Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

HASNA (MFU ANAE ISHI) - 3

   

Simulizi : Hasna (Mfu Anae Ishi)

Sehemu Ya Tatu (3)


Aliitikia mama Ujugi. Alimtambulisha Hasna kama ni mtoto wa marehemu rafiki yake.

Alimuelezea kilicho wakuta hadi kufoka hapo.Shangazi yake ambaye alikua ni MTU mzima,aliwapokea na kuwatoa wasi wasi kuwa wake tu hapo nyumbani.

Zilipita miezi miwili wakiwa pale pale Nyakitonto .Siku moja alikuja binti wa shangazi yake na mama Ujugi.Ambaye alikua kaolewa Kigoma mjini,

Alikuja kwa mama yake kwa lengo la  kutafuta binti wa kazi.Mama yake alimwambia Hasna ni binti mtaratibu na mwenye ni dhamu.

Basi binti huyo wa shangazi yake mama Ujugi aitwaye  Neema, alikubaliana na mama yeke na kumchukua Hasna, na kwenda nae kigoma mjini.




Neema alikua na watoto wawili mmoja mdogo wa kiume anasoma darasa la  nne,na mwingine ni binti anasoma  kidato cha pili.

Pia alikua na mume aliye kua mfanya biashara wa kawaida .kwa upande wa maisha haya kuwa mabaya  sana ,wala mazuri sana yalikua ni yakawaida.

Basi Hasna alianza kazi,kwa muda mchache  waajiri wake walitoka kumpenda sana.kwa uchapaji kazi wake, na upole aliokuwa nao  hata majirani walimpenda sana Hasna.     

Watoto wa muuajiri wake walikua ni watundu sana. Na hata darasani walikua wana shika nafasi za mwisho.  

Hasna alikua akimaliza  kazi zake zote mida ya jioni.Alikua anawachukua na kuanza kuwafundisha masomo mbali mbali.Japo watoto  hao walianza kumchukua Hasna.Lakini kama ujuavyo Hasna alikua anapenda kusoma.Lakini nafasi ya kuendelea na kitadato cha tano ,aliikosa baada ya baba yake, kumuozesha kwa nguvu.

Lakini Hasna hayo Alikua haya kumbuki kabisa.Na sazingine alikua akijishangaa,jinsi anavyoelewa masomo mbali mbali.

Hakutaka kuona watoto hao wakiwa na matokeo mbaya kabisa.Alijitahidi hadi akawabadilisha tabia.Walianza kupenda kusoma napia walimpenda sana Hasna.

Wazazi wao Neema na mumewe Robati walikua niwatu wakutoka sana.Natoka Neema apate binti wakazi alimuachia  majukumu yote Hasna.

“Dada Hasna cheki Leo nilivyopata hesabu“

Aliongea binti yule wa Neema.Aliwakuta wamekaa sebureni,Hasna na Neema.

“Heburete huku tuone ,unafurahia kupata ziro”

Aliongea Neema.Alipopelekewa alishangaa  kuona mwanae kapata tisini,wakati sio kawaida yake akijitahudi sana huwa anapata kumi na tano.

“Wewe justina umeigilizia,toka lini  ukapata hivi”

Alisema Neema.

"Mama nimefanya kwa akili yangu"

Mama ake alimfukuza na kumwambia amtoleeujinga wake,tokalini anaweza kufanya hivyo.Basi Justina aliingia zake ndani akiwa mnyonge sana.

Zilipita wiki mbili wazazi wa Justina waliitwa shuleni na mkuu wa shule.

“Jamani karibuni naimani nyinyi  ndio wazazi wa Justina“

Alisema mkuu wa shule huku akiwa anafunua funua mafaili yake.

“Jamani nimewaita hapa ilikuwapa pongezi”

Alisema mkuu wa shule .Baba Justina na mama Justina walibaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa.

“Mwalimu hizo pongezi ni za nini”?

Aliuliza baba Justina.Mkuu huyo wa shule alianza kuwaelezea ,kuwa binti yao ndani ya hizi wiki chache kaonesha mabadiliko ya hali ya juu.kuanzia tabia hadi upande wa masomo yake .kwa sasa anafanya vizuri.kafanya  majaribio mbali mbili na Sasa anachezea tano bora arasani.

Aliendelea kuongea huku akiwapa matokeo yake ya majaribio mbali mbali.

Wazazi hao hawakuweza kua mini.Maana watoto wao hawa kuwa na tabia ya kujisomea.Walipenda  michezo na kuangalia runinga.

“Jamani mimi niliwaitia hayo, mumkazanie aendelee hivi hivi maana zimebaki miezi michache, afanye mtihani wa taifa".

Aliongea mwalimu mkuu.Kisha waliagana na wazazi wa Justina walirudi nyumbani.

Walimuita Justina na kumuuliza .Ni nani aliefanya kuwa na mabadiliko hayo .Justina aliwaeleza kila kitu.Kuwa ni Hasna ndiye aliyeweza kuyafanya yote hayo.

Lakini mama yake Justina hakuweza kuamini,maneno ya Justina.

Maana aliijua vema sitori ya Hasna .Aliweza kusimuliwa kipindi anamchukua kijijini.

Miezi zilipita Hatimaye Justina alifanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili.Na matokeo alitoka kafahuru kwa wastani mzuri.

Baba yake na Justina aliongeza  upendo kwa Hasna,Nakuwa anampatia zawadi mbali mbali.

Lakini kitendo kile kilianza  kumchkiza mama Justina.

Siku moja Baba Justina alimuita Hasna.Na kuanza kumuuliza  Hasna kuhusu maisha yake ya nyumba.

“Baba mi sijui chochote kama alivyo kuambia mama.Zaidi nachojua ndio hicho nilicho  waeleza nikiwa Shunga hadi nimefuka hapa”

Aliongea Hasna.

“Mi unacho nishangaza kujua mambo mengi.Hasa  masomo wakati haujawahi hata kusoma”

Aliongea baba Justina.Alimruhusu Hasna akaendelee na kazi jikoni.Alimuita mke wake na kuanza kuongea kuhusu Hasna.Kuwa anataka ampeleke shule.

“Hapana siwezi kukubaliana na wewe. Hauwezi kumpeleka shule kijakazi”

Aliongea mama Justina.

“Mke wangu angalia alivyo weza kuwasaidia watoto.unadhani tutampa. Zawadi gani huyu binti”?

Aliongea baba Justina. Kwa msisitizo.Lakini mama Justina hakutaka kumsikiliza.Zaidi alimpa maneno makali  .

“Kama una taka awe mke wa pili huyo Hasna basi umekwama.Hakuna yakusikia kila kukicha Hasna Hasna nimechoka”

Aliongea mama Justina kwa ukali.Huku akinyanyuka ,Hasna alisikia lile neno LA mwisho.

Alimfata mama yake na kwenda kujua shida nini.

“mama kuna nini mbona hivyo”?

Aliuliza Hasna.

“Nitokee hapa nawewe unaweza kuwa na mama kama mimi”?

Aliongea mama Justina kwa hasira hadi Hasna aliogopa.

Zilipita siku kadhaa nyumba ilikua sina maeleweno.

Siku moja Hasna alishangaa  kuchanga mkiwa na mama Justina.Wakati alikua anamchukia sana.

“Hasna muda wote nakuita kumbe humo  chumbani”

Aliongea mama Justina. Alimwambia Hasna kuwa Leo kamundalia chakula kizuri  mezani.

Waliongizana wote mama Justina mbele na Hasna akifata kwa nyuma.

Lakini ghafla mama Justina alishituka na kupiga kelele.

“Mama yangu. mwanangu Justina nani kakuambia  ile hicho chakulaa”


Alisema huku akikimbia kuelekea alipo Justina. Justina alibaki kumshangaa mama yake,maana hakuweza kuelewa kuna tatizo gani.

Robati nae alitoka ndani  baada ya kelele za mama Justina.

“Jamani leteni maziwa”

Alisema mama Justina.

“Kala nini si useme  mama Justina, mbona hatukuekewi ”?

Aliuliza baba Justina. Mara ghafla Justina alianza kutoa povu mdomoni.kila mmoja alishituka ,baba  Justina. Justina alianguka chini na kuanza kuminya minya tumbo lake Kwa maumivu.Huku akisugua sugua miguu kwenye sakafu.

Mama Justina alikua kasimama huku akiwa kama anachezea muziki wa kwaito vile. Mara ende  mbele arudi nyuma .Aweke mikono  kichwani huku miguu yake kama mtu anae piga kwata,akiwa anairusha rusha.

“Mwanangu Mimi jamani baba Justina,mwanangu ”

Alisema mama Justina.Huku akiwa bado anae endelea kutapatapa.

“Mama Justina asema tatizo nini.Hasna nenda chumbani niletee simu yangu.”

Aliuliza baba Justina. Huku akimuagiza Hasna.

“Sumu, nisamehe mume wangu alikua lengo”

Alisema mama Justina. Baba Justina alipiga  simu ili kuita usafiri lakini Aliye mpigia akikua hapatikani .Alimbeba Justina ili kuelekea nje kutafuta usafiri amkimbize hospital. Lakini alipofika mlangoni alikua Hasna kalegea mwili mzima.Aka muweka  chini damu zilianza  kutoka mdomoni na masikioni.Na mapigo ya moyo yaliacha kupiga.

“Mwanangu kafa”.

Alisema baba Justina. Hasna alishuka na kwenda kumuangalia Justina.

Alipofika alimuangalia  Justina usoni.ghafla  kuna mwanga mweupe ulitoka macho mwa Hasna, na kwenda kuingia machoni mwa Justina.

Mwanga huo hakuna aliye uona  zaidi ya Hasna. Nae alijikuta kashangaa nini kimetokea .

“Hasna pisha hapo kaisha  kufa huyo”

Alisema baba Justina. Lakini Hasna alikua kakaa bado akimtazama Justina. Mara akapeleka mkono wake kichwani mwa Justina.

Baba Justina na mama Justina wakabaki kumtaza Hasna .kumuona anachofanya ni nini?.

Dakika kumi zilipita Justina alianza kukohoa.

Mama Justina baada ya kuona hivyo alienda mbio kwa Justina.

Hasna akinyanyuka na kuelekea chumbani kwake.Justina aliamka na kua kama mtu ambaye hajapatwa na kitu.

Baba Justina alimwita mama Justina nakuanza kumuuliza nini kimetokea.Mama Justina alimuomba mume wake msamaha.Na akakili aliweka sumu  kwenye chakula kwa lengo la kumuua Hasna .Lakini kwa bahati mbaya akala  Justina baada ya Hasna.

“Sasa nacho kuomba ingia ndani chukua kila kilicho chako na uondoke hapa kwangu.Mwanamke gani wewe uliyekosa chembe ya utu moyoni mwako.Binti wa watu kakukosea nini ,mama Justina naomba utoke kwangu”

Aliongea baba Justina.huku akimuwasha vibao mama Justina.Mama Justina alikua akilia huku akisema  ,muwe wangu Mimi unaenda wapi usiku wote huu.

Ungomvi wote aliusikia  Hasna .Alitoka chumbani kwake huku akiwa kashika  begi lake mkononi.

“Baba nakuomba usimfanyie hivyo mama,msamehe kwa alichokifanya wala usimfukuze hapa ni kwake.Mnamiaka mingi sana toka mmeona  na kuishi kwa amani na upendo ,hadi leo  mmepata watoto. Tuseme baba haujagundua tu tatizo?.Tatizo ni Mimi baba,ndio chanzo.ni Mimi ,mama asingeweza kufanya jaribio hilo kuniwekea simu.Naomba  niondoke amani  itawale kama awali”

Aliongea Hasna kisha alifungua mlango na kuanza. Kuondoka mama Justina pamoja na Justina walimkimbilia kumzui .lakini Hasna aligoma na kuondoka zake.

Alitembea asijue anaenda  wapi.maana mji wenyewe alikua sio mwenyeji. Na muda wato  aliyokaa kwa mama Justina alikua ni wakushinda ndani. kutoka kwake ilikua Mara moja moja sana.

Alikua na visenti kidogo aliona atafute  gest  alale ili ajue cha kufanya ifikapo kesho.

Alienda kwenye gest  moja hivi .Ile anaingia mlangoni aliona mtu  akiwa kakaa kando kando ya mlango. Akionekana na hali mbaya Huku mate yakimtoka mdomoni.

Hasna alimungalia  sana alimuonea  huruma.Lakini mtu  huyo alikua bize na kuita wateja .

Hasna alifika mapokezi na kumkuta dada wa mapokezi.

“Dada samahani hivi huyo mtu hapo unamoa chakula kweli”

Hasna alimuuluza  dada huyo wa mapokezi.

“Dada mbona hakuna mtu utakuwa umeona vibaya”

Aliongea dada wa mapokezi.

“Dada Mimi siomjinga Yule ni nani si mtu.”

Aliendelea kuonesha Hasna. hadi yule dada alitoka na kwenda kule mlangoni lakini hakuna kitu Hasna akishangaa sana .

Nakujiukiza macho yake yamekuaje.Hasna alipata chumba .

Alivyo fungu chumbani alikua binti wa lika lake akiwa anatandika kitanda.

Hasna alishituka kidogo kisha amuuliza.

“We dada walikua wamekufungia humu? mbona mimi  ndio nafungua sahizi nafunguo ninayo hapa”

Aliongea Hasna lakini yule binti akionekana .kupata na mshituko,baada ya Hasna kuongea hivyo.

“Kumbe unaniona  jamani”



Aliuliza yule binti.

“Kwanini nisikuone kwanini Mimi kipofu”?

Alisema Hasna.

“Hapana sina maana hiyo.Lakini binadamu wa kawaida hawezi kuniona mimi”

Aliongea binti huyo.Mara mlango uligongwa,Hasna alimkaribisha alikua ni muhudumu wa gest.Alikua kaleta sabuni na taoulo.

“Lakini dada mbona nimesikia unaongea na mtu”

Aliuliza yule muhudumu.

“Ndio siu...”

Alikua anaongea  Hasna lakini hakumalizia .baada ya kugeuka na kuto muona  yule binti.

“Yani dada yangu wewe una matatizo sana,au unakalibia kuchizi si bure”

Aliongea  huyu dada ,huku akifunga mlango na kutoka nje.

Baada ya dakika moja Hasna alisikia kicheko.

“Haaaa unaelekea kua chizi”

Hasna alipo geuka baada ya kusikia kicheko hicho.Alimkuta yule binti kakaa kitandani.

"Dada yangu wewe sio mtu  wa kawaida kabisa”

Alisema binti huyo.

”Kwa nini Mimi sio wa kawaida ”?

Aliuliza Hasna .

“Dada Mimi nimekufa mwaka mmoja uliopita"

Alisema binti huyo. Hasna alishituka aliyapikicha macho kwa mikono kuona kama ni ndoto ama laa.

“Umekufa ”

Aliuliza Hasna kwa mshangao.

“Ndio mimi  ni Mfu  nae ishi”

Aliongea dada huyo.Na Alianza kumuhadithia Hasna.

“Baba yangu alitutoa kafara Mimi na kaka yangu.Kaka yangu yupo mlangoni anaita  wateja ,na Mimi niko  ndani nikifanya  mambo mbali mbali. Ikiwepo  kuuwa  baadhi ya wateja kwa ajili ya kafara ya baba”

Aliongea binti huyo .Hasna aliogopa sana baada ya kusikia hivyo.

“Dada yangu we lala usiku umenda naomba uwe  na amani”

Aliongea binti huyo. Hasna alikua na wasi wasi sana.Usingizi ulipo mpitia  alikuja kushituliwa.Na mtu  aliye kua akigonga mlango kwa fujo.

Hasna alishituka na kwenda kufungua.Alipofungua Alimkuta baba wa makamo kasimama.

“Binti nakupa onyo ,nimeambiwa yote sasa naomba ufate mambo ya liyokulete hapa ya watu achananayo”

Aliongea yule baba kwa ukali sana.

“Mzee wangu mbona mimi sikuelewi”

Aliuliza Hasna .

“Utanielewa tu nini  na maanisha”

Alisema mzee huyo ,huku akiwa anatika nje.Hasna nae alioga na kwenda  kutafuta kifungua  kinywa.

Alifika kwenye mgahawa mmoja uliokuwa na watu wengi wakipata chakula.

Nae alifika akagiza supu ya kuku.Ilipokucha alishituka kuona .

“We dada hiki nini ”?

Aliuliza Hasna.

“Dada si umeagiza supu ya kuku ”?

Alisema muhudumu.

“we dada si mikono ya mtoto mchanga  na huu mchuzi ni damu tupu”

Aliongea Hasna huku akiwa anavimwaga chini.Wateja waote  waligeuka na kushangaa kuona kweli mikono ya mtoto.

“ona watu wanavyokula vitu vya ajabu”

Aliongea Hasna huku akionesha baadhi ya meza. Wateja wote waliondoka mahala pale.

Hasna alirudi gest  akiwa kakaa chumba, akitafakali mambo aliyo yaona nje yanatusha.

Akiwa kwenye dimbwi la mawazo , Mara alishituka baada ya kusikia upepo mkali .Kisha akitikea mtu  kimaajabu.

“Binti utajuta kwa kitendo ulicho kifanya  Leo,Hauwezi kunihalibia biashara yangu. haujui nimetumia muda gani na gharama kasi gani kutafuta wateja.sasa leo  lazima ufe”

Aliongea mtu  huyo. kisha akanyoisha mkono wake kumuelekezea Hasna na miale ya mwanga ilitoka.na kumkuta Hasna usoni.

Hasna alipiga kelele na kuanguka chini, akaanza kurusha miguu huku na kule. huku akipiga kelele za kuomba Masada.



Mara Hasna alitulia kabisa ,na damu zikaanza kutoka puani mdomoni na masikioni.

Upande wa pili wa  katika kijiji cha Mbika .kilichopo wilayani Kahama mkoni  Shinyanga.

Wanakiji walionekana kuteseka sana.Baada ya  mzee Jafari  ambaye ni  baba yake Hasna. Kujisimika utemi wa kijiji hicho.

Aliwatumikisha kazi watu alivyo jisikia  yeye. walilima mashamba yake bila malipo na kila baada ya wiki moja, kila mwana kijiji anatakiwa  ampelekee Mtemi huyo debe la  mahindi.

Kila mmoja alikua anamuogopa mtemi huyo.kwa ajili ya uchawi mkubwa aliona nao.

Hakuna aliye weza kumpiga  na ikitokea umempinga basi ni lazima ufe.

“Jamani hivi haya mateso mpaka lini”

Walikua wamekaa baadhi ya kikundi cha vijana,wakijadiliana 

“Sasa Jose unadhani tunafanyaje.Tukubali tu kuwa tumerudi enzi za utumwa”

Alisema kijana mmoja kwenye kundi hilo.

“Mimi nasapoti alichosema Jose.Alafu na wewe acha umama sisi ndio vijana tunaotakiwa kuleta mapinduzi hapa kijijini ”

Aliongea kijana mwingine kwenye group hilo.walijadiliana  wakapanga usiku wakachome mto  kwenye ngome yake Kitemi.

Walikua vijana watano.Walifika hadi kwenye ngome hiyo. iliyokuwa imejengwa tujumba twa  misonge twingi .na tulikua ndani ya ngome iliyo zungurushiwa nyasi.

Kulikua na ulinzi mkali lakini cha ajabu walikua walinzi wote wamelala.

Vijana hao walipenya nakufani kuwa kuwasha moto kwenye kijumba cha mtemi.Moto ulipamba wakaanza kuchoma sasa na vile jumba vingine.

Cha ajabu hakuna hata mtu mmoja aliyepiga kelele wala hakuna hata mlinzi mmoja aliye weza kuamka.

Walikuja kushitu upande pili wa kijiji hicho .kulikua na kelele na mwanga wa moto. ukionekana kuwaka sehemu tofauti ya kijiji hicho.

Vijana hao walitoka hapo kwa mtemi nakuanza kukimbia kila mmoja akifata moto anao ona unamuhusu.

Vijana hao walishangaa baada ya kukuta nyumba zao zimeungua na kubaki majivu.

Mwingine aliacha mke na watoto ndani wote wameungua,mwingine wazazi wake na ndugu zake wote wameungua,mwingine mke wake alikua mjamzito nae pia kaugulia ndani.

Walilia  sana kupoteza familia zao.Miili ya ndugu zao ilikua imeungua na kubaki majivu.

Hivyo walichua majivu hayo na kwenda kuyazika.

Zilipita siku tatu. ngoma ya kuashikia mkutano ilipigwa na wanakijiji wote walikusa  nyika  nyumbani kwa mte.

Mtemia alikuja kabebwa juu juu.Kwenye kitu kilichotengenezwa kwa miti huku kikiwa  kina mishikio minne mbele miwili na nyuma miwili.Kati kati kulikua na kiti kikubwa alichokalia mtemi.

Watu wawili wamebeba mbele ,na wawili wengine wamebeba kwa nyuma.

Alipita  katika ya watu huku zikisikia sauti zikimtakia maisha marefu mtemi huyo.

Alifika hadi sehemu aliyotakiwa kukaa.watu waliweka migongo kama viti ,kisha mtemi akakaa.

“Nachotaka kusema hakuna yoyote ayeweza kufanya jambo ndani ya aridhi yangu bila Mimi kujua.Iwe mchana iwe usiku ulipo nipo.Kuna baadhi ya watu wanakiuka utaratibu tuliojiwekea.  

Kama kawaida yangu mtu  au watu wakienda  kinyume na mimi  basi adhabu yao kifo tena mbele ya uma.”

Mtemi aliamuru walinzi wake .wawalete baadhi ya watu walikua sio waaminifu.

Waliletwa vijana wale walioenda kuchoma kwenye imaya ya kitemi.

“Mme hawa vijana na dhani hakuna asiye jua walichokifanya.Sasa nawahukumu mbele yenu kama ilivyo kawaida yangu siku zote”

Aliongea Mtemi huku akinyanyuka.Alimshika kijana mmoja kisha akamnyofoa mkono.Wana kijiji wote walibaki kimya huku midomo yao ikiwa wazi.

Kijana huyo alipiga kelele kwa maumivu.Huku wenzake wakionekana kutetemeka.

Mtemi alinza kula nyama hiyo ya mtu,ikiwa mbichi hivyo hivyo.kisha kipande kingine  akawarushia wafuasi wake wa kichawi.

Alimtoboa macho kijana huyo kwa kutumia vidole vyake vya mikono.

Kisha alimchana chana  vipande na nyama yake wakala pale pale.

Mtemi alimsogelea mwingine huku muonekano wake ulizidi kubadilika na kua kiumbe cha ajabu.Hiyo hali inamtokeaga pindi hasira inapo mjaa.

Maana vijana hao walitaka  kumpoteza

 Duniani.

Ile anataka kumshika kijana wa pili,ilisikika sauti ikitoka  nyuma ya umati ya wana kijiji.na wote wakishituka na kugeuka kutazama ni nani mwenye jeuri ya kumzuia mtemi.

Mtemi Mwenyewe alishanga wana kijiji walipisha pembeni nakuacha uwazi ulikua kama barabara. Wakabaki wa naona mtemi na huyo mtu aliye ongea.

“Huna mamlaka hayo wewe hapa Duniani ”

Aliongea alikua ni msichana wa makamo


" haa  hahahahahah"

Alicheka Mtemi kwa dharau .kuhu akisogelea msichana huyo.

“Mwisho wako umefika  sasa ,umezidi kunyanyasa wana kijiji”

Aliongea msichana huyo.

“Binti kama una taka uwaponze wana kijiji basi endelea na upuuzi wako”

Aliongea Mtemi huyo.

Kisha msichana yule akawaamuru wana kijiji wa ondoke eneo hilo.

Lakini Mtemi alisema kwa yeyote  atakaye toka basi.kifo kinamuhusu.

Msichana huyo alipaa juu na hakuweza kuoneka kana kabisa.Baada ya dakika kadhaa ulivuma upepo mkali,kilisikika  kitu kimepua alizini hadi alizi ikatetemeka kama kuna tetemeko limepita.

Kilionekana kiumbe cha ajabu nimesimama mbele ya Mtemi.Mtemi nae alibadilika na kua kiumbe cha ajabu chenye  mapembe na mkia mrefu, na alikua ni mkubwa Mara tatu ya tembo

Mtemi alitema vitu vya njano lakini msichana  yule aliejigeuza, na kua kiumbe cha ajabu alianza kuvipangua huku akisogea kwa mtemi.

Wana kijiji walikua  wakiangalia mpambano huo.Binti yule alianza kurusha moto ukiambatana  miale ilio unguruma kama radi.

Mtemi alianza kuzidiwa  kisha akaanguka chini. Wana kijiji wote walianza kushangilia huku wakimba .

“mkombozi wetu kaja, mkombozi wetu kaja”

Binti yule aligeuka na kurudi kwenye umbo lake.

Mtemi nae akiwa pale chini alikua kaisharudi kwenye umbo lake.

Msichana huyo alimsogelea  mtemi. alitoa kitu kilicho kakaa mfano wa kisu, akamtobao mtemi .kisha akakivuta kwa juu .kilionesha kunyonya  damu kidogo ya mtemi.

Kumbe mtemi alitumia ujanja  ili kutaka  kujua ,msichana huyo anashida gani hasa. Anataka  kuchukua  uongozi wa kijiji hicho au laa. 

Alipo gundua kua lengo la  msichana huyo ilikua ni kumchukua damu tu.

Na damu ya mtemi ilikua na nguvu kubwa sana .na pia ilikua na uwezo wa kufanya mambo makubwa.

Mtemia akiwa pale chini alinyanyuka na watu wote.Walikaa kimya wakimtazama .Msichana yule alitaka  kupotea  kimazingara, lakini Mtemi alimuwahi kwa sikadi.Lililomtupa mbali ,akinyanyuka alitoa moto tena Lakini haikua chochote kwa Mtemi.

Mtemi aliunguruma kisha akapiga piga kifuani mwake, kwa kutumia mikono yake. Alirusha tena sikadi ilimpata yule 

msichana kisha akaanguka chini damu zilimtoka mdomoni na puani.

Mtemi alikua na hasira  alimsogelea msichana huyo ,aliye kua kalala pale chini. Alinyanyua mkono yake juu kisha akaikutanisha kama,kama kashika kitu ulitokea mkuki.Alirudisha mikono yake nyuma.kwa.lengo la kukusanya nguvu iliamchome msichana huyo.

Kabla hajashusha mkuki huo ,alitokea  ndege mkubwa sana .Aliefanania kama tai,kisha akampitia msichana huyo.

Mtemi alikua kajawa hasira sana. Aliwageukia wana kijiji walionekana.wakiwa na hofu,mtemi alitema  moto upande mmoja ya wana kijiji walipokua wamekaa.

Walianza kuungua  na moto huwo walitapatapa mwisho walikufa  wote.

Mtemi aligeukia  upande mwingine walipo kua wamekaa wana kijiji. Aliwatazama na wote walipiga makoti chini nakuinamisha paji la  uso  chini.

Walianza kuongea maneno ya kumtakia  maisha marefu kiongozi wao.

“ kuanzia sasa natoa  amri ,kaya  zote za hapa kijijini.Mpo kwenye kifungo kisicho  julikana muda wake.Mtakula mlo mmoja kwa siku,tena jioni tu yeyote atakaye kula zaidi ya Mara moja atakufa” 

Aliongea Mtemi huyo. Kwa sauti Kali iliyo jawa  na hasira.

“Kitu kingine  nimechoka kutembea na wanawake hapa kijijini, kuanzia sasa naanza kutembea na wanaume .Hiyo ni amri na zoezi hilo linaanza  sasa.Mimi ndio Mtemi Jafari wa Jafari,Afrika mashariki na kati hakuna anaye  niweza kwa uchawi.Ndomaana nafanya chochote nacho jisikia.”

Aliongea Mtemi huyo.Aliwaruhusu watu waondoke ,walikua na uzuni sana hasa  upande wa  wanaume  wa kijiji hicho.

Siku hiyo jioni kuna mgeni aliingia kwenye kijiji hicho. Na alionekana anaulizia ofisi za kata.

“Hodi hapa”

Alipisha mgeni kwenye ofisi hiyo ya kata.Lakini hakuweza ujibiwa na mtu .mlango ulikua wazi alisukuma na kuingia.

Ofisi ilikua inavumbi mazingira yake alikua ni machafu.Baada ya muda alikuja mzee mmoja na kumkuta mgeni huyo ndani ya ofisi hiyo.

“Habari yako kija”

Alisalimia mzee huyo.lakini huyo kija  hakurudisha salami yoyote kwa mzee huyo.Alivua muwani wake kisha akawa anamuangalia mzee kwa dharau.

“wewe nini na nani”?

Aliuliza kijana huyo.

“Mimi naitwa Mabula ni mtendaji wa kijijini hiki”

Aliongea yule mzee.

“Oooh mtendaji wa kijiji, mbona mchafu mchafu sana”

Aliongea kijana  huyo.Nae alijitambulisha alikua anaitwa Tomasi ni Mtendaji wakata  Mpya aliye kuja kulipoti.

Alikua nikijana wa sasa mwenye dharau na alikua ni bishoo. Alipelekwa sehemu ya kupunzika na mwenyeji wake mzee Mabula.

Ilifika majira ya saa  mbili za usiku.Tomaso alienda kupata chakula cha usiku kwa mzee Mabula.

Walipo maliza kula walikua wamekaa wakiongea mambo ya ofisi yao .Mara ghafla walikuja mabinti wawili walifika nyumbani hapo kwa Mabula.

“Mzee tumeagizwa na Mtemi,kusema mida ya saa nne  umpeleke mgeni wako anashida nae”



Walisema mabinti hao alafu wakaondoka .

“Mzee wangu huyo Mtemi anashida gani na mimi”

Aliuliza Tomasi.

“Kiukweli kijana wangu Mimi sijui anacho kuitia, sema Mtemi wetu ni hatari sana”

Alisema Mzee Mabula.

“Hatari kivipi kwangu atanyooka tu.Tu taenda kumsikiliza tujue anashida gani”

Alisema Tomasi. Lakini mzee Mabula akimuangalia sana Tomasi.Na alikua kaishaelewa shida ya Mtemi ilikua ni nini.

Mzee alimuelezea kijana huyo matatizo yote ya kijijini hapo.Ikiwemo na hilo la  kula mlo mmoja kwa siku.Lakini kuhusu tamko lake la kutaka  kulala na wanaume kijijini hapo, hakuweza kumwambia kabisa.

Muda ulipofika waliondoka na kwenda kwa Mtemi.Walipofika   walimkuta Mtemi kakaa nje ,na baadhi ya wachawi wenzake walionekana kunajambo wakijadiliana.

“Kaeni hapo kwenye kigogo hicho”

Aliongea miongoni mwa kijakazi cha Mtemi.Walikaa mzee Mabula na Tomasi,lakini baada ya nusu saa  alikuja Mtemi huku akiwa anacheka.Mzee Mabula alipo muona  alipiga  magoti huku sura yake akiiangalizisha chini.

Lakini kwa upande wa Tomasi alikua kasimama  akimtazama mzee Mabula kwa kitendo hicho.

“Kijana piga magoti”

Aliongea Mzee Mabula.

“Muache tu kijana mtanashati,Usimchoshe kwa sasa maana anakazi nzito ya kufanya usiku waleo”

Aliongea Mtemi huku akionesha tabasa mdomoni mwake.

“Ni kazi gani hiyo mzee unayotaka  kunipa”?

Aliuliza Tomasi kwa mshangao.

“Kijana acha haraka utajua tu.Kwa leo  utalala  hapa kwangu”

Aliongea Mtemi Jafari.

“Nilale hapa kwako?,kwa mzee Mabula nimepatiwa chumba pale”

Aliuliza Tomasi.Mzee Mabula alimwambia Tomasi asijali alale tu kwa Mtemi. Tomasi alikubali ,Lakini moyo wake ulikua na wasi wasi sana.

Alipelekwa kwenye chumba kilichokua kimeandaliwa kwa ajili yake.Mtemi alibaki nje aliongea na Mzee Mabula.

Baada ya lisaa limoja, Tomasi aliona mlango ukisukumwa  na alitaamaki ,kumuona Mtemi akiwa kifuwa wazi  akiwa kavaalia penzi.

Mtemi alifika hadi pale mahala alipo kuwa kalala Tomasi.Ali panda na kumwambia Tomasi asogee nae alale.

“Mzee hiyo kazi unayo taka kunipa,  ni lazima uongelee hapa si ukae hata pale kwenye kigoda”?

Aliongea Tomasi.Mtemi alicheka kidogo.

“Kijana kazi nayotaka kukupa  ipo hapo hapo na si sehemu nyingine”.

Aliongea Mtemi huku akiishusha kaptula yake.Mara alizima kibata kilichokua kikiwaka, na kuleta muangaza ndani.Kulibaki giza  ambayo  hata ukodoe macho vipi hauwezi kuona kitu chochote.

“Wewe mzee kuna nini jamani”

Alisikika Tomasi akipiga kelele Mara zikazima ghafla.

Kesho yake palipo kucha Mzee Mabula akiamka, na kwenda kwenye chumba alichokua kamuandalia Tomasi.

Lakini cha ajabu alikuta mzigo ya Tomasi haipo ndani.

“Mke wangu njoo”

Aliita mzee Mabula.Mkewe haraka alifika .

“Abee mume wangu”

Aliitikia mke wa mzee Mabula.

“Mke wangu mlitoa mizigo  ya yule kijana, humu ndani”?

Aliuliza mzee Mabula. Lakini mkewe alisema hakuna aliieingia kwenye chumba hicho.

Walitoka nje,lakini mzee Mabula alihisi Tomasi atakua alirudi asubuhi, na kuchukua  mizigo  yake na kuondoka kijijini hapo.

Ilikua majira ya saa  saba za mchana ,Mzee Mabula alikua kakaa nje ya nyumba yake,akijiuliza  kijana Tomasi ni wapi alipoelekea.Alitaka  kunyanyuka na kwenda kwa Mtemi .Mara ghafla alitokea  Mtemi na wafuasi wake kimazingara.

“Mabula yule kijana yuko wapi”?

Aliuliza mtemi akionekana ni mtu ambaye mwenye jaziba Kali.Mzee Mabula alibaki kalitoa jicho lake kwa mshangao.

“Lakini Mtemi ,wewe ndio alikua kwako,?Mimi sijui kabisa, na hapa ndio nilikua najianda nije kwako.Maana hata sisi tumeamka asubuhi hatukukuta mizigo yake”

Aliongea Mzee Mabula akionekana kujawa na wasi wasi.

“Usinitanie kabisa ,sasa adhabu yako ni hii”

Aliongea Mtemi kisha akamkata kichwa Mzee Mabula. Kwa kutumia mkono yake iliyokuwa na kucha ndefu.

Kisha akamchana chana na nyama akawarushia  wafuhasi wake.

“Sasa nawaamulu mtafuteni kijana huyo pande zote za dunia,Na msipo mleta hapa msirudi.Na mkimpata wote nawapa cheo kwenye ushilika wetu wa kichawi.

Wafuhasi hao walipokea akigizo hilo kisha wakapotea kimazingara. Na mtemi  nae apotea na kurudi kambini kwake.



Mtemi akiwa kwenye ngome yake alikua hajatulia,alionekana ni mtu mwenye wasi wasi na jambo flani.Alikua akitembe huku na kule.

Upande wa Hasna alionekana kalala kwenye chumba chenye  Giza.Na kulikua na kadirisha.Ndika kalikua  kakipitisha mwangaza ndani ya chumba hicho.

“Pole dada utapona sahizi naona una endelea vizuri”

Aliongea binti yule aliyetolewa kafara na baba yake kwenye ile gest aliyofikia Hasna.

Hasna alipigwa fataki la  kichawei na mmiliki wa sehemu ya chakula.Lililo mfanya apoteze fahamu, lakini akiwa pale chini kalala alianza kupata kumbukumbu ya toka ana olewa hadi siku anakufa akiwa kwa Zuberi.

Hasna alipoteza fahamu ya patayo masaa kumi na mawili,na alipewa msaada na binti ambaye ni mfu  anae ishi. Alimchukua na kumpeleka kwenye chumba. Ambacho kilionekana kuwa ni stoo , na chumba hiyo alikua akiishi binti huyo.

Kilikua kichafu na kilikua kikinuka sana.Hasna alishituka na kujikuta kalala sehemu asiyo ifahamu na alikua hana kumbukumbu ya kilicho kilichimtokea.

Aliangaza pembeni alimuana mtu  kakaa pembeni yake.Hasna alishituka kidogo kisha akataka  kunyanyuka, lakini alishindwa baada ya kuisi  maumivu makali  miguuni.

“dada niko  wapi hapa ,wewe ni nani na nimefanya nini”?

Aliuza Hasna. Yule msichana alimuelezea Hasna yaliyo mkuta yote mpaka kua hapo.

"Dada kuna tiba yako pia nimeelekezwa na mwana mke mmoja wa makamo aliye jitambulisha kua wa ni mama yako"

Alisema binti huyo.

“Tiba yangu na mbona Mimi sina mama”?

Aliongea Hasna huku akiwa anakumbuka  mambo aliyo kua akiyaona kipindi kapoteza fahamu.Ya nyuma yote na kumbu kumbu zilikua zimeanza kumrudi ,ambazo alikua kapotezewa na wale wa chawi  kwa lengo la kuto waumbua pindi wamrudishapo Duniani.Kwa hiyo alipo ambiwa kuhusu mama yake alijumbuka mama yake akijufa miaka mingi iliyopita.

“Ndio najua hauna mama lakini nilitokewa na mzima wa mama yako.Ukasema  nikikusaidia basi na mimi atanisaidia ni rudi tena kuwa hao maana Kwa sasa Mimi ni Mfu nae ishi”.

Alisema msichana huyo.Huku Hasna akiwa ana msikiliza kwa makini.

“Najua hali yako kuwa wewe kwa sasa si binadamu wa kawaida.Sasa huo Masada unatakiwa ni upi"?

Aliuliza Hasna.

“Kupona kwako na kurudi kwenye hali yako,maana hapo hauwezi kusimama wala kutembea tena.Hivyo inatakiwa ipatukane damu ya baba yako ndio itakayo kuponya”

Aliongea binti huyo.Hasna alivuta na kushusha punzi kwa kasi kisha akatulia sekunde kadhaa.

“Dada baba yangu unamjua?.Baba yangu ni mtu  hatari sana sidhani kama damu yake utaweza  kuipata”

Alisema Hasna.Huku akionesha kukata  tamaa baada ya kusikia tiba yake ni damu ya baba yake.

“Dada usiwaze kuhusu damu yenyewe ineishapatikana”

Aliongea msichana huyo.Huku akitia kichupa kidogo kilichokua na damu hiyo.Hasna alishangaa sana.

“Dada damu ya baba uneipataje”?

Aliuliza Hasna Kwa mshangao.

Msichana huyo alianza kumuhadithia jinsi ilivyokua.

?.            ?.           ?.        

Baada ya mzimu wa mama yako kunitokea ,ulinipa maelekezo yote kuhusu wewe na maelekezo yote jinsi ya kumpata  baba yako.

Nilienda kijijini kwenu nikiwa kwenye umbo langu la  kawaida .Nilimjuta baba yako ambaye ni Mtemi wa kijiji hicho.Alikiwa na wanachi wake alikua akiwapa adhabu ya kifo.

Basi ndio na mimi nilitokea  kisha nikampinga kwa kitendo hicho anachofanya.Mtemi huyo alikasilika sana tukaanza kuoambana nilionekana kumzidia.Lakini kumbe alikua akipumbaza nione kuwa namuweza,baada ya kujua lengo langu ni nini kwake.Ndio alipoamsha nguvu zake zote nakuanza kunishambulia,Alinizidia lakini ile anataka kunimaliza kabisa.Ulitokea mzimu wa mama yako kwa umbo la  ndege,na kunibeba tukapaa juu.

Tulipo fika hapa  tuliapanga shambulizi lingine.Maana Mtemi Alikua ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kichawi.

Mama yako alitoa mbinu nyingine.Alinibadilisha na kuwa kijana mtana shati. nikarudi tena kwenye kijiji hicho kama mtendaji wa kata mpya, niliyenda  kuripoti.

Nilikutana na mzee mmoja Alikua ni mtendaji wa kijiji.Nilianza kumletea dharau na kumpa maneno ya kashifi,ili achukie  na kuzagaza maneno kijijini hapo,Lengo langu ya mfikie Mtemi najua yakinfikia tu basi lazima aniite na akiniita basi kazi yangu ingekua nyepesi.

Lakini nikiwa nayapanga hayo ,kumbe Mtemi siku hiyo alitangaza kutembea na wanaume. yani kuwaingilia kinyume na maumbile.

Nasiku hiyo aliwatuma vijakazi wake wawili na kunitaka niende nyumbani kwake.Nilienda na mzee Mabula, Nilipo fika Aliniambia leo  inatakiwa nilale kwake.Nilijivunga vunga kukataa lakini mzee Mabula nae alinishawishi.Nikawa sina jinsi nikakubakubali.

Aliita vijakazi wake na kunipeleka sehemu niliyo  andaliwa. Huku yeye nikimuacha nje akizungumza na mzee Mabula.kwa kuwa nilikua najua lengo lake ni nini kwangu.

Nilipo ingia ndani kuna dawa alinipa mama yako.Niliichukua na kuipaka kwenye viganja vya mikono yangu.

Baada ya muda mtemi aliingia na kuvua  buksa yake kisha akazima kibatali.Alinifata nakuanza kunivamia kwa lengo la  kutaka kuniingilia kinyume na maumbile.Nilipiga kelele huku nikimshika usoni mwake,kama mtu  anae jiokoa kwenye tukio hilo.

Nikifanikisha kumgusa macho na puani.Akawa kaivuta dawa hiyo niliyo  ipaka kwenye vinganja vya mikono . baada ya dakika kadhaa alianza kuishiwa nguvu.Na akalala usingizi mzito.

Hapo Ndipo nililifanya zoezi la kuichukua damu ya Mtemi. Nilipo maliza  mama yako alikuja kimazingara na kisha tukaondaka sehemu hiyo kimazingara.

?.              ?.            ?

Alimaliza  kutoa simulizi jinsi alifanikiwa kuchua damu.

“Pole ana dada,sijui hata cha kukupa"

Alisema Hasna.Lakini dada huyo alimwambia Hasna asuwaze kuhusu cha kumlipa .Alichomuambia mama Hasna kinatosha na nifura kubwa sana kwake kurudi na kua binadamu.

“Hasna unakibarua kizito sana, baada ya kupata matibau, unatakiwa kurudi kwenu ili uwasaidie wana kijiji.Baba yako anawatesa sana hakuna amani.Na hiyo ni lazima,ni agizo alilo  niachia mama yaoko”



Aliongea binti huyo.Alipo maliza alianza kumpatia Hasna matibabu.Kwa kufata maelekezo aliyopewa na mama yake Hasna.

Zilipita siku kadhaa Hasna alikua kapata nafuu.

Upande wa pili wa katika mji wa Kahama.Alionekana  Jimmy akiwa na baadhi ya washilika wenzake wa kichawi.

“Jamani tumeitana hapa tujadiliane kuhusu hii nafsi ya Zuberi, pia kuhusu Jafari (baba Hasna).

Aliongea mtu  miongoni wa washilika hao.

Zuberi alionekana kuwa tishio kwa sasa ,baada ya kuendelea kuuwa  watu wa karibu kwa wale wote walio shiliki hadi yeye kuingia chama hicho cha kafara.

Walijadili  pia kuhusu Jafari, ambaye aliwenza kuwasaliti na kuunda ushilika wake.Ambao aliondoka na watu wengi sana.

“Mi naona kuhusu Zuberi,Tumrudishie mwili wake hapo ndio itakua rahusi tumuondoe kabisa Duniani ”

Alitoa wazo mshilika mmoja wa kundi hilo ka kafara.

“kweli hilo ni wazo zuri  sana, lakini sasa mwili wa Zuberi utakua umeisha halibika”

Alichangia mshilika mwingine.

Walifikia  muhafaka kuwa Zuberi wa mrudishe kwenye mwili wake ,ili waweze kumua kwa uwepesi.

Pia kuhusu Mzee Jafari waliona swala hilo waachane nalo kwa sasa.Watalifanyia kazi baada ya la  Zuberi kuisha

Zilipita siku kadhaa walifanikiwa kuurudisha mwili huo kwenye nafasi yake.

Mwili wa Zuberi ulikua umehalibika sana,Ulikua umeisha oza na pia Alikua ananuka sana.

“Jamani ndio nimekua hivi”

Alikua ni Zuberi alianza kujishanga baada ya kuona yuko vile.

“Ha ha ha ha majirani msaada”

Zilikua kelele za mama yake Zuberi. Baada ya kumuona  Zuberi akiwa kwenye hali ile.Lakini haikuwa lahisi kumfahamu kwa jinsi alivyo halibika.

Pia Zuberi alikua ajagundua kama mwili wake umerudi.kilicho sababishe agundue kuwa mwili umerudi nipale mama yake, alipo muona na kupiga kelele.

Kwa siku zote Zuberi ndio yalikua makazi yake,kwenye nyumba ya mama yake kwa muda wote huwo.Toka isemekane kafari Dunia.Na kulikua hakuna mtu  yoyote ambaye anaweza kumuona.Kutokana na na mwili wake kuzikwa na kubaki nafsi yake ikitembea.

“Mama Mi mwanao  Zuberi”

Alisema Zuberi huku akiwa kasimama mlango mama yake asiweze kutoka nje.

“Mama usifanye lolote watu watajaa,tulia mama yangu nikuhadithie  yote mi sijafa,wala baba hajafa”

Aliongea Zuberi .Mama yake  alibaki akishangaa tu maana alikua ni mtu  wa ajabu kama zombi vile.

Mama yake alikua nae chini lakini alikua na wasi wasi na hofu kubwa sana.

Zuberi alimuelezea mama yake mambo yote yalivyo kuwa.

“Mwanangu Zuberi tamaa ya maisha sio nzuri ona  sasa ulivyotoa roho za watu,umepata faida gani”?

Aliongea mama Zuberi huku akiwa analia.

“Sasa baba yako yuko wapi ”?

Aliuliza mama Zuberi.

“Baba yuko kwenye mgodi wangu.lakini ilikumsaidia baba inatakiwa kwanza Mimi nitoke kwenye hii hali mama”

Aliongea Zuberi.Mwili wake ulikua unatokwa na funza.

“Sasa hiyo hali tunafanyaje iliuondokane nayo”

Aliuliza mama Zuberi.

“Mama kuna binti yule niliyemuoa Mara ya mwisho sijui unamkumbuka”?

Aliuliza Zuberi.

“Ndio namkumbuka si alishafariki”?

Aliongea Mama Zuberi.Lakini Zuberi aliendelea kumuelekeza mama yake,kua binti huyo hakufa yuko hai  na akimpata binti huyo basi.Yeye ndiye mwenye uwezo wa kumponesha.

Alimuelekeza kijiji anacho patikana binti huyo ,ambaye ndio Hasna.

Lakini Zuberi alimwambia hana hakika  kama binti  huyo  yuko kijijini.Maana walimtupa mkoa wa kigoma kwenye kijiji cha Shunga.

Basi Zuberi alimpa mama yake jina la  shangazi ya Hasna.  kama atamkosa Hasna basi shangazi yake anaweza jua cha kumsaidia.

Napia alimuomba mama yake ajitahidi  kufanya haraka hata ikiwezekana aanze safari leo .Maana muda wowote anaweza kuuliwa na washilika wenzake.

Kweli mama Zuberi aliondoka na kuelekeaKijiji hicho cha Mbika alifika salama ,Alianza kwa kumuulizia Hasna.

"Kijana habari za sahizi”

Alisalimia mama yake na Zuberi.

“Salama bibi shikamoo”

Alisalimia huyo kijana.

“Marhaba kinaja wangu.Samahani nilikua napaulizia kwao na binti mmoja anaitwa Hasna”

Aliuliza mama Zuberi.Lakini yule kijana hakuweza kujibu swali aliloulizwa na mama yake Zuberi. Badala  yake alimtazama  kwa kumsusha na kumpandisha.

“Bibi kama hauna kingine  cha kuniukiza  Mimi naenda”

Aliongea kijana huyo huku akizipiga hatu.Mama yake Zuberi alibaki kushangaa mbona kijana huyo hakumjibu swali lake badala  yake kaondoka.

Kitu kingine  kilicho mshangaza mama huyo.Nikuona  kijiji kimepoa hakuna watu kabisa.

Aliendelea kusonga mbele huku nacho yake akiangaza huku na kule.

Lakini macho yake yaligota kwenye nyumba moja.baada ya kumuona mama mjamzito akiangakia huku na kule.

Mama zuberi alifika hadi mahara hapo,nakuanza kumsaidia mama huyo.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG