Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

WAKALA WA SIRI - 2

  

Simulizi : Wakala Wa Siri 

Sehemu Ya Pili (2)


Kitambo kidogo aliingia mtu wa pili, Sajenti akajua amekwisha kwa maana kadiri muda unavyoenda wanazidi kuongezeka jambo ambalo ni hatari kwa usalama wake. Aliwaza; Sipaswi kuendelea kusubiri mpaka wawe wengi, watanishinda, ikiwa sitafanya kitu. Kwa upesi alitoka chini ya kitanda, akawafyatulia wote risasi wakadondoka chini, kabla hajakaa sawa wengine wawili walikuwa wanakuja mlangoni akawawahi kwa kuwapiga risasi za vichwa wakaanguka chini. Chapu chapu akachukua bunduki moja ya wale watu aliowaua, muda wa kuondoka ulikuwa umewadia, alitoka mule wodini akatokea kwenye korido ambapo alikutana na wanajeshi wawili wakamrushia risasi ambazo zilimkosa kosa akauvamia mlango wa wodi nyingine akaufunga, sasa kazi ilikuwa imeanza, tayari walikuwa wamemuona. Wale watu waliitana waje upande ule ambao Sajenti yupo. Vikosi kwa vikosi viliandamana, kuzingira wodi aliyokuwa ameingia Sajenti, kwa ndani aliufunga mlango huku akifikiria namna ya kuepa eneo lile. Hatari ya maisha yake aliiona, alijua kama ataleta mchezo anaweza siku ile kupoteza maisha.

Vikosi vya kijeshi vilikuwa mlangoni vikipiga mahesabu ya kuuvunja mlango ili kumnasa Sajenti. Punde si punde kishindo kilisikika na mlango ukafumuliwa fumu fumu! Moshi ukatawanyika na kuzingira eneo lote la chumba, mianga mikali ya tochi iliishambulia wodi aliyokuwa ameingia Sajenti Warioba, kwa uchu wa roho mianga ile ilienda huku na huku ikitafuta roho ya Sajenti. Vishindo vya miguu ya wale watu vilikuwa vishindo vya mauti vikimuita Sajenti kwa sauti ya ghadhabu na Jeuri. Wale watu walishangaa kuona wodi ipo tupu bila ya Sajenti kuwapo, waliliona dirisha lipo wazi hapo wakadhani huenda Sajenti aliruka kutoka dirishani. Kiongozi wa wale watu alisogelea lile dirisha na kutazama nje kwa chini, hapo akaangaza macho yake huku na huko kuona uwezekano wa Sajenti kuruka pale dirishani, alimuliika mpaka kule chini kabisa lakini akili yake ikamuambia Sajenti hajapitia pale dirishani, atakuwa mule mule ndani. Sasa atakuwa kajificha wapi, hilo ndio swali ambalo wote walikuwa wakijiuliza huku macho yao yakijaribu kutafuta majibu kwa kuangalia huku na huko kwa usaidizi wa tochi zilizomo katika bunduki zao na nyuso zao.

“Sajenti Warioba, tunajua upo humu humu ndani, na unanisikia. Jitokeze mara moja. Huwezi kuikimbia serikali. Jitokeze haraka, unafahamu kulisumbua jeshi adhabu yake ni kubwa sana. Jitokeze upesi” Sauti kavu ya kibabe ilisema huku ikitoa maneno ya vitisho.

“ Unajidanganya Sajenti, huwezi kimbia tusikukamate, jitokeze huenda utaonewa huruma, kulisumbua jeshi ni kutafuta matatizo, haya jitokeze upesi” Sauti ile ile iliendelea kumtisha Sajenti ili ajitokeze lakini Sajenti aligoma kujitokeza. Akiwa kajificha Upande wa pili wa wodi ambapo kuna mlango wa siri uliofanana na ukuta alisikia kila kitu, maneno ya mtu Yule yalimfanya achanganyikiwe, anatafutwa na jeshi kwa sababu gani, kwani kafanyaje mpaka atafutwe, wasiwasi uliongezeka. Yeye alitumwa na Kamanda Mkuu kuja kumlinda Mateka wa ushahidi, ambaye alipofika hakumkuta zaidi ya kukuta mauaji ya kinyama. Sasa hili jeshi linatoka wapi. Sajenti aliikumbuka ile gari aina ya Verosa aliyoiona ikitoka getini wakati yeye akija katika hospitali hiyo. Alikumbuka pia kuwa gari ile haikuwa na Plate namba. Nani atakuwa nyuma ya jambo hili. Sajenti alijiuliza, alihisi kuchanganyikiwa, aliona jambo lile ni gumu na zito linalomshinda. Tangu aanze kazi hajawahi kuona ugumu kama aliouhisi wakati huu.

Kinachomfanya achanganyikiwe ni kuwa mpaka muda ule hamjui adui yake ni nani, hajui nani yupo nyuma ya mambo yote yale. Kwanza, ni nani aliyeiba chipu ya darubini, aliiba ya nini, na kama katumwa katumwa na nani, alijuaje kama hospitali ya Boreti ndio yenye hiyo darubini nchi nzima, na chipu hiyo ipo moja tuu. Kama hiyo haitoshi, mwizi wa sampo za uchunguzi ni nani, Nani aliyeiba Cadava, nani aliyewateka wakiwa pale hotelini akiwa yeye, Fernanda na Kamanda Mkuu, na sasa ni kina nani wamemtorosha Mateka wa ushahidi ambaye huenda angetoa mwanga wa maswali yote. Hata wanajeshi hawa hakujua ni wanajeshi kweli au wanajeshi wa maadui. Sajenti alihisi kuchoka, kichwa kilivurugika huku moyo ukiwa hoi kwa wasiwasi na mashaka.


Punde akiwa ndani upande wa pili ya wodi aliwasikia wale wanajeshi wakijadiliana jambo lililomfanya akili yake ikose utulivu. Aliwasikia wakijadiliana kuwa wodi ile inamlango wa siri, kisha akasikia wakishika kuta za ile wodi hapo akajua amekwisha, alichungulia juu ya dari akaona dari ya ubao. Akapata wazo la kupanda juu ya dari na kutokea kwa upande wa juu. Wazo hilo akaliafiki. Kwa upesi akapanda, kwenye ukuta kikomando kama mjusi Kupitia pembe ya chumba kile. Haikuzidi dakika, alipokuwa akimalizikia juu ya dari wale watu walikuwa washavunja ule mlango wa siri, wakatokea kwenye kile chumba alichokuwepo, walipotazama juu walimuona akimalizikia miguu wakaanza kumrushia risasi.


Sajenti kwa haraka alitambaa juu ya dari kwenye mbao akatokea upande wa pili, kisha akatambaa dari kwa dari mpaka wodi ya nne ghorofa ya tatu, kisha akaruka na kuanza kukimbia kushuka chini ghorofa ya pili. Alipita ghorofa ya pili salama salimini, kimbembe kikatokea alipofika chini, milio ya risasi ilimlaki naye kwa upesi akajihifadhi kwa kujificha kwenye ukuta, akajiweka sawa na kuikoki bunduki yake. Kisha akajitokeza, aliwapiga risasi wote watano wakafa. Hapo akatoka nje ambapo aliwakuta wanajeshi wawili wakiwa juu ya gari, akakimbia kimya kimya bila ya wao kumuona lakini kabla hajafika getini alisikia mlio wa risasi kwa nyuma kule alipokuwa ametokea, walikuwa ni wale watu wabaya aliowakimbia kule juu ghorofa ya tatu. Alijitahidi kukimbia kuliwahi geti ili atoke lakini bahati haikuwa yake, alipigwa risasi ya mguuni, akajirusha na kujikokota mpaka nje kabisa ya geti, kwa nyuma wale watu waliendelea kumfukuza huku wakimrushia risasi. Sajenti alijikokota akikimbia mguu mmoja akichechemea kuokoa uhai wake. Alihisi maumivu makali sana, hata hivyo hakutaka kufa kijinga, alijikaza kisabuni akazidi kukimbia kwa kuchechemea nyuma yake wale wanajeshi wabaya wakiwa wamemkaribia, alikata kushoto ulipo uchochoro akaanza kukimbia huku akihema kama mtu anayemaliza pumzi yake ya mwisho. Uchochoro ule kwa mbele aliona barabara ya lami, alijikaza ili walau afike kwenye ile barabara ya lami kama ndio ukombozi wake lakini ilikuwa ni faraja kwa marehemu. Alikuwa akikimbia huku akigeuka nyuma kuwarushia risasi ili wasimfikie kwa urahisi, nao wale watu walikuwa wakimfukuza huku wakijificha kwenye kuta kukwepa risasi walizokuwa wakirushiwa na Sajenti.

Bahati haikuwa yake, alishangaa bunduki yake ikinyamaza bila kutoa risasi.




Looh! Alishusha

pumzi, risasi zilikuwa zimeisha. Hapo akazidisha mbio, wale maadui waliokuwa wamejificha

nyuma ya kuta kukwepa risasi walipoona kimya, wakajua Sajenti kaishiwa na Risasi, kwa upesi

walijitokeza na kuanza kumkimbiza kwa kasi zaidi. Sajenti alikimbia akiwa anamalizia nguvu

zake za mwisho, muda huu walikuwa hawamrushii risasi tena, hii ilimaanisha walitaka

kumkamata akiwa hai. Walimkimbiza, punde si punde mbele ya ile barabara ya lami ilisimama

gari ya kijivu, kisha mlango wa mbele ukafunguliwa.

“Otiti mpenzi, kimbia uingie ndani, jikaze tuondoke” Ilikuwa ni Sauti ya Fernanda iliyotoka

ndani ya lile gari la kijivu. Sajenti alivyosikia sauti ya Fernanda alipata nguvu upya, aliongeza

kasi wakati huo wale watu wabaya wakianza kurusha risasi zao kumfuata Sajenti na kulipiga lile

gari. Sajenti alijitahidi kukimbia akikoswa koswa na risasi mpaka alipojirusha ndani ya gari na

hapo hapo Fernanda alitia gia na gari likaondoka kwa kasi huku likiachia moshi mweusi eneo

lile. Wale watu wenye kiu ya damu walilisindikiza lile gari kwa risasi mpaka lilipokatisha kona

na kupotea katika upeo wa macho yao.


*****************************

Fernanda alimsafisha Sajenti Warioba Mguu wake, na kuitoa risasi iliyomjeruhi mguuni.

Bahati nzuri risasi ile haikuvunja mifupa isipokuwa iliharibu vibaya nyama za mguu wake wa

kushoto. Baada ya hapo, alimuacha Sajenti warioba apumzike baada ya kuhakikisha amempaka

madawa ya kukausha jeraha. Fernanda hakutaka kumpelekea Sajenti nyumbani kwake

Mikocheni, alijua wale watu wabaya wangemfuatilia, pia hakutaka kumpeleka nyumbani kwake,

alichokifanya ni kwenda Hotelini. Walichukua hoteli yenye hadhi ya nyota tatu iliyokuwepo

Maeneo ya Ubungo. Muda ulikuwa umeenda yapata majira ya saa saba za usiku. Usingizi

uliwachukua mpaka kesho yake asubuhi ambapo wa kwanza kuamka alikuwa ni Sajenti,

alichechemea kwenda kuwasha Luninga iliyokuwa mule ndani, ilikuwa ni taarifa ya habari ya

saa kumi na mbili asubuhi. Hapakuwa na habari ya maana, alichukua simu yake akaiweka chaji,

kisha akaiwasha kwani ilikuwa imezima. Alivyoiwasha tuu ikaita, namba aliyoiona kwenye kioo

cha simu ilikuwa ni namba ya kamanda Mkuu. Alihisi ubaridi ukipanda shingoni mpaka kwenye

uso wake. Alijishauri aipokee au aache kuipokea.

“Pokea mpenzi, mbona unawasiwasi” sauti ya Fernanda ilimshtua Sajenti, kutokana na kuwa

Sajenti alimuacha Fernanda kitandani amelala.

“ Sajenti Warioba, umeamua kumtorosha Mateka wa ushahidi, umeamua kuwa msaliti wa nchi

na kuungana na adui zetu, utakiona cha mtema kuni, kumbuka kiapo ulichokula siku ile

ulipoingia katika kulitumikia taifa, Umekwenda, tutakutafuta kila kona, lazima tukufundishe

adabu” Sauti ya Kamanda Mkuu iliyokuwa ikizungumza kwenye simu ilimaliza, kisha simu

ikakatika. Sajenti alibaki ameshikwa na bumbuwazi ambalo lilimfanya midomo yake kuwa

mizito isiweza kusema chochote, bado simu alikuwa kaiweka sikioni ingawaje ilikuwa

ishakatika. Aliiondoa simu sikioni taratibu kisha akamgeukia Fernanda ambaye naye alikuwa

ameshtushwa na simu hiyo.

“…..Umeamua kumtorosha Mateka wa ushahidi, umeamua kuwa msaliti wa nchi na kuungana

na adui zetu..” Sajenti aliyarudia maneno ya Kamanda Mkuu aliyoyasikia kwenye simu.


“ Haiwezekani, hii ni njama. Mimi..! Ati nimekuwa adui wa nchi, ati nimemtorosha Yule mateka,

hapana….! Hii ni njama ya kuniangamiza. Haiwezekani..” Masikini Sajenti aliongea kwa sauti

ya huzuni hasira zikimkaba shingoni huku machozi yakimlenga lenga, wakati mguu wake

ukichokoza na maumivu ya jeraha la risasi alilopigwa usiku wa jana.

Alimpiga Kamanda Mkuu simu, ikaita mara mbili, mara ya tatu ikapokelewa;

“ Mkuu, mbona sielewi unazungumzia nini, mimi sijamtorosha Yule Mateka wa ushahidi.,

nikisema….”

“Sajenti huna haja ya kujitetea, hila yako tumeijua, tumekufuatilia kwa siku nyingi sana.

Tumegundua pia, wewe ndiye uliyeiba chipu ya darubini, sampo za uchunguzi, na Cadava, mtu

mbaya sana. Subiri utaeleza yote tukikuweka chini ya ulinzi” Kamanda Mkuu alimkatisha

Sajenti aliyekuwa akijitetea.

“ Chipu…! Cadava tena! Kamanda Mkuu Mimi sijui chochote…” Sajenti alisema, lakini kabla

hajaongea zaidi simu ikakatwa.

“ Aliyeichonga hii njama atalipia, atalipia mara elfu, huu sasa ujinga” Sajenti aliongea kwa

sauti huku akiyatoa macho yake akimtazama Fernanda. Maneno ya Sajenti yalimchoma sana

Fernanda, kama kuna mambo ambayo Fernanda alikuwa hapendi, ni kumuona Sajenti akiwa na

huzuni. Fernanda alikuwa akimpenda sana Sajenti Warioba,tangu siku ya kwanza walivyokutana

kule Brazil, kwenye mji wa Juquei ndani ya Meli ya Ambagon mpaka muda huu ambao wapo

pamoja hakupenda kumuona Sajenti anamajonzi. Sajenti kwake ndio alikuwa furaha ya maisha,

yeye ndiye mwanaume pekee aliyemuwezea. Hivyo kumuona Sajenti kwenye hali ile kulimfanya

naye akose amani.

“ Otiti mpenzi, tumepitia mambo mengi mazito, hata hili litapita. Usiumie mume wangu, hapa

tufikiri namna ya kukabiliana na tatizo hili” Fernanda alisema.

“ Mambo mengi mazito tumepitia lakini sio kama hili Fernanda, sikuwahi kufikiri kuwa siku

moja nitaitwa adui wa taifa, nilizoea kuwakimbia maadui zangu, nimekimbia wanyama wakali

wa kutisha porini, nimeepa kwenye midomo ya mamba na papa kwenye mito na baharini,

jangwani nimeushinda upepo wa vumbi la jangwa, lakini bado uhodari wangu huo hautafua

dafu nitakapokimbizwa na serikali. Unajua kabisa serikali inamikono mirefu na miguu yenye

kasi, tena inambawa zenye nguvu kama tai, na mapezi mepesi ya kuchanja maji baharini,

sitoweza kukimbia Fernanda, nahisi mwisho wangu umefika” Sajenti aliongea kwa sauti ya

huzuni, macho yake yalisema maneno elfu ya kukatisha tamaa, uso wake ulijawa na ishara zote

za mtu aliyekosa tumaini, hata pumzi yake ilitoka kama mtu anayeaga na kutoa mkono wa kwa

heri.

Ukimya kwa kitambo ulitokea, walitazamana huku kila mmoja machozi yakibisha hodi katika

milango ya macho yao

“Wewe ni shujaa, nimewahi kuonana na watu hodari lakini wewe umewazidi wote, nafahamu

huwezi kuwa hodari na shujaa kwa kiwango cha kuishinda serikali. Lakini unaweza kutumia

uhodari wako kuionyesha serikali kuwa wewe ni mtu mwenye haki, mtu bora usiye na hatia.

Otieno, sitaki niwe mbali nawe, ukiondoka nami nitaondoka, ukipotea nami nitapotea, embu


nambie tufanyeje ili serikali ijue kuwa wewe sio adui, wewe sio mtu mbaya, sema tufanyeje?”

Fernanda alisema huku akimsogelea karibu Sajenti

“ Serikali inajua mimi ni mtu mwema, tena muungwana. Nimeitumikia kwa miaka kumi na tano

nikiwa mwaminifu. Serikali haina shida na mimi , ila kuna watu baadhi ndani ya serikali

wanataka kunivalisha kombora ili linilipue peke yangu. Nahitaji nikaonane kwanza na Dokta

Beatus, nikifika kwake nitajua wapi pakuanzia, najua Kamanda mkuu kaamua kunifanyia njama

na kunibebesha huu mzigo ili yeye aonekane ni mwema” Sajenti alisema, kisha akameza fumba

la mate na kuendelea;

“ Sitaki uingie katika matatizo Fernanda, nataka ufanye jambo moja ikiwa wanipenda na

kunisikiliza” Sajenti alisema sauti ikiteleza bila kuwa na vishikizo.

“ Wewe unajua jinsi gani ninavyo kupenda, tena wajua kuwa nakusikiliza kuliko mtu yeyote,

hata mama yangu sikuwa namsikiliza hivi, tafadhali niambie, unataka nifanye jambo gani Otiti

Mume wangu” Fernanda alisema sauti yake akiizuzua na kuipeperusha mdomoni ikawa kama

inatoa mwangwi wa hisia za mapenzi.

“ Nataka uwe mbali na mimi kwa wakati huu, nataka uniache kwa muda”

“Otiti umechanganyikiwa, hata usingethubutu kuwaza jambo hilo, ikawaje ukaweza kutamka

kabisa?” Fernanda alisema akiwa ameghadhibika.

“ Tumekuwa kama mfupa na nyama siku zote, neno hili sikulipenda Fernanda lakini ndilo lenye

usalama wa penzi letu. Kukaa karibu na mimi kwa wakati huu ni kukaa juu ya kaburi

linalozungukwa na majinamizi wabaya. Sipendi udhurike, nahitaji uishi kwa amani” Sajenti

aliongea huku akiwa anashika nywele za fernanda bado wakiwa wamesimama.

“ Kaburi nitalibusu, tena nitaliimbia nyimbo za mapenzi ikiwa ni kaburi lako. Hata sanda

nitavaa, nitatembea nayo njiani ikiwa ni sanda yako Otiti. Nakupenda Mume wangu, tafadhali

isiwe mjadala usio na mwisho, sikia sauti yangu Otiti” Fernanda alisema huku akilazimisha

kumkumbatia Sajenti hali iliyopelekea kumtonesha kwenye jeraha lake lililoko mguuni mwake.

Aligugumia kwa maumivu, Fernanda akamtuliza kwa kumpa busu zito lililofubaza maumivu ya

risasi, japo aliumia lakini maumivu hayakufua dafu mbele ya busu matata kutoka kwa Fernanda.

“ Wananifuatilia, sitoshangaa ikiwa watajua nipo hapa, wakifuatilia mawasiliano ya simu

hawatoshindwa kujua nilipo, sipaswi kuendelea kuwa mahali hapa. Naomba niondoke” Sajenti

alisema huku uso wake ukiwa umezingirwa na wasiwasi.

“Uondoke..! Uende wapi? Alafu uniache, hiyo haiwezekani, Otieno hilo kamwe haliwezeni.

Tutaondoka wote, popote pale tutakuwa wote’’ Fernanda aliongea uso wake akiupeleka mbele na

kuurudisha nyuma huku mkono wake mara auweke kiunoni mara amnyooshee kidole Sajenti.

Sajenti alibaki kimya, alikuwa kwenye wakati mgumu sana. Alihisi akili yake ikimuacha,

asingeweza kujiongopea kuwa yupo katika hatari ya kuingia chini ya mikono ya serikali, kwa

kosa la usaliti na kutoa siri za nchi ingawaje lilikuwa kosa la kusingiziwa.

“ Usiwe na wasiwasi mpenzi, tulia mambo yatakuwa sawa, pumzika, ngoja niagize chakula cha

asubuhi tusafishe matumbo” Fernanda alisema akisogelea simu ya mezani iliyokuwa mule


chumbani, simu ya hoteli. Alibonyeza namba na kuagiza wahudumu wawaletea chakula.

Kitambo kidogo mlango uligongwa, Fernanda akaenda kufungua, alikuwa ni mhudumu akiwa

kabeba supu ya kuku, chapatti mbili, mayai manne na sambusa nne pamoja na chupa kubwa ya

wine nyekundu. Alichukua, akashukuru kisha akafunga mlango wakati mhudumu wa hoteli

akiondoka.


Baada ya kupata kifungua kinywa, walienda wote kuoga, Sajenti alifurahia mahaba

aliyoyapata bafuni akiwa na Fernanda, japo alikuwa na jeraha mguuni la risasi lakini hakuyasikia

maumivu yake. Ilikuwa raha bila karaha, walimwagiana maji huku wakicheza tadhani watoto wa

bata. Fernanda aliyajua mapenzi, ilifikia kipindi mpaka Sajenti alikuwa amesahau habari za

kusakwa na serikali chini ya Kamanda mkuu kwa kesi ya kuiba chipu ya darubini. Sajenti

alizamishwa katika kilindi kirefu cha mapenzi na Fernanda, alipelekwa kwenye kiza kizito cha

mahaba. Hakukumbuka ingawa alikuwa na ubongo, hakuona ingawa alikuwa na macho, hata

kusikia hakuweza kusikia. Sajenti alikuwa ametekwa kimapenzi na jinamizi jike la mapenzi

kutoka Brazili, ndiye Fernanda mwanamke aliyeshindika kwa utaalamu wa kutupa kete za

mahaba kwa kuku wake, Sajenti.

Sajenti alimbeba Fernanda licha ya kuwa na Jeraha mguuni, akambwaga kitandani Pwaa! Wote

walikuwa wapo uchi kama walivyozaliwa, rangi nyeupe ya Fernanda iliyavuta macho ya Sajenti

kama sumaku. Iliyalaghai na kuteka hisia zake. Hisia za Sajenti zilienda mbiombio bila uelekeo

maalumu. Udenda wa hamu ulimtoka. Mwili ulimsisimka, hamu ya kufanya mapenzi ilimvaa

kwa nguvu, akamrukia Fernanda pale kitandani na kuanza kumtomasa bila mpangilio, hii

ilimshangaza sana Fernanda, aliziona hisia kali na uchu wa kufanya mapenzi aliokuwa nao

Sajenti, Fernanda alijibinjua na kujiweka kijike shupa, akajishengendua na kujibetua kisha

akamgeuza ghafla na kumuweka Sajenti kwa chini. Akamkalia kisha akaanza kumrubuni kwa

kuzungusha kiuno chake laini kilichokuwa kimeshikiliwa na mkufu wa rangi ya silva. Alilegeza

macho yake makubwa hali iliyozidi kumpagawasha Sajenti. Shughuli ya kupeana mapenzi

ilianza rasmi, walipeana uroda kwa upendo usiokifani. Baada ya dakika thelasini wote walikuwa

hoi wakiwa wametosheka. Japokuwa kulikuwa na kiyoyozi lakini bado jasho liliwatoka.

“ Umenipa mbingu, nami nikakupa ardhi yangu yenye Rutuba uinyeshee na mvua yako. Natumai

tunaweza pata mazao msimu huu sio kwa mvua hii uliyoninyeshea. Nakupenda Otieno”

Fernanda alisema akiwa anampepea Sajenti huku akimchezea kifuani.

Maneno hayo yaliufungua moyo wa Sajenti akatabasamu, alielewa kile alichomaanisha

Fernanda, alijua Fernanda alikuwa akizungumzia suala la yeye kupata ujauzito. Jambo ambalo

Sajenti alilitamani kutokana na kuwa mpaka muda ule hakuwa na mtoto Licha ya kuwa na umri

wa miaka zaidi ya arobaini. Alimtazama Fernanda kisha akasema;

“ Nazeeka sasa, nywele zangu mpaka zinabadilika rangi, ona zilikuwa nyeusi lakini sasa moja

baada ya nyingine zinakuwa za kijivu. Uzee unanguvu kama upepo wa bahari, unanivuta kwa

nguvu. Tena wanivuta kwa hasira, huenda ningekuwa na mtoto ungenihurumia, lakini ninataka

kuondoka mwenyewe kama nilivyokuja bila ya uzao. Ningejivunia mengi, tena ningesifiwa kwa

mengi kama ningekuwa na mrithi. Lakini nimegeuka shamba lisilo na mazao, habari ya mtoto

imenikumbusha huzuni zote nilizowahi Kupitia….” Sajenti alisema, hapo uso wake ulikuwa

umebadilika sana, sura yake ilijawa na simanzi.


“ Inatosha, huna haja ya kusema yote, maneno yako hayafurahishi, ni kama wimbo wa huzuni

unaokaribisha upepo wa majonzi moyoni mwangu. Sitovumilia tena. Mungu ataotesha mbegu

katika shamba ulilopanda na kulinyeshea mvua, nawe utayaona matunda yako na kuyafurahia.

Moyo usife ganzi wala usikome kudunda kwa jambo hilo, jipe Moyo Otieno” Fernanda alisema,

sauti yake ikiwa imepoa yenye nguvu ya tumaini.

Otieno ndiye huyo huyo Sajenti Warioba, Fernanda hupenda kumuita Otieno kwa sababu ndilo

jina la kwanza alilomfahamia Sajenti Warioba siku ya kwanza walipokutana kule kwenye ile

Meli ya Ambagon, meli ya watu hatari, ambapo simulizi hii ipo kwenye kitabu cha “MLIO WA

RISASI HARUSINI” huu ukiwa ni mwendelezo wake. Hata hivyo Fernanda hupenda

kulifupisha jina hilo yaani Otieno na kuliita Otiti.




Walikumbatiana kwa huzuni penzi zito likiwazunguka, walikuwa wakipendana mithili ya njiwa.

Walijaliana na kuhurumiana, mapenzi yao yalikuwa kama kamusi ya kuelezea neno Upendo.

Kila mmoja alitamani kuwa na mwenzake.


Fernanda akiwa kifuani mwa Sajenti huku akichezea ndevu ndogo ndogo zilizomea kwenye

kidevu cha Sajenti, akasema; Mungu atakusaidia Mume wangu, yote yataisha. Nasi siku moja

tutaishi kwa furaha kama watu wengine. Umesikia Mume wangu?

“ Nashukuru kusikia hivyo Mke wangu Fernanda, umekuwa faraja kwangu, umekuwa kwangu

kama zawadi kuu. Siwezi kueleza namna ninavyoshukuru kukupata Fernanda. Nakupenda Mke

wangu” Sajenti alisema, wakakumbatiana mpaka pale usingizi ulipowapitia.

Jioni ilifika, Fernanda alizinduka kutoka usingizini. Alishtuka kutokumuona Sajenti Warioba

pale chumbani. Alitoka kitandani akaelekea chooni na bafuni kumtazama lakini hakumuona,

alichanganyikiwa akamuangalia mpaka chini ya uvungu, napo hakumuona. Akaenda dirishani

ambapo miale ya jua la magharibi lililokuwa linazama likimmulika usoni na miale isiyo na

nguvu. Alichungulia dirishani kwa nje, hakumuona. Sajenti alikuwa ameondoka.

Fernanda alilia sana, alilia kama mtoto mdogo akijigaragaza kitandani. Hakutakia kabisa kuwa

mbali na Sajenti, hakutaka Sajenti aondoke na kumuacha, alichotaka yeye ni kuwa naye kila

mahali kama mtu na kivuli chake. Sasa iweje Sajenti amuache peke yake. Aliamka akatafuta

simu ya Sajenti nayo hakuiona, akachukua simu yake akampigia simu lakini ikawa hapatikani.

Baadaye aliamua kuondoka pale hotelini na kuelekea nyumbani kwake, Mbezi Beach.


Siku, wiki na sasa Mwezi mmoja ulipita bila ya Fernanda kumuona wala kuwasiliana na Sajenti

Warioba, baada ya kumtafuta na kumkosa sehemu zote alizohisi kuwa angekuwepo. Fernanda

alikata tamaa kabisa ya kuweza kukutana naye. Leo Fernanda alikuwa amejipumzisha nyumbani

kwake, ilikuwa siku ya jumamosi akiwa sebuleni kajilaza kwenye sofa akitazama muziki wa

kizazi kipya, Fernanda alipenda muziki wa bongofleva licha ya kuwa yeye alikuwa ni chotara wa

Kibrazil na kitanzania. Alipenda sana utamaduni wa kitanzania, ndio maana mara nyingi

hupendelea kuweka miziki ya kibongo na filamu zake.


Punde mlango wake ulifunguliwa bila ya kubishwa hodi, alishtuka kuona mtu mmoja mrefu

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG