Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

WAKALA WA SIRI - 3

  

Simulizi : Wakala Wa Siri 

Sehemu Ya Tatu (3)


mweusi aliyevalia Tisheti Nyeusi na Suruali ya jinsi. Fernanda alikaa vizuri uso wake ukiwa na

taharuki;

“ Wewe ni nani, unaingia nyumbani kwangu bila ya hodi? Umepitaje pale getini na umewezaje

kufungua mlango huu wakati nilikuwa nimeufunga?” Fernanda alisema macho yake yakiwa

yanacheza cheza kwa hofu.

“ Naitwa Stanslaus Mahige, naingia popote, hakuna mlango ambao utafungwa nisiufungue.

Hata hivyo sijaja hapa kueleza habari hizo. Kilichonileta ni jambo moja tuu. Tafadhali nambie,

Sajenti Warioba Yupo wapi?” Yule mtu alijitambulisha, kisha kwa sauti ya ubabe akausogelea

uso wa Fernanda akamtisha.

“ Tokea lini Sajenti Warioba anaishi hapa? Au kuna mtu kakuambia Sajenti yupo hapa?

Mmeenda kwake hamjamkuta?” Fernanda alisema.

“ Sikiliza wewe Mwanamke, sijaja hapa kujibishana na wewe, nambie Sajenti yupo wapi?”

Stanslaus Mahige alisema uso wake akiwa ameukunja tofauti na awali. Alivyoukunja mikunjo

yenye dalili zote za hila na ukatili zilizokuwa zimejificha zilionekana. Hakuwa mtu wa mchezo.

Fernanda aliweza kuona macho ya mtu Yule jinsi yalivyoficha udhalimu na ufedhuli alioufanya

kipindi cha nyuma. Hata hivyo hilo halikumfanya Fernanda aogope kutokana na ujasiri wake.

“ Sijui Sajenti yupo wapi? Mwenyewe namtafuta, nani kakutuma umtafute Sajenti, na

unamtafuta kwa nini?” Fernanda alimtupia swali.

“ Hakuna asiyejua kuwa Sajenti ni adui wa nchi, yeye ndiye aliyeiba chipu ya Darubini ya

maabara, yeye ndiye kaiba Cadava, yeye ndiye kaiba sampo za uchunguzi, tena akamtorosha

Mateka wa ushahidi, sasa kaamua kutoroka. Huyajui mambo haya au upo pamoja naye kwenye

uovu wake? Embu niambie Sajenti yupo wapi hiyo ndio salama yako, usiponiambia utajiingiza

kwenye matatizo makubwa” Stanslaus Aliongea huku akichuchumaa kuufuata uso wa Fernanda

“ Sikiliza, usinitishe…..! Mimi sio mtu wa kutishwa tishwa. Au unaniona kwa vile ni mwanamke?

Nimeshakuambia kuwa sifahamu Sajenti alipo. Haya ondoka nyumbani kwangu kabla sijapiga

kelele za mwizi” Fernanda aliongea uso wake ukitazamana na uso wa Stanslaus.

“ Hahahha! Ikiwa wewe uliyemwanamke hutishwi, mimi ndio nitatishwa na kelele zako za

mwizi? Haya sema Sajenti Yupo wapi?” Stanslaus alicheka kwa dharau kisha akakamata nywele

za Fernanda kwa nguvu akiwa ameichomoa bastola yake upesi akamnyooshea Fernanda.


Maumivu makali ya kuvutwa nywele yalimfanya Fernanda akunje sura yake kama mtu aliyekula

ndimu ya handeni.

“Piga hizo kelele za mwizi, mimi si mwizi, piga hizo kelele sasa. Unadhani nimekuja hapa

kukubembeleza, nambie Sajenti alipo, sitaki kukudhuru lakini wewe ndio unataka tufikie huku”

Stanslaus alisema.

Ghafla Fernanda kwa upesi usiozidi sekunde moja alijinasua na kumpiga teke la makende,

Stanslaus akamuachia na kuiangusha bastola yake, akatoa ukelele wa maumivu akiwa kashika sehemu zake za siri. Lilikuwa ni pigo la kiufundi ambalo kamwe Stanslaus asingelitarajia

kutokana na kuwa Fernanda alikuwa kakaa na kubinua kichwa chake upande kwa maumivu ya

kuvutwa nywele.

Fernanda kwa upesi alimuongeza teke jingine la uso, Stanslaus akaangukia kwenye meza ya kioo

iliyokuwa pale sebuleni ikapasuka. Tayari Fernanda alikuwa ameokota ile bastola ya Stanslaus

aliyokuwa ameiangusha. Stanslaus alikuwa pale chini akijivuta huku maumivu yakimsengenya.

Alifanya kosa kubwa sana kumdharau Fernanda, kama angekuwa anamjua Fernanda Vizuri wala

asingethubutu kumkalia karibu huku akimsemesha maneno kama mtoto mdogo.

Stanslaus aliamka, Fernanda akawa anamuamrisha aweke mikono kichwani lakini Stanslaus

alimpuuzia akasimama. Kisha akapiga makofi ya dhihaka kumpongeza Fernanda kwa kuonyesha

uwezo ule. Fernanda alimtishia kumpiga risasi lakini Stanslaus akawa anacheka.

“ Piga…! Piga kama wewe ni jasiri. Hahahah! Naitwa Stanslaus Mahige, mtu mbaya nisiye na

huruma. Muuaji wa watu ishirini na tisa. Sitaki wewe uwe mtu wa thelasini. Lakini ikiwa

hautanambia alipo Sajenti Warioba, basi leo hii nitatimiza idadi ya watu thelasini niliyowaua

kwa mkono wangu huu” Stanslaus aliongea huku akimuonyeshea Fernanda mkono wake.


Fernanda kwa hasira akidhamiria kuonyesha ujasiri wake, akaikoki bastola ili ampige risasi ya

kichwa lakini bastola haikuwa na risasi. Hapo akajua amechezewa akili kama mtoto mdogo.

Wakati huo Stanslaus alikuwa akitazama uso wake akiwa katengeneza tabasamu la dharau.

“ Nilijua wewe ni mjinga, ndio maana sikutaka kuweka risasi kwenye hiyo bastola, na hata

nitakapokuua nitakuua kwa mkono wangu huu, sitatumia bastola wala kisu. Niliapa sitamua

mwanamke kwa silaha. Haya unataka kupigana nami ndipo unambie alipo Sajenti au unanambia

kwa amani?” Stanslaus alisema.

Fernanda alibaki ameduwa, akili yake ilimzunguka, asingeweza kujiongopea kuwa amezidiwa

ujanja. Hakutaka kuyaamini na kuyaogopa maneno ya Stanslaus muuaji lakini pia hakutaka

kuyapuuzia. Macho yake yalianza kumkagua Stanslaus, alimuona ni jitu lenye mikono yenye

mishipa mingi iliyojazia, uso wa stanslaus ulikuwa mweusi juu akiwa amenyoa kipara, urefu

wake ulikuwa futi sita, mwenye umbo lililojengeka kimazoezi hali iliyofanya Tisheti aliyoivaa

kumbana. Macho yake yalikuwa mekundu ambayo Fernanda aliyaona kama macho ya mtu

anayefurahia kumwaga damu. Kufikia hapo Fernanda hakutaka kuamini kama ataweza kupigana

na jitu lile akalishinda lakini pia angemuambia nini ikiwa yeye mwenye hakujua mahali alipo

Sajenti.


“ Nimepigana na watu wengi, nimeua watu wengi, weupe kwa weusi, warefu kwa wafupi. Wenye

hatia na wasio na hatia. Nimefunzwa kupiga na kuua. Hiyo ndio kazi yangu niliyokuwa naipenda tangu nikiwa mtoto mdogo licha ya kuwa napenda muziki na kucheza, lakini kuua watu kama

wewe ndiyo furaha yangu. Aliyekutuma amefanya makosa makubwa kutokukwambia mimi ni

nani. Sikumbuki nikikuua wewe utakuwa mtu wa ngapi. Lakini kama wewe sio mpumbavu na

hautaki kufa ni bora uondoke, maana sitaki kuua mtu ambaye anataka kuishi” Fernanda alisema,

sauti yake ilitoka kwa kufoka, alimtazama Stanslaus na wote macho yao yakawa yanaongea,

tayari mioyo yao ilishaanza kupigana, kilichobaki ni miili yao kukutana.

Kwa upesi Fernanda alimrushia ile bastola, Stanslaus akaikwepa lakini kabla hajajiweka sawa

Fernanda alikuwa ameshamfikia akampiga ngumu mchongoko shingoni, kisha akamchanganyia

ngumi na kumparua usoni upesiupesi, ndani ya sekunde ishirini alishampiga ngumi za uso

zisizopungua kumi na tano kisha akampiga kichwa kimoja kichojaa kwenye uso wa Stanslaus.

Hapo Stanslaus akapiga ukelele akiwa anapepesuka akitaka kuanguka lakini alijizuia. Kasi ya

upiganaji wa Fernanda ilimchanganya sana Stanslaus, lakini Fernanda bado alipaswa achunge

sana, kwani Stanslaus ni kweli alikuwa mtu hatari mwenye uzoefu wa kuua watu na anayependa

kuvuta roho za watu kwa mikono yake bila kutumia silaha.

Fernanda alivuta pumzi kisha akaiachia, ni kama alijipa nguvu mpya, Stanslaus bado

alikuwa anamawenge. Fernanda alirusha teke lakini hila yake iligundulika, likakwepwa na hapo

kwa upesi Fernanda akageuka nalo kumpiga stanslaus lakini napo halikumpata, alilikwepa tena.

Kisha Stanslaus akamsukuma kwa nguvu Fernanda akaangukia kwenye sofa, kwa upesi

Stanslaus alimrushia teka pale kwenye sofa, holaa! Fernanda akasogea upesi pembeni likapiga

sofa. Kisha Fernanda akamkamata lile teke lililopiga kwenye sofa na kulinyanyua juu kisha

akampiga mtama ule mguu mwingine, Stanslaus akaanguka chini kama gunia la mahindi.


Fernanda akamrukia, looh! Alifanya kosa kubwa, Stanslaus alimdaka kama mpira kisha

akampiga kichwa wote wakiwa palepale sakafuni, Fernanda aliona kiza kilichopambwa na nyota

bila ya mwezi, kilikuwa kichwa kizito kilichofanya pua ya Fernanda kuvuja damu.

Stanslaus akamsukuma Fernanda kwa pembeni kisha akaamka, muda huo Fernanda alikuwa hoi,

hakumbuki ni lini aliwahi kupigwa na kitu kizito kichwani, alihisi uso unadondoka. Akiwa pale

chini Stanslaus akamfuata kisha akamnyanyua, kwa upesi Fernanda kwa kutumia vidole vyake

vyenye kucha akaviingiza kwenye macho ya Stanslaus, safi sana, lilikuwa ni pigo makini

lililomfanya Stanslaus apige yowe huku akishika macho yake na kumuachia Fernanda. Huo

ulikuwa ni muda wa Fernanda kumdhibiti Stanslaus na kumchosha. Fernanda alichukua chupa ya

wine iliyokuwa chini pembeni ya Sofa aliyokuwa anakunywa akampiga nayo kichwani,

Stanslaus akachanika na damu zikavuja kutoka kichwani. Kwa upesi sana bila kupoteza muda,

alichukua sindano yenye dawa maalumu, kisha akamchoma Stanslaus kwenye shingo, hapo hapo

Stanslaus akapoteza fahamu.


Fernanda alipumua kwa kasi, akiwa anageuka huku na huku kama mtu aliyechanganyikiwa.

Alimburuza kisha akamuingiza kwenye kichumba kidogo ambacho kilikuwa kama stoo lakini

hakikuwa na kitu chochote wala hakikuwa na dirisha. Alimfunga kamba za miguu na mikononi,

kisha akaenda kuchukua gundi akagundisha kwenye mdomo wake. Hapo akamfungia mlango

akaondoka kwenda kufanya usafi sebuleni.

Baada ya masaa matatu, Stanslaus alizinduka. Alijikuta yupo kwenye kichumba kidogo kisicho

na dirisha chenye giza. Alikumbuka mara ya mwisho alikuwa akipigana na Fernanda, sasa

akajiuliza yupo wapi, na nani aliyemleta. Kabla hajafika mbali katika kujiuliza, mlango

ukafunguliwa na Fernanda akatokea.


siri.jpg



WAKALA WA SIRI 07

Mtunzi; Robert Ng'apos Heriel

0693322300


ILIPOISHIA

Baada ya masaa matatu, Stanslaus alizinduka. Alijikuta yupo kwenye kichumba kidogo kisicho

na dirisha chenye giza. Alikumbuka mara ya mwisho alikuwa akipigana na Fernanda, sasa

akajiuliza yupo wapi, na nani aliyemleta. Kabla hajafika mbali katika kujiuliza, mlango

ukafunguliwa na Fernanda akatokea.


INAENDELEA

“ Habari yako, Stanslaus Mahige, muuaji mahiri. Unajionaje?” Fernanda alimsalimia Stanslaus huku akitabasamu kwa dharau.

“ Nimekaa na wewe zaidi ya masaa matatu ukiwa huna fahamu, kama ningeamua kukuua ningekuwa nimeshakuua, sasa hivi ungekuwa ni maiti, tena maiti iliyokosa maziko. Lakini nimekuacha hai kwa sababu ya jambo moja tuu. Hilo ndilo litakuwa dhamana yako. Usiponambia nakuhakikishia utakufa kwa uchungu mwingi sana” Fernanda alisema, kisha akamburuta Stanslaus mpaka kwenye chumba kingine kikubwa kilichokuwa na madirisha mawili. Alafu akambandua ile gundi aliyompachika mdomoni ili asiongee. Kisha akatoka akamuacha pale chumbani, kitambo kidogo alirejea akiwa na chupa ya wine na glass mbili. Akaiweka ile chupa kwenye stuli iliyokuwa pale chumbani, akamimina ile wine kwenye zile glass mbili. Kisha akaenda kumnyanyua Stanslaus na kumuegemeza kwenye ukuta.

“ Karibu Rafiki yangu, kunywa tufurahi, sisi ni marafiki kwa sasa, tusahau vita vyetu, fungua mdomo basi rafiki” Fernanda aliongea akiwa anajaribu kumnywesha Stanslaus wine. usisahau Stanslaus alikuwa amefungwa mikono na miguu.

“ Nambie nani amekutuma, unajua lolote kwenye jambo hili? Nambie rafiki muuaji usiye na huruma, nambie kisha nitakuruhusu uifyonze roho yangu itoke kwenye mwili wangu. Hautafurahi? Si ulisema wewe ni muuaji mahiri, sasa nataka unambie ukweli kisha uniue. Je hapo sitatenda haki kwako?” Fernanda aliongea akiwa anazunguka zunguka ndani ya kile chumba huku akiwa ameshika glass iliyojaa Wine.

“ Unataka nikuambie nini, mimi namtafuta Sajenti, adui wa nchi, huyo ndiye namtafuta, na sipaswi kurudi bila kuwa naye. Mimi ni muuaji mahiri, lakini leo nimenaswa na mshale laini wa mabua” Stanslaus alisema, macho yake yalikuwa yamejeruhika kwa kucha alizoshambuliwa na Fernanda wakati ule wakiwa wanapigana.

“ Mshale wa mabua! Haloo! Unamaneno sana rafiki muuaji. Haya tusipoteze muda, nambie unachojua kuhusu jambo hili” Fernanda alicheka kishambenga kisha kwa ghafla akabadilika uso wake ukawa wa mwanamke katili.


“ Kila usemalo wanalisikia, unajiingiza kwenye matatizo makubwa, ingefaa ungenambia alipo Sajenti huenda hiyo ndio ingekuwa ponapona yako” Stanslaus aliongea, maneno hayo Fernanda aliyaelewa. Akajua huenda Stanslaus amefungwa vifaa vya kurekodi sauti na wasiwasi uliongezeka pale alipohisi kuwa huenda hata muda ule kulikuwa na watu wanaomfuatilia na hawapo mbali.

“ Kelele nguruwe wewe! Utasema au husemi, eehe! Unadhani mimi natishwa na maneno yako ya kipuuzi, sasa utasema kwa mateso, wewe si hautaki kusema” Fernanda alisema huku akimshika Stanslaus sehemu nyeti. Stanslaus alipiga yowe kwa maumivu makali aliyoyasikia.

“ Nasema! Tafadhali niachie nitasema sasa, uuwhi!” Stanslaus alisema akijaribu kujitingisha mikono yake iliyofungwa na kubana mapaja ili kumzuia Fernanda asibinye nyeti zake. Maumivu ya kubinywa nyeti hayalinganishwi na maumivu yoyote yale, kubinywa nyeti ni adhabu kubwa na inayokaribia adhabu ya mwisho kwa mwanaume. Ilikuwa ni afadhali Fernanda amchinje lakini sio kumbinya makende yake.

“ Sema sasa, usifikiri nipo hapa kukuchekesha. Nambie nani kakutuma?” Fernanda alisema, akiwa kamuachia Stanslaus Nyeti zake.

“ Watu wabaya, wenye nia ovu na wasiolitakia mema taifa letu. Hao ndio wamenituma” Stanslaus alisema jasho likiwa linamtoka.

“Watu gani hao, sitaki maelezo mengi, wataje..” Fernanda alisema.

Ajabu ni kuwa kabla hajasema chochote Stanslaus alianza kulegea mwisho akapoteza maisha, Fernanda alishangazwa na hali hiyo, awali hakutaka kuamini kuwa Stanslaus amekufa, alidhani anamfanyia maigizo lakini ni kweli kabisa Stanslaus alikuwa ameaga dunia. Kilichomshangaza zaidi ni kuwa, stanslaus alianza kubadilika uso wake, macho yake yalibadilika na kuwa meusi tii. Hapo Fernanda akajua kuwa kilichomua Stanslaus kilikuwa ni sumu. Fernanda alienda kuchukua Gloves za mikononi akazivaa, kisha akarudi, ndipo akamkagua Stanslaus ili apate kujua kilichomuua ni kitu gani japo alishahisi ni sumu lakini alitaka kuhakikisha, akamgeuza kwa nyuma, looh! Alishtuka kuona chini ya kichwa karibu na shingo kwa nyuma ilikuwepo chipu ya kurekodia sauti. Akaigusa na mkono wake, alishangaa kuona kwa pembeni damu ilikuwa ikivuja kidogo kama kaupele kaliko tumbuka, aliposhika kale kaupele aligundua ndani kuna pini, hapo hapo Fernanda akaelewa ni kwa nini Stanslaus amekufa. Kilichomuua ilikuwa ni ile pini, ambayo iliwekwa makusudi nyuma ya kichwa karibu ya kisogo pamoja na ile chipu ya kurekodia. Pini ile huwekwa sumu maalumu ambayo endapo jasusi au mpelelezi akikamatwa na adui basi hujigongesha kwa nyuma kisha pini humchoma, na mara moja mtu hupoteza maisha. Basi Fernanda alihuzunika sana kwa kitendo cha Stanslaus kujiua kabla hajamwambia siri ya nani aliyemtuma na nani yupo nyuma ya uovu wote ule. Kwa upesi akamtoa stanslaus ndani ya nyumba na kumuingiza kwenye gari, nyuma ya buti. Kisha alirudi ndani, akasafisha nyumba kusudi kuondoa ushahidi wa aina yoyote ile. Ile meza ya kioo iliyopasuka kutokana na wao kupigana aliokota vipande vya vioo na kwenda kuvitupa kwenye shimo la taka lililokuwa nyuma ya mabanda ya kuku ya nyumba hiyo.

Jioni ilifika, Fernanda alitoka akiwa na gari alilobeba maiti ya Stanslaus. Alikuwa anaenda kuitupa katika mapori ya Bagamoyo. Aliendesha gari kwa uangalifu mpaka alipouacha mji wa Dar es salaam na sasa alikuwa ameingia katika mapori makubwa ya Bagamoyo. Njiani alipishana na magari machache na hii ndio sababu ya kuchagua mapori ya Bagamoyo ambayo magari yanayotumia njia hiyo kwa mida ya jioni yalikuwa ni machache ukilinganisha na Morogoro Road. Hivyo ingekuwa vigumu kushtukiwa.


Aliona barabara ya vumbi ikikata kulia akaamua kuifuata, akaangalia huku na huku kuona kama kuna gari inamfuata lakini hali ilikuwa shwari. Akaendesha umbali wa kilometa mbili kutoka Bagamoyo Road, hapo akaona sehemu nzuri ambayo ingemfaa kutupa ile maiti ya Stanslaus. Alisimamisha gari, kisha akaangalia huku na huku kwa Mbele hakuona mtu, alafu akachungulia kwa nyuma Kupitia vioo vya pembeni ya gari, pia hakuona mtu. Akashuka akiwa kavaa suruali nyeusi, raba nyeusi zenye soli nyeupe, juu akiwa kavalia blauzi ya rangi ya damu ya mzee na uso wake ukiwa nyuma ya miwani ya rangi ya hudhurungi.

Upepo mwanana ulimpuliza, tayari jua lilikuwa limezama, mwanga wa jua uliokuwepo ni ule wa buriani. Fernanda alisimama kama mlingoti kisha akatulia tuli kusikiliza kama kuna uwepo wa mtu eneo lile, hali ilikuwa shwari, eneo lilikuwa kimya ndege wakiimba nyimbo za kuiaga siku ile. Alienda kwenye buti la gari akafungua, kisha akaitoa ile maiti kwa kuivuta, ikatoka ikaanguka chini. Fernanda hakuweza kuibeba, hivyo aliiburuza kwa kuivuta mpaka nje kidogo ya barabara, kisha akaiburuza tena umbali wa mita thelasini, muda wote alikuwa kavaa Gloves mikononi. Alijua kuwa ile maiti muda mchache ujao itaonekana na uchunguzi utaanza. Baadaye alirejea ndani ya gari, akachukua kikopo kidogo kwenye mkoba wake. Akatoka nacho na kwenda kule kwenye ile maiti ya Stanslaus. Alipofika akaimwagia ile maiti kemikali iliyokuwa ndani ya kile kikopo. Kazi ya kemikali ile ni kupoteza fingerprint zilizogusa mwili wa marehemu, hivyo Fernanda hakutaka alama zake za vidole zibaki kwenye maiti ya Stanslaus ili kupoteza ushahidi kuwa yeye anahusika kwenye kifo cha Stanslaus.

Hatimaye alimaliza, na safari ya kurudi nyumbani kwake ikaanza. Akiwa njiani Fernanda alijaribu kumpigia simu Sajenti Warioba lakini namba ikawa haipatikani. Huzuni ilimkumba, simanzi ikamkumbatia. Alikumbuka mambo yote mema aliyokwisha kufanya akiwa na Sajenti. Hakuona mwanaume afananaye na Sajenti. Alimpenda Sajenti kuliko kitu chochote kile, alitamani muda wote awe naye, lakini leo alikuwa pekeyake bila kujua ni wapi Sajenti alipo. Punde si punde alikumbuka jambo muhimu lililomfanya asimamishe gari kwa ghafla. Wakati huo alikuwa keshakaribia Bunju, alipata wazo, akageuza gari kurudi Bagamoyo. Muda huu aliendesha kwa kasi kidogo akiwa kawasha taa za gari kutokana na giza lilikuwa limeingia. Ndani ya lisaa limoja na dakika chache alikuwa kaingia Bagamoyo, ilikuwa mida ya saa mbili na nusu. Bado maduka yalikuwa hayajafungwa, alienda kwenye vibanda vya kutolea pesa. Hapo akataka kutoa pesa kutoka kwenye simu yake. Alishangaa kuona kila akitaka kutoa pesa inakataa, alipewa ujumbe kuwa akaunti yake ilikuwa imefungwa hivyo afike ofisini kwa ajili ya kushughulikia jambo hilo. Akili ya Fernanda ikakosa utulivu, tayari alijiingiza kwenye mkondo wa balaa. Alijua kuwa akaunti zake zimefungwa makusudi ili asiweze kutoa pesa zitakazo msaidia kutoroka.


Lakini hiyo isingeweza mzuia hata kidogo, Fernanda alikuwa jasusi mbobezi wa kimataifa, tayari ameshafanya kazi nchi nyingi hivyo anauzoefu wa matata na hekaheka za namna ile. Alisonya, kisha akatoa zile laini na kuzivunja vunja, alitoa simu nyingine ambayo aliisajili kwa majina NADIA BANDA. Alijua ni muhimu kuwa na laini za simu tofauti tofauti na majina yasiyofanana ili ikitokea siku ya matatizo aweze kujinasua. Alijua ni rahisi kudhibitiwa ikiwa utakuwa na laini za simu zenye jina moja tuu, lakini ukiwa na laini zenye majina tofauti sio rahisi kudhibitiwa. Hivyo kwenye laini ya kawaida aliweka pesa lakini hakuweka pesa nyingi tofauti na laini aliyojisajilia kwa majina mengine asiyotambulika nayo.

Alitoa milioni moja na nusu kisha akaziweka kwenye mkoba, huyo akatoka na kuingia ndani ya gari lake. Akiwa njiani kutafuta Lodge ya kupumzika alitupa zile simu zilizokuwa na laini zenye majina ya Fernanda kwa kuhofia kuwa wapo watu wanamfuatilia, Moja kwa moja alichukua chumba kwenye moja ya Lodge nzuri zilizokuwa pale Bagamoyo. Aliandikisha jina Nadia Banda kisha akapewa chumba.


Aliingia kuoga alafu akatoka akakaa kitandani akazikausha nywele zake ndefu za kibrazil. Baadaye akapumzika. Akili yake ilimrejesha asubuhi alipovamiwa na jitu jeusi, ndilo Stanslaus. Kisha akakumbuka habari za Sajenti Warioba, alikumbuka penzi zito alilopewa na Sajenti mwezi mmoja uliopita. Alitamani raha zile. Alijikuta akitabasamu, alafu akasema; Nakupenda sana Otieno.

Usingizi ulimpitia akalala.




SURA YA 3


KIJIJI CHA MAKANYA, SAME KILIMANJARO.


Sajenti alikimbilia kwenda kujificha katika kijiji cha Nkwini kilichopo kata ya Makanya, wilaya ya Same iliyoko Mkoa wa Kilimanjaro. Huko alienda kwa Babu yake mzaa Mama. Babu yake alikaa nje kidogo ya kijiji cha Nkwini, alikuwa kazeeka sana. Mwenye umri wa makadirio ya miaka themanini hivi.

Mzee Mkwizu alishtuka kusikia mlango ukibishwa yapata saa tisa za usiku. Alipofungua mlango alishangaa kumuona mtu aliyevalia kofia iliyoficha uso wake, Mzee Mkwizu alifunga mlango kwa upesi kwa hofu. Hakutambua kuwa mtu Yule alikuwa ni Sajenti Warioba. Ni mpaka Sajenti alipojitambulisha kuwa yeye ni nani ndipo alipofunguliwa na Mzee Mkwizu.

“Karibu sana Mjukuu wangu, Kulikoni, mbona unakuja usiku mnene kama huu? Usalama upo?” Mzee Mkwizu aliongea huku akimkaribisha Sajenti ndani.

“ Nitakusimulia kila kitu Babu, kwa sasa naomba nipumzike, nimechoka sana” Sajenti Warioba alisema, kisha akatazamana kwa kitambo na Mzee Mkwizu bila kusema chochote, alafu akampita Mzee Mkwizu akaelekea chumbani. Mzee Mkwizu aligeuka kumtazama Mjukuu wake, alishangaa kumuona Sajenti akichechemea, akili yake ilishtuka, moja kwa moja akatambua kuwa kuna tatizo kubwa linalomkabili mjukuu wake. Sajenti aliingia katika chumba kisichokuwa na mlango isipokuwa pazia, akatoma ndani akimuacha Mzee Mkwizu akimshangaa.

Sajenti alijibwaga kitandani, kilikuwa kitanda kidogo cha futi tatu kwa sita. Alivua nguo alizokuwa amezivaa akabakiwa na kaptura juu akiwa kifua wazi. Kisha akajinyoosha kitandani, hapo akakumbuka mambo yaliyomtokea mchana.

Alikumbuka jinsi alivyomtoroka Fernanda pale kwenye Hotel ya nyota tatu iliyopo Ubungo. Akatoka, moja kwa moja akiwa kashika simu yake akiwa karibu na Kituo cha mabasi ya Mkoani Ubungo. Mfukoni alikuwa na shilingi laki mbili, hiyo isingemtosha hivyo akatoa laki tano, ikamfanya akawa na jumla ya shilingi laki saba za Kitanzania. Alichukua boda boda akamwambia ampeleke Stendi ya daladala ya Mbezi mwisho, hakutaka kupandia Mabasi pale Ubungo kwa kuogopa kufuatiliwa. Hiyo ilikuwa yapata saa kumi na moja za jioni.


Akiwa kwenye bodaboda mara kwa mara alichungulia kwenye vioo vya pikipiki, jambo hilo alilifanya kila mara hali iliyomfanya dereva wa bodaboda kumshtukia. Dereva wa Bodaboda alitamani kumuuliza swali kuwa mbona anachungulia mara kwa mara kwenye vioo lakini akili yake ilimuonya, aliona lingekuwa swali la kichokozi ambalo halina msingi wowote. Sajenti alibaini hofu ya dereva macho yao yalipokutana kwenye kioo cha pikipiki. Dereva aliondoa macho yake haraka, na kuuliza swali la kukaribisha mazungumzo.

“ Bwana Mkubwa, Nikushushie Mbezi mwisho ndani kabisa ya Stendi ya Daladala au nje?”

“ Nishushie mbele kidogo ya kituo cha daladala cha mbezi mwisho” Sajenti alijibu macho yake yakichungulia kwenye kioo kutazama magari yaliyokuwa yanakuja kwa nyuma.

“Huku ndio nyumbani , boss? Au umekuja tuu mara moja?” Dereva wa bodaboda aliuliza.

“ Hapana, nimekuja tuu mara moja, kuna mtu nataka kuonana naye ” Sajenti aliongea.

Tayari walikuwa wamefika Mbezi mwisho mbele kidogo ya Stendi ya daladala. Sajenti akatoa elfu ishirini kisha akampa Yule Dereva Bodaboda na kumuambia achukue tuu yote bila kurudisha chenchi ingawaje walipatana nauli ni shilingi elfu kumi na mbili. Dereva bodaboda alifurahi sana, uso wake ulishindwa kuzuia furaha ya kupata ofa ile.

“Shukrani Boss, sijui naweza kurudi kukuchukua au nikusubiri hapa hapa mbezi ili nikurudishe Ubungo?” Dereva Bodaboda alisema huku tabasamu shawishi la kibiashara likiuzingira uso wake.

“ Usijali, nitakaa huku mpaka kesho, Ahsante kwa huduma yako, jioni njema rafiki” Sajenti alimuaga Dereva bodaboda, akaondoka huku akichechemea. Alitembea hatua kumi kisha akageuka nyuma kumtazama Yule bodaboda, hakumuona tayari alikuwa keshaondoka. Hakutaka mtu yeyote ajue ni wapi anaelekea, kama angeweza hata yeye hakutaka ajue ni wapi anaelekea, alihisi hiyo ndio salama yake.

Alitembea akichechemea akaingia ndani ya stendi ya Daladala, hakuna aliyekuwa akimtilia maanani licha ya kuchechemea kwake. Tayari ilishahitimu saa kumi na mbili jioni kigiza cha usoni kikiwa kinafukuza mwanga wa mchana. Sajenti alisoma mienendo ya watu wa pale Stendi, hakuona ishara yoyote ya hatari. Hapo akaingia chapuchapu kwenye Daladala zinazoelekea Mlandizi. Kutokana na Kuwa tayari Daladala ilikuwa imejaa gari haikumaliza dakika tano ikatia moto na kuondoka.


Sajenti alikuwa amekaa siti ya nyuma kabisa, huku watu wengine wakiwa wamesimama kutokana na gari kujaa. Hapo alitulia akisoma mienendo ya abiria mmoja baada ya mwingine, aligundua abiria wengi walikuwa ni watu wa tabaka la chini, wasakatonge ambao wanajishughulisha na shughuli za ujasiriamali na baishara ndogo ndogo. Wengi wa abiria walikuwa ni wakazi wa Kibaha na mlandizi ambao kila siku hujihimu asubuhi na mapema kwenda Dar es salaam kufanya biashara, kisha jioni hurejea makwao. Hivyo ndivyo maisha yao yalivyo, hata hivyo jambo jema ni kuwa kutokana na ubora wa miundombinu ya barabara ndio unaochochea maendeleo na ustawi wa shughuli zao. Jambo kuu ambalo lilikuwa linalalamikiwa ni suala la foleni za magari katika barabara ya Mlandizi, hata hivyo tayari serikali imeshaanza kuipanua barabara hiyo iwe ya njia nne.

Sajenti alikumbuka jambo, hapo akageuka nyuma akachungulia Kupitia dirisha la nyuma la gari. Alipagawa, akili yake ilipoteza utulivu. Alimuona Yule dereva bodaboda akiwa nyuma ya gari alilokuwa amepanda. Awali hakuamini macho yake lakini baadaye alijihakikishia ndio Yuleyule bodaboda aliyekuwa amembeba akamleta mbezi mwisho. Hapo tayari walishakuwa wamepita mji wa kibaha giza likiwa limeshafunika nchi.

Sajenti sasa alihisi ipo hatari kama ataendelea kukaa ndani ya ile daladala, alimhofia Yule dereva kuwa huenda anamfuatilia. Hilo peke yake lisingemuogopesha lakini vipi kama dereva Yule katoa taarifa kwa watu wanaomtafuta Sajenti, hiyo ndio ilikuwa hofu yake. Sajenti alijua fika watu wanaomtafuta ni watu wakubwa wenye nyadhifa kubwa serikalini. Hivyo kitendo cha yeye kujulikana alipo kingehatarisha maisha yake.


Akachungulia tena nyuma ya gari kwenye kioo cha nyuma hapo alimuona Yule Dereva bodaboda akiongea na simu aliyoichomeka kwenye helmet aliyoivaa kichwani, hisia zake moja kwa moja zikamtuma kuwa dereva Yule anawasiliana na watu wanaomtafuta.

Akili ya Sajenti ikamuambia ashuke, hapo hapo akamuagiza konda wa ile daladala asimamishe gari ili ashuke. Konda akagomba akisema pale hakuna kituo wala mji wowote isipokuwa mapori, lakini Sajenti aliomba afanyiwe msaada tuu. Basi gari ikapunguza mwendo, kisha ikasimama na Sajenti akashuka. Hapo Sajenti aliiona ile Bodaboda ikipunguza mwendo ikiwa umbali wa mita hamsini.

Daladala ikamuacha Sajenti, na ile bodaboda ikapita na kwenda kusimama umbali wa hatua mia moja kama urefu wa kiwanja cha mpira.

Sajenti alitamani mguu wake wa kushoto ungekuwa mzima amkimbize Yule Dereva wa Bodaboda lakini hakuweza, mguu wake ulikuwa na jeraha kubwa la risasi aliyoipata kule katika hospitali ya Boreti. Alichechemea, kisha akapotelea kwenye mapori akimzuga Yule dereva bodaboda, punde akiwa kajificha kwenye kichaka alisikia kwa mbali sauti ya pikipiki ikiwashwa, hapo akajua Yule dereva anakuja kule alipo. Kitambo kidogo dereva wa bodaboda alikuwa amesimama pale alipokuwa ameshukia Sajenti, alishuka na kuanza kumulika mulika huku na huko, Sajenti yeye alikuwa kajibanza kwenye kichaka chenye majani mazito yaliyomfanya asionekane.

Punde alimsikia Yule dereva akiongea na simu;

“Fanyeni haraka kabla hajapotea, ameshuka muda huu, anaonekana anajeraha mguuni, kaingia kwenye mapori, mimi siwezi kumfuata mwenyewe….” Dereva Bodaboda aliongea lakini kabla hajamaliza Sajenti alijitokeza akiwa kamshikia bastola yule dereva akakata simu na kuweka mikono juu, muda huo pikipiki ilikuwa ikinguruma huku ikiwamulika.


Sajenti akamfuata, kisha akampiga kitako cha bastola Yule dereva akaanguka chini, Sajenti akaichukua simu ya dereva kisha akaikariri namba aliyokuwa anaongea nayo Yule dereva, akaingia kwenye uwanja wa meseji hakuona la maana. Akamsogelea Yule dereva pale chini aliyekuwa anagugumia kwa maumivu ya kupigwa na kitako cha bastola, akamuwekea mdomo wa bastola mdomoni,

“nambie ulikuwa unaongea na nani?” Sajenti alimuulzia Dereva.

“Tafadhali naomba usiniue, mimi sio mtu mbaya. Tafadhali nakuomba boss…”

“Kama wewe sio mtu mbaya nambie umetumwa na nani, nahesabu mpaka tatu, usiposema napasaua kichwa chako” Sajenti alisema akiufikicha mdomo wa bastola kwenye mdomo wa Yule dereva.

“ moja..! Mbili…..! Taaatu…! PAAH!” Sajenti aliongea kisha akaachia bastola iliyolenga kwenye paja la bodaboda. Hapo dereva akapiga makelele lakini Sajenti akamkemea anyamaze.

Ghafla bin vuu kwa mbali Sajenti aliona gari ikija kwa kasi ikitokea upande wa Dar es salaam, hakutaka kujiuliza maswali , alikimbilia pikipiki ya Yule dereva akapanda juu yake na kuanza kuiendesha kwa uelekeo wa Chalinze. Alichanganya gia mwendo ukawa mwendo, kasi ikawa kasi, alipishana na upepo huku akilichana giza na mwanga wa pikipiki. Ilikuwa pikipiki aina yo Boxer, moja ya pikipiki nzuri zenye mwendo mzuri usio na shaka ziwapo kwenye barabara ya lami.

Wale watu nao hawakuwa nyuma walimfungia mkia wakimfukuza kwa kasi kama mshale. Tayari walikuwa wamemkaribia kama hatua ishirini na tano tuu. Ilikuwa ni Difenda iliyokuwa ikimjia kama jini pori.


Wakaanza kumrushia risasi zilizokuwa zikimpunyua punyua, naye hakuwa nyuma kuhakikisha anazikwepa kwa kuhamisha pikipiki upande huu na upande huu, Sajenti alikoswa koswa na magari aliyokuwa anapishana nayo hata hivyo bado alichanja mbuga, akiyapita magari yaliyokuwa mbele yake, jambo ambalo Difenda iliyokuwa ikimfukuzia ikichelewa kufanya hivyo kutokana na kuhofia kusababisha ajali ya kugongana uso kwa uso na magari yaliyokuwa yanayokuja mbele yao. Hii kwa Sajenti ilikuwa nafasi nzuri ya kuwaacha wale maadui walioisaka roho yake kwa hamu bila ya nidhamu.

Punde aliingia mji wa Mlandizi, bahati mbaya pikipiki ikaisha mafuta.....




Wakaanza kumrushia risasi zilizokuwa zikimpunyua punyua, naye hakuwa nyuma kuhakikisha anazikwepa kwa kuhamisha pikipiki upande huu na upande huu, Sajenti alikoswa koswa na magari aliyokuwa anapishana nayo hata hivyo bado alichanja mbuga, akiyapita magari yaliyokuwa mbele yake, jambo ambalo Difenda iliyokuwa ikimfukuzia ikichelewa kufanya hivyo kutokana na kuhofia kusababisha ajali ya kugongana uso kwa uso na magari yaliyokuwa yanayokuja mbele yao. Hii kwa Sajenti ilikuwa nafasi nzuri ya kuwaacha wale maadui walioisaka roho yake kwa hamu bila ya nidhamu.

Punde aliingia mji wa Mlandizi, bahati mbaya pikipiki ikaisha mafuta.....


INAENDELEA


, akaingia vichochoro vya mlandizi akiwatoroka wale watu wabaya, aliitupa pikipiki kisha akakimbia akichechemea, tayari alikuwa ameshawapoteza. Alisimama mbele ya moja ya Bar za pale Mlandizi, akiwa pale Bar aliwaona mwanaume mmoja na mwanamke wakiwa wanaingia ndani ya gari aina ya Suzuki, akawafuata kabla hawajafunga mlango akawavamia. Kisha akawaweka chini ya Ulinzi, Yule mwanaume akamvalisha pingu na Yule mwanamke akampiga kidogo kwenye kisogo akapoteza fahamu.

“ Samahani Brother, sikujua kama Leah ni Mke wa mtu, Nisamehe. Nipo tayari kukupa kitu chochote lakini tafadhali naomba usinidhuru” Yule mwanaume alisema huku akilia. Hapo Sajenti akajua kuwa kumbe Yule mwanaume na Yule mwanamke hawakuwa mke na mume bali walikuwa wanafanya uzinzi.

” Sitaki kusikia kelele zako, umenichukulia mke wangu, bado unipigie kelele? Bado unataka nikusamehe” Sajenti aliongea hukua akichanganya na kupangua gia akiitafuta Chalinze. Hapo utulivu ukatokea, huku Sajenti akitafakari mambo mengi ambayo yalimfanya awe na huzuni. Malipo ya kulitumikia taifa ndio yale. Mambo yote mema aliyoyafanya leo ndio anakimbizwa na kuwindwa kama digidigi. Amegeuka mkimbizi wa nchi yake mwenyewe.

“Nawezaje kuiibia nchi yangu, nawezaje kuwa adui wa nchi, ati nimeiba chipu ya darubini ya hospitali ya Boreti, chipu ambayo imebeba siri nyingi za nchi, nimeiba Cadava na sampo mbili za uchunguzi, wakaona hiyo haitoshi sasa wanasema nimemtorosha mateka wa Ushahidi. Sitokubali, siwezi nasema”

Sajenti alisema maneno hayo akiwa kitandani baada ya kumbukumbu hizo kukatika, usingizi ulimpitia, hatimaye akalala.

*******************************


Asubuhi ilifika, siku mpya ilimkuta Sajenti akiwa katika nyumba ya Babu yake, Mzee Mkwizu. Akiwa kitandani alisikia mbuzi, kondoo na ng’ombe wakilia kwa nje. Sajenti alivaa nguo kisha akatoka nje, alimkuta Mzee mkwizu akimkamua ng’ombe maziwa. Sajenti aliwaona ng’ombe wengine wakiwa zizini, walikuwa ng’ombe wazuri walionona. Pia aliona zizi la pili, hili lilikuwa na kondoo na mbuzi, zizi la tatu lilikuwa na ndama na vitoto vya mbuzi na kondoo ambavyo vilikuwa vikililia mama zao huku vingine vikicheza cheza.

Mzee Mkwizu alikuwa mfugaji mkubwa katika kijiji cha Nkwini ndio maana aliamua kujitenga nje kidogo ya mji. Mbali na kondoo, mbuzi na Ng’ombe pia Mzee Mkwizu alikuwa anafuga kuku wa kienyeji. Vyote hivyo vilimpatia Mzee mkwizu kipato cha kuendesha maisha yake.

Kupitia ufugaji Mzee Mkwizu aliweza kujenga nyumba nzuri ya matofali ingawaje bado haikuwa na umeme wala baadhi ya vyumba ilikuwa haina milango, lakini aliweza kuweka sakafu nzuri ya vigae, bati na madirisha ya chuma. Nyumba yake ilizungushiwa na uzio wa milingoti inayotokana na zao la mkonge..

Sajenti alitaka naye ajaribu kukamua maziwa lakini alishindwa.

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG