hii hospitali. Nikamuita mmoja kwa ishara, akaingia ndani ya bajaji yake kwa haraka na kutufwata hapa nilipo simama na mwanangu.

“Kuna gari moja kubwa nyeusi pamoja na gari la wagonjwa yametoka hapa. Umeona yameelekea wapi?”

“Ahaa…kule”

Dereva huyu alinionyesha barabara ya upande wa kulia kwetu.

“Okya unaweza kuyafukuzia?”

“Ndio, chombo kimpya hichi kaka”

“Poa twende”

Nikaingia ndani ya hii bajaji na dereva huyu akatazama pande zote za barabara kisha tukaingia na kuanza kuzipita gari zinazo kwenda taratibu. Nikamtazama mwanangu na kumuona jinsi anavyo tabasamu kwa furaha, kidogo akanipa matumaini na kupunguza wasiwasi wangu, japo jambo lililo fanyika ndani ya chumba cha hospitali ni kubwa sana.

“Mbona hatuzioni?”

Nilimuuliza Dereva huku tukiwa tumesamama kwenye mataa ya barabarani yanayo ruhusu magari ya upende mwengine kuweza kupita.

“Ika kaka kwa mwendo wa zile gari zilivyo toke pale hospitalini, sidhani kama tunaweza kuzipata. Unajua ubaya mbele imetangulia ile gari ya wagonjwa, huwa inapishwa barabarani hivyo ni nguvu sana kuweza kuwadaka. Ila ngoja tujaribu”

“Unawanja wa ndege nipeleke?”

“Wa mwalimu Julius Nyerere?”

“Kwani kuna viwanja vingapi vya ndege hapa Dar”

“Poa poa kaka nimekusoma”

Taa za upande wetu zilivyo ruhusiwa dereva akaondoka kwa kasi na kuzidi kufanya kila liwezekanalo kuelekea uwanja wa ndege. Simu yangu ikaita, nikaitazama na kukuta ni mama ndio anaye nipigia, nikaitazama kwa muda kidogo, nikataka kuikata ila nikaipokea.

“Randy mwanangu”

“Zungumza”

“Ninakupenda sana, nimefanya makosa makubwa sana kwenye maisha yangu. Mimi ni mama mpumbavu, mimi ni mama ambaye sistahili kuigwa kwenye jamii yangu”

“Nani akuige, kwani kuna mtu anatazama filamu ya maisha yetu mama. Hembu niache kwanza hali ya mke wangu ni mbaya na kichwa changu kipo hovyo sitaki kuendelea na haya maisha. Tafadhali sana”

“Randy naomba unisikilize”

“Mama, nitakusikiliza ila hali ya mke wangu ni mbaya. Narudia mke hapa nipo njiani kuelekea uwanja wa ndege ninayapigania maisha ya mke wangu. Kama ulimtesa kwa ajili yangu na kumfanya apatwe na maradhi ya ajabu ambayo kwa hali yake hakupaswa kuweza kuyapata. Nakuomba sana mama yangu, nipe nafas ya kupambana na hali ya familia yangu sawa”

Nilizungumza huku machozi yakunichuruzika usoni. Mwanangu taratibu akaanza kunifuta machozi yangu huku akitabasamu, japo ni mtoto mdogo sana ila sijui kwa nini anafanya hivi.

“Sawa. Ninakuja”

“Wapi?”

Mama akakata simu. Dereva bajaji akanitazama kwa macho ya kuiba tu ila hakuweza kuzungumza kitu chochote.

“Hei”

Nilimsemesha mwanangu huku nikitabasamu. Dereva bajaji akazidi kukoleza moto wa bajaji hii. Tukafanikiwa kufika uwanja wa ndege salama salimini na katika maegesho ya magari, ya hapa uwanja wa ndege, nikaona gari la wagonjwa pamoja na gari la Dany. Tukamuona Jojo akiwa amesimama, akionekana kutusubiria sisi.

“Bei ngapi kaka”

“Hamsini”

“Jojo mpe elfu hamsini”

Nilizungumza huku nikishuka kwenye bajaji hii, Jojo akatoa kiasi hicho cha pesa na kumkabidhi dereva. Akambeba mwanangu na tukaanza kuelekea ndani ya uwanja huu wa ndege. Nikakutana na bi Jane na akanikabidhi bahasha ya kaki.

“Ndani kuna hati zenu za kusafiria, kuna kadi ya beki ambayo unaweza kutoa pesa sehemu yoyote duniani. Pia kuna kiasi cha pesa humo ndani, kuna barua ya maelezo ambayo mutapokelewa uwanja wa ndege nchini India na wahusika wa hospitali ile ambayo nimeagiza mgonjwa aweze kupelekwa huko sawa”

Bi Jane alizungumza, huku tukitembeea kuelekea kwenye eneo la ukaguzi.

“Nashukuru sana”

“Ahaa kitu kingine. Ninaomba ukifika tu uweze kutujulisha sawa”

“Sawa, namuomba mtoto”

“Randy mtoto ana baki”

Jojo alizungumza huku akinitazama usoni kwa msisitizo.

“Anabaki kwa nini?”

“Randy unakwenda kumuuguza mngojwa, sio jambo dogo na endapo utakuwa na mtoto unahisi itakuwaje. Hembu jaribu kufikiria hilo kwa sekunde kadhaa”

“Jamni ndege ibegakisha dakika tano tu kuondoka na Randy wewe ndio unasubiria. Hivyo mambo mengine mutazungumza kwenye simu”

Ikanilazimu kukubaliana na Jojo kishingo upande tu. Nikatoa hati yangu ya kufaria, ikakaguliwa vizuri kisha ikapigwa muhuri na nikarudishiwa. Wahudumu wawili wa kike wa shirika la ndege tunalo safiria wakanihimiza niweze kuongeza mwendo kwani ndege inatakiwa kuondoka. Nikajumuika nao wahudumu hawa kuingia nao ndani ya ndege, na mlango taratibu ukafungwa.

“Huku”

Muhudumu mmoja alizungumza huku tukikaza kwenye siti zilizo jaa abiria. Nikaingia kwenye daraja la V.I.P na kukuta Marieta akiwa amelazwa kwenye kitanda chake, huku eneo hili lote likiwa halina abiria.

“Mbona hakuna abiria hapa?”

“Mumekodishiwa eneo zima kwa ajili yenu”

“Sisi wawili?”

“Ndio muheshimiwa. Tunakuomba uweze kufunga mkanda wako ndege sasa inaingia kwenye run way”

Nikaka kwenye moja ya siti kisha nikaifunga mkanda na kumtazama jinsi Marieta alivyo fungwa vizuri kwenye kitanda hicho huku akiwa amelala usingizi fofofo na puani mwake amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua. Taratibu ndege hii ikaanza kupaa angani na kuacha ardhi ya jiji la Dar es Salaam. Ndege ilipo kaa sawa nikafungua mkanda wangu na kumsogelea Marieta alipo lazwa kwenye kitanda chake. Nikamchunguza vidole vyake ila sikuweza kuona jambo lolote la tofauti.

“Kaka unaweza kurudi tu kwenye siti yako, mgonjwa hapo yupo salama kabisa”

Muhudumu mmoja wa kike aliniseemesha huku akinitazama usoni mwangu.

“Huyu ni mke wangu ndio maana nipo naye hapa”

“Sawa, sahamani kwa hilo. Nikuletee kinywaji gani?”

“Nitakuambia nikihitaji”

Muhudumu huyu akaondoka, nilipo jiridhisha kwa kumtazama mke wangu, nikarudi na kukaa kwenye siti yangu. Nitoa simu yangu mfukoni na kuwasha wi-fi. Nikampigia Jojo kupitia katika mtandao wa whatsapp video call. Baada ya muda kidogo simu yake ikapotelewa.

“Vipi umemuona mgonjwa?”

“Ndio nimemuona. Hivi ni nani aliye fanya tukio lile la hospitalini?”

“Mke wako”

“Mke wangu?”

“Ndio yeye ndio alimsukumia mchungaji dirishani, akawanyonga wauguzi wa watu. Yaani hapo laiti kama ingekuwa si Dany na Livna kuwahi kuwemo ndani ya chumba hicho basi angetoka nje na kuanzisha sokomoko ambalo kwa kweli sijui kama kuna watu wangepona.”

“Sasa mchungaji si alikuwa anamuombea?”

“Sawa, si ameyaamsha mashetani yake, ndio maana akaanza kufanya hivyo. Sijui mchungaji huyo alikuwa anampima Mungu, yaani hata sielewi”

“Mmmmm hembu niambie ukweli si Dany aliye fanya hivyo?”

Nina apa kwa jila la mama yagu, si Dany aliye fanya vile kwani Dany hana akili yeye”

“Sasa mume mfanya nini hadi ametulia?”

“Alichomwa na sindano tatu za usingizi hapo atalala ndani ya msaa zaidi ya 72 ndio atazinduka”

“Mmmmm Jojo?”

“Ndio hapakuwa na jinsi. Nina imani kwamba ndani ya masaa hayo atakuwa amesha fika nchini India”

“Sawa muangalie mwanangu”

“Yupo mikono salama wala usijali katika hilo kaka yangu”

Nikakata simu hii, nikamtazama Marieta jinsi alivyo lala. Nikanyanyuka kwenye siti yangu na kuingia kwenye choo cha ndege hii na kuanza kujisaidia haja ndogo taratibu. Nilipo hakikisha kwamba nimemaliza haja yangu, nikanawa mikono yangu kwa sabani kisha nikaisafisha mikono yangu vizuri kisha nikatoka ndani ya choo hichi na kurudi katika siti yangu. Nikastuka sana mara ya kuto kutomuona Marieta kitandani kwake huku mikanda ambayo ilikuwa imezungushiwa kitandani kwake kwa ajili ya kumzuia asianguke kitandani hapo yote ikiwa imekatwa katwa jambo lillo nifanya nianze kujawa na mashaka mengi sana moyoni mwangu.


Nikatoka kwenye eneo hili na kuhamia eneo la abiria wengine huku nikiwa makini sana katika kumtafuta Marieta ambaye sifahamu ni wapi alipo elekea.

“Vipi tunaweza kukusaidia kitu?”

Muhudumu wa ndege hii aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“K.una….kuna….Mke wangu simuoni kitandani pale”

Nilizungumza kwa kubabaika sana, muhudumu akabaki akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Huku hujamuona?”

“Sijamuona hembu twende huku”

Muhudumu huyu alizungumza huku akinipita na kutangulia mbele. Tukarudi katika daraja la VIP. Jinsi nilivyo kiacha kitanda hichi ndivyo jinsi tulivyo kitukuta. Mikanda yote ambayo ilikuwa imemfunga Marieta imekatika. Dada huyu akatazama eneo la linalo elekea katika chumba cha marubani, akaanza kuelekea huko huku nami nikimfwata kwa nyuma. Akafungua pazia hili jeusi na sote tukashuhudia mlango wa marubani ukiwa wazi kidogo jambo ambalo si la kawaida kwa marubani wa ndege kubwa kama hizi za abiria kuacha mlango wazi. Tukatazamana na dada huyu kwa sekunde kadhaa kisha taratibu tukaanza kuusogelea mlango huu, kabla muhudumu hajaufungua mlango huu, nikamgusa bega huku nikitingisha kichwa na kumuomba asiweze kufungua yeye. Dada huyu akanielewa na taratibu, nikausogelea mlango huu, nikakishika kitasa cha mlango huu taratibu, nikaufungua mlango huu kwa umakini. Sote tukastuka sana mara baada ya kuona rubani msaidizi akiwa amevunjwa shingo yake. Nikamalizia kuufungua mlango huu na nikamshuhudia Marieta akiwa ameshika jicho la rubani mkuu wa hii ndege ambaye tayari na yeye amesha kufa. Niasikia kishindo kizito nyuma yangu, nikastuka sana na kumkuta muhudumu huyu wa kike akiwa ameanguka chini. Nguvu zote mwilini mwangu zikaniishia, kwenye maisha yangu hakika sikuwahi kutegemea kukutana na kitu kama hichi. Mikono ya Marieta imejaa damu nyingi sana.

“Randy”

Marieta alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Samahani mume wangu”

Marieta aliendelea kuzungumza kwa upole sana huku akinitazama usoni mwangu. Nikakosa hata nguvu ya kunyanyua kinywa changu ili kujibu samahani hiyo aliyo izungumza Marieta.

“Sijafanya hivi kwa kutegemea”

Marieta alizungumza huku akilitupa chini jicho la rubani huyo aliye fariki. Marieta akaanza kunisogelea mlangoni hapa nilipo simama. Nikatamani kurudi nyuma ila nikashindwa kabisa, jasho jingi linaendelea kunichurizika kila kona ya mwili wangu.

“Randy, nina kupenda sana mume wangu”

Marieta alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu. Marieta akaanza kulia kwa uchungu sana. Akili yangu hakika imesimama kwa dakika kadhaa, sijui hata nifanye jambo gani katika ndege hii ikiwa kuna tatizo kubwa kama hili.

“Randy”

“Mmm!!”

“Zungumza nami basi mpenzi wangu”

“Ehee”

“Ongea basi”

Marieta aliendelea kuzungumza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Ni…in..i..on..ge…e”

“Ndio zungumza. Una nipenda?”

“Ehee?”

“Unanipenda?”

“Ndio”

Sauti ya moja ya kipaza sauti humu chumba cha rubani ikaanza kusikika na kutustua sote. Sauti hii inaonyesha ni ya watu wanao ongoza ndege hii kutoka chini ya ardhi.

“Munatupata”

Mtu huyo aliendelea kuzungumza, nikatazama ndani ya chumba hichi na kuona kamera kama nne hivi zikiwa katika hichi chumba na kila kitu ambacho kimetokea ndani ya hichi chumba wameweza kukishuhudia.

“Rudi kwenye siti yako”

Nilimuambia Marieta huku nikimtoa mwilini mwangu. Marieta akanitazama kwa macho ya huruma, akamtazama muhudumu huyu hapa chini kisha akamruka na kutoka katika chumba hichi. Nikazitazama maiti za marubani hawa kisha nikaitoa maiti ya rubani mkuu na kumkalisha pembeni. Nikaitoa maiti ya rubani msaidizi na kuiweka pembeni ya maiti ya rubani mkuu. Nikamnyanyua muhudumu huyu wa kike na kumkalisha katika kiti cha rubani msaidizi na kumfunga mkanda wa siti hii. Nikafunga chumba hichi kisha nika kaa kwenye chumba cha rubani mkuu. Nikavaa earphone hizi kubwa.

“Haloo unanisikia”

“Ndio ninakusikia, kwa jina nina itwa Randy Dany”

“Tumeshuhudia kila jambo ambalo limetokea katika chumba hicho. Tunakuomba uweze kufwata maelekezo ambayo tunakuambia”

“Sawa”

“Kwa sasa ndege mbil za kijeshi aina ya Jet zipo njiani kuja kukusaidia kuhakikisha kwamba hiyo ndege unairudisha katika kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Kambarage nyerere salama. Ninaomba uweze kunipa ushirikiano mzuri kuhakikisha kwamba unaokoa mamia ya abiria waliomo ndani ya ndege hiyo. Umenielewa bwana Randy”

“Ndio nimekuelewa, ninazungumza na nani?”

“Unazungumza na Godzbert Mgogo. Ni muongozaji mkuu wa ndege hapa jijini Dar es Salaam”

“Sawa, ila sijui ni kitu gani nifanye hapa”

“Okay ninahitaji uweze kushika hiyo control wheel umeiona?”

“Ndio”

“Sasa kabla ya hujafanya chochote anza kuwatangazia abiria wote waweze kufunga mikanda yao na uwaeleze kwamba ndege inatakiwa kurudi jijini Dar es Salaam. Kutokana na dharura za kiufundi. Kuna kinasa sauti hapo pembeni umekiona?”

“Ndio nimekiona”

“Sawa bwana Randy ninaomba uweze kufanya hivyo”

Nikashusha pumzi nyingi sana huku nikikichukua kinasa sauti hichi. Nikakitazama kwa sekunde kasha na kuminua moja ya batani ambayo inaweza kuruhusu sauti yangu kuweza kusikika kwa abiria wote ndani ya hii ndege.

“Habari zenu ndugu abiria. Muna zungumza na Randy Dany, rubani wa dharura katika ndege hii. Ninawaomba kila mmoja wenu aweze kufunga mkanda wa siti yake. Ndege inarudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya marekebisho ya kiufundi ambayo tunaomba radhi kwani safari yetu haito weza kuendelea hadi pale matengenezo hayo yaweze kukamilika.”

Nikaminya batani hii na kuifanya sauti yangu isiweze kusikika kwa abiria.

“Kazi nzuri bwana Randy. Sasa ninaomba uweze kuzungusha hiyo control wheel taratibu upande wako wa kushoto hadi director finder iweze kukuonyesha kaskazini mangaribi, nina imani kwamba unaweza kusoma vizuri dira?”

“Ndio”

“Fanya hivyo nina imani kwamba umeziona ndege za kivita zikwia pembeni yako”

Nikatazama kwenye kioo na kuona cha upande wa kulia kwangu na kuona ndege moja ya kuvita huku upande wa kushoto napo nikiona ndege nyingine. Rubani wa ndege ya kulia akanipa ishara ya dole gumba akiashiria kwamba kila jambo litakuwa safi. Nami nikamjibu kwa ishara hiyo hiyo ya dole gumba, taratibu nikaanza kuzungusha control wheel taratibu huku nikitazama direction finder, ndege hii taratibu ikaanza kuzunguka hadi ikafikia usawa ambao muongozaji aliyopo chini aliweza kunielekeza.

“Safi sasa unaweza kuuweka sawa control wheel”

Muongozaji alizungumza na nikafanya alicho niambia na ndege hii ikaka sawa.

“Una dakika arobaini na tano kabla ya ndege hiyo kuweza kutua aridhini hivyo unapasawa kuendelea kuwa nami hadi pale ndege itakapo tua aridhini”

“Sawa ila nina ombi moja muhimu sana na nina hitaji kuhakikishiwa hili ombi”

“Zungumza”

Nikaka kimya huku nikijifikiria hichi ambachi ambacho ninataka kukizungumza.

“Maisha ya mamia ya watu, watoto, wanaume na wanawake waliomo kwenye hii ndege yapo mikononi mwangu kwa sasa. Mke wangu ndio aliye sababisha matatizo haya yote katika hii ndege na ninajua sheria ya Tanzania moja kwa moja lazima atashtakiwa akiwa katika hali yake hii ya ungojwa. Ninaomba muweze kunahakikishia kwanza usalama wa mke wangu kwamba hato shatikiwa, pili nina hitaji mke wangu akapatiwe matibabu ya matatizo ya ugonjwa ambayo yana msumbua.”

Nikamsikia bwana Gozbert akishusha pumzi.

“Bwana Randy kutokana mimi nina husika tu kwenye maswala ya kuongoza ndege labda hili swala uweze kuzungumza na waziri wa Mkuu yupo hapa uwanja wa ndege”

“Sawa ni jambo zuri naomba kuzungumza naye”

“Dakika moja”

Sikuweza kusikia mazungumzo ya aina yoyote, ndege hizi za kijeshi bado zipo pembeni ya ndege hii huku tukienda sawa sawa. Nikamtazama muhudumu wa hii ndege niliye mkalisha siti ya pembeni na kumkuta akiwa anafumbua fumbua macho. Taratibu akanitazama huku akionekana kama kuvuta kumbukumbu ili aweze kufahamu ni eneo gani ambalo yupo.

“Hei”

Nilimuonglesha kwa sauti ya chini huku nikiendelea kumtazama usoni mwake.

“Nipo wapi?”

“Upo ndani ya ndege”

Akataka kutazama nyuma ila nikamzuia.

“Kwa sasa ni mimi na wewe ndio tunaiongoza hii ndege hivyo nina kuomba uweze kuwa makini”

“Tunaiongoza ndege!! Kwani rubani Tomy yupo wapi?”

“Vaa earphone”

Nilizungumza huku nikimuonyesha muhudumu huyu earphone kubwa ambazo zilikuwa zikitumiwa na rubani msaidizi. Taratibu msichana huyu akazivaa earphone hizi.

“Ninaitwa Randy”

Nilizungumza huku nikimpa mkono wangu wa kulia, akautazama kwa sekunde kadha akisha akaupokea.

“Nina itwa Delila”

“Delila jina zuri”

“Nashukuru”

Delila alizunguza huku akitazama ndege hizi za kivita zilzopo pembeni yetu.

“Bwana Randy sasa unaweza kuzungumza na waziri mkuu wa nchi ya Tanzania.”

“Nashukuru. Muheshimiwa nina imani kwamba una nisikia”

“Ndio nina kusikia Randy Dany. Zungumza”

“Mke wangu ndio amesababisha haya matatizo yote ndani ya ndege nina imani kwamba uweza kushuhudia kila jambo ambalo limetokea kwenye chumba hichi cha marubani. Ila jambo ninalo hitaji kuweza kukuomba, ni kwamba mke wangu hajafanya hivi kwa kukusudia ni matatizo aliyo nayo. Hivyo ninahitaji kwanza aweze kupewa msamaha wa kisheria na mbili ninahitaji aweze kupewa matibabu ili aweze kurudi kwenye akili yake ya kawaida”

“Ila mke wako ameua marubani wawili na anahatarisha maisha ya abiria zaidi ya miambili na stini ndani ya hiyo ndege”

Delila akageuka nyuma na kutazama marubani walio uwawa na mke wangu na kujikuta akishika mdomo wake kwa kuhamaki sana.

“Nalitambua hili waziri mkuu, ila ombi hilo ninakuomba wewe nina imani kwamba lipo ndani ya uwezo wako na kumbuka kwamba hivi sasa maisha ya hawa abiria wote yapo mikononi mwangu. Hivyo ninawezakufanya jambo la iana yoyote tuhakikisha kwamba mke wangu haingii katika vyombo vya dola. So haya ni maamuzi yako waziri mkuu, kumsamehe mke wangu au nifanya maamuzi yangu ninayo yajua mimi mwenyewe”

Ukimya ukatawala huku ikonyesha kwamba waziri mkuu anafikiria jambo la kunijibu.

“Nasubiri jibu lako muheshimiwa waziri mkuu”

“Ninakujibu”

Mazunguzo haya yakakatishwa.

“Unataka kufanya nini?”

Delila aliniuliza huku akiwa ameshikwa na mshangao mkubwa sana.

“Chochote”

“Kama?”

“Utafahamu baada ya jibu la waziri mkuu”

“Tafadhali nakuomba usiweze kufanya kitu chochote kibaya. Tafadhali ninakuomba sana”

“Yule aliye fanya yale ni mke wangu, sihitaji mke wangu aingie kwenye vyombo vya dola ikiwa hali yake ni mbaya. Ana umwa mke wangu kama zingekuwa ni akili zake wala asinge weza kufanya jambo lolote kama hilo”

“Ila kumbuka amewaua marafiki zangu wa muda mrefu. Hawa hawakuwa na hatia yoyote, hembu tazama jinsi alivyo mfanya Tomy, amemng’ofoa jicho kabisa”

“Nalitambua hilo. Mimi na wewe hapakuwa na mtu aliye tegemea kuona hili jambo. Hivyo nahitaji mke wangu kuwa salama”

“Bwana Randy”

“Ndio waziri mkuu”

“Nimezungumza na raisi na ameahidi kumpatia msamaha wa kisheria na amenihakikishia kwamba atapewa matibatu ya aina yote ambayo wewe utahitaji mkeo aweze kupatiwa”

Nikashusha pumzi taratibu huku nikitafakari juu ya hii kauli.

“Kama ni hivyo, nipo tayari kuhakikisha kwamba ndege na abiria wote wanatua salama”

“Tunashukuru”

Dakika zikazidi kuyoyoma mbele na muda wa kutua ardhini ukawadia. Kutokana nipo na Delila ambaye mwenzangu kidogo ana uwelewa na mambo haya ya urubani. Taratibu nikashika throttle levers, na taratibu nikaanza kuivuta nyuma taratibu huku matairi ya ndege hii yakiwa tayari nimesha yachomoza kwenye ndege. Ndege hii ikaanza kugusa ardhi ya jiji la Dar es Salaam. Ndege taratibu huku nikikanyaga brake pedals na kuyafanya matairi ya nyuma kufunga breki huku ndege ikiendelea kupunguza mwendo wake. Taratibu nikaanza kuiendesha kwenye hii run ways hadi nikafika eneo ambalo muongozaji wa ndege akaniomba niisimamishe. Ndege ikasimama na kujikuta nikitazamana na Delila ambaye naye hakuamini kama nina weza kufanikiwa kuisimamisha ndege hii. Nikafungua mkanda wa siti yangu na kutoka chumbani humu kwa haraka. Nikafika katika level ya VIP ambayo nilimuagiza Marieta akakae, sikuweza kumuona zaidi ya nguo zake zilizo angukachini huku begi la nguo ambalo Jojo alimletea likiwa na nguo likiwa limewekwa kwenye moja ya siti huku likiwa limefunguliwa na dhairi inaonyesha kwamba Marieta amebadilisha nguo nyingine kwa lengo la kutoroka humu ndani.



Nikaelekea kwa haraka daraja jengine na kukuta abiria wakiwa wamesha anza kushuka. Nikajaribu kuangaza macho yangu kwa abiria waliomo ndani humu ila sikuweza kumuona Marieta jambo ambalo likanifanya nizidi kuchanganyikiwa. Nikaanza kushuka kwenye ngazi ndefu na kukuta askari wengi sana wakiwa wamekusanyika katika eneo hili huku wakiwa wameizunguka ndege hii na kila abiria anaye shuka wanamuweka pembeni kuhakikisha kwamba wana wakagua mmoja baada ya mwengine ili mradi wampate Marieta.

‘Fuc**’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikigeuza na kurudi ndani ya ndege nikaanza kukagua vyoo vya humu ndani na wala sikuweza kumuona Marieta.

“Kaka vipi?”

Muhudumu mwengine wa kike aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kuna dada mmoja hivi mrefu, ana shepu shepu na ni maji ya kunde fulani hivi. Umemuona?”

“Hapana labda atakuwa ameshuka”

“Huko nyuma hakuna mtu?”

Nilimuuliza dada huyu huku nikitazama chumba kilichopo nyuma kabisa ya hii ndege ambacho ukiingia kina elekea chini kabisa ya ndege hii eneo ambalo mizigo ina hifadhiwa.

“Hapana”

“Ngoja”

Nikampita muhudumu huyu na kuingia katika chumba hicho. Nikafungua mlango na kuchukua moja ya tochi kisha nikashuka ngazi hizi nne na kuingia eneo hili lenye mizigo mingi sana.

“Marieta”

Nilizungumza huku nikianza kuita taratibu. Nikaendelea kumulika mulika kila eneo la eneo hili la mizigo. Nikatembea eneo hili lote na sikuweza kufanikiwa kumuona mtu wa aina yoyote, nikatoka ndani ya ya eneo hili na gafla nikakutana na askari wawili wakiwa wameshika mitutu ya bunduki. Wakaniamrisha kunyoosha mikono yangu juu na nisifanye jambo la aina yoyote.

“Mimi sijafanya kosa lolote”

“Nyoosha mikono juu”

Askari hawa walio valia nguo nyeusi pamoja na kofia ngumu nyeusi walizidi kuniamrisha. Nikaitii amri huku nikiwatazama kwa umakini. Kitendo ch ammoja wao kunikaribia, ili anifunge pingu, ikawa ni kosa kubwa sana kwake. Nikamvuta kwa haraka na kumpiga kigoti cha tumboni, mwezake akajaribu kunivamia ila nikamrudisha alipo toka kwa teke zito la kifua na kumfanya anguke chini mzima mzima. Askari niliye anza kumpiga kigoti, nikammpiga shingoni mwake kwa ubapa wa mkono wangu na kumkufanya apoteze fahamu zake hapo hapo. Huyu askari mwengine nikamshindilia mateke mawali ya kichwani naye akapoteza fahamu hapa hapa.

“Unafanya nini?”

Sauti ya Delila ikanistua sana kwani ndani ya ndege hii tupo sisi wanne, askari wawili na Dalila. Abiria wengine wote tayari walisha shuka.

“Wao wameanza kunivamia”

“Kukuvamia ndio uwapige. Tambua kwamba una vunja sheria?”

“Sheria gani. Mimi nina kosa gani, unajua ni makubaliano gani ambayo tuliweza kuyafanya na hawa watu. Imekuwaje wame izingira ndege. Wanataka kumkamata mke wangu eheee?”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Delila usoni mwake. Delia akakosa la kuzungumza mara baada ya kuchungulia dirishani na kuona wingi wa askri hawa.

Kwa haraka nikamvua nguo mmoja wa askari kisha nikvua nguo zangu na kuzivaa za kwake. Nikachukua bunduki yake huku askari hawa wote nikiwaingiza eneo ambalo ni la mizigo.

“Unawaacha humu?”

Delila aliniuliza kwa shauku kubwa sana.

“Ndio maana yake, sina la kufanya”

“Mmmm!!”

“Sasa nitatoka na wewe naomba usionyeshe dalili yoyote ya kuonyesha kwamba kuna jambo lililo tokea kwa maana hawa wanahitaji kunikamata na mimi”

“Sawa”

“Sio sawa tu. Umenielewa?”

“Ndio nimekuelewa”

Delila alatangulia na kuanza kushuka kwenye ngazi ndefu zilizo wekwa. Nami nikaanza kufwatia kwa nyuma. Hapakuwa na askari aliye weza kutufwatilia. Macho yangu yote yapo kwa abiria wanao endelea kukaguliwa kwa umakini sana. Katika kundi la abiria ambao wanasubiri kukaguliwa ili kuingizwa kwenye basi kubwa lililopo hapa, nikamuona Marieta akiwa amejipamba sana na amebadilika sana kiasi cha kwamba kwa mtu ambaye hamfahamu si rahisi kuweza kumfahamu. Marieta amevalia gauti jeusi refu na lenye mpasuo mkubwa, huku usoni mwake akiwa amevalia wigi moja refu huku baadhi ya vijinywele vikiwa vimeufunika uso wake.

“Vipi huyo binti yupo ndani?”

Mzee mmoja aliye valia nguo hizi za kiaskari aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Jamaa anendelea kukagua nimempata huyu muhudumu”

Nilizungumza kwa kujiamini huku nikimkazia macho mzee huyu, ambaye akatingisha kichwa chake kuonyesha kujawa na hasira ya kumkosa mtu anaye mtafuta.

“Hakikisheni kwamba wana patikana wote”

“Sawa mkuu”

Niliendelea kuzungumza kwa kujiamini. Jambo zuri ni kwamba nilisha wahi kupitia jeshini hivyo nina jua mambo yote ya kiaskari na endapo kuna tokea msako wa namna hii kuna hali ambazo askari wanao husika katika msako wana kuwa nazo.

“Hei sasa unakwenda wapi?”

Delila aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Nimemuona mke wangu nina hitaji kufanya mpango wa kuondoka naye hapa uwanjani”

“Umemuona?”

“Ndio”

“Ni yupi?”

“Siwezi kukueleza kwa sasa”

“Unashindwa kuniamini?”

Delila alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Nikamtazama kwa sekunde kadha huku nikimkazia macho.

“Siwezi, mke wangu amefanua uhalifu wa kukuulia rafiki zako. Unahisi kwamba nikikuonyesha itakuwa ni jambo rahisi kwa wewe kuweza kumsamehe?”

Swali langu likamuweka Delila katika mabano ya kushindwa kufahamu anijibu nini.

“Kajumuike na wafanyakazi wezako kule”

Nilimuambia Delila huku nikimuonyesha wahudumu wezake wa kike walio kaa sehemu nyingine. Delila akanitazama kwa macho ya hasira kisha akaanza kutemeba kuelekea walipo wezake. Nikamtazama Marieta na kumuona ni kama mtu wa tatu kabla ya kukaguliwa na askari wanne wanao fanya kazi hiyo huku askari hao wakionekana kutazama picha ya msichana huyo. Nikatazmaa moja ya gari la hawa askari wa kikosi cha Interpol. Nikalisogelea gari hili aina ya Ford Ranger. Nikalichunguza ndani kwa bahati nzuri nikakuta likiwa na funguo yake.

‘Nitamtoaje mke wangu hapa’

Niliwaza huku nikimtazama Marieta. Wingi wa askari pamoja na magari yao hapa uwanjani yana nifanya nizidi kuumiza kichwa kuweza kufahamu ni jinsi gani nina weza kumtoa mke wangu. Nikamtazama Delila na kumuona akizungumza zungumza na mmoja wa askari. Yeye na askari huyo wote wakanitazama mimi.

‘Mseng** amenichomesha kwa askari huyu.’

Nilizungumza kimoyo moyo, huku nikiingia ndani ya gari. Nikamshuhudia askari huyo akiwajulisha askari wezake wawili na wakaanza kunifwata kwenye gari hili huku wakikimbia. Kwa haraka nikaliwasha gari hili, nilalizungusha kwa kasi sana na kuanza kuwalenga askari na watu wanao kaguliwa, jambo lililo wafanya kutawanyika huku kila mmoja akiokoa maisha yake. Nikafunga breki za gari hili eneo la pembeni alipo angulia Marieta, nikafungua mlango wangu.

“Ingia”

Nilizugumza kwa sauti ya msisitizo. Marieta wala hakuhitaji kujishauri mara mbili mbili. Akarukia ndani huku nikiufunga mlango. Akapita kwenye siti ya pembeni, nikakanyaga mafuta na kuondoka eneo hili kwa kasi sana huku nikiwaacha askari hawa wakilishambulia gari hili kwa risasi na uzuri ni kwamba gari haliingizi risasi.

“Umejuaje kama ni mimi?”

Marieta aliniuliza huku akivua wigi lake na kubaki na nywele zake halisia.

“Unahisi kuna mtu ambaye ana mshau mke wake?”

“Ohoo your so amaizing mume wangu”

“Shukrani. Funga mkanda”

Nilizungumza mara baada ya kuona gari zipatazo sita zikija kwa kasi nyuma yetu. Marieta kabla ya kufunga mkanda akanitandika busu zito la shavuni mwangu.

“Nakupenda sana mume wangu”

“Nakupenda pia mke wangu. Funga mkanda sasa”

Marieta akafunga mkada, ubaya ni kwamba kwa hapa uwanja wa ndege sifahamu ni wapi ninaweza kutoka ili niwakimbie hawa askari. Nikazidi kuendesha gari hili kwa kasi huku nikipita katika njia maalumu ambazo ndege hutumia kupita.

“Randy angalia mbele”

Marieta alizungumza huku akipiga kelele. Nikashuhudia ndege kubwa sana ikiwa inatua katika usawa huu wa gari letu lilipo.

“Ohoo boy”

Nilizungumza huku macho yakiendelea kunitoka kwani ndege hii imeziba njia hii yote hii ni kutokana na ukubwa wake. Nikazidi kukuanganya mafuta huku nikitazama jinsi ndege hii inavyo kuja kwa kasi, Marieta macho yakazidi kumtoka, nikazidi kuendelea kuongeza mwendo kasi wa gari hili, mita chache kutoka ndege ilipo nikalitoa gari hili pembezoni mwa kabisa mwa hii barabara na kusababisha gari za askari wana fukuzana nami kubamizwa vibaya na ndege hii. Nikaanza kujitahidi nina liweka sawa gari hili, kwani lina yumba kwa kiasi kikubwa sana hii yote ni kutokana na kasi ambayo nilikuwa nayo.

Jambo la kusmhukuru Mungu, nikafanikiwa kuweza kulihimili gari na kurudi katika njia hii ya ndege. Nyuma hapakuwa na gari hata moja ambalo linaendelea kunifukuzia, zaidi ya moto mkubwa sana unao ambatana na moshi mwingi kutawala eneo la nyuma yetu.

“Ile ndege imepata ajali?”

Nilizungumza huku nikitazama nyuma. Marieta naye akageuka nyuma na kutazama eneo tulipo toka na akabaki akishika mdomo wake kwa mshangao mkubwa.

“Yote ni kutokana na mimi mume wangu”

“Wewe ndio umesababisha hiyo ajali au?”

Nilimuuliza Marieta kwa ukali huku nikimkazia macho. Tukafanikiwa kutoka katika uwanja huu wa ndege na kuingia mitaani. Tukafika katika moja ya mtaa na kusimamisha gari hili.

“Unafanyaje?”

Marieta aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Kutembea na gari hili inaweza kusababisha kukamatwa kirahisi”

“Kwa nini?”

“Nina hisi katika gari zao wana weka track divice nina imani wanaweza kufwatilia magari yao popote yanapo elekea”

“Sasa tunafanyaje?”

“Tutembee kwa miguu hadi pale nitakapo pata huduma ya simu kwa maana simu yangu kwa bahati mbaya nime iacha ndani ya ndege”

“Sawa”

Tukashuka kwenye gari hili na kulitelekeza. Tukaanza kutembea katika mtaa huu ulipo karibu kabisa na uwanja wa ndege.

Hadi inafika saa moja usiku tukafika katika eneo la Tazara. Nikamuona dada mmoja akiminya minya simu yake, nikamsogelea kwa ukaribu kabisa.

“Habari, ninaomba nisaidie simu yako”

Dada huyu akabaki akiwa ameshangaa, kwani sikusubiria hata aitike salamu yangu.

“Nitakupaje ikiwa sikufahamu?”

“Natambua unifahamu, nawasiliana na mtu mara moja kisha ninakurudishia simu yako”

Dada huyu akanitazama kwa sekunde kadhaa huku akijishauri. Marieta bila hata ya kuuliza akamichukua simu ya dada huyo na kunikabidhi.

“Tuna shida ndio maana tuna fanya hivyo”

Dada huyu akabaki na kigugumizi kilicho mfanya ashindwe hata kupiga kelele. Nikaingiza namba ya Jojo na kumpigia simu na kumueleza kwamba nipo Tazara. Jojo akaniahidi ndani ya muda mchache atafika katika eneohili.

“Shukrani kwa msaada wako”

Nilizungumza huku nikimrudishia simu dada huyu.

“Alafu nyinyi si munatafutwa!”

Msichana huyu alizungumza kwa mshangao mkubwa sana. Marieta akataka kumvamia ila nikawahi kumshika mkono wake.

“Dada funga kinywa chako. Nina uwezo wa kukufanya jambo bada ila sihitaji kukufanyia hivyo. Endelea na safari yako mama”

Dada huyu akaondoka kwa haraha huku kwa mara kadhaa akitazama nyuma.

“Yule atawapigia polisi unajua?”

“Natambua, ila hawawezi kutukamata hapa”

“Hapana bwana Randy acha nikamuue, kwa maana lazima atatuchomesha na isitoshe namba ya Jojo hukuifuta ndani ya simu yake”

Marieta alizungumza na kuanza kukimbilia alipo elekea dada wa watu ambaye naye mara baada ya kumuona Marieta akimkimbiza naye akaanza kukimbia ili kuyaokoa maisha yake.


 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG