Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

HASNA (MFU ANAE ISHI) - 2

   

Simulizi : Hasna (Mfu Anae Ishi)

Sehemu Ya Pili (2)




Sauti hiyo ilisikika kwa mwangwi na ilikua nzito sana.

“NHAKUBHI SANA MULEHAYA KUGAGALAJA MININGA GISA KULWA SABHABHU YA MIHAYO YINGWE YANYALOGI.IHAHA NALEFUNYA ADHABHU NHALE KUKWA KILA UMO WING'WE"

(Mekisea sana mnataka kuidhalilisha damu yetu kwa ajili ya mambo yenu ya kishilikina .Sasa natoa  adhabu  Kali kwa kila mmoja wenu.)

Ilisikika sauti hiyo ikiongea kwa lugha ya kisukuma.

“MASAMVYA GI GUNGULI LYA MBIKA TULELOMBA MSAMAHA GETE KULWA LENILE TWA LILEKELAGA WIYABYE NA HANGE TWANSHOKEJAGA WELELO KWANDEJA IHAHA TULEOMBA MTWIZE TWINAA EADHABHU”

(Mizimu ya himaya ya Mbika tunaomba msamaha sana kwa hili, tuna muachia huru  napia tuna mrudishia Duniani  kuanzia  sasa .Tunaomba msitupe adhabu.)Alimjibu kwa lugha hiyo hiyo yakisukuma.Basi ile sauti ilisikika kicheka na kicheko chake hicho kiliashilia wamesamehewa kupewa adhabu.

Hali ilirudi kama ilivyo  kuwa awali.huku pale chini zikionekana maiti nyingi sana za washilika.walikufa  kutokana naule upepo mkali.

Waliitana kikao cha dharula viongozi  ilikujadili swala la  binti Hasna.

“Niliwaambia toka mwanzo swala la kutoa kafara Hasna litatuletea shida ona  sasa zaidi ya washika ishirini wamepoteza maisha”

Aliongea baba yake na Hasna 

“Jafari tuache kulaumiana kwanza,tujadili Hasna anarudije Duniani”?

Aliongea mmoja wa viongozi  hao.

"Kurudi Dunia sio shida shida watu wamejua kafa  pili watu wote tulio  mfanyia hivi anatujua na siri nyingi kazifahamu. ikiwemo baba yake kumtoa kafara mama yake.Jamani amuoni kama tutaumbuka hasa  baba yake”

Aliongea kiongozi wa ngazi za juu.

" Jamani mi nimepata  wazo,tuna mrudisha duniani lakini tuna ufutia kumbukumbu zote akumbuke jina lake tu”

Alipo maliza kuongea  .mmoja wa kiongozi wa ngazi ya chini wote walipiga makofi.kuashilia kukubaliana nae.

“Jamani na lakuongezea hapo baada ya kumtoa kumbukumbu,tunampeleka mbali na mkoa huu wa Shinyanga ili asionekane na watu wanao mfahamu"

Alipo maliza kuongea moja wa viongozi  hao .Basi walikubaliana wakapanga wakutane siku nyingine ilikumrudisha Hasna Duniani kutoka kuzimu.Na pia wajabidili wanampeleka mkoa gani.

Walipo ongea hao kila mmoja aliondoka zake.Zuberi alimbeba Hasna NA kisha wakarudi nyumbani.Na alipo  mfikisha alienda kumfungia kwenye kile chumba cha misukule.

Kesho yake palipo kucha  Zuberi kama kawaida yake alienda kwenye kile chumba na kuwapa chakula.Lakini alikua anamuogopa sana Hasna,yeye alimpa chakula safi kwenye sahani la peke yake.

Ilikua majira ya sanane za mchana Zuberi alipokea simu kutoka kwa mdogo wake ,aliye kua akisoma chuo cha SAUTI mwanza.

“Hallo kaka Mimi Habiba nyoo unichue hapa sitendi,simu yangu ilizima hii nimeazima"

Aliongea mdogo wake na  Zuberi .basi alienda kumchua na mdogo wake huyo huwa anapenda kufikia kwa Zuberi.wakiwa njiani waliendelea kupiga sitory.

“Hivi kaka kwanini mama asije kukaa kwako,?maana na uzee ule  nyumba lote yuko yeye na mfanyakazi wake tu“

Aliongea Habiba.

“Nadhani mama yako unamjua kwa ubishi.Sawa lakini wazo zuri talifanyia kazi”

Aliongea Zuberi. Baada ya muda walifika nyumbani kwa Zuberi.

Habiba alikua na chumba chake, aliingia na kwenda kuweka mizigo yake ,nakupata maji ya kuoga iliatoe uchovu.

Ilipofika majira ya jioni Zuberi na mdogo wake, walielekea nyumbani kwa mama yao kumchukua.Maana waliongea nae kwa njia ya simu mchana,aliwakubalia japo haikua rahisi kama unavyo dhani.Basi walimchukua na kurudi nyumbani kwa Zuberi.

Ilifika mida ya saa  nane za usiku, ilikua ni siku ya kwenda kumrudisha Hasna Duniani, na kumpeleka mbali na mkoa huo wa Shinyanga.

Zuberi alifanya kama kawaida yake, aliacha kivuli chake alimchukua Hasna ,kisha wa kaondoka kwenda kwenye ule  msufi wanapofanyiaga kafara zao.

Huku nyuma Habiba mdogo wake na Zuberi, mida ya saa  tisa  kichwa kilianza kumuuma sana alianza kulia ,hadi mama yake aliamka na kwenda chumbani kwake.

“Habiba una nini mwanangu"

Aliuliza mama yake.

“Mama kichwa kina niuma sana yani kama mtu  anagonga na nyundo”

Alisema  Habiba huku akiwa analia.

“Ngoja nikamuamshe kaka yako atupe dawa  ya kutuliza maumivu”

Mama Zuberi aliondoka, alipifika mlangoni aligonga sana Lakini hakujibiwa.Aliamua kuufungua mlango na kuingia,alipo ingia alijalibu kumsemesha lakini hakuitika.

Alisikiliza mapigo ya mbele.Alishituka akaenda kumchukua simu na kumpigia mtu.

Kama nusu saa alifika  huyo mtu  alikua ni daktari alimchukua vipimo .kisha akasema  sioni dalili yoyote kama ana pumua .



Aliskiliza mapigo ya moyo.Alishituka akenda kuchua simu na kumpigia MTU.

Kama nusu saa alifika huyo mtu alikua ni daktari alimchukua vipimo.kisha akema 

"Sioni dalili yoyote kama ana pumu"

Alisema daktari huyo. Kisha wakashaulia ana kwenda hospital kwa uchunguzi zaid.

Daktari alikua kaja na gari yake ,hivyo walimpakia Zuberi na kumpeleka Hospital.

Walipofika walimchunguza na kuona kuwa kafariki. Maiti ya Zuberi ikaenda kuifadhiwa mochwari.

Huku nyuma Zuberi akiwa karudi na kukuta mwili wake haupo  pale kitanda alianza kuutafu.Mara muda ulipita kidogo waliingia mama Zuberi na mdogo wake wakiwa wanalia .

“jamani mimi  nimekukosea nini mungu,misiba  kwangu kila siku”

Alikua analia  mama Zuberi huku akiongea  maneno hayo.Zuberi alikua namfata mama yake.

“Mama usilie Mimi sijafa Niko mzima,nionesheni mwili wangu”

Aliongea Zuberi huku akiwa analia.Lakini hakuna mtu  aliye kua akimsikia wala kumuona.

Zuberi aliondoka hadi kwa mkuu wao wa kichawi.

“Mkuu nimekuta wamebeba mwili wangu wana jua nimekufa”

Aliongea Zuberi huku akiwa analia.

“Zuberi nadhani unajua kuwa hilo ni tatizo, na auwezi  kurudi kwenye hali yako.na mtu  wa kukusaidi kwa hili ni Hasna peke yake”

Aliongea mkuu huyo na Zuberi aliondoka .Mashariti ya kuuacha mwili na nafsi yako ikiwa  imendoka ,ikitokea watu wakauamisha mwili wako, basi kurudi hadi nafsi yako inyweshwe damu ya mtu  mwenyewe nguvu, na aliekubaliwa na kupewa baraka na heshima yote na mizimu  jamii yao.  Na mwenye  vigezo hivyo ni Hasna.Na Hasna alikua katolewa kumbukumbu .na wamempeleka mkoa mwingine tofauti na mkoa huo wa Shinyanga.

Zuberi alikua kizunguka tu mule ndani sijue  anafanya  je .Mara asubuhi ilingia na watu walianza kujaa pale msibani  .Zuberi alikua anatembea  huku na kule asijue Cha kufanya .

Muda wakuosha  mwili ulifika, wakati watu wakiwa kwenye chumba hicho chakuoshea .Alitokea  mzee mmoja kichawi kwenye chumba hicho.Alichua nywele za mwili huo wa Zuberi na kisha akapote .

Waliuandaa mwili kwa ajili ya kwenda kuuzika .Hatimaye walianza safari ya kuelekea makaburi, Zuberi nae alikuwa  

 tu akiufata mwili wake.Walizika walipo maliza waliondoka. Zuberi alibaki akiangalia tu kaburi lake.

Alikaa Zuberi hadi Usiku uliingia alienda nyumbani kwake .

Ilipita miezi mitatu  mambo kwa kina mama Zuberi yalianza kua magumu.Alianza kuuza gari moja moja mama yake Zuberi.

“Mama usize chochote ,”

Zuberi alikua akimwambia  mama yake sema ndio hasikii.

Muda mrefu ulipita .Rafiki zake na Zuberi baada ya kujua Zuberi awezi tena kurudi.

Walitengeneza dokumenti feki kuwa walimkopesha Zuberi  milioni mianane na akaweka dhamana  nyumba.

Walienda walimkuta mama yake Zuberi. Walikuja   na wakili wao.wakaonyesha dokumenti hizo na maneno mengi ya uongo

Hatimaye waliweza kuwapokonya nyumba.Zuberi alikua analia  tu kwa uchungu jinsi Mali zake zinavyo potea.Mama Zuberi alirudi kwenye nyumba yake ya mwanzo

Baada ya wiki mbili Rafiki yake huyo na Zuberi kwa jina anaitwa jimi.Aliweza kuhamia na familia yake.

Kitendo hicho kilimuumiza sana Zuberi 

Na kusema atafanya jambo kubwa na hatokuja kusahau huyo rafiki  yake.Siku moja Mke wa Jimi akiwa kaka sebureni anangalia tv .ana mtoto mdogo wa mwaka mmoja na nusu kamlaza chumbani.

Akiwa pale alisikia vyombo jikoni vinapigwa kama ngoma .

Aliondoka na kwenda kuangalia nini ,lakini kila anapozidi kusogea sauti ilipungua na alipo sogea kabisa haikusikika. 

Akiwa huko jikoni alisika sebreni mtu anacheka kwa sauti kubwa sana Mara akasikika mtoto analia kama kafinywa .Yule mama aliogo naalipo  elekea chumba alikua mtoto kalala fofofo.

"Jamani hii nyumba ina nini?”

Aliongea mke wa jimi.Alichukua  simu nakumoigua mumewe ,alimueleza kila kitu.

Upande wa sasa ilikua Kasulu kwenye kijiji cha Shunga Mkoa wa Kigoma

“Baba kuna mtu kafa  huko njia ya kwenda kisima"

Walikua ni watoto waliokuja mbio nakumpa taarifa baba yao.Basi baba huyo aliongozana nawane kwenda kuakikisha.Nikweli alikua ni binti.


Upande wa pili wa kijiji hicho  cha Shunga kuna watoto wengine walionekana,wakimpa  taarifa hizo babu yao ambaye alikua ni mzee alikua kaka a mgeke wake wakikamua mawese.

“Yebhagaa halilo umuntu yaleye kunzila yigenda kumugezi nyomba  agihema”

(Jamani kuna mtu kalala mule njia ya kwenda kisimani sijui kafa.)

“Nihehe iyo  tugende kumulabha”(wapi huko twendeni tukamuone sasa).

Walikua wanaongea lugha ya kiha. Waliondoka walipo fika walikuta watu wamekusanyika wakimtaza akiwa pale pale chini hajielewi.

Alipofika yule mzee  pale watu walianza kumpisha

Alimsogelea yule binti. Akamshika kichwani .kisha aliwaomba vijana wa mbebe hadi nyumbani kwake.Walipo mfikisha yule mzee ,alitwanga majani ya miti  mbali mbali kisha akachemsha na kuanza kumkanda binti huyo mwili mzima.

Yalipita masaa sita  hakiwa bado hajaamka binti huyo.Mzee huyo aliendelea na kazi zake za kukamua mafuta ya mawese.Baada ya muda mjukuu wa yule babu alikuja na kumwambia kitu babu yake .Babu aliinuka  haraka haraka nakuingia ndani ,sehemu aliyokua  kamlaza  binti huyo.

Alikuta  Binti kanyanyuka kakaa akiangaza huku na kule.  hakuna chochote anacho kielewa .

“Habari yako binti,unajisikiaje kwa sasa”

Alimuuliza  yule mzee.

“We ni nani na hapa wapi”

Aliuliza binti huyo.

“binti usiwe na hofu,upo sehemu Salama ”

Alimwambia mzee huyo.Bi huyo alicheka kisha akanza kutoka nje, kuna watu walikua wamekaa nje, wakiendekea na shunguli zao za kukamua mawese

Wote walianza kumshangaa .Huku huyo binti yeye alikua akishangaa mazingira Yale.

Kama ujuavyo sheria za vijijini kama kuna mgeni yoyote lazima watu watalifiwe,na pia wamuhoji ili kujua   taarifa zake .Hata tatizo likitokea basi wajue wanaanzia wapi wanaishia.

Basi ilipofika majira ya saa kumi, watu wote wana kua wametoka mshambani.Iligongwa kengele iliyo ashilia kuna dharula ,na wote walikusanyika kwa mwenyewe kiti  wakijiji.

Hakuna aliweza kukaidi maana tamaduni hiyo ilikua imezoeleka.

“Jamani nyinyi wenza  mnajua ,kengele hii ina  Maana gani”.?

Waliukiza baadhi ya kundi la  vijana lililokua limekaa mahala hapo.

“Mi nahisi itakua ni mambo ya michango ya zahanati ya kijiji.”

Alijibu  kijana mmoja kwenye hilo kundi.

Baada ya muda alikuja mwenyekiti wakiwa na wajumbe wake.Akiwa kaambatana na yule mzee pamoja na binti aliyeokotwa.

Alisimama mwenyekiti na kuwaekeza wananchi wake alicho  waitia.

“Jamani binti mwenyewe ndio huyu mbele yenu.Lakini kama nilivyo waambia hakuna anacho kujua zaidi ya jina lake.Inaonekana maswahibu aliyota, yemempelekea kupoteza kumbukumbu. Hivyo tutakaa nae hapa kijijini, hadi ndugu zake watakapo kuja kumtambua.Jina lake anaitwa Hasna."

Aliongea hayo mwenyekiti watu walishangilia hasa  vijana walionekana kufurahi sana.Lakini kwa upande wa mabinti, baadhi yao walionekana kuchizwa na ujio wa binti Hasna, kwenye kijiji chao.Hasna  alikua ni mrembo sana.

Basi mwenyekiti aliendelea.

“Jamani sisi wana kijiji wa Shunga, Kama mnavyojua ukarimu ndio nguzo .Hivyo tungeomba mtu ajitolele kukaa nae, hadi pale uongozi wa kijiji utapo mtengenezea

Mazingira ya kukaa binti huyu."

Alimaliza kuongea mwenye kiti.lakini waliojitokeza wengi walikua ni vijana ,tena ambao hawajaoa.

Lakin baada alijitokeza mama mmoja ambaye ni mtu  mzima kidogo na kuomba kukaa nae.Mwenyekiti alimkubalia  mama huyo kwani alimfahamu vyema ana alikua anajiheshi.

Mama huyo anaitwa  Ujugi ,na alikua ni mjane alifiwa na mumewe miaka mitatu iliyopita.Ujugi alikua ni binti mwenye umri wa miaka ishirini na Kwa sasa alikua hayupo kijijini hapo.Alikua kaenda kwa mjomba wake Dar es laamu .

Basi kikao kikawa  kimeishia hapo na Mama Ujugi alimchukua Hasna na kumpeleka kwake.

Kuna vikao vidogo  vidogo  viliendelea mtaani.

“eeh bhana Hasina  ni bhonge ra murembo"

Walikua wanaongea vijana hao kwa lafudhi ya kiha  kama ujuavyo wenyewe kwenye L wana weka R.Kila kona  vijana walikua wanamuongelea Hasna.Hicho kiliwakela mabinti wengi , Hasa kuna binti mmoja ndio alikua akikisumbua, kijiji hicho kwa urembo.

Walikua wana muita Bionce.

“Mwanangu mbona Leo hauna  raha kuna nini"?

Alieuliza ni mama Bionce.

“Mama ni masaa machache huyu binti kaingia hapa.lakini utafikilia mzawa wa hapa kila mtu  ni huyo binti”

Aliongea Bionce. 

“Kwahiyo mwanangu una taka nimfanye nini?.Si unajua we ndio mwanangu wa pekee unaataka tumfanye nini”?

Aliuliza Mama Bionce.

“Eeeh mama nimekumbuka kitu mfanye kipofu tuone nani atampenda”

Walikubalia  Bionce na mama yake. 

Ilikua imefika mida ya Saa tatu za usiku.Mama Ujugi aliandaa chakula  wakala na Hasna kisha akampeleka sehemu ya kupunzika. Nyumba ya mama Ujugi ilikua imejengwa kwa udogo,imeezekwa kwa kutumia makuti ya migazi.

Ilifika majira ya sanane za usiku kuna mwanga ulionekana angani kisha ukaja kutua Kwenye nyumba ya mama Ujugi......



Ule  mwanga ulivyo  tua  ukapote nakuingia ndani.Azikupita hata dakika mbili ilisikika kelele ya mtu  .Mara ghafla ule  mwanga ulitoka kwa kasi, na kwenda kudondoka nje ya nyumba ya kina Bionce.

“Mwanaje Bionce Ingo"

(Mwanangu Bionce njoo)

Aliita mama Bionce.Alikua nje ya nyumba na Bionce akiwa ndani kalala.

"Kuliniki mama”

(Kuna nini mama”

Aliuliza Bionce. huku Akiwa anafungua mlango ,uliotengenezwa kwa bati.

“Ndawehwe ingo”

(Nakufa  Mimi njoo)

Alisema mama Bionce .Akiwa chini anagalala.

"Ugizente mama"?

(Umefanya nini mama)

Aliuliza Bionce .huku akiwa anamshika shika mama yake aliye kuwa chini akionekana kuhisi  maumivu makali  sehemu ya macho yake.

“uwo mkobwa alineza nukumule gusa”

(Huyo binti yuko vizuri sio wa kumchezea kabisa)

Aliongea mama Bionce. Huku akiwa analia .Bionce alimchua mama yake na kumpeleka ndani,akiwa kamshika mkono .Macho yake yalikua hayaoni.

Alienda akamchukulia majani ya mrumba rumba. kisha akachanganya na unga unga mweusi akampaka mama yake usoni.Hali yake ikarudi sawa.

Kesho yake palipo kucha mama Bionce .Alimuagiza mwanae Bionce akaenda kuwaita wazee   wawili na mama mmoja. Nao walifika kwa muda bila kuchelewa. 

" Yemga ndabhahamagaye ngaha mbhabwile huwu mukobwa latwononela amagambo yachu su muntu”

(Jamani nimewaita hapa niwaambie huyu binti atatuvurugia mambo yetu sio wa kawaida)

Aliongea mama Bionce. Akiwapa habari watu hao wakionekana  ni washilikina.Jana mama Bionce alienda nyumbani kwa mama Ujugi. kwa lengo LA kumpofua macho Hasna,kwa agizo alilipewa na mwanae Bionce. Ilikumkomesha Hasna.

"None tugilente ave ngaha mkijiji”?

(Sasa tunafanyaje ili aondoke hapa kijijini?)

Aliongea mama mmoja anae fahamika kwa jina la  mama kampakasa.

“Hiyo ni sawa  vilashobhoka,none izoezi litanguke dyali”

(Hilo ni sawa kabisa,kwahiyo zoezi hili linaanza  lini)

Aliuza mzee wa makamo.Alieonekana  alikua kakaa kimya muda akiwasikiliza tu.

“Hili izoezi lilatangula isiku  zitatu si mbele”

(Zoezi hili llitafanyika siku tatu mbele )

Aliongea mama Bionce .Walikubaliana kwa pamoja na kisha waka  sambaa .

Hasna alikua na mama Ujugi wakitoka  mtoni kuuchota maji.

“Hasna mwanangu kijiji hiki , wanawivu sana napia kunauchawi sana"

Alikua anaogea mama Ujugi. Pia alianza kumuhadithia kifo cha mume wake.Alikufa  kifo cha kutatanisha cha kuliwa na mamba wakati mto  wa Shunga hauna mamba kabisa.

“kwani mama Uchawi ndio nini”

Aliuliza Hasna.Kumbuka Hasna alikua hana kumbu kumbu yote .Hata hayo anayo hadithiwa na mama Ujugi kwake yalikua mageni.Maana hata Jana usiku yeye akujua chochote kilichokua kina endelea alipo kuja kuwangiwa na mama Bionce. Naakijulikani kilimpata nini au alikutana na kitu gani.

Zilipita siku mbili. Hasna alikua peke yake akielekea mtoni kuchota maji.Alipo fika alimkuta Bionce ndio alikua akijitwika ndio ya maji.

Lakini Bionce alipo muona  Hasna aliangusha ndoo chini kisha akaanza kukimbia.

Hasna alianza kushanga na kujitazama.Nakuanza kujiuliza mbona hamna kitu alafu anakimbia.

Basi Hasna aliamua kuendelea  kuchota maji .Alimaliza alipiga  hato  kadhaa kuelekea mbele kulikua na mlima wa nawe.Mara alisimamishwa na vijana wa tatu.

“We Hasina  Jana ulijifanya mujanja, ulipokua unaenda gengeni tukakuita kudengua, sasa rete nyodo zako na huku"

Aliongea kijana moja kati ya wale kwa rafudhi ya kiha. huku aki shusha mfuko aliokuwa kaubeba bega.

.“We bhana una muchelewesha ,muchuzi wa mubwa  uliwa  wa moto bhana"

Alidakia kijana mwingine huku akimvaagaa Hasna.Hasna aliangusha ndoo chini akataka kukimbia,lakini waka  mtaimu nakumuangusha chini.

Walimchania nguo  lengo lao nikumbaka .Alitangulia mmoja akavua haraka nguo lakini alionekana kama kanganda bale .Hasna alikua anapiga kelele za kuomba msaada  lakini hakuweza kupata msaada  wowote.

“We Michael bado tu mbona hautoki”

Aliongea kijana mmoja miongoni mwa wale vijana watu.Aliye simama akiwa kajianda, akimaliza mwenza nayeye aende.

“Eeeeh haka kadada mbona hakana”

Aliongea Michael huku akinyanyuka. Alipo nyanyuka tu na yule mwingine alimrukia Hasna .dakika mbili alinyanyuka akashika nguo mkononi nakuanza kukimbia.Huku maiko alikua kafika mbali.Yule mwenzao alibaki anajiuliza wenzake nini kilicho wakimbiza.

Hasna nae alibaki akishangaa, hawakuweza kumfanya  chochote alafu wamekimbia .Hasna akinyanyuka akaenda kuchukua  ndoo yake. huku nguo zake nikiwa zimechanika.

Alipita  karibu na yule kijana  mwingine. Aliye kua kabaki akiwashangaa wenzake wakikimbia.alianza kusogea kwenye majani huku akiwa na hofu.

Hasna alienda kuchota maji na kurudi nyumbani .Akimuhadithia mama Ujugi yote.

Upande wa wale vijana warifika  makwao.Yule mwenzao waliye muoacha kule nae arifika.

“jamani mlikimbia nini sasa". 

Kijana yule aliwauliza wenzake.

"Eeeh bhana hauwezi kua mini kare  kadada ni karembo rakini  akana kikojolio"

Aliongea maiko Lakini mwenzao alitaka  kumbishia .yule kijana alietaka kumuingilia Hasna Mara ya pili alimsibitishia hilo.

Ni kweli hawakuweza kuona chochote ndomaana walimuona ni mtu wa ajabu.

Maneno yalianza kuzangaa kuwa Hasna nimchawi.

Siku moja kulitokea vifo vya watu wawili,vilivyo  kuwa na utata .Watu walijikusanya na mapanga wakidai toka huyo binti kaingia pale kumekuwa na matatizo.Na hata mvua zimegoma kunyesha yeye ndio sababu.

Ilikua ni usiku waliizingira nyumba ya mama Ujugi na kiwasha moto.



Nyumba ili endelea kupamba moto ,huku wana kijiji wakiwa  pembeni wakushuhudia.

"Ilazima bhahwele bhose humo  nyene mulugo bwabhu wene huwo mkobwa 

Nuwo muntu wage yamusize munzu”

(Lazima wafe  humo  humo  ndani pamoja,na huyo mtu  anaemfuga).

Nimaneno ya baadhi ya wana kijiji.

Wana kijiji hawakuweza kutoka hapo hadi walipo akikisha nyumba yote imeungua na kubaki majivu.

Baadhi ya watu ambao hawa kupendezewa na tukio hilo, walimfata mwenyekiti wa kijiji hicho, nakupeleka malalamiko  hayo ya ukatili na  unyama.Ulifanywa na wana kijiji hao.Lakini mwenye kiti  huyo hakuwa jali zaidi aliwafukuza kwake.

Upande wapili kwenye nyumba ya Zuberi, Alionekana akiwa kaa  akiitaza nyumba yake huku machozi yakimtoka.

“Eeeh mungu waku nimetoa  roho za watu wengi, bila kujali maumivu yao wala machungu ya familia zao.Tamaa imeniponza,eeh mungu nimejifunza kwa mateso haya ninayo yapata.Natamani unipe hata dakika moja ya kurudi duniani.Ni tubu  na kuomba masamaha kwa yote niliyo  yatenda.Nipo kuzimu natumikia adhabu  ya matendo yangu.”

Yalikua ni maneno ya Zuberi.Naalihapa kulipa kisa kwa wote waliomshawishi kuingia kwenye chama hicho.

Aliingia ndani na kumkuta mtoto mdogo akiwa kalanzwa  kwenye sofa.Alikua ni mtoto wa Yule rafiki yake,yeye ndiye alikua mshawishi mkubwa wa Zuberi kuingia kwenye chama hicho.

Zuberi alimnyanyua mtoto .Mtoto huyo alianza kulia kwa saut.Mama yake alikua jikoni,alikuja mbio mbio alivyo sikia mtoto analia.Lakini alijikuta akishangaa na kubaki mdomo wazi  alipo mkuta mtoto wake akiwa anaelea juu juu.Maana yeye hana uwezo wa kumuona Zuber.Alichokua anakiona ni mtoto.Alianza kusogea taratibu mama huyo .Lakini alipokaribia Zuberi alikigawa kitoto hicho vipande viwili na damu nyingi zilimrukia yule mama.Mama yule alipo ona  vile alipoteza fahamu pale pale.

“Na huu ndio mwanzo lazima wote mpate machungu, niliyo  yapata mimi ,nilikua naishi  maisha ya furaha ya umasikini wangu nimemuua mke wangu na watoto wangu.Mlitumia ujinga wangu ili mnufaike nyinyi  pasipo kutoa hata  damu za ndugu zenu."

Aliongea Zuberi akiwa ka shika vipande vya yule mtoto.

Zuberi hapo nyuma alikua naishi na familia yake .Alikua na mke pamoja na watoto wawili.Zuberi alikua anafanya kazi ya kubeba watu kwenye baiske daladala kwa wasukuma wanaita ganagana.

Maisha ya Zuberi yalikua magumu sana, muda mwingine familia yake ililala bila kupata chakula.

Zuberi aliona bora abadilishe kazi na kujikita machimboni.Kwenye  machimbo ya kakola yalioko nje kidogo ya kahama mjini.

Kidogo maisha yake yalikua angalau.

Zilipita Miezi miwili kuna MTU alipoteza maisha kwenye shimo (longo bezi) alililokua akichimba Zuberi na wenzake .Mtu huyo alifariki kwa kukosa hewa alipo kua chini ya longobezi hiyo.Hivyo selikari ilichukua jukumu la kuwafungia wachimbaji wadogo wadogo.

Maisha ya Zuberi yalirudi kuwa magumu sana.Siku moja Akiwa njia akitokea  machimboni ambako kwa sasa walikua wakichimba kwa kuibia ibia kutokana na kufungiwa. Alikutana na mtu mmoja Aitweye Jimi,alikua nisimati alionekana kuwa napesa hata usafiri aliokuwa nao ulidhilisha hilo.Alikua na BMW ya mwaka elfu mbili kumi na  mbili.

Basi alimpa lifuti Zuberi walipo fika mjini  waliingia kwenye hoteli moja kubwa.Zuberi aliogopa kuingia kwa jinsi alivyo kua mchafu.

“Usiogope ndugu ingia tukae hapo”

Aliongea Jimi.Zuberi alifuta kiti  akakaa,Jimmy aliagiza dompo. 

Zuberi aliagiza chakula maana Alikua na njaa.Alipo maliza kula walianza kupiga sitori.wakatambulishana  majina yao.

“Ndugu yangu nashukuru sana.Nilikua naomba nikuache, maana nimeacha familia yangu aina kitu ,siwezi kukaa hapa nakula raha wakati familia yangu inashinda njaa."

Aliongea Zuberi huku akiwa ana nyanyuka.

“bwana mdogo acha haraka hebu subiri kidogo."

Aliongea Jimmy. Huku akitoa waleti yake mfukoni.Aliehesabu lakimoja na kumkabidhi Zuberi ,ambaye alikua akisita kuzichua pesa hizo.Mwisho wasiku alichua.Jimmy alimuomba kesho ajitahidi  waonane.

Zuberi aliondoka akiwa  nafuraha.Kesho ilipofika Zuberi alimtafuta Jimmy.

“Zuberi nataka nikuambie kitu,siku zote siri ya hela anaijua mwenye hela"

Aliongea Jimmy .

“Una maana gani Jimmy kusema hivyo”

Aliuliza Zuberi.

“Zuberi haupendi maisha mazuri”?

Aliuliza Jimmy.

“Maswali gani hayo kaka tunaulizana kwa maisha haya hata Leo nipate maisha mazuri.”

Aliongea Zuberi huku akiwa anatabasamu.

“Sasa unaroho ngumu mzee au una roho yakike”?

Aliuliza Jimmy.

“Hebu nicheki unanionaje nafanana na demu.”?

Aliongea Zuberi.Basi Jimmy alimwambia kesho mapema ajiandae kuna sehemu anampeka.



Zuberi alirudi nyumbani kwake akiwa na furaha.

“Mume wangu furaha huyo kulikoni leo”

Aliuliza mke wa Zuberi.Zuberi hakumjibu chochote yeye Alikua akitamani kesho iwahi kufika.

Hatimaye kesho iliwadia na zuberi alijiandaa.

Na kwenda nyumbani kwa Jimmy .Alimkuta Jimmy akiwa tayari akimsubiri yeye.

Basi safari ilianza,ilikua ni mida ya saa  mbili za asubuhi.

Waliekea barabara ya kuelekea Kigoma,walipo fika maeneo ya Mlima Sinai walikatisha kuelekea kulia.kulikua na msitu mzito na ulio weka giza.Zuberi alionekana kuanza kupatwa na wasi wasi ,Lakini Jimmy Aliweza kumtuliza.

Walifika sehemu wakapaki gari,na kuanza kutembea kwa mguu.kati kati ya msitu huo kulikua na mji mzuri.Na nyumba za kifahari ,Zuberi alikua akishangaa .Ukiwa unaingia hapo kunakibao kikubwa ,kimeandikwa “KARIBU MJI WA KULA BILA KUVUJA JASHO”

Basi walifika moja kwa moja ,kwenye nyumba kubwa sana,na nje ya jumba hilo kuna mzee alikua kakaa Kwa nje.Alikua na ndevu nyingi hadi anatisha .Macho yake alionekana muda wote yamejifumbu.

Walifika aliwa  karibisha,Lakini Zuberi akishangaa na kujiuliza mzee huyo anaonaje?wakati kafumba macho muda wote.

“Mzee nimemleta yule kijana niliye kuambia”

Aliongea Jimmy lakini yule mzee aliongea chochote. Alinyanyuka  na kuingia ndani Jimmy na Zuberi nao  wakafata nyuma.

Zuberi alishangaa  kuingia ndani kukuta kuna mti mkubwa wa msufi.

Alikuta watu wengi wamevalia majoho meusi wakiwa wamepiga magoti chini.

Yule mzee alifika akakaa kwenye kiti kikubwa kilichokua mbele ya watu wale.

Zuberi na Jimmy walikua wamesimama.

“Jimmy unahuwakika na huyu mtu  uliye tuletea anafaa”

Aliuliza mzee huyo.

“Ndio anafaa,na kalizia kufanya chochote ”

Aliongea Jimmy. Lakini Zuber alishangaa  kusikia Jimmy anaongea  hivyo alimkazia macho na kumuambia.

“Jimmy mwambie mimi nataka dawa  tu,sitaki mambo mengine”.

Aliongea Zuberi kwa sauti ya chini.Basi yule mzee aliendelea kusema ,Kama yuko tayari apite mbele .Jimmy alimwambia Zuberi apite mbele.Zuberi alisogea kisha akapiga  goti mbele ya yule mzee.

Alianza kuongea mzee huyo. Kuanzia  sasa umejiunga kwenye ushilika wa kafara. Kwa sababu umekubali mwenyewe ukiwa na akili timamu,bila kulazimishwa na mtu.Jimmy alikua akimjibia Zuberi kila alicho sema chenye  kuhitaji majibu.Hilo swala lilibaki likimshangaza sana Zuberi.

Sasa tuna kupa sheria zetu ukikiuka basi utapatiwa adhabu kubwa na Kali.

Kisha yule mzee akampatia Zuberi kitabu kikubwa cheusi.Nakuambiwa akisome ili azijue sheria vizuri.

“kwahiyo unatakiwa utoe kafara ya mbuzi mwenye masikio mafupi na ambaye hana mkia”

Aliongea mzee huyo.Lakini Zuberi hakuelewa mzee ana Maana gani.?Zuberi alimwangalia Jimmy .Jimmy alimpa ishala kuwa akubali.

“Ndio nimekubali”

Alipo sema hivyo washirika wote walifurahi kwa pamoja.Kisha yule mzee alimchukua kisu na kumkabidhi Zuberi, akamuonesha mti uliokua  mdogo  na kumuambia aukate.

Zuberi alipokua anakata alisikia sauti ya mwanae wa kwanza.Akipiga kelele ikisema  baba usiniue.Zuberi alishituka alipo sikia hivyo alibaki kazubaa asijue cha kufanya.Alisikia sauti ya yule mzee ikisema kata,unatuchelewesha hatujaja kucheza hapa.

Zuberi alipo kata naile sauti hakuisikia tena.Zuberi alianza kuwa na wasi wasi moyoni mwake.

Yule mzee alimkabidhi Zuberi kichupa kidogo.na kumwambia maelekezo ya kichupa hicho anayo  Jimmy. Mwisho mzee huyo alimalizia kwa kusema, Zuberi chochote hutakacho kikuta  huko usijaribu kutoa chozi hata kidogo.

Basi walirudi. Lakini walipo fika  nyumbani alipo panga Zuberi .Zuberi alishangaa kuona watu wengi. alianza kupata na wasi  

“Jimmy mbona kuna watu wengi”?

Aliuliza Zuberi.Lakini Jimmy hakumjibu alicho ulizwa .Na kumuambia nadhani unakumbuka  ulichoambiwa na mzee.

Zuberi akishuka haraka na kwenda kuukiza nini kimetokea ,aliambiwa mwanae kagingwa na pikipiki hivyo kapoteza maisha.Zuberi alianza kulia kwa uchungu, huku akikumbuka yale aliyo yaona kule kwa yule mzee.

Zilipita siku kadhaa baada ya mazishi.Jimmy alienda kwa  Zuberi.Zuberi alipomuana Jimmy alimfukuza na kumwambia hatakia amuone akikanyaga pale.

Zilipita wiki mbili Zuberi alifusha tena mwanae wapi. Alibumbukia kisimani akawa kapoteza maisha.

Zuberi aliachanganyikiwa   na asijue cha kufanya.Pesa hana na nisiba inemuandama.

Zilipita miezi miwili,  mke wa Zuberi mimba yake ilikua imeishakua kubwa .Walikua wanamuhesabia siku tu.

Hatimaye siku zilifika mke wa Zuberi alishikwa na uchungu.Walimkimbiza hospital.Taarifa zilikuja zingine mbaya kwa upande wa Zuberi.

Mke  wake nakiumbe kilicho kuwa tumboni, kwa pamoja wamepoteza maisha.

Zuberi alichanganyikiwa.Mara hakiwa kwenye hali hiyo ya mawazo.Alitokewa na yule mzee.

“kijana sisi huwa hatuchezewi ,Ukitaka uwe na amani  basi urudikuomba msamaha, na uendelee  na ushilika.La sivyo tunateketeza familia na ukoo  mzima.”

Aliongea yule mzee kisha akapotea.

Zuberi alimtafuta Jimmy na kurudi kuomba msamaha .Alipewa mashariti kila baada ya miezi miwili awe anatokea kafara ya damu, ya msichana ambaye hajawahi kukutana na mwaume ya bikira.  

Ndio hayo yaliomkuta Zuberi na sasa analipiza kisasi.

Hata kuzikwa kwa mwili wake ,na kuachwa kwa nafsi yake ikitapa tapa,ni mpango uliopangwa na Jimmy na baadhi ya washilika.Iliwampoteze baadae asijue kutoa siri zao.Maana kaingia kwenye chama hicho kwa Mara ya pili ili kunusuru familia yake isiendelee kuisha.

*     *       *        *         *       

Jimmy baadae alipo rudi nyumbani kwake alikuta  mkewe kalala chini huku akiwa katapakaa na damu.Jimmy alipo angalia pembeni aliona damu nyingi NA vipande viwili vya mwanae.

U pande wakasuliu katika kijiji cha Shunga.Alionekana mama Bionce na wenzake wakipongezana. kwa zoezi walilo lifanya  la kumuundia Hasna njama na kuonekana yeye ndiye mchawi.Na wana kijiji wenyewe hasira Kali kumteketeza Kwa moto.

Mara wakiwa pale walishangaa kumuona Hasna akiwa kasimama mbele yao huku akitokwa  na machozi ya damu.



"Ye nyina  Bionce kuliniki wichaye kimya ighafula gusa"?

(Wewe mama Bionce kuna nini mbona umekaa kimya ghafla)

Aliuliza mzee mmoja kwenye kile kikunda waliochokaa cha watu wanne.

“Ndamubhonye wa mukobwa alahagaze ngaho”

(Nimemuona yule binti kasimama hapo”

Aliongea mama Bionce. Huku akiwa anasonesha kwa kibole.

“Alihehe kuki  atabhoneka ngaha?.Leka ugutinya yalamaze uguhwela”

(Mbona hakuna mtu?,acha woga kaisha teketea na moto huyu”

Aliongea tena yule mzee.

”Ye mga tulabhonana baadaye  jewe ndagihe imuhila ukuruhuka ndiyumva nabhi”(jamani tutaonana baadae mi unaenda kupunzika najisikia vibaya)

Aliongea mama Bionce. Huku akinyanyuka na kuingia ndani.

Nawale  wenzake walibaki kumshangaa .Nakuona kama mwenzao kachanganyikiwa.

 Kwenye mashamba mbali na kijiji hicho cha Shunga. Alionekana mzee  mmoja akiwa anaokota kuni.Na hapo kulikua na  kinyumba kimoja tu ,kilichojengwa kwa kutumia miti  na juu kimeezekwa kwa nyasi.

Mzee huyo aliona watu wawili wakiongozana kuelekea mahala alipo kuwa yeye.

“Babu shikamo"

Walisalimia watu hao.Mzee alibaki kawatazama bila kuitikia hata salamu.

“Samahani mzee unaweza kutusaidia maji ya kunywa”?

Aliongea mmoja kati ya hao watu wawili.Mzee akuongea  kitu.Alichukua mzigo wake wakuni na kuanza kuongoza njia ya kuelekea kwenye mji wake.

Walimfata nyuma,mmoja kati yao aliomba kumsaidia lakini mzee alikataa.

Walifika kwenye mji wa mzee huyo.aliingia ndani nakuwaketea maji kwenye kata.

Walipo maliza kunywa maji walishukuru lakini mzee.kama kawaida yake akujibu chochote.Walianza kuondoka wakifata kanjia ,alikokua kanapita nyuma ya nyumba ya mzee huyo.

Walishituka walipo sikia sauti ya yule mzee akiwasemesha.

“Nyinyi mabinti hebu rudini hapa”

Walishangaa nakujiuliz kumbe  mzee anongea.

“Hivi mnapajua mko  kwenda”?

Aliwauliza mzee.

“Ndio mzee tunaelekea Nyakitonto”

Aliongea mmoja kati ya wale watu wawili alikua ni mama wa makamo.Na ndio alionekana kuwa ni mwenyeji hapo.

“Huko nikubaya sana kwa sasa,na muda huu hamtofika popote”

Aliongea yule mzee .

“kwani kuna nini mzee”?

Aliuliza yuke mama mtu mzima  kidogo.Mzee aliendelea kuwaambia huko nikubaya na kuna mambo ya ajabu.

Aliwapa hifazi kwa siku hiyo ,ilipofika jioni walienda shamba na mzee waka  chimba  viazi.Walivichemsha walikula  wakisukumia na maji.

Mzee aliwaomba wakae siku tatu, amalize mambo yake ya palizi ili awavushe kwenye msitu huo mkubwa, na pia aliwambia.Atawapa sababu kwanini kawakaza kuendelea na safari.

Ulipo ingia usiku ,mzee aliwasha moto mkubwa wa kuni.Walikaa  wote kwenye moto na mzee, wakanza kupiga sitori aliwauliza mzee kwanini wameondaka.

Alianza kuhadithia yule mama mtu mzima.

Ilikua usiku majira ya saa tano,nikiwa nimelala Mara kidogo alikuja binti huyu kuni amsha.

Akaniomba tu toke nje lakini sikuelewa kwa nini,lakini na Mimi sikua mbishi nilimsikiza tu.Aliendelea kuelezea  yule mama.Walipo toka nje alimuomba wakajifiche, kuna kicha  jirani na nyumba hiyo.

Japo mama huyo alianza kupata wasi wasi,kutokana na binti huyo kuwa mgeni kijijini hapo.Hakujua lengo lake ni nini,alitaka  kugoma  maana huku walipokua  wanaelekea kulikua na kiza  kikubwa.Binti huyo alimbebeleza ,mama huyo akajikuta akikubali.

Walikua kwenye kichaka huku wakiwa wanaiagalia nyumba ndipo hapo walipo waona watu wengi wakiizingira nyumba ,na kuichoma moto.

“Mzee wangu hivyo ndivyo nilivyo kuwa”

Alimaliza kuzungumza mama huyo.Mzee alitazama binti huyo kisha akawapa pole.

“Samahani sikuwauliza hata majina yenu,Mimi naitwa mzee bungi”

Alijimbulisha mzee huyo.

“Mimi naitwa uwiga(Mama Ujugi),Na huyu binti anaitwa Hasna"

Alitoa utambulisho huo mama Ujugi.

“Basi karibuni sana pia nashukuru tumefahamiana”

Aliongea mzee bungi huku  akiwa anchochea moto.

“Mzee kwanini unaishi huku porini tena pekeako na mazingira yana tisha hivi”

aliuliza mama Ujugi .Mzee yule aliinama chini kisha alipo inua macho yake ,yalibadilika na kua mekundu sana kama nyanya iliyoiva.

Kisha na machozi yakanza kutililika.Hasna na mama Ujugi walianza kuogopa nakurudi kwa kujivuta kutumia makalio yao.

“Katika watu wenye  bahati na nyinyi ni miongoni mwa hao”

Aliongea mzee bungi.

“Kwanini babu unasema huvyo”

Aliuliza mama Ujugi.

“Hasna una weza kuniambia  wewe ni nan”?

Aliuliza mzee Bungi.Kisha Hasna na mama Ujugi waliangaliana kwa mshangao swali hilo.




Walishindwa kuelewa kwanini kauliza hivyo mzee Bungi.Hasa  kwa upande wa Hasna alibaki kutokua  na sito fahamu.

“Hasna nakuuliza naomba jibu”

Aliuliza mzee Bungi Kwa sauti ya juu na yaukali sana.Hasna alianza kutetemeka.Kiukweli swali hilo kwa Hasna lilikua  gumu  kwake ,na alikua hajui  chochote kinachomuhu, yeye ni nani nakatokea wapi hadi kufika  hapo kwenye kijiji cha Shunga.Anacho kumbuka ni jina lake tu.Hasna alibaki kumuangalia mzee bungi, huku asijue cha kujibu.

“Mzee wangu huyu tulimuokota hakiwa ajitambui,na alikua akumbuki  chochote kile zaidi ya jina”

Alisema mama Ujugi. Lakini mzee Ujugi alimuangalia kwa jicho la  ukali hadi mama Ujugi alianza kuogopa.

“Siongei na wewe naomba ukae kimya”

Aliongea mzee Bungi.

“Mzee  wangu Mimi sijui  chochote kinacho nihusu.Nimejikuta nikiwa huku hata kumbukumbu nikijaribu kuvuta, hakuna picha yoyote nayoipata”.

Aliongea Hasna huku akitokwa na machozi.

“Kama mmetumwa mwambieni aliye watuma haniwezi.Kuanzia sasa sitaki niwaone Hapa kwangu ”

Aliongea mzee Bungi huku akiwa kanyanyuka.

“Sasa mzee wangu  usiku wote huu, sisi tutaelekea wapi”?

Aliongea mama Ujugi.

“Nimesema ondakeni kwanguuuu.Tawafanya usiku huu muuone mchungu kwenu”

Aliongea mzee Bungi hakiwa kabadirika kwa Hasra.

Mama Ujugi na Hasna walinyanyuka mbio mbio,nakuanza kuondoka .

“Sasa mama tunaenda wapi”

Aliuliza Hasna .

“Tena naomba usiongee lolote ukae kimya mchawi mkubwa wewe,kila sehemu wanatufukuza kwa ajili yako.Umesababisha nyumba yangu imechomwa kwa uchawi wako.Najuta hadi kwa nini nilikupokea kwangu.

Sasa nacho kuambia kuanzia sasa kila mtu  aende na njia yake.”

Aliongea mama Ujugi .Nakuanza kuondoka na kumuacha Hasna akiwa kasimama  pale pale. Na asijue  wapi aelekee,maana ilikua  usiku na msitu umefunga sana.

Mama Ujugi alitembea hadi sehemu, aliona moto mbele kidogo alipata faraja.Akajua kuna miji ya watu.

Lakini alipozidi kusogea alianza kushangaa kuona watu wa ajabu.Wakiwa wanazunguruka moto kwa mduara ,huku wakicheza na kuimba  nyimbo.Kwa lugha walioijua wenyewe.

Mama Ujugi alianza kuogopa.Kisha akasogea mbele na kujificha,huku akiwa ana tizama kinachoendea.

Hakiwa pale akishanga. Alishituka alipo sikia kitu  kikimgusa mgongoni.

Upande wa Hasna aliendea  kutembea,alikua akifata mama Ujugi nyuma nyuma bila ya yeye kujua.

Alipo endelea kutembea alisikia kelele za watu kushangilia.Alizifata kelele hizo.Na hapo alishindwa kuelewa mama Ujugi kaelekea  wapi.

Alisongea Hadi jirani na eneo hilo aliwaona watu wengi,wakiwa wanacheza na kuimba  kwa furaha.

“Nyama imejileta ,nyama imejileta.uuuuuuwi,uuuuuuuwi”

Watu wale walikua wanaimba na kushangilia.

Hasna alipo taza  kwa umakini ,ule  moto ulivyo  waka  kwa kasi na kuweka mwanga.Aliweza kumuona mama Ujugi kiwa  akiwa kalazwa chini na watu wale.  

Wakimzunguka na kumshangilia.

Hasna alivyo ona  vile.Alisogea hadi pale walipo kuwa wale watu.Kwa lengo la kumsaidia mama Ujugi.

Lakini cha ajabu alipo sogea pale wale watu ,walikaa kimya  wote na kuanza kurudi kinyume nyume .Na kisha  wote wakakimbia.

Lakini Hasna alianza kushangaa kwa nini wamemkimbia.?Alifaka akamnyanyua mama Ujugi,mama Ujugi alikua namuagalia Hasna kwa wasi wasi.

“Hasna mbona ulikua kiumbe cha ajabu wakati unakuja hapa”

Aliongea mama Ujugi huku akimtazama Hasna  kwa wasi wasi.

“Mama Ujugi utakua  ulikua unaota,Mimi mbona Niko vile vile”

Aliongea Hasna Huku akitabasamu.

“Hasna na kwambia  kweli ulikua unatisha,na Mimi nilijua ndio nakufa  baada ya kuona kiumbie cha ajabu, nikajua Masada na kosa na wale watu wote wakakimbia.”

Hasna alianza kukumbuka ,baada ya wale watu kukimbia nakubaki akijiuliza  wanakimbia nini.Alifikilia lakini hakupata  jibu.

Kitu kimoja  ambacho Hasna alikua ajagundua kutoka  kwake,nipale  anaposhikwa na  hasira anabadilika, na kuwa kiumbe cha  ajabu.Na chakutisha sana.Lakini yeye kwa upande wake ujiona wa kawaida tu.

Basi walianza kuondoka na mama Ujugi wakitafuta njia.Ilikua bado usiku mzito.Walitembea kwa muda mrefu ,kidogo palianza  kupambazuka.  

Walitembea kwa masaa kadhaa ,wakawa wamefika kwenye kijiji cha Nyakitonto.

Walikua wamechoka sana walielekea hadi nyumba moja pale kijijini.Walipokelewa lakini watu wa nyumba hiyo walionekana kumfahamu mama Ujugi.

“Karibu shangazi za masiku”?

Aliwakaribisha mama wa mji huo.

“Asante shangazi za siku”


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG