Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

MASHARIKI YA MBALI - 5

   

Simulizi : Mashariki Ya Mbali

Sehemu Ya Tano (5)


Akajifanya mjuaji angali alitambua wazi kuwa yeye ni majinuni tu!

Ile siku aliyowatukana waalimu waliompatia sifuri katika mitihani yake. Sasa alitamani watokee ili wamsaidie huu mtihani uliokuwa mbele yake.

Akakiri kimyakimya kuwa, sifuri haijawahi kuwa na maana nd’o maana hata yai liligoma kufanana nayo.

Lakini sasa anatakiwa kuitumia hiyohiyo sifuri iliyomuongoza awali kulitengenea tatizo. Hiyohiyo ilisawazishe!

Pagumu!


________


LILIKUWA wazo la Chuma, baada ya kumshirikisha kwa kina juu ya nduguye kusemekana yu matatani, akibebeshwa tuhuma za kuuza madawa ya kulevya.

Kama alivyotabiri mzee Machache kuwa Chuma na Daniel akili yao bado ni changamfu.

Alikuwa sahihi!

Chuma akalipindua wazo la Daniel la kuutafuta ukombozi kwa kutumianguvu.

Hakuacha kumdhihaki kuwa hata hao mgambo wanne aliowachakaza na kutoweka na virungu vyao, ni vile tu walikuwa wametoka kunywa pombe za kienyeji. La si hivyo wangeweza kumgeuza asusa.

Daniel akaipokea ile dhihaka huku akijibu mashambulizi kidogo.

Wakacheka kisha wakarejea katika lengo.

“Daniel! Judo yetu ya asili, ibaki kutusaidia katika misala midogomidogo tu, tusijifanye wababe. Zama zetu zilipita….. kwa sasa kitu tulichonacho ni akili. Tuzitumie.” Alizungumza Chuma huku wakizifaidi karanga mbichi walizoandaliwa na mke wa Chuma.

“Wewe na akili ulizokuwanazo mbona umeishia kuwa mbanguaji korosho.” Daniel akalipiza ile dhihaka.

“Harakati bila pesa kaka! Harakati bila kuwa na timu walau ya kukufanyia ‘back up’ ukizidiwa?” alizungumza kwa kumaanisha.

“Sawa, mimi ninazo dolali za Semedari, nikizibadilisha hizi zote. Inapatikana pesa ya kutosha kabisa kuwapagawisha mabinti wote wa Chikwa.”

Hili likawafanya wacheke!

Kisha Chuma akauelezea mkakati wake.

“Hakuna asiyezijua sifa za huyo jamaa yenu wa huko Fununu. Ni mshenzi mshenzi tu. Sasa tunatakiwa kuzizimisha hizo sifa”… akaweka pumziko kisha akaendelea.

“Hakosi kuwa na ndugu hukuhuku vijijini, maana tunajua kuwa alizaliwa na kuishi vijijini. Kama sio yeye basi mkewe, maana ipo hivi hawa watu wanaopenda sifa, wanaendeshwa kishenzi na wake zao. Tunaweza tukapiga panga kwa mkewe. Kisha tuwaache wafarakane, sisi tunachotaka ni jina kwanza tuwe na uhakika. Tusije kujiingiza matatani kumbe hata sio mtu wetu.”

Mkakati ukaelezewa vyema, kwa mapana na marefu. Penye kukosoana wakakosoana, penye kudhihakiana wakafanya hivyo.

Mwisho wa maongezi, lengo lao lilikuwa moja.

Lengo imara kabisa.

Lengo la marafiki.


Siku iliyofuata wakaanzia katika ‘intaneti cafĂ©’. Wakajipa muda wa kuwasoma, mkuu wa jiji la Fununu Mark Dunguli na mkewe Ester Mark Dunguli.

Kidogo tu, ilitosha!

Wakazibadili zile pesa za semedari.

Lundo! Zikapatikana pesa za Mashariki ya mbali.


Baada ya siku nne, wakamkumbatia Mzee Machache, wakamuaga pia mke wa Chuma. Huku wote wakiwaachia pesa ya kutosha, pesa ambayo ni miaka mingi ilikuwa imepita bila kuitia mikononi.

Hii walipewa kwa ajili ya matumizi.

Shangazi yake Daniel, alifurahia sana lakini mzee Machache alimvuta Daniel na Chuma akawanong’oneza.

“Iwapo hii pesa mmeithaminisha na uchungu nitakaoupata nikiwapoteza ninyi vijana wangu. Ni heri mbaki nayo na mbaki hapa kijijini.” Alizungumza kwa sauti ya chini.

“Tutarejea!” walijibu kwa pamoja.


Kisha kwa uchungu mkubwa wakakiaga kijiji cha Chikwa.

Kama alivyorejea kwa kumwaga chozi, safari hii tena likamtoka na kumezwa na ardhi yenye ukame.

Kwaheri Chikwa! Tutarejea, kufurahi na kuteseka pamoja.

Daniel alijisemea!


Sawa, angeweza kumuachia tena kwa ujumbe mmoja tu wa maandishi.

Ukweli atakaousema, walau nusu tu hauwezi kuacha kuwatia wazimu watu wake. Na huenda hii ikawa na malipo machungu zaidi.

Watakuwa na mtu wao tayari, watakuwa wanagonga na kukimbia. Kabla hapajapoa wanagonga pengine wanapotea.

“Walinikamata, wakanifunga kitambaa cheusi, wakanivua nguo zangu, wakanisimamisha mbele ya shimo refu kuliko kaburi, wakanipiga teke kali la tumbo, nikaangukia shimoni, nikichubuka na kuvunjika shingo, wakanifukia kisha wakanifukua, wakanitia kitanzi…….” Mkuu wa mkoa alijisemea yote haya kwa sauti ya kunong’ona akijaribu kujenga picha jinsi Danstan atakavyokuwa anawasilimulia wenzake.

Simba wa jiji la Fununu, akaanza kulia kama mtoto mdogo ndani ya gari lake la kifahari sana.

Majuto yakafunga ndoa upesiupesi pasi na kufuata sheria zinazotakikana.

Hayakungoja sana yakapata mtoto na kumsihi naye afunge ndoa upesi. Mtoto wa majuto akatii nasaha za wazazi, alipopata kichanga akawarudishia wazee wake mjukuu.

Na wao bila hiyana wakamsafirisha kama furushi la zawadi.

Hili hapa katika gari la muheshimiwa Mark Dunguli!



WALIKUWA mbele kwa masaa mengi yajumlishwapo huunda siku kadhaa. Aliyekuwa anakimbizana nao, alikuwa ameketi akiamini hana mshindani.

Alitafuna na kumeza bila wasiwasi!

Alipokuja kushtuka, vumbi lilikuwa likitimka, hakuiona sura ya mbele wala kichogo cha mtimua vumbi.

Akasimama ili aendelee kukimbia.

Ama! Alikuwa amevimbiwa tayari. Asingeweza kukimbia.

Akabaki kutapatapa huku akitafuta yeyote wa kula naye lawama.

Aanze kumlilia nani?

Nyumbani hakuendeki, mke amechachamaa. Ofisini hakukanyaga, akili ya kufanya kazi ilijipa likizo.

Akaghairi kila kitu, sasa amejilaza katika kiti cha gari lake.

Mark Dunguli, alikuwa amedunguliwa.


---------------------


DANSTAN McDONALD

Jina likatajwa, mke akalituma katika nambari zilizokuwa zikiwasiliana naye.


“Ni yeye aisee!” Daniel Katunzi akaingia katika taharuki ndogo. Awali alikuwa akijiuliza huenda ndie, ama labda siye.

Sasa ni uhakika, Danstan alikuwa yungali katika mikono ya polisi kwa miezi kadhaa kwa shutuma za uuzaji wa madawa ya kulevya nchini Mashariki ya mbali.

“Kwa hiyo huyu mama tunamuachia?” Chuma aliuliza akionekana kutolihitaji jibu la ‘ndio’.

“Tunamuachiaje wakati Danstan hajaachiwa, kwani kulijua jina lake tunakuwa tumesaidia nini. Akinyongwa tutasema tulifanya jitihada za kulijua jina? Haachiwi huyu!” alizungumza akiwa katika hamaki.

“Tuliza jazba Salu..aaahm! Danny. Siwezi kusema ni kwa asilimia mia moja, lakini hakuna jambo lililowahi kutafutiwa suluhu kwa jazba likapata matokeo chanya. Tunapambana na mpuuzi mmoja mwenye madaraka makubwa, anaweza kuajiri watu wenye akili kutuzidi wampambanie. Sasa ukitanguliza jazba wao wakatumia akili kidogo tu. Tumekwisha!” alizungumza kwa utulivu Chuma.

Daniel akakiri kuwa anatakiwa kuwa mtulivu sana, hisia zisiwe mbele yake bali katika kiganja cha mkono wake akiziongoza.

“Kwa hiyo sasa hatua gani unashauri ifuate?”

“Twende tukaimaliziea ngwe ya pili jijini Fununu.”

“Aaaah! Bwana we, lile jiji lake, si tutakuwa tumejipeleka jirani naye atatuweza kirahisi. Si bora huku!” Daniel akapinga.

“Ni rahisi kufunga magoli mengi ukiwa karibu na lango la mpinzani wako, ukibaki katika lango lako ni rahisi kujifunga mwenyewe. Hakuna kujifunga hapa Danny!” Chuma alizungumza.

Danny akatikisa kichwa, na hapo akatia akili kuwa Chuma alikuwa ameikamia ile vita zaidi na anaicheza kwa akili.

Akachukua maamuzi ya kumsikiliza zaidi!

Mwanamama akaachiwa kutoka katika maficho ya nyumba ya kupanga. Nyumba ambayo Danny aliilipia maalumu kwa ajili ya kazi mmoja tu. Akajiandikisha jina bandia, wakafanikiwa kumteka mwanadada yule majira ya usiku akitokea shambani.

Wamemuachia na kuiacha nyumba katika upweke, ikibaki na godoro na mashuka mawili.


___________________________


NIMUUE?

Swali hili lililopita katika kichwa cha mkuu wa jiji la Fununu, halikumshtua kabisa. Haikuwa mara ya kwanza kutoa amri nyepesi tu kisha watu wanapoteza maisha.

mungu wa Fununu!!

Alidhani hivyo!

Akasahau kuwa Mungu anaweza kuua na kuhuisha!

Yeye alijitamba kwa sababu anaweza kutoa amri ya kuua na ikawa.

Fedhuli wa nafsi!


Amri zote alizowahi kuzitoa kisha mtu ama watu wakapoteza maisha, hakuwahi kupata adui wa kumshutumu moja kwa moja kuwa yawezekana anahusika.

Watu waliuwawa kisha wakatupwa mitaroni, taarifa ya serikali za mitaa itadai ni ulevi umesababisha.

Watakutwa ufukoni mwa bahari wameuwawa na alama za mateso makali zikibaki katika miili yao.

Serikali itasema kuwa upelelezi unaendelea.

Uzuri huwa hawasemi utaendelea mpaka lini.

Mwezi mmoja, mwaka? Miaka?


Kuhusu Danstan, alikwisha mtupa kaburini, alishamtia kitanzia, alimkanyanga kila eneo la mwili wake, matusi yote alitukanwa.

Akapigwa akachakaa, akakata tamaa!

Anao uwezo wa kusema, muueni! Watamuua.

Ataanzia wapi, ulimi ulikuwa mzito.

Domo limeshikwa na ganzi kubwa kupita zote tangu azaliwe.

Danstan akaanza kuwa kijimchanga kidogo kilichotwama katika jicho la Mark Dunguli.

Ukipekecha kulia, kinahamia kushoto. Ukijifumba jicho linapotea, ukifumbua kinaisumbua mboni.

Unalisugua jicho, linakuwa jekundu!

Hakitoki, kinakera!!

Hakina ubabe wowote kikiwa nje ya jicho, lakini sasa kinatawala pasi na kujua kama kinatawala mtu anayeogopwa.

Danstan hakujua hata kidogo amegeuka kuwa mtawala katika maisha ya Mark Dunguli.

Mark hawezi kumuua kwa sababu hajui ni akina nani hao walioifikia familia ya mkewe, wakamteka dada yake na ndani ya siku chache kabisa wamefanikiwa kulipata jina la zungu la unga!

Jina sahihi kabisa!

Vipi akimuua, wapandwe na hasira waifikie familia yake.

Wamuue baba yake, waifyeke shingo ya mama yake mzazi, wasitosheke wakambaka dada yake, wakaichoma nyumba yao kubwa ya kijijini!

Jasho likaanza kumtiririka!


NIMUACHIE?

Sawa, angeweza kumuachia tena kwa ujumbe mmoja tu wa maandishi.

Ukweli atakaousema, walau nusu tu hauwezi kuacha kuwatia wazimu watu wake. Na huenda hii ikawa na malipo machungu zaidi.

Watakuwa na mtu wao tayari, watakuwa wanagonga na kukimbia. Kabla hapajapoa wanagonga pengine wanapotea.

“Walinikamata, wakanifunga kitambaa cheusi, wakanivua nguo zangu, wakanisimamisha mbele ya shimo refu kuliko kaburi, wakanipiga teke kali la tumbo, nikaangukia shimoni, nikichubuka na kuvunjika shingo, wakanifukia kisha wakanifukua, wakanitia kitanzi…….” Mkuu wa mkoa alijisemea yote haya kwa sauti ya kunong’ona akijaribu kujenga picha jinsi Danstan atakavyokuwa anawasilimulia wenzake.

Simba wa Fununu, akaanza kulia kama mtoto mdogo ndani ya gari lake la kifahari sana.

Majuto yakafunga ndoa upesiupesi pasi na kufuata sheria zinazotakikana.

Hayakungoja sana yakapata mtoto na kumsihi naye afunge ndoa upesi. Mtoto wa majuto akatii, alipopata kichanga akawarudishia wazee wake mjukuu.

Na wao bila hiyana wakamsafirisha kama furushi la zawadi.

Hili hapa katika gari la Mark Dunguli!

Majuto ni mjukuu!


Simu yake ikaunguruma!

“Wife!” jina likasomeka.

Akaitazama ikiita kwa muda mrefu, akaipokea ikiwa anakaribia kurejea katika kimya.

“Brenda amerejea nyumbani salama.” Alizungumza kwa sauti iliyopoa.

“Sawa, baadaye.” Alimaliza maongezi.

“Nipeleke nyumbani!” hatimaye alimweleza dereva wake aliyekuwa kimya muda wote.

Dereva akafunga mkanda na kumsihi Muheshimiwa Mark pia afanye hivyohivyo.

Akaingiza gari barabarani!

“Sio nyumbani huko….” Akamuwahi alipoona uelekeo wake.

“Sawa muheshimiwa, nielekee wapi?” aliuliza kwa nidhamu.

“Nyumbani kwetu, Kinguru.” Alizungumza kwa upole, tofauti na kawaida yake.

“Samahani muheshimiwa unamaanisha, kijijini Kinguru.”

“Jaza mafuta kabisa…. Tunaenda sasa hivi!” Mark Dunguli akasisitiza.

Yalikuwa maamuzi ya ghafla sana.

Aliamua kuwahi kijijini alipokuwa akiishi mama na baba yake.

Aliamini fika kuwa watesi wake wapo njiani kuelekea huko ili wampe pigo jingine.

Akaamua kuwawahi!

Mlinda mlango akaachia lango wazi akidhani ameliziba.

Washambuliaji wakalikuta lango wazi.

Kifuatacho…..

________________


MAWASILIANO yalifanyika ipasavyo. Kila lililohitajika kufanyika lilifanyika.

Mke alielezwa juu ya safari hiyo juu kwa juu!

Mzee wake kijijini akalezwa juu ya ujio huo, huku akielezwa pia hatari iliyopo. Akasisitizwa awe mlinzi mkuu wa familia, wakati wakiendelea kumngoja.

Usiku mnene, wakati muheshimiwa Mark Dunguli akiifikia ngome yao kijijini, tayari palikuwa na ulinzi mkali sana.

Hapakuwa na taarifa yoyote ya kitisho. Hapakuwa na ndugu yeyote ambaye amekuwa katika kimya kisichofahamika.

Wote walikuwa salama!

Muheshimiwa Mark Dunguli akashusha pumzi kwa nguvu sana, akarejea kujiona kuwa amepigana kwa kiasi kikubwa sana.

Akajitangazia ushindi kwa usiku huo.

Akapumzika kijijini kwao, majukumu ya jijini Fununu akiyakabidhi kwa mkurugenzi wa jiji hilo.

Jogoo la kwanza likawika, hili hakulisikia.

Adhana ya mnadi swala alfajiri, hii nayo hakuisikia. Alikuwa amechoka sana.

Kelele za punda waliokuwa wanalalamika kwa kukurupushwa asubuhi ili waende mashambani. Hizi aliweza kuzikisikia, akafumbua macho.

Kumekucha!

Alipoketi kitako na kuishika simu yake aweze kupata taarifa mbalimbali. Simu ikatoa mwanga, na mlio kwa mbali.

Jina lililosomeka pale alilifahamu fika.

Mkuu wa gereza alilohifadhiwa Danstan.

Haikuwa mara ya kwanza kupigiwa simu ama kuwasiliana na mzee yule mtiifu. Ambaye busara zake zimezikwa katika shimo la nidhamu ya uoga.

“Heshima yako mzee!” akaanza kumsalimia kwa sauti inayokoroma.

Kimya!

“Mzee!, unanisikia…” akauliza alipoona hajibiwi.

“Hakuna cha mzee hapa, nisikilize kwa makini kabisa, sitaki kujua mlikubaliana nini. Na sitaki itokee tena mnafanya makubaliano ya hovyohovyo wakati mahakama zipo. Nahitaji hii kesi ya huyu kijana wa Semedari ya madawa ya kulevya iende mahakamani na haki itendeke! Upesi sana…. Wiki moja kuanzia sasa!.”

Ilikuwa sauti kali ya raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Mashariki ya Mbali!




Ilikuwa sauti kali ya raisi wa jamuhuri ya demokrasia ya Mashariki ya Mbali!

Simu ilikatwa pasi na mzungumzaji kuhitaji majibu aina yoyote ile.

Hali ya hewa ya kijiji cha Kinguru, haikuwa ya ubaridi sana lakini ulihitajika kukimbia mita kadhaa ili uweze kuliona jasho likikuchuruzika.

Pasi na kukimbia, Mark Dunguli alikuwa anatiririka jasho akiwa ameketi kitandani. Simu ile ilikuwa imeleta aina ya kitisho kikubwa sana kuliko uwezo wake wa kuchanganua mambo.

Mwili ukiwa bado haujasahau suluba ya safari ya masaa zaidi ya kumi na nane hadi kukifikia kijiji, anaamka na simu ya kutisha kutoka kwa raisi wa nchi. Licha ya ukaribu aliokuwa ameujenga baina yake na raisi wake, hakuacha kuzitambua sifa za utendaji wake.

Alikuwa ni mtu wa maamuzi ya ghafla, maamuzi ambayo atayasimamia hata kama wengine watampinga.

Alizijua vyema ziara zake za kushtukiza, na waliweka tahadhari ya muda mrefu sana juu ya jambo hilo kutokea. Wakajipanga namna yamkumkwepa raisi na mitego yake, tahadhari ikaishi kwa muda mrefu bila kutumika.

Wakamtesa Danstan, wakamdhihaki kwa kila namna. Mchezo ukawanogea, wakamsahau raisi na ziara zake za ghafla.

Ghafla hii ikaacha gumzo.

Gumzo lililomfikia Mark Dunguli kwa njia ya simu. Simu iliyopigwa na mke wa mkuu wa gereza la ukwama. Gereza lililozuia jua lisimfikie Danstan!

“Mzee amefukuzwa kazi!” kwa sauti iliyojaa masikitiko na lawama alizungumza mama yule.

Mark Dunguli akastaajabu kwa jinsi mambo yalivyokuwa yanakwenda kasi. Yote yakimuelemea yeye.

Simu hii nayo ikakatwa pasi na kuagwa!

“Jamaa kamueleza mkewe kuwa mimi nd’o nimemponza!” Mark alijisemea huku akijaribu kuvinyoosha viungo vya mwili wake.

Akili kidogo iliyokuwa inafanya kazi katika kichwa chake ilibaki kulala licha ya mmiliki wake kuamua kujitoa kitandani.

Amshirikishe nani ili aweze kumsaidia kufikiri na kuleta hitimisho zuri.

Angeweza kwenda kwa mama yake mzazi, lakini licha ya umri kumtupa mkono. Mama huyu hakuwa mtu mwepesi, unampelekea shauri lako, anakutupia maswali manne ya msingi ambayo ukikurupuka kuyajibu unakuwa umejifunga.

Baada ya hapo itamtoka kauli yakemaarufu ‘Nitolee ujinga wako hapa’.

Alikuwa hivyo tangu Mark Dunguli anaazimisha kichwa chake kuielewa elimu ya msingi, akafanikiwa kupenya huko akaangukia katika elimu ya upili. Huku napo mama alimkalia kooni, aiendelea kukaguliwa madafari yake hata alipofika kidato cha nne.

Yawezekana ukamwelekeza punda mahali maji yalipo, lakini katu huwezi kumlazimisha.

Kichwa cha Mark kilikuwa kizito, kichwa ambacho hatimaye mama mzazi aikiri kuwa kimeshindikana.

Siasa!

Hizi zikamuunganisha na baba yake mzazi, urafiki ukaanza kushamiri. Huku alipapenda kwa sababu hapakuhitaji kuitafuta thamani ya ‘x’ katika minganyo unaotisha. Huku ni maneno yako tu.

Mark alikuwa amejaliwa maneno, akaongezewa na elimu ya kujipendekeza. Akafuzu shahada ya kwanza ya siasa za Mashariki ya mbali.


Mark akamwendea baba yake, akamweka kitako na kumeleza kuwa amelikoroga tawi la muarobaini akidhani anaenda kumnywesha mtu mwingine.

Upepo unabadilika na anapaswa kulinywa!

“Sasa wewe ulimchukua mtu bila ushahidi na kumpa shtaka zito kama hilo!” baba alimuuliza kwa upole.

“Popularity! Umaarufu baba, umaarufu wangu kisiasa ulipungua sana. Kweli baba ikawa inapita hadi siku nne hakuna gazeti lililoniandika, hakuna televisheni iliyonizungumzia.” Alijibu kwa kulalama.

“Uiwapa kitu cha kukuzungumzia, ama uitaka warejee kusema ambayo wameyasema tayari”

Kimya! Hana jibu.

“Unakumbuka nilikueleza nini wakati nakufundisha juu ya umaarufu wa kisiasa? Hususani hizi siasa za Mashariki ya mbali?” baba Mark akamswalika.

Kimya! Amesahau tayari…

Angelikuwa ni mama yake, angelishamwambia ‘nitolee ujinga wako hapa!’.

Ujinga huu baba aliubeba.

“Nilikueleza hivi, na itabaki kuwa hivi. Hapa nchini kwetu, ukifanikiwa kuwa na mamlaka katika Nyanja za kisiasa. Ili uvume, unapaswa kulitengeneza tatizo iache kwa muda kidogo kisha litatue huku ukihakikisha watu hawajajua kama ni wewe ulilitengeneza.” Baba alizungumza, Mark akajifanya aliyekumbuka vyema.

“Halafu nilitaka kusema hivyohivyo!” Mark akadakia

“Achana na habari za nilitaka kufanya hivi angai haujafanya, past tense hazina maana kabisa katika siasa na ukilemaa zitakuua. Fanya yote lakini ukitaka kujiua katika siasa uje uropoke, nilitaka kufanya hivi!” kidogo, baba alifoka.

“Sawa baba, na mimi niliunda hilo tatizo. Akini ugumu umeanza katika kulitatua.” Mark Dunguli alijieleza tena.

“Mark! Mark! Sitaishi miaka mia ili niwe nakukumbusha, unawezaje kulitengeza tatizo kisha nawe ukabaki kuwa ndani ya hilo tatizo, na utegemee kulitatua? Haiwezekani? Wewe umempa shtaka, halafu mapema unajitapa mbele ya vyombo vya habari. Unadhani lini utawapa wananchi nafasi ya kukupa ushindi. Ulipaswa kumuachia yule mkuu wa polisi kanda maalumu. Apambane mpaka atakapoelekea kushindwa wewe unajitokeza unamaliza mchezo.” Bwana Dunguli aliendelea kuzungumza. Akamuelewesha kijana wake masuala lukuki.

Kisha wakarejea katika tatizo!

“Sasa hapo unachotakiwa kufanya, hizo siku sana ulizopewa hakikisha anafikishwa mahakamani. Hapo hakuna namna zaidi ya kumchinja kama unataka kubaki salama. Ila ukijichanganya unachinjwa wewe katika hili. Na mwanangu nikueleze ukweli, mimi ni baba yako na sijafurahishwa hata kidogo na hili ulilomfanyia huyo kijana!!”

Mark, kimya!

“Kwa hiyo ahukumiwe nd’o unachomaanisha?”

“Eeeh! Hakuna namna!..... na hapo anafungwa maisha… aaah! Mark, umemkosea sana Mungu wangu. Gemu la siasa halichezwi hivyo….” Dunguli alilalama.

“Lakini kuna tatizo jingine mzee.” Mark alizungumza huku akimsogelea baba yake, kwa tuo akamueleza juu ya tukio la watu wanaojiita kwa kutumia alama ya ‘CD’, kumteka shemeji yake, kisha wakalazimisha wapewe jina la zungu la unga.”

Toba!

Dunguli alisimama, akabaki kujishika kiuno. Mark akabaki katika kuinama.

“Baada ya kuwapa jina, hawajawahi kutuma ujumbe wowote. Sasa sijajua nia yao…” Mark, alijileza kinyonge. Dhahiri, ubaridi wa hofu ulikuwa unamtawala.

“Kwa hiyo, ukaamini kuja kwako huku nd’o ulinzi tosha kwetu dhidi ya hao watu waliokuzidi maarifa? Kama unadhani umekuja kutulinda si kwei, labda kama umeamua kuja nyumbani ili tufe pamoja. Unadhani wakitupa bomu hapa kuna ambaye atapona. Kwanini unakuwa mpuuzi kiasi hiki Mark eeh! Kwanini? Hao watu umewahi kufanya nao mawasiiano ya moja kwa moja?”

“Aaah! Hapana walizungumza na mama!”

“Mama gani?”

“Aaah mke wangu…”

“Wewe ni mjinga Mark, unawezaje kumuita mke wako mama wakati mama yako bado anaishi. Si ungoje afariki kwanza alaa! Nd’o maana mama yako mnagombana sana… unafanya mambo ya kizembe. Kwa hiyo umemuita mama… sasa umeona kila kitu anaweza, unawaachaje maharamia wanawasiiana na mwanamke. Akienda kukuchoma polisi, unapata vitisho kama hivyo na haujashtaki! Akili huna… naomba unitolee ujinga wako hapa!” baba akawa mbogo akasimama na kumwacha Mark asiamini na baba yake ametumia kali ya mama yake.


________________________


SIKU ZOTE alikitamani kile kiti ambacho sasa alikuwa amekabidhiwa.

Kanali mstaafu Omari Nzegekunuka.

Tayari alikuwa ameapishwa na alikuwa amekichukua rasmi cheo cha ukuu wa gereza la Ukwama.

Wakati Muheshimiwa Mark Dunguli akiwa katika gari lake, safarini kurejea jijini Fununu. Yeye Kanali alikuwa akilipitia faili ya kesi iliyotajwa kama ya moto kupita zote.

Kesi ya zungu la unga!

Maelezo ya awali polisi, hayakuonekana. Maelezo ya msingi akiwa gereza la mahabusu yalikuwa na walakini.

Cheo cha kupewa na raisi moja kwa moja, sio masihara!

Hakutaka kufanya uzembe, hakutaka kona kona!

Akaagiza Danstan na washtakiwa wengine waliounganishwa katika kesi ile, wafikishwe mbele yake aweze kuzungumza nao ana kwa ana.

Alipanga kukutana huko iwe baada ya siku mbili tu.

Hizo zikimaanisha ni siku tano kabla ya siku aliyoitaja raisi.

Siku ya mahakama!

Kila kilichokuwa inaendelea, kilimfikia mkuu wa mkoa. Vijana wake waliokuwa wanafanya kazi katika gereza lile na wengine waliokuwa na haki ya kuingia gerezani. Walimfikia taarifa, taarifa waliyoipa majina ya matunda.

Hii ya siku hii waliita piipili kichaa!

Mkuu wa gereza alikuwa amekubaliana na ombi la Danstan McDonald kufanya mawasiliano nchini Semedari, ambapo atazungumza na wakili msomi wa familia yao.

Asafiri na kufika nchini Mashariki ya mbali kwa ajili ya kumtetea katika kesi yake.

Taarifa hii ilikuwa pilipili kweli.

Ikamtia wazimu Mark Dunguli.

Hana ushahidi wowote wa kumshtaki Danstan, na bora asingekuwa na ushahidi pekee. Alikuwa ana wasiwasi, Danstan akizungumza na kutaja madhira yote aliyotendewa.

Ni bomu la aina gani litamlipukia katika kifua chake?

“Aisee endesha gari basi, Fununu mbali!” alimkurupua dereva wake.kati huo alikuwa katika mwendo mkali.

Labda alitaka apaishe gari!


Hakuwa peke yake katika uharaka wa kufikishwa mahali.

Yeye alihitaji kulifikia jiji la Fununu.


Ndani ya jiji la Fununu, Daniel na Chuma walikuwa wanamsisitiza dereva wa taksi iliyowabeba ajitahidi kuongeza mwendo.

Walikuwa wanahitaji kufika mahali, wautekeleze mpango nambari mbili katika orodha yao. Baada ya mpango wa KITISHO kupata mafanikio makubwa.

Mpango huu uliobatizwa kwa jina la SANA na NANA!




SAA NNE USIKU.


LICHA ya kuamini kuwa haitakuwa shughuli pevu, hawakufikiria hata kidogo yawezekana kuwa nyepesi kiasi hiki. Ulikuwa umebadilika kuwa kama mchezo unaofurahisha, mchezo ambao kila mara mshindi anajulikana kuwa ni wewe.

Ilikuwa inashangaza, licha ya matukio ya kijangili na kigaidi ulimwenguni, bado lilikuwa ni suala jepesi sana kuweza kupangishwa nyumba nchini Mashariki ya mbali.

Kwa kipindi kirefu alichokuwa ametoweka aliamini fika kuwa nchi yake itakuwa imejifunza jambo hili kutoka nchi nyingine.

Nchini Semedari lilikuwa jambo jepesi kujijengea nyumba yako mwenyewe, kuliko nyumba ya kupangishwa.

Utalazimika kupitia hatua takribani tano kabla haujakabidhiwa nyumba uishi. Kwa mgeni anaweza kudhani anagandamizwa kutendewa hivyo!

Mashariki ya mbali bado mambo yalikuwa yaleyale, na ule wimbo wao unaoimbwa pasi na kutoa sauti uliendelea kuvuma ‘Tunasubiri majanga ndipo tuchukue hatua’.

Hata katika hili la nyumba yumkini walikuwa wanangoja majanga yawakumbe wananchi ndipo kiongozi wa ngazi ya juu, atatoka mbele akiwa na hotuba fupi aliyoandikiwa na katibu muhtasi wake. Ataanza kuisoma kama ilivyo.

“Sisi kama serikali tumepokea kwa masikitiko sana…..” zitaendelea porojo zilizozoeleka. Wakati anaisoma, katibu muhtasi atamtazama katika luninga na kujiuliza “unayesikitika ni wewe ama mimi?”.

Daniel na Chuma walikuwa wanaufurahia mchezo, walikuwa na masaa machache sana jijini Fununu na tayari walikuwa wanamiliki nyumba tatu za kupangishwa.

Walikuwa mbiombio kuwahi kufanya umiliki wa nyumba ya nne. Kirahisi tu, hakuna barua ya serikali ya mitaa, hakuna alama za vidole, hakuna picha za kumbukumbu ya ushahidi, mkataba hauna muhuri wowote, dalali hana ofisi wala kitambulisho cha kazi.

Ajabu ya yote, biashara ilifanyika kwa uhalali kabisa na dalali alipewa posho yake.

“Nchi yangu Mashariki ya mbali, kwa utaratibu huu mmefuga magaidi wangapi kihalali? Mmefuga wahamiaji harama wangapi?” Daniel alijiuliza kwa sauti.

“Acha usiwaamshe mpaka tumalize na sisi jambo letu!” Chuma akadakia, wakaangukia katika kicheko.

Ndani ya masaa sabini na mbili, tayari nyumba sita zilikuwa katika umiliki wa Chuma na Daniel.

Kelvin, Mansham, Muhsin, Muhando, Bwana Mushi, Dadu, Philipo! Haya yakawa majina yao ya upangishwaji wa hizo nyumba. Baadhi ya nyumba waliingia bila hata kuiona mikataba, pengine wakaingia pasi na kumfahamu mmiliki, walichoamriwa ni kutuma pesa tu!

Kisha, mkakati ukawashwa rasmi.

SANA na NANA!

_________________


INJINI ya gari iliendelea kuunguruma kwa dakika tano zaidi, kila akitaka kushuka miguu inamuwia mizito. Hakufanania na mtu ambaye ndani ya masaa kumi na sita yaliyopita alikuwa akimuharasi dereva wake, akimsisitiza aendeshe gari kwa mwendokasi maradufu ili wawahi kulifikia jiji la Fununu.

Huyu hapa sasa katika jiji la Fununu, mbele ya nyumba ambayo alihitaji kuifikia. Ameifikia na anapatwa uzito katika kushuka.

Baada ya dakika kumi, akakata shauri!

Mlango ukafunguliwa akautanguliza mguu wake wa kuume chini, wa kushoto ukifuata baada ya dakika moja nyingine.

Walinzi ambao gari lilipofika tu waliwahi na mitutu yao kuchungulia kulikoni, walimsogelea tena na kutoa heshima zao kwake.

“Karibu kiongozi!” sauti ya kishupavu ilisikika. Hii haikufanania na sauti ya mlinzi.

Muheshimiwa Mark Dunguli akageuka, akatazamana moja kwa moja na Kanali mstaafu Omari Nzegekunuka.

Ujasiri ukagoma kusimama pamoja naye, hofu ikaonyesha urafiki wa dhati.

“Shkamoo mzee wangu!” akatokwa na salamu ile, kwa mara ya kwanza kwenda kwa Nzegekunuka.

“Naona umenivamia, kwema?” Kanali Nzegekunuka hakuijibu ile salamu.

“Mwanajeshi naye anavamiwa?” Mark akajaribu kutupa utani kidogo. Ukagonga mwamba.

Nzegekunuka hataniwi, wala hatanii!

“Mwanajeshi ni nyama tupu kama wanadamu wengine” alijibu huku akibaki kusimama imara mbele ya Mark Dunguli.

“Mguu huu ni wako mzee wangu!..” Mark alianza kuzungumza, mdomo ukiwa mzito.

“Hadi kulifikia geti langu, kusalimiana na vijana wangu wakakamavu, bado tu walazimika kujieleza kuwa huu mguu umekuja kwangu Mark!! Hata mtoto wangu mdogo akitoka hapa atajua huyu ni mgeni wa baba…. Nieleze Mark unasemaje…” Haya yalimtoka Kanali mstaafu Omari huku amemkazia macho Mark Dunguli.

Mark akakwepa!

Nzegekunuka akamchapa kibao chepesi begani Mark Dunguli, ishara ya uelekeo aliopaswa kuufuata.

Wakasogea pembeni!

“Ni kuhusu Danstan McDonald bila shaka, upo hapa kwa sababu umepenyezewa taarifa kuwa nimeanza kulipitia upya jalada lao?” Nzegekunuka akaendelea kutamba katika ulingo wa daiolojia baina yao.

Kitu kama ngumi kali ikatua katika kifua cha Mark, uzito wa kauli ile ulimzuzua kiasi kwamba akahisi pumzi zikipambana kumkimbia. Akafanikiwa kuweka udhibiti katika hali ile.

“Ni hili tu limesababisha uweze kunipatia heshima finyu ya ‘shikamoo’, uniite mimi mzee wako na unitembelee usiku kama huu!” Kanali aliendelea kugandamiza. Awali Mark alikuwa na zege zito katika mdomo wake, baada ya kauli hizi zilizoshiba, mdomo ukaunganishwa na gundi kali.

Hawezi kuufungua, hawezi kuuchezesha!

Nzegekunuka anatamba.

“Zungumza sasa nakusikiliza. Ni nini huu mguu wako unataka usiku huu??”alimpa nafasi ya kuzungumza kupitia swali.

“Nataka kesi ya Danstan isitazamwe upya! Nataka unisaidie kwa hilo.” Alizungumza.

“Tazama ulivyo, haupo katika ujeuri, haupo katika ushamba, haupo hata katika ujinga. Sijui upo kundi gani wewe mtoto, unaniambia ‘unataka’, eti! Nataka kesi isitazamwe, sijui nataka unisaidie. Ni kweli huwezi kuiga hata jambo moja kwa wananchi wako wanapokuja kwako na kusema ‘samahani tunaomba utusaidie’ wewe unataka, kipi ulichonipa sasa unakitaka?” Kanali mstaafu alimfokea Mark Dunguli, hii ikiwa ni fursa yake ya kufanya malipizi dhidi ya bwana huyu, mjivuni wa tabia. Aliyewafokea askari wenye umri sawa na wa baba yake, akawakejeli huku wake zao wakitazama katika luninga ama wakisikiliza redioni.

Laiti kama angepatikana mtu wa kurekodi siku hii! Lingekuwa lipizi sawa sawia.

“Nisamehe mzee wangu, nimechanganyikiwa….”

“Baradhuli wa tabia, umewahi kumwona aliyechanganyikiwa? Hajachanganyikiwa Danstan mliyemvesha bomu akalipuke mbele nyie mkicheka. Unachanganyikiwa wewe unayepokea mshahara sawa na raisi wetu!... hebu niambie, kuna akina Danstan wangapi ndani ya gereza langu. Niambie mwenyewe kabla haujafunga safari usiku wa manane kuja kwangu kuniambia tena ‘nataka uache hiki na kile…” Kanali Omari Nzegekunuka aliendelea kuzungumza.

Mark! Kimya….

“Sikiliza nimezungumza na mzee wako, kabla hata haujafika hapa. Mzee wako nimeiona sura yake katika gazeti tu, lakini ni mmoja kati ya wazee wa kuigwa. Ana busara sana, laiti kama ningeambiwa nifanye uchaguzi, ningekutoa wewe katika hicho kiti na kumkabidhi mzee wako. Ngoja nikueleze jambo Mark kijana wangu, laiti kama mzee wako asingenipigia simu, ungepiga honi, ungebisha hodi, nisingetoka mpaka nihakikishe mimi na wewe tunakutana mahakamani. Mawakili wakutoe akili mbili ulizobaki nazo, ujibu hovyo kama ulivuozoea. Ukafungwe walau miaka miwili ukavune akili mpya gerezani. Busara za baba yako, zimebadilisha kila kitu!

Mpigie simu umshukuru sana.” Nzegekunuka akaweka kituo kikubwa.

Mark akashusha pumzi zake kwa nguvu, hakuamini kuwa baba yake aliye kijijini amempigania katika hili.

Licha ya kwamba kauli za kanali zilikuwa zinamvua nguo, lakini ni heri tupu yake kuonekana mbele ya watu wachache kuliko kuvuliwa nguo mahakamani kisha nchi nzima ikaziona tupu zake.

“Asante sana mzee wangu, nashukuru.” Mark alizungumza.

“Nakutakia heri katika mechi ya jumapili. Nakusihi usije ukaleta siasa tu uwanjani! Umealikwa kama mkuu wa jiji na sio vinginevyo!” Kwa mara ya kwanza Nzegekunuka alizungumza huku anatabasamu.

Ilimgharimu Mark sekunde kadhaa kukumbuka kuwa alikuwa ni mgeni rasmi katika mpambano wa kukata na mundu baina ya timu ya SANA dhidi ya ile ya NANA.

Akashusha tena pumzi, akakumbuka alivyompanga katibu muhtasi wake kuandika barua ya udhuru juu ya tukio hilo, kisha aitume asubuhi ya siku inayofuata.

Bila kujalisha kuwa ule ni usiku, na mama yule yu katika majukumu ya ndoani. Akampigia simu, sasa akiwa katika gari lake. Simu ikaita mara kadhaa kabla ya kupokelewa na mwanaume.

“Nipe niongee na huyo mama.” Akazungumza Mark, kwa lugha zilezile alizotoka kuonywa na kanali mstaafu.

Ama kwa hakika tabia ni kama bikira, ikifyatuka imefyatuka.

“Achana na ile barua ya udhuru. Nitaenda..” akazungumza na katibu muhtasi wake. Kisha akakata simu hata asipate sekunde chache za kujilaumu juu ya usumbufu aliouleta kwa kupiga simu usiku.

“Unadhani SANA na NANA nani atashinda?” Dereva akamtupia swali Mark wakiwa garini.

“Hilo sio swali, NANA tunashinda mapema tu.” Mark alijibu huku anacheka.

__________


“Hivi unahisi SANA na NANA nani atachukua pointi tatu?” Chuma alimuuliza Daniel wakiwa nje ya mojawapo ya nyumba waliyokuwa wanaimiliki.

“Mechi haichezwi hiyo! Mechi itakayokuwepo ni ya wajuzi kushindana kutambua nini maana ya CD huku wananchi wakililia kurudishiwa viingilio vyao.” Daniel alijibu huku akimtazama Chuma usoni.

Chuma akatabasamu kisha akajisemea, ‘oparesheni SANA na NANA imewashwa!’.





Suala hilo ikatupwa katika mzani wa gharama.

Kuwa upande wa Danstan na kumpatia haki zake, hii ilimaanisha kuwa wametia kidudu mtu kilichoenda kupeleleza madhaifu ya gereza la Mashariki ya mbali, ubakaji wa sheria za kibinadamu na mengineyo mengi yatakayoishtua dunia.

Kumwachia Danstan, ilikuwa ni sawa kabisa na kufanya makubaliano na nyoka, kuwa ukimkanyaga mkia basi asikugonge kisigino chako. Kisha unafanya jaribio hilo kwa nyoka aina ya koboko mwenye meno timilifu kinywani mwake.

Kubaki upande wa mkuu wa jiji la Fununu, muheshimiwa Mark Dunguli. Ilikuwa na uzito wa bomu ambalo unafahamu vyema kuwa likilipuka litawatekeza watu wengi, lakini kujiamini kunasababishwa na kufahamu ni wapi ilipo pini ya bomu hilo. Hivyo umakini unawekwa zaidi katika ile pini kuliko madhara ya bomu lenyewe.

Maamuzi yakatoka, lifanyike jambo lolote lile ushindi uwe upande wa Mark Dunguli kwa masilahi ya chama, kisha baada ya upepo huu mchafu kupita, atapewa onyo kali kwa siri na baadaye atatafutiwa kosa lolote lile ambalo litaweka rehani madaraka yake.

Kosa ambalo jamii nzima italiona kwa macho ya kulazimishwa! Jamii itapiga kelele, Mark aadabishwe.

Atateuliwa mkubwa mmoja kulikemea kosa hilo vikali, kisha uamuzi utatoka katika mamlaka ya juu.

Mark Dunguli atavuliwa madaraka.

Tengeneza tatizo kisha tatua tatizo!

Sifa zitaendelea kuzunguka humohumo ndani ya chama.

Sifa zitakazowasahaulisha wananchi wa Mashariki ya mbali kuwa, hata Mark Dunguli ni mtoto wa kuzaliwa katika chama hicho.

Katika kuusuka mpango huu wa kumpatia mpira Mark kisha kumpokonya ghafla, hakuna aliyekuwa anatambua kuwa lipo jingine la kufahamu.

Hakuna aliyefahamu fika kuwa suala sio kumgandamiza Danstan pekee kwa masilahi ya chama, ama kumsafisha muheshimiwa Mark Dunguli kisha kumchafua tena.

Lilikuwepo pia fukuto lililopachikwa alama ya ‘CD’.

Fukuto lililokuwa limeingia mjini pasi na kubisha hodi




“Hivi unahisi SANA na NANA nani atachukua pointi tatu?” Chuma alimuuliza Daniel wakiwa nje ya mojawapo ya nyumba waliyokuwa wanaimiliki.

“Mechi haichezwi hiyo!” Daniel alijibu huku akimtazama Chuma usoni.

Chuma akaielewa maana ya Daniel.

“Sawa hii mechi yetu, pasi na shaka washindi ni sisi hakuna kipingamizi katika hilo. Tunachukua alama zote tatu.” Chuma akajazia.

______________


HALIKUWA jambo la kwanza kujadiliwa kisha masilahi ya chama yakawekwa mbele zaidi kuiko utu. Huu ukawa ni muendelezo wa tabia komavu.

Chama kwanza!

Aliyekuwa mkuu wa gereza la Ukwama, licha ya kutolewa katika madaraka yale. Pia raisi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya watu wa Mashariki ya mbali, alihitaji kupata maelezo yake juu ya sababu ya kuchelewesha mahabusu kwa muda mrefu pasi na kuwafikisha mahakamani.

Suala la Danstan Mcdonald akilipa kipaumbele.


Ili kulinda ugali wake, bwana yule hakutaka kuchelewesha maelezo.

Akayaandika na kuyafikisha yalipohitajika.

Yakapitiwa na watu wanne tofauti kabla haijanyanyuliwa simu na kufikishwa kwa mkuu wa nchi. Taarifa ikionyesha bayana kuwa ukifanyika uzembe wa aina yeyote ile basi chama kitachafuliwa sana.

Mark Dunguli!

Huyu akatajwa kama muhusika mkuu katika uchafuzi huu.

Bila kupitia nyaraka zozote zile, ilifahamika wazi kuwa kinachohitajika hapo ni kulindana. Kuacha kumlinda Mark basi ni kujiandaa kukisafisha chama kwa gharama kubwa zaidi.

Suala hilo ikatupwa katika mzani wa gharama.

Kuwa upande wa Danstan na kumpatia haki zake, hii ilimaanisha kuwa wametia kidudu mtu kilichoenda kupeleleza madhaifu ya gereza la Mashariki ya mbali, ubakaji wa sheria za kibinadamu na mengineyo mengi yatakayoishtua dunia.

Kumwachia Danstan, ilikuwa ni sawa kabisa na kufanya makubaliano na nyoka, kuwa ukimkanyaga mkia basi asikugonge kisigino chako. Kisha unafanya jaribio hilo kwa nyoka aina ya koboko mwenye meno timilifu kinywani mwake.

Kubaki upande wa mkuu wa jiji la Fununu, muheshimiwa Mark Dunguli. Ilikuwa na uzito wa bomu ambalo unafahamu vyema kuwa likilipuka litawatekeza watu wengi, lakini kujiamini kunasababishwa na kufahamu ni wapi ilipo pini ya bomu hilo. Hivyo umakini unawekwa zaidi katika ile pini kuliko madhara ya bomu lenyewe.

Maamuzi yakatoka, lifanyike jambo lolote lile ushindi uwe upande wa Mark Dunguli kwa masilahi ya chama, kisha baada ya upepo huu mchafu kupita, atapewa onyo kali kwa siri na baadaye atatafutiwa kosa lolote lile ambalo litaweka rehani madaraka yake.

Kosa ambalo jamii nzima italiona kwa macho ya kulazimishwa! Jamii itapiga kelele, Mark aadabishwe.

Atateuliwa mkubwa mmoja kulikemea kosa hilo vikali, kisha uamuzi utatoka katika mamlaka ya juu.

Mark Dunguli atavuliwa madaraka.

Tengeneza tatizo kisha tatua tatizo!

Sifa zitaendelea kuzunguka humohumo ndani ya chama.

Sifa zitakazowasahaulisha wananchi wa Mashariki ya mbali kuwa, hata Mark Dunguli ni mtoto wa kuzaliwa katika chama hicho.

Katika kuusuka mpango huu wa kumpatia mpira Mark kisha kumpokonya ghafla, hakuna aliyekuwa anatambua kuwa lipo jingine la kufahamu.

Hakuna aliyefahamu fika kuwa suala sio kumgandamiza Danstan pekee kwa masilahi ya chama, ama kumsafisha muheshimiwa Mark Dunguli kisha kumchafua tena.

Lilikuwepo pia fukuto lililopachikwa alama ya ‘CD’.

Fukuto lililokuwa limeingia mjini pasi na kubisha hodi.


________________________


ALIISUBIRI siku ya kuzungumza na wakili kutoka Semedari. Siku haikufika, labda itafika siku ya kwenda mahakamani. Hii nayo haikufika.

Danstan alikuwa ameondolewa katika kile chumba alichokuwa amehifadhiwa kwa ajili ya kupambania kurudisha afya yake, ili aweze kuwa na muonekano mzuri mahakamani.

Sasa alikuwa amechanganywa na mahabusu wenzake pamoja na wafungwa waliokata rufaa.

Hakuwa akinyanyaswa tena kama zamani, lakini bado hakuwa huru na hakusikia jambo lolote lile tena linalohusu uendelevu wa ule moto wa mkuu wa gereza mpya, kanali mstaafu Nzegekunuka.

Danstan ambaye alikuwa ameanza kupata walau chembe ya tumaini, alirejea katika kukata tamaa. Alibaki kuwa mahabusu mkongwe ambaye aliijua kesho yake.

Kesho ya kuendelea kuwa mahabusu mpaka walioamua iwe hivyo watakavyoridhika. Kila kukicha aikuwa akirudia kiapo chake cha kutokanyaga tena Mashariki ya mbali ikiwa atafanikiwa kuupata uhuru wake.

Kuna siku ambayo alibaki katika kulaumu, alimlaumu yeyote atakayepita katika kumbukumbu zake.

Atamlaumu Daniel kwa kumsimulia juu ya nchi yake, simulizi zilizomvutia na kusababisha atamani kuifikia nchi hii ya maajabu.

Hata kabla hajaizoea mitaa, ghafla anapokonywa uhuru wake na kuhamishiwa katika maisha mengine. Ni kama aliambiwa kwa vitendo, aanze kuijua Mashariki ya mbali kuanzia gerezani kisha ajifunze kuhusu nchi hii katika uhuru.

Ya gerezani yalikuwa machungu, hakutaka tena mpango huu wa ukombozi utembee pamoja naye. Ni zaidi ya mara mbili kuna mabazazi waliwahi kujaribu kummendea kwa ajili ya kumgeuza asusa. Bahati ilikuwa kwake alipata watetezi na hakuna aliyefanikiwa kum-bashia.

Atatetewa mara ngapi kabla halijatokea bazazi lenye kila aina ya ubabe na kufanikiwa kumtenda vibaya?

Hili, lilimsumbua sana kichwa chake.

Lilipomchokonoa sana, akajikuta akiangukia katika wazo la kuweka mgomo mpaka apelekwe mahakamani.

Angeweza kulifanyia kazi pia wazo la kutoroka. Lakini ameshuhudia mara mbili waliojaribu kufanya hivyo wakiishia kushindiliwa risasi na kupoteza maisha, na zaidi ya mara nne watu walisimuliana mabalaa mengine makubwa yaliyowakuta wafungwa na mahabusu waliojaribu kutoroka.

Hili la kutoroka, Danstan akaliweka mbali naye.

Akachagua kugoma.

Lakini mgomo wa peke yake? Huu ungehesabika kama utovu wa nidhamu. Labda atapewa adhabu?

Adhabu ipi ambayo hakuwahi kupewa hapo kabla!

Danstan akachagua kuwashirikisha wengine waliokuwa na maalamiko kama yake, huku akijiapiza kuwa hata wasipomuunga mkono. Yeye ataweka mgomo.

Tena mgomo ambao hautakuwa na kurudi nyuma bali kupata ufumbuzi.

_________________


YALIBAKI masaa thelathini kabla mpambano wa kukata na shoka, baina ya vilabu vya soka maarufu zaidi nchini Mashariki ya mbali, Sana na Nana havijaingia dimbani kupepetana ili kumpata mshindi atakayeondoka na alama zote tatu, ama la kugawana alama.

Jiji lilikuwa limependeza tayari, mashabiki walikuwa wanatambiana huku kila mmoja akivutia upande wake. Wengi wakiwa wanamiliki tikiti zao mikononi.

Wasiokuwanazo wakiendelea kupambana kuzipata.

Kama ilivyokuwa ada, mpambano huu ulitarajiwa kulijaza dimba linaloweza kuwahudumia viti vya kuketi mashabiki wasiopungua elfu themanini.

___________


WATU Elfu themanini!

Hii ndiyo hesabu iliyokuwa ikiwapa kiburi Chuma na Daniel, kuwa kwa namna yoyote wamelishika jambo lililokuwa sahihi kabisa. Kuna muda walipata mashaka kuwa mpango wao ukianguka na wakatiwa mikononi mwa polisi basi wasingeliona tena jua la uhuru na amani. Wangeangukia katika shimo la mateso ambalo kila mara kivuli cha mauti kitakuwa kando yao.

Mawazo haya ya kukamatwa yaliwatikisa!

Walikiri kuwa hakuna mtu asiyeupenda uhuru.

Wakafanya walilotakiwa kufanya.

Wakafanya mawasiliano na mke wa mkuu wa jiji, Ester Mark Dunguli.

“Jina pekee halitoshi, tunamtaka Danstan akiwa hai na mwenye afya. La sivyo, watu zaidi ya elfu themanini watapoteza maisha. Ni juu yako wewe na mume wako kupima, je? Awe katika orodha ya maziko ya majivu ya watu elfu themanini? ama akubali kupoteza mpambano huu kwa kumuachia Danstan asiye na hatia?” Sauti kavu ya Chuma ilizungumza. Akaweka kituo kusikiliza jibu la upande wa pili, kimya! Anamsikia mwanadamu anayepambana kuziongoza pumzi zake zilivyokuwa zinapishana kwa kasi.

“Sio rahisi kuwa mjane huh!... Aaah! Kwako ni rahisi sana, kama alivyotueleza dada yako. Upo pamoja na huyo jamaa kwa sababu ya kuzichuma pesa zake tu! Nadhani akifa, kwako itakuwa furaha. Unarithi kila kitu. Lakini usiangukie katika wazo la urithi pekee. Kuna wadogo zako watakuwa uwanjani, wajomba zako, na huwezijua hata bwana uliyemuandaa kumrithi muheshimiwa, naye anaweza kwenda uwanjani.

Unayo masaa machache ya kuamua, aidha kuwapa taarifa watu wako wote wa muhimu wasiende uwanjani, ama la masaa mengi kabisa ya kumshauri mume wako amuachie Danstan. Vita havina macho, nasi tumejiandaa kwa hilo.”

Simu ikakatwa!

“Braza, mambo yakienda vizuri kabisa, anzisha kikundi cha sanaa kijijini kule. Unafaa kuigiza…. Sitaki kufikiria ni jinsi gani anatetemeka.” Daniel akiwa amekipakata kichwa chake mapajani huku anamtazama Chuma alizungumza.

Chuma hakujibu kitu bali akamfanyia ishara kwa kutumia kichwa chake.

Wakatoka na kuifunga nyumba ile wakatoweka.

“Kule Semedari, hapa tungetakiwa kuwa makini zaidi. Alama za vidole tulizoacha ndani ya ile nyumba hususani katika kitasa, hizo tungetakiwa kuzifuta. Sauti uliyotumia ingeweza kukukamatisha ndani ya dakika sitini tu.

Ajabu sana, hapa kwetu mambo yanaenda kienyeji enyeji tu.sijui kama magaidi hawajaitambua fursa hii. Ama nd’o wakoloni walibeba kila kitu kiasi kwamba magaidi hawana cha kufanya na nchi hii zaidi ya kukiacha kifo kiwe hakimu wa haki?” Daniel alizungumza.


“Ndugu yangu, nchi hii ina madeni makubwa mno. Ina viongozi ambao wanajipendekeza kila kukicha kwa nchi tajiri, yaani ukoloni bado upo. Ni jambo la kushukuru kuwahuwa tunasikia tu wamepewa mikopo tayari, hatujui ni kiasi gani huwa wanawalamba miguu mabepari!! Yawezekana ikawa zaidi ya enzi za utumwa.” Chuma naye akachangia hoja.

Wakatoweka eneo lile na kuelekea katikati ya jiji.

Wakanunua fulana na kofia za pande mbili za timu hizi zilizotarajia kuchuana baada ya masaa yasiyozidi thelathini.

Chuma akichagua kuwa upande wa NANA na Daniel akiangukia upande wa SANA.


Danstan yeye alikuwa amechagua upande wa mgomo.

Serikali ikichagua upande wa kumgandamiza Danstan.

Alikuwa anasubiriwa Mark Dunguli achague upande wake.


MWISHO WA SEASON 1

ENDELEA KUFUATILIA SEASON 2


0 comments:

Post a Comment

BLOG