Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SAMAIRAH - 3

  

Simulizi : Samairah

Sehemu Ya Tatu (3)


Oya bajaji njoo ,yule jamaa aliita ile bajaji ambayo ilikuwa imewabeba akina Aryan baada ya kutoka hospitalini kwa mara nyingine ikawarudisha hospitalini wote watatu wakiwa hoi.


Walipelekwa kwenye ile hospitali ambayo walitoka kumtibu Gwae,walipokelewa upesi kisha wakaanza kufanyiwa matibabu

Aryan alikuwa anafahamu zake ila damu nyingi ndio zilikuwa zinamtoka

Gwae alipelekwa tena kwenye chumba cha kufunga p.o.p huku Abbas na Aryan walisafishwa yale majeraha ambayo walipigwa na chupa.

Saa tisa usiku ndio Abbas alizinduka na kumkuta Aryan yuko pembeni yake ,Aryan alisikia maumivu makali alivyopeleka mkono kichwani alikutana na pandeji ndipo akakumbuka jana alipigwa na yule kijana ambae ndio anatembea na mama yake.


Abbas aliuliza mama yangu yuko wapi? Lile swali lilimfanya Aryan ainamishe kichwa kisha akasema mama yako amewakana mbele ya yule kijana ambae ulimwona yuko nae na amesema hawajui wala hawatambui.

Yale majibu yalimfanya Abbas alie kama mtoto ,ndipo Aryan alichukua jukumu la kumnyamazisha hadi aliponyamaza.


Asubuhi palipo kucha Aryan alimwendea daktari na kumweleza kuwa awaruhusu wakamalizie mtihani halafu watakuja kulipa pesa ambazo zimetumika katika matibabu, yule dakatari alikuwa muelewa aliwaruhusu ndipo waliondoka wote watatu ,huku Gwae amefugwa mhogo ama gamba gumu mikono yote miwili.


Aryan alikuwa na hasira alienda hadi nyumbani alimwacha Gwae kwa mama yake kisha wao wakaingia darasani wakiwa na bandeji,

Ile Aryan anaingia darasani

Jesca alikuwa wakwanza kumwona alimkimbilia na kwenda kumkumbatia,ile anayapeleka macho yake kwenye paji la uso ndipo alikutana na bandeji kubwa aliyageuza macho yake na kumwangalia na Abbas alishangaa kumwona ana bandeji usoni,


Mara Nanaa akaja pamoja na mwenzake Lusi walimsalimia kisha wakamwambia pole Aryan umefanyeje? Kabla hajawajihu Joyce akaingia darasani taratibu akiwa anachechemea maana tokea alivyochomwa bisi bisi mguu wake bado hujapona.


Joyce alikuwa kashika zawadi ya Aryan alivyomwona Aryan na bandeji Joy alijikuta akibaki mdomo wazi ,mara kundi la akina Kudra likaingia darasani kwa fujo walishangaa kuwaona Aryan na Abbas wamesimama huku wanafunzi wenzao wakiwashangaa.


Mara mkuu wa shule akaingia huku kashika fimbo ,mkuu aliongea kwa ukali nani kavunja kioo cha nyumba yangu usiku na kuniibia pesa.


Kudra na Mussa waliwanyoshea mikono Abbas na Aryan ,mkuu hawa ndio wezi angalia usoni wanabandeji bila shaka hao ndio wezi maana inaonekana wamepasuliwa na vioo walikuwa wakiiba


Mara polisi wakaingia wakiwa wameshikilia pingu ,mkuu wa shule aliwanyoshea mkono akina Aryan na kusema wezi wenyewe ndio wale


Tulipoishia jana baada ya mkuu wa shule kuingia darasani akiwa kaongozana na polisi , aliuliza mwizi aliyevunja dirisha na kuiba pesa zake,akina Kudra waliwanyoshea mikono Abbas na Aryan kuwa hao ndio walioiba maana hata kwenye vichwa vyao walikuwa na bandeji tena zinaonekana bado mpya,


Polisi waliwafuata Aryan na Abbas kisha wakawaambia mpo chini ya ulinzi,Aryan hakupenda kabisa kubisha alinyoosha mikono yake na kufungwa pingu huku Abbas nae akitii amri ya polisi

,Aryan aliwaangalia wabaya wake wanao yasakama maisha yake alijua kuwa hii ni njama imefanywa na akina Kudra ili wafukuzwe ,kazi na ndio ilikuwa siku ya mwisho wamalizie mitihani,

Akina Jesca walimshika Aryan huku wakilia na kusema Aryan hajaiba jamani Aryan hajaiba,Joyce nae alianza kulia taratibu maana mtu ampendaye ndo hivyo anasemekana ni mwizi hivyo hatomwona tena.


Mara walimu walibidi wakaongee na polisi ili wawaachie akina Aryan wamalizie mitihani ,halafu wakishamaliza watawachukua na kuwapeleka kituoni, mkuu wa shule aliwaka na kusema hapana kunifundisha kazi pelekeni kituoni.


Walipakiwa kwenye difenda kabla gari haijawasha kuna gari ya wawekezaji walio wekeza kwenye hio shule ,waliomba wanafunzi waachiwe kisha uchunguzi ufanyike kwanza halafu waachiwe wakamalizie mtihani,

Aryan na Abbas waliruhusiwa kisha wakaingia darasani ,ile wanaingia darasani ndipo na Samairah aliingia darasani ,lakini Samairah kabla hajaingia darasani alimfuata muwekezaji mmoja na kumpatia flashi kisha akasema baada ya kumaliza mtihani ataichukua.


Basi polisi hawakuweza kuondoka walikaa mlangoni kabisa na chumba ambacho akina Aryan wanafanya mtihani,Aryan alifanya mtihani wake kama kawaida.

Tukirudi nje wawekezaji walitoa laptop kisha wakaweka ile flash waliopewa na Samairah, kila mmoja alibaki kukodoa macho hatimae waliita na walimu waje kushuhudia wakati huo mkuu wa shule yupo kwenye ofisi yake.


Kwenye laptop kulikuwa na video iliyorekodiwa majira ya saa kumi na moja alifajiri ,kulikuwa na kijana Mussa pamoja na Kudra wakiwa katika nyumba ya mkuu wa shule.


Mkuu wa shule ndio aliwaambia akina Mussa ,sasa tutafanyaje ili tumfukuze Aryan shule,Kudra alitoa wazo mkuu sisi tunakupa pesa kisha tunabomoa haya madirisha yako ya vioo na kuyapasua halafu ,tutasingizia Aryan kaiba pesa sababu yeye kwao ni masikini na kibaya zaidi hana nyumba,nyumba yao ishaunguaga moto kitambo,'

Mkuu wa shule alitabasamu na kusema hakika ninyi mnaakili alipewa kiasi cha pesa kisha Mussa na Kudra wakabomoa vile vioo vya madirisha ,


Wakati wanafanya hayo bibie Samairah aliwanasa na kuchukua mkanda kupitia kamera ,na kuhifadhi kwenye flashi , wawekezaji walipata ukweli kuhusu mkuu wa shule ,walichokifanya walichukua polisi na kwenda kumkamata mkuu wa shule na kumpeleka kituo cha polisi aeleze kwanini anashiriki katika masuala ya rushwa tena na wanafunzi wake.

Aryan alimaliza mtihani akatoka nje cha ajabu hakukuta polisi wala mkuu wa shule, alivyouliza polisi wako wapi ,wanafunzi wakidato cha kwanza walimweleza kuwa kesi imegeuka kwa mkuu wa shule na ashakamatwa ,Aryan alishidwa kuelewa , ,


Samairah alimaliza mtihani na kumfuata Aryan ,kisha alimsalimia na kumweleza kila kitu walichokifanya akina Mussa ,Aryan aliuliza sasa akina Mussa wanataka kunifanya nini mimi, kuniua ama kuniachisha shule, Samairah alitabasamu na kusema safari bado ndefu ,

Aryan umefanyaje hapo kwenye paji la uso ,Samairah aliuliza ,Aryan nae hakupenda kumficha kilichotokea alimweleza kila kitu kilicho wakuta jana.


"Pole" ndio neno alilolisema Samairah kisha akaondoka ,tukirudi kwa Aryan aliwaza sasa "tushamaliza mtihani na kesho ndo siku ya kupewa matokeo na kufunga shule" , Aryan alifurahi ili aweze kukaa mbali na akina Mussa.


Hatimae masaa yalienda jua likazama na siku nyingine iliwadia siku hio wanafunzi walipendeza na wengine walifurahi maana ndio ilikuwa siku ya kufunga shule

Kengele iligongwa na wanafunzi walikusanyika mahali wanakofanyiaga shughuli za kishule kama ilivyokawaida kulikuwa na wageni wawekezaji wa hiyo shule ,mwalimu wa zamu aliwaambia wanafunzi wakae kimya na wasikilize kwa makini maneno yatakayosemwa na waalimu pamoja na wageni waliopo mbele yao.


Kudra alimnong'oneza Mussa na kumwambia mhula huu tunaosha sababu nishaongea na mkuu kila kitu ,mimi nitashika nafasi ya kwanza wewe wapili halafu na Jesca watatu. Basi walikaa kwa makini ili waweze kushinda hizo zawadi .

Mwalimu wa taaluma alisimama na kuanza kusoma matokeo ya kidato cha kwanza kama ilivyo kawaida ,walisoma wanafunzi watatu bora na kumi bora,waliobahatika kupata nafasi ya kwanza hadi ya tatu walizawadiwa begi na makaunta book na kupigiwa makofi na shule nzima,ila kwa msimu huu wawekezaji waliboresha vizuri mshindi wa kwanza anapata shilingi laki mbili wapili laki moja na watatu elfu hamsini.


Wanafunzi walifurahi sana ,hatimae mtaaluma alisoma matokeo ya kidato cha pili na alivyomaliza alihamia matokeo ya kidato cha tatu,kwanza mwalimu wa taaluma alisema katika shule hii darasa la maajabu ni kidato cha tatu,kwanza wanafunzi wana akili sana pili wana ushindani mkubwa


Mtaaluma alitaja nafasi ya kwanza mhulaa huu imeshikwa na watu wawili wamegongana ,Aryan ,pamoja na bibie Samairah,wanafunzi walishangilia kwa fujo hasa hasa wanafunzi wakike wanavyompenda Aryan ,basi walianza kutaja Aryan ,Aryan,nakuwafanya hadi wawekezaji kutabasamu,

Aryan na Samairah wakiwa na ufaulu sawa sawa ,walibeba zawadi zao.

Mtaaluma aliendelea nafasi ya pili wamefungana watatu ,,mwalimu wa taaluma alivyosema hivyo Mussa na Kudra walijiuliza hio nafasi ni yetu ,watatu mimi wewe na Jesca, halafu Kudra akauliza hivi mkuu wa shule kala pesa zetu alafu hajafanya sawa wala hapa simwoni ,"mtaaluma alianza kutaja majina ,wakwanza ni "j" yaani alitaja "J" Jesca kasimama ,ndipo akamalizia Joyce basi Jesca alikaa kwa hasira na kuwaangalia akina Mussa

Walikuwa Joyce,Abbas,na Nanaa

Basi makofi yalipigwa nderemo na vifijo vikatawala, ndipo Mussa akaanza kukunja sura, nafasi ya tatu alikuwa Jesca pamoja na Lusi

Hakika kidato cha tatu kiliweka historia

Nafasi ya nne alikuwa Amina ,kuanzia nane na kumi ndio zilikuwa namba zao akina Mussa na Kudra.


Kudra wala hakusubiri waalimu wamalizie aliondoka akiwa na hasira na kwenda kukaa kwenye nyumba ya mkuu wa shule, hili li mkuu wa shule naenda kumtoboa hicho kitambi anipe pesa zangu ni maneno aliyoongea Kudra.


Baada ya waalimu kumaliza maongezi hatimae walipewa tarehe ya kufungua shule ,ndipo mwalimu Farida alisema naomba wanafunzi wakiume wa kidato cha tatu ,

Waje hapa ,walienda kama walivyoambiwa.


Mwalimu aliwaambia wapande kwenye gorofa ya nne ya jengo la hapo shuleni ,halafu kwa juu yake kulikuwa na sehemu ya kuhifadhi maji walikuwa wameweka matanki ya maji


Jamani wanafunzi nane naomba mpande mkateremshe lile tank la lita 2000 mtalisukuma tu halafu litaashuka taratibu mkiwa huko juu muwe makini msisukumane mtadondoka ,kati ya walio chaguliwa Mussa na Aryan walikuwemo ,


Mussa akiwa na hasira hajapata nafasi ya kwanza halafu Aryan kaongoza, 'Mussa aliwaza leo Aryan ndio siku yake ya mwisho tukipanda juu naenda kumsukuma adondoke chini ,leo ndio leo ,ni mawazo aliyoyawaza Mussa

Walipanda kwenye gorofa la pale shuleni hadi gorofa ya nne halafu kwa juu yake.walifanikiwa kuteremsha lile tank,

Lakini walivyomaliza wanafunzi walianza kuteremka ngazi na kushuka,

Mussa alimvuta Aryan shati na kumwambia wewe boya naona unajifanya kisa unashika namba moja ,Aryan ukweli sikufichi na unaona hapa tulipo nakusukumiza chini udondoke

Leo ndio siku yako ya kufa Mussa aliongea huku akitoa kisu chake kidogo mfukoni mwake.


Alimshika shati ,Aryan,na kumwambia nimekutafuta sana leo ndio nimekupata mahali pake unaona hichi kisu nakuchoma nacho tumboni.

Aryan alimwangalia Mussa ambae yupo siriazi ,kiukwelii kabisa ,Aryan aliona akizubaa anaweza kufa alitoa sauti kwa nguvu jamani msaada naku......

Aryan hakuweza kumalizia tayari Mussa alikizamisha kisu tumboni,Aryan alifumba macho akiwa ameshikilia mpini wa kile kisu kilichopo tumboni,Aryan alijikuta anakuwa kimya

Halafu Mussa akatabasamu na kusema wewe boya nimekuwinda sana alimsukumiza chini,

Tambua wapo gorofa ya nne kwa juu yeke sehemu ambayo ilikuwa na matanki ya maji sasa amesukumizwa chini,

Na chini pana umbali, kibaya zaidi sehemu anayosukumizwa chini kulikwa na mawe makubwa mfano wa yale ya kujengea msingi.


Aryan ndio anashuka kisu kikiwa tumboni na chini ni mbali na mahali anakokwenda kkudondokea pana mawe

Mussa alimchungulia na kuona Aryan anavyoteremka alitabasamu na kusema kuanzia sasa hakuna tena Aryan ,dakika sifuri tutaita marehemu



Tulipo ishia jana,baada

ya Aryan kufanyiwa unyama na Mussa alichomwa kisu tumboni,na kurushwa chini toka kwenye gorofa ya nne ,hatimae Aryan akiwa na hali mbya alifumba macho na kubaki kimya , alihisi kama roho inanyofoka tumboni kisu kimekitwa mahali pabaya.


Maeneo hayo jirani na hilo gorofa bibie Jesca walikuwa wapo na Samairah walikuwa wanapeana sweta,Jesca alikuwa kavaa sweta ya Samairah, Samairah alimwambia Jesca hebu nipe sweta yangu niwahi nyumbani kabla hajalivua lile sweta ndipo walisikia kicheko cha Mussa akicheka kwa dharau baada ya kumrusha Aryan.


Jesca aligairi kuvua sweta na kusema nani huyo anataka kunichungulia aone chuchu zangu (jesca anavopenda kujishaua) sasa ndipo walipogeuza macho ,juu walimwona Aryan akishuka toka gorofa ya juuu,Jesca alikuwa wakwanza kuogopa baada tu yakuona alisema mama yangu uwiii yule si Aryan ,alifumba macho na kulala chini huku kaziba masikio" mawazo yake yote aliyahamisha na kusema Aryan ndo unakufa bado sijaonja penzi lako", wakati anaendelea kuwaza pale Samaira alikimbia upesi na kuwahi mahali ambako Aryan atadondokea.


Huwezi amini Samairah alisimama na kukinga mikono yake ,pale pale Aryan alitua mikononi mwa Samairah kutokana na uzito alionao Aryan ,hata ingekuwa warushiwa kitu cha kilo tano toka gorofani ukikidaka lazima mkono ushuke chini

Lakini kwa Samairah lilikuwa jambo la kushangaza alimdaka Aryan wala mikono yake haikutetereka ,

Samaira akiwa kamdaka Aryan aliita" Aryan uko salama ",ndipo alipoyapeleka macho yake tumboni mwa Aryan aliona kisu kikiwa kimekitwa tumboni.


Samairah alimtizama Mussa juu gorofani wala hakumwona , Mussa alijua tayari ashagundulika alianza kushuka ngazi upesi

Hio sehemu ilikuwa mbaya kuna mawe makubwa ,Samairah alianza kupiga hatua akiwa kambeba Aryan, Jesca nae alifumbua macho yakiwa yametawaliwa na machozi na kujua tayari Aryan kama si kupasuka kichwa basi mwili wake ungevunjika nyang'a nyang'a, Jesca hakuamini macho yake baada ya kumwona Samairah akimlaza Aryan akiwa anahema kwa tabu,


Mwalimu Farida hakuwa mbali na eneo hilo nae aliweza kushuhudia lile tukio aliwahi mahali aliko Aryan, na kuuliza "Aryan nini kimekusibu" kabla hajajibiwa nae aliona kisu tumboni mwa Aryan,

Ile hali ilikuwa yatia huruma Aryan alishidwa kuongea na kusema jamani kuna watu wenye roho mbaya alipo ulizwa nani kamfanyia kitendo hicho Aryan hakusema hata kidogo aliishia kulia.


Jesca nae alikuwa akilia na kuwaza kimoyo moyo,itakuwa si vyema Aryan anapoteza maisha na sijaonja lips zake ,nipate walau busu la handsome maana nampenda hadi sijielewi Jesca aliupeleka mdomo wake na kugandisha na mdomo wa Aryan kisha akampiga busu zito,

Aryan anafumbua macho alishangaa kumwona Jesca akimbusu ,,Aryan aliyafumba macho yake tena, ,mwalimu Farida alimpigia dereva wake alikuja na gari upesi hawakupenda kupoteza muda maana walijua wakizubaa Aryan anapoteza maisha.


Gari lilikuja na Aryan alipakiwa ndipo mwalimu Farida,Jesca pamoja na Samairah walipanda na kuanza safari ya kuelekea massana hospital. Hatimae Aryan alipokelewa upesi na kupelekwa chumba cha watu mahututi, madaktari bingwa walishika zana zao na kuanza kuushughulikia mwili wa Aryan


'Tukirudi kwa mtaalamu wa roho mbaya naweza sema Mussa baada ya kushuka kwenye lile gorofa alikimbia alipo toka nje ya jengo la shule alimkuta Kudra akiwa kasimama mahali Aryan anapitaga wakati anarudi nyumbani ,Kudra nae alikuwa kajifunga kitambaa usoni ,huku mkononi kashika kisu kama kile ambacho Mussa alimkita nacho Aryan tumboni.


Mussa alikuwa anakimbia kujiokoa maana akigundulia lazima angefukuzwa shule kwa kitendo alicho kifanya ,

Mussa alikuwa anacheka na kujisemea lini mtu akichomwa kisu cha tumbo akapona ha ha ha Aryan fanya kuwasalimia kuzimu kuanzia sasa tuko huru .

Mara Mussa alisikia anaitwa alivyogeuka Kudra alishusha kitambaa alichofunga usoni na kuongea " oya mwanangu yule boya yuko wapi" ,Mussa alicheka na kuonekana mwenye furaha baada ya kumwona rafiki yake Kudra alisema huyo kuanzia sasa hivi hesabu marehemu kisha akamwelezea tukio zima jinsi alivyomfanyia ,Kudra alifurahi kisha wakasema sasa tuko huru ,tufanye jambo moja tukavue haya manguo ya shule halafu baadae tukawatafute akina Joyce,Nanaa na Lusi wanako ishii ili tukiwapata nawao tuwafanyie kitu kibaya ikiwezekana tuwachukue tuwapeleke bahari beach ili tukaogelee ,hapo ndipo tutapata bahati yakuwazamisha kwenye maji hadi kufa kwao.

Ni mawazo aliyoyatoa Kudra kisha wakaondoka na kuelekea majumbani kwao,

Tukirudi hospitali ya massana baada ya Aryan kufikishwa hapo,madaktari walishidwa kumtibu na kusema hili tatizo wao hawataweza labda apelekwe muhimbili na kwamba akicheleweshwa muda wowote anaweza akapoteza maisha ,mwalimu Farida wala hakupenda kuchelewesha walichukua ambulesi ya pale hospitali kisha safari ya kuelekea mhimbili ilianza hawakuchukua muda sana hatimae waliweza kufika na kupokelewa ,Aryan alianza kufanyiwa matibabu kwa umakini wa hali ya juu.


Wakati huo Samairah kabaki na mwalimu Faridi huku Jesca aliondoka na kurudi kwao,njia nzima aliwaza Aryan hawezi kupona ila hata akifa sawa nishaonja busu lake tamu ila ndio hivyo atapoteza maisha ,Jesca aliwaza na kuingia kitandani kwake kulala.


Siku zilizidi kuyoyoma huku Abbas akiendelea kumhudumia mdogo wake Gwae,,maana mikono yake miwili yote imevunjika ilikuwa ni kazi kubwa kumvulia nguo kumwogesha na kumlisha hio kazi aliifanya Abbas, huku mama yao akiendelea na tabia yake yakutoka nyumbani na kushinda baa asirudi nyumbani hadi siku tatu,


Ilikuwa siku ya juma pili ndipo Abbas alikaa na mama yake sebuleni ,alimuuliza mama lini utaacha pombe na tuishi maisha mazuri kama kipindi cha nyuma.


Lile swali alilouliza Abbas lilimkera mama yake kisha akainuka na kufunga kitenge vizuri kiunoni,we Abbas siku hizi wajifanya umekuwa ee na umefikia hadi umri wa kuniuliza maswali hayo ,we mtoto nimekuzaa mwenyewe sitaki unifuatilie, nitalala na mwanaume yeyote nitakae mpenda na hamna mtu yeyote wa kunikataza ,na ukiendelea kunifatilia mwanangu oohoo sikufichi nitakuua hata kama nimekuzaa ,tena nitakuua kifo kibaya tofauti na cha baba yako nilimuua kwa sumu,.mama aliongea na kuingia chumbani kwae ,yale maneno ya mama yake yalimuuma sana,nakujikuta akilia ,


Abbas akimwangalia mdogo wake ambae bado mdogo ndio wanaishi katika maisha ya shida namna ile alizidi kuumia ,kilichomchanganya zaidi rafiki yake Aryan ambae alikuwa mstari wa mbele nae hali yake si nzuri bado yuko hospitali,


Mama yake Aryan alikuwa anaenda kumtembelea mwane hospitali kila siku huku Samairah nae alijitahidi kuhudhuria walimpelekea chakula ,na mahitaji mbali mbali, kutokana na upasuaji aliofanyiwa alibahatika kuokolewa maisha yake na alitumia mwezi mzima hadi akapona ndipo wakaruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani,

Mwalimu Farida alitumia gari yake kumrudisha Aryan nyumbani pamoja na mama yake ,


Siku hiyo wakati Aryan wanarejea nyumbani toka hospitalini ," bibi aliwaza akiwa amebaki peke yake nyumbani,, mwanangu Ramso umenifanya hadi leo maisha yangu ya kutanga tanga namna hii umenitapeli nyumba yangu ukauza na kwenda kula raha .


Bibi alionekana siku hiyo amemkumbuka sana mwanae basi na alivyochoka kukaa nyumbani bibi alibidi atoke nyumbani na kutembea tembea kunyoosha miguu ,bibi alitoka zake na kutembea hadi barabara kuu ,bagamoyo road bibi alifika barabarani na kuona magari mengi yakipita ,bibi alijikuta anakumbuka maisha ya nyuma na kujisemea zamani nilikuwa naendesha gari langu binafsi leo hii nasimama barabarani naangalia magari ya watu ,mimi sina hata nyumba ya kukaa ndo natanga tanga hivi.

Bibi alijikuta anawaza wakati huo alikuwa anataka kuvuka bara bara upande wa pili,

Kelele za watu zilisikika zikisema "uwiii bibi anagogwa na gari sasa huyu bibi na uzee wake atavukaje barabara peke yake.?" Haikupita dakika moja baada ya bibi kufika kati kati ya barabara kuna gari ndogo aina ya V8 ili mgonga bibi na kumrushia mtaroni kisha gari hio ili hama bara bara na kujibamiza kwenye henga za bara barani.


Derava alijibamiza kwenye kioo cha mbele na kuning'inia huku uso wake hutamaniki na damu huku bibi amevunjwa kiuno na miguu yote,

Gari ambayo ilikuwa nyuma ya ile iliyomgonga bibi ,kumbe ndio gari ambayo Aryan alikuwemo.

Dereva alishika breki ,Aryan alifungua mlango na kushuka alivyomwangalia dereva wa ile gari ya mwanzo iliyopata ajali alimgundua kuwa ndio yule kijana siku ile alikuwa na mama yake Abbas na walikuwa wanaitana baby.


Mara bibi mtaroni alijaribu kutupa macho na kubaini nani kamgonga japo alikuwa kaumia mno damu zikimvuja kwa wingi alijikakamua na kutazama kwenye gari alimwona mwanae Ramso akiwa katokeza kichwa kwenye kioo ,bibi aliita "Ramsooo mwananguuu nini hiki umefanya" pale Aryan aligeuka na kutizama mtaroni akamwona bibi akiwa nyang'any'a hoi bini tahabani




Tulipo ishia jana baada ya ile ajali kutokea ,na aliyemgonga bibi ni mtoto wake kabisa wakumzaa ,na ndiye huyo huyo kijana alimpiga Abbas chupa ya kichwa huku akisema mama yake na Abbas ni mpenzi wake,

Bibi kwa kilio cha kwikwi alimwangalia mwanae ambae hajitambui kaning'inia kwenye dirisha aliita Ramso Ramso ,bibi alijaribu kuinuka na kujikuta akibaki pale pale ,bibi alikuwa kavunjwa miguu yote miwili kibaya zaidi kiuno nacho kilikuwa kimevunjika.


Aryan alipiga hatua za kwenda kumpa bibi msaada ile anapiga hatua kuelekea mtaroni Aryan alijikuta akisimama na kufumba macho ile gari iliyomgonga bibi ilikuwa imelala upande mmoja sasa tairi zilirudi nyuma na gari kwenda kitako na kwenda kutua mahali bibi alipo ,

Mpenzi msomaji na msikilizaji siwezi elezea kamwe mwonekano wa bibi jinsi ulivyokuwa ,bibi alikufa kifo kibaya,lile gari lilimkandamiza na kufanya bibi kichwa kipasuliwe na kifua kuwa kama chapati ,

Aryan alijikuta akilia kama mtoto , akiita bibi bibi

Mjukuu wako nimepona amka unione ,Aryan wakati akilia alikumbuka maneno ambayo bibie Samairah alishawahi kumwambia siku za nyuma


"Mogy usinione nipo kimya nakuonea huruma ipo siku utapoteza mtu ambae upo karibu nae sana" ,leo hii yametimia.

je Samairah aliyajuaje? Haya yote hayo yalikuwa mawazo ambayo yapo kichwani kwa Aryan.


Gari iliyopata ajali ilivutwa, watu walijaa na kusikitika jinsi vifo vya watu hao wawili vilivyotokea,tena mama na mwanae ,bibi alifanikiwa kutolewa na yule mwanae wote walikuwa wamepoteza maisha ,ni msiba uliomliza sana Aryan pamoja na mama yake maana ndiye alikuwa amejenga ukaribu nao mkubwa,Aryan alilia sana akiwa pamoja na bibie Samairah, msiba ulifanyika maeneo ya kunduchi hatimae waliwazika.Aryan alirudi nyumbani pamoja na Samairah akaenda kwao.


Tukija maeneo ya kawe beach tunawaona akina Mussa pamoja na Kudra wakiwa wanacheza mpira kwenye fukwe za bahari ,wakiwa sambamba na wadada watatu ambao muda wote walitembea pamoja si wengine ni Joyce,Nanaa na Lusi ,

Mussa alianza kuongea jamani sisi ni marafiki ambao tumejuana kwa muda mfupi,nimewaita tuje tufurahi wote hapa beach tucheze mpira tukichoka tunaingia baharini tuogelee

Nanaa alifurahi na kusema jamani mimi napenda kuogelea leo ndio mmenipatia ila na Aryan angekuwepo hapa beach pangenoga mno maana huyo mwanaume nampenda hadi sijielewi,ni maneno aliyoyaongea bibie Nanaa na kumfanya Joyce aachie mpira na kuanza kuwaza.


We Nanaa tena usithubutu kukaa karibu na Aryan maana nampenda hadi sijielewi ,yale yalikuwa mawazona aliyeyawaza ni bibie Joyce.


Kudra aliufuata mpira na kuuchukua huku nae akiwa na wazo lake rohoni ,nyie wazeni ujinga kwanza leo ndio mwisho wenu wa kuishi maana huyo Aryan hamtamuona tena ngoja muda wa kuingia kuogelea ufike ,wapuuzi nyie ,

Musaa alimsogelea Kudra na kumuuliza hivi Aryan yupo? Maana toka nilivyomchomaga kisu sijawahi kumwona yeye wala kale kademu Samairah , nahisi atakuwa amefariki maana kisu cha tumboni si cha kawaida.


Kudra alicheka na kusema aah kama ivyo poa wala usijali na hivi vijiwanawake vinajifanya vinampenda huyo boya leo tunawazamisha kwenye maji

Wakati akina Kudra wapo zao baharini wanaogelea ,

Tukija maeneo ya tegeta ,tunamwona mama yake Abbas akiwa anaingia nyumbani na kijana mdogo huku wameshikana viuno ,mara anamkiss ,

Walizama ndani ya nyumba ile wanafika sebuleni walijiachia kwenye sofa ,yule kijana alianza kumtomasa mama yake na Abbas huku akimpapasa mgongoni ,mara Abbas akaingia akiwa ameongozana na mdogo wake Gwae ,alichokiona Abbas alijikuta akidondosha machozi ,yaani mama yake mzazi alikuwa na kijana mdogo ambae huyo kijana anasoma darasa moja na wanajuana.


Abbas aliita Issa kwanini unanifanyia hivi? Isaa alicheka kwa dharau na kusema alafu wewe dogo jiangalie hebu ondokeni mie nifaidi vitu vya kikubwa, ki ukweli ilimuuma sana Abbas ,itawezekana vipi mama yake atembee na kijana mdogo tena anaumri sawa na wake,kibaya zaidi huyo Issa ndio kundi moja na akina Mussa wabaya wao wa maendeleo.


Abbas alijikuta analia na kutoka hapo nyumbani , aliondoka moja kwa moja hadi maeneo ya mbezi na kumkuta rafiki yake Aryan,alimwelezea kila kitu ambavyo mama yake anavifanya kwa sasa ,hata Aryan pia aliumia na kuwaza kwa kina.


Abbas sikia wewe ni muislamu yawezekana mama yako ana matatizo makubwa ama kuna jini mbaya ka mwingia ndio maana mama yako anafanya vitendo vibaya sasa sikia usijali wewe ni rafiki yangu nakuahidi tutasaidiana hatimae mama yako atakuwa sawa.


Inabidi tukamtafute ostadhi Othumani ili aje amsomee mama yako dua kama kuna mapepo ama majini yaweze kutoka ,Abbas alicheka na kusema sasa wewe umetoa wazo zuri tutaanzaje kumshawishi mama hadi akubali kukaa kitako na kusikiliza dua ya ostadh Othumani ,Aryan alimwangalia rafiki yake na kumwonea huruma ,kisha akamwambia usijali tutapata wazo lingine ila kwa sasa twende tukamwone huyo ostadh ,

Walitoka na kwenda kumtafuta ostadh ili waweze kumsaidia mama yake aondokane na huyo pepo mubaya,


Tukirudi maeneo ya baharini tunawaona akina Kudra na Mussa wakiwa wanacheza michezo mbali mbali kwenye fukwe za kawe ,wakiwa na lengo lao la kuwauwa akina Joyce Nanaa na Lusi wawazamishe kwenye maji hadi wapoteze maisha.


Hatimae Nanaa aliingia ndani ya bahari huku wakiogelea na aakina Mussa mara Joyce nae akajikuta ananogewa aliingia kwenye bahari na yeye kuendelea kuogelea ,Lusi nae hakupenda kupitwa aliingia kwenye maji huku wakiwa wanacheza michezo mbali mbali kama kukimbizana ,akina Joyce hawakuwa na mashaka hata kidogo na akina Mussa kama wanamawazo mabaya ya kuwaua.

Wao walicheza na kuonesha ukaribu kama marafiki wanao soma darasa moja, alianza Mussa akamshika mkono Joyce na kuanza kumvuta kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari, huku Kudra kawashika mikono Lusi na Nanaa ,na yeye alianza kuwavuta kuelekea kwenye kina kirefu, Mussa na Kudra walikonyezana kwa kubinyiana jicho.


Wakati huo kajua ndo kanaendea kuzama ufukwe ulikuwa kimya mno hapakuwa na watu ,Mussa alimgeukia Joyce na kumshika shingo kisha akamvuta na kumzamisha kwenye maji wakati huo Kudra nae kawazamisha akina Lusi na Nanaa.


Kudra alijisemea kimoyo moyo nyie wasalimieni kuzimu mnajifanya mnahamia shuleni kumbe nia yenu mapenzi yamewachanganya mnamtaka Aryan ,halafu mnakuja na kushika nafasi za juu kwenye masomo wapuuzi nyie.


Masikini wadada wawatu walianza kunywa maji taratibu huku wakijaribu kujiokoa lakini hawakufanikiwa , matumbo yalizidi kutanuka jinsi walivyokuwa wakinywa maji.


Hatimae waliishiwa nguvu za kujikomboa mikononi mwa wauwaji wale ,walianza kuona mwili ukikosa nguvu.


Gafla yalitokea mawimbi makubwa baharini yaliwazamisha hadi akina Mussa na Kudra nawao walifunikwa na mawimbi wakajikuta wanawaachia akina Joyce bahari ilianza kuwavuta na wao kuwapeleka kwenye kina kirefu zaidi kibaya zaidi Mussa pamoja na Kudra walikuwa si wazoefu wa kuogelea wakajikuta na wao wakianza kuyanywa maji ya bahari taratibu jinsi yalivyo na chumvi nyingi sasa mmh.

Bahari ilizidi kuwavuta na kuwapeleka zaidi kwenye kina kirefu wakati huo Joyce ,Nanaa na Lusi ndio walikuwa wamezama kabisa hata hawaonekani sijui ndo washakufa ama laaa.


Lakini pembeni mwa bahari kulikuwa na binti mrembo kasimama huku akishuhudia jinsi akina K.udra wakitapatapa



Tulipo ishia jana baaada ya mawimbi makubwa kutokea baharini na kuwazamisha akina Kudra kisha bahari ikaanza kuwavuta taratibu kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari wakati huo akina Joyce na wenzake ndio kabisa walikuwa hawaonekani.

Kudra alianza kutapa tapa na kujikuta akizidi kuzama ,ndipo likatokea wimbi kubwa na kuwasomba akina Mussa pamoja na akina Joyce walirushiwa pembezoni kabisa mwa bahari ambapo palikuwa na maji kidogo .


Mussa na Kudra wakiwa na matumbo makubwa baada ya kunywa maji mengi walipozamishwa na mawimbi ,walikuwa hawajitambui lakini mahali walikotupwa na maji kulikuwa na mrembo kasimama huku nywele zake ndefu hadi mgongoni akiwa amezitindua ,alikuwa kavalia gauni jekundu na refu ,alikuwa ni bibie Samairah aliwaza mambo mengi moyoni mwake " hivi ninyi akina Mussa ni nini hasa mnataka ,kwanini mnataka kuwaua wenzenu tena pasina hatia ,Samairah alitikisa kichwa kisha akamfuata Joyce ambae alionekana kupoteza fahamu kabisa alimgusa maeneo ya puani na kugundua kuwa bado anapumua ,aliinama na kumpuliza mdomoni huku kaziba pua za Joyce ,pale pale Joyce alikohoa na kuanza kutapika maji ,huku akipiga piga kifua chake ,hatimae Samairah alimfanyia Nanaa na Lusi kisha waliweza kuzinduka.


Joyce na wenzake walishangaa kumwona Samairah maeneo haya ,Joyce aliuliza huku akifuatiwa na kikohozi " Samairah umekuja peke yako ama upo na Aryan" lile swali lilimfanya Samairah atabasamu kisha akawashika mikono wote watatu na kuwaambia naombeni mnifuate maana sasa hivi naona mshapata ahueni.


Samairah aliwatupia jicho Mussa na Kudra kisha akatikisa kichwa na kuwaambia akina Joyce twendeni tuondoke na hawa wapuuzi waacheni hivi hivi ,

Akina Joyce walianza kumfuata Samairah,ndipo Nanaa aliuliza ,Samairah kwani nawe ulikuwa hapa baharini? Maana kwa kumbukumbu zangu mara ya mwisho niliona Kudra amenikaba shingo kwa nguvu na kunizamisha kwenye maji, ndipo nilianza kunywa maji na hatimae sikujua nini kiliendele,


Samairah aliwaangalia na kuwaambia ,kuanzia leo iwe mwanzo na mwisho wa kutembea na akina Kudra si watu wema hata kidogo maana hawa akina Kudra walinifuatilia mimi na kunishawishi kuja beach nao niliwagomea,

Nilivyogoma Mussa alimnong'oneza Kudra na kumwambia huyu Samairah tumwache kwanza tuanze na akina Joy tukahakikishe wanafia baharini ,

Maneno ya Samairah yaliwafanya akina Joyce wapate picha kamili jinsi walivyozamishwa kwenye maji ,akina Joy walimkumbatia Samairah na kumshukuru kisha wakamuahidi kuanzia leo sisi tutakuwa marafiki zako ila mwanzoni tulikuwa tunakuchukia kwa sababu upo karibu na Aryan

Samairah aliwaambia sawa ila kuweni makini,walifika maeneo ya kawe na hatimae kila mmoja alichukua usafiri na kwenda makwao .

Mida ya saa mbili usiku ndipo akina Mussa walipiga chafya na kuzinduka ,kila mmoja alivyoangalia tumbo lake ,walishangaa kuwa na matumbo yamejaa maji ,

Kudra alikuwa wakwanza kurudisha kumbukumbu alimwambia ,oya Mussa mpaka sasa tuko fresh Aryan tushamuua na akina Joyce naimani washafia ndani ya maji ,Mussa alidakia na kusema kesho zamu ya kumtafuta Samaira nae tutapanga mbinu ya kumnasa

Walijipongeza na kuondoka baharini baada ya kuzunguka ,lakini Kudra alikumbuka kitu,

Oya Mussa hivi wakati tumewazamisha akina Joyce baada ya wimbi kubwa kutokea ,tulizamishwa na maji chini lakini tulivyoibuka niliona kama mwanamke kasimama pembezoni mwa bahari na akiwa kanyoosha mkono mahali tulipo

,Mussa alicheka na kumwambia wewe acha zako labda ulikuwa ndotoni twenzetu tukachukue bajaji tuondoke

Waliondoka zao .


Tukirudi maeneo ya tegeta tunawona Aryan na Abbas wakigonga geti kwenye nyumba flani hatimae walifunguliwa ,walimsalimia yule mkaka aliyewafungulia geti kisha Aryan akauliza braza ivi tumemkuta ostadh Othumani ? Yule kijana aliitikia yupo tena kakalia kibarazani anasoma Qur'an ,Aryan alisema ooh afadhali waliingia na kumsalimu ostadh

"Assalaam alaykum ,"(ikiwa na maana amani iwe juu yako) Aryan alisalimu kisha Othumani aliitikia ,"waalaykum salaam Warahmatullah Wabarakatuh"(amani , rehma na baraka ziwe nanyi pia) karibuni mashekhe. walikaribishwa kwenye jamvi kisha akina Abbas walikaa na kukunja miguu "hiyo style ya kukunja miguu huitwa tahiyatu,"

Othumani aliwaangalia akina Aryan kwa makini na kugundua huenda wanamatatizo labda wamegombana maana Abbas alikuwa kakunja sura mno ,yote akifikiria mambo anayofanya mama yake.


"Ehe karibuni shekhe "Othumani aliwaambia ndipo Aryan akakohoa kidogo kuweka sauti yake vizuri na kuanza kuongea, ostadh tumekuja kukuona wewe tunashida tena si shida imekuwa tatizo na kumsababishia rafiki yangu kuwa na mawazo ,ehee shida ipi hio Othumani aliuliza huku akizinyoosha ndevu zake.


" ostadh mama yake na Abbas nadhani hata habari zake hapa mtaani umezipata siku hizi anafanya vitu vya ajabu anatembea na waume za watu ,na watoto wadogo kiukweli ostadh inatia aibu haswaa, tulikuwa tunaomba ukatusaidie walau kumsomea dua ,maana kadri siku zinavyozidi kusonga ndipo anazidi kubadilika tunakuomba sana.


Ostadh wala hakuwa na maneno mengi aliuliza kwani sasa hivi yuko wapi"? Abbas aliinua kichwa na kumjibu kuwa yupo nyumbani , ostadh aliinuka na kuvaa kubaz zake kisha wakaanza safari ya kuelekea kwa akina Abbas

,wakiwa njiani kuna gari aina ya kirikuu lilipita huku likitangaza kuwa kuna kongamano kubwa litakalofanyika kwenye viwanja vya tegeta nyuki atakuwepo mchungaji Petro atawaombea wakazi wote wa tegeta pamoja na viunga vyake ,wenye mapepo ,majini ,wagumba mikosi na nuski zote wataombewa na kupokea neno la mungu.


Ni maneno waliyoyasiki kwenye gari likitangaza na kutaja siku ya juma pili,Abbas aliwaza ostadh akishidwa kumponyesha mama na dua zake itabidi nitumie mbinu nimpeleke mama kwa huyo mchungaji Petro huenda angeweza kuyatoa hayo majini.


Haikua mbali walifika nyumbani walimkuta mama yake na Abbas yuko na mwanaume mwingine tofauti na Issa ,tena walikuwa wamekaa sebuleni wakipapasana ,Abbas kitendo cha kuingia ndani na kuwakuta mama yake akiwa katika pozi la kimapenzi aliumia sana na kutoka nje ya nyumba ,maana kulikuwa na mwarobaini mkubwa Abbas alienda zake kukaa nje ili kutoa aibu, ile anafika kwenye mwarobaini alisikia sauti ya mdogo wake Gwae akilia.


Abbas aliinua kichwa juu alihisi kuchanganyikiwa baada ya kumkuta mdogo wake kafugwa miguu juu kichwa chini kaning'inizwa kama mtu anae uza mkungu wa ndizi,Gwae alilia lakini hakupata msaada wakati huo mama yake ndio akibadilisha wanaume ,

Hakika kile kitendo kilikuwa kinauma mno ,Abbas ilibidi achukue ngazi na kumfungulia kamba mdogo wake kisha akamuuliza , Gwae nani kakufunga juu ya mti " mama kasema nifugwe na yule mbaba aliyekuja nae ndio kanifunga.

Abbas alimwangalia mdogo wake ambae mikono yote imevunjika halafu bado anateswa aah Abbas alizidi kuwaza mama katoa wapi hiyo roho ya kinyama,


Ostadh alikaribishwa ndani na Aryan kisha akamwambia ostadh aanze na kisomo , kitendo cha mama yake na Abbas kumwona ostadh alitabasamu na kumwambia subiri ni malize na huyu kisha zamu yako itafuata ,Othumani alimsogelea mama yake na Abbas na kumwambia ,mama nimekuja hapa kwa lengo moja la kukutoa katika mateso ya jini mbaya jini mahaba tuweze kukusomea dua hilo pepo litoke na urudi katika hali yako.


Maneno ya ostadh ndio kama yalimvuruga mama Abbas aliinama chini ya kochi na kutoa chupa ya bia alinyanyua ili ampige ostadh lakini Aryan aliwahi akaudaka mkono wa mama yake na Abbas yule mwanaume ambae alikuwa yupo na mama Abbas


Alinyanyua shati lake upande wa ubavu wa kulia kisha akatoa bastola na kumnyoshea ostadh,we ndo unajifanya unasomea watu dua ili kuwatoa majini ee ,sasa sikia huyu ni mpenzi wangu ,nakupa dakika mbili uwe ushapotea la sivyo nitasambaratisha kichwa.


Ostadh hakuwa na neno hata moja aliinuka kisha akatoka nje taratibu na kuvaa kubaz zake huyo kuelekea kwake ,sasa walibaki Abbas ,Aryan na Gwae ,pamoja na mama yao.

Yule mwanaume ambae alikuwa kajazia kwa mazoezi aliwaambia akina Abbas watoke nje kisha wao wafanye mambo yao wakimaliza watawaita waiingie ndani.


Abbas na mdogo wake walitoka na kukaa nje ,lakini chumbani kwa mama Abbas alianza kuzungumza na yule mwanaume,

JOSHUA ,sikia huyu mwanangu siku hizi kajiona kakua sitaki kumuua kwa kumpa sumu kwakuwa hizi kazi wewe unaiweza naomba uwanyonge pamoja na Gwae wafe tu maana naona kama wananikera kera tu hapa nyumbani nataka nibaki peke yangu nikitaka kufanya jambo lolote na fanya ,


Kwanza najuta kwanini nilizaa hizi taka taka , ,Joshua kwa sauti yake nzito alisema sawa hio kazi mbona dakika siruri tu ngoja niwafuate hata nje niwatwage risasi halafu nikimbie.


Wakati mama Abbas anapanga na Joshua Aryan alikuwa kasimama karibu na dirisha alisikia kila kitu ambacho mama yao anataka kuwaua ,Aryan kwa mwendo wa haraka aliwaendea akina Abbas na kuwaambia


"Abbas nakuomba hapa hatuna muda wa kukaa mama yako si mama tena nimemsikia kwa masikio yangu akimwambia yule mwanaume aje awaue naomba tukimbie ,Abbas nae alishaanza kuwa na hofu na mama yake alivyoambiwa hivyo alikimbia pamoja na Gwae .


Gwae kwakuwa amevunjika mikono yake miwili na alikuwa bado hajapona vizuri alikimbia kidogo alibanwa na vichomi na kushidwa kukimbia kabisa na kujikuta anasimama na kuinama huku akiugulia maumivu wakati huo Aryan ashakimbia na kuondoka zake ,

Abbas alivyoona mdogo wake kashidwa kukimbia alimrudia ili amshike mkono amsaidie kukimbia .


Ile anageuka tu alishangaa anadakwa mkono na Joshua ,"Joshua alikuwa kashika upanga huku akihema juu juu " , Joshua aliongea kwa ubabe " we dogo unaweza kushindana na mimi ? Sasa unaona hili panga nakufyeka",wakati huo Gwae kadondoka chini kwenye kauchochoro flani cha pale mtaani kwao ilimbidi kutembea na magoti ili ajibane vizur kwenye gogo la mti ili Joshua asiweze kumuona na anusuru maisha yake "wakati huo

Ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku palikuwa na giza giza huku taa za nyumba za majirani zilikuwa zimeangaza ,

Gwae akianza kujiburuza ili ajifiche kwenye sehemu ambayo hataweza kuonwa ,wakati anasogeza goti la mguu wa kushoto huku akigeuka kumwangalia Joshua kumbe maeneo hayo kulikuwa na nyoka,Gwae akajikuta anamgusa mkia wa nyoka tena alimkandamiza na goti ,kawaida ukimgusa nyoka kwenye mkia huwa anakuwa mwepesi kurusha kichwa ili kubaini mbaya wake ama kuuma chochote kile

Sasa , masikini Gwae aliudondokea ule mkono ambao ulikuwa umevunjika na bado hujapona kisha akalala chali.

Yule nyoka alirusha kichwa na kutua shingoni mwa Gwae ,huku Gwae anajitahidi kutokutoa sauti ili Joshua asimkamate .....



TULIPO ISHIA JANA bĂ ada ya Abbas kukamatwa na Joshua na Fwae kudondoka chini ,kisha nyoka alitua kichwa chake shingoni mwa Gwae.., na Gwae alijikuta akinyanyua mikono yake iliyofugwa mhogo ama gamba gumu (p.o.p) yule nyoka aliliuma hilo ganga kisha akaruka na kuondoka zake ,.Gwae alijikuta kama kagandishwa na theluji,

Wakati huo Abbas kashikiliwa shati na Joshua "we mtoto inaonekana unamfuatilia mama yako sana na ndio kanipa pesa nikuue ,ila najua hii ni dunia" ,Joshua aligeuka nyuma na kumwona mama yake na Abbas akija kushuhudia jinsi mwanae anavyouliwa ,kumbe Joshua hakupenda kitendo cha mama yake na Abbas kutaka kuwaua wanae.


"Joshua alimnong'oneza Abbas ,sitakuua ila nikinyanyua upanga kisha nitakupiga na ubapa halafu udondoke chini kisha mimi nitakubeba na kwenda kukutupa ,Abbas baada ya kuambiwa vile alianza kutetemeka maana Joshua mwenyewe anatisha kwanza uso wake unangeu za kila aina huku mikono yake ikiwa imekomaa mno.


Mama yake na abbas aliita Joshua fanya kama nilivyokuambia hatuna muda wa kupoteza ,Joshua alinyanyua upanga kisha aliugeuza ubapa kisha alimpiga Abbas maeneo ya begani kisha akamshika maeneo ya shingo na kubonyeza mshipa wa fahamu,pale pale Abbas alidondoka chini na kupoteza fahamu

Joshua alitoa kichupa kidogo ambacho kilikuwa na damu ,ila haikuwa damu ya binadamu bali ilikuwa damu ya mnyama

Alimpaka Abbas maeneo ya shingoni na kumwagia damu kwenye shati kisha ,akawekea na upanga wake damu.


Kisha alianza kumfuata mama yake na Abbas alimwonesha upanga,mama Abbas alivyoona damu akajua kazi tayari imeisha ,alifurahi na kusema mwanangu nenda salama huko uendako afadhali mimi nimepata uhuru sasa


Haya Joshua shika kiroba hichi kamfungie humu kisha ukamtupe huko hata baharin samaki wale ama ile mindege ya baharini ,kisha mama Abbas akarudi na kuondoka zake,

Joshua alianza kuwaza " ukweli dunia imeisha japo mimi naishi mjini kwa kazi hizi za kutumwa kuua watu ,kukaba na kuwafanyia watu vitendo vya kinyama ila leo siwezi wafanyia hawa watoto yawezekana huyu mama kuna mtu kamloga ama amekubwa na jini mahaba ,sasa kwanini anataka kuwaua watoto wake ,daah.


Joshua alijiwazia na kuingiza upanga wake ndani ya suruali kisha alimchukua Abbas na kumfunga kwenye roba ,mama Abbas aliagiza gari ikaja na Abbas akapakiwa kwenye buti kisha safari ya kuelekea kutupwa baharini kuanza.


Wakati huo Aryan alirudi na kumkuta Gwae kalala chini alimshika mkono na kumwambia tukimbie ,lakini Aryan alivyopiga jicho aliona Abbas akipakiwa nae bila kuchelewa alikodi piki piki na kuanza kulifuatilia hilo gari ,Aryan alitaka ajue ni wapi rafiki yake anaenda kutupwa ,wakati huo Aryan alikuwa akidondosha machozi na kujua kuwa rafiki yake tayari ashauliwa.


Na Gwae baada ya kuachwa na tayari ilikuwa ni usiku aliogopa kwenda nyumbani maana alijua huenda akauliwa alibaki amekaa nje huku baridi kali likimpiga ,

Gwae aliwaza aende kwa rafiki yake Rashidi lakini alivyokumbuka jinsi mama Ashura alivyo mvunjaga mkono basi aliamua akae nje tu usiku kucha ,

Kibaya zaidi mikono yake yote imevunjika na bado haijaanza kuimarika ,

Tukija maeneo ya mbezi ya afrikana lile gari lililompakia Abbas lilikata kona na kuingia kwenye barabara ya vumbi kisha walifika mahali kulikuwa na miti mikubwa halafu katikati ya hiyo miti palikuwa na nyumba ,haikuwa hata na geti ,Abbas alishushwa na kutolewa lile roba alilofugwa nalo ,kisha dereva aliwasha gari na kuondoka wakati huo Aryan nae alikuwa maeneo hayo alitaka apate uthibitisho ili hata akienda polisi aweze kuwapa maelezo kamili,

,

Joshua alimshitua Abbad maeneo ya shingoni na ndipo pale alizinduka na kujikuta yupo katika mazingira mapya kabisa ,Abbad akiwa haelewi aliuliza "wewe ni nani na hapa niko wapi " Joshua alimwangalia Abbas kisha akafungua mlango na kuingia ndani

Kisha akamwita Abbas nae aingie ndani ,

Abbas alikubali na kuingia ndani kisha alipewa kiti kidogo na kukaa.


Joshua alitoa upanga wake na kuutupia chumbani mwake kisha akavua shati na kuwasha mshumaa ,Abbas alijikuta akitoa macho makubwa baada ya kuona kovu kubwa mgongoni mwa Joshua ,na Abbas kuwaza huyu atakuwa jambazi nini

Wakati Abbas yupo ndani Aryan nae alikuwa kwa nje ya hiyo nyumba alivyochungulia kwenye upenyo mdogo wa dirisha alishangaa kuona Abbas yupo salama ,Aryan alijikuta akishusha pumzi na kusema inamana pale yule mtu alivyoinua panga alimkata au alifanyaje ,Aryan aliwaza kwa haraka na kusema yawezekana huyu mtu alimchukua Abbas si mtu mbaya wacha nigonge mlango nipate kujua

Wakati huo Abbas kakaa huku wameangaliana na Joshua kwa nje walisikia mlango ukigongwa ,Joshua aliinuka na kuufungua mlango,na kumkuta Aryan kasimama nje ,kabla Joshua hajaongea chochote Aryan aliwahi kujitambulisha na kusema

Mimi ni ndugu yake na Abbas huku akilia ,Joshua hakuwa na kipingamizi alimwambia aingie kisha awasimulie kwa nini ameamua kufanya hivyo.


Aryan nae alikaa chini kisha Joshua alianza kueleza ," mimi kwa jina nafahamika kama buda ,hili jina nililipewa na watu hasa kwa kazi zangu za kuua watu ,nimepewa kazi na mama yake Abbas kanipa laki tano hiii hapa ,Joshua alizimwaga pesa chini kisha akaendelea kuongea ,katika maisha yetu ama familia yetu ,baba yetu ni tajiri mkubwa sana tu hapa mjini anaitwa Kizza ,

Akina Abbas na Aryan walivyosikia Joshua kasema yeye ni mtoto wa Kizza walishituka maana na wao wana mwanafunzi mwenzao wanaosoma nae anaitwa Kudra Kizza ,ambae muda wote huwa anajitapa kuwa ni mtoto wa kitajiri.


Joshua aliendelea kusimulia, mimi wa wapili kuzaliwa ,wakwanza ni kaka yangu alikuwa mkandarasi ila kwa sasa kawa kilema tena kilema cha kudumu hata baba yangu hamtaki kumwona machoni mwake ,"Joshua baada ya kutaja kaka yake mkandarasi " Aryan alikumbuka yule mkandarasi aliyedondokewa na gorofa,na kujua huenda ndio kaka yake na Joshua ,

Joshua aliendelea kueleza mdogo wetu wa mwisho anaitwa Kudra ila kanasoma sasa ivi,baada ya Joshua kutaja ivo Aryan alijua fika hapa muda wowote anaweza kuuliwa maana anajua fika Kudra huwa anamchukia ,

Joshua aliendelea, katika familia yetu tushapewaga laana kubwa sana watoto wote wa Kizza watakuwa na roho mbaya kupita maelezo ,ndio maana mimi nilijikuta naingia kwenye kazi ya kuua binadamu ,natumwa na watu kamuue fulani ,nami naenda naua.


Ila kwa huyu kijana sijui shetani gani kanipitia roho yangu imekataa kata kata kukuua hivyo tambua mama yako si mtu mwema chukua hizi pesa alizonipa nikuue ,kapange chumba uanzishe maisha yako , na uhakikishe mdogo wako unamtumza mama yako si mtu mwema kuanzia hivi sasa.


Joshua alimpa Abbas pesa zote alizopewa na mama yake ili amuue ,lakini akina Aryan walivyokuwa ndani kwa Joshua walikuwa wakisikia kaharufu kama cha mzoga ama kitu kilichojifia na kuanza kutoa harufu,

Joshua aliwaangalia na kuwaambia hii nyumba yangu nakaaga mwenyewe hapa na nimeiwekea zindiko hamna mtu yeyote anaeweza kuiona lakini nimeshangaa wewe kijana umeionaje?

Joshua alimuuliza Aryan "Aryan alifikiria na kusema mbona inaonekanika tu ,Joshua aliguna na kusema we dogo usinidanganye hii nyumba hamna mtu yeyote anae weza kuiona labda jini na wachawi Lakini binadamu wakawaida hawezi kuona ila dogo sitaki kukuhoji sana ipo siku tutakutana naomba muondoke".


Abbas alitangulia kusimama kisha akatoka lakini Aryan alivyosimama alitupa macho kwenye chumba kimoja ambacho mlango wake ulikuwa wazi alishangaa kuona mwili wa mtu ukiwa umevimba tumbo halafu kinywa kipo wazi


Aryan alijua fika kuwa Joshua akiua watu anakuja kuwaweka katika hii nyumba maana kasema hamna mtu anaeweza kuiona,Aryan nae alitoka walitembea haraka haraka na kutoka eneo ambalo Joshua anakaa.


Abbas hebu simama vua hilo shati vaa sweta langu ,Aryan alimwambia Abbas nae alifanya hivyo maana shati lake lilikuwa limepakwa damu kisha walianza safari ya kurudi tegeta kwa ajili ya kumtafuta Gwae tayari ilikuwa ishatimia saa saba usiku

Waliweza kufika maeneo ya tegeta walipitia mahali ambako palikuwa nyumba ya akina Aryan walikuwa wakinyata kwa umakini.


Maana Aryan wakati anamfuatilia Abbas alimwambia Gwae asiende kulala kwenye nyumba ya mtu yeyote akiona wanachelewa aende akalale kwenye hilo gofu la akina Aryan


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG