Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

RANGI YA CHUNGWA - 4

  

Simulizi : Rangi Ya Chungwa

Sehemu Ya Nne (4)



Hata yule Dokta alishangaa yale maneno ya Dickson. "Dickson umeanza kuchanganyikiwa, maneno gani unayo zungumza mwanangu. Kwa nini umekuwa hivi, nini shida mwanangu" Aliongea Mama yake na Dickson huku nae akianza kutokwa na machozi, halikuwa kitu cha kawaida mtu kuzungumza maneno kama yale, kulionekana kuwa na jambo kubwa ambalo lilikuwa linamsibu Dickson. "Mama mimi siwezi tena kuwa na mtoto, hata huyu ambae niliona atakuwa tumaini langu nae sidhani kama atakuwa hai" Dickson alishindwa kuendelea kuongea kutokana na kilio alichokuwa akilia. Yale maneno yaliwafanya wazazi wa Dickson kushtuka huku midomo yao ikiwa wazi, ilidhihirusha kushtushwa na yale maneno.


"Ni kweli anavyo sema Dickson lakini sina maana kama haitowezekana bali ni kumuomba Mungu aweze kuponya, maana uwezo wetu madaktari umefikia mwisho, ila si mwisho wa Dunia. Cha muhimu kwa sasa ni kujaribu kumsaidia huyu msichana ili kuokoa maisha ya msichana huyu" Aliwasisitizia yule Dokta na kuwafanya kuduwaa na kutoa macho. "Dokta naomba usinifiche maana mimi mwanangu hakuwa akiumwa ugonjwa wowote, sasa iweje leo unaniambia maneno kama haya.


Embu niambie ukweli Dokta!" Aliongea Mama yake na Dickson akiwa kama mtu alieanza kuchanganyikiwa, hali ya hewa ya pale ofisin kwa yule Daktari ilibadilika, japo kuwa kulikuwa na feni pamoja na AC lakini jasho lilikuwa likimtoka Mama yake na Dickson. Yule Dokta alihisi akiwaambia ukweli angeweza kuleta matatizo maana alianza kuona mabadiliko kutoka kwa Mama yake na Dickson. Dickson alimwangalia Mama yake pamoja na Baba yake walivyo onekana kuwa na huzuni kwa kile walichokisikia, lakini Dickson hakutaka kuwaficha maana alijua hata akiwaficha bado isingekuwa msaada kwake au kupona kwake, ndipo alipoamua kuzungumza ukweli.



"Mama na Baba. Najua hili linawauma sana lakini si kama ninavyo umia mimi, ila siwezi kuyapata maji yaliokuwa tayari yamemwagika na kumezwa na ardhi. Kila kitu kina mapungufu yake na kila jambo lina mwisho wake, naweza kusema kila kitu Mungu huwa anapanga, lakini hili la kwangu mimi siwezi kusema mungu amepanga. Kweli Mama hili jambo Mungu hajapanga kabisa, sijui nitakuwa mgeni wa nani na sijui ni kwanini haya yote yananipata mimi. Nimemkosea nini Mungu, mbona hakuna dhambi nilio ifanya inayo lingana na adhabu hii. Haya yote na weza kusema ni kwa sababu ya Johar, Johar ndiyo chanzo cha yote haya, angalia leo hii siwezi kumpa mwanamke ujauzito.


Bora kufa tu Mama maana hata huyu ninaemdhania nae sizani kama atakuwa hai" Aliongea Dickson maneno yalimfanya hadi yule Daktari kutokwa na machozi, kila mmoja wao alikuwa akitokwa na machozi na kusikitishwa na maneno ya Dickson. Kiukweli Dickson alikuwa na maumivu makali katika nafsi yake, hakuonekana kuwa na hata chembe ya furaha. Sura yake ilijawa na huzuni kila kona, machozi nayo yalitawala katika uso wake.

"Dokta, Dokta?"

Ilikuwa ni sauti ya kike iliokuwa ikimuita yule Daktari aliekuwa akiongea na Dickson pamoja na wazazi wake. Yule Dokta alinyanyuka na kuanza kuelekea kwenye mlango wa kutokea ofisini kwake huku akifuta machozi yaliokuwa yakimtoka. Mama yake na Dickson alibaki kumbembeleza Dickson na kumtia moyo.


************

Mzee Tarimo akiwa ofisini kwake huku taarifa za mwanae kuto onekana zilikuwa zikimsumbua kichwa chake na kumfanya kushindwa hata kazi zake. Akiwa anajitahidi kupitia baadhi ya ma file pale ofisini simu yake iliita, aliichukua na kuipokea na kuiweka masikioni na ndipo yule aliempigia alivyoanza kuongea. "Baba ni mimi Johar nilikuwa nakuambia kesho nitakuwa kwenye ndege kuja huko" Baada ya kuzungumza yale maneno simu ilikata. Mzee Tarimo alishtuka sana maana sauti aliokuwa ameisikia ilikuwa ni ya mwanae Johar, ambae alikuwa akimtafuta kwa kipindi kirefu bila mafanikio. Hakuweza kuamini kama yule aliekuwa akizungumza ni mtoto wake, ndipo alipoamua kupiga ile namba kwaajili ya kupata uhakika, lakini alipopiga ile namba ilisadikika namba hiyo haikuwa hewani. Kitu ambacho kilimsanganza mzee Tarimo na kushindwa kuelewa nani aliekuwa anamchezea akili yake ni zile namba za simu.


Code za namba zile zilikuwa ni code za Tanzania, lile jambo lilimuumiza kichwa maana alitambua kila nchi huwa na code zake. Mara ghafla akiwa kwenye mawazo ya kutaka kujua zile namba zilikuwa ni za nani alisikia simu yake inaita, alipoangalia ni nani, alikuta ni mkewe. Aliamua kuipokea na kuiweka sikioni. Hello mme wangu? Nimeweza kupigiwa simu na Johar na kuniambia kesho anakuja Tanzania, ila sikuwa na huakika na yale maneno nikaamua kumpigia lakini ile namba haikuwa ikipatikana. Sasa sijui ni kweli au sikweli. Aliongea Mama yake na jihari baada tu ya mume wake kupokea simu. Mzee Tarimo alishindwa kuelewa ni Johar yupi anazungumziwa, hakuweza kuamini, yeye aliamini kulikuwa na mtu anamchezea mchezo na hilo alitambua baada ya kungalia zile namba.


Mzee Tarimo alishindwa kumjibu mkewe na kuamua kuiweka simu yake juu ya meza huku mkewe akiwa anauliza bila kujibiwa, kiukweli mzee Tarimo alikuwa mfano wa mtu aliekuwa ameanza kuchanganyikiwa. Alishindwa kuelewa ni nani aliekuwa amemchezea mchezo ule, alibaki pale ofisini akiwa anakwenda huku na kule huku akiwa anatafakari kile alichokuwa ameambiwa. Aliamua kutoka pale ofisini na kuingia ndani ya gari na kuelekea nyumbani kwake, hakuchukua muda mrefu kufika nyumbani kwake kutokana na kuwa na usafiri. Alipofuka nyumbani kwake alimuita mke wake na kuelekea chumbani kwake.


"Hiyo namba iliokupigia iko wapi, embu nionyeshe!" Aliongea mzee Tarimo baada ya kufika chumbani.

"Hii hapa" Alimjibu mkewe huku akiwa anamkabidhi simu ili kuweza kuiangalia namba hiyo. Alipoingalia na kuifananisha na ile iliompigia kwake ndipo alipogundua kuwa hazikuwa zikifanana, aliziangalia mara mbili mbili lakini ukweli ulibaki pale pale.

"Ni nani anaejaribu kkunichezea akili yangu. Mke wangu baada ya kuziangalia hizi namba umegundua nini?" Alilalama mzee Tarimo na kumuuliza mkewe swali.

"Nigundue nini sasa wakati mimi nimepigiwa simu na mwanangu Johar na Kuniambia anakuja kesho kutoka kwenye masomo yake"


"Mke wangu naona hujaelewa namaanisha nini kukuuliza juu ya hizi namba. Embu angalia code za hizo namba alafu uniambie ni za nchi gani?" Aliongea mzee Tarimo kwa utaratibu na kwakusisitiza, mke wake alipoangalia zile namba bado hakuelewa nini maana ya kuulizwa vile.

"Code ni za Tanzania, kwanini umeniuliza hivyo mme wangu?" "Kama ni za Tanzania na ni mwanao kakupigia na mwanao anasoma wapi?"

Mzee Tarimo alimuuliza mkewe ili kumuelewesha ili kutaka mkewe kugundua kuwa alikuwa anachezewa mchezo. Mke wa Mzee Tarimo alionekana kukaa kimya huku akiwa anazitazama zile namba asijue nini chakufanya.


Dickson alibaki akitokwa na machozi huku Mama yake akiwa na kazi ya kumfuta machozi. Haikupita muda mrefu yule Dokta alirejea ofisini kwake na kuwakuta Dickson na wazazi wake wakiwa wenye kujawa na huzuni na majonzi katika nyuso zao.

"Samaha kwa kuwaweka hapa ila nina taarifa nzuri kwa Dickson"

Aliongea Dokta huyo na kuwafanya Dickson pamoja na wazazi wake kuweka masikio yao vizuri kwaajili ya kusikiliza kile yule Dokta alichotaka kukisema. "Hongera Dickson kwa kuitwa Baba na ninavyo ongea sasa mkeo amejifungua salama"

Aliongea yule Daktari na kufanya Dickson pamoja na Wazazi wake kushangaa na kubaki wakiwa wantizama yule Dokta. Dickson alivyosikia vile alitoka anakimbia kuelekea chumba alichokuwa Angely kwenda kushuhudia alichoambiwa.


Alipotika nje ya ofisi ya yule Dokta alianza kupita kwenye kordo ya ile hospitali kwaajili ya kuelekea kwenye chumba alichokuwa Angely. Alipofika mlangoni mwa chumba kile alimuona msichana aliekuwa amevaa nguo za kawaida akiwa anatoka kwenye chumba hicho, hakujali sana akaamua kuingia ndani na kumkuta angely akiwa anavuja damu nyingi katika ubavu wake huku akiwa anarusha rusha miguu, kile kitendo kilimshtua na kumfanya kuduwaa kwa dakika kadhaa badala ya kumwita Dokta alijikuta anapoteza muda kumshangaa Angely huku akiwa anajaribu kumtafuta mtoto aliekuwa ameambiwa.


Alizunguka chumba kizima lakini hakuweza kumuona mtoto, alishindwa kuelewa nini kilichokuwa kinaendelea. Damu zilizidi kuvuja huku Angely akiwa ametulia kimya, ndipo Dickson alipopata wazo la kumuita Dokta, alitoka haraka haraka ili kwenda kumuita Daktari. Alipotoka nje ya kile chumba aliona Dokta pamoja na wazazi wake wakiwa wanakuja kule alipokuwa, Dickson aliona Dokta anatembea pole pole ndipo alipoamua kumkimbilia na kumshika mkono na kumvuta kwa haraka hadi kwenye chumba alichokuwa Angely. Kile kitendo kiliwashangaza hata wazazi wake na kuhisi mtoto wao ameanza kuchanganyikiwa.


ule Dokta alipofika ndani alionekana kupata mshtuko baada ya kumuona Angely akiwa anavuja damu nyingi. Bila kuchelewa yule Dokta aliwaita watu wa kumsaidia na kumtoa Angely na kumwingiza kwenye chumba cha wagonjwa mahuti huti. Dickson alibaki pale chumbani huku akiwa anajaribu kujua mtoto alieambiwa amezaliwa mahali alipo kuwa. Dickson aliamini mtoto alieambiwa amezaliwa ndiyo tegemeo lake maana kwa wakati huo madaktari walikwisha mpa majibu ya kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke mimba, alitamani kumuona lakini hakuweza kumuona maana yule dokta aliingia kwenye chumba cha wagonjwa mahuti huti kwaajili ya Angely. Akiwa pale kwenye chumba hicho huku akiwa anasubiri polisi kwaajili ya usalama wa pale hospital simu yake iliita na kumfany akuingiza mkono mfukoni na kuipokea.


"Hello mpenzi napenda kukujuza kuwa kesho nitakuwa kwenye ndege nikiwa nakuja huko, sawa eeh?" Ni sauti ya kike ambayo ilimfanya Dickson kujiuliza kabla ya kumjibu, alishindwa kuelewa ni nani aliempigia ile simu, alipotaka kumjibu alijikuta amekwisha kuchelewa maana simu ilikwisha kukata. Ile sauti alioisikia kwenye simu ilimpa maswali mengi na kuanza kufikiria aliwahibkuisikia wapi, aliamua kuipigia ile namba kujua nani aliekuwa amepiga namba ile.


Alipojaribu kupiga kwa mara nyingine ile namba ilionekana kuto kuwa hewani, aliahindwa kuelewa akaamua kujaribu tena na tena bila mafanikio.

"Siyo Johar kweli huyu, mbona sauti kama yakwake au nimeifananisha"

Alijuliza Dickson na kujijibu mwenyewe, Dickson alizidi kuchanganyikiwa na kuonekana kuwa kama mtu aliekuwa na vitu vungi kichwani.

Ile sauti ilimpa maswali mengi sana Dickson na kubaki ameshikilia ile simu huku akiwa anatafakari yale maneno. Hakuweza kujua nini kilichokuwa kinaendelea, hadi polisi walipofika bado Dickson alikuwa ameshikilia ile simu.


******

Mzee Tarimo alihisi kulikuwa na kitu kinaendelea, hakutaka kuumiza akili sana, alichoamua ni kunyanyua simu yake na kuibonyeza vitufe kadhaa kwenye ile simu na kuiweka katika sikio lake la kushoto na kuonekana kusubiri majibu ya upande wa pili.

"Ndiyo boss"

Sauti ya upande wa pili ilisikika baada ya simu kupokelewa.

"Sasa hivi nahitaji kuonana na nyinyi" "

Sawa boss" Aliongea mzee Tarimo huku huku akionekana kuongea na kundi flani la watu. Baada ya kukata simu ile aliingia ndani kwake na kumkuta mke wake akiwa amejilaza kitandani, taratibu alimsogelea mkewe kwaajili ya kumfariji maana zile taarifa zilionekana kumuathiri kwa kiasi kikubwa katika ubongo wake.


Mzee Tarimo alimsogelea mkewe na kumkumbatia kisha kumlaza juu ya mapaja yake na kuanza kuchezea nywele zake, ile hali ilionekana kupunguza mawazo japo hakukuwa na mabadiliko. Taratibu wakaanza kupigana denda zito lililo mfanya kila mmoja kupata hisia za mapenzi, ile hali iliendelea ndipo mzee Tarimo alipoanza kumtoa nguo moja baada ya nyingine na kuanza kumchezea mkewe huku akijaribu kumuondoa mawazo aliokuwa nayo



Taratibu wakawa katika tendo muhimu kabisa kwenye ndoa, baada ya dakika kadhaa mbele wakawa wamejilaza kitandani huku kila mmoja aliwa amemfurahiya mwingine.

Dickson alizidi kuwa na maswali mengi katika kichwa chake mpaka pale yule Dokta alipokuja kumuita na kumrudisha hadi ofisini na kuwakuta Baba yake na Mama yake Dickson wakiwa kwenye hali ya uoga na hofu kubwa, ni kutokana na kile walichokuwa wamekiona kwa Angely. Kiukweli kilikuwa ni kitendo cha kinyama, hadi wakati huo hakuna aliekuwa amapata taarifa zozote juu ya mtu aliekuwa amefanya jambo kama lile.


"Angely anaendelea vizuri mabisa ila kuna itilafu kidogo imetokea kwenye maeneo ya mbavuni maana alionekana kuchomwa na kitu chenye ncha kali. Hivyo nilikuwa nawaombeni muende mkamwandalie mgonjwa chakula kisha mtarejea kwa wakati mwingine"

Aliongea Daktari huyo huku akiwa mwenye haraka, zile taarifa zilionekana kutokamilika kwa jinsi yule Dokta alivyokuwa akizungumza.

"Dokta na mtoto mbon."

"Mtoto yupo salama kabisa, hana tatizo hata kidogo"

Yule Daktari alijibu kwa ufupi na kutoka nje haraka haraka. Kile kitendo kiliwapa wasi wasi Dickson pamoja na Wazazi wake na kuhisi kulikuwa na tatizo kubwa limemkuta Angely. Dickson alitoka haraka haraka kumuwahi Dokta ili amwambie ukweli, alipofika nje hakuweza kumuona yule Daktari. Alishindwa kuelewa ni upande gani yule Dokta alipokuwa ameelekea maana ile hospital ilikiwa kubwa, hivyo ilikuwa ngumu kugundua alipokuwa ameelekea yule Dokta.


Dickson alibaki akiwa njia panda, hakujua aelekee wapi, ikamlazimu arudi kule walipokuwa wazazi wake.

Safari ya kuelekea nyumbani ilianza huku kila mmoja wao akiwa na maswali mengi juu ya kile kilichokuwa kimetokea, Dickson alipokuwa akitafakari alikumbuka wakati alipokuwa anaingia kwenye chumba alichokuwa Angely alipishana na msichana aliekuwa amevaa nguo za kawaida. Kumbu kumbu za Dickson zilikumbuka tukio lile vizuri, alikumbuka pindi alipomuona yule msichana hawakuweza kuonana nyuso zao maana yule msichana alikwepesha uso wake.


"Yule msichana ni nana, na mbona alionekana kuwa na wasiwasi baada ya kuniona. Anawza akawa yeye ndiye aliesababisha haya yote"

Dickson alikuwa akijiuliza maswali mengi bila kupata majibu, walizidi kusonga mbele huku wakiwa wanaongelea kile kilichokuwa kimetokea. Mara ghafla wakiwa hawaelewi hili wala lile, walishangaa gari linakuja kwa kasi upande wao. Walibaki wanahamaki na kushangaa wasijue nini chakufanya, kwa jinsi lile gari lilivyokuwa linakuja kasi walishindwa kulikwepa. Dickson alipoangalia kwenye lile gari alishangaa sana baada ya kumuona Johar huku akiwa amevaa nguo kama zile alizokuwa amevaa yule msichana aliemuona pale hospitali.


lile gari liliongeza kasi na kuwafikia wakina Dickson pamoja na Wazazi wake, ilikuwa kama mchezo wa kuigiza maana Johar hakuwa anatani alipofika aliongeza kasi na kuwagonga wote watatu na kuanguka chini huku kila mmoja akiwa anatokwa na damu nyingi. mama yake na Dickson alipogongwa kichwa chake kilijipigiza kweny jiwe kubwa na kumfanya kichwa chake kutokwa na damu nyingi.Baba yake pia aliweza kupitiwa na lile gari na kuonekana kuumia sana kwenye upande wa begani na kifuani.


Dickson aligongwa vibaya maana yeye alikuwa mbele hivyo damu nyingi zilimtoka kichwani huku akiwa anatokwa na damu mdomoni na kifuani, hali ya Dickson ilionekana kuwa mbaya sana maana damu nyingi zilikuwa zikimtiririka. Akiwa pale chini huku akiwa anajitahidi kuamka alimuona Johar mbele ya macho yake huku Johar akionekana kuwa na hasira kali na Dickson. Dickson hakuamini macho yake aliamini kile alichokuwa anakiona kilikuwa ni ndoto, hakuamini kama Johar angeweza kumfanyia kitu kama kile. Johar alipomfikia Dickson alichomoa Bastola ambayo ilikuwa ngumu kugundua msichana kama yule angeweza kumiliki kitu cha hatari kama kile.

Dickson alizidi kushangaa, alihisi pengine Johar alikuwa anatania lakini haikuwa hivyo.

Dickson alibaki akigugumia kwa maumivu aliokuwa nayo, Johar hakuonekana kuwa na huruma hata kidogo kwa Dickson, alionyesha chuki ya wazi wazi huku akionekana kumchukia sana Dickson. "Wewe si unajifanya unajifanya malaya, sasa endelea na umalaya wako na hili litakuwa fundisho kwa wanaume wengine, wenye taaria kama yako" Aliongea Johar kwa hasira huku akiwa anaelekezea bastola yake katika nyeti za Dickson, kabla hajafatua risasi kwaajili ya kusambaratisha nyeti za Dickson alisikia sauti nyuma yake na kumfanya kugeuka kwa haraka ili kupata kufahamu aliekuwa akimuita.


Alipogeuka alishangaa kumuona Baba yake mzee Tarimo, Johar alishtuka sana na kubaki akihamaki, mapigo ya moyo wake yalianza kuenda kasi. Mzee Tarimo alionekana kushtushwa na lile tukio, hakuwahi kufikiria kama mwanae angeweza kufanya unyama kama ule. Alishindwa kuelewa nini kilichokuwa kinamsibu mwanae mpaka kufanya jambo kama lile, alitaka kumuuliza ila kabla ya kutamka neno lolote alisikia sauti ya magari ya polisi ndipo akaamua kumvuta mtoto wake hadi ndani ya gari na kuondoka nae, japo alijua mtoto wake ndiye aliesababisha yale lakini kutokana na kumpenda ilimlazimu amsaidie .


Yote hayo Dickson aliyashuhudia kwa macho yake lakini kutoka na maumivu aliokuwa nayo pamoja na damu zilizomtoka zilimfanya kupoteza fahamu. "Johar ni wewe au nilikuwa naota, Mungu wangu, ni roho gani uliokuwa nayo wewe mtoto. Sikufikiria kama ungekuja kubadilika na kuwa muuwaji, sijui hiyo roho umeitoa wapi. Kwanini Johar, sinakuuliza. Ni kitu gani kimekufanya kubadilika hivi, mimi Baba yako mwenyewe sikuwahi kufanya unyama kama uliokuwa umeufanya wewe" Alikuwa akiongea mzee Tarimo Baada ya kufika nyumbani, kile kitendo kilionekana kumkera na kumuogopesha sana. Wakati akiwa anaongea hayo yote mkewe nae alikiwa akisikia Mume wake jinsi alivyokuwa anaongea na mwanae, yale maneno yalimfanya hata Mama yake na Johar kubaki mdomo wazi.


Hakikuwa kitendo cha kibinadamu alichokuwa amekifanya Johar, lisha ya yote na mzee Tarimo kuongea bado Johar hakuwa na hata lepe ya kusikiliza aunkutaka kuwaelewa wazazi wake. Mzee Tarimo alibaki akiwa haelewi nini kilichokuwa kikimsibu mtoto wake, ukimya ulitawala katika nyumba ya mzee huyo.

"Lazima nimuuwe hata ikinigharimu kufa, ni kwajinsi gani nilivyopata shida hadi mimi kubakwa na kufanyiwa unyama wa kila aina kisa Dick, nahisi anifahamu. Nitahakikisha ninamuuwa ikibidi hata mimi pia kufa, maana sina thamani tena katika maisha yangu. Angely wewe nitakuuwa pole pole maana wewe huwezi nisumbua akili yangu, najua kile nilichokufanyiahospital hakikuto au kulingana na mlichonifanyia.


Sitoweza kuwasamehe hata siku moja, nitahakikisha mnakufa wote" Yalikuwa ni maneno ya Johar akiwa chumbani kwake, yale maneno yalionekana kuwa kama utani lakini Johar hakuwa anatania kabisa. Alionekana kuchafukwa katika moyo wake, hakuwa nafuraha katika uso wake. Yale maneno aliokuwa akiyazungumza yalimfanya machozi kumtoka, kiukweli Johar alikuwa mwenye kuwa na roho ya kutaka kuuwa wazi wazi. Polisi walipofika eneo la tukio wali walikuta majeruhi watatu huku wote wakiwa hawajitambui, walijaribu kuangalia ile ajali ilivyotokea hadi wale kugongwa lakini hawakupata jibu. Waliliangalia lile gari lililo wasababishia ajali Dickson pamoja na Wazazi wake na kukuta likiwa na paspoti za nchi mbalimbali, walizidi kukagua lile gari na ndipo walipo pata Kitambulisho kilichokuwa na picha ya msichana.


Yule afande alipokiangalia kile kitambulisho alionekana kushtuka na kufeuka nyuma kama kunae aliemuona, alipoangalia hakuona dalili ya mtu au afandi yeyote aliekuwa amemuona, ndipo alipoamua kukiweka mfukoni. Lakini wakati anakiweka mfukoni kna afande mwenzake alimuona, lakini hakutaka kusema jambo lolote maana alikuwa amemzidi nafasi juu kwake. Dickson pamoja na wazazi wake walichukuliwa na kuwaishwa hospital, mara moja madokta waliwachukuwa na kuwapeleka katika vyumba vya wagongwa mahuti huti. Hali ya Dickson pamoja na wazazi wake ilikuwa mbaya kiasi kwamba hata madokta walipata wasiwasi mkubwa, ubize wa madokta na ufanyaji kazi kwa kuwashuhulikia wagonjwa watatu wenye hali mbaya ulionekana kugonga mwamba, kila walipojaribu kutumia akili na maarifa waliokuwa nayo bado hali zao zilionekana kuwa mbaya.


Johar akiwa anavua nguo zake ambazo alifanyia mauaji muda siyo mrefu alipoangalia vitu vyake alishangaa kutoona kitambulisho chake, alikagua kila kona katika nguo zake lakini hakufanikiwa kukiona, alivua nguo zote na kubaki kama alivyo zaliwa huku akikagua katika nguo alizokuwa amevaa lakini hakufanikiwa kuona chochote. Johar alihisi kuchanganyikiwa, mapigo ya moyo yalionekana kwenda kasi alihisi kama askari wangeweza kukagu lile gari wangeliweza kukikuta kitambulisho chake.

"Mungu wangu sasa nifanyaje, kila kitu kimejulikana bora ningewahi kumuwa ili hata nikienda jela niwe nimesha maliza kazi yangu. Haya yote amesababisha Baba maana bila yeye kija pale haya yote yasinge tokea"


Ni katika chumba cha msichana johar akiwa kama mtu aliekuwa amechanganyikiwa, kwa jinsi alivyokuwa na maneno aliokuwa akiyazungumzia yalimfanya aonekane kama mtu aliekuwa amechanganyikiwa. Akiwa kwenye dibwi la mawazo, mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa na kuingia Mama yake. Mama yake alipoingia chumbani kwa mtoto wake alishangaa kukuta pamevurugika huku akimkuta Johar akiwa hana nguo hata moja katika mwili wake. Kile kitendo kilimuogopesha sana na kumfanya ashangae, alibaki ameduwa huku akimtazama mtoto wake bila kusema jambo lolote. Alipokuwa anamwangalia mwanae aliweza kugundua kitu katika mwili wa Johar, kwa jinsi alivyokuwa anamjua mwanae alishangaa sana na kutamani kujua nini kilichompata Johar katika mwili wake



Mama yake na Johar alimsogelea Johar huku akiwa anajaribu kumwangalia vizuri ili kupata huakika kwa kile alichokiona, Johar alionekana kuwa na makovu ya aina tofauti tofauti huku akionekana kuwa na baadhi ya vidonda katika mwili. Mama yake na Johar alibaki akimshangaa mwanae jinsi alivyokuwa, kila upande katika mwili wa Johar kulionekana kuwa na makovu.

"Johar mwanangu nini kimekupata huko ulipokuwa, na mbona mwili wako unaonekana kuwa na majeraha mengi. Nini tatizo mwanangu?" Mama yake na Johar alimuuliza mwanae Johar kwa upole, mama huyo alionekana kuwa na machungu sana, ni baada ya kumuona mwanae akiwa katika hali kama ile. Roho yake ilimuuma pengine kuliko Johar, alionekana kuwa na hofu kubwa kutokana na kile alichokuwa amekiona kwa mtoto wake.


"Ni story ndefu Mama ila kwa sasa naomba uniache maana nahisi kufa kwa hili lililo mbele yangu" Alijibu Johar kwa ufupi na kumfanya Mama yake kushangaa na kuona jinsi gani mwanae alivyokuwa amebadilika, mama yake Johar alipotaka kumuuliza kitu Johar alionekana kunyamaza kimya na macho yake yakiwa juu ya kitanda cha Johar. Kile alichokiona kilitosha kabisa kumfanya ashangae, alifanikiwa kuona bastola ambayo aliifahamu vizuri ndipo alipokumbuka maneno ambayo Mume wake alikuwa akimwambia Johar, hakuamini kile alichokiona mapigo yake ya moyo yalianza kwenda kasi hadi akaweka mkono wake wakulia katika kifua chake. Mama huyo alishindwa hata kuzungumza chochote na kubaki ameikodolea ile bastola. Taratibu mama yake na Johar alitoka na kumuacha Johar pale ndani, alipotoka ya mlango wa Johar alimuona Mume wake akiwa anakuja haraka haraka katika chumba cha Johar. Mke wake alipomuona anakuja ilimlazimu kumzuia asiingie ndani kwanza maana alijua akiingia ndani angeweza kumkuta Johar akiwa mtupu.


Lakini cha kushangaza hata kabla ya kuongea lolote walishangaa Johar akiwa anatoka huku akiwa tayari amekwisha kubadilisha nguo zake. Mama yake na Johar alishangazwa na kile kitendo maana hazikupita hata dakika tatu tayari Johar alikuwa amekwisha badilisha nguo zake. Mzee Tarimo alipofika alimvuta Johar hadi nje na kumkuta yule afande alie onekana kukificha kile kitambulisho cha Johar. Johar alishindwa kuelewa Baba yake alikuwa akifanya nini kuvuta kwa haraka namna ile, Johar alipofika nje na kumuona yule askari alishtuka sana na kutamani kurudi ndani, lakini Mzee Tarimo alivuta kwa nguvu na kumsogeza hadi karibu na askari yule. Johar alionekana kuwa na hofu na kuhisi Baba yake ndiye alimtuama yule Askari kuja kumkamata.

"Johar mwanangu nakuomba ondoka na huyu afande atakusaidia maana yeye ndiye mwenye kuifuatilia kesi ya Dickson pamoja na wazazi wake" Aliongea mzee Tarimo na kumfanya Johar kushangaa na kushindwa kuelewa Baba yake alikuwa na maana gani kumkabidhi kwa askari wa polisi. Mzee Tarimo hakutaka kuongea chochote maana alijua askari wangeweza kufika pale nyumbani kwake muda si mrefu, hivyo ingeleta shida kama wangeweza kumkuta Johar pale nyumbani.


Bila kupoteza muda Johar pamoja na yule askari waliingia kwenye gari na kuondoka katika nyumba ya mzee Tarimo. Walipo toka hazikupita hata dakika tano wakaingia maaskari katika nyumba ya Mzee Tarimo, mzee Tarimo hakuwa na mshtuko hata kidogo maana alijua walichokuwa wakikihitaji hakikuwepo, alijua moja kwa moja alie kuwa akitafutwa ni mwanae Johar. Askari wale walipofika waliruhusiwa kusachi kila kona katika nyumba ile na baada ya dakika kadhaa wakawa wametoka bila kupata ushahidi wowote. Mzee Tarimo alifurahi sana na yote ni kutokana na kumpenda mwanae wa pekee, wale askari waliondoka na kumuacha mzee Tarimo akiwa ameachia tabasamu kubwa na kuhishi kuwashinda wale askari kiakili.



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG