Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

POWER SEHEMU YA 2/10

 

 


 POWER

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 2 KATI YA 10

 

Mzee mmoja alizungumza huku akito kalamu kwenye mfuko wake wa koti. Akasaini sehemu anayo takiwa kusaini, inayo mpa kiapo kwamba amekubaliana na masharti ya mkataba wangu. Baada ya kila mtu kutia saini ya mkataba, mwanasheria akaikusanya na kunipatia. Nikaanza kuupitia mkabata mmoja baada ya mwengine huku nami nikitia saini kama mtoaji masharti hayo.

“Naona tumemaliza na asanteni sana baba zangu na babu zangu. Niwatakie usiku mwema”

Nilizunugmza huku nikimkabidhi mwana sheria kalamu ambayo aliitoa meneja mmoja.

‘Ethan kalamu hiyo ina ushahidi wa kila kitu milicho kizungumza’

‘Kalamu gani?’

‘Hiyo muliyo saini’

Nikageuka nyuma na kumuona mwana sheria akimkabidhi meneja huyo kalamu hiyo na taratibu mzee akaaweka katika mfuko wake wa suti, huku sura yake kidogo ikonyesha kuwa na furaha. Nikarudi hadi katika kiti alicho kaa, akanitazama kwa wasiwasi, nikamnyooshea mkono huku nikimtazama usoni mwake.

“Nini mkuu?”

“Kalamu”

Mzee huyu nikamuona jinsi anavyo babaika, wasiwasi mwingi ukamjaa na kujikuta akinisukuma na kuanza kukimbilia mlangoni, kwa kasi ambayo hata mimi mwenyewe sifahamu nimeitolea wapi nikajikuta nikiwa nimesimama mlangoni huku nikimsubiria kufika hapa mlangoni. Nikamshika mzee huyu shingoni mwake na kumnyanyua juu kwa mkono mmoja hadi mimi mwenyewe nikajishangaa hii nguvu niliyo nayo.

“Naomba kalamu”

Meneja huyu akatoa kalamu na kunikabidhi mkononi mwangu huku mwili mzima ukimtetemeka.

‘Ethan huyu amenisaliti nimfanyaje?’

‘Mrushie kwenye meza kule’

Nikamrusha mzee huyu hadi mezani ambapo ni mita kama ishirini kutoka hadi hapa nilipo simama. Watu wote wakaka kimya wakimshuhudia mwenzo jinsi anavyo angukia katika viti. Nikashusha pumzi taratibu huku nikiminya kalamu hii katika eneo la kifuniko, mazungumzo niliyo kuwa nikiyazungumza ndani humu yote yakaanza kusikia kwa kila mtu.

“Yoyote mwenye ujinga kama huu, labda umeurekodi kwenye simu yako. Toa simu yako sasa hivi na ufute kile kitu mbele yangu. Mameneja na mchungaji wakaanza kutazamana.

‘Hakuna aliye fanya hivyo’

‘Kweli Ethan?’

‘Niamini mimi’

NIkamuona meneja akijitahidi kunyanyuka kwenye viti hivyo alivyo vivunja.

“Nenda kamsaidieni mwenzenu”

Nilizungumza kisha nikafungua mlango na nikatoka ndani humu, huku mwanasheria akinifwata kwa nyuma kwa mwendo wa haraka.

“Ethan”

“Naam”

“Hembu niambie ni wewe au ni macho yangu yaliona vibaya kitu ulicho kifanya”

Nikasimama na kumgeukia mwana sheria.

“Ulicho kiona ndani ya ofisi nahitaji kibaki ndani ya ofisi. Umenielewa?”

“Sawa sawa mkuu”

Tukarudi katika jumba ambalo watu mbalimbal wamakusanyika na wapo kwa ajili ya kutupatia pole kwa msiba ulio tupata.

“Ethan”

Muandishi wa habari wa BBC aliniita, nikakumbuka ahadi niliyo mpatia, nikasimama na akanifwata nilipo.

“Samahani naona nusu saa nililo kuahidi lilipita dada yangu”

“Usijali, sijui tunaweza kufanya mahujiano?”

“Ndio tunaweza, kutoka nilikuahidi inabidi nitimize ahadi yangu niliyo kuambia”

“Nashukuru kusikia hivyo. Tunaweza kutoka nje na kuelekea katika gari letu la kurusha matangazo”

“Sawa”

Nikaongozana na dada huyu hadi kwenye gari lao kubwa la kurusha matangazo. Vijana wake wakasha kamera, akachukua maiki yake, akajiweka vizuri kwenye zake. Kamera man, akaanza kuhesabu vidole vyake kuanzia moja hadi tatu.

“Habari za muda huu watazamaji wa BBC, tupo katika nyumba ya mzee Klopp, mchezaji wa zamani wa nchi ya Ujerumani na timu ya B. Dotmund. Hapa nipo na mwanaye wa kiume, Ethan Klopp atatuelezea ni kitu gani kilicho tokea hadi baba yake mzaza akapoteza maisha. Karibu sana”

Kabla sijalijibu swali la muandishi wa habari huyu, nikashuhudia gari la wagonjwa likisimamishwa kwa haraka aneo la mbele la nyumba hii. Wauguzi wakashuka kwa haraka kwenye gari hilo huku wakiwa na kitanda cha kusukuma na kukimbilia ndani ya nyumba hii. Wasiwasi mwingi ukanijaa moyoni mwangu, makamera man wakageuzia kamera zao katika eneo lilipo gari hilo la wagonjwa. Nikaanza kutembea kueleka katika eneo hilo la gari huku nikifwata kwa nyuma na waandishi hao wa habari. Kabla sijalifikia gari hili nikawaona wauguzi wakitoka ndani humu huku juu ya kitanda wakiwa wamemlaza bibi Jane Klopp huku akihemea pumzi ya oksijeni jambo lililo nistusha sana kwani sifahamu ni kitu gani ambacho kimempata mama yangu, bi Jane Klopp.



“Daktari ni kitu gani kinacho endelea?”

Niliuliza huku nikiwa na shauku kubwa ya kuhitaji kufahamu.

“Mama yako amepoteza fahamu gafla, tunatakiwa kumwahisha hospitalini sasa hivi”

“Camila kaa na Mery sawa”

“Sawa”

Nikaingia ndani ya gari la wagonjwa huku nikiwa nimekaa pembeni nikimtazama bibi Jane Klopp jinsi anavyo hema kwa kutumia gesi maalumu ya oksijeni. Gari likaanza kuondoka katika eneo la jumba hili, njia nzima madaktari kazi yao ni kuhakikisha kwamba hali ya bibi Jane Klopp haiwi mbaya kabisa. Tukafika hospilini na bibi Jane Klopp akashushwa kwenye gari huku nami nikishuka na tukaanza kutembea kelekea katika chumba cha matibabu. Nikaikunja vizuri mikataba niliyo wasainisha mameneja kisha nikasimama pembeni ya mlango wa chumba hichi.

‘Ethan ni nini kimempta mama?’

‘Ni mstuko’

‘Haliya kae itakaa vizuri?’

‘Ndio usiwe na waasiwasi mkubwa rafiki yangu’

‘Sawa’

Hadi ina inatimia majira ya saa kumi na moja alafajiri bibi Jane Klopp akafanikiwa kupata fahamu zake. Nikakaa naye chini ya uangalizi mzuri wa madaktari hadi majira ya saa moja asubuhi ndipo nikarudi nyumbani huku daktari mkuu anaye mtibu akiahidi majira ya saa nne asubuhi ataruhuusiwa kurudi nyumbani.

***

Kutokana na kifo cha mzee Klopp utaratibu wa nazishi yake ukatuchukua wiki nzima hadi kukamilika. Hii ni kutokana na umaarufu wake kuanzia kwa wananchi hadi taifa kwa ujumla. Siku ya mazishi ikawadia huku karibia watu wote tukwia tumevalia nguo nyeusi huku wengine wakiwa wamevalia miwani nyeusi ili kuficha huzuni waliyo nayo juu ya kifo cha mzee Klopp. Viongozi mbalimbali kutoka bara hili la Ulaya nao ni miongoni mwa watu ambao wameudhuria mazishi haya.

“Mama jikaze”

Nilizungumza huku niiwa nimemuegemeza bibi Jane Klopp kichwa chake kwenye bega langu. Mchunganji akaendelea kuongoza ibada hii fupi, wana familia tukamuaga kwa mara ya mwisho huku tukiwa tumejawa na huzuni kubwa. Baada ya ibada kuisha, tukaondoka eneo hili la makaburini na kuwaachia wazikaji kufanya kazi yao ya kuuweka mwili wa mzee Klopp katika nyumba yake ya milele.

“Ethan”

Bibi Jane Klopp aliniita kwa sauti ya ungonge huku tukiwa katika gari tukirudi nyumbani.

“Ndio mama”

“Muangalie dada yako Mery kwa maana siku si nyingi nitamfwata mume wangu kule alipo elekea”

Mimi na Mery tukajawa na mshangao mkubwa sana huku tukimtazama mama usoni mwake.

“Mama huwezi ukafa”

Mery alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Bi Jane Klopp akatabasamu kwa muda.

“Mery mwanangu, mama yako siku zangu za kuishi hapa duniani zina hesabika. Mimi na baba yako tuliweza kudumu sana kwneye ndoa yetu, upendo wetu ulianza toka tulivyo kuwa watoto wadogo na hadi tumekuwa watu wazima.”

Bibi Jane Klopp alizungumza huku akijipangusa machozi usoni mwake kwa kutumia kitambaa chake.

“Yeye ndio alikuwa rafiki yangu wa karibu. Naona kifo kikiwa mbele yangu, nawaomba sana muweze kushikamana, nawaomba sana muweze kupenda na Ethan nakuomba usiweze kusahau asili yako”

“Kivipi mama?”

“Ujerumani ni nchi ambayo umekua tu, ila Tanzania ndio nchi ambayo umezaliwa, najua hapo mbeleni utakuwa mchezaji mkubwa sana wa mpira wa miguu. Ila nakuomba ukicheza timu ya taifa, usiichezee Ujerumani, hakikisha unaichezea timu yako ya nchi ya Tanzania. Hata kama ni vikombe basi unailetea sifa nchi yako sawa”

“Sawa mama”

Nilimjibu bibi Jane huku nami machozi yakinimwagika usoni mwangu.

“Mery hakikisha kwamba una chagua mwanaume sahihi kwenye maisha yako, si kila mwanaume anaye kuja kwako ana kupenda, wengi wao wanapenda pesa zako na mali zako, hakikisha kwamba hivyo unaweza kuvihimili kwenye maisha yako ya kila siku.”

“Sawa”

“Ethan kwa upande wako natambua umepata mwnaamke sahihi, ila endapo utamuacha Camila maisha yako yatapoteza muelekeo hata kama utakuwa na pesa nyingi kiasi gani ila maisha yako yatayumba”

“Siwezi kumuacha mama nitakuwa naye maisha yangu yote”

“Nashukuru kusikia hivyo”

Bibi Jane Klopp alijibu kwa upole na unyonge wa hali ya juu. Tukafika nyumbani, bibi Jane akatumbo aeleke chumbani kwake kulala kwani anajihisi kuchoka sana.

“Ethan naomba tuzungumze”

Dada Mery alizungumza huku akitangulia nje, tukaa kwenye moja ya benchi la kumpumzikia lililpo katika moja ya bustani.

“Ethan kuna vitu nahitaji kufahamu kuhusu wewe”

“Vitu gani dada yangu?”

“Mama pale alisema kwamba umetokea Tanzania, je unapafahamu kwenu hata tukisema twende tukatembekee huko?”

Nikaka kimya huku nikitafakari maisha yangu ya nyuma.

“Nafahamu mkoa nilio tokea”

“Ni mkoa gani huko Tanzania?”

“Kilimanjaro ndio mkoa nilio tokea, mzee na mama ndiopo walipo nikuta huko”

“Je unaweza kuwakumbuka mama na baba yako au ndugu zako wengine?”

Nikajaribu kurudisha kumbukumbu zangu nyuma, ila kitu ninacho kikumbuka ni siku nilipo kuwa nimelala kitandani na kuwasikia mzee Klopp na mke wake wakizungumza.

“Ethan”

“Sikumbuki mtu wa ina yoyote.”

“Hata mama yako humkumbuki?”

“Kwa kweli simkumbuki”

“Mmmm”

“Ila mzee na mama waliniambai kwamba waliniokota pembezoni mwa mto mmoja hivi nahisi huko ndipo nilipo kuwa nimepata matatizo”

“Huo mto walikuambia jina lake?”

“Hawakuniambia na wala siufahamu ni mto gani”

“Inabidi siku moja tupange safari na kwenda nchini Tanzania, natamani sana kuiona hiyo nchi”

“Tuombe Mungu dada yangu mambo yasiwe magumu”

“Ila ushauri wa mama alio kueleza hakikisha kwamba una ufanyia kazi”

“Sawa”

“Poa mimi nipo ndani”

Dada Mery akandoka na kuniacha nikiwa na mawazo mengi sana juu ya kuifikiria nchi yangu ya Tanzania.

***

Siku zikazidi kusonga mbele huku nami nikizidi kujitahidi kuutenga muda wangu katika masomo na kuongoza mali za mzee Klopp ambazo kwa sasa ni mali zangu. Ethan hakusita kunisaidi kwa kila jambo ambalo ninalifanya kwenye maisha yangu. Nikiwa mwaka wa mwisho katika masomo yangu ya sekondari, Camila na wanafunzi wezake wakapata safari ya kuelekea barani Afrika kwa ziara ya wiki mbili katika nchi ya Somalia na Tanzania.

“Unafurahia safari yako?”

Nilimuuliza Camila huku tukiwa tumekaa kwenye bustani ya shule ninayo isoma mimi.

“Ndio nina furaha”

“Hivi unafahamu kwamba Tanzania ndipo nilipo zaliwa?”

“Weee?”

“Hivi sikuwahi kukuambia hicho kitu?”

“Hapana”

“Mmmm mabona nahisi kwamba nimesha wahi kukuambia?”

“Hapana au kama umeniambia basi nitakuwa nimesahau”

“Tuachane na hayo. Mimi kwetu ni mkoa wa Kilimanjaro”

“Kwenye mlima wa Kilimanjaro?”

“Ndio”

“Ohoo huko ndipo tunapo kwenda”

“Ni mlima mmoja mzuri, naamini utakwenda kufurahia safari ya huko”

“Kweli”

“Camila muda wa kuondoka umefika”

Mmoja wa waalimu aliye kuja na Camila alizungumza huku akitutazama.

“Tunakwenda mwalimu”

“Camila hakikisha unakuwa muangalizi huko, kwa nchi ya Somalia huwa sina uhakika nayo katika usalama wake”

“Usijali mume wangu, tumehakikishiwa ulinzi mzuri”

“Sawa, ila vipi baba yako kampeni zake zinaendeleaje?”

“Mmmm vizuri, tuna matumaini anaweza kuchukua kiti cha uraisi”

“Sawa, nenda usije ukamuudhi mwalimu”

Camila taratibu akanibusu mdomoni mwangu kisha akaanza kutembea kueleka kwa mwalimu wake. Hakika Camila ni mzuri kuanzia juu hadi chini. Kiunoni mwake amefungashia makalio makubwa kiasi huku hipsi zake zikiwa zimenona kisawa sawa. Mguu wa bia ndio kabisa umezidi kunichanganya akili yangu.

“Una mwanamke mzuri kaka”

Sauti ya rafiki yangu Frenando ikanistua, nikajikuta nikitabasamu huku nikimtazama usoni mwake.

“Yaaa Mungu amenibariki”

“Tukimaliza masomo hakikisha una muoa?”

“Huo ni mpango uliopo mbele yangu, baba yake ameniahidi akipata kiti cha uraisi basi nitamuoa”

“Naamini nitakuwa msimamizi wako”

“Hahaa hilo wala usijali, vipi leo tunaelekea uwanjani?”

“Yaa ndio nilikuja kukustua twende tukaanze mazoezi”

Nikaondoka na Frenando, rafiki yangu kutoka nchini Mexco. Tumekuwa ni marafiki toka kidato cha kwanza hadi muda huu na uwanjani mwezangu anacheza nafasi ya golikipa huku nami nikicheza nafasi ya mshambuliaji. Tukiwa katikati ya mazoezi, tukamuona mwalimu mkuu akifika uwanjani hapa jambo amlao sio kawaida yake.

“Ethan na Frenando njooni”

Tukatoka uwanjani na kuwaacha wezetu waendele na michezo.

“Natambua kwamba sasa hivi muna jiandaa na masomo yenu ya mwisho, ila nina jambo moja nina hitaji kuwaomba”

Mwalimu mkuu alizungumza huku akitutazama usoni mwetu, nikatingisha kichwa kidogo ikiwa ni ishara ya kumruhusu mwalimu mkuu aweze kuzungumza kile anacho kihitaji kukizungumza.

“Kuna mashindano ya shule za sekondari za bara la Ulaya. Shule yetu ni moja ya shule zilizo chaguliwa kushiriki kugombani kombe hilo. Kuna shule kutoka, Uingereza, hapa Ujerumani, Hispain na kadhali. Ndio shule yetu ina kikosi kizuri cha wachezaji, ila pasipo nyinyi kuwepo hakuna jambo linalo weza kufanyika na sidhani kama shule yetu inafuzu na kufika mbali”

Mwalimu mkuu alizungumza kwa upole sana na ushawishi mkubwa kwani wachezaji wanao soma kidato chetu wote wametolewa katika kikosi cha timu ya shule ili wapate muda mzuri wa kujiandaa na mitihani ya mwisho. Nikamazama Frenando usoni mwake.

“Mkuu hapo inabidi tusaidiane, kama unavyo jua mitihani ya mwisho inavyo kuwa migumu na inahitaji muda mwisngi wa kujiandaa sasa tukishiriki ina maana kuna asilimia stini ya sisi kufeli”

“Una maanisha nini Frenando?”

“Maana yangu ni kwamba inabidi utuhakikishie juu ya kuvujisha mtiani kwa sisi wawili. Nasi tutajitoa kwa ajili ya shule na utapata sifa timu yako kuchukua ubingwa na pili utapata sifa ya wachezaji wako kufaulu kwa kiwango cha juu”

Mwalimu mkuu macho yakamtoka, akavua miwani yake na kujipangusa macho yake kidogo kisha akaivaa tena.

“Hilo ni kosa la jinani na ikijulikana lazima nifungwe na mutafutiwa matokeo”

“Siri itakuwa ni ya watu watatu, mimi wewe na Ethan?”

“Nipeni muda niwee kulifikiria hilo”

“Utakapo kuwa tayari basi nasi tutakuwa tayari”

Mwalimu mkuu akaondoka bila hata ya kuaga na kumfanya Ethan kuangua kicheko cha chini chini.

“Pumbavu, tumemkamata anapenda kujipatia ujiko kupitia sisi na mwisho hatunufaiki na chochote”

Frenando alizungumza huku akiendelea kumsindikiza mwalimu kwa macho.

“Turudi uwanjani”

Nilimuambia Frenando huku nikikimbilia ndani ya uwanja na tukaendelea na mazoezi ya kawaida ambayo tunayafanya kila siku. Baada ya siku tatu mkuu wa shule akatuita ofisini kwake, akatueleza kwamba amekubaliana na makubaliano yetu tuliyo muagiza na atahakikisha kwamba hakuna kati yetu atakaye weza kufeli.

“Kama ni hivyo, anda mashabiki tu”

Frenando alizunugmza huku akinyanyua kwenye kiti alicho kalia na tukatoka ofisini humu. Kitu ninacho mpendea Frenando ni mtu anaye jiamini na huwa hayumbishwi na msimamo wake anao jiwekea. Amekuwa ni msaada mkubwa sana wa kwangu wa kuwakataa wasichana wote wanao mtumia yeye kunisumbua katika swala la mahusiano huku akiamini kwamba Camila ndio mwanamke sahihi kwenye maisha yangu na si hawa wengine wanao nipenda kutokana na pesa pamoja umaarufu wangu.

Wanafunzi wa kidato chetu wakashangaa sana kutuona nasi tumeitwa kwenye kikosi cha timu ya shule. Maswali mengi yakaibuka kwa baadhi ya wachezaji wa darasa letu, ila hatukuweza kuwajibu kitu cha kueleweka huku nasi tukiwaambia hatujui ni kwa nini kocha wa shule ameamua kufanya hivyo. Tukajumuika na wanafunzi wa vidato tofauti tofauti katika kufanya mazoezi na timu ya shule.

“Frenando”

“Mmmm”

“Umepata barua yangu yoyote kutoka kwa shemeji yako?”

“Hapana kwa nini?”

“Aliniahidi kwamba akifika nchini Tanzania atanifahamisha kwamba amefika”

“Labda hajapata simu, si unajua huko alipo kwenda maisha ni tofauti na hapa Ujerumani”

“Ni kweli”

Kocha akatukabidhi ratiba ya nchi tulizo pangwa nzao katika kundi letu hili ambalo ni ‘F’

“Nchi ya kuwa nazo makini sana hapo ni Uingereza na Italy, tukifanya makosa hatuto songa mbele na wezetu wamejiandaa kisawa sawa, kwani wachezaji wao wana vipaji na wana uwezo mkubwa. Ethan wewe ni jicho langu, Frenando wewe ni kifua changu na mulio salia nyinyi ni mikono yangu. Nawaomba musiniangushe, nawaomba mufanye kile munacho paswa kufanya kwa miaka yote ya nyuma kwenye mashindano mengine. Haya ni mashindano mapya kabisa kwa timu za sekondari, hapa ndipo kwa kujiuza nyinyi wewenyewe kwani mameneja na makocha kutoka timu kubwa duniani watakuwa wakifwatilia mashindano hayo ambayo yatarushwa moja kwa moja kwenye televishion. Tulinde heshima ya nchi, na heshima na shule pia. Kwa pamoja tutakiwa kishinda sawa”

Wachezaji wote tukamuitikia kocha wetu kwani amezungumza maneno hayo hadi machozi yanamwagika usoni mwake, ikiashiria kwamba ana uchu na hamu sana ya kutuona vijana wake tunashinda na kuwa timu bora katika bara zima la Ulaya.



Siku iliyo fwata tukaingia kambini rasmi huku kila mmoja akiwa amesha jiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano haya.

“Frenando hembu fanya mpango wa kupata simu ni wasiliane na Camil”

“Poa kaka, ila namba yake unayo?”

“Nitawapigia shuleni kwao, ili waweze kunipatia namba wanayo itumia nchini huko”

“Ingekuwa vizuri ukatumia hiyo simu ya chumbani kwetu kuwasiliana nao?”

“Hizi si zimeunganishwa na hapa hapa hotelini, au zinaweza kutoka nje ya hii hoteli?”

“Sijajua ila ngoja tujaribishe tuone itakavyo”

Frenando, akaingiza namba ya mama yake iliyopo nchini Mexco kwenye simu hii, akaisikilizia kwa muda kisha akatingisha akimaanisha kwamba hii simu haina uwezo wa kutoa simu nje ya hoteli hii.

“Badae tutoroke tuende tukatafute simu mjini”

“Hapana hakuna haja ya kutoroka, tumuombe kocha ruhusa kisha tutoke”

“Tatizo lako Ethan wewe ni muoga”

“Sio uwoga Frenando”

“Ila?”

“Sura yangu kila sehemu inajulikana, umaarufu muda mwengine ni shida”

“Mmmm, ngoja nina mpango”

“Mpango gani?”

“Nina kuja”

Frenando akatoka chumbani humu na kuniacha mimi peke yangu.

‘Mutakwenda kushinda michezo yote ila fainali sijajua’

Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu huku akiwa amekaa kwenye moja ya sofa humu ndani, nikanyanyuka kitandani na kukaa sofa la mbele yake huku tukitazamana.

“Ina maana fainiali hatushindi?”

“Sijajua kwa maana timu ambazo mutaingia fainali zote ni ngumu na kuna hati hati ya nyinyi kuto shinda”

Nikakaa kimya kwa muda huku nikimtazama Ethan kwa maana ni jini ambaye ana nitabiria vitu vingi sana vya mbeleni.

“Tuachane na maswala ya mpira, vipi mpenzi wangu Camila yupo sehemu salama?”

“Ndio, ukizungumza naye leo usiku hakikisha kwamba unamsisitizia haendi nchini Somali”

“Kwa nini?”

“Somali sio nchi salama kwa wao kwenda, kuna matukio ya kila aina ambayo yanaweza kumkuta. Ukiachilia mbali na matatizo hayo, baba yake anagombania kiti cha uraisi, zinaweza kutumiwa njama za kutekwa kwake, kisha baba yake akashinikizwa kuendelea kugombania uraisi na kama unavyo jua siasa za hapa Ujerumani, watu wana misimamo na niwaelewa wa mambo. Mzuie mpenzi wako kwenda huko na hata ikiwezekana apande ndege mara tu ya kumaliza ziara yao nchi Tanzania.”

Nikashusha pumzi taraibu huku nikimtazama Ethan usoni mwake.

“Naamini huto hitaji kukiona kifo cha mpenzi wako, fanya hivyo nilivyo kuambia”

“Nimekuelewa na ninashukuru sana Ethan”

“Karibu”

“Asante”

“Rafiki yako ana kuja ngoja niondoke”

Ethan akapotea kwenye uepo wa macho yangu. Frenando akaingia huku akiwa ameshika mfuko mweusi.

“Ume beba nini?”

“Haya ni makofia ambayo tutavaa tukitoroka”

“Frenando akili yako ipo wapi rafiki yangu. Ninacho taka mimi ni simu na sio makofia”

Nilizungumza kwa kufoka kidogo hadi Frenando mwenyewe akanishangaa kwa maana katika kipindi chote cha urafiki wetu hakunishuhudia siku hata moja nikiwa nimekasirika.

“Ethan kuna jambo lolote baya nililo kufanyia”

“Samahani rafiki yangu. Akili yangu haipo sawa nina hisia mbaya kuhusiana na Camila”

“Hisia mbaya? Hisia gani?”

“Wana ziara ya kwenda nchi Somali wakitoka nchini Tanzania hivyo nahitaji asiende Somali”

“Somali si ndio kule kwenye kundi la Al-Shubabu sijui Al-Shabibi?”

“Ndio huko huko”

“Mmmmm hili swala ni muhimu Ethan, sio la kimapenzi tena ni kweli unatakiwa kumzuia kwenda”

“Ndio hivyo nahitaji simu”

“Twende tukamuombe kocha simu yake, kwa maana sisi si wametuzia kuwa na simu”

Nikamtazama Frenando usoni mwake kwa muda kidogo kisha nikaanza kutembea kuelekea nje, akanifwata kwa nyuma na tukaingia kwenye chumba cha kocha bila hata ya kubisha hodi. Tukamkuta kocha akifanya mapenzi na mmoja wa wahudumu wa hoteli hii ambaye alitopokea kwa bashasha sana.

“Ohoo Mungu. Ethan ndio nini hicho”

Kocha alizunguzma huku akijifunika shuka na muhudumu huyo.

“Waoooo!!”

Frenando alizungumza huku akijawa na tabasamu pana usoni mwake.

“Simu”

Nilizungumza kwa ufupi tu huku nikimtazma kocha usoni mwake.

“Nini?”

“Nataka simu yako”

Nilimfokea kocha kana kwamba ni kijana mwenzangu. Kocha kwa ishara akanionyesha simu yake ilipo ni ndani ya koti la suti yake aliyo kuwa ameivaa. Nikaingiza kiganja kwenye mfuko wa kushoto, ila sikuikuta, ila katika mfuko wa upande wa kulai nikaikuta. Nikaitoa simu hiyo aina ya Samsung S8.

“Mke wako anapiga”

Nilimuambia kocha huku nikimtazama usoni mwake, kwani ni kweli mke wake anapiga simu na ameizima mlio wake ili isisikike pale anapo pigiwa. Kocha akabaki akiwa amenitumbulia macho huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Nikaipoke simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.

“Ndio mama Philipes”

“Nani mwenzangu”

“Ethan mmoja wa wachezaji wa mume wako”

“Ethan Klopp?”

“Ndio”

“Ohoo nafurahi kusikia hivyo mwanangu habari yako”

“Salama tu mama Philipes”

Nilizungumza huku nikiwa nimekazia macho kocha pamoja na muhudumu huyu wa hoteli huko wote wakiwa wamekaa kimya huku miili ikiwatetemeka.

“Yupo wapi kocha wako?”

“Nimetoka na simu yake mara moja na nipo mjini nikirudi nitakufahamisha uzungumze naye”

“Ohoo sawa sawa Ethan, ninafurahi kuzungumza nawe”

“Hata mimi mama nina furahi kuzungumza nawe”

“Sawa nikutakie mchana mwenma”

“Nawe pia”

Nikakata simu na kumtazama kocha na nikamuona jinsia navyo shusha pumzi nyingi. Sikumsemesha kitu chochote zaidi ya kutoka chumbani humu na kurudi chumbani kwetu.

“Ethan umemuachia mzee wa watu hali mbaya”

“Kwa nini?”

“Si tazama jinsi vile alivyo pata wasiwasi mwingi jamani.”

“Hahaaa…..umalaya unamsumbua na anatusisitiza sisi tusiwe na wapenzi sijui anatuona sisi sio watu”

“Anatamatatizo”

Nikaingiza namba ya shuleni kwa kina Camila, nikaipiga simu hiyo. Ikaanza kuita na baada ya sekunde kadhaa ikapolewa.

“St Lilian High school. Mery ninazungumza nani mwenzangu”

“Unazungumza na Ethan Klopp”

“Ohoo habari yako”

“Salama, ninaweza kupata mawasiliano ya mpenzi wangu kwa nchi waliyo kwenda?”

“Tanzania?”

“Ndio”

“Sawa ngoja nikutumie kwa njia ya meseji”

“Nashukuru sana, je wamefika salama?”

“Ndio wamefika salama”

“Naomba msaada wako Mery”

“Usijali Ethan”

Nikakata simu kwani sio mara yangu ya kwanza kuzungumza na sekretari wa shule hii. Haikuisha hata dakika moja meseji ikaingia ikiwa na maelezo ya namba ambayo inatumiwa na uongozi walio ongozana nao kwenye safari hiyo nchini Tanzania.

“Duu kumbe nchi ya Tanzania code namba yake ni +225”

Nilizunugmza huku nikimuonyesha Frenando namba hiyo

“Wemechelewa sana kupata huduma za simu”

“Yaaa”

Nikaingiza namba hiyo, ila nikapewa taarifa kwamba simu hii haina salio la kutosha, niongeze tena kisha nipige tena.

“Kocha mzima hana salio kwenye simu yake”

“Mmmm sasa tunafanyeje?”

“Inabidi tutoke tukanunue”

“Umeona sasa”

Frenando akanikabidhi moja ya kofia aliyo nunua. Tukatoka chumbani kwetu na kufunga mlango wetu na kuondoka. Tukaanza kuzunguka mitaani huku ni baadhi ya watu wachache sana ambao waliweza kutugundua na wengine walituomba waweze kupiga picha nasi. Tukaingia kwenye moja ya duka la kununu simu, nikatia kadi yangu ya malipo ambayo ina kiasi cha kutosha na sehemu yoyote katika nchi hii ya Ujerumani, nina weza kuitumia kununua kitu cha ina yoyote ile na katika duka lolote.

“Tununue simu zetu na tumrudishie yule mwehu simu yake”

Nilizungumza huku tukizunguka katika duka hili ambalo simu zote zilizomo humu ndani ni simu za garama sana. Kila mtu akanunua simu yake, tukasajiliwa laini zetu kama kanunu na taratibu za nchi hii. Tulipo maliza maunuzi yetu tukaingia kwenye moja ya mgahawa, tukanunua vyakula na vinywaji kisha tukarudi hotelini.

“Shika mrudishie simu yake”

Frenando akachukua simu ya kocha na kumpelekea chumbani kwake, nikaipiga namba niliyo kabidhiwa na sekretari. Namba hiyo ikaanza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.

“Habari yako?”

“Salama, ninaitwa Ethan Klopp ninahitaji kuzungumza na Camila Marco”

“Ohoo hivi sasa ni usiku sana, labda kukipambazuka atakutafuta”

“Sawa sawa mwalimu, ila ana endeleaje?”

“Anaendelea vizuri tu ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli”

“Asante basi kukipambazuka utanifahamisha”

“Sawa Ethan”

Nikakata simu huku nikiwa na faraja kuba sana moyoni mwangu, kwani mwalimu huyo aliye pokea simu ni mlenzi wao kwa upande wa wanawake.

“Vipi umesha zungumza naye?”

Frenando alizungumza huku akiingia ndani ya chumba hichi

“Ndio ila kule ni usiku amepokea matron wao”

“Ahaa, hivi sasa na huko masaa huwa yana pishana sana ehee?”

“Ndio ila sijajua yanapishana kwa masaa mangapi mangapi”

Tukapata chakula cha mchana. Jioni tukaelekea katika viwanja vya karibu kabisa na hoteli hii kwa ajili ya mazoezi ya hapa na pale.

“Ethan na Frenando nina waomba”

Kocha alituita mara baada ya kumaliza mazoezi, tukasimama mbali kidogo na basi letu la timu.

“Naamini mumeona kilicho tokea mule chumbani”

“Ndio”

“Ninawaomba iwe siri yenu. Ninaomba musiweze kuitoa siri hiyo kwa mtu yoyote”

Kocha alizungumza kwa msisitizo huku akitutazama kwenye nyuso zetu.

“Mke wako ana kasoro gani?”

Nilimuuliza kocha kwa upole sana huku nikimtazama usoni mwake.

“Ethan”

“Usiseme Ethan kocha. Tambua nimebeba dhambi kubwa sana ya kumdanganya mke wako. Je dhambi hiyo mimi nina ilipaje eheee?”

“Ethan natambua nyinyi bado ni wadogo, ila muikingia kwenye ndoa mutaweza kujua ni nini kinacho tokea hadi wanaume tunaamua kuwa na wake wa nje”

“Wacha weeee”

Frenando alizungumza kwa kejeli huku akimtazama kocha usoni mwake. Gafla simu yangu ikaanza kuita ikiwa ndani ya kibegi changu mgongoni. Kocha akatoka na macho ya hasira kwani moja ya sheria tukiwa kambini ama shuleni haturuhusiwi kuwa na simu.

“Ethan kwa nini una simu?”

Kocha aliniulza kwa kunifoke sana.

“Acha upuuzi wewe mzee. Muache apokee simu la sivyo tunakwenda kuzungumza uchafu wote kwa mke wako na ushahidi wapicha ninao”

Frenando alizungumza kwa kujiamini na kumfanya kocha kukodolea macho na kukosa jambo la kuzungumza kwa muda huu.



Nikamtazama kocha kwa muda kisha nikachukua simu yangu ndani ya kibegi na kukuta ni namba kutoka nchini Tanzania. Nikaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwangu.

“Haloo”

“Ethan”

“Niambie mke wangu”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na furaha sana huku nikiondoka katika eneo hili na kumuacha Frenando na kocha.

“Safi Ethan wangu, samahani sana kwa kushindwa kuweza kuzungumza nawe mpenzi wangu baada ya kufika”

“Usijali mpenzi wangu, ila si mumefika salama?”

“Ndio tumefika salama na asubuhi ya leo tutaanza rasmi ziara yetu ya kimasomo”

“Sawa mpenzi wangu ila ninahitaji nikuombe kitu kimoja”

“Kitu gani tena mpenzi wangu?”

“Utanikubalia?”

“Ndio mpenzi wangu nitakukubalia wewe ni mume wangu lazima ninacho kuomba niweze kukubalia.”

“Ni jambo gumu lakini”

“Niambie tu Ethan, kumbuka mimi nipo kwa ajili yako mume wangu”

“Nakuomba mukimaliza ziara yenu nchini Tanzania, usiende nchini Somalia”

“Kwa nini?”

“Nahisi kuna hali ya hatari itakwenda kuwatokea huko mpenzi wangu”

“Usijali mume wangu, hapa nilipo tu kuna walinzi walitangulia wiki moja kabla ya kuja nchini hapa Tanzania kwa ajilli ya kunilinda na hata huko Somalia walisha tangulia walinzi kama mia moja hivi. Wapo kwa akili yangu mume wangu”

Camila alizungumza kwa kujiamini sana na kunifanya nishushe pumzi taratibu huku nikifikiria cha kumuambia.

“Usiwe na wasiwasi Ethan wangu, tamua nina lindwa sana na hakuna wa kuniletea ubaya wa aina yoyote sawa mume wangu”

“Sawa ila nakuomba ikiwezekana usiende”

“Usijali nitakuwa nikikujulisha kwa kila hatua ambayo nina fikia”

“Sawa mke wangu”

“Ngoja nijiandae kesho nitakupigia mchana tukiwa tuna rudi”

“Sawa sawa”

Camila akakata simu na taratibu nikashusha pumzi na kurudi alipo simama Frenando.

“Mzee wako anatetemeka, amesha ingia ndani ya gari”

“Kwani ushahidi wa picha unao kweli au?”

“Ndio cheki hizi hapa”

Frenando akanionyesha picha za kocha na muhudumu wa hoteli jambo lililo ishangaza sana.

“Umezipiga piga vipi?”

“Muda ule nilivyo mrudishia simu, niliingia kwa kunyata ndani kwao papiso wao kujijua kwani walikuwa wapo katikati ya dimbwi la mapenzi basi nikawapiga picha za kutosha kisha nikawastua”

Tulizungumza huku tukiingia kwenye basi la wachezaji wezetu. Safari ya kurudi hotelini ikaanza taratibu huku kocha wetu akiwa amekaa siti ya mbele kabisa akionekana sio mtu mwenye furaha kabisa.

“Frenando futa hizo picha”

“Kwa nini?”

“Isije baadae zikaleta matatizo si unajua tupo kwenye kipindi cha mashindano na mwalimu anahitaji furaha na akili yake iweze kutulia ili aweze kufanya kazi yake kwa umakini”

“Sasa Ethan unahisi huyu katika makocha kweli ni kocha. Tunacho kifanya uwanjani ni juhudi zetu tu. Acha kwanza tumpe tumbo joto akipata akili basi atanitafuta na kukaa nami kwa upole na kuniomba msamaha”

“Msamaha wa nini tena?”

“Si unamfahamu yule mwanaye wa kike?”

“Ndio”

“Mzee alinichimba biti siku moja, sikutaka kukuambia tu. Akaniahidi akiniona naye atanipiga risasi”

“Weee”

“Ndio hataki niwe mkwe wake”

“Ila vipi mwanaye anakupenda?”

“Ndio ananipenda, na hata yeye anajisikia vibaya sana juu ya baba yake kutukataza kuwa katika mahusiano”

“Duuu”

“Yaa mzee analeta swaga eti mimi Mmexco siwezi kumuoa Mjerumani”

“Ana wazimu, kwa hiyo mimi Mtanzania nisioe Mjerumani?”

“Ndio maana yake”

“Poa endelea kuzishikilia ila hakikisha kwamba simu yako hupotezi wala hakuna mtu mwengine wa kuziona”

“Poa poa”

Tukafika hotelini, tukaingia kwenye vyumba vyetu vya kulala. Tukaoga kisha tukaijiandaa kwa chakula cha usiku, ambacho tunakula kwa pamoja na siku inayo fwata tunaanza mechi yetu ya kwanza. Tukiwa katika eneo la chakula, kocha hakuwa na furaha kabisa. Hata mipango ya kupanga kesho tucheze mfumo gani kocha hazungumza kabisa jambo ambalo lilianza kuwashangaza hadi wachezaji wengine kwani si kawaida yake, kwani katika kipindi cha nyuma huwa hutumia muda wa chakula kuweza kupanga mipango na sisi wachezaji wake.

“Ethan”

“Mmmm”

“Hembu mfwate kocha kwa maana anaonekana hayupo sawa”

Mchezaji mmoja aliniambia kwa upole huku akinitazama usoni mwangu.

“Sawa”

“Tunakutegemea Ethan kumbuka wewe ndio timu kapteni”

Nikanyanyuka na kumfwata kocha alipo kaa, nikavuta kiti cha pembeni na kukaa huku nikimtazama usoni mwake.

“Kocha kuna tatizo gani?”

Kocha akanitazama kwa muda kisha akashusha pumzi nyingi.

“Kuna mambo ninatafakari”

“Mambo gani kocha, unaweza kunishirikisha”

Kocha akaingiza mkono mfukoni na kutoa karatasi nyeupe na kunikabdhi. Akanyanyuka kwenye kiti alicho kikalia na kunitazama.

“Hakikisha unawapa maelekezo wezako juu ya mchezo wa kesho”

Kocha baada ya kuzungumza hivyo akaondoka na kuniacha nikimsindikiza kwa macho. Nikafungua karatasi hii na kuoona ikiwa imeandikwa mfumo wa jinsi gani tunavyo takiwa kucheza kesho nani aanze na nani apumzike. Nikaikunja vizuri karatasi hii na kuiweka mfukoni mwangu.

“Mukimaliza kula tukutane chumbani kwangu wote”

“Sawa”

Wachezaji waliitikia kwa pamoja huku wakionekana kujawa na furaha.

“Dokta hembu kazungumze na kocha tujue ana sumbuliwa na nini?”

“Alisha nieleza anahitaji muda wa kupumzika kidogo ndio maana nilimuacha akae peke yake”

Kocha wa timu alinijibu huku akinitazama usoni mwangu.

“Kocha msaidizi anakuja lini?”

“Kesho asubuhi”

“Sawa”

Nikamfwata Frenando alipo kaa.

“Mzee sijui ni wewe ndio umemchanganya?”

“Kivipi?”

“Si umemuona leo alivyo nyeshewa na mvua”

“Ohoo pale nahisi anafikiria juu ya makubaliano tuliyo wekeana”

“Yapi tena?”

“Mara moja hii umesha sahau”

“Niambie”

“Nimemuambia, anipe mwanaye kiroho safi nami nifute picha hizi la sivyo tuna haribiana”

“Hiyo unahisi ni njia sahihi ya kuanzisha mahusiano na baba mkwe wako?”

“Ethan kuna njia gani nyingine zaidi ya hiyo. Mimi nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kwamba mzee ananikubali, ila wapi. Hata golini ninavyo jituma nisifungwe magoli, si kwamba ni kwaajili ya timu hapana. Nikwaajili yake, ili aone kwamba mkwe wake nina muhitaji mwanaye ila ananiletea upuuzi tu”

Frenando alizungumza kwa msisitizo mkali huku akinitazama usoni mwangu.

“Achagua moja tu, mtoto kunikabidhi au nizimwage kwenye mtandao na ikitokea nimeziachia kwenye mtandao basi ukocha anapoteza, ndoa inakufa. Hata huyo mwanaye anaye hisi kunibania pia atamkosa na kiulaini nitamchukua mwanaye”

Nikamtazama Frenando kwa muda kidogo jinsi anavyo ipanga mipango yake, nikajikuta nikicheka mwenyewe.

“Nini kinacho kuchekesha?”

“Mipango unayo ipanga ni ya mbali sana pasipo kufikiria madhara kwa upande wako”

“Upande wangu madhara yake yapo vipi?”

“Tambua akiamua kukufungulia hatua za kisheria anaweza kukufunga”

“Wapi, ana ushahidi gani kwamba mimi ndio nimefanya tukio hilo na akitaka kunistaki usihisi kwamba nitabaki mwenyewe”

“Una maana gani?”

“Wewe ni rafiki yangu naamini watakuchunguza na wewe wakiamini huu ni mpango wetu sisi wawili, ila ni wangu mimi kama mimi. Natambua kwamba wewe una makampuni mengi sana, sasa hii inaweza kuleta skendo kubwa kama mmiliki wa makampuni amehusika kwenye urushaji wa picha za nguno mtandaoni”

Maneno ya Frenando kidogo yakanistua sana na kunikasirisha kwa kiasi ila nikajaribu kuizuia hasira yangu kwa kutabasamu huku nikimtazama usoni mwake.

“Nakutania bwana Ethan, siwezi kukuhusisha katika maswala yangu haya ya kipuuzi. Kumbuka mama yako ni waziri mkuu Mexco hata likitokea la kutokea, kesi itakwenda kufunguliwa Mexco na si hapa”

“Sawa, maliza kula twende chumbani”

“Sawa kapteni”

Nilipo hakikisha kwamba wachezaji wezangu wote wamepata chakula, tukaelekea chumbani kwangu. Kutokana vyumba vyetu ni vikubwa, wachezaji wote waliweza kuenea ndani ya chumba hichi.

“Habari zenu”

“Safi kapteni”

“Kesho ndio tunaanza michuano yetu rasmi. Tukumbuke kwamba tuna maadui wengi sana kwenye haya mashindano. Maadui ambao wapo tayari kuhakikisha kwamba timu yetu inatoka mapema sana kadri wao wanavyo amani.”

“Ushikamano wetu, muunganiko wetu. Ujasiri wetu na kujituma kwetu ndio misingi kamili ya kuwaangusha maadui. Tumezoeleka kuwa na mifumo minne ya kimichezo. Mifumo ambayo makocha wengine wa timu nyingine ni lazima watakuwa wamesha ifanyia kazi na kujua ni nani na nani ambaye atakabwa ili timu isitembee”

Nilizungumza kwa upole huku wachezaji wezangu wote wakinisikiliza kwa umakini sana. Nikatoa karatasi ambayo alinikabidhi kocha nikaifungua mbele yao na kumkabidhi mmoja wao ili atazame nini kilicho andikwa na kocha kisha amkabidhi na mwenzake.

“Tutazame haraka haraka hiyo mifumo ndugu zangu”

Karatasi hiyo ikaendelea kupita kwa kila mchezaji na hadi mwisho ikarudi kwangu.

“Mfumo huo alio panga kocha, unafahamika sana kwa kila mmoja wetu. Pia kwa wachezaji wa timu pinzani. Jambo ambalo litatusababishia kutumia nguvu nyingi sana katika kutafuta magoli na inawezekana pia tukashindwa kupata magoli.”

“Ninahitaji mfumo ubadilike. Sisi sote humu ndani kila mmoja anaweza kucheza nafasi zaidi ya mbili si ndio?”

“Ndio”

“Tuachane na mfumo wa 4, 4,2 tucheze mfumo wa 4,3,1,2”

“Mchezo huu utawawezesha viungo kumpa mipira Lukas. Lukasi utasimama hapo kwenye moja, na kutokana una nguvu, kasi na unaweza kukaa na mpira muda mrefu, kazi yangu mimi na Pilo itakuwa ni kupokea mipira kutoka kwako na mipira usiilete kwa njia ya pasi za chini, wataizuia sana. Ilete kwa pasi za juu. Mimi ninaweza kuruka na kuichukua hata Pinto ni hivyo hivyo. Mabeki naamini munafahamu kazi yenu. Apite mtu mpira ubaki au upite mpira mtu abaki. Nyinyi viongo wa katikati, kazi yenu ni kuhakikisha Lukas anakuwa huru, kabeni watu wasielekee kwa mabeki. Kipa, sina wasiwasi na Frenando. Mumenielewa jamani”

“Ndio kapteni”

Wachezaji wezangu wakapiga makofi wakionyesha kukubaliana nami katika hili nilio waambia.

“Mwenye swali?”

“Kampteni je mfumo huu ukituwia ugumu tunafanyaje?”

“Tutakuwa tunabadilisha mifimo ya uchezaji kila baaada ya dakika kumi. Tuanze na mfumo wa kawaida wa 4,4,2 kisha tutabadilika kadri mchezo unavyo zidi kwenda. Kikubwa ninacho kitegemea ni kasi, na Pinto yake mambo yako ya ubishoo wa kupiga chenga ukiwa golini ukitegemea penati sitaki kuyaona. Ukifika golini piga shuti golini, na kipa atajuana yeye mwenyewe na mpira wake. Sijui umenielewa Pinto?”

“Nimekuelewa kocha”

“Weweee mimi sio kocha ni kapteni”

Kauli yangu ikawafanya wanafunzi wachezaji wezangu kucheka. Gafla mlango wetu ukafunguliwa na sote tukastuka, akaingia daktari wa timu huku akionekana kujawa na wasiwasi.

“Kuna nini?”

“Njooni kocha amejinyonga”

Kauli ya daktari ikatufanya tutoke humu ndani kwa kasi sana na kikimbilia chumbani kwa kocha, kitendo cha kuingia ndani humu nikajikuta miguu ikiniishia nguvu kabisa kwani ni kweli kocha amejinyonga bafuni kwenye bomba kubwa la maji kwa kutumia tai yake.



Tukiwa katika hali ya sinto fahamu, akaingia meneja wa hoteli hii huku akiwa ameongozana na baadhi ya wafanyakazi wa kiume. Wakaanza kufanya juhudi za kumtoa kocha kwenye bomba hilo, wakafanikiwa na kumlaza kocha sakafuni, daktari akainama na kuweka sikio lake katika kifua cha kocha, akatutazama.

“Bado mapigo yake ya moyo yanadunda”

Daktari alizungumza huku akianza kuminya kifua cha kocha. Wakaingia madaktari wakiwa na machela, wakampakiza kocha juu ya kitanda hicho, wakamfunga mikanda ya kitanda hicho ili asipate mitikisiko. Wakamuwekea mashine maalumu ya kupumulia na kuanza kukisukuma kitanda hicho kuelekea katika lifti za gorofa hili. Mimi na wachezaji wezangu tukaingia kwenye lifti nyingine na tukaanza kuelekea chini. Tukafika chini na kukuta madaktari wakimuingiza kocha kwenye gari la wagonjwa na kuondoka naye katika eneo hili huku gari hiyo ikiwashwa ving’ora vya kuashiria hatari. Gari mbili za polisi zikafika katika eneo hili la hotelini. Wakashuka askari kumi na kuelekea katika chumba ambacho kocha alijinyonga.

“Nani kiongozi wenu hapa”

Mmoja wa askari alizungumza.

“Mimi”

Nilijibu huku nikimtazama askari huyu usoni mwake na kwa kujiamini.

“Unaweza kutuambia ilikuwaje?”

Nikashusha pumzi taratibu ili kuyarudisha mapigo yangu ya moyo kwenye mfumo wake wa kawaida, kwani wasiwasi na woga ndivyo vilikuwa vimenitawala.

“Tulikuwa chumbani kwangu na wachezaji wenzangu, daktari yeye ndio aliye kuja kutuita na kutuambia kwamba kocha amejinyonga”

“Daktari gani?”

“Daktari wetu wa timu”

“Anaitwa nani?”

“Ruben”

Kila nilicho kizungumza askari huyu anakiandika kwenye kijikitabu chake kidogo.

“Daktari yuppo wapi?”

“Amepanda gari la wagonjwa na ameambatana na mgonjwa”

“Sawa, wakusanye wezako ili tuweze kuwahoji mmoja baada ya mwengine?”

“Maeleo ambayo wao watakupa ndio niliyo kupa mimi, unavyo hitaji niwakusanye kwa pamoja ni kuzidi kuwapa presha na isitoshe kesho tuna mechi ya kwanza mchana. Sinto penda wachezaji wezangu wazidi kupatwa na presha”

Nilizungumza kwa kujiamini sana hadi askari huyu akanikodolea macho ya mshangao.

“Naomba ufanye hivyo kwa maana ni mahojiano ya kawaida kabisa”

Nikashusha pumzi huku nikitabasamu kidogo, nikaingia chumbani kwangu na bahati nzuri nikawakuta wachezaji wezangu wote. Frenando akanifwata huku mwili mzima ukimtetemeka.

“Ethan naogopa”

“Unaogopa nini?”

“Mimi naweza kutiwa hatiani kwa tukio hili?”

“Hakuna kitu kama hicho kwani wewe ndio ulimpa tai ajinyonge?”

Niliendelea kuzungumza kwa kujiamini japo kwa namna moja ama nyingine nami nina wasiwasi mwingi sana na kama ni kweli Frenando atahisiwa juu ya picha za nguno alizo mpiga kocha basi matatizo yanaweza kuwa makubwa sana.

“Futa picha hizo kwenye simu yako na ikiwezekana simu pia iviunje kabisa”

Nilizungumza kwa sauti ya chini sana pasipo wachezaji wengine kuweza kusikia na wote kila mmoja yupo katika hali ya majonzi na mashaka.

“Polisi wanahitaji kufanya mahojiano na sisi hivyo naomba mujiandae kila mmoja akajibu kitu sahihi kama atakavyo ulizwa. Mumenielewa?”

Wachezaji wezangu wakaanza kulalama huku wengi wao wakitetemeka. Hali hii ikaniogopesha sana kwa maana kesho ndio siku ambayo tunatakiwa kucheza mechi yetu ya kwanza na hali ndio kama hivi.

“Hei nawaomba mutulie musiwe na wasiwasi wa aina yoyote kila kitu kitakwenda kuwa sawa. Mumenielewa?”

Hapakuwa na mchezaji aliye weza kunijibu, nikafungua mlango na kuwatazama askari watatu ambao wananisubiria mlangoni hapa.

“Nitahitaji mutakapo wahoji wachezaji wangu, mimi mwenyewe niwepo?”

“Hilo sio jukumu lako kuwepo, tunacho hitaji ni kuzungumza na wacheji mmoja baada ya mwengine”

“Nimezungumza hivyo nikiwa nina maana kubwa sana na kama mutashindwa kukubaliana nami basi sinto ruhusu mchezaji wangu hata mmoja kuhojiwa na mahijiano mutayafanya pale atakapo kuja mwanasheria wa shule au mwalimu mkuu sawa”

Kujiamini kwangu kidogo kukateteresha msimamo wa hawa maaskari ambao walisha kazana kumuhoji mchezaji mmoja baada ya mwengine.

“Sawa”

“Mahojiano yatafanyika kwenye moja ya chumba ambacho wachezaji wangu wanakaa, tena chumba hicho hapo mbele yangu”

Nilizungumza huku nikiwaonyesha chumba kinacho tazamana na chumba changu.

“Tungehiji majina ya wachezaji wako yote”

“Nendeni mapokezi, mutaweza kuona majina hayo”

Majibu yangu dhairi yakaonyesha kuto wapendeza hawa askari. Tukamuona mkuu wa shule na mwanasheria wakifika katika eneo hili. Wakasalimiana na askari hawa na kuanza mazungumzo yao ambayo sikuhitaji kuyasikia kwani ninacho kihitaji hivi sasa ni akili ya vijana wangu kuweza kuwa sawa.

“Jamani mahojiano yamesimama kwa muda, ila nina jambo ninahitaji kuzungumza nawe, naomba tukusanyike”

Wachezaji wezangu wakanitiia na wote wakaanza kukusanyika na kunizunguka.

“Frenando yupo wapi?”

“Bafuni”

“Samahani nisubirini”

Nikapita katikati ya wezangu hadi bufani, nikamkuta Frenando akiwa amekaa kwenye sinki huku akilia kwa uchungu sana. Nikamtazama kwa muda kisha nikachuchumaa mbele yake.

“Hei Frenando”

 


“Mmmm”

“Unalia nini rafiki yangu”

“Ethan ninakwenda jela mimi”

“Nisikilize kitu kinacho itwa jela hivi sasa fanya kukisahau. Kumbuka kwamba hujahusika kwenye jambo la aina yoyote ile. Kumbuka kwamba maamuzi ya kujinyonga ni ya mtu mwenyewe na bahati nzuri kocha hajakufa, na hawezi kukutaja wewe katika hili swala kwamba umehusika na tukio lake. Umenielewa”

Frenando akaka kimya huku akinitazama usoni mwake.

“Pia mimi rafiki yako nina pesa, nitahakikisha hakuna jambo lolote ambalo linaweza kutoka kwenye maisha nakuahidi hivyo”

“Kweli Ethan”

“Niamini mimi rafiki yangu, ninaapa kwa jila la mwenyezi Mungu siwezi kukuacha upate matatizo.”

Frenando akanikumbatia kwa furaha sana huku akijipangusa machozi usoni mwake.

“Njoo tuwape wezetu mioyo ya kucheza mechi ya kesho. Ukiwa na huzuni wewe unahisi mimi nitafanya nini kwa hawa wachezaji. Tafadhali Frenando”

“Sawa kaka nimekuelewa”

Frenando akasimama nami nikasimama, tukakumbatia kwa sekunde kadhaa.

“Ulifuta zile picha?”

“Ndio na simu nimeivunja vunja na kuidumbukiza huku chooni”

“Sawa”

Tukatoka chumbani humu na kumkuta mkuu wa shule akizungumz ana wachezaji. Tukajisogeza katika eneo hilo.

“Kocha wenu ndio kama hivyo amepata matatizo hakuna haja ya kuendelea kuwemo katia mashindano haya ni vyema tukakubaliana kwa pamoja, mujitoe na mutashiriki mwakani. Hali zenu hapa wote mumejawa na wasiwasi mwingi sana. Ili kuto itia shule na taifa aibu basi ni vyema musishiriki”

Maneno ya mkuu wa shule yakanikere sana na kujikuta nikikatiza katikati ya wachezaji wezangu na kusimama mbele yake.

“Kwani kocha ndio anacheza uwanjani?”

Nilimuuliza mwalimu mkuu huku nikimkazia macho.

“Kocha ndio kiongozi wa timu sasa nyinyi kama nyinyi mutafanya nini?”

“Mkuu nakuomba katika timu yangu usiweze kuendelea kuzungumza ujinga na upuuzi wa kuwakatisha tamaa wachezaji wangu. Rudisha tumbo lako shuleni kule ukakae na walimu wezako mkacheke cheke. Sawa”

Mwalimu mkuu akanitazama kwa hasira kwani maneno niliyo yazungumza yana udhalilishaji ndani yake kwani ana kitambi kikubwa.

“Niachie timu hii nitaiongoza mimi mwenyewe na nitahakikisha kwamba siku moja inaweka heshima katika nchi hii na dunia. Huna taaluma ya kuongoza mpira sawa”

“Ethan tazama kinywa chako”

“Siwezi kutazama kinywa changu kwa ujinga na uzembe unao zungumza. Mimi hapa ni timu kampteni na sio mwalimu mkuu na sizungumzi kama Ethan, nazungumza kama kiongozi wa wezangu. Kama wao wamekuogopa kuzungumza kile wanacho kihisi katika mioyo yao, basi mimi nitakuambia ukweli kwanza ninakuomba uweze kutoka humu ndani”

“Unanifukuza?”

“Sikufukuzi, ila hatukuhitaji humu ndani”

“Sasa ninapiga simu kwa waandaaji wa hii michezo na ninawambia timu yangu inajitoa na wachezaji wangu haw…….”

Kabla ya mwalimu mkuu kumaliza kuzungumza jambo lolote nikajikuta nikimkaba kooni mwake na kumsukomia hadi ukutani na kumkazia machohuku nikiendelea kumtazama kwa hasira sana hadi wachezaji wezangu wakashangaa.

“Kwenye maisha yangu sipendi kuyumbishwa, sipendi mwanaume asiye jiamini kwa maamuzi yake. Uliamua timu ije kwenye michuano na si timu ije kuyumbishwa na mpuuzi mwenzako aliye jinyonga na kuanzia hivi sasa hatuhitaji kocha wa aina yoyote. Nitasimama kama kocha mchezaji umenielewa?”

Nilizunugmza huku nikiendelea kumkaba mwalimu mkuu koo lake, akatingisha kichwa akimaanisha kwamba amenielwa, nikamuachia taratibu na kumfanya anza kukohoa sana huku akihema kwani kama ningeongeza dakika mbili katika kumkaba koo lake basi angepoteza maisha.

“Potea ndani ya chumba chetu”

Mwalimu mkuu akatia amri niliyo muamuru na akatoka chumbani kwangu na kuwafanya wachezaji wangu wote kupiga makofi.

“Hatuwezi kuyumbishwa, sisi ni wanaume na hakuna mwanamke humu ndani, hakuna mseng** humu ndani. Tukiachana na swala zima la kuleta heshima ya shule, ila tucheze kwa ajili ya heshima zetu sisi wenyewe. Kesho na kesho kutwa tutajenga historia yetu sisi wenyewe. Historia ambayo haito jengwa na mwalimu mkuu, bali ni kwa juhudi zetu sisi wenyewe. Mawazo juu ya kocha yapotee, tufikirie mechi ya kesho na hata kocha msaidizi akifika kesho alfajiri hakuna haja ya kumpa nafasi ya kuvuruga kile tulicho kipanga. Mumenielewa?”

“Tumekuelewa kiongozi”

Nikanyoosha mkono wangu wa kulia katikati ya duara hili tulilo zunguka na kila mchezaji akanyoosha mkono wake na tukaiweka kwa pamoja ikiwa ni ishara ya mshikamano wetu na umoja wetu.

“Mechi ya kwanza hadi ya mwisho, tuhakikishe kwamba tunachezwa kwa ajili ya kuchukua kombe. Kila mmoja acheze kwa uwezo wake wote anao jua yeye. Siku moja mutanikumbuka mukiwa katika klabu kubwa za mpira. Hakuna siri ya mafanikio kama kujituma kwa juhudi pasiopo kukata tamaa. Mumenielewa?”

“Tumekuelewa kapteni”

Tukaachanisha mikono yetu. Nikawaruhusu wachezaji wote kwenda kulala. Nikajaribu kumpigia Camila ila nikakuta simu haipatikani.

“Hivi kocha alikuwa anafikiria nini hadi kujinyonga?”

Frenando aliniuliza huku akiwa amelala kwenye kitanda chake.

“Sifahamu kwa kweli. Ila kuna mambo yake mengine aliniambia kwamba anayatafajari, nahisi hayo ndio yamempekekea kuwa katika hali aliyo kuwa nayo”

“Mmmm, Mungu amsaidie apote tu”

“Ni kweli”

“Poa Ethan usiku mwema”

“Nawe pia ndugu yangu”

Nikajifunika shuka langu na kulala usingizi fofofo.

***

Muda wa kueleka katika uwanja ambao ndio zinafanyika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya kombe la bara la Ulaya kwa shule za sekondari. Kila mchezaji akabeba kifaa chake anacho hitaji kwenda kukitumia uwanjani.

“Ethan nakuomba”

Koch msaidizi aliniita kabla ya kuingia ndani ya basi. Tukasimama pembeni ya basi hili na kuwaacha wachezaji wengine waendelea kuingia ndani ya basi.

“Ndio kocha”

“Mfumo ambao umekubaliana na wezako kweli mutaweza kuuhimili uwanjani kwa maana timu munayo kwenda kukuata nayo inacheza mfumo wenu?”

Kabla sijamjibu kocha simu yake ikaingia meseji. Nikaa kimya huku nikimtazama kocha anavyo soma meseji hiyo. Akashusha pumzi huku akinikabidhi simu simu yake ili niisome meseji hiyo.

‘Shule haito husika kwa chochote kwenye swala la mshahara wako wa ukocha, malezi na matumizi ya timu yako la sivyo jiudhuru ukocha tumuachie huyu mpumbavu timu tuoneka kama ataweza kuiongoza. Bili ya hotelini, leo ndio itakuwa siku yenu ya mwisho kukaa, nimeisitisha na muthithubutu kurudisha miguu yenu kwenye hiyo hoteli sawa Robert’

“Kocha ni nani huyu?”

“Mwalimu mkuu wenu”

Nikajikuta nikiachia msunyo mkali sana kwani sijui ni kitu gani mwalimu mkuu huyu anakifikiria kwenye ufahamu wake wa akili hadi kuamua kumshinikiza kocha kuacha ufundishaji wa timu hii.



ENDELEA

“Usijali, nakuomba usimueleze mchezaji yoyote kuhusiana na hili swala. Ngoja niwasiliane na dada yangu ili aweze kushuhulika na hili swala”

“Sawa”

“Ila ushindi wowote utakao patikana asilimia hamsini itakuwa yangu na zifwatazazo zitakuwa kwa ajili ya timu na hakuna hata asilimia itakayo ingia kwenye akaunti ya shule umenielewa?”

“Nimekuelewa”

Tukaingia kwenye gari na nikakaa kwenye siti aliyo kaa Frenando.

“Vipo kocha anasemaje?”

“Ngoja tutazungumza tukipata muda”

“Sawa”

Nikatoa simu yangu mfukoni na kuingiza namba ya dada Mery kisha nikampigia. Simu yake ikaanza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.

“Ethan”

“Naimbie dada yangu”

“Safi, nasikia upo kwenye kiosi cha timu ya shule yako”

“Ndio dada. Upo wapi?”

“Mimi ndio ninajiandaa kutoka hospitalini hapa. Vipi?”

“Kuna jambo moja nahitaji kukuomba unisaidie”

“Zungumza tu mdogo wangu”

“Nahitaji uniwekee oda kwenye hoteli nzuri, nina idadi ya wachezaji ishirini na mbii pamoja na kocha mmoja”

“Ahaa sawa hilo halina shida kuna la ziada?”

“Hapana ni hilo tu, ila hoteli iwe ya kimichezo, viwepo viwanja vya michezo”

“Sawa sawa, nimekuelewa ndani ya dakika tano nitakupatia jibu lako”

“Poa”

Nikakata simu kisha nikasimama katikati ya basi hili, wachezaji wezangu wote wakanitazama.

“Naomba tusikilizane ndugu zangu”

“Kunzia hivi tunavyo toka hivi sasa. Hatuto rudi kwenye hoteli hiyo. Moja ni kutokana na maswala ya usalama wetu kwani kwa tukio la jana nina imani kila mmoja wetu emekuwa ni mtu mwenye wasiwasi na mashaka. Tumeamua kutafuta hoteli nyingine kwa garama zangu, na kila huduma ambayo timu kama timu itahitaji basi nipo tayari kugaramia”

Wachezaji wezangu wote wakapiga makofi na kushangilia

“Ngoja niwaeleza kitu kimoja. Ninawapenda sana”

“Hata sisi tunakupenda kapteni”

“Tunakwenda kupambana na tuhakikishe kwamba tunashinda sawa jamani”

“Sawa”

Wachezaji walitikia na mmoja wao akianzisha nyingo za kushangilia. Gari likafurika kwa shangwe huku kila mchezaki akipata munkari wa kwenda kucheza mechi iliyopo mbele yetu. Simu yangu ikaanza kuita, nikaipokea kuiweka sikio la upande wa kuhosto huku na nikiziba sikio la upande wa kulia ili niweze kumsikiliza dada Mery atazungumza kitu gani.

“Mbona makelele?”

“Utawaweza wachezaji, niambie umefanikiwa?”

“Ndio nimefanikiwa kupata hoteli moja ila ipo nje ya mji, ina kila sifa ulizo zihitaji”

“Hembu nitumie picha zake”

“Sawa, mechi munaanza kucheza saa ngapi?”

“Mida ya saa kumi na moja jioni”

“Ahaa sawa, nitafanikiwa kuiwahi kwa maana hivi sasa ninaelekea kwenye hiyo hoteli na wamehitaji kulipwa dola elfu ishirini na tano kwa siku”

“Sawa hilo halina tatizo, kikubwa iangalie na kama ipo vizuri muambie muhasibu atoe pesa hiyo kwenye akaunti yangu”

“Poa”

“Vipi mama?”

“Yupo vizuri hapa anategemea kuangalia mechi yenu”

“Poa badae basi”

“Poa”

Nikakata simu na kuzisubiria picha za hoteli hiyo. Baada ya muda kidogo picha hizo zikaingia kwenye simu yangu, nikamuonyesha Frenando.

“Duu hapa pazuri kaka”

“Eti ehee?”

“Yaa hapa pazuri kuliko hata pale”

“Poa poa”

Tukafika katika uwanja mkubwa wa mpira wa Olympiastadion Berlin ambao ndio shuhuli za ufunguzi wa kombe hili zinafanyika. Uwanja huu unaingiza mashabiki zaidi ya 74,475 kwa wakati mmoja. Basi letu likasimama katika eneo maalumu na sikuamini macho yangu baada ya kukuta idadi kubwa ya mashabiki ambao ni watu wazima wakiwa wamekusanyika kuipoke timu yetu. Waandishi wa habari ambao ni wengi sana wakaendelea kupiga picha mbalimbali huku wengine wakirekodi kila kinacho endelea. Tukashuka hutu nikuwa tumevaa makoti ya jezi zetu za shule.

“Ethan Klopp, Ethan Klopp”

Baadhi ya waandishi wa habari waliniita kwa ajili ya mahojiano. Nikasimama na wakanizunguka huku wakiniwekea vinasa sauti karibu na mdomo wangu.

“Kwanza poleni sana kwa kile kilicho tokea kwa kocha wenu”

“Tunashukuru sana”

“Je mumejiandaaje kwa mechi ya leo pasipo kuwa na kocha mkuu”

“Mimi na wachezaji wezangu tumejiandaa vizuri sana na nina imani kwamba tutawapa mashabiki wetu kitu kizuri kile wanacho kitarajia kutoka kwetu”

“Nimepata habari ya chini ya kapeti, ni kweli shule imejitoa katika kuihudumia timu kutokana na tukio la kukosekana kocha mkuu?”

Nikaka kimya huku nikimtazama muandishi huyu, nikatabasamu kidogo.

“Hapana ni uongo mtu. Kama shule ingejitoa katika kuhudumia timu basi leo hii tusinge kuwepo hapa”

“Mbona kuna hii meseji hapa imetoka kwa mwalimu mkuu wako, alininitumia na kudhibitisha kwamba shule imekata huduma zote juu ya timu yenu?”

“Kwa mimi hilo sifahamu na sina maoni juu ya hilo”

“Je mutafanikiwa kushinda kwa mbinu za kocha msaidizi?”

“Kija kitu ni mipango. Asanteni”

Nikaanza kuondoka na wakaanza kunifwata ila wakazuiwa na askari wanao imaeisha ulinzi katika eneo hili. Tukaingia kwenye vyumba vya kubadilishia mazoezi na kukuta jezi zetu zikiwa zimepangwa vizuri kila mtu kwenye sehemi yake. Tukabadilisha nguo, zetu na kuvaa jezi hizi na viatu.

‘Ethan’

Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu, nikaangaza macho ndani ya chumba hichi ila sikuweza kumuona.

‘Upo wapi?’

‘Siwezi kujitokeza kwenye kundi hili la watu’

‘Vipi?’

‘Leo jitahidi kwani timu pinzani ina mikakati mizito dhidi yenu na inaweza kuwa moja njia ya kuwadhalilisha’

‘Kutudhalilisha tena?’

‘Ndio’

‘Kivipi?’

‘Mutakwenda uwanjani utajionea’

‘Unanipa presha rafiki yangu’

‘Usijali’

‘Ethan’

Ethan hakuitika na ukimya ukatawala ndani ya nafsi yangu. Nikaendelea kumtazama kocha jinsi anavyo endelea kupanga mipango yake ya jinsi gani tuweze kucheza.

“Hei mbona unaonekana kama huna raha?”

Frenando aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hakuna ninawazia tu mechi”

“Usiwaze sana, tunakwenda kuwafunga hawa wajinga”

“Nakuomba usiruhusu goli Frenando”

“Usijali kaka”

Tukaendelea kukaa ndani ya chumba chetu hichi, tukisubiria maonyesho kadhaa yaweza kumalizika uwanjani. Saa kumi na moja kasoro kumi tukatoka ndani ya chumba chetu cha michezo na kuelekea katika mlango wa kutokea. Wachezaji wengi wa shule hii kutoka Italy ni warefu na wana miili mkubwa kiasi cha kuwafanya baadhi ya wachezaji wezangu kujawa na hofo. Kama timu kapteni nikaka mbele ya mstari huku nuyuma yangu akinifwatia Frenando na wengineo. Kocha msaidizi na madaktari wa timu wakatangulia uwanjani. Refa na wasaidizi wake wawili, wakasimama mbele kabisa na ilipo timu saa kumi na moja kasoro tano tukaanza kutembea na kutoka uwanjani humu. Uwanja mzima umejaa mashabiki wengi sana na katika maisha yangu sijawahi kucheza mpira kwenye wingi wa mashabiki wengi kama hawa.

‘Ehhh Mungu nisaidie’

Nilizungumza huku mapigo ya moyo yakiniende kasi. Hata mimi mwenyewe wasiwasi mwingi umenijaa moyoni mwangu. Tukapanga mstari mmoja, na sisi kama wenyeji, tukaanza kuwapa mikono marefa kisha tukafwatia wachezaji wa timu pinzani. Kila mchezaji ninaye mtazama naona ananizidishia wasiwai mwingi san. Baada ya kuwamaliza kuwapa mikono wapinzani wezetu, nikawaita wachezaji wezengu na kukusanyika duara moja.

“Hei jamani hawa wana ukuwa tu wa miili ila nina imani tunakwenda kushinda sawa”

“Sawa kapteni”

“Kapteni tayari kule”

Mchezaji mmoja alizungumza huku huku akinionyesha sehemu walipo simama marefarii. Nikakimbilia katika eneo hilo na kukuana na kapteni wa timu pinzani. Refarii akatuonyesha shilingi yenye pande mbili huku akituomba kila mmoja achague upande wake.

“Kichwa”

Nilizungumza huku nikimtazama refa, akairusha shilingi hiyo juu kisha akaibana na viganja vyake. Kwa bahati timu yangu inaanzia upande wa mashariki mwa uwanja huku tukupeleka mashambulizi kaskazini mwa uwanja.

“Asante”

Nilizungumza huku tukibadilishan nembo za shule na mpinzani wangu. Tukawa marefarii mikono pamoja na wasaidizi wao na kwa ishara nikawaomba timu yangu tuelekee upande wa mashariki. Tukapiga picha ya pamoja na kila mchezaji akatawanyika upande wake huku mimi nikisimama peke yangu katikati ya uwanja nikiwa na mpira kwa ajili ya kuanzisha mpira huu. Refarii akatazama saa yake ya mkononi na ilipo timia saa kimi na moja kamii akapiga kipenga cha kuanzisha mpira. Nikampigia Pilo na taratibu tukaanza mchezo huu huku wapinzani wetu wakitufwata kwa kasi, kwa bahati mbaya mchezaji mwezetu mmoja akapokonywa mpira. Wapinzani wezetu wakimbia kwa kasi kuelekea golini kwetu na mmoja wao akapige shuti moja kubwa sana, Frenando akajaribu kulifwata kwenye pembe ya goli, ila akashindwa kuuzuia kwa mkono mmoja na mpira ukaingia nyavuni.

Robo ya uwanja wakanyanyuka na kushangilia, nikatazama saa kubwa hapa uwanjani ndio kwanza ni dakika ya pili. Nikastuka mara baaya kuwana mabeki wakiwa wamemzunguka Frenando, kwa haraka nikakimbilia hadi golini na kumkuta Frenando akilia kwa uchungu huku akiwa ameshika kiganja cha mkono wake wa kulia. Nikamvua gloves ya mkono huo, kidole kimoja cha mwisho cha Frenando kimefunjika jambo ambalo ni pigo kubwa kwetu kwani ndio kipa tegemezi naninaye muamini. Refarii akafika eneo hili huku madaktari wetu nao wakifika wakaanza kumpa Frenando huduma ya kwanza.

“Siwezi kuendelea”

Frenando alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, jambo lililo nifanya na mimi machozi kunilengea lenga usoni mwangu. Nikatazama nje ya uwanja na kumuona kipa namba mbili akijiandaa na kipa huyu udhaifu wake mkubwa ni kunyaka mipira ya chini, huwa hajiwezi kabisa kuruka chini.

‘Ethan upo wapi?’

Nilimuita Ethan mwezangu ila hakuweza kuitikia, nikajiona kwenye tv kubwa la hapa uwanjani jinsi nilivyo jawa na wasiwasi mwingi sana. Frenando akatolewa uwanjani hapa kwa kigari maalumu na kukimbizwa hospiyalini kwa matibabu zaidi. Akaingia kipa namba mbili anaye itwa Antoniyo Jr.

“Hakikisha huonyeshi udhaifu wako sawa”

Nilizungmza na kipa huyu huku nikimtazama usoni mwake.

“Sawa kapteni.”

Tukaanza mpira kwa kasi sana huku nikijitahidi kupeleka mashambulizi mbele, ila zaidi ya wachezaji wanne wananikaba mimi peke yangu na kunifanya nipate wakati mgumu wa kumiliki mpira hata kwa sekunde kumi. Kila nilivyo jaribu kutoa pasi kwa Pilo, hakuweza naye kutembea kwani kuna benki mmoja mkubwa anamzuia. Katika maisha yangu ya mpira leo ndio siku ambayo ninajihisi kukata tamaa mwanzo tu mwa mechi. Wachezaji wezangu hapo katikati ya uwanja wamepoteana kabisa, kwani wachezaji wanao cheza kati wa timu pinzani wana uwezo mkubwa, kwanza kumiliki mpira na pili kupiga chenga. Dakika ya kumi na tisa tukafunga goli la pili, tena kipa alipigiwa shoti lililo mchanganya akaruka upande mwengine na mpira ukaingia upande mwengine.

‘Ethan nisaidie, nipe uwezo basi rafiki yangu’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiwatazama wachezaji wa timu pinzani wakishangilia goli hilo. Kwa dakika hizi kumi na tisa za hapa awali wachezaji wezangu wote wamechoka na wamechoka na wanaonekana kukata tamaa kabisa. Tukaanza tena mpira huku nikijitahidi kukimbia kidogo na mpira na kupiga katika goli la wapinzani, ila mipira yangu haikuweza kufika kwani mabeki ni mahiri kwa kuzuia mipira ya juu. Dakika ya ishiri na mbili tukafungwa goli la tatu. Dakika ya ishirini na nane tukafungwa goli la nne. Dakika ta arubaini na tano tukafungwa goli la tano ambalo liliyafanya machozi yangu kushindwa kujizuia na kuanza kutiririka machoni mwangu kwani mchezaji wa timu pinzani aliwapiga chenga mabeki wanne na akampiga tobo kiba na kufunga goli hili na kwa dharau ya ajabu akaanza kupiga piga kifua chake kwamba sisi na mashabiki wetu hatuna chochote mbele yao.



Kitendo cha kuanza mpira, refarii akapuliza kipenga akiashiria ni muda wa mapumziko. Tarati bu tukatoka uwanjani huku nikiinamisha uso wangu chini, kwani nina huzuni kubwa kwa kweli. Tukaingia kwenye vumba vya kubadilishia nguo. Kila mchezi hakika amechoka na hakuna ambaye anaonyesha ana matumaini ya kufanya vizuri.

“Goli ni tano hadi sasa”

Kocha msaidizi alizungumza kwa unyonge sana huku akitutazama.

“Kipa namba moja hali yake kidogo sio nzuri. Kipa namba mbili ninakuomba ujitahidi sana kuwapanga mabeki wako. Katikati munapotea sana, mipira haimfikii Ethan. Jaribuni kupanda na si kukaa tu nyuma kusubiria mashambulizi”

Kocha alizungumza kwa msisitizo. Nikanyanyaka na kuingia bafuni huku nikiwa nimejawa na hasira.

‘Kama ni urafiki wenyewe wa kuniacha kwenye matatizo peke yangu ni bora uishie hapa’

Nilizungumza kimoyo moyo nikiamini kwamba Ethan yupo ananisikia. Nikamuoa akiwa amesimama mlangoni huku akicheka sana.

‘Ni nini kinacho kuchekesha?’

‘Leo mumekula maharage ya wapi?’

‘Ethan tambua kwamba sipo katika wakati wa utani, tumedhalika kipindi cha kwanza’

‘Ni kweli mume dhalilika, maelfu ya mashabiki wenu wamekuwa hoiii. Imani yao imepotea kabisa kwenu’

‘Kwa hiyo, nipe basi njia nijue ni nini nafanya ili niweze kufanikiwa?’

‘Hahahaa. Njia ni moja tu’

‘Ipi?’

‘Vua hicho kitambaa cha timu kapteni na umkabidhi kipa wenu na wewe ubaki kama mchezaji huru’

‘Kwa kufanya hivyo tutashinda au?’

‘Unaniamini au huniamini?’

Nikakaa kimya kwa muda huku nikimtazama Ethan usoni mwake.

‘Fanya hivyo la sivyo, leo mutaoga mvua ya magoli hadi muone dunia chungu’

‘Poa’

Nikavua kitambaa hichi kabla ya kutoka humu ndani, Ethan akanigusa kifuani mwangu kwa mkono wake wa kulia, nikahisi msisimko mkubwa sana kifuani mwangu. Uchovu ambao ulitokana na kukata tamaa, ukanipotea hali ya kujiamini na munkari vikanitawala. Ethan akanitazama kwa muda kidogo kisha akatingisha kichwa kunirudi nitoke ndani humu. Nikatoka na kuwakuta wachezaji wezangu wakiwa tayari wamesha simama kujiandaa kurudi uwanjani. Nikamuita kipa na kumvisha kitambaa cha timu kapteni.

“Kwa nini kapteni”

Kipa aliniuliza huku akinitazama.

“Hii ni moja ya mbinu ya kuwapa kiburi wapinzani wetu. Wakikuona wewe umevaa hichi watajiamini na kujisahau sana”

Kocha akanitazama kwa muda kisha akakosa cha kuzungumza.

“Tunakwenda kushinda, mumenielewa”

“Ndiooo”

Wachezaji wezangu waliitikia huku wakionekana kujawa na matumaini ya kupambana upya. Tukarudi kiwanjani huku baadhi ya mashabiki wakianza kutuzomea kwa kushindwa kufanya vizuri kipindi cha kwanza. Wapinzani wakaweka mpira kati na refarii akapuliza filimbi na mechi ikaanza upya. Nikamfwata mchezaji mwenye mpira na kwa kasi nikampokonya mpira miguuni mwake na kuanza kukimbia huku nikiwapita mabeki wao kirahisi sana, nikapaki mimi na kipa. Kwa mguu wangu wa kushoto nikapiga shuti moja zito lililo mbabatiza kipa na kumuingiza golini yeye na mpira wake.

Uwanja mzima ukafurika kwa shangwe, Wajerumani wote wakanyanyuka, kwenye viti vyao, tukapeana mikono ya kupongezana na wachezaji wezangu huku nikiwahakikishia kwamba ni lazima tushinde. Wapinzani wetu wakaanza mpira kwa kasi, ila kwa bahati mbaya wakaponywa na mmoja wa mchezaji wetu, alicho kifanya ni kupiga mpira mrefu, nikaruka juu na kuutuliza kifuani mwangu. Mabeki wawili wakanifwata kwa pupa. Mmoja nikampiga tobo huku mwengine nikimpitishia mpira juu yake, huwa tumezoea kuita kitendo hichi ‘Kanzu’. Nikaaza kukimbia kwa kasi, nikia mita chache kutoka golini, nikajikunjua mguu wangu wa kulia na kupiga shoti moja la chini ambalo kiba alibaki akisimama akiutazama mpira na kukaingia nyavuni.

Nikakimbia kwa kasi, kisha nikaburuzika kwa magoti yangu kwa mita kadhaa kisha nikalala chali na wachezaji wezangu wakaniangukia kwa juu huku kila mmoja akiwa na furaha kubwa.

“ETHAN, ETHA, ETHAN’

Jina langu lilitawala uwanja mzima. Wachezaji wezangu wakazidi kupata nguvu na matumaini.

“Tumebakisha goli tatu sawa”

“Sawa sawa”

Shangwe zikazidi kuwachanganya wapinzani wetu, kwani kila walivyo jaribu kushambulia, wakakutana na safu ya mabeki walio tulia na kila mchezaji wetu aliye pata mpira akiwa eneo la nyuma, alicho kifanya ni kuupiga mpira mbele. Wyne ambaye ni mchezaji namba nane katika timu yetu, akapata mpira mmoja kutoka kwa beki namba tano, akaanza kuwakimbiza wapinzani wetu hadi eneo la kona. Akaingiza krosi moja, na Pinto bila ya makosa akaruka hewani na kupiga kichwa kizito kilicho ufanya mpira kuingia nyavuni, na kuinua shangwe za mashabiki wetu.

Tukamkumbatia Pinto kwa furaha sana, kwani tayari mashabiki wetu tumesha washika sehemu ambayo hata wao wamesha jawa na hofu.

“Bado mbili”

Nilizungumza huku nikipiga makofi ili kuwahimiza wachezaji wezangu. Kocha wa timu pinzani akabadilisha mabeki wa wili na kuwaingiza wengine ambao wana miili mikubwa kulio hata walio anza toka.

“Pinto kuwa makini wale wameingia kuzuia tu na wapo tayari kucheza rafu hata kumvunja mtu. Sawa”

“Nimekupata kapteni”

Wapinzani wakaanza mpira katikati ya uwanja. Wakajaribu kuleta mashambulizi ila Lukas, akamzuia mpira na kunipigia pasi ya chini ambayo sikutaka kuiweka mguuni mwangu hata kwa sekunde mbili, nikampasia Wyne. Wyne kwa kasi aliyo barikiwa na Mungu akaanza kuwafwata mabeki wawili walio ingizwa katikati ya boksi la mabeki. Beki mmoja pasipo kujua ni nini maana ya Wyne kufanya hivyo akajikuta akimchota kwa miguu yake miwili na Wyne akaanguka chini. Refarii pasipo ubishi, akaweka penati huku beki huyo akionywa kwa kadi ya njano.

“Wyne piga”

Nilizungumza kwani mimi ndio nimezoeleka kupiga petani zozote zinazo toke. Wyne akaweka mpira kwenye kidura maalumu cha kupigia penati. Wachezaji wote tukajipanga nje ya boksi la makipa tukisubiria Wyne apige penati hiyo. Wyne akarudi hatua mbili nyuma huku akishika kiono chake kwamikono miwili, akisubiria refarii kupuliza kipenga.

Refarii akapuliza kipenga, Wyne akapiga penati hiyo kwa bahati mbaya ikapiga mwamba wa pembeni kisha ikarudi katika eneo nililo simama mimi. Nikampasia Wyen mpira huo na akamalizia kwa kuupigia nyavuni na kufanya ubao wa matangazo kusoma goli nne kwa tano. Nikatazama ubao wa matangazo unaonyesha ni dakika ya sabini na mbili.

“Tubadilisheni mfumo, tucheze ule nilio waambia jana usiku sawa”

“Sawa kampteni”

Mpira ukanza huku wapinzani wetu wakipoteana kwa mashaka makubwa sana. Nikaletea pasi moja nzuri sana na nikaanza kukimbia pembenozi mwa uwanja kila beki aliye nifwata alijikuta akishindwa kunizuia, nilipo fika karibu na eneo la kona, nikapika krosi. Kama kawaida ya Pinto akaruka hewani na kupiga kichwa kimoja kizito kilicho ingiza mpira huo golini na sasa tukawa tupo sawa kimagoli na wapinzani wetu.

“Mechi tunashinda hii Ethan”

Pinto alizungumza huku akinikumbatia kwa furaha sana.

“Ndio tunashinda”

“Sikieni bado goli tatu za mwisho”

“Dakika ni ya themanini na mbili”

“Ndio zinatosha, Pinto utacheza nyuma yangu. Wyne Lukas na wengine hakikisheni hakuna anaye panda huko kwetu sawa”

“Sawa”

Wapinzani wakaanza mpira, kwa kasi nikamfwata mwenye mpira, katika kukabana ili niuchukue mpira nikampiga kipushi kidogo akaweweseka na kuacha mpira, nikaanza kukimbia kwa kasi yangu yote, nikaanza kumchenga mchezaji wa kwanza, wa pili, wakaja wawili nikawapita, akaja wa tano, nikampita akaja mchezaji wa saba nikampita, kisha nikabaki mimi na kipa tu, kipa akajaribu kinifwata huku akiliacha goli mita kadhaa, nikampiga chenga na kukimbia hadi kwenye mstari wa goli hili nikaukanyaga mpira huku nikiwatazama wachezaji na mabeki wao wanavyo kuja kwa kasi huku wakionekana kujawa na hasira sana. Walivyo nikaribia nikaupiga mpira kwa kisigino na ukaingia nyavuni.

Nikaanza kujipiga kifuani mwangu huku nikirudia ishara za unyanyasaji alio ufanya mfungaji wao mmoja mara baada ya kutufunga goli la kwanza kipindi cha kwanza.

Uwanja ukafurika kwa shangwe, timu pinzani wakazidi kunyong’onyea. Wakajaribu kupiga shuti golini, ila kipa akadaka mpira wa kwanza toka tuingie kipindi cha pili. Kipa akapiga mpira mrefu na ukanikuta nipo mita chache kabla sijafika katikati ya uwanja. Nikamtazama kipa wao na kumuona yupo mbele kidogo kutoka lilipo goli lao. Nikapiga shuti moja refu lililo ambaa ambaa hewani kipa akajaribu kurudi nyuma ili kuunyaka mpira huo ila akajikuta akichelewa na mpira ukaingia golini.

Nikasimama sehemu hii hii na wachezaji wazangu wote wakanifwata na kunikumbatia, kwani magoli kama haya yanafungwa na wachezaji wachache sana duniani. Hadi tunafika mwisho wa mechi hii, tukaibuka na magoli saba huku nami nikiwa nimefunga magoli manne na nikakabidhiwa mpira ikiwa nikama pongezi ya kufunga magoli zaidi ya matatu.

“Hongera sana Ethan”

“Asante kocha”

Tukakumbatiana na kocha kwa muda kidogo kisha tukaendelea kushangilia upande wa mashabiki wetu. Waandishi wa habari kadhaa wakanifwata kwa ajili ya kunihoji maswali mawili matatu.

“Ethan unazungumziaje goli lako la mwisho ulilo funga”

“Nimoja ya goli la ndoto yangu, nilitamani siku moja nifunge vile na nikafanikiwa”

“Kwa sasa wewe ndio mchezaji unaye ongoza kwa goli nne, je utazidi kupanda au utabaki hapo hapo?”

“Hayo yote ni ya kumuachia mwenyezi Mungu, unajua mpira unaweza kusama unapanda na kesho ukapata majeruhi na ukashindwa kufanya chochote”

“Hongereni sana kwa mchezo mzuri ulio uonyesha natimu yako”

“Tunashukuru”

Nikasogea pembeni na wachezaji wengine wakaendelea kuhojiwa na waandishi mbalimbali. Pinto akanimwagia maji ayaliyomo kwenye chupa aliyo ishika na kunifanya nifurahi.

“Hongera kaka”

“Asante”

“Sikutarajia kama inaweza kuwa hivi”

“Yaa tumefanya kazi nzuri hata wewe hongera”

Nikaanza kutembea kueleeka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, mashabiki wakazidi kunishangilia kila nilipo pita. Mechi yetu ya leo unaweza kusoma ni kama fainali kwani tunafuraha kubwa sana.

“Kaeni tupige picha”

Nilizungumza huku nikiishika simu yangu, tukapiga picha kadhaa na timu nzima.

“Ethan”

Kocha aliniita huku akinitazama”

“Ndio kocha”

“Kuna pongezi”

“Kutoka wapi?”

“Kwa baba mkwe wako, ametwitte kupitia akaunti yake hii hapa”

Kocha alinionyesha ujumbe wa baba Camila aliio uweka kupitia akaunti yake ya Twitter. ‘Ni furaha kuwa na mkwe kama Ethan, naamini mwanangu hajakosea kuwa naye. Hongera sana Ehan Klopp na hongereni sana shule ya CJD Christophorusschule Königswinter’

Nikajisikia kufarijika sana mara baada ya kusoma ujumbe huu wa baba mkwe wangu ambaye yupo katika kampeni za kugombania uraisi wa nchi hii kupitia chama cha Social Democratic Party of Germany(SPD) na kama atashinda basi atatawala nchi hii kwa miaka mitano ya mwanzo kabla ya uchaguzi kufanyika tena.

“Shukrani kocha kwa kunionyesha”

“Asante nawe pia. Jamani tukitoka hapa inabidi kuelekea hospitali kwenye kumuona rafiki yetu Frenando sawa jamani?”

“Sawa kocha”

Tukaingia kwenye mabafu na kuanza kuoga huku tukiwa tumejawa na furaha. Tukavaa nguo tulizo kuja nazo na safari ya kuekejea hospitalini ikaanza huku basi letu likipata uzindikizwaji wa pikipiki moja polisi. Simu yangu ikaanza kuita na kwa bahati nzuri ni namba inayo toka nchini Tanzania, nikaipokea kwa haraka huku nikiwa na shauku ya kuisikia sauti ya Camila. Camila akaanza kwa kunipatia mabusu mototomo ambayo yaliyo ufanya mwili wangu wote kusisimka kimahaba.

“Nakupenda sana Ethan wangu”

“Nakupenda pia mpenzi wangu”

“Yaani sikuamini kama unaweza kutoa timu yako kidedea hakika sijakosea kuwa nawe Ethan nakupenda sana, tena sana mpenzi wangu na ninakuomba tukimaliza masome unioe”

Camila alizungumza kwa hisia kali sana huku nikihisi machozi yakimwagika.

“Etha nakuomba unioe”

“Nitakua mpenzi wangu”

Kelele za gafla zikaibuka kwenye basi na wachezaji wezangu wakaanza kunifwata kwenye siti niliyo kaa huku basi likifunga breki kali sana na kunisababisha hofu na mashaka makubwa sana kwani sijua ni kitu gani kilicho sababisha dereva kufunga breki za gafla.



“Ngoja ninakupigia mpenzi wangu”

Nilipo maliza kuzungumza maneno hayo nikakata simu na kuiingiza mfuoni simu yangu. Nikashuhudia gari mbii nyeusi kubwa zikiwa zimesimama mbele ya basi letu huku pikipiki aliyo kuwa ikiendeshwa na askari, ikiwa pembeni mwa barabara huku ikiwa imegongwa vibaya. Watu walio valia nguo nyeusi, huku wamezificha sura zao na mikononi mwao wakiwa na bunduki. Wakalizunguka basi letu kwa haraka huku wakimuamrisha dereva kufungua mlango huu wa basi.

“Nyote rudini nyuma”

Nilizungumza kwa amri huku nikitembea kuelekea mbele alipo dereva. Dereva mwili mzima unamtetemeka, hata mimi mwenyewe japo nimajitahidi kufika hapa mbele ila mwili mzima umejawa na jasho litokanalo na woga. Nikauona mkono wa dereva ukielekea kwenye kitufe cha kufungulia mlango.

“Usiminye”

Nilimuambia dereva huyu na kwa haraka akaurudisha mkono wake nyuma huku akiendelea kutetemeka sana kwa woga. Watekaji mmoja akapiga risasi kwenye kioo cha mlango wa gari hili na kikavunjika. Woga ukazidi kututawala, dereva pasipo kipingamizi cha aina yoyote akaminya batani hiyo na mlango ukafunguka, wakaingia watekaji wanne, wawili wakanifwata mimi na kunipiga na kitako cha bunduki usoni mwangu na kusababisha gizo zito kwenye mboni zangu za macho na kuanzia muda huu sifahamu ni kitu gani kinacho endelea.

***

Sauti ya za wanaume wawili wakizungumza lugha ya Russia, zikanistua kutoka katika dimbwi zito la kulala. Nikajaribu kunyanyua mkono wangu mmoja ila nikashindwa kutokana na kufungwa nyuma katika kiti hichi nilicho kalia.

“Munahitaji nini kutoka kwangu”

Nilizungumza kwa hasira sana huku nikiwatazama wanaume hawa wawili wenye bunduki mikononi mwao. Wakanitazama kwa muda ila hawakunijibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya.

“Nawauliza nyinyi washenzi muna hitaji nini kutoka kwangu”

Mmoja wao akanisogelea, akasimama mbele yangu kwa sekunde kadhaa. Kisha akanitandikia kofi moja jito sana hadi nikaanguka na kiti changu mzima mzima. Akaninyanyua na kunikalisha tena huku akionekana kujawa na hasira kali sana. Akatoa kitambaa chake kikubwa mfukoni, akakikunja kunja vizuri kisha akanifunga mdomoni mwangu kwa nguvu na ujanja wote wa kuzungumza ukaniishia.

“Kaa kimya la sivyo utakufa”

Baada ya kuzungumza maneno hayo akaondoka katika eneo hili na kurudi mlangoni alipo simama mwenzaje na wakaendelea kuzungumza mazungumzo wanayo yajua wao wenyewe.

‘ETHAN UPO WAPI RAFIKI YANGU’

Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimwagikwa na machozi mengi sana. Ethna hakuweza kunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ukimya kutawala. Nikarudia kumuita Ethan mara kwa mara ila sikuweza kumpata hadi ikafikia hatua nikapoteza matumaini yangu kabisa. Baada ya nusu saa, wakaingia wanaume wawaili mmoja akiwa ni mzee sana huku mwengine akiwa ni kijana ila amevalia suti nyeusi.

“Ethan Klopp habari za siku nyingi”

Mzee huyu alinisalimia huku akinitazama usoni mwangu. Nikamtazama kwa muda huku nikijitahidi kuvuta kumbukumbu za wapi niliweza kumuona.

“Naamini itakuwa ni vigumu sana kunikumbuka si ndio”

Alizungumza huku akinivua kitambaa hicho mdomoni mwangu.

“Unataa nini kwangu”

“Ni kitu kidogo sana ninacho kihitaji kwako”

“Kitu gani?”

“Nahitaji boksi jeusi”

“Boski jeusi!!?”

“Ndio boksi jeusi, baba yako Mzee Klopp alilichukua kwetu na hatujui ni wapi alipo liweka hivyo basi nalihitaji”

“Kwa kweli sifahamu unazungumza nini mzee, naomba uniachie kabla ya nchi yangu ya Ujerumani haijachukua hatua kali sana dhidi yako”

“Hahahaaa……upo mbali sana na Ujerumani. Hapa ni Russia na hutoweza kwenda popote hadi pale nitakapo pata boksi langu”

Nikashusha pumzi nyingi sana huku nikimtazama mzee huyu usoni mwake. Akanyoosha mkono kwa mwanaume aliye ingia naye humu ndani, mwanaume huyu akamkabidhi simu na akaweka video.

“Huyu ni dada yako Mery hapa watu wangu wanamuangalia popote pale anapo kwenda, ukifanya mchezo wa aina yoyote basi dada yako nitamuua”

“Ole wenu mujaribu kumgusa dada yangu nitahakikisha kwamba ninawachinja mmoja baada ya mwengine”

“Haahahaa Ethan acha hasira zisikudanganye, huna uwezo wa kufanya jambo lolote juu yangu. Tutakuachia huru ila kwa sharti la kuniletea boksi hapa nchini mwangu”

Kwa ishara mzee huyu akamuamrisha mmoja wa watu wake walio simama mlangoni, akanifwata na kunifunga kitambaa cheusi mdomoni na kukirudisha kitambaa alicho kifunga mdomoni mwangu na kunifanya nishindwe kuona wala kuzungumza chochote. Wakaanza kunitembea, hatua kadhaa mbeleni mwangu nikasiki mngurumo wa helicopter. Nikaingizwa kwenye helcopter hii na taratibu safari ya kuondoka katika eneo hili ikaanza. Ukimya mwingi ukatawala ndani ya hii helicopter sikuweza kusikia sauti za watu wakizungumza.

‘Ethan upo wapi rafiki yangu?’

Nilizungumza kimoyo moyo ila sikuweza kuhisi uwepo wake. Safari hii ikazidi kuchukua masaa mengi sana hewani.

“Tunakaribia kutua”

Niliisikia sauti ya mwanaume huyo ambaye kwa haraka haraka akili yangu inahisi kwamba anazungumza na simu.

“Sawa bosi”

Nikahisi kitu chenye ncha kali kikinichoma kwenye mkono wangu wa kulia, na baada ya sekunde kadhaa nikapitia na usingizi mmoja mzito sana ambao umenifanya nisijue ni kitu gani kinaendelea.

***

“Ethan…..Ethan”

Niliisikia sauti ya Mery akizungumza huku akilia, nikajaribu kufumbua macho yangu ila ukungu mwingi ulio nitawala usoni mwangu, ukanifanya nishindwe kuweza kuomuona Mery. Sauti za kuzungumza zikaongezeka huku nikisikia madaktari jinsi wanavyo elezana vitu vya kufanya. Nikapatia huduma ya haraka sana na baada ya muda kidogo nikaanza kujihisi nafuu huku nikimuona Mery akiwa amekaa pembeni ya kitanda changu huku amenishika mkono wangu wa kulia.

“Ethan”

“Mmmmm”

“Unajisikiaje?”

“Kidogo afadhali”

“Pole sana”

“Asante”

“Ni nini kilicho tokea?”

“Ehee?”

“Nini kilicho tokea?”

“Kwani imekuwaje?”

“Tulikuokota leo asubuhi katika hoteli ambayo uliniagiza niwachukulie wachezaji wezako”

“Muliniokota?”

“Ndio”

“Wachezaji wezangu wapo wapi?”

“Wapo nje huku wanakusubiria”

“Ni siku ya ngapi toka nipotee?”

“Ya tatu leo, nchi nzima kumekuwa na msako wa kukutafuta na ukipata nafuu basi wana usalama watakuhoji maswali kadhaa”

“Umesema ni siku ya ngapi leo?”

“Ya tatu?”

“Mungu wangu leo usiku timu yangu si inacheza?”

“Ndio ila huto weza kwenda kucheza Ethan, umenipa hofo kubwa sana kwa kupotea kwako. Huwezi amini ndani ya siku hizo tatu nimekuwa ni mtu wa kushindia maji tu, chakula hakikuweza kukatiza kabisa kwenye koo langu”

Kabla sijazungumza chochote, mlango ukafunguliwa, akaingia Camila na kwa haraka akanifwata kitandani nilipo na kunikumbatia kwa nguvu sana huku akilia kwa uchungu. Tukakumbatia kama kwa dakika tano hivi, kisha taratibu Camila akaanza kuninyonya midomo yangu.

“Umerudi lini kutoka nchini Tanzania?”

“Yaani sasa hivi ndio ninatoka uwanja wa ndege, nilighairisha safari yangu nikiwa nchini Kenya, ilimlazimu baba kutuma private jet kuja kunichukua Kenya na ndio nimefika. Nilistushwa sana na kutekwa kwako mpenzi wangu, tambua siwezi kwenda mbali nawe kwenye maisha yangu”

Camila alizungumza huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.

“Nipo nje”

Dada Mery alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kikalia. Camila akamshika mkono, kisha wakakumbatiana kwa muda.

“Samahani Ethan wachezaji wezako wanahitaji kukuona”

Daktari alizungumza huku akiwa amesimama mlangoni mwa chumba hichi.

“Waruhusu tu waingie”

Wachezaji wezangu wakaingia kwa utaratibu huku wakinitazama, nikaweka tabasamu usoni mwangu ili kuto waogopesha kama nina matatizo.

“Vipiti mimu kapteni”

“Safi, mbona mumekuwa wanyonge sana, mutaweza kucheza kweli mechi ya leo?”

“Bila ya sisi kufahamu afya yako kaka hatuwezi kufanya kitu chochote, na tutashindwa kuingia uwanjani na tupo tayari kwa wapinzani wetu wapewe point tatu kwa sisi kushindwa kuingia uwanjani”

Kapteni msaidizi alizungumza kwa unyonge sana huku machozi yakiwalenge lenga usoni mwao. Hakika kwa hali waliyo nayo dhairi inaonyesha kwamba wananipenda sana na kunikubali.

“Hatuwezi kuwapa nafasi maadui zetu kushinda. Tunatakiwa kufanya jambo katika hili”

“Ila kapteni haupo sawa”

“Ndio sipo sawa, ila nahitaji nyinyi muwe sawa. Kwa umoja wenu, kwa kushikamana kwenu na kwa kupambana kwenu nahitaji mechi ya leo wote mukacheze kwa pamoja. Mukacheze kwa umoja na mushinde kwa pamoja. Lazima tuimarishe uhodari wetu. Wapinzani wetu wasitumie udhaifu wa kuto kuwepo mimi uwanjani, kuwashindwa nyinyi. Munatakiwa kuwa na NGUVU. Nguvu ya mshikamamo wa pamoja, nilazima tushinde sawa?”

Nilizungumza kwa msisitizo huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Wachezaji wezangu nikawaona wakimwagikwa na mchozi.

“Mimi ni kama tawi katika mti, nikikatika ni lazima mzizi usimame imara kuhakikisha unanizaa tena na tena. Nyinyi ni mzizi, ingieni leo uwanjani na ninahitaji mechi hii ya leo mushinde kwa ajili yangu sawa”

“Sawa timu kapteni”

“Nilazima mushinde kwa ajili yangu. Sawa”

“Sawa”

Nikazidi kuwahimiza wachezaji wangu. Nguvu na faraja ambayo hapo awali waliipoteza ikarejea upya kabisa.

“Kwa ajili ya mpenzi wangu. Ninawaomba muhakikishe munashinda mechi hii, nina imani mukishinda hata yeye kesho tu hapa atapona sawa jamani”

Camila alizungumza huku akiwatazama wachezaji wezangu.

“Sawa shemeji ni kwa ajili yenu tutashinda”

“Frenando yupo wapi?”

“Kesho atatoka hospitalini na ataanza mazoezi na timu kesho kutwa”

“Naamini nami pia nitaanza mazoezi hivi karibu. Ila ninacho waomba leo mushinde goli nyingi zaidi ya munavyo weza. Pinto hakikisha mambo yanakwenda vizuri”

“Usijali kapteni”

Tukaagana na wachezaji wezangu na wakaondoka hospitalini hapa na moja kwa moja wakaelekea uwanjani kwa ajili ya mechi ya leo. Camila akawasha tv iliyomo humu ndani na kuweka stesheni inayo onyesha mpira huu moja kwa moja kutoka uwanjani(Mubashara).

“Dada Mery unaweza kunisaidia chakula?”

“Ndio ngoja nikakuchukulie”

Dada Mery akanyanyuka hapa kitandani na kutoka humu chumbani, mlangoni akapishana na Ethan pasipo yeye kumuona. Ethan akatembea kwa kujiamini hadi karibu kabisa mwa kitanda changu. Akamtazama Camila kwa muda kisha akamshika mkono wake pasipo Camila yeye mwenyewe kujijua, hazikupita hata dakika tano Camila akakilaza kifua chake kifuani mwangu huku akilala usingizi fofofo.

“Umemfanya nini mpenzi wangu?”

“Tunacho takiwa kuzungumza sisi wawili yeye hakimuhusu”

“Hakimuhusu vipi?”

“Umesahau masharti yetu. Endapo utamueleza mtu yoyote kuhusiana na mimi basi nitakwenda kumuua huyo mtu pasipo huruma ya aina yoyote”

Ethan alizungumza huku mboni za macho yake zikibadilika badilika rangi, mara nyeusi, mara rangu ya blue na akazidi kutisha zaidi, zilipo badilika kuwa rangi nyekundu, huku machozi ya rangi nyekudu yakimwagika usoni mwake jambo lililo nifanya nijawa na woga mkubwa sana na wasiwasi.

“Najua uliniita sana, ila kila jambo lililotokea kwa sababu ya huyu mwanamke wako. Kwa ajili yake yeye nilazima sadaka ya damu za wanadamu zitolewe ili furaha yako izidi kudumu zaidi na zaidi”

Ethan alizungumza kwa sauti nzito sana iliyo jaa utetemeshi mithili ya radi hadi nikajikuta mimi mwenyeweni nikiogopa sana kwani kila analo lizungumza linasababisha vitu vilivyomo ndani ya hichi chumba kupeperushwa na kuanguka chini.



“Una maanisha nini?”

Nilizungumza huku nikiwa na wasiwasi mwingi sana. Ethan akaisogelea tv kubwa iliyomo humu chumbani, akainyooshea mkono wa kushoto na ikabadilisha matangazo ya kituo cha ESport niliyo kuwa nikiyatazama na kuonyesha kundi kubwa la wasichana walio valia sare za shule zinazo fanana na sare za shuleni kwa Camila.

“Hawa ni wasichana wezake ambao kwa sasa wapo nchini Somalia”

Ethan alizungumza kwa sauti ya kawaida na kusababisha hali ya upepeo humu ndani kutulia kabisa na hata mingurumo ya radi sikuweza kuisikia tena.

“Angalia”

Ethan aliniambia na nikazidi kutazama safari hiyo ya wanafunzi wezake Camila. Gafla basi walilo panda likazingirwa na gari nne ina za pick up zilizo jaa watu wenye silaha huku wakiwa wamevalia vitambaa kichwani huku wakiwa na mavazi ambayo si rasmi. Wakampiga dereva wa basi hilo risasi nyingi sana kisha wakaingia ndani ya basi hilo huku wakiwa na mitutu yao mikubwa ya bunduki.

“Laiti mpenzi wako angekusikiliza haya yasinge wakuta wezake”

“Ila Ethan si uliniambia asiende na hakwenda kweli?”

“Moyo…..Moyo wake ulisha dhamiria na safari ali ighairi mara tu ya kusikia wewe umetekwa, la sivyo angeenda”

Ethna alizungumza kwa msisitizo mkubwa sana.

“Naomba basi uwasaidie wasipate matatizo?”

“Kwa kosa hilo la mpenzi wako ni lazima wezake walipe kwa damu zao na hilo tukio linatokea sasa hivi nchini Somalia, na wote wanafunzi kumi na tisa na waalimu wao wanne lazima watauwawa kikatili sana”

Nikashuhudia mwalimu mmoja wa kiume akipigwa risasi kichwani mwake na kuanguka chini.

“Ethan fanya jambo rafiki yangu?”

“Snna uwezo wa kufanya jambo hilo, nimekusaidia ili uweze kuwa na furaha yako kwa maana huyu mwanamke ndio furaha yako laiti angekufa huyu usinge kuwa na furaha maisha yako yote”

“Je na wale wanao hitaji boksi jeusi ni kina nani?”

Mlango ukafunguliwa, akaingia Mery akiwa ameshika kifuko cha rangi ya kaki. Ndni ya sekunde tano kila kitu kikarudi katika hali yake na wala Mery hakuweza kuelewa ni kitu gani kilicho tokea humu ndani. Ethan akanitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akapotea.

“Wifi amelala?”

“Yaaa nahisi alichoka na safari”

Mery akaka kwenye kiti kilichopo karibu kitanda hichi.

“Nimekuchukulia kuku wa kuchoma na ndizi za kuchoma kama unavyo penda”

“Nashukuru”

“Wifi amka ule”

Tartaibu Camila akaamka huku akipiga miyoyo mingi itokanayo na uchovu mwingi sana.

“Ehee nimechoka jamani”

“Pole sana mke wangu”

Nilizungumza huku nikimtazama Camila usoni mwake, nikatupia macho yangu kwenye tv hii na kuona maandalizi ya mechi ya timu yangu ambayo inakwenda kuanza muda si mrefu. Nikatamani kumueleza Camila juu ya matatizo ambayo yanawakuta rafiki zake kwa muda huu ila nikashindwa kabisa kwani ataniuliza nimejuaje.

“Samahani kunwa wana usalama kutoka serikalini wanahitaji kuzungumza na Ethan tunaweza kuwaruhusu?”

“Kama ni maswala ya mahojiano waambie wamuache mume wangu ale kwanza”

“Sawa”

Daktari akafunga mlango na kutuacha, tukaendelea kula taratibu huku nikimtazama Camila usoni mwake. Mpira ukaanza, huku uwanja ukiwa umemimimika mashabiki wengi sana ambao wengi wao wameshika mabango yanayo nitakia afya njema na nipone haraka ili nirudi uwanjani.

“Watu wanakupenda sana mume wangu”

Camila alizungumza huku akinilisha kipande cha ndizi.

“Kweli”

“Sasa baadae inabidi ufanye mpango uwashukuru watu hao”

“Nitawashukuru vipi dada yangu?”

“Hata kwa kuwaandikia kwenye ukurasa wako wa Twitter”

“Sawa, vipi hali ya mama?”

“Mama yupo na nesi wake nyumbani, bado hali yake ndio ile ile”

“Habari ya kutekwa kwangu anaifahamu?”

“Sikuthubutu kumueleza kwa maana na uzee ule na hali aliyo nayo tungempoteza kabla ya siku zake”

“Sawa dada yangu nashukuru kwa hilo”

“Usijali”

Pinto akafunga goli la kwanza na kutufanya wote ndani ya hichi chumba kushangilia kwa furaha. Wachezaji wote wakajipanga mstari mmoja, kisha wakafunua tisheti zao na kila tisheti moja ina herufi moja zilizo anaindikwa ETHAN KLOPP. Nikajikuta nikijawa na furaha kubwa sana. Hadi wanakwenda kipindi cha kwanza wanaongoza goli moja. Walinzi wa wili wa Camila wakaingia chumbani humu.

“Unatakiwa kuondoka madam”

“Kuna nini!!?”

Camila aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana.

“Utakwenda kufahamu ukifika nyumbani, mzee anakuhitaji”

“Likini mpenzi wangu ana umwa jamani”

“Tunalifahamu hili madam ila ni amri kutoka kwa baba yako na hatuna la kufanya”

Camila sura yake dhairi ikaonyesha imejawa na masikitiko makubwa sana, akanitazama huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Taratibu akaninyonya lipsi zangu, kisha akakumbatiana na dada Mery kidogo.

“Kesho pajapo majaliwa ya Mungu nitakuja sawa”

“Sawa mpenzi wangu”

Camila akatoka ndani huku na walinzi wake hao wawili ambao ninawafahamu na wamekuwa wakimlinda toka alipo kuwa shule ya msingi.

“Inabidi na wewe Ethan utafute walinzi”

“Wa nini dada?”

“Kwa ajili ya usalama wako, hembu tazama jinsi ulivyo tekwa, hadi sasa hivi sijajua huko wallikufanya kitu gani hadi kukuachia na kukutupa mbele ya hoteli”

“Usijali dada yangu usiwe na wasiwasi kila jambo litakwenda vizuri”

“Lini Ethan, unanipa wasiwasi mwenzio unajua?”

“Nalitambua ila wewe kuanzia leo inabidi uwe na walinzi wa karibu sana ambao watakulinda kila sehemu unayo kwenda”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama dada Mery usoni mwake.

“Watu walio niteka wanahitaji bosky jeusi, wanasema ni boksi ambalo ni mali yao na baba alilichukua”

“Boski jeusi, ndio lipi?”

“Hata mimi sifahamu hata lipo vipi, nashindwa hata kufahamu ninaanzia wapi kuwatafutia, isitoshe wanasema nisipo wapelekea tu, basi wanaanza kukuangamiza wewe”

“Ohoo Mungu wangu!!!”

“Ndio maana nahiyaji ulinzi uongezwe nyumbani. Maswala ya kwenda kwa shemeji sasa hivi hembu yakatishe kwanza, mimi nitawatafutia hili boksi kisha nitawapelekea”

“Ethan naogopa mwenzio”

Taratibu nikamshika dada Mery mkono wake wa kulia huku nikimtazama usoni mwake.

“Nipo kwa ajili yako, siwezi kukuacha wewe na mama mukapata tatizo lolote dada yangu umenielewa?”

Dada Mery alizungumza huku akitingisha kichwa chake akimaanisha kwamba amenielewa.

“Vizuri, naomba umpigie mwanasheria wa familia namuhitaji hapa hospitalini”

“Sawa”

Dada Mery akampigia simu mwanasheria huyu aliye ahidi atafika hospitalini hapa mara baada ya nusu saa. Tukaendelea kuangalia mpira huu, kusema kweli timu yangu inacheza kwa umoja na mshikamano hadi wanamaliza kipindi cha pili, wakaibuka na ushindi wa goli moja bila.

“Kazi nzuri wamefanya”

“Yaa”

Mlango ukagongwa, nikamruhusu anaye gonga kuingia ndani. Mwanasheria wa familia akaingia ndani, tukamsalimia kutokana ni mzee sana. Akaka kwenye kiti cha pembeni, akaniomba nimsimulie ni kitu gani kilipelekea hadi mimi kutekwa. Nikamueleza kila kitu, kuanzia tulivyo kuwa ndani ya basi na wachezaji wezangu hadi pale nilipo jikuta nipo nchini Russia.

“Sasa wao wanahitaji hilo boksi jeusi, unalifahamu kweli?”

Mwanasheria akaka kimya huku akinitazama na macho yanayo maanisha kwamba anafahamu kile nilicho mueleza.

“Tafadhali niambie ukweli unafahamu hilo boski jeusi?”

“Ndio”

Nikashusha pumzi taratibu.

“Ila siwezi kukuambia lipo wapi kwa maana ni hatari sana hilo boksi Ethan”

“Kwa nini ushindwe. Maisha ya dada yangu, yangu na mama yangu yapo kwenye hatari. Walio niteka wanataka hilo boksi. Sema ni wapi lilipo ili tujue tunajitoa vipi kwenye huu mpango”

“Ni jambo la hatari sana kufanya hivyo Ethan. Ukiwakabidhi boksi hilo hakika dunia nzima itakwenda kuangamia kwa ajili yako”

Tukatazamana na dada Mery huku tukiwa na wasiwasi mwingi sana.

“Kivipi?”

“Samaani kwa kuwaingilia. Ninaitwa Agent Thomas. Ninamaswali kadhaa ninahitaji kukuhoji bwana Ethan”

Alizungumza mwanaume mmoja wa kijerumani, huku akituonyesha kitambulisho chake kinacho mtambulisha yeye kama mpelelezi mkuu kutoka katika kitengo cha Bundesnachrichtendienst (BND).

“Bila sahamani”

Nilizungumza huku nikikaa vizuri kitandani.

“Wengine sijui munaweza kutupisha kwa muda”

“Mimi ni mwanasheria wake, kama ni maswala ya kiusalama unaweza kuzungumza nikiwemo nami ndani humu”

Mwanasheria wa familia alizungumza huku akimtazama bwana Thomas. Bwana Thomas akamtazama Mery kwa muda, dada Mery hakuhitaji hata kusemeshwa neno, akanyanyuka na kutoka chumbani humu na kutuacha sisi.

“Ilikuwaje mukatekwa?”

Nikaanza kuwaadisia jinsi basi lilivyo zuiwa na watekaji hao. Mwanasheria kwa ishara ya kidole akanikataza kuzungumzia kuhusiana na bosky jeusi.

“Je ni kitu gani walihitaji kwako hadi wakaamua kukuteka?”

“Hawakunieleza kitu chochote”

“Kweli Ethan?”

“Ndio hawakuniambia kitu cha aina yoyote ile”

“Je unaweza kuwakumbuka sura zao watu hao?”

“Mzee mmoja ninaweza kumkumbuka”

“Unaweza kuingi”

Bwana Thomas alizungumza kwa kutumia kinasa sauti kilichopo mkononi mwake. Akaingia mwana dada aliye valia miwani kubwa kidogo huku mkononi mwake akiwa ameshika laptop.

“Unaweza kumuonyesha picha za wale washutumiwa”

“Sawa mkuu”

Akafungua laptop yake kisha akaanza kunionyesha picha za wahalifu mbalimbali, hadi anafika mwisho hapakuwa na picha ya hata mualifu mmoja ambaye nina mfahamu.

“Je unaweza kumuelezea mzee huyo jinsi alivyo?”

“Ndio”

“Ehee muelezee”

Nikaanza kumuelezea mzee huyo jinsi anavyo onekana huku dada huyu akiwa makini katika kumchora kila ninacho kieleza, hadi ninamaliza kumuelezea mzee huyo, huyu dada naye akawa amemaliza na kunigeuzia picha aliyo ichora.

“Yupo hivi”

Nikajikuta nikishangaa sana kwani huyu dada ana kipaji cha hali ya juu, kwani mzee huyo amemtoa vile vile alivyo kuwa amenieleza.

“Ndio”

“Itume hiyo picha makao makuu na msako uanze kufanywa nchi nzima.”

“Sawa mkuu”

“Tunashukuru Ethan kwa muda wako, tutakapo kuwa na hitaji lolote basi tutakutafuta na kuzungumza nawe”

“Sawa sawa”

Thomas na dada huyu wakaondoka na dada Mery akaniingia ndani, nikamueleza dada Mery kile kitu ambacho nimehojiwa.

“Hii ishu ni kubwa sana, ndani ya serikali hii na dunia, hilo boksi jeusi linatafutwa. Na mtu pekee ambaye alikuwa anafahamu ni baaba yenu”

“Mbona hunyooshi maelezo, wewe si umesema kwamba unafahamu lilipo boksi hilo?”

“Ninacho fahamu ni njia ya kuweza kulipata boksi hilo seheu lilipo fichwa”

“Ni njia gani?”

Mwasheria akaka kimya kwa muda huku akitazama chini.

“Nakuuliza njia gani?”

“Njia ya kulipata ni wewe Ethan”

Maneno ya mwanasheria huyu yakatuacha mimi na dada Mery midomo wazi kwani sifahamu mimi nina njia gani ikiwa sifahamu hata muonekano wa boksi hilo jeusi.



“Mimi?”

“Ndio”

“Kivipi?”

“Vua shati lako”

Mwanasheria aliniambia kwa utaratibu, nikatazamana na dada Mery kwa sekunde kadhaa, kwa ishara ya macho akaniruhusu kuvua shati langu. Mwanasheria akasimama na kunitazama mgongoni mwangu.

“Sehemu hii hapa, alifanyiwa upasuaji mdogo na kuwekewa ramani ramani inayo muwezesha kufahamu ni wapi lilipo boksi jeusi na mimi ndio mtu wa pekee niliye weza kufahamu kuhusiana na hili jambo toka ulipo kuwa na umri wa mika nane”

Sehemu ambayo mwanasheria anaizungumzia mgononi mwangu kwa mimi sio rahisi kuiona na sikuwahi hata sikumoja kufahamu kama nilifanyiwa upasuaji mgongoni mwangu.

“Haito kuwa imeharibika hiyo karatasi?”

“Hapana iliwekwa ndani ya kimfuko cha nailon ambayo si rahisi kuoza”

“Inabidi munitoe hicho kikaratasi”

“Kwa sasa haiwezekani Ethan?”

“Kwa nini haiwezekani?”

“Boksi hilo ni hatari endapo litakuwa mikononi mwa mtu yoyote yule”

“Kwani ni boksi la nini jamani?”

Mwanasheria akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akitutazama.

“Lina siri nyingi za kiserikali, lina mbinu za utengenezaji wa nyuklia. Babu yenu alikuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kubuni vitu hususani kwenye maswala ya silaha. Alitumiwa na Adofl Hitler katika kutengeza silaha za vita ya kwanza ya dunia na ya pili”

“Babu yenu aliweza kuunda mfumo wa bomu la kwanza la nyuklia na hakuihitaji kulitumia kwani alihofia lingeuaa mamilioni ya watu duniana na ingesababisha hata mabara kadhaa kupotea kwenye ramani ya dunia, kutokana ni bomu ambalo lilikuwa na uwezo mkubwa la kusababisha sehemu inayo shambuliwa kugeuka chini juu na juu huingia chini”

“Mmmmm”

Babu yenu aliuwawa akiwa ktika harakati za kuificha fumula hiyo. Aliye kuwa babu mzaa baba yenu ambaye baba yake ndio alihusika katika utengenezaji wa fomula hiyo aliridhishwa huyo aliitwa Klopp Jr. Yeye alililitengeza hilo bomu kisiri sana, jaribio lake alilifanya kwenye moja ya kisiwa kimoja Uingereza na kusababisha kisiwa hicho kufutika kwenye ramani ya dunia.”

“Alianza kuwindwa sana na mataifa makubwa ambayo kwa kipindi hicho yalisha jipatia nguvu kama Marekani na Russia. Babu yenu huyo alitengeneza hilo boksi jeusi, akaweka siri kubwa sana ambayo mimi siifahamu na hata fumola hiyo ya kutengeza hilo bomu imo ndani yake. Alirisishwa baba yenu naye karatasi hiyo aliiweka ndani ya mwili wake katika eneo la paja upande wa kulia”

“Nimekumbuka kitu”

Mery alizungumza huku akitutazama.

“Nini?”

“Kipindi nilipo kuwa mdogo, nilikuwa ninamuuliza baba alama aliyo kuwa nayo kwenye paja. Alikuwa akiniambia, kwamba alipata ajali ya pikipiki na aliweza kuchanika katika eneo hilo”

“Yaa haikuwa ajali bali ni karatasi ambayo inatoa maelekezo lilipo hilo boksi na endapo litavumbuliwa duniani, basi magaidi wengi watakuwinda na si wao tu bali hata nchi kubwa duniani zitakuwinda kuhakikisha kwamba wanalipata hilo boksi na endapo watalipata, basi vita ya tatu ya dunia inakwenda kutokea kwa maana mwenye nguvu atajaribu kumdhibiti asiye na nguvu”

Taratibu nikashusha pumzi nyingi sana kwani kwenye maisha yangu sikuweza kufahamu kama nimebeba siri kubwa sana ambayo nikiamua kuitoa hadharani basi ni damu nyingi sana na watu wasio na hatia zitanijaa mikononi mwangu.

“Unatakiwa kuwa makini sana Ethan na ikiwezekana unda timu ya walinzi wako, watakao kuwa wakikulinda popote uendapo, kama wamekuteka na kukuacha huru, basi kinacho fwata ni kukua”

Ukimya ulii tawaliwa na hofu, ukatawala kati yetu. Amani ya kuishi katika nchi hii taratibu inaanza kupotea na sehemu ya pekee mimi ya kukimbilia ni Tanzania. Taarifa ya dharura iliyo anza kuonyeshwa kwenye hii kitua cha tv tunayo itazama ikamfanya mwanasheria kusimama huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Taarifa hii inahusiana na kutekwa kwa basi la wanafunzi na inasadikika mtoto wa mgombea uraisi nchini hapa Ujerumani ambaye ni Camila hakuwemo ndani ya basi hilo. Picha vya video iliyo tumwa kwenye mtandao inaonyesha mwalimu mmoja wa wanafunzi hao akichinjwa kama kuku huku watu wanao fanya tukio hilo wakiwa wamezificha nyuso zao.

Sikushangaa sana kwani tayari Ethan alisha nieleza juu ya hili swala. Nikajikuta machozi yakinitiririka usoni mwangu kwani ni tukio la kinyama sana ambalo kwa binadamu wa kawaida ni ngumu sana hata kumaliza kulitazama lote.

“Ohooo Mungu wangu, mwanangu yupo pale, mwanangu ametekwa”

Mwanasheria alilia kwa uchungu sana na kutufanya tushangae sote. Nikachomoa sindano ya dripu la maji na kushuka kitandani. Nikatambea kwa haraka hadi karibu ya tv hii.

“Ohoo mwanangu wanakwenda kumuu jamani. Ohoo wanakwenda kumuu”

Mwanasheria aliendelea kulia huku akiweka mikono yake juu ya kichwa.

“Naomba simu yako”

Nilimuambia dada Mery, akanikabidhi simu yake. Nikaingiza namba za mama Camila, nikaiweka sikioni na simu yake ikaanza kuita.

“Habari Mery”

“Sio Mery ni mimi mama”

“Ohoo Ethna pole sana kwa matatizo ambayo yamekukumba”

“Nashukuru mama, umetazama tevishion yoyote?”

“Hapana kuna nini?”

“Upo karibu na tv?”

“Ndio, nipo ndani ya gari labda niwashe tv humu ndani ya gari”

“Hembu washa mama yangu”

“Sawa”

“Ohoo Mungu wangu Wangu”

Nilisikia sauti ya mama Camila akizungumza huku akionekana kustuka sana.

“Nakupigia Ethan”

Simu ikakatwa. Nikamgeukia dada Mery na kumtazama usoni mwake.

“Tunatakiwa kuondoka hapa hospitalini sasa hivi”

“Tutakwenda wapi?”

“Mwanasheiria akakurupuka na kutoka humu ndani huku akikimbia. Dada Mery kwa haraka naye akatoka na kuanza kumkimbiza.

“Ethan nahitaji kuzungumza na wewe”

Nilizungumza kwa hasira sana, haukupita muda mrefu Ethan akasimama kwenye moja ya kona humu chumbani huku akiwa amevalia suti nyeusi.

“Naokuomba ufanye jambo dhidi ya wale watoto wa kike. Tafadhali ninakuomba sana Ethan”

“Huwa nikizungumza neno langu alianguki chini. Nimefanya yote kwa ajili yako wewe na mpenzi wako. Kusudia kubwa lilikuwa ni mpenzi wako kukamatwa. Sasa changua moja kati ya mpenzi wako Camila kufa au wale wezake ndio wafe na kila kitu kinawezakana kwangu?”

Nikashusha pumzi huku nikimtazama Ethan usoni mwake.

“Hakuna jinsi Ethan, ni lazima Camila apone kwa ajili ya maisha yako ya baadae”

“Hivi huwezi hata kumponyesha mtoto mmoja hivi?”

“Hicho kitu hakipo Ethan, kila jambo linalo tokea hapa duniani, lazima liwe na sababu. Hakikisha kwamba unakuwa mvumilivu na mstahimilivu katika hili. Usizungumze chochote juu ya hili cha kufanya niwewe kuwa kimya na kutoa pole kwa wafiwa”

Ethan alizungumza kwa sauti ya upole sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Je unafahamu kuhusina na boksi jeusi?”

“Ndio”

“Maelezo niliyo pewa ni sahihi?”

“Ndio ni sahihi. Hiyo ni sababu ya mimi kuwa rafiki yako. Lazima boksi hilo lilindwe kwa manufaa ya baadae”

“Unaweza kunipeleka na kuliona lilipo?”

“Muda wake bado haujafika”

“Lini muda wake utafika?”

“Ukifika nitakufahamisha sawa”

“Sawa”

“Nahitaji kuondoka na kaa hospitalini hadi utakapo ruhusiwa na hakuna kutoka nje ya hii hospitali kabla hujaruhusiwa”

“Sawa”

Ethan akaondoka na dada Mery akaingia huku jasho likimwagika sana usoni mwake.

“Vipi umempata?”

“Hapana, nimemkosa. Ameingia ndani ya gari lake na kuondoka kwa kasi”

“Mmmm sawa”

“Jamani sijui kwa nini wametekwa?”

“Hilo swala tuiachie serikali, hivi huna mtu unaye mfahamu au kampuni unayo ifahamu ikatusaidia kupata walinzi wa kutosha”

“Zipo kampuni ninazo zifahamu, ila kampuni nzuri wa walinzi binafsi mimi ninaona ni bora tuende Japan”

“Japana wapo wazuri?”

“Sana, uzuri wa Japan, kwanza mlinzi ana uwezo binafsi wa kupigana yeye kama yeye. Pili anauwezo wa kutumia kila aina ya silaha hivyo utakuwa salama zaidi tukiwachukua hao. Na hata wanaweza kukufundisha kujilinda mdogo wangu”

“Naomba basi utafute kampuni nzuri leo hii tuweze kuwasiliana nao dada yangu”

“Sawa usijali”

Dada Mery akanichoma sindano ya dripu la maji kisha tukaanza kuperuzi peruzi kwenye mtandao kuhakikisha kwamba anapata kampuni nzuri ya ulinzi kwa watu binfasi.

“Nimepata hii kampuni inaitwa Ging Jang Ging”

“Mmmm mbona jina gumu”

“Wee acha tu mdogo wangu. Nimepata namba yao ngoja nizungumze nao”

Dada Mery akapiga namba hiyo.

“Habari, unazungumza na Mery Klopp, ninapiga simu kutoka nchini Ujerumani”

Dada Mery akaanza kueleza shida yake, na nikamueleza kwamba tunahitaji walinzi wanne kwanza wa kuanza kufanya nao kazi.

“Wananitumia video za walinzi hao”

Dada Mery alizungumza mara baada ya kukata simu. Video ikaingia kwenye email yake na tukaanza kuitazama. Mafunzo ya walinzi mbali mbali wanayo fanya huku wakiwemo walinzi wa kike. Mafunzo yao hakika ni mazuri na yanatia hamasa hata kwa muajiri.

“Tuchukue wakike wawili na wanaume wawili”

“Sawa hakuna tatizo wakike watakulinda wewe na wakiume watanilinda mimi”

“Ngoja niwatumie picha za wale ninao wahitaji”

Tukakubaliana na dada Mery katika kuwachagua walinzi tunao wahitaji kisha akawatumia picha zao.

“Wanasema kila mlinzi atalipwa dola milioni moja kwa mwaka”

“Mwaka mzima?”

“Ndio”

Nikakaa kimya kidogo kwa maana kiwango hicho cha pesa ni kikubwa kiasi.

“Kwani tuna kiasi gani bwana. Mimi ninawakubalia na kama inawezekana tunaanza kufanya malipo ya awali dola milioni mbili, baada ya miezi sita tunalipa dola milioni mbili iliyo salia”

“Sawa”

“Poa ngoja nikalishuhulike hili swala”

Dada Mery akaondoka na usku huu nikabaki hospitalini hapa peke yangu huku nikitafakari mambo mengi sana kwenye maisha yangu na hususani hilo boksi jeusi ambao wanadai lina siri nyingi sana. Majira ya saa nne usiku mlango ukafunguliwa na akaingia nesi mmoja mrefu kiasi na mwenye asili ya Afrika.

“Mambo Ethan”

Nesi huyu alinisalimia kwa sauti iliyo jaa furaha sana huku akiweka chombo maalumu cha kubebea chakula, mezani.

“Poa tu”

“Inabidi ule chakula cha usiku”

Nesi huyu alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu sana, nikamtazama kifuani mwake, kifungu kimoja cha gauni alilo livaa kipo wazi jambo lililo nifanya niyaone maziwa yake vizuri. Nikajikuta mwili wangu ukianza kujawa na msisimko ulio mfanya jogoo wangu kuanza kusimama taratibu. Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kumsaliti Camila ila kwa mitego anayo ifanya huyu nesi hakika kila mwanaume lazima ajihisi msisimko wa kimapenzi. Nesi huyu hakuishia hapa, akaangusha kichupa kidogo cha dawa na akainama taratibu na kuzidi kunipagawisha pale nilipo yaona mapaja yake yaliyo nona.

“Unataka nikulishe au utakula mwenyewe?”

Nesi alizungumza kwa sauti iliyo jaa mahaba mengi sana.

“Ehee…”

Nilizungumza huku nikihisi koo langu likikosa mate, nesi huyu taratibu akaka kitandani hapa huku akiwa ameshika hotpot hili lenye chakula, akanilegezea macho yake huku akizilamba lamba lipsi zake. Akazidi kunibabasha zaidi baada ya kuushika mkono wangu wa kushoto na kuuweka juu ya paja lake jambo lililo nifanya nipagawe sana.

“Usiogope wewe nishike tu”

Taratibu nikapandisha kigauni chake juu kidogo huku jogoo wangu akiwa amesimama kisawa sawa. Galfa nikastuka sana mara baada ya kumuona nesi huyu akiwa na tattoo kwenye hili paja lake, inayo fanana sana na tattoo ya mezee aliye niteka akiniamrisha kuhakikisha kwamba ninamletea boksi jeusi. Kabla sijafanya chochote kwa huyu nesi feki taa za chumbani humu zikazima na giza totoro likatawala.



Nikawahi kuishika mikono ya nesi huyu, ili kuhakikisha kwamba hanidhuru kwa jambo lolote lile. Tukaendelea kukurupushana na nesi huyu huku akionyesha dhairi kwamba analengo la kunidhuru humu. Gafla taa za humu ndani zikawaka.

“Mikono juu”

Sauti kali ya askari walio ingia ndanu humu walizungumza huku wakitutazama. Nikawatazama askari hawa wenye bastola mikononi mwao. Nesi huyu akaniachia taratibu huku akitabasamu. Nesi huyu kwa haraka akaokota sindano iliyopo chini na kujichoma kifuani mwake, hazikuisha hata sekunde stini akaanguka chini huku mapovu meupe yakimwagika usoni mwake.

“Upo salama Ethan?”

Askari mmoja aliniuliza huku akimsogelea nesi huyu kwa utaratibu

“Ndio”

Jasho jingi likazidi kunimwagika usoni mwangu huku nikimtazama nesi huyu aliye hitaji kuniua. Wakaingia madaktari wawili, kwa haraka wakanza kumpatia matibabu nesi huyu feki kabla hajafariki duniani. Wakaingia wana usalama wengine humu chumbani wakiwa na bastola mikononi mwao. Wanausalama hawa wakanionyesha vitambulisho vyao na kunieleza kwamba wapo hapa kwa ajili ya kunilinda. Nikatolewa ndani ya hichi chumba na kuhamishiwa chumba kingine.

“Nahitaji kuzungumza na dada yangu”

“Sawa”

Mwana usalama mmoja akanipatia simu yake, nikaingia namba ya Mery kwenye simu hiyo kisha nikipiga namba hiyo. Simu ya Mery ikaanza kuita taratibu, baada ya sekudne kadhaa ikapokelewa.

“Haloo”

“Ni mimi, upo wapi?”

“Ndio ninafika nyumbani”

“Hakikisha kwamba hautoki nje na waeleze walinzi wazidi kuimarisha ulinzi sawa”

“Ethan kuna nini kilicho tokea?”

“Kuna nesi alitumwa kuniua humu ndani, hivyo fanya kama ninavyo kuambia dada yangu sawa”

“Sawa”

Mery aliitikia kwa woga sana akionyesha dhairi kujawa na wasiwasi mwingi sana kwani maisha yetu hivisasa hayapo kwenye hali ya usalama.

“Ethan naogopa”

“Usiogope, fanya kama nilivyo kuambia dada yangu”

“Sawa”

Nikakata simu na kumpigia mama Camila, simu ya mama kamila ikaita hadi ikakatika, nikarudi kumpigia tena nayo majibu yakawa ni hayo hayo.

“Hii namba ikipiga naomba unifahamishe”

Nilimueleza mwana usalama huyu huku nikimuonyesha namba ya mama Camila.

“Sawa”

Hadi kua pambazuka, sikuweza kufahamu ni kitu gani kinacho endelea kwa nesi aliye hitaji kuniokoa. Akaingia mkuu wa kitengo cha usalama ambaye jana alikuja kunihoji. Tukasalimiana kisha akakaa pembeni ya kitanda changu.

“Pole sana kwa lile lililo tokea jana usiku”

“Nashukuru sana”

“Hivi huna wazo lolote kuhusiana na hawa watu wanahitaji kitu gani kutokea kwako?”

“Hapana sifahamu kwa kweli”

Niliamua kumdanganya mkuu huyuwa upelelezi kwa maana hivi sasa sifahamu ni nani ambaye ni muwazi au mkweli kwangu.

“Una uhakika?”

“Ndio, laiti kama wangekuwa wana hitaji kitu fulani kwangu basi wangenieleza mapema sana, ila hadi hivi sasa sijaambiwa chochote zaidi ya kuhitaji kuuwawa na yule nesi. Ila vipi yupo hai?”

“Ndio, ila hali yake sio nzuri”

“Naweza kumuona?”

“Hapana kwa sasa hutaki kumuona na usalama wako ni mdogo sana hivyo unatakiwa kuto kuonekana onekana hovyo”

Nikaka kimya huku nikimtazama mpelelezi huyu.

“Nikuombe kitu?”

“Niombe”

“Nahitaji dada yangu kuwa salama kwanza. Pili nahitaji kueleeka nyumbani baba yangu mkwe”

“Sawa nitakufanikishia cha pili, ila chwa kwanza, ulinzi wa dada yako tulisha uimarisha tayari. Akaingia mwana usalama ambaye jana nilitumia simu yake. Akanikabidhi simu yake inayo ita, na namba inayo piga ni ya mama Camila. Taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.

“Hei Ethan pole sana mwanangu, nimepata habari kwamba jana usiku kuna watu walihitaji kukua?”

“Ndio mama”

“Ohoo jamani pole, ila ulinzi si umesha imarishwa?”

“Ndio mama na ninahitaji kuja kwako”

“Sawa, nitawasiliana na mkuu aliyopo hapo, kama yupo mkabidhi simu”

“Haya”

Nikamkabidhi simu mkuu huyu wa upelelezi simu, akaiweka sikioni mwake na kuisikilizia kwa muda.

“Ndio”

“Sawa madam”

“Haya”

Mkuu huyu wa upelelezi akakata simu na kunitazama usoni mwangu.

“Ngoja nizungumze na dokta kama kuna matibu yoyote aweze kukupatia ili tuondoke”

“Sawa”

Mkuu huyu wa upelelezi akatoka ndani humu na kuniacha peke yangu. Ethan akaka pembeni yangu huku akinitazama usoni mwangu.

“Ethan kuna hali mbaya ambayo inaendelea hivi sasa”

Ethan alizungumza huku akionekana kujawa na wasiwasi mwingi sana usoni mwake.

“Hali gani?”

“Kuna muda ninajihisi kupoteza nguvu kwenye utawala wangu”

“Sijakuelewa?”

“Ni hivi kuna kaka yangu kwenye ufalme wa kishetani, anahitaji kuchukua nguvu zangu kwa nguvu ikiwa mimi ndio mtawala halali ambaye nilikabidhiwa madakaraka na baba yetu”

“Mmmm sasa hapo utafanyaje rafiki yangu?”

“Sijui Ethan na sitaki niwe karibu nawe kwa kipindi hichi kwa maana ataihamishia vita yake kwako kutokana hapendi kabisa wanadamu, hapendi kabisa hata kuwasikia na akishikilia utawala basi mimi nimekwisha”

Habari hii ya Ethan ikanifanya nikae kimya huku nikiwa nimejawa na wasiwasi mwingi sana, kwani yeyey ndio tegemezi langu kwenye mambo mengi.

“Ethan naogopa mwenzio na ninaomba unisaidie kunishauri jambo basi”

“Kwani katika huo ulimwengu wenu hauna majeshi yako?”

“Yeye ndio alikuwa mkuu wa majeshi yote toka baba alipo kuwepo, hivyo amri kubwa zote za kijeshi wanajeshi huwa wanasikiliza kwake. Sasa hivi nimebakiwa na majeshi machache sana ambayo hakika hayawezi kufanya chochote kwa kaka yangu”

“Ohoo Mungu wangu”

“Ndio hivyo na ili niweze kupata nguvu zaidi inabidi nianze kumwaga damu za binadamu jambo ambalo sihitaji kulifanya kabisa”

“Uzimwage kivipi?”

“Ninywe damu zao na nikianza kunywa sinto kuwa kama hivi, nitakuwa mbaya, nitakuwa muuaji rafiki yangu”

Mlango ukafunguliwa na akaingia daktari pamoja na mkuu wa upelelezi. Wakanitazama usoni mwangu huku daktari akitabasamu kidogo.

“Samahani bwana Ethan kwa kile kilicho tokea jana usiku”

Daktari alizungumza huku akisimama mbele yangu, Ethan hakupotea kuelekea sehemu yoyote zaidi ya kukaa hapa pembeni yangu huku macho yake akimkazia daktari huyu. Daktari na mkuu wa upelelezi hawamuoni Ethana kwani macho yao hayana uwezo wa kumuona kabisa.

“Nashukuru sana dokta”

“Tumeutazama mwili wako naona hauna tatizo lolote lile.”

‘Ethan nahitaji kumnyonya huyu dokta damu yake, nahitaji nguvu Ethan’

Ethan alizungumza huku akinyanyuka kwenye kitanda, nikamshika mkono na kumkalisha chini, jambo lililo mfanya mkuu wa upelelezi kunitazama kwa muda kidogo kwani kitendo cha mkono wangu kunyanyuka amekishuhudia vizuri ila hajaona ni kitu gani nilicho kishika. Ikanibidi nikurudia tena kitendo hicho ili maradi kumpoteza mawazo anayo yafikiria.

“Nashukuru dokta”

“Au unajihisi hali mbaya?”

“Hapana kabisa”

“Sawa, tunashukuru kwa kuwepo kwenye hospitali yetu”

“Nashukuru sana dokta”

Daktari huyu akonodoka ndani huku huku Ethan akiwa amemkazia macho.

“Tayari magari yapo tayari kwa safari”

“Sawa ninaomba dakika moja”

“Sawa”

Mkuu huyu wa upelelezi akatoka ndani humu na nikabaki na Ethan.

“Ethan unataka kufanya jambo gani. Tambua yule ni binasamu”

“Nahitaji damu Ethan”

“Sawa natambua hilo, ila kunywa damu yangu”

Ethan akanitazama kwa mshangao kwani maamuzi yangu niliyo yachukua sijui kama nitakuwa hai au laa.

“Siwezi?”

“Jaribu, ukinywa damu ya mimi unaye nipenda, nina imani huto kuwa na mazoea ya kwenda kunywa damu za watu wengine”

Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Ethan alinitazmaa huku akiwa hana la kuzungumza, nikamukabidhi mkono wangu wa kulia ili hata kama ni kuninyonya damu basi aninyonye kwenye mshipa wa damu. Taratibu Ethan akaanza kuupeleka mkono wangu mdomoni mwake. Meno yake manne, mawili ya chini na mawili ya juu yakaongezeka uwefu. Jataribu akauweka mkono wake kwenye meno yake ila kabla ya kuunyonya, akaushusha mkono wangu chini huku jasho jingi likimwagika usoni mwake.

“Siwezi, siwezi Ethan”

Alizungumza Ethan huku akihema sana.

“Safi, naomba uweze kuiongoza hiyo tamaa yako vizuri kama ulivyo weza kuiongoza kwangu. Sihitaji umdhuru mtu yoyote. Ethan wewe ni kiumbe kizuri, sio kila kiumbe cha asili yenu kina wema kwa binadamu kama unavyo nionyesha wewe. Tafadhali usifanye baya kwa mtu yoyote sawa”

“Sawa”

Nikamshika bega Ethan kisha nikatoka ndani humu. Nikaongozana na walinzi hawa hadi kwenye gari mbili nje ya hospitali ambapo nikakuta waandishi wa habari wengi. Waandishi wa habari wakaanza kutuzonga zonga huku wengi wakuhitaji kupata habari yoyote kwangu.

“Tuambie juu ya kutekwa kwako”

Muandishi mmoja alizungumza.

“Vyombo vya usalama vitazungumza hilo baada ya upelelezi wao kukamilika, nikaingizwa ndani ya gari na walinzi hawa na safari ikaanza huku nikiwaacha waandishi wa habari wakiwa na maswali mengi sana ya kuniuliza.

“Umewajibu vizuri waandishi wa habari”

“Nashukuru, vipi wale wanafunzi walio tekwa kuna jambo lolote kama serikali ambalo limewafanyia?”

“Ndio kuna vikosi ambayo vimeagizwa kwenda nchi Somalia, kuwakomboa wasichana hao”

“Kuna kitu chochote ambacho wanahitaji watekaji?”

“Hakuna wanacho kihitaji”

“Wamewateka tu?”

“Yaa ila kama watakuwa wanahitaji chochote basi tutaweza kuwapatia hicho wanacho kihitaji.

“Sawa”

Niliuliza maswali hayo kutokana ninahitaji kufahamu ukweli wa mambo. Tukafika nyumbani kwa kina Camila, nikakuta ulinzi ukiwa umeimarishwa maradufu. Camila akatoka ndani na kunikumbatia kwa nguvu huku akionekana kutokuwa na furaha kabisa.

“Ethan ninaogopa mwenzio”

“Usiogope mpenzi wangu”

Nilizungumza huku tukiwa tumekumbatiana na Camila. Tukaachiana na kuingia ndani na kumkuta baba Camila, na mama yake wakiwa wamekaa sebleni humu pamojana watu wengine wengine wa kiserikali wakitazama taarifa za habari. Nikasalimiana nao huku nao nyuso zao zikiwa zimejawa na majozi mengi sana.

“Kuna kitu gani kinacho endelea?”

Nilimuuliza Camila kwa sauti ya unyonge.

“Wamesema kwamba baada ya nusu saa watamuua msichana mmoja kwa kumchinja na hadi sasa hivi zimebaki dakika tano”

“Ohoo Mungu wangu”

Nilizungumza huku nikitazama Tv hii kubwa iliyomo humu ndani. Ndani ya dakika walizo ahidi magaidi hao, kweli Tv hiyo ikaonyesha video ya magaidi wanne waiwili wakiwa wamesimama mbele ya tambaa moja jeusi huku likiwa na maandishi ya kiarabu. Sura zao wamezificha kwa kuzifunika vinyago na kuaacha macho tu. Gaidi mmoja amemshika mwanafunzi huyo kichwa chake huku mwengine akiwa ameshika jambia kali sana. Wakaanza kuzungumza maneno ya kiarabu huku mmoja kati ya watu humu sebleni ana tutafsiria, kwamba wanamuomba Mungu kwa sadaka ambayo wanakwenda kuitoa. Simu ya gaidi aliye shika jambia ikaanza kuita, akaipokea na kuiweka sikioni mwake. Akaitikia baada ya muda akairudisha mfukoni mwake.

“ETHAN KLOPP, unatakiwa kuleta boksi jeusi la sivyo vifo vya wasichana hawa wote vitakuwa mikononi mwako”

Baada ya gaidi huyo kuzungumza maneno hayo, video hiyo ikaishia hapo na kuwafanya watu wote sebleni kunigeukia mimi na kunitazama kwa mshangao mkubwa sana.



Butwaa lililo nipata hakika toka kuzaliwa kwangu sina kumbukumbu ni lini liliwahi kunishika. Kila mtu ninaye mtazama ninaona mawenge mawenge ambayo yamenifanya niweke mikono yangu kichwani huku machozi yakinilenga lenga. Camila akanishika mkono wangu wa kulia na tukaanza kuondoka eneo hili na kuingia ndani kwake. Camila akanikumbatia kwa nguvu sana huku machozi yakitumwagika sote.

“Ethan”

“Mmmmm”

“Unajua chochote kuhusiana na hili jambo?”

Swali la Camila likaniacha mdomo wazi huku mapigo ya moyo yakizidi kunienda kasi sana. Camila akanitazama kwa muda kidogo kisha akaniomba nilale kitandani kisha akatoka chumbani humu. Nikanyanyuka kitandani kwa haraka, nikatembea hadi kwenye kioo, nikavua shati langu na kuanza kujichunguza sehemu ambayo mwanasheria alizungumza kwamba niliwekewe ramani ambayo itanisaidia kulipata boski hilo. Nikafanikiwa kuiona sehemu hiyo jambo lililo nifanya nijawe na woga mkubwa sana. Mlango ukafunguliwa na akaingia baba Camila. Taratibu akatembea hadi hapa nilipo simama.

“Ethan”

Baba Camila aliniita kwa sauti ya upole huku akikaa kwenye kiti maalumu cha dreasing table hii.

“Naam”

“Naomba uniambie mwanangu, kuna nini kinacho endelea kati yako na magaidi?”

Nikakaa kimya huku nikimtazama baba Camila usoni mwake. Nafsi moja inanisukuma nizungumze ukweli, huku nafsi nyingine ikinikataza kuzungumza jambo la aina yoyote.

“Naomba uniambie ukweli mwanangu. Tumeshangazwa sana na magaidi hawa kuweza kukutaja katika hili swala. Kama unafahamu ni wapi lilipo hilo boksi jeusi basi naomba uwapatie ili wale watoto waweze kuwa salama”

“Siwezi”

Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama baba Camila. Nikavaa shati langu na kuanza kutembea kuelekea mlangoni. Baba Camila akaniwahi na kunikamata mkono wangu wa kulia.

“Ethan zungumza tu ukweli ili tuweze kukusaidia katika hili. Tambua ninakwenda kuwa raisi. Okoa maisha ya wale wasichana”

“Siwezi kufanya hivyo. Mamilioni ya watu wanakwenda kufa duniani, wakifahamu ni wapi lilipo hilo boksi ni bora wafe hawa. Itatuuma ila si kwenda kuona dunia ikiangamia kwa ajili ya wachache”

Nilizungumza kwa ujasiri sana huku nikimtazama baba Camila usoni mwake. Nikafungua mlango wa chumba hichi na kutoka, nikakutana na Camila kwenye kordo, nikampita kwa kasi pasipo kumsemesha kitu cha aina yoyote.

“Ethan, Ethan”

Camila alainiita huku akinikimbilia, nikakatiza sebleni kwa kasi na kutoka nje na kumfanya Camila naye azidi kunifwata. Nikafika kwenye gari nililo kuja nalo hapa nyumbani, Camila akanishika mkono na kunigeuza kwa nguvu.

“Ethan una tatizo gani mpenzi wangu?”

“Siwezi kuaiacha dunia iangamie kwa ajii ya watoto wachache. Acha wale waangamie ili dunia iwe salama”

“Una maanisha nini Ethan mbona sielewi unacho kizungumza?”

Camila aliniuliza kwa mshangao kidogo ambao sikuhitaji kuujali. Nikafungua mlango wa gari na kuingia ndani, Camila naye akaingia ndani ya gari hili na kwa bahati mbaya hatukumkuta dereva.

“Ettha niambie ni nini kinacho endelea, hembu niamini basi mpenzi wangu”

Camila alizungumza huku akinishika mashavu yangu. Nikatazamana naye kwa muda kidogo huku nikiwa ninamwagikwa na machozi usoni mwangu.

“Tafadhali Ethan niambie ukweli”

“Hii yote ni kwa ajili yako Camila”

“Kivipi mpenzi wangu”

“Nilifahamu juu ya kutekwa kwa wale wezako, ndio maana nilikumabia usiende kwenye ile nchi. Lengo lao kubwa ilikuwa ni wewe”

Camila akajawa na mshangao mkubwa sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Unakumbuka kuna siku nilikupigia simu nikakuambia kwamba usiende Somalia?”

Camila akatingisha kichwa akimaanisha kwamba anakumbuka.

“Nilikuwa na maana ya kuzungumza vile ila hukuhitaji kunisikiliza mke wangu, uliamua kwenda huko?”

“Ngoja kwanza Ethan ulijuaje juaje kama nitatekwa?”

Swali la Camila likanifanya nikae kimya, nikakumbuka masharti ya Ethan, kwamba sipaswi kumuambia mtu yoyote juu ya uhusiano wangu wa kirafiki kati yangu na yeye na kufanya hivyo ni kosa kubwa ambalo yule atakaye fahamu basi ni lazima atakufa.

“Ethan wewe ni nani?”

Camila alizungumza huku uso wake ukianza kujawa na ndita nyingi zinazo ashiria kwamba ana hasira. Taratibu akaanza kuniachia huku akirudi nyumba nyuma hadi akagota kwenye mlango wa gari.

“Mimi ni Ethan, kwani umenifaamu leo Camila?”

“Hapana Ethan wewe ni nani, na kwa nini umesema wasichana wale wafe ili dunia iwe salama eheee?”

Camila alizungumza kwa ukalis ana huku akinitazama usoni mwangu.

“Wewe ndio chanzo cha wezako kutekwa Camila na hii yote ni kwaajili ya uhai wako. Mimi sijawahi ona hilo bosky jeusi, ila mwilini mwangu nina ramani ya kuninyesha ni wapi lilipo. Boksi hiyo jeusi limejaa kanuni na mbinu za kutengenezea mabomu hatari ya nyuklia, ambayo hao magaidi wakiweza kuyapata, mamilioni ya watu watakufa duniani”

Nilizungumza huku nikimtazama Camila usoni mwake.

“Wanatumia kigezo cha wasichana hao ili niweze kuwapatia hizo kanununi za kutengezea mabomu ya nyuklia.”

“Wewe hizo kanuni umezitolea wapi?”

“Ehhee?”

“Umezitolea wapi?”

“Babu yake mzee Klopp ndio alikuwa muanzilishi wa hizo kanununi, alikuwa ni genius wa kutengeza mabomu ya nyuklia katika utawala wa Adolf Hitler. Si serikali inayo paswa kuwa na mabomu hayo, bali haitakiwi mtu yoyote kuwa na mabomu hayo mke wangu”

Camila alizungumza huku akishusha pumzi taratibu. Nikavua shati langu na kumgeukia Camila, nikamuonyesha sehemu hii ambayo nimehifadhiwa ramani hii.

“Hapa ndipo nilipo hifashiwa ramani ya kuniwezesha kufahamu lilipo hilo boksi jeusi mpenzi wangu. Tafadhali ninakuomba hii siri usimueleze mtu wa aina yoyote. Endapo utanisaliti katika hili naapia kwa mwenyezi Mungu, haki ya Mungu sinto kwenda kukusamehe kamwe sawa Camila?”

Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Camila usoni mwake. Camila hakunijibu chochote zaidi ya kunikodolea macho tu, jambo ambalo kidogo likaanza kunipa wasiwasi naye.

“Siwezi kuachia hii fomula kwenye maisha yangu. Sitaki dunia iweze lia kwa ajili yangu. Sitaki dunia iangamie kwa ajili yangu. Tafadhali nakuomba unielewe hilo jambo Camila”

“Kwa hiyo unahitaji marafiki zangu wafe kwa ajili ya dunia si ndio?”

“Ndio”

Camila kwa haraka akashuka kwenye gari hili na kuubamiza mlango kwa nguvu. Akaanza kutembea kuelekea ndani, nikamshuhudia akiingia ndani, nikashusha pumzi taratibu huku nikiwa nimejawa na mawazo mengi sana. Baada ya dakika kama mbili nikawaona walinzi zaidi ya kumi wakilizunguka gari hili huku wakiwa wameshika bastola mikononi mwao. Nikamuona Camila na wazazi wake wakitoka ndani mwao huku wakishuhudia tukio hili. Mlinzi mmoja akaniamrisha kushuka ndani ya gari, nikamtazama Camila kwa macho makali sana kwa maana yeye ndio mtu aliye kwenda kutoa siri hii. Nikafungua mlango kwa nguvu na walinzi wawili wakanivamia huku mmoja akanipiga mtama na kuniangusha chini. Nipigwa pingu mikononi mwangu huku mikono ikiwa imerudishwa nyuma.

Camila akanifwata hadi hapa nilipo lazwa chini kama muhalifu mkubwa.

“Siwezi kuwaacha rafiki zangu wafe kwa ajili yako. Mpelekeni na muhakikishe kwamba anazungumza ni wapi lilipo hilo boski sawa?”

“Sawa madam”

Sikuamini kama Camila anaweza kubadilia kiasi hichi. Camila si wakutoa amri ya namna hii.

“CAMILAAAAA CAMILAAAA”

Niliita huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, walinzi hawa wakaanza kunipeleka mpute mpute hadi kwenye moja ya chumba chenye kiti kimoja tu. Nikaufunga miguu yangu na mikono yangu kwenye kiti hichi, mlinzi mmoja mwenye mwili mkubwa kiasi, akavua koto lake la suti, akakunja mikono na shati lake jeupe huku akinitazama usoni mwangu.

“Lipo wapi boksi jeusi?”

Mlinzi huyu aliniuliza kwa sauti nzito kama vile hanifahamu kabisa. Akanitandika kofi zito la shavu na kunifanya nihisi maruwe ruwe kwani toka kuzaliwa kwangu sijawahi kukutana na kofi zito kama hili.

“Ni wapi lilipo boksi jeusi?”

“Sifahamu”

“Akanitandika makofi mawali mfululizo hadi macho yakapata kiza kidogo”

“Sifahamu”

Nilijikaza kuzungumza, mlango ukafunguliwa, akaingia Camila huku akiwa ameongozana na mwananume mmoja aliye shika kibegi kidogo chenye msalaba mwekundu.

“Dokta angalia mgongoni mwake”

Camila alizungumza huku akinikazia macho usoni mwake. Damu zinazo nichuruzika pembeni ya mdomo wangu zikanifanya nizidi kumchukia Camila.

“Wapi?”

Daktari huyu alizungumza na kumfanya kamila kuzunguka nyuma ya mgongo wangu.

“Hapana”

Akanigusa sehemu ambayo ndio nilifanyiwa upasuaji na kuhifadhiwa ramani hii ya siri. Daktari huyu akafungua kibegi chake, kisha kisha akatoa bomga la jipya la sindano na kuvuta dawa ya ganzi na kunichoma katika sehemu hiyo.

“Kwa nini unafanya hivi Camila”

“Funga kinywa chako Ethan, nimesha kuambia siwezi kuwaacha marafiki zangu wafe kwa ajili yako”

“Kwa hili sinto kusamehe Camila”

“Potelea pote, maisha ni muhimu kuliko mapenzi”

Camila alizungumza kwa dharau huk nikihisi ninavyo pasuliwa sehemu hiyo ya mgongoni mwangu.

“Mbona hakuna kitu?”

Daktari alizungumza mara baada ya kunifanyia upauaji huo.

“Hembu angalia vizuri?”

“Hakuna kitu cha aina yoyote humu ndani, si unajionea mwenyewe”

“Mchane zaidi”

Camila alizungumza bila ya huruma yoyote. Daktari akatii amri hiyo na kuendelea kunifanyia upasuaji huu ambao ni batili kwa upande wangu, kwani sikurishia kufanyiwa hivi. Baada ya dakika kama mbili hivi daktari akatoa jibu kile like kwamba hakuna kitu chochote alicho kiona nyuma ya mgongo wangu.

“Shiittii wewe nguruwee zungumza ni wapi ilipo ramani”

Camila alizungumza huku akinishika mashavuni mwangu na kunigandamiza mashavu yangu kwa vidole vyangu. Nikatabasamu kwa dharau huku nikimtazama usonii mwake, kama amekosa kuona sehemu hiyo basi hata mimi mwenyewe sifahamu ni sehemu gani ambayo hiyo ramani imefichwa. Camila akanitatika makofi kadhaa kusoni mwangu pasipo kuangalia ni wapi anapiga kwani, makofi mengine yametua usoni mwangu.

“Sema Ethan ni wapi ilipo ramani”

Camila alizungumza kwa hasira huku akilia. Akaanza kunitingisha tingisha mwili wangu mzima hadi akasababisha kiti hichi nilicho kualia kikaanguka.

“Mnyanyueni”

Camila aliwaambia walini wake, wakaninyanyua na kiti changu kizima na kukalishwa sawa.

“Camila ni miaka mingapi mimi na wewe tumefahamiana. Ni miaka mingapi mimi na wewe tumekuwa pamoja, ni miaka mingapi tumeishi mapomoja na kufanya mambo mengi pamoja. Leo hii utu wangu haupo, leo hii sina dhamani kabisa mbele yako si ndio?”

Nilizungumza kwa upole sana huku machozi yakinimwagika usoni mwangu.

“Yote yametokea kwa ajili yako wewe uwe hai, kwa nini lakini. Unanihukumu kwa vitu ambayo havina msingi”

“Nyamaza”

Camila alizungumza huku akinitandika kofi jengine la sikuo la upande wa kushoto. Mwili mzima wa Camila umebadilika rangu na kuwa mwekundu.

“Nilikupenda mtu mweusi nikiamini kwamba una roho mbaya. Unakuja kuniambia kwamba eti niache wezangu wafe kwa ajili ya dunia. Sitaki kujua dunia ina nini, dunia ina mambo gani. Ninacho taka ni rafiki zangu wawe hai”

Camila alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu sana.

“Camila mimi sifahamu ni wapi lilipo boksi hilo”

“Ethan usitake kujua nina roho mbaya kiasi gani, ninataka boksi jeusi ili wezangu wakaokolewe”

“Sifahamu ni wapi lilipo hilo boksi”

“Ufahamu si ndio?”

“Ndio”

Camila akatoa simu yake mfukoni na kuniwekea video inayo onyesha dada Mery akiwa amewekwa chini ya ulinzi mkali huku macho yake yakiwa yamefungwa na kitambaa cheusi.

“Dada yako yupo njiani analetwa hapa. Haki ya Mungu usipo nieleza ukweli Ethan ninakwenda kumuua mbele yako, sinto jali wewe ni mtu ninaye mpenda au laa. Ila nilazima nitamuua”

Camila alizungumza kwa msisitizo na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa, kiasi cha kuzidi kumchukia Camila. Hazikupita hata dakika tano dada Mery akaingizwa ndani humu, akasukumizwa chini huku mikono yake ikiwa imefungwa na kamba.

“Ethan ni wapi lilipo boksi jeusi?”

Camila alizungumza huku akikabidhiwa bastola na mmoja wa walinzi wake. Camila akaielekeza bastola hiyo kweye paja la dada Mery.

“Wifi”

Dada Mery aliita huku akijaribu kuangaza angaza ilipo simama Camila. Mlio wa risasi ukanifanya nilie kwa nguvu sana, kwani risasi hiyo imempiga dada Mery kwenye japa la mguu wake wa kulia na kumfanya agaregare chini kwa maumivu makali sana.



Machozi mengi yakazidi kunimwagika machoni mwangu, hasira yangu ikazidi kupanda hadi ikafikia kiwango nikaanza kumwagikwa na makamasi puani mwangu. Sikuamini kama Camila ninaye ishi naye siku zote na kumchukulia kama mtu wa maana kwangu, kumbe ana roho mbaya sana.

“Sema boksi lipo wapi?”

Camila alizungumza kwa hasira huku akiwa amemuelekezea dada Mery bastola ya kichwani. Kilio cha dada Mery kikazidi kunipagawisha kabisa, kwani kila jinsi anavyo lia ndivyo jinsi damu inavyo mwagika kwenye kidonda chake.

“Nipo tayari kuwasaidia kuhakikisha kwamba tunalipata hilo boksi”

“Zungumza wapi?”

Gafla mlango wa kuingilia humu ndani ukavunjwa. Akasimama Ethan mlangoni huku kucha za vidoleni mwake zikiwa zimechongoka kwa sentimita kadhaa. Walinzi wa Camila wakaanza kumshambulia kwa kumpiga risasi mfululizo ila hapakuwa na risasi hata mmoja ambayo iliweza kumdhuru Ethan. Risasi zilivyo waisha, Ethan kwa kasi ya ajabu akaanza kuwaua walinzi hawa wa Camila huku akiwachomoa miayo yao jambo lililo mfanya Camila kuogopa sana hadi haja ndogo ikaanza kumwagika. Ndani ya sekunde kadhaa walinzi wote wa Camila wakawa chini huku wakiwa tayari ni marehemu. Ethan akaanza kumfwata Camila aliye zidi kurudi nyuma nyuma hadi akafika ukutani na kukosa sehemu ya kwenda. Ethan akanitazama usoni mwangu huku akisubiria amri ya kufanya kama ni kumuua Camila au laa.

Nikamuita kwa ishara ya macho Ethan, akanifungulia kamba na pingu nilizo kuwa nimefungwa, kwa haraka nikamuwahi dada Mery chini alipo kaa. Nikataka kumfungua kitambaa chake ila nilivyo angalia maiti hizi nikaona hakuna haja ya kumfungua kitambaa chake. Nikamuacha na kuanza kutembea hadi alipo Camila.

“Nilikuambia kwamba sinto kusamehe kwa kuitoa siri yangu.”

Nilizungumza huku nikimkazia macho Camila usoni mwake.

“Sikujua kwamba nipo na jini. Ni hivi kuanzia hivi sasa hivi mimi na wewe basi kwenye kila jambo, si mahusiano na wala si kwa mambo mengine. Umenielewa?”

Camila akatingisha kichwa akimaanisha amenielewa. Ving’ora vya gari za polisi vinavyo kuja katika eneo hili vikanifanya nimtazame Ethan mwenzangu ambaye tayari amesha fanya mauaji makubwa sana.

“Ondoka na dada yangu”

“Na wewe?”

“Nahitaji kuwepo hapa hapa, sitaki kukimbia na kuwa mtu anaye tafutwa”

Ethan akanitazma ausoni mwangu, kwa haraka akanirudisha kwneye kiti changu, akanifunga kama nilivyo kuwa nimefungwa hapo awali. Akamshikisha Camila bastola na kumsimamisha mbele yangu na kuninyooshea.

“Unafanya nini?”

“Utaona”

Ethan baada ya kufanya anacho kifanya, akamkumbatia dada Mery na kuondoka naye katika eneo hili. Polisi wakaingia ndani humu huku wakiwa na silaha. Polisi wote wakabaki wakiwa wameshikwa na bumbuwazi kubwa sana, kwa haraka wakamuwahi Camila na kumpokonya bastola aliyo nielekezea.

“Ethan upo salama?”

Askari mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu. Askari hawa wakaanza kunifungua pingu pamoja na kamba, sehemu ambalo alikuwepo dada Mery kuna mwili wa mlinzi mmoja. Camila kila anacho ulizwa na askari hawa juu ya hichi kilicho tokea hapa anashindwa kuzungumza.

Nikatolewa nje na madaktari wa kitengo hichi cha polisi wakaanza kunishuhulikia jeraha lililopo mgongoni mwangu huku wote wakiwa na shauku ya kuhitaji kunihoji maswali. Sikuweza kuwaona wazazi wa Camila katika eneo hili zaidi ya watu wengine.

“Mumejuaje nipo hapa?”

Nilimuuliza mmoja wa askari anaye nishuhulikia jeraha langu.

“Tulipigiwa simu na mama Camila, akisema kwamba mtoto wake amekuteka na amesikia milio ya risasi ikitokea huku”

“Mama?”

“Ndio, ilikuwaje hadi imekuwa hivi?”

Nikashusha pumzi sana huku nikifiria usaliti alio ufanya mama Camila kwa mwanaye. Nikawaona wazazi wa Camila wakimkimbilia mtoto wao aliye wekwa chini ya ulinzi mkali wa askari.

“Una uhakika mama yake ndio aliye piga simu kwenu?”

“Asilimia mia moja”

Nikamtazama Camila jinsi anavyo kumbatiwa na wazazi wake. Kitu kinacho nishangaza ni kulia kwa mama yake, jambo lililo nifanya nijiulize swali kama aliamua kumsaliti mwanaye sasa hivi kwa nini ameamua kulia. Camila akaingizwa kwenye moja ya gari la askari. Baba Camila akaonekana kuzungumza na askari hao ila hapakuwa na askari ambaye anamsikiliza na kila askari anafwata sheria za nchi zinavyo kwenda. Hata kama wewe ni mtoto wa kiongozi, ukifanya makosa ni lazima watakukamata. Mama Camila akaanza kutembea huku akitufwata kwa kasi katika eneo hili ninalo patiwa matibabu.

“Ethan ni nini ulicho kifanya eheee?”

Mama Camila alizungumza kwa ukali sana huku akinitazama usoni mwangu.

“Mwanao ndio aliye niteka mimi na kunisababishia majeraha mgongoni mwangu”

Mama Camila akanizaba kofi zito la shavuni mwangu na kuwafanya askari wa kike walio karibu na eneo hili kumzuia, kwani kufanya hivyo navyo ni kuvunja sheria.

“Ole wako mwanangu afungwe nitahakikisha na wewe unafungwa”

Mama Camila alizungumza kwa hasira sana huku akiondolewa katika eneo hili. Hapa ndipo nikatambua kwamba mchezo wote wa kupiga simu ameufanya Ethan, jini mwenye uwezo wa kujibadilisha kila aina ya mtu amtakaye yeye. Nilipo maliza kupatiwa matibabu na mimi nikaingizwa kwenye gari la polisi na safari ya kuelekea makao makuu ya polisi ikaanza. Ukimya ndani ya gari hili umetawala kiasi cha kunifanya nizidi kusongwa na mawazo kichwani mwangu. Mahusiano yangu na Camila yamebadilika sana na kuzalisha uaduia mkubwa sana. Mipango yote ambayo tulikuwa tumeipanga kwenye maisha yetu pale tutakapo ingia kwenye ndoa, ndio tayari imesha vurugika.

Nikafika katika kituoa cha polisi na kukuta kundi kubwa la waandishi wa habari wakitusubiria hadi nikajikuta nikishangaa na kujiuliza wametokea wapi hawa. Wandishi wa habari wakandelea kufanya kazi yao ya kuchukua kila tukio linalo endelea huku wengine wakiwa na shahuku ya kunihoji ila polisi waliwazuia na nikafanikiwa kuingia ndani ya jengo hili kubwa lenye gorofa zaidi ya thelathini. Nikaingizwa kwenye chumba cha mahojiano na kuachwa peke yangu. Nikaanza kukumbuka tukio la Ethan jinsi alivyo kuwa akiwaua walinzi hao na mbaya zaidi amewachomoa chomoa mioyo yao.

‘Ethan’

Niliita kimoyo moyo, baada ya sekunde kadhaa Ethan akakaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu na tumetenganishwa na meza tu.

‘Vipi dada yangu yupo sehemu salama?’

‘Ndio nimemuweka sehemu salama kabisa, na kidonda chake kimepona’

‘Camila je?’

‘Bado unamkumbuka huyo mpuuzi?’

‘Hapana, ila nataka kufahamu kwamba yupo wapi?’

‘Yupo kwenye chumba cha mahojiano’

‘Ni kitu gani ambacho kimempata hadi kuwa vile?’

‘Ni hasira tu ndio imepelekea yeye kuwa vile’

‘Mmmm sasa hii kesi si ataibeba yeye?’

‘Nakusikiliza wewe, kama unahitaji apotelee jela, nipo tayari hii kesi kumgeuzia yeye?’

Nikaka kimya huku nikimtazama Ethan usoni mwake. Uzuri mazungumzo yetu hakuna binadamu yoyote anaye yasikia. Nikasimama kwenye kiti na kuanza kuzunguka ndani ya chumba hichi huku nikitafakari ni kitu gani nimjibu Ethan. Nikakumbuka maisha ya nyuma ambayo tuliishi na Camila, maisha ambayo kila mmoja alikuwa akituzungumzia sisi. Nikakumbuka kipindi cha utoto jinsi alivyo kuwa akinitetea shule kutokana na ubaguzi wa rangi ulivyo kuwa kipindi hicho.

‘Fanya mamuzi sahihi’

Ethan alizungumza huku akiwa amesimama nyuma yangu.

‘Mbeleni hato kuja kunidhuru?’

‘Ni ngumu sana kuzungumzia vitu vya mbeleni, kwani dunia hubadilika kila kukicha’

‘Iue kesi kwa upande wake’

‘Sawa nitambambikia kesi daktari aliye kufanyia upasuaji huko nyuma.’

‘Kwani hukumuua?’

‘Yupo hai, utaona nitakacho kifanya, na hata ukiiulizwa maswali hakikisha kwamba unamtetea Camila kwamba bastola aliishika kwa ajili ya kujitetea mara baada ya kukuta dokta akiwaua walinzi wake kwa kuwachomoa mioyo yao’

‘Hilo linaweza kukubalika kweli?’

‘Ndio linakubalika, huku mimi nitatengeneza ushahidi wote na kila jambo litakwenda vizuri sawa’

‘Sawa’

Ethan akanishika bega kisha akapotea katika eneo hili. Mlango ukafunguliwa na akaingia mzee mmoja wa makamo. Mzee huyu akakaa kwenye kiti alicho kuwa amekalia Ethan.

“Habari yako bwana Ethan”

Alisalimia huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu nikarudi na kukaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia.

“Nahitaji kufahamu ni kitu gani kilitokea?”

“Wapi?”

“Kwenye eneo la tukio?”

Nikakaa kimya kwa sekunde kadha huku nikiwa nimeinamisha kichwa changu chini. Nikamtazama mzee huyu.

“Nilipo toka hospitalini leo asubuhi, nilielekea nyumbani kwa wakwe zangu. Nikiwa pale jina langu lilitajwa na magaidi, nina imani kwamba utakuwa umeona video ile”

“Ndio nimeiona”

“Nilichanganyikiwa kwa kweli, na niliingia chumbani kwa Camila kwa muda kidogo. Baba yake aliingia chumbani mule akihitaji ufafanuzi juu ya boksi hilo jeusi ambalo kwa kweli mimi silifahamu”

Nilizungumza kwa upole sana huku nikimtazama mzee huyu usoni mwake.

“Baada ya kutoka nje nikiwa ndani ya gari, Camila naye aliingia. Ila baada ya muda kidogo alitoka na kuelekea ndani”

“Kwa nini alitoka?”

“Tulipishana kauli za kimapenzi”

“Kauli gani hizo?”

“Mzee mahusiano yangu na Camila si ya kuhojiwa, kwani wewe na mke wako hamkuwahi kugombana?”

“Sawa, endelea”

Walinzi walinizunguka huku wakiwa wamenishikia bastola, wakaniamrisha kutoka ndani ya gari. Mmoja wao akanipiga mtama na nikaanguka chini. Wakanifunga pingu na kunipeleka katika ile nyumba ya pembeni mulipo nipata. Mlinzi mmoja alinipiga sana huku akinilazimisha kunihoji ni wapi lilipo hilo boksi jeusi, ila sikuweza kumjibu chochote zaidi ya kuendelea kunipiga”

“Ilikuwaje walinzi walikufa?”

“Daktari aliingia ndani ya chumba hicho kwa kuvunja mlango, sijui alikuwa na nguvu za aina gani. Walinzi walijaribu kumshambulia kwa risasi, ila cha kushangaza hakufa. Alianza kuwatoa mioyo yao mmoja baada ya mwengine. Hadi anaingia Camila pale alikuta watu wote wapo chini, akashika moja ya bastola huku akijaribu kumshambulia dokta yule kwa maana alikuwa katika hatua za kuniua mimi kwa kunitoa moyo”

“Unataka kusema kwamba Camila hausiki na chochote?”

“Atahusikaje na tukio hilo ikiwa yeye ndio alikuja kuniokoa”

“Kwa nini ulikamatwa na walinzi wao?”

“Hilo sio swala langu, ungemuuliza mgombea uraisi, ni kwa nini walinzi wake walinikamata”

“Unakumbuka chochote juu ya daktari?”

“Ndio baada ya kuwaua wale walinzi, alinipasua hapo nyuma ya mgongo wangu, sikujua anatafuta nini ila kabla hajamaliza anacho kifanya ndipo Camila alipo tokea”

“Tunashukuru”

“Nipo tayari kuondoka?”

“Tutakufahamisha mara mahojiano yetu yatakapo kishwa”

Mzee huyu akatoka chumbani humu na kuniacha peke yangu. Ethan akarudi tena na kuiweka miguu yake juu ya meza huku akitabasamu sana.

“Ethan rafiki yangu naomba kitu kimoja”

“Kitu gani?”

“Namuhitaji nimuoe dada yako”

“Merry au dada yangu yupi?”

“Huyo huyo, sikuwahi kufahamu kama ni mzuri kiasi kile”

Nikamtazama Ethan huku nikiwa nimemkazia macho.

“Sawa ni wewe na yeye mimi sipo hapo”

“Nashukuru”

Ethan akaondoka na kuniacha peke yangu, mlango ukafunguliwa, akaingia mwanasheria wa kampuni huku akiwa ameongozana na mzee ambaye alikuwa ananihoji maswali. Nikaruhusiwa kuondoka eneo hili.

“Pole sana bosi”

“Nashukuru”

Tukatoka nje na kukutana na kundi la waandishi wa habari ambao wanamuhoji Camila na wazazi wake. Waandishi wa habari walipo niona mimi wakakimbilia wote kwangu na wakanizingira huku kila mmoja akihitaji kunihoji swali lake. Sikuwajibu kitu chochote hawa waandishi wa habari, nikatembea hadi walipo simama Camila na wazazi wake.

“Mumenionyesha uhalisia halisi wa familia yenu nawashukuru sawa. Ila CAMILA kuanzia hivi sasa sahau kama kuna mwanaume ulisha wahi kumpenda anayeitwa Ethan. Na mzee ninatoa asilimia zangu za mchango nilizo kuchangia kwenye kampeni zako tusijuane kuanzia hivi sasa. Asanteni”

Mara baada ya kuzungumza maneno hayo huku mwanasheria wangu akiwa amesimama nyuma yangu tukaondoka eneo hili na kumuacha Camilia akiangua kilio kizito sana ambacho sikuhitaji kukijali kwani alicho kua anakitafuta kwangu tayari amesha kipata.



Tukaingia ndani ya gari la mwana sheria na kuondoka katika eneo hili.

“Una simu ya ziada ambayo huitumii?”

“Ndio ninayo”

“Naomba uniazime kwa muda”

Mwanasheria wangu akanikabidhi simu yake. Nikaingia katika mtandao wa Twitter na kuandika neno kwamba ‘MIMI NA WEWE, IMEKWISHA’

Ndani ya dakika mbili, nikapata ujumbe wa maswali mengi sana, kwani watu wengi nimewaacha njia panda. Wapo walio hisi labda matatizo yatakuwa yamekwisha na wapo walio hisi kwamba mimi na Camila mahusiano yetu yamekwisha. Sikuhiyaji kujibu swali la mtu yoyote na nikaawacha hewani. Tukafika nyumbani, na kuwakuta dada Mery na mama wakiwa wamekaa sebleni. Kidogo bibi Jane Klopp macho yake hayaoni vizuri, ila ni mtu makini anaye ifahamu harufu yangu.

“Ethan mwanangu”

Bibi Jane Klopp alizungumza huku akiitanua mikono yake, nikamfwata alipo kaa na nikamkumbatia kwa nguvu.

“Pole sana mwanangu”

“Asante sana mama”

Dada Mery akanitazama kwa macho makali sana.

“Ethan naomba tuzungumze”

Dada Mery alizungumza huku akinyanyuka kwenye sofa alilo kalia. Tukaongozana hadi chumbani kwake.

“Ethan ni kitu gani ambacho kinaendelea.”

Dada Mery alizungumza huku akiwa amenikazia macho. Nikaka kimya huku nikijifikiria ni kitu gani ambacho ninaweza kumuambia dada Mery akakielewa.

“Sijakuelewa?”

“Ethan kuna mambo yametokea kwenye masaa kadhaa hapa nyuma, sijaelewa na sijui ilikuwaje hembu niambie”

“Kuna mambo yanayo endelea, ila nakuomba unipe muda kila jambo likikaa vizuri basi nitakujulisha”

“Ethan nahitaji kujua sasa hivi”

Akatokea Ethan ndini ya chumba hichi na kumfanya dada Mery kupiga kelele, ila nikawahi kumziba mdomo wake ili kelele zake zisimstue mama aliye kaa sebleni. Dada Mery macho yakamtoka kwa maana katika maisha yake hakuwahi kuona mtu akijitokeza gafla mbele yake.

“Nakuomba utulie dada”

“Halooo Mery”

Ethan alizungumza huku akikaa kwenye moja ya kiti humu ndani huku akiwa amevalia suti ya dhahabu.

“Wewe ni nani?”

Dada Mery alizungumza huku akiutoa mkono wangu mdomoni mwake.

“Ni wajina wa mdogo wako”

“Wajina ndio nini?”

“Ninaitwa Ethan, nimekuwa na urafiki na mdogo wako toka kipindi alipo kuwa mtoto mdogo na nimekuwa ni msaada mkubwa sana kwake”

“Shindwa na ulegee kwa jina la Yesu?”

“Kumbuka hata mimi nina mfahamu Yesu na tumepewa mamlaka ya hapa Duniani. Siwezi kushindwa pale ninapo kuwa na nia nje kwako”

Ethan alizungumza kiustarabu huku akiwa amejawa na tabasamu pana. Muonekano wa Ethan wa leo kidogo ni wa tofauti. Umri wake unaendana na dada Mery tofauti ni siku nyingine anavyo nijia katika makamu yangu. Amependeza sana kwa muonekano wake ambao hakika una mvutia dada Mery.

“Dada zungumza naye mimi ninakuja”

Dada Mery akataka kunifwata ila Ethan akamnyooshea mkono na kumtuliza na kumfanya ashindwe kwenda popote, taratibu dada Mery akamfwata Ethan sehemy alipo kaa na wakaendelea kuzungumza. Nikafika sebleni na kumkuta mwanasheria wa kampuni akizungumza na mama.

“Ethan kuna habari njema”

“Habari gani?”

“Wanafunzi wameokolewa ma majeshi ya Marekani, Ufarana an Uingereza”

Mwanasheria alizungumza huku akinionyesha picha za matukio hayo kwenye simu yake.

“Hawa walio pigishwa magoti ndio watekaji?”

Nilizungumza huku nikimtazama mpiganaji mmoja baada ya mwengine wa kundi hili la Al-Shabab.

“Ndio”

“Mmmm ni wengi aisee”

“Yaa ni wengi, sana. Watoto wa kike wanapandishwa kwenye helicopter ya jeshi. Watapelekwa Afrika kusini. Wanafanyiwa uchunguzi wa kiafya kisha wataletwa huku Ujerumani”

“Mungu ni mwemama kwa kweli. Je hawa wapiganaji nao wanapelekwa wapi?”

“Hayo ni mambo ya kijeshi, sijaweza kufahamu kwa kweli.”

“Ethan”

“Naam mama”

“Naomba tuzungumze”

Taratibu nikakaa pembeni ya mama. Nikamuomba kwa ishara mwanasheria atupishe na atangulie katika ofisi katia jengo moja nje ya jumba hili.

“Ndio mama”

“Umesha wahi kuzungumza na dada yako, kuhusianana swala lake la kuolewa?”

“Hapana mama, sijawahi kuzungumza naye”

“Hembu basi jaribu kuzungumza naye. Unajua umri wa dada yako unakwenda sasa. Hajapata mtoto wala hajawahi niletea mwanaume wa kunitambulisha au anataka nife ndio azae”

“Nitazungumza naye mama yangu, wala usijali”

“Hembu ongea naye bwana, nahitaji kufa nikiwa nimemshika mjukuu wangu. Au kama yeye ana chelewa muwahi basi. Umpatie Camila ujauzito”

Kauli hii ikanifanya nikae kimya kwa muda kdigo. Nikatazama katika mlango wa kuingilia humu ndani, nikamuona Camila akiwa amesimama kwa unyonge sana huku mikononi mwake akiwa ameshika kipocho kidogo.

“Huyo ni Camila?”

Bibi Jane Klopp aliniuliza huku akinitazama. Nikamkazia macho kamila, kwa maana mimi na yeye tayari mahusiano yetu yalisha kwisha.

“Ndio mama”

“Ohoo karibu mkwe wangu”

Camila akaanza kutembea kwa unyonge hadi alipo mama, akamkumbatia na kuanza kuangua kulia jambo lililo nifanya nizidi kukasirika.

“Unalia nini mwanangu”

“Mama ni Ethan”

Camila aliendelea huku akiendelea kumkumbatia bibi Jane Klopp. Nikatamani kuwaachanisha, ila nikashindwa kufanya hivyo, kwani sihitaji bibi Jane Klopp afahamu kwamba mimi na Camila tuna tofauti kati yetu.

“Amefanyaje Ethan?”

“Camila njoo tuzungumze”

“Ethan mbona sauti yako imebadilika, umegombana na mwenzako?”

Bibi Jane Klopp alizungumza kwa upole huku wakiachiana na Camila.

“Hapana mama ni mambo ya kawaida?”

“Mbona mwenzio analia, sijamzoea kumuona Camila akiwa hivi na amekuwa mnyonge sana. Eti Camila niambie ni kitu gani kimetokea”

Camila akanitazama kw amacho ya woga huku akijawa na wasiwasi mwingi sana. Macho yangu ninayo mtazama nayo, dhairi yanaonyesha kwamba nimekasiria na ninamzuia kwa ishara ya macho kuto kumuambia bibi Jane Klopp kitu cha aina yoyoye.

“Ethan……”

Camila akaka kimya mara baada ya kukiweka kidole changu kimoja mdomoni na kumuashiria kwamba akae kimya.

“Amefanya nini?”

“Mama nilimuambia Camila kwamba nina acha kucheza mpira maisha mwangu na ninataka kusimamia biashara za baba, ndio maana kitu hicho kimemuumiza”

Ilibibi niongopee ili mradi kuficha tofauti zetu mimi na Camila, kwani bibi Jane endapo atafahamu juu matatizo yanayo endelea hivi sasa, nina imani kwamba ndio utakuwa mwanzo wake wa kufa kwa presha.

“Kwa nini Ethan, ikiwa marehemu baba yako alikuwa ni mchezaji mzuri. Hembu fwata nyayo zeka bwana usiwe hivyo. Uje ni wengi utawaumiza, si yeye tu hata wale mashabiki wako Ethan”

“Kweli mama, nilsha muambia hilo, na timu yake imekataa kuingia uwanjani kwa mechi zilizo baki kwa ajili yake, wanahitaji arudi uwanjani”

Camila naye aliendeleza uongo wangu, ili mradi kumfunga akili bibi Jane Klopp.

“Ohoo Ethan sio vizuri bwana, kumbuka hizi kampuni zina wasimamiaji. Hembu sikiliza kilio cha mpenzi wako, na fanya maamuzi ya kuto kumuumiza Camila. Tambua kwamba Camila anakupenda na kukuhiji ndio maana ana umi sana kwa maamuzi yako sawa mwanangu”

Bibi Jane alizungumza kwa suati ya upole na iliyo jaa hekima ndani yake.

“Sawa mama”

“Unajua siku ambayo baba yako alikuwa ana stafu kucheza mpira. Tulilia sana, nilisha zoea kukaa uwanjani na kumshangilia, nilijisikia furaha zaidi pale alipo kuwa akifunga goli. Hivyo natambua maumivu ya kama mke wa mchezaji mpira. Ethan mwanangu, ninakupenda sana tena sana. Hembu jaribu kufurahisha moyo wa mpenzi wako sawa mwanangu”

“Sawa mama nimekuelewa sana na ninakuahidi nitahakikisha kwamba nina rudi uwanjani”

“Kweli mume wangu?”

Camila alijaribu kuzungumza huku akiwa na furaha ya uongo.

“Ndio mke wangu”

Nilizungumza neno hilo huku moyo wangu ukiwa umejawa na hasira na maumivu makali sana.

“Haya nyanyukeni mukatafute mtoto”

Bibi Jane Klopp alizungumza maneno yaliyo mshangaza sana Camila, ila sikuhitaji kumuonyesha Camila sura ya furaha. Tukiwa kwenye kordo ya kueleka chumbani kwangu, kwenye mlango wa dada Mery nikasikia miguno ya kimahaba, nikajikuta nikitabasamu tu, kwani Ethan naye anafanya mambo yake. Nikaingia chumbani kwangu na Camila akaingia na kufunga mlango kwa ndani.

Camila akapiga hatua moja mbele kisha akapiga magoti chini huku machozi mengi yakiwa yanamwagika usoni mwake.

“Nimevumilia japo kukaa kwa nusu saa peke yangu na kujiaminisha kwamba sina mwanaume ninaye mpenda kwneye maisha yangu, ila nimeshindwa Ethan”

Camila alizungumza huku nikiwa nimekaa kitandani na kumtazama usoni mwake.

“Ni bora ningekuwa nimewahi kuwa na mwanaume mwengine zaidi yako, ningesama basi acha niende kwake nitulize moyo wangu. Ila Ethan sina, Ethan ninakupenda sana mume wangu, nakuhitaji sana mpenzi wangu. Nilihisi njia niliyo itumia itakuwa ni rahisi kwangu kujua ni wapi lilipo boksi jeusi, ila kumbe ndio ninakupoteza Ethan. Ninakupenda sana”

“Ndiovyo jisni baba yako alivyo kutuma ili nisitoe asilimia thelathini ya pesa zangu nilizo wekeza kwenye kampeni zake si ndio?”

Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo kadhaa inayo dhihirisha kwamba nina hasira.

“Ethan, sipo hapa kwa ajili ya baba yangu. Nipo hapa kwa ajili ya upendo wangu kwako. Kumbuka nilisha weka ahadi kwenye maisha yangu. Nikikukosa wewe ni lazima nitajiua. Kumbuka siku nilipo hitaji kujitupa gorofani kwa ajili ya penzi lako”

“Ungejitupa tu. Sasa hivi tungekuwa tumesha kusahau wewe”

Nilimjibu Camila kwa dharua iliyo changanyikana na hasira. Camila akanitazama kwa macho yaliyo jaa huruma huku akionekana ni mtu anaye jutia kwa maamuzi yake.

“Ulinishika bastoka kama jambazi. Ulinidhalilisha na walinzi wako. Walinipiga wakanifunga pingu pasipo huruma ya aina yoyote. Nilikupa kipimo kidogo kama mwanamke kwenye maisha, nikihitaji kufahamu je nina mwanamke sahihi kwenye maisha yangu kumbe hapana. Umenionyesha moyo wa kishetani ambao hata mtu wa kawaida anashangaa kwa kweli, kwani nini lakini eheee?”

Nilizungumza huku machozi ya hasira yakinimwagika usoni mwangu.

“Mangapi ambayo tulifanya siri Camila, mangapi ambayo tulipanga kwenye maisha yetu. Okay kwa mfano sasa mimi ni gaidi, na wewe mke wangu umeulizwa na polisi ni wapi nilipo, kwa hiyo ungewapa ushirikiano wa kunikamata si ndio?”

Camila akatingisha kichwa akimaanisha kwamba asinge wapa ushirikiano polisi.

“Acha unafki mtoto wa kike. Umenionyesha dhairi kwamba wewe sio mwanamke wa kuoa. Umenibagua kirangi na kuniiita sokwe. Sawa mimi ni sokwe, nakuomba usinipende na usokwe wangu. Nitatafuta sokwe mwazangu, niishi naye na nitavumiliana naye kwenye shida na raha, tabu na majanga kama uliyo nifanyia leo. TOKA NYUMBANI KWETU”

Nilizungumza kwa kufoka sana hadi mishima ya damua ikavimba katika mikono yangu. Camila taratibu akasimama na akaanza kunifwata kwa hatua za taratibu, jambo lililo nifanya niamke kiatandani na kumfwata sehemu nilipo, ili nimrudishe mlangoni n aondoke zake. Kitendo cha kumshika mkono wake, akachomoa kisu cha kukunjua ndani ya kipochi chake. Akanichoma kisu cha tumboni mwangu, jambo lililo nifanya nihisi maumivu makali sana ambayo toka kuzaliwa kwangu sikuwahi kuyapata.

“Ni bora tufe wote kuliko kuendelea kukukosa wewe”

Camila mara baara ya kuzungumza maneno hayo, akakichomoa kisu hicho kwa nguvu tumboni mwangu kisha naye akajichoma tumboni mwake na akawa wa kwanza kuanguka chini huku nami nikianguka pembeni yake.



Camila taratibu akaanza kuuleta mkono wangu kwangu huku machozi yakiwa yanamwagika usoni mwake. Taratibu giza zito likaanza kunitawala usoni mwangu, kabla sijaipoteza nuru ya macho yangu. Nikamuona Ethan akisimama mbele yangu huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Ethana akatuwekea mikono yake kwenye majeraha yetu ambayoa baada ya sekunde chache, maumivu makali amnbayo tulikuwa tunayahisi, yakapotea na Camila akawa mtu wa kwanza kukaa kitako huku akijishangaa.

“Kwa nini umefanya hivi binti?”

Ethan alimuuliza Camila kwa sauti nzito sana hadi Camila akaanza kutetemeka.

“Nipo mbinguni ehee…..!!?”

Camila aliuliza swali ambalo lilizidi kumkasirisha Ethan, kwani alishika kwa mikono yake na kurushia kitandani na kutaka kumuadhibu.

“Ethan usifanye hivyo, nitalishuhulikia”

NIlizungumza huku nikijinanyua kitandani taratibu, Ethan akanitazama kwa macho yaliyo jaa hasira, kwa ishara ya kutingisha kichwa nikamuomba tena asiweze kufanya jambo lolote baya. Ethan akapotea ndani humu, taratibu nikasimama na kuanza kumfwata Camila kitandani alipo lala huku akiwa amejionea mauza uza.

“Ethan tupo mbinguni, etii?”

“Umeona wapi mbinguni kukiwa na vitanda, acha upuuzi Camila”

Nilizungumza kwa kufoka kidogo huku nikimtazama Camila usoni mwake.

“Kwa nini unakuwa mjinga, umeona kuniua ndio suluhisho la tatizo”

“Bila wewe Ethan tambua siwez…………”

Nikamzaba Camila kofi la shavuni mwake, ikiwa ndio mara yangu ya kwanza kumpiga toka tuanze mahusiano. Camila akaa kimya huku akitazama chini na machozi yakimbubujika.

“Unakuwa mpumbavu, unakuwa mjingia, wewe ni mwanamke wa aina gani usiye elewa kwamba kuna maisha na kufa. Kuna kitu gani kimeingia kwenye ubongo wako. Au huko Tanzania walikuroga si ndio?”

Nilizungumza kwa kufoka sana hadi Camila akaanza kutetemeka, taratibu akanitazama huku nikishuhudia jinsi vidole vyangu vilivyo acha alama shavuni mwake.

“Nilikupenda, nilikujali na nikakueleza vitu vyangu vingi kwa ajili yako. Leo hii unataka kuniua nikiwa bado mdogo ili iweje eheeee”

Nilizungumza huku nikimtingisha Camila mwili wake. Camila kwa haraka akanishiaka mashavu yangu na kuanza kuninyonya midomo yangu, nikajaribu kumtoa, ila akaendelea kuning’ang’ania kwa nguvu sana. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi Camila alivyo zidi kuipoteza hasira yangu hadi mwishowe nikajikuta nikilainika na kuendelea kumnyonya midomo yake.

Kweli mapazi yana nguvu sana kwenye mioyo ya watu wengi. Ndani ya muda mchache tu, tumejikuta tukisahau kila kitu ambacho kilitokea. Tukaanza kuvuana nguo zetu na ndani ya muda mchache tukajikuta tukiwa tupo kama tulivyo zaliwa.

Tukaanza kupeana burudani huku kila mmoja akiwa katika furaha kubwa ya kurudisha penzi lililo kuwa limeyumba kwa muda. Hadi tunamaliza mzunguko wa kwanza kila mmoja alijawa na furaha.

“Nataka tena mume wangu”

“Ngoja kidogo nivute pumzi”

Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na tabasamu pana sana. Camila akaanza kumshika jogoo wangu, ambaye hakumaliza hata sekunde stini akasimama tena. Camila akanitazama huku akijilamba lipsi zake kwa ulimi. Akaninyonya lipsi zangu kidogo kisha akamkalia jogoo wangu huku akitoa miguno milaini ya kimahaba. Akaanza kumkatikia jogoo wangu, jambo ambalo kwake ni adimu sana kulifanya, toka mimi na yeye tulivyo juana.

“Camila”

Nilizungumza huku nikiwa nimeshika kiuno chake ambacho bado kinaendelea kuzunguka kama gurudumu la cherehani.

“Mmmm…..”

“Nani kakufundisha mambo haya?”

“Ohoo Tanzania hiyo mume wangu”

“Tanzania?”

“Eheee?”

“Ndio imekufundisha?”

“Yaaa….kun…a….aiiiss….ohooo….dada….”

“Dada mmoja alikuwa akitumfundisha maswala ya chumbani na hapa ndio ninafanya kwa vitendo”

“Mmmm….”

“Niamini mume wangu”

Camila hakutaka hata kunipa nafasi ya mashambulizi, alicho fanya ni kuzidisha kasi ya kiuno chake hadi nikajikuta waarabu wangu wakishindwa kujizuia na kutoka bila idhini yangu.

“Ohooo….ahaaaa”

Camila alitoa miguno hiyo kisha taratibu akanilalia kifuani mwangu na kuanza kuninyonya midomo yangu taratibu kwa hisia kali sana. Katika mapenzi yetu toka nimfahamu Camila, leo hii ndio nimeweza kufurahia penzi lake kwa asilimia mia moja.

“Hii ni mbinu namba moja tu mume wangu tuliyo fundishwa. Kuna mbinu nyingine tisa bado sijazitumia”

“TISAAAAA…..!!!?”

“Ndio mume wangu”

“Ohoo Mungu wangu, utaniua mke wangu, si kwa utamu huu”

“Haa, sasa ulipo kuwa unataka kuniacha ulidhani kwamba mautamu haya ningempa nani jamani?”

Camila alizungumza kwa sauti ya kudeka hadi mimi mwenyewe nikabaki nikiwa na kigugumizi kizito.

“Leo sihitaji kurudi nyumbani, nata tupeane usiku kuacha na kama mama jisni alivyo sema, lazima unipatie mtoto”

“Ila kumbuka kwamba bado tupo shuleni?”

“Hivi kwa hili lililo jitokeza unahisi nitarudi tena shule. Siwezi kurudi shule, kwa sasa nataka kusimamia kampuni za baba yangu, mara baada ya kushinda kiti cha uraisi”

“Ohoo tena nimekumbuka kitu”

“Kitu gani?”

“Ngoja ninakuja”

Nilizungumza huku nikishuka kitandani, nikafungua kabati langu la nguo. Nikachukua tisheti pamoja na pensi fupi kiasi.

“Ethan unakwenda wapi?”

“Ninakuja sasa hivi mke wangu”

Nilizungumza huku nikivaa nguo hizi, nikatoka chumbani humu na kumuacha Camila kitandani. Nikampita bibi Jane Klopp sebleni pasipo kumsemesha chochote, nikaelekea kwenye jengo la ofisi, nikamkuta mwana sheria akiwa anazungumza na simu. Nikaka kwenye kiti changu na ofisini humu na nikamsubiria amalize kuzungumza.

“Mkuu nimesha weka taratiu zote za kutoa asilimia thelathini tulizo weka kwenye kampeni za mgombea uraisi ninasubiria tamko lako la mwisho tu nipitishe”

Mwanasheria alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.

“Umesema umesha andaa jinsi ya kuzitoa asilimia zangu?”

“Ndio”

“Hembu ongeza asilimia ishirini na ziwe hamsini?”

“NIONGEZEE……!!??”

Mwanasheria aliniuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana, kwani maamuzi aliyo kuwa akiyategemea kutoka kwangu yamekuwa ni tofauti.

“Fanya kama nilivyo kuambia. Nina mipango mikubwa ambayo nimeifikiria, akikosa uraisi, mambo ninayo yafikiria nina imani kwamba hayato weza kwenda sawa”

Mwanasheria akajawa na kigugumizi kikubwa sana ambacho hakika kinaonyesha dhairi kumuweka njia panda.

“Piga simu na waambie kwamba Ethan Klopp ameongeza asilimia za kumdhamini mgombea uraisi na kama watahitaji kampeni yangu kubwa kwake, basi nitampatia”

“Kuna kitu gani kinacho endelea mkuu?”

“Nitakueleza. Niakwenda kulala sasa hivi, ukimaliza unaweza kwenda tu nyumbani sawa”

“ETHAN, ninakufahamu, hembu zungumza ni kitu gani kinacho endelea”

“Mimi na Camila tumesha rudiana”

“Nini!!!?”

Mwanasheria alizungumza kwa mshangao mkubwa sana.

“Ndio tumerudiana na sasa hivi huko ndani tunatafuta mtoto kufuta matatizo yetu. Hichi ninacho kifanya, ninawekeza kwa mwanangu na sio kwao umenielewa”

Mwanasheria akabaki akitabasamu, nikaanza kutembea hadi mlangoni mwa ofisi hii, kisha nikamgeukia.

“Iwe siri yako, mambo yanayo endelea kwenye mitandao ya kijamii, wewe yapotezee sawa”

“Sawa mkuu”

Nikatoka humu ndani na kuanza kuelekea ndani huku nikiwa nimejawa na furaha huku kichwani mwangu, nikiwa nawazia mbinu tisa zilizo bakia kwa Camila, kwani kama ni mbinu ya kwanza imenipagawisha namna hii, nina imani kwamba mbinu hizo tisa, zitanifanya niwe zuzu kabisa.

Nikamkuta dada Mery na mama wakiwa wamekaa sebleni, huku Mery akionekana kuwa na furaha kubwa sana na mazungumzo ambayo walikuwa wakizungumza na mama waliyakatisha mara baada ya kuniona.

“Nini?”

Dada Mery aliniuliza mara baada ya kuona nimemkazia macho sana.

“Hamna jamani”

“Mbona una cheka cheka?”

“Hata wewe mbona una cheka cheka. Hembu nenda ndani huko kuna mambo nahitaji kuzungumza na mama”

Nikatabasamu tu kisha nikaanza kupandisha ngazi, nilipo fika katkati ya ngazi, nikasimama kisha, nikanyata na kutega siko langu ili niweze kumsikiliza dada Mery ni kitu gani ambacho anakizungumza na mama.

“Yaani huwezi kuamini mama. Toka ulivyo nizaa na nijitambue kwenye mambo ya mapenzi, leo hii ndio nimekojo*** katika tendo la ndoa”

Nikajikuta nikitabasamu, na nikaendelea na mambo yangu huku nikijisemea kimoyo moyo kwamba Ethan amefanya yake. Nikaingia chumani na kumkuta Camila akiwa amejifunga shanga kiunoni.

“Za nini tena hizo?”

“Hii ni mbinu namba mbili mpenzi wangu”

Camila alizungumza huku akinishika mkono kuelekea kitandani, kabla hatujafika kitandani, akainama na kushika kitanda, taratibu akaanza kukatika, jambo lililo sababisha hisia zangu kurudi kwa kasi sana. Nikajikuta nikivua nguo zangu zote na kuanza tena kumshuhulikia, ushirikiano ambao Camila ananipa hakika kama ningemuacha, ningeenda kumnufaisha bwege mwengine ambaye hajui hata jinsi nilivyo itoa bikra ya Camila.

“Nakupenda sana mume wangu”

“Nakupenda pia”

Simu ya Camila ikaanza kuita, akashuka kitandani taratibu, akaokota kipochi chake chini na kuitoa.

“Ni nani?”

“Baba”

“Ahaaa sawa”

“Ndio baba”

“Kweli?”

“Ohooo asante sana mume wangu”

Camila alizungumza kwa furaha huku akinikimbilia akanikumbatia kwa nguvu sana hapa kitandani nilipo lala.

“Huyu hapa zungumza naye”

Camila akaniwekea simu hii sikioni mwangu na nikaisikia sauti ya baba yake.

“Ndio baba”

“Nashukuru sana kwa kiwango ulicho kiongeza kwenye kampenzi zangu. Mungu azidi kukubariki”

“Nashukuru sana”

“Naomba pia unisamehe kwa yale yote yaliyo pita kwani ni tatizo letu”

“Nashukuru pia baba, tupo pamoja”

“Asante, haya endeleni kufurahia muda wenu”

“Nashukuru”

Nikamabidhi Camila simu yake.

“Ndio baba”

“Sawa, tutaonana kesho”

“Nakupenda pia baba”

Camila akakata simu huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.

“Baba amefurahi sana kwa kuongeza asilimia zako kwenye kampeni zake za uchaguzi”

“Usijali, na ninawazo nimelipata”

“Wazo gani mume wangu?”

“Nahitaji kufanya matangazo ya kampeni yake. Umaarufu unaweza kumsaidia kuzidi kupata wafuasi wanao muamini”

Camila akanikumbatia kwa nguvu sana huku akiwa amejawa na furaha.

“Ndio maana ninakupenda sana Ethan wangu, nakuahidi sinto fanya ujinga wa aina yoyote kwenye mapenzi yetu”

“Usijali mke wangu, yaliyo pita acha yapite, ila kwa sasa tutazame haya yaliyopo mbele yetu”

“Nashukuru na ninafuraha kusikia hilo”

Taratibu tukakumbatiana na Camila huku nyuso zetu zikiwa zimejawa na furaha. Tukaingia bafuni na kuoga kwa pamoja kisha Camila akavaa nguo zangu za michezo na tukatoka sebleni. Bi Jane Klopp alipo tuona, usoni mwake akajawa na furaha kubwa sana.

“Atakuwa wa kike”

“Nani?”

Niliuliza huku nikitabasamu.

“Huyo muliye mtafuta”

“Jamani mama”

“Kweli vile atakuwa wa kike”

Bibi Jane alizungumza katika hali ya utani. Dada Mery naye akaja sebleni hapa na furaha ikaendelea kutawala katikati yetu. Dada Mery na Camila wakaandaa chakula cha usiku. Muda ulipo wadia wa chakula tukala pamoja na nikasaidiana na Camila kumrudisha mama chumbani kwake.

“Ethan”

“Naam mama”

“Usije ukamuacha huyu binti. Mukiendelea kuwa pamoja mambo yenu mengi yatafanikiwa. Camila, natambua una hasira za karibu na unajiamini sana, hembu jaribu kidogo kuzizuia hata kama kuna jambo kubwa limetokea katikati yenu. Hakika mutadumu kwa miaka mingi sana”

Bibi Jane Klopp alizungumza huku akiwa ametushika mikono yetu.

“Nashukuru sana mama na nitafanya hivyo”

“Sawa, naweza kulala sasa”

Nikambusu bibi Jane Klopp kwenye paji lake la uso kisha tukatoka ndani humu. Usiku mzima tuliutumia katika kuburudishana kwa kila aina ya kimapenzi. Asubuhi na mapema, kama kawaida yangu nikaanza kufanya mazoezi mepesi mepesi ili kuendelea kuuweka mwili wangu sawa. Jioni ya siku ya leo nikarudi kambini hukun ikiwa nimeongozana na Camila ambaye kwa sasa ahitaji hata niwe mbali naye. Wachezaji wezangu wakazidi kufurahi mara baada ya kuniona nimerudi nikiwa na afya njema.

“Mwanangu shavu limekuwa, au ndio maisha mazuri?”

Frendando aliniuliza huku akiwa amejawa na furaha usoni mwake.Tukakumbatiana kwa muda kidogo.

“Ni shemaji yako ndio msababishaji wa haya yote”

“Samahani Ethan”

Muhudu wa hoteli hii tuliyo fikia, alizunumza huku akiwa amesimama pembeni yetu.

“Bila samahani”

“Kuna mzee pale anakuita”

Nikageuka nyuma yangu na kumuona mzee mwenye asili ya Kichina akiniita.

“Sawa”

Nilimjibu muhudumu huyu, kisha nikaanza kutembea hadi kwa mzee huyu, nikamsalimia kwa heshima zote kwa maana sifahamu ni nani.

“Ninaitwa Mr Shing Jing, nimetokea China”

“Nashukuru kufahamu”

“Kuna jambo kidogo nataka kushirikiana nawe, kama hoto jali naomba nafasi nikuonyeshe”

“Bila samahani”

Mzee huyu akachukua brufcase yake iliyopo pembezoni mwa miguu yake. Akaiweka mezani na kuifungua, akatoa bahasha ya kaki kubwa kiasi na kunikabidhi. Akaifunga brufcase yake na kuirudisha chini.

“Unaweza kufungua tu hiyo bahasha”

Nikaifungua bahasha hii, nikakuta picha nne ndani ya bahasha hii, nikaanza kutoa moja baada ya nyingine. Picha hizi zinamuonyesha mwana mama wa kiafrika akiwa amefungwa mikonono yake pamoja na mdomo wake na pembeni yake kuna wanaume wawuli walio shika mitutu ya bunduki.

“Hizi picha za nini kwangu?”

Mzee huyu akatabasamu huku akinitazama usoni mwangu.

“Huyo ni mama YAKO MZAZI, ana siku ya tatu toka vijana wangu wamshikilie. Biashara iliyopo hapa ni ndogo sana. Boksi jeusi, kwa uhai wa mama yako mzazi”

Maneno ya mzee huyu yakanitusha sana, nikazitazama picha hizi kwa umakini sana, taratibu taswira ya sura yangu nikaanza kuiona kwa mwanamama huyu jambo lililo nifanya nistuke huku mwili wangu ukisisimka hadi vinyweleo vyangu vya mwili vikaanza kunisiamama kwa mstuko huu nilio upata.



“Mama yangu!!?” Nilimuuliza mzee huyu huku nikimtazama kwa mshangao. Akanijibu kwa kutingisha kichwa, ila kila ninavyo jaribu kukumbuka kwamba nishawahi kuwa na mama katika maisha yangu, sina kumbukumbu hiyo.

“Nashukuru sana na sifahamu boksi hilo lililopo” Nilipo maliza kuzungumza maneno hayo nikamsogezea mzee huyu picha zake pamoja na bahasha.

“Muda mwengine usinijaribu kwa mambo ya kijinga na kipuuzi kama haya” Nilizungumza kwa msisitozo kisha nikanyanyuka na kaunza kuondoka.

“Kesho nitakuletea kidole chake” Neno la mzee huyu likanifanya nisimame kwa muda kidogo, nikamgeukia na kumtazama kwa umakini sana kisha nikaendelea na safari yangu. Nikajumuika na wachezaji wezangu kwenye mazoezi ya asubuhi.

“Ethan mbona unaonekana huna raha?” Kocha aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hapana kocha nipo sawa” “Una uhakika?” “Ndio nipo sawa”

Hata uchezaji wa uwanjani haukuwa mzuri kabisa, kwani mawazo ya maam mzazi yamenichanganya kabisa. Ila jambo ambalo lina nitatiza ni kwamba sina kumbukumbu ya aina yoyote inayo husiana na mama wala baba yangu mzazi, japo ninatambua kwamba mzee Klopp na bi Jane Klopp ni wazazi wangu.

“Kocha nakuomba nipumzike kidogo” Nilimuomba kocha huku nikimtazama usoni mwake.

“Hakuna tatizo, pumzika” Nikatoka nje ya uwanja na Camila akanikabidhi kitaulo kidogo cha kujifutia jasho mwilini mwangu.

“Mbona kama una mawazo mpenzi wangu” “Akili yangu haipo sawa” “Kuna nini kinacho kutatatiza?” “Hembu twende huku” “Mazoezi una acha?” “Nitashiriki jioni, twende huku” Nilizungumza huku nikianza kutembea kuelekea katika eneo ambalo nilikaa na mzee yule. Tulipo fika tukakua kuna watu wengine ambao walio kaa. Watu hawa wakajawa na furaha kubwa sana mara baada ya kutuona. Kila mtu akaanza kutamani tupige picha ya mapamoja.

“Tupige tu mpenzi wangu” Camila aliniambai kwa sauti ya chini kiasi, tukaanza kupiga picha kadhaa na watu hawa kisha tukawaaga na kuondoka.

“Tunakwenda wapi Ethan?” “Nahitaji kuingia kwenye chumba kinacho ongoza kamera za ulinzi katika hii hoteli” “Mmmm niambie mume wangu kuna jambo gania mbalo lina endele?” “Nitakueleza naomba uniazime simu yako” Camila akanipatia simu yake, nikampigia mwana sheria wa kampuni na kumuomba aweze kufika hotelini hapa. Kutona sehemu hii tulipo ni mbali na mjini, ikamlazimu mwana sheria kupanda helicopter ya kampuni yake na kufika katika hoteli hii.

“Ethan naomba uniambie ni jambo gani linalo endelea au huniamini?” Camila alizungumza kwa kulalama.

“Nitakuambia mpenzi wangu, nakuomba uweze kuwa mvumilivu katika hili ninalo kwenda kulifanya sawa” “Sawa” Camila alinijibu kwa unyonge, nikampokea mwana sheria na moja kwa moja tukaongozana naye hadi kwenye ofisi ya meneja wa hii hoteli. Meneja huyu akafurahi sana kuniona ofisini kwake. “Ndio Ethan niwasiaidie nini?” “Nahitaji kwanza ulinzi wa wachezaji wezangu, na sisi uweze kuongezwa” “Kwa nini unazungumza hivyo Ethan?” “Kuna hali ya hatari ambayo nimekutana nayo masaa kadhaa hapa hotelini kwako. Jambo hili litanifanya niweze kuiondoa timu yangu hapa. Nakuomba sana meneja uweze kufanya hivyo” “Sawa, tutaongeza ulinzi, ila ningependa kufahamu ni hatari gani ambayo ulikutana nayo” “Nakuomba twende kwenye chumba cha kuongozea kamera” Meneja huyu akatafakari kwa sekunde kasha akisha akakubali. Tukatoka ofisini hapa huku mwanasheri na Camila wakionekana kujawa na shahuku ya kuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea kwangu. Tukaingia katika chumba hichi kikubwa ambacho kina tv nyingi sana ambapo kila tv inaonyesha video ya kamera inayo rekodi eneo hilo.

“Karibuni, hichi ndio chumba chetu cha kuongozea kamera zote” Meneja huyu wa hoteli alizungumza.

“Nashukuru. Nakuomba uweze kuonyesha video iliyo rekodiwa katika eneo lile ambalo lipo pembezoni mwa swimming pool” “Turudishe majira ya saa ngapi?” “Saa moja na nusu hivi asubuhi leo” Kijana huyu ambaye tumemkuta ndani ya chumba hichi, akafanya kazi niliyo muagiza. Video ya mimi na mzee huyu wa kichina ikaanza kuonekana.

“Hembu hiamihshie kwenye tv kubwa” Meneja alizungumza na video hii ikaanza kuonekana kwenye tv kubwa kupita zote iliyopo katika chumba hichi. Nikaonekana jinsi ninavyo fungua bahasha na kutoa picha hizo.

“Hembu zoom kwenye hizo picha” Nilimuambia kijana huyu na akafanya hivyo na picha hizo zikaonekana vizuri sana. Watu wote wakaonekana kustuka sana kwani hizo picha zinaonyesha mwanamke huyo akiwa ametekwa.

“Nahitaji hizo picha na pia sura ya huyo mzee” “Sawa Ethan” “Baby kwani alikuambia yeye ni nani?” “Hakuniambia yeye ni nani aliniwekea hizo picha……” Mwanasheria akanitazama kwa macho yanago nikataza nisizungumze kitu cha aina yoyote kwa maana kuna watu hapaswi kufahamu nilicho kizungumza.

“Je munaweza kumsaka mzee huyo taarifa zake” Camila alizungumza huku akimtazama kijana huyu.

“Ndio inawezekana” “Basi ninaomba muweze kunisaidia katika hilo” Kijana huyu akaanza kazi hiyo ambayo haikuchukua muda mrefu sana akafanikiwa kupata taarifa muhimu za mzee huyu. Taarifa zinaonyesha kwamba mzee huyu uraia wake ni nchini China, na inaonyesha kwamba ametokea nchini Nigeria na kufika hapa Ujerumani, wiki moja iliyo pita. Taarifa zikaonyesha kwamba alingia nchini kama mfanya bishara kutoka katika shirika moja la simu lililopo nchini Nigeria.

“Makazi yake yapo nchini Nigeria?” Kijana huyu alizungumza.

“Inabidi tuwataarifu askari” “Hapana, tusiwaafahamishe askari kwa sasa. Tunahitaji kuzungumza na Ethan mara moja ndio tuamue” “Musimpeleke polisi, naomba hizo taarifa zake, umtumie Camila hapa kwenye simu yake pamoja na hiyo picha.” “Huoni kwamba anaweza kukudhuru?” “Tutajua nini cha kufanya, kesho atakuja aliniahidi hivyo. Hakikiseni kwamba kesho akija tu basi macho yenu yanakuwa makini kuhakikisha kwamba muna mpata” “Sawa” “Hili swala ni sisi watu watano munalifahamu, nawaomba wewe na kijana wako musiweze kutoa siri yoyote?” “Hatuwezi kuvujisha sira muhimu kama hizi na kesho asipo kuja basi muna haki ya wewe kututulia mashaka juu ya hili” “Ninashukuru sana” “Karibu sana Ethan” Tukatoka chumbani humu na moja kwa moja tukaeleka katika chumba changu na Camila, ambacho tutakitumia hapa hadi pale mashindano yatakapo kwisha.

“Wamekutumi hizo taarifa na picha?” “Ndio mume wangu” Nikaichukua simu ya Camila na kumtazama mzee huyu, nikarudi kumtazama mama huyu anaye onekana kwenye picha kisha nikampatia mwana sheria.

“Alikuwa anakuambiaje?” “Aliniambia kwamba huyo ni mama yangu na wamemteka.Hivyo ameniagiza kwamba nichague kati ya boksi jeusi au uhai wa mama yangu” “Mmmmm” Camila aliguna aliguna huku akinitazama usoni mwangu. “Ndio maana yake” “Hivi hilo bosky jeusi Ethan ndio nini?” Camila aliniuliza kwa shahuku kubwa na kumfanya mwanasheria kunitazama machoni mwangu kwa macho ya kunikataza nisizungumze chochote.

“Hata mimi sifahamu” “Ethan hili swala nitalishuhulikia, hadi inafika usiku kila kitu kitakuwa kimekamilia, nipe mchana huu” “Sawa” “Utatumia simu hii, nikifika mjini nitakupigia niweze kukufahamisha ni kitu gani ambacho kinaendelea” “Sawa, ila hakikisha kwamba huyu mzee munamkamata, nina hitaji kuonana naye kabla ya yeye hajanifwata kesho” “Sawa mkuu” Mwanasheria akaniaga na akaondoka, kabla hata sekunde stini hazijaisha, meseji ikaingia kwenye simu hii aina ya iphone seven. Nikaifungua meseji hii na kukuta imetoka kwa mwanasheri.

‘USIMUAMINI CAMILA KWA KILA JAMBO’

Baada ya kuisoma meseji hii nikaifuta na kumtazama Camila kwa tabasamu kubwa sana, kwa maana hapo awali alisha nisaliti na isitoshe alisha nichoma kisu kwa madai anahitaji kufanya mwenyewe.

“Tutafanyaje Ethan?” “Usijali kila jambo litakwenda vizuri”

“Au nimuambie baba atusaidie katika kumtafuta?” “Hapana usimbebeshe mzee mizigo mingi sana. Tunaweza kulifanya kazi hii sisi kama sisi” Taratibu Camila akanikumbatia kwa hisia kali sana.

“Ninakupenda sana mume wangu” “Ninakupenda pia mke wangu” Mlango ukagongwa, tukaachina na Camila na nikaufungua, nikamkuta Frenando ndio anaye bisha hodi.

“Vipi Ethan una umwa?” “Hapana ndugu yangu, karibu ndani?” “Shem yupo?” “Ndio” “Basi siingii. Shem” Frenando aliita kwa sauti ya juu kidogo. “Beee” “Naomba nimuibe mumeo kidogo” “Usijali wewe muibe ila umrudishe akiwa salama kama ulivyo mchukua” “Usijali shemeji yangu” Nikarudi chumbani na kumnyonya Camila lipsi zake kidogo, ikiwa ni ishara ya kumuaga.

“Uwe makini mpenzi wangu” “Usijali, ninakuja” “Poa” Nikatoka chumbani humu. Nikaongonzana na Frenando hadi kwneye moja ya bustani ya kupumzikia, kwa maana huyu ni rafiki yangu na ni mtu ambaye ana fahamu siri zangu nyingi, nikaona sio mbaya nikamshirikisha matatizo yangu. Hadi ninamaliza kumuadisia, macho yakwa yamemtoka sana.

“Kaka kwa matatizo yako una haja ya kupata muda wa kupumzika, uwanjani si unafahamu kwamba mtu hutakiwi kuwa na mambo mengi kichwani” “Usijali nitacheza, ila tambua watu ninao waamini kwa sasa ni wachache sana.” “Pole sana ndugu yangu, ila kama alivyo kuambia mwana sheria wako, usimuamini Camila kama alikufanya yale yote na bado akaamua kurudi basi kuwa makini” “Kweli, hapa ni mwendo wa kuchezeana akili, akileta ujinga sasa hivi nakuapia haki ya Mungu, nitahakikisha kwamba ninamuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”



“Kaka kama ukimuua kwa mikono yako huoni kwamba itakuwa ni kesi ya dunia. Baba yake anakwenda kuwa raisi hii hii nchi, ulitambua hilo” “Nalitambua” “Na kumbuka wewe ni maarufu. Una makampuni mengi, una kipaji kizuri cha mpira. Utatakiwa siku moja uwe na mtoto wako naye afwate nyayo zako. Hakikisha kwamba hufanyi maamuzi ya kipuuzi Ethan” Frenando alizungumza kwa upole sana huku akinitazama usoni mwangu. Siku zote huwa ninampenda Frenando kwani ni mtu ambaye akili yake imetulia sana na hata akikushauri jambo basi anakushauri kwa ajili ya maisha ya baadae.

“Nimekuelewa kaka, ila leo usiku ninaweza kutoka” “Unakwenda wapi?” “Nitakuambia safari kama itakuwepo kwa maana nimekaa mguu mmoja ndani mguu mmoja nje” “Sawa, tuongozane?” “Nitakujulisha” “Poa poa kaka. Mwanangu nimepata kitoto cha Kimerxco hapa hotelini yaani weee acha tu kitamu kishenzi” “Weee umesha mla?” “Oohoo unahisi kwamba ninachelewa jamaa yangu. Kitoto ni kihudumu, leo kataingia shifti ya usiku. Yaani asikuambie mtu” “Hahaaa rafiki yangu wee mbaya” Tulizungumza huku tukiwa tumejawa na furaha sana. Tukaendelea kuzungumza mazungumzo mbalimbali. Kocha akajumuika nasi huku akionekana kuwa mtu wa furahas ana.

“Ethan nina habari nzuri, ila ni mbaya kwa wapinzani wetu” “Ehee tuambie kocha” “Leo niliweka hii picha yako kwenye akaunti yangu ya Twitter, na nikaangindika. ‘Mashine yangu imerudi’ Weee wapinzani wamejawa na presha balaa” “Hahaaa kocha ungewaacha tuwafanyie suprize bwana” “Tungewafanyia Suprize wangekufa kwa presha, kwa maana si kwa kukuogopa huku” “Hahaa kazi wanayo” “Kocha una mipango gani baada ya hapa?” Frenando alimuuliza kocha huku akimtazama usoni mwake.

“Mipango ipo mingi sana. Kama mukichukua kombe, basi ninakwenda kuongeza taaluma yangu ya ukocha na ninampango wa kufindisha timu kubwa duniani” “Ni mipango mizuri kocha, siku ukipata nafasi kwenye timu yoyote, tungependa kucheza chini yako” “Haki ya Mungu, lazima niwachukue kwa garama yoyote na nitakuwa tayari hata kuvunja rekodi ya Pogba katika manunuzi yenu” “Sawa kocha tutakuunga mkono, ila ningependa upate timu kama za Uingereza hivi kwa maana ligi ya hapa Ujerumani mimi naona kama haina changamoto kiviele” “Ni kweli unacho kizungumza Ethan, ligi ya ujerumani, ina mtawala mmoja ambaye ni Munich. Ila Uingereza kwa sasa hakuna mbabe, kila mwenye kisu kikali basi ndio anaye kula nyama” “Kweli kocha, natamani siku moja tubebe kombe mikononi mwako” “Hahaa muta beba tu wala musijali” “Sawa kocha” Simu niliyo achiwa na mwanasheria ikaingia ujumbe mfupi wa maneno. Nikaufungua na kuusoma kwa umakini.

‘TUMEMPATA, SAA NNE USIKU NITAKUJA KUKUCHUKUA’

Nilipo maliza kusoma ujumbe huu, nikaufuta kwenye simu yangu.

“Vipi kuna tatizo?”

Frenando aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.

“Hapana hakuna tatizo” “Sawa”

“Kocha kesho mazoezi yataanza saa ngapi?” “Majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi” “Sawa” “Mechi ya kesho kutwa nina waomba muweze kujituma sana. Kumbukeni kwamba mechi iliyo pita hamkuwepo na tulifunga goli moja tu. Goli ambalo lilizua maneno mengi kwenye mtando huku watu wengine wakitukashifu kwamba bila nyinyi timu haina uwezo wowote” “Usijali kocha kila kitu kitakwenda sawa. Unataka nikufungie goli ngapi?” “Sita” “Mmmmm” “Unaguna nini Frenando, mbona ina wezekana” “Haya mwaya, mimi langu ni goli. Nitazuia kuto kufungwa kwa uwezo wangu wote” “Ulinde vidole vyako wasije wakakutengua tena” “Tena sasa hivi nipo makini sana kwa maana kuan watu kama vile wanachezea timu ya taifa. Yaani kazi yako ni kudungua tu mashuti utadhani aliye kaa golini ni roboti” Maneno ya Frenando yakatufanya tucheke. Nikawaaga wezangu na kurudi chumbani. Nikamkuta Camila akiwa amelala kitandani, nikajilaza pembeni yake huku nikimkumbatia.

“Niambie” Nilizungumza huku nikimbusu shavuni mwake.

“Safi tuu mume wangu” “Usiku kuna sehemu nitakwenda mpenzi wangu” “Wapi tena Ethan?” “Yule mzee amapatikana” “Kweli?” “Ndio, nitahitaji kwenda kuzungumza naye uso kwa uso” “Mume wangu huoni kwamba inaweza kuwa hatari sana kwako?” “Usijali kila kitu kimewekwa chini ya uangalizi mzuri.”

Camila akanitazama usoni mwangu kisha akaninyonya midomo yangu kwa muda kidogo huku akishusha pumzi taratibu.

“Nitapenda usimfungulie mlango mtu yoyote zaidi yangu” “Usijali mume wangu, siwezi kumfungulia mtu mlango na nitawamfahamisha baba aweze kunitumia walinzi wake waje kunilinda” “Itakuwa ni vizuri” Masaa yakazidi kwenda. Usiku ukawadia, tukapa chakula cha usiku, mwanasheria wangu akafika hotelini hapa na helicopter. Tukaagana na Camila huku nikimkabidhi Frenando jukumu la kumlinda shemeji yake kisha mimi nikaondoka. Tukiwa ndani ya helicopter, mwana sheria akanikabidhi bahasha kubwa kidogo ya kaki.

“Homo ndani ya bahasha kuna taarifa za mzee huyo. Tumeweza kufwatilia hadi familia yake iliyopo nchini China” “Kazi nzuri, kazi umeifanya na nani?” “Kuna vijana wangu nimewatumia. Wapo wanne wao ni wapelelezi maalumu na wenye uwezo wa juu sana na huwa wanafanya kazi zao wao kama wao” “Ahaaa sawa sawa” Nilizungumza huku nikitazama picha kadhaa za mzee huyu, huku nyingine zikimuonyesha famili yake. Tukafika katika moja ya msitu, tukaona kiwanja kidogo cha helicopter ambacho kwa pembezoni mwake kimewashwa moto. “Ni wapi hapa?” “Hapa ndipo walipo vijana wangu” Mwanasheria wa familia alizungumza huku helicopter ikishuka taratibu. Helicopter ilipo fika ardhini. Tukafunguliwa mlango na jamaa mmoja mrefu aliye jazia mwili wake. Akanisalimia kwa kunipa mkono kisha tukaanza kuongozana kuingia msituni. Tukakuta mfuniko mzito wa chuma, kijana huyu akaufungua kisha akanza kuingia ndani humu huku akiwa amewasha taa. Wasiwasi kwa mbali ukaanza kunitawala huku nikijifikiria endapo kama mwana sheria ataamua kunigeuka basi, ataniulia humu ndani na hakutokuwa na mtu wa aina yoyote ambaye atafahamu kuhusiana na kifo changu. ‘Ehee Mungu nisaidie’

Nilizungumza kimoyo moyo huku tukishuka kwenye ngazi hizi, zipatazo hamsini. Tukakuta kordo ndefu iliyo washwa taa zenye mwanga hafifu kidogo. Tukaendelea kutembea huku tukimfwata kijana huyu nyuma nyuma. Tukatokea kwenye ukumbi mkubwa ambao umejaa tv kubwa sana zipatano kumi. Katika ukumbi huu kuna vijana watatu pamoja na mzee yule wa kichini akiwa amekalishwa kwenye kiti huku amefungwa kamba za mikononi mwake na miguuni. Usoni mwake anamwagikwa na damu na inaonyesha kwamba amepata kipigo kimoja kikali sana. Nikasalimiana na vijana hawa huku wakionekana kujawa na furaha sana ya kuniona.

“Mtu wako mkuu huyu hapa. Tumeweza kumuhoji na ametupa ushirikiano wa kutosha” “Amewaeleza juu ya sehemu alipo huyo mwana mama aliye mteka?” “Ndio amesema kwamba mwana mama huyu yupo katika nchi moja inaitwa Tanzania katika bara la Afrika Mashariki” Kidogo nikastuka huku nikimtazama mzee huyu wa kichina. Taratibu nikamsogela na kumtazama usoni mwake.

“Nimewahi kufika kabla ya wewe kufika. Nahitaji kufahamu mwanamke huyo yupo wapi ndani ya Tanzania?” Mzee huyu akanitazama kwa muda kisha akanitemea mate jambo ambali lilimfanya kijana mmoja atake kumpiga ila nikamzui kwa ishara ya mkono. Nikajifuta mate yake usoni mwangu, kisha taratibu nikavua koti langu hili kubwa na kumkabidhi mwana sheria anishikie.

“Yupo wapi mama yangu” Nilizungumza kwa kauli hii kwa maana tayari mwili wangu umesha anaza kupata hisia ya kutambua kwamba mwanamke huyu ni mama yangu.

“Yupo Tanzania, ila sinto kuambia ni wapi alipo hata uniue” ‘Ethan naomba nguvu’

Nilizungumza kimoyo moyo pasipo mtu yoyote kuweza kusikia. Mwili wangu ukapata msisimko ambao siku zote nikihitaji kuwa na nguvu basi Ethan hunipa nguvu kwa njia hiyo. Nikakinyanyua kiti hichi na mzee akiwa amekikalia jambo lililo washangaza watu wote humu ndani, kwani kwa umri wangu sina nguvu ya kumnyanyua mzee huu na kiti chake. Nilipo mpikisha kimo cha kama ng’ombe dume hivi. Nikamtupa chini kwa nguvu mzee huyu hadi kiti chote kikapasuka vipande vipande.

“Yupo wapi mama yangu?” Nilizungumza kwa ukali na sauti iliyo jaa besi kidogo. Mzee huyu mwili mzima ukazidi kumtemeka. Nikaokota moja ya koande cha mbao ya kiti kilicho chongeka kiasi. Nikamkita nacho kwenye paja la mguu wake wa kulia na kumfanya mzee huyu kupiga ukunga mmoja mzito sana.

“Nitakutajiaaaa…….” Mzee huyu alizungumza hukua kilia kwa uchungu sana.

“Wapi alipo….” “Tanzania katika mkoa mmoja uaitwa Tanga…..” “Itafuteni Arusha hapo” Nilimuambia kijana mmoja aliye kaa katika kiti huku pembe yake kukiw ana computer ya kampuni ya Apple. Kijana huyu akautafuta mji huo wa Tanga na baada ya muda kidogo, akafanikiwa kuupata.

“Tanga sehemu gani?” “Katika mji Mmoja unaitwa Lushoto” “Umeipata Lushoto” “Ndio mkuu” “Lushoto eneo gani?” “Kuna mji mdogo unaitwa Lukozi” “Lukozi?” “Ndio” Mzee alizungumza huku akilia kwa maumivu makali sana kwani bado nina endelea kumshindilia ubao huu ambao hadi sasa umezama kama nusu hivi. Nikauchomoa ubao huu huku nikimtazama mwanasheria usoni mwake.

“Nahitaji lifanyike kila linalo wezekana ndani ya siku mbili hizi mama yangu awe amepatikana. Utawapa kiasi chochote ambacho watakihitaji kwenye hii kazi. Mutakwenda Tanzania, sasa sijui mutakwenda wangapi?” “Tutakwenda sisi wawii mkuu” “Basi nawaombeni muwe makini na endapo mutampata basi nawaomba muweze kumleta hapa Ujerumani. Natamani sana kuzungumza naye mambo mengi sana” “Sawa mkuu kazi itaisha ndani ya siku nne” “Nashukuru kwa umoja wenu na ushirikiano wenu” Nilizungumza huku nikitoa kitambaa changu mkononi. Nikajifuta damu za mzee huyu.

“Mkuu kuna swala moja hatujakujilisha” “Swala gani?” “Huyu mzee ana bosi wake ni mwanamama tajiri sana kutoka nchini Nigeria katika viwango vya utajiri kwa wanawake barani Afrika yeye ni namba moja na kidunia kwa wanawake yeye ni namba nane” “Anaitwa nani?” “Yemi. Hilo ndio jina lake linalo pendelewa na watu wengi kuitwa” “Ina maana bosi wake ndio aliye mtuma hilo boksi jeusi?” “Ndio mkuu” Nikashusha pumzi taratibu, nikamsogelea mwana sheria na kumtaza usoni mwake.

“Hii ni vita ambayo tumesha ianzisha. Ni lazima damu za watu ziweze kumwagika. Nahitaji kuwa pamoja nawe kwenye kila jambo” “Usijali mkuu, baba yako alinipa jukumu la kukuangalia nami nitakuangalia hadi mwisho wa maisha yangu” “Sawa nashukuru kusikia hivyo. Huyo mwana mama tunamfanyaje?” “Kwa sasa ngoja tumtafute kwanza mamam mzazi. Tukisha mpata tunamgeukia na yeye” “Nashukuru” “Huyu mzee mkuu tunamfanya nini?” Kijana mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwake. Nikamuonyesha ishara ya kuchinja, kijana huyu akachomoa bastoka yake na kumpiga risasi nne za kifua mzee huyu na kumfanya afe hapo hapo.



“Hakikisheni kwamba mwili wake hauonikani sehemu yoyote katika dunia hii. Ikiwezekana mumuingize kwenye pipa la tindikali”

Nilizungumza huku nikiwatazama vijana hawa.

“Sawa mkuu”

“Kitu kingine, naamini kwamba leo hii mimi na nyinyi ndio tumeonana. Naomba haya mambo yabaki humu ndani, juu ya nguvu zangu mulizo zishuhudia pia liwe jambo la siri sawa”

“Sawa mkuu, kati yetu hakuna mtu ambaye anatatoa siri yoyote. Tuamini katika hilo”

“Nafurahi na ninashukuru kusikia hivyo”

Mara baada ya kuzungumza hivyo nikaagana na vijana hawa. Kijana aliye kuja kutupokea akatuto na kutupeleka hadi sehemu ilipo helicopter tulio.

“Ninawategemea katika hii kazi”

“Usijali mkuu, tutaifanya katika muda mfupi snaa na kwa umakini wa hali ya juu kisha tutakueletea ripoti”

“Sawa”

Akafungua mlango wa helicopter hii, nikawa wa kwanza kupanda kisha akapanda mwanasheri. Mlango ukafungwa kisha rubani wetu taratibu akawasha helicopter hii na safari ya kurudi hotelini ikaanza. Ukimya ukatawala ndani ya helicopter hii, huku mwanasheria akionekana kujawa na mawazo mengi sana.

“Unawaza nini mzee?”

“Nawaza jinsi ulivyo mnyanyua yule mzee na kiti chake hadi sasa hivi ninakosa jibu?”

“Hahaa usijali katika hilo, nina uwezo binafsi ambao Mungu amenijali”

“Kweli, Mungu ashukuriwe katika hilo”

“Wale vijana una waamini?”

“Asilimia mia moja wala usiwe na mashaka nao mkuu”

“Sawa, sinto penda kutokee matatizo kwenye hii kazi”

“Usijali”

Tukafika hotelini majira ya saa saba usiku. Nikashuka kisha mwanasheria akaondoke na kurudi kwake. Nikafika kwenye mlango wa chumba changu, nikaminya kengele, nikaisikia sauti ya Camila akiniuliza ni nani, nikaguna kidogo na baada ya sekunde tano mlango ukafunguliwa. Camila alipo niona akanikumbatia kwa furaha sana huku akininyonya midomo yangu.

“Umenipa hofu mwenzako”

“Kweli?”

“Ndio, nimeshindwa hata kulala”

“Pole mpenzi wangu, ninamshukuru Mungu nimefanikiwa kulimaliza jambo lililo nipeleka kule”

“Vipi umemuona mzee?”

“Yaa nilimuona, amebananishwa kidogo na ametaja ni sehemu gani alipo mama yangu”

“Duuu sasa mama utampataje?”

“Kuna watu nimewakabidhi kazi ya kwenda kumleta, nina imani kwamba watafanikisha kumleta akiwa salama”

“Yupo nchi gani?”

“Tanzania”

“Ahaaa sawa mume wangu, twende bafuni tukaoge”

Camila alizungumza huku akinishika kiuno kwa nyuma. Tukaingia bafuni, akanivua nguo zangu zote kisha naye akavua nguo hizi za kulalia. Tukaoga kisha tukarudi chumbani, kutoka na uchovu nilio nao, sikuweza kufanya kitu chochote na usingizi uliwahi kunipitia. Asubuhi na mapema nikawahi kuamka na kumuacha Camila akiwa amelala, nikavaa nguo zangu za mazoezi kisha niakelekea uwanjani. Nikaanza kufanya mazoezi peke yangu hata kabla ya wachezaji wezangu. Baada ya nusu saa wachezaji wezangu wakajumuika nami katika kufanya mazoezi. Jinsi ninavyo cheza leo, kumewafanya wachezaji wezangu kunisifia kwani jana sikuwa sawa kabisa. Kocha akatupa mipango ya jinsi gani tunatakiwa kucheza mechi yatu ya kesho, kwani hadis asa hivi tunaongoza kundi letu kwa pointi sita.

“Tunatakiwa kushinda kila mechi iliyopo mbele yetu. Ethan nahisi hili ninalo kwenda kuzungumza sio jambo zuri kidogo, ila naomba ulivumilie kwa leo tu”

“Zungumza tu kocha”

“Leo naomba usifanye chochote na bibie, asije akakumaliza nguvu sawa”

Mimi na wachezaji wezangu tukajikuta tukicheka huku tukimtazama kocha.

“Kweli vile, ninalo lizungumza lina maana Ethan”

“Usijali kocha”

“Haya sasa ni muda wa kupata kifungua kinywa”

Tukaondoka uwanjani hapa na kurudi eneo la hotelini, tukamkuta Camila akisiaidiana na wafanyakazi wa hapa katika kuandaa vifungua kinywa. Camila alipo niona akanifwata kunilaki, akanikumbatia pasipo kujali kama nina jasho liilo nilowanisha nguo zangu zote.

“Vipi, umecheza vizuri?”

“Ndio mke wangu na kesho nitafunga magoli kwa ajili yako”

“Kweli mume wangu?”

“Ndio”

“Utanifungia magoli mangapi?”

“Kama sita hivi”

“Huuhuhu, sita?”

“Ndio, kwani nashindwa?”

“Hamna hushindwi mume wangu, ila inabidi ufanye kazi kubwa. Tena leo inabidi nikubanie nisikupe utamu”

Camila alizungumza kwa kuninong’oneza sikioni mwangu na kunifanya nitabasamu.

“Sawa mama”

“Mbona umeitikia kinyonge?”

“Hamna mke wangu, mbona sijaitikia kinyonge”

“Kweli?”

“Ndio mke wangu”

“Nimeandaa kifungua kinywa kwa ajili yako, twende ukanywe.”

“Sawa”

Tukaa kwenye meza yetu pamoja na rafiki yangu Frenando. Tukapata kifungua kinywa kisha tukarudi mavyumbani mwetu. Siku nzima hii ya leo, kocha alikaa nasi karibu sana huku akituhimiza sana tusipoteze mchezo ulipo mbele yetu kwani ana malengo makubwa sana nasi kwa maisha ya baadaye ya soka.

***

Siku ya mechi ikawadia, tukaingia kwenye basi letu maalumu kwa timu hii kisha safari ya kuondoka nje ya mji ikaanza huku tukipewa usindikizaji wa gari mbili za polisi. Moja ipo mbele ya basi letu huku nyingine ipo nyuma ya basi letu. Daktari wa timu akampa Camila nafasi ya kuwa msaidizi wake, hivyo naye amejuimuika kuungana nasi katika basi hili.

“Utaimudu kazi ya udokta?”

“Ndio, kwa nini nishindwe”

“Hahaaa haya mwaya”

“Tena ukianguka wewe, nitakufwata na kukuhudumia hadi upone”

“Haya bwana mke wangu, ngoja nizungumze na wachezaji wangu”

Nikanyanyuka kwenye siti yanguna kusimama katikati ya basi. Wachezaji wezangu wote wakanitazama.

“Ni siku nyingine, tunakwenda kupambana, tukiwa pamoja. Ninawaomba tucheze kwa umoja, na tuhakishe tunashinda. Ninawategemea sana na kwa pamoja tutashinda sawa”

“Sawa kapteni”

Wachezaji wezangu waliitikia kwa pamoja kisha safari ikaendelea. Hadi kufika uwanjani, ilitugarimu masaa mawili. Tukashuka na kuwakuta waandishi wa habari pamoja na mashabiki wakiwa tayaru kwa kutupokea. Waandishi walipo niona ninashuka kwenye gari huku nikiwa na Camila, wakapiga shangwe ambayo hakika sikuitaraji.

“Ethan na Camila tunawapenda”

Ni maneno yaliyo sikika katika kundi moja kubwa la wamashabiki wa kike. Nikagairi kuelekea ndani na kuwafwata mashabiki wangu hao huku walinzi na askari wakiwa wametangulia mbele yetu. Nikaanza hukuchua kalamu ya kila mshabiki, wapo wengine walihitaji niweke saini yangu kwenye mikono yao huku wegine wakihitaji niweke saini kwenye tisheti zao walizo zifanya. Camila naye aliweka saini kwa mashabiki wake wanao muomba kufanya hivyo.

“Ethan muda sasa umefika”

Mlinzi mmoja alizungumza pembeni yangu. Nikawapungia mkono na kuanza kuongozana na walinzi huku nikiwa nimeshika Camila mkono. Tukaingia katika chumba chetu cha kubadilishia nguo.

“Camila naomba clipbandeji”

“Ya nini mume wangu?”

“Nahitaji kujifunga kwenye mguu wa kulia, nahisi kama nyayo kidogo inavuta vuta kwa chini”

“Sawa”

Camila akaanza kunifunga mguu wangu kulia.

“Kaza kidogo”

Camila alafanya kama nilivyo mueleza. Akanivisha soksi, nikavua koti langu pamoja na suruali hii ya mazoezi niliyo ivaa, kisha nikavaa jezi yangu, ambayo mgongoni imeandikwa namba sana pamoja na jina langu. Kocha akaanza kupiga piga makofi, ikiwa ni ishara ya kutunyamazisha. Baada ya sekuende kadhaa kila mmoja akanyamaza na kumsikiliza kocha ni kitu gani ambacho anahitaji kuzungumza.

“Naamini kwamba kila mmoja anatambua nafasi yake si ndio”

“Ndio kocha”

“Kasi, na mashuti ya mbali ndio mchezo wa leo. Wamezoea kutuona tunacheza mchezo wa pasi fupi fupi, kumbukeni wezetu wana nguvu, wana kasi pia. Hivyo ni lazima tuweze kukubaliana na mwendo kasi wao la sivyo tutachemsha leo sawa”

“Sawa sawa kocha”

“Ethan, Pinto ninawategemea. Hakikisheni kwamba munayengeneza mfumo mzuri wa kushirikiana. Katikati, Chris na wezako hakikisheni hamtawaliwi. Chukueni mipira nyuma kisha muipeleke mbele sawa”

“Sawa sawa kocha”

“Tunadakika tano kabla ya kuingia uwanjani. Munaweza kuendelea na shuhuli zenu”

“Kocha suti ya leo imekutoa?”

Nilimtania kocha na kumfanya acheke kidogo.

“Nashukuru capten”

Camila taratibu akanifunga kitambaa cha ukapten katika mkono wangu wa kushoto.

“Hakikisha unaongoza timu na inashinda, sihitaji ushindwe mume wangu sawa”

“Sawa mke wangu

Camila akanipiga busu la mdomoni. Nikamuachia, kisha yeye na benchi la ufundi wakaanza kutoka katika chumba hichi. Taratibu tukaanza kutoka katika chumba chetu na kuelekea katika mlango wa kutokea, huku makaera man wakiwa makini sana kuhakikisha kwamba wana turekodi vizuri. Nikakonyeza kamera moja ambayo inanichukua kwa ukaribu sana usoni mwangu. Refarii na wazaidizi wake wakasimama mbele yangu, katoto kamoja ka kike kaliko valia jezi ya timu yetu kakanipa mkono na nikakashika.

“Unaitwa nani?”

Nilimuuliza huku nikiwa nimeinama.

“Camila Alexander Diaz”

Kalinijibu kwa ufasaha kabisa huku akitabasamu sana.

“Kweli?”

“Ndio”

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG