Search This Blog

Saturday, February 26, 2022

THE WORLD HATES ME (DUNIA INA NICHUKIA) - 2

   

Simulizi : The World Hates Me (Dunia Ina Nichukia)

Sehemu Ya Pili (2)


"unaitwa nani unakaa wapi" aliuliza beka, na abdul alimtajia jina na kumuelekeza kwao,

abdul na beka walikaa kwa muda wa dakika saba wakiongea story zisizo eleweka, na badae abdul alimuaga beka, beka akamsindikiza rafiki yake abdul ambae alimpunguzia njaa ya siku hiyo, beka akamuongoza abdul mpaka walipofika kwenye geti la kina abdul wakaagana abdul aka muahidi beka atakuwa akitoka nje kumtafuta, beka akarudi kwao ambako alienda kusubiri njaa kali ya usiku, abdul akaingia ndani ya geti akiwa amejaa furaha kwani alikuwa amepata rafiki tangu azaliwe beka akawa ndo rafiki yake wa kwanza.


siku zilisonga huku siku mojamoja abdul akitoka nje ya geti kwa kisingizio cha kwenda kununua juice, na akitoka alienda kumtafuta beka na kunywa nae juice pamoja, urafiki ukazidi kukuwa kwa hao watoto wawili.


ilikuwa ni juma pili jioni ambapo abdul alishtukizwa na mama yake kwa kuambiwa anaogeshwa na siku hiyo ndio alikuwa anarudi shuleni likizo ilikuwa imekwisha,

mtoto abdul alilaani kitendo kile alitamamani angalau amuage beka

lakini muda haukuruhusa hata sekunde moja,abdul alipakizwa kwenye gari yao, na safari ikaanza huku abdul akiangalia dirishani kama ange muona beka lakini kamwe hakikutokea kitu kama hicho.

abdul alikabidhiwa shuleni na jumatatu wakaanza masomo huku wanafunzi wakubwa kwa siku hiyo ilikuwa ni siku ya usafi,

walimu wa shule hiyo walipanga kabla wanafunzi hawajaanza shule rasmi waandae shindano la mpira wa miguu ambayo lingeshirikisha darasa la sita alience pamoja na darasa la sita la shule ya msingi nyakato,

ndani ya wiki hilo walimu waliweza kufanya mikakati yote na kupanga shindano hilo lifanyike ijumaa ya wiki hiyo.


ijumaa saa tano asubuhi wanafunzi walialifiwa kujiandaa kwenda uwanja wa mpira wa shule ya mahina ili wakashangilie timu yao, walezi wali waadaa na kuwavisha sale zao za michezo, baada ya muda kidogo wakaanza kutoka nje ya geti wakielekea uwanjani.,

abdul alijawa na furaha sana kwani alijua siku hiyo lazima angeeda kucheza mpira wa dobo na wale wanafunzi alio waona siku ile,

wanafunzi wa alience uwanjani na kwakuwa mda washindano ulikuwa bado walimu waliwaruhusu wanafunzi wa alience wa cheze michezo michezo mingina, wanafunzi wa chekechea wao waliendelea kukimbizana kwenye manyasi, abdul akaona ule ulikuwa muda muafaka wa yeye kwenda kuwatafuta wale wanafunzi wa mahina, abdul alitoka mbio kupitia mulemule alimopita siku ile, alipoinua macho kwa mbali kidogo aliona vumbi eneo lilelile alilo ona siku ile, abdul akaogeza mwendo mpaka akasogea kabisa .

"ha abdul umekujaje huku?" nisauti ya mtoto beka alisema kwa kuhamaki baada ya kumuona abdul, abdul alishangaa na hapohapo moyo wake uliripuka kwa furaha, hakutegemea kama angemuona beka eneo lile

"heh mi nasoma mule, na unafanyaje huku" alisema abdul huku akisonta ngome ya alience,

"mi nasoma hapa mahina" alisema beka, na hapo abdul akatambua ndie yeye alie muona siku ile na ndomaana alikuwa ana hisi kumfananisha,

"nime kuja kucheza mpira"alisema abdul,

"lakin hii ni dobo kipigo" alisema beka,

"si ile ya kukimbizana mpaka ushike sehemu"

"ndio"alijibu beka,

"basi na mimi na cheza" alijibu abdul huku akianza kuingia uwanjani, beka hakutaka rafiki yake abdul acheze mchezo huo kwani aliujua madhara ya mchezo ule,

"jamani huyu ndugu akiomba poo mnamuacha" alisema beka kuwaambia wenzake,

"ah, we nawe una ndugu anae soma alience au shobo, mwambie avue viatu vyake vya six " alisema mmoja wa wale watoto,

abdul akavua viatu vyake, na akaingia ndani ya uwanja.

Abdul akaendelea kucheza huku muda mwingi akiwa anacheka kwa furuha.


shindano la mpira liliisha na walimu wakaanza kukusanya wanafunzi kuwa rudisha bwenini, lakini hawa kumuona abdul ikabidi waanze kumtafuta huku na kule.


walimu walishangaa kumkuta abdul akicheza mchezo hatari na wanafunzi wa mahina tena akicheza kwa furaha, abdul alionekana kuwa na furaha kupita kiasi, walimu walishangaa.

walimu wakamchukua abdul na kuanza kumrudisha bwenini, abdul akawaaga kina beka na aliwambia siku nyingine atarudi, abdul akarudishwa bwenini akiwa kachafuka muda wote akiwa na furaha .


kila siku abdul ] muda wa mapumziko akawa anaenda kusimama kwenye senyenge ambapo aliwaita kina beka wakawa wakiongea abdul akiwa ndani ya ngome na kina beka wakiwa nje, abdul aliwambia kina beka wawe wanacheza dobo karibu na senyenge ili awe ana waona na kina beka walikubali.


abdul akawa mtu wa furaha muda wote mpaka walimu wakashangaa ,

wimbi kubwa la upendo lili wafunika watoto hawa wawili beka na abdul.


ingekuwa abdul kajiunga urafiki na watoto wenzake wakitajiri walio soma alience ingekuwa ni furaha kubwa kwa mama yake abdul,

lakini abdul alikuwa kajiunga urafiki na beka mtoto wa kimaskini tena mtoto mtundu,

unafikiri nini kitajiri?

mama yake abdul atakubari abdul aendelee kuwa na urafiki na beka mtoto wa mtaani?




walimu hawa kujua ni vipi abdul kawa mchangamfu kiasi kile, walimu ikabidi kumfuatilia maana kila siku muda wa mapumziko abdul hakuonekana sehemu walio zoea kumuona,

baada ya walimu kufuatilia walifanikiwa kujua abdul alikuwa ana urafiki mkubwa na wanafunzi wa shule ya msingi mahina na kila siku abdul alionekana akiongea nao akiwa kwenye senyenge na wakati mwingine walimu walimuona abdul akijaribu kukwea senyenge ili avuke upande wapili lakini alishindwa kukwea uzio ule,

walimu ikawalazimu kumpa taarifa mama yake abdul na walimpa zile taarifa za kumkuta abdul akicheza mchezo hatari wa dobo kipigo ,

mama abdul alishindwa kujua abdul kaanza vipi urafiki na watoto wale ambao kwa hakika ni watoto wenye maisha ya hali ya chini kabisa, mama abdul alimuuliza mfanya kazi wa ndani kama kuna siku alimuona abdul akitoka nje na kwenda kucheza nje mpira , mfanya kazi wandani akasema hakuwahi kumuona, mama abdul akashindwa kujua ni kwa namna gani mtoto wake kafikia hatua ile,

mama abdul ambae alikuwa bado mdada tena mrembo akawa haamini maneno yale ya waalimu,

walimu kwa kumthibitishia hilo walimuambia ijumaa itakuwa siku ya michezo na wata watoa wanafunzi wote nje kwenye uwanja wa mahina,walimu waka mwambia yeye afike mida ya saa nne na akae pembeni halafu wanafunzi wakisha toka halafu amuangalie abdul atakapo elekea,

mama yake na abdul na walimu wakakubaliana kuwa watafanya kama walivyo kubaliana


juma tano ilifika na wanafunzi wakaandaliwa kwa ajili ya kwenda kwenye michezo baada ya wanafunzi kuvaa sale za michezo geti lilifunguliwa na wanafunzi wakaanza kutoka nje kuelekea uwanjani,

mama abdul yeye alikuwa amesha fika kasimama pembeni akisubiria kushuhudia kile alicho kisikia, akiwa kasima pale kwa mbali akaanza kuona wanafunzi wa alience walio pendeza wakija uwanjani na hapohapo akaona wanafunzi wa chekechea wakija huku wakikimbizana hatua mbili mbele ya wale watoto wa chekechea alimuona mtoto mmoja akiwa anakimbia kwa kasi kuwaacha wanafunzi wenzake mama abdul alipomuangalia vizuri akamtambua alikuwa ni abdul, na hapohapo alimuona abdul akisimama kwenye kundi la watoto walio vaa mashati meupe na kaptula za khaki, mama abdul akamuona mwanae akipokelewa kwa furaha na kina beka .abdul akavua viatu vyake kina beka waka weka mpira kati na vumbi likaanza kutimka eneo hili huku abdul na kina beka wakiendelea kulikoleza vumbi lile kwa kucheza mpira wenye vurugu.

mama yake abdul alishuhudi alicho ambiwa, na hapohapo akashindwa kuvumilia na kuanza kumfuata mwanawe mpendwa abdul , na walimu na walezi waka ungana na mama abdul kusogea pale alipokuwepo abdul,

"we abduuul" sauti nyembamba nzuri iliita kwa ukali nisauti ya mama abdul,

abdul alisikia sauti hiyo alivyo geuka hakuamini kumuona mama yake ,

"heh mama yangu yule subirini nakuja" alisema Abdul kuwa ambia kina beka, abdul akatoka mbio kwenda kukumbatia miguu ya mama yake kama ilivyo kuwa kawaida yake,

"we usinikumbatie usije kuchafua suruale yangu,.. eeh nani kukufundisha kucheza michezo ya kijinga" mama yake abdul alimfokea mwanae, abdul furaha yake ikasambaratika, abdul hakujibu kitu akawa kimya, abdul akamuangalia mama yake usoni kisha akawatazama wale walimu waliokuwa wameshika viboko. wale wanafunzi aliokuwa anacheza nao abdul baada ya kuona ile hali waliondoka mmoja mmoja akabaki beka peke yake ambae mguu wake wakulia ulikuwa umekanyaga mpira huku mikono ya yote ikiwa imeshika kiunoni macho yake yakiangalia alipokuwa rafiki yake kipenzi

"wewe unaacha kucheza na wanafunzi wenzako wa alience unakuja kucheza na watoto wa mtaani eeh" mama abdul alizidi kufoka, abdul alishindwa kuvumilia japo alikuwa ni mtoto ila hisia kali zili mkumba kitendo cha mama yake kuwaita kina beka watoto wa mtaani kilimfanya abdul alengwe na machozi aliona kama unyanyasaji.,

"wanafunzi wa alience sina urafiki nao rafiki yangu ni huya hapo beka ni kaka yangu" alisema abdul na machozi ya lianza kumtoka, mama yake abdul alichukia jibu lile akamuangalia pale beka aliye simama kama mchezaji messi,

beka nae kile kitedo cha kuitwa mtoto wa mtaani kilimfedhehesha, lakini aliposikia abdul akisema yule ni kaka yake beka alitoa machozi ya furuha kuna kitu kiliugusa moyo wa beka baada ya kutajwa kama kaka yake na abdul.


"walimu hemu mleteni yule mtoto aliesimama huyu ndie ana haribu tabia ya mwanangu" alisema mama abdul na walimu wa kiume wawili wakaanza kumsogelea beka ambae alikuwa kasimama kana kwamba ana wasubiri, kitendo cha walimu wale kumsogelea beka wakiwa na fimbo mkononi angekuwa mtoto mwingine angekimbia ,lakini beka hakukimbia alisimama na walimu wa kaja kumshika, kitendo hiki cha beka kuto kukimbia walimu wale wenye fimbo mkononi kilitabiri urafiki mkubwa kati ya abdul na beka [REJEA:- SEHEMU YA KUMI YA RIWAYA HII, BEKA ALIPIGWA SANA NA ROBERT LAKINI HAKUSEMA ABDUL ALIPO JIFICHA]


walimu wale walimshika beka na kumpeleka mbele ya mama abdul , .

"unaitwa nani unakaa wapi?" aliuliza mama abdul.

"naitwa beka nakaa nyakato mama" alisema beka kwa nidhamu huku machozi yaki mlenga,

"we koma nani mama yako hapa, kwanini unamfundisha mwanangu michezo ya kijinga?" alifoka mama abdul, wakati huu abdul alikuwa analia,

"mama huyu nirafiki yangu kama kaka yangu" alisema abdul,

"pumbavu kaka yako wa kutoka wapi huwezi kuwa na urafiki pamoja na mtoto wa mtaani" alisema mama abdul na kumpi kofi dogo abdul ambae alianza kulia,

"mama usimpige abdul ni mimi mwenye makosa ni mimi mtoto wa mtaani niliejipendekeza kwa mtoto wa tajiri, mama sita rudia kucheza na mwanao abdul kwaheri abdul" alisema beka na kuondoka taratibu huku akilia,

"ondoka na usirudie kuniita mama... hivi mwalimu hamuwezi kumuazibu yule mtoto?" alisema mama abdul ,

"mama hatuwezi sio mwanafunzi wa shule yetu" alisema mwalimu mmoja aliekuwa pale,

beka aliondoka akachukua mpira wake na kuanza kuondoka eneo lile, tayari beka ameshagundua tatizo ye ni maskini ndo maana kapigwa marufuku kuwa rafiki wa abdul, beka alikuwa anampenda sana abdul lakini tayari alisha tenganishwa hakuwa na jinsi zaidi ya kulia.


abdul alirudishwa bwenini akiwa analia na mama yake akaenda kwenye ofisi ya mwalimu mkuu wa shule ya mahina ,mama abdul akamueleza kila kitu mwalimu mkuu kuhusu beka anavyo mlaghai abdul ,beka akaitwa akapewa onyo asionekane akiwa na abdul na asionekane kwenda kuongea na abdul kupitia kwenye senyenge ya shule ya alieance, beka akachapwa fimbo nne beka akarudi darasani akiwa na huzuni kubwa, mama abdul akawaaga walimu na kuondoka.


kuna baadhi ya walimu wali sikitishwa na kwa kutenganishwa kwa beka na abdul, na wengine wali uzunishwa na maneno ya beka aliyo ya sema wakati anaondoka yalikuwa ni maneno yaliyo beba uzuni.


hari ya abdul ilibadiri na ukimya pamoja na uzuni ukachukuwa sehemu kubwa ya abdul, abdul akawa kuongea mpaka atakapo ulizwa kitu na mwalimu ndio alikuwa akifungua kinywa chake na kuongea kimya kikateka maisha ya abdul ukimya huu ulikuwa zaidi ya ule wa mwanzo .


beka nae alibadilika sana beka akawa mtoto anaekaa peke yake kila wakati, rafiki zake beka walipo jaribu kumshawishi waka chezo mchezo wowote beka ali kataa na kuwaambia hato cheza, beka akawa mtoto mpweke asiependa kujichanganya na rafiki zake,

walimu wali shangaa sana ile hari ya beka ,kwani beka hakuwa vile beka huwa ni mchangamfu kila muda,




walezi wali jaribu kila njia ile kumuweka sawa abdul lakini ilikuwa kazi bure, walimu ikabidi wa peleke taarifa hizi kwa wazazi.


taarifa zilimfikia mama abdul ambae nae aliona tatizo lilikuwa lina umuhimu kumjulisha baba abdul I.G.P Ibrahim,

mama yake abdul akamuambia kila kitu ibrahim na ibrahim alimuambia mke wake kuwa hakufanya vyema kuchukua maamuzi kama alio ya chukua, chakufanya ni kuruhusu ule urafiki uendelee na kama kuwatenganisha abedul na beka wata weka mazingira ambayo yata punguza uhusiano kwa watoto hao ,. mama abdul yeye hakutaka ule urafiki uendelee hata kidogo kwani hakutaka mtoto wake ajiunge na mtoto wa mtaani hata kidogo lakini kwakuwa imelazimu ikabidi wafanye hivyo na wakapanga juma tatu waende wote kufanya utaratibu wa kuurudisha urafiki wa watoto wale,


juma tatu ilifika , baba na mama abdul wakaenda shuleni wakafanye kitu ambacho kingerudisha furaha ya mtoto wao abdul.


beka ni mtoto mwenye miaka saba lakini akiri yake ilijua baya na zuri, beka tayari alikuwa amesha gundua tatizo ni hali ya kimaisha ndio ilikuwa chanzo cha mama abdul kuutenganisha urafiki,

"KAMA MAMA YANGU ANGEKUWEPO NA MIMI NINGE KUWA NASOMA ALIENCE NA MAMA ABDUL ASINGE TUTENGA NISHA" alisema bekal akiwa chini ya mwembe kajiinamia na hapohapo akashikwa begani na mkono mkubwa mzito ,beka akiinua macho na kumuona mtu mwenye mwili mkubwa alievaa nguo za kipolisi. alikuwa ni baba yake abdul aliemfuata beka baada ya kuelekezwa.

baba yake abdul alimuuliza beka anaitwa nani na anaishi wapi na ilikuwa vipi mpaka wakajuana na abdul , beka alitaja jina lake na anapoishi kwa uoga kwani hakuwahi kuongea na polisi, beka alieleza kila kitu jinsi ilivyokuwa mpaka wakawa marafiki ,

baba yake abdul baada ya kusikia story ile kutoka kwa beka alie onekana kuwa na nidhamu, baba yake abdul aliona sio haki kuwatenganisha watoto wale kisa hali ya kimaisha.


yeye mama yake abdul alienda kumfuata abdul shuleni ambae alimkuta akiwa tofauti kabisa na siku zote , akamchukua mwanawe abdul na kuanza safari kwenda pale alipokuwa beka na na baba abdul,

ibrahimu alievaa nguo za kipolisi alimuambia beka kuwa yeye ni baba yake abdul, beka alishituka kwani alijua kama mama yake abdul anamchukia lazima na baba abdul angekuwa anamchukia, na beka alihisi baba abdul kaja kumchukua kumpeleka kituoni , kipindi beka anaendelea kubabaika hapohapo akamuona mama abdul akija na abdul, beka alitaka kukimbia kwani alikuwa anamuogopa sana mwanamke huyo, asinge kuwa baba abdul beka angetimka mbio, mama abdul akaja akamsimamisha abdul Karibu na beka , abdul alionesha furaha lakini beka hakuonesha furaha kwani alihisi kama kuna hatari.

ibrahim alichutama mbele ya wale watoto wawili na kuwaambia kuanzia siku hiyo watakuwa marafiki na wasi sahau masomo. ibrahimu akaingiza mkono mfukoni na kutoa shilingi elfu mbili na kumshikisha beka mkononi akawambia wakanunue juice, beka alikuwa haamini muda wote woga ulimtawala ,tangu mama abdul aingie pale beka hakumtazama usoni hata mara moja, ibrahimu akawaambia waende wakanunue wanacho kipenda beka na abdul wakeanda huku abdul akiwa na furaha kumpita beka,

ibrahimu na mke wake wakaelekea kwenye ofisi ya mwalimu mkuu wa shule ya mahina,

ibrahimu cha kwanza aliulizia maendeleo ya masomo ya beka, mwalimu mkuu akamwambia muhura wakwanza alikuwa wapili kati ya watoto miamoja na thelasini na muhura wa pili alikuwa wa kwanza kati ya watoto walewale kwa ujumla beka alikuwa ana muelekeo mzuri wa kima somo ,ila ilionesha mazingira anayo ishi yana onesha si mazuri kwani marakwamara walimu walimpa barua beka ampelekee mlezi alieishi nae lakini beka alipo peleka barua mjomba wake hakuitikia wito ule,

ibrahimu akauliza kuhusu tabia ya beka, mwalimu alisema beka alikuwa na nidhamu tena mcheshi, ibrahimu akauliza "beka sio mgomvi?"

"ugomvi umechukua sehemu kubwa ya shule hii so kumkuta mwanafunzi akipigana sio swala la ajabu" alijibu mwalimu mkuu.

majibu yali mlizisha ibrahimu na akamwambia mwalimu itabidi beka na abdul urafiki wao uendele maana kuna sababu zisizo zuilika,

ibrahimu na mke wake wakatoka nje ya ofisi na kwenda alipokuwa beka na abdul ambao wali wakuta wakinywa juice wakawaaga na kumuambia abdul ikifika saa saba atakuja kuchukuliwa na mlezi kwajili ya chakula cha mchana ,

Ibrahimu na mke wake wakaingia kwenye gari na kuwaacha abdul na beka,

Abdul na beka siku hiyo hawakucheza ila walikaa wakisimuliana mambo yao ya kitoto siku hiyo muda kwao ulienda kwa haraka kama mshale kwani wakiwa pale wanaongea mambo yao alikuja mlezi wa abdul ilikumchukua kwajili ya chakula, abdul alimbembeleza sana beka wakale pamoja mpaka beka akakubali na mlezi hakuwa na shida aka wachukuwa wote ,

Abdul na beka wakaanza kuingia ndani ya bweni abdul akiwa kavaa kaptula yenye rangi ya damu ya mzee na shati la drafti jekundu ,na beka akiwa na kaptula ya khaki na shati jeupe, beka alikuwa mrefu kidogo kwa abdul,

Wanafunzi wa alience walishangaa kumuona abdul akiingia na mwanafunzi asiekuwa wa shule ile,

Wakaenda wakakaa sehemu ambayo huwa wana subiria chakula na muda mchache abdul na beka wakapatiwa chakula wakala wote kwapamoja kwa furaha na kuwa shangaza wanafunzi wa alience,

Walipo maliza kula abdul alimuongoza beka mpaka kwenye viwanja vya michezo ambapo kulikuwa kuna bembea na sehemu ya kutelezea pamoja na kujipima uzito, abdul na beka walicheza kila mchezo huku beka akiwa na uoga flani, walicheza sana ilipo fika saa kumi beka alitambua kuwa kachelewa kwa beka akamuaga abdul ambae aliekuwa anahitaji waendelee kucheza. beka akaondoka haraka huku akijua lazima siku hiyo angechapwa na mjomba wake.


siku zilikwenda miezi ilisogea urafiki wa beka na abdul ulizidi kuwa mkubwa huku kila mmoja akitamani kama angesoma shule moja na mwenzake.


mika ilisogea mpaka abdul anaingia la tano alikuwa akiendelea vizuri kimasomo, beka nae akiwa la sita aliendelea kuwa wa wanne au watatu kwenye mitihani huku akionekana kuna kitu kinacho msibu na kumfanya muda mwingine awe mpweke na muda mwingine alionekana kuwa na furaha ya kulazimisha, walimu walihisi kuwa kuna mambo yanayo msibu beka na kumuasili kisekorojia beka alipo ulizwa alisema hamna kitu kuna wakati walimu walipo mdadisi sana beka alilia bila kutaja sababu ya kulia .ILIONESHA KUNA MAMBO YALIYO KUWA YANA MSIBU BEKA TENA MAKUBWA.


beka akaingia darasa la saba na abdul akaingia darasa la sita,

urafiki wa beka na abdul ukawa mkubwa tena wenye pendo la dhati, si mama abdul wala baba abdul wote wali shindwa kuutenganisha urafiki ule, kuna wakati binamu zake beka walimsema maneno mabaya kwamba anajifanya kujipendekeza kwa mtoto wa kishua, lakini beka hakujibu kitu kwani kama maneno alishazoea,

abdul kuna kitu alishaanza kuhisi kutoka kwa rafiki yake ,alihisi kuna mambo yanamsibu rafiki yake lakini hataki kuya sema, mara kadhaa abdul alishamkuta beka akilia peke yake na kuna siku alimkuta beka kakaa peke yake katulia na akiwa kafinya macho yake kana kwamba kunakitu alikuwa anajilazimisha kukumbuka 'kama..na mfahamu...lakini... simkumbuki vizuri..but yale maneno ...kama... ' ni maneno aliyo yasikia abdul kutoka kwa beka aliejiongelea peke yake , abdul kama rafiki mkubwa wa beka alihisi kuna mambo makubwa yanayo mtatiza rafiki yake, abdul akanuia kumdadisi rafiki yake mpendwa.




ilikuwa ni jumapili asubuhi ambapo abdul aliamka na kabla ya kunywa chai alienda kumtafuta beka, abdul alipanga siku hiyo amuulize rafiki yake nikipi kinacho mtatiza,

abdul alipo kalibia kwa kina beka alikutana na beka aliekuwa na biblia mkononi,

"eh mbona asubuhi na bible" aliuliza abdul baada ya kumuona beka,

"ah naenda church siunajua leo juma pili" alijibu beka .

"duh we pastor nini? yani saa moja kasoro unaenda church?" abdul alisema huku akicheka,

"ah kuna some where na pita" alijibu beka, kawa kingreza na kiswahili , abdul na beka wote walipenda kuchanganya lugha.

"ah poa but nina maongezi flani hemu tusogee mbele tukaongee" ,alisema abdul na kumshika beka mkono na kutembea mpaka sehemu iliyo kuwa kimya wakakaa kwenye msingi ambao ulikuwa bado hujawekwa tofali.

" unajua best sikuelewi" alisema abdul baada ya kukaa kwenye msingi,

"kivipi" alijibu beka na kuonesha wasi wasi,

"bado siku chache sana ufanye mtihani wa kumaliza la saba ,then unakuwa na stress , au we unaona kukaa kimya ndio njia ya kuondoa stres mi ni mdogo wako na sio rafiki sito penda kuona una fichaficha kitu ambacho badae kitakualibia kila kitu, au mi siyo ndugu yako" alisema abdul huku akimuangalia kwa mtazamo wa kumchunguza,

kitendo cha abdul kumuita beka kaka yake kilimfanya beka atoe chozi la furaha beka alijisikia faraja kubwa kuitwa kaka na abdul,

" nothing abdul... mimi sina stress mdogo wangu" alisema beka huku akionekana kuficha kitu,

"ukiwa unatatizo then unanificha kaka inaonekana udungu wetu tuna ektiana na sio udungu bali badae udungu kama huu hugeuka kuwa uadui kwa kitu kidogo sana best" alisema abdu huku akioneshwa kuchukizwa na kitendo cha beka kuficha mambo yanayo msibu, abdul akawa anaanza kusimama maana hakuona faida ya kuwa pale,

"no abdul nitakuambia"alisema beka na abdul akabaki kasimama,

"abdul mimi nina matatizo ambayo ninayo kabla hata ya urafiki wangu mimi na wewe.......wanasema mama yangu umalaya ndo ulimponza...... Sawa hata kama ....kwanini uwe kama wimbo kwangu kila siku wana niambia mama yangu umaraya wake ndio umenifanya mimi niwe mazingira haya .. Why ."alisema beka huku akilia kwa hasira ,abdul aliekuwa kasimama akakaa chini huku machozi yakimlenga maneno ya beka yali mnyong'onyesha abdul,

Akakaa kwenye msingi na kumshika beka begani ,huku akimbeleza ndugu yake huyo abdul.

"abdul si ajabu hata mimi ningekuwa nasoma alience kama wewe... na siajabu hata mimi ningekuwa mtoto waki sure kama wewe, ..naikumbuka sana siku hiyo wao wanasema baba alimua mama kwa kosa la kumfumania lakini ule niogo japo nilikuwa mdogo but baba haku muua mama ila alie muua mama ndie huyo alie muua baba na kisha kumuua kijana wanaesema alikuwa hawala yake na mama.... niuuugooo"alisema beka na kupiga ngumi kwenye msigi ule, abdul alianza kuogopa kwani yale maneno yalikuwa mazito kwake alijuta kumdadisi beka, abdul nae akaanza kulia huku akiwa kamshika beka begani,


"abdul mi nakumbuka kila kitu... naikumbuka sana hiyo siku ...ilikuwa nijioni nikiwa nimo ndani ya gari ambalo marehemu mama aliliendesha tulikuwa tumetoka kununua baskeli ndogo ya watoto ambayo ilikuwa nizawadi yangu alio ninunulia mama kwa sababu nilikuwa wa kwanza kwenye mitihani ya nursery moja ilioko huko nyegezi, mama yangu alikuwa na furaha kubwa kwani nilikuwa najua kusoma na kuandika katika umri wangu mdogo , baada ya kufika nyumbani kwetu nyegezi ,mama alinichukua na kunipeleka chumbani kwangu akanilaza kitandani kwangu na kunishushia neti, akataka kuondoka lakini akasita na akarudi pale nilipokuwa akafunua neti na kunibusu kwenye paji la uso wangu,

"i love you my son god bless you in that night" alisema mama yangu huku akitabasamu ,

"i love too my mother see tommorow" nili sema na kujifunika shuka mama akaondoka na kufunga mlango wa chumba changu,

nikiwa karibu kusinzia nikasikia mlango wa sebuleni ukigogwa na nikamsikia mama akisema 'karibu' huku akienda kufungua mlango.

" mume wangu kuna nini .... nyie mme mfanya nini mume wangu..." hiyo ni sauti ya mama yangu nilio isikia na mimi nikajua kulikuwa kuna tatizo, kabla sija fanya lolote ni kitu kiki dodoka kama mzigo na hapo nikasikia mama akilia kwa uchungu, ina onekana alisukumwa na watu walioingia ndani, hapo hapo nikasikia mlipuko wa risasi,

"mume wanguuu... kwanini mume muua mume wanguu" hiyo nisauti ya mama ilio sikika baada ya mlipuko wa risasi nikaamka harakaharaka kitandani ili nikajue niyapi yanayo msibu mama, lakini nilivyo sogea karibu na mlango nilisikia mama akiongea kwa kukoroma kana kwamba alikuwa kakabwa , "ka...k.... siamini kama niwewe unae tufanyia hivi" nisauti ya mama ilionesha alimtambua muuaji ambae kwa hakika ilionesha walifahamiana..

"wewe....E " PAH PAH kabla mama haja malizia kusema kitu kilicho onesha kuwa ni jina la mtu lilionzia na herufi "E" hapo hapo nikasikia milipuko miwili kikafuata kilio kikubwa kutoka kwa mama, mi nili shindwa kuvumilia maana nilimpenda sana mama, nikataka kufungua kitasa cha mlango ule lakini nilishindwa kufikia kitasa kilikuwa juu na mimi nilikuwa mfupi, nikaanza kupiga mlango huku nikilia wamuache mama.

"hemu fuateni kitoto chao na chenyewe mkiuwe" nisauti ambayo ilikuwa sio ngeni kwangu ilio sema alikuwa kanisikia na sasa ilikuwa zamu yangu,

"hamuwezi kumuua mwanangu.." nisauti ya mama iliokuwa dhaifu, na hapo nikasikia vishindo vikija kwenye mlango nilimukuwemo nikasikia mtu akishika mlango na kisha kuufunga kwa nje harafu nikasikia kitu kama chuma kidogo kikitupwa mbali na aneo hilo, alikuwa ni mama aliefunga mlango kwa nje na kuutupa mbali ufunguo, nikasikia mama akigumia kana kwamba amekabwa na kitu,

"pumbavu huyu malaya ananiumaaa" hiyo nisauti ya kiume ili lalama kwa uchungu, hii ilimaanisha mama alikuwa kamuuma muuwaji yule,

nika sikia mlipuko wa risasi ,

"pumbavu kaniuma begani"ilisema sauti ya kiume.

"SOMETIME INA BIDI KUMGEUZA NDUGU KAFALA KWA AJIRI YA FAIDA YA WATU WENGI PUMBAVU" pah pah pah, ni maneno niliyo ya sikia kutoka kwa yule muaji kisha ikafuata milio ya risasi mfululizo siku msikia tena mama yangu. na akiri zangu zika niambia mama hayupo, nikachutama ili nichungulie kupitia uwazi uliokuwa chini ya mlango ikawa ndio salama yangu kwa nikiwa nimechutama pale chini risasi mfululizo zilitoboa mlango niliokuwemo, mimi nikalala pale pale chini, kupitia uwazi ulikuwepo pale chini niliona viatu ambavyo havikuwa vigeni machoni kwangu , milipuko ya risasi ikatawala masikioni mwangu nikaanza kusikia kizungu zungu, kichwa kikawa kizito nikaendelea kukodelea macho viatu vile vilivyo kuwa vikipiga hatua viatu vile kuna sehemu nili wahikuviona, macho yangu yakawa mazito ya kapoteza mwanga sura ya mama yangu ikipita kichwani mwangu ...sikujua kilichotokea,(mama yangu akawa kauwawa kikatiri huku mwili wake ukiwa na matobo ya risasi zaidi ya matano)


nilikuja kujikuta nikiwa kwenye kitanda cha hosptal ya bugando, ambapo mjomba alikuja kuni chukua na kunileta ninapo ishi sasa,

tarifa zikazagaa kwamba mama yangu alifumaniwa na baba yangu ,eti baba yangu akampiga risasi mama yangu pamoja na mtu aliekuwa hawala wa mama, kisha baba akajipiga risasi . kwa mazingira hayo abdul eti ni kweli mama yangu aliuliwa na baba?"

beka akawa kamtupia swali abdul ambae macho yake yalikuwa mekundu kwa kulia,

"hapana beka ... wazazi wako wameuwawa... pole beka nimakubwa uliyo yaona" alisema abdul huku akilia , beka nae alikuwa akilia,

"muuaji ilionesha walifahamiana na wazazi wangu one day i'll know that swine, vile viatu alivyokuwa amevaa siku ile nilikuwa kama na vifahamu na hata sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwangu mama kabla ya kufa alimng'ata begani mwake ambako sijui ni bega la kulia au kushoto, tatizo nilipoteza fahamu... ..vile viatu na sauti yake... kumbukumbu ndio sina vizuri ila nita mjua tu" alisema beka huku akilazimisha ubongo wake kukumbuka vizuri,

"beka inabidi usahau yote japo sio rahisi kwani mitihani imekalibia jitahidi ukimaliza kufanya mitihani ...tutakuwa pamoja .... usijipe stress fanya kwanza mitihani " alisema abdul huku akijifuta machozi,

"abdul swa la kumjua muaji halinipi stress lingekuwa linanipa stress nisingekuwa nafanya vizuri kwenye masomo tangu zamani KUNA MAMBO MENGINE YANAYO NIONGEZEA MAUMIVU " alisema beka na kumshangaza abdul,

"yapi hayo tena?"abdul aliuliza kwa mshangao,

beka akashusha pumzi ndefu kujiandaa kumueleza abdul,





"Hivi abdul ingekuwa wewe mama yako ndio limemkuta janga hilo, halafu kila siku watoto wa mjomba wako kila siku kwao ndio umekuwa wimbo kila ukifanya kosa wanakuambia 'we mtoto malaya kama mama yako , mama yako kafanya umalaya mpaka kajisababishia kifo kafa kakuacha' ungekuwa ungefanyaje" beka alisema na kumuachia swali abdul,

"ninge piga mtu" alijibu abdul

"utampiga nani utamuacha nani " alisema beka akatulia kidogo akaendelea,

" hata shangazi na mjomba nao kila siku wanasema 'mama yangu kawaachia mzigo ' wanasema umalaya wa mama imekuwa shida kwao" alimaliza kuogea beka,

"sasa unahisi ni kwanini wanafanya hivyo"

"nyegezi tuna nyumba nzuri tena kubwa nahisi mimi ndio kikwazo cha wao kuichukua nyumba alio iacha mama na baba" alisema beka na kutulia,

"kwanza pesa za kwenye acount ya wazazi wako nani alizi chukua, au walikuwa hawana acount" abdul aliuliza akijaribu kuhisi kitu ,

"et taarifa zinasema masaa matano kabla ya vifo vya wazazi wangu, eti baba alitoa hela zote milioni hamsini kwenye acount yake, et na milio ishirini kwenye acount ya mke na mume, inakuja akirini masaa matano kabla ya vifo vya wazazi wangu milioni sabini zilitolewa kwenye acount mbili kwa wakati mmoja" alisema beka kwa uzuni

"no baba yako achukue then akazipeleka wapi, alie ua wazazi wako ndie alie chukua hizo pesa" aliema abdul kwa hisia kali

"mawazo yako na hisia zangu zimeendana, baba yangu hakutoa pesa" abdul na beka wakakaa kimya kidogo,

"sasa hapo sijui ufanye nin pole sana beka" alivunja ukimya abdul,

"siku moja nitamgundua alie mwaga damu nyumbani kwetu, sauti ya mtu yule haikuwa ngeni kabisa masikioni mwangu ..tatizo nilivyo zinduka baada ya kupoteza fahamu nimejikuta sauti ile siikumbuki kila kila nikijilazimisha kuikumbuka nashindwa" alisema beka akiwa katulia,

" kwa saivi jisomee kwanza kuhusu swala la binamu zako kukusimanga fanya kama ulishazoe mimi ndio ndugu yako sio rafiki, tatizo lako ni tatizo langu tuta lifuatilia baada ya wewe kufanya mitihani.... " alisema abdul huku akisima na abdul akasimama wakakumbatiana,

"we si unakwenda church" alisema abdul baada ya kukumbatiana,

"ah nime hairisha lakini mimi kila jumapili naenda kwenye makaburi ya wazazi wangu huko mahina"

"twende wote pamoja" alisema abdul na wakaanza kuondoka,

walitembea kwa mguu mpaka kwenye makaburi ya mahina ambako walisogea kwenye makabuli mawili yalio kuwa yamekaribiana , makaburi hayakuwa na majani maana beka kila jumapili beka alienda kufanyia usafi wa makaburi ya wazazi wake ,

hawakuchukua muda wakataka waanze kuondoka lakini abdul akiwa ameanza kutangulia aligeuka nyuma baada ya kuto sikia nyayo za rafiki yake, abdul akamuona beka akiwa kapiga magoti na alikuwa kama anaongea kitu ila hakutoa sauti,

"mama mara ya mwisho ulinibusu ukasema mungu anibariki ndio ukawa umeniaga, mama na muomba nipate kumjua alio dhurumu uhai wenu" alisema beka kisha akafanya ishara ya msalaba akainuka wakarudi nyumbani.


baada ya siku kadhaa abdul alirudi shuleni rikizo ilikuwa imekwisha abdul akamsihi beka ajisomee mengine yatafuata badae beka akamuahidi abdul kuwa lazima atafaulu kwa kishindo kwenye mitihani , abdul akarudi shule ambako waliendelea kuonana na beka,

mwezi wa tisa ulifika na tarehe za mtihani zilibaki siku saba kina beka wafanye mitihani,

beka na binamu zake wawili walikuwa wanasoma wote la saba lakini paka zina baki siku mbili beka alikuwa haja wasilisha shuleni pesa kwa jili ya chakula siku ya mtihani lakini binamu zake wawili walikuwa wamesha wasilisha yeye alinyimwa na mjomba wake akimuambia akamuombe best wake abdul, mwalimu wa darasa baada ya kuona beka haja wasilisha pesa ya chakula aliamua kumtolea kwani alishajua beka aliishi mazingira ambayo si mazuri.

**ilikuwa ni saa mmoja asubuhi siku ya juma tano shule ya mahina wanafunzi walikuwa wachache sana ,walikuwa ni darasa la saba A NA B waliokuwa wakisubiri muda ufike waingie kwenye chumba cha mtihani,

*beka alikuwa kasimama kwenye ngome ya shule ya alience akiongea na abdul aliekuwa ndani ya ngome hiyo , abdul alikuwa akimsihi sana beka atulize akiri kwenye mtihani kwani elimu ndio kila kitu , waliongea sana baadae mazungumzo yao yaka katika baada ya kuona wanafunzi wakiingia kwenye chumba cha mtihani, beka akaagana na abdul,

abdul akabaki ana muangalia beka aliekuwa akikimbia kuelekea kwenye chumba cha mtihani.


***beka baada ya kumaliza mitihani alikuwa mtaani akitafuta pesa kwa ajili ya kushiriki sherekhe ya kuhitimisha shule ya msingi .

Beka alijitahidi kutafuta pesa kwa bidii kwani alitaka kumtolea abdul ambae alipanga kumualika siku ya sherekhe ile,

hatimae beka aliwasilisha shilingi elfu nane ambayo ilimtoa jasho, kawaida alitakiwa kutoa shilingi elfu nne lakini kwakuwa alipanga kumuaalika abdul ilibidi atoe elfu nane ,

beka akaenda kumualika abdul ambae alipokea mualiko ule kwa furaha.


***shule ya mahina ilependeza kwa shamla shamla wasichana wavulana walio vaa vizuri walizagaa eneo lile ilkuwa ni sherehe ya kumaliza la saba, wanafunzi wengi wakiume walikuwa wamejichanganya na wasichana . beka na abdul walikuwa pembeni wakiendelea na maongezi yao mara nyingi walionekana wakicheka kwa furaha.

baada ya kula chakula , wanafunzi wote waliambiwa waingie kwenye chumba cha mziki , beka na abdul walikuwa wa mwisho kuingia kwenye chumba cha muziki mziki ambao ulikuwa wa kanda na sio cd,

asilimia kubwa ya wanafunzi wale walicheza mvulana na msichana . ila beka na abdul walikuwa pembeni wakinywa soda na kufurahia mziki.


** wakati wa matokeo ya walio chaguliwa kuingia sekondari ulifika na abdul alikuwa nyumbani kwa rikizo fupi abdul baada ya kusikia matokeo yameshatolewa aliamka asubuhi na kwenda kumtafuta beka ambae nae alimkuta akienda kwenye ofisi za serekali za mtaa akaangalie matokeo,

"ebwana bora nimekuona hapa naenda kuaangalia matokeo yamesha toka si unipe suport" alisema beka baada ya kumuona abdul,

"hah mimi ndo nimekufuata twende ndani tuka angalie kwenye internet" alisema abdul kwa shauku, beka alitaka kukataa kwani tangu urafiki wao uanze hakuwahi kuingia ndani kwa kina abdul na kubwa zaidi alimuogopa sana mama abdul

Abdul akafanikiwa kumshawishi beka na kumuambia kuwa mama yake hakuwepo ndani, beka akawa kamkubalia abdul.

beka alivyokuwa anaendelea kuingia ndani alipo angalia mazingira yale alikumbuka sana nyumba yao ilioke nyegezi

abdul alimkaribisha beka kwenye sebule kubwa ilio pendeza kwa vigae vya thamani , beka alishtuka kumuona mama abdul akiwa amekaa kwenye kochi la mtu mmoja beka akakilaani kitendo cha abdul kumdanganya kuwa mama yake hakuwepo kumbe yupo,

"mama tunaomba laptop yako tuangalie matokea ya darasa la saba" alisema abdu kumuambia mama yake,

"ah karibuni wanangu ,karibu beka" alisema mama abdul baada ya kuinua uso wake, tayari mama abdul alikuwa hana kinyongo na beka kwani alisha gundua beka hakuwa na matatizo, natayari alishagundua kuwa beka aliishi kwenye mazingira magumu,

"ahsante...shikamoo..mama" alisema beka kwa kubabaika na hapo akakumbuka kitu 'usirudie kuniita mama yako' ni maneno alio mbiwa na mama abdul miaka sita iliyopita, beka akajua kaisha fanya kosa,

"marahaba mwanangu ...ngoja nikawaletee muangalie matokeo yako" alisema mama abdul na kuelekea chumbani kwake.

beka alijisikia faraja kuitwa mwanangu na mtu ambae zamani aliwahi kumuambia asimuite mama yake.

muda mchache mama abdul akaja na laptop akamkabidhi abdul ambae alianza kubonyeza batani za laptop ile kwa shauku kubwa akitafuta jina la beka john.

"ebwana hila hapa jina lako" alisema abdul kwa sauti tena kwa furaha kubwa huku akiwa amegusisha kidole kwenye kioo ambapo kulikuwa na jina la beka, beka alifurahi sana hata mama abdul nae alisogea aangelie alama za beka , mama abdul alishangaa kwani beka alikuwa na alama zuri ni masomo mawili aliyo pata B nayo ni maarifa ya jamii na hisabati mengine yote alipata A.

"Heh we mtoto mmh ...subiri ni kupe zawadi yako"alisema mama abdul kwa furaha huku akiinuka na kuingia ndani na kuwaacha kina beka wakifurahia matokeo yale, mama abdul akarudi na noti mkononi

beka hakuamini kupokea noti ya shilingi elfu tano kutoka kwa mama abdul kama zawadi,

"ahsante mama.... abdul mi siamini acha niende serekali za mtaa nika hakikishe" alisema beka,

"ah twende wote.. mama tunarudi sasa hivi" alisema abdul

"haya wanangu"


abdul na beka walitoka nje wakikimbia hawakuchukua mda wakawa wamesha fika yalipo bandikwa matokeo, walisogea mpaka kwenye ukuta ulio bandikwa matokeo ambapo kulikuwa na watu wengine wakitafuta majina yao, beka alivyo tupia macho kwenye karatasi lililojaa majina aliliona jina lake likiwa la kwanza kabisa Hapo moyo wa beka ulipuka kwafuraha beka akamgeukia abdul kwa furaha na kumkumbatia wote walikuwa na furaha kubwa isio fichika wakiwa wamekumbatiana ghafla tabasamu la beka likapoteza muelekeo baada ya kumuona binamu wake aliekuwa anamzidi kidogo umri, binamu yake beka alipita mbele yao huku akiwatazama kwa husda akaenda mpaka palipo bandikwa matokeo,

beka na abdul wakabaki kimya wakimtazama, binamu wa beka alisimama kwa mda lakini hakuona jina lake akarudia tena kuangalia huku mkono wake mmoja ukikuna kichwa lakini hakuona, tayari beka na abdul walisha gundua jamaa hajaona jina lake, beka na abdul wakamuona jamaa akiondoka akiwa mnyonge, abdul akishindwa kuvumilia akaangua kicheko hata beka pia ilimshinda wakacheka kwa sauti binamu aligeuka na kumuangalia beka kwa macho ya kumsubiri beka nyumbani binamu akaondoka bila kugeuka nyuma,




"ah lazima usome beka kamwambie kwanza mjomba wako then tumsikie atasema nini" alisema abdul kumpa beka matumaini

"mmh nahivi mtoto wake amefeli sidhani kama nitasomeshwa"alisema beka kwa unyonge.

"ah beka kwa vyovyote vile lazima usome, mimi leo narudi shule nenda ukamwambia mjomba wako juu ya swala lako la kufaulu majibu atakayo kupa uje uniambie kesho shuleni" alisema abdul kwa msisitizo

"pouwa tutakutana kesho" alisema beka huku akiwa hana uhakika na matumaini aliyopewa.


************

binamu yake abdul alipoondoka alifika nyumbani akiwa amefura akampita mama yake nje bila kumsemesha akaingia chumbani mwake akaanza kulia mama yake akawa kaisha tambua kuwa mwanae analia basi matokeo yamekuwa tofauti alijua mwanawe amefeli , mama huyu aliwapenda sana wanawe na hakupenda kuona wakiwa kwenye udhuni , kitendo cha kumsikia mwanae analia kwa kwikwi chumbani alishindwa kuvumilia ikambidi aende kumbembeleza akafungua mlango na kuingia ndani ambako alimkuta mtoto wake akiwa kainamia goti akilia,

"mwanangu usilie kama umefeli baba yako atakupeleka private" alisema mama yule aliejulikana kwajina la mama yona, na yona ndie aliekuwa analia pale,

"mama sawa nimefeli lakini silii kwa sababu hiyo" alisema yona na kumshangaza mama yake ..

"sasa kinacho kuliza ni kipi"

"si huyu mbwa mnaemfuga hapa yani nimemkuta huko na abdul wakaanza kunicheka na kunizomea eti kisa nimefeli, yani beka ananicheka mbele za watu labda ahame humu ndani... leo atamtaja mama yake " alisema beka na kuongeza uongo na kusababisha hasira kubwa kwa mama yake

"huyu mshezi... atanikuta " alisema mama yona na kumuambia mwanawe asilie kisha akaondoka kwenda kufanya kazi zake za nyumbani mama huyu alikuwa na watoto wa tatu wakiume wawili wakike mmoja wakike aliitwa joyce wakiume peter na huyu yona alie kuwa analia, tangu beka aanze kuishi pale hakuwahi kuinua mkono kumpiga hata mtoto mmoja wa mama huyu ila ni yeye aliegeuka ngoma ya kupigwa na binamu zake wale kila kukicha , na leo alikuwa kapaniwa na yona.


mjomba wa beka aliporudi kutoka kazini salamu ilikuwa ni malalamiko kutoka kwa mke wake akimwelezea jinsi beka alivyo mfedhehesha mtoto wao yona.

"sasa na nyie yani anamdhalilisha mwanangu na nyie mnamuangalia kwanini mlishindwa kumpiga mpaka ashindwe kutembea?" alisema mjomba yake beka kwa hasira,

"sasa tupige hewa na wakati mpaka sasahivi saa mbili usiku bado hajarudi " mama yona ambae ni shangazi yake beka alisema akiwa amefura

"atanikuta leo atapigwa na yona mpaka ashindwe kutembea hemu mwiite yona" alisema mjomba wake beka na mama abdul akapaza sauti kumuita yona,


**beka na abdul baada ya kuafikiana waliondoka kurudi nyumbani abdul akamuambia beka siku ile wakanywe chai kwa kina abdul beka hakukataa kwani hakuwa na uhakika wa chakula cha mchana siku hiyo, na kila alipo kumbuka kuwa alimcheka binamu yake yona alijua kulikuwa kuna uwezekano wa kushinda na kulala njaa .

beka na abdul wakiingia nyumbani wakapatiwa chai wa kanywa wakiwa kwenye meza kubwa ya chakula, beka alikumbuka miaka nane iliyopita alikuwa akinywa chai ile na baba na mama yake,

siku hiyo beka na abdul walishinda wakicheza game la G.T.A vice city ambalo lilikuwa kwenye computer ya kina abdul, abdul akamfundisha beka jinsi ya kucheza.

mama abdul alipendezwa na urafiki wa watoto wale japo zamani hakutaka beka awe na urafiki na mtoto wake, kwakuwa siku hiyo abdul alitakiwa kurudi shuleni ilimpendeza mama abdul kwenda kuwafanyia shopping watoto wale wawili ambao walikuwa wameanza kuwa vijana.

baada ya chakula cha mchana beka na abdul waliingia kwenye gari abdul akiwa na begi lake lililo jaa vifaa vya shuleni mama abdul nayeye akaingia ndani ya gari na kuanza kuondoa gari kutoka getini na kuelekea mjini mwanza penye maduka ya nguo nzuri za duka.


shopping ilikuwa nzuri tena iliojaa furaha , abdul alinunuliwa nguo za kubadilisha akiwa shule, beka akanunuliwa begi la mgongoni suruale ya jinsi na mashati mazuri pamoja na viatu vya shule na shati jeupe la shule.

baada ya shopping kuisha waliingia kwenye gari na kuanza kurudi ili wampeleke abdul shuleni.

mama abdul aliendesha gari kwa muda akawa amesha mfikisha abdu shuleni, abdul na beka wakaagana kwa furaha "usisahau tulivyo ongea "alisema abdul akimkubusha beka kuhusu ahadi yao ya kukutana siku ya pili yake beka alinyoosha kidole gumba kwa ishara ya kuafiki , mama abdul akawasha gari na kuanza kurudi nyumbani akiwa na beka ndani ya gari.

muda ulikuwa ni saa moja jioni na giza lilikuwa limeshaanza kuingia mama abdul akiwa anaendesha gari huku akiwa ana muuliza beka mswali tofauti tofauti ya kuvunja ukimya uliojengeka kwa beka,

mara ghafla beka aliingiwa na kumbukumbu za miaka nane iliyopita, kitendo cha kuwa yeye na mama abdul ndani ya gari kilimfanya akumbuke siku ile aliyo kuwa na marehemu mama yake ndani ya gari akitoka kununuliwa beskeli ambayo ilikuwa zawadi yake, na siku ile ilikuwa ni jioni kama hii, matukio yalikuwa yame fanana kati ya tukio la mama abdul kumnunulia za wadi beka na kurudi nae nyumbani jioni wakiwa wa wiwili ndani ya gari, na tukio la mama beka kumnunulia beka beskeli na kurudi nae nyumbani mida ya jioni ambayo ndio ilikuwa jioni ya mwisho ya yeye kuwa pamoja na mwanawe.

kumbukumbu hizi zika mfanya beka akumbuke tukio la mauji ya wazazi wake.

"beka tumesha fika mwanangu" sauti ya mama abdul ilimtoa beka kwenye wimbi kubwa la kumbukumbu,

"ah kumbe tumefika ahsante mama ...ngoja ni wahi nyumbani" alisema beka kwa kubabaika na kufungua mlango wa gari na kuanza kuondoka,

"haya kesho mwanangu" alisema mama abdul na kuanza kuingiza gari ndani ya geti.

beka akaanza kuhesabu hatua kuelekea kwao huku kumbu kumbu za mauaji ya wazazi zikitawala kichwa chake.

beka alipo fika nyumbani kwao akachungulia dirishani na kumuona mjomba na shangazi yake wakiwa na yona, alimuona mjomba wake akihesabu noti nne nyekundu akimkabidhi yona,

"hii utapeleka kwenye ofisi niliyo kuagiza" beka alimsikia mjomba wake akisema, hapo hapo beka akaingia ndani akiwa na begi lake mgongoni "shikamoo mjomba" beka alisalimia lakini hakuna alie jibu walimuangalia kwa macho ya hasira, beka akamuona yona akiinuka na kuingia chumbani, beka akakaa kwenye kochi na bila kuchelewa akamwambia mjomba wake juu ya swala lake la kufaulu ,

"HAPA HAKUNA ATAKAE KUSOMESHA KAMFUFUE MAMA YAKO AMBAE NI KAFALA AJE AKUSOMESHE" ni maneno ya mjomba wake abdul, hapohapo abdul kuna kitu kilianza kuzunguka kichwani mwake huku kumbu kumbu ya sauti ya yule muuaji alie wauwa wazazi wake ikaanza kumrudia beka akahisi kuitambua sauti ile , 'KAMFUFUE MAMA YAKO AMBAE NI KAFALA' haya maneno yali jirudia rudia mwa beka, kichwa kikaanza kumuuma beka akahisi kizungu zungu, beka akashindwa kuvumilia alihisi muda ule akikaa peke yake angeweza kuikumbuka ile sauti ya muuaji ilikuwa ya nani, beka aliondoka na kuingia chumbani mwake ambapo kulikuwa na mkeka alio kuwa ana lalia pamoja na stuli mbili alizo tumia kusomea usiku , beka akajitupia kama mzigo kwenye ule mkeka huku kumbu kumbu ya ile sauti ya muuaji ikisumbua kichwa chake, "SOME TIME INABIDI KUMGEUZA NDUGU KAFALA KWA FAIDA YA WATU WENGI" haya yalikuwa ni maneno ya muuaji aliyo yasema kipindi ana muua mama beka "KAMFUFUE MAMA YAKO AMBAE NI KAFALA" haya ni maneno ambayo beka kaambiwa na mjomba wake, maneno haya ya mjomba wake na ya muuaji yali jirudia kwa pamoja kwenye kichwa cha beka na sauti zili fanana , kichwa kikawa kina muuma beka huku akihisi kuchanganyikiwa,

mara mlango ukafunguliwa,

"eh we mtoto wa malaya si uli nicheka ukiwa na abdul leo utalia mpaka mama yako atakusikia huko kaburini" alisema yona akiwa kashika mkanda mkono wa kulia na kuanza kumfuata beka alipo lala, beka alimsikia yona na neno 'WE MTOTO WA MALAYA' likasabisha maumivu makubwa kichwani mwa beka, beka alipo taka kugeuka amuangalie yona hapohapo chuma cha mkanda kilitua kichwani mwa beka alicho pigwa na yona, beka kichwa chake kilikua kimesha chafuka , hapo hapo kwa wepesi ambao yona hakuutarajia beka alisimama na kuchukua stuli iliyo kuwa pembeni , yona kabla haja tanabahi stuli ilitua kichwani mwake na yowe kubwa lika sambaa nyumba nzima, , ,

vishindo vikaanza kusikika vikielekea kwenye chumba alicho kuwemo beka na yona....




kipindi beka alivyo ondoka sebuleni akiwa ana sumbuliwa na kichwa , yona alitoka ndani akiwa na mkanda ,

"kamshikishe adabu mi na kwenda kuoga nikimaliza ndio nimuongezee kichapo mpaka ajihisi dunia ina mchukia"alisema mjomba wake beka huku akivua shati na kubaki na pensi, yona akaenda kwenye chumba alimukuwemo beka , mama yona akiwa na baba yona wakieleke bafuni mara walisikia yowe la mtoto wao yona wakaanza kukikimbia kuelekea kwenye chumba alicho kuwemo beka na yona huku mjomba wake beka akiwa kifua wazi ,

yona alivyo pigwa na stuli kichwani yowe lili mtoka akihisi kifo mbele yake akataka ageuke na kukimbia chumbani mule lakini alichelewa kwani alivyo geuka tu na kumpa beka mgongo beka alimuwahi na kushika shati la yona kwa nyuma kisha beka akainua mkono uliokuwa na stuli juu ya kichwa cha yona na kumpiga na stuli ile kichwani kwa nguvu kuzidi alivyo mpiga mara ya kwanza, yona akatoa mguno hafifu na kuanguka kama mzigo.

hakuwa beka tena alikuwa mtu mwingine kabisa, kwani yale matukio mfululizo yali iasili akili ya beka , kwanza kauli ya mjomba wake iliyo sema 'KAMFUFUE MAMA YAKO AMBAE NI KAFALA' halafu na yale maneno ya muuaji 'KUMGEUZA NDUGU KUWA KAFALA YA WATU WENGI' ukijumlisha na kipigo cha chuma cha mkanda alicho pigwa na yona mambo hayo yali sababisha maumivu makubwa kwenye ubongo wa beka.

yona alivyo anguka beka akaziona noti za shilingi elfu kumi kumi zikiwa zimetokeza kwenye mfuko wa shati la yona akiri ya beka ikamtuma kuzichukua na beka akizichuka na kuziweka mfukoni na hapohapo mlango ukafunguliwa akaingia mjomba wake akiwa kifua wazi , beka akamtupia macho mjomba wake alie kuwa kifua wazi na hapo beka kuna kitu alikiona kwenye bega la mjomba wake akiri ya beka ikaanza kufanya kazi kwa kasi isiyo ya kawaida kile kitu alichokiona beka kwenye bega la mjomba wake kiliingiliana na kumbu kumbu za mauaji ya wazazi wake hapo hapo beka kichwa kikaanza kumuuma na kwa mbali akakumbuka ile sauti ya muuaji ' HUYU MALAYA AMENING'ATA BEGANI' nisauti ya muuaji iliyo jirudia kichwani mwa beka , beka akaanza kuona kama ukungu mbele yake,

"wewe umemfanya nini yona" alisema mjomba wake beka baada ya kumuona yona akiwa kalala chini bila kujitikisa , mjomba wake beka akawa anamsogelea abdul kwa hasira, mawazo ya beka yalikuwa mbali mno lakini aliona kama watu wawili walimfuata mbele yake huku sura ya watu hao ikiwa nimoja,

"NI NANI ALIE MUUA MAMA YANGU? ni sauti ya beka iliyo mshitua mjomba wake beka na akabaki kashangaa,

beka alikuwa ana muona mjomba wake kama watu wawili hii ilisababishwa na maumivu yakichwa, mjomba akahisi mambo yanaenda tofauti hakujua ni kwa namna gani beka kadiliki kumuuliza swali hilo, beka alikuwa amesha gundua kuwa lile kovu lililo kuwa kwenye bega la mjomba wake alilo ng'atwa na marehemu mama yake,

"NI WEWE ULIE MUUA MAMA YANGU NA BABA YANGU " beka aliendelea kusema huku kichwa kikiendelea kumuuma, mjomba wake ambae anaitwa EDWARD alibaki ameganda kama sanamu la posta.

"yah na ni wewe jina lako lina anza na herufi 'E' ambayo mama alitakukutaja ukamkaba na mama yangu akashindwa kusema akaishia kusema "E"" beka aliendelea kuongea kwa hisia kali huku kichwa chake kikiwa bado kwenye hali mbaya,

"na vile viatu ulivyo kuwa umevaa siku una fanya mauaji niliwahi kukuona navyo kabla ya tukio ...sauti yako haikuwa ngeni ...umempakaza marehemu mama kashifa ya umalaya na kutengeneza mazingira yalionesha baba ndie alie ua ...wewe ndio ulie muua mama why you killed your sister ...why you killed my mother" abdul alisema kwa sauti ya chini kama ana mnong'oneza mjomba wake.


<<<* * * * *

mama yake na beka na mjomba wake beka walikuwa mtu na dada yake lakini walikuwa hawa pendani tokea utotoni , mama yake beka alifanikiwa kupata elimu ya juu kwani alifika chuo kikuu lakini kaka yake alieitwa edward aliishia darasa la saba kutokana na upeo wake mdogo wa akili,

uadui wa tangu utotoni kati ya mama beka na edward ulidumu mpaka wakiwa wa kubwa, mpaka mama beka anapata mchumba na mpaka anaolewa bado uadui mkubwa kati ya watu hawa ulikuwa una endelea, john alie kuwa mume wa mama beka ambae ni baba beka hakupendezwa na chuki iliokuwa ikiendelea .

john alikuwa mtu wa dini na alithamini sana amani kuliko kitu chochote ikambidi john aanze kuondoa tofauti zilizo kuwepo kati ya edward na mama beka.

john alkuwa mfanya biashara wa madini mkubwa alie julikana kwenye mgodi wa madini geita ulioko jijini mwanza .

john akaamua kuanzisha uhusiano mkubwa na shemeji yake edward ambae mpaka muda huo alikua ameoa na alikua anafanya biashara za kuungaunga, john akawa ana mkaribisha edward mara kadhaa nyumbani kwake lakini edward alikataa kabisa,,,

mama beka nae hakujusumbua kabisa kuji komba kwa edward,.. john akaona njia nzuri ilikua ni kujenga mazoea ya kwenda kumtembele edward nyumbani kwake mara kwa mara,

"mke wangu leo tunaenda kumtembelea kaka yako"alisema john baada ya kunywa chai asubuhi.

"wewe nae kwa kupenda kumbembeleza mtu...yule mi namjua tangu zamani alikuwa hapendi maendeleo yangu tangu nipo shule ya msingi....na saivi amesha ona tumejenga nyumba hii ndo kabisa anazidi kuweka husda... ya nini kubebeleza mtu mwenye wivu wa kijinga " alisema mama beka kwani alijua kisa cha yeye kuchukiana na kaka yake ilikuwa tangu alipokua anamzidi kimasomo wakiwa chekechea.

"ah mke wangu, ukishindwa kumpenda ndugu yako unaemuona huwezi kumpenda mungu ambae huja wahi kumuona au ukristo wako ni wa juu juu" alisema john maneno yenye hekima ,

"haya kwa kua umenipiga andiko tutaenda but yule.. mmh"

siku hiyo walienda mkuyuni ambapo alikuwa amepanga edward ,,,

john alipata nafasi nzuri ambapo aliwakalisha chini chini edward na mama beka na kuwasihi waondoe tofauti zao,

"nyie ni ndugu na wazazi wenu wapo kayenze mbali na hapa mwanza inabidi muishi kwa upendo hivi mtaishi hivi mpaka lini?" alisema john huku akiwatazama usoni. hatimae john alifanikiwa kuwaonganisha ndugu hao walio kuja mjini mwanza kutoka kayenze, edward alikuja kutafuta maisha na mama beka alikuja kwa ajili ya masomo hatimae kupata kanzi na bahati ya kuolewa na tajiri john.


john akawa na uhisiano mkubwa na edward, john akamfungulia duka kubwa shemeji yake edward.

edward akafanikiwa kujenga nyumba kwa msaada wa john ambae ni baba beka...


john alimuamini edward na siku moja john alimuambia edward kuwa kesho yake alikuwa anasafirisha madini mengi ya thamani kwenda kuuza south afrika.. john akawa amefanya kosa kubwa kumuambia edward. kwani edward alikua na hamu ya utajiri mkubwa akawa amepanga kumfanya kitu kibaya john.


ilikua mida ya saa kumi ambapo john edward alikua anaagana na mama beka pamoja na beka mwenyewe na ni muda huo ndipo beka aliviona vile viatu aina ya safari buti alivyo kuwa amevaa edward, john alimwambia edward amsindikize uwanja wa ndege kwa ajili ya kusafirisha madini alio kuwa nayo kwenye begi la mkononi.

john edward pamoja na kijana ambae alikuwa dreva wa gari la john waliondoka na kuanza safari, na mama na beka wakaeleke mjini kwa ajili ya shopping.


john akiwa ndani ya gari alishtukaa kushangaa akiwekewa bastola kichwani na edward na kuambiwa atulie. " dreva simamisha gari" alisema edward. na wakaingia watu watatu ghafla baada ya edward kutoa rock za milango.

john hakuamini kama edward ndie aliekua akimfanyia vile pamoja na wema wote alio mtendea.

" geuza gari tuka waulie nyumbani kwake...no acha kwanza atoe pesa zake zote kwenye akaunt afe akiwa kafirisika" alisema edward.


baada ya masaa mawili gari lilo kuwa na edward pamoja na majambazi alio wakodi lili ingia ndani ya nyumba ya john ambamo wali muua john akafuata mama beka ambae aliuawa kikatiri huku beka akisikia mama yake alivyoteseka. edward baada ya kufanya ukatiri huo wali mwaga risasi kwenye mlango chumba alichokuwemo beka kwania ya kummaliza lakini beka alikuwa kalala chini ambapo hakupatwa na risasi hata moja, waka ishikisha bastola maiti ya john aonekane kajiua mwenyewe, na waka muua yule dereva , edward akachukua kalamu na karatasi akaandika wosia ulio onyesha john ndio kaua mke wake pamoja na dereva wake baada ya kuwafumania , walitaka waingie kwenye chumba cha beka ili wahakikishe kama wamemua beka lakini waka hofia kukutwa na polisi wakaondoka mbio wakiwa na madini .

***hivyo ndivyo mjomba wake beka alivyo waua wazazi wabeka na sasa beka amesha tambua na wapo chumba kimoja***

*****

edward alibaki kasimama akiwaza kumuua beka asije kutoa siri ile akawa ana waza kumuua.

"ni wewe ulie ni ulia wazazi wangu"

"eh ndio nili waua hakuna anaependa kufa maskini... kwanza na wewe unamfuata mama yako utuachie tule mali za wazazi wako" alisema edward huku akimfuata beka kwa hasira.

Edward alikua amesha zamilia kumuua beka na aliona kwake ilikua kazi rahisi kwani beka alikua anamiaka kumi na nne tu! sema alikua na mwili mkubwa kidogo, edward akawa ana msogelea beka amuue kikatiri ,

beka alijua wazi pale kilicho fuata kilikua ni kifo macho ya beka yalikua yamesha poteza mwanga yakawa yana muona edward akija akiwa kwenye moshi huku akiwa haonekani uso vizuri beka akatikisa kichwa chake na kukaza macho yake ili asiuone ukungu ule lakini bado ile hari ilimpa wakati mgumu , beka aliona pale cha muhimu ni kukimbia lakini alipoangalia mlangoni alimuona shangazi yake akiwa amesimama mlangoni na mlango umefungwa na komeo......




Edward alikua amesha zamilia kumuua beka na aliona kwake ilikua kazi rahisi kwani beka alikua anamiaka kumi na nne tu! sema alikua na mwili mkubwa kidogo, edward akawa ana msogelea beka amuue kikatiri , beka alijua wazi pale kilicho fuata kilikua ni kifo macho ya beka yalikua yamesha poteza mwanga yakawa yana muona edward akija akiwa kwenye moshi huku akiwa haonekani uso vizuri beka akatikisa kichwa chake na kukaza macho yake ili asiuone ukungu ule lakini bado ile hari ilimpa wakati mgumu , beka aliona pale cha muhimu ni kukimbia lakini alipoangalia mlangoni alimuona shangazi yake akiwa amejaa mlangoni beka hakutaka kusita kwani kitendo cha yeye kuto kujaribu kuimbia kinge gharimu maisha yake. edward kabla haja mshika beka .. ..beka aliruka hatua moja kubwa na kumtoka mjomba wake beka akaipitia stuli iliyo kuwa chini akaruka hatua nyingine kuelekea mlangoni alipokuwa shangazi yake. "mzuie asitoke huyo mshezi" edward alipaza sauti kumuambia mke wake lakini alisha chelewa kwani beka alikuwa amesha mfikia mke wa edward na hapohapo beka akamtwanga stuli ya uso mke wa edward akatoa yowe kubwa, beka akageuka haraka nyuma yake na kumuona edward akija kwa kasi pale alipokuwa beka , kwa kasi aliyo kuwa nayo edward kamwe beka asinge weza kufungua mlango na kukikimbia lazima edward angemfikia na kumkamata... beka akajirusha pembeni huku akitupa stuli kuelekea kule alipokua akija edward......


**kipindi yote hayo yanatokea joyce mtoto wa edward hakuwepo alikua ameenda twisheni na hata peter pia nae hakuwepo, siku hiyo joyce alichelewa sana kurudi nyumbani alikua kwa marafiki zake , alipofika tu nyumbani ndio akasikia balaa lilio kua linaendelea alisogea mpaka karibu na mlango akawa ana sikiliza yaliyo kuwa yakiongelewa ndani kati ya beka na edward na ndipo joyce alimsikia baba yake akisema "eeh ni mimi nilie wuua hakuna mtu anae kubali kufa maskini ...na wewe utamfuata mama yako" joyce alishtuka sana kusikia baba yake ndie alie muua wazazi wa beka. ni kweli walikuwa wanamtesa beka na kumnyanyasa lakini wao walijua mama yake beka aliuliwa na baba beka kwa sababu ya umalaya, swala la kusikia edward ambae ni baba yake kuwa ndie aliewaua wazazi wa beka lili mshtua joyce akahisi kama donge kubwa lime mkwama kohoni, akiwa katika hali ile ndipo alipo sikia mama yake akitokwa na yowe na akasikia zile purukushani na vishindo ndani ya chumba joyce akaenda kwenye mlango ili afungue lakini mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani akajaribu kwa nguvu zake lakini haku fanikiwa kuvunja mrango ikabidi atoke mbio akaite majirani waje watoe msaada , lakini alivyotoka tu akakutana na kaka yake alie itwa peter joyce akamwambia peter kuwa kuna balaa nyumbani joyce na peter wakaanza kukimbia kuelekea kwenye chumba alicho kuwemo beka na mama na baba yao.


*********


stuli alio ilusha beka ilimkuta edward usoni edward akapata maumivu usoni na kupoteza mwelekeo mikono ya edward ikawa usoni mwa edward akiugulia maumivu beka haku laza damu aliinuka pale alipo jitupa akachukua stuli nyinge akaishika kwa mikono miwili beka akamrukia edward stuli ikiwa mkononi beka akawa kama ameruka juu kidogo kupita urefu wa edward kisha beka akashusha stuli juu ya kichwa cha edward alie kuwa bado kashika uso wake kwa maumivu, beka na edward waka piga mweleka chini kama mizigo huku edward akitoa yowe lenye sauti hafifu huku akitaka kuamka pale chini, beka kwa haraka akachukua kipande cha mbao (mguu wa stuli) kilicho toka kwenye stuli aliyo mpigia edward, beka akampiga nacho kichwani edward aliekua akitaka kuinuka kipigo kile kili mrudisha edward chini ,beka akampiga tena edward kichwani edward akatulia , mambo yote beka alikua akiyafanya alikua kama kachanganyikiwa kitendo chakujua kuwa mjomba wake ndie aliemwaga damu ya wazazi wake kilimfanya beka awe kama mwendawazimu na akili ya beka ilikua imemtuma amuue edward, beka akachukua ule mkanda aliokuja nao yona beka akamuinua mjomba waka na kumkalisha kisha akazungusha ule mkanda shingoni mwa edward na kuanza kumniga na mkanda ule beka akiwa nyuma ya mgongo wa edward aliekua amekaa huku beka akiwa kapiga goti moja chini nyuma ya mgongo wa edward. "ulimua mama yangu kwa risasi.... leo mimi nakuua kwa mkanda wa mtoto wako yona ulio nunua mwenyewe" beka alisema karibu kabisa na sikio la edward, edward alifulukuta lakini vile vipigo viwili vya stuli vilikua vime mmaliza nguvu , edward akafurukuta huku akirusha mikono yake nyuma ili ampige beka lakini haikusaidia kitu edward macho yakamtoka akamuona islael akijianda kuchukua uhai wake edward akaanza kusaga miguu chini, muda wote huo walikuwa wame upa mgongo mlango. "pumbavu .......kufa ...ukajibu ukajibu mashitaka kwa mama" aliseme beka huku akiendelea kukanza mkanda kwa nguvu kwenye shingo ya edward, , ,puuh ghafla mlango ulipigwa ukafunguka na kumpipa beka mgongoni ambae alisukumwa na mlango ule, beka alishituka akahisi itakuwa majirani beka akiinua uso na ndipo aka muona peter , peter na joyce walikuwa wamevunja mlango na kuingia ndani peter akapigwa butwaa kwa hali alioikuta kwani yona na mama yake pamoja na baba yake walikua chini huku baba yake akikohoa na mbele yake alikuwa anatazamana na beka aliekuwa amelowa kwa jasho na macho ya beka yalikuwa yame geuka rangi na kuwa mekundu, "we.. umewafanya ni wazazi . . wangu? " aliuliza peter kwa kigugumizi huku akiwa na woga na akiwa kachanganyikiwa kwa hali alio ikuta. " mmejileta leo .,ni siku ya kumaliza kizazi cha nyoka ." alisema beka kwa sauti ya kukwaluza huku akiangalia mguu wa stuli ulio kuwa mbele yake na wakati huo akimtazama peter usoni . "peter tukimbie atatuua"alisema joyce hukuakiangalia mlango, peter aligeuka na kumuangalia dada yake lakini kitendo chayeye kugeuka kilimrahishia beka kazi "peter unapigwaaaa" joyce alipiga kelele kumtahadharisha peter kwani alimuona beka akiogota mguu wa stuli na kumfuata peter, peter kelele za joyce zilimbabaisha akawa anataka kugeuka kule alipokuwepo beka lakini hapo hapo alipigwa na mguu wa stuli kichwani peter akahisi maumivu na akiri zake zikamwambia kifo kilikuwa kipo njiani kinaifuata roho yake , peter akaona asipo jitetea pale yanaweza kumkuta mengine beka alivyo inua mguu wa stuli ampige tena peter hapohapo peter akamvaa beka peter akiwa kajikunja kutokea kiunoni halafu bega lake moja likawa kwenye tumbo la beka na kichwa chake kikawa kwenye ubavu wakulia wa beka na mikono ya peter akawa imekutana kwenye mgongo wa beka kwa mtindo wa kukumbatia hapo peter akawa kammiliki beka na kuanza kumsukuma beka kurudi kinyumenyume nia ya peter ilikuwa ni kumbwaga chini beka. beka alihamaki kwani hakutegemea kitu kile kutoka kwa peter beka akajua kama ange angushwa chini na peter basi angekuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha , peter alicho kosea nikwamba alikua kaicha mikono ya beka ikiwa huru kama peter angekuwa ameibana mikono ya beka basi beka angekuwa hana la kufanya .., kipindi peter anaendelea kumsukuma beka beka aliangalia kichwa cha peter na hapo beka akaona kulikuwa kuna uwezokano wa kumkaba peter ,beka akashusha mkono wake mpaka kwenye kichwa cha peter na kuuzungusha chini mkono wa beka ukawa chini kidogo ya kidevu cha peter beka akawa amemkaba peter ambae aliacha kumsukuma na kuanza kuangaika kuitoa roba ya beka peter alihangaika kuitoa ile roba lakini ilikuwa ni ngumu kutoka kwani mwili wake wote ulikuwa umeinama na akashindwa njisi ya kutoka kwenye mikono ya beka ,"leo ni siku ya kumaliza kizazi cha nyoka.... mtatoka humu ndani mkiwa maiti " alisema beka huku akikema kwani alikuwa ametumia nguvu zake kwa kumkaba peter ,peter akawa anarusha mikono hewani ili ampige beka lakini ilikuwa ni kazi bure peter akawa hana ujanja mwigine . joyce aliendelea kusimama huku akishindwa amsaidie vipi kaka yake peter na sehemu kubwa ya mwili wa joyce ulitawaliwa na woga ,"baba ...msaidie kaka" alsima joyce baada ya kumuona baba yake akiianza kuinuka . " ..,ngoja nije nimtwange risasi..." alisema edward huku akianza kuondoka kwa kusunta . beka alimsikia na kumuona edward akianza kuondoka , beka akajua wazi edward alikuwa anaendea bastola chumbani mwake, beka akajua wazi edward akishika bastola ni kifo tu, beka akamuachia peter beka akarudi nyuma hatua moja na kwa hara viganja vya beka vikaifumbata shingo ya peter kwa nyuma na hapohapo beka akainua kwa nguvu goti lake na kupiga kwa nguvu kifuti ambacho kilimpata peter kwenye paji la uso wake ,kelele nyingi zikamtoka peter kitendo hiki kili fanyika ndani ya sekunde tatu ..."tukimbimbie mwanangu nikachukue bastola" alisima edward huku akiwa wa kwanza kuanza kutoka kwenye chumba kile. beka muda huohuo akamuachia peter ambae alikuwa ana ugulia maumivu akiwa anaona nyotanyota na aliona Kile chumba kikizunguka, beka akamuacha peter na kuruka hatua moja kubwa na kufikia mlangoni ambapo alimkuta joyce ambae alihamanika beka akamshika joyce kichwani na kubamiza paji la uso wa joyce kwenye ukuta na kumuacha akiangauka na kupoteza fahamu , edward akiwa anakaribia chumba chake ili akachukue bastola ndipo akamuona beka akitoka akiwa na mguu wa stuli mkononi mwake na akimfuata kwa kasi edward alijua hawezi kuingia ndani na kufanikiwa kuchukua bastola ni lazima beka angemfikia edward aliona kukimbia ndio ilikuwa njia pekee, edward hakuwahi kuwaza hata siku moja kuwa angekuja kukibizwa na beka lakini leo mambo yalikuwa yamemuendea vibaya edward akaanza kukimbia huku akihisi kizunguzungu ,beka nae alipoona edward anakimbia nae akaongeza mbio ili amfikie na kutimiza azima yake beka alikuwa amekusudia kuua, edward alifanikiwa kufungua mlango wa nje na akaanza kukimbia huku akipiga kele kuwaita majirani edward akawa anakimbia ili avuke barabara na atafute nyumba ya jirani ambamo alihisi angepata msaada ,edward alikimbia na alipokaribia kwenye barabara aligeuka nyuma na kumuona beka kama hatua stini edward akavuka barabara kwa haraka na kuingia mtaa wapili, beka alivyo muona edward amevuka barabara na alikuwa ameanza kutokomea beka aliongeza mwendo akiwa ana wahi nae avuke barabara beka alivyo karibia akaongeza mwendo kwani alishahisi anaweza kuachwa na mjomba wake . beka akaingia barabarani lakini kabla haja vuka akapigwa na kitu kikubwa akatupwa hewani ........



kosa alilo lifanya beka nikuingia kwenye barabara bila kuangalia kushoto na kulia beka wakati anakatiza barabara kulikuwa na gari linakuja mwendo kasi na dreva ghafla alimuona beka kama hatua nane dreva alijitahidi kufunga brek lakini alikuwa kaisha mfikia beka na hapohapo gari lilimgonga beka na kumtupa pembeni kama hatua nne kutoka gari lilipokuwa beka akapiga kichwa chini na hapohapo hakujitikisa kana kwamba alikuwa hakimbii dakika kadhaa zilizopita beka akawa katulia dreva alipigwa na butwaa pamoja na woga na akajua tayari amekwisha ua dereva aliangalia eneo lote lilikuwa kimya akawasha gari na kuanza kuondoka kipindi anaanza kuondoka taa za gari lake zili mmulika pale beka alipo angukia beka na ndipo aligundua alikuwa ni kijana ambae hajafikisha miaka kumi na nane na kingine beka alikuwa ana tokwa na damu nyingi , yule dreva aliekuwa baba wamakamo aliona kama angemuacha pale beka na hari ile ingekuwa ni uaji kwani pale kulikuwa na uwezekano mkubwa wa beka kutogundulika na wananchi kuwa alikuwa eneo lile angeweza kuwa pale hadi asubuhi na hii ingepelekea kifo cha beka , dreva akaangalia hakuona mtu eneo lile dreva akashuka akatembea mpaka pale alipokuwepo beka na kumbeba huku akiendelea kuvuja damu dreva akamlaza beka kwenye viti vya nyuma ya gari kisha dreva akafunga milango na kuondoa gari kwa kasi na kushika barabara inayo elekea mjini dreva akaendesha mpaka kituo cha polisi mabatini kilichopo pembeni kidogo na barabara kubwa inayo elekea mjini ,hapo kituoni alimkuta afande alie julikana kama hussen dreva akatoa taarifa kituoni na ambapo alisema amemkuta barabarani kapata ajali na alie mgonga kakimbia uongo wa dreva ukafanikiwa akapewa P.F3 na kuanza safari ya kuelekea bugando hosptal kubwa ya mwanza, dreva aliendesha gari kwa kasi muda mchache gari likaacha barabara ya mjini na kukata kona ya agakhani na kushika barabara ya bugando dakika chache zilizofuatwa beka alikuwa juu ya kitanda chenye magurudumu akipelekwa kwenye chumba cha matibabu daktari alipoagalia hari ya beka ilikuwa mbaya sana damu nyingi zilimtoka na alikuwa hana fahamu hata kidogo na mwili wake ulikuwa wa baridi A na B yalikuwa nimajibu yanayo weza kuwa jibu mojawapo kwa beka yani kifo na uzima kwa beka huku uwezekano wa kifo kuchukuwa maisha ya beka ulikuwa wazi machoni pa madaktar.


************


edward alivyo vuka barabara hakugeuka nyuma na wala hakujua kama beka aligongwa na gari yeye edward muda wote alijua anafukuzwa nyuma na beka edward kipindi anakimbia aliona nyumba moja iliokuwa mlango wazi hapo edward akawa kaona msaada wa maisha yake edward akaingia moja kwa moja hadi ndani ambapo alikuta familia ya nyumba ile ikiwa inapata chakula cha jioni wale watu walikuwemo ndani walishituka kumuona edward akiingia bila hodi na kufunga mlango baadhi ya watoto ndani ya nyumba hiyo waliamka na kukimbia,

"jamani msikimbie....kuna mtu anataka kuniua...." alisema edward huku akitweta, mwenye nyumba akapigwa na butwaa akajua kama edward alikuwa ana kimbizwa na majambazi basi alikuwa amewaletea zakhama, "nenda kituo cha polisi ...kwani wapo wangapi usituletee matatizo" alisema mwenye nyumba huku akiwa na wasiwasi ,

"sio majambazi ..,ni mpwa wangu mtoto wa marehemu dada anataka kuniua beka? jamani twendeni mkasaidie familia yangu"

"mpwa wako beka!?"

"eh huyo huyo anataka kuniua" kila mtu mule ndani alipigwa na butwaa kwani hakuna aliekuwa hamjui kuwa edward ni mjomba wa beka na hakuna asie jua kuwa beka ni yatima na alikuwa ananyanyasika na kuteswa kila siku na mjomba wake, hakuna alie amini kuwa edward ni mzima wa akiri kwani walimjua beka alikuwa kijana wa miaka kumi na nne ingewezekana vipi edward akimbizwe na beka.

"we sio mzima...ila maralia acha tuka muite mke wako akupeleke hospital" alisema mwenye nyumba huyo ,

"ebwana mi sio chizi mi nina akiri zangu naomba mkaisaidie familia yangu" alisema edward akiwa kama analia, ilikuwa kazi kubwa kwa yule mwenye nyumba kuamini maneno ya edward hakuamini hata kidogo na muda huo wapangaji walikuwa karibu na nyumba ile walianza kusogea kwenye nyumba ile kwani walimsikia edward akilalimika, wapangaji waka gonga mlango na kuuliza kama kulikuwa na usalama lakini edward akawaeleza balaa alilo liamsha beka, "mmh beka huyu huyu mpwa wako ?" kila mpangaji alisema maneno hayo kwa wakati tofauti, edward aliendelea kutilia mkazo huku akiwa hasemi sababu ya beka kuamsha balaa lile. mwishowe wakaafikiana kuwa waende wakahakikishe alicho kisema edward wakaanza kuifuata njia kuelekea nyumbani kwa edward,

"jamani mbona hapa kuna damu..nini tena"alisema mmoja kati ya wale majirani waliokuwa wanaelekea kwa edward ilikuwa ni pale ambapo beka aligogwa na gari kisha kutupwa pembeni, "asije akawa kamchinja mwanangu"alisema edward huku akilia baada ya kuona zile damu .

"jamani tuwahi isije ikawa kweli anayo yasema jamaa" alisema yule mwenye nyumba kwa hamaki na muda huo wakaanza kuelekea haraharaka kwenye nyumba ya edward.

kila mtu hakuamini eti kuwa ni beka peke yake alie angusha chini familia ya edward . walikuta yona akiwa amelala pembeni ya mlango huku mchiririzi mkubwa wa damu ukitokea kwenye kichwa cha yona chini alie lala bila kujitikisa pale chini, peter nae alikuwa ukutani kabisa akipumua kwa shinda akihisi dunia ikizungaka na kuna wakati alijaribu kuinuka lakini kizungu zungu kilimshindana nae na kumrudisha chini joyce nae alikuwa kapoteza fahamu kwa mshtuko huku akiwa na kidondo kwenye paji la uso wake ,mama yona nae alikuwa pembeni ya mlango akiwa hana fahamu hata moja . chumba kilikuwa kinatisha edward akawa analia huku akimtikisa mke wake ,

"ebwana tufanye mpango tuwawaishe hosptal ....acha mi nikachukwe tax" alisema mmoja wa wale jirani

"oya nenda kituoni ili uje na tax tatu tuwapeleke kwa pamoja"alisema baba wa makamu.


muda mchache yule aliendea tax alifika akiwa ndani ya tax huku akifuatwa nyuma na tax mbili akashuka na kuanza kusaidiana na majirani kuingiza majeruhi ndani ya gari muda wote edward alikuwa ana mlilia mke wake aliepoteza fahamu walianza kumbeba yona lakini walivyo mshika na kumuinua yona majirani wakaangaliana! yona alikuwa wa baridi kama barafu na hii ilimaanisha kuwa mwili wa yona ulikuwa umetengana na roho majirani hawakutaka kumuambia edward taarifa zile mbaya zile stuli mbili alizo pigwa na beka zilitosha kuya chukua maisha ya yona , wakamuweka yona ndani ya gari moja kisha wakafuata pale alipokuwa joyce wakamuinua lakini walivyo mbeba akawa kazinduka wakamuambia atulie anapelekwa hospital wakasaidiana kumuingiza peter na mama yona ambae alikalishwa seat moja na edward , msafara wa magari matatu ukaanza safari ya kuokoa familia ya edward

gari zikaelekea mpaka kituo cha polisi mabatini ambapo kama nusu saa iliyopita beka alipitishwa hapo akiwa hajitambui,

"he leo mbona ajali zimefuatana mda mchache uliopita kuna kijana kapitishwa hapa na hari mbaya.... eh nanyie ajari yenu mmeipatia wapi ?" aliuliza afande hussen ambae siku hiyo alikuwa na kazi maalumu.

"ah afande kuna mpwa wangu ...ametushambulia na kutoweka samahani afande tupatie PF3 ni wawaishe hosptal wana hari mbaya" alisema edward.

"so unataka kuniambia amefanya tukio hili bila sababu yoyote?"aliuliza hussen akiwa na mashaka ..

"ndio afande itakuwa makundi na bangi ndio vime mshauri afanye hivyo"

"sawa tuna kupa PF3 lakini kesho asubuhi unatakiwa uriport ili utoe maelezo zaidi maana ni tatizo kubwa ok?"

"sawa afande hakuna tatizo " alisema edward . wakapatiwa PF3 na wakaingia kwenye gari na kuanza kuendesha kwa speed kuelekea bugando na muda mchache wakawa wamefika geti la bugando na wakapokelewa na walinzi.


*****


upande wa beka


madaktari waliona hari ya beka ilikuwa mbaya sana ikabidi apelekwe ghorofa ya nane chumba C118 madakatari wakaanza kumpatia huduma muhimu beka za kwanza na kwa kuwa alikuwa ametokwa na damu nyingi ikabidi awekewe dripu ya damu na madaktari waligundua alikuwa anahema kwa tabu sana wakaleta mashine ya kumsaidia kupumua beka akawa katika hari iliyo tazamiwa majibu mawili kutokea huku jibu moja ambalo ni baya likichukwa nafasi kubwa kutazamiwa.


****upande edward .


edward na majirani pamoja na wauguzi walipo kuwa wanashusha familia ya edward ,.." huyu mmoja hayupo tena amesha kufa" alisema muuguzi mmoja baada ya kumshika yona bila kujua baba wa mtoto huyo alikuwa ndie edward

"ninii?" aliropoka edward huku akishika kichwa na kuanza kulia bila kujali walio mbembeleza na joyce nae aliekuwa na fahamu aliangusha kilio kikubwa ikawa hamna kuskilizana..

"we kaka,.unataka na hawa wengine wafe..unaacha kuwawaisha hawa wazima kwenye matibabu unakaa kulia kama mwanamke!"alisema yule nesi huku akifyonza na kuanza kusukuma kitanda chenye magurudumu kilichokuwa kime mbeba peter akaanza kuelekea ndani na huku nyuma wakaafuata edward na majirani wakisukuma kitanda kilicho mbeba mama yona ,na baadhi ya majirani wakimbembeleza joyce aliekuwa analia, wakaingia kwenye lifti na kuekekea juu majirani wengine waliambiwa watumie ngazi ambako wangekutana ghorofa ya nane. muda mchache badae peter na mama yona wakapokelewa na madaktari muda wote joyce alikuwa analia kwa kwikwi joyce akaoneshwa sehemu ya kukaa akakaa na kuendelea kumlilia kaka yake yona, mama beka akapelelwa kwenye wodi yakike na peter akapelekwa chumba C114! haya beka kalazwa ghorofa ya nane chumba C118 na peter ghorofa hiyohiyo chumba C114 ,beka na peter wametenganishwa na vyumba vitatu tu! na edward yupo ghorofa hilohilo .

edward akawa kwenye wodi alimo peter mda wote edward alikuwa alikuwa akitembea huku na huku akiwa na machungu kitu ambacho hakujua ni kwamba beka nae alikuwa kalazwa chumba cha nne kutoka chumba alicho lazwa peter ,edawar alikuwa na hasIra na beka na alitamani akimuona popote amuue.................




edward akawa anatembea tembea mwishowe akaamua kukaa kwenye kitanda alicho lazwa mtoto wake alipokaa akamkumbuka mwanae yona edward akakumbuka niyeye aliemtuma yona akamshikishe adabu beka lakini mambo yaligeuka na hatimae yona kapoteza maisha kwa kupigwa na stuli mara mbili kichwani edward alilia sana usiku ule ni yeye aliemponza mwanawe, edward akazidisha hasira kwa beka usiku huo edward haku lala kabisa ila badae yeye na mwanawe joyce waliwekewa dawa kwenye majeraha yao madogo joyce akawa amewekewa plasta kwenye paji la uso wake na edward bandeji kwenye utosi.


asubuhi ilipofika edward akaelekea mochwari ilipokuwa maiti ya mwanawe akauliza taratibu zote za kuchukua mwili wa mtoto wake baada ya kupata maelekezo akaondoka kwenda nyumbani kwake nyakato ili akatowe taarifa ile kwa majirani lakini akiwa njiani alikumbuka kuwa aliambiwa ariport kituo cha polisi kwa ajili ya maelezo zaidi ,ikambidi aende huku akitunga uongo ambao atausema kituoni, edward akafika na baada ya salamu na kumkumbusha polisi aliemkuta jana yule pOLISI afande hussen akachukua karamu na jarada akamuambia edward aanze kueleza.

"sisi tulikuwa tumekaa sebuleni mara huyo beka akaingia ndani bila hata salamu akapitiliza chumbani mwake ...mimi nikamtuma marehemu mwanangu yona akamuulize beka nikipi kime msibu yona akaenda chumbani alimukuwa beka... na mara tukasikia yona akipiga yowe, ikabidi na sisi tuende tuelekee chumbani mule tulivyo ingia beka akatushambulia kwa ghafla" edward alimaliza kusema uongo wake. yalifuata maswali mengine machache ambayo edward aliya jibu kwa uongo mwingi.

"ana miaka kumi na nne tu...ila alikuwa ameshaanza kuvuta bangi....makundi yamemuaribu" alimaliza edward.

"sawa we nenda ukafanye mpango wamazishi ila unatakiwa kutuletea picha ya huyo beka ili aanzwe kusakwa na jeshi la polisi" alisema hussen edward akakubali na kuondoka kuelekea nyumbani.

edward alipofika nyumbani alitoa taarifa ya kifo cha mwanawe majirani wakampa pole na kuanza kuwa nae pamoja kwa kila jambo, , , muda kidogo edward akaanza kurudi bugando akiwa na wababa saba kwaajili ya mikakati ya kuuchukua mwili wa yona.


*****


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

BLOG