Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

GENGE - 4

    *

Simulizi : Genge 

Sehemu Ya Nne (4)



JIJI LA DAR ES SALAAM lilikuwa katika hali ya utulivu. Wingu zito lilitanda na kuleta giza hafifu. Kama kawaida, wakazi wa jiji hilo walianza kujiandaa kwa kuipokea mvua kubwa waliyoitabiri.

Adha ya mvua katika jiji hili huwa ni mbaya hata kupelekea vifo na mafuriko katika maeneo Fulani. Hii yote ni kutokana na miundombinu mibovu isiyoendana na mahitaji ya jiji hilo.

Upande wa pili wa jiji hilo, yaani Kigamboni, Madam S alilitoa gari lake katika pantone na kuanza safari ya kuelekea Gezaulole. Mwendo wake wa wastani ulimcukua takribani dakika arobaini na tano kufika eneo hilo. Akayaaca makazi ya watu na kuanza kupita mashambani mpaka kijiji kidogo ambacho kwacho ndipo waliweka makazi yao ya siri, ‘Shamba’. Alipofika tu getini hakusimama maana geti hilo lilifunguka lenyewe. Magari yote waliyokuwa wakiyatumia kiofisi, yalifunwa kifaa maalumu ambacho kiliwasiliana na sensa ya geti umbali wa mita ishirini na kufanya lifunguke atomatiki.

Ndani ya jumba hilo alikosekana Jasmini pekee, kwa kuwa alikuwa katika kazi maalum.

Madam S akaingia na kupokea heshima zote kutoka kwa vijana wake. Alistahili kwa kuwa alikuwa Spymaster makini katika taifa. Head Of TSA ‘HOT’. Aliyeaminika kubeba ulinzi wa siri wa Rais na urais wake.

Ndani ya jumba hilo hilo, katika vyumba viwili tofauti; kimoja alilazwa Mariamu na kingine Andrew Makita. Wote wawili walilazwa katika vitanda vya Chuma tupu bila hata godoro. Vitanda hivyo vilikuwa na uwezo wa kubadili hali tatu kwa nyakati tofauti. Ama viwe vya baridi sana au moto wa kubandua ngozi au shoti kali za umeme. Mikono na miguu vilifungwa katika mwisho huu na ule. Mwilini kila mmoja alibaki na nguo ya ndani tu. Ngozi ilikutana na chuma moja kwa moja.

Andrew alikuwa wa kwanza kuamka kutokana na ubaridi mkali katika vyuma hivyo vy akitanda. Akavuta mkono huu, umefungwa, akatikisa mwingine , vivyo hivyo. Na miguu nayo alkadhalika. Akagwaya. Akapepesa macho na kugeuza shingo huku na huko, akapambana na maumivu makali. Akakumbuka alivyopigwa na Brian kwa kitu hasichokijua. Chumba kilikuwa na ukubwa wa wastani. Zaidi ya kitanda hicho kulikuwa na mashine nyingine ndogo pembeni. Andrew aliijua vyema mashine ile. Ukuta wa kile chumba, ulitisha. Alama za damu za watu waliouawa kwa risasi zilitapakaa kila kona, hewa nzito iligubika. Hakukuwa na dirisha isipokuwa tundu dogo la kupita kalamu juu kabisa ya paa lake.

“Shiiit!” Andrew alilalamika. Hakuwahi kufika sehemu kama hii tanu azaliwe. Aliogopa. Moyo wake ukaanza kupunguza kasi ya mapigo yake.

Brian amenileta huku? Mshenzi huyu wanataka kuniua! Akawaza. Akajitahidi kupiga kelele, lakini sauti yote alijisikia mwenyewe tu. Mlango mzito wa chuma ulikuwa upande wa kichwa chake, hivyo asingeweza kuona nani anaingia ndani ya chumb hicho.

Katika chumba kingine, Mariamu alishtuka ghafla baada ya kujikuta akipigwa shoti ya umeme. Akapiga ukelele wa nguvu lakini haukusaidia chochote kutokana na kile chumba kilivyojengwa. Mariamu alianza kutetemeka kwa hofu, maumivu makali ya majeraha ya kile kipigo kutoka kwa Brian yalianza upya mara baada ya kurudiwa na fahamu.

“Niko wapi! Niko wapi miye…?” akaanza kuongea mwenyewe. Kila akiutazama ule ukuta alizidi kuchanganyikiwa. Damu mbichi ilikuwa sakafuni, na ile iliyoganda ilikuwa chini sakafuni. Katika moja ya kona ya chumba hicho aliona mkono wa mtu na upanga uliolowa damu chini yake. Akaanza kutweta huku macho yakiwa yamemtoka pima. Hofu ile ikamfanya apoteza fahamu kwa mara nyingine.

* * *




Niko wapi! Niko wapi miye…?” akaanza kuongea mwenyewe. Kila akiutazama ule ukuta alizidi kuchanganyikiwa. Damu mbichi ilikuwa sakafuni, na ile iliyoganda ilikuwa chini sakafuni. Katika moja ya kona ya chumba hicho aliona mkono wa mtu na upanga uliolowa damu chini yake. Akaanza kutweta huku macho yakiwa yamemtoka pima. Hofu ile ikamfanya apoteza fahamu kwa mara nyingine.

* * *

Katika chumba maalumu kilichofungwa mitambo mbalimbali ya mawasiliano, Gina alikuwa ameketi huku vidole vyake vikigongagonga meza ambayo juu yake kulikuwa na kompyuta kubwa na ukuta wa mbele yake ulikuwa na luninga iliyokuwa ikionesha chumba kile alichofungwa Mariamu. Ni hapa alipokaa kwenye hii meza palikuwa na kitu kama kichakata cha kompyuta amacho kilibeba batani kumi. Alipoona mwanamke yule bado yupo kwenye mzimio alibonyeza tu batani moja na shoti kali ya umeme ilimchapa, akaamka.

“Safi sana msichana mzuri!” Gina akatamka kwa sauti ya chini, akaanza kuiongoza kamera iliyofungwa kwa siri ndani ya chumba hicho kumwangalia vizuri mwanamke huyo. Gina alitazama mahangaiko yote ya mwanamke huyo na kuanza kucheka kwa hofu waliyomtengenezea.

Katika ofisi hiyo hiyo, meza kubwa ya upande wa pili, Chiba naye alikuwa mbele ya lunina nyingine akamtazama Andrew Makita katika mahangaiko yake ile ndani. Kwa kutumia kamera yake ya siri, iliyofungwa ndani ya chumba hicho, Chiba aliweza kumchunguza kijana huyo atakavyo. Dakika hiyo hiyo, Kamanda Amata na Madam S wakaingia katika ofisi hiyo.

“Haya vijana. Nataka kujua uhusiano wa Mariamu na Andrew,” Madam S akawaambia.

Chiba akamtazama Gina na kumpa ishara. Gina akaminya tenaile swichi na kumpiga shoti ya umeme Mariamu. Akashtuka na kupiga kelele, akajivuta kama anataka kukaa lakini vile vifungo vilimrudisha chini.

“Mariamu!” akasikia sauti ya kike yenye mwangwi ikimwita. Akageuka huku na huko, hakumwona mtu.

“Be-e-e!” akaitika kwa shida.

“Hicho kitanda ulicholalia, kina uwezo wa kukupiga shoti ya umeme, kina uwezo wa kukubanika kwa moto kama kuku na kina uwezo wa kukugandisha barafu… sasa chagua kati ya hivyo vitatu unataka nikufanye kipi sasa hivi?” Gina akamuuliza.

“Ha-ha-pana, usini-fa-nye cho-cho-te…” Mariamu akajibu.

“Sawa, sintokufanya chochote kama utanipa majibu ninayotaka…” Gina akamwambia kwa sauti ya upole.

“Sawa!” Mariamu akajibu huku akitweta kama mbwa aliyekimbizwa.

“Unamjua Andrew Makita?” Gina akaamuliza.

“Ndi-yo, uhhh!”

“Ni nani kwako?”

“Alikuwa mpenzi wangu…” akajibu na kuanza kulia.

“Alikuwa mpenzi wako? Kwani sasa mmeachana?”

“Siiimmmtaki hata kumuona…… ah!” Mariamu akaanza kulia.

“Nyamaza, sitaki makelele yako,” Gina akamkaripia. Mariamu akanyamaza na kubaki na kwikwi za kilio. Alionekana tangu usoni kutomtaka kabisa mwanaume huyo.

“Hebu nambie mara ya mwisho ulimuona wapi?” Gina akauliza.

“Ahaaaa dah, mara ya mwi-sho jana, nime-pi-gwa na rafiki yake, hakunitetea… wewe ni nani kwanzzza?” akajibu. Kitendo cha kuamka ‘jana’ kilimfanya Gina agundue kuwa mwanamke amepoteza kumbukumbu kiasi fulani.

“Wapi ulikuwa ukipigwa nay eye akiwepo?”

“Kinondoni,” Mariamu akajibu kwa utulivu.

“Hapo ndipo ulikuwa unaishi?”

“Hapana…”

“Unaishi wapi?”

“Mburahati NHC,”

“Kwenye nyumba ya nani?” Gina akamtupia swali ambalo lilimfanya Mariamu atulie kidogo.

“Naikiaga jina tu Kihwelo, hata simjui, sijawahi kumuona,” akajibu.

Gina akamtazama Madam S. Madam S akampa ishara aendelee kumuuliza. Wakati huo mashine ya kurekodi sauti ikiendelea kufanya kazi.

“Nikikwambia kuwa Andrew na huyo rafiki yake wana mpango mmoja kwako, utakataa au utakubali?”

“Ntakubali tu…”

“Kwa nini?”

“Yeye ndo amenipeleka kwa rafiki yake, napigwa hanitetei… maana yake nini sasa? wale majambazi kwanza, majambazi kabisa,” Mariamu akaanza kulia tena.

Madam S akampa ishara ya kuzima ile microphone, Gina akafanya hivyo. Madam S akamgeukia Chiba.

“Mpe disprin kwanza, pumbavu huyo!” akamwambia. Chiba akaminya batani na kumpiga shoti moja mbaya ya umeme. Andrew alipiga kelele na kujitikisa huku kauma meno kisha akarudi kitandani na kuanza kutweta kwa nguvu.

“Chiba! Unafanya nini?” Madam S akang’aka.

“Si umenambia nimpe disprin, hii ndiyo disprin Madam!” Chiba akajibu.

“Shenzi kabisa wewe! Unataka kumuua mwenzio!” Madam akamwambia Chiba huku akiketi vyema kitini, “Endelea!” akamwambia.

“Umetugeuka Andrew!” Sauti ya Chiba ikasikika ndani ya chumba kile kwa mwangwi. Andrew aliisikia. “Mimi sijawageuka ila mnahisi hivyo,” Andrew akajibu kwa sauti tetemeshi.

“Sisi tuna akili, na tunajua umetugeuka… na wale uliokwenda kuwapa taarifa zetu juu ya kesi hii wamekugeuka!” Maneno hayo ya Chiba yalimshtua Andrew. Akashindwa kuongea na kubaki akimwemwesa midomo, “Ninyi ni nani?” akauliza huku akihema. Chiba akaangua kicheko kirefu ambacho upande ule wa pili kinakuwa cha kutisha.

“Sisi ni kaka zako tuliokulea, mpumbavu wewe! Haya nieleze kwa Mariamu ulikuwa unafuata mapenzi au kitu kingine?” Chiba akauliza. Andrew akaendelea kuhema na kubaki kimya.

“Hutaki kunijibu! Kumbuka kitanda ulicholalia kina kazi kubwa tatu, kukupiga kwa umeme, kukubanika kama kuku au kukugandisha kama barafu. Usiponipa majibu kimoja wapo kitachukua nafasi,” Chiba akaweka mkono wake kwenye batani tayari kuruhusu kimojawapo. Akaanza kuzungusha taratibu.

“No! no! no! Nooooooo!!!” Andrew akapiga kelele baada ya kuhisi vyuma vya kile kitanda vikipata moto.

“Semaaaaaa!!!” sauti mbaya yenye mwangwi ikasikika masikioni mwake.

“Ravennnnn!” akajibu kwa kutumia lugha ya kiintelijensia.

“Kwa ajili ya nani?” Chiba akauliza.

“Nilitaka yule mwanamke anipe siri iliyofichwa ndani ya ile nyumba…”

“Nani aliyekwambia mle ndani kuna siri?” Chiba akahoji haraka haraka.

“Godfather!”

“Godfather ni nani?”

“Simjui, nimesikia sauti yake mara moja tu! Noooooo tafadhali msinichome!” Andrew akaanza kulia kama mtoto. Kamanda Amata akaukamata mkono wa Chiba na kuutoa kwenye ile batani.

“Acha tafadhali, inatosha!” Amata akasema huku macho yake yakiwa yamejawa machozi yasiyotaka kumwagika. Madam S akamtazama Amata, wakagongana macho.

“Hata wewe una huruma leo?” Madam akamuuliza Amata.

“Sometime yes! Sometime no!” akajibu kisha akageukia tena kwenye ile luninga na kumtazama Andrew akihangaika pale kitandani. Amata akatikisa kichwa kushoto kulia.

“Tuambie wajibu wako kwao, ulikuwa unawanyia nini?” Amata akamuuliza.

“Nilikuwa na kazi ya kuiba siri za serikali dhidi yao… pamoja na yote walikuwa wanataka kabrasha lenye Top Secret kuhusu mapinduzi ya mwaka 1980 dhidi ya serikali,”

“Uliwapa?”

“Sikufanikiwa kulipata, lakini nakala yake ilisemekana imefichwa nyumbani kwa marehmu Dastan Kihwelo,” Andrew akajibu vizuri kabisa.

“Tunaitaka hiyo uliyokuwa unaitafuta kwa Kihwelo,” Amata akamuuliza.

“No! sijaipata pia, iliibwa usiku na watu wasiojulikana. Inaonekana kuna watu wengine pia walikuwa wanaitaka na walijua ni wapi ipo,” Andrew akaeleza kwa uwazi.

“Dastan Kihwelo yuko wapi?” Amata akauliza.

“Huyu jamaa aliuawa miaka kama kumi na mbili nyuma…”

“Nani aliendesha mauaji yake?”Amata akahoji.

“Hawa jamaa wana timu kubwa na mbaya katika mauaji. Mauaji ya Dastan yalisimamiwa na mwanamke wa Kirusi anaitwa Barbier Saratov,” akaeleza. Haraka Chiba akaandika jina lile.

“Maiti yake ilizikwa wapi?” akamuuliza tena.

“Kwa kweli sifahamu, ninachojua ni kuwa wakiua mtu wanamyeyusha kwenye tindikali ili kupoteza ushahidi,” Andrew akaeleza. Amata na Chiba wakatazamana huku Madam S akitikisa kichwa juu chini.

“Umeshawahi kumsikia Kibwana Mtokambali na James Msambamagoya?” Amata akauliza.

“Hao wote ni marehemu, na wanaheshimiwa sana na lile genge…”

“Mkuu uliyeongea naye ni nani?”

“Simjui!”

Madam S akawapa ishara ya kusitisha zoezi. Wakati huo simu ya mezani ilikuwa ikiita kwa fujo.

“Wafungulieni kwa muda, kisha warudishwe uraiani,” madam S akamwambia Chiba. Kwa kidole chake akabonyeza batani moja tu na vile vifungo alivyofungwa Andrew kwenye kile kitanda vikaachia kwa mara moja. Bila kuchelewa akajitupa chini sakafuni huku akiugulia maumivu. Gina naye akafanya vivyo hivyo na Mariamu akawa huru.

Madam S aliifikia simu ile na kuinyakua, akaiweka sikioni, “Ground Zero!” akaitikia.

“D.I.A terminal two. Mzigo umefika, ova and out!”

“Copy!” Madam akajibu na kukata simu. Akawatazama, Amata, Chiba na Gina kwa zamu.

“Dana amefika!” akawaambia.

* * *

Dana aliwasili uwanja wa ndege majira ya saa kumi jioni. Mara baada ya kumaliza taratibu zote za uhamiaji na kuchukua mabegi yake, alijiandaa tayari kwa kutoka nje ya uwanja huo. Aliangaza macho kwenye vioo vinavyoonesha watu walioko nje kwa minajiri ya kuwaona ndugu na jamaa waliokuja kumpokea. Akawaona, japo wao hawakumuona. Dana alijawa na furaha sana kwa kurudi nyumbani baada ya kuondoka kikazi miaka mitatu na kwenda kuhudumu katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Ureno.

Akiwa tayari kila kitu kimekamilika alipakia mizigo yake kwenye kitoroli tayari kwa safari ya kuondoka uwanjani hapo. Akiwa ndani ya chumba cha kufikia wageni, Dkt. Jasmini tayari alikwishamuona mwanamke huyo ambaye kwaye ametumwa kuhakikisha anafika shamba. Akaingia msalani, akafungua begi lake na kuchukua koti lake la kidakitari. Akalivaa. Kishapo akachukua sindano yake ndogo, akavuta dawa kidogo na kuifunga. Akaitia mfukoni na mkono wake ukabaki huko. Akatoka na kuangaza macho kujua ni wapi ameelekea. Akamuona. Akavuta hatua kumfuata na alipomfikia akasimama sentimeta chache nyuma yake. Akahakikisha hakuna mtu anayemuona kwa kile atakachokifanya. Akachuku ile sindano kwa siri na kumdunga ubavuni. Dana akasikia kitu kikimchoma, akageuka kutazama akakutana macho na mwanamke huyo.

“Unajisikiaje Dana?” jasmine akamuuliza.

“Ummmennnifanya nnnninnnni?” akamuuliza kwa kuvuta maneno. Tayari dawa ile ilisafiri haraka sana na kuanza kukata mawasiliano ya fahamu za mwaDanada huyo. Sekunde hiyo hiyo, Dana akaanza kutokwa na povu kinywani. Akaishiwa nguvu na kulegea. Dkt Jasmini akachukua simu yake ya upepo.

“Mgonjwa wetu amezidiwa, msaada wa kitanda tafadhali! Ova!” akaita.

“Msaada unakuja mara moja! Ova!” akajibiwa upande wa pili.

Kutoka kwenye maegesho ya magari, nje ya uwanja huo, Scoba akatia moto injini gari lake la wagonjwa alilokuwa nalo siku hiyo. Akapiga king’ora na kupata msaada wa njia haraka mpaka karibu kabisa na mlango mkubwa wa kutokea wageni. Akaupita na kulizungusha gari upande wa ndani wa jingo hilo. Walinzi hawakuwa na shaka kwani walishapewa taarifa ya mgonjwa huyo, lango likafunguliwa. Akaingiza gari na kuliegesha salama. Akateremka na kufungua milango ya nyuma, akatoa kitanda cha magurudumu na kuwahi kuingia nacho ndani. Dana akapakiwa juu ya kile kitanda na kufungwa barabara akiwa hana lepe la fahamu. Kwa haraka kitanda kile kikaingizwa garini. Kikawekwa mahala pake na safari ikaanza.

Nusu saa baadae, gari lile likaingizwa kwenye maegesho maalumu huko Shamba. Madam S, Kamanda Amata, Chiba, Gina, wote walikuwa hapo maegeshoni wakimsubiri mgeni wao.

“Kazi nzuri Jasmini na msaidizi wako Scoba,” Madam S akawaambia huku akiwapa mkono kila mmoja. Dana akaingizwa ndani katika chumba maalumu, akaondolewa kwenye kile kitanda na kuwekwa juu ya kitanda kingine cha chuma. Akalazwa hapo akiwa kafungwa mikono na miguu kwa vifungo maalumu. Baada ya hapo timu nzima ikaingia kwenye chumba maalumu cha mawasiliano. Ndani ya chumba hicho, waliweza kumwona vyema mgeni wao. Wakasubiri aamke.

“Dozi ya saa ngapi uliyompatia?” Madam S akamuuliza.

“Masaa mawili tu,” Jasmini akajibu huku akijiegemeza kitini.

“Nafikiri kutoka kwake, tutapata mengi sana…” Madam S akamwambia Amata.

“Kabisa, huyu alitaka aniuze kule Lisbon,” Amata akajibu.

TSA, wote wakaketi kila mmoja katika kiti chake. Mbele yao kulikuwa na luninga moja kubwa inayoonesha mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaama hasa zile sehemu nyeti kama

Muhimbili, Uwanja wa ndege, Bandarini, Ikulu na maeneo mengine. Huko shughuli ziliendelea kama kawaida, pilikapilika za watu zilishika hatamu. Wakati mazungumzo hayo yakiendelea katika chumba hicho, Chiba alikuwa ametingwa kwenye kompyuta yake akipekua hili na lile. Cyber Intelligency.

“Hapa tulipokwama, huyu mwanamke atatukwamua tu… anajua mengi sana,” Amata akasema na wengine wakatikisa vichwa kukubaliana naye.

* * *



Hapa tulipokwama, huyu mwanamke atatukwamua tu… anajua mengi sana,” Amata akasema na wengine wakatikisa vichwa kukubaliana naye.

* * *

Chiba aliendelea na kazi yake katika kompyuta hiyo bila kubughudhiwa na mtu. Aliendelea kuchimbua mafaili waliyoyapata kwenye ile Hard Disk waliyoichukua kule Mtaa wa Galu. Miongoni mwa hayo yalikuwepo yenye taarifa anuai juu ya mmpango wa mapinduzi. Lakini kila moja lilikosa mambo mengi na kumtaka msomaji apate taarifa kutoka katika faili kuu.

Faili kuu! Chiba akawaza na kujaribu kupekua hilo faili kuu, asilipate. Akamgeukia Madam S aliyekuwa akizungumza na Amata na wengine.

“Madam!” akaita, mwanamama huyo akageuka kumtazama kijana wake, TSA 2, “Naweza kupata sauti ya Kibwana Mtokambali? Kama aliwahi kurekodiwa mahali akiongea…” akauliza.

“Bila shaka, kwa kuwa yeye alikuwa kiongozi wa serikali, lazima RTD watakuwa nayo. Ngoja kidogo,” Madam akamjibu na kuchukua simu yake. Akabofya namba fulani na kuiweka sikioni. Akaongea na mtu wa upande wa pili kwa dakika chache kisha akakata simu ile. Akamgeukia Chiba, “Subiri kama dakika tano hivi, wanaangalia kwenye maktaba yao. Unataka ya nini?” akamjibu na kumtupia swali.

“Kuna sauti hapa nimeipata ya mazungumzo kati ya Andrew na huyo anayemwita mkulu. Ijapokuwa sauti yenyewe ina mwangwi lakini si tatizo. Nataka kuifananisha na hiyo, nione, kama ni ya mtu mmoja au vipi,” Chiba akaeleza. Madam S akaitika kwa kutikisa kichwa juu-chini.

“Ok, unaamini kuwa Kibwana atakuwa hai?” Madam akauliza.

“Ninaamini kwa asilimia sitini. Sikilizeni! Hawa watu wanajua wanachokifanya. Kama wao wangekufa nani sasa anayeplan kuendeleza mapinduzi?” akawajibu kwa swali. Madam S akawatazama vijana wake, kila mmoja alitikisa kichwa kama ishara ya kukubaliana na Chiba.



Saa Tatu Baadae


Bado TSA wote walikuwa kwenye chumba kilekile wakijadiliana hili na lile. Dana akionekana juu ya kitanda kile amelala kwa utulivu.

“Jasmini! Ina maana Dana ulimpa dawa ya muda gani?” Madam S akawa wa kwanza kuingiwa shaka na jambo hilo.

“Nimempa ya masaa mawili tu, nashangaa hili ni saa la tatu hajaamka!” Jasmini akajibu.

Madam S akashusha pumzi ndefu. Kabla hajasema lolote, simu yake ikaita. Akaipokea na kuiweka sikioni, “Yes!” akaitikia.

“Mzigo tayari, unauchukuaje?”

“Namtuma kijana sasa hivi!” Madam S akajibu na kumtazama Scoba. Kijana huyo akainuka mara moja kitini na kusimama, tayari kusikiliza .

“Fika RTD, muone Jamila Msemakweli, atakupatia mzigo, nausubiri hapa…” akamwambia.

“Sawa madam!” Scoba akajibu kwa nidhamu ya hali ya juu na kuiacha ofisi hiyo. Madam S akarudisha akili yake tena kwa hawa waliobaki.

“Huyu inatupasa kumwamsha, hivihivi atajilaza pale kutupotezea muda!” Gina akasema. Madam S akatikisa kichwa kumpa ishara Gina kuwa afanye hivyo. Bila kuchelewa, akaminya kitufe cha kwanza, cha pili na baadae akaminya nobu nyingine. Shoti kali ya umeme ikampiga Dana. Akatoa ukulele wa maumivu. Gina hakuachia nobu ile mara moja mpaka Madam S alipomvuta mkono kwa nguvu.

“Gina! Hivi hujui kuwa unaweza kuua?” akamuuliza.

“Najua!”

“Sasa?”

“Lazima apate adabu kidogo kwa kusaliti nchi yake.

Dana alitulia kimya kitandani baada ya shoku ile ya umeme. Kifua chake kilionekana wazi kupanda na kushuka haraka haraka. Akatazama huku na kule kwa kugeuzageuza kichwa chake.

“Dana!” sauti iikamwita, akatulia kuisikiliza. Hakujibu chochote. Sauti ile yenye mwangwi ikarudia kuita karibu mara tatu, lakini mwanamke yule hakuitika, wala hakuonesha kuwa anajali.

“Jeuri huyu!” Gina akasema na kubonya tena kile kitufe. Shoku nyingine ya volti nyingi ikampiga Dana takribaki sekunde kumi hivi. Kelele kali ikasikika katika spika ndogo ndani ya kile chumba. Gina akaachia ile nobu.

“Dana!” ile sauti ikaita.

Dana akabaki kimya. TSA wakatazamana wote kwa mara moja.

“Amekula yamini, hawezi kusema…” Jasmini akadakiza kwa kauli hiyo. Kamanda Amata akamtazama Madam S aliyekuwa kimya akimtazama msichana huyo kwenye luninga kubwa ukutani.

“Nunda!” Madam S akasema na kumtazama Amata, “Nahitaji wanawake kama hawa kwenye idara yangu,” akamalizia huku akisimama kitini.

Vijana wake wote wakamfuata kwa macho kumtazama. Hawakuwahi kumsikia akisema kitu kama hicho hata siku moja.

“Unataka kumpa kazi?” Kamanda Amata akauliza.

“Mh! Mwanaume hupitwi… haya mi natoka nahitaji Dana azungumze. Nitakaporudi nipewe taarifa ili kazi ianze rasmi muda huohuo!” Madam S akatoa maagizo na kukiacha kile chumba. Kamanda Amata akageuza macho yake na kutazama luninga ile, hakujali alichosema bosi wake. Chiba bado alikuwa akiiweka mitambo yake vyema, tayari kurekodi kila kitu ambacho atakisema mwanamke huyo.

“Dana, kuna mambo matatu tu ambayo naweza kukufanyia endapo hutosema lolote,” Amata akamwambia na sauti ile iliyojaa mwangwi ikamfikia mwanamke huyo vyema kabisa.

“Sina la kuwaambia,” Dana akajibu kwa kauli fupi.

“Tunataka kujua, uhusiano wako kati yako na genge la akina Mwanachia,” Amata akamwambia.

“Mwanachia alikuwa mpenzi wangu, hakuna lingine,” akajibu. Amata akatulia kwa sekunde kadhaa.

“Bob Marley alisema ‘Only your friend know your secret’ kwa maana hiyo unajua siri na nyendo za marehemu Mwanachia,” Amata akamwambia.

“Negative,” Dana akajibu akimaanisha hapana.

“Mara baada ya kuuawa Mwanachia, ulienda kufanya nini pale Rua Camarante, lote 25?” Amata akamtupia swali ambalo lilimfanya ababaike kidogo.

“Wewe! Unapajua Rua Camarante, lote 25?”

“Jibu swali Dana!” ile sauti ikamwambia.

“Nilienda kwa mpenzi wangu,” Dana akajibu kwa sauti kavu kana kwamba hakuna hatari yoyote iliyomzunguka. Alijua, tayari yupo safe house, kwenye mikono ya watu wanaoijua kazi yao. Hakuumiza kichwa kwa maana alijua kati ya waliopo ndani humo lazima Amata anahusika kwa kuwa ndiye aliyekuwapo kule Lisbon.

“Nani alikuwa mpenzi wako?” Amata akauliza kwa sauti ileile.

“Yule uliyemuua!” Dana akajibu. Jopo la TSA likatazamana.

“Amejua anaongea na sisi?” Gina akauliza.

“Bila shaka. Ni mwanausalama huyo, lazima anajua yuko wapi...” Chiba akajibu. Kamanda Amata akatulia kimya akimtazama pale kwenye luninga. Wakati wote wapo kimya, Gina akawasha umeme volteji ya juu. Shoku mbaya ikampiga Dana, akapiga yowe moja na kukata sauti.

“Najua sasa utanieleza,” Amata akamwambia.

“Si-siwezzzzi... siammmini ka-ma nchi ya-ngu inawe-za kkkkunifanya hivi,” Dana akaongea kwa shida. Gina akawasha nobu nyingine. Kile kitanda kikaanza kupata moto.

“Umeisaliti!” Amata akamwambia.

“Nnnnnnoooooooo!!!!” Dana akapiga kelele. Akajaribu kujigeuza, wapi! Vifungo vya kitanda hicho vilimkamata barabara. Vyuma vya moto vikaanza kuichoma ngozi yake kwa uchu.

“Nnnnnnoooooooooooo, nnnnaaaasemmma!” akapiga kelele.

“Niambie, wako wapi washirika wa Mwanachia?”

“Uhhh! Saratov, Russia” akaongea kwa akionekana kuwa na maumivu makali. Dana aliuma meno wakati upande wa pili Gina alikuwa akitabasamu. Kamanda Amata akampa ishara Gina apunguze moto. Akafanya hivyo.

“Saratov, Russia!” Chiba akarudia jina lile.

“Nataka utambue picha mbili, na unipe majibu yake haraka!” Amata akamwambia. Dana akatikisa kichwa juu-chini kuitikia. Amata akamtazama Chiba na kumpa ishara kwa kichwa. Chiba akabonya mahala fulani. Luninga ndogo ikajitokeza katika kile chumba. Picha ya kwanza ikaonekana ya mwanamke wa kadiri ya miaka hamsini hivi, Mzungu.

“Unamjua huyo?” Amata akauliza.

Dana akatulia kwa sekunde kadhaa, kisha akajibu, “Namjua, anaitwa Barbier!”

“Ana uhusiano gani na hili genge?” Amata akauliza.

“Babier ni muuaji mwenye taaluma hiyo. Ni mtu wa karibu sana katika genge hili... ana akili nyingi sana,” Dana akajibu kana kwamba si yule aliyekuwa akilia maumivu dakika chache zilizpita.

“Mfungue!” Amata akaamuru na Gina akabonyeza kitufe cha kufungua vile vifungo vya kitanda. Dana akainua mikono na kujinyoosha, kisha akajiangusha chini sakafuni.


MSOCOW – URUSI


K


kochi kubwa la von o. Kochi lililompakata vyema na kumnyemeleshea usingizi mtamu usi ATIKA HOTELI ya kifahari ya Moscow Mariot Trevaskaya, Mc Tee alitulia kimya juu ya

kifani. Alikuwa ndani ya chumba cha ukubwa wa wastani, chenye makochi mawili tu yanayofanana. Aliletwa ndani ya chumba hichi na mhudumu wa hoteli hiyo, akitakiwa kumsubiri mwenyeji wake. Mbele ya kochi hilo, kulikuwa na meza moja iliyotengenezwa kwa kioo tupu. Juu yake paliwekwa chupa mbili za pombe kali zenye chapa ya Whisky 73.

Nusu saa baadaye, mlango wa chumba kile ukafunguliwa, akaingia mwanamke wa makamo ambaye alitambuliwa mara moja na Mc Tee.

“Mr. Mc Tee karibu sana Moscow!” yule mwanamke akamkaribisha. Akavua gloves zake na kuziweka kando. Jaketi nalo vivyo hivyo. Akachukua chupa moja wapo kati ya zile mbili. Akaifungua na kummiminia Mc Tee kwenye bilauri yake. Kisha vivyo hivyo akafanya kwake. Akaiinua bilauri yake na kuipunga hewani.

“Cheers! Kwa afya yako…” Yule mwanamke akasema wakati wakignganisha bilauri zao. Kisha kila mmja akapeleka kinywani na kugugumia.

“Huko nje kuna baridi kali sana. Huwezi kutka bila kupata Whisky au Vodka”.

“Najua vyema maisha yenu Babier…” Mc Tee akamwambia yule mwanamke. Kisha wakapiga mafunda mengine kadhaa kabla ya kuanza mazungumzo.

“Anasemaje Colonel Ivan Chernyakhovsky?” Mc Tee akamuuliza Barbier.

“Hajambo kabisa, anajiandaa kukutana na wewe kwa dakika ishirini tu. Alikuwa huko Afrika ya Kati amerudi leo,” Barbier akaeleza, “Na vipi maendele ya kazi yetu? Ni Tanzania tu ambako mnatuangusha hatujui mnakwama wapi,” akaongeza swali

“Kuna kazi kubwa!” akajibu. Baada ya kupiga fundwa lingine na kuliskmezea tumboni, akamtazama Barbier, “Umakini wa kwenye maswala ya kiintelijensia unanitia hofu, wanatuchokna mpaka wajue tulipo,” akaongeza jibu. Barbier, akainama chini. Baada ya sekunde kadhaa akainua us wake.

“Ina maana wamewagundua?” akauliza kwa sauti ya chini.

“Bado, ila nana wanapita kwenye njia ambay, tukichelewa, watatutia mkononi,” Mc Tee akaeleza.

“Lakini nyinyi mna makosa! Tuliwaambia kuwa Afrika haiwezi kugeuzwa kirahisi kama yai kwenye kikaango, mkatuhakikishia inawezekana. Look! Mtaingia kwenye mikono ya serikali sasa hivi!” Barbier akazungumza kwa uchungu.

“…Kote tulikopanga mapinduzi, tumemaliza. Tanzania tu, tunakwama. Hebu kuweni wanaume kidogo, mlijaribu kuitikisa nchi kipindi kile, sasa hivi, mmezeeka? Andaeni vijana tulete mzigo mfanye kazi,” Barbier aliongea kwa mamlaka kama anaongea na mdogo wake.

“Najua…”

“Hata Ivan hajafurahi kabisa baada ya kusikia habari ya Brian…” Barbier akamkatisha sentensi yake. Ukimya ukatawala kati yao, hakuna aliyeongea wala kutikisika.

“So?” Mc Tee akauliza kwa kifupi.

“Tuna dakika kumi za kwenda kumwona Ivan… lazima ukubaliane na atakachokisema…” Barbier akamwambia Mc Tee na wakati huo huo kijana momja wa Kizungu akaingia katika chumba kile. Unadhifu wake ulimnadi waziwazi kuwa ni mlinzi wa mwanamke huyu. Mc Tee alimtazama mwanamke yule, akamkumbuka miaka mingi nyuma akiwa msichana mbichi. Akamkumbuka jinsi alivyofanikisha mauaji ya Dastan kwa mtindo wa kipekee kabisa. Alimkumbuka, Barbier, ndani ya Mazda jekundu.

Baada ya mazungumzo machache na yule kijana safari ikaanza. Mc Tee alivaa koti lake kubwa na zito ili kujikinga na baridi kali ya jiji hilo.

Aurus Senat, gari la kifahari, zalisho la Urusi, lilikuwa tayari likiwasubiri. Mc Tee alilitazama kwa makini na uchu jinsi lilivyopendeza.

Huwezi kulimiliki ndinga kama hiiAfrika! Akawaza. Barbier akaingia kwanza na Mc Tee akafuatia. Milango ikafungwa. Mshangao wa Mc Tee haukujificha mbele ya Barbier.

“Utalimiliki ukiwa Rais,” akamwambia.

“Na sura langu hili?” naye akauliza.

“No! kama tuliweza kukuua hatutashindwa kukufufua,” Barbier akamjibu na lile gari likaiacha ile hotel taratibu. Taa za nje, barabarani na majengo yaliyojengewa mapaa mithili ya ice cream zilivutia katika dutu la giza jepesi.

* * *




No! kama tuliweza kukuua hatutashindwa kukufufua,” Barbier akamjibu na lile gari likaiacha ile hotel taratibu. Taa za nje, barabarani na majengo yaliyojengewa mapaa mithili ya ice cream zilivutia katika dutu la giza jepesi.

* * *


Iliwachukua takriban dakika arobaini na tano kuwasili katika Msitu wa Khimki, uliyo nje kidogo ya Jiji la Moscow. Msitu wenye takribani ukubwa wa hekta elfu moja. Ndani ya msitu huu kulikuwa na nyumba kadhaa za kupumzikia wageni wanapenda kutembelea uoto wa asili. Babier na Mc Tee waliwasili katika moja ya nyumba kuukuu iliyojengwa ndani ya msitu huo. Utulivu na ukimya vilitosha kumfanya aliyesimama hapo kuingiwa na hofu. Barbier akapiga mbinja mara tatu kisha akafuata mlango wa nyumba hiyo uliyosongwasongwa na mimea itambaayo.

Kuna biDanamu anaishi humu? Mc Tee akajiuliza. Barbier akasukuma ule mlango, nao ukafunguka bila shida.

“Nifuate!” akamwambia Mc Tee. Akaingia ndani ya ile nyumba na kuufunga mlango nyuma yake. Yule mwanamke akachukua taa ya kandili na kuiwasha, akaiweka kwenye kiango na kuendelea mbele kama mita kumi hivi. Hapo palikuwa na mlango mwingine uliofuatiwa na ngazi zilizoteremka chini. Wakateremka pamoja mpaka walipokuta mlango mwingine. Barbier akabofya kengele na ule mlango ukafunguka. Mara tu walipoingia, macho ya Mac Tee yakapokelewa na sebule pana yenye kila aina ya samani za thamani. Taa nzuri za umeme zenye urembo wa aina aina zilikuwa zikining’inia darini. Sebule hii haikuwa na mtu zaidi yaw a wawili tu. Katika ukuta mmoja wapo palitundikwa picha kubwa sana ya mtu ambaye Mc Tee alimfahamu fika, Vladimir Ilyich Ulyanov au wengi walimtambua kama Lenin.

“Keti hapa!” Barbier akamwambia Mc Tee, naye akatii na kuketi mkabala na picha ile kubwa. Picha ya mwanamapinduzi wa Kirusia, mwanasiasa na mnadharia wa siasa aliyeamini katika mapinduzi. Aliyesimika nadharia yake ya Leninism, iliyojikita katika jinsi ya kuunda vyama vya kimapinduzi. Aliyejenga kaulimbiu ya ‘Kifo cha Uhuru’.

Yote haya Mc Tee aliyakumbuka pindi alipokuwa akisimuliwa na rafiki yake huyu, Colonel Ivan, walipokuwa huko Kiev katika mafunzo ya kijeshi na medani za usalama. Mc Tee akajikuta akibebwa na usingizi baada ya kusubiri kwa muda mrefu.

“Pasipo na nadharia ya mapinduzi, hapawezi kuwa na vuguvugu la mapinduzi”. Mc Tee akashtuka kutka usingizini, macho yake yakagongana na yale makali ya Colnel Ivan. Hakujua wala hakuwa na uhakika kama sentensi ile iliyonukuliwa kwenye moja ya hotuba za Lenin ilitamkwa na Ivan au alikuwa ndotoni tu.

“Mc Tee…” Ivan akaita huku akiwa kajiegemeza kwenye kochi lililokuwa mkabala na lile aliloketi Mc Tee.

“Comrade Ivan,” akaitikia.

“Mapinduzi hayawezekani bila kuwa na hali ya kimapinduzi; alikadhalika, siy kila hali ya kimapinduzi itatuongoza kwenye mapinduzi,” Ivan alinukuu manen mengine ya mwanamapinduzi Vladimir Lenin. Mc Tee hakushangaa, alimjua swahiba wake huyo jinsi alivyoishiba falsafa ya Lenin, falsafa ya mapinduzi.

“Kwanini unashindwa kufikia ndoto zako mpaka umri unakutupa?” Ivan akamuuliza. Mc Tee akabaki kimya kwa muda.

“Nashindwa kujua, kama nashindana na serikali ileile ya Tanzania au la!” akajibu.

“Mbinu zote tumekupa, watu wa kuwatumia tumekupa, shabaha tumekunesha, shida nini?” Iva akamuuliza swali jingine.

“Medani ya usalama Tanzania imekuwa na weledi wa hali ya juu sana. Anayetutafuta hatumwoni lakini anatupunguza taratibu,” akajibu.

“Nimekuficheni ninyi wawili, hakuna anayejua mlipo, lakini mpo palepale… sasa kama mbinu zte zimeshindikana, twende msituni…” Ivan akamsisitizia.

“Na ndilo lililonileta,” akajibu Mc Tee. Colonel Ivan akatikisa kichwa kama ishara ya kukubali. Babier akaingia sebuleni hapo akiwa na chano iliyobeba pombe kali na bilauri mbili. Akawamiminia. Wawili hawa wakagonga cheers na kujimiminia matumboni mwao. Walipoweka bilauri zile mezani, wakatazamana.

“Hiyo ndiyo mbinu ambayo washirika wangu wote wameitumia na kufaulu… kwa kuwa umeamua, utafaulu. Tanzania haitaweza kuziona nyayo zetu zilizobaki. Walipofika wamefika ukomo, na katika hili nitajua tu nani yupo nyuma yao…” akapiga funda jingine na kuitua bilauri ile mezani. Mc Tee, akaigiza mkono katika mfuko wa koti na kuchomoa picha moja. Akaiweka mezani. Ivan akainyakua na kuitazama kwa makini, akavuta kumbukumbu ya sura anayoiona kwenye picha hiyo. Akatikisa kichwa kama ishara ya kutokumjua.

“Huyu ndiye anayetutesa, muuaji wa siri anayetumiwa na serikali kukamilisha hukumu yetu,” Mc Tee akamweleza Ivan. Colonel Ivan, akachukua kitu kama simu ya mkononi, akaipiga picha ile picha na kuiingiza katika mtandao wa siri wa utambuzi. Dakika tatu baadaye, kile kifaa kikatoa mlio.

Akakichukua na kutazama majibu gani yamekuja.

“Amata Ric, au Kamanda Amata. Agent wa siri asiyeonekana, code ya kijasusi 005…” Ivan akasoma kwa sauti yale yote yaliyoandikwa kwenye kidubwasha hicho. Akakitua na kushusha pumzi ndefu.

“Kuna lolote?” Mc Tee akauliza.

“Lazima auawe haraka iwezekanavyo. Kuna mambo mawili ya hatari kwa huyu kiumbe, na ndiyo maana nasema lazima auawe; ajenti wa siri na code 005,” akamweleza Mc Tee, “Hizo peke yake zinatosha kumfanya awe kiumbe hatari, kuliko hatari hyenyewe,” akamaliza kusema. Alipobonyeza kitufe fulani chini ya meza yake, Babier akaingia haraka. Ivan akampatia Babier kile kifaa.

“Erase him!'' akamwambia amfutilie mbali. Barbier akainamisha kichwa chake kama ishara ya kutii agizo hilo. Akaondoka na kuwaacha wawili wale wakiendelea na mazungumzo. Alipopotelea katika mlango mwingine, Ivan akamgeukia Mc Tee na kumwambia, “Kuna njia mbili tu za kumwondoa mtawala madarakani”. Mc Tee akamtazama na kumkazia sura.

“Ama kumwondoa kwa kura, au kwa chuma cha moto,” Ivan akamwambia Mc Tee. Wakaendelea kupata pombe kali kama walivyoanza kwa dakika kadhaa zilizofuata. Na baadae wakaagana wakiwa tayari wameweka sawa mikakati ya awali.




Dar Es Salaam Shamba


Madam S alikuwa tuli mbele ya meza yake kubwa. Ukimya wake ulivunjwa na mbisho wa hodi ya Kamanda Amata. Mara baada ya mlango kufunguka, alishusha pumzi ndefu na kumkaribisha kijana huyo kitini.

“Amata…” akaita.

“Yes Mom!”

“Kichwa changu kimevurugika kabisa na hili swala,” Madam S akamwambia Amata huku akijifikicha jicho kwa mkono wake wa kuume.

“Najua, ila nahisi tumekaribia ukingoni…” akasema Amata.

“Kwa nini wasema hivyo?”

“Dana ametupatia funguo nzuri ya kuanzia…” Amata akaeleza.

“Babier?” Madam akauliza.

“Ndiyo… na nimeshatuma taarifa na picha yake katika ubalozi wetu kule Moscow waanze uchunguzi kujua wapi anapatikana,” Amata akaeleza kwa urefu.

“Safi sana, ndiyo maana nakupenda we mtoto, huwa wakati mwingine unanitangulia katika kile ninachotaka kufanya au kusema,” Madam S akaeleza. Akajikohoza kidogo kusafisha koo kisha akarejesha utulivu wa awali.

“Mmemaliza na hao watu?” akamuuliza Amata.

“Ndiyo, kwa sasa hawana la kutuambia,”

“Ok, fanyeni mpango muwarudishe uraiani. Dana mumpeleke Muhimbili ICU aamkie huko. Hawa wengine warudisheni mnapopajua nyie,” akatoa maagizo.

“Timamu!” Amata akajibu.

“Jambo lingine… kama nilivyokudokeza awali, inabidi ufike Moscow. Fanya mbinu zote za kijasusi mpaka mwanamke huyu akupe siri ya anachokijua au mahusiano yake na hili genge,” Madam S akamwambia Amata kisha wakaagana.

* * *

Alfajiri ya siku iliyofuata ikawakuta Mariamu na Andrew wakiwa kitandani katika chumba cha mwanamke huyo kule Mburahati. Wa kwanza kuamka alikuwa Mariamu, akajishangaa. Akainuka na kukimbilia dirishani. Jua la asubuhi lilipendezesha nchi. Hakujua amerudije. Akarudi kitandani na kumwamsha Andrew. Naye alipoamka akajishangaa, akatazama dirishani, akatambua yupo Mburahati kwa mpenzi wake, Mariamu.

“Tumerudi vipi sweetie?” Mariamu akauliza.

“Hata mimi sifahamu, kila kitu kama muujiza!” akamjibu huku akivuta hatua kuelekea bafuni. Mariamu bado hakuamini. Alipovuta kumbukumbu, alijikuta akiishia tu kuvuta kitu kama hewa iliyochanganyika na moshi, akalala.

Dana alirudiwa na fahamu saa sita baadae na kujikuta kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Akapepesa macho huku na kule.

Muhimbili! Akawaza. Amefikafikaje, hajui. Alichokikumbuka yeye ni tukio lililofanyika kabla ya hapo. Dana alifumba macho yake na kuanza kuvuta kumbukumbu.

* * *

Wakati huo huo, Kamanda Amata alikuwa akijiweka tayari kwa safari ya Urusi. Begi lake na mkoba wa mkononi, tayari vilikuwa vikisubiri safari. Wakati yeye akihangaika kuchukua hiki na kile tayari kwa safari Gina alitingwa kwa kujitazama kwenye kioo. Aligeuka huku, akageukia huko, akavaa nguo hii, akavua, akachukua ile, ilimradi tu apendeze. Yote hayo yakifanyika, Amata alikuwa tayari keshakamilika.

“Gina!” akaita. Gina akageuka kama kashtuliwa, alishajisahau. “Tunaenda au unaendelea kuchagua nguo?” akamtupia swali.

“Tunaenda mpenzi!” akajibu huku akijiweka sawa gauni lake. Dakika ishirini baadae, wakaanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege.

“Uende salama, urudi salama mpenzi!” Gina akamwambia Amata wakati akiiacha barabara ya Nyerere na kuingia ile ya kufika katika uwanja huo.

“Bila shaka! Cha msingi na kuniombea… maana kazi hii hapa ilipofika ni pagumu kuliko ilipotoka,” Amata akajibu. Gina akaegesha gari vizuri. Wote wawili wakateremka. Gina akamkumbatia Amata, akambusu huku chozi likimtoka.

“Rudi na roho yako!” akamwambia. Amata akajibu kwa kutikisa kichwa. Akachukua mkoba wake na kuuweka begani. Dakika tatu baadae akawa tayari ndani ya jengo la uwanja huo.




Rudi na roho yako!” akamwambia. Amata akajibu kwa kutikisa kichwa. Akachukua mkoba wake na kuuweka begani. Dakika tatu baadae akawa tayari ndani ya jengo la uwanja huo.



MOSCOW - URUSI


Alfajiri ya saa kumi na nusu, Kamanda Amata aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sheremetyevo - A.S. Pushkin na kupokelewa na swahiba wake Laabib Hussein.

“Karibu sana swahiba!” Laabib alimkaribisha Amata, wakapeana mikono.

“Shukrani… naona Moscow imekupenda, umetakata sana!” Amata akamtania, kisha wote wakacheka na kugonganisha viganja vyao. BMW 3 Saloon, iliwameza watu hawa na safari ya keulekea mjini ilianza. Iliwachukua dakika kumi na tano tu kufika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ndani ya jiji la Moscow, katika barabara ya Nikitskaya.

“Karibu nyumbani!” Laabib alimkaribisha mgeni wake, “Hapa hatukai Swahiba, tuna mazungumzo machache ya kikazi halafu utaamua kama unataka kutalii jiji la Moscow au unaendelea na safari,” akamweleza. Amata akaitikia kwa kutikisa kichwa. Baada ya kusalimiana na maofisa wachache wa ubalozi. Kamanda Amata na mwenyeji wake wakaingia katika chumba kimojawapo. Hakikuwa chumba kikubwa. Kilikuwa kidogo cha wastani, chenye meza moja na viti vinne. Zaidi ya hapo hakukuwa na kitu kingine chochote. Mara tu baada ya kuketi, Kamanda Amata akainua mkono wake na kuangalia muda. Akaishika pete ya saa hiyo na kuizungusha kidogo kisha akaiacha kwa sekunde kadhaa, ikifuatiwa na taa ndogondodo zilizokuwa zikiwaka.

Nipo salama! Akawaza. Muda huo huo mlang ukafunguliwa, Laabib akaingia na kuketi.

“Yes Kamanda Amata,” akasema na kuliweka kabrasha moja katikati yao. Amata akalivuta kwake na kulifungua. Kurasa ya kwanza tu akakutana na picha ya kuvutia ya msichana Barbier.

“Ndiye huyo! Sivyo?” Laabib akauliza.

“Swadakta! Ni yeye… nipe tafutishi zako!” Amata akamwambia Laabib.

“Kazi mlonipa nimeifanya kikamilifu na taarifa zote ndizo hizo… Barbier anapatikana sana kuliko mlivyofikiria. Hajifichi, hata ukitaka kufanya biashara naye, msichana huyu hana tabu. Ni mcheshi, anapendwa na watu na ni mwema sana!” Laabib akaeleza. Amata akatikisa kichwa kushoto kulia.

“Sikubaliani na wewe!” Amata akasema, “Barbier ni mwanamke anayeshiriki njama chafu za kuiangusha serikali ya Tanzania. Amehusishwa na genge hili haramu tangu akiwa na miaka kumi na saba mpaka sasa anakaribia uzee. Taarifa zetu zinamwonesha kama muuaji hatari aliyeshindikana!” akaeleza.

Laabib akashusha pumzi na kujiweka vyema kitini, “Barbier yupi unayemsema wewe?” akauliza. Amata akachomoa picha na kuiweka mezani. Laabib akaitazama, kisha akamtazama Amata. Laabib akaichukua ile ya kwenye kabrasha na kuziweka pamoja. Zinafanana kila kitu.

“Endelea…” Amata akamwambia Laabib.

“Kama ulivyosema. Babier amelelewa katika kituo cha watoto yatima huko Kirov kabla hachukuliwa na Afisa wa jeshi la Urusi aliyekuwa akikaa huko Saratov na kumlea kama binti yake,” akaeleza. Maneno haya yakaanza kumwingia Amata kwa namna fulani. “Katika chunguzi zangu nimeweza kupata mpaka wapi alisoma lakini kuna miaka mitatu au mine nimeshindwa kujua huyu Barbier alikuwa wapi…” akamaliza kusema.

“Sikiliza Laabib, niambie Barbier anapatikana wapi, nitajua mimi kama ni yeye au la…” Amata akasema.

“Sawa! Fika Saratov, mtafute Dimitri Gobenskiv, anapatikana katika casino la Faraon. Ukimpata yeye, habari zote atakupa… isitoshe ndiye aliyenipa habari hii yote. Beba na picha hii umpatie, atakutambua kirahisi zaidi!” Laabib akampatia ile picha Amata. Naye akatia kwenye mfuko wa koti. Dakika chache baadae wakaagana.

* * *


Dimitri Gobenskiv, kijana tajiri katika matajiri wa Saratov, kama kawaida yake, aliketi katika ofisi yake pana nay a kisasa ndani ya Casino Faraon. Hakuwa na makuu kama matajiri wengine wa jiji hilo. Alifikika ijapokuwa alikuwa na ulinzi mkali sana. Siku zote alikuwa na kilio kikubwa ndani yake baada ya wazazi wake wote wawili kuuawa kikatili kwa mkono wa mwanamke hatari, Barbier.

‘Ukijaribu kufanya lolote juu ya maisha yangu, nakuua!’ Ni ujumbe wa mwisho aliopewa na Barbier mara baada ya kugundua kuwa ndiye muuaji wa wazazi wake. Alitamani kulipa kisasi, lakini kila alipokumbuka onyo hilo, aligwaya. Kupitia luninga yake kubwa pale ofisini aliweza kuona kila eneo katika casino hiyo. Kila aliyeingia na kutoka, alimwona. Vijana waliokuwa wakimsaidia upande wa kuongoza kamera hizo waliijua kazi yao vyema. Taarifa zote zilimfikia kwa wakati kama kuna hatari au la. Hakupenda wageni hasiyowajua. Dimitri, alikuwa na wageni wake maalum. Wanawake wazuri wa gharama, matajiri kadhaa kutka nchi mbalimbali wanaopenda kuja hapo kibiashara au kucheza kamari.

Mlango wa ofisi yake ukafunguliwa, kijana shababi, mkakamavu, aliyevalia suti safi nyeupe, aliingia.

“Sir, kuna mgeni amefika anataka kuonana nawe!” akamwambia. Wakati huo, Dimitri alikuwa akimtazama mgeni huyo kupitia luninga ile. Hakuwa na ratiba ya kupokea mgeni yeyote kwa

siku hiyo. Akamtazama vizuri kupitia luninga. Kijana wa Kiafrika, aliyevalia suti safi nyeusi iliyotanguliwa na shati jeupe. Usoni mwake alipachika miwani ya kisasa sana, nyeusi, iliyomkaa vyema.

“Ana namba?” akamuuliza kijana wake.

“Hana, ila amesisitiza kama anaweza kukuona leo hii…” yule kijana akasema.

“Msafi?” akauliza akimaanisha kama hana silaha yoyote.

Kila mgeni aliyekuja kwa Dimitri alipaswa kuwa na namba ya miadi. Naye aliwapokea kwa wakati kadiri ya maelekezo ya namba hizo.

Waafrika! Atakuwa anataka msaada tu! Akawaza.

“Mpeleke chumba namba tatu, nitamkuta huko,” akamwambia. Yule kijana akatoka kwenye kile chumba na kumwacha Dimitri peke yake.

* * *

Kamanda Amata alifikishwa chumba namba tatu. Hakikuwa chumba kikubwa, ila kilikuwa cha gharama sana. Samani zake zilivutia macho, meza lkubwa ya kioo iliyotenganisha kochi la vono upande huu na ule, ilikuwa ya aina yake. Amata akaketi kwenye kochi mojawapo huku nyuma yake kukiwa na vijana wawili wakakamavu, wamesimama. Vijana hawa walikuwa wamefanana kwa sura, vichwa vyao vikiwa havina nywele, hawakucheka wala kuongea chochote. Dimitri akaingia akisindikizwa na yule kijana aliyempelekea taarifa kule ofisini.

“Karibu sana kijana!” akamkaribisha Amata kwa kumwita ‘kijana’ ilhali ukiwatazama, wamekaribiana umri. Pesa tatizo.

Amata hakujibu ile salamu badala yake akaondoa miwani usoni mwake na kuikunja, akaitia mfukoni.

“Tuna biashara ya kuzungumza!” Amata akaongea kwa kiingereza safi.

“Biashara? Unataka kuniletea wanawake kutoka Afrika ili niwauze humu? Au we ni mcheza kamari? Maana hata suti yako huvaliwa na gamblers, wacheza kamari…” Dimitri akaongea kiingereza kilichozungukwa na lafudhi ya Kirusia.

“Afrika hatuna dhambi kama zenu!” Amata akamjibu Dimitri huku akiwa kamkazia macho.

“Dhambi zipi?”

“Za kuwafanya dada zetu kuwa biashara kama ninyi mfanyavyo,” Amata akamjibu.

“Ha ha ha haaaaaaa!” Dimitri akacheka sana na yule kijana wake naye akaangua kicheko. Lakini Amata hakucheka hata kidogo. Alipoingiza mkono ndani ya koti lake, vijana wale wa nyuma yake wakachomoa bastola na tayari zilikuwa zikimlenga Amata. Akachomoa picha na kuiweka mezani.

“Hii ndiyo biashara ambayo nataka tuizungumze, na si upumbavu unaoongea!” Amata akamwambia. Dimitri akawapa ishara vijana wake, wakarudisha bastola kwenye makoti yao. Akaivuta ile picha na kuigeuza.

“Barbier Kermikov!” Dimitri akatamka jina la mwanamke yule wa pichani.

“Namhitaji, nimeambiwa ni wewe tu unayeweza kunambia ni vipi na wapi naweza kumpata…” Amata akamwambia. Dimitri akakunja sura yake na kuikunjua tena.

“Hii picha umeipata wapi?” akamuuliza.

“Uliyempa, ndiye aliyenipa kwa kuwa ni mimi nilimtuma kwako…” Amata akaongea.

“Huwezi kumfikia kirahisi, huyu ni mwanamke hatari sana… analindwa na watu hatari vilevile. Anajua mtu gani wa hatari na mwema. Ni muuaji aliyepitiliza…” Dimitri akasema huku chozi likimdondoka, “Yeyote atakayeweza kumuua mwanamke huyu, nitampa pesa nyingi sana… naaihitaji damu yake,” akamaliziakusema.

“Nimetumwa kwake…” Amata akamwambia Dimitri.

“Wewe ni nani?” Dimitri akamuuliza Amata.

“Mr. Spark!” akajitaja kwa utambulisho bandia kama kawaida yake.

“Mr. Spark, Barbier ni mwanamke kahaba… si ngumu kumpata. Lakini nenda kama mteja wa kawaida unayetaka kufanya naye ngono… japo hapendi watu weusi, tumia ujanja wako. Ni mwanamke mwenye siri nyingi sana, na zote zipo kifuani mwake kazining’iniza kwa mkufu wa dhahabu na kuzifificha kwa jiwe la emerald,” Dimitri akaeleza. Amata alikuwa kimya akisikiliza kila hatua ya maneno ya mwenyeji wake.

“Huwezi kumuua, Spark!” Dimitri akasema.

“Sitaki kumuua… naihitaji information moja tu kutoka kwake,” Amata akasema.

“Nimeshakwambia siri zake anaweka wapi, nina uhakika hata information hiyo itakuwa humo humo. Kifua chake, hubaki wazi awapo kitandani tu… ukiipata hazina hiyo, niletee na mimi kuna kitu nakihitaji pia. Nilishatuma watu watatu na wote wameuawa hakuna aliyerudi… na sasa ananitafuta mimi aniue!” Dimitri akasema na kusimama, “Subiri hapa!” akamwambia Amata na kukiacha kile chumba.

Dakika tano baadae, yule kijana aliyekuwa na Dimitri akarudi na kikasha kidogo mkononi mwake, akamkabidhi Amata.

“Dimitri anakutakia kazi njema sana… anasema kama ukifanikiwa muonane kabla hujarudi kwenu,” yule kijana akasema na kumkabidhi kike kikasha.

“Asante!” Amata akachukua miwani yake na kuivaa, akakipokea kile kikasha na kukikamata vizuri mkononi mwake. Akatoka huku akiongozwa na wale jamaa wawili mpaka mlango mkuu wa jumba lile la starehe.

“Take Care!” jamaa mmoja kati ya wale wawili akasema. Amata akampa ishaya ya dole gumba kwamba anaafiki asemacho. Moja kwa moja akaliendea BMW alilokuja nalo na kuingia ndani yake. Akaketi nyuma ya usukani, na jambo la kwanza, akafungua kile kikasha. Macho yake yakapokelewa na bulungutu la noti, dola za Kimarekani. Chini kabisa ya kikasha hicho akakutana na kadi iliyoandikwa kwa kalamu nyekundu.

Park-Hotel, Vineshvaya Gora

2nd Aptechnyi proezd 11,

410009 Saratov, Russia

Chini ya anwani hiyo kukawekwa maelezo mafupi tu ya kumpa tahadhari. Akakisoma na kisha anwani ile akaiingiza katika kifaa chake kinachoweza kutambua uelekeo wa mahali uendako kwa msaada wa satelaiti. Akatia ufunguo na kuwasha gari. Injini ikakubali. Akalitoa kwenye maegesho na kuingia barabarani taratibu.

* * *




Chini ya anwani hiyo kukawekwa maelezo mafupi tu ya kumpa tahadhari. Akakisoma na kisha anwani ile akaiingiza katika kifaa chake kinachoweza kutambua uelekeo wa mahali uendako kwa msaada wa satelaiti. Akatia ufunguo na kuwasha gari. Injini ikakubali. Akalitoa kwenye maegesho na kuingia barabarani taratibu.

* * *

Barbier Kelmikov akatikisa kichwa juu chini na kumtazama dereva wake.

“Vipi?” yule dereva akauliza.

“Apelekwe chaka nakuja kumshughulikia,” Barbier akamwambia yule dereva. Wakati wote ambao Kamanda Amata alikuwa katika casino lile, Barbier alikwishapata taarifa ya ujio wa mtu huyo hatari. Kwake ikawa rahisi kuimaliza kazi kama alivyoamuriwa na mzee wake, Colonel Ivan. Kama ingebidi asafiri kwenda Tanzania basi anayemfuata alijipeleka mwenyewe.

* * *

Kamanda Amata mara tu baada ya kusoma ujumbe na kuweka tayari ramani yake ya safari, alilitoa gari maegeshoni na kuondoka taratibu kuwelekea katikati ya jiji la Saratov. Akiwa tayari kalivuka geti la casino hiyo na kuingia barabara kuu, macho yake yalikuwa kwenye taa kuongozea magari zilizo mbele yake. Hakuwa na wasiwasi, akili yake yote ilikuwa ni kumtia mkononi Barbier na kuweza kujua nini kipo katika sakata hilo. Honi kali na nzito zikamfikia masikioni, alipogeuka kutazama kulia aliliona lori kubwa aina ya Liaz likiwa umbali mdogo kutoka pale alipo yeye. Akajitahi kuepa kwa kukunja kona kushoto, lakini hakufanikiwa kwani lile lori lililigonga gari la Amata sehemu ya nyuma ubavuni. Likaizungusha na kulitazamisha lilikotoka. Matairi ya nyuma ya lori lile yakalikanyaga boneti na kuliharibu vibaya likiacha vyoo vikivunjikavunjika na kutuka huki na huko. Kamanda Amata aliyatazama yote hayo kama mkanda wa filamu.

Sekunde chache tu, gari la polisi likawasili pamoja na lile la kubeba wagonjwa. Haraka sana, wahudumu wa gari lile wakateremka na machela, na kumtoa Amata ambaye alikuwa tayari keshapoteza fahamu. Dakika moja baadae lile gari likaondoka eneo lile. Kutoka katika chumba cha dereva cha gari lile la wagonjwa, Barbier alisogeza kioo cha kumuwezesha kuona katika chumba cha mgonjwa.

“Vipi?” akawauliza vijana wake waliojifanya wahudumu wa afya kumbe la. Kamanda Amata alikuwa tayari mikononi mwa Barbier.

“Amezimia tu, na ana majeraha madogo madogo!” akajibiwa huku gari lile likichanja mbuga kuelekea nje ya jiji la Saratov.



Kumysnaya Polyana


Katika msitu huu mkiubwa ambao watu hupenda kwenda kwa mapumziko na harakati

nyingine, lile gari la wagonjwa likaingia. Baada ya kufuata ujia mrefu unaotosha gari moja tu wakafika mahali penye kizuizi. Mlinzi wa eneo hili alikuwa mzee sana kadiri ya miaka sitini au sabini.

“Safari ya wapi?” akamuuliza Barbier ambaye alikuwa ameketi upande wake.

“Shimoni!” Barbier akajibu. Yule mzee kabla ya kufungu lile geti la mbao, akauendea ufagio wa wima ulioegemezwa katika ukuta wa kibanda chakavu langoni hapo. Akauchukua na kuugeuza, akazungusha pale kwenye kiungo cha mpini na ufagio wenyewe. Kwa ndani hapo palikuwa na simu ya upepo iliyofichwa kiufundi sana. Akaongea maneno machache tu na mara lile geti likafunguka lenyewe. Lile gari likapita na kuendelea na safari.

Haikuwa nyumba kubwa, bali ndogo ya kizamani, iliyochoka kiasi kwamba haikuwa na uhai ndani yake. Lile gari likasimama nje yake, Barbie akateremka na kufuatiwa na yule dereva. Wale vijana wa nyuma nao wakateremka. Amata bado alikuwa kimya kitandani.

Barbier alisimama kimya mikono yake ikiwa kiunoni. Sura yake ya kiutu uzima kwenda uzeeni ilionesha dharau ya paka. Si yule aliyekuwa akijidai na Mazda jekundu nyakati zile za miaka ya themanini, si yule aliyekuwa na sura ya kuvutia ya binti mbichi yenye kuvutia marijali. Huyu alikuwa Barbier mwingine kabisa, mtu mzima, mwenye macho yaliyojaa ukatili wa miongo kadhaa. Akamtazama Amata pale alipolala.

“Mshusheni, mpelekeni shimoni haraka,” akaamuru. Wale vijana wakamshusha Amata na kumbeba akiwa hana fahamu. Wakaingia nae ndani ya ile nyumba chakavu, nyuma yao wakifuatiwa na Barbier. Katika sebule ya nyumba hiyo, kukafunguliwa kitu kama mfuniko wa tanki la maji machafu. Baada ya kufungua mfuniko huo wakateremka chini ambako ghala kubwa liliwakaribisha. Amata akabwagwa chini kama mzigo. Ndoo ya maji baridi ikafuatia juu yake. Akashtuka kutoka katika mzimio huo, akatikisa kichwa na kujaribu kujiinua.

“Waoh! Vizuri sana, umeamka ee?” Barbier akasema huku akimzunguka Amata na alipofika upande wa kichwani , akasimama na kujishika kiuno. Amata akainua uso wake na kumtazama mwanamke huyo. Macho yake yakatua kifuani mwa mwanamke huyo. Kidani cha gharama kilikuwa kikining’inia kifuani mwake. Barbier akayatazama macho ya Amata, kisha akajitazama kifuani.

“Ni mwanamke mwenye siri nyingi sana, na zote zipo kifuani mwake kazining’iniza kwa mkufu wa dhahabu na kuzifificha kwa jiwe la emerald,”

Wakati akiwaza hayo akajikuta ghafla akipokea teke zito lililtua usoni na kumwangusha upande wa pili. Amata akainua mkono na kujifuta damu zilizokuwa zikitoka puani mwake. Barbier akaachia sonyo kali.

“Na utafia ndani ya ghala hili shetani mweusi we!” akasema. Amata hakujibu kitu akabaki kimya.

“Mfundisheni adabu,” akawaambia. Wale vijana wakamwinua Amata na kuanza kumsulubu. Vipigo vizito viliufikia mwili wake. Dakika saba zilimwacha nyang’anyang’a akiwa hana hali.

“Good! Mfungeni kwenye kiti cha ufalme…” Barbier akawaamuru wale vijana, wakamtutusa kutoka pale chini na kumkalisha kwenye kiti. Mikono yake ikafungwa kwa vifungo vya chuma, miguu yake pia na kifungo kingine kikafungwa kuzunguka shingo yake. “Utakaa hapa na kifo chako kitakukuta humu ndani,” Barbier akamwambia na kuwapa vijana wale ishara ya wote kutoka mle ndani. Mara baada ya wote kutoka, ule mlango ukafungwa na giza likatawala chumba kile chote. Kamanda Amata akafumbua macho vizuri, hakuweza kugeuza shingo yake kutokana na kifungo kile kilichowekwa shingoni mwake. Kila alipojaribu kujitikisa, vile vifungo vilimbana na kumpa maumivu makali. Alijaribu kutumia macho yake tu kwa kuyapepesa kwa nyuzi aziwezazo. Mwanga mdogo na mwembamba sana ukapita kati ya macho yake kutoka upande wa kushoto. Akili yake ikasoma haraka sana.

Camera! Akawaza. Kisha akatulia. Hakuwa na cha kufanya kwani alikuwa amefungwa barabara. Hana ujanja. Alitulia kimya akisubiri mwisho wake.

Upande wa juu, nje ya ile nyumba, katikati ya msitu wa Kumysnaya Polyana, Barbier na vijana wake walikuwa wakizungumza jambo. Dakika mbili baadae, kukasimama gari la kisasa, BMW. Ndani yake akatoka mwanaume aliyekula chumvi nyingi, Mzungu, aliyechakaa kichwa chake kwa mvi lukuki. Barbier akamsalimu kwa kumpa mkono. Mzee huyo akapokea salamu hiyo pasi na kusema neno. Fimbo yake ya kutembelea alikuwa ameining’iniza kwenye mkono wake, upande wa nyuma ya kiwiko. Barbier akampa ishara yule mzee ya kuwa ‘amfuate’, akafanya hivyo. Wakateremka shimoni, alikohifadhiwa mateka wao.

Dakika tano baadae, Colonel Ivan Chernyakhovsky, alisimama imara mbele ya Kamanda Amata. Kanali wa jeshi la Kirusi aliyeasi na kuanzisha shughuli zake za siri. Kuwekeza katika tawala nyonge zilizojawa tamaa huko Afrika. Kamanda Amata, akamtazama mwanaume huyo, mzee, mwenye macho makali. Kinywani pake alikuwa na cigar ya gharama sana. Akaibana kwa vidole vyake viwili, akaiondoa katika midomo yake na kuining’iniza vidoleni.

“Finally, hatujatumia nguvu kukutafuta! Umekuja mwenyewe kwenye himaya ya mtu mwenye mikono michafu” Ivan akamwambia Amata huku akitembea huku na kule. Amata hakuweza kugeuza sura yake kumtaza kila upande aliyokuwa akienda. Macho yake yalibaki kutazama mbele tu lakini poopoo zake ziliweza kuzunguka kadiri ziwezavyo. Muda wote huo Barbier alikuwa kasimama kando ya chumba mahali ambapo palikuwa na swichi kubwa ya taa na vibonyezo vingine.

“Nani aliyekudanganya kuja huku? Nani kakutuma?” Ivan akamuuliza Amata. Ukimya ukatawala. Barbier akabonyeza moja ya zile swichi. Vile vifungo vikaanza kukaza kwa nguvu. Kile cha shingoni kikawa kinamkaba zaidi na kuliminya koromeo taratibu. Kamanda alimwagikwa na jasho, akakosa pumzi, akahangaika kuitafuta, akaanza kukoroma huku vidole vyake vya mikono vikiwa vimechanua kutafua msaada.

“Aaaa hah hah hah hahaaa hakuna kitu kizuri kama kumuona biDanamu akikata roho!” Ivan akasema baada ya kutoa cheko lake la kifedhuli. Cheko lile lilimtia hasira Amata lakini hakuweza kufanya lolote. Barbier akaminya swichi nyingine, kile kifungo cha shingoni kikalegea kabisa. Amata akakohoa mfululizo. Nuru iliyoanza kumpotea ikarejea taratibu. Akakohoa na kutema damu iliyochafua shati lake. Akabaki akihema kwa nguvu huku macho yake dhaifu yakimtazama mzee yule katili. Sura yake ikawa inakuja na kutoka katika kumbukumbu za Amata lakini hakujua ni wapi amewahi kumuona.

Sebastiano Moznich! Akamkumbuka. Huyu ndiye key point yetu! Akakumbuka nini walizungumza shamba walipoiona sura hii katika tafutishi zao.

“Amata Ric, mnajifanya mnaweza kuzuia mapinduzi! Nani kawaambia? Na sasa ndugu zako watashuhudia nchi ile inageuka. Vijana wangu wataiangusha kwa mtutu wa bunduki wakati wewe tayari ukiwa nyama ya udongo!” Ivan akasema kwa sauti yake kavu. Akiwa katika kusema yote hayo, Amata alibaki kimya kabisa bila kujibu.

Ivan akainua ile fimbo yake na kuibonyeza kwa juu. Katika ile ncha ya fimbo kikajitokeza kitu kama kisu chembamba. Akamchoma nacho pajani.

“Aaaagh!” Amata akatoa ukelele.

“Hah! Kumbe una sauti?” Ivan akauliza huku akitabasamu, “Haya nambie nani kakutuma kwangu?” akamsindikiza na swali huku akimchomachoma na kile kisu mapajani huku na huko. Kamanda Amata aliuma meno kwa maumivu.

“Mmmnnnnnhhhhh!” akagugumia kwa maumivu, “Aaaaaaghhh Sebastianoooooo!” akapiga kelele na kulitaja lile jina. Ivan akaacha kile alichokuwa akifanya na kukodoa macho, akimtazama Amata. Barbier akatoka pale kwenye ile swichi na kusogea karibun na mzee huyo.

“Umesema nani kakutuma?” Ivan akauliza.

“Sebbbastiano Moznich!” Amata akataja jina lile kwa urefu. Moyo wa Ivan ukabadili kasi ya mapigo. Akili yake ikahama, akamtazama Barbier kifuani, macho yake yakakutana na ule mkufu wa dhahabu.

“Unamjua? Kanipa ujumbe wako!” Amata akamuuliza Ivan kwa kuwa sasa aliona wazi kuwa mzee yule kachanganyikiwa. Sebastiano Moznich lilikuwa ni jina lake la bandia lililoficha mambo mengi sana nyuma yake. Mzee huyu aliyefungua duka kubwa sana la kuuza magari ya Ferarri huko Toscana, Italia.

“Lock him well!!” akamwamuru Barbier amfunge sawasawa. Ivan akatoka kwenye kile chumba na kuelekea katika sebule ndogo upande mwingine. Baada ya kurudisha kile kifungo cha shingoni, Barbier akatoka na kumfuata Ivan. Ivana akageuka na kumtazama mwanamke huyo aiyemlea tangu akiwa na miaka kumi na saba.

“Nataka huyu jamaa afe, sihitaji kuju chochote kutoka kwake, na ile program yetu iharakishwe ili kusudi mipango isiharibike,” Ivan akatoa maelekezo huku mwili wake ukitetemeka. Alielewa kuwa siri yake kubwa imefichwa katika jina hilo la Sebastiano Moznich. Yeyote anayejua jina hilo basi anakuwa ameingia kwenye kiini cha mipango na mikakati yake.

“Na vipi kuhusu mjinga Dimitri?” Barbier akamuuliza Ivan.

“Kill him,” Ivan akajibu bila kusita. Barbier akaondoka zake. Giza lilikwishauvamia mzitu huo, wakati vijana wa Barbier walipokuwa njiani kwenda kumkusanya Dimitri.


SIKU SABA BAADAE


Mc TEE, Big J na Madam Jesca walikutana tena kwa kikao katika kisiwa kilekile. Wenyewe walikiita ‘kikao cha mafanikio’. Kama ilivyo ada, kilikuwa kikao cha siri na cha watu watatu tu huku wakiunganishwa na mfadhili wao Colonel Ivan kwa njia ya mtandao.

“Bwana Ivan amekasirishwa sana na uendeshaji wetu wa mapinduzi, aDanai tumechelewesha mambo ndiyo maana sasa tumeanza kugundulika…” Mc Tee akawaeleza wenzake.

“Analolisema ni kweli… lakini sisi kilichotutawala ni huruma kwa ndugu zetu. Tungemwaga damu, tungeua dada zetu, kaka zetu, shemeji zetu, shangazi na wajomba. Uamuzi wetu wa wakutumia nguvu kipndi kile cha ujana wetu ilikuwa sahihi lakini kwa sasa imekuwa ngumu,” Big J akasema huku sura yake ikionekana wazi kusawajika kwa mawazo lukuki.

“Sasa inabidi tutumie nguvu tu kuiondoa serikali hii madarakani. Tufumbe macho, cha muhimu ni kuwalinda wale wa damu yetu…”

“Nani anakukumbuka wakati wewe umeshakufa?” Jesca akamuuliza Mc Tee. Mzee huyo mtu mzima, mwanausalama wa jeshi aliyehasi, akatabasamu akimwangalia mwanamke huyo.

“Ni kweli usemayo, lakini hata Yesu alipofufuka aliwatambua ndugu zake japo wao wakati mwingine hawakumtambua,” Mc Tee akamjibu Jesca.

“Jesca!” Big J akaita, “Kama kaututambua wangefanya hivyo sasa, lakini wamefeli wakati tumesimama katika miguu yao…” akamwambia.

“Ok, sasa katika mwezi huu, tutegemee mzigo silaha nzito utakaoingia kwa siri, tayari kwa kazi…” Mc Tee akawaambia na taarifa hiyo ikamgutusha kila mmoja. “Jesca, inabidi uende Dar es salaam, nitakupa barua yenye kifungo maalum ukwapatie watu nitakaokuelekeza,” Mc Tee akatoa maelekezo kwa mwanaharakati huyo wa kike. Bi Jesca alijizolea umaarufu sana miongoni mwa Watanzania kwa harakati zake za kuiponda na kuikosoa serikali. Alipoanza kutafutwa akafanikiwa kutoroshwa na Vincent Mwanachia.

“Lazima ubadilike kidoko!” Big J akamwambaia Jesca, “Utatoka hapa utaenda India, pale utafanyiwa mambo yote kisha utaingia Dar’ kama utakavyoelekezwa. Hautatakiwa kufanya lolote kwa maamuzi yako isipokuwa yetu. Ukikiuka hilo, utakamatwa kirahisi, wanausalama wa Tanzania ni wakali sana siku hizi, wananusa kuliko mbwa,” akamwambia.

Wakiwa katika mazungumzo hayo, simu ya mezani ikaita. Simu hii iliyounganishwa na satelaiti iliweza kuwaunganisha hapo Camp Site na Saratov bila kuingiliana na kampuni yoyote ya mtandao. Mc Tee akawasha luninga ndani ya chumba hicho na kuifyatua ile simu. Katika luninga ile, akaonekana mzee wa makamo, nywele nyeupe, fimbo ya kutembelea mkononi mwake. Nyuma yake, mitya kama mbili hivi alisimama mwanamke mwenye umri kidogo, midomo yake myekundu ilimfanya aonekane kama mtu wa kuchora.

“Comrades! Nina habari nzuri sana kwenu na kwetu pia!” Upande wa pili , Ivan alizungumza. Mc Tee na jopo lake wakakaa tayari kusikiliza. “Tunaye huyu bwana hapa!” akageuka nyuma na kutoa ishara. Akaletwa mbele ya camera, mwanaume, mwafrika, akiwa tumbo wazi, damu ilionekana dhahiri shahiri mwilini mwake. Uchovu aliyokuwa nao ulionesha wazi kuwa mwanaume huyo alipigwa na kuteswa haswa.

“Anaitwa Kamanda Amata kutoka TSA huko Tanzania, huyu ndiye mwaribifu wa mipango yetu siku zote. Ndiye aliyepokea kijiti kutoka kwa mshenzi Dastan. Tumemkamata, na leo hii mtakishuhudis kifo chake kupitia luninga hii…” Ivan akaongea kwa uchungu huku akitetemeka kwa hasira. Mc Tee na wenzake walibaki kimya kabisa wakimtazama mtu yule ambaye hata sura haikuonekana sawasawa.

“Nataka mjue kwamba, huyu bwana kufika hapa ina maana kuwa amekwishajua siri nyingi sana za genge hili. Huyu ndiye aliyeiangusha Brussels, huyu ndiye aliyeiangusha Lisbon, na bado alikuwa katyika mikakati ya kuigusa ngome kuu. Ninyi mlikuwa mnamchekea tu wakati mnamjua fika! Nimemtia mkononi na hapa ni kifo tu,” Ivan akasema kwa Kiingereza chake kilichotawaliwa na lafudhi ya Kirusia. Mc Tee, Big J na Jesca hawakuamini nini wanachokiona. Mtu aliyekuwa akiwaumiza kichwa na kuwanyima usingizi alikuwa mikononi mwa jitu katili, Ivan, na mwanmke muuaji, Barbier. Ilikuwa kama ndoto.

“Hakuna jinsi tunasubiri kushuhudia kifo chake!” akasema Mc Tee.


* * *


OFISI NDOGO


Ilikuwa siku ya tatu tangu Kamanda Amata atoweke, Madam S alipopata nukushi ya kujulishwa habari hiyo mbaya. Nukushi hiyo iliingia asubuhi kabisa ambapo ofisi hiyo ilikuwa ndiyo kwanza inafunguliwa. Madam S baada ya kuisoma alijikuta akikaa kitini huku akiwa haamini.

Nini kimetokea? Akajiuliza. Baada ya kutumia dakika kumi za kutafakari, uamuzi ukafika akilini mwake. Akainua simu yake na kubofya namba kadhaa. Baada ya kuongea maneno machache akakata na kutulia akisubiri. Dakika kumi baadae Chiba na Gina walikuwa tayari ndani ya ofisi hiyo. Ukimya ulitawala kwa maana kila mmoja alijua nini maana ya simu ile. Kazi nyeti, kazi nzito.

“TSA!” akatamka.

“For my people. For my nation!” wakaitikia pamoja.

“Kamanda Amata amepotea. Na nyote mnajua ugumu wa mchezo huu… hatutakiwi

kujiuliza wala nini. Gina na Chiba haraka sana mkamate ndege mchana au jioni ya leo, mtapokelewa Moscow na Laabib. Mambo mengine yote tayari huyo bwana keshapanga… na ubalozi utawakirimia yatayobakia,” Madam S akawaambia huku macho yake yakiwa wazi yametona machozi. Alimwamini sana Amata lakini mara nyingi ilikuwa endapo inatokea kuwa katika mikono ya watesi, raha humuondoka. Akajifikicha macho na kuirudisha miwani yake usoni.

“Madam!” Chiba akaita, “Unatukutanisha na ubalozi tena? Umesahau yaliyotokea Lisbon?” akauliza.

“Nakumbuka, lakini nchi ile ipo makini sana na mambo ya usalama na kijasusi. Mkiingia viabaya mnaweza kujikuta pabaya. Lakini kuna mambo ya kidiplomasia ambayo lazima yafanyike, hivyo Laabib ambaye ndiye aliyempokea Amata , atawapokea na ninyi. Mkiona mauzauza basi akili vichwani mwenu,” Madam akawaambia.


Siku iliyofuata


Jioni ya siku iliyofuata iliwakuta Chiba na Gina ndani ya jiji la Moscow. Ndani ya moja ya ofisi za siri katika viunga vya jiji hilo, Laabib aliwakaribisha watu wake.

“Unataka kunambia Spark katoweka au katekwa?” Chiba aliuliza mara tu baada ya salamu na mazungumzo machache.

“Nilichokigundua ni gari lake lilipata ajali, na askari katika eneo lile wanasema alichukuliwa na gari la wagonjwa. Unajua huku kwa wenzetu, magariya wagonjwa yanafanana isipokuwa kuna namba maalumu ambayo hutofautisha kuwa hili ni la wapi na lile ni la wapi…”

“…Enhe, hilo lilikuwa na namba za wapi?” Gina akadakiza swali kwa shauku.

“Lile halikuwa na namba ubavuni, na tumefatilia kwenye camera za barabarani tumeliona likielekea nje ya mji wa Saratov ambako kumejawa misitu tu…”

“…ametekwa, lazima tukafunge kazi,” Chiba akawaambia.

“Kama ametekwa, basi yuko mikononi mwa Barbier…” Laabib akasema.

“Barbier!” Chiba na Gina wakatamka kwa pamoja.



Msitu wa Kumysnaya Polyana


Barbier, mwanamke katili, alisimama mbele ya Amata aliyekuwa amefungwa barabara. Macho yake makali yalikuwa makini kumtazama kijana huyo. Kamanda Amata alikuwa kimya, ingawaje aliteswa kwa kipigo kikali lakini alibaki hivyo pasi na kujibu swali lolote aliloulizwa.

“Endelea kuwa bubu hivyo hivyo… umeshatelekezwa, na humu hutoki. Aliyekuelekeza amekuingiza kuzimu kwenye shimo la mauti, si kwamba alikusaidia. Dimitri ni mshirika wetu na tumemuweka pale makusudi kabisa,” akamwambia Amata huku akitembeatembea ndani ya chumba kile kichafu na cha kuogofya. Kuta zake zilichafuka kwa damu ya biDanamu, sakafu nayo iliganda damu ya muda mrefu. Harufu nzito iliyotokana na damu hiyo ilikijaza chumba hicho. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na makolokolo mengi na kukifanya kionekane kana ghala. Amata aliyavumilia yote. Kukaa ndani ya chumba hicho kwa siku saba haikuwa rahisi.

“Leo ndiyo mwisho wako… na huyo mjinga mwenzio Dimitri anakuja hapa kuungana nawe maana anajifanya anajua sana,” Barbier akasema. Sekunde chache baadae, Amata akasikia kelele za mtu anayelia kwa uchungu huku akitukana matusi yote ya Kirusia. Sauti ile haikuwa ngeni sana kwake. Hisia zake hazikukosea. Mita chache mbele yake, Dimitri aliangushwa vibaya na kupigiza uso chini.

“Shiiit!” Amata akatamka kwa sauti ya kichovu. Vijana wa miraba mine, watatu wakafuatia nyuma yake. Wakamwinua Dimitri na kuanza kumsulubu kwa makonde mazito mazito yaliyotua tumboni na kifuani. Dimitri alitapika damu nyingi sana, macho yake yalimtazama Amata kuomba msaada lakini minyororo iliymfunga mikononi na miguuni ilimkatisha tamaa.

“Stop!” Barbier akawaamuru. Wale vijana wakamwacha Dimitri. Akaanguka chini na kulala kimya. Barbier akachutama na kumgeuza kwa kumshika ukosi wa shati lake. Dimitri alikuwa kimya kabisa. Akampapasa kwa mkono wake maeneo ya shingoni, kisha akamtazama Amata, “Bado ana uhai kidogo unaoweza kumfikisha masaa matatu yajayo, hah hah hah…” akatoa cheko lake la kifedhuli. Sekunde chache zilizfuata, akanyamaza na kubadilika sura.

“…saa ya hukumu,” akasema na kutoa tabasamu baya na la kuchukiza. Kamanda Amata alihisi kakutana na shetani. Sura ya mwanamke huyu ilimfanya kusadiki kuwa watu-majini wapo duniani.

Nitakuua vibaya wewe mwanamke shetani! Amata akawaza kwa hasira. Chuki ndani ya moyo wake ikajijenga na kufanya donge kubwa la gadhabu liuzunguke moyo wake. Amata alipogeuza sura kuwatazama wale vijana waliokuwa wakimsulubu Dimitri, akapata ganzi kidogo. Hakuyaamini macho yake yaliyovimba kwa kipigo na kufumbwa kwa damu iliyoganda huku akiachiwa eneo dogo la kuweza kuona. Kati ya wale vijana alikuwapo mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni kabisa. Akajaribu kuvuta kumbukumbu ya wapi amemuona kijana huyo ambaye daima alikuwa akikwepesha kukutana macho na Amata.

Take care! Sauti hii ikamrudia tena. Akamkumbuka, ni yeye aliyemtamkia neno hili pale katika Casino la Pharaon. Mmoja wa walinzi wa Dimitri katika casino lile. Akamtambua bila kificho.

Alijua nini kitanipata, alijua kila kitu. Dimitri ameuzwa na watu wake, ama kweli kikulacho ki ng… Hakumaliza hata kuwaza huko, akashtushwa na taa kali zilizommulika usoni.

“Tungeweza kukuua muda mrefu sana, lakini tulikuacha ili ipatikane saa maalum ambayo wapendwa wako watashuhudia kifo chako kwa njia ya mtandao,” ilikuwa ile sauti kavu ya mzee Ivan, Colonel muasi wa jeshi la Urusi. Sauti yake ilitangulia kabla ya yeye kufika. Barbier akamwendea mzee huyo na kumvua koti la ngozi alilokuwa amelivaa. Moyo wa Amata ukaanza kudunda mfululizo bila mpangilio, kifo kilikuwa dhairi shahiri mbele yake. Minyororo yenye nguvu ilimdhibiti asiweze kufanya lolote. Mbele yake kukasogezwa kitu kama beseni kubwa la kioo ambalo mwaDanamu mwenye urefu wa futi sita angeweza kusimama wima ndani yake. Beseni hilo lilikuwa juu ya kifaa maalumu chenye magurudumu na lilisogezwa pale kwa kuongozwa na mitambo maalumu. Ndani ya beseni lile kulikuwa na kimiminika ambacho Amata alikitazana na kutokuelewa ni cha aina gani. Kijana mwingine, akatega camera ili kuchukua matukio yote. Kompyuta iliyokuwa juu ya meza ndogo ilionesha kuwa matukio yale yanatazamwa mubashara sehemu fulani. Ivan akakusanya mikono yake kifuani na kumtazama Amata.

“Hii ni kemikali itakayotumika kukuteketeza na hutoonekana duniani isipokuwa nguo zako tu ulizoziacha Tanzania. Kwa mkono wa Ivan utateketezwa mwili na roho… kisha ndugu zako watashuhudia mapinduzi yenye umwagaji damu mkubwa katika nchi yako,” akamwambia. Ivan akachukua pande la nyama kutoka katika chano iliyokuwa imeshikwa na kijana mwingine. Akalitumbukiza ndani ya lile beseni. Pande lile la nyama likateketea taratibu na kupotea kabisa. Na kemikali ile ikanbaki safi kama mwanzo. Ni kitendo cha dakika mbili tu jambo lilifanyika.

“Mwili wako utateketea namna hii baada ya ule wa Dimitri,” Ivan akamwambia Amata. Akasogea pembeni na kumpisha Barbier. Mwanamke huyu akatoa amri Dimitri atumbukizwe kwenye ile kemikali.

Ni kemikali hii ilitumika kumteketeza Dastan na mkewe? Amata akajiuliza huku akihema kwa nguvu. Bila kificho, alijua wazi kuwa mwisho wa maisha yake umefika.



Juma moja baadae


Ndani ya Ofisi ndogo timu nzima ya TSA ilikutana kwa kikao kifupi. Ni mara chache sana Madam S kukutana na vijana wake wote kwa pamoja. Mara nyingi hukutana ama na mmoja mmoja au wachache wao kwa sababu maalum.

Siku hii, ikiwa ni juma moja tu tangu Kikosi cha wokovu kilichoundwa na watu watatu; Gina,

Chiba na mwanausalama wa ubalozi wa Tanzania huko Urusi, Laabib, kuiangusha sehemu ya ngome ya Colonel Ivan Chernyakhovsky, Madam S aliwaita kwa kikao cha pamoja. Mara hii ilionekana wazi kuwa kazi inayowakabili si ya mtu mmoja mmoja tena bali ya wote kama timu.

“Tumefikia pazuri…” Madam S akawaambia vijana wake ambao kila mmoja alikuwa kimya katika kiti chake, “hatua chache zijazo, ukweli uliojificha utajulikana”. Aliposema hayo akawatazama kwa zamu. Vijana wake wote walionekana kuwa katika umakini wa hali ya juu kusikiliza nini kitasemwa na mwanamama huyu, mwanamke wa chuma, kama wao walivyomwita. Akaendelea kusema, “nyote mnajua kuwa bado tupo kwenye kutekeleza hukumu ya kifo ambayo genge hatari lililotaka kuipindua serikali ya awamu ya kwanza mara mbili kama si tatu lilihukumiwa kwayo. Tumefanikiwa kuangusha watu wawili, bado wawili. Lakini punde tu tutakamilisha kazi hiyo. Sasa nimewaita hapa ili kupata taarifa za tafutishi zetu ambazo kwa pamoja tutazichambua ili zitupe mwanga wa kusonga mbele. TSA 2, endelea…”

TSA 2, Chiba wa Chiba, akajiweka tayari kitini mwake na kufungua laptop yake. Kitendo hicho kiliwafanya kila mmoja kuvuta kabrasha lilil mbele yake, lililosomeka kwa maandishi makubwa ‘GENGE’ na kulifunua ndani yake. Chiba alieleza kwa ufasaha sana jinsi ambavyo operesheni hiyo inaendeshwa kwa usiri na utaalamu wa hali ya juu. Kila mmoja alikubaliana naye kwa kile anachokisema.

“Na kilichotufanya tuwe hapa sasa si haya niliysema ambayo yapo kwenye kurasa kumi za kwanza za kabrasha hilo. No! ninachotaka kukisema na kilichotuleta hapa ni kuwa Kibwana Mtokambali aliyekuwa Waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na James Msambamagoya ambaye alikuwa mwanausalama wa juu kabisa ndani ya Ikulu ya Magogoni, wapo hai na uhai wao,” Chiba akaeleza. “Naomba tufungue ukurasa wa kumi na moja…” wote wakafungua kwenye yale makabrasha. Katika ukurasa huu kulikuwa na picha ya mwanaume, mzungu, mtu mzima. Ukurasa uliyofuatia ulionesha picha za Mzungu yuleyule akiwa katika mavazi ya kijeshi na kiraia, picha zilionesha utofauti wa miaka zilivyopigwa.

“Huyu anaitwa Kanali Ivan Chernyakhovsky. Alikuwa mwanajeshi mahiri wa jeshi la Urusi, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani na nje ya jeshi la Urusi. Amekuwa mwanausalama asiyeonekana wa KGB ndani ya jeshi hilo, na ndiye aliyefanikisha uvamizi wa eneo la Mashariki mwa Ukraine na kuiteka rasi ya Crimea. Ivan amekuwa mfuasi mkubwa wa falsafa ya kimapinduzi ya Lenin. Ameshiriki kubomoa serikali nyingi za nchi za dunia ya tatu na kuweka vibaraka wao. Na katika hili ndipo alipoifikia Tanzania miaka hiyo ya themanini akirithi mafaili na mafaili ya waliomtangulia…” akanywa maji kidogo, na kuendelea, “katika ukurasa wa kumi na tatu…” wakafunua, “tunaona akiwa pichani na bwana Kibwana Mtokambali… mara tu baada ya kupata uhuru, serikali yetu ilianza kupeleka vijana katika mafunzo tofautitofauti ili kuja na kuwa viongozi wa kuijenga nchi. Mwaka 1975 Mtokambali akiwa kijana aliyeaminiwa sana na Mwalimu, akapelekwa Urusi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa mambo ya kiusalama, na hapa ndipo alipokutana na Ivan na kuwa marafiki wa kutupwa akimlisha sumu kali za kimapinduzi. Aliporudi nchini na kushiriki vita vya Kagera, ndipo naye alipowalisha sumu ileile vijana watiifu wa jeshi. Miaka miwili baada ya vita tukashuhudia wakitaka kupindua serikali. Ivan ndiye tuliyemgundua kwa jina la Sebastiano Moznich. TSA 1 akiwa tekoni, anasema alipotaja jina hilo huyu mzee alishtuka”. Alipofika hapo kila mtu alichukua kalamu na kuanza kuandika kitu fulani katika kabrasha lile isipokuwa yeye na Amata tu. Chiba akatulia kimya na kumtazama Madam S.

“Nafikiri mpaka hapo mmepata picha ya nani tunapambana nao. Ili kumpata Kibwana Mtokambali na James Msambamagoya imebidi tupambane na huyu mtu. Amata shahidi kwa kuwa ameonana naye uso kwa uso. Anamwelezea kama mtu mmoja makini sana ambaye akizungumza jambo akili yake huwa nusu saa mbele ya wote. Mtu hatari! Lakini eleweni kwamba hakuna mtu hatari katika mikono ya TSA… Chiba endelea,” Madam S akasema na kumruhusu Chiba kuendelea na taarifa yake.

“Ukurasa wa kumi na nne,” akawaambia, nao wakafunua. Kwenye ukurasa huu kulikuwa na picha ya mwanamke katika sura mbalimbali za ujana na utu uzima. Gina akatikisa kichwa juu chini na kumtazama Chiba. “Huyu mwanamke Mrusi anajulikana kwa jina moja tu, Barbier. Barbier ndiye kibaraka wa Ivan, amemfundisha upiganaji na uuaji tangu akiwa msichana mdogo. Sasa ni muuaji asiyeogopa kitu. TSA 1 anakiri na anasema ‘anakuua huku anatabasamu, ana mikono ya chuma na kucha ngumu kama misumari’”. Wakacheka wote kwa sifa hiyo. “Huyu mwanamke tumegundua kuwa, japo hatuna uhakika, ndiye aliyemuua Dastan Kihwelo kwa kumtumbukiza kwenye kemikali mbaya kabisa inayoyeyusha nyama na mfupa,” Chiba aliongea kwa msisitizo, kila mmoja akajikuta akikunja sura. “Nimefanya utafiti wa kina, huyu mwanamke alifika Tanzania mwaka 1991katika harusi ya Dastan na ndiye aliyeendesha operesheni ya kumteka Dastan na mkewe akishirikiana na Brian ambaye tayari ni marehemu. Haya mnayoyasikia tumeyapata katika nyumba ile namba 73A ya Mtaa wa Galu, tuliigundua nyumba hiyo baada ya kupata lile kabrasha la ‘SIRI’ katika chumba cha marehemu Dastan,” Chiba akakatishwa na Jasmin aliyepiga meza kwa kofi lake. Hii ilikuwa ni ishara yao kwa mtu anayetaka kusema jambo katika vikao kama hivyo.

“Unataka kutuambia kuwa Dastan ameuawa na tuondoe dhana kuwa ametoweka?” Jasmini akauliza.

“TSA 3, upo sahihi kabisa. Dastan ameuawa ila mkewe ndiyo hatujui mpaka sasa…” Chiba akajibu.

Dastani amekufa, nina uhakika kwa kuwa ametekwa leo jioni na mbinu zangu za kumwokoa zimefeli. Dastani amekufa! Wengi watasema ‘ametoweka’ lakini mimi nasema amekufa. Madam S akajikuta anaikumbuka kauli ya Chameleon aliyomtamkia miaka kadhaa nyuma walipokuwa wawili tu ndani ya ofisi ya siri. Akamtazama Chiba alipokuwa akisisitiza kauli hiyo. Kamanda Amata naye akapiga meza kwa mtindo uleule.

“Wale jamaa hawafai, wanakuyeyusha kwenye kemikali unatoweka kabisa duniani…” Amata akakazia. Wote wakamtazama maana tangu kikao kianze hakuwa ameongea chochote. Baada ya hapo masikio yakarudi kwa Chiba.

“Katika kurasa ya kumi na tano ndipo tunapopata uthibitisho kuwa Mtokambali yuko hai. Rekodi za sauti za hotuba zake ambazo nilizichukua pale RTD kwa maagizo ya HOT, nimezioanisha na sauti za simu zilizokuwa zikipigwa kwenye nyumba namba 73A, na crossmatch yake imeshahabiana kwa asilimia themanini na tano. Hilo la kwanza, la pili, ni kutoka katika huu mkufu,” akauchomoa mkufu kutoka katika mkoba wake na kuuning’iniza mkononi.

“Huu, kifuani mwa Barbier haukuwa mkufu kama mkufu bali ni kifaa cha teknolojia ya kisasa sana kilichohifadhi zaidi ya makabrasha elfu kwa maelfu. Ndani ya mkufu huu ambao TSA 1 ameuleta tumebaini mpango mzima ulivyopangwa na jinsi unavyopangwa kutekelezwa ndani ya ardhi yetu wenyewe. Katika kurasa ya kumi na sita mpaka kumi na tisa, inatudihirishia kuwa Mtokatambali na Msambamagoya wamefanyiwa upasuaji wa sura zao na kuvikwa sura nyingine na kuwabadili hapa na pale ili wasitambulike kiurahisi. Na zoezi hili limefanyika katika kliniki binafsi ndani ya jiji la Athens huko Ugiriki. Kwa maana hiyo hawa watu wawili wapo, si ajabu wapo Kariakoo au Magomeni au popote pale. Tutawapataje?” Chiba akaishia hapo, na lile kabrasha likawa limeishia pale, zaidi ya hapo kukawa na kurasa kumi nyingine zisizo na maandishi. Ndani ya mkufu ule wa Barbier kulikuwa na makabrasha mengine mengi na mazito ambayo ilikuwa ni vigumu kwa macho ya kawaida kuhimili kuyasoma kabla hayajapofuka.

“Ili kuzuia kila lililopangwa, tuna mambo matatu ya kufanya,” Madam S akasema, “mosi, Mtokambali na Msambamagoya lazima watambulike, pili, watekelezewe hukumu yao kama ilivyokuwa kwa Mwakibinga na Mwanachia, tatu, mpango wa mapinduzi ulioainishwa katika moja ya makabrasha hayo na ambao utekelezaji wake unatakiwa ufanyike mara moja lazima ukomeshwe. Kazi hii inatakiwa ifanyike haraka na kwa umakini wa hali ya juu sana… Hili genge lifutiliwe mbali,” Madam S akawaambia vijana wake.

“Ivan na huyo mwanamke shetani hawajafa! Na kama wao ni wafadhili wa mpango huu basi lazima nao wafutiliwe mbali. Nina uhakika ngome ya Saratov tumeisambaratisha. Na nina uhakika pia kuwa kuna ngome ya siri ambayo hawa watu wawili wamehifadhiwa, hii ndiyo ya kuitafuta. Chiba lazima tukae chini tuchambue hayo makabrasha mpaka tujue hawa wawili wamejificha wapi, kwa sura gani. Lazima tuiokoe Tanzania na watu wake kwa mara ya nyingine,” Amata akaongea kwa uchungu. Madam S akabaki kimya kumwangalia kijana huyo akiongea. “Wale washenzi wana siri nyingi sana sana sana na nina uhakika katika huo mkufu kuna mambo mengi ambayo hatujayaelewa. Madam, nafikiri tupatie siku kama nne hivi tuendelee na kufukuafukua mengine kama tutapata, na kuyaelewa,” akamalizia.

“Sawa, nawapa hizo siku nne, tukutane hapa tu nitakapowaita. Kwa sasa kila mmoja aendelee na majukumu yake ya kawaida,” Madam S akafunga kikao na kuagana na vijana hao.

* * *

“Wameweza kuigundua ngome yetu?” Ivan akamuuliza Barbier aliyekuwa kitini huku uso wake umesawajika kwa mawazo.

“Hata sijui… najaribu kutafakari sipati jibu,” Barbier akajibu. Mara tu baada ya kufanikiwa kutoroka eneo lile, Ivan na Barbier walijificha kwenye nyumba nyingine ndogo iliyopo nje kidogo yam situ ule wa Kumysnaya. Wakiwa katika nyumba hii, Ivan alirusha camera ndogo mfano wa nyuki na kuweza kufuatilia kila kinachoendelea katika nyumba yake hiyo iliyofumuliwa vibaya kwa bomu la kutegwa. Juma hili, lilikuwa gumu sana kwa wawili hawa, wakiwa wamepoteza vitu viwili vikubwa; ngome na mkufu wenye siri nyingi sana.

“Nani alikuwa anajua kama mkufu wako una nyaraka zetu za siri?” Ivan alimuuliza Barbier.

“Sijui kwa kweli, maana ni mimi na wewe tunaolijua hili. Isitoshe hawawezi kufanya chochote na mkufu ule. Kila kabrasha limefungwa kwa kodi ngumu kuzijua…”akaeleza.

“Mmmmhhh sawa, ila dunia ina mambo mengi, lazima tuhakikishe hizo data hawazipati,”

Ivan akasema, “kwa sasa hatutakiwi kuwa hapa, mpango mkuu wa kimapinduzi huko Tanzania lazima ufanyike si kwa matakwa yao ila lazima sasa tushike usukani wenyewe na ndani ya miezi mitatu hii, damu lazima imwagike. Tuondoke, twende nje ya bara la Ulaya tukapange mipango,” Ivan akamwambia Barbier. Saa chache baadae walikuwa kwenye ndege binafsi wakielekea kusikojulikana.

Tukio la kugundulika na kusambaratishwa kwa ngome ya Ivan huko Saratov lilimfanya mzee huyo aamue kubadili mipango yake. Liliiwasha hasira yake na kumfanya aanze kupanga mipango ya siri kabisa kichwani mwake. Daima, msiri wake alikuwa Barbier, aliyemtuma hapa akaue au pale akadhulumu. Na kazi zote hizo alizifanya kwa umakini wa hali ya juu kiasi kwamba vyombo vya usalama vingi duniani vilimshuku lakini havikupata ushahidi wa kumtia hatiani. Kila alikopita, mwanmke huyo hakuacha nyayo. Ni mara hii tu Ivan alipoanza kupata wasiwasi wa mipango yake kwenda kombo. Akaanza kuwahofia wanausalama wa Tanzania. Habari alizokuwa akizikia aliziona kama riwaya tu lakini sasa alijikuta jasho likimtoka.

Wapi nimekosea? Alijiuliza kila wakati tangu ngome yake ya siri ilipovamiwa na kusambaratishwa.

Private Jet iliyowabeba Ivan na Barbier iliendelea kukata anga kuelekea upande wa Kusini Maghalibi mwa dunia. Wakati Ivan akiendelea kuperuzi katika kompyuta yake, Barbier alikuwa akitafakari jinsi maisha yalivyomuwia magumu sekunde chache alizokuwa akipambana na Amata na jinsi alivyotumia ufundi na muda mfupi kuuondoa mkufu shingoni mwake. Akajikuta akisonya na kujiapia kama akikutana naye tena basi atahakikisha anamtunukia kifo kibaya sana.




Private Jet iliyowabeba Ivan na Barbier iliendelea kukata anga kuelekea upande wa Kusini Maghalibi mwa dunia. Wakati Ivan akiendelea kuperuzi katika kompyuta yake, Barbier alikuwa akitafakari jinsi maisha yalivyomuwia magumu sekunde chache alizokuwa akipambana na Amata na jinsi alivyotumia ufundi na muda mfupi kuuondoa mkufu shingoni mwake. Akajikuta akisonya na kujiapia kama akikutana naye tena basi atahakikisha anamtunukia kifo kibaya sana.

* * *

Big J akamtazama Mc Tee, akajikuta anakosa nguvu ya kusema neno na kubaki kimya tu. Wawili hawa walikuwa ndani ya jengo moja refu katika jiji la Port Louis huko Mauritius. Ilikuwa ofisi ndogo, ya kisasa, iliyosheheni samani za kupendeza. Picha mbalimbali zilikuwa zimetundikwa ukutani kwa ustadi mkubwa. Picha za viongozi, na watu mashuhuri duniani. Ni picha moja tu ilikuwa ya mtu asiyejulikana, kijana, mweusi, aliyevalia suti ya Kaunda, mwenye macho dadisi. Kila picha ilikuwa na jina kasoro hiyo tu. Ubora wa picha hiyo ulionesha wazi kuwa si picha iliyopigwa kwa kamera ya kisasa bali ni teknolojia ya nyuma kabisa. Inaweza kuwa ya miaka ya themanini au hata sabini huko. Wawili hawa, maswahiba wa damu walikuwa ndani ya jengo la Telecom Tower katika jiji hilo la Port Louis. Simu ya Big J ikapokea ujumbe mfupi wa maneno. Akainyakuwa kutoka juu ya meza na kuusoma.

Labourdonnais Waterfront Hotel, 1600hr

Big J akainua mkono wake na kuitazama saa yake ya mkononi. Bila ubishi, ilimwonesh kuwa ni saa tisa na dakika hamsini. Akamtaarifu Mc Tee aliyekuwa kimya muda wote.

“Tutatumia muda gani na sasa tuna dakika kumi tu?” akauliza.

“Si mbali kutoka hapa, ni mwendo wa dakika tano au sita kwa gari,” Big J akajibu huku akitungua koti lake na kujituypia mwilini. Mc Tee naye akafanya vivyo hivyo. Wakachukua lifti na kuteremka chini kutoka ghorofa ya kumi na moja. Kwa kupitia Mtaa wa D’Entrecasteaux na Caudan Access waliifikia hotel hiyo kwa dakika kama sita hivi. Mara tu walipowasili wakakaribishwa na kuongozwa na mhudumu mpaka katika chumba maalum chenye viti vinne tu. Sekunde ishirini na saba tangu waketi chini, Mzee Ivan na mwanamke Barbier wakawasili katika chumba hicho. Vinywaji vikali vikaletwa katika chumba hicho ili kutuliza makoo yao.

“Mmeona kilichotokea Kumisnaya?” Ivan akawauliza, na wote wakatikisa vichwa, “hii inaashiria tunaenda kuharibikiwa mipango katika miezi mine ijayo. Kwa sababu kadiri siri zetu zilivyokaa itawachukua miezi mine kuweza kugundua mipango yetu. Miezi minne kwa sababu ya udhaifu wa kiintelijensia huko Tanzania. Kama ingelikuwa CIA ningesema juma moja tu watakuwa wamegundua tulipo. Haya yote ni ninyi mnasababisha!” akaongea kwa hasira. Kila mtu alinyamaza. “Kwa maana hii, inabidi ndani ya miezi mitatu tuwe tumeshaangusha serikali ya Tanzania kwa kuilazimisha ifanye uchaguzi kabla ya wakati,” akaongeza kusema kisha akajiegemeza kitini. Barbier akachukua chupa kubwa ya GIN na kummiminia bosi wake.

“Kuilazimisha kufanya uchaguzi, kivipi? Na uchaguzi ni mwakani tu,” Big J akauliza.

“Wewe ni mwanausalama, umefanya kazi hiyo kwa miaka na miaka, unashindwaje kunielewa? Alichotakiwa akifanye Komandoo Jairosi Simbamwene, sasa kinatakiwa kitekelezwe ndani ya siku tisini. Hatuna budi kutekeleza item namba 117 katika kabrasha la sitini na tano. Wanunuliwe wanajeshi kadhaa wenye kujiamini si kama wa wakati ule. Wapewe sumu ya mapinduzi kisha kitakachofanyika ni coup detant. Mwenye serikali anatiwa risasi ya kichwa na wale wanajeshi wanamweka chini ya ulinzi Makamu wa Rais, Spika wa Bunge na Jaji mkuu. Mkuu wa majeshi alikadhalika, kisha wale vijana wetu wanakuwa tayari, mara tu kazi ikianza wanaiteka RTD na hapo tunatangaza ushindi na nchi inakuwa mikononi mwetu. Kazi ndogo ya kuifanya kwa siku saba hadi kumi tumemaliza,” Ivan akaeleza mpango mzima na wote wakauafiki.

“Ninautilia shaka mpango!” Mc Tee akasema.

“Kivipi?” Ivan akauliza mshangao ukiwa wazi usoni mwake.

“Kwa kuwa watu wanaoratibu safari za Rais kwa sasa wako na umakini wa hali ya juu sana…”

“Usitie shaka, hilo niachie mimi… siku kumi na nne zijazo mzigo wetu wa kwanza utafika kisiwani, pale kwa Mc Tee, tayari kufanya ugavi,” Ivan akamjibu.

“Sawa!” Mc Tee na Big J wakajikuta wamejibu kwa pamoja. Ukimya ukatawala kwa sekunde kadhaa kati yao. Mara Mc Tee akajikohoza ili kusafisha koo, ishara ya kutaka kusema neno.

“Colonel Ivan, nimekuelewa vizuri sana… mimi sina shaka na hilo na nipo tayari. Naahidi kuifanya kazi hiyo kwa miezi miwili kama nitachelewa sana,” akamwambia.

“Nahitaji maamuzi kama hayo! Maamuzi ya kiume… miezi mitatu ijayo tunatakiwa tumtangaze Rais wetu,” Ivan akaongezea kusema.

Kikao cha wanne hawa kilikamilika kwa kuweka mipango yote sawa kwa kupindua ile ya kwanza ambayo ilisheheni katika ule mkufu wa Barbier. Ivan alielewa wazi kuwa kama adui zake wataweza kutegua kitendawili kile basi watachukua miezi minne kuzuia mapinduzi. Na hii miezi minne ni kwa wale wenye weledi wa hali ya juu katika medani za kijasusi. Yeye kwa akili yake pevu, ya kijasusi aliamua kubadili mpango, akaufupisha ili utekelezeke ndani ya miezi mitatu tu. Huyu ndiye Ivan, mwanajeshi muasi wa jeshi la Urusi, asiyetabirika. Amefanikisha mipango yake mingi ya kiuhalifu kwa kubadili mbinu dakika ya mwisho. Ivan Chernyakhovsky.

Wakiwa wamekwishaagana na watu wake, Ivan akamwita karibu Barbier na kumnong’oneza, “futa nyayo zote kokote tulikokanyaga kuhusu swala hili”.

“Sawa!” akajibu.

* * *

“Huu ni mpango kabambe aisee!” Chiba akamwambia Amata wakati wakiwa Shamba, wawili tu, wakichambua makabrasha waliyoyaprinti kutoka kwenye ule mkufu.

“Ndiyo hivyo, kiukweli hapa tulikwama ila Dimitri, Mungu amrehemu… alinambia ‘siri ya mwanamke yule ipo kifuani mwake’, nilitafakari na kumwelewa vyema ana maana gani. Nilipokuwa napambana naye nia yangu ilikuwa ni huu mkufu tu,” Amata akamjibu Chiba. Juu ya meza, mbele ya Amata kulikuwa na karatasi kama tano hivi ambazo alizitandaza. Macho yake yaliikodolea karatasi mojawapo. Karatasi ile iliprintiwa kutoka katika kabrasha namba ishirini na tano lililoandikwa kwa mtindo wa kuficha au kuchengesha herufi za neno ama kwa kutumia namba au kuzigeuzageuza au kuzibadili nafasi zake unaojulikana kama Cipher. Hili lilimvutia Amata, hata macho yake yote aliyahamishia hapo.

“Kaka vipi, mbona umenyamaza ghafla?” Chiba akauliza.

“Kuna kitu hapa! Ciphertext imetumika kuficha jambo nyeti sana…”

Chiba akasogea kutazama hicho kinachosemwa na Amata. Naam, macho yake yakapokewa na kile alichoambiwa.

“Subiri!” akamwambia Amata. Hatua tano zikamfikisha kwenye rafu ya vitabu. Akagusa hiki na kuacha kile. Mwishowe akachukua kitabu kikubwa kilichoandikwa siri mbalimbali za lugha za kijasusi. Chiba akakibwaga mezani kisha wote wawili wakaanza kukipitia kuona kama wanaweza kung’amua chochote. Haikuwa rahisi kama unavyofikiri.

“Pamoja na kusoma kwangu vitu hivi lakini hapa najikuta nagonga ukuta,” Amata akasema.

“Tunafanyeje sasa?” Chiba akamuuliza Amata huku akiegemea kiti chake. Amata akashusha pumzi na kuzitupia macho zile karatasi kwa mara nyingine.

“Kazi ipo!” Amata akasema na kuchukua simu yake kutoka mfukoni. Akabofya dijiti kadhaa na kuiweka sikioni. Upande wa pili ikapokelewa.

“HOT hapa!” ikajibiwa.

“Tumekwama katika ciphertext na plaintext, msaada tafadhali…” Amata akamwambia HOT, yaani Madam S.

“Nilikwambia, ipo siku utakutana na hicho kitu, ukaona nakutania… umekwama! Haya mfike hapa Ofisi ndogo haraka na hayo makabrasha,” Madam S, kutoka upande wa pili akawaambia. Chiba na Amata wakakusanya zile karatasi na kuzitia kwenye bahasha. Safari kuelekea Ofisi ndogo ikaanza.

Iliwachukua dakika arobaini na tano kufika katika ofisi hiyo. Wakamkuta bosi wao akiwasubiri kwa shauku. Moja kwa moja wakabwaga yale makaratasi mezani. Madam S akachukua na kuyatazama haraka haraka, akayapanga la kwanza mpaka la mwisho. Akabaki kimya kwa sekunde kadhaa huku akiyabadili la juu kwenda chini na linalofuatia kuwa juu. Macho ya Amata daima yalikuwa yakiusoma uso wa mwanamama huyo na kugundua kuwa akisomacho kilikuwa ni siri nzito.

Alipomaliza akawatazama vijana hao kwa zamu. Uso wake ulionekana wazi kuwa una jambo la kusema.

“Ni yale yale mliyoyasoma mwanzoni… Kibwana Mtokambali na James Msambamagoya wapo hai… na matekelezo ya kuipindua serikali yako palepale,” akasema.

“Unasema?” wakajikuta wanauliza kwa pamoja.

“Hivyo mlivyosikia ndivyo… katika haya maandishi inaeleza kuwa hawa jamaa wapo hai isipokuwa wamefanyiwa upasuaji wa kubadili sura zao na kuwapandikizia hata nywele ili wapoteze muonekano wao. Taarifa hii inaeleza kuwa hawa watu wawili, mmoja wao yupo hapahapa Tanzania na anaendesha shughuli zake hapa…” Madam S akaeleza.

“Ina maana ni taarifa ileile ya kwanza? Kwa nini waindike kwa lugha ya kificho…”Chiba akasema.

“Kwa vyovyote, kuna jipya. Naendelea kusoma…”

“Shiiiit! Ina maana bado wapo katika mpango uleule?” Amata akauliza.

“Inawezekana sana, lakini tutamtambuaje au tutawatambuaje? Ni mpaka tupate sura zao mpya ikiwezekana na utambulisho wao mpya…”

“Kazi mpya inaanza…”

“Na lazima kitendawili kiteguke” Madam akaongeza.

Amata akatazamana na Chiba, kisha wote wawili wakageuza sura zao kumtazama Madam S. Amata akashusha pumzi ndefu zilizoashiria jambo.

“Vipi?” Madam akamuuliza.

“Huu ni mpango kabambe sana…” akasema na kutulia kwa sekunde chache, “endelea kuidadavua labda nitagundua jambo,” akamaliza. Madam S akaendelea kupitia zile karatasi ambazo ziliandikwa lugha isiyoeleweka.

“Dr. Prakesh Chamarakuz!” akatamka. Chiba akachukua ubamba wake na kuanza kuperuzi kitu katika mtandao.

“Gleneagles Global Hospital,” Madam S akatamka tena. Akakusanya yale makaratasi na kuyaweka kando. “Vingi nimevielewa ila nahitaji muda kuviweka pamoja. Lakini mambo matatu ya msingi ya kuzingatia na kuyajua ni hayo. Mosi, Dkt. Prakesh Chamarakuz, ndiye surgeon aliyefanya kazi hii miaka mingi nyuma. Sijui kama ni mzima au amekufa. Pili Gleneagles Global Hospital ndiyo iliyotumika kutekeleza kazi hiyo na tatu, hawa watu wapo hapa nchini. Sasa cha kufanya ni lazima tujue sura gani wamepewa, na mwonekano walio nao kwa sasa…” Madam S akawaambia. Kamanda Amata alikuwa kimya kabisa akisikiliza. Chiba akauweka ule ubamba mezani, juu katika kioo kulikuwa na picha ya mzee wa Kiindi, aliyevalia koti jeupe la kidaktari na stethoscope shingoni mwake. Amata akauchukua ule ubamba na kutupia macho. Maandishi machache yaliyoisindikiza ile picha yalimweleza Daktari Chamarakuz kuwa ni bingwa katika aina hiyo ya upasuaji, upandikizaji na utengenezaji wa sehemu mbalimbali za mwili wa biDanamu. Wasifu wake ulitosha kumweleza kuwa ni daktari bingwa kabisa ulimwenguni. Amata akatikisa kichwa.

“Nahitaji kufika India… hatuwezi kupiga hatua kama hatujapata sura halisi za watu hawa kwa sasa…” akasema huku akirudisha ule ubamba kwa Chiba.

“Panga kila kitu chako, unipe taarifa saa nne zijazo,” Madam S akamaliza na kuwaaga vijana wake. Dakika tano zilizofuata, alibaki pekee ofisini humo. Akachukua zile karatasi na kuzisoma tena kwa makini. Ijapokuwa alikuwa anafahamu sana kusoma na kuandika aina hiyo ya lugha ya kificho lakini safari hii alijikuta akisoma maandishi ya mtu aliyebobea kwenye kazi hiyo. Akainua simu yake na kubofya tarakimu kadhaa kisha akaiweka sikioni.

“Njoo ofisi ndogo haraka!” akakata simu na kuirudisha mezani.














Chiba aliwasili ofisi ndogo kama alivyotakiwa na Madam S. kikao cha wawili hawa kilifanyia saa moja baada ya kile cha wote. Mara tu baada ya kuingia ndani ya ofisi ile alimkuta Madam S akiwa katulia kitini kwake huku meza yake ikiwa imejaa yale makabrasha aliyokuwa akiyasoma.

“Nimeitika wito,” akamwambia Madam.

“Vizuri, tusipoteze muda… katika kuendelea kupitia hizi tafutishi kuna codes nimekutana nazo, nahitaji uzitambue kwa haraka sana. Wameweka tovuti ya kutumia ila nahisi zitakuwa na nywila za kufungulia,”

“Hiyo kazi ndogo,” Chiba akajibu. Baada ya kutajiwa aina hiyo ya codes akainakili pembeni pamoja na ile tovuti ambayo kwayo angeweza kupata jibu. Akajaribu kwenye kompyuta yake ndogo. Kama alivyosema Madam S, alihitajika kuweka Jina tumizi na nywila. Akajaribu kuidanganya kwa kuweka majina ya uongo lakini mtandao ule uligoma. Baada ya takribani dakika kumi na tano, akapata wazo la kutumia jina la Barbier, akaingiza kama jina tumizi, ikakubali. Nywila ikawa ni tatizo lingine, hakukubali.

Chiba alikuwa jasusi mzuri wa mtandao, baada ya kuzipat kodi za tovuti hiyo akazitumbukiza kwenye mtandao wake anaotumia kuvunja vifungo vya mitandao kama hiyo. Bado hakuweza kuona chochote. Akamtazama Madam S.

“Vipi?” Madam akauliza.

“Jamaa wakali, kila mbinu nimeshindwa, inabidi nitulize akili. Ila mzuie kwanza Amata asiende India, tunaweza kupata jibu hapahapa,” akamjibu.

“Of coz nimeshamwambia asubiri kwanza… nafikiri kwenye hizo kodi kuna siri nyingine kubwa,” Madam S akaeleza na Chiba akaitika kwa kutikisa kichwa, “kwa hiyo tunafanyaje?” akamwongezea swali.

“Nipe dakika chache,” Chiba akasema kisha akachukua simu yake na kuwasiliana na mtu mwingine.

* * *




Of coz nimeshamwambia asubiri kwanza… nafikiri kwenye hizo kodi kuna siri nyingine kubwa,” Madam S akaeleza na Chiba akaitika kwa kutikisa kichwa, “kwa hiyo tunafanyaje?” akamwongezea swali.

“Nipe dakika chache,” Chiba akasema kisha akachukua simu yake na kuwasiliana na mtu mwingine.

* * *

Abigail Andrew, mwaDanada mahiri katika TEHAMA ndani ya kitengo cha siri cha kijasusi cha Israel aliipokea simu ya Chiba. Hakuuliza wala kushangaa, alimfahamu Chiba in and out na alijua mpaka kupiga simu basi kulikuwa na shida kubwa. Aliitazama simu yake, akatabasamu na kutikisa kichwa.

Amekamatika! Akawaza. Binti huyu aliyekuwa akihudumu ndani ya Mossad, shirika la kiintelijensia la Isarel, alikuwa mahiri sana katika Nyanja hiyo. Simu ile haikuongea chochote, akaelewa maana yake nini. Akachukua kitu kama waya na kuiunganisha na kompyuta yake kubwa ofisini hapo, kwa haraka akaifunga ili isiingiliane na mtandao mwingine wowote au kufukuliwa.

“Endelea,” akamwambia kwa lugha ya Kiebrania ambayo Chiba aliifahamu kwa kiasi kikubwa. Maelekezo kadhaa yakafuata na Chiba akaomba msaada wa kufunguliwa zile kodi pamoja na kupata maana zake.

Abigail, akazichukua na kuingiza katika mfumo wao wa utambuzi. Mfumo ulitumiwa na Mossad ulikuwa wa kisasa Zaidi kuliko wowote ule ulimwenguni. Haikuchukua hata dakika kumi kwa mwaDanada huyo kukusanya maelezo na kodi za QR zilizofichwa kwa namba maalumu. Hakuhitaji kujua ndani kuna nini, akazirudisha kwa Chiba mara moja ili kazi iendelee.

Chiba akazipokea taarifa zile ndani ya dakika thelathini tu. Akamshukuru mwaDanada huyo na kutazama kwenye zimu yake maelezo yote.

“Wanasemaje?” Madam akauliza kwa shauku ya kutaka kujua.

“Kazi imeisha mama,”

“Nini?”

“Kazi imeisha… hawa jamaa nafikiri hizi kodi za QR zitakuwa na maelezo Zaidi ngoja niziskani,” Chiba akajibu kisha akachukua zile Quik Response Code, na kuziweka kwenye mfumo wa kompyuta yake. Naam! Siri ikafichuka. Kodi moja kati ya hizo ilitoa maelezo stahiki kuhusu Kibwana Mtokambali, ubadilishwaji wake wa sura mpaka ile aliyoichagua.

“Madam!” Chiba akaita.

“Sema…”

“Haya hapa maajabu ya Mungu,” akachukua kompyuta yake na kuiunganisha na luning kubwa iliyokuwa ofisini hapo.

“Mama yangu! Kibwana huyu huyu?” akauliza.

Kwenye kioo kile ilionekana picha halisi ya Kibwana Mtokambali iliyopigwa miaka ya themanini ikiambatana na maelezo yote kuhusu yeye. Chini yake kulikuwa na maelezo na viambatanisho vya fomu alizojaza kukubali kufanyiwa upasuaji huo. Na sura aliyoichagua mwenyewe ilikuwa pale, jina lake jipya la Mc Tee lilijiandika na kumtambulisha kama raia wa Australia. Vivyo hivyo kwa James Msambamagoya maelezo yake yote yalikamilika, picha yake iliyopigwa miaka ya themanini ilionekana wazi pamoja na ile sura mpya atakayoonekana nayo mara baada ya upasuaji. Alikadhalika, jina lake jipya la Big J lilionekana wazi kabisa akiwa raia wa Mauritius.

Chiba na Madam S wakatazamana.

“Tumemaliza,” Chiba akasema. Madam S akatikisa kichwa kushoto kulia kuashiria kazi bado.

“Sawa, tumepata maelezo na kila utambulisho wao mpya… je yupi yupo Tanzania na yupo wapi, maelezo hayajadadavua…” Madam S akaeleza, “mwite Amata tukutane Shamba haraka iwezekanavyo,” akaamuru.

* * *

Katika ofisi kuu za TSA, Kigamboni, au kama panavyojulikana Shamba, Kamanda Amata alikuwa mbele ya Madam S na Chiba pembeni yake. Picha zile zilizotolewa kwenye lile kabrasha laini ndani ya mkufu wa Barbier zilikuwa mezani. Kamanda Amata alikuwa akiziangalia kwa zamu picha zile.

“Sawa!” akatamka, “hatruna haja ya kwenda India bali Mauritius… hawa jamaa ni mamafia aisee, yaani siri zao wanatembea nazo mwilini. Nikioanisha nay ale makabrasha niliyoyapata katika ile laptop ya Mwanachia kule Lisbon, nahisi sasa tunakaribia kupata mpango kamili,” akaeleza.

Madam S akatikisa kichwa juu chini, “tuna taarifa mbili, Rua Camarante na Saratov…” akasema.

“Yeah, na ukiziangalia, bado kuna vitu zinaficha, nafikiri bado kuna kabrasha lingine,” Amata akasema. Chiba akamkodolea macho TSA 1 kana kwamba hakuelewa kinachosemwa.

“Yaani…” akataka maelezo zaidi.

“Amata, jambo unalolizungumza nafikiri lina ukweli… unakumbuka taarifa ulizopata toka Brussels, zikatusaidia kufika Lisbon, ila kutoka Lisbon kwenda hatua nyingine tumepata tabu kwa sababu kulikuwa na Saratov,” Madam S akaeleza.

“Ndiyo,” Amata na Chiba wakajibu pamoja na kutazamana.

“Baada ya kumbana Dana katupa mwanga wa Saratov, na mzigo ndo huu, sasa hapa bila shaka kumebaki na taarifa mbili muhimu, kati yazo moja ni ya pili kutoka mwisho na nyingine ndo yenye kila kitu…” akaeleza Zaidi.

“Hiki kitendawili chepesi sana, James Msambamagoya, au Big J kwa jina jipya ametambulishwa kama raia wa Mauritius. Ina maana huyu Mtokambali au Mc Tee atakuwa hapa Tanzania… kazi imeisha,” Amata akasema.

Chiba akagonga meza, “inawezekana na vipi kama wametuzungusha tena katika hili wakitegemea kuwa ipo siku tungeweza kupata taarifa hii ili tuiamini na kumbe siyo?” akauliza.

“Negative,” Amata akatamka, “huyu mshenzi Ivan, kwa vyovyote alijuwa kuwa hatutaweza kuifikia hii taarifa, kwa hilo basi, hii ina ukweli,” akasema.

“Ok, kwa hiyo taarifa moja ipo Mauritius?” Madam akauliza.

“Fifty fifty Madam,” Chiba akadakiza.

Ukimya ukatawala kwa jozi la sekunde, watatu hawa, kila mmoja alikuwa akiwaza jambo lake kichwani mwake.

“Dana anahitajika tena?” Amata akatamka.

“Haswaaa!” Chiba akaunga mkono hoja.

“Pamoja na hayo lazima tufanye uchunguzi wa ndani nan je yaani huko Mauritius, na tukijua alipo, Amata, utatekeleza agizo. Nilikupa watu wanne, hujamaliza,” Madam akamwambia. Naye akajibu kwa kutikisa kichwa.

“Niachie mimi…” Amata akajibu huku ananyanyuka kitini.

“Tayari?” Madam akauliza.

“Ndiyo, naenda kumalizia hao wawili…”

“All the best!”

* * *

Kamanda amata aliwasili katika ofisi za jeshi la uhamiaji saa moja baada ya kikao na Madam S. Moja kwa moja akalifikia dawati analolihitaji. Katika dawati hilo kulikuwa na wanadada wawili waliokuwa wakiendelea kuhudumia wateja kwa kupokea simu, na kuwasikiliza ana kwa ana.

“Karibu kaka nikusaidie nini?” akaulizwa.

“Nahitaji kuonana na Lulu,” akamwambia.

Yule mwanadada, akainua simu na kubofya namba kadhaa akaiweka sikioni.

“Kuna mgeni wako, nimruhusu?” akamuuliza mtu wa upande wa pili. Baada ya kupata jibu, akakata ile simu na kumwonesha Amata mlango wa kuingia.

Lulu, mwanausalama mwenye kifuniko katika idara ya uhamiaji ya Tanzania, mara nyingi aliwasaidia TSA katika kazi mbalimbali hasa walipokuwa wakihitaji kujua kuhusu wageni au nani kaingia nchini na nani katoka. Miaka kadhaa nyuma alikuwa akihudumu katika Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na mara hii alihamishiwa katika ofisi za makao makuu, jingo la Wizara ya Mambo ya ndani.

“Waoh! Amata!” Lulu alifurahi kumuona kamanda. Akainuka na kumkumbatia kwa nguvu, “karibu Amata, za siku nyingi…”

“Salama, naona sasa upo kwenye kiyoyozi, umeachana na kelele za ma boeing…”

“Kabisa,”

“Nisipoteze muda nimekuja nina shida,”

“Shidika kaka yangu,”

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG