Search This Blog

Wednesday, November 18, 2020

MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE) SEHEMU YA 9/10

 

 


 MKE WA RAISI (PRESIDENT‘S WIFE)

WRITER…………………………………………EDDAZARIA G.MSULWA
WEBSITE………………………………………… www.storyzaeddytz.com
CONTACT……………………………………….. 0657072588/0768516188
AGE……………..18+ 

SEHEMU YA 9 KATI YA 10

 


K2 alizungumza huku akianza kulipapasa paja la upande wa kulia la Livna Livba huku mkono wake huku taratibu akiupelekea kwenye ikulu ya Livna jambo lililo msangaza sana Livna Livba japo hisia za kimapenzi taratibu zimeaanza kumpanda.

***

“Hivi unahisi raisi Dustan anaweza kutuacha hai kwel?”

Dumbe alimuuliza Dumpe huku akiendelea kuongeza mwendo wa gari hili analo liendesha.

“Unahisia gani katika hilo”

“Ninacho kihisi, atatutafuta na kuhitaji kutua kwa manaa kama aliweza kutufungia katika ile sehemu na tukaishi kifungo cha ndani kwa miaka kadhaa, japo huduma ya chakula na vinywaji alikuwa anatupatia. Najua hashindwi kututafutia namna ya kututumikisha na mwishowe tutajikuta tukifa vibaya na kijinga sana”

Dumbe alizungumza kwa msisitizo

‘Unahitaji tufanye nini?”

“Nahitaji tumuue sisi kwanza kabla ya yeye kutuua sisi”

“Unahitaji tumue?”

“Ndio.”

Mawazo na maneno ya Dumbe yakampa Damp kukaa kimya akiyataakari. Akamtazama rafiki yake huyo ambani yaw a muda mrefu sana toka walivyo kuwa katika shule ya chekechea, miaka mingi sana ya nyuma na wameshirikiana katika mambo mengi kiasi cha kuzoea sasa na kuwa kama ndugu na mmoja huwa akitoa wazo basi ni lazima mwengine alitekeleze hata kama ni wazo la kijinga.

“Sawa tuifanye hii kazi, ila niahidi kitu”

“Kitu gani?”

“Hii ndio itakuwa ndio kazi yetu ya mwisho na hatuta fanya kazi nyingine yoyoye ya hatari?”

“Nakuahidi kwa mana natambua hisia zao zote kwa sasa zipo katika mapumziko na kujificha”

“Sawa”

***

Furaha ya Raisi Dustan ikatoweka mara baada ya kukata simu. Msaidizi wake akamtazama kwa macho yaliyo jaa maswali mengi huku akimsogelea hata kabala hajamfikia karibu, akastusha wa tukio la raisi Dustan kuanza kutupa kila kitu kilichopo juu ya meza ya kwa hasira sana jambo lililo zidi kumshanganza bwana Silvester ambaye ni kwa kipindi kikubwa sana hajawahi kumuona raisi Dustan akipandwa na hasira kama hiyo ambayo kwa mara nyingi humpelekea akili yake hata kuchanganyikiwa, japo ni siri ambayo anaifahamu yeye mwenyewe na pamoja na daktari wa raisi huyo, na endapo siri hiyo itaweza kufahamika wa wabunge wa upinzani wa chama chake, basi ni lazima raisi Dustan aweze kuachia madaraka mara moja kwani sifa kubwa ya nchi hiyo ya Marekani ni kuongozwa na kiongozi mwenye akili timamu na asiye umwa na ugonjwa wa aina yoyote ile.



“Muheshimiwa ninakuomba, ninakuomba sana upunguze jazba hili ni tatizo muheshimiwa”

Mshauri wa raisi Dustan alizungumza kwa sauti iliyo jaa unyenyekevu mwingi sana huku akimtazama Raisi Dustan aliye zidi kufura kwa hasira.

***

“Sihitaji kuufanya ujinga unao uhitaji kunifanyia”

Livna alizungumza huku akiutoa mkono wa K2 kwenye paja lake.

“Kwani kuna ubaya?”

K2 alizungumza kwa sauti iliyo jaa msisimko wa kimapenzi sana huku akijitahidi kuhakikisha kwamba anajaribu kushika sehemu zenye msisimko wa kimapenzi katika mwili wa Livna. Livna kwa haraka akashuka kitandani huku akimkazia macho K2. Akatembea kwa haraka hadi mlangoni mwa chumba chake, akaufungua kwa haraka, kwa ishara ya mkono akamuomba Livna kutoka ndani ya chumba hicho. K2 taratibu akashuka kitandani na kuanza kutembea kuelekea nje ya chumba hichi.

“Livna ila jua kwamba kundi lako sasa hivi linatakiwa kufanya kazi ki professional zaidi”

K2 alizungumza kwa suati ya upole na msisitizo kidogo.

“Nahitaji kupumzika kichwa changu kimechoka kwa sasa”

“Ila nina wazo moja”

“K2 nimekuambia kwamba nahitaji kupumzika”

Msimamo wa Livna ukamfanya K2 kutoka kwa hasira ndani ya chumba hicho na moja kwa amoja akaeleka chumbani kwake. K2 moja kwa moja akapitiliza hadi chumbani kwake, akaanza kuzunguka zunguka huku akipanga mipango ni jinsi gani ambavyo weza kumuangamiza raisi Rahab ili azidi kuikaribia ikulu ya Tanzania na siku moja yeye na kaka yake waweze kuchukua madaraka ya nchi hiyo.

“Nimepata mbinu. Mimi mwenyewe ni lazima nihakikishe kwamba kaka yangu anaingia madarakani”

K2 alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu pan asana usoni mwake.

***

Usiku wa siku hii furaha ikatawala ndani ya nyumba ya makamu wa raisi Eddy Godwin. Ukubwa wa familia yake kwa sasa umeongezeka. Vyakula vilivyo andaliwa katika meza kubwa vinamtamanisha kila mmoja aliye kaa katika katika viti vilivyo izunguka meza hii. Taratibu Eddy akasimama huku akiwa amejawa na tabasamu, akawatazama Phidaya na Shamsa ambao kila mmoja amebeba mtoto wake mikononi mwake.

“Habari za usiku huu”

“Salama”

“Ni furaha kwangu na kwenu kuwaona mukiwa mumejumuika mami kwenye chakula hichi cha usuku, kusema kweli ni jambo kubwa nililo kuwa ninalitamani katika maisha yangu ya kila siku”

“Karibuni sana wageni ambao mumeweza kusaidia na mdogo wangu Adrus hapo kuhakikisha kwamba familia yangu inarudi katika umoja kama huu. Ninaswashukuru sana”

“Ni jukumu langu muheshimiwa”

Adrus alijibu kwa heshima zote.

“Nisizungumze mambo mengi sana karibuni katika chukula hichi cha usiku. Mungu abariki chakula hichi”

“Amen”

Kila mmtu akaanza kujitengea chakula anacho kihitaji. Mazungumzo ya hapa na pale yakazidi kupamba moto. Mama Adrus alipo maliza kupata chakula akawa mtu wa kwanza kuaga mezani na kutoka nje na kudai kwamba anakwenda kupunga upepo . Jambo hili likamfanya Adrus kumtazama mama yake jinsia navyo malizikia kuelekea nje, kitu ambacho Eddy naye aliweza kukielewa. Taratibu Eddy akavuta kiti chake nyumba na kuchukua glasi yake ya juisi na kuanza kutembea kwa kuchechemea kuelekea nje. Akamkuta mama Adrus akiwa amesimama pembezoni mwa swimming pool lililopo katika eneo hilo.

“Mama mbona unaonakena kama huna furaha?”

Sauti ya Eddy kidogo ikamstua mama Adrus ambaye kila anapo muona Cookie nafsi yake inachafukwa sana kwani mapenzi yake yote kama mama yapo kwa Naomi mwanamke wa kwanza aliye uteka moyo wa mwanaye.

“Ahaa nipo sawa tu muheshimiwa”

“Hapana mama, najua ni nini kinacho kusumbua”

Mama Adrus akabaki akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana huku akimtazama Eddy usoni mwake.

“Najua ni jinsi gani au maumivu ya namna gani mama anayapata pale kijana wake anapo kuwa na mwanamke ambaye hajampenda”

Mama Adrus akazidi kustuka kwani hakutarajia kama Eddy anaweza kuzungumza maneno kama hayao.

“Najua kuna kipindi mama yangu alikuwa na moyo kama wa kwako, kwa maana mama yangu hakupenda niwe hata na huyu mwanamke ambaye sasa hivi ndio mke wangu. Ila nilipambana kwa ajili ya upendo wangu, nilipambana kwa ajili ya kile nilicho kihitaji kwangu na hadi leo maisha yangu yamekuwa na mwanamke ambaye nipo naye.”

Mama Adrus akainamisha kichwa chini kwa aibu, kwani alihisi maamuzi ya kumkataa Cookie basi yatabaki kati yake yeye na Adrus.

“Ila muheshimiwa, mwanangu hawezi kuwa na mwanamke kama huyu. Mwanamke anaonekana dhairi ni muuaji, mwanamke anaye onekana dhairi ni gaidi”

“Hata mwanao ni muuaji”

Mama Adrus akamtolea macho sana Adrus aliye zungumza kwa msisitizo.

“Yaa kazi ayayo ifanya mwanao kuua kwao sio dhambi, kwenye uso wa binadamu, japo siujui huko mbinguni watakuwa wanahesabiwaje. Kwa maana usipo ua, basi huuliwa yeye.”

“Mpe nafasi mwanao ya kupenda, usimuangalie mtu kwa macho, mpe nafasi aweze kuonyesha ni jinsi gani ambayo anaweza kupigania maamuzi ya moyo wake, sawa mama yangu”

“Nimekuelewa muheshimiwa”

“Najua hujapenda maneno yangu na….”

“Hapana muheshimiwa, kila binadamu ana maono yake, ila ushairi wako pia ni muhiamu. Nitampa nafasi mwanangu, na nitaona ni jinsi gani binti huyo atakavyo simama katika kuutetea upendo wa mwanangu”

“Nashukuru sana mama kwa kuweza kusikia hivyo”

Kumbe muda wote walivyo kuwa wakizungumza, Adrus alikuwa amesimama nyuma yao mita chache na alikuwa anasikia kila kitu ambacho Eddy alikuwa analizungumza na mama yake. Kitendo cha maam Adrus kugeuka nyuma macho yake yakakutana na macho ya mwanaye ambayo yamejaa machozi. Eddy naye akageuka na kumkuta Adrus, taratibu akapiga hatua hadi sehemu alipo simama na kumshika bega.

“Hakikisha kwamba huyumbi katikamaamuzi yako ambayo unayafanya dogo sawa”

“Sawa mkuu”

“Poa zungumza na mama”

Eddy akaondoka katika eneo hilo na kumuacha Adrus na mama yake, taratibu Adrus akamsogelea mama yake sehemu alipo simama.

“Kwa nini umemuambia makamu wa raisi juu ya maamuzi yangu?”

Mama Adrus aliuliza huku akiwa amejawa na hasira kiasi.

“Mama”

“Sio mama, Adrus umekuwaje wewe, kwa nini unataka kunizika mama yako nikiwa na uchungu wa kitu ambacho hakipo moyoni mwangu Adrus kwa nini lakini?”

Mama Adrus alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Japo mama Adrus aliweza kusikiliza ushauri wa makamu wa raisi, Eddy Godwin, ila maamuzi ya moyo wake kamwe hayakuweza kubadilika kabisa.

“Mama kwa nini unamkataa Cookie ana nini lakini?”

“Cookie si mwanamke wa kudumu naye, nina hisia naye mbaye moyoni mwangu atakuja kukuua siku wewe shauri yako tu”

“Kuniaua vipi?”

“Umekutana naye vipi kwanza, eheee niambie”

Adrus akainamisha kichwa chake chini kwani kukutana kwake na Cookie. Cookie alikuwa katika kazi maalimu ya kumuua yeye mwenyewe.

***

“Nawaomba”

Eddy aliwanong’oneza Shamsa na Phidaya kwa pamoja. Wote wakaondoka katika eneo hilo la sebleni na moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha Eddy na Phidaya wanacho lala huku kila mmoja akiwa emembeba mwanaye.

“Tuambie babaa”

Phidaya alizungumza huku wakikaa kitandani.

“Najua sasa nyinyi ni mama wa waanangu kwa sasa. Kikubwa ninacho kiomba na ninacho kihitaji kuweza kukipata kwenu ni amani ya moyo wangu, amani ya familia yangu”

“Kusitokee mtoto mmoja akathaminiwa na akaonekana kwamba ana thamani kubwa kuliko mwengine, sinto penda kabisa hilo jambo. Camila na Junion Jr wote ni wanangu na wote ni damu yangu, atakacho kipata Camila ni sawa sawa ana atakacho kipata Junion Jr. Mumenielewa”

“Kwa upande wangu mimi sina tatizo na mama Junion Jr najua amekamilisha furaha ambayo mimi kwa upande wangu naamini nisinge ikamilisha kwa miaka hii ya karibu”

“Una maana gani?”

“Nisinge weza kukuzalia mtoto wa kiume kwa muda wa hivi sasa”

“Hata mimi jamani nina amani katika hilo, kwa hapo awali nilijihisi ni mwenye wivu na mwenye mawazo mabaya juu ya mama Camila ila ninamshukuru Mungu hicho kitu kwa sasa kimefutika katika moyo wangu”

“Nashukuru kusika hivyo na kila kitu ninahitaji hivi sasa kiende katika amani, haijalishi watu nje watachukuliaja maisha yenu au kuzungumzia ila kikubwa ni heshima na upendo utawawale kati yenu”

“Sisi tupo sawa na tunashukuru kwa hilo.”

Eddy wakamaliza mazungumzo na wake zake hao wawili alio zaa nao. Shamsa akatoka chumbani humo na kuwaacha Phidaya na Eddy.

“Eddy”

“Naam”

“Lile wazo la wewe kuwa raisi nililo wahi kukuambia limeishia wapi?”

“Hii miaka miwili ya mwisho ikiisha sinto ingia tena kwenye maisha ya uongozi, nahiji sasa kupumzika na familia yangu”

“Hapana mume wangu, umri wako una ruhusu wewe kuja kuwa kiongozi wa hii nchi”

“Kuwa makamu wa raisi inatosha Phidaya”

“Hapana nahitaji ndoto zako zitumie, nahitaji uwe raisi wa Tanzania”

“Kwa nini unahitaji niwe raisi”

“Kwa heshimwa ya wanao, kwa heshima ya historia yako, kwa nini historia yako iishie katikati”

“Kikubwa ni historia yangu tu?”

“Ndio, wanao watajivunia nini? Kuwa raisi ili uweze kufuta maovu ya baba yako aliyo wahi kuifanya katika hii nchi kuwa raisi uweze kufuta historia mbaya ya baba yako”

Eddy akaka kimya huku akimtazama Phidaya usoni mwake. Eddy akatingisha kichwa na kukubaliana na wazo ambao mke wake anamsisitizia kulifanya.

***

Majira ya saa nne asubihi ndege aliyo panda Naomi ikatua katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage nyerere. Naoami akajuimika na abiria wengi kushuka katika ndege hiyo, akafwata taratibu zote na kutoka ndani ya uwanja huo.

“Habari yako kaka?”

Naomi alimsalimia mmoja wa dereva taksi mara tu baada ya kuingia ndani ya taksi hiyo.

“Salama”

“Nipeleke katika hoteli moja ya kawaida tu, iliyopo katikati ya jiji hili”

“Sawa dada”

Dereva wa taksi akawasha gari lake na kuondoka katka eneo hilo.

‘Adrus upo wapi mpenzi wangu. Nipo nchini kwenu Tanzania’

Naomi alizungumza kimoyo moyo huku akitazama magofa a jiji hili la Dar es Salaam.

“Dada unahitaji hoteli iliyo tulia sana au yenye mchanganyiko wa watu?”

“Nitumie yenye mchanganyiko wa watu”

“Sawa sawa”

“Jiji lenu lina foleni sana eheee?”

“Ndio lina foleni nyini sana”

Dereva taski alizungumza huku akisimamisha gari lake pembeni ya gari jengie aina ya Toyota Land Cruser. Naomi macho yake yote akayelekezea kwa dereva wa gari hilo ambaye si mwengine ni Adrus huku pembeni yake akiwa amempakiza mwanamke mwengine ambaye hamfahamu ni nani.



Taratibu mataa ya barabara zikaruhusu magari kuanza kuondoka.

“Dereva fwatilia hilo gari hapo”

“Lipi?”

“Hilo lenye rangi nyeusi, wahi hakikisha kwamba hatuliachi”

“Sawa dada”

***

Asubuhi mama Adrus akawa ni mtu wa kwanza kuamka katika nyumba ya Eddy. Moja kwa moja akaelekea hadi kwenye chumba alicho lala Adrus na Cookie. Miguno ya mapenzi ambayo anaisikia ikitokea ndani humu ikazidi kuchanganya mama Adrus kwa maana swala la mwanaye kuwa katika mahusiano na Cookie linamchanganya sana. Akapiga hatua mbili mbele ili aondoke katika eneo hilo, ila roho yake ikasita kabisa na kujikuta akirudi mlangoni hapo na kuanza kugonga. Akagonga mara nne na mlango ukafunguliwa na Cookie ambaye amajifunga taulo mwilini mwake.

“Mama shikamoo”

Mama Adrus akamtazama Cookie kwa macho makali yanayo onyesha dhairi kwamba yamejaa chuki dhidi ya Cookie ambaye hadi sasa hivi haelewi ni kitu gani kinacho endelea.

“Huyo mwenzako amelala?”

“Hapana, ila nimekusalimia mama hujaitikia salamu yangu”

“Marahaba, niitie”

Cookie aliita baada ya muda Adrus akatoka akiwa amevalia bukta na tisheti.

“Mama”

“Nahitaji kuzungumza na wewe”

“Sasa hivi?”

“Ndio”

Adrus akamtazama mama yake jinsi alivyo nunu. Akatazama ndani na kumuona Cookie akiwa amejiinamia kwenye kitanda akionekana amejawa na mawazo kiasi. Adrus akatoka ndani humo, moja kwa moja wakaongozana hadi nje ambapo walinzi wa serikali wanendeleza usalama.

“Hivi nikuambie na nini ili uweze kuelewa wewe mtoto”

Mama Adrus alifoka hadi walinzi wawili walio karibu yao wakawatazama. Kwa ishara Adrus akawaomba alinzi hao kuweza kusogea pembeni ili aweze kuzungumza na mama yake.

“Ila mama mbona unataka nifanye maamuzi ya haraka haraka sana, nimekuambia kwamba nitamuacha, sasa asubuhi kama hii unanifwata asubuhi mama kama tupo uswahilini”

“Sijali upo uswahilini au upo wapi, ila siwezi kukubalia kukuona unaendelea kulala na huyo jini humo ndani”

“Ila mama siku hizi umekuwaje lakini, kwa nini wewe, kwa nini lakini unapingana na maamuzi ya moyo wangu”

“Nimekuambia sitaki, kama mimi ni mama yako niliye kuweka tumboni miezi tisa na kukulea hadi leo umekuwa na mkifua kama tofali na hao wadada wanakung’ang’ania ninataka uachane naye. Sasa hivi ni saa kumi na mbili, nenda Airpoet kamaktie tiketi na aondoke sawa”

“Mama ninakuheshimu na sijawahi kukufichia heshima siku hata moja, ila kama kweli umeamua nifanye hivyo, basi nitaondoka Tanzania na ubaki wewe mwenyewe, nife nisife jua kwamba huna mtoto wa kiume sawa”

Adrus mara baada ya kuzungumza maneno hayo, akaingia ndani huku akiwa amejawa na jazba. Akakutana na makamu wa raisi sebleni.

“Vipi dogo umeamkaje?”

“Salama mkuu, samahani naomba uniazime moja ya gari nahitaji kuelekea uwanja wa ndege?”

“Saa ngapi?”

“Sasa hivi”

“Kwema lakini?”

“Yaa kwema”

Eddy akamtazama Adrus kwa muda kidogo, kutokana ni mtu mwenye upeo mkubwa akatambua kabisa kwamba si kwema ila hakuhitaji kuuliza swali jengine mara baada ya kumuona mama Adrus akiwa ameingia ndani huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Eddy akatingisha kichwa akikubalia na ombi la Adrus kumuomba gari, moja kwa moja Adrus akapitiliza hadi ndani kwake na kumkuta Cookie akiwa anatoka bafuni.

“Vipi mama mbona anaonekana kama amekasirika kuna nini kinacho endelea?”

Cookie aliuliza kwa sauti iliyo jaa upole mwingi huku akimtazama Adrus.

“Vaa nguo tuondoke”

“Tuondoke, kwend wapi?”

“Nimekuambia kwamba vaa tuondoke”

Adrus alizungumza huku wakielekea bafuni na kumuacha Cookie akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Mama Eddy, kisha akaelekea chumbani kwake na kumuacha sebleni Eddy akishusha pumzi nyingi sana, kwani ushauri alio weza kumshauri mama huyo umekuwa bure.

“Weee Sa Yoo”

Eddy alimuita Sa Yoo aliye katika kwa haraka akielekea jikoni.

“Bee”

Sa Yoo aliitikia huku akirudi nyuma na kumtazama Eddy aliye simama sebleni.

“Mbona spidi vipi kwema?”

“Kwema nakuja”

Sa Yoo mara baada ya kumaliza kuzungumza hivyo akakimbilia jikoni, akafungua friji kwa haraka, akachukua chupa ya maji ya baridi akafungua mfuniko na kwa haraka kisha akaanza kunywa kwa haraka huku akihema. Hamu yake ya maji ya baridi ilipo isha kwa haraka akarudi sebleni.

“Ehee niambie baba Camila Junion Jr”

“Hee umamua kuniita majina yote mawili?”

“Ndio, vipi mbona mapema, unatoka nini?”

“Hapana ulikuwa unakimbilia wapi?”

“Nilikuwa naenda kunywa maji, nimeamka na kiu sana”

“Sogea hapa karibu”

Eddy alizungumza na kumfanya Sa Yoo kumsogelea kwa haraka sana ili aweze kusukiliza ni kitu gani Eddy anacho hitaji kumuambia.

“Adrus na Cookie watatoka sasa hivi, hakikisha wakitoka tu unachukua gari na kuwafwatilia”

“Wanakwenda wapi?”

“Sijajua ila ninaomba uweze kuwafwatilia”

“Sawa, ngoja nikavae kwanza”

“Poa”

Sa Yoo akakimbila hadi katika chumba anacho lala na Shamsa. Akafungua kabati na kuanza kutoa nguo.

“Unakwenda wapi?”

Shamsa alimuuliza huku akijigeuza na kujiweka sawa.

“Kuna kazi Eddy amenipa?”

“Kazi ya gani?”

“Yeye ameniambia kwamba niwafwatile yule Adrus na mpenzi wake wanatoka”

“Mmmm haya, ila kuwa makini”

“Usijali”

Sa Yoo alizungumza huku akivuta suruali nyeusi anayo ipende sana kuivaa. Adrus akatoka bafuni, akaanza kujifuta maji na taulo.

“Ila Adrus naomba uniambie ni kitu gani ambacho kinaendelea na kama ni kuondoka tunaondoka kwa kustukia bala hata kuaga”

“Kumuaga nani, ni kwako au ni kwenu hapa?”

Adrus alizungumza kwa hasira maneno yaliyo mfanya Cookie kushangaa. Adrus akavaa nguvo zake na wakatoka chumbani humu huku Cookie akiwa amejawa na maswali mengi.

“Muheshimiwa tunatoka”

“Sawa, utachukua gari lolote hapo nje”

“Sawa”

Adrus na Cookie wakatoka nje, wakaingia kwenye garia aina ya Toyota Land Cruser na kuondoka eneo hilo. Sa Yoo akatoka chumbani na kumkuta Eddy akiwa amesimama.

“Wamesha ondoka wawahi”

“Sawa, ila wana na nini?”

“Sa Yoo acha maswali mengi wewe wafwatilie”

Sa Yoo akatoka nje, akaingia kwenye gari aiana ya Ferrali na kuaondoka kwa kasi ili awaweze kuwawahi Adrus na Cookie. Machozi yakazidi mama Adrus mara baada ya kumuona mwanaye akiondoka katika jumba hili la makamu wa raisi.

‘Jamani baba Adrus kwa nini mwanao amekuwa hivi?’

Mama Adrus alizungumza kimoyo moyo huku machozi yakiendelea kumwagika.

“Adrus ila sijapendezewa na jibu ambalo umenijubu kule chumbani”

“Wewe ulitaka nikujibuje sasa”

“Hata kama ila unatakiwa kuniambia ukweli tu, kama mama yako umekosana naye niambie tu mimi ndio mke wako”

Adrus hukumjibu kitu chochote Cookie zaidi ya kumtazama tu usoni mwake.

“Adrus”

“Naam”

“Unanipenda kweli?”

“Ndio”

“Kwa nini unanificha kitu kinacho endelea wewe na mama yako, jana nilimuona akikupiga kibao, leo hii amekuja asubuhi amegonga mlango, nimemfungulia nimemsalimia ila hajaniitikia kwa furaha. Hembu zungumza basi maisha gani haya ambayo unaishi na mama yako”

Adrus akatamani sana kumueleza ukweli Cookie ila akajikuta akishindwa, wakafika uwanja wa ndege, wakasimamisha gari katika megesho.

“Nisubirie hapa”

Adrus alizungumza huku akishuka kwenye gari. Moja kwa moja akalekea hadi kwenye ofisi za shirika la ndege la KLM. Akasimama kwa muda huku akitafakari maneno ya mama yake kichwani mwake anaye mshinikiza kuachana na Cookie.

“Kaka, kaka”

Muhudumu alimuita Adrus na kumfanya astuke kidogo.

“Ndio”

“Nikusaidie nini?”

“Eheeee?”

Adrus akawa kama mtua ambaye ajui ajibu kitu gani kwani kuja kwake hapo uwanja wa ndege hajui hata aelekee wapi.

“Ninakusikilizia kaka yangu”

“Ahaa ratiba ya ndege zenu kwa leo zipo?”

“Hapana kwa leo hatuna, ndege zinaingia tu Tanzania, ila kwa kesho zipo”

“Kwa kesho?”

“Ndio, ndege zinazo ingia leo, moja imefika hapa saa nne hii asubihi na nyingine itafika hapa saa nane mchana ikitokea nchini Uingereza”

Adrus akiwa katika mazungu na muhudumu wa shirika hilo la ndege. Naomi mpenzi wake wa kwanza kwneye maisha yake akampita mita chache sana kutoka alipo na kwa bahati mbaya hawakuweza kuonana.

“Kesho ndege zenu zinaondoka saa ngapi?”

“Ya kwanza itaondoka Tanzania, ikipitia Kenya na safari yake ya mwisho itakuwa nchini Marekani”

Adrus akashusha pumzi nyingi sana kwani katika nchi ambayo hatamani kwenda wala kuzisikia kwenye maisha yake ya sasa ni Marekani

“Asante”

Adrus alijibu huku akielekea katika ofisi nyingine za shirika la fly emirates. Kabla hajaifikia ofisi hiyo akasimama kwa muda huku matukio mazuri ambayo mama yake aliwahi kumfanyia kipindi alipo kuwa mtoto yakianza kujirudia kichwani mwake.

‘Siwezi kufwata moyo wangu, ikiwa mwanamke anaye nipenda, kabla na baada ya kuwa mtu anaumia kwa ajili yangu’

Adrus alijisemea kimoyo moyo huku akiondoka na kuelekea katika magesho ya magari. Akaingia kwenye gari lake, jambo lililo mfanya Sa Yoo aliye simamisha gari alilo panda akiendelea kushangaa shangaa.

“Tuondoke”

“Tunakwenda wapi?”

“Nyumbani tunarudi”

“Adrus hembu niambie basi mume wnagu ni kitu gani kinacho endelea”

“Ni hivi. Mama……”

Adrus akasitisha sentensi yake akawasha gari na kuondoka kw amwendo wa kasi katika eneo hilo la uwanja wa ndege hadi Sa Yoo akashangaa. Kwa haraka Sa Yoo akawasha gari lake na kuanza kuwafwatilia, simu ya SaYoo ikaanza kuita akaitoa kwenye mfuko wa suruali yake na kukuta ni Eddy ndio anaye mpigia.

“Haloo”

“Mbona hunipi ripoti?”

“Tunatoka uwanaja wan dege hapa. Naona Adrus anaendesha gari kwa kasi, sijui amekerwa na nini”

“Munaelekea wapi?”

“Naona tumeshika njia ya kurudi nyumbani”

“Sawa endelea kuwafwatilia”

“Sawa”

Sa Yoo akakata simu na kuendelea kuwafwatilia. Adrus akafunga breki kwenye foleni kubwa ya magari akisubiria taa maalumu zinazo ongoza mataa ya barabarani kuwaruhusu upande wao na aendelee na safari.

“Alfu kuna gari nyekundu ile ferali inatufwatilia toka tulipo toka nyumbani”

Cookie alizungumza hukua kitazama kwenye kioo cha pembeni gari ambayo amepanda Sa Yoo. Adrus akaitazama kwa muda na kugundua kwamba anaye wafwatilia ni Sa Yoo.

“Ameagizwa”

“Nani?”

“Huyo binti, ni yule pale nyumbani nahisi atakuwa anatufwatilia”

“Ila kwa nini anatufwatilia sasa?”

“Sijajua”

Taa zikaruhusua na Adrus akaondoka kwa kasi eneo hilo. Dereva taksi aliye pokea amri ya kulifwatilia gari la Adrus, akamchumekea Sa Yoo ambaye naye alisha anaza kuondoka kwa mwendo wa kasi kwani akimpoteza Adrus itakuwa sio jambo zuri kwake.

“Weee mshenziii”

Sa Yoo alizungumza kwa kufoka huku akifunga breki za gari lake na kuiacha taksi hiyo kupita mbele yake. Naomi akageuka nyumba, hakuamini macho yake mara baada ya kumuona dereva wa gari hiyo ndogo, waliyo ipita ni miongoni wasichana wawilio alio pewa kazi ya kuwaua na raisi Dustan na inavyo onyesha, msichana huypo anamfukuzia Adrus mpanzi wake na mawazo ya Naomi moja kwa moja yakapelekea kwamba Sa Yoo anahitaji kumuua Adrus, jambo lililo mfanya Naomi kuchomoa bastola yake ndani ya begi na kuikoki vizuri tayari kwa kumshambulia Sa Yoo.



Sa Yoo kwa haraka akafunga breki za gari lake na kusabisha gari zinazo kuja nyuma yake nazo kufunga breki za gafla huku nyingine zikigongana kwa nyuma kwani tayari mataa yalisha ruhusu gari hizo kuondoka. Dereva taksi akabaki akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana kwani hakuamini kama abiria wake anaweza kuwa na silana na wala hajui amfungua fungua vipi kioo cha upande wake alio keti na kuanza kushambulia gari la nyuma yake. Honi za magari zikazidi kutawala huku, Sa Yoo akijaribu kufikiria nini cha kufanya kwani gari lake ndio limesababisha foleni hiyo. Sa Yoo akaitazama taksi hiyo kwa macho makali huku aking’ata meno yake, kwa haraka akaanza kuondoka eneo hilo huku akiifwata taksi hiyo kwa mwendo wa kasi sana.

Naomi akajitoa tena kwenye gari lake na kuanza kufyatua risasi kuelekea katika kioo cha gari la Sa Yoo, ugumu wa kioo hicho ukafanya risasi hizo kuto weza kupenya na kumpata Sa Yoo ambaye lengo na nia yake ni kuigonga taksi hiyo kwa nyuma. Kama alivyo dhamiria ndivyo alivyo fanya kwa nguvu Sa Yoo akaingonga taksi hiyo na kuifanya ianze kuyumba.

“Wee dada, mambo gani hayo, gari sio langu hili”

Dereva taksi alilalama na kumfanya Naomi kukaa vizuri kwenye siti yake ili kuhimili kuyumba huko kwa gari. Adrus akapunguza mwendo kasi wa gari huku akijaribu kutazama nyuma na kuto kuiona gari ya Sa Yoo ambaye tayari walisha gundua kwamba alikuwa akiwafwatilia.

“Vipi?”

“Sioni gari la yule dogo?”

“Labda ulivyo ondoka hivi kwa kasi amempoteza”

“Hapa hakuna kona ambayo nimekunja siwezi kumpoteza”

“Twende zetu tu nyumbani yeye si mwenyeji hapa mjini?”

“Ngoja”

Adrus alizungumza huku akigeuza gari hilo kwa utaalamu mkubwa sana na kuanza kurudi walio kuwa wametoka. Naomi akahamia siti ya mbele, akamnyooshea dereva taksi huyu bastola ya kichwa.

“Toka ndani ya gari unashangaa shangaa nini?”

Dereva taksi macho yakamtoka, hakuamini dada mzuri kama Naomi anaweza kwua jambazi ambaye anaweza kumpokonya gari. Dereva taski akafungua mkanda wa siti yake aliyo kalia huku machozi yakimlenga lenga, akafungua mlango na gari na kujirusha barabarani, na kwa bahati nzuri akafanikiwa kutua vizuri japo amepata michubuko ya hapa na pale iliyo sababishwa na kubingiria barabarani ila mwisho akafanikiwa kusimama na kuanza kuikimbizia taski yake kwa miguu akionyesha dhairi kwamba amepagawa na tukio hilo.

Naomi akahamia kwa haraka kwenye siti ya dereva huku akifunga mlango wa dereva, akaongeza spidi ya taksi hiyo na kuliacha gari la Sa Yoo mita kadhaa.

‘Pumbavu’

Sa Yoo alizungumza huku akiongeza tane mwendo wa gari lake, akaikaribia taski hiyo kidogo, kisha akaigonga kwa pembeni na kusababisha taksi hiyo kuyumba sana na kuanza kuzunguka, huku Naomi akijitahidi sana kuhakikisha kwamba ana ihimili isianguke.

“Hee ni nini kile?”

Cookie aliuliza mara baada ya kuona taksi ikizunguka barabarani. Wakashuhudia jinsi gari analo endesha Sa Yoo ikiibamiza taksi hiyo maeneo ya ubavuni na kuisabahisha ipinduke na kuzunguka mara mbili barabani na kwa bahati nzuri ikatula kwa kugonga bomba la taa za barabarani na kulisababisha bomba la taa hiyo kupinda. Kama kawaida ya Watanzania kukusanyika inapo tokea ajali ndivyo jinsi walivyo anza kukimbilia katika taksi hiyo kwenda kushuhudia ni nini kilicho tokea. Sa Yoo mara baada ya kuona raisi wanaongezeka na yeye dhairi anaonyesha kwamba ndio msababishaji wa ajali hiyo, hakuona haja ya kushuka kwenye gari lake, alicho kifanya ni kuhakikisha kwamba anaondoka eneo hilo kwa mwendo wa kasi sana na kuwafanya watu wabaki wakiwa wameshikwa na maswali yaliyo kosa majibu.

“Huyu mtoto amechanganyikiwa nini?”

Adrus aliuliza huku akishuhudia jinsi Sa Yoo anavyo zidi kutokemea katika eneo hilo.

“Hembu twende tukaangalie amemgonga nani?”

Cookie alishauri na Adrus hakuwa na ubishani wa aina yoyote zaidi ya kusimamisha gari lao mita chache kutoka sehemu iliyo poteka ajali. Kwa haraka wakashuka na kukimbilia katika eneo hilo. Adruds akawapangua pangua watu hadi akafika katika taksi hiyo, akajumuika na wanaume watatu wanao jitahidi kufungua mlango wa taksi hiyo, ulio pondeka pondeke huku tanki la mafuta likiwa linamwaga mafuta barabani na kuna cheche cheche za nyanya za bomba hilo la taa zikiruka huku na kule.

“Sogeeni mbali nyinyi watu”

Adrus alizungumza kwa ukali huku akiwatazama raia walipo katika eneo hili. Raia hawa wala hawakujali sauti ya Adrus, zaidi ya kuzidi kukogoa macho huku vibaka nao wakijichanganya wakiona ni kitu gani wanacho weza kukifanya ili kujipatia japo ridhiki kutoka katika ajali hii, na mashuhuda wengine ambao nao wapo wakishangaa kinacho endelea, wanaibiwa na vibaka hao pasipo wao wenyewe kujijua.

Kwa bahati nzuri Adrus akaoiona bastola iliyo ndani ya gari hilo, akaingiza mkono wake na kuichukua huku macho yake yakiwa bado hayajamuangalia Naomi aliye poteza fahamu. Adrus akachomoa magazine ya bastola hiyo na kukuta ikiwa na risasi za kutosha, akairudisha na kuikoki bastola hiyo na kufyatua risasi mbili hewani.

Si raia mwema wala kibaka hakuna ambaye alithubutu kubaki katika eneo hilo, kila mmoja akapotelea anapo jua yeye mwenyewe na aliye bakia katika eneo hilo ni Adrus na Cookie ambaye alishuhudia jinsi Adrsu anavyo piga risasi hizo hewani.

“Nisaidie”

Adrus alizungumza kwa haraka Cookie akamsogelea na wakasaidiana kumchomoa Naomi ndani ya gari hilo, jambo lililo mfanya Adrus kuhisi ni ndoto na labda msichana huyo atakuwa amemfananisha.

“Pochi yake”

Cookie alizungumza huku akiivuta pochi ya msichana huyo, ambaye kwa yeye hamfahamu ila Adrus anamfahamu vizuri sana. Kwa haraka Adrus akambeba mikononi mwake, na kuanza kukimbia naye katika gari lao, huku Cookie akimfwata kwa nyuma akiwa amebeba pochi. Kitendo cha kuingia tu ndani ya gari lao, taksi hiyo ikalipuka, kwani cheche nyingi zilitua juu ya mafuta yaliyo kuwa yamesambakaa barabarani.

Adrus akawasha gari na wakaondoka eneo hilo kwa kasi, huku akili yake kwa haraka ikimtuma kumuwahisha mwanamke huyo anaye mpenda katika hospitali ya Muhimbili.

***

Sa yoo akafunga breki kali kwenye geti za kuingilia katika geti la jumba la Eddy huku akipiga honi kubwa na kuwafanya walinzi kutoka nje kwa haraka huku wakiwa na silaha, hawakuamini kuona jinsi gari la Sa Yoo, likiwa limebondeka bondeka huku kioo cha mbele kikionyesha dhairi kimeshambuliwa na risasi japo hakijapasuka. Mlindi mmoja akaruhusu geti hilo kufunguliwa, Sa Yoo akapita hadi katika geti la pili ambalo nalo lilifunguliwa na moja kwa moja akasimamisha gari hilo usawa wa mlango. Akashuka huku akihema na kumfanya Eddy aliye kuwa amesimama katika kibaraza akilishuhudia gari hili jinsi linavyo ingia humo ndani kumfwata kwa kasi huku akiwa na shauku kubwa ya kuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kimempata Sa Yoo.

“Vipi ni nini kimetokea?”

“NImevamiwa”

“Na nani?”

“Sijui na nani ila alikuwa kwenye taksi”

“Kwenye taksi, ni nani?”

“Sifahamu”

Eddy kwa haraka akakimbilia kwenye gari hilo, akaminya moja ya batani na tv ndogo iliyomo ndani ya gari hilo ikasoegea mbele kidogo. Akachomoa card ndogo ya kuhifadhia vitu, kisha akashuka.

“Nenda ndani kamuite yule, yule mchina mwenzako”

“Wapo wawili?”

“Yule mwembamba kumzidi mwenzake”

Sa Yoo akagundua kwamba anaye zungumziwa hapo ni Lee Ji.

“Muambie aje na laptop yake”

“Sawa”

Sa Yoo akaingia ndani, kwa bahati nzuri akakutana na Lee Ji akiwa anashuka kwenye ngazi zinazo tokea goroafani huku akiwa ameshika laptop yake.

“Sa Yoo mbona una wasiwasi vipi kwema?”

“Si kwema, ila Eddy anakuita huko nje”

“Yupo nje eneo gani?”

“Hapo kibarazani, twende wote”

Wakatoka nje kwa pamoja na kumkuta Eddy akiwa anaelekea katika bustan ya mapumziko. Lee Ji akaonekana kulishangaa gari hilo la kifahari lililo bondeka bondeka.

“Mbona hili gari limebondeka hivi?”

“Yaani weee acha nimevamiwa huko barabarani, nusu nife”

“Heee wewe ndio ulikuwa unaliendesha?”

“Eheee”

“Eheee pole sana”

“Asante”

Walizungumza huku wakimfwata Eddy katika sehemu alipo kaa.

“Lee Ji kuna hii chipu hapa nimeitoa kwenye gari langu pale huwa inarekodi matukio yote jinsi gari linavyo kwenda mbele, hembu angali ni kitu gani ambacho kimempata Sa Yoo”

Eddy alizungumza huku akimkabidhi Lee Ji chipu hiyo, Lee Jing akaitazama chipu(memory card) akaona ina uweza wa kuingia kwenye laptop yake bila mashaka ya aina yoyote. Akawasha laptop yake na kuichomeka chipu hiyo.

“Matukio ya leo si ndio?”

“Ndio”

Lee Ji akaweka video inavyo onyesha jinsi Sa Yoo alivyo kuwa anatoka asubuhi ya leo.

“Pelekea pelea mbelea”

Sa Yoo alizungumza huku naye akitazama video hiyo.

“Hapa”

Sa Yoo alizungumza huku akionyesha jinsi alivyo kuwa kwenye foleni. Wakamshuhudia msichana huyo jinsi alivyo kuwa akimfyatulia risasi Sa Yoo. Eddy akajaribu kuvuta kumbukumbu ya wapi amemuona msichana huyo, ila akakosa jibu sahihi katika kichwa chake, kwani msicha huyo sura yake sio ngeni kabisa kwake.

“Unaweza kutafuta maelezo ya huyu msichana kwa kupitia picha yake?”

Eddy aliuliza.

“Ndio”

“Nisaidie katika hilo”

Lee Ji akaanza kuifanya kazi hiyo kwa umakini sana, haikuchukua muda mwingi sana kafanikiwa kupata maelezo ya msichana hiyo anaye itwa Naomi na ni mwanajeshi wa Marekani.

“Ina maana Wamarekani wametuma watu kwa ajili ya kutuua?”

Sa Yoo aliuliza swali ambalio si Eddy wala Lee Ji aliye weza kulijibu kwa wakati huo. Kwenye maelezo ya mahusiano Lee Ji akajikuta akitazamana na Eddy, kwani mtu ambaye anaonekana kwamba yupo kwenye mahusiano na msichana hiyo ni Adrus Maldin mtu ambaye wapo naye katika jumba hilo.

“Wana mahusiano na Adrus?”

Sa Yoo aliuliza huku macho yakizidi kumtoka.

“Ndio sasa hapa nimekumbuka”

Eddy alijibu kwa msisitizo, kwani huyu ndio msichana ambaye Adrus anampenda sana kwenye maisha yake na ndio msichana ambaye kipindi cha mwaka mmoja na Nuru, Adrus alimuomba aweze kumsaidia katika kufwatilia juu ya afya yake hiyo ni mara baada ya shambulio likilo fanywa na kikundi cha Al-quida na waliondoka na mtoto wa raisi wa Marekani, Charity Dustan.

“Sasa kwa nini alikuwa ananishambulia mimi?”

“Hili swali kwa sasa ni ngumu kuweza kufahamu, kwani yupo wapi?”

“Kwa ajali aliyo ipata sidhani kama anaweza kuwa hai”

Maneno ya Sa Yoo kidogo yakamstusha Eddy ambaye, anafahamu vizuri jinsi hisia za Adrus zilivyo juu ya msichana huyo.

“Adrus ana simu?”

“Sidhani”

Lee Ji alijubu swali hilo la Eddy.

“Hembu tafuta gari namba T666JRT”

Eddy alimtajia Lee Ji namba ya gari hilo kwani ndilo gari walilo ondoka nalo Cookie na Adrus. Lee Ji akafanikiwa kufahamu ni wapi gari hilo linapo elekea.

“Limemefika katika hospitali ya Muhimbili”

“Muhimbili?”

“Ndio”

Kwa ishara Eddy akamuta mmoja wa walinzi, akafika eneo hilo.

“Niandalieni msafara wangu haraka ninahitaji kuelekea Muhimbili.”

“Sawa muheshimiwa”

“Lee Ji tunakwenda pamoja, Sa Yoo wewe baki hapa nyumbani”

“Ninataka niende huko, nataka kujua ni kwa nini msichana huyo alihitaji kuniua mimi”

Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku akimkazia macho Eddy aliye kaa kimya huku akishindwa kumjibu kitu chochote.

***

Machozi yanayo mwagika Adrus usoni mwake, yakaanza kujenga maswali mengi sana kichwani mwa Nuru kwani hajui ni kwa nini mume analia mara tu baada ya kumpakiza msichana huyo waliye msaidia kwenye ajali. Akatamani kumuuliza swali Adrus, ila kwa hali ambayo Adrus anayo anashindwa hata kumuliza chochote. Wakafika katika hospitali ya Muhimbili, kwa haraka Adrus akawa mtu wa kwanza kushuka kwenye gari akafungua mlango wa siti ya nyuma na kumtoa Naomi na kumbeba mikononi mwake huku akiomba kimoyo moyo mpenzi wake huyo asiweze kupoteza maisha yake.

Cookie akawafwata kwa nyuma huku akiwa ameshika pochi ya msichana huyo. Manesi wawaili wakakiweka kitanda cha matairi sawa na Adrus akamlaza Naomi juu ya kitanda hicho.

“Ehee Mungu msaidie”

Adrsu alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Akamshuhudia Naomi akiingizwa katika chumba cha matibabu na nesi mmoja akawaomba waweze kusubiria nje.

“Adrus”

“Nini?”

Naomi akasita kidogo kwani kuitikia kwa Adrus kumemkatisha tamaa kidogo.

“Samahani mpenzi wangu. Unamfahamu huyo binti?”

“Sijui”

Adrus alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekikalia na kumfanya Cookie abakiwa na mshangao.

“Akifa. Lazima na yeye afee”

Maeneno hayo ya Adrus yakazidi kumduwaza Cookie, ambaye kwa haraka akapata wazo la kuipekua pochi ya msichana huyo waliye msaidia, akatoa hati ya kusafiria, akaitazama vizuri. Jina la Naomi sio ngeni kabisa kwenye masikio yake. Naomi ni msichana wa kwanza wa Adrus ambaye anampenda kuliko kitu chochote, na hilo Cookie analifahamu.

‘Mungu wangu, sina changu hapa’

Cookie alizungumza huku mikono ikimtetemeka kwa wasiwasi na mapigo ya moyo nayo yanazidi kumuenda kasi.

‘Hapana siwezi kumpoteza Adrus wangu, ninampenda sana. Naomi na wewe ni lazima ufee, ninakuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe’

Cookie alizungumza huku akimtazama Adrus anaye zunguka zungua kwenye kordo hiyo ikionyesha dhairi kwamba amechanganganyikiwa na ajali iliyo mpata Naomi.



Adrus kwa haraka akarudi mlangoni hapo, akataka kuufungua ila Cookie akamuwahi na kumzuia kuingia ndani.

“Baby unataka kufanya nini jamani ikiwa madaktari wakiwa wametukataza kuingia humu ndani”

Cookie alizungumza kwa sauti iliyo jaa mahaba ili mradi kuhakikisha kwamba ana mshawishi Adrus kuto kufanya chochotye katika kuingia ndani. Adrus akamtazama Cookie kwa muda kidogo kisha akapiga hatua hadi kwenye viti vilivyopo katika eneo hilo na kukaa.

***

Eddy na msafara wake wakafika katika hospitali ya Muhimbili, moja kwa moja wakapelekewa hadi katika chumba cha matibabu anayo fanyiwa Naomi na hapo ndipo wakakutana na Adrus pamoja na Cookie wakiwa nje ya chumba hicho. Adrus macho yake yote yanamtazama Sa Yoo anaye onyesha ana shauku kubwa sana ya kufahamu hali ya binti huyo.

“Mgojwa ana endeleaje?”

Eddy aliuliza huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Bado madaktari hawajatoka ndani ya chumba hichi”

Sauti ya Adrus dhairi inaonyesha ni mtu aliye jawa na uchungu mwingi ndanye yake ulio ambatana na hasira kali.

“Kwa nini huyo dada alitaka kuniua?”

Sa Yoo aliingilia mazungumzo hayo na kumfanya Cookie kushangaa kidogo.

“Kukuua…..!!?”

Adrus aliuliza kwa mshangao huku akimtazama Sa Yoo usoni mwake. Kabla ya Sa Yoo kujibu kitu cha aina yoyote. Lee Ji akafungua laptop yake na kuiweka video inayo onyesha jinsi Naomi alivyo kuwa akimshambulia Sa Yoo na kuhitaji kumuua. Hasira yote ambayo Adrus anayo ikaanza kuyayuka taratibu, laiti kama angefahamu taksi ambayo alisimamisha gari pembeni yake ilikuwa imembeba mpenzi wake Naomi wala asinge chukua maamuzi ya kuondoka katika eneo hilo kwa kasi, kisa tu kumkimbia Sa Yoo aliye kuwa akiwafwatilia.

‘Kwa nini ameteka kuua.

Adrus alijiuliza kimoyo moyo huku akijaribu kuirudia rudia video hiyo mara kadhaa.

“Inabidi aweze kufanyiwa mahojiano akiamka haraka iwezekanavyo”

Eddy alitoa maagizo ambayo kwaupande mmoja hayajamfurahisha kabisa Adrus, ila nashindwa kuyakataa kwamaana ni maamuzi ya makamu wa raisi.

“Sawa mkuu”

“Mimi nitamuhoji, ni kwa nini alitaka kuniua kwa maana simjui, ila inavyo onekana yeye ananijua mimi”

Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo ulio wafanya Eddy na Adrus kushangaa sana.

“Sa Yoo we…”

“Hapana Eddy, ulinituma hii kazi acha niimalizie, mtu akihitaji kuku ua ina maana yeye ni adui na anastahili kuhukumiwa.”

“Sawa tumpe nafasi ya kurudisha kumbukumbu zake”

Eddy alizungumza, simu yake ikaanza kuita kwa haraka akaitoa mfukoni mwake na kukuta ni namba ya raisi Rahab ndio anaye mpigia. Akaipokea na kuiweka sikioni mwake huku akiondoka katika eneo hilo.

“Ndio Rahab”

“Nimepata habari kwamba upo Muhimbili, kuna nini kinacho endelea?”

“Kuna binti wa Kimarekani, ninavyo hisi ametumwa na serikali yake kuja kumuangamiza Sa Yoo na ninavyo hisi zaidi ni mtu mwengine atakuwa ni Shamsa, naamini bado wana visasi juu ya majasusi wao walio weza kuwatuma kwetu”

“Mmmmm hiyo ni hatari kidogo”

“Sio kidogo ni kubwa, hii inaweza kupelekea kuua mahusiano yetu mazuri kati yetu na wao”

“Ni kweli sasa huyo binti imekuwaje kuwaje hadi awepo hapo Muhimbili?”

“Katika juhudi za Sa Yoo kujiokoo, kwa bahati nzuri alifanikiwa kuweza kumsababisha ajali kwa maana mashambulizi yenyewe yalifanyika wakiwa kwenye magari”

“Ahaaa hembu endelea kufanya upelelezi na mimi huku nizidi kufanya upelelezi kwa makachero wetu walipo katika nchi ya Marekani”

“Sawa muheshimiwa.”

“Poa baadae”

Eddy akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake.

Ndani ya chumba cha matibabu, Naomi akayafumbua macho yake, na madaktari wote ambao bado walikuwa wakiendelea kumfanyia uchunguzi wa vipimo vya mwili wake wakabiki wakiwa wameshangaa.

“Dada jaribu kuwa mpole, kidogo una majeraha kati….”

Naomi akamsukuma daktari huyo na kuvua tafarani ndani ya chumba hicho cha matibabu, manesi wengine wakaungua mlango na kutoka chumbani humo kwa kasi na kuwaduwaza Adrus na wezake wote walio kuwa wakisubiria taarifa nzuri kutoka chumba hicho. Adrus akawa mtu wa kwanza kuingia ndani ya chumba hicho cha matibabu na kumkuta Naomi akishuka kitandani.

Adrus na Naomi wakatazamana kwa muda huku wote wakiwa kwenye usikivu, ulio wafanya machozi yaanze kuwamwagika. Kwa haraka wakakumbatia huku machozi yakiwamwagika.

Kitendo cha Naomi kukumbatiana kimahaba na Adrus kikamuumiza sana Cookie ambaye amesimama mlangoni mwa chumba hicho na anashuhudia jinsi wanavyo lia kwa furaha. Maumivu ya moyo wa Cookie yakazidi kuongezeka mara tu Adrus alipo anza kunyonya midomo ya Naomi pasipo kujai kama Cookie yupo au hayupo katika eneo hilo.

Sa Yoo na Lee Ji wakazidi kushangaa tukio hilo, kwani wote wanafahamu kwamba Cookie ndio mpenzi sahihi wa Adrus. Cookie akataka kuingia ndani ya chumba hicho, ila Eddy akamuwahi na kumshika mkono.

“Usiende”

Eddy alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Cookie usoni mwake, ambaye tayari amesha anza kufura kwa hasira. Cookie akamtazama Eddy kwa macho yaliyo jaa hasira, kisha kwa nguvu akautoa mkono wake ktika kiganja cha Eddy, kisha akaingia ndani humo na kuwaachanisha Adrus kwa nguvu hadi, Naomi akaangukia kitandani.

“Adrus hii ni dharau, hii ni dharau tena kubwa”

Cookie alizidi kuzungumza huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake.

“Ahaaa wewe ndio uliye mshawishi Adrus kuniacha si ndio?”

Naomi naye alizungumza kwa dharua huku akimpandisha kwa macho na kumshusha Cookie.

“Adrus ni mume wangu”

“Hahaaa, angekuwa mume wako asinge ninyonya midomo yangu, hujui ni wapi mimi na Adrus tumetoka”

Naomi alizidi kuzungumza kwa kejeli, iliyo mfanya Cookie azidi kupandwa na hasira iliyo pelekea kurusha kibao kilicho mpiga Naomi cha shavu. Adrus akatamani kuingilia ugomvi huu ila akashindwa kabisa kutokana na kushikwa na kigumizi ch amwili mzima, kwani kwenye maisha yake yote hakuwahi kukutan ana tukio kama hili.

Naomi naye akarudisha kofi zito lililo mfanya Cookie kurudi nyuma kidogo huku akisikilizia maumivu ya kofi hilo. Kwa karaka Cookie akamerukia Naomi na wakaangushana kitandani kitendo kilicho wafanya waanze kukwidana huku kila mmoja akijitahidi kumkandika mangumii mwenzake.

Eddy kwa haraka akaingia ndani ya chumba hicho na kuanza kuwaachanisha Naomi na Cookie, hapo kidoho Adrus naye akapata nguvu ya kusaidiana na Eddy katika kuwaachanisha wanawake hawa ambao wote wivu ndio unawasumbua. Adrus alaka,shika Cookie na kutoka naye nje kwa nguvu huku kwa mara kadhaa akinyanyua nyanyua kutokana na Cookie kibisha kabisa kutoka katika eneo hilo.

“Umeridhika kuona unanyonyana denda na mwanamke mwengine mbele yangu si ndio?”

Cookie alizungumza kwa hasira ila Adrus hakumjibu chochote zaidi ya kuzidi kumbeba kwa nguvu na kuelekea naye eneo walipo liacha gari lao.

“Niachie nikamkomeshe yule malaya wako”

“Tulia acha upumbavu, unanidhalilisha mbele za watu”

“Ninakudhalilisha au unajidhalilisha mwenyewe eheee…..”

Cookie alizidi kuzungumza huku akifoka.

“Tulia binti”

Eddy alizungumza huku akimshikilia Naomi ambaye naya anajaribu kufurukuta kujitoa mikononi mwa Eddy ili akapambane na Cookie. Naomi taratibu akaanza kutulia huku akimtazama Sa Yoo aliye simama mlangoni.

“Kwa nini umeta kuniau?”

Sa Yoo aliuliza kwa hasira huku akiendelea kumtazama Naomi aliye shikiliwa na Eddy. Naomi akashindwa kujibu chochote kwani kuna walinzi zaidi ya nane wamesimama nyuma ya Sa Yoo.

“Mchukueni na mumpeleke katika chumba cha mahojiano”

Eddy aliwaambia walinzi wake na kwa haraka wakaingia ndani chumba hicho akamfunga pingu Naomi na kuanza kutoka naye ndani humo huku Sa Yoo na Lee Ji wakiwafwata kwa nyuma.

“Ila kwa nini Cookie unataka kunidhalilisha mbele za watu?”

“Ninakudhalilisha au unajidhalilisha mwenyewe. Kwa nini lakkini umeamua kuumiza moyo wangu mbele za watu eheee?”

Cookie aliendelea kufoka huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Ila…..”

“Ila nini, unahisi sifahamu, eheee yule si ndio Naomi wako si ndio?”

Adrus akaka kimya na kushindwa kujibu swali hilo.

“Nilijitolea maisha yangu kwa ajili yako, nilihakikisha kwamba ninamsaliti bosi wangu na kuamua kuanzisha maisha yangu kwa ajili yako, sasa nakuambia ukweli toka moyoni mwangu, ukiendelea kuwa na yule msichana, nakuhakikishia kwamba nitamuaa. Aniue mimi au mimi nimue yeye sawa”

Maneno ya Cookie taratibu yakaanza kutengeneza picha mbaya kichwani mwa Adrus na kujikuta akitamani kufanya tukio moja baya ambalo litamnyamazisha Cookie maisha yake yote.

***

“Ninaushauri kwako bwana John”

Mkuu wa kikosi cha CIA, alizungumza huku akimtazama John usoni mwake.

“Ushauri gani?”

“Kuna makomandoo wawili hatari sana ambao wametumiwa na raisi wetu Dustan katika kumuokoa mwanye hivi juzi na wamesha fanikiwa kuifanya kazi hiyo kwa muda mfupi sana na wamesha pote ana ninavyo zungumza hivi sasa raisi Dustan amepagawa juu ya kutoweka kwao hao makomandoo”

“Amepagawa kwa nini?”

“Ni watu hatari ambao ukiwapa kazi ya kumuangamiza mtu fulani huwa hawana masihara na ndani ya muda mchache, na wewe umeweza kuniadisia kwamba makamu wa raisi wa Tanzania ametuma vijana wake wamekuulai mwanamke uliye kuwa unampenda na baba yako mkwe, basi unaweza kuwapa hiyo kazi”

“Nitawapatia wapi?”

“Mimi ninajua ni wapi kwa kuwapata na ninawafahamu vizuri na wanaweza kunisikilizaa katika kile ambacho tutawakabidhi ila kikubwa unatakiwa kuandaa kiasi kikubwa cha kuwapa ili kazi yako iweze kutendeka vizuri”

“Kama kiasi gani?”

“Dola bilioni moja na kuendelea?”

“Dola bilioni moja……..!!!?”

“Yaa hilo ndio dau lao, nahisi watu wenyewe utakuwa umesha wahi kuwasikia, wanaitwa Dump na Dumbe”

“Sijawahi kuwaisikia, ila wanaweza kweli kuifanya kazi ya kuwaua Eddy na timu yake?”

“Ndio ninakua uhakika wa asilimia mia moja wanaweza kuifanya hiyo kazi na pesa ulizo ibiwa nazo zitarudishwa”

“Kweli”

“Sikudaganyi na niamini mimi”

“Sawa nahitaji kuonana nao na hii kazi nahitaji waweze kuifanya haraka iwezekanavyo sawa?”

“Nimekupata, wewe andaa kiasi cha pesa ambacho nimekuambia.”



John akashusha pumzi nyingi sana huku akiwazia ni jinsi gani anaweza kuipata hiyo pesa ambayo ameambiwa kwamba aanze kuianda.

“Unauhakika kwamba pesa yangu ambayo imeibiwa wanaweza kuirudisha kwa maana hiyo pesa hapa nafikiria ni katika kampuni gania mbayo ninaweza kwenda kuikopa”

“Nakuhakikishia hilo nipe masaa mawili nitakuwa nimesha wapata”

***

“Nahitaji kurudi Tanzania?”

Maneno ya K2 yakamstua sana Livna, hadi akajikuta akiacha kunywa chai ambayo ipo kwenye kikombe chake.

“Tanzania?”

“Ndio”

“Hivi unahisi kwamba sura yako itakuwa imesahaulika katika siku mbili tatu hizi?”

“Najua ni nini ninacho kifanya, ni muhimu sana kwa mimi kurudi Tanzania leo hii”

“Nahisi hujui unacho kifanya?”

“Ninajua. Kumbuka kwamba mimi sio mwanachama wako uniye takiwa kuniongoza kama unavyo waongoza hawa vijana wako hapa, nina maamuzi yangu ya kufanya na nitakiwa kurudi Tanzania, niende nikafanye mipango yangu, kwa maana nikikuomba msaada wowote naona sipati msaaha huo ninao utarajia”

“Sawa nitakusaidia katika kukupatia vijana wataka kurudisha Tanzania kisha wao watarudi”

“Sawa, itakuwa ni vizuri sana ikiwa ni muda huu kwa maana mipango yangu naona inakwenda kulala”

“Sawa”

Livna akawasiliana na vijana wake wawili wana shuhulika katika maswala ya kuendesha boti zinazo kwenda kwa kasi wanazo zimiliki. K2 hakuhitaji hata kuimalizia. K2 akaongozana na vijana hao walio kuja kumfwata ndani ya chumba hicho. Livna kwa haraka akanyanyuka akatoka katika chumba hicho na kuanza kumfwata K2 kule anapo elekea.

“K2, K2”

Livna aliita huku akimfwata K2 kwa nyuma.

“Ndio”

“Ahaaa….kama utakuwa unahitaji msaada wangu basi utawasiliana nami, nitakusaidia katika jambo lolote ambalo utahitaji nikusaidie sawa”

“Nashukuru kwa ukarimu wako”

“Ila angalizi, hakikisha kwamba sura yako haionekani kirahisi, tambu kwamba hali ya nchi ya Tanzania bado itakuwa inatutafuta”

“Usijali nitahakikisha kwamba hawanikamati”

“Sawa, hivi hukuniambia juu ya kikosi chako unacho kimiliki”

“Tutalizungumzia hilo kwa wakati mwengine, ila kwa sasa ninahitaji kwenda kufanya kitu kingine kinacho weza kusumuma juhudi zangu”

“Sawa, ila jambo la kukushauri la mwisho, vaa baibui”

Livna akamuagiza kijana wake mmoja kwenda kuchukua baibui. Wakamletea K2 baibua, na akalivaa, na kuifunika sura yake vizuri. Walipo hakikisha kwamba si rahisi kwa K2 sura yake kuonekana, vijana hao wawili wakaingia kwnye boti huku wakiwa wameongozana na K2. Safari ya kuelekea nchini Tanzania ikaanza taratibu.

***

“Wewe tu niangalie ila ninakuambia ukweli, nitahakikisha kwamba nina muua huyu malaya wako”

Cookie aliendelea kuzungumza kwa hasira, kwani wivu wa mapenzi tayari umesha mtawala. Wakiwa ndani ya gari hili Adrus akashushudia jinsi Naomi akiwa ameshikiliwa na walinzi wa makamu wa raisi na kuingizwa kwenye moja ya gari la walinzi hao na kuondoka eneo hilo.

“Washa gari umfwatilie huyo malaya wako ujue ni wapi anapo peletwa”

“Cookie usione nipo kimya ukahisi siwezi kuzungumza, heshima itawale sawa”

“Itawale vipi, itawale vipi, mwanaume gani usiye jua thamani ya mtu, kazi umeendekeza umalaya tu”

Adrus akamtazama Cookie kwa macho ya hasira sana, hapa sasa ndipo akaanza kuyakumbuka maneno ya mama yake ambayo yalimsisitizia kwamba aachane na msichana huyu.

“Cookie”

“Nini?”

“Unapesa ya kutosha ya kwenda popote unapo pahitaji, hivyo basi nakuomba uachane na mimi sawa”

Maneno ya Adrus yakamfanya Cookie kutulia, hasira ambayo ilikuwa ikimfanya kuzungumza chochote anacho jisikia, ikaanza kutoweka, upole na unyonge ukaanza kumtawala.

“Adrus……”

Cookie aliita huku machozi yakianza kumlenga lenga usoni mwake.

“Naamini umeelewa, nitakusaidia kwa kutafuta sehemu yoyote ambayo utahitaji kwenda, ila swala la mahusiano mimi na wewe na kuomba liishia leo hii, sahau kama ulisha wahi kuwa na mwanaume kama mimi sawa”

“Unaniacha kwa ajili ya yule mwanamke kweli Adrus, kumbuka ni mambo mangapi tumeyafanya mimi na wewe?”

“Hata yeye tumeweza kupambana na mambo mengi sana hadi kufika hapa tulipo fikakia, hivyo basi nakuomba uachane na mimi”

Adrus alizidi kuzungumza kwa msisitizo jambo lililo zidi kumsonenesha sana Cookie na kujutia kwa nini alishindwa kuzizuia hisia zake za kimapenzi na amejikuta akiwa katika hali hiyo ya kuachwa.

“Adrus ninakupenda, ninakuhitaji”

“Hata Naomi ananipenda, ana nihitaji”

“Sawa anakuhitaji ila hata mimi nakuhitaji Adrus wangu”

“Koma mimi sio wako wewe, endelea na maisha yako sawa”

Kila neno linalo toka mdomoni mwa Adrus linamshangaza sana Cookie na kuhisi kwamba yupo kwenye ndoto moja kubwa sana ambayo haina muda maalumu wa kuisha ili atoke kwatika usingizi huo.

“Ukihitaji kuondoka nchini Tanzania utaniambia sawa”

“Nipeleke nyumbani”

“Sawa”

Adrus akawasha gari na kwa mwendo wa taratibu wakaanza kuondoka katuka eneo hilo, na hakuwa na wasiwasi mwingi sana kuhusiana na Naoami na anaamini kwamba Naomi eneo analo pelekwa, itakuwa ni rahisi kwa yeye kuweza kulifahamu eneo hilo endapo atamuuliza makamu wa raisi.

Safari ya kuelekea nyumbani kwa jumbaa la makamu wa raisi haikuchukua muda mrefu sana, wakafika katika jumba hilo na Adrus hakuhitaji kuingia ndani zaidi ya kusimamisha gari lake nje ya jumba hilo.

“Shuka uende ndani kuna sehemu nahitaji kwenda”

Cookie akamtazama Adrus kwa muda, kisha akashuka taratibu na kuufunga mlango. Adrus akawasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi sana. Cookie akajifuta machozi yanayo mlenga lenga na taratibu akaanza kuingia ndani, kutokana walinzi wanamfahamu, hapakuwa na haja ya wao kuweza kumkagua.

“Vipi mulikuwa wapi?”

Jing alimuliza Cookie mara baada ya kumuona akiingia ndani humo, ila Cookie hakumjibu chochote zaidi ya kumpita tu jambo ambalo lilimfanya Jing kushangaa kidogo. Jing akaanza kumfwata Cookie kwa nyuma hadi wakaingia kwenye chumba anacho lala na Adrus.

“Cookie una tatizo gani, mbona umekuwa mnyonge na unaonekana kama ni mtu uliye kuwa unalia?”

“Ni Adrus”

“Adrus amefanyaje?”

“Ameniacha”

“Amekuacha, amekuacha kwa nini?”

“Leo hii amekutana na mwanamke wake wa zamani, yule anate itwa Naomi”

“Naomi yupo nchini Tanzania!!!?”

Jing aliuliza kwa mshangao mubwa sana.

“Ndio yupo nchini Tanzania, nimepokonywa tonge mdomoni mwangu”

Cookie alizungumza huku machozi yakiendelea kumwagika usoni mwake. Jing akaka kimya huku akimtazama rafiki yake huyu anavyo umia kwa ajili ya mapenzi.

“Adrus yaani ana mla denda mwanamke huyo mbele yangu, kweli, kweli jamani hiyo ni haki eheee?”

“Jamani hapo alipo fikia si pazuri”

“Kwa nini likini, au kwa sababu hapo nyuma sikuwahi kuwa na familia eheee?”

Cookie alizungumza kwa uchungu sana huku akiendelea kuliwa sana. Jing machozi yakaanza kumlenga lenga usoni mwake.

“Inabidi uzungumze na mama juu ya hili?”

“Naanzia wapi, ikiwa hata sijatambulishwa kwa muda wote ambao nimekaa hapa, nimekuwa nikikaa kaa tu”

“Ngoja”

Jing alizungumza huku akijifuta machozi usoni mwake. Akatoka katika chumba hicho na moja kwa moja akaelekea hadi katika chumba cha mama Adrus. Akagonga mara mbili na mlango ukafunguliwa.

“Shikamoo”

“Marahaba Jing mbona unaonekana huna furaha”

“Mama nahitaji kuzungumza na wewe”

“Sawa, karibu ndani, vipi kuna tatizo?”

“Hapana, nahitaji tukazungumzie huku”

Jing alizungumza huku akimtazama mama Adrus usoni mwake. Mama Adrus akakubaliana na Jing wakaanza kutembea hadi walipo fika katika mlango wa chumba cha Adrus, kidogo mama Adrus akasita kuingia.

“Ni chumbani kwa mwanangu, kuna nini tena?”

“Wewe mama njoo tuzungumze”

Jing alizungumza kwa msisitizo. Taratibu wakaingia ndani ya chumba hicho, wakamkuta Cookie akiwa amekaa kitandani huku amejikunyata na kuukumbatia mto mkubwa alio kuwa nao.

“Mama naomba ukae hapo kitandani”

Jing alizungumza kwa msisitizo hadi mama Adrus akashangaa kidogo. Taratibu mama Adrus akakaa taratibu kitandani huku akijiuliza maswali mengi sana juu ya hali inayo endelea kwa wasichana hawa.

“Mama wewe ndio msemaji wa mwisho kwa mwanao Adrus, si ndio”

“Ndio, ila yeye ana maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume”

“Ndio ni mwanume ila una maamuzi juu yake si ndio?”

Jing aliendelea kuuliza kwa msisitizo huku hasira ikwia memtawala ndani yake.

“Ndio”

“Mwanao Adrus amemuacha rafiki yangu, anamuumiza mtoto wa mwanamke mwezetu, kisa kumpenda kwa nini mwanao anafanya hivyo eheee?”

Mama Adrus kidoo akastuka, kwani yeye ndio mtu wa pekee ambaye amemsisitizia mwanaye kuhakikisha kwamba anaachana na Cookie kutokana tu hajampenda.

“Ila sijawaelewa?”

“Hujatuelewa nini, hivi unajua ni jinsi gani mwanao anavyo mtesa Cookie?”

“Nikiwa kama mama na ninaye mpenda mwanangu, siwezi kukubaliana naye katika maamuzi ambayo alihitaji kuyafanya”

Meneno ya mama Adrus yakamfanya Cookie kunyanyua kichwa kidogo na kumtazama mama Adrus usoni mwake.

“Maamuzi gani?”

“Sijapenda Adrus kuwa katika mahusiano na Cookie. Cookie ninakupenda kwa kukuona tu, ila si kwa kuwa kimahusiano na Adrus mwanangu, najua ni swala linalo kuumiza, ila mimi kama mama sijapenda”

Meneno ya mama Adrus yakamfanya Jing kukunja ngumi mkononi mwake, huku akiwa amejawa na hasira sana, alihisi labda mam huyo atazungumza maneno ya bura kumbe ndio kwanza amezugumza kitu kibaya pasipo kujali upande mmoja. Cookie akazidi kuangua kilio kilicho zidi kumchanganya Jing.

“Adrus ana mpenzi wake, Adrus moyo wake upo kwa Naomi. Naomi ndio mwanamke ambaye ninampenda awe mama wa wajukuu wangu”

Kwa hasira Jing akamshika mama Adrus na kumnyanyua akamgandamiza ukutani huku akimtazama usoni mwake kwa hasira sana.

“Hivi wewe mama unaja maumivu ya mapenzi eheee?”

Jing alizungumza kwa hasira sana huku akiendelea kumkwida kisawa sawa.

“Hivi unajua huruma ya Cookie yule pale ndio iliyo mfanya hadi leo mwanao kuendelea kuwa hai, unalijua hilo eheee?”

Jing alizidi kuzungumza huku akimtingisha tingisha mama Adrus ambaye woga tayari umesha anza kumtawala mwilini mwake.

“Sasa ukweli ni kwamba, mimi na Cookie tulitumwa kumuua mwanao. Ila kwa ajili ya upendo wa Cookie tukagairi hilo jambo na tukasaidiana naye kufa na kupoka katika kila jamboa mbalo tunahitaji kulifanya. Ila wewe na mwanao sasa mumetugeuka. Ni hivi mpango wa kumuua mwanao utaendelea na wewe ndio utakaye anza”

Jing alizungumza kwa hasira na kuanza kulikaba koo la mama Adrus na kumfanya azidi kujawa na woga hadi haja ndogo ikaanza kumchuruzika kwenye mapaja yake taratibu.



Kwa haraka Cookie akashuka kitandani na kumfwata Jing na kumshika mkono, akimuomba asiendelee kumdhuru mama Adrus.

“Acha, Jing acha”

Cookie alizungumza huku akiendelea kulia na kuutoa mkono wa Jing unaendelea kumgandamiza mama Adrus. Jing akamuachia mama Adrus na kumfanya mama Adrus taratibu kukaa chini huku akilia kwa woga.

“Mama kwa nini lakini usiongee na Adrus, mimi ninampenda, ninempenda kutoka moyoni mwangu. Nina kasoro gani lakini mama yangu?”

Cookie alizungumza huku akikaa pembeni ya mama Adrus huku akiendelea kulia. Mama Adrus akashindwa kujmjibu kabisa Cookie na kuendelea kuzidisha kilio.

Jing akatoka chumbani humo kwa hasira sana na kukutana na Shamsa sebleni, wala hakumsemesha chochote zaidi ya kumpita kwa kasi. Shamsa akabaki akiwa amejawa na mshangao kiasi, akasikilizia vilio vya wanawake wawili vikitoka katika chumba alicho uwa amekabidhiwa Adrus. Akaingia ndani ya chumba hicho na kumkuta mama Adrus na Cookie wakiwa wamekaa chini.

“Jamani kuna nini kinacho endelea?”

Shamsa aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Mama Adrus akaanza kuyafuta machozi yake mara tu ya kumuoan Shamsa, taratibu mama Adrus akasimama na kuanza kutoka chumbani humo kitu kilicho zidi kumuweka Shamsa njia panda.

“Etii Cookie ni nini kinacho endelea?”

“Adrus”

“Adrus amefanyaje?”

Shamsa aliuliza huku mapigo ya moyo yakizidi kumuenda mbio huku hisia zake zikimpeleka moja kwa moja kwenye kifo.

“Adrus, jamani ohooo…..”

Cookie aliendelea kulia na kumfanya Shamsa kuchuchumaa pembeni yake akihitaji kufahamu ni kipi kilicho mpata Adrus

“Niambie Adrus amefanyaje?”

“Ameniacha”

“Amekuacha, kivipi?”

“Adrus amekutana na mpenzi wake wa zamani na ameamua kuniacha mimi moja kwa moja”

Kasi ya mapigo ya moyo ya Shamsa, taratibu ikaanza kupungua, kwa maana alicho kuwa anakifikiria na hichi anacho elezwa hapa ni vitu viwili tofauti.

“Yupo wapi huyo Adrus?”

“Sifahamu, alinishusha hapo getini, na amekwenda nisipo pajua”

“Usilie mwaya nitakusaidia kuzungumza naye sawa”

“Kweli Shamsa?”

“Yaa nitakusaidia wewe kuwa na amani katika hilo”

Taratibu Shamsa akamnyanyua Cookie na kumkalisha kitandani na kuendelea kumbembeleza.

***

K2 akafikishwa hadi kwenye fukwe za koko bichi na vijana wa Livna Livba. Akatembea kwa hatua chache hadi kwenye maegesho ya waendesha bajaji. Akamsalimia mmoja wao aliye mkuta ndani ya bajaji yake akisikiliza mziki.

“Nipeleke masaki”

“Poa sister thelathini”

Dereva bajaji alijibu huku akijiweka sawa.

“Wewe nipeleke”

Dereva taksi akawasha bajaji yake na kuiweka sawa na taratibu akaiingiza barabani huku kwa mara kadhaa akitumia kioo cha pembeni yake kumtazama abiria aliye mpakiza kwani baibui alilo livaa kitu kinacho onekana ni macho yake tu.

“Dada naona umeianza ramadhani kabla haijaanza”

Dereva takisi alizungumza kwa utani huku akitabasamu.

“Una maana gani?”

“Naona umejitundika baibui kubwa nini ehee?”

“Fanya kazi yako acha kuingilia yasiyo kuhusu, au munapenda kuwabeba hivyo vijisichana vinavyo tembea mapaja wazi si ndio?”

K2 alizungumza kwa ukali kidogo kwani dereva huyu amemvurugia mipango yake aliyo kuwa akiipanga kichwani taratibu.

“Samahani dada kama nitakuwa nimekuudhi au kuku kwaza”

“Poa”

“Ni Masaki gani?”

“Wewe twende mimi nitakua ninakuelekeza wapi kwa kwenda”

“Sawa”

***

Adrus akatoa simu yake na kuanza kuitafuta namba ya makamu wa raisi. Simu ya Eddy ikaanza kuita baada ya muda ikapokelewa.

“Muheshimiwa, Adrus hapa”

“Ndio Adrus”

“Naomi amepelekwa wapi?”

“Kwa sasa tunaelekea naye katika ofisi zangu”

“Sawa ninashukuru”

“Kama unakuja hakikisha kwamba huji na huyo mpenzi wako, alicho kifanya pale hospitalini sijakipenda”

“Sawa muheshimiwa nipo peke yangu”

“Poa”

Adrus akakata simu na kuendelea kundesha gari lake huku akiendele kuhakikisha kwamba anafika ofisi za makamu wa raisi haraka iwezekanavyo. Hakuchukua muda mwingi sana kaafanikiwa kufika katika ofisi ya makamu wa raisi, akasimamisha gari lake kwenye maegesho maalumu mara tu baada ya kuvuka katika geti la kuingilia katika ofisi hizo. Kitendo cha kushuka kwenye gari akaona gari za makamu wa raisi zikisimama katika maegesho maalumu. Adrus akatembea kwa haraka hadi karibu kabisa katika gari hizo, akashuka Eddy, Sa Yoo pamoja na Lee Ji.

“Muheshimiwa”

Adrus alizungumza huku akimpa Eddy mkono.

“Ndio”

“Yupo wapi ?”

Adrus aliuliza huku akionekana kuwa na shahuku kubwa sana ya kuhitaji kumuona Naomi.

“Amesha pelekwa katika chumba cha mahojiano”

“Naomba ruhusa yako ya kwenda kumuona”

“Nahitaji kumuona kabla yake”

Sa Yoo alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Eddy usoni ambaye hakuweza kuyajibu maombi hayo, akaanza kutembea na kuwafanya waanze kumfwata kwa nyuma. Moja kwa moja wakaelekea katika ofisi maalumu za mahojiano. Wakamkuta Naomi akiwa katika chumba hicho huku akiwa amefungwa pingu mikononi mwake.

“Subirini hapa”

Eddy alizungumza huku akiingia ndani ya chumba hicho. Akawaomba walinzi wawili ambao walipewa jukumu la kulinda ndani ya chumba hicho.

“Habari yako”

Eddy alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Naomi usoni mwake. Naomi hakujibu kitu cha iana yoyote zaidi ya kumtazama Eddy usoni mwake.

“Lee Ji”

Eddy aliita na Lee Ji akaingia ndani ya chumba hicho.

“Naiomba ile video”

Lee Ji akaifungua laptop yake na kuiweka juu ya meza, Eddy akamgeuzia Naomi video hiyo inayo muonesha jinsi anavyo mshambulia Sa Yoo.

“Kwa nini umelifanya hili tukio?”

“Nahitaji kuzungumza na balozi wangu kwanza kabla sitajibu hayo mambo mengine”

“Ahaa, ubalozi wako ndio ulikufanya uje Tanzania na kufanya matukio hayo si ndio”

“Nimesema kwamba sinto jibu chochote, wasiliana na ubalozi wangu wa Marekani”

“Okay”

Eddy taratibu akanyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekikalia, akatoka katika chumba hicho na kuwakuta Adrus na Sa Yoo wakiwa na shauku ya kuhitaji kuingia ndani ya chumba hicho.

“Adrus ingia”

“Ila Eddy nilitaka nianz…….”

“Sa Yoo”

Eddy alizungumza huku akimtazama Sa Yoo usoni mwake. Adrus akaingia ndani ya chumba hicho huku macho yake yakimtazama Naomi. Kwa haraka Naomi akasimama kwenye kiti chake na kumkimbilia Adrus, wakakumbatiana kwa sekunde kadhaa. Furaha na machozi yakawatawala wote wawili.

“Ulikuwa wapi Adrus wangu?”

Naomi alizungumza kwa sauti ya upole huku machozi yakiendelea kumiminika.

“Usijali mpenzi wangu upo hapa, nipo kwa ajili yako”

Taratiu wakaachiana, Adrus akamkalisha Naomi katika kiti chake, kisha akaka katika kiti kilichopo upande wa pili na wakatenganishwa na meza kati yao.

“Umekuja kunihoji?”

Naomi alizungumza huku akijifuta machozi usoni mwake. Adrus akaka kimya kwa muda huku akiendelea kumtazama Naomi, ishara za macho anazo zifanya Adrus, zikamfanya Naomi kuanza kuzielewa.

“Usijali kila jambo ni la kuzungumzika.”

“Sawa”

Adrus akasimama na kutoka katika chumba hichi na kuwakuta Sa Yoo, Lee Ji na Eddy wakimsubiria.

“Muheshimiwa ninaomba kuzungumza nawe”

“Ninahitaji kwenda kumuhoji mimi”

Sa Yoo aliendelea kushikilai msisitizo wake, Eddy kwa ishara ya mkono akamruhusu Sa Yoo kuingia katika chumba hicho. Eddy na Adrus akasogea mbali kidogo na chumba hicho.

“Kwa nini ulihitaji kuniu?”

Sa Yoo aliuliza kwa ukali sana huku akimtazama Naomi usoni mwake.

“Hata hapa nikihitaji kukuua ninaweza kukuua”

Naomi alizungumza kwa ujasiri na kumfanya Sa Yoo azidi kukasirika. Kwa haraka Sa Yoo akamshika Naomi shingo yake na kuanza kumkaba. Kitendo hicho Naomi hakuweza kukubaliana nacho, akatandika Sa Yoo kisukusuku cha tumbo na kumfanya ajikunje huku akiugulia maumivu makali sana.

“Muheshimiwa, ninakuomba unisaidie katika hili, naomba umueachie huru Naomi, naamini kwamba unatambu ni jinsi gani ninavyo mpenda sana tena sana”

“Hilo ninalitambua, ila ninahitaji niweze kupata sababu ya kwa nini aliamua kumuua Sa Yoo, tukiifahamu sababu hiyo basi nipo tayari kumuachia huru hii yote itakuwa ni kwa ajili yako”

“Nashukuru sana muheshimiwa”

Eddy na Adrud wakashangaa kuona walinzi wakiingia katika chumba hicho. Kwa haraka wakakimbilia katika chumba hicho na kumkuta Sa Yoo akiwa amelala chini huku damu za mdomoni zikimtoka.

“Naomi unafanya nini sasa?”

Adrus aliuliza kwa ukali huku akimtazama Naomi usoni mwake. Sa Yoo akasaidiwa kunyanyuliwa na walinzi wengine.

“Mpatieni huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo”

Eddy alizungumza kwa msisitizo unao endana na hasira ndani yake.

“Siwezi kujilegeza kwa mtu ambaye anahitaji kuniaua mimi”

Naomi alizungumza huku walinzi wakiendelea kumshikilia.

“Hata kama ila kwa nini unafanya haya mambo ni kwa sababu gani?”

“Nilituma kuja kuwaangamiza hawa wasichana kwa sababu waliwaangamiza makachero wane wa kimarekani”

Maneno ya Naomi yakamfanya Eddy kumsogelea karibu sana. Akamtazama kwa macho yaliyo jaa hasira kubwa sana.

“Nilipanga kukusamehe ila kwa hili sinto kusamehe. Na kitu muhimu kwenye maisha yangu ni familia yangu, endapo utadhubutu muda mwengine kunyanyua mkono wako kwa ajili ya hii familia yangu, nitakuuaa umenielewa”

“Jiangalie ukidhubutu na wewe kuniua mimi, basi siku zako zitakuwa zinahesabika ni lazima utauwawa”

Eddy akatabasamu kwa dharau kidogo, kisha akamtandika Naomi, kofi la shavu lake hadi Adrus akafumba macho yake akiyasikilizia maumivi ya moyo wake kwa jinsi mpenzi wake alivyo sulubiwa kwa kofi hilo.

“Chunga kinywa chako binti umenielewa?”

Naomi akamtemea Eddy mate usoni mwake.

“Raisi, firauni uniye fuga waalifu na kuita ni familia yako. Sheta…..”

Eddy hakumpa Naomi nafasi ya kuimalizia sentensi yake hiyo, akampiga naye ngumi ya tumbo iliyo mfanya Adrus kutetemeka mwili mzima kwa hasira kali. Taratibu akaanza kukunja ngumi, hukua kitamani kufanya jambo ili mradi kumukoa mpenzi wake ambaye tayari amesha bananishwa na makamu wa raisi. Miguno ya maumivu ya Naomi, ikazidi kumchanganya Adrus. Eddy akamshika Naomi koo lake na kumnyanyua huku akimtazama usoni mwake.

“Raisi wako ndio amekutuma uje kufanya ujinga huu. Eheeee?”

Eddy alizungumza kwa ukali huku akiendelea kulikaba koo la Naomo ambaye hawezi kuuzuia mkono huo kutoana na kushikiliwa na walinzi wa kiume wenye uwezo mkubwa kuliko yeye. Adrus machozi ya hasira yakaanza kumtoka, akafikiria kiasi cha pesa ambacho anakimiliki na akajiaminisha kwamba ana uwezo wa kufanya chochote katika maisha haya kinacho hitaji pesa. Kwa haraka akaichomoa bastola aliyo ichomeka kiunoni mwake na kumnyooshea Eddy kichwani. Jambo hilo likamshangaza snaa Eddy na kuwafanya walinzi wa Eddy nao kumnyooshea Adrus banduki zao.



“Muheshimiwa samahani sana”

Adrus alizungumza huku mikono ikimtetemeka. Eddy akatabasamu huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Umekusidia kufanya hivi si ndio?”

“Muheshimiwa huyo ni mwanamke ninaye mpenda, namuhitaji na ninamthamini, nakuomba umuache mpenzi wangu niondoke naye nakuomba umuachie huru”

Eddy akamtazama Adrus kwa muda, kisha kwa ishara akawaomba walinzi wake washushe silaha chini.

“Muachieni”

Edddy aliwaamuru walinzi walio mshikilia Naomi kumuachia. Kwa haraka Naomi akamkimbilia Adrus na kumkumbatia kwa nguvu huku akilia. Taratibu Adrus akaishusha bastola yake chini na kuendelea kumkumbatia.

“Siku nyingine usija ukarudia ujinga kama huu ambao umeufanya. Umenielewa?”

Eddy alizungumza huku akimtazama Adrus usoni mwake.

“Sawa, sahani pia kwa hilo muheshimiwa”

Eddy akatoka katika chumba hicho cha mahojiano pamoja na walinzi wake na kuwaacha Adrus na Naomi wakiendelea kukumbatiana. Adrus akamshika mkono Naomi, akabeba na begi la Naomi na kutoka katika eneo hilo na kumfanya Lee Ji kubaki na mshangao tu.

Adrus akaondoka pasipo hata kumuaga mtu yoyo, akatoka nje na wakaingia kwenye gari na kuondoka katoka ofisi hizo za makamu wa wairi kwa mwendo wa kasi sana.

“Eddy mbona umemuachia mualifu?”

Lee Ji aliuliza kwa shauku sana mara baada ya kuingia katika ofisi ya Eddy.

“Sioni sababu ya kuingia katika bifu na Adrus, ikiwa nimtu ambye aliifanya kazi yangu kikamilifu”

“Ila yule binti amempiga kale kabinti kadogo?”

“Nalitambua hilo kikubwa ni kuweza kusamehe yaliyo tokea”

“Ila yule binti ataendeleza uovu wake wa kuhitaji kuwaua wale wasichana?”

“Hapana hawezi kufanya hivyo”

“Kweli?”

“Ndio, naamini Adrus anaweza kulishuhulikia hilo jambo na likaenda vizuri”

“Sawa”

***

Adrus na Naomi wakafika katika hoteli ya Nemax Rayal Kinondoni. Wakakodisha chumba na moja kw amoja wakaelekea gorofani kilipo chumba chao. Kitendo cha kuingia ndani, kwa haraka Adrus akamvuta Naomi karibu yake na wakanza kunyonyana midomo yao huku kila mmoja akiipitisha mikono yake katika mwili wa mwenzake. Wakaanza kuvuana nguo zao walizo zivaa, ndani ya sekunde kadhaa wote wakawa wapo kama walivyo zaliwa.

“Nimekumiss mume wangu”

“Hata mimi Naomi”

Adrus baada ya kumjibu hivyo wakaendelea kunyonyana midomo yao. Taratibu wakaanza kupeana utamu huku kila mmoja akihakikisha kwamba ana mpa mwenzake kitu roho inataka. Kila mmoja akazidi kumuonyesha mwenzake ujuzi hususai Adrua ambaye hapo awali alipo kuwa mekutana na Naomi alikuwa ni mwanamfunzi katika nyanja nzima ya mahusiano hususani mahusiano ya kitandani. Mzunguko wa kwanza ukaisha huku kila mmoja akiwa anamwagikwa na jasho mwilini mwake.

“Huu huku kwenu Tanzania kweli kuna joto sana”

“Yaani wee acha tu mpenzi wangu, ila unajisikiaje mwilini mwako. Una maumivu eneo lolote?”

“Hapana, nashukuru Mungu ile ajali ilivyo tokeana kwa bahati nzuri zikiweza kuumia”

“Ila ni kwa nini ulihitaji kumua yule Sa Yoo?”

“Nilipewa majukumu ya kikazi ya kuwaangamiza na raisi wangu, ila kutokana kwa sasa nipo na wewe sinto hitaji kuendelea kuifanya kazi hiyo. Kwani lengo langu kubwa lilikuwa ni kuja Tanzania na kukutafuta wewe”

“Usijali mpenzi wangu, ila nahitaji ndani ya wiki hii hii nikuoe”

“Kweli mpenzi wangu?”

“Yaa nahitaji kukuoa, sihitaji kukupoteza tena”

“Nashukuru sana mpenzi wangu, yaani mimi nipo tayari hata kabla hujaniuliza kama nipo tayari kwa jambo hilo”

“Hahaaa kweli”

“Ndio mpenzo wangu”

“Ila inabidi nimshirikishe makamuw a raisi”

“Kwa nini, ikiwa anaonekana kuto kunipenda?”

“Anakupenda, ila kwa kosa la kumpiga binti yake nina amini kwamba hili ndio limekasirisha na kusababisha akafanya kama vile alivyo kufanyia”

“Mmmmmmm”

“Yaa niamini mpenzi wangu, huoni kwa nini amekuachia huru”

“Sawa kwa ajili yako inabidi niweze kuamini”

“Nashukuru kusukia hivyo”

***

“Nisubiri hapa”

K2 alizungumza huku akishuka kwenye bajaji, akaingia katika jumba kubwa lililo zungushiwa ukuta mkubwa na kuna ulinzi wa kutosha. Akapitiliza moja kwa moja hadi sebleni na kumkuta kaka yake akiwa na mmoja wa washauri wake.

“Nipatie elfu hamsini hapo”

K2 alizungumza huku akivua baibui hilo na kumfanya kaka yake kushaa sana, kwani kuingia kwake ndani ya nyumba hiyo hakuwa na taarifa yoyote .

“Umeigiaje?”

“Naomba bwana pesa hayo mengine tutazungumza”

Bwana John akatoa waleti yake na kuchomoa noti tano na kumkabidhi K2, akatoka ndani humo huku akivaa tena kitambaaa chake cha baibui ili kuificha sura yake, akamkabidhi muendesha bajaji kiasi hicho cha pesa japo sio kiasi ambacho walikuwa wamekubaliana. K2 akarudi ndani huku akilifunga geti na kuingia seblenI huku akivua nguo zake zote.

“Inabidi uite mafundi waweze kulirekebisha geti lako, wewe unahisi linafanya kazi ila ni bovu”

“Duu ndio maana nilikuuliza umeingiaje ingiaje?”

“Nitakuonyesha tukitoka nje, ehee niambieni ni nini kinacho endelea?”

“Kwanza pole, sijui ulikimbilia wapi?”

“Yaani wee acha tu, ila kikubwa ni kwamba nipo salama”

“Ni kweli, hapa nimemuita Rama ili anishauri katika mpango wa kuingia katika siasa, sasa hapa nilikuwa ninahitaji kujua ni chama gani ambacho ninaweza kuingia na kugombania”

“Maswala ya kufikria kuingia kwenye siasa kwa wakati huu hembu achana nayo kwanza”

“Kwa nini?”

“Mpango wa kumuangamiza raisi huyu wa sasa upo pale pale, na nina wazo jengine, najua endapo tutamua katika kipindi hichi basi atakaye tawala nchi kwa miaka hii michache iliyo baki basi atakuwepo makamu wa raisi, na kwa kupitia makamu wa raisi nahitaji kutengeneza nafasi ambayo itakufanya kuingia kwa amani na kishindo bila ya kipingamizi cha aina yoyote”

K2 alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama kaka yake pamoja na Rama.

“Kwa hiyo mpango ni kumua raisi aliyopo madarani?”

“Ndio”

“Kikosi chako si umekitoa sadaka wewe, unahisi kwa hilo unalo lizungumza kweli litawezekana?”

“Niamini mimi kaka kila jambo litawezakana na nitahakikisha kwamba kila kitu kinakwenda kuwa poa”

“Rama una la kuzungumza?”

“Ninalo muheshimiwa, ila hilo jambo ambalo analizungumza K2 hapa kwa upande mmoja ni zuri, ila kwa upande mwengine sio zuri, kwa maana anaye kwenda kuuwawa ni kiongozi wa nchi. Nimeweza kumfwatilia Rahab kwa kipindi kirefu sana toka mume wake raisi Praygod alivyo kuwa akiongoza.”

Rama akameza mate kidogo kisha akaendelea kuzungumza.

“Kwanza Rahab yeye ndio alikuwa mlinzi wa karibu kabisa wa mume wake”

“Mlinzi kivipi?”

K2 aliuliza huku akiwa na shahuku kubwa ya kuhitaji kuweza kufahamu.

“Kuna kitabu cha siri sana, kiliweza kundika na muandishi mmoja hivi ambaye alikuwa anayafwatilia san akwa ukaribu maisha ya Rahab na kundi lake. Kitabu hicho kinaitwa She is My wife, hakijatolewa hadharani hadi hivi ninavyo weza kukizungumza, ila muandishi huyo aliweza kunihadithia mambo muhimu muhimu juu ya huyu raisi ili muwe kufahamu kwamba una shuhulika na mtu wa aina gani na musiwe tu muna kurupuka”

“Kwa jinsi alivyo niadisia muandishi yule alikuwa akidai kwamba Rahab slikuwa ni jambazi wa hatari”

“Jambazi?”

K2 aliuliza huku macho yamemtoka

“Ndio alikuwa ni jambazi hatari, kiasi kwamba hata serika za kipindi hicho zilishndwa kumzuir katika kazi yake hiyo na ana kikosi chake ambacho hufanya kazi nyuma yake”

“Duuu ila hata kama alikuwa ni jambazi ni lazima tutamuangamiza?”

“Hilo linawezeakana ila ukumbuke kwamba yeye ndio ndio aliye ongoza harakati za kumtoa dikteta Godwin madarakani munakumbuka?”

John kaka yake K2 akatingisha kichwa akishiaria kwamba anakumbuka juu ya hilo jambo.

“Kama aliingia madarakani kwa mtutu, basi ni lazima na sisi tumtoe kwa mtutu”

“Mmmmm, sawa ila kuna siri moja kubwa ambayo muandishi huyo anaifahamu, na hakuhitaji kuniambia kwamba ni siri gani ambayo anayo Rahab, sasa endapo tunatifahamu hiyo siri ni lazima tutakuwa tumefanikiwa sana katika kumuangamiza”

“Ni siri gani hiyo?”

K2 aliuliza huku akimtazama Rama usoni mwake.

“Mimi na wewe sote sisi ni wageni, kikubwa tumtafute huyo muandishi aweze kutupatia hiyo siri, la sivyo mipango yetu yote tunayo ipanga hapa ni sawa na bure.”



“Sasa huyo muandishi yupo wapi?

K2 aliuliza huku akiwa amejawa na shauku kubwa sana.

“Kuna sehemu nitawapeleka na mutaweza kuonana naye”

“Lini?”

“Leo usiku”

“Sawa fanya hivyo”

***

Livna akaitazama simu iliyopo mezani kwake ndani ya ofisi yake. Taratibu akaunyanyua mkongo wa simu hiyo, akaingiza namba za mtu ambaye hajazungumza naye siku nyingi sana. Simu ikaanza kuita, baada ya muda ikapokelewa.

“Haloo”

Ilisikiaka sauti ya kiume iliyo jaa mikwaruzo mingi sana na dhairi sauti ya inaonyesha kwamba ni mzee wa miaka mingi sana.

“Ni mimi”

“Rahab?”

“Ndio dokta, nahitaji kuonana na wewe”

“Kuna usalama?”

“Ndio usalama upo, ila ninahisi nahiji kuona na wewe”

“Mimi nipo kule kule unapo pafahamu”

“Basi usiku huu wa leo nitakuja huko huko kuonana na wewe”

“Sawa karibu”

Raisi Rahab akairudisha simu hiyo sehemu alipo itoa huku mawazo mengi yakimtawala kichwani mwake, kwani hajui ni kwa nini siku ya leo anamuwaza sana dokta Wiliam, daktaria ambaye aliweza kumtoa kwenye maisha ya kimasikini na kumuingiza katika maisha ya utafutaji pesa kwa juhudi japo pesa hiyo walikuwa wakiitafuta kwa kuiba kwenye baadhi ya mabenki na kwa njia hiyo ndio ilimfanya hadi kukutana na raisi Praygod aliye kuwa mume wake. Mawazo ya Rahab yakamfanya kuitoa simu yake mkononi na kuitafuta namba ya makamu wake wa raisi na kumpigia. Simu ya Eddy ikaita kwa muda kisha akaipokea.

“Ndio Rahab”

“Nakuomba uje ikulu”

“Muda huu?”

“Ndio”

“Kuna nini kilicho tokea?”

“Eddy nakuomba tu njoo ikulu, nina jambo la muhimu sana nahitaji kukuambia?”

“La kikazi au binafsi?”

“Ni binafsi ila ninahitaji sana kukuona muda huu”

“Sawa, ila yule binti nimemuachia?”

“Binti gani huyo?”

Eddy akanyamaza kidogo huku akiisikilizia sauti ya Rahab jinsi anavyo zungumza kwa upole na unyonge sana ambao tangu wafahamiane hajawahi kumsikia akizugumza hivyo kwa sauti inayo onyesha dhairi kwamba amekata tamaa.

“Rahab upo poa lakini?”

Eddy aliuliza kwa upolea sana.

“Nakuomba uje ikulu”

“Sawa najiandaa sasa hivi ninakuja”

***

“Niatamuagiza dereva akupeleke nyumbani, mimi nahitaji kuelekea ikulu sasa hivi”

Eddy alizungumza huku akimtazama Lee Ji usoni mwake mara tu ya kukata simu yake hiyo.

“Nahitaji kwenda kumuangalia Sa Yoo”

“Oooho sawa, basi taratibu zote nitamuachia sekretari wangu”

“Sawa”

Eddy akampigia simu sekretari wake na kumyomba aingie ndani ya ofisi yake, baada ya muda sekretari akaingia.

“Ndio mkuu”

“Mchukue Lee Ji, mpeleke sehemu alipo Sa Yoo, na wakimaliza matibabu hakikisha wanakwenda nyumbani salama”

“Sawa muheshimiwa”

Eddy akatoka ofisini kwake, na kuongozana na walinzi wake hadi kwenye maegesho ya magari. Wakaingia na kumuelekeza dereva wake mkuu na kumueleza kwamba wanaelekea Ikulu. Safari ikaanzahuku Eddy kwa mara kadhaa akijiuliza ni kitu gani ambacho kinamsumbua raisi Rahab.

Wakafikia ikulu, akashuka kwenye gari na moja kwa moja wakaelekea katika ofisi ya raisi Rahab na kumkuta akiwa amejikalia kwenye moja ya sofa akionyesha dhairi kwamba amechoka sana. Kwa haraka Rahab akasimama na kumkumbatia Eddy.

“Vipi?”

“Sio safi Eddy”

“Kuna tatizo gani tena mpenzi wangu?”

“Eddy kuna siri kubwa nahitaji uweze kuifahamu”

“Siri, siri gani hiyo?”

Taratibu Rahab akamuachia Eddy huku machozi yakimlenga lenga.

“Niambie tafadhali”

“Eddy, nahitaji unisindikize sehemu moja hivi ya siri. Nahitaji twende sisi wawili tu”

“Sisi wawili, pasipo walinzi wetu?”

“Ndio pasipo walinzi wetu”

“Ndio ni sehemu ya siri sana. Eddy naona kuna hali mbaya inakuja mbele yangu. Ninahisia na kitu hicho”

“Hali gani?”

“Sijui tu ila nahisi kwamba kuna jambo baya linakuja”

Eddy akaka kimya huku akimtazama Rahab usoni mwake. Taratibu akamvuta na kumkumbatia kwa nguvu.

“Hakuna jambo baya linalo weza kujitokeza, mpenzi wangu”

“Sawa”

Rahab aliendelea kujibu kinyonge sana. Wakaanza kupanga mikakati ya jinsi gani wanvyo wea kwenda katika eneo hilo pasipo walinzi wao kuweza kufahamu kitu cha aina yoyote.

”Eddy kuna mlinzi yoyote unaye weza kumuamini?”

“Ninaye muamini kwa sasa ni Adrus peke”

“Naomba umshirikishe katika hili”

“Una uhakika?”

“Ndio mshirikishe, nahitaji yeye ndio aweze kututoa hapa ikulu kisiri pasipo walinzi wengine waweze kufahamu”

“Sawa”

Eddy akatoa simu na kumpigia Adrus. Simu ya Adrus ikaita hadi ikakatika, akajaribu kupiga kwa mara ya pili ikapokelewa.

“Ndio muheshimiwa”

“Kuna kazi nahitaji unisaidie”

“Kazi gani muheshimiwa”

“Nahitaji uje kunitoa hapa ikulu majira ya saa tatu usiku pasipo walinzi wowote kuweza kufahamu”

“Kukutoa kisiri kivipi?”

“Ukija hapa ikulu muda huo nitakueleza”

“Sawa muheshimiwa”

“Hakikisha kwamba umuelezi mtu yoyote juu ya hilo swala”

“Sawa muheshimiwa”

***

“Inabidi wewe ubaki hapa hotelini, kuna kazi ninakwenda kumsaidia makamu wa raisi”

“Kazi gani teja jamani mpenzi wangu?”

Naomi alilalamika huku akiwa amejilaza kifuani mwa Adrus.

“Naamini kwamba ni kazi muhimu”

“Ila huyo makamu wako wa raisi mimi wala simuamini, sijui kwa nini wewe una mauamini sana?”

“Wewe ni wewe na mimi ni mimi, katika maswala ya kumuamini mtu siangalia kama wewe humuamini au laa. Alfu kuna jambo moja japo tulilizungumzia juu juu, ila sinto hitaji kuja kuliona linajitokeza. Kama ulikuja kwa kazi ya kuwaangamiza Sa Yoo na Shamsa, hembu sahau hilo swala. Acha amani itawale katika familia za watu, usihitaji kuwapa watu machungu sasa hivi na mwishoni mambo yaje kuwa mabaya sijui umenielewa?”

“Nimekuelewa”

“Poa”

 ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG