Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

THE WORLD HATES ME (DUNIA INA NICHUKIA) - 3

   

Simulizi : The World Hates Me (Dunia Ina Nichukia)

Sehemu Ya Tatu (3)


upande wa beka


mida ya saa tisa usiku tangu beka awekewe mashine ya oxegen , kichwa cha beka kilikuwa kwenye maluweluwe kabla ya kuzinduka alikuwa akiona kama sura ya mtu alie mfahamu ikija na kupotea hakuikumbuka vizuri sura hiyo ..akawa anaona mauaji ambayo hakukumbuka ambayo hakukumbuka aliyaona wapi picha ya mama yake ikapita kichwani mwake....hapo hapo akazinduka .

"mamaaaa" alipiga kelele beka baada ya kuzinduka, muuguzi akaenda kuwaita madaktari wakaja kumtolea ile mashine ya kupumulia.

"unaitwa nani mtoto mzuri?" aliuliza daktari wakike baada ya kujua beka amezinduka na ana uwezo wa kujielezea ili waandike riport maana yule alie mleta hakutoa riport yoyote yeye alidanganya kuwa amemuogota beka akiwa kapata ajali na siye yeye alie mgonga.

"..mmh...b.,beka kwani nipo wapi hapa ..." beka alisema huku akijilazimisha kukumbuka mambo.

"ah beka ulipata ajali jana ...unaweza kuelezea ilivyokuwa?" alisema yule doctor wakike

"hapana sikumbuki mama... mi nakumbuka mara ya mwisho nikiwa nyumbani nyegezi chumbani mwangu nilisikia wazazi wangu waki uwawa kwa kupigwa risasi ... na mimi nikalala chini na kuchungulia kwenye uwazi uliokuwa chini ya mrango na hapohapo nikasikia milipuko ya risasi na risasi nyingi zikatoboa mlango ule" alisema beka. masikini yamungu

beka alikuwa kapoteza kumbukumbu ya maisha yake, tukio analolisema beka nitukio la mauaji ya wazazi wake lililotoke nyegezi miaka kumi iliyo pita. beka kipindi anapata ajali ile kichwa chake kilikuwa kimevurugika na alipo gongwa na gari alitupwa na kupiga kichwa chini, hii ikapelekea kuaribu kilakitu kwenye kichwa cha beka, na kumfanya ajione yupo kwenye lile tukio lililotokea miaka kumi iliyo pita.

dakatari alishangaa kwani yule baba alie mleta hosptal alisema beka kagongwa gari na beka anasema mara ya mwisho alikuwa kwenye tukio la mauji ya wazazi wake, doctor akaondoka na kurudi ofisini ambapo alipiga simu kutoa taarifa ile. beka akaendelea kulala kitandani huku akijiuliza ninani alie uwa wazazi wake beka akawa anatoa machozi akimlilia mama yake, yaani beka kumbukumbu zake zilirudi nyuma na kuambatana na tukio la mauaji ya wazazi wake.

mganga mkuu aliingia asubuhi kwenye wodi ya beka na kumuuliza maswali beka juu ya ajali yake beka akajibu vile vile kama alivyo mjibu doctor wakike jana usiku . mganga mkuu ikabidi achukuwe kifaa maalumu na kumpima kwani alishaanza kuwa na wasiwasi juu ya tukio la beka .

doctor baada ya kuupima ubongo wa beka alitambua kitu na akachukua file na kuanza kuandika vitu na baadae akamuita pembeni doctor wakike na kuongea nae faragha...

"ina onesha masaa kadhaa yaliyo pita ubongo wa beka uliweza kutambua kitu cha mda mrefu kidogo... na baada ya kugundua hicho kitu akiri yake ikachanga nyikiwa....na mambo anayo ya sema hapa ni mambo ya nyuma kidogo.. ..na anaonekana hanakumbukumbu nzuri" alisema mganga mkuu na kumuambia mwenzake aendelee kumpa beka matibabu mengine muda huo wakitafuta njia ya kutatua tatizo.


****


upande wa edward


edward na watu saba wakafanya taratibu zote za kuchukuwa mwili wa yona, na edward akaamua kwenda kuiangalia kwanza familia yake ambapo alimkuta mke wake akiwa amesha zinduka lakini alikuwa na hari nzuri kidogo, peter nae alikuwa kapata nafuu mama yona alivyo sikia yona kafariki alilia na kupoteza fahamu ikawa ikawa patashika nyingine lakini baadae alipo mwagiwa maji akapata fahamu lakini aliendelea kulia kwa uchungu, edward akaamua kuondoka ili wapeleke mwili wa yona nyumbani peter na mama yona wakabaki kwani walikuwa bado hawajaruhusiwa na joyce akabaki na mama yake aliendelea kuombeleza mpaka ikawa kero kwa wagonjwa wengine,

edward akachukua mwili ambao uliwekwa kwenye jeneza na kupakiwa kwenye toyota na wakaanza kurudi nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

taarifa zilikuwa zimesha zagaa kwa dungu jamaa rafiki na majirani watu walikuwa wamejaa nyumbani kwa edward huku minong'ono mingi na mtazamo wa kutokuamini kilichotokea ukitawala, "et, beka ndio kafanya balaa hili.... japo alikuwa anateswa lakini siamini ... beka hawezi kupiga familia yote" yalikuwa ni maneno ya watu walio kuwa eneo la msiba,

baada ya edward kukaa na wazee ndipo wakaamua kuwa yona atazikwa siku ya pili jioni . edward akaona ule ndo ulikuwa wakati muafaka wa yeye kupeleka picha ya beka kwenye mikono ya jeshi la polisi edward alifika kuiwasilisha picha kwa yule askari, afande hussen alipopewa picha ya beka alishtuka na kuanza kuvuta kumbukumbu,

"huyu kijana mbona aliletwa hapa akiwa mahututi jana usiku kabla ya nyie kuja alikuwa kagonwa na gari" alisema hussen na kumshangaza edward

"mmh sasa itakuwa kilimkuta nini ...maana mi nilivyo mkimbia sikumuona tena"

"tulimpa pf3 akapelekwa bugando ... kwakuwa hili ni tatizo kubwa acha niwasiliane na vyombo vya habari atangazwe na sisi twende tukamtafute bugando maana ameshakuwa muuaji" hussen akachukua radio call akampigia kwanza mkuu wake wa kazi na kumueleza na mkuu wa kazi akaruhusu taarifa hiyo itangazwe , hussen akachukua simu na kuwapigia wamiliki wa vyombo vya habari na muda kidogo akakata kisha akaipiga picha ile picha ya beka kupitia simu yake alipo maliza akaingia kwenye mtandao na kuituma kwenye blog flani ya tv.

na muda kidogo askari pamoja na edward wakaingia ndani ya gari aina ya toyota na kuanza safari ya kwenda kumtafuta beka bugando

dakika kumi na tano walifika bugando na kuwaonesha picha ya beka walinzi wa kampuni la K SECURETY walio linda hapo bugando na kuwaambia wakimuona kijana aliekuwa kwenye picha wakimuona wamkamate na polisi wakaanza kuingia ndani ya bugando.


****

upande wa beka


beka aliendelea kuwa kitandani huku akiwa anasumbuliwa na maluweluwe kichwani mwake beka aliinuka na kujaribu kutembea akajiona kama anajimudu ila alisikia maumivu ya kichwa na mgongo beka akarudi kukaa kwenye kitanda , kitanda cha jirani ya beka kuna babu aliekuwa na radio na muda huo ilikuwa on...

"taarifa ya habari kijana beka john mwenye umri wa miaka kumi na nne anatafutwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumuua binamu yake yona edward na kujeruh watu wa tatu wa familia ya edward"


beka alishituka kuisikia radio ikitoa taarifa ile, beka alihisi kulitambua tukio linalo taarifiwa na radio na alihisi kumfahamu YONA EDWARD, kingine kilicho mshituwa ni kutambua jina lake kuwa ni yeye aliekuwa akitafutwa beka akahisi kuchanganyikiwa


"hah yani mimi jana wazazi wangu ndio wameuliwa then leo et me ndo natafutwa sijui nime muua yona ambae simjui ...hii ni njama" beka alijisemea moyoni huku akiwa hakumbuki hata kidogo kuwa jana alisababisha balaa na kumuua yona, hakika akiri ya beka ilikuwa kwenye ulimwengu wa miaka kumi iliyo pita.

beka akahisi ile ilikuwa njama ya mtu alie ua wazazi wake ..akiri ya beka ikamshauri beka atoroke hosptalini pale , beka hakupoteza mda akavaa tshirt yake kwa kuigeuza maana ilikuwa na damu alivyo igeuza ikasaidia damu kuto onekana akavaa viatu na kuanza kutoka wodini,

"mwenzetu unaenda wapi?" aliuliza kaka mmoja ndani ya wodi ile,

"ah naenda kula upepo najisikia joto "alisema beka na kutoka na kuanza kutembea kuelekea kwenye lifti .

beka alifika kwenye sehemu ya kusubiri lifti akamkuta dada aliekuwa kampa mgongo nae akisubiri lift huku dada akiwa anajifuta machozi kwa kitambaa, beka alikuwa nyuma ya dada huyo muda mchache lift ikaonekana mbele yao na yule dada akaingia kwenye bila kugeuka nyuma na beka akaingia na mlango wa lifti ukafunga ,yule dada alipo geuka alishtuka kukutana na sura ya beka huyu dada alikuwa ni joyce binamu yake."mamaaaaaaa" joyce alipiga kelele na lift ilikuwa imeanza kushuka .


***

muda huu ulikuwa ni mda wa chakula cha mchana na manesi na baadhi ya madoctor walikuwa sehemu ya kulia chakula na eneo ilo kulikuwa na tv na muda huo tv ilikuwa inatangaza taarifa ya kutafutwa kwa beka..."...aidha mkuu wakituo cha polisi mabatini amesema kijana huyo mara ya mwisho alipitishwa kituoni akiwa mahututi alikuwa kapata ajari na alipewa PF3 na kupelekwa bugando,,,,kwa mtu yoyote atakae fanikiwa kumuona kijana huyo apige na hii namba atoe taarifa " ilisema tv ile "hah huyu kijana yupo kwenye wodi yangu" alisema nesi mmoja aliekuwa anakula chakula eneo lile baada ya kuiona picha ya beka kwenye tv. na hapohapo akatowa simu yake ya mkono na kupiga namba zilizokuwa kwenye kioo cha tv na kupiga bahati nzuri namba aliyo piga ilikuwa ni ya hussen ambae aliingia bugando na wenzake .

"Hallow me ni nesi nafanya kazi bugando natoa taarifa kuwa yule kijana beka anae tafutwa yupo kwenye wodi yangu ghorofa ya nane" alisema yule nesi .

"whaat... sasa sikia mi nipo ghorofa ya tano nakuja...nenda kwenye wodi yake mumzuie asitoke"alisema afande hussen huku akipandisha ngazi akiwa na askari wenzake pamoja na edward wakawa wanakimbia kupundisha ngazi.

nesi nae aliondoka na wenzake kwenda kwenye wodi ya beka...nesi alishangaa kumkuta beka hayupo alipoulizia sana baadhi ya watu waliokuwa sehemu ya mapumziko walisema walimuona akiingia kwenye lifti . nesi haraka akatoa simu na kumpigia afande..

"afande hayupo ila yumo kwenye lifti...ana shuka chini" alisema nesi .......



afande alikuwa amesha fika ghorofa ya saba alipo enda kwenye sehemu ya kusubiri lift akabonyeza kitufe kilicho kuwepo ukutani na kwa ajili ya huduma ya lifti na ndipo akatambua kuwa lift imesha pita. hussen na wenzake wakaanza kushuka ngazi yule hussen kwa kutumia radio call akampigia na kumuomba yule nesi atoe taarifa ya tukio lile na lifti isimamishwe haraka "sawa lifti itasimamishwa muda sio mrefu" alisema yule nesi .. askari wakaanza kushuka chini wa muwahi beka kwenye lifti....


****

beka & joyce ndani ya lifti...


joyce alishituka sana kumuona beka aliekuwa na bandeji kichwani joyce alijua tayari kifo chake kime fika kwani kama beka alimua yona basi na yeye alikuwa anafuata kwa jinsi kina joyce walivyo kuwa wanamtesa beka na kumtukania mama yake kila siku joyce alijua beka kaja kulipa kisasi ., joyce akapata mshituko na akapoteza fahamu na kuanguka na kupiga kichwa kwenye kuta za lifti ile.

beka alishangaa sana hakujua msichana kwanini alishituka na kupiga kelele na kisha kupoteza fahamu na kuanguka....beka hakuwa na kumbukumbu hata kidogo akashindwa kumtambua kabisa joyce alie anguka chini kengele ya hatari ikagonga kichwani mwa beka akahisi kuwa yule msichana kamuongezea matatizo kwani kama joyce angeonekana kaanguka pale chini kapoteza fahamu na yeye beka yupo ndani ya lifti ile ingekuwa hatari na beka angeshindwa kutoka ndani ya hospatal , beka alipo angalia ndani ya lifti ile akaona pembeni kulikuwa na kiti ambacho huwa ni cha mlinzi lakini muda ule mlinzi hawa kumkuta ndani ya lifti ,,, beka akapata wazo akamuinua joyce na kumkalisha kwenye kiti beka akawa kama anakumbuka kuna sehemu aliwahi kumuona mschana huyo beka alipo tazama uso wa joyce akaona alikuwa kaumia kwenye paji la uso wa joyce... kichwa cha beka kikaanza muluweluwe huku picha za mtu akiwa kwenye vurugu ya watu wengi ikipita kichwani mwake ikiwa kwa muonekano wa nagetive kichwa kikaanza kumuuma beka akafungua mkoba wa joyce na kukuta tishirt ya peter beka akaona bora aivae kwani yake ilikuwa na damu akavua yake akava ya peter hii tishirt ni ile aliyokuwa kaivaa peter siku ya tukio la beka. beka akahisi kuitambua tishirt ile .. na hapohapo lift ikasimama mlango ukafunguka beka alivyo gundua yupo ghorofa namba tatu na muda huo hakuona dalili ya mtu kutaka kuingia kwenye lifti akaamua kutoka akamuacha joyce akiwa amekaa kwenye lifti hana fahamu na lifti ikaendelea kushuka chini ,beka akaangalia eneo lile akaona watu wachache wakiwa wamekaa kwenye mabechi sehemu ya mapumziko lakini hapohapo akatupia macho yake kwenye ngazi zilizokuwa zinaenda ghorofa ya nne akaona viatu na miguu ya wale askari wakipandisha juu kuelekea ghorofa namba nne [muda huo askari walikuwa bado hawajapigiwa simu na yule nesi] beka akajua kuna hatari beka akaanza kuondoka haraka kuelekea ghorofa namba mbili ,.,.

beka alipo fika namba mbili akanyoosha njia iliyokuwa inaelekea carteen akavuka ile carteen ya bugando na kuanza kuelekea kwenye geti la kutokea nje....


****

maaskari..


hussen na askari kipindi wanaendelea kushuka wakiwa na edward mara radio call ya yule hussen ikaanza kukoroma hussen akapokea..."afande nakujurisha kuwa lifti imesha simamishwa ipo ghorofa namba mbili wahini " ilisema sauti ya nesi ..."sawa tunawahi..." alisema yule afande hussen huku akiongeza speed kushuka kwenye ngazi "...wahini maana mlango wa lift umelokiwa na hawezi kutoka nje...wahini siunajua mtumwenyewe mgonjwa asije akafa kwa kukosa pumzi" alisema nesi akiwa anajua beka amefungiwa kwenye lift na hawezi kutoka...

"sawa mmefanya kazi nzuri ahsante kwa ushirikiano.." alisema afande hussen na kuanza kushuka huku akiruka ngazi mbili nyuma akifuatiwa na edward...moyo hussen ulikuwa na furaha isiyo pimika kwani alijua lazima angepandishwa cheo kwa kitendo cha kumkamata beka ambae alijaribu kutoroka. na edward nae kichwani mwake akaanza kupanga mipango ya kumua beka pindi akikamatwa na polisi edward alipo kumbuka kuwa beka amemuuwa yona hasira zilizidi kumpanda...

askari walifika kwenye chumba namba mbili cha lifti wakazunguka eneo la lifti na afande hussen akaenda kubonyeza kitufe ukutani kwa ajiri ya kufungua mlango wa lift lakini mlango haukufunguka akatoa radio call yake na kupiga kwa nesi...."eeh tumefika mbona mlango haufunguki?" aliongea afande hussen kwa mshangao kwa mshangao..

" ..ah tuli urock kwaajili ya kuto ruhusu mtu mwingine kuingia ...utafunguliwa sasa hivi " ilesema sauti ya yule nesi.

edward na askari wakawa wanakodolea macho mlango wa lifti na mara mlango ukaanza kufunguka na mara ukafunguka kabisa...

kila mtu alipigwa butwaa hawakumuona beka na cha ajabu walimuona msichana aliekaa kwenye kiti huku shingo yake ikiwa imelalia upande mmoja..."mh" afande hussen aliguna na kuanza kumsogelea msichana huyo na edward nae alimfuata nyuma afande .."mbona kama huyu msichana kama amekufa" alisema afande hussen na edward akasogea kumuona msichana huyo "mungu wangu....joyceeeee" alipiga kelele edward baada ya kungundua ni mwanawe "joyce mungu wangu..beka amekufanya nini mwanangu amka.." aliendelea kupiga kelele edward huku akimtikisa mwanaye polisi wote pamoja na hussen wakachanganyikiwa kwanza wamemkosa beka...pili kwenye lifti alimokuwemo beka wamekuta msichana wanaezania amekufa ..cha ajabu zaidi huyo msichana ni mtoto wa edward...beka akaanza kuwa picha mpya kwenye mtazamo wa maaskari ..."mwanangu,. beka amekukamataje na kufanyia haya kwenye lifti....na kawezaje kutoka kwenye lifti na wakati mlango ulikuwa umerockiwa..no beka ni jini sio mtu huyu mtoto mzimu beka ni jini!" alisema edward huku akiendelea kulia na kuhisi beka ni mzimu muda huo watu waliendelea kujaa eneo lile.

hata maaskari walianza kuhisi kama anavyo hisi edward kwani na wao walijiuliza beka beka katokaje kwenye lifti wakati mlango ulikuwa umerokiwa na wao wakahisi labda beka alikuwa jini [kitu ambacho hawakujua askari nikwamba beka alishuka kwenye lifti akiwa ghorofa ya tatu kabla lift haija rokiwa] .

afande afande hussen alie kuwa aki wania kupandishwa cheo baada ya kumkamata beka aliona ni bora aanze kuuliza watu kama walimuona beka akitoka kwenye lifti na alielekea wapi? afande hussen akaacha edward akimlilia joyce yeye akaanza kuuliza watu ambao walikuwa eneo lile kwa mda mrefu.

"mmh afande tangu lifti ilipofika mlango haukufunguka mpaka nyie mlipo kuja kufungua.." alisema kijana mmoja baada ya kuulizwa na afande kama alimuona beka akitoka kwenye lifti .

kazi ikawa ngumu kwa afande , lakini afande hakukata tamaa alimpigia simu yule nesi na kumuuliza kuwa beka alikuwa kavaa nguo gani nesi akasema hakumbuki ila cha muhimu nikwamba beka alikuwa kaumia kichwani so alikuwa na bandeji kichwani , afande hussen baada ya kusikia vile akatoa picha ya beka mfukoni na kuanza kuulizia baadhi ya watu huku akakazia kwamba mtu wanae mtafuta ameumia kichwa na anabandeji "... mmh huyu kijana alipita hapa kuelekea carteeni" alisema mlinzi ambae huwa anakaa kwenye mlango wa kuingilia carteen "...amepita kama mda gani hapa" aliuliza afande hussen kwa shauku "mmh kama dakika ishirini hivi" alisema yule mlinzi na akawa kamshitua afande hussen. beka na maaskari walikuwa wamepishana kama mda wa dakika ishirini kwani kipindi askari wanatoka ghorofa ya tatu kwenda ghorofa ya nne ndio mda huo beka alitoka kwenye lift na kushuka kuelekea namba mbili.

afande hussen na askari wakaanza msako kuelekea carteen na kumuacha edward akisaidiana na wauguzi kumpeleka joyce kwenye matibabu kwani waligundua joyce alikuwa anapumua kwa mbali sana.


polisi wakaendesha msako eneo lote la carteen bila kumuona beka afande akaenda kuuliza walinzi wa geti la kutokea nje ya bugando .. "afande una uwakika beka hajatoka kupitia hapa getini ?" afande hussen alimuuliza mlinzi wa getini " afande hapa hajapita...labda atakuwa ameenda kuruka senyenge...maana wagonjwa wengi ambao hukimbia malipo ya hosptal hupitia huko nyuma kwenye eneo la chuo na kuruka senyenge" alisema yule mlinzi na kumuelekeza afande hussen eneo lile naa afande na askari wake wakaanza kukimbia kuelekea eneo lile walilo elekezwa..


***

upande wa beka..


beka alipo toka ndani ya carteen moyo wake ulikataa asipite getini kwani alihisi walinzi wangemuomba karatasi ya kuruhusiwa kutoka wodini ...beka akaamua kukata kona na kushuka kwenye ngazi akaanza kufuata barabara ambako alihisi angeweza kutoka nje ya hosptal bila kukaguliwa na walinzi.

beka alitembea mpaka eneo la chuo cha bugando ambapo palikuwa kimya alipo angalia aliona senyenge ambazo zilikuwa zime tenganisha mtaa na eneo hilo la chuo beka akaanza kuzisogelea ili akwee na kuondoka eneo lilie " wewe kijana unatafuta nini hapo na mbona unaonekana mgonjwa.. hemu njoo hapa" beka alishituliwa na sauti ya mlinzi aliekuwa amekaa pembeni karibu na vijana flani, beka akawaza akwee senyenge haraka haraka na akimbie wazo hilo akaliona ni hatarishi kwani lazima mlinzi ange mkimbiza beka akakata shauri la kwenda kuongea na mlinzi..beka akaanza kutembea kuelekea kwa mlinzi huku akiwa na woga...

"wewe si nimgonjwa unafanya nini huku?" aliuliza mlinzi

"mzee naomba unisaidie mimi juzi nilipata ajali ya boda boda nikiwa nimeletwa hosptal sasa najisikia nafuu nataka nitoroke...sina pesa ya kulipia matibabu na mimi ni mtoto wa mtaani" alisema beka uongo kwa kutia huruma..

"nyie watoto wa siku hizi...pouwa niache na kitu kidogo kimtindo" alisema mlinzi kumaanisha alitaka pesa kidogo

" mzee sina hata mia hapa penyewe sijui nikifika mtaani nita kula nini"

"hah we mtoto dhalau yani huna hata mia halafu unataka kupita hapa...walai hupiti nakurudisha wodini" alifoka mlinzi ,beka alilalamika sana na kumuomba mlinzi beka akaanza na kulia ,muda wote yanatendaka hayo wale vijana walio kuwa pembeni walikuwa wanaangalia..

"haya ondoka usije ukanifia" alisema mlinzi baada ya kuona hawezi kupata kitu kwa beka "ahsante"alisema beka na kuenda kukwea senyenge japo aliumia na kupata maumivu lakini alifanikiwa kuwea na kutua upande wapili beka akaanza kuondoka eneo lile....


***

upande wa asakari..


askari walikimbia haraka na baada ya dakika tano wakafika eneo la chuo cha bugando yule afande akaenda mpaka alipokuwa yule mlinzi alie mruhusu beka kuruka senyenge.. yule afande alitoa picha na kumuonesha yule mlinzi ,mlinzi alishituka kujua kijana alie mruhusu kukwea senyenge alikuwa anatafutwa na polisi ,mlinzi akakataa haja muona beka kwani angesema amemuona na kumruhusu kukwea senyenge ange poteza kazi yake.

yule askari aliuona mshituko wa yule mlinzi akawa ana mashaka nae afande hussen akaenda kwa vijana waliokuwa pembeni na kuwauliza na kuwaonesha picha ya beka...."hah ...huyu si yule kijana alieruhusiwa na mlinzi kukwea senyenge...ndio huyu" alisema kijana mmoja baada ya kuiona picha ya beka mlinzi akaanza kutetemeka alijua kibarua kilikuwa kinaenda kuota nyasi...afande akamgeukia mlinzi.."ameondoka kama dakika ngapi na amepitia ameelekea wapi?" alisema afande hussen kumuuliza mlinzi

"kama dakika kumi na tano..aliekea kule"alisema mlinzi huku akisonta alipo elekea beka.

"tuki mkosa beka itabidi ukasaidie polisi...askari vukeni senyenge tuka msake" alisema afande hussen kwa hasira na kuanza kuvuka senyenge .

askari wakaanza msako kuelekea alipo elekea beka...




askari walianza kumtafuta beka huku hussen akionesha picha ya beka kwa watu wa mtaa ule huku akisisitizia kwamba kijana huyo alikuwa na bandeji kichwani

"ah huyu kija amenipita hapa kama dakika kumi na tano kanyoosha hiihii barabara" alisema mzee mmoja aliekuwa anauza kahawa pembeni ya barabara baada ya kuulizwa na husseni , hussen baada ya kusikia vile aliondoka na askari wengine huku akikimbia kuifuata ile barabara

hatimae wakafika sehemu moja yenye kituo cha boda boda ambapo walikuta baadhi ya pikipiki eneo lile

"samahani ndugu kuna kijana tuna mtafuta inasemekana alielekea huku sijui mme muona ana bandeji kichwani.."alisema hussen na kumpa picha mtu mmoja aliekuwa amekaa juu ya pikipiki

"ah afande huyu dogo alikuja hapa..na akaomba apelekwe mjini kwa bodaboda...bodaboda mwenzetu amempeleka"alisema yule mtu aliekuwa amekaa juu ya pikipiki. moyo wa hussen uliripuka na akiri ya hussen ikaanza kufanya kazi kwa kasi kupita kiasi ......hussen akajiuliza afanye nini na ndipo akapata wazo hussen akaona kama atapata namba ya dereva aliembeba beka na kumuambia dereva amshikilie beka ingekuwa rahisi kumpata beka..ama hakika hussen alikuwa kadhamilia kumkamata beka

"mna namba ya simu ya huyo mwenzenu? "aliuliza hussen"

"ndio" alijibu mtu aliekuwa juu ya pikipiki na kumtajia hussen

hussen baada ya kuandika zile namba akapiga ...simu ikaita kidogo kisha ikapokelewa

"halow nani mwenzangu?" iliuliza sauti ya upande wa pili.

"naitwa afande hussen... kuna kijana umembeba kwenye pikipiki yako tunaomba umshike na kumzuia kwani anatafutwa na jeshi la polisi" alisema hussen na kumshitua yule bodaboda

"ah..afande...mbona nimesha mshusha kama dakika tatu zilizopita na sasa narudi kituoni" alisema dereva wa bodaboda na kumshitua hussen

"sikia nikwambie rudi ulipo mshusha umkamate amri sio ombi...kwanza umemshushia sehemu gani" alisema hussen kwa kufoka

"zinapo paki gari za airpot afande"

"haya rudi fasta nasisi tunakuja sasahivi"

alisema hussen na kukata simu

"sawa" alisema bodaboda na kugeuza pikipiki kurudi alipo muacha beka.

...hussen akawambia wale boda boda wachache waliokuwa pale wawa bebe wawapeleke mjini na madereva wakatii bila shuruti

bodaboda saba zikawapakia kina hussen na kuanza kuondoka kuelekea huku baadhi ya askari wakiwafuata kwa miguu,

msafara wapikipiki saba zilizo beba askari ukaanza kuelekea alipo shushwa beka na bodaboda.


*upande*wa*beka*


beka alipo vuka senyenge alianza kutembea harakaharaka huku akiwa na lengo la kwenda kwenye nyumba yao nyegezi ...alikuwa anahisi maumivu makali kwenye mwili wake ila alikuwa hana jinsi beka alikuwa kaamua atembee kwa mguu mpaka nyegezi.

wakati beka anatembea aliweka mikono yake mfukoni na ndipo beka alipohisi kashika kitu kama karatasi ngumu akazitoa... beka hakuamini na kuona shilingi elfu arobaini [zilikuwa nizile alizochuka kwenye mfuko wa yona] beka aliona kama miujiza hakukumbuka kabisa kama alizichukua kwenye mfuko wa shati wa marehemu yona... .

beka akatembea mpaka kwenye kile kituo cha bodaboda na kuomba apelekwe mjini ambapo alipanga angepanda daradara na kwenda kwao nyegezi.


beka alishushwa mjini zinapo paki daradara za airpot beka akamlipa pesa dereva wa bodaboda , dereva wa bodaboda akaondoka kurudi kituoni beka akaanza kuulizia zilipo gari zinazoenda nyegezi, hatua kadhaa beka akakutana na machinga aliekuwa anauza kofia aina ya kapelo beka akanunua kapelo moja na kuivaa kwa ajiri ya kufuniki bandeji kichwani .

beka akaenda kwenye kituo cha daradara zinazo kwenda nyegezi beka akaona basi dogo ambalo lilikuwa limejaza na kuanza kuondoka beka akaikimbilia na kuingia ...safari ya kwenda nyegezi ikaanza beka akiwa kasimama huku kofia aliyo ivaa ikiwa imefunika sehemu ya uso wake.


*hussen*na *askari*


yule dereva wa bodaboda alirudi alipo muacha beka lakini hakumkuta akajiribu kumtafuta eneo lile lakini hakumuona...hussen na askari wakiwa kwenye bodaboda waliwasili eneo lile na kumkuta yule dereva wa bodaboda ambae aliwaambia kuwa hakumkuta beka...

hussen akiwa na askari wakaanza kumtafuta beka mjini pale kwenye mchanganyiko wa watu wengi lakini hawa kumuona beka

hussen alijaribu kuulizia sana na kuwaonesha watu picha ya beka lakini ilikuwa ni kazi bure kwani pale mjini kulikuwa kuna pita watu wakila namna hivyo ni vigumu mtu kumuona mtu walie mtafuta kina hussen na kumkariri.

beka akawa amemuacha hussen katika mazingira ya mzaha huku wakiwa wameachana dakika chache sana ... moyo ulimuuma sana hussen kwani alihisi kumkosa beka kwenye mazingira yaliyo mruhusu kumkamata kijana beka.

hussen akakata shauri la yeye kurudi bugando ili akachukue maelezo yaliyo muhusu beka na askari wenzake warudi kituoni.


hussen alienda bugando ambapo alifanikiwa kujua chumba alichokuwemo edward na joyce..hussen akamkuta edward alikuwa na mawazo mengi juu ya matukio yanayo fanywa na beka

"afande mmemkamata?"aliuliza edward kwa shauku

hussen akamwambia edward hali harisi..na hussen hakukaa sana akamwambia edward kuwa atamtafuta siku nyingine kwani hussen alihitaji kujua mengi ya beka kutoka kwa edward, hussen akaondoka kwenda kwa madoctor walio mpokea beka ili apate maelezo yatakayo msaidia na hussen alifanikiwa kuonana na yule mganga mkuu alie mpima beka na kujua kuwa kapoteza kumbukumbu.

mganga mkuu alimweleza hussen kuwa kumbukumbu ya kijana beka ilikuwa haipo sawa ..."inaonekana kabla hajapata ajari kunakitu alikigundua cha mda mrefu ...na baada ya kupata ajari amepoteza kumbukumbu" alisema mganga mkuu na kusababisha hussen ahisi vitu tofauti juu ya beka.

hussen akachukua karatasi na karamu na kuanza kuandika maelezo ya mganga mkuu ambayo alihisi yatamsaidia , hussen alimaliza kuandika akaondoka akiwa amedhamilia ajue nikipi kilimkuta beka.!


*upande*wa*beka


beka akiwa ndani ya hiace hakuamini pale aliposikia kwa mara yapili radio ilyokuwa ndani ya hiace ile ikimtangaza kuwa anatafutwa kwa kosa la kumuua yona .

beka akajua sasa alikuwa yupo kwenye hati hati ya kutafutwa na polisi wazo likamuijia beka akimbie jijini mule aende mbali na mwanza alihisi kama angeendelea kuwa mwanza bado angekuwa matatani.

gari aliyo kuwemo beka ilisimama stendi ya nyegezi na beka alikuwa wa kwanza kushuka kwenye gari lile beka akatembea mpaka eneo la stend ya basi zinazo kwenda mikoani beka akakata tiket na kuingia ndani ya basi kusubiri muda ufike safari ianze.


basi alilokuwemo beka lilianza kuondoka na kuliacha jiji la mwanza na kushika barabara ya shinyanga.


ilikuwa ni saa tatu ndani ya stend ya shinyaga...basi alimokuwemo beka liliingia katika stend ya shinyanga na msululu wa watu ukaanza kushuka kutokea kwenye lile basi beka nae alishuka na kuenda palipokuwa na pikipiki za bodaboda, beka akaomba apelekwe kwenye stesheni ya treni beka akatoa elfu mbili akapakiwa kwenye bodaboda mpaka stesheni ya treni.

bahati nzuri ilikuwa ipo upande wa beka kwani alikuta ratiba ambayo ilionesha kuwa treni ya kutoka mwanza kwenda tabora hatimae dar es salaam itapita pale saa tano za usiku ile.

beka akafanya mpango wa teketi akafanikiwa kupata tiketi ya kumfikisha dar es salaam ...beka akawa amekaa anasubiria tren ili akimbie mbali na mwanza, beka mwili wake ulikuwa na maumivu ya ajali lakini aliamua kuvumilia...beka aliumwa na mbu na kupigwa baridi sana siku hiyo akiwa anasubiri tren beka akaanza kuhisi homa kali mwilini mwake.


ilikuwa ni saa sita za usiku mlio mkubwa wa honi ya treni na mtikisiko ulisikika eneo la steshen na kila abiria wakaanza kuandaa mizigo yao baada ya kuiona treni wakaanza kuingia beka aliingia ndani ya tren mfukoni akiwa na elfu nne tu.,

huku akiwa anatetemeka kwa baridi na dalili zote za kuwa alikuwa na homa kali zikazihilika kwa kijana beka.

beka akakaa kwenye siti ya dirishani huku akiwa na kofia yake kichwani ambayo hakutaka kuivua kabisa

mara tren ikaanza safari beka akiwa ndani ya tren akiwa na malengo ya kuingia dar es salaam akiwa hajui ata fikia wapi...




********

ilikuwa ni saa nane ndani ya mtaa wa nyakato katika nyumba ya edward vilio na maombolezo

vilisikika katika nyumba ya edward watu walikuwa wamejaa eneo hilo kwa upande wapili kulijaa vijana na watu wazima wa mtaa ule minong'ono mingi ilisikika kutoka kwa watu wale "...jamani hata siamini et dogo beka ameisababisha familia ya familia ya edward... sipati picha."alisema kijana mmoja aliekuwa katika kundi la watu walio subiri muda ufike wanyenyue jeneza alimokuwemo yona na kumpelekakwenye makazi ya milele ..

"ila wajomba beka alikuwa anateswa na mshua edward ... yaani atakama niyeye aliuwa ...." aliongea mvulana mmoja na kushindwa kumalazia...


inspector hussen alikuwa amefika muda mrefu eneo lile la msiba na alikuwa kajichanganya kwa hawa watu waliokuwa wanamjadili beka,.. hussen alikuwa kimya akisikiliza maneno ya wale wana zengo waliokuwa pale wakijadili habari za beka

"ila mimi nakataa ...unajua beka alikuwa mpole mwenye tabia nzuri...we mpaka mama abdul akamruhusu kuwa na ukaribu na abdul mtoto wageti kali.."


"duh kweli mwanangu na sikia beka na abdul walikuwa mabest kama ndugu" alisema kijana mmoja na hapo hussen akataka amfahamu huyo abdul wanae msema kuwa ni rafiki mkubwa wa beka ambae mpaka muda huo alikuwa hajulikani alipo...

".....kwanza huyo abdul yuko wapi..." sauti ya hussen iliuliza kana kwamba nayeye ni mwenyeji wa eneo lile

"yupo bording ...huko alience" kijana mmoja alisema alie mfahamu abdul...

"na anaishi wapi?" swali kutoka kwa hussen .kijana mmoja akaelekeza kwenye nyumba ya kina abdul.. hussen akaanza kufanya mikakati ya kwenda kumtafuta abdul hussen alitaka kufahamu mambo mengi kuhusu beka kwani alishaanza kuhisi kulikuwa kuna kitu kati ya beka na edward.


upande wapili edward mama yona na peter walikuwa kwenye chumba kimoja wakiwa wamegubikwa na huzuni kubwa hakika beka alikuwa amewatupia wimbi zito la simanzi muda huo joyce alikuwa bugando hali yake haikuwa nzuri , edward alikuwa katika maumivu na hasira zidi ya beka ,edward bado alikuwa bado haamini kuwa beka ame waletea simanzi na kumuondoa duniani mwanawe mpendwa yona, edward akakumbuka jinsi beka alivyo wachomoka ndani ya bugando ,edward akawa anahisi beka anatumia nguvu za giza, kilio cha peter na mama yona kiliendelea ndani ya chumba cha wafiwa..


******abdul****


abdul akiwa bwenini alishangaa kuona beka hakufika pale kama walivyo ahidiana ..abdul akahisi kuna mambo yalimzuia beka asifike kumpa taarifa za mjomba wake..

abdul akaendelea kujipa moyo kuwa beka atakuja ,

lakini siku zikakatika bila kumuona beka ,abdul akaanza kuwa na wasisi wasi juu ya rafiki yake mpendwa.

abdul akashindwa kuvumilia ikabidi aende kwa mwalimu na kumuomba kuwa alihitaji kuongea na mama yake kwahiyo aliomba ruhusa siku ya michezo ambayo ni ijumaa ataenda nyumbani kwao na baada ya masaa mawili atakuwa amesharudi, kwakuwa abdul alikuwa ameshakuwa mkubwa kiasi na anajielewa walimu waka mruhusu.

siku ya ijumaa ilifika na abdul akabdilisha nguo na na muda mchache baadae abdul alikuwa njiani kuelekea kwao nyakato.

abdul alivyo fika nyumbani kwao alitaka kwenda kwanza kwa kina beka lakini kwakuwa alikuwa na kiu ikabidi aingie kwanza nyumbani mwao akanywe maji na ndo aanze kumtafuta beka..

"ha wow mwanangu..mbona umekuja kabla ya shule kufungwa?" alisema mama abdul baada ya kumuona abdul kaingia ndani

"nimekuja mara moja kumuulizia beka kuhusu masomo maana..." kabla abdul hajamaliza akaona badiliko kwenye sura ya mama yake...

"heh mama mbona umeshtuka?"

"mwanangu... beka siku uliyo achana na beka siku kuna matatizo aliya fanya kwao...so hata usimtafute utajilete matatizo" alisema mama abdul.. abdul akaanza kuhusi mama yake kuna mpango ana uadaa ili atenganishe urafiki wake na beka. mama abdul akasimulia kila kitu juu ya mambo aliyo yafanya beka abdul akawa bado mbishi mama abdul akaingia ndani na kutoka na gazeti na kumpa abdul... abdul haku amini kile alicho kuwa anakisoma..kwenye gazeti kulikuwa na picha kubwa ya beka na maandisha " atafutwa na jeshi la polisi kwa kuua binamu yake" mwili wa beka ukaingiwa na baridi...

"yaani mwanangu baba yako asingekuwa I.G.P sasa hivi ungekuwa kituoni unaisaidia polisi kwani wewe ndie rafiki mkubwa wa beka...kuna inspector alikuwa amekuja kwa ajili ya kutaka maelezo kutoka kwako...lakini waka malizana na baba yako" alimaliza mama abdul.

abdul moyo wake uliingia simanzi kubwa kibaya ni kwamba inasemekana beka amekimbia pasipo julikana , abdul akawa yupo kwenye simanzi.

abdul hakutaka hata kula chakula cha mchana akamuaga mama yake ambae alimsihi kuwa asiwaze sana na awe makini na masomo abdul akamkubalia mama yake akaondoka huku akihisi miguu yake kuishiwa nguvu , mama abdul akawa na wasiwasi kwa abdul kulikuwa na hatari ya abdul kuuridia ukimya wake wazamani na hata kutokufanya vizuri kwenye masomo .

abdul akarudi shuleni huku akiwa na mawazo tele juu ya rafiki yake kipenzi beka .


***hussen***


baada ya mazishi ya yona kufanyika hussen alimuaga edward na kumuambia siku nyingine atakuja kwa ajili ya maelezo machache...

hussen akaondoka hapo msibani na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwa abdul .

hussen alishtuka kukutana na I.G.P ibrahim mkubwa wake wa kazi na hata ibrahim akashangaa na kujiuliza hussen alikuwa amefuata nini kwake.

hussen bila kuficha alimuambia ibrahim kuwa alikuwa anafanya uchunguzi juu ya swala la beka na pale alikuja kupata maelezo kutoka kwa abdul kwani abdul ndie rafiki mkubwa wa beka.

"abdul nimwanangu na urafiki wao ulikuwa wa kombolela sidhani kama mwanangu atakuwa na majibu mazuri yatakayo fanikisha uchunguzi wako" alisema ibrahimu akimaanisha hakuna haja ya kuhojiana na abdul, hussen akaagana na ibrahim huku akiwa anawaza njia nyingine ya kupata maelezo kutoka kwa abdul. hussen huwa akidhamilia kitu huwa si mwepesi wa kukata tamaa.


baada ya siku tano tangu mazishi ya yona hussen alimtembelea edward na kumuambia aelezee juu ya beka na wazazi wa beka hussen alikuwa na kalamu na diary ndogo..

edward akaeleza uongo wake huku hussen akiandika

"baba yake beka alimua mama beka na yeye kujiuwa baada ya kumfumania" alimaliza edward

"mali za marehemu baba beka zipo mikononi mwa nani " aliuliza hussen

"ziliendelea kuwa mikononi mwangu bila kutumiwa...ila siku chache zinazo kuja itakuwa mali yangu mimi ndie ndugu pekee wa marehemu mama beka" alisema edward, hussen yale maelezo yalimtosha akakunja diary yake na kuanza safari ya kwenda alience alipo kuwa anasoma abdul.


***abdul***


ukimya mkubwa ulimgubika abdul muda mwingi akawa anajiuliza kwanini beka aliamua kufanya mauji ya yona na vp aliweza kusambaratisha familia ya edward.

abdul alikuwa amekaa pembeni ya kiwanja cha michezo.

"haujambo abdul" sauti ya hussen ilimshitua abdul kutoka kwenye mawazo mazito abdul akainua macho na kukutana na tabasamu la hussen ..

"sijambo shikamoo" abdul alisalimia na hussen aliitikia.

hussen akamwambia abdul kuwa alikuwa na lengo la kumsaidia beka..na ili kumsaidia aliitaji maelezo machache juu ya beka.

"aliwahi kukusumilia chochote juu ya vifo vya wazazi wake?" aliuliza hussen. abdul kwakuwa alijua hussen anataka kumsaidia beka ikambidi abdul asimulie jinsi mauji ya wazazi wa beka yalivyo fanyika kama alivyo simuliwa na beka..

"..but beka alisema baba yake hakumua mama yake...alie muua mama yake ndio huyo aliemua baba yake...na alisema sauti ya huyo muuji haikuwa ngeni masikioni mwake...tatizo ni kila alipo jaribu kuikumbuka sauti ile alishindwa maana baada ya tukio alizimia...afande wazazi wa beka waliuwawa" abdul alimaliza kwa msisitizo , hapo hussen akiri ikaanza kumzunguka kuna mambo yalianza kufanana na kuleta maana kubwa mganga mkuu wa bugando alisema "beka inaonekana kuna kitu alikigundua kabla ya kupata ajali...na baada ya kupata ajali kumbukumbu yake ikawa imerudi nyuma..na hosptal beka alikuwa akiongelea tukio ambalo abdul kamfafanulia hussen kwa ufasaha" akaendelea kuumiza kichwa.. "inaweza ikawa beka alimgundua muuaji na baada yahapo akapata ajari na kuirudisha nyuma kumbukumbu...na je huyo muuaji ni nani?....kwanini beka alimua yona na kutaka kumuua edward? "husen aliendelea kujiuliza huku akianza kuona kuna jambo kubwa tena zito katika kesi hiyo..

"kabla ya mama beka kufa alimng'ata muuaji kwenye bega na .... muuaji alisema "sometime inabidi kumgeuza ndugu kafala kwa faida ya watu wengi'" abdul aliendelea kutoa maelezo huku akilia na hussen akazidi kuya fananisha baadhi ya mambo yaliyo kuwa yakifanana.

hussen akaandika maelezo yale ya abdul kisha akasimama

"nitamsaidia beka...usiwe na wasi wasi..na usimwambie baba yako kama nilikuja kuchukua some info kutoka kwako " alisema hussen na kumuahidi abdul kumsaidia beka.

hussen akaondoka huku akihisi kama atayafanyia kazi vizuri yale maelezo ya abdul na akichanganya na yale ya mganga mkuu wa bugando akahisi kuna uwezekano wa kumjua mtu alie uwa wazazi wa beka na angejua sababu muhimu ya beka kumuua yona kwani maelezo ya edward hayakujitosheleza na haya kuleta maana .

hussen kaanza kazi.....




maisha ya abdul ndani alience yalikuwa ya upweke sana japo alikuwa anafanya vizuri kimasomo lakini upweke ulikuwa sehemu kubwa ya maisha ilikuwa ni ukimya hakuwa na rafiki wa dhati kama alivyo kuwa beka.


upande wa hussen alifanya uchunguzi na ile kesi ilikuwa na utata sana kwani kulikuwa kuna kitu kikubwa katikati ya beka na edward kuna kitu hussen alianza kukihisi kwa edward lakini shahidi mkubwa na kithibitisho cha mwisho alikuwa ni beka . beka ndo angeweza kumuambia kila kitu hussen na kukamilisha kwani uchunguzi unasema beka kuna kitu alikitambua kitu chenyewe cha mda mrefu na ndipo ikafatia ajali aliyo ipata na kupoteza kumbukumbu swali kubwa kwa hussen ilikuwa ni kwanini beka baada ya kugundua kile kitu alifanya vurugu kwenye familia ya edward? na nikitu gani alicho gundua ? haya maswali yote majibu alikuwa nayo beka.

hussen alijua lazima kama beka angepatikana na kusema ukweli lazima mtu aliefanya mauaji ya wazazi wa beka angejulikana . hussen akawa anafanya kazi ya kumtafuta beka ili akamilishe uchunguzi wake na hussen hakurudi tena kwa abdul kwani swala lile lilikuwa zito na sio vema kumshirikisha mtoto kama abdul.


mahakama ilimruhusu edward kuzimiliki mali za wazazi wa beka kwani mlisi wa zile mali ndo ameshakuwa mtuhumiwa na kibaya ameuwa mtoto wa edward.


familia ya edward yenye watu wanne huku watano akiwa pengo kubwa walihamia kwenye jumba kubwa la kifahari la wazazi wa beka joyce alikuwa amesha pona na kurudi nyumbani familia yote ilikuwa ina makovu walio achiwa na beka , peter na joyce walikuwa wana makovu usoni na edward na mkewa walikuwa na mkovu kichwani yaliyo tokana na kupigwa na stuli.

muda huo edward ndo alio utumia kuuza zile almas alizo muibia john baba yake na beka na kufungua miradi mikubwa edward akawa tajiri mkubwa jijini mwanza ,gari la wazazi wabeka ndio litumiwa na familia ya edward wakiendeshwa na dereva wa kulipwa huku edward akitumia gari aina ya prado aliyo inunua kwa pesa za damu ya wazazi wa beka.

siku zote edward alikuwa ana umiza kichwa jinsi ya kumpata beka na kumuua ili amalize familia yote.

edward akawa anamtafuta beka kimya kimya. [edward & hussen wakawa wanamtafuta beka kwa nia mbili tofauti]


abdul mpaka anafanya mtihani wa darasa la saba alikuwa bado hajapata taarifa zozote za beka kutoka hussen , japo abdul alifanya vizuri kwenye mitihani lakini kila siku alimuwaza beka na kuingiwa simanzi iliyo pelekea abdul kuwa mpole kuzidi watu wote shuleni.


abdul alifaulu kwa matokeo mazuri na abdul aliikumbuka sana ile siku walipo kuwa wanafurahia ufaulu wa beka ..maskini beka ameachishwa shule kwa matatizo abdul alitamani beka angekuwepo siku hiyo angefanya bonge la sherehe washerekee pamoja na beka lakini muda huo beka hakuwepo.


mpaka abdul anaingia form four alikuwa hajaanza kujihusisha na mahusiano waschana wali jaribu kumfuata abdul walie muita handsome lakini kwa abdul ilikuwa kazi bure kwani hata kuwachangamkia kwa ucheshi ilikuwa kazi kwa abdul kwa ufupi abdul hakujiusha na mahusiano kabisa.


violla alikuwa mschana mweupe mzuri wa umbo na mrembo wa sura .

yeye alihamia shuleni aliyo kuwa akisoma abdul akiwa mkubwa form three.


violla katika wavulana wote aliwaona shuleni pale alishangazwa na kijana mmoja abdul kwani alikuwa ni kijana tofauti kabisa na vijana wingine muda mwingi abdul alikuwa anajitenga peke ya na muda mwingi alikuwa anajiinamia violla aliaulizia wanafunzi wenzake kuhusu abdul "..ah huyo tangu yupo chekechea yupo hivyo..hanaga rafiki...alikuwaga na rafiki mmoja tu ila huyo rafiki imekuwa mda mrefu hajulikani ALIPO...si tunamuitaga mwanaume suluale mwanaume gani hata salamu kwa watoto wazuri hamna" ndio majibu aliyo yapata violla.


violla aliwahi kumfuata abdul zaidi ya mara tatu akiwa peke yake darasani violla alimfuata kwa kujifanya kuna swali la mathe limemshinda.

abdul hakuwa na kinyongo alimuelekeza jinsi ya kufanya swali hilo, violla akadhani kwakuwa abdul ameonesha ushirikiano kufanya swali lilio mshinda basi ataonesha ushirikiano wa kirafiki ,lakini haikuwa kama alivyo tarajia abdul aliendelea kuwa serious bila kuonesha ucheshi wowote kwa violla.

viola akajikuta katoka kwenye hali ya kumshangaa abdul na kuingia kwenye hali ya kumpenda abdul! na kumuhitaji kimahusiano.


violla akaanza kufanya kila kitu ili asimkose abdul moyo wa violla ulimsukuma kwa abdul na violla akajikuta akionesha kila dalili kwa abdul ya kuonesha kuwa anampenda. mara nyingi violla alienda kukaa kwenye dawati la abdul na kujifanya kuna swali limemshinda violla alipokaa na abdul aliacha wazi viungo vya sehemu ya mwili wake ambavyo mara nyingi huwatia kiwewe wanaume wangi, violla maranyini akiwa amekaa na abdul alifungua vifungo viwili vya juu vya shati lake na kufanya sehemu kubwa ya kifua chake cheupe kuonekana na muda mwingine aliivuta sketi yake na kufanya mapaja yake meupe ya onekane wazi kwa abdul, violla aliweza kuutambua uoga wa abdul kwani abdul alivyoona mambo yale na alitetemeka na kujifanya kama hana habari.


mpaka wanafanya mtihani wa kuitimu form four violla alikuwa bado haja fanikisha adhima yake kwa abdul kwani violla alisubilia abdul amtakie kuwa anampenda lakini kamwe haikutokea ,violla akapanga siku ya sherehe ya kumaliza kidato angemuomba abdul wacheze muziki,

lakini ajabu siku ya sherehe abdul hakuoneka na kufanya violla akose raha siku ile violla alikuwa ameshampenda abdul kwa upendo wa kweli na sio tamaa za kimwili. wazo likamuingia violla kuwa aende kwenye mabweni ya wavulana alijua abdul ndiko aliko kuwa na nilazima angekuwa peke yake, violla akaanza kwenda kwenye mabweni


wakati sherehe inaendelea abdul alikuwa chumba chake bwenini akiwa amekaa kwenye kitanda kavua shati lake kajiinamia akikumbuka siku ile alipo kuwa kwenye party ya rafiki yake beka ,"kama beka angekuwepo leo ningekuwa nae kwenye party yangu lakini kwakuwa hayupo kwenye party nikafanye nini sina rafiki" alijisemea abdul na muda huo mlango ulifunguliwa abdul alishtuka kumuona violla akiingia mule chumbani alimukuwemo peke yaka, violla akaenda mpaka alipokuwa abdul..

"abdul...mbona umekaa peke yake...na kwanini unalia...abdul una matatizo gani...niambie ...abdul ujue nakupenda" aliongea violla kwa mfulilizo na kumaliza kwa kusema dhamila yake , violla aliona ule ulikuwa muda mzuri wayeye kueleza hisia zake zidi ya abdul, kimya kikatanda.

"et abdul nini kinachofanya uwe hivi" violla aliuliza hata kabla ya kujibiwa swali la kwanza, violla alikuwa amekaa pembeni ya abdul na bila woga akapeleka mkono wake kwenye bega la abdul violla alikuwa kaamua kwani alichoka kusubiri kuambiwa anapendwa na abdul kitu ambacho alijua kisinge tokea. 'leo makubwa' abdul alijiwazia.

abdul akaona ni bora amsimulie maana alikuwa hana njia nyingine abdul alishaanza kutetemeka hakuwahi kuwa na msichana mazingira kama yale tena wakiwa wawili.


abdul alimsimulia juu ya urafiki wake na beka ambae hajulikani alipo lakini abdul hakusimulia habari ya vifo vya waza wabeka.

"..beka alikuwa kaka yangu na sio rafiki..mpaka sasa sijui alipo" alimaliza abdul.

"nataka kuziba pengo la beka" sauti nyembamba ya violla iliongea karibu kabisa na sikio la abdul.

"...huwezi kuziba pengo...ila utakuwa rafiki pekee ndani ya shule hii" alisema abdul na hapohapo violla kwa furaha alimkumbatia abdul kwa nguvu "wow thanks" alisema violla huku akizidi kumkumbatia kwa nguvu, abdul macho yalimtoka mwili ulimsisimuka kifua cha violla kilikuwa kimeshikana kabisa na kifua cha abdul ,abdul akawa anahema harakaharaka huku moyo wake ukidunda hakuwahi kabisa kukumbana na tukio hilo , violla nae alitambua kuwa abdul alikuwa akiwewe seka, violla aliendelea kumkumbatia abdul kichwani mwa violla akawaza ule ulikuwa muda muafaka kwani alihisi asinge pata nafasi nyingine na alijua abdul asinge chomoka pale , violla akiwa anajifikiria aanze na hatua gani kwenye mwili wa abdul mara mlango ulifunguliwa kwa nguvu !

abdul na violla walishituka na kuangalia kwenye mlango mungu wangu!

wanafunzi walikuwa wametoka kwenye sherehe na wamerudi kulala walishangaa kumkuta msichana aleikuwa miongoni mwa wasichana warembo shuleni hapo akiwa ame kumbutiana na abdul mtu ambae walizoea kumuona akiwa peke yake mda wote na mtu seriuos.

abdul na violla walipigwa butwaa huku wanafunzi wakiume wakizidi kujaa walimokuwa.

violla yalikuwa yamemkuta .

.

violla aliona chamaana nikuinuka na kuondoka kwani angeendelea kukaa pale wanafunzi wange zidi kujaa na hatimae ingekuwa noma zaidi.

violla akainuka na kuanza kuondoka taratibu akapita katikati ya wavulana walio valia nadhifu macho ya wavulana wengi yalimsindikiza violla kwa mshangao violla akaondoka akiwa kainama kwa aibu na kumuacha abdul.


kesho yake neno 'abdul jana kaopoa violla' lilikuwa ndo habari ya shuleni pale huku wasichana wa shule ile walishangaa sana mwenzao kawezaje .

upande mwingine violla aliona powa habari zile japo zilileta picha mbaya lakini kwake zilimzidishia urahisi wakuwa na abdul.


wanafunzi walifanya mtihani wa kuhitimu sekondari na wanafunzi walikuwa wanaagana kurudi majumbani kwao, violla alifanikiwa kupata nafasi ya kukutana na abdul na kumuomba namba ya simu na abdul hakuwa na kinyongo alimtajia na za simu ya mezani kwao na wakaagana huku violla akiwa na furaha iliyo pitiliza.


abdul akarudi kwao na violla akarudi kwao.


abdul alivyofika nyumbani baba yake alimpeleka kwenye mafunzo ya udereva baada ya wiki kadhaa abdul alihitimu mafunzo yote na abdul akarudi nyumbani na kuchukuwa nafasi kubwa ya kuendesha gari ya nyumbani kwao. abdul alipenda sana kuendesha gari kwa umahiri wa hari ya juu abdul alikuwa na uwezo mkubwa wakuendesha gari kwa kasi na style za ajabu.


abdul alimpenda sana mama yake abdul kila siku alikuwa wakwanza kuamka kwao na kufanya baadhi ya kazi kisha kumpeleka mama yake kazini kwake huku akiendesha kwa kasi na kwa umakini wa ajabu mpaka mama yake akawa anaogopa ila alipenda kwani alikuwa anafikishwa kazini kwa mda mchache sana

siku za mapumziko abdul alienda kwenye uwanja mkubwa ulioukwa karibu na nyumbani kwao kwa ajili ya kujifunza kila aina ya kuendesha gari kwa utundu , yote haya yaliendelea lakini ukimya na upweke uliendelea kumuandama huku mawazo mengi juu ya beka yakijenga makazi kwenye kichwa cha abdul.


mawasiliano kati ya violla na abdul yaliendelea mpaka siku moja violla alifanikiwa kuongea na mama abdul.......... mama abdul akajua kuwa mwanawe alikuwa kwenye mahusiano . kila siku violla alimwambia abdul maneno mazuri ya kimapenzi na kumuambia alikuwa anampenda kwa dhati.

safari ya uhisiano kupitia simu ikaanza kati ya abdul na violla na abdul akajikuta kwenye wimbi la kumpenda violla , yote yaliendelea lakini abdul hakuacha kumkumbuka beka.


matokeo ya walio faulu kuingia form five yalitoka na abdul alikuwa kafaulu na violla nae alikuwa kafaulu na habari njema wote walichagua shule moja ya bording.


maandalizi yalipo kamilika abdul akaagana na wazazi wake na mama yake alisema atamkumbuka mwanawe abdul kwani alizoea kila siku kupelekwa kazini na abdul. abdul akaanza safari ya kwenda shule ambako alikuwa na furaha ya kwenda kukutana na violla.





abdul alifika shuleni ambapo alikutana na violla na kila siku waliongelea mambo mengi kuhusu upendo wao ambao ndo kwanza ulikuwa unachipukia , abdul alimsimulia story fupi ya maisha yake na alimuambia kuwa yeye nimtoto wa I.G.P ibrahim na violla alisimulia maisha yake kuwa yeye wazazi wake na familia yake ipo jijini dar es salaam ila yupo mwanza kwa ajili ya masomo na anaishi kwa shangazi yake.

masomo yaliendelea huku upendo kati ya violla na abdul ukizidi kukuwa.


hatimae waliingia form six huku kila mmoja akiwa anafanya vizuri kwenye mitihani.


ikiwa bado kama miezi miwili wafanye mitihani ya kuhitimu form six kila mmoja tamaa za kimwili zili mshawishi kufanya mapenzi na mwenzake lakini mazingira ikawa kikwazo.


ilikuwa kama saa mbili usiku wanafunzi wote walikuwa kwenye ukumbi wa music wakiburudika siku hiyo kulikuwa na hafla.

kama kawaida yake abdul huwa hahudhulii kwenye sherehe ya aina yoyote alikuwa bwenini kajipumzisha.

siku hii violla alikuwa anaisubiria kwa hamu alijua lazima abdul angekuwa chumbani peke yake na kwake ilikuwa siku pekee ya kutimiza hitaji la mwili wake.

abdul akiwa amekaa kitandani akijisomea mlango wa chumba kile ulifunguliwa na abdul akamuona violla akiingia kavaa sketi fupi na violla akafunga mlango na komeo la ndani na kuenda alipokuwa abdul.

hakuna alie muuliza mwenzake kwani kila mmoja alijua kilichokuwa kinatakiwa kiendelee chumbani mule.

siku hiyo abdul na violla walitimiza maana nzima ya mahusiano .


***


hatimae walifanya mitihani na ulikuwa mda wa wanafunzi kurudi nyumbani kwao upande wa violla na abdul walikuwa kwenye udhuni kwani violla alidai atarudi dar es salaam ambako atakuwa ana subiria matokeo violla alionekana kuna kitu alitaka kumwambia abdul ila alisita lakani aliamua tu kumuambia.

"abdul..unanipenda?" aliuliza violla kwa hudhuni.

"zaidi ya kukupenda" alijibu abdul huku akitabasamu.

"nina mimba yako" alisema violla na kuanza kutoa machozi

"whaaat" alihamaki abdul, abdul hakuamaki kwa kuogopa kulea mimba ila hakuamini aliyo ya sikia, violla akawa anasubili kukanwa na kusalitiwa na abdul.

"serious?... nitaamini vipi?" aliuliza abdul kwa furaha.

"twende tukapime" alisema violla na wakaondoka kwenda kutafuta maabara,

baada ya kupima majibu ilikuwa ni kweli violla ana mimba

"wow kumbe hatari one day mimba ..." alisema abdul kwa furaha na kumfanya violla nae afurahi

"eeeh sikumoja tu..we unadhani siku ile ilikuwa mchezo" alisema violla na wote wakakumbatiana kwa furaha abdul alikuwa anahitaji mtoto.

"sasa abdul tuna fanyaje" violla aliongea akiwa bado amekumbatiana na abdul.

"please violla nilelee hiyo mimba...nampenda mwanangu mtalajiwa na hata wewe soon utakuwa mke wangu" alisema abdul kwa kubembeleza

"hata mimi nahitaji kuwa na mtoto ..but vipi kuhusu masomo yangu...na baba yako akijua umesha mpa mimba mtu ...na hivi baba yako I.G.P ....mmh" alisema violla kwa uzuni

"wife.. mi ndio mtoto pekee kwetu na nina pendwa.... mama akijua amekalibia aitwe bibi atafurahi....kwanza twende sasa hivi nyumbani" alisema abdul na kumshika mkono violla na kuanza kuondoka, violla alikuwa haamini kwani yeye alicho tegemea kwa abdul ni kukanwa.


abdul na violla walifika kwa kina abdul ambapo walimkuta mama abdul.

abdul bila kuchelewa akamuambia mama yake hali halisi kuhusu yeye na violla, muda wote violla alijawa na woga.

mama abdul alifurahi sana kwa alijua muda mchache angeitwa bibi.

"mwanangu violla upo nyumbani hiyo mimba hata ukifukuzwa kwenu haraka njoo uishi hapa na ukisha jifungua tu mjukuu wangu ataishi hapa na kwa gharama zetu utaendelea na masomo ya chuo kikuu" alisema mama abdul na kusababisha moyo wa violla ulipuke kwa furaha, siku hiyo violla na abdul walishinda wakiwa na furaha kubwa . hata I.G.P alipo pewa taarifa zile hakuwa na kipingamizi ,

violla akaondoka kurudi dar es salaam na kumuacha abdul mwanza huku wakiwa wamewekeana ahadi kemkem .


abdul aliendelea kuishi mwanza huku kila siku akiwasiliana na mpenzi wake violla.

abdul aliendelea na kawaida yake ya kuleta utundu wa kuendesha abdul alipenda mchezo wa kuendesha sana gari , hata baba yake aligundua kuwa mwanawe alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchezea gari akiwa barabarani tena akiwa mwendo kasi.


MEJA george mwakasege alikuwa mwanajeshi aliekuwa rafiki wa karibu na I.G.P ibrahimu walikuwa na urafiki mkubwa sana.

meja george aliekuwa karibu astafu tangu alipo jua abdul alikuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha gari george akajikuta akimuhitaji sana abdul!

meja george mwakasege aliweza kugundua abdul kuwa anauwezo mkubwa wa kuendesha gari ni siku ile ....

hiyo siku george na ibrahimu walikuwa na safari na walitakiwa wasafari kwa ndege.

ticket walikuwa wamesha kata na ndege ilikuwa ikiondoka saa tisa alaasiri , lakini kwa sababu zisizo zuilika ibrahimu na george mpaka saa nane na nusu walikuwa wapo nyumbani george alikuwa kakata tamaa alijua wasinge iwahi ndege, lakini ibrahim akamwambia acha wajaribu huwenda wakaiwahi, ibrahim akamuita mwanawe abdul na kumuambia walitakiwa wawahi airpot .

wakaingia kwenye gari na abdul akaanza kutoa gari nje.

baada ya sekunde arobaini na tano abdul alikuwa barabarana akiongeza mwando kana kwamba mwendo aliokuwa nao ulikuwa mdogo.

george aliweza kuona uhodari wa abdul ,abdul aliendesha gari kama barabara haikuwa na gari nyingine george alishuhudia abdul anavyo overtake magari na kuna wakati aliingia barabara ambayo si upande wake na kuzidi kuyapita magari kana kwamba yalikuwa yamesimama.

mwendo aliokuwa nao abdu ulikuwa mwendo hatarishi mpaka george akawa na hofu na kumshangaa abdul aliekuwa ameangalia mbele bila kupepesa macho.


baada ya dakika ishirini na nane tangu waondoke nyumbani abdul alifunga breki mbele ya uwanja wa ndege mwanza ,ibrahim na george wakashuka na kuiwahi ndege, sehemu ya kutumia mwendo wa saa moja abdul alikuwa katumia dakika ishirini na nane.

hicho kitendo ndicho kilicho mfanya george amtake sana abdul nakumtamani kwenye kazi zake binafsi lakini george alishindwa kujua angempata vipi abdul.


abdul aliendelea na maisha yake ya kila siku huku mara kwa mara george akienda kwakina abdul kwa ajiri ya kumsalimia rafiki yake ibrahim, mara zote alienda akiwa kavaa nguo zake nadhifu za kijeshi.

abdul nae alitamani kuwa mwana jeshi tena kila alivyo muona george akija kavalia nguo zake za kijeshi alizidi kutamani.

ikiwa ni miezi minne tangu abdul amalize form six abdul alisikia kuna nafasi za mafunzo ya jeshi kwa walio hitimu form six, hapo abdul akaona bora aende jesheni wakati anasubiri matokeo ya kuingia chuo.

abdul akamwambia baba yake kuwa alitaka aende jeshi wakati akisubiria matokea ya chuo kuliko kukaa bure nyumbani. ibrahim aliona mwanawe kachukuwa uamuzi wa busara kwani kama angeeda jeshi angekuwa mkakamavu na hata angekuwa na hekima,

mfunzo yalio tangazwa kwa ajili ya form six yalipangwa kufanyika hukohuko mwanza, ibrahim alitaka kama ni mafunzo ya mwanawe akayafanyie mkoa mwingine na sio humohumo jijini, ibrahim akabidi amuite george na walizungumzie hilo swala , george alifika na baada ya kuambiwa taarifa zile alishangaa sana maamuzi ya abdul na george akafurahishwa na maamuzi ya abdul


"sehemu nzuri na yenye mafunzo bora mwaka huu itakuwa ni arusha. ujue sehemu nyingine huwa ni mateso na sio mafunzo...na kitu kizuri ni kwamba na mimi nimepangiwa kwenda kufundisha arusha" alisema george


"basi hamna shida mwanangu huya hapo...nataka awe john rambo" alisema baba abdul na wote wakacheka


baada ya wiki moja abdul alikuwa na meja george ndani ya basi maalumu la JWT wakielekea arusha kwenye mafunzo ya kijeshi na ukakamavu.


***violla***


violla alipo fika kwao aliendelea na maisha na siku zilivyo kwenda ndivyo mimba ilivyo zidi kuonekana , alivyo ulizwa na wazazi wake kuwa huyo alie mpa mimba anampango gani na ana maisha ya hali gani, violla hakuficha alieleza kila kitu juu ya abdul na akwambia kuwa wazazi wa abdul hawana matatizo wanasubiria muda ufike ndoa ifungwe wazazi wa violla wakmuelewa mtoto wao.


***abdul jeshini***


Mafunzo ya kijeshi yaliendelea kwa kijana abdul akiwa na wenzake wengi, miezi miwili ya kwanza kwa abdul ilikuwa kama ya mateso lakini baadae alianza kuzoea .

mazoezi yalikuwa yavikwazo vya kila aina na kuzidi kuwa jenga wanadepo kwa kima zoezi.

baada ya miezi mitano tangu abdul aaingie kwenye mafunzo ya kijeshi waliaanza kufundishwa jinsi ya kupambana na watu zaidi ya watano kwa wakati mmoja hata kareti pia walifundishwa na abdul akatoka kwenye mwili wa kitajiri akawa na muili wa mazoezi tena wa kijeshi.

hatimae waliingia kwenye mazoezi ya kulenga shabaha ambapo baada ya siku chache abdul akawa mlengaji mzuri na mtumiaji mzuri wa bunduki, muda mwingi george alikuwa pamoja na abdul huku akifurahishwa na muenendo mzuri wa abdul george alikuwa anamuhitaji sana kwenye kazi flani lakini alishindwa atampata vipi ,kuna baadhi ya siku george alimpa abdul gari la jeshi na kufanya nae mizunguko midogo, uendeshaji wa gari wa abdul ulizidi kumtamanisha george kumchukua abdul kwenye kazi yake..


ilikuwa nimiezi tisa na siku kadhaa tangu abdul aachane na violla abdul akiwa kajipumzisha kambini ndipo alipoitwa na kuambiwa kuna simu yake, abdul akainuka na kuelekea kwenye hema iliyo kuwa ina radio ilio tumika kwa mawasiliano ya jeshi abdul akafika na kushika mkonge wa radio ile na kuweka sikioni.

"hellow" sauti ya kijeshi ya abdul

"eh baba...sisi ni wazazi wa violla..violla yupo hosptal kajifungua mtoto wa kiume" moyo wa abdul uliliripuka kwa furaha hakuamini

"heh mama vp hali yake..ni nzuri...basi mimi naenda kuaga jeshini ili niende arusha mjini kwa ajili ya kuwatumia pesa ya matibabu" alisema abdul kwa furaha.

"sawa baba"

Abdul akawa anatoka ili aende akaombe ruhusa ,lakini alivyotoka tu nje akakutana na mwana jeshi mmoja

"abdul unaitwa na meja george kwenye hema haraka" alisema mwanajeshi yule na abdul akaanza kukimbia kuelekea kwenye hema ya george.

"ndio meja nimefika" alisema abdul kumuambia george aliekuwa kaka kwenye kiti nyuma ya meza.

"kaa kwenye kiti abdul" alisema george, na abdul akaona george alikuwa anamchelewesha kwani alikuwa anataka akatume pesa kwa ajili ya violla.

"unajua abdul wewe ni mwanaume..na kikubwa zaidi wewe ni kama mwanajeshi" alisema george

"ndio"

"sasa inabidi uwe na moyo wa kijeshi na sio moyo wakike" alisema meja george abdul akazidi kushangaa.

"kwanza naomba unisamehe but mi nilifanya vile kama maamuzi ya kijeshi" george alizidi kumuweka abdul kwenye hali ya sitafahamu

"ni kama wiki moja iliyo pita baba yako alipata matatizo...alikutwa na tuhuma za kujishirikisha na mtandao wa madawa ya kulevya,... mimi sikutaka kukwambia maana wewe ulikuwa kwenye mafunzo na zile taarifa zinge kufedhesha na kukuletea msongamano wa mawazo ni kingine niliona hazikuwa na umuhimu kwako..." kufikia george alinyamaza abdul akaaza kuchanganyikiwa akajua baba yakea atakuwa mahabusu abdul akataka kuuliza kitu kwa george lakini kabla abdul hajauliza..george akaendelea

"...ni jana ambapo mwili wa baba yako umekutwa ukiwa chini kwenye sakafu....huku ikionesha kuwa amejikata mshipa wadamu kwenye mkono wake wa kushoto"


"whaaaat " abdul alipiga kelele huku moyo wake ukipata mshituko mkubwa.


abdul alikuwa katoka kupokea taarifa njema kutoka kwa violla kuwa amejifungua na hapohapo anapata taarifa mbaya juu ya kifo cha baba yake mpendwa je nini kitaendelea?

je? ni kweli baba abdul alikuwa anajihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya?

je? nani kafanya mauaji ya baba abdul?

meja george anaonekana anamtaka abdul kwa ajili ya kazi yake binafsi je?nikazi gani hiyo?





abdul hakutaka kuamini kile alicho kiskia kutoka kwa meja . abdul alionesha dalili zote za kuchanganyikiwa alishindwa kuyazuia machozi yake abdul akaanza kulia alihisi kichwa kikimzunguka.

george aliamka kutoka pale alipokuwa na kwenda alipokuwa amekaa abdul

"pole sana abdul ...nipo pamoja nawe yote ni ya dunia nisamehe kwa kutokupa taarifa za awali" alisema george, abdul hakujibu kitu aliendelea kulia.

george alikaa kwenye meza akiwa kimya kwa mda

"abdul nilisha fanya mpango baada ya nusu saa tutaondoka wote kwa usafiri wa anga... jikaze abdul mazishi yana tusubiri jikaze abdul japo sio rahisi" alisema george na kumuinua abdul kisha george akamuongoza mpaka kwenye gari ndogo ya jeshi aina ya landrover akafungua milingo na kumuambia abdul apande kisha george akaenda kuchukua begi la nguo za abdul na kumchukua mwanajeshi mmoja na safari ya kwenda uwanja wa ndege ikaanza.


walifika uwanja wa ndege na kuliacha gari kwa yule mwanajeshi na wao wakaingia kusubiri ndege ambayo ilikuwa inasafari binafsi za shirika, muda mchache baadae ndege ndogo ilifika ambayo ilikuwa inasafari binafsi kwa ajiri ya shirika george na abdul wakaingia ndani ya ndege na safari ya kurudi mwanza ikaanza kwajinsi alivyo changanyikiwa abdul alikuwa kasahau kabisa kama alipewa taarifa ya mpenzi wake violla kuwa kajifungua na alisahau kama aliwaahidi wazazi wa violla kuwa atawatumia pesa.


walitua uwanja wa ndege wa mwanza na bila kuchelewa waka kodi tax na kuanza kuelekea nyakato, muda wote abdul alikuwa kimya japo george alijitahidi kumfariji abdul lakini ilikuwa kazi bure kwa abdul.

tax iliyo wabeba abdul na george ilisimama mbele ya geti la nyumba ya kina abdul na george baada ya kumlipa dereva walifungua geti na kuingia ndani abdul miguu yake ilikuwa inatetemeka na kuishiwa nguvu ndani ya geti watu wengi ndugu zake baba abdul walijaa askari aliekuwa analinda geti lile hakuwepo kabisa alikuwa kahamishwa baada ya kujilikana mtu aliekuwa anamlinda hakuwa mwaminifu na serekali, abdul akiwa kashikwa mkono na george huku chozi likimtoka alipita katikati ya ndugu waliokuwa pale ambao walimwangalia kama hawa muoni ndugu wa baba abdul hawakumpenda abdul hata kidogo kwani walisema abdul alikuwa anajisikia sana na kingine baba abdul alimpenda abdul kuliko ndugu zake kilicho fanya ndugu wa marehemu I.G.P ibrahimu wazidi kumchukia abdul nipale walipo tambua abdul ndie mlisi mkubwa wa mali za baba yake. kidogo walio mpenda abdul ni ndugu wa mama abdul ambao walikuwa wachache eneo lile. abdul na george wakati wanazidi kusogea ndipo baadhi ya watu walio mfahamu walimpokea na kuingia nae ndani ya jumba lao abdul mawazo yake yote yalikuwa kwa mama yake, baada ya kuingia ndani sebuleni aliona wa kina mama wakiwa wamejitanda ushungi abdul aliangaza macho pote hakumuona mama yake!

"mama yuko wapi" sauti ya abdul iliyo kwaruza aliuliza watu wale waliompokea.

"twende kwanza ukakae abdul tukueleza kwa kirefu" alisema baba mmoja . george akaanza kuwa na wasiwasi na hata abdul pia. baada ya abdul kukaa sehemu husika aliuliza tena yuko wapi mama yake.

"abdul mama yako baada ya kupata taarifa hizi za kifo cha baba yako mama yako alianguka na kupata mshtuko akapoteza fahamu yupo hosptal " taarifa hii ilikuwa pigo lingine kwa abdul akazidi kuchanganyikiwa hapohapo akasimama,

"yupo hosptal gani na chumba namba ngapi niende kumuona mama yangu" abdul alisema huku kilio kikimtoka , george nae akasima na kumshika beka begani

"abdul subiri mazishi yafanyike ...hapa tulikuwa tunakusubiri wewe ili tufanye mazishi ya baba yako...abdul kuwa na moyo wa kiume mama yako mzima" alisema mzee mmoja , abdul ikabidi atulie na hapohapo simu ya abdul ikaita mfukoni mwake abdul aliitoa akapokea na kuweka sikioni bila kuangalia jina

"haloo"

"sasa baba ndo umetufanyaje si tunasubiria utume hela kwa ajili ya matibabu ya violla hari yake sio nzuri kidogo" sauti ya mama violla iliongea kwenye simu. hapo abdul ndio akakumbuka kuwa mpenzi wake violla alikuwa amejifungua, abdul alipotaka kuongea kitu akashindwa ndoge zito lilikuwa limemkaba abdul kooni abdul akashindwa kabisa kuongea huku simu ikiwa sikioni. george aliliona lile tatizo kwa abdul george akamnyang'anya abdul simu na kuiweka sikioni mwake "haloo baba yake mdogo na abdul naongea ... na hapa nyumbani kuna matatizo... sijui nani mwenzangu?" aliongea george kwa sauti ya kijeshi, kina mama violla wakajitambulisha kwa george na george bila kuficha aliwaambia mambo yaliyotokea hapo nyumbani...wazazi wa violla walishtuka sana na kuhuzunika...


baada ya muda kidogo abdul alichukuliwa na kuongozwa mpaka kwenye chumba ulimokuwemo mwili wa baba yake.

kilio kikubwa kilimtoka abdul baada ya kuona mwili wa baba yake ukiwa kwenye sanda kama pipi ,abdul alilia sana george akimbembeleza sana mtoto wa rafiki yake george alikuwa yupo bega kwa bega na abdul kana kwamba alikuwa ndugu yake


kama ilivyo kawaida ya dini ya kiislam maiti ikishafungwa kwenye sanda huruhusiwi kuifungua na kuiona sura ya marehemu, hivyo abdul aliishia kumuona baba yake akiwa kwenye sanda hakuruhusiwa kuina sura ya baba yake kwa mara ya mwisho.


baada ya taratibu zote kufanyika mwili wa baba abdul uliwekwa kwenye jeneza, na baada ya kusaliwa jeneza lilibebwa na safari ikaanza ya kumpeleka I.G.P ibrahimu kwenye makazi ya milele huku george akiwa kamshika abdul waki usindikiza mwili wa ibrahim.

miongoni mwa watu waliokuwa wakisindikiza msafara ule kwa miguu mmoja wao alikuwa ni afande hussen! ambae mara ya mwisho aliagana na abdul miaka saba iliyopita wakiwa mahina huku akimuahidi abdul kuwa atamsaidia beka .

hussen alikuwa kaja kwa ajili ya uchunguzi wa chini kwa chini, hussen alikuwa na na maswali mengi juu ya kifo cha I.G.P , hussen alikuwa hana sehemu nyingine ya kuanzia uchunguzi wake zaidi ya kuanzia uchunguzi wake kwa abdul, muda wote akawa anatafuta nafasi ya kuonana na abdul lakini ilikuwa ngumu hussen akawa anaendele kutafuta nafasi ya kuweza kuongea na abdul.


mazishi ya I.G.P ibrahim yalifanyika kama mazishi ya watu wengine na sio I.G.P ,alikuwa hana heshima yoyote serekalini tena alikuwa kavuliwa vyeo vyote kwa tuhuma za kujishirikisha na mtandao wa waingizaji wa madawa ya kulevya nchini.


abdul aliendelea kulia huku macho yake yakishuhudia koleo nyingi zikiufukia mwili wa baba yake ndani ya kaburi bila heshima yoyote kutoka serekalini.

hussen muda wote macho yake yalikuwa kwa mtu mmoja tu abdul ,

hussen alimuona george akimshikisha koleo abdul aliekuwa kalegea na kumsaidia kutupa koleo mbili kwenye kaburi , abdul akaliachia koleo na kushika udongo kwa viganja vyake na kuutupia kwenye shimo alimokuwepo baba yake mpendwa.


baada ya mazishi abdul na george pamoja na mzee mmoja wa makamu waliondoka kuelekea bugando aliko lazwa mama abdul.

yule mzee aliwaongoza kina george mpaka kwenye wodi za private alimukuwemo mama abdul, abdul pamoja na george waliingia kwenye chumba alichokuwemo mama abdul, kwanza walikuta baadhi ya ndugu wa mama abdul wakiwa wamekaa kwenye benchi maalumu mule ndani wakiwa na masikitiko walimpokea abdul na kumkumbatia na kumpa pole.

"mama yuko wapi?" aliuliza abdul,

"hatakiwi kuingia mtu kwenye chumba alimokuwemo mama yako...wanaingia madaktari tu wakijaribu kuokoa maisha ya mama yako ana hari mbaya" hili ilikuwa pigo lingine kwa abdul ambalo lilimpa wasi wasi mkubwa.

kwa mara ya kwanza abdul alianza kukutana na shinda za dunia baba yake amekufa katika mazingira ya kutatanisha, mama yake yupo hosptal ana hari mbaya sababu ya mshtuko, mpenzi wake violla kajifungua na hari yake sio nzuri kidogo, abdul akakaa kwenye benchi huku akiona dunia ina zunguka hakika abdul alikuwa kwenye hari ya kuchanganyikiwa.


walikaa pale mpaka saa tatu usiku na muda wote abdul alikuwa kajiinamia na mara akashtushwa na viatu vya doctor.

"jamani hari ya mgonjwa sio nzuri ...tangu mumlete jana mpaka sasa hajazinduka kwa ufipi hari yake nimbaya mno kwani anasaidiwa kupumua na mashine ya oxegen.... kuna dawa zita hitajika ...thamani yake kama laki mbili" alisema doctor na kufanya simanzi kubwa iwa gubike ndugu wa mama abdul na kumsababisha abdul azidi kulia.

mpaka muda huu ndugu wa mama abdul walikuwa wamesha changachanga na kutoa laki nne kwa madoctor ili mama abdul afanyiwe huduma haraka na sasa hivi hawakuwa na pesa.

"doctor hii apa laki tatu...please jamani jitahidini kuokoa maisha yake" alisema george na kutoa laki tatu badala ya laki mbili.


"hamna tatizo ndugu...muda huu nyie rudini nyumbani mje kesho saa nane" alisema doctor huku akifurahi alikuwa kapata cha juu.

kwa mara ya kwanza meja george akawa msaada mkubwa kwa abdul. siku hiyo abdul alienda kulala kwa george kwani george aliamua kumchukua alijua abdul alikuwa kwenye stress hakutakiwa kwenye ile hari.


***ilikuwa ni saa saba abdul alikuwa anapandisha ngazi kuelekea kwenye wodi ya mama yake alikuwa peke yake kwani george kuna sehemu alienda yeye alisema ataenda kumuona mama abdul mida ya saa kumi.

abdul hakukuta hata ndugu mmoja kwani saa nane ilikuwa bado

"samahani doctor naweza kumuona mama yangu" alisema abdul kumuambia mtu alie mkuta pale

"yah...amezinduka ..lakini hari yake mmh! ..... nenda tu ukamuone" alisema yule doctor, na abdul akaingia alipo lazwa mama yake.

abdul alipofika akaangalia pale alipo lala mama yake abdul hakuamini !

mdomo wa mama yake ulikuwa umeenda upande! huku mkono wake wakulia ukiwa umejikunja kwenye ungio la kiganja! maskini ya mungu mama yake abdul alikuwa amepata ungonjwa wa kiharusi yaani upande wa mmoja wa mwili wake ulikuwa umepooza.

sura ya mama abdul haikuwa ile sura ya mama abdul aliekuwa anakila sifa za kupendwa na I.G.P , mdomo wa mama abdul ulikuwa umeenda upande.

abdul alishindwa kujizuia kulia, ulemwengu ulikuwa umeanza kumuelemea abdul kwani matatizo yalikuwa yanamfuata kwa mfululilizo.

"mama polee nini kimekukuta mama...mama aaaaa" abdul alisema huku akilia hakujua nini kimemkuta mama yake mpaka kufikia hari ile, moyo ulimuuma abdul huku akihisi kutengwa na dunia.

" baba amekufa ....na mamaaa" hakika ilikuwa nipigo kubwa kwa abdul ambae alikuwa hajawahi kukumbana na shida na hila za dunia.


mara ndugu wa mama abdul waliingia na kumkuta abdul akiwa analia amekaa kwenye kitanda alicho lala mama yake. hata baadhi ya ndugu walilia kumuona mama abdul akiwa kwenye ile hari ,na muda kidogo akaingia doctor kutoa taarifa

"dungu yenu amepata ungonjwa wa kiharusi hii imetokana na pale alipopata taarifa mbaya za mume wake alipata mshituko mkubwa na kuanguka vibaya sana .,. hapo alipo yupoyupo hajielewi hata kama anakuangalia usifikiri kwamba anatambua chochote....kiukweli huu ugonjwa ni mbaya sana na matibabu yake ni gharama sana.... hapa inatakiwa tumrudishe kwanza kwenye hali ya ufahamu....matibabu pamoja na dawa ita gharimu kama laki saba" alisema doctor na kusababisha ndugu wote wainamishe vichwa chini hakuna aliekuwa na uwezo wa pesa hiyo kama jana walisaidiwa na george kutoa laki mbili leo ndo wangeweza kutoa laki saba? ilikuwa haiwezekani.

"... please doctor endeleeni kumfanyia mama yangu matibabu...na ileta hiyo pesa ndani ya masaa manne" alisema abdul na kuinuka nakuondoka na kutoka nje na kuanza kukimbia.

dakika chache baadae abdul alikuwa njiani akikimbia huku akiongea peke yake, kichwani mwake alikuwa na wazo la kwenda kuuza gari la baba yake.


abdul alifika nyumbani kwao ambapo alikuta ndugu wa upande wa baba ambao walikuwa wengi na walimuangalia abdul kama hawa muoni abdul akaangaza eneo lote hakuliona gari la baba yake! ikabidi aulize japo alio wauliza alijua hawa mpendi.

"baba yako kabla ya kukamatwa na mapolisi alikuwa anakimbia akiwa na hilo gari akapata ajali gari lipo kituoni halitamaniki" alijibiwana shangazi yake.


abdul akahisi dalili zote za kupoteza fahamu miguu yake ikakosa nguvu.....


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG