SIN SEASON 2
WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+
SEHEMU YA 1 KATI YA 10
ILIPOISHIA MSIMU WA KWANZA
Kijana huyo akatoka ofisini hapo. Raisi Mtenzia akampia simu sekretari wake na akaingia ndani hapo.
“Niandalie kikao na mkuu wa mkoa. Meya wa jiji, mkuu wa majeshi pamoja na waziri wa mambo ya ndani. Nina hitaji kuzungumza nao baada ya lisaa moja wawe hapa”
“Sawa muheshimiwa raisi. Alafu mama yupo hapo nje ana hitaji kuonana na wewe”
“Mruhusu aingie”
“Sawa”
Sekretari huyo akatoka, akaingia mrs Mtenzi ambaye uso wake una onyesha kuto kuwa na furaha.
“Mume wangu nina pata simu za usumbufu. Watu wana niuliza kwa habari hizi za kuondoka jijini Dar hadi nina pata hofu”
“Mke wangu usimjibu mtu yoyote juu ya mambo hayo. Tambua kwamba nchi ipo kwenye hali ya usalama na hili ndio jiji letu na ulinzi ni mkali sana”
“Sawa mume wangu. Je hawa wananchi wanao hoji na kuulizana maswali huko kwenye mitandao ya kijamii tuna watuliza vipi?”
“Nchi yetu ni ya kidemokrasia. Kila mtu ana uhuru wa kuzungumza anacho jisikia, ili mradi asienende kinyume sheria za nchi. Jambo la msingi ni wewe kuhakikisha kwamba una tuliza akili na kesho harusi ipo kama kawaida, hakuto kuwa na hata panya wa kukatiza mtaani. Umenielewa mke wangu”
“Sawa mume wangu”
“Njoo”
Mrs Mtenzi akasimama kutoka kwenye kiti alicho kalia na kuzunguka meza ya mume wake na kusimama pembeni yake. Taratibu raisi Mtenzi akasimama na kumshika kiuno mke wake.
“Tambua kwamba mimi ndio raisi. Nina jukumu la kuilinda nchi yangu na watu wake, huwa una jua nikizungumza nina maanisha. Hivyo maneo ya kimtandao yasikuumize kichwa, sawa mama watoto”
“Sawa mume wangu”
Raisi Mtenzi akambusu mke wake mdomoni kisha akamuachia.
“Wewe nenda kazungumze na wageni wetu, nikitoka ofisini nita jumuika nanyi”
“Sawa mume wangu”
“Nina kupenda”
“Nina kupenda pia”
Mrs Mtenzi akambusu mumewe shamvuni kisha akatoka ndani hapo. Akapisha na sekretari mlangoni.
“Muheshimiwa, nimesha wajulisha na wana kuja”
“Sawa wakifika wote waambie nikutane nao kwenye ukumbi namba moja”
“Sawa muheshimiwa”
Raisi Mtenzi akashusha pumzi taratibu, akaichukua simu yake na kuanza kutazama kutazama kurasa ya Intergram ambayo ina wahimiza watu kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam na ndoa ya Jery na Julieth ni haramu. Simu ya mezani ya raisi Jery ikaanza kuita, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akachukua mkonga wa simu na kuiweka sikioni mwake.
“Halooo”
“Habari muheshimiwa raisi”
“Una hitaji nini The Brain?”
“Natambua kwamba ume nitoa nje ya nafasi ya ushauri. Ila nina imani kwamba una weza kuona ni mambo gani ambayo yana endelea kunywe mtandao si ndio”
“Ndio”
“Hapa nilipo nami nipo kwenye harakati za kuondoka jiji la Dar es Salaam. Ukiachilia mbali kwamba wewe ni raisi au bosi wangu, ila wewe ni rafiki yangu na pia ni mdogo wangu. Nitakueleza ukweli, uwe una penda ua hupendi,ila huu ni ukweli. Hili ambalo una ona lina endelea kwenye mitando ya kijamii, sio jambo la kulipuuzia hata kidogo. Fukua fukua ili uone ni kipi kipo nyuma ya pazia, nina imani kwamba uta kuwa una watafuta waanzilishi wa kurasi hizi kwa ajili ya kuwakamata. Ila jambo moja Chinas, una paswa kuwa na busara, waulize ni kitu gani ambacho kina wafanya wahimize watu kuondoka jiji la Dar es Salaam na endapo uta pata sababu uta jua ni njia gani utatue, ila ukiendelea kuwa mbabe mdogo wangu. Hata mimi sijui ni nini kita tokea, ndio maana nina hamasika na mimi kuondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam. Nikutakie ndoa njema ya vijana wako”
Simu ikakatwa na kumfanya raisi Mtenzi kuishusha simu hiyo chini taratibu. Jambo hili ambalo hapo awali alilichukulia kama mzaha sasa lina anza kumkaa akilini mwake vizuri. Raisi Mtenzi akampigia simu mr THE Brain.
“Ndio muheshimiwa”
“Nahitaji uje ikulu sasa hivi?”
“Muheshimiwa uta nisamehe kwa maana na mimi nina ondoka Dar es Salaam”
“Tafadhali nina kuomba sana ugahiri hiyo safari nina kuomba uje ikulu sasa hivi”
Mr the Brain akaka kimya kwa sekunde kama thelathini.
“Sawa nina kuja ila nita kaa lisaa moja, kisha nita endelea na safari yangu”
“Nashukuru kwa kuitikia wito wangu”
Raisi Mtenzi akakata simu yake kisha akampigia simu makamu wa raisi ambaye yupo nchini China kwa ziara ya kikazi.
“Habari muheshimiwa”
“Salama, kuna jambo linalo endelea kwenye mitandao ya kijamii. Je ume fanikiwa kuliona?”
“Ndio muheshimiwa, nime jaribu kuomba msaada kwa serikali hii kujaribu kutusaidia kuwapata waanzilishi wa page hizo”
“Wame semaje?”
“Wana lishuhulikia muheshimiwa, ila sija taka kuwaambia kwamba kitengo chetu cha NSA, kina tatizo”
“Kazi nzuri ndugu yangu”
“Watakapo fikia basi nita kujulisha muheshimiwa”
“Sawa sawa”
Sekretari akagonga na raisi Mtenzi akamruhusu kuingia ndani kwa ishara.
“Muheshimiwa wageni wote wamesha fika”
“Sawa twende ila wasiliana na mr the Brain na umuambie aje kwenye ukumbi namba moja”
“Mr the Brain ame rudi kazini?”
“No nime muita kwa ajili ya hili jambo”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Raisi Mtenzi akaingia ndani ya ukumbi huo na kuwafanya viongozi alio waita hapo kusimama kwa heshima. Alipo kaa kwenye kiti chake na yeye akakaa.
“Nime waita hapa wa ajili ya hili swala linalo endelea kwenye mitandao ya kikamii. Wana nchi bado wana hofu kwenye hili, je kuna hata mmoja wenu ambaye ana weza kuwaza au kufikiria ni kitu gani ambacho kita kwenda kutokea?”
“Muheshimiwa kwa upande wangu najaribu kutafuta sababu ya hawa watu au mtu kufungua hizo kurasa, ila nina shindwa kupata jibu la uhakika katika hili.”
Mkuu wa mkoa alizungumza, mlango ukafunguliwa na akaingia mr the brain akawasalimia watu wote, kisha akatafuta kiti na kukaa.
“Nashukuru kwa kuja ndugu yangu”
“Usijali muheshimiwa”
“The Brain swala tunalo jadili ni kuhusiana na hili jambo la wananchi kuhimiza kuondoka jiji la Dar es Salaam nawe ni mmoja wapo ya watu walio kuwa wana ondoka jijini. Tuambie una maoni gani juu ya jambo hili?”
“Muheshimiwa nchi ipo kwenye shambulizi na eneo ambalo lime pangwa kutoka kwa mashambulizi hayo ni jiji la Dar es Salaam”
Mr the Brain alizungumza kwa kujiamini na kuwafanya viongozi wote kustuka.
“Shambulizi gani na nani ambaye ana kwenda kuishambulia nchi?”
“Dakika tano kabla sija ingia hapa ndani, nilikuwa nina zungumza na mr Mbogo uliye mfukuza kwenye kitengo cha NSA. Yeye na timu yake wamesha ondoka jijini Dar es Salaam na ameniambia kwamba kesho kwenye harusi ya mwanao. Kundi la Al-Shabab ambalo uli lishambulia kima kosa wata fanya shambulizi, hivyo muheshimiwa, haijulikani ni wapi na wapi wata shambuli na wala kati yetu hakuna anaye fahamu ni saa ngapi wanavyo shambulia. Kiufupi muheshimiwa, kesho haito kuwa siku nzuri kwako na taifa kwa ujumla”
Maneno ya mr the Brain yaka wafanya viongozi wote macho kuwatoka, huku raisi Mtenzi mapigo ya moyo yakianza kumuenda kasi sana kwani wamebakisha muda mchache sana kabla ya harusi ya kijana wake kufanyika.
ENDELEA
ENDELEA
Macho ya viongozi wote yapo kwa raisi Mtenzi ambaye jasho la uso lime anza kumtiririka. Akilini mwake akakumbuka jinsi mzee Mbogo alivyo kuwa ame kataa kabisa kufanya shambulizi kwa Al-Shabab pasipo kuwa na kidhibitisho kwamba wao ndio wame husika katika shambulizi la kuwaua askari wake wa majini.
“Muheshimiwa raisi”
Mkuu wa mko alimuuia raisi Mtenzi, ila hakuitika.
“Muheshimiwa”
“Mmmmm!!!”
“Tuna fanyanye mkuu”
Waziri wa mambo ya ndani aliuliza huku akimtazama raisi Mtenzi usoni mwake.
“The Brain ulizingumza na na…na na nani?”
“Mbogo?”
“Ndio muda gani?”
“Kwa sasa zita kuwa ni dakika kumi zilizo pita”
“Yeye amepata wapi hizo habari?”
“Hakuniambia sorce ya habari yake, ila kama unavyo fahamu. Mbogo ni mtu mzuri sana kwenye maswala ya upelelezi muheshimiwa. Isitoshe kwa sasa yupo nje ya serikali yako hivyo ana weza kuwa na vyanzo vingi vya habari nyeti kama hizo ndio maana aka nieleza kama rafiki yake”
“Una weza kumpigia simu”
“Alafu nimuambie nini?”
“Aje hapa ikulu”
“Kabla sija mpigia ila ukweli muheshimiwa ni kwamba hayupo ndani ya jiji la Dar es Salaam”
“Wewe mpigie simu”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa msisitizo huku akiwa na wasiwasi mwingi sana moyoni mwake. Mr the Brain, akampigia simu mzee Mbogo.
“Ndugu yangu umesha anza safari?”
“Hapana, nipo ikulu sasa hivi na nipo na raisi. Nime mfikishia ile habari ambayo ume niambia na ame kuomba uweze kuja ikulu”
“Najua ume weka loud speeker si ndio?”
“Ndio”
“Raisi ana nisikia vizuri si ndio?”
“Ndio ana kusikia”
“Ngoja niwe muwazi, siwezi kurudi Dar es Salaam kwa sasa hivi. Pia siwezi kufanya kazi kwenye serikali ambayo haiwezi kunisikiliza. Mimi nime kuwa professional kwenye hii kazi sasa una kwenda mwaka wa arobaini na tano. Nime fanya kazi na maraisi wa awamu kama nne hivi na wote waliheshimu mawazo yangu na hapakuwa na kitu chochote kilicho weza kutokea katika serikali zao.”
“Muheshimiwa raisi nilikuwa nipo very disappointed kwa maamuzi uliyo yafanya kwenye kundi la Al-Shabab. Ningekuwa sija kushauri hapo kweli unge sema nina makosa. Ila nime kushauri na nikaenenda kinyume ana oder yako ya kuwashambulia, ila ulicho kifanya ni kunifukuza kwenye nafasi ambayo nilihitaji kustafu kwa heshima, ila ile siku nilistafu kwa kudhalikishwa mbele ya wafanyakazi wangu ambao wote wame amua kuungana na mimi kwa manaa kilicho fanyika hakikuwa sawa. Una yule binti uliye mkabidhi kitengo cha NSA. Muambie ahakikishe ana tafuta ni wapi Al-Shabab watakapo fanyia mashambulizi yao. Ila kwa mimi kurudi tena kazini siwezi hata mukiniua siwezi kutoa ujuzi wangu, ni heri kufa kuliko kudharualiwa. Kama nime zungumza maneno mabaya nina kuomba uni samehe muheshimiwa raisi”
Mzee Mbogo alizungumza kwa msisitizo na uchungu mkali sana. Viongozi wote wakatazamana na nyuso zao waka zidurisha kwa raisi Mtenzi ambaye amekaa kimya huku mikono iki mtetemeka.
“Ila Mbogo ndugu yangu, hapa tuna angalia taifa na si kumuangalia raisi alifanya vipi. Ita kuwaje wana mama, watoto, wazee wakafa kwenye mashambulizi hayo?”
“Ndio maana kume anzishwa page za kuwasisitiza watu waondoke jiji la Dar es Salaam. Japo sifahamu ni kina nani ambao wame anzisha page hizo. Ila ukweli ni kwamba lengo na nia ya hao watu ni kuwaomba watu wasihudhurie harusi ya mtoto wa muheshimiwa kwani kuna asilimia kubwa kwa Al-Shabab kufanya mashambulizi huko. Hivyo msaada wangu ndio huo nilio wapa wa kuwafafanulia hali halisi inayo kwenda kutokea. Baada ya hapo pambeneni na hali zenu, siku njema”
Mzee Mbogo akakata simu na kila kiongozi aliyopo hapo, akaanza kupata tumbo joto. Kila mmoja akaanza kuiwazia familia yake. Wapo walio tamani kupiga simu hapo hapo kwa familia zao ili waambie waondoke Dar es Salaam, ila kutokana na kumuogopa raisi, ikawabidi kuvumilia wasiwasi unao watafuna kwenye mioyo yao.
“Muheshimiwa tuna subiri maamuzi yako. Tuna fanyaje?”
Mr the Brain alizungumza huku akimtazama raisi Mtenzi.
“Waziri wa mambo ya ndani”
“Ndio muheshimiwa”
“Zungumza na askari wako. Wape maagizo ya kufanya msako nyumba hadi nyumba. Wahakikishe wana wakamata Wasomali wote, awe mwamke, mwanaume au mtoto wa kisomali. Wote wakamatwe na wahojiwe asiye zungumza apigwe risasi afe”
“Sawa muheshimiwa, ila kwenye hilo swala la kuwaua kidogo hapo tuna weza kukiuka haki za kibinadamu muheshimiwa?”
“Nimesema waueni wote. Maswala ya haki za binadamu nita jibu mimi na sio nyinyi ume nielewa?”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa kufoka.
“Ndio mkuu nime kuelewa”
“Wewe mkuu wa majeshi. Hakikisha jiji zima na mipaka yake una mwaga wanajeshi wako. Endapo ata onekana mtu wa kutiliwa shaka, basi hakikisheni kwamba muna waaua”
“Sawa muheshimiwa”
“Mkuu wa mkoa nataka, narudi tena nataka wananchi wote wanao ondoka jijini kisa uvumi wa kimitandao. Wazuiwe na wasiingie ndani ya huu mkoa. Wale walio toka wasiingie ndani ya huu mkoa, ume nielewa?”
“Ndio muheshimiwa nime kuelewa”
“Chinas”
Mr the Brain alimuita raisi Mtenzi jina lake na kuwafanya viongozi wote kumshangaa kwani kumuita raisi jina lake halisi pasipo kutanguliza cheo au heshima yake ni kosa.
“Ume niita kwa ajili ya kukushauri si ndio?”
“Ndio”
“Basi nina kuambia ukweli. Maagizo yote uliyo yatoa kwa hawa viongozi wako yana makosa. Waziri wa mambo ya ndani pekee tu ndio aliye jitahidi kuuliza swali, ila kutokana na ukali wako ata kwenda kuwavisha Polisi wa watu joho la dhambi wazizo husika. Usitake kuigeuza nchi Sodoma na Gomora na Mungu ata tuhukumu kwa moto. Nikiwa kama mshauri wako nina pigana na wewe kwenye kila agizo ulilo wapatia hawa viongozi wako. Sio kila Msomali aliyopo ndani ya nchi yetu ni gaidi na pia na sio kila Mtanzania aliyopo ndani ya hii nchi ni mwema na nchi yake.”
“Acha kunihubiria Brain. Nenda kwenye ushauri wako nini tufanye kama hizo njia hapo una hisi kwamba hazipo sawa”
Raisi Mtenzi alizidi kuzungumza kwa hasira.
“Ushauri wangu ni kwamba. Askari na jeshi, wahakikishe wana pita mtaa kwa mtaa wakiwa na vipimo vyao vya kutafuta mabomu pamoja na mbwa wenye utambuzi wa kunusu mabomu. Hayo mambo ya kuua na kumwaga damu kwa kweli yata iweka nchi katika sifa mbaya na hata hiyo serikali yako haito pendwa.”
“Ni kweli muheshimiwa alicho kizungumza mr brain”
Mkuu wa mkoa alizungumza kwa sauti ya unyonge huku akimtazama raisi Mtenzi.
“Basi kafanyeni hivyo alivyo zungumza bwana Brain na muwe muna nipatia ripoti kila baada ya dakika kumi na tano”
“Sawamuheshimiwa”
Viongozi hao wakatoka ndani hapo huku kila mmoja akiwa na wasiwasi na mashaka makubwa sana juu ya familia yake.
“Mtenzi ni lini uta acha kufanya maamuzi ya hasira?”
“Ndivyo nilivyo”
“Badilika na kama una chindwa uta ipeleka nchi shimoni. Mimi nina ondoka zangu kazi njema”
“Hutaki kuhudhuria harusi ya kijana wangu?”
“Duu ndugu yangu hadi sasa bado una fikiria kuhusiana na ndoa ya kijana wako. Hembu fikiria ni shambulizi gani linalo kwenda kutokea. Kumguka wewe ndio raisi wa hii nchi. Ume nielewa?”
“Sawa”
Bwana the Brain aka nyanyuka, akatembea hadi mlangoni kisha akasimama. Akageuka na kumtazama raisi Mtenzi jinsi alivyo jawa na unyonge mwingi sana. Hali aliyo kuwa nayo raisi hakika ika mtia simanzi na huruma ika mtawala. Ukiachilia kwamba utendaji wao wa kazi wa pamoja, ila ni marafiki wa kipindi kirefu sana, mr the Brain akarudi na kukaa kwenye kiti chake.
“Nilihisi kwamba una weza kumuomba msamaha Mbogo, ili arudi madarakani, ila kumbue huna hata huo mpango”
“Siwezi kumuomba msamaha”
“Kwa nini?”
“Wewe una nijua kwamba siwezi kumuomba mtu msamaha. Mimi ni raisi na ana paswa kuniheshimu?”
“Kumbuka kwamba ukiachilia mbali kwamba wewe ni raisi, ila wewe pia ni binadamu. Unakosea na una paswa kumuomba msamaha kila mtu unaye mkosea”
“Siwezi badilika ndugu yangu. Nilibadilika kidogo tu pale alipo niaombea Sanga, ila kwa sasa siwezi badilika”
“Mmmm haya. Sinto ondoka nita kusaidia kwenye kukushauri kwa maana niki kuacha peke yako, nita shangaa nchi ikianguka hivi hivi”
“Una hofu na uwezo wangu wa kuongoza?”
“Tena sana. Afadhali pale mara ya kwanza nilikuwa nina uhofia kidogo ila kwa sasa, nina uhofia sana tena sana”
Raisi Mtenzi akamtazama mr the Brain kwa macho makali sana kisha akasimama na kutoka ndani ya ofisi hiyo pasipo hata kuaga na kumfanya mr the Brain kutabasamu tu kwa maana ana tambua tayari raisi Mtenzi amesha karisika.
***
“Ulinzi nina ona ni mkali sana huko nje, hivyo tusiwe na wasiwasi wowote”
Nabii Sanga alimuambia ndugu zake na ndugu wa wake zake walio fikia nyumbani kwake kwa ajili ya kushuhudia harusi ya binti yao.
“Shemeji tuna shukuru kwa taarifa kwa maana tulisha jawa na wasiwasi.”
“Ni kweli shemeji, ila muna jua kwamba mambo haya ya kimitandao siku hizi huwa yana tatizo. Kila mtu ana kuwa ana post kile anacho jisikia. Ila musiwe na mashaka kabisa. Muheshimiwa ame nihakikishia usalama wa hali ya juu”
Nabii Sanga aliendelea kuwafariji wageni hao. Mrs Sanga akasimama mara baada ya simu yake kuanza kuitwa, moyo wake uka stuka sana mara baada ya mtu anaye mpigia ikiwa aime andikwa unknown number. Akatoka nje na kusimama eneo ambalo hakuna ambaye ana msikia mazungumzo hayo.
“Haloo”
“Habari yako mrs Sanga”
Sauti mbaya inayo kwaruza kwarudha na nzito ilisikika na kumfanya mrs Sanga kuishusha simu yake kutoka sikioni na kuitazama vizuri namba hiyo.
“Nani wewe?”
Mrs Sanga alizungumza kwa ukali mara baada ya kuirudisha sikioni mwake.
“Natambua hunijiu ila mimi nina kujua. Ume muua Tomas kwa kumchoma sindano ya sumu, machungu ambayo ulinipatia moyoni mwangu hakika siwezi kukuacha uka sherekea sherehe ya huyo msichana wako”
Mrs Sanga akahisi tumbo likimvuruga, akahisi haja kubwa ikimbana kisawa sawa, ila hakuwa na la kufanya zaidi ya kuendelea kumsikiliza.
“Mimi ndio niliye fungua page zote za kuikashifu harusi ya mwanao. Sasa nina kwenda kuiweka video yako ya ngono kwenye kurasa zote. Dunia nzima ita kwenda kuona jinsi ulivyo kuwa una fir** ofisini kwa mume wako. Hahahahaahahaaaaaaaaa”
Sauti hiyo mbaya ilicheka na kumfanya mrs Sanga kutetemeka mwili mzima. Mrs Sanga akajikuta akikaa kwenye kiti kilichopo kwenye moja ya kibanda. Mrs Sanga akamshuhudia mume wake, akija eneo hilo huku akionekana kuwa ni mtu mwenye mashaka.
“Mrs Sanga”
“Be…e.e..e.e..e..e.ee”
Nabii Sanga akaka kiti cha pembeni huku akimtazama mume wake.
“Naona mume wako ame kuja hapo”
Mrs Sanga akazidi kustuka na kuangaza kila eneo la nyumba yao huku akihisi kwamba mtu anaye zungumza naye yupo ndani ya jumba lao.
“Usipate shida ya kunitafuta. Ila nina waona jinsi mulivyo kaa, weka simu yako loud speaker”
Mrs Sanga akaiweka simu yake loud speaker huku mikono yote ikitetemeka.
“Ifikapo saa mbili kamili usiku nina kwenda kuipandisha video hiyo kwenye kurasa sangu zote. Una onaje wakwe zako wakijua kwamba wewe kahaba”
Nabii Sanga kwa haraka akaikwapua simu ya mke wake na kuiweka karibu yake.
“Wewe ni nani ambaye una mtishia mke wangu kirahisi rahisi”
“Hahahahahahaaaaa nabiii Sangaaa. Nawe nina dhambi zako nyingi sana, dhambi za kumf** mwanaume mwenzako Tomas. Isitoshe mke wako aka muuua. Hahahaaaaaaaa nina kwenda kuwadhihirishia dunia kwamba nyinyi sio watumishi wa Mungu bali ni watenda DHAMBI namba moja duniania. Hahahahahaaaahahahahaaaa, subirini na muoneeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Hahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa!!!”
Mtu mwenye sauti hilo baya alizungumza huku akicheka kwa dharuau na akaikata simu na kuwacha nabii Sanga na mke wake mapigo yao ya moyo yakiwaenda kasi sana kwani ubaya ni kwamba simu hiyo haijakuja na namba na wala hawajui ni nani aliye wapiga.
“Mume wangu tuna fanyaje?”
Mrs Sanga aliuliza huku aklengwa lengwa na machozi usoni mwake.
“Sijui mke wangu tuna fanya nini na mbaya zaidi ni kwamba aliye piga ame tumia private number na hatuwezi kumjua.”
“Ehee Mungu ni aibu gani hii inayo kwenda kutukumbuka”
Mrs Sanga alizungumza kwa unyonge mkubwa sana huku akiifikiria aibu atakayo ipata kwa mamioni ya watu walio likes page hizo.
***
Levina akaachi kicheko kikali hukua kigongesheana mkono na Josephine. Mtindo alio utumia wa kutengeneza sauti ya ajabu ambayo hakika ana amini ime mzuzua mrs Sanga na mume wake.
“Hiyo saa mbili uta ziweka video zao kwenye hiyo page?”
Magreth aliuliza kwa upole hukua kiwatazama wezake.
“Kesho kama munavyo jua, mambo yanaweza kuwa sio mambo Dar. Jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba tuna vuna pesa zao kabla mambo hayajawa mabaya”
“Hapo Levina ume nena jambo. Alafu uile mzee ana pesa nyingi sana”
Magreth alitilia msisitizo jambo hilo.
“Kwa hiyo tuna fanyaje?”
“Nina fungua akaunti nje ya nchi.”
“Nchi gani?”
“Canada”
“Una weza kufungua akaunti ukiwa nchi tofauti”
Josephine aliuuliza huku akiwa na mshangao.
“Ndio tuna fungua kwenye mtandao.”
“Basi fanya hivyo”
Levina akaianza kazi hiyo na ndani ya dakika hamsini, akawa amekamilisha taratibu zote za kibeki huku akitumia baadhi ya vitambulisho feki vya Frank ambavyo alikuwa ame mtengenezea.
“Jamani mambo tayari je tuna wachukulia kiasi gani?”
“Mmmm kwa haraka haraka nabii Sanga ana weza kuwa na utajiri wa kiasi gani?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Yule mshenzi ana pesa nyingi sana. Tuwapige dola milioni mia”
“Mmmmm dola milioni mia kweli si nyingi sana?”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole.
“Awe nazo asiwe nazo lazima atoe. Tena dola mia na ishiri, kila mmoja ana chukua milioni arobaini, aisee wakizitoa hizo tuna kuwa tupo level nyingine za kimaisha jamani”
Magreth alizungumza kwa msisitizo.
“Kwa hiyo niwapigie tena”
“No watumie kila mmoja video yake kwenye simu yake, si haito onekana namba ehee?”
“Ndio namba haito onekana”
“Sawa fanya hivyo kisha baada ya dakika tano una wapigia”
Levina akamtumia nabii Sanga na mrs Sanga video zao na zote zikaonekana kufunguliwa katika wakati mmoja.
“Naona wata kuwa wana haha sasa hivi”
“Ndio, tuwape muda wa kutazama madhambi yao”
Magreth alizungumza huku akilini mwake akianza kufikiria kiasi hicho cha pesa ambacho ni kikubwa sana.
“Wapigie sasa”
Magreth alizungumza. Levina akaiunganisha simu yake na mfumo ambao una toa sauti mbaya na za kutisha. Simu ya mrs Sanga aikaanza kuita na baada ya sekunde tano ikapokelewa.
“Nina ona mume pata zawadi zenu sasa?”
Levina alizungumz akwa sauti yake ya kawaida, ila kwa upande wa mrs Sanga ana isikia sauti nzito yenye mikwaruzo na ina tisha.
“Ndio tuambie ni nini tuna paswa kufanya Kama una taka pesa zungumza”
“Hahaaaa una hisi pesa zina weza kurudisha uhai wa Tomas?
“Nakuomba unisikilize wewe mtu. Kama una fanya haya mambo kwa ajili ya pesa ni heriuka zungumza, una nielewa. Usitake kutu black mail mimi na mke wangu kwa ajili ya shida zako.”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti kali sana.
“Mzee usiwe jeuri sana kwa maana tuna weza kuishusha hiyo heshima yako uliyo jitengenezea kwa muda mredu ndani ya dakika moja tu tuna iharibu”
“Sawa sawa, sema una hitaji nini?”
“Kabla haijafika saa mbili usiku nina hitaji kwenye akaunti yangu kuwe na kiasi cha dola milioni mia moja hamsini”
“Dola milioni mia moja na hamsini?”
“Ndio. Sasa chagua pesa au heshima yako ya mke wako na familia yako kwa ujumla. Kumbuka kuna waumini wako wanao kusujudia na kukuona wewe ni mwema sana, kumbe ni mtu mwenye dhambi kuliko hata mtengeneza dhambi shetani. HahahaaahahHAHA”
Levina alizungumza kwa kujiamini sana kisha akakata sim hiyo.
“Hapo ume wakomesha. Sasa watumie hiyo akaunti namba na jina”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Josephie akafanya kama vile alivyo agizwa na wote wakaka mkao wa kusubiria mamilioni ya pesa ambayo endapo wata yapata basi maisha yao yana kwenda kubadilika kwa asilimia kubwa sana.
***
“Milioni mia moja na hamsi dolar ni nyingi sana mke wangu. Mimi siwezi kuzitoa”
“Mume wangu, heshima tuliyo nayo sio sawa na hiyo pesa. Piga picha hizi video zikiwa mtandaoni una hisi kwamba ni nani ambaye ata kanyaga pale kanisani kwetu”
“Nina waza kitu”
“Kitu gani?”
“Magreth ndio mtu wa pekee amabaye ana hizi video na yeye ndio aliye tuambia kuhusiana na kufa kwa Tomas na yeye ndio mtu wa pekee ambaye ana tishia juu ya hizo video. Nina imani yeye ndio ana fanya huu mchezo”
“Sawa mume wangu. Kama ni yeye je tuna fanyaje, ikiwa hatujui ni wapi alipo na wala hatujui ata fanya nini hiyo saa mbili, ikiwa sasa hivi yame baki maaa sita hadi ifike saa mbili usiku”
“Nita kuambia”
Nabii Sanga mara baada ya kuzungumza hivyo akanyanyuka na kuondoka eneo hilo na kumuacha mke wake akiwa katika wakati mgumu sana. Nabii Sanga akaingia chumbani kwake huku akiwa amejawa na hasira kali sana. Akilini mwake ana muwazo Magreth ni kwa nini ana msumbua kwa kiasi hichi.
‘Wewe malaya lazima nita kuua’
Nabii Sanga alizungumza huku hasira ikiwa imemtawala kisaswa sawa. Akachukua funguo ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8. Akaanza kushuka kwenye gari na akakutana na mtoto wake wa kwanza.
“Baba mbona speed speed wapi tena”
“Kuna swala nina kwenda kulishuhulikia mara moja.”
Nabii Sanga alijibu kwa ufupi kisha akaendelea kushuka kwenye ngazi hizo. Akatoka nje na kuanza kutembea kuelekea kwenye gari lake. Mke wake akamfwata kwa haraka.
“Una kwenda wapi mume wangu?”
“Nina kwenda kwenye mgahawa wa yule malaya na nikimpata hakika nina muu”
“Twende wote”
“Ingia kwenye gari sasa, acha kushangaa shangaa”
Wote wakaingia kwenye gari, kitendo cha nabii Sanga kuwasha gari lake tu, simu yake ikaanza kuita, akaitoa mfukoni na kukuta ni watu wanao wasumbua. Akaipokea na kuweka loud speker.
“Sanga Sanga, una kwenda wapi?”
Sauti hiyo ilizungumza na kumfanya nabii Sanga na mke wake kuanza kuangaza angaza kila eneo la nyumba yao.
“Nina kwenda kukutafutia pesa unazo hitaji?”
“Nyuso zenu zime jaa hasira. Sidhani kama una kwenda kutafuta pesa”
“Kwani wewe una taka tutabasamu ili iweje?”
Nabii Sanga alizungumza kwa kufoka sana.
“Hahaaaaahahaaa nabii Sanga Sanga Sanga, usinifokee kabisa. Haya nenda katafute hizo pesa”
Simu hiyo ikakatwa na kuwafanya nabii Sanga kuzidi kushangaa.
“Huyu mshenzi yupo hapa ndani”
Nabii Sanga akizungumza huku akitazama tazama watu waliopo hapo kwao.
“Ndio hata mimi nina hisi hivyo kwa maana ame juaje kwamba tumeingia ndani ya gari?”
Nabii Sanga akashuka ndani ya gari na kuanza kumtazama ndugu na jamaa walipo eneo hilo. Kila mmoja ana onekana kuwa yupo bize. Nabii Sanga akaingia sebleni na kuwaangalia wageni ila wote wana onekana kuwa bize na mambo yao. Akarudi kwenye gari alipo muacha mke wake.
“Kila mtu namuona yupo bize na mambo yake”
“Hembu twende kwanza kwenye mgahawa wa yule mpuuzi”
Wakaondoka nyumbani hapo na wakafika katika mgahawa na Magreth. Jambo la kushangaza wakakuta mgahwa huyo ukiwa ume fungwa na hakuna mtu hata mmoja.
“Umamini mke wangu kwamba ni Magreth”
“Ndio, kama ingekuwa sio yeye tunge mkuta hapa. Ila ana fanya makosa kisha ana kimbia”
“Tuna fanyaje mke wangu?”
Nabii Sanga aliuliza kwa sauti ya upole huku akiwa amejichokea.
“Tumpatie hizo pesa alafu najua ni jinsi gani ya kuzirudisha”
“Sawa mke wangu, ila dola milioni mia moja na hamsini ni nyingi sana. Hapo tuna zungumzia billions of shilingis baby”
“I know honey. Ila ita tulazimu kulinda heshima yetu. Ona hizi video zikienda hewani ita kuwaje. Kesho tutatazamwa vipi na jamiii. Ukiachilia mbali jamii, je watoto wetu wata tuangalia vipi mume wangu. Tupo kwenye bad position.”
Nabii Sanga akashusha pumzi huku kitafakari kutoa kiasi hicho cha pesa. Japo wana pesa nyingi sana zaidi ya dola bilioni ihirini ambazo ni pesa halali, ila kwenye akaunti zao za siri ambazo zina ingiza pesa zipatikanazo na biashara haramu, ni nyingi zaidi ya pesa zao halali.”
“Hili swala kama lingekuwa sio la aibu, ninge mshirikisha raisi”
“Ni kweli, ila hatuwezi kumshirikisha yule ni mkwe wetu laiti akijua sisi tuna tabia kama hizi nina imani ata leta ukinzani katika ndoa ya mtoto wetu”
“Haki ya Mungu kama ingekuwa sio harusi ya binti wetu hakika nisinge toa hii pesa”
“Ndio hivyo mume wangu. Alafu kabla ya kuwapa pesa hizo ina bidi watuhakikishie kwamba wana futa video zetu na hawazitumii kama chanzo cha kutuchafua tena”
“Yaani ukisikia kucheza kamari ndio leo”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwasha gari lake na kuondoka eneo hilo.
***
Polisi wakisaidiana na wanajeshi wakazidi kusambazwa mitaani huku wakiwa na vifaa vya kutafuta mabomu pamoja na mbwa walio funzwa uwezo wa kutambua bomu. Msako huo ukazidi kuwashangaza wananchi wengi, kila mmoja alijawa na swali lake ambalo halikuwa na jibu. Msako huo haukuweza kuza matunda yoyote kwa maana wengi wao wana hisi kwamba mabomu hayo ni makubwa au ya kutega kama yaliyo zoeleka. Ripoti ya msako huo ikatolewa kwa waziri wa mambo ya ndani naye akawasiliana raisi Mtenzi na kumueleza hali ya usalama iliyopo ndani ya jiji zima.
“Kwa hiyo hakuna bomu lolote?”
“Ndio muheshimiwa, vijana wangu wamefanya kazi ya mtaa kwa mtaa na hakuna ambaye ameweza kukuta hata kipisi cha bomu”
“Kazi nzui sana waziri kwa hiyo kesho harusi ya vijana wangu iendelee kama kawaida”
“Nina kuhakikishia muheshimiwa ulinzi uta kuwa ni asilimia mia moja. Furaha itawale ndani yako muheshimiwa na kama ni hawa Al-Shabab nina kuhakikishia muheshimiwa, tuta kwenda kuwa bamiza endapo tu wana onyesha nyuso zao”
“Basi kazi nzuri sana.”
“Nashukuru muheshimiwa”
Raisi Mtenzi akakata simu huku akiwa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Hofu na mashaka ikamuisha kabisa. Akatoka ofisini kwake na kuelekea katika nyumba anayo ishi ndani ya ikulu hiyo hiyo. Akakuta shamra shamra za maandalizi ya harusi zikiwa zina endelea kama kawaida.
“Baba vipi ume fanikiwa kufahamu ni kina nani wanao eneza upuuzi?”
Jery aliuliza huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana.
“Wala usijali katika hilo. Wewe jiandae kesho una chukua mke wako”
“Nashukuru sana baba”
“Usijali mwanangu”
Raisi Mtenzi akamkumbatia kidogo Jery kisha akamfwata mama yake mzazi ambaye ame zeeka sana na akaka pembeni yake na wakanza kuzungumza kilugha.
***
Levina, Magreth na Josephine kila muda macho yao wana yatupia kwenye saa zao. Kila mmoja ana ona saa mbili usiku ni mbali. Kila mmoja wao ameingiwa na tamaa ya utajiri na hakuna hata mmoja wao ambaye ana fikiria umakisikini tena.
“Zime baki dakika ishirini kufika saa mbili na hawajatuma chochote”
Levina alizungumza huku akiwatazama wezake.
“Labda tuwapigie tena na kuwasisitizia”
Josephine alishauri.
“Hapana tusiwapigie endapo wapipo tuma. Ikifika saa mbili kambili Levina uta zipandisha video zao zote kwenye mtandao. Sisi tutakosa pesa na wao wata kosa heshima, na sidhani kama raisi na familia yake akiwaona wakwe wezie ata kubali kuwaozesha”
Magreth alizungumza kwa msisitizo kutokana yeye ndio kiongozi wao hapakuwa na mtu aliye pinga wazo hilo kwani lengo lao la toka mwanzoni ni kuhakikisha kwamba wana ichafua heshima ya nabii Sanga na mkewe.
ENDELEA
Levina akajifikiria kwa sekunde kadha akisha akanyaua simu yake na kumpigia kumpigia nabii Sanga.
“Unwa fanya nini Levina”
Magreth aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.
“Pesa ni muhimu kwetu. Mambo ya heshima zao sisi hayatuhusu ni lini sii tuta kuwa na pesa nyingi ni lini nasi tuta heshimika na kuwa watu wenye hadthi ndani ya hii nchi hii?’
Maswali mfululizo ya Levina yakamfanya Magreth kukaa kimya na kumuacha afanya kile anacho hisi kwamba ni sahihi. Simu ya nabii Sanga ikapokelewa.
“Naamini mume jianda kwa nyeti zenu kuonakena hadhariani”
Levina alizungumza kwa msisitizo.
“Hiyo pesa ipo na tupo kwneye hatua za kuzituma. Ila hatuwezi kuzituma pasipo wewe kutu hakikishia kufuta video hizo kwa maana muna weza kuzitumia siku nyingine kudai pesa, sasa uta uwani mchezo wa kitoto”
Levina akawatazama wezake. Magreth akazungumza bila ya kutoa sauti na Levina akamuambia.
“Nyinyi muna taka tuwadhibitishie vipi kwamba tuna zifuta video hizo?”
“Nina hitaji kuonana nawe ili kama ni kuzifuta basi uta zifuta mbele yangu na mke wangu”
Matakwa ya nabii Sanga yakazidi kumbada Levina, akakosa cha kujibu zaidi ya kuwatazama wezake, Magreth akachukua simu ya Levina na kumfanya Levina kushangaa.
“Saa tisa kamili usiku tukutane katika fukwe za koko beach. Hakikisha una kuja na mke wako enapo uta kuja na mtu zaidi ya mmoja basi viche vyenu kesho ita kuwa ni zawadi za maharusi wenu”
Magreth mara baada ya kuzungumza hivyo akakata simu.
“Tuna rudi Dar es Salaam”
Levina alizungumza huku akichukua funguo ya gari lake juu ya meza.
“Dar!!?”
Josephine alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka.
“Ndio hau hamjanisikia”
“Ila Levina Dar si mabomu yana lupika?”
“Munataka pesa au hamtaki pesa?”
Josephine na Levina wakatazamana.
“Tuna taka”
Levina akajibu kwa sauti ya upole.
“Tuondokeni”
Magreth alizungumza hukua kitangulia mlangoni. Levina na Josephine kila mtu akachukua kilicho chake na wakatoka ndani hapo huku wakiwa na wasiwasi na mashakama mengi sana. Wakaingia kwenye gari huku kila mmoja akitamani kumuuliza swali Magreth ila wana hofia kwa maana ana onekana kukasirika.
“Fungeni mikanda kwa maana spidi nitakayo tembea nayo kuna mawili, tuwahi kufika Dar es Salaam au tuwahi kufika mbiguni. Tumeelewana?”
Magreth aliuliza kwa ukali kidogo. Levina akajikuta akihamia siti ya nyuma alipo Josephine, akajifunga mkanda wa siti na safari ikaanza huku Magreth akihakikisha kwamba ana fanya kila liwezekanalo, ana tumia masaa mawili au mawili na nusu kufika Dar es Salaam wakitokea Morogoro.
***
“Nilikuambiaje mke wangu. Hawa watu wana taka pesa na ni lazima wangepiga simu”
Nabii Sanga alizungumza huku akimtazama mke wake.
“Sasa wana hitaji tukutane koko hiyo saa tisa mume wangu si hatari?”
“Ndio ni hatari, ila ina tubidi tuwaambie vijana wetu. Hatuwezi kwenda sisi kama sisi”
“Sasa vijana ukiwaambia si lazima watatumia njia ya baharini kuja huku. Je ulinzi ulio imarishwa, ita kuwaje mume wangu”
“Ila yupo Tyson acha niwasiliane naye”
“Huyo si alishindwa kumpata Evans je hao watu wengine kwelia ata weza kuwapata?”
“Namuamini Tyson na isitoshe jambo la Evans liliingiliwa na watu ambao hatuwajui”
“Sawa mpigie”
Nabii Sanga akampigia Tyson, simu ikapokelewa.
“Ndio muheshimiwa”
“Upo Dar es Salaam”
“Ndio”
“Kuna kazi, ikiwezekana tuonane muda huu”
“Wapi?”
“Niambie nikufwate”
“Nipo Kimara kwa sasa”
“Sogea hadi Ubungo”
“Sawa mkuu”
Nabii Sanga akakata simu. Wakatoka chumbani kwao na mke wake, wakaingia kwenye gari na kuoandoka, wakafika Ubungo sheli, Tyson akashuka kwenye gari lake na kuingia kwenye gari la nabii Sanga ambalo vioo vyake ni vyeusi kasoro tu kioo cha mbele.
“Habari yako Tyson”
“Salama mkuu, heshima yako. Mama heshima yako”
“Nashukuru”
Mrs Sanga alijibu huku wote wakiwa wame mgeukia nabii Tyson aliye kaa siti ya nyuma.
“Nina imani una mualiko wa harusi ya binti yangu?”
“Ndio mkuu na kesho Mungu bariki ni lazima nifike”
‘Sawa, ila kabla ya kesho kufika, tume pata mtihani kidogo. Kuna watu wana tupigia simu za vitisho wana hitaji pesa nyingi sana na sisi hatuna mpango wa kuwapatia hizo pesa. Wana hitaji tukutane nao koko bichi mida ya saa tisa kamili usiku. Nahitaji ufanye jambo, tuna hitaji udungue huyo mtu na nahitaji kumjua kwa maana ana ifanya siku yangu nzima kuenenda vibaya”
“Sawa mkuu hilo swala lina wezekana. Malipo nina imani kwamba yata kuwa ni makubwa”
“Siwezi kukuangusha kwenye hilo”
“Sawa saa tisa kasoro usiku nita fika pale. Nita jiweka sehemu ambayo sio rahisi kwa huyo mtu kuniona”
“Hakuna shaka tuta onana huo muda”
“Sawa sawa muheshimiwa”
Tyson akashuka kwenye gari hilo, akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo.
“Kazi ime kwisha mke wangu twende tuka ungane na familia yetu”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana moyoni mwake. Wakandoka eneo hilo na kurudi nyumbani kwao.
***
“Hakuna hata simu yetu moja iliyo okotwa na askari hivyo kesho mpango wetu upo pale pale. Ifikapo kesho saa tisa kamili alasiri Dar es Salaam yote ita geuja na kuwa tanuri la jehanamu”
Omary alizungumza kwa furaha kwa maana walikuwa wakiufwatilia msako wa wanajeshi pamoja na mbwa wao kuhakikisha wana tafuta kama kuna mabomu yoyote yale yaliyo tegwa ardhini. Omary na wezake usiku huo waka utumia katika kusoma baadhi ya dua za kujikabidhi mikononi mwa mwenyezi Mungu kwani wana amini kwamba jambo wanalo kwenda kulifanya kesho lita kuwa ni jambo la kishujaa na wata kubukwa sana kwenye familia zao miaka na miaka.
Walipo maliza kusoma dua hizo, wakaanza kula vyakula vizuri ambao mwenyeji wao aliwaandalia, ikiwa ndio vyakula vyao vya mwisho mwisho kula wakiwa hai.
“Najua kwamba kesho tuna kwenda kufa si ndio”
“Ndio”
“Mwenyezi Mungu ata tupokea na tuna ingia peponi tukiwana furaha sana”
Omary alizungumza kwa msisitizo huku furaha ikiwa ime mtawala.
“Kesho nina hitaji kila mmoja uso wake uwa na furaha. Kesho ni siku yetu ya ushindi, je tupo pamoja”
“Ndio tupo pamoja”
Vijana hao walishangilia kwa furaha sana kana kwamba kesho wana kwenda kucheza fainali za kombe la dunia.
***
Majira ya saa sita Magreth akasimamisha gari lake mbele ya nyumba amba yake ya Kigamboni. Levina na Josephine wakamshukuru Mungu kwa kufika salama eneo hilo kwa maana spidi aliyo kuwa ana tembea nayo Magreth barabarani hakika haikuwa ya kawaida. Kitu kilicho wasaidia ni foleni ya magari kidogo ndio ime wafanya wasiende mwendo wa kasi sana.
“Levina nahitaji uchukue gari lako. Tuna ondoka hapa”
“Kumbe hatuingii ndani?”
“Kwani kuna kitu cha kuchukua tofauti na gari lako?”
“Hakuna”
“Basi chukua gari lako na tuna elekea nyumba ya kule”
“Sawa”
Levina akashuka kwenye gari, akaingia ndani hapo, moja kwa moja akapitiliza hadi chumbani alicho kuwa naa kaa. Akachukua fungua ya gari lake akatoka nje na kukuta Josephine akiwa tayaria mesha fungua geti kubwa. Levina akaingia kwenye gari lake na kulitoa ndani hapo. Magreth akafunga nyumba yake, kisha wakaondoka eneo hilo. Wakafika katika nyumba iliyopo pembezoni mwa habari na imejitenga na nyumba nyingi.
“Ehee tume rudi Dar tuna mpango gani Mage”
Levina alizungumza huku akifunga mlango wa gari lake.
“Nifwateni”
Magreth alizungumza na wakaingia kwenye banda kubwa la gereji iliyopo nyumbani hapo. Magreth akafunua turubai kubwa lililo ifunika pikipiki yake ambayo ni kubwa.
“Waooo hii pikipiki ni ya nini?”
Josephine alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana
“Ni yangu na nimpya kabisa”
“Duu hizi pikipiki hivi bongo zimesha ingia?”
“Tanzania nzima tupo watu wawili tu ambao tuna mikili hizi pikipiki. Sasa pointi yangu ni kwamba nina kwenda mimi mwenyewe Coco kwa kutumia hii pikipiki. Nahitaji wewe Levina unisaidie kwenye jambo moja, sihitaji kuitumia sauti yangu hii, je una uwezo wa kuibadilisha sauti yangu na ikawa kama sauti uliyo kuwa una zugumza na hawa viajuza?”
“Sauti kubadilishwa ina wezekana.”
“Kweli?”
“Ndio, kuna mfumo fulani hivi una tumika, na kuna viji plasta vina tumika kubadilisha sauti, huwa una vifunga hapa shingoni. Sasa vipo nyumbani kwangu”
“Sasa hivi ni saa saba kasoro, tuna weza kwenda kuvichuku”
“Hakuna noma”
Wakaingia kwenye gari la Levina na kuondoka nyumbani hapo. Wakafika nyumbani kwa Levina na wakaingia ndani wakiwa na tahadhari kubwa kwani toka Levina aondoke nyumbani kwake hapo leo hii ndio ana rudi. Walipo hakikisha kwamba kuna usalama wa kutosha wakawasha taa za ndani.
“Njooni huku”
Levina alizungumza huku akielekea chumbani kwake. Wakaingia katika chumba hicho, Levina akaminya moja ya batani na kitanda chake kikaanza kusogea pembeni.
“Heee kitanda mbona kina sogea”
Josephine aliuliza kwa mshangao.
“Usishangae”
Levina alijibu huku akiwa amejawa na tabasamu. Mlango wa siri ambao upo chini ya kitanda hicho ukafunguka. Wakaanza kushuka kwenye ngazi na wakaingia katika chumba kilichopo ardhini.
“Karibuni, katika chumba hichi ndipo ninapo fanya kazi zangu za kutengeneza sura za bandia pamoja na mambo mengine mengine kama vyeti vya bandia hati za bandi na kadhalika”
“Ahaa hongera”
Josephine alizungumza kwa furaha sana.
“Magreth ni sauti ya aina gani ambayo una hitaji uwe una zungumza nayo?”
“Nzito yaani kama uliyo kuwa ana isikia nabii Sanga”
“Sawa”
Levina akawasha laptop yake na kumuomba Magreth azungumze neno lolote na akalirekodi, akaanza kuitengeneza sauti hiyo. Mara baada ya kumaliza kuifanya kazi hiyo, akamuwekea Magreth kiji plasta shingoni mwake eneo la koromeo.
“Sema mama”
“Mama”
Magreth na Josephine wakajikuta wakishangaa kwa maana sauti yake ime kuwa nzito.
“Hichi kiplasta ume weka nini?”
“Ni utaalamu, ukikibandua, sauti yako ina rudi kuwa ya kawaida. Ila ukikiacha basi sauti yako ina kuwa nzito.”
“Hapa nahitaji nirushe ndege ndogo isiyo na rubani, ambayo ita kuwa ina kufwatilia kila unapo kwenda”
“Ipo wapi?”
Levina akafunua kitambaa kilicho ifunika ndege hiyo ambayo ni ndogo ila ina urefu wa futi nne.
“Hii ina uwezo wa kuzunguka kila eneo la nchi na nje ya nchi hii na nina weza kuiendesha nikiwa sehemu yoyote ile”
“Ume itengeneza wewe?”
Josephine aliuliza.
“Ndio, nime itengeneza mimi. Pia ina uwezo wa kwenda juu usawa wa ndege hizi kubwa zinapo pita. Kiufupi ni nzuri nime ifanyia majaribio kama mara nne hivi na ime fanya vizuri”
“Hapo rafiki yangu uta kuwa ume nisaidia sana kwa mana ninavyo mjua nabii Sanga ni lazima ata jaribu kutafuta msaada wa pembeni. Endapo ata fanya hivyo, ina bidi unipe taarifa nihakikishe nina anza na hao ambao wana msaidia, kisha baada ya hapo nina dili naye”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akiwatazama wezake hao.
“Sasa Mage, je ikiwa hivyo uta muua nabii Sanga na mke wake?”
Swali la Josephine kikamfanya Magreth kujifikiria kwa muda kisha akashusha pumzi na kumtazama Josephine kisha akatingisha kichwa akimaanisha hato fanya hivyo na kuwafanya wezake wamshangae kwa maana kama ni nafasi ya kumuua nabii Sanga na mke ndio hiyo hapo.
“Kwa nini sasa usiwaue?”
Levina aliuliza kwa mshangao.
“Nataka kuwatesa kwa maumivu ya moyo kama niliyo kuwa nina pitia mimi. Nitakapo ridhika na mateso hayo basi uta kuwa ni wakati wa wao kufa”
Josephine akajikuta akiangua kicheko sana kwa maana jinsi sauti ya Magreth ilivyo badilika hakika ina chekesha.
“Sawa kama ume amua kufanya hivyo kwa maana sisi tuna kusikiliza wewe. Sasa hivi ni saa nane ina kubidi ukaonane naye”
“Ni kweli, tuondokeni”
Levina akasaidia na Josephine kubeba vifaa vyake ambavyo ana amini kwamba vita wasaidia katika kazi hiyo. Wakafika katika nyumba ambayo kwa sasa wana isha. Magreth akaanza kujiandaa na kuivaa nguo yake hiyo inayo mfunika mwili mzima na eneo la machoni line tengenezwa na miwani ngumu ambayo haipitishi risasi yoyote. Miwani hiyo ina uwezo wa kumsaidia Magreth kuona hata kwenye giza nene. Magreth akachukua upanga wake mrefu ambao ume chomekwa kwenye kibebeo chake. Akavaa kibebeo cha upanga huo mgongoni mwake. Cheni yake ndefu yenye kisu kilicho jikunja mbele kidogo akaizungusha kuinoni mwake na kuifunga vizuri. Akabeba silaha ndogo ishirini zenye umbo la nyota.
“Magreth hii ni kifaa cha mawasiliano, kivae sikioni mwako. Tuta kuwa tuna wasiliana na nita kupatia taarifa ya kula kitu ambacho uta pitia sawa”
“Sawa”
Magreth akafungua vizipu vya nguo hiyo na kuivua eneo la kichwani mwake kisha akavaa kifaa hicho na kuirudishia nguo hiyo.
“Hii ndio simu ambayo ina video zao na na namba zao. Hakikisha kwamba una wakabidhi na wana futa wao wenyewe”
“Pesa”
“Mimi nipo online, mukifika pale muta kubaliana muingiziane hicho kiwango cha pesa kisha pesa zikiingia huku uta wapatia hiyo simu wazivute au waende nayo kabisa”
“Hakuna kitu kinacho onyesha kwamba ni wewe ndio mmiliki wa hiyo simu?”
“Hakuna”
“Ila jamani kama wakifiria kwmaba hizo video zita kuwa kwenye simu nyingine ita kuwaje?”
Josephine alitoa wazo hilo na kuwafanya wajifikirie kwa sekunde kadhaa.
“Wata amini hivyo hivyo, hatuna muda wa kujieleza sana kwao”
“Sawa kama ni hivyo”
Magreth akaaingiza simu hiyo mfukoni. Akafungua sanduku lenye vifaa vyake, akachukua bastola moja pamoja na magazine iliyo jaa risasi, akaichomeka magazine hiyo na kuichomeka hiyo kwenye mfukoulipo kwenye paja la mguu wa kushoto. Uzuri wa nguo hiyo ime tengenezwa na viatu vyake maalumu ambavyo vime unganishwa na suruali ya chini.
“Kuwa makini Mage”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole”
“Usijali”
Wakatoka nje, Magreth akapanda kwenye pikipiki yake, Josephine akafungua geti na Magreth akaondoka eneo hilo. Levina akawasha ndege yake hiyo ndogo inayo endeshwa bila rubani, akairukisha hewani na ilipo fika kimo fulani akarudi ndani kwa haraka na kuanza kuiongoza kwa kupitia laptop yake na kila eneo ambalo Magreth ana pita wana liona vizuri kwa maana ndege hiyo ina mfwatilia.
***
Raisi Mtenzi akamimina wyne kidogo kwenye glasi yake na kuanza kunywa taratibu akiwa amekaa eneo la kupumzikia ndani ya ikulu. Jery kutokana na kiweru weru cha ndoa, siku hiyo naye hakupata usingizi kabisa, akatoka chumbani kwake na katika kukatiza katiza akamuona baba yake akishusha mvinyo huo taratibu. Akatembea hadi eneo hilo na kukaa.
“Baba huja lala?”
“Yaa sija lala bado vipi una fanya nini nje usiku huu?”
“Yaani baba hapa akili yangu yote ina muwaza Julieth”
“Haha yule ni wako. Ila una jua hiyo hali yako ina nikumbusha kipindi hicho ambacho nili kuwa nina muoa mama yako. Usiku ule wa kuamkia harusi, kwa kweli sikuweza kupata hata lepe la usingizi”
“Wee!!”
“Haki ya Mungu vile, yaani ile siku nilijikuta nikiwa katika wakati wa kuwaza ita kuwaje kanisani. Ila nina mshukuru Mungu nilimuoa mama yako akiwa bikra kabisa”
“Duuu kwa hiyo mimi na wewe tume pata bahati ya kuoa wana wake bikra?”
“Yaa ni bahati kwa kweli hususani kwenye hii dunia yenu ya sasa iliyo jaa mitandao ya kijamii ya kila aina”
“Ni kweli. Ehee baba nipe experience yako kwenye ndoa ilikuwaje?”
“Mmmm mama yako jambo la kwanza ambalo lime nivutia kweke ni kwamba ana nisikiliza na kunitii. Mwanamke akiwa ana kusikiliza wewe mume ndani na kutii kile unacho zungumza basi huyo ni mwanamke mzuri. Hata kama ata kuwa ana pinga kauli yako basi ana ipinga kwa unyenyekevu ambao akikuambia wewe mwaume kweli una jikuta una kubaliana naye”
Raisi Mtenzi alizungumza kwa suati ya upole. Akapiga fumba la wyne hiyo.
“Chuku glasi unywe na wewe”
Jery akanyanyuka na kuelekea jikoni, akachukua glasi na kurudi eneo hilo. Baba yake akamiminia kiasi hicho cha wyne na wakaendelea na mazungumzo.
“Kipindi nilipo kuwa nina jiunga na jeshi la polisi, nilikuwa kijana mmoja machachari sana. Nilikuwa nina ruka sarakasi sana kwa hiyo mabinti wengi walinipenda sana pale chuoni. Aisee nili wachinja”
“Hahahaaaa”
Jery alicheka kwa furaha sana kwani toka azaliwe hajawahi kuzungumza na baba yake mazungumzo kama hayo.
“Haki ya Mungu vile, yaani niliwachinja, sema nilikuwa nina akili sana. Sikuwahi kukamatwa hata siku moja na mkufunzi yoyote pale chuoni. Hadi nina maliza na kupewa ajira, nika endelea kuwatafuna hadi nilipo kuja kumpata mam yako na akaniwekea mkazo nisi mle hadi tufunge ndoa, hapo ndipo nilipo weza kuyaelewa maana ya mapenzi na toka nimuoe mama yako sikuwahi kutoka nje ya ndoa yangu”
“Kweli?”
“Haki ya Mungu vile, nami nina kuasia usiruke ruke, magonjwa ni mengi na si una jua kwamba haya jali kama wewe ni mtoto wa raisi au ni dokta”
“Yaa nalitambua”
“Wewe kaa na yule binti, isitoshe ni mzuri na amekamilika kila idara. Ila angalizo moja, asikupande kichwani, endapo uta ona ana dalili fulani ya kukupanda kichwani, mtulize kwa ukali au hata kumtandika makofi mawili matatu. Ila ukisema kwamba uwe mpole na mnyonge mwanamke ata kupanda kichwani”
“Usijali baba nita kuwa kiongozi bora wa familia yangu”
“Sawa, unajua japo kumpiga mwamke sio jambo zuri. Ila kwa hichi kizazi chenu kwa kweli usipo mlamba makofi kadha ana weza kupeleka puta”
“Nime kuelewa baba”
Nabii Sanga akamtazama Jery ambaye ndio mwanaye wa pekee kwani kwenye maisha yake ame bahatika kupata watoto wawili wa kime na mtoto wake wa kwanza alikuwa ni jambazi na akaagiza polisi wake kipindi ni RPC kumuu ili kuli tawanyisha kundi hilo la kihalifu lililo kuwa lina pora magari na mali za watu katika mkoa wa Kagera.
***
Majira ya saa tisa kasoro usiku nabii Sanga na mke wake wakaanza safari ya kuelekea Coco beach. Safari yao haikuwachukua umbali mrefu kwa maana hawapo mbali sana na beach hiyo. Wakafika karibu beach hiyo, nabii Sanga akampigi simu Tyson.
“Vipi sisi ndio tuna karibia”
“Mimi nimesha fika eneo la tukio n anime jitegea sehemu ambayo nina weza kuona kila kitu”
“Sawa hakikisha una mtandika risasi ya mguu, nina imani kwamba hato kuwa na uwezo wa kunikimbia”
“Hakuna shaka muheshimiwa”
Nabii Sanga akakata simu huku akimtazama mke wake usoni. Akaliendesha gari lake taratibu hadi kwenye maegesho ya beach hiyo. Akazima taa za gari hilo na hawakushuka kabisa.
“Mume wangu nahisi kuogopa”
“Usiope mke wangu, huyu mjinga lazima nimuue leo”
“Sawa mume wangu”
Wakaendelea kukaa ndani ya gari huku wakiendelea kuangaza angaza eneo hilo wakisubiria kuonana na mtu aliye ahidi ana naye kufika eneo hilo.
“Punguza mwendo”
Sauti ya Levina ilisikika vizuri kabisa masikioni mwa Magreth ambaye tupo kasi na pikipiki yake hiyo, taratibu Magreth akapunguza mwendo kasi wa pikipiki hiyo.
“Ume ona nini?”
“Ngoja kwanza nivute kwa ukaribu eneo hilo”
Levina alizungumza huku akilivuta eneo zima la coco beach kwa ukaribu kwa kutumia kamera iliyo fungwa kwenye ndege hiyo.
“Hei nime ona mtu”
Levina alizungumza huku akiwa amehamaki.
“Wapi?”
“Eneo la mashariki mwa beach. Tena mtu huyu ana bunduki….Ohooo Mungu wangu, ana onekana ni mdunguaji”
“Okay ngoja nifanye jambo”
Magreth akasimamisha pikipiki yake kwenye moja ya mti ambao upo mbali kido na beach hiyo.
“Umesema kwamba yupo eneogani?”
“Hapo ulipo ni upande wako wa kulia. Songa mbele uta tokea nyuma yake”
“Poa”
Magreth akaanza kukimbia pembezoni mwa barabara. Akamuona Tyson kwa mbali kidogo akiwa amelala kwenye moja ya jiwe kubwa huku bunduki yake akwia ame ielekezea eneo la beach hiyo. Magreth akajibanza kwenye moja ya mti, akatoa simu yake na kumpigia nabii Sanga.
“Upo wapi?”
Sauti ya Magreth alikuwa ni mbaya hadi nabii Sanga akaitazama simu yake mara mbili.
“Tumesha fika beach hapa jitokeze”
“Nime waona”
Magreth akakatasimu na kusubiria kwa sekunde kadhaa. Nabii Sanga kwa haraka akampigia simu Tyson.
“Amesha vika jiandae”
“Sawa mkuu”
Magretha akashuhudia jamaa huyo akishusha simu yake sikioni na kuiweka pembeni huku akiongeza umakini wa kuangalia eneo zima la beach. Magreth akakimbia kwa kasi kabla hajafika eneo la karibi na alipo Tyson, Tyson akageuka kwa haraka kwani hata yeye ana machale ya hali ya juu. Akachomoa bastola yale, ila kabla haja fyatua risasi tayari Magreth alisha rusha teka lililo ipiga basola hiyo pembeni.
Uharaka wa Magreth uka mshangaza sana Tyson ambaye akajipanga kwa kupigana kwa mkono kwa mkono kuhakikisha kwamab ana mkabili mtu huyo aliye valia mavazi ya ajabu.
“Una nafasi ya kuondoka eneo hili na ukamuachia nabii Sanga kisanga chale la sivyo nita kuua”
Sauti nzito na yenye mikwaruzo, ikamshangaza sana Tyson kwani katika ujasusi wake wote hajawahi kukutana na mtu anaye fanania hivyo.
“Una hisi kwamba nina kuogopa?”
Tyson alizungumza huku akijiandaa kufanya shambulizi. Magreth akamtazama Tyson kwa umakini, usimamaji wake kati kupigana akajua kabisa kwamba ana weza kumuhimili.
“Mage una muweza?”
Levina aliuliza huku yeye na Josephine wakifwatilia mtanange huo moja kwa moja kupitia laptop yake. Tyson akaanza kurusha ngumi mfululizo. Magreth akazikwepa ngumi hizo, huku naye akituma makombora ya nguvu ambayo mengi yalimpata Tyson mwilini mwake.
“Nina kupa nafasi ondoka”
“Siwezi kupigwa na kiumbe cha ajabu kama wewe”
Kauli hiyo Tyson ilio jaa dharau ndani yake, ikamfanya Magreth kuchomoa mnyororo wake huo, mrefu, Tyson akiwa katika kushangaa jinsi Magreth anavyo zungusha zungusha myororo huo mkononi mwake, akastukia myororo huo ukizunguka shingoni mwake. Mgreth akamvuta Tyson kwa karibu na kumfanya ajitahidi kutoa myororo huo ila akajikuta akishindwa. Magreth akaivunja shingo ya Magreth kwa kutumia mnyororo huo Tyson taratibu akafariki. Magreth akautoa mnyororo huo huku akimtazama Tyson ambaye ame ingilia vita ambayo haimuhusu.
Magreth akapiga hatua mbili mbele kisha akasimama, akautazama mwili wa Tyson, akachomoa upanga wake ambao una kata pande zote mbili. Akakishika kichwa cha Tyson na kukikata na upanga huo, Levina na Josephine wakastuka sana hawakuamini kama Magreth ana roho ya kikatili namna hiyo. Magreth akatazama eneo la fukwe hiyo na akaona gari la nabii Sang na mke wake. Akaanza kukimbia kwa umakini huku mkono wake wa kushoto ukiwa ume bebe kichwa cha Tyson. Alipo fika eneo la karibu la gari hilo, akachomoa nyota nne na kuanza kuzirusha kwenye tairi la moja la mbele na tairi moja la nyuma na kusababisha gari hilo kuanza kupungua upepo hali iliyo wastua sana nabii Sanga na mke wake.
“Nini hicho mume wangu?”
Mrs Sanga aliuliza huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.
“Nahisi gari lime pata pancha.”
Nabii Sanga alizungumza huku akichomoa bastola yake kiunoni, akaifunga kiwambo cha kuzuia risasi. Gafla wakastukia kioo cha upande wa nabii Sanga kikigongwa kidogongwa, hali ya hofu ikawatawala nabii Sanga na mke wake. Gafla wakamuona mtu aliye valia mavazi meusi yaliyo mfunika hadi uso wake akiwa amesimama upande huo wa nabii Sanga. Magreth akagonga kioo tena, na kuwafanya nabii Sanga na mke wake kuchachawa.
“Mume wangu washa gari tuondoke”
Mrs Sanga alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Nabii Sanga akajaribu kupeleka mkono wake kwenye batani ya kuwashia gari lake, gafla kioo cha upande wa nabii Sanga kikavunjwa na kuwafanya wachanganyikiwe, nabii Sanga akajaribu kufyatua risasi, iliyo tua kifuani mwa Magreth, ila haikuweza kumdhuru Magreth kwani nguo alizo zivaa haziingizi risasi. Magreth kwa haraka akafungua mlango wa gari hilo na kuwafanya nabii Sanga na mke wake kupiga makelele ya woga.
“KIMYA”
Sauti nzito ya Magreth ikawafanya nabii Sanga na mke wake kuacha kupiga kelele na kukaa kimya huku haja ndogo ikaanza kumtoka.
“Muna hisi huyu mtu ana weza kupambana na mimi?”
Magrerth alizungumza huku akikirushia kichwa cha Tyson ndani ya gari na kikatua mapajani mwa mrs Sanga mstuko walio upata wa kukiona kichwa cha Tyson ndani ya gari lao kika mfanya mrs Sanga kuzimia kwani hawakutarajia kama Tyson ambaye walikuwa wame mpa kazi hiyo ame uwawa kikatili namna hiyo.
Nabii Sanga mwili mzima ukazidi kumtetemeka kwa woga. Swali alilio ulizwa hakuweza hata kulijibu, ujanja wote ukamuisha.
“Nimekuuliza una hisi ana weza kuni ua?”
“Ha..h…a…p….ana”
“Nahitaji pesa”
Magreth alizungumza kwa ukali sana na kumfanya nabii Sanga kujibu kwa kutingisha kichwa kwamba ana ingiza kiasi hicho. Nabii Sanga akachukua laptop yake iliyopo siti ya nyuma, akaiwasha na kuingia kwenye tovuti ya moja ya akauti ya benki iliyopo inchini Afrika kusini.
“Kwa kosa kama hili nahitaji dola milioni mia mbili hamsini”
Nabii Sanga macho yakamtoka, jasho la woga likazidi kulowanisha mwili wake. Hakika alihisi kwamba hili jambo ni la kawaida sana ila mambo yame kuwa tofauti saba, Nabii Sanga akaanza kujaza fomu ya uhamisho wa pesa kwa njia ya mtandoa. Alipo kamilisha fumo hiyo ambayo ameandika namba ya akaunti inayo onyesha jina la Tomas, akaminya neno lililo andikwa ‘SEND’
Nabii Sanga akaanza kushuhudia jinsi asilimia za uhamishaji wa pesa zinavyo kwenda taratibu taratibu.
“Mage pesa ina aanza kuingia”
Levina alizungumza na kumfanya Magreth kujawa na tabasamu pana usoni mwake, japo nabii Sanga haioni sura yake halisi. Gari moja aina ya defender ililiyo jaza askari kumi ikakatiza kwenye barabara iliyopo eneo hilo la Coco beach. Ila gafla gari hilo likasimama.
“Jamani mume ona lile gari pale?”
Mkuu wa kikosi hicho cha oparesheni alizungumza huku akimuuliza dereva wake.
“Ndio mkuu”
“Usiku huu ina fanya nini?”
“Sijafahamu”
“Heii tuichekini gari hiyo”
Mkuu huyo alizungumza na kumfanya dereva wa gari hiyo kuirudisha nyuma gari hiyo kwa kasi. Kitendo cha gari hiyo kusimama, askari wote waka ruka huku wakiwa na bunduki zao. Magreth aliweza kushuhudia jinsi askari hao wanavyo kuja.
“Zimebaki asilimia ngapi ikamilike?”
Magreth alimuuliza nabii Sanga kwa ukali, nabii Sanga akamgeuzia Magreth laptop na akaona zime baki asilimia thelathini na tano kabla ya pesa hizo kuhama. Magreth taratibu akaanza kuukunjua mnyororo wake ambao kwa mbele una kisu kikali na kinacho kata pande zote mbele.
“Mage uta weza kupambana na hao askari!!?”
Levina aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana kwa maana askari hao wapo wengi.
“Wangapi wapo?”
“Kumi na wana smg mikononi mwao”
“Wana kufa”
“Eheee?”
Magreth akampiga nabii Sanga eneo la shingoni mwake na akazimia. Magreth akaichukua laptop hiyo na kuiweka siti ya nyuma ya gari hilo, ili kama ni zoezi hilo lisiweze kukatishwa na mtu yoyote. Magreth kwa haraka akapanda juu ya gari hilo huku akiwa ameshika mnyororo huo unayo ng’aa hata kama kuna giza. Askari wote wakashangaa kuona mtu wa aina hiyo.
“Ime fika asilimia ya ngapi?”
Magreth alizungumza kwa sauti ya chini.
“Asilimia sabini”
“Poa hakikisha isikatike”
Magreth akachuchumaa huku akiandaa nyota nne huku akiwatazama askari walio tangulia mbele.
“Muna nafasi ya kuondoka eneo hili kabla hamjapata madhara?”
Magreth alizungumza kwa sauti kubwa na kuwafanya askari wanne walio tangulia mbele kusimama kidogo huku wakijiuliza juu ya sauti mbaya na nzito ya mtu huyo.
“Mkuu ume sikia?”
“Ndio nime sikia, sijawahi kuona mtu wa aina hii”
“Moja…..Mbili….”
Magreth alizungumza ili kuwapa onyo askari hao.
“Mage usiue askari, una jua ukiiua askari wata kusaka dunia nzima”
Levina alisiitiza kwani hali ilipo fikia ni lazima askari wafanye mashambulizi kwa Magreth. Mkuu wa kikosi hicho kwa wenge akafyatua risasi moja, iliyo tua kifuani mwa Magreth. Risasi hiyo haikuweka kuingia mwilini mwa Magreth, kitendo hicho kikazidi kuwachanganya na kuwashangaza askari hao.
“Shambulia”
Mkuu wao alizungumza na kuwafanya askari wake kuanza kufyatua risasi kuelekea eneo alipo Magreth. Magreth kwa kasi ya ajabu akaruka sarakasi kadhaa huku akishuak kutoka juu ya gari hio. Magreth akaanza kurusha nyota hizo zilizo anaza kutua kwenye miili ya askari hao. Kila askari aliye kutana na silaha hiyo iliyo kaa kwenye umbo la nyota alianguka chini na mwili wake ukazizima na kushindwa kufanya chochote. Magreth kwa kutumia cheni hiyo akaanza kuwashambulia askari hao huku akiwajeruhu kwa kuwakata baadhi ya sehemu za miili yao kwa kisu hicho. Japo askari wana bunduki ila wakashindwa kabisa kumuhimili Magreth ambaye ana onekana kuwa ni mwiba kwao. Ndani ya dakika mona na sekunde hamsini, askari wote wapo chini wakiugulia maumivu makali sana. Magreth hakuhitaji kuwaua wala kuwapunguza viongo vyao kwani ana tambua jukumu la askari hao ni kulinda raisi. Magreth kwa haraka akarudi kwenye gari la nabii Sanga akaifungua laptop hiyo na kuona zikiwa zime baki asilimia mbili.
Akampapasa nabii Sanga mifukoni mwake na kuichukua simu yake. Akaivunja simu hiyo vipande vipande kisha akavitupia ndani ya gari lao. Ilipo fika asilimia mia mia moja, tiki la kijani lililo ambatana na neno complete, vikaonekana kwenye laptop hiyo. Magreth akaivunja laptop hiyo vipande vipande na kuirushia ndani ya gari la nabii Sanga.
“Waoo zime ingia”
Levina alizungumza kwa furaha sana.
“Salio lipo kweli?”
“Ndio”
“Poa”
Magreth akaanza kuondoka eneo hilo kwa kukimbia. Akafika sehemu alipo iacha pikipiki yake, akapanda na kuondoka eneo hilo.
“Ondokeni eneo hilo na tukutane Morogoro”
“Tuondoke na magari yote”
“Ndio”
“Poa”
Magreth hakuwa na mpango wa kurudi kwenye nyumba hiyo kwani kama ni kazi amesha ikamilisha na kilicho baki ni yeye kutoka nje ya mji huo.
***
“Beba kila kitu”
Levina alizungumza na wakaanza kukusanya kila kitu na Josephine na kuviingiza kwenye gari la Levina. Josephine akaingia kwenye gari la Magreth, akaliwasha na kulitoa ndani hapo. Levina naye akalitoa gari lake na wakazima taa za nyumba nzima, wakafunga geti na kuanza kuondoka kuelekea mkoani Morogoro.
“Mume fikia wapi?”
Magreth aliwauliza wezake.
“Sisi tuna itafuta kibaha”
“Mimi nimesha fika Moro”
“Ume fika?”
Josephine aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.
“Ndio nime fika”
“Acha utani bwana Mage”
“Haki ya Mungu, kwani Levina ukiniangalia location yangu una ona nipo wapi?”
Levina akafunua laptop yake na kweli eneo ambalo lina someka alipo Magreth ni Morogoro.
“Hiyo pikikipi ume iendeshaje jamani?”
“Nime izoea tayari ina spidi kubwa sana”
“Je kuna askari njiani?”
“Hapana, barabara ipo nyeupe”
“Poa sasa tuna fikizia wapi?”
“Hoteli ile ile, ila wahini kuna sehemu nina wasubiria nahitaji muni patie nguo”
“Sawa”
Levina na Magreth wakazidi kuongeza mwendo wa magari hayo. Wakafika kwenye msitu mmoja na kusimama, Magreth akatoka ndani ya msitu huo alipo jificha, wakampatia nguo za kwaida, akabadilisha haraka haraka, kisha Magreth akaongoza msafara wa wezake wakiwa na gari hizo. Majira ya saa kumi na moja alfajiri wakafika kwenye hoteli waliyo panga. Wakashuka na kuelekea kwenye chumba chao, hapakuwa na muhudumu aliye wahofia huku wahudumu hao wakiamini kwamba mabinti hao walikwenda disko kama wafanyavyo baadhi ya wateja wao pangisha ndani ya hoteli yao.
“Mage wewe ni mtu wa ajabu sana”
Levina alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Kwa nini?”
“Cheki hizi video jinsi ulivyo kuwa una pambana na huyu Tyson. Hembu angalia jinsi ulivyo kuwa una pambana na hawa askari. Yaani your so amaizing”
Levina alizungumza huku akimuonyesha Magreth video hizo. Magreth hata yeye mwenyewe akajishangaa kwani alikuwa ana jichukulia ni mtu wa kaiwada tu, ila kumbe ana uwezo mkubwa namna hiyo.
“Ila Mage wewe huja ogopa kumkata huyo jaa kichwa?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Niogope nini sasa. Endapo ninge muacha ange nidhuru mimi”
“Mmmm ila kwa kweli una ujasiri. Ehee ime kuwaje kwa nabii Sanga na mke wake kwa maana tulikuwa tuna sikia makelele tu”
“Ohoo mrs Sanga alikata moto mara baada ya kumrushia kichwa cha jamaa kwenye mapaja yake.”
Josephine na Levina wakajikuta wakicheka kana kwamba walicho kifanya ni kitu cha kawaida sana.
“Weee”
“Ohoo wee acha tu”
“Naona kuna gari za polisi zime fika Coco”
Levina alizungumza na wote wakaanza kutazama gari nne za polisi zikisimama eneo la Coco beach kwani ndege hiyo isiyo na rubani bado ipo eneo hilo.
***
Kila askari aliye waona wezake wakiwa wame lala chini huku wakiwa wame jeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao wakajawa na mshangao sana. Wakaanza kuwasaidia wezao na kuwapatia huduma ya kwanza.
“Mzee, mzeee”
Askari mmoja alimuamcha nabii Sanga ambaye yeye na mke wake wote wame zimia. Nabii Sanga aka kurupuka huku akipiga makelele.
“Tulia tulia mzee”
Askari huyo alizungumza huku akimshikilia nabii Sanga. Askari huyo akawaita wezake na wakashangaa kuona kichwa cha mtu kikiwa mapajani mwa mrs Sanga.
“Ime kuwaje mzee?”
“Mmmmm?”
“Ime kuwaje?”
Nabii Sanga akakosa hata cha kujibu.
“Kwa sasa hawezi kuelewa ime kuwaje ana wenge. Kitoeni hicho kichwa hapo”
Askari mmoja alizungumza, mmoja wao akavaa gloves na kukitoa kichwa hicho mapajani mwa mrs Sanga. Mrs Sanga akamtingisha mke wake naye akakurupuka huku akiwa na mawenge.
“Tuna kufa mume wangu tuna kufa.”
Mrs Sanga alizungumza huku akibabaika.
“Hayupo ame ondoka mke wangu”
Nabii Sanga alizungumza huku akimkumbatia mke wake. Mrs Sanga alilia kwa uchungu sana kwa maana hakuwahi kushuhudia tukio la kikatili kama hilo japo kuwa amefanya matukio mengi ya mauaji ila hakuwahi kumkata mtu yoyote kichwa chake. RPC na mlinzi wake wakafika eneo hilo.
“Mume jua ni kitu gani kilicho tokea?”
“Hapana muheshimiwa, ila tume mkuta nabii Sanga na mke wake wakiwa aneo hili”
RPC Karata akashtuka kidogo kwa maana watu hao walipaswa wae majumbani kwao kwa maana leo hii ndio siku ya harusi ya mtoto wao. RPC Karata akatembea hadi kwenye gari la nabii Sanga. Akatazama tairi ya nyuma jinsi ilivyo chomwa na silaha ambayo kwa Tanzania sio maarufu sana kutumiwa na wahalifu.
“Pigeni picha hapa ni ushahidi huu”
RPC Karata alizungumza huku akimuonyesha kijana wake mmoja. Akasimama kwenye mlango wa nabii Sanga. Akawatazama jinsi walivyo kumbatiana na mke wake huku mrs Sanga akilia kama mtoto mdogo.
“Nabii Sanga habari yako?”
RPC Karata alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama nabii Sanga. Taratibu nabii Sanga akamuachia mke wake na kumtazama RPC Karata ambaye kwa sasa hawapatani kabisa.
“Kime wakuta nini waheshimiwa?”
“Karata tusaidie tusaidie baba”
Mrs Sanga alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu na kumfanya RPC Karata kujawa na mshangao kwa maana watu mashuhuri na matajiri kama hao ambao hapo awali walikuwa wana mpa vitisho ime kuwaje leo hii wana muomba msaada tena kwa machozi mengi sana.
“Wazee wangu shukeni kwenye gari. Tuelekee kituoni”
Nabii Sanga na mke wake wakashuka kwenye gari huku wakitetemeka kwa woga. Wakatazama damu za askari walio jeruhiwa zikiwa zime tapakaa chini, huku askari hao wakiwa wame wahishwa hospitalini.
“Mkuu tume kuta mwili wa mtu kule juu ya jiwe, tuna imani kwamba mwili huo ndio wa kichwa kike”
Kijana huyo alizungumza na kumfanya nabii Sanga na mke wake kuzidi kuogopa.
“Uchukueni huo mwili na muupeleke hospitali kuu ya taifa”
“Sawa muheshimiwa, ila tume mkuta akiwa na bunduki mbili. Ina onekana ni mdunguaji”
“Sawa pigeni picha kisha muelekee naye mochwari. Hili eneo nahitaji lisafishwe, sinto hitaji wananchi wala waandishi wa bahari wafahamu ni kitu gani ambacho kime tokea.”
“Sawa mkuu”
RPC Karata akwafungulia mlango wa siti za nyuma nabii Sanga na mke wake. Wakaingia ndani ya gari hilo aina ya Toyota land cruiser V8. RPC Karata na dereva wake ambaye ndio mlinzi wake, wakaondoka eneo hilo.
“Tuelekee nyumbani kwa nabii Sanga”
“Sawa muheshimiwa”
RPC Karata akageuka nyuma na kumtazama nabii Sanga na mke wake ambao wame jawa na hofu kubwa sana. Simu ya mrs Sanga aikaanza kuita, akaitazama na kukuta ni Julieth ndio anaye mpigia.
“Pokea simu”
RPC Karata alizungumza huku akimtazama mrs Sanga usoni mwake. Taratibu mrs Sanga akapoke simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Haloo”
“Mama mupo wapi jamani. Tume jaribu kuwapigia toka jana mulipo ondoka hampokei simu zenu”
“Tuna kuja”
“Mbona simu ya baba haipatikani”
“Ime zima chaji”
Mrs Sanga aliongopea huku akizungumza kwa sauti ya upole sana.
“Sawa mama wahini si muna jua maandalizi ya harusi yana anza asubuhi hii”
“Ndio”
Mrs Sanga akakata simu. Akajitazama damu zilizo tapakaa kwenye suruali yake ya jinzi aliyo ivaa.
“Jamani naombeni nikatafute nguo nyingine”
Mrs Sanga alizungumza na RPC Karata akakubaliana na jambo hilo. Wakasimama kwenye moja ya dula la nguo.
“Una vaa size gani kiuno?”
RPC Karata alimuuliza mrs Sanga huku akimtazama.
“Kuino arobaini na mbili”
“Sawa”
RPC Karata akashuka kwenye gari lake na kuingia ndukani hapo. Akanunua suruali ya jinzi pamona na tisheti na kurudi navyo kwenye gari. Akamkabidhi mrs Sanga nguo hizo kisha dereva wake akashuka ili wabadilishe nguo.
“Mkuu hivi una hisi ni kitu gani kilicho wapata?”
“Yaani hata mimi sielewi, ilikuwaje na wala sijui kulikuwa na tukio gani pale.”
“Daa una jua ina ogopesha. Askari wote wale hakuna aliye pigwa risasi, ila wame katwa katwa kiasi kwamba sijui ili kuwaje waka shindwa kujitetea”
“Ndio hivyo upelelezi uta tusaidia katika kufahamu ni kitu gani kinacho endelea”
Nabii Sanga akashusha kioo kidogo.
“Tayari ame maliza”
Mara baada ya nabii Sanga kuzungumza hivyo. RPC Karata na kijana wake wakaingia ndani ya gari hilo na kuendelea na safari hiyo. Wakafika nyumbani kwa nabii Sanga na kukuta watu wakiwa katika heka heka za maandalizi ya harusi hiyo.
“Mzee tuna weza kuzungumza”
RPC Karaka alizungumza huku akimtazama nabii Sanga. Wakashuka kwenye gari na kukaa kwenye moja ya kibanda cha kupumzikia.
“Ehee mzee niambie ni kitu gani kimetokea?”
Nabii Sanga akashusha pumzi taratibu huku akimtazama RPC Karata.
“Akili yangu kwa sasa haipo sawa. Una weza kunipa muda na hayo maswali uka nihoji baadae”
“Ila mzee kumbuka wewe na mke wako mume kutwa eneo la tukio na mbaya zaidi mume kutwa na kichwa cha marehemu ndani ya gari lenu”
Julieth akafika eneo hilo, akamsalimia baba yake kisha akamsalimia RPC Karata.
“Baba raisi ana kupigia simu yako haipo hewani”
“Ime zima chaji”
“Ngoja nimpigie kwangu ana hitaji kuzungumza nawe.”
Julieth alizungumza na akampigia raisi Mtenzi. Simu ikapokelewa.
“Baba mkumkwe mzee huyu hapa”
Julieth alizungumza kisha akampatia baba yake simu.
“Ndio muheshimiwa”
“Habari za asubuhi ndugu yangu”
“Salama tu muheshimiwa”
“Ratiba ya kufungisha ndoa kanisani ime badilika. Nilizungumza na mchungaji na ame tuambia saa sita mchana ibada ifanyike, Hivyo nina omba muweze kujiandaa kwa hilo na muwapatie taarifa ndugu na jamaa mbao walijiandaa kwa ajili ya saa tisa alasifi”
“Sawa ndugu yangu nime kuelewa”
“Ila samahani bwana kwa kutengua ratiba”
“Hakuna tabu ndugu yangu kwa maana ripoti ime kuja asubuhi basi nina weza kuwasiliana na watu na wakafahamu hilo”
“Nashukuru sana kwa kunielewa ndugu yangu”
“Sawa sawa”
Nabii Sanga akakata simu na kumrudishia Julieth.
“Naamini ume ambiwa muda wa harusi ni saa ngapi?”
“Saa tisa au?”
“Ni saa sita. Waambie na watu wengine sawa”
“Sawa baba”
Julieth akaondoka eneo hilo huku akiwa na furaha sana moyoni mwake.
“Naamini kwamba ume ona ratiba ime badilika hivyo nakuomba niweze kujianda akwa ajli ya shuhuli ya mwangu”
“Sawa, je una weza kuniambia aliye sababisha mauaji yale na kuwajeruhia askari wangu yupo vipi?”
“Sio mtu wa kawaida. Mtu ambaye mwili wake haingizi risasi ana zungumza sauti mbaya. Basi sio mtu wa kaiwada. Nahisi mke wangu ata kuwa hayupo sawa, acha nika ungumze naye. Nitafute kesho akili yangu ikiwa ime tulia”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akimtazama RPC Karata usoni mwake. RPC Karata akamtazama nabii Sanga kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa kwamba ame mkubalia.
“Hakikisha una wasiliana na mimi pale utakapo ona jambo la tofauti”
“Sawa”
Nabii Sanga akanyanyuka kwenye kiti na kuelekea chumbani kwake. Akasikia maji yakiwa yana mwagika bafuni, akafungua mlango na kumkuta mke wake akiwa amekaa kwenye sakafu huku maji ya mbomba la mvua yakimwagikia mwilini mwake. Taratibu nabii Sanga na yeye akakaa pembeni ya mke wake na kumkumbatia.
“Sijawahi kukutana na tukio la ajabu maishani mwangu kama hili”
Mrs Sanga alizungumza kwa sauti ya upole sana.
“Hata mimi, nime shindwa kumfahamu mtu huyo ni wa aina gani”
“Ila niliona ukimpiga risasi, kwa nini hakufa?”
“Hilo ndio swali ninalo jiuliza na wanavyo dai ni kwamba hata askari wenyewe wame shambuliwa kiasi cha lile eneo kujaa damu”
“Mmmmm sasa ina kuwaje mume wangu kama akirudi tena?”
“Hilo ni jambo gumu. Ila ngoja tuangalie itatavyo kuwa, ila kwa sasa ina bidi tubadilishe namba zetu za simu. Sawa”
“Sawa mume wangu”
“Jiandae muda wa harusi ume badilika. Sio saa tisa tena ni saa sita”
“Kwa nini?”
“Sijamuuliza muheshimiwa, ila kutokana wao ndio wenye harusi wana mamlaka ya kuzungumza chochote wanacho jisikia. Sisi tuta fwata”
“Sawa yaani nikikumbua kile kichwa cha yule kijana. Yaani mwili wangu una ishiwa nguvu kabisa”
“Usiwe hivyo, jikaze mke wangu”
“Mmmmm”
“Ndio jikaze mke wangu. Polisi nina imani kwamba wata kuwa wana tufwatilia ila tuwe na kauli moja. Wakituhoji tuwaeleze kwamba tulipigiwa simu ya mtu asiye julikana. Alitupa vitisho vya kutuvamia kwenye harusi ya binti yetu na alihitaji kiasi cha pesa cha milioni hamsini za kitanzania. Hivyo muda huo tulikuwa tume kwenda kuonana naye. Sawa”
“Mmmm hilo mume wangu lita tupeleka mbali sana. Tuwaambie hivi polisi, tulikuwa tuna toka kwenye hoteli yetu. Njiani tuliweza kutekwa na watu wasio julikana, wakatupeleka pale Coco na wakataka kutua.”
“Hilo nalo halijaa vizuri. Jambo la msingi tusubirie akili zetu zikae sawa kisha tuta jua nini cha kufanya”
”Sawa”
Nabii Sanga akamvua mke wake nguo kisha na yeye akavua nguo zake na wakaanza kuoga kwa pamoja.
***
“Muheshimiwa raisi tukio hizi ndio picha za tukio lililo tokea Coco beach”
RPC Karata alizungumza huku akiweka picha hizo za askari wake kujeruhiwa na maiti ya mtu mmoja aliye katwa picha. Raisi Mtenzi akaanza kutazama picha moja baada ya nyingine.
“Hizi star si zina tumiwa na manija wa Kijapani?”
“Ndio muheshimiwa. Ndio muheshimiwa na tume jaribu kufanya mahojiano na askari wetu walio jeruhiwa na waka dai kwamba mtu aliye wavamia kwanza ana sauti mbaya nzito mithili ya radi na tatu mtu huyo haja mwili wake hauingii risasi”
“Mwili wake hauingii risasi?”
“Ndio, vijana wetu walimshambulia kwa risasi za kutosha, ila uwezi amini muheshimiwa kitu walicho kutana nacho ndio hichi”
“Mmmmm!!”
Raisi Mtenzi aliguna huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana usoni mwake.
“Je wame sema mtu hiyo ana tumia silaha gani tofauti na hizi nyota”
“Ana tumia mnyororo ambao kwa mbele una kisi kikali sana. Kiufupi huyu mtu ni muhalifu mpya Tanzania na ana uwezo mkubwa sana kwani kupambana na askari zaidi ya kumi tena wakiwa na silaha sio jambo rahisi muheshimi”
“Ni kweli. Je hii habari ime wafikiwa waandishi wa habari?”
“Hapana haija wafikia kwani niliwaeleza vijana waweze kufuta kila kitu kilicho tokea, ili waandishi wa habari wasije waka leta hofu kwa watu wa jiji letu”
“Ni kweli, hapo ume fanya jambo la maana. Sasa hakikisheni kwamba mtu huyu ana sakwa na akipatikana nahitaji nimshuhudie kwa macho yangu”
“Sawa muheshimiwa”
“Hili gari ni la nani?”
Raisi Mtenzi aliuliza huku akitazama picha ya gari la nabii Sanga.
“Hilo gari mkuu ni la wakwe wezako na wao tuliwakuta eneo la tukio wakiwa wame zimia”
Raisi Mtenzi alishangaa.
“Wamezimia?”
“Ndio tena na mbaya zaidi, maiti ya mtu huyu aliye katwa kichwa. Kichwa chake kilikuwa kimetupiwa mapajani mwa mrs Sanga.”
“Ohoo Mungu wangu. Una taka kuniambia mtu huyu aliwateka?”
“Kitu kama hicho, nime jaribu kuzungumza nao, kidogo wana onekana kwamba hawapo sawa hivyo nime waacha harusi hii ipite kisha tuta kaa nao chini na kuzungumza. Pia kwenye gari lao tume kuta laptop ikiwa ime funjwa, simu ya mzee ikiwa ime vunjwa na bastola ya mzee ikiwa ime tumika risasi moja. Tairi zikiwa zime chomwakwa hizi star”
“Ila wao ni wazima na hawajeruhiwa?”
“Yaa ni wazima hakuna mwenye jeraha mwilini mwake na hali tuliyo ikuta ni wao kuzimia”
“Mmmm kwa mtazomo wako wana weza kusherekea hii harusi kwa furaha?”
“Naamini wana weza”
“Sawa Karata, hakikisha kwamba ulinzi una kuwa ni imara, nikipata muda nita watembelea vijana wako walio jeruhiwa”
“Sawa muheshimiwa”
RPC Karata akatoka ofisini kwake. Akaingia kwenye gari lake huku akitafakari ni kitu mtu wa aina gani ambaye ana weza kufanya mashambulizi kama hayo. Akampigia simu Magreth na ikapokelewa.
“Mage habari yako”
“Salama muheshimiwa”
“Tuna weza kuonana?”
“Lini?”
“Muda huu?”
“Hapana muheshimiwa kwa maana nipo nje ya mkoa wa Dar es Salaam. Vipi kwema?”
“Sio kwema. Adui zako jana usiku walivamiwa na mtu wa ajabu aisee. Ila haya mazungumzo sio mazuri kuzungumzia kwenye simu. Ni heri tukutane na kuzungumza kwa kina”
“Usijali, ila nina jambo moja nahitaji kukueleza kabla ya kukutana”
“Jambo gani?”
“Kama mke wako na familia yako ipo bado jiji la Dar es Salaam nina kuomba uweze kuwahamisha na uwaondoke kabisa ndani ya jiji la Dar”
“Kwa nini?”
RPC Karata alizungumza kwa mshangao wa hali ya juu.
“Al-Shab wana vamia jiji la Dar saa tisa alasiri. Nime kuambia kama kaka yangu ambaye nina penda kukuona una ishi maisha marefu. Tafadhali nina kuomba unisikilize na kuniamini”
RPC Karata akaka kimya kwa muda kidogo huku akianza kujiuliza ni kwa nini muda wa harusi ya mtoto wa raisi Mtenzi ime badilishwa kutoka saa tisa alasiri na kuwa saa sita mchana.
‘Ina maana raisi ana jua hili ndio maana ame badilisha na haja nifahamisha’
RPC Karata alijiuliza kimoyo moyo huku akitazama jengo hilo la ikulu. Taswira ya mke wake ika mjia usoni mwake na kujikuta akimuamrisha mlinzi wake kuwasha gari na kuelekea nyumbani kwake kuhakikisha ana ondoka na familia yake, kama majanga yakitokea, basi asiwepo ndani ya jiji hilo la Dar es Salaam lililo pangwa kuvamiwa.
“Halooo”
Magreth alizugumza mara baada ya kusikia ukimya wa dakika moja.
“Ndio Mage”
“Ume nielewa?”
“Ndio nime kuelewa. Nashukuru kwa taarifa”
“Asante”
RPC Karata akakata simu na kumuhimiza dereva wake wawahi kuelekea nyumbani kwake. Ndani ya dakika arobaini na tano wakafika nyumbani kwa RPC Karata.
“Nisikilize Basesa kama una ndugu yako au rafiki yako na mademu zako. Waambie waondoke jiji la Dar es Salaam sasa hivi Umenielewa”
RPC Karata alizungumza huku akimtazama mlinzi wake huyo ambaye pia ni dereva wake.
“Kuna nini muheshimiwa?”
“Dar es Salaam ifikapo saa tisa ita shambuliwa na Al-Shabab hatujui wata shambulia kwa anga au kujitoa muhanga ila ni lazima wata shambulia. Ndio maana jana iliendeshwa oparesheni ya kusaka mabomu na maumbwa. Mbaya zaidi niliagizwa tu vijanawafanye kazi ila hatukuambiwa sababu ya kitu gani kinacho endelea. Ume nielewa?”
“Ndio mkuu”
“Chukua gari yangu ile nyeusi na ondoka nayo. Tukutane Morogoro”
“Sawa mkuu”
RPC Karata akaingia ndani na kumkuta mke wake akiwa jikoni akiandaa chakula cha mchana.
“Mke wangu acha kupika na ninahitaji ukusanye nguo, pesa na watoto wapo wapi? Tuna ondoka ndani ya jiji la Dar es Salaam”
“Kuna nini mume wangu?”
“Al-Shabab wana kwenda kushambulia jiji hili. Hivyo nahitaji wewe na wanangu muwe nje ya jiji hili. Umenielewa”
RPC Karata alizunguma kwa akimtazama mke wake usoni kwa msisitizo.
“Sawa, watoto wapo wana cheza huko uwani”
“Kawaite”
Mrs Karata akazima jiko hilo la gesi na kukimbilia eneo la nyumba hiyo ambapo kuna uwanja mdogo wa mpira. RPC Karata, akafungua shelf yake akatoa vibunda vya pesa kisha akatoa na bastola yake ambayo ina kaa nyumbani hapo. Mke wake akaingia ndani hapo akiwa na watoto wake wawili.
“Waandae haraka haraka”
Mrs Karata akaanza kuwaandaa waneye huku RPC Karata akihakikisha ana kusanya nguo zao watakazo zitumia wakiwa nje ya mkoa. Wakaingiza mizigo kwenye gari hilo la serikali na kuanza kuondoka Mkoa Dar Es Salaam na kuelekea mkoani Tanga.
***
“Jamani bado tu bibi harusi hajamaliziwa kupambwa?”
Nabii Sanga alizungumza huku akiwa amesimama mlangoni mwa chumba cha Julieth.
“Tuna mmalizia baba”
Mpambaji alizungumza, nabii Sanga akamtazama mwanaye jinsi alivyo mrembo na akajikuta akitabasamu. Maandalizi yote ya kumuandaa bi harusi yakakamiika. Bi harusi na wana familia wote wakaingia kwenye gari za kifahari zipatazo ishirini na kuondoka nyumbani hapo. Mrs Sanga akamshika mkono mume wake huku wakiwa wame kaa siti ya nyuma kwenye gari lao aina ya Range Rover Sport.
“Vipi mbona kama una wasiwasi?”
Nabii Sanga alimuuliza mke wake huku akimtazama usoni.
“Yaani nina kumbuka yale ya usiku, kila nikifumba macho nakiona kile kichwa”
“Usijali mke wangu, yata kishwa na hii harusi ikiisha nita hakikisha kwamba nina imarisha ulinzi kwa familia yangu na hapato kuwa na mtu ambaye ana weza kutu gusa”
“Sawa mume wangu”
Julieth akaifungua picha aliyo tumiwa na Jery. Akaanza kuitazama huku akiwa amejawa na furaha kwani ni picha inayo muonyesha akiwa ame valia suti yake.
‘Nitumie basi na wewe picha yako mke wangu’
Julieth aliisoma meseji hiyo huku akiwa amejawa na tabasamu.
‘Sikutumii uta niona kanisani’
‘Mmm acha hizo mke wangu, nitumie bwana’
‘Kweli vile sikutumia. Vipi mume sha toka ikulu?’
‘Ndio tuna jiandaa si una jua raisi kutoka kwake ni kwa maandalizi’
‘Ni kweli, sisi ndio tupo njiani kuelekea kanisani’
‘Sawa mke wangu nita kukuta huko. Natamani nikuone sema ndio hivyo ume nibania’
‘Usijali mume wangu uta niona tu na nitakuwa wako milele na milele’
Nafurahi kusikia hivyo, nina kupenda sane mke wangu’
Julieth akafurahi sana kuziona meseji hizo. Wakafika kanisani na bi harusi moja kwa moja akeleekea katika ofisi ya mchungaji akiwa na waziazi wake, kuwasubiria wakwe zao kufika..
***
Ulinzi wa barabarani ulipo kamilishwa. Raisi Mtenzi na wana familia yake wakaanza kuondoka ikulu. Waandishi wa habari nao hawakucheza mbali juu ya kurusha matangazo yao ya moyo kwa moja kwenye vituo vyao vya televishion. Wananchi wengi walishangazwa juu ya linado;ola lwa ratiba ya harusi hiyo.
“Jery mwanangu una kwenda kuoa. Jana sikupata muda wa kuzungumza na wewe”
Mrs Mtenzi alizungumza huku akiwa ana mtazama Jery usoni.
“Nina kuomba sana mwanangu ukawe ni kielelezo cha maisha ambayo tulikulea mimi na baba yako. Una muona baba yako, nilikuwa naye toka yupo askari wa kawaida. Ila leo hii ame kuwa ni raisi, kwenye ngazi zote za vyeo nilipanda naye. Una weza kugundua nguvu ya mwanamke kwa mwanaume. Laiti kama baba yako angekuwa ni mtu wa starehe kama wanaume wengine basi leo hii nina imani hata yale maombi yangu ya kufunga na kuomba kwa ajili yake yasinge fanya kazi”
Raisi Mtenzi akatabasamu tu huku wakiendelea kumsikiliza mke wake kwa umakini.
“Najua nyinyi nyote mume toka kwenye familia za kitajiri. Wotte muna ujua utajiri, isitokee mmoja wenu akajigamba kisa pesa za wazazi wake, hakuto kuwa na ndoa”
“Hili mama halito weza tokea”
“Nami nina ombea lisije likatoka. Pili hakikisha muwe muna chukuliana mapungufu. Ifikie hatua kila mmoja awe ana weza kujishusha kwa mwenzake. Wewe ukikosea, usisite kumuomba mke wako msamaha, hivyo hivyo na yeye akikosea asisite kukuomba msamaha. Mukiyamuda hayo, nina imani mwanangu uta fanikiwa zaidi ya haya mafanikio tulio kuwa nayo sisi wazazi wako”
“Nashukuru mama kwa nasaha zako nzuri”
“Jery sisi wawili tulisha malizana jana usiku”
“Ndio baba”
“Basi ukiyashika maneno yetu tuliyo kueleza basi nina kuhakikishia kwamba uta kuwa na ndoa yenye furaha na mfano kwa watu wengine”
“Asanteni sana wazazi wangu”
Wakafika kanisani, ulinzi ukaendelea kuimarishwa. Wakashuka kwenye gari hilo na moja kwa moja wakaelekea ofisini kwa mchungaji na kuwakuta wakwe wezao pamoja na mkwe woa. Wakasalimiana kwa furaha kisha wazazi waka omba kutoka nje ili kuwapisha wana ndoa wakiwa na mchungaji.
“Utaratibu wetu wa kanisa, huwa tuna wauliza wana ndoa kabla ya kufika pale madhabauni. Je kuna mtu yoyote kati yenu ambaye ame lazimishwa kuingia kwenye ndoa hii?”
“Hapana”
“Hapana”
“Je kuna mmoja kati yenu ambaye amewahi kuzini huku nyuma au muliwahi kuzini?”
“Hapana”
“Hapana mchungaji”
Julieth alijibu kwa kujikaza tu ila ukwelia na ufahamu kwani hata hiyo bikra aliyo kuwa nayo hivi sasa ni ya bandia.
“Sawa je muna penda na kweli au mume kuwa kwenye mahusiano kwa ajili ya matamanio ya kihisia?”
“Nina mpenda sana mume wangu”
“Bwana harusi”
“Hata mimi nina mpenda sana mke wangu kwani nilikuwa naye kwa kipindi cha mahusiano toka tulipo kuwa tuna soma na niliweza kumsubiria na kumvumilia hadi sasa tuna kwenda kufunga ndoa”
“Nafurahi kusikia hivyo na nina shukuru kwa wote kuwa wavumilivu. Leteni mikono yenu niwaombee”
Wakamkabidhi mchungaji mikono yao ya upande wa kulia na akaanza kuwaombe taratibu. Sala ilipo malizika akawaachia mikono.
“Sasa ni wakati wa kuelekea kwenye ibada”
Julieth na Jery wakanyanyuka. Jery akamtazama mke wake kuanzia chini hadi juu, uzuri wa Julieth ume zidi kuongezeka mara dufu. Mchungaji akatanguli mbele kutoka ofisini hapo na wao wakamfwata kwa nyuma huku wakijumuika na wasimmizi wao wa kike na wakiume.
***
“Shitii tume pigwa chenga ya mwili”
Omary alizungumza huku akiwasa tv iliyopo chumbani hapo. Vijana wote wa Al-Shabab wakashuhudia jinsi harusi ya mtoto wa raisi ikiendelea kanisani.
“Sasa tuna fanyaje mkuu ikiwa mabomu yote tuliyo yagega kwenye simu yana lipuka saa tisa kamili alasiri”
Omary akatazama saa yake ya mkononi na ina muonyesha ni saa saba na dakika moja.
“Yamebaki masaa mawili kabla ya kufika saa tisa, hatuwezi kuzikusanya simu zote na kufanya mashambulizi”
“Sasa ita kuwaje?”
“Saa tisa hiyo hiyo tuta fanya mashambulizi, haijalishi ni nani ata kufa ila ni lazima tufanye mashambulizi”
“Ni muda wa sisi kuondoka na kusambaa kila eneo la jiji la Dar es Salaam sawa”
“Sawa mkuu”
“Tuta toka moja mmoja”
Omary alizungumza kwa msisitizo na wakaanza kutoka kijana mmoja baada mwengime. Omary akawa wa mwisho kutoka eneo hilo. Akakodisha pikipiki na kuomba impelekea kwenye kanisa inapo fungishwa ndoa ya mmtoto wa raisi.
Muendesha pikipiki akmtazama Omary kwa sekunde kadhaa kisha akamruhusu apande. Wakaondoka na kufika karibu kabisa na kanisa hilo.
“Dogo ulinzi ume imarishwa hapo. Wewe shuka utembee kwa miguu”
“Sawa”
Omary akalipa kiasi alicho kubaliana naye, kisha dereva huyo akaondoka. Omary akaungana na wana nchi wengien kuingia kanisani hapo. Aka kaa kwenye benchi la mwisho huku akishuhudia ibada hiyo jinsi inavyo endelea.
Omary akaendelea kutazama jinsi ulinzi ulivyo imarishwa ndani ya kanisa hilo. Muda wa maharusi kula kiapo cha kuishi milele ikawadia. Akaanza Jery kiapo cha kumpokea Julieth kuwa mke wake hadi kifo kitakapo watengenisha kisha akamvisha pete. Julieth naya alaka kiapo hicho na akamvisha pete mume wake. Shangwe zikazidi kutawala ndani ya kanisa hilo huku wazazi na ndugu wa pande zote wakiwa wamejawa na furaha.
***
“Josephine hivi hao Al-Shabab watavamia au maono ni ya siku nyingine?”
Levina aliuliza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Kwani saa tisa imesha fika?”
“Bado”
“Subiri uone”
“Naona harusi ina kwenda kwisha na ndio tayari wamesha kuwa mume na mke”
“Jery kumuona Julieth hilo mimi sikuonyeshwa, nilicho onyeshwa ni Dar es Salaam kulipuka”
“Levima una onekana una hamu sana ya kushuhudia maono ya Josephine ehee?”
“Ndio nina hamu ya kuona kama alicho kizungumz ani kweli au laa”
“Usijali, uta ona”
Wakaendelea kutazama matangazo hayo ya kurushwa moja kwa moja kwenye tv. Maharusi wakaelekea kwenye hoteli moja ya hadthi tano kwa ajili ua mapumziko kabla ya kuelekea ukumbini. Josephine akatazaama saa yake ya mkononi na ina onyesha ni saa tisa kasoro ishirini.
“Ehee Mungu wangu!!!”
Josephine alihamaki.
“Kuna nini?”
“Zime baki dakika ishirini kabla ya kile jambo kukamilika”
“Acha likamilieke tu, sisi si tupo mbali”
Levina alizungumza kana kwamba kitu kinacho kwenda kutokea ni cha kawaida kabisa.
“Levina kumbuka kuna watoto na wana wake ambao wana kwenda kufa pasipo hatia ya aina yoyote”
Josephine alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakimlenge lenga usoni mwake. Magreth akashusha pumzi na kumuona jinsi rafiki yake anavyo pata maumivu ya moyo. Josephine akaanza kusali na kumuomba Mungu kama ikiwezekana basi kisasi hicho cha Al-Shabab aweze kukiepusha kwenye ardhi ya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
ITAENDELEA
Haya sasa, Josephine ana jitahidi kuomba je maombi yake yata fanikiwa kuepusha balaa lililopo mbele yao? Usikose sehemu ya 115.
SIN 115
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Website……………………………………………… www.storyzaeddytz.com
ILIPOISHIA
“Ehee Mungu wangu!!!”
Josephine alihamaki.
“Kuna nini?”
“Zime baki dakika ishirini kabla ya kile jambo kukamilika”
“Acha likamilieke tu, sisi si tupo mbali”
Levina alizungumza kana kwamba kitu kinacho kwenda kutokea ni cha kawaida kabisa.
“Levina kumbuka kuna watoto na wana wake ambao wana kwenda kufa pasipo hatia ya aina yoyote”
Josephine alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakimlenge lenga usoni mwake. Magreth akashusha pumzi na kumuona jinsi rafiki yake anavyo pata maumivu ya moyo. Josephine akaanza kusali na kumuomba Mungu kama ikiwezekana basi kisasi hicho cha Al-Shabab aweze kukiepusha kwenye ardhi ya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
ENDELEA
Gafla Josephine akaanza kuhisi kizungu zungu, akajaribu kusimama ila akastukia akiaanguka chini na akazimia. Magreth na Levina wakajikuta wakishangaa sana kwani hali kama hiyo hawajawahi kumuona nayo Josephine. Wakamnnyanyua kwa haraka na kumlaza kitandani, wakafungua vifungo vya shati lake pamoja na suruali ailiyo ivaa.
“Amezimia hiyu”
Levina alizungumza huku akiwa ana mpima Josephine mapigo yake ya moyo.
“Vipi tumpelekea hospitali?”
“Hapana ata kaa sawa tu”
Levina alizungumza kwa kujiamini kwa maana ana ujuzi kidogo kwenye maswala ya udaktari kwani marehemu mama yeke elikuwa ni dokta.
***
Omary hakucheza mbali sana na hoteli ambayo maharusi na familia zao wamekusanyika eneo hilo. Wapambe pamoja na waandishi wa habari nao pia wapo hotelini hapo kuhakikisha wana shuhudia kila kinacho endelea katika sherehe hiyo. Omary akaitazama saa yake ya mkononi na ima bakisha dakika tano kabla ya mambo waliyo tatege kwenye simu zaina za Nokia, kulipuka.
“Hii hoteli ni nzuri sana”
Julieth alizungumza huku akitazama tazama eneo la hoteli hiyo.
“Baba aliichagua hoteli hii kw amaana ni mpya na pia upo pazuri sana”
“Hei baby una jua ni watu wengi wapo nje wana tusubiria. Njoo uone”
Jery akasogea dirishani hapo na kutazama nje, akaona jinsi watu walivyo kusanyika wakiwa wana wasubiria japo wawaone tu kwa macho.
“Harusi yetu ime weka historia Tanzania”
“Ni kweli ime weka historia.”
“Mke wangu una weza kunipa kidogo?”
“No baby acha totoke ukumbini, nitakupa hadi uchoke mwenyewe. Tambua zime baki dakika mbili tu tuelekee eneo la kupiga picha”
Mlango wa chumba chao uka gongwa. Jery akatembea hadi mlangoni na kuufungua.
“Baba”
“Ahaa nina weza kuingia?”
“Ndio”
Raisi Mtenzi akaingia ndani hapo.
“Nina imani mume pumzika vya kutosha?”
“Ndio baba”
“Basi twendeni kuna viongozi nina hitaji kuwatambulisha kwao”
Jery akamshika mkono Julieth kisha wakatoka chumbani hapo. Wakaingia ndani ya lifti wakiwa na walinzi wao wawili. Galfa mtikisiko mkubwa ukatokea katika jengo hilo, umeme uka katika na kusababisha hofo kubwa kwa raisi Mtenzi pamoja watu wote.
Mlipuko mkubwa ulio tokea eneo alilo kuwa amesimama Omary na kumgawanyisha vipande vipande, ukawadhuru watu wote walipo eneo hilo. Magari na kila kitu kilichopo eneo hilo kiliweza kulipuka vibaya sana. Maeneo mbali mbali ndani ya jiji la Dar es Salaam ambapo zilitupwa simu na maeneo ambayo vijana hao wa Al-Shabab walisambaa maeneo yote yalilipuka kwa mabomu hayo ambayo ni makubwa sana. Vilio vilizidi kutanda na kutawala maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Majengo mengi yalivunjika mithili ya biskuti zinavyo vunjwa vunjwa. Hapakuwa na eneo la kukimbilia kwani milipuko hiyo ni mikubwa sana na ime dhuru eneo kubwa sana.
***
Mzee Mbogo na vijana wake wote macho yamewatoka. Kila mmoja alihisi kwamba habari za mashambulizo hizo ni propaganda tu katika mitandoa ya kijamii. Wengi wao machozi yalianza kuwamwagika, video inayo rekodiwa na satelati, ina onyesha milipuko mbalimbali jinsi inavyo tokea ndani ya jiji la Dar es Salaam.
“Mkuu”
John alimuuita Mzee Mbogo huku akimtazama usoni mwake.
“Mmmm”
“Hali ime tokea kama hivyo. Tuna fanyaje?”
“Hatuna la kufanya ila kusema katika hili”
Mzee Mbogo akaondoka ndani hapo na kuingia chumbani kwake. Kila akifumba macho ana ona jinsi milipuko hiyo ikiendelea kulipuka katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam. Mzee Mbogo akatoa simu yake, akaitafuta namba ya Evans, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akampigia. Simu ya Evans ikapokelewa.
“Kijana”
Mzee Mbogo alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyonge ndani yake.
“Ndio muheshimiwa”
“Wewe ni nani?”
“Kivipi mzee wangu mbona sija kuelewa?”
“Ulijuaje kama Al-Shabab wata shambulia leo?”
“Kama nilivyo kuambia nilipewa maono na Mungu ndio maana niliweza kukupa habari hiyo. Niliyo yazungumza yame timia”
“Malaki wa watu wame teketea na moto ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa nini hii habari hukuizungumza toka wiki iliyo pita ili hili janga lisiangamize watu wengi”
“Mzee wangu ilipaswa kutokaa hivi ili raisin aye aweze kujifunza. Kazi yangu mimi ni kutabiri tu na siwezi kuzia mambo kama hayo kutokea”
“Nahitaji kuonana na wewe. Niambie upo wapi?”
“Nita kufwata wewe ulipo ila usije nilipo.”
“Sawa nipo Morogoro”
“Natambua upo shambani kwako”
“Ume juaje?”
“Mungu akiwa na uwezo wa kumfunilia mtumishi wake basi ana uwezo wa kuona hata yaliyo jificha. Kama nina uwezo wa kuwaona mizimu, vibwengo ma majini basi nina weza kukuona hata wewe”
“Sawa nina kusubiria”
Mzee Mbogo akakata simu huku akiwa na huzuni kubwa sana. Kwenye maisha yake yote aliyo wahi kuishi duniani hajawahi kuona shambulizi kama hilo na baadhi ya mashambulizi ambayo kidogo yana endana na hilo, aliyashuhudia Iraq kipindi alipo kuwa chini ya jeshi la umoja wa mataifa, UN.
***
“Sasa ni wakati wa wewe jina lako kukua na huduma yako pia kukua”
Jini Maimuna alizungumza huku akimtazama Evans usoni mwake.
“Nini nina paswa kufanya?”
“Una paswa kupona wagonjwa, una paswa kutoa misaada kwa watu na una paswa kuanzisha taasisi yako ambayo ita tambulika kitafita na uta wajengea watu wote nyumba zao zilizo bomoka. Ukifanya hivyo uta pata wafuasi wengi na wata kusujudia na hato kuwa Evans huyu wa sasa, bali uta kuwa ni Evans mwenye nguvu na mamlaka hata ndani ya serikali”
Jini Maimuna alizungumza msisitizo.
“Nina imani uta kuwa nami kwenye kila hatua?”
“Ndio sinto weza kukuacha”
“Sawa ina bidi leo hii niondoke na nielekee Morogoro nikaonane na mzee Mbogo.”
“Hakuna shaka tuta ondoka wote”
Mlango wa chumba cha Evans uka fungulia na akaingia mdogo wake.
“Kaka una zungumza na nani?”
“Kuna rafiki yangu nilikuwa nina zungumza naye kwenye simu”
“Ahha…..ume ona kilicho tokea leo Dar es Salaam?”
“Rafiki yangu ndio alikuwa ana nina taarifa hiyo”
Evans alizungumza huku akimtazama jina Maimuna ambaye mdogo wake hawezi kuomuona zaidi yake yeye pake yake.
“Daa yaani kuna ogopesha. Watu wame kufa hao, mabomu yame lipuka”
“Ndio hivyo mdogo wangu nina shukuru Mungu nilisha ondoka”
“Ni kweli?”
“Mama yupo wapi?”
“Mama yupo sebleni ana tazama habari hiyo”
“Sawa mimi nina hitaji kuondoka leo na kuelekea Morogoro”
“Mmmm kaka Morogoro na Dar si karibu, usije uka lipuka na wewe?”
“Hakuna kitu kama hicho siwezi kulipuka”
“Mmm sijui kama mama ana weza kukubalia”
“Usijali nita zungumza naye. Hakikisha una simamia mafundi wana maliza kujenga hiyo gorofa ya mwisho pamona na ukuta uta jengwa vizuri”
“Sawa, je hakuna fundi ambaye ana tudai?”
“Mafundi wote nilisha walipa hakuna anaye dai”
“Sawa kaka”
Mdogo wa Evans akatoka ndani hapo.
“Jiandae sasa tuondoke”
Evans akaingiza nguo kadhaa kwenye kibegi chake kisha akatoka ndani hapo. Akamueleza mama yake juu ya safari hiyo na hakuweza kupinga kwa lolote. Evans na jini Maimuna wakaingia kwenye gari jipya la Evans aina ya Toyoter Harrier new model na wakaianza safari ya kuelekea mkoani Morogoro
***
Magreth na Levina nao wakawa kama watu walio shikwa na bumbuwazi. Walihisi mlipuko una weza kuwa ni mmoja ila hawakuamini kuona jiji ambalo lilikuwa na magorofa makubwa na majumba ya kifahari kwa sasa lina teketea kwa moto huku magorofa hayo yakiwa yame katika katika. Levina akajaribu kuminya japo batani moja kwenye laptop yake hiyo ila akajikuta mikono yote ikimtetemeka kwa woga.
Hadi sasa rafiki yao Josephine bado jaja zinduka na wakaanza kuhisi kitu kilicho mfanya azimie ni hii hali wanayo iona hivi sasa.
“Levina”
“Mmmmm”
“Sa…sa…aa tuna fanya nini?”
“Sijui rafiki yangu. Nime amini Josephine ana tumiwa na Mungu. Piga picha na sisi tunge kuwepo eneo hilo”
“Ila hawa Al-Shabab wame wau watu wasio na hatia kwa nini wame fanya hivi?”
“Sijui”
“Nahitaji kukiteketeza kikosi chote cha Al-Shabab”
Magreth alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Una hisi ni jambo rahisi kama hivyo”
“Ita wezekana tu nilazima niwewe kufanya jambo”
“Mage usije uka sababishia watu balaa jengine.”
“Haijalishi ila nikiwa kama mtanzani ni lazima niwe na uchungu. Wale walio kufa pale sio panya au kuku, ni watu wale Levina. Kuna ndugu zetu pale, kuna rafiki zetu pale na pia kuna watoto na vichanga ambavyo havina hatia yoyote. Kwa nini wawaue, kwa nini wasinge lipiza kisasi kwa raisi Mtenzi mwenyewe na serikali yake”
Magreth alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Levina naye machozi yakaendelea kumwagi. Josephine akakurupuka na kuwakuta weake wakiwa katika haliya huzuni kubwa.
“Jose Jose ime tokea kweli”
Levina alizungumza huku naye akilia. Josephine kwa haraka akashuka kitandani na kusogea ilipo laptop ya Levina, akashika mdomo wake kwani dakika za mwisho hali hiyo ndio aliyo weza kuiona kwenye maombi yake na ilimstua sana hadi akazimia.
“Josephine muombe huyo Mungu wako na akuonyeshe ni wapi lilipo kundi la Al-Shabab nina taka kwenda kuwaua wote. Nina taka kwenda kuchinja kundi zima la Al-Shabab na kiongozi wao nina hitji kumleta hapa nchini Tanzania na kumkabidhisha kwa wananchi waweze kumtandika mawe hadi afe”
Magreth alizungumza huku akimshika Josephine mikono yake. Josephine hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kuendelea kuduwaa mithili ya mtu anaye anza kupandwa uwenda wazimu.
***
Gorofa ya hoteli waliyopo raisi Jery pamoja na familia yake, japo ime tengeneza kwa uimara wa hali ya juu, ila haikuweza kuhimili mlipuko huo wa bumo kubwa. Gorofa hilo likaanza kukatika vipande vipande huku nabii Sanga, Jery, Julieth na walinzi wawil wakipigizw a pigizwa ndani ya lifti hiyo na kila mtu aliweza kumuomba Mungu wake aweze kumsaidia.
“Mungu wangu ni nini kimetokea ume usikia huo mtikisiko?”
Mrs Sanga ali hamaki huku wakiwa wamo ndani ya boti ya kifahari ambayo walikuwa wana ifanyia majaribio kabla ya kuinunua.
“Ndio, sijui hembu turudi”
Nabii Sanga alimuambia nahodha wa boti hiyo, kugeuza kwani hapo walio ni mbali na fukwe ya hoteli hiyo. Nahonda wa boti hiyo taratibu akaigeuka na wakaanza kurudi eneo lilipo hoteli.
“Mapigo yangu ya moyo yana nienda kasi mume wangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana.
“Usijali labda ita kuwa ni tetemeko la ardhi”
“Baharini?”
“Ndio”
Nabii Sanga alimtia matumaini mke wake, ila na yeye ame tawaliwa na wasiwasi mkubwa sana. Kila jinsi walivyo karibia nchi kavu ndivyo jinsi walivyo weza kushuhudia moshi mwingi mweusi ukiwa ume tanda kwenye anga la hoteli hiyo.
“Ohoo Mungu wangu”
Nahonda wa boti hiyo ambayo nabii Sanga walipanga kuinunua na kumpatia mtoto wao zawadi katika sherehe ya usiku, alizungumza huku akiwa ana tazama eneo la fukweni kwa kutumia darubini yake. Nabii Sanga kwa haraka akampokonya darubini hiyo na kuiweka machoni mwake. Nabii Sanga akajawa na mstuko mkubwa sana kwani hoteli ya gorofa hamsini, ime katika na zime baki gorofa tatu tuu huku kipande chote cha juu kikiwa kimetapakaa chini.
Nabii Sanga hakurusubiria nahonda wa boti hiyo kutua nanga. Akajirusha ndani ya maji kwa haraka na kuanza kuogelea kuelekea nchi kavu. Akafanikiwa kutoka ndani ya maji na akaanza kukimbilia eneo la hoteli hiyo ambalo uzuri wake ume badilika na kuwa kama jehanamu ya moto.
”Oooohhh Mungu wangu”
Nabii Sanga alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Hakuelewa ni kitu gani kilicho tokea kwani miili ya watu iliyo katika katika viungo ime tapakaa kila mahali. Nahodha wa boti hiyo akamsaidia mrs Sanga kushuka kwenye boti hiyo na wakakimbilia alipo nabii Sanga. Kila mmoja alihisi kama ana ota ndoto isiyo isha kwenye upeo wa macho yao.
Mrs Sanga akajikuta akikaa chini huku akiendelea kulia kwa uchungu sana kwani hatambui wana familia wake wata kuwa wapi kwani eneo hilo lina onyesha hakuna mtu aliye weza kusalia.
***
“Ohoo Mungu wangu”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr alijikuta akitahamaki huku akitazama tv iliyopo chumbani kwake akiwa katika ziara ya kikazi nchini China. Msaidizi wake naye macho yame mtoka kwani shambulizi linazo lililo tokea jijini Dar es Salaam lime washangaza wote.
“Muheshimiwa raisi kwa sasa si yupo kwenye hiyo hoteli?”
“Ndio muheshimiwa”
“Ohoo Mungu wangu kwa hiyo ata kuwa ame fariki dunia?”
“Hatuwezi kukadiria hilo muheshimiwa, ina bidi tuwasiliane na mkuu wa majeshi”
“Basi fanya hivyo”
Kijana huyo kwa haraka, akachukua simu yake na kumpigia mkuu wa majeshi. Simu ya mkuu wa majeshi nayo kwa bahati mbaya haipatikani.
“Hapatikani mkuu”
“Niandalie ndege yangu, nahitaji kurudi nchini Tanzania sasa hivi”
“Sawa muheshimiwa”
Kijana akawasiliana marubabi wa ndege ya makamu wa raisi, kisha akawasiliana na raisi wa nchi ya chini ambaye ndio mwenyeji wao.
“Raisi Jing Hoo ana hitaji kuzungumza nawe”
Bwana Madege Jr akaichukua simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Ndio muheshimiwa”
“Nimeona shambulizi la kigaidi lililo tokea hapo nchini kwako. Kwakeli nime fadhaika kuona maelfu ya watu wakiteketea. Hivyo mimi na serikali yangu tupo tayari kukupa full support utakayo hitaji, ikiwemo ujenzi mpya wa jiji la Dar es Salaam”
“Nina shukuru sana muheshimiwa. Nami nina omba niweze kuikatisha ziara yangu nirudi nchini kwa maana hadi sasa hivi hatutambu kama raisi yupo hai au laa”
“Sawa nafanya mawasiliano na uwaja wa ndege ili ndege yako ipewe kipambele katika kupaa”
“Nashukurus ana muheshimiwa”
“Pole sana rafiki yangu”
“Nina shukuru”
Bwana Madenge Jr akakata simu huku macho yote yakiwa mekundu. Wakatoka hotelini hapo na walinzi wake pamoja na walinzi wa kichina. Moja kwa moja wakaelekea uwanja wa ndege, raisi Madenge na wasidizi wake pamoja na walinzi wake wakangia kwenye ndege yake na wakaondoka nchini China huku kila mmoja akiwa amejawa na mawazo ya ni kitu gani ambacho kime zipata familia zao zinazo ishi jijini Dar es Salaam.
“Muheshimiwa, waziri mkuu yupo kwenye laini namba moja”
Bwana Madenge Jr akanyanyua mkonga wa simu ya mezani iliyopo pembeni yake.
“Ndio bwana Makongoro?”
“Muheshimiwa nime tuma vikosi vya jeshi na zima moto kwa njia ya anga kufika katika jiji la Dar es Salaam kwa maana miundo mbinu ime haribika vibaya sana na milipuko”
“Kabla hawajafanya jambo lolote hakikisheni kwamba wana fika katika kwenye hoteli aliyopo raisi na wana hakikisha wana mpata akiwa hai au ame kufa”
“Sawa muheshimiwa na ndio agizo ambali tume wapatia?”
“Je mume weza kufahamu ni kina nani ambao wame husika na shambulizi hilo?”
“Hadi sasa hivi muheshimiwa hatuja weza kufahamu ni kina nani na hakuna kikundi hata kimoja na kigaidi ambacho kime andika statmente yoyote ya shambulizi hilo”
“Sawa nipi njiani nina kuja Tanzania, nita tua kwneye uwanja wa KIA kisha nita elekea Dar es Salaam”
“Sawa mueshimiwa”
Bwana Madenge Jr akakata simu huku picha ya milipuko ya mabomu hayo ikiendelea kumtawala kichwnai mwake. Akawatazama wasaidizi wake alio kuwa nao ndani ya ndege hiyo na kila mmoja ana onekana kujawa na wasiwasi mwingi sana huku wengie wakishindwa kuzuia machozi yao.
***
Nabii Sanga, nahodha wa boti pamoja na mrs Sanga wakaanza kuona helicopter nyingi zikikatiza eneo hilo. Helicopter hizo zikaanza kumwaga maji mengi kwenye gorofa hillo linalo teketea kwa moto. Vikosi maalumu vya ukozi vya wanajeshi vikaanza kushuka kwenye helicopter hizo huku wakitumia kamba.
“Nabii Sanga, nina itwa captain Homba. Eneo hilo kwa sasa sio salama, ina bidi tuwaondoe”
Kaptain Homba alizungumza huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Siwezi kwenda popote kampteni, watoto wangu watatu wote wapo ndani ya hicho kifusi hapo. Siwezi kuwaacha na kuondoka. Nahitaji kusaidiana nayi”
Nabii Sanga alizungumza kwa msisitizo huku machozi yakiendelea kumwagika. Kapteni Homba akamtazama mrs Sanga aliye jichokea, na akawaagiza madaktari wa jeshi alio ambatana nao kumuondoa mrs Sanga aneo hilo kwani ana weza kufa kwa presha. Shuhuli ya kutoa vifusi vya jengo hilo ikaanza huku wanajeshi wangine wakijaribu kuondoa miili ya watu walio poteza katika eneo hilo. Waandishi wa bahari wa jeshi wakaanza kurusha matangazo ya kufukua kifusi hicho kwenye chaneli tofauti tofauti za nchi ya Tanzania. Zoezi hilo halikuwa jepesi kwani madhara yaliyo tokea ni makubwa sana.
Waziri mkuu naye na walinzi wake wakafika eneo hilo majria ya saa mbili usiku. Akakuta wana jeshi pamoja na polisi wakiendelea kujitahidi katika kutoa vifusi hivyo. Kapteni Homba akamfwata waziri mkuu, akampigia saluti kisha wakapeana mikono.
“Karibu muheshimiwa”
“Nashukuru je kuna mtu yoyote ambaye ame patikana?”
“Hapana muheshimiwa. Hatujafanikiwa kupata mtu aliye hai hivyo pia hatujui kama raisi na familia yake kama wapo hai”
Waziri mkuu akashusha pumzi huku akitazama vijana wanavyo jitahidi kufunua vifusi hivyo kwa kutumia vifaa visivyo na uwezo wa kuifanya hiyo kazi iende haraka haraka.
“Kapteni hakuna uwezekano wa kuleta Matinga tinga kuja kufukua hili eneo?”
“Hapana muheshimiwa. Barabara zime haribika hapa nime weza kuwasiliana na mkuu wa jeshi la majini. Nime muagiza kutumia boti zake kubwa kuleta japo vikoko viwili viweze kusaidia na kika hili swala”
“Sawa jambo zuri. Makamu wa raisi ata fika eneo hili muda si mrefu”
“Hakuna shaka muheshimiwa”
Wziri Mkuu akaanza kukatiza katiza eneo la hoteli hiyo na kuangalia uharibifu mkubwa ulio weza kutokea eneo hilo.
‘Nashukuru Mungu sikuwepo eneo hili’
Waziri mkuu alizungumza kimoyo moyo moyo kwani bomu hilo halijamucha mtu salama.
***
Evans akasimamisha gari lake aneo la kuingilia katika shamba kubwa la mzee Mbogo. Akatoa simu yake na kumpigia mzee huyo.
“Nime fika njia ya kuingilia shambani kwako”
“Ingia tu”
Evans akakata simu huku akimtazama jini Maimuna amabaye muda wote ame kuwa naye ndani ya gari hilo.
“Hawato kuona kweli?”
“Wewe pekee ndio mwenye uwezo wa kuniona mimi.”
Evans akaanza kuifwata barabara hiyo inayo ingia ndani ya shamba hilo na akafika katika nyumba ya mzee Mbogo na kukuta ulinzi ukiwa ume imarishwa. Evans akashuka kwenye gari, akakagulia na walinzi wa mzee Mboo kisha akasindikizwa ndani hadi sebleni alipo mzee huyo.
“Heshima yako mzee”
“Nashukuru. Una weza kukaa”
Evans akaka kwenye moja ya sofa linalo tazamana na mzee Mbogo.
“Ndio mzee nime kuja”
“Nime kuita hapa nahitaji kufahamu mambo mengi kutoka kwako. Ulicho kizungumza ndio kitu kilicho tokea”
“Ndio ni maono niliyo onyeshwa.”
“Je ni kitu gani kinacho kwenda kutokea sasa”
“Wapi?”
“Kwenye nchi”
“Kilichopo hivi sasa ni kuhakikisha una jengwa mji mpya wa Dar es Salaam”
“Vipi raisi na familia yake ipo salama”
Evans akamtazama jini Maimuna aliye simama pembeni yake, akatingisha kichwa.
“Swala hilo kwa siwezi kulijibu kabisa kwa maana ni jambo gumu kulitabiri”
“Nahitaji umuombe Mungu wako huyo na akuonyeshe”
“Siwezi kufanya hivyo kwa sasa”
“Nahitaji”
Mzee Mbogo alizungumza kwa kufoka na kuwafanya hadi wasaidizi wake kumshangaa.
“Kama hili ndio ulilo niitia nina ondoka”
“Huwezi kuondoka. Nahitaji uweze kunifahamisha kila kitu. Au wewe una shirikiana na hao Al-Shaba?”
“Ninge kuwa nina shirikiana nao basi nisinge kuambia jambo la iana yoyote kuhusiana na tukio ambalo lingetoka, pia kama ume kuja kunifokea, basi acha niondoke. Sina haja ya kuendelea kukaa hapa kwako”
Evans mara baada ya kuzungumza kanyanyuka na kuanza kueleeka mlangoni. Mzee Mbogo akamtazama Evans kwa macho makali sana yaliyo jaa hasira na uchungu.
“Hivi wewe ni mtanzania kweli?”
Swali la mzee Mbogo likamfanya Evans kusimama na kugeuka.
“Wewe una nionaje?”
“Uso wako una onysha dhahiri kwamba huna uchungu kwa yale yaliyo tokea”
“Una hisi kwamba sina uchungu. Wale walio kufa pale ni ndugu zangu na rafiki zangu na nilazima niwe na uchungu. Jambo jengine haya yote yaliyo tokea ni kwa ajili ya raisi wako na una jua kabisa kwamba ni raisi wako ndio alikuwa ana lipiziwa kisasi. Maamuzi yake ndio yame mponza, kwa heri”
Evans akatoka eneo hilo, akaingia kwenye gari lake na kuaianza safari ya kuelekea Morogoro mjini.
“Hivi raisi ni kweli yupo hai?”
Evans alimuuliza jini Maimuna.
“Sifahamu kwa kweli”
Evans akamtazama jini Maimuna kisha akaweka umakini wake barabani.
***
Josephien akaanza kushika kichwa chake huku huku akianza kuona giza lililo mfanya kutingisha kichwa chake na kuwafanya Magreth na Levina kumshangaa. Josephine akaanza kuona eneo ambalo raisi Mtenzi, Jery, Julieth na walinzi wawili walipo. Akayafumbua macho yake huku akihema sana, akatazama kwenye tv na kuona watu wakiendelea kufukua sehemu ambazo sio ambayo wana weza kumkuta raisi.
“Ina tubidi kwenda Dar sasa hivi?”
Josephine alizungumza kwa msisitizo.
“Kufanya nini?”
Levina aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Nime fahamu sehemu raisi alipo na yakipita masaa kumi yeye na watu wote waliomo ndani ya lifti hiyo wata kufa”
Magreth aliweza kumuelewa kwa uharaka Josephine anacho kizungumza.
“Ahaa kwa mabomu hayo mimi kwa kweli siwezi kurudi Dar”
Levina alizungumza huku akiwa amejawa na woga.
“Ina bidi kwenda kweli”
Magreth alitilia msisitizo.
“Tuna kwendaje, ikiwa barabara zitakuwa zime haribika, muna hisi mabomu hayo ni madogo kweli?”
“Levina kama huitaji kwenda, kaa hapa hatujakulazimisha”
Magreth alizungumza kwa kufoka na kumfanya Levina kushusha pumzi nyingi huku akijishauri juu ya kwenda au kuto kwenda.
“Tuta kwenda na pikipiki. Vaa nguo zako”
Magreth alizungumza huku akichukua fungua ya pikipiki hiyo.
“Msaada tunao omba kwako. Uweze kutuelekeza sehemu gani ya kupita, sawa”
Magreth alizungumza huku akimtazama Levina usoni mwake.
“Sawa hilo nita fanya kwa roho moja”
Magreth na Josephine wakajiandaa na kutoka nje ya hoteli hiyo. Wakapanda kwenye pikipi hiyo.
“Naomba unishikilie”
“Sawa”
Magreth akavaa kofia ngumu(helment) kisha wakaianza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam. Gafla Magreth akafunga breki za gafla mara baada ya gari ndogo kukatiza mbele yake. Gari hiyo ikasimama na kumfanya Magret kujawa na hasira kubwa sana kwani mwenye gari huyo ame mchomekea na asinge kuwa makini basi ange wasababishia ajali mbaya sana. Mageth akazima pilikipi yake na wakashuka na wakatembea hadi kwenye gari hiyo. Magreth akagonga kioo cha pembeni cha dereva huyo na kumfanya ashushe kioo cha gari hilo.
“Samahani sana dada yangu”
Magreth akastuka sana mara baada ya kumuona Evans ndio dereva wa gari hiyo. Hasira zote alizo kuwa nazo zikamshuka na kujikuta akivua helment hiyo na kumfanya Evans kujawa na mshangao mkubwa sana.
“Evans!!?”
Magreth aliita huku akiwa amejawa na mshangao. Evans akamtazama jini Maimuna aliye kaa pembeni yake, jini Maimuna muda wote macho yake yana tazamana na Josephine aliye simama upande wake. Josephine akazunguka na kumshika mkono Magreth.
“Waache waondoke”
“Jose una jua ni jinsi gani nilivyo kuwa nina mpatuta Evans”
“Hapana sio Evans yule ambaye una mjua”
Josephine alizungumza huku akimkazia macho jini Mariam ambaye hana uwezo wa kumdhuru Josephine kwa lolote kwani Josephine ana ulinzi wa Mungu.
“Kwa nini?”
“Nita kuambia sio leo”
Josephine akamshika mkono Magreth na wakarudi kwenye pikipiki yao. Taratibu Evans akafunga kioo cha gari lake na kuondoka eneo hilo huku akimtazama jini Mariam ambaye muda wote amekuwa kimya. Magreth akaikremisha namba ya gari la Evans kisha taratibu akapanda kwenye pikipiki hiyo.
“Jose niambie ni kwa nini ume nizuia kuzungumza na Evans ikiwa una jua nina mpenda?”
“Ana tumiwa na jini”
“Jini?”
“Ndio na pale alipo Evans hawezi kuwa na mahusiano na mwamke ambaye sio bikra”
“Ume juaje?”
“Ume sahau nina uwezo gani?”
Magreth hakutaka kubishana au kuuliza swali jengine, akavaa kofia ya pikipiki yake. Josephine akapanda na wakaendelea na safari yao. Wakafanikiwa kufika maeneo ya Kihaba, hakika ni sehemu kubwa ya jiji la Dar es Salaam lime weza kuathiri kwa asilimia kubwa sana.
“Tuna elekea wapi?”
“Kwenye hoteli ambayo alikuwepo raisi na familia yake”
Magreth akajitahidi kuendesha pikipi yake katika meneo yaliyo kungoroka hadi wakafanikiwa kufika tika hoteli hiyo.Wakakuta ulinzi mkubwa ukiwa ume imarishwa katika eneo hilo huku taa kuwa zikiwa zime fungwa eneo hilo ili kuhakikisha kazi ya kuokoa walio fukiwa na kifusi hicho ina endelea kama kawaida.
“Hamruhusiwi kuingia hili eneo?”
Mwanajeshi mmoja aliwazuia Magreth na Josephine kuingia eneo hilo.
“Nani ambaye ni kiongozi wenu”
Magreth alimuuliza mwana jeshi huyo.
“Una muhitaji wa nini?”
“Kuna jambo muhimu sana nina hitaji kumuambia”
“Dada kama una shindwa kuzungumza kilicho waleta basi ondokeni”
“Kaka nime kuja hapa nina tambua ni wapi raisi alipo. Tuonyeshe nani ni mkuu wako tuzungumze”
Josephine alizungumza kwa msisitizo na kumfanya mwanajeshi huyo kustuka kidogo. Akatwazama kwa sekunde kadhaa kisha akaanza kuongoza sehemu alipo kapteni wa kikosi chake hicho.
“Mkuu kuna hawa wasichana wana hitaji kuzungumz ana wewe”
“Ehee mabinti jitambulisheni”
“Mimi nina itwa Magreth”
“Mimi nina itwa Josephine nina fahamu sehemu raisi Mtenzi alipo”
Kauli ya Josephine kidogo ika mstua kapteni Homba. Akamtazama Josephine kwa umakini huku akimkazia macho.
“Ndio nina fahamu sehemu raisi Mtenzi alipo. Yame baki masaa matano tu, mukishindwa kumukoa basi ana weza kufa na watu wote walipo ndani ya lifti hiyo”
Kapteni Homba kabla hajafanya maamuzi yoyote akamuita kijana wake kumuita waziri mkuu. Waziri mkuu akafika eneo hilo.
“Muheshimiwa kuna hawa wasichana hapa, huyu ana itwa Josephine ana dai kwamba ana fahamu ni sehemu gani raisi Mtenzi yupo”
“Ume muona wapi raisi Mtenzi?”
Waziri mkuu aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Nifwateni”
Josephine akaanza kutembea na kuwafanya watu kumfwata kwa nyuma. Josephine akapanda kwenye moja ya kifusi na akasimama.
“Eneo hili kwa chini ndipo alipo raisi”
Watu wote wakashangaa kitu anacho kizungumza Josephine, wengi walihisi ata waonyesha eneo tofauti na gorofa hilo.
“Hapa ndipo alipo raisi?”
Waziri mkuu aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.
“Ndio, tena ina bidi mutoa kifusi hichi”
Kapteni Homba akamuamini Josephine kitu anacho kizungumza na shuhuli ya kuanza kupasua kifusi hicho ika anza.
“Wewe kenge upo hapa?”
Sauti ya nabii Sanga ika mstua sana Magreth, akageuka nyuma kwa haraka na kumkumta nabii Sanga akiwa amejawa na vumbi jingi usoni mwake.
“Mzee samahani ume changanyikiwa au?”
Magreth alizungumza kana kwamba hamfahamu nabii Sanga.
“Ume fwata nini hapa?”
“Samahani dada mzee kidogo hayupo sawa. Muheshimiwa tuna kuomba uka pumzike kule”
Mwanajeshi mmoja alizungumza huku akimtoa nabii Sanga kwenye eneo hilo. Nabii Sanga akamtazama Magreth huku akiwa na hasira kali sana.
“Ume muona nabii wako?”
Magreth alimuuliza Josephine.
“Yupo wapi?”
“Yule kule anaye pelekwa. Naona ame ponea chupu chupu”
“Masikini ana tia huruma”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama nabii Sanga. Mwanajeshi huyo akamkalisha nabii Sanga kwenye moja ya eneo lililo tulia. Nabii Sanga machozi yakaendelea kumwagika usoni mwake kwani hadi sasa hatambu ni wapi walipo. Simu yake ikaanza kuita, akaitoa mfukoni mwake na kukuta ni mke wake ndio anaye mpigia.
“Ndio”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti iliyo jaa huzuni kubwa.
“Vipi mume wangu kuna lolote?”
“Hakuna mke wangu”
“Ohoo Mungu wangu, tuna fanyaje?”
“Sijui nina endelea kusikilizia. Vipi nyumba yetu?”
“Ipo salama”
“Upo na nani?”
“Peke yangu”
Nabii Sanga akafumba macho kwani katika kundi kubwa la watu alio kuwa nao nyumbani kwake hapo lime teketezwa na mabomu hayo.
“Sawa usitoke pumzik”
“Uni fahamishe kile kinacho tokea mume wangu”
“Sawa”
Nabii Sanga akakata simu huku akimtazama Josephine aliye simama mbele yake.
“Mtumishi”
Josephine alizungumza huku akichuchumaa mbele ya nabii Sanga.
“Jose una fanya nini hapa?”
“Nime kuja kuwaonyesha eneo ambalo raisi yupo”
“Wa….w….a.aaa..nang…u je?”
“Sehemu atakayo patikana raisi ndipo alipo Julieth na mume wake”
“Je na wanangu wa kiume?”
Nabii Sanga alizungumza huku akimkodolea macho Josephine kwa maana ana utambua uwezo wake. Taratibu Josephine akafumba macho yake, Josephine akafumbua macho yake na kumtazama nabii Sanga huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana.
“Nini?”
“Samahani kwa kuzungumza haya”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole huku malengo yakimlenga lenga usoni mwake.
“Zungumza tu”
“Watoto wako wote wa kiume wame fariki dunia”
Nabii Sanga macho yakamtoka huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi sana kwani habari hiyo sio nzuri hata kidogo kwake.
***
Ndege ya makamu wa raisi bwana Madenge Jr, ikatua katika kiwanja cha kimataifa KIA. Akapanda kwenye helicopter na moja kwa moja safari ya kuelekea jiji la Dar es Salam ikaanza.
“Wama patikana watu wangapi hai hadi sasa?”
Bwana Madenge alimuuliza mkuu wa mkoa wa Moshi aliye mpokea katika kiwanja hicho.
“Bado hatuja pata taafira mkuu”
“Daa hawa washenzi ni lazima tushuhulike nao kisawa sawa”
“Ni kweli muheshimiwa, wame tuharibia sana sifa ya nchi yetu”
Helicopter hiyo ikatua katika eneo la hoteli hiyo na makamu wa raisi akapokelewa na waziri mkuu.
“Karibu sana muheshimiwa”
Waziri mkuu alizungumza huku wakipenda mkono na makamu wa raisi.
“Nashukuru, aisee hii gorofa ndio ime kuwa hivi?”
“Ndio muheshimiwa na lile eneo pale kuna bintu ametueleza kwamba ndipo alipo raisi Mtenzi”
“Binti!! Binti gani?”
“Yule msichana yupo wapi?”
Mwanajeshi mmoja akaenda eneo alipo Josephine.
“Sinte una hitajika”
Josephine akamtazama nabii Sanga anaye weweseka kwa uchungu wa kufiwa na watoto wake wa kiume. Akasimama na kuanza kumfwata mwanajeshi huyo huku Magreth naye akiambatana naye. Wakafika katika eneo walipo viongozi hao.
“Binti mwenyewe ndio huyo hapo”
Makamu wa raisi akamtazama Josephine kuanzia juu.
“Shikamoo”
Josephine alizungumza huku akimpa mkono makamu wa raisi”
“Marahaba ume tambuaje kwamba raisi yupo eneo hilo?”
“Ni maono yangu”
“Maono?”
“Ndio”
“Je uliweza kufahamu juu ya hili shambulizi?”
Josephine akamtazama Magreth ambaye alishindwa kumpa ishra yoyote kwa maana viongozi wote wana mtazama yeye.
“Ndio, nilionyeshwa juu ya shambulizi hilo na nilitambua muda na saa ambalo lita tokea”
Watu wote wakamshangaa Josephine.
“Kwa nini sasa usiwaambie watu au ulitoa ripoti kwenye chombo gani?”
“Hata ninge zungumza nisinge aminika. Hakuna mtu ambaye anaweza kuamini, yamebaki masaa manne endapo muta shindwa kumtoa raisi, mwanaye, mkwe wake pamoja na walinzi wake wawili waliomo ndani ya lifti basi wote wata kufa”
Kauli za Josephine zikazidi kuwashangaza watu wote hapo na hawakuna na namna ya kufanya zaidi ya kuendelea kuongeza juhudi za kuifukua sehemu hiyo walio onyeshwa na Josephine kwamba ndipo alipo raisi Mtenzi.
***
“Mbona una mawazo mengi”
Jini Maimuna alimuuliza Evans aliye jilaza kwenye sofa huku akimfikiria Magreth aliye kutana naye.
“Hei Evans”
“Mmmm”
“Nakuuliza mbona una mawazo mengi kiasi hicho, au una muwaza Mgareth?”
“Yaa nina muwaza yeye”
“Kumbuka kwa sasa wewe ni nani, hupaswi kumuwaza na wala hupaswi kumpenda kabisa”
“Maimuna tambua kwamba mimi ni binadamu. Endapo ninapo kutana na hali kama hizo basi nina kuwa katika hali kama hiyo”
Taratibu jini Maimuna akakaa pembeni ya Evans, akamtazama kwa sekunde kisha taratibu akamshika mashavu yake na kumnyonya lipsi zake na kumfanya Evans kushangaa sana.
“Sihitaji umfikirie tena Magreth”
Jinsi Maimuna mara baada ya kuzungumza hivyo, akampulizia Evans pumzi ailiyo ingia hadi ndani ya moyo wake na kusabaisha chuki kubwa sana juu ya Magreth na hata mawazo yake mazuri yakabadilika na kuwa mabaya.
“Magreth ni adui yako nauna paswa kumuua yeye na yule rafiki yake”
Jini Maimuna alizidi kumpandikiza Evans chuki hadi akatamani kumuua Magreth wakati huo huo.
“Nita muua Magreth na rafiki yake sehemu yoyote nitakayo muona”
Evans alizungumz akwa msisitizo huku akimtazama jini Maimuna usoni mwake na kumfanya atabasamu kwa maana uwezo alio kuwa nao rafiki wa Magreth ni mkubwa sana na una weza kumkwamisha kwenye mipango yake mingi.
“Bado wana jeshi wana endelea kufukua kisiki kwani hii ndio sehemu ya mwisho ambayo raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania bwana Chinas Mtenzi alikuwepo na familia yake katika harusi ya kijana wake.”
Evans na jini Maimuna wote walimsikiliza muandishi huyo wa habari anaye onekena kwenye luninga huku akionyesha jinsi wanajeshi wakeindelea kufanya jitihada katika kuhakikisha wana upate mwiliwa raisi Mtenzi.
“Yule si Mage na rafiki yake?”
Evans alizungumza huku macho yakiwa yame mtoka.
“Ndio, sija jua wana fanya nini pale”
“Twende basi”
“Ngoja kwanza hatuwezi kwenda Dar es Salaam usiku huu acha kupambazuke”
Jini Maimuna alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Evans kukubaliana na kila jambo.
***
Jitihada zikazidi kuongezeka na wakafanikiwa kuikuta lifti lilyo fukikwa na kifusi hicho. Wakaanza wakaanza kumtoa raisi Mtenzi ambaye yupo kwenye hali mbaya sana, wakamtoa Julieth pamoja na mume wake kisha wakawafwatia walinzi huko wote wakiwa wamezimia. Kila mmoja akajikuta akimuamini Josephine kwani ndio mtu wa pekee aliye walekeza kwamba raisi Mtenzi ata kuwepo eneo hilo.
“Binti je wana familia wengine wapo hai?”
Makamu wa raisi alimuuliza Josephine huku akimtazama usoni mwake. Josephine akafumba macho yake huku Nakijaribu kumuomba Mungu kumuonyesha ni nani ambaye ame salimika katika jengo hilo.
“Vipi?”
Makamu wa raisi aliluliza mara baada ya Josephine kufumbua macho.
“Hakuna wote walio baki ni marehemu”
Makamu wa raisi akashusha pumzi huku akitazama jengo hilo la gorofa lililo vunjika vibaya sana.
“Muheshimiwa ina bidi kwa sasa uelekee ikulu.”
Mlinzi wa makamu wa raisi alizungumza.
“Ikulu haijapata madhara?”
“Hapana”
“Nahitaji kuondoaka na huyu binti”
Makamu wa raisi alizungumza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Mimi nime ongozana ndugu yangu muheshimiwa hivyo kama ni kwenda nahitaji twende wote”
“Hakuna shaka”
“Sisi tuna usafiri wa pikipiki”
Magreth alizungumza na makamu wa raisi. Magreth na Josephine wakapanda pikipiki na kuanza kuelekea ikulu huku raisi na wapambe wake wakipanda helicopter na kuelekea ikulu. Magreth na Josephine wakafika ikulu na kupokelewa na makamu wa raisi.
“Ahaa samahani muheshimiwa ninge penda kufahamu lengo la wewe kutuita hapa”
Josephine alimuuliza makamu wa raisi huku wakiwa wamekaa kwenye ofisi ya raisi Mtenzi.
“Nahitaji kufahamu raisi ata pona?”
“Ndio hato kufa”
“Ata kaa kitandani kwa muda gani?”
“Muda mfupi hawajapata majeraha ya kuwafanya wakae kitandani kwa kipindi kirefu”
“Je mke wake na wana familai wake wengine ime kuwaje?”
“Wote wame kufa”
Josephine alizungumza kwa kukiamini na kumfaya makamu wa raisi kuzidi kumuamini kwa kila jambo.
“Una weza ni wapi tunapo weza kuwapata wahusika wa kundi hili la kigaidi”
“Hilo ina nibidi nimuombe Mungu ili aweze kunionyesha”
“Basi nina kuomba ufanye hivyo. Hii ni namba yangu ya mawasiliano, chochote utakacho onyeshwa basi hakikisha kwamba una wasiliana na mimi”
Josephine akaipokea bussines card hiyo.
“Sawa muheshimiwa”
“Kwa sasa muna jishuhulisha na nini?”
“Nina mgahawa”
Magreth aliwahi kulijibu swali hilo huku akimtazama makamu wa raisi usoni.
“Basi nina shukuru kwa muda wenu”
“Asante nawe muheshimiwa”
Magreth na Josephine wakaondoka ikulu majira ya saa kumi na moja alfajiri na moja kwa moja wakaelekea kwenye nyumba ya Magreth iliyopo Kigamboni na kwa bahati nzuri mtaa wao hakuweza kupata madhara ya aina yoyote.
“Hili jambo Josephine siwezi kuliacha kilapita hivi hivi. Ina tupasa kuisaidia nchi yetu kwa kila jambo”
“Ni kweli ila watu ambao wana shuhulika na hili jambo kwao hawaogopi kabisa kufa. Kufa ni dhawabu kwa mwenyezi Mungu”
“Potelea pote ila ni heri kuwaua kuliko hichi walicho kifanya hapa Dar. Wewe mwenyewe una ona ni jinsi gani raisi wasio na hatia walivyo fariki”
“Mmmmm acha tuone huko mbeleni mambo yatakuwa vipi”
Hapakuwa na hata mmoja wao aliye patwa na usingizi, kwani hali walio iona kwa kweli ina wanyima usingizi.
***
Huduma zikazidi kuendelea kwa raisi Mtenzi, Jery, Julieth na walinzi wake wawili. Madaktari wa hospitali ya taifa ya Muhimbili wakazidi kujitahidi wana hakikisha kwamba wana wanaokoa maisha yao pamoja na wananchi wanao letwa hapo wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Nabii Sanga muda wote hakuweza kukaa kabisa kwani ana tamani hata kusikia sauti ya mwanaye Julieth kwa mara nyingine.
Majira ya saa mbili asubuhi wakatolewa katika vyumba vya matibabu na kuingizwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.
“Mwanangu hali yake ipo vipi dokta?”
Nabii Sanga alimuuliza daktari huyo.
“Wana endelea salama, ni jambo la kumuomba Mungu hali zao ziweze kurudi na kuwa fiti”
“Nashukuru dokta”
Nabii Sanga alizungumza huku akichungulia kwenye kioo cha dirishani jinsi Julieth anavyo wekewa mashine za kumsaidia kuhema vizuri. Mrs Sanga akafika hospitalini hapo na wakakumbatiana na mume wake hukua kilia sana
“Vipi watoto wetu wengine hawajapatikana?”
“Ndio mke wangu”
Nabii Sanga alijibu kwa upole na hakuhiji kumueleza mke wake kwamba wame fariki kwani ana weza kumsababishia mke wake huyo matatizo ya presha.
“Wamesemaje juu ya Julieth?”
“Ana endelea vizuri hapa tumuembe Mungu”
Tv iliyopo kwenye kordo hiyo inayo rusha matangazo mabalimbali ikaanza kuwafanya watu kadhaa walipo hapo kutulia kutazama video hiyo.
‘TUME LIPIZA KISASI CHA KARNE. TANZANIA ILITUSHAMBULIA KATIKA BANDARI YETU SASA HICHO WALICHO KIPATA NI HAKI YAO INAYO WASTAHILI.”
Video hiyo fupi ya mkuu wa kikundi cha Al-Shabab ikaishia hapo na kumfanya kila mtu aliye iona video hiyo kukasirishwa.
“Ina maana Al-Shabab ndio walio tushambulua hivi?”
Mrs Sanga alimuuliza mume wake.
“Ndio”
Nabii Sanga alijibu kwa ufupi kisha akaanza kutembea akitoka hapo na kuelekea nje huku mke wake akimfwata kwa nyuma. Nabii Sanga akatafuta namba ya vijana wake wakazi ambao wana fanya kazi za kijasusi.
“Ohoo tuna shukuru Mungu muheshimiwa upo salama”
“Nina imani kwamba mume weza kuona hiyo video iliyo tangazwa kwenye tv?”
“Ndio muheshimiwa ndio tume iona”
“Wame haribu harusi ya binti yangu na wame sababisha maafa ya vifo vya ndugu zangu na wana familia yangu. Ninacho kihitaji musambaratishe kikundi hicho ila namuhitaji kiongozi wao akiwa hai. Mume nielewa”
“Ndio muheshimiwa”
Nabii Sanga akakata simu huku akiwa amejawa na hasira na uchugu mwingi sana.
“Mume wangu una hisi wana weza kuifanya hiyo kazi?”
“Ndio”
“Ila wale ni drugs dealers. Una wapa majukumu magumu sana mume wangu. Hembu jaribu kulifikiria hilo mara mbili mume wangu”
“Sasa una taka mimi nifanye nini ikiwa wewe mwenyewe ume ona hili jambo lilivyo tuharibia kila kitu tulicho kuwa tume panga”
“Ndio nime ona ila mume wangu hii vita sio ya sisi peke yetu. Vita hii ni ya nchi nzima na lazima serikali ita fanya jambo kwenye hili. Hembu jaribu kuwaza hili”
Mrs Sanga alizungumza kwa msisitizo, akachukua simu ya mume wake na kumpigia kijana wake.
“Bory”
“Ndio madam”
“Musifanye chochote hadi pale nitakapo waambia. Ume nielewa?”
“Ndio, ila kwa ni nini ikiwa muheshimiwa ame toa amri?”
“Ame itoa akiwa na hasira. Hatuhitaji kuwapoteza na nyinyi pia”
“Sawa madam”
Mrs Sanga akakata simu na kuanza kuelekea ndani na kumfanya mume wake kumtazama kwa macho makali laiti kama ange jua kwamba ange jua wanaye wa kiume wame fariki basi asinge wazuia vijana hao.
***
“Muheshimiwa una uha kika hiyo video haito tuletea shida?”
Msaidi za karibu wa kiongozi cha Al-Shabab alizungumza huku akimtazama bosi wake ambaye ameituma video hiyo kwenye mitandao ya kijamii dakika kadhaa zilizo pita.
“Najua wata tutafuta ila kwa sasa ina tubisi kubadilisha makazi yetu”
“Una hitaji twende wapi?”
“Leo tuna elekea nchini Nigeria na tuta ungana na kundi la Boko haramu”
“Mmmmm muheshimiwa, ume kubali tuwe chini yao?”
“Ni kwa muda, hili sekeseke likiisha basi tuta hakikisha kwamba tuna rudi kwenye mamlaka yetu”
“Ila muheshimiwa tume jipalia makaa ya moto. Kuna nchi kama Marekani ni mshirika mzuri sana wa Tanzania na raisi wa Marekani ni siku kadhaa alikuwa nchini Tanzania. Huoni wata tuwinda”
“Hatuwezi kukamatwa. Niamini mimi, vijana wame maliza kufunga kila kitu?”
“Ndio mkuu”
“Ni muda wa kuondoka sasa”
Mkuu huyo wa kundi la Al-Shabab aliwamba vijana wake na safari ya kueleke nchini Nigeria kwenye kundi la Boko Haramu ikaanza huku ikiwa hiyo ndio shabaha yao ya mwisho kabisa katika kujificha ili kukimbia hili mikono ya usalama.
***
“Hili swala la vikundi vya kigaidi vya bara la Afrika sasa lime fikia pabaya sana. Japo sisi tupo mbali sana ila ina tupasa kuhakikisha tuna saidiana na ndugu zetu katika kuteketeza na kuvifuta kabisa vikundi kama Al-Shabab , Boko haramu na vikundi vingene vinavyo fanania na hivyo”
Raisi wa Marekani alizungumza na washauri wake.
“Ndio muheshimiwa, hilo ni wazo zuri sana. Je tuna anzia wapi ikiwa hadi sasa hivi serikali ya Tanzania haijatoa statement ya aina yoyote?”
“Tuwape muda, kwani raisi pia alikumbwa na shambulizi hilo.”
“Muheshimiwa una weza kuwasha tv”
Sekretari wa raisi wa Marekeni alizungumza akiingia ofisini hapo. Raisi akawasha tv iliyopo ofisini kwake hapo. Wakatazama makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania akizungumza na waandishi wa habari.
“Ndugu zangu Watanzania. Ni majonzi makubwa sana ambayo kwa sasa tuna kabiliana nayo. Tume weza kufahamu adui yetu aliye sababisha, ndugu zetu, rafiki zetu, wazazi wetu na watoto wetu kufa vifo vya kinyama sana.”
“Ninacho kwenda kuwaahidi. Sisi kama serikali ya jamuhuri na Muungano wa Tanzania. Tuta kwenda kuhakikisha tuna lipa kwa haya yote yaliyo tokea. Tuta watafuta Al-Shabab iwe ni ardhini, majini, angani au nchi kavu nina wahakikishia kwamba tuta wapata. Tuta tumia nguvu na uwezo wote ambao tunao kuhakikisha tuna watawanyisha kundi lote la Al-Shabab.”
Makamu wa raisi alizungumza kwa msisitizo.
“Familia zote ambazo zime patwa na matatizo ya kufiwa na wapendwa wao au kuharibikiwa na rasilimali zao ikiwemo makazi yao ya kuishi. Serikali yangu ita hakikisha kwamba ina toa ushirikiano wa asilimia mia moja ili kuijenga Dar es Salaam mpya na Tanzania mpya. Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Afrika, asante kwa kunisikiliza”
Hotuba hiyo fupi ikaishia hapo.
“Mpigieni simu makamu wa raisi wa Tanzania nahitaji kufahamu hali ya rafiki yangu raisi Mtenzi”
“Sawa muheshimiwa”
Simu ikapigwa na sekretari. Ikapokelewa na sekretari wa Tanzania ambaye kwa haraka akaiunganisha simu hiyo na simu ya ofisi ya raisi ambayo kwa sasa makamu wa raisi ndio anaye iongoza.
“Muheshimiwa makamu wa raisi yupo hewani”
Raisi wa Marekani akachukua mkonga wa simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Habari yako makamu wa raisi?”
“Nina shukuru muheshimiwa”
“Nime toka kuona hotuba yako yako na waandishi wa habari sasa hivi. Mimi pamoja na wananchi wote wa Marekani tuna toa pole kwa nchi yako ya Tanzania”
“Nina shukuru sana muheshimiwa”
“Natambua kwa sasa ni kipindi kigumu ambacho muna pitia. Vipi hali ya rafiki yangu Mtenzi ina endeleaje?”
“Hali yake bado yupo ICU. Ila madaktari wame tuhakikishia kwamba ana weza kurusi kwenye hali yake hivi karibuni”
“Kama hali yake ipo mbaya sana nina kuomba aweze kuletwa nchini Marekani kwa matibabu zaidi. Tuta hakikisha kwamba tuna fanya kila liwezekanalo hali yake ina rudi na kuwa salama”
“Sawa muheshimiwa, nita kujulisha muda wowote kuanzia hivi sasa”
“Pia nahitaji kutoa msaada wa kijeshi. Nahitaji kutuma jeshi langu lije nchini kwako kuhakikisha wana toa msaada wa ujenzi wa majengo ya kisasa na afya kwa ujumla”
“Nina shukuru sana muheshimiwa na nina wakaribisha muda wowote ule”
“Sawa basi nita wasiliana nawe baada ya masaa mawili”
“Karibu sana muheshimiwa”
Raisi wa Marekeni akakata simu na kuwatazama washauri wake na akaachia tabasamu kwani kile alicho kuwa ana kihitaji kutoka Tanzania sasa kina kwenda kutimia.
“Nahitaji viongozi wote wa ngazi za juu wa muwaarifu juu ya kikao hichi cha dharura. Sawa”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Sekretari akatoka ndani hapo na kumuacha raisi na washauri wake.
“Tuna kwenda kujenga magorofa ya kisasa, ila kuna hadithina kubwa ipo chini ya ardhi ya Dar es Salaam. Hadhina hiyo ita tuongezea utajiri mara dufu na huu tulio nao kwa maana Watanzania wenyewe hawajui kama kuna mali nyingi sana zipo katika mji huo”
Raisi wa Marekani alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana, kwani ziara yake aliyo ifanya Tanzania miezi kadhaa ilikuwa ni kuchunguza juu ya hadhina hiyo na hakujua ni jinsi gani anaweza kumshawishi raisi Mtenzi katika kuitoa hiyo hadithina.
***
Kengele ya getini ikawafanya Magreth na Josephine kutazamana.
“Ni nani huyo?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth. Magreth akatoa simu yake mfukoni na kuangalia upande wa video za cctv kamera na akamuona Juma akiwa ame simama mlangoni hapo. Magreth kwa haraka akatoka nje na kufungua geti lake.
“Juma”
Magreth alizungumza kwa kuhamaki na akakumbatiana na Juma.
“Bosi upo salama?”
“Ndio, wewe je?”
“Nimepo salama, ila jengo la mgahawa wetu nalo lime angukaka”
Juma alitoa taarifa iliyo mstua kidogo Magreth.
“Ila kati ya wafanyakazi wetu hakua aliye poteza maisha?”
“Yaa wengi niliweza kuwadanganya na kwenda nao Bagamoyo hivyo tulikuwa salama japo wapo walio wapoteza ndugu zao”
“Ohoo Mungu wangu. Karibu ndani”
“Nashukuru”
Wakaingia hadi sebleni, Josephine akasalimiana na Juma huku wote wakiwa wamejawa na furaha kwa maana kila mmoja ana hisia za kimapenzi na mwenzake, ila wana ogopa kuambiana ukweli.
“Upo salama Juma”
“Ndio wewe je?”
“Mimi nipo salama kabisa. Ahaa jana niliwaona kwenye tv ndio nika hisi kwamba asubuhihi hii muna weza kuwa hapa”
“Ni kweli, tulikuwa katika hoteli ambayo raisi alifukiwa”
“Ahaaa sawa sawa”
“Juma uta kula nini?”
“Chochote tu bosi”
Magreth akanyanyuka na kuelekea jikoni na kuwaacha wawili hao ambao ana tambua kwamba wana penda. Ukimya ukatawala kati yao huku macho yao wote wakiwa wame yageuzia kwenye tv iliyopo sebleni hapo.
“Ahaa mgahawa wetu ume lipuliwa”
“Weee kweli?”
“Ndio”
“Poleni sana, ila si muliondoka kama tulivyo waambia?”
“Ndio”
“Duu maisha ni bora kuliko majengo”
“Ni kweli”
Magreth akarudi akiwa amebeba glasi tatu za juisi na kuziweka mezani.
“Japo ni asubuhi, ina bidi tupate juisi kidogo au kuna mtu ana hitaji chai hapa?”
“Hapana juisi ina tosha”
Juma alizungumza huku akipokea glasi hiyo ya juisi. Josephine akachukua glasi yake kitendo cha kuanza kuiepeleka glasi hiyo mdomoni mwake akajikuta mkono wake huo wa kulia ukitetemeka sana na glasi hiyo ikaponyoka na kuanguka chini na kuwashangaza Magreth na Juma.
“Vipi?”
Magreth alimuuliza Josephine. Magreth akafumba macho yake kwa haraka huku akiaanza kuonyeshwa kitu kingine ambacho kika mfanya astuke sana. Magreth akafumbua macho yake huku mapio yake ya moyo yakimuenda kasi sana hadi akajihisi maumivu.
“Kuna nini Josephine”
Juma aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Raisi”
Kauli hiyo ika mstua sana Magreth.
“Raisi ame fanyaje?”
“Ina bidi tumsaidie raisi sasa hivi”
“Kwa nini?”
“Kuna mtu ame pangwa kumuua raisi”
Josephine alizungumza huku jasho likimtiririka usoni mwake na kuwafanya Magreth na Juma wote wakajawa na mshangao.
***
“Natambua hii kazi ninayo kupatia ni ngumu ila nina hitaji uweze kuifanya kikamilifu”
Makamu wa raisi alizungumza huku akimtazama mmoja wa madaktari wana muhudumia raisi Mtenzi.
“Kazi gani muheshimiwa?”
“Nahitaji umchome sindano ya sumu raisi Mtenzi ambayo ita muua taratibu ndani ya msaa sita na isitokee mtu yoyote kuweza kufahamu kwamba ame kufa kwa sindano hiyo ya sumu”
Daktari huyo akastuka sana, hakuamini kama makamu wa raisi bwana Madenge Jr ana weza kumuambia maneno kama hayo.
“Usistuke hii pia ita kuwa nafasi kwako kupanda cheo na kuwa daktari mkuu wa hospitali au uihitaji hiyo nafasi?”
“Na…itaka”
“Basi kazi hiyo hakikisha una ifanya leo. Ila nahitaji iwe siri yako na mimi tu. Ume nielewa?”
“Ndio muheshimiwa”
“Nime kuandalia milioni mia moja pamoja na kazi kukupandisha cheo. Ukishindwa basi kila kitu kina yayuka”
Dokta Masawe, akatingisha kichwa huku akiwa amejawa na tamaa ya pesa hizo ambazo kwenye maisha yake ya utendaji wa kazi haja wahi kufanikiwa kushika kiwango kikubwa kama hicho cha pesa.
“Sawa muheshimiwa nita ifanya ila nina kuomba ahadi iwe ya kweli”
“Nina imani kwamba una nifahamu vizuri si ndio?”
“Ndio”
“Basi mimi ni mtu wa kutimiza ahadi zangu. Fanya hivyo”
“Sawa”
“Kazi njema na kazi itakapo malizika basi hakikisha kwamba tuna onana uso kwa uso na usinipigie simu na kunieleza habari kama hizo”
“Sawa muheshimiwa”
Dokta Masawe akapena mkono na makamu wa raisi Madenge kisha akatoka ofisini hapo. Taratibu makamu wa raisi akanyanyuka na kuitazama ofisi hiyo ilivyo nzuri.
‘Siku zote nilikuwa nina tamani sana kukalia hichi kiti. Sasa huu ni wakati wangu, Mtenzi hapo ulipo fikia sinto ruhusu urudi tena duniani’
Dokta Masawe akaingia kwenye gari lake na kuondoka ikulu hapo huku akilini mwake akifikiria ni jinsi gani anavyo weza kuitekeleza kazi hiyo kwa maana raisi Mtenzi yupo chini ya uangalizi mkali sana wa jopo kubwa la madaktari wezake na mara kwa mara huwa wana ifwatilia afya ya raisi.
‘Ila nilazima niondoke na hichi kitita cha pesa. Nime fanya kazi miaka yote ila sija wahi kushika kiasi hicho kwa kumkupuo ni lazima nizishike sasa’
Dokta Msangi aliendelea kujifariji huku akipita kwenye barabara ambayo haijaadhirika na mashambulizi hayo ya mabomu.
***
“Ni nani huyo ambaye ame panga kumuua raisi?”
Magreth alizungumza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Sijajua na sijaonyeshwa ni nani, ila kuna mtu ame kusudia kabisa kumuua raisi Mtenzi.”
“Ohoo Mungu wangu ni nini hichi tena”
“Samahani bosi na Josephine. Ume juaje kama raisi ana taka kuuwawa?”
Juma aliuliza kwa maana hatambui kabisa uwezo wa Josephine.
“Nina uwezo wa kuona maono ya mambo yanayo taka kutokea kabla hata hayajatokea”
“Mmmmm!!”
“Anacho kizungumza Jose ni kweli, ana uwezo huo”
“Mage hatuna muda wa kutosha ina tupasa kwenda Muhimbili kumsaidia raisi”
“Sawa, ila ni lazima tuwe na plan nina imani kwamba raisi ana lindwa sana”
“Ndio ana lindwa, ila hatuna jinsi na hatujui ni nani ambaye ata muua”
Magreth akajikuta akikaa kwenye sofa huku akijaribu kutafakari ni jambo gani ambalo ana weza kulifanya kama ni kazi basi hiyo ina kwenda kuwa kazi ngumu sana. Magreth akatoa simu yake mfukoni na kuitafuta namba ya Levina, akampigia, ila kwa bahati mbaya akakuta simu ya Levina ikiwa haipo hewani. Akajaribu kupiga tena ila simu yake bado haipatikani.
‘Huyu naye amepatwa na nini?’
Magreth alizugumza huku akijaribu kumpigia simu Levina kwa mara ya tatu na majibu yakawa ni yake yale.
“Nina wazo”
Juma alizungumza na kuwafanya Josephine na Magreth kumtazama.
“Kama ni kumuokoa raisi ina bidi tutafute mavazi ya madaktari wa hospitali ya Muhimbili na tuhakikishe kwamba tuna mtoa ndani ya hospitali pasipo mtu yoyote kuweza kuona”
“Ni wazo zuri, ila nina fikiria ni jinsi gani ambavyo tuna kwenda kumtoa ingali wewe mwenyewe una jua hali hakisi iliyopo hivi sasa?”
“Mage sisi twendeni tuta jua huko huko”
Josephine alisisitizia na Magreth hakuwa na kipingamizi. Wakatoka ndani hapo na kuingia kwenye gari ndogo ya Juma ambayo ameinunua siku za hivi karibuni na wakaianza safari ya kuelekea hospitali ya Muhimbili.
***
“Wakija wale wezangu wawili uta wakabidhi funguo. Muda wetu wa chumba si bado haujaisha?”
“Ndio bado hauja isha”
“Basi uta wakabidhi funguo”
“Sawa”
Levina alizungumza na muhudumu huyo kisha akaondoka eneo la mapokezi huku akiburuza begi lake la matairi lenye nguo zake pamoja na vifaa vyake muhimu. Akaingiza begi hilo ndani ya gari lake, akazunguka upande wa dereva, akafungua mlango na kuingia ndani. Akatoa hati zake tatu za kusafiria ndani ya pochi yake, akaanza kuzipitia moja baada ya nyingine.
‘China pata nifaa’
Levina alizungumza kimoyo moyo kisha akawasha gari na kuanza safari ya kueleke katika kiwanja cha ndege KIA, huku simu yake ya mkononi akiwa ameizima na kuicha ndani ya chumba hicho cha hoteli. Kiwango cha pesa ambacho walishirikiana na wezake kukipata, ana amini kita mfanya kuishi maisha ya starehe hadi kufa kwake katika nchi hiyo ya china.
“Siwezi kuwa na watu ambao akili zao haziwazi yale ninayo yawaza mimi”
Levina alizungumza huku akizidisha mwendo kasi wa gari lake ili kuwahi kufika Moshi kabla ya mambo haya rafiki zake hao hawaja stukia juu ya wizi huo ambao ana ufanya.
***
“Mzee”
Daktari mmoja alimuita nabii Sanga na wakasogea pembeni na kumuacha mke wake aliye kaa kwenye kiti akiendlea kusali ili mwanaye Julieth aweze kupata nafuu.
“Ndio”
“Nina kuomba tuongozane kama hotajali”
“Tuna kwenda wapi?”
“Nahitaji kukuonyesha baadhi ya maiti ili uweze kutambua wana ndugu wako”
Nabii Sanga akamtazama mke wake ambaye ana onekana kukosa raha, kisha msogele mke wake.
“Mke wangu nina kuja sasa hivi”
“Una kwenda wapi?”
“Nazungumza na daktari mara moja”
“Sawa”
Nabii Sanga na dokta huyo wakaondoka eneo hilo na wakaongozana hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Hakika ndani ya chumba hicho kume jaa maiti nyingi sana hadi baadhi zime lazwa sakafuni kwani watu walio fariki ni wengi na hadi sasa idadi yao haijaweza kufahamika.
“Kuna hizi maiti hapa zime letwa kutoka kwenye jengo la hoteli hivyo tuna kuomba uweze kuzitambua kama zina husia na wewe”
Daktari akafungua shuka la maita ya kwanza na kumfanya nabii Sanga kufumba macho yake kwani huyo aliye muona hapo ni mdogo wake wa tumbo moja ambaye ni wa kike.
“Nina mjua ni dada yangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujikaza ila machozi yana mlanga lenga usoni mwake.”
Daktari akamuagiza muhudumu wa chumba hicho kuapachika kibao cha namba maiti huyo. Akafunua shuka la pili nabii Sanga akahisi moyo wake ukiraruriwa na kitu chenye ncha kali sana. Hakuamini kumuona mwanaye wa kwanza akiwa amelala eneo hilo huku kifua chake kikiwa ime fumuka na mbavu zote zime chomoza nje.
“Ni…ni…first born wangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa uchungu sana na huku akishindwa kabisa kuyazuia machozi yake. Akafuniliwa maiti ya tatu na kumfanya nabii Sanga kushindwa kustahimiki kabisa na kuanza kuangua kilio kwa sauti kwani mwanaye wa pili wa kiume naye mwili wake ume pondeka pondeka vibaya na hapo alipo kiwili wili cha kuanzia kiunoni kuelekea miguuni hakipo kabisa.
Daktari akataka kufunua shuka lililo funikia maiti nyingine ila nabii Sanga hakuwa na uvumilivu wa kuendelea kutazama. Akatoka nje hakufika mbali katika jengo hili akajikuta akiinama na kuanza kutapika huku akilia kwa uchungu sana.
“Mzee upo sawa”
Daktari alimuuliza nabii Sanga, jicho alilo tazamwa na nabii Sanga likawa ni jibu tosha kwamba hayupo sawa. Nabii Sanga akajjifuta mdomo wake huku yaswira za maiti za watoto wake wa kiume pamoja na dada yake zina endelea kumrudia mara nyingi kichwani mwake hadi akatamani kupiga makelele ila ana shindwa.
“Ndani paking za magari zime jaa”
Juma alizungumz ahuku aki simisha gari lake nje ya geti la hospitali ya Muhimbili. Akaanza kushuka Josephine huku akiangaza angaza eneo hilo la hospitalini. Honi iliyo pigwa nyuma ya gari lao ika mfanya Juma kutazama nyuma. Dokta Masawe akashusha kioo cha gari lake na kuchungulia nje.
“Binti mwambie dereva aingize gari ndani”
Dokta Masawe alimuambia Josephine na kumfanya Josephine kumtolea macho daktari huyo. Mapigo yake yakaanza kumuenda kasi sana.
“Binti vipi mbona una nitumbulia macho?”
Dokta Masawe alizungumza kwa ukali sana. Juma akashuka kwenye gari huku akiongozana na Magreth.
“Mzee ndani paking zime jaa”
“Sasa ndio usimamishe gari getini. Litoea bwana”
Dokta Masawe aliendelea kufoka.
“Juma litoe tu gari”
Magreth alizungumza. Juma akaingia ndani ya gari na kulitoa gari hilo, mlinzi akafungua geti hilo na taratibu akaliingia gari hilo ndani ya eneo hilo la hospitali. Askari wa ulinzi akamuelekeza Juma ni eneo gani anapo weza kulisimamisha gari lake.
“Mage Mage”
Josepghine aliita huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana.
“Nini?”
“Nime Muangalia yule mzee mapigo yangu yana nienda kasi sana”
“Mzee gani?”
“Si yule aliye kuwa ana foka kwenye gari”
“Mmmm labda ni kutokana na kufoka kwake au kuna kitu umeweza kuona kwake?”
“Hapana, ila nime jikuta tu mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi”
“Tuachane naye. Magreth alizungumza huku akisimama na kumtazama Juma anaye shuka ndani ya gari lake.
“Raisi yupo wapi?”
Juma aliuliza, Josephine akatazama majengo hayo kisha akanyooshea mkono jengo moja la gorofa. Wakaanza kutembea kuelekea katuka jengo hilo.
“Ulinzi ni mkali sana”
Juma alizungumza huku akitazama wanajeshi wanao katiza katiza katika jengo hilo.
“Musiogope”
Magreth alizungumza huku wakiingia ndani ya jengo hilo, wakaanza kupandisha ngazi kuelekea juu gorofani. Wakafika katika kordoa mbayo moja ya chumba ndipo alipo lazwa raisi Mtenzi, Julieth na Jery.
“Duu wapo wanajeshi arobaini”
Juma alizungumza huku akiwa amesha hesabu idadi ya wanajeshi walipo eneo hilo.
“Jose tuna kutegemea wewe?”
“Ngojeni kwanza….Yule si mrs Sanga?”
“Ndio”
Magreth alijibu huku wakimtazama mrs Sanga aliye kaa kwenye moja ya kiti huku akiwa amejiinamia.
“Nisubirini hapa”
Josephine alizungumza huku akielekea katika eneo alilo kaa mrs Sanga. Baadhi ya wanajeshi wana mfahamu Josephine kwani yeye ndio mtu wa pekee aliye waonyesha ni wapi alipo kuwa raisi.
“Shikamoo mama”
Josephine alizungumza kwa heshima zote huku akikaa pembeni ya mrs Sanga.
“Marahaba Jose. Ume salimika?”
“Ndio mama nipo hai vipi baba yupo wapi?”
“Ame ondoka hapa na daktari. Nashukuru nasikia kwamba kwa kupitia maono yako uliweza kusaidia kupatikana kwa raisi mwanangu na mkwe wangu”
“Sifa ni kwa Mungua ambaye yeye ndio amenipatia kipawa hichi. Si kwa uwezo wangu wa kibinadamu”
“Ni kweli, je katika lile jengo ukiachilia na hao walipo patikana je kuna watu wengine ambao wame salimika?”
Josephine akashusha pumzi huku akimtazama mrs Sanga kwani anavyo onekana hafahamu kama watoto wake wa kiume pamoja na ndugu zake wengine wamefariki dunia.
***
“Hali inayo endelea nchini Tanzania hivi sasa nina imani kila mmoja wenu ameweza kuiona”
Raisi wa Marekani alizungumza na viongozi wa ngazi za juu ikiwemo viongozi wa kijeshi. Huku wengine waliopo mbali wakifwatilia kikao hicho nyeti kwa njia ya video call.
“Kama unavyo fahamu ziara yangu ya mwisho nilikwenda nchini Tanzania. Tuna hitaji sana kuhakikisha tunawasaidia ndugu zetu kwa hali na mali”
“Muheshimiwa raisi, tuna tambua ni nguvu gani ambayo nchi yetu inayo. Ila hatuta weza kupelekea majeshi yetu tukaingia vita na vikundi vya ajabu alafu tuka shindwa kunufaika na chochote. Ina tupasa tunufaike na misaada yetu”
Makamu wa raisi alizungumza pointi iliyo mfanya raisi kutabasamu.
“Ni kweli, katika jiji la Dar es Salaa kuna hadihina kubwa ambayo ipo chini ya ardhi. Hadihina hiyo ina weza ika tufanya tuzidi kuwa matajiri mara dufu. Ndio maana tume ridhia katika kutoa majeshi pamoja na pesa za kutosha kwa kwenda kujenga jiji jipya la Dar es Salaam”
“Je wanajeshi wetu wata pambana na hivyo vikundi vya kigaidi?”
“Ndio, mission yetu ni kuifanya dunia kuwa sehemu salam”
“Muheshimiwa raisi, mimi nina pinga hilo. Kumbuka ni juzi tu tume weza kuwarudisha wanajeshi wetu kutoka Iraq na Telebani. Wanajshi wetu wameweza kufariki, wengine kupoteza viongo vyao, muheshmiwa raisi ifikie hatua wanajeshi wetu waweze kupumzika na familia zao.”
Mkuu wa jeshi alizungumza na kuwafanya viongozi wengine kuungamkono jambo hilo.
“Kama lengo ni kwenda na kujenga mji wao na kupata hadhina hiyo basi hatuwezi kubisha. Hilo la kupambana na Al-Shabab tafadhali tuwa pumzishe wana jeshi wetu”
“Sawa nime waelewa na wanejeshi wetu wata fanya kama tulivyo zungumza”
“Sawa mkuu”
Kikao hicho kikashia hapo na raisi akarudi ofisini kwake pamoja na wasaidizi wake ambao ni washauri wake.
“Mpigieni makamu wa raisi wa Tanzania”
“Sawa muheshimiwa”
Sekretari akapiga simu kwa makamu wa raisi wa Tanzania na simu hiyo ikapokelea.
***
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Tume kaa na viongozi wezangu na tume fikia muafaka wa kutoa msaada wa wanajeshi wetu katika ujenzi wa Dar es Salaam na kuimarisha ulinzi wa jiji hilo hadi pale litakapo kamilika”
“Nashukuru sana muheshimiwa. Nimeitisha kikao na wakuu wa usalama kisha nita kufahamisha ni kiipi tulicho kubaliana na lini muweze kuja nchini kwentu”
“Sawa nina subiria makubaliano yako”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr akakta simu kisha akanyanyuka. Akaongozana na sekretari wake hadi kwenye ofisi ukumbi wa kikao. Akamkuta waziri mkuu pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu ambao siku ya jana ya shambulizi hawakuwepo jijini Dar es Salaam.
“Habari za muda huu”
“Salama muheshimiwa”
“Tume weza kupokea maombi mawili kwa marafiki zetu Marekeni. Ombi la kwaza kabisa ni kuleta vikosi vya vya jeshi katika kujenga mji wetu ambao ume haribika na kama munavyo fahamu, nchi yetu haina Malighafi za kutosha katika kulirudisha jiji letu liwe kama lilivyo kuwa awali. Pili wana hitaji raisi Mtenzi kupelekwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi. Je mume afikiana na hilo”
“Makamu wa raisi nina swali moja tu?”
“Uliza waziri mkuu”
“Ina kuwaje wana tuletea wana jeshi ikiwa nchi kama ya kwao ina makampuni mengi yenye ubunifu mkubwa wa ujengaji wa majengo”
“Wanajeshi wana jitolea, sidhani kama kuna kampuni ita kuwa tayari katuka kujenga bure ikiwa wata tumia vifaa vyao. Nina imani waziri mkuu nime kujibu vizuri”
“Ndio muheshimiwa”
“Jiji letu lina paswa kurudi katika ubora wake. Mukumbuke kwamba jiji hili ni jiji la kibiashara. Likiendelea kuwa kama magofu hakika uchumi wetu uta dhorota”
“Sawa muheshimiwa, je afya ya raisi ina endeleaje?”
“Bado yupo ICU hadi sasa hivi bado sijapata ripoti yoyote ya afya yake”
“Sawa muheshimiwa kwa upand wangu mimi sina pingamizi katika hilo”
“Hata mimi sina pingamizi”
Viongozi wote wakakubali kwamba wanajeshi wa Marekani waweza kufika nchini Tanzania kwa ajili ya kulijenga upya jiji la Dar es Salaam ambalo lime shambuliwa vibaya sana. Makamu wa raisi akajibu makubaliano hayo kwa barua pepe ili kutulia usisitizo katika makubaliano hayo ya kujengwa kwa jiji la Dar es Salaam.
***
“Niambie tu ukweli”
Mrs Sanga alizungumza kwa upole huku akimtazama Josephine usoni mwake. Kabla Josephine hajazungumza chochote nabii Sanga akafika eneo hilo huku macho yake yakiwa mekundu sana.
“Mume wangu vipi?”
Mrs Sanga alizungumza huku akisimama. Nabii Sanga akamkumbatia mke wake huku akimwagikwa na machozi hali iliyo mfanya mrs Sanga kujawa na wasiwasi mwingi sana.
“Mume wangu kuna nini?”
“Tumepoteza watoto wetu wa kiume”
Mrs Sanga taratibu akamuachia mume wake huku macho yakiwa yamemtoka. Mrs Sanga taratibu akakaa chini huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.
“Una…na….taka kuniambia wanangu wame kufa?”
Mrs Sanga alizungumza kwa wasiwasi.”
“Ndio mke wangu”
Mrs Sanga akashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio kwa sauti ya juu na kuwafanya wanajeshi wote kumtazama. Nabii Sanga hakuweza hata kumbembeleza mke wake kwani hilo walilo lipata ni pigo kubwa sana.
“Masikini wee”
Juma alizungumza huku wakimtazama mrs Sanga kwa mbali.
“Nahisi ata kuwa ame fiwa”
“Na nani?”
“Sija jua”
Josephine akarudi sehemu alipo simama Juma na Magreth.
“Vipi nani ame kufa?”
“Watoto wao wa kiume wame fariki”
“Duuu”
“Yaa sasa hapa ina bidi turudi kwenye plan yetu. Kumtoa raisi pale ni ngumu sana ila ina bidi mutafute makoti nyinyi wawili ili muweze kuingia katika chumba cha dokta”
Josephine alizungumza huku akiwatazama Juma na Magreth.
“Sawa”
“Mimi nita kuwepo pale kwa mrs Sanga na mume wake. Chumba kile ndipo eneo lilipo lazwa raisi Mtenzi, Jery na Julieth”
“Sawa”
Juma na Magreth wakaondoka eneo hilo na kuanza kutafuta chumba cha kuhifadhia makoti ya madaktari wote.
“Aisee mimi huwa siijui vizuri hii hospitali”
Magreth alizungumza huku wakiendelea kuangaza angaza kila eneo la gorofa hilo.
“Tuingie hapa”
Juma alizungumza huku akifungua mlango ulio andikwa dreasing room. Wakaingia ndani na kwa habahati nzuri wakakuta makoti ya madaktari ambayo yame fuliwa, yapo ndani ya chumba hicho.
“Ina bidi mimi nivalie kama nesi”
“Yaa ita pendeza”
Juma akachukua koti jeupe na kulivaa huku Magreth akivalia kiji gani ambacho ni kifupi ambacho kidogo kime acha maeneo ya mapaja yake kuwa wazi. Dokta Masawa akafungua droo ya ofisini kwake, akachukua chupa ndono ya sumu ambayo ina weza kumuua mtu ndani ya msaa matatu. Akakiingiza kichupa hicho katika mfuko wa koti lake, akatoka ofisini kwake na kuanza kuelekea katika chumba cha wagonjwa mahututi. Akafika nje ya chumba hicho na kumkuta mrs Sanga akiendelea kulia kwa uchungu sana.
“Ahh samahani sana, muna weza kumsogeza mama mbali na hapa kwa maaana hili eneo halitakiwi kuwa na kelele kabisa”
Dokta Masawe alizungumza, kitendo cha Josephine kumtazama mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda kasi, huku wasiwasi ume mjaa na kujikuta akimshangaa hadi dokta Msawe akahisi binti huyo ata kuwa ame hisi jambo ambalo wote wawili hawalifahamu.
“Samahani dokta”
Josephine alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama dokta Masawe usoni mwake. Gafla mrs Sanga akaangukana kuzimia. Kitendo hicho kikamfanya dokta Masawe kugairi kuingia ndani hapo, akamkimbilia mrs Sanga na kuanza kumpatia huduma ya kwanza.
“Mke wangu amepatwa na nini?”
“Nabii Sanga alizungumza huku macho yakiwamekundu sana usoni mwake kwani tukio hilo lina zidi kumkosesha amani.
“Tulia nina muhudumia”
Dokta Masawe alizungumza na akawaomba wanajeshi wamsaidia kumbebea mrs Sanga na kumuingiza kwenye moja ya chumba.
“Mbona wanajeshi wame pungua?”
Juma aliuliza huku wakiwa wana tambea kwenye kordo hiyo ya kuelekea kwenye chumba cha ICU alipo lazwa raisi Mtenzi huku nyoso zao wakiwa wamezifunika na vitambaa vyeupe ambavyo wana vitumia madaktari wengi katika kipindi hicho ambacho hali ya kuwapokea wagonjwa ni wengi sana.
“Sifahamu kume tokea jambo gani”
Magreth alizungumza huku wakizidi kuwapita baadhi ya wanajeshi wanao imarisha ulinzi eneo hilo. Magreth akamkonyeza Josephine kisha wakaingia katika chumba hicho chenye wagonjwa watano, mmoja wapo akiwa ni raisi Mtenzi. Magreth akatembea hadi dirishani na kuchungulia..
“Hapa hatuwezi kumshusha ni mbali sana”
Magreth alizungumza huku akitazama umbali ulipo dirishani hapo.
“Sasa tuna fanya nini?”
“Ngoja kwanza”
Magreth alizungumza hukua kiangaza angaza kila sehemu ya chumba hicho. Akamsogelea raisi Mtenzi na kumuangalia jinsi mashine za kupimulia zinavyo msaidia katika kuhema.
“Nahitaji kusafisha njia na wewe huku nyuma hakikisha kwamba una toka na kitanda cha raisi”
“Una maanisha nini?”
Magreth akamtazama Juma kwa sekunde kadhaa, kisha akajifunga kitambaa hicho cha usoni ambacho kimebakisha macho pamoja na paji lake la uso. Akatoka kwenye kordo hiyo, akampiga mwanajeshi mmoja ngumi nzito ya shingoni mwake na kumfanya mwanayeshi huyo kuweweseka na akaanguka chini huku akiwa ana shika koo lake. Kitendo hicho kikawashangaza wanajeshi wengine pamoja na Josephine, mshangao huo wa wanajeshi, ukazidi kumpa Magreth kasi ya kuwashambulia kwa kuwapiga sehemu muhimu ambazo hawatoweza kusimama katika muda huo.
Juma akachungulia nje ya chumba hicho na akaona shuhulia ya Magreth inavyo kwenda na akajikuta akimshangaa bosi wake jinsi anavyo piga wanajeshi hao wambao ni wauame walio shiba kisawa sawa. Juma kwa haraka akaikweka kitanda alicho lazwa raisi Mtenzi sawa akaitoa mashine hiyo inayo msaidia kupumua, puani mwake. Akategesha saa yake dakika kumi kuhakikisha kwamba ndani ya dakika kumi hizo ana pata kifaa cha hewa ya oksijeni kitakacho msaidi raisi Mtenzi kupumua.
Juma akakisukuma kitanda hicho hadi mlangoni, akachungulia nje na kuwakuta wanajeshi wote wakiwa chini. Juma akakisukuma kitanda hicho na kwa haraka akaanza kukisukuma kwenye kordo hiyo huku wakisaidiana na Magreth anaye mwagikwa na jasho jingi. Wakamuingia raisi Mtenzi kwenye moja ya chumba wakamkalisha kwenye kiti cha magurudumu na kutoka ndani hapo huku wakiwa wame mfunika na koti jeupe mwili mzima ili watu wasimtambue.
“Ina tubidi tumtafutie mashine yoyote ya oksijeni pasipo kufanya hivyo ana weza kufa”
Juma alizungumza huku wakiendelea kuelekea nje. Wakakuta gari moja ya wagonjwa ikiwa ime washwa, huku dereva akiwa hayupo. Magreth akafungua mlango wa nyuma na wakakuta kitanda na kwa bahati nzuri gari hiyo ya wagonjwa ina kitanda ndani na ina mashine ndogo inayo weza kumsaidia mtu kupumua. Juma akamuingiza raisi Mtenzi ndani ya gari hilo, akamuwekea mashine hiyo na upumuaji wake ukaendelea kama kawaida. Magreth akawasha gari hilo na wakaondoka eneo hilo.
“Kume tokea nini?”
Dokta Masawe alizungumza huku akimtazama Josephine ambaye muda wote wa matukio hayo yaliyo endelea alibaki kuwa kama mshangaaji na hakutaka kujihusisha hata kidogo kuhofia kuhisiwa kwamba yeye naye ana husika kwenye jambo hilo.
“Aisee kume tokea nini?”
Dokta Masawe alimuuliza mwana jeshi mmoja aliye kaa chini huku akisikilizia maumivu hayo ya kupigwa na mtu ambaye hawamfahamu. Mwajeshi huyo alinyoosha mkono kwenye chumba cha ICU. Dokta Masawe kwa haraka akasimama na kukimbilia chumbani hapo. Macho yakamtoka mara baada ya kukuta kitanda cha raisi Mtenzi akiwa hayupo ndani hapo.
“Mungu wangu raisi hayupo”
Dokta Masawe alizungumza huku akikimbilia kipaza sauti akaminya batani na kuanza kuzungumza.
“Kume tokea tatizo, raisi ame toweka chumba cha ICU narudi raisi ametoweka chumba cha ICU. Wana jeshi wote na wana usalama wote tusaidiane katika kumtafuta”
Dokta Masawe mara baada ya kutoa taarifa hiyo akatoka ndani hapo huku akiwa amechanganyikiwa. Wanajeshi, askari pamoja na madaktari wakaanza msako wa kimtafuta raisi Mtenzi kika kona ya hospitali hiyo pasipo kufahamu kwamba tayari alisha tolewa hospitali hapo.
Josephine akaondoka eneo hilo, akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Magreth.
“Ndio”
“Mupo wapi?”
“Tumesha toka siku nyingi hapo”
“Muna kwenda wapi?”
“Tuta kuambia. Wewe chukua pikipiki uelekee nyumbani”
“Sawa”
Josephine akakata simu, akamkodisha muendesha pikipiki mmoja na wakaondoka eneo hilo huku akiwaacha wanajeshi, madaktari wakiwa katika hali ya wasiwasi mkubwa sana.
“Nilikuambia usinipigie simu ukimaliza kazi”
“Nalitambua hilo muheshimiwa. Hadi ninavyo zungumza hivi sasa, raisi ametowesha hapo hospitalini na watu wasio julikana”
“Nini?”
“Ndio ame toweshwa na watu wasio julikana”
“Ila kazi ume ifanya?”
“Sija ifanya muheshimiwa”
“Shitii mtafuteni hadi muumpate mume nielewa?”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr alizungumza kwa ukali sana kwani mpango wake ume kwenda vibaya. Dokta Masawe akakata simu huku woga ukiwa ume mtalawa sana.
***
“Boss tuna kwenda wapi?”
Juma alizungumza huku akimtazama raisi Mtezi aliye lala kimya.
“Tuna elekea nyumbani kwangu, ndio eneo salama zaidi”
“Kwako, hawato tufwata?”
“Hakuna ambaye ana weza kutufwata huko”
“Sawa”
Magreth akasimamisha gari hilo nje ya geti lake wakamshusha raisi Mtenzi na kumuingiza ndani, wakamlaza katika chumba cha Josephine wakamuweka mashine hiyo ya kupumulia waliyo ikuta ndani ya gari kisha Magreth akaliondoa gari hilo na kwenda kulitelekeza kwenye moja ya eneo ambalo lime pata majanga ya kuharibiwa na milipuko. Akarudi nyumbani kwake na kumkuta Josephine akiwa amesha rudi.
“Vipi hospitalini?”
“Wee kume chachamaa. Wanajeshi wana katiza kila sehemu, yule daktari woga ume mjaa alafu nina hisi yule doktaa na jambo la kufanya katika hili”
“Dokta yupi?”
“Yule mzee aliye kuwa ana foka pale getini kumbe ni dokta. Ila nilipo muona moyo wangu ulinienda kasi kama mara ya kwanza.”
“Kwa nini?”
“Sijui ikiwa watu wa kawaida ukiwaangalia nina kuwa sawa tu”
“Ina bidi tumpate yule dokta”
Magreth alizungumza kwa msisitizo.
“Tumpate wa nini?”
“Mashaka ya Levin….nani Josephine ni lazima kuna jambo yule dokta atakuwa ana lifahamu juu ya mpango wa raisi Mtenzi kuuwawa”
“Hata mimi nina hisi hivyo”
Josephine alitilia mkazo.
“Alafu huyu mjinga hadi sasa hivi hajatutafuta”
“Nani?”
Juma aliuliza.
“Levina”
Josephine akafumba macho yake kidogo na akajikuta akistuka.
“Nini?”
“Nime ona Levina ana panda ndege inayo kwenda Kenya”
“Ina maana ana toroka au?”
“Ndio ana toroka”
“Huyu mtoto chok** kweli vipi pesa zetu”
Magreth alizungumza kwa ukali huku akionekana kuchanganyikiwa kwani usaliti alio ufanya Levina una yeyusha ndoto zao zote za kumiliki pesa nyingi zime toweka.
Levina akajawa na tabasamu pana mara baada ya ndege aliyo ipanda kuanza kuiacha ardhi ya Tanzania taratibu. Ndege hiyo ilipo kaa sawa, akafungua mkanda wa siti yake na kujikalisha vizuri kwenye siti hiyo huku akiaanza kuwaza ni jinsi gani anavyo weza kuanza kuzitumia pesa hizo alizo wadhulumu na wezake.
Akafungua laptop yake na kuanza kutafuta hoteli ambazo zina patikana nchini China. Akapata hoteli moja ambayo watalii wengi wana fikizia, akafanya malipo ya awali akiamini kwamba ndani hato kaa muda mrefu nchini Nairobi.
“Tuna fanyaje sasa ili tumpate Levina?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Josephine usonimwake.
“Hatuna namna na pesa yetu ndio imesha kwenda hivyo”
“Duuu huyu mjinga haki ya Mungu niki mshika nita muu. Una namba ya pale hotelini?”
“Ndio”
Magreth akainakili namba hiyo kwa haraka ndani yas imu yake kisha akaipiga. Simu ikapokelewa.
“Nina itwa Magreth nilipangisha chumba kwenye hoteli yenu hapo majuzi”
“Ndio dada Magreth”
“Huyo rafiki yetu tuna jaribu kumpigia ila hatumpati hewani kuna tatizo lolote?”
“Ohoo rafiki yenu aliondoka asubuhi ya leo. Ila ame acha funguo”
“Basi nina kuja chumba chetu si kipo salama?”
“Ndio”
Magreth akakata simu, akaingia bafuni akaogo. Akabadilisha nguo haraka haraka kisha akanza safari ya kuelekea mkono Morogoro kwa kutumia pikipiki yake.
“Hivi huo uwezo wako una utolea wapi?”
Juma aliuliza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Hahaa, ni kipawa ambacho mwenyezi Mungu alinipatia toka utotoni”
“Ahaa hicho kipawa chako hakiendani na swala la kukoko?”
“Yaa ila ina nibidi niwe sana karibu na Mungu kwani yeye ndio anayesha mambo yajayo na yanayo weza kutika sasa hivi”
“Ahaa sawa sawa”
Ukimya ukatawala katikati yao huku kila mmoja akimtazama mwenzake kwa macho ya aibu. Juma akashusha pumzi na taratibu akahamia kwenye sofa alilo kaa Josephine. Akamshika Josephine katika paja lake la kushoto na kumfanya Josephine kukaa kimya kidogo. Juma akazidi kujikaza japo mapigo yake ya moyo yana muenda kasi sana. Akasogeza lispi zake karibu na lispi za Josephine na akaanza kumnyonya na Josephine hakuwa na ujanja wa aina yoyote zaidi ya kutulia na kumruhusu Juma afanye anacho jisikia
***
Macho yakazidi kumtoka makamu wa raisi Madenge Jr. Video iliyo rekodi tukio zima lililo fanyika katika kordo ya kuelekea katika vyumba vya ICU. Mapigo waliyo kuwa wana pigwa wanajeshi walio kuwa wame imarisha ulinzi wa eneo hilo hakika yakazidi kumuacha mdomo wazi makamu wa raisi.
“Huyu hadi sasa hivi hamjamjua huyu mwanamke ni nani?”
Makamu wa raisi alimuuliza daktari mkuu wa hospitali ya taifa Muhimbili.
“Hapana muheshimiwa”
“Sio mfanyakazi wenu?”
“Hapana sio mfanyakazi wetu”
“Hakikiesheni huyu binti muna mpata.”
Makamu wa raisi alitoa maagizo hayo kwa mkuu wa kiosi cha wanajeshi walio kuwa wana mlinda raisi Mtenzi hospitalini hapo.
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi na walinzi wake wakatoka ofisini hapo. Akamtazama dokta Msangi kisha akamuita kwa ishara, akasogea eneo ambalo halina mtu yoyote ambaye ana weza kuwaisikia chochote.
“Ulishindwaje kumdhuru?”
“Muheshimiwa nilichelewa kufika eneo la tukio. Samahani sana kwa hilo”
“Sasa funga kinywa chako na usijaribu kumueleza mtu yoyote juu ya hili swala na kuanzia hivi sasa mpango wa kumuua Mtenzi haupo tena mikononi mwako. Umenielewa?”
Makamuwa raisi alizungumza kwa suati ya chini ila iliyo jaa umsisitizo ndani yake.
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaondoka eneo hilo na kumuacha dokta Masawe akiyang’ata meno yake kwa hasira kwani hakutarajia kama dili hilo lina weza kukatishwa ikiwa alisha anza kuipangia bajeti pesa hiyo.
ITAENDELEA
Haya sasa, dili la dokta Masawe lime katishwa je ata jitahidi kuhakikisha kwamba ana muua raisi Mtenzi ambaye hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo? Usikose sehemu ya 122.
SIN 122
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
Website……………………………………………… www.storyzaeddytz.com
ILIPOISHIA
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi na walinzi wake wakatoka ofisini hapo. Akamtazama dokta Msangi kisha akamuita kwa ishara, akasogea eneo ambalo halina mtu yoyote ambaye ana weza kuwaisikia chochote.
“Ulishindwaje kumdhuru?”
“Muheshimiwa nilichelewa kufika eneo la tukio. Samahani sana kwa hilo”
“Sasa funga kinywa chako na usijaribu kumueleza mtu yoyote juu ya hili swala na kuanzia hivi sasa mpango wa kumuua Mtenzi haupo tena mikononi mwako. Umenielewa?”
Makamuwa raisi alizungumza kwa suati ya chini ila iliyo jaa umsisitizo ndani yake.
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaondoka eneo hilo na kumuacha dokta Masawe akiyang’ata meno yake kwa hasira kwani hakutarajia kama dili hilo lina weza kukatishwa ikiwa alisha anza kuipangia bajeti pesa hiyo.
ENDELEA
“Hakikisha kwamba dokta huyu ana toweka duniani”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr alimuambia mlinzi wake huku akiingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo la hospitalini.
***
Magreth akafika mkoni Morogoro. Akaingia eneo la mapokezi na kukutana na muhudumu wa hoteli.
“Habari yako”
“Salama dada. Funguo yako hii hapa”
“Nashukuru”
Magreth akapandisha gorofani na kuingia kwenye chumba chao. Kila kitu chao akakikuta chumbani hapo kasoro vitu vya Levina. Magreth akakusanya vitu vyake na vitu vya Josephine, akaviingiza kwenye gari lake. Alipo hakikisha kwamba vitu vyao vyote vipo kwenye gari, akampigia simu Josephine.
“Vipi?”
“Nimefika n anime mkuta hayupo. Sasa naliancha hili gari hapa, hembu mpatie simu Juma”
“Ndio boss”
“Naacha gari langu hapa Morogoro, nina hitaji uje kulichukua”
“Ahhaa sawa bosi so nipande basi?”
“Hivi kuna mabasi yanago anza safari kutoka Dar?”
“Hapana, ina bidi nikapandie Mlandizi naona basi zote zinazo tokea mlandizi”
“Sawa fanya hivyo mimi nina rudi Dar es Salaam na fungua nina iacha mapokezi hapa”
“Sawa”
“Mage”
“Nina hitaji kwenda Muhimbili nita hitaji kumpeleleza yule dokta uliye na mashaka naye”
“Njoo kwanza nyumbani”
“Poa”
Magreth akamkabidhi muhudumu wa mapokezi funguo ya gari lake na akaianza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam. Ikamchukua masaa manne kufika Dar es Salaam.
“Juma alisha ondoka?”
Magreth alimuuliza Josephine mara baada ya kuingia ndani.
“Ndio aliondoka muda ule ule ambao ulimpigia simu”
“Una onekana una furaha sana vipi?”
Swali la Magreth likamfanya Josephine kubaki akitabasamu.
“Au mume sha kubaliana nini?”
Magreth aliendelea kumtania Josephine.
“Bwana Mage”
“Haya bwana vipi raisi ame jitingisha hata kidogo?”
“Hapana ina bidi tumtafute daktari la sivyo ana weza kufa humu ndani”
“Sasa ni dokta gani ambaye ana weza kumfanyia matibabu?”
“Hata mimi sifahamu kwa kweli, au kumachukue yule dokta ninaye mtilia mashaka”
“Sasa kama una mtulia mashaka akija hapa si ina weza kuwa ni shida kwetu”
“Yule yule ndio anaye tufaa sisi”
“Mmmm sawa”
Magreth na Josephine wakakubaliana kumpata dokta Masawe. Magreth akaelekea hospitali ya Muhimbili na kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona dokta Masawe akiwa ana elekea kwenye maegesho ya magari. Mlinzi wa makamu wa raisi aliye kabidhiwa kazi ya kumuua dokta Masawe ili kuhakikisha siri ya kumuua raisi Mtenzi haivuji naye yupo eneo hilo la maegesho huku akiwa amevalia kofia nyeusi kuificha sura yake.
“Samahani dokta”
“Magreth alimuita dokta Masawe aliye shika fungu mkononi mwake kwa ajili ya kufungua mlango wa gari hilo.
“Bila samahani”
“Ahaa nina weza kupata dakika moj…..”
Gafla Magreth akamuangusha dokta Masawe chini na risasi iliyo kuwa imefyatuliwa kwa ajili ya kumpiga dokta Masawe, ikapiga kwenye kioo cha gari lake na kika pasuka. Tukio hilo Magreth alilifanya kwa uharaka sana kwani aliweza kumuona muuaji kwa kupitia kioo hicho ambacho kwa sasa kime funja.
“Nini?”
“Lala chini”
Magreth alizungumza huku akijaribu kuchungulia. Mlinzi wa makamu wa raisi bwana Madenge Jr akafyatua risasi mfululizo na uzuri ni kwamba bastola yake ameifunga kiwambo ambacho kina zuia sauti kutoka hivyo watu wengine walio eneo la hospitali wana endelea na shuhuli zao. Magreth akabundigika chini ya uvungu wa gari la pembeni aina ya Ford Range. Akatokea upande wa kijana huyo. Akamvuta mguu kijana huyo na akaanguka chini. Kabla Magreth hajafanya shambulizo lolote, kijana huyo akampiga teke la shingo na kumfanya Magreth kuona mawenge mawenge. Kijana huyo akasimama na kukimbia eneo hilo huku akimuacha dokta Masawe akimfwata Magreth aliye alal chini kwa ajili ya kumpa huduma ya kwanza.
“Una jisikiaje?”
Dokta Masawe alizungumza hukua kimuamsha Magreth.
“Kidogo nafuu”
“Wana taka kuniua washenzi hawa”
Dokta Masawe alizungumza kwa hasira.
“Kina nani?”
Dokta Masawe akaka kimya kwa maana bado hamuamini Magreth.
“Ahaa acha tu”
Dokta Masawe kalizunguka gari hilo, akatoa chupa ya maji na kumkabidhi Magreth kwa ajili ya kunawa uso wake kwani ume chafuka kidogo.
“Nashukuru binti”
“Usijali dokta. Nina mgonjwa wangu yupo nyumbani nina kuomba sana uweze kwenda kumfanyia matibabu”
“Ana sumbuliwa na nini?”
“Naye aliweza kuudhurika na mashambulizi ya mabomu.”
“Sasa kwa nini usimlete hospitalini”
“Nina imani hata wewe mwenyewe una ona jinsi gani ambavyo hospitali zilivyo jaa na wagonjwa wa kawaida huwa hawapati kipaumbele kama jinsi wenye huwezo na mali wanavyo pewa kipaumbele”
Dokta Masawe akamtazama kwa sekunde kadhaa Magreth.
“Alafu wewe kama nina kujua. Wewe si yule mmiliki wa ule mgahawa pake Kinondoni?”
“Ndio”
“Ahha mimi ni mteja wenu huwa mara kwa mara huwa nina pata chakula pale. Basi ingia kwenye gari langu twende”
“Mmmm kule ninapo ishi mimi kidogo barabara ime haribika. Kama ina wezekana tuondoke na pikipiki yangu”
Dokta Masawe akajishauri kwa sekunde kadhaa kisha akakubaliana na Magreth.
“Hivi ni wapi ume sema?”
“Kigomboni”
“Ahaa sawa sawa twende.”
Magreth na dokta Masawe wakaondoka eneo hilo huku matarajio ya Magreth yame kwenda kiwepesi sana tofauti na alivyo kuwa ana fikiria.
Nabii Sanga akamtazama mke wake aliye wekewa mashine na kumsaidia kupumua mstuko alio upata kwa kweli ni mkubwa sana. Taratibu nabii Sanga akasimama na kutoka ndani hapo, hapo ndipo akaanza kutambua kwamba utajiri wake hauwezi kufanya kila jambo kwani, laiti kama roho zinge kuwa zina nunuliwa basi ange wanunulia vijana wake roho ambazi zinge wafanya warudi tena duniani. Akaitoa simu yake mfukoni, akaingia upande wa video na kuanza kuangalia video za sherehe ya send off ya mwanaye. Furaha iliyo kuwa ime watawala watoto wake hao watatu hakika ika zidi kumfanya moyo wake kupatwa na maumivu ambayo kwenye maisha yake yote hakuwahi kuyapata.
Madaktari wanne wakiwa wana kimbia wakingia katika chumba cha ICU na kumfanya nabii Sanga kusimama na kuanza kuelekea karibu na chumba hicho.
“Huruhusiwi kuingia ndani hapa”
Daktari mmoja alizungumza huku akimtoa nabii Sanga ambaye ana mshuhudia Julieth akiwa ana jirushua rusha kitandani mithili ya mtu mwenye kifafa huku mashine inayo msiaida kupumua ikitoa mlio wa kuashiria uhatari wa hali ya mgojwa. Nabii Sanga akazidi kuchanganyikiwa kwa maana hatambui ni jambo gani ambalo lina msumbua mwanaye hadi hali hiyo kumtokea.
***
“Vipi ume fanikiwa?”
Makamu wa raisi aliuliza mara baada ya mlinzi wake huyo kuingia ofisini kwake.
“Ime shindikana”
“Ime shindikana vipi ikiwa ni kazi rahisi sana”
“Aliweza kusaidia na yule binti ambaye jana alikuwa na mwenzake aliye onyesha eneo ambalo raisi alifukiwa”
“Yule msichana mrefu, maji ya kunde”
“Ndio muheshimiwa”
“Ilikuwaje hadi amsaidie”
“Walikuwa wana zungumza eneo la maegesho ya magari na laiti kama ninge mkosa pale nisinge mpata tena”
“Bado huja nijibu alimsaidia vipi?”
“Alimkumba na akaanguka pembeni na risasi zilimkosa”
“Hakikisha kwamba una mpata huyu mpumbavu ume nielewa”
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi alizungumza kwa hasira na kijana wake akatoka ndani hapo kwani kama ni mpango wake sasa una anaza kuwa mgumu.
“Je una fahamu ni sehemu gani ambapo yule binti ambaye ni mtabiri tabiri ana ishi?”
“Sifahamu ila tuna weza kupapata”
“Nitamfutie leo usiku nahitaji kwenda kuonana naye na kuzungumza naye”
“Sawa”
Mlinzi wake huyo akatoka ofisini hapo na baada ya dakika kumi akarudi akiwa ame tambua ni eneo ganiambalo Josephine ana ishi.
***
“Karibu sana dokta hapa ndio nyumbani”
Magreth alizungumza hukuwakishuka kwenye pikipiki. Dokta Masawe akamtazama kwa sekunde kadhaa Josephine na akamkumbuka.
“Wewe leo ulikuwepo pale hospitalini?”
“Ndio, nilikuwepo”
Dokta Masawe akamtazama Magreth aliye muonyeshea ishara ya kuingia ndani. Dokta Masawe taratibu akaanza kutembea kuelekea ndani huku akimuacha Josephine akifunga geti hilo vizuri. Wakamkaribisha sebleni hapo, Magreth akaingia ndani kwake, akachomeka bastola yake kiunoni na kurudi sebleni.
“Dokta ni nani aliye hitaji kukua na kwa nini alihitaji kukuua?”
Swali la Magreth kidogo likamstua dokta Masawe.
“Ahaa ni watu fulani ambao kidogo tumepisha kwenye mambo ya kibiashara kwa maana ukiachilia kazi yangu ya udaktari, pia nina nina fanya biashara.
“MUONGO”
Josephine alizungumza kwa kujiamini na kumfanya dokta Masawe kumshangaa.
“Samahani binti naamini hatujuani. Nime kuja hapa kwa ajili ya msaada alio utenda dada yako sijui nani yako, ila tambua kwamba sijakuja kuhojiwa”
Magreth akachomoa bastola yake na kumnyooshea dokta Masawe na kumfanya aanze kutetemeka mwili mzima.
“Ukweli wako ndio utakufanya uwe huru. Niambie ni kwa nini ulihitaji kuuwawa?”
Dokta Masawe akaanza kutetemeka mwili mzima.
“Ku…mb….e na nyinyi ni wale wale?”
“Dokta nijibu sina utani nita kifumua kichwa chako ukidanganya?”
“Ni…i…ima kamu wa raisi”
“Makamu wa raisi ana nini?”
“Yeye ndio ameagiza mtu kwa ajili ya kuniua mimi”
Josephine na Magreth wakajawa na mshangao mkubwa sana.
“Kwa nini ana hitaji kukuua?”
“Dokta Masawe macho yakamtoka huku akiogopa sana kutoa siri hiyo ambayo aliapa kwamba hato itoa.
“Zungumza dokta kumbuka kwamba maisha yako mimi ndio muamuzi sasa hivi. Ufe au uendelee kuishi”
“Ni…ni..ni kutokana na…na….”
“Na na na na nini?”
“Alihitaji nimchome sindano ya sumu raisi Mtenzi ili afe”
Macho yakawatoka Josephine na Magreth.
“Acha utani wewe”
Magreth alizungumza huku akitabasamu huku akihisi kwamba anacho kizungumza dokta Masawe ni uongo.
“Haki ya Mungu dini yangu ni mkristo. Makamu wa raisi aliniahidi kunipandisha cheo na kunipa milioni mia moja ikiwa kama malipo ya kazi hiyo”
Taratibu Magreth akaishusha bastola hiyo.
“Ndio maana nilipo kuwa nina kutazama mapigo yangu ya moyo yalikuwa yana kwenda kasi sana”
Josephine alizungumza huku akimtazama dokta Masawe.
“Moyo wako bado una hitaji kumuua raisi Mtenzi?”
“Hapana kwa kweli, siwezi kufanya jambo hilo kwenye maisha yangu.”
Dokta Masawe alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Magreth akampa ishara ya kusima na akatii. Wote watatu wakaondoka sebleni hapo na kuingia chumbani alichopo raisi Mtenzi. Macho yakamtoka dokta Masawe huku kwa mara kadhaa akimwatazama Josephine na Magreth usoni mwake.
“Nina kupa jukumu la kuhakikisha raisi Mtenzi ana pona endapo uta fanya ubabaishaji wowote, au akafa basi tambua kwamba na wewe nina kuua. Kama niliweza kuwapiga wanajeshi zaidi ya kumi na tano na nika mtoa raisi pale Muhimbili basi hakika kuitoa roho yako ni kitendo cha sekunde. Tumeelewana?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama dokta Masawe usoni mwake na akamfanya atingishe kichwa akimanisha kwamba ame muelewa vizuri sana.
“Ila haya hali ya raisi sio salama ina weza kuleta shida”
“So una hitaji tumpeleke wapi ikiwa raisi ana hitaji kumuu”
Dokta Msangi akaka kimya huku akimtazama raisi Mtenzi aliye lala kitandani hapo huku hali yake ikiwa bado hajitambui kabisa.
“Sema tukuletee nini na nini ili kumuhudumia”
“Nikiwataji hamuto weza kuvifahamu. Nina omba muniletee kalamu na karatasi ili niwaandikie”
Josephine akatoka ndani hapo na baada ya sekunde kadhaa akarudi akiwa na kalamu na karatasi. Dokta Masawe akaorodhesha vitu vyote ambavyo ana hitaji katika kumuhudumia raisi Mtenzi.
“Vitu hivyo sio rahisi kuvipata madukani ni hadi muende kwenye hospitali kubwa kama Agakhan”
“Wao wame salimika na milipuko?”
“Yaa hawajaguswa hata kidogo nendeni pale kuna daktari mmoja ana itwa dokta Khan muambie kwamba nime agizwa na dokta Masawe hivi vitu nina uha kika ata kupatia”
Dokta Masawe alizungumza huku akimkabidhi karatasi hiyo Magreth.
“No ata kwenda Jose.”
“Sasa dokta kwa nini usimpigie kwa maana endapo nika mkuta hayupo ina kuwaje?”
“Simu yangu hapa sina, nina hisi ime angukia eneo la tukio pale tulipo shambuliwa”
Magreth akampapasa dokta Masawe na kweli hakuwa na simu yake mfukoni.
“Akikataa kunipatia?”
“Muambie ni muhimu sana na kama akihitaji kuzungumza nami basi una weza kuwasiliana na dada yako hapa na nina weza kuzungumza naye”
“Sawa. Mage nita tumia pikipiki?”
“Una weza kuiendesha?”
“Ndio, ila sio sana”
“Hivyo vitu nilivyo waagiza sio rahisi kubebwa na pikipiki, mukipata gari pickup kidogo ina weza kusaidia kubeba hivyo mizigo kwa maana ni kuna life mashine hapo kubwa itakayo weza kumsaidia raisi katika siku hizi”
“Hiyo gari ndogo hapo nje ina weza kujitahidi kubeba?”
“Hapana, ukienda kule una weza kuina”
“Basi hadi Juma arudi na gari Aud Q7 si ina beba?”
“Yaa”
Magreth akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Juma.
“Vipi?”
“Ndio nina fika hapa hotelini, funguoa ume iacha kwa nani?”
“Dada mmoja mrefu hii, ni mweupe kidogo”
“Okay nina muona ngoja nizungumze naye usikate simu”
“Sawa”
“Samahani dada, nina itwa Juma. Kuna funguo ya gari aina ya Aud q7 ime acha hapa?”
“Mmm una mtambua aliye iacha?”
“Ndio ni boss wangu”
“Ana muonekano gani?”
“Ni mwana dada mrefu, maji ya kunde na nimwembamba kiasi”
“Una weza kumpigia”
“Simu ipo hewani, una weza kuzungumza naye”
Juma alizungumza huku akimkabidhi mwana dada huyo simu.
“Haloo”
“Ni mimi, nime muagiza huyo ni kijana wangu, mpatie funguo”
“Sawa”
“Nashukuru”
Magreth alimsikia Juma akizungumza.
“Amenikabidhi”
“Una weza kufika Dar es Salaam saa ngapi?”
“Mmmm nita chukua kama masaa manne hadi matano kufika hapo nyumbani?”
“Sasa hivi ni saa mbili, okay jitahidi basi uwahi si una jua tuna mgonjwa hapa ndani?”
“Yaa natambua bosi”
“Sawa”
Magreth akakata simu hiyo.
“Hivi tatizo lake haswa ni nini?”
“Amekosa pumzi, na amevuta hewa chafu hivyo endapo hewa hivyo ita weza kutoka kwenye mapafu yake basi kidogo ana weza kuwa sawa.”
“Jose vipi mbona kama ume kosa raha galfa?”
“Hata mimi sielewi, ila nina hisi kuna ugeni uta kuja hapa nyumbani”
“Ugeni kutoka wapi?”
“Sifahamu, ila nina hisi kwamba kuna ugeni uta fika hapa”
Magreth na dokta Msangi wakatazamana kwenye nyuso zao na wakakosa kutambua ni mgeni gani ambaye ata fika nyumbani hapo.
***
“Dokta vipo hali ya mwanangu?”
Nabii Sanga aliuliza huku akiwa amejawa na simanzi.
“Tuna mshukuru Mungu ameweza kuzinduka kutoka kwenye kifo na tuta muhamisha wodi hii na kumpeleka katika wodi ya kwake peke yake”
“Ohoo asante Mungu”
“Pia mke wako amezinduka, sasa je tuwaweka katika wodi moja au tuwatenganishe”
“Wawekeni wodi moja”
“Sawa”
Daktari huyo akaingia katika chumba hicho cha ICU, akawaeleza manesi kumuandaa Julieth kwa ajili ya kumtoa katika chumba hicho cha ICU.
“Waziazi wangu wapo wapi?”
Julieth alimuuliza mmoja wa manesi hao.
“Baba yako yupo hapo nje ana kusubiria”
“Mama yangu je?”
“Naye yupo uta muona”
Walipo hakikisha wame kiandaa vizuri kitanda cha Julieth wakaanza kukisukuma ili kumtoa nje.
“Mume wnagu hali yake ina endeleje?”
“Bado ila naye muda si mrefu ata zinduka”
Julieth akamtazama Jery ambaye naye hadi sasa hivi hajitambui, kisha akwaruhusu manesi hao kumtoa katika chumba hicho. Nabii Sanga tabasamu pana likamtawala usoni mwake, taratibu akamkumbatia Julieth.
“Mama yupo wapi?”
“Yupo huku chumbani?”
Manesi wakamuingiza Magreth katika chumba alicho lazwa Mrs Sanga.
“Julieth”
Mrs Sang alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake.
“Mama”
“Bee mwanangu”
Mrs Sanga aliitikia huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Baba kaka wapo wapi?”
Nabii Sanga akamtazama mke wake ambaye kidogo akatingisha kichwa akimaanisha kwamba wasizungumze kitu chochote.
“Wame toka kidogo kuna mambo wana yashuhulikia”
“Sawa, kulitokea nini mbona tupo hospitalini?”
Nabii Sanga taratibu akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Julieth usoni mwake.
“Mwanangu kuna moja ya shambulizi lilitokea kwenye ile hotel pale na kwa bahati mbaya mambo yame kuwa kama hivyo yalivyo kuwa je una kumbuka mara ya mwisho ulikuwa wapi?”
“Ndio, baba mke alikuja kutuita chumbani kwetu tukaingia kwenye lifti na baada ya hapo tukapata mtetemeko mkubwa na hatukujua kilicho endelea baada ya hapo. Je mume wajua walio fanya shambulizi hilo?”
“Ndio”
“Ni kina nani?”
“Al-Shabab”
“Al-Shabab!! Walikuwa wana tafuta nini kwenye harusi yetu?”
“Bado hatuja jua chanzo kamili, ila woa ndio walio husika”
“Ila baba ina bidi tufanye jambo juu ya hili. Hatuwezi kuacha hili swala lipite kirahisi hivi’
“Usijali mwanagu, kila jambo lipo chini ya uangalizi”
“Ungalizi gani baba. Watu walio tuvurugia shuhuli yetu haiwezekani kuwaacha, watumie wanachama wote email na waambie nahitaji kuonana nao kesho usiku”
Jlieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama baba yake usoni.
“Ila huja pona bado?”
“Baba, sijavunjika sehemu yoyote ya mwili wangu, ninacho kihitaji kwa sasa ni kukutana na wanachama wangu na hayo mengine muniachie mimi sawa”
“Nime kuelewa”
Nabii Sanga alijibu kwa upole kwani mwanaye Julieth amejawa na hasira mithili ya Simba jike aliye uliwa watoto wake.
***
“Muheshimiwa kila kitu kipo tayari tuna weza kuondoka sasa”
“Sawa”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr, akasimama na kuongozana na mlinzi wake huyo, wakaingia ndani ya gari na wakaondoka eneo hilo la ikulu huku wakiwa na walinzi kumi watano wakiwa gari ya mbele na watano wakiwa katika gari la nyuma.
“Muheshimiwa naweza kukuuliza swali?”
“Uliza”
“Kwa nini una kwenda kuonaan na yule msichana?”
“Kuna mambo nahitaji kumuuliza, naona ana jambo fulani ndani yake. Hivi alikufahamu yule binti ambaye ni rafiki yake?”
“Sidhani”
“Basi tukifika pale ina bidi ukae ndani ya gari sinto hitaji akuone ukiwa ume ambatana nami”
“Sawa muheshimiwa”
Gari hizo zikazidi kusonga mbele na wakafanikiwa kufika nyumbani kwa Magreth.
“Ni kina nani?”
Magreth alizungumza huku akitazama kwenye simu yake video zinazo rekodiwa kupitia cctv kamera alizo zifunga getini kwake.
“Kuna nini?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Kuna gari tatu nyeusi zime simama hapo nje?”
Magreth alizungumza huku akimuonyesha Josephine video hizo.
“Mungu wangu!!”
Josepghine aliye shika simu hiyo alihamaki. Magreth akamsogele na kutazama video hiyo. Wakamuona makamu wa raisi Madenge Jr akishuka kwenye gari la katikati.
“Ame kuja kufanya nini?”
“Hata mimi sifahamu ame kuja kufanya nini?”
Magreth akakimbilia katika chumba alipo lazwa raisi Mtenzi na ndipo alipo dokta Masawe.
“Dokta kuna jambo lime tokea. Ila nakuhitaji ukae ndani ya chumba hichi na mgonjwa na mujifungie kwa ndani, sinto hitaji kukuona una toa pua yako nje. Sawa”
“Jambo gani?”
Magreth akamuonyesha dokta Masawe video hizo na kumfanya aanze kutetemeka mwili mzima.
“Ume nielewa lakini?”
“Ndio so ame kuja kufanyaje, au ame gundua kwamba nipo hapa na mgonjwa?”
“Nina imani kwamba hajajua chochote, ila kaa ndani hapa na usitoe”
“Sawa”
Magreth akatoka chumbani hapo na kwa haraka dokta Masawe akafunga chumba hicho kwa ndani. Magreth akamkuta Josephine akiwa ana haha sebleni hapo.
“Hei nahitaji utulie usionyeshe wasiwasi wa aina yoyote. Sawa”
“Sawa”
“Niangalie, endapo uta kuwa na wasiwasi basi tambua kwamba uwepo wa dokta Masawe pamoja na raisi Mtenzi uta julikana”
“Sawa”
Magreth akaichomeka bastola yake kiunoni mwake na kuifunika na tisheti yake ndefu aliyo ivaa. Akatoka ndani hapo huku akisikilizia jinsi kengele ya mlangonimwake jinsi inavyo toa mlio, akafungua geti dogo na akajifanya akishangaa uwepo wa makamu wa raisi Madenge Jr.
“Muheshimiwa”
“Yaa je tuna ruhusiawa kuingia ndani?”
Makamu wa raisi Madenge Jr alizungumza huku akiwa amejawa na tanasamu pana sana usoni mwake. Magreth akawatazama walinzi hao kumi walio simama pembeni ya raisi Mtenzi na katika sekunde hizo chache akaweza kugundua uwezo wao pamoja na udhaifu wao na hata likitokea jambo lolote basi ata weza kulihimili.
“Yaa karibu sana muheshimiwa. Hii ni big suprize kwangu”
“Ni kweli, sikuhitaji kuwafaamisha nikaona nije mwenyewe”
“Ume pajuaje hapa muheshimiwa?”
“Ahaa…niliagiza vijana wangu waweze kuwafwatilia. Kama muliweza kuja ikulu basi nami nikaona sio mbaya leo nije kuonana nanyi”
“Tuna shukuru sana, muheshimiwa karibu sana ndani”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Makamu wa raisi akaingia sebleni na walinzi wake wawili huku wengine wakibaki nje kuimarisha ulinzi.
“Shikamoo muheshimiwa”
Josephine alisalimia kwa heshima zote.
“Marahaba habari ya wewe?”
“Nina smshukuru Mungu ana saidia”
“Karibu ukae muheshimiwa”
“Nashukuru. Mume jitahidi, eneo hili ni zuri sana”
“Asante sana muheshimiwa. Je nikuandalie nini muheshimiwa?”
Magreth alizungumza kw afuraha iliyo mfanya Josephine naye kujiamini.
“Nime toka kula usiku huu, hivyo musi sumbuke sana. Ahaa Jose nime kuja kwanza kukushukuru kwa kuweza kutuonyesha ni wapi raisi Mtenzi alipo kuwa ame fukiwa na kile kifusi cha hoteli. Pili tume pata tatizo ambalo kwa kweli tuna amini kwamba wewe uta kuwa ni msaada mkubwa sana kwetu”
Makamu wa raisi alizungumza kwa sauti ya utaratibu na iliyo jaa hekima kubwa sana. Ukimtazama kwa haraka haraka una weza kusema ni mtu mwema na mwenye roho ya upendo. Ila sumu na tamaa inayo endelea kuchemka moyoni mwake kwa kweli ni jambo la hatari sana.
“Tatizo gani muheshimiwa?”
“Leo mchana raisi Mtenzi aliweza kuondolea hospitalini na watu ambao tuliweza kunyaka matikio yao kwenye cctv camera, ila kwa bahati mbaya hatukuweza kuona sura zao. Watu hao mmoja wao alikuwa ni mwanamke ambaye ana oneana ana uwezo mkubwa sana wa upambanaji na mtu wa pili ni mwanaume. Walimuondoa raisi Mtenzi hospitalini na hadi sasa hivi hatufahamu ni wapi walipo, pia nina imani kwamba ulikuwepo kwenye eneo la tukio na ulishuhudia jinsi mwanamke huyo alivyo kuwa ana wapiga wanajeshi wangu?”
“Ndio muheshimiwa na pia nili muadisia rafiki yangu juu ya jambo hilo”
“Kwa kweli, nina shinda hata hii taarifa kuitoa kwenye vyombo vya habari kwani watu wata niona kwamba sio muwajibikaji. Ila nilipo kaa sana na kutafakari, nika kumbuka kwamba upo wewe mwenye uwezo wa maono yajayo au yaliyopo. Basi kwa heshima zote, nina kuomba uweze kumuomba Mungu wako aweze kutuonyesha sehemu alipo raisi wetu mpendwa bwana Mtenzi”
Josephine akashusha pumzi huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Laiti kama ninge kuwa na uwezo wa kupambana basi ninge pambana na yule aliye muiba raisi pale hospitalini ila sikuwa na uwezo wa kupigana.”
“Ni kweli, na hata kwenye cctv camera niliweza kuona ni jinsi gani ulivyo kuwa una duwaa”
“Nita muomba mwenyezi Mungu na akinionyesha ni wapi alipo raisi Mtenzi basi nita kuambia muheshimiwa”
“Je huna hisia zozote za sehemu alipo?”
“Mmmm hapana muheshimiwa. Ila ngoja nisali kidogo”
Josephine akafumba macho yake kwa dakika moja nzima kisha akaafumbua.
“Nime pata jambo muheshimiwa”
“Jambo gani?”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment