Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SAMAIRAH - 5

  

Simulizi : Samairah

Sehemu Ya Tano (5)


Jesca akazidi kukumbuka na sasa baba yake amemtamkia kuwa sharti la mganga aliyempa utajiri alikwisha kumwambia mama yake atakufa kwa ajili ya wivu wa mapenzi ,ndipo Jesca alijikuta akigonga kichwa chake kwa nguvu

Kwanini mimi nimekuwa na wivu ,ona nimempoteza mama yangu ,kwanini Samairah ,kwanini Samairah,Jesca alianza kupiga makelele huku baba yake , akimwangalia tu ,

Jesca alikuwa kavalia suruali ,aliingiza mkono mfukoni aliweza kutoa


Kikaratasi kidogo ambacho kilikuwa na unga ,tena unga ule hatari sumu ,ambayo Aryan alipuliziwa kwenye macho na mkandarasi ili awe kipofu ,maana huo unga ukigusana na maji ya aina yeyote na kugusa mwili wa binadamu basi mwili lazima ukatike katike vinyama ,


Jesca alijiona hana bahati pia kwenye ulimwengu hastahili kuishi upesi alikifungua kile kikaratasi alitoa ule unga akatia mdomoni ,kwa pembeni kulikuwa na chupa la maji lilikuwa na maji kidogo aliokota na kufungua upesi aliyanywa yale maji.


Dakika hazikupita hata mbili ki ukweli ile ilikuwa sumu kali mno ,alianza kukatika katika ulimi ,baba yake akimwongelesha mwanae ,aliita Jesca umekula nini mwanangu ,mwanangu nini umekula ,


Jesca tayari alishaanza kulegea alimwangalia baba yake kisha akamjibu ,baba nilisoma kwa dharau na kujiona mimi ndio mimi ,nikijua baba yangu unautajiri wa jasho lako kumbe utajiri wa kupitia waganga ,nimepata laana nyingi kwa watu niliringia utajiri wa kichawi baba mimi sifai kuisha kwa...


Jesca hata hakumalizia tayari alianza kutema vipande vya ulimi ,ulimi wa Jesca uliorojeka na kukatika katika ndani ya dakika mbili meno yalianza kutoka moja moja ,ile sumu ilikuwa haifai hata kidogo kila ikigusa kiungo kilikatika


Jesca alijikuta anadondoka chini utumbo wote ulisagika sagika baada ya kuimeza ile sumu ,baba yake alizidi kuchanganyikiwa ,aliita gari ili amuwahishe hospitali ya pale mwenge aliwahishwa na kupelekwa chumba cha watu mahututi ,kutokana na ile hospitali kuwa na uhaba wa vyumba ililazimika apelekwe chumba ambako Aryan yupo anatibiwa baada ya kuchoamwa na kisu.


Na Aryan alikuwa anatibiwa mahali alikochomwa na kisu,wakati Aryan ameshapoteza kumbu kumbu ,huku madaktari wakijitahidi kumpatia huduma .

Upande wa Jesca alivyoingizwa kwenye kile chumba aliko Aryan ,pale Aryan alijikuta akifungua macho alianza kupata ahueni alivyogeuza macho aliweza kushuhudia mwili wa Jesca ukifunikwa na madaktari kusema tayari ashakufa ila inaonekana amemeza sumu kali mno ,madaktari ilibidi wampasue tumbo Jesca waweze kujua nini hasa ama hio ni aina gani ya sumu ,kitendo cha kugusa tumbo la Jesca tayari lilikuwa lishaanza kuoza na kukatika katika ,ili bidi wamfunike na kupelekwa kwenye sehemu ya kuifadhia miili yaani mwochwari.


Baada ya Aryan kupata ahueni ,ndipo Samairah aliruhusiwa kuja kumwona ,Samairah alikuja akiwa katabasamu ila alikuta Aryan akiwa katika dimbwi la mawazo mazito akiwaza ,

Samairah aliuliza Aryan unaendeleaje? Aryan alimwangalia Samairah na kumwambia nashukuru mungu niko salama lakini Jesca kapatwa na nini mbona nimeshuhudia kama amekufa?


Samairah alimwangalia sana Aryan na kuguna " mmmmmmh we hujui ki ukweli Jesca kafariki na kajiua mwenyewe kwa kujua maovu yake aliyowatendea watu ,Samaira alimwambia Aryan.


Aryan aliuliza tena ,maovu gani hadi ajiue ?


"Samairah alitabasamu na kusema Aryan huwezi elewa kwa sasa ila ... Samairah hakumalizia na kuwaza itakuweje endapo Aryan atajua mimi si binadamu kamili?


Mara Samaira alitabasamu na kusema ,Aryan wacha leo nikuweke uwazi ,kiukweli ile ajali ambayo uliiona pale baada ya wewe kuchomwa na kisu ,ile ajali ndo ingetakiwa nife mimi ,ila mimi sikufanikiwa kufa wala kudhurika

Aryan alidakia sasa ni nani aliyekufa pale maana mie niliona viungo vimetengana mara miguu imenasa kwenye matairi ya gari utumbo ulidumbukia mtaroni ,

Sasa ni nani alokufa ?

Aryan aliuliza ili aweze kuelewa ,Samairah alikaa kidogo kimya kisha akamwangalia Aryan huku akahofia kusema ,lakini aliona akiendelea kumficha Aryan kwake itakuwa tabu kidogo maana Aryan anaandamwa na watu pasina sababu.


Samairah aliangalia kucha zake kisha akashika nackless aloivaa shingoni aliangalia chini na kumwambia Aryam

"Mtu alokufa sio mtu hilo lilikuwa boksi tu tena lenye taka taka ,hivyo mama yake na Jesca yupo hai tena yuko nyumbani

Ila Jesca ndio kafa sababu kajiua mwenyewe kwa kujutia aliyoyafanya.


Aryan ilibidi ainuke kitandani na kusema ile ajali ndo ilikuwa box?

Na si mtu kugongwa na gari?

Hebu niweke wazi Samairah nielewe....



Samairah aliangalia kucha zake kisha akashika neckless aloivaa shingoni aliangalia chini na kumwambia

Mtu alokufa sio mtu hilo lilikuwa boksi tu tena lenye taka taka ,hivyo mama yake na Jesca yupo hai tena yuko nyumbani

Ila Jesca ndio kafa sababu kajiua mwenyewe kwa kujutia aliyoyafanya .


Aryan ilibidi ainuke kitandani na kusema ile ajali ndo ilikuwa box Aryan alizidi kukodoa macho alijaribu kusimama ila mgongoni mwake palikuwa na jeraha alilochomwa kisu,

Samaira alisema ndio hilo lilikuwa box kwani wewe uliona nini?,Samairah alimuuliza swali Aryan,Aryan alisema "mbona niliona mwili wa mwanamke umesagwa sagwa na gari" ,kabla Samairah hajaeleza mama yake na Jesca aliingia hospitalini akiwa analia ,jamani mwanangu kwanini umeamua kujiua ,mimi mama yako bado niko hai ,

Kwanza hospitali nzima kila mtu aliacha kufanya shughuli zake na kumshangaa mama Jesca ,ki ukweli sura ya marehemu aliyeletwa kuwa amegongwa na gari ,ndio ile ile mama Jesca anaonekana mzima hali iliyowafanya watu kupata hofu na kujua labda maiti kafufuka.


Hata baba Jesca alimuogopa mkewe na kusema sielewi hata kidogo ,mama aliendelea kulia kwa kwikwi mno huku akitaja jina la mwanae, daktari ilibidi aondoke na madaktari wengine kwenda sehemu ya kuhifadhia miili ya marehemu ,walienda sehemu ambako walihifadhi mwili wa mama Jesca walifungua kila mmoja alibaki mdomo wazi na kuzidi kubaki njia pamda .


Ki ukweli walikuta mabox ,ilibidi watoke na kusema kweli huyu ndio mama halisi wa mtoto aliyekufa na ile ajali iliyotokea si ajali ya kawaida kama mlivyozoea ile ni miujiza ama mambo ya kishirikina lilikuwa box ambalo limegongwa na gari ,daktari alitoa ufafanuzi huku watu wakizidi kushangaa tukio hilo.


Wakati baba yake na Jesca anamwogopa mkewe alitoka nje na kutaka kukimbia japo alikuwa kavalia mavazi ya polisi usalama wa barabarani ,lakini wakati anatoka kwenye geti la hospitali alishangaa kuona njemba moja akiwa amefunika uso ,yule njemba hakupenda kupoteza muda alitoa kile kitambaa ambacho amefunika macho , ki ukweli hali aliyoiona kamanda wa polisi alianza kutetemeka ni mtu ambae anamjua vizuri

Si mwingine alikuwa Joshua ,ambapo kwenye vipande vilivyopita alipewaga kazi ya kuwaua akina Abbas na mdogo wake Gwae ,lakini hakuwaua na alishaeleza kazi yake huwa anapewa tenda za kuua watu.


Sasa leo kakutana na baba yake Jesca, ki ukweli baba Jesca alianza kukumbuka miaka ya nyuma iliyopita alikuwa anatembea na mke wa Joshua kisha alimpa mimba mke wa Joshua na kumtishia endapo atasema atamuua ,mke wake Joshua hakusema hadi alivyobanwa na Joshua alieleza kuwa ameahidiwa kununuliwa gari na kamanda Jacob ambae ni baba yake na Jesca ,


Ndipo Joshua alimuuaga mke wake baada ya kugundua anatembea na kamanda Jacob na kuahidi kuwa atamtafuta Jacob nae atampa malipo ya kutembea na mke wake ,sasa wamekutana .

Joshua alitabasamu na kusema kamanda, mimi muda wangu wa kuishi umekisha hivyo siwezi kukuacha tunakufa wote ,


Joshua aliongea kisha alifunua koti lake alitoa nondo iliyochogwa ncha kali kisha aliirusha na kuikita kwenye kitambi cha Jacob,pale pale Jacob alitoa jicho kubwa na kubaki ameganda kabla hajatulia Joshua alitoa panga na kumfyeka Jacob huku watu wakishuhudia.


lakini Joshua alipo maliza alitoa kachupa kadogo kalikuwa na ule unga ambao Jesca aliula na kufa papo hapo ,na Joshua aliuchukua ule unga akatia mdomoni akasukumizia na maji.


Joshua alikaa chini na kusema polisi nikamateni ,mara difenda ya polisi ikiwa imejaa polisi walifika pale hospitalini na kukuta Joshua kalala huku kafumba mdomo ,ki ukweli polisi walikuwa hawajui chochote walifika na kumwambia upo chini ya ulinzi bila yakujua kama amekula sumu ,

Huku wameshikilia bunduki zao ,mmoja alimsogelea Joshua alimgeuza Joshua akiwa hoi alitikisa kichwa kisha aliachama mdomo wake na kutema ulimi ukiwa na rangi nyeusi pale pale akafumba macho tayari alikuwa ameshafariki ,huku Jacob nae kauliwa pale pale hospitani. Ni matukio yaliyoacha historia na kuongelewa kwenye vyombo vya habari na mitaani.


Mama Jesca alitoka hospitali akiwa analia ,aliita mume wangu ile anataka kutoka alipishana na madakatari wakiwa wamebeba mwili wa mume wake ,pale pale mama alipoteza fahamu ,ki ukweli lile tukio liliweka historia kubwa mno .


Aryan aliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupata nafuu ,akiwa kaongozana na Samairah aliendelea kuuliza ,hivi ulishawai kuona ajali inatokea mtu amegongwa halafu unakuja kusikia mtu kagonga box? Aryan aliuliza huku akimwangalia Samairah ,


Samairah alianza kuwaza ni heri niondoke hapa duniani maana hata Aryan akigundua mimi si binadamu kamili ataniacha ,Samairah alikosa kabisa furaha na kukosa la kufanya ilibidi amchukue Aryan hadi nyumbani anakoishi alimkabidhi mama yake na kuwaaga Aryan na mama yake kuwa yeye anaenda mbali na hadhani kama atarudi tena waweze kuonana katika hii dunia.


Mama Aryan aliumia sana maana ametokea kumpenda sana Samairah alimpenda na wote hawajui kama yeye ni nusu mtu nusu jini ,Aryan nae alianza kuwaza matukio ya zamani wakiwa shuleni ,walikuwa pamoja alimletea chapati alimsaidia pesa za matumizi leo hii Samairah anasema anaondoka kwa nini ? Na anaenda wapi Aryan alizidi kujiuliza maswali pasina kupata majibu


Samairah alivyomaliza kuwaaga aliondoka lakini nyuma Aryan alimfuata na kutaka kujua kwanini Samairah anataka kuondoka ,

Aryan aliita "Samairah kwanini wataka kuondoka na waenda wapi?" Samairah alimwangalia Aryan na kumwambia naenda mahali aliko mama yangu na baba yangu ,Aryan alikaa kimya na kumuuliza wewe si uliniambia unaishi mikocheni sasa mama yako yuko wapi, Samairah alimwangalia Aryan kisha akaendelea kutembea ,maana anahofia kumweleza ukweli ,


Samairah aliuliza Aryan kwa mfano ukapedwa na jini na akataka muoane utakubali ? ,Aryan alicheka na kusema hata kwa dawa siwezi kukubali kupedwa na jini mimi, ki ukweli lile jibu lilimfanya Samairah adondoshe machozi maana mtu mwenyewe anayempenda hataki kusikia habari za majini halafu yeye ni jini.


Samairah alimwambia nenda kwa akina Abbas kamuulize gwae akuelezee kitu flani kuhusu mimi nakupa hiyo kazi ,Samairah aliongea kisha akapanda piki piki na kumwambia Aryan kwaheri hatuwezi tena kuonana , Samairah akiwa kwenye piki piki alikuwa analia na kujutia moyo wake kwanini ulimpenda Aryan wakati Aryan hataki hata kuoana na jini.

Samairah aliondoka hadi baharini ,alivyofika alikaa akajiinamia kisha alipangusa machozi yake na kusema naondoka mie sitakuona tena Aryanalikaa kimya kwa muda kisha alimuita mama yake kisha akaongea lugha isiyoeleweka alipotea na kwenda aliko mama yake ,aliumia sana maana Aryan kamwambia hawezi kuoa jini ,na swali lile Samairah aliuliza kwa mtego .


Tukirudi upande wa pili

Mama Jesca alizinduka kisha taratibu za mazishi ya mtoto wake pamoja na mume wake yalianza kuandaliwa akina Mussa walipata hizo taarifa za kupotelewa na Jesca na wao walienda kwenye msiba ,walifanikiwa kuwazika Jacob pamoja na mwanae Jesca, kiukweli ulikuwa msiba mkubwa sana kwa mama yake Jesca


Baada ya kumaliza mazishi walikaa siku kama kumi nyumba ya mama Jesca iliungua moto ,magari na kila kitu vyote viliteketea ki ukweli watu walijitahidi kuokoa vitu lakini vitu vilikuwa havibebeki hata kidogo vilikuwa vizito mno,yote sababu ya utajiri ulikuwa wakichawi ,mali zakamanda Jacob ziliisha na mama Jesca kuishi kama masikini ,alianza kutanga tanga mitaani nae alivyoona maisha magumu aliamua kujinyonga ,hivyo familia yote ilifariki.

Siku zilikatika hadi shule zilifunguliwa ,Aryan akiwa darasani alimkumbuka sana Samairah ,alianza kukumbuka jinsi alivyomuokoa alivyotekwa na akina Mussa ,


Jinsi alivyomdaka alivyotupwa toka gorofani na akina Mussa ,Aryan alizidi kusema hapana lazima nimtafute Samairah nimemkumbuka halafu nimeanza kuwa nae na hisia za kumpenda ,


Hatimae yalifika majira ya saa nane waliruhusiwa na kurudi nyumbani , siku hiyo Aryan alikumbuka alivyoambiwa na Samairah siku wakati anaondoka ,Samaira alimwambia ukitaka kujua yeye ni nani akamuulize Gwae ,maana Gwae ndio anamjua Samairah ni nani

" oyaa Abbas ndugu yangu leo sijielewi najikuta nimemkumbuka Samairah na sijui nitampata wapi maana aliaga anaondoka na mimi nilikosea sikumuuliza anaenda wapi ,hebu twende kwenu nikamuulize Gwae jambo flani ,

Waliondoka hadi kwa akina Abbas walifika na kumkuta mama Abbas akiwa na mama Ashura wamekaa kibarazani wakiwa wamejitanda vizuri mitandio yao wamefunga ushungi

Huku wakichambua njegere ,waliendelea na kupiga story zao.


Aryan alifika na kuwasalimia kwanza mama Ashura alivyomuona Aryan alitabasamu na kusema Aryan baba Assalam alaykum pole na masomo ,ki ukweli mama Ashura alikuwa kabadilika kawa mkarimu anaswali swala tano pamoja na mama Abbas huku wakiwa na chuo cha kufundisha mafunzo ya kiislamu.


Aryan aliitikia na kusema yes hadi raha watu ambao walikuwa wanaongoza kwa tabia mbaya mtaani leo hii wamekuwa watu wa dini ki ukweli inatia furaha sana.


Mara Gwae alirudi kutoka shule ,cha kwanza alienda hadi kwa mama Ashura alimsalimia ndipo mama Ashura akamsaidia kumtua begi la shule mama Ashura aliinuka na kwenda kumtengea chakula Gwae ,ki ukweli upendo ulizidi maana hata Gwae ashaponaga mikono yake iliyovunjika.


Baada ya Gwae kumaliza kula,Aryan alimwita Gwae kisha wakatoka nje lengo lake alitaka kujua Samairah ni nani , kwanza alimuuliza Gwae hivi tokea umemuona Samairah ulishawahi kuona kitu gani ambacho kipo tofauti na watu wengine ,

Gwae alishituka na kuinuka alianza kukimbia na kusema Samairah sio binadamu huyoo ile Gwae anakimbia ili asimweleze Aryan maana alishapewa onyo kali na Samaira asieleze chochote kuhusu Samairah aliambiwa asiseme chochote

Lakini Gwae alijikuta anamparamia kilema mmoja ambae alikuwa amekokotwa na kibaiskeli huku kaongozana na vijana saba.


Aryan kuangaalia mbele alijikuta amezungukwa na vijana saba waliojazia huku kwa mbele yake kuna kilema asiyekuwa na miguu wala mikono si mwingine alikuwa ni mkandarasi.


Mkandarasi alicheka kwa nguvu na kusema wewe kijana unanini mbona hufi nakufanyia kila kitu kibaya lakini hadi sasa hujadhurika sasa leo nimekuja ,mzima mzima ,sina mikono wala miguu ila leo lazima nikuue mwenyewe ha ha ha mkandarasi alicheka kwa dharau.........


Mkandarasi alicheka kwa nguvu na kusema wewe kijana una nini ? mbona hufi ?,nakufanyia kila kitu kibaya lakini hadi sasa hujadhurika sasa leo nimekuja ,mzima mzima ,sina mikono wala miguu ila leo lazima nikuue mwenyewe ha ha ha mkandarasi alicheka kwa dharau kubwa mno ,Aryan akiwa bado kahamaki wale vijana sita waliokuja nao walimshika Aryan upesi kisha wakamsukumiza matambara mdomoni ili asiweze kupiga kelele ,walimfunga kitambaa machoni kisha wakampakia kwenye gari ,mkandarasi alikuwa akichekelea wakati huo Abbas alikuwa yupo ndani anavua nguo za shule ,


Lakini mkandarasi aliamuru hata Gwae akamatwe na yeye sababu alishuhudia Aryan, wakimkamata wanahofia taarifa kuja kusambaa kutekwa kwa Aryan ,masikini Gwae bado mtoto mdogo lakini akaingia kwenye matatizo kama yale,

Abbas anatoka nje akiwaita Aryan na Gwae hakuona kitu ,alivyoangalia chini aliona kuwa kuna gari imekuja maeneo yale, Abbas hakuwa na mashaka sana alijua labda Aryan ameondoka na Gwae ,maana huwa anapenda kutembea nae.


Safari ya mkandarasi kilema iliishia maeneo ya salasala kuna jumba moja kubwa geti lilifunguliwa kisha akaingia ndani,Aryan akiwa kafugwa macho pamoja na Gwae walishushwa na kuingizwa ndani ,Gwae alikuwa akilia tu ,machozi ndio yalikuwa yakibubujika lakini sauti haikutoka yote sababu ya kufugwa matambara mdomoni,


Aryan alishushwa na mkandarasi kwakuwa ni kilema huwa anabebwa juu juu ama kutembea na baiskeli yake ,Aryan alishushwa chumba kimoja pamoja na Gwae na kile chumba kilikuwa na giza totoro. walitolewa matambara mdomoni kisha wakaambiwa nawapa dakika kumi kwa ajili ya sala ya mwisho .msali maana leo lazima mfee ,"mkandarasi aliongea" na kupelekwa kwenye meza ya chakula .alilishwa kama mtoto yote sababu hana mikono wala miguu.


Aryan alijua fika leo hawezi nusurika kamwe alimshika Gwae mkono na kumuuliza ,Gwae leo ndo tumeambiwa tunauliwa naomba unieleze chochote kuhusu Samairah japo ashaondoka ila ningependa kujua ,yeye ni nani ,

Gwae alimshika Aryan mkono kisha akasema ,kaka Aryan ,mi najua Samairah si kiumbe mbaya ,alitusaidia sana pale mama yetu alivyokuwa akinywa pombe na kutaka kutufukuza ,Samairah alikuwa yupo upande wetu ,vile vile mimi nampenda sana aunt Samairah kwanza anapenda kucheka cheka muda wote . Gwae aliongea huku akionesha sura ya huzuni ,aliendelea kueleza.


"Kunasiku mliniacha nyumbani kwenu mbezi Samairah alikuja na kunikuta nimekaa ndani ,Samairah alisema anahisi joto ,na siku hiyo hapakuwa na umeme ,alitoka zake nje na kuzunguka nyuma ya nyumba,.


Mimi nilijua labda kaondoka nilianza kuzunguka nyumba ya kwenu taratibu nikishangaa maua ,ki ukweli nilishituka baada ya kumwona aunt Samairah kajiachia, kwanza

Miguu yake ni kwato kama za farasi alikuwa na manyoya mepesi na meupe mazuri ,ila alikuwa na kichwa cha binadamu ila kichwani alikuwa na masikio makubwa ,

Nilivyomuona tu alishituka na kurudi kwa umbo lake la kawaida ,na kuinuka upesi, kuja kushituka kanishika mkono ,


Ki ukeli nilimuogopa sana ila aliniambia nisiseme chochote kuhusu umbile lile nililo liona ,ndipo nilipataga ujasiri na kumuuliza wewe ni nani ,aunt Samairah aliniambia kuwa yeye ni jini ila jini asiyedhuru watu ovyo.Basi tokea siku ile sikumuogopa tena ,


Gwae alimalizia kuelezea na kumfanya Aryan akumbuke kabla Samairah hajaondoka alimuuliza swali mfano ikitokea ukipendwa na jini utaweza kumuoa ,Aryan alitabasamu na kusema khaa kumbe lile swali alikuwa anajiongelea yeye , moyoni Aryan aliwaza Samairah nakupenda hata kama wewe ni kiumbe tofauti na mwanadamu.

Ile Aryan kusema kimoyo moyo kuwa anampenda Samairah ,chini ya bahari ndipo makazi ya Samairah yalipo pamoja na familia yake ,ujumbe aliupata ,kipindi chote Samairah toka aondoke kwenye ulimwengu hakuwa na furaha lakini siku hiyo alijikuta akitabasamu baada tu ya Aryan kusema na nafsi yake anampemda Samairah.

Yaani Samairah alikuwa akisikia kila kitu Aryan anachozungumza na aliamini huenda ipo siku Aryan atasema anampenda hatimae ndoto zake zimetimia.


Samairah alitabasamu na kusema kama kweli Aryan ameridhia kunipenda ,basi sina budi ya kuishi mwenyewe acha nianze safari ya kurudi duniani tena kwa ajili ya Aryan,

Samairah alimuaga mama yake kuwa anatoka kidogo mama yake alimruhusu kisha alijiandaa kuondoka kuja duniani kwa ajili ya Aryan.

Maana kwenye moyo wake alisikia Aryan alivyojisemea kimoyo moyo kuwa anampenda yeye.


Turudi mahali Aryan na Gwae walipo taa ziliwashwa kisha mkandarasi akiwa kaongozana na vijana watatu aliingia chumbani akiwa amekokotwa kwenye baiskeli ,hatimae aliingia hadi ndani.

Mkandarasi alimwangalia Aryan na kumwambia wewe kijana mimi nishakuambia hadi kufa kwangu lazima nikuue,,najua nitakufa nikiwa na chuki mbali mbali nimeua watu wengi sana najua nitaenda kuchomwa moto siku yangu ya mwisho .


Mkandarasi aliomba Aryan akamatwe kisha asogezewe shingo ya Aryan karibu na mdomo wake ,wale vijana walifanya kama alivyowaambiwa ,mkandarasi alicheka na kusema nakung'ata kwenye koo halafu damu yako niinywee ili ujue kuwa nina hasira na wewe,umenisababishia nipate ukilema sasa sitaki kukuona kwenye hii dunia, mkandarasi aliupeleka mdomo wake ili amng'ate Aryan koo ili afe yote sababu hana mikono na hataweza kumshika ,wala kumpiga


Lakini kabla hajamng'ata kuna mdada alikuja na kumwita baba samahani nakuomba mara moja , mkandarasi aligeuka na kuuliza kunanini mwanangu? Aryan aliachiwa na kusimamishwa ,ukweli Aryan alibaki ameduwaa baada ya kumwona Joyce akiwa kavalia suruali iliyo mbana ,Aryan alishangaa imekuwaje asome na Joy kumbe baba yake ndio mkandarasi.


Aryan alishidwa kujizuia aliita Joy,pale Joy kugeuka alimwona Aryan maana hata Joy anampenda balaa alikimbia na kutaka kumkumbatia lakini alizuiliwa na kuambiwa atoke kwenye kile chumba. Ki ukweli Joy alilia baada ya kuona kuna panga kwenye kile chumba mahali aliko Aryan na anamjua baba yake akiletaga mtu nyumbani ujue kuna jambo,

Joyce aliondoka na kwenda kuchukua simu aliwapigia akina Mussa na kuwaomba waende nyumbani kwao wakamsaidie,

Joy aliwapigia cm wabaya wake Aryan ,akina Kudra na Mussa ,ukweli Kudra anajua kuwa Joy ni mtoto wa kaka yake ila huwa anamchukia sana Joyce maana yeye ndio wa mwisho katika familia ya mzee Kiza na yeye ndie atakae achiwa mali nyingi ndio maana anakuwaga na kiburi kibaya sana.


Mkandarasi aliwaamuru vijana wake wamlaze Aryan chini walitekeleza, Aryan alilazwa na kukandamizwa miguu na mikono ,kisha nondo mbili zilizochongoka zililetwa kisha wakaambiwa waziingize machoni mwa Aryan ,

Basi kijana mmoja aliinama ili azipigilie machoni mwa Aryan,ndugu msikilizaji yaani nondo inagongelewa kwenye jicho na inaurefu wa sentimita 40 Aryan akiwa kapoteza tumaini aliyafumba macho yake kisha akasubiri kitakachotokea kitokee ,

Jamaa aliiweka nondo kwenye jicho la kushoto kisha akachukua nyundo agongelee ,lakini kila akipeleka nondo kwenye macho ya Aryan anajihisi kizungu zungu kikali na kushidwa kugongelea kila akijitahidi ndipo kizungu zungu kinazidi kuongezeka , yule jamaa ilibidi amwambie mkandarasi sielewi kila nikitaka kugonga hii nondo nasikia kizungu zungu mno kidogo nidondoke.


Kwa nje ya hiyo nyumba tunamwona mwanadada akiwa amejitanda ushungi mweupe pee alitembea huku akiangalia huku na kule ,mara kuna gari iliingia nyumbani kwa mkandarasi Jaoy alitoka upesi na kuwafungulia walikuwa ni akina Mussa Joy aliwaelekeza mahali aliko Aryan ili wakamuokoe.


Lakini Joy alivyowaambia kuwa anaenda kuwaokoa akina Aryan na Gwae pale pale Kudra alicheka na kusema kumbe tumemnasa huyo choko kirahisi walienda upesi na kuingia chumba aliko Aryan akiteswa.


Kwanza walikuta amechanjwa na wembe mwili mzima ,huku akipigwa virungu kwenye magoti ila kila wakitaka kumdhuru macho walikuwa wanashidwa mkandarasi alimwagiza kijana wake mmoja akalete ile dawa ya unga ili wamwekee Aryan kwenye macho ,

Mkandarasi aliendelea kuongea" we kijana nimetokea kukuchukia umenisababishia ukilema hadi nami nikupatie ukilema ile sumu ililetwa na wakaambiwa wamuwekee machoni lakin Mussa alikataa na kusema haihitaji hivyo inabidi tumchinje ,Mussa alitoa wazo Aryan achinjwe maana na wao waliingilia kati.


Mussa alitoa kisu na kutaka kumchinja walishangaa Aryan akainuka zile kamba walizomfunga zilifunguka.

Kwa nje walisikia sauti zikiwaita Kudraa ,Kudraa njoo na Mussa upesi Kudra alitoka kuwahi mahali anakoitwa ki ukweli ile sauti Kudra aliifahamu na alikimbia huku akisema mama umepatwa na nini?

Wakati Kudra anakimbia kutoka nje akidhania anaitwa na mama yake. Huku Mussa nae alimfuata akiwa kashika kisu baada ya kugairi kumchinja Aryan.


Pale pale Aryan alipata nafasi ya kutoka na ili akimbie ,wakati Kudra akiwa nje aliona kama mama yake anamwita huku akikimbilia kwenye korongo flani na kinachomshangaza alikuwa anakimbia kwa kasi sana toka azaliwe hakuwahi kumwona mama yake akikimbia namna hiyo hilo jambo lilimtia wasiwasi "inawezekana vipi mama yangu akimbie namna hii?"

Mussa na kudra walianza kukimbia ili kubaini mama yake amefanyaje mbona anakimbia.


Kwa mama Kudra akiwa anakimbia huku anageuka nyuma bahati mbaya kwa mbele kulikuwa na korongo refu mno ,gafla mama Kudra alijikwaa na kudumbukia kwenye lile korongo lilikuwa refu mno ,uwiiiiiiiiiiii mama alipiga yowe huku akibiringita na kwenda kujibamiza kwenge gogo la mti chini pwaaa ,mama alipasuka kichwa kikajigawa mara mbili

Wakati huo akina Mussa na Kudra nao wamefika eneo hilo wakati wanachungulia kwenye lile korongo refu ,bahati mbaya Kudra nae aliteleza wakati anataka kujiokoa nae asidumbukie alimshika Mussa akamvuta na Mussa nae akayumba akadaka kimti kidogo wakati huo Kudra kashikilia mguu wa Mussa na Mussa kashikilia kimti kidogo mno.


Walianza kupiga kelele jamani msaada msaada

Kudra aliangalia chini anamwona mama yake kalala chini huku kichwa kimepasuka kati kati na ubongo umemwagika akiangalia juu kashikilia mguu wa Mussa na Mussa kashika kimti kidogo.

Mara Aryan baada ya kuwakimbia wale vijana wanaotaka kumuua ili kujiokoa asiuliwe na mkandarasi alitokea kwenye lile korongo na kuwakuta Mussa na Kudra wamening'inia, endapo Mussa ataachia kale kamti .wakidondoka chini lazima wafe

Maana chini palikuwa na umbali mrefu ,sasa Aryan kasimama anawaangalia wakilia na kuomba msaada ,

"Aryan tusaidie ndugu yangu" Mussa alianza kujitetea na kumwita ndugu yake wakati huo alishika kisu na kutaka kumchinja mara gafla kale kamti alokuwa amekashikilia kalianza kung'ooka mizizi mara kakakatika ......




Tulipo ishia jana baada ya akina Mussa kuning'inia kwenye poromoko ama korongo refu walianza kupiga kelele jamani msaada msaada !!!!! .

Kudra aliangalia chini anamwona mama yake kalala chini huku kichwa kimepasuka kati kati na ubongo umemwagika akiangalia juu kashikilia mguu wa Mussa na Mussa kashika kimti kidogo.

Mara Aryab baada ya kukimbia ili kujiokoa asiuliwe na mkandarasi alitokea kwenye lile korongo na kuwakuta Mussa na Kudra wamening'inia, endapo Mussa ataachia kale ka mti wakidondoka chini lazima wafe maana kuna magogo kwa chini .

Na chini palikuwa na umbali mrefu ,sasa Aryan kasimama anawaangalia wakilia na kuomba msaada ,

"Aryan tusaidie ndugu yangu" Mussa alianza kujitetea na kumwita ndugu yake. wakati huo alitaka kumkata na kisu na kutaka kumchinja.


Wakiwa wanahangaika kujiokoa mara gafla kale ka mti alokuwa amekashikilia kalianza kung'ooka mizizi mara kakakatika


Aryan aliwaza kwa haraka na kujisemea mimi sio mtoa hukumu japo wanayaandama maisha yangu ,bila sababu wacha niwasaidie Mungu ndiye anaetoa baraka na hukumu ,Aryan aliwahi na kuudaka mkono wa Mussa na kuanza kuuvuta huku Kudra kashikilia mguu wa Mussa , Aryan alijikaza kwa nguvu zake zote na kuanza kuwavuta taratibu taratibu hatimae alifanikiwa kuwatoa nje wote wawili .wakiwa hawaamini kama wametoka salama ,Mussa na Kudra wakiwa wanahema juuu juu ,baada ya kunusurika kufa.

Lakini Aryan aliinuka ili aondoke maeneo yale maana anajua fika licha ya kuwasaidia pia wataweza kumdhuru ,mara kikundi cha mkandarasi kilikuja wakiwa wamembeba Gwae juu juuu ,Aryan aliwaza hawa watu hawana nia njema huenda wanakuja kumrushia Gwae kwenye hili korongo ,na kweli waliweza kufika maeneo yale Aryan alitaka kukimbia ila Mussa alimshika shati na kumwambia oya we boya sisi hatujakuomba utusaidie kwenye hili korongo .kwanza sisi tungejiokoa wenyewe halafu mie nimejifunza makareti hatari hapa ningejibinua na sarakasi wala nisingekufa sasa Mussa aliongea huku kamshika Aryan mkono.

Unaliona hili korongo tuna kudumbukiza sasa zamu yako kudumbukia kiherehere chako tu cha kutusaidia sisi hatunaga huruma ,wakati huo mkandarasi nae kafika akiwa amekokotwa kwenye baiskeli yake ,alimwona Aryan na kumwambia we kijana huwezi nikimbia kamwe hapa lazima ufe leo bado kauli yake ilibaki pale pale lazima Aryan afe.

Wakati huo Kudra alikimbia na kwenda chini ya lile korongo pale ambako alihisi mama yake kaangukia na kupasuka kichwa lakini cha ajabu alifika wala hakuona damu wala aina yeyote ya mtu ,Kudra aliita mama ,mama!!!!!!! Lakini hapakuwepo na mtu wa aina yeyote aliangalia chini ya lile korongo akaona nyayo tu za pundamilia zimepita eneo hilo la korongo.

Kudra ilibidi atoke kwenye lile korongo hadi nje kabisa alijaribu kumpigia mama yake simu,mama alipokea simu na kusema yupo salama tena yupo kwenye kikao ,cha kushangaza mama yake alikuwa yupo kwenye kikao tena mzima wa afya Kudra alizidi kuchanganyikiwa ,mbona nilimwona mama yangu kabisa kadondokea kwenye hili korongo sasa mbona simwoni ,Kudra hakuelewa ni mchezo gani anauchezewa alihisi yupo ndotoni lakini hakuwa amelala.


Alitoka hadi kwa akina Mussa alifika mahali pale mara kwa mbali aliwaona Joyce akiwa na Samairah wanatembea huku wakielekea mahali aliko Aryan pamoja na kundi la akina mkandarasi.


Aryan aliweza kumwona Samairah aliwaza huenda atamsaidia lakini aliwaza atawezaje kumsaidia angali yeye ni mwanamke? Aryan alikuwa bado hana tumaini la kupona ama kujiondoa mikononi mwa wabaya wake.

Aryan aliwaomba wa mwachie Gwae aondoke ili kama wataweza wamuue yeye ila Gwae abaki ,

Mara Gwae alimwona Samairah aliita antiii umerudi??? Antiii antiii ,Gwae alifurahi kumwona Samairah kwa mara nyingine.


Pale ndipo Mussa alipomuona Samairah akaanza kufanya masifa alimshika Aryan ili amsukumize korongoni kwa bahati mbaya kamba ya kiatu chake ilikuwa imetoka sasa aliikanyaga na mguu mwingine ile anafanya rafu amrushie Aryan kwenye korongo

Mussa alijikuta kayumba na kuporomoka kwenye korongo huku akipiga kelele za kuomba msaada jamani nakuuuu faaaa

Hapakuwa tena na msaada alienda mzima mzima korongoni.


Huku akina Kudra wakiwa wanashangaa baada ya Mussa kuteleza kwenye korongo ,wakiwa bado hawaja kaa sawa gafla kalizuka ka upepo chenye vumbi jingi kaliwazunguka mahali waliko akina Kudra ,mkandarasi na kikundi chake

Kibaiskeli alichokuwa nacho mkandarasi kalianza kuserereka taratibu na kufika kwenye korongo unaambiwa mkandarasi alitangulia na kuanza kubiringita kwenye lile korongo ,hakuwa na mikono wala miguu hivyo alikwenda kujibamiza kwenye aridhi unaambiwa shingo yote iliingia tumboni .


Huku utumbo wake ulipasuka pale pale mkandarasi alipoteza maisha huku pembeni Mussa nae kavunjika vunjika kila kiungo nae alipoteza maisha,,kale kaupepo kalichozuka gafla kaliisha wakati huo Gwae ashafika kwa Samairah na kumkumbatia,Aryan akimwangalia Samairah na kukosa nini afanye

Joy alimkimbilia Aryan na kumkumbatia huku kikundi cha mkandarasi wakishuka bondeni kwenye like korongo kwenda kuutoa mwili wa mkandarasi na Mussa.


Kudra alinusurika pale pale alimpigia magoti Aryan na kumwomba msamaha kwa yale yote mabaya aliyoyafanya na kumshukuru kumuokoa kwenye like korongo ,wakati Kudra akiomba msamaha huku rohoni akiwaza wewe mpuuzi kaka yangu Yusuph amefariki ambae ndio mkandarasi na Mussa rafiki yangu amefariki yote sababu yako sasa endapo utakubali kunikumbatia ili tusameheane itakuwa imekula kwako na ndio utakuwa mwisho wa uhai wako,,ni wazo alilowaza Kudra moyoni mwake.


Basi aliendelea kuomba msamaha huku akilia machozi ya kinafiki ,siku zote Aryan huwa ni mtu anaependa amani ,alimsogelea Kudra alimshika mkono na kumwambia yaishe nishakusame....

Kabla hajamalizia ni kosa kubwa mno alilo fanya ,kumpa Kudra mkono ,Kudra alimvutia kwenye korongo,Aryan aliserereka mzima mzima lakini kabla hajadumbukia alishangaa mkono wake umedakwa

Kucheki nani kaudaka mkono wake alikuwa ni mrembo Samaira akiwa amemkodolea macho ,Samairah alianza kuwaza ,wewe ndiye umenifanya nimerudi kwenye huu ulimwengu sasa hawa watu wanaokufanya ukose amani leo ndio mwisho wao.


Samairah alianza kumvuta Aryan taratibu huku akisaidiana na Joyce ,pale ndipo Kudra aliwaza kwa mara nyingine ya kumuua Aryab pale pale korongoni,nyie mnajifanya mnamsaidia ee sasa nawasukumiza wote Kudra aliwaza huku akionekana mwenye hasira na kulipiza kisasi.


Ile anapiga hatua akawasukumize alishangaa tumbo linamkamata huku anajisikia kizungu zungu kikali ,alijaribu kusimama alijikuta anayumba huyoooo aliporomokea kwenye korongo wakati huo Aryan ashatolewa na Samairah waliondoka eneo hilo upesi na kuanza kukimbia wakiwa wanne ,Arysn,Gwae Joyce na Samairah ,baada ya kufika mbali ,Aryan ilibidi amuulize Joyce ,

Vipi Joyce mbona umeungana na sisi? Wakati baba yako nae kafia kwenye korongo, Joyce alitabasamu na kuwaambia

Ni story ndefu mno ila kwa ufupi yule si baba yangu kabisaa

Baba yangu walishakufaga kwenye ujenzi wa gorofa moja maeneo ya mbezi kimara wakati huo Yusuph alikuwa mkandarasi ,wa hilo gorofa ,mama yangu alikuwa akiuza chakula kwenye lile gorofa alikuwa akiwapikia wajenzi na vibarua lakini cha ajabu Yusuph ambae ni mkandarasi alisababisha kifo cha

,mama yangu alikuwa akipika chakula chini na yeye akiwa juu alichukua tofali toka juu na kwenda kumpiga mama yangu kichwani mama yangu alifia hapo ,huku baba yangu alipigwa shoti ya umeme siku hiyo hio kwenye hilo gorofa ,

Mimi sikuwa na ndugu ndipo huyu mkandarasi alijitolea kunilea.


Aryan bana naomba tuishie hapo maana nikiendelea kuwapa story nitajikuta naanza kulia ,basi waliacha na kuondoka wote hadi maeneo ya mbezi mahali anakoishi Aryan ,njia nzima Aryan alikuwa akiwaza ina maana Samairah ni jini? Au wamemsingizia maana wanaona mzuri na kaumbika ,Aryan aliwaza na kujikuta akitabasamu ,na kusema yes Samairah ni kisura kiukweli hamna mfano ,japo nilisema sitopenda tena wanawake ila Samairah hata nikiambiwa ni vempare nitakuwa nae.

Wakati Aryan anayawaza hayo alikuwa ameshikilia mkono wa Samairah huku wakitembea taratibu ,alijikuta hisia za mapenzi zinaanza kumtembelea Aryan alishidwa kujizuia alimwangalia Samaira na kumwambia

Samairah wew ni nani?


Lile swali lilimfanya Samairah akose tena furaha na kuhofia akimwambia tu yeye ni jini Aryan hatakubali kuwa nae ,sasa Aryan kasimama kwenye njia katikati na kumuuliza Samairah wewe ni nani?

Samairah alimwangalia Aryan kwa huruma na kujisemea moyoni "yaani Aryan ungejua ninavyokupenda wala usingenitesa hivi nimekuja kwa ajili yako ila kama bado unaniuliza maswali hayo heri nirudi zangu tu nikae mbali na wewe"


Wakati Samairah anawaza Aryan alimshika mkono Samairah na kumvutia kwake ,hapo hapo Samairah yeye alikuwa anasikia raha mno akiangalia macho ya Aryan na kusema wewe mwanaume kwanini ulipendelewa uzuri namna hiii

Pale Samairah alianza kulegeza macho na kusahau kama kaulizwa swali na Aryan.


Gafla Aryan alivutwa mkono na Joyce ,"Joyce aliwaangalia Aryan na Samairah na kushangaa hivi ninyi mnapendana eee ,Mungu wangu ,ila kama Samairah unampenda Aryan mimi sina kinyongo na wewe kuanzia leo nitakuwa rafiki yako japo nampenda sana Aryan ila nitakuachia.


Wakiwa wamesimama njiani kandokando ya barabara ,kuna mtu akiwa kavalia mavazi meusi tiii alishuka kwenye gari akiwa ameongozana na vijana wawili wakiwa wamevalia suti nyeusi

Yule mzee alitoa miwani yake na kuuliza ndio hawa ? Mbona wanaonekana wadogo ,aliongea huku akitoa bastola mfukoni.


Kijana mmoja alidakia na kusema Mr Kizaa ndio hawa waliowaua watoto wako kwenye korongo.


Aryan kugeuka tu mlio wa risasi ulisikika tii tiii tii tiii zilipigwa risasi nne ,akina Aryan,Samairah ,Joyce na Gwae wote wakawa wameshalala chini ,Mr Kizza alisema hapo vipi kawakagueni kama bado wako hai na hata mkikuta wanahema wapigeni tena risasi zingine wafe pale pale haiwezekani waue watoto wangu Kudra na Yusufu nami nimewaua wabaya wenu mkakutane kuzimu pamoja .

Yule mzee Kiza baada ya kuwapiga risasi akina Aryan,aliondoka na kuingia kwenye gari kisha akaiangalia bastola yake na kusema ,wasalimieni kuzimu...




TULIPOISHIA Aryan kugeuka tu mlio wa risasi ulisikika tii tiii tii tiii zilipigwa risasi nne ,akina Aryan ,Samairah ,Joyce na Gwae wote wakawa wameshalala chini ,Mr Kizza alisema hapo vipi ,hebu kakagueni kama bado wako hai waongezeeni risasi na kuhakikisha wamekufa kisawa sawa ,aliongea kisha akakaa kwenye gari yake.


Yule mzee alikuwa anajiona vibaya mno aliangalia saa yake mkononi kisha akasema harakisheni nikazike wanangu ,wale vijana wake walienda kukagua kama Mr Kizza kafanya kazi yake ,

Kijana mmoja alimwangalia Kizza na kusema boss ndio maana umepewaga jina Kiiza au kisa wavaaga mavazi meusi kama giza nini ,wale vijana waliwakagua akina Aryan kama kweli waoivyopigwa risasi na Kizza wahakikishe kama wamekufa. Huku Kiza anawaza mambo yake ,Samaira aliinuka na kuwaangalia wale vijana ndani ya sekunde moja wale vijana walianza kucheia damu huku kila mmoja kashika kifua chake ,ndipo Mr Kizza alishuka kwenye gari na kwenda kuwatazama vijana wake aone wamekubwa na nini ki ukweli walikuwa wamepigwa risasi kifuani ,jambo lililomfanya Kiiza kuhamaki ,aligusa masikio yake na kusema mbona sijasikia mlio wa risasi hawa vijana wamefanyajwe? Kizza aligeuka kuwatazama akina Samairah ni kosa moja alilofanya,Samairah aliiangalia ile bastola yake kwa sekunde kisha akacheka ha ha ha.


Kiza aliangalia bastola yake huku kuonekana kuchanganyikiwa na kujisemea ina maana sijamlenga huyu bint? Kisha akamnyoshea bastola Samaira ,wakati huo Aryan ,Gwae na Joy wamedondoka chini wakiwa hawajitambui ,

Samairah alicheka na kutabasamu kila mara , Mr Kizza kafyatua risasi nyingine pale Samairah aliiangalia ile risasi upesi kisha akamtizama Mr Kiiza kwenye paji la uso.

Yaani Samaira alikuwa na uwezo wa ajabu akikuangalia mahali kama wataka kumfanyia ubaya basi ubaya unakurudia wewe mwenyewe.

Basi alivyo mtizama Mr Kizza kwa umakini ,kitendo cha Kiza kufyatua risasi ile risasi ilimgeukia mwenyewe na kutua kwenye paji la uso pale pale Kiza alidondoka kama gunia la mkaa chini huku damu nyingi zikiwa zinamtoka kwenye paji la uso.

Taratibu Mr Kiza alijinyoosha na kukata roho na kuwaacha akina Samairah wako salama kabisa wala hawakuguswa na risasi ya aina yeyote zile risasi ambazo Kiza aliwapiga ,hazikuwapiga akina Aryan bali Samairah kwa uwezo wake alizigandisha hewani ndipo wale vijana wa Kiza walivyoenda kuwakagua ,zile risasi aliziachia na kuwapiga vifuani hatimae kusababisha kucheua damu na kupelekea kufa pale pale.


Samairah aliwainua akina Aryan na Joy wakiwa hawaelewi kilichotokea walikuwa na kumbu kumbu kuna mtu alikuja na gari alishuka na kuwanyooshea bastola lakini kilichoendelea hawakikumbuki. Basi Samairah aliwaambia twendeni nyumbani walienda hadi kwa akina Aryan ,walipofika waliingia bafuni kila mmoja akaoga kisha Samairah alisema ana maongezi na akina Aryan pamoja na Joy.


Wakati huo mapolisi walifika eneo la tukio na kumchukua Mr Kizza akiwa tayari ashapoteza maisha na vijana wake walienda kuwapima hospitalini ili kubaiini muuaji lakini cha ajabu kila wakijaribu vipimo ,majibu yalitoka giza totoro hapakuwa na picha wala mtu alowaua kesi ikawa imeishia hapo .


Tukirudi kwa akina Aryan walivyomaliza kula kisha mama yake na Aryan alifurahi kumwona Samairah kurudi ,Samairah aliomba awaeleze nia yake ya kurudi tena na kuwa karibu na Aryan ,kwanza kabisa alimwambia Joyce ,kuanzia leo utaishi hapa kwa akina Aryan sisi tutakutunza utaishi utakavyo ki ukweli Joyce alifurahi maana hana wazazi zamani alikuwa akiishi kwa mkandarasi nae ashakufa.


Ndipo Samairah alilitoa lile bangili aliliweka mezani ,kisha akamwita Gwae na kuuliza umeliona hili bangili? Gwae alitabasamu na kufanya upengo wa magego mawili ya juu uonekana na kusema ndio aunt nimeiona,Samairah alishusha pumzi na kumuuliza Aryan hii bangili uliiokota wapi ,

Aryan alivuta kumbukumbu na kusema kuwa aliiokota baharini kipindi walipoenda baharini na baba yake kwa ajili ya kupata utajiri , Samairah alitabasamu na kueleza kuwa hii bangili inamilikiwa na majini ,ila nawaomba msiniogope ukweli mimi ni jini ila nusu mtu nusu jini ,tokea nilipozaliwa nilipewaga hii bangili kwa ajili kuwa malikia wa viumbe aina ya majini wekundu lakini ilikuja kutokea vita kubwa sana ya majini ndipo nilinyang'anywaga hii bangili ,siku ambayo watu walishuhudia mwezi ukimezwa na jua na ndio huwa siku ya watu kupata utajiri ukienda kwenye kingo za bahari unaweza okota madini ama vito vya dhahabu ,na vya thaman sana.


Lakini siku hio bahari ilikuwa tofauti iliweza kuwameza watu wote alinusurika Aryan ambae aliachwa na baba yake mbali na bahari ,ndipo kuna ndege wa blue anae tokea katika falme za majini weupe alipopita usawa alikokaa Aryan aliidondosha hii bangili na Aryan alifanikiwaga kuiokota hivyo hii bangili ndio utajiri wenyewe ndio maana siku mama yangu alipoiona hii bangili aliwanunulia hii nyumba na kusema kuwa mnatakiwa muishi pazuri kila kitu mnachotaka mtakipata ,pia mama Aryan pole kwa kupotelewa na mume wako ambae ni baba yake na Aryan .


Hii bangili huwa haipotei ndio maana siku ya kwanza mama aliponiona kwa marehemu Jesca ulinivalisha yote sababu hii bangili ni yangu,na mateso yote anayoyapitia Aryan ya yametokana na waganga walikuwa wanawaelekeza watu katika familia yenu mtu akitaka utajiri,walipewa sharti yeyote akifanikiwa kumuua Aryan lazima ataipata hii bangili na akisha imiliki anaeweza kuwa tajiri wa dunia.


Samairah aliwakumbatia wote kisha akaaga anarudi aliko toka maana anahofia kujitambulisha kuwa yeye ni jini ,lakini cha ajabu kila mmoja alimkumbatia na kumwambia hapana kurudi huko tunaomba uishi huku uishi na sisi.


Gwae alimwangalia na kumuuliza aunt nasikia majini wanaweza kupotea kama upepo ni kweli? Samairah alimwangalia Gwae na kumshika mashavu na kumwambia ndio tuna uwezo wa kupotea ,Gwae alimwambia huwezi aunt kama kweli wewe ni jini hebu potea nione maana mie nilikuona kama vile farasi na zile kwato zako

Samairah aliwaangalia wote na kuwauliza mnaniruhusu nipotee?

Mama Aryan alimwangalia mwanae kisha akamwangalia na Joy kisha wote walimwambia potea tuone.

Samairah alifumba macho sekunde akatoweka kila mmoja alishtuka baada ya dakika moja walisikia akitoka ndani ya chumba akiwa ameshikilia jagi la juice basi ilikuwa furaha kubwa ,walimzoea na wakawa wanaishi nae akitaka kupotea anapotea na akirudi anarudi wala hamna mtu anaeogopa.


Gwae akawa anapenda kukaa na Samairah alikuwa akiondoka tegeta na kwenda mbezi kwa ajili ya kumwona Samairah ,ndipo Samairah aliamua kununua nyumba mbili zikiwa zimefuatana tena za kisasa ndipo alimuhamisha na mama yake Abbas, walianza kuishi wote mbezi walikuwa marafiki toka zamani na mama Aryan. Maisha yalizidi kusonga mbele huku penzi la Aryan na Samairah likizidi kukua .


Samairah hakuishia hivyo alimfungulia duka kubwa mama Ashura la nguo yote sababu alijuwa rafiki na mama Abbas ,maisha yaliendelea shuleni Aryan ,na Joy ndio waliendelea kusoma ila ,Samairah hakurudi tena shule maana yeye alikuwa akisoma kwa ajili ya kumlinda Aryan .


Baada ya akina Jesca kufariki na Mussa pamoja na Kudra darasa lilibaki na vinara wa tatu nafasi ya kwanza alikuwa an a chukka Aryan yapili Abbas na tatu alikuwa Joyce, alifuatiwa na Nanaa pamoja na Lusi ,masomo yaliendelea walifanikiwa kufaulu kidato cha nne hatimae cha tano na cha sita,

Aryan aliamua kusomea kazi ya uandishi wa habari kutokana na kipaji chake, huku Samairah akiendelea kusimamia biashara mbali mbali jijini dar es salamu , hatimae mahusiano yao na Aryan yalizidi kunoga miezi kadhaa ilikatika hatimae miaka sasa Samairah alishika ujauzito wa Aryan.


Aryan aliweka juhudi zake za kuwa mwandishi wa habari hodari na hatimae aliajiriwa katika kituo cha Mwai tv na alikuwa repota aliyeaminika ,yote kutokana na kujituma kwake na bidii katika kazi zake.


Maisha yaliendelea familia ilikuwa ya furaha kila siku ,siri ili baki kuwa siri ,hamna mtu mwingine aliyejua kama Samairah ni jini tofauti na akina Arya ,mama ake ,Joyce na Gwae ,waliifunga siri ambayo ilidumu.


Hatimae Samairah alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume hakika ilikuwa furaha hasa kwa Aryan na Samairah bila kumsahau mama Aryan,pamoja na Joyce , Joyce aliishi maisha anayoyataka alibadilisha gari kila alitakalo ,hatimae alikuja kubadili dini na kuitwa Sabrinah ,


Kutokana na mfanano wa Aryan na Abbas, alivyomkosa Aryan alijikuta akidondokea mikononi mwa Abbas ,ila hakujutia kamwe penzi lake kumpa Abbas ,walipendana hatimae walifunga ndoa ,watu walisherekea sana.


Mtoto wa Samairah na Aryan walimpa jina Mukhusin ,hakika Samairah aliweza kumlea mwanae vizuri na kumtunza vyema .


Hii ndio stori yetu ya

***** samairah******

Na ndio imefikia mwisho


MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG