Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

SEKESEKE (ROHO MKONONI) - 5

   

Simulizi : Sekeseke (Roho Mkononi) 

Sehemu Ya Tano (5)


"Wote kimyaaa..."


Ghafla sauti kali tena ya amri ikasikika kutoka nje ya selo ile kubwa ya wa babe triple c,wengi waliijua sauti ile aikuwa ya mwingine zaidi ya ya mkuu wa gereza lile Gerald Dunga.


"Umefanya kosa sana kumpiga nyapara wako ni kama umenipiga mimi,sasa hukumu yako ni hapa hapa iwe fundisho kwa wengine"


Dunga aliongea kwa ukali akachomoa bastola yake ndogo na kumuelekezea Butu,akipanga amtandike na kumuulia palepale kama alivyoambiwa na mkurugenzi wa usalama wa taifa mr Zidu kite.akaikoki bastola tayari kuiruhusu kuchomoka,Butu alibaki katika bumbuwazi kutokuamini kile kinachotokea,kupata adhabu ya kifo kisa kosa la kupigana?!,hakika jambo hili lilimshangaza sana...


Sasa kidole cha pili baada ya dole gumba cha Dunga,kikawa kinaenda kushika kinasulio,kuruhusu risasi kuchomoka.


Majanga!.



Sekeseke la hatari bado lina ya andama Maisha ya alokuwa Inspekta wa jeshi la polisi John Butu, baada ya kusalimika ndani ya lango la jehannamu anapelekwa katika selo ijulikanayo kwa jina la trple c,huko anakutana na nyapala Manzua,nyapala alopewa kazi ya kumtesa Butu ikiwezekana kumuua kabisa,kazi inakuwa ngumu kwa Manzu hatimaye anapigwa yeye,kitendo cha kupigwa kinawafurahisha wafungwa na hata maaskari pia kwani wengi walimchukia Nyapara yule,je nini kitaendelea?!,tusonge katika hatua inayofuata...


HATUA YA ISHIRINI NA NNE


Kabla Mkuu wa Magereza Dunga ajaruhusu risasi kutoka katika bastola yake,ghafla ikasikika sauti nyuma.


"Hapana mkuu usifanye ivyo!.."


Ikabidi mkuu yule wa gereza ageuke nyuma,macho yake yakatua kwa kijana mdogo alokuwa ndani ya sare nadhifu za jeshi la magereza,mabegani kwake akiwa na nyota mbili akipishana naye kwa nyota moja tu yeye alikuwa na cheo cha kapteni akimiliki nyota tatu.


Usoni mwa kijana yule alipambwa na tabasamu jepesi,akamfikia Kapteni Dunga bado tabasamu likipamba mdomo wake.


"Unataka kuniambia nini Luteni?!"


Dunga akaongea kishari mkono wake wenye silaha ukiwa una angalia chini,kijana yule alojulikana kwa jina la Luteni Johnson Mamba ndo alikuwa msaidizi wake,alimfikia akamshika mkono na kumkokota mpaka nje.


"Mkuu punguza hasira kumbuka huyo ni mwanausalama tena inspekta wa polisi je unadhani ukimtandika risasi jeshi lita acha kufatilia na mashahidi niwafungwa utakaa pabaya mkuu"


Wakati wakielekea ofisini Johnson akatumia wasaha huo kumshauri mkuu wake,hata Dunga alipofikiria ni kweli,jeshi la polisi lazima lingechunguza kijana wake kafa katika mazingira gani!,na ingejulikana kuwa yeye ndo kamtandika risasi tena hadharani angejiweka pabaya!.


"Lakini ilikuwa ni oda ya usalama wa taifa!,"


Dunga akaongea kwa sauti ndogo,sauti ilojaa wasiwasi tele!,


"Hata kama mkuu ni oda ya usalama wa taifa ndo si umuue hadharani,lazima upange mpango kabambe ikiwemo kuamishwa gereza then njiani gari ivamiwe auwawe,au njia nyingine yeyote ambacho kifo chake akitokuwa cha utata!"


Wazo lile dunga moja kwa moja akakubaliana nalo,alipofika ofisini kwake akaongea na Zidu juu ya mpango aloupanga kwamba ata andika barua kwa general kuomba kuamisha wafungwa kadhaa sababu ikiwa wingi wa watu,siku ambayo hata amisha wafungwa atamjulisha aandae vijana wake wavamie msafara na wajifanye kumtorosha Butu hapo askari wake wamuue kwa kumtandika risasi,hii isingeleta shida wala upelelezi ndani ya jeshi la polisi.

Pasina kupoteza muda Kapteni Dunga akaandika barua kwa General,ambapo baada ya kuituma siku ilofatia,kesho yake akapokea majibu kwamba Gereza la keko lishajulishwa hivyo aandaye hao wafungwa katika karandinga wasafirishe...


***


Kwa upande wa Butu maswali mengi bado yaliushambulia ubongo wake hasa tukio la mkuu wa magereza kumnyooshea silaha.


'ina maana kama si kutokea Jonson,Dunga angemtandika risasi na kumuulia mbali?!,kisa tu kampiga nyapara?!'


Jambo hilo alilifikiria sana alikumwingia akilini!,alijua lazima kuna kitu kinachoendelea dhidi yake!,akakumbuka yani yeye kuja tu,pasina kosa lolote akaswekwa lango la jehannamu tena ndani ya masaa 24 sawa na siku mbili za kifungwa,lango la jehannamu mahali wawekwao magaidi,majambazi sugu makatili,na viumbe visivyo stahili kuishi!,iweje awekwe yeye?!,yeye aloitumikia serikali tena idara ya polisi ulinzi na usalama wa raia na mali zake leo wamlipe vile?!,yeye ilipaswa awekwe triple A,iweje awekwe triple c?!,kwa uzoefu wake wa kipolisi akamtilia shaka mkuu wa magereza,akajua lazima anatumika,na maisha yake si salama,akajua ilipaswa afanye kitu haraka,kukaa pale ni sawa na kukisubiria kifo,na kingemkuta!.


Sasa angetokaje hali ya kuwa hata kazi nje akuruhusiwa kwenda kufanya pengine angefikiria kutorokea huko.


Japo kwa sasa Gereza lilimuheshimu hakukuwa na alothubutu kumtishia si nyapara,wala magwa,katu akujua hatari aloandaliwa...


Siku ilofatia asbuh alishangaa akiitwa akaelekea mpaka kwa mkuu wa magereza ndani alikuta pia wafungwa wa kutosha,huko ndipo walipoambiwa wa na amishwa gereza,hivyo wakatolewa chini ya ulinzi mkali,wakapakiwa katika karandinga lililozungushiwa nondo ndogondogo kwenye bodi,safari ikafatia wakisindikizwa na gari mbili za polisi


Tayari Zidu alisha waandaa vijana wake wa kutosha eneo la tukio tayari kwa uvamizi pale gari la magereza litakapowafikia.


Butu akujua hili wala lile,safari ikaendelea!....




Gari ilobeba wafungwa ilizidi kukata mbuga huku mbele yake pakiwa na kitara cha polisi na nyuma ikiwepo cruzar ya polisi ikiwa na maaskari takribani wa tano wenye mitutu waloivaa vifuani mwao,kitara cha polisi kilikuwa na askari wa tatu tu pale mbele,safari iliendelea na sasa walikuwa wakiikaribia keko,ila wakiwa katika eneo moja nyuma kidogo ya daraja Swami kitara cha polisi kilisimama,mbele yake paliwekwa mawe makubwa,dizaini kama kuzuia njia,


Askar wale wawili wakashuka kwa lengo la kwenda kutoa yale mawe yaliyopangwa chiani!.


Kosa!.


Ng'afla milio ya risasi ikasikika punde watu wasopungua kumi waloficha nyuso zao wakatokea toka chini ya daraja na kuanza kuwashambulia wale maaskari,wale walokuwa nyuma kuona hivyo nao wakashuka na kuwatupia risasi wavamizi,ila askari walizidiwa na mwisho kusamli amri,wavamizi wale wakaomba wapewe Butu gari ikafunguliwa Butu akatolewa,kisha maaskari wakaruhusiwa kuendelea na safari.


Kitendo kile kiliwashangaza sana wale wafungwa,askari kusamli amri,kukubali kuachia mfungwa pasina kupata jeraha hata moja,kila mmoja alisema lake,ila safari iliendelea.


Hawakuwa na uhuru ni wapi wangepeleka wasiwasi wao?!.


Kwa upande wa Butu machale mapema yalishamcheza hasa baada ya kuona urushianaji wa risasi kati ya pande mbili zile,ulikuwa ni wa uangalifu kuto mlenga mwenzake,kichwani mwake akajenga picha kuna kitu kinachoendelea pale,alikamilisha wazo lake baada ya kuona maaskari eti wanasamli amri na mwisho kukubali kumtoa nao kuendelea na safari yao.


Kipo wapi kiapo walichokula?, kupambana kufa kupona kulinda raia na mali yake,kivipi wakubali kumtoa kwa watu wasojulikana?!,alijiuliza pia je wale ni watu wa aina gani waloamua kumsaidia?!,alijua kwa kipindi kile hapakuwa na msaada wowote kwake asitegemee.


Watu wale walimswaga mpaka mahali walipoifadhi magari yao,walikuwa na magari matano,wakamwingiza katika gari moja wapo wengine wakaingia katika magari yao,yeye bado alibaki na butwaa akitafakari wale ni watu gani na li lipi lengo la wao kumchukua?!...


"Unapaswa ufungwe macho upaswi kujua ni wapi unapelekwa,kingine kaa utulie atutakufunga miguu wala mikono ila tuki gundua unataka ulete janja ujanja fulani hatutosita kukumaliza hata kabla ya muda tulokupangia kukuua nadhani tume elewana?!".


Mtu mmoja alimuongelesha Butu hata hivo kijana yule akujibu kitu,mtu yule akampa ishara mwenzake amfunge macho Butu kusudi asijue anapopelekwa,naye akatii hilo safari ikaendelea.


Redio ikawashwa njia nzima watu wale wakawa wakizungumzia maswala ya wasanii,Butu hakazidi kushangaa kwani alijua labda hata angepata chochote katika maongezi yao,alikaa kwenye gari mpaka akachoka,akujua ni wapi anapelekwa njiani ni kama alitembea masaa matatu hatimaye gari ilisimama.


Akajua sasa kashafika,akashushwa akakokotwa pasina kujua ni wapi anapelekwa ila aliweza kung'amua kuwa yupo msituni kwani alizisikia sauti za wanyama,na hata ndege pia aliundua kuna muda alikanyaga majani kuna muda alipishana na miti mwisho akasikia mmoja akisema...


"Dula hapa panatosha!"


Palepale akabwagwa chini akafunguliwa kitambaa sasa alipata kuona vizuri mazingira ya pale alipokuwepo.


Ni katikati ya msitu,tena katikati ya vichaka mbele yake akizungukwa na wale watu kumi tena wakiwa na silaha.


"Una dakika tano za kuvuta pumzi ilobakia,ndani ya dakika hizo waweza zitumia,'a' kwa kusali Allah aipokee roho yako na kuitunza mahali pema peponi amin,'b'kujitetea ama kwa kupambana na sisi au tukuruhusu ukimbie na che tunakupa nafasi uliza chochote,swali moja tu!,tutakujibu.


Butu alijua sasa anaenda kufa lakini huzuni yake kubwa anakufa bila kumlipizia aloiteketeza familia yake,anakufa na kinyongo,akajikuta machozi yakimchuruzika,ila

akakumbuka ana dakika tano tu alizopaswa achague,alitamani amjue mbaya wake,ila akuona uhafadhali huo hali ya kuwa anaenda kufa akaona ni bora tu asali sala zake za mwisho roho yake ipokelewe,baada ya dakika zile kuisha ndipo silaha zilipo mwelekea ni kwamba angetandikwa zote kumi kwa mara moja uwezekano wa kuendelea kuishi kwake usingekwepo.


"Kabla atujakuua nimeona ni vyema pia kukupa nafasi ya upendeleo uzitambue sura zetu sisi wauwaji wako!"


Palepale watu wale waka anza kuvua sox zile walizovaa vichwani.


Butu kuwaona tu watano kati ya kumi wale aliwatambua.


vipara.


Ndiyo ni wale waloshuka kwenye ndege siku ile wakiwa na madawa ya kulevya akawakamata na kuwatia ndani,simanzi ikamtawala upya,mabwana wale vipara,walimtazama kwa matabasamu mabaya,yalojaa dharau,kisha wakapeana ishara palepale milio ya risasi ikasikika.


Risasi kumi zikikishambulia kifua cha Butu akaporomoka chini,na kutulia tuli,mmoja wa watu wale akaenda na kusikiliza mapigo ya moyo yalitulia,akageuka na kumwonesha mwenzake ishara ya dole,mmoja mwenye kamera akaupiga mwili ule picha kadhaa.


"Mkuu tushaikamilisha kazi vipi huu mwili tuache huku?!".


"No! hiyo ni mali ubebeni muulete hapa kwangu haraka kesho usafirishie mzigo"


Palepale mwili wa Butu ukabebwa na kuwekwa nyuma ya buti kwenye tax moja wapo kati ya zile gari,safari ya kurudi mjini ikafatia...





John Butu anatandikwa risasi kumi na kupoteza fahamu,watu wale wakijua wamesha muua wanambeba na kumuingiza ndani ya Buti ya gari yao,je unadhani nini kiliendelea?!...


Tusonge katika hatua inayofatia


Baada ya kuuingiza ule mwili ndani ya Buti safari ikafatia.


Mwisho wa safari ulikuwa ni katika jumba la kifahari la Zidu,jumba ambalo ulitumia kufanya mambo yake ya siri,mwili ule ukatolewa na kuingizwa katika chumba maalumu,vijana wale wa usalama wa taifa hatimaye wakaondoka.


MASAA MATATU BAADAYE


Walinzi walifungua lango gari kadhaa zikaingia,zilielekea mpaka maeneo ya maegesho zikapakiwa vizuri kisha walokuwa ndani ya magari yale wakashuka,wa kwanza akiwa Zidu mwenyewe akaenda kufungua mlango,vijana wale waloshuka walielekea nyuma ya buti zao walipofungua na kutoa miili ya watu wakaingiza ndani,kule alipowekwa Butu,baada ya kukamilisha kazi yao wakarudi katika gari zao wakaingia na kutoka.


Zidu alielekea mpaka sebuleni kwake akaketi kochini,sasa alihitaji kumjulisha mh Rais walipofikia,akashika simu yake na kutafuta namba alizohitaji alipozipata akazitwanga,zilihita hatimaye zikapokelewa...


"Mh Raisi nimefanikiwa kuileta ile miili mpaka hapa pardon je kipi kifatie?!"


"Vizuri sana,ngoja niongee na dk Stanley aje aipasue hiyo miili na kuiyewekea mizigo mara moja kesho asubuh isafirishwe,then itapaswa iondoke na wamama wa tano ambapo watarudi nayo ikiwa na mizigo mingine sawa?!"


"Sawa mkuu!"


Kweli baada ya nusu saa gari ya dokta ikawasili,akiwa na msaidizi wake,dokta alikuwa kakunja sura akuipenda ile kazi sasa angefanyaje na ni amri ya kiongozi wa nchi,haraka wakaingia katika chumba kile cha siri,waka anza kuifanyia operesheni miili ile mitano na kuiweka kiasi kikubwa cha madawa katika matumbo yao,dokta alishtuka baada ya kuukuta ule mwili wa mwisho ukiwa na uhai,japo mapigo yake yalipiga kwa mbali!.


Akajikuta moyo ukimsuta,wajibu wa kazi yake ukamvaa,dhima ya kazi yake ni kupigania maisha ya kiumbe kilicho mahututi kuhakikisha kinakuwa hai,hapo ndipo ilipofuraha ya daktari yeyote ulimwenguni,akampa ishara msaidizi wake,operesheni ikaanza,kwanza kwa kumtolea risasi zote kumi,mwisho maswala ya kitabibu yakafatia,masaa manne wakaitimisha operesheni ile,sasa Butu alilala kitandani akitumia mashine za oxygen hali yake bado ilikuwa mbaya.


Masaa yakakatika hatimaye Zidu akawasili toka kazini alipoelekea ile mida ya mchana,baada ya kuwasili kwa daktari.


"Vipi kazi imekamilika?!"


Zidu akamuhoji daktari yule huku akiketi sofani.


"Ndiyo mkuu ile miili mitano mfu nimeipandikiza viroba vya unga ulivyo nipatia ila ule mwili mmoja nimeukuta una uhai nimeufanyia operesheni japo hali yake bado mbaya kupona ni kudra za Mungu..."


Zidu akakunja sura,hasira zikampanda.


"Kwani uliambiwa uje utibu hapa au upasue matumbo utie unga ndani yake na kuyashona?!"


"Lakini tahaluma yangu ainitumi kufanya hivyo kwa kiumbe hai!"


Dk Stanley naye akaja juu,.


"Kwa hiyo pakiti moja ujaliweka ndani ya tumbo la mtu?!"


"Yah nimefata maelekezo kama ulivyo nambia kila mwili nitie kiroba kimoja na ndivyo nilivyofanya,kasoro tu kwa huyo kiumbe hai,nimemtoa risasi nikamfanyia opereshen now nimemtundikia dripu na anasaidiwa na mashine za kupumulia".


"Aaah!,comon dk unafanya nini?,ujui yule mtu ana hatari gani kwa taifa ingali akiwa hai,yapaswa ukamuue mara moja na utie hayo madawa katika tumbo lake muda wowote mheshimiwa anawasili sijui tutamjibu nini!?"


"Hapana mkuu utanisamehe bure kazi yangu mimi ainitumi kuua,kwa hilo sitokuwa tayari!".


Daktari akazidi kubishana na Zidu pasina kujua yule ni kiumbe katili kwa kiasi gani,mapigo ya moyo yakazidi kumwenda kasi akazidi kujiuliza yule dokta ni wa aina gani mpaka awe na ujasiri wa kubishana naye?!,kipi kinacho mfanya ajiamini kwa namna ile?,akajikuta akiwaza sasa kutumia nguvu kuiendesha ile kazi hata ikibidi kuua aue kama ato muelewa!,.


"Dokta kama unayapenda maisha yako,naomba fanya kazi nilokuagiza taratibu geuka twende chumbani ukaue yule kiumbe umwekee hiyo pakiti ilobakia hapana muda tena wa kupoteza."


Tofauti na mategemeo yake dk aka achia tabasamu tena lile la madharau,kisha kwa sauti ndogo ila ya kujiamini akageuka...


"Unantisha siyo?,unadhani nina nidhamu ya uoga siyo?!,tandika risasi uzitakazo lakini siwezi badilisha ukweli,siwezi ua kiumbe kilicho hai nilichopoteza muda wangu kukitibu,jasho limenitoka pale labda uue wewe lakini mimi akaa utansamehe tu bure."


Kuongea vile akawa kampa wazo Zidu,kuliko kubishana na kupoteza muda mbona yeye ana weza kwenda na kumuua kwa sekunde chache kwa kumtandika risasi nyingine zisizo na idadi?!


Kwa haraka akageuka na kuelekea chumbani,dokta akimfata nyuma alipofika akafungua mlango bastola mkononi akaielekezea kitandani pale alipo Butu,alijua labda dokta angemzuia ila dokta alibaki tu kumwangalia,taratibu akapeleka kidole chake katika kifyatulio kwa lengo la kuruhusu risasi ichomoke safari hii kwa hali alokuwa nayo Butu sijui kama angepona!..


Sijui kwa kweli.......





Butu anachukuliwa kwa lengo mwili wake ukatumike kubebea na kusafirishia madawa ya kulevya nchi za nje ikiungana na mihili mingine kumi.


Kwa bahati nzuri Dokta ajulikanaye kwa jina la Dokta Stanley anagundua Butu yu mzima haraka sana anamfanyia operesheni ya kumtoa risasi zote kumi kitendo hiki kinazua Sekeseke jipya kwa Zidu,


Anamjia juu daktari.


Maisha ya Inspekta Butu yanakuwa Roho mkononi,mabishano makali yanaendelea mwishoni Zidu mwenyewe ana amua kuzama ndani ya chumba kile akamalize kazi mwenyewe bastola mkononi anaielekeza pale alipo Butu je atammaliza?!....


Ungana nami katika hatua inayofatia kuzidi kuburudika zaidi


HATUA YA ISHIRINI NA SABA.


Kabla ajamtwanga ile Risasi ghafla akasikia sauti nyuma yake.


"Zidu achaaaaa...."


Kisha hatua tena zikipigwa haraka haraka kuja ule upande wao.


Sauti ile aliijua fika,ilikuwa ni ya mheshimiwa Rais,mapigo ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi si yeye tu lah hata kwa daktar Stanley naye alitetemeka binafsi aliutambua ukatili wa Raisi wake yule akajua hapo pangenuka tu na si kwake hata kwa Zidu pia ila hata ivyo akujali.


Moyo wake ulisimama katika haki,alikuwa tayari kufa ila si kuua kiumbe kisicho na hatia hiyo kuziwekea tu zile mwili viroba vya madawa moyo wake ulikuwa ukimchuruzika machozi kwa uchungu sembuse kuua?!.


Hapana hakuwa tayari kwa ilo.


Itakavyokuwa na iwe,akawa tayari kupokea lolote lijalo.


Raisi Patrick Bisau akawafikia pale walipo.


" Zidu amna haja ya kumuua huyo kwani inatakiwa miili Kama hii mitano kwa ajili ya kusafirisha mizigo USA hivyo dokta katufanyie mchakato ya miili minne katika hospitali yako dokta Julias atafanya hiyo kazi ya kuiwekea mzigo sawa?!,Zidu hii itangulie uwanja wa ndege kwa Safari ya kuelekea hapo kenya wale wa mama wa msiba si ushaongea nao?!..."


"Ndio mkuu nishawapanga watakuwepo KEIA kuipokea miili Kama ya ndugu zao"


"Very nice kazi nzuri mpigie Isack,Kinampa waje mkaipakie hii miili DIA haraka sana na Isack asafiri nayo wewe utaelekea USA na hii miili mahututi na madokta hawa sawa?!"


"Sawa mkuu"


Zidu akaitika,palepale Raisi aka aga na kuondoka,mzigo wote ulikuwa katika jumba lile la Zidu na kazi ilifanyikia pia palepale.


Baada ya muheshimiwa Bisau kuondoka Zidu na dokta wakatazamana hakuna alotoa neno kwa mwenzake kila mtu akaendea na shughuli yake.


Dokta Silvestar akaelekea mpaka mahali alipo msaidizi wake akampa maelekezo.


"Doto mimi natoka hakikisha usalama wa mgonjwa wangu mpaka hapo dokta Julias atakapowasili badiliko lolote litakalotokea utanijulisha sawa?!"


"Sawa dokta"


Binti yule nesi akaitikia kwa heshima,daktari akatoka zake,tayari kwa kwenda kutekeleza jukumu jipya alilopewa na mkuu wake.


Zidu mapema sana yeye alishaondoka yeye hakuwa na wa kumpa maelekezo pale.


***


*SURA YA SITA*


*UNITED STATES OF AMERICA*


*WASHINGTON DC*


Ndani ya taifa la marekani katika mji mkuu katikati ya jiji katika jengo moja kubwa lenye ghorofa zaidi ya 30 jengo hilo kubwa lilimilikiwa na bilionea alotambulika kwa jina la Mernly Max Arthur.


Ndani ya chumba kimoja juu kabisa ya ghorofa kulikuwa na kikao cha siri ni baada ya taharifa nyeti kutua kwa bilionea huyu Merly kwamba kuna kiasi kikubwa Cha madawa ya kulevya kinaingia nchini kwa njia ya magendo kutoka nchini Tanzania akakumbuka miaka mingi nyuma alishawai kutapeliwa na huyo mwenye mzigo huo kipindi hiko Bisau akiwa mgombea pesa hizo akazitumia kuimarisha chama na kuendeshea kampeni.


Kwa muda mrefu sasa Merly amekuwa akimfatilia Raisi Bisau kwa kusudi la kulipiza kisasi bila mafanikio ila mtafutaji huwa akosi siku hiyo hatimaye habari zikamfikia kuwa watu mzigo unaingizwa na wagonjwa mahututi haraka akaweka kikao kujadili swala Lile.


Alikuwa kavimba kwa hasira,


"Niliapa siku moja kulipiza kisasi kwa kile Bisau alichonitendea na muda ni Sasa sitokuwa na msamaha kwa hili!,alinirudisha nyuma sana Sasa Agent Bray hakikisha unakusanya vijana wako wakakamavu mnawasili uwanjani na ambulance mnawapokea hao wagonjwa Mimi nishawapanga Madison's Hospital ndo walikuwa wawapokee watachelewa kwa dakika tatu nanyi mtazitendea haki kumbuka ni dakika tatu tu..


Agent Bray nakuamini nimekusomesha na Sasa ni mpelelezi unaye tegemewa, na taifa letu la Marekani usije ukaniangusha kwa hili nitampiga huyu fala pigo ambalo hatokaa alisahau katika maisha yake na huu ni mwanzo naapa one day nitahakikisha anakufa na Tanzania inatawaliwa na kiongozi safi Raisi gani anauza madawa ya kulevya?!"


Max Merly aliongea kwa uchungu.


Agent Bray alitabasamu akamtoa khofu mkuu wake kwamba kazi ataifanya Vizuri.


Kwa upande wa Tanzania miili ile mitano ilipasuliwa ikatiwa madawa siku ilofatia ikapakiwa kwenye ndege binafsi Safari ya kuelekea Washngtone Dc ikafatia,wakijua watakaowapokea ni wale walowapanga wao.


Ila kumbe mkuu wa kundi hatari la Mafia nchini Marekani Max Arthur Merly alishamuwekea mtego akimtumia kijana wake jasusi hatari Agent Bray.


Ndani ya ndege kidume Zidu kiliketi pasina wasiwasi madaktari Wawili Stanley na dokta Julias na wasaidizi wao wakizidi kutazama usalama wa wagonjwa wao walolala vitandani pasina ufahamu tena wakitumia mashine za hewa ya Oxygen kupumulia....




Wagonjwa mahututi wanapandikiziwa unga wa madawa ya kulevya katika matumbo yao na kusafirishwa kuelekea nchini Marekani Butu akiwa mmoja happy wakisindikizwa na Zidu kijana katili aliyoko ndani ya usalama wa Taifa nchini Tanzania...


Pia tuliona habari hizi nyeti zinamfikia tajiri Merly Max Arthur mkuu wa mafia nchini Marekani haraka anaitisha kikao cha siri na kazi ile anamwachia kijana wake aitwaye Agent Bray kuhakikisha mzigo ule unafikia kwenye mikono yake je ATAFANIKIWA?!


Tusonge katika hatua ifuhatayo kuzidi kuburudika zaidi tiririka nayo


HATUA YA ISHIRINI NA NANE


*UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA WASHNGTONE DULLES*


Ndege binafsi ilomilikiwa na Raisi Bisau ilitua katika kiwanja kikubwa cha ndege Dulles mjini Washngton Dc nchini Marekani.


Kama ilivyo ada mlango ukafunguliwa na machela zilibeba wagonjwa haraka zikashushwa,madaktari maalumu waloandaliwa tayari walisogea kusaidia kupokea wale wagonjwa na kwenda kuwapakia katika magari yao ya wagonjwa.


Walipokamilisha safari sasa ya kutoka uwanjani kuelekea hosptal ikafatia....


Zilikuwa ambulance tatu moja ikipakia wagonjwa wa nne na hizo mbili zilipakia wagonjwa wa tatu wa tatu.


Ambulance ilokuwa mbele kabisa ndiyo alokuwepo Agent Bray kijana aliyekuwa na asili ya 'black America' akiwa ndani ya koti zuri jeupe la kidaktari nywele zake fupi alizichana Vizuri huku kidevu chake akiwa kakipendezesha kwa kuchonga ndevu mtindo wa 'O' macho yake akiyaficha kwa mawani ilomzidishia utanashati shingoni akitupia kipimo maalumu Cha kupimia mapigo ya moyo kiitwacho...........


Kamwe usingeweza kukubali kwamba yule si daktari kwa muonekano tu alokuwa nao tena alionekana Kama daktari mkuu katika jopo lile maalumu waloandaliwa kuja kuwapokea.


Ambulance ya pili walikwepo madaktari wale Wawili Silvester pamoja na Julias masikioni mwao wakiwa na earphone kwa ajili ya mawasiliano maalumu.


Na Ambulance ya mwisho alikwepo Zidu Katili yeye alipiga tisheti ilombana na suruali yake ya jeans na chini akitupia 'simple' Raba alipendeza hakika masikioni mwake alikuwa na 'earphone'alizounganisha na simu yake pembeni yake walikwepo madaktari wale walokuja kuwapokea wote lengo lao kuhakikisha hali za wagonjwa zinakuwa nzuri japo hata wangekufa kwao isingeleta shida yeyote.


Safari iliendelea gari mbili zile zikilifata gari ile ya mbele ambapo ndipo alipokwepo Agent Bray ambaye tayari dereva wake alishajua aneo analopaswa kuwapeleka.


Mbaya Zaidi Zidu akujua ni wapi miili ile inapopelekwa wala ilipo hiyo hospital ya Madison's Hospital ambayo ndio ilotumika kuwapokea wagonjwa mahututi na kuwafanyia upasuaji na kuwatoa hayo madawa kabla ya kusambazwa na mawakala maalumu waloandaliwa,kabla ya miili ile kuwekewa aina nyingine ya madawa na kusafirishwa tena Kama maiti ikitua jijini Dar watu maalumu uipokea kwa majonzi ivyo upita bila kukaguliwa.


Wakati safari ikiendelea ghafla simu ya Zidu ikaita kuangalia ni mheshimiwa Raisi haraka akapokea.


"Mmeenda wapi mbona amuonekani hapo uwanjani?!...."


"Ndo tupo njiani mkuu tushapokelewa?!."


"Unasemaje?!...mbona hapa madaktari kutoka Madison's Hospital wamefika hapo uwanjani awajawakuta."


Zidu akaduwaaa....


"Embu subiri muheshimiwa,...


Akamwangalia moja wa madaktari alokuja kuwapokea Kisha akamtwanga swali.


....Samahani daktari eti tunaelekea hospitali gani?!"


Daktari akageuza shingo kumtazama Zidu,akaachia tabasamu la kumtoa khofu.


"Madison's Hospital"


Daktari yule mmama unayeweza kukadiria miaka yake kwenye thalathini na nane au arobaini akajibu kwa sauti tulivu kisha akageuka kuendelea na shughuli yake.


"Mkuu wala usijali ni Madison's Hospital"


"Hapana umekosea fanya juu chini urudi uwanja wa ndege sasa hivi!,"


Raisi aliongea huku dhahiri alionekana kuwa na wasiwasi,pale pale Zidu akafikiria kuchomoa silaha yake amwelekezee dereva na kumpa amri ageuze gari ile anataka kuingiza mkono mfukoni alishtuka akitazamana na bastola ndogo wale madaktari wakiwa wamezishika Vizuri hapo Zidu akajua kumekucha ya kumepambazuka.


Simama yao,nyuso zao sasa zilibadilika,kwa haraka Zidu akajua wale si madaktari wa kawaida Kama alivyodhani awali.


Wana kingine zaidi ya udaktari.


Haraka akajitahadharisha kabla ya kutahadharishwa kuwa makini.


Akatulia tuli.


"Tulia hivyo hivyo usijiguse hata kujikuna tutausambaratisha ubongo wako..."


Yule dada aliyeonekana kuwa na tabasamu mwanzo aliongea kwa amri akiwa tayari kwa chochote.


"Mikono juu...."


Mwingine akatoa amri,Zidu alitaitika ikabidi atii haraka kijana mwingine akamsogelea na kuichukua silaha Kisha pale pale akapewa amri atoe mkono akachomwa sindano iloenda na fahamu zake....


No 29


Msafara ule wa gari za wagonjwa zilizidi kusonga mbele tayari Madamu Mery mwanadada hatari jasusi alisha mdokeza Agent Bray kilichotokea na walivyofanikiwa kumdhibiti Zidu kilaini tu....


"Congrats comred nilijua sikukosea kukuacha na huyo mtu!"


Agent Bray alimpongeza mwanadada yule,kwa kipindi hiki bilionea Max Arther Merly ndio aliyosadikika kulishika taifa la Marekani na yeye ndo alikuwa mdhamini mkuu wa chama tawala Cha American People 'AP' yeye ndo alopanga Raisi awe nani katika chama chake.


Na toka chama hiko kiingie madarakani Miaka 15 Raisi alimsikiliza yeye,alitumia wapelelezi maalumu na muhimu wa taifa Kama Kina Agent Bray,mwanadada Machachari Merry,na wengineo kwa mambo yake binafsi.


Arthur kazi yake kubwa ni usambazaji wa madawa ya kulevya duniani na kwa kuwa taifa lake lilikuwa kubwa akupata ukinzani wa aina yeyote na alikuwa na mawakala dunia nzima kundi lake likiitwa Mafia gengstar.


Miaka kibao nyuma wakala wake wa Tanzania akiwa ni waziri Patrick Bisau alituma mzigo wa ma bilioni,ghafla katika hali isiyo ya kawaida fedha zilichelewa kurejeshwa baadaye akasikia Bisau kachukua tiketi ya kugombea nafasi ya Uraisi na hata alipo ipata Bisau alimwambia pesa zake anazitumia katika kampeni akishinda Basi atazireuesha mara mbili yani na kiasi kile kile cha riba.


Kwa kuwa chama cha Patrick kilikuwa na nguvu Max alikubaliana naye,Bisau akapiga kampeni pa kuonga akionga mwisho wa siku akashinda tena kwa kishindo.


Kuwa Raisi Patrick kukamtia kiburi,Max alipoitaji hela yake akawa akizungushwa mwisho wa siku akatamkiwa wazi kutopatiwa hizo hela.


Mazoea ni mzigo kuutua ni ngumu , kwa kuwa Bisau alishazoea kazi ile ya magendo aliendelea nayo japo ni kwa usiri sana,kwa muda mrefu alitamani kuuza Marekani ila alishindwa kwa kuhofia mzigo wake kuingia mikononi mwa Max ila kwa kuwa taifa la Marekani soko lake lilikuwa juu akajipa muda wa kutengeneza mazingira.


Siku hiyo alialikwa kugawa vyeti kwa madaktari kadhaaa waliomaliza masomo yao,zoezi la ugawaji vyeti lilipokamilika Raisi akaomba aitiwe mwanafunzi mmoja punde kijana mmoja mchangamfu akaja.


"Ok unaitwa nani?!..."


"Madisoni Shemweta muheshimiwa!"


"Katika udaktari upo katika tahaluma gani?!"


"Upasuaji muheshimiwa Raisi"


Raisi Bisau akatabasamu,ndo mtu alokuwa akimtaka,kijana yule alikuwa ni yatima alolelewa na kusomeshwa na kituo Cha watoto yatima Cha Mkombozi, historia yake ya maisha pia ikamvutia Muheshimiwa Raisi.


"Nataka nikufungulie hospital nchini Marekani privet unaonaje?!"


Kijana yule akuamini ila Raisi alimpanga akapangilika,Madisoni akasafirishwa na kupitia balozi wa Tanzania nchini Marekani akafanyiwa mchakato wa uraia nchini Marekani,hospitali kubwa ilobeba jina lake Madison's Hospital ikajengwa na kuajiri madaktari wengi wakiwa wa Tanzania na wahindi.


Mpango ukakamilika.


Upasuaji ukawa ukifanyika pale watu wakawa wakipachikwa madawa ya kulevya na kusafirishwa Tanzania,hakuna alogundua hili kwa muda mrefu Bisau akawa akifanya kazi kwa uhuru huku Max akichunguza bila mafanikio.


Ila hakuna siri inayodumu milele ya mtu zaidi ya mmoja,siku ya siku Max akagundua siri ile naye kwa siri akakutana na dk Madison akampa fedha na kumpanga ampe Siri tofauti na ivyo angemuua Madison akaingia upepo,pesa akachukua na Siri akaitoa,mpango ukapangwa ukapangika,Max akaandaa vijana wake akiwemo Agent Bray wakawah uwanja wa ndege na kuwapokea kina Zidu baada ya kuondoka tu ndipo dk Madison alipowasili alipokuta wameondoka ndipo akampigia muheshimiwa Raisi Bisau na kumjulisha.


Raisi alichanganyikiwa,naye kwa haraka akampigia Zidu na kumuomba haraka arudi uwanja wa ndege.


Zidu akamuhaidi kufanya hivyo simu ikakatwa.


Zilipita dakika tano,Bisau akapiga tena kabla ya kukutana na sauti 'mteja unayempigia kwa Sasa apatikani tafadhali jaribu tena baadaye'.


Hata alipojaribu tena jibu likawa lile Lile.


Raisi akazidi changanyikiwa, ulikuwa Ni mzigo wa mabilioni...


Wasiwasi wake ulikuwa ni kwa mtu mmoja tu!....


Max Arthur Merly.


Akukosea,punde sms ikaingia katika simu yake haraka akaifungua kutaka kujua imetoka kwa nani.


Namba ilikuwa ni ya nje,


+1 859-962-3177


'Kwa kuwa umekuwa Raisi ukajua umekuwa Mungu wa dunia ukanidhulumu pesa zangu,Vizuri,ila usiangaike kutafuta mzigo wako pamoja na hawa Raia wako vyote kwa Sasa vipo chini yangu hii ni mwanzo rasharasha mvua inakuja....'


Ujumbe ule Raisi aliusoma zaidi ya mara tatu ila aukubadilika akapiga zile namba kabisa lakini pia azikupokelewa

Mwisho kwa hasira akaitupa ile simu na kuipasuapasua.


Ni Hasara kubwa sana aloenda kuipata!...


No 30


Hatimaye siri kubwa ilojificha kati ya bilionea mkubwa nchini Marekani Max Arthur Merly na Raisi Patrick Bisau tunaitambua,juu ya bifu lao la muda mrefu hatimaye Max Arthur Merly anafanikiwa kuiteka miili ya watu kumi ikiwa na madawa ya kulevya ndani,Bisau anachanganyikiwa kupata taharifa hizo je unadhani nini kiliendelea?!, Tusonge katika hatua ifuatayo nayo ni....


HATUA YA THALATHINI:


Haraka sana Raisi Bisau akamtwanga simu waziri mkuu wake Benson Sai na kuhitaji waonane haraka sana ikulu.


Muheshimiwa Sai alijiuliza ni nini kitakuwa kimetokea bila kupata jibu mwishoni akaona aende tu akasikie wito kwani ndo yalipo majibu ya maswali yake.


Dereva wale akampeleka mpaka ikulu,baada ya kusalimiana wakaingia katika chumba maalumu maongezi yakafuata.


Raisi Bisau alimweleza rafiki yake kila kitu kuanzia Madison alipompigia simu na kumtaharifu kutowakuta wagonjwa pale uwanjani,alipompigia Zidu na majibu alompa mpaka naye alipopigiwa simu na Max,hata waziri pia alichoka ila akakumbuka jukumu lake ni kuto kuonesha udhaifu na badala yake kumtia moyo kiongozi wake yule.


"Ni ku haidi tu muheshimiwa Raisi hakuna baya litakalotokea lazima Zidu ataukomboa mzigo wetu ni kijana ninayemwamini usijali kwa hilo muheshimiwa."


"Kwa hiyo kwa sasa yapaswa tufanyaje Sai"


"Tuwe na subira Muheshimiwa."


"Hapana Mimi na wazo."


"Wazo gani?!"


Sai akahoji akionekana kuwa na hamu ya kujua wazo hilo.


"Tumtume kk yeye pekee ndo anauwezo wa kurejesha mzigo pamoja na kumkomboa mumewe."


Kumbukumbu za waziri Sai azikufuta kazi alizowah kufanya Katarina,kumbukumbu zake ziliandikwa toka kuipatia uhuru Kinte,kupambana na mumewe Zidu uhodari wake wakaona wamtumie akauoneshe kwa bilionea yule.


"Haraka Katarina apigiwe simu nionane naye aingie kazini."


Mwisho Raisi akamaliza,waziri Sai akatoka sasa akiwa na matumaini.


**************


Mwili wote ulimsisimka,hatari ilishagonga katika kichwa chake si kawaida ya mume wake huwa akisafiri akifika salama umpigia na kumwambia mume wangu nimefika salama,ila safari hii mpaka muda huu akupigiwa.


Haraka aka amua akanunue vocha akatia katika simu yake akajiunga vifurushi vya nje akaitafuta namba ya mume wake anayoitumia Marekani akaipiga aikupatikana.


Akajaribu laini yake ya Tanzania pia jibu lilikuwa lile lile au simu imeisha chaji?!...


Hapana,alipingana na wazo hilo baada ya kugundua hata ndani ya ndege angeweza kuchajisha,alijua lazima mumewe atakuwa kaingia kwenye matatizo japo akujua Marekani kaenda kwa shughuli gani,pia alielewa mumewe alitumika kiuhalifu mara kibao alishamuomba abadilike bila mafanikio.


Wakati akiwa katika hali ya sintofahamu ghafla simu yake ikaita kuangalia alompigia ni 'privet namba' huku akiwa na wasiwasi akaipokea...


"Ni waziri mkuu Bisau hapa naongea unaitajika Ikulu na muheshimiwa Raisi kuna gari inakuja kukuchukua hapo nyumbani muda huu ivyo haraka sana jiandae ndani ya dk 5 uwe mbele ya Raisi"


Sauti ile ya waziri mkuu ikaitimisha,mwili wote wa Katarina ulimlegea jasho lilimtiririka akajua lazima mumewe kapatwa na matatizo je ni kafa?!,maswali mengi yakatiririka mawazoni,woga ukamtawala ila akajikaza haraka sana akaanza kujiandaa alipomaliza gari ikawasili akapanda Safari ya ikulu ikafatia.


Sasa kilikuwa ni kikao cha watu wa tatu, Raisi Bisau, waziri mkuu Sai na Katarina akiwa kaongezeka, Raisi hakuwa na budi kumsimulia kila kitu Katarina,mwisho akamueleza wazi kuwa kuitwa kwake ni kwa kazi moja tu,hata kuua ikibidi ila aokoe mzigo ikiwezekana na watu wale kumi wakiwa hai au maiti zao.


Akakabidhiwa paspoti na siku ilofatia ndiyo ilipaswa Katarina asafiri kuelekea nchini Marekani.


Kikubwa yeye alichofikiria ni kumkomboa tu mumewe katika mikono ya watu wale hatari.


Ni kazi ngumu itakayo yaweka maisha yake rehani


Roho mkononi!!!


Alilijua hilo, sekeseke analoenda kukumbana nalo alijua si la kawaida!


Ila je angefanyaje?!...


Mafia Ni kundi lililo ogopwa ulimwenguni.


Akaaga akiahidi kuifanya kazi Vizuri,akapewa baraka akatoka,tumaini kwa viongozi wale wa Taifa likarejea upya.


**********


Katika moja ya jumba la kifahari,jumba lenye ghorofa zaidi ya tano ndani pakiwa pamezungushiwa ukuta mkubwa wenye nyaya za shoti kamera za ulinzi na pakiwa na geti tatu zenye walinzi wa kutosha wenye silaha mabegani walojaza risasi.


Geti ya kwanza ikafunguliwa gari zile za wagonjwa zikaingia ndani pakiwa pamejengwa pakajengeka nyumba ndogo ndogo zikiwa pembeni zenye ghorofa moja mbili mpaka tatu yani kalikuwa Kama ka mtaa cha kitajiri gari zile zikaendelea kwenda hatimaye wakaingia geti la pili napo kulikuwa na walinzi maalumu pembeni pakiwa na banda la mbwa walobweka kwa ukali geti likafunguliwa wakaingia katika mtaa wa pili nao aukuwa tofauti na ule mtaa wa kwanza gari zile zikaendelea na safari hatimaye wakakutana na geti la tatu walinzi wakafungua na gari zile zikapita.


Mtaa huu ulikuwa tofauti na mtaa wa kwanza na wa pili mtaa huu ukuta wake ulikuwa mrefu zaidi kupita kuta za mtaa wa kwanza na wa pili pia ndani palionekana Kama pori miti ya matunda ilitawala si maembe machungwa migomba mbele kidogo wakaikuta bustani nzuri mbele ya bustani ile upande wa kushoto palikuwa na bwawa la kuogelea mbele nyuma ya bwawa Lile kulikuwa na jengo kubwa la ghorofa zaidi ya 50 ukitazama juu uoni mwisho wake.


Hili ndo jumba la bilionea Max Arthur Merly lililopo jijini Washngtone dc japo alikuwa na majumba Kama haya zaidi ya hamsini nchini Marekani,yani mitaa yake mwenyewe,pakiwa na hospital zake ndani maduka,masoko kwa kifupi katika mtaa huu wa tatu wa ndani hawakuruhusiwa kutoka nje,.


Japo mitaa hiyo miwili aliipangisha.


'Max Arthur Merly hospital'


Ambulance zilizimama mbele ya jengo ilo miili ile ikashushwa haraka na kuingizwa wodini.


"Haraka ipasuliwe na mizigo itolewa hakikisheni wanakuwa hai"


Agent Bray aliwa ambia madaktari walokuwa bize kuishusha miili ile.


Mwili wa Zidu kwa kuwa yeye alikuwa kalala akapelekwa katika chumba maalumu akafungwa kitandani kwa pingu maalumu akisubiriwa kuzinduka.


Tayari alikuwa ni mateka.....


Mwili wa Inspekta Butu na wenzake upasuaji ukaanza mara moja hali zao bado zilikuwa mbaya....


Merly Max Arthur mafia mwenye mtandao mkubwa hakupata tabu kugundua kutumwa kwa Katarina.


Alipotua tu uwanja wa ndege akaingia mikononi mwa wanausalama na taharifa akapewa.


Akacheka kwa kiburi akista ajabu upumbavu wa Rais Bisau na Mawazo mabovu ya kumtuma Mwanamke


Akaagiza Katarina apelekwe kwake akachanganywa na mateka wale kumi.


BAADA YA MWEZI MMOJA


Hali za mateka wale ziliendelea vizuri walipona kabisa Merly Arthur alishajua cha kufanya akawasiliana na shirika la habari la BBC na kuandaa kipindi Maalumu Cha watu wale kujielezea historia ya maisha yao.


Zidu na Katarina nao ili kuwa hai na mtoto wao Mdogo Sebastian aliyekuwa akademy Nchini humo kutodhuriwa ikawapasa waeleze ukweli wote Zidu akaeleza kutumika na Raisi kumtesa afisa wa Jeshi la Polisi Butu mbinu alizotumia kuiteketeza familia yake.


SEKESEKE likazaliwa nchini Tanzania watu wakaanza kuandamana wakishinikiza Rais Bisau sambamba na Waziri Mkuu wake kujiuzulu,


Jeshi likaingilia Kati kweli Bisau na Waziri Mkuu wakajiuzulu na kushtakiwa katika mahakama ya kimataifa na mwishowe wabaya wote Raisi Waziri Mkuu wake wakafungwa kifungo cha maisha.


Zidu naye alifungwa miaka mitano jela kwa kuwa alikuwa chini ya Rais ilikuwa lazima afate maagizo yake.


Inspekta Butu akarudi Kazini akipandishwa cheo na kuteuliwa mkuu wa Polisi ' IGP ' na Raisi aliyechaguliwa baada ya uchaguzi wa haki na amani ulosimamiwa na Jeshi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba na umoja wa mataifa.


Hakika mafia japo lilikuwa ni kundi baya Ila kisasi chake kikaliletea mwanga Taifa la Tanzania.


Amani sasa ikatawala katika maisha ya Butu alopita yakabaki Kama historia ambayo asingeweza kuisahau katika maisha yake.


Alimshukuru Mungu tu kwa kuwa bado yupo hai tena akiwa mkuu wa Polisi huru katika taifa lake.


***************


MWISHO


0 comments:

Post a Comment

BLOG